239
DIBAJI Mara nyingine maisha huonekana kama sumaku yenye nguvu, ambayo humshurutisha mtu sawasawa na mfano wa kifaa kinachofanya kazi kwa mbali. (remote control) Hata ikiwa Karma ana usemi wa mwisho, kwa nini hutokea kwamba watu wengine wana bahati kuliko wengine? Mawazo yetu, maneno, chaguzi, tabia na mienendo huendelea kugeuza na kutia nguvu mazingira, matukio na watu, ambayo matokeo yake hugusa na kutengeneza hatima yetu. Hata hivyo mara nyingi hujikuta tumeingia katika machafuko, mahali ambapo maisha hayawi na maana tena. Je bado ‘kanisa la mapokeo’ lina sauti ya uhai katika jamii? Tofauti na hali ya wakati wa mageuzi katika siku za Luther, mimbari ambayo kanisa la kwanza lilikuwa nayo, hasa miongoni mwa vijana, ilipoteza mvuto wake kwa watu. Malipo ya toharani (purgatory indulgences) yaani ‘tenda dhambi sasa, lipa baadaye;’ au kwa hakika ‘lipa sasa, tenda dhambi baadaye!’ Zilinunuliwa kwa gharama yoyote, na sasa zinampa nafasi buibui yule yule kutengeneza utando mpya, yaani, Uzembe wa kidini. Kusudi la uwongo huu wote ni kuendelea kumfuga mtu katika ujinga wa kutokujua utambulisho wake wa kweli.

Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Discover yourself in the mirror of God's love

Citation preview

Page 1: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

DIBAJI

Mara nyingine maisha huonekana kama sumaku yenye nguvu, ambayo humshurutisha mtu sawasawa na mfano wa kifaa kinachofanya kazi kwa mbali. (remote control)

Hata ikiwa Karma ana usemi wa mwisho, kwa nini hutokea kwamba watu wengine wana bahati kuliko wengine? Mawazo yetu, maneno, chaguzi, tabia na mienendo huendelea kugeuza na kutia nguvu mazingira, matukio na watu, ambayo matokeo yake hugusa na kutengeneza hatima yetu. Hata hivyo mara nyingi hujikuta tumeingia katika machafuko, mahali ambapo maisha hayawi na maana tena.

Je bado ‘kanisa la mapokeo’ lina sauti ya uhai katika jamii? Tofauti na hali ya wakati wa mageuzi katika siku za Luther, mimbari ambayo kanisa la kwanza lilikuwa nayo, hasa miongoni mwa vijana, ilipoteza mvuto wake kwa watu. Malipo ya toharani (purgatory indulgences) yaani ‘tenda dhambi sasa, lipa baadaye;’ au kwa hakika ‘lipa sasa, tenda dhambi baadaye!’ Zilinunuliwa kwa gharama yoyote, na sasa zinampa nafasi buibui yule yule kutengeneza utando mpya, yaani, Uzembe wa kidini. Kusudi la uwongo huu wote ni kuendelea kumfuga mtu katika ujinga wa kutokujua utambulisho wake wa kweli.

Ninaamini kuwa katika kufikia upeo wa mioyo yetu, sauti ya roho yetu huitikia ukweli. Tumeumbwa kupeleleza na kuvumbua undani wetu, utajiri wa nuru, na maisha katika kufikia hali yetu. Hata hali ya kutokuwa na matumaini katika shida itatuhimiza kuchimba chini zaidi ili kutafuta msingi wa Mwamba ndani yetu.

Ninaomba kwamba maandiko haya yalete changamoto na kuamsha hali ya undani wako na imani yako kuondoa kila alama ya kuwa mbadala, iliyotengenezwa na watu, mfano binafsi pamoja na kichwa cha utukufu wa mng’ao wa dhahabu na sanamu yake ya fedha na mwili wa shaba. Jiwe dogo lililochongwa bila kazi ya mkono limewekwa kipiga ile sanamu ya ubatili wa uchaji wa Mungu juu ya nyayo zake za chuma na

Page 2: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

udongo, na badala yake kuwa Jiwe lililoijaza dunia yote; sura ya kweli na mfano wa Mungu, uliorejeshwa na kufunuliwa ndani ya mwanadamu. (Dan.2:32-35)

NYANGUMI NA MCHANGA WA SABI

Mimi na jamaa yangu tunaishi Hermanus, karibu na Cape Town. Kwa kweli huu ni mmoja wa miji mizuri sana ndani ya Afrika ya kusini, na maarufu kwa maeneo ya kuwaangalia nyangumi. Shirika la Haki za Nyangumi hutembelea ufukwe wetu kila mwaka kati Juni na Desemba ili kushiriki na kutulia huko. Kwa miaka mingi Hermanus ulibaki kuwa mji wa uvuvi na kijiji cha mapumziko. Lakini huwezi kumficha mnyama wa mita 14 na tani 40 milele. Kwa kweli ni zaidi ya watu 200 huchezea, huvunja sheria, kufanya ujangili na kuitupa mikia kwa wingi!

Tuliondoka hapa miaka saba iliyopita, baada ya mwaka wa shida ya uharibifu mkubwa. Katika mwaka wa 1996 shughuli zetu, na ndoa yetu vilikuwa karibu na kuvunjika. Ilikuwa kama tumeanguka katika shimo refu. Si kwamba nilimpoteza baba yangu tu, bali na mmoja wa rafiki zangu wapendwa alikufa kwa ajali ya pikipiki. Kwa miaka mingi hakuna mtu wa karibu aliyekuwa amefariki. Ghafula, katika miezi michache, watu sita tuliowafahamu walifariki katika ajali tano tofauti za ndege. Mimi mwenyewe nilianguka na ndege yangu katika hifadhi za Mchanga wa Sabi, lakini nilitoka katika ajali bila mkwaruzo. Bado wanasema kuwa ardhi yoyote unayoweza kutoka kwa kutembea (au kukimbia) ndiyo iliyo nzuri! Wakati wa mwaka ule, tulikuwa tumeanzisha uwekezaji wa ‘ajabu,’ ambao uligeuka na kuwa kama chungu cha mashauri. Zilihitajika Randi milioni nyingi, na watu wengi waliumizwa vibaya!

Lakini miaka minne kabla ya mambo haya, tuliishi kwa ndoto yetu. Nilifanya makubaliano na mmoja wa wamiliki wa shamba la mifugo katika hifadhi binafsi ya Mchanga wa Sabi, lililopakana na hifadhi maarufu ya Kruger. Tulibuni, tulijenga na kusimamia nyumba ya wageni ya kijijini yenye vyumba vitano

2

Page 3: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

ambavyo viliongezeka mara mbili. Kituo kilikuwa mashambani, na joto lenye tabia ya kubadilika-badilika. Wakati Lyidia alifurahiwa sana na wageni kwa uwezo wake wa kupika kwa moto wa nje, mtoto wa ndugu yangu pamoja nami, tuliwachangamsha kwa mwendo mrefu katikati ya tembo na simba. Wakati wa mwisho wa juma na siku kuu za shule, watoto wetu wanne walijizoeza katika kazi ya kukaribisha watu. Shinga ulikuwa katika eneo zuri la Afrika safi. Kwa kweli huu ulikuwa wakati wa ujuzi wa ajabu na utajiri wa kumbukumbu nyingi. Tulikutana na watu wa ajabu na kushirikiana nao nyakati zisizoweza kusahaulika.

Nilimshirikisha mwenzi wangu ambaye alimhimiza mmiliki wa shamba la mifugo kwa mambo ya kifedha. Ndipo tulifikia makubaliano ya kuendelea kuipandisha hadhi, hatimaye ilikuwa ni hoteli kubwa katika Mchanga wa Sabi. Mipango ya kuiendeleza hoteli mpya ilikamilika, na uandikishaji wote uliotangulia Shinga ulifutwa.

Tukiwa katika mapumziko Rooi Els karibu na Hermanus, mwezi Desemba ya 1996, tulipata habari ambazo zilitufunga; kamati ya Mchanga wa Sabi iliikataa mipango yetu yote ya kuwa na hoteli mpya. Tulijulishwa kwamba tusingeruhusiwa kufungua tena Shinga kwa kuwa wamiliki wa Mchanga wa Sabi waliamua kuzuia idadi ya vitanda katika shamba. Mpaka hapo tayari tuligundua kuwa tulikuwa tumepoteza kila kitu kuhusu mambo ya uwekezaji, kwa mbadiliko wa matukio yasiyotegemewa; tulilazimika kufanya ubunifu na maamuzi ya haraka.

Wazazi wa mama yangu pamoja na wazazi wa baba yangu waliishi Hermanus kwa miaka mingi. Tulitumia muda mwingi wa mapumziko hapa. ‘Nyumba ya maonyesho ya sanaa ya De Wets-huis’ ilikuwa nyumba ya nyanya yangu. (Hakutaka kwamba watoto wake wafundishwe na mwalimu wa kiingereza, kwa hiyo alimleta Hermanus Pieters kutoka Holland). Mpaka miaka ya 1890 aliendesha mashua sita kutoka bandari ya zamani. Mvuto wa bahari na uwezekano kwa watoto wetu kuishi mjini kwa mara ya kwanza katika maisha yao, pamoja na elimu

3

Page 4: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

ya msingi na ya sekondari kama kizuizi tu, vilitusaidia kutengeneza akili zetu.

Wakati uo huo, ‘katika shamba la mifugo,’ mwenzi na mmiliki wa shamba alizuia mipango ya hoteli mpya. Kwa kuwa wakati huo tuliishi kijijini kilometa 2000, habari za mambo mapya zilitufikia baada ya miezi sita kwa njia ya usafirishaji zabibu kwenda rasi ya mizabibu.

Lakini hakuna awezaye kukusikitikia iwapo unaishi Hermanus. Na pia haisaidii kujisikitikia wewe mwenyewe. Nilijitahidi kwa miaka miwili. Nilinuna na kunung’unika hata siku moja mke wangu aliona kuwa mazungumzo yangu yalishuka na kuwa ni ya kuhema sana! Tulikuwa tumezungukwa na uzuri mkubwa wa asili; je, tulipaswa kuupata kwanza kabla ya kuufurahia? Kwa kweli, hatukuwa na kitu chochote katika vitu vya ulimwengu mbali ya kuwa na muda mfupi au kumbukumbu.

Siku moja nikiwa njiani kwenda Cape Town kuweka mifuniko ya bwawa la kuogelea, hali ya kukata tamaa na kutokuwa na matumaini ilinikandamiza; hakuna lililokuwa la maana tena. Nilikuwa na shauku angalau ya kusikia sauti ambayo kwa namna yoyote ingeniongoza katika kuchanganyikiwa kwa mawazo yangu. Nilipofungua redio, nilisikia msitari mmoja tu wa wimbo wa Mike na Mafundi, ‘…wewe ni ombaomba wa pwani ya dhahabu!’ Hakuna kitu utakachoweza kupoteza na kujiona maskini, mnyong’onyevu na mkiwa, kuliko kupoteza ufahamu wa kuijua mali iliyo ndani yako.

Kinacholala nyuma yako na kinacholala mbele yako ni vitu vidogo ukilinganisha na kilicho ndani yako. [Ralph Waldo Emerson]

Kwa muda wa mwongo mmoja, nilichukuliwa katika jangwa la giza la kiroho na ukiwa. Nilianza kuandika mihutasari ambayo hatimaye ilitoa kitabu hiki mwezi Desemba 2000.Minong’ono ya upepo ilifanyika kuwa mpasuko wa wingu wa fikira. Kutaka kwangu ni kwamba somo hili litakuwa taa kwa kiongozi, hasa

4

Page 5: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

kwa wale wote wanaopita mahali pa giza. Tazamia siku itapambazuka kwako kama nyota ya asubuhi ikiangaza ndani ya moyo wako. (2Pet.1:19)

NGUVU YA UVUTANO

Kila jambo huanzia mahali fulani. Wakati mwingine ni vigumu kujua chanzo na muda, lakini mara kwa mara ghafula hutokea kujua kwamba umeshikwa na chanzo cha utelezi wa jambo. Ama unawinda kitu fulani, au kuna kitu kinakuwinda wewe. Hili linanikumbusha kuhusu habari ya mtu aliyefika akiwa ameishiwa pumzi kwa mshituko katika nyumba ya shamba la mifugo. Alikuwa amemkimbia simba. Mwenye shamba alimwuliza kwa nini hakupanda katika mti…, Alijibu, ‘Huh! Nilikuwa kasi mno!

Kuhusu chanzo cha utelezi, daima chanzo cha wazo hufanya nguvu ya haraka kuunda uwanja wa sumaku pamoja na mvuto wake au nguvu ya uvutano. Katika mazingira maalumu, sheria ya uvutano hufanya kazi kwa hiari. Kwa kadiri unavyokuwa karibu na chanzo, ndivyo kadiri nguvu ya matokeo huonekana. Mara kwa mara wazo linalofurahiwa huwa ndio njia ya kukanyaga katika uwanja wa fikira zako. Ni ufahamu wa kawaida kwamba wazo la kinyume huwa ndio sababu kubwa ya kukandamizwa. Wazo linaweza kuwa siri na kutokuonekana kwa muda fulani, lakini sharti litaathiri mazungumzo yako, hali yako na afya yako. Mwenendo wako, kama ni lugha ya mwili au tabia, siku zote itayasaliti mawazo yako. Tabia ya kila mtu na jazba huambukiza nguvu zinazoleta mvuto kwa wengine. Mara kwa mara katika familia ya ajabu, muda wa chakula unaweza kuharibiwa na tabia mbaya ya mtu mmoja, iwapo hakuna mtu anayejua vema.

Tunaiepukaje tabia ya kufikiri kinyume? Juhudi ya kushinda wazo la kinyume au hata kubadilisha na wazo la kweli, linaweza kumaliza na mara nyingine kufadhaisha, na kumwacha mtu na

5

Page 6: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

hisia za kupigana vita vya kushindwa. Unakuwa mzunguko mbaya. Kupigana na hali ya kushushwa moyo kwa njia hii inaweza kuwa vigumu zaidi kuliko kujaribu kuacha sigara. Wote tunajua kwamba nuru huondoa giza bila shida, lakini mtu anaiwashaje nuru? Je kuna sheria ambayo inaweza kuizuia nguvu ya uvutano?

Niliposomea leseni ya urubani, mkufunzi alieleza jinsi sheria ya kuinua, katika akili, huwa badala ya sheria ya uvutano. Sheria moja inabatilisha matokeo ya sheria nyingine, na hivyo ni kama kusema. Kuendelea mbali kabisa katika anga la dunia, kunaleta hali ya kukosa uzito. Sheria ya uvutano hutoa malinganisho ya kupendeza, ili kusaidia kuelewa jinsi sheria nyingine zifanyavyo kazi. Sheria haifanyi kazi kwa kubahatisha. Hata hivyo hufanya kulingana na kanuni maalumu na za kutabirika. Uchaguzi hautoi matokeo ya uvutano. Wala uvutano hauna upendeleo; kwamba wewe ni mwembamba, au mzito zaidi, maarufu, mwenye mvuto au maskini, mkatoloki au mwislamu, uvutano utaiweka miguu yako ardhini; unapobakia katika hali ya kufikia mvutano; hata hivyo, daima unaweza kujifunza kuruka!

Tunataka kushikwa sana na kushughulishwa katika mzunguko wa siku kwa siku ambao, mara kwa mara tunashindwa kumtambua rafiki katika majirani, mbali na kuta zilizomiminwa. Kuvunja mipaka inayojulikana, kuutambua muda na nafasi katika mtazamo na viwango tofauti, kwa kweli kutaleta changamoto kwa eneo tulivu.

Sayansi inaturuhusu kutafiti chanzo na hatima yetu kwa kadiri iwezekanavyo, katika mipaka iliyofungwa kwa yale tunayoyajua kwa akili zetu kuwa kipimo halisi cha nafasi na muda. Hata hivyo, nidhamu hii, inafikia mahali ambapo teknolojia ya kisasa isiyo ya asili, inashindwa kufanya hesabu za kina na upeo wa macho yetu.

Darubini aina ya Hubble hukamata sura za vitu kwa namna nzuri sana zenye rangi mbalimbali, miaka milioni nyingi kabla yetu, umbali ambao macho ya kibinadamu hayawezi kupenya

6

Page 7: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

katika uumbaji wa ulimwengu. Mwanga wa nuru hupima umbali wa mwendo wa nuru ukisafiri kwa kasi ya kilomita 300,000 kwa nukta moja kwa kipidi cha mwaka mmoja! Kama mtu angeweza angalau kuhesabu nyota, kwa kipimo cha nyota moja kwa nukta, ingemchukua kiasi cha miaka 3000!

Kwa uvumilivu, wachunguzi wa mambo ya kale wanavumbua mabaki na mifupa ya watu kutoka ardhini, na kupata muda kwa njia ya carbon, hufunua ushahidi wa kihistoria wa miaka milioni nyingi iliyopita. Tunaendelea kuboresha njia zetu, na mara nyingine kufanya madai ya mwaka wa jana kuonekana hayana maana. Kimsingi, vitu vyote duniani vimeumbwa kwa chembe-chembe ndogo ziitwazo atom. Kiini cha atom ni sauti za mawimbi, zilizotiwa nguvu kwa umeme, na kutikiswa taratibu kunakoendelea. Mamilioni na mamilioni ya atom ni chembechembe ndogo sana kuonekana, isipokuwa kwa kiona mbali cha nguvu, kuingia katika ulimwengu usioonekana ili kufunua siri zake. Tunagundua kuonekana kwa ushindi umbali, nguvu, na mwendo ambao unaonyesha nafasi ya nje. Juu ya mizani, umbali kati ya mzunguko wa nguvu ya umeme na kiini kizungukacho ndani ya atom, ni zaidi ya umbali kati ya dunia na jua. (Kilomita milioni 220!) Hatimaye tunatazamia kufanya hesabu ya nguvu ya umeme, hushuka chini katika mitetemo ya nguvu ambayo inametameta ndani na nje ya kuona kwetu mara milioni nyingi kwa nukta.

Kutambua ulinganifu wa kipimo cha atom, mifano ifuatayo itakushangaza: Ikiwa maktaba mia moja na thelathini, na kila moja ina vitabu milioni nane, vyenye kurasa elfu moja, na kila ukurasa ukiwa na nukta 50,000, na jumla ya nukta katika vitabu hivi zingekuwa sawa na idadi ya atom katika chombo kimoja cha oksijeni kipimo cha punje ya haradali! Basi fikiria punje ndogo inayoonekana kama moshi ikigawanyika miongoni mwa watu milioni nane. Kazi yao katika maisha ingekuwa kuhesabu atom zilizomo katika vipande vyao! Kama ingewezekana

7

Page 8: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

kuhesabu atom nne kwa nukta kwa saa nane katika siku moja, ingelichukua miaka mia moja na hamsini kufanya kazi hiyo!

Muda hupima ulinganifu wa mwendo unaoendelea kubadilika, wakati unakuwa mchana, usiku, na majira yake; mzunguko wa maisha umesajiliwa milele. Kutoka nje ya ufahamu wetu wa muda, tunakuwa na hatari ya kukamata mtazamo wa haraka wa milele; tunachunguza nafasi kwa vyombo butu, kupima mwendo na umbali katika shauku yetu ya upelelezi na kupata hoja.

VIFAA VYA PEPO

Hakuna uchawi zaidi kuliko kushuhudia madirisha ya kiroho yakiwa wazi, mbali kabisa na uharibifu wa akili na maarifa yaliyo katika jamii yetu. Mvutano unaahidi kukutana na thawabu kubwa sana. Ufahamu wa kiroho unafunua ulimwengu usioonekana wa mawazo na fikira. Hapa, matokeo yanapunguzwa kuwa kama sauti ya mlio tu, na hatima yake kuwa ni tunda la imani. Unaporekebisha sauti ya chombo cha nyuzi, waya mwingine utaanza kutetema peke yake wakati pigo kamili linapoitikia.

Wanadamu wamejengewa uwezo kuutambua ukweli. Ndani yetu tuna uwezo tofauti wa kutambua thamani. Hili ni zaidi ya ushawishi au majadiliano, nao hushinda mashaka. Kuna mambo ya ziada katika maisha kuliko yale yanayoonekana katika mwili huu wa nyama. Usemi wa kwamba mtu hataishi kwa mkate tu, unaonyesha kuwa kufurahia maisha yaliyokamilika, kunahitajika zaidi kuliko kuulisha mwili tu. (Luka 4:4). Hata kama unakula mkate uliopakwa siagi pande zote, hauna faida. Watu wengi walio matajiri siku za leo, wanategemea mambo yaliyo kinyume kabisa na kushuka. Utajiri na umaarufu, kwa kweli havitoi uhakika wa maisha makamilifu; badala yake, huleta shinikizo amblo limekuwa ugonjwa wa kisasa. Hata hivyo, bado hatujisikii uzuri wowote katika akili zetu. Maarifa ya elimu yametupa mambo ya tiba

8

Page 9: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

muhimu kutuwezesha kuishi maisha marefu na salama kuliko wakati wa nyuma. Kuna watu wengi zaidi wanaoishi leo kuliko jumla yote ya watu waliokufa katika historia ya wanadamu. Pamoja na msisitizo maarufu juu ya chakula cha kuleta afya na mazoezi, wengine hata wanakaribia kuishi milele!

Kufurahishwa kwa akili kumekuwa ndio utendaji mkubwa sana katika ulimwengu wetu; kwamba ni biashara haramu na kutisha za madawa ya kulevya na pamoja na jitihada za kuzuia, au mchezo maarufu wa fedha nyingi, filmu, muziki, igizo, safari, au chakula na kileo, tumejikamilisha katika hali ya kujifurahisha sisi wenyewe. Hiki kinaweza kuwa kipindi cha utimilizo wa kileleni kabisa. Tunaharibu akili zetu kwa taarifa na hisia. Hatujapata kujua zaidi; hatujasafiri kwa haraka zaidi. Watoto wetu wanatushangaa wakiwa na ujuzi wao wa kompyuta na uwanja wa michezo. Tangu miaka ya 1700 mpaka miaka ya 1800, kingo za dunia zinapungua kutoka umbali wa miezi sita hadi majuma sita. Mwanzoni mwa miaka ya 1900, muda huo umekuwa ni siku tatu tu. Bibi yangu alisafiri kutoka Cape Town mpaka Pretoria kwa mara ya kwanza, alipokuwa na umri wa miaka sita, kwa gari la kukokotwa na ng’ombe Safari ya ujasiri ya kilomita 3000 ilichukua miezi kadhaa. Mwaka wa 1961, akiwa na miaka zaidi ya 80, baba yangu alimchukua kutoka Hermanus, na waliruka kwa ndege kutoka Cape Town mpaka Johannesburg katika muda wa saa mbili! Leo tunasafiri popote duniani kwa saa chache, na kujisifu kwa kuufikia limwengu ndani ya nukta. Hata nafasi ya nje inaweza kuwa sehemu ya utalii! Maisha yamekuwa ni yenye manufaa. Tunapata mambo mengi mno kwa kiasi cha kugusa ufunguo tu. Lakini bado kuna uchoyo na hali ya kupungukiwa inayowatawala watu wote, maskini na tajiri.

Kwa watu wengi, wajibu wao umekuwa ni uzuri wa mitindo ya ulimwengu, mikanda ya picha, mambo ya sanamu na mashujaa wa michezo. Kwa namna fulani, tumetwaa misisimko ya kuendesha maisha yetu, na kuifanya kivuli cha kuona mafanikio ya wengine. Kupata kwao au kushindwa kwao kunakuwa ni kwetu na sisi pia! Mamilioni ya watu wameshikwa

9

Page 10: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

katika ulimwengu wa mazingaombwe. Maisha yamepunguzwa na kuwa mchezo mwingine wa LOTTO. Tunahesabu siku ili kufikia mapato ya bahati nasibu, nakuendelea kuota ndoto za kupata mamilioni.

Tunawapuuza watengenezaji wa takwimu wanaotusumbua au kutudharirisha: Magereza yamefanyika kuwa malundo ya takataka katika jamii yetu. Tunashindwa kutambua kwamba mfumo wetu wa urekebishaji wa mambo hauwezi kuwabadilisha wafungwa. Mwaka wa 2003, asilimia 85 ya wafungwa wote wa Afrika ya kusini walioachiliwa huru, walirejea tena katika makosa yao na kurudi katika magereza ambayo tayari yalikuwa yamefurika kwa 70%. Baadhi ya magereza ndani ya Afrika ya kusini yamefurika kwa karibu asilimia 300. Inawagharimu walipa kodi zaidi ya Randi milioni 500 kwa mwezi kuwafanya wafungwa waishi. Ni kiasi cha Randi 3000 kwa mwezi kwa kila mfungwa, kiasi ambacho ni mara tatu ya kiwango cha chini cha mshahara wa mtu. Gharama hizi zinamlenga mfungwa moja kwa moja, bila kujumlisha gharama nyingine zinazohusiana na polisi, uendeshaji mashitaka na bima, ambazo ni wajibu, katika ongezeko la mzunguko wa makosa. Kwa namna fulani, juhudi zetu za kurudisha hali nzuri, nguvu zote zinatumika kulenga utando wa buibui badala ya kumwua buibui. Makosa ya jinai, makosa ya kitoto, madawa ya kulevya, matumizi mabaya ya kileo, unyanyasaji wa wanawake na watoto, kupeana talaka, kuvunjika kwa familia, ufisadi na vita, huleta aibu katika jamii, miundo ya kidini, na kisiasa.

Hakuna sehemu iliyo na maisha yasiyo na maana kama mazingira ya vita. Sauti ya ukatili kwa uchache kama ule wa al-Qaeda au Boeremag, au wingi kama vile utawala wa Bush na Blair, wanavyosema mamoja: Tuna jamii inayougua na ubinafsi unaougua. Kupuuza thamani ya roho ya mwanadamu ni kukufuru uadilifu wa kuumbwa kwetu.

Jambo hili huwa la utata; tumejiandaa kutumia mamilioni kuokoa maisha, na wakati uo huo tunatumia mamilioni kuharibu maisha. Tunashindwa katika elimu yetu ya msingi, wakati

10

Page 11: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

tunaposhindwa kutambua au kuheshimu maisha tuliyo nayo. Heshima yetu sisi kwa sisi inaweza kupewa changamoto, thamani ya uadilifu wetu wa juu uko hatarini.

Hakuna mtu aishiye kwa furaha akijali mambo yake mwenyewe, ageuzaye kila jambo kwa faida yake mwenyewe. Mtu lazima aishi kwa ajili ya mwingine iwapo anataka kuishi kwa ajili yake mwenyewe. Marafiki wa kweli ni ulimwengu wote kila mmoja kwa mwingine. Yeye ambaye ni rafiki mwenyewe, pia ni rafiki wa wanadamu wote. Seneca K.K.3 - B.K.65 Rumi.

UELEWA WA IMANI

Katika somo hili ninataka kufungua na kujadili juu ya siri ambayo ninaamini itamwimarisha kila mmoja kuishi mbali na vifungo vya vizuizi vya mfadhaiko wa kuonekana duni. Itakufungua ili uishi mbali na hali ya kukata tamaa na kukuweka huru kutokana na mashaka, hofu ya kushindwa, na hofu ya mauti.

Kuna sheria, ambayo kiutendaji inaleta changamoto na kufuta matokeo ya nguvu ya uvutano wa hukumu, hatia, unyonge na kuendelea kuvuta kwa tabia zilizo kinyume.

Tunaambatanisha thamani nyingi kwa kusifu na kumtambua mtu aliye mwenzi wetu. Tendo la pekee linakufanya kuwa mali ya wazi. Bado kundi lile lile linalokusifu leo, ndilo litakalokusulibisha kesho; mtazamo wa kitendo unafifia, kukatisha tamaa au kushindwa. Wakati wengi wanaota ndoto za utajiri na umaarufu, wengine wanajificha ndani ya nafasi iliyofungwa ya majina maarufu: kuvaa mavazi sahihi, kuendesha aina fulani ya gari, na kuonekana na kundi sahihi n.k; ‘mchanganyo’ huwa kama neno la kichawi. Kwa sababu ya hofu ya kukataliwa, kila mtu hajaribu kuwa wa tofauti. Hisia za kukubalika na kundi humpa mtu hali ya usalama na vitu vyake;

11

Page 12: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

hata hivyo, kuyatafuta mambo haya, baada ya muda fulani hufanyika kuwa mtego unaomdhoofisha kila mtu.

Makundi husalimika na kulazimika kuishi chini ya amri bila wazo lolote la kweli au nafasi ya kuweza kubadili au kuepuka mazoea ya kila siku yaliyokufa. Vizazi vya watu wote, tajiri na maskini wanaishi na kufa wakiwa ndani ya akili walizojengewa.

Kwa kuwa ni kweli kwamba, kimsingi mwanadamu ni roho, halafu tukigundua asili yetu ya roho na utambulisho wetu, tutakuwa na hali mpya ya kufikiri na kuonekana bila kipingamizi! Mawazo yako yanaongoza njia kwa roho yako, hali ya ndani ya utu wako. Hapa kuna utaratibu wa mwanzo wako, na utambulisho wa roho umehifadhiwa kwa wingi, kwa namna ile ile ambayo chembechembe za mwili wako zinatunza taratibu za DNA kuhusiana na uzazi.

Maisha ni kitu cha kuharibika kirahisi yakiwa ndani ya umbo la mwili, lakini yakiwa na mwako wa milele katika roho. Hata hivyo katika mwili mtakatifu na wa udongo, unafunua uthabiti ambao kwa ukaidi huokoa na kushinda mashambulizi ya muda na changamoto.

Tunaweza kufuatilia mababu na vizazi vya wanadamu wa kale, lakini je, baada ya hapo, inawezekana kuelewa asili yetu ndani ya Mungu? Je sisi ni uzao unaotokana na mshindo tu, au muda na mageuzi, hatimaye kufanyika mwili, au tunashiriki asili ya akili za kawaida zilizo tofauti na historia yetu ya vizazi?

Katika mtandao tunamiliki mawasiliano ya ulimwengu wote na wapendwa wetu, bila kujali vizuizi vya hali ya kijiografia, kisiasa, kimila hata lugha. Bado tunabaki kuwa na mashaka kuhusu uwezo wetu wa mwunganiko wa kiroho na Mwumba wetu, na kukutana na matokeo ya maana, tunapobisha hodi kwenye mlango wake, au tunatambua kuwa ni hakika yeye anabisha hodi katika milango yetu? Katika mambo ya sayansi, daima tunajaribu kukana juu ya kuwepo kwa Mungu, wakati ukweli pekee ni kwamba, sisi tupo kama ushahidi wake hasa

12

Page 13: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

kuonyesha kwamba Mungu yuko, ushahidi unaodharauliwa kwa nguvu za makusudi. Hatuwezi kuukataa ushahidi. Sisi ndio ushahidi huo.

Zuria la maisha huanza na uzi mmoja. Yai moja lililorutubishwa (zygote), kiasi cha ncha, huchukua maelezo ya dawa ambazo zingeweza kujaza zaidi ya machapisho kurasa 500,000! Taarifa za kizazi zilizomo ndani ya “encyclopaedia” hutegemea namna ya nguvu za mwili kuhusu maendeleo ya mwanadamu, tangu urefu mpaka rangi ya nywele. Halafu yai lililorutubishwa hugawanyika katika chembe-chembe trilioni 30 ambazo zinaufanya mwili wa mwanadamu, pamoja na chembe-chembe za ubongo bilioni 12, na uwezo wa kuunda zaidi ya viunganishi trilioni 120. Na A.E.Wilder-Smith.

Katika hali ya mazingira yaliyozuiliwa hata kuweza kutumiwa chini ya asilimia 10 ya uwezo wa ubongo wake.

Kila mara tunapenda kukutana na furaha, au kuona dokezo la asili ya Mwumbaji wetu ikionekana ndani yetu. Uwezo wetu wa kuelewa na kutambua thamani ni upanuzi wa tabia zake. ‘Jicho la kuona na sikio la kusikia, ni Bwana ameviumba vyote.’ (Mith.20:12). Kutaka sana na hali ya kutimizwa kwa maana kamili, kunatuzuia tusitafiti mambo zaidi ya kuupendeza mwili. Ikiwa Mungu yupo, na ndiye aliyeubuni ulimwengu wote, kuwajibika kwa mambo yote, na kutiwa nguvu ya umeme ya atom na uhalisi wa muundo wa sehemu ya kila mmoja; halafu hakuna anayeuliza ukweli kwamba, huyu lazima awe Mungu wa kuogofya na wa mvuto mkubwa! Halafu kumjua na kukutana naye kiundani, ni lazima iwe thawabu kubwa ya maisha. Kumwonea mashaka, nikubaki wapungufu wa elimu ya fursa na upweke. Hakuna hesabu ya muda ambayo inaweza kutoa fursa njema, ya kufanya japokuwa moja tu ya sehemu muhimu iliyo rahisi ya protini. “Kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.” (Ebr.11:6). Thawabu yake ni yeye mwenyewe. (Mw.15:1). Mwanadamu hakuumbwa ili kuishi katika upweke na ukiwa wa kiroho.

13

Page 14: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Siri iko ndani yetu na ndani ya kila kiumbe kilicho hai, hata katika miili ya samaki wadogo waliomo bwawani, mna siri ya kuwapo kwa Mungu. Hakuna kiumbe kinachopumua pumzi ambayo ni mwitikio wa upendo wake; hakuna ua linalometa-meta kwa aina yoyote ya mwanga, bali mwanga wake; hakuna sauti inenayo katika wema, isipokuwa ni kwa upole wake mwenyewe. Elizabeth Goudge.

Kujitambua katika kuakisi kama kwa kioo, asili yako iliyo ndani yake, ndio ufunguo unaofungua mlango wa kuingia katika mambo ya mbinguni. Uhakika zaidi wa kugusa mwanzo na uwepo wetu umefunuliwa. Shauku yetu muhimu na ya ndani inatoshelezwa tunapogundua asili yetu ya kweli na utambulisho wetu unaoonekana ndani yake.

Kwa kadiri ambavyo ulimwengu wa sayansi unategemea juu ya kuelewa, kipimo cha kuzihesabu kweli na kufanya hitimisho la kuaminika; imani huelewa uhalisi wa Mungu na kupanua ushahidi wa kufikiri. Imani ni kwa ajili ya roho, kama vile akili zako zilivyo kwa ajili ya mwili. Tazamia ufunuo wa Mungu ndani yako.

KUPIMA UZITO WA MANENO

Ninafurahia utajiri wa maana ya maneno iliyomo katika lugha za kale za Biblia, lakini yamkini huhitajiki kuwa mwanafunzi wa Kiyunani au Kiebrania kabla hujafikia kukutana na Mungu, sawasawa na ambavyo huhitajiki kuelewa mambo ya ufundi wa ndege kabla hujafurahia kupanda.

Maneno ni magari ya roho. Popote ambapo mtambo wa upepo umesimamishwa, upepo ambao ulibakia bila kupimwa kwa vizazi, sasa unaweza kuvunwa na kuongozwa katika chanzo cha nguvu muhimu. Tumegundua na kimiliki teknolojia ya mpisho na mapokezi. Leo mawimbi ya anga yanapasuka kwa taarifa za kiakili katika rangi kamili. Zote zinabakia bila kuonekana na bila kusikika mpaka chombo cha kupokea

14

Page 15: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

kiwekwe katika kituo maalumu. Sikio liliumbwa ili kusikia sauti ya Mwumba wake; ‘Yeye aliye na sikio la kusikia na askie.’

Nukuu ifuatayo inaeleza habari ya msichana mdogo aliyemsikiliza baba wa kambo akisoma Biblia: Katika kitabu chote, hata katika sehemu za kutisha, sasa lugha itamgeuza mara kama uchawi. Tofauti zilizotolewa na baba Sprigg hazikumtisha hata kidogo. Ilikuwa kama vile sauti yake ya ukali iliyokuwa ikirusha maneno ovyo hewani, ilitenganisha visehemu visivyo na maana, na mara yalianguka tena yakiwa yamegeuzwa, kama muziki wa mlio wa kengele au matone ya mvua yaliyoanguka pamoja na mwako wa jua, na maono zaidi yenye uzuri usiofananishwa, uliofunguliwa mbele ya ufahamu wake. Ilikuwa ni siri kwa Stela kwamba, ni maneno tu yaliweza kufanya jambo litokee. Alidhani kuwa muundaji wa maneno haya alikuwa ameyatengeneza kukamata maono yao kama mtu afanyavyo sanduku la kushikia hazina, na sauti ya baba Sprigg ulikuwa ndio ufunguo ulioparuza-paruza ndani ya kufuri, ili kwamba sanduku liweze kufunguka na kumweka huru. Mageuzi katika anga bado yalibaki kuwa ya kutokuelezeka kama mabadiliko ya haraka ndani yake, wakati katika muda huo, anguko la kichawi lilimpumbaza akili na ghafula kumeta-meta kwa maajabu, na roho yake kuruka-ruka ndani yake kama vile ndege…’ (Gentian Hill, imeletwa na Elizabeth Goudge)

Katika lugha yoyote ile, neno linaweza kuleta madhara zaidi. Mbegu huhifadhi nguvu ya uhai na kuonekana kwa kizazi cha aina ya mmea, ndivyo mawazo na fikira yanavyofungwa katika lugha na maneno. Wakati ambao mbegu inaota, inafunua udhihirisho mpya wa nguvu ya uhai. Majira yanapobadilika, hata kupita wakati, miti iliyokuwa kana kwamba imekauka na kufa huchanua kwa harufu mpya ya kunukia sawa na mmea mchanga.

Mazingira yanayokubalika ndio mchango pekee ambao mbegu inauhitaji. Baba yangu alitunza kuku wachache katika ua wa nyuma. Tukiwa kama watoto, mara kwa mara tulikuwa hodari zaidi wakati wa kuanguliwa vifaranga, ili kuanza kuhesabu siku

15

Page 16: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

za kuatamia mayai. Mara nyingine tuliweza kumfunika kuku na kasha la mbao juu ya kiota chake, ili kumlazimisha kuangua, lakini hayo yote hayakusaidia kitu. Walakini, tulielewa kuwa, yai lilikuwa na ahadi zaidi kuliko kuwa na kifungua kinywa kingine.

Hivi karibuni nilishiriki katika mradi mdogo wa bustani ya mboga katika eneo la Zwelihle huko Hermanus. Nilijifunza kanuni rahisi kwamba, juhudi nyingi hutumika katika kutayarisha udongo, kutengeneza matuta, na kuitunza bustani; na zaidi sana ndivyo inavyokuwa hata kuzaa mara mia. Hatuwezi kuongeza ubora wa mbegu. Mbegu iliyokanyagwa au kuliwa na ndege, au mbegu ambayo ilitoa mazao mengi, zote zilikuwa na uwezo ulio sawa. Hakuna mtu awezaye kutoa kile ambacho ni mbegu peke yake iwezayo kukitoa. Hata hivyo, bado tunaweza kufanya zaidi katika udongo kwa kutayarisha mazingira ambayo mbegu inayahitaji. Sisi tunafanya kwa udongo, lakini mbegu hufanya mambo yaliyosalia.

Kufuatana na Injili ya Mathayo, Marko, Luka na Yohana, wote wameandika kuhusu jinsi Yesu alivyotangaza habari njema, alivyofundisha na matumizi ya nguvu yake, na kuwaponya watu wengi. (Math.4:23,24; 9:35). Mahubiri yake na mafundisho yake yalitayarisha udongo wa imani katika akili na mioyo ya watu. Mara kwa mara aliangalia mwitikio wa imani ya mkutano. ‘Na iwe kwako sawasawa na imani yako’ [Angalizo, Sio sawasawa na mapenzi au nguvu ya Mungu ya kuponya]. Alizungumza juu ya imani kubwa na imani ndogo, na daima alikubaliana na imani iliyoonekana; ‘…Alipoiona imani yao…’ Hata mtu aliyezaliwa kipofu alisikia kiasi cha kutosha kuona kwamba anaona. Imani ni uwezo wa kujiona wewe mwenyewe sawa na akuonavyo Mungu. Imani inaumba mazingira ya kukutana kwa njia ya ki-Mungu isiyo ya kawaida. Imani yako ni ufunguo; imani ya namna hii chanzo chake ni katika Mungu. ‘Imani huja kwako kupitia yale unayoyaskia’ (Rum.10:17). ‘Kutoka imani hata imani’ (Rum.1:16,17). ‘Yeye ndiye mwanzilishi wa imani yetu’ (Ebr.12:2). Imani ya Mungu ndani yako, inasugua juu yako! ‘Paulo alihubiri kwa njia ambayo wengi waliamini’ (Mdo 14:1). Alitilia mkazo msimamo maalumu wa mafundisho, ambao

16

Page 17: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

haukutoa nafasi ya mashaka au kujichanganya. Tafsiri ya Dodrich inasema, ‘Mfano wa mafundisho, unawaelekeza ninyi kama vile kielelezo cha chapa’ (Rum.6:17). “Na huko Listra palikuwa na mtu mmoja , dhaifu wa miguu, kiwete tangu tumboni mwa mamaye, ambaye hajaenda kabisa. Mtu huyo alimskia Paulo alipokuwa akinena; ambaye alimkazia macho na kuona ya kuwa ana imani ya kuponywa, akasema kwa sauti kuu, ‘Simama kwa miguu yako sawasawa.’ Akasimama upesi akaenda. Na makutano walipoona aliyoyafanya Paulo wakapaza sauti zao, wakisema kwa Kilikaonia, ‘Miungu wametushukia kwa mifano ya wanadamu.” (Mdo 14:8-11). Mahubiri ya Paulo yalimpa nguvu kupitia sauti yake ambayo ilipita kelele zote za kutokuamini ambazo huenda zingeweza kumzuia.

Katika Marko 11:22 Yesu anasema, ‘Mwe na imani ya Mungu.’ Kwa bahati mbaya tafsiri nyingi zinasema, ‘mwamini Mungu;’ pana tofauti kubwa. Imani ya Mungu ndani yako huipa imani yako uhalisia. Habari njema hufunua imani ya Mungu ndani ya mtu. Imani yako ni kama kuakisi kwa kioo kwa maono ya Mungu juu yako. Imani yako inafunua thamani unayoiweka juu ya imani ya Mungu iliyo juu yako. “Na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu” (Gal.2:20). (Katika Kiyunani, ni imani ya; sio imani katika).

Moja ya maandiko ya kusikitisha katika Biblia liko katika Waebrania 4:2, “…Lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa hao, kwa sababu halikuchanganyika na imani ndani yao waliosikia.” Kamwe Mungu hatamlazimisha au kumshurutisha mtu. Uhusiano hauna wema ulio nje ya mmoja kwa mwingine. Jambo la kutisha zaidi kuhusu mwanadamu ni ukweli wa kwamba, kama wakala huru wa maadili, mwanadamu ana uwezo kushupaza moyo wake na kuzipinga baraka na makusudi ya Mungu! Leo kama mtaisikia sauti yake, msifanye migumu mioyo yenu. Ninaomba kuwa macho ya ufahamu wako umulikiwe, ili kugundua kipimo kamili cha Mungu ndani yako!

17

Page 18: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

SHERIA YA HIARI YA MOYO

Kutenda vizuri kwa sababu ni wajibu wa mtu ni vema; lakini tendo jema ambalo ni matokeo pasipo sheria ya kuwajibika, hung’aa zaidi kuliko tendo lingine lolote. (Na Thomas Hardy).

Katika Agano jipya, Yakobo ndugu mdogo wa Yesu, anaandika juu ya dhana ya nguvu, anayoiita ‘sheria kamilifu iliyo ya uhuru.’ (Yak.1:17,18,23-25). Kiutendaji, sheria hii inatoa changamoto juu ya namna tunavyofikiri na kujihisi. Yakobo anazungumzia kuhusu neno la kweli linalorudisha nuru ya sura ya uzao wa mwanadamu (mwanzo) kama katika kioo. Analitaja neno hili, linalomtangaza Mungu kuwa ndiye asili ya kweli, sheria kamilifu illiyo ya uhuru. Kumtambua Mungu kama ndiye asili yetu, kunaleta mpango mpya na ubora wa maisha ya hiari ya moyo. Sheria kamilifu ya uhuru katika Kiyunani ni, nomon teleion eleutherias, yana maana ifuatayo: nomon, ni sheria, amri; teleios, ni kamilifu, kamili; eleutherias, ni lisilo na mipaka, mbali na wajibu au kustahili.

Kwa desturi, dini hutangaza na kuinua wajibu wa mtu wa kutazama mwonekano wa kanuni thabiti za mwenendo. Ni katika utii wa ndani tu ambamo mtu anaweza kutaka kujipatia maana. Kwa kadiri tunavyojitahidi kufanya jambo jema, ndivyo hali ya hukumu na hatia inapozidi kwa nguvu na kushindwa. Hata ukifikiria maisha pasipo wajibu, na kuwa na mambo yaliyo mbali na mambo yakupasayo, kunaleta hali ya kutokujali na kutokuwajibika. Kwa kweli sheria hii ya hiari ya moyo ni zaidi ya fikira za kutaka. Lakini matokeo ya sheria hii yanatoa uhakika wa kuwapo kwa maisha ya uwezo wa kukamilika na uhuru, kuwa mkamilifu bila kupungukiwa na kitu. (Yak.1:4). Sisi sote tunajua kuwa uzoefu wa maisha ‘halisi’ yapo katika upinzani mkubwa. Tumekwisha kupokea ukweli wa kwamba sisi hatujakamilika, na hivyo daima kuwa na upungufu.

18

Page 19: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Je, maisha haya ya ukamilifu yanapatikana kwa mtu wa kawaida mtaani, au yamewekwa kwa ajili ya kuhani pekee au kwa ajili ya Papa, au labda kwa Dalai Lama?

Sheria kamilifu ya uhuru haitegemei uwezo wa mtu na utendaji wa nidhamu kwa kutii na kutenda mazoea ya maagizo na amri. Kama ilivyo sheria ya nguvu ya uvutano, sheria hii inafanya kazi kwa hiari ndani ya uwanja maalumu wa mvutano wa ‘sumaku.’ Kuishi chini ya sheria ya Musa au sheria yoyote ya maadili kwa ajili ya jambo husika, hutegemea kikamilifu matakwa ya mtu, na kuwa na kiasi cha kuwa na mwambatano, na kutii mahitaji ya sheria. Kwa hiyo, sheria ya kuwajibika ilifanyika kuwa msingi wa hali ya mtu ya hukumu, hatia, na hisia za kushindwa, kupungukiwa na kuwa duni. Kinachofanya dini ifungwe na sheria hii ni hofu ya adhabu na tumaini la thawabu, kwamba ni wazo la kuepuka jehanamu na kuipata mbingu siku moja, au hisia za uchaji wa Mungu na kusifu na kujulikana sasa. Kila kipimo cha mafanikio yaliyopatikana, yalizaa tabia ‘takatifu zaidi,’ ambayo kwa urahisi ilifanyika kuwa ardhi ya damu kwa ajili ya unafiki. Hitaji la kutambuliwa na kusifiwa lilikuwa muhimu zaidi kwa Mafarisayo kuliko matendo mema. (Math.6:1-8).

Chini ya sheria ya uwajibikaji, utendaji unabaki kuwa wajibu na wala si mtindo wa maisha ya hiari. Juhudi nyingi sana na nguvu zinahusika kwa mtu kujaribu kufanya mambo ambayo yanatumainiwa kumpa sifa ya kukubalika na Mungu. Lakini huzuni ni kwamba, mazoea ya watu wengi ya siku kwa siku, hali ya umbali uliopo kati ya Mwumbaji na kiumbe unabakia kuwa wa kweli. Hatimaye, mwanadamu anaendelea kuwa mpweke kwa njia ya hisia za hatia, unyonge na kukata tamaa, na kubakiwa na tumaini lenye mashaka, kwamba Mungu atawaonea huruma kwa rehema zake, na hatimaye, maskini viumbe wake siku moja atawaingiza katika mbingu yake ya uzuri milele. Hii ina kwamba, ikiwa Mungu yuko. Kwa kadiri tunavyokutana na matokeo madogo ya kiroho, ndivyo kadiri tunavyozidi kutegemea taratibu za mipango yetu na mifumo ya kidini na mapokeo, angalau kuendeleza mchakato wa kwenda

19

Page 20: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

bila Mungu. Kwa kweli haijalishi kile tunachoamini, kwa kadiri tunavyoamini, ndivyo tunavyodhania.

Mungu ni mkuu sana kuliko dini, kwa kadiri tunavyozidi kumjua, ndivyo alivyo mkuu kuliko tunavyoweza kumwelezea. Kuna mmoja alisema, ‘Mtu mwenye kukutana hayuko katika rehema ya mtu mwenye mabishano.’

