72
KANUNI ZA UCHAGUZI NA UTEUZI CHAMA CHA WALIMU ZANZIBAR (ZATU)

SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

  • Upload
    others

  • View
    4

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

KANUNI ZA UCHAGUZI NA UTEUZI

CHAMA CHA

WALIMU ZANZIBAR (ZATU)

Page 2: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

2012

ii

Page 3: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

SEHEMU YA KWANZA1. UTANGULIZIa) i).Kanuni hii itajulikana kama

“KANUNI YA UCHAGUZI NA UTEUZI” ya Chama cha Walimu Zanzibar (ZATU) na imetayarishwa na Baraza Kuu Taifa chini ya ibara ya 32(2) (vii) na 48.(3) ya Katiba ya Chama cha Walimu Kanuni itaanza kutumika kuanzia tarehe 4 Februari 2010

ii) Pamoja na mambo mengine, Chama kinaelewa kuwa uongozi bora ni hii inakusudia kuweka mwongozo na ufafanuzi utakaoweka taratibu mbali mbali za kuwapata viongozi bora, mahiri na wenye uwezo mkubwa wa kuwatetea na kuwatumikia walimu kama ilivyoainishwa kwenye madhumuni ya Chama.

1

Page 4: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

b) Nyenzo muhimu katika kuleta umoja wa walimu wa Zanzibar ni UMOJA ni NGUVU. Aidha uongozi bora utajenga mshikamano utakao wezesha Walimu kutekeleza azma yetu ya kutimiza Wajibu na kutetea Haki zetu ipasavyo kwa wanaotuajiri.

i). Ili kupata Viongozi bora ndani ya chama, lazima kuwa na taratibu bora zitakazosimamia zoezi zima la kuwapa Viongozi katika ngazi zote za chama.

ii) Chama kitakuwa na aina mbili (2) za uongozi:-a. Uongozi wa kuchaguliwa.b. Uongozi wa kuteuliwa.

iii). Katika mchakato mzima wa Uchaguzi na Uteuzi, Chama kitahakikisha kuwa hakuna mtu anashikilia zaidi ya nafasi moja ya uongozi katika Chama kwa kuchaguliwa au kuteuliwa.

iv) Mwalimu Mwakilishi au Naibu wake anaweza kuchaguliwa au kuteuliwa kushika nafasi

2

Page 5: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

nyengine moja (1) ya uongozi na hatapoteza uwakilishi wake.

SEHEMU YA PILI

2. UCHAGUZI WA VIONGOZI

Chama kinaamini kuwa njia ya kuwapata viongozi wanaokubalika kwa wanachama ni uchaguzi wa kidemokrasia. Hivyo Chama kitaendelea na jukumu lake la kujenga, kusimamia na kuendeleza demokrasia ya kweli ndani ya chama kwa kuzingatia yafuatayo:

3

Page 6: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

i) Uchaguzi unakuwa wa haki, huru na wazi kwa wanachama wote na kwa mujibu wa Katiba ya Chama.

ii) Wanachama watapata fursa ya kuchaguliwa au kuchagua viongozi wao moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi na hivyo kuamua hatma ya Chama chao.

iii) Kunakuwepo uwiano unaoeleweka kwa wajumbe na unaozingatia hali halisi ya kijiogarafia, kijinsia na makundi mengine kama itakavyoonekana inafaa

iv) Kuhakikisha kuwa nafasi chache za Uongozi zilizopo zinagawanywa vizuri na si kwa maslahi ya wachache.

v) Kunakuwepo mtiririko mzuri wa mawasiliano kuanzia ngazi ya chini hadi juu kutokana na mfumo wa uongozi uliopo.

4

Page 7: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

3. NAFASI ZA UONGOZIa) Ibara ya 19(2) na (3)(iii) ya

Katiba ya Chama inatoa mamlaka kwa Mkutano Mkuu wa wanachama wote wa Skuli/ Taasisi kumchagua mwanachama mmoja kuwa Mwalimu mwakilishi.

b)Skuli/Taasisi yenye wanachama zaidi kumi na tano (15) Mkutano utamchagua mwanachama mwengine kuwa Naibu Mwalimu mwakilishi.

c) Ibara ya 24(2)(v) ya Katiba ya Chama inatoa fursa kwa Wawakilishi na Manaibu wao wa kila wilaya husika kuwachagua wajumbe kumi (10) miongoni mwao kuingia katika Mkutano Mkuu wa Kanda.

d) Ibara ya 26(2)(v) ya Katiba ya Chama inatoa mamlaka kwa

5

Page 8: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

Mkutano Mkuu wa kila Kanda kumchagua Mwenyekiti wa Kanda, Wajumbe sita (6) wa Baraza Kuu Taifa, Wajumbe wawili kutoka kila Wilaya kuingia katika Kamati Tendaji ya Kanda na wajumbe ishirini wa Mkutano Mkuu Taifa kwa (Jinsia itazingatiwa).

e) Ibara ya 32(3)(v) ya Katiba ya Chama inatoa mamlaka kwa Mkutano Mkuu Taifa kumchagua Mwenyekiti wa Taifa, Makamo Mwenyekiti wa Taifa, Wajumbe watano wa Kamati Tendaji Taifa na Wajumbe wengine wa kuwakilisha katika shirikisho la Wafanyakazi Zanzibar.

