8

Panga uzazi, watoto - The Compass for SBC · 2016. 11. 7. · Panga uzazi, watoto wapate malezi bora! Kwa maelezo zaidi nenda kwenye kituo cha afya kilichopo karibu nawe au tuma SMS

  • Upload
    others

  • View
    6

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Panga uzazi, watoto - The Compass for SBC · 2016. 11. 7. · Panga uzazi, watoto wapate malezi bora! Kwa maelezo zaidi nenda kwenye kituo cha afya kilichopo karibu nawe au tuma SMS
Page 2: Panga uzazi, watoto - The Compass for SBC · 2016. 11. 7. · Panga uzazi, watoto wapate malezi bora! Kwa maelezo zaidi nenda kwenye kituo cha afya kilichopo karibu nawe au tuma SMS

Panga uzazi, watotowapate malezi bora!

Kwa maelezo zaidi nenda kwenye kituo cha afya kilichopokaribu nawe au tuma SMS “m4RH” kwenda 15014 - BURE!

Chagua. Tumia njia ya uzazi wa mpango inayokufaa.

Page 3: Panga uzazi, watoto - The Compass for SBC · 2016. 11. 7. · Panga uzazi, watoto wapate malezi bora! Kwa maelezo zaidi nenda kwenye kituo cha afya kilichopo karibu nawe au tuma SMS
Page 4: Panga uzazi, watoto - The Compass for SBC · 2016. 11. 7. · Panga uzazi, watoto wapate malezi bora! Kwa maelezo zaidi nenda kwenye kituo cha afya kilichopo karibu nawe au tuma SMS
Page 5: Panga uzazi, watoto - The Compass for SBC · 2016. 11. 7. · Panga uzazi, watoto wapate malezi bora! Kwa maelezo zaidi nenda kwenye kituo cha afya kilichopo karibu nawe au tuma SMS

Namshauri kila mwanamkekutumia huduma za uzazi wa mpango kwa ajili ya familia bora!

Kwa maelezo zaidi nenda kwenye kituo cha afya kilichopokaribu nawe au tuma SMS “m4RH” kwenda 15014 - BURE!

Chagua. Tumia njia ya uzazi wa mpango inayokufaa.

Page 6: Panga uzazi, watoto - The Compass for SBC · 2016. 11. 7. · Panga uzazi, watoto wapate malezi bora! Kwa maelezo zaidi nenda kwenye kituo cha afya kilichopo karibu nawe au tuma SMS

Mwandishi: Jina lako halisi?Mama Ushauri: Naitwa Beatrice Makani. Mwandishi: Unafanya kazi gani?Mama Ushauri: Ninafanya kazi mamlaka ya bandari Tanzania na pia ninafahamika kama mama ushauri ambapo

pia nimekuwa nikishiriki kipindi cha redio cha mama ushauri kinachotoa ushauri wa jinsi ya kutumia uzazi wa mpango.

Mwandishi: Katika kipindi cha mama ushauri huwa unatoa ushauri gani hasa? Mama Ushauri: Kipindi cha mama ushauri kinawaelimisha wanajamii katika mambo mbalimbali ywanayokabiliana

nayo kama vile ushauri wa namna ya kupambana na maambukizi ya ukimwi, uzazi wa mpango na mambo yote yanayoihusu jamii

Mwandishi: Unadhani uzazi wa mpango ni sahihi hata kwa ambao hawajaoa au kuolewa? Mama Ushauri: Kwa kuwa uzazi wa mpango ni kwa mwanamke na mwanaume mwenye umri wa kuweza kuzaa ni

vizuri kwa kila mtu kuanza kutumia hata kabla hajaoa au kuolewa kwa kufanya hivyo kutafanya mtu aweze kujipanga na mambo yake vizuri na kujua ni lini ataanza kuzaa.

Mwandishi: Ni kwa nini una�kiri hivyo? Mama Ushauri: Kwasababu kila mtu anahitaji kuwa tayari kupata mtoto wakati akiwa tayari kwa hiyo ni muhimu

kwa kila mtu awe ameolewa au hajaolewa kutumia njia za kisasa za uzazi wa mpango. Ingawa watu wengi wanaamini kwamba uzazi wa mpango unasababisha ugumba hasa pindi mwanamke anapochelewa kupata mimba imani hiyo ni potofu. Kama mwanamke unaweza kutumia njia za kisasa kwa kipindi ambacho haupo tayari kupata mimba na pindi utakapohitaji kupata mimba unaacha kutumia na hapo utaweza kupata mimba na ni vizuri kabla ya kufanya hayo uende kwenye kituo cha afya kilichopo karibu nawe ili kupata ushauri ulio sahihi.

Mwandishi: Umewahi kutumia njia za kisasa za uzazi wa mpango? Kama ndio kwa nini? Mama Ushauri: Ndio na nimeanza kutumia tangu nikiwa msichana nimekuwa nikitumia njia za kisasa za uzazi wa

mpango na umekuwa ukinisaidia sana kujipanga na siku zote kuwa mwenye furaha.Mwandishi: Ni ushauri gani unaweza kumpa mtu ambaye ana wasiwasi kuhusu madhara

yanayosababishwa na uzazi wa mpango.Mama Ushauri: Njia za uzazi wa mpango ni salama na zina manufaa kama zitatumiwa kwa ufasaha. Wanawake

wengi hupata maudhi madogomadogo ambayo huonekana kwa kipindi kifupi sana na mara nyingi hupungua taratibu na kuisha kabisa. Maudhi hayo sio dalili ya kuugua na mara nyingi huwapata wanawake wachache kuna wengine hawayapati kabisa.

