Ukweli ni huu,(kuusuta uwongo) -Aman Thani Fairooz

Embed Size (px)

Citation preview

  • 8/8/2019 Ukweli ni huu,(kuusuta uwongo) -Aman Thani Fairooz

    1/76

    1

    http://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli.html

    UKWELI NI HUU(KUUSUTA UWONGO)Aman Thani Fairooz

    DibajiKitabu HichiUkweli Ni Huu (Kuusuta Uwongo)Utukufu Na Neema Ya ZanzibarZanzibar Na Ubaguzi Kabla Ya MavamiziUbaguzi Umeanzishwa Zanzibar Wakati Wa Serikali Yenye Kujiita Ya "Mapinduzi"Elimu Na Matibabu Bure!TaalimuMatibabuHali Za MaishaNeema ZilikuwepoKuanza Harakati Za SiasaSheikh Ali Muhsin Kwenda Nchi Za Ulaya Ikiwemo Na Uingereza Kupigania Uchaguzi Wa "CommonRoll" (Mtu Mmoja Kura Moja).Kuasisiwa HizbulWattan (Zanzibar Nationalist Party)Wakoloni Dhidi Ya Hizbu, Uhuru Na Umoja Wa ZanzibarMakao Makuu Ya HizbuHizbu Kumleta Zanzibar Seyyid AbdulRahman (Babu)Natija Ya Safari Ya Sheikh Ali MuhsinWakoloni Na Nyerere Ndio Waasisi Wa AfroShiraziUchaguzi Wa Mwanzo Juni 1957Kwanini Sheikh Ali Muhsin Aliamua Kusimama N'gambo Badala Ya Majumba Ya Mawe?Kwenye Shari Huzaliwa KheriKukuwa Kwa Harakati Za SiasaAti Husemwa Kuwa Hizbu Imefeli!Kugawanyika Kwa AfroShirazi

    Kuasisiwa Kwa Zanzibar And Pemba Peoples' Party (ZPPP)Tume Ya Sir Hillary BloodUchaguzi Wa Pili, Januari 1961Uchaguzi Wa Tatu Juni 1961Ushirikiano Wa ZNP/ZPPPKutokufaulu Mazungumzo Ya Mwanzo Ya Katiba Ya UhuruAfroShirazi Iliandaa Machafuko Siku Ya UchaguziMuungano Wa ZNP/ZPPP, Waunda SerikaliKutokufaulu Mazungumzo Ya Mwanzo Ya Katiba Ya UhuruBabu Kutoka Katika HizbuDhamiri Za BabuKufungwa Gerezani Kwa Seyyid AbdulRahman BabuKutolewa Gerezani Babu

    Babu Na Fisadi Yake Ya MwishoKipi Kilicho Mpelekea Babu Kuchukua Khatua Kama HizoUchaguzi Wa Julai 1963Nyerere Anasema Wakoloni Walipendelea Kuiacha Serikali Ya Zanzibar Mikononi Mwa HizbuMkutano Wa Katiba Ya Uhuru.Uhuru Wa ZanzibarSherehe Za UhuruYaitwayo "Mapinduzi"Kuuliwa Kwa Muhsin, Suleiman Na Ahmed

    http://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli.htmlhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli.htmlhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli.html#DIBAJI#DIBAJIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli.html#DIBAJI#DIBAJIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli.html#KITABU%20HICHI#KITABU%20HICHIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli.html#KITABU%20HICHI#KITABU%20HICHIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli.html#UKWELI%20NI%20HUU#UKWELI%20NI%20HUUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli.html#UKWELI%20NI%20HUU#UKWELI%20NI%20HUUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli0.html#UTUKUFU%20NA%20NEEMAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli0.html#UTUKUFU%20NA%20NEEMAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli0.html#UBAGUZIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli0.html#UBAGUZIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli0.html#UBAGUZI%20MAPINDUZIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli0.html#UBAGUZI%20MAPINDUZIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli0.html#ELIMU%20NA%20MATIBABUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli0.html#TAALIMUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli0.html#TAALIMUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli0.html#MATIBABUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli0.html#MATIBABUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli0.html#HALI%20ZA%20MAISHAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli0.html#HALI%20ZA%20MAISHAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli0.html#NEEMA%20ZILIKUWEPOhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli0.html#NEEMA%20ZILIKUWEPOhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli1.html#KUANZA%20SIASAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli1.html#KUANZA%20SIASAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli1.html#SHEIKH%20ALIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli1.html#SHEIKH%20ALIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli1.html#SHEIKH%20ALIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli1.html#HIZBUL-WATTANhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli1.html#HIZBUL-WATTANhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli1.html#WAKOLONI%20DHIDIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli1.html#WAKOLONI%20DHIDIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli1.html#MAKAO%20MAKUUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli1.html#MAKAO%20MAKUUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli1.html#KUMLETA%20BABUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli1.html#KUMLETA%20BABUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli1.html#SAFARI%20YA%20%20ALI%20MUHSINhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli1.html#SAFARI%20YA%20%20ALI%20MUHSINhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli1.html#WAKOLONI%20NA%20NYEREREhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli1.html#WAKOLONI%20NA%20NYEREREhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli1.html#UCHAGUZI%201957http://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli1.html#UCHAGUZI%201957http://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli1.html#KUSIMAMA%20N'GAMBOhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli1.html#KUSIMAMA%20N'GAMBOhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli1.html#KWENYE%20SHARIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli1.html#KWENYE%20SHARIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli2.html#KUKUWA%20SIASAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli2.html#KUKUWA%20SIASAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli2.html#HIZBU%20IMEFELI!http://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli2.html#HIZBU%20IMEFELI!http://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli2.html#KUGAWANYIKA%20ASPhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli2.html#KUGAWANYIKA%20ASPhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli2.html#KUASISIWA%20ZPPPhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli2.html#KUASISIWA%20ZPPPhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli2.html#SIR%20HILLARY%20BLOOD.http://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli2.html#SIR%20HILLARY%20BLOOD.http://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli2.html#UCHAGUZI%20WA%20PILIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli2.html#UCHAGUZI%20WA%20PILIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli2.html#UCHAGUZI%20WA%20TATUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli2.html#UCHAGUZI%20WA%20TATUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli2.html#MUUNGANO%20%20ZNP/ZPPPhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli2.html#MUUNGANO%20%20ZNP/ZPPPhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli2.html#KUTOKUFAULU%20MAZUNGUMZOhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli2.html#KUTOKUFAULU%20MAZUNGUMZOhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli2.html#ASP%20Machafukohttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli2.html#ASP%20Machafukohttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli2.html#MUUNGANO%20%20ZNP/ZPPPhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli2.html#MUUNGANO%20%20ZNP/ZPPPhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli2.html#KUTOKUFAULU%20MAZUNGUMZOhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli2.html#KUTOKUFAULU%20MAZUNGUMZOhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli3.html#BABU%20KUTOKA%20HIZBUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli3.html#BABU%20KUTOKA%20HIZBUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli3.html#DHAMIRI%20ZA%20BABUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli3.html#DHAMIRI%20ZA%20BABUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli3.html#KUFUNGWA%20BABUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli3.html#KUFUNGWA%20BABUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli3.html#KUTOLEWA%20BABUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli3.html#KUTOLEWA%20BABUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli3.html#BABU%20FISADIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli3.html#BABU%20FISADIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli3.html#BABU%20KUCHUKUA%20KHATUAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli3.html#BABU%20KUCHUKUA%20KHATUAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli4.html#UCHAGUZI%20WA%20JULAI%201963http://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli4.html#UCHAGUZI%20WA%20JULAI%201963http://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli4.html#NYERERE%20ANASEMAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli4.html#NYERERE%20ANASEMAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli4.html#MKUTANO%20WA%20KATIBAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli4.html#MKUTANO%20WA%20KATIBAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli4.html#UHURUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli4.html#UHURUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli4.html#SHEREHEhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli4.html#SHEREHEhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli5.html#YAITWAYO%20MAPINDUZIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli5.html#YAITWAYO%20MAPINDUZIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli5.html#MUHSIN,%20SULEIMAN%20%20NA%20AHMEDhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli5.html#MUHSIN,%20SULEIMAN%20%20NA%20AHMEDhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli5.html#MUHSIN,%20SULEIMAN%20%20NA%20AHMEDhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli5.html#YAITWAYO%20MAPINDUZIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli4.html#SHEREHEhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli4.html#UHURUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli4.html#MKUTANO%20WA%20KATIBAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli4.html#NYERERE%20ANASEMAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli4.html#UCHAGUZI%20WA%20JULAI%201963http://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli3.html#BABU%20KUCHUKUA%20KHATUAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli3.html#BABU%20FISADIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli3.html#KUTOLEWA%20BABUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli3.html#KUFUNGWA%20BABUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli3.html#DHAMIRI%20ZA%20BABUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli3.html#BABU%20KUTOKA%20HIZBUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli2.html#KUTOKUFAULU%20MAZUNGUMZOhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli2.html#MUUNGANO%20%20ZNP/ZPPPhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli2.html#ASP%20Machafukohttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli2.html#KUTOKUFAULU%20MAZUNGUMZOhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli2.html#MUUNGANO%20%20ZNP/ZPPPhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli2.html#UCHAGUZI%20WA%20TATUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli2.html#UCHAGUZI%20WA%20PILIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli2.html#SIR%20HILLARY%20BLOOD.http://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli2.html#KUASISIWA%20ZPPPhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli2.html#KUGAWANYIKA%20ASPhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli2.html#HIZBU%20IMEFELI!http://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli2.html#KUKUWA%20SIASAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli1.html#KWENYE%20SHARIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli1.html#KUSIMAMA%20N'GAMBOhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli1.html#UCHAGUZI%201957http://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli1.html#WAKOLONI%20NA%20NYEREREhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli1.html#SAFARI%20YA%20%20ALI%20MUHSINhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli1.html#KUMLETA%20BABUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli1.html#MAKAO%20MAKUUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli1.html#WAKOLONI%20DHIDIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli1.html#HIZBUL-WATTANhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli1.html#SHEIKH%20ALIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli1.html#SHEIKH%20ALIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli1.html#KUANZA%20SIASAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli0.html#NEEMA%20ZILIKUWEPOhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli0.html#HALI%20ZA%20MAISHAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli0.html#MATIBABUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli0.html#TAALIMUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli0.html#ELIMU%20NA%20MATIBABUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli0.html#UBAGUZI%20MAPINDUZIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli0.html#UBAGUZIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli0.html#UTUKUFU%20NA%20NEEMAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli.html#UKWELI%20NI%20HUU#UKWELI%20NI%20HUUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli.html#KITABU%20HICHI#KITABU%20HICHIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli.html#DIBAJI#DIBAJIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli.html
  • 8/8/2019 Ukweli ni huu,(kuusuta uwongo) -Aman Thani Fairooz

    2/76

    2

    Kifo Cha Ali Mzee Mbalia"Skolashipu" Za MisriYaliyo Nifika Nafsi Yangu Na Hayo Yenye Kuitwa "Mapinduzi"Maafa Ya GerezaniKufungwa Kifungo Cha Miaka 10 GerezaniKiasi Cha Kazi Alichokuwa Akifanyishwa MfungwaMaovu Waliyotendewa "Wafungwa Wa Kisiasa"Kutolewa GerezaniNakimbilia DarEsSalaamMahabusi Wadhulumiwa Wa Mwalimu NyerereMateso Ya "Kwa Ba Mkwe"Maisha Ya Gereza LangoniNyakati Za Kufanyishwa Kazi "Wafungwa Wa Sisasa"Ufungwa Wa Karume Ni Zaidi Ya UtumwaKurejeshewa Uhuru WetuKuuliwa Wananchi MsikitiniKuuliwa Kwa Wananchi WengineNamna Walivyo UliwaWafungwa Waliyokufa Gerezani(1) Mzee Mohammed Mbaba(2) Maalim Harun Ustadh(3) Idi Hassan(4) Ramadhan Ibrahim SaadallaWameuliwa VifungoniWafungwa Wengine Wauliwa"Wafungwa Wa Siasa" Bado Waendelea KuuliwaAliyonizungumziya TwalaYalomfika Othman ShariffKuteswa Na Kuuliwa Othman ShariffKufungwa Na Kuuliwa Saleh SaadallaKarume Kuanza Kumbadilikia TwalaMwisho Wa TwalaMakomred Wamechangia Maafa Yaliopo Nchini

    Kwanini Mwalimu Nyerere Alikataa Kuwapeleka Zanzibar Watuhumiwa Wa Kesi Ya Ukhaini?Siri Hii Ni Kubwa Sana!!Serikali Ya Mavamizi Ya Zanzibar Bado Imo Na Ubaguzi WakeNilitakiwa Nitoke NchiniNamna Nilivyoondoka Kuukimbia Wattani WanguKuleta Ahli Zangu DubaiMengineyo Kwa UfupiMwalimu Na UislamuMwalimu Na UtumwaPorojo La MitaaniDemokrasi Ya Vyama Vingi (MultiParty Democracy)Vipi Kuifikilia DemokrasiShukrani

    DIBAJINamshukuru Mwenye Enzi Mungu Mwenye Wingi wa Rehema Kubwa na Ndogo kuniwezesha kuandikakijitabu hiki ambacho nimejaribu kiasi nilichoweza kuyaeleza yale yaliyotokea katika Nchi yetu,Zanzibar. Na yaliyonitokelea mimi mwenyewe na yaliyowatokelea Wananchi wenzangu kutokana nahayo yenye kuitwa, "Mapinduzi" yaliyofanyika katika Visiwa vyetu mnamo taarikh 12 Januari, 1964.Haya ninayoyaandika ni kiasi ya hayo niyajuayo mimi tu; hapana shaka yapo mengi ambayo sikupatakuyajuwa. Bali nataraji watatokea wenzangu nao, wakayaeleza waliyotendewa au waliyoyaonayakitendwa.

