39

Ukweli ni Huu - Shia Maktab

  • Upload
    others

  • View
    13

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Ukweli ni Huu - Shia Maktab
Page 2: Ukweli ni Huu - Shia Maktab

ukwelini

huuMwandishi:

Dr. Sheikh Ahmad al-Waaili

Mtarjumi:

Sheikh Abdulmajid Nassir

Kimetolewa na Kuchapishwa na:Bilal Muslim Mission of Tanzania

S.L.P. 20033 Dar es Salaam,Tanzania

Page 3: Ukweli ni Huu - Shia Maktab

Haki za kunakili imehifadhiwa na:Bilal Muslim Mission of Tanzania

ISBN: 9987 620 43 4

Chapa ya Kwanza: Ramadhan 1427 / Octoba 2006

Idadi: Nakala 2,000

Kimetolewa na Kuchapishwa na:BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA

S.L.P 20033DAR ES SALAAM

TANZANIA

Page 4: Ukweli ni Huu - Shia Maktab

YALIYOMO

1. Dibaji . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 12. Uadui na Uzushi Dhidi ya Ushia . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 23. Sababu za Uadui Dhidi ya Mashia . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 54. Baadhi ya Uzushi Unao Nasibishwa kwa Mashia . . . . . . . . . . . . 135. Mfano wa Kwanza: Madai ya Kupotoshwa Qur’ani . . . . . . . . . . 136. Mfano wa Pili: Uzushi wa Kukosea Jibril Kuteremsha Wahyi

kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w.) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 217. Mfano wa Tatu: Kuvuka Mipaka Katika Itikadi ya Maimamu . 28

Page 5: Ukweli ni Huu - Shia Maktab

1

DIBAJI

Tunamshukuru Allah (s.w.t.), na kwa Baraka za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Watukufu wa Ahlul~Bait (a.s.) kwa kutujaalia kuweza kufanikisha juhudi zetu hizi katika kuchapisha kitabu hiki “Ukweli Ni Huu”. Kitabu kilichopo mikononi mwako ni kile ambacho kimeandikwa na Dr. Sheikh Ahmad al-Waaili na kutarjumiwa na Sheikh Abdulmajid Nassir na kusahihiswa na Shiekh Musabbah Shabaan Mapinda. Kwa jitihada zao hizi na nyingine, Mwenyezi Mungu awalipe malipo mema hapa Duniani na kesha huko Akhera.

Sababu iliyoifanya Bilal Muslim Mission isimamie kazi hii ni kama zile za mwanzo. Nia na madhumuni ni kutaka wale watu wazungumzao kiswahili waelewe na kufahamu zaidi itikadi za ki-Shia.

Bilal Muslim Mission inatoa shukurani zake za dhati kwa wale wote ambao kutokana na juhudi zao kitabu hiki kinawafi kia wasomaji wetu mikononi mwao. Vile vile taasisi ya Bilal Muslim Mission inawashukuru wote wanaoiunga mkono kwa njia moja au nyingine katika kazi zake za Tabligh. Tunamuomba Allah (s.w.t.) awalipe malipo mema hapa Duniani na baadaye huko Akhera. Amin

12 Octoba, 2006 Sayyid Murtaza Rizvi Dar es Salaam Bilal Muslim Mission

Page 6: Ukweli ni Huu - Shia Maktab

2

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHMA MWENYE KUREHEMU

UADUI NA UZUSHI DHIDI YA USHIA

Kila mwenye kufuatilia historia ya ummah au kikundi fulani, atakubali ya kuwa hakuna ummah au kikundi kilicho zushiwa mambo kadha wa kadha, au kugeuzwa maana ya mafundisho yake kama ulivyofanyiwa Ushia.

Hakika mashia na ushia wamezushiwa mambo mengi mabaya, pengine wamenasibishiwa na kuhusishwa na mambo ya aibu ambayo hawanayo Wakati mwingine wamenasibishiwa mambo ya watu wengine; na si hivyo tu, bali wamekuwa wakihusishwa na mambo ya maadui zao. Katika kurasa hizi chache tutakutajieni kwa ufupi baadhi ya mifano juu ya mambo hayo.

Ni wengi waliyoelezea na kuandika vitabu kwa marefu na mapana juu ya maudhui hii. Kwa hiyo katika kitabu chetu hiki tutayaelezea hayo kwa kifupi.

Kama ingekuwa malengo ya wale wanao andika kuhusu ushia au itikadi za kishia wanafanya hivyo kwa niya nzuri, au wanafanya hivyo kwa lengo la kutafuta ukweli, yangetosha kwao yale yaliyo andikwa na mashia wenyewe. Au yangetosha majibu waliyojibiwa waulizaji kubainisha ukweli wa itikadi za kishia na hata kubatilisha utata na kuondoa kiza kilicho kusudia kufi cha historia ya mashia na usahihi wa itikadi zao.

Lakini inavyo onekana malengo ya wale wanao andika kuhusu ushia na mashia yako mbali na (lengo la) kutafuta ukweli. Bali kilichopo ni majaribio ya wazi wanayo yafanya ili kufuta na kubadilisha mafundisho na ukweli ulivyo. Pia ni majaribio ya kutaka kuwabana mashia na ushia na kuwatoa katika jengo la uislamu kwa gharama yoyote ile.

Page 7: Ukweli ni Huu - Shia Maktab

3

Pamoja na majaribio yao ya muda mrefu, hawajaweza kufanikiwa. Lakini pamoja na kutofanikiwa kwao bado wanaendeleza juhudi zao kwa nguvu zao zote ili kuona kuwa ushia na mashia wanawatoa ndani ya uislamu.

Baadhi ya jumuia zinasisitizia jambo hili kwa malengo yasiyo dhahiri, na hata wale walio ajiriwa ili kufanya kazi hii pia wanasisitiza bila ya kudhihirisha malengo yao hayo. Hata hao wafanyao kazi hii wamepotezwa kwa kupandikiziwa fi kra potovu dhidi ya ushia, na wakazijenga imani zao ya kuwa ushia sio uislamu. Wakaamini hivyo na kuyajengea dhana nzuri yale waliyopandikiziwa, na wakaendelea kuamini hivyo na kutumikishwa bila kuyafanyia utafi ti mambo hayo.

Na baadhi ya watu waliyo lelewa katika uzushi huo, waliyachukua mambo hayo kama urithi mtukufu; kiasi kwamba inawawia vigumu kutia shaka juu ya mambo hayo ili wasiziudhi dhamira zao za kidini ambazo wamelelewa nazo katika kuwazulia mashia na kuitakidi ya kuwa yanayo nasibishwa kwa mashia ni mambo yasiyo na shaka.

Ni wachache ambao dhamira zao nzuri na kuwa kwao na ghera ya dini yao, imewafanya wahisi hatari na matokeo mabaya katika umma wa kiislam kwa kuenezwa uzushi kama huu. Watu hawa wamezipaza sauti zao juu ya mambo haya na kuwalingania waislamu wawafanyie uadilifu mashia.

Wamefanya juhudi na majaribio ya kusahihisha sifa mbaya walizo pachikwa mashia kinyume cha uislamu mbele ya madhehebu zingine za kiislam.

Majaribio yao yalikuwa ni kuonesha ya kuwa, baadhi ya mambo yanayo nasibishwa kwa mashia hayana uhusiano wowote na ushia na mashia, isipo kuwa ni mambo ya watu fulani au vikundi fulani ambavyo tayari vimekwisha futika (kwa maana hovipo tena katika ulimwengu huu). Pia walijaribu kuonesha kwamba, baadhi ya rai za mashia ni ijitihadi za

Page 8: Ukweli ni Huu - Shia Maktab

4

maulamaa ambao walikosea katika ijitihadi zao na inabidi washauriwe ili waepukane na rai hizo.

Kuna wengine nao waliwalingania waislamu kuyanyamazia mambo hayo na kuongeza mashambulizi yao kwa njia ya taratibu ili kuwafuta (mashia) katika historia. Na kufanya hivyo ni kwa ajili ya kuunganisha na kuhifadhi jengo la uislamu ili lisiharibike.

Pamoja na majaribio yote hayo sijamuona yeyote kati ya hawa aliye fi kiria kurejea na kusoma vitabu walivyo virithi ambavyo vimeandikwa kwa ajili ya kuwashutumu mashia na wakafanya utafi ti juu ya ukweli wa yale yaliyo andikwa ndani ya vitabu hivyo ili waweze kuona usahili wa hayo yaliyo andikwa.

Na ili waone kuwa: Je! Yaliyo andikwa ni kutokana na matakwa ya waandishi na hayana ukweli wowote bali yame vishwa tu sura ya dini au itikadi? Au kuwa, waliyo nayo wao ndani ya vitabu vyao ni ukweli usio na shaka na usio hitaji kufanyiwa mjadala wowote wala utafi ti?

Nime tangulia kusema hapo kabla ya kuwa, ni wachache sana walio toa wito wa kuwafanyia (insaafu) mashia, na sauti zao ziko mbioni kutoweka au kufi fi zwa ndani ya anga hili pana na refu. Na amani yao inakaribia kuyayuka katika mawimbi haya makali yanayotoa wito wa kuuteketeza ushia na mashia na kuwatoa katika uhai kiukamilifu. Yanafanyika hayo wakati ambapo tunawaona ahlu sunna pamoja na madhehebu zao wanakwenda mbio kumvuta angalau mtu mmoja awe katika safu yao. Na wanatoa pesa na juhudi kubwa kufanikisha hilo, lakini wao hao hao wana kwenda mbio na kusisitiza kuwatoa waislamu milioni miatatu walio mashia katika umma wa kiislamu kwa vigezo ambavyo Mwenyezi Mungu hakuviteremshia dalili ndani ya Kitabu (Chake) kitukufu.

Vigezo ni vile ambavyo ikiwa watafi ti watajika lifi sha na wakafanya uchunguzi au utafi ti juu ya ukweli wake au usahihi wake, watagundua

Page 9: Ukweli ni Huu - Shia Maktab

5

yakuwa ni vigezo vilivyo tegemea matakwa yao binafsi, si vigezo vyenye dalili, na kwamba, natija waliyo ipata inatokana na msingi dhaifu. Kama ambavyo hawakuangalia kwa upana na kuona ya kuwa matendo wayafanyayo yatatoa natija mbaya katika umma wa kiislamu.

