49
HADITHI Y A MAISHA Y ANGU Hebu tuinamishe vichwa vyetu kidogo kwa maombi. Baba yetu wa Mbinguni Mwenye neema, kweli kabisa ni kwa majaliwa kwamba tunakukaribia Wewe, Mungu na Mwokozi wetu. Tunaposikia wimbo huu wa ajabu, Jinsi Wewe Ulivyo Mkuu, unatusisimua kwa sababu tunajua kwamba Wewe u mkuu. Na tunaomba kwamba ukuu Wako utadhihirishwa kwetu upya, adhuhuri hii, wakati tunapozungumza. Na kura imeniangukia, kwa mara ya kwanza katika miaka mingi, kujaribu kurudi nyuma kwenye mambo yaliyopita ya maisha, nami naomba kwamba Wewe utanipa nguvu na—na ninalohitaji, Bwana, kuwa katika saa hii. Na makosa yangu yote katika maisha yawe tu jiwe la kuvukia kwa wengine, jambo ambalo lingewaleta karibu zaidi na Wewe. Tujalie hilo, Bwana. Jalia wenye dhambi waone zile nyayo kwenye mchanga wa wakati, na wajalie waongozwe Kwako. Mambo haya tunaomba katika Jina la Bwana Yesu. Amina. (Mnaweza kuketi.) [Ndugu Glover anasema, “Ungeweza kuombea leso hizi kabla ya kuanza?”—Mh.] Nitafurahia. [“Kuna zile na hizi za kuombea.”] Sawa, bwana, asante. Kama vile huyu mtu mwema sana, Ndugu Glover, ambaye nimemjua sasa kwa miaka kadha, nimepata majaliwa ya kuwa pamoja naye kwa kitambo kidogo jana jioni. Naye ameniambia alikuwa hawezi kwa kitambo kidogo, akipumzika. Na sasa hivi, kwenye umri wa miaka sabini na mitano, anarudi kwenye utumishi wa Bwana. Mimi sijafikia nusu ya uchovu kama nilivyokuwa kabla ya kusikia jambo hilo. Nilifikiria nilikuwa nimechoka, lakini si—siamini nimechoka. Hivi punde alikuwa ameniwekea hapa leso kadhaa, katika namna ya bahasha, na kadhalika, ambazo ziko ndani na tayari zimefungwa. Sasa, ye yote wenu mnaosikiliza redio, au mliopo hapa, ambao mnataka kupata mojawapo ya hizi leso, na mngetaka, Angelus Temple huzituma daima, wakati wote. Ungeweza kuwaandikia hapa Angelus Temple na wao wataiombea, kwa sababu nitakuhakikishia kwamba ni Maandiko. Ni ahadi ya Mungu. Na iwapo ungetaka mimi niiombee moja kwa ajili yako, mbona, nitafurahia kufanya jambo hilo. Ingekupasa tu kuniandikia kwa sanduku la posta 3-2-5, 325, Jeffersonville, huendelezwa J-e-f-f-e-r-s-o-n-v-i, l mbili, e. Jeffersonville, Indiana. Au iwapo huwezi kukumbuka sanduku la posta, andika tu “Jeffersonville.” Ni mji mdogo, yapata kama wakazi thelathini na tano elfu. Kila mtu ananijua kule. Na kwa hiyo tungefurahia kuombea leso na kukutumia.

SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

  • Upload
    others

  • View
    42

  • Download
    10

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

HADITHIYA MAISHAYANGU

Hebu tuinamishe vichwa vyetu kidogo kwamaombi.

Baba yetu wa Mbinguni Mwenye neema, kweli kabisani kwa majaliwa kwamba tunakukaribia Wewe, Mungu naMwokozi wetu. Tunaposikia wimbo huu wa ajabu, Jinsi WeweUlivyo Mkuu, unatusisimua kwa sababu tunajua kwamba Weweu mkuu. Na tunaomba kwamba ukuu Wako utadhihirishwakwetu upya, adhuhuri hii, wakati tunapozungumza. Na kuraimeniangukia, kwa mara ya kwanza katika miaka mingi,kujaribu kurudi nyuma kwenye mambo yaliyopita ya maisha,nami naomba kwambaWewe utanipa nguvu na—na ninalohitaji,Bwana, kuwa katika saa hii. Na makosa yangu yote katikamaisha yawe tu jiwe la kuvukia kwa wengine, jambo ambalolingewaleta karibu zaidi na Wewe. Tujalie hilo, Bwana. Jaliawenye dhambi waone zile nyayo kwenye mchanga wa wakati, nawajalie waongozwe Kwako. Mambo haya tunaomba katika Jinala Bwana Yesu. Amina. (Mnaweza kuketi.)

[Ndugu Glover anasema, “Ungeweza kuombea leso hizikabla ya kuanza?”—Mh.] Nitafurahia. [“Kuna zile na hizi zakuombea.”] Sawa, bwana, asante. Kama vile huyu mtu mwemasana, Ndugu Glover, ambaye nimemjua sasa kwa miaka kadha,nimepata majaliwa ya kuwa pamoja naye kwa kitambo kidogojana jioni. Naye ameniambia alikuwa hawezi kwa kitambokidogo, akipumzika. Na sasa hivi, kwenye umri wa miakasabini na mitano, anarudi kwenye utumishi wa Bwana. Mimisijafikia nusu ya uchovu kama nilivyokuwa kabla ya kusikiajambo hilo. Nilifikiria nilikuwa nimechoka, lakini si—siamininimechoka. Hivi punde alikuwa ameniwekea hapa leso kadhaa,katika namna ya bahasha, na kadhalika, ambazo ziko ndani natayari zimefungwa.

Sasa, ye yote wenu mnaosikiliza redio, au mliopo hapa,ambao mnataka kupata mojawapo ya hizi leso, na mngetaka,Angelus Temple huzituma daima, wakati wote. Ungewezakuwaandikia hapa Angelus Temple na wao wataiombea, kwasababu nitakuhakikishia kwamba ni Maandiko. Ni ahadi yaMungu.

Na iwapo ungetaka mimi niiombee moja kwa ajili yako,mbona, nitafurahia kufanya jambo hilo. Ingekupasa tukuniandikia kwa sanduku la posta 3-2-5, 325, Jeffersonville,huendelezwa J-e-f-f-e-r-s-o-n-v-i, l mbili, e. Jeffersonville,Indiana. Au iwapo huwezi kukumbuka sanduku la posta,andika tu “Jeffersonville.” Ni mji mdogo, yapata kama wakazithelathini na tano elfu. Kila mtu ananijua kule. Na kwa hiyotungefurahia kuombea leso na kukutumia.

Page 2: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

2 NDUGU BRANHAM

Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katikakulitenda jambo hili, kwa sababu…Utapata barua ndogoikiambatana nayo, kwamba watu ulimwenguni pote huombakila asubuhi saa tatu, na saa sita, na saa tisa. Nawe unawezakufikiria, huko upande wa pili wa ulimwenguni, inawabidikuamka saa ngapi usiku kufanya maombi haya. Kwa hiyo iwapohawa wote makumi elfu, na mara elfu, wanapeleka maombikwa Mungu wakati huo huo kwa ajili ya huduma hii, ugonjwawako, Mungu hawezi kukataa hilo. Na kwa hiyo sasa sisi, kamaninavyosema, hatuna mipango yo yote, hatutaki hata peni moja.Tuko tu…Iwapo tunaweza kukusaidia, hili ndilo lililotuletahapa. Basi hebu…

Mtu fulani analeta kifurushi kingine cha leso.

Sasa, iwapo huna leso ambayo ungetaka kutuma, vema,basi wewe andika tu, kwa vyo vyote. Kama huihitaji sasahivi iweke katika kitabu cha Matendo, katika Biblia, suraya 19. Na itakuwa namna ya utepe mdogo mweupe ambaoutatumwa kwako, na maelezo jinsi ya kuungama dhambizako kwanza. Na (asante) jinsi ya kuungama dhambi zako.Usithubutu kamwe kupata kitu cho chote toka kwa Mungubila kwanza kusawazisha mambo na Mungu. Unaona? Na kishaunaagizwa katika jambo hili kuwaita majirani zako waje, namchungaji wako. Kama una kitu cho chote moyoni mwako dhidiya mtu ye yote, nenda kakisahihishe kwanza, ndipo urudi. Kishaomba, fanya mkutano wa maombi nyumbani mwako, halafuishikize leso hii kwa pini kwenye nguo yako ya ndani, ndipoumwamini Mungu. Na kwenye vipindi hivyo vya masaa matatu,kila siku, kutakuwako na watu kote ulimwenguni wanaomba,mfungamano kuzunguka dunia.

Na sasa ni yako, bila malipo kabisa, itume tu. Na—na,sasa, hatutakuwa tukikuandikia kukutoza fedha au kukuambiamiradi ya maendeleo tuliyo nayo. Tunakutaka uunge mkonomiradi, lakini hatuna—hatuna wo wote kwako wewe kuungamkono. Unaona? Kwa hiyo wewe…Si kwa madhumuni yakupata anwani yako, ni kwa ajili ya kuratibisha tu na hudumaya Bwana ambayo tunajaribu kuendeleza.

Sasa hebu tuinamishe vichwa vyetu. Na iwapo unasikilizaredio, weka leso yako hapo, hebu weka tu mkono wakomwenyewe juu yake tunapoomba.

Bwana Mwenye Neema, tunakuletea Wewe vijifurushihivi vidogo, pengine baadhi yavyo vinaonekana kuwa labdavijifulana vidogo vya mtoto mchanga, au—au kijishati chandani, au pengine jozi ndogo ya viatu, au—au kitu fulani,leso, inayopelekwa kwa mgonjwa na anayeteseka, Bwana nikulingana na Neno Lako kwamba tunatenda hili. Kwanitunasoma, katika Kitabu cha Matendo, kwamba walichukuatoka mwilini mwa mtumishi Wako, Paulo, leso na vitambaa,

Page 3: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

HADITHI YA MAISHA YANGU 3

kwa sababu waliamini kwamba Roho Wako alikuwa juu yamtu yule. Na roho wachafu waliwatoka watu, na mateso namagonjwa yaliwaondoka wao, kwa sababu waliamini. Na sasatunatambua, Bwana, kwamba sisi sio Mtakatifu Paulo, balitunajua kwamba Wewe bado ungali Yesu. Nasi tunaombakwambaWewe utaikirimu imani ya watu hawa.

Na ilinenwa wakati mmoja kwamba wakati Israeli(wakijaribu kumtii Mungu) walinaswa mtegoni, bahari mbeleyao, milima pande zote mbili, na jeshi la Farao linakaribia.Na mtu mmoja amesema, kwamba “Mungu aliangalia chinikupitia Nguzo ile ya Moto, kwa macho yenye hasira, nayo bahariikaogopa na ikajifingirisha ikarudi nyuma, na kufanyiza njiaIsraeli wapate kuvuka kwenda nchi ya ahadi.”

Ee Bwana, angalia chini tena, wakati vifurushi hivivitakapowekwa juu ya miili ya wagonjwa kwa kumbukumbu laNeno Lako lililo hai. Ugonjwa na uone hofu, angalia kupitiaDamu ya Mwanao, Yesu, Ambaye alifia upatanisho huu. Aduina aogope na aondoke, kusudi watu hawa waweze kuingiakatika ile ahadi, kwamba “Zaidi ya mambo yote,” kwambani mapenzi Yako “kwamba tufanikiwe katika afya.” Tujaliehilo, Baba, kwani tunalipeleka kwa hiyo—kwa hiyo nia moyonimwetu. Na hilo ndilo kusudi letu. Tunalituma katika Jina la YesuKristo. Amina.

Asante, Ndugu Glover. Asante, bwana.

Sasa, usiku wa leo ukiwa ni wa kumalizia sehemu hii yaufufuo, sijui iwapo itatangazwa kwa redio au la, bali ningetakakusema (kama sivyo) kwa watu wanaosikiliza redio, kwambahuu umekuwa mmoja wa mikutano mizuri sana niliyopata kuwanayo kwa miaka kadha wa kadha. Umekuwa mkutano wenyenguvu, dhabiti, wenye upendano sana na wenye ushirikianoniliopata kuhudhuria kwamuda mrefu.

[Ndugu fulani anasema, “Tunatangazwa kwa redio hadisaa kumi na robo, ndugu. Nao wanakusikiliza, kila mahalihuko California ya kusini, nje huko visiwani, na kwenyemeli. Wanatupasha habari. Na kwa hiyo unao watu wengiwanaokusikiliza, maelfu namakumi elfu.”—Mh.] Asante, bwana.Hilo ni zuri mno. Ninafurahi kusikia hilo. Mungu awabarikinyote.

Na hakika sikuzote nimekuwa na shauku moyoni mwangukwa Angelus Temple, kwa msimamo wake wa Injili kamiliya Yesu Kristo. Na, sasa, li—linaonekana la kibinafsi zaidikwangu sasa. Inaonekana kama, baada ya kukutana na kilammoja na kuona roho zao nzuri, yaelekea kama kwamba mimini mmoja wenu zaidi kuliko nilivyokuwa. Mungu awabariki,ndilo ombi langu. Na…[Wasikilizaji wanapiga makofi—Mh.]Asanteni, sana.

Page 4: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

4 NDUGU BRANHAM

Sasa, imetangazwa kwamba leo ningezungumza nanyi kwakitambo juu ya: Hadithi ya Maisha Yangu. Hilo ni—ni jambogumu kwangu. Hii itakuwa ni mara ya kwanza mimi nimejaribukuiendea kwa miaka mingi. Na nisingekuwa na muda wakuisimulia kwa undani, lakini tu sehemu yake. Na, humu ndani,nimefanya makosa mengi, nimefanya mambo mengi yaliyokuwamakosa. Na nitatamani, kwamba ninyi mnaosikiliza kwenyeredio na ninyi mliomo humu, kwamba hamtachukulia makosayangu kuwa ni mawe ya kujikwaa, bali mawe ya kuvukia ilikuwaleteni karibu zaidi na Bwana Yesu.

Basi, usiku wa leo, kadi za maombi zitatolewa kwa ibadaya kuponya usiku wa leo. Sasa, tunapozungumzia kuhusuibada ya kuponya, haimaanishi kwamba tutamponyamtu fulani,“tutamwombea mtu fulani.” Mungu ndiye anayeponya. Yeyeamekuwamwema sana kwangu, kujibumaombi.

Nami nilikuwa nikizungumza na meneja wa mwinjilistimaarufu, hapa juzijuzi, na—na iliulizwa kwa nini mwinjilistihuyu alikuwa haombei wagonjwa. Ndipo yule mwinjilisti alitoajibu kwa yule—yule meneja wa mikutano yangu, kasema,“Kama…Huyu mwinjilisti anaamini katika kuponya Kiungu.Lakini kama yeye angeanza kuombea wagonjwa, ingetatizaibada yake kwa sababu anadhaminiwa na makanisa. Makanisamengi na wengi wao hawaamini kuponyaKiungu.”

Kwa hiyo nina staha na heshima kwa mwinjilisti yulekwa sababu yeye ameshikilia mahali pake, wajibu wake.Yeye angeweza labda…Nisingeweza kamwe kupachukuamahali pake, na ninashuku kama angeweza kuchukua mahalipangu. Sote tuna sehemu katika Ufalme wa Mungu. Sotetumeunganishwa pamoja. Vipawa tofauti, bali Roho yeye yule.Madhihirisho mbalimbali, nilimaanisha kusema, bali Roho yeyeyule.

Na, sasa, usiku wa leo ibada zitaanza…Nafikiri walisemauimbaji unaanza mnamo saa kumi na mbili u nusu. Na, sasa,iwapo unasikiliza redio, njoo uusikilize. Ni…Utakuwa mzuri,ndivyo ilivyo sikuzote.

Na kisha nataka kusema kwamba kadi zamaombi zitatolewamara baada ya ibada hii, mara tu ibada hii inapokwisha, iwapoupo hapa nawe unataka kadi ya maombi. Niliarifiwa ndanihapo muda mfupi tu uliopita, mwanangu au Bw. Mercer au Bw.Goad, watakuwa wakitoa kadi za maombi. Msiondoke kwenyeviti vyenu. Mara tu ibada inapokwisha, hebu bakini kwenye vitivyenu ili wale vijana waweze kupita katika mstari na kutoakadi za maombi haraka iwezekanavyo. Hilo litakuwa kwenyeroshani au chumbani, po pote pale, vyumba vya chini au po poteulipo, basi endeleeni kuketi na hao wavulana watajua kwambamnahitaji kadi za maombi. Na ndipo usiku wa leo tutawaombeawagonjwa. Na iwapo Bwana hatabadili mawazo yangu, nataka

Page 5: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

HADITHI YA MAISHA YANGU 5

kuhubiri juu ya somo usiku wa leo, Kama Utatuonyesha Baba,Itatutosha.

Sasa nataka kusoma fungu la maneno adhuhuri hii,kuanza tu Hadithi ya Maisha, lipatikanalo katika Kitabu chaWaebrania, sura ya 13, na tuanzie hapa kwenye…ningesemakwenye aya ya 12.

Kwa ajili hii Yesu naye, ili awatakase watu kwa damuyake, mwenyewe, aliteswa nje ya lango.Basi na tutoke…tumwendee nje ya kambi,

tukichukua shutumu lake.Maana sisi hapa hatuna mji udumuo, bali twatafuta

ule ujao.Sasa hicho ni namna fulani ya fungu la maneno. Kwa

maana, unaona iwapo ni hadithi ya maisha, au jambo lolote linalohusiana na mwanadamu, hatutukuzi jambo hilo, nahasa sana ma—maisha ya mtu yaliyopita, kama yamekuwameusi kama yangu yalivyokuwa. Bali niliwaza, kama tukisomaMaandiko,Mungu angebarikiMaandiko yale. Nawazo langu ni:

Kwamba hapa hatuna mji udumuo, bali twatafuta uleujao.Sasa, ninajua kwamba mnapenda sana Los Angeles. Mna

haki ya kuupenda. Ni jiji maarufu, jiji zuri. Pamoja namchanganyiko wake wa moshi na ukungu na kadhalika, hatahivyo ni jiji zuri, hali nzuri ya hewa. Lakini jiji hili haliwezikudumu, halina budi kuwa na mwisho.

Nimesimama huko Rumi (ambako wafalme wakuu) na ilemiji ambayo walidhani wangejenga idumuyo, na kuchimba chinifuti ishirini kupata hata magofu yake.

Nimesimama ambapo Mafarao walikuwa na milki zao kuu,na ungechimbua chini katika ardhi kupata ambapo haoMafaraowakuu walitawala.

Sisi sote hupenda kufikiria kuhusu jiji letu na mahali petu.Bali, kumbuka, haviwezi kudumu.

Nilipokuwa mvulana mdogo nilizoea kwenda kwenye mtimkubwa wa mepoo. Nchini mwangu tuna miti mingi migumu.Basi tulikuwa na huu mti wa mepoo, mepoo sukari, na tunaoita“mepoo mgumu” na “mepoo laini.” Mti huu mkubwa mno,ulikuwa mti mzuri zaidi ya yote. Na wakati ningerudi kutokamakondeni, katika kazi ya nyasi za malisho na—na mavuno,nilipendelea kwenda kwenye mti huu mkubwa na—na kuketichini yake na—na kuangalia juu. Na ningaliweza kuona matawiyake makubwa na imara yakipepea kwenye upepo, shina kubwamno. Na nikasema, “Unajua, ninaamini kwamba mti huuutakuwepo hapa kwa mamia na mamia ya miaka.” Si mudamrefu uliopita nilivangaliamti ule wa kale, ni kisiki tu.

Page 6: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

6 NDUGU BRANHAM

“Maana hapa hatuna mji udumuo.” La, hakuna kituhapa duniani ambacho unaweza kutazama kitakachodumu.Hakina budi kiwe na mwisho. Kila kitu ambacho hufalazima kitoe nafasi kwa kisichopatikana na mauti. Kwa hiyohaidhuru barabara zetu kuu tunazijenga vizuri vipi, jinsi ganitunatengenezamajengo yetu, vyote havina budi kuharibika, kwamaana hapa hakuna kitu kinachoweza kudumu. Kinachodumuni kile tu kisichoonekana.