Mtu anaposhikwa na mapenzi, mara moja hukutana na hali ya kuona sheria ya hiari. Halafu, huwezi kufanya kiasi cha kutosha kumpendeza mwenzi wako; hakuna sadaka iliyo kubwa zaidi, kila kitu hushirikishwa bila unyimivu. Unaanza kumwangalia mtu mwingine kwa macho ambayo ni mapya. Huenda labda hata mlikuwa pamoja lakini kamwe hamkujuana; lakini sasa huwezi kumtoa mtu huyo katika akili yako. Unasisimka kwa furaha ya wazo tu la kuwa pamoja na kushikamana na mmoja ambaye unampenda. Maisha huchukua maana mpya kabisa. Unajikuta kwamba unakuwa mvumilivu zaidi hata kwa watu wanaokuzunguka, ambao kwa kawaida wangekufanya uchanganyikiwe. Tabia yako yote na mtazamo juu ya maisha unakuwa mpya. Maisha ni upeo wa furaha. Watu husema hakuna mtu aliye mkamilifu mpaka aingie katika kupenda!

Ni masikitiko kwamba, ingawa bata anajigonga na kuonekana kutoweka kidogo kidogo, lakini tunaukubali ukweli wa kwamba kamwe maisha hayakukusudiwa kuwa ya hali ya juu daima. Tulikuwa tumeanza kuruka katika hali mpya tuliporudi duniani kwa kishindo. Labda maisha ni kama riadha na kujitahidi, wakati ni wachache tu watakaochaguliwa kufikia mwisho wa taabu!

Kama tunaweza kugundua na kugota ndani ya chanzo cha siri ya uvuvio na huruma, tunaweza kuvunja yale mazoea ya kuendelea katika kushindwa, kukata tamaa na majuto.

Kwa kawaida moja ya mambo manne yafuatayo yanaweza kutuhamasisha:

Hofu ya kushindwa au adhabu. Mvuto wa thawabu au kutambuliwa.

20

Page 21: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Msukumo wa tabia au mazoea. Maisha ya hiari, yaliyovuviwa, huruma isiyo na ubinafsi.

Unaweza kumfanya mtu karibu na kutokufanya chochote, ikiwa utamnyima chakula au kumwogofya kiasi cha kutosha au kumwahidi zawadi kubwa ya kutosha.

Kuna mtu aliyekuwa amembeba mgonjwa kwa mwendo mrefu, wakati mtu fulani alipomwuliza ikiwa mzigo alioubeba haukuwa mzito. Alitoa jibu jepesi, ‘Si mzito, huyu ni ndugu yangu.’ Mtazamo wa mtu huyu ulikuwa na kiini cha sheria ya uhuru. Sheria ya upendo humweka mtu katika uhuru wa maisha yenye kiwango kilicho tofauti. Lugha yake haiwi ya ‘kutakiwa kufanya’ bali ‘kutaka kufanya.’ Kuna tofauti kubwa baina ya nguvu ya kutakiwa na kutaka. Sheria hii inatawala matakwa ya mtu, sio kwa namna ya kuwajibika bali uvuvio na huruma, pamoja na upendo ambao unatamani kumpendeza. Uvuvio wa imani ni nguvu sahihi ya nafsi. Kiwango hiki cha uvuvio hakitokani na maswali ya kujiuliza, bali kwa ufunuo. Imani ya Mungu ndani yako inatangaza thamani yako; thamani iliyotambuliwa huleta huruma. Maisha ya desturi huondoa sehemu ya huruma; desturi hubatilisha huruma; kujihesabu mwenyewe au watu wengine kuwa bure kunatenda mambo yayo hayo.

Kulisikia neno la kweli ni kuona uso wa uzao wako kama katika kioo. Huwezi kuikosoa sura au kuupunguza mfano; hata kuchunguza kwa karibu kila jambo la uumbaji wako wa asili kunabakia kuwa kamili na kuthibitisha kuwa wewe ni mkamilifu pasipo upungufu. Hii ni nguvu ya imani inayoleta furaha ya kushinda upinzani wote. (Yak.1:2-4,17,18,23-25).

MWANZO

Kuamini kuwa Mungu yuko, na kwamba yeye ndiye mwanzo hasa wa kuwepo kwako, kunafanya hatua ya kumfahamu. Kukutana naye uso kwa uso na kuakisi kwa asili yako ya kweli katika kioo iliyohifadhiwa na kutambuliwa katika wazo la chapa

21

Page 22: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

ya Mungu, husababisha nguvu ya sheria hii ya uhuru. Sawa sawa na kifaranga cha bata, mara kinapotambua katika kuakisi kwa mfano wake kwamba alikuwa ni ndege mkubwa.

“Kazi ya sanaa ni kama mwanadamu, kwa kadiri inavyofurahiwa ndivyo kadiri inavyokua na kuwa nzuri zaidi, ikiakisi kipawa cha upendo kama vile mwanga ukirudi kwa mtoaji.” Na Elizabeth Goudge.

Katika kila uhusiano wako, unaanza kwa kugundua thamani na kutangaza thamani ya mtu mwingine. Mungu anapenda ukaribu, na sio umbali. Umeumbwa kuishi maisha yenye utimilifu kabisa. Kutegemezwa, usiri wa ndani na furaha kamili sio madanganyo, bali yenye maana hasa kwako.

Moja ya haki za mwanadamu za msingi kabisa ni kutambuliwa. Tunatamani kutambuliwa. Hakuna kinachoathiri uhusiano au mfano wa sura zaidi kuliko kuhisi kukataliwa na kuhesabiwa kuwa ni bure. Upendo na urafiki huchanua katika mazingira ya kukubaliwa. Uko katika asili ya upendo kuheshimu bila chuki. Hata hivyo, upendo unaweza kufanikiwa hata bila kueleweka, kudharauliwa, mabishano ya ana kwa ana, kuonewa na vita, na bado ukashinda. Kutambua kazi ya mtu maana yake ni kudhihirisha na kuwasilisha thamani. Lakini thamani lazima itambuliwe, iheshimiwe katika kweli, heshima inayozidi ubora wetu, au utendaji mbaya.

Huruma yangu na utume katika maisha ni kuwasaidia watu wa kawaida kuelewa uadilifu wa thamani halisi ya kila mmoja na kuepuka upinzani wa desturi na mapokeo ya kuwapo katika mwili tu. Kuna mambo mawili tunayohitaji kuyajua juu yetu: Sote tunafanana; na bado wakati uo huo sisi sote tu wa kipekee. Hakuna kinacholeta thawabu zaidi kuliko kutambua utu uliomo ndani ya mtu mwingine. Ni kutambua utu ulio ndani yako tu unafananisha mambo haya. Tumetengenezwa kwa mfano mmoja, udhihirisho wa wazo hilo moja. Sahihi ya mwanzilishi wetu na sura isiyoonekana hakuna mahali ilipohifadhiwa au

22

Page 23: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

kuonyeshwa vema kuliko ilivyo ndani ya dhamiri zetu. Asili yetu inafuatisha hasa kusudio la Mungu.

Kila ubunifu huanza na wazo la mwanzo. Sisi tu wazo lake la mwanzo. Sisi tu ubunifu wake. Tunda la uvuvio wa uumbaji wake. Uumbaji wake wa ndani na ndoto ya upendo. (Neno la kwanza katika Biblia, Bereshet, maana yake’ katika kichwa.’) Sisi ni udhihirisho wa fikira zake kuu zilizokuwapo! Mungu alikufikiria! Amka kwa sura yake ndani yako! Kama vile mbegu itungavyo ndani ya tumbo, ndivyo anavyojifunua ndani ya utu wako. Wakati wazo linapoanzishwa, huumba nafasi yake na mwendo.

Wakati wa miaka ya huzuni, mhubiri alisimulia habari ya talanta katika kusanyiko lake, na baada ya ujumbe alimpa kila mmoja aliyekuwepo nusu ya taji. Mara mmoja wa wanawake alikwenda na kununua baadhi ya maua na aliendelea kuoka aina ya biskuti chini ya mazingira magumu sana ya umaskini ndani ya jiko dogo. Watu wachache leo wanaelewa kuwa chipsi za Simba na biskuti za Ouma ambazo wanazinunua katika soko bora na Migahawa kule Afrika ya Kusini, zilikuwa zimefichwa na kulala ndani ya ile nusu ya taji ya kwanza.

Kitu kilicholala bila kazi ndani ya moyo wa kila mwanadamu ni dhamiri yenye nguvu isiyoonekana ya mfano na sura ya Mungu. Katikati ya utu wetu sote tunashiriki mfano pamoja na Mungu, na pia sisi kwa sisi. Kuielewa sura ya Mungu ndani ya kila mmoja ni kutambua asili yetu ya kawaida. Kwa sura ya nje, kila mtu huonekana kuwa tofauti na mwenzake. Lakini unapofikia ndani ya chembe ya uzao wetu, jambo ambalo linaweza kuwatofautisha watu wawili litakuwa ni aslimia moja tu. Ni asilimia 0.01 tu ya uzao wetu hujitokeza kwa mwonekano wa nje; vyovyote vile, iwe kitaifa au kihistoria.

Tunashiriki mambo mengi sana ya msingi ambayo kwa kawaida ni asilimia 99.9 zinazomfanya mtu kuwa rafiki wa mwingine! Hata hivyo, hakika ya kuwa sisi tuko tafauti inatupa thamani zilizo tofauti. Kila mmoja wetu anaweza kufanya mchango wake

23

Page 24: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

wa kipekee ambao hakuna atakayeweza kuurudia au kushindana nao! Maisha yanatafuta udhihirisho wa kipekee ndani yako, mbali na alama za vidole. Kwa kweli wewe ni mtu asiye na mbadala!

Kweli hizi mbili ndizo zilizo msingi na rejea kwa thamani yote ya kweli. Zimefungwa ndani na nguvu yake imekaa ndani ya asili ya mtu, ambayo humpa kila mmoja wetu thamani ya kipekee. Uhalisi huu unaelezea msalaba; Kwani Mungu alijisumbua kupitia njia hii ndefu ya kumwokoa mwanadamu? Thamani ya soko huimarishwa tu kwa gharama ambayo mtu amejiandaa kuilipa. Wema na upendo wa jinsi hii hauwezi kuhesabiwa kwa hali ya huzuni tu kwa kizazi cha wanadamu, au huruma ya Muumba. Mungu aliona hesabu ya thamani ya kutosha ndani ya kila mtu ili kutoa haki ya gharama aliyoilipa kwa ukombozi wa wanadamu kutoka katika dhambi, hatia na hofu. Kwa mafanikio makubwa alikomboa sura yake na mfano wake ndani ya mwanadamu. ‘Ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyofichwa katika shamba, ambayo mtu aliigundua na kuificha; na kwa furaha yake, alikwenda na kuuza vyote alivyokuwa navyo na kulinunua shamba.’ (Math.13:44). Paulo anafunua katika 1Wakorintho2:7,8; kwamba kwa nini hazina ilifichwa. (Angalia sura ya 22, “Siri imefunuliwa”).

Kwa njia ya dhabihu ya kifo cha Yesu Kristo, Mungu alimthibitishia mwanadamu zaidi ya kitu chochote ambacho kingeweza kumwondolea haki au kumhukumu tena. Kosa la Adamu haliwezi tena kushika rehani kizazi cha wanadamu (Rum.5:7,8,12-21). Wanatheolojia wengi ni wepesi wa kuamini kuathirika kwa ulimwengu kutokana na anguko la Adamu, lakini wanashindwa kuutumaini msalaba na kusudi lake lililo kubwa, mbali na malinganisho yote ya dhambi ya Adamu. Mungu anakuamini, ikiwa wewe wamwamini au la! Shilingi iliyopotea kamwe haikupoteza utambulisho au thamani yake. Kupotea kwake kuliizuia tu kuwapo katika mzunguko. “Au kuna mwanamke gani mwenye shilingi kumi, akipotewa na moja, asiyewasha taa na kufagia nyumba, na kutafuta kwa bidii hata aione?” (Luka15:8-10). Katika fundisho lake lingine, Yesu

24

Page 25: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

anatoa mfano wa mwana mpotevu. Usiku mmoja Mungu alinifunulia katika ndoto sura ya mama yangu yenye machozi. Alikuwa amepiga magoti, akifagia nyumba kwa kutafuta sarafu yake iliyokuwa imepotea! “Nionyesheni dinari. Ina sura na anwani ya nwani? Luka 20:20-26. Pia angeweza kusema “Nileteeni mtu….” Sura na kuonekana kwa Mungu imechorwa katika utu wetu wa ndani. “Basi, vya Kaisari mpeni Kaisari, na vya Mungu mpeni Mungu.”

Kwa kadiri unavyozidi kujikumbusha mwenyewe au mtu mwingine juu ya upungufu au kushindwa, ndivyo kadiri unavyojipa nafasi ndogo wewe mwenyewe au mtu mwingine ya kuepuka thamani ya maisha yanayoendelea na uumbaji wako wa asili. Maisha yako yanaweza kuvuviwa na upendo au kutawaliwa na hofu. Walakini, hofu siyo nguvu ya msukumo pekee; ni kukosekana kwa ufahamu wa dhamiri ya upendo. Giza siyo nguvu ya msukumo; ni kukosekana kwa nuru. Lakini tunaweza kuipa hofu nguvu. Tunatoa uzoefu, mazingira, uvumi au nguvu za watu dhidi yetu na namna ya mwitikio wetu kwao. Maudhi, uchokozi, hasira, na kujihurumia ni mitego pekee itakayokudhoofisha. Chochote kilichotokea katika maisha yako kukuletea hasira, uchungu, kujihurumia au majuto, sasa ni mambo yaliyopita na historia; kuendelea kuyatunza mawazo haya ndani yako, yanakutia sumu katika mfumo wako. Msamaha hufungua mtiririko na wema wa uponyaji wa upendo wa Mungu.

Kitabu cha zamani sana katika Biblia kimeandikwa habari ya Ayubu; hapa palikuwa na mtu tajiri sana alijiyenasa katika hofu. Anatoa sababu ya anguko lake: “Maana jambo hilo nichalo hunipata, Nalo linitialo hofu hunijilia.” (Ay.3:25). Akili ya Ayubu ilikuwa katika machafuko na kushikwa na hofu hata kupoteza macho ya kuona kwamba yeye ni nani na alikuwa na nini. Hofu yake ilifanyika kuwa uwanja wa sumaku ulioleta maafa. Hakika hofu ilimfanya Ayubu kupoteza mali zake hata kabla ya kuzipoteza kweli.

25

Page 26: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Mtazamo wa hofu huleta fadhaa, kupungukiwa, uwongo, hitaji, mashaka, shauku, wivu, hasira, unyonge, shuku mbaya, hatia, mkandamizo, kukosa shukurani, ugumu wa moyo n.k. Imani huchochewa na upendo. Upendo huamini. Upendo huthamini uwezo juu ya utendaji au kukata tamaa.

Kwa kadiri unavyoweza kumpata mmoja au mtu wa kumlaumu, unabaki kuwa katika mtego. Kumlaumu mtu au kitu, udhaifu hujipatia nafasi ya utetezi na kubakia kuwa utetezi. Unawekwa huru wakati unapotambua kuwa hakuna awezaye kutwaa thamani ya maisha kutoka kwako, iwapo hakuna awezaye kukuzuia kufikiri mawazo ambayo huvuviwa na ukweli. Kutokujua kwetu na kutokuamini kunatoa nguvu kwa udanganyifu. “Mkikaa katika neno langu, mtaifahamu kweli, nayo kweli itawaweka huru. Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.” Uwana hukuweka huru! (Yoh.8:31-36).

Kama unaweza kuelewa na kuuamini ukweli kuhusu wewe mwenyewe, jinsi gani umekuwa mkamilifu katika roho yako, utatambua kuwa kila kitu ambacho ungekihitaji kukufanya ufurahi, tayari kiko ndani yako. Maisha si juu ya yale unayofanya, bali ni juu ya wewe kuwa ni nani. Mwendo wa maisha yako, kuonekana kwa kazi au mafanikio, hayawezi kamwe kukupa hali kubwa ya kustahili na kuridhika kuliko urahisi wa kujua kuwa wewe ni nani. Hakuna ambacho ungetamani kukipata au kufanikiwa ambacho kingeweza kukuongezea zaidi thamani ya maisha yako. Kujua wewe ni nani ndio kitu halisi kwa wema wote. Kila jambo alilolikusudia Mungu kwako, liko ndani yako na katika yale unayoyafikia. Mungu alijualo kuhusu wewe, ni zaidi ya mambo unayoyatamani mwenyewe. Jinsi tayari tulivyo, ni zaidi ya vile ambavyo tungetamani kuwa! Wewe ni ndoto ya upendo wa Mungu!.

Miaka mingi iliyopita baba yangu alinunua Land Rover. Katika safari yake ya kwanza kutoka nje alipata mkwamo mkubwa katika matope. Tulijitahidi kuikwamua bila mafanikio. Msafiri

26

Page 27: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

mmoja alisimama kwa huruma ili kutupa msaada. Alipoangalia ndani ya kebini, mara alitambua kuwa gia ya 4x4 haikupangwa vema! Kwa muda mfupi baada ya kutambua hivyo, gari lilitoka katika matope. Ulikuwa usumbufu mkubwa sana, lakini lilikuwa ni fundisho kubwa na kufunguliwa. Gari la barabara za vijijini kwa nafasi ya kwanza lilitengenezwa kuhimili mikiki-mikiki, ni jinsi gani ilivyo zaidi kwa mwanadamu! Maisha yana maana, na kuwa jambo la kusisimua. Hakuna awezaye kukuvunja moyo, kukushusha au kukudhalilisha pasipo kibali chako. “Pendo kamili huitupa nje hofu… Katika hili pendo limekamilishwa kwetu… Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini.” (1Yoh.4:16-19). Mungu ameweka thamani juu ya maisha yako ambayo haina mashindano; thamani yako ya kweli si ya mapatano. Kusahau kwamba wewe ni mtu wa namna gani, kila unapokutana na upinzani, ni kujidanganya wewe mwenyewe. Hakuna awezaye kukudhuru zaidi. Wewe ni Roho. Katika hali halisi roho yako haipaswi kubadilika. Lakini akili yako, tabia yako, mwili wako na mazingira yako vinaweza kubadilika. Wewe ni wa milele.

Katika miaka ya 1890 Pierre na Madamme Curie walivumbua Radium. Radium huhamisha nguvu ya utendaji ya redio kwa hiari na kwa kudumu. Chanzo hiki cha thamani ni kama asilimia moja ya milioni iliyomo katika jiwe moja linaloibeba. Hata hivyo jiwe huchukua thamani yake kutokana na hazina ambayo limeibeba. Hivi ndivyo ilivyo kuhusu maisha ya mtu. Hata katika maisha yaliyoharibika na mabaya sana, ni lazima tuamini kuwa thamani ya roho ya mwanadamu inabakia kuwa kamili katika uwezo wake. Maandiko yaliyo katika sarafu yanakifanya kipande cha chuma kuwa malipo halali. Utambuzi wa utajiri wa kiroho hubadili maisha. Imani inajua ukweli kuhusu wewe; imani ni kukubaliana na Mungu kuhusu wewe. Kwa sababu imani inajua ukweli kuhusu mtu, imani inatazamia na inayatia moyo mabadiliko sahihi kwa saburi. Imani huchochea nguvu za kukua na mabadiliko. Imani haivumilii kitu chochote katika akili yako, tabia, mwili au mazingira ambacho hakipatani na uumbaji wako wa asili. Hata tabia za zamani zinatiwa changamoto. Mambo ya

27

Page 28: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

kinyume, na tofauti za kurithiwa na vizazi, zinapoteza nguvu. Imani huumba mazingira ya mabadiliko.

Kuku mwenye kuatamia kwa shida anatunza joto liliopo kwenye mayai yake lisivurugwe, bila kujali changamoto za hali ya hewa au michanganyo yoyote kwa silika (imani) yake ijuavyo. Anaendelea kuona thawabu. Anahesabu vifaranga hata kabla havijaanguliwa. Ingekuwa kosa kusema kuwa hawezi kungoja hata vianguliwe; ndiyo anaweza; anajua! Anakilinda kiota chake kwa uhai wake. Imani sio kukosa hisia; imani inajua.

“Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.” (Mith.4:23). Furahia yaliyomo katika moyo wako kuliko thamani zote. Kila uwezo unaokubalika wa maisha ndilo fungu lako. Moyo wako unashika siri ya mwanzo na asili ya uhai wako. Tazamia maisha yanayotokana na thamani za moyo wako. Moyo hushikilia hazina kwa wazo na maneno kama mtofaa (apple) unavyoshikilia matunda yake kwa mwenye njaa. Mawazo unayofikiri hufanyiza nguvu ambazo huamurisha matokeo ya uzoefu wako wa siku kwa siku. Tengeneza kielelezo cha wazo ambalo hutoa picha ya maisha ya baadaye. “Maisha ya mtu yatakuwa ni ya tabia ya mawazo yake.” Na John G. Lake.

“Ni wazo la kitabia linalojiumba ndani ya maisha yetu na kutuathiri zaidi hata kuliko uhusiano wa ndani wa kijamii unavyoweza kufanya kazi. Marafiki zetu wa siri hawana cha kufanya zaidi katika kuyachonga maisha yetu kama yalivyo mawazo tunayoyatunza.” Na Teale.

Mtazamo wenye dhamiri ya thamani utaendelea kuvunja katika maisha yako na mivuto ya nia, ambayo labda ingeweza kukuzuia katika kukumbatia ubora wa maisha. Mawazo yako ndipo patakatifu pako, nafasi takatifu na mahali pa siri.

Mawazo yetu ni ukimya wa maneno ambayo ni Mungu tu pamoja na sisi tunayasikia, lakini maneno hayo yanaathiri utu

28

Page 29: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

wetu wa ndani, afya yetu, furaha yetu na mwenendo wetu mzima. [Na asiyejulikana].

Imani inasema kweli kuhusu wewe. Imani huwasilisha tu ambayo hutokana na upendo. Badala ya kulaumu, hubariki; badala ya kulalamika, husifu. Hata kushindwa kukubwa huhisi kutiwa moyo na kupewa changamoto kuliko kutishwa au kuhukumiwa katika uwepo wa imani. Yesu alijulikana kuwa rafiki wa wenye dhambi. Hakuna aliyejihisi kuhukumiwa au kuonekana hana thamani. Aliwahukumu tu wanafiki na wasioamini.

Imani inasamehe; msamaha huona mbali zaidi ya maumivu au kukatishwa tamaa. Huchochewa na upendo, msamaha hufuta yaliyopita, unaangalia yajayo na kubadilisha yaliyopo. Msamaha hupendelea ambayo imani inayajua. Kutokutaka au kutokupenda kuwasamehe wale ambao wamekukosea, kutazuia baraka za Mungu katika maisha yako na kukuvuta, kukuchelewesha au kuharibu hatima yako. Chuki na uchungu kutakuingiza katika maisha yasiyozaa. Badala ya kuleta faraja yoyote, ni majuto na lawama tu vinazidisha maumivu. Imani inashinda kuvunjika moyo. Mengine unapata, mengine unajifunza; na kujifunza kwako kote unapata ufahamu. Imani huifadhi wazo la kipekee na kwa moyo huwasilisha shukurani kuthamini, upendo na thamani.

Maisha ya baadaye yanapatikana tu katika moja ya viwango viwili: utimizo au mvunjiko. Utimizo huanza na kuthamini. Shughulisha akili yako kwa shukurani badala ya shutuma na majuto. Tunda la kushukuru ni kuridhika na furaha; hili litakuweka mbali na chuki, husuda, mashindano au mabishano. Kuridhika kunajengwa juu ya kujua wewe ni nani hasa, kunakuweka mbali na vitisho. Mashindano, majaribu na kuvunjika moyo havitakuingilia wala kukuchanganya. Ipalilie tabia ya shukurani. Leo ni zawadi yako; kila muda unahitaji kusheherekewa, shukurani ni kichocheo cha furaha. “Shukurani hufungua utimilifu wa maisha; inaweza kugeuza mlo kuwa

29

Page 30: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

sherehe, nyumba kuwa nyumbani, mgeni kuwa rafiki.” Na Melody Beath.

“Nafsi iliyoshiba hukinai sega la asali; bali nafsi yenye njaa huona kila kitu kichungu kuwa kitamu.” (Mith.27:7). Hakuna kinachokufanya kushindwa zaidi kuliko kuongozwa na hali ya uhitaji na kupungukiwa. Hakuna kinachokufanya mzuri zaidi na thabiti kuliko hali ya utimizo kamili. Kujua kwamba sisi ni nani hasa na ukuu unaokaa ndani yetu ni mbali na ulinganifu wote kwa uongo wa upungufu na hitaji.

Wema wenye maana kuu sana na wa msingi kwa wanadamu sio uwezo wa akili zao, wala ujuzi wa teknolojia au mafanikio, wala udhihirisho wao wa maendeleo ya kisasa na mawasiliano, bali uwezo wa kila mmoja kuelewa na kuakisi chapa ya sura na mfano wa Mungu! Umbo lako kuu sio mvuto wa sura au jinsia ya mwili wako au umaarufu wako au gari la fahari, bali utukufu wake, wazo lake likionekana ndani yako! Ushawishi huu hufanyika kuwa ufahamu ndani yako unaofanya maisha yako kutokushindwa na mvuto!

Sisi wenyewe tunaweza kuwa na mambo ya kufurahisha mawazo ya Mungu kuhusu sisi tulivyo wa pekee.

‘KIOO, KIOO, UKUTANI…’

“Mbele za uso wako (Kiebrania: ana kwa ana na wewe) ziko furaha tele.” (Zab.16:11). Furaha tele ni kuona uso wa Baba katika kioo ukionekana katika macho yake. Hili lilikuwa wakati, katika filamu iitwayo ‘Mfalme Simba’ mtoto alitambua utambulisho wake wa kweli.

‘Kwa kupenda kwake mwenyewe alituzaa sisi kwa neno la kweli… kwa kuwa kila asikiaye neno hili, ni kuona uso wa uzao wake ukionekana katika kioo.’ (Yak.1:18,23-25). Neno la kweli ni neno linalobeba chapa ya uumbaji wa mtu wa asili, na

30

Page 31: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

kutangaza thamani halisi ya mtu. Ukijiona kwa njia hii, halafu ukaondoka na kusahau kuwa wewe ni mtu wa namna gani unapokutana na upinzani wa kwanza, ni kujidanganya nafsi yako. Kusahau kwamba wewe ni mtu wa namna gani hakubadilishi jinsi ulivyo, lakini kwa kweli kunakupa kikomo. Huku ni kupoteza maisha ya thamani! (2Pet.1:8,9). Kwa muda ambao upinzani unaonekana kuwa ni wa kusadikika kuliko ukweli. Unabakia uamuzi wako, unaokuhimiza kushikilia kweli.

“Lakini aliyeitazama sheria kamilifu (parakupto) iliyo ya uhuru, na kukaa humo (parameno) asiwe msiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi (aliyevuviwa na kutambua yeye ni nani hasa) huyo atakuwa heri katika kutenda kwake” (Yak.1:23-25). Badala ya kujitahidi kutenda yaliyo mema kutokana na hali ya sharti na wajibu, utendaji unakuwa ni wa furaha. Kutenda mambo kwa kujitahidi, maana yake ni kushindwa kuona. Kutenda kwa moyo moja kwa moja kunahusiana na kutambua au kuelewa uwezo wa utambulisho wa kila mtu na thamani yake. Sasa utendaji unakuwa ni tunda la kuhitimisha mambo.

Kutazama katika mwanga wa sura ya mwanzo wako na asili ya kweli, na kuona ukamilifu wake kama katika kioo, huleta sheria kamilifu ya uhuru. Ni sawa na kuchukua sarafu ya zamani yenye kutu na uchafu na umri mkubwa, na halafu kuisafisha sarafu, ili kuyatambua maandishi yake ya asili kuwa bado ni kamili!

Parakupto, ni kuegemea na kujiinamisha chini kama kuchungulia ndani na kujifunza kwa uchunguzi wa kutumia kiona mbali. Parameno, kubaki chini ya msukumo wake. Hili linaelekeza kuvutwa na kitu, kufikia hatua ya kuwa mzoefu, na hatimaye kubakia ndani ya eneo la sumaku la kuvutwa na nguvu ya uvutano ya maono haya. (Yak.1:25).

Katika eneo lolote la kujifunza, kumekuwapo shule mbalimbali za wazo fulani. Muda mwingi, nguvu na kipaji vimewekezwa kupanua na kutoa haki na kuunga mkono fundisho maalumu. Matoleo yameandikwa na vita vimepigwa vya kuzuia ushawishi.

31

Page 32: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Haki huwa sababu ya kulihesabia haki tendo ambalo linaaminika. Makundi ya watu huishi na kufa mara kwa mara katika ufuatiliaji mgumu wa mambo ya uongo.

Mwanafunzi wa muziki yeyote aliye makini atatafuta kuelewa na kutafsiri kipande kimoja kwa uangalifu bila kuharibu wazo la asili na mwendo mzima kutoka kwa mtunzi wa wimbo. Kupata hitimisho lenye usahihi katika somo la asili yetu, kutahusisha na kuchunguza juu ya Mungu kama alivyo, ili kutazama kwa kupitia macho yake na kustajabia mpango wake wa mbele. Wosia binafsi au imani ya kijadi haina msingi wowote dhidi ya upya wa chemchemi ya wazo lake. Neno la kweli linahifadhi kwa usahihi wazo lake la asili ndani ya mioyo yetu.

Yesu alivuvia kiwango cha kusikia na kutenda juu ya neno lake ambacho kingelifananishwa na mtu aliyechimba chini sana ili msingi wa nyumba yake ukae juu ya mwamba. Nyumba hii inaweza kusimama dhidi ya dhoruba na mashambulizi ya namna yote. Mwamba unaelezea tabia yake kwa njia ya msingi unaofanya muundo kuwa sawa na mwamba ambao umejengwa juu yake. (Math.7:24-27). Tambua utambulisho wako, “Uangalieni mwamba ule ambao mlitolewa kwa kuchongwa.” Mwamba unahifadhi kielelezo na chapa ya uumbaji wetu wa kwanza. (Isa.51:1). “Simoni mwana wa Yona, nami nakuambia, wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu.” (petros = sehemu ya mwamba kutokana na petra = wingi wa mwamba). “Mpeni ukuu Mungu wetu, yeye ni Mwamba, kazi yake ni kamilifu. Je, yeye Baba yako aliyekuumba, Amekufanya na kukuweka imara? Lakini humkumbuki Mwamba aliyekuzaa, Mungu aliyekuzaa umemsahau.” (Kumb.32:3,4,6,18). Ukuu wa mfinyazi mkuu umedhihirika katika kazi ya mwanadamu. “Kazi yake ni kamilifu!” (:4) “Sisi tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu.” (Ef.2:10). “Na nyumba ilipokuwa ikijengwa, ikajengwa kwa mawe yaliyokwisha kuchongwa chimboni; wala nyundo, wala shoka, wala chombo cha chuma chochote, sauti yake haikusikiwa ilipokuwa ikijengwa nyumba.” (1Wafal.6:7). “Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya

32

Page 33: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Roho….” (1Pet.2:5). “Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka. Kwa kupenda kwake mwenyewe alituzaa sisi kwa neno la kweli. Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo. Lakini anapokutana na jaribu (:2) ndipo hutenda kinyume na uumbaji wake, mara husahau jinsi alivyo na kujidanganya mwenyewe.” (Yak.1:17,18,23,24). Kuelewa kwamba sura ya Mungu imehifadhiwa katika roho ya mwanadamu, kama vile alama ya maji iliyo katika makaratasi, ndivyo ulivyo wakati wa kuijua kweli. Kutambua na kuheshimu mwanzo wako wa kweli na asili yako hufanya kisiwepo kitu chochote cha kuushawishi uumbaji wako wa asili.

Upendo, furaha, amani, uvumilivu, wema, upole, uadilifu, unyenyekevu na kiasi si mambo ya kuharibika, misisimko inayozimika, inayotokana na matakwa ya mtu. Hayo ni tunda la mambo unayoyajua ndani ya roho yako kuwa ni kweli kuhusu hali yako. Tunda si juhudi za mtu, ni udhihirisho wa moyo wa tabia ya mti. Ufahamu huu huleta sheria kamilifu ya uhuru. “Juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.” (Gal.5:13-15,22,23). Thamani hizi za tabia si thawabu ya juhudi kubwa na nidhamu miongoni mwetu, wala si madanganyo ‘ya hewani, fikira za matakwa ya mtu.’ Kwa kweli, huonyesha kabisa asili na chapa yetu, sura ya kioo ya asili yetu.

Mapenzi ya Mungu ni kufunua ndani yako hazina yenye utajiri usiopimika. Utajiri unaozidi maombi ya mahitaji maarufu! Kuna tofauti kubwa kati ya fikira za matakwa na ukweli wa mtu. Watu wengi wamenaswa katika ujinga wa kujitahidi kuwa vile ambavyo tayari wamekwisha kuwa! Hakuna litakalokufurahisha zaidi kuliko kujua na kuamini ushuhuda wa kweli unaokuhusu wewe. Maisha ya mvuto mkubwa unayoweza kuishi ni dhamiri ya maisha juu ya jambo hili. Maana kamili ya ukweli huu itawale katika nia na mazungumzo yenu. Kama vile usukani mdogo uzungushavyo na kuongoza chombo kizito, ndivyo mawazo na mazungumzo kuhusu hali zetu yanavyotawala hatima yetu juu

33

Page 34: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

ya bahari ya maisha. Uangaliaji wa mali dirishani unakusumbua tu kwa ndoto na shauku usizoweza kuzifikia. Walakini, kutazama sura yako katika kioo, kunafunua uhalisi wa asili yako ya kweli, sura na mfano wa Mungu ndani yako. (2Kor.3:18). Uone katika huo mtazamo mtakatifu, uso wa uzao wako ulioumbwa ndani ya wazo lake kabla ya wakati haujakuwako.

Kujitahidi kuupata upendo, amani na furaha; au kumwomba Mungu akupe thamani hizi zote, ni kupoteza nguvu za kidini. “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa….” (Hos.4:6). Ufahamu hutokea kwamba Mungu anahitaji kunenwa kwa kufanya mambo kwa ajili yetu. Kutambua uwepo wake na asili yake ndani yako, ndiko kunakokuweka wewe kuwa huru kama vile ulivyo. Kwa kadiri tunavyozidi kumjua Mungu ndani yetu, ndivyo kadiri tunavyozidi kushinda katika hali ya utimilifu na ukamilifu. Tunahitaji kuondosha hali isiyo na maana. Yeye si Mungu aliye mbali; Imanueli maana yake, “Mungu yu pamoja nasi.”

Hakuna unachoweza kutafuta kufanya au kutaka kwa kuomba, kinachoweza kukupa maisha mazuri. Hakuna kitakachoweza kuyafanya maisha yako yawe ya maana zaidi kuliko kuwa na ufahamu wa asili yake na uwepo wake ndani yako na upendeleo wake kwako.

Maombi na kuabudu kwetu sasa hupatana katika umoja na kuakisi kwa milele na kupaa kwa sifa za duniani; kusujudu si kwa wanadamu tu bali hata viumbe vyote. (Na E. Goudge)

Kama wimbo wa ndege au harufu ya maua na uvumba, kila dakika, kuna chembe-chembe na mtetemo wa atom ambao una sauti, ya kumheshimu Muumba. Sikiliza! Pamoja na ukimya sauti zao husikika kama sauti ya maji mengi, radi yenye nguvu.

34

Page 35: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

KUFANYIKA MWILI

Mungu huwafurahia wanadamu. Utukufu wake unazidi vitu vyote ambavyo huenda vingeweza kumshusha mtu. Amebomoa kila ukuta wa kila uadui na kila sababu ya kujiona kuwa mbali naye. Miaka mia saba kabla ya Kristo, nabii Isaya alitangaza, “…. Itengenezeni nyikani njia ya Bwana; Kila bonde litainuliwa, na kila mlima na kilima kitashushwa; Palipopotoka patakuwa pamenyoka, na palipoparuza patasawazishwa; Na utukufu wa Bwana utafunuliwa; Na wote wenye mwili watauona pamoja.” (Isa.40:4,5; Luka 3:4-6). Jangwa ni tunda la laana, kamwe haikukusudiwa kuwa ndio hatima ya mwanadamu.

Mungu anaongea lugha ambayo wenye mwili wote wanaielewa. Katika Kristo, Mungu anafunua njia mpya ya kuishi. Neno lililofanyika mwili humfanya Mungu asiyeonekana, kuonekana na kwa hali iyo hiyo huonyesha katika kioo cha sura ya mwanadamu. (Kol.1:15-23). Kufanyika mwili ni njia kuu ya Mungu! Sasa, sababu yoyote ambayo labda tungekuwa nayo kuendelea katika maisha ya ukame wa kiroho, upweke, dhambi, kutostahili, hatia na unyonge imefutwa. Wanadamu hawanaswi tena jangwani; kuna njia kuu ya kuepuka.

Katika Yohana 14:2 anatabiri jinsi ambavyo kifo na ufufuo wake vilivyoweza kutuandalia mahali, ili tuweze kuwa mahali alipo, yeye pamoja na Baba yake, amefungwa katika umoja pamoja naye. Kwa njia hiyo, Yesu alikuwa hajifanyi kuwa mkandalasi wa majengo mbinguni. Hayuko katika shughuli ya kujenga makao, kama fasiri nyingine zinavyomaanisha! Katika kifo na ufufuo wake aliandaa mahali kwa ajili yetu, penye umoja wenye usiri pamoja naye pia na Baba. Filipo anahisi kuwa kama angeweza kumshawishi Yesu ili awafunulie Baba tu, na ingetosha. Yesu anajibu, “Aliyeniona mimi amemwona Baba….Siku ile ninyi mtatambua ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu, nanyi ndani yangu, nami ndani yenu.” (Yoh.14:2,8-12,20). Wakati mwingine wazo la Mungu wa utatu linatuchanganya. Kufanyika mwili hakukuingilia au kugawa umoja wa Mungu. Katika baadhi ya desturi za kipentekoste

35

Page 36: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

tumefundishwa juu ya Roho Mtakatifu kwa njia ambayo karibu inamwondoa kabisa kutoka kwa Mungu Baba na Mungu Mwana. Wakati Yesu anapotutambulisha kwa Roho Mtakatifu, anamfunua kama kuonekana kwake katika kioo sawa na yeye mwenyewe, alivyo kioo cha kuonekana kwa Baba! Anasema katika Yohana 14:18, “Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu! Sura ya kioo inatupa maelezo ya usahihi; mmoja anamfunua mwingine, bila wasiwasi! Huu ni umoja wa milele. Wanamuziki wa ulinganifu wa sauti, kila kifaa kinaakisi sauti ya kingine. “Maana kwa ajili yetu amezaliwa mtoto, Naye ataitwa jina lake:..Baba wa milele!’ (Isa.9:6). Ufunuo wa Mungu kama Baba, asili ya kweli ya mwanadamu, ndio kiini kikuu cha Injili. Vile alivyo Yesu na yote yaliyokamilishwa, yanathibitisha jambo hili.

‘Nuru ya Injili ni utukufu wa Kristo, ambaye ni mfano wa Mungu. Na sisi sote tunautazama utukufu wa Bwana kama katika kioo, tukibadilishwa katika sura yake. Mungu ambaye alisema, ‘Nuru iangaze katika giza, imeangaza ndani ya mioyo yetu ili kuleta nuru ya ufahamu wa utukufu (shauri) wa Mungu katika uso wa Kristo!’ Katika uso wa mwili, Kristo hufunua shauri la Mungu juu ya mwanadamu! (2Kor.3:18; 4:1-7). “Lakini tuna hazina hii katika vyombo vya udongo.” Mungu anaona mwili wako kuwa chombo cha thamani!

Kufanyika mwili kunafunua kwamba neno lilipofanyika mwili, Mungu alirejesha miliki iliyopotezwa na Adamu. Mungu alirejeza udhihirisho wa sura yake na uwepo wake katika hekalu la udongo. Hakuna tatizo la kuwa chombo cha udongo! Mwili wa kibinadamu sio mpango wa B; sababu za unyonge ambazo zitatakiwa kuwa badala ya kukosekana kitu fulani kilicho bora. “Katika Kristo kuna kila kilicho cha Mungu ndani ya mwili wa mwanadamu” (Na Kenneth Taylor). ‘Ndani yake yeye tunaupata ukamilifu; yeye ni kichwa cha chemchemi ambamo enzi yote na mamlaka vinakaa.’ (Na Knox. Kol.2:9,10). Sisi sote tumepokea utimilifu wake. (Yoh.1:14,16). Chombo hupata thamani kutokana na hazina ambayo kimeibeba! Hivi karibuni niliuza gari aina ya Isuzu kwa R 18,000. Nilipolitoa lile gari, yule mtu alinilipa fedha taslimu zikiwa katika bahasha chakavu rangi ya

36

Page 37: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

kikahawia. Niliikunja na kuiweka mfukoni. Kaptura ya khaki niliyoivaa niliinunua kwa R 79.99; sasa kwa ghafla kulikuwa na gharama ya R 18,079.99!! Ukweli huu na matokeo ya kutambua huku, kutashinda katika ulimwengu!

“Na utukufu wa Bwana utafunuliwa , na wote wenye mwili watauona pamoja!” (Isa.40:5). “Kwa maana dunia itajazwa maarifa ya utukufu wa Bwana, kama maji yaifunikavyo bahari” (Hab.2:14). “Taa ya mwili ni jicho; basi jicho lako likiwa safi, mwili wako wote utakuwa na nuru.” Ufunuo wa kufanyika mwili kwa Kristo utakuangaza mwili wako wote. (Math.6:22).

Katika Mathayo 16 tunasoma jinsi jina la Simoni lilivyobadilishwa kuwa Mwamba (Petro) wakati alipomkiri Yesu kuwa ni Mwana wa Mungu aliye hai. Na wakati ule ule alitambua asili yake ya kweli na utambulisho, mbali na ule wa baba yake wa mwili, yaani Yona, alipogundua Mwamba ambao mwanadamu alichongwa kutoka ndani yake. (Kumb.32:18; Isa.51:1; 1Wafal.6:7).

Baada ya kuangalia na kuzungumza juu ya maana ya ufunuo kama huu kwa kirefu, yeye pamoja na wavuvi wawili, Yakobo na Yohana, walialikwa kujiunga na Yesu juu ya mlima mrefu, siku sita baadaye (Math.17:1-9). Mara walipofika kileleni, Yesu anabadilika mbele yao; sura yake ikang’aa kama jua, na mavazi yake yakametameta kama nuru; na tazama wakatokea Musa na Eliya, wakizungumza naye. Siku sita baada ya Simoni kutambua utambulisho wake mpya katika ufunuo wa Kristo, Mungu alimfunua mtu katika sura yake, kwa mfano ule ule aliofanya siku ya sita katika Mwanzo sura ya kwanza, wakati ule kwa mara ya kwanza katika historia ya ulimwengu, Mungu asiyeonekana alipojionyesha katika mwili wa nyama na damu.

Adamu na Hawa walipoteza utukufu na kuanguka kutoka katika utaratibu wa maisha, na kudumaa na kulala katika roho zao. Bali katika Kristo, utukufu ule ule unarudi katika mwili wa kibinadamu. Sasa Yesu ndiye udhihirisho kamili katika nafsi moja ya harufu ya wazo la Mungu kuhusu utambulisho wa kweli

37

Page 38: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

wa mtu na ukombozi, kama ulivyoelezwa katika torati na manabii. (Ebr.1:1,2). Wakati huu sio kuonekana kwa sura na mfano wa Mungu katika nafsi tofauti, bali Mungu mwenyewe anaonekana akiwa katika mwili. Siku ya saba iliyo mpya ya milele itapambazuka, ambayo ni sabato mpya. Mwanadamu sasa anaalikwa kujiunga na Mungu katika pumziko lake. Mungu hachoki; pumziko lake ni la juu zaidi sana kuliko siku kuu maalumu; ni sherehe ya milele ya ukamilifu wa yote aliyoyakamilisha kwa ufanisi; wakati msanii mkuu anaongeza mguso wake, kazi yake bora inafunua mambo yote. “Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu.” (Ef.2:10). Pumziko la Msanii ni sherehe ya kuridhika. “Atakushangilia kwa furaha kuu, Atatulia katika upendo wake, atakufurahia kwa kuimba.” (Sef.3:17). Neno la Kiyunani kuhusu upendo, agape linatokana na maneno mawili: ago, lenye maana ya kuongoza kama mchungaji aongozavyo kondoo wake; na pao, lenye maana ya kupumzika! (Zab.23). “Leo kama mtasikia sauti yake, msifanye migumu mioyo yenu.” (Ebr.3:13-19; 4:1-11). Sasa ndio utimilifu wa wakati. Sasa ndio wazo la milele, sio wazo la wakati. Kila wakati katika historia ya mwanadamu, ni sasa ya Mungu; pia kila wakati ujao wa mwanadamu, ni sasa ya`Mungu! Wakati ambao kila mmoja anaikumbatia sauti yake, ndio sasa ya mkakati wake wa milele inapoanza kufunguka.

Ukombozi ni kitu halisi. Mungu alifuta kila dai halali dhidi yetu katika mwili wake wa nyama alipoangikwa msalabani. (Kol.2:14,15). Aliondoa madai na utawala wa mshitaki wetu (Shetani) juu ya mwili wa mwanadamu! Hukumu ya Mungu ya milele katika upendeleo wa mwanadamu ni zaidi ya mabishano na hoja isiyo na mjadala. “Maana, upendo wa Kristo watubidisha; maana tumehukumu hivi, ya kwamba mmoja alikufa kwa ajili ya wote, basi walikufa wote….Hata imekuwa , sisi tangu sasa hatumjui mtu awaye yote kwa jinsi ya mwili.” (2Kor.5:14,16). Mbali na mapendekezo yote ya matokeo ya kosa la Adamu, ni matokeo ya kipawa cha neema yake katika Kristo Yesu. (Rum.5:15-19).

38

Page 39: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Kama Mwimba zaburi na mchaji wa Mungu, Daudi, alijua uwepo na mpango wa Mungu. Roho ya unabii ilimfunulia kuugua na mateso ya Kristo juu ya msalaba miaka mia nyingi kabla ya tukio kuu la kihistoria halijatokea. “Mungu wangu, Mungu wangu, Mbona umeniacha? Mbona U mbali na wokovu wangu, na maneno ya kuugua kwangu? Ee Mungu wangu, nalia mchana hujibu, na wakati wa usiku, lakini sipati raha. Nimemwagika kama maji, mifupa yangu yote imeteguka, moyo wangu umekuwa kama nta, na kuyeyuka ndani ya mtima wangu. Nguvu zangu zimekauka kama gae, ulimi wangu waambatana na taya zangu; unaniweka katika mavumbi ya mauti. Kwa maana mbwa wamenizunguka; kusanyiko la waovu wamenisonga; wamenizuia mikono na miguu. Naweza kuihesabu mifupa yangu yote; wao wananitazama na kunikodolea macho. Wanagawanya nguo zangu, na vazi langu wanalipigia kura! Tumemdharau na kumkataa, bali yeye hakulidharau teso la mteswa, wala hakuchukizwa nalo; wala hakumficha uso wake, bali alipomlilia akamsikia. Wapole watakula na kushiba. Miisho yote ya dunia itakumbuka, na watu watamrejea Bwana; jamaa zote za mataifa watamsujudia. Maana ufalme una Bwana, naye ndiye awatawalaye mataifa. Wakwasi wote wa dunia watakula na kusujudu, humwinamia wote washukao mavumbini. Wazao wake watamtumikia; zitasimliwa habari za Bwana, kwa kizazi kitakachokuja. Nao watawahubiri watakaozaliwa haki yake, ya kwamba ndiye aliyeyafanya. (Zab.22). Ni ajabu sana kujua kwamba Zaburi ya 23 inakuja baada ya Zaburi ya 22! Ushindi wa msalaba unasherehekewa. “Sitapungukiwa na kitu….Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya” (Zab.232:4). Miaka mia saba kabla ya kutokea katika historia yetu, Isaya anauona mpango wa Mungu, siri ambayo hakuna mmoja wa watawala wa giza aliyeweza kuielewa. Maana kama wangaliijua, wasingalimsulubisha Bwana wa utukufu, wangemwacha asije akajichubua mguu wake katika jiwe!” (1Kor.2:8-10). Kwa sababu ya sheria ya kufanyika mwili kwa Kristo, kila jambo lililotokea kwa Yesu, mara moja liliwajumlisha wanadamu wote. Mwanadamu ameshirikishwa milele katika Kristo. (Ef.1:3,4). Neno la kushirikisha lina maana ya kutokea

39

Page 40: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

pamoja katika umoja wa karibu, kama kushikanisha kwa njia ambayo, hatimaye mmoja wapo akiingizwa akilini, wengine huwa tayari kuletwa katika wazo. Hili lina maana kwamba haiwezekani kwa Mungu kufurahia wazo la Mwana wake, na kwa wakati uo huo kumtenga mwanadamu! Katika nia ya Mungu, tumeshirikishwa katika Kristo kwa maana ya usawa! “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya!” Ni muhimu kuelewa kwamba neno “ikiwa” katika mtiririko huu, si neno la sharti bali ni hitimisho! Hatuko “ndani ya Kristo” kwa uchaguzi binafsi, “kwa Mungu mmepata kuwa katika Kristo, ambaye Mungu alimfanya kuwa ukombozi wetu, haki yetu na utakaso.” (1Kor.1:30). “Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye alitupa huduma ya upatanisho; yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho. Basi tu wajumbe kwa ajili Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu.” (2Kor.5:17-20).

