64
Halmashauri ya Wilaya ya Singida Vijijini Novemba 2012 Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)

Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

  • Upload
    others

  • View
    9

  • Download
    3

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Halmashauri ya Wilaya ya Singida VijijiniNovemba 2012

Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)

Page 2: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia
Page 3: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Halmashauri ya Wilaya ya Singida Vijijini

Imeandaliwa na Timu ya SamNovemba 2012

Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)

Page 4: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Hakimiliki © 2013Shirika la Sikika, Haki zote zimehifadhiwaTarehe ya kuchapishwa 2013Imeandaliwa na Timu ya UUJ Singida na Shirika la Sikika

Imechapishwa na: Digitall Ltd.

Page 5: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-i-

SHUKURANITimu ya UUJ wilaya ya Singida Vijijini inatoa shukrani za dhati kwa uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Singida kwa ushirikiano waliouonyesha tangu kuanza kwa zoezi hili hadi mwisho hasa katika ushiriki wa watumishi wake na upatikanaji wa taarifa mbalimbali zilizochambuliwa katika zoezi zima la mafunzo ya UUJ.

Pili timu ya UUJ inatoa shukrani kwa wakuu wa wilaya za Singida na Ikungi kwa utayari wao wa kushiriki na kuhakikisha timu ya UUJ inachaguliwa, inapata mafunzo na kwa kukamilisha zoezi lililokusudiwa.

Tatu timu ya UUJ inatambua na kushukuru mchango mkubwa wa baraza la madiwani na wananchi wa wilaya ya Singida Vijijini ambao umesaidia kukamilika kwa zoezi zima ikiwa ni pamoja na kutoa wawakilishi walioingia kwenye timu ya Uwajibikaji Jamii.

Nne timu ya UUJ wilaya ya Singida inapenda kutoa shukrani za dhati kwa vyombo vya habari vyote vya ndani na nje ya Singida kwa ushirikiano wao waliouonesha katika kuripoti matukio yote yaliyokuwa yanaendelea katika zoezi zima la UUJ.

Tano timu ya UUJ inapenda kutoashukrani kwa wadau wote wa sekta ya afya wilayani, ikiwa ni pamoja na watumia huduma za afya na asasi za kiraia kwa ushiriki wao katika hatua mbalimbali za zoezi la UUJ

Mwisho kabisa timu ya UUJ wilaya ya Singida Vijijini inalishukuru shirika la Sikika na wafanyakazi wake hususani ndugu Zakayo Mahindi, Aisha Hamis, Theresia Kapinga, Fredrick Ngao kwa kuiwezesha timu ya UUJ katika maandalizi na mafunzo ambayo yaliwezesha kuundwa kwa timu ya UUJ na kukamilika kwa zoezi zima

Page 6: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-ii-

YALIYOMO

SHUKURANI i

ORODHA YA VIFUPISHO iv

MUHTASARI v

UTANGULIZI vi

SEHEMU YA I: UUNDWAJI WA TIMU YA UUJ 11.1 Kikao Baraza la Madiwani wa Singida Vijijini 11.2 Mkutano wa Wadau wa Afya na UKIMWI Wilaya ya Singida 21.3 Uzinduzi wa timu ya UUJ 3

SEHEMU YA II: MAFUNZO NA UCHAMBUZI WA NYARAKA MBALIMBALI 4

2.1 Mafunzo kwa timu ya UUJ 42.2 Uchambuzi wa Mpango Mkakati na Mgawanyo wa Rasilimali 52.3 Mgawanyo wa rasilimali sekta ya afya 82.4 Uchambuzi wa Ripoti ya Mkaguzi wa Ndani Robo ya Kwanza 2010/2011 92.5 Uchambuzi wa ripoti ya mkaguzi wa ndani robo ya pili (2010/2011) 132.6 Uchambuzi wa ripoti ya mkaguzi mkuu wa serikali mwaka wa fedha 2009/2010 17

SEHEMU YA III: HOJA ZILIZOIBULIWA NA TIMU YA UUJ KUHUSU HALI YA HUDUMA 24

3.1 Hoja kuhusu umakini na ufanisi wa halmashauri kutekeleza bajeti 243.2 Kuhusu Bakaa Kubwa katika Sekta ya Afya kwa Mwaka 2010/2011 243.3 Kuhusu Upatikanaji wa Taarifa za Utekelezaji za Halmashauri na Idara ya Afya kwa Ujumla 253.4 Kuhusu Ukaguzi wa Ndani na wa Nje katika Halmashauri 253.5 Kuhusu Wafanyakazi Kutokuwa na Mafaili ya Kumbukumbu zao 25

Page 7: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-iii-

3.6 Hoja kuhusu utekelezaji wa shughuli katika vituo vya huduma 263.7 Majibu ya jumla kwa hoja mbalimbali 40

SEHEMU YA IV: MAONI YA WADAU JUU YA UBORESHAJI WA HUDUMA 47

4.1 Maoni Ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali 474.2 Zoezi la UUJ Liwe Endelevu 474.3 KuwezeshwaOfisiyaMkaguziwaNdaniwaHalmashauri 474.4 Timu ya UUJ Ipewe Ushirikiano 474.5 Ushiriki Wa Baraza la Madiwani 484.6 Ushiriki Wa Wananchi 484.7 Hitimisho 48

VIAMBATISHO 49Hotuba ya Mkuu wa Wilaya 49Majina ya timu ya UUJ 51Hotuba ya mwenyekiti wa timu ya UUJ ya mkutano wadau wa halmashauri singida 52

Page 8: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-iv-

ORODHA YA VIFUPISHO

CHF Community Health Fund (Mfuko wa afya wa jamii)

CHMT Council Health Management Team (Timu ya uendeshaji wa shughuli za afya katika halmashauri)

CMT Council Management Team (Timu ya uendeshaji wa shughuli za halmashauri)

MSD Medical Store Department (Bohari kuu ya madawa)

UUJ Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii

WAVIU Waishio na Virusi vya Ukimwi

FGM Female Genital Mutilation (Ukeketaji wa wanawake/wasichana)

SAM Social Accountability Monitoring (Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii)

Page 9: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-v-

MUHTASARINdugu msomaji, ripoti hii ya timu ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ) wilaya ya Singida vijijini itakuwezesha kuelewa dhana nzima na lengo la UUJ ikiwa ni pamoja na kuelewa mchakato na hatua zote zinazotakiwa kupitiwa ili kukamilisha zoezi la UUJ kwa ufanisi.

Ripoti hii imeeleza mchakato mzima wa uundwaji wa timu ya UUJ, uliowezesha kupatikana kwa timu ya UUJ wilaya ya Singida vijijini.

Katika ripoti hii, inaonyesha taarifa za mafunzo yote yaliyotolewa na Sikika kwa timu ya UUJ na matokeo ya uchambuzi wa nyaraka mbalimbali za halmashuri zilizotumika katika uchambuzi na timu ya UUJ zimeelezwa kwa uwazi kabisa.

Ripoti hii imebainisha changamoto zilizojitokeza katika vituo vya huduma ya afya ambavyo timu ya UUJ ilitembelea pamoja na mambo ambayo timu ya UUJ ilijifunza. Pia, ripoti inaonyesha hoja za timu ya UUJ kwa halmashauri ya wilaya ya Singida pamoja na majibu ya halmashauri kwa timu ya UUJ. Ripoti inaoonyesha mtazamo wa wadau mbalimbali wa afya juu ya huduma za afya zinazotolewa katika vituo vya huduma.

Mwisho, ripoti hii ya timu ya UUJ imetoa mapendekezo kadhaa kwa halmashauri, wadau na wanachi kwa ujumla juu ya zoezi zima la UUJ. Timu inaamini iwapo mapendekezo hayo yatazingatiwa zoezi la UUJ litaleta tija na maendeleo katika upatikanaji wa huduma bora za afya katika halmashauri.

Ni matumaini yetu kuwa ripoti hii itasaidia kuongeza uelewa wa wakazi wa Singida vijijini kuhusu zoezi zima la ufuatiliaji wa uwajibikaji.

Bruno M. Natalis Mwenyekiti - Timu ya UUJ Singida Vijijini

Page 10: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-vi-

UTANGULIZISerikali imepewa dhamana kubwa kusimamia na kutumia rasilimali mbalimbali za uma ili kuwahudumia wananchi. Rasilimali hizi zinazotokana na kodi, mikopo na misaada ya wahisani mbalimbali. Ni vema pia tukumbuke kwamba, rasilimali hizo ni za wananchi, na hivyo wanayo madaraka makubwa ya kuhoji matumizi yake aidha mwananchi mmoja mmoja au kupitia viongozi wao. Hata hivyo, ni mara nyingi watendaji wanajisahau kwamba ni haki ya wananchi kufanya hivyo kisheria.

Kwa kutambua umuhimu wajibu huu wa wananchi katika kusimamia na kuleta maendeleo kwa jamii, shirika la Sikika lilitekeleza zoezi la Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ) katika wilaya ya Singida. Zoezi hili la UUJ lilitekelezwa na Timu iliyoundwa kwenye mkutano wa pamoja wa wadau wote wa sekta ya afya wilayani. Timu iliwakilisha makundi yote muhimu katika sekta ya afya wakiwemo madiwani, wawakilishi wa taasisi zisizo za kiserikali, mashirika ya dini, wawakilishi wa kamati za uendeshaji za vituo vya kutolea huduma za afya, watendaji wa vijiji pamoja na wawakilishi wa timu ya uendeshaji wa huduma ya afya ya wilaya. Kwa niaba ya wananchi wa Singida vijijini, timu ya UUJ imefanya ufuatiliaji wa uwajibikaji katika sekta ya afya na kuja na mapendekezo yaliyodai ufafanuzi, uthibitisho na uhalalisho wa maamuzi yanayofanywa na watendaji katika sekta ya afya na halmashauri kwa ujumla.

Timu ilipata mafunzo ya ufuatiliaji wa uwajibikaji (UUJ). Mafunzo haya yalihusu uwajibikaji wa jamii kupitia ufuatiliaji wa mipango na mgawanyo wa rasilimali katika halmashauri (planning and resource allocation), usimamizi wa matumizi (expenditure management), usimamizi wa utendaji wa shughuli mbalimbali za halmashauri (performance management), usimamizi wa uadilifu (public integrity) na usimamizi wa uwajibikaji (Oversight). Timu ilipata nafasi ya kujifunza kuwa usimamizi mzuri wa hatua tano za mfumo wa ufatiliaji wa uwajibikaji hupelekea upatikanaji wa haki za binadamu na mahitaji ya jamii.

Page 11: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-vii-

Kielelezo 1: Mfumo wa Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii

Aidha, baada ya mafunzo, timu ilifanya uchambuzi wa nyaraka mbalimbali ili kujiridhisha juu ya utendaji na uwajibikaji kwa jamii katika kuhakikisha upatikanaji wa mahitaji na haki za msingi ya jamii. Nyaraka za halmashauri zilizochambuliwa ni pamoja na Mpango Mkakati wa Halmashauri, Ripoti ya Utekelezaji ya Halmashauri, Mpango Kabambe wa Afya wa Halmashauri, Ripoti ya Utekelezaji wa Mpango Kabambe wa Afya wa halmashauri, Ripoti ya Mkaguzi wa Ndani wa Halmashauri, Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali kwa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Miuhtasari ya Vikao vya Madiwani, Mpango Kazi wa Kazi za UKIMWI na Ripoti ya Utekelezaji wa Huduma za UKIMWI.

Baada ya uchambuzi wa kina wa taarifa mbalimbali, timu ilitembelea vituo ishirini na moja vya kutolea huduma za afya vya umma vilivyo katika wilaya ya Singida vijijini. Dhumuni la ziara hii lilikuwa ni kutathmini hali ya utekelezaji wa shughuli za afya za halmashauri kulinganisha na taarifa zilizoandikwa katika ripoti za utekelezaji na kubainisha changamoto. Timu ya UUJ ilibainisha maeneo mbalimbali ambayo yalihitaji ufafanuzi kutoka kwa watendaji. Pia timu inatarajia kuona hatua za marekebisho na zenye uwazi “za watendaji” kwa wadau wa afya na jamii kwa ujumla zikifanyika katika halmshauri ya Singida, na hatimaye kupatikana kwa huduma bora za afya kwa wananchi wote.

Ripoti hii ina sehemu kuu nne ambazo ni; Uundwaji wa timu ya UUJ, Mafunzo na uchambuzi wa nyaraka mbalimbali za halmashuri kwa timu ya UUJ, Changamoto zilizodhihirika, hitimisho na mapendekezo.

1. Mipango na mgawanyo wa

Rasilimali

2.Usimamizi wa Matumizi

3. Usimamizi wa Utendaji

4. Usimamizi wa Uadilifu

5. Uangalizi Upa kanaji wa haki

za Binadamu za kijamii na kiuchumi

Page 12: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-viii-

Uundwaji wa timu ya UUJ: Sehemu hii inaelezea mchakato mzima uliowezesha kupatikana kwa timu ya UUJ wilaya ya Singida vijijini.

Mafunzo na uchambuzi wa nyaraka mbalimbali za halmashuri kwa timu ya UUJ: sehemu hii inaelezea mafunzo yaliyotolewa kwa timu ya UUJ kutoka kwa Sikika pamoja na taarifa zote za halmashauri zilizotumika katika uchambuzi na timu ya UUJ.

Changamoto zilizodhihirika: sehemu hii inaonyesha changamoto zilizobainishwa katika vituo vya huduma ya afya na zahanati zote ambazo timu ya UUJ ilitembelea na mambo ambayo timu ya UUJ ilijifunza. Pia inaelezea hoja za timu ya UUJ kwa halmashauri ya wilaya ya Singida pamoja na majibu ya halmashauri kwa timu ya UUJ.

Hitimisho na mapendekezo: Sehemu hii inajadili mapendekezo ya UUJ kwa halmashauri, wadau na wananchi kwa ujumla juu ya namna walivyoliona zoezi zima la uundaji wa UUJ. Timu inaamini kuwa iwapo mapendekezo hayo yatazingatiwa, zoezi la uundaji, mafunzo, uchambuzi wa timu za UUJ na maelezo ya ufafanuzi kutoka kwa watoa huduma litaleta tija na maendeleo katika upatikanaji wa huduma bora za afya katika halmashauri.

Page 13: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-1-

SEHEMU YA I: UUNDWAJI WA TIMU YA UUJ

1.1 Kikao Baraza la Madiwani wa Singida Vijijini

Kikao baina ya waheshimiwa madiwani na wawakilishi wa Sikika kilifunguliwa na Mkuu wa wilaya ya Singida Bi. Singida Queen Mwanshinga ambaye Katika hotuba yake ya ufunguzi (kiambatanisho 1) aliwahimiza madiwani kushiriki kikamilifu katika mpango wa ufuatiliaji wa uwajibikaji kwa kufuatilia na kusimamia matumizi ya rasilimali za wananchi katika halmashauri. Hii ni kwa sababu madiwani ndio watunga sera na wanayo mamlaka kisheria kusimamia utendaji wa halmashauri. Pia, katika hotuba hiyo, mkuu huyo wa wilaya alisisitiza umuhimu wa kila kiongozi hasa waheshimiwa madiwani kushiriki katika kusimamia na kuwawajibisha watendaji pale wanapoona rasilimali za umma zinatumika kinyume na matarajio ya wananchi.

Ufunguzi wa kikao ulifiatiwa namadambalimbali zilizowasilishwa nawakufunzikutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia uwajibikaji wa watendaji katika halmashauri husika.

Madiwani waliishukuru asasi ya Sikika na wawezeshaji kwa mafunzo mazuri ya dhana nzima juu ya uwajibikaji jamii. Akishukuru kwa niaba ya wenzake, diwani wa Dung’unye Mheshimiwa Bruno Natalis alisisitiza kuwa wao kama madiwani wana uwezo wa kufatilia matumizi na uwajibikaji katika ngazi ya halmashauri. Aliendelea kusema kuwa kuna vitengo kama vile MSD ambavyo wao kama madiwani hawawezi kuvifikikia kiurahisi. Alishauri kuwa asasi ya Sikika ingesaidia kufikiavitengo hivyo na kuhakikisha wanawajibika kama inavyopaswa ili kuleta tija katika sekta ya afya.

Baadhi ya waheshimiwa madiwani walishauri pia kuwa ingefaa mafunzo haya ya UUJ yapelekwe katika ngazi ya chini kabisa ya jamii, yaani kata ili wananchi walio wengi wapatekufikiwanaelimuhiyo.Hiiitawawezeshakuanzakuitumiakuanziangaziyavijijini, kata, tarafa na hatimaye wilaya.

Madiwani waliwachagua wawakilishi wao kuingia katika timu ya UUJ ya Wilaya ambao ni Mheshimiwa Bruno M. Natalis na Mheshimiwa Bi. Salima A. Kundya

Page 14: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-2-

1.2 Mkutano wa Wadau wa Afya na UKIMWI Wilaya ya Singida

Mkutano wa wadau wa afya Singida uliandaliwa kwa lengo la kutoa fursa kwa wadau wa afya kutoka makundi mbalimbali kufahamu dhana nzima ya uwajibikaji na kutoa fursa kwa wadau kujadili jinsi ya kutekeleza majukumu yao ili kuleta uwajibikaji katika utoaji wa huduma za afya. Wadau hao ni wawakilishi kutoka timu ya uendeshaji ya wilaya (CMT), timu ya uendeshaji wa huduma za afya ya wilaya (CHMT), madiwani, na wawakilishi wa wananchi. Wadau wengine ni kamati za usimamizi wa vituo vya huduma, AZAKI, vyombo vya habari pamoja na viongozi wa dini.

Mkutano huu ulifunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Singida Queen Mwanshinga kwa kusisitiza umuhimu wa watendaji na viongozi kuwa makini na kutunza muda katika kutekeleza majukumu yao kwani muda ni rasilimali muhimu na ikitumiwa vibaya hurudisha nyuma maendeleo ya jamii.

Vilevile Mkuu huyo wa wilaya alitoa rai kwa watendaji kuwa, kuhoji ni haki ya msingi ya wananchi hivyo ni wajibu wao kuhakikisha haki hiyo inatekelezwa kwani hata rasilimali zinazohojiwa ni za wananchi. Aliwakumbusha watendaji kuhakikisha wanasoma taarifa za mapato na matumizi kwani kutokufanya hivyo ndio chanzo cha matumizi mabaya na kudorora kwa shughuli za kiuchumi na kijamii. Pia watendaji walisisitizwa kuzingatia maadili ya kazi zao ili watoe huduma zilizo bora kwa jamii.