4. MUDA WA UONGOZIa) Muda wa Uongozi utakuwa wa

kipindi cha miaka mitano (5) au kama mkutano wa uchaguzi

6

Page 9: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

utaitishwa kiongozi aliyemaliza muda wake anaweza kuchaguliwa tena.

b) Kiongozi aliyechaguliwa atahesabiwa kuwa amemaliza muda wake iwapo Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa ngazi inayomuhusu imeitishwa

c) Iwapo Mwakilishi au Naibu wake atahamishiwa au atakuwa nje ya kituo chake cha kazi kwa zaidi ya miezi sita (6) atapoteza Uwakilishi wake lakini ataendelea kushika ile nafasi nyengine ya uongozi kama atakuwanayo.

d) Iwapo nafasi wazi itakuwa ya Mwalimu Mwakilishi, Naibu wake atashika nafasi hiyo.

e) Iwapo Skuli / Taasisi haitakuwa na Naibu Mwakilishi au kama ameshika nafasi ya Mwalimu Mwakilishi, mkutano Mkuu wa

7

Page 10: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

wanachama utajaza nafasi iliyokuwa wazi

5. SIFA ZA WAGOMBEAi) Wanachama haiii) Awe ametimiza miaka miwili

(2) katika kufundishaiii) Awe amaethibitishwa kazi

6. WASIORUHUSUSIWA KUGOMBEA UONGOZIKwa mujibu wa Ibara ya 16, 17 na 50 (iii) ya Katiba ya Chama cha Walimu inawataja wafuatao kuwa hawatakuwa na haki ya kugombea:

i) Wanachama wa heshima.ii) Wanachama shiriki.iii) Wanachama ambao ni viongozi

wa vyama vya siasa.Watumishi wa Chama hawatakuwa na haki ya kugombea Uongozi wa Chama lakini wanaweza kuchaguliwa

8

Page 11: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

nafasi za Mwalimu mwakilishi au Naibu wake katika Taasisi zao.

7. RATIBA YA UCHAGUZIa) Kamati Tendaji Taifa itatoa

ratiba ya Uchaguzi kwa ngazi zote siku sitini (60) kabla ya uchaguzi wa mwanzo kuanza.

b) Ratiba itataja tarehe ya kuchukua na kurudisha Fomu, tarehe ya Vikao vya maandalizi, kupachika orodha ya Wagombea na tarehe ya mkutano wa Uchaguzi

c) Fomu zianzie uchaguzi wa Mwalimu Mwakilishi na Naibu wake, Kanda na Taifa.

8. VIKAO VYA MAANDALIZI VYA UCHAGUZI

Kutakuwa na Vikao vya maandalizi kwa ajili ya

9

Page 12: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

kufanikisha Uchaguzi kama vifuatavyo:-

i) Kamati Tendaji ya Kanda na Taifa zitakaa kufanya mambo mbali mbali ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na .

ii) Kuhakikisha kuwa orodha ya wajumbe wa mkutano wa Uchaguzi wa ngazi yake ya chini imeandaliwa na Vifaa vya uchaguzi vinavyohitajika vimeandaliwa.

iii) Uhai wa wapiga kura umehakikiwa.

iv) Kuhakikisha kuwa Fomu zote za wagombea wa nafasi zote zimepokelewa na kuorodheshwa na Katibu husika.

v) Kuhakikisha kuwa wagombea wote wamearifiwa kwa maandishi na Katibu husika kukiri kupokea fomu zao za

10

Page 13: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

kuwajuilisha tarehe, mahali na saa ya uchaguzi.

vi) Kuhakikisha kuwa wagombea wametimiza sifa za kugombea nafasi hiyo Kamati Tendaji inaweza kuunda Kamati ndogo ndogo ndogo ndogo ndogo za maandalizi ya Mkutano wa Uchaguzi kama itakavyoona inafaa.

9. TARATIBU ZA KUGOMBEAa) MGOMBEA KUJAZA FOMU.i) Kila mgombea atalazimika

kujaza fomu maalum ya kuomba uongozi kwa kila nafasi anayotaka kugombea kikamilifu

ii) Fomu zitatolewa katika Afisi za Kanda kwa nafasi za ngazi ya Skuli /Taasisi na Kanda. Kwa nafasi ya Taifa, fomu zitapatikana Makao Makuu na kwa Pemba katika Afisi ya

11

Page 14: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

Kanda kwa utaratibu utakaowekwa na Katibu Mkuu.

iii) Kila mgombea ataruhusiwa kugombea si zaidi ya nafasi mbili katika mkutano mmoja wa uchaguzi.

iv) Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa hataruhusiwa kugombea nafasi ya Kamati Tendaji Taifa isipokuwa wale tu wanaotetea tena nafasi zao.

v) Mjumbe wa mkutano Mkuu wa Kanda hataruhusiwa kugombea nafasi yoyote katika mkutano Mkuu wa Kanda, isipokuwa wale wanaotetea nafasi zao.

10. ORODHA YA WAGOMBEA KUPACHIKWA

i) Orodha ya majina ya wagombea Ngazi ya Kanda itapachikwa Afisi ya Kanda. Kwa ngazi ya Taifa orodha kama hizo

12

Page 15: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

zitapachikwa Makao Makuu na Afisi ya Kanda Pemba.

ii) Kila mgombea atatakiwa kuona kama jina lake limeorodheshwa kwenye orodha ya wagombea katika nafasi aliyoomba.

iii) Mgombea ambae jina lake halimo katika orodha ya wagombea atamuarifu Katibu husika kwa masawazisho

iv) Iwapo itabainika nafasi ambayo haina Mgombea au Wagombea hawakufikia idadi inayotakiwa, mara baada ya tarehe ya mwisho ya kurudisha fomu, wanachama husika wataombwa kujaza fomu za kuzirudisha katika kipindi cha siku saba au kama itakavyo agizwa na Katibu Mkuu.