    http://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli5.html#ALI%20MZEEhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli5.html#ALI%20MZEEhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli5.html#SKOLASHIPUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli5.html#SKOLASHIPUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli6.html#YALIYO%20NIFIKAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli6.html#YALIYO%20NIFIKAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli6.html#MAAFA%20YA%20GEREZANIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli6.html#MAAFA%20YA%20GEREZANIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli6.html#KUFUNGWA%20MIAKA%2010http://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli6.html#KUFUNGWA%20MIAKA%2010http://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli6.html#KAZI%20MFUNGWAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli6.html#KAZI%20MFUNGWAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli6.html#MAOVU%20WALIYOTENDEWAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli6.html#MAOVU%20WALIYOTENDEWAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli6.html#KUTOLEWA%20GEREZANIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli6.html#KUTOLEWA%20GEREZANIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli6.html#NAKIMBILIAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli6.html#NAKIMBILIAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli7.html#MAHABUSI%20WADHULUMIWAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli7.html#MAHABUSI%20WADHULUMIWAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli7.html#KWA%20BA%20MKWEhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli7.html#KWA%20BA%20MKWEhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli7.html#GEREZA%20LANGONIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli7.html#GEREZA%20LANGONIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli7.html#NYAKATI%20ZA%20KUFANYISHWA%20KAZIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli7.html#NYAKATI%20ZA%20KUFANYISHWA%20KAZIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli7.html#UFUNGWA%20WA%20KARUMEhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli7.html#UFUNGWA%20WA%20KARUMEhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli8.html#KUREJESHEWA%20UHURU%20WETUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli8.html#KUREJESHEWA%20UHURU%20WETUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli8.html#KUULIWA%20WANANCHI%20MSIKITINIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli8.html#KUULIWA%20WANANCHI%20MSIKITINIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli8.html#KUULIWA%20KWA%20WANANCHI%20WENGINEhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli8.html#KUULIWA%20KWA%20WANANCHI%20WENGINEhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli8.html#NAMNA%20WALIVYO%20ULIWAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli8.html#NAMNA%20WALIVYO%20ULIWAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli8.html#WAFUNGWA%20WALIYOKUFA%20GEREZANIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli8.html#WAFUNGWA%20WALIYOKUFA%20GEREZANIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli8.html#WAFUNGWA%20WALIYOKUFA%20GEREZANIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli8.html#WAFUNGWA%20WALIYOKUFA%20GEREZANIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli8.html#WAFUNGWA%20WALIYOKUFA%20GEREZANIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli8.html#WAFUNGWA%20WALIYOKUFA%20GEREZANIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli8.html#WAFUNGWA%20WALIYOKUFA%20GEREZANIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli8.html#WAFUNGWA%20WALIYOKUFA%20GEREZANIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli8.html#WAFUNGWA%20WALIYOKUFA%20GEREZANIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli8.html#WAFUNGWA%20WALIYOKUFA%20GEREZANIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli8.html#WAMEULIWA%20VIFUNGONIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli8.html#WAMEULIWA%20VIFUNGONIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli8.html#WAFUNGWA%20WENGINEhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli8.html#WAFUNGWA%20WENGINEhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli8.html#WAFUNGWA%20WA%20SIASA%20WAULIWAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli8.html#WAFUNGWA%20WA%20SIASA%20WAULIWAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli9.html#ALIYONIZUNGUMZIYA%20TWALAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli9.html#ALIYONIZUNGUMZIYA%20TWALAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli9.html#YALOMFIKA%20OTHMAN%20SHARIFFhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli9.html#YALOMFIKA%20OTHMAN%20SHARIFFhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli9.html#KUTESWA%20NA%20KUULIWA%20OTHMAN%20SHARIFFhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli9.html#KUTESWA%20NA%20KUULIWA%20OTHMAN%20SHARIFFhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli9.html#KUFUNGWA%20NA%20KUULIWA%20SALEH%20SAADALLAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli9.html#KUFUNGWA%20NA%20KUULIWA%20SALEH%20SAADALLAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli9.html#KARUME%20KUMBADILIKIA%20TWALAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli9.html#KARUME%20KUMBADILIKIA%20TWALAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli9.html#MWISHO%20WA%20TWALAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli9.html#MWISHO%20WA%20TWALAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli10.html#MAKOMRED%20WAMECHANGIAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli10.html#MAKOMRED%20WAMECHANGIAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli10.html#NYERERE%20ALIKATAA%20KUWAPELEKAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli10.html#NYERERE%20ALIKATAA%20KUWAPELEKAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli10.html#SIRI%20HII%20NI%20KUBWA%20SANA!!http://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli10.html#SIRI%20HII%20NI%20KUBWA%20SANA!!http://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli10.html#SERIKALI%20BADO%20IMO%20NA%20UBAGUZIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli10.html#SERIKALI%20BADO%20IMO%20NA%20UBAGUZIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli11.html#NILITAKIWA%20NITOKE%20NCHINIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli11.html#NILITAKIWA%20NITOKE%20NCHINIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli11.html#KUUKIMBIA%20WATTANI%20WANGUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli11.html#KUUKIMBIA%20WATTANI%20WANGUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli11.html#KULETA%20AHLI%20ZANGU%20DUBAIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli11.html#KULETA%20AHLI%20ZANGU%20DUBAIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli12.html#MENGINEYO%20KWA%20UFUPIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli12.html#MENGINEYO%20KWA%20UFUPIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli12.html#Mwalimu%20Na%20Uislamuhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli12.html#Mwalimu%20Na%20Uislamuhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli12.html#Mwalimu%20Na%20UTUMWAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli12.html#Mwalimu%20Na%20UTUMWAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli12.html#POROJO%20LA%20MITAANIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli12.html#POROJO%20LA%20MITAANIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli12.html#DEMOKRASI%20YA%20VYAMA%20VINGIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli12.html#DEMOKRASI%20YA%20VYAMA%20VINGIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli12.html#VIPI%20KUIFIKILIA%20DEMOKRASIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli12.html#VIPI%20KUIFIKILIA%20DEMOKRASIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli12.html#SHUKRANIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli12.html#SHUKRANIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli12.html#SHUKRANIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli12.html#VIPI%20KUIFIKILIA%20DEMOKRASIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli12.html#DEMOKRASI%20YA%20VYAMA%20VINGIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli12.html#POROJO%20LA%20MITAANIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli12.html#Mwalimu%20Na%20UTUMWAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli12.html#Mwalimu%20Na%20Uislamuhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli12.html#MENGINEYO%20KWA%20UFUPIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli11.html#KULETA%20AHLI%20ZANGU%20DUBAIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli11.html#KUUKIMBIA%20WATTANI%20WANGUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli11.html#NILITAKIWA%20NITOKE%20NCHINIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli10.html#SERIKALI%20BADO%20IMO%20NA%20UBAGUZIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli10.html#SIRI%20HII%20NI%20KUBWA%20SANA!!http://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli10.html#NYERERE%20ALIKATAA%20KUWAPELEKAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli10.html#MAKOMRED%20WAMECHANGIAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli9.html#MWISHO%20WA%20TWALAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli9.html#KARUME%20KUMBADILIKIA%20TWALAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli9.html#KUFUNGWA%20NA%20KUULIWA%20SALEH%20SAADALLAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli9.html#KUTESWA%20NA%20KUULIWA%20OTHMAN%20SHARIFFhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli9.html#YALOMFIKA%20OTHMAN%20SHARIFFhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli9.html#ALIYONIZUNGUMZIYA%20TWALAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli8.html#WAFUNGWA%20WA%20SIASA%20WAULIWAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli8.html#WAFUNGWA%20WENGINEhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli8.html#WAMEULIWA%20VIFUNGONIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli8.html#WAFUNGWA%20WALIYOKUFA%20GEREZANIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli8.html#WAFUNGWA%20WALIYOKUFA%20GEREZANIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli8.html#WAFUNGWA%20WALIYOKUFA%20GEREZANIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli8.html#WAFUNGWA%20WALIYOKUFA%20GEREZANIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli8.html#WAFUNGWA%20WALIYOKUFA%20GEREZANIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli8.html#NAMNA%20WALIVYO%20ULIWAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli8.html#KUULIWA%20KWA%20WANANCHI%20WENGINEhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli8.html#KUULIWA%20WANANCHI%20MSIKITINIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli8.html#KUREJESHEWA%20UHURU%20WETUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli7.html#UFUNGWA%20WA%20KARUMEhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli7.html#NYAKATI%20ZA%20KUFANYISHWA%20KAZIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli7.html#GEREZA%20LANGONIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli7.html#KWA%20BA%20MKWEhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli7.html#MAHABUSI%20WADHULUMIWAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli6.html#NAKIMBILIAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli6.html#KUTOLEWA%20GEREZANIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli6.html#MAOVU%20WALIYOTENDEWAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli6.html#KAZI%20MFUNGWAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli6.html#KUFUNGWA%20MIAKA%2010http://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli6.html#MAAFA%20YA%20GEREZANIhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli6.html#YALIYO%20NIFIKAhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli5.html#SKOLASHIPUhttp://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli5.html#ALI%20MZEE
  • 8/8/2019 Ukweli ni huu,(kuusuta uwongo) -Aman Thani Fairooz

    3/76

    3

    Nafanya haya si kwa makusudio yoyote mengine zaidi ya kutaka kueleza ukweli wa yaliyotendeka katikaNchi yetu ili Wananchi wenzangu (na ndugu zetu wa Tanganyika, bali na ulimwengu, pia) na khasa walewaliokuwa wadogo, na wale ambao hawajaja duniani wakati huo waweze kuyafahamu japo kwauchache yaliyotendeka katika Nchi yao kwa hayo yenyekuitwa "Mapinduzi". Ikiwa katika kuyaelezeahaya, kutahitajia kumtaja mtu au watu kwa njia yoyote, itakuwa nafanya hivyo kwa kutokana namaudhui ninayo izungumza wala si kwa ajili ya kusengenya au kukejeli au kudharau au kwa kutia illa zanamna fulani, hashaa! Bali kwa vile dhamiri ya kukiandika kijitabu hiki ni kuelezea ukweli wa mamboyalivyokuwa, basi sitochelea kulieleza lolote madhali kwa kufanya hivyo ndio itakuwa natimiliza lengonililolikusudia, nalo ni kuueleza ukweli. Kutokana na hayo, nachukuwa nafsi yangu masuliya yoteyatayotokea katika maandishi haya.

    Muhimu, nawaomba wasomaji wangu wajishughulishe zaidi na hayo niliyokusudia kuyaeleza, kwani hayohayana shaka yoyote, ni kweli tupu. Na nawaomba wasijishughulishe na makosa madogo madogo, kamavile ya upigaji chapa, makosa ya lugha au juu ya utaratibu wa uwandishi. Ikiwa litatokea suala lolote,au ikiwa lolote halitafahamika, basi wakurejelewa ni mimi. Inshallah, nitajaribu kama nitavyowezakutanzua kila lililotanzika na ikiwa nitashindwa, basi sitoona taabu kutaka msamaha. Mwenyekukamilika kwa yote ni Mwenye Enzi Mungu. Tunamuomba Mwenye Enzi Mungu ajaaliye hayatunayoyaeleza yapate kusomwa, kuzingatiwa na kufahamika na ipatikane faida ndani yake kwakutumiwa kwa kheri. Kubwa ya kheri hizo ni kusahihisha palipo haribika, kuiondosha haramu, kuombatoba na kutenda mema, kwani mema huondowa mabaya. Mwenye Enzi Mungu atupe taufiq, Amin.

    Aman Thani FairoozP.O. Box 10836Telephone 04850802Dubai United Arab EmiratesJanuari, 1995

  • 8/8/2019 Ukweli ni huu,(kuusuta uwongo) -Aman Thani Fairooz

    4/76

    4

    KITABU HICHIKidogobasi, Chungutamu.Kwa hakika Kitabu hichi ni kidogo basi. Lakini, kama alivyosema muandishi kuwa kaandika kwaufupi, bali ufupi wa kutosheleza faida yake. Yoyote atakaye kisoma kitabu hichi kwa kutakakufahamu na bila ya mawazo yake kudhibitiwa na kupenda au kuchukiya, basi hapana shakaatapata faida. Atafahamu jinsi wananchi wa Zanzibar walivyokuwa katika harakati zao zakuwania uhuru wa nchi yao kutokana na ukoloni wa Muingereza. Harakati ambazo zalianzakabla ya miaka ya 1940. Pia ataweza kufahamu ni nani walioanzisha harakati hizo, namnazilivyopata kuungwa mkono na wananchi na namna zilivyokuwa zikiendeleya. Pia atapatakufahamu jinsi ya pingamizi zilivyokuwa. Atafahamu pingamizi hizo zilivyoanzia, nanialiyezianzisha na kuzipalilia na kuzikuza. Atafahamu natija yake! Pia atafahamu vipi wananchichini ya uwongozi wa vyama vyao ZNP/ZPPP walivyokuwa wakizikabili pingamizi hizo. Na zaidiatafahamu juhudi za waongozi wa ZNP/ZPPP katika kutaka mafahamiano na ushirikiano nawananchi wenziao ASP na nini ulikuwa muelekeo wa waongozi wa ASP, muelekeo ambao maranyingi ulikuwa ukiathirika kwa uwongozi na fikra zilizokuwa zikipangwa na kuletwa kutoka njeya nchi.