Katika hotuba yake, Mkuu wa Wilaya alitoa taarifa fupi juu ya taarifa za bajeti na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2010/11; mwaka ambao timu ya UUJ ilitarajia kufaya ufuatiliaji wa uwajibikaji. Alihoji kwa vipi Halmashauri iliweza kutumia 89% ya fedha zote walizopokea huku wakishindwa kabisa kutekeleza 17% ya miradi ya maendeleo (miradi 21 kati ya 121 iliyopangwa). Pia alihoji iwapo madiwani walikuwa na taarifa juu ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kata zao, na kama wanashirikishwa katika hatua zote za mipango hadi utekelezaji. Aliendelea kuhoji kama miradi iliyopangwa ilitekelezwa kwa wakati na kama ililingana na thamani ya fedha zilizotumika. Akiendelea, mkuu huyo wa wilaya aliwahimiza madiwani kufuatilia taarifa hizo kwa kina ili waweze kutoa majibu sahihi kwa wananchi mara wanapohojiwa.

Alimaliza kwa kutoa wito kwa Sikika kuwawezesha wananchi wa Singida kutambua wajibu wao hususani juu ya uwajibikaji, bila kujali changamoto wanazokabiliana nazo

Page 15: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-3-

katika utekelezji wa majukumu ya shirika. Pia aliahidi kushirikiana bega kwa bega na Sikika katika kuleta maendeleo kwa wananchi wa Singida. Wawakilishi kutoka makundi ya wadau mbalimbali kama yalivyoainishwa kwenye kipengele kinachofuata waliteuliwa kuingia katika timu ya UUJ.

Uzinduzi wa timu ya UUJ

Madiwani wawili (2), wananchi (6) na wawakilishi wa asasi za kiraia (2), waliteuliwa kujiunga na timu ya UUJ. Wajumbe wengine walichaguliwa kutoka katika makundi yao ni watendaji wa Kata (1), wawakilishi wa kamati za vituo vya afya (1) na wawakilishi wa dini (1) na wawakilishi wa halmashauri (1). Orodha kamili ya majina ya wajumbe wa timu ya ufuatiliaji inapatikana katika kiambatanisho namba 2. Baada ya uteuzi huo, timu ya UUJ ilitambulishwa rasmi kwa wadau wa afya wa Singida.

Page 16: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-4-

SEHEMU YA II: MAFUNZO NA UCHAMBUZI WA NYARAKA MBALIMBALI

2.1 Mafunzo kwa timu ya UUJ

Timu ya UUJ ya wilaya ya Singida ilipata mafunzo ya siku 10 juu ya dhana ya ufuatiliaji wa uwajibikaji jamii. Katika mafunzo hayo, wajumbe wa timu walipata fursa ya kujadili kwa kina hatua tano muhimu za UUJ. Mafunzo yaligusia dhana ya utoaji huduma kwa mtazamo wa HAKI za msingi za Binadamu na kuangalia mahitaji ya dola ama serikali katika kuhakikisha upatikanaji wa haki za msingi za kijamii na kiuchumi zikiwemo huduma za afya.

Wajumbe walijifunza mchakato wa UUJ ambao umegawanyika katika hatua kuu tano. Wajumbe walipata fursa ya kufafanuliwa kwa kina juu ya kila hatua ya dhana, umuhimu na nyenzo zinazostahili kutumika katika kila hatua.

Timu ilijifunza hatua ya kwanza ambayo ni Mgawanyo wa Rasilimali na Mpango Mkakati na kwanini wananchi wafuatilie mchakato wa mgawanyo wa rasilimali. Timu ya UUJ pia iliangalia mchakato wa Mgawanyo wa rasilimali nchini Tanzania; na kujadili kwa kina mchakato wa maandalizi ya mipango ya muda mrefu, muda wa kati na mipango ya muda mfupi ikiwemo mipango ya mwaka ya afya katika ngazi ya vituo na halmashauri kwa ujumla. Katika mjadala huu, timu ilipata fursa ya kusikia uzoefu wa wajumbe wawakilishi wa kamati za usimamizi wa vituo juu ya namna wanavyoandaa mipango na njia za kuanisha mahitaji ya jamii, muda wa maandalizi na wadau wanaoshiriki katika mchakato wa maandalizi ya mipango ya mwaka ya vituo vya huduma zikiwemo kata. Timu pia ilijifunza hatua zote muhimu kabla ya kupitishwa mipango ikiwemo mipango kuwasilishwa kwa timu ya Mipango ya halmashauri na hatimaye baraza la madiwani la halmashauri. Pamoja na hayo, timu ilifahamishwa zana za usimamizi katika kusimamia mgawanyo wa rasilimali.

Usimamizi wa matumizi ni hatua inayohusisha ufuatiliaji wa karibu wa jinsi halmashauri/taasisi inatumia fedha zilizoidhinishwa na kutolewa katika mipango ya wakati husika. Katika hatua hii, wajumbe wa timu ya UUJ walijadili ni muhimu kusimamia matumizi na uwajibikaji kwa jamii pamoja na kuangalia Miongozo inayosimamia matumizi ya fedha za umma. Pia wajumbe walijifunza juu ya taarifa za mifumo ya Usimamizi wa Fedha na wajibu wa kitengo cha ukaguzi wa ndani

Page 17: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-5-

katika kusimamia matumizi sahihi ya rasilimali ili kuzuia ama kuepusha matumizi mabayayarasilimalinakufikiaupatikanajiwahakizamsingizabinadamuikiwemohaki ya huduma bora za afya.

Usimamizi wa Ufanisi/Utendaji ni hatua ya tatu ya mfumo wa usimamizi wa uwajibikaji. Timu ya UUJ ilipata fursa ya kujifunza mambo muhimu katika hatua hii ikiwemo maswali ambayo timu ya UUJ wanapaswa kujiuliza.

Mfano, Je, Halmashauri na watoa huduma wanatekeleza shughuli na malengo ya mpango kwa ufanisi na ufasaha? Je, wanawajibika kwa makosa au udhaifu wa mfumo wa Usimamizi wa Utendaji au katika utoaji huduma? Je, Halmashauri zinahakikisha ufikiwaji wa haki za kijamii na kiuchumi kwa kutoa huduma kulingana na rasilimali zilizopo?

Ni kupitia majibu ya maswali haya na mengine mengi timu ingeweza kubaini ufanisi wa utendaji wa halmashauri yao

Usimamizi wa Uadilifu ni kitendo cha kuwawajibisha watendaji wa serikali kusimamia maamuzi/shughuli zao kwa kuwajibika dhidi ya kanuni za ufanisi, uaminifu na unyoofu katika utendaji. Timu ilipata nafasi ya kujifunza juu ya hatua hii ya nne na kujadili vyombo mbalimbali vya kusimamia uadilifu

Usimamizi wa uwajibikaji: Timu ilipata fursa ya kujifunza juu ya hatua hii ya tano ya dhana ya uwajibikaji jamii na vyombo vyenye wajibu ama mamlaka ya kikatiba na ya kidemokrasia kusimamia mipango, mgawanyo wa rasilimali, matumizi, utendaji, uadilifu na uwajibikaji. Vyombo hivi ni pamoja na Bunge, Baraza la madiwani, Taasisi za Ukaguzi (Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu), wakaguzi wa ndani, kamati za huduma ya afya, kamati za maadili na Kamati za UKIMWI.

2.2 Uchambuzi wa Mpango Mkakati na Mgawanyo wa Rasilimali

Mpango Mkakati wa Singida unaonesha dira na dhamira, shughuli na bajeti zake. Ni mpango ulioshirikisha jumla ya wananchi 110 katika mchakato wa uandaaji wake. Pia umeweza kuzingatia mahitaji ya wananchi, sera na miongozo ya kitaifa katika uundwaji wake (uk 3). Aidha, mpango mkakati umefanya uchambuzi wa hali halisi ya wilaya kiuchumi, kiutawala na kijamii.

Utawala:Watumishi34walipatiwamafunzoyakompyuta,ofisizakata8naofisizavijiji5zilijengwa,vifaambalimbalivyaofisivilinunuliwa:viti60,kitimaalumu1,

Page 18: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-6-

meza 27, kompyuta 4, machine ya kutoa nakala 4. Watumishi wa kada mbalimbali 413 walipatiwa mafunzo mbalimbali, jumla ya watumishi 339 wa kada mbalimbali waliajiliwa. Halmashauri imeainisha masanduku ya maoni yalitengenezwa na kuwekwa katikamaeneoyafuatayohalmashauri(masanduku6),ofisizakata(masanduku28),ofisizavijiji(masanduku146),zahanati(masanduku42),vituovyaafya(masanduku5), shule za msingi (masanduku 188) na shule za sekondari (masanduku 56).

Huduma za kijamii – Afya:Halmashaurikatikampangomkakatiwakeiliainishavikwazo mbalimbali katika sekta ya afya. Uhaba wa fedha za kutekelezea miradi ni changamoto inayokwamisha utekelezaji wa shughuli mbalimbali. Vikwazo vingine vilivyoainishwa ni pamoja na usambazaji duni wa madawa na vifaa, upungufu wa rasilimali watu wenye utaalamu au ujuzi na ukosefu wa masurufu kwa wafanyakazi waliopo.Pia,ukosefuwausafiriwauhakikanamazingiramabayakatikavituovyakutolea huduma za afya kutokana na majengo mengi na miundombinu ya vituo kuwa mibovu. Mpango mkakati umeelezea kwa kina hali ya utoaji wa huduma za afya kwa mwakawafedha2011nashabahazilizotarajiwakufikiwakupitiampangohuu.

Idara ya Fedha: Halmashauri inachangia 7% tu ya bajeti kutoka katika vyanzo vya ndani. Vikwazo vinavyobainishwa ni pamoja na ukosefu ama kutokuboresha mifumo ya udhibiti wa fedha na kutokuwepo kwa muunganiko kati ya mipango mkakati na mifumo ya usimamizi wa fedha katika kuandaa ripoti za fedha na zisizo za kifedha. Mpango mkakati umebainisha kuwa halmashauri imeanzisha kitengo cha ukaguzi wa ndani pamoja na kamati ya ukaguzi ya wilaya. Katika utekelezaji wa mpango mkakatihuu,halmashauri imepatahatisafikwamiaka3mfululizo(2007-2010).TimuyaUUJinaaminikwamba,pamojanakupatahatisafi,badokunauwezekanowa kuwepo mapungufu katika utendaji na watendaji, yanaweza pelekea kutokuwepo kwa uwajibikaji. Hali hii inaweza kusababisha kutokupatikana ama kupatikana kwa hudumahafifuzajamii,hasahudumazaafya.

Maendeleo ya Jamii: Mpango umeainisha kuwa maambukizi ya VVU/UKIMWI ni asilimia 1.9, na shabaha ya utekelezaji wampango katika eneo hili ni kufikiaasilimia 1.5. Mpango wa kupunguza matatizo yanayotokana na VVU/UKIMWI katika Halmashauri unaonyesha kuwa, katika kipindi kilichopita, jumla ya WAVIU 258 wamegawiwa lishe (wafanyakazi na wanajamii) na vikundi 7 vya mtandao wa WAVIU vimeanzishwa. Mpango wa Halmshauri umebainisha jumla ya watoto 1,500 wanaoishi katika mazingira magumu. Katika kuhamasisha ushiriki wa jamii katika shughuli za maendeleo, mpango unaeleza kuwa mipango shirikishi imetekelezwa katika vijiji 146.

Page 19: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-7-

Uwezeshaji Jamii: Mafunzo kwa WAVIU, watoto na wanawake juu ya haki zao yamefanyika katika kata 28. Vikundi vya kiuchumi 424 vya wanawake na 100 vya vijana vimeanzisha ingawa vingine sio hai. Mikopo imetolewa kwa vikundi hivi. Hakuna uwezeshwaji wa kifedha uliotolewa kwa vikundi vya walemavu

Kuimarisha usawa wa kijinsia: Mpango unaeleza kuwa elimu/mafunzo juu ya afya na uzazi na haki yametolewa katika kata 14. Lakini hakuna elimu ya kina iliyotolewa kwa wanawake kugombea nafasi za uongozi. Mpango wa halmashauri unaeleza kuwa, kampeni dhidi ya ukeketaji (FGM) imefanyika kwenye kata 14. Uchambuzi wa timu ya UUJ umebaini kutokuwepo kwa bajeti inayozingatia jinsia katika idara zote za halmashauri. Pia hauonyeshi kuwepo kwa kwa timu ya jinsia halmashauri.

Mgawanyo wa rasilimali katika halmashauri: Katika mwaka wa fedha 2010/11 halmashauri ya Singida vijijini ilikisia kutumia kiasi cha shilingi 24,124,486,183.00 kwaajiliyautekelezajiwamiradimbalimbali.Hatahivyo,hadikufikiamwishowamwaka, jumla ya shilingi 22,291,073,382.00 (sawa na asilimia 92.4) kutoka vyanzo mbalimbali ndizo zilipatikana ambapo Halmashauri ilichangia kiasi cha shilingi 2,021,46,873.00 kutoka mapato yake ya ndani (sawa na asilimia 0.9).

Halmashauri ilitenga kiasi cha shilingi 612,099,240.00 (sawa na asilimia 2.7) kwa ajili ya maendeleo na shilingi 1,912,990,026.00 (sawa na asilimia 8.6) kwa ajili ya matumizi mengineyo na shilingi 13,848,340,716.00 (sawa na asilimia 62.1) kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa halmashauri. Hata hivyo, halmashauri iliweza kutumia kiasi cha shilingi 19,853,936,015.00 katika mwaka wa fedha wa 2010/2011 ambayo ni sawa na asilimia 89.

Ripoti ya utekelezaji inaonyesha kwamba, katika mwaka wa fedha wa 2010/2011, jumla ya miradi 121 ilitarajiwa kutekelezwa kwa kutumia fedha zilizopokelewa. Hata hivyo, ni miradi 52 tu ndiyo iliyokamilika, 48 ilikuwa bado inaendelea kutekelezwa na miradi 21 (sawa na asilimia 17.4) ya miradi yote haikutekelezwa kabisa. Timu ya UUJ ilitaka kujua kwanini halmashauri imekamilisha miradi 52 tu wakati fedha zilizopatikana ni zaidi ya asilimia 92.

Utekelezaji wa shughuli katika halmashauri unalenga (hadi kufikia 2015) kuifanyahalmashauri ya wilaya ya Singida kuwa kati ya halmashauri bora katika utoaji wa huduma za kijamii na kiuchumi kwa wananchi. Kwa mtazamo huo, katika mwaka wa fedha 2010/2011 mipango na bajeti inaonyesha, zaidi ya asilimia 90 ya rasilimali za halmashauri zilipangwa kutumika katika sekta ya elimu, maji, afya, kilimo na mazingira. Utekelezaji mkubwa uliopangwa kufanyika kwa kutumia rasilimali zilizopatikana ni

Page 20: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-8-

uboreshaji wa mazingira ya kazi kupitia ujenzi na matengenezo kwenye sekta za elimu, maji,afya,kilimonausimamiziwamazingira,ujenzinaukarabatiwaofisizakatanavijiji pamoja na kuboresha mfumo wa ukusanyaji wa mapato na usimamizi wa fedha zahalmashauri,n.k.(Rejea:Ripotiyautekelezaji2010/2011).Aidhahalmashauriilitakakuhakikisha kunakuwepo upatikanaji wa ripoti za utekelezaji za mwaka na zile za robo-mwaka ili kuwezesha ufuatiliaji na usimamizi wa utekelezaji wa shughuli kulingana na malengo yaliyowekwa.

2.3 Mgawanyo wa rasilimali sekta ya afya

Katika mwaka wa fedha wa 2010/2011 sekta ya afya wilayani ilipata takribani shilingi bilioni moja milioni mia mbili na sitini na tano (1,265 b). Kiasi hiki cha fedha kilikuwa sawa na asilimia 98 ya makisio. Vyanzo vya fedha hizi vilikuwa ni; Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) shilingi 274.5 millioni (sawa na asilimia 112 ya makisio), mfuko wa bima ya afya ya jamii (Mfuko wa afya wa jamii) kiasi cha shilingi milioni 134 na Kamati za UKIMWI shilingi 115,776,000.00.

Ripoti ya utekelezaji ya robo ya nne ya 2010/2011 (uk 4) inaonyesha kuwa idara ya afya(hadikufikiamwishowaroboyatatu)ilikuwaimebakiwa na jumla ya shilingi 833,650,392.54 kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli mbali mbali. Aidha idara ilipokea jumla ya shilingi 985,590,585.18 katika robo ya nne. Hadi mwisho wa mwaka wa fedha wa 2010/2011, halmashauri ilibakiza jumla ya shilingi 799,707,804.00 (sawa na asilimia 5.5) ambazo hazikuwa zimetumika. Mpaka mwisho wa robo ya tatu, mfuko wa afya ya jamii (Mfuko wa afya wa jamii) ulikuwa na jumla ya shilingi 179,467,366.54. Katika robo ya nne mfuko huo ulipokea shilingi 148,212,668.18 na kufanya jumla ya shilingi 327,680,034.72. Hata hivyo, katika robo ya nne halmashauri iliweza kutumia shilingi 21,382,502.00 na kubakiza jumla ya shilingi 306,297,532.72. Kiasi kilichotumika ni kidogo sana na kiasi kilichobaki ni kikubwa mno ukizingatia kwamba vituo vya huduma vinakumbwa na uhaba wa mara kwa mara wa dawa na vifaa tiba, mafuta ya magari ya wagonjwa, n.k.

Hali hii pia hupelekea wananchi wengi kukosa mwamko wa kuchangia mfuko huu kwa kuwa kuna uwezekano wa kukosa huduma tarajiwa. Uchambuzi huu unaonyesha kuwa si kweli halmashauri hazipati fedha kwa wakati, bali zinashindwa kutumia fedha kutokana na sababu zingine ambazo timu ilihitaji kuzijua. Timu inataka kupata ufafanuzi kwanini matumizi ya mfuko huu ni ya chini, chanzo chake na hatua za marekebisho na uwajibikaji zilizochukuliwa kwa wahusika.