Dhambi iliwapotoa na kuwageuza wanadamu kutoka katika mfano wao wa kweli. (Wafil.2:15). Tulikusudiwa kuonyesha ukamilifu wa uzuri bila waa au kovu la makosa. Sasa, yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika yeye. (2Kor.5:21). “Kama vile walivyokustaajabia, (uso wake ulikuwa umeharibiwa sana zaidi ya mtu yeyote, na umbo lake zaidi ya wanadamu), ndivyo atakavyowasitusha mataifa mengi; wafalme watamfumbia vinywa vyao; maana mambo wasiyoambiwa watayaona; na mambo wasiyoyasikia watayafahamu.” (Isa.52:14,15). “Ni nani aliyesadiki habari tuliyoileta? Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani? Maana alikua mbele zake kama mche mwororo, na kama mzizi katika nchi kavu; yeye hana umbo wala uzuri; Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani. Alidharauliwa na kukataliwa na watu; mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu. Hakika ameyachukua masikitiko yetu, amejitwika huzuni zetu; lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, amepigwa na Mungu, na kuteswa. Bali

40

Page 41: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

alijeruhiwa kwa makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu; adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.” (Isa.53:1-5). “Ataona mazao ya taabu ya nafasi yake, na kuridhika. Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye haki, atawafanya wengi kuwa wenye haki; naye atayachukua maovu yao.” (Isa.53:11). Tunaishi katika kipindi ambacho kimegeuzwa kutoka katika mfano wake wa kweli, tukiangaza kama nguzo za nuru. (Wafil.2:15).

Juu ya mlima wa kugeuka sura, Musa hakuona tena ahadi kutoka mbali; aliangalia katika macho ya Kanaani ya Mungu. Nchi ya ahadi siyo anwani ya kijiografia iliyo juu ya sayari, bali ni mtu mpya mmoja ambaye anawakilisha na kukumbatia kizazi chote cha wanadamu!

Kipindi chote cha torati na manabii kimewakilishwa katika Musa na Eliya. Waliona wakati huu na kutangaza maana yake. “Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi. Mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu. Yeye kwa kuwa ni mng’ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu.” (Ebr.1:1-3). Neno hili lililofanyika mwili ndio kikomo cha wazo la Mungu; uwana ni tamko dhahiri la nia ya Mungu. Hebu fikiri, Mungu akitafuta neno, linalofaa kushika hatima ya wazo lake; Neno la mwisho, la undani wa milele kwa mwanadamu. Analifanya neno hili siyo kwa lugha ya kale ya wanadamu au malaika, bali katika chombo cha udongo, Yesu, Adamu wa mwisho, mtu mpya, na kwa wakati uo huo, kuangaza kwa kioo kwa utimilifu wa Uungu wake katika mwili wa mwanadamu. Lugha ya Mungu ni uzima katika mwili ambao unafunua utukufu wake. (2Kor.3:3). Mungu alisema kila jambo na kutokea, lakini akiisha kumwumba mtu kwa sura yake na mfano wake, sasa anautengeneza mwili wa udongo kwa mikono yake kutoka katika mavumbi ya ardhi. “Lakini sasa, Ee Bwana, wewe U Baba yetu; sisi tu udongo,

41

Page 42: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

nawe u mfinyanzi wetu; sisi sote tu kazi ya mikono yako!” (Isa.64:8).

(Katika mwaka wa 1947, kijana mchungaji wa kondoo Bedouin kule Uarabu, aligundua magombo katika vyungu vya udongo ndani ya pango! magombo haya yalihakikishwa kuwa ni ya zamani sana na yalikuwa maandiko halisi, ili kuthibitisha uadilifu wa kihistoria wa Isaya na vitabu vingine vingi vya Biblia. Zaidi ya magombo (scrolls) 800 yanawakilisha maktaba ya maandiko yaliyofichwa katika mapango karibu na Qumran wakati wa kuvunjika kwa vita baina ya Wayahudi na Warumi mwaka wa 66 B.K. Maktaba hii, ilikuwa ya kundi lililoitwa Essenes lililoongozwa na kuhani aliyeitwa “mwalimu wa haki.” Leo, udhihirisho halisi na dhahiri wa uwepo na nafsi ya Mungu, ni uzima wake uliohifadhiwa na kufunuliwa pia katika chombo cha udongo, mwili wa mwanadamu. (2Kor.3:2).

Miaka mingi baada ya kugeuka sura juu ya mlima, Petro anaandika, “Katika habari ya wokovu huo manabii walitafuta-tafuta na kuchunguza-chunguza, ambao walitabiri habari za neema itakayowafikia ninyi. Wakatafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwako baada ya hayo. Wakafunuliwa ya kuwa si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yenu walihudumu katika mambo hayo, ambayo sasa yamehubiriwa kwenu na wale waliowahubiri ninyi Injili kwa Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni. Mambo hayo malaika wanatamani kuyachungulia.” (1Pet.1:10-12).

Kazi ya Mungu ya ukombozi ina nguvu kwa matokeo ya haraka. “Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe.” (2Pet.1:1,3). Petro anamtakia kila mwamini kukutana na Yesu mwenyewe, ili kumjua kuwa yeye ni nani hasa, na wala sio kama mtu asiyejulikana, aliye mbali na wa kihistoria tu. Anaandika katika waraka wake wa mwisho kwamba alikuwa hafuati hadithi

42

Page 43: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

zilizotungwa kwa werevu, bali ulikuwa ushahidi wa kuona kwa macho ukuu wake; aliona mwili wake ulipobadilika kuwa nuru na kusikia sauti mlimani siku ile; “Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.” Sasa neno la unabii limethibitishwa bila mashaka. Tunaweza kuhoji, ‘sawa, hayo ni mambo makuu kwako Petro; ulikuwa mmoja wa wenye bahati wa kushuhudia kwa macho. Na sisi je?’ Hili ndilo alilokuwa nalo Petro akilini mwake hasa alipoandika waraka huu; “….Nasi tuna neno lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo mkiliangalia, kama taa ing’aayo mahali penye giza, mwafanya vema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.” (2Pet.1:16-21). Kusoma Biblia na maandiko ya kiroho hufanya kazi kama taa ili kuamsha ufunuo wa Mungu ndani yenu. Haiwezekani kupika chakula katika joto la njiti moja ya kiberiti, lakini ni njiti moja tu hutumika kuwasha moto wa jiko! “Lakini nasema ya kuwa mrithi, wakati wowote awapo mtoto, hana tofauti na mtumwa, angawa ni bwana wa yote; bali yu chini ya mawakili na watunzaji, hata wakati uliokwisha kuamriwa na baba, bali sasa wakati mkamilifu umekuja.” (Gal.4:1-11).

Kijana wa uzao wa kiungwana, Sauli, mwenye juhudi kwa mapokeo ya dini yake, akiwa na shauku kubwa na kutambuliwa kuliko wengine wa hirimu yake, alifuatilia utumishi wake kufuta kabisa wafuasi na ushawishi wa huyu Yesu. Ghafla, nuru kubwa kuliko jua ilimwangusha. Akawa kipofu kwa siku tatu, lakini Kristo alijifunua ndani yake. Mungu yule aliyesema, ‘Nuru na iangaze katika giza’ ameangaza mioyoni mwetu ili kuleta nuru ya maarifa ya utukufu (ushauri) wa Mungu katika sura ya Kristo. “Tuna hazina hii katika vyombo vya udongo.” (2Kor.4:7). Sasa, Paulo hamjui tena kwa jinsi ya mwili; ukweli hamjui tena mtu yeyote kwa jinsi ya mwili. (2Kor.5:16). Katika nuru hii haitokei tena tofauti ya watu, hata watu wake walio wateule walipoteza umaarufu wao ghafla na utambulisho wao wa asili. Hapa hakuna tena Myahudi wala Mmataifa, wala mtu mume au mke, mtu huru au mtumwa, bali mtu mpya mmoja! (Ef.2:14-22; Gal.3:28). Ufunuo huu hufanyika kuwa shauku ya utume wake mpya; kumfunua Kristo ndani ya kila mtu. Kuna tofauti kama

43

Page 44: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

hiyo baina ya kumhubiri Kristo kwa mtu na kumfunua Kristo ndani ya mtu. Andiko la Kiyunani linasema kwa wazi kabisa kwamba, alitumwa kumfunua Kristo kwa wapagani. (Gal.1:16).

Ufunuo wa utambulisho wao wa kweli na jua la wema wa upendo wa Mungu, liling’aa kwa nguvu juu ya mitume wakati ule, hata kivuli kilipoanguka juu ya watu waliweza kuponywa kwa ajabu! (Mdo 5:12-16). Nguvu ya Mungu ndani yao, iliweza kuhamishiwa hata katika nguo na mavazi yao waliyoyagusa, na haya yaliweza kuwekwa juu ya wagonjwa na watu waliopagawa na mapepo, nao waliponywa. “Bali njia ya wenye haki ni kama nuru ing’aayo, ikizidi kung’aa hata mchana mkamilifu.” (Mith.4:18). “Nimekuweka uwe nuru ya mataifa, upate kuwa wokovu hata mwisho wa dunia.” (Mdo 13:47). “Na wote wenye mwili watauona utukufu wa Bwana” (Isa.40:5). “Kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu, ukombozi wa miili yetu!” (Rum.8:19). “Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, na utukufu wa Bwana umekuzukia! Na mataifa wataijilia nuru yako, na wafalme kuujia mwanga wa kuzuka kwako!” (Isa.60:1-3).

MKATE WETU WA KILA SIKU

Mungu ni mbunifu. Tunampenda kwa sababu alitupenda kwanza. Kuelewa na kupokea ubunifu wake, kunafuta namna zote za mashaka; uwepo wake na kusudi huwa la kutabirika.

Ili kuwasiliana na Mungu, ni wito wa kawaida. Hakuangalii kutoka mbali. Dini ya umbali mrefu imepitwa na wakati! Mjue Mungu; Imanueli maana yake Mungu pamoja nasi. Anaweka uwepo wake miongoni mwa watu. Anakaa pamoja nasi; anwani ya Mungu ni wewe; daima ana mawasiliano kukufikia kwa haraka. Furaha yako na upendo vinamwonyesha yeye; uwepo wake ndilo fungu lako, wewe uko katika mpango wa wazo lake, ndani ya mtazamo wa moyo wake. Utajiri wako ni kujua ukaribu wake. Mkiri yeye, mwabudu yeye…. Au umdharau! Unabaki

44

Page 45: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

kuwa uchaguzi wako kuisikia sauti yake. Wewe ni kusanyiko lake; msikilize!

Mara nyingine tunapata wazo kwamba Mungu husema katika njia ya pekee na kiuchumi; maneno yake ni adimu, na tunahitajika kumlipa kuhani au mchungaji ili amsikie Mungu kwa niaba yetu. Lakini ukweli, wala hutakiwi hata kungoja hadi Jumapili nyingine! “Hekima hupaza sauti yake katika njia kuu, hutoa sauti yake katika viwanja. Hulia penye mikutano mikubwa ya watu, mahali pa kuyaingilia malango; ndani ya mji hutamka maneno yake. Enyi wajinga, hata lini mtapenda ujinga? Na wenye dharau kupenda dharau yao, na wapumbavu kuchukia maarifa? Geukeni kwa ajili ya maonyo yangu; Tazama, nitawamwagia roho yangu, na kuwajulisheni maneno yangu! (Mith.1:20-23).

Ikiwa uumbaji wa mwanadamu na matengenezo ya ndani yako hivyo, kwamba tunapaswa kutegemezwa kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu, ndipo neno lake lazima lisomwe zaidi, lipatikane kuliko mkate wetu mpya wa kila siku!

“Mbingu zahubiri utukufu wa Mungu, Na anga laitangaza kazi ya mikono yake.Mchana husemezana na mchana,Usiku hutolea usiku maarifa.Hakuna lugha wala maneno,Sauti yao haisikilikani. Sauti yao imeenea duniani mwote, na maneno yao (au makubaliano) hata miisho ya ulimwengu. (Kiebrania: kawv kutokana na kawva –kamba inayounganisha pamoja, kufunga pamoja kwa kuviringa, uzi wa muziki au ulinganifu, au msitari wa kupimia.)Katika hizo ameliwekea jua hema,Kama bwana arusi akitoka chumbani mwake,Lafurahi kama mtu aliye hodari,Kwenda mbio katika njia yake.Kutoka kwake lautoka mwisho wa mbingu,Na kuzunguka kwake hata miisho yake, wala kwa hari yake,Hakuna kitu kilichositirika.

45

Page 46: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Sheria ya Bwana ni kamilifu, huiburudisha nafsi. (sheria kamilifu ya uhuru). Ushuhuda wa Bwana ni amini, humtia mjinga hekimaMaagizo ya Bwana ni adili, huufurahisha moyo.Amri ya Bwana ni safi, huyatia macho nuru. Kicho cha Bwana ni kitakatifu, kinadumu milele. Hukumu za Bwana ni kweli, zina haki kabisa.Ni za kutamanika kuliko dhahabu, kuliko wingi wa dhahabu safi. Nazo ni tamu kuliko asali, kuliko sega la asali.Maneno ya kinywa changu, na mawazo ya moyo wangu,Yapate kibali mbele zako, Ee Bwana,be acceptable in thy sight, Mwamba wangu, na mwokozi wangu.” (Zab.19). Neno lake hung’aa katika kutafakari kwa moyo wangu na maneno ya kinywa changu.

Inaweza kuonekana kwamba katika wingi wa kupatikana na kumiminwa kwa mawazo ya Mungu na maneno, hata wahubiri maarufu watakwenda nakufanya kazi katika makusanyiko. Lakini kufunguliwa kwa mawazo yake na kufunua siri zake, kunawahusu tu wale ambao wanayakumbatia maneno yake, wanaosikia sauti yake; anayetega sikio lake kusikia hekima; anayeuelekeza moyo wake apate ufahamu; anaita kwa busara, na kupaza sauti yake apate ufahamu, na kuutafuta kama fedha na kuutafuta kama hazina iliyositirika. (Mith.2:1-4). Mitume, manabii, wainjilisti, wachungaji na waalimu ni vipawa kwa waamini ili kuwaimarisha katika imani na kuwafikisha kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo. (Ef.4:11-16). Kuna tofauti kubwa sana baina ya kipawa na thawabu! Sisi ni vipawa vya Mungu kila mmoja kwa mwenzake. Jinsi tulivyo kila mtu katika mwonekano wetu, ni kipawa wala sio thawabu inayotokana na juhudi binafsi au mafanikio. Vipawa hivi havikukusudiwa kamwe kuwa vyeo rasmi, bali ni kutambulisha kazi na huduma maalumu kwa watu wote ili kufikia kutambua utimilifu wa kipimo cha Kristo ndani yao!

Katika kanisa la kwanza, mitume walikuwa katika mahitaji makubwa wakati ishara nyingi na maajabu yalifanywa katika mikono yao. (Mdo 5:12). Zaidi kwamba baadhi ya huduma za kila siku, zikiwa pamoja na mgawanyo wa mahitaji ya chakula

46

Page 47: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

miongoni mwa wajane ambao walisahauliwa. Walifikiri juu ya ya ufumbuzi wa utendaji: watu wengi wenye sifa nzuri, waliojaa Roho, hekima na imani waliteuliwa kwa kazi hii. Jambo hili liliwapa uhuru mitume wa kutumia muda zaidi katika kuomba na kuhubiri.

Lakini mipango ya Mungu na mkakati kwa maisha yetu ni mkubwa sana kuliko nembo tunazozivaa! Stefano alikuwa mmoja wapo wa kwanza kuteuliwa kama shemasi. Aliitwa kuhudumia meza wakati ghafula alikuwa ameingia mbali katika kazi nyingine! “Na Stefano, akijaa neema na uwezo, alikuwa akifanya maajabu na ishara kubwa katika watu…. Lakini hawakuweza kushindana na hiyo hekima na huyo Roho aliyesema naye.” (Mdo 6:8,10). Pia huduma ya Filipo yenye nguvu, ilimweka mbali na wajibu wa huduma ya shemasi! Alivuka mipaka ya kisiasa ya siku zake na kuendeleza huduma ya Yesu miongoni mwa Wasamaria. (Mdo 8:38). Kumbuka, Wayahudi waliwaona Wasamaria kama mbwa, wala hawakuweza hata kusema nao. “Na makutano kwa nia moja wakasikiliza maneno yale yaliyosemwa na Filipo, walipoyasikia na kuziona ishara alizokuwa akizifanya. Kwa maana pepo wachafu wakawatoka wengi waliopagawa nao, wakilia kwa sauti kuu; na watu wengi waliopooza, na viwete, wakaponywa. (Mdo 8:6,7). Katika msitari wa ishirini na sita, malaika wa Bwana anamwongoza kwenda kusini! Habari njema zinakwenda kusini! Afrika inakwenda kuzipata! Tazama jinsi mkakati wa Mungu unavyowaendea watu wengi kwa makundi; Filipo anaongozwa kwa njia ya pekee kumhudumia mtu mmoja! Ndipo anasafirishwa kimwujiza kwenda mji mwingine baada ya kumwongoza Mwafrika mmoja kwa Kristo. (Mdo 8:26-40). Thamani ya mtu mmoja haipimiki kwa kiwango cha chini kamwe! Mungu aliliona bara ndani ya mtu mmoja. Ni katika asili ya mbegu kutoa mazao kulingana na aina yake. Mguso wa thamani iliyo sawa inapaswa kumwendea mtu mwingine ili kumwaanda mtu huyo, naye agundue uwezo usioonekana ulio ndani yake.

47

Page 48: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Paulo anaona umuhimu wa kuwatia moyo waamini kutambua kikamilifu maana halisi ya wokovu wao, katika safari yake ya kujitegemea au waraka kwao. “…. Si wakati mimi nilipokuwapo tu, bali sasa zaidi sana mimi nisipokuwapo, utimizeni wokovu wenu kwa kuogopa na kutetemeka.” (Wafil.2:12). Huku ni kuhusika kwa kweli, kwa kuwa mmoja anaweza kunaswa kirahisi katika mwendo na kuondosha ujuzi wa mwingine.

Huduma haikukusudiwa kamwe kuwafurahisha makundi juma baada ya juma, na mwaka baada ya mwaka katika ukanda wa starehe wa kujihisi vizuri. Mungu haonekani katika hali ya kujihisi vizuri! Wakati uwepo wa Mungu na kutembea kwa Roho wake juu ya roho yako, ndio hali ya kufurahisha zaidi ambayo mtu atafikiria kwamba sisi hatuko katika shughuli ya kujifurahisha! Ikiwa huduma haikuhamasishi, inakuharibu! Ikiwa kipimo cha cheo chake kinaeleweka ndani yako, sio zao la mahubiri yangu au mafundisho yangu, basi nafanya kazi bure!

Petro alikuwa anahakikisha kuwa kwa njia ya kuwakumbusha, maandiko yake yangefanya kazi ya kuwatia moyo na kuwaamsha waamini kuufikiri ushuhuda wake, ili kwamba ufahamu juu ya kweli uwe kwa kila mmoja, hali ya kukutana ana kwa ana. “….Mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.” (2Pet.1:12-15,19). Yesu anamsaidia mwanamke kisimani kuelewa asili yake ya kweli, chemchemi iliyo ndani yake. Hakuna ziara ya ufuatiliaji au mawasiliano zaidi yanaahidiwa. (Yoh.4:6-42). Chemchemi ya ndani hufuatia yenyewe na kuongoza katika ushirika na kuongeza hiari ya moyo, huduma yenye mafanikio tofauti na mtu mwenyewe. “Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.” (Yoh.7:38). Mto hupenya katika milima na kujifanyia njia yake, na kuleta uhai kila unapotiririkia.

Kiwango na mchanganyiko wa mafundisho ambayo mwamini anayatii, hutegemea thamani ya kukutana binafsi na ushirika anaotakiwa kuwa nao kwa Mungu. (Rum.6:17). “Ninaomba

48

Page 49: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

kwamba ushirika wa imani yako ufanye kazi yake, katika ujuzi wa kila kitu chema kilicho kwetu, katika Kristo.” (Filem.6).

“Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu…. Mara kwa mara tunaishia kusoma hapo, halafu tunatumia andiko hili kuelezea kwa nini hatuzielewi njia za Mungu; lakini msitari unaofuata unasema, “….Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula; ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.”Isa.55:8-11). Mbegu na udongo vinaelewa lugha ya mvua. Kufanyika mwili kwa Kristo, milele kunaweka daraja kati ya umbali ambao labda ungeweza kumtenga mwanadamu na Mungu. Mungu yuko katika sura yetu! Neno lake limefanyika mwili! (Yoh.1:1,14; Ebr.1:1,2).

“Watu wale waliokaa katika giza, wameona mwanga mkuu” (Math.4:16). “Nuru halisi, amtiaye nuru kila mtu, amekuja ulimwenguni.” (Yoh.1:1-5,9,14,16). “Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima. Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.” Watu wanapoyaona mambo ambayo Mungu anatenda kupitia kwako, wanatambua shauri la Mungu kuhusu wao! (Math.5:16). “Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, na utukufu wa Bwana umekuzukia. Maana, tazama, giza litaifunika dunia, na giza kuu litazifunika kabila za watu; bali Bwana atakuzukia wewe, na utukufu wake utaonekana juu yako. Na mataifa wataijilia nuru yako, na wafalme kuujia mwanga wa kuzuka kwako.” (Isa.60:1-3). Anazungumza juu ya kuishi maisha ya mvuto! Mungu anajitahidi kukamilisha mapenzi yake ulimwenguni kupitia kwako.

49

Page 50: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Kusikia kwamba kila kilicho chema na kipawa kamili hutoka kwa Mungu, Baba wa mianga, aliyetuzaa kwa ubunifu wake mwenyewe na upendo, ni sawa na kuona sura ya uzao wako, utu wako wa ndani kama vile ulivyo hasa, kama katika kioo. (Yak.1:17,18). Sisi ni kipawa chake kilicho kamili kila mmoja kwa mwingine. Sisi ni roho; tumezaliwa kutoka juu; kuonekana kwetu kwa nje katika mwili ni kama chombo cha udongo kinachovunjika, lakini unashikilia hazina isiyo na mwisho. Chombo kinapata thamani yake kutokana na hazina inayobebwa. Thamani ya chombo cha udongo haitegemei umbo lake, ukubwa au rangi. Unaweza kuubadili mwili wako na kuupamba uso wako na kupendeza, na mavazi ya thamani na dhahabu, lakini utu hauko nje bali ndani!

Kama vile alama ya maji ndani ya karatasi, mtu wa ndani anabeba chapa halisi ya tabia ya Mungu. “Yeye ni mng’ao wa utukufu wa Mungu, na kuchukua chapa halisi ya asili yake.” Ebr.1:3. (Neno la Kiyunani la utukufu ni doxa kutokana na dokeo =shauri). Sisi sote tuna asili moja. Ndio sababu Yesu haoni haya kutuita sisi ndugu (Ebr.2:11). “Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja. Ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu. Maana sisi sote tu wazao wake.” (Mdo.17:26,27,28). Usawa wa ‘alama ya maji’ hii hung’aa katika wazo la mbegu. Kila mbegu hutoa taarifa zote za aina ya uzao. Kinachochochea mzunguko wa uhai na udhihirisho unaoonekana wa aina ya mbegu ndicho chenye maana.

Chemchemi ndani yetu zinaachiliwa tunapogundua asili yetu ndani ya Mungu. Uumbaji wetu wa msingi na kupambwa asili yake ni kutoka katika wazo lile lile moja. Ndani ya roho zetu uumbaji wetu wa asili unabakia kuwa kamili. Kufikiria sura ya Mungu ndani ya mtu kunaongeza thamani ya mtu inayozidi akili zote, ujuzi au mafanikio, au kukatishwa tamaa kwa ajili ya jambo fulani. Kugundua utajiri uliomo ndani, ndiko kunamfungua na kumtia nguvu mtu kuwa rasilimali na siyo tegemezi. Hili pekee litavunja vifungo vya umaskini, uchoyo na uharibifu. Ulazima wa kuchukua na kupata unachukuliwa nafasi yake na shauku ya kushiriki na kutumiwa. Kila uvumbuzi una

50

Page 51: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

asili yake katika wazo. Kufuatilia asili yako ya uumbaji katika fikira za Mungu ili kutambua uhalisi wa neno la kweli, neno lililo na wazo la asili la Mungu, kichwa cha chemchemi ya kweli. Hili ni neno lililokuwako tangu mwanzo kabla ya wakati au kuwako kwa lugha, neno ambalo ni Mungu, neno lililofanyika mwili, chapa ya uumbaji wetu. Ni kama vile DNA zinavyohifadhi utaratibu wa mtu, utambulisho wa pekee kimwili, roho yetu ina utaratibu wa asili yetu ulioonyeshwa katika wazo la Mungu. Alituumba na kututengeneza na kutuunganisha pamoja katika tumbo la mama yetu. Katika mazingira ya ukweli huu, tunaepuka matokeo ya sheria ya dhambi, hatia na unyonge. Huwa rahisi sana kuamini jambo ambalo unaweza kulishika. Mara kwa mara tunafikiri kuwa imani ni kuamini mambo tusiyoyaelewa. Imani yenye upofu ni udanganyifu; imani inaona. Kuku jike huhesabu vifaranga vyake kabla havijaanguliwa; tayari anaviona ndani ya ganda la yai. Kweli mbili zilizo ufunguo zinaunga mkono sheria hii: Ukweli kwamba Mungu alimwumba mtu kwa sura na mfano wake, sawa na ilivyo katika Kristo; Mungu aliupatanisha ulimwengu na nafsi yake. (Mw.1:26; 2Kor.5:18,19).

Ujumbe wa kujumlishwa kwa mwanadamu katika yote ambayo Kristo aliyapata kwa niaba ya wanadamu, hushika maana ya haraka na ya lazima kwa viumbe wote. Kuelewa wewe ni nani katika hali zote, katika umoja wako na Mungu na ubinadamu, na katika upekee wa mtu, ni ukweli wa kusisimua sana kuliko ambavyo akili yako ingeweza kufikiri. Kichwa kilichoanguka juu ya kisigino katika upendo na uzima, ni kumpenda na kumfurahia Mungu, mwanadamu mwenzi wako na nafsi yako kwa upendo ulio sawa. (Math.22:38,39; Yak.2:8-12; 3:9,10; Rum.13:7-10). Kioo hufunua umoja wetu. Paulo anasema kuwa tunaposhindana sisi kwa sisi na kuendelea kujitahidi ili kutambuliwa, na kupima na kujilinganisha sisi wenyewe, tunafanana na watu wasio na akili. (2Kor.10:12). Ni mashindano ya aina moja tu yanayotiwa moyo, ‘kwa heshima mkitangulizana.’ (2Kor.12:10). “Tangu sasa hatumjui mtu tena mtu awaye yote kwa jinsi ya mwili.” (2Kor.5:16).

51

Page 52: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Tumekuwa wenye kushindwa sana na nguvu ya sura yake ndani yetu kiasi kwamba hali yote ya uhitaji, kupungukiwa au unyonge vinapewa changamoto, hata katika hali ya upinzani mzito.

NI ZAIDI YA KISIMA CHA YAKOBO

Siku moja, akiwa ametembea kwa muda usiopungua maili ishirini mchana wa jua kali, Yesu aliwatuma wanafunzi wake kwenda Sikari, mji wa Samaria, ili kununua chakula. Aliwangojea akiwa amechoka, akiwa na njaa na kiu kando ya kisima cha Yakobo pembezoni mwa kijiji. Hatimaye, mwanamke Msamaria alifika kisimani kuchota maji, na mara akamwomba maji ya kunywa. Hakuwa na chombo cha kutekea, na kisima kilikuwa na kina kirefu kama futi 150. Akimtambua Yesu kama Myahudi, alianza kufunua shida iliyokuwepo na kumkumbusha kwamba Wayahudi hawakupaswa kuzungumza na Wasamaria. Alitazamia angalau kupata majibu ya kisiasa katika siku ile.

Yesu aliishi maisha yenye ushawishi na dhamiri ya asili yake ya kweli na utambulisho wa roho. Katika mazungumzo naye, mwanamke alianza kutambua kuwa Yesu alikuwa zaidi ya Myahudi, na kwamba naye alikuwa zaidi ya Msamaria. Ghafla alielewa kuwa, kwa kweli watu wote wanashiriki asili yao moja. Chemchemi ya maji ya uzima haikuwa mbali naye kuifikia, bali ilikuwa ndani yake. Hakuna ndoa yoyote kati ya zile tano zilizotangulia, au hata desturi za dini ambazo zingeweza kuondoa kiu yake. Sio kwa sababu alishindwa kukutana na ‘Aliye Mkamilifu’ au walishindwa kukutana na matazamio yake, bali ni kwa sababu ya ukweli kwamba, mwenzi hakuwa na maana ya kukamilisha maisha yake kamwe. Hakuna kitu wala mtu anaweza kufananishwa na utajiri ambao mtu anautambua anapogundua asili yake kuwa ni chemchemi ya uzima. Hapa, habakii tena mwenzi, au siasa, au ujuzi uliotangulia wa kulaumu au kushindana nao, bali ni uzima mpya tu ulio ndani yako, ambao ni wa kuutambua, kuupeleleza, kushiriki na kuufurahia. Chanzo chako ndicho kitakutegemeza. Ukweli wa kuponya haujaribu kuondoa hisia nzito zenye kuumiza na matatizo

52

Page 53: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

yaliyopita; badala yake, ukweli hufunua uadilifu wa uzima wa asili, msingi wa chemchemi wa asili yetu! “Je wewe ni mkubwa kuliko baba yetu Yakobo aliyetupa kisima hiki? “Saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu! Ninyi mnaabudu msichokijua; (mapokeo ya kidini yanafawanya makundi ya watu waendelee kunaswa katika ujinga); Sasa waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli.” Baba ndiye chemchemi yetu ya kweli! Baba yako siye Yona au Yakobo, kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili. Mwisho wa makosa umewadia! Rudi kwenye chanzo chako. “Mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu.” (Ebr.12:2). “Kwa Mungu, mmepata kuwa katika Kristo; yeye ndiye chanzo cha uzima wako katika Kristo Yesu. (1Kor.1:30). “Yote hutokana na Mungu.” 2(Kor.5:18). “Tu watenda kazi pamoja naye, tuliumbwa katika Kristo Yesu.” (Ef.2:10).

Huduma zote hutokea kwa kusudi moja: Kuwafunulia wanadamu kujumlishwa kwao katika Kristo na maana yake kamili; thamani zilizorejeshwa sawasawa na ushirika uliorejeshwa. Wengine husema, “Mimi ni wa Paulo, au mimi ni wa Apolo,’ ni kuwa na kiburi katika kufanya malinganisho, ugomvi na wivu. (1Kor.3:4). Wakati Paulo alipofika mara ya kwanza Efeso aliwakuta wanafunzi wa Yohana Mbatizaji kule, miaka mingi baada ya kiongozi wao kuuawa. Wala hawakuwahi kusikia kuhusu Roho Mtakatifu, lakini bado walihubiri fundisho la dhamiri ya dhambi. (Mdo 19:1-6). Wanafunzi wa Yesu walipofanya sherehe na kunywa, wanafunzi wa Yohana walikuwa wanafunga na kuomba. (Luka 5:33). Yohana Mbatizaji alimtangaza Yesu kuwa Mwana-kondoo wa Mungu, azichukuaye dhambi za ulimwengu, aliona mbingu zikifunuka juu yake na kushuhudia Roho Mtakatifu juu yake kwa mfano wa hua na kuisikia sauti ya Mungu. Lakini badala ya kuwa mwanafunzi wa kwanza wa Yesu, aliendeleza huduma yake mwenyewe. Aliendelea kuhubiri juu ya dhambi na hukumu kana kwamba Mwana-kondoo hakuchukua dhambi za ulimwengu. Kichwa cha ujumbe wake kinaonyesha yote: “Enyi uzao wa nyoka….!” Fungu la maneno aliyohubiri chini ya upako wa Roho, kutoka Isa.40:3, anaanza kwa maneno katika msitari wa

53

Page 54: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

1 na 2 anasema, “Watulizeni mioyo, watulizeni mioyo, watu wangu, asema Mungu wenu. Semeni na moyo wa Yerusalemu, kauambieni kwa sauti kuu ya kwamba vita vyake vimekwisha, uovu wake umeachiliwa!” Jambo la huzuni, huduma ya hatia na hukumu, inaonekana kuwa ni ya upofu ukilinganisha na uzuri wa Injili. Kuihukumu tamaa ya Herode kwa mke wa ndugu yake, ilimpeleka gerezani. Shaka na kosa vinaanza kurudia mara nyingi, na kutoka gerezani anawatuma wanafunzi wake kumwuliza Yesu, “Wewe ndiwe yule ajaye, au tumtazamie mwingine?” Yesu anawajibu, “Nendeni mkamweleze Yohana mnayoyasikia na kuyaona; vipofu wanapata kuona, viwete wanakwenda, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa habari njema. Naye ni heri awaye yote asiyechukizwa nami.” (Math.11:2-6). Chochote kikukwazacho ndicho kinachokuharibu.

Maamuzi ya Yohana gerezani ni tofauti sana na yale ya Paulo; wala hawakuwa gerezani kwa sababu za aina moja. Yohana hakufungwa kwa ushirikiano wake na Yesu. Wakati Yesu alijifanya kuwa rafiki wa wenye dhambi, Yohana aliwahukumu. Paulo alikwenda gerezani mara kwa mara, na kila wakati kwa sababu zile zile na kwa watu wale wale wa dini waliomsulubisha Yesu. Anaeleza habari zake mwenyewe, “Katika vifungo kuzidi sana; katika mapigo kupita kiasi; katika mauti mara nyingi. Kwa Wayahudi mara tano nalipata mapigo arobaini kasoro moja. (Katika filamu ya ‘Shauku ya Kristo,’ Mel Gibson, anafunua kijiografia yale yanayotokea katika mwili wa mwanadamu akipigwa mara thelathini na tisa!) Mara tatu nalipigwa kwa bakora; mara moja nalipigwa kwa mawe; mara tatu nalivunjikiwa jahazi; kuchwa kucha nimepata kukaa kilindini; katika kusafiri mara nyingi; hatari za mito; hatari za wanyang’anyi; hatari kwa taifa langu; hatari kwa mataifa mengine; hatari za mjini; hatari za jangwani; hatari za baharini; hatari kwa ndugu za uongo; katika taabu na masumbufu; katika kukesha mara nyingi; katika njaa na kiu; katika kufunga mara nyingi; katika baridi na kuwa uchi.” (2Kor.11:23-28). Ushuhuda huu unamjaza mtu hofu kuu, lakini Paulo anaona kwa njia hii: Katika mambo hayo yote tunashinda. Anaona uzima uliojaa

54

Page 55: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

furaha katikati ya kila aina ya upinzani! “Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi!” (2Kor.4:17). Tumepewa mtazamo wa mara moja kuhusu maono ya Paulo juu ya siri iliyofunuliwa ndani yake. “Furahini katika Bwana siku zote, tena nasema furahini! Si kwamba nasema haya kwa kuwa nina mahitaji; maana nimejifunza kuwa radhi na hali yoyote. Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yoyote, na katika mambo yote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa. Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.” (Filip.4:4,11-13).

Kuwa na vitu vingi sio uthibitisho wa wema wa Mungu; wala kupungukiwa sio ishara ya kumkosa Mungu!

SHINDA UPINZANI

Mashindano si ndiyo yakufanyayo uwe mshindi, kutambua jinsi ulivyo kamili mbele ya upinzani, bila uthibitisho wowote wa nje au sifa, bali ni tabia ya kweli ya shujaa.

Hivyo imani hutwaa mfano wake ndani yako, hiyo hufanyika kuwa upumbavu unaposahau kuwa wewe ni mtu wa namna gani, hata katikati ya uadui mkubwa na majaribu ya kukupinga: “Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu bila kupungukiwa na neno.” (Yak.1:4,24). Neno la kweli, linalofunua uadilifu na ukamilifu wa asili yako, huzaa imani. Imani huleta saburi, saburi huleta uthibitisho! (Yak.1:17,18). “Lakini mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo.” (Ef.4:7). Mfano wake ndani yetu ni kipimo cha ukamilifu wetu. “Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema.” (Yoh. 1:16). Kiyunani, xarin anti xarin, ni neema dhidi ya ukweli kwamba hatukustahili neema, kuwa kama matokeo ya utendaji binafsi au mafanikio. Neema ni kipawa, wala sio thawabu. (Rum.4:3,15,16).

Kuna vipimo vya namna mbili, kipimo binafsi na kipimo cha maisha. Vipimo vyote huuliza swali la aina moja na kuleta

55

Page 56: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

hitimisho moja. Katika waraka wa mwisho wa Paulo kwa Wakorintho, anawapa changamoto waamini ya kujijaribu wenyewe ili kujua kama wanaishikilia imani yao. Anasema, “Jijaribuni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu?” (2Kor.13:5). Hii ndiyo maana ya imani ilivyo. Ukweli huu ndio hitimisho pekee lililo sahihi la imani yako. Hiki ndicho kipimo cha kwanza na mwisho cha kumkamilisha mwamini, sawa na mfano wa mwanafunzi wa uganga, anavyopaswa kuelewa kwa usahihi na kujibu maswali yote yanayomhusu, katika mtihani wake wa mwisho kabla hajafuzu kukabiliana na mambo ya maisha halisi kimatendo katika huduma ya madawa. Kwa nini ni lazima tufikie katika hitimisho la Kristo ndani yetu? Yamkini, si kwa furaha binafsi tu au kujihisi vizuri, bali kwa kazi na huduma yenye nguvu na mafanikio! Baraka za ukaribu wake, uwepo wake na utisho haviepukiki!

“Mungu akiwepo upande wetu, ni nani aliye juu yetu? Kwa kuwa Mungu alitukusudia mapema ili tutengenezwe pamoja katika mfano na sura ya Mwana wake, (‘Tunaona sura ya asili iliyokusudiwa kwa maisha yetu ndani yake,’ mstari wa 29. Tafsiri ya Message). Ni nani atakayetushitaki au kutuhukumu? Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je, ni dhiki, au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga? La! Katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.” (Rum.8:29-39).

“Hesabuni kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali (kupingana na utambulisho wenu wa kweli), mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. (Yak.1:2-4). Saburi ni tunda la mchakato unaosukumwa na majaribu na kupimwa; kumbatia mchakato kwa shauku na furaha badala ya kuchoka. Huwezi kununua saburi wala huwezi kurithi saburi; haiji kwa njia nyingine yoyote. Hakuna njia

56

Page 57: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

ya mkato ya kupata saburi; haipatikani kwa makubaliano. Saburi katika imani yako, kuwa na hakika ya umoja wako na Mungu, ni kiunganishi chako cha juu cha thamani inayotafutwa; uzoefu wa maisha mbali na upungufu. Kipimo au jaribu katika mtiririko huu maana yake ni chochote kinachokufanya ujione kuwa si mkamilifu na mpungufu; chochote kinachopingana na hakika ya kwamba Kristo yu ndani yako. Kumbuka, Mungu hamjaribu mtu yeyote; Mungu hana agenda ya siri, hana kivuli cha kugeuka-geuka au kubadili nia yake. Mungu ana uhakika juu yako. Nia yake iko kwa ajili yako. Shauri lake kwako halipo kwa sababu ya kushinda au kushindwa jaribio. Yeye hahitaji kukufanyia jaribio kabla hajakuthibitisha. Kwako wewe kuwa na nia mbili ni kupotoka katika saburi na kujidanganya nafsi yako; huwezi kufanikiwa, si kwa sababu yoyote, bila kujali ni sababu ngapi muhimu ulizo nazo. “Saburi na iwe kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu bila kupungukiwa na neno.” Neno la Kiyunani kwa ukamilifu, holokleroi. Lina maana ya kumiliki kikamilifu sehemu ya mgawo wako. Linganisha na Yakobo 1:15, hamartia, kutokana na ha-meros: kushindwa kutwaa mgawao wako, kipimo kamili cha uzima uliokusudiwa na Mungu kwa ajili yako. Kwa kawaida hutafsiriwa kuwa ni dhambi. Kwa kawaida kile kinachotangazwa kuwa dhambi, mara kwa mara huwa dalili tu za maisha yasiyotimilika. “Nafsi iliyoshiba hukinai sega la asali, bali nafsi yenye njaa huona kila kitu kichungu kuwa kitamu.” (Mith.27:7). “Kamba zangu zimeniangukia mahali pema, naam, nimepata urithi mzuri. (Zab.16:6). Ndio sababu Mungu anapenda kuwaonyesha kwa uhakika zaidi warithi wa ahadi, tabia isiyobadilika ya kusudi lake! (Ebr.5:17). “Hesabuni yote kuwa ni furaha tupu” ni neno la Kiyunani, hegeomai ni muundo wa neno uliotiwa nguvu, ago, kuongoza kama mchungaji aongozavyo kondoo wake. Mchungaji katika siku za Biblia alikuwa na sura ya mamlaka. Alitakiwa kulilinda kundi lake dhidi ya mazingira, wanyang’anyi na wanyama wa mwitu. Kwa hiyo, hegeomai lina maana ya kuteuliwa rasmi, ili kuwa katika amri na mamlaka maalumu ya kutawala. ‘Furaha na itawale juu ya mazingira yenu.’ Furaha siyo jaribio dhaifu la kutabasamu, wakati unaumizwa na vidonda na kujisikitikia.

57

Page 58: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Furaha ni nguvu inayotawala roho yako mbele ya upinzani. Hesabu kubwa ya kiasi anayoweza kuifanya mtu ni hitimisho, ambalo daima matokeo yake ni furaha. Kumbuka kuwa, furaha si jambo fulani unalotenda; ni tunda la jambo ambalo unalijua. Furaha inaelewa kuwa wewe huna mwisho pamoja na Muumba wako. Furaha ni sauti ya imani. Furaha inaitikia katika yale ambayo imani inayajua. Furaha inapokuwa na mamlaka rasmi, ndipo shauku, kuondolewa taabu, kujihurumia nafsi yako, kulalamika, kutafuta kuhurumiwa, kuzungumza juu ya matatizo yako na kulinganisha matatizo yako na ya wengine, yote yanatawaliwa. Miitikio hii itakunasa kukuingiza katika udhaifu na unyonge.

Moja ya matatizo makubwa ya Afrika ya kusini tangu falsafa ya upotoshaji na ubaya wa ubaguzi, ni rejea ya kisasa ya kuendelea kwa ‘Hasara iliyotangulia.’ Ingwa ina maana nzuri, hatutafanikiwa kamwe kuwatia nguvu watu kwa kusisitiza na kutia moyo hisia za kujihurumia na lawama. Hakuna kilicho kibaya zaidi kuliko kujihurumia mwenyewe na kumlaumu mwingine. Kizazi cha watu ambacho huzidi kuwa tegemezi katika kupokea, kina matokeo yasiyoepukika. Hili ni shambulio lingine baya juu ya heshima ya mwanadamu. Huwa rahisi sana kuyanyoshea kidole yaliyopita na nini na nani wa kulaumiwa. Ukweli wa kusikitisha ni kwamba, kadiri tunavyohisi kuhalalisha kufanya hivyo, ndivyo tunavyozidi zaidi kuharibikiwa, kupooza na kufirisika kwa shutuma. Maisha hayatokani na vitu tusivyo navyo, bali ni yote tunayofanya na tuliyo nayo! Gundua utajiri ulio ndani yako!

Furaha ni sauti ya imani; furaha huimba badala ya kuhuzunika. Matokeo ya kutamka kwetu kunafananishwa na usukani wa meli, chombo kizito kinaweza kuongozwa bila kutumia nguvu; kamwe usidharau nguvu ya mazungumzo. (Yak.3:2-4). Hata mawazo yetu ni maneno yasiyosikika ambayo yanaumba afya yetu na msimamo mzima wa maisha. ‘Kunena kweli katika upendo, ili kwamba ushirika wa imani yako ufanye kazi yake, katika ujuzi wa kila kitu chema kilicho kwetu, katika Kristo.’ (Ef.4:15,29; Filem.6). Kiwango hiki cha mazungumzo kinaumba

58

Page 59: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

mazingira ambayo yanatukamilisha kufikia cheo cha Kristo ndani ya kila mmoja. Ukweli ambao unaonyeshwa katika Yesu ndio kielelezo chetu pekee kilicho cha kweli. (Ef.4:20-27). “Neno la Kristo likae kwa wingi ndani yenu.” (Kol.3:1-4,10,11,16). Utajiri wa neno hili huwa ndio kiini cha mazungumzo; ni uvuvio wa kila fundisho na faraja, kila zaburi na wimbo wa sifa, au hata nyimbo mpya katika roho. Neno laKristo ni neno linalofunua uadilifu wa kujumlishwa kwetu ndani yake na utambulisho wetu wa kweli. Neno la kweli kama lilivyo katika Yak.1:18; Kol.1:5,6; Ef.1:13; ni neno ambalo daima hujenga na kuleta neema. Watu wengi makini hufikiri kuwa kuna wema katika kujadili matatizo na kusimulia giza chini ya dhana ya ukweli na uwazi. Ukweli wa habari njema ya Injili hauhusiani na jinsi mtu alivyo mwenye dhambi, bali jinsi alivyo mzuri, mkamilifu na mtu aliyekombolewa! Hili ni neno la kweli ambalo Roho wa kweli anasema. (Yoh.16:13). “Mkikaa katika neno langu, mtaifahamu kweli, na hiyo kweli itawaweka huru!” (Yoh.8:31,32).

NGUVU YA ROHO Nia yako, na ujuzi wa akili, hujenga wazo kutokana na vyanzo viwili: hisia (pamoja na kumbukumbu), au roho. Ufahamu wa Roho hutokea ndani, wakati hisia zako huhusiana tu na mazingira ya nje. Mawazo yetu hujaza hisia zetu. Utambuzi huleta tofauti.

Ufahamu wa Roho unajulikana kwa njia ya tamko na imani. Imani ni kwa roho yako wakati hisia ni kwa mwili wako. Imani inatambua ukweli tofauti na upeo wa hisia. Neno la Kiyunani la kuelewa ni, sunieimi, maana yake ni ufahamu uliounganika; kutiririka pamoja kama vijito viwili. Neno la dhamiri ni, suneidesis kutokana na neno sun+oida, maana yake ni karibu ile ile; ufahamu uliounganika au kuakisi.

Isaya 40:29-31 anasema juu ya mtu kufikia kikomo cha nguvu zake za mwili na uwezo. Katika ujana wake, nguvu zake hufikia kilele, bali hata vijana wanachoka na mara kwa mara huzimia kwa kuishiwa nguvu. Wengi wanaweza kuhusisha na uzoefu wa

59

Page 60: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

kufikia mahali ambapo mtu huhisi kushindwa na kupooza kabisa kwa udhaifu. Lakini hapa kuna habari njema kwa wale wanaohisi kwamba wamefika mwisho wa njia; “Bali wamngojao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.” Kwa kweli linatupa ujuzi wa mazingira mapya; wakati roho inapaa juu, mwili wako unaonekana kama unakwenda pamoja na nguvu mpya iliyopatikana kukabiliana na mzunguko wa maisha ya siku kwa siku hata kushughulika na ongezeko la hatua ya siku ya madai au upeo.