    Chungutamu. Kweli ni chungu! Lakini ni wajibu isemwe na kubainishwa. Uchungu uliyomo ndaniya kitabu hichi ni kuona jinsi wananchi walivyohangaika kwa jasho, mali na hata damu zao kwakuwania uhuru wao kutokana na ukoloni wa Muingereza, lakini kwa sababu ya husda, chuki naufisadi uhuru huo haukuachiwa kuishi zaidi ya siku thalathini! Isitoshe, sio kuwa uhuru huoulipotezwa kwa kutumiliwa njiya za usalama, sivyo, bali kwa fujo! Fujo ambalo natija yake nikupotezwa Dola ya Zanzibar, roho za wananchi, heshima ya binaadamu, mali za watu namwisho kuwachwa wananchi kuishi ndani ya haramu. Utamu japo kwa hakika sio utamu ni kwavile kuweza wananchi kupata kuufahamu UKWELI ambao kwa muda wa zaidi ya miaka thalathiniumekuwa ukifunikwa kwa UWONGO. Lakini, kama yalivyo maumbile, kweli daima huibuka.

    Tunamshukuru Mwenye Enzi Mungu kwa kudhihiri kitabu hichi na kuweza kuufahamisha umma,bali na ulimwengu, maafa yaliofikishiwa Zanzibar, Nchi na Wananchi. Msomaji, na pengine hataasimuliwaye haya, huenda akasema, yaaleiti yalielezwa haya kiasi cha miaka ishirini liyopita,au kabla ya hapo. Hivyo ni kweli! Lakini kila kitu kwa majaaliwa, na kuchelewa kwengine kunakheri zake kama kwengine kunavyo shari zake. Kheri katika kuchelewa kudhihiri kitabu hichi nikuwa vijana waliokuwa wadogo wakati wa maafa ya Zanzibar leo ni watu wazima, wenye uwezo

    wa kufikiri, kuamua na kutenda. Kwa hivyo wanahitajia kuujuwa Ukweli. Wao si kwa ajili yaKuusuta Uwongo, hashaa!! Bali ni kwa ajili ya kuujuwa ukweli, kisha iwe ni mafunzo kutokanana yaliotendeka. Watasoma, na Inshallah watayafahamu na kuyatumia. Na haya ndio khasamakusudio na faida ya kitabu hichi. Kutumia kwao huko kwanza iwe ni kwa kuepushayasitendeke tena maafa yaliyotendwa, kufuatilia hilo au yote mawili sambamba ni kwakufanyakazi katika kujenga palipo bomolewa. Kubomowa daima ni rahisi kuliko kujenga,kujenga kunataka umoja na ushirikano wa kila mmoja wetu. Kwa hivyo ni waajibu wa kilammoja wetu kushirikiana, bega kwa bega, kwa nia na nguvu moja kufanyakazi kuirejeshaZanzibar. Kwanza, kuirejesha katika ramani ya ulimwengu ili iwe na jina na pahala pake kuwani Dola kaamili na iliyo huru. Kisha, bali ndio la muhimu, kuirejesha katika neema zake.

    Hichi ni kitabu cha kusomwa na kila Mzanzibari, bali na ndugu zetu wa Tanganyika, pia.Abdulla Ali (Baba)

  • 8/8/2019 Ukweli ni huu,(kuusuta uwongo) -Aman Thani Fairooz

    5/76

    5

    UKWELI NI HUU (KUUSUTA UWONGO)

    Nimelichagua jina hili la UKWELI NI HUU KUUSUTA UWONGO, baada ya kuyasikia na kuyasoma me ngi yauwongo na hata yakafika kusomeshwa watoto wetu katika maskuli ya Zanzibar kukhusu hayo yenyekuitwa "MAPINDUZI" yaliyofanyika katika visiwa vyetu vya Zanzibar mnamo taarikh 12 Januari 1964.Kabla ya kuingia katika hayo, ningependa ku waambia wasomaji wangu wote kuwa mimi si mjuzi hatakidogo wa fani hii ya uandishi; tena ni mbovu sana katika "spellings" na ka tika "nahau" za Kiswahili chakisasa. Pia nawaomba radhi kwa Kiswahili changu cha kizamani. Bali, kutokana na huo uzushi nakupotezwa kwa makusudi ukweli wa hayo yaliofanyika kukhusu hayo yenye kuitwa "mapinduzi" nimeonasina budi illa ni kujitolea hivyo hivyo juu ya upungufu wangu katika fani hii ya uandishi. Lakini ukwelilazima niudhihirishe ili vichipukizi vyetu viweze kuyaelewa vilivyo yaliyotendeka katika nchi yao. Kwaniwengi walikuwa wadogo na wengine walikuwa hata hawajazaliwa katika wakati huo.

    Ilivyokuwa Kiswahili ni lugha yangu ya kuzaliwa, basi ninaiandika kama ninavyoisema. Si shughuliki na"kua au kuwa, aliniambia au aliniambiya, ameuawa au ameuwawa kenda au kaenda, amekwenda auameenda". Hayo kwa wataalamu wa lugha ni mambo muhimu lakini kwa mimi nakutakeni msamaha juuya hayo. Muhimu ya kuyaangaliya na kuyazingatiya ni yale nikusudiayo kuyaeleza, kwani hayo ndiomuhimu na ndio ya kweli tupu isiyokuwa na dosari hata chembe.

    La mwanzo nitakalo kuombeni mlifahamu uzuri ni ile hakika kuwa hayo yaliyofanyika katika visiwavyetu taarikh 12 Januari 1964, hayakuwa "MAPINDUZI" wala hayafai hata kidogo kuitwa 'mapinduzi' kwamaana asili ya neno. Bali kwa maana zote yalikuwa khasa ni "MAVAMIZI", yaani kwa Kiingereza"INVASION". Mapinduzi lazima yapangwe, yaongozwe na yatekelezwe na wananchi wenyewe kwamaslaha ya nchi na wananchi wake. Sasa tukiangalia hayo yaliotendeka Zanzibar, yalipangwa,yaliongozwa na yalitekelezwa na WAGENI kutoka nchi za nje za jirani zetu. (Ni wao wala si wananchindio waliochukua ngawira kubwa kubwa). Haya yanathibitika zaidi kwa vile kuwa huyo jamadarialiyeyaongoza hayo 'mavamizi' ni John Okello na wa chini yake walikuwa Injini na Mfaranyaki. Nani katiya hao aliyekuwa kitovu chake kimezikwa visiwani? Okello amezaliwa na amekulia kwao Uganda, Injiniamezaliwa na amekuliya kwao Kenya na Mfaranyaki amezaliwa na amekuliya kwao Tanganyika. Wotehao walikuja Zanzibar wakiwa watu wazima na shughuli zao, wamekuja kutafuta kibarua na kukimbiakodi za kichwa katika nchi zao.

    Liangalie hilo waliloliita "Baraza la Mapinduzi". Utaona sehemu kubwa ya wanachama wa Baraza hilo

    walikuwa si Wazanzibari, laa kwa kuzaliwa wala kwa kuchukua Tajnisi (Kuandikisha Uraia). John Okello,Khamis Darweshi, Seif Bakari, Said Natepe, Said Washoto, Muhammed Mfaume, Edington Kisasi,Mohammed Abdalla Kaujore. Ukiwaacha wengineo ambao nao vile vile walikuwa si wananchi waZanzibar kwa kuzaliwa, bali wao walikuja Zanzibar wakiwa katika migongo ya wazee wao nawaliendelea kuishi humo visiwani kwa maisha yao yote. Na wakachukuliwa kama ni Wazanzibari.

    UTUKUFU NA NEEMA YA ZANZIBARMwenyezi Mungu amevipa visiwa hivi viwili yaani Unguja na Pemba bahati ya utukufu kwa kila jambolake. Hayo yaliendelea tokea karne na karne mpaka pale ulipotendwa ufisadi wa taarikh 12 Januari1964, ndipo neema na utukufu wa Zanzibar ulipoanza kutoweka. Hapo tena, badala ya zumari kuwalikipulizwa Zanzibar, watu wa maziwani (Bara) walikuwa wakihemkwa, ikawa linapulizwa Bara, tuliopovisiwani tunahemkwa!

    ZANZIBAR NA UBAGUZI KABLA YA MAVAMIZINathubutu kusema bila ya wasiwasi wowote kuwa Zanzibar hakukuwepo ubaguzi wa namna yoyote kwamaana khasa na ya wazi ya neno UBAGUZI. Kwanza Wazanzibari ni watu waliochanganya sana damuhata sio rahisi kuweza kumtambua mtu kuwa ni mwenye kutokana na asili ya kabila fulani kwakuangalia rangi yake au pua yake au masikio yake au kimo chake au kwa jina lake. Jee, watu haowatabaguana namna gani? Malipo ya wafanyakazi serikalini yalikuwa hayakupangwa kiukabila. Walaserikali haikuwa na sehemu maalumu katika maskuli wala katika mahospitali kuwa zimetengwa kwaajili ya watu wa makabila fulani.

  • 8/8/2019 Ukweli ni huu,(kuusuta uwongo) -Aman Thani Fairooz

    6/76

    6

    Katika nchi za jirani zetu, Tanganyika, Kenya na Uganda kote huko kulikuwepo na ubaguzi uliyokuwaukiongozwa na serikali za nchi hizo. Malipo ya mishahara ya wafanyakazi yalikuwa yakilipwa kutokanana makabila yao wala si kutokana na ujuzi wao wa kazi. Kulikuwepo "African Scale, Asian Scale naEuropean Scale". Madaktari, Mainjinia, Waalimu na wowote nawawe wana elimu na ujuzi na maarifa yanamna moja, yaani wote sawa sawa kwa elimu na ujuzi wa kazi zao, lakini mishahara yao ilikuwatafauti kutokana na makabila yao. Waafrika ndio wenye kulipwa malipo ya chini kabisa kuliko wote.Wazungu walikuwa ndio wenye kulipwa mishahara minono (hata baadhi yao walikuwa hawana elimuyoyote isipokuwa huwo Uzungu wao), waliowafuatia ni Waasia.

    Vyoo vya njiani (Public Toilets) na sehemu za kungojelea usafiri wa reli navyo vile vile vilikuwavikitumika kwa ubaguzi wa kikabila. Waafrika waliekewa vyoo vyao na sehemu zao za kungojeleausafiri. Wazungu walikuwa na sehemu zao na Waasia walikuwa na sehemu zao, wote mbali mbali.Lilikuwa ni kosa na kuvunja sheria ikiwa imetokea kwa yoyote kuingia katika sehemu isiyo kuwaamekhusika nayo. Khasa Muafrika awe ameingia au amekaa katika sehemu za Waasia au za Wazungu.Katika Tanganyika, Kenya na Uganda kote huko kulikuwa na Kodi ya Kichwa. Kodi hiyo ilikuwa ikilipwana kila mtu aliyekwishafika balegh katika umri wake. Nayo pia ikitekelezwa kwa njia za ubaguzi wakikabila. Waasia na Wazungu, wao hata ikiwa wamechelewa kulipa kodi zao, basi walikuwahawakamatwi majiani wala hawaendewi majumbani mwao kukamatwa. Lakini, Waafrika walikuwawakisakwa majiani na wakiendewa majumbani mwao mnamo pinga pinga za usiku. Na wakikamatwa,basi walikuwa wakifungwa kamba za viunoni au hufungwa ncha ya shati la huyu na la huyu kishawalikuwa wakiongozwa mmoja nyuma ya mmoja na huku wakipigwa mateke na kusukumwa mpakawakifikishwa Bomani. Huko ikiwa hawatokuwa na cha kulipa basi walikuwa wakihukumiwa na kufungwa.Kutokana na hali kama hizo, ndipo wengi kati ya wananchi wa nchi hizo, khasa kutoka Tanganyikawalikimbia kutoka makwao na kuhamia Zanzibar kwa sababu ya kufuata hali njema za kimaisha.Zanzibar hakukuwepo kodi za kichwa wala ubaguzi wa vyooni wala malipo ya mishahara wala wa namnayo yote. Ilikuwa njema atakae naaje.

    UBAGUZI UMEANZISHWA ZANZIBAR WAKATI WA SERIKALI YENYE KUJIITA YA "MAPINDUZI"Mara tu baada ya kufika hiyo serikali ya 'mavamizi' katika Zanzibar ubaguzi wa ukabila ulianzishwa. Kila"mrangi rangi" kama walivyokuwa wakiwaita wenyewe, yaani wenye asili za Kiarabu, za Kihindi na zaKingazija walianza kutolewa makazini bila ya kupewa hata haki zao za ufanyaji wa kazi. Mashamba,majumba na hata mabiashara yao yalichukuliwa kwa nguvu na kupewa wageni ikiwa ni tunzo la ukatilina maovu waliyowafanyia wananchi katika nchi yao. Serikali ya 'mavamizi' ya Zanzibar ilitangaza rasmi

    kupitia vyombo vya khabari vya serikali kukhusu ubaguzi katika Taalimu. Waafrika, wakipasi au wasipasibali idadi yao ya kuingia katika "Form One" ya "secondary school" ilikuwa ni 77 katika mia (77%),Waarabu 16 katika asili mia (16%), Wahindi 6 katika mia (6%), na Wangazija MMOJA katika mia! (1%).Si hayo tu, bali serikali ya 'mavamizi' imetumia fedha za umma kwa ajili ya kujijengea hospitali yao waotu Wanachama wa Baraza la Mapinduzi na familia zao na wameita, "Mapinduzi Wing". Vitanda,mabetishiti, foronya za mito, vyombo vya kulia kama sahani, vikombe, visu na nyuma (forks) vyoteviliagiziwa kutoka Ulaya. Ilikuwa ikitokea Mheshimiwa kulazwa huko, basi na mkewe alikuwa akihamiahuko huko na kulala kitanda kimoja kama kwamba wamo katika siku za fungati! Haya yakitendekawakati wananchi wanyonge hawana hata dawa mahospitalini! Huo ulikuwa ndio usawa, sio ubaguzi!