Kwa ufupi matendo hayo yanawaandalia njia wale wenye kutaka kuwagawa waislamu na kuufarakanisha umma wa kiislam, kwa malengo ya kuzinufaisha nafsi zao, na wenye kutaka kuingiza shaka katika nyoyo za baadhi ya watu ya kuwa uislamu sio dini ya umoja, bali ni dini inayo lingani’a utengano. Na zaidi ya hapo ni kuwa, kwa kufanya hivyo Mwenyezi Mungu atatuepusha na kutunyima rehma zake na tawfi ki yake.

Mwenyezi Mungu anasema: “Wamemsahau Mwenyezi Mungu naye akawasahaulisha nafsi zao.”

SABABU ZA UADUI DHIDI YA MASHIA

Katika kulielezea tatizo hili, tujiulize kama ambavyo wengine wamekuwa wakijiuliza sababu na siri ya kuwa na msimamo dhidi ya mashia na ushia.

Katika kulijibu swali hili, nitaelezea kwa ufupi sababu ambazo zimenidhihirikia, nikitarajia ya kuwa sababu hizi zitatosha kwa kiasi fulani kuonesha kiini cha uadui wanao fanyiwa mashia.

1. Tangu ushia ulipoanza katika zama za Mtume (s.a.w.w.) na baadhi ya watu wakafahamika kuwa ni mashia, na kwa wakati huo walijulikana kwa jina la Shiiatu Ali (yaani wafuasi wa Ali) kwa mfano: Salman, Abu Dhar, Miqdad ibnil-As’wad na Amar bin Yassir na wengineo. Ushia ulianza ukiwa umewajumuisha watu fulani tu, kwani kuanza kwake kulitokana na tathmini ya Mtume (s.a.w.w.) kwa Ali (a.s.).

Page 10: Ukweli ni Huu - Shia Maktab

6

Tathmini hii ya Mtume ilikuwa inalenga kumtofautisha Ali (a.s.) na watu wengine. Mambo haya tuna yashuhudia katika msimamo wa Mtume (s.a.w.w.) kumuelekea Ali (a.s.), na yote hayo yalitokana na mambo mbali mbali aliyo yafanya Ali (a.s.) katika kuutumikia Uislam. Amma kuhusu dalili ni kuwa, kuna aya kati ya sabini hadi mia tatu katika Qur’ani tukufu kama alivyo eleza Abdullah bin Abbas na jamaa wengine ya kuwa aya hizi zinamuelezea Ali (a.s.) peke yake juu ya mambo aliyo yafanya na aya zingine zinamuelezea yeye pamoja na watu wengine. Vitabu vya Asbaab al-Nuzul1, vimebainisha idadi kamili ya aya hizo na kueleza kila aya na muhusika wake. Pia katika hadith za Mtume (s.a.w.w.) kuna dalili nyingi zinazomuhusu Ali (a.s.) na wamezithibitisha wanazuoni wa Hadithi.

Ama misimamo ya Ali (a.s.) katika vitabu vya historia ni mingi sana, kwani kuna matukio mengi ndani ya historia yaliyo fanywa na Ali (a.s.). Matukio ambayo husisimua nyoyo na kushangaza, kiasi kwamba kila mwenye kuyasoma ataungana na Ali (a.s.) kimoyo na kifi kra.

Mambo haya ndio yaliyo wapelekea baadhi ya maswahaba kuwa karibu na Ali (a.s.) na wakawa ni watu wenye kumpenda na wenye kumtukuza kuliko wengine. Na kuna maswahaba wengine wakawa na msimamo wa upinzani, na walijulikana kuwa ni kikundi cha upinzani.

Upinzani huo ulidhihirika zaidi baada ya upande huo wa upinzani kuchukua utawala na kujizatiti kwa kila uwezo dhidi ya Ali (a.s.) kama ambavyo siku zote upande unao tawala hujiimarisha dhidi ya mpinzani wake.

2. Sababu ya pili ni kwamba: Kwa kuwa madeni ya Ali bin Abi Talib (a.s.) yalikuwa ni mazito kutokana na yeye kuzimwaga damu za makuraishi na washirikina, ukianzia vita vidogo hadi vikubwa, vita ambayo vilifi kia thamanini na tatu (83) ukivijumuisha vyote kwa

1 Vitabu vya Asbaab al-Nuzul ni vile vitabu vinavyoelezea sababu za kushuka kwa Aya za Qur’an. Hii ikiwa na maana kwamba, Aya fulani ilishuka kutokana na tukio fulani au baada ya tukio hilo.

Page 11: Ukweli ni Huu - Shia Maktab

7

ujumla, utakuta kuwa, nafasi ya Ali (a.s.) katika vita hivyo ilikuwa ni kubwa zaidi. Kwa mfano, katika tukio la Badri peke yake, nusu ya waliouliwa katika jeshi la washirikina waliuliwa kwa upanga wa Ali (a.s.). Na katika tukio la Uhudi waliyo uliwa na Ali (a.s.) walikuwa ni watu kumi na nane ukiongezea na nyumba za waarabu ambao watu wao aliwajeruhi.

Pamoja na kuwa vita hivi vilikuwa ni vita vya kiislam dhidi ya ukafi ri kiasi kwamba hapakuwa na sababu nyingine iliyopelekea kuwepo kwa vita kati ya Ali (a.s.) na watu hao isipokuwa uislamu, lakini zile damu zilizo mwagwa katika vita hivyo (kumwagika kwake) hakukuhusishwa na uislamu bali moja kwa moja kulihusishwa na Mtume (s.a.w.w.) na familia yake, yaani wao ndio wanaobeba majukumu ya damu hizo.

Na Ali (a.s.) alibebeshwa majukumu hayo baada ya Mtume (s.a.w.w.), na wala jambo hilo halikuishia kwa Ali (a.s.) tu, bali lilizidi kupanuka na kawajumuisha hata wale walio kuwa na mahusiano naye.

Kutokana na sababu hiyo wafuasi wa Ali (a.s.) wakaanza kupata misukosuko ya ulipizaji kisasi uliyo vishwa sura mbalimbali. Damu zao zikamwagwa, wakanyang’anywa haki zao na kuvunjiwa heshima zao, na mwisho waliandamwa na milolongo ya tuhuma na uzushi mwingi dhidi yao.

Tuhuma moja wapo kati ya nyingi walizo tuhumiwa nazo nikuwa mashia si waislam. Na yote hayo yalifanywa na watawala wa kiquraishi ambao utawala wao ulidumu kwa muda mrefu.

Tunaweza kusema kuwa, hiyo ilikuwa ni kazi iliyo fanywa ili kuwaangusha mashia na ni kazi iliyo tokana na wale walio jeruhiwa katika matukio tuliyo yaeleza hapo kabla.

3. Sababu ya tatu inatokana na kuenea nadhariya ya Shia kuhusu utawala na kuwa ni nani mwenye haki ya utawala baada ya Mtume

Page 12: Ukweli ni Huu - Shia Maktab

8

(s.a.w.w.)? Na hapo ikadhihiri hali ya kisiasa katika upande huu na ikajenga mazingira ya mapambano ya fi kra na nadharia katika upande huu.

Waandishi wa pande zote mbili wakaanza kuandika juu ya suala hili na kila upande ukijikusanyia nyenzo na uwezo wa kifi kira. Na katika hali hii yakaanza mapambano kati ya pande hizi mbili: upande mmoja ukijitetea na upande mwingine ukifanya mashambulizi nao ni ule upande uliokuwa kwenye madaraka.

Ama (tukitazama) upande wa raia wenye kutawaliwa, ambao kwa desturi hufuata dini ya watawala wao, tutanaona kuwa huo ndiyo upande wenye nguvu na wenye nyenzo kiasi kwamba haiwezekani kulinganishwa kati ya nyenzo zitumikazo katika pande hizi mbili.

Hapana shaka kwamba miongoni mwa nyenzo zilizotumika ni waandishi walio andaliwa na kupewa majukumu ya kufanya mashambulizi yasiyo na huruma (dhidi ya wapinzani wa tawala zilizokuwa madarakani).

Hayo yalitendeka kiasi kwamba misingi ya uaminifu na maadili ya uandishi katika historia ikavunjwa. Maadili ya uandishi na maneno mazuri pia yalitoweka, na yakabadilishwa yote hayo kuwa ni matusi ambayo hata uislamu kamwe hauyaridhii.

Hali hii iliendelea kiasi ikafi kia mahala pa kuhuzunisha mno, ambapo kila muislamu mwenye ghera na dini yake lazima hali hiyo itamsikitisha. Na matokeo yake ilikuwa ni kukithiri uzushi mwingi dhidi ya mashia. Hali hii iliendelea tokea kipindi hicho hadi leo hii, na hwenda hivi sasa imezidi kuota mizizi inayo onekana kutokana na mambo mawili yanayo toa msukumo ambayo ni mali na chuki. Vitu hivi viwili vimezidi kuwapa msukumo waandishi na kuongeza kuwasha moto kwa kuni zilizo imara ili usiweze kuzimika. Ni Allah peke yake ndiye mwenye uwezo wa kuwakunjulia waislamu rehma Zake na kuwaokowa kutokana na moto huu.

Page 13: Ukweli ni Huu - Shia Maktab

9

4. Sababu ya nne: Ni kule kuwepo kwa imani iliyokita mizizi yake katika ulimwengu wa kiislam ya kuwa utawala wa dola ya kiislamu ulikuwa milki ya Ahli Sunna peke yao. Pia hali za kijografi a na kiitikadi zili saidia kulifanya jambo hili liote mizizi. Hali hii inayo maelezo marefu. Hatuhitaji kuielezea kwa kirefu katika kurasa zetu hizi isipokuwa tunaashiria tu.

Ni jambo lililo wazi ya kuwa utawala unao uwezo wa kukusanya nguvu zote kufanikisha jambo hili, na hivi ndivyo ilivyo fanyika; kwani watawala walitumia hali iliyo kuwepo kiasi wakawatenga mashia na utawala kwa kutumia njia tofauti tofauti.

Hali hiyo ilipelekea kuimarika kwa utawala wa Ahli Sunna na kuwafanyia uadui mashia, uadui ambao ulitokana na wale waliokimbilia madaraka na kuchukuwa utwala kiislamu.