Hapa kuna ufunguo: MNGOJE Bwana. Kungoja hakujawahi kuwa shughuli ya kuipendelea. Hakika, siwezi kufikiri chochote kilicho cha kuchosha kukifanya zaidi kuliko kungoja. Ni mpaka wakati nilipoelewa maana ya neno la Kiebrania lililotafsiriwa ‘kungoja.’ Neno ‘KAWVA’ maana yake kuviringa au kusokota pamoja kama kutengeneza kamba au uzi wa muziki, kwa hiyo, huzidisha uimara wake wa kukatika, au kubadili sauti ya wimbo! Hakuna kinachosisimua zaidi kuliko kuyasokota mawazo yako pamoja na mawazo ya Mungu. Kanuni ya KAWVA inafanana na kanuni ya Sabato. Hii ndio siri ya utendaji wa kioo; kung’aa kwa ukweli wa shauri la Mungu kuhusu mimi kuimarisha tafakari yangu, mazungumzo na uzoefu wa jumla na mwenendo. Matokeo yake ni kama mvua ilainishavyo ardhi kwa unyevu-nyevu wake, kuiamsha mbegu, kuchanua kwa nguvu na mtikisiko wa maisha.. Isaya 55:6-11, anapenya ndani ya dhamiri yangu na kuchochea utu wangu kwa nguvu zake.

Paulo anaongea juu ya kusumbuka na kujitahidi kwa nguvu zote ili kwamba Mungu aweze kuleta uvuvio ndani yake. (Kol.1:25-29). Anahisi kumalizwa na mguso na shauku ili kumfikishia kila mmoja kipimo kamili na kimo cha Kristo. ( Pia angalia katika Efeso 1:17-20; 2:7). Anaona uwezo ule ule ndani ya kila mmoja, ili kufunua tabia ya Mungu katika mwili, kwa namna ile ile alivyofanya Yesu.

60

Page 61: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Katika Mathayo 6:22, Yesu anasema kwamba jicho ni taa ya mwili. Ikiwa jicho lako ni safi, mwili wako wote utakuwa na nuru! Neno lililotafsiriwa ‘safi’ ni haplous, hutokana na neno la Kiyunani, kufuatana na Itifaki ya Biblia ya Strong, ni ha, ambalo kwa suala hili hutoa sehemu ya mwungano, + pleko, lenye maana ya kusokotwa au kuviringwa, yaani kilichosokotwa au kufungwa pamoja! Huu ni muda mrefu kabla ya kuvumbua umeme! Kwa hiyo, ikiwa jicho lako limewashwa na shauri la Mungu kuhusu wewe, mwili wako wote utakuwa na nuru. “Maana kwako wewe iko chemchemi ya uzima, katika nuru yako tutaona nuru” (Zab.36:9). Hakuna kitakachounufaisha mwili wako zaidi ya nuru hii. Hakuna kiasi cha shauku kinachoweza kukuongezea thamani ya maisha yako. Kutambua uadilifu wa uhalisi wako, thamani ya utu wako kutokana na mtazamo wa Baba yako, hutajirisha maisha yako zaidi ya tamaa yako. Tulicho nacho tayari kinapita hali yote ambayo tungependa kuwa nayo!

Katika habari hii, Yesu anasema msisumbukie mtakula nini au mtakunywa nini, hata kufadhaika kuhusu mavazi yenu. (Math.6:25-34). Huu ndio msingi unaoweza kuupata, lakini la kushangaza ni kuwa msingi huu mara kwa mara unazishughulisha akili na muda na kujali kusiko kwa lazima.

“Waangalie ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kuliko hao? Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja? Na mavazi ya nini kuyasumbukia?” Hii haina maana kwamba tunastahili kuwa maskini. Kuvaa mavazi ya kifukara sio ishara ya kiroho. “Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti; nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo.”

Kwa kweli hakuna ubaya wowote wa kupanda, kuvuna na kukusanya; ni sheria ya uzima. Lakini ni upumbavu kutatanishwa na uchoyo na mchakato katika tamaa.

61

Page 62: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Kuongozwa na hisia za kupungukiwa na uhitaji kunazaa uchoyo, kutokuridhika na kuvunjika moyo. Sheria ya uhuru inapanda kwa furaha na kuvuna kwa shangwe. Imani hupanda hata wakati wa njaa. (Mw.26:1-12).

Huwezi kumpenda na kuambatana na Mungu na kupenda fedha kwa wakati mmoja; Kila moja huchukua nafasi ya mwingine. Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. Elekeza akili zako kwake na sio kusumbukia vitu. Kupenda fedha kunawafanya watu kuwa kichekesho. Ni kipimo dhaifu cha kupimia thamani. Utajiri wako ni mkubwa zaidi kuliko cheo chako cha kazi au mshahara wako. Katika kufuatilia utimilizo anasema, “Haya kila aonaye kiu, njoni majini, naye asiye na fedha; njoni, nunueni mle; Naam, njoni, nunueni divai na maziwa, bila fedha na bila thamani. Kwani kutoa fedha kwa ajili ya kitu ambacho si chakula; na mapato yenu kwa kitu kisichoshibisha? Nisikilizeni kwa bidii, mle kilicho chema, na kujifurahisha nafsi zenu kwa unono. (Isa.55:1-3).

Kutembea katika nuru kama yeye alivyo katika nuru, maana yake ni kuona maisha yako na kila jambo linalokuhusu kwa njia ya pekee kutoka katika mtazamo wa Baba. Hakika wewe ndiwe mtazamo wa wema wa Mungu. Kuwa na hakika ya asili yako katika Mungu, ndio nguvu ya maisha ya sheria ya uhuru. Kuakisi shauri la Mungu hukupatia mwanga ambao utakufanya maisha yako kuwa na mvuto usiozuilika.

Siku za kale, kujifunza ili kufanya kazi ya fedha katika benki, ilihusisha mazoezi ya kushika noti ili kupata uzoefu wa kuhisi kitu halisi, ili kwamba noti bandia iweze kugunduliwa haraka. Kuwafundisha watoto wako kwamba mbili kuongeza mbili sio nini, ni kichekesho. Wafundishe ukweli nao watajua tofauti. Kwa miaka mingi tumepigwa na dhambi, hukumu na hatia, na tumekwishaambiwa jinsi tusivyofaa na wanyonge; matokeo yasiyoepukika ni ya dhambi nyingi, hukumu, hatia na unyonge. Uovu si wa milele, bali nuru ni ya milele. Nuru inabakia kuwa ndio mamlaka ya mwisho dhidi ya dhambi. Hakuna kitu

62

Page 63: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

kitakachokuwa badala ya nuru. Kujitambua kuwa ndani ya nuru ya shauri la Mungu, ndiko kunakufanya kuwa huru.

“Kufa kila siku” hakuna maana yoyote iwapo wewe tayari umekufa kwa heshima. Katika nia ya Mungu, wewe ukiwa mtenda dhambi ulikufa wakati Yesu alipokufa, mara moja kwa ajili ya wote. Ili kufikia hitimisho moja la kuzihesabu dhambi zako, nafsi isiyoangaziwa nuru ya Mungu, kufa katika kifo chake ni kukubaliana na Mungu; kazi hii ndivyo ilivyo rahisi. (Rum.6:5,6,10,11). Msalaba wako si mwenzi wako, au mtoto wako, au mkuu wako; msalaba wake ni msalaba wako. Umesulubiwa pamoja na Kristo.

Mateso ya Paulo yasiyochukulika, hayakuongeza thamani kwa mateso ya Kristo; hakuna mateso yanayoweza kuchangia ustahili wowote kwa kuwepo na maana iliyo hai ya mateso ya Kristo kwa niaba ya wanadamu. Kuuadhibu mwili wako kwa kung’oa macho yako, kukata mikono yako au hata kwa kujihasi, hakuwezi kamwe kuongeza maana ya kifo cha kutisha ambacho Yesu alipata mateso kwa niaba yako.

Dalili za mafua, shinikizo, au ugonjwa mwingine wowote au maradhi, kwa kawaida ni za kuendelea. Tajiri au maskini, maarufu au la, dalili huonekana zile zile kwa kila mmoja. Dalili ya namna yoyote, kamwe haichukui nafasi ya utu wako, kwa namna yoyote haifanyiki kuwa wewe; inabakia kuwa mdukizi. Mwili umeumbwa kwa mfumo wa kinga za akili kupigana na kupingana na udakizi kutoka nje. Kuhukumu au kushutumu mwili wako unapojihisi kuwa mgonjwa au kuchoka kutakuwa kichekesho. Jifunze kujipenda mwenyewe sawasawa na wazo la Mungu kuhusu nafsi yako. Haiwezekani kujipenda na kufa nafsi yako kwa wakati mmoja. Hakuna kabisa uzuri wowote kwa kujaribu kufa nafsi yako bila kutambua kuwa ulikufa kifo kile kile alichokufa Yesu. Ufufuo wake unafunua uzao wako mpya. (1Pet.1:3).

63

Page 64: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

“Baada ya siku mbili atatufufua; siku ya tatu atatuinua, nasi tutaishi mbele zake.” Hos.6:2. (Miaka 800 baada ya Kristo). “Umeumbwa kwa njia ya ajabu ya kutisha. (Zab.139:14). ‘Wewe ni kazi yake’ (Ef.2:10). ‘Kazi yake ni kamilifu’ (Kumb.32:4).

Ikiwa mtu mmoja atakulipia deni lako tu kwa sababu mtu huyo anaona thamani ya kutosha ndani yako na kuona ni haki kukufanyia hivyo, halafu wewe usiipokee zawadi hiyo kwa shukurani, litakuwa ni tusi. Amini kuwa Mungu yuko sahihi kuhusu wewe, anakuamini.

Kupaa katika hali ya kiroho na kushiriki maono yake kwa ajili ya maisha yako, ndilo fungu na hatima yako sasa!

ZAIDI YA UNUNUZI WA KUTAZAMA DIRISHANI

Yaliyotokea kihistoria na kiroho Yesu alipopata mateso, alikufa na kufufuka katika wafu, wanajumlishwa wanadamu wote, kwamba wanaamini hayo au la. “Mungu alikuwa ndani ya Kristo akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake.” Mungu hakuchezea kamari uzima wa Mwana wake. Haki ya Mungu haipo katika hatari. Upendo wake umejengwa katika thamani, na siyo katika huruma. Aliona thamani ile ile ndani yako. Aliikomboa sura yake na mfano wake. Aliona tunda la uchungu katika nafsi yake, na lilimridhisha. Imani ya Mungu inakuona wewe ukiwa huru! Uzao wako mpya siyo matokeo ya uamuzi wako makini ulioufanya kumfuata Yesu, bali ilikuwa ni kuamshwa kwa roho yako kuuendea ukweli wa lile ambalo tayari lilitokea miaka elfu mbili iliyopita, Mungu alipomfufua Yesu katika wafu. Kufufuka kwake kutoka kwa wafu kulileta namna mpya! (1Pet.1:3).

Kumwona Yesu aliyekufa kihistoria tu kama mtu, hakuleti maana yoyote ya zaidi kuliko simulizi za kidini. Yesu sio mfano kwa mtu; yeye ni mfano wa mtu! “Kumtazama kama katika kioo, kunambadilisha mtu kuwa katika mfano wake, kutoka utukufu [shauri] hata utukufu [shauri]” (2Kor.3:18). Shauri lake linatengeneza hatua. Kioo kinaonyesha kifo na ufufuo wa yule

64

Page 65: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

unayemtazama. Kioo kinamwonyesha mwanadamu ndani ya Kristo. Huu ni ufunguo wa kuielewa Injili. Ujione ukiwa ndani ya kioo katika kifo chake na katika ufufuo wake. (Rum.6:6).Kuamini katika utajiri wa madini yaliyowekezwa katika ardhi sio hakika ya kuushinda umaskini. Kugundua dhahabu ndani ya bustani yako mwenyewe, ndiko kunakoleta tofauti na kukuweka huru. Upatikane ndani ya Biblia! Huku kutafanya usomaji wa Biblia uwe wa kusisimua na kubadilisha maisha. Kila tunapoisoma Biblia, mara kwa mara tunakuwa na mtu mwingine katika akili! Gombo lilipotolewa kwa Yesu, alitafuta mahali palipoandikwa, “Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema….” Maelezo yake yaliyofuata, yaliwashitua makutano; walidhani kuwa walimfahamu vema. “Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu!” (Luka 4:17-22). Biblia nzima inamhusu Yesu, na Yesu mzima anakuhusu wewe! “Katika gombo la chuo nimeandikiwa” (Ebr.10:7). Ufunuo wa kuonekana katika kioo, unabadilisha mambo yote. Yeye ni mwonekano wa kioo kwangu. Hivi ndivyo Mungu anionavyo! Alipokufa, sababu yoyote ambayo ningekuwa nayo ya kuishi maisha manyonge ilikufa, na alipofufuka, wanadamu walifufuka pamoja naye katika upya wa uzima. Katika nia ya Mungu, kila jambo alilolifanya Yesu, na kila namna alivyo, kunajumlisha kizazi cha wanadamu wote. Habari njema, ni stakabadhi rahisi iliyotolewa kwa wanadamu kama uthibitisho halali wa kuachiliwa kwao.

Inashangaza jinsi tunavyojitahidi kupokea kitu ambacho hatukukitendea kazi, au labda tuseme hatukustahili, hata hivyo tusingepata tatizo lolote kudai fedha tulizoshinda mchezo wa LOTTO. Pia hatuna tatizo kupokea ushindi wa timu yetu au mshindi wa mchezo kama ni wetu sisi wenyewe. ‘Tumeshinda!’ Hata ingawa tuliangalia tu mchezo kama watazamaji. Lakini bado tunaendelea kujiuliza kana kwamba hatimaye itatuchukua kifo chetu cha mwili kutuweka huru kutokana na masumbufu ya mwili wetu, kana kwamba kifo cha Yesu kilikuwa na maana na huruma ya kiroho tu. Inakuwa kama kuja kwa mara ya kwanza kwa Kristo kulikuwa ni kwa kushindwa kidogo, mtego mwingine maarufu wa mawazo na maono ya kidini sasa ni kwa kukata

65

Page 66: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

tamaa, kungojea unyakuo na kuja kwake mara ya pili kutuokoa. Imani yako katika kifo na ufufuo wake kama ni wako, sio nafasi yako ya kwanza kukupa sifa ya siku moja kwenda mbinguni, bali ni kuachilia uzima wake ndani yako ili kukuandaa kwa maisha ya sasa, hapa hapa, katika sayari hii ya dunia. Anapenda kuwasiliana na kufunua utukufu wake ndani yako. Katika hali na mtiririko huu, wewe ndio kuja kwake mara ya pili! Chembe ya ngano ambayo itawalisha wanadamu kwa mkate wa kweli kutoka mbinguni imeshuka duniani na kufa. Haikubaki peke yake, bali ilizaa mavuno yasiyopimika! (Yoh.12:24). Mavuno haya yameiva na yako tayari! Wewe ni mavuno ya Mungu. Mara baada ya ufufuo, Petro na Yohana walimpa kiwete kile walichokuwa nacho kama matokeo wa ushindi wa Kristo. Kujumlishwa kwa wanadamu katika uzima wa Kristo, kifo na ufufuo, ni kurejeshwa kwa mambo yote waliyoyaona manabii. “Walihubiri habari za siku hizi…. Mungu , akiisha kumfufua mtumishi wake Yesu, alimtuma kwenu ninyi kwanza.” Yesu hakufa na kuondoka, bali yu hai na salama ndani ya kila mwamini anayemkumbatia kama mwonekano wa kweli wa mtu. Mwujiza wa Matendo sura ya 3 haukuwa hasa kwa uponyaji wa kiwete, bali ulikuwa ni hakika ya Kristo aliyefufuka akijifunua katika maisha ya kawaida, watu wasio na elimu na wa kawaida! (Mdo 3:7,13,18-21,24,26; 4:13).

Wakati ningali ninaijua sheria ndani yangu, inayonilazimisha kufikiri, kusema au kufanya mambo ambayo yatawaumiza wengine au mimi mwenyewe, tayari nimekwisha sahau neno la kweli linalofunua sura ya utambulisho wangu wa kweli katika kioo. Halafu, kugeukia tena chemchemi ya kweli, na kutambua kwa kicho uadilifu wa sheria kamilifu ya uhuru, kunanithitishia ndani yangu furaha isiyoneneka ya kuwa na umoja na Muumba wangu. Kipawa cha Mungu kwa wanadamu katika Kristo, ni mbali na mapendekezo ya matokeo ya kosa la Adamu. (Rum.5:12-21; 1Kor.15:21,22). Tuna uhakika kwamba mmoja alikufa kwa ajili ya wote, kwa hiyo wote walikufa. Tangu sasa, hatumjui mtu awaye yote kwa jinsi ya mwili. (2Kor.5:14,16). Kusikia kwamba kila kitolewacho kilicho chema hutoka kwa Mungu, na kwamba sisi ni ndoto yake ya upendo, iliyo katika

66

Page 67: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

sura yake, ni kuona uso wa mwanzo wetu kama katika kioo. (Yak.1:18,23,24). Sheria ya kifalme huwa na maana tu katika mazingira haya: Kushiriki mwanzo mmoja kunaniweka huru kumpenda na kumthamini jirani yangu, kama ninavyojipenda na kujithamini nafsi yangu. Kuwa mkarimu bila kuonyesha upendeleo ndio hitimisho lenye maana. Tambua hali ya kifalme, iliyo katika mavazi mabovu! (Yak.2:1-4,8). Tunawezaje kumbariki Bwana na Baba, halafu kwa kinywa hicho hicho kuwalaani watu walioumbwa kwa mfano wa Mungu (Yak.3:9). Haijalishi ni kiasi gani mtu anatokea kustahili laana, hukumu na mashutumu, katika nia ya Mungu, na kulingana na yale aliyoyafanya Yesu, anastahili kuachiliwa zaidi. Hizi ni habari njema ndani ya ganda. “Lakini ijapo ile iliyo kamili, iliyo kwa sehemu itabatilika. Nilipokuwa mtoto mchanga, nalisema kama mtoto mchanga, nalifahamu kama mtoto mchanga, nalifikiri kama mtoto mchanga; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto. Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule (nikiwa mtu mzima) nitaona uso kwa uso; wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana” (1Kor.13:10-13). Mungu, kamwe hakumjua mtu kwa namna nyingine! Uhai wa Injili ni kujijua sisi wenyewe kama vile tulivyojuliwa daima. “Bali mimi nikutazame uso wako katika haki, niamkapo nishibishwe kwa sura yako” (Zab.17:15). Siri ya ukweli ni kuona uso wa Mungu katika uso wa mtu!

INUKA!

Binti mdogo aliyekuwa amepoteza jino lake la mbele, alimwomba mwalimu wake aume tunda lake la mtofaa, ili amsaidie kuanza njia.

Bila kuingia katika kiburi cha ‘fanya na usifanye,’ au kuanguka katika mtego wa mchanganyiko mwingine wa kidini, kwa ujasiri kabisa ningekutia moyo katika mtazamo ufuatao: Maombi yana mchanganyiko wa vitu vinne: kuabudu, maombezi, mahitaji na shukurani. Zingatia katika kuabudu mbali na mazoea ya kidini. Inashangaza jinsi mahitaji yako yanavyokuwa madogo,

67

Page 68: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

unapozingatia juu ya Mwenye enzi yote, na ukweli wa utisho wa kukaa kwake ndani yetu. Mara nyingine mtu anaweza kujua zaidi mahitaji na maombi kuliko Mungu. Mungu anapenda kuwa zaidi ndani yako kuliko ‘tengenezo la haraka.’ Kuwepo kwake na ufunuo wa madaraka yake na kujumlishwa kwako katika Kristo, unakupa nguvu. Sio kadiri au ukubwa wa mahitaji yetu unaohamasisha bidii na maombi yenye ufanisi, bali ni ushawishi na uthabiti wa imani yetu katika kazi iliyokamilika na utimilifu wake ndani yetu. “Aa! Bwana Mungu, tazama, wewe umeziumba mbingu na nchi, kwa uweza wako mkuu na kwa mkono wako ulionyoshwa; hapana neno lililo gumu usiloliweza. Mungu aliye mkuu na aliye hodari. Tazama, mimi ni Bwana, Mungu wa wote wenye mwili; je, kuna neno gumu lolote nisiloliweza?” (Yer.32:17,19,27). Kuna thamani isiyopimika katika kutafuta ufalme wake na haki yake kwanza, sio kwa sababu ya agenda ya siri, bali kwa sababu amekuwa ndiye shauku yako pekee. (Math.6:33). “Nawe utajifurahisha kwa Bwana, naye atakupa haja za moyo wako.” (Zab.37:4). Usiingie katika mtego wa udanganyifu wa mali. Hakuna kigusacho zaidi undani wako na Mungu. Heshimu mwanzo wako kwa kicho kikuu na heshima. Yeye ni mpole. Anatufundisha katika tumbo la subira. Anatuwezesha na kututia mafuta. Anakuzungushia wema kama ngome. (Zab.5:12).

Anza kuishi kwa utajiri wako. Kwa yale ambayo umeyaona, tayari unaweza kumtajirisha na mtu mwingine pia. Kumbuka jinsi ambavyo kifungua kinywa cha mvulana mmoja kilivyowalisha makutano! Ishi maisha ya dhamiri yenye thamani. Ishi ukijua utajiri uliomo ndani yako. Wakati watu wanapokuwa matajiri wa kweli, watasimama kwa ujasiri, bila mashaka au kiburi. Wanaweza kufanikiwa kuwa wanyenyekevu; hakuna haja kwao ya kutambuliwa au kusifiwa. (Math.6:2-4).

Mungu anapendezwa nawe kwa sababu yeye anaamini zaidi kuwa ndani yako. Imani yako inafunua thamani unayoiweka juu ya imani ya Mungu ndani yako. Kushikwa na nguvu ya kujua ukaaji wa Mungu ndani yetu, kunaichochea na kuiamsha roho ya mtu na shauku ya kutumiwa. Mara moja, mahitaji yako

68

Page 69: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

binafsi yanaonekana kutokuwa ya maana ukilinganisha na uwezo wa Mungu ulio ndani yako wa kuwafikia na wengine. Kwa kadiri anavyotamani kukubariki, ndivyo anavyopenda kuwabariki wengine kupitia kwako. Si ajabu kwamba Yakobo anahitimisha kuwa, dini ya kweli ni kwatembelea wajane na yatima. Unaweza kufikiri jinsi ambavyo huzuni zao na upweke wao unaweza kuijaribu dhana ya kuwa mkamilifu bila kupungukiwa na kitu?

Onyesha shukurani, kuthamini, kupenda, kufurahia, kutia moyo na thamani. Uwe mjumbe wa habari njema wa kipekee. Usibishane. Kuna maana gani kushinda mabishano, lakini ukampoteza mtu? Sasa unaweza ‘kutoa bila kusita, kupoteza bila kujuta, na kupata bila uchoyo.’ Na George Sand.

Uwezo wetu wa kuona thamani ndani ya watu wengine ni lazima uwe kwa wema, hata kama thamani hizo zimekuwa ngumu kwa uharibifu, hofu, kukata tamaa na chuki. Roho ya binadamu huangazwa na mng’ao wa Roho wa Muumba wetu, huendelea kuwa nguvu ya kutawala dhidi ya uharibifu na aina zote za giza. Shuku na wivu hushindwa kwa njia ya msamaha, uadilifu na urafiki. Hizi ni nguvu za msukumo wa nuru na maisha ambayo hayawezi kudharauliwa kamwe.

Kupata zaidi kwa mtu ni kupenda kutoa pasipo wazo la ubinafsi, kuishi kwa kutoa, pasipo nia ya pembeni au agenda iliyofichika. Je, unaweza kufikiri juu ya jamii ambayo mtazamo huu unatawala?

Ninaendesha mabasi mawili ya zamani ya Leyland. Moja lina umri wa miaka 30 na lingine lina miaka 50. Kinachonishangaza daima ni jinsi mabasi haya zamani yanavyotegemewa. Kwa kubonyeza tu kitufe, mashine inawaka, inatoa hewa na muungurumo wa nguvu na kuwaka; Yalitengenezwa kufanya namna hiyo. Watu wameumbwa kutoa mwitikio wa mguso. Mafundisho haya na yakuguse kama mvua ya upole juu ya mapigo mororo, na kama manyunyu juu ya mimea mikubwa. (Kumb.32:2).

69

Page 70: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Nitanong’ona maneno ambayo upepo utayapeleka ng’ambo; wakati utageuzwa kuwa ngurumo katika mgongano wa mawingu ya mawazo. Wakati ni mwenzi wa tumbo.

Mwana wangu mdogo Stefan, alipokuwa na umri wa miaka minne, alisimamia vidole ili kukifikia kinanda cha piano na kukipiga kwa sauti ile ile ambayo alimsikia kaka yake Renaldo akipiga. Nilishitushwa na kuuliza jinsi gani aliweza kufanya vile. ‘….Ni rahisi baba, ninabonyeza tu kibao kinachotoa sauti ya wimbo!’

MUDA WA MWANADAMU WA UTUKUFU

Kwa njia hiyo, Yakobo huyu anayeandika kuhusu sura ya mfano wa kioo ya asili yetu katika Mungu, alikuwa ndugu mdogo wa Yesu. Walifanya kazi kama maseremala pamoja na baba yao, na kuongozwa maisha ya kawaida katikati ya muundo wa kijamii uliokubalika kwa wakati wao kwa miaka mingi. Lakini Yesu alipofikisha miaka 30, maisha yake na huduma isiyo ya kawaida ilianza. Mwanzoni,Yakobo lazima alijitahidi kwa shida na ugumu wa kutambulika. Ni wapi ndugu yake alipata ufahamu huu wote, kwa mara moja?

Makutano walivutwa kumsikiliza akihubiri na kushuhudia miujiza yake. Maji ya kawaida yanaitwa jina bora katika arusi. Kwa njia hiyo hiyo, watu wa kawaida maisha yao yalibadilishwa. Magonjwa mengi yaliyokuwa sugu yaliponywa. Vipofu walilia kwa furaha, mara walipoanza kuona. Viziwi, viwete waliruka na kucheza. Wakoma walitangaziwa utakaso, na hata wafu walifufuliwa.

Sifa zake zilienea mbali, kiasi kwamba watu walisafiri kutoka ng’ambo ya bahari ili kuonana naye. Utalii unaongezeka. Usafiri katika siku zile haukuwa mzuri. Yalikuwa maisha ya vitisho! Hata hivyo, Wayunani walifika na kutaka kumwona Yesu. (Yoh.12:19-24). Wanafunzi wake wanafurahi; ni lazima wawape thamani kwa fedha zao. Huenda wangemfanyia hila moja au

70

Page 71: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

hata mbili, kama vile kutembea juu ya maji, au wangeanza kupanga mistari ya wagonjwa. Ni fursa ilioje kumtangaza Yesu kimataifa!

Lakini Yesu anakubali ombi la Wayunani kwa maelezo haya ya kushitusha: “Saa imefika atukuzwe Mwana wa Adamu” Je, sasa atanyakua mamlaka na kufanywa Mfalme wa kipindi kipya? Huenda angekuwa kiongozi wa kisiasa mkuu wa wakati wote. Hata hivyo huu usingekuwa wakati mkuu kwa ajili ya mtu mkuu; huu ni wakati mkuu kwa ajili ya wanadamu!” Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi.” Haiwezekani kwa chembe moja ya ngano kuzaa kipande cha mkate, isipopandwa kwanza katika udongo wa mbolea na kuvunwa, wala haukuwa ubanifu wa Mungu ambapo mikate mitano na samaki wawili walilisha maelfu. Kwa kuwa mtu hakuumbwa kuishi kwa mkate pekee, hakuna kiasi cha hali ya kufurahisha, wala kushuhudia mambo ya ajabu na miujiza inayoweza kuiridhisha roho ya mwanadamu.

Katika habari hii, Wayunani wanawawakilisha mataifa walio mbali na watu wa Uyahudi. Yesu alielewa kuwa ufunuo wa Mungu asiyeonekana ndani ya mwili wa kibinadamu, kamwe haukuwa na maana ya kubakia kuwa ufunuo pekee wa Mungu, ndani ya mtu mmoja wa kipekee, ambapo ungefika wakati, na maana yake ingeharibika na kuwa jambo la kishujaa tu, kihistoria, na maono ya kidini. Wala hakuwa na maana ya kuwa Masihi wa taifa moja maalumu. Maisha yake, kifo na ufufuo wake uliwajumlisha na kuwawakilisha wanadamu wote, ili kwamba wao wafanyike kuwa mavuno ya kifo chake na ufufuo wake.

Hitaji kuu la wanadamu ni kuikumbatia sauti ijulikanayo na kutambua ukaribu wake; na kujua kwamba Mungu si mgeni, si duni, wala si Mungu aliye mbali, bali kwamba yu karibu nasi kuliko hewa tuivutayo!

71

Page 72: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Saa imefika ili Mwana wa Adamu atukuzwe. Wakati wa utumwa na wa giza umekwisha. Mavuno ya wote ambao aliwakusudia na kuwakamilisha katika dhabihu ya kifo chake yapo hapa! Shauri na utukufu wa Mungu katika uso wa Kristo sasa unang’aa ndani ya mioyo yetu, ili kuleta maarifa ya ukombozi wa umoja wetu pamoja naye. Kioo cha ukweli kinafunua na kuonyesha utukufu (shauri la asili) wa Mungu uliorejeshwa katika Mwili. Inuka uangaze, kwa kuwa nuru yako imekuja!

KANISA

Mafundisho, miujiza na umaarufu wa Yesu vilifanyika kuwa somo la mjadala mkubwa. Maana ya haya yote ilikuwa nini?

“Watu hunena Mwana wa Adamu kuwa ni nani?’ Yesu aliwauliza wafuasi wake. (Math.16:13). Kila mmoja alijua kuwa Yusufu na Mariamu walikuwa wazazi wa Yesu. Au labda Yesu aligeuka kutokana na mwili wa Musa, au wa nabii Eliya! Mara Simoni alijibu kwa uhakika, “….Wewe ni Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai!” Neno la Kiyunani la Kristo ni xristos, linatukumbusha juu ya neno la xeir, yaani, mkono. Upana wa mkono ulikuwa aina ya kipimo cha zamani na asili. Bado tunatumia vipimo kwa mfano, urefu wa mikono 17. Neno Kristo au Masihi lina maana ya mpakwa mafuta. Yesu lina maana ya Mwokozi; alitabiriwa kuwakoa kizazi cha wanadamu, tangu mwanzo wa kuandikwa kwa historia. Yeye ni mkono wa Mungu ambao ungedakiza wakati na kufunua chapa ya milele, na kipimo cha uumbaji wao wa asili. “Tunaona asili na sura iliyokusudiwa ya maisha yetu tukiwa ndani yake. (Tafsiri ya’The message’ Rum.8:29).

“Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye Mbinguni.” Wewe ni zaidi ya kuwa mwana wa Yona tu. Asili ya mtu inakwenda mbali zaidi ya mwili! “Nami nakuambia, wewe ndiwe Petro, na juu ya Mwamba huu (petra, mwamba mkuu, kwa hiyo, petros imechimbuliwa kutoka petra; Isa.51:1) nitalijenga kanisa langu;

72

Page 73: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

wala milango ya kuzimu haitalishinda” (ekklesia). Kanisa ni sauti ya utambulisho wa Mungu katika mwili; ‘Neno alifanyika mwili!’ Ufunuo wa kwamba Mwana wa Adamu ni Mwana wa Mungu kweli ndio msingi kwa nafasi hii ambayo Baba anatuita kuingia ndani yake. Neno lililotafsiriwa kanisa, ni ekklesia, lina maana zaidi kuliko picha ya desturi ambayo inakuja akilini, ikimaanisha, ‘ekklesia’ yaani, kuita kwa jina, au mwaliko muhimu na mguso. Tumeitwa kutoka katika nafasi ya kuzuiliwa na kusalimika na kuwepo katika mwili kuingia katika nafasi mpya ya maisha yasiyo na mwisho. Tumeitwa kuujua utambulisho wetu wa kweli katika Kristo. Maneno mawili yanaunda neno la ekklesia: ek, ambalo ni la utangulizi, likiashiria asili; na neno kaleo, lenye maana ya kualika kwa sauti kuu, au kumpa mtu jina, kuamkia kwa jina. Hivi ndivyo hasaYesu alivyofanya, alifunua asili ya kweli ya mtu na kumpa Simoni jina jipya!

Neno hades, (kuzimu) linatokana na ha + ideis maana yake, kutokuona. Kuyaona maisha kama ni hali ya kuonekana katika macho ya kawaida tu, ni kuingia katika mtego wa nia na kuonekana kibinadamu. Usemi, “milango ya kuzimu haitalishinda” lina maana kuwa, wito wa kutoka katika mji huu uliofungwa na ukuta wa maisha ya mwili, uliohifadhiwa katika hali kama ulivyokuwa, utasababisha vipingamizi vyote kuharibiwa. Kuzimu kunawakilisha chochote kinachomfunga mtu katika mawazo duni kuhusiana na yeye mwenyewe. Yanangojewa maisha ya kupendeza sana yasiyofikirika nje ya ukuta wa mji. Kuta ambazo zilikuwa na maana ya kuuweka na kuulinda mji na kuufanya gereza.

Mkakati wa Mungu kwa ajili ya kanisa lake sio jengo, bali ni mwili! Ushirika ni zaidi sana kuliko mikutano rasmi; ni mazungumzo yanayoendelea; “katika ujuzi wa kila kitu chema kilicho kwetu katika Kristo.” (Filem.6). Majengo yote ya makanisa leo, ya madhehebu yote, na nafasi zilizojaa, hayawezi hata kuchukua asilimia 2% ya idadi ya watu duniani. Mungu anaona zaidi kuliko shirika au jengo; anauona mwili wako, utendao kazi, chombo kinachosogea, ambacho kinabeba

73

Page 74: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

na kufunua uwepo na asili ya Mungu asiyeonekana. Huruma zake zinadhihirika katika macho yako na mguso; neno lake linapata sauti ndani yako. Mungu huona uwezo usioonekana ndani ya mtu sawa na alivyoona ndani ya Yesu. Chembe ya ngano huzaa mavuno yenye thamani inayofanana. Mavuno hayajapunguzwa nguvu, nakala duni ya mbegu ya asili; ni sura ya kioo halisi ya mbegu ile ile. “Kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.” Yesu aliweza kuwa mahali pamoja kwa wakati mmoja, kwa miaka mitatu ya huduma. Sasa amejizidisha ndani yetu bila shida ya wakati na mipaka. Huu ni mkakati wa Mungu. Haya ni mavuno anayoyatazamia. Kwa kusudi hili, analiandaa kanisa kwa mambo yote yanayomleta kila mtu kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo. (Ef.4:11-13). Kusudi la Mungu ni kukuandaa wewe kwa ufunuo wa utimilifu wake ndani yako ili kwamba, maisha yako yaguse maisha yajayo kwa maana ile ile. Watu wanahusiana na watu. Paulo aliuelewa mkakati huu, “….Bali tukiwa na tumaini ya kwamba, imani yenu ikuapo, tutakuzwa kwenu kwa kadiri ya kipimo chetu na kupata ziada, hata kuihubiri Injili katika nchi zilizo mbele kupita nchi zenu. (2Kor.10:15,16). Mungu asiyeonekana, anaonekana; kugusika na kusikika ndani yako! Ah! Mwili wako na nafsi yako ni gari lake. Wewe ni mkakati wa Mungu! Fikiri kuwa Mungu anawaza mawazo yake ndani ya akili yako. Fikiri, Mungu anasema neno lake kupitia midomo yako. Fikiri, Mungu anafanya kazi yake kupitia mikono yako! Fikiri, aliye wa milele anautaka muda wako! “Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema; wafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona tena, kuwaacha huru waliosetwa.” Luka 4:18,19). Ujumbe huu hauji kwako kamani namna ya njia nyingine ya pili, au tazamio la kufurahisha, au tafsiri mpya ya mafundisho ya kidesturi. Wala haikupi uchaguzi wa kufanya biashara katika bima kwa ajili ya Mercedes. Tunaongea hapa juu ya nafasi kubwa! Hali mpya ya maisha yenye nguvu ya hapa na sasa, yenye uamsho ndani yako.

74

Page 75: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Tukiwa katika mapumziko ya ndoa yetu kule Blydepoort, Mpumalanga, Januari 1979, mimi na Lyidia tulikutana na afisa kutoka hifadhi za mali asili aliyetuambia juu ya tukio la kufurahisha; alishuhudia tendo la kuachiliwa kwa Tai Mweusi majuma machache kabla ya kufika kwetu. Tai huyu alikuwa mfungwa katika shamba la Pretoria kwa miaka kumi. Alitueleza jinsi walivyokuwa na msisimko, furaha na matazamio, wakati hatimaye tai alipowasili akiwa katika kisanduku na kilango chake kufunguliwa. Lakini ni baada ya kazi ngumu, hatimaye walifanikiwa kumtoa ndege huyo katika kisanduku chake. Lilikuwa suala moja kumtoa ndege katika kisanduku, lakini ni jinsi gani ya kukitoa kisanduku ndani ya ndege, lilikuwa ni suala lingine! Katika akili ya huyu tai, alikuwa bado ni mfungwa wa shamba la Pretoria! Kila mmoja alikuwa akishusha pumzi yake, lakini huyu ndege mwenye nguvu alibaki kuwa mfungwa wa akili duni. Hakukuwa na badiliko mpaka baada ya muda mrefu wakati tai mwingine alipoanza kuita katika eneo lile. Macho ya tai wa kufugwa yaliangaza, na mara alichukua hatua ya kuruka katika anga lisilo na mipaka. Unaposikia sauti unayoifahamu, huhitaji tena sababu za kuruka. Milango ya gereza imefunguliwa. Kuzimu hakuwezi kukurudisha nyuma. EKKLESIA.

‘NDINYI MIUNGU; NA WANA WA ALIYE JUU NYOTE PIA

Jambo la pili la kweli ni kwamba, Mwanzo 1:26, linatangaza kuwa Mungu alimwumba mtu kwa mfano wake na kwa sura yake, maneno haya yanakuzwa miongoni mwa wengi na kuwa maelezo ya kushitusha katika maandiko yote. Kinachosababisha mshituko ni wasikilizaji waliohutubiwa na Yesu: Viongozi wa dini wa siku zake walichukizwa naye sana hata kutaka kumpiga kwa mawe kwa kukufuru. Alithubutuje, mwana wa mtu tu kujifananisha na Mungu? Maelezo yake kama vile, “Mimi na Baba tu umoja” hayakueleweka vema kwa Mafarisayo! (Yoh.10:30-39). Waliweza kumhesabu kuwa mwenda wazimu au aliyepagawa na mapepo, au vizuri zaidi, kumharibu na kumnyamazisha milele. Kwa hawa washika dini

75

Page 76: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

wasioangaziwa nuru, Yesu alinukuu maneno ya nabii Asafu, “Mimi nimesema, ndinyi miungu, na wana wa Aliye juu, nyote pia, lakini hamjui wala hamfahamu; kwa hiyo, mtakufa kama wanadamu, mtaanguka kama wanadamu tu.” (Zab.82:5-7).

Ijapokuwa ufahamu wa mtu umetiwa giza, ni lazima kuwe na jambo ndani ya mtu linalomfanya mtu awe wa aina ya Mungu. Mtu si kiumbe tofauti kilichotengwa kutoka kwa Mungu; yeye ni mbebaji wa mfano wa Mungu unaofanana katika sura na uwezo wa kutunza roho. Kwa kweli yeye ni sehemu ya Mungu mwenyewe.

Andiko katika Waebrania 2:6-12 lina nguvu inayofanana. Hata watafsiri wa andiko hili hapa wanaonekana kutokupenda hata kumjulisha mtu kwa Mungu; wanaona ni vizuri zaidi kutumia neno ‘malaika.’ Zaburi ya nane ya Daudi imenukuliwa; “Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, na binadamu hata umwangalie? Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu” ndivyo lisemavyo andiko la asili. (watafsiri wanapendelea kusema ‘mdogo kuliko malaika’). Umemvika taji ya utukufu na heshima, umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.” Tunashiriki katika uwepo na hali ya Mungu; tumekuwa na kikomo tu katika ufahamu na utambuzi. Hata hivyo, anguko la dhambi liliwatosa wanadamu mahali ambapo badala ya mtu kutawala ulimwengu wa wanyama, asili ya mnyama inatawala ndani ya mtu.

Ni pale tu ukweli wa ukombozi utakapopambazuka katika ufahamu wetu, utawala wa asili ya unyonge utakuwa umevunjwa.

Katika kitabu chake cha MUNGU-MTU, Dr John G Lake, anaandika yafuatayo: Tuna mwili wa kibinadamu wenye milango mitano ya fahamu, na kupitia milango hii, tumeletwa katika uhusiano wa shabaha fulani ya utendaji ambayo ni ya kimwili kabisa. Lakini hayo yote ni kwa mtu. Mungu anapenda kuamshwa kwa ufahamu wetu kutambua kwamba mtu wa ndani ndiye mtu halisi. Mtu wa roho ni mtu asiyekufa milele. Ni mtu ambaye Mungu mwenyewe

76

Page 77: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

hawezi kumharibu, kwa sababu Mungu hawezi kujiharibu mwenyewe. Mtu ni wa asili ya Mungu.

Mtu anapokuwa chini ya huyo Mungu-mtu wa kiroho na kumshushia heshima kwa tamaa za mtu wa nje wa nyama, ni kwa jinsi gani mtu wa ndani lazima augue! Mungu hakukusudia kamwe kwamba mtu wa nje wa nyama awe mtawala wa mtu wa ndani wa roho. Kama vile mtu wa nje wa nyama hupokea kwa kuona, kwa njia ya mgusano, mambo yatokeayo kuhusu yeye, na kama yalivyoandikwa katika nafsi, ndivyo shabaha ya utendaji ilivyo kuu kuliko mtu wa mwili. Mtu wa mwili na wa roho kwa pamoja, huandika mambo yao katika dhamiri ya nafsi.

Maendeleo ya mtu wa ndani kuingia katika sura na kimo cha Kristo, ndio msingi mkuu na kusudi ambalo linaweza kuendesha maisha yetu. Nguvu mpya ya msukumo inayoshika mioyo yetu ni dhamiri ambayo kwa hiyo, Mungu ana kusudi la milele katika maisha yetu. Utume wa ki-Mungu na kusudi ambalo litaendelea kujinua hata zaidi ya maisha yetu katika mwili.

Mimi ni mwamini katika muungano baina ya mtu na Mungu. Kuna kuchanganya, ulinganifu wa Mungu na mtu; wawili kuwa mmoja. Sio mtu aliyeokoka na Mungu wa utukufu. Lakini mtu hujichanganya katika Mungu, na Mungu hujichanganya katika mtu, na kuwa uumbaji mmoja wa ki-Mungu. Musa aliposimama katika Bahari ya Shamu, hawakuwa Musa na Mungu, alikuwa ni Mungu tu. Tunasema, “Mungu nifanye kuwa njia ya kupitia” kuondoka kwetu na kujitenga na Mungu katika mawazo yetu, huku tukimtazamia kumimina nguvu zake za kiroho na baraka kupitia sisi; hilo si jambo la juu kabisa. Kuna ujuzi ulio mkuu zaidi kuliko ulio katika neno. Ni pale wewe na Mungu mnapokuwa wamoja. Mwili wako wote, nafsi yako yote, akili zako zote, moyo wako wote, roho yako yote inaanza kutembea katika makubaliano na mchanganyiko na ulinganifu wa Mungu wa milele; wamoja katika moyo, wamoja katika akili, wewe na Mungu kama mmoja. Musa alijaribu kuurudisha uhusiano huu. Mungu alimwambia kunyamaza na kuacha kuomba ili

77

Page 78: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

kuendelea na kazi! “….ukaunyoshe mkono wako juu ya bahari na kuigawanya!”

Mungu hatafuti tu mahali pa kuishi; anatafuta haki ya matendo katika mwili na roho ya mtu. Mungu anatazamia umoja wa upendo ule ule ambao ulitendeka kati ya nafsi yako na yeye mwenyewe ili uongezeke, ili kwamba uukumbatie umoja huo pamoja na nafsi za watu wengine. Nyumbani mwako, ofisini mwako, popote ulipo, acha maono ya mawazo yako huko. Popote ulipo, uudhihirishe utamu wake na ishara ya nguvu zake.

Maneno ya mwisho ya Injili ya Yesu Kristo ni kuzalisha na kumfanya kila mtu aliyefungwa na dhambi na kushikwa na mambo ya mwili na kuwa mtumwa wa mwili, awe kama yeye katika matendo na kweli, Mwana wa Mungu. Sio wana wa Mungu kwa kiwango cha chini, bali wana wa Mungu kama Yesu alivyokuwa. Mwanadamu ni chombo cha kustaajabisha na cha ajabu katika uumbaji wake wote na uwezo wa kumfunua Mungu.

Watu wamekuwa na tabia ya kumweka Yesu katika daraja lake mwenyewe, kiasi kwamba wameshindwa kutambua kuwa, amekwisha kutoa nafasi kwa Roho hai wa Mungu aliyeishi katika maisha yake mwenyewe, ambayo yeye mwenyewe alikuwa udhihirisho hai, kuishi ndani yao na akili zao. Wewe ni wa lazima kwa Mungu katika mpango wake kwa ajili ya wokovu wa wanadamu, kama Mungu alivyo wa lazima kwako. Pasipo mtu, Mungu asingekuwa na njia ya kupitia, ambayo kwayo angejidhihirisha kwa ulimwengu.

Umemfanya Roho wa Mungu aliye wa thamani kana kwamba ni njia ya kujifurahisha kiroho. Kusudi la Mungu ni la nguvu zaidi kuliko hilo. Yesu alipokuwa karibu na kuondoka, alisema, “ Utukufu ule alionipa Baba, nawapa ninyi. Kazi nilizozifanya, nanyi mtafanya , na kubwa kuliko hizo mtazifanya.” Yesu angekuwa mmiliki wa siri ya mbinguni, siri ambayo wengine hawakuielewa, maneno kama haya, yangekuwa ni maneno ya

78

Page 79: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

uenda wazimu. Lakini kwa sababu Yesu alielewa siri ya ahadi ya Baba na kusudi lake, alikuwa na uwezo wa kusema maneno haya ya ajabu.

John G. Lake alikuwa mhubiri wa ki-Amerika, aliyetumiwa sana na Mungu katika Afrika ya Kusini, pia nchini Amerika mwanzoni mwa miaka ya 1900.

Watu wa kizazi chake walisema nini kuhusu John Graham Lake?‘Hatimaye, mafundisho ya Dr Lake, yatakubaliwa na ulimwengu wote.’ Na Mahatma Ghandi, kiongozi wa kitaifa wa Hindu.

‘Ujumbe wake umeifagia Afrika. Amefanya zaidi kwa ajili ya amani ya baadaye kwa Afrika ya Kusini kuliko mtu mwingine yeyote.’ Na Cecil John Rhodes, Mjenzi wa Dora.

‘Huduma ya uponyaji ya Dr John Lake, ni moja yenye sifa kubwa ambayo dunia imepata kuona.’ Na Dr William T.Gentry, Mwandishi wa kitabu, “Materia Medica” (vifaa vya utabibu), chenye matoleo 27, kinapatikana karibu maktaba zote za utabibu.

‘Ni mtu ambaye anamfunua Mungu kuliko mtu yeyote katika Afrika.’ Na Rev. Andrew Murray.

SABATO

Hakuna kabisa kazi yoyote inayoruhusiwa siku ya Sabato. Amri hii imerudiwa zaidi ya mara arobaini katika Agano la kale. Kwa nini? Sabato ina maana gani?

Maelezo ya uumbaji wa Mungu yanakomea siku ya sita, katika kumfanya mtu kwa sura yake na mfano wake. Hii ndio siku ambayo historia imekuwa ikiingoja. Kwa mara ya kwanza, Mungu asiyeoneka anaonyesha sura yake na mfano wake katika mwili wa nyama. Adamu anasimama akiwa mrefu, anaakisi mfano wa Muumba wake kama katika kioo. Kwa hiyo

79

Page 80: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Mungu anaitakasa siku ya saba kuwa Sabato takatifu, siku ambayo ilikuwa kivuli cha unabii wa pumziko lake la milele. Mungu hachoki, na kwa hiyo hahitaji kupumzika ili kukusanya nguvu zake tena; msanii anapofanya hatua ya mwisho ili kukamilisha kazi yake bora, picha yote ambayo fikira zake ziliiona kabla, sasa inamridhisha kwa furaha! Katika Sefania 3:17, hili ni onyesho la kupendeza: “Atakushangilia kwa furaha kuu, atatulia katika upendo wake. Atakufurahia kwa kuimba na shangwe.”