    ELIMU NA MATIBABU BURE!Tunaambiwa na serikali yenye kujiita ya 'mapinduzi' kuwa elimu na matibabu yameanza kuwa bure kwawananchi baada ya kupatikana kwa Serikali ya 'mapinduzi'! Huu ni uwongo uliokuwa hauna hata

    kifuniko. Toka lini elimu na matibabu yalikuwa kwa malipo katika Zanzibar? Tangu kuanzishwa kwaskuli ya serikali na Sayyid Ali bin Hamoud na toka kuanzishwa kwa matibabu katika mahospitali, kamwehayajapata kuwa ya malipo. Toka kwa kuangaliwa na madaktari mpaka kwa madawa, chakula, nampaka kulala kwa kutibiwa katika mahospitali kulikuwa bure.

    TAALIMUWananchi na wageni, kuanzia chumba cha kwanza yaani (standard one) mpaka kufikia chumba cha nane(standard eight), masomo yalikuwa bure kwa wote. Sio hivyo tu, kila mwanafunzi alikuwa na deski lakepeke yake la kukalia na kila mwanafunzi alikuwa akipewa madaftari ya kuandikia bure, vitabu vya

  • 8/8/2019 Ukweli ni huu,(kuusuta uwongo) -Aman Thani Fairooz

    7/76

    7

    kusomea bure, kalamu za kuandikia bure, vidawa vya wino na wino wake bure hata blotting papers (lakukaushia wino) pia wakipewa bure. Na kila Ijumaa wanafunzi walikuwa wakipewa sabuni za kufuliabure. Skuli za mashamba, wanafunzi walikuwa wakipewa kifungua kinywa kunde na uji kabla yakuingia katika vyumba vya masomo, bure.

    Kuanzia chumba cha tisa mpaka cha 12, na baada ya muda katika miaka ya 1950 kuanzia chumba chasaba mpaka cha 12, wazee walitakiwa wasaidie kitu kidogo katika masomo ya watoto wao. Malipo hayoyalikuwa ya kitu kidogo sana na si kila mzee alikuwa akilipa ada hizo. Wengi sana katika wazeewalikuwa hawalipi hata senti moja. Na hao waliokuwa wakilipa, wengi wao walikuwa wakilipa kuanziaShs. tano mpaka Shs. 20 kwa wingi kila baada ya miezi mitatu au mine. Kabla ya mzee kuwa alipe auasilipe, kulikuwepo taratibu maalumu zilizokuwa zikifanywa. Mzee wa mtoto alikuwa akipelekewa"questionnaire" (karatasi) yenye masuala yaliyokhusu mapato yake, kazi yake na idadi ya watu wake wanyumbani. Kwa kutaka kuhakikisha uwezo wa mzee huyo, basi akipelekewa waraka huo kwanza Shehawa mtaa kuhakikisha yale yalioandikwa na akisha Sheha humpelekea Mudiri wake na Mudiri humpelekeaD.C. wake. Baada ya khatuwa hizi ndio tena hapo hutolewa uamuzi wa kulipa au wa kutokulipa, nakama kulipa alipe kiwango gani.

    Kutokana na mipango kama hiyo, zaidi ya 70 katika mia (70%) ya wazee watoto wao walikuwa wakisomabila ya kulipiwa kitu chochote na kiasi cha 20 katika mia (20%) walikuwa wakilipiwa kitu kidogo na kiasicha 10 katika mia (10%) ndio waliyokuwa wakilipiwa idadi kamili ambayo ilikuwa chini ya Shillingi 200,kwa mwaka mzima. Wengi waliokuwa wakilipa kima hicho, walikuwa ni wazee wenye asili za Kihindi.Wanaoitwa Waafrika na wanaoitwa Waarabu hayo yalikuwa si maji yao. Muhimu katika hayo si kulipa aukuto kulipa, muhimu ni thamani (quality) ya elimu iliyokuwa ikipatikana siku hizo, jee leo inapatikana?Hilo ndilo suala muhimu la kujiuliza na kulizingatia. Ikiwa hiyo isemwayo leo kuwa elimu bure, naimekuwa wanafunzi hawana madeski ya kukalia, hawana vitabu vya kusomea, wala chochote chakusomea, bali zaidi hawana hata walimu wenye ujuzi wa kusomesha; basi bure kama hiyo ni "bureghali". Kwa hiyo bure, basi watoto wetu leo wametokwa na vibyongo kwa kuinama wakati wa kuandika.Wakirejea kutoka maskuli utadhania wanatoka kuchimba makaburi kwa mavumbi yalivyo watapakaakwa kusota chini.

    Elimu bure! Wanafunzi wakipotezewa wakati wao wa masomo kwa kuchezeshwa ngoma za sindimba nakuimbishwa majimbo ya kanisani ati huitwa, "Kwaya". Kuanzia Disemba wanafunzi walikuwawakianzishwa mazowezi ya kucheza ngoma na kuimba hizo kwaya pamoja na magwaride kwa ajili ya

    kujiweka tayari kwa sherehe za hayo yenye kuitwa 'mapinduzi' katika mwezi wa Januari. Wakimaliza tu,hawawahi hata kushusha pumzi wanangojewa kwa sherehe za kuasisiwa kwa Chama cha AfroShirazi, 22 (February 2). Wakimaliza tu, hawawahi hata kunywa maji, wanazolewa tena kwa mazowezi yasherehe za "Muungano" April 26. Hawawahi hata kukaa kitako, wanabebwa tena kwa mazowezi yaSikukuu ya Wafanyakazi "May Day". Hapo hupumua kidogo kisha huzolewa tena kwa mazowezi yakusherehekea, "Saba Saba", July 7. Hawawahi hata kwenda chafya, hunyakuliwa tena kwa mazowezi yasherehe za "Elimu Bure"! Septemba. Wakimaliza hapo wanazolewa tena kwa mazowezi ya sherehe za"Uhuru wa Tanganyika" Desemba. Ukiangalia utaona kuwa mwaka mzima badala ya watoto wetukusomeshwa, walikuwa wakichezeshwa ngoma, kuchezeshwa magwaride na kuimbishwa manyimbo yakanisani. Bado ati husemwa ELIMU BURE, kweli bure, lakini BURE KWA MJINGA!

    Kwa kweli kiwango cha elimu Zanzibar kimeanguka kiasi kikubwa sana, kiasi cha kuitwa, "chini yasufuri". Imefika hadi leo kuwa mwanafunzi aliyemaliza hicho wanachokiita, "kidato cha nne" (Form IV),

    ukimwambia aandike barua ya kuomba kazi kwa lugha ya Kiingereza, anashindwa hata kujaribukuandika na ikiwa atajaribu, basi kichwa huwa miguu na miguu huwa kichwa. Hapo yalipokuwepomasomo ya kweli na walimu wa kweli wenye kufunzwa wakafunzika katika fani ya kusomesha,wanafunzi waliyomaliza chumba cha nane ilikuwa wakiandika Kiingereza, utawavulia kofia.

    MATIBABUTukija katika matibabu, ndiko tutakako kukuta kumeporomoka vibaya kabisa. Hospitali hazina madawa,hazina vifaa vya matibabu, hakuna hata vitanda na mabetishiti ya kutosha. Wagonjwa wanatakiwawakenda kutaka matibabu, wachukue zana zao wenyewe tokea pamba, gauze, vijembe vya kunyolea na

  • 8/8/2019 Ukweli ni huu,(kuusuta uwongo) -Aman Thani Fairooz

    8/76

    8

    hata chupa za "Drips" pia wende nazo. Shuka za kutandika vitandani, mito na foronya zake na nguo zakujifunikia wakati wa kulala vyote hivyo lazima wendenavyo mwenyewe; kama si hivyo basi hatapatamatibabu. Ubavuni mwao wakitazama wanaiyona "Mapinduzi Wing" bwana na bibi wanaingia na kutoka!Tokea miaka yalipoanzishwa mahospitali ya serikali Zanzibar, matibabu yalikuwa bure kwa wote. Kwawananchi, kwa wageni na hata kwa wapita njia. Kuangaliwa na daktari kulikuwa bure, dawa bure,ukilazwa kwa ajili ya matibabu, bure. Na hospitali zilikuwa hospitali kweli kwa kila kitu. Madawa yakila maradhi yalikuwepo. Madaktari wenye ujuzi wa kazi zao, waliosomeshwa wakakhitimu walikuwepowa kutosha. Sivyo kama ilivyo hivi sasa, wauguzaji (Staff Nurses) ndio madaktari, tena wa kufikakuuchana na kuupasua mwili wa binadamu! Kwenye nchi yenye sheria, pindi likitokea lolote, basiushahidi wa watu kama hao, hauwezi kukubalika katika mahakama za sheria, kuwa ni ushahidi wakidaktari. Lakini ndio kama ule msemo wa Kiswahili, "likikosekana la mama, hata la punda hufaa".

    Ni kweli kulikuwepo katika hospitali kuu ya serikali sehemu maalumu za kulala wagonjwa wa kulipa.Lakini hayo yalikuwa kwa kupenda kwake mwenyewe huyo mgonjwa. Malipo yenyewe yalikuwa kwawatu wenye kufanyakazi za serikali, walikuwa wakilipa Shs. sita kwa siku, na waliyokuwa hawafanyikazi za serikali, walikuwa wakilipa Shs.12 kwa siku. Kwa hakika hakukuepo tafauti kubwa baina ya hukokwa malipo na kwa bila ya malipo. Tafauti ziliyokuwepo baina ya sehemu za kulala wagonjwa kwamalipo na sehemu za bure ni za nyongeza tu, sio kwa ya lazima. Kwa mahitajio ya kimatibabu kulikuwahakuna tafauti hata kidogo. Tafauti zenyewe zilikuwa kama hizi: Katika upande wa malipo, wagonjwawalikuwa wakipewa panjama za kulalia, vyakula vyao wakiletewa katika sinia na sahani zao zilikuwa zakaure na walikuwa wakipewa chai ya kitandani (bedtea) na pia walikuwa wakipewa chai ya alaasiri(afternoon tea). Pia walikuwa wakipewa taula ya kujifutia maji baada ya kukoga. Chakula kikubwakilikuwa wali na mchuzi wa nyama na kibakuli cha puding.

    Upande wa wagonjwa wa bure, wao walikuwa wakiletewa vyakula vyao bila ya kutiliwa katika sinia nasahani zao zilikuwa za senti (aluminium), chai walikuwa wakitiliwa katika makopo ya senti. Hapakuwana tafauti kubwa ya chakula isipokuwa wao badala ya kupewa chai ya kitandani, wakipewa uji.Wagonjwa wote wa kulipa na wa bure walikuwa wakipewa matunda na mboga. Na ikiwa mgonjwaameandikiwa na daktari chakula maalumu kutokana na maradhi yake, basi alikuwa akipewa chakulahicho (bila ya malipo) sawa sawa na mgonjwa aliyekuwa katika sehemu za malipo ikiwa maradhi yao niya namna moja. Madaktari na wauguzaji walikuwa ndio hao hao na matibabu yalikuwa ndio hayo hayokwa wote, wa kulipa na wa bure.

    Leo tuambiwayo kuwa matibabu bure, mgonjwa akenda hospitali baada ya kuangaliwa na daktari(pengine na muuguzaji "nurse" tu) na akaandikiwa dawa, akifika kwa watoa dawa jawabu analolipata nikuwa, "dawa hizi hazipo. Kanunue nje"! Jawabu kama hizo ni za kila siku. Ukenda kuwaangaliawagonjwa waliolazwa, ukianza tu kupanda ngazi, unakaribishwa na harufu za mikojo na za mashondekutoka vyooni. Hospitali haina maji ya kutosha. Ukiingia katika vyumba vya kulala wagonjwa,unawakuta mapaka wanacheza foliti kwa jinsi ya uchafu uliomo ndani. Makunguru wanaruka huku nahuku humo vyumbani, wanapitia dirisha hili na kutokea jengine. Sakafu zinanata kwa uchafu. Sasawatizame hao wagonjwa namna walivyo lala humo vitandani. Vichekesho khasa. Wengine wamejifunikakanga za kisutu, wengine za mkeka, wengine za visima, na za namna mbali mbali. Utadhania watoto wakizamani walipokuwa wakitiwa kumbini (kutahiriwa) Mabetishiti yaliyotandikwa vitandani kwailivyokuwa kila mmoja amekuja na lake, basi, huyu katandika jeupe la mfuto, huyu lililofumwa tausi nahuku limeandikwa KARIBU MGENI, na kwa kipembeni ya chumba utaona mengine yameandikwa FURAHAYA BIHARUSI, na jengine limeandikwa kwa maandishi ya nakshi SINA MWENGINEWE, au MAPENZI YETU

    YA UTOTONI, au MIMI NA WEWE HATULISHANI YAMINI, mradi huwa rangi rangire. Hospital zimepotezajina na thamani yake kwa kila upande, haziwezi hata kidogo kutowa huduma zitarajiwazo.