5. Sababu ya tano: Inafahamika wazi jinsi fi kra na fi qhi ya kishia zinavyofungamana na dalili ya Aya au hadithi kiasi cha kupelekea kutobadilisha dalili kwa kuzingatia vigezo vingine. Kama vile kutoifanyisha kazi dalili ya Aya au Hadithi ikiwa itapingana na maslahi. Au kutoifanyisha kazi dalili ikiwa itapingana na rai ya madhehebu. Maana ya maneno haya ni kuwa: Hakuna nafasi kwa mtu yeyote atakaye taka kuibadilisha dalili ya Qur’an au Sunna ili mradi tu iwafi kiane na matakwa yake au maslahi yake.

Wakati ambapo tunaona upande wa pili wakipanua maana ya dalili na kuyafungulia milango maoni yao wanayoyakusudia kuyatekeleza. Yote hayo ni kwa kutaka kuyafanya maoni yao hayo yaingie katika mafh um yao ili tu, waweze kuyafi kia maslahi yao kwa gharama yoyote iwayo, hata kama dini itadhurika.

Kwa hivyo basi, hali ya watu kutozichukua fi kra za ushia kulitokana na sababu hizi ukiongezea na sababu nyingine zilizo changia hali hii. Hawakuishia hapo tu, bali walikwenda mbele zaidi wakajitenga mbali

Page 14: Ukweli ni Huu - Shia Maktab

10

na fi khi ya kishia kwa kuzihujumu fi kra zake, huku wakitoa madai kuwa haziambatani na Qur’ani na Sunna, misingi ambayo haifai kuikiuka. Madai kama haya hayana tofauti na yale mwanzo kwa kuwa nyuma yake kulikuwa na maslahi yanayolengwa, hata kama yame vishwa nguo nyingine na yaka onekana katika sura ile.

Waanzilishi wa fi kra hii potovu waliacha nyuma vitabu vingi vilivyobaki kama urithi uliorithiwa, na ambao ilikuwa si rahisi kuepukana nao. Wafuasi wa urithi huu wakafanya kazi ya kumshambulia kila mwenye kuupinga hata kama ni fatwa inayo ambatana na haki, na kukubaliwa na Waislamu wote.

Hii ni baadhi tu ya mifano na nyenzo mbali mbali zilizopelekea kupatikana hali hii ya kuwazulia mashia na ushia, kwa uzushi mwingi tunaousikia. Na kutokana na haya tuliyo yataja, ilikuwa ni lazima kudhoofi ka harakati za mashia kifi kra na kijamii. Kwani mashambulizi yalikuwa yakiwalenga wao na yalikuwa yakija mfululizo katika zama na hali tofauti.

Vyombo vya habari vimo mikononi mwa maadui zao kama vile magazeti, vitabu, redio, runinga na vinginevyo. Pia mitaala ya masomo ni njia nyingine iliyo tumika na inayotumika kuzishambulia fi kra za ushia na kuziendeleza fi kra za upande wa pili. Vile vile fursa za kujijenga zimefunguliwa kwa wanaobeba fi kra za kisunni, na zimefungwa kwa wale wabebao fi kra za kishia. Bali hata wale wenye kuwafanyia upole mashia hawana fursa hiyo isipokuwa tu kwa mtu mmoja mmoja aliefanya harakati na kuhangaika huku na kule na kufanikiwa kujitengenezea maisha yake kwa juhudi zake chache.

Na lau si Allah kuyahifadhi madhehebu na fi kra za kizazi cha Mtume Muhammad (s.a.w.w.), basi hata hiki kikundi tukionacho kingetoweka na kuangamia.

6. Sababu ya sita: Kwa mfano tuchukulie kwamba msomaji hakuzitilia maanani sababu tulizozitaja hapo kabla, kama vigezo

Page 15: Ukweli ni Huu - Shia Maktab

11

na dalili za hujuma hizi zinazo fanywa siku zote dhidi ya Mashia katika karne zilizo pita, basi itabakia sababu moja tu ifuatayo:

Vikwazo walivyowekewa Mashia tangu siku za mwanzo, ambavyo vilitokana na tawala zilizopita sababu yake ilikuwa ni hali ya kisiasa iliyolenga kuwafuta katika ramani ya ulimwengu kwa kutumia njia ya kuwaondoa Maimamu wao kwenye nafasi ya utawala. Na ilikuwa ni lazima kutengenezwe visingizio kama tulivyo ashiria hapo awali. Na visingizio muhimu ni visingizio vya itikadi na baada ya muda mrefu ukachipukia umma uliolishwa na kulelewa katika hali ya kuwachukia Mashia. Malezi ambayo vyombo vya habari ndivyo vilikuwa vikiyaeneza ili wachukiwe, eti kwa madai kuwa “Mashia wako kinyume na dini ya kiislam.” Umma huu ukawa ukiendelea kuzaliana na kukua na kurithishana mambo haya. Nao ni urithi wa kuitakidi ya kuwa yale mambo yanayo nasibishwa kwa Mashia ni mambo ya kweli wakati ambapo tunayakuta mambo hayo ni upotovu na uzushi usio na ukweli wowote.

Na kwa kuwa watu hawa wanaghera ya dini yao ya kiislamu hali hii (ya uzushi uliozuliwa dhidi ya Mashia) inawafanya wawe na msimamo dhidi ya Mashia hasa ukizingatia kuwa bado kuna waandishi wengi wanaoendelea kuzitumia kalamu zao kuchochea moto huu. Hakuna wanachokikusudia bali lengo lao ni kutaka kuonesha muungano wao na fi kra (ya dhehebu) iliyokuwa ikitawala. Vile vile ni kwa ajili ya ghera ya maslahi yake na nafasi yake ya utawala. Vitu ambavyo huenda vitakuwa mbioni kutoweka na kupotea ikiwa haki itazungumzwa au kurakibishwa hii njia iliyopo vinginevyo huenda watakuwa hatarini ikiwa watawafanyia insafu mashia.

Msimamo wa watu wa Sham (Syria) kwa Imam Nasai hauko mbali na kumbukumbu zetu wakati walipo muuliza kati ya Ali (a.s.) na Muawiya ni yupi bora? Akawajibu: “Ni kwa lipi Muawiya ataweza kuwa sawa sawa na Ali (a.s.), seuze kuwa bora zaidi yake.?” Kutokana na maneno haya ya kufanywa Ali (a.s.) kuwa ni mbora kuliko Muawiya, watu wa Sham (Syria) walimponda ponda Imam Nasai hadi wakamuuwa.

Page 16: Ukweli ni Huu - Shia Maktab

12

Pamoja na yote hayo inabakia amana ya historia na jukumu la uandishi na kauli ya haki vikiwaita wanafi kra na wafuasi halisi wa dini kuidhihirisha haki na kuyaandika mambo kama yalivyo. Na vinawaita katika kuhisi umuhimu wa kulinda maslahi ya umma wa kiislamu na kuinua heshima yake na kuwa na nguvu moja na kulifanya jepesi lile lililo fanywa kuwa zito na kutaka radhi za Allah na maisha mazuri ya Akhera.

Hapana shaka kwamba faida zitokanazo na umoja wa waislamu ikiwa zitathibiti, basi hilo ndilo tumaini la kila nafsi iliyo epukana na machafu ya ubaguzi na ikamtakasia niya Mwenyezi Mungu hata kama ni jambo zito kupatikana.

Historia inatuonesha kuwa mafanikio hayapatikani bila kupambana na matatizo mbalimbali yaliyo mazito, hasa ukizingatia kuwa ukweli umedhihiri kutokana na kuenea vyombo vya habari na kupatikana vyombo vilivyo wafahamisha watu fi kra za kishia. Na pia kuwepo maingiliano kati ya Waislamu.

Yote haya tuliyo yataja tumeyataja kwa sababu ya kuondoa giza lililo tanda katika umma wa kiislamu, na kwa sababu ya kufahamu hali halisi ilivyo kuwa. Laiti madai hayo yangekuwa na ukweli ingetosha kuithibitisha hiyo Qur’ani inayo daiwa kuwanayo mashia tofauti na Qur’ani waliyonayo waislam wengine. Mpaka sasa zimepita karne kumi na nne tangu yaanze madai hayo na bado hawajaweza kuithibitisha Qur’ani hiyo inayodaiwa kuwa Mashia wanayo. Na ikiwa hakuna uwezekano wa kupatikana nakala mojawapo ya Qur’ani hiyo, basi hivi vitabu mama2 vya kishia vinapatikana, pia vitabu vya fi qhi ya kishia vinapatikana. Yewezekana kabisa kuvirejea na kupata ukweli wa fi kra zao zilizo wazi. Na hatafanya hivyo ila yule aliye shupavu na mwenye kuitaka haki.

Kwa hivyo basi, sababu hii kwa mukhtasari ni kuwa uadui dhidi ya

2 Vitabu mama: Maana yake ni vitabu vikubwa vya rejea.

Page 17: Ukweli ni Huu - Shia Maktab

13

Mashia na ushia na kuwazulia Mashia ni jambo lililotokana na nia ya wale waliyokusudia kuwatoa mashia katika jamii ya kiislamu.

BAADHI YA UZUSHIUNAO NASIBISHWA KWA MASHIA

Baada ya utangulizi huu nitaelezea maudhui yenyewe ambayo ndio malengo yangu. Nayo ni kutoa baadhi ya mifano ya mambo yanayo nasibishwa kwa mashia kwa lengo la kuwatoa kwenye uislamu na kuwafanya wawe ni wenye kuchukiza mbele ya Waislamu. Pia nitataja mifano mitatu tu kama vielelezo na kipimo cha hayo mengine waliyo nasibishiwa.

MFANO WA KWANZA:MADAI YA KUPOTOSHWA QUR’ANI

Qur’ani tukufu ni kitabu cha Mwenyezi Mungu kilicho teremshwa ambacho hakikuingiliwa na batili kabla ya kuteremshwa na baada ya kuteremshwa. Kitabu ambacho ndio msingi wa utamaduni wetu na ni katiba yetu na chemchem ambayo umma huirejea.