Page 21: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-9-

Pia, ripoti ya utekelezaji ya robo ya nne (uk. 4) inaonyesha kuwa mfuko wa MMAM ulikuwa na kiasi kikubwa cha fedha mwishoni mwa robo ya tatu (shs. 356,595,925.56).Mwishowa robo ya nne kiwangohiki kiliongezeka hadi kufikiashilingi 423,778,986.00. Hii pia inathibitisha kuwa si kweli halmashauri hazipati fedha kwa wakati, bali zinashindwa kutumia fedha kutokana na sababu zingine. Hivyo timu ya UUJ inataka kujua ni sababu zipi hasa zilipelekea kushidwa kutumia fedha ambazo zimekuwepo halmashauri tangu robo ya tatu, na pengine kabla ya hapo.

2.4 Uchambuzi wa Ripoti ya Mkaguzi wa Ndani Robo ya Kwanza 2010/2011

Kipengele hiki kinahusu uchambuzi wa ripoti ya mkaguzi wa ndani wa halmashauri ya wilaya ya Singida katika robo ya kwanza 2010/2011. Hii ni sehemu ya ufuatiliaji wa uwajibikaji wa jamii katika hatua yake ya tano, ambayo ni usimamizi. Katika kipengele hiki, timu ya UUJ imechambua ripoti ya mkaguzi wa ndani kama chombo kimojawapo katika usimamizi, imeangalia mapendekezo yake na jinsi gani halmashauri imetekeleza mapendekezo hayo.

Lengo kuu la ukaguzi wa ndani katika halmashauri katika mwaka wa fedha 2010/2011 ilikuwa ni kuhakikisha kuwa halmashauri ya wilaya ya Singida imeandaa taarifa za hesabu kwa kufuata taratibu, sheria na sera za matumizi ya fedha ya halmashauri, yaani kama ziliandaliwa kwa kuzingatia mahitaji ya mfumo wa kimataifa wa viwango vya hesabu za sekta za umma (IPSAS).

Ukaguzi wa ndani hufanyika kwa mujibu wa kifungu 45 (1) cha sheria zinazosimamia fedha za serikali za mitaa namba 9 ya mwaka 1982. Kifungu hiki pia kinatoa majukumu kwa muidhini mkuu wa halmashauri, kuanzisha na kutumia mfumo wa ukaguzi wa ndani. Majukumu ya mkaguzi wa ndani ni pamoja na kufanya ukaguzi na kutoa ripoti juu ya mapato na matumizi ya rasilimali za halmashauri, kuangalia kama taratibu, sheria na sera za fedha zinafuatwa, kukagua na kuripoti juu ya utendaji na program mbalimbali ili kujihakikishia kama matokeo ya shughuli zilizopangwa yanapatikana kulingana na shabaha zilizowekwa na halmashauri, kuangalia kama wakuu wa idara wanachukua hatua za kutosha katika kutekeleza mapendekezo ya mkaguzi wa ndani na kutoa ushauri zaidi juu ya utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa katika ripoti za ukaguzi, nk.

i. Mfumo duni wa ukusanyaji wa mapato ya halmashauri:

Katika mwaka wa fedha 2009/10, halmashauri ilikadiria kukusanya kupitia kwa wakusanyaji wa nje ya halmashauri kwa mkataba wa kuipatia halmashauri kiasi

Page 22: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-10-

cha shilingi 6,500,000.00 kwa mwezi sawa na shilingi milioni 78 kwa mwaka. Mkaguzi wa ndani anakadiria kiasi cha shilingi 1,469,320,000.00 zingekusanywa kama kungekuwepo na mfumo mahususi wa vituo vya masoko. Mkaguzi anaendelea kubainisha kuwa masoko haya yangeweza kuwasaidia wakulima na wanunuzi wa mazao kufanya biashara kwa urahisi na halmashauri kupata mapato yake. Uchambuzi wa timu ya UUJ unaonyesha kuwa, halmashauri inakosa mapato ya takribani shilingi 1,391,320,000.00. Halmashauri pia ilikisia kupata kiasi cha shilingi 253, 666,000.00 katika mwaka wa fedha 2010/2011, kiasi ambacho bado ni cha chini ukilinganisha na makadirio ya mkaguzi wa ndani wa halmashauri yaliyoainishwa hapo juu.

Timu ya UUJ inakubaliana na mapendekezo ya mkaguzi wa ndani, lakini inashangaa kuona ripoti ya ufuatiliaji wa mapendekezo yake haionyeshi hatua gani za utekelezaji zimefikiwa. Katika taarifa yake ya (kipengele 3.1 uk 9),mkaguzi anaonyesha (katika hatua zilizofikiwa katika utekelezaji) kwambawamekubaliana kwa utekelezaji. Taarifa hii haionyeshi wala haisaidii katika kuchukuliwa kwa hatua za uwajibikaji. Ripoti ya ufuatiliaji ya mkaguzi wa ndani ilitakiwaionyeshehatuazilizofikiwakatikakutekelezamapendekezoaliyoyatoakwa halmashauri, kitu ambacho hakikufanyika.

Timu ya UUJ ilitaka kupata ufafanuzi juu ya mambo yafuatayo; Hatua zilizochukuliwa mpaka sasa na halmashauri katika kushughulikia mapendekezo ya mkaguzi wa ndani juu masoko, mfumo wa risiti, na mfumo wa ruhusa toka kwa mkurugenzi kwa wanunuzi wa mazao; Kwa nini mkaguzi wa ndani anatoa taarifa za utekelezaji wa mapendekezo yake kwa uzito mdogo usio na tija katika kuletauwajibikaji(yaani,ripotiyakehaionyeshihatuazilizofikiwa);Jehatuazipiatafanya kuleta marekebisho?; Ni kiasi gani cha pesa zilikusanywa na mzabuni katika mwaka wa fedha 2009/2010? (yaani, kiasi gani alitoa kwa halmashauri na kiasi gani alibakiza); Je vijiji husika vimepata kiasi gani kama mrejesho kutokana na makusanyo hayo?

ii. Halmashauri kupoteza jumla ya shilingi 71,500,000.00 za ushuru wa leseni na adhabu zake

Taarifa ya mkaguzi wa ndani inaonyesha kuwa, jumla ya biashara mbalimbali zipatazo 1,430 kati ya 1,606 (sawa na asilimia 89) zinafanyika bila kuwa na leseni. Hii ni kinyume cha sheria ya biashara no. 25 ya mwaka 1972 (iliyofanyiwa marekebishomwaka2004).Mkaguzialitoamapendekezokuwaafisabiasharanamhasibu wa mapato wa wilaya wakishirikiana na watendaji wa vijiji wahakikishe kwamba watu wanaoendesha biashara bila leseni wapigwe faini kwa mujibu wa

Page 23: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-11-

sheria. Ripoti ya ufuatiliaji ya mkaguzi wa ndani haionyeshi ni hatua zipi za utekelezajizimefikiwa.Taarifayaufuatiliajiyamkaguziwandanihaitoimwelekeowowote juu ya hatua za uwajibikaji kupitia utekelezaji wa mapendekezo yake.

Timu ya UUJ ilitaka kupata ufafanuzi juu ya mambo yafuatato katika kipengele cha 3.2 cha ripoti ya mkaguzi;

• Kwaninimkaguziwandanianatoamapendekezonahatuazilizofikiwakwa uzito mdogo ambao hauleti tija katika uwajibikaji?;

• Ni kwanini biashara ziendelee bila ulipiaji wa lesseni wakati watendaji wapo?

• Hatua zipi zilichukuliwa kwa watendaji hawa?

• Je kati ya wafanyabiashara 1,430 wasiolipia lesseni, ni wangapi walipigwa faini kufuatia mapendekezo ya mkaguzi wa ndani, na kiasi gani cha fedha kilipatikana?

• Je katika mwaka wa fedha 2010/2011, jumla ya wafanyabiashara wangapi walilipia lesseni zao na kiasi gani cha fedha kilipatikana?

• Je wangapi hawakulipa na halmashauri imechukua hatua gani?

• Je hatua zipi za uwajibikaji zimechukuliwa kwa watumishi wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao na kuisababishia halmashauri hasara.

iii. Halmashauri kukosa jumla ya shilingi 21,500,000/- kutokana na kutokufanyika malipo kutoka mzabuni kinyume na mkataba

Taarifa ya mkaguzi wa ndani inaonyesha kuwa mzabuni alishindwa kuilipa halmashauri kiasi cha shilingi milioni 21.5 kwa mujibu wa mkataba. Fedha hizi ni za ushuru wa mifugo (mil 7), mazao (6.5 m), mazao ya asili (1.5m) na uvuvi (800,000) katika mwaka wa fedha 2009/2010. Mkaguzi wa ndani alimtaka mzabuni huyu kuilipa halmashauri kiasi hicho kama mkataba ulivyotaka. Uchambuzi wa timu ya UUJ unaonyesha kuwa ripoti ya ufuatiliaji ya mkaguzi wa ndani haionyeshi hatua zilizofikiwa na halmashauri katika kutekelezamapendekezo hayo.

Timu ya UUJ ilitaka kupata ufafanuzi juu ya mambo yafuatayo yaliyojitokeza katika kipengele cha 3.4 cha ripoti ya mkaguzi

• Kwanini mkaguzi wa ndani anatoa mapendekezo na haonyeshi hatua zilizofikiwakwauzitounaotakiwakatikakuletatijakatikauwajibikaji

• Je halmashauri imeshalipwa kiasi hiki cha pesa? na kimetumikaje?

Page 24: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-12-

Kama hakijalipwa, ni hatua zipi zimeshachukuliwa?

• Je kiasi gani cha fedha kimerejeshwa katika vijiji kama sheria za serikali za mitaa zinavyotaka.

iv. Mapungufu katika taarifa ya hali ya fedha za halmashauri 2009/2010

Taarifa ya mkaguzi wa ndani (uk. 11, 3.1) inaonyesha upungufu wa shilingi milioni 26.9 katika ziada ya halmashauri. Mkaguzi anataarifu kuwa hii inatokana na upotevu wa nyaraka zilizotumika kurekodi ziada. Aidha uongozi wa halmashauri uliahidi kufanya marekebisho ili kuweza kuondoa tofauti iliyobainishwa.

Timu ya UUJ ilitaka kupata ufafanuzi juu ya mambo yaliyojitokeza katika kipengele hiki cha ripoti ya mkaguzi wa ndani.

• Je wahusika walichukuliwa hatua zipi za uwajibikaji?

• Je, hatua zipi zimefikiwa katika kutekeleza mapendekezo yamakaguzi wa ndani? Ni tofauti ya kiasi gani iliweza kufanyiwa marekebishio?

v. Ukirimu (honoraria)

Halmashauri ilitumia jumla ya shilingi milioni 97,393,000.00 kama honoralia katika mwaka wa fedha 2009/2010 (uk 20 kipengele 13). Kwa wastani halmashauri ilitumia shilingi 8,160,083.00 kwa mwezi. Pia halmashauri ilitumia shilingi 21,000,000.00 kwa ajili ya kukirimu (uk 21, kipengele 14). Kiasi hiki ni kikubwa mno hasa kwa kuzingatia mahitaji ya huduma zingine muhimu. Timu ya UUJ ilihitaji kupatiwa mchanganuo wa matumizi haya.

Uwekezaji kwenye bodi ya mikopo ya serikali za mitaa

Halmashauri ilipanga kutumia kiasi cha shilingi 16,386,000.00 katika mwaka wa 2008/2009, na shilingi 44,040,000.00 katika mwaka wa fedha 2009/2010 kwa ajili ya bodi ya mikopo. Kiasi hichohicho (44 m) kilitumika katika mwaka wa fedha 2010/2011.

Timu ya UUJ ilitaka kupatiwa ufafanuzi juu ya matumizi haya. Mfano watumishi wangapi walipata mikopo hii na kwa kiasi gani kila mmoja kwa miaka yote miwili ya fedha. Je watumishi wangapi wa sekta ya afya walinufaika na mikopo hii. Timu pia inaomba kufahamishwa nini malengo ya mikopo hii na kiasi gani tayari kimesharudishwa.

Page 25: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-13-

2.5 Uchambuzi wa ripoti ya mkaguzi wa ndani robo ya pili (2010/2011)

i. Mapendekezo yaliyotolewa na mkaguzi wa ndani katika robo ya kwanza

Taarifa ya mkaguzi wa ndani (uk. 11, 3.1) inaonyesha upungufu ya shilingi milioni 26.9 katika ziada ya halmashauri. Mkaguzi anataarifu kuwa hii inatokana na upotevu wa nyaraka zilizotumika kurekodi ziada. Aidha uongozi wa halmashauri uliahidi kufanya marekebisho ili kuweza kuondoa tofauti iliyobainishwa. Katika ukaguzi wa robo ya pili, mkaguzi wa ndani anaarifu kuwa mapendekezo aliyoyatoa ili kusahihisha suala hili hayakufanyiwa kazi.

Timu ya UUJ ilitaka kujua ni nani wanahusika moja kwa moja na suala hili. Pia ilitaka kujua ni hatua zipi za uwajibikaji zimechukuliwa kwa watendaji hawa. Mwisho timu ilitaka kujua kama hatua zozote za marekebisho zimeshafanyika ili kuleta uwajibikaji kwa kutolea maelezo ya kina juu ya upungufu huu uliobainishwa wa fedha.

Mapendekezo yaliyotolewa na mkaguzi wa ndani katika robo ya kwanza juu ya mapungufu katika utendaji kifedha hayakufanyiwa kazi (uk 9). Mkaguzi wa ndani ameonyesha kutoa ushauri mzuri katika kuboresha shughuli za uendeshaji wa halmashauri kwa kupendekeza hatua za marekebisho. Menejimenti kwa upande wake imekuwa ikishindwa kutekeleza mapendekezo ya mkaguzi wa ndani aidha kwa makusudi ama kwa sababu zingine. Timu ya UUJ ilitaka kujua kwa nini menejimenti haikutekeleza ushauri na mapendekezo ya mkaguzi. Pia timu ilitaka kujua kama marekebisho haya yamefanyika.

Mkaguzi wa ndani aliishauri halmashauri kuwa na mfumo wa kutambua na kutoa taarifa juu ya mali zilizoharibika baada ya kugundua kuwa mali zenye thamani ya shilingi milioni 19,531,184,000.00 hazikuwa zimeripotiwa katika mfumo wa IPSAS 21 (uk. 10). Hata hivyo taarifa ya ufuatiliaji ya halmashauri katika robo ya pili (uk. 10) inaonyesha halmashauri kutokutekeleza mapendekezo haya. Timu ya UUJ inataka kujua kama utekelezaji wa mapendekezo haya ulifanyika. Na kama haujafanyika, nani anahusika na utoaji wa taarifa hizi, na hatua zipi zimechukuliwa na menejimenti kwa wahusika.

ii. Wafanyakazi kutokuwa na mafaili ya kumbukumbu zao

Mkaguzi wa ndani alifanya ukaguzi wa taarifa za malipo kati ya mwezi Agosti na Septemba 2010. Jumla ya rekodi za wafanyakazi 110 ziliangaliwa. Wafanyakazi 38 (sawa na asilimia 34.5) hawakuwa na mafaili ya taarifa za wafanyakazi; kati yao, wafanyakazi 10 walitoka sekta ya afya. Ripoti pia inaonyesha jumla ya wafanyakazi 53 (sawa na asilimia 48 ya walioangaliwa) hawakuwa na barua za kuajiriwa,

Page 26: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-14-

kinyume na taratibu za ajira, miongoni mwa hao, wafanyakazi 12 ni kutoka idara ya afya. Mkaguzi wa ndani alikadiria upotevu wa shilingi 126,850,680.00 kupitia mishahara hewa. Mkaguzi alipendekeza menejimenti ichukue hatua za kukagua wafanyakazi wake, na kwamba mafaili na taarifa za wafanyakzi ambazo hazikupatikanazitafutwe.Menejimentinaofisiyautumishiiliahidikulifanyiakazikatikamwakawafedha2011/2012nakuongezausimamizimakinikatikaofisiyamasijala.

Timu ya UUJ ilitaka kujua kama taarifa za wafanyakazi hawa zimepatikana. Kama bado, ni hatua zipi za uwajibikaji zimechukuliwa kwa wahusika. Timu pia ilitaka kujua ni kwa kiasi gani wafanyakazi hawa wameathirika katika masilahi yao kama vile kupandishwa madaraja, kupatiwa vyeo, mishahara, pensheni na stahiki zingine mbalimbali.

iii. Wafanyakazi kukaa katika muda wa uangalizi kwa kipindi kirefu

Katika kuchambua ripoti ya mkaguzi wa ndani, timu ilibaini kuwa jumla ya wafanyakazi 65 kati ya wafanyakazi 110 waliochunguzwa (sawa na asilimia 59) wamekaa kwa muda mrefu bila kuthibitishwa kazini. Idara ya afya pekee ilikuwa na wafanyakazi 14 ambao hawakuwa wamedhibitisha kazini. Ikumbukwe kwamba, mkaguzi alichukua sehemu tu ya taarifa za wafanyakazi na kuzifanyia kazi, na si wafanyakazi wote. Hivyo, idadi yaweza kuwa ni kubwa zaidi kama ukaguzi ungejumuisha wafanyakazi wote.

Timu ya UUJ ilitaka kujua kama hatua za uwajibikaji na marekebisho zilichukuliwa namenejimenti kwa pamoja na ofisi ya utumishi yawilaya, nakama wafanyakazi hawa tayari wamethibitishwa kazini. Timu pia ilitaka kujua ni jinsi gani wafanyakazi wameathirika katika masilahi yao kutokana na mapungufu haya. Mfano, kupandishwa madaraja/vyeo na mishahara, pensheni na stahiki zingine mbalimbali.

iv. Manunuzi kufanyika bila ridhaa ya bodi ya wazabuni ya halmashauri

Ripoti ya mkaguzi wa ndani inaonyesha kuwa wakuu wa idara na muidhini mkuu waliidhinisha jumla ya manunuzi 11 yanayozidi kiwango wanachoruhusiwa kisheria. Manunuzi haya yalifanyika bila kuyapitishwa kwenye bodi ya manunuzi ya halmashauri kinyume na taratibu za manunuzi, na kifungu cha sheria za manunuzi ya umma cha (2004). Mkaguzi aliwataka watendaji hawa kutoa taarifa kwenda kwa bodi ya manunuzi kuhusu manunuzi yote yaliyofanywa kinyume cha taratibu.

Page 27: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-15-

Timu ya UUJ ilitaka kupata ufafanuzi juu ya kiasi cha fedha kilichotumika kufanya manunuzi hayo. Aidha, timu inataka kujua aina ya manunuzi yaliyofanyika, na kwa nini wahusika waliyafanya kinyume cha taratibu za manunuzi. Vilevile timu ilitaka kujua kama wakuu hawa wa idara walitoa taarifa kimaandishi kama mkaguzi wa ndani alivyotaka.