Sabato ni sherehe ya milele ya Mungu ya ukamilifu wa kazi yake. Analoliona Mungu ndani ya Sabato huimarisha pumziko lake. “Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana.” (Mw.1:31). “Mpeni ukuu Mungu wetu! Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu; Je, yeye siye Baba yako aliyekuumba, aliyekufanya, na kukuweka imara? ….Humkumbuki Mwamba aliyekuzaa, na Mungu aliyekuzaa umemsahau.” (Kumb.32:3,4,6,18). “Na nyumba ilipokuwa ikijengwa, ikajengwa kwa mawe yaliyokwisha kuchongwa chimboni; wala nyundo, wala shoka, wala chombo cha chuma chochote, sauti yake haikusikiwa ilipokuwa ikijengwa nyumba.” (1Wafal.6:7). “Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili hutoka juu. Alituzaa sisi kwa neno la kweli.” (Yak.1:17,18). Hakuna ambacho mtu anaweza kukifanya ili kuongeza ukamilifu wa kazi ya Mungu iliyokwisha kukamilika. “Mpenzi wangu u mzuri pia pia, wala ndani yako hamna ila.” (Wimbo 4:7). “Tangu nyayo za miguu yake hata utosi wa kichwa chake, hapakuwa na ila kwake.” (2Sam.14:25).

Katika kuitakasa siku hii maalumu ya kupumzika, Mungu anapanua fursa kwa mtu ili kuingia katika raha yake, kwa kuona vile aonavyo. Anapenda mwanadamu atambue na kuikumbatia maana kamili ya ukamilifu wa kazi yake. Hakuna mchango wa mtu unaoweza kuongeza thamani yoyote au wema kwa yale ambayo Mungu aliyafanya; hakuna ambacho labda mtu anaweza kukifanya ili kujibadilisha, kubadili njia zake, kuongeza, au kuhimiza upendo na thamani ambao tayari Mungu anao kwa viumbe wake! Imani ni uwezo wa kuona kama

80

Page 81: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

vile Mungu aonavyo. Imani yetu ni thamani tunayoiweka juu ya imani ya Mungu iliyo ndani yetu. Raha ya Mungu haipo katika hatari. Raha yake inafunua uadilifu wa ushawishi wake kuhusu sisi. Jinsi tulivyo tayari kuwa kuliko vyovyote vile ambavyo tungependa tuwe!

Ni nini, basi, ikiwa baadhi yao hawakuamini? Je, kutokuamini kwao kutaubadili uaminifu wa Mungu? Hasha! Mungu aonekane kuwa amini na kila mtu mwongo!” (Rum.3:3,4). Ujuzi wa mtu haumthibitishi Mungu kuwa ni wa haki au hapana. “Hatuwezi kufanya chochote dhidi ya kweli” (2Kor.13:5,8). “Ikiwa hatuamini, anabaki kuwa mwaminifu, kwa kuwa hawezi kujikana mwenyewe” (2Tim.2:13). “Mungu alipotaka kuwaonyesha zaidi wale wairithio ile ahadi, jinsi mashauri yake yasivyoweza kubadilika, alitia kiapo katikati; kwa sababu alikuwa hana mkubwa kuliko yeye mwenyewe wa kumwapia, aliapa kwa nafsi yake.” (kama vile hakuweza kuaminika!) Kwa maneno ya kibinadamu, ilikuwa haiwezekani kwa Mungu kusema uongo. Kwa kweli wanadamu huapa kwa aliye mkuu kuliko wao, na katika maagano yote, kiapo ndicho cha mwisho kwa uthibitisho, na kufuta kila namna ya mashindano. (Ebr.6:11-18). Msalaba ni mafanikio! Mungu ameshawishika sana kuhusu sisi, wala hahitaji uthibitisho wowote wa zaidi; sasa anajihusisha na kutushawishi kuhusu maisha yetu sisi wenyewe.

Taratibu za desturi za dini kama vile siku kuu maalumu na sherehe, sheria na maagizo kuhusiana na kufunga, vyakula maalumu, mabatizo, kanuni na maadhimisho mbalimbali, vilibeba thamani za kinabii mpaka wakati wa yule ambaye zililenga kwake, ulipotimia. Wakati wengi bado wamegawanyika kwamba, Sabato inatakiwa kuadhimishwa siku ya kwanza au siku ya saba, lakini Sabato tayari imekuja kikamilifu ndani ya mtu. Yesu ni nani, na yale aliyoyafanya; yanaonyeshwa yote ambayo Mungu anayaona katika Sabato!

Wakati wa Mungu ni dhana ya milele; tangu zamani maandiko yanaelekeza kwa Mwana-kondoo wa Mungu ambaye alichinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia. Uf.13:8. (Kiyunani: kataballo,

81

Page 82: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

kutupwa chini, hili linaelekezwa kwenye anguko la mwanadamu) Yesu ndiye utimilifu wa wakati. Mungu alitupata sisi ndani ya Kristo kabla ya kutupoteza katika Adamu. “Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo” (Kol.2:8). (Mapokeo hushika vipande tu vya ukweli kama waonyeshaji waelekeao kwenye ukweli mkubwa). “Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili.” (Ni ndani yake ambamo Mungu hutupa udhihirisho wake kamili katika mwili wa kibinadamu. Ni tafsiri ya Phillips). Kwa sababu ya umoja wako na yeye, wewe unadhihirisha utimilifu wake ule ule. Yeye ni kichwa cha chemchemi ambamo usultani wote na mamlaka yoe yanakaa.

Katika mwunganiko na kifo chake, wewe ulitahiriwa kiroho, wakati kwa njia ya ubatizo, ulitupa mbali uonevu na utawala wa dhambi juu ya mwili wake. Katika nia ya Mungu, pia ulifufuliwa kwa nguvu zile zile ambazo Mungu alimfufua Yesu katika wafu. (Kiyunani: imani ya Mungu). Kuunganishwa kwako katika kifo chake, kuzikwa na ufufuo vinaonekana kwa nguvu katika ubatizo wa maji, ambao katika mtiririko wa habari hii, unakuwa badala ya desturi ya tohara. “Kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu, aliwafanya hai pamoja naye, akiisha kutusamehe makosa yote; Akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani. Kol.2:13-15. (Kila teso alilolipata Yesu, mara moja kizazi cha wanadamu wote kilijumlishwa). Kristo alifuta kabisa vielelezo vya hukumu ya kuvunja sheria na amri, ambazo daima zilivitundika vichwa vyetu (Tafsiri ya Phillips). Alizishusha nguvu za giza hata kufikia sifuri, alipofuta madai yake dhidi ya mwili wa mwanadamu! Alipofuta vielelezo vilivyo dhidi yetu, alinyang’anya silaha za usultani na mamlaka. Hatia yetu ilitoa nguvu ya hukumu. Tafsiri ya Knox inasema, “Aliwanyang’anya mateka yao! Ndipo alizionyesha hadharani na kuziweka wazi katika ushindi wa ufufuo wake.

82

Page 83: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Kufuatana na haya yote, basi mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya siku kuu au mwandamo wa mwezi, au Sabato; (Katika mambo ya sherehe za kidini za kila mwaka, kila mwezi, au kila juma. Tafsiri ya TCNT). Mambo hayo yalikuwa ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo. (Mambo haya yote zaidi yana thamani ya mifano tu. Tafsiri ya J.B Phillips). Mtu asikudharau, kwa kunyenyekea kwa mapenzi yake mwenyewe tu, hata kudai kukutana na malaika ambao wanamtokea, lakini hakuona kitu chochote, isipokuwa anajivuna tu kwa fikira zake. (Hakuna malaika kutoka kwa Mungu atakayepingana na Kristo). Mafundisho hayatoki kwa Kichwa, ambaye kwa yeye mwili wote unalishwa na kuungamanishwa pamoja kwa viungo na mishipa, na kukua na kuwa kimo kamili kitokacho kwa Mungu. Basi ikiwa mlikufa pamoja na Kristo mkayaacha yale mafundisho ya awali ya ulimwengu, kwa nini kujitia chini ya amri, kama wenye kuishi duniani. “Msishike, msionje, msiguse!” Mambo hayo yote huharibika wakati wa kutumiwa, hali mkifuata maagizo na mafundisho ya wanadamu? Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kunyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali; lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili.” (Kol.2:8-23).

Katika habari hii, ni wazi kuwa Sabato imetimia katika Kristo, hatusherehekei tena siku, bali uzima! Neno la kinabii ni kama kondo la nyuma litunzalo mtoto kabla hajazaliwa. Baada ya kuzaliwa mtoto, linakuwa halina maana.

Mungu anatualika kuingia katika raha yake juu ya msingi ule ule ambao anaifurahia raha yake. Anatutia moyo ili tuone kama vile aonavyo yeye, kutembea katika nuru kama yeye alivyo katika nuru. Tunatakiwa kujiona kama anavyotuona yeye kwa namna ya pekee. Wanadamu hawawezi kujiumba wala kujikomboa wenyewe. “Yote haya yanatoka kwa Mungu,” (1Kor.1:30). Yeye ni Alfa na Omega. (Uf.1:8). Mafanikio binafsi kwa njia ya kujitoa kwa dini na nidhamu, haviwezi kuleta upendo na wema wa Mungu. Ni bure kutafuta kupata kitu

83

Page 84: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

ambacho tayari unacho! Uhalisi wa maono ya Injili ni hakika kwamba Mungu anapendezwa na mwanadamu. Hili si jambo la majadiliano. Hakuna kitakachomtenga mwanadamu na upendo wa Mungu!

Malaika walitangaza wema wa Mungu wakati wa kuzaliwa kwa Kristo, na kutoa sauti ya neno la unabii kabla hakujawa dalili zozote za imani au maisha yaliyobadilika.

‘Ili katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu sisi katika Kristo Yesu. Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu! Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza tuenende nayo.” (Ef.2:7-10). “Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake; usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu? (Neno toba katika Kiyunani, metanoia, maana yake ni kufikia akili nzuri, kubadilishwa namna ya kufikiri). Rum.2:4. “Lakini kwa mtu afanyaye kazi, ujira wake hauhesabiwi kuwa ni neema, bali kuwa ni deni.” (Rum.4:4). “Sisi ni matunda ya taabu ya nafsi yake” (Isa.53:11).

Kila juhudi ya mtu ya kujikomboa au kujihesabia haki mwenyewe, ni kushindana na Mungu moja kwa moja. Kwa kweli ni kama kuukufuru msalaba, kana kwamba ulishindwa kuuleta wokovu kwa ufanisi. “Kwa kurudi na kustarehe mtaokolewa; nguvu zenu zitakuwa katika kutulia na kutumaini, lakini hamkukubali.” Isa.30:15). Sabato maana yake ni kuona na kusherehekea pamoja na Mungu. Ni sherehe ya milele ya shukurani, sherehe ya ukamilifu.

MATENDO MEMA

Matendo mema yanakubalika mahali gani katika picha hii? Tumekwisha kuona katika sura iliyotangulia kwamba matendo yetu mema hayawezi kutuokoa; wala hayawezi kumshawishi

84

Page 85: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Mungu kwa namna yoyote ili atupende na kutupokea zaidi kuliko ambavyo tayari alikwisha kufanya. Mungu hawapendi watu kwa upendeleo, anataka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli. (1Tim.2:4). “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Yesu; Hakuja ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.” (Yoh.3:16,17). “Kwa maana upendo wa Mungu watubidisha; maana tumehukumu hivi, ya kwamba mmoja alikufa kwa ajili ya wote, basi walikufa wote. Yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake.” (2Kor.5:14,19). “Je, mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye? Hiki ni kifungo cha nguvu kilichopo katika uhusiano wa mwanadamu. Hata hili litawezekana, lakini mimi sitakusahau wewe. Tazama nimekuchora katika vitanga vya mikono yangu!” (Isa.49:15,16). Upendo wa Mungu kwa mtu mwenye dhambi, unaonyesha thamani ambayo Mungu anaiweka juu ya kila mtu. Mwenendo mzuri wa mtu hauchangii wema wowote kuushawishi moyo wa Mungu.

Walakini, matendo mema ni ya moyo, na ni matokeo yenye nguvu ya ukombozi: “Lakini tunda la Roho ni utu wema.” (Gal.5:22). “Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, watendeeni mema wanaowachukia ninyi, waombeeni wale wanaowadharau ninyi na kuwaudhi; ili mweze kuonyesha tabia ya Baba yenu, anayewaangazia jua lake waovu na wema, na kuwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.” (Math.5:44,45). “Kwa kuwa tunda la nuru ni katika wema wote na haki na kweli.” (Ef.5:9). “Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.” (Ef.2:10). “Nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.” (Math.5:16). Matendo mema yanafunua utukufu na shauri la Baba. Matendo yetu mema yanawaonyesha watu jinsi Mungu anavyowaona. “Baba wa yatima na mwamuzi wa wajane. Mungu huwakalisha wapweke nyumbani; huwatoa wafungwa wakae hali ya kufanikiwa.” (Zab.68:5,6). Huu ndio uhai wa dini ya kweli;

85

Page 86: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

kuwatazama wajane na yatima katika dhiki zao.” (Yak.1:27). Mungu huvutwa na wapweke.

“Tufanyeje ili tupate kuzitenda kazi za Mungu? Yesu akajibu, akawaambia, Hii ndiyo kazi ya Mungu, mmwamini yeye aliyetumwa na yeye.” (Yoh.6:28). Hii ina maana kwamba, kuona ndani ya Kristo kama vile Mungu aonavyo ndani yake. Yeye si mfano kwa ajili yetu, bali ni mfano wetu! “Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba. Nanyi mkiomba lolote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lolote kwa jina langu , nitalifanya.” (Yoh.14:12-14). “Kwani kutoa fedha kwa ajili ya kitu ambacho si chakula? Na mapato yenu kwa kitu kisichoshibisha?” (Isa.55:2). “Ikiwa ndugu mwanamume au ndugu mwanamke yu uchi na kupungukiwa na riziki, na mtu wa kwenu akamwambia, Enendeni zenu kwa amani, mkaote moto na kushiba, lakini asiwape mahitaji ya mwili, yafaa nini? Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake. Nionyeshe imani yako pasipo matendo, nami nitakuonyesha imani yangu kwa njia ya matendo yangu.” (Yak.2:14-18).

Yesu akatoka, akaona mkutano mkuu, akawahurumia, akawaponya wagonjwa wao. Hata kulipokuwa jioni, wanafunzi wake wakamwendea, wakamletea, si viti vyao vilivyovunjika na meza kwa seremala ili avikarabati, bali viwete, wenye kupooza, vipofu, mabubu, na wengine wengi, wakawaweka chini ya miguu yake, naye akawaponya. Ndipo Yesu aliwaita wanafunzi wake na kuwaambia, Nawahurumia makutano kwa sababu wamekuwa nami kwa muda wa siku tatu sasa, na hawana chakula; Nami sipendi kuwaruhusu waende zao na njaa, wasije wakazimia njiani. Lakini wanafunzi wakasema, “Tutapata wapi chakula cha kutosha kuwalisha kundi kubwa hili hapa nyikani? Jibu la kukubalika ambalo mmoja alihoji, hata hivyo Yesu alitaka kuwafunulia kwamba kuna hali ya utoaji wa ki-Mungu ulio karibu nasi zaidi, kuliko soko bora lililo karibu zaidi. Alisema, “Wapeni mlicho nacho” Mungu ametuita katika

86

Page 87: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

ushirika wa mbinguni mahali ambapo hubadili mchango wetu kuwa katika hali mpya kabisa, kwa wingi, kuliko yote tuwezayo kumwomba, au hata kuwaza! (Math.14:14-21; 15:30-38; Ef.3:20).

“Naye Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina. Na alipowaona makutano, aliwahurumia, kwa sababu walikuwa wamechoka na kutawanyika kama kondoo wasio na mchungaji.” Kwenye hatari ya mbwa mwitu. (Katika Zaburi 105:37 tunaiona picha tofauti kama hiyo: Israeli walipookolewa kutoka Misri, hapakuwa na mtu mwenye haki miongoni mwao; sasa, baada ya miaka mingi, wakawa wabaya zaidi katika Kanaani, na mfumo wa dini uliokuwa umeimarishwa kuliko walivyokuwa jangwani!). “Ndipo aliwaambia wanafunzi wake, ‘Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache; basi mwombeni Bwana wa mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake. Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu, wawatoe, na kupoza magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.” (Math.9:35-10:1). “Basi, baada ya hayo Bwana aliweka na wengine, sabini, akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenda kila mji na kila mahali alipokusudia kwenda mwenyewe.” (Luka 10:1).

Kabla ya kupaa kwake, Yesu aliwaambia wanafunzi wake, mia moja na ishirini wakati ule, kungojea Yerusalemu ahadi ya Baba, mpaka wavikwe uwezo utokao juu. (Luka 24:49). “Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.” (Mdo 1:8).

Kuyahukumu matendo mema: Biblia inasema juu ya hukumu ya aina tatu: Ya kwanza ni hukumu ya dhambi, ambayo Yesu aliichukua juu yake mwenyewe kwa niaba ya wanadamu. ‘Alipata mateso ambayo yalituletea amani’ (Isa.53:5) Yesu alipolia, “Imekwisha!”

87

Page 88: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

alisema juu ya hukumu ya Mungu; wanadamu wamekwisha kuachiliwa! Hukumu ya pili, ni hukumu ya wale ambao waligeuka kabisa na kuikataa habari njema. Ni wazi kuwa hii inawahusisha wale ambao walikuwa na nafasi nzuri ya kuisikia Injili ya kweli, lakini walimkataa. Aina ya hukumu ya tatu ni hii inayotuhusu sisi katika sura hii. Paulo anaisema katika 1Kor.3:8-16, “Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu; basi yeye apandaye, na yeye atiaye maji ni wamoja, lakini kila mtu atapata thawabu yake mwenyewe sawa-sawa na taabu yake mwenyewe.” Ukweli wa kwamba sisi sote tu wamoja, hauna maana kuwa sote tutapokea thawabu zilizo sawa, maana kila kazi ya mtu itadhihirishwa; kwa kuwa hiyo siku itaifunua, kwa kuwa itafunuliwa kwa moto, na ule moto wenyewe utaijaribu kazi ya kila mtu, ni ya namna gani. Yesu ndiye msingi; basi, kazi ya mtu aliyoijenga juu ya msingi ikikaa, atapata thawabu. Kazi ya mtu ikiteketea, atapata hasara; ila yeye mwenyewe ataokolewa; lakini ni kama kwa moto. “Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya.” (2Kor.5:10).

Kumbuka, mwili wako ni mkakati wa Mungu! “Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi tupokee taji isiyoharibika. Mungu tayari ndiye thawabu yetu izidiyo sana! Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye; napigana ngumi vivyo hivyo, si kama apigaye hewa; bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.” (1Kor.9:1-27). Mara kwa mara kuna muda mwingi sana, juhudi na fedha zimepotea katika kuanzisha huduma, ambazo matokeo yake hakuna zaidi ya ‘kupiga hewa.’ Daima fikiria andiko hili sawasawa na sheria kamilifu ya uhuru. Mtindo huu wa maisha ya ukombozi ambayo yanadhihirisha nguvu ya Mungu katika mwili wa kibinadamu, ambayo itakupeleka zaidi ya mipaka ya waajibu wa dini tu na nidhamu. Kwa nini utumie nguvu zako na kazi ngumu kwa thawabu ambayo inakuachia fadhaa na utupu! (Isa.55:2). Kazi

88

Page 89: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

zetu zote zitahukumiwa: miti, nyasi, majani, au fedha, dhahabu na mawe ya thamani! (1Kor.3:12). “Vema, mtumwa mwema na uaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako” (Math.25:21). “Ni nani, basi, aliye wakili mwaminifu, mwenye busara, ambaye bwana wake atamweka juu ya utumishi wake wote, awape watu posho kwa wakati wake? Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta anafanya hivyo. Kweli nawaambia, atamweka juu ya vitu vyake vyote.” (Luka 12:42-44). Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu. (Gal.6:10).

Mungu awafanye ninyi kuwa wakamilifu katika kila tendo jema, mpate kuyafanya mapenzi yake; naye akifanya ndani yetu lile lipendezalo mbele zake. (Ebr.13:16,21). “Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema” (Filipi 2:13). “Nimefanywa mhudumu wake, sawasawa na uwakili wa Mungu, niliopewa kwa faida yenu, nilitimize neno la Mungu; siri ile iliyofichwa tangu zamani zote na tangu vizazi vyote, bali sasa imefunuliwa kwa watakatifu wake; ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika Mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu! Ambaye sisi tunahubiri habari zake, tukimwonya kila mtu, na kumfundisha kila mtu katika hekima yote, tupate kumleta kila mtu mtimilifu katika Kristo. Nami najitaabisha kwa neno lilo hilo, nikijitahidi kwa kadiri ya kutenda kwake atendaye kazi ndani yangu kwa nguvu.” (Kol.1:25-29).

Paulo anakutana na umhimu wa wito wake wa kuhubiri Injili, zaidi sana kuliko uchaguzi wa kutaka tu, uliovutwa kutokana na faida zilizo na mvuto; “Maana nimewekewa sharti; tena ole wangu nisipoihubiri Injili! Basi, thawabu yangu ni nini? Ni hii, ya kuwa nihubiripo, nitaitoa Injili bila gharama, bila kutumia kwa utimilifu uwezo wangu nilio nao katika Injili.” Anatoa maneno haya ya kiutendaji ili kusisitiza ukweli kwamba sheria ya uhuru na hiari ya moyo, inaachilia msukumo mkubwa zaidi kuliko sheria yoyote iliyojengwa juu ya hofu au thawabu au wajibu wa

89

Page 90: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

maadili ambavyo ingeweza kufanya. Chini ya sheria hii, kutembea maili ya pili huwa jambo la kawaida kufanya! Mafundisho ya kweli huleta hiari ya moyo. Ikiwa yale unayosikia yanakuingiza katika matakwa yako tu na kukuacha ukiwa na hatia na fadhaa, basi unaisikia Injili potofu!

Sheria hii ya upendo imedhihirishwa kwa nguvu katika eneo la fedha: Paulo anajisifia juu ya makania ya Makedonia jinsi ambavyo, “Kwa dhiki nyingi, wingi wa furaha yao na umaskini wao uliokuwa mwingi, uliwaongezea utajiri wa ukarimu wao. Maana nawashuhudia kwamba, kwa uwezo wao, na zaidi ya uwezo wao, kwa hiari yao wenyewe walitoa vitu vyao; wakituomba sana pamoja na kutusihi kwa habari ya neema hii, na shirika hili la kuwahudumia watakatifu. (Katika makanisa ya leo, mara nyingi wachungaji wanawaomba washirika kutoa!) Lakini kama mlivyo na wingi wa mambo yote; imani, na usemi, na elimu, na bidii yote, na upendo wenu kwetu sisi; basi vivyo hivyo mpate wingi wa neema hii pia.” (2Kor.8:1-7). Katika Wafilipi 4:17, anaona kustahili zaidi katika matunda ambayo kutoa kunaachilia faida ya mwamini, kuliko kipawa peke yake.

Hatimaye anasisitiza, “Nimevipiga vita vilivyo vizuri , mwendo nimeumaliza, imani nimeilinda; baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.” (2Tim.4:7,8). Ufunuo wa wema wa Mungu ndio nuru ambayo Paulo alitembea ndani yake. Kiini cha ujumbe wake ulikuwa neema ya Mungu iliyomletea mwanadamu haki. Neema katika akili ya Paulo ni ufunuo wa jumla ya hesabu ya mambo yote aliyoyafanya Mungu kwa niaba ya wanadamu ndani Kristo Yesu. Ni zaidi sana kuliko rasimu ya msaada wa kutetea dhambi. Neema ya Mungu ni uwezo wake wa kuishi maisha yake ndani yetu na kupitia kwetu.

Neema inatupa maana mpya kwa maisha yetu. Maisha yetu hayamo tena katika fikira za kujihisi unyonge. Waamini wengi wazuri, wanaishi maisha yasiyo ya ufanisi na yasiyo na matunda, wamekuwa vipofu wa kutokuona mbali katika utajiri

90

Page 91: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

ambao umo ndani yao. Kuona kunamwandaa na kumtia nguvu mwamini. (2Pet.1:8,9). Ujinga na mafundisho mabaya vinawadhoofisha watu na kuongeza udanganyifu. Fundisho lolote ambalo linasisitiza wajibu na mchango wa mtu kutenda mambo ili kupata kibali kwa Mungu, linamweka mtu katika utumwa. Fundisho la jinsi hii linaisaidia dhamiri ya dhambi na kumweka mtu kuwa mfungwa wa kujihisi unyonge na hatia. Kustahili wema wa Mungu, upendo, kibali na uwepo, havitegemei kiwango cha upeo wa mtu au hata katika juhudi ya mtu kujipa haki au kustahili; bali ni katika kutambua thamani ambayo Mungu aliiweka juu yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.

Mungu hawezi kujipa talaka kutoka sura yake na mfano wake ndani ya mtu. Wewe huna kitu mbadala; wewe ni wazo lake la asili; unatenda kazi kwa nia ya Mungu milele yote! Tunashughulika na upendo wa milele usiokwisha kamwe!

SIRI IMEFUNULIWA

JE, HEKIMA INAPATIKANA WAPI? Mungu hakumficha chochote mwanadamu, bali alificha kwa ajili ya mwanadamu. Utajiri wa madini uliwekwa katika ardhi kwa faida yetu na kwamba tugundue. Mtu anamiliki mali ya kushangaza na kuitafuta bila kizuizi chochote wala upeo wa macho; yeye yuko katika uhalisi wa thamani ya dhamiri, akivutwa na uzuri na kufuata uchunguzi.

Kitabu cha zamani sana katika Biblia, Ayubu, anaandika moja ya andiko linalokata-kata vipande, katika sura ya 28, “Hakika kuna shimo wachimbako fedha, na mahali wapatapo dhahabu waisafishayo. Binadamu hukomesha giza; huyatafuta-tafuta hata mpaka ulio mbali, mawe ya giza kuu, giza tupu. Hufukua shimo (wakienda chini sana kuliko ambavyo upeo wa kawaida ungewaruhusu kwenda) mbali na makao ya watu; husahauliwa na nyayo zipitazo; huning’inia mbali na watu, huyumba-yumba huko na huko. (Kiwango cha mzunguko wa maisha ya kijamii, kujisifu, masengenyo, kutetana, michezo inayochezwa na watu,

91

Page 92: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

vimepoteza mvuto wake na msaada. Haja yao kutafuta thamani katika mazingira mbalimbali, imewapeleka mbali zaidi ya mchezo wa kuruka, na kutafiti matukio kwa juu juu; zaidi ya, ’nilikuwa pale, nimefanya, nimepata T-shirt’ aina ya dhana ya kitalii).

Katika ardhi, (upeo unaoonekana, au udongo wa juu) ndimo kitokamo chakula; (Hii ndio sababu ya utafiti wa mwanadamu; kwa sababu mtu yuko katika hali halisi ya roho, kuulisha na kuuchochea mwili na hisia, haviwezi kamwe kuutosheleza na kumtimizia matakwa kwa ukamilifu au kwa muda. “Mtu hataishi kwa mkate tu….” Sasa ni kwamba amekula ujazo wake kutoka katika mavuno ya ardhi, tamaa yake inaendelea kumwendesha kutafuta zaidi ya riziki ya kila siku, hata kwa hatari ya kupoteza maisha yake).

Na chini yake hupinduliwa kama kwa moto. Mawe yake ni mahali zipatikanapo yakuti, nayo ina mchanga wa dhahabu, (kama kuna mchanga, ni lazima uwe zaidi!) Njaa hii ndani ya mtu, humtofautisha na ulimwengu wa wanyama; Njia ile hapana ndege mkali aijuaye, wala jicho la tai halijaiona. Wanyama wakali wajivunao hawajaikanyaga, wala simba mkali hajaiona. Huunyoshea mwamba wa gumegume mkono wake; huipindua milima hata misingi yake. Hukata mifereji kati ya majabali, na jicho lake huona kila kitu cha thamani. (Baba yangu alikuwa na rafiki yake wa Kiitalia, alifanya kazi katika machimbo ya Tsumeb, kule Namibia kwa miaka 21. Mara nyingi alituambia juu ya uzuri wa rangi usioelezeka unaoonyesha zaidi ya maandishi, kutoka chumba kimoja kwenda kingine cha vito vya thamani vya aina mbalimbali! Mgando wa maji, rangi nyekundu, kijani, Yakuti samawi, kahawia, nyavu za amethesto, nyavu za nyuzi safi rangi ya shaba, kama zile za buibui!)

Mtu amepata njia kuvifunga vijito vilivyo chini ya ardhi kiasi kwamba havitiririki, (hakuna kizuizi cha kawaida kiwezacho ku kuzuia utafutaji wake). Kitu chochote kilichojificha, anakitoa katika mwanga.

92

Page 93: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Bali hekima itapatikana wapi? Na mahali pa ufahamu ni wapi? Mwanadamu hajui thamani yake. Vilindi vyasema, Haimo ndani yangu, na bahari yasema, Haiko kwangu. (Jaribio la mtu kubadili juhudi zake na kitu kisichodumu, linamwacha na akiwa na mwitikio mtupu wa kushindwa). Haipatikani kwa dhahabu, wala fedha haitapimwa iwe thamani yake. Haiwezi kutiwa thamani kwa dhahabu ya ofiri, wala kwa Shohamu ya thamani nyingi, wala kwa yakuti ya samawi. Dhahabu na vioo haviwezi kulinganishwa nayo; wala kubadili kwake hakutakuwa kwa vyombo vya dhahabu safi. Naam, kima cha hekima chapita marijani. Utafutaji wa mwisho wa mtu ni kugundua Muumba wake kama thawabu yake kubwa izidiyo. Kumcha Bwana (Utisho wa Mungu) ndio chanzo cha hekima. Hitaji la mtu ni kugundua thamani ambayo itafanana na hali ya utajiri, thamani ambayo itaonyesha kwa wazi kabisa undani wa asili yake ya milele na matengenezo.

MWAMBA –CHAPA YA UUMBAJI WETURejea ya Mwamba katika maandiko huchochea mwendo mgumu katika Kompyuta; inashikilia maelezo ya kina ya chapa ya asili yetu na uumbaji wetu. Ukuu wa utisho wa Mungu umefunuliwa katika kazi yake na ushirika wa milele wa mwanadamu katika Kristo. (Ef.1:4; 2:10). Paulo anaongea kuhusu “Kupata utajiri wote wa ufahamu kwa hakika, kupata kujua kabisa siri ya Mungu, yaani, Kristo; ambaye ndani yake yeye hazina zote za hekima na maarifa zimesitirika.” (Kol.1:15-17,26,27; 2:2,3).

“Kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.” (Ebr.11:6). “Nisikilizeni, ninyi mnaoifuata haki; ninyi mnaomtafuta Bwana; uangalieni Mwamba ule ambao mlitolewa kwa kuchongwa, na tundu la shimo ambalo mlitolewa kwa kuchimbuliwa.” (Isa.51:1).

Mungu hajapotea, wala hajajificha ili atafutwe; kwa kawaida, watu ndio wanaopoteza macho ya ki-Mungu ndani yao.

93

Page 94: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Kumtafuta Mungu nje ya mtu, ni kutafuta ubatili! Sura yake na mfano wake vimehifadhiwa katika kazi yake ndani ya mtu.

“Mpeni ukuu Mungu wetu; Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu; Humkumbuki Mwamba aliyekuzaa, Mungu aliyekuzaa umemsahau.” (Kumb.32:3,4,18). “Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka. Kwa kupenda kwake mwenyewe alituzaa sisi kwa neno la kweli; mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo.” (Yak.1:17,18,23-25).

Kioo ni kitendawili kilicho na siri ya uso wa Mungu ndani ya uso wa mtu! “Nilipokuwa mtoto mchanga, nilitambua sura yangu iliyoonekana katika uso wa mama yangu, sawasawa na kuangalia katika siri ya kioo, lakini sasa, baada ya kuitazama sheria kamilifu ya uhuru, ninaona uso kwa uso; sasa ninajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana.” (Mtoto mchanga anawakilisha kipindi cha unabii kabla Yesu hajafunuliwa katika mwili; wakati ambao mwanadamu alinaswa katika uchanga, na alitegemezwa kwa maziwa ya sehemu ya unabii na matamko. ‘Ebr.1:1,2’ Kuwa mtu mzima ni kutimizwa kwa unabii; kimo cha utimilifu wa Kristo, uliofunuliwa ndani ya maisha ya mtu wa kawaida!) ‘Yak.1:17,18,23-25; 1Kor.13:10-12.’ Daima Mungu ananijua kwa namna hii!

“Zamani zilizopita aliwaacha mataifa yote waende katika njia zao wenyewe. Lakini hakujiacha pasipo ushuhuda, kwa kuwa alitenda mema, akiwapeni mvua kutoka mbinguni, na nyakati za mavuno, akiwashibisha mioyo yenu chakula na furaha.” (Mdo 14:16,17). Mema yanamshuhudia Mungu!

THAMANI INAYOFANANA Yesu anasema katika Mathayo 5:44-48, kwamba, njia sahihi zaidi na kamilifu ambayo tunaweza kuwakilisha ufunuo wa Mungu ndani ya mtu (watoto wakamilifu wa Baba mkamilifu) tutatakiwa kuwapenda maadui zetu, kuwaombea wale wanaotuudhi. “Maana yeye huwaangazia jua lake waovu na

94

Page 95: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.” (Pasipo jua na mvua hakutakua na maisha duniani). “Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi, mwapata thawabu gani? Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, (wale ambao wanakubaliana nasi katika kila eneo la mafundisho ya imani) mnatenda tendo gani la ziada?

Paulo anamwandikia Tito na kumtia moyo, “Wasimtukane mtu yeyote, wasiwe wagomvi, wawe wema, wakionyesha upole wote kwa watu wote. Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi, tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi; tukiishi katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana. Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa; si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi, bali kwa rehema yake.” (Tito 3:2-5).

Si ajabu kwamba Yesu alikuwa na sifa nzuri ya kuwa rafiki wa wenye dhambi, hawakujihisi kushutumiwa, kuhukumiwa kwa kutokufaa au kutengwa katika ushirika wake. “Watoza ushuru na wenye dhambi wote walivutiwa naye kumsikia akihubiri.” (Luka 15:1). Viongozi wa kidini walipomlaumu kuhusu jambo hili, aliwaambia mifano mitatu ya kusisitiza ukweli huu: mwana mpotevu, shilingi iliyopotea na mwana mpotevu, kuwakilisha mtu mmoja. Hali yao ya kupotea haikufuta thamani yao au utambulisho wao wa asili.

Mungu ndiye Baba pekee wa kweli na asili ya mwanadamu; yeye ni Baba ambaye kwa jina lake ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa. (Ef.3:14,15) Shetani siyo baba wa kweli wa mwanadamu; yeye ni baba wa uongo. (Yoh.8:44). Neno la Kiyunani satanos maana yake, mshitaki. Mwili wa Yesu msalabani ulikuwa ni hati ya hatia ambayo iliwakilisha kizazi cha wanadamu wote, na katika kifo chake Mungu aliupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao. Kuachiliwa kwa wanadamu kulithibitishwa na nguvu za giza ziliondolewa.

95

Page 96: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Katika Warumi 2:4 Paulo anasema, “Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu?” Neno lililotafsiriwa la toba, katika Kiyunani ni metanoia, lenye maana ya mabadiliko ya kukubalika ya akili na utambuzi, lakini watu wengi wana utambuzi juu ya Mungu, ambao umepinduliwa kwa njia ulivyowasilishwa kwao.

Yesu hakuishi maisha au kuhubiri Injili ya kujichanganya; mvuto wa maisha yake kwa makusanyiko, ulikuwa ni ukweli kwamba, alimfanya Mungu asiyeonekana, kuonekana, na wakati uo huo alionyesha chapa ya asili ya kila mtu.

Wenye dhambi walisikia vya kutosha katika neno lake, na kuona vya kutosha katika maisha yake, ili kujihisi kikamilifu kutambuliwa na kujumlishwa ndani yake. Ndani yake waliona onyesho la tabia ya utambulisho wa uumbaji wao wa asili na mapambo; waliyatambua maisha ambayo walipaswa kuishi: yaliyotimizwa kikamilifu, maisha ya ukarimu na upendo na uadilifu wa maadili. Walishuhudia mguso wa msamaha usio na masharti, uliorejesha zaidi kuliko kufutiwa tu dhambi za muda uliopita, bali ulifungua thamani mpya ya maisha na udhihirisho wa uadilifu.

Yeye hakuwa mfano kwetu, bali alikuwa mfano wetu. Kahaba alihisi kusafishwa kwa upendo wake na kuachiliwa kwa uwezo mpya ndani yake; kuondoka akiwa huru bila kutenda dhambi tena. Mwizi alihisi kutokuiba tena, bali badala yake kutafuta kazi ya uaminifu na kutoa kwa wengine. (Ef.4:28). “Maana katika nyika maji yatabubujika, na vijito jangwani” (Isa.35:6).

SIRI IMO NDANI YA MBEGU Siri ya maelezo ya uzao wa maisha, utata na ya hiari, imefichwa ndani ya mbegu. Mbegu ni ukweli ambao huonekana katika kioo kwa mti uzaao matunda. Neno ‘siri’ ni musterion, katika Kiyunani, limetumika mara tatu tu katika Injili. Mathayo, Marko na Luka, wanatumia neno hili kila wakati ndani ya habari ya siri

96

Page 97: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

ya mbegu. Mavuno makubwa sana zaidi ya hesabu yoyote imefichwa katika mbegu moja.

Siri iliyokuwa imefichwa kwa miaka mingi na vizazi, ilifikia wakati wa kutoka katika udongo katika hali isiyoonekana ya kweli katika Roho, na kubadili udhihirisho wa maisha milele, na hatima ya mwanadamu. “Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake.” (Yoh.12:24). Hatima ya mbegu moja ya ngano, ilikuwa ni kufungua siri yake na kuwa mavuno ya maisha, ilijizidisha kulingana na aina yake, ndani ya mwanadamu; mkate wa uzima ambao uliwalisha wenye njaa katika mataifa. Hakumaanisha kamwe kuwa ni maelezo ya mafundisho ya kidini na desturi, lakini maisha ya udhihirisho wa juu kabisa wa wema na uadilifu wa Mungu yakifunuliwa ndani ya kila mtu. Kwa sababu hiyo, Paulo alijitaabisha na kujitahidi kwa kadiri ya kutenda kazi, kwake atendaye kazi ndani yake kwa nguvu! (Kol.1:27-29).

Daima tumedhani kwamba uzuri mkamilifu ni kitu kidogo, kama vile Absalomu ambaye hakuwa na mawaa, tangu nyayo za miguu yake, hata utosi wa kichwa chake, (2Sam.14:25). Lakini, bado Mungu alihifadhi ukamilifu wa uzuri, chapa ya uumbaji wetu wa asili, katika Kristo na kwa njia ya Injili, sasa anaifunua katika maisha yetu!

SHERIA YA KUJUMLISHWA“Ambayo wenye kuitawala dunia hii hawaijui hata mmoja; maana kama wangaliijua, wasingalimsulubisha Bwana wa utukufu!” (1Kor.2:7,8). “Mmoja alikufa kwa ajili ya wote, basi walikufa wote!” (2Kor.5:14) Hakuwa Adamu wa pili, bali uzao wa Adamu wa mwisho! (1Kor.15:22,45).

Ufufuo wake kwa kweli ulikuwa ni uzao wa namna mpya! (2Kor.5:17; 1Pet.1:3). “Ni nani aliyesikia neno kama hili? …. Je nchi yaweza kuzaliwa siku moja? Taifa laweza kuzaliwa mara?” (Isa.66:8; Hos.6:2).

97

Page 98: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Watawala wa giza hawakuelewa kuwa mtoto aliyekuwa amezaliwa kwa ajili yetu, kwa kweli alikua ni Baba wa milele! Mwenyezi, Mungu wa milele katika hali ya mwili wa udhaifu! (Isa.9:6). “Ndani yake ndimo ulimokuwamo uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. Nayo nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza.” (Yoh.1:4,5,9). “Ondoka, uangaze, kwa kuwa nuru yako imekuja, na utukufu wa Bwana umekuzukia. Maana, tazama, giza litaifunika dunia, na giza kuu litazifunika kabila za watu; bali Bwana atakuzukia wewe, na utukufu wake utaonekana juu yako. Na mataifa wataijilia nuru yako; na wafalme kuujia mwanga wa kuzuka kwako” (Isa.60:1-3). Mataifa watavutwa kwako bila kizuizi kwa sababu nuru ya kweli ndiyo imwangazayo kila mtu, nuru ambayo inayofunua kujumlishwa kwao.

Ujinga ulionyang’anya mamlaka ya giza na nguvu zao juu ya wanadamu, hivi sasa, ndio silaha pekee dhidi ya mtu. Kwa kadiri mtu anavyobaki kuwa mjinga juu ya ukweli wa ukombozi, ambao ni utambulisho wa kweli, na kujumlishwa katika Kristo, kutokuamini kwao kunazipa nguvu za giza kuendelea kupunga fimbo ya ufalme wa udanganyifu juu yake. Kristo, ambaye ni sura ya Mungu, pia ni onyesho la kioo la mtu; hii ni nuru ya Injili. Yeye ni onyesho halisi la utukufu (shauri) wa Mungu (2Kor.3:18; 4:4,6; 2Tim.1:9,10). Maarifa ya ya kweli hufungua kwa hakika ile nuru iondoavyo giza.

Katika kila aina ya giza, iwe ni kushindwa na madawa ya kulevya, tamaa au ulevi, kila aina ya misisimko, maumivu, uvunjifu au mkandamizo ya namna yoyote, umaskini, hofu na kujiona duni, pia kila ugonjwa na maradhi, hupoteza madai yake na utawala juu ya mwanadamu. Ukweli huleta ushawishi; imani huja kwa kusikia ukweli. Ni katika habari hii ambapo kufaa kwa habari njema kunakuwa ni nguvu ya ajabu. (Rum.1:16,17; 10:17).

“Paulo alihubiri kwa njia ambayo wengi waliamini! (Mdo 14:1,9,10). Paulo alisema kuwa ufunuo wa Mwana wa Mungu ndani yake, ulimtenga katika maana ya kuwa na mpaka wa

98

Page 99: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

maisha yake kwa njia ya uzao wake wa kimwili. Utume wake sasa ulikuwa ni kumtangaza Kristo kwa kila mtu! (Gal.15-17). Alishangazwa sana na ufunuo wa Mungu katika mwili, ukamilifu wa Uungu katika mwili wa kibinadamu, akikaa ndani yake, kiasi kwamba hakuona umuhimu wa kutetea ufunuo huu dhidi ya imani yoyote ya desturi maarufu.

KRISTO NDANI YA KILA MTU Katika Athene, alihutubia mkutano wa kufurahisha wa Wayunani, na wanafalsafa wa kigeni; alitamka ukweli ambao ulionekana kuutunza udhihirisho wa Uungu ulio mpana na wa ulimwengu wote, ulionyeshwa katika namna nyingi za ibada.

Kuhakikisha kwamba hakuna dini au mungu ambaye angejisikia kuchukizwa au kutengwa, pia walitengeneza madhabahu yenye maandishi, “Kwa mungu asiyejulikana.” Hii ililipua ujumbe wa Paulo kwao; “Basi mimi nawahubirini habari zake yeye ambaye ninyi mnamwabudu bila kumjua. Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono; wala hatumikiwi kwa mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji kitu chochote; kwa maana ndiye anayewapa wote uzima na pumzi na vitu vyote. (Mungu huyu si wa mvuto mwingine au uchaguzi mwingine unaofaa kwa mafundisho yetu ya imani sisi tulio wengi. Wala hashindani na maana au udhihirisho mwingine wowote wa kidini wa ‘kumulika katika giza!) Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao; ili wamtafute Mungu ingawa ni kwa kupapasa-papasa, wakamwone.”

Ndipo alisema maneno haya mazito: “Ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu; kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu, kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, maana sisi sote tu wazao wake! (Aratus, mkulima wa Kiyunani wa mtume, na mtangulizi wake katika nchi kama tatu; pia mawazo ya Cleanthes, mwanafalsafa asiyejali furaha wala huzuni).

99

Page 100: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Basi, kwa kuwa sisi tu wazao wa Mungu, haitupasi kudhani ya kuwa Uungu ni mfano wa dhahabu, au fedha au jiwe, vitu vilivyochongwa kwa ustadi na akili za wanadamu. Basi zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hazioni.” (Katika uhalisi wa kufanywa kwetu, sisi ni aina ya ki-Mungu! Tusitamani kamwe kutaka kumjua Mungu katika hali nyingine yoyote nje ya utu wetu).

Mungu hakuziangalia nyakati za ujinga, lakini sasa anawataka watu wote wa kila mahali kubadili nia zao kuhusu wao wenyewe. (Kiyunani, metanoia, ni badiliko kamili la akili kuwa na ufahamu mpya). “Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa mtu yule aliyemchagua (kuachiliwa kwa wanadamu), naye amewapa watu wote uthabiti wa mambo haya kwa kumfufua katika wafu.” (Mdo 17:22-31). Uhakika wa ufufuo wa Yesu Kristo katika wafu ni ushuhuda wa mwisho wa uthibitishi wa Mungu kwa wanadamu. (Rum.4:25; 1Kor.15:17). Mungu aliweza kumrejesha mwanadamu katika hali ya kutokuwa na lawama wala hatia mbele zake.

Kusudi la Injili ni kwa ajili ya mtu kujitambua kuwa ameunganishwa katika Kristo! Ufufuo wa Yesu katika wafu, unamhimiza kila mmoja kuwa na utambuzi mpya, ili kuona mavuno ambayo Mungu aliyatazamia wakati chembe ya ngano ilipoanguka katika nchi na kufa! (Yoh.12:24). Petro anasema, “Kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili, ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu.” (1Pet.1:3).

HAKI IPATIKANAYO KWA IMANI Ubora mpya wa maisha unaelezwa katika maandiko kama, “Haki kwa njia ya imani.” Neno haki, linamaanisha msingi halali wa uhusiano wa uadilifu kabisa, ambapo hapapatikani namna yoyote ya unyonge, hatia, shuku mbaya, mashitaka au hukumu. Ubunifu wa Mungu, kumrejesha mtu kwake bila kutegemea mchango wowote wa thamani kutoka kwa mtu, ndio kiini cha

100

Page 101: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Injili. (1Kor.1:30; 2Kor.5:18,21). Kutangazwa kwa ujumlisho wa wanadamu katika Kristo, ndio msingi wa imani. Ushirika huu unapatikana katika nia ya Mungu milele yote! (Ef.1:4; Rum.1:16,17). Siri ya kioo inaonyesha na kufunua ujumlisho kamili wa mtu ndani ya mafanikio ya Kristo. (2Kor.3:18). Kristo anabaki kuwa ushuhuda wa milele wa chapa ya uumbaji wetu wa asili.

Litakuwa jambo la huzuni sana kujifunza kwa juhudi kubwa na uchunguzi mwingi, uadilifu katika historia, na kielelezo cha maisha, ujumbe, miujiza, kifo na ufufuo wa Yesu Kristo, bila kugusia habari ya mbadiliko wa maisha mapya, au nguvu ya Injili. Ni katika ufunuo wa kuunganishwa kwetu tu, kulikothibitishwa kwa njia ya ushuhuda wa roho zetu kwamba tunashiriki asili yetu ndani yake, na kwamba Mwana wa Mungu amefunuliwa ndani ya mwanadamu. (Gal.1:15,16).

Roho Mtakatifu hushuhudia pamoja na roho zetu kwamba tumezaliwa kutoka juu. (Rum.8:16). Mwaka 1995, mtu mmoja alijipatia pointi katika dakika za majeruhi za mchezo, ulioifanya Afrika ya Kusini kuwa mshindi wa kombe la dunia la mchezo wa Rugby. Afrika ya Kusini yote ilijumlishwa katika ushindi huo, ikiwa tulitazama, au kucheza au kuudharau mchezo. Hali ya wengine kutokushiriki na kuufurahia wakati huo, hakukuufanya ushindi kuwa batili. Bila dhana ya ushirikiano, hakuna mchezo hata mmoja unaoleta maana!

Ikiwa haki ina kitu chochote cha kuhusishwa na mchango wa mtu, basi haiwi tena kwa imani, na wala hatutafurahia tena ule usawa wa kuingia ndani yake.

UZIMA HALISI Mtu ameumbwa na uwezo wa “kumtafuta Mungu na kumwona! Hayuko mbali na kila mmoja wetu.” Mungu hataki kuendelea kuwa siri kwa mtu, anapenda kujifunua katika njia halisi kwa kila mtu!

101

Page 102: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

“Lile lililokuwako tangu mwanzo (huu si ufunuo wa hivi sasa), tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya neno la uzima; na uzima huo ulidhihirika , nasi tumeona, tena twashuhudia. Nanyi pia mpate kushirikiana nasi; na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake, tumehakikisha juu ya kuunganishwa kwenu katika ushirika huu; Ninayaandika haya, ili furaha yenu itimizwe.” (1Yoh.1:1-4).