Nakumbuka nyumba ambayo tuliishi, ilikuwa nyumba yakale ya magogo iliyokandikwa kwa matope. Mimi…Penginehuenda wengi hawajawahi kuona nyumba iliyokandikwa kwamatope. Lakini yote ilikuwa imekandikwa kwa matope, na yalemagogo makubwa mno yaliyokuwa katika hiyo nyumba ya kale,nilifikiri nyumba ile ingedumu kwa mamia ya miaka. Bali,unajua, leo pale nyumba ile iliposimama pana mradi wa ujenziwa nyumba. Pamebadilika sana.Kila kitu kinabadilika. Bali…

Nami nilizoea kumwona baba yangu, alikuwa mtu mfupihivi, mwenye maungo, ana nguvu sana, naye alikuwa mmojawa watu wadogo wenye nguvu sana niliopata kujua. Nilikutanana Bw. Coots, mtu ambaye alikuwa akifanya kazi naye katikamagogo, alikuwa mkata magogo, basi yapata mwaka mmojauliopita, na Bw. Coots ni rafiki yangumsiri, na ni shemasi katikakanisa la First Baptist, naye akasema, “Billy, huna budi kuwamtu mwenye nguvu sana.”

Nami nikasema, “La, sina, Bw. Coots.”Akasema, “Kama ulichukua maungo ya baba yako,

ungekuwa hivyo.” Kasema, “Nilimwona mtu huyo, mwenyeuzito wa ratili mia moja na arobaini, akipandisha gogo kwenyebehewa peke yake, lenye uzito wa ratili mia tisa.” Yeye alijuatu jinsi ya kufanya hivyo. Alikuwa na nguvu. Ningemwonaakija mahali pa kunawia na kujitayarisha kwa chakula, mamaanapomwita.

Nasi tulikuwa na mtofaa wa zamani nje katika uwanja,na halafu kulikuwa na mitatu au minne midogo upande wanyuma. Na pale penye mti wa katikati kulikuwa na kioo chakale cha kujiangalia, kimevunjika, kioo, kikubwa. Na kilikuwakimebandikwa ubavuni mwa ule mti kwamisumari iliyokunjwa.Ni kama ambayo baadhi yenu ninyi maseremala mnaosikilizamngeita “misumari ya kutundikia koti.” Umekunjiwa kwandani kushikilia kile kioo mahali pake. Na kulikuwa na kitanakikuukuu cha bati. Wangapi wamewahi kuona bati…kitanacha bati mtindo wa kale? Naweza tu kukiona.

Na halafu kulikuwa na benchi dogo la kunawia, ubao mdogotu uliokuwa na mguu chini yake uliokaa upande, umepigiliwakwenye ule mti. Bomba dogo kuukuu, la nusu salfa pale ambalotulivutia maji, nasi tuliogea kwenye mti huu wa zamani. Namama alizoea kuchukua magunia ya unga na kutengeneza taulo.

Page 7: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

HADITHI YA MAISHA YANGU 7

Kunamtu aliyewahi kutumia taulo ya gunia la unga? Naam, ninahakika ninajisikia niko nyumbani sasa. Na hizo taulo kubwa zakale zinazoparuza! Nawakati alipotuogesha sisi watotowadogo,ange…ilisikika kama alikuwa anasugua ngozi itoke kila wakatialiposugua. Na ninakumbuka gunia hilo la zamani la unga.Naye angechomoa baadhi ya nyuzi zake na kutengeneza vifundovidogo, ili kulipamba kwa namna fulani.

Ni wangapi wamewahi kulala kwenye godoro la nyasikavu? Vema, nita—nitasema! Wangapi wamewahi kujua mto wamakapi ulikuwa nini? Vema, Ndugu Glover, niko nyumbani sasa,bila shaka! Godoro la nyasi kavu, vema, haujapita muda mrefusana tangu niache kulalia moja, na ilikuwa…Loo, ni—ni zurila kulalia, baridi kidogo. Katika majira ya kipupwe huchukuakitanda cha zamani cha manyoya wakakilalia, unajua, halafuinabidi kutufunika kwa kipande cha turubai kwa sababu thelujiiliingilia katika zile—zile—zile nyufa kwenye nyumba, unajua,ambapo mbao kuukuu za kuezekea nyumba zingepishana,unajua, na theluji ingepenya mle. Na, lo, naweza kulikumbukahilo vizuri sana.

Na halafu Baba alipata kuwa na burashi ya kunyolea.Mimi…Sasa hili litawachekesha. Ilitengenezwa kwa magandaya mahindi, brashi ya kunyolea ya maganda ya mahindi.Angechukua sabuni ya kale ya mama ya magandi ambayoalitengeneza, akaitayarisha na akajipaka usoni kwa brashi hiiya maganda ya mahindi, na kuzinyoa kwa wembe mkubwawa kale ulionyoka. Na Jumapili angechukua vi—vipande vyakaratasi, akavibandika kuuzunguka ukosi wake, walivaa ukosiwa karatasi ngumu na kuizungushia kwenye ukosi namna hiikuhifadhi po—po—povu lisiguse ukosi wa shati lake. Mmewahikuona hilo likifanywa?Mbona, jamani, jamani!

Ninakumbuka chemchemi ndogo chini huko, tulikozoeakwenda kuchota maji ya kunywa, na kuchota maji yetu kwa kataya kale ya kibuyu. Wangapi wamewahi kuona kata ya kibuyu?Naam, wangapi wenu wanatoka Kentucky, basi? Ndiyo, vema,hebu waangalieni Wakentucky walio hapa. Vema, jamani, niko—niko katikati…Nilifikiria wote walio hapa ni Okies na Arkies,bali inaonekana kama Kentucky inaingia. Naam, walivumbuamafuta huko Kentucky miezi michache iliyopita, mwajua, kwahiyo pengine hao ni baadhi yao wanaokuja huku.

Na halafu ninakumbuka wakati Baba alipokuwa anakuja nakunawa kwa ajili ya chakula, angekunja mikono ya shati lake,na hiyo mikono mifupi na minene. Na alipokunja mikono yakeapate kunawa, akajitupia maji usoni mwake, hiyo misuli ilijaatu kwenye mikono yake midogo. Nami nikasema, “Unajua, babayangu ataishi miaka mia moja na hamsini.” Alikuwa na nguvusana! Lakini alikufa akiwa na umri wamiaka hamsini namiwili.Unaona? “Hapa hatuna mji udumuo.” Hiyo ni kweli. Hatuwezikwendelea.

Page 8: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

8 NDUGU BRANHAM

Sasa hebu na tusafiri kidogo, sisi sote. Kila mmoja wenuhapa ana hadithi ya maisha yake, kama niliyo nayo mimi, nani vizuri kutembea katika barabara ya kumbukumbu mara kwamara. Sivyo? Kurudi tu, na hebu sote turudi kwa muda, nyumakwenyemaisha sawa na hayo kamawatoto wadogo.

Na sasa sehemu ya kwanza ya hadithi ya maisha. Nitaigusiakidogo tu, maana iko katika kile kitabu na wengi wenu mnakitabu hicho.

Nilizaliwa katika kibanda kidogomlimani, juu huko kwenyemilima ya Kentucky. Walikuwa na chumba kimoja ambamotuliishi, hapakuwa na zulia sakafuni, hakuna hata mbaosakafuni, ilikuwa tu udongo mtupu. Na gogo, sehemu ya juuya gogo iliyokatwa yenye miguu mitatu, hiyo ndiyo iliyokuwameza yetu. Na hao watoto wote Wabranham wangekusanyikakuizunguka, na huko nje mbele ya kile kibanda kidogo cha kale,na kugaagaa kabisa, ilionekana kama kwamba kundi la kombawamekuwa wakigaagaa kule nje kwenye vumbi, mwajua, walendugu wadogo wote. Sote tulikuwa tisa, na msichana mmojamdogo, na kwa kweli alikuwa na wakati mgumu miongoni mwakundi lile la wavulana. Inatubidi tumheshimu leo kutokana namambo ambayo tulifanya katika siku zile. Hakuweza kufuatananasi mahali po pote, tungelimfukuza arudi, alikuwa msichana.Kwa hiyo asingeweza kuyastahimili hayo, unajua. Kwa hiyotulikuwa…Na wote…

Kumbuka kwamba huko nyuma ya meza tulikuwa na vitiviwili tu, na vilitengenezwa kutokana na gome la tawi. Nivitawi vidogo vya mti mgumu vikiunganishwa pamoja, nasehemu ya chini imesukwa pamoja kwa gome la mti huo.Yupo aliyewahi kuona kiti cha gome la mti mgumu? Ndiyo.Na bado naweza kumsikia Mama. Loo, baadaye tulipofikiamahali ambapo angeweza kupata sakafu ya mbao, akiwa nawale watoto wachanga pajani mwake namna hii, na akibembeakile kiti cha kale huku kinalia bankti, bankti, kishindosakafuni. Na ninakumbuka ili kuwazuia watoto wasitoke njeya mlango, wakati yeye anafua au kitu fulani, angelaza kitichini na kukigeuza kwa namna fulani kikingame mlangoni,ili kuwazuia watoto wasitoke nje wakati ilipombidi kwendakwenye chemchemi kuchota maji, na kadhalika.

Basi Mama alikuwa na umri wa miaka kumi na mitanonilipozaliwa, naye Baba alikuwa na kumi na minane. Naminilikuwa wa kwanza kati ya watoto tisa. Nao waliniambiakwamba asubuhi hiyo niliyozaliwa…

Naam, tulikuwa fukara sana, maskini wa maskini. Nahatukuwa hata na dirisha kwenye kibanda hiki kidogo. Kilikuwana kitu kama mlango mdogo wa mbao ambao mnafungua.Sijui kama mmewahi kuona kitu kama hicho. Mlango mdogowa mbao ambao ulifunguka badala ya dirisha, unauacha

Page 9: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

HADITHI YA MAISHA YANGU 9

wazi mchana na kuufunga usiku. Hatukuweza kuwasha taaza umeme au hata za mafuta ya taa siku hizo, tulikuwa nainayoitwa “taa ya shahamu.” Sasa, sijui kama uliwahi kujuataa ya shahamu ilikuwa nini. Vema, ninyi mna…Na uliwahikununua…kuwasha fundo la msonabari? Maana unachukua tufundo la msonabari na kuliwasha na kuliweka juu ya kifuniko,litawaka. Na hiyo ni…lilifuka moshi kidogo, lakini hawakuwana fanicha, hata hivyo, ya kutia masizi. Kwa hiyo kili…kibandakilipata masizi. Ulitoka vizuri sababu kulikuwa na paa lakutosha juu kule kwa huo kutokea. Kwa hiyo u…

Basi nilizaliwa Aprili ta—tarehe 6, 1909. Bila shaka, mnajua,hilo lanifanya niwe na umri uliozidi kidogo miaka ishirini namitano sasa. Na kwa hiyo, asubuhi niliyozaliwa, Mama alisemakwamba walifungua lile dirisha. Sasa, hatukuwa na madaktari,kulikuwa na mkunga. Tu…Na huyo mkunga alikuwa ninyanyangu. Na kwa hiyo nilipozaliwa na kulia kwangu kwakwanza, na—na Mama alitaka kumwona mtoto wake. Na—nayeye alikuwa mwenyewe ni mtoto tu. Na walipofungua hilodirisha dogo, wakati wa mapambazuko, yapata saa kumi namoja. Na yule…Alikuweko maskini robin ametua kando yakichaka kidogo. Kama ninyi nyote mlivyokwisha kuona pichayake katika—katika kitabu changu cha hadithi ya maisha yangu.Maskini robin alikuwa ametua pale akiimba kwa bidii sana.

Nimewapenda robin sikuzote. Sasa, ninyi wavulanamnaosikiliza redio huko nje, msiwaue hao ndege wangu.Mnaona, wao ni—wao ni—wao ni…Wao ni ndege wangu.Mmewahi kusikia hadithi ya robin, jinsi alivyopata kifua chakechekundu? Nitasimama hapa kwa muda. Jinsi alivyopata kifuachake chekundu…Kulikuwa na Mfalme wa wafalme anakufasiku moja Msalabani, na Yeye alikuwa anateseka na hakunamtu aliyekuja Kwake. Hakuwa na mtu wa kumsaidia Yeye. Napalitokea ndege mdogo mwenye rangi ya kahawia aliyetakakuiong’oa hiyo misumari Msalabani, basi akaendelea kurukapale Msalabani na kuvuta misumari ile. Alikuwa mdogo mnoasingeweza kuing’oa, basi kifua chake kidogo kikalowa damu.Na tanguwakati huo kifua chake kimekuwa chekundu.Msimuueenyi wavulana. Mwacheni.

Alikuwa ameketi kando ya dirisha, akiimba kamawaimbavyo robin. Basi—basi Baba alifungua dirisha. Nawalipolifungua lile dirisha la mlango mdogo, Nuru ile ambayomnaiona kwenye picha ikaja inazunguka dirishani, asemamamangu, na ikaning’inia juu ya kitanda. Nyanya hakujuala kusema.

Sasa, tuna…hatukuwa familia yenye dini. Watu wangu niWakatoliki. Mimi ni Muairishi pande zote mbili. Baba yangu niMuairishi halisi, Branham. Mama yangu ni Mharvey; ni kwambatu, baba yake alimuoa Mhindi wa Cherokee, kwa hiyo hilolilivunja huo ukoo mdogo au damu ya Kiairishi. Na Baba na

Page 10: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

10 NDUGU BRANHAM

Mama hawakwenda kanisani, na walioana nje ya kanisa nahawakuwa na dini hata kidogo. Na nyuma huko kwenye milimahakukuwa hata na kanisa la Kikatoliki. Kwa hiyo walikujawakati wa masetla wa kwanza, Wabranham wawili wakaja, nakutoka kwa hao kukatokea kizazi kizima cha Wabranham; ndioukoo wa familia.

Ndipo akafungua…Walipofungua dirisha hili na Nuruhii ikaning’inia mle ndani, hawakujua la kufanya. Babaaliishajinunulia (Mama alisema) ovaroli mpya kwa ajili yatukio hili. Alikuwa amesimama na…huku ametia mikono yakekwenye sehemu ya mbele ya hiyo ovaroli kuukuu, kama vilewakata miti na wakata magogo walivyozoea katika siku zile. Nailiwaogopesha.

Naam, baada ya kufikia labda umri wa siku kumi, aukitu kama hicho, walinipeleka kwenye kanisa dogo la Kibatistilinaloitwa “Possum Kingdom,” kanisa la Kibatisti la PossumKingdom. Hilo ni jina kwelikweli. Kulikuwa na mhubiri wakuzunguka huku na huko, mhubiri wa Kibatisti wa mtindowa kale alizuru mahali hapo mara moja kila miezi miwili.Kuhusu…Watu wangefanya ibada ndogo pamoja, wangeendawaimbe nyimbo, bali walikuwa na mahubiri mara kwa maratoka kwa mhubiri yule wa mzunguko. Walimlipa kila mwakakwa gunia la maboga na vitu vichache kama hivyo, unajua,ambavyo watu walilima wapate kumpa yeye. Na huyo mhubirimzee akaja, na hapo alinifanyia maombi kama mvulana mdogo.Hiyo ilikuwa safari yangu ya kwanza kanisani.

Kwenyemwakawa kama…kitu kama umri unaozidi kidogomiaka miwili, ono la kwanza lilitokea.

Naam, walikuwa wamelitangaza sehemu zote za milimanikule kwamba “Nuru hii iliingia.” Kwa hiyowalijaribu kuliwazia.Baadhi yao walisema lazima ilikuwa nuru ya jua ikirudisha nurutoka kwenye kioo humo nyumbani. Lakini hapakuwepo na kioomle ndani. Na jua halikuwa limechomoza, kwa hiyo ilikuwamapema mno, saa kumi na moja. Hivyo basi, loo, wakaipuuzaHiyo. Nami nilipokuwa na kama…nadhani kuwa na umri wakaribu miaka mitatu…

Sasa, yanipasa niwemwaminifu. Kunamambo hapa ambayositaki kuyasema, nami laiti ningeweza kuyaruka na isinibidikuyasema. Bali hata hivyo, kusema kweli, yakubidi usemeukweli kama ni juu yako mwenyewe au watu wako. Uwemwaminifu kuhusu jambo hilo, ndipo sikuzote ni jambo lile lile.

Baba yangu alikuwa mbali na kuwa mtu wa dini. Yeyealikuwa mvulana halisi wa mlimani ambaye alikunywa pombedaima, wakati wote. Naye aliingia katika matatizo ya kupigana,na kulikuwa na watu wawili au watatu karibu wauawewakati wao walipopigana, wakitupiana risasi, na kukatanavisu, kwenye namna fulani ya tafrija huko milimani. Na Baba

Page 11: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

HADITHI YA MAISHA YANGU 11

alikuwa mmoja wa viongozi wa kundi la mapigano haya, kwasababu kulikuwa na rafiki yake aliyeumizwa, na amempigamtu fulani kwa kiti. Na ame…Huyo mtu alichomoa kisu naalikuwa anataka kumchoma rafiki ya Baba kwa kisu sakafuni,kumchomamoyoni, basi Baba akashiriki. Na kwa kweli vilikuwavita vikali sana, kwa sababu wao, kutoka mbali chini hukohadi Burkesville, umbali wa maili nyingi, walimtuma liwalikumfuatilia Baba, juu ya farasi.

Kwa hiyo mtu huyo alikuwa amelala akiwa nusura kufa.Yawezekana baadhi ya watu wake wanasikiliza. Nitataja jinalake, jina lake aliitwa Will Yarbrough. Wao labda…Nadhaniwao wako California, baadhi ya wanawe. Lakini alikuwamjeuri,mtu mnene mwenye nguvu, alimuua mwanawe kwa ufito waua. Kwa hiyo yeye—yeye alikuwa mtu mwenye nguvu sana namwovu. Na kwa hiyo palikuwa na vita vikali vya visu kati yakena Baba. Na baba yangu karibu amuue yule mtu, kwa hiyoilimbidi akimbie aondokeKentucky avukemto hadi Indiana.

Basi yeye alikuwa na kaka ambaye aliishi, wakati huo, hukoLouisville, Kentucky, alikuwa kaimu msimamizi wa Kiwandacha Mbao cha Mosaic huko Kentucky, huko Louisville. Na kwahiyo Baba akaja kumkuta kaka yake. Baba alikuwa kitindamimba katika wavulana, kwa watoto kumi na saba. Na kwahiyo alikuja kumtafuta kaka yake, na wakati ambapo alikuwaameondoka kwa karibu mwaka mmoja. Hangeweza kurudi,kwa sababu sheria ilikuwa inamtafuta. Na ndipo tulipopatahabari kutoka kwake kwa barua, iliyotiwa sahihi kwa jinajingine, lakini kwamba yeye alikuwa amemwambia mama jinsiangewasiliana naye.

Kisha ninakumbuka siku moja chemchemi ile (kibanda hikikidogo) ilikuwa tu nyuma ya nyumba. Na—na mnamo wakatihuo baada ya…Kuna tisa…tofauti ya miezi kumi na mmojakati yangu na ndugu yangu anayenifuata, na yeye bado alikuwaanatambaa. Basi nilikuwa na jiwe kubwa mkononi mwangu,na nilikuwa nikijaribu kumwonyesha yeye jinsi ambavyoningeweza kulitupa jiwe hili kwenye matope, mahali ambapochemchemi ilibubujika toka ardhini na kuifanya ardhi iwetopetope. Ndipo nikasikia ndege, na alikuwa akiimba juu yamti. Basi niliangalia juu kwenye mti ule na yule ndege akarukaakaenda zake, na, wakati alipoondoka, Sauti ilinena nami.