Mkaguzi wa ndani alilipoti kwamba halmashauri haikuwa ikiandaa ripoti za robo mwaka za manunuzi na kuwataka wafanye hivyo (uk 13). Timu ya UUJ ilitaka kujua kama kitengo cha manunuzi kiliweza kuanda ripoti hizi na kuziwasilisha kwa muidhini mkuu, mkaguzi mkuu wa serikali (NAO), IA na PPRA.

v. Mapungufu katika usimamizi wa mfumo wa malipo

Mkaguzi wa ndani alipitia malipo 387 kati ya jumla ya malipo yote yaliyofanywa na halmashauri (uk 14). Ripoti yake inaonyesha kuwa malipo sita (sawa na asilimia 1.6) yalifanyika bila ukaguzi wa awali na malipo 62 (sawa na asilimia 19) hayakuonyesha stakabadhi za kukubali kupokea kwa waliolipwa. Hii ni kinyume cha taratibu za malipo na sheria zinazosimamia fedha za serikali za mitaa. Na pia inatoa mwanya kwa matumizi mabaya na kuwepo kwa maswali mengi ya kiukaguzi. Mapendekezo ya mkaguzi yaliitaka halmashauri kuhakikisha kuwa inafanya ukaguzi wa kila mwezi na robo mwaka katika vocha za malipo.

Timu ya UUJ inaona kuwa mapendekezo haya hayaleti uwajibikaji kwa makosa yaliyofanyika. Timu ilitegemea kuona mkaguzi wa ndani akishauri risiti za malipo zipatikane ili kujiridhisha kama malipo haya yalifanyika kwa kufuata taratibu za fedha. Aidha timu ilitaka kujua ni kiasi gani cha fedha kililipwa bila kufuata taratibu za fedha za serikali za mitaa (LGAFM) kwa kuwa kiambatanisho (uk 24) katika ripoti ya mkaguzi wa ndani ya robo ya pili hakionyeshi kiasi cha fedha.

Pia, ripoti ya mkaguzi (kiambatisho II, uk. 24) inaonyesha jumla ya malipo 68 yalifanyika bila kuwa na nyaraka za uthibitisho. Hiki ni kinyume cha taratibu na sheria za usimamizi wa fedha za halmashauri (LAFM). Timu ilitaka kujua ni hatua zipi za uwajibikaji zilichukuliwa kwa watendaji husika.

2.6 Uchambuzi wa ripoti ya mkaguzi mkuu wa serikali mwaka wa fedha 2009/2010

Halmashauri ya wilaya ya Singida ilipata hati safi ya mkaguzi mkuu wa serikalikatika mwaka wa fedha 2009/2010, ikiwa na maeneo kadhaa ya msisitizo yaliyoitaka halmashauri kufanya marekebisho. Eneo mojawapo la msisitizo ni lile la halmashauri kuingia mikataba na kampuni binafsi kukusanya mapato kwa niaba ya halmashauri.

Page 28: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-16-

Mkaguzi mkuu alibainisha kuwa, pamoja na kutakiwa kuwasilisha makusanyo hayo kila tarehe 25 ya mwezi kwa mujibu wa mkataba, wakusanyaji hawakufanya hivyo. Timu ya UUJ ilitaka kujua kama utekelezaji wa mapendekezo ya mkaguzi mkuu ulifanyika na hatua zipi za uwajibikaji zilichukuliwa kwa wahusika.

Katika kipindi cha mwaka wa fedha kinachoishia Juni 30 mwaka 2011 Mkaguzi mkuu wa Serikali Aligundua mambo yafuatayo katika taarifa ya matumizi ya fedha katika halmashauri ya wilaya ya Singida.

i. Fedha za maendeleo hazikutumika

Mkaguzi mkuu wa serikali aligundua kwamba halmashauri ilikuwa na kiasi cha shilingi 2,744,797,960 ambazo kati ya hizo shilingi 1,058,418,000 zilitumika katika kukamilisha miradi ya maendeleo, na kuacha kiasi kisichotumika cha shilling 1,686,561,960 ambacho ni sawa na asilimia 61.4. Kutotumika kwa kiasi hicho cha fedha kunamaanisha kwamba baadhi ya miradi ya maendeleo ilikamilika nusu ama haikukamilika kabisa.

Jambo linalopelekea kucheleweshwa kwa maendeleo ya upatikanaji wa huduma za jamii na haki za msingi. Pia, inaweza kuongeza gharama zaidi kama fedha hazikutumika katika muda husika kutokana na mfumko wa bei. Maswali yanayohitaji ufafanuzi ni kwa nini halmashauri inashindwa kutumia fedha hizi wakati inakabiliwa na changamoto nyingi za utoaji wa huduma kwa jamii. Ikumbukwe kwamba changamoto hizo zimeainishwa kwenye mpango mkakati wa halmashauri.

• Nini majibu na menejimenti kwa mkaguzi mkuu wa serikali?

• Hatua zipi za marekebisho ama uwajibikaji zimechukuliwa na watendaji?

ii. Kucheleweshwa kuhamishwa fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo

Jumla ya kiasi cha shilingi milioni 820,648,000.00 hazikuhamishwa kwa muda uliopagwa kutoka kwenye mfuko wa pamoja wa fedha za wadhamini wa afya (HBF) kwenda kutekeleza shughuli mbalimbali zilizopangwa. Hii ilipelekea kuchelewa kwa fedha hizo kati ya kipindi cha mwezi mmoja hadi miezi miwili. Kutokana na kucheleweshwa huku, pia ilipelekea kuchelewa kwa utekelezaji wa kazi zilizopangwa.

• Je, ni sababu zipi zilizopelekea kuchelewa kwa fedha hizi?

• Ni hatua zipi za uwajibikaji zilichukuliwa kwa wahusika ?

• Je, halmashauri imejipanga vipi kuzuia tatizo hili lisijirudie tena?

Page 29: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-17-

iii. Fedha za mfuko wa afya wa jamii (Mfuko wa afya wa jamii) ambazo hazikutumika

Ripoti ya mkaguzi mkuu wa serikali inaonyesha kwamba halmashauri ilikuwa haijatumia kiasi cha shilingi milioni 306,298,000/- ambazo ni fedha za mfuko wa afya wa jamii. Hii inamaanisha kwamba huduma za afya zilizotarajiwa kuwafikiawananchiwahalmashaurihiikupitiamfukowaafyayajamiihazikufikaipasavyo. Hali hii ni kutowatendea haki wachangiaji kwa kukosa huduma zao za msingi. Pia, inaweza kuwa ndio inayosababisha matokeo hasi katika uchangiaji wa mfuko huu (kushuka kwa mwamko wa uchangiaji).

Timu ya UUJ ilitaka kujua sababu zilizofanya fedha hizi zisitumike wakati vituo vya afya vikikabiliwa na ukosefu mkubwa wa dawa, mafuta kwa ajili ya magari ya kuhudumia wagonjwa na changamoto nyingine nyingi katika sekta ya afya.

iv. Kuchelewa Kurejeshwa Benki Mishahara ambayo haikulipwa

Kulikuwa na ucheleweshwaji wa urejeshaji (kati ya siku 6 hadi miezi 2) wa mishahara ambayo haikulipwa, kiasi cha shilingi milioni 36,539,700.00. Hii ni kinyumenautaratibuuliowekwa juuyamishahara ambayohaijalipwa (Rejea:barua ya mweka hazina yenye kumbukumbu namba EB/AG/5/03/01/Vol.VI/136 ya 31/08/2007).

Timu ya UUJ ilitaka kujua ni nini kinachokwamisha fedha hizi kuhifadhiwa benki kwa wakati. Je ni kiasi gani cha pesa kilirudishwa? Je uongozi hauoni kwamba hali hii inaweza kuchochea ubadhirifu wa fedha za umma? Hatua zipi za uwajibikaji zilichukuliwa kwa wahusika.

v. Mfumo Duni wa Usimamizi wa Ndani

Mfumo wa usimamizi wa ndani wa halmashauri umeonekana kuwa duni kwa kiasi fulani kutokana na kutofanya kazi vizuri kwa kitengo cha ukaguzi wa mahesabu ya ndani pamoja na kamati ya ukaguzi wa ndani. Kutokana na hali hiyo mapungufu mengi hujitokeza kama vile kutolewa kwa ripoti za fedha zenye makosa, kushikiliwa kwa muda mrefu mishahara ambayo haikulipwa na kushikiliwa kwa fedha za vijiji pasipo kuingiliwa na uongozi wa halmashauri. Mambo yote haya yaliyotajwa yanaonyesha jinsi gani usimamizi wa ndani wa halmashauri ulivyo na mapungufu.

Timu ya UUJ inaona kuwa iwapo hatua za haraka za marekebisho hazitachukuliwa kadri muda unavyokwenda, mfumo wa ukaguzi wa ndani wa halmashauri utashindwa kabisa kulinda mali na uendeshaji wa halmashauri hii. Na matokeo

Page 30: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-18-

yake ni kutoa mwanya wa matumizi mabaya ya rasilimali za umma. Timu ya UUJ ilitaka kufahamu hatua za marekebisho na uwajibikaji zilizochukuliwa na watendaji dhidi ya mapendekezo ya mkaguzi mkuu wa serikali. Pia, halmashauri imejipanga vipi kuimarisha mfumo wake wa usimamizi wa ndani ili kuepuka madhara yaliyoainishwa na mkaguzi mkuu wa serikali.

vi. Mawakala wa Ukusanyaji Mapato Kukosa Kuwasilisha Fedha za Makusanyo ya Halmashauri

Makusanyo ya mapato ya ndani kiasi cha shilingi milioni 21,680,000.00 hayakuwasilishwa kwenye halmashauri na mawakala mbalimbali wa ukusanyaji mapato walioingia mkataba na halmashauri. Aidha ripoti ya mkaguzi mkuu inaonyeshakuwepokwamawakalaambaowalifikishwamahakamanikutokanana kushindwa kutimiza mikataba yao. Hii ni moja kati ya mambo yanayoonyesha mapungufu katika usimamizi wa mikataba ambayo hupelekea kupotea kwa mapato ama fedha za halmashauri.

• Jenimawakalawangapiwalifikishwamahakamaninawanadaiwakiasigani cha fedha?

• Mashauri mangapi yameshakamilika na halmashauri imefaidika vipi?

vii. Kulipwa kwa Makosa kwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) Kiasi cha Shilingi 7,380,562/-

Jumla ya kiasi cha shilingi 7,380,562/- iligharamiwa na halmashauri kwa ajili ya program ya ASDP kinyume cha utaratibu na maelekezo ya kifungu namba 13.2.2 cha makubaliano (MOU) cha ASDP. Halmashauri inatakiwa kudai kiasi hicho kutoka kwa ASDP.

• Je, halmashauri imechukua hatua gani hadi sasa ya kudai fedha hizo kutoka kwa ASDP?

• Je, kwa nini malipo yalifanyika pasipo uongozi wa halmashauri kufuata taratibu za makubaliano yake na ASDP?

• Ni hatua zipi za uwajibikaji zilichukuliwa?

viii. Kujumuishwa kwa Akaunti za Halmashauri bila Maelezo ama Taarifa

Ripoti ya mkaguzi mkuu wa serikali inaonyesha kuwa akaunti tatu zilijumuishwa kwenye akaunti za serikali na kuchukuliwa kwenda benki kuu ya Tanzania bila taarifa yoyote kwa halmashauri. Akaunti hizi zilikuwa na kiasi cha shilingi 18,216,234/- ambacho mpaka leo hakijarudishwa kwenye halmashauri ya Singida.

Page 31: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-19-

• Je ni akaunti gani zilihusika na zoezi hili?

• Je, halmashauri ilichukua hatua gani kuhakikiksha fedha hizo zinarudishwa katika akaunti yake ili zisaidie katika miradi mbalimbali ya maendeleo?

• Je fedha hizi zimesharudishwa, na kama ndiyo zimetumika kwa malengo yaliyokusudiwa?

ix. Fedha za Michango ambazo hazikuhamishiwa kwenye Serikali za Vijiji

Ripoti ya mkaguzi mkuu wa serikali inabainisha kuwa, kwa kipindi cha miaka mitatu (3) iliyopita uongozi wa halmashauri haukupeleka kwenye serikali za vijiji kiasi cha shilingi 177,398,290.00. Kiasi hiki cha fedha ni asilimia ishirini ya fedha zote ziliyopokelewa kama mbadala wa kodi za usumbufu. Hivyo halmashauri ilienda kinyume na maelekezo ya mweka hazina kifungu 9 (e) cha kifungu cha sheria cha uendeshaji wa fedha wa serikali za mitaa (LGFA) namba 9 cha mwaka 1982. Pia ni kinyume cha agizo namba 91 la makubaliano ya matumizi ya fedha ya serikali za mitaa (LAFM) ya mwaka 1997 ambalo linaainisha vyanzo vya mapato kwa ajili ya halmashauri za vijiji.

Aidha, fedha hizo hazikuonyeshwa kwenye taarifa ya fedha chini ya matumizi ya muda. Madhara ya kuvunjwa utaratibu huu ni pamoja na kushindwa kutekeleza kazi mbalimbali zilizopangwa na serikal za vijiji kutokana na kukosekana kwa fedha.

• Je ni sababu gani zinafanya fedha hizi zisipelekwe serikali za vijiji kwa miakamitatumfululizo ikiwamisaada hii inaifikia halmashauri kamainavyotakiwa?

• Je ni vijiji vingapi (kwa majina) havikupata fedha hizi? Na kiasi gani cha fedha kwa kila kijiji?

• Je fedha hizi zilitumika kwa shughuli gani?

• Na kama hazikutumika je halmashauri iko tayari kuzipeleka fedha hizi kwa vijiji husika?

x. Kazi ambazo hazikufanyika kutokana na mpango kazi kiasi cha shilingi 4,934,318,716.00

Ripoti ya mkaguzi mkuu wa serikali imebainisha kuwa kazi za maendeleo zenye thamani ya shilingi 4,934,318,716.00 hazikutekelezwa kama ilivyopangwa. Aidha mkaguzi huyu alibainisha pia kuwa kucheleweshwa ama kutotekelezwa kabisa kwa miradi kunaweza kupelekea gharama za miradi kubadilika hivyo kufanya

Page 32: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-20-

miradi kutekelezwa kinyume cha matarajio ya hamlashauri. Kiasi hiki kikubwa cha fedha hakikutumika wakati jamii zikikabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa dawa katika vituo vya kutolea huduma.

• Je nini kinasababisha halmashauri isitekeleze mpango kazi wake kama ilivyokusudiwa?

• Na kwanini tatizo hili linaonekana kujirudia bila kuchukuliwa hatua zozote za marekebisho?

xi. Mishahara Iliyocheleweshwa Kwenda kwa Afisa Tawala wa Mkoa

Kulikuwa na ucheleweshwaji wa kati ya miezi 2 hadi 8 wa malipo ya mishahara kwendakwaAfisaTawalawamkoakinyumenamaelekezoyawizarayaTawalaza Mikoa na Serikikali za mitaa na maelekezo ya mweka hazina.

• Je nini chanzo cha tatizo?

• Je ni nani walipelekea ucheleweshaji huu na hatua zipi za uwajibikaji zilichukuliwa?

• Yepi madhara ya ucheleweshaji huu?

xii. Kukwama kwa Matokeo ya Ukaguzi na Maelekezo ya Ndani

Kumekuwepo na udhaifu katika kutekeleza matokeo, mapendekezo na maelekezo ya ukaguzi wa ndani. Halmashari ilihitaji kiasi cha shilingi 16,664,734,404. Hii inakwamisha juhudi kuongeza mazingira bora zaidi ya usimamizi wa ndani pamoja na usimamizi mzuri wa kifedha ndani ya halmashauri. Timu inaamini kuwa mengi ya mapendekezo ya mkaguzi wa ndani hayahitaji kiasi kikubwa cha fedha kuyatekeleza.

• Je kwanini kunakuwa na ukwamishaji wa pesa kwa ajili ya kutekeleza wajibu na shughuli za mkaguzi wa ndani?

• Je halmashauri haioni kuwa kutotekelezwa kwa majukumu hayo kunasababisha matumizi mabovu ya fedha za umma?

xiii. Ripoti za Utekelezaji wa Shughuli Mbalimbali za Sekta ya Afya 2010/2011

Tathmini ya utoaji wa huduma ilifanyika kwa kurejea shughuli zilizotekelezwa na halmashauri kwa mwaka 2010/2011. Timu ilifanya mapitio ya mpango ya afya (2010/11) na taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali za halmashauri katika mwaka wa fedha. Baada ya mapitio ya taarifa hizo, timu ilitembelea vituo vya kutolea huduma za afya vinavyohudumiwa na halmashauri. Zahanati 21, vituo vya afya vitano na hospitali teule ya Makiungu vilitembelewa. Zoezi hili lililenga kufuatilia na

Page 33: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-21-

kutathmini hali ya utekelezaji wa miradi mbalimbali kama ilivyoainishwa katika ripoti za utekelezaji. Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi ama ukarabati wa vituo, nyumba za watumishi pamoja na vyoo. Vilevile uwepo na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba na samanizaofisi.Timupia ilifuatiliauwepowawatumishiwaafyakatikavituo,ilitathmini suala zima la huduma zitolewazo katika kituo husika na changamoto mbalimbali zinazokabili utoaji wa huduma za afya katika wilaya.

Katika ripoti za utekelezaji wa miradi ya afya (2010/2011), halmashauri ilionesha kutekeleza ujenzi na ukarabati wa vituo vya huduma, nyumba za watumishi pamoja na vyoo kutoka vyanzo mbalimbali vya fedha ikiwemo MMAM na basket fund. Jumla ya shilingi 614,672,550.00 (ambazo ni 438,821,550.00 bakaa ya 2009/10 na 175,851,000.00) zilipokelewa katika mwaka 2010/11. Kiasi hiki cha fedha kilitengwa kwa ajili ya ukarabati wa majengo mbalimbali zikiwemo nyumba za watumishi, vituo vya huduma na vyoo. Hata hivyo, ni shilingi 237,738,550.40 tu, ambazo ni sawa na asilimia 38.7 ya jumla ya fedha zilizokuwepo ndizo zilitumika. Hii inaonyesha kuna kiasi kikubwa cha fedha hakikutumika

Page 34: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-22-

SEHEMU YA III: HOJA ZILIZOIBULIWA NA TIMU YA UUJ KUHUSU HALI YA HUDUMA

Kwa kuptitia Uchambuzi wa nyaraka, timu ya UUJ ya Singida iliibua masuala na ama shughuli mbalimbali zilizoripotiwa kutekelezwa katika Hospitali, vituo vya afya na zahanati za umma na kuandaa dodoso maalum lililoonesha shughuli na hali ya utekelezaji kama zilivyoripotiwa katika mipango ya mwaka ya afya pamoja na ripoti zake za utekelezaji kwa kila kituo.