11. TARATIBU ZA KAMPENI

13

Page 16: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

Kwa kuzingatia ibara ya 11 (iii) ya Katiba ya Chama inayotoa haki kwa Mgombea kupiga, kupigia, au kupigiwa kampeni, wapiga kampeni wote wanapaswa kuzingatia yafuatayo:-

i) Kuepuka lugha chafu au shutuma zenye lengo la kumpaka matope au kumchafulia jina mgombea yoyote.

ii) Kuepuka kukosoa au kushutumu uongozi uliopita au walionesha msimamo tofauti nay a kwao

iii) Kuepuka rushwa na vitendo vyote vinavyoashiria rushwa

iv) Kampeni ya aina yoyote ikiwemo ya mtu na mtu haitaruhusiwa wakati mkutano wa Uchaguzi unaendelea kuepuka kutumia Ukabila,

14

Page 17: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

Uzawa, au Udini kama njia ya kujipatia ushindi

v)Kuepuka kufanya Kampeni dhidi ya Mgombea usiyemtaka

12. WASIMAMIZI WA UCHAGUZIi) Kutakuwepo wasimamizi wa

Uchaguzi na Wasaidizi wao katika ngazi zote za uchaguzi wasiozidi wawili kama itakavyoamuliwa na Kamati Tendaji Taifa .

ii) Ngazi ya Skuli/ Taasisi zitasimamiwa na Kamati Tendaji ya Kanda husika kama itakavyoelekezwa na Kamati Tendaji Taifa.

iii)Ngazi ya Kanda na Taifa Wasimamizi watakuwa Mwanasheria na Afisa kutoka Idara ya Kazi kama itakavyoamuliwa na Kamati Tendaji Taifa.

15

Page 18: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

14. MUJUKUMU YA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI

i) Kuhakikisha kwamba Katiba na Kanuni ya Uchaguzi zinafuatwa:

ii) Kuhakikisha kuwa Wajumbe wamekaa katika nafasi zao zilizoandaliwa kabla ya Uchaguzi kuanza

iii) Kuhakikisha kuwa watu wengine ambao si wapiga kura kama vile waalikwa na wagombea wanatengewa nafasi maalum na hawachanganyiki na wapiga kura.

iv) Kutatua matatizo au malalamiko yoyote yatakayojitokeza wakati wa uchaguzi na kushauriana na Katibu husika

v) Kuhakiki wajumbe halali wanaopiga Kura kwa kuangalia majina na vitambulisho vyao na

16

Page 19: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

kwamba kama akidi ya mkutano imetimia

vi) Kushirikiana na Mwenyekiti wa muda kuona kwamba uchaguzi unafanyika kwa haki, uwazi na kiungwana na kwamba wakati wote amani na utulivu inatawala Mkutano.

vii) Kutoa ripoti ya Uchaguzi ndani ya wiki moja.

15. KAMATI YA UCHAGUZIi) Kamati ya Uchaguzi itaundwa

kwa mujibu wa kanuni hizi chini ya Uwenyeviti wa Msimamizi wa Uchaguzi.

ii) Kwa ngazi ya Kanda na Taifa Mwanasheria atakua ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi na Afisa kutoka Idara ya Kazi atakuwa Makamo wake.

iii)Wajumbe wengine watachaguliwa na Mkutano

17

Page 20: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

Mkuu husika miongoni mwao na watakuwa ni wasaidizi wa Msimamizi wa uchaguzi.

iv)Kamati itakuwa na jukumu la kusimamia zoezi zima la uchaguzi, kugawa na kukusanya kura, kuhesabiwa kura na kutoa matokeo.

16. MIIKO YA UCHAGUZIi) Rushwa au vitendo vyovyote

vyenye lengo la aina hiyo ni marufuku wakati wote wa mchakato wa uchaguzi Mkiukaji wa kanuni hii hataruhusiwa kugombea nafasi yoyote katika Chama endapo kwa bahati mbaya atabainika baada ya kumaliza uchaguzi, basi kuchaguliwa kwake kunaweza kubatilishwa na Kamati Tendaji Taifa.

18

Page 21: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

ii) Wajumbe, wagombea au mtu mwengine yoyote ndani ya ukumbi wa Mkutano wa uchaguzi hataruhusiwa kwa kauli au vitendo vyake kuvunja utaratibu wa uchaguzi. Endapo kwamakusudi atabainika kukiuka, Mwenyekiti wa Uchaguzi anaweza kumtoa nje mtu huyo baada ya kushauriana na Kamati ya uchaguzi. Mpiga kura aliyetolewa nje atapoteza haki yake ya kupiga kura.

17. KUONDOA JINAi) Mgombea anaweza kuondoa

jina lake siku saba kabla ya tarehe ya uchaguzi kwa maandishi akieleza nafasi anayokusudia kujiondoa na sababu zake.

ii) Mgombea anaweza kuondoa jina lake siku ya uchaguzi kwa

19

Page 22: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

kumikabidhi Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi barua yake inayokusudia kufanya hivyo au wakati wa kujieleza mbele ya Mkutano Mkuu husika.

iii)Mgombea anayejiondoa wakri wa kujieleza atatakiwa kutaja jina lake, nia yake ya kujiondoa na si zaidi ya hapo.

iv)Wagombea wote waliojiondoa baada ya karatasi ya Kura kuchapishwa, majina yao yatafutwa kwenye karatasi ya kura hawatapigiwa kura au kuhesabiwa.