Sasa, najua mnafikiri nisingeweza kufikiri na kukumbukajambo hilo. Bali Bwana Mungu Ambaye ndiye Hakimu, wambingu na nchi na yote yaliyomo, anajua ninasema kweli.

Ndege yule, aliporuka kwenda zake, Sauti ilikuja kutokamahali yule ndege alipokuwa juu yamti, kama upepo ulioshikwakatika kijiti, na Hiyo ikasema, “Utaishi karibu ya mji unaoitwaNew Albany.” Na nimeishi, tangu nilipokuwa na umri wa miaka

Page 12: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

12 NDUGU BRANHAM

mitatu hadi wakati huu, umbali wa maili tatu toka New Albany,Indiana.

Niliingia ndani nikamwambia mama kuhusu jambo hilo.Naam, alifikiria nilikuwa tu ninaota au kitu fulani.

Na baadaye tulihamia Indiana na baba akaenda kufanyakazi kwa mtu mmoja, Bw. Wathen, mtu tajiri. Ni mwenyeKiwanda cha Wathen cha kutengenezea mvinyo. Basi alikuwana hisa nyingi sana. Yeye ni milionea kwelikweli katikaLouisville Colonels na—na gofu, na kadhalika. Na basi tuliishikaribu na mahali pale. Na Babangu akiwa maskini, hatahivyo hangeweza kuacha ulevi wake, kwa hiyo aka—akaanzakutengeneza chang’aa kwa—kwa chombo cha kutengenezeachang’aa.

Ndipo tukio hili likanilemea sana kwa sababu nilikuwandiye mkubwa wa watoto wote. Ilinibidi nije niteke majikupeleka kwenye chombo hiki cha kutengenezea chang’aa,kupoza mifereji ile wakati walipokuwa wanatengenezachang’aa. Basi akawa anaiuza, na halafu akapata vyombo viwiliau vitatu vya chang’aa. Sasa, hiyo ndiyo sehemu nisiyotakakusimulia, bali ni kweli.

Ndipo nakumbuka siku moja, toka kwenye ghala la nafaka,nikipanda kwenda nyumbani, nikilia. Kwa sababu nje hukonyuma ya mahali hapo kulikuwa na kidimbwi, ki…ambapowalitumia kukatia barafu. Wengi wenu mnakumbuka wakatiwalipozoea kukatakata barafu na kuiweka kwenye unga wambao. Naam, hiyo ndiyo namna Bwana Wathen alivyohifadhibarafu nje huko kijijini. Na Baba alikuwa de—dereva wake,dereva wa binafsi. Na dimbwi hili lilipojaa samaki wakatiwangeenda kukatakata barafu na kuileta na kuiweka kwenyeunga wa mbao, basi wakati barafu ile ilipoyeyuka wakati wamsimu wa kiangazi wakati ilipokuwa inazama, nadhani ilikuwasafi kidogo, zaidi kama ziwa la barafu, nao waliweza kuitumia,sio kwa kunywa, bali kwa kuyahifadhi maji baridi, waliiwekakandokando ya ndoo zao namaziwa yao na kadhalika.

Basi siku moja nilipokuwa nikibeba maji toka nyumanje kwenye bomba hili, ambalo lilikuwa umbali wa kamajengo moja la mji. Nilikuwa namlilia kwa nguvu mtu ambayehangenisikiliza, kwa sababu nilikuwa nimetoka shuleni nawavulana wote walikuwawamekwisha kwenda bwawani, kuvuasamaki. Nilipenda sana kuvua samaki. Na kwa hiyo wotewalienda kuvua isipokuwa mimi, na ilinibidi kubeba maji yachombo hiki cha chang’aa. Bila shaka, jamani, lilibidi lifanywekisirisiri, ilikuwa imepigwa marufuku. Na mimi…Lilinilemeasana. Nami nakumbuka nikija pale huku kidole gumba chamguuwangu kimepondwa, na nimefunga gunzi chini ya gumba langukulikinga na vumbi. Uliwahi kufanya jambo hilo? Kuweka tugunzi la mahindi chini ya kidole gumba chako namna hii na

Page 13: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

HADITHI YA MAISHA YANGU 13

kulifunga kwa kamba. Linakishikilia kidole gumba chako juukama vile kichwa cha kasa, unajua, kikitokeza juu. Ungewezakunifuatilia kila mahali nilipoenda, nikiwa na gunzi hili lamahindi chini ya kidole gumba; mahali nilipokanyaga, unajua.Sikuwa na viatu vyo vyote vya kuvaa. Kwa hiyo tulikuwa hatuvaiviatu, wakati mwingine nusu ya msimu wa kipupwe. Kamatulivaa, sisi…ilikuwa tu ambavyo tuliweza kuokota, mtu fulaniangetupa sisi. Na nguo ambazo mtu fulani, ambazo tungezipatakwa hisani.

Nami nikasimama chini ya mti huu, na nilikuwa nimekaapale nikilia sana (ilikuwa Septemba) kwa sababu nilitakakwenda kuvua. Ilinibidi kujaza maji mapipa kadha kwa ndoo zasukari guru, kama urefu huu tu, nusu galoni, sababu nilikuwamvulana mdogo tu wa kama umri wa miaka saba. Naminingezimwaga kwenye pipa kubwa halafu nirudi na kuchotandoo nyingine mbili na kurudi, kuyasukumiza kwenye bomba.Hayo ndiyo maji tuliyokuwa nayo. Nao walikuwa watengenezechang’aa ya mahindi usiku ule, watu hawa pamoja na Babangu,kule nyumbani.

Basi nilikuwa nikilia, mara nikasikia kitu kikifanya uvumikama wa upepo wa kisulisuli, kitu kama hiki (sasa, natumainisi mkubwamno), ukivuma, “Whoooossssh, whoooossssh,” uvumitu kama huo. Naam, kulikuwa kimya sana, nami nikaangaliapande zote. Wajua, upepo mdogo wa kisulisuli, naaminimnauita vimbunga vidogo? Kwenye majira ya kupukutikamajani vinabeba kwenye shamba la mahindi, unajua, majani nakadhalika, katika msimu wa masika kule, majani yanapoanzatu kugeuka. Nami nilikuwa chini ya mti mkubwa mweupewa mtakawa, nikisimama karibu kati ya ghala na ile—ilenyumba. Basi nikasikia ule uvumi. Nami nikatazama pande zote,kulikuwa kimya tu kama ilivyo katika chumba hiki. Hakuna janilinalopeperukamahali po pote, au cho chote kile. Basi nikawaza,“Uvumi huo unatoka wapi?” Naam, nikawaza, “Lazima uwembali na mahali hapa.” Nikiwa mvulana mdogo tu. Ukazidikuwa mkubwa.

Nikachukua ndoo zangu na nikalia mara nyingi zaidi kishanikaanza kutembea nikipanda kwenye kile kijia, nilikuwaninapumzika. Ndipo nikatembea futi chache tu toka pale,kutoka chini ya matawi ya mti huu mkubwa, na, loo,jamani, ulitoa sauti ya upepo wa kisulisuli. Nami nikageukakuangalia, na yapata urefu wa nusu ya mti ule kulikuwepona upepo mwingine wa kisulisuli, umenaswa kwenye ule mtiukizungukazunguka, ukitikisa majani yale. Naam, sikuwaziacho chote kigeni kuhusu hilo kwa sababu ni katika wakati ulewa mwaka, na masika, mbona, hizo pepo za kisulisuli huja.Ndogo…Tunaziita “pepo za kisulisuli.” Na hizo—na hizo huzoamavumbi. Mmeziona kwenye jangwa namna hiyo. Jambo lile lile.Kwa hiyo niliangalia, lakini haukuondoka. Kwa kawaida huwa

Page 14: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

14 NDUGU BRANHAM

ni mngurumo kwa muda mfupi sana, kisha huondoka, lakiniulikwisha kuwepo hapo dakikambili au zaidi.

Naam, nikaanza kutembea nikipanda kwenye kile kijiatena. Ndipo niligeuka kutazama hili tena. Na Huo ulipofanyahivyo, Sauti ya kibinadamu inayosikika tu wazi kama yanguinavyosikika, ilisema, “Usinywe pombe kamwe, kuvuta sigaraau kuuchafua mwili wako kwa namna yo yote. Kuna kaziutakayofanya utakapokuwa mtu mzima.” Mbona, ilinitishanusura nife! Ungeweza kuwazia jinsi mtoto mdogo alivyojisikia.Niliangusha ndoo zile, nikatimuambio kuelekea nyumbani upesinilivyoweza, nikipigamayowe kwa upeowa sauti yangu.

Na kulikuwa na vichwashaba nchini, nyoka, nao wana sumusana. Mama alifikiria, ati nimemkanyaga huyo kichwashabanilipokuwa nikija kando ya bustani, ndipo akakimbia akijakunichukua. Basi nikaruka juu hata kwenye mikono yake, hukuninapiga mayowe, nikimkumbatia na kumbusu. Naye akasema,“Kuna nini, umeumwana nyoka?”Akaniangalia kilamahali.

Nikasema, “Hapana, Mama! Kuna mtu kwenye mti ulekule chini.”

Naye akasema, “Loo, Billy, Billy! Wacha?” Kisha akasema,“Ulisimama ukasinzia?”

Nikasema, “La, mama! Kuna mtu kwenye ule mti, na Yeyeameniambia nisinywe pombewala nisivute sigara.”

“Kunywa mvinyo na—na kadhalika.” Nami nilikuwaninabeba maji kupeleka kwenye chombo cha kutengenezeachang’aa, wakati uo huo. Naye akasema, “Usinywe pombekamwe au kujichafua mwili kwa namna yo yote.” Hiyo nikusema uchafu, unajua, na utoto wangu…ujana na wanawake.Na nijuavyo mimi, sijawahi hata wakati mmoja kuwa nahatia ya jambo hilo. Bwana alinisaidia kwa mambo hayo, nanikiendelea mbele mtafahamu. Kwa hiyo basi, “Usinywe pombewala usivute sigara, au usiuchafue mwili wako, kwani kuna kaziutakayofanya utakapokuwamkubwa zaidi.”

Naam, nilimwambia hilo Mamangu, naye ali—alinicheka tu.Nami nilikuwa na kiwewe sana. Aliita daktari, naye daktariakasema, “Vema, yeye yuna wasiwasi tu, hivyo tu.” Kwa hiyoakanilaza kitandani. Na kamwe, tangu siku ile hata sasa, sijapitakaribu ya mti ule tena. Niliogopa sana. Ningeshuka kupitiaupande wa pili wa ile bustani, kwa sababu niliwaza kulikuwana mtu juu kwenye ule mti na Yeye alikuwa anazungumza nami,Sauti nzito mno ambayo ilinena.

Na halafu wakati fulani yapata mwezi mmoja baadaye,nilikuwa ninacheza gololi kule nje na ndugu zangu wadogo,mbele ya nyumba. Mara nikahisi hali ya ajabu ikinijia. Basinikatulia na kuketi chini kando ya mti. Nasi tulikuwa huko juuya ukingo toka kwenye Mto Ohio. Nikaangalia chini kuelekeaJeffersonville, na nikaona daraja likiinuka na kukingama huo,

Page 15: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

HADITHI YA MAISHA YANGU 15

mto huo, kuvuka mto huo. Kisha nikaona watu kumi na sita(niliwahesabu) ambao walianguka kutoka huko na kupotezamaisha yao kwenye daraja lile. Nilikimbia ndani haraka sanana kumwambia mama, naye akadhani nililala usingizi. Balijambo hilo waliliweka moyoni, na miaka ishirini na miwilitangu wakati huo Daraja la Manispaa sasa (ambalo wengi wenumnalivuka mnapoenda ng’ambo ya pili) lilikingama mto ulemahali pale pale, na watu kumi na sita walipoteza maisha yaowakijenga daraja lile kukingama ule mto.

Haijashindwa kamwe kuwa kweli kabisa. KamamnavyoionaHiyo hapa kwenye jumba la mikutano, ndivyo imekuwasikuzote.

Naam, walifikiri nilikwa tu na wasiwasi. Ambalo, mimini mtu mwenye wasiwasi, hilo ni kweli. Na, iwapo umewahikuchunguza, watu ambao ni—wanaelekea kuwa wa kiroho wanawasiwasi.

Waangalie washairi na manabii. Hebu mwangalie WilliamCowper ambaye aliandika wimbo ule maarufu, “Damuimebubujika, ni ya Imanueli.” Uliwahi…Unajua wimbo huo.Nilisimama karibu na kaburi lake si muda mrefu uliopita.Ndugu Julius, ninaamini, sijui, la…ndiyo, hilo ni kweli,alikuwa pamoja nasi kule kwenye kaburi lake. Na—na hapo,baada ya yeye kuandika wimbo huo, uvuvio ulikuwa umemtoka,akajaribu kuutafuta ule—ule mto ajiue. Unaona, ile rohoilikwishamwacha. Na watu kama washairi na waandishi na…au sivyo…ninamaanisha manabii.

Mwangalie Eliya, wakati aliposimama juu ya mlima nakuagiza moto kutoka mbinguni na kuagiza mvua kutokambinguni. Halafu wakati Roho alipomtoka, alikimbia kwa tishola mwanamke. Na Mungu alimkuta amejificha pangoni, sikuarobaini baadaye.

Mwangalie Yona, ana uvuvio wa kutosha wakati Bwanaalipompaka mafuta kuhubiri kule Ninawi, mpaka m—mji wenyeukubwa wa Saint Louis ukatubu kwa nguo za magunia. Nahalafu Roho alipomwacha, ilitukia nini kwake? Tunamwonayeye juu ya mlima baada ya Roho kumwacha, akimwombaMungu auchukue uhai wake. Na, unaona, ni uvuvio. Na mambohaya yanapotukia lina—linatenda jambo fulani kwako.

Halafu ninakumbuka nilipoendelea kukua. Nikawa kijanamwanamume. (Nitaharakisha kuwahi katika muda mfupi ujao)Nilipokuwa kijana mwanamume nilikuwa na mawazo kamavijana wengine wote. Mimi…nikienda shuleni, niliwaona haowasichana wadogo. Unajua, nilikuwa na haya sana, na unajua.Basi ha—hatimaye nikajipatia rafiki mdogo msichana. Na kamawavulana wote wadogo, kama umri wa miaka kumi na mitano,nadhani. Na—na kwa hiyo, loo, alikuwa mrembo. Jamani,

Page 16: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

16 NDUGU BRANHAM

alikuwa na macho kama ya hua, na alikuwa na meno kama lulu,na shingo kama ya korongo na a—alikuwamrembo kweli.

Na mvulana mwingine mdogo, yeye…tulikuwa marafiki,kwa hiyo alichukua Ford aina ya T ya zamani ya baba yake,tukapeana miadi na wasichana wetu. Na tulikuwa tunaendakuwachukua kwenda matembezini, kwa gari. Tulikuwa na zakutosha kununua galoni mbili za petroli. Ilitubidi kuwekea jekigurudumu la nyuma tupate kupiga hendeli liondoke. Sijui kamamwaweza kukumbuka hilo au la, unajua, kupiga hendeli. Balitu—tulikuwa tunaendelea vizuri sana.

Na kwa hiyo nilikuwa na hela chache mfukoni mwangu, natulisimama kituo fulani kidogo tukanunua…ungeweza kupatasambusa ya nguruwe kwa hela moja. Na kwa hiyo, loo, nilikuwatajiri, ningeweza kununua nne! Unaona? Na baada ya kula zilesambusa na kunywa koka kola. Nilianza kurudisha chupa. Basinikashangaa, nilipotoka kule, (wanawake walikuwa wameanzatu kupungukiwa na neema wakati ule, au kuacha utu uke)maskini hua wangu alikuwa anavuta sigara.

Naam, sikuzote nilikuwa na wazo langu kuhusu mwanamkeambaye angevuta sigara, na sijabadilisha kipengele kimojatangu wakati ule. Hilo ni kweli. Ni kitu duni sana awezachokutenda. Na hilo ni kweli kabisa. Nami ni—nilidhani mimi…Sasa, kampuni ya sigara ingeweza kunichukulia hatua kwajambo hili, bali, ninawaambia, huo ni mkogo wa Ibilisi. Ndiyomuuaji mkubwa sana na mhalifu taifa hili liliye naye. Afadhalimwanangu awe mlevi kuliko awe mvuta sigara. Huo ni ukweli.Afadhali nimwone mke wangu amelala sakafuni, amelewa,kuliko kumwona na sigara. Hivyo ndivyo…

Sasa, huyu Roho wa Mungu ambaye yuko pamoja nami,kama Huyo ni Roho wa Mungu (kwa kuwa huenda mkatiliashaka), ninyi mnaovuta sigara mna nafasi ndogo mtakapofikakule, sababu hiyo tu…kila wakati. Mnaona kwenye jukwaa,jinsi Yeye anavyoilaani. Ni kitu cha kuchukiza sana. Achaneni nakitu hicho. Mabibi, iwapo mmekuwa na hatia katika kitu hicho,tafadhalini, katika Jina la Kristo, kiacheni! Kinawaangamiza.Kitawaua. Kita-…Ni—ni kansa chungu nzima.

Madaktari wanajaribu kukutahadharisha. Na halafu jinsiwanavyoweza kukuuzia takataka hiyo! Kama ungeenda kwenyeduka la dawa na kusema, “Nunua…nataka kununua kansaya senti hamsini.” Mbona, wangekuja na kuwafunga. Baliunaponunua sigara za senti hamsini, unanunua kitu kile kile.Madaktari wanasema hivyo. Loo, taifa hili lenye kichaa chafedha. Ni jambo bayamno. Nimuuaji. Limethibitishwa.

Naam, nilipomwona msichana yule mrembo akijifanyamjanja, sigara hii mkononi mwake, hilo nusura liniue, maanakwa kweli nilifikiria nilimpenda. Nami nilifikiri, “Vema…”

Page 17: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

HADITHI YA MAISHA YANGU 17

Sasa, mimi huitwa “mchukia-wanawake,” mnajua hilo, kwasababu sikuzote kwa namna fulani nawapinga wanawake,bali mimi si dhidi yenu ninyi akina Dada. Ninachukia jinsiwanawake wa kisasa wanavyotenda. Hilo ni kweli. Wanawakewazuri wanapaswa kusifiwa.

Lakini naweza kukumbuka wakati chombo cha baba chakutengeneza chang’aa juu kule kilipokuwa kinafanya kazi,ilinibidi kuweko nje huko na maji na kadhalika, kuona bibiwadogo ambao hawakuwa na zaidi ya umri wa miaka kumi nasaba, kumi na minane, juu kule na wanaume wa umri wangu wasasa, wamelewa. Na iliwabidi kuwalevusha kwa kuwapa kahawanyeusi, wapate kurudi nyumbani kuwapikia chakula cha jioniwaume zao. Loo, kitu kama hicho, nilisema, “Mimi…” Nilitoatamshi hili wakati huo, “Hawastahili risasi safi na nzuri yakuwaua.” Hilo ni kweli. Nami niliwachukia wanawake. Hiyo nikweli. Nami yanibidi nichunguze kila hatua sasa, kujiepusha nakuwaza jambo lile lile.

Kwa hiyo, bali sasa, mwanamke mzuri ni lulu katika tajiya mwanamume. Anapaswa aheshimiwe. Yeye…Mama yanguni mwanamke, mke wangu vile vile, nao ni wazuri sana.Nami ninao maelfu ya Dada Wakristo ambao ninawaheshimusana. Bali kama—kama wanaweza kuheshimu kile Mungualichowafanya, umama na malkia wa kweli, hilo ni sawa.Mwanamke ni moja ya mambo mazuri zaidi kuliko yote ambayoMungu angeweza kumpa mwanamume, ilikuwa ni mwanamke.Kando ya wokovu, mwanamke ndicho kitu kizuri zaidi yavyote kama yeye ni mke mzuri. Bali iwapo yeye sivyo alivyo,Sulemani alisema, “Mwanamke mwema ni lulu katika tajiya mwanamume, bali aliye m—mkaidi au asiyefaa ni majidamuni mwake.” Na hiyo ni kweli, ndilo jambo baya mnolinaloweza kutukia. Kwa hiyo mwanamke mwema…Kamauna mke mwema, ndugu, yakupasa kumheshimu sana. Hiloni kweli, yakupasa kufanya hivyo. Mwanamke halisi! Pia,enyi watoto, kama mna mama halisi ambaye hukaa nyumbaniakijitahidi kuwatunza, kuwasafishia nguo zenu, anawapelekashuleni, akiwafundisha habari za Yesu, yawapasa kumheshimumama mzuri huyo mwenye upendo kwa yote yaliyo ndani yenu.Yakupasa kumheshimu mwanamke huyo, ndiyo, bwana, kwasababu yeye ni mama halisi.

