54

UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

  • Upload
    others

  • View
    9

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab
Page 2: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

UTETEZI WA SHERIA ZA KIISLAMU

Muhtasari Nne Juu YaSheria Mbali Mbali Binafsi za Kiislamu

Kimeandikwa na:

Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi

Kimetafsiriwa na:

Dr. Mohammad Said Kanju

Kimetolewa na: Bilal Muslim Mission of Tanzania

S.L.P. 20033 Dar es Salaam - Tanzania

Page 3: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

Haki za kunakili imehifadhiwa na:Bilal Muslim Mission of Tanzania

ISBN 9987 620 26 4

Toleo la Kwanza : 2001 Nakala: 2000 Toleo la Pili : 2004 Nakala: 2500

Kimetolewa na:BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA

S.L.P 20033DAR ES SALAAM - TANZANIA

Kimechapishwa na:TANZANIA PRINTING SERVICES LTD

S.L.P 9661DAR ES SALAAM - TANZANIA

Page 4: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

YALIYOMO

Dibaji . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . i

Utangulizi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .1

1. Muhtasari juu ya Sheria za ndoa uliwasilishwa mbele ya Tume ya Serikali ya Kenya juu ya Sheria za ndoa n.k . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .6

2. Muhtasari juu ya Sheria za mirathi uliwakilishwa mbele ya Tume ya Serikali ya Kenya juu ya Sheria za ndoa n.k . . . . . . . . . . . . . . . . . 15

3. Muhtasari juu ya Waraka wa Tanzania juu ya Sheria ya ndoa inayofanana sawa kwa wote Imechapishwa katika Standard (DSM) Jumatatu, 8 Desemba 1969 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 26

4. Muhtasari juu ya Hijabu na Mirathi uliwasilishwa kwa Mheshimiwa Al-Haj Sheikh Ali Hassan Mwinyi . . . . . . . . . . . . . . . .38

5. Barua ya Wizara ya Elimu Juu ya Hijabu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 45

6. Mahkama ya Kadhi: Baadhi ya Mapendekezo Imechapishwa katika The Democrat (DSM) 17-23, Aug, 1999 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 46

Page 5: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

i

DIBAJI

Tunamshukuru Allãh (s.w.t.), na kwa baraka za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Ahlul~Bayt (a.s.), kwa kutujaalia tuweze kufanikisha juhudi zetu hizi katika kuchapish kitabu hiki juu ya sheria za ki-Islamu.

Kitabu hiki kilochopo mikononi mwako ni tafsiri ya kitabu cha kiingreza kiitwacho In Defense of Islamic Laws kilicho andikwa na marehemu Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi, Muasisi na Mhubiri Mkuu wa Mission hii. Kitabu hiki kimekua maarufu katika ulimwengu wa ki-Islamu. Watu wengi kutoka Africa ya Mashriki wametuomba kukitafasiri katika lugha ya kiswahili.

Tunamshukuru Dr. Mohammad Salehe Kanju kuitafsiri kitabu hiki katika lugha ya kiswahili.

Kwa manufa ya wasomaji wetu tumeongeza makala juu ya Mahakama ya Kadhi ambae ilityariswa na Mwandidhi bada ya kitabu asili ya kiingreza kuchapiswa.

Mission inatoa shukurani zake za dhati kwa Bwana Mahmood Khimji ambae kwa juhudi zake kitabu hiki kinawafikia wasomaji wetu mikononi na Sayyid Murtaza Rizvi kuipanga vizuri katika kompyuta na wale wote wanaotuunga mkono kwa njia moja au nyingine kwa kufanikisha kuchapiswa kitabu hiki, Tunamuomba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) awalipe malipo mema hapo Duniani na baaday huko.

Wamaa Tawfeeqi Illah Billah

BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA

Page 6: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

1

UTANGULIZI

﷽الحمد للہ رب العلمین و الصلوة والسلام علی

خیر خلقه محمد واله الطا ھر ین

Katika mwaka wa 1964, Bunge la Tanganyika lilipitisha Sheria ya “ki-Islamu” (Taarifa mpya) ambayo ilimpa uwezo Waziri anayehusika na mambo ya Sheria kutengeneza na kutangaza Taarifa ya Sheria ya ki-Islamu baada ya kushauriana na Wasomi wa sheria katika madhehebu ya ki-Islamu. Kwa mujibu wa Gazeti la Standard Tanzania (13/7/67) liliandika: “Inafahamika kwamba Tanganyika ni nchi ya kwanza kupata kutekeleza zoezi la kupanga kanuni ya sheria ya ki-Islamu katika mfumo wa sheria iliamriwa halali. Taarifa hizi zitasaidia sana Mahakama ambazo hutegemea juu ya vitabu vya kiada.”

Khoja Shia Ithna-asheri territorial council of Tanzania (Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheri) walilichukulia uzito suala hili. Bwana Mohamed G. Dhirani, aliyekuwa wakati huo Rais wa Baraza ya Jumuiya iliyotajwa, alinichukuwa mpaka kwenye Ofisi za Mwanasheria Mkuu, ambako nilimkuta wakili mkuu wa mradi huo. Alikuwa ni mwislamu wa Zanzibar. Alinishauri niandike kwa Kiingereza, sheria zote za Shia zihusikanazo na masuala haya kwa matumizi ya Ofisi yake. Hivyo niiandika “sheria za ki-Islamu zinazohusika na ndoa, kuvunjika kwa ndoa, makubaliano ya ndoa, wosia, mirathi na waqf.” Bwana Fida Hussein Abdallah Hameer, aliyekuwa Katibu wa Baraza wakati huo alitayarisha Sekretariati kwa ajili ya kusaidia.

Miwishowe makaratasi (yenye taarifa) yalimfikia Bwana Bashir Rahim, aliyekuwa mrasimu wa Bunge Muandamizi ambaye alikamilisha sura nne za ndoa (kama inavyokubalika na madhehebu makubwa matatu

Page 7: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

2

ya Sheria ya Uislamu - Shafii,Hanafi na Shia). Ilichapishwa chini ya mamlaka ya bwana Rashid Kawawa, aliyekuwa wakati huo makamu wa rais wa Tanzania, ambaye alikuwa anapasika vile vile na Idara ya Sheria. Ilitokea kama sheria ndogo zilizotungwa chini ya Taarifa rasmi mpya ya Sheria ya ki-Islamu (Na. 56 ya 1964) (Katika) Nyongeza ya Gazeti (la Serikali Na. 34 la 27 Juni 1967). Ilieleweka zile sura zilizobakia zinazohusu utunzaji wa watoto na talaka nk. zitachapishwa mwishoni mwa mwaka, na kisha hapo Sheria zitaanza kutekelezwa.

KUELEKEA KENYA

Sasa mandhari inahamia Kenya. Serikali ya Kenya wakati huo iliunda Tume juu ya sheria za ndoa, talaka na mirathi, chini ya uwenyekiti wa Mheshimiwa Jaji Spry wa Mahakama Kuu ya Kenya. Tume ilitakiwa itoe mapendekezo kwa ajili ya sheria mpya yenye uwezo mkubwa na kwa kadiri itakavyoweza kutumika kama sheria inayofanana ya ndoa, na talaka itumikayo kwa watu wote nchini Kenya. Ambayo itakuwa badala ya Sheria iliyopo juu ya suala lihusianalo na Sheria ya mila, Sheria ya “ki-Islamu”, (haswa ya kwetu) Sheria ya Baniani na Sheria za Bunge zinazohusika na kutayarisha rasimu ya Shria mpya; ikitoa kipaumbele mahususi kwa hadhi ya wanawake kuhusiana na ndoa na talaka katika jamii huru ya kidemokrasia.

Nilikwenda Mombasa Julai 1967 kwa mintaarafu fulani mingine na wahusika wa Supreme Council (Halmashauri Kuu ya Shia Ithna-asheri) walinichukuwa nikaonane na wakili ambaye alikuwa bingwa katika sheria binafsi za Uislamu. Kwa kuelezewa matukio ya Tanzania, aliniomba nimplekee nakala ya Sheria za “Ki-Islamu” ambayo nimeiandika kwa ajili ya Tanzania. Nami niliahidi hivyo.

Kabla ya hii, niliandika majibu kwa maswali ya Tume ambayo yalipelekwa kabla kwenye Tume.

Kurudi Dar es Salaam, nilikusanya taarifa ya Sheria za “Ki-Islamu” zilizotajwa (karibu karatasi ndefu mia moja, kurasa zilizopigwa

Page 8: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

3

mashine kwa karibu karibu) zikiwa zimerudufiwa, na kutumwa Halmashauri Kuu ya Khoja Shia Ithna-asheri.

Katika juma la tatu la Augusti 1967, niliitwa haraka Mombasa ambako tume ilikuwa ikae kwa ajili ya kusikiliza kuanzia 21/8/1967. Niliandika muhtasari (au taarifa) kwa ajili ya kuwasilisha mbele ya tume, ambayo ilikamilishwa baada ya majadiliano na maofisa wakuu watendaji (wa Halmashauri Kuu).

Muhtasari ule uliwasilishwa kwenye tume na kisha ukachapishwa katika “The Light” ya Julai – Augusti 1967. (Marehemu) Haji Mohamedali Meghji, Rais wa Halmashauri Kuu ya Khoja Shia Ithna-asheri aliandika barua iliyoambatanishwa ya maelezo (ya ziada) dondoo ambayo imechapishwa marudufu kabla ya muhtasari wa kwanza.

Mheshimiwa Jaji Spry alisikika akiwaambia wenzake baadae kwamba “watu hawa walijua kuhusu walichokuwa wakiongea.”

Muhtasari mwingine juu ya Sheria ya Mirathi ambao ulioandikwa na mimi, ulitumwa kwenye tume na kuchapishwa katika “The Light” ya Januari – Aprili 1968. Ni Muhtasari wa pili katika mkusanyo huu.

KURUDI TANZANIA:

Wakati matukio hayo hapo juu yalipokuwa yanafanyika nchini Kenya, ghafla Serikali ya Tanzania ilisimamisha zoezi la upangaji wa Kanuni (wa Sheria ya “ki-Islamu”).

Tume ya Kenya iliwasilisha taarifa yake na mapendekezo wakati fulani katika mwaka wa 1969. Tarehe 10/9/69 Serikali ya Tanzania ilichapisha waraka (White Paper) No. 1 wa 1969 uliosema kwamba inataka kutunga Sheria ya Ndoa iliyo sawasawa (kwa wote), na ikatoa maelezo ya masharti iliyoyataka yawekwe kwenye Sheria iliyokusudiwa.

Pamoja na kuchapishwa kwa waraka, Serikali ilikaribisha maoni na mapendekezo kutoka kwenye Jumuiya na watu binafsi. Wakristo,

Page 9: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

4

Mabaniani na Maismailiya walichapisha maoni yao katika magazeti. Niliwafuata Bakwata kwa madhumuni haya; walikataa kwa mkato kabisa kuingilia mpango wa Serikali. Nilikuwa sina njia nyingine bali kuandika kwa niaba ya Shia Ithna-sheri tu. Maoni yalikuwa ya ukweli na pengine kifungu cha mwisho kilikuwa kikali kidogo. Nilipeleka mswada kwa Bwana Anverali M. Rajpar, aliyekuwa wakati huo Rais wa Khoja Shia Ithna-asheri Territorial Council of Tanzania, aliniambia niendelee na niuchapishe kwenye Gazeti la Standard kwa niaba ya Tanzania Council. Ilitokea katika Standard (Dar es Salaam) tarehe 8 Desemba 1969 (Jumatatu) na baadaye dondoo zake zilichapishwa katika “The Light” ya Desemba 1969. (Mswada) huu hutokea kama muhtasari wa tatu katika kijitabu hiki.

Wakati wa miezi ya baadaye, Halmashauri Kuu (Supreme Council) ilinitumia taarifa mbili za tume ya Kenya, nilishangazwa kuona kwamba karibu mapendekezo mengi ya waraka wa Tanzania yaliondolewa kutoka kwenye mapendekezo ya Tume ya Kenya.

Wakati naandika muswada wa Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971, katika mwanga wa waraka wa Serikali na maoni niliyopokea, Bwana Bashir Rahim, aliyekuwa wakati huo msawidi mkuu wa Bunge, alijaribu kwa uwezo wake kuingiza masharti ya Sheria za “ki-Islamu”. Kabla ya kukamilisha muswada huo, ulionyehswa kwa wanachuoni wa kila dini na madhehebu, na mabadiliko fulani yalifanywa kwa kutegemea juu ya ushauri wao.

HALI ILIYOPO SASA:

Serikali ya Tanzania sasa inataka kutunga Sheria ya Mirathi iliyo sawa kwa wote; ambayo itawapa wanawake kigawanyo sawa na kile cha wanaume. Wakati wanachuo wa “ki-islamu” (sio Bakwata) walipotoa kauli zao dhidi ya sheria hiyo, aliyekuwa wakati huo Rais (wa Jamhuri ya Tanzania) Mheshimiwa Al–Haji Ali Hasani Mwinyi aliwahakikishia kwamba rai haikuwa kubadilisha sheria ya “ki-Islamu”, bali kuweka haki ya mirathi kwa wanawake wale ambao hawana haki kama hizo kabisa – bali wao wenyewe wanachukuliwa kama bidhaa za mirathi.