Timu ya UUJ ilitembelea jumla ya vituo 21 ili kujiridhisha juu ya hali ya utekelezaji wa miradi/shughuli hizo kwa kulinganisha kilichoripiotiwa katika vitabu kwa kulinganisha fedha zilizotumika na muda wa utekelezaji na baadaye kutoa maoni yao juu ya hali halisi ya miradi/shughuli hizo kama walivyozikuta kipindi cha ziara.

Baada ya kuandaa ripoti, timu ya UUJ iliiwakilisha katika timu ya Uendeshaji wa Huduma za afya ya halmashauri na kutoa ufafanuzi, uthibitisho na uhalalisho juu ya masuala yote yaliyoibuliwa na timu. Baadaye timu ya UUJ iliandaa mkutano wa pamoja na uongozi wa halmashauri na wadau wa afya na UKIMWI ili kutoa mrejesho wa utekelezaji wa zoezi la UUJ na kuweka mikakati ya pamoja juu ya namna ya kuboresha huduma wilayani Singida.

3.1 Hoja kuhusu umakini na ufanisi wa halmashauri kutekeleza bajetiMwakilishi wa idara ya afya daktari Mbando kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Singida alieleza kuwa sababu ya miradi mingi kutotekelezwa kwenye kipindi cha mwaka wa fedha 2010/2011 ni kutokana na kuchelewa kupatikana kwa fedha, ambapo Serikali ilileta fedha katika robo ya nne ya mwaka ; hivyo kufanya fedha isiweze kutumika kikamilifu na hivyo kufanya miradi iliyotekelezwa kuwa michache tofauti na ilivyopangwa.

3.2 Kuhusu Bakaa Kubwa katika Sekta ya Afya kwa Mwaka 2010/2011Mwakilishi wa Timu ya Afya ya Wilaya alieleza kuwa fedha iliyobaki hadi Juni 30 2011 ilikuwa ni shilingi 799,707,804.12 kama ifuatavyo:-OCTsh.4,520,000BasketTsh 24,290,000, MMAM Tsh 423,778,986.68,Tunajali Tsh 3,207.60 na BMAF Tsh. 90,266.52, Fedha nyingine zilizobaki ni za MMAM na Mfuko wa afya wa jamii, Alifafanua kuwa malipo ya fedha za MMAM yanategemea kasi ya ukamilishaji wa

Page 35: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-23-

miradi husika kwa kuwa miradi ya MMAM inategemea mchango wa jamii. Aidha alisema kuwa fedha za Mfuko wa afya wa jamii hazitumiki tu ili zionekane zimeisha kwenye akaunti bali matumizi yake hutegemea mahitaji ya vituo, ambapo kituo husika huomba fedha pale kunapokuwa na haja ya kufanya hivyo.

Mwaka 2010/2011 Idara ya afya ilipanga kutekeleza shuguli 155 na ilitekeleza shuguli 141(91%) na bajeti ilikuwa Tsh. 5,361,059,911, Idara ilipokea sh 4,432,923,143.17 sawa na 82.69% na zilitumika Tsh 4,285,900,212.59 sawa na 84.3%.

3.3 Kuhusu Upatikanaji wa Taarifa za Utekelezaji za Halmashauri na Idara ya Afya kwa Ujumla

Taarifa zote za utekelezaji huwasilishwa katika vikao mbalimbali vya kisheria kuanzia bodi ya huduma za afya ya halmashauri, kamati ya huduma za jamii, kamati za fedha, mipango na uongozi na baraza la madiwani kila robo kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za utoaji taarifa za serikali ili kudumisha utawala bora.

3.4 Kuhusu Ukaguzi wa Ndani na wa Nje katika HalmashauriKuhusu hoja za ukaguzi wa ndani na wa nje katika halmashauri Dk. Mbando alieleza kuwa hoja hizi zilikwishafungwa na mdhibiti na makaguzi mkuu wa serikali (CAG), baada ya ukaguzi kufanyika na majibu kutolewa. Alifafanua kuwa hakuna chombo kingine kinachoruhusiwa kisheria kuhoji kazi za CAG. Alihitimisha kwa kueleza kuwa ufungaji wa hoja hizi ulifuata taratibu za kisheria za kujibu ufungaji wa hoja za ukaguzi.

3.5 Kuhusu Wafanyakazi Kutokuwa na Mafaili ya Kumbukumbu zaoDkt. Mbando alieleza kuwa sio kweli kwamba wafanyakazi 38 hawana mafaili ya kumbukumbu zao na 53 hawana barua za ajira, na sio kweli kuwa kuna upotevu wa Tsh 126,850,680 kupitia mishahara hewa. Watumishi wote wanayo mafaili na barua zaajiranazakuthibitishwakazini,piaofisihaijapokeamalalamikoyoyotekutokakwawatumishi kupitia dawati la malalamiko la watumishi kuwa wamekaa katika kipindi cha uangalizi kwa kipindi kirefu kama timu ya UUJ ilivyoeleza kutokana na taarifa ya CAG.

3.6 Hoja kuhusu utekelezaji wa shughuli katika vituo vya huduma

i. Hospitali ya Makiungu Ripoti ya utekelezaji ya idara ya afya ileleza kuhusu ukarabati jego la TB katika hospitali hii kwa gharama ya shilingi 26,100,900. Timu ya UUJ ilipotembelea ili kujionea ukarabati uliofanywa na kuona kuwa jengo lilikuwa linatumika. Timu iliipongeza idara ya afya kwa jitihada za kuhakikisha kuwa ukarabati ulifanyika kama ilivyopangwa.

Page 36: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-24-

ii. Kituo cha afya cha Ikungi Katika ripoti yake ya utekelezaji Idara ya Afya ilieleza kuwa kulikuwa na ujenzi wa jengo la huduma ya mama na mtoto katika kituo cha Ikungi pamoja na ukarabati wa kituo cha Matunzo na Matibabu.

Timu ya UUJ ilipotembelea ilithibitisha kuwepo kwa jengo la huduma ya mama na mtoto na inafanya kazi ingawa hakuna huduma ya uhakika ya maji hivyo kulazimu Wajawazito kutumia vyoo vya nje ambavyo havikuwa katika hali ya kuridhisha kiafya. Ilielezwa kuwa kituo kilikuwa kimeruhusiwa kutumia maji kutoka Mfuko wa afya wa jamii na kuyaingiza jengo la huduma ya mama na mtoto lakini kazi hiyo ilikuwa haijafanyika. Pia kulikuwa na changamoto ya dawa kupelekwa kidogo, wakati mwingine zilipelekwa tofauti na walizoagiza. Kituo cha Matunzo na Matibabu kilikuwa kimekarabatiwa kama ilivyobainishwa na kinafanya kazi ambapo Timu ilipongeza jitihada hizo.

Tofauti na vituo vingine, katika kuboresha rufaa kwa wagonjwa kituo cha afya Ikungi kina magari mawili ya kubebea wagonjwa ambapo moja ni gari/bajaji yenye magurudumu matatu. Hata hivyo, gari/bajaji hiyo iliyopo katika hali mbaya haijawahi kufanyakazi tangu ikabidhiwe kituoni hapo, huku sababu zilizotolewa ni ubovu wa betri pia kutokuwepo na dereva wa kuendesha gari/bajaji hiyo.

Kushoto: Mjumbe wa timu ya UUJ akifunua blanketi lililofunikiwa gari ya wagonjwa ya magurudumu matatu

Kulia: Gari ya kubebea wagonjwa ikiwa imevunjika vioo na kutelekezwa katika kituo cha afya Ikungi

Page 37: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-25-

Majibu ya Menejimenti: Kuhusu changamoto zilizoonekana, Dkt. Mbandoalieleza kuwa mchakato wa uingizaji maji katika jengo la huduma ya mama na mtoto ulikuwa unaendelea kufanyika kupitia mfuko wa Mfuko wa afya wa jamii. Ilielezwa pia kuwa gari la kubeba wagonjwa lililopo kituo cha afya Ikungi lililetwa kama msaadanaBMAF.Kwavilekituohikikwasasakinagarilawagonjwa,idarainafikiriakuhamishia gari hilo la magurudumu matatu katika kituo kingine mara itakapopata kibali toka BMAF.

iii. Kituo cha afya Sepuka

Katika mpango wa afya, halmashauri iliripoti kufanya ukarabati wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) na nyumba ya watumishi; pamoja na ujenzi wa jengo jipya la wagonjwa wa nje kwa bajeti ya shilingi 66,901,811/-. Katika ripoti ya utekelezaji, halmashauri iliripoti kuwa ukarabati wa OPD na nyumba ya watumishi umekamilika vilevile ujenzi wa jengo jipya la wagonjwa wa nje mpya limepauliwa na kuwekwa milango na madirisha kwa kiasi cha shilingi 44,074,982/-. Halmashauri pia ilipanga kufanya Ujenzi wa nyumba 1, choo 1, bafu 1, jiko 1, stoo 1 na uzio na kutenga bajeti ya shilingi 20,000,000/= pamoja na ununuzi wa dawa na vifaa tiba vikiwemo vitanda vya kuzalishia na vya kupumzikia, magodoro pamoja na mashuka.

Hali halisi: Timu ya UUJ ilipotembelea kituo hicho ilikuta mapungufu mengi katika kituo kama vile nyufa katika kuta za vyoo pia vyoo hivyo vikiwa vimejaa. Timu pia ilibainisha changamoto ya upungufu wa dawa na watumishi katika kituo hicho. Timu ya UUJ ilitaka sababu ya kuwepo kwa hali hiyo, pia kupata ufafanuzi juu ya uwepo wa vikundi vya WAVIU na kama wanawezeshwa kwa kupewa lishe.

Majibu ya menejimenti: Mwakilishi wa menejimeti Dokta Mbando, alitoa ufafanuzi kuwa nyumba moja ilikuwa kwenye mpango wa ukarabati wa kubadilishwa kutoka Jengo la wagonjwa wa nje na kuwa nyumba ya watumishi. Ujenzi huo umefanyika na kukamilika ikiwa ni pamoja na kujenga upya uwa wenye jiko pamoja na vyoo, bafu na stoo.Ufauliojitokezaumesababishwanakuhitilafianakulikotokananakuunganishwajengo jipya na la zamani. Nyumba nyingine pamoja na kuwa ni chakavu hazikuwa kwenyempangowaukarabatikwamwakahusika,hiinikutokananaufinyuwabajeti.Kila mwaka idara inaomba fedha kwa ajili ya ukarabati wa nyumba za watumishi.

Kuhusu hoja ya vyoo vilivyojaa Dk. Mbando alieleza kuwa vyoo hivyo ni vya nyumba za zamani, na ushauri ulitolewa kuwasilisha hoja hiyo kwenye baraza la maendeleo la katanapindifedhaikipatikanaofisiitajengavyoovingine.

Page 38: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-26-

Vikundi vya WAVIU vipo na ni hai, pia lishe ipo na inatolewa kupitia vikundi hivyo kwa utaratibu maalumu kwa sasa kuna chakula cha RUTF na vyakula vya ziada kama mchele, maharage, mafuta, sukari na unga. Vyakula hivi hutolewa tu pindi fedha zinapopatikana, na hugawiwa kupitia vituo vya matunzo na matibabu.

iv. Kituo cha afya Ihanja

Katika kituo cha afya Ihanja, halmashauri iliripoti kufanyika kwa ukarabati wa nyumba tatu za watumishi, jiko 1, bafu 1 na stoo 1 na Jengo la wagonjwa wa nje pamoja na upanuzi wa TB clinic ambayo iliwekwa marumaru kwa gharama za shilingi 47,793,000/-.Hata hivyo timu ilipotembelea, ilikuta nyumba za watumishi zilizofanyiwa ukarabati na sio ujenzi kama ilivyoainishwa kwenye taarifa, vilevile hapakuwa na stoo wala bafu. Kazi ya upanuzi wa jengo la TB na kuweka marumaru sakafuni hazijafanyika kabisa.

Kituo hakikuwa na uzio, zaidi ya hayo ubao wa matangazo na sanduku la maoni havitumiki. Kulikuwa na upungufu wa watumishi watatu na 10% ya CHF hazirejeshwi kituoni. Timu pia ilitaka ufafanuzi kwa nini gari la kituo halikuwepo kwa muda wa miezi miwili kituoni.

Majibu ya menejimenti: Timu ya UUJ ilipohoji juu ya maswala haya, Dkt. Mbando alieleza kuwa katika mpango hakukuwa na mradi wa ujenzi wa nyumba bali kulitengwa fedha kwa ajili ya ukarabati wa nyumba tatu za watumishi. Kazi hii ulifanyika pamoja na kujenga vyoo na stoo katika nyumba mbili za watumishi. Aliendelea kueleza kuwa hakuna fedha iliyotengwa kwa ajili ya kujenga uzio wa kituo na upanuzi wa jengo la TB kama ilivyoelezwa kwenye ripoti ya timu ya UUJ.

v. Zahanati ya Mwaru

Halmasahuri iliripoti kukamilisha ukarabati wa jengo la huduma ya mama na mtoto pamoja na ujenzi wa uzio wa nyumba ya mganga wa zahanati ya Mwaru. Vilevile Ripoti ya utekelezaji wa Miradi ya Afya ilionesha kuwa kituo kilipokea kitanda cha kujifungulia na magodoro 2 yenye thamani ya shilingi 350,000 vitanda viwili vya kupumzishia wagonjwa (kila kimoja kwa shilingi 170,000) pamoja na Screen fold na mapazia mawili (kila moja kwa shilingi 100,000).

Hali halisi: Katika ziara ya tathmini, timu ilibaini kutokutekelezwa kwa baadhi ya shughuli za ujenzi kama ilivyooneshwa katika ripoti za utekelezaji kwani hakuna ukarabati wowote uliofanyika kwani jengo halina sakafu, lina nyufa, dari imeharibika na paa linavuja wakati wa mvua. Nyumba ya mganga haikuwa na uzio ulioripotiwa kujengwa. Katika bajeti ya 2011/12, kituo kiliidhinishiwa tena kutumia kiasi cha

Page 39: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-27-

1,000,000/- kutoka mfuko wa Bima ya afya ya Jamii hali inayozua wasiwasi kuhusu zilivyotumika fedha zilizotengwa kutumika mwaka 2010/11. Timu imebaini kuwa hakuna vitanda wala vifaa tiba vilivyopelekwa kituoni kwa mwaka 2010/2011. Vitanda vilivyopo kimoja cha kujifungulia na kingine cha uchunguzi ni vya zamani.

Zahanati inakabiliwa na upungufu wa dawa na vifaa tiba kwani zinazoletwa hazitoshelezi mahitaji ya kituo. Vilevile uhifadhi wa dawa si salama kwani stoo ya kuhifadhia ni chakavu na inavuja, pia hakuna matrei ya kuwekea dawa hivyo dawa zinawekwa juu ya meza. Kituo kina ubao wa matangazo lakini upo ndani ya chumba cha mganga hivyo hautumiki na wananchi kupata tarifa mbalimbali kama ilivyokusudiwa na wala hakuna sanduku la maoni. Hakuna uwezeshaji wa WAVIU wanapopata rufaa.

Halmashauri iliripoti kutumia jumla ya shilingi 90,336,000/- kwa ajili ya ujenzi wa wodi za wazazi katika vituo vinne, ikiwemo zahanati ya Ntuntu. Hata hivyo, baada ya timu kutembelea, haikukuta ujenzi wowote ulioanza na wala mganga wa kituo hakuwa na taarifa juu ya shughuli hiyo.

Majibu ya menejimenti: Mwakilishi wa menejiment, Daktari Mbado alieleza kuwa kazi ya ukarabati wa jengo la kliniki ya huduma za mama na mtoto ilikuwa ifanyike kwa fedha za Mfuko wa afya wa jamii na kamati ya afya ya Zahanati iliomba Tsh 1,000,000 na ziliidhinishwa, lakini timu ya usimamizi ilipotembelea jengo hilo iliona kuwa fedha zilizoombwa ni kidogo kulingana na uchakavu wa jengo, na kushauri mhandisi aende kufanya makisio ya kitaaluma (BOQ) kazi ambayo bado haijatekelezwa na fedha ziilizoombwa awali hazijatolewa.

vi. Zahanati ya Wibia

Taarifa ya utekelezaji ya idara ya afya ilionesha kuwa kumefanyika ujenzi wa nyumba ya wafanyakazi kwa gharama ya shs 105,851,000, pia kulifanyika ujenzi wa vyoo katika zahanati tano ikiwemo Wibia kwa gharama ya shs 16,800,000/-.

Hali halisi: Timu ya UUJ ilipotembelea ilikuta hakuna nyumba ya mfanyakazi iliyojengwa kama ilivyoelezwa kwenye taarifa, badala yake ilijengwa nyumba ya mfadhili kwa ajili ya shule, zahanati ilijengwa kwa nguvu ya wananchi, halmashauri na mfadhili. Choo kilichokuwepo ni cha shimo cha kawaida na sio VIP kama ilivyoainishwa katika ripoti. Vilevile mganga wa kituo anakaa umbali wa km 4 kutoka kituoni hali ambayo huleta ugumu mara inapotokea dharura, ilidhihirika kuwa kituo kina upungufu wa wafanyakazi.