Qur’ani ni kitabu kitakatifu kwa kila Muislamu, na ni kitabu ambacho hakilinganishwi na chochote. Ni jambo lililo wazi yakuwa Qur’ani ndio chimbuko la msingi wa sheria za kiislamu ambapo vyanzo vyote vya sheria ndani ya Uislamu marejeo yake ni Qur’ani.

Kwa hivyo basi, ikiwa kutakuwa na madai ya kuwa Qur’ani imepotoshwa au kuwepo mabadiliko ndani yake, mabadiliko hayo yawe ni ya kuzidi aya au kupungua, au kugeuzwa kwa baadhi ya sentensi. Muislamu yeyote hawezi kuwa na uhakika juu ya usahihi na usalama wa sheria za kiislamu kwa sababu kauli kama hizi tayari zinakitia dosari kitabu hiki.

Page 18: Ukweli ni Huu - Shia Maktab

14

Hapana shaka kwamba Mwenyezi Mungu amesema: “Hakika sisi tumeiteremsha Qur’ani, na hakika sisi ndio wenye kuilinda.” Qur’ani 15:9.

Kutokana na nafasi ya Qur’ani na utukufu wake uliyomo ndani ya nafsi za Waislamu, kikundi chochote au madhehebu yoyote yatakayo thubutu na kudai ya kuwa Qur’ani ilifanyiwa mabadiliko, hayo yatakuwa ni madhehebu ya ajabu katika umma wote. Na pia madai kama hayo yatakuwa ni sababu ya kuchukiwa kwa madhehebu hayo. Kwa hivyo basi jambo la kwanza lililo tengenezwa na kuzushwa na tawala zilizopita na kuwapa mawakala wao jukumu la kulieneza, ni kuwanasibishia mashia kauli ya kuwa Qur’ani ilifanyiwa mabadiliko. Na inshaallah tutaona ukweli wa maneno hayo. Pia tutaziona kauli za masunni juu ya suala hili ili kuona usahihi wa yale wanayo nasibishiwa mashia.

Kuna kauli nyingi za Maulamaa wetu na mufassirina wetu zinazopinga madai haya kunasibishwa na ushia na wameubatilisha uzushi mwingi katika vitabu vya kishia, kiasi kwamba huwezi kupitia kitabu chochote kinacho zungumzia elimu za Qur’ani na maudhui zake isipo kuwa utakuta kuna kurasa kadhaa zimetengwa maalumu kwa ajili ya kubatilisha madai ya kuwa Qur’ani imebadilishwa.

Sio lengo langu kuorodhesha yote yaliyo andikwa katika maudhui haya isipokuwa ni kuashiria kwako wewe msomaji baadhi tu ya vyanzo vinavyo onesha rai za mashia kwa uwazi. Nitataja baadhi tu ikiwa ni dalili kwa hayo niliyoyasema, kwa kiasi cha kutosheleza.

Rai za maulamaa wote wa kishia ni kuwa: Qur’ani tukufu imehifadhiwa; haikuingiliwa na mabadiliko yoyote kama kuzidi aya au kupungua katika sura zake na hata herufi zake, bali Qur’ani tuliyo nayo ndio ileile iliyo teremshwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w.) tuionayo kwenye majalada mawili na iliyo enea katika jamii ya kiislamu. Na unaweza kuyathibitisha maneno haya kwa kurejea katika utangulizi wa Tafsir at-Tibyan ya Shaykh Tusi, pia katika utangulizi wa Tafsir Majma

Page 19: Ukweli ni Huu - Shia Maktab

15

al-Bayan ya Shaykh Tabarsi. Kadhalika Tafsir Kashful Ghitaa ya Sheikh Ustaadh ul Fuqahaa Sheikh Ja’far katika mlango wa Bahthul-Qur’ani. Pia waweza kurejea kwenye kitabu kiitwacho Haqq al-Yaqin cha Mulla Muhsin al-Faydh ambaye ni mashuhuri kwa jina la al-Muhaddithul-Kashani. Pia rejea kwenye kitabu Ala-ur-Rahman cha Sheikh Muhammad Jawad al-Balaghi.

Si hivyo tu bali waweza kusoma al-Bayan fi Tafsir al-Qur’an cha Ayatullah Abul-Qasim al-Khui. Na hiyo ndio rai ya Sheikh Mufi d na Sheikh Bahai na Qadhi Nurullah. Na wala si hawa tu bali muhaqqiqina wote.

Amma kauli inayo nasibishwa kwa Sheikh Kulayni Th iqatul-Islam katika kitabu cha “al-Kafi ” ya kuwa amepokea riwaya zinazo zungumzia kuwepo mabadiliko ndani ya Qur’ani yeye mwenyewe anazipinga riwaya hizo na anasisitiza mambo yafuatayo:

Kwanza: Hadith zinazoelezea kuwa Qur’ani imebadilishwa alizitaja kwenye mlango wa hadithi ambazo ni nadra. Hii ikiwa na maana kwamba hadithi hizo ni chache mno katika vitabu vya hadithi, pia ni hadithi ambazo hazitumiki. Ni hadithi zisizotumika kwa sababu hadithi kama hizi zinapotofautiana na Qur’ani na Sunna, au hadithi zenyewe zikawa sahihi lakini zikapingana na hadithi nyinginezo ambazo ni mashuhuri kuliko hizo, basi hadithi hizo huwa hazitumiki. Msimamo huu ndiyo wanaouthibitisha Maulamaa wetu katika mlango wa Attaadilu wa Atarjiihu3. Na kwa kuwa riwaya zinazo elezea kugeuzwa kwa Qur’ani zinapingana na Qur’ani yenyewe na Sunna, na zinapingana na kauli mashuhuri na zenye nguvu zaidi ikaamuliwa kutotumiwa hadithi hizo.

Kisha (ifahamike kwamba) hadithi hizo amezitaja katika kupambanua 3 Hii ina maana kwamba: Ikiwa kutakuwa na makundi mawili ya hadithi

zinazopingana, na kundi moja lina nguvu zaidi kuliko lingine, basi litatumika kundi ambalo hadithi zake zina nguvu zaidi. Kanuni hii ni miongoni mwa istilahi za elimu ya usul.

Page 20: Ukweli ni Huu - Shia Maktab

16

kati ya Riwaya sahihi na isiyo Sahihi. Lakufanywa hapa ni kuzipima na Qur’ani na Sunna na zikiwafi kiana na vitu hivyo wiwili huchukuliwa na zikipingana navyo huachwa. Hapa kuna dalili ya wazi kuwa, Sheikh Kulayni hakuzipa uzito riwaya hizo bali yeye alizisimulia kama Bukhari na Muslim walivyo zisimulia zile riwaya zinazosema kuwa Qur’ani imefanyiwa mabadiliko.

Vile vile ameitaja riwaya ya Saadul-Khair iliyopo kwenye kitabu kiitwacho “Raudhatul Kafi ”. Riwaya ambayo imeeleza wazi kutokuwepo upungufu ndani ya Qur’ani kama riwaya ifuatayo. Imam Baqir (a.s.) akasema kumwambia Saadul-Khair: “Na miongoni mwa kukipuuza kwao kitabu ni kuzibakiza herufi zake na kubadilisha hukumu zake.” Riwaya hii inabainisha wazi kukamilika kwa herufi za Qur’ani.

Sio kila msimulizi wa riwaya huweza kuyataja madhumuni ya riwaya vilivyo, kama ambavyo jambo hili linavyofahamika kwa mujibu wa viwango vya juu vya elimu.

Hizi ni baadhi tu ya fi kra zinazo elezea juu ya kuwepo suala la kubadilishwa kwa Qur’ani tukufu. Msimamo wa Mashia juu ya suala hili ukowazi na tunazo dalili nyingi zinazo thibitisha ya kuwa, Mashia hawasemi ya kuwa Qur’ani imebadilishwa. Isipo kuwa wasemao ya kuwa Qur’ani ilibadilishwa kwa maana ya kuzidi au kupungua maneno na aya ni wengine (na siyo Shia).

Ama kugeuzwa kwa maana ya kubadilishwa maana ya maneno na aya na hata sababu za kateremshwa aya fulani, Mashia wanayo rai iliyo wazi juu ya jambo hili. Nayo ni kuwa, wanakubali ya kwamba mabadiliko kwa maana ya kugeuzwa maana ya maneno, na ya baadhi ya aya na hata ya sabab un-Nuzul yali tokea katika riwaya nyingi, mabadiliko ambayo yalifanywa na wenye kutafsiri kwa sababu ambazo ziko wazi.

Tutataja kundi la wanachuoni wa Kisunni wanaosema ya kuwa Qur’ani imepungua kwa mujibu wa vitabu vyao.

Page 21: Ukweli ni Huu - Shia Maktab

17

Jambo la kushangaza ni kuwa masunni wenyewe ndiyo wasemao ya kuwa Qur’ani ilibadilishwa. Na kauli zao ziko wazi juu ya kupungua kwa Qur’ani waliyo nayo Waislamu. Ukiwachilia mbali ya kuwa wao wanaulazimu usemi huu au la. Hapana shaka kwamba wametuzowesha ya kuwa wao wao siku zote ni watu wasiyojilazimisha kushikamana na kauli zao wenyewe katika mambo yao mengi. Mambo haya hapa si mahala pake kuyatolea dalili, lakini kuna sehemu yake nyingine huenda tukayataja Insha-Allah.

Nina kariri ya kuwa kauli zao ziko wazi juu ya kuzidi au kupungua kwa Qur’ani, lakini wao hao hao wanawatuhumu wenzao kwa jambo hilo kama tutakavyoona katika mifano tutakayoitoa.

Kwanza tutatoa kauli zao kisha tutaashiria vitabu ambavyo kauli hizo zinapatikana kwa mwenye kutaka kufanya utafi ti zaidi.1. Suyuti katika kitabu chake (Al-Itqan Fi Ulum al-Quran) amesema

katika mlango wa idadi ya sura, maneno, na herufi za Qur’ani katika riwaya iliyo pokelewa kutoka kwa Umar bin al-Khattab ya kuwa: “(Yeye Umar) alikuwa akisema kwamba herufi za Qur’ani ni milioni moja na ishirini na saba elfu”. Na riwaya hii ameiandika Tabarani kwa sanadi iliyokubaliwa na hali ya kuwa ni Hadithi Marfuu’4 kutoka kwa Umar bin al-Khattab.

