94
[Woga ] SURA YA KWANZA MAANA YA WOGA You can not teach a man anything; you can only help him find it with himself – huwezi kumfundisha mwanadamu kitu chochote; unaweza tu kumsaidia kutambua yeye mwenyewe. Galileo Galilei Woga au hofu ni hali inayomkumba mtu endapo anakosa matumaini na kuwa na wasiwasi katika vitu, maswala au matukio fulani ya maisha yaliyopita au yatakayotokea. Kila mtu ana silika ya woga na kila mtu kwa jinsi alivyoumbwa anao woga ndani mwake. Woga ulio wa kawaida haumuathiri mtu isipokuwa woga ambao umezidi au kupungua. Woga kama woga sio mbaya ila namna tunavyoutumia 1

Vyanzo vya woga, kakitabu

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Vyanzo vya woga, kakitabu

[ ]

SURA YA KWANZA

MAANA YA WOGA

You can not teach a man anything; you can only help him find it with himself – huwezi kumfundisha mwanadamu kitu chochote; unaweza tu kumsaidia kutambua yeye mwenyewe. Galileo Galilei

Woga au hofu ni hali inayomkumba mtu endapo anakosa matumaini na kuwa na wasiwasi katika vitu, maswala au matukio fulani ya maisha yaliyopita au yatakayotokea. Kila mtu ana silika ya woga na kila mtu kwa jinsi alivyoumbwa anao woga ndani mwake. Woga ulio wa kawaida haumuathiri mtu isipokuwa woga ambao umezidi au kupungua. Woga kama woga sio mbaya ila namna tunavyoutumia huu woga ndio unaotupa matatizo. Katika kitabu chake cha How to Overcome Fear, M.K. Gupta anaeleza kuwa, Woga au hofu daima ipo tu katika wakati uliopita na wakati ujao lakini sio kwa wakati

1

Page 2: Vyanzo vya woga, kakitabu

Eugene kawau

uliopo. Mwanasaikojia Sweet Marden anasema kuwa, Woga unaumbwa na mtu mwenyewe na kwa namna yeyote ile hamna mtu anayeweza kueleza woga unapatikana wapi. Woga au hofu juu ya jambo fulani hujikuta ndani ya mtu bila hata yeye mwenyewe kutarajia ila mtu hujitambua katika hali ile ya kuogopa. Kila mtu anayo adrenaline homoni ambayo inaratibu swala la woga katika mwili wa binadamu na kumfanya aweze kupambana na mazingira ya woga. Kuna aina nyingi za woga ambazo tunakumbanan na nazo katika maisha yetu. Kuna woga wa mitihani, woga wa kufa, woga wa kukosa mchumba, woga wa kufeli jambo la muhimu, woga wa kukosa kazi, woga wa kutembea usiku, woga wa kuzaa, woga wa kuendesha gari, woga wa kuongea mbele za watu, woga wa kulala peke yako, woga wa kutoamini kazi zako na kile unachokifanya, woga wa kuachwa au kuacha, woga wa kupingwa au kuulizwa maswali,woga wa kuongea na wazazi au watu wengine, woga wa mapepo, woga wa kula mbele za watu, woga wa adhabu n.k. Katika uhalisia, kuna mambo mengi ambayo tunayaogopa katika maisha ila tukiulizwa huu woga upo wapi, inaweza kutupa shida kubwa sana kumuelezea mtu woga unakaa wapi na ukoukoje. Woga hupatikana

2

Page 3: Vyanzo vya woga, kakitabu

[ ]

ndani ya mawazo ya mtu na woga kama woga huundwa na mtu mwenyewe. Mmojawapo wa wanawake maarufu duniani katika saikolojia, Maria Curie, anasema kuwa, ujinga wa kuelewa mambo yalivyo ndio unaotufanya kuogopa. Kama tungefahamu kukosea ni jambo linalotokea katika maisha na la kawaida, tusingekuwa na woga wa kuongea mbele za watu. Au, kama tungelifahamu, madhara ya woga tusingeliendekeza tabia ya woga katika maisha yetu. Kuweza kutawala tabia ya woga ni hatua kubwa sana katika kujitafutia hekima kama anavyotueleza Bertrand Russel.

Nukuu: “If you willingly plan on being less than you are capable of being, then I warn you that you will be sad for the rest of your life (Kama umeamua mwenyewe kuwa katika hali ya chini kuliko ambavyo ungeweza kuwa, nakuonya kuwa utakuwa bila raha siku zako zote za maisha yako) – Abraham H. Maslow

1.1 Hisia Zinazofanana na Woga kwa Mwanadamu

1.1.1 Worry – Udhi, Sumbua Ni mahangaiko yanayompata mtu

kutokanana kufikiria juu ya suala fulani ambalo 3

Page 4: Vyanzo vya woga, kakitabu

Eugene kawau

hajui hatima yake itakuaje. Mahanganiko haya ni ya muda mrefu na mtu anafahamu ni nini kinachomsumbua. Kwa mfano, mfanyakazi ambaye anakaribia kustaafu, huwa na hofu nyingi kuhusu jinsi atakavyoishi bila ajira. Ni jambo ambalo huwakumba watu wengi katika hali kama hii. Hata hivyo, woga huu haumsaidii mtu kutatua tatizo la jinsi atakavyoishi baada ya kustaafu kwani kitakachotoa majibu ni akili na wala sio woga. Kuna wakati mwingine mtu husumbuka sana anapofikiria ataishije endapo atafukuzwa shule; au atakula nini miaka kumi ijayo; au atafanya nini endapo atafukuzwa kazi; au atafanya nini endapo hatapata mtoto n.k. Huu ni usumbufu ambao mtu anakuwa nao akilini bila kutambua kuwa una madhara makubwa katika maisha. Wakati mwingine mtu anaweza kuishi katika hali hii ya kuudhi au kuwa na usumbufu au wasiwasi katika kipindi kirefu bila kutambua kuwa ni mambo ya kawaida katika maisha. Hivi mtu ataogopaje kufukuzwa shule kama hana kosa? Au mtu utaogopa kufa kwa sababu gani kama anaishi vizuri na watu na anazitii amri za Mola wake?1.1.2 Anxiety – Wasiwasi, dukuduku

Ni hofu inayowapata watu wakati wanasubiria jambo fulani muhimu katika maisha. Wanafunzi wengi baada ya kumaliza

4

Page 5: Vyanzo vya woga, kakitabu

[ ]

mitihani huwa na shauku kubwa ya kutaka kujua wamefaulu au la. Ingawa kuna ambao wanajiamini walifanya vizuri, bado wanakuwa na ile hali ya kuogopa. Mtu ambaye anasubiri vipimo vyake vya H.I.V. baada ya kupima, hujikuta akiwa katika hali fulani ya woga ambao ukitazama hutaona sababu za kimsingi za kuogopa, maana kuna majibu mawili ambayo tayari mtu anafahamu atapewa, kuwa ameathirika au hajaathirika. Kwa upande mwingine, hali hii pia inaweza kutokea pale mtu anapomsubiria mgeni kutoka mbali. Wakati akimsubiria mgeni wake, moyoni huwa na furaha lakini huwa na wasiwasi, yeye pamoja na anayesubiriwa kama kweli wataonana au la. Ukijaribu kuangalia kwa umakini utagundua kuwa, wasiwasi huu hutengenezwa na mtu mwenyewe na wala hamna faida ya woga wa namna hii kama asemavyo Bacon, ‘we invite what we fear because fear is acknowledgement of weakness.’ (Tunakaribisha yale tunayoyaogopa kwa sababu woga ni kukubali madhaifu)1.1.3 Nervousness – Wasiwasi mkubwa juu ya jambo lijalo

Ni hali ya kuogopa juu ya jambo fulani ambalo linatarajiwa kufanyika muda ujao. Ni ile hali ya kutojiamini kuhusu suala ambalo

5

Page 6: Vyanzo vya woga, kakitabu

Eugene kawau

litafanywa muda mchache ujao. Kwa mfano, watu wengi huwa na woga wa kuwekeza hela zao benki au katika vikundi vya ushirika kwa sababu ya kuhofia kuwa hela zao zitapotea. Mwanafunzi ambaye anajiandaa kufanya mtihani wa Interview huwa na woga fulani kabla hajaingia kufanya mtihani huo. Mtu anayeamini mapepo hugopa kupita karibu na makaburi au kulala peke yake. Hali kadhalika na mwanamke au mwanaume ambaye anategemea kufanyiwa vipimo vya H.I.V. huwa na woga fulani kabla ya kupima. Ndio maana watu wengi hawataki kuchukua vipimo vya miili yao kwa sababu ya woga wa aina hii. Nervousness ni ile hali ya kutojiamini katika kufanya jambo ambalo lipo katika wakati ujao. Hali hii ni hatari sana katika maisha maana mtu hukata tamaa na kushindwa kufanya lile alilolipanga kiufasaha.1.1.4 Panic – Woga au hofu inayomjia mtu ghafla

Ni woga au hofu inayompata mtu ghafla wakati anajiandaa kufanya jambo fulani au wakati analifanya jambo hilo. Panic ni aina ya woga ambao humfanya mtu kujisahau kabisa na kumfanya ashindwe kueleza kile alichokiandaa au kukitenda kama inavyotakiwa. Watu wenye matatizo ya panic,

6

Page 7: Vyanzo vya woga, kakitabu

[ ]

mara nyingi hushindwa kumalizia yale ambayo walipanga kuyafanya na kujikuta wakishindwa katika yale ambayo walijiandaa kwayo. Kwa mfano, kuna watu wanapewa nafasi ya kutoa maneno ya shukrani kwa wageni rasmi. Endapo mtu aliandaa neno la shukrani kwa lugha ya Kiswahili na akaambiwa atumie kiingereza, hujikuta akitetemeka na kuingia kwenye dilemma kana kwamba ni jambo la ajabu sana. Katika mazingira mengine, mtu anapokutana na tatizo ambalo hakulitegemea, hujikuta akiwa na woga au hofu kubwa ya ghafla ambayo inamfanya mtu huyu kushindwa kuamua mapema. Kwa mfano, kufiwa na ndugu au rafiki, kufeli mtihani, kushtushwa na mtu au mnyama n.k. Woga wa aina hii ni hatari sana katika afya na maisha kiujumla kwani unamfanya mtu adharaulike au aonekane asiye na msimamo mbele za watu na yeye binafsi.Nb: A nxiety, panic na nervousness ni woga wa muda mfupi ila worry huwa ndani ya mawazo ya mtu kwa muda mrefu.1.1.5 Phobia – Woga wa mazoea

Ni aina ya woga ambao mtu huwa nao katika mazoea. Ni ile hali ya mtu kuogopa kitu au vitu ambavyo mtu wa kawaida ambaye hana tatizo la phobia hawezi kuogopa. Kwa

7

Page 8: Vyanzo vya woga, kakitabu

Eugene kawau

mfano, kuna watu ambao wana tabia ya kuogopa vitu ambavyo havina madhara yoyote kwa binadamu kama panzi, mbu, sisimizi, giza, miti mingi, jinsia tofauti, watu weusi, watoto wadogo, walimu, wazazi, vivuli vyao wenyewe au hata wakati mwingine kusafiri na gari, kusafiri kwa ndege, kuongea mbele za watu na kuogopa kuchomwa sindano hospitalini. Inafikia hatua ya mtu kuwa na hofu kubwa anapokumbana na hali mojawapo ya hizi. Inaweza tokea kabisa mtu anaogopa kuingia ndani ya nyumba na kulala kwa sababu kuna panzi, au sisimizi, au ndege ndani ya chumba. Kuna baadhi ya mambo ambayo humfanya mtu awe na woga wa aina hii kama, kumbukumbu za ajali, masimulizi hasi na ujinga.