18. ORODHA ZA UCHAGUZIi) Orodha ya wanachama

ii) Orodha ya wapiga kuraiii) Orodha ya wagombea

Katibu Mkuu atakabidhi kwa wasimamizi wa uchaguzi

20

Page 23: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

orodha ya wapiga kura, orodha ya wagombea, fomu za wagombea, kwa nafasi zao, Katiba, Kanuni ya uchaguzi, vifaa vyote vya uchaguzi pamoja na barua za kujiondoa katika ugombea.

a) Wakati wa uchaguzi ukiwadia Mwenyekiti wa Taifa, Mwenyekiti wa Kanda au Mwalimu Mwakilishi kwa niaba yya viongozi wote waliochaguliwa na Mkutano Mkuu husika atatangaza kujiuzulu ili kutoa nafasi uchaguzi ufanyike.

b) Viongozi wote waliojiuzulu kwa mujibu wa kifungu (a) cha hapo juu wataendelea kuwa wajumbe wa mkutano husika na watakuwa na haki ya kupiga kura.

21

Page 24: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

c) Mara baada ya kujiuzulu kwa viongozi husika Msimamizi wa Uchaguzi atachukua nafasi yake na kuwataka wajumbe kumchagua Mwenyekiti wa Mkutano wa Uchaguzi na kuwachagua wajumbe wasiozidi watano kuunda Kamati ya Uchaguzi.

d) Mwenyekiti na wajumbe wa uchaguzi atachaguliwa miongoni mwa wajumbe wa Mkutano husika ambao hawatakuwa wagombea wa nafasi yoyote katika mkutano huo.

e) Mwenyekiti ataongoza mkutano na atamtaka Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi kuendesha uchaguzi.

19. ORODHA YA WAPIGA KURA

22

Page 25: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

i) Katibu wa ngazi husika ataandaa Orodha ya wapiga Kura katika kila Mkutano wa uchaguzi na kumkabidhi Msimamizi wa uchaguzi siku ya uchaguzi.

ii) Katibu wa ngazi husika ataandaa vitambulisho kwa kila mpiga kura vikionesha jina la mpiga kura na kumkabidhi mpiga kura mara atakapoingia katika ukumni wa mkutano wa uchaguzi.

20. TARATIBU ZA KUENDESHA UCHAGUZI

Kamati ya Uchaguzi itahakikisha kuwa Katiba na Kanuni ya uchaguzi zitafuatwa wakati wa uchaguzi kwa kufanya yafuatayo;-

23

Page 26: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

i) Kuhakikisha akidi ya wajumbe halali kwa mujibu wa Katiba imetimia.

ii) Kuhakikisha kuwa kila mgombea aliyewasilisha fomu, jina lake limewekwa katika karatasi ya kupiga kura kwa nafasi aliyoomba.

iii) Iwapo kuna mgombea ambaye jina lake halikuorodheshwa, kamati italifuatilia suala hilo na kufanya uwamuzi sahihi kabla ya uchaguzi wa nafasi hiyo.

iv) Wagombea wote wanapata nafasi sawa na kujieleza na kujibu maswali

v) Wajumbe wamepata nafasi ya kuwauliza maswali wagombea.

vi) Kuhakikisha kuwa uchaguzi unakuwa wa SIRI na HAKI.

vii) Kuhakikisha kuwa karatasi za kura zinatolewa kulingana na idadi ya Wajumbe.

24

Page 27: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

viii) Kuhakikisha kuwa vifaa vyote vya uchaguzi vinavyohitajika vinakuwepo.

21. TARATIBU ZA KUJIELEZAi) Kila mgombea atapewa muda

usiozidi dakika tatu (3)wa kujieleza mbele ya wajumbe wa Mkutano husika au kama itakavyoamuliwa na Mkutano

ii) Kila mgombea ataweza kuulizwa maswali yasiozidi matatu au kama Mkutano utakavyoamua. Mgombea atatakiwa kulijibu suala aliloulizwa iwapo Mwenyekiti ataridhika nalo.

iii) Mgombea ambaye hayupo atasomewa maelezo yake kama alivyo jieleza katika fomu ya mgombea.

25

Page 28: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

22. TARATIBU ZA KUPIGA KURAKura zote za uchaguzi zitakuwa za siri na kwa kutumia karatasi maalum zilizowekwa kwa ajili hiyo.

Karatasi za kurai) Itataja nafasi inayogombaniwa

na itaorodheshwa majina kamili ya wagombea kwa kufuata alfabeti na itakuwa na muhuri wa chama

ii) Kila Mjume atapata karatasi moja ya kura kwa wakati mmoja na atapiga kura kwa idadi maalum inayohitajika.

iii) Kila mjumbe atatakiwa kuingiza kura yake katika kisanduku cha kura yeye mwenyewe mara upigaji kura ukimaliza

iv) Iwapo nafasi ya uongozi itagombaniwa na mgombea

26

Page 29: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

mmoja (1) tu, atapigiwa kura ya NDIO au HAPANA.

v) Karatasi ya kupigia kura hazitagawanywa mpaka wagombea wote wamemaliza kujieleza.

23. TARATIBU ZA KUHESABU KURA

Baada ya upigaji na ukusanyaji kura kumalizika. Wasimamizi wa uchaguzi watahakikisha kuwa.

i) Kura zinahesabiwa kwa umakiniii) Kila mgombea atapata nafasi

ya kuteuwa mwakilishi wake kama atataka wakati wa kuhesabu kura kwa nafsi aliyogombea.

iii) Kuhakikisha kuwa idadi ya kura zilizopigwa zinalingana na idadi ya wajumbe waliopiga kura.

27

Page 30: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

iv) Kutakuwa na karatasi za kuhesabia kura kwa kura za makundi ambazo zitakuwa na orodha sawa na karatasi za kura.

v) Karatasi zote za kura zitahifadhiwa kwa muda wa miezi kumi na mbili (12) na baadae zinaweza kuharibiwa.

vi) Kura zilizopigwa kwa wagombea ambao majina yao yamefutwa, zitahesabiwa kuwa ni kura zilizoharibika.

