8
Programu ya Panda Miti Kibiashara inatekelezwa kwa pamoja na Serikali ya Tanzania na Serikali ya Finland Panda Miti Kibiashara Toleo No. 2 Februari, 2015

Panda Miti Kibiashara

  • Upload
    others

  • View
    10

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Panda Miti Kibiashara

Programu ya Panda Miti Kibiashara inatekelezwa kwa pamoja na Serikali ya Tanzania na Serikali ya Finland

Panda Miti Kibiashara

Toleo No. 2 Februari, 2015

Page 2: Panda Miti Kibiashara

Wapendwa msomaji,

Ninayo furaha kukuletea Toleo hili la Jarida la Panda Miti Kibiashara ambalo limesheni habari za uandaaji wa mashamba ya kupanda miti na shughuli za upandaji miti katika vijiji 11 vya majaribio vinavyopatiwa msaada na Programu ya Panda Miti Kibiashara (PFP).

Shughuli za kupanda miti zinaendelea vizuri, na jambo la kutia moyo ni kuona kuwa Vikundi vya Wakulima wa Miti vimekuwa kitovu cha mafanikio ya shughuli zinazoendeshwa kwa Msaada wa Programu ya Panda Miti Kibiashara kama ilivyotarajiwa. Nimevutiwa na jinsi wakulima wa miti wanavyotekeleza shughuli za kupanda miti kwa kufuata vigezo vya kitaalam vilivyowekwa na PFP.

Vilevile wakulima wa miti wamezingatia ipasavyo utekelezaj wa miradi midogo ya kuwaongezea kipato wakati wakisubiri miti ikue (IGA). Pia wakulima wa miti wametekeleza kwa hiyari kilimo cha maharage na parachichi ili kujiongeza kipato (IGA).

Upandaji miti unaendelea vyema, na ni matumaini yangu kuwa lengo la kupanda hekta 1,000 katika msimu huu litafikiwa, na kuwa katika msimu ujao tutaweza kuandaa mipango yetu kwa ufanisi zaidi kutokana na uzoefu utakaopatikana.

PANDA MITI KIBIASHARA

Sangito SumariMeneja wa Mashamba

Panda Miti Kibiashara2

Uzinduzi Rasmi wa Programu ya Panda Miti Kibiashara waashiria Mafanikio Siku Zijazo

Yaliyomo

3

SERA YA UHARIRIMadhumuni ya Jarida la PANDA MITI KIBIASHARA ni(i) Kuhabarisha na kuelimisha kuhusu masuala yanayohusu Programu ya Panda Miti Kibiashara.(ii) Kuwa Jukwaa la mawasiliano kwa wadau wa Programu ya Panda Miti Kibiashara.(iii) Kufafanua mipango na utekelezaji wa Programu ya Panda Miti Kibiashara.

WAHARIRI:George MatikoLillian Mrema

Hutolewa na:Programu ya PANDA MITI KIBIASHARAS. L. P. 1060, Njombe Email: [email protected]: www.pandamiti.or.tz

UJUMBE KUTOKA KWA MENEJA WA MASHAMBA

PFP yasaidia Vijiji vya Majaribio4Uandaaji mashamba na Upandi miti Unaaendelea Vema5Wajumbe wa Kamati Elekezi ya PFP Washuhudia Miti Ikipandwa6Mkuu wa Mkoa wa Njombe Ahimiza Panda Miti Kibiashara7Habari Katika Picha8