Ingawa ilikuwa karibu miaka sitini tangu Yohana alipomwona rafiki yake mkuu kwa mara ya mwisho, Yesu katika mwili, anaongea kwa usemi wa wakati uliopo. Inaonyesha kwamba aliandika kutoka kisiwa kilichojitenga, hata hivyo hapunguzi furaha yake ya ushirika hata kidogo. Ufunuo wa Mungu katika mwili, ni wa zaidi sana kuliko mafundisho ya imani ya dini nyingine tu; unaeleweka, ni uzima halisi! “Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu; Mungu alidhihirika katika mwili!” (1Tim.3:16). “Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua.” (Yoh.1:18). Mungu, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote, “Yeye ni mfano wa Mungu asiyeonekana. (Mfano wa asili na chapa ya uumbaji wetu).

Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake. Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye.” (Kol.1:15-17). Yohana mwanafunzi wa Yesu, aliutumia muda mwingi wa maisha yake ya baadaye (kama miaka 30) kuishi Asia ndogo, na hasa katika Efeso; msisitizo zaidi wa mafundisho ya Paulo, unaonekana katika maandiko ya Yohana. Aliandika Injili ya Yohana akiwa tayari na umri wa miaka karibu 96! Hii ilitokea ama katika Efeso au katika kisiwa cha Patmo, alikoishi miaka michache ya utumwa. (Linganisha Kol.1:15-17 na Yoh.1:1-3,16,17; 1Yoh.5:20). “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye neno alikuwa Mungu;. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika. Ndani yake ndimo

102

Page 103: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. Nayo nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza. (Kiyunani: katalambano, maana yake kutwaa, kufahamu) Kulikuwako Nuru halisi amtiaye nuru kila mtu, akija katika ulimwengu. Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua. Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea. Bali kila mmoja ambaye, kwa imani alimtambua kuwa ndiye asili yake ya kweli, (Kiyunani, lambano, kuelewa, kufahamu, kutambuliwa na) ndani yao aliwathibitishia uadilifu wa uwana wao, kujua kuwa ni wake, waliozaliwa kutoka juu, utu wao uko ndani yake!” (Kiyunani: eksousia, uhalali, mamlaka, misingi halali).

Ndani yake tunatambua kuwa hatupo hapa kwa bahati au ajali, au kwa kupenda kwa mzazi wa kidunia, wala uzao wa dhana ya kimwili tu; tupo kwa udhihirisho wa kutaka kwa Mungu kujidhihirishwa katika mwili. (Yakobo anasema, “Kwa kupenda kwake mwenyewe alituzaa sisi kwa neno la kweli…. Mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo.” (Yak.1:17,18,23).

Neno lilifanyika mwili na kupata makao ya kudumu (kufanya hema) ndani yetu, na tulimtazama kwa ajabu na mshangao juu ya siri ya ujumlisho ndani yake; (theaomai, kutazama, kuelewa). Tuliuona utukufu wake (Kiyunani, doxa, onyesho la shauri lake), utukufu kama wa asili, halisi, wa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli.” (Nia ya asili, au shauri la Mungu, lilitunzwa na kujulikana katika Kristo). Tumefahamu kuwa yeye ni ufunuo wa utimilifu wetu. “Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema.” (Neema tusiyoistahili). “Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo. Yeye aliye katika kifua cha Baba, Mwana pekee (asili, halisi) atokaye kwa Baba; yeye ni kiongozi wetu ambaye anatangaza na kumtafsiri Mungu asiyeonekana kwa usahihi ndani yetu.” (Yoh.1:1-5,9-14,16-18).

103

Page 104: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

NURU YA INJILI Hitimisho la neema ni ufunuo wa mwunganiko wetu ndani ya Kristo. “Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili. Na ninyi mmetimilika katika yeye aliye kichwa cha enzi yote na mamlaka. (Kol.2:9,10). Kristo anapotufunulia, huwa ndio kiini cha Injili! Hili ni neno la Kristo linalokaa ndani yetu kwa wingi wa utajiri. (Kol.3:1-16). “Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukirudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu.” (Kutoka nia ya unyonge sisi wenyewe, uliojengwa juu ya umbo la nje na utendaji, kufikia shauri la imani, lililojengwa juu ya uumbaji wetu wa asili na neema ya Mungu, iliyoonyeshwa katika Kristo.)

Hii ni nuru ya Injili! “Kutokuamini kunampa nguvu mungu wa dunia hii kukupofusha akili zako, na kukufanya usiione nuru ya Injili ya utukufu wa Kristo, ambaye ni sura ya Mungu. Kwa kuwa Mungu aliyesema, Nuru itang’aa toka gizani, ndiye aliyeng’aa mioyoni mwetu, atupe nuru ya elimu ya utukufu (doxa, maana yake utukufu) wa Mungu katika uso (kurudishwa katika kioo) ndani ya Kristo.” (2Kor.3:18; 4:1-7).

Jambo pekee ambalo huenda linaweza kututenga na Mungu, ni ujinga wetu na kutokuamini! Wala Shetani au dhambi haziwezi kumtenga mtu na Mungu, ikiwa lile alilolifanya Kristo katika kifo na ufufuo wake, lilikuwa ni la mafanikio; “Alizivua enzi na mamlaka.” (Kol.2:15).

Yesu anatangaza kwa uhakika: “Ninyi mkikaa katika neno langu, mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru. Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.” (Yoh.8:31,32,36). Uwana unakuweka huru! Ufunuo wa kwamba Mwana wa Adamu, ni Mwana wa Mungu, ni jambo la msingi kwa ujumbe wa Injili. (Math.16:13,16-19; Luka15; Mal.2:10; Zab.82:6; 22:27,30,31; Kumb.32:18; Isa.51:1; Ef.3:14,15).

Ufunguo wa kumjua Mungu umehifadhiwa katika siri ya kufanyika mwili kwa Kristo, ufunuo wa Kristo kama ndiye asili

104

Page 105: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

yetu; Mungu katika mwili, mfano wa kioo wa mwanadamu; “Maana sisi sote tu wazao wake” (Mdo 17:28). Neno la kweli linaonyesha uso wa kuzaliwa kwetu, kama katika kioo; huwezi kuukosoa mfano au kuidharau sura hata kwa uchunguzi wa karibu, maelezo yote ya uumbaji wako wa asili, unathibitisha kuwa wewe ni mkamilifu na mtimilifu, bila upungufu. Hili linakuchochea imani yako kuzaa furaha ambayo inashinda mapingamizi yote. (Yak.1:4,17,18,23-25).

KUWAFANYA WATU WOTE WAONE “Kulikuwako Nuru halisi, amtiaye nuru kila mtu, akija katika ulimwengu.” (Yoh.1:9). “Bwana Mungu amenipa ulimi wa hao wafundishwao, nipate kujua jinsi ya kumtegemeza kwa maneno yeye aliyechoka, huniamsha asubuhi baada ya asubuhi; huniamsha, sikio langu lipate kusikia kama watu wafundishwao.” (Isa.50:4).

“Mkituombea na sisi pia, kwamba Mungu atufungulie mlango kwa lile neno lake, tuinene siri ya Kristo; ili niidhirishe, kama inipasavyo kunena.” (Kol.4:3,4).

“Akiisha kutujulisha siri ya mapenzi yake, sawasawa na uradhi wake, aliokusudia katika yeye huyo. Yaani kuleta madaraka ya wakati mkamilifu, atavijumlisha vitu vyote katika Kristo, vitu vya mbinguni na vitu vya duniani pia. Na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, ….Nanyi pia katika huyo, mmekwisha kulisikia neno la kweli.” (Ef.1:9,10,13). “Sisi ni mawakili wa siri za Mungu.” (1Kor.4:1). Paulo alijua kuwa elimu ya siri ya kusudi la Mungu la milele, ilidhaminiwa kwake. “Kwa hayo, myasomapo, mtaweza kuutambua ufahamu wangu katika siri yake Kristo.” (Ef.3:4).

“Nalipewa neema hii ya kuwahubiri mataifa utajiri wake Kristo usiopimika; na kuwaangaza watu wote wajue habari za madaraka ya siri hiyo, ambayo tangu zamani zote ilisitirika katika Mungu aliyeviumba vitu vyote; ili sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho. (Milki ya kiroho).

105

Page 106: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Kwa kadiri ya kusudi la milele alilolikusudia katika Kristo Yesu Bwana wetu.” (Ef.3:8-11,14-21).

Ekklesia, mwitikio wa wito wa Mungu katika kila jiwe, lililochimbuliwa kutoka katika Mwamba, sasa umekuwa ni onyesho la kusudi la Mungu la milele. (Math.16:16-19; Isa.51:1). “Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe, na hao wawili watakuwa mwili mmoja. Siri hiyi ni kubwa; ila mimi nanena habari ya Kristo na ekklesia.” (Muungano mpya,jina jipya, utambulisho mpya ulio mbali na uzao wa mwili). ‘Ef.5:31,32.’ “Bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu! “Kristo amefunuliwa kuwa ndiye ufafanuzi sahihi na kipimo cha uzima ambao Mungu aliukusudia kwa ajili yetu kabla ya wakati. Kiyunani: prohoritso, maana yake, kukusudia mapema, kuweka upeo wa macho wa kweli; wakati neno, doxa, lilitafsiriwa kuwa ni utukufu, shauri, linaloleta ubora wa uzima ambao Mungu alikuwa nao katika nia yake kwa ajili yetu). “Wenye kuitawala dunia hii hawaijui hata mmoja; maana kama wangaliijua, wasingalimsulibisha Bwana wa utukufu!” (Kor.2:7,8).

Siri imefichuliwa! Wanadamu wote walijumlishwa katika Kristo! “Mmoja alikufa kwa ajili ya wote, basi walikufa wote! Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo; Yeye asiyejua dhambi alimfanya dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika yeye.” (2Kor.5:14-21). “Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao. Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho; Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho.” (Maneno ya Roho hunenwa katika kweli mbali na mjadala wa kiakili). ‘1Kor.2:9-13.’

“Ambalo nimefanywa mhudumu wake, sawasawa na uwakili wa Mungu, nililopewa kwa faida yenu, nilitimize neno la Mungu. Siri ile iliyofichwa tangu zamani zote na tangu vizazi vyote, bali

106

Page 107: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

sasa imefunuliwa kwa watakatifu wake. Je, siri takatifu ya utajiri wa utukufu kwa mataifa ni nini? Ni Kristo ndani yenu! Hili ni tumaini la shauri la Mungu kuhusu wewe! (Tumaini la utukufu). Ambaye sisi tunamhubiri habari zake, tukimwonya kila mtu na kumfundisha kila mtu katika hekima yote, tupate kumleta kila mtu mtimilifu katika Kristo. Nami najitaabisha kwa neno lilo hilo, nikijitahidi kwa kadiri ya kutenda kazi kwake atendaye kazi ndani yangu kwa nguvu.” (Kol.1:25-29).

“Ninajitahidi kwa ajili yao, ili wafarijiwe mioyo yao, wakiunganishwa katika upendo, wakapate utajiri wote wa kufahamu kwa hakika, wapate kujua kabisa siri ya Mungu, yaani, Kristo; ambaye ndani yake yeye hazina zote za hekima na maarifa zimesitirika.” (Kol.2:2,3). Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu.” (2Kor.3:18). Hii ni nuru ya Injili, kujumlishwa kwetu, ambaye ni sura ya Mungu. Sura ya Mungu imerejeshwa tena katika mwili. “Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili. Na ninyi mmetimilka katika yeye.” (Kol.2:9,10). “Kwa kuwa Mungu, aliyesema, Nuru itang’aa toka gizani, ndiye aliyeng’aa mioyoni mwetu, atupe nuru ya elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo. Lakini tuna hazina hii katika vyombo vya udongo.” (2Kor.3:18-4:7).

TUMEFUFUKA PAMOJA NAYE, ILI KUTAWALA PAMOJA NAYE“Baada ya siku mbili atatufufua; siku ya tatu atatuinua.” (Hos.6:2). “Lakini tangu sasa Mwana wa Adamu atakuwa ameketi upande wa kuume wa Mungu Mwenyezi!” (Luka 22:69). “Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu.” (Ef.2:6). “Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu, Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu.” ‘Kol.3:1.’ (Haya ni mamlaka ya utawala ambayo amehifadhi kwa ajili yako, ili kwamba alipo nawe uwepo. (Yoh.14:3).

“Ishughulishe akili yako na utaratibu huu mpya wa maisha; Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo

107

Page 108: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

katika Mungu. Siri ya uhai wako ni umoja pamoja na Kristo katika Mungu.” (Kol.3:1-4).

(Wewe pamoja na Kristo aliyetukuzwa kama wamoja mmekuwa udhihirisho mtakatifu wa Mungu. Njoni katika kiti cha enzi ninyi mpendwao. Maisha ya enzi na upendo wa enzi na nguvu za enzi na roho ya enzi vikutawale, na kukanyaga kwako kutakuwa ni kutembea kwa mshindi, taji yako itakuwa taji ya utukufu, na nguvu zako zitakuwa nguvu za Mungu. Sio mtu aliyeokoka na Mungu wa utukufu, Bali mtu aliyejichanganya ndani ya Mungu na Mungu amejichanganya ndani ya mtu, uumbaji mmoja wa mbinguni. wamoja katika moyo, wamoja katika akili, wamoja katika nafsi, wewe na Mungu kama mmoja. “Ulivyo navyo vyote ni vyangu, na vyote nilivyo navyo ni vyako. Sisi ni wamoja wasiogawanyika.” (Na John G. Lake).

Sasa wewe ni ufunuo wa Kristo katika mwili; huruma yako, wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu, kuchukuliana, furaha, kusameheana, kupendana, na amani ya Kristo kuamua katika nia zenu, ni udhihirisho wa uzima wa Kristo ndani yako; “Mkivaa utu mpya unaofanywa upya upate ufahamu sawasawa na mfano wake yeye aliyeuumba. Hapo hapana Myunani wala Myahudi, kutahiriwa wala kutokutahiriwa, mgeni wala mshenzi, mtumwa wala mwungwana, bali Kristo ni yote, na katika yote!” (Kristo yuko ndani ya wote, katika kila mmoja, hata ndani ya mshenzi!) ‘Kol.3:10,11.’

“Hata imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awaye yote kwa jinsi ya mwili!” Mawazo ya mtu ya unyonge juu yake mwenyewe na wenzake, hufanyika kuwa kivuli kwa ufunuo wa uadilifu wa ushawishi wa Mungu kuhusu sisi. 2Kor.5:16. (Tulikufa pamoja naye, tulifufuka pamoja naye, tumeketishwa pamoja naye katika chumba cha kiti cha enzi cha Mungu, sasa pia tunaonekana pamoja naye, kila wakati anapoonekana! (Kol.3:4).

Katika kitabu cha Matendo, sura ya 3, Kristo anajionyesha katika maisha ya watu wawili wa kawaida, wavuvi wasio na elimu, wanamponya mtu aliyekuwa kiwete tangu kuzaliwa!

108

Page 109: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Wangeweza kusema, “Ndugu, tulimjua mtu ambaye angeweza kukupatia mahitaji yako zaidi kuliko ulivyotazamia kupokea kutoka kwetu, lakini kwa bahati mbaya umemkosa kama miezi miwili iliyopita!” Lakini tunamshukuru Mungu kwa ufunuo wa ufufuo; walielewa kwa hakika kwamba, kile walichokuwa nacho, kile ambacho Mungu alifanya kwa niaba ya mwanadamu katika Kristo, kilijumlisha na mwujiza wa mtu huyu! (Mdo 3:26; 4:13).

MAPENZI YA MBINGUNI

Kiini kikuu na ufunuo wa Biblia kinafurahia uhusiano baina ya Mungu na mtu kwa kiwango cha juu sana, muunganiko wa uadilifu kabisa, pasipo aina yoyote ya kujitenga, unyonge, hatia, hukumu au shuku mbaya. Muda wa Mungu, wakati kwa mara ya kwanza katika historia ya ulimwengu, Muumbaji asiyeonekana alionyesha mfano wake na sura yake ndani ya chombo cha udongo cha mwili, ikawa ni kumbukumbu na uwepo wake na kusudi katika dunia, ambayo ilitawala historia ya mwanadamu na hatima yake. (Mw.1:26,27,31). Ufunuo wa Injili unaonyesha jinsi Mungu alivyotunza chapa ya uumbaji wetu katika Kristo, japokuwa mwanadamu alianguka dhambini. Ushirika wetu wa milele katika Kristo tangu msingi wa dunia, ulikombolewa. (Ef.1:4,5). Mungu alitupata sisi ndani ya Kristo kabla ya kutupoteza ndani ya Adamu! Mengi yamefanyika kutokana na anguko la Adamu, wakati jambo lingine lenye maana kubwa zaidi limestahilisha mtazamo wetu usiogawanyika. (Yoh.10:10). Ujumbe wa upatanisho unasisitiza ubunifu ambao Mungu aliufanya, na unafunua jinsi Mungu alivyofanikiwa kumrejesha kwake mwanadamu aliyeanguka bila hatia yoyote. (1Kor.1:30; 2Kor.5:18,19; Rum.1:16,17; 5:12-20).

Mtu anaonekana kuwa katika muungano na Muumba wake katika uumbaji wake; uumbaji huu ni wa aina ya ki-Mungu hasa, aliumbwa kwa urafiki na kukutana ki-mbingu. Mwanadamu ni ndoto ya upendo wa Mungu. (Ef.1:4,5). “Mimi nimesema, Ndinyi miungu, na wana wa Aliye juu, nyote pia. Lakini mtakufa kama wanadamu, mtaanguka kama mmoja wa wakuu.” (Zab.82:6,7).

109

Page 110: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

“Humkumbuki Mwamba aliyekuzaa, Mungu aliyekuzaa umemsahau.” (Kumb.32:18). Katika Zaburi 22, Daudi anatabiri kifo cha Masihi-Kristo, na anayaona matokeo ya ushindi katika msitari wa 27, “Miisho yote ya dunia itakumbuka, na watu watamrejea Bwana; jamaa zote za mataifa watamsujudia!” Katika Kristo, Mungu alishughulikia kila sababu ambayo ingeweza kumfanya mtu ajihisi kutengwa au kuwa mbali na Mungu; Yeye ni njia kuu jangwani aliyoiona Isaya, kila kilima kilishushwa, na kila bonde liliinuliwa, palipopotoka palinyoshwa, na hata palipoparuza palisawazishwa! (Isa.40:3-5; Luka3:4-6). Katika kifo chake msalabani, alitutengenezea mahali kwa ajili yetu, ili alipo nasi tuwepo: (Yoh.14:2,3,20). “Siku ile ninyi mtatambua ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu, nanyi ndani yangu, nami ndani yenu!” “Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake.” (Kol.1:21,22; 3:3; 2Kor.5:19).

Paulo anaelezea shukurani zake zisizozuilika kwa Mungu kwa ajili ya waamini wa Korintho, kila anapofikiri juu ya umoja wa imani yao ndani ya Kristo. Anawaona wakiwa wamejaa wema na neema, na kwa hiyo wanaweza kuwasilisha kwa uhuru ili kuwafikishia na watu wengine vivyo hivyo. (1Kor.1:4,5). “Mmepata maarifa yote na maneno yote, kwa sababu ndani yenu ushuhuda wa kweli ya Kristo umepata uthibitisho.” (Tafsiri ya New English Bible, msitari wa 6). Tafsiri ya King James inasema, Hata kama vile ushuhuda wa Kristo ulivyothibitishwa ndani yenu.” Paulo anawatia moyo kukumbatia kwa matumaini ya ujasiri, ufunuo wote wa Yesu ulio ndani yao. Sasa mwamini apate kujua bila shaka kuwa, kila atakachokihitaji, tayari ni sehemu iliyofungwa katika hiki kipawa cha neema. Ushuhuda wa Kristo uliothibitishwa ndani yako hautakuacha uhangaike njiani, bali unaweza kukutegemeza bila hatia mbele zake hata siku ya mwisho. Yesu ndiye uhakika wa kuachiliwa kwako, uzima wake na ushuhuda ni stakabadhi na hati ya uthibitisho dhidi ya mashitaka yote na shuku mbaya. (Tafsiri ya Biblia iliyofafanuliwa inasema: “yeye ni hakikisho la uthibitisho wako; yeye ni kibali chako dhidi ya mashitaka yote.”

110

Page 111: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Katika jambo hili Paulo anawasihi waamini kila mmoja kushawishika katika nia moja; anawaonya kila mmoja wetu, kunena lugha moja ya kipekee (kunena mamoja), hasa kwa sababu tunashiriki hofu ya aina moja na hukumu. (1Kor.1:4-13). Mtazamo wa Mungu ndio nuru pekee ya kutembea ndani yake. Matengano hayawezi kuvumilika! “Kama yamkini, kwa upande wenu, makae katika amani na watu wote.” (Rum.12:18). “Maana kwako iko chemchemi ya uzima, katika nuru yako tutaona nuru.” (Zab.36:9). Kulingana na kazi ya Mungu ya neema ya kumtambua na kumuunganisha kila mtu ndani ya Kristo, hakuna nafasi tena ya kuwa na wazo jingine. Hakuna mkazo maalumu wa mafundisho ya imani au mtindo binafsi kutoka kwa mtu yeyote, kwamba ni Paulo au Petro au Apolo, unaoweza kuingilia kiini kikuu cha Injili ya neema yake. Hatukuitwa kutambua ujuzi wa mtu yeyote, mafundisho yake ya imani, au tafsiri, kwa gharama ya ukweli kama ulivyo ndani ya Kristo. Chemchemi huhifadhi na kulinda asili, wazo la Mungu lisilopunguzwa; Yeye ndiye neno litokalo katika kinywa cha Mungu; Yeye ndiye asili yetu na vijito vyetu vya furaha viko ndani yake!

Michanganyo mitano ifuatayo ni thamani za urafiki wa maana ambao hauwezi kujichanganya:

1. Upendo usio na masharti hutengeneza hatua. (kukubaliwa, wema, kutambuliwa, kufurahiwa).

2. Uadilifu huleta kuaminiwa. 3. Bila hatia, msamaha, kuachiliwa kabisa, bila shuku

mbaya, lawama au hatia. 4. Umoja wa nia. 5. Tumaini lidumulo na taarifa za kutegemewa.

1. Ufunuo wa ubunifu wa Mungu unatofautisha ukristo wa kweli na dini nyingine yoyote. Huku sio kujaribu kwa mtu kupata upendeleo wa uungu, au kujaribu kushawishi hali ya mungu mwenye hasira; hapa, Mungu anaupatanisha ulimwengu wenye uadui na nafsi yake! (Rum.5:10). Wala sio dhabihu ziletwazo na mtu; wala sio mtu na mwana-kondoo wake mzuri; Injili

111

Page 112: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

inafunua ubunifu wa Mungu; “Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukiaye dhambi ya ulimwengu.” (Mw.22:13,14; Isa.53:7; Yoh.1:29). “Twampenda, kwa kuwa alitupenda sisi kwanza.” (1Yoh.4:19). “Alitupenda tulipokuwa tungali wenye dhambi.” (Rum.5:8). Kama dhambi iliweza kumtenga mtu na upendo wa Mungu, basi ukombozi ulikuwa hauwezekani.Yesu Kristo ndio kipimo cha thamani ambacho Mungu huweka juu ya kila mtu. “Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo.” (Ef.4:7). Aliukomboa mfano wake na sura yake ndani yetu. (Luka 15:8:9). “Tulinunuliwa kwa thamani.” 1Pet.1:18,19). “Je, mtu ni kitu gani, hata ukamtukuza na kumtia moyoni mwako?” (Ayu.7:17). “Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, na binadamu hata umwangalie?” (Zab.8:4). “Mungu, fikira zako zina thamani nyingi kwangu; jinsi ilivyo kubwa jumla yake! Kama ningezihesabu ni nyingi kuliko mchanga; niamkapo nikali pamoja nawe.” (Zab.139:17,18). Mungu anaona matunda ya taabu ya upendo wake, na kusherehekea juu ya mawazo ya ukombozi wetu na urejesho wetu kwake.” (Isa.53:4,5,11). “Atakushangilia kwa furaha kuu, atatulia katika upendo wake, atakufurahia kwa kuimba.” (Sef.3:17). “Upendo huifanya imani kuwa na matendo.” (Ga.5:6).

2. Pasipo mashindano. Mungu mwenyewe anatuhakikishia uadilifu wa mwungano huu; “Kama sisi hatuamini, yeye hudumu wa kuaminiwa, kwa maana hawezi kujikana mwenyewe.” (2Tim.2:13). “Ni nini, basi, ikiwa baadhi yao hawakuamini? Je, kutokuamini kwao kutaubatili uaminifu wa Mungu? Hasha! Mungu aonekane kuwa amini na kila mtu mwongo.” (Rum.3:3,4).

Anapenda kutushawishi bila mashindano kuhusu uwazi na uadilifu wa kusudi lake la milele; (katika hali yetu ya kibinadamu, tulipaswa kuapa kwa mamlaka ya juu sana ili kuongeza uzito wa hitimisho la kusudio letu.) Mungu hutumia njia iyo hiyo ili kurudisha uhakika wake usioyumba-yumba kuhusiana nasi, na hufanya mambo kana kwamba neno lake lisingetumainika; kwa hiyo anaapa kwa nafsi yake, kwa kuwa

112

Page 113: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

hakuna mamlaka iliyo juu zaidi ya kiti chake cha enzi; kwa hiyo uungu wake unafanyika kuwa uthibitisho wa haraka kwa neno lake. (Ebr.6:9-20).

Ukombozi wa wanadamu hauko katika uwiano, wala hauko katika hatari! Yesu ndiye ndiyo ya Mungu ya milele na ya mwisho kwa mtu; katika ubinadamu wake mwenyewe alifanyika kuwa hakika na utimilifu wa kila ahadi ambayo Mungu alikuwa nayo akilini kwa ajili ya wanadamu! (2Kor.1:18-22). “Mungu hawezi kusema uongo.” (Tito1:2,3). “Neno ni la kuaminiwa na linastahili kukubalika kabisa” (2Tim.2:11).

“Abrahamu akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu (Kiyunani, doxa, shauri), huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi. Imani yake ikahesabiwa kuwa haki.” (Rum.4:20,21. Tafsiri ya Knox). “Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa.” (1Tim.4:9). “Kwa kuwa mlipopata lile neno la ujumbe la Mungu mlilolisikia kwetu, mlilipokea si kama neno la wanadamu, bali kama neno la Mungu; na ndivyo lilivyo kweli kweli; litendalo kazi pia ndani yenu ninyi mnaoamini.” (1Thes.2:13. Tafsiri ya The Message). Yesu ndiye mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu.” (Ebr.12:2). Imani ya Mungu ndio kiini cha imani yetu; “Kutoka imani hata imani.” (Rum.1:16,17).

Mtu ni wa asili ya imani; “Lakini kwa kuwa tuna roho ile ile ya imani, kama ilivyoandikwa, Naliamini, na kwa sababu hiyo nalinena; sisi nasi twaamini, na kwa sababu hiyo twanena.” (2Kor.4:13). Mfuatano wa maelezo haya ni 2Kor.3:18; 4:1-18. “Kwa sababu hiyo, kwa kuwa tuna huduma hii, kwa jinsi tulivyopata rehema, hatulegei.” Hakuna kujichanganya kuna jambo la kutushawishi.

Kilichomo katika imani yetu na mchanganyiko mkuu wa imani yetu, ni kuonekana kwa kioo kwa wanadamu katika uso wa Kristo ambaye ni sura ya Mungu. Kufuatana na uadilifu wa Mungu, Biblia hufanyika kuwa hati ya uthibitisho wa hakika

113

Page 114: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

kuanzisha jukwaa halali na uhakika wa utambulisho wa kweli na wa kuachiliwa kwake.

Maandishi na picha ya Kaisari inatofautisha kipande cha chuma kama malipo halali; kwa namna iyo hiyo, Injili inafunua maandishi na picha ya Mungu katika sura ya Kristo kama malipo halali ya kuwakomboa wanadamu.

3. Bila hatia. Dhamiri ya dhambi inabatilisha matokeo ya msalaba na kuharibu namna yote ya uhusiano wa kweli. Uhusiano uliojengwa juu ya hatia, shuku mbaya, au hukumu hauna matumaini ya wakati ujao. Urafiki wa kustahili, hali ya kuwa bila hatia ni ya lazima. Hali ya kutokuwa na hatia kwa Adamu aliyotembea nayo ndani yake kabla ya anguko, ni hali ile ile ambayo Kristo anaifurahia katika mwungano na Baba yake, na sasa ni fursa iliyorejeshwa kwa kila mtu. Kila shitaka dhidi ya mtu limefutwa; mwanadamu amethibitishwa na kuachiliwa kwa uhakika. Mwana mpotevu hayuko katika kujaribiwa, bali amehesabiwa haki, kana kwamba hajawahi kutenda dhambi! “Kristo alitolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kufufuliwa ili mpate kuhesabiwa haki. Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii, ambayo mnasimama ndani yake.” (Rum.4:25; 5:1,2).

Kazi ya Mungu katika Kristo kwa niaba ya wanadamu, imefanya mambo mengi mno zaidi ya msamaha wa dhambi, amevunja utawala wa dhambi katika maisha yetu! (Rum.8:1-5). “Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa makosa yenu, (Kutokutahiriwa kwa mwili; Kiyunani: maisha yaliyotawaliwa na via vya uzazi!) Mungu aliwafanya hai pamoja naye, akiisha kutusamehe makosa yote; akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani. Akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akazishangilia katika msalaba huo!” (Kol.2:13-15). Tafsiri ya “The contemporary

114

Page 115: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

English Version” inasema, “Mungu aliutumia mwili wa Kristo kuihukumu dhambi.”

Sifa ya dhambi ya kutawala mwili wa wanadamu, imekanushwa milele na kushindwa katika mwili wa Kristo! Tafsiri ya Knox inasema, “Alitia sahihi katika hati ya kifo cha dhambi katika asili yetu.” (Rum.8:3). Injili inafunua kuwa imani huleta dhamiri ya haki badala ya dhamiri ya dhambi. (Ebr.9:9-14; 1o:1-4,14,22). “Kifo huleta mwisho wa dhambi, kwa kuwa Kristo aliteswa kwa ajili yetu, (alikufa kifo chetu; tulikuwa katika nia yake yote) fikiri maana ya kujumlishwa ndani yake; kwa hiyo, husaidia akili yako kusimama imara ukiwa na silaha kinyume cha kila shambulio.

Unaweza kuishi kwa ujasiri muda wako uliobaki katika mwili ukiwa umevuviwa na kusudi la Mungu lililoainishwa pasipo wajibu zaidi na kupotoshwa na tamaa za kibinadamu. (1Pet.3:18; 4:1,2). “Kifo alichokufa, aliifia dhambi, mara moja kwa ajili ya wote; bali uzima anaoishi, anamwishia Mungu.” “Maana kwa kule kufa kwake, aliifia dhambi mara moja tu; lakini kwa kule kuishi kwake, amwishia Mungu. Vivyo hivyo nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu. (Kiyunani: logitzomai, hitimisho lenye maana). Kila shitaka dhidi ya mwanadamu limefutwa kwa ushindi. (Yoh.12:31,32; Uf.12:8-11; Zab.103:2,3,10-12; Zek.3:1-9).

4. Umoja wa nia, sio uchaguzi wa anasa; bali ni hitimisho la imani. Umoja huu huweka urafiki bila ugomvi. Paulo anaona kuwa umoja ndani Kristo unasababisha marekebisho katika mazungumzo yetu; “Basi nawasihi kwamba ninyi nyote mnene mamoja!:

Endeleza roho ya makubaliano, inayosababisha matengano yasiwezekane kabisa, kwa kuwa sisi sote tumeunganishwa kikamilifu pamoja kwa njia ya kujua yale ambayo Mungu aliyafanya katika Kristo, ili tufurahie uhakika wa shauri moja.” (1Kor.1:10). “Twaamini, na kwa sababu hiyo twanena.” (2Kor.4:13). “Ili kwamba ushirika wa imani yako ufanye kazi

115

Page 116: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

yake, katika ujuzi wa kila kitu chema kilicho kwetu, katika Kristo.” (Filem.6). “Nina matumaini kwenu katika Bwana, ya kwamba hamtakuwa na nia ya namna nyingine.” Gal.5:10). Injili nzima inafunua mwunganiko wetu ndani ya Kristo. Si ajabu kwa kusema kuwa, kwetu sisi kushindana sisi kwa sisi, au hata kujipima au kujilinganisha na wengine, ni kutokuwa na akili. (2Kor.10:12).

Hili linahitimisha kwamba hakuna tofauti za binafsi, au matakwa ya mtu au chuki, inaweza kuvumilika nje ya ukweli wa ajabu wa kazi ya Mungu ya neema na upatanisho wake. Paulo anamkumbusha Tito, ”Wasimtukane mtu yeyote, wasiwe wagomvi, wawe wema, wakionyesha upole wote kwa watu wote. Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi, tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukiishi katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana. Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa; si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, iliyoonyeshwa katika Kristo.” (Tito 3:2-5).

“Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote. (Kiyunani: pronoeo, ni kutazamia, fikiri au kujua mapema; kalon, ni uzuri, ambao ni wa ubora mwingi). Ninyi ni zaidi ya wenye uwezo, na ndani yenu mna kila namna ya kuwafanya mwe na amani na kila mmoja, bila kujali jinsi wanavyowatendea ninyi! Usijisumbue kujilipiza kisasi, hata kama mnahisi kutendwa vibaya. Hapa kuna mbinu nzuri: Uwe mwangalifu kwa mahitaji ya adui zako na wote wanaokuchukia, walishe wawapo na njaa, na uwanyweshe wawapo na kiu! (Rum.12:17-20). Hapa, Paulo ananukuu katika Mithali 25:2i,22; “Kutia makaa ya moto kichwani pake” kunamaanisha jinsi ambavyo mhunzi anavyoweza kuyeyusha chuma ndani ya kalibu, na si kwa kukiweka tu juu ya moto, bali kwa kupalia makaa ya moto juu yake, hivyo kuzidisha joto na kuharakisha mchakato! Kwa hiyo, haya matendo ya wema, yataweza kumwokoa katika uovu uliomo ndani ya adui yako, na kumpata

116

Page 117: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

kama rafiki! Mungu anaona dhahabu katika kila uhusiano. Alitupata sisi tulipokuwa tungali maadui kwake! (Rum.5:8,10).

“Wema wa Mungu wakuvuta wewe kwa ushawishi wa nguvu ili kukugeuza kabisa nia yako. (Rum.2:4). “Maana, upendo wa Kristo watubidisha; maana tumehukumu hivi, ya kwamba mmoja alikufa kwa ajili ya wote, basi walikufa wote. Hata imekuwa, sisi tangu sasa, hatumjui mtu awaye yote kwa jinsi ya mwili.” (2Kor.5:14,16). Jifunze na kukariri maandiko yafuatayo kwa juhudi na uangalifu: 1Kor.1:30; 2:2,7,8; 2Kor.1:18-20; Ef.4:7; Filem.6; Yak.3:9; Ebr.2:11; Mdo 10:15,28; 1Yoh.1:7; 2:8,9,10; 5:9,10,20; Zab.36:9. Kwa kuwa Mungu hajachanganyikiwa kuhusu sisi, tunaweza kumudu kuwa wamoja katika nia zetu, na kuunganika katika nia moja.

5. Baada ya hayo, kuishi kwa furaha: Huu si mwako wa ghafula ndani ya chungu, kitu cha kupiga na kukimbia! Injili hii inapima mwungano ili ufurahiwe bila kizuizi, bila mpaka, bila kuingiliwa na wakati ujao! Kwake Ayubu, wazo hili lilikuwa jema sana na la kweli. Hofu ilitawala uhusiano wake na Mungu. (Ayu.1:5; 3:25). Anapoangalia maisha yake, anazungumza kuhusu “Siku za kukomaa kwa urafiki wa Mungu.” (Ayu.29:2-4; RSV). Hii inaonyesha kuwa, aliishi katika hofu ya kuendelea, na masika yaliingilia ghafla kipeo cha furaha ya urafiki huu!” Mungu anayo mengi zaidi katika akili yake, kuliko kuwa na baraka za msimu tu. Waefeso 1:4,5; inafunua kuwa sisi ni ndoto ya Mungu ya milele. Ndani ya Kristo, raha ya Sabato sio siku tena, bali ni sherehe ya ukombozi mkamilifu; ni mahali pa furaha ya Mungu kwa ajili ya mwanadamu isiyozuiliwa, na furaha ya mwanadamu kwa ajili ya Mungu isiyozuiliwa.

Mtume Yohana, rafiki wa Yesu wa karibu, anaandika, (miaka 60 baada ya Yesu kujitenga nao katika mwili), juu ya ushirika usioharibiwa kwamba, hadumu kwa kuufurahia tu, bali anataka kila mwamini ashiriki ndani yake. “Ujumbe wetu unahusu lile Neno, ambalo ni uzima; ambaye alikuwako tangu zamani, ambaye tumesikia, na kumwona kwa macho yetu, tulimtazama, na mikono yetu ikampapasa. Ndiyo, uzima umepambazuka, na

117

Page 118: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

sasa tu mashahidi wake. Ninawaandikieni haya, ili furaha yenu itimizwe kwa wingi! (Tafsiri ya Knox).

“Mungu ni nuru, na ndani yake hamna giza hata kidogo!” Kutembea katika nuru kama Mungu alivyo katika nuru, kunaonyesha jinsi ya kujiona kwa namna ya Mungu. Sasa kuungama dhambi kunaleta maana mpya. Neno la Kiyunani lililotafsiriwa la kuungama, limeunganishwa kwa maneno mawili: homo + logeo, lililo na maana ya kunena mamoja; kwa hiyo badala ya kumwambia Mungu habari za dhambi zako, unaiambia dhambi habari ya ukombozi wako. Mungu hahitaji taarifa, bali mamlaka ya giza hufanya hivyo!

Huwezi kumudu kujidanganya mwenyewe kwa kuishi maisha yenye nia mbili, na “kuigiza ushirika” wakati bado unaficha dhambi ndani ya maisha yako! Iamuru dhambi kwa mamlaka sawasawa na utendaji wa Mungu katika Kristo; damu yake inatusafisha na dhambi zetu zote. Yohana anawaandikia waamini katika viwango tofauti vya kukua kwao; watoto wadogo, vijana na akina baba. (1Yoh.2:12-14). Kwa watoto wadogo anasema, “Nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi; na kama mtu akitenda dhambi, (dhambi ni kasoro) tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki, naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote.” Hakuna mwenye sifa ya kukuwakilisha kuliko yeye! (1Yoh.1:1-10; 2:1,2). Jifunze na kukariri pia maandiko yafuatayo: Ebr.9:12; Kol.2:13-16; 3:1-3; Rum.6:1,6,7,11,12,17; 8:1-4; 1Pet.4:1,2.

MAFANIKIO YA MSALABA

Injili inafunua jinsi Mungu alivyoweza kuondoa matokeo ya anguko la Adamu. Ili Injili iwe habari njema, ni lazima iweze angalau kuwasilisha ukombozi ambao unamrejesha mwanadamu kwenye ndoto ya upendo wa Mungu wa asili. Katika Waefeso 1:4 Paulo anamwona mtu ameshirikishwa katika Kristo kabla ya kuwekwa misingi ya dunia. Maneno

118

Page 119: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

“Katika Kristo” huenda ndio maneno mawili muhimu sana katika Biblia; kwa sababu ya mwungano huu, kila jambo linalotokea ndani au kupitia Kristo, linamjumlisha mwanadamu. Paulo anasema, “Kwa Mungu ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu.” (1Kor.1:30). Umoja huu sio matokeo ya kudhania kwa mtu, au fikira za kutaka, “Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, ambaye katika Kristo aliupatanisha ulimwengu na nafsi yake! (2Kor.5:18,19).

Jambo kubwa zaidi na lenye matokeo makubwa zaidi lilitokea kwa mwanadamu katika Kristo, kuliko lolote ambalo lilisemwa dhidi ya mtu kama matokeo ya anguko la Adamu. Yote yaliyoandikwa katika historia, hayakuweza kuleta ushahidi wa kutosha dhidi ya mwanadamu kupinga au kufuta hukumu ya Mungu ya kuachiliwa! Kipawa cha bure cha Mungu kisichoweza kupimika kinaondoa makosa katika matokeo. Kwa maana ikiwa kwa makosa ya mtu mmoja, wengi wamekufa, ukarimu mkuu usio na mwisho ambao ni neema ya Mungu, na kipawa kimefungwa ndani ya neema yake, kimeelezwa ndani ya mtu mwingine, Yesu Kristo, kimewekwa katika wanadamu wengi. Halafu kinachofuata ni kwamba kwa kadiri ya matokeo ya kosa moja hukumu ilienea kwa kizazi chote cha wanadamu.” (Rum.5:15,18; Tafsiri ya Weymouth). “Tendo moja la Adamu, na tendo moja la Kristo yanafanana, katika mambo yote ya mwanadamu yameathiriwa na hilo; ingawa matokeo yana tofauti.” (Rum.5:18; Tafsiri ya Johnson). Wanadamu hao hao walionguka chini ya dhambi ya Adamu, sasa wameingizwa katika Injili ya Yesu Kristo! Yale aliyoyakamilisha Mungu katika Kristo ni zaidi ya malinganisho na nje ya mapendekezo yote katika matokeo ya dhambi ya Adamu.

J.B.Phillips aliandika mwaka 1955, katika dibaji ya tafsiri yake ya kitabu cha Matendo, haya yafuatayo: Hivi sasa katika uinjilisti mwingi wa kileo, matangazo makuu ya majukwaa ni msisitizo wa tena na tena, juu ya matamko ya uovu wa wanadamu. Biblia inasema, “Wote wametenda dhambi” Wainjilisti wa siku hizi watapaza sauti zao na kusema, “Biblia inasema, Hakuna mwenye haki hata mmoja.” Biblia inasema,

119

Page 120: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Haki yetu yote ni sawa na mavazi machafu.” Lakini Luka akiandika kitabu cha Matendo ya Mitume, inaonyesha kutokujua lolote kuhusu msisitizo huu. Badala yake anaainisha uzoefu wa Petro na Kornelio, Mungu alipomwambia asimwite mtu yeyote kuwa najisi! Kwa kweli njia ya kisasa ya kuamsha hatia kwa kunukuu vifungu vya maandiko visivyojitosheleza, haipatikani katika kitabu cha Matendo ya Mitume hata kidogo.” Mafanikio ya msalaba na mguso mpya na matumizi ya ufufuo, ulikuwa ushuhuda katika kitabu cha Matendo wa waamini wa kwanza. Roho Mtakatifu alitoa ushuhuda kwa neno la neema pamoja na ishara na maajabu vilivyofuatana na mahubiri yao, na neno likaenea na idadi ya wanafunzi iliongezeka kwa nguvu! (Mdo 6:7; 14:3.

Injili inatangaza kutokuwa na hatia kwa mwanadamu; ni stakabadhi inayothibitisha kuachiliwa kwa wanadamu. Katika shughuli yoyote, stakabadhi inawakilisha hati ya maelezo na kumbukumbu halali kwa malipo yanayostahili; ni ukiri wa maandishi wa malipo hayo. Sasa badala wanadamu kukabiliana na shutuma na hukumu, hukumu ya mwisho: msamaha wa Mungu na wema wake! Misingi halali kwa hukumu kama hii, imeelezwa kirefu katika mahubiri na mafundisho ya Injili ya neema. Wazo la kuachiliwa maana yake ni kwamba misingi yote ya mashitaka, hukumu na shutuma vimeondolewa; mwanadamu ametangazwa kutokuwa na hatia kuachiliwa rasimi kutokana na deni! “Aliwafanya hai pamoja naye, akiisha kutusamehe makosa yote; akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani! (Kol.2:13,14). Shetani hawezi tena kumfunikamtu kwa hatia! Mungu amefanya mambo ya kutosha kumthibisha mwanadamu; ufufuo wake katika wafu, unatangaza haki yetu kwa ushindi. (Rum.4:25).

Ufunuo wa haki ya Mungu ni siri ya nguvu ya Injili. (Rum.1:16,17). “Kutoka imani hata imani” maana yake ni kwamba Mungu anaamini yale ambayo Injili inayafunua, na tunaitumia imani yetu kuanzia hapo; Injili inatangaza kwa

120

Page 121: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

namna tofauti, hasa yale ambayo Mungu anasema juu ya mtu, aliyoyatangaza katika Kristo. Vipeperushi vingi kwa miaka mingi vilitangaza Warumi 3:23 nje ya mtirirko wa habari husika, wakati mistari ya 21,22 na 24-26, inafunua ushindi wa msalaba! Jinsi ambavyo Mungu anatafsiri kifo na ufufuo wa Yesu, kunatupa ufafanuzi wa mwisho na mguso wa Injili. Sasa anapenda kukamata mtazamo wetu, kuona aliyoyaona katika mazao ya uchungu wa nafsi yake, na kujua sisi wenyewe kama vile tulivyojuliwa sana! (Isa.53:11). Jambo kubwa katika Yohana 10:10, sio ukweli wa kwamba mwivi huja kuiba, kuua na kuharibu, bali kwamba Yesu alikuja ili tuwe na uzima tele! “Maana kwako wewe iko chemchemi ya uzima, katika nuru yako tutaona nuru! (Zab.36:9). Ushuhuda wa Mungu ni madai pekee ya utukufu! (1Yoh.5:9-11,20).

“Hata imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awaye yote kwa jinsi ya mwili!” (2Kor.5:16). “Lakini Mungu amenionya, nisimwite mtu awaye yote mchafu wala najisi.” (Mdo 10:28). Hakuna tamaa ya mtu, sifa, uzao wa kiungwana au mafanikio yanayoleta tofauti zaidi au maana kwa mtu, kuliko ukweli wa utambulisho wa mtu na kujumlishwa kwake katika Kristo! (Filipi 3:4-9). Paulo anailinda kwa juhudi na wivu Injili hii. (Gal.1:6,7,11,12; 2:5). “Injili yangu na kwa kuhubiriwa kwake Yesu Kristo, sawasawa na ufunuo wa ile siri (kujumlishwa kwa kila mtu katika yeye, 1Kor.2:6-8; Hos.6:2), ambayo ilisitirika tangu zamani za milele; ikadhihirishwa wakati huu kwa kwa maandiko ya manabii, ikajulikana na mataifa yote.” (Rum.16:25-27). Watawala wa giza walishindwa kuelewa kwamba watu wote waliwakilishwa katika kifo na ufufuo wa Yesu Kristo; yale walioshindwa kuyaona yalileta madai ya nguvu juu yao hata kufikia sifuri. Neno la Kiyunani, katargeo, maana yake ni kutolewa bila faida kabisa! (1Kor.2:6). Mungu alihitimisha na kuagiza yaliyotokea katika Kristo kuwa ni urejesho wa mtu kwenye wazo la asili (utukufu) la Mungu. Adui hawezi kufanya lolote bila kuruhusiwa na mtu; nguvu pekee inayowezekana ambayo adui aliyeshindwa sasa anaweza kudhania, ni kuruhusu kutokuamini kwa mtu na ujinga kumshawishi mtu ajidanganye mwenyewe na kusahau yeye ni mtu wa namna

121

Page 122: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

gani. (Yak.1:8,18,22-25). Yesu alisema kukaa katika neno lake, ni kuifahamu kweli, na kuijua kweli ya uwana ni uhuru wa kweli. (Yoh.8:31,32,35,36). Kwa kawaida kweli huzaa imani; imani huhuishwa katika kusikia kwetu; huu ni mtiririko wa hiari unaotazamiwa na ushawishi wa uadilifu wa mpango wa Mungu kama ulivyofunuliwa katika Kristo. (Rum.10:17; Ef.1:13; 4:21). Kusudi la Mungu la milele daima limekuwa kwa ajili ya watu kushiriki katika utukufu wake; imaini huona ushindi wa msalaba katika matumizi yake yote. (1Pet.1:10-13). Ukombozi hupata mkazo wake na maana katika ukweli wa kwamba, mwanadamu aliumbwa kwa mfano na sura ya Mungu; mwonekano wa kweli wa Muumba wetu unangoja kuamshwa ndani yetu kwa njia ya Injili ya imani. (Mw.1:26,31). Injili inathibitisha zaidi ya mabishano kwamba Mungu alikomboa mfano na sura yake ndani ya mwanadamu.