Page 40: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-28-

Majibu ya menejimenti: Timu ya UUJ ilipotaka maelezo, daktari Mbado kwa niaba ya idara ya afya alieleza kuwa ni sahihi kutolewa taarifa ya nyumba ya watumishi iliyojengwa na mfadhili kulingana na makubaliano ya serikali ya kijiji na mfadhili, ambapo nyumba ilijengwa kwa ajili ya mganga na mwalimu katika eneo la zahanati na mganga mfawidhi anakaa upande mmoja. Vilevile Ilielezwa kuwa mtumishi mwingine wa zahanati amepewa nyumba shuleni ambayo ipo umbali wa chini ya kilometa moja toka kwenye zahanati na siyo umbali wa kilometa 4 kama ilivyohojiwa na timu ya UUJ.

vii. Zahanati ya PumaZahanati ya Puma iliripotiwa kufanyiwa ujenzi wa choo na ukarabati wa nyumba ya mtumishi, choo 1 (VIP), bafu 1, jiko 1 na stoo kwa gharama ya shilingi 14,000,000. Wakati wa kutembelea vituo, timu ilikuta ujenzi umefanyika ingawa haikuridhishwa na ubora na kiwango cha ukarabati kulingana na thamani ya fedha zilizotumika. Vilevile timu ilikuta ujenzi wa tanki la maji ambalo mganga alieleza kuwa hakushirikishwa katika mchakato wa ujenzi wake. Pia katika kuboresha huduma za VVU na UKIMWI, jumla ya shilingi 5,256,000/- zilitengwa kwa ununuzi wa dawa na vifaa tiba kwa kituo cha Matunzo na Matibabu, timu ilitaka kujua ni vifaa na dawa zipi zilizonunuliwa

viii. Zahanati ya TupendaneHalmashauri iliripoti kujenga vichomea vitatu katika zahanati za Msosa, Ighombwe na Tupendane kwa gharama ya shilingi 5,400,000/- (1,800,000/- kila kichomeo) hata hivyo hakuna kichomeo kipya kilichojengwa. Katika zahanati ya Tupendane, timu ilibaini kutumika kichomeo cha zamani huku zahanati ya Ighombwe haikuwa na kichomeo. Tatizo la kituo kukosa kichomeo pia limebainika katika zahanati za

Chumba cha kuhifadhia mitungi ya gesi ambacho hakijakamilika kwa muda mrefu

Kichomeo taka cha zamani katika zahanati ya Tupendane

Page 41: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-29-

Mudida, Ghalunyangu, Sambaru, Wibia na Mtunduru. Vilevile ujenzi wa kibanda cha kuhifadhia mitungi ya gesi haujakamilika tangu ulivyosimama zaidi ya miaka minne iliyopita, hali inayolazimu kituo kushindwa kutoa huduma ya chanjo kwa mama na mtoto.

Matatizo mengine yaliyopo kituoni hapa ni pamoja na uhaba mkubwa wa watumishi kituoni, kwani wahudumu wawili waliopo hawatoshelezi mahitaji ya kituo. Kuvuja kwa jengo, kukosekana kwa kadi za mama na watoto pamoja na kukosekana kwa huduma ya chanzo za mnyororo baridi. Timu pia ilikuta idadi kubwa ya neti za kujikinga na malaria zikiwa zimerundikwa stoo.

Majibu ya menejimenti: Timu ya UUJ ilipohoji juu ya maswala hayo, Dkt. Mbando alieleza kuwa kichomea taka kilijengwa katika bajeti ya mwaka 2009/2010 na kinatumika, na jengo la zahanati litakarabatiwa mara fedha zitakapopatikana. Ilielezwa pia kuwa kibanda cha kuhifadhia mitungi ya gesi kipo katika hatua ya kupauliwa na kitakapokamilika huduma ya mnyororo baridi itaanza kupatikana katika kituo hiki. Kuhusu neti ilielezwa kuwa zilizopo zinaendelea kutolewa kwa wananchi walengwa wa Tupendane na uhamasishaji utafanyika ili wananchi waone umuhimu wa matumizi yake.

ix. Zahanati ya Irisya

Ripoti ya utekelezaji inaonyesha kuwa Tshs. millioni 16.8 zilitumika kwa ujenzi wa vyoo katika zahanati 5 na ukarabati wa nyumba na jengo la wagonjwa wa nje.

Wakati wa ziara yake, timu ya UUJ ilikuta ujenzi wa vyoo hivyo umetekelezwa kwa kiwango cha kuridhisha. Hata hivyo, choo kilichojengwa (pamoja na zahanati zingine)siorafikikwamazingiranamatumiziyawananchikwanivinginivyasinkivinavyohitaji maji mengi hivyo kuleta usumbufu katika kuvitumia na kuvitunza pia kuta tayari zilikuwa na nyufa.

Zahanati hiyo ya Irisya pia ilitengewa jumla ya shilingi 17,231,754 kwa ajili ya ukarabati wa nyumba ya mganga, na Jengo la wagonjwa wa nje pamoja na ujenzi wa jiko, choo, bafu, stoo na uzio wa nyumba na choo cha Jengo la wagonjwa wa nje. Timu iligundua kuwa ujenzi wa choo cha Jengo la wagonjwa wa nje ulitengewa bajeti mbili, na vilevile choo, bafu, jiko, stoo na uzio wa nyumba ulifanyiwa ukarabati tu na sio ujenzi kama ilivyoripotiwa.

Kituo kina upungufu mkubwa wa watumishi kwani wapo wawili tu. Hakuna sanduku la maoni wala ubao wa matangazo. Utambuzi wa wazee kupata huduma bure hauko

Page 42: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-30-

wazi ingawa wazee wanapata huduma kwa vitambulisho. Halmashauri hurudisha 10% ya Mfuko wa afya wa jamii kawa ajili ya matumizi ya uendeshaji wa kituo.

x. Hali ya uwepo na upatikanaji wa dawa, vifaa na vifaa tiba katika vituo vya huduma

Inaridhisha kwani vituo vyote vilivyotembelewa vimeripoti kuwa na kiasi kikubwa cha dawa muhimu. Hata hivyo, kuna changamoto ya ucheleweshwaji wa usambazaji wa dawa vituoni pamoja na kuletewa dawa tofauti na zilizoagizwa hivyo kupelekea wananchi kukosa baadhi ya dawa.

Timu pia ilibaini tatizo la upungufu wa samani vituoni vikiwemo makabati ya kuhifadhia dawa ingawa Halmsashuri imeripoti kusambaza mashelfu ya kuhifadhia dawa katika vituo.

Timu ya UUJ imeshuhudia vituo vingi vikikosa kabisa matrei (dressing and dispensing trays) hivyo kupelekea dawa kuhifadhiwa sakafuni, kwenye mabenchi ama juu ya meza. Vituo hivi ni pamoja na zahanati ya Unyankhanya, Misinko, Irisya, Mdida, Puma, Mwaru na nyinginezo.

Zahanati ya Irisya pia inakabiliwa na uhaba wa kitanda cha kuzalishia kwani kilichopo ni kimoja tu ambacho ni cha zamani. Hakuna vipimo vya kupimia VVU, hakuna kadi za kina mama na watoto, madaftari yanatumika badala ya kadi.

Majibu ya menejimenti: Ufafanuzi uliotolewa na mwakilishi wa menejimenti ni kuwa ukarabati wa zahanati ya Irisya na nyumba ya mtumishi ulifanyika mwaka 2010/2011 na kukamilika ukiwa katika hali nzuri na kufanyiwa ukaguzi wa kiuhandisi na mkandarasi kulipwa. Isipokuwa hali ya nyufa inayojitokeza katika mkoa wa Singida ni kuwepo kwa matetemeko ya mara kwa mara pamoja na kuwa maeneo mengine kuwanaudongowamfinyanziambaohupasukawakatiwakiangazi.

Kuhusuvyoovisivyorafikinamazingirakatikakituo,Dk.Mbandoalielezakuwa,vyoo vinavyojengwa sasa ni vile vya kutumia maji kidogo ili kuvifanya viwe katika mandhari nzuri na elimu kwa sasa inaendelea kutolewa kwa jamii.

Kuhusu dawa zinazowekwa chini katika kituo, Dokta Mbando alieleza kuwa idara imepeleka kabati na shelfu mbili za kutunzia vifaa na dawa katika vituo vya kutolea huduma; hivyo ufuatiliaji utafanyika kwa watoa huduma wa kituo hiki ili kubainisha vya Irisya vimepelekwa wapi .

Ucheleweshwaji wa taarifa za usambazaji wa dawa vituoni; vituo vimelalamikia halmashauri kutokutoa taarifa mapema kwa waganga wafawidhi wa vituo muda na

Page 43: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-31-

siku ya kupeleka dawa hali inayolazimu waganga hao kupokea dawa bila kuwepo kamati ya usimamizi ya kituo. Hii inaathiri mamlaka ya kamati kukagua na kuthibitisha dawa zilizopokelewa na kutoa maamuzi kama dawa zinaletwa pungufu ama tofauti na zilivyoagizwa.

Halmashauli ilipanga kujenga jengo la Jengo la wagonjwa wa nje na ilieleza kuwa ujenzi wa Jengo la wagonjwa wa nje unaendelea na hali ni nzuri. Jumla ya shs 21,573,375/ sawa na 65% zimetumika, timu ya UUJ ilipotembelea ilijionea kuwa jengo limepauliwa na kupigwa plasta, kuwekwa dari, milango na madirisha tu mpaka sasa bado ujenzi unaendelea. Timu ilipotaka kujua ni lini jengo hilo litakamilika, Dkt Mbando kwa niaba ya halmashauri alieleza kuwa kazi ya ukamilishaji wa zahanati ya Nduru unaendelea na kwa sasa kazi iliyobaki ni kuweka top za milango na madirisha na ujenzi wa nyumba ya mtumishi.

xi. Zahanati ya Ighombwe

Halmashauri iliripoti kutekelea ujenzi wa vichomeo taka katika zahanati 3 kwa bajeti ya 5,400,000/-. Katika zahanati ya Ighombwe, ripoti ilionesha kuwa kichomeo taka kimekamilika kwa gharama ya shilingi 1,800,000/-. Vilevile ripoti ilionesha kuwa vifaa tiba vikiwemo kitanda kipya cha kujifungulia (350,000/), vitanda viwili vya wagonjwa (@170,000/-) pamoja na screen fold na mapazia mawili (100,000/-) vilipelekwa kituoni hapo.

Hali halisi: Wakati wa ziara kituoni, timu ya UUJ ilikuta Kitanda cha kujifungulia kilichopo ni kichakavu na kisichofaa kwa matumizi kwani licha ya kuwa na kutu, kitanda hicho kina tundu kubwa katikati huku kikiwa na vipande vichakavu vya magodoro visivyotumika hali inayohatarisha usalama wa mama na mtoto atakayezaliwa. Kituo hakikuwa na kichomeo taka hali iliyolazimu kuchimba Shimo la kawaida ambalo linatumika kuchomea taka.

Kama ilivyo katika vituo vingi vilivyotembelewa, timu ilishuhudia nyufa katika kuta na sakafu za majengo ya zahanati pamoja na nyumba za waganga. Pamoja na zahanati ya Ighombwe, tatizo hili limeonekana vituo vya Irisya, Sepuka, Mdida, Mwaru, Zahanati za Misinko, Ikiwu, Kituo cha afya Ikungi, Tupendane, Mwaru. Zaidi ya uchakavu wa miundombinu, vituo vingi havina nafasi za kutosha kwani majengo yakenifinyuikiwemozahanatiyaTupendane,Ighombwe,Misinko.Majengokatikazahanati hizi hayatoshelezi mahitaji hali inayolazimu chumba kimoja kutoa huduma zaidi ya moja. Mfano chumba cha kujifungulia kinatumika kuhifadhia jokofu, kupima wajawazito na huduma nyinginezo.

Page 44: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-32-

Changamoto nyingine zilizopo kituoni hapo ni pamoja na upungufu wa dawa na kutoshirikishwa kwa kamati za afya katika kuhakiki dawa wakati wa kupokea .

Majibu ya menejimenti: Timu ya UUJ ilipohoji hali hiyo ilipata ufafanuzi kuwa kichomea taka kilijengwa katika bajeti ya mwaka 2009/2010 na kinatumika na jengo la zahanati ya Ighombwe lilikuwa limeombewa fedha kwenye mpango wa ukarabati wa mwaka 2013/2014. Udogo wa jengo la zahanati umetokana na ramani ya wizara ya wakati huo, ambayo huboreshwa mara kwa mara na kuendana na ongezeko la huduma zitolewazo, ndio maana kwa kuzingatia hilo vituo vinavyojengwa sasa ramani yake ni kubwa.

x. Zahanati ya Mtunduru

Ripoti ya utekelezaji inaonyesha kuwa, kiasi cha Tshs 14,883,934/= kilitumika kwa Ukarabati wa nyumba 1 na Jengo la wagonjwa wa nje, Ujenzi wa choo kilichoboreshwa, jiko, stoo, na bafu.

Hata hivyo, Timu ya UUJ ilipotembelea kituo hicho iliridhishwa na ukarabati uliofanyika ingawa nyumba moja ya mtumishi iliyopo haikidhi mahitaji ya kituo. Zahanati hii, ni moja ya vituo vilivyoripotiwa kupatiwa vifaa tiba vikiwemo vitanda vya kujifungulia na vya uchunguzi.

Hali halisi: Timu ya UUJ ilikuta ujenzi wa Jiko, choo, bafu na stoo umekamilika na vinatumika. Hatahivyo, Zahanati haina kichomeo taka wala vitanda vipya vilivyopelekwa na vile vilivyopo vilipokelewa mwaka 2008. Hakuna kadi za mama na mtoto, sanduku la maoni wala ubao wa matangazo. Changamoto kubwa inayokabili kituo ni kutokuwepo na umeme jua wala umeme hivyo kuwalazimu wauguzi kutumia taa za chemli kutoa huduma usiku haswa za kujifungua. Kituo hakipati uwezeshwaji wa vocha kwa ajili ya mawasiliano ya simu kituoni na pia Ulipwaji wa stahili za watumishi una matatizo ingawa halmashauri iliripoti kulipa stahili za watumishi wake katika mwaka wa fedha 2010/2011.

Majibu ya menejimenti: Timu ya UUJ ilitpotaka maelezo juu ya namna pesa hizo zilivyotumika, mwakilishi wa menejimenti alieleza kuwa kazi iliyofanyika ni ukarabati wa jiko la zahanati, nyumba ya mtumishi, choo, jiko, na stoo kwa Tshs.14,883,934 tu. Lakini Kichomea taka na vitanda ni vya zamani na si vipya kama ilivyoelezwa na timu ya UUJ kupitia taarifa za utekelezaji za idara ya afya. Hata hivyo, halmashauri imeahidi hapo baadaye fedha zikipatikana, maboresho muhimu yatafanywa ili kituo kitoe huduma kwa ufanisi na kiwango kinachokubalika.

Page 45: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-33-

xi. Zahanati ya Nkoiree

Halmashauri ilitenga jumla ya Tshs 33,000,000/- kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la wagonjwa wa nje na kutumia kiasi cha shulingi 11,000,000/- sawa na 33%. Hali ya utekelezaji iliyoripotiwa ni jengo limepauliwa, kupigwa plasta, kuwekwa dari pamoja na kuwekwa milango na madirisha.

Timu ya UUJ ilipotembelea kujiridhisha ilikuta ni kweli upauaji ulifanyika, lakini kulikuwa na mapungufu kama vile mbao kutokuwa na dawa ya kuzuia wadudu, pia wananchi walilalamika kuwa hawakushirikishwa katika mipango ya ujenzi.

Majibu ya menejimenti: Ujenzi wa zahanati mpya ya Nkhoiree ulishirikisha wananchikwakiwangochahaliyajuu,kwavilewamechangianguvuzaohadikufikiahatua ya renta bila halmashauri kuchangia kifedha. Mkataba wa ujenzi ulifanywa na Serikali ya kijiji kwakusaidiwanamhandisi na afisaugavi, nambao zilizotumikazinakubalika kiuhandisi kulingana na nafasi iliyoachwa katika kenchi.

xii. Zahanati ya Ikiwu

Katika zahanati ya Ikiwu, Halmashauri ilionesha kutekeleza ujenzi wa nyumba ya mganga wa kituo kwa gharama ya shilingi 6,800,000/- pamoja na ununuzi wa dawa na vifaa tiba zikiwemo vitanda, screen fold na mapazia. Timu ya UUJ ilipotembelea kituo hiki iliona huduma za afya zinavyotolewa, ilikuta ujenzi umekemilika na kituo kipo katika hali nzuri ya kuridhisha. Hata hivyo kituo kinakabiliwa na changamoto zikiwemo upungufu wa watumishi 6.

Vilevile, watumiaji wa huduma katika zahanati hiyo walimlalamikia mganga wa kituo kutoza kiasi kikubwa cha malipo ya dawa tofauti na vituo vya jirani, kutoza gharama za matibabu kwa wazee na watoto walio chini ya miaka mitano na wajawazito pamoja na kutumia lugha mbaya kwa wagonjwa. Hali hii inapelekea wagonjwa kuacha kituo hicho na kutumia vituo vya jirani ikiwemo zahanati ya Misinko hivyo kuongeza wingi wa watumiaji katika kituo hicho.

Changamoto nyingine ni kutokuwepo kwa Sanduku la maoni, ubao wa matangazo ulikuwepo lakini haukuwa ukitumika. Kamati ya afya ilikuwepo lakini haikuwezeshwa kwa mafunzo, pia wananchi walilalamika kuwa walitakiwa kulipia huduma za afya kwa watoto na wazee. Asilimia 10 ya Mfuko wa afya wa jamii haijawahi kutolewa kituoni, na pia hapakuwepo na huduma za VVU na UKIMWI.

Majibu ya menejimenti: Halmashauri inasisitiza kuwa Vituo vyote vya kutolea huduma za afya vinazingatia muongozo wa Wizara ya afya; ambapo huduma za

Page 46: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-34-

matibabu kwa watoto chini ya miaka mitano, wajawazito na wazee hutolewa bila malipo. Alifafanua pia kuwa vituo 53 vinatoa huduma za upimaji wa VVU na Ukimwi ikiwa ni pamoja na zahanati ya Ikiwu. Huduma inayotolewa kwenye zahanati hizi ni upimaji wa hiari na ushauri nasaha wa VVU.

xiii. Zahanati ya Mjughuda

Ripoti ya idara ya afya ilibainisha kuwa kuna ujenzi wa nyumba tatu, choo, stoo, bafu na jiko kwa bajeti ya 75,601,000 za MMAM. Pia shughuli nyingine iliyopangwa kutekelezwa ni ujenzi wa wodi ya wazazi na fedha zilizotolewa ni 131,560,000/- za LCDG. Ripoti ya utekelezaji ilionesha kuwa nyumba moja imejengwa na kupauliwa kwa kutumia gharama ya shilingi 9,766,000/- ambazo ni sawa na 15%. Huku wodi ya wazazi ikiripotiwa kujengwa na fedha zilizotumika ni 90,336,000/-.