Page 3: Panda Miti Kibiashara

Panda Miti Kibiashara 3

Wakulima wa Miti katika Nyanda za Juu Kusini wame-

pongezwa kwa utamaduni wao wa kupanda miti na wametakiwa kuifanya shu-ghuli hiyo kuwa ya kibiasha-ra. Ili upandaji miti uwe wa mafanikio, wakulima wa miti wanashauriwa kuunda Vi-kundi vya Wakulima wa miti (TGAs). Kwa njia hiyo Progra-mu ya Panda Miti Kibiashara (PFP) itaweza kuwafikia na kuwapa misaada kupitia vi-kundi hivyo. Ushauri huo wa kuunda vi-kundi ulitolewa na wageni rasmi walioshiriki katika uzinduzi rasmi wa PFP uli-ofanyika Njombe tarehe 5, Novemba 2015. Uzinduzi huo uliongozwa kwa pamoja na Naibu Waziri wa Wizara ya Mali Asili na Utalii, Mhe. Mahmoud Hassan Mgim-wa na mwakilishi wa Balozi

wa Finland Bw. Mikko Lep-panen. Kwa ufadhili wa Serkali ya Finland mradi wa Panda Miti Kibiashara unayo nia ya ku-wapatia msaada wakulima vijijini ili kuinua kipato chao kwa kupanda miti kibiashara.

aliainisha miradi ambayo il-itekelezwa na serikali kwa misaada iliyotoka Finland kuwa ni pamoja na: Miradi ya Misitu ya Hifadhi, Taasisi za Mafunzo, Kuandaa Sera ya Taifa ya Misitu, Kuandaa na kutekeleza Programu ya Taifa ya Misitu na Nyuki na Mradi wa Tathmini ya Rasli-mali Misitu (NAFORMA).Mwakilishi wa Balozi wa Finland Bw Leppanen ali-wapongeza wakulima wa miti wote katika eneo la mradi wa Panda Miti Kibi-ashara kwa kuunda vikundi vya upandaji miti mwanzoni kabisa mwa PFP. Alisema ‘Programu ya Panda Miti Kibiashara itatoa misaada kwa wepesi zaidi kupitia vi-kundi hivyo’. Vilevile Bw Lep-panen alisisitiza kuwa Fin-land imedhamiria kwa dhati kuendelea kuisaidia sekta ya misitu, Tanzania.

Uzinduzi Rasmi wa Programu ya Panda Miti Kibiashara Waashiria Mafanikio Siku Zijazo

Mwakilishi wa Balozi wa Finland Bw. Mikko Leppanen na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mgimwa wakizindua kwa pamoja Programu ya Panda Miti Kibiashara.

Katibu Mkuu , Wizara ya Maliasili na Utalii, wa wakati huo, Bibi Maimuna Tarishi pamoja na mwakilishi wa Balozi Bw Mikko Leppanen (katikati) wakiwa kwenye picha ya pamoja kuonyesha mshikamano kati ya Finland na Tanzania.

Wanafunzi ni kati ya watu waliohudhuria kwenye uzinduzi wa Panda Miti Kibiashara uliofanyika

tarehe 5 Novemba, 2014.

Naibu Waziri alitumia fursa hiyo kuishukuru serkali ya Finland kwa kuendelea kui-saidia sekta ya misitu kwa zaidi ya miaka 40.Naibu Waziri Mgimwa

Page 4: Panda Miti Kibiashara

Panda Miti Kibiashara4

PFP YasaidiaVijiji vya MajaribioProgramu ya Panda Miti Kibiashara

imeanza shughuli zake kwa kuvisaidia vijiji 11 vya majaribio

moani Njombe. Mafanikio yatakayotokana na msaada huo yatawezesha mipango ya baadaye ya Panda Miti Kibiashara kutekelezwa kirahisi.Vijiji hivyo ni Usagatikwa kilichoko wilayani Makete, Mavanga na Lusala vilivyoko wilayani Ludewa. Vingine ni Ngalanga, Mgala, Kifanya, Ng’elamo na Iboya katika wilaya ya Njombe Mji. Vilevile, katika Wilaya ya Njombe Vijijini vijiji vya majaribio ni Ikang’asi, Matembwe na Itambo. Vijiji hivyo vilichaguliwa kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo:• Kijijikuwanakiwangochamvuacha

mm 1000 au zaidi kwa mwaka,• Kijiji kuwa na Mpango Endelevu wa

Matumizi ya Ardhi (VLUP),• Wanufaikaji wa Programu

wanapaswa kujiunga na Kikundi cha Wakulima wa Miti (TGA),

• Kijiji kiwe na ardhi ya kutosha yakupanda miti.