Historia imeandika juu ya kifo na ufufuo wa mtu mmoja; hali ya milele inatoa habari ya kifo na ufufuo wa kizazi cha Adamu! Mungu anaona ndani ya kifo cha Yesu, kuna kifo cha kila mtu! (2Kor.5:14; 1Kor.15:22). Kujumlishwa kwa wanadamu katika Kristo ndio ukamilifu wa neema. Manabii waliona hivyo: “Ni nani aliyesikia neno kama hili? Ni nani aliyeona mambo kama haya? Je, nchi yaweza kuzaliwa siku moja? Taifa laweza kuzaliwa mara? (Isa.66:8). “Baada ya siku mbili atatufufua; siku ya tatu atatuinua, nasi tutaishi mbele zake.” (Hos.6:1,2,7). Kujumlishwa kwetu katika kifo chake na ufufuo wake, kulitabiriwa miaka 800 K.K. kwa njia ya Hosea, na miaka 700 K.K. na Isaya. “Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani?” (Isa.52:10; 53:1,4,5,11). Petro aliona hivyo: “Tulizaliwa upya katika ufufuo wake!” (1Pet.1:3). Luka aliona hivyo: “Na sisi tunawahubiri habari njema ya ahadi ile waliyopewa mababa, ya kwamba Mungu amewatimizia watoto wetu ahadi hiyo kwa kumfufua Yesu; kama Daudi alivyotabiri katika zaburi ya pili akisema, “Wewe ndiwe Mwanangu, mimi leo nimekuzaa.” Hapa Luka anamnukuu Daudi katika Matendo 13:30-33). Ufufuo wa Yesu ni sawa na uzao mpya wa wanadamu. Paulo aliona hivyo: “Hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo.” (Ef:2:5).

122

Page 123: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

“Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai” Nimeunganika pamoja naye katika kifo chake. (Gal.2:20; 3:26; 4:7; 2Kor.5:16-19;Rum.6:5; Kol.2:11-13; 3:1-4). Yohana aliona hivyo: “Nasi twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mwana wa Mungu wa kweli, na uzima wa milele.” (1Yoh.5:20). “Neno lilio la kweli ndani yake, ni la kweli ndani yenu.” 1Yoh.2:7,8). Yesu aliona hivyo: “Saa imefika atukuzwe Mwana wa Adamu; chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi.” (Yoh.12:23,24). Sasa sisi tunaona hivyo: “Paulo anatuombea kwamba macho ya mioyo yetu yatiwe nuru, ili tuweze kujua siri ya kusudi lake. (Ef.1:9,10,17-19; 2:1-10). “Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake.” (Rum.6:5,6). “Vivyo hivyo nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi.” (Tafsiri ya Knox, Rum.6:11). Neno la Kiyunani logizomai lina maana hitimisho lenye maana; huu ni ukamilifu wa imani, unaotushauri kwamba, si kwa mawazo ya kutaka kwetu, au kwa kufikiri kwetu wenyewe namna hii! Kwa kweli, hakuna njia nyingine ya kujiona wenyewe bila kujidanganya au kupindua ukweli! Mahali ambapo sheria iliwataka kuwa na wajibu wa kutii kwa nguvu zao; Injili ya neema inatutaka kuwa na hakika ya imani. Hali hii inafungua aina mpya ya utii: utii wa imani. (Rum.1:5,16,17; 16:25,26). Torati ilifunua jinsi mwanadamu alivyokuwa mwenye dhambi, wakati Injili inafunua jinsi mwanadamu alivyo mwenye haki. (Rum.7:13). Miisho ya dunia itayaona haya! Habakuki (ambaye jina lake lina maana ya kukumbatia), ni nabii aliyeiona haki ipatikanayo kwa imani. 2:4; Katika sura ya 2:2 anasema, “Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma kama maji.” Halafu katika msitari wa 14 anatoa tamko hili zito, “Kwa maana dunia itajazwa maarifa ya utukufu wa Bwana, kama maji yaifunikavyo bahari.” Zaburi 98:1-3, umeandikwa wimbo ufuatao: “Mwimbieni Bwana wimbo mpya, kwa maana ametenda mambo ya ajabu! Mkono wa kuume wake mwenyewe, mkono wake mtakatifu, umemtendea

123

Page 124: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

wokovu. Bwana ameufunua wokovu wake; Machoni pa mataifa ameidhihirisha haki yake. Miisho yote ya dunia imeuona wokovu wa Mungu wetu.” Falme zote na mamlaka zitauona: “Ili sasa kwa njia ya kanisa (wale ambao wanasikia na kuitikia sauti ya asili yao ya kweli na utambulisho wao) hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka.” Katika miaka ijayo, ataendelea kuonyesha ndani yetu utajiri usiopimika wa neema yake katika wema kwetu katika Kristo Yesu. (Ef.2:6,7; 3:10).

Paulo anaiona huduma na utume kama zao la neema, ambalo sasa linamhimiza kuleta utii wa imani. (Rum.1:5). Neno la Kiyunani la utii ni, hupakouo, (upo, kujitiisha chini ya + akouo, kusikiliza kwa ajili ya) , kusikia kwa kutofautisha na kuelewa kwa usahihi. Paulo anatamani kuwafanya watu wote waone hivyo. (Ef.3:9). Yakobo anaona siri ya kioo, mahali ambapo utambulisho wetu wa kweli umefunuliwa, kama sheria kamilifu ya uhuru. (Sheria ya hiari ya moyo) ‘Yak.1:23-25.’

Kutenda kwetu kunasukumwa na kuuona ukweli kuhusu hali yetu sisi wenyewe; kutenda hakuwi kitu tena au kutenda ili kujihakikisha wenyewe, bali kutenda kwa sababu ya imani yetu ijuavyo kuwa sisi ni nani. Kuwa na hakika kuhusu utambulisho wako mbele ya upinzani, ndio siri ya maisha makamilifu. (Yak.1:2-4,17,18). Injili inadumu katika nafasi ya kwanza ya kile ninachokiona, sio kile ninachokifanya; hata kufa kwangu sio kutenda, bali ni kuona; daima kuona kunavuvia utendaji.

Sheria ya imani inafunua jinsi utii wa Kristo ulivyoyafuta matokeo ya kutokutii kwa Adamu. (Rum.5:19). Maana ya haraka ya utii wa Kristo, inatufungulia mamlaka, ambayo kwa hayo tutaweza kuziharibu ngome na kuteka kila fikira inayotufanya tuwe watumwa wa mawazo manyonge, au utambulisho mnyonge. (Angalia 2Kor.10:3-5; mahali ambapo Biblia ya King James ina tafsiri nzuri zaidi, “utii wa Kristo” badala ya kusema, “utii kwa Kristo” kama tafsiri nyingine nyingi zinavyoeleza kimakosa. Hili linafanya tofauti inayofanana: Kumtii Kristo kunamweka mtu abakie katika hali ile ile na

124

Page 125: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

mfadhaiko aliouzoea chini ya sheria; kutokuendelea kwake mwenyewe na kutokuwa na uwezo kunaleta hali isiyoepukika ya hatia na kushindwa; mahali ambapo utii wa Kristo unamwunganisha mtu na mafanikio yasiyo na mipaka ya kutenda kwa Kristo kwa niaba ya wanadamu; alitenda kwa niaba yetu!). Hakuna upinzani wa maana kwa utii wake na uvumilivu. Wakati wa imani ni kama nuru ifukuzavyo giza, bila kutumia nguvu! Giza haliuondoi ukweli, ila linauficha ukweli kutoka katika mtazamo ambao tayari ndivyo ulivyo, wakati nuru inaufunua.

Bado inawezekana kwa mtu kudharau au kupuuza ukweli wa wokovu na kuufanya uwe mdogo sana, lakini haiwezekani kuufanya wokovu uwe mkubwa sana. Ukombozi unaweza kushushwa thamani, lakini sio kuuzidisha. (Ebr.2:3; 2nyak.9:5,6; Luka 11:31). Gundua hali isiyopimika ya upendo wa Mungu, unaopita maarifa yote. (Ef.3:18-20). “Waamini wote wawili wanaweza kuthamini kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi, na kufurahia katika msamaha; mmoja wao badala yake, huona kwa kina na kuelewa kwamba, pia Kristo alikufa kwa ajili ya uovu wetu.” (Na George Peck, 1880). Je, inawezekana kuwa sasa tunayo ruhusa kutenda dhambi ili kupata faida ya neema? Ni upuuzi kiasi gani! Hatuwezi kufa na kuwa hai kwa dhambi kwa wakati huo mmoja.” (Rum.6:1,2). “Kusulibiwa pamoja na Kristo kuna maana kwamba, dhambi imepoteza haki yake ya kutumia miili yetu kama gari lake. Mtu aliyekufa ana kinga ya nguvu dhidi ya dhambi. Kwa kuwa tumeunganishwa katika kifo cha Kristo kwa njia ya imani, halafu kwamba huo ni msingi ambao juu yake na sisi pia tunashiriki katika uzima wake.” (Rum.6:6; Tafsiri ya Way). Sasa tunaweza kuhitimisha kwa ujasiri kwamba, kwa kweli sisi tumeifia dhambi, na kuishi katika mwungano na Mungu katika Kristo. Miili yetu ni mizuri kama iliyokufa kwa kadiri ya utawala wa dhambi unavyohusika. (Rum.6:11,12). “Juu ya msalaba, mwili wake ulichukua uzito wa dhambi zetu. (Na Knox). Hivyo tuliifia dhambi, na sasa tunajihesabu kuwa hai kwa haki; Kwa kupigwa kwake, sisi tumepona!” (1Pet.2:24; 4:1,2). Ndani ya Kristo, Mungu alishughulika na dhambi kwa namna ambayo alizihukumu

125

Page 126: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

nguvu zake katika mamlaka ambayo ilidai kuwa ni ngome yake, yaani, mwili wa binadamu! (Rum.8:3).

YESU – UFUNUO WA UTAMBULISHO WA KWELI WA MTU (Ushuhuda wa ukweli)

Asili ya mtu imechapwa milele katika nia ya Mungu. (Mw.1:26). “Kabla sijakuumba katika tumbo, nalikujua.” (Yer.1:5). Ushirika usiotenganishwa ulitokea kabla ya msingi wa dunia ambao unamtambua mwanadamu katika Kristo. (Ef.1:4). Katika Kristo tunaona mfano wa asili, na umbo lililokusudiwa la maisha yetu. (Rum.8:29; Tafsiri ya Message). Maneno mawili yaliyo muhimu sana katika Biblia ni maneno, “Katika Kristo.” Mwungano huu ni ufunguo unaofungua siri ya Biblia; haiwezekani kuielewa Biblia au ukombozi, katika nuru nyingine yoyote.

Neno “shirikisha” lina maana kuwa kunatokea mwungano kati ya sehemu mbalimbali, unaofanya isiwezekane kudharau au kuondoa sehemu yoyote kutoka kwa nyingine wakati zikiwa akilini. Katika nia ya Mungu, ghafula Yesu anawawakilisha wanadamu; ushirika huu unafanya isiwezekane Mungu kumwacha au kumtenga mtu katika maisha, kifo, ufufuo na kutukuzwa kwa Mwana wake. Mungu ameunganishwa kiundani na mwanadamu katika uhalisi wa wazo lake la milele. Katika kina cha uwepo wake, anamwona mtu katika mfano wake na sura yake. “Mungu alipotuumba na kutufanya katika mwungano na Kristo, alikuwa na jambo bora katika akili ambalo lilikuwa la kuendelezwa pamoja na matumaini yake ya kweli kwa ajili ya uumbaji wetu wa asili.” (Ef.2:10).

Neno la Kiyunani, hetimatzo, lina maana ya kuandaa kabla ya wakati; limechukuliwa katika desturi za mashariki za kuwatuma watu mbele ya wafalme katika safari zao ili kutayarisha njia na kuifanya ipitike. Katika Kristo, Mungu aliifanya njia kuu ya kifalme kwa ajili yetu, kila kizuizi kimeondolewa ili kwamba tutembee kama wafalme! (Isa.40:3,4). Katika mtiririko wa Efeso 2, Paulo anafunua jinsi Mungu alivyoturejesha katika utawala wa mkono wake wa kuume kwa njia ya mwungano wetu na

126

Page 127: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Kristo katika kifo na ufufuo wake. Sasa tumeketishwa pamoja naye na kushiriki ushindi wake na enzi juu ya dhambi na mamlaka zote za giza.

Historia haikuweza kamwe kuleta upinzani wa kutosha ili kubatilisha au kuondosha mfano wa Mungu ndani ya mtu. Asili yetu inafunua mwanzo wa matokeo makubwa kuliko vile ambavyo upinzani wowote ungeweza kukana; wakati muda na historia vinaweza tu kuandika na kutunza nyakati na matukio ya muda mfupi, imani inafunua ukweli katika roho na hali ya milele. Utajiri wa ushirika huu wa ndani, unatengeneza msingi wa kukutana kiroho. Hii ndiyo nguvu ya ushawishi wa imani yetu na udhihirisho kamili wa maisha yetu. Kufuatana na mwungano huu, kunapatikana siri na ukweli wa Injili. Yesu haoni haya kumwita mwanadamu ndugu yake, kwa kuwa wanashiriki asili moja. (Ebr.1:1-3 na 2:11).

Maana ya kuunganishwa kwa mtu katika Kristo inakamilika katika ufunuo wa kifo chake kufanyika ni kifo chetu, na ufufuo wake wa ushindi kama uzao wetu mpya. Yesu kama Adamu wa mwisho anakifikisha mwisho kizazi cha anguko la Adamu. (1Kor.15:45; 1Pet.1:3). Alipofufuka kwa nguvu za Mungu, aina mpya ilizaliwa, mambo ya kale yamepita, tazama yote yamekuwa mapya! “Hata imekuwa mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya.” Neno “kama” au “ikiwa” sio la sharti bali ni hitimisho! (2Kor.5:17). “Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu?” (Rum.31).

Habari njema zinafunua kwamba Mungu ni kwa ajili yetu! Malaika wanatangaza wema wake na kupendezwa katika wanadamu walipotangaza kuzaliwa kwa Yesu. Hizi ni habari njema za furaha kuu, zitakazowajia watu wote! (Luka 2:10,14). “Kwa Mungu ninyi mmepata kuwa katika Kristo.” (1Kor.1:30). “Alituhuisha pamoja naye; akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho katika Kristo Yesu.” (Ef.2:5,6; Hos.6:2). “Kwa kupenda kwake mwenyewe alituzaa sisi kwa neno la kweli.” (Yak.1:18).

127

Page 128: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Kusikia neno la kweli ni kuona uso wa kuzaliwa kwako mwenyewe kama ulivyo. (Yak.1:22-25). Ukweli kuhusu mtu umefunuliwa katika Kristo; hii ni siri ya neema; Mungu alitufunua ndani ya Kristo! “Mmoja alikufa kwa ajili wote, jambo ambalo linatupa hitimisho moja tu kwamba, wote walikufa!” (2Kor.5:14). Injili ni ukweli unaotuhusu sisi kama ulivotunzwa katika Kristo. (Ef.1:13; 4:21). Ndani ya Injili hii, hakuna mtu anayebaki kuwa mhukumiwa; hukumu ya wanadamu iliangukia juu ya mtu mmoja, mara moja, kwa ajili ya wote. Mungu alitoa ushahidi wa haki ya mwanadamu kwa kumfufua Kristo katika wafu. (Mdo 17:31; Rum.4:25). “Hata imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awaye yote kwa jinsi ya mwili.” J.B. Phillips anatoa tafsiri inayosomeka hivi, “Kuwajua watu hakuwezi kuwa kwa maisha yao ya nje.” (2Kor.5:16). “Maana yale yasiyowezekana kwa sheria (Tusingeweza kuyakamilisha haya kwa sheria, kwa kuwa sheria ilituwekea mipaka ya mwili; aliyoyafanya Mungu katika Kristo, yamefungua hali mpya ya kutufikiria sisi, sasa tuweze kujiona ndani ya utambulisho wetu wa roho, tukiwa huru kutokana na nguvu ya utawala wa mtu wa dhambi wa kale wa mwili). Kristo aliihukumu dhambi katika mwili, ili kwamba mahitaji ya torati yatimizwe ndani yetu.”Kristo aliweka sahihi hati ya kifo cha dhambi ndani ya asili yetu.” (Rum.8:3-5; Tafsiri ya Knox).

Mtu anaendelea kuwa mwenye uwezo wa kuhoji kinyume cha ukweli na hivyo kujidanganya mwenyewe na kubatilisha matokeo ya imani; wanahitajika kuwa na nia ya dhamiri iliyofanyika kwa mambo ya roho. Kuwa mwenye nia mbili kuhusu utambulisho wako wa kweli, kutakufanya uchanganyikiwe na kutokuwa imara. (Yak.1:7,8). Sheria kamilifu ya uhuru inakuweka huru kuona ukweli wako mbali na upinzani wote! (Yak.1:25). “Enyi Wagalatia, kwa nini mnaruhusu kuchukuliwa na udanganyifu wa kifalsafa? Katika kupoteza imani ya mguso wa kwanza wa kweli, unapoteza mambo yote uliyoyapata akilini mwako! Kristo aliyesulibiwa alihubiriwa kwa kuwekwa wazi na maana, kwa hiyo yaliyotokea kihistoria, vile vile yalitokea ndani yako! Ukweli ulitangazwa kwa kiasi kwamba mlikishuhudia kifo chake kuwa kama chenu wenyewe. (Gal.3:1).

128

Page 129: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Kwanza, Injili ni “kuona” kabla ya “kutenda,” hata kufa kwako ni kutenda, kwa kuwa ni kuona kwamba umekufa katika kifo chake; kwa kweli alikufa kifo chako! (Rum.6:11; 1Kor.1:30). Kwa hiyo, nguvu nyingi za kidini zinapotezwa katika majaribio yasiyo na maana, ya kufanya mambo ambayo tayari yalikwisha kutendwa; kujaribu kuwa mtu ambaye tayari ndivyo ulivyo!

Kwa sababu ya ujinga, Ukristo umekuwa kama imani ya Buddha; watu wamekuwa hawana kabisa kuzaa matunda, lakini wameendeleza juhudi za kuufisha ukristo. Unapogundua ukweli kuhusu mfano wa Mungu ndani yetu na uhalisi wa Kristo ndani yetu, utampenda jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe! Kuona kunavuvia utendaji; sheria ya ushirika ni kanuni ya imani. (Rum.3:27; Yak.1:25). Sheria ya imani, inafanana na sheria kamilifu ya uhuru; pia Paulo anaiita sheria hii kuwa ni sheria ya roho, na sheria ya uzao mpya. (Rum.8:2; Gal. 6:15,16).

Kamwe ukweli hauwi chini vitisho; ujinga na upinzani haviwezi kuufuta ukweli. “Maana hatuwezi kutenda neno lolote kinyume cha kweli, bali kwa ajili ya kweli!” (2Kor.13:8; Rum.3:3,4). Kukata tamaa, kuvunjwa moyo, kuvutwa kifikira, uzoefu binafsi, au shauri la mtu mwingine, haviwezi kamwe kukushawishi kinyume cha ukweli! Hakuna haja ya kujifanya au kulikasirikia neno la Mungu ili kulibana shauri la Mungu kulichanganya kama ilivyo kwa wengine, ili kumfanya Mungu akubaliane na mtu kuhusu kushindwa kwake. Ujuzi wa kibinadamu sio kipimo cha ukweli. ”Pamoja na maelezo wazi ya ukweli, Naishuhudia dhamiri ya kila mtu.” (Neno la Kiyunani la dhamiri ni, suneidesis, ni kuona kwa pamoja), na Kristo kama onyesho la kioo la utambulisho wa kweli wa mtu, kuitaka dhamiri ya mtu, ni kwa ulimwengu wote.” (2Kor.3:18; 4:2). Paulo anaelewa kuwa watu wote wana asili ya kuwa na dhamiri; anatazamia mwitikio wao wa kupendeza kwa matakwa ya ukweli.

Mafundisho ya imani nyingi za watu, yamejengwa juu maandiko yasiyojitosheleza, yakiwa nje ya mtirirko wa habari ya kazi ya Mungu ya ukombozi kama ilivyofunuliwa katika Kristo. Kila

129

Page 130: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

wazo linalozitenga habari njema za mambo aliyoyafanya Mungu kwa niaba ya wanadamu katika Kristo, basi halifai, bila kujali ni maandiko mangapi yanaweza kunukuliwa. Ukombozi ndio mazingira ya maandiko, wala sio historia yake, au matengenezo ya kidesturi. Tafsiri nyingi kwa miaka mingi zimefanyizwa kuonyesha shauri la wanadamu na tafsiri ya kimapokeo, kuliko ukweli wa ukombozi kamili kutoka dhambini na urejesho wa mfano wa Mungu.

Hali ya mtu ya hatia na kupungukiwa vimeenezwa, vibaya sana kupitia taasisi za kidini kwa miaka mingi. Mahekalu mengi sana ya Kikatholiki yaliyo ya zamani, yanashuhudia ukweli wa jambo hili. Uuzaji wa vibali vya ruhusa vilivyoitwa, “indulgence” viliingiza mapato mengi kama miradi katika majengo hayo. Hiki kilikuwa kipande cha karatasi kilichotolewa kwa niaba ya Papa, au Askofu wa eneo kwa mamlaka ya kanisa, chenye ahadi zilizoandikwa ili kupunguza muda wa kukaa toharani! Uongo huu uliwapa watu uhuru kwa fedha kuendelea kuendekeza kila aina ya tamaa ya dhambi bila kupata hatia, kwa kuwa alinunua kiasi cha kuachiliwa kwake mwenyewe pamoja na ndugu zake waliofariki. Hofu ya kukuza na kuuza ilikuwa ndio mkazo wa kanisa, hasa wakati watu wengi walikuwa hawawezi kuisoma Biblia ambayo ilikuwa imeandikwa katika lugha ambazo hakuna aliyezijua, bali viongozi wa kanisa ndio walizielewa. Inapofikia kwenye hatia, mashaka na hofu ya wakati ujao, daima mwanadamu amekuwa mjinga kwa ajili ya hukumu; si ajabu majengo makubwa na marefu siku za zamani yalikuwa makanisa au mahekalu; na katika kila mji wa kisasa siku hizi, ni majengo ya makampuni ya bima; na bado yanaendelea kuuza mazao yale yale, yaani hofu. Miongoni mwa makanisa ya kiprotestanti, ujumbe wa dhambi, jehanamu na hukumu ya milele, umekuwa ndio mtindo maarufu wa kuwashawishi watu kufanya maamuzi kwa ajili ya Kristo. Daima inanishangaza mimi jinsi ambavyo watu wenye akili wawezavyo kudhania juu ya uhusiano wenye maana kujengwa juu ya hofu na dhana ya kushindwa, unyonge na hatia. Kwa namna fulani, msisitizo juu ya kosa la Adamu na tamko la dhambi za mwanadamu, unaonekana kuwa ndio mchanganyiko mkubwa wa “habari

130

Page 131: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

njema.” Wakati Injili ya kweli inafunua kwamba kipawa huru cha Mungu cha neema katika Kristo, kilifuta nguvu na maana ya dhambi. Yesu alisema, “Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; BALI MIMI NALIKUJA ILI WAWE NA UZIMA, KISHA WAWE NAO TELE.” (Yoh.10:10).

Katika Kristo, Mungu hufunua thamani ya kweli ya mtu. “Amenionya nisimwite mtu yeyote kuwa mchafu na najisi!” (Mdo 10:15,28; 1Yoh.5:9-11; 2Kor.5:16).

Kutokuamini kunamjaza mtu ujinga na ufahamu mbaya na kumfanya mtu anaswe akilini mwake kwa mashauri ya unyonge kuhusiana na yeye mwenyewe. Ujinga wa mtu haubadili ukweli wa kwamba wanadamu wanajumlishwa na kusamehewa sawasawa mbele ya macho ya Mungu; hata hivyo upinzani wa mtu kwa neno la kweli, kwamba ni kwa sababu ya ujinga au ni ugumu wa kichwa chake mwenyewe na moyo wake, vinamwibia ile hali ya kufurahia upendo wa Mungu, uzima uliojaa nuru. “Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita; maana yeye asiyekuwa na hayo ni kipofu, hawezi kuona vitu vilivyo mbali.” (2Pet.1:3,9). Kutokuona kitu fulani , si kwamba kile kitu hakipo! Ufahamu unapoamshwa unakuwa sawa na kugundua.

Picha na maandishi vinabaki katika busara iliyo juu ya sarafu iliyopotea, haiwezi kamwe kupoteza utambulisho wake wa kweli au thamani yake. (Mak.12:15-17; Mdo 17:27-29). Kama ilivyo katika sarafu, picha na jina la Mungu vimechorwa ndani ya kila mtu; utambulisho wa kweli wa mtu ulitunzwa ndani ya Kristo, ijapokuwa kulikuwa na anguko la Adamu. Asili ya mkanda inatunza asili ya picha; hivyo Yesu ndiye chapa ya kweli ya asili ya mtu.

Watu hunena Mwana wa Adamu kuwa ni nani? Mwana wa Adamu ni Mwana wa Mungu. (Math.16:13-18). Swali linaonyesha fumbo lililomo katika utume wa Kristo; anatoa ufafanuzi sahihi wa asili ya kweli ya mtu na utambulisho wa kiroho. Katika kumwona mbali na mawazo maarufu yanayotokana na mtazamo wa kibinadamu tu, tunagundua uso wa uzao wetu kama katika kioo! (2Kor.5:16; Yak.1:18,23). Simoni, mwana Yona,

131

Page 132: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

wewe ni Petro (Mwamba) mwana wa Petra (Mungu, Mwamba mkuu aliyekuzaa, Kumb.32:18). Katika lugha ya kompyuta za kisasa, Mwamba unafanana na Mwendo Mgumu, akiba ya kumbukumbu za kudumu. Juu ya Mwamba huu, nitalijenga kanisa langu (ekklesia) Kanisa ni neno lililobuniwa na watafasiri wa Biblia ya King James! Hakuna ambacho kinaelezwa na neno kwa kumbukumbu za desturi zetu zinazofahamika, kimeendelea kuwa na mazingira ya maana ya kweli ile ile. Ni maneno mawili ya Kiyunani yanaunda neno la ekklesia: ek, ni utangulizi unaotoa asili; na neno, kaleo, lenye maana, kualika kwa sauti kuu, au kumpa mtu jina, au kumtambua mtu kwa jina, kumsalimu mtu kwa jina. Hii ni sawa kabisa na Yesu alivyofanya; alifunua asili ya mtu ya kweli (Mwana wa Mungu), na kumpa Simoni jina jipya! Ni juu ya ufunuo wa utambulisho wa kweli wa mtu, ambapo Yesu analijenga kanisa (ekklesia) lake. Hili si jengo au shirika lililojengwa kwa mikono ya watu, bali ni mawe yaliyo hai yaliyofunuliwa pamoja na kuwa makao ya Mungu duniani. “Ambaye kwa jina lake ubaba wote wa mbinguni na duniani unaitwa.” (Ef.3:15; Mal.2:10,15; Isa.51:1). “Tunapata asili yetu kutoka kwake” (1Kor.1:30; Tafsiri ya Knox). “Maana yeye atakasaye na hao wanaotakaswa wote pia watoka kwa mmoja. Kwa ajili hii haoni haya kuwaita ndugu zake.” (Ebr.2:11,12). “Maana sisi sote tu wazao wake.” (Mdo 17:28). Yesu ni zaidi ya kuwa Myahudi. (Yoh.4:9,10). Yeye ni kipawa cha Mungu kinachoamsha chemchemi ya uzima (asili) ndani ya kila mtu. “Naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.” (Kol.1:15). Vitu vyote asili yao ya kweli imo ndani yake. (Yoh.1:3). “Tukimtazama kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano wake.” (2Kor.3:18).

“Lakini Mungu aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, alipoona vema kumdhihirisha Mwanawe ndani yangu , ili niwahubiri mataifa habari zake!” (Gal.1:15,16). Tafsiri nyingi zinasema kwamba, Kristo lazima ahubiriwe kwa mataifa. Kuna tofauti kubwa kati ya kuwasilisha wazo la kigeni na kufunua sauti inayofahamika ya Kristo ndani yako, kutazamia utukufu ambao daima umekuwa na maana kwako (tumaini la utukufu). Ufunuo huu unapindua dhana ya uinjilisti! “Hata imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awaye yote kwa jinsi ya mwili!” (2Kor.5:14,16). Uzao wa kiungwana wa Paulo katika hali ya mwili, hauleti maana yoyote ya zaidi! (Filipi 3:3-9). “Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke; maana ninyi nyote mmekuwa

132

Page 133: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

mmoja katika Kristo!” (Gal.3:28). Ni wakati wa vifaranga vya bata kujitambua vyenyewe katika ukweli wa kioo!

Ekklesia ni mwitikio wa sauti ambayo inatangaza asili na utambulisho wa kweli wa mtu. Maisha ya mwamini ni barua iliyo hai inayoitaka kila dhamiri ya mtu; kujulikana na kusomwa na watu wote. (2Kor.3:2,3; 4:2). “Nalipewa neema hii ya kuwahubiri mataifa utajiri wake, kuwaangaza watu wote wajue habari za madaraka ya siri hiyo, ambayo tangu zamani zote ilisitirika katika Mungu aliyeviumba vitu vyote; ili sasa, kwa njia ya kanisa (ekklesia) hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho. Kwa kadiri ya kusudi la milele alilolikusudia katika Kristo Yesu.” (Ef.3:8-11). Hatupaswi kuishi tena chini ya utawala wa asili ya dhambi, wala kuambiana uongo kwa njia ya madanganyo, bali kwa kufanywa upya kabisa, sawasawa na mfano wake yeye aliyetuumba.” (Kol.3:9-11).

MKAKATI WA MUNGU – ASIA NDANI YA MTU MMOJA

“Nisalimieni Epaineto, mpenzi wangu aliye malimbuko ya Asia kwa Kristo.” (Rum.16:5). Mungu huwaona watu wengi katika mmoja. Anamwambia Abrahamu, “Katika wewe mataifa yote watabarikiwa!” (Gal.3:8,9). Yeye ni Mungu ayatajaye yale yasiyokuwako (kwa sababu bado hayajatokea) kana kwamba yamekwishakuwako (kwa sababu yapo!) ‘Rum.4:17’ Torati ilifunua jinsi watu wengi walivyounganishwa katika Adamu; lakini sasa kwa matokeo makubwa zaidi, Injili inawafunulia watu wale wale walio wengi ambao walikuwa wamehukumiwa katika Adamu, sasa wameunganishwa katika tendo la mtu mmoja la haki. “ (Rum.5:15-19). “Miisho yote ya dunia imeuona wokovu wa Mungu wetu.” (Zab.98:1-3). “Miisho yote ya dunia itakumbuka, na watu watamrejea Bwana; jamaa zote za mataifa watamsujudia; wazao wake watamtumikia, zitasimliwa habari za Bwana kwa kizazi kitakachokuja. Nao watawahubiri watakaozaliwa haki yake, ya kwamba ndiye aliyeyafanya.” (Zab.22:27,30,31).

133

Page 134: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Nabii Habakuki anaiona imani ipatikanayo kwa imani; mwanadamu akiwa amekumbatiwa na kurejeshwa kabisa katika wema wakiwa bila hatia, kwa sababu ya utendaji wa Mungu. (Jina la Habakuki lina maana ya aliyekumbatiwa). Maono haya yalitakiwa kuenezwa kwa usahihi mkubwa na uwazi ili kwamba asomaye asome kwa haraka. Kwa maana dunia itajazwa maarifa ya utukufu wa Bwana, kama maji yaifunikavyo bahari. (Hab.2:2,4,14). Hitilafu mbaya sana haiwezi kubatilisha shauku na furaha ambayo inaletwa na kujua kweli inayookoa: “Ingawa mtini hautachanua maua, wala mzabibuni hamtakuwa na matunda; Taabu ya mzeituni itakuwa bure, na mashamba hayatatoa chakula. Zizini hamtakuwa na kundi, wala vibandani hamtakuwa na kundi la ng’ombe. (Hii inaonekana kama laana ya Kumb.28!) Lakini kwa sababu ya kile kinachofunuliwa na haki ipatikanayo kwa imani, badala ya hatia na kukata tamaa, anasema, Walakini nitamfurahia Bwana, nitamshangilia Mungu wa wokovu wangu. Yehova, aliye Bwana, ni nguvu zangu; yeye huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu, naye ataniendesha katika mahali pangu palipoinuka!” (Hab.3:17-19; Yak.1:2-4).

“Kwa kadiri ninavyolifikiria, ndivyo kadiri ninavyofikia hitimisho kukaa juu yangu, kwamba jambo kubwa ambalo nafsi ya mtu hufanya katika ulimwengu huu ni kuona jambo, na halafu kueleza linaonekanaje katika njia ya wazi.” (Na Ruskin, miaka ya 1800).

“Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili aisomaye aisome kama maji!” (Hab.2:2). “Kwa hayo, myasomapo, mtaweza kutambua ufahamu wangu katika siri yake Kristo.” (Ef.3:4). “Yafahamu sana hayo nisemayo, kwa maana Bwana atakupa akili katika mambo yote.” (2Tim.2:7). “Nayo twayasema, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, (hekima sio mwalimu wa kweli) bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri (kuunganisha) mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni.” (1Kor.2:13). “Paulo, kwa vile alivyonena, kundi kubwa la watu waliamini.” (Mdo 14:1). “Basi imani (ushawishi) chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa

134

Page 135: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

neno la Kristo.” (Rum.10:17). “Lakini kwa kuwa tuna roho ile ile ya imani; kama ilivyoandikwa, Naliamini, na kwa sababu hiyo nalinena; sisi nasi twaamini, na kwa sababu hiyo twanena!” (2Kor.4:13).

“Watu wale waliokwenda katika giza, wameona nuru kuu; Wale waliokaa katika nchi ya uvuli wa mauti, nuru imewaangaza. Umeliongeza taifa, umezidisha furaha yao; wanafurahi mbele zako, kama furaha ya wakati wa mavuno, kama watu wafurahivyo wagawanyapo nyara. Kwa maana umeivunja nira ya mzigo wake, na gongo la bega lake, na fimbo yake yeye aliyemwonea, kama katika siku ya Midiani. (Mungu alipotenda ushindi mkubwa kupitia Gideoni, bila silaha yoyote, bali tarumbeta tu na mienge ndani ya mitungi tupu, katika siku ambayo walihesabiwa kwa namna ya kipekee). “Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume; na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwanye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani. Maongeo ya enzi yake na amani hayatakuwa na mwisho kamwe. Wivu wa Bwana wa majeshi ndio utakaotenda hayo.” (Isa.9:2-4,6,7). Wivu wa Bwana ni tofauti kabisa na wivu kwa ajili ya Bwana.

Wivu wa Bwana unasukumwa na ufunuo wa haki ipatikanayo kwa imani. (Hab.2:2,4; Rum.10:2,3). “Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako.” (Zab.2:8). Miisho ya pembe za dunia itashuhudia wokovu ambao Mungu ameuleta. (Isa.42:6,7; 52:7-10; 60:1-3,21,22; 61:1,2). Milango ya kuzimu haitaweza kuuzuia ufunuo wa utambulisho wa mtu. (ha+ideis, kutokuona, ujinga wa kiroho). ‘Math.16:13-18.’ Kama jiografia ingekuwa kipimo cha ukuu wa wokovu, ndipo miisho ya dunia ingekuwa ndio mwisho pekee. Upana, urefu, kimo na kina cha upendo wa Kristo, upitao akili, unamtaka kila mtu aunganishwe katika kundi la Mungu. Injili hii ni fungu la kila mmoja. “Tazama, tunawaletea habari njema ya furaha kuu, itakayokuwa kwa watu wote” (Luka 2:10,14). Hitimisho la habari njema ni kuupata ulimwengu. “Ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya

135

Page 136: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

duniani na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa Yesu Kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.” (Filipi 2:10,11).

Watu wote walifanyika kuwa wenye dhambi zaidi kupitia anguko la mtu mmoja, Adamu; hawakulielewa jambo hili mpaka pale torati ilipolifunua. Lakini watu wote walifanyika kuwa wenye haki zaidi kupitia kifo cha mtu mmoja na ufufuo wake; lakini bado watu hawaelewi mpaka pale Injili inapofunua. (Rum.5:12,13; 7:7,13). Utambuzi huu unachochea bidii na shurutisho la kutaka kumuunganisha mtu mwingine katika maisha haya yenye mwungano na Mungu! (Ef.3:9; 2Kor.5:14-21). “Maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia.” (Mdo 4:20). Kutangaza habari njema kunaleta maana ya maisha. “Lakini imo roho ndani ya mwanadamu, na pumzi za Mwenyezi huwapa akili. Kwa kuwa nimejaa maneno; roho iliyo ndani yangu hunihimiza. Tazama, tumbo langu ni kama divai iliyozibwa; kama viriba vipya li karibu na kupasuka. Nitanena, ili nipate kutulia.” (Ayu.32:6-8,18-20). “Moyo wangu ukawa moto ndani yangu, na katika kuwaza kwangu moto ukawaka; nalisema kwa ulimi wangu!” (Zab.39:3). “Je, mioyo yetu haikuwaka ndani yetu hapo alipokuwa akisema nasi njiani, na kutufunulia maandiko?” (Luka 24:32).

“Hilo tuliloliona na kulisikia , twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi; na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana, ili furaha yetu itimizwe! (1Yoh.1:3). Paulo anaongea juu ya nguvu za ndani ambazo zinamchochea kwa nguvu na shauku na bidii ya kumshawishi kila mtu kikamilifu katika ufunuo wa siri ya Mungu. (Kol.1:24-29). Ufunuo wa neema unahimiza moto ndani! (1Kor.15:10). Imani inapata uvuvio wake katika kuujua ufunuo; Paulo anasema kuwa, siri ya huduma yake haipo katika maneno ya hekima, au maneno ya ushawishi, bali ufahamu wa imani. (2Kor.4:13; 11:6; 5:14; Ef.3:4; 1Kor.2:1-5). Huduma ya Paulo ilikuwa ni ya juu sana zaidi ya kuwa na uchaguzi wa maisha mazuri tu; alikuwa mtu aliyetembea katika dhamiri ya ukamilifu wa furaha, kwa sababu ya yale aliyoyajua kuwa ni ya kweli, katikati ya upinzani. (2Kor.11:23-30; Filipi 4:11,12).

136

Page 137: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Maisha ya muda yalitengeneza mambo ya mbele, na kupungukiwa hakukumtisha katika uhakika mkubwa wa upendo wa Mungu aliokuwa nao. (Rum.8:37-39). Alihisi kuhimizwa na kuwiwa ili kuwashawishi watu wote, Wayunani waliosoma, sawasawa na wasiosoma kuhusu kujumlishwa kwa wingi wao katika Kristo. (Rum.1:5,14,15).

Alifanya kazi kwa mikono yake mwenyewe, bila kuwatwisha mzigo wowote watu aliowahudumia, hata hivyo hakupata kujulikana kuwa Paulo alikuwa mshonaji wa mahema, hata utume wake hakikuwa cheo rasimi, walakini kielelezo cha juhudi yake; alisukumwa na neno kuwaonya watu wote wapate waone. (Mdo 18:3,5; 20:33; 1Thes.2:7-9; 1Thes.4:11,12; 2Thes.3:6-13). Kwake maisha katika mwili yalimaanisha matunda ya kazi; chochote kilichotokea kwake, kilitumika tu kuieneza Injili. (Filipi 1:12,21-25). Hakuna hata kifungo kilichoweza kumshusha au kufadhaisha maono yake; aliendelea kuona kwamba neno kuwa halifungwi katika mazingira yake. (2Tim.2:9). Alihakikisha kuwa huduma yake kamwe haiwi bila matunda au kuwa ya bure; wala hakuwa kama mpiga ngumi asiye na shabaha apigaye hewa. (1Kor.9:26 na sura ya 15:58). Alielewa thamani ya mtu, na alijua kuwa ufunguo wa kuwafikia watu wengine ulikuwa katika kumfikia mtu mmoja. (2Kor.5:16; 10:12-16; 2Tim.2:2).

Yesu hakumshusha mtu kamwe, bila kujali sifa zao; anafika mji wa Sikari kwa kupitia mwanamke mmoja. (Yoh.4:40-42). Katika Marko 5:19,20; anaona miji kumi katika ushuhuda wa mtu mmoja! (Dekapoli = miji kumi). Filipo anaongozwa na Roho katika njia ya pekee, kumtambulisha Mwithiopia mmoja kwa Kristo; kuna bara zima katika mtu mmoja! (Mdo 8:26-40). Mungu anahutubia mkutano ndani ya mtu mmoja ambaye anaunganishwa na mataifa; anawaona wanadamu katika mtu mmoja! (Zab.2:7,8).

Paulo hakuongozwa kwa milango wazi, bali kwa kujua kuwa Mungu anatuongoza daima katika ushindi, na kwa kupitia sisi, anaeneza harufu ya kumjua yeye kila mahali. (2Kor.2:12-14). Mungu aliona mambo mengi zaidi ndani ya Gideoni kuliko Gideoni alivyojiona mwenyewe. Kabla ya kukutana na neno la Bwana, maisha yake yalishushwa kufikia kujisalimisha tu. (Waam.6:11,12,14-16).

137

Page 138: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Mungu analiangalia neno lake ili alitimize (Yer.1:5-12). Yeremia anaona ufito wa mlozi; jina la kiebrania kwa mlozi, lina maana ya mti ulioamka; kwa kuwa ndio mti wa kwanza kuchanua na kuzaa matunda wakati miti mingine yote bado inalala! “Hamsemi ninyi, bado miezi minne, ndipo yaja mavuno? Tazama, mimi nawaambieni, inueni macho yenu myatazame mashamba, ya kuwa yamekwisha kuwa meupe, tayari kwa mavuno. Mimi naliwatuma myavune yale msiyoyataabikia; wengine walitaabika, nanyi mmeingia katika taabu yao.” (Yoh.4:35,38). “Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye alitupa huduma ya upatanisho; yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake. Nasi tukitenda kazi pamoja naye, twawasihi msiipokee neema ya Mungu bure! Tazama, wakati uliokubalika ndio sasa; tazama, siku ya wokovu ndio sasa!” (2Kor.5:18-20; 6:1). Haki kwa njia ya imani inasema, “Mungu amelitenda; kwa Mungu, mmepata kuwa katika Kristo; amelitenda, tunaingia katika kazi yake iliyokwisha kukamilika, tunaingia katika raha yake (mazao ya kazi yake) mahali tunapoacha kazi zetu! Leo, kama mtaisikia sauti yake, msifanye migumu mioyo yenu. (Ebr.4:2,7,10; Isa.26:12).

Watu wasio na elimu na wa kawaida waliupindua ulimwengu. (Mdo 1:5-8; 4:13; 5:5-7,26,27,40; 10:1,5,28; 17:6; 1Kor.1:26-31; Ebr.12:1-3). “Kisha zinasalia nchi nyingi sana ambazo bado kumilikiwa!” (Yosh.13:1). Asia yote ilisikia neno katika muda wa miaka miwili, yakiwa ni matokeo ya huduma iliyokusudiwa kutoka katika shule moja! (Mdo 19:8-11). “Panda juu ya mlima mrefu wewe uhubiriye habari njema; paza sauti yako kwa nguvu!” (Isa.40:9). Hebu fikiria juu ya lugha ya malaika akirudi kutoka uwanja wa vita na habari njema za ushindi! “Jinsi ilivyo mizuri juu ya milima miguu yake aletaye habari njema, aitangazaye amani, aletaye habari njema ya mambo mema, yeye autangazaye wokovu!” (Isa.52:7).

HITIMISHO

138

Page 139: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Anza kuishi maisha ya Mungu anayofikiria kwa ajili yako. Tumeumbwa ili kuishi kwa kudhihirisha mashauri ya Mungu, “Kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.” (Math.4:4).

“Katika hali ya kawaida ya mwili, hatumiliki kitu chochote, bali wakati; ung’arishe kama kito cha thamani.” (Na E.Goudge). Kuthamini kunaung’arisha wakati na kuleta mng’ao wa kila uzuri uliofichika. Ndani ya wakati, kuna nguvu isiyoonekana ambayo inaweza ama kukudhuru au kukubariki. Palilia tabia ya kushikilia uzuri. Nyakati huhifadhi uwezo katika kumbukumbu. Jifunze jinsi ya kutumia nguvu ya lazima. Kuthamini, kufurahia na kupenda kunaonyesha wema na thamani; hiki ni kiini cha maisha.

Nuru ya wema wa Mungu iyafukuze mambo yaliyo kinyume na ya kushindwa. Hali ya kushindwa itaharibu mfumo wako na kuidumaza imani yako. Jitie nguvu katika Mungu. Mawasiliano ya imani yako yatainua ufahamu wa mema yote yaliyo ndani yako katika Kristo Yesu. (Filem.6).

“Zitambue nyakati za mpenyo na ushindi. Yakumbuke matukio ya furaha. Kumbuka ulinzi wake na matayarisho yake. Jikumbushe kinachokufanya ujihisi kuwa kushikwa kabisa na wema wa Mungu na uwepo wake. Kweli halisi za kiroho na za milele, daima huweka mambo ya mwili na muda wake katika uzoefu na matazamio.

Jizungushie shukurani; hali hii itasababisha kujihurumia mwenyewe, hasira, na kukata tamaa visiweze kupata nafasi. Furahia mafanikio ya msalaba. Ukombozi bado una nguvu.

Mungu alimpa Yesu jina lililo juu ya kila jina, mamlaka, nguvu au falme. Sifa yake ya kuokoa na kuponya inapita sifa ya ulevi, athari za madawa ya kulevya, ukimwi, saratani au maradhi yoyote au utumwa, yenye kuua na kuangamiza.

Shikilia ukiri wa imani yako;Mimi ni roho.

139

Page 140: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Nina mwili wa afya. Nimebarikiwa kwa kuwa na akili nzuri. Maisha yanaleta maana yenye nguvu. Ninaamini kuwa Mungu ni ‘Niko ambaye Niko’ Huwapa thawabu wale wamtafutao kwa bidii. Yeye ndiye thawabu yangu kuu, na mimi ni wake.Mfano wake na sura yake vinaonekana ndani yangu. Katika kioo cha roho yangu, ninaona uso wake. Pia ninamwona kila mtu ameunganishwa katika kumbatio lake.Nimezaliwa na yeye. Mimi ni umoja naye.Yeye ndiye asili yangu na Baba yangu wa kweli.Mimi ni uzao wake kweli kweli, mzao wa fikira zake za ndani.Nilikuwa pamoja naye tangu mwanzo.Pia yeye ndiye hitimisho la uzima na hatima yangu ya milele.Kutoka kwake na kwa njia yake na ndani yake vitu vyote vimekuwako.

KUJENGA BILA KUTA Je, mvua ina baba?Au ni nani aliyeyazaa matone ya umande? Je, umeiamuru asubuhi tangu siku zako zilipoanza?Umeyajulisha mapambazuko mahali pake? Je, umeelewa gharama ya dunia?Je, unaelewa asili yake?

Anakujua kwa jina lakoUumbaji wake ndio dai lakeAnatangaza kwa ujasiri, “Nipime”Je, umeupima moyo wako?Je, umeupima ukubwa wa utu wako? Amekuchagua ili auweke utimilifu wa ndoto yake.

Je, umeyaelewa? Yeye yuko nyumbani ndani ya moyo wako; Maskani yamejengwa ndani yako pasipo kuta; Uchukue upendo wangu mpaka mwisho.Uchuke upendo wangu kwa kila mmoja, Zihesabu nyota, uhesabu mchanga,

140

Page 141: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Yapime mataifa mkononi mwangu, Njoo sasa, unipime; Ninatimiza umilele wako. (Na ANTHEA van der Pluym Acts Team, mwaka 19986 – 1990).

Hakuna wazo kubwa linaloweza kushughulisha akili zangu kuliko wazo ambalo mimi ni tunda na kifaa cha wazo la Mungu.

Ninajizoeza na kuonyesha uhalisi wa wema wote – umoja na asili yangu. Hili ni jambo la kushangaza, ndani ya ufahamu wangu juu yako, Inatokea hali ya ghafula ya kuwa mali ya mwingine na kuwa mmoja pamoja nawe.

Ninakuheshimu kwa wema Mwanzilishi wa uzima wangu, Mtawala wa mwisho wangu..

Mungu anazunguka-zunguka juu ya maisha yako Pamoja nakutazamia kwa saburi.

Mungu ni kuhusu maisha yote jinsi yalivyo.Ikiwa Mungu haleti maana, basi hakuna chenye maana. Mtu aliumbwa kwa ajili ya uwepo wa Mungu, wala si kwa kutokuwepo kwake.