1.1.6 Recipes for knowledge – Dondoo za maarifa

The only place where fear exists is in your mind and outside that has no other existence – Woga huishi ndani ya mawazo yako tu, nje ya hapo hauna makao mengine. Swami Sivananda

The only feara allowed is the fear of God and fear of doing evil – Woga unaoruhusiwa ni ule wa

8

Page 9: Vyanzo vya woga, kakitabu

[ ]

kumwogopa Mungu na kutenda mabaya tu. M.K. Gandhi.

Nothing in life is to be feared but only to be understood – Hamna chochote kinachostahili kuogopwa,ila kinatakiwa kueleweka. Maria Curie

Good actions give strength to ourselves and inspire good actions in others – Matendo mazuri hutupa nguvu na kutia moyo matendo mazuri kwa wengine. Plato

We must believe in ourselves or no one else will believe in us: we must master our aspirations with competence, courage and determination in succeed – Tujiamini sisi wenyewe au hamna yeyote atakayetuamini: ni lazima tuzingatie malengo yetu kwa uhodari, kujiamini na kwa kujituma. Rosalyn Sussman Yalow

1.2 Aina za Woga kwa Mwanadamu

Kuna mambo mengi ambayo yanasababisha watu kuwa katika hali ya hofu. Ni vigumu kuelezea mambo yote ambayo huwasababisha watu waogope ila tutajaribu kuyaangalia kwa uchache. Ni vizuri pia kutambua kuwa, kila mtu ana uwezo wa kudhibiti woga alio nao kama atakuwa tayari

9

Page 10: Vyanzo vya woga, kakitabu

Eugene kawau

kufanya hivyo kwa imani. Woga ni kama mgeni ambaye humjia mtu bila yeye kumtaka. Hamna mtu anayependa kuwa na woga ila hujikuta ndani yake. Endapo mtu hatachukua maamuzi ya haraka kujizuia woga usimtawale, anaweza kuathirika kisaikolojia na kibaolojia kama tutakavyoangalia katika aya zijazo. Zifuatazo ni baadhi ya aina za woga ambazo huwakumba watu kwa uchache katika mazingira tofauti na kwa watu mbalimbali:-

(a)Woga wa kuongea mbele za watu, woga wa macho ya watu

(b)Woga wa kufanya mtihani au woga wa kufeli mitihani,

(c) Woga wa kuongea na wanawake au wanaume,

(d)Woga wa kula au kunywa mbele za watu, (e)Woga wa kutoa ushauri kwa mtu,

kufundisha n.k. (f) Woga wa kufukuzwa kazini, shuleni au

nyumbani, (g)Woga wa adhabu ya Mungu, au walimu

au wazazi na mahakama (h)Woga wa kutembea usiku na woga wa

wanyama kama simba, nyoka n.k. (i) Woga wa kukaa na watu wa aina na rika

mbalimbali,

10

Page 11: Vyanzo vya woga, kakitabu

[ ]

(j) Woga wa kutoa maoni, woga wa kuolewa au kuoa,

(k)Woga wa kutumia dawa, woga wa kupima afya ya mwili,

(l) Woga wa kuumwa, woga wa mashetani, madini au misukule,

(m) Woga wa kuwekewa sumu kwenye chakula,

(n)Woga wa kubakwa, kuuawa, kufukuzwa, kusengenywa

(o)Woga wa majanga kama mafuriko, matetemeko ya ardhi na milipuko ya magonjwa.

(p)Woga wa kufa, woga wa giza, woga wa mapepo, misukule, majinamizi, wachawi n.k

(q)Woga wa kukataliwa na jamii, woga wa watu

(r) Woga wa kupokea maoni na mapingamizi kutoka kwa watu,

(s) Woga wa kupata magonjwa kama Ukimwi na Malaria,

(t) Woga wa kuonekana mchafu, woga wa kazi fulani

(u)Woga wa kusema ukweli, woga wa viongozi

(v)Woga wa kuishi maisha ya uhuru na kujitawala,

11

Page 12: Vyanzo vya woga, kakitabu

Eugene kawau

(w) Woga wa kutenda dhambi, (x)Woga wa wa wanyama, (y)na katika mazingira mengine mtu

anaweza hata kuogopa kivuli chake mwenywe na baadhi ya sehemu za mwili wake kama sehemu za siri, rangi ya ngozi, mikono, miguu, macho, tumbo, matiti n.k. Inafikia hatua ya mtu kujibadilisha ili kuondoa kero ya mwili wake mwenyewe.

Kiujumla, kuna aina nyingi za woga ambazo zinawapata watu kiasi kwamba haziwezi kuandikwa zote hapa na kutosheleza. Jinsi watu walivyo na tabia tofauti ndivyo na watu hougopa vitu tofauti katika nyakati tofauti. Cha msingi ni kutambua kuwa, woga wa aina yeyote ile haumsaidii mtu kutatua tatizo bali unamfanya mtu kushindwa kuendelea mbele. Hamna sababu ya kuogopa hali au vitu katika maisha bali kilicho cha muhimu ni kuvielewa vitu unavyoviogopa na utakuja kuona ni vitu vya kawaida katika maisha. Marie curie anasema kuwa ‘Nothing in life which is to be feared but only to be understood’, (Hamna kitu kinachostahili kuogopwa maishani ila tu chatakiwa kueleweka)

12

Page 13: Vyanzo vya woga, kakitabu

[ ]

1.3 Recipes for knowledge – Dondoo za maarifa

There can be as many fears as number of stars, even to extent of fearing youself – Kunaweza kuwa na aina nyingi za woga, hata ya mtu kujiogopa mwenyewe. M.K. Gupta.

We invite what we fear because fear is the agree of weakness – Tunakaribisha yale tunayoyaogopa kwa sababu woga ni kukubali udhaifu. Bacon

A man is unhappy as he has convinced himself he is – Mtu atakuwa bila raha kwa jinsi alivyojishawishi kuwa bila raha. Seneca

Our false idea is that any one can hurt you – Mawazo yetu potofu ni kwamba mtu yeyote anaweza kukuumiza. Vernon Howard

‘What a person believes’ is not as important as ‘how a person believes’ – Kile anachoamini mtu’ sio muhimu kama ‘jinsi anavyoamini mtu.’ Timothy Virkkala

13

Page 14: Vyanzo vya woga, kakitabu

Eugene kawau

SURA YA PILINothing which occurs by chance; every thing has a reason – hamna kitu kinachotokea bila sababu, kila kitu kina sababu.

ASILI YA WOGA AU VYANZO VYA WOGA KWA MWANADAMU

Bila shaka hamna jambo lolote ambalo hutokea bila kuwa na chanzo chake. Watu hupigana kwa sababu walishindwa kuelewana,watu huenda husali kwa Mola wao kwa sababu kuna baadhi ya mambo ambayo kwa akili za kibinadamu hawawezi kuyafanya; watu husafiri kwa sababu mbalimbali, watu huongea kwa sababu mbalimbali, watu pia husoma kutokana na sababu mbalimbali; hali kadhalika watu wengi huogopa na baadae kupatwa na mishtuko katika maisha kwa sababu mbalimbali. Ukijaribu kuwauliza watu wengi ambao wana phobia au matatizo ya pressure watakupa sababu ambazo ziliwafanya wakajikuta katika hali hiyo ingawa sio wote. Hata watoto wadogo wana sababu ambazo zinawafanya waogope baadhi ya mambo ingawa hawawezi kutoa sababu hizo kwa

14

Page 15: Vyanzo vya woga, kakitabu

[ ]

kuongea barabara. Kwa ujumla, kuna sababu nane ambazo zinawafanya watu wengi kuogopa watu, vitu na hali mbalimbali katika maisha ya kila siku hapa duniani. Mambo hayo ni pamoja na:-

2.1 Kutojiamini/ kujikataa/kukata tamaaMtu anapojikataa kuwa anao uwezo wa

kufanya jambo fulani analolitaka, anajitengenezea mazingira ya kuogopa lile alilotaka kulifanya. Mara nyingi watu ambao hawajiamini katika yale wayasemayo na kuyafikiria, hata yale wayatendayo hawayaamini. Kuna kuamini kwa namna mbili kunakofaa zaidi, kuamini kwamba naweza au kuamini kwamba siwezi. Hakuna njia ya katikati kwamba naweza-siwezi. Katika kufanya maamuzi, mtu ambaye yupo katika naweza-siwezi hajiamini, na kwa sababu hiyo anajikuta akifanya lile analotaka kulifanya kama alivyolifikira, yaani naweza-siwezi. Katika hali hii, mtu hujichanganya katika maamuzi au mpangilio wa hoja na hatimaye hushindwa kabisa kufanya kile ambacho alitaka kukifanya. Hata hivyo, namna ya pili ya kujiamini yaani, siwezi kufanya jambo peke yangu, humfanya mtu aogope kuyafanya yale ambayo anaamini hawezi kuyafanya. Kwa mfano, anayeamini

15

Page 16: Vyanzo vya woga, kakitabu

Eugene kawau

kuwa hawezi kuwa tajiri, hatakaa awe tajiri maana hana matumaini ya kuwa tajiri na endapo akiwa sio lengo lake. Tatizo la kutojiamini linamfanya mtu kukosa ile hali ya kujitambua kifikra na kimaumbile. Kutojiamini kifikra ni kule kujiona kuwa hamna chochote ambacho unaweza kukifanya, kukiongea au kukiandika bila kutumia mawazo ya watu wengine yapatikanayo kwa kuyasoma, kuyasikia au kuyaona. Ni jambo zuri sana kutumia mawazo ya watu wengine katika kuandika au kusema yale tunayotaka kusema ila sio lazima. Sio lazima kwa sababu kila mtu anao uwezo wa kufikiri na kutoa mawazo mazuri ya kuisaidia jamii. Jinsi mtu anavyozidi kukua ndio anavyozidi kukosa imani na uwezo wake wa kufikiri. Hudhani kuwa, kuna haja kubwa ya kutegemea tu mawazo ya watua wengine maarufu na kuyaachilia mbali mawazo na fikira zao. Katika hali kama hizi, itafikia sehemu mtu atashindwa kabisa kuongea mambo kutoka akilini mwake bila kutumia yaliyosemwa na watu wengine. Mazingira haya yanamfanya mtu kushindwa kujiamini maana mtu hudhani akiongea au kufanya tofauti na kile alichosoma au kuona ataonekana muongo. Hapa simaanishi ni vibaya kusoma na kutumia mawazo ya