Programu imeweka utaratibu wa kuzingatiwa ili wakulima wa miti waweze kupata misaada. Kwanza Programu huwataka wanachama wa Vikundi vya Wakulima wa Miti kutuma maombi ofisini PFP. Baada ya kupokelewa maombi hayo huchambuliwa na uteuzi kufanyika kwa kushirikiana na Halmashauri za Wilaya. Kisha waombaji wote huarifiwa juu ya matokeo ya maombi yao. Waombaji wanaofanikiwa huambiwa kuingia mikataba kati yao na Programu ya Panda Miti Kibiashara. Katika mikataba hiyo inasisitizwa kuwa hakuna pesa taslimu itakayotolewa. Kinachotolewa ni misaada ya hali na mali tu. Vilevile kutokana na ufinyu wa bajeti, Programu ya Panda Miti Kibiashara haiwezi kumpatia msaada kila mwombaji.

Baadhi ya waombaji ambao wanastahili kuomba msaada ni Watu binafsi, Kaya, wafanya biashara wadogo na wakubwa, Taasisi za umma, Taasisi za Elimu, naAsasi za jamii (CBO).Ingawaje Panda Miti Kibiashara kwa sasa inatoa misaada kwa vijiji vya majaribio, eneo lake kijiografia linahusisha mikoa mitatu ya Njombe, Iringa na Morogoro. Wilaya husika katika mikoa iliyotajwa ni : Mkoa wa Njombe (Ludewa, Makete na Njombe), Mkoa wa Morogoro (Kilombero) na Mkoa wa Iringa (Mufindi na Kilolo). Imeonekana kuwa vijiji vingi vya Nyanda za Juu Kusini vinakidhi vigezo vya kuweza kusaidiwa. Hali hiyo inaashiria uwepo wa vijiji zaidi kupewa msaada katika msimu ujao.

Wanachama wa TGA ya Ngalanga wakiwa katika mkutano

Wanachama wa TGA ya Mavanga wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutayarisha shamba la kupanda miti

Page 5: Panda Miti Kibiashara

Panda Miti Kibiashara 5

Uandaaji mashamba na Upandi Miti Unaendelea Vema

Wakulima wa Miti katika vijiji vya majaribio wamedhamiria kukamilisha shughuli za kupanda

miti ifikapo mwisho wa mwezi Februari 2015. Huo ndio msimamo uliotolewa na viongozi wa Vikundi vya Wakulima wa Miti (TGA) katika vijiji vya majaribio. Aidha viongozi wa makao makuu ya Panda Miti Kibiashara, Juhani Pekkala na Gerge Matiko wamethibitisha msimamo huo wa viongozi wa vikundi kuwa sahihi walipofanya ziara vijijini. Vijiji vya majaribio vilivyotembelewa mwezi Januari 2015 ni vijiji vya: Ng’elamo, Kifanya, Mgala, Usagatikwa na Ikang’asi. Vijiji vingine ni Itambo, Lusala, Mavanga, Iboya na Ngalanga. Ilivyoonekana ni kuwa vijiji vingi vimetenga meneo ya pamoja kwa ajili ya miti kibiashara ambapo kila mwana kikundi anamiliki shamba lake binafsi mahali hapo. Ni vijiji viwili tu vya Lusala na Ngalanga ambako maeneo ya kupanda miti hayakutengwa eneo moja. Maeneo hayo yamesambaa vijijini kufuatana na Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi (VNUP).Aidha, wakulima wa miti waliwasihi viongozi wa Panda Miti Kibiashara waliotembelea vijiji vya majaribio, kuzishawishi Halmashauri kuwapatia wakulima hao hati miliki ya ardhi ili kuwa na uhakika wa umilki wa mashamba yao ya miti kisheria.