Page 10: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

5

Wakati huo huo katika mwaka wa 1990, mashirika mabalimbali ya “ki-Islamu” (Mbali na Bakwata) yalianza kufanya kampeni kwa ajili ya washichana wa “ki-Islamu” kuruhusiwa kuvaa Hijab mashuleni. Wawakilishi wao walikutana mara nyingi, na kutegemea juu ya majadiliano yao, niliandika Muhtasari juu ya Hijab na mirathi, ambao hatimaye uliwasilishwa kwa Rais Al-Haj Ali Hassan Mwinyi. (Muhtasari huo) umewekwa katika kijitabu hiki kama Muhtasari wa nne. Inafurahisha kuona kwamba Rais alitamka katika hotuba ya hadhara tarehe 10/8/1995 kwamba wasichana wa “ki-Islamu” sasa wanaruhusiwa kuvaa Hijab mashuleni; na Kaimu Kamishina wa Elimu alitoa mwongozo kwenye suala hili kwa taasisi za Elimu, ambao barua yake halisi yaweza kuonekana katika ukurasa ufuatao, na tarjuma yake ya kiingereza imetolewa mwiso wa kitabu hiki.

Bilal Muslim Mission of Tanzania inaona kwamba muhtasari hizi zina hoja zilizo wazi kuthibitisha kwamba Sheria za “ki-Islamu” zilizoanzia kutokana na hekima ya Mungu haziwezi kubadilishwa, na kwamba Sheria ya “ki-Islamu” ni mfumo pekee ambao huweza kutoa haki na uhuru katika jamii.

Ni kwa sababu hii kwamba Misheni hii imeamua kuchapisha Muhtasari nne pamoja katika kijitabu hiki. Nawashukuru kwa ari hii, na kuomba kwa Allah Subhanahu wa Ta’ala kuwapa tawfiq zaidi, na akifanye kitabu hiki kuwa njia ya mwongozo kwa Waislamu na kwa wasio Waislamu hali kadhalika.

و ما تو فیقی الا با اللہ علیه تو کلت و الیه انیب

Dar es Salaam Sayyid Saeed Akhtar Rizvi31st October 1998

Page 11: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

6

1MUHTASARI JUU YA SHERIA ZA NDOA*

Dondoo kutoka barua iliyoambatanishwa : Muhtasari ufuatao uliandikwa na Maulana Sayyid Saeed Akhtar Rizvi kwa ajili ya kuwasilisha mbele ya tume juu ya Sheria za Ndoa, Talaka na Mirathi, iliyowekwa na Serikali ya Kenya chini ya uweneyekiti wa Mheshimiwa Jaji Spry wa Mahakama Kuu ya Kenya.

Masharti ya Rejea kwa ajili ya Tume ni:-

“Kufikiria Sheria iliyopo ihusikananyo na Ndoa, Talaka na mambo yahusianayo na hayo;” “Kutoa mapendekezo kwa ajili ya Sheria mpya itoayo uwanja mpana na, kwa kadiri itakavyoweza kutekelezwa sheria ya Ndoa sawa kwa watu wote, na talaka itumikayo kwa watu wote nchini Kenya, ambayo itachukuwa nafasi ya sheria iliyopo juu ya suala lihusianalo na Sheria ya mila, Sheria ya ki-Islamu, Sheria ya ki-baniani na amri zinazohusika za Bunge na kutayarisha muswada wa Sheria mpya.”

“kutoa kipaumbele mahususi kwa hadhi za wanawake katika kuhusiana na ndoa na talaka katika jamii huru ya kidemokrasia”.

Tume ilituma maswali mapema kwa pande zote zinazohusika, na Halmashauri Kuu (Supreme Council) ikapeleka majibu yao (yalioandikwa na Maulana Sayyid Saeed Akhtar Rizvi) kwenye Tume kabla.

Tume ilikaa kwa ajili ya kusikiliza mjini Mombasa kuanzia tarehe 21

* Uliwasilishwa mbele ya Tume ya Serekali ya Kenya juu ya Sheria za Ndoa, Talaka na Mirathi; kwa niaba ya Khoja Shia Ithna–asheri (Supreme Council of Africa, Mombasa) 22/8/1967

Page 12: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

7

Augasti 1967. Ujumbe wetu ulitokea mbele ya tume tarehe 22 Augasti. Pamoja na Muhtasari, taarifa iliyobeba mambo mengi ya sheria za ki-Islamu na mkusanyo wa hotuba juu ya Usul-Din “Islam” zote zikiwa zimeandikwa na kukusanywa na Maulana Sayyid Saeed Akhtar Rizvi, ziliwasilishwa mbele ya Tume.

Ni wazi kwamba juhudi ya Maulana katika suala hili imestahiki kusifiwa mno, na sisiti kukiri kwamba uwasilishaji ufuatao usingelifanikiwa bila muongozo na msaada wake.

Wajumbe wa msafara walikuwa, Maulana Sayyid Saeed Akhtar Rizvi, Mulla Asgherali M. M. Jaffer (Mh. Katibu Mkuu), Bw. Hassan A. M. Jaffer (Mh. Mhazina Mkuu), Maulana Sheikh Maqbool Hussain (Mombasa), Bw. Bashir H. Pira na mimi mwenyewe.

Mh. Katibu Mkuu wa Halmashauri Kuu ya Khoja Shia Ithna-asheri Mulla Asgheri M. M. Jaffer aliwasilisha kama msomaji wa Shia Ithna-asheri, na alisoma wasilisho mbele ya Tume. Vile vile alijibu maswali yaliyoulizwa na Tume, na kufafanua nukta mbali mbali zinazohusika na Ndoa, Talaka n.k. kwa mujibu wa madhehebu ya Shia.

MOHAMEDALI MEGHJI:Rais, Shia Ithna-ashri-Halmashauri Kuu (ya Khoja)P. O. Box 1085, Mombasa.

*****

1. Kwa niaba ya Jumuiya ya Shia Ithna-asheri ya Kenya, tunachukuwa fursa hii ya kufanya uwasilishaji huu kwa ajili ya kufikiriwa na Tume.

2. Katika uwasilishaji huu, tunakomea maelezo yetu kwenye Sheria za dini zilizofungana na Ndoa, Talaka, Wosia na Nirathi ya Madhehebu ya ki-Islamu ya Shia Ithna-asheri.

3. Inafahamika kwamba matatizo ya kijamii aina mbalimbali yatokeayo kwa kutmia vibaya au tafsiri potofu za mila, desturi au sheria za dini katika utekelezaji wa jumla, hutoa sababu kwa uwajibikaji wa

Page 13: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

8

makini kwa Serikali, na Serikali katika hamu yake kuwapatia watu wake ustawi katika suala hilo inakabiliwa na jukumu ngumu la Serikali la kutokomeza maovu ya kijamii. Juhudi yoyote katika muelekeo huu yafaa kuungwa mkono na hustahiki ushirikiano wote. Lakini tunahisi kwamba wazo la kutunga Sheria ya wote kuchukua mahali pa Sheria ya ki-Islamu iliyopo sasa sio sahihi.

Hata desturi za kimila (zisizo na mamlaka ya kidini) ni ngumu kubadilisha. Hii huwa hatari mno zaidi katika suala kama la Sheria ya ki-Islamu ambayo ni sehemu muhimu ya dini yetu, ambayo haikomei kwenye ibada tu. Sheria hizi haziwezi kuvunjwa bila ya kupata hisia ya hatia na dhambi.

Kwa hiyo, tunahisi kwamba njia nzuri “itakuwa kuacha mamia ya maua kuchanua.” Umoja wa Kitaifa hauhitaji kwamba raia wote yawapasa kuwa na lahaja inayofanana au imani ya dini inayofanana. Hivyo kwa nini inafikiriwa kwamba ni muhimu kuwa na Sheria ya Ndoa inayofanana na talaka ya kutumika kwa watu wote wa Kenya.

4. Sheria zetu za Shia Ithna-asheri hazikutegemezwa juu ya “Rai” (maoni) au “Qiyas” (anolojia). Zimetegemea kabisa juu ya Qur’an Tukufu na Hadith za Mtukufu Mtume na Maimamu wetu Kumi na Mbili.

Kwa vile tume inahusika na mambo ya Ndoa na Mirathi, lazima tuonyeshe kwamba kanuni za msingi na mambo mengi namna kwa namna ya mirathi yanaelezwa katika Qur’an Tukufu. Kusema kweli, maudhui hii imeshughulikiwa zaidi kwa ukamilifu katika Kitabu Kitukufu. Hali kadhalika, kanuni za msingi za ndoa na talaka zimetegemezwa juu ya Qur’an Tukufu.

Mambo ambayo hayako wazi katika Qur’an Tukufu yanaelezwa katika Hadithi kama ilivyotajwa hapo juu.

Wanachuoni wetu ambao wanaitwa MUJTAHID hawatoi hukumu yoyote kwa maoni yao, analojia (Qiyas) au (kwa) ijimai. Hakuna

Page 14: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

9

mamlaka kama hayo yaliyotolewa kwa yeyote katika Sheria ya madhehebu yetu. Wanaweza kutofautiana katika kutafsiri Hadith fulani zinazohusu baadhi ya mambo madogo, lakini hata hivyo tofauti hiyo ni tofauti katika tafsir, sio ya maoni.

Madhehebu ya Shia Ithna-ashri hufuata katika mambo yote ya dini hukumu za Mujtahid mkubwa wa zama. Anachukuliwa kuwa yeye ni mwakilishi wa Imamu wetu wa Kumi na Mbili na ni mtu wa mwisho juu ya mambo yote ya dini. Kwake yeye amekabidhiwa katika masuala fulani, mamlaka za ulezi wa watoto, ulinzi katika ndoa na talaka, utekelezaji wa Wosia na mali ya marehemu na mambo kama hayo.

5. Sheria ya ki-Islamu ya madhehebu ya Shia Ithna-asheri ni chombo kilichofumwa vizuri. Hatuwezi kubadilisha au kurekebisha, moja au mbili ya mambo yake bila kuharibu ufumaji wote.

Kwa Mfano:-

Hivyo ni wazi kwamba mfumo wa Sheria ya ndoa, talaka na mirathi hauwezi kubadilishwa; vinginevyo hii itaanzisha muingilio wa moja kwa moja katika dini yetu.

6. Kuhusu hamu ya Tume “Kutoa kipaumbele kwa hadhi ya

i. Hukumu za Ndoa na Talaka zinabeba uzito wa moja kwa moja juu ya uhalali au vinginevyo wa mtoto; juu ya wema au dhambi ya pamoja ya mwanaume na mwanamke; katika haki ya wao wenyewe kwa wenyewe ya mirathi na ile ya mtoto; mbali na kutokana na jamii na shida za kisheria.

ii. Katika sheria za ki-Islamu mtu hawezi kutumia kitu chochote kilichopatikana kiharamu (kwa maana ya kidini) amma kwa kilimwengu au kwa madhumuni ya kidini. Kwa hiyo, kama mabadiliko yanafanywa katika sheria za mirathi na mtu fulani anapewa zaidi kuliko mgao wake kwa mujibu wa Qur’an Tukufu, maisha yake yote yatakuwa duni. Maisha yake ya kila siku yatakuwa ni orodha ndefu ya kuchupa mipaka, Sala zake, Hija, chakula na mavazi vitakuwa haramu katika maana ya kidini.

Page 15: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

10

wanawake katika kuhusiana na Ndoa na Talaka katika jamii huru ya kidemokrasia”.

7. Mgao wa mwanamke kwa kawaida ni, nusu ya ule (mgao) wa mwanaume. Lakini hii ni mantiki kabisa. Uislamu umemfanya mwanaume kuwa na jukumu la kutunza familia. Hakuna mzigo kama huo uliowekwa juu ya mwanamke. Hata mke tajiri anahusika kupata matunzo yake kutoka kwa mume wake ingawa anaweza kuwa ni maskini. Kwa vile matunzo ya familia ni jukumu la mwanaume, amepewa mgao marudufu karibu katika mirathi yote.

Vile vile, mwanamke hupata mahari ambayo hutoka kwa mume kwenda kwa mke. Kwa hiyo uwiyano wa mgao uliowekwa katika Qur’an Tukufu ni wa haki zaidi.

Tunataka kuwakilisha kama ifuatavyo:-

a. katika sheira ya madhehebu yetu mwanamke anazo haki hizo upendeleo na ulinzi wa salama tangia Karne ya Kumi na nne, nyingi ya hizo hazikufikiriwa katika Jamii zisizo za ki-Islamu mpaka Karne iliyopita na baadhi ya hizo ziko mbele ya inayoitwa zama ya kisasa.

b. Uislamu kwa mujibu wa madhehebu ya Shia, umempa mwanamke haki ya kufanya mkataba yeye mwenyewe katika Ndoa kama ni mtu mzima na makanifu.

c. Uislamu umempa mwanamke kitambulisho cha kujitegemea. Mwanamke wa ki-Islamu anamiliki mali yake mwenyewe hata baada ya kuolewa, na mume hawezi kuingilia.

d. Mwanamke anaweza kumfungulia mume wake mashtaka, anaweza kutoa ushahidi dhidi yake. Anarithi kutoka kwa mume kwa haki na mwanaume kutoka kwa mwanamke.

Haki hii, ya wote pamoja ya mirathi (kurithiana) ilitolewa wakati hakuna jamii kamwe ilifikiria kuhusu haki hii.

Page 16: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

11

8. Sheria ya Uislamu ihusianayo na Wosia haimruhusu mtu kuusia zaidi ya thuluthi moja ya mali yake kamili. Hivyo hali ya kifedha ya wale watakao kuwa warithi siku zote inalindwa na mbali ya kutwaliwa kokote isivyo haki na yeyote. Usalama huu bado unakosekana katika jamii nyingi ambazo huruhusu mtu kutoa mali yote kwa mgeni haswa.