16

Page 17: Vyanzo vya woga, kakitabu

[ ]

watu wengine, ila mawazo hayo yasifanywe ndio tegemeo lako, bali yatumike katika kuboresha yale mawazo yako ambayo naamini kila mtu anayo akilini mwake kama mwanafalsafa Socrates alivyosema, kila binadamu amezaliwa na utashi. Katika mazingira mengine ambayo sio ya kawaida, baadhi ya watu hushindwa kujiamini na maumbile yao. Kuna baadhi ya watu hawapendezwi na miili yao wenyewe. Hujiona kuwa wao ni wabaya na walikosewa katika kuumbwa ukilinganisha na watu wengine. Katika hali kama hizi, watu wa namna hii hujikuta wakiogopa kupita mbele za watu, huogopa kuongea na watu, hutumia madawa kujibadilisha maumbile ya miili yao, na hata huogopa kuangalia sehemu za miili yao ambazo wanadhani ni mbaya au hazifanyi kazi. Kwa mfano, kuna watu ambao huogopa kuangalia sehemu zao za siri, miguu, macho au hata nyuso zao kwa sababu wanajiona wabaya. Huu ni woga usio na msingi kwani haumbadilishi mtu bali unamuongezea madhara.

2.2 Kutegemea sana watu na vitu mbalimbali

17

Page 18: Vyanzo vya woga, kakitabu

Eugene kawau

Kuna watu ambao huweka mategemeo yao yote kwa watu fulani au vitu fulani ambavyo wanadhani wakivikosa ni kama kupungukiwa na kitu kikubwa sana katika maisha. Kwa mfano, mtu anayemtegemea mtu mwingine katika kukamilisha mambo yake huwa anaogopa kumkosea, ili aendelee kusaidiwa. Mbali na hivyo, kuna watu ambao wanategemea sana vitu kama pombe na sigara ili kutatua matatizo yao; na pale wanapokosa huogopa kufanya yale wanayotegemea kuyafanya. Katika mazingira mengine, kuna watu wanategemea sana ushauri na mawazo ya watu wengine ili kukamilisha malengo yao. Wanaogopa kufanya kosa kwa wale watu ambao wanawategemea kiushauri na kimawazo katika kufanikisha au kukamilisha mambo yao. Huu ni woga ambao hauna msingi maana kinachotakiwa hapa sio kuogopa bali ni kuelewa hali, watu na vitu jinsi vilivyo na inavyotakiwa kuviishi. Lililo la msingi sio kuogopa vitu au watu maana kuogopa kwako hakutamsaidia yule ambaye unamuogopa, tena kama ni mtu muelewa atakudharau maana hizo ni dalili ya kutokukomaa kiakili na kimwili. Ni vizuri kujiweka katika hali ya kujitambua wewe unaweza na wala hupendi kuomba ila ni kwa

18

Page 19: Vyanzo vya woga, kakitabu

[ ]

vile tu unajiandaa kufanya jambo ambalo linahitaji msaada kwa wakati huo. Ni vizuri kutambua kuwa, kila kitu katika hii dunia kinabadilika na hamna kitu au hali ambayo itatawala milele, kama alivyosema mwanafalasafa maarufu, Heracletus wa Ugiriki. Kama tukitambua kila kitu kinabadilika kutoka hali moja kwenda nyingine, hata machungu ambayo tunayo leo, inawezekana kabisa kesho yasiwepo. Katika kutambua hili, hamna sababu ya kuogopa hili au lile litatokea kama uko sahihi, bali lililo la msingi ni kutambua kuwa, ili kuepukana na yale unayoyaogopa ni sharti kuyachukulia kama mambo ya kawaida na ambayo yanawapata wengi. Itakuwa ni vyema sana, endapo kila mtu atajitahidi kuishi maisha yake kama mtu anayeweza kujitegemea katika maisha, maana hata yule ambaye unamtegemea yawezekana amekuchoka lakini anaamua tu kukusaidia maana unamsumbua. Wakati mwingine kumtegemea sana mtu katika kila jambo ni kama kupoteza dira ya maisha; hebu fikiria mtu huyo unayemtegemea akifukuzwa kazini au akifa ghafla utaishije? Ni vizuri sana kufanya maamuzi yako wewe kama wewe lakini usipuuze ushauri kutoka kwa watu

19

Page 20: Vyanzo vya woga, kakitabu

Eugene kawau

wanaokuzunguka. M.K. Gandhi, alisema ujasiri ni kuwa bila woga na kuwa bila woga ni kutokuogopa kifo, njaa, kusingiziwa, kukosolewa,mapepo, watu, vitu, hasira za watu n.k., kutokudhamini mambo haya na mengineyo kama haya ni kuwa huru bila woga. 2.3 Imani dhaifu kwa Mungu

Binadamu huamini uwepo wa Mungu maana kuna baadhi ya mambo ambayo yapo nje ya uwezo wake wa kuelewa. Pia huamini uwepo wa Mungu ambaye haonekani kwa macho bali kwa njia ya imani na yale ambayo huyafanya. Bila shaka kwa watu wengi ambao wana imani kwa Mungu, wanapatwa na woga pale ambapo wanaenda nje ya yale anayotaka Mungu. Mtu anapotaka kuvunja amri mojawapo ya Mola wake, huwa na woga kabla na baada. Kabla mwizi hajaenda kuiba huwa na woga ila hujitahidi kuusahau ili akamilishe kuiba; mtu anayetaka kuzini huwa na woga kabla ya kufanya jambo hilo lakini hujifanya kasahau amri ya Mola wake ili atimize kuzini; mtu anayetaka kuua huwa na woga ila hujikaza ‘kisabuni’ ili kutimiza mauaji; mtu anayetaka kumfanyia mwenzake kitendo chochote kibaya huogopa kabla hajafanya kitendo hicho ila hujitahidi kukamilisha alilolipanga n.k. Hali kadhalika baada ya

20

Page 21: Vyanzo vya woga, kakitabu

[ ]

kuvunja amri ya Mola wake, mtu huogopa zaidi ya kabla hajaivunja amri ya Mola wake. Hujutia alilolifanya na huwa na wasiwasi kwamba Mungu atamuadhibu. Mfano, mtu aliyezini baada ya kuzini, huumia rohoni na hatamani tena kuzini; tena huishi na wasiwasi huenda amepatwa na magoniwa hatari kama H.I.V – AIDS, Kisonono au Kaswende. Pia baada ya mtu kufanya uovu huogopa kila mara na kila anapopata tatizo husema kuwa ni Mungu anampa adhabu; na kwa vile Mungu ni roho, kabla na baada ya kufanya uovu binadamu huwa na wasiwasi kwamba Mungu anamuoana. Kuepukana na woga wa namna hii mwanadamu hana budi kusheshimu amri za Mungu wake na kutambua ukuu wa Mungu kwa kuacha kufanya mabaya. Kwa namna hii binadamu anaachana na woga na kuingia katika maisha ya raha. Katika mtizamo mwingine, kuna watu ambao hawaamini kabisa uwepo wa Mungu. Watu walio katika mazingira haya hupatwa na mishtuko mingi kwani hawana wa kumtegemea katika matatizo yao. Watu wa namna hii huamini hali walizo nazo hazitakaa zibadilike. Ikifikia katika kusafiri au kufanya kazi yeyote ya hatari huwa na hofu ya kufa saa yeyote maana hawana imani kuna Mungu

21

Page 22: Vyanzo vya woga, kakitabu

Eugene kawau

anayeweza kuwasaidia. Kuamini kuwa Mungu yupo na anaweza kufanya kila kitu, kunamfanya mtu kuwa huru na kumwezesha kufanya mambo yake kikamilifu. ‘Kumweka Mungu mbele katika maisha yetu ndio kuishi huru.’ 2.4 Malezi, misemo na maneno ya watu mbalimbali

Maisha ya mtu huanza tangia tumboni mwa mama yake. Kuna uhusiano mkubwa kati ya mama mjamzito na mtoto aliye tumboni mwake. Malezi ya mtoto yanatakiwa kuanza tangia mtoto akiwa tumboni mwa mama yake. Mtoto aliye tumboni mwa mama yake anaadhirika moja kwa na yale ambayo mama yake anafanya. Kwa mfano, kama mama hana furaha, hata kichanga kilicho tumboni mwake kitakuwa hakina raha; kama mama ana furaha na upendo, mtoto naye anakuwa na furaha na upendo. Kuna akina mama ambao wana tabia ya kushtuka mara kwa mara. Hali hii inaweza kusababisha mtoto atakayezaliwa kuwa na tabia ya kushtuka. Kama mama alikuwa anaishi na hali ya woga katika ujauzito wake, hata mtoto atakayezaliwa anaweza kurithi hali hii kutoka kwa mama yake. Katika hali nyingine, ikiwa mama alikuwa anataka kumuua mtoto wake kabla hajazaliwa (to make

22

Page 23: Vyanzo vya woga, kakitabu

[ ]

abortion), mtoto huyo atakapozaliwa atakuwa anamuogopa mama yake maana tayari alishamuona mama yake kuwa adui tangia akiwa tumboni. Uchunguzi uliofanyika, unaonesha kuwa, watu wengi ambao hujinyonga au kunywa sumu wakiwa watu wakubwa huchangiwa na woga ambao ulisababishwa na mama zao walipotaka kuwaua wakiwa bado hawajazaliwa. Baada ya kuzaliwa mtoto asipopata malezi mazuri ya awali, baadaye anaweza kuwa na tabia ya kushtuka. Mtoto wa kiume ambaye alilelewa katika malezi ya kubembelezwa kila wakati, akifikia hatua ya utu uzima huwa na tabia ya woga kwa watoto wenzake wa kiume. Wazazi wenye tabia ya kuwakemea watoto wao kwa kuropoka huwafanya watoto hao washtuke na kuogopa. Mtoto ambaye hugombezwa kwa makelele mengi na kupigwa na wazazi wake kila mara, humfanya kuwa na tabia ya woga kwa wazazi na watu wakubwa kwani hudhani watampiga. Kuna watu wengine huogopa kuongea na watu wa nyumba za jirani kutokana na kulelewa na wazazi wao vibaya, hasa katika kuamini ushirikina. Katika mazingira haya mtu hujikuta akiogopa jamii fulani au familia fulani kutokana na malezi mabaya kutoka kwa wazazi au nudge wengine.