24. TARATIBU ZA KUTANGAZA MATOKEO

i) Msimamizi wa uchaguzi atajaza fomu maalum za matokeo kwa kila nafasi iliyogombewa.

ii) Mshindi atatokana na wingi wa kura na kwa kufuata Katiba na Kanuni ya Chama, mshindi wa

28

Page 31: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

kura ya NDIO atahitajika kupata zaidi ya nusu ya kura zote zilizopigwa.

iii) Mwenyekiti wa Mkutano wa uchaguzi atatangaza matokeo ya uchaguzi kama alivyokabidhiwa na msimamizi wa uchaguzi.

iv) Matokeo ya kura za Mwenyekiti yatatangazwa mwanzo.

v) Jina la mgombea lililofutwa katika orodha ya wagombea litapigwa matokeo.

vi) Baada ya matokeo Mwenyekiti au Mwalimu Mwakilishi aliyechaguliwa atapewa nafasi ya kutoa shukrani kwa niaba ya wenzake.

vii) Fomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina

29

Page 32: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

lake katika orodha sawa na karatasi ya kura.

25. MALALAMIKO YA UCHAGUZIa) Ngazi ya Skuli / Taasisii) Malalamiko yote yatokanayo na

uchaguzi ngazi ya Skuli /Taasisi yatawasilishwa kwa Katibu wa Kanda husika katika kipindi kisichozidi siku saba (7) tokea siku ya uchaguzi.

ii) Katibu wa Kanda atayafuatilia malalamiko hayo na kuyatolea maamuzi katika kipindi kisichoziidi siku kumi na nne tangu muda wa malalamiko kufikishwa.

iii) Iwapo mlalamikajii hakuridhika na uamuzi huo atapeleka rufaa yake kwa Kamati Tendaji ya Kanda husika siku saba (7)

30

Page 33: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

tangu apate majibu ya Katibu wa Kanda.

b) Ngazi ya Kanda.i) Malalamiko yote yatokanayo na

uchaguzi ngazi ya Kanda yatawasilishwa kwa Katibu Mkuu Taifa kupitia Kanda husika katika kipindi kisichozidi siku (14) tokea siku ya uchaguzi kumalizika.

ii) Katibu Mkuu ataunda kamati ndogo ya Wajumbe wasiozidi watatu kusikiliza malalamiko hayo na kuyatolea mapendekezo ili atoe uamuzi katika kipindi kisichozidi siku (21) tangu muda wa malalamiko kumalizika

iii) Iwapo mlalamikaji hakurudhika na maamuzi ya Katibu Mkuu atakata rufaa kwa Kamati

31

Page 34: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

Tendaji ya Taifa kwa uamuzi wa mwisho.

c) Ngazi ya Taifai) Malalamiko yote yatokanayo na

Uchaguzi ngazi ya Taifa yatawasilishwa kwa Katibu Mkuu kipindi kisichozidi mwezi mmoja (siku 30) tangu uchaguzi ulipofanyika.

ii) Kamati Tendaji itasikiliza malalamiko hayo na kuyatolea uamuzi katika kipindi kisichozidi miezi mitatu (siku 90) tangu muda wa malalamiko utapoisha. Katibu Mkuu atawaarifu wahusika maamuzi ya Kamati Tendaji mara ya baada maamuzi kutolewa.

iii) Iwapo malalamikaji hakuridhika na maamuzi hayo, atakata rufaa kwa Baraza Kuu Taifa kwa maamuzi ya mwisho. Baraza Kuu litakaa kuipitia na kuitolea

32

Page 35: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

maamuzi rufaa hiyo ndani ya kipindi cha mwaka mmoja tangu uchaguzi ulipomalizika.

iv) Malalamiko yoye ya uchaguzi yatakuwa ya maandishi na yataonyesha ni kwa jinsi gani Mgombea au Mkutano wa Uchaguzi ulivyokiukwa Katiba au Kanuni za Uchaguzi.

v) Malalamiko yote ya uchaguzi yatakuwa ya maandishi na yataonyesha wazi jina na anuani yake nafasi anayoilalamikia au Mgombea anaye mlalamikia

vi) Malalamiko yatakayowasilishwa kinyume na Kanuni hizi hayatashuhulikiwa.

26. UTATUZI WA MALALAMIKOi) Malalamiko yote ya uchaguzi

yatashughulikiwa bila kuchelewa na Kikao husika na

33

Page 36: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

kutoa Uamuzi juu ya malalamiko hayo

ii) Iwapo maamuzi ya malalmiko yaliyotolewa yatahitaji kuchukuliwa hatua na vyombo vya juu, chombo kinachohusika kitapeleka mapendekezo yake kwa chombo husika chenye uwezo wa kuchukua hatua hiyo.

iii) Malalamiko yote ya uchaguzi lazima yawe yameshughulikiwa na kumalizika katika kipindi cha miezi kumi na mbili (12) tangu Uchaguzi Mkuu ulipomalizika.

iv) Mlalamikaji ni lazima ajuilishwe maamuzi ya kila hatua iliyofikiwa ya malalamiko yake.

v) Mlalamikaji anaweza kutakiwa kutoa maelezo ya ziada au kuitwa mbele ya chombo kinachohusika, kutoa ushahidi wa malalamiko yake.

