8
HALAFU CAMP Siku 3 mfululizo BAAB KUBWA!! Toleo la Novemba, 2015 Jarida kuhusu Kila kona ya Pangani Filamu mpya ya AISHA... ...ndio ‘habari ya mujini!’ Y A L I Y O M O Nani Kasema Haiwezekani? “Badiliko la Uongozi wangu linatoka wapi?” Inaendelea Uk. 2 Wanakamati wa shule ya Mikinguni wakijadiliana kwa pamoja, ili kujua haswa nini kinachokwamisha jamii kushiriki hata kama jambo lenyewe linaonekana wazi kuwa lina manufaa kwenye maisha yao ya kila siku na ya baadae. M aendeleo ya kweli katika sekta ya elimu ni zaidi ya madaſtari, vitabu, waalimu, kamati na wanafunzi. Zaidi ya hayo ni lazima kuwa na mazingira mazuri ya kitaaluma yanayojali maendeleo ya mwanafunzi kiafya, kimwili na kisaikolojia pamoja na mwalimu kuifanya shule kuwa eneo rafiki na muhimu katika makuzi na malezi. Kupitia Halafu Camp na mafunzo ya kamati za shule, UZIKWASA imefanikiwa kuwezesha kamati 20 toka Julai 2014 hadi Agosti 2015. Lengo la mafunzo hayo ni kuwezesha Bw. Shaban Ally, Mtendaji wa Kijiji Mbulizaga (mwenye fulana nyeusi pichani) ni miongoni mwa viongozi waliofaidika na mafunzo ya Uongozi wa Mguso. Kabla ya kuhamia Mbulizaga alikuwa kiongozi kijijini Mikinguni. Wakati wa kutembelea utekelezaji wa Halafu Camp alikuwa na haya ya kusema: “...haitakuwa haki kama sitasema na kuishukuru UZIKWASA kwa kazi yenu. Kama wengi mnavyoweza kuona, mimi ni kiongozi yule yule ambaye nilidhaniwa sifai Mikinguni. Lakini leo mmeshuhudia wenyewe jinsi watu walivyokubali utendaji wenu na kutekeleza mpango kazi. Asanteni sana kwa kazi mnazozifanya...“ Uk. 3 Uk. 4 Uk. 5 Uk. 6 Uk. 7 Uzinduzi wa PANGARITHI Badiliko ni Mimi na Huanza na Mimi! Je, Uwezo Wangu wa Kuongoza Wengine Unatoka Wapi? Kujifunza na ‘Kujifunzua’ - Nguzo Kuu ya Mafanikio UZIKWASA Mpango Mkaka wa UZIKWASA 2014 - 2018

Siku 3 mfululizo BAAB KUBWA!! Nani Kasema Haiwezekani ... · (mwenye fulana nyeusi pichani) ni miongoni mwa viongozi waliofaidika na mafunzo ya Uongozi wa Mguso. Kabla ya kuhamia

  • Upload
    others

  • View
    2

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Siku 3 mfululizo BAAB KUBWA!! Nani Kasema Haiwezekani ... · (mwenye fulana nyeusi pichani) ni miongoni mwa viongozi waliofaidika na mafunzo ya Uongozi wa Mguso. Kabla ya kuhamia

HALAFU CAMPSiku 3 mfululizoBAAB KUBWA!!

Toleo la Novemba, 2015

Jarida kuhusu

Kila kona ya PanganiFilamu mpya ya AISHA...

...ndio ‘habari ya mujini!’

YALI

YOMO

Nani Kasema Haiwezekani?

“Badiliko la Uongozi wangu linatoka wapi?”

Inaendelea Uk. 2

Wanakamati wa shule ya Mikinguni wakijadiliana kwa pamoja, ili kujua haswa nini kinachokwamisha jamii kushiriki hata kama

jambo lenyewe linaonekana wazi kuwa lina manufaa kwenye maisha yao ya kila siku na ya baadae.