9. Sasa tunakuja kwenye baadhi ya mambo ya Ndoa:-

Kwa mfano, kama mke ana ugonjwa sugu au ni mgumba au kwa sababu nyingine fulani haiwezekani kwa wawili hao kuishi kama mume na mke. Suluhisho litolewalo na jamii fulani ni kumtaliki mke na kuoa mwingine. Lakini je, hii ni haki? Je, ni wema au uadilifu kumfukuza mwanamke katika hali ya uzee au katika umri wake wakati kutoka kwenye nyumba yake, kwa sababu ame kuwa mgonjwa siku zote au ametokea kuwa mgumba? Uislamu hupinga ukatili huo kwa kuruhusu mitala.

10.

a. MITALA: Jamii ya Waafrika ilikuwa, na kwa kiwango fulani ni, jamii ya kimitala. Uislamu vilevile huruhusu mitala. Umeruhusu wake wanne kwa wakati mmoja na imeamuru usawa katika kuwahudumia wake wote.

b. Yapasa ikumbukwe kwamba mitala sio kitu cha lazima wala sio kitu kinachotetewa. Ni ruhusa tu pamoja na ukomo fulani na masharti. Na katika baadhi ya mazingira ruhusa hii imethibitisha manufaa mazuri mno.

a. TALAKA: Hakuna haja kusisitiza kwamba katika hali fulani talaka ndio suluhisho pekee lililobakia kwa wawili hao (mume na mke). Manufaa ya mfumo wa talaka yanaweza kuonekana kutokana na ukweli kwamba hata Baniani na Wakristo wengi wamelazimika kwa nguvu ya moja kwa moja isio epukika kutunga sheria za talaka.

b. Ni lazima tuonyeshe kwenye wakati wa mwanzo kwamba madhehebu ya Shia-Ithanaseri ya ki-Islamu imeweka kanuani ngumu zilizotegemea juu ya Qura’n Tukufu na Hadithi, kuhusiana na talaka.

Page 17: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

12

Zaidi ni lazima vile vile kwamba mume awe mtu mzima, mwenye akili timamu na mwenye kuelewa vizuri atendaye kwa utashi wa uhuru wake mwenyewe, na sio katika mshituko wa hasira au kutishwa. Na kwamba lazima awe na nia ya dhahiri ya kuvunja ndoa.

Kwa kadiri mwanamke anavyohusika, yeye wakati wa Talaka lazima awe katika hali ya tohara na kwamba talaka haiwezi kutamkwa hata wakati wa tohara ambao kwamba mume amekutana naye kimwili.

Kama moja ya masharti yaliyotajwa hapo juu yakivunjwa Talaka itakuwa batili na kutenguka.

c. Talaka imetangazwa na Mtukufu Mtume kuwa ni kitu kilichotwezwa katika halali zote.

d. Qur’an Tukufu imeweka mfumo wa usuluhisho wakati wowote kukiwa kuna kutokuelewana kati ya mume na mke.

e. MASHARTI YA TALAKA: Talaka inaruhusiwa mradi tu inatamkwa mbele ya watu wawili mashahidi. “Adil” (watu wamuelekeo thabiti) ambao husikiliza maeneno na kuelewa asili au chanzo cha talaka. Talaka lazima itamkwe katika utaratibu uliothibitishwa,

f. Talaka tatu haziwezi kutolewa kwa wakati mmoja. Kama mtu atasema kwamba anatoa talaka tatu, hata moja haitakuwa halali.

g. Katika hali nyingi, talaka inaweza kutenguliwa, na mume ana lazimika kumtunza mke aliyetalikiwa wakati wa kipindi cha “Iddat” (kwa kawaida ni miezi mitatu) katika nyumba yake; vinginevyo ahiari kutoka (mwenyewe).

h. Wakati wa kipindi kilichotajwa cha “IDDAT” mume anayo haki ya kutengua talaka kwa maneno au kitendo na kutakuwa hakuna haja ya taratibu zozote.

Page 18: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

13

Kanuni hizi ngumu zimekuwa siku zote zikitekelezwa na madhehebu yetu. Shukurani kwa Shariat yetu, talaka katika madhehebu ya Shia Ithna-asheri ziko mara chache sana.

11. HAKI YA MWANAMKE KUHUSIANA NA UVUNJANI WA NDOA: Mwanamke hakupewa haki ya kumpa talaka mume wake. Sababu yeneyewe sio ngumu sana kuelewa. Familia ni msingi wa jamii ya binadamu na kwa vile kila jamii huhitaji mamlaka ya mwisho kuiweka katika mpango ulioandaliwa vizuri. Familia lazima vile vile ipate kiongozi mkuu. Sheria ya ki-Islamu imetoa nafasi hiyo kwa mume, na mume amepewa haki ya kutoa talaka.

Lakini mke ana haki ya kudai talaka katika hali nyingi: Km:

12. Katika uwasilishaji wetu, tulionyesha mapema kwamba sheria sawa kwa wote katika jamii ya kilimwengu kama hii ya Kenya haina umuhimu kwa umoja wa kitaifa. Sasa tunaomba kuwasilisha kwamba kuishi pamoja, kwa amani na urafiki miongoni mwa watu walioambatanishwa kwenye imani za dini mbalimbali na sheria kunaweza kupatikana tu kama uhuru utatolewa kwao kutekeleza sheria kama hizi, na kutenda kimujibu (kama itakikanavyo).

Haitakuwa nje ya sehemu (ya maudhui) kutaja hapa kwamba Uislamu una seti ya theolojia inayojumuisha mambo yote ya maisha. Na kwamba

a. Anaweza akaomba Khula ambayo inaweza kukubalika juu yake na mume;

b. Anaweza kumuomba Mujtahidi kumpa talaka katika hali ambako mume ametoweka, au akapuuza kumtunza.

c. Katika hali ya mume yakuwa mwenda wazimu, imma imetokea kabla au baada ya ndoa, ana haki ya kuifuta ndoa bila haja yoyote ya kupeleka kesi kwa Mujtahid.

d. Na anaweza kuibatisha Ndoa baada ya kuipeleka kesi kwa Mujtahid, kama mume ni hanithi.

Page 19: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

14

amri zake na maelekezo hayakomei kwenye ibada za sala za kila siku na maombi pekee. Ni mfumo wa maisha ambao hutoa huduma ya mipangilio namna namna kwa jaamii, ndoa, maadili, na hali kadhalika uendeshaji wa biashara katika maisha ya kibinadamu.

Pengine itakuwa ni kitu cha kuvutia kwamba hivi karibuni Tanzania imechapisha “Taarifa ya sheria ya ki-Islamu.” Huu ni utungaji mdogo wa Sheria chini ya “Taarifa mpya ya sheria ya ki-Islamu” (No. 56 ya 1964). Nyongeza ya Gazeti (la Srikali) No. 34 ya 27 Juni, 1967 yahusika. Hatua hii iliyokuja wakati mzuri katika Tanzania imethibitisha kwamba nchi yoyote inayopigania uhuru wa kuabudu na utekelezaji wa dini inaweza kwa usalama kuweka sheria mbali mbali kuhusiana na Ndoa, Talaka, Mirathi au mambo yoyote kama hayo. Vile vile huonyesha kwamba hatua kama hiyo inatekelezeka. Tunaweza kuongeza kwamba vile vile hudokeza kwamba mpangilio kama huo unasaidia kwenye kuelewa vizuri na uhusiano katika nchi ambako mazingira ya maridhia yanatakiwa yafanyike, na tunaweka mikononi mwa tume kupendekeza hatua kama hiyo nchini Kenya.

13. Kujaribu kuweka mpaka kati ya Qur’an Tukufu na Sheria ya ki-Islamu kamwe hakuwezi kufikirika. Jaribio lolote la kuvuruga au katika maneno ya masharti ya rejea ya Tume, “Kubadilisha Sheria ya ki-Islamu” kutakuwa hakukubaliki. Kama ilivyoelezwa hapo juu, sheria ya ki-Islamu imetegemezwa juu ya Qur’an Tukufu na kubadilisha Sheria ya Kiislamu ni sawa sawa na kubadilisha Qur’an Tukufu.

14. Tumewasilisha maswali yaliyotumwa na Tume yakiwa yamekamilishwa ipasavyo sambamba pamoja na mpangilio wa sheria ya ki-Islamu (katika Kiingereza) kwa mujibu wa Sheria ya Madhehebu ya Shia kuhusiana na Ndoa, uvunjaji wa Ndoa, Wosia, Mirathi, Makubaliano na Wakf; na tutafurahi kujibu maswali yoyote yajitokezayo kutoka humo na kuwasilisha ufafanuzi utakiwao.

MOMBASA, 22 AGOSTI 1967.

Page 20: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

15

2MUHTASARI JUU YA SHERIA ZA MIRATHI*

ANGALIA: Tuna furaha kufunga pamoja na huu muhtasari uliowasilishwa kwenye tume juu ya sheria ya mirathi iliyoteuliwa hivi karibuni na Serikali ya Kenya. Masharti ya rejea yakiwa, kufirikiria sheria zilizopo sasa zinazohusu ndoa, talaka na mambo yanayohusika pamoja na hayo na kupendekeza Sheria inayofanana ya kutumika kwa watu wote wa Kenya ikitoa kipaumbela kwenye hadhi ya wanawake kuhusiana na ndoa na talaka katika jamii huru ya kidemokrasia.

Sekritariati hii ina wiwa na Maulana Sayyid Saeed Akhtar Rizvi, mwanachuo mkazi wa Dar es Salaam, Muasisi na Mhubiri Mkuu, wa Bilal Muslim Mission of Tanzania kwa juhudi zake kubwa katika kuandaa muhtasari huu. Vile vile tuna viwa na Mulla Hussein A. Rahim M.B.E. wa Zanzibar, kwa muongozo wake wenye thamani.

Tunaomba Allah (s.w.t.) kwamba awalipe kwa wingi hapa duniani na kesho akhera.

ASGHARALI M. M. JAFFAR,Mh. Katibu Mkuu,Halmashauri Kuu K. S. Ithna-AsheriP. O. Box 1085, MOMBASA

*****

1. Kwa niaba ya Jumuiya ya Shia Ithna-Asheri ya Kenya tunaomba ruhusa ya kutoa uwasilishaji huu kw aajili ya kufikiriwa na Tume.

* Uliwakilishwa mbele ya Tume ya Serikali ya Kenya juu ya Sheria za Ndoa, Talaka na Mirathi: kwa niaba ya Khoja Shia Ithna-Asheri Supreme Council of Afrika Mombasa, 1967.

Page 21: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

16

2. Maelezo yetu yanakomea kwenye Sheria za dini zinazohusika na wosia na Mirathi kwa mujibu wa madhehebu ya ki-Islamu ya Shia Ithna-asheri, isipokuwa ambako palipokuwa na maana kutoa maoni ya madhehebu nyingine ili kuifanya nukta yetu kuwa wazi.

3. Tayari tumewasilisha maswali yaliyotumwa na Tume yakiwa yamekamilishwa ipasavyo pamoja na mpangilio wa sheria za ki-Islamu (kwa Kiingerza) kwa mujibu wa Sheria ya Madhehebu ya ki-Islamu ya Shia Ithna-asheri ihusianayo na Mirathi na Wosia miongoni mwa mambo mengine. Katika wasilisho hili tutajitahidi kueleza kanuni za msingi chini ya hukumu hizo.

4. Tunaelewa kwamba tume hii itatoa kipaumbele kwenye hadhi ya wanawake. Tunajasiri kutumaini kwamba Sheria ya ki-Islamu inayotajwa kwa mujibu wa madhehebu ya Shia, itakuwa ya msaada mkubwa kwa Tume katika kazi yake juu ya suala hili.

Haitakuwa nje ya sehemu (ya maudhui) kutaja kwamba mila ya ki-Arabu ya zamani ilikuwa na lengo moja la msingi katika mtizamo, yaani, uzuiaji wa kudumu wa mali katika familia. Pamoja na lengo hili katika mtizamo, urithi ulikomea kwa ndugu wa kiume pekee tu, na hata miongoni mwao ni kwa wale tu ambao walikuwa na uwezo wa kubeba silaha.

Hatukusudii kushughulika sana juu ya nukta hii; itoshe tu kusema kwamba tabia kama hii, zaidi au kidogo ilikuwepo katika jamii zote katika wakati huo na imebakia katika jamii nyingi mpaka sasa. Uislamu ulitoa kwa kudhihirisha uwekaji wa sheria ya haki ya kurithi kwa wale ambao walienguliwa na taasisi za zamani. Moja ya matokeo ya faida ya sheria mpya ya Mungu ilikuwa kunyanyua hadhi ya wanawake katika mizani ya ustaarabu, kwa kunyanyua uchumi wao na nafasi ya kijamii, na kuwapa wajane, mama, mabinti na dada na ndugu wengine wa kike haki ya kurithi.