    Hiyo ndio hali ya hayo yanayoambiwa matibabu ya bure! Lakini haya yote yanaowapata ni wananchi wakawaida tu. Ama wenyewe wakina fulani na fulani pamoja na watoto wao, wao bukheri wa sururu hatahawana khabari nayo wala hawayasikii licha kuyaona. Khalafu kwa kuudanganya umma ati husema,"Tumeondoa serikali ya kisultani na kibwanyenye!". Wakati wa huo Usultan, Mfalme wa nchi hajapatakuwa na hospitali yake peke yake. Yeye pamoja na ukoo wake wakenda katika hospitali hiyo hiyowanayokwenda watu wa kawaida. Aliyekuwa Mfalme wa nchi, Seyyid Abdulla Bin Khalifa Bin Haroub,

  • 8/8/2019 Ukweli ni huu,(kuusuta uwongo) -Aman Thani Fairooz

    9/76

    9

    alipopata maradhi, alilala katika hospitali hiyo hiyo na alifanyiwa operesheni katika hospitali hiyo hiyowanayotibiwa watu wa kawaida.

    Wakoloni wa Kiingereza waliweka sehemu yao ya kutibiwa waliita "European Wing". Kutokana namakelele ya wananchi, khasa kutokana na makala yaliyokuwa yakiandikwa katika gazeti la wananchi la"Mwongozi", sehemu hiyo ilibadilishwa jina na badala ya kuitwa "European Wing", ikaitwa "West Wing".Kutokea wakati huo ilikuwa wazi kwa yoyote mwenye kupenda kwenda katika sehemu hiyo ikiwayutayari kulipa ada zilizowekwa. Leo baada ya mapinduzi ya kuleta usawa na kuondoa usultani naubwanyenye, mheshimiwa akiumwa na mdudu upande basi mbio anachukua ndege anakwenda zakeUingereza au Ujarumani kwa matibabu. Ikiwa matibabu yapo nchini bure, mbona wao wanayakimbia nakuyafuatia ya malipo, tena katika nchi za n'gambu na kwa kutumia pesa za wanyonge kwa matibabuyao? Sasa ipi inayostahiki kuitwa serikali ya kibwanyenye? Hii ya waheshimiwa waliyojitenga mbali naumma au ile ya waliyokuwa wakiishi pamoja na umma? Mwenye macho haambiwi tizama! Unawezakuwadanganya baadhi ya watu baadhi ya siku, lakini huwezi kuwadanganya watu wote siku zote.

    HALI ZA MAISHAMatunda makubwa waliyopata wananchi wa visiwani wa Unguja na Pemba kutokana na hayoyenyekuitwa, 'mapinduzi', ni shida za kimaisha katika kila upande. Vyakula havinunuliki, nguohazikamatiki. Mradi wananchi wamo katika kuhiliki kwa maisha yalivyo magumu. Vijana wamekuwawazee kwa shida. Sokoni kunaitwa, "Uwanja wa Mapambano". Na kweli, ukenda sokoni basi upaniekweli kweli kwani fungu la mihogo sita ikiwa huna Shs.200, hulichukui. Mkungu wa ndizi ya mtwike,Shs.3000, nazi moja Shs.50, pilipili za mchuzi fungu Shs.30 mpaka 50, kicha cha mboga ya mchichakuanzia Shs.70 mpaka kuteremka Shs.50. Fungu la machungwa sita yaliyotukuka kidogo, Shs.200 nayaliyokuwa madogo, Shs.100. Takriban watu wote wamekuwa Mabaniani, hawali nyama kwani kilo yanyama ni Shs.1200!

    Mishahara ya wafanyakazi wa serikali ya kiwango cha chini ambao ndio wengi, ni Shs.7000! Mtu, yeyena mkewe na watoto wawili, inambidi, tena kwa kujibana, atumie Shs.1000 kwa siku kwa chakula chaasubuhi na cha mchana. Kwa hivyo inamlazimu apate Shs.30,000 kwa mwezi. Ikishakuwa mshaharawake ni Shs.7000 kwa mwezi, hizo 23,000, atazipata wapi? Kutokana na hali kama hizo za kimaisha,ndio utaona kuwa toka waongozi wa serikali mpaka wafanyajikazi wa chini wanaishi kwa magendo."Corruption" (rushwa) katika nchi imefika katika kilele cha juu kabisa. Tunakubali kuwa ulimwenguwote umeingiwa na shida za kimaisha lakini huwepo sababu maalumu ambazo kwa Zanzibar

    Alhamdulillahi hazijatokea na Inshallah zisitokee. Mara nyingi watu hukutwa na shida za kimaishakatika nchi zao kwa kutokana na hali za mabadiliko kama kutokupata mvua, kutokea mifuriko ya maji,kutokea moto wa misituni, kutokea mitetemeko ya ardhi au vita vya wenyewe kwa wenyewe. Kamanilivyo tangulia kusema shida kama hizo, Alhamdulilah hazikufika katika nchi yetu.

    Sasa kipi kilicho sababisha taabu na dhiki zote hizi za kimaisha? Hili ni suala ambalo kila mwananchilazima ajiulize, ikiwa tutajiuliza kwa insafu basi jawabu halitokuwa zito kulipata. Mpaka Januari 11,1964, pishi moja ya mchele ilikuwa baina ya Shs. nne mpaka tano. (Pishi moja ni sawa na kilo tatu). Inamaana ya kuwa kilo tatu za mchele zilikuwa Shs. nne mpaka tano. Na zilikuwepo kabila mbali mbali zamchele yaani namna kwa namna. Neema zote zilizokuwepo Visiwani Zanzibar, Mwenyezi Munguameziondosha kwa kutokana na maovu yaliyoletwa na hayo yenye kuitwa "Mapinduzi". Ni kama walewatu waliyo mchinja bata aliyekuwa akitaga mayai ya dhahabu. Dhulma zilizofanywa za kupoteza rohoza viumbe wa Mwenyezi Mungu, bila ya kuwa na kosa lolote la kisheria, mali za watu zimechukuliwa

    kwa nguvu kutokana na wenye haki nazo. Natija ya hayo imekuwa leo sehemu kubwa sana ya vyakulavinavyouzwa masokoni vinatokana na ardhi zilizoporwa.

    Kwa hivyo, wananchi wanalishwa vyakula vya haramu. Na wale waliokuwa wamenunua majumbaambayo wanajua ni yenye kutokana na kuibiwa kutoka kwa wenye haki nayo, basi wajue kuwa Sala zaowanazo zisali katika majumba hayo, Mwenyezi Mungu hazikubali. Na ni hivyo hivyo, kwa walewalionunua mashamba yaliyoporwa kutokana na wenye haki nayo, basi na wao wajue kuwa vyakulawanavyo vivuna katika mashamba hayo ni vyakula vya haramu. Kwa hivyo, wao wanakula haramu nawakiviuza, wao, ndio watao chukua dhima ya kuwalisha wenziwao vyakula vya haramu. Kutokana na

  • 8/8/2019 Ukweli ni huu,(kuusuta uwongo) -Aman Thani Fairooz

    10/76

    10

    hali kama hizo zilizokuwa zimefanyika katika nchi, ndio ikawa kila lifanywalo haliwi. Na ikiwahapatofanywa TOBA ya kweli, basi nawaje wowote wataokuja, ikiwa wataendelea na mwendo wakurithi mwendo wa kidhalimu waliyoukuta, basi hapana litalo weza kutengenea ila itakuwa kuzibakiraka hapa na kupasuka pengine. Kauli ya Mwenyezi Mungu kattu haiwezi kwenda kombo. MwenyeziMungu Anasema kuwa: "Hazidi mwenye kudhulumu illa khasara".

    NEEMA ZILIKUWEPOKatika huo wakati unaoitwa wa kikoloni, Serikali ya Zanzibar ilikuwa ikiendesha mambo yake yote kamakujenga maskuli, mahospitali, mabarabara, kununua meli za usafiri, pamoja na kuyahudumia na kulipamishahara ya wafanyakazi tokea wa kigeni mpaka wananchi. Na hao wafanyakazi wa kigeni ambaowengi wao walikuwa Wazungu, basi juu ya mishahara yao walikuwa wakipewa posho maalumu(Inducement Allowances), pia walikuwa wakilipiwa nauli za kuwaleta na kuwarejesha na za wakati walikizo zao. Yote hayo na mengineyo yakifanywa kutokana na mapato ya ushuru tu wa forodha.

    Serikali hii yenye kujiita ya "Mapinduzi", ni wao peke yao ndio wenye kununua bidhaa muhimu zote zanchi kama vile, karafuu, mbata na pilipili hoho kutoka kwa wananchi kwa bei wazitakazo wao wenyewena wakaziuza kwa bei ziliopo katika masoko ya ulimwengu. Isitoshe, serikali hii haina gharama zakuwalipa hao Wazungu kama ilivyokuwa hapo zamani, sasa ilikuwaje hata ifike serikali kuwa hainafedha hata za kuwalipa mishahara wafanyakazi wake wa kienyeji? Hapana shaka sababu kubwa ya hayoni hii dhulma iendeleayo hadi hii leo, uwendeshaji mpotofu, ukiongozwa na siasa ya husda na uroho wamadaraka na kipato, siasa ya "Chukuwa Chako Mapema"! (CCM). Siasa ambayo immefanya mwananchikuwa hana uwezo wala itibari yoyote katika nchi yake. Kwa hali za kimaisha nchini mwananchi hawezikukaa akatua na kufikiri na kupanga juu ya maendeleo ya nchi yake, yeye anafikiri juu ya cha jiyo tu!Siasa mbovu hii iliopangwa makusudi imemzuiliya na kumnyima mwananchi uwezo na njia zakujiendeleza, laa si katika kimaisha, walaa si katika kiutamaduni au kielimu. Inatilia nguvu mizizi yasiasa yake ile ile ilioanziwa, nayo ni "Mwenye Elimu ni Aduwi"

    KUANZA HARAKATI ZA SIASAKabla ya Serikali ya Kiingereza kuiingiza Zanzibar chini ya Himaya yake, Zanzibar ilikuwa ni Dola kamiliiliyokuwa ina shughuli zake (ikiamiliana) na ulimwengu wote. Mara tu Muingereza alipoitia Zanzibarkatika makucha yake mnano mwaka 1890, kila jambo kubwa na dogo lilikuwa lazima liamuliwe kutokaUingereza. Mfalme wa nchi alifanywa kuwa ni alama tu ya Dola, hakuwa na uwezo katika kukata shaurijuu ya uwendeshaji wa nchi. Kama ilivyo kawaida ya wakoloni popote ulimwenguni wanapotawala,

    lazima watumie mbinu za kuwagawa wananchi (ili waendeleze utawala wao) kutokana na hali za namnafulani ziliopo katika nchi. Ikiwa kwa njia za kidini, ukabila, urangi, utajiri, uwezo wa kimaisha na hataumadhehebu.

    Katika Zanzibar Muingereza alitumia njia za kuwagawa wananchi kwa kutumia asili za makabila yao.Aliwafanya wenye asili za Kiarabu wajione kuwa wao tu ndio wenye haki za utawala kwa vile ilivyokuwaMfalme wa nchi anatokana na asili zao. Aliwafanya Washirazi yaani, Wahadimu, Watumbatu naWapemba wajione kuwa wao tu ndio wenye kila haki za nchi kwa vile ilivyokuwa wao ndiowaliyokwenda kuwaita Waarabu (kutoka kwao Oman) kuja kuwasaidia kumuondoa Mreno. AliwafanyaWaafrika (weusi) wajione kuwa wao tu ndio wenye kusitahiki utawala wa Zanzibar kwa vile Zanzibarimo katika Bara la Afrika. Na alichukua uchumi wote wa nchi na kuuweka katika mikono ya wenye asiliza Kihindi kuwa wao ndio raia wa Kiingereza sahihi wa tangu asli, kwa uwezo wao wa kimaishawakajiona kuwa wao ni wabora kuliko wengine katika nchi. Kutokana na hali kama hizo, wananchi

    walianza kujigawa mafungu kwa mafungu na walianza kufungua Jumuiya zao za Kikabila. Waarabuwalifungua yao, Washirazi walifungua yao, Waafrika walifungua yao na Wahindi walifungua yao naWangazija wakafungua yao. Na ndani ya hizo hizo, zilijitokeza zengine na kila moja ilikuwa ikijitapakwa upande wake.

    Kwa muda mkubwa jumuiya hizo zilikuwepo katika nchi na hazikuweza kupata wala kufanya lolote kwamaslahi ya nchi. Kubwa walilokuwa wakilipata ni kualikwa chai ya alaasiri kwenye Bustani ya Jumba laBalozi wa Kiingereza, na kualikwa katika siku ya kuzaliwa Mfalme wa Kiingereza na Mfalme wa nchi nakualikwa kutembelea manuwari za Kiingereza zinapofanya ziara kuitembelea Zanzibar. Katika miaka ya

  • 8/8/2019 Ukweli ni huu,(kuusuta uwongo) -Aman Thani Fairooz

    11/76

    11

    1920 Muingereza katika njama zake za kuzidi kuwafarikisha wananchi ili aendelee kuwatumia katikakuendeleza utawala wake, alianzisha kuwateuwa (appoint) wananchi kwa kuwatia katika Baraza laKutunga Sheria (Legislative Council) kwa njia za kikabila. Aliwateua hatimaye Waarabu wane, Waafrikawane, Wahindi watatu na Mzungu mmoja. Na upande wa Serikali walikuwemo wakurugenzi wa idara waKiingereza kutoka idara mbali mbali za serikali walioteuliwa vile vile, hao walizidi kwa wingi katikabaraza hilo kuliko raia. Mwendo huo uliendelezwa kwa muda wa miaka 28 na hapakuweza kupatikanalolote la maslaha ya nchi. Miaka nenda miaka rudi, nchi haikuwa na maendeleo yoyote kukhusumabadiliko ya Katiba itayo wawezesha wananchi kuendesha wenyewe shughuli za nchi yao bila yakuingiliwa na yoyote.