34

Page 37: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

27. KUFUTA MATOKEOa) Kiongozi au mgombea anaweza

kulalamikiwa kufuatiwa matokea kwa sababu zifuatazo:-

i) Atapoteza sifa yakuwa mwanachama

ii) Atabainika kuwa hakuwa na sifa za kuwa mgombea au alidanganya.

iii) Atavunja kifungu chochote cha Katibu au Kanuni hizi.

b) Kiongozi au mgombea atakaethibitika kuwa malalamiko dhidi yake ni ya kweli atachukuliwa hatua zifuatazo:-

i) Atafutiwa ushindi wake.ii) Hataruhusiwa kugombea au

kuteuliwa kuwa kiongozi kwa muda wa miezi thelathini (30) tangu tarehe ya uamuzi huo kutolewa

35

Page 38: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

SEHEMU YA TATUUTEUZI WA VIONGOZI

28. UTEUZIChama kinaelewa mapungufu yanayoweza kujitokeza katika kuwapata viongozi wazuri hasa watendaji kwa njia ya uchaguzi. Hivyo sambamba na uchaguzi Chama kitaendelea na utaratibu wa kuwateuwa baadhi ya Viongozi wake ili kuimarisha safu za watendaji na vyombo vya maamuzi.

29. NAFASI ZA UTEUZIi) Ibara ya 27 a (x) ya Katiba

Chama, imeipa Kamati Tendaji ya Kanda mamlaka ya kumteuwa Mratibu wa Kitengo cha Wanawake Kanda.

ii) Ibara ya 33 b (vi) ya Katiba imelipa mamlaka Baraza Kuu

36

Page 39: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

Taifa kuwateua Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Mtunza Hazina, Mratibu wa kitengo cha Wanawake Taifa, Makatibu wa Kanda na Wajumbe wanne wakuteuliwa na Baraza Kuu Taifa

30. SIFA ZA KUTEULIWAKanda atakuwa ni mwanachama hai mwenye sifa zifuatavyo:-i) Awe na sifa ya kuwa Mgombea

wa Chama cha Walimu.ii) Awe ni mwanachama ambaye

anakubalika na wanachama.iii) Awe na uwezo wa kuandika na

kuzungumza lugha ya kiingereza kwa ufasaha.

iv) Awe na uwezo wa kuifanya kazi kwa nafasi anayoiyomba.

v) Awe ana uwezo wa kutumia kompyuta.

vi) Awe mwanamke.vii) Awe na Elimu ya darasa la kumi

na mbili (FIV) na amesomea ualimu.

37

Page 40: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

c) Mjumbe wa kuteuliwa wa Baraza Kuu Taifa atakuwa mwanachama hai mwenye sifa zifuatazo:

i) Awe na sifa ya kuwa Mgombea wa Chama cha Walimu

ii) Awe ni mwanachama mzoefu katika Vyama vya Wafanyakazi.

iii) Awe mzoefu na anasifa ambayo inahitajika katika kuimarisha shughuli za Chama .

iv) Awe na sifa ya uongozi wa walimu.

a) Katibu wa Kanda atakuwa mwanachama hai mwenye sifa zifuatazo:-

i) Awe na sifa za kuweza kugombea uongozi wa chama.

ii) Awe na uzoefu wa Vyama vya Wafanyakazi.

iii) Awe na uwezo wa kuandika na kuzungumza lugha ya kiingereza kwa ufasaha.

38

Page 41: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

iv) Awe na uwezo wa kufanya kazi pahala popote bila ya kujali wakati

v) Awe na uwezo wa kutumia kompyuta.

vi) Awe na Elimu ya darasa la kumi na mbili (FIV) na amesomea ualimu.

b) Mratibu wa kitengo cha Wanawake Taifa atakuwa mwanachama hai mwenye sifa zifuatazo:-

i) Awe na sifa za kuweza kugombea uongozi wa Chama

ii) Awe ni mwanacham ambae ana elimu isiyopungua kiwango cha Digrii

iii) Awe na uwezo wa kuandika na kuzungumza lugha ya kiingereza kwa ufasaha

39

Page 42: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

iv) Awe na uwezo wa kubuni mbinu katika kutekeleza majukumu ya kazi

c) Mtunza hazina atakuwa mwanachama hai mwenye sifa zifuatazo:-

i) Awe na sifa za kuweza kugombea uongozi wa Chama

ii) Awe na uwezo wa kuandika na kuzungumza lugha ya kiingereza kwa ufasaha

iii) Awe na taaluma ya fani ya uhasibu na utawala wa fedha

iv) Awe na uwezo wa kutumia Kompyuta

d) Naibu Katibu Mkuu atakuwa mwanachama hai mwenye sifa zifuatazo:

i) Awe na sifa za kuweza kugombea uongozi wa Chama

40

Page 43: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

ii) Awe na elimu isiyopunguwa kiwango cha digrii au inayolingana

iii) Awe na uwezo wa kuandika na kuzungumza lugha ya kiingereza kwa ufasaha

iv) Awe na uwezo wa kutumia Kompyuta

v) Awe na uzoefu wa uongozi wa walimu.

e) Katibu Mkuu Taifa atakuwa mwanachama hai mwenye sifa zifuatazo:-

i) Awe na sifa za kuweza kugombea uongozi wa Chama

ii) Awe na Elimu isiyopunguwa kiwango cha Digrii au inayolingana

iii) Awe na uwezo wa kuandika na kuzungumza lugha ya kiingereza kwa ufasaha.

41

Page 44: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

iv) Awe na uzoefu wa kuongoza katika Taasisi za Kijamii si chini ya miaka miwili (2)

31. MUDA WA UTEUZIi) Muda wa kushikilia nafasi ya

uongozi wa kuteuliwa utakuwa miaka mitano(5)

ii) Kiongozi wa kuteuliwa atahesabiwa kuwa amemaliza muda wake mara baada ya uchaguzi Mkuu kufanyika hata kama mteuliwa huyo hajafikisha miaka mitano (5) tangu kuteuliwa kwake.

iii) Kiongozi aliyemaliza muda wake wa kuteuliwa anaweza kuteuliwa tena kushika nafasi aliyokuwa anayo au nafasi nyengine kama Baraza Kuu litakavyoona inafaa.