Uchunguzi uliofanyika wakati wa ufuatiliaji umeonyesha kuwa vijiji vyote vya mfano vimefikia vigezo vilivyowekwa na Panda Miti Kibiashara. Kwa mfano wakulima wote waliopewa msaada ni wanachama wa vikundi vya Panda Miti Kibiahara. Ni dhahiri kuwa vikundi hivyo ndiyo kitovu cha shughuli zinazopewa msaada na Programu ya Panda Miti Kibiashara vijijini.Aidha wakulima hao waliopanda miti wamezingatia vigezo vyote vilivyowekwa na PFP. Kwa mfano, vijiji vya Lusala, Kifanya na Ngalanga viliandaa mashamba kwa kutumia madawa ya kuua magugu na kuondoa vichaka na miti isiyostahili kadri walivyoelekezwa.Changamoto pekee inayowakabili ni miteremko na miinuko mikali inayotokana na vijiji kuwa na vilima vingi. Hata hivyo, wakulima wanashirikiana kurekebisha njia na barabara za kuelekea kwenye maeneo ya kupanda miti ili yaweze kufikika kwa urahisi. Baadhi wameamua kutumia mikokoteni inayovutwa na ng’ombe kupeleka miche ya miti mashambani.

Miche ya kutoka kitalu cha Mgololo ikiwa tayari kusambazwa kwa Trekta kupelekwa kwenye

maeneo ya upandaji miti kijijini Lusala

Akwilino Mluwili, mmojawapo wa vijana waliopanda miti katika kijiji cha Lusala

Wakulima wa miti wa Iboya katika picha ya pamoja baada ya kuandaa shamba la kupanda miti

Page 6: Panda Miti Kibiashara

Panda Miti Kibiashara6

Wajumbe wa Kamati Elekezi ya PFP Washuhudia Miti Ikipandwa

Shughuli za kupanda miti zimepamba moto katika vijiji vyote 11 vya majaribio katika programu ya Panda

Miti Kibiashara mkoani Njombe. Wajumbe wa Kamati elekezi walishuhudia hayo walipokuwa wakihudhuria mkutano wao wa siku mbili uliofanyika Njombe Mjini, mwanzoni mwa mwezi Februari, 2015. Mkutano wao uliambatana na kufanya ziara katika vijiji vya Ngalanga na Iboya vilivyopo katika Wilaya ya Njombe Mji.Programu ya Panda Miti Kibiashara hutoa msaada wa hali na mali kwa wakulima wa miti kupitia Mpango wa kutoa Motisha kwa Wakulima wa Miti (TGIS). Vilevile Programu hutoa misaada kupitia shughuli za kujiongezea kipato (IGA), ambapo wakulima wa miti huibua miradi midogo ya kutekeleza wakiwa wakisubiri miti yao waliyoipanda kukomaa. WajumbewaKamatiElekeziwalipotembeleaKikundi cha Panda Miti cha Nyambera kijijini Ngalanga, walionyeshwa shamba la Bw Reginald Danda lenye ukubwa wa Hekta 26. Danda amepanda miti aina ya misindano jamii ya Pinus patula. Wakulima wengi walipanda Misindano na baadhi walipanda Mikaratusi (Milingoti).

Mashamba ya miti katika kijiji cha Ngalanga hayapo pamoja bali yametawanyika sehemu mbalimbali kijijini kama inavyoanishwa katika Mpango Endelevu wa Matumizi yaArdhi (VLUP) ya kijiji hicho. Pia, wajumbe wa Kamati Elekezi walipatafursa ya kuona shamba la Bw Mario Lyanzile ambalo lilikuwa limepandwa miti ya misindano siku mbili tu kabla ya Kamati kufika kijijini Ngalanga. Kamati ilipotembelea kijiji cha Iboya ambacho kiko umbali wa km 34 toka Njombe mjini, walikagua shamba la Parachichi lenye ukubwa wa Hekta 2.5 linalomilikiwa na Shule ya Sekondari ya Ilowola. Shamba hilo ni mfano wa miradi ya kujiongezea kipato (IGA) kwa wakulima wa miti.Hatimaye wajumbe wa Kamati Elekeziwalitembelea eneo la kikundi cha Wakulima wa Miti katika kijiji cha Iboya. Wakiwa Iboya wajumbe walijionea kuwa Kijiji kimetenga eneo kubwa la pamoja kwa ajili ya Kikundi cha Wakulima wa Miti ambapo kila mwanachama analo shamba lake binafsi la kupanda miti. Hivyo mashamba yote ya kikundi yanapatikana eneo moja kijiografia.