Maendeleo ya kweli katika sekta ya elimu ni zaidi

ya madaftari, vitabu, waalimu, kamati na wanafunzi. Zaidi ya hayo ni lazima kuwa na mazingira mazuri ya kitaaluma yanayojali maendeleo ya mwanafunzi kiafya, kimwili na kisaikolojia pamoja na mwalimu kuifanya shule kuwa

eneo rafiki na muhimu katika makuzi na malezi. Kupitia Halafu Camp na mafunzo ya kamati za shule, UZIKWASA imefanikiwa kuwezesha kamati 20 toka Julai 2014 hadi Agosti 2015. Lengo la mafunzo hayo ni kuwezesha

Bw. Shaban Ally, Mtendaji wa Kijiji Mbulizaga (mwenye fulana nyeusi pichani) ni miongoni mwa viongozi waliofaidika na mafunzo ya Uongozi wa Mguso. Kabla ya kuhamia Mbulizaga alikuwa kiongozi kijijini Mikinguni. Wakati wa kutembelea utekelezaji wa Halafu Camp alikuwa na haya ya kusema: “...haitakuwa haki kama sitasema na kuishukuru UZIKWASA kwa kazi yenu. Kama wengi mnavyoweza kuona, mimi ni kiongozi yule yule ambaye nilidhaniwa sifai Mikinguni. Lakini leo mmeshuhudia wenyewe jinsi watu walivyokubali utendaji wenu na kutekeleza mpango kazi. Asanteni sana kwa kazi mnazozifanya...“

Uk.

3Uk.

4Uk.

5Uk.

6Uk.

7Uzinduzi waPANGARITHI

Badiliko ni Mimi na Huanza na Mimi!

Je, Uwezo Wangu wa Kuongoza Wengine Unatoka Wapi?

Kujifunza na ‘Kujifunzua’

- Nguzo Kuu ya Mafanikio UZIKWASA

Mpango Mkakati wa UZIKWASA 2014 - 2018

Page 2: Siku 3 mfululizo BAAB KUBWA!! Nani Kasema Haiwezekani ... · (mwenye fulana nyeusi pichani) ni miongoni mwa viongozi waliofaidika na mafunzo ya Uongozi wa Mguso. Kabla ya kuhamia

2

Nani Kasema

Haiwezekani?

Nafasi ya Pangani FM kama Sauti ya Jamii

Inatoka Uk. 1

Ili kukuhabarisha kwa habari zenye uhakika hatuwi nyuma. Watangazaji wakiperuzi kwenye mtandao kujua nini kimejiri ulimwenguni ikiwa ni maandalizi ya kipindi.

Bango la mmoja wa wasikilizajiwa Pangani Fm kuonyesha mwamko walionao kuhusu kujishughulisha.

Watangazaji wa Pangani FM wakiwa studio

wanaendesha kipindi.

kamati kufahamu majukumu yao, kubaini fursa na changamoto zinazowakabili wanafunzi na kuzitumia ili kufikia malengo yaliyokusudiwa:

1.Ukuaji wa taaluma, 2.Ustawi wa mwanafunzi hususani mtoto wa kike.

Kwa wanakamati waliopatiwa mafunzo na kutambua hili wameweza kuongeza ufaulu, kupunguza utoro, udhalilishaji wa kijinsia. Pia mwamko wa jamii kitaaluma umeongezeka. Mafanikio mengine yalikuwa kujenga vyoo bora, upatikanaji wa maeneo na vifaa vya michezo na chakula. Inafurahisha kwamba kauli nzuri na rafiki toka kwa waalimu, kutungwa kwa sheria ndogo ndogo zenye kumlinda mtoto wa kike na wa kiume zimekuwa nguzo imara katika shule zetu. Haya yote ni hatua muhimu dhidi ya udhalilishaji na ukandamizaji, ili kumpatia haki mwanafunzi kwa kuimarisha na kuboresha anga la kitaaluma.