23

Page 24: Vyanzo vya woga, kakitabu

Eugene kawau

Pia, kuna watoto wakubwa ambao huogopa kuongea na wazazi wao kuhusu mambo ya mahusiano maana wazazi wao waliwalea katika mazingira ya kuwaficha kuhusu maswala hayo. Katika ujumla wake, tunaweza kuona kuwa malezi ya wazazi kwa kiasi kikubwa huichangia katika kumfanya mtu awe na tabia ya woga katika maisha yake.Kwa upande mwingine, kuna watu ambao wana tabia ya kuogopa baadhi ya mambo au vitu baada ya kusikiliza maneno ya watu na ushauri kutoka kwa watu mbalimbali. Kwa mfano, wazazi wengi wamekuwa wakiwasimulia watoto wao hadithi za kuogopesha kama za watu waliowahi kung’atwa na nyoka, nge, nyuki, ajali au watu waliouawa baada ya wizi, au za wanyama wakali, au za watu waliofukuzwa nyumbani baada ya kuoa, za kichawi n.k. Mtu ambaye amekulia katika mazingira kama haya hujenga tabia ya woga katika yale ambayo husikia kwa watu wakiongea wenyewe au kuwasimulia. Mpaka wakati huu, kuna watu ambao wakiona nyoka, mbwa, paka au hata panya hukimbia. Ni vizuri kutambua kuwa, kila kitu katika hii dunia kina sababu ya kuwepo na kila kitu kina matumizi yake. Hamna sababu ya kumuogopa nyoka au vitu vingine tunavyoambiwa ni vikali

24

Page 25: Vyanzo vya woga, kakitabu

[ ]

kwani lililo la msingi ni kutambua kuwa ni hatari, hivyo kujifunza namna ya kupambana navyo pale tunapokutana navyo.2.5 Kuwa mbali na watu au vitu/ kukosa mazoea na watu au vitu

Kuna watu ambao wanajikuta katika hali ya woga kwa watu na vitu mbalimbali kutokana na kuwa mbali na watu au na vitu hivyo. Wakati mwingine, kuna baadhi ya watu huogopa watu au vitu katika maisha yao kwa kuwa hawana mazoea navyo. Wengine huogopa watu au vitu kwa sababu hawajawahi kuviona katika maisha yao. Kwa mfano, kuna watu wanaoogopa mbilikimo (watu wafupi mfano, hadzabe na tindiga wanaopatikana Arusha) kwa sababu sio kawaida kuwaona; wengine huogopa watu kutoka mataifa mengine kama Ulaya na Amerika; wengine huogopa watu kutokana na maumbile yao mfano, watu wanene au wembamba sana; wengine wamezaliwa na kukulia eneo moja, hivyo hushangaa na kuogopa watu wa sehemu nyingine wanavyoishi. Kabla magari hayajawa mengi, watu waliokuwa nje ya miji, yaani vijijini walikuwa wakikimbia pale wanapoona magari n.k.Katika hali nyingine, mtu anapopewa au kuona kitu ambacho hajawahi kukiona na kuambiwa

25

Page 26: Vyanzo vya woga, kakitabu

Eugene kawau

akitumie huwa anakuwa na woga fulani maana hana mazoea na kitu hicho. Katika mazingira kama haya, watu hujikuta wakiogopa vitu na watu bila kujijua. Mtu anapokuwa na tabia ya kuogopa vitu mara kwa mara, mwishowe atakuja kupata mshtuko maana kuna vitu vingi sana katika hii dunia ambavyo bado wengi wetu hatujavifahamu. Ni vizuri kujitahidi sana kuwachukulia watu kama walivyo, na vitu kama vilivyo huku tukijitahidi kuvifahamu. Namna mojawapo ya kuondokana na woga wa aina hii ni kujitengenezea mazoea ya kuwa karibu na vitu unavyoviogopa mara kwa mara, kuuliza watu wengine juu ya mtu au kitu ambacho unakiogopa. Ni vizuri kutambua kuwa, akili ya mwanadamu inao uwezo mkubwa wa kuelewa mambo mengi kadiri siku zinavyoenda. Hakuna sababu ya kumuogopa mtu au watu ambao hujawahi kuwaona, au vitu ambavyo hujawahi kuviona kwani woga sio namna ya kutatua matatizo bali ni namna ya kujiongezea matatizo ya kiroho na kimwili. Lililo la msingi ni kuwa na ile roho ya kuamini kuwa, hawa ni watu, au hivi ni vitu, na ni watu kama watu wengine au ni vitu kama vitu vingine, hivyo inanibidi nielewe namna ya kuishi na watu hawa au na vitu hivi.

26

Page 27: Vyanzo vya woga, kakitabu

[ ]

2.6 Kumbukumbu ya mambo yaliyopita na matazamio yajayo Kuna watu ambao walishawahi kushuhudia au kijikuta katika jambo la kutisha katika maisha yao kama ajali, ugonjwa, kufumaniwa, kuibiwa, mauaji ya kutisha n.k. Kumbukumbu ya matukio kama haya na mengineyo humfanya mtu aogope pale anapoyakumbuka. Hujitengenezea mazingira ya kuwa katika tukio hilo katika dhamira yake kila anapokumbuka. Kwa mfano, mtu anapokumbuka jinsi alivyopata ajali ya gari au moto humfanya aogope kupanda magari au kuwa karibu na moto. Wengine huogopa pale wanapokumbuka mateso yaliyowapata ndugu au jamaa zao wa karibu kama gonjwa la Ukimwi, kansa, kubakwa, au hata kukatwa miguu. Mambo haya humfanya mtu ashtuke pale anapoyakumbuka. Katika mazingira mengine, watu hujikuta wakiogopa pale wanapofikiria mipango yao ya baadaye. Hushtuka pale wanapoona kuwa malengo waliyojipangia huenda yasifanikiwe kama walivyotarajia. Hii ndio sababu kubwa ya wanafunzi, viongozi na wafanya biashara kupatwa na mishtuko (stresses) pale wanapoarifiwa jambo lolote liwezalo kuwaletea hasara katika mipango yao na kuharibu

27

Page 28: Vyanzo vya woga, kakitabu

Eugene kawau

malengo waliyojipangia. Katika mazingira haya, ni vizuri kutambua kuwa, kila jambo lina wakati wake na kila tunalolitegemea katika maisha laweza kutokea au kutotokea. Kuna kupanda na kushuka katika maisha; kuna shida na raha katika maisha; hali kadhalika kuna kufanikiwa na kufeli katika maisha. Mambo haya hutokea katika nyakati tofauti. Hauwezi kufanikiwa na kufeli kwa wakati mmoja au kuwa na raha na shida kwa wakati mmoja. Hali hizi hufuatana, kama leo shida kesho yaweza kuwa raha, au kama leo nimefeli kesho nina uwezo wa kufaulu. Ndio maana waswahili husema, ‘leo kwangu kesho kwako.’ Lililo la msingi hapa ni kujua kuwa juhudi za mtu ndizo zinazoweza kumkomboa kutoka hali mbaya kwenda nzuri. Woga hausaidii jambo lolote, tena humuongezea mtu hofu na panic katika kutatua matatizo aliyo nayo. Ili kuepukana na woga wa namna hii, yatupasa kuachana na mawazo hasi kwa yale yaliyopita na yajayo na kufikiria mawazo chanya. Tujiepushe na mawazo hasi kwa kufikiria na kujishughulisha na mambo menginine yaletayo furaha katika maisha huku tukijitahidi kutafutia ufumbuzi wa yale tunayofikiri ni chanzo cha woga. Ni vizuri kuchukulia kila tukio katika maisha kuwa lina

28

Page 29: Vyanzo vya woga, kakitabu

[ ]

sababu zake, linapita na wala halitakaa milele na hivyo hatuna sababu ya kuogopa.2.7 Uelewa mbovu wa matatizo na imani potofu kifikra

Kuna watu ambao hudhani shida walizo nazo ni kubwa kuliko za watu wengine. Hudhani kuwa wamepungukiwa na kitu kikubwa sana katika maisha na hawatarajii mafanikio tena. Huchukulia tatizo dogo kuwa kubwa kwa kulitengenezea hoja nyingi kichwani bila kuangalia uhalisia wake. Kwa mfano, mwanafunzi aliyefeli mtihani anadhani ndio mwisho wa maisha yake bila kuangalia kuwa, anao uwezo wa kujitahidi na kufaulu au pia ana uwezo wa kujishulghuisha na kazi nyingine za mikono. Mgonjwa wa kikohozi anaogopa kuwa atakufa au atakonda bila kufikiria kuwa kuna wanoteseka kuliko yeye kama wagonjwa wa ukimwi na kansa. Watu wengine huunda hoja za uwongo akilini mwao kwamba, tatizo walilo nalo au la rafiki zao sio rahisi kutibika na kuisha. Hivyo wanakuwa wakiwaza tatizo hilo mara kwa mara. Wengine hujitengenezea mazingira ya kupata magonjwa kama kansa, ukimwi, ukichaa, BP, n.k. kwa kuyawaza na kuyaogopa magonjwa haya kila wakati. Kisaikolojia mtu anayeogopa hali fulani au kuamini kuwa hali aliyo nayo

29

Page 30: Vyanzo vya woga, kakitabu

Eugene kawau

haiponyeki, basi huwa kama anavyowaza. Kwa mfano, mgonjwa wa malaria, kaswende, B.P, kisonono, kuharisha, kansa, upugufu wa nguvu za kiume za uzazi, kuumwa tumbo, Ukimwi n.k. asipoamini atapona, itamchukua muda mrefu kupona au kupata nafuu. Katika mazingira mengine ya hatari zaidi, kuna watu ambao hawaumwi kabisa ila huanza huamini kwa kuhisi kuwa huenda wakapatwa na magonjwa kama kansa, malaria, typhoid, kaswende, Ukimwi, upungufu wa nguvu za kiume au za kike, ukichaa, mafua n.k. kulingana na sababu zao za binafsi nje na ndani ya miili yao. Watu wa namna hii hujijengea mazingira ya kupata magonjwa haya kwani tayari walishajiandaa kisaikolojia kuyapata. Mtu anayejihisi kwa kuwa na woga au wasiwasi kuwa ana H.I.V. au ana tatizo la Pressure, au kisukari, au kansa na hajaenda hospitalini kuhahakisha hukosa raha, hukonda na hatimaye hufariki ingawa inawezekana kabisa kwamba mtu huyo hakuwa na tatizo lolote bali ni woga tu. Ni vizuri kujua hali za miili yetu kwa kujua uhakika wa afya zetu pale tunapohisi tuna tatizo. Tabia ya kujiundia na kuamini uwepo wa kasoro katika miili yetu kutokana na woga, husababisha matatizo ya kibaiolojia na kisaikolojia katika maisha ya

30

Page 31: Vyanzo vya woga, kakitabu

[ ]

mwanadamu. Namalizia kwa maneno ya kisaikolojia kutoka kwa Beryl Pfizer kuwa, sio kazi inawaua watu bali ni woga na mishtuko. Kazi kama kazi ni afya; hufanywa na mtu kadiri ya uwezo wake.