42

Page 45: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

iv) Katibu wa Kanda ataendelea na Uteuzi wake mpaka pale uteuzi wake utakapofutwa lakini ataweza kuhamishiwa kufanya kazi katika Kanda nyengine au kupangiwa kazi nyengine kama Baraza Kuu litakavyoona inafaa.

32. NAFASI KUWA WAZIa)Nafasi ya kuchaguliwa itakuwa

wazi kwa mambo yafuatayo:i) Kiongozi atamaliza muda wakeii) Ataacha kuwa mwanachama

kwa hiari, atapoteza uwanachama wake au atafukuzwa uwanachama.

iii) Atafariki kabla ya muda wake kumalizika

iv) Atafikia umri wa kustaafu kazi

43

Page 46: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

v) Atajiuzulu nafasi yake ya uongozi

33. KUJAZA NAFASI ZILIZOWAZIa) Nafasi za Kuchaguliwai) Iwapo nafasi wazi ni ya

Mwenyekiti wa Kanda, Kamati Tendaji ya Kanda itamteua mtu mwengine miongoni mwao kuikimu nafasi hiyo

ii) Iwapo nafasi wazi ni ya Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Kanda, Kamati Tendaji itamtangaza mwanachama mwengine kushika nafasi hiyo kwa kufuata Orodha ya matokeo ya Uchaguzi uliopita na kanuni hizi.

iii) Iwapo nafasi wazi ni ya Mwenyekiti wa Taifa, Makamo Mwenyekiti atakaimu nafasi hiyo.

44

Page 47: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

i) Iwapo nafasi wazi ni ya Makamo Mwenyekiti, Baraza Kuu litamteuwa mtu mwengine miongoni mwao kukaimu nafasi hiyo kwa kuzingatia Katiba ya chama.

ii) Iwapo nafasi wazi ni ya Mjumbe wa Kamati Tendaji Taifa au Baraza Kuu Taifa Baraza Kuu litamtangaza mwanachama mwengine kwa kufuata orodha ya matokeo ya Uchaguzi uliopita kushika nafasi hiyo.

iii) Muda wa kukaimu kwa nafasi ya Mwenyekiti Taifa, Makamo Mwenyekiti na Mwenyekiti wa Kanda anaendelea mpaka Mkutano Mkuu wa Kawaida wa ngazi husika utakapoitishwa. Iwapo mkutano utakuwa katika kipindi cha miezi (30) ya mwanzo (uchaguzi mdogo

45

Page 48: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

utafanywa kujaza nafasi zilizokaimiwa)

iv) Kiongozi atakae kaimu nafasi ya uongozi, nafasi yake haitakaimiwa na mtu mwengine wakati wote atakapokuwa anakaimu.

b) Nafasi ya Uteuzii) Kamati Tendaji ya Kanda

itamteua mwanachama mwengine mwenye sifa baada ya kukamilisha taratibu zote za uteuzi kwa nafasi ya Mratibu wa kitengo cha wanawake Kanda.

ii) Kwa ngazi ya Taifa, iwapo nafasi ya Katibu Mkuu ipo wazi, Naibu Katibu Mkuu atakaimu nafasi hiyo kwa muda mpaka uteuzi mwengine utakapo fanyika.

iii) Iwapo nafasi wazi ni ya Naibu Katibu Mkuu, Mtunza Hazina, Mratibu wa Kitengo cha

46

Page 49: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

wanawake Taifa au Katibu wa Kanda, Kamati Tendaji Taifa au Katibu Mkuu kwa kushauriana na Mwenyekiti Taifa na wajumbe wa Kamati Tendaji, atamteuwa mjumbe wa Kamati Tendaji Taifa kukaimu nafasi hiyo kwa kufuata taratibu za uteuzi

iv) Muda wa kukaimu nafasi ya uteuzi ni miezi sita (6).

34. TARATIBU ZA UTEUZIa) Sambamba na uchaguzi wa

Viongozi wa Chama, mchakato wa uteuzi utachukua mkondo wake kwa kufuata taratibu zifuatazo:-

i) Kamati Tendaji husika itatangaza nafasi wazi ya uongozi wa kuteuliwa ikitaja sifa zinazohitajika kwa waombaji na muda wa maombi.

47

Page 50: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

ii) Wanachama wenye sifa za kujaza nafasi hizo watatuma maombi yao kwa kuzingatia sifa walizonazo na muda wa kupokelewa maombi yao.

iii) Kwa nafasi ya Mratibu wa kitengo cha Wanawake Kanda, maombi yatatumwa kwa Katibu wa Kanda husika. Kamati Tendaji ya Kanda baada ya kupokea maombi itayachambua na hatimae itafanya uteuzi wake.

iv) Kwa ngazi ya Taifa maombi yatatumwa kwa Katibu Mkuu.

v) Iwapo hakuna mtu aliyeomba kuteuliwa au kama waombaji hawakufikia viwango vya vigezo na sifa zilizowekwa, Kamati Tendaji itapendekeza majina ya wanachama wengine wenye sifa zinazotakiwa na kuyaongeza kwenye orodha ya waombaji.