    Katika mwaka 1953 na 1954, Jumuiya ya Waarabu (Arab Association) iliamua kumpelekea Balozi waKiingereza madai ya kutaka yaletwe mabadiliko ya Katiba yatayo wawezesha wananchi wa Zanzibarkuchagua wajumbe wao wa kuwapeleka katika Baraza la Kutunga Sheria kwa njia ya uchaguzi wa KuraMoja Kwa Mtu Mmoja (One Man One Vote). Na miongoni mwa madai yao, walidai uondolewe mtindo wakuwateua wananchi kwa njia za kikabila katika kila jambo la nchi. Pia walitaka baada ya kupatikanakwa matokeo ya uchaguzi huo, paanzishwe mazungumzo ya taratibu za kupatikana kwa Uhuru kamili waZanzibar.

    Balozi wa Serikali ya Kiingereza aliyekuwepo Zanzibar wakati huo akiitwa Mr. Renkin. Balozi huyoalikataa hata kuyatia maanani madai hayo. Jumuiya ya Waarabu walipoona hawakuweza kupata natijayoyote katika madai yao, bali hata hayakuzingatiwa, waliamua kuanzisha mgomo kwa kuwazuiawajumbe wao kushiriki katika vikao vya Baraza la Kutunga Sheria na katika vikao vya Kamati zaMabaraza yote waliyoteuliwa kushiriki. Mgomo huo ulichukua muda wa miezi 18 bara bara. Jambo lakulizingatia katika suala hili ni kuwa, madai hayo kutokana na Jumuiya ya Waarabu hawakuyafanya kwamaslahi yao binafsi zao, bali kwa maslahi ya Zanzibar na Wazanzibari wote bila ya kujali asili zamakabila yao. Haya yanajithibisha zaidi kwa vile ukiangaliya idadi ya hao waliyokuwa wakiitwa (auwanaoitwa) Waarabu katika Zanzibar, walikuwa ni kiasi cha 16 katika 100 (16%). Juu ya hivyo waliamuakuziachilia mbali nyadhifa walizopewa, sio hivyo tu, bali kutoa muhanga nafsi zao wakiweka mbelemaslahi ya nchi. Bahati mbaya hawakupata kuungwa mkono na wananchi wenziwao wenye asili zamakabila mengine juu yakuwa walizungumza nao na waliwataka washirikiane katika madai hayo.Mmoja kati yao (alioteuliwa kushiriki katika Baraza la Kutunga Sheria akiwa ni mwenye asili yaKiarabu), alipinga uamuzi wa Jumuiya yake na alihudhuria katika kikao cha Baraza la Kutunga Sheriawakati wenzake walipokuwa wamesha amua kugomea. Matokeo yake, alitokea mwananchi mwenye

    uchungu na nchi yake na kumpiga bwana huyu kwa visu. Kwa bahati mbaya alikufa kutokana na pigohilo.

    SHEIKH ALI MUHSIN KWENDA NCHI ZA ULAYA IKIWEMO NA UINGEREZA KUPIGANIA UCHAGUZI WA"COMMON ROLL" (MTU MMOJA KURA MOJA).Wakati Jumuiya ya Waarabu ilipokuwa katika hekaheka za mgomo wao wa kuto kushiriki katikaMabaraza yote ya Serikali kwa madai ya kutaka papatikane mabadiliko ya Katiba yatayo wawezeshawananchi kuchagua wawakilishi wao wa Baraza la Kutunga Sheria kwa njia ya uchaguzi wa "One ManOne Vote" na kusita kuteuliwa kutokana na asili ya makabila yao, mwananchi mwenzao mwenyeuchungu wa nchi yake alifunga safari (kwa gharama zake mwenyewe) kwenda kupigania maslahi ya nchiyake, akiendeleza madai ya wananchi wenziwe huko nyumbani. Wakati Sheikh Ali Muhsin alipokuwakatika hekaheka hizo huko Uingereza, alikutana na Seyyid AbdulRahman Mohammed (Babu) nawaliweza kushirikiana katika juhudi hizo. Katika harakati hizo Sheikh Ali alikutana na waongozi mbali

    mbali wa kisiasa na wengi wao walimshajiisha juu ya kuendelea na juhudi za ugombozi wa nchi yake nawalimpa kila msaada (moral support). Huko Uingereza alipata kuzungumza na wakuu wa Serikali yaKiingereza, wakuu wa upande wa Upinzani na wakuu wa Vyama vya Wafanyakazi. Pia alikutana nawakuu wa vyama na jumuiya mbali mbali zenye kupigania kuondoka kwa ukoloni katika Afrika na katikasehemu zengine za ulimwengu.

    KUASISIWA HIZBULWATTAN (ZANZIBAR NATIONALIST PARTY)Wakati Sheikh Ali Muhsin akiwemo katika safari zake huko nchi za Ulaya, huko nyumbani walichomozawananchi wengine waliokuwa nao na ghera na mapenzi ya nchi yao. (wote, isipokuwa mmoja tu kati

  • 8/8/2019 Ukweli ni huu,(kuusuta uwongo) -Aman Thani Fairooz

    12/76

    12

    yao Sheikh Abdalla Mahmoud walikuwa si Waarabu) Wananchi hao walikutana kuzingatia na kutafakarijuu ya kupotea kwa nchi yao kutokana na mbinu za mkoloni za kuwagawa wananchi kwa kutumia asiliza makabila yao. Wananchi hao waliibuka na amuo la kuanzisha Umoja wa Wananchi wa Unguja naPemba. Umoja ambao kila raia wa Zanzibar atastahiki kuwemo bila ya kujali asili ya kabila yake walaImani ya Dini yake, la umuhimu ni URAIA wake. Hichi kilikuwa ndio chama cha kwanza na pekee katikanchi kuasisiwa kwa kufuatia misingi ya Uwananchi.

    Wananchi waasisi hao walikuwa ni, Sheikh Vuai Kiteweo, Sheikh Miraj Shaalab, Maalim Zaid Mbarouk,Maalim Maksud Fikirini, Maalim Mwandoa Khamis, Maalim Wazir Ali bin Maalim, Sheikh Haji HussainAhmed, Sheikh Othman Soud, Sheikh Abdulla Mahmoud Kombo (wa Makunduchi), Sheikh RamadhanTosir (Ramadhan Madafu), Maalim Hija (wa Ndijani), Sheikh Ame, Sheikh Abdulla Mali, Sheikh HajiKombo (wa Kiboje), Sheikh Abdalla Mahmoud na wenziwe wachache. Kwahivyo wale wenye kusema nakutangaza kuwa Hizbu (ZNP) iliasisiwa na Waarabu au kilikuwa chama cha Waarabu, hapana shakawanakosea, amma kwa kutokujuwa ukweli ulivyo au wanasema hivyo kwa makusudio ya kutafutamaslaha yao. Ukweli na hakika ilivyo ni kuwa Hizbu haikuasisiwa na Waarabu wala hakijapata kuwaChama cha Waarabu. Na kama Hizbu kingelikuwa ni Chama cha Waarabu, basi kisingeweza kupataushindi katika chaguzi zilizofanyika za (One Man One Vote) kwani idadi ya hao wenyekuitwa Waarabunchini ilikuwa ndogo; kwahivyo idadi yao hiyo haingaliwezesha kukipa (hicho kisemwacho ni chamachao) voti za ushindi.

    Madai hayo ni miongoni mwa maneno na mbinu za kufitinisha na kuwagawa wananchi kwa kuuwogopaumoja wao. Hapana shaka zimetungwa na wakoloni na kuimbwa na vibaraka vyao, kwa maslahi yao.Mabwana hao tuliowataja hapo juu wakiwa ndio waasisi wa Chama cha HizbulWattan, wao ndiowaliyomuendea Sheikh Ali Muhsin nyumbani kwake baada ya kurejea kutoka safarini na kumuelezakukhusu kuasisi kwa chama chao na nini dhamiri zilizo wapelekea kuasisi chama hicho. Baada yakumueleza, walimtaka na yeye awaunge mkono kwa kujiunga katika chama. Sheikh Ali Muhsin alipoonakuwa hayo wayatakayo wananchi wenzake ndio hayo hayo ayatakayo na kuyapigia mbio daima basi,hapo hapo aliamua kujiunga na kushirikiana nao. Baada yakujiunga, waasisi hao walimtaka Sheikh AliMuhsin aanze kuzungumza na nduguze wenye asili za Kiarabu bali na kila anaefahamiana nae iliwajiunge na wananchi wenziwao. Sheikh Ali aliupokea na kuanza kuutekeleza ujumbe huo.Miongoni mwa wa mwanzo (kati ya hao wenye kuitwa Waarabu) kujiunga na Umoja huo ni, Sheikh BadrMuhammed Barwani, Sheikh Ahmed Seif Kharusi, Sheikh Amour Zahor Ismaily, Sheikh Ali Ahmed RiyamySheikh Nassor bin Isa Ismaily na Sheikh Ahmed Khalfan Naamani haikuchukuwa muda ila nao walijiunga.

    WAKOLONI DHIDI YA HIZBU, UHURU NA UMOJA WA ZANZIBARSerikali ya kikoloni ilipoona Umoja wa Hizbu umesimama na kila siku unazidi kuungwa mkono nawananchi wa kila pembe na kila aina, walizidi kuogopea maslahi yao. Kwa kuhifadhi maslahi yaowalianza kuuandama Umoja huo HizbulWattan nje ndani, usiku na mchana kwa kuwatumilia baadhi yawananchi wafanyakazi wa Idara ya Utawala khasa Mamudiri na Masheha. Vitumishi hivyo vilifunga njugana kuingia mitaani na viamboni katika juhudi za kuuvunja Umoja huo wa HizbulWattan. Kwa kiasi fulanihapo mwanzoni waliweza kufanikiwa, kwani walitumilia mbinu za kuwatisha wananchi; baadhi kwakuwaambia kuwa, chama hiki azma zake ni kuleta michafuko katika nchi na kwa baadhi ya wananchiwakiwaambia kuwa chama hiki kinataka kumuondoa Mfalme. Kila mmoja wakimpigia mdundowaliofikiria kuwa utaweza kumshitusha na kukiepuka chama hiki. Bali wananchi hawakuchukuwa mudailla waliweza kuzielewa mbinu zao hizo na kuwaepuka na badala yake kuzidi kuungana na wananchiwenziwao.

    MAKAO MAKUU YA HIZBUKabla ya uchaguzi wa mwanzo wa "Common Roll Election, yaani, "Mtu Mmoja Kura Moja", katikaZanzibar mnamo mwaka 1957, mwananchi, mzalendo Sheikh Mahmoud wa Mtendeni aliyekuwamwishoni akijishughulisha na utengezaji wa saa, alijitolea kwa kukipa Chama jumba lake la ghorofamoja lililokuwepo mtaa wa Mwembetanga kuwa ni Makao Makuu ya Chama. Alilitoa jumba hilo bila yakupokea kodi hata senti moja. Baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa mwanzo wa 1957, Hizbuiliyaondoa Makao Makuu yake kutoka Mwembetanga na kuhamia Mkunazini karibu na Msikiti Gofu.Baada ya kuwepo hapo kwa muda, ndio iliweza kununua jumba lake wenyewe katika mtaa wa Darajani

  • 8/8/2019 Ukweli ni huu,(kuusuta uwongo) -Aman Thani Fairooz

    13/76

    13

    na kulifanya ndio Makao Makuu ya Chama. Jumba hilo, baada ya 'Mavamizi' ya Januari 12, 1964,liliporwa na Serikali ya 'Mavamizi' na kufanywa Makao Makuu ya AfroShirazi Youth League. Kama ilivyohali ya majengo mengi mengineo humo nchini, jumba hilo limetupwa bila ya matengenezo walamatumizi ya faida. Na linaachwa kubomka pole pole. Haya sio ajabu, bali haya yanazidi kuthibitishajinsi hao viongozi wa Zanzibar walivyokuwa hawana uchungu na Nchi bali na chochote cha nchi.

    HIZBU KUMLETA ZANZIBAR SEYYID ABDULRAHMAN (BABU)Miezi michache kabla ya uchaguzi wa mwanzo wa 1957, Chama cha HizbulWattan kilimleta BabuZanzibar ili ashirikiane na wananchi wenziwe katika harakati za kisiasa. Baada ya kufika Zanzibar,Hizbu ilimteuwa kuwa Katibu Mtendaji wa Chama (Excutive Secretary). Kutokana na maarifa aliyokuwanayo katika mipango ya kuendesha chama cha kisiasa, Babu baada ya muda mdogo alianzisha Umoja waVijana (Youth Own Union) (YOU). Kwa msaada na ushirikiano wa waongozi wenziwe na wananchi Babualifanya kazi kubwa katika kukijenga Chama cha Hizbu ndani na nje ya nchi. Lakini, kwa bahati mbaya,kama alivyokuwa hodari katika kukijenga, ndivyo alivyojaribu kwa uhodari au ilivyo khasa kwa kiujanjakutaka kukibomoa baada ya kushindwa kufikilia maslahi yake binafsi kwa kukitumilia chama. (Baadaetutaeleza aliyoyatenda katika kukibomoa chama na kuifisidi nchi).