Kumekuwa na ushirikiano mzuri kati ya kamati na Dawati la Jinsia la Polisi. Wameshirikiana kuinua na kukuza uelewa wa jamii kuhusu masuala ya kisheria, haki na wajibu. Kwa kipindi cha Julai 2014 hadi Agosti 2015 jeshi la Polisi Pangani limeweza kurusha vipindi 48 kwenye radio yetu. Hii imerahisisha kuripotiwa kwa visa mkasa hasa kuhusu ukatili na unyanyasaji wa kijinsia, mimba za utotoni na ndoa za kulazimishwa. Mfano ni kisa hai kilichoripotiwa wakati wa mkutano wa wadau wa Novemba 2014 kuhusu mwanafunzi wa Pangani aliyefaulu darasa la saba na kujikuta yuko njia panda baada ya baba yake kukataa kumlipia ada ya shule ya sekondari. Badala yake akakusudia kumwozesha. Mkewe alipopata habari hizo aliamua kuripoti Polisi. Hatimaye baba mzazi akaamuriwa kuhakikisha analipa ada, na mwanawe anaendelea na masomo. Kwa hakika Pangani FM Redio imekuwa zana muhimu katika kupashana habari, jamii kupaza sauti zao, kuzungumzia na kujadili masuala na changamoto mbali mbali za kimaendeleo. Pia ni zana muhimu katika kupeleka mrejesho kwenye jamii kuhusu mada za kimaendeleo kupitia simu na ujumbe mfupi wa maneno. Njia nyingine ya mrejesho ni kuwepo kwa vikundi vya wasikilizaji wa redio. Imesaidia kujua usikivu, changamoto na namna bora ya kuendesha vipindi.

Page 3: Siku 3 mfululizo BAAB KUBWA!! Nani Kasema Haiwezekani ... · (mwenye fulana nyeusi pichani) ni miongoni mwa viongozi waliofaidika na mafunzo ya Uongozi wa Mguso. Kabla ya kuhamia

3

Uzinduzi wa Kituo cha Urithi wa Kihistoria na Utamaduni Pangani (PANGARITHI) ulifana!

Wanapangani wakisubiri shughuli za uzinduzi kuendelea.

Ngoma za asili pia zilikuwepo.

Anko Mo na Pili Mlindwa wa Pangani FM wakiwachangamsha Wanapangani na wageni

waliohudhuria.Mkurugenzi wa UZIKWASA Dr. Vera Pieroth

akielezea usuli wa kuwepo Pangarithi.

Vijana wa Pangani wakisukumana ili kuingia na kuona maonesho ndani ya kituo.

Mtaalamu wa Akiolojia Dr. E. Mjema akielezea kuhusu mabaki ya zamani yaliyopatikana kutokana

na utafiti uliofanyika kwenye jengo ili kufahamu historia yake kikamilifu.

Page 4: Siku 3 mfululizo BAAB KUBWA!! Nani Kasema Haiwezekani ... · (mwenye fulana nyeusi pichani) ni miongoni mwa viongozi waliofaidika na mafunzo ya Uongozi wa Mguso. Kabla ya kuhamia

4

Badiliko ni Mimi na Huanza na Mimi!

Igizo na Jarida la HALAFU bado ‘vinabamba’ mitaani!

Mwenyekiti wa Halmashauri ya kijiji cha Stahabu akionesha choo kipya walichojenga kwa nguvu ya wanajamii ngazi ya kitongoji kwa jitihada za mwenyekiti wa kitongoji.

Mwenyekiti wa kijiji cha Stahabu akimwonesha Mratibu wa Shughuli

za ndani na nje za UZIKWASA Nickson Lutenda choo kilichokuwa kikitumika na wanafunzi kabla ya

Halafu Camp kijijini hapo.