5. Moyo huu umehifadhiwa katika Sheria ya madhehebu ya Shia ambayo, kwa kunukuu maneno ya mwanachuoni mkubwa Sayyed Amir Ali, “Ni ya wepesi mkubwa mno na haihusishi mjadala wowote

Page 22: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

17

kuhusiana na haki za ndugu wa kiume na wa kike - “Asabah na Zav-il-Arham”. Kisha aliendelea kusema kwamba “Tofauti kubwa, kusema kweli, kati ya Shia na Sheria ya mirathi ya Sunni iko katika suala la jinsia ya Kuumeni. Shia wanakataa kwa kupinga itikadi ya Taasib au jinsia ya Kuumeni; hatimaye uhusiano wa Kuumeni wa jinsia ya kiume, au inayoitwa “Asbah Sahihi” katika fikihi ya Sunni (Sheria ya Sunni), hawana upendeleo maalum wala hawafadilishwi kwenye kuunganisha mahusiano na marehemu kupitia wanawake. Kwa mfano, Shia wanaona ni kinyume cha uadilifu kuwatoa watoto wa binti kwa kupendela kizazi cha mbali cha kaka, kwa msingi wa kubunia kwa kuwa kwao kuungana na marehemu kupitia mahusiano ya kuumeni.” (Mohammeden Law, by Ameer Ali Vo. 2; P. 128).

6. Kanuni zinazoongoza zinaweza kuelezwa kwa ufupi katika maneno yafuatayo:-

Kwa mfano:

a. Kama Muislamu Sunni akifa akiacha nyuma yake binti wa binti yake pamoja na mtoto wa kiume wa kaka yake, mtoto wa kiume wa kaka yake atachukuwa urithi wote kama ASABAH (ndugu wa kuumeni wa jinsia ya kiume). Kwa kumuondoa mjukuu mwenyewe wa marehemu. Chini ya Sheria ya Shia Ithna-asheri, mjukuu wa kike (anayezaliwa na binti yake) wa marehemu, kama mtoto kwa nasaba, huchukuwa mali yote kwa kumuondoa mtoto wa kiume wa kaka yake.

b. Kama Muislamu Sunni akifa, akiacha nyuma binti na kaka, binti huchukuwa mgao ulioainishwa, yaani moja kwa mbili za mwanaume na inayobakia huenda kwa kaka kama Asabah. Chini ya Sheria ya Shia Ithna-asheri, huchukuwa mali yote, nusu kama kiainisho cha mgao wake, na nusu nyingine kwa itikadi ya kurudisha.

a. Mrithi mwenye uhusiano wa karibu na marehemu hurithi kwa kumfadhilisha zaidi kuliko yule mwenye kufungamana naye kwa mbali;

b. Yeyote yule anayehusiana na marehemu kupitia mtu yeyote harithi

Page 23: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

18

Inaweza ikaulizwa kwa nini mgao wa mwanamke, kwa kawaida ni nusu ya ule wa mwanaume? Kusema kweli, ni yenye mantiki kabisa. Uislamu umemfanya mwanaume kuwajibika kwa ajili ya matunzo ya familia. Hakuna mzigo kama huo uliowekwa juu ya mwanamke. Hata mke tajiri anapasika kupata matunzo yake kutoka kwa mume wake ingawa anaweza akawa masikini. Kwa vile anatakiwa kubeba gharama zote, amepewa mgao marudufu karibu katika kila mirthi. Vile vile mwanamke hupata mahari ambayo hutoka kwa mwanaume kwenda kwa mwanamke. Hivyo uwiyano wa migao uliowekwa na Qur’an Tukufu ni wa haki zaidi.

7. MAKUNDI NA TABAKA ZA WARITHI:

Katika Shariat za Shia Ithna-asheri, warithi wamegawanywa katika makundi mawili, yaani, wale ambao hurithi kwa haki ya “Nasab” (nasaba); na wale ambao wanarithi kwa haki ya “Sabab” ambao kwamba muhimu ni wa ndoa (kuoana). Makundi yote hurithi kwa pamoja.

Kundi la kwanza yaani mahusiano ambayo yanapasika kurithi kwa sababu ya unasaba limegawanyika katika tabaka tatu:-

wakati mtu yule anaishi;

c. Kaka na dada wa kuzaliwa mama mmoja, baba mmoja wanapendelewa kuliko kaka na dada wa kinasaba; lakini kaka na dada wa tumbo mmoja watarithi pamoja nao.

d. Wakati uhusiano ni sawa, mwanamume kwa kawaida hupata marudufu ya mgao wa mwanamke, isipokuwa katika hali ya warithi wanaohusiana kwa mama ambao kwa ujumla hugawanya urithi miongoni mwao kwa sawa sawa bila tofauti ya jinsia.

a. Tabaka la Kwanza:

(i) Wazazi na (ii) Watoto (au katika kukosekana kwao, wajukuu wowote kwenda chini: yaani: kilembwe, kitukuu na kuendelea).

Page 24: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

19

Kama ilivyoelezwa hapo juu mume au mke au wakeze marehemu watarithi pamoja na tabaka zote hizi.

8. Dhul – Fardh na Dhul Qarabat:

Ni muhimu kutaja kwamba, chini ya sheria ya Shia, warithi katika kundi au tabaka lolote watakalokuwa wamegawanywa katika mafungu matatu, kuhusiana na haki ambayo wanapasika wao kushiriki katika mirathi:-

b. Tabaka la Pili:

Kama hakuna mrithi kabisa katika tabaka la kwanza, basi wazazi na dhuria wa wazazi wa marehemu watarithi: Ina maana:

(i) Babu zake marehemu (wowote kwenda juu).(ii) Kaka na Dada (au katika kukosekana kwao, dhuria wa kaka na dada).

c. Tabaka la Tatu:

Kama hakuna mrithi aliyepo si katika tabaka la kwanza au la pili, basi dhuria wa mababu (wowote kwenda juu) watarithi. Ina maana: ndugu wa upande wa kiume na upande wa kike wa marehemu, ami, wajomba na shangazi wa marehemu (au katika kukosekana kwao, basi watoto wao kwenda chini).

i. DHUL-FARDH: wale ambao wana haki kwenye mgao ulioainishwa katika mirathi ni hawa:

ii. DHUL-QARABAT: Wale ambao huchukuwa urithi kwa sababu ya uhusiano wao na marehemu, lakini ambao mgao wao hushuka na kupanda kwa kutegemea idadi ya warithi na mazingira. Hawa ni:-

a. Mamab. Mume c. Mjane au Wajaned. Mtu au watu wanaohusiana kwa mama yuleyule tu

a. Mtoto au watoto wa kiume

Page 25: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

20

Angalia : Wakati kukiwa na mrithi mmoja tu, imma Dhul-Fardh au Dhul-Qarabat, au mwenye kupasika kwa sababu ya uhusiano maalum wa Sabab (kuoana-ndoa), mrithi kama huyo huchukuwa mirathi yote. Kwa mfano, binti pekee huchukua mgao wake uliopangwa, yaani, nusu moja na iliyobakia huenda kwake kwa kurudisha. Mtoto wa kiume pekee huchukua mali yote kwa haki ya Qarabat, hakuna mgao ulioainishwa uliowekwa kwake kwa Sheria. Wakati marehemu ni mwanamke na hakuacha nyuma yake jamaa anayehusiana na yeye isipokuwa mume, ambaye anahusika na kurithi kwa sababau ya ndoa, anachukuwa urithi wote kwanza kama mgao wake ulioainishwa, na uliobakia kwa kurudisha.

iii. DHUL – FARDH WAL-QARABAT: Hawa ni warithi ambao wakati mwingine hurithi kwa sababu ya uhusiano wao na wakati mwingine hutegemea migao yao iliyopangwa; hawa ni:

b. Kaka kamili au katika kutokuwepo kwao ndugu kwa upande wa baba (mama mbali mbali)

c. Mababud. Ami na Shangazie. Wajomba na mama wadogo.

a. Baba ambaye hurithi mgao uliopangwa kama kuna mtoto wa marehemu; na huchukuwa kwa uhusiano kama hakuna mtoto wa marehemu.

b. Binti au Mabinti ambao hupata mgao wao uliopangwa bila kuwepo baba wa marehemu au kaka yake au kaka zao wenyewe; na wanachukua kwa ushusiano wakati wakiwa pamoja na yeyote kati yao.

c. Dada kamili au dadaze au katika kutokuwepo kwao, dada wa nasaba au dadaze, ambao hupata mgao uliopangwa wakati bila kuwepo babu au kaka, kakaze wa daraja moja kama wao wenyewe, na huchukuwa kwa uhusiano wakati wakiwa pamoja na yeyote kati yao.

Page 26: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

21

9. MIGAO: Kwa kadiri migao inavyohusika iko sita kwa idadi, yaani:- (1) Nusu moja (2) Moja ya nne (3) Moja ya Nane (4) Moja ya tatu (5) Mbili ya tatu (6) Moja ya sita.

i. NUSU MOJA : Wafuatao wanapasika kwenye nusu moja ya urithi:

ii. MOJA YA NNE : Wafuatao wanahusika kwenye moja ya nne:

iii. MOJA YA NANE : Hii huchukuliwa na mjane au wajane wakati kuna nasaba ya dhuria ya mume.

iv. MOJA YA TATU : Wafuatato wanapasika kwenye moja ya tatu:-

v. MBILI YA TATU : Wafuatao wanapasika kwenye mbili ya tatu:

vi. MOJA YA SITA : Moja ya Sita inachukuliwa na wafuatao:

a. Mume wakati mke hakuacha mtoto;b. Binti wakati hakuna mtoto wa kiume;c. Dada kamili kwa kukosekana warithi wengine ambao

wametajwa mapema;d. Dada wa nasaba wakati hakuna kaka na dada kamili.

a. Mume, wakati kuna nasaba ya dhuria ya mke;b. Mke, wakati hakuna nasaba ya dhuria ya mume;

a. Mama, wakati hakuna nasaba ya dhuria ya marehemu, wala hakuacha kaka wawili, au dada wanne au kaka mmoja na dada wawili.

b. Kaka na dada tumbo moja, wakati wakiwa wawili au zaidi katika idadi.

a. Mabinti wawili au zaidi, wakati hakuna mtoto wa kiume;b. Dada kamili wawili au zaidi wakati hakuna kaka kamili au

hakuna kakaze (baba mmoja mama mabali mbali).

a. Wote baba na mama wakati marehemu ameacha nasaba ya dhuria.

b. Mama, wakati wanakuwepo pamoja naye kaka wawili au zaidi wa damu kamili au kaka mmoja na dada wawili au dada wanne wa damu kamili (au kwa baba yule tu, baba yule akiwa yupo).

c. Kaka mmoja au dada wa tumbo moja.

Page 27: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

22

10. MGAWANYO WA MALI: Wakati kuna mmoja tu wa warithi waliotajwa hapo juu akiwa mwanaume au mwanamke hupata mali yote. Kama ni Dhul-Qarabat, huipata kwa sababu ya uhusiano; kama ni Dhul-Fardh, kwanza anapata mgao wake uliopangwa, na kisha mabaki anapewa yeye kama kurudisha (Radd).

Kama wako warithi wawili au zaidi, itagawanywa katika utaratibu ufuatao: Kwanza mume; au mke au wake watachukuwa mgao wao; kisha ndugu Dhul–Fardh watapata mgao wao; kisha mabaki yatagawanywa miongoni mwa warithi Dhul-Qarabat.

Mfano: Kutoa mfano wa utaratibu wetu, ngoja nichukulie kwamba mtu anakufa anamuacha baba yake, mama, mke, watoto wanne wa kiume, mabinti watano, wajukuu watatu, babu, kaka watatu na shangazi wawili.

Kwa vile ameacha wazazi na watoto wakiume na mabinti, ambao wanahusika na tabaka la kwanza la warithi, babu na kaka (ambao wanahusika na tabaka la pili) na mashangazi (ambao wanahusika na tabaka la tatu) wataondolewa kwenye urithi.

Hali kadhalika, wajukuu wataondolewa kwa sababu ya kuwepo watoto, juu ya msingi wa karibu kuwaondoa wa mbali zaidi.

Mfumo huu wa kuondoa hutuacha na warithi wafuatao: Mke, Baba, Mama, Watoto wanne wa kiume na mabinti watano.

Mke atapata 1/8 ya mali kwa sababu marehemu ameacha watoto; Baba na Mama wote watapata kila mmoja, moja ya sita 1/6.

Kigawanyo cha kawaida cha 8 na 6 itakuwa 24. Hivyo mali itagawanywa katika migao 24 – ambapo kutoka hiyo mke atapata 3 (yaani 1/8), baba 4 (yaani 1/6) na mama vile vile 4 (yaani 1/6). Itaonekana kuwa baba ameshughulikiwa hapa kama Dhul–Fardhi, sio kama Dhul–Qarabat, kwa sababu ya watoto wa marehemu, na mama kupata mgao pungufu (yaani 1/6 badala ya 1/3) kwa sababu ya mantiki hiyo hiyo.

Vyovyote vile, baada ya kupunguza 3 + 4 + 4 (yaani 11/24) tumebakiwa

Page 28: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

23

na migao 13. Hii itagawanywa miongoni mwa watoto, mtoto wa kiume akipata marudufu ya mgao wa binti. Ina maana kwamba – kila mmoja wa watoto wanne wa kiume atachukuwa migao miwili (kufanya 8) na kila mmoja wa mabinti atapata mgao mmoja (kufanya 5). Hivyo migao yote imekwisha.

11. DHUL-FARDH LAZIMA WAPATE MGAO WAO ULIOPANGWA:

Katika mfano wa hapo juu, migao imelingana na mahitaji ya mafungu ya mirathi. Lakini kuna weza kuwa na hali wakati migao iliyopangwa yaweza kuzidi kigawanyo cha kawaida cha migao. Kwa mfano, kama mwanamke ataacha mume nyuma yake mabinti wawili na mama, migao yao kwa kuhusiana itakuwa moja ya nne, mbili ya tatu na moja ya sita. Kigawanyo cha kawaida 3, 4, na 6 ni 12, ambacho huwakilisha migao ambayo kwayo mali itagawanywa – 3 ikiwa mgao wa mume, 8 wa mabinti na 2 wa mama. Lakini 3 + 8 + 2 hufanya 13, sio 12.