48

Page 51: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

vi) Muombaji anaweza kuombwa kutoa vielelezo vyake vya sifa alizonazo na ushindi wake au kuitwa mbele ya vyombo vya uteuzi kwa kutoa maelezo.

b)Kwa nafasi ya Wajumbe wa Baraza Kuu wa kuteuliwa na Baraza Kuu Taifa, utaratibu ufuatao utafuatwa:-

i) Kamati Tendaji Taifa itapendekeza Kwa Baraza Kuu majina yasiyozidi sita (6) ya Wanachama wenye sifa kuomba kuteuliwa kwa nafasi hizo.

ii) Kamati Tendaji itaweka vigezo na sifa za kuwapata wateuliwa kwa kuzingatia hali halisi ya Baraza lilivyo, uwiyano wa kijografia na jinsia, uzoefu na uwezo alionao.

49

Page 52: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

iii)Baraza Kuu litazingatia mapendekezo ya Kamati Tendaji ya majina ya wanachama, vigezo na sifa walizonazo.

iv) Baada ya kuchambua kwa makini orodha ya majina waliyonayo, na kwa kuzingatia mahitaji halisi yaliyopo, Baraza Kuu litawateuwa wajumbe wane kuwa Wajumbe wa Baraza Kuu Taifa.

c) Baraza Kuu linaweza kutumia kura ya siri au namna nyengine yoyoyte watakayoona inafaa katika kuwapata Wajumbe wa kuteuliwa. Mara baada ya uteuzi kumalizika

i) Mwenyekiti wa kikao atawatangaza walioteuliwa kwa mujibu wa nafasi za uteuzi wao

ii) Katibu Mkuu atawandikia barua kuwaarifu kuteuliwa kwao na

50

Page 53: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

wataanza kushika nafasi zao tangu tarehe ya uteuzi wao.

35. KUFUTA UTEUZIa) Baraza Kuu Taifa linaweza

kufuta uteuzi wa mjumbe yoyote aliyeteuliwa kushika nafasi ya Uongozi kwa mambo yafuatayo.

i) Atapoteza sifa ya kuwa mwanachama.

ii) Atabainika kuwa hakuwa na sifa za kuteuliwa kwake au alidanganya.

iii) Atashindwa kuhudhuria vikao zaidi ya viwili mfululizo bila kutoa maelezo yanayokubalika.

iv) Atabainika kuwa hana uwezo wa kumudu kazi zake au amefanya kwa makusudi.

51

Page 54: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

b) Katika kufikia uamuzi wake, Baraza Kuu litachambuwa kwa makini ombi la kufuta uteuzi wa mjumbe, sababu na ukubwa wa kosa lake kama litakavyo wasilishwa na Kamati Tendaji Taifa na hatimae kupiga kura. Maamuzi ya Kura yafikie zaidi ya nusu ya Wajumbe halali wa Baraza Kuu.

SEHEMU YA NNEMENGINEYO

52

Page 55: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

36. UTEUZI WA WANACHAMA WA HESHIMA

a) Ibara ya 16 ya Katiba ya Chama inatoa mamlaka kwa Baraza Kuu kuwatunukia uwanachama wa heshima watu waliowahi kutoa mchango mkubwa katika kada ya ualimu au mtu yoyote ambaye Chama kitaona anastahiki kutunikiwa heshima hiyo. Katika kufanya kazi yake hiyo, utaratibu ufuatao utatumika:-

i) Kamati Tendaji itapendekeza majina ya watu wanaostahiki kutunukiwa uwanachama wa heshima wakitaja sifa na sababu za mapendekezo yao kwa Baraza Kuu la Taifa.

ii) Baraza Kuu litazingatia mapendekezo ya Kamati na kutoa uamuzi wake.

53

Page 56: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

iii) Mtu atakaye kubali atapewa cheti kinachoonesha kutunukiwa kwake uwanachama wa heshima pamoja na kutolewa maelezo mafupi ya wasifu wake na sababu zilizopelekea kupewa heshima hiyo.

37. UCHAGUZI MDOGOi) Uchaguzi mdogo unaweza

kufanyika iwapo nafasi ya Mwenyekiti Taifa, Makamo Mwenyekiti au Mwenyekiti wa Kanda itakuwa wazi.

ii) Iwapo nafasi ya Mwenyekiti Taifa na Makamo wake kwa pamoja au nafasi ya Kaimu Mwenyekiti zitakuwa wazi, uchaguzi mdogo unaweza kuitishwa.

iii) Uchaguzi Mdogo utafuata taratibu zote za uchaguzi Mkuu.

54

Page 57: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

38. UFAFANUZI WA KANUNIIkiwa kutakuwa na matatizo yoyote ndani ya kanuni hizi, Kamati Tendaji Taifa itakuwa na uwezo wa kutoa muongozo wa kufafanua na kuweka utaratibu bora zaidi wa utekelezaji wa kanuni hizi.

39. MABADILIKO YA KANUNIi) Kanuni hizi zinaweza

kubadilishwa na Baraza Kuu Taifa baada ya theluthi (2/3) ya Wajumbe wote wa Baraza Kuu kukubali mabadiliko hayo.

ii) Mapendekezo ya mabadiliko na masahihisho ya kanuni hizi yapelekwe kwa Katibu Mkuu na kujadiliwa na Kamati Tendaji Taifa.

55

Page 58: SEHEMU YA KWANZA YA UCHAGUZI NEW BK 2012… · Web viewFomu ya matokeo itaonesha idadi ya kura zilizopigwa idadi ya kura zilizoharibika na kura za kila mgombea mbele ya jina lake

iii) Iwapo mjadala wa marekebisho ya kanuni unaendelea, mjumbe anaweza kutoa mapendekezo mengine ya marekebisho lakini lazima yakubalike na theluthi mbili (2/3) ya Wajumbe.

Tamati

56