Baada ya kukosa nakala yao ya jarida la HALAFU mitaani, iliwalazimu vijana kufika hadi UZIKWASA. Hapa mmoja wao anajieleza kwa niaba ya wote furaha yao baada ya kupata nakala.

Kumekuwepo na ongezeko la wanawake kumiliki

rasilimali. Kwa mfano idadi ya akina mama waliopeleka maombi wapatiwe ardhi vijijini imeongezeka kwa kiasi kikubwa: Wanawake 184 waliomba na kupewa ardhi kwa mwaka 2013. Mpaka Juni 2014 idadi iliongezeka tena kufikia 393. Na kisha Disemba 2014 wanawake 542 walikuwa wamepatiwa ardhi. Hii ni tofauti kubwa kabisa na ilivyokuwa awali mwaka 2008 ambapo wanaume ndio walipewa vipaumbele vya umilikaji wa ardhi. Pia walikuwa na mamlaka juu ya rasimali na matunda ya kazi za mikono ya wanawake. Tunapongeza viongozi kwa kujali na kukidhi maombi ya wanawake wilayani kwetu.

Wanawake wazidi kudai haki zao

wilayani Pangani Mafanikio makubwa ya Halafu Camp sio kutoa mafunzo tu bali pia kujenga ushirikiano mzuri kati ya wadau mbali mbali wilayani kwetu. Kwa mfano, kamati za shule kwa muda mrefu zilikuwa zimesahaulika na kuonekana kutokuwa na umuhimu. Hata badhi ya ajenda zao zilipuuzwa zilipofikishwa kwenye Halmashauri za vijiji. Mchanganyiko wa viongozi wengi kutoka shule, halmashauri ya kijiji, Polisi pamoja na wakilishi wa Halmashauri ya wilaya kwenye mafunzo ya Halafu Camp umesaidia sana kupeana mawazo, kushauriana na kuchukua hatua kwa pamoja. Kwa njia hii ajenda za kamati ya shule zimeanza kubebwa katika moyo wa kila mmoja kwa ajili ya utekelezaji bila lawama.

Page 5: Siku 3 mfululizo BAAB KUBWA!! Nani Kasema Haiwezekani ... · (mwenye fulana nyeusi pichani) ni miongoni mwa viongozi waliofaidika na mafunzo ya Uongozi wa Mguso. Kabla ya kuhamia

5

pangani fm: michezo huimarisha ushirikiano!

JE, UWEZO

WANGU WA KUONGOZA

WENGINE UMETOKA

WAPI?

Viongozi wa shirika l a U Z I K W A S A BwanaNovatus Urassa na Joseph Peniel wakiwapa

mawaidha, hamasa na mbinu za kuishinda timu pinzani siku ya mchezo huo ambapo Pangani FM ilichomoza na ushindi wa bao moja kwa nunge.

Mwenyekiti mstaafu wa kijiji cha Mtonga aliyeshika tama (kushoto kwenye picha) anaonekana akifuatilia kwa makini igizo kwenye Halafu Camp kijijini Mwera. Anajivunia kuwa sehemu ya mafunzo ya kamati ya shule pamoja na Uongozi wa Mguso yanayoendeshwa na UZIKWASA. Kwa mfano, kijijini kwake Mtonga ameweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kwenye maendeleo. Ameweza kupata ufadhili wa matenki manne ya kukingia maji ya mvua ya lita 5000 kila moja na kuondoa kero ya maji kwa wanafunzi. Kwa kuwa yeye mwenye amefaidika sana kutokana na mafunzo ya Halafu Camp na Uongozi wa Mguso ndio maana aliamua kuenda takriban kilometa 20 huko Mwera kuona kinachoendelea.

Timu ya soka ya Pangani FM The Dream ikiwa katika maandalizi ya mchezo wa kirafiki dhidi ya

timu ya Mapo FC katika uwanja wa Kirumba mjini Pangani. Lengo lilikuwa ni kudumisha ushirikiano mzuri baina ya wadau wa Pangani FM na watan-gazaji, pamoja na kusherehekea siku ya kufunguli-wa kwa Redio. Sherehe hizi hufanyika tarehe 8 ya

Agosti kila mwaka.