    Alipojiunga Sheikh Ali Muhsin katika chama cha HizbulWattan Zanzibar Nationalist Party (ZNP) aliwapashauri wakuu wa Chama kumtaka Babu achukue mafunzo katika kuendesha chama na baadae ajeasaidie katika uendeshaji wa ZNP. Wakuu wakapendezewa na shauri hiyo, na Babu akawafik. Sheikh Alihapo tena aliiomba Labour Party ya huko Uingereza kwa kupitia kwa (wasta wa) Mr. John Hatch na Mrs.Eirene White M.P. na Labour Party ikakubali kumpokea Babu kwa mafunzo. Mafunzo hayo yalikuwa yamuda wa miezi sita. ZNP (Hizbu) ililipia gharama zote za kimaisha kwa muda huo na za safari. Katikamuda huo pia aliendelea kulipwa mshahara akiwa ni Executive Secretary wa Chama ZNP. Utaonadhahiri kuwa imani ya Hizbu juu ya elimu na maarifa haikufungika sehemu mmoja tu, bali ilikuwa nikwa kila upande. Hizbu iliamini kuwa uwongozi mwema wa chama na nchi utapatikana kutokana nawatu wenye ujuzi na maarifa, kwa hivyo iliona umuhimu wa kumpatia mafunzo na elimu ifaayo KatibuMtendaji wake khasa, na wengine wafuatie.

    NATIJA YA SAFARI YA SHEIKH ALI MUHSINKama tulivyoeleza hapo mwanzoni kuwa Sheikh Ali Muhsin alizitembelea baadhi ya nchi za Ulayapamoja na Uingereza kwa ajili ya kugombania kupatikana kwa mabadiliko ya Katiba ya Kuanzishwa kwauchaguzi wa "Common Roll" yaani "One Man One Vote" katika Zanzibar. Natija ya safari hiyo, Serikali ya

    Kiingereza, ilimleta Zanzibar Mr. Coutts akiwa ni mchunguzi juu ya maendeleo ya Katiba. Mchunguzihuyo alifika Zanzibar kati ya mwaka wa 1956. Chama cha Hizbu kilifanya maandamano makubwa kwakumpokea Mr. Coutts hapo kiwanja cha Ndege cha Kiembe Samaki siku aliyofika Zanzibar.Waandamanaji walichukuwa mabango yaliyokuwa yameandikwa:

    "TUNATAKA UCHAGUZI WA ONE MAN ONE VOTE" "TUNATAKA UHURU WA NCHI YETU" "TUMECHOKAKUTAWALIWA'' ''TUNAPINGA "UBAGUZI WA RANGI NA WA UKABILA"

    Mjumbe huyo alipokuwa nchini alikutana na wananchi pamoja na wakaazi mbali mbali wa nchini.Alionana hata na watu binafsi. Na alipokea risala (za maandishi na za mdomo) kutoka vyama mbalimbali vya kikabila na vya kidini. Chama cha Hizbu nao walionana na mjumbe huyo na walimkabidhirisala yao yenye kutilia nguvu matakwa yao, matakwa ambayo ndio msingi wa ujumbe wake wa kujaZanzibar. Inafaa ifahamike kuwa tangu kufika kwa mchunguzi huyo na mpaka kuondoka hapakuwepo

    chama cha kisiasa nchini isipokuwa kimoja tu HizbulWattan. Vyama vyote vya kisiasa vyengineviliasisiwa baadae. Kwahivyo HizbulWattan ndicho chama cha mwanzo cha kisiasa kuasisiwa Zanzibar.

    Mr. Coutts alipomaliza shughuli zake alirejea kwao. Baada ya muda alileta mapendekezo ya uchunguziwake kwa Balozi wa Serikali ya Kiingereza aliyekuwepo Zanzibar. Katika mapendekezo yake hayo, Mr.Coutts alikubali kuwa Zanzibar inafaa kuanzishwa uchaguzi wa "Common Roll" yaani uchaguzi wa kwapamoja, bila ya kujali khitilafu za kabila. Lakini alipendekeza kuwa uchaguzi uanzie kwa viti sita navilivyobakia viendelee katika mpango ule ule wa kuteuliwa na Balozi wa Serikali ya Kiingereza kwakushauriana na Mfalme wa nchi. Pia katika mapendekezo yake, Bwana Coutts alitaka Balozi wa

  • 8/8/2019 Ukweli ni huu,(kuusuta uwongo) -Aman Thani Fairooz

    14/76

    14

    Kiingereza aendelee kuwa Mwenye Kiti wa Baraza la Kutunga Sheria na watumishi wa Serikali yaKiingereza waendelee kuwa waongozi wa upande wa Serikali.

    Hizbu haikuridhika hata kidogo na mapendekezo hayo, kwa vile asli ya madaai yao ni kuwa Wawakilishiwote wa Baraza la Kutunga Sheria wawe ni wananchi waliyo chaguliwa na wananchi kwa uchaguzi wa"One Man One Vote". Juu ya hivyo, Hizbu ilikubali kushiriki katika uchaguzi huo kwa kuona kuwa msingiwa matakwa yao ulipatikana; nao ni kuanzishwa kwa uchaguzi wa "Common Roll". Kwa kukubaliwamisingi hii Zanzibar ikawa ndiyo nchi ya mwanzo katika Afrika Mashariki, Afrika ya Kati na ya Kusinikuanzishwa uchguzi kama huo. Baada ya kupatikana haya HizbulWattan ilizidisha juhudi zakuwafahamisha wananchi misingi na faida ya kuchaguwa Wawakilishi wao kwa kupitia uchaguzi huo.

    WAKOLONI NA NYERERE NDIO WAASISI WA AFROSHIRAZIWakuu wa Serikali wa Idara ya Utawala, Zanzibar baada ya kuona kuwa mpaka kuondoka kwamchunguzi Coutts Zanzibar na mpaka kuleta mapendekezo ya uchunguzi wake, hapakuweza kuasisiwachama chengine cha kisiasa nchni ili kipate kushindana na HizbulWattan (ZNP), waliamua kumtumiliaMwalimu Julius Kambarage Nyerere. Wakoloni walimtumilia Mwalimu kwa kuja Zanzibar kujaribukuwashawishi waongozi wa vyama viwili vya kikabila waweze kuungana na kuasisi chama kimoja chakisiasa ili kiweze kushiriki katika uchaguzi na kiweze kuwa pingamizi kwa Chama cha Hizbu. Katikaripoti ya Mr. Penny aliyekuwa Muangalizi wa Uchaguzi aliandika, "Ofisi yangu na Idara ya Utawalazilisaidia kuundwa kwa AfroShirazi na kwahivyo ikaokolewa Zanzibar na kuwa na utawala wa chamakimoja wa namna ya khatari."

    Mwalimu Nyerere alikuja Zanzibar pamoja na Sheikh Zubeir Mtemvu mnamo mwisho wa mwaka 1956.Mwalimu pamoja na ujumbe wake alikutana na waongozi wa African Association, Sheikh Abeid AmaniKarume, Bwana Mtumwa Borafia na Bwana Boniface. Waongozi wa Shirazi Association aliokutana naoNyerere katika ujumbe wake huo ni, Sheikh Ameir Tajo, Sheikh Thabit Kombo Jecha na Sheikh OthmanShariff Musa. Mkutano huo ulifanyika katika nyumba ya Sheikh Abeid Amani Karume iliyokuwepo mtaawa Kachorora, Mwembe Kisonge. Nyumba hiyo kwa wakati huo, ilikuwa ikikaliwa na Maalim Haji AliMnoga na Bwana Hija Saleh Hija. Njama hizo za wakoloni pamoja na Mwalimu Nyerere zilifanikiwa.Taarikhi 2 Februari 1957, miezi michache tu kabla ya kufikia uchaguzi wa mwanzo wa Juni, 1957 Chamacha AfroShirazi kiliasisiwa rasmi (kikiwa ni muungano wa jumuiya mbili za kikabila yaani "AfricanAssociation na Shirazi Association"). Karume akawa Rais wa chama, Sheikh Ameir Tajo Makamo wa Raisna Sheikh Thabit Kombo Katibu Mkuu. Uwongozi wa chama haukwenda kwa mzalendo, haukwenda laa

    kwa Sheikh Ameir Tajo walaa kwa Sheikh Thabit Kombo, walaa kwa Sheikh Othaman Shariff, bali kwaMzee Karume. Mbinu na njama za kuuwangamiza Uzanzibari zilianzwa zamani.

    UCHAGUZI WA MWANZO JUNI 1957Kutokana na mapendekezo ya uchunguzi wa Bwana Coutts kukhusu uchaguzi, uchaguzi wa mwanzoulifanyika, June, 1957. Na kwa uchaguzi huo ndio wananchi wa Unguja na Pemba kwa mara ya kwanzawaliweza kushiriki katika kuwachagua Wawakilishi wao wa Baraza la Kutunga Sheria la nchi yao.Uchaguzi huu ulikuwa wa viti sita. Majimbo mane yalikuwa kwa Unguja na mawili Pemba. Majimbo sitahayo yaligaiwa kama hivi:

    Unguja: Majumba ya MaweUnguja: N'gamboUnguja: Kaskazini

    Unguja: KusiniPemba: KaskaziniPemba: Kusini

    Sheikh Ali Muhsin alisimama katika jimbo la N'gambo akiwa ni Mwakilishi wa HizbulWattan, akishindaniana Sheikh Abeid Karume akiwa Mwakilishi wa AfroShirazi, na Sheikh Ibuni Saleh alisimama katika jimbohilo hilo akiwa ni mgombea huru. (independent candidate). Bwana Rutti Bulsara alisimama katika jimbola Majumba ya Mawe akiwa Mwakilishi wa Hizbu na washindani wake wakiwa, Bwana Choudhry,Mwakilishi wa Muslim Association, Bwana Anverali Hassan Virji, mgombea huru na Bwana AbdulQadir

  • 8/8/2019 Ukweli ni huu,(kuusuta uwongo) -Aman Thani Fairooz

    15/76

    15

    Mukri, akiwa naye pia ni mgombea huru. Sheikh Amour Zahor alisimama jimbo la Kusini akiwa niMwakilishi wa Hizbu na Sheikh Ameir Tajo akiwa ni Mwakilishi wa AfroShirazi katika jimbo hilo. SheikhHaji Muhammad alisimama katika jimbo la Kaskazini akiwa mgombea huru akiungwa mkono na Hizbu,Sheikh Daud Mahmoud yeye alikuwa Mwakilishi wa AfroShirazi katika jimbo hilo. Hizbu ilimuunga mkonoSheikh Haji Muhammad kwa kuamini kuwa ana fikra za kizalendo, na kutarajia kuwa hayuko mbali balinaye atajiunga na wananchi wenziwe ndani ya HizbulWattan; na hakika ikawa hivyo.

    Pemba Kusini alisimama Sheikh Rashid bin Ali Khaify akiwa Mwakilishi wa Hizbu na Sheikh MuhammedShamte Hamad alisimama jimbo hilo akiwa mgombea huru. Pia alisimama katika jimbo hilo SheikhAbdalla bin Suleiman Busaidy, akiwa naye ni mgombea huru. Pemba Kaskazini, alisimama Sheikh RashidHamad Othman akiwa Mwakilishi wa Hizbu, Sheikh Ali Shariff Musa akiwa mgombea huru na SheikhShaaban Soud Mponda akiwa Mwakilishi wa AfroShirazi. Matokeo ya uchaguzi huo, Chama chaAfroShirazi kilipata viti vitatu Unguja na hakikuweza kupata hata kiti kimoja Pemba. HizbulWattanilishindwa kupata hata kiti kimoja laa Unguja wala Pemba. Viti viwili vya Pemba vilichukuliwa nawagombea huru wake, yaani Sheikh Muhammed Shamte na Sheikh Ali Shariff, baadae waliviunga vitivyao kwenye AfroShirazi na kuwa na viti vitano katika Baraza jipya la Kutunga Sheria. Kiti kimoja chaNyumba za Mawe, kilichukuliwa na Bwana Chodhry Mwakilishi wa Muslim Association. Natija hii yauchaguzi inathibitisha kuwa Hizbu ni chama kilicho asisiwa bila ya kutokana na asili ya chama aujumuiya ya kikabila iliyokuwepo nchini kwa muda, kama vile ilivyokuwa hali kwa AfroShirazi. Na kwavile HizbulWattan ilikuwa ndio kwanza chama kichanga haikustaajbu kwa kutopata hata kiti kimojakatika uchaguzi huu, kwani kilikuwa bado hakijawafikilia wananchi kwa wingi. Amma AfroShiraziambayo ni muungano wa jumuiya mbili za kikabila, jumuiya ambazo kwa muda zilikuwa zishakuweponchini hakikupata taabu kupata ushindi wa uchaguzi huu, kwani wanachama wake ndio walewale.Tafauti na HizbulWattan ambayo ilibidi ikuwe kwa kupitia kwa wananchi pole pole.