Wanazungumzia kuhusu kutokujua kusoma na kuandikakwa wenyeji wa milima ya Kentucky. Mnaliona katika jambohili ovu hapa. Baadhi yao mama wazee nje kule wangewezakuja hapa Hollywood na kuwafundisha ninyi mama wa kisasajinsi ya kuwalea watoto wenu. Hebu mtoto wake aingie usikummoja na nywele zake zimechafuliwa, na midomo…atoroke,(mnaiitaje hiyo?) takataka ya kujipodolea wanayopaka usonimwao, na nguo yake imebanwa upande mmoja, na amelala njeusiku kucha, amelewa, ndugu, atakata fimbo toka juu ya mti wa

Page 18: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

18 NDUGU BRANHAM

hickory naye hatatoka kwendamatembezini tena. Ninawaambiakweli, ange…Na kama ungekuwa na zaidi ya hao, ungekuwa naHollywood nzuri zaidi hapa, na taifa zuri zaidi. Hilo ni sawa. Nikweli. “Jaribu tu kuwa wa kisasa,” hiyo—hiyo ni moja ya hilaza Ibilisi.

Sasa, msichana huyu mdogo, nilipomtazama, moyo wanguukamwonea huruma sana.Na nikawaza, “Maskinimtoto huyu.”

Naye akasema, “Aa, unataka sigara, Billy?” Nikasema, “La,mama.” Nikasema, “Sivuti.”

Akasema, “Sasa, wewe ulisema huchezi dansi.” Walitakakwenda kwenye dansi na nisingelitenda jambo hilo. Kwa hiyowalisema kulikuwa na dansi chini kule, ambako wanakuitaBustani za Mikuyu.

Nami nikasema, “La, sichezi dansi.”Akasema, “Sasa, huchezi dansi, huvuti, hunywi.

Unajifurahisha vipi?”Nikasema, “Vema, ninapenda kuvua samaki na kuwinda.”

Hilo halikumpendeza.Kwa hiyo akasema, “Chukua sigara hii.” Nami nikasema,

“La, mama, asante. Sivuti.”Nami nilikuwa nimesimama kwenye mandigadi ya gari.

Walikuwa na ubao mrefu kwenye Ford za zamani, mnakumbuka,nami nilikuwa nimesimama kwenye ubao ule, tukaketi kwenyekiti cha nyuma mimi na yeye. Naye akasema, “Wataka kusemahutavuta sigara?” Kasema, “Na sisi wasichana tuna ujasirikuliko wewe.”

Ndipo nikasema, “La, mama, siamini ninataka kufanyahivyo.”

Akasema, “Ala, jike mkubwa wee!” Loo, jamani! Nilitakakuwa Bill mkubwa mbaya, kwa hiyo mimi—mimi hakikasikutaka cho chote cha kike. Unaona, nilitaka kuwa mwanandondi mashuhuri, hilo lilikuwa kusudio la maisha yangu. Kwahiyo nikasema…“Jike! Jike!”

Singeweza kuvumilia jambo hilo, kwa hiyo nikasema, “Nipehiyo!” Nikinyosha mkono wangu, nikasema, “Nitamwonyeshakama mimi ni jike au la.” Nikachomoa sigara ile na nikaanzakuwasha kiberiti. Sasa, najua mna…Sasa, mimi siwajibiki kwajambo mnalofikiria, wajibu wangu tu ni kuwaambieni kweli.Nilipoanza kuwasha sigara ile, nikiwa tu nimeamua kuivutakama ninavyoamua kuitwaa Biblia hii, unaona, nilisikia kitukikifanya, “Whoooossssh!” Nilijaribu tena, sikuweza kuifikishakinywani. Basi nikaanza kulia, nikatupa takataka ile chini.Wakaanza kunicheka. Nikaondoka kwenda zangu nyumbani,nikapanda kwenda nikipitia shambani, nikaketi chini kule,nikalia. Na—na yalikuwa ni maisha ya kutisha sana.

Page 19: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

HADITHI YA MAISHA YANGU 19

Ninakumbuka siku moja Babangu alikuwa anashukakwenda mtoni pamoja na vijana. Mimi na ndugu yangu, ilitubidikuchukua mashua na kwenda huku na huko mtoni, tukitafutachupa za kutilia chang’aa. Tulipata dazeni ya hizo kwa helamoja, kuziokota mtoni. Na Babangu alikuwa pamoja nami, nayealikuwa na moja ya zile chupa ndogo bapa…naamini zilikuwachupa za kama nusu kibaba. Na kulikuwa na mti ulioangushwana upepo, na Babangu…Basi mtu huyu alikuwa pamojanaye, Bw. Dornbush. Nilikuwa na ninino yake…Alikuwana mashua nzuri, nami nilitaka kufanya urafiki naye sababunilitaka kutumiamashua ile. Ilikuwa na usukani mzuri na yanguhaikuwa na usukani kabisa. Tulikuwa na mbao za zamani zakupigia kafi. Na iwapo ataniruhusu nitumie mashua ile…Kwa hiyo, alikuwa akiunganisha vyuma hata akamtengenezeababa vyombo vya kutengenezea chang’aa. Kwa hiyo yeye…Walinyosha miguu yao kukingama mti ule, kisha Babanguakaingiza mkono katika mfuko wake wa nyuma akachomoachupa ndogo bapa ya chang’aa, akampa naye akanywa kidogo,akamrudishia Babangu naye akanywa kidogo, na akaiwekachini kwenye chipukizi dogo kando ya mti ulioanguka. Basi Bw.Dornbush akaitwaa, akasema, “Haya, Billy.”

Nikasema, “Asante, sinywi.”Akasema, “Mbranham, na hunywi?”Kilammojawao alikufa

kiume, karibu kila mmoja. Naye akasema, “Mbranham, na etihunywi?”

Nikasema, “La, bwana.”“La,” baba akasema, “nilizaa jike moja.”Babangu aniite jike! Nikasema, “Nipe hiyo chupa!”

Nikafungua kile kizibo, nimeamua kuinywa, bali nilipoanzakuitia kinywani, “Whoooossssh!” Nikairudisha ile chupanikatimua mbio nikishuka kupitia kwenye shamba nikiendakasi nilivyoweza, huku ninalia. Kitu fulani kisingeniruhusunifanye hivyo. Unaona? Nisingeweza kusema kwamba nilikuwamwema kwa vyo vyote (nilikuwa nimeamua kulitenda), balini Mungu, neema, neema ya ajabu ambayo ilinizuia nisitendemambo hayo. Nilitaka kuyatenda, mimi mwenyewe, bali Yeyeasingeniruhusu niyatende.

Baadaye nikapata msichana nilipokuwa na umri wa kamamiaka ishirini na miwili, alikuwa kipenzi. Alikuwa msichanaambaye alienda kanisani, Mluteri wa Kijerumani. Jina lakelilikuwa Brumbach, B-r-u-m-b-a-c-h, linatokana na jina laBrumbaugh. Naye alikuwa msichana mzuri. Hakuvuta walakunywa, au—au hakucheza dansi au cho chote kile, msichanamzuri. Nilifuatana naye kwa kipindi kidogo, nami wakatihuo nilikuwa na kama miaka ishirini na miwili. Nilikuwanimekusanya fedha za kutosha hata nikajinunulia Ford kuukuu,na ni…tungepeana miadi tukafuatana pamoja. Na kwa hiyo,

Page 20: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

20 NDUGU BRANHAM

wakati ule, hapakuwa na kanisa la Kiluteri lililo karibu,walihama toka Howard Park juu kule.

Na kwa hiyo kulikuwa na mhudumu, yule aliyenitawazakwenye kanisa la Kimisionari la Kibatisti, Daktari Roy Davis.Dada Upshaw, yule hasa aliyempeleka Ndugu Upshaw kwangu,au aliyezungumza naye kunihusu mimi, Daktari Roy Davis. Nakwa hiyo alikuwa akihubiri, na alikuwa ana kanisa la Kwanzala Kibatisti, au ile—ile…Siamini lilikuwa kanisa la Kwanza laKibatisti, mojawapo, lilikuwa la Kimishenari…liitwalo kanisala Kimishenari la Kibatisti kule Jeffersonville. Naye alikuwaakihubiri mahali hapo wakati huo, nasi tungeenda kanisaniusiku, kwa hiyo…nasi tungerudi. Na kamwe sikujiunga nakanisa, bali nilipenda tu kwenda naye. Kwa sababu wazo kubwalilikuwa tu “kuambatana naye,” ni vema niwemwaminifu.

Kwa hiyo basi nikiambatana naye, na siku moja ni…Alikuwa anatoka kwenye jamaa nzuri. Basi nilianza kufikiri,“Unajua, unajua, hainipasi kupoteza wakati wa msichana yule.Siyo—siyo sawa, kwa sababu ni msichana mzuri, na mimi nimaskini na—na mimi…” Baba yangu alikuwa na afya mbaya,nami—nami…Hapakuwepo na njia kwangu mimi kumtunzamsichana kama yule, ambaye amezoea nyumba nzuri na mazuliasakafuni.

Ninakumbuka zulia la kwanza nililowahi kuona, sikujualilikuwa ni nini. Nilipitia kando yake. Nilifikiria lilikwa kitukizuri sana nilichowahi kuona maishani mwangu. “Mbonawameweka kitu kamahicho sakafuni?” Lilikuwa zulia la kwanzanililowahi kuona. Lilikuwa—lilikuwa moja ya haya—naaminilinaitwa “mazulia yaliyosukwa.” Naweza nikosee hilo. Ainafulani ya kama “kirago” au kitu fulani kilichosukwa pamoja, nakulazwa sakafuni. Zulia zuri la kijani na nyekundu, na waridikubwa lililochorwa katikati yake, unajua. Kilikuwa kitu chakupendeza sana.

Na kwa hiyo ninakumbuka ni—niliamua kwamba auilinibidi kumwomba nimuoe, au itanilazimu niondoke nakuacha mtu anayefaa amuoe, mtu ambaye angekuwa mzurikwake, ambaye angeweza kumtunza na angekuwa mwemakwake. Ningeweza kuwa mwema kwake, bali ni—ni—nilikuwatu ninapata senti ishirini kwa saa. Kwa hiyo nisingeweza kupatafedha za kutosha kumtunza vizuri. Nami…Tukiwa na jamaayote hiyo tuliyopaswa kutunza, na Babangu amekuwa na afyambaya, basi ilinibidi mimi kuwatunza wote, kwa hiyo nilikuwana wakati mgumu kweli.

Kwa hiyo nikafikiri, “Naam, jambo pekee linipasalo kufanyatu ni kumwambia kwamba mimi—mimi (yeye) mimi—mimisitarudi, kwa sababu nilimthamini mno nisingetaka kuharibumaisha yake na kumwacha apoteze wakati akinifuata mimi.”Halafu niliwazia, “Kama mtu fulani angeweza kumpata na

Page 21: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

HADITHI YA MAISHA YANGU 21

kumuoa, awe na nyumba nzuri. Na pengine kama nisingewezakumpata, ningeweza—ningeweza kujua kwamba alikuwa nafuraha.”

Na kwa hiyo niliwaza, “Bali mimi—mimi si—siwezikumwacha!” Na mimi—mimi nilikuwa katika hali mbaya sana.Na siku baada ya siku ningefikiria jambo hilo. Kwa hiyo nilionahaya sana nisingemwomba nimuoe. Kila usiku ningeamua,“Nitamwomba.” Na, wakati mimi, ah, ni kitu gani kile, vipepeo,au kitu fulani unachopata katika…?Wote ninyi ndugu nje hukolabda mlipata tukio lilo hilo katika jambo hilo. Na hali fulanihalisi ya ajabu, uso wangu ungepata joto. Mimi—mimi sikujua.Sikuweza kumwomba.

Kwa hiyo nadhani mnashangaa jinsi gani nimepata kuoa.Unajua nini? Nilimwandikia barua nikamwomba. Na kwa hiyoyeye…Sasa, haikuwa “Bi mpendwa,” ilikuwa zaidi kidogo(unajua) upande wa mapenzi kuliko hilo. Haikuwa tu ma—mapatano, ilikuwa…ni—niliiandika vizuri sana nilivyoweza.

Nami kidogo nilimwogopa mama yake. Mama yakealikuwa…alikuwa mkali kidogo. Na, lakini baba yake alikuwamzee mpole wa Kidachi, mzee mzuri tu. Alikuwa msimamiziwa udugu na wafanya kazi wa garimoshi kwenye njia ya reli,akipokea kama dola mia tano kwa mwezi kwenye zama hizo. Namimi nikipokea senti ishirini kwa saa moja, kumwoa binti yake.Aha! Nilijua singefanikiwa kabisa. Na mama yake alikuwasana…Sasa, yeye ni bibi mzuri. Na yeye—yeye alikuwa kwanamna fulani mmoja wa hawa watu wa tabaka ya juu, unajua,kama mwenye kisirani, unajua, na kwa hiyo sikumfaa kitu kwavyo vyote. Nilikuwa tu maskini kijana mshamba asiye na mbelewala nyuma, naye alifikiria Hope anapaswa kuambatana namvulana wa tabaka bora zaidi, nami na—na—nafikiri alikuwasahihi. Na kwa hiyo…Bali si—sikulifikiria wakati huo.

Kwa hiyo nikawaza, “Vema, sasa, sijui vipi. Si—siwezikumwomba baba yake, na ni—nina hakika sitamwomba mamayake. Na kwa hiyo yanibidi nimwombe yeye kwanza.” Kwahiyo nikaandika barua. Na asubuhi ile njiani nikienda kazini,niliitumbukiza kwenye sanduku la barua. Kuituma…Tulikuwatunaenda kanisani Jumatano usiku, na hiyo ilikuwa Jumatatuasubuhi. Nilijaribu Jumapili nzima kumwambia kwambanilitaka kuoa, nami sikuweza kabisa kupata ujasiri wa kutosha.

Kwa hiyo basi niliitumbukiza kwenye sanduku la barua.Basi huko kazini siku hiyo nikawaza, “Na mama yake akiipataile barua je?” Loo, jamani! Ndipo nilijua nitajuta kama—kama akiwahi kuipata, sababu hakunijali sana. Naam, nilikuwanikiwaza na kuliwazua tu jambo hilo.

Na Jumatano ile usiku nilipokuja, loo, jamani, nikawaza,“Hivi nitaendaje kule juu? Iwapo mama yake aliipata baruaile kweli atanishambulia, kwa hiyo natumaini yeye aliipata.”

Page 22: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

22 NDUGU BRANHAM

Niliiandika kwenye bahasha “Hope.” Hilo lilikuwa ndilo jinalake, Hope. Na kwa hiyo nilisema, “Nitaiandika tu juuhapa Hope.” Na kwa hiyo…Na nalifikiri labda yawezekanahakuipata.

Kwa hiyo nilijua vyema kuliko kusimama nje na kupiga honikusudi yeye atoke. Loo, jamani! Na mvulana ye yote ambayehana ujasiri wa kutosha kutembea hadi nyumbani na kubishamlangoni na kumwomba msichana, haimpasi kamwe kutokanaye nje kwa vyo vyote. Hilo ni sawa kabisa. Huo ni upuzimkubwa sana. Hiyo ni tabia duni.

Na kwa hiyo nilisimamisha Ford yangu kuukuu, unajua,na nilikuwa nimeisafisha vizuri sana. Na kwa hiyo nilipandanikaenda nikabisha mlangoni. Salala, mama yake akaufunguamlango! Ilikuwa vigumu kwangu kupumua, nikasema, “U—u—uhali gani, Bibi Brumbach?” Ndiyo.

Akasema, “Sijambo, William.”

Nikawaza, “Loo, ‘William’!”

Ki—kisha akasema, “Karibu?”

Nikasema, “Asante.” Nikaingia ndani. Nikasema, “Hopeyuko tayari?”

Mara tu huyu hapa Hope anapita upesi mle nyumbani,msichana tu wa umri upatao miaka kumi na sita. Naye akasema,“Hujambo, Billy!”

Na nikasema, “Sijambo, Hope.” Kisha nikasema, “Ukotayari kwenda kanisani?”

Akasema, “Hebu kidogo.”

Nikawaza, “Loo, jamani! Hakuipata kamwe. Hakuipatakamwe. Sawa, sawa, sawa. Wala hata Hope hajaipata, kwahiyo itakuwa barabara, sababu angeliigusia kwangu.” Kwa hiyonilijisikia vizuri kabisa.

Na halafu nilipotoka kanisani, ikawa nikawaza, “Na, kamaameipata je?” Unaona? Basi sikuweza kusikia ambacho DaktariDavis alikuwa anasema. Nikamtazama, nikawaza, “Kamapengine analinyamazia jambo hilo, na kwa kweli atanikaripianitakapotoka hapa, kwa kumwomba yeye jambo hilo.” Namisikuweza kusikia alilokuwa akisema Ndugu Davis. Na—naminikamtazama, nikawaza, “Lahaula, ninachukia kumwacha,lakini…Namimi—mimi…ukweli hakika utajidhihirisha.”

Kwa hiyo baada ya ibada tukaanza kutembea tukishukabarabarani pamoja, tukienda nyumbani, na—na kwa hiyotulitembea hadi kwenye ile Ford kuukuu. Na huko njiani kotembalamwezi inawaka kwelikweli, unajua, nikamwangalia nayealikuwa mzuri kweli. Jamani, ningemwangalia, na kuwaza, “Lo,jinsi ningefurahi kumpata, bali nafikiri siwezi.”

Page 23: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

HADITHI YA MAISHA YANGU 23

Na kwa hiyo nilitembea mbele zaidi, unajua, naningemwangalia tena. Nikasema, “Je, u—unajisikiaje usiku waleo?”

Akasema, “Loo, ni mzima.”Nasi tukasimamisha ile Ford kuukuu chini na tukaanza

kutoka, unajua, kuzunguka kando, kutembea kuzunguka konana kuelekea nyumbani kwao. Na nilikuwa ninapanda kuelekeamlangoni pamoja naye. Nikawaza, “Unajua, labda hakuipatakamwe ile barua, kwa hiyo afadhali nisahau jambo hilo tu.Nitakuwa na juma jingine la kulifikiria haidhuru.” Kwa hiyonikaanza kujisikia amani kabisa.

Akasema, “Billy?”Nikasema, “Naam,”Akasema, “Nilipata barua yako.” Loo, jamani!Nikasema, “Uliipata?”Akasema, “Aha.” Naam, akawa anaendelea kutembea,

hakusema kamwe neno jingine.Nikawaza, “Ewe mwanamke, niambie kitu. Nifukuze au

uniambie unachowazia juu ya jambo hilo.” Ndipo nikasema,“Uli—uliisoma?”

Akasema, “Aha.”Jamani, unajua jinsi mwanamke anavyoweza kukutia

wasiwasi. Loo, si—sikumaanisha hilo namna hiyo, unaona.Unaona? Bali, hata hivyo, unajua, ni—niliwaza, “Kwa niniusiseme kitu?” Unaona, basi nikazidi kusonga mbele. Nikasema,“Uliisoma yote?”

Na yeye…[Sehemu tupu kwenye kanda—Mh.] “Aha.”Kwa hiyo tulikuwa tunakaribia mlangoni, nami nikawaza,

“Jamani, usinifikishe kwenye baraza, sababu singewezakuwatoroka, kwa hiyo niambie sasa.” Basi nikaendeleakungojea.