2.8 Recipes for knowledge – Dondoo za maarifa

Fear is created by man himself out of his own mind – Woga huumbwa na mtu mwenyewe katika mawazo yake mwenyewe. M.K. Gupta

Truth fears no trials – Ukweli hauogopi majaribu – M.K. Gupta

We would accomplish many more things if we did not think of them as impossible – Tungefanikisha mambo mengi zaidi kama tusingeliyafikiria kutowezekana. Chretien Malesherbes

The thing happens the way you believe it and a believe in a thing makes it happen –Kitu kitatokea jinsi ulivyoamini na kuamini kitu kunakifanya kitokee. Frank Lloyd Wright

The greater the knowledge, the greater the doupt – Maarifa mengi, wasiwasi mwingi. Johann Wolfgan Von Goethe

A great deal of talent is lost in the world for the want of little courage – Vipaji vingi

31

Page 32: Vyanzo vya woga, kakitabu

Eugene kawau

hupotea duniani kutokana na ujasiri mdogo. Sydney Smith

There is nothing worse in this world than wasted talent – Hamna kitu kibaya huku duniani kuliko kipaji kilichopotea. Anonymous

There are only two ways to live your life. One as though nothing is a miracle and the other is as if everything is a miracle – Kuna njia mbili za kuishi. Ya kwanza ni kuona hamna kitu cha ajabu na nyingine ni kuona kila kitu ni cha ajabu. Albert Einstein

We are what we believe we are (Tuko vile tunavyoamini tupo) - Benjamini Cardozo

Much of the fears comes from the fact that man always fears the unknown – Woga mwingi hutokana na ukweli kwamba mwanadamu huogopa asiyoyajua. Anonymous

32

Page 33: Vyanzo vya woga, kakitabu

[ ]

SURA YA TATU

DALILI ZA WOGA NA MADHARA YA WOGA

3.1 Yanayompata mtu akiwa katika hali ya woga

Mtu anapokuwa katika hali ya woga huonesha dalili mbalimbali, ambazo huambatana na mtu kukosa imani na anachokifanya. Woga unapomtawala mtu, husababisha baadhi ya sehemu mbalimbali za mwili kushindwa kufanya kazi zake kama inavyotakiwa. Woga humletea mtu mishtuko (stresses) ambazo husababisha matatizo kwenye mfumo wa neva wa binadamu unaoratibu shughuli mbalimbali za mwili (Sympathetic Nervous System). Baadhi ya mabadiliko ambayo hutokea kwa mtu ambaye amepatwa na mshtuko ambao husababishwa na hali ya woga ni kama haya yafuatayo; mapigo ya moyo huongezeka maradufu, mtu huhema kwa jazba kama mtu aliyetoka katika mazoezi ya kukimbia ingawa mtu hajafanya

33

Page 34: Vyanzo vya woga, kakitabu

Eugene kawau

zoezi lolote, ubongo kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja, mate hupungua mdomoni na husababisha mtu kupata kiu ya ghafla, kutetemeka kama vile mtu aliye katika eneo la baridi, homoni ya adrenaline ambayo inasaidia kupambana na ajali huongezeka ghafla, mfumo wa uzazi husimama kwa muda (mtu aliye katika hali ya mshtuko huadhirika sana katika suala zima la mapenzi), mmeng’enyo wa chakula katika mwili husimama (kutokana na hali hii mtu huhisi njaa ghafla pale anapokuwa na mshtuko utokanao na woga), msukumo wa damu huongezeka (high blood pressure), damu inaweza kushindwa kutembea ndani ya mwili (blood clot may occur) na kusababisha baadhi ya viungo vya mwili kupata ganzi, mfumo wa hewa hushindwa kufanya kazi zake kawaida, kutokwa na jasho, mishipa ya damu hupanuka kuruhusu damu kupita haraka, kuumwa na tumbo kutokana na kuzalishwa asidi nyingi wakati wa mshtuko, seli nyekundu za damu huzalishwa kwa haraka zaidi mwilini, na pia mtu hujikuta njia panda katika kufanya maamuzi. Matatizo haya ni ya kisaikolojia zaidi, hivyo kuyatibu kwahitaji zaidi ushauri wa kisaikolojia kotoka kwa wataalam. Pia kuna baadhi ya madawa ambayo husaidia

34

Page 35: Vyanzo vya woga, kakitabu

[ ]

kupunguza tatizo hili kwa kiasi fulani ila sio vizuri sana kuyategemea.

3.2 Madhara ya Woga kwa mwanadamu

Kuna madhara mbalimbali yatokanayo na woga usio wa kawaida kwa mwanadamu. Woga hupelekea watu kupatwa na mishtuko, msongo moyo, mawazo mengi n.k. Madhara haya yapo katika nyanja kuu mbili, yaani kisaikolojia na kibaolojia.Yafuatayo ni madhara ya woga kwa mwanadamu

(a)Kushindwa kutimiza malengo kimaisha kama kufeli katika mitihani, biashara na maisha kiujumla kutokana na kukata tama.

(b)Kuonekana mjinga mbele za watu kwa kutetemeka ovyo na kushindwa kuongea kwa ufasaha kutokana na panic.

(c) Kukosa amani rohoni na kuishi katika hali ya kutokuwa huru kutokana na mawazo yasiyo na majibu kiuhalisia. Yaani mawazo haya huanza kichwani na kuishia kichwani bila utimilifu wake kimatendo

(d)Kuona aibu mbele za watu na vitu. Mwanaume mwoga huona aibu kubwa

35

Page 36: Vyanzo vya woga, kakitabu

Eugene kawau

kuzungumza mbele za watu na hudharaulika sana ikilinganishwa na mwanamke.

(e)Kukosa ajira kutokana na woga wa kushindwa kufanya mitihani ya kuandika au interviews na pia kushindwa kupata ajira kutokana na woga wa kuonyesha vipaji vyao mbele za watu

(f) Kukonda na kukosa raha kutokana na kuwa na mawazo mengi yasiyo na msingi endapo yangewekwa wazi

(g)Kupungua uwezo wa kufikiri kutokana na mawazo mengi. Katika hali kama hii wengi hufeli kimaisha maana badala ya kujitahidi kutatua matatizo yanayowakumba katika matendo, wanaishia kuyatafutia majibu kichwani huku wakishindwa pia kupata majibu sahihi na kuyaweka katika matendo.

(h)Kushindwa kufanya maamuzi sahihi katika maisha kutokana na kushindwa kujiamini.

(i) Kujiundia magonjwa au hali fulani za kutisha akilini ambazo zaweza kumtokea mtu baadae na kumuathiri kiafya.

(j) Kuchanganyikiwa kiakili na kushindwa kufanya mambo katika mpangilio maalum kama inavyotakiwa

36

Page 37: Vyanzo vya woga, kakitabu

[ ]

(k)Kupatwa na ukichaa endapo mtu atakuwa na mawazo mengi yanayosababishwa na woga juu ya jambo lililopita au lijalo kwa muda mrefu

(l) Kukosa marafiki wengi kutokana na kushindwa kuongea kwa ufasaha na kwa ucheshi na watu.

(m) Kujiua kwa kunywa sumu au kujinyonga kutoka na ugumu wa maisha au matatizo ya kutokuelewana katika maswala mnbalimbali ya maisha

(n)Kujenga chuki na watu kwa kuwadhania wachawi kutokana na kusikiliza maneno ya watu au hata kuwaota unaodhani ni wachawi, na kuishia kuwaogopa kwamba ndio maadui zako.

(o)Kuonewa na watu hasa pale wanapotambua kuwa una tabia ya kuogopa watu, na hata wanyama watakuonea kama unawaogopa

Yafuatayo ni magonjwa yatokanayo na tabia ya woga

(a)Magonjwa ya akili kama kuchanganyikiwa, ukichaa na wendawazimu

(b)Magonjwa katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kama ulcers,

37

Page 38: Vyanzo vya woga, kakitabu

Eugene kawau

kuharisha, tumbo kunguruma, tumbo kusumbua bila sababu, kukojoa ovyo n.k.

(c) Magonjwa ya ngozi kama ukurutu, kiseyeseye, lijabu n.k.

(d)Magonjwa ya mishipa na misuli kama kuvimba kwa mishipa

(e)Magonjwa ya uzazi kama kupungua nguvu za kiume, kupungua nguvu za kike, kukosa hamu ya tendo la ndoa, kubadilika kwa siku za hedhi n.k.

(f) Magonjwa ya moyo kama mapigo ya moyo kuongezeka na mshtuko wa moyo.

38

Page 39: Vyanzo vya woga, kakitabu

[ ]

SURA YA NNE

Every problem has its own solution – kila tatizo lina namna yake ya kutatuliwa. Anonymous

NAMNA NA NJIA ZA KUONDOKANA NA TATIZO LA WOGA

Baada ya kuona sababu mbalimbali ambazo zinachangia watu kuogopa pamoja na matatizo yake, ni vizuri kujua ni namna ipi ya kuponya na kuondokana na tatizo la woga katika maisha yetu. Kuna namna tofauti za kuondokana na tatizo la woga kulingana na chanzo cha woga, kiasi cha woga na mazingira ya woga wenyewe. Zifuatazo ni baadhi ya njia za kuepukana na tatizo la woga katika maisha yetu.4.1 Kutambua chanzo cha woga ulio nao Hamna mtu anayeogopa bila sababu. Kila mtu anayeogopa kuna mazingira ambayo yamemfanya awe katika hali ile. Vyanzo vya woga ni vingi sana katika maisha na vinatofautiana baina ya watu kama ilivyoelezwa katika sura ya kwanza. Chanzo

39

Page 40: Vyanzo vya woga, kakitabu

Eugene kawau

cha woga chaweza kuwa mtihani, ugonjwa, simulizi, Mungu, watu, vitu n.k. Kutambua chanzo cha woga, kunamsaidia mtu kujua ni njia ipi haswa ya kutibu aina hiyo ya woga. Bila kujua chanzo cha ugonjwa, huwezi kutibu ugonjwa huo ukaisha na vivyo hivyo kwa tatizo la woga. Ni vizuri, kufanya kile ambacho kinakuogopesha na hapa utagundua kuwa, woga uliokuwa nao ni kikwazo. Kwa mfano, pale mtu anapogundua kuwa, anaogopa kuongea mbele za watu, yambidi ajaribu kuongea mbele za watu mara kwa mara na baada ya muda ataona ni jambo la kawaida. Vivyo hivyo na kwa mambo mengine tunayoyaogopa, yatupasa kuyafanya kwa kujiamini na kujituma kwa manufaa ya jamii na mtu binafsi.4.2 Kujiamini na kuwa na ujasiri