Huvishika vitu vyote pamoja kwa neno la nguvu zake. (Ebr.1:3). Ndani yake tunaishi, tunakwenda na kuwa na uhai wetu. Sisi tu wazao wake kweli kweli. [Paulo alimnukuu mwanafalsafa wa Kiyunani, Aratus, katika sura ya Mdo 17].

Mungu sio egemeo zuri la kushikilia wakati fulani tu, bali wakati wote. Yeye ni uzima wako….Kumdharau yeye, ni kujifanya uonekane kama kichekesho.

Mtakatifu Augustine alizaliwa mwaka 354 katika Afrika ya kaskazini alisema, “Na ni nani aliye Mungu bali Mungu wetu, Mungu aliyeziumba mbingu na nchi, na kuwajaza, sababu ya

141

Page 142: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

kuwajaza, ni kwa ajili yake mwenyewe, kuonyesha kwamba aliwaumba.”

Miaka mia sita iliyopita, Dame Julian alisema, “Yeye ni vazi letu anatufunika na kutupepea kwalo, anatukumbatia na kutupatia yote, kwa ajili ya upendo….udumu katika hili na utajua zaidi kama hayo….pasipo mwisho.”

Kamwe usipoteze tumaini. Tumaini linaona mbele. Tumaini linaona mavuno. Tumaini linaelewa wema na saburi, na linauleta wakati kuwa kama rafiki na mwenzi.

Nilisimama katika kiwanja juma lililopita, niliaza kufikiri nini nilichotakiwa kufanya juu ya kiwanja hicho ili niweze kufurahia namna isiyozuiliwa na sharti yoyote iliyofichwa au namna ya utumwa na vyanzo visivyozuilika! Fikiria ni nini angeweza kufanya Muumba mwenye nguvu – Mungu ndani yako na kupitia kwako kama mtu mmoja; angeifurahia njia isiyozuilika katika akili yako, muda, kipaji na mwili!

Fikiri muziki ambao unaoendelea kufa ndani ya zeze moja. Nitumie Bwana.

Sura zifuatazo zimetolewa katika barua ambazo niliwaandikia watu mbalimbali:

TABIA YA ZAMANI – MAWAZO MAPYA

Usiku mmoja niliota ndoto kwamba nilikuwa katika chumba cha mhadhara nikiandika mihutasari ifuatayo: Kumbukumbu ina michanganuo ya aina 3:

Tukio kamili au wazo Mwitikio wangu au ujuzi maalumu wa tukio, na Matokeo chanya au hasi ambayo kumbukumbu

zinaendeleza katika maisha yangu. Tukio haliwezi kukataliwa, ni la kihistoria, liko katika maandishi, lakini matokeo yaliyomo ndani yangu, sasa yanaweza kuwa

142

Page 143: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

changamoto.

Msisimko mkuu sana na furaha katika maisha yangu ni kujua matokeo ya ki-Mungu kutokana na mawazo ambayo Mungu anayavuvia ndani yangu. Hakuna jambo linaloshinda na kunitimizia zaidi kuliko kujua uwepo wake ndani yangu. “Yeye ndiye thawabu yangu kubwa.” Wakati uo huo, ninapigana pamoja na fadhaa za kushughulika na miingiliano ya kukutana na mambo matakatifu. Sio lazima, miingiliano ya watu na mazingira, lakini mara nyingi hasira zangu zilionekana kama kuharibu na kuchafua ufahamu wangu wa ajabu na hisia za upeo. Ninashangazwa kwamba, mtu mmoja anaweza kufurahia zaidi kukutana na Mungu, na ufahamu mkubwa wa uwepo wake na kukaa ndani, halafu baadaye unamkuta akichukizwa na kusumbuliwa na jambo fulani au na mtu fulani. Bado ninaitikia kwa hasira au wasiwasi ninapojua kuwa jambo linaweza kunivunja moyo pale tu ninapoliruhusu. Inaonekana kuwa mimi nimekamatwa na tabia fulani ya upumbavu, hasa ninapohisi kuchoka na kuwa chini ya mkandamizo, inatokea kuwa na mwitikio mkali, na kulichua jambo kwa watu ninaowajali zaidi. Ah!!

“Michanganyiko mitatu ya kumbukumbu” ilinifanya mimi kutambua kuwa akili ya mtu iko sawa na kompyuta, na kuna “mafaili mengi ya kumbukumbu” ambayo bado yana matokeo ya dhamiri katika maisha ya mtu. Ndipo tabia za zamani zinazijaza hizi kumbukumbu na kuleta msukumo wa miitikio mbalimbali ambayo inaweza kumnasa mtu katika wasiwasi na masumbufu. Tabia zinaweza kuwa ni urithi katika ukoo zilizoambukizwa, au matokeo ya maamuzi na vielelezo vya mawazo yaliyoendelezwa kwa muda mrefu. Nina uhakika kwamba njia pekee ya kupambana na tatizo hili kwa ujasiri na mamlaka, ni kufikiria juu ya mambo mawili kutoka katika mapendekezo yote ya kweli za ujuzi wa historia ya mwandadamu:

1 Kama roho iliyo hai, nimeumbwa katika mfano na sura ya Mungu mkamilifu, ananipenda, na hahangaiki kuhusu

143

Page 144: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

mimi. Mfano wake na sura yake vimehifadhiwa ndani ya roho yangu; na kila kitu kinaweza kubadilika.

2 Kifo na ufufuo wa Yesu kwa niaba ya wanadamu ndio ushuhuda wa milele wa kuachiliwa kwa mtu.

Kutafakari juu ya kweli hizi kunaleta ushindi wa haraka. Imani inaamsha na kufungua upendo wa Mungu, na kutuwezesha kujisamehe sisi wenyewe, pamoja na wote waliotukosea. Kila namna ya hatia, kuvunjika moyo, hasira au hata huzuni zimeondolewa kwa ushindi. Ni lazima tuamue kujiona sisi wenyewe tukiwa watu wa pekee sawasawa na shauri la Mungu. “Katika nuru yake tunaona nuru?” Daima nuru inafukuza giza. Akili iliyofanywa upya inashinda nafasi ambayo mara ya kwanza ilijihusisha na kutafuta mambo yasiyofaa.

Kuyashinda matokeo ya kumbukumbu zilizo hasi na tabia mbaya kunakuwa ni ushindi wa kweli wa kushinda kumbukumbu mbaya katika maisha. Mahali pa udhaifu sasa panakuwa ni nguvu; badala ya hofu, hali ya matazamio chanya yanatawala.

Wakati nikiwa kama tai, ninakaa kimya ukingoni mwa genge, mruko wa kwanza unakuwa ni mpya katika akili yangu. Tayari kuna mlipuko pamoja na matazamio kwa ajili ya tukio lingine. Neno la Kiebrania ‘KAWVA’ katika Isaya 40, “….kumngojea Bwana” lina maana ya kujichanganya pamoja. Sasa maisha yanakuwa ya maana. Sio lazima kila mara uzimie kwa mifadhaiko. Kujua siri ya kuruka kama tai kunamfanya mtu awe mtulivu katika hali yoyote. Barua hii ilikuwa ya mazungumzo ya mwisho niliyokuwa nayo na mama yangu kabla hajafa, mwezi Februari, 2003.

KIPUPWE – Tumbo la mwanzo mpya

Nitajitahidi kujifunza kutokana na majira:

144

Page 145: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Huko ni kuruhusu kipupwe kuendelea katika maisha yangu kwa heshima, sio kujutia hasara ya majani. Afadhali kukumbatia nafasi pamoja nguvu ya siri kutoka katika mizizi yangu.

Kisima cha uzima kinachoendelea kuwa ushuhuda usioonekana kwa mabadiliko ya majira yasiyoepukika. Pamoja na mvua ya vuli na mvua ya masika, kwa mara nyingine tena tutasherehekea kwa wimbo wa mavuno.

Katika uwepo wako, hata usiku ni nuru. Ninalikaribisha jangwa. Wakati wa baridi utanikuta nikiwa nimejificha katika furaha yako.

“Akisimama mbele ya meza imara ya mti mvinje, iliyokuwa maalumu kwa saa yake kubwa, moyo wake ulipiga kwa furaha kuu kwa kile alichokiona. Hakuna mwingine aliyekuwa ameona chochote isipokuwa kuchanganyikiwa na mchanganyiko wa mitambo; lakini Isaka aliiona saa yake kama ambavyo ingekuwa. Aliona jambo lililokamilika. Kama wabunifu wote, alijua vema kwamba hisia ngeni za mwondoko ndani ya roho, unafananishwa tu na mwondoko wa kwanza wa mtoto ndani ya tumbo, unaosababisha mhusika kusema labda kwa msisimko, labda kwa kukasirika, labda kwa uchovu, “kuna shairi jipya, picha mpya, ulinganifu mpya wa sauti unakuja, mbingu nisaidie!” Picha iliyokamilika tayari ilikuwa ndani ya akili yake, ilifanyika maono kwa mizani ya mwisho juu ya samaki wa fedha aliyemetameta wakati wa saa 6. Isaka alikuwa na namna ya akili iliyopenda kukusanya vipande vyenye rangi nzuri vya hadithi zilizolala juu ya sakafu ya dunia kwa ajili ya watoto ili waiokote. Kama mtu na fundi stadi alijua kwamba angegusa kimo cha uwepo wake kwa kutengeneza saa hii. Moyo wake ulienda mbio na kengele ziligonga kichwani mwake. Alifunika kitu kipendwacho kwa nguo na kugeuka. Haikuwa rahisi kuiacha ingawa hakukuwa na chochote ndani ya nguo isipokuwa sauti za mapigo ya chuma na baadhi ya matumbawe ya mafuta. (Na E.Goudge, kitabu cha “Saa ya mkuu wa chuo”).

Mungu aligusa kimo cha uwepo wake aliponiumba!“Giza nalo halikufichi kitu, bali usiku huangaza kama mchana; Giza na mwanga kwako ni sawasawa. Maana wewe ndiwe

145

Page 146: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

uliyeniumba mtima wangu, uliniunga tumboni mwa mama yangu. Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, na nafsi yangu yajua sana. Mifupa yangu haikusitirika kwako, nilipoumbwa kwa siri, nilipoungwa kwa ustadi pande za chini za nchi. Macho yako yaliniona kabla sijakamilika. Chuoni mwako ziliandikwa zote pia, siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado. Mungu, fikira zako zina thamani nyingi kwangu; jinsi ilivyo jumla yake! Kama ningezihesabu ni nyingi kuliko mchanga; niamkapo nikali pamoja nawe.” (Zab.139:12-18).

Yafuatayo yametolewa katika barua niliyomwandikia rafiki yangu mpendwa aliyepoteza mume wake katika ajali mbaya:

KUSHUGHULIKA NA HUZUNI

Wakati mwingine ni vigumu sana kwetu kuelewa hasa maumivu ya mtu mwingine na uchungu. Kuna nyakati ambazo ni lazima huzuni iwe changamoto ya mwisho ili kuifikia busara.

Hata hivyo, jeraha zilizo mbaya sana, zitaponyeka tena. Tumeumbwa kwa uwezo wa kushangaza kwa jinsi hii ili kuyashinda majanga katika maisha.

Kifo kinaleta maana ndogo sana, hasa ule mwisho wake na kuwa ghafula ya kutisha. Lakini ni lazima tuamini kuwa, maisha yataleta maana tena, na hali yake ya ajabu itaharibu hofu ya huzuni ya sasa.

Rafiki yangu alivunja mfupa wake wa nyonga katika ajali ya pikipiki, na alilala kwa kufungwa muda wa majuma sita. Jambo la kushangaza kuhusu mwili ni ule udhaifu wake, na bado, wakati uo huo, unaweza kujirudi na kuwa na uwezo wa kujijaza tena. Kwa kweli ni jambo lisiloeleweka.

Katika ajali ya Rick, ilikuwa haiwezekani tena kufanya kazi, kwa sababu mfupa ulivunjika vipande elfu, kwa hiyo kumning’iniza ilikuwa ndilo jawabu pekee. Ninafikiri kwamba wakati fulani akili

146

Page 147: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

zetu zinahitaji sana kuning’inizwa kwa kufungwa kama ilivyokuwa kwa mtu huyu, inaweza kuwa hakuna starehe, lakini kutoa muda na uthabiti, vinaweza kuponya. Katika mchakato wa ‘kuning’iniza’ ndio unafuu wa kujua mahali pa kuponea katika uwepo wake. Ukaribu wake mkuu ndilo fungu lako sasa, naye atakuinua katika matazamio mapya.

Mungu hatazamii kwamba kila mara utatafuta majibu ya haraka kwa maswali magumu, lakini angalau kuingiza wazo ambalo litakurutubisha kwa faraja katika mateso yako yote. Wazo la umoja wetu na Mungu na sisi kwa sisi, ni uvuvio wa jinsi ya ajabu na faraja. Yeye ni chemchemi kuu ndani yako. Vijito vyote vya furaha yako viko ndani yake.

Katika kila jambo la ‘kawaida’ linalotokea kwetu, siku kwa siku, katika mambo mdogo na pia kutoka wakati hata wakati; katika mambo makubwa kama vile kifo na kuzaliwa, huja pamoja, kwa fursa pekee na ya milele ili kumjua Mungu katika njia isiyo ya kawaida!

Ninaamini kuwa Mungu anapenda kujionyesha yeye mwenyewe kuwa ni wa nguvu kwa niaba yako. Nina ujasiri kwamba hali ile ya kutengenezwa kwako na mizizi yako ndani yake, itaendelea kukusimamisha.

Yeye aliyesema, “Nuru iangaze gizani,’ ameangaza ndani ya mioyo yetu!

Mungu yuko tayari kukutia mafuta kwa njia mpya pamoja na hekima ambayo inatoka juu na kulipuka kutoka ndani.

Niliandika yafuatayo katika wakati wa matatizo makubwa kifedha, wakati wa kipupwe cha mwaka 2002:

KUPAMBANA NA MATATIZO KWA UJASIRI

Ujasiri wa imani unavuta chanzo cha nguvu na kuazimia zaidi kuliko changamoto. Ni uhuru wa nguvu wa uwezo wa ndani

147

Page 148: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

unaotiririka kutoka akili zilizozoezwa katika maisha chanya. Akili zilizozoezwa katika mchakato wa vielelezo vya mawazo yanayoendelea pamoja na chapa ya uumbaji wetu kama kwa kioo katika uso wa asili ya kweli ya mtu.

Tumetengenezwa katika mfano mmoja, udhihirisho wa wazo moja. Sahihi ya mwanzilishi wetu na mfano usioonekana, hakuna ulipohifadhiwa vema au kuonyeshwa kuliko ilivyo ndani ya dhamiri zetu. Asili yetu inafuatia hasa fikira ya Mungu. Kila ubunifu huanzia na wazo la asili; mimi ni wazo lake la asili.

Hali hii ya akili humfungua mtu kutenda na kuitikia kwa njia tofauti kabisa katika jambo lililo baya; furaha inatenda kazi. Ni hesabu ya tulivu sana inayoweza kufanywa ili kufikia hitimisho ambalo daima huleta matokeo ya furaha.

Ndani ya wakati, na nafasi, kuna ujuzi unaohusiana na uletaji wa ukweli ulio maana kubwa. Maana iliyo karibu, ndani ya ufahamu wa kila mtu. Ukweli ambao umetambuliwa, unaweza kugeuza kila aina ya nguvu hasi, na kuingia ndani ya msukumo wa nuru inayofukuza giza bila kutumia nguvu. Hakuna ujuzi, mazingira au mtu aliye na uwezo wa kukuondolea sifa, au kukushusha, au kukukwaza, au hata kukuvunja moyo, pasipo kibali chako mwenyewe.

Ujasiri unakuandaa pamoja na mtazamo ambao utavuta ufumbuzi utakaokushangaza!

BARUA KWA WASOMAJI

Mpendwa msomaji ulimwenguni pote;

Pamoja na heshima kubwa katika vyeo vyenu vyenye kuheshimiwa, ninawaletea maandishi haya:

148

Page 149: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Kuwekwa katika cheo cha kufanya maamuzi ambayo yatagusa hata kubadilisha historia ya wanadamu lazima uwe mwenye kicho na heshima.

Wengi wetu tunaamini kuwa kila mtu hufanya sehemu yake ndogo katika mchakato wa maamuzi ya walio wengi, ambayo wanatunukiwa viongozi wa kuwakilisha ndoto zetu katika jamii ambayo hatimaye, katika uundaji wa sehemu moja moja unaonyesha mvuto wetu wa msingi sana.

Heshima yetu ya kila mtu kwa mwenzie imekuwa changamoto, na thamani ya uadilifu wetu iko katika hatari. Ni katika habari hii, napenda kunukuu mawazo haya ya kutatanisha:

“Hakuna mtu awezaye kuishi kwa furaha iwapo anajijali Mwenyewe; yeye ageuzaye kila kitu kwa faida yake.

Mtu lazima aishi kwa ajili ya mtu mwingine, iwapo kuna mtu anapenda kuishi kwa ajili yake mwenyewe. Rafiki wa kweli ni mtu aliye na mwenzi wake duniani pote; Na ambaye ni rafiki kwake mwenyewe, ni rafiki kwa wanadamu wengine pia.” (Na Seneca).

Jambo hili linaonyesha kuwa haiwezekani mtu kuishi maisha yenye maana akiwa mtu mmoja-mmoja bila gharama ya watu wengine.

Haiwezekani kujiheshimu kwa kweli bila kuwa na heshima baina ya mtu na mtu, kwa ndugu yako sawasawa na kwa Muumbaji wako. Amri kuu kuliko zote inabakia kuwa ni “Kumpenda Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote; na kumpenda jirani yako kama nafsi yako.”

Hii itakuwa kazi isiyowezekana bila kuwepo thamani zinazoeleweka. Pia kumpenda adui yako, kwa kweli ni

149

Page 150: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

changamoto ya mwisho chini ya sheria hii. Uwezo wetu wa kuona thamani ndani ya mtu mwingine lazima uthaminiwe, hata kama thamani hizo zimegandishwa na uharibifu, hofu, kuvunjika moyo na chuki.

Roho ya mwanadamu, iliyoangaziwa nuru na kuonekana katika Roho wa Mwumba wetu, inaendelea kuwa ndio nguvu ya utawala dhidi ya uharibifu na aina zote za giza.

Shuku mbaya na chuki zinashindwa na nguvu ya msamaha, uadilifu na urafiki. Hizi ni nguvu za nuru na maisha ambayo hayawezi kudharauliwa kamwe.

Pato kubwa zaidi la mtu ni kupenda na kutoa bila wazo lolote kwa ajili ya pato binafsi. Je, unaweza kufikiri juu ya jamii ambayo mtazamo huu unatawala? Wala hii sio vita inayoweza kutulazimisha zaidi.

Ninaamini kuwa mtazamo mkuu wa elimu yetu lazima uwe “kuvuta kitu kile kinacholala ndani yetu” (Maana halisi ya neno ‘elimisha’) ni zaidi ya “kutia ndani” tu ukubwa wa taarifa.

Akili yetu, kama uwezo wa kichwa, kuhimiza wazo na kuonyesha msisimko kutokana na moja ya vyanzo viwili, hisia au roho. Ufahamu wa roho unakuja kutokea ndani, wakati hisia zetu zinaweza tu kuhusiana na mazingira yetu ya nje. Ufahamu wa roho unajulikana kwa njia ya usikivu wa sauti na imani, (Neno “kuelewa” katika Kiyunani ni neno, sunieimi, lenye maana halisi ya kujua kwa pamoja, kutiririka pamoja kama vijito viwili. Pia neno la dhamiri, suneidesis kutokana na sun oida, lenye mana ya ufahamu au kujua kwa pamoja, au kuakisi).

Upendo, furaha, amani, uvumilivu, upole, utu wema, uadilifu, unyenyekevu na kiasi, si mambo ya kuharibika, wala si misisimko ipoteayo, inayoletwa na matakwa ya mtu. Ni udhihirisho wa nguvu wa nafsi; ni tunda la kujua kwa roho. Ubora wa tabia hizi si thawabu kwa juhudi kubwa na nidhamu miongoni mwetu, wala si “jambo la hewani, madanganyo ya

150

Page 151: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

kutaka kwa kufikiri.” Kwa kweli yanaonyesha asili yetu hasa ya uumbaji. Ni chapa yetu, mfano wa kioo wa asili yetu. Kutazama tu katika dirisha la duka kunamsumbua mtu kwa ndoto za kutaka zaidi ya upeo wa mtu. Walakini, kutazama katika kioo, kunafunua uhalisi wa asili yetu ya kweli, mfano na sura ya Mungu. (2Kor.3:18). Kujitahidi kupata upendo, amani na furaha, n.k. au kumwomba Mungu ili atupe ubora huu kumepoteza nguvu za kidini. Kutambua kwa urahisi kuwepo kwa watu ndani, ndiko kunatuweka huru ili kuwa kama tulivyo.

Hadithi bora ya kifaranga cha bata inafaa sana; kuonekana kwa kioo kunafunua kwamba sisi sote tulikuwa kama ndege. Pia chama cha simba katika filamu iitwayo, “Mfalme simba” inatukumbusha ukweli uo huo. Alipoingia katika bwawa la maji , kuonekana kwake katika maji kulikuwa ni uso wa baba yake. Sawa na alama ya maji katika maandishi ya karatasi, hali yetu ya kweli inabeba chapa halisi ya tabia ya Mungu. Ulinganifu huu wa “alama ya maji” pia unaonekana katika dhana ya mbegu. Kila mbegu hubeba taarifa zote za aina ya kizazi chake.

Kinachochochea mzunguko wa maisha na udhihirisho wa kuonekana kwa aina yake, ndio ulio muhimu. Chemchemi iliyo ndani yetu inafunguliwa wakati tunapotambua asili yetu ya kawaida. Uumbaji wetu kimsingi na kufanyizwa kwetu, asili yake ni kutokana na wazo la kawaida. Kila ubunifu huanzia na wazo la asili. Ndani ya roho zetu, uumbaji wetu wa asili unabaki kuwa mkamilifu. Kila jambo linalohusiana nasi linaweza kutiwa changamoto na kubadilika, hasa katika akili zetu, hali yetu na mazingira yetu.

Kufikiria mfano wa Mungu ndani ya mtu, kunaongeza thamani ya kila mtu inayozidi kipaji chochote, ujuzi au mafanikio. (Au kukatishwa tamaa kwa jambo hilo). Hakuna thawabu iliyo kuu kuliko kutambua utu uliomo ndani ya mtu mwingine. Ni kule kutambua utu wa mtu pekee, ndiko kunakofanana nayo.

“Hakuna wazo wala hisia, hakuna tendo la uzuri au kiungwana, ambalo linampa mtu uwezo; bali anaweza kupata ukamilifu

151

Page 152: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

katika kuwa rahisi, na wa maisha ya kawaida sana.” (Na Maeterlinck).

“Mwanadamu ni sawa na kazi ya sanaa, kwa kadiri inavyofurahiwa, ndivyo kadiri inavyozidi uzuri, ikionyesha kipawa cha upendo, kama mwanga, ikirudisha kwa mtoaji.” (Na Elizabeth Goudge).

Hatimaye, msomaji anaitwa kuwatumikia watu wake. Huduma kubwa zaidi inayoweza kutolewa kwa wanadamu sio kumfanya mtu mmoja awe tegemezi zaidi na zaidi kwa mwingine; wala hata kuwaacha wategemee juu ya upendeleo wa uongozi na miundo ya kijamii wanayojitoa kwayo; bali kuwatia moyo na kumruhusu kila mtu akutane na chemchemi iliyo ndani yake.

Kugundua utajiri huu ulio ndani yetu, ndiko kunamweka mtu kuwa huru na kumtia nguvu mtu kuwa rasilimali na si tegemezi. Ni hili tu litakalovunja vifungo vya umaskini, uchoyo na rushwa. Sharti la kuuchukua utajiri huu na kuwa nao, linabadilishana na ile shauku ya kuwa mshiriki na mwenye kutumika.

Ufahamu wa kujua sisi ni nani hasa, na ukuu unaokaa ndani yetu, ni zaidi ya mapendekezo yoyote ya uongo ya kuwa wapungufu na wahitaji.

Mwanamke pale kisimani alikutana na ufahamu kwamba Yesu alikuwa zaidi ya kuwa Myahudi tu, na kwamba yeye alikuwa zaidi ya kuwa Msamaria tu. Mara moja, alielewa kuwa watu wote wanashiriki asili moja. Chemchemi ya maji ya uzima haikuwa mbali naye, au mbali na upeo wake, bali ilikuwa ndani yake. Hakuna hata ndoa mojawapo ya zile tano zilizotangulia, au hata mapokeo ya dini yake yaliyoweza kutuliza kiu yake. Si kwa sababu alishindwa kukutana na “mume mkamilifu” au walishindwa kutimiza matazamio yake, bali ni kwa sababu ya ukweli kwamba, mwenzi au hata mzunguko wa desturi za kidini, kamwe havikuwa vya kukamilisha maisha yake.

152

Page 153: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Hakuna kitu na hakuna mtu awezaye kufananishwa na utajiri anaoupata mtu wakati anapoitambua asili yake kuwa chemchemi ya uzima. Hapa, habakii mwenzi, wala siasa au uzoefu uliopita wa kulaumu au kushindana nao; ni maisha mapya ya ndani tu, kuyapeleleza, kuyashiriki na kuyafurahia. (Injili ya Yohana sura ya 4).

Ndani ya habari hii, utume wetu katika maisha ni kuwasaidia watu kutambua uadilifu wa uhalisia wao, na thamani ya mtu.

Sisi sote tuko sawa, hata hivyo maisha yanapata udhihirisho wa pekee ndani ya kila mmoja wetu, ambao hakuna mtu awezaye kuukariri tu au kushindana nao.

Matendo makubwa daima hayakai katika njia zetu;Bali kila wakati tunaweza kutenda yaliyo madogo vizuri zaidi;Hayo ni pamoja na upendo mkuu. (Na St Francis de Sales).

Kutoka moyoni mwangu na kuja mioyoni mwenu.

MBALI NA MASHAKA!

Mtu aliyekuwa kiwete tangu kuzaliwa kwake, akikaa katika kusanyiko, siku moja aliposikia maneno yaliteka usikivu wake. Wazo lililoamsha ndani yake kama mvua juu ya udongo mkavu. Uchungu wote, hasira na aibu vilivyomfunga katika kumbukumbu zake za kwanza, vinatiwa changamoto. Sauti mpya, na kwa njia mpya, sauti inayojulikana, inaongea ndani ya moyo wake.

Ghafula, imani iliujaza uso wake; alijiona kujumlishwa katika ujumbe huu wa upendo, wa tumaini na wa nguvu. Mungu wa dunia yote anajidhihirisha kama kiini macho katika mwili wa udhaifu. Kufa kwake msalabani kuliwakomboa wanadamu walioanguka katika utukufu wa asili ya uumbaji wao. Huyu mtu Yesu, ambaye alikuwa amesikia habari mbalimbali kuhusu yeye, anawakilisha kizazi chote cha wanadamu katikia uzima

153

Page 154: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

wake, kifo na ufufuo wa mwujiza! Je, inawezekana kuwa nguvu ya roho yule yule aliyemfufua katika wafu, sasa inaweza kurejesha miguu yake?

“Mtu huyo alimsikia Paulo alipokuwa akinena; ambaye alimkazia macho na kuona ya kuwa ana imani ya kuponywa, akasema kwa sauti kuu, ‘Simama kwa miguu yako sawasawa.’ Akasimama upesi akaenda!” (Mdo 14:8-10).

Imani ni kwa roho yako na hisia zako ni kwa mwili wako. Imani huona na kusema! Paulo alihubiri kwa njia ambayo wengi waliamini. (Mdo 14:1). Chochote kinachokufanya uwe mtumwa wa maisha ya unyonge, kinafichwa kutokana na upendo wa Mungu, ulioonyeshwa katika Kristo kama katika kioo. “Na sisi sote, pamoja na ufahamu mpya, tunajiona katika yeye kama katika kioo; hivyo tunabadilishwa kutoka nia ya unyonge hata kufikia shauri lililofunuliwa la asili yetu ya kweli. ‘2Kor.3:18’ (Kiyunani: doxa, yaani, utukufu, nia au shauri). 2Kor.5:14,16-21.

Mambo yote ya Biblia yanamhusu YESU, na yote ya YESU yanakuhusu WEWE!

UTAMBULISHO WA ROHO

Ni furaha kuu kujua kwa kulingana na ndoto ya upendo Mungu wa milele na kupata ushirika wetu hapo!

Kuwa na uhakika kuhusu lile linaloushawishi moyo wa Mungu, kweli ndio jambo linalodumu ambalo Mungu anapenda kwa ajili ya kila mmoja wetu kutembea na kuishi ndani yake; mahali pa furaha ya Mungu isiyozuilika kwetu, na furaha isiyozuilika kwake, na kila mmoja na mwenzake!

Sisi wenyewe tunaweza kulifikiri shauri la Mungu kuwa ndio anasa yetu ya pekee!

154

Page 155: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Kazi yetu ni kufanya mawazo yake yawe ndio tafakari yetu na kiini cha mazungumzo yetu. “Ili kwamba ushirika wa imani yako ufanye kazi yake, katika ujuzi wa kila kitu chema kilicho kwetu katika Kristo.’ (Filem.6). Ni jambo la utukufu kugundua kwamba mambo yaliyomo katika maandiko sio ya kihistoria au ya kidesturi tu, bali ni ukweli ulio mkubwa zaidi uupasao uwana wetu! (Heb.!:1,2).

Maandiko yote yanakuwa na maana tu katika ufunuo wa Kristo kama utambulisho wetu wa kweli! “Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia.” (Yoh.5:39). Maandiko yanatuelekeza kwa Kristo, na Kristo anatufunulia! (2Kor.3:18). Imani pekee inayostahili kufuatwa, ni imani ya Mungu; Mungu anavyoamini kuhusu sisi kunatustahilisha msimamo usiogawanyika. Imani ya Mungu inaonyeshwa ndani ya mtu; maisha, kifo na ufufuo wa Kristo. Mungu anaamini katika kuunganishwa kwetu ndani yake! “Imani huja kwa kusikia; namna ya kusikia ambako kunaleta ufunuo wa Kristo.” (Rum.10:17; Tafsiri ya RSV, na nakili za kale).

“Mkikaa katika neno langu, (neno lililokuwako tangu mwanzo, neno ambalo ni Mungu, neno lililofanyika mwili na kukaa ndani yetu), mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli; nanyi mtaifahamu kweli, na hiyo kweli itawaweka huru. Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli! (Yoh.8:31,36).

Kulitukuza andiko nje ya mtririko wake wa habari, ni kuukosea ufunuo wa Kristo ndani yako! “Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo. Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu kwa jinsi ya mwili. Yeye peke yake anatupa ukamilifu wetu!! (Kol.2:8-10). Pia soma mistari ya 16-23. Mifano yote na vivuli vya agano la kale, sasa imekuwa badala ya ukweli mkubwa, kiumbe kipya katika Kristo! “ Sisi tu watenda kazi wake, tuliumbwa katika Kristo Yesu.

155

Page 156: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Aliumba ndani ya nafsi yake mtu mpya mmoja! (Ef.2:10,15; Pia soma 2Kor.5:14,16,17).

Kiini cha maandiko yote yanamhusu Mwumbaji wa wanadamu, aliyefunuliwa kama Baba yao wa milele, aliyekomboa sura yake na mfano ndani ya mtu kwa njia ya utii wa mtu mmoja! Kwa matokeo makubwa ya kosa la Adamu, ni ushindi wa kifo cha Kristo na ufufuo uliotambuliwa ndani yetu!  Furaha iliyo kubwa sana ni kufikiri juu ya yale ambayo sasa Mungu anaweza kuwasiliana nasi kwa njia ya maisha yaliyoangazwa kweli, kwa kukaa kwake ndani yetu, hazina ya Mungu ndani ya vyombo vya udongo. Ukweli unastahili kuonekana ndani ya maisha yako, sawasawa na kutukuzwa kwake katika maisha ya Kristo!

“Tunakupa kile tulicho nacho! Kwa jina la Yesu, simama uende!” (Mdo 3:6). Jina lake sio neno la uchawi. (Mdo 19:13). Jina lake linatufunulia utambulisho wetu wa kweli! “Ambaye kwa jina lake ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa.” (Ef.3:15). Petro alitembea katika ujazo wa kujua utambulisho wake wa kweli, (jiwe lililochimbuliwa katika Mwamba, Math.16:18; Isa.51:1); kwamba hata kivuli chake kiliweza kuleta uwepo na nguvu za Mungu! (Mdo 5:15).

TAZAMIA WAKATI UJAO

Katika miaka ijayo, Mungu anapenda kuuonyesha utajiri usiopimika wa neema yake katika wema kwetu ndani ya Kristo Yesu. Nataka kukupa changamoto kuishi maisha yako katika mtazamo kamili wa fikira za Mungu! Anapenda wewe kujijua kama vile siku zote unavyojulikana . Ujione kama ni ndoto yake ya upendo. Fikiria uwezo wako kamili usioonekana ndani yake! Mfikirie yeye na wewe katika mwungano wenye maana isiyo na mwisho.

156

Page 157: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

Mojawapo wa mchanganyiko muhimu sana katika huduma ya Paulo na msukumo wake, ulikuwa ni kuona mbele na uwezo wake wa kuona kwa matazamio ya imani, ukamilisho na kusudi la Injili hii katika maisha ya wengine. Aliona maisha ya wengi yakiguswa na kubadilishwa pamoja na ufunuo wa uzuri wa hii habari njema. Alikuona wewe na mimi! Mchanganyiko uo huo wa Injili, uliomvuvia Paulo kusema yale aliyosema, na kuishi katika furaha aliyotembea ndani yake, ijapokuwa alikutana na ugumu na majanga. Uwezo huu uko ndani yetu ili kuwafikia watu kwa haraka!

Watu wengi watatambua ukweli kuhusu wao wenyewe, na kuelewa uhalisi wa Muumba wao anavyoonyesha upendo wake na maisha katika kuonekana kama kwa kioo cha Kristo ndani yetu.

Maombi yangu ni kuwa na ule mtazamo wa huduma yetu katika neno, maandishi na matendo ambayo yatakuwa mchanganyiko maalumu uliofunuliwa katika maneno yaliyo hai, yakiandikwa katika akili na mioyo ya watu wa kawaida, na kujulikana na kusomwa na watu wote. Maisha ambayo alituumbia sisi, na kuyakusudia kwa viumbe vyake ili vifurahie na kushiriki ndani yake, sasa yako ndani ya uwezo wetu, tunapotambua ukweli wa ajabu wa Kristo ulio ndani yetu! “Neno li karibu nawe, katika kinywa chako na katika moyo wako.” Hii ndiyo nuru itakayoyavuta mataifa na wafalme wao na viongozi, kuingia katika mng’ao wa kuangaza kwetu, ukombozi wa kweli wa wanadamu unaonyeshwa katika lugha ambayo inaitaka dhamiri ya kila mtu; lugha ya maisha ya siku kwa siku, yaliyo huru kutokana na chuki, unyonge, shuku mbaya, hukumu au lawama; maisha yaliyojaa nuru, matumaini, furaha, thamani, msamaha, uadilifu na upendo. Haya ndiyo matumaini kwa mataifa; kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu!

“Uwezo wa maana sana na wa kina wa wanadamu sio kiwango cha akili, wala ujuzi wa kiteknolojia au mafanikio, wala si kuonekana na mawasiliano ya kisasa yaliyoendelea, bali ni

157

Page 158: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

uwezo wa kila mtu wa kuelewa na kudhihirisha chapa ya mfano na sura ya Mungu! Mwonekano wako mkubwa sio mvuto wa sura yako au jinsia ya mwili wako, wala umaarufu wako au gari zuri; bali ni utukufu wake, shauri lake likionekana ndani yako! Ushawishi huu unakuwa ndio ufahamu ndani yako, unaoyafanya maisha yako kuwa na mvuto usiopingika! Tunaweza kuwa na uwingi wa kufurahisha mawazo ya Mungu kuhusu sisi, kwa njia ya pekee.” (Mwano sura ya 8).

Mtendee kila mtu unayeshughulika naye, kwa adabu na heshima. Ishi maisha yako kwa juhudi ya moyo na ushawishi! Epuka mabishano na kuwajadili watu wengine kwa namna yoyote, bali ukweli wa maisha yetu ufunuliwe ndani yao.

SHAMBULIO LA LONDON 2005

Barua kwa Tanswell na Portia baada ya shambulio la mabomu:

Ni jambo la furaha na la kutia moyo kuisikia sauti yako ya imani! Ni tamko gani ulilofanya katika barua yako; nina maana, ikiwa tendo la ugaidi linaweza kutetemesha jiji na taifa kwa hofu, itakuwaje kutetemesha jiji na taifa kwa imani?

Ilitokea katika siku za matendo ya waamini; “Na kwa vile walivyonena, watu wengi waliamini.” (Mdo 14:1). “Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri.” (Mdo 4:31). “Maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia.” (Mdo 4:20). “Na neno la Mungu likaenea; na hesabu ya wanafunzi ikazidi sana.” (Mdo 6:7). Shemasi mpya aliyeteulia, Filipo, alishuka mpaka mji wa Samaria, akawahubiri Kristo; na makutano kwa nia moja (Ufunuo wa Kristo kama ukweli umo ndani ya Yesu, akifunua umoja na mwunganiko wa watu wengi) wakasikiliza maneno yale yaliyosemwa na Filipo walipomsikia na kuziona ishara alizokuwa akizifanya. Kwa maana pepo wachafu wakawatoka

158

Page 159: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

wengi waliopagawa nao, wakilia kwa sauti kuu; na watu wengi waliopooza, na viwete, wakaponywa. Ikawa furaha kubwa katika mji ule! ‘Mdo 8:5-8.’ (Kitendo cha ugaidi kiliwajeruhi wengi na wengine kufa, na kulikuwa na hofu kubwa na majonzi ndani ya mji).

Fikiria kuwa umepewa nguvu na Mungu; unafanya kazi ambazo Yesu alizifanya! Ni lini tutakuwa na fedha za kutosha ili kumwalika mwinjilisti mkuu ili aje kutuhubiria katika jumuia yetu?

“Haki ipatikanayo kwa imani yanena hivi, “Usiseme moyoni mwako, Ni nani atakayekwenda mbinguni kumshawishi Mungu ili amtume Yesu mara nyingine tena (angalau hata kwa mkutano wa siku 10 katika mji wangu?). Mambo yanaweza hata kuwa mabaya zaidi kwa sababu tunapoteza ufunuo wetu wa ufufuo, kwa sababu haki ipatikanayo kwa imani pia haisemi, “Ni nani atakayeshuka kwenda kuzimu, huko ni kumleta Kristo kutoka kwa wafu!” Lakini haki ipatikanayo kwa imani yanenaje? Haki kwa imani yanena hivi, “Lile neno li karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako! Ukaribu wa neno katika kinywa chako na katika moyo wako, ni sawa na uwepo wa Kristo duniani; ni sawa na ufunuo wa ufufuo wake kutoka kwa wafu! Haki kwa imani hufunua kwamba tulisulibiwa pamoja naye; tulikufa pamoja naye; pia tulifufuka pamoja naye; na sasa tumeketi pamoja naye katika mkono wa kuume wa Mungu ili kuyashinda mataifa pamoja naye! Wakolosai 3:4 anasema, kila wakati Yesu anajifunua, pia tumefunuliwa pamoja naye! Matendo 3, Petro haombi radhi kwa mtu kiwete kwa kutokuwepo kwa Yesu! Hasemi, “Samahani, ila umemkosa Yesu kama miezi miwili iliyopita, yuko mbinguni sasa, utatakiwa kungojea wakati wa kuja kwake mara ya pili, wakati ambao kutatokea miaka elfu kadhaa tangu sasa! Lakini badala yake alisema, “Tunakupa kile tulicho nacho katika mwungano na jina lake! (Jina lake linafunua utambulisho wetu wa kweli). Tulicho nacho ni pamoja na wewe! Petro anatangaza kwa ujasiri kwamba, katika ufufuo wake kutoka kwa wafu, Mungu aliyarejesha mambo yote kwa mwanadamu, mambo ambayo

159

Page 160: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

manabii wote waliyanena kuhusu siku hizi wakisema, “Mungu akiisha kumfufua mtumishi wake Yesu, alimtuma kwenu ninyi kwanza.” Hapa Yesu amefunuliwa tena katika maisha ya watu wa kawaida wasio na elimu! (Mdo 3).

Fikiri kwamba unamgusa mtu mwingine kwa imani! Fikiri kwamba unageuza huzuni ya mji kuwa furaha! Amka uangaze kwa kuwa nuru yako imekuja! Simama kwa imani na kupaza sauti yako isikike! Panda juu ya mlima mrefu na uinue sauti yako kwa nguvu! “Watu hawa walioupindua ulimwengu wamefika huku nako! (Mdo17:6).

Paulo hakuwahi kuona Injili dhaifu; hakuwahi kufikiria juu ya Injili isiyo na mguso wa maana, ambayo iliwataka watu wachache hapa na pale! Hukuona hitaji kuwa lilipunguzwa kwa watu waliokata tamaa na wapweke, ambao hatimaye hawakuwa na mtu mwingine wa kuwageuza; kwa hiyo walidhani kuwa walimgeukia Yesu kwa kumtendea wema kama ilivyokuwa! Badala ya hayo, utume wa Paulo ulikuwa kuwafanya watu wote waone, na kuwaleta watu wote katika utimilifu wa kimo cha Kristo. Paulo aliona na kutangaza bila kusita wala kutaka radhi kwa ajili ya Injili ambayo ni uweza wa Mungu, ikifunua haki ya Mungu kutoka imani hata imani. (Yeye ni mwenye kuanzisha na mwenye kuikamilisha imani yetu; imani yake inaichochea imani yetu). Alitangaza ukweli wa kuunganishwa kwetu ndani ya Kristo kwa namna ambayo ilikuwa kama kuonekana kwa kioo. (Kwa maelezo yasiyotiwa utaji ya kweli, tunaishuhudia kila dhamiri ya mtu.” (Ef.3:9; Kol.1:28; Rum.1:16,17; 2Kor.3:18; 4:2).

Nilikumbushwa asubuhi ya leo juu ya Warumi 4, "Abrahamu akiiona ahadi ya Mungu, hakusita (diakrino) kwa kutokuamini! (hakuchanganyikiwa katika uamuzi wake, hata baada ya miaka ya upinzani, hakushawishika kufanya maamuzi kufuatana na hali iliyokuwapo, bali kwa kile alichokijua kuwa ni kweli, ndicho kiliendelea kumshawishi). Hii ndio sababu imani yake ilihesabiwa kwake kuwa ni haki.” Lakini maneno haya, “Ilihesabiwa kwake” hayakuandikwa kwa ajili yake peke yake,

160

Page 161: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

bali na kwa ajili yetu pia! Hii inaonekana kama ilivyo katika 2Kor.4:13, “Lakini kwa kuwa tuna roho ile ile ya imani, kama ilivyoandikwa, ‘Naliamini, na kwa sababu hiyo nalinena;’ sisi nasi twaamini, na kwa sababu hiyo twanena, tukijua ya kwamba yeye aliyemfufua Bwana Yesu, atatufufua sisi nasi pamoja na Yesu!” Hapa Paulo alimnukuu Daudi katika Zab. 116. Msitari wa 7, Daudi anaonekana akijisemea mwenyewe, (wewe ni kusanyiko la kwanza la imani!) “Ee nafsi yangu, urudi rahani mwako, kwa kuwa Bwana amekutendea ukarimu” Msitari wa 10, “Naliamini, kwa maana nitasema, (baadhi ya tafsiri zinasema, “Mimi nimeteswa sana” kana kwamba ulikuwa ni ukiri wa Daudi; lakini katika Kiebrania inasema, “Nitaimba kwa sauti kuu!)

Kama ujuavyo imani ya kuwa ni kweli, inapata sauti katika kinywa chako, na nafasi katika moyo wako, ambayo kwa kweli inawakilisha upendo wa ndoto ya Mungu ya milele, na mpango wake kwa wanadamu kama ulivyojulikana katika Kristo, kwa wakati mkamilifu!

Ndugu yangu Hanri alinishirikisha andiko zuri usiku uliopita kutoka Ebr.12:3, “Maana mtafakarini sana yeye aliyestahimili mapingamizi makuu namna hii….” Neno la Kiyunani la kutafakari, ni analogitzomai, lenye maana ya kuendelea, tena na tena, kufikia hitimisho lile lile!

Haki ya imani inaona kitu na ushahidi wa yote tunayoweza kutazamia kuhusu tangazo la Mungu juu yetu, lililofunuliwa, limetambuliwa na kutimizwa katika Kristo kama katika kioo! Tusingoje siku nyingine, wimbi lingine, au ufunuo mwingine, au wazo kubwa; hebu na tufikirie jinsi ya kupepea mwali wa moto ulio ndani yetu, na jinsi ya kuchocheana sisi kwa sisi, na kuamshana sisi kwa sisi kwa njia ya kukumbushana.

“Wivu wa Bwana ndio utakaotenda haya.” (Isa.9:7). Tusichanganye kati ya wivu wa Bwana na wivu kwa ajili ya Bwana. Paulo aliwaambia Wayahudi, “{Kwa maana nawashuhudia kwamba wana juhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si

161

Page 162: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

katika maarifa. Kwa maana wakiwa hawaijui haki ya Mungu, na wakitaka kuithibitisha haki yao wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya Mungu.” (Rum.10:1-3).

Injili inafunua imani ya Mungu, upendo wa Mungu, amani ya Mungu, furaha ya Mungu, haki ya Mungu, na kadhalika; na haya yote yamefunuliwa ndani yetu kama katika kioo! Haiwezekani kuwa na ubora kuliko huu! Mazungumzo yetu yote, kuabudu kwetu, ushirika wetu unakuwa ni udhihirisho wa neno lake la milele, lililofanyika mwili ndani yake ili kwamba lile lililo la kweli ndani yake, liwe la kweli ndani yetu. Ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, yaani ndani ya Mwana wake. Tukiupokea ushuhuda wa wanadamu, ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi! (1Yoh.2:7,8; 5:9,20).

“Basi nikatabiri kama alivyoniamuru; pumzi ikawaingia, wakaishi, wakasimama kwa miguu yao, jeshi kubwa mno!” (Ezek.37:10). “Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha” (1Kor.15:45).

CHUNGUZA TOVUTI YETU! www.mirrorreflection.net Barua pepe: [email protected]

S.L.P. 1428 Hermanus South Africa 7200

(Maandiko yamenukuliwa kutoka Biblia ya: RSV, isipokuwa iwapo imeelezwa vinginevyo, vile vile kama tafsiri huru kutoka maandiko ya asili yaliyotolewa na mwandishi).

Kimetafsiriwa na Mch. Z.E.Mwalusambo

162

Page 163: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

FAHIRISI

Dibaji: uk. 1 1. Nyangumi na mchanga wa Sabi: Uk. 22. Nguvu ya uvutano: Uk. 5 3. Vifaa vya pepo: 8 4. Uelewa wa imani: Uk. 11 5. Kupima uzito wa maneno: Uk. 146. Sheria ya hiari ya moyo: Uk.17 7. Mwanzo: Uk. 218. Kioo, kioo, ukutani: Uk. 29 9. Kufanyika mwili kwa Yesu: Uk. 3310. Mkate wa kila siku: Uk. 43 11. Zaidi ya kisima cha Yakobo: Uk. 51 12. Shinda upinzani: Uk. 5213. Nguvu ya roho: Uk. 58 14. Zaidi ya ununuzi wa dirishani: Uk. 6315. Inuka: Uk. 66 16. Muda wa mwanadamu wa utukufu: Uk. 69 17. Kanisa: Uk.7118. Ninyi ndinyi miungu: Uk. 7519. Sabato: Uk. 7920. Matendo mema: Uk. 8321. Siri imefunuliwa: Uk. 8922. Mapenzi ya mbinguni: Uk. 10723. Mafanikio ya msalaba: Uk. 117 25. Yesu, ufunuo wa utambulisho wa kweli: Uk.124 26 Mkakati wa Mungu- Asia ndani ya mmoja: Uk.132 27 Hitimisho: Uk. 137 28 Tabia za zamani, mawazo mapya: Uk. 141 29 Kipupwe: Uk. 14330 Kushughulika na huzuni: Uk. 145 31 Kupambana na matatizo: Uk.146 32 Barua kwa wasomaji: Uk. 147 33 Mbali na mashaka: Uk. 152 34 Utambulisho wa Roho: Uk. 153

163

Page 164: Swahili Translation GOD BELIEVES in YOU[1]

35 Tazamia wakati ujao: Uk. 155 36 Shambulio la London: Uk. 157

164