2. Vile vile muandishi wa Muntakhab Kanzul Ummal ametaja katika riwaya yake kutoka kwa Zur bin Hubaish amesema: “Ubay aliniambia: ‘ewe Zur vipi unaisoma Suratul Ahzaab?’ Nikamjibu: ‘Suratul Ahzaab ni aya Sabini na tatu’. Akasema: ‘Sura hii ilikuwa kama Suratul-Baqarah au zaidi ya al-Baqarah’.”

Kutokana na riwaya hizi mbili tunafaidika ya kuwa hii ndio rai ya Khalifa kama alivyo sema katika riwaya yake ya kuwa herufi za Qur’ani zilizoko ni chini ya theluthi ya herufi zote.

4 Hadithi Marfuu’, maana yake ni hadithi ambayo haina kiunganishi hadi kufi ka kwa mwenyewe Mtume (s.a.w.w.)

Page 22: Ukweli ni Huu - Shia Maktab

18

Na riwaya ya pili iliyotolewa na Ubay inaonesha kuwa, Suratul Ahzaab iliyopo (sasa hivi ndani ya Qur’an) ni chini ya theluthi ya sura iliyo teremshwa.

3. Pia Ahlu Sunna wamesema ya kuwa Sura al-Hafd na al-Khal’ ni miongoni mwa Sura ndogo ndogo ambazo hazimo ndani ya Qur’ani na ni sura ambazo Khalifa Umar bin al-Khattab alikuwa akizitumia kwenye kunuti zake. Nazo ni kama zifuatazo:

اللهم إنا نستعينك ونستغفرك ونثني عليك ولا نكفرك ونخلع وغترك من يفجركMaana yake.“Ewe mola Hakika sisi tuna kuomba msaada, na tunakuomba msamaha, na tunakusifu. Na wala hatukukufuru. Na tunajiepusha na kumuacha mwenye kukuasi”

نقمتك إن عذابك ك نسعى ونحفد نرجو رحمتك ونخ اللهم إياك نعبد ولك نصلي ونسجد وإبالكافرين ملحق

Maana yake. “Ewe Mwenyezi Mungu wewe tu ndiye tunaye kuabudu, na kwa ajili yako tuna Sali na kusujudu na kwako ndiko tunako kimbilia. Tunataraji rehma zako na tunaogopa adhabu zako. Hakika adhabu yako itawapata makafi ri.”

Angalia katika kitabu cha Suyuti kwenye mlango wa idadi ya sura. Imepokelewa riwaya hii katika njia nyingi pamoja na kuwa sura hizi mbili hazimo ndani ya Qur’ani.

4. Imam Ahmad bin Hambal ametaja katika Musnad juzuu ya kwanza kwa sanadi yake kutoka kwa Ibn Abbas, naye kutoka kwa Umar ibn al-Khattab ya kuwa amesema; “Hakika Mwenyezi Mungu alimtuma Muhammad na haki na akamteremshia kitabu na miongoni mwa aliyo mteremshia ni aya ya Rajm (kumpiga mawe mzinifu). Mtume (s.a.w.w.) akawapiga mawe wazinifu nasi tukawapiga mawe baada yake na tulikuwa tukisoma kama ifuatavyo:

Page 23: Ukweli ni Huu - Shia Maktab

19

ولا ترلبوا عن آبائكم فإنه كفرا بكم أن ترلبوا عن آبائكمMaana yake “Na wala msijiepushe na wazazi wenu ikiwa watakukufuruni, kujiepusha na wazazi wenu”; na aya hii haimo ndani ya Qur’ani.

5. Suyuti katika kitabu chake Al-Itqan ametaja riwaya ya Naafi ’ kutoka kwa mtoto wa Umar amesema; “Asiseme yeyote ya kuwa nimeichukua (nimeihifadhi) Qur’ani yote; ni jambo gani linalo kujulisha ya kuwa ni yote. Hakika ilitoweka sehemu kubwa ya Qur’ani, lakini mwenye kusema aseme yakuwa hakika nimechukuwa katika Qur’ani iliyo dhihiri.”

Vile vile imepokelewa kutoka kwa mwana Aisha mkewe Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Suratul Ahzaab ilikuwa ikisomwa katika zama za Mtume (s.a.w.w.) aya mia mbili. Uthmani alipouandika msahafu hatukusoma isipokuwa kama ilivyo hivi sasa.” Riwaya hizi mbili ziko wazi kabisa juu ya suala hili.

6. Imam Muslim amepokea katika kitabu chake Sahih Muslim juzuu ya tatu kwa sanadi yake kutoka kwa Abi Harb ibn Abi Aswad ya kuwa: “Baba yake Musa al-Ashari alisema kuwambia wenye kuihifadhi Qur’ani huko Basra. Sisi tulikuwa tukiisoma sura fulani tukiifananisha kwa urefu wake na uzito wa maneno yake, na Suratul-Baraa. Lakini nimeisahau isipo kuwa ninakumbuka sehemu hii

جوف ابن آدم إلا الترابلو كان لابن آدم واديان من مال لانتغى واديا ثاكخا ولا فملأ

“Lau kama mwana Adam angekuwa na mapango mawili ya mali angetaka apate la tatu na hakuna kinachoweza kulijaza tumbo la mwana Adam isipo kuwa udongo.”

Vile vile tulikuwa tukiisoma sura tukiifananisha na mojawapo ya sura za al-Musabbihaati na nimeisahau isipo kuwa sehemu hiiلون قنها يوم القيامة

ين آمنوا لم يقولون ما لا يفعلون فتكتب شهادة في أعناقكم فتسأ يا أيها ا

Page 24: Ukweli ni Huu - Shia Maktab

20

Maana yake “Enyi mlio amini kwa nini mna sema msiyo yafanya zikaandikwa shahada katika shingo zenu na mkaulizwa siku ya kiyama.”

Aya hizi mbili na sura mbili alizozitaja hazimo ndani ya Qur’ani, na hii ina maana zilitoweka kufatana na rai yake. Ukiongezea na mifano tuliyo tangulia kuitaja, kwani katika njia ya kuikusanya Qur’ani kama walivyo pokea Ahlu Sunna na katika njia ya kuandikwa kwake na kutokana na kauli yao ya kuwa kuna visomo vilivyofutwa, katika aya nyingi sawa kufutwa hukumu ya aya au haikufutwa, yote haya yanapelekea kukiri kuwepo mabadiliko ndani ya Qur’ani na kuwepo upungufu pia.

7. Ibnu Majah ameandika hadithi kutoka kwa mwana Aisha mkewe Mtume (s.a.w.w) amesema: “Iliteremka aya ya Rajm na aya ya kunyonyeshwa mtu mzima mara kumi. Na aya hizi mbili zilikuwa kwenye nyaraka chini ya kitanda changu. Alipokufa Mtume (s.a.w.w) tukawa katika hali ya kushughulikia kifo chake akaingia mnyama akazila nyaraka hizo”. Vile vile riwaya hii ameisimuliya Ad-Dumairi katika kitabu kiitwacho Hayatul Hayawan chini ya neno Ad-Daajin.

Wanachuoni wetu katika sehemu mbalimbali wamekuwa wakijadiliana na wale wasemao ya kuwa Qur’ani imegeuzwa, na kubatilisha kauli zao hizo. Ili kuyapata hayo waweza kurejea katika vitabu tulivyo vitaja hapo mwanzo. Pamoja na yote hayo, tuliyo yataja ni baadhi tu ya mifano kwani tuna vyanzo vingine ambavyo tukiyakusanya yote basi itatulazimu kutunga vitabu vingi ili kubainisha kauli zao zote zinazo zungumzia kuwa Qur’ani imegeuzwa. Pamoja na yote hayo tuliyoyabainsha, uzuishi huu umekuwa ukiendelea bila kukoma.

Na mimi nina itakidi na kuamini ya kuwa tunayo yaandika na kuyaeleza kubatilisha uzushi huu yatawanufaisha wachache sana nao ni wale watafi ti na wenye nyoyo zenye kutakasika na ambao wanapenda kuitafuta haki. Ama walio wengi si watafutaji wa haki bali wao

Page 25: Ukweli ni Huu - Shia Maktab

21

hung’ang’ania waliyo nayo hata kama ni batili na katika ung’ang’anizi wao hufi kia hatua ya kuliita jua kuwa ni jiwe jeusi na si jua.5

Pamoja na hayo, juhudi zetu ni kuwafafanulia wale wenye kuutafuta na kuutaka ukweli, na kwa kufanya hivyo huwenda Mwenyezi Mungu akamnufaisha nao mwenye kutaka kuongoka.

MFANO WA PILI: UZUSHI WA KUWA JIBRIL ALIKOSEA KUTEREMSHA WAHYI KWA MTUME

MUHAMMAD (S.A.W.W.)

Miongoni mwa mambo ya msingi katika itikadi ya waislamu ni kuwa Mwenyezi Mungu alimtuma Mtume Muhammad (s.a.w.w.) kwa viumbe wote na akaukamilisha utume kwa Muhammad (s.a.w.w). Na dalili za Qur’ani zinathibitisha hivyo. Mwenyezi Mungu anasema “Ewe Mtume, hakika sisi tumekutuma ukiwa ni mwenye kushuhudia na mwenye kubashiria na mwenye kuonya”. Kisha amesema “Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu.” Na katika aya nyingine amesema: “Ni Yeye (Mwenyezi Mungu) ndiye aliye mtuma Mtume kwa watu wasiyojuwa kusoma anaetoka miongoni mwao”.

Jambo hili liko wazi kwa waislamu ya kuwa Mtume alitumwa na Mwenyezi Mungu na ni Mtume wa mwisho. Ikiwa atatokea anayedai ya kuwa Mtume Muhammad hakuwa ametumwa na Mwenyezi Mungu bali Jibril, ambae ni kiunganishi kati ya Mwenyezi Mungu na watu, alifanya khiyana akapeleka utume kwa Muhammad (s.a.w.w.) badala ya kuupeleka kwa Ali bin Abi Talib (a.s.) hapana shaka mwenye kusema hivyo atakuwa kafi ri na atakuwa ametoka kwenye uislamu. Na hapana shaka waislamu watamlaani kwani atakuwa amekwenda kinyume na dalili za Qur’ani.5 Kuliita jua kuwa ni jiwe jeusi: Maana yake ni ung’ang’anizi na ubishi usiyokuwa na

hoja. Mtu hata kama utamuelekeza vipi, kamwe hakubali, lake ni lake tu la mwingine hasikii.