Watu wengi wanaoogopa hali, vitu au watu wanakuwa na imani ndogo katika matarajio yao. Hudhani kuwa kwa jinsi walivyo hawawezi kufanya yale wanayoyaogopa. Ni vizuri kutambua kuwa, kila mtu anao uwezo wa kufanya jambo lolote ambalo ni gumu kama ataamini kuwa ataweza. Hamna sababu ya kusitasita katika kufanya mambo ambayo ni muhimu katika maisha yetu. Kukosa matumaini katika maisha ni sawa na kufa bado

40

Page 41: Vyanzo vya woga, kakitabu

[ ]

unaishi maana mtu ambaye hana imani dhabiti kuwa anaweza, atabakia kutegemea sana mawazo ya watu wengine au msaada wa vitu vingine na kushindwa kutoa maamuzi ya binafsi katika maisha. Sio lazima, na wala sio kila unalolifikiri liwe sawa kabisa na analofikiri mtu mwingine. Kukosea ni jambo la kawaida katika maisha na hivyo hili lisikufanye uogope. Ni watu wengi hufanikiwa katika maisha baada ya kukosolewa na kurekebishwa katika yale waliyosema na kuyafanya. Usiogope kufanya jambo la muhimu katika maisha yako kama haujavunja sheria za Mungu, nchi au jamii. Kwa kutumia imani dhabiti, mtu anao uwezo wa kuwa anavyotaka na kufanya anayoweza kufanya bila kuwa na woga wa aina yeyote au kusumbuliwa na mishtuko ya mara kwa mara.4.3 Kupenda kuongea na kushirikiana na watu mbalimbali (socialization)

Watu wengi ambao huogopa binadamu wenzao au hali mbalimbali katika maisha ni kutokana na kukosa mazoea na watu au hali hizo. Kwa mfano, watu wanaoogopa kuongea na wenzao wa jinsia tofauti, huweza kusababishwa na kukosa mazoea na jinsia hizo. Watu wanaoogopa kuongea mbele za watu wengi, yaweza kusababishwa na kutokuzoea kuongea na umati mkubwa au

41

Page 42: Vyanzo vya woga, kakitabu

Eugene kawau

mdogo wa watu. Mtu anapokuwa katika kundi la watu, mara nyingi hushirikishana mambo mengi, mojawapo yakiwa ni yale anayoyaogopa. Hivyo basi, mtu anayependa kuongea na kushirikiana na watu wa aina mbalimbali anayo nafasi kubwa sana ya kupunguza na kuepukana na tatizo la woga katika maisha.4.4 Kuepuka mawazo hasi juu ya maisha yako na ya watu wengine Baadhi ya watu hujiundia mawazo ambayo wanadhani ndio ilivyo katika uhalisia. Hudhani kuwa, shida walizo nazo ni kubwa sana na haziwezi kuepukika. Hujiandaa kushindwa katika wanayoyatarajia au yaliyokwisha tokea katika maisha yao na kuona kuwa hamna namna yoyote ya kupona. Kwa mfano, kuna baadhi ya wagonjwa huendelea kuogopa kuwa hawatapona na hawaamini kama watakaa wapone. Wengine huamini kuwa hawatakaa wafanikiwe katika mitihani au biashara zao kwa vile kuna ambao wapo juu yao. Mazingira haya humuongezea mtu hali ya woga katika maisha yake. Ili kuondokana na tatizo kama hili ni vizuri sana kuacha mawazo hasi katika maisha yetu. Willbard Samboti, ni mwanfuzi katika chuo kikuu cha Jordan. Alinisimulia jinsi rafiki yake alivyokonda karibia kufa kwa

42

Page 43: Vyanzo vya woga, kakitabu

[ ]

sababu ya woga. Rafiki yake huyo, aliota kiupele kidogo mguuni. Baba yake alikufa kutokana na kansa. Naye alianza kuhisi kuwa ana kansa na hatapona tena. Aliacha masomo na kukaa nyumbani huku akisubiria kufa. Kwa bahati nzuri alitembelewa na Mwanafunzi mwenzake aliyemshauri aende hospitalini kupima na vipimo vilionesha kuwa ulikuwa ni upele tu wa kawaida. Alipewa dawa na baada ya muda mfupi alipona. Sio kila unaloliwaza ndivyo lilivyo kiuhalislia kwani mambo mengi hutambulika kwa vitendo. Epuka kuwa na mawazo na mitizamo hasi katika hali uliyo nayo. Jitahidi kujiwekea mitazamo chanya, kwamba matatizo hali niliyo nayo yaweza kabisa kubadilika.

4.5 Kuchukulia kila jambo jinsi lilivyo na kulikabili kwa njia muafaka

Kuna mambo ambayo watu huogopa kutokana na kushindwa kuelewa namna ya kuyakabili. Katika mazingira mengine, watu huona mambo fulani kuwa ni balaa kubwa sana kwao na hawawezi kukaa na kuyakabili. Ni vizuri kuelewa kila jambo kwa jinsi lilivyo na kulikabili kwa kutumia njia sahihi. Hamna sababu ya kuogopa matukio yanayotupata katika maisha kwani, kila linalotukia lina

43

Page 44: Vyanzo vya woga, kakitabu

Eugene kawau

sababu na linaweza kukabiliwa kwa kutumia maarifa. Hamna sababu ya kuogopa matukio, hali, vitu au watu bali lililo la msingi ni kuyaelewa matukio hayo, au hali hizo, au watu hao, au vitu hivyo na hivyo kujijngea mazingira mazuri ya kuyazoea. “Don’t complicate things, face them as they are,” (usifanye mambo kuwa magumu, yakabili jinsi yalivyo)4.6 Kuondokana imani potofu ya mizimu, mashetani, misukule na mengineyo yaendanayo na hayo.

Ni watu wengi sana huogopa kutokana na kushtushua na uwepo wa nguvu za mizimu. Wengine huamini kuwa, mizimu ina nguvu kubwa sana na kwamba inaweza kufanya lolote katika maisha yao. Ni vizuri kutambua kuwa, kwa jinsi mtu anavyoamini na kuogopa nguvu za mizimu, misukule au mashetani, ndivyo anavyosumbuliwa kisaikolojia na nguvu hizi. Kuna watu, kila wanapoumwa hudhani kuwa wamelogwa ingawa ni magonjwa ya kawaida kabisa yanayoweza kutibiwa hospitalini. Wakati mwingine, kuna watu wanaoumwa kutokana na tatizo la kisaikolojia mfano, kuwaza sana kwamba umelogwa tumbo, kichwa, miguu, kifua, akili n.k., kunamfanya mtu ahisi kuumwa sehemu hizo na kama akienda hospitalini vipimo vitaonesha

44

Page 45: Vyanzo vya woga, kakitabu

[ ]

hana ugonjwa maana tatizo ni la kisaikolojia na njia pekee ya kuponya ugonjwa wa aina hii ni ushauri wa kisaikolojia kutoka kwa wataalam. Kuna ulazima wa kuamini uwepo wa Mungu ambaye anakulinda wakati wowote na mahali popote. Imani dhabiti kwa Mungu inamfanya mtu aondokane na imani za ukuu wa nguvu za mashetani mfano, uchawi na misukule. Kama mtu anaumwa ni vizuri akaanza kujitibu mwenyewe kisaikolojia kwa kuamini kuwa atapona na pale atakapoenda hospitalini atapona mapema. 4.7 Kumwamini Mungu na kufuata sheria zake na za nchi au jamii unayoishi

Imani kwa Mungu humwondoloea mtu woga wa mambo ya dunia hii ambayo hayana uwezo kama Mungu. Ni Mungu pekee anayetakiwa kuogopwa kwa kuacha kutenda yale yanayomchukiza. Endapo mtu anazifuata sheria za Mungu na za nchi au jamii anayoishi anakuwa huru katika maisha yake, na kwa namna hii huondokana na matatizo ya woga katika maisha. Mara nyingi watu ambao hawamwamini Mungu, hawafuati hata sheria za nchi au jamii wanazoishi. Katika mazingira haya, watu hawa huishi katika mazingira ya wasiwasi na mwishowe hufa katika mazingira ya kutatanisha. Daima mtu ambaye ana imani

45

Page 46: Vyanzo vya woga, kakitabu

Eugene kawau

iliyo ya kweli kwa Mungu, huishi huru na kufanikiwa katika yale ayafanyayo. Watu wanaoishi huru ni wale ambao wanazitii sheria za Mungu, nchi pamoja na jamii inayowazunguka. Wanaokiuka sheria hizi, mara nyingi hupata matatizo katika maisha yao kama kukosa raha, kufungwa gerezani, kukataliwa na jamii. Mambo haya yote humfanya mtu kuwa huru katika shughuli zake na maisha yake kwa ujumla.4.8 Kupumzisha akili na mwili (relaxation)

Ili kuondokana na matatizo ya woga, ni vizuri kutumia muda maalum katika kupumzisha akili na miili yetu. Kuna aina tatu za kupumzisha akili na miili yetu. Njia ya kwanza ni tafakari (meditation). Njia hii humfanya mtu kujikusanya na kutafakari juu ya jambo moja maalum, na kufanya yale anayoyaogopa kufutika akilini mwake. Mtu anayetafakari mara kwa mara, hujijengea tabia ya kutatua shida zake kwa njia hii badala ya kuziwazawaza kila mara. Mara nyingi, tafakari hufanywa wakati mwili haujachoka sana na katika sehemu ambayo imetulia bila usumbufu. Njia ya pili ni namna ya kutumia pumzi. Wakati mtu yupo katika hali ya woga, hupumua kwa haraka na bila mpangilio maalum. Kuna sababu ya kupumua kwa

46

Page 47: Vyanzo vya woga, kakitabu

[ ]

utaratubu ili kurudisha hali ya kawaida ya mwili. Pia ijulikane kuwa, wakati akili imetulia, mtu hupumua taratibu na kwa mpangilio maalum. Kwa namna hii, kuna umuhimu wa kupumua kwa namna ambayo hewa huzunguka katika mfupo wake ili kutuliza akili na mwili. Njia ya tatu ni kufanya mazoezi ya viungo yenye lengo la kupumzisha akili na mwili (Hatha Yoga). Mazoezi haya huiweka akili bize katika mazoezi na pia viungo vya mwili huchangamshwa. Mtu anayependa kufanya mazoezi, hupunguza mawazo na kupata afya ya akili na mwili tofauti na asiyefanya mazoezi.4.9 Matumizi ya Dawa za Kuondoa Woga.Katika mazingira ambayo woga umemtawala mtu kwa kiasi kikubwa, na kumfanya ashindwe kujizuia, kuna ulazima wa kwenda hospitalini ili kupimwa na kupewa dawa. Woga mwingi humfanya mtu kuwa na mawazo mengi kiasi kwamba hawezi tena kuwa na hali ya furaha. Mara nyingi watu hawa hutembea wakiongea peke yao na kama hali hii isipodhibitiwa mapema, watu hawa huishia kupata ukichaa au magonjwa mengine ya akili. Hospitalini, watu hawa hupewa ushauri kama tatizo halijawa sugu sana, na kama limeshakuwa sugu, watu hawa hupewa dawa ambazo huwasaidia kupunguza tatizo la woga kwa

47

Page 48: Vyanzo vya woga, kakitabu

Eugene kawau

muda maalum. Kuna madawa ya aina mbalimbali ambayo husaidia kupunguza tatizo la woga kwa binadamu. Madawa hayo yapo katika makundi makuu mawili, nayo ni yale yanayopunguza nguvu ya ubongo (Tranguillizers) kama Nitrazepam na Diazepam, na yale yanayoharibu mfumo wa neva (Beta blockers). Kundi la kwanza ni hatari sana kwa afya maana linamfanya mtu ategemee hayo madawa ili kuratibu woga (makes one addicted to them) lakini kundi la pili ni tofauti maana haliharibu ubongo bali mfumo wa neva.