Masunni hugawa mali kwenye migao 13, na kuleta upungufu kwa wote. Lakini miongoni mwa Shia, Mama na mume, wao wakiwa ni Dhul-Fardh, lazima wapate mgao wao kamili, yaani 3 + 2. Na mabaki yaani 7/12 yatagawanywa sawa sawa miongoni mwa mabinti, kwa sababu watoto vile vile ni miongoni mwa Dhul-Qarabat.

Hivyo wakati wowote kunapokuwa na upungufu katika migao iliyopangwa, huangukia juu ya Dhul–Qarabat, ambao migao yao hupasika na kupanda na kushuka, sio juu ya Dhul-Fardh.

12. IMAM : Mrithi wa Marehemu asiye na mrithi:

Kama hakuna mrithi katika tabaka yoyote na makundi yaliyotajwa hapo juu, Imam atakuwa mrithi wake. Kwa vile Imamu wetu yuko kwenye ghaibu kwa wakati huu, Mujtahid atapokea mali ile kwa niaba ya Imamu na ataitumia katika utangazaji wa imani na unyanyuaji wa dini ya Jumuiya ya Shia kwa kupendelea zaidi katika eneo lile lile alilokuwa akiishi marehemu.

Page 29: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

24

Mtu ambaye hana mrithi isipokuwa Imamu, ameruhusiwa katika Sheria ya Shia kutoa kwa wosia mali yake yote ili mradi utoaji huo ni kwa ajili ya faida ya Shia Ithna-asheri masikini, Ithna-asheri mayatima au Ithna-asheri wasafiri mafukara tu.

13. KUONDOA KUTOKA MIRATHI :

Hakuna mwandishi wa wosia mwenye haki yoyote ya kumzuiya yeyote katika warithi wake kutokana na haki yake ya mgao wa mirathi. Hata kama anafanya wosia kuhusu suala hili, utakuwa umetenguka na batili katika sheria. Lakini mrithi atazuiwa kutoka kwenye mirathi kama akitokea kuwa sio Mwislamu au kwa makusudi na kwa dhulma amemuua marehemu ambaye kwamba mali yake angerithi.

14. HATI ZA WOSIA :

Ufanyaji wa wosia unatambuliwa na kuhimizwa na Sheria ya Ki-Islamu. Wosia unaweza ukawa wa mdomo au katika maandishi. Mwandishi wa Wosia ameruhusiwa kurithisha mpaka theluthi moja ya mali yake halisi. Kurithisha kokote kunakozidi theluthi moja ni batili, vinginevyo mpaka ikubaliwe na warithi. Mpangilio ya hukumu juu ya suala hili unatolewa katika kitabu kilicho andamana “ISALAMIC LAW-Sheria za Ki-Islamu” na sio muhimu kueleza kwa kinaganaga hapa.

15. ULIPAJI WA MADENI NA GHARAMA KUTOKA KWENYE MALI:

Inaweza kuonyeshwa hapa kwamba katika hali zote, madeni ya halali yampasayo marehemu pamoja na gharama fulani fulani lazima yapewe umuhimu wa kwanza katika ulipaji wa urithi na migao ya warithi.

Neno “Deni”, Maana yake madeni ya kawaida ailiyoyaingia mwenyewe au kwa niaba ya marehemu na hujumuisha vile vile madeni ya kidini kama Zakat (kodi ya maskini), Khumus (hutolewa moja ya tano), Kaffara (malipo ya kosa au fidia), Nazar (nadhiri) nk., na neno “gharama” hujumuisha wajibu wa kupeleka wakili kwa gharama za mali ya

Page 30: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

25

marehemu, kutekeleza Hija Makka kama ilikuwa wajibu juu ya marehemu na haikutekelezwa na yeye wakati wa uhai wake. Gharama za mazishi vile vile zinatakiwa kupewa umuhimu wakulipwa.

Baada ya kulipa madeni yaliyotajwa na gharama na urithi ulioelekezwa na wosia wa marehemu kufikia mwisho wa theluthi moja ya mali halisi, mabaki yatagawanywa miongoni mwa warithi.

16. Katika kuhitimisha, tungependa kurudia tuliyoyasema mapema mbele ya Tume juu ya Sheria ya mambo ya Ndoa. Tunahisi kwamba wazo la kutunga Sheria ya wote kuchukua mahali pa Sheria ya ki-Islamu iliyopo sasa sio makosa tu bali ni kufuru kwa mtizamo wetu wa kidini. Itakuwa ni sawa sawa na kuweka dini inayofanana juu ya wote ambapo litakuwa ni wazo lisilo na maana. Sheria za ki–Islamu ni sehemu ya dini yetu. Sheria hizi haziwezi kubadilishwa au kuvunjwa bila kupata hisia ya hatia na dhambi.

17. Hukumu zinazohusu mirathi zimewekwa kwa usahihi wa juu mno na Qur’an Tukufu na zinaelezewa kiukamilifu kwa uwazi katika Hadithi za Mtukufu Mtume na Maimamu kumi na mbili na hakuna shaka hata kidogo kwamba hukumu hizi ni kwa mujibu wa kanuni pana ya undugu wa mtu ambao Uislamu unataka kuanzisha.

18. Sheria ya ki-Islamu ya madhehebu ya Shia Ithna-asheri ni kitu kilichofumwa vizuri. Hatuwezi kubadilisha au kurekebisha moja au mambo yake mawili bila kuharibu ufumaji mzima. Kwa mfano, katika Sheria ya Ki-Islamu mtu hawezi kutumia kitu chochote kilichopatikana kiharamu (katika maana ya kidini) amma kwa kidunia au kwa madhumuni ya kidini. Kama kwa mfano mabadiliko yanafanywa katika sheria ya mirathi, mtu fulani kwa maana hiyo kikawaida atapata zaidi kuliko haki ya mgao aliogawiwa na Qur’an Tukufu na pato hili la haramu litafanya maisha yake yote kuwa duni. Maisha yake ya kila siku yatakuwa ni orodha ndefu ya kuchupa mipaka; Sala zake, Hija yake, hata chakula chake na mavazi vitakuwa haramu, katika maana ya dini. Hivyo hawezi kutegemea amani katika maisha ya kesho akhera.

Page 31: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

26

3MUHTASARI JUU YA WARAKA WA TANZANIA

JUU YA SHERIA YA NDOA INAYOFANANA (SAWA) KWA WOTE*

ANGALIA: Muhtasari huu kwa kutoepukika imeunganisha baadhi ya ibara kutoka kwenye Muhtasari uliowasilishwa kwenye Tume ya Serikali ya Kenya.

*****

Kwa niaba ya Jumuiya ya Shia Ithna-asheri ya Tanzania, tunachukuwa fursa hii ya kuwaslisha maoni yafuatayo kwa mapendekezo ya Serikali juu ya sheria inayofanana kwa wote ya Ndoa (Waraka wa Serikali Na. 1 wa mwaka 1969).

Madhumuni yaliyodaiwa na mapendekezo haya ni kuondoa hali iliyopo ambayo kwayo “Sheria zilizopo hazitambui Ndoa zote zilizofungwa chini ya Sheria tofauti kama zinazolingana sawa”.

Lakini je, ni lazima kwa madhumuni haya kutunga sheria ya ndoa inayofanana kwa wote? Je, suala hili haliwezi kufikiwa kirahisi kwa kuleta pamoja Ndoa zote chini ya mamlaka ya kisheria ya mahakama moja chini ya rejesta moja?

Katika mwaka wa 1964 “Taarifa mpya ya Sheria za ki-Islamu” ilipitishwa inayosema kwamba hukumu za sheria za ki-Islamu za Ndoa ziwekwe katika mpango ulio wazi. Sheria ndogo chini ya amri hiyo ilichapishwa kama nyongeza ya Gazeti Na. 34 la 27 Juni 1967. Hii ndio ilikuwa iwe ni awamu ya kwanza.* Imechapishwa katika Standard (Dar es Salaam) Jumatatu, 1969 kwa niaba ya Khoja

Shia Ithna-asheri Territorial Council of Tanzania.

Page 32: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

27

Tunashangaa kwa nini sera hii haikuweza kuendelezwa, au angalau kupanuliwa kujumlisha tofauti za sheria za ndoa za kimila hali kadhalika na za ki-Baniani na za Kikiristo. Sheria hizi zingeweza kupangiwa kanuni na kuwekwa chini ya mamlaka ya kisheria ya Mahakama moja.

Hapo, na hapo tu, sura yenye mambo mengi ingeweza kuongezwa kushughulikia migongano ya sheria; (ni) baadhi ya mifano ambayo kwamba imetolewa katika Waraka wa Serikali.

Tunatambua kwamba matatizo mbalimbali ya jamii yanayojitokeza ya matumizi mabaya au tafsiri potofu za sheria za kimila au za kidini kwa ujumla hutoa sabau kwa Serikali kuhusika kwa makini. Serikali katika juhudi za kuwapatia watu wake ustawi katika suala hilo, inakabiliwa na jukumu la kutokomeza maovu ya kijamii.

Juhudi yoyote katika muelekeo huu yafaa kuungwa mkono na kustahiki ushirikiano wote. Lakini tunahisi kwamba wazo la kutunga Sheria ya wote kuchukuwa mahali pa taarifa mpya ya sheria ya Ki-Islamu sio sahihi.

Hata desturi za kimila (zisizo na mamlaka ya ki-Mungu) ni ngumu kubadilisha. Hii huwa hatari mno zaidi katika suala la sheria ya ki-Islamu ambayo ni sehemu muhimu ya dini yetu. Sheria hizi haziwezi kuvunjwa bila kupata hisia ya hatia na dhambi.

Kwa hiyo tunahisi kwamba njia nzuri ingelikuwa “kuacha mamia ya maua kuchanua.” Umoja wa kitaifa hauhitaji kwamba raia wote lazima wawe na lahaja inayofanana au imani ya dini inayofanana. Hivyo kwa nini inafikiriwa kwamba ni muhimu kuwa na Sheria ya Ndoa na Talaka inayofanana ya kutumika kwa watu wote wa Tanzania?

Sheria zetu za Shia Ithna-asheri hazikutegemezwa juu ya “Ra’i” (maoni) au “Qiyas” (analojia). Zimetegemezwa kabisa juu ya Qur’an Tukufu na Hadithi za Mtukufu Mtume na Maimamu wetu Kumi na Mbili.

Page 33: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

28

Kwa vile waraka unahusika na mambo ya Ndoa, lazima tuonyeshe kwamba kanuni zetu za msingi za Ndoa na Talaka zimetegemezwa juu ya Qur’an Tukufu. Mambo ambayo hayako wazi katika Qur’an yanaelezwa katika Hadithi.

Wanachuoni wetu ambao wanaitwa MUJTAHID hawatoi hukumu yoyote kwa maoni yao, analojia (Qiyas) au (kwa) ijimai. Hakuna mamlaka kama hayo yaliyotolewa kwa yoyote katika sheria ya madhehebu yetu. Wanaweza kutofautiana katika kutafsiri Hadithi fulani zinazohusu baadhi ya mambo madogo, lakini hata hivyo tofauti hiyo ni tofauti katika tafsiri, sio ya maoni.

Shia Ithna-asheri hufuata katika mambo yote ya dini hukumu za Mujtahid mkubwa wa zama. Anachukuliwa kuwa yeye ni muwakilishi wa Imamu wetu wa kumi na mbili na ni mtu (mwanachuoni) wa mwisho juu ya mambo yote ya kidini.

Kwake yeye mumewekwa ndani yake masuala fulani, uwezo wa ulezi wa watoto, ndoa na talaka, utekelezaji wa wosia na mali ya marehemu na mambo kama hayo.

Sheria ya ki-Islamu ya madhehebu ya Shia Ithna-asheri ni chombo kilichofumwa vizuri. Hatuwezi kubadilisha au kurekebisha moja au mbili ya mambo yake bila kuharibu ufumaji wote.

Kwa mfano, hukumu za ndoa na talaka zinabeba uzito wa moja kwa moja juu ya uhalali wa mtoto; juu ya dhambi ya pamoja ya mwanaume na mwanamke katika haki ya wao kwa wao wenyewe ya mirathi na ile ya mtoto. Mbali na mambo mengine ya jamii na matatizo halai.

Katika sheria ya ki-Islamu mtu hawezi kutumia kitu chochote kilichopatikana kiharamu (kwa maana ya kidini) amma kwa kidunia au kwa madhumuni ya kidini. Kwa hiyo, kama mabadiliko yanafanywa katika sheria za mirathi, kwa mfano, mtu fulani anapewa zaidi kuliko haki ya mgao wake kwa mujibu wa Qur’an Tukufu, maisha yake yote yatakuwa duni. Maisha yake ya kila siku yatakuwa ni orodha ndefu ya

Page 34: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

29

kuchupa mipaka, Sala zake, Hija, chakula na mavazi vitakuwa haramu katika maana ya dini.

Hivyo ni wazi kwamba mfumo wa Sheria ya ndoa, talaka na mirathi hauwezi kubadilishwa. Vinginevyo hii itaanzisha muingilio wa moja kwa moja katika dini yetu.