    KWANINI SHEIKH ALI MUHSIN ALIAMUA KUSIMAMA N'GAMBO BADALA YA MAJUMBA YA MAWE?Sheikh Ali alikuwa na hakika mia juu ya mia kuwa hatoweza kumshinda mpinzani wake katika sehemuhiyo kama alivyokuwa na hakika kuwa angeweza kupata ushinde ingekuwa amesimama katika Jimbo laMajumba ya Mawe. Lakini alitaka kuthibitisha kuwa kura chache za wananchi wenye asili mbali mbalizilikuwa pia nazo zina umuhimu katika kuendeleza siasa ya chama, si kasoro kuliko kura nyingi ambazoangeweza kuzipata katika Majumba ya Mawe. Lengo lilikuwa ni kuondoa ukabila na urangi. Kura 918ndizo alizozipata, lakini zilikuwa na umuhimu mkubwa kwa chama na ziliongezea kumpa moyo zaidikatika kuendelea na juhudi za ugombozi wa nchi.

    Uchaguzi ulifanyika kwa salama na ulimalizika kwa salama ingawa wakoloni walijaribu kutaka zitokeefujo wakati wa uandikishaji wa uchaguzi. Kwani badala ya wao (wakiwa ndio serikali) kuchukuadhamana ya kuchunguwa na kuhakikisha ni nani mwenye kustahiki kuchagua na kuchaguliwa, kazi hiyowaliitupia vyama vya siasa. Kweli sheria waliziweka za kuwa ni raia wa Zanzibar tu ndiye mwenye hakiya uandikishaji na upigaji wa kura, lakini sharia hizo hawakuzilinda na kuhakikisha kuwa zinatekelezwa.Matokeo yake kulitokea kupingana na kuzozana baina ya watu wenyewe kwa wenyewe na hayo ndiyoyaliyozidi kupalilia chuki na ukhasama. Katika uchaguzi huu, wageni wengi khasa kutoka Tanganyikaambao walikuwa wakiishi Zanzibar walipenya katika kujiandikisha na walipiga kura. Hata hivyo, si habauchaguzi uliweza kufanyika kwa salama bila ya kutokea fujo la namna yoyote.

    KWENYE SHARI HUZALIWA KHERIKushindwa HizbulWattan katika uchaguzi wa mwanzo, ndiko kuliko zidi kuwazinduwa wananchi na

    kujitokeza paruwanja katika kusimama bega kwa bega na wananchi, wazalendo wenziwao katika juhudiza kuigomboa nchi yao kutokana na ukoloni wa Kiingereza. Baada ya kumalizika kwa machofu ya pirikapirika za uchaguzi, Chama cha Hizbu kilitayarisha mkutano maalumu wa hadhara katika Jumba laSeyyid Khalifa Hall (sasa ati linaitwa "Karume House"). Umma wa kike na wa kiume uliomiminika sikuhiyo ulikuwa wa aina ya peke yake. Haukupata kutokea tangu kuanza kwa harakati za kisiasa katikaZanzibar. Kwa jinsi mabibi walivyokuja kwa wingi kwenye mkutana huo, ililazimu wanaume wotewaliyokuwemo katika ukumbi wa jumba hilo watoke nje kwa kuwapisha mabibi. Wanaume, wao walikaakatika uwanja wa Bustani ya jumba hilo. Siku hiyo ndipo wanawake walipodai wawe na Sehemu yaokatika Chama, na wapate kura sawa na wanaume. Waliopiga kifua mbele kati yao ni BiZuhura bt Saleh,

  • 8/8/2019 Ukweli ni huu,(kuusuta uwongo) -Aman Thani Fairooz

    16/76

    16

    BiSharifa Ahmed na BiZamzam Sultan. Kuanzia siku hiyo, kila usiku uchao, wananchi wake kwa waumewalikuwa wakijitokeza kwa wingi katika kujiunga na Chama cha Wazalendo wenziwao. Waongozi wachama kwa kulingana na umma unavyozidi kujiunga na chama kila siku ilibidi watengeneze mipangokukhusu kueneza mafunzo na siasa ya chama kila upande.

    KUKUWA KWA HARAKATI ZA SIASABaada ya kumalizika kwa uchaguzi wa Juni 1957, Hizbu ilianza kutayarisha mipango ya kueneza fikra nasiasa ya chama kwa Unguja na Pemba kwa mjini na mashamba. Natija ya juhudi hizo haikuchukuwamuda illa zilidhihiri. Matawi ya Hizbu yalikuwa yakifunguliwa kila siku Unguja na Pemba, mjini namashamba. Kila Tawi lilikuwa na skuli ya kusomeshea vijana na watu wazima (wa kike na wa kiume)waliokuwa hawakuwahi kuingia skuli wakati wa udogo wao. Vilevile kila Tawi lilikuwa ni kituo cha kutoa"Huduma ya Kwanza" (First Aid) kwa wenye kufikwa na maradhi madogo madogo. Vijana wa Youth OwnUnion ndio waliyokuwa walimu wa kusomesha na ndio waliyokuwa waganga wa kutibu maradhi madogomadogo.

    Sheikh Juma Aley, aliyekuwa Waziri wa Fedha katika Serikali ya ZNP/ZPPP, yeye ndiye aliyekuwaakiwapa vijana hao mafunzo ya haraka juu ya namna ya kusomesha. Dr. Said Aboud Bin Tahir, yeyealikuwa akiwapa mafunzo juu ya matibabu madogo madogo. Sheikh Ali Makka na Sheikh Juma Ali (dogodogo), wao wakijitolea kwa kuwapa wogonjwa matibabu katika kituo cha matibabu cha Hizbukilichokuwepo katika jumba la Makao Makuu ya Chama, hapo Darajani. Katika kituo hicho vilikuwepokila vifao vyenye kuhitajika kwa matibabu. Wagonjwa walikuwa wakiangaliwa na wakitibiwa bila yamalipo yoyote na bila ya kutizamwa msimamo wao wa kisiasa. MuHizbu na MuAfro wote walikuwawakipata matibabu sawa sawa.

    Pia katika Makao Makuu hayo ya chama kulikuwepo na sehemu ya "Welfare" ambayo ilikuwaikijishughulisha na mambo ya kutoa misaada ya dharura kwa mwananchi yoyote (si kwa wananchamawa Hizbu tu). Sehemu hiyo ya "Welfare" ilikuwa na gari mbili za kuchukulia wagonjwa (ambulance)kutoka majumbani mwao kwa wale waliokuwa hawawezi kwenda kwa miguu yao au wanaishi katikasehemu zilizo mbali na hospitali, kama mashamba na sehemu zengine. Pia sehemu hiyo ya "Welfare"ilikuwa ikishughulikia kuweka majina ya wananchi wanaojitolea kutoa damu kwa kuwasaidia wagonjwa.Ilifika hadi hospitali kuu ya serikali wakihitajia damu kwa sababu ya wagonjwa, wakenda katika sehemuhiyo ya "Welfare" ya Hizbu kuomba watu wa kutoa damu. Vilevile ilifika wakati mmoja hospitali yaserikali kuazima dawa fulani kutoka katika kituo cha Hizbu cha matibabu. Sehemu hiyo ya "Welfare"

    ilikuwa chini ya uangalizi wa Seyyid Hashim Bin Abubakar Bin Salim, Bibi Aisha Salim (maarufu BibiAisha wa YOU au Aisha Mtumbatu) na Bibi Azza Mohammed Seif (mamewatoto wa Sheikh Ali Muhsin).

    Miongoni mwa harakati za Hizbu katika kuwahudumia wananchi, wazee na vijana wa kiume na wa kikewalijitolea bila ya malipo kwa ujenzi wa njia ya Nungwi. Mwishowe Serikali ikaingia kusaidia katikaujenzi huo kwa kuleta mipango ya siku moja kuwalipa na siku moja ya kujitolea. Yaani katika siku 30,wakilipwa siku 15. Mpango huo ukiitwa "Jisaidie Nikusaidie". Vilevile Mahizbu kwa kuendeleza hudumakwa wananchi wenziwao walijitolea kuijenga njia ya Uzi toka mwanzo mpaka mwisho, kwa kuunganishakisiwa cha Uzi na kisiwa kikubwa cha Unguja hapo Unguja Ukuu. Pia walijitolea kuwapelekea majindugu zao wa Tumbatu. Wakati wananchi wa Tumbatu walipokuwa na shida kubwa ya maji Chamakilikodi matishali na kupakia mapipa ya maji kutoka mjini mpaka Tumbatu. Ikiwa nitaendelea kutaja yakheri yaliokuwa yakifanywa na Chama cha Hizbu katika kuwahudumia wananchi, basi itanifanyanisiendelee na hayo niliyo yakusudia khasa kuzungumza na wananchi wenzangu. Kwahivyo, haya

    machache yanatosha kukupeni sura na fikra namna gani Chama cha Hizbu kilivyokuwa kikiendeshwa. Nakutokana na maendesho kama hayo, ndipo kila uchao wananchi walikuwa wakijiunga na Wazalendowenziwao.

    ATI HUSEMWA KUWA HIZBU IMEFELI!Ikiwa Hizbu imefeli, iliyofuzu ni ipi!? Yaliyofanywa na Hizbu kikiwa ni chama tu cha siasa, basi serikaliya Zanzibar hii iliyokuwepo ya "Mavamizi" kwa muda wa miaka 30 (1964 - 1994) haijaweza kuyafanya.Hospitali za serikali kuwa hazina hata vidonge vya Panadol licha ya Penicillin, ndio kufuzu huko? Skuliza serikali kuwa hazina hata madeski ya kukalia, licha walimu wajuzi wa kusomesha, ndio kufuzu huko?

  • 8/8/2019 Ukweli ni huu,(kuusuta uwongo) -Aman Thani Fairooz

    17/76

    17

    Wanafunzi wa Chuo cha Kujifunza Uwalimu hawana hata matandiko wala mashuka katika vitanda vyao.Chakula ni cha mipango mipango na wakati mwingi wanafunzi wanalala na njaa kwa ukosefu wa chakulacha kutosha. Huko, ndiko kuffuzu! Barabara hazipitiki kwa uchafu wa maji ya makaro. Katika kila taa10 za njiani, taa mbili tu ndizo zinazowaka na muwako wenyewe utadhani globu ya kurunzi (tochi)uchwara. Huko ndio kufuzu? Baada ya miaka 30 ya utawala wa Serikali yenye kujiita ya 'mapinduzi',kiwanja cha ndege cha Zanzibar hakina hata kiti kimoja cha kukalia wajao kuwashindikiza wasafiri wao.Ikiwa huko ndio kufuzu, basi hatujui kufeli kutakuwa na sura gani! Inaweza kuwa huko ndio kufuzu,yategemea nia na azma za waongozi wa hizo serikali. Bali kwa nchi na wananchi huko hata kwa lughagani hakuitwi kufuzu, bali ni kudamirika. Kudamirika ambako ni sawa na kuteremkiwa na balaa, kwaniiteremkapo balaa ya Mwenye Enzi Mungu (kwa maasi ya binaadamu) humfika mwema na mbaya. Maafaya Zanzibar yamemteremkia kila mwananchi, mwema na mbaya, (Inshallah wako hao wema). Sababukubwa ya hivyo ni kuwa juu ya maovu yaliofanywa na yaendeleayo kufanywa hakuna tena kukatazanamaovu na kufahamishana kutenda mema, na hapo ndipo Mwenye Enzi Mungu azidishapo nakama Zake.Mwenye Enzi Mungu tunakuomba utunusuru.

    KUGAWANYIKA KWA AFROSHIRAZIMwanzoni mwa 1959 kulitokea mgawanyiko wa waongozi wa Chama cha AfroShirazi. Sheikh MohammedShamte na Sheikh Ali Shariff waliamua kujitoa katika chama na kwa kutoka kwao, kulifuatiwa nawanachama wengi nyuma yao khasa Pemba. Katika wakati huo huo, Chama cha AfroShirazi kilimfukuzakatika chama Sheikh Ameir Tajo kwa singizio la kuwa alikwenda kuwaombea msaada wa fedha vijanawa YASU (Young African Social Union) kwa Sir Tayabali Karemjee kwa ajili ya ujenzi wa klabu (club) yaoiliyokuwepo Miembeni, bila ya kuiarifu kamati kuu ya AfroShirazi. Sababu kubwa zilizompelekea SheikhMohammed Shamte na wenziwe kujitoa katika Chama cha AfroShirazi ni zenye kutokana na hisia zauwananchi khalisi kwa nchi yake. Hisia zake za kisiasa na nyendo zake pamoja na matarajio yake juu yanchi yake yalikuwa ya kutaka kutumikia upatikane uhuru wa Zanzibar. Uhuru utaongozwa naWazanzibari wenyewe bila ya kuchukua amri au shauri kutoka pahala pengine popote.

    Sheikh Karume yeye alikuwa hawezi kufanya lolote bila ya kuzungumza na Mwalimu Nyerere na kamaitavyoamuliwa na Mwalimu, ndivyo hivyo hivyo atavyofuata hata ikiwa si maslahi kwa Zanzibar (na maranyingi hivyo ndivyo ilivyokuwa). Sheikh Mohammed Shamte, hayo yeye alikuwa hayakubali; kwahivyodaima walikuwa wakibuburushana mpaka mambo yalipofika hadi ya kufanywa mikutano ya Kamati Kuuya Chama bila ya kuarifiwa Sheikh Mohammed kwa kukhofiwa kuwa akiwepo ataleta upingaji juu yabaadhi ya mambo. Ilipofika kiwango hichi, maji kuzidi unga, Sheikh Mohammed na Sheikh Ali Shariff

    walijitoa katika AfroShirazi.

    KUASISIWA KWA ZANZIBAR AND PEMBA PEOPLES' PARTY (ZPPP)Chama cha Z.P.P.P. kiliasisiwa Novemba, 1959. Raisi wa Chama alikuwa Sheikh Mohammed ShamteHamad na