48

Page 49: Vyanzo vya woga, kakitabu

[ ]

4.10 Njia Mbaya Ambazo Watu Hudhani Huondoa Tatizo la Woga

4.10.1 Unywaji wa pombe, uvutaji wa sigara na matumizi ya dawa za kulevya

Kuna baadhi ya watu ambao huweka matumaini yao kwenye unywaji wa pombe kama njia ya kuondokana na woga wa kufanya maswala mbalimbali katika maisha yao. Kwa mfano, kuna watu ambao hawawezi kuongea mbele za watu kabla hawajanywa pombe, na wengine hawathubutu kuongea na jinsia tofauti kabla hawajanywa pombe. Wengine hawawezi kabisa kufanya kazi ngumu kabla ya kuvuta sigara kama bangi. Kuna wengine ambao hutumia madawa ya kulevya kwa sababu za kuogopa hali ngumu za kimaisha. Hudhani kuwa wanatatua matatizo yao kumbe ndio wanayaongeza. Mambo haya yote, hayamsaidii mtu kuondokana na tatizo la kuogopa bali humjengea imani hewa ambayo humuathiri baadae kisaikolojia na kimwili pia. Watu wa namna hii hawawezi kufanya mambo yao bila kutumia vitu hivi, hasa pale wanapoathirika navyo (being addicted to them) na pia huwa katika hatari kubwa ya

49

Page 50: Vyanzo vya woga, kakitabu

Eugene kawau

kupatwa na magonjwa mbalimbali kama kansa, mapafu, figo kushindwa kufanya kazi, kupungua nguvu za uzazi na madhara mengineyo kama kujiua, kuharibika kwa mimba na kushindwa kuishi vizuri na watu. Kutumia madawa ya kulevya, sigara au pombe kama njia za kuondokana na matatizo ya woga, sio sahihi kwani faida zake ni chache na za muda mfupi ila madhara yake ni mengi na ya muda mrefu.4.10.2 Kukimbia mazingira ya woga

Sio sahihi kukimbia mazingira ya woga kwani tatizo litabakia pale pale kwamba unaogopa mazingira yale. Kwa mfano, mtu anayeogopa kutembea usiku hastahili kujifungia chumbani usiku, bali anatakiwa kujifunza na kuzoea namna ya kutembea usiku. Hali kadhalika, kukimbia mitihani, wanyama, miti, giza, watu, mizimu n.k., sio namna sahihi ya kutatua matatizo ya woga wa vitu hivyo, maana kila utakapokutana na vitu hivyo utakuwa unashtuka. Namna pekee ya kutatua matatizo ya woga wa namna hii ni kuvielewa vitu vyenyewe, kuzoea vitu vyenyewe na kuvichukulia vya kawaida katika maisha.4.11 Recipes for knowledge – Dondoo za maarifa

50

Page 51: Vyanzo vya woga, kakitabu

[ ]

Social life through sharing creates a feeling of openeness and fearlessness – Maisha ya kijamii katika kushirikiana husababisha hisia za uwazi na uhuru. M.K. Gupta

Negative things should only be faced and not thought – Vitu vinavyoudhi vinatakiwa kukabiliwa na sio kufikiriwa. Anonymous

The whole world may leave you but God wont leave you – Dunia yote inaweza kukuacha lakini Mungu hatakuacha. Anonymous

Put all excuses aside and remember this: YOU ARE CAPABLE – Weka visingizio vyote pembeni na kumbuka hili: UNAWEZA. Zig Ziglar

Every success is built on the ability to do better than good – Kila fanikio hujengwa na uwezo wa kufanya vizuri zaidi kuliko vizuri ya kutosha. Anonymous

We can not choose our external circumstances, but we can choose how we respond them. Hatuwezi kujichagulia hisia zetu za nje bali tuna uwezo wa kujichagulia namna ya kuzipokea/kuzikubali. Epictus

Be not afraid of life. Believe that life is worth living and your belief will help create the fact – Usiogope maisha. Amini kuwa maisha ni mazuri kuyaishi na imani itakusaidia kuunda ukweli. Willium James

The more experiments you make the better – Unavyojaribu zaidi ndivyo unavyofanya vizuri zadi. Ralph Waldo Emerson

51

Page 52: Vyanzo vya woga, kakitabu

Eugene kawau

Knowledge is knowing that we don’t know – Maarifa ni kufahamu kuwa hatufahamu. Ralph Waldo Emerson

Better to be ignorant of matter tha half know it – Ni vizuri kuwa mjinga wa jambo kuliko kulifahamu nusu. Publilius Syrus

52

Page 53: Vyanzo vya woga, kakitabu

[ ]

SURA YA TANO

UTAFITI KUHUSU WOGA

(2010 – 2011)

Seek councel from the aged for their eyes have seen many, and their ears have heard a lot in faces of years. Even if their councel is not pleasing to you, pay heed to them – Tafuta ushauri kutoka kwa wazee maana macho yao yameona mengi, na masikio yao yamesikia mengi katika miaka mingi. Hata kama ushauri wao haukufurahishi, wasikilize. Khlil Gibran

Ufuato ni utafiti nilioufanya kuhusu woga katika maeneo mbalimbali na matokeo yake

5.1 Njia nilizotumia katika kufanya utafiti huu

Njia ya kujionea watu ambao wameathirika na tatizo la woga (Observation)

53

Page 54: Vyanzo vya woga, kakitabu

Eugene kawau

Njia ya kuuliza maswali na kujibiwa (Questionare)

Njia ya maongezi ya ana kwa ana (Interview)Njia ya kujadili katika makundi (group discussion)

5.2 Watu niliowatumia katika utafiti huuWatoto, vijana, watu wazima na wazee niliokutana nao mashuleni, kazini, katika matembezi na majumbani.

5.3 Maswali yaliyofanyiwa kazi

Maana ya woga Aina za woga na mazingira ya

woga Vyanzo vya woga katika maisha ya

mwanadamu Madhara/matokeo ya woga katika

maisha ya mwanadamu Njia za kutibu tatizo la woga katika

maisha ya mwanadamu Faida za woga katika maisha ya

mwanadamu Mahusiano ya woga usio wa

kawaida kielimu, kijamii, kisiasa na kiuchumi

Mengineyo: ushauri, maoni, experience na nyongeza kutoka

54

Page 55: Vyanzo vya woga, kakitabu

[ ]

kwa watu binafsi kuhusiana na swala la woga.

5.3 Matokeo ya utafiti wenyewe

Jina: Nobert Mwijage (25) Eneo la kuzaliwa: Bukoba ila anaishi Dar es SalaamCheo au kazi: Mwanafunzi wa Theology, Segerea Seminary, Dar es Salaam

Baada ya kusalimiana na kujuliana hali mkoani Dar es Salaam, nilimkaribisha katika mazungumzo ya ana kwa ana kuhusiana na swala zima la woga na baadae kuandikwa kwenye karatasi maalum. Yeye alikuwa na haya kuhusiana na woga;

Woga ni hali ya kutojiamini katika kufanya jambo fulani. Kuna woga wa aina nyingi na watu huogopa katika mazingira tofauti mfano, kuna watu wanaoogopa kuongea mbele za watu na wengine huogopa kufanya mitihani n.k. Chanzo cha woga kwa mwanadamu ni mambo anayokutana nayo katika ukuaji, anasema kuwa mtoto mdogo anaweza kujua chanzo cha woga wake au asijue ila kwa mtu mzima sio rahisi kutokujua.

55

Page 56: Vyanzo vya woga, kakitabu

Eugene kawau

Madhara ya woga kwa binadamu ni pamoja na kukosa kujiamini na kuaminiwa na jamii inayomzunguka, kuwa na wasiwasi, kujenga chuki na watu pasipo sababu. Ni vizuri kujiamini ili kuondokana na tatizo la woga. Faida ya woga wa kawaida alio nao mwanadamu ni kuepukana na mabaya bila kumletea matatizo. Kwake yeye hakana uhusiano wowote kati ya woga na kukua kielimu, kiuchumi na kijamii. Akahitimisha kwa kusema; Woga wa kushindwa kufanya mambo kama inavyotakiwa sio mzuri katika maendeleo. Hivyo basi, kila mtu anaweza kuondokana na tatizo la woga kama akiamua kufanya hivyo kwa kujituma na kujiamini katika maisha ili aweze kujijengea nafasi nzuri ya kufanikiwa zaidi.

Jina: Mosha Change; baba wa familia (39) Eneo la kuzaliwa: MorogoroCheo au kazi: Mchoraji na Mpambaji, Dar es Salaam

Nilikutana na baba huyu katika mojawapo ya duka dogo, mtaa wa mango garden wilayani Kinondoni katika mkoa wa Dar es Salaa. Baada ya kusalimiana na

56

Page 57: Vyanzo vya woga, kakitabu

[ ]

kufahamiana, nilimkaribisha katika uwanja wa mahojiano, naye bila kusita alianza kwa kuelezea;

Woga ni hali ya kukata tamaa na maisha. Hakuweza kutaja aina za woga. Kulingana na maelezo yake, chanzo kikubwa cha woga katika maisha ya mwanadamu ni pamoja na kushindwa kujiamini, watu wenye vyeo, kukata tamaa, wivu, elimu ndogo ya kufahamu watu na mazingira. Kwake yeye, mtu ambaye ana tabia ya kuogopa mara kwa mara, huenda akapatwa na madhara kama, ukichaa, kujiua, panic, mgonjwa ya mwili kama tumbo na kichwa. Kwake yeye haoni faida yoyote ya woga katika maisha na hajui ni kwa nini watu huogopa bila kujua kuwa ni matatizo makubwa na dhambi kubwa sana kuogopa. Aliendelea kusema kuwa, mtu mwoga ataogopa kufanya mambo ambayo yangemsaidia kufaulu kielimu, kijamii, kiuchumi na kisiasa. Kwa mfano, kama mgombea ana tabia ya woga, hataweza kunadi sera zake kiufasaha na kama akijaribu kwa woga, watu watamuona ovyo. Hali kadhalika katika masomo na biashara, mtu mwenye wasiwasi wa kufanikiwa atashindwa kufanya maamuzi sahihi na kumfanya kushindwa katika yale anayoyaogopa. Alimalizia kwa kusema kuwa, kuna siku aligongwa na gari akiwa juu

57

Page 58: Vyanzo vya woga, kakitabu

Eugene kawau

ya baiskeli yake, lakini hakushtuka bali alijirusha upande uliokuwa salama na wala hakudhani kuwa aliumia ila baadae aligundua ameumia mguu. Alinionyesha kovu hilo katika mguu wake na akahitimisha kwa kusema kuwa, kujiamini ni dawa kubwa sana katika kuponya magonjwa na hali za hatari maishani.