Kuhusu haki ya mwanamke katika sheria ya ki-Islamu tunataka kuwakilisha kwamba:

Katika sheria ya madhehebu yetu mwanamke anazo haki hizo, upendeleo na ulinzi kwa muda wa Karne Kumi na Nne zilizopita, nyingi ya hizo hazikufikiriwa katika jamii zisizo za ki-Islamu mpaka kwenye Karne iliyopita na baadhi ya hizo mbele ya inayoitwa zama ya kisasa.

Uislamu kwa mujibu wa madhehebu ya Shia umempa mwanamke haki ya kufanya mkataba yeye mwenyewe katika ndoa kama ni mtu mzima na makanifu.

Uislamu umempa mwanamke kitambulisho cha kujitengemea. Mwanamke wa ki-Islamu anamiliki mali yake mwenyewe hata baada ya kuolewa, na mume hawezi kuiingilia.

Mwanamke anaweza kumfungulia mume wake mashitaka, anaweza kutoa ushahidi dhidi yake. Anarithi kutoka kwa mume kwa haki na mwanaume kutoka kwa mwanamke. Haki hii ya wote pamoja ya mirathi (kurithiana) ilitolewa wakati hakuna jamii kamwe ilifikiria kuhusu haki hii.

Mgao wa mwanamke kwa kawaida ni nusu ya ule (mgao) wa mwanaume.Lakini hii ni mantiki kabisa. Uislamu umemfanya mwanaume kuwa na jukumu la kutunza familia. Hakuna mzigo kama huo uliowekwa juu ya mwanamke. Hata mke tajiri anahusika kupata matunzo yake kutoka kwa mume wake ingawa anaweza kuwa ni masikini. Kwa vile matunzo ya familia ni jukumu la mwanaume, amepewa mgao marudufu karibu katika mirathi yote.

Page 35: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

30

Mwanamke hupata Mahr (sio bei ya kuziba pengo ambalo ni geni kwenye fikira za Ki-Islam) ambayo hutoka kwa mwanaume kwenda kwa mwanamke. Uwiyano wa mgao uliowekwa katika Qur’an Tukufu kwa hiyo ni wa haki zaidi.

Sheria ya Uislamu ihusikanayo na Wosia hairuhusu mtu kuusia zaidi ya thuluthi moja ya mali yake kamili. Hivyo hali ya kifedha ya wale watakaokuwa warithi (pamoja) na mke siku zote inalindwa na kutwaliwa isivyo haki na yeyote. Usalama huo bado unakosekana katika jamii nyingi ambazo huruhusu mtu kutoa mali yake yote hata kwa mgeni.

Sasa tukija kwenye waraka wa Serikali wenyewe, kuna pendekezo moja ambalo katika mfumo wake uliopo, hukata ndani kabisa kwenye mzizi wa dini zote. Ni ule ushauri wa kwamba, “kama mwanaume anakaa na mke kinyumba kwa muda wa zaidi ya miaka miwili basi atachukuliwa kwamba amemoa mwanamke huyo, na kama wamepata watoto, (basi) watoto hao watachukuliwa kuwa watoto halali wa mume na mke huyo.”

Kama nia ni kutoa usalama kwa mke halisi ambaye Ndoa yake haikusajiliwa au ambaye Cheti chake cha Ndoa kilipotea, neno kinyumba halileti maana.

Itapaswa libadilishwe kwa (maneno), “Kuishi pamoja kama mume na mke katika mazingira ya kifamilia, mradi inawezekana kwa wao kuoana na mmoja wao akadai ndoa ambayo haikukataliwa na mwingine; au katika hali ya kifo cha mmojawapo, kwa kawaida inajulikana kwamba walikuwa wameoana na haithibitishwi kwamba hakukuwa na ndoa kabisa.”

Vile vile, tulitaja mapema, katika Uislamu mke hana wajibu wa kumtunza mume. Hivyo, makusudio ya Waraka kumfanya mke apasike kumtunza mume wake inakwenda kinyume kabisa na maamrisho ya Qur’an Tukufu.

Kwa vile mjadala unaendelea juu ya suala la mitala, ni muhimu kuthibitisha tena kwamba tumeridhishwa vya kutosha na hali yenye kutaka kwa hakika umuhimu wa mitala katika hali nyingi. Jamii ya

Page 36: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

31

ki-Afrika, kama Waraka kwa usahihi unavyothibitisha, ni jamii ya ki-Mitala. Uislamu unakubaliana nao. Lakini Uislamu umeweka mpaka kwa wake wanne kwa wakati mmoja na umeamrisha, kwa taratibu makhsusi, usawa katika huduma na haki ya wake wote kama waraka unavyotaka iwe.

Inapasa ikumbukwe kwamba mitala sio kitu cha lazima wala hakitetewi. Ni ruhusa tu yenye mipaka fulani na mashariti. Na katika baadhi ya mazingira ruhusa hii imeonyesha kuwa yenye manufaa mno.

Kwa mfano: kama mke ana ugonjwa sugu, au mgumba au kwa sababu nyingine fulani haiwezekani kwa wawili hawo kuishi kama mume na mke. Suluhisho litolewalo na jamii fulani ni kumtaliki mke na kuoa mwingine. Lakini, je ni haki? Je, ni wema au uadilifu kumfukuza mwanamke katika hali ya uzee, katika umri wake wa kati kutoka kwenye nyumba yake, kwa sababu amekuwa mgonjwa siku zote au ametokea kuwa mgumba?.

Uislamu hupinga ukatili huo kwa kuruhusu mitala.

Hii ni mbali kabisa na utafiti wa kitakwimu kwamba wanawake wanawazidi wanaume katika Tanzania, wanawake 100 kwa wanaume 95; au katika ile misiba fulani kama vita, wanaume hukumbana na kifo zaidi kuliko wanawake. Kama mitala hairuhusiwi na jamii, italazimisha asilimia tano ya wanawake nchini kujiingiza katika ukahaba.

Tunafikiri kiasi hiki kitatosha kuonyesha hekima ya Waraka wa Serikali katika kutambua mitala kama halali na desturi yenye “manufaa”. Lakini, katika mfumo wake wa sasa, Waraka hautakidhi madhumuni yanayohitajiwa. Je, itatokea nini kama pamoja na hali kuruhusu ndoa ya pili, mke wa kwanza akakataa kwa “hiari na kwa uhuru kukubali kuigeuza ndoa ya mke mmoja” kuwa ya mitala? Je; haitamlazimisha mwanaume kuwa “kwenye hali ambapo ama amtaliki mke wake wa kwanza au akae kinyumba (isvyo halali) na mke mwingine”, pamoja na athari zake zote zisizofaa zisizoepukika?.

Page 37: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

32

Njia nzuri ni kumtaka mwanaume aende kwenye baraza (au mahakama) iliyopendekezwa ya ndoa au kamati ya jumuiya yake na kuwathibitishia haja zake. Kama wakikubali, kukataa kwa mke wa kwanza hakupasi kufikiriwa kabisa.

Tunachukulia kwamba, kwa vile hakuna suala la kubadilisha asili ya ndoa katika ndoa ya Mwislamu, Mwislamu hatahitaji idhini ya mke wa kwanza (au wake) kabla ya kuoa mke mwingine.

TALAKA: Hakuna haja ya kusisitiza kwamba katika hali fulani talaka ndio suluhisho pekee lililobaki kwa wanandoa. Manufaa ya mfumo wa talaka yanaweza kuonekana kutokana na ukweli kwamba hata mabaniani na wakristo wamelazimika kwa nguvu ya moja kwa moja isiyoepukika kutunga sheria za talaka. Waraka umetambua hoja hii. Vile vile lazima ikumbukwe kwamba Uislamu, wakati ambapo unakubali hoja hii katika hali fulani, umetamka kwamba ni “Sheria halali yenye kuchukiza mno”, (makuruhu), itumikayo tu katika hali zilizo ngumu mno.

Qur’an Tukufu imeweka chombo cha usuluhisho na jumuiya nyingi za ki-Islamu zina kamati kama hizo. Kwa bahati mbaya baadhi ya pande fulani hawakupendelea kabisa mfumo huu muhimu. Matumizi haya mabaya ya uhalali wa talaka lazima yaachwe na jaribio la waraka kudhibiti hali hii linakaribishwa sana.

Masharti ya Talaka: Lazima tuonyeshe katika mwanzo kwamba madhehebu ya Shia Ithna-asheri ya Sheria ya ki-Islamu imeweka kanuni ngumu zilizotegemezwa juu ya Qur’an Tukufu na Hadithi kuhusiana na talaka. Talaka inaruhusiwa mradi tu inatamkwa mbele ya watu wawili mashahidi “Adil” (watu waliothibitishwa uaminifu wao) ambao husikia maneno na kuelewa chanzo cha talaka. Talaka lazima itamkwe katika utaratibu uliothibitishwa.

Zaidi, ni lazima vile vile kwamba mume awe mtu mzima, mwenye akili timamu na mwenye kuelewa vizuri, atendaye kwa utashi wa uhuru wake mwenyewe na sio katika mshituko wa hasira au kutishwa, na kwamba lazima awe na nia ya dhahiri ya kuvunja ndoa.

Page 38: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

33

Kwa kadiri mwanamke anavyohusika, yeye wakati wa talaka lazima awe katika hali ya tohara na kwamba talaka haiwezi kutamkwa hata wakati wa tohara ambao kwamba mume amekutana naye kimwili.

Kama moja ya mashariti yaliyotajwa hapo juu yakivunjwa, talaka itakuwa batili na kutenguka.

Sheria ya ki-Islam haimpi mwanamke haki ya kutoa talaka, maoni yoyote kwamba mwanamke apasa kupewa haki ya kumtaliki mumewe yatakuwa ni kuingilia maadili ya dini, ambayo waraka umekariri kusema, sio nia ya Serikali.

Familia ni msingi wa jamii, na kama ilivyo kila jamii, huhitaji mamlaka ya mwisho kuhifadhi nidhamu na ustawi wa jamaa (wa familia). Uislamu umetoa nafasi hiyo kwa mume ambaye amepewa haki ya kutoa talaka.

Lakini mwanamke wa ki-Islamu anapasika kutoa maombi ya kuvunja ndoa au kuibadilisha yeye mwenyewe katika mazingira yafuatayo:-• Anaweza kuomba (Khula) ambayo yaweza kukubaliwa juu yake na

mume.

• Anaweza kumuomba Mujtahid (ambaye ni Kadhi katika Sheriat za Shia Ithna–asheri) kumpa talaka kama mume ametoweka, au anakataa kumtunza.

• Anaweza kuifuta ndoa kama mume ni mwenda wazimu au akawa mwenda wazimu baada ya ndoa.

• Na anaweza kuibatilisha ndoa (baada ya kupeleka suala lake kwa Mujtahid) kama mume ni hanithi.

Itakuwa muhimu, wakati wa kuandika hati ya rasimu, kutambua talaka iliyotolewa na Mujtahid na ubatilisho wa ndoa kwa kadiri ambavyo ndoa za Shia Ithna-asheri zinavyohusika.

Hukumu zilizotajwa hapo juu zinauhusiano juu ya masharti ya waraka

Page 39: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

34

kuhusiana na mume aliyetoweka. Kutoa talaka kwa Mujtahid (au hakimu katika suala la wasio kuwa Shia Ithna–asheri au wasiokuwa Waislamu) ni sahihisho bora zaidi kuliko kudhania kwamba mume kafa (kwa madhumuni ya ndoa yake) na kudhani anaishi (kwa madhumuni mengine, pamoja na ndoa nyingine kama ipo yoyote) wakati mmoja na huo huo!

Kwa vile Waraka kwa usahihi hutambua talaka iliyotolewa na mume mwislamu kama mwisho (wa ndoa), na kuitaka mahakama kusajili talaka hiyo bila uchunguzi wowote zaidi, tunataka kusisitiza kwamba talaka kama hiyo iwe inafanya kazi kuanzia tarehe ya kutamkwa kwa utaratibu wa talaka na mume, na sio tarehe ya kusajiliwa.

Waraka humtaka Mwislamu akusudiaye kutoa taarifa ya kusudio lake siku 21 kabla kwa “Sheikh aliyeruhusiwa na Waziri kufungisha Ndoa.”

(Waraka) umepuuza ukweli kwamba Mvulana wa ki-Islamu na msichana wanaweza kufunga Ndoa wao wenyewe bila kuwa na haja ya “kumwita Sheikh na kumuomba afungishe ndoa”. Tuna hakika sio nia ya Serikali kutengeneza Sheria mpya ya Uislamu ambayo ingelianzisha wachungaji kama wa Kikristo. Basi nini hii maana ya kutajwa Sheikh aliyeruhusiwa na Waziri? Ni wazi kwamba wazo hili linakwenda kinyume kabisa na Uislamu.

Vile vile tunashindwa kuona haja yoyote kwa ajili ya pendekezo hili la taarifa ya siku 21. Tuchukulie msichana kutoka Kigoma na mvulana kutoka Pangani (wote wanaishi Dar es Salaam). Wakamjulisha Sheikh wa Jumuiya yao mjini Dar es Salaam kwamba wanataka kuoana. Sheikh yule hatarajiwi kuchapisha au kutangaza kusudio la ndoa katika magazeti au radio. Basi, vipi ataweza kujua kama kuna kikwazo chochote cha halali dhidi ya ndoa ile?

Na hata hivyo, hakutakuwa hata ndoa moja kama hiyo ya kusudio la kiharamu katika ndoa elfu moja. Tunafikiri, ni bora kuiondoa sheria hii na kuibadilisha na nyingine kwa maana kwamba kama itakuja kufahamika hata baada ya kuona kwamba wasingeweza kuona kihalali, ndoa itakuwa batili na kutenguka kuanzia mwanzo.