Page 6: Siku 3 mfululizo BAAB KUBWA!! Nani Kasema Haiwezekani ... · (mwenye fulana nyeusi pichani) ni miongoni mwa viongozi waliofaidika na mafunzo ya Uongozi wa Mguso. Kabla ya kuhamia

6

Kujifunza na ‘kujifunzua’ - Nguzo kuu ya mafanikio ya UZIKWASA

Baadhi ya wafanyakazi wa UZIKWASA walifanya ziara Mkoani Mwanza kwa lengo la kujifunza kupitia mashirika mbalimbali yanayofanya kazi za kijamii. Miongoni mwao ni shirika la Usimamizi wa Mazingira na Maendeleo (EMEDO), Tandabuhi na Redio Afya FM. Kama shirika linalojifunza ni muhimu kwa UZIKWASA kufahamu mengi

kutoka kwa mashirika mengine. Iko haja ya kujua nini kimechangia kwenye mafanikio yao na zipi ni sababu za kukwama. Mkurugenzi wa EMEDO Bi. Editrudith Lukanga aliishukuru UZIKWASA kwa kufanya safari ndefu na kuchagua EMEDO kati ya mashirika mengi kwa ajili ya kujifunza na kupeana usoefu na mawazo. Kwetu sisi UZIKWASA mara nyingine ni muhimu kuwa tayari kuweka pembeni tunachoamini tunajua. Hii inatusaidia tuwe wazi kupokea mawazo mapya. Hiyo ndio maana ya kujifunzua. Na jambo la kutembelea mashirika mbalimbali huko Mwanza limetusaidia kuelewa zaidi kazi zetu nyumbani Pangani. Vilevile mashirika haya yamefurahishwa kupata fursa kujifunza kuhusu shughuli nyingi zilizofanywa na UZIKWASA. Wakati wa kuagana mkurugenzi wa EMEDO alisema kwamba na wao wana hamu ya kutembelea Pangani ili kujifunza zaidi kupitia uzoefu wa UZIKWASA. Tunatarajia kwamba kutokana na kutembeleana huku sisi sote tutaweza kuelewa zaidi uwezo wetu, kutambua udhaifu wetu na kuufanyia kazi.

Page 7: Siku 3 mfululizo BAAB KUBWA!! Nani Kasema Haiwezekani ... · (mwenye fulana nyeusi pichani) ni miongoni mwa viongozi waliofaidika na mafunzo ya Uongozi wa Mguso. Kabla ya kuhamia

7

Mpango Mkakati wa UZIKWASA 2014 - 2018

Je, Mafunzo ya Uongozi na Jinsia yamesaidiaje kupambana na

Ukatili wa Kijinsia? Ushirikiano mzuri wa viongozi kwa umoja wao na jamii baada ya kuingiza masuala ya jinsia kwenye mipango kazi yao yote kwa vijiji 33 ni chachu ya mabadiliko. Katika kutafuta mshindi bora wa VMAC miongoni mwa vigezo ilikuwa idadi ya kesi za unyanyasaji na ukatili wa kijinsia zilizoripotiwa kwa kamati na kuchukuliwa hatua.

Kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2014, jumla ya kesi 77 ziliripotiwa na kati ya hizo, 52 zilishughulikiwa katika ngazi ya kijiji na 25 kupelekwa ngazi ya wilaya kwa maamuzi . Hii inafanya jumla ya kesi 143 kushughulikiwa katika ngazi ya kijiji na 34 kupelekwa ngazi ya wilaya kwa mwaka 2014 kuanzia Januari mwaka huo.

Huu ni mwamko mkubwa kwa jamii kutofumbia macho masuala ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia. Mfano mzuri ni kijiji cha Mkwaja ambapo viongozi wameunda kikosi kazi cha siri kuchunguza masuala ya ukatili wa kijinsia kisha kujulisha mamlaka husika.