Timu ya UUJ ilipotembelea kituo hiki ilikuta ujenzi wa wodi ya wazazi ukiendelea vizuri na Jengo lilikuwa limepauliwa. Hata hivyo, timu ilibaini changamoto kwani kuta zimepasuka kabla hata nyumba zenyewe hazijaanza kutumika. Ujenzi umetumia bati geji 30 badala ya 26/28, vitasa ni vya ubora wa chini na baadhi yake ni vibovu. Matatizomengineyaliyodhihirikani;kukosekanabarabarayakufikakituoninakituokuwa mbali na makazi.

Timu ya UUJ ilipotembelea kituo hicho ilikuta ni ujenzi wa Jengo la wagonjwa wa nje tu uliokuwa unaendelea kukamilishwa na hapakuwa na ujenzi wa wodi kama ilivyoripotiwa, aidha vitasa vilivyowekwa vilikuwa ni vya mkandarasi kwa lengo la kutunzia mali yake; ambavyo ni vitatu tu, vitasa rasmi vilikuwa bado havijawekwa.

Pamoja na kupongeza ujenzi kuendelea timu ya UUJ ilitaka kujua sababu za changamoto zilizojitokeza

Majibu ya menejimenti: Eneo la kituo lilipendekezwa na serilkali ya kijiji baada ya kuridhiwa na kikao cha Maendeleo ya kijiji (WADC) kwa kuzingatia kuwa kituo hicho kitahudumia vijiji vinavyozunguka kata za Ikhanoda na kuzingatia ukubwa wa eneo ambalo linaweza kutosheleza majengo ya kituo cha afya.

xiv. Zahanati ya Sambaru

Katika ripoti yake ya utekelezaji, idara ya afya ilieleza kuhusu ujenzi wa nyumba ya mtumishi, choo, bafu, jiko na stoo kwa gharama ya shilingi 20,665,370.80. Timu ya UUJ ilithibitisha kujengwa kwa nyumba ya mtumishi pamoja na choo, bafu, jiko, stoo na uzio. Nyumba ni nzuri lakini ina nyufa, ukarabati wa Jengo la wagonjwa wa nje umefanyika vizuri, ujenzi wa choo cha Jengo la wagonjwa wa nje umekamilika.

Page 47: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-35-

Hata hivyo kituo kilikuwa na mtumishi mmoja tu na hakukuwapo na sanduku la maoni wala ubao wa matangazo. Kichomea taka hakikuwapo wala vitanda vipya vilivyopelekwa kama ilivyoelezwa kwenye ripoti ya utekelezaji. Timu ya UUJ ilipongeza jitihada hizo na kutaka ufafanuzi kuhusu mapungufu yaliyojitokeza

Majibu ya menejimenti: Wilaya ilipeleka masanduku ya maoni katika vituo vyote, hivyo idara itafanya ufuatiliaji ili kujua sanduku hilo la maoni lilikuwa wapi. Katika kuboresha huduma kituoni hapo, halmashauri itajenga kichomea taka pindi fedha zitakipatikana.

xv. Zahanati ya Unyankhanya

Katika ripoti yake ya utekelezaji idara ya afya ilielezea ujenzi wa kituo cha afya cha Unyankanya, Timu ya UUJ ilipotembelea kituo hicho iliona hitilafu mbalimbali; sakafu ya jengo, milango na vitasa vilikuwa vibovu sana pia choo kisicho rafikikwa mtumiaji, hakikuwa na maji na ni choo cha sinki. Hakukuwa na barabara ya kufikiakituoni.Vilevilehakukuwanahudumayamnyororobaridi.Kwakuwakituokilikuwa hakijafunguliwa rasmi, kilikuwa hakina samani za kutosha; kama vile kabati la kuwekea dawa.

Majibu ya menejimenti: Kuhusu changamoto zilibainishwa kituoni hapo, Daktari Mbando alikubali mapungufu yaliyojitokeza na kueleza kuwa hayo yanatokana na ukweli kuwa zahanati ya Unyankhanya ilikuwa bado katika mchakato wa kumalizia ujenzi, kwa vile kituo kilikuwa hakijakamilika rasmi.

xvi. Zahanati ya Ntuntu

Taarifa ya utekelezaji ya idara ya afya kuhusu kituo cha Ntuntu ilionyesha kuwa kulikuwa na ujenzi wa nyumba 1, choo 1, bafu 1, stoo 1, jiko 1 (vimepauliwa) kwa gharama ya shilingi 18,500,000/- Ilipotembelea kituo hicho, timu ya UUJ ilijionea milango ikiwa imeachia; hakukuwa na wodi ya wazazi iliyojengwa kwa fedha za MMAM kulingana na taarifa; nyumba ilikuwa haina dari na ukarabati uliokuwa ukifanyika ulisimama, pia ilidhihirika kuwa kituo kilikuwa ni kidogo ikilinganishwa na matumizi yake, vilevile ujenzi wa nyumba za watumishi ulikuwa haujamalizika vizuri hasa upande wa choo na stoo. Timu ya UUJ ilipohoji changamoto hizo;

Majibu ya menejimenti: Daktari Mbando alieleza kuwa mradi wa nyumba mbili za watumishi umekamilika na malipo yote yalikuwa yamekamilika. Hakukuwa na mradi wa ujenzi wa wodi ya wazazi katika zahanati ya Ntuntu. Ilielezwa pia kuwa ukarabati wa nyumba za zamani ulisimama baada ya mkandarasi kushindwa kukamilisha kazi kulingana na mkataba, kwa hiyo mkataba ulivunjwa, badala yake ikajengwa nyumba moja mpya.

Page 48: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-36-

3.7 Majibu ya jumla kwa hoja mbalimbali

3.7.1 Upungufu wa dawa vifaa tiba katika vituo vya Huduma

Katika ufuatiliaji uliofanyika vituoni, timu ilibaini tatizo kubwa la uwepo na utendaji kazi wa vifaa tiba ingawa halmashauri iliripoti kutumia jumla ya shilingi 49,000,257.00 kutoka mfuko wa Mfuko wa afya wa jamii kununua dawa na vifaa tiba vilivyopelekwa katika vituo vya afya vitano (5) na zahanati 41. Vituo vingi havina vipimo muhimu ama vipo lakini havifanyi kazi hususani BP mashine, microscopes, baiskeli za wagonjwa, n.k. Vilevile vituo vimeripoti tatizo kubwa la upungufu wa vipimo vya VVU hususani Uni gold hivyo kupelekea huduma hiyo kukosekana kwa vipindi.

Upungufu na Uchakavu wa vitanda vya uchunguzi, vitanda vya kujifungulia, seti za vifaa vya kujifungulia, screen folding na toroli za dawa (dressing & dispensing) ingawa halmashauri iliripoti kupeleka vifaa hivi katika vituo 46 vya huduma. Screen folding hazipo kwenye vituo vingi na zile zilizopo katika baadhi ya vituo ni za zamani (chakavu)

Kielelezo Na 3: Kushoto; Vifaa havifanyi kazi na Kulia ni seti moja ya kujifungulia iliyopo katika Zahanati ya Tupendane

Kielelezo Na 4: Vifaa vya kujifungulia, Zahanati ya Tupendane

Page 49: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-37-

Majibu ya menejimenti juu ya upungufu wa Dawa na Vifaa Tiba

Upungufu upo wa baadhi ya dawa na vifaa tiba ambavyo havipatikani katika bohari ya dawa ya serikali (MSD). Hivyo upungufu hautokani na halmashauri kutoagiza dawa na vifaa tiba ila ni kutokana na vifaa hivyo kuwa havipo MSD. Akifafanua tatizo hili,daktariMbando,alielezakwamfano,kuwampakakufikiamwishowamweziJune 2012, Halmashauri ilikuwa ikidai MSD dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya takribani shilingi milioni 400.

Dokta Mbando alieleza kuwa vitanda hubadilishwa vinapokuwa vimechakaa. Baadhi ya vitanda vilivyonunuliwa vilipelekwa kwenye vituo vipya vilivyofunguliwa badala ya vituo vilivyokuwa vimekusudiwa awali. Aliendelea kueleza kuwa kila kituo kina kitanda cha kujifungulia.

Halmashauri ilifanya ununuzi wa majokofu na mitungi ya gesi 450 kwa shilingi 10,625,000/- kwa ajili ya kutolea huduma za chanjo kwa mama na mtoto. Katika huduma hii, halmashauri imefanikiwa kusambaza mitungi hiyo hivyo kufanikisha utolewaji wa huduma kwa mama na mtoto. Hata hivyo, timu ya UUJ ilibaini baadhi ya vituo ambavyo havitoi huduma ya chanjo kwa kukosa majokofu ya kuhifadhia chanjo hivyo kulazimisha wananchi kufuata huduma hizo vituo vya jirani, mfano zahanati ya Tupendane ambapo wananchi wanapata huduma Mang’onyi.

3.7.2 Upungufu wa Kadi za akinamama na Watoto katika Vituo

Halmashauri iliainisha kutumia jumla ya shs 11,200,000/- kwa ajili ya ununuzi wa kadi za wajawazito na watoto namba 1 5600 na kadi za wajawazito na watoto Namba. 4 zenye idadi ya 5600 kwa ajili ya hospitali ya Makiungu, huku zahanati na vituo vya afya kutokuwekewa bajeti kwa shughuli hiyo. Katika ufuatiliaji uliofanyika vituoni, timu ilibaini tatizo kubwa la kutokupatikana kwa kadi za watoto na wajawazito. Kina mama na watoto hulazimika kununua madaftari kwa matumizi hayo, hali inayoathiri kujua maendeleo ya afya ya mtoto.

Majibu ya menejimenti: Ilithibitishwa kuwa ni kweli idara haikuwa inajua jambo hilo; hivyo Dkt. Mbando kwa niaba ya idara iliishukuru timu ya UUJ kwa taarifa na hadi majibu haya yanatolewa tayari kadi hizo zilikwisha nunuliwa na kusambazwa vituoni.

3.7.3 Uhaba wa watumishi wa afya

Wilaya ya Singida inakabiliwa na changamoto kubwa na uhaba wa watumishi wa afya, kwani wastani wa watumishi waliopo katika vituo ni 1 hadi 4 kwa zahanati na

Page 50: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-38-

6 hadi 25 kwa vituo vya afya. Changamoto nyingine ni ukosefu wa wataalam wenye vigezo miongoni mwa watumishi waliopo.

Majibu ya menejimenti: Upungufu wa watumishi kwenye vituo ni suala la kitaifa na halmashauri kila mwaka hutenga fedha za kuajiri watumishi wapya lakini wanaopatikana ni wachache.

3.7.4 Nidhamu na Maadili ya Watumishi

Wakati wa kutembelea vituo, wananchi waliripoti tatizo la ucheleweshwaji wa huduma vituoni kutokana na waganga kutokuwepo kazini wakati wa kazi, matumizi ya lugha chafu kwa wagonjwa na ulevi kazini.

Wananchi pia waliripoti kutozwa shilingi 2,500/- kwa mama mjamzito kujifungulia nyumbani ingawa mganga mfawidhi wa kituo na mtendaji kata wakidai kutokufahamu juu ya gharama hizo, huku muuguzi mkunga akithibitisha kuwepo kwa gharama hizo. Swali ni kuwa, inakuwaje wananchi wanalipishwa bila mganga wa kituo kuwa na taarifa, na je fedha hizi zinaingia katika mfuko gani?

Majibu ya menejimenti: Wakati wa usimamizi tegemezo wa CHMT, watumishi wenye utovu wa nidhamu, kama vile walevi na wasiozingatia maadili huonywa kwa mdomo na wasipojirekebisha huandikiwa barua ya onyo, na baadaye hatua stahiki za kinidhamu kulingana na makosa yaliyofanywa huchukuliwa.

Ilielezwa kuwa stahili ya watumishi kisheria ni mshahara na wanalipwa kwa wakati na hakuna mtumishi anayedai, pia wanastahili malipo ya masaa ya ziada, likizo, matibabu na kujiendeleza na hulipwa kutegemeana na upatikanaji wa fedha.

3.7.5 Uwepo na matumizi ya Sanduku la Maoni

Timu ilibaini baadhi ya vituo kutokuwa na masanduku ya maoni ingawa halmashauri iliripoti kuchongesha masanduku ya maoni 471 na kusambaza mashuleni, ofisiza kata na vijiji pamoja na vituo vya huduma 42. Kwa vituo vyenye masanduku, hayatumiki ipasavyo kwani hayafunguliwi ama hayajapachikwa sehemu muafaka ili wananchi wayatumie.

Majibu ya menejimenti: Kila kituo cha afya kilipewa sanduku la maoni, hivyo basi ni wajibu wa idara kufuatilia kila kituo kujua iwapo masanduku hayo yapo na yanatumika.

Page 51: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-39-

3.7.6 Mbao za Matangazo

Hali ya Upashanaji wa taarifa katika vituo vya huduma hairidhishi kwani vituo vingi havina mbao wa matangazo. Kwa vichache vyenye mbao, timu haikukuta matangazo/taarifa za utendaji zilizobandikwa katika mbao hizo. Vilevile mbao hizo hazikuwekwa katika maeneo ya wazi yatakayowezesha wananchi kupata taarifa mbalimbali zikiwemo za mapato na matumizi na huduma mbalimbali zinazotolewa kituoni.

Kielelezo Na 5: Ubao wa Matangazo bila taarifa yoyote

3.7.7 Uwepo na Utendaji Kazi wa Kamati za usimamizi za vituo vya huduma

Kamati za usimamizi za vituo hazioneshi ufanisi kwani nyingi hazikutani na kutekeleza majukumu yao kama inavyotakiwa na muongozo. Ingawa taarifa ya utekelezaji inaonesha halmashauri ilitumia shilingi 14,214,000/- kwa ajili ya kuhamasisha kamati za vituo vya huduma 62. Mchanganuo wa matumizi katika taarifa ya utekelezaji ulionesha kulipa posho ya shilingi 10,000/- kwa washiriki 620, wawezeshaji 16@35,000/- kwa siku 16 na kutumia lita 1,763.5 za mafuta kwa gharama ya shilingi 3,527,000/-. Hatahivyo, wakati wa kutembelea vituo, timu ilibaini ni vituo vichache sana vinavyowezeshwa na gharama ya posho kwa wanakamati ni 2,500 hadi 10,000/-. Mfano, zahanati ya Irisya walipatiwa 25,000/- kwa ajili ya uwezeshaji wa kamati.

Wakati huohuo, timu imebaini kuwa halmasahuri huwezesha Bodi ya afya ya halmashauri kwa kiasi kikubwa kwani kwa mwaka 2010/11, jumla ya shilingi 10,270,000/- ilitumika kutekeleza vikao vyote vya mihula. Mchanganuo wa matumizi unaonesha waheshimiwa madiwani kumi (10) wamelipwa jumla ya shilingi 6,400,000/- za posho za vikao kama wajumbe wa kamati, hali iliyozua maswali kwa timu juu ya uhalali wa madiwani kuingia katika kamati (wajumbe ama waalikwa)

Page 52: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-40-

3.7.8 Malipo ya Asilimia 10 ya Mfuko wa afya wa jamii

Ufafanuzi wa menejimenti: Malipo haya hutolewa kila baada ya miezi mitatu, baada ya kwanza kuidhinishwa na kikao cha bodi ya huduma za afya cha halmashauri ya wilaya, kisha kuidhinishwa na kikao cha huduma za jamii na hatimaye baraza la halmashauri ya wilaya. Mpaka sasa fedha za 10% zimetolewa kwa vituo vyote vilivyochangia hadi mwezi June 2012.

3.7.9 Uimarishaji wa Kamati za Afya za kata

Halmashauri ilitumia kiasi cha 7,358,000/- kwa ajili ya uhamasishaji wa kamati za afya za kata juu ya Mfuko wa afya wa jamii yaliyohudhuriwa na wajumbe 310 waliolipwa 10,000/- kila mmoja, wawezeshaji 6 kila mmoja 35,000/- kwa siku 8, huku mafuta yakigharimu 2,012,000/- (lita 1,006). Hatahivyo, taarifa za kutembelea maeneo ilibainisha kuwa uhamasihaji wa Mfuko wa afya wa jamii uliofanyika haukuwa na posho.

3.7.10 Uboreshaji wa Huduma za VVU na UKIMWI

Timu ilibaini kuwa Huduma za Ushauri Nasaha na Upimaji wa hiari hutolewa katika vituo vya afya huku zahanati zikitoa huduma za PMTCT tu. Watumishi walieleza timu kuwa kuna changamoto katika upatikanaji wa vipimo vya VVU hususani Determine (uni gold vinapatikana). Baadhi ya vituo viliripoti kukosa vipimo kwa muda mrefu mfano zahanati ya Tupendane.

Katika kupunguza matatizo yanayotokana na VVU/UKIMWI katika Halmashauri, ripoti imeonesha kuwa lishe imegawiwa kwa WAVIU 258 (wafanyakazi na wanajamii). Mtandao wa WAVIU umeanzishwa (vikundi 7). Pia, ripoti zimebainisha watoto wapatao 1,500 wanaoishi katika mazingira magumu. Hata hivyo, ni vituo vya afya vya Sepuka, Ikungi, ndivyo vyenye vikundi vya WAVIU na kupokea misaada kwa WAVIU hao.

Majibu ya menejimenti: Lishe kwaWAVIU: wote wanapewa chakula na dawakwa kufuata vigezo vilivyokubalika, na sasa kuna chakula dawa cha RUTF ambacho hutolewa kwenye vituo vyote 10 vinavyotoa huduma za tiba na maangalizi.

Page 53: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-41-

3.7.11 Uwepo na utendaji kazi wa Kamati za Kudhibiti Ukimwi za Halmashauri

Tofauti na wilaya nyingine, halmashauri ya Singida haina kamati za kudhibiti UKIMWI kwa ngazi ya vijiji. Hii ni kinyume na muongozo wa serikali unaotaka kila halmashauri kuunda kamati za kudhibiti UKIMWI ngazi ya kitongoji, kijiji, mtaa, mji mdogo, kata na wilaya ili ziweze kusimamia shughuli zote za udhibiti UKIMWI na kutoa elimu katika jamii. Kamati zilizopo zinaanzia ngazi ya kata hata hivyo kamati hizo hazitekelezi majukumu yake ipasavyo kutokana na uwezeshwaji duni kutoka halmasahuri.