Page 26: Ukweli ni Huu - Shia Maktab

22

Pili: Mtu huyo atakuwa amepinga dharura6 moja wapo kati ya dharura za dini.

Tatu: Atakuwa amemtuhumu yule ambaye Mwenyezi Mungu kampa sifa ya kuwa ni muaminifu, naye ni Jibril.

Nne: Atakuwa amemnasibishia Mwenyezi Mungu sifa ya kunyamazia kosa lililofanywa na Jibril.

Tano: Atakuwa amemtuhumu Mtume (s.a.w.w.) yakuwa alichukua haki ya mtu mwingine.

Sita: Atakuwa amefungua mlango wa shaka katika wahyi wote na Maudhui yake. Kwa sababu mwenye kufanya khiyana katika kufi kisha, inawezekana vile vile kufanya khiyana katika maudhui ya wahyi huo pia.

Kwa hivyo basi kunasibishwa akida kama hii tuliyo itaja kwa kundi lolote inatosha kulitoa kundi hilo katika Uislamu. Na haya ndiyo wanayo yanasibisha Masunni kwa Mashia na kusisitiza hivyo.

Baada ya kuazinukuu kauli zao (Masunni), tutazijadili ili tuone jinsi wanavyo wanasibishia Mashia kauli hizo na tutaona athari zitokanazo na kauli zao hizo.

Kama maneno hayo yangekuwa yanasemwa na mtu wa kawaida kusingekuwa na tatizo kiasi hicho, lakini jambo la kuhuzunisha ni kuona kuwa wasemao maneno kama haya ni watu wenye nafasi zao, na ni miongoni mwa watu ambao maneno yao husomwa kila siku na pia ni wasomi wa Ki-Islam mashuhuri kama hawa wafuatao:

6 Dharura za dini ya Ki-Islamu, ni mambo ambayo mtu anapoyakanusha huwa nisababu ya yeye kutoka katika dini. K.m. Kukanusha kuwepo kwa Mwenyezi Mungu, kumkanusha Mtume (s.a.w.w.), kukanusha ulazima wa kusali sala tano au kufunga Ramadhan, kwenda hija n.k.

Page 27: Ukweli ni Huu - Shia Maktab

23

1. Fakhrul Razi:Amewasingizia Mashia mambo hayo katika Tafsiri yake ya aya hii.

رون ه إلا المطه لا فمسMaana yake: “Hapana atakayeigusa (Qur’ani) ila waliotakaswa.” (Qur’ani, 56:79)

Kwa hakika sitaacha kumzinduwa msomaji ya kwamba, Ahlu Sunna hupata wakakitaja kikundi fulani na wakakinasibisha na Mashia, wakati ambapo kikundi hicho ni kikundi kinachojitegemea kisicho na uhusiano wawote na Mashia. Ahlu Sunna hufanya hivyo ili kuonesha ya kuwa yanayo husishwa na kikundi hiki ni mambo makubwa na ili yaenee na ionekane kuwa huo ni mtazamo wa Mashia wengi. Kwa mfano kuwaita Mashia kuwa ni Muhammadiyah, kwa kuwanasibisha kwa Muhammad bin Abdullah mtoto wa Imam Hassan mjukuu wa Mtume (s.a.w.w.) wakati ambapo kikundi hiki hakipo kamwe.

Mambo haya amejaribu kuyataja Abdul Qahir ibn Tahir al-Baghdadi katika kitabu Al-Farq Bayn Al-Firaq. Kwa hakika kila mwenye maarifa ya vitabu vya Ki-Islamu atakuwa anamfahamu Fakhrul Razi kuwa ana daraja gani katika nyanja za kielimu. Mwanachuoni kama huyu pindi anapotaka kukihusisha kitu au rai fulani kwa mtu fulani, basi kamwe haiwezekani ikadhaniwa kuwa yeye hakukithibitisha kitu hicho na au pengine ametegemea uvumi tu wa jambo hilo. Na ikiwa atafanya hivyo ina maana nafasi yake ya kielimu itatoweka.

Hapo baadaye tutaeleza kuna ukweli kiasi gani wa haya aliyowanasibishia Mashia.

2. Qurtubi al-MalikiVile vile huyu bwana ni kama yule tuliye muelezea mwanzo. Huyu si mtu mdogo, na tafsiri yake ni miongoni mwa tafsiri muhimu, pia na daraja yake kielimu ni ya juu. Ni mara chache mno kukuta maudhui fulani ya Qur’ani imeandikwa ambapo ndani ya maudhui hiyo tafsiri yake haikutajwa. Basi ni upi msimamo wa msomaji ikiwa atayaona maneno ya huyu bwana aliyowanasibishia Mashia?

Page 28: Ukweli ni Huu - Shia Maktab

24

3. Ibnu Taymiyah:Katika kitabu chake kiitwacho Minhaj as-Sunnah juzu ya kwanza amesema alipokuwa akili nganisha kati ya mayahudi na Mashia: “Mayahudi wanamchukia Jibril na wanasema, miongoni mwa Malaika yeye ni adui yetu, Vile vile marawaafi dhi (yaani Mashia) nao wanasema Jibril alikosea kupeleka wahyi kwa Muhammad …” Mtu huyu (Ibnu Taimiyyah) anayo mengi mazito aliyowazulia Mashia. Mimi ninamuomba Mwenyezi Mungu awalipe Mashia (malipo stahiki) ikiwa ni ya kweli hayo waliyohusishwa nayo. Kadhalika Mwenyezi Mungu amlipe bwana huyu (malipo stahiki) ikiwa hayo aliyowahusisha nayo Mashia ni uzushi mtupu.

Sijawahi kuona mtu mkorofi kuliko huyu ambaye mafunzo yake yanachanganya kufru na imani.

Baada ya hawa mabwana tuliowataja, wako wengine waliofuata nyayo zao kama ibn Jabhan katika kitabu chake kiitwacho Tabdidudhilami, na mwenzake akiitwa Muhibbuddin al-Khateeb na wengineo.

Kama ambavyo wako na wengine walioanza kuziratibu athari zinazohusu madai ya kuwa Mashia siyo Waislamu.

Kutokana na itikadi hii waliyonayo mwanachuoni mmoja ajulikanaye kwa jina la Abdul Qahir al-Baghdadi katika kitabu chake al-Farq Bayn al-Firaq, amaefi kia kusema kuwa: “Haifai kumsalia Shia, wala haifai kusali nyuma yake na mnyama aliyechinjwa na Shia siyo halali kuliwa na wala haifai kumuoza Shia binti wa kisunni”. Bali amesema kuwa siyo halali kuowa kwao ikiwa binti huyo ana itikadi kama za Mashia.

Na hivi hivi ndivyo alivyoeleza pia mwenye kitabu kiitwacho Al-Ankihatul Faasidah. Dr. Amir na wengineo waliyo watangulia katika kikundi cha salafi yya ambao walikuwa ni mamuft i wa miji ya Ki-Islam. Na mas’ala haya yamekuwa mashuhuri hakuna haja ya kuyaeleza zaidi.

Page 29: Ukweli ni Huu - Shia Maktab

25

Na mwisho tuna sema: Mabwana hawa mambo waliyo wahusisha nayo mashia kama ni ya kweli na sahihi basi hakuna haja ya kutafuta dalili ya kuonesha ukafi ri wa yule mwenye kupinga dharura moja wapo kati ya dharura za dini kama hii, lakini kwa jambo hili tunasema:1. Ni vigezo gani walivyo vitegemea juu ya madai yao hayo ya

kuwahusisha Mashia na kauli ya kukosea kwa Jibril katika kushusha wahyi kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w.)?

Sisi tuna wataka watuoneshe vigezo hivyo, na ni haki yetu kuwadai hawa walio toa madai haya chanzo moja wapo kati ya vitabu vyetu ambamo yanapatikana maneno hayo, na je wanaweza katupatia vitabu hivyo? Ikiwa hawawezi kupata chanzo cha maneno hayo ndani ya vitabu vyetu je wako tayari kuacha na kujiepusha na uzushi wao huo? Je wataona haya juu ya madai hayo?

Na dhana kubwa ni kuwa hawawezi kujizuia kutoa madai hayo kwani vitu vinavyo wapa msukumo wa kufanya hivyo vina fahamika.

2. Hata kama wangepata kitabu kimoja kinacho sema hivyo, je! Ni Sahihi kuunasibishia Ushia na Mashia wote kauli kama hiyo kwa sababu tu mtu mmoja kasema hivyo, wakati vitabu vyote vya Mashia vina pingana na jambo hilo? Na ukitaka uthibitisho soma vitabu vyao vya fi khi na akida, vimejazana katika maktaba na vina sema wazi ya kuwa Mwenyezi Mungu alimtuma Mtume Muhammad (s.a.w.w.) na akamfanya kuwa ni Mtume wa mwisho na kwamba Jibril ni Muaminifu katika wahyi utokao kwa Mwenyezi Mungu na Qur’ani ina thibitisha ya kuwa Jibril ni mtiifu kisha muaminifu.

Hapana shaka kwamba, kuna mwanazuoni mmoja aitwaye al-Karkhi ambaye ni miongoni mwa maimamu wa madhehebu ya Hanafi , yeye anasema kuwa: Qur’ani na Sunna ikiwa vitapingana na kauli za wanazuoni wa kihanafi , basi ni lazima vifanyiwe tawili, (yaani Qur’ani na Sunna).7

7 Kufanya Tawili: Inakusudiwa ni kutowa tafsiri itakayokubaliana na hizo kauli zawanachuoni wao

Page 30: Ukweli ni Huu - Shia Maktab

26

Je Ahlu Sunna wanaridhia tutangaze ya kuwa wao wanayohukumu ya kuwa Qur’ani ni lazima ifuate kauli zao? Na je! Ikiwa tutasema kauli kama hii hivi itaonekana ni kauli yenye mantiki inayokubaliana na akili?