Naye akasema, “Billy, ningependa kufanya jambo hilo.”Akasema, “Ninakupenda.” Mungu na abariki nafsi yake sasa,yuko Utukufuni. Akasema, “Ninakupenda.” Kasema, “Nafikiriyatubidi kuwaambia mzazi wetu, wazazi kuhusu jambo hilo.Unaonaje?”

Ndipo nikasema, “Mpenzi, sikiliza, hebu na tuanzejambo hili kwa pendekezo la nusu kwa nusu.” Nikasema,“Nitamwambia baba yako kama utamwambia mama yako.”Nikijiondolea sehemu iliyo nzito na kumwekelea, kwanza.

Akasema, “Sawa, iwapo utamwambia Baba kwanza.”Nikasema, “Sawa, nitamwambia Jumapili usiku.”

Na kwa hiyo usiku wa Jumapili ukafika, nikamletanyumbani kutoka kanisani na mimi…Akaendelea kunitazama.

Page 24: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

24 NDUGU BRANHAM

Ndipo niliangalia, na ilikuwa saa tatu u nusu, wakati wanguwa kuondoka umewadia. Kwa hiyo Charlie alikuwa ameketimezani mwake, akipiga taipureta. Bibi Brumbach ameketipembeni, akifuma, mnajua, au vijigurudumu unavyoweka juuya vitu, unajua. Sijui unaziitaje. Na kwa hiyo alikuwa akifanyavitu kama hivyo. Basi Hope aliendelea kuniangalia, nayeangenikunjia uso, unajua, akielekeza kwa baba yake. Namimi…Loo, jamani!Nikawaza, “Vipi kama atasema ‘La’?”Kwahiyo nikaanza kutoka nje, nikasema, “Vema, nadhani afadhaliniende.”

Basi nikaenda mlangoni, na—na akaanza kwenda mlangonipamoja nami. Sikuzote anakuja mlangoni na kuniambia “lalasalama.” Kwa hiyo nikaanza kwenda kuelekea mlangoni, nayeakasema, “Hutamwambia?”

Nami nikasema, “Ha!” Nikasema, “Hakika ninajaribukumwambia, bali si—si—sijui jinsi nitakavyomwambia.”

Naye akasema, “Nitarudi tu nawe umwite aje nje.” Kwa hiyoalirudi nyuma naye akaniachamimi nimesimama pale.

Na nikasema, “Charlie.”Akageuka naye akasema, “Ndiyo, Bill?”Nikasema, “Naweza kuzungumza nawe dakikamoja tu?”Akasema, “Hakika.” Akageuka nyuma akiwa mezani.

Bibi Brumbach akamwangalia, akamwangalia Hope, kishaakaniangalia.

Ndipo nikasema, “Tafadhali uje nje barazani.”Naye akasema, “Ndiyo, nitakuja.” Kwa hiyo akatoka akaja

barazani.Nikasema, “Hakika ni usikumzuri, sivyo?”Naye akasema, “Ndiyo, ni mzuri.”Nikasema, “Hakika kumekuwa joto.”“Bila shaka,” akaniangalia.Nikasema, “Nimekuwa nikifanya kazi sana,” nikasema,

“unajua, hata mikono yangu imepata sugu.”Akasema, “Unaweza kumchukua, Bill.” Loo, jamani!

“Unaweza kumchukua.”Nikawaza, “Loo, hilo ni afadhali.” Nikasema, “Hivi kweli

unamaanisha hivyo, Charlie?” Akasema…nikasema, “Charlie,angalia, najua kwamba yeye ni binti yako, nawe una hela.”

Naye akaunyoshamkonowake akanishikamkono. Akasema,“Bill, sikiliza, hela siyo mambo yote yaliyo katika maisha yabinadamu.” Akasema…

Nikasema, “Charlie, ni—ninapata senti ishirini kwa saa,lakini ninampenda naye ananipenda. Nami ninakuahidi,Charlie, kwamba nitafanya kazi mpaka hizi…mpaka sugu

Page 25: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

HADITHI YA MAISHA YANGU 25

ziondoke mikononi mwangu, nipate kumtunza. Nitakuwamwaminifu kwake niwezavyo kuwa.”

Akasema, “Ninaamini hilo, Bill.” Akasema, “Sikiliza, Bill,nataka kukuambia.” Kasema, “Unajua, furaha, kwa jumlahaihitaji hela kuwa na furaha.” Kasema, “Uwe tu mwemakwake. Nami najua utafanya hivyo.”

Nikasema, “Asante, Charlie. Hakika nitafanya jambo hilo.”Ndipo wakati wake wa kumwambia mama ukawadia. Sijui

jinsi gani alifaulu, bali tulioana.Kwa hiyo, tulipooana, hatukuwa na kitu, hakuna cho chote

cha kununulia vyombo vya nyumbani. Nafikiri tulikuwa na dolambili au tatu. Kwa hiyo tulikodi nyumba, ilitugharimu dolanne kwa mwezi. Kilikuwa kijumba kidogo, cha zamani chenyevyumba viwili. Basi mtu mmoja akatupa kitanda cha kale chakukunja. Sijui kama kuna mtu ye yote aliyewahi kuona kitandacha kale cha kukunja? Na wakatupa sisi hicho. Kisha nikashukakwenda kwa Sears na Roebucks nikanunua meza ndogo naviti vinne, na ha—haikupakwa rangi, unajua, nasi tuliipatahiyo kwa wakati mzuri. Na kwa hiyo basi nilikwenda kwaBw. Weber, mfanya biashara wa vyombo vikuukuu, nikanunuajiko la kupikia. Nililipa senti sabini na tano, na dola moja nakitu kununulia nondo zake. Tukaweka vyombo vya nyumbani.Nakumbuka nilipovichukua vile viti na kuvichora mmea washamrock, nilipokuwa nikivipaka rangi. Na, loo, tulikuwa nafuraha, hata hivyo. Tulikuwa pamoja, kwa hiyo hilo ndilolililokuwa la lazima. Naye Mungu, kwa rehema Yake na wemaWake, tulikuwa mume na mke wachanga wenye furaha sanaduniani.

Niliona hili, kwamba furaha haipo katika kiasi ulicho nachocha mali ya ulimwengu, bali ni jinsi ulivyoridhika na sehemuambayo umegawiwa.

Na, baada ya kitambo kidogo, Mungu akashuka akajaakabariki nyumba yetu ndogo, tukapata mtoto mwanamume.Jina lake lilikuwa Billy Paul, yuko humu ibadani sasa hivi.Na baadaye kidogo tokea hapo, kama miezi kumi na mmoja,Yeye alitubariki tena na mtoto wa kike jina lake Sharon Rose,lililotokana na neno “Waridi la Uwandani.”

Basi nakumbuka siku moja nilikuwa nimeweka akiba fedhazangu na nilikuwa nataka kwenda likizoni, niende mahalifulani, Ziwa Paw Paw, kuvua samaki. Basi nilipokuwa njianinikirudi…

Na mnamo wakati huu…Ninaacha kuongoka kwangu.Niliongoka.Na nilitawazwa naDaktari RoyDavis, katika kanisala Kimishenari la Kibatisti, na nilikuwa mhudumu na ninaMaskani ambayo sasa ninahubiria kule Jeffersonville. Naminilikuwamchungaji kwenye hilo kanisa dogo. Nami…

Page 26: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

26 NDUGU BRANHAM

Hakuna fedha, nilifanya kazi ya uchungaji kwenye kanisalile miaka kumi na saba na kamwe sikupata hata sentimoja. Sikuamini katika kuchu…Hapakuwa hata na sahaniya sadaka ndani yake. Na fungu la kumi ambalo nilipatakutokana na ile kazi, na kadhalika, kulikuwa na sanduku dogonyuma ya jengo, yalisema, maandishi yaliyokuwepo juu yake,“Kadiri mlivyowatendea mmojawapo wa hao walio wadogoWangu, mlinitendea Mimi.” Na basi hivyo ndivyo jinsi kanisalilivyolipiwa. Tulikuwa na mkopo wa miaka kumi kulilipia,na lililipiwa chini ya miaka miwili. Nami sikuchukua kamwesadaka ya namna yo yote.

Na halafu nilikuwa, loo, na dola chache nilizoweka akibakwa ajili ya likizo yangu. Mke wangu alifanya kazi, pia,kwenye Kiwanda cha Fine Shirt. Msichana mzuri mpenzi. Nakaburi lake labda lina theluji leo hii, bali yeye bado yukomoyoni mwangu. Nami ninakumbuka wakati alifanya kazi sanakunisaidia kupata fedha za kutosha kwenda kwenye ziwa hilikuvua samaki.

Na nilipokuwa ninarudi kutoka ziwani, nikaanza kuona,nikija Mishawaka na South Bend, Indiana, basi nikaanza kuonamagari ambayo yalikuwa na maandishi upande wa nyuma,yakisema, “Yesu Pekee.” Ndipo nikawazia, “Hilo linaonekanageni, ‘Yesu Pekee.’” Basi nikaanza kuona yale maandishi. Nayalikuwa juu ya kila kitu tokea baiskeli, Ford, Kadilak, nakadhalika, “Yesu Pekee.” Basi nikafuatilia baadhi yao kule chini,nao wakafika kwenye kanisa kubwa mno. Nami nikatambuakwamba walikuwaWapentekoste.

Nilikuwa nimesikia kuhusu Wapentekoste, bali walikuwakundi la “watakatifu wanaojifingirisha ambao walijitupasakafuni na kutoka povu vinywani mwao,” na kila kitu ambachowaliniambia kuwahusu. Kwa hiyo sikutaka kuhusiana nao.

Kwa hiyo niliwasikia wote wakiendelea na mamboyao mle, nami nikawaza, “Naona nitaingia ndani.” Kwahiyo nilisimamisha Ford yangu kuukuu nikaingia, nakuimba kwote ulikowahi kusikia maishani mwako! Naminikatambua kulikuwa namakanisamakubwamawili, mojawapoliliitwa P.A la J.C., na P.A. la W., wengi wenu ninyi watumwaweza kukumbuka madhehebu hayo ya zamani…Nafikiriyameungana, sasa yanaitwa, yanaitwa kanisa la UnitedPentekostal. Vema, nikasikiliza baadhi ya waalimu wao. Naowalikuwa wakisimama pale, loo, walikuwa wakifundishakuhusu Yesu na jinsi Yeye alivyokuwa Mkuu, na jinsi kila kitukilivyokuwa kikuu, na kuhusu “ubatizo wa Roho Mtakatifu.”Nikawaza, “Wanazungumzia nini?”

Na, baada ya muda kidogo, mtu fulani akaruka juu akaanzakunena kwa lugha. Naam, sijawahi kusikia jambo kama hilomaishani mwangu. Na hapa akaja mwanamke fulani anakimbia

Page 27: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

HADITHI YA MAISHA YANGU 27

mbio sana awezavyo. Halafu wote wakasimama wakaanzakukimbia. Basi nikawaza, “Naam, ndugu, hakika hawanataratibu za kanisa!” Wakipiga yowe na kupaza sauti na kufanyavurugu, nikawaza, “Kundi gani hili!” Lakini, unajua, jambofulani kuhusu hilo, kadiri nilivyoendelea kuketi pale, ndivyonilivyozidi kulipenda. Kulikuwa na jambo fulani lililoonekanakuwa zuri sana. Ndipo nikaanza kuwaangalia. Na ikaendelea.Nikawaza, “Nitawavumilia kwa muda kidogo, sababu nita…niko karibu na mlango. Kama likianza jambo la hatari,nitakimbia nje. Najuamahali gari langu dogo limeegeshwa, hapapembeni tu.”

Basi nikaanza kusikia baadhi ya hao wahubiri, walikuwawasomi nawanafunzi. Mbona, nikawaza, “Hilo ni zuri.”

Kwa hiyo ukaja wakati wa chakula cha jioni, wakasema,“Kila mtu amealikwa kwenye chakula cha jioni.”

Bali niliwaza, “Ngoja kidogo. Nina dola moja na sentisabini na tano za kwenda nyumbani, nami…” Hizo ndizotu nilizokuwa nazo kwa fedha ya petroli. Nilichukua hizo tukunifikisha nyumbani. Nami nilikuwa na Ford yangu kuukuu,ilikuwa Ford nzuri sana iliyo kuukuu. Haikuwa mbovu, ilikuwatu kama hii hapa nje, ila tu imechakaa. Na hiyo…Kwa kweliniliamini Ford ile ingeenda maili thelathini kwa saa, bali bilashaka hizo zilikuwa kumi na tano upande huu na kumi na tanoupande huu. Unaona, zijumlishe pamoja, utapata thelathini. Nakwa hiyo hiyo…Nikawaza, “Vema, usiku ule nafikiri nitatokanje na baada ya ile…”Nilikuwa nangoja ibada ya usiku.

Na, loo, yeye akasema, “Wahubiri wote, bila ya kujalimadhehebu, njoni kwenye jukwaa.” Naam, tulikuwa kama watumia mbili juu pale, nikapanda juu. Na kwa hiyo akasema, “Sasa,hatuna muda wa kutosha kwenu nyote kuhubiri.” Akasema.“Hebu pita hapa na usemewewe ni nani na unatokawapi.”

Naam, ikafika zamu yangu, nikasema, “William Branham,Mbatisti. Jeffersonville, Indiana.” Nikapita.

Ningewasikia wengine wote wakijiita, “Mpentekoste,Mpentekoste,Mpentekoste, P.A. waW., P.A.J.C., P.A.W., P…”

Nikapita. Nikawaza, “Naam, nadhani mimi ndiye mgeniasiye namwenziwe.”Kwa hiyo nikaketi chini, nikangojea.

Na, siku ile, walikuwa na wahubiri wazuri, vijana mbelepale, nao walihubiri kwa nguvu. Ndipo wakasema, “Atakayeletaujumbe usiku huu ni…” Naamini walimwita, “Mzee.” Nawahudumu wao, badala ya “Kasisi,” ilikuwa “Mzee.” Naowakamleta mzee mweusi pale, naye alikuwa na moja yamakoti haya ya mhubiri ya mtindo wa kale. Sidhani mmewahikuona moja. Mkia mrefu wa njiwa nyuma, unajua, lenye ukosiwa mahameli, naye alikuwa na kishungi kidogo tu cha mvikinachozunguka kichwa chake. Maskini mzee huyo, alikujanamna hii, unajua. Naye akasimama pale kisha akageuka. Na

Page 28: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

28 NDUGU BRANHAM

ambapo wahubiri wote walikuwa wakihubiri kuhusu Yesu namambo makuu…jinsi Yeye alivyo mkuu, na kadhalika, yulemzee alichukua fungu lake la maneno kutoka katika Ayubu.“Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi, au hapo nyotaza asubuhi zilipoimba pamoja na Wana wa Mungu walipopigakelele kwa furaha?”

Na maskini mzee yule, nikawaza, “Kwa nini hawakuwekabaadhi ya hao vijana juu kule kuhubiri?” Kuu…mahali palepalijaa watu hata wakasongamana. Basi nikawaza, “Kwa ninihawakufanya hivyo?”

Kwa hiyo basi huyu mzee, badala ya kuhubiri yaliyokuwayakiendelea humu duniani, alianza kuhubiri yaliyokuwayanatendeka Mbinguni wakati wote. Naam, alimchukua Yeyepale mwanzo pale mwanzo wa wakati, kisha akamrudisha Yeyekwenye Kuja mara ya Pili akishuka chini kwenye upinde wamvua. Mbona, sijawahi kusikia mahubiri ya jinsi hiyo maishanimwangu! Yapata wakati huo Roho akamjilia, akaruka urefukama huu huku anagongesha visigino vyake pamoja, akatupamabega yake nyuma akajifiringisha pale jukwaani, kasema,“Hamna nafasi ya kutosha hapa kwangu mimi kuhubiria.” Nayealikuwa na nafasi kubwa kuliko niliyo nayo hapa.

Nikawaza, “Iwapo Kitu hicho kitamfanya mzee atendejinsi hiyo, je kingefanya nini kama Chenyewe kingenipatamimi?” Ni—nikawaza, “Labda ninahitaji sehemu ya kituHicho.” Mbona, alitoka hapa, nikamsikitikia jamaa yule mzee.Bali, alipoondoka, nilikuwa ninajisikitikia. Nami nilimtazamaakiondoka pale.

Nilitoka usiku ule, nami nikawaza, “Sasa, asubuhiinayofuata sitamruhusu mtu ye yote ajue wapi, mimi ninani.” Kwa hiyo nikaondoka nikaenda, na usiku ule nilinyoshasuruali yangu. Nilichukua ile…nilikwenda kwenye shamba lamahindi kulala, nami nikashuka kwenda kujinunulia sambusazilizochacha. Wewe…Nilinunua fungu zima kwa hela moja.Kulikuwa na bomba la maji chini pale, nikachota maji kidogo.Kwa hiyo nilijua kwamba hizo zingenichukua muda kidogo, kwahiyo nikachukua maji nikanywa, nikaondoka nikala sambusazangu. Kisha nikarudi nikanywa maji tena. Nikaenda kwenyeshamba la mahindi, nikachukua viti viwili na kulaza surualiyangu ndogo ya pamba yenye milia mle ndani, nikaibananiinyoshe kwa kiti.

Na, usiku ule, niliomba karibu usiku kucha. Nikasema,“Bwana, kitu gani hiki nimekutana nacho? Sijawahi kuonawatu wa kidini kama hao maishani mwangu.” Kisha nikasema,“Nisaidie kujua maana ya haya yote.”

Na asubuhi iliyofuata nilishuka nikaenda kule.Tulikaribishwa kifunguakinywa. Bila shaka, singekuja kulapamoja nao, kwa sababu sikuwa na kitu cha kutolea sadaka.

Page 29: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

HADITHI YA MAISHA YANGU 29

Nilirudi tu. Na asubuhi iliyofuata nilipoingia, mbona (nimekulasambusa zangu), basi nikakaa chini. Na mmoja wao alikuwakwenye maikrofoni. Nami sijawahi kuona maikrofoni hapokabla, na niliogopa kitu hicho. Kwa hiyo wao…Na ilikuwana kamba ndogo inayoning’inia hapa juu, nayo ikining’iniachini. Moja ya hizo maikrofoni za kushusha, namna hiyo. Nayeakasema, “Usiku uliopita, kwenye jukwaa, palikuwa na mhubirikijana hapa, Mbatisti.”

Nikawaza, “Salala, watanipa kazi kubwa sasa.”Naye alisema, “Yeye alikuwa mhubiri mdogo kuliko wote

kwenye jukwaa. Jina lake lilikuwa Branham. Kuna mtu yeyote anayejua aliko? Mwambie aje, tunamtaka alete ujumbe waasubuhi.”

Loo, jamani! Nilikuwa nimevaa T-shati, suruali ya pambayenye milia, unajua. Nasi Wabatisti tunaamini yakubidi uvaesuti, upate kwendamimbarani, unajua. Kwa hiyo…Basi mimi—mimi nilikaa kimya kabisa. Na wakati huo…Waliufanyia hukoKaskazini wakati huo sababu (mkutano wao wa kimataifa)watu weusi hawangeuhudhuria kama ulifanyiwa huko Kusini.Walikuwa na watu weusi pale, nami nilikuwa wa Kusini,nilikuwa na kiburi bado, unaona, nilifikiri nilikuwa bora kulikomtu mwingine. Na ilitokea kuwa asubuhi ile, papo hapo karibunami aliketi m—mtu mweusi. Kwa hiyo niliketi nikamwangalia.Nikawaza, “Vema, yeye ni ndugu.”

Naye akasema, “Kuna ye yote anayejua aliko WilliamBranham?” Nikainama chini kitini namna hii. Kwa hiyoakasema, akalitangaza mara ya pili, kasema, “Kuna mtu hukonje” (akavuta ndani hii mikrofoni ndogo) “ajuaye alipo WilliamBranham? Mwambie tunamtaka aje jukwaani atoe ujumbe waasubuhi. Yeye ni mhubiri wa Kibatisti kutoka Indiana yakusini.”