Mojawapo ya majukumu ya kamati hizi ni kuendesha uchanganuzi wa hali halisi ya VVU/UKIMWI katika eneo husika la kijiografia ili kupata; idadi ya watuwalioathirika, wagonjwa, yatima, wajane, kiwango cha uambukizo, mambo maalumu ya kimazingira ambayo yanachangia katika kuongeza maambukizo. Hivyo basi kutokuwepo kwa kamati za kudhibiti UKIMWI katika vijiji kunapelekea halmashauri kukosa takwimu sahihi hivyo kuathiri mipango na upatikanaji wa huduma za VVU na UKIMWI. Hivyo basi timu ya UUJ inashauri halmashauri kuunda kamati za Kudhibiti UKIMWI ngazi ya vijiji na kuziwezesha kifedha na mafunzo ili ziweze kutekeleza majukumu yao.

Page 54: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-42-

SEHEMU YA IV: MAONI YA WADAU JUU YA UBORESHAJI WA HUDUMA

Wadau wa afya na UKIMWI wa wilayaya Singida wameona kwamba zoezi hili la kufuatilia uwajibikaji jamii hasa katika huduma za afya litasaidia sana katika kurekebisha mapungufu katika sekta ya afya na kuongeza ubora wa huduma katika vituo vya afya na zahanati katika wilaya ya Singida vijijini. Hivo timu ya UUJ pamoja na wadau wengine wanatoa mapendekezo yafuatayo;

4.1 Kutekeleza naoni Ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali

Uongozi wa halmashauri ufuate maoni ya mkaguzi mkuu wa serikali na kuyafanyia kazi ili kuepuka matumizi mabaya ya fedha za wanachi na kuboresha huduma mbalimbali za kijamii hususani huduma za afya.

4.2 Zoezi la UUJ Liwe Endelevu

Inapendekezwa kuwa zoezi hili la ufatiliaji wa uwajibikaji jamii linakuwa endelevu na linafanyika mara kwa mara ili kuweza kubaini matatizo na kupata hali halisi ya utekelezaji wa miradi ya halmashauri hususani katika mgawanyo wa rasilimali, mipango, uwajibikaji na usimamizi wa matumizi. Hii italeta ufanisi katika sekta ya afya, ambalo ni muhimu sana kwa maisha ya kila mwananchi.

4.3 Kuwezeshwa Ofisi ya Mkaguzi wa Ndani wa Halmashauri

Inashauriwa kuwa ofisi yamkaguziwa ndaniwa halmashauri iwezeshwe kifedhakulingana na bajeti husika ya halmashauri ili iweze kufanya kazi zake kwa ufanisi na ili kuzuia matumizi mabaya ya fedha za umma.

4.4 Timu ya UUJ Ipewe Ushirikiano

Uongozi wa halmshauri na watendaji wake kwa ujumla hususani wa idara za afya, mipango, fedha na ukaguzi wa ndani watoe ushirikiano zaidi kwa timu za uwajibikaji jamii na kushirikiana nao katika hatua zote ili kuweza kuibua matatizo yanayokabili sekta muhimu kama ya afya. Vilevile washirikiane katika kutatua matatizo hayo ili kufikialengolakutoahudumaborazakijamiikatikawilaya.

Page 55: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-43-

4.5 Ushiriki Wa Baraza la Madiwani

Timu ya UUJ ya wilaya ya Singida vijijini inatoa wito kwa baraza la madiwani hususani madiwani kushiriki zaidi na kutoa ushirikiano mkubwa kwa timu za uwajibikaji jamii kwani wao ni nguzo muhimu sana katika kuleta maendeleo katika maeneo yao kwa kuwa ndio viongozi waliochaguliwa na wananchi ili wawawakilishe.

4.6 Ushiriki Wa Wananchi

Wito umetolewa kwa wananchi wote wa Singida Vijijini kushiriki katika kufuatilia uwajibikaji wa jamii nzima katika kuhakikisha mipango na utekelezaji wa miradi hasa katika sekta ya afya inaenda kama ilivyokusudiwa, kwani ni jukumu la kila mwananchi kuhakikisha anapata huduma bora ya afya katika eneo analoishi.

4.7 Hitimisho

Ni matumaini yetu kuwa iwapo watendaji watawajibika kwa maamuzi yote waliyofanya, mazuriamamabaya,hakizamsingizajamiikatikahalmshauriyaSingidazitafikiwa,hatimaye kupatikana kwa huduma bora za afya kwa wananchi wote.

Page 56: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-44-

VIAMBATISHO

Hotuba ya Mkuu wa Wilaya

Hotuba ya Mkuu wa Wilaya katika ufunguzi wa warsha ya kuhimiza uwajibikaji kwa jamii, tarehe 24/10/2012, Wilayani Singida Vijijini.

Mheshimiwa Mwenyekiti wa Halmashauri, waheshimiwa wawakilishi wa Baraza la Madiwani, waheshimiwa wa kuu wa idara, wafanyakazi wa idara ya afya, waheshimiwa watendaji wa kata, wawakilishi wa asasi mbalimbali, wawakilishi wa wananchi na wafanyakazi wa Sikika, mabibi na mabwana, Hamjambo?

Ninayo furaha ya dhati kujumuika nanyi leo katika mkutano huu muhimu kwa wadau wa afya wilayani Singida vijijini. Napenda kutumia nafasi hii kuwashawishi wajumbe wote juu ya umuhimu wa dhana ya uwajibikaji wa serikali kwa wananchi. Uwajibikaji huu ni kupitia upatikanaji wa huduma mbalimbali zinazotolewa na Serikali kwa wananchi wake. Ni matumaini yangu kuwa mshiriki atatumia fursa hii iliyotolewa leo na wenzetu wa Sikika ili kuifahamu dhana ya kufuatilia uwajibikaji katika jamii (Social Accountability Monitoring-UUJ). Lengo kuu likiwa ni kuleta uwazi na uwajibikaji si katika sekta ya afya tu, bali katika sekta zote.

Ndugu, ni vema tukumbuke kwamba, tumepewa dhamana kubwa na wananchi ya kusimamia na kutumia rasilimali mbalimbali ili kuwahudumia wananchi wetu. Rasilimali hizi zinatokana na kodi, mikopo na misaada mbalimbali. Ni vema pia tukumbuke kwamba, rasilimali hizo ni za wananchi, na hivyo wanayo madaraka makubwa ya kuhoji matumizi yake aidha mwananchi mmoja mmoja au kupitia viongozi wao. Hata hivyo, ni mara nyingi tunajisahau kwamba ni haki ya wananchi kufanya hivyo kisheria.

Hivyo basi, naomba kila mmoja wetu atumie fursa hii tuliyopata leo kujifunza ama kukumbushanayafuatayo:

• Dhana ya mfumo wa uwajibikaji wa jamii

• Haki ya msingi ya kila mwananchi kuhoji na kupewa maelezo ama ufafanuzi juu ya maamuzi yanayofanywa na watoa huduma

• Nini nafasi ya kila mdau katika utekelezaji wa uwajibikaji jamii

• Umuhimu wa uwajibikaji katika kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi

Page 57: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-45-

Ndugu wajumbe, katika mwaka wa fedha 2010/11 halmashauri ya Singida Vijijini ilikisia kutumia kiasi cha Tshs. 24,124,486,183/= kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali. Hata hivyo halmashauri ilifanikiwa kupata Tshs. 22,291,073,382/= kwa ajili ya kutekeleza shughuli mbalimbali za halmashauri. Katika fedha hizi, kiasi cha shilingi 2,021,46,873/= zilitokana na mapato ya ndani ya halmashauri. Hii ikumbukwe kwamba fedha hizo zilizopatikana ni sawa na takribani asilimia 92.4 ya makadirio ya Halmashauri.

Katika fedha hizi, kiasi cha shs 612,099,240/= kilitengwa kwa ajili ya maendeleo; 1,912,990,026/= kwa ajili ya matumizi mengineyo na shilingi 13,848,340,716/= kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa halmashauri. Hata hivyo, halmashauri iliweza kutumia kiasi cha shilingi 19,853,936,015 katika mwaka huo wa fedha wa 2010/2011 ambayo ni sawa na asilimia 89.

Ripoti ya utekelezaji inaonyesha kwamba, katika mwaka wa fedha wa 2010/2011, jumla ya miradi 121 ilitarajiwa kutekelezwa kwa kutumia fedha iliyopokelewa. Hata hivyo, miradi 52 ndiyo ilikamilika, 48 ilikuwa bado inaendelea kutekelezwa na miradi 21 (sawa na asilimia 17.4 ya miradi yote) haikutekelezwa kabisa.

Sekta ya Afya

Katika mwaka huo wa fedha wa 2010/2011, sekta ya afya hapa wilayani ilipata takribani shilingi bilioni moja milioni mia mbili na sitini na tano. Kiasi hiki cha fedha kilikuwa sawa na asilimia 98 ya makisio. Vyanzo vya fedha hizi vilikuwa ni; Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAAM) shilingi milioni 274.5 (sawa na asilimia 112 ya makisio), mfuko wa bima ya afya ya jamii (Mfuko wa afya wa jamii) kiasi cha shilingi milioni 134.044 na Kamati za UKIMWI shilingi 115,776,000/=.

Katika dhana nzima ya uwajibikaji inabidi tujiulize au wananchi wanapaswa kutuulizayafuatayo:

• Je, fedha hizi zilitumika kwa malengo yaliyokusudiwa?

• Je, utekelezaji wa miradi ulimalizika kwa muda uliokusudiwa?

• Je, utekelezaji wa miradi hiyo uliboresha huduma za afya na huduma zingine?

• Je, taarifa za upatikanaji wa rasimali hizi pamoja na matumizi yake viko wazi kwa madiwani ambao ndio wawakilishi wa wananchi,

• Je taarifa hizi ziko wazi kwa wananchi ambao ki-msingi ndio walengwa wa rasilimali hizo?

Page 58: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-46-

• Ndugu wadau, naomba tutambue kuwa uwepo wa mfumo sahihi wa uwajibikaji unatoa fursa ya kupata majibu ya maswali haya kwa urahisi.

Ushirikianao kwa Sikika

Tunatambua kuwa Sikika imeanza kufanya kazi katika wilaya yetu ya Singida Vijijini. Hivyo basi, naomba tuwape ushirikiano wa kutosha ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kuleta tija inayohitajika. Natoa rai kwa wakuu wa idara kutoa ushirikiano mkubwa kwa Sikika pale wanapohitaji msaada.

Ndugu wadau, Sikika kwa kushirikiana na wadau wa afya hapa wilayani wataunda timu ya UUJ (Ufuatiliaji wa Uwajibikaji) lengo likiwa ni kuhimiza uwajibikaji. Zoezi hili litaangalia utekelezaji wa miradi katika sekta ya afya, hasa mwaka wa fedha 2010/2011. Ni matumaini yangu kuwa zoezi hili litakalofanywa na Sikika kwa kushirikiana na baadhi yetu hapa litaleta mafanikio makubwa kwetu kwa sasa na hata siku za usoni. Hivyo basi ninaelekeza wapatiwe taarifa mbalimbali watakazohitaji ambazo ziko ndani ya uwezo wa halmashauri.

Taarifahizinipamojanahizizifuatazo:

• Mipango Mkakati wa halmashauri ili tuweze kujipima ni kwa kiwango gani tumeweza kuutekeleza

• Bajeti ya Halmashauri 2010/2011• CCHP na taarifa zake za utekelezaji za mihula na mwaka mzima kwa miaka ya

2009/10, 2010/2011, 2011/12• Taarifa za Mkaguzi wa Mahesabu (Ndani na Nje)• Ripoti za utekelezaji wa shughuli za halmashauri za robo na za mwaka• Ripoti za vikao mbalimbali vya Baraza la Madiwani, Kamati ya Maadili, Bodi

ya Afya na taarifa nyingine watakazohitaji kwenye mchakato wa mafunzo na uchambuzi.

Rai Nitoe pia rai kwa Sikika kutekeleza shughuli zao kwa uadilifu ili mafunzo yatakayotolewa yawe na tija kwa wananchi wa Singida Vijijini.

Page 59: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-47-

Hitimisho

Mwisho ni matumaini yangu kuwa sote kwa pamoja tutaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wenzetu na timu yetu ya wilaya itakayoundwa na wadau wote ili waweze kutekeleza majukumu tutakayowakabidhi ya kufuatilia uwajibikaji wa jamii.

Nawatakia mafunzo yenye mafanikio na asanteni kwa kunisikiliza

Majina ya timu ya UUJ

Na. Jina Kundi Kata Anuani

1 Salima A. Kundya Diwani Ilongero 0787 513 478

2 Michael A. Moses Jamii Mjini 0756 799 813

3 Penina Lungwa HAPA Mjini 0754494854

4 Josephina Omari Jamii Ikungi 0718945222

5 Amour Hamisi Jamii Sepuka 0755074134

6 Zahara J. Mwiru Jamii Ihanja 0718674781

7 Salumu A. Masaka Dini Msinko 0768866785

8 Juma H. Ntantau CHMT Singida

9 Omari Missanga Jamii Ihanja 0757095538

10 Julius R. Ntangu Jamii Isuna 0765840288

11 Moses Njaghuri – Mtee Jamii Kituntu 0714 409 921

12 Abdallah Swalehe WEO Ikungi 0758 589 497

13 Machemba Mghewa Kamati afya Ikungi 0715 086 809

14 Bruno M. Natalis Diwani Dung’unye 0782 954 335

15 Leonard Munna Kamati afya Ihanja 0765 423 889

Page 60: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-48-

Hotuba ya mwenyekiti wa timu ya UUJ ya mkutano wadau wa halmashauri singida

Mheshimiwa Mgeni Rasmi, waheshimiwa madiwani (Kamati ya Huduma za Jamii), watendajiwahalmashauri,nduguwaalikwa:

Kwa niaba ya wananchi wa Singida vijijini, timu ya SAM imefanya ufuatiliaji wa uwajibikaji katika sekta ya afya na kuja na mapendekezo yanayodai ufafanuzi, uthibitisho na uhalalisho wa maamuzi yanayofanywa na watendaji katika sekta ya afya na halmashauri kwa ujumla. Timu hii iliundwa kupitia mkutano wa pamoja wa wadau wote wa sekta ya afya wilayani na inawakilisha makundi yote muhimu katika sekta ya afya. Makundi haya ni madiwani, wawakilishi wa taasisisi zisizo za kiserikali, mashirika ya dini, wawakilishi wa kamati za uendeshaji za vituo vya kutolea huduma za afya, watendaji wa vijiji, wawakilishi wa CHMT, nk.

Timu hii ilipata mafunzo ya ufuatiliaji wa uwajibikaji (SAM) yenye lengo la kutathmini ni jinsi gani halmashauri inapanga na kutekeleza shughuli za afya kwa kuzingatia haki za msingi za kijamii na mahitaji muhimu ya wananchi.

Mafunzo haya yalihusu uwajibikaji wa jamii kupitia ufuatiliaji wa mipango na mgawanyo wa rasilimali katika halmashauri (planning and resource allocation, usimamizi wa matumizi (expenditure management), usimamizi wa utendaji wa shughuli mbalimbali za halmashauri (performance management), usimamizi wa uadilifu na usimamizi wa uwajibikaji (oversight).

Aidha, baada ya mafunzo, timu ilifanya uchambuzi wa nyaraka mbalimbali ili kujiridhisha juu ya utendaji na uwajibikaji kwa jamii katika kuhakikisha upatikanaji wa mahitaji ya jamii. Baada ya uchambuzi huu wa kina wa taarifa mbalimbali, timu ilitembelea maeneo ya utekelezaji wa shughuli za halmashauri katika vituo vya huduma za afya. Lengo lilikuwa kujiridhisha na hali ya utekelezaji huo kama hatua mojawapo ya kuchochea uwajibikaji na kusimamia matumizi sahihi ya fedha za umma. Hii itawezesha wananchi wapate huduma inayokidhi mahitaji yao.

Mheshimiwa Mgeni Rasmi, waheshimiwa madiwani (Kamati ya Huduma za Jamii), watendajiwahalmashauri,nduguwaalikwa:

Katika kutekeleza majukumu yake, timu ilikumbana na changamoto nyingi zikiwemo ushirikiano duni/hafifu kutoka kwa baadhi ya watendaji wa halmashauri haliiliyosababisha timu kuchelewa kumaliza kazi zake kwa wakati. Vilevile mapokeo hasi ya watendaji iliyopelekea baadhi yao kutumia lugha za kubeza ama kejeli kwa timu

Page 61: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-49-

na kusababisha timu kuona kazi yao haithaminiki na kuvunja moyo wananchi katika kutimiza wajibu wao wa kusimamia rasilimali zao.

Ndugu wadau wa afya, ni vema tukumbuke kwamba, watendaji wamepewa dhamana kubwa kupanga, kusimamia na kutumia rasilimali mbalimbali za umma ili kuwahudumia wananchi. Rasilimali hizi zinazotokana na kodi, michango ya wananchi/wadau, mikopo na misaada ya wahisani mbalimbali. Ni vema pia tukumbuke kwamba, rasilimali hizo ni za wananchi, na hivyo wanayo madaraka makubwa ya kuhoji matumizi yake aidha mwananchi mmoja mmoja au kupitia viongozi wao.

Hivyo basi, timu imeainisha maeneo mbalimbali ambayo yanahitaji ufafanuzi kutoka kwa watendaji. Pia timu inatarajia kuona hatua za marekebisho na zenye uwazi “za watendaji” kwa wadau wa afya na jamii kwa ujumla zikifanyika.

Mwisho, tunaamini kuwa kama watendaji watawajibika kwa maamuzi waliyofanya, mazuriamamabaya,hakizamsingizajamiikatikahalmshauriyaSingidazitafikiwa.Hatimaye huduma bora za afya zitapatikana kwa wananchi wote.

Page 62: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

-50-

Page 63: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

-51-

Page 64: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ)...kutoka Sikika. Mada hizo zilikuwa ni juu ya umuhimu wa uwajibikaji wa jamii, nafasi ya waheshimiwa madiwani katika kusimamia na kufuatilia

Ripoti ya UUJ Singida

-52-

Sikika inafanya kazi kuhakikisha usawa katika

upatikanaji wa huduma bora za afya, kwa kutathimini

mifumo ya uwajibikaji katika ngazi zote za serikali.

Nyumba Na.69Ada Estate, KinondoniBarabara ya TunisiaMtaa wa WaverleyS.L.P 12183Dar es Salaam, Tanzania.

Nyumba Na. 340Mtaa wa KilimaniS.L.P 1970Dodoma, Tanzania.Simu: 0262321307Faksi: 0262321316

Simu: +255 22 26 663 55/57 Ujumbe mfupi: 0688 493 882Faksi: +255 22 26 680 15Barua pepe: [email protected]: www.sikika.or.tzBlog: www.sikika-tz.blogspot.comTwitter: @sikika1Facebook: Sikika Tanzania