Kwao Ahlu Sunna yapo maoni binafsi ya mtu mmoja mmoja ya wanachuoni wao kuhusu mambo ya hukumu na itikadi. Na hukumu hizo zinatofauti kubwa na wala haziwiani na mwendo wa Ki-Islamu. Kwa mfano mtazamo wa Bukhari ya kuwa: Maziwa ya ng’ombe yana sababisha kupatikana uharamu, yaani ikiwa watu wawili watashirikiana kunywa maziwa ya ng’ombe mmoja watakuwa ndugu wa kunyonya. Sasa je! Ni sawa kauli kama hii kuinasibisha kwa masunni wote? Pamoja na yote hayo sisi tuna wataka angalau watoe ushahidi wa mtu mmoja anayesema ya kuwa Jibril alikosea au alifanya khiyana na kuupeleka wahyi kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w.) kama upo ushahidi tuna waomba watuoneshe.

3. Ni jambo lililowazi kwamba Imam Ali (a.s.) alikuwa na Mtume wakati wote, kwani ni mtu aliyekuwa na mapenzi mno kwa Mtume, hata malezi yake yalifanywa na Mtume (s.a.w.w.). Na tukiiangalia historia yake tunakuta kuwa ni mtu aliejitolea kumtetea Mtume na Dini ya Allah na alikuwa ni nafsi ya Mtume kwa dalili ya Qur’ani. Ikiwa ni kweli utume ulikuwa ni wa Ali mbona hatuoni kwamba Ali alikata mawasiliano na Mtume au kutoa maneno mabaya dhidi ya Mtume? Je! Unadhani Mashia pamoja na wanachuoni wao waliyobobea na wasiyo hesabika hawayafahamu hayo isipokuwa anaye yafahamu ni ibn Jabhan na wenzi wake tu, watu ambao Mwenyezi Mungu amewapiga mihuri juu ya nyoyo zao? Kama kweli wangekuwa wanaitakidi hivyo wangeona athari zake kati ya uhusiano uliyo kuwepo kati ya Mtume na wasii wake (a.s.).

4. Ulipoteremshwa wahyi Imam Ali (a.s.) alikuwa na umri kati ya miaka saba au kumi, kutokana na riwaya mbili zilizopokelewa. Je! Unadhani inawezekana kutumwa Mtume akiwa na umri wa miaka saba au kumi? Na je kuna mfano wowote wa Mtume kabla ya

Page 31: Ukweli ni Huu - Shia Maktab

27

Mtume Muhammad (s.a.w.w.) aliyepewa Utume akiwa na umri kama huu? Na je! hili ni katika mambo magumu yasiyoweza kufahamika?

Ni ajabu iliyoje kwa watu hawa wasio na elimu na wasiyo fahamu maneno ya Allah!

5. Qur’ani tukufu inasema:رسلنا من قبلك إلا رجالا

وما أ

Maana yake: “Hatukuwatuma kabla yako isipokuwa watu walio kamilika.”

Katika Aya hii limetumika neno Rijaalan, neno hili hutumika kumuashiria mtu aliefi kia utu uzima kisheria, yaani aliefi kia kubalehe na mwenye miaka kati ya ishirini na tano. Na Imam kama tulivyo tangulia kusema alikuwa bado ni mtoto.

Na mengine mengi ambayo yalitakiwa yaangaliwe vizuri kabla ya kutangaza uzushi huu ndani ya jamii. Katika kitabu chetu kiitwacho Hawiyat al-tashayyu’ tulikwisha kuyabatilisha madai hayo.

Baada ya yote hayo tunasema; “Misikiti yetu na vipaza sauti vyetu, hupaza sauti ya adhana siku zote wakati wa sala tano pembe zote za dunia tunanadi na kusema:

د الرسول االله اشھد ان محم“Ninashuhudia ya kuwa Muhammad ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu.”

Je adhana zote hizi zitolewazo si dalili tosha ya kubatilisha uzushi huu? Watasema ya kuwa nyinyi mnasema hayo kwenye adhana kwa taqiya na hapa tunawajibu kabla hawaja yasema hayo. Tunasema yakuwa katika adhana zetu tuna dhihirisha kauli ifuatayo:

االله أشهد أن عليا و“Nina shuhudia ya kuwa Ali ni wali wa Mwenyezi Mungu.”

Page 32: Ukweli ni Huu - Shia Maktab

28

Na katika hili hatutumii taqiya.

Kwa maoni yangu basi, tunge yadhihirisha hayo katika misikiti yetu iliyopo ulaya ikiwa tunaogopa kuyadhirisha kwenye misikiti iliyopo kwenye bara la Asia au sehemu zenye Waislamu wengi.

Kama ambavyo tungeweza kuyadhihirisha hayo katika nchi ambazo zilitawaliwa na Mashia k.m. Misri iliyotawaliwa na dola ya Faatimiyah, na au Iraq iliyo kuwa ikitawaliwa na Buwayhiyiin au Iran ambayo ni dola ya Kishia au sehemu zingine zisizo hizo.

Basi kote huko tungeweza kutangaza hilo bila ya khofu yoyote. Sasa je! mbona hatufanyi hivyo? Je wanaweza kutujibu? Kinachoonekana ni watu wanao pandikiziwa na watu wenye shubuha au wenye lengo la kuufarakanisha umma wa kiislamu na kuvunja umoja wao.

Jibu sahihi ni kuwa watu hawa hawataki ukweli. Na kama kweli wangekuwa ni watafutaji wa ukweli wasinge thubutu kusimama juu ya uzushi kama huu.

Japokuwa hawakosekani baadhi wenye dhamira nzuri ya kupinga uzushi kama huu, kwa mfano Sheikh Muhammad al-Ghazali katika kitabu chake Difau anil-Akida na Dr. Abdul-Wahid Katika kitabu chake, Baynas-Shiah was-Sunnah.

MFANO WA TATU:KUVUKA MIPAKA KATIKA ITIKADI YA MAIMAMU

Vitabu vya Ahlu Sunna katika fani zao mbali mbali zenye uhusiano na elimu za ki-Islamu, wamekuwa wakiwatuhumu Mashia ya kuwa wanavuka mipaka katika imani zao kwa Maimamu wao, kiasi kwamba wanawapa daraja wasizo zistahiki na wanavuka mipaka katika kuwasifi a.

Page 33: Ukweli ni Huu - Shia Maktab

29

Na huenda baadhi yao wamekuwa wakitutuhumu ya kuwa tunasema kuwa wao wanafahamu mambo ya ghaibu kwa dhati zao (yaani kwa uwezo wao wenyewe) na kuwa wanao uwezo kibinafsi wa kugundua yaliyomo ndani ya ghaibu. Na kwamba sisi tunawapa utawala wa kuviendesha viumbe vyote kwa kuviathiri kwa dhati zao na mengine mengi. Kwa ufupi wanadai ya kuwa tunawatoa Maimamu wetu kwenye hali ya ubinadamu wa kawaida na tunawaweka nafasi ya juu zaidi.

Katika sehemu hii nitaanza kwa kuashiria ya kuwa, watu wengi wasomao fi kra za Mashia huwa hawasomi kupitia maandiko yaliyoandikwa na Mashia wenyewe, bali husoma fi kra zilizoandikwa na maadui zao au zilizoandikwa na watu ambao hawajaiva kifi kra vizuri katika kufahamu mifumo ya dini.

Na huenda wanasoma maandiko ya Mashia ambao hawajawiva vizuri kielimu kiasi cha kuwa na uwezo wa kupambanua istilahi zake au fi kra zake, au ni watu waliyojichanganya na kushindwa kupambanua kati ya kuwa Maimamu huletewa ujuzi huo kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa njia hii au ile. Kama ambavyo pia ndugu zetu Masunni wanavyowapandikiza fi kra potofu watu wa kawaida juu ya Shia8, hali ya kuwa wanafahamu wazi kwamba ni jambo gani lililopelekea kufahamika kimakosa hizi fi kra za kishia.

Ninapenda kuligusia jambo jingine nalo ni kuwa: Baadhi ya waandishi wana weza kuiona rai fulani ambayo ni moja tu kati ya nyingi na ni ya mtu mmoja au kundi fulani ambalo halipo tena (yaani limekwisha toweka), wao huichukua rai hiyo na kuifanya kuwa ni rai ya Mashia wote. Kama ambavyo baadhi ya waandishi wanaweza kuiona riwaya fulani pamoja na kuwa wao si watu wenye ujuzi na maarifa ya uwanja huu wa riwaya. Na wakisha kuiona riwaya hiyo hawafuatilii kutaka kujua kama kuna riwaya nyingine inayo ipinga au inayo toa tafsiri yake au ufafanuzi wake na kubainisha mambo yaliyo fungika ndani ya riwaya hiyo. Mtu kama huyo huchukua hatua ya kuiandika bila

8 Tutaliezea baadaye jambo hili.

Page 34: Ukweli ni Huu - Shia Maktab

30

uchunguzi, na matokeo yake ikawa ni kutoa hukumu ambazo hazipo ndani ya Uislamu au hukumu zisizo za kweli.

Na pengine huenda akawepo mwenye ujuzi wa elimu hizo, lakini ndani ya moyo wake kuna magonjwa kiasi kwamba akatumia njia isiyo ya haki kuiandika na kutoa hukumu zisizo faa mfano wa aliye sema “Hakuna apasaye kuabudiwa.” Bila kusema; “Isipokuwa Allah.”

Pamoja na yote hayo nitaonesha katika sehemu hii japo kwa muhtasari rai za Mashia katika maudhui haya, zikiwa ni dalili tosha ya kuthibitisha msimamo wao juu ya suala hili, na mwisho nitanukuu rai za Ahli Sunna kwa Maimam wao ili tuone ni watu gani wanao vuka mipaka.

1. Shia Imamiyya wametoa dalili inayo dhihirisha ukafi ri wa maghulati9 na kwamba wao hawana uhusiano wowote na kikundi hicho na miongoni mwa dalili hizo ni kauli ya Mwenyezi Mungu, aya ya sabini na saba ya Suratul – Maaidah, Mwenyezi Mungu amesema:

ضلوا هواء قوم قد ضلوا من قبل وأ

هل الكتاب لا يغلوا في دينكم لير الحق ولا تتبعوا أ

قل يا أ

بيل كثيرا وضلوا قن سواء السMaana yake.“Waambiye: (Ewe Muhammad), Enyi watu wa kitabu msivuke mipaka katika dini yenu kwa kuyachukua yasiyo ya haki, wala msiyafuate matamaniyo ya watu fulani waliyopotea toka zamani na wakawapoteza wengi na wakapotea njia ya kweli.”