Nilikaa kimya kabisa na kuinama chini, unajua. Hakunamtualiyenijua, kwa vyo vyote. Yule mvulana mweusi akaniangalia,akasema, “Je, wewe unajua aliko?”

Nikawaza. Mimi—mimi aidha itanilazimu kudanganya aukufanya jambo fulani. Kwahiyo nikasema, “Inama hapa chini.”

Akasema, “Ati nini, bwana?”Nikasema, “Nataka kukuambia jambo fulani.” Nikasema,

“Mimi—mimi ndiye.”Akasema, “Vema, nenda juu kule.”Ndipo nikasema, “La, siwezi. Unaona,” nikasema, nimevaa

suruali hii ndogo kuukuu ya pamba yenye milia na T-shati hiindogo.” Nikasema, “Singeweza kwenda juu kule.”

Akasema, “Hao watu hawajali jinsi unavyovalia. Nendakule juu.”

Page 30: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

30 NDUGU BRANHAM

Nikasema, “La, la.” Nikasema, “Nyamaza kimya, usisemekitu sasa.”

Nao wakaja tena kwenye maikrofoni baada ya kitambokidogo, kasema, “Kunamtu anayejua alikoWilliamBranham?”

Akasema, “Huyu hapa! Huyu hapa! Huyu hapa!” Loo,jamani! Hapo nilisimama huku nimevaa ile T-shati ndogo,unajua. Na hapa mimi…

Akasema, “Njoo huku juu, Bw. Branham, tunakutaka uleteujumbe.” Loo, jamani, mbele ya hao wahubiri wote, lo, watuhao wote! Basi nikaenda haraka, unajua. Uso wangu umeiva,na masikio yangu yakiwasha. Basi nikaenda haraka kule juu,suruali ya pamba yenye milia, na T-shati, mhubiri, mhubiri waKibatisti akienda kwenye maikrofoni, hajaona moja hapo awali,unaona.

Nami nikasimama juu kule, nikasema, “Vema, si—si—sijuijambo hili.” Nilikuwa nikihangaika, wasiwasi kweli, unajua.Ba—basi nikafungua hapa katika Luka 16, nami nikawaza,“Vema, sasa…” Ndipo ni—nikapata somo, Basi akayainuamacho yake kuzimuni, ndipo akalia. Nikapata…Kwa hiyo ni—nikaanza kuhubiri, unajua, basi nilipoanza kuhubiri nikajisikiaafadhali kidogo. Nami nikasema, “Yule tajiri alikuwa kuzimuni,basi akalia.” Hayo maneno madogo matatu, kama nilivyo namahubiri mengi kama hayo, “Wewe Unaamini Hili,” na “Nenana Mwamba,” mmenisikia mimi nikiyahubiri. Nami nilikuwana, “Ndipo akalia.” Nami nikasema, “Hakuna watoto kule,hakika siyo huko kuzimuni. Basi akalia.” Nikasema, “Hakunamaua kule. Basi akalia. Hakuna Mungu kule. Ndipo yeye akalia.Hakuna Kristo kule. Ndipo akalia.” Ndipo nami nikalia. Kitufulani kilinishika. Jamani! Loo, jamani! Baada ya hapo, sijuiilitokea nini. Basi nilipopata kujirudia, nilikuwa nimesimamakule nje. Hao watu walipiga yowe na kupaza sauti na kulia,pamoja nami, tulikuwa nawakati wa ajabu sana.

Nilipotoka nje alitokea mtu aliyenijia huku amevaa kofiakubwa ya Texas, buti kubwa, akanijia, kasema, “Mimi ni Mzeefulani wa fulani.” Mhubiri, buti za cowboy, amevaa nguo zacowboy.

Nikawaza, “Vema, suruali yangu ya pamba yenye milia siyombaya basi.”

Kasema, “Nataka wewe uje huko chini Texas ukanifanyizieufufuo.”

“Enhee, hebu niandike hilo, bwana.” Nami nikaliandikanamna hiyo.

Hapa akajamtu akiwa amevaamoja ya namna ya hizi surualindogo za mpira wa gofu, hapo walipozoea kucheza gofu, unajua,walikuwa wanavaa suruali ndogo fupi. Akasema, “Mimi ni Mzeefulani wa fulani kutokaMiami. Nakutakawewe…”

Page 31: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

HADITHI YA MAISHA YANGU 31

Nikafikiri, “Jamani, pengine mavazi si jambo kubwa.”Nikalingalia, na nikawaza, “Sawa.”

Kwa hiyo nikanyakua vitu hivi, na huyoo nikaenda zangunyumbani. Mke wangu akanilaki, kasema, “Mbona unaonekanakuwa na furaha namna hiyo, Billy?”

Nikasema, “Loo, nimekutana na kundi halisi. Jamani, ndilozuri kuliko yote uliyowahi kuona. Hao watu hawaionei aibudini yao.” Na, loo, nikamwambia yote kuhusu jambo hilo. Naminikasema, “Tazama hapa, mpenzi, ratiba nzima ya makaribisho.Hao watu!”

Kasema, “Hao siowatakatifuwanaojifingirisha, sivyo?”Nikasema, “Sijui wao ni wafingirikaji wa aina gani, bali

wanacho kitu nilichohitaji.” Unaona? Nikasema, “Hilo—hilo nijambo moja ninalojua yakini.” Nikasema, “Nilimwona mzeemmoja, umri wa miaka tisini, akiwa kijana tena.” Nikasema,“Sijasikia mahubiri ya namna hiyo maishani mwangu. Mbona,sijawahi kumwona Mbatisti akihubiri namna hiyo.” Nikasema,“Wanahubiri mpaka wanakosa pumzi, na hukunja magotiwakainama mpaka sakafuni, wakainuka, wakapata pumzitena. Unaweza kuwasikia umbali wa majengo mawili, badowanahubiri.” Kisha nikasema, “Si—Sijawahi kusikia jambo lanamna hiyo maishani mwangu.” Basi nikasema, “Wananenakwa lugha isiyojulikana, na yule mwingine anafasiri. Kamwesijawahi kusikia jambo la namna hiyo maishani mwangu!”Nikasema, “Utaenda pamoja nami?”

Akasema, “Mpenzi, uliponioa, nitaambatana nawempaka kifo kitakapotutenganisha.” Akasema, “Nitakwenda.”Akasema, “Sasa, tutawaambia jamaa zetu.”

Basi nikasema, “Sawa, wewe mwambie mama yakonami nitamwambia mama yangu.” Kwa hiyo tu…Nikaendanikamwambia mama.

Mama akasema, “Naam, bila shaka, Billy. Lo lote Bwanaalilokuitia kufanya, nenda kafanye.”

Na kwa hiyo Bibi Brumbach akaniomba niende kwake.Nikaenda. Kasema, “Ni kitu gani hiki unachokizungumzia?”

Basi nikasema, “Loo, Bibi Brumbach,” nikasema, “lakinininyi nyote hamjaona watu kama hao.”

Akasema, “Tulia! Tulia!”Nikasema, “Ndiyo, mama.”Nikasema “Nasikitika!”Naye akasema, “Unajua hilo ni kundi la watakatifu

wanaojifingirisha?”Nikasema, “La, mama, mimi sikujua jambo hilo.” Nikasema,

“Wao—wao hakika ni watu wazuri.”Akasema, “Hata wazo lenyewe! Unadhani unaweza

kumkokota binti yangu umpeleke katika upuzi huo!” Kasema,

Page 32: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

32 NDUGU BRANHAM

“Dhihaka hii! Hilo si cho chote bali takataka ambazo makanisamengine yametupa nje.” Akasema, “Kweli! hutampeleka bintiyangu mahali kama hapo.”

Basi nikasema, “Lakini, unajua, Bibi Brumbach, kwenyekilindi cha moyo wangu naona kwamba Bwana ananitakanifuatane na hao watu.”

Akasema, “Rudi kanisani kwako mpaka watakapowezakukupatia nyumba ya kasisi, ukaishi kamamtu aliye na busara.”Kasema, “Hutamchukua binti yangu nje umpeleke kwenyemambo hayo.”

Nikasema, “Ndiyomama.”Nikageuka nikaondoka.Ndipo Hope akaanza kulia. Akatoka nje, akasema, “Billy,

hata mama aseme nini, nitaambatana nawe.” Ubarikiwemoyo wake.

Basi nikasema, “Loo, hilo ni sawa, mpenzi.”Basi nikaliachilia. Asingelimruhusu bintiye aende na watu

kama hao sababu “Haikuwa kitu ila takataka.” Na kwahiyo kwa namna fulani nikaliachilia. Lilikuwa ni kosa bayazaidi nililowahi kufanya maishani mwangu, moja ya yaliyomabaya sana.

Baadaye kidogo, miaka michache baadaye, watoto wakaja.Na siku moja tulikuwa…Yakatokea mafuriko ya maji,mwaka 1937. Yakatokea mafuriko. Na ninino yetu…Nilikuwakwenye doria wakati ule na nilikuwa ninajaribu kwa uwezowangu wote kuwaokoa watu kutoka kwenye mafuriko yale,nyumba zikivunjwa-vunjwa na kuanguka. Na mke wangumimi akashikwa na ugonjwa, naye alikuwa mahututi sanakwa numonia. Nao wakamtoa…Hospitali ya kawaida yenyeweilijaa sana kiasi kwamba hatukuweza kumweka mle, kwa hiyotulimpeleka kwa—kwa ya serikali ambako walikuwa na chumbahuko. Ndipo waliniita nirudi. Na siku zote niliishi mtoni,nikiwa nahodha halisi wa boti, kwa hiyo nilikuwa ninajaribukuwachukua watu, kuwaokoa na yale mafuriko. Na halafuninge…mmoja…

Wakaniita, kasema, “Kuna nyumba huko kwenye Barabaraya Chestnut, nusura izame. Kuna mama na watoto kadhamle,” kasema, “kama unafikiri boti yako, mota yako inawezakuwafikia.” Nikasema, “Vema nitafanya yote niwezayo.”

Nami, nikiabiri kasi kwenye mawimbi yale. Boma lakuzuia maji lilikwisha bomoka juu kule, na, loo, jamani,ile…yakibubujikia mjini. Nami ningejitahidi niwezavyo, nahatimaye kule chini kuvuka vichochoro vyamji na kupitamahalimbalimbali. Nami nikafika pale karibu na mahali ambapopalikuwa na ukuta wa boma la kale, maji yakibubujikia mle.Ndipo nikasikia mtu akipiga mayowe, kisha nikamwona mamafulani amesimama nje barazani. Na kulikuwa na mawimbi

Page 33: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

HADITHI YA MAISHA YANGU 33

makubwa yakipita hivyo. Naam, nilikwenda juu upande huu,kadiri nilivyoweza, nikakumbana na mkondo wa maji nikarudihata upande ule. Nilikuwa nimesimamisha boti yangu nikiwanimewahi tu kuifungia kwenye nguzo, nguzo ya mlango, nguzo,au nguzo ya baraza. Basi nikaingia ndani mbio nikamnyakuayule mama na kumwingiza mle, na watoto wawili au watatu.Ndipo nikaifungua boti yangu na nikaipeleka hadi…kurudi.Nikaenda hata kule chini kabisa, nikampeleka hadi ufukoni,yapata maili moja na nusu kuvuka mji, mpaka nikamfikishaufukoni. Ndipo nilipofika kule, alikuwa amekwisha zirai. Naalikuwa ameanza…alikuwa anapiga mayowe, “Mwanangu!Mwanangu!”

Naam, nikafikiri kwamba alimaanisha ameacha mtotoyule kule nyumbani. Loo, jamani! Nikarudi tena wakatiwalipokuwa wanamwangalia. Na, nikagundua, ilikuwa…aualikuwa akitaka kujua iwapo mtoto wake alikuweko. Kulikuwana jamaa mdogo wa kama miaka mitatu, nami nilifikiriaalimaanishamtotomchanga anayenyonya au kitu fulani.

Na kwa hiyo nikarudi nikafika kule. Na niliposhuka kwenyeboti ile nikaingia mle ndani na sikuweza kuona mtoto ye yotemchanga, ndipo ile baraza ikavunjika na nyumba ikazama. Basinilikimbia mbio, nikakamata kile—kile kipande pale ambachokilikuwa kinaelesha motaboti yangu, nikaingia katika ile botinikakivuta hicho na kuifungulia.

Basi ikanipeleka kwenye mkondo wa mto mkubwa. Nailikuwa kama saa tano u nusu za usiku, huku inanyeshamvua ya theluji. Nami nikashika kamba ya kuipiga stati nanikajaribu kuvuta ile mashua, nayo haikuwaka, nikajaribu tenana haikuwaka, nikajaribu tena. Nikaenda mbali zaidi kwenyemkondo ule, nimekaribia sana yalemaporomoko. Nami nilikuwanikijaribu kwa nguvu sana, na nikawaza, “Loo, jamani, huu—huu ndio mwisho wangu! Ndio huu hapa!” Nami ningejaribukwa nguvu sana. Ndipo nikasema, “Bwana, tafadhali usiniachenife kifo kama hiki,” nami ningevuta na kuvuta.

Basi likanijia tena, “Vipi kuhusu kundi lile la takatakaambalo usingeliendea?” Unaona? Enhee.

Nikarudisha mkono wangu kuuweka kwenye mashua, nanikasema, “Mungu, nirehemu mimi. Usiniache niwaache mkewangu na mtoto mchanga namna hii, nao wako nje huko wakiwawagonjwa! Tafadhali!” Nami nikaendelea tu kuvuta namnahiyo, nayo haikuwaka. Nami niliweza kusikia ile ngurumochini kule, sababu mimi…Dakika chache tu, na, loo, jamani,huo ungekuwa ndio mwisho. Basi nikasema, “Bwana, iwapoWewe utanisamehe, ninakuahidi Wewe nitafanya jambo lo lote.”Nikapiga magoti ndani ya mashua ile huku mvua ya thelujiikinipiga usoni, nikasema, “Nitafanya jambo lo lote ambaloWewe unataka mimi nifanye.” Ndipo nikavuta tena, na ikawaka.

Page 34: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

34 NDUGU BRANHAM

Basi nikafungulia petroli yote niliyoweza, na hatimaye nikafikaufukoni.

Nami nikarudi kutafuta lori, lori la doria. Ndipo nikawazakuhusu…Kulikuwa na baadhi yao waliosema, “Aisee, ilehospitali ya serikali imechukuliwa na mji hivi punde.” Mkewangu na mtoto mchanga wakiweko mle ndani, watoto wotewawili.

Basi nikaendambio kwenye ile ya serikali upesi nilivyoweza,na maji yalikuwa yamefikia kina cha yapata futi kumi na tanokila mahali. Na palikuwa nameja pale, na nikasema, “Meja, ninikimeikumba hospitali?”

Kasema, “Sasa, usiwe na wasiwasi. Ulikuwa na mtu ye yotemle ndani?”

Nikasema, “Ndiyo,mkem—mgonjwa nawatotowawili.”Akasema, “Wote walitoka.” Kasema, “Wako kwenye gari la

mizigo na wameelekea Charlestown.”Nikakimbia, nikaigia katika mashua yangu na…au

nikaingia katika motokaa yangu, na mashua yangu nyumayake, nikakimbilia kule ku…Ndipo basi ghuba zilikwishapungua zikawa na upana wa maili mbili na nusu au tatu. Nausiku kucha nilijaribu ku…Baadhi yao walisema, “Gari, garilamizigo, lilichukuliwa namaji huko kwenye daraja.”

Naam, nikajikuta nimeachwa peke yangu kwenye kisiwakidogo, nikakaa pale siku tatu. Nilikuwa na muda wakutosha kufikiria kama kundi Hilo lilikuwa ni takataka au la.Nikipigapiga tu, “Mke wangu yuko wapi?”

Hatimaye nilipompata, mnamo siku chache baada ya kutokakule na kuvuka, alikuwa huko mbali Columbus, Indiana, katikaJumba la Mikutano la Kibatisti ambako wamefanya na—namnaya hospitali, vyumba vya wagonjwa kwa machela madogoya serikali. Basi nikamkimbia mbio nilivyoweza, nikijaribukutafuta mahali alipokuwa, nikipiga mayowe, “Hope! Hope!Hope!” Ndipo niliangalia, huyo hapo amelala kwenye machela,pia ameugua kifua kikuu.

Akainua maskini mkono wake uliokonda sana akasema,“Billy.”

Na nikamkimbilia, nikasema, “Hope, mpenzi.”Akasema, “Ninaonekanambaya sana, sivyo?”Nikasema, “La, mpenzi, huonekani mbaya.”Kwa yapatamiezi sita tulifanya kazi kwa bidii sana, kujaribu

kuyaokoamaisha yake, lakini aliendelea kudhoofika.Sikumoja nilikuwa kwenye doria na nilikuwa nimeifungulia

redio yangu, nami nilifikiria nilisikia wakisema, wakiitakwenye redio, kasema, “Kwa William Branham, unatakiwahospitalini mara moja, mkeo yuafa.” Nikarudi hospitalini

Page 35: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

HADITHI YA MAISHA YANGU 35

haraka nilivyoweza, nikawasha kimulimuli na kupiga king’oranikaondoka. Ndipo ni—nikafika hospitali nikasimama,nikaingia ndani haraka. Nikashuka nikaenda ho—hospitalini,nikamwona maskini rafiki yangu ambaye tulivua samakipamoja, tulicheza pamoja kamawavulana, SamAdair.

Daktari Sam Adair, yeye ndiye ambaye lile ono lilikuja kwaajili yake si muda mrefu uliopita na kumwambia kuhusu ilehospitali. Naye alisema, kama mtu ye yote alitilia shaka lileono, hebu ampigie simu bila malipo kama wanataka kujua kamailikuwa kweli au la.

Na kwa hiyo basi huyu hapa anakuja hivi, naye alikuwaameshika kofia mkononi. Aliniangalia akaanza tu kulia.Na nikamkimbilia, nikamkumbatia. Akanikumbatia, akasema,“Billy, anaaga dunia.” Akasema, “Ninasikitika. Nimetendayote nilivyoweza kutenda, nimemletea wataalam maalum nakila kitu.”

Nikasema, “Sam, hakika haagi dunia!”Kasema, “Ndiyo, anaaga dunia.”Ndipo akasema, “Usiingie mle ndani, Bill.”Nami nikasema, “Yanibidi niingie, Sam.”Basi akasema, “Usifanye hivyo. Usiingie, tafadhali usifanye

hivyo.”Nikasema, “Tafadhali niruhusu niingie.”Kasema, “Nitaenda pamoja nawe.”Nikasema, “La, wewe kaa hapa nje. Nataka kukaa pamoja

naye katika dakika zake za mwisho.”Kasema, “Amezirai.”Nikaondoka nikaingia mle chumbani. Naye mwuguzi

alikuwa ameketi pale, naye alikuwa analia sababu yeye na Hopewalikuwa wakisoma pamoja. Na kwa hiyo nikamtazama, nayeakaanza kulia, akainuamkonowake akaanza kuondoka.

Basi nikamtazama, kisha nikamtikisa. Huyo hapo, alikwishapungua toka kama ratili mia moja na ishirini, hadi yapata sitini.Nami ni—nikamtikisa. Na kama nitaishi nifikie umri wa miakamia, sitasahau kilichotukia. Aligeuka, na yale macho makubwamno na mazuri yakanitazama. Akatabasamu. Akasema, “Kwanini uliniita nirudi, Billy?”

Nikasema, “Mpenzi, hivi punde nimepata…fedhatasilimu.”

Ilinibidi kufanya kazi. Tulikuwa na deni kubwa sana namamia ya dola za bili ya daktari, na hatuna kitu cha kulipia.Nami ilinibidi tu kufanya kazi. Nami nilienda kumtazama marambili au tatu kwa siku, na kila usiku, na hapo alipokuwa katikahali ile.