Mwishoni mwa kijarida hiki tunapenda kufahamisha wadau wetu kuhusu msingi wa Mpango Mkakati wetu wa sasa 2014-2018 ili kujenga uhusiano mzuri zaidi katika kazi zetu wilayani Pangani. Dira yetu ni kuona wilaya ya Pangani panakuwa mahali ambapo wanawake, wanaume, na watoto wao wanaishi na kufanya kazi pamoja kwa kuheshimiana, kufurahia haki zao za kibinadamu na kuongoza maendeleo yao wenyewe. Dhamira yetu ni kwamba UZIKWASA inawajengea uwezo jamii ili wasimamie maendeleo yao kupitia mbinu za ushirikishwaji kwenye miradi, kukuza haki za kijinsia, kuimarisha vitendo vya uongozi wenye mabadiliko na uhusiano wa kimkakati ili kupata jamii yenye mabadiliko na inayojitambua. Hatimaye heshima ya pamoja, haki za kijinsia na kibinadamu ziwe zinaongoza. Tunaamini kwamba:

1. Mabadilliko yanawezekana kwa kujenga utamaduni wa kujadiliana, kusikilizana na kuwajibishana kati ya jamii na viongozi.

2. Mabadiliko yanaanza na kila mtu mwenyewe na kujitambua kwenye maendeleo yake binafsi.

3. Uongozi mzuri na unaowajibika umejengwa juu ya msingi wa kujituma na kujitambua.

4. Miradi ya maendeleo inapaswa kufuata maadili na kwa hiyo inaweza kujenga uaminifu na uwajibikaji wenye uendelevu kwa viongozi na wanajamii.

Yote haya yanaongoza shughuli za UZIKWASA na mbinu zake za utekelezaji.

Page 8: Siku 3 mfululizo BAAB KUBWA!! Nani Kasema Haiwezekani ... · (mwenye fulana nyeusi pichani) ni miongoni mwa viongozi waliofaidika na mafunzo ya Uongozi wa Mguso. Kabla ya kuhamia

Kijarida hiki kinatoa mifano mingi ya mchakato wa mabadiliko ambayo ingeweza kuangaliwa miongoni mwa jamii za Pangani katika

kipindi cha miaka 6. Katika kipindi hiki UZIKWASA kwa msaada wa wadau wote imefanya juhudi kubwa katika kuchangia kuimarisha uwezo wa jamii kuchukua jukumu la maendeleo yao. Kazi yetu pia ilishirikisha kufanya kazi na uongozi wa ngazi ya chini kabisa kuwa bora zaidi na kuwa viongozi wanaojitambua wanaoweza kushughulikia mahitaji ya kijinsia na kujenga usawa wa kijinsia katika jamii zao. Pamoja na hayo, kampeni ya mawasiliano ya Banja Basi imekuwa ikishughulikia tabia za kijamii na kitamaduni ziletazo changamoto miongoni mwa jamii za Pangani na zikadumisha mjadala mzuri miongoni mwa watu wa Pangani katika miaka 6 iliyopita. Mafanikio haya yalithibitishwa na tathmini ya nje iliyofanywa na mwana Anthropolojia kutoka London School of Hygiene and Tropical Medicine inayosema kuwa harakati za UZIKWASA zimezaa matunda na zimeleta ushahidi madhubuti wa mabadiliko na mageuzi wilayani Pangani. Mafanikio yetu yametujengea imani na kutambulika miongoni mwa wana Pangani, na ni imani yao ndiyo iliyoleta kutambulika hata zaidi: Julai 14 2014 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. J. Kikwete ametutunukia cheti cha kuthamini mchango uliotolewa na UZIKWASA katika maendeleo ya wilaya ya Pangani. Jambo la kuvutia zaidi katika mwaka 2015 ni uzinduzi wa kituo cha urithi wa Pangani, Pangarithi hapo tarehe 21 Machi 2015. Tangu siku hiyo hadi

tarehe 30 Septemba 2015 zaidi ya watu 1600 walifika kutembelea na ninayo furaha kusema kuwa wengi wa watu hao waliotembelea kituo ni watu wa Pangani wenyewe. Tunafurahi sana kuwaona vijana wetu kupenda sana kujifunza historia ya Pangani na tunaona fahari kwa