2. Imam Ali (a.s.) amesema; “Wameangamia kwa ajili yangu watu wawili: Mwenye kunipenda na akavuka mipaka ya kunipenda na mwenye kunichukia na akaniona si chochote.”

3. Pia Imam Sadiq (a.s.) amesema: “Hatukuwa sisi ispokuwa ni watumwa wa Mwenyezi Mungu ambao alituumba na akatuchagua, na ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba, mbele ya Mwenyezi Mungu hatuna hoja na wala hatuwezi kuepukana nae.

9 Ghulati ni watu waliyovuka mipaka ya dini.

Page 35: Ukweli ni Huu - Shia Maktab

31

Hakika sisi tutakufa na tutasimamishwa na tutaulizwa. Yeyote mwenye kuwapenda Maghulati atakuwa ametuchukia na mwenye kuwachukia Maghulati atakuwa ametupenda. Maghulati ni makafi ri na Mufawidha10 ni washirikina. Mwenyezi Mungu awalaani Maghulati, kwani walikuwa kama Manasara walikuwa kama Qadaria, walikuwa kama Murjiyyah walikuwa kama Haruriyyah”

4. Pia Wanachuoni wetu kwa pamoja wamekubaliana ya kuwa Maghulati ni najisi na haifai kuiosha maiti yao. Pia haifai kuzika maiti yao, na ni haramu kuwapa zaka. Pia haifai kuwaoza mabinti wa ki-Islamu na haifai wao kumrithi Muislamu isipo kuwa inafaa Muislamu kuwarithi wao.

5. Sheikh Mufi d katika kitabu chake Sharh aqaid al-Sadiq amesema: “Maghulati ni miongoni mwa watu wanaojionesha ya kuwa ni Waislamu, nao ni wale waliomnasibishia Uungu na utume Imamu Ali (a.s.) pamoja na Maimamu wa kizazi chake na wakawatukuza ndani ya dini na dunia kiasi kwamba wakafi kia hatua ya kuvuka mipaka na kutoka kwenye njia ya sawa. Kwa hiyo wao ni watu waliyopotea na ni makafi ri”.

Na dalili hizi tulizozitanguliza ni kama vielelezo vinavyobainisha mtazamo wa Mashia katika suala hili linalowahusu maghulaati na kuvuka kwao mipaka katika imani ya Maimamu.

Na sidhani yakuwa wale wanaowatuhumu Mashia kuwa wanavuka mipaka hawaja ziona dalili hizi, bali yaliwashinda matamanio yao kiasi kwamba wakawanasibishia Mashia kuwa wamevuka mipaka. Mwenyezi Mungu ndio mwenye kutegemewa kwa hayo wayasemayo.

Na tutaonyesha kwa ufupi mwendo wa fi kra za Ahlus-Sunna ili tuone 10 Mufawidha ni kikundi ambacho kimekwisha toweka, lakini itikadi ya kikundi hiki

ni kwamba: Mwenyezi Mungu amempa binadamu uhuru usiyokuwa na mipaka, na ameondosha Uwezo Wake na Qadar Yake juu ya mwanadamu.

Page 36: Ukweli ni Huu - Shia Maktab

32

je kwao kuna hali ya kuvuka mipaka katika masuala ya Imam au hapana?

1. Bwana Alauddini al-Sikatwari al-Basnawi Ali Dede katika kitabu chake Muhadarat al-Awail wa Musamarat al-Awakhir amesema: “Kulitokea tetemeko la ardhi katika mji wa Madina, Umar akapiga juu ya Ardhi kwa upanga wake na akasema kuiambiya ardhi: Tuliya!! Basi ardhi ikatuliya na tetemeko likatoweka.” Na amesema vile vile maji ya mto Naili yalipungua na mtawala wa Misri kwa wakati huo alikuwa Amr ibn al-A’as. Basi watu wa Misri wakataka kumtosa bibi harusi ndani ya mto Naili kama kawaida yao. Amr ibn al-A’as akawazuwiya na akamuandikia Umar bin al-Khattab barua. Umar bin al-Khattab katika jibu lake akamtumia barua iliyokuwa imeandikwa mambo fulani akaitupia kwenye mto Naili na mto ukafurika. Kisha ametaja tukio la vita vya mlimani, Sariyatul Jabal, na tukio jingine la kuzima moto kuliko fanywa na khalifa Umar, Mwisho akasema: “Hakika Umar alikuwa na uwezo wa kuvitawala vitu vinne: maji, hewa, mchanga, na moto.” Na maana iliyomo katika maneno haya ni Wilayat e Takwiniyya (yaani utawala katika viumbe na kuviathiri atakavyo). Sasa je riwaya kama hizi zimepata kutoa hisia fulani kwa Ahlus-Sunnah baada ya kuzisoma ndani ya vitabu vyao? Ukweli ni kuwa ni hapana!! Lakini riwaya kama hizi lau moja tu ingelisimuliwa kutoka kwa mmoja wapo kati ya Maimamu wa Ahlul Bayti ingeonekana kuwa, ni ghuluw yaani ni kuvuka mipaka bali ingeonekana kuwa ni kufru.

2. Ibnu Jawzi katika Manaqib al-Imam Ahmad Ibn Hanbal kutoka kwa Ali bin Ismail amesema: “Niliona katika ndoto kana kwamba kiyama kimesimama, na watu wakija kwenye kivuko na hapo haruhusiwi yeyote kuvuka mpaka aje na muhuri – na pembeni mwake kuna mtu amekaa akiwapigia mihuri. Nikasema ni nani huyo? Waka jibu ni Ahmad bin Hanbal”.

3. al-Makki ametaja katika kitabu chake Manaqib al-Imam Abi Hanifa

Page 37: Ukweli ni Huu - Shia Maktab

33

juzuu ya pili ya kuwa Abu Hanifa amesema: “Aliona katika ndoto ya kuwa yuko kwenye bustani akiwa na kipande cha karatasi huku akiandika ijaza ya watu fulani akaulizwa sababu ya kufanya hivyo akajibu: “Hakika Mwenyezi Mungu amekubali matendo yangu na madhehebu yangu na amenifanya niwe muombezi wa umma wangu na nina andika ijaza zao.” Akaulizwa: “Wale unaowaandikia ijaza, elimu zao yapasa ziwe zimefi kia kiwango gani?” Akasema: “Wakielewa ya kuwa tayamamu haijuzu kwa kutumia majivu.”

4. Pia Khatib al-Baghdad katika tarekh yake juzu ya kumi na nne amesema kwa sanadi ya kutoka kwa Abi Umama kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Niliingia peponi… kisha akasema: Nilipokuwa mlangoni kikaletwa kiganja cha mizani nikawekwa juu yake na umma wangu ukawekwa upande wa pili upande wangu ukawa mzito zaidi kuliko umma wangu. Kisha akaletwa Abu Bakr akawekwa upande mmoja na umma wangu upande mwingine upande wa Abu Bakar ukawa mzito kuliko umma wangu. Kisha akaletwa Umar akawekwa upande na umma wangu upande mwing-ine, upande wa Umar ukawa mzito kuliko umma wangu, kisha mizani ikainuliwa.” Maneno haya yana maana ya utukufu wa mabwana hawa juu ya umma wa Mtume (s.a.w.w.). Na maneno haya ameyasimuliya al-Hakim al-Tirmidhi kwenye kitabu chake kiitwacho Nawadir Al-Usul.

5. Pia al-Abidi al-Maliki katika Umdat al-Tahqiq, amesema: “Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa karibu na Mwenyezi Mungu alipo kwenda miraji alishikwa na woga akiwa mbele, ghafl a akasikia sauti ya Abu Bakr moyo wake ukaingiwa na utulivu na akaliwazika kwa kusikia sauti ya swahibu wake.”

Mpaka hapa ninawaambia wale wanaotutuhumu kwa kuvuka mipaka kwa kusema tunavyo vitabu vyenu vinavyoelezea mambo kama haya bila kuongeza chochote. Sisi hatutaki kupoteza wakati wetu kwa kuya nukuu yote hayo na wala hatutaki kutekeleza malengo yenu ya

Page 38: Ukweli ni Huu - Shia Maktab

34

kuyaandika mambo hayo na kuyaeneza miongoni mwa Waislamu badala ya kuzishughulisha kalamu zenu kwa kutetea dini au kueneza mafundisho mazuri ya dini. Na sina shaka ya kuwa malengo ya watu wengi waliyoandika mambo hayo ni watu walio pandikiziwa shubuha zikawafanya wawe na lengo la kuufarikisha umma wa ki-Islamu. Na ni watu ambao ndani ya nyoyo zao kumejaa chuki ambazo ilikuwa ni lazima ziondoke kwa sababu ya kuwa kwao ni watu wenye kuamini. Chuki hizo zingeondoka tu kama wangekuwa na malengo mazuri ya kuwaita watu kwenye neno kumpwekesha Mwenyezi Mungu.

Na asitie dhanna yeyote ya kuwa tunayasema haya kwa kuogopa. Hakuna sababu ya kutufanya tuogope na hatuna matumaini ya kuwa mtarudi nyuma na kufanya uadilifu, isipokuwa wachache wenye nyoyo safi na wenye kuitaka haki. Kwa ajili yao tunatoa juhudi tunafanya juhudi ya kuyaandika haya ili waweze kunufaika huku tukimuomba Mwenyezi Mungu aliye tuhimiza na kutuadabisha kwa kusema: “Hakika umma wenu ni umma mmoja, nami ni Mola wenu, basi ni abuduni.” Ewe Mola hakika sisi tunakuabudu na wala hatu kushirikishi na chochote na tuna kiamini Kitabu Chako na Mtume wako Muhammad (s.a.w.w.) na dini yako. Wewe ni Mola wetu na Mtawala wetu tuenezee (utupe) Rehma zako ewe Mwingi wa kurehemu.

Page 39: Ukweli ni Huu - Shia Maktab

Kimetolewa na Kuchapishwa na:Bilal Muslim Mission of Tanzania

S.L.P. 20033 Dar es Salaam,Tanzaniaa

ISBN 9987 620 43 4