Page 36: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

36 NDUGU BRANHAM

Nikasema, “Unamaanisha nini, ‘Kukuita’ ‘urudi’?”

Akasema, “Bill, umehubiri kuhusu Huko, umezungumziahabari Zake, bali huwezi kuwazia jinsi kulivyo.”

Nikasema, “Unazungumzia kuhusu nini?”

Akasema, “Mbinguni.” Akasema, “Angalia,” akasema,“nilikuwa ninasindikizwa Nyumbani na watu fulani, wanaumeau wanawake au wo wote wale ambao walivaa nguo nyeupe.”Ndipo akasema, “Nilikuwa nimestarehe na mweye amani.”Kasema, “Ndege wakubwa wazuri wakiruka toka mti hadimti.” Akasema, “Usidhani nimerukwa na akili.” Akasema,“Billy, nitakuambia kosa letu.” Akasema, “Keti chini.” Sikuketi;nilipigamagoti, nikashikamkonowake, Akasema, “Unajua kosaletu liko wapi?”

Nami nikasema, “Ndiyo, mpenzi, ninajua.”

Akasema, “Laiti tusingalimsikiliza Mamangu. Hao watuwalikuwa sahihi.”

Na nikasema, “Ninajua jambo hilo.”

Akasema, “Niahidi hili, kwamba utakwenda kwa watuhao,” kasema, “kwa sababu wako sahihi.” Naye akasema,“Walee watoto wangu namna hiyo.” Nami…Akasema, “Natakakukwambia jambo fulani.” Akasema, “Ninakufa, bali” kasema“ni…si—siogopi kwenda.” Kasema, “Ni—ni kuzuri.” Akasema,“Ila tu, nachukia kukuacha, Bill. Nami najua una watoto hawawawili wachanga wa kulea.” Akasema, “Niahidi kwamba—kwamba hutakaa bila mke na kuwaacha watoto wanguwachukuliwe huku na huko.” Hilo lilikuwa jambo la busara kwamama wa miaka ishirini na mmoja.

Nami nikasema, “Siwezi kuahidi hilo, Hope.”

Akasema, “Tafadhali niahidi.”Kasema, “Nataka kukuambiajambo moja.” Kasema, “Unakumbuka ile bunduki aina yaraifo?” Ninapenda bunduki sana. Basi akasema, “Ulitakakununua raifoo ile siku ile nawe hukuwa na fedha za kutoshakwa malipo ya kwanza.”

Nikasema, “Ndiyo.”

Akasema, “Nimekuwa nikiweka fedha yangu, hela zangu,kujaribu kutoa malipo ya kwanza ya raifoo ile kwa ajiliyako.” Akasema, “Sasa, haya yatakapomalizika nawe urudinyumbani, angalia kwenye kile kitanda cha kukunja…aukitanda cha kukunja, chini ya kipande kile cha karatasi hukojuu, nawe utazipata hizo fedha humo.” Akasema, “Niahidikwamba utanunua raifoo ile.”

Hujui jinsi nilivyojihisi wakati nilipoona ile dola na sentisabini na tano (katika hela) zimewekwa mle. Nikanunua ilebunduki.

Page 37: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

HADITHI YA MAISHA YANGU 37

Naye akasema, “Unakumbuka hapo ulipokuwa ukishukakwenda mjini kuninunulia jozi ya soksi ndefu, nasi tulikuwatunakwenda Fort Wayne?”

Nikasema, “Ndiyo.”Nilikuwa nimerudi toka kuvua samaki, naye akasema…

Ilitubidi kwenda Fort Wayne, ilinipasa kuhubiri usiku ule. Nayeakasema, “Unajua, nilikwambia, ‘Kuna aina mbili tofauti.’”Moja iitwayo “chiffon.” Na ile nyingine ni nini, rayon? Hiloni sawa? Rayon na chiffon. Vema, lo lote lile, chiffon ndiyoiliyokuwa nzuri kuliko zote. Sivyo? Ndipo akasema, “Sasa, hebuninunulie chiffon, mtindo kamili.” Unajua kitu kile ambachokina kitu kidogo nyuma ya soksi sehemu ndefu, juu? Namisikujua kitu kuhusu nguo zawanawake, kwa hiyo ni…

Nami nilienda barabarani nikisema, “Chiffon, chiffon,chiffon, chiffon, chiffon,” huku nikijaribu nisije nikasahau, hukunasema, “chiffon, chiffon, chiffon.

Mtu fulani akasema, “Habari zako, Billy!”Nikasema, “Loo, sijambo, sijambo.” “Chiffon, chiffon,

chiffon, chiffon, chiffon.”Basi nikafika pembeni nikakutana na Bw. Spon. Akasema,

“Habari zako, Billy, unajua sangara wanadonoa sasa upande ulewa gati?”

Nikasema, “Bila shaka, hilo ni kweli?”“Ndiyo.”Nikawaza sasa, nilipomwacha, “Kitu kile kilikuwa ni nini?”

Nimekisahau.Kwa hiyo Thelma Ford, msichana niliyemjua, alifanya kazi

kwenye duka la rejareja. Basi nilijua waliuza soksi ndefu zawanawake pale, kwa hiyo nilikwenda huko. Nikasema, “Habarizako, Thelma.”

Akasema, “Njema, Billy. U hali gani? Habari zaHope?”Basi nikasema, “Mzima.” Nikasema, “Thelma, nataka jozi ya

soksi kwa ajili ya Hope.”Akasema, “Hope hahitaji soksi.”Nikasema, “Ndiyo, mama, hakika anazihitaji.” Kasema,

“Unamaanisha soksi ndefu.”“Loo, hakika,” nikasema, “ndizo hizo.” Nikawaza, “Lo-ehee,

nilikwisha onyesha ujinga wangu.”Naye akasema, “Anataka za aina gani?”Nikawaza, “Lo-enhee!” Nikasema “Unazo za aina gani?”

Akasema, “Naam, tuna rayon.”Sikujua tofauti. Rayon, chiffon, yote inasikika sawa.

Nikasema, “Nataka hiyo.” Akasema…Nikasema, “Nifungiejozi yake, staili kamili.” Na yeye…Nilikosea hilo. Ni nini?

Page 38: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

38 NDUGU BRANHAM

Mtindo kamili. “Mtindo kamili.” Na kwa hiyo nilisema,“Nifungie jozi ya hizo.”

Naye aliponipa, zilikuwa kama senti thelathini tu, sentiishirini au senti thelathini, kama nusu ya bei. Vema, nikasema,“Nipe jozi mbili.” Unaona?

Nami nikarudi nyumbani, na nikasema, “Unajua, mpenzi,ninyi wanawake mnazunguka mji mzima kubishana bei yabidhaa.” Unajua jinsi unavyopenda kuwika. Ndipo nikasema,“Lakini hapa, angalia hapa, nimenunua jozi mbili kwabei ambayo mnanunulia jozi moja. Unaona?” Nikasema,“Loo, huo—huo ni uwezo wangu binafsi.” Unaona, nikasema—nikasema, “Unajua, Thelma, aliniuzia hizi.” Nikasema, “Pengineameniachia nizichukue kwa nusu ya bei yake.”

Akasema, “Ulipata chiffon?”Nikasema, “Ndiyo, mama.” Yote yanasikika ni mamoja

kwangu, sikujua kulikuwa na tofauti yo yote.Basi akaniambia, akasema, “Billy.” Nilishangaa wakati

alipofika FortWayne, ilibidi anunue jozi nyingine ya soksi ndefu.Alisema, “Nilimpa mama yako hizo,” kasema, “ni za wanawakewazee.” Kasema, “Ninasikitika nilitenda jambo hilo.”

Ndipo nikasema, “Hilo ni sawa, mpenzi.”Naye akasema, “Sasa, usi—usiishi peke yako.” Naye

akasema…Hakujua ambacho kingetukia katika masaamachache tokea hapo. Nami nikashika mikono yake mizuriwakati Malaika waMungu walipomchukua.

Nikaenda zangu nyumbani. Sikujua la kufanya. Nililalachini pale usiku kisha nikasikia…Nafikiri ilikuwa panyamdogo, alikuwa katika nondo za lile jiko kuukuu ambamotuliweka makaratasi. Basi nikafunga mlango kwa mguu wangu,na hapo palining’inia nguo yake ya kimondo hapo nyuma, (nayeamelala chini kule kwenye kile chumba cha maiti). Na mudakidogo tu mtu fulani akaniita, kasema “Billy!” Na ilikuwa niNdugu FrankBroy. Akasema, “Mtotowakomchanga yuafa.”

Nikasema, “Mtoto wangumchanga?”Kasema, “Ndiyo, Sharon Rose.” Kasema, “Dakt yuko

juu’Anae sasa, kisha akasema, ‘Ana homa ya uti wa mgongo,aliambukizwa namama yake.’” Kisha akasema, “Anakufa.”

Nikaingia kwenye gari, nikapanda kwenda kule. Huyo hapo,kitoto kipenzi. Nao wakamkimbiza hospitalini.

Nikaenda kumuona. Sam akaja akasema, “Billy, usiingie mlechumbani, yakubidi umfikirie Billy Paul.”Kasema, “Anakufa.”

Nikasema “Dakt, ya—yanipasa kumwona mtoto wangumchanga.”

Akasema, “La, huwezi kuingia.” Kasema, “Ana homa ya utiwamgongo, Billy, nawe ungemwambukiza Billy Paul.”

Page 39: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

HADITHI YA MAISHA YANGU 39

Basi nikangojea mpaka alipotoka nje. Sikuweza kuvumiliakumwona akifa, na mama yake amelala chini kule kwenyechumba cha maiti. Nakwambia, njia ya mkosefu ni ngumu. Basini—nikaenda, nikapenyeza mlangoni, basi Sam alipotoka njepamoja namwuguzi, nilienda kwenye orofa ya chini. Ni hospitalindogo. Alikuwa mahali palipotengwa, na inzi walikuwa kwenyemacho yake. Nao walikuwa na ninino ndogo…tunayoita“kizuizi cha mbu,” au chandalua kidogo kwenye macho yake.Naye angeninino…na mshtuko mdogo, mguu wake mdogomnene ulikuwa unasogea juu na chini namna hiyo, na mikonoyake midogo, na mshtuko ule. Nami nikamwangalia, na yeyealikuwa mkubwa vya kutosha kuwa mrembo, kama umri wamiezi minane.

Na mama yake alizoea kumweka nje kule na gari lakelenye magurudumu matatu, wajua, uwanjani, nilipokuwa nikija.Na ningepiga honi, naye angefanya, guu—guu, guu—guu,akininyoshea mikono, unajua.

Na hapo alilala mpenzi wangu, anakufa. Nikamtazama palechini, nami nikasema, “Sharry, unamjua Baba? Unamjua BabaSharry?” Naye alipotazama…Alikuwa anateseka sana mpakamoja la hayo macho madogo ya samawati lilikengeza. Karibujambo hilo linivunje moyo kabisa.

Nikapiga magoti, nikasema, “Bwana, nimefanya nini?Sikuhubiri Injili kwenye kila sehemu mitaani, na kufanya kilanijuacho kufanya? Usinipatilize kwa jambo hilo. Sikuwaitakamwe hao watu ‘takataka.’” Bibi huyo ndiye aliyewaita haowatu ‘takataka.’” Nikasema, “Ninasikitika yote hayo yalitukia.Nisamehe. Usi—usimchukue mwanangu.” Na wakati nilikuwaninaomba, ilionekana kama kitu cheusi…kama shuka au nguoilitelemka. Nilijua Yeye amenikatalia.

Sasa, huo ulikuwa ndio wakati mgumu zaidi na wa wahatari sana maishani mwangu. Nilipoinuka na kumtazama, basinikawaza…Shetani akaninong’onezea, “Vema, wataka kusemajinsi ulivyohubiri kwa bidii, na jinsi ulivyoishi, na sasa inapofikakwamtotowako binafsi aliyemchanga, Yeye atakukatalia?”

Ndipo nikasema, “Hilo ni kweli. Kama Yeye hawezikumwokoa mtoto wangu mchanga, basi siwezi…”Nikanyamaza. Si—sikujua tu la kufanya. Halafu basi nikasemahivi, nikasema, “Bwana, Wewe ulinipa huyu na Weweumemchukua, na libarikiwe Jina la Bwana! Hata kamautanichukuamimi, bado nitakupendaWewe.”

Ndipo nikaweka mkono wangu juu yake, nikasema,“Ubarikiwe, kipenzi cha moyo. Baba alitaka kukulea, kwamoyo wangu wote nilitaka kukulea, na kukulea ukampendeBwana. Lakini Malaika wanakuja kukuchukua, kipenzi chamoyo. Baba atachukua mwili wako mdogo aupeleke kule chiniakauweke mikononi mwa Mama. Nitakuzika pamoja naye. Na

Page 40: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

40 NDUGU BRANHAM

siku moja Baba atakutana nawe, basi ngojea tu juu kule pamojana Mama.”

Mama yake alipokuwa anakufa, alisema, maneno ya mwishoaliyosema, alisema, “Bill, usiache kuhubiri.”

Nikasema, “Nita…” Akasema…nikasema, “Kamanitakuwa ninahubiri wakati Yeye ajapo, nitawachukua watototukamlaki. Kama sitafanya hivyo, nitazikwa karibu na wewe.Nawe nenda upande wa kuume wa lile lango kuu, na hapoutakapowaona wote wakiingia, simama pale uanze kupigakelele, ‘Bill! Bill! Bill! kwa nguvu uwezavyo. Nitakutana nawekule.” Nikambusu kwa heri. Niko kwenye uwanja wa vita leo.Hiyo imekuwa karibu miaka ishirini iliyopita. Nimepeana miadina mke wangu, nitakutana naye.

Basi nikamchukua yule mtoto mchanga, na alipokufa,nikamweka kwenye mikono ya mama yake, nasi tukamchukuakwenye makaburi. Ndipo nilisimama pale kumsikia NduguSmith, mhubiri wa Kimethodisti ambaye aliongoza ibada yamazishi. “Majivu kwa majivu, na mavumbi kwa mavumbi.”(Nami nikawaza, “Moyo kwamoyo.”) Huyo akaenda.

Si muda mrefu baada ya jambo hilo, nilienda huko na Billyasubuhi moja alipokuwa mchanga, yeye alikuwa mtoto mdogotu. Alikuwa…

Hiyo ndiyo sababu haniachi nami simwachi, ilibidiniwe vyote viwili Baba na Mama (wote wawili) kwake.Ningeichukua chupa yake ndogo. Hatukumudu kuwa na motousiku kuchemsha maziwa, yake, na ningeiweka chini ya mgongowangu namna hii na kuyapashamoto kwa joto lamwili wangu.

Tumeshikana pamoja kama marafiki wazuri sana, na sikumoja nikiondoka uwanjani nataka kumkabithiNeno, na kusema,“Endelea, Billy. Kaa Nalo.” Baadhi ya watu wanashangaa kwanini niko pamoja nayewakati wote. Siwezi kumwacha. Yeye hataameoa, lakini bado ninakumbuka aliloniambia, “Usimwache.”Na tumeshikana pamoja kamamarafiki wazuri sana.

Nakumbuka nikitembea mjini, chupa kwapani mwangu,angeanza kulia. Usiku mmoja alikuwa—alikuwa anatembea njeuwani ambako tu…(Wakati alipokuwa anajiandaa kumzaa,yeye alikuwa anasongwa moyo, nami…msichana tu, unajua.)Nami ningetembea huku na kule toka kwenye ule mwalonikwenye uwanja wa nyuma. Naye alikuwa anamlilia Mama yake,nami sina Mama wa kumpelekea. Basi ningembeba, ningesema,“Loo, mpenzi.” Nikasema…

Akasema, “Baba, mama yangu yuko wapi? Je, weweulimweka katika ardhi?”

Nikasema, “La, mpenzi. Yeye hana tatizo, yuko juuMbinguni.”

Page 41: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

HADITHI YA MAISHA YANGU 41

Naye akasema jambo fulani pale, nusura liniue alasirimoja. Alikuwa analia, ilikuwa karibu usiku, nami nilikuwanimembeba mgongoni mwangu namna hii, nikimbeba beganimwangu na kumpigapiga hivi. Naye akasema, “Baba, tafadhalinenda ukamchukueMama umlete hapa.”

Na nikasema, “Mpenzi, siwezi kumpataMama. Yesu…”Kasema, “Vema, mwambie Yesu aniletee mama yangu.

Namtaka.”Nami nikasema, “Vema, mpenzi, mimi…mimi na wewe

tutamwona siku moja.”Ndipo akanyamaza, akasema, “Baba!”Nami nikasema, “Ndiyo?”Kasema, “NimemwonaMama juu kule kwenyewingu lile.”Jamani, nusura’Nimemwonakawaza, “Jamani! ‘Nimemwona

mama juu kule kwenye wingu lile.’” Karibu nizimie.Nikamkumbatia jamaa mdogo huyo kwenye kifua changu hivi,na kuinamisha kichwa changu chini, nikaingia ndani.

Siku zikapita. Sikuweza kulisahau. Nikajaribu kufanyakazi. Singerudi nyumbani, haikuwa ni nyumbani tena. Naminilitaka kukaa. Hatukuwa na kitu ila tu fanicha ile kuukuuna iliyochakaa, lakini ilikuwa ni kitu ambacho mimi na yeyetulifurahia pamoja. Ilikuwa ni nyumbani.

Nami ninakumbuka siku moja nilikuwa ninafanya kazi yaserikali. Nilikuwa nimekwenda kutengeneza waya dogo kuukuuza umeme, zilikuwa zinaning’inia, ilikuwa asubuhi na mapema.Nami nikapanda hadi hapa zinapopitana. (Nami sikuwezakumsahau mtoto yule. Nilivumilia kumwona mke wangu akiagadunia, lakini yule mtoto mchanga akiaga dunia, kitoto kichangatu.) Nami nilikuwa juu pale, nilikuwa ninaimba, “Kwenye kilimachambali, palisimamaMsalaba ulioparuza.” Na zile waya ndogoza umeme zilishuka chini kwenye transfoma na kutoka katika(unajua) kwenye zile kubwa. Nami nilikuwa ninaning’iniakule juu yake. Na ikatukia kwamba nilitazama, huku jualinachomoza nyuma yangu.Na pale,mikono yangu imenyooshwahuku ishara ya Msalaba ule ka—kando ya kilima. Nikawaza,“Ndiyo, dhambi zangu ndizo zilizomweka Yeye pale.”

Nikasema, “Sharon, mpenzi, Baba yako anataka sanakukuona, mpenzi. Jinsi ningependa kukushika mikononimwangu tena, maskini kipenzi changu.” Nikachanganyikiwakabisa…Imepita majuma kadhaa. Nikavua mifuko yangu yamikono ya mpira. Kuna voti elfu mbili na mia tatu zinatiririkakaribu kabisa nami. Nikavua mifuko yangu ya mikono ya mpira.Nikasema, “Mungu, ninachukia kutenda jambo hili. Mimi nimwoga.” “Lakini, Sherry, Baba anakuja kukuona pamoja naMama mnamo dakika chache tu.” Nikaanza kuvua mifukoyangu, kuweka mkono wangu kwenye zile voti elfu mbili na mia

Page 42: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

42 NDUGU BRANHAM

tatu. Ingevunja…Mbona, hata usingekuwa na damu iliyobakiandani yako. Na kwa hiyo ni—ni—nikaanza kuvua ile mifuko,ndipo kitu fulani kikatukia. Nilipopata kujirudia, nilikuwanimekaa chini ardhini na mikono yangu juu namna hii, kwenyeuso wangu, nikilia. Ilikuwa neema yaMungu, la sivyo singekuwaninaendesha ibada ya kuponya hapa, nina hakika na jambo hilo.Ilikuwa ni Yeye akilinda kipawa Chake, si mimi.

Nikaanza kwenda nyumbani. Nikaacha, nikaweka vyombovyangu. Nikarudi, nikasema, “Ninakwenda nyumbani.”