©UZIKWASA - SLP 1, Mtaa wa Jamhuri , Pangani, Tanzania. Simu +255-27-2630303 au 2630203 Baruapepe: [email protected] Tovuti: www.uzikwasa.or.tz Facebook: https://www.facebook.com/aisha2015swahilimovie Trela ya AISHA: https://www.youtube.com/watch?v=JdWO-xxRm-k

kukua umaarufu wa Pangarithi, hususan miongoni wa wana Pangani. Onesho la kwanza la filamu Aisha ambayo ni filamu ya tatu ya UZIKWASA yenye maudhui halisi lililofanyika tarehe 31 Julai 2015 limezidi matarajio ya kila mtu. Watu wapatao 6000 walihudhuria onesho hilo wakiwa na hamu ya kuiona filamu iliyokuwa ikizungumzwa sana. Tukio hilo lilihitimishwa kwa tamasha ya kuvutia ya kuwasha mishumaa, iliyoongozwa na msanii mkuu Godliver Gordian aliyeigiza kama Aisha. Madhumuni ya kitendo hiki

cha ishara ni kumulika vitendo vingi vya kikatili na uonevu dhidi ya wanawake na wasichana visivyoripotiwa katika wilaya yetu na kwingineko duniani, na kumtaka kila mtu achukue hatua. Wakati ambapo filamu ya AISHA itatembelea vijiji vyote vya wilaya ya Pangani, imekwishavutia watazamaji wengi zaidi huko Dar es Salaam. Filamu hii ilijaza sinema ya

Mlimani City mpaka kiti cha mwisho hapo tarehe 2 Oktoba 2015. Hii ni hali ya nadra sana hata kwa filamu za kigeni katika cinema za Dar es salaam. Tunaelewa kuwa mafanikio yetu si sababu ya kubweteka, bali ni dhima ya kuhakikisha kuwa mafanikio yaliyofikiwa yanaenziwa na kufikishwa kwenye ngazi mpya. Na hii haiji bila ya changamoto. Wakati dunia inakabiliwa tatatizo la wakimbizi katika nchi nyingi, kukusanya pesa kwa ajili ya mipango ya maendeleo katika bara letu kumekuwa kugumu zaidi. UZIKWASA haikuachwa na changamoto hizi. Hata hivyo, kwa kuwa tunaridhika kuwa kazi yetu inaendelea kuwa ya faida kwa jamii mbalimbali, hatutakata tamaa, wala kupoteza nguvu yetu wakati tunaendelea mbele kishujaa. Tunawashukuru wote wale waliotusaidia katika kazi zetu, waliotoa utaalamu wao na kuungana nasi katika safari yetu ya kutufanya bora zaidi katika tuyafanyayo. Hawa ni pamoja na watu ambao hawakupuuza kutembelea Pangani na kukutana nasi, kutupa walichojifunza na kubadilishana nasi mawazo. Pia inahusu mashirika wenza na watu binafsi walioimarisha timu yetu katika jukumu lao la kuwezesha na kusaidia mchakato wa mabadiliko katika jamii. Tunazishukuru sana jamii za Pangani na viongozi wao, mamlaka za wilaya na washirika wa Pangani kwa imani yao, kutupa moyo na ushirikiano wao.

Dr. Vera PierothMkurugenzi Mtendaji, UZIKWASA.

Kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Gr

aphi

cs &

Des

ign

by M

arco

Tib

asim

a