Mwandishi: Je endapo mwanamke atapata maudhi yoyote afanye nini? Mama Ushauri: Kama mwanamke ukiona maudhi yoyote inakupasa kwenda kwenye kituo cha afya uonane na

mtoa huduma kwa ajili ya ushauri na pengine kubadili njia ya uzazi wa mpango uliyokuwa unaitumia.

Mwandishi: Unamshauri nini mtu anayehisi matumizi ya njia za kisasa za uzazi wa mpango yanaweza kusababisha mwanamke akachelewa kuzaa mtoto?

Mama Ushauri: Njia za uzazi kama vidonge, kitanzi, kipandikizi pamoja na kondomu ni njia ambazo mwanamke anaweza kupata mimba wakati wowote atakapoacha kuzitumia. Kwa upande wa sindano kwa kawaida mwanamke huchukua mda kidogo kabla ya kupata mimba hivyo hapaswi kuwa na wasiwasi. Vilevile kuna njia za kisasa za kufunga kizazi za kudumu ambazo mara nyingi hutumiwa na wale ambao hawataki kuzaa tena.

Chagua. Tumia njia ya uzazi wa mpango inayokufaa.

Page 7: Panga uzazi, watoto - The Compass for SBC · 2016. 11. 7. · Panga uzazi, watoto wapate malezi bora! Kwa maelezo zaidi nenda kwenye kituo cha afya kilichopo karibu nawe au tuma SMS

Ni vema kujipangia, watoto umri wapishane.

Kwa maelezo zaidi nenda kwenye kituo cha afya kilichopokaribu nawe au tuma SMS “m4RH” kwenda 15014 - BURE!

Chagua. Tumia njia ya uzazi wa mpango inayokufaa.

Page 8: Panga uzazi, watoto - The Compass for SBC · 2016. 11. 7. · Panga uzazi, watoto wapate malezi bora! Kwa maelezo zaidi nenda kwenye kituo cha afya kilichopo karibu nawe au tuma SMS

Mwandishi: Jina lako halisi? Yusuph: Naitwa Mzee Yusuph.

Mwandishi: Unafanya kazi gani? Yusuph: Ninajishughulisha na muziki wa taarabu.

Mwandishi: Mbali na kazi ya muziki ni kazi gani nyingine unafanya? Yusuph: Mbali na kazi ya muziki pia najishughulisha na biashara zangu ili niweze kujiongezea

kipato na kuboresha maisha yangu na familia kwa ujumla.

Mwandishi: Unazungumziaje wanaume kujihusisha katika matumizi ya uzazi wa mpango? Yusuph: Ni wajibu kwa kila mwanaume kujihusisha na masuala ya uzazi wa mpango kwani

kwa kufanya hivyo kutasaidia kupata familia ambayo utaweza kuihudumia.

Mwandishi: Unawaambia nini wanaume wenye �kra potofu kuhusu njia za kisasa za uzazi wa mpango?

Yusuph: Wanaume wengi wanadhani kuwa uzazi wa mpango ni wa wanawake peke yao, mimi nawaambia kuwa uzazi wa mpango ni kwa wote wanawake na wanaume, hivyo ni jukumu letu sote kuhakikisha tunashirikiana na wake zetu katika kupanga familia zetu na tutaona manufaa yake. “Ukitaka kujua uhondo wa ngoma uingie ucheze”

Mwandishi: Kitu gani kimekuvutia mpaka ukashiriki katika kampeni hii ya uzazi wa mpango? Yusuph: Mimi kama msanii na msanii kama kioo cha jamii ni jukumu langu kuhakikisha natoa

elimu kwa jamii yangu hivyo nilivyopata nafasi hii ya kushiriki katika kampeni hii nimeona ni nafasi nzuri kutoa elimu kwa jamii yangu.

Mwandishi: Kwa kutumia muziki wako, Je umewezaje kuwaelimisha wanajamii kuhusu uzazi wa mpango?

Yusuph: Kwa kutumia muziki wangu nimeweza kushiriki kwenye kampeni hii na kama ulivyoona katika tangazo la jiamini umeweza kusikia tungo ya wimbo wenye ujumbe wa kuhamasisha matumizi ya njia za kusasa za uzazi wa mpango na faida zake pia.

Mwandishi: Kitu gani unadhani kifanyike kuwavutia watu wengi zaidi kutumia njia za kisasa za uzazi wa mpango?

Yusuph: Kwa upande wangu nahisi elimu zaidi itolewe ili watu wengi waelewe umuhimu wa uzazi wa mpango. Jambo jingine ni kutoa mwanga zaidi kwa wanaoishi vijijini kwani huko elimu huwa inachelewa sana ku�ka ukilinganisha na mijini.

Mwandishi: Kuna faida gani hasa mtu anaweza kuipata akiwa na watoto waliopishana? Yusuph: Kuwa na watoto waliopishana ni jambo zuri sana kwani itakusaidia kuwapa malezi

bora pamoja na mahitaji yao itakuwa ni rahisi kwako. Pia itaongeza mapenzi katika familia .

Chagua. Tumia njia ya uzazi wa mpango inayokufaa.