Nikaanza kuzunguka nyumba, kisha nikachukua baruanyumbani, ilikuwa baridi kidogo, basi nikaingia ndani.Tulikuwa na chumba kimoja kidogo, nilikuwa ninalala kwenyekitanda kidogo pale, na ukungu ukija, na jiko hilo kuukuu.Nikachukua zile barua na nikazisoma, na jambo la kwanza palelilikuwa hela zake chache za akiba kwa ajili ya Krismasi, sentithemanini, “Bi Sharon Rose Branham.” Hilo hapo, limeruditena.

Nimekuwa mlinzi wa wanyama pori. Nikaunyosha mkonomle ndani nikachukua bunduki yangu, bastola, kutoka kwenyemfuko wake. Nikasema, “Bwana, si—siwezi kuendelea hivi tena,ni—ninakufa. Nina—ninateseka sana.” Nikafungua usalamawa bunduki, nikailenga kichwani, huku nimepiga magotipale kwenye kitanda kile katika chumba hicho chenye giza.Nikasema, “Baba yetu Uliye Mbinguni, Jina Lako litukuzwe.Ufalme Wako na uje, mapenzi Yako yatimizwe,” ndiponilipojaribu, nikafinya mtambo wa kufyatulia kwa nguvu kadirinilivyoweza, nikasema, “duniani kama huko Mbinguni. Utupeleomkate wetuwa kila siku.” Nayo haingefyatuka!

Basi nikawaza, “Ee Mungu, Wewe unanirarua vipande-vipande? Nimefanya nini? Hata hutaniruhusu nife.” Naminikaitupa bunduki ile chini, nayo ikafyatukia chumbani. Ndiponikasema, “Mungu, kwa nini nisife na kuachana na jambo hilo?Siwezi kuendelea mbele zaidi. Huna budi kunifanyia jambofulani.” Nami nikaanguka chini na kuanza kulia kwenye kitandachangu kidogo na kichafu cha kale pale.

Na lazima nilichukuliwa na usingizi. Sijui kama nilikuwanimelala au nini kilitukia.

Sikuzote nimetamani kwendaMagharibi. Sikuzote nimetakamoja ya hizo kofia. Baba yangu aliwafundisha farasi katika sikuza ujana wake, nami nilitaka moja ya hizo kofia. Na NduguDemos Shakarian alininunulia moja jana, ya kwanza niliyopatakuwa nayo (niliyowahi kuwa nayo) ya namna hiyo, moja ya hizokofia za magharibi.

Nami nikawaza ninashuka nikipitia mbugani,nikiimba wimbo ule, “Kuna gurudumu la gari la farasilililovunji’Linauzwa.” kwenye ranchi, ‘Linauzwa.’” Basinilipoendelea, nikaona gari kubwa la farasi lenye turubai, kama

Page 43: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

HADITHI YA MAISHA YANGU 43

gari la kale la mbugani, huku gurudumu lake limevunjika.Bila shaka, hiyo iliwakilisha familia yangu iliyovunjika. Naminilipokaribia, nikaangalia, na hapo palisimama m—msichanamdogo na mrembo sana, yapata umri wa miaka ishirini,nywele nyeupe zinazoning’inia chini na macho ya samawati,amevaa nguo nyeupe. Nikamwangalia, nikasema, “Hujambo?”Nikaendelea.

Akasema, “Sijambo, Baba.”Nami nikageuka nyuma, nikasema, “Ati Baba?” “Mbona,”

nikasema, “vipi, Binti, unaweza…ninawezaje kuwa baba yakona huku tuna umri mmoja?”

Akasema, “Baba, hujui kabisa uko wapi.”Ndipo nikasema, “Unamaana gani?”Akasema, “Hapa ni Mbinguni.” Kasema, “Duniani nilikuwa

mtoto wako Sharon.”“Mbona,” nikasema, “mpenzi, ulikuwa tumtotomchanga.”Kasema, “Baba, watoto wachanga si watoto wachanga

humu, wao hawapatikani na mauti. Hawazeeki wala kukuakamwe.”

Nami nikasema, “Vema, Sharon, mpenzi, u—u kijanamwanamke mrembo.”

Akasema, “Mama anakungojea.”Nikasema, “Wapi?”Akasema, “Huko juu kwenye nyumba yakompya.”Na nikasema, “Ati nyumba mpya?” Wabranham ni watu wa

kutangatanga, hawanamakao, wao tu…Basi nikasema, “Vema,sijawahi kuwa na nyumba, mpenzi.”

Akasema, “Lakini unayo moja huku juu, Baba.” Simaanishikuwa mtoto mchanga, lakini ni halisi sana tu kwangu. [NduguBranham analia—Mh.] Ninapoanza kufikiria jambo hilo, yoteyanarudi tena. Kasema, “Unayo moja huku, Baba.” Najuaninayo moja kule juu, siku moja nitaenda mle. Akasema, “Yukowapi Billy Paul, ndugu yangu?”

Nami nikasema, “Naam, nimemwacha kwaBibi Broy, dakikachache tu zilizopita.”

Kasema, “Mama anataka kukuona.”Basi nikageuka na kutazama, na kulikuwa na majumba

makubwa mno ya kifalme, na Utukufu wa Mungu ukijakuyazunguka. Kisha nikasikia kwaya ya Malaika ikiimba,“Makao yangu, Makao mazuri.” Nikaanza kupanda vipandionikipiga hatua ndefu, nikikimbia mbio nilivyoweza. Nanilipofika mlangoni, huyo hapo amesimama, amevaa vazijeupe, zile nywele nyeusi na ndefu, zinazofunika mgongo wake.Akainua mikono yake, kama alivyofanya sikuzote nilipokuja

Page 44: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

44 NDUGU BRANHAM

nyumbani nimechoka kutoka kazini au kitu fulani. Nikamshikamikono, nikasema, “Mpenzi, nimemwona Sharon chini kule.”Nikasema, “Amekuwamsichanamrembo, sivyo?”

Akasema, “Ndiyo, Bill.” Akasema, “Bill.” Akanikumbatia,(naye akasema) kwenye mabega yangu, akaanza kunipigapigaakasema, “Acha kunifadhaikia mimi na Sharon.”

Nikasema, “Mpenzi, siwezi kujizuia.”Akasema, “Sasa mimi pamoja na Sharon tuna hali nzuri

zaidi kuliko uliyo nayo.” Kisha kasema, “Usitufadhaikie sisitena. Utaniahidi?”

Ndipo nikasema, “Hope,” nikasema, “nimekuwa na ukiwasana kwa ajili yako wewe na Sharon, na Billy anakulilia wewewakati wote.” Nikasema, “Sijui nifanyeje naye.”

Basi akasema, “Mambo yatakwenda sawa, Bill.” Akasema,“Niahidi tu hutafadhaika tena.” Naye akasema, “Tafadhaliketi.” Basi nikaangalia pande zote na palikuwa na kiti maarufukikubwa mno.

Basi nikakumbuka nilijaribu kununua kiti. Sasa, katikakufunga. Nilijaribu kununua kiti wakati mmoja. Tulikuwa tu nahivyo viti vikuukuu—viti vya kawaida vyenye vikalio vya mbaokwa ile seti ya kifunguakinywa. Ilibidi tuvitumie, ndivyo vitipekee tulivyokuwa navyo. Na tungeweza kununua moja ya vitihivi ambavyo unavikunjua viegemee nyuma, kama…ninasahauni kiti aina gani cha kustarehe. Nacho kiligharimu dola kumina saba, na ungeweza kulipa dola tatu kwanza na dola mojakwa juma. Nasi tukapata kimoja. Na, loo, wakati ningerudi…Ningefanya kazi mchana kutwa, na kuhubiri mpaka usiku wamanane barabarani na po pote nilipoweza kuhubiri.

Na—na siku moja nikachelewa kulipa malipo yangu.Hatungeweza kulipa, basi ikawa hivyo siku baada ya siku,hatimaye siku moja wakaja wakachukua kiti changu wakaendanacho. Usiku huo, sitasahau kamwe, aliniokea sambusaya matunda. Maskini mama huyo, yeye—yeye—yeye alijuaningehuzunika. Na baada ya chakula cha jioni nikasema,“Kitu gani kinakufanya uwe mwema namna hiyo usiku waleo, mpenzi?”

Naye akasema, “Aisee, niliwaleta vijana majirani hapakukuchimbulia vyambo vya kuvulia samaki. Si ni afadhalitwende chini mtoni tukavue kwamuda kidogo?”

Basi nikasema, “Ndiyo, lakini…”Naye akaanza kulia. Nilijua kuna jambo limeenda kombo.

Nilikuwa na fununu sababu walikuwa tayari wameishanipelekea notisi wangekuja kukitwaa. Nasi hatungaliwezakufanya malipo ya dola moja kwa juma. Hatungeweza,hatungeweza tu kukigharimia. Alinikumbatia, na nikaendamlangoni na kiti changu kilikuwa kimechukuliwa.

Page 45: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

HADITHI YA MAISHA YANGU 45

Akaniambia kule Juu, akasema, “Unakumbuka kile kiti,Bill?”

Nami nikasema, “Ndiyo, mpenzi, ninakikumbuka.”Kasema, “Hicho ndicho ulichokuwa unafikiria, sivyo?“Ndiyo.”Kasema, “Vema, hawatakichukua hiki, hiki kimelipiwa.”

Akasema, “Keti chini kidogo, nataka kuzungumza nawe.”Nami nikasema, “Mpenzi, sielewi jambo hili.”Naye kasema, “Niahidi, Billy, niahidi kwamba hutafadhaika

tena. Unarudi sasa.”Kisha akasema, “Niahidi hutafadhaika.”Nami nikasema, “Siwezi kufanya hilo, Hope.”Mara nikapata jirudia, kulikuwa giza chumbani.

Nikaangalia kila upande, huku ninausikia mkono wakeumenikumbatia. Nikasema, “Hope, umo humu chumbani?”

Akaanza kunipigapiga. Akasema, “Utanipa ahadi hiyo, Bill?Niahidi hutaoa…hutafadhaika tena.”

Nikasema, “Ninakuahidi.”Na kisha aliponipigapiga mara mbili tatu, akaondoka.

Nikaruka juu na kuwasha taa, nikatazama kila mahali, aliishakwenda. Bali alitoka tu mle chumbani. Hajaondoka, badoanaishi. Alikuwa Mkristo.

Mimi na Billy tulikwenda kwenye kaburi hapa wakati fulaniuliopita, tukibeba maua machache kwa ajili ya mama yakena dada yake, kwenye asubuhi ya Pasaka, nasi tukasimama.Mtoto huyo akaanza kulia, akasema, “Baba, mama yangu yukochini kule.”

Nikasema, “La, mpenzi. La, hayuko chini kule. Dada hayukochini kule. Tuna kaburi lililofunikwa hapa, bali huko mbaling’ambo ya bahari kuna kaburi lililo wazi ambamo Yesualifufuka. Na siku moja Yeye atakuja, Yeye atamleta dada namama pamoja Naye.”

Niko kwenye uwanja wa vita leo, marafiki. Si—siwezikusimulia zaidi. Mimi [Ndugu Branham analia—Mh.] Munguawabariki. Hebu tuinamishe vichwa vyetumuda kidogo.

Ee Bwana! Mara nyingi, Bwana, nina hakika watuhawaelewi, wanapofikiria mambo haya huja kwa urahisi. Balikuna siku kuu ijayo Yesu atakapokuja na huzuni hizi zotezitafutiliwa mbali. Naomba, Baba wa Mbinguni, kwamba Weweutatusaidia kujiandaa.

Na ahadi ile ya mwisho, nilipombusu kwenye shavuasubuhi ile, kwamba ningekutana naye huko siku ile. Naaminiatakuwa amesimama kwenye ile nguzo, akiliita jina langukwa sauti kubwa. Nimeishi mwaminifu kwa ahadi ile tanguwakati huo, Bwana, ulimwenguni kote, katika sehemu za kila

Page 46: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

46 NDUGU BRANHAM

aina, nikijaribu kuileta Injili. Ninazeeka sasa na kuchoka,nimechakaa sana. Sikumoja hivi punde nitafunga Biblia hii kwamara yamwisho. Basi, Mungu, niwekemwaminifu kwa ahadi ile.Nizungushie neema Yako, Bwana. Jalia nisiyatazame mambo yamaisha haya, niishi kwa ajili ya mambo yaliyo kule ng’ambo.Nisaidie kuwa mwaminifu. Siombi maisha yaliyo rahisi, la,Bwana, na huku Kristo wangu alikufa matesoni. Na hao wotewalikufa namna hiyo. Siombi kitu rahisi. Nijalie tu kuwamwaminifu, Bwana, mtu wa kweli. Wajalie watu kunipendakusudi niweze kuwaongoza Kwako. Ndipo sikumoja wakati yoteyameisha nasi tumekusanyika pamoja chini ya miti isiyokauka,nataka kumshika mkono na kumpandisha juu, kuwaonyeshawatu waAngelus Temple na wengine wote. Utakuwa basi wakatiwa furaha kuu.

Naomba kwamba rehema Zako zikae juu ya kila mmojawetu hapa. Na wale waliopo hapa, Bwana, hata huenda ikawahawakujui Wewe. Na pengine baadhi ya maskini wapenzi waowako kule ng’ambo ya bahari. Iwapo hawajatimiza ahadi yao,hebu na wafanye hivyo sasa, Bwana.

Huku vichwa vyetu vimeinamishwa. Sijui katika jengohili kubwa mno la mikutano adhuhuri hii, ni wangapi wenuwanasema “Ndugu Branham, ninataka kukutana na wapenziwangu, pia. Ni—ni—ninao baadhi ya wapenzi wangu kuleng’ambo ya pili ya mto.”? Pengine uliahidi kwamba utakutananao, pengine ulipomwambiamama “kwa heri” juu kule kaburinisiku ile, pengine ulipomwambia dada mdogo “kwa heri,”au Baba, au baadhi yao kaburini, ukaahidi utakutana nao,na wewe—wewe hujafanya matayarisho hayo bado. Hudhanikwamba ni wakati mzuri sasa kufanya jambo hilo?

Samahani kwa kububujika machozi. Bali, loo, jamani,hamtambui, marafiki. Hamjui ni—ni kujitolea jinsi gani! Hiyohata si hata nuktamoja ya hadithi ya hayomaisha, haifikii.

Ni wangapi wenu mngependa kuinuka sasa na kutembeakuja hapa kwa maombi, mseme, “Nataka kukutana na wapenziwangu?” Simama utoke kwenye makutano uje hapa. Utafanyahivyo? Kama mtu ye yote hajafanya matayarisho hayo bado.Mungu akubariki wewe, bwana. Ninamwona mzee mweusiakitoka, wengine wakija. Tokeni, ninyi mlio kule juu kwenyeroshani, sogeeni mje kwenye marefu ya kanisa. Au msimame,ninyi mnaotaka kukumbukwa katika maombi mafupi sasahivi tu. Sawa. Simama moja kwa moja kwa miguu. Sawa.Simameni, kila mahali, ninyi ambao mngesema, “Nina babahuko ng’ambo, ninaye mama au mpenzi ng’ambo huko. Natakakwenda nikawaone. Nataka kukutana nao katika amani.”Tafadhali simama, hebu simama kwa miguu yako, po potekatika kusanyiko. Simama kwa miguu yako, useme, “Natakakukubali.”

Page 47: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

HADITHI YA MAISHA YANGU 47

Mungu akubariki, bibi. Mungu akubariki nyuma kule. Naakubariki juu kule. Bwana akubariki wewe hapa, bwana. Hilo nisawa. Juu kwenye roshani, Bwana akubariki. Kila mahali, kilamahali, simameni kwa miguu yenu sasa tupate kuomba maombimafupi, wakati Roho Mtakatifu yupo hapa na anatenda kazimioyoni mwetu, ku—ku—kuivunjavunja.

Unajua, kanisa linachohitaji leo ni kuvunjika. Tunapaswakushuka kwenda katika nyumba ya Mfinyanzi. Theolojia yetungumu ya kujitengenezea wakati mwingine haifanyi kazi vizurisana. Tunachohitaji ni kuvunjika kwa mtindo wa kale, tobamioyoni mwetu, kuwa wasio wagumu mbele za Mungu. Hao tusasa ndio walio tayari kusimama?

Na tuinamishe vichwa vyetu basi kwamaombi.Ee Bwana, Wewe uliyemfufua tena Yesu kwa—katika wafu,

kutuhesabia haki sisi sote kwa imani, tukiamini. Naomba,Bwana, kwamba hawa ambao wanasimama sasa kwa miguu yaokukukubali Wewe, naomba kwamba msamaha utakuwa kwao.Pia, Ee Bwana, naomba kwamba watakukubali Wewe kamaMwokozi wao na Mfalme na Mpenzi. Na pengine wana mama aubaba au mtu fulani ng’ambo tu ya bahari. Kuna jambo moja lahakika, wanaMwokozi. Nawasamehewe dhambi zao, namakosayao yafutwe, nafsi zao zipate kuoshwa katika Damu ya Mwana-Kondoo, na waishi kwa amani tangu sasa.

Na siku moja tukufu hapo yote yatakapokwisha, hebuna tukusanyike Nyumbani Kwako, tukae mle kama jamaaisiyotengana, kukutana na wapenzi wetu ambao wanangojeang’ambo ya pili. Hawa, tunawakabidhi Kwako, kwamba“Utamlinda katika amani kamilifu yeye ambaye moyo wakeumemtegemea Yeye.” Tujalie, Bwana. Tunapowatoa Kwako,katika Jina la Mwanao, Bwana Yesu. Amina.

Mungu awabariki. Nina hakika watenda kazi wanaonamnaposimama, na watakuwa pamoja nanyi katika dakikachache.

Na sasa kwa wale ambao watakaopokea kadi za maombi.Billy, wako wapi Gene na Leo, wako kule nyuma? Wapohapa kutoa kadi za maombi katika dakika chache. Nduguatawaruhusu watu wafumukane kwa maombi, na kadi zamaombi zitatolewa. Tutarudi hapa punde tu, kuwaombeawagonjwa. Vema, Ndugu.

Page 48: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

HADITHIYA MAISHAYANGU SWA59-0419A(My Life Story)

Ujumbe huu uliohubiriwa na Ndugu William Marrion Branham, uliotolewahapo awali katika Kiingereza mnamo Jumapili alasiri, tarehe 19 Aprili, 1959,kwenye Hekalu la Angelus huko Los Angeles, California, Marekani, umetolewakwenye kanda ya sumaku iliyorekodiwa na kuchapishwa bila kufupishwa katikaKiingereza. Tafsiri hii ya Kiswahili ilichapishwa na kusambazwa na Voice OfGod Recordings.

SWAHILI

©1992 VGR, ALL RIGHTS RESERVED

VOICE OF GOD RECORDINGS

P.O. BOX 950, JEFFERSONVILLE, INDIANA 47131 U.S.A.www.branham.org

Page 49: SWA59-0419A Hadithi Ya Maisha Yangu VGRdownload.branham.org/pdf/SWA/SWA59-0419A My Life Story VGR.pdf · 2 NDUGUBRANHAM Na, sasa, tumekuwa na mafanikio makubwa katika kulitenda jambo

Ilani ya haki ya kunakili

Haki zote zimehifadhiwa. Kitabu hiki kinaweza kuchapishwa kwa matbaa ya nyumbani kwa matumizi ya kibinafsi ama kusambaza, bila malipo, kama chombo cha kuitangazia Injili ya Yesu Kristo. Kitabu hiki hakiwezi kikauzwa, kunakiliwa kwa wingi, kuwekwa kwenye mtandao, kuhifadhiwa kikatolewe tena, kufasiriwa katika lugha zingine ama kutumiwa kuomba fedha bila idhini halisi iliyoandikwa moja kwa moja kutoka Voice Of God Recordings®.

Kwa habari zaidi ama kwa vifaa zaidi, tafadhali wasiliana na:

Voice of God RecoRdinGsP.o. Box 950, JeffeRsonVille, indiana 47131 U.s.a.

www.branham.org