Jina: Alex Silvest Silayo Eneo la kuzaliwa: Nairobi - KenyaCheo au kazi: Mwanafunzi, Chuo cha Afya Muhimbili

Baada ya kutembelea wagonjwa kadhaa pale hospitalini Muhimbili, niligundua kuwa, wengi walikuwa wakiogopa kama watapona au vipi. Wengine walikuwa wakimtumaninia Mungu awasaidie kwani walishakata tamaa na maisha. Kiujumla, wengi wao walikuwa na woga isipokuwa wachache waliokuwa na nafuu. Ndipo nilipoamua kumuona kijana huyu ambaye ni mwanafunzi karibu na hospitali. Tulisalimiana na baada ya muda nilimkaribisha kuzungumzia swala zima la watu kukata tamaa za kuishi kutokana na woga; naye alianza kusimulia,

58

Page 59: Vyanzo vya woga, kakitabu

[ ]

Woga ni hali ya kutojiamini. Woga humpata mtu kabla au baada ya jambo fulani kumtokea. Alieleza kuwa, panic, hofu, wasiwasi, fobia na kuchanganyikiwa ni dalili za woga katika maisha ya mwnadamu. Vyanzo vya woga ni pamoja na kutojiamini, watu, hali, umaskini, mahusiano (kwa mfano, watu walio katika mahusiano ya mapenzi huogopana kiafya endapo hawajui hali zao na pia huogopa kuachwa, kuachana, kuingiliwa na watu wengine n.k.), imani potofu za mizimu, matendo mabaya (kwa mfano, watu wanaofanya maovu kama wizi, umalaya, usengenyaji, umbeya n.k., huishi katika hali ya woga wakifikiria mtu au jamii itawachukuliaje endapo watagundulika) na mengineyo kutegemeana na mazingira. Aliendelea kusema kuwa, woga una madhara mengi sana kwa mwanadamu endapo utamtawala. Madhara hayo ni kama ukichaa, kuathiri mtoto aliye tumboni, kukonda, kukosa raha, ngozi kukunjamana, kuumwa kichwa kutokana na mawazo mengi yanayosababishwa mishipa ya damu kupanuka, kifafa, ulcers, kupungua kwa nguvu za kiume au za kike, kupungua kwa kinga ya mwili kutokana na kuwaza mambo mengi, kukosa uhuru na mengineyo. Mtu anayetaka kukua kielimu, kijamii na kiuchumi

59

Page 60: Vyanzo vya woga, kakitabu

Eugene kawau

hana budi kuelewa hali halisi ya mambo na sio kujijengea hofu sizizokuwa za lazima. Alihitimisha kwa kusema kuwa, ili kuponya tatizo la woga mtu anastahili kujiamini, kujumuika na watu wa rika tofauti na jinsia tofauti, kupata utaalam wa kisaikolojia, kwenda hospitalini kwa matibabu ila hakupendelea njia hii maana alisema kutumia madawa ili kuondokana na tatizo la woga humfanya mtu ashindwea kabisa kujiamini na mwisho aliwashauri watu wenye tabia ya woga kujenga mazingira ya kufahamu mambo mengi na kutambua kuwa, kushindwa ni jambo la kawaida katika maisha.

Jina: Sist. Bernadette Kimario Eneo la kuzaliwa: Kilimanjaro - TanzaniaCheo au kazi: Mtawa wa Shirika la Maria wa Kakamega

Baada ya kukutana naye pale Parokiani Ananasif, tulisalimiana na kutambulishana. Katika maongezi, nilimgusia kuhusu tatizo la woga kwa wanadamu walio wengi. Alitoa mchango wake kwa maelezo mengi, ndipo nilipoamua kumpa kopi ya karatasi iliyokuwa na maswali juu ya woga. Aliyajibu maswali hayo kama ifuatavyo ndani ya siku tatu,

60

Page 61: Vyanzo vya woga, kakitabu

[ ]

Woga ni hisia fulani iliyopo ndani ya nafsi zetu ambazo hutujia katika hali tofauti na katika mazingira tofauti. Chanzo kikubwa cha woga kulingana na maelezo yake ni kutojiamini, kupatwa na jambo ambalo mtu hakulitegemea, kukosa uaminifu kwa mambo ya binafsi na ya watu wengine na kutojituma katika kazi kwa kukata tama na kuhisi kuwa haitaweazekana. Madhara ya woga ni pamoja na kukosa raha, kuharibu vitu ovyo kutokana na panic au kuwa na wasiwasi, kukosa marafiki kutokana na kuogopa kuongea na watu na pia woga unamfanya mtu akose kazi kwa maana kazi nyingi zinahitaji kujiamini na kujituma. Ili kuepukana na tatizo la woga hatuna budi kutafuta njia za kuepukana na kuogopa kusiko na faida katika maisha yetu, kubwa zaidi ikiwa ni kujituma na kusali. Kwa namna fulani woga una faida, haswa ule ulio na lengo zuri la kumsaidia mwanadamu kama kuogopa kutenda mabaya kwa kuutambua uwepo wa Mungu. Woga huu hauna madhara kwani mtu hashtuki au kupatwa na magonjwa, tofauti na woga wa aina nyingine ambao humkumba mtu bila kutaka ila anaweza kuuratibu. Nawashauri wale ambao wana tatizo la kuogopa wajitahidi kujua chanzo cha woga wao na kuacha tabia

61

Page 62: Vyanzo vya woga, kakitabu

Eugene kawau

hiyo kwani ina madhara mengi katika maisha kuliko faida.

Jina: Magret Peter (mama wa familia)Eneo la kuzaliwa: Moshi ila kwa sasa anaishi Dar es SalaamCheo au kazi: Mfanyabiashara mdogoNilikutana na mama huyu jijini Dar es Salaam, ni muumini wa kanisa katoliki na makazi yake ni Kinondoni. Baada ya kusalimiana na kutambulishana, katika maongezi yetu, nilimgusia kuhusu suala la woga katika jamii tunazoishi. Kw avile alikuwa na haraka, aliniomba nimwachie kopi ya maswali na baada ya siku nne alinirudishia ikiwa na majibu yafuatayo:-

“Woga ni ile hali ya kutojiamini au kutokuwa na uhakika wa jambo unalohitaji kufanya. Kuna aina mbili za woga, nazo ni woga wa mema na woga wa mabaya ila watu huogopa zaidi wakati wanatenda mabaya. Chanzo cha woga ni kushindwa kujiamini wakati mtu anapotaka kufanya jambo. Woga humwathiri mtu katika ngazi zote za kimaisha yaani, kielimu, kijamii, kisiasa, kiuchumi na kisaikolojia na kumfanya ashindwe kufanikiwa kama inavyotakiwa au kushindwa kabisa. Ili

62

Page 63: Vyanzo vya woga, kakitabu

[ ]

kuondokana na tatizo la woga hatuna budi kujiamini na kufanya mambo kwa umakini. Faida ya woga ni kuepuka kufanya mabaya. Nawashauri watu wasiwe na tabia ya kuogopa kueleza mambo ambayo ni ya ukweli kwani kukaa na mambo rohoni kunatengeneza magonjwa ya roho na kimwili.”

Jina: Akhy SalimEneo la kuzaliwa: Dodoma, anaishi Kinondoni-Dar Cheo au kazi: Ustadhi na Mwanachuo DRS-KI

Nilikutana naye akiwa katoka msikitini kuswali sala ya mchana. Baada ya kusalimiana na kujuliana hali, tulitambulishana na kilichofuata ni mazungumzo ya moja kwa moja kuhusu swala zima la woga kama ifuatavyo:Eugene: Bila shaka ushawahi kuogopa, lakini

woga ni nini?Akhy: Woga ni ile hali ya kuwa na hofu na

wasiwasi mwingiEugene: Kuna aina zozote za woga? Kama

zipo zitaje tafadhali.

63

Page 64: Vyanzo vya woga, kakitabu

Eugene kawau

Akhy: Ndio zipo, mojawapo ni kuogopa kukutana na mambo mapya au kuogopa kitu kama mitihani n.k. ila kuna nyingi.

Eugene: Unadhani ni nini haswa kinawafanya watu kuogopa?

Akhy: Ni mambo kama ujinga, adhabu, kutojiandaa, mapepo na woga wa Mola.

Eugene: Kuna madhara yoyote ya woga?Akhy: Yapo, tena mengi tu kama kutofikia

malengo, mishtuko inayosababisha magonjwa kama pressure, tumbo, kichwa kuuma, upunguvu wa nguvu za uzazi, kisukari, ulcers na mengineyo nisiyoweza kuyataja maana mimi sio mtaalam sana.

Eugene: Asante, lakini kuna uwezekano wa kuponya tatizo hili?

Akhy: Braza, kila tatizo lina chanzo na kwa vile lina chanzo laweza kuponywa. Kwa mfano woga unaweza kuepukika kwa kujiamini, kusoma kwa bidii, kumwamini Mungu na kuondokana na hofu za maneno ya watu.

Eugene: Kuna watu wameniambia woga una faida katika maisha. Wewe unasemaje Mh. Ustadhi kuhusiana na maneno haya?

Akhy: Ni kweli woga una faida lakini, kumuogopa Mungu tu! Hata maandiko

64

Page 65: Vyanzo vya woga, kakitabu

[ ]

yanaweka bayana ya kwamba Mungu tu ndiye wa kuogopwa na sio mwanadamu na kumuogopa Mungu sio kumkimbia au kushtuka bali ni kuacha mabaya na kufuata amri zake.

Eugene: Kuna mahusiano kati ya woga na kukua kielimu, kijamii na kisiasa?

Akhy: Sidhani ila yanaweza kuwepo.Eugene: Nakuomba uongee kwa maneno yako

mwenyewe, machache kuhusu woga.Akhy: Woga uko ndani ya mtu naturally, na

woga kama woga sio mbaya ila jinsi tunavyoupokea na kuuendekeza ndio unatuletea matatizo.

Eugene: Asante sana Mh. Ustadhi kwa ushirikiano