Page 40: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

35

Kwa kadiri usajili wa Ndoa na Talaka unavyohusika, katika Jumuiya yetu rejesta za ndoa zimekuwepo kwa zaidi ya miaka 125 na tunatoa vyeti kwa wanandoa.

Lakini lazima tusisistize kwa nguvu sana kwamba uhalali wa ndoa au talaka hauwezi kufanywa kwa kupasishwa na usajili. Yaweza ikafanywa kuwa ni kosa kwa zile ambazo hazikusajiliwa; lakini isije ikaathiri uhalali wa ndoa au talaka.

Hivyo hivyo, katika hali nyingine pia, kama ndoa ni sahihi kwa mujibu wa dini, isije ikachukuliwa kuwa ni batili kama inapingana na masharti yoyote yaliyowekwa na waraka. Vinginevyo, itakuwa ni uingiliaji wa moja kwa moja katika dini.

Madhumuni ya muhtasari huu ni kuidhihirishia Serikali kwamba utungaji wa sheria lazima ufanye juhudi ya kuhifadhi sheria za dini za Jumuiya mbalimbali zinazoishi chini ya bendera moja, hususani wakati sheria hizo zikiwa ni zenye athari nyingi juu ya misingi hiyo kama ndoa na maisha ya kifamilia.

Kama tulivyoonyesha mapema, katika Uislamu Sheria na dini havitenganishwi, kwa vile sheria zetu zimeanzia kutoka kwenye Qur’an Tukufu ni wazi kwamba kama sheria yoyote inatungwa ambayo umma hupingana na maamrisho ya Qu’ran au Hadithi; kwa kawaida itasababisha vurugu kubwa katika akili za Umma wa ki-Islamu na kwa hiyo Jumuiya yote ya Uislamu itakuwa katika usumbufu.

Mwishoni, tunapenda kufanya muhtasari wa maoni yetu kwa ifuatavyo:

Tunahitaji kwamba badala ya kutunga Sheria inayofanana kwa wote, “Amri ya Taarifa mpya ya Sheria za ki-Islamu” lazima ziwe katika matumizi kwa ajili ya Waislamu na uandikwe muswada wa Sheria ndogo chini ya Amri hiyo, uchapishwe na ifanywe itumike kwa mapema iwezekanvyo.

Kwa kadiri mapendekezo ya Waraka yanavyohusika tunakubali kabisa

Page 41: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

36

kwamba “Ndoa lazima iwe muungano wa hiari” (ibara ya 6 ya waraka maelezo ya Kiingerza) kwamba wanandoa wasije wakawa ndani ya hadhi iliyokatazwa ya undugu au unasaba (ibara ya 9); kwamba “yeyote kati ya mume au mke anweza kumiliki mali yake mwenyewe.” (ibara ya 19); kwamba mke awe na uwezo wa kutoa ushahidi dhidi ya mumewe (ibara ya 21); kwamba kuwe na masharti ya talaka “kama ndoa imevunjika kabisa” na kwamba “Talaka zisishughulikiwe juu juu (ibara ya 24); na kwamba kuwe na mabaraza ya usuluhisho” na “utambulisho kamili upewe mabaraza kama hayo ambayo yapo katika Jumuiya mbali mbali kabla ya sheria hii mpya unayokusudiwa” (ibara 25).

Tunakubaliana na mapendekezo yafuatayo pamoja na masharti na sifa fulani:-

Umri wa chini wa miaka 15 na 18 kwa wasichana na wavulana mtawalia (ibara ya 7) na usajili wa ndoa (ibara ya 17), na wa talaka (ibara ya 27) ni mambo mazuri tunakubaliana nayo ilimradi, kuvunja au kukiukwa kwao hakufanyi ndoa au talaka batili na kutenguka.

Matamshi ya Mwislamu ya Utaratibu (formula) ya talaka yanatambuliwa na Waraka kama ushahidi wa kuvunjika kabisa kwa ndoa na mahakama inapaswa “kutoa cheti cha kuvunja ndoa”. Tunakubali pendekezo hili, ilimradi cheti kinachosemwa kinaanzia nyuma kuanzia tarehe ya kutamkwa kwa utaratibu wa talaka na mume.

Tuko katika maafikiano kamili na pendekezo kuruhusu Ndoa ya mke mmoja kubadilishwa kuwa ya mitala. Lakini hatufikirii kuwa ni busara kusisistiza juu ya idhini ya mke wa kwanza (ibara ya 12). Mume anapaswa kuwa na haki ya kwenda kwenye baraza la Ndoa lililopendekezwa na uamuzi wao utakuwa wa mwisho.

Vile vile, tunaona kwamba Ndoa ya Mwislamu ikiwa yenye uwezekano wa mitala, mume wa ki-Islamu hatatawaliwa na sharti hili.

Tunafikiri kwamba pendekezo la kudhania mume (aliyetoweka kwa muda wa miaka 5) kama aliyekufa sio la busara. Njia nzuri ni kumruhusu Hakimu (au Mujtahid) kutoa talaka kama mazingira yatahitajia hivyo.

Page 42: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

37

Haki ya mwanamke kudai talaka au kuvunja au kutengua ndoa lazima ikomee kwenye mazingira yaliyotajwa mapema katika muhtasaari huu. Utungaji wowote wa sheria uendao kupita mpaka huo, utakuwa ni uingiliaji wa moja kwa moja katika dini yetu.

Tunakataa kwa nguvu pendekezo kwamba kukaa kinyumba na mwanamke kwa muda wowote (mpaka wa miaka 2 ni wa kiholela kabisa) huwafanya hao wawili mume na mke kihalali. Vinginevyo mpaka utamkaji unabadilishwa kama, ilivyopendekezwa katika ibara ya 11 ya muhtasari huu, pendekezo hili haliwezi kukubaliwa.

Tunakataa kabisa pendekezo la kumfanya mke kuwajibika kumtunza mume wake (ibara ya 19).

Tunafikiri kwamba pendekezo la kutaka taarifa ya siku 21 halina maana kabisa, na kuunganisha katika hali ya Waislamu pamoja na usemi “taarifa itapelekwa kwa Sheikh, ambaye ameruhusiwa na Waziri kufungisha ndoa” huhitaji kuangaliwa kwa tahadhari sana, kwani huonyesha kuanzishwa kwa sheria mpya ya uchungaji ambao ni kinyume kabisa na misingi ya Ki–Islamu. Kwa hiyo hatuwezi kukubaliana nalo.

Page 43: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

38

4MUHTASARI JUU YA HIJABU NA MIRATHI*

Mheshimiwa Rais,

1. Kwa niaba ya Jumuiya na mashirika mbali mbali ya ki-Islamu, tunachukua fursa ya kufanya wasilisho hili kwa ajili yako wewe Mheshimiwa kulifikiria kwa huruma.

2. Katika wasilisho hili tunakomea wenyewe kwenye masuala mawili ambayo yalikuwa yakikera akili zetu kwa muda mrefu. Nayo ni: Hijabu kwa ajili ya wasichana wa ki-Islamu katika taasisi za elimu na Sheria za ki-Islamu zinazohusu Wosia na Mirathi.

3. Mheshimiwa: Sisi wote ni raia wa nchi huru, na tumejipa katiba ambayo, pamoja na mambo mengine kuhakikisha uhuru wa kuabudu, dini, muungano na kuzungumuza. Hususan tanarejea kwenye Ibara 18 (1), 19 (1) (2) na 20 (1) ya Katiba ambazo ni kama ifuatavyo:-

18 (1) Bila chuki kueleza sheria za nchi, kila mtu anao Uhuru wa kutoa maoni na kuzungumza, na kutaka, kupokea, kugawa au kusambaza habari na maoni kupitia chombo chochote cha habari bila kujali mipaka ya kitaifa, na vile vile ana haki kutokana na kuingiliwa mawasiliano yake.

19 (1) Kila mtu ana haki ya Uhuru wa mawazo au dhamira, itikadi au imani, na hiari katika mambo ya dini, pamoja na uhuru wa kubadili dini au imani yake.

* Uliwasilishwa kwa Mheshimiwa Al-Haj Sheikh Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Muungano wa Jamhuri ya Tanzania, kwa niaba ya wawakilishi wa Mashirika (Taasisi) mbali mbali ya Ki-Islamu ya Dar es Salaam mwaka 1990

Page 44: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

39

19 (2) Bila chuki kwenye sheria zinazohusika za Jamhuri ya Muungano, taluma ya dini, ibada na utangazaji wa dini utakuwa huru na jambo la binafsi la mtu binafsi, na mambo na uendeshaji wa vyombo vya Dini hautakuwa sehemu ya shughuli za mamlaka ya Dola.

20 (1) Kila mtu ana haki ya kupewa uhuru, kutegemea Sheria za nchi, kukusanyika kwa uhuru na kwa amani, kuunganika na kushirikiana na watu wengine, kutoa maoni hadharani, na muhimu zaidi kuunda au kujiuunga na mashirika au vyama (vikundi) vilivyoundwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza itikadi zake au masilahi yoyote mengine.

4. Allah (swt) amesema katika Qur’an Tukufu neno lake la mwisho:“Na sikuwaumba majini na watu isipokuwa kwamba wanitumikie mimi”. (Sura 51, aya 56) Waislamu wote kuanzia mwanzo kabisa wanakubali kwamba neno “li ya budun” ambalo linatokana na (neno) “Ibadah” na linatafsiriwa hapa kama “tumikia”, maana yake unyenyekevu kamili.

Mheshimiwa: Hakuna awezaye kufahamu zaidi kuliko busara zako nzuri kwamba “Ibadah” katika Uislamu sio kawaida ya baadhi ya ibada zenye kutekelezwa katika nyakati au siku makhususi. Huzunguka maisha yote ya Mwislamu. Uislamu maana yake kujisalimisha kwenye majaaliwa ya Allah (swt) na wakati tunapoahidi kufanya hivyo tunaitwa Waislamu (ili) kutuongoza katika maisha yetu ya kidunia, na kutusaidia kufika karibu Yake katika maisha ya kesho akhera Allah (swt) ametuma kwetu kupitia kwa Mtume Wake wa mwisho (s.a.w.) mfumo wa sheria wenye mambo mengi unaojumuisha mambo yote ya maisha … ya nyumbani, ya kijamii ya kifedha, ya kimaadili na ya kiroho.

5. Mheshimiwa unajua vizuri sana kwamba Qur’an Tukufu haikushughulikia suala lolote la sheria kwa ufafanuzi zaidi (na uanagalifu) na katika namna ya utaratibu kwama sheria ya ndoa, wosia, mirathi na mambo mengine yanayohusika nayo, pamoja na adabu ya mavazi kwa wanawake.

Page 45: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

40

6. HIJAB: Ni lazima iwekwe wazi kuanzia mwanzo kwamba hukumu zinazoelekeza Wanawake kuvaa katika namna ambayo hufunika mwili wote na kuhifadhi muruwa wao zimetajwa kwa wazi katika Qur’an Tukufu. Ni urithi wa kawaida kwa Waislamu wote na haukukomea kwenye madhehebu au Jumuiya fulani. Vile vile, sio mila ya kitamaduni, ni sheria ya lazima ya Mungu, na haiwezi kuachwa bila kupata hisia ya dhambi na hatia.

7. Kuna aya si chini ya tisa katika sura mbali mbali za Qur’an Tukufu zinazofafanua hukumu ya Hijab. Kwa ruhusa yako Mheshimiwa tunanukuu mbili ya hizo hapa chini:-

“Nasema (Ewe Mtume) kuwaambia waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasidhihirishe viungo vyao isipokuwa vinavyodhihirika; na waangushe shungi zao mpaka vifuani mwao, na wasionyeshe mapambo yao ila kwa waume zao, au baba zao, au baba za waume zao, au watoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au wanawake wenzi wao, au wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume, au watumishi wanaume wasio na matamanio ya kijinsia au watoto wadogo ambao hawajapata elimu ya siri za wanawake; wala wasipige miguu yao ili yajulikane wanayoyaficha katika mapambo yao; na tubieni nyote kwa Allah; enyi waumini, ili mpate kufudhu (kesho akhera).” (Sura 24 Aya 31).

“Ewe Mtume. Waambie wake zako, na binti zako na wanawake wa waumini wateremshe chini “Jilbab” zao, ili kwamba wapate kuhishimiwa ….” (Sura 33, Aya 59).

(Jilbab = Joho Kubwa kuliko shela na fupi kuliko kashida, ambayo hufunika kichwa na kifua cha mwanamke).

8. Kwa kutegemea juu ya aya hizi na aya nyingine za Qur’an Tukufu na Hadithi sahihi za Mtukufu Mtume (s.a.w) Wanachuoni wa ki-Islamu, bila utengano wowote wa hitilafu, wameamuru kwamba:-

a. Wanawake wa ki-Islamu lazima wafunike mwili mzima wakati

Page 46: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

41

9. Mheshimiwa! Wizara ya Elimu katika nchi yetu imechagua sare kwa ajili ya wasichana wa shule za msingi, ambayo ni mfano wa vazi la kimagharibi. Tunashangaa kwa nini uamuzi kama huo ulichukuliwa. Blauzi na sketi sio vazi la ki-Afrika, wala si la kikristo au la ki-Islamu. Kwa nini mtindo huo ni mtakatifu mno kiasi kwamba hauwezi kubadilishwa? Ingelikuwa vizuri zaidi kuwa na hamu yetu yakitaifa badala yake kuamuru (kuvaa) gauni refu na bui bui. Kwa vile ni vazi linalovaliwa na mamilioni ya wanawake wa ki-Afrika. Je, si wakati muafaka kwamba wenyewe tunaondokana na tabia kwamba yote yale yanayokuja kutoka nchi za Ulaya (Magharibi) ni mazuri kwetu, ambapo maadili yetu wenyewe ni ya “kishenzi”?