WajumbewaKamatiElekeziyaPFPwakiwakatikapichayapamoja baada ya mkutano wao wa tarehe 5 Februari 2015.

MwenyekitiwaKamatiElekeziyaPFP,MariamMrutu akipanda mche wa Parachichi katika shama la IGA la Sekondari ya Ilowola kijijini Iboya.

Page 7: Panda Miti Kibiashara

Panda Miti Kibiashara 7

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Ahimiza ‘Panda Miti Kibiashara’

Wakulima wa Miti mkoani Njombe wamehimizwa kupanda miti Kibiashara.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dr. Rehema Nchimbi alitoa wito huo akiwa Mgeni Rasmi siku ya maadhimisho ya Siku ya Mkoa ya Kupanda Miti iliyofanyika tarehe 10 Januari wilayani Makete. Kauli mbiu ya Siku ya Mkoa ya Kupanda Miti ilifanana sawia na jina la Programu la ‘Panda Miti Kibiashara’. Aliwataka wakulima wa miti kutoivuna miti hiyo hadi itakapokua na kukomaa. Jumla ya miche 3,000 ilipandwa na wananchi wa Mjini Makete katika eneo la hifadhi ya Dombwela iliyoko karibu kabisa na mji wa Makete.Mkuu wa Mkoa wa Njombe aliziagiza Halimashauri zote katika Mkoa wa Njombe kuhakikisha zinatenga maeneo na kupanda miti kwa wasiojiweza. Alisema ‘Miti hiyo itakapokomaa na kuvunwa, mapato yake yatatumika kulipia ada katika shule na vyuo kwa watoto wanaotoka katika familia za wasiojiweza.Dr. Nchimbi alizishauri Halmashauri kuhakikisha zinakuwa va vitalu vya kukuza

miche ya kutosha na kuisambaza kwa wingi kwa wananchi kwa kusudi la kuigeuza miti kuwa mojawapo ya mazao ya biashara mkoani Njome.Mkuu wa Mkoa aliwaasa wakazi wa Njombe waishio nje ya mkoa kuwekeza katika upandaji miti ili kukuza uchumi wa mkoa wao.Mkuu wa Mkoa aliwasifu wananchi wa Mkoa wa Njombe kwa kuendeleza tabia ya upandaji miti , ambayo ni shughuli muhimu kiuchumi na katika kutunza mazingira. Alisisitiza ‘Msiishie kupanda miti tu bali hakikisheni mnaitunza na kuikinga na majanga ya moto’.Dkt Nchimbi aliwahimiza wananchi kutunza vyanzo vya maji kwa kuepuka shughuli za binadamu zinazoathiri vyanzo vya maji. “Kwa hiyo mchaguapo miti ya kupanda zingatieni pia kupanda miti inayohifadhi vyanzo vya maji badala ya miti ya kibiashara pekee’ alisisitiza.Aina ya miti iliyopandwa katika maadhimisho ya Siku ya Mkoa ya Kupanda Miti ilikuwa Mizambarau na Miturunga ambayo inahifadhi vyanzo vya maji, pia inatoa mbao.

Dr. Rehema Nchimbi, Mkuu wa Mkoa wa Njombe akipanda mti Siku ya Mkoa ya Kupanda Miti, tarehe 10, Januari 2015.

Page 8: Panda Miti Kibiashara

Panda Miti Kibiashara8 Panda Miti Kibiashara8

Wakulima wa miti wa kijiji cha Ikang’asi wakiwa katika picha ya pamoja

Bustani iliyoko Mgololo

Habari Katika Picha

Eneo la kupanda miti la kijiji cha Usagatikwa (linaloonekana) ndiyo mfano wa maeneo mengi chini ya Programu