10. Kwa mtazamo wa ukweli hapo juu, kwa unyenyekevu Mheshimiwa tunaomba uielekeze Wizara ya Elimu kuagiza (uvaaji) wa sare kama hizo kwa wasichana wa shule zenye kufunika vichwa vyao na mwili mzima, kuacha wazi nyuso na viganja. Inaweza kurahisishwa kwa kuvaa: skafu, gauni, suruali na soksi.

Tunaamini kwamba itakuwa ni sare yenye heshima zaidi, na itaruhusu hata wasichana kushiriki katika riadha na michezo kwa uhuru bila hofu ya kuonekana aibu yoyote.

wanapotoka majumba yao. Uso tu (lakini sio kichwa na nywele) na viganja vya mikono vinaweza kuwa wazi.

b. Kuna hukumu maalum na za shuruti za mavazi kwa ajili ya Sala na Hajj.

c. Nguo isiwe yenye kubana kuonyesha mikunjo kunjo ya mwili, wala nyepesi, (na kuonekana) kuyashinda madhumuni ya vazi (kama ilivyokusudia).

d. Wanawake hawapaswi kuvaa vazi ambalo kwa ujumla hutumiwa na wanaume, wala wanaume kuvaa za wanawake.

Page 47: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

42

11. Mheshimiwa:Kama kwa sababu yoyote ni vigumu kuanzisha sare hizi kwa wasichana wote, basi wasichana wa ki-Islamu waruhusiwe nchi nzima kuvaa sare hizo bila pingamizi au kizuizi chochote, kwa vile ni sheria ya dini yao na sio kikabila au mila ya kitamaduni.

12. Kabla hatujaendea masuala mengine, tungependa kwa huruma zako Mheshimiwa kutoa taarifa kwako kwamba wasichana wa ki-Islamu wanaoishi Uingereza na Ufaransa wamepata haki yao ya kuvaa Hijab mashuleni, ingawa ilichukuwa hatua za kimahakama (na katika suala la Ufaransa, uingiliaji kati ya Tume ya haki za binadamu ya Uingereza) kuipata haki hiyo. Karibu na nyumbani nchini Kenya, mwaka huu (1990) msichana Mwislamu wa ki-Afrika alishinda kesi mahakamani dhidi ya mamlaka za shule waka-ti zilipokataa kumruhusu kuingia shule na Hijab. Gazeti rasmi la KANU (liitwalo) the Kenya times (Nairobi) liliandika tahariri tarehe 2/2/1990 ambayo kwayo pamoja na mambo mengine liliandika:

“Kwa nchi ya Kidemokrasia kama hii yetu, ambako uhuru wa kuabudu kwa dini zote umehifadhiwa katika Katiba, ni vigumu kuamini kwamba baadhi ya watu wanaona ni sawa kuwanyima wengine uhuru huu”.

“Dini, kama tujuavyo, ni jambo lililo karibu sana na mioyo ya baadhi ya watu kuwanyima uhuru wa kuelezea hisia zao wakati wowote wanapotaka kufanya hivyo ni kuwa dhidi ya juhudi zote katika kujenga jamii yenye amani na upendo”.

“Chukuwa Uislamu kwa mfano, ni mfumo kamili wa maisha. Kumtaka mfuasi yeyote muaminifu wa dini hii kuacha baadhi ya mambo ya maisha haya, hakika ni kumuambia akatae yale yalioandikwa katika Qur’an Tukufu. Na sisi ni nani, katika wadhifa wowote ule uwao tunaoundesha, kuingilia maisha ya ndani ya watu wengine na dini zao? Suala la msichana huyu wa ki–Islamu kuambiwa afunue kichwa chake wakati akiwa katika eneo la Shule halipaswi kutokea. Hali kadhalika kuwanyima watoto haki yao ya elimu kwa sababu wanavaa vilemba si ya kuvumiliwa.”

Page 48: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

43

13. SHERIA YA KIISLAMU YA MIRATHI:Tumepata kuelewa kwamba Serikali inakusudia kufanya mabadiliko katika sheria ya ki-Islamu ya mirathi. Tulikerwa mno na habari hizi: Kama tulivyo wasilisha mapema, Qur’an Tukufu imeweka kwa usahihi na uwazi mno zaidi hukumu zinazohusiana na mirathi, kwa ufafanuzi kabisa ikitoa kwa warithi mbali mbali migao yao katika mali ya Mwislamu marehemu. Sheria ya ki-Islamu ni chombo kilichofumwa vizuri. Hatuwezi kubadilisha au kurekebisha moja au mbili ya mambo yake bila kuharibu ufumaji wote. Kwa mfano, katika sheria ya ki-Islamu mtu hawezi kutumia kitu kilichopatikana kiharamu (katika maana ya dini), amma kwa kidunia au kwa madhumuni ya kidini. Kwa hiyo kama madiliko yanafanywa katika Sheria ya mirathi, kwa maana hiyo mtu fulani kwa kawaida atapata zaidi kuliko mgao wake (ule ambao amegaiwa na Qur’an Tukufu). Pato hilo la haramu litafanya maisha yake yote kuwa duni. Maisha yake ya kila siku yatakuwa ni orodha ndefu ya madhambi na kuchupa mipaka. Sala zake zitakuwa batili; Hija yake itakuwa batili na kutenguka; hata chakula chake na mavazi vitakuwa haramu katika maana ya dini. Mtu kama huyo kamwe hawezi kutarajia amani katika maisha ya kesho akhera.

14. Hatujui ni nini maana halisi ya zoezo hili. Kwa hiyo hatuwezi kusema zaidi kwa sasa. Lakini tunarudia kusema kwamba sheria hizi zimeegemezwa juu ya Qur’an Tukufu na haiwezekani kuweka mpaka baina ya Sheria hizi na Qur’an Tukufu. Jambo lolote la kubadilisha migawanyo ya ki–Qur’an itakuwa sawa na kubadilisha Qur’an Tukufu.

15. Hata hivyo, katika mintaarafu hii, tungetaka kuvuta nadhari yako Mheshimiwa kwenye Amri ya Taarifa mpya ya Sheria ya ki-Islamu ya Serikali ya Tanzania (Na. 56 ya 1964), ambayo chini yake, kazi ilianzishwa ya kupanga kanuni za Sheria za ki-Islamu, ikitoa utambulisho halisi kwa madhehebu. Sura nne zinazo husika na Ndoa, Ulinzi wa watoto n.k. zilichapishwa pia kama sheria ndogo chini ya sheria hiyo katika nyongeza ya Gazeti Na 34 la 27 Juni 1967. Ilikuwa ni hatua ambayo ilifurahisha Umma wote wa Ki-Islamu

Page 49: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

44

wa nchi hii. Kwa bahati mbaya mpango ule uliachwa. Bado, kama mpango ule utahuishwa, ambao kwayo hukumu za kila Madhehebu zinatambuliwa kama Sheria zitumikazo kwenye Jumuiya hiyo, na sheria hizo zikapangiwa kanuni katika juzuu moja kwa rejea za urahisi kwa Mahakama za Sheria, itakuwa hatua ya kusifia sana ambayo kwamba Umma wote wa Waislamu wa Tanzania watakuwa siku zote na shukurani kwako wewe Mheshimiwa.

Page 50: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

45

Page 51: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

46

MAHAKAMA YA KADHI:BAADHI YA MAPENDEKEZO*

Waislamu nchini kwa muda mrefu wamekuwa wakidai kuwepo na Mahakama ya Kadhi katika Tanzania itakayoangalia na kushughulikia mambo maalum ambayo yanajumuishwa zaidi na Sharia za Kiislamu kuliko Sheria za Mahakama za kawaida.

Ukweli kwamba tayari ipo Mahakama ya Biashara (Uchumi), ni uthibitisho tosha kwamba mambo maalum (ya aina moja) yanahitaji kushughulikiwa na Mahakama maalum ambayo vitabu vya Sheria vya kawaida huyafafanua kwa nadra (uchache).

Hata hivyo, tayari inakubalika kimsingi kwamba hakuna utata katika suala hili, kwani Rais Benjamin Mkapa ameshasema atayashughulikia matatizo yote yanayowakera Waislamu na kuhakikisha kuwa Waislamu wote nchini hawajisikii kunyanyaswa kwa vile sera ya Chama tawala (Serikali) ni Usawa miongoni mwa Wananchi wake, bila kujali jinsia, rangi (Utaifa), au Dini.

Kwa mantiki hii, mapendekezo kadhaa yanatolewa kuisaidia Mahakama ya Kadhi iweze kufanya kazi zake kwa ufanisi na kupatikana madaraka kamili ya kisheria ya Mahakama ya Kadhi.

Ili Mahakama iweze kupata hadhi yake, haya ni mapendekezo ambayo yangeweza kusaidia kufikia lengo hilo.

Mswada unalenga kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi katika kila Wilaya ya Tanzania, ili kuangalia mambo yote yahusianayo na Sharia ya Kiislamu katika masuala ya Ndoa, talaka, haki ya kulea watoto, mgawanyo wa mali, Urithi n.k. pale ambapo wahusika wa utata * Imechapishwa katika The Democrat (Dar es Salaam) Aug 17-23,1999.

Page 52: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

47

huo ni Waislamu, waliooana kwa mujibu wa sharia na desturi ya ndoa za Kiislamu.

Ukweli ni kwamba makusudio ya mswada huu ni mazuri, lakini upo uwezekano mkubwa kwamba kutokana na ukosefu wa Kitabu makhususi cha Sheria za Kiislamu, Makadhi katika wilaya mbali mbali wakifikia kwenye uamuzi wa kesi zinazofanana, wanaweza wakatoa hukumu zinazopingana.

Hivyo, upo umuhimu wa kukiandaa kitabu makhsusi kitakachotumika kama Mwongozo wa Makadhi ili kuiepuka migongano.

Hapo zamani mwaka 1964, Bunge la Tanganyika kwa wakati huo lilipitisha “Sharia ya Kiislamu (Sheria ndogo)” iliyompa madaraka Waziri aliyehusika na mambo ya Sheria kuandaa na kuchapisha kipengele cha Sharia ya Kiislamu baada ya kushauriana na wanachuoni wa Sharia za Madh-hebu za Kiislamu.

Katibu Mkuu wa Bunge wakati huo, alikamilisha kuandika Mswada wa ndoa wenye sehemu 4 (kama ulivyokubaliwa na wanachuoni wa Sharia za Kiislamu kutoka Madh-hebu matatu ya Kiislamu Shafi’i, Hanafi na Shia).

Mswada huu uliotolewa kama Sharia ndogo chini ya kifungu kidogo cha Sharia ya Kiislamu (Na: 56 ya mwaka 1964) ikiwa ni sehemu ndogo ya Gazeti la Serikali na Na: 34 la tarehe 27, Juni, 1967.

Ilifahamika kuwa sehemu zilizosalia, kuhusiana na kuwalea watoto na talaka n.k. zingechapishwa mapema. Lakini zoezi hili lilisitishwa na badala yake serikali ilitunga sheria ya ‘Ndoa’ kupitia Mswada wa Ndoa wa mwaka 1971.

Hata hivyo, kanuni ya Sheria ya Ki-Islamu 1964 bado haijafutwa na bado ni sehemu ya Kitabu cha Bunge. Na kwa sababu sasa serikali inakusudia kuanzisha Mahakama za Makadhi katika kila Wilaya, ni wakati muafaka wa kufufua tena mswada wa sheria ya Kiislamu ya mwaka 1964 ili ufanyiwe kazi na kazi hii ianzie pale ilipoachiwa.

Page 53: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

48

Jambo muhimu hapa ni kuepusha uwezekano wa Makadhi kutoa hukumu zitakazoleta utata. Vinginevyo, mzigo wa kazi za Mahakama Kuu utaongezeka kwa kuwa rufani kutoka Mahakama za Makadhi zitajazana kwenye Mahakama ya Rufaa.

Madhehebu za Makadhi wa Wilaya:

Kwa vile Waislamu wengi wa Tanzania ni wafuasi wa Madhehebu ya Shafii ni vizuri makadhi wa Wilaya watokane na Madhehebu ya Shafii.

Lakini iwapo wahusika au mhusika wa mgogoro ni wa Madhehebu isiyo ya Shafii, inapendekezwa kuwa Kadhi wa Wilaya asaidiwe na wanachuoni wa madh-hab inayohusika.

Hii itafuta uwezekano wa kutolewa hukumu isiyo sawa na itawapa imani ya kutendewa haki wahusika au mhusika. Wasaidizi wa Kadhi wa Wilaya waliotajwa hapo juu itabidi watayarishwe katika kila Wilaya na wanaweza kuangaliwa upya (kuteuliwa) muda baada ya muda.

Iwapo mapendekezo mawili muhimu yaliyotajwa hapo juu katika makala haya yatakubalika na kufanyiwa kazi, itakwenda hatua kubwa kuwatendea haki na usawa Waislamu wote nchini.

Page 54: UTETEZI WA SHERIA - Shia Maktab

Kimetolewa na Kuchapishwa na:Bilal Muslim Mission of Tanzania

S.L.P 20033Dar es Salaam

ISBN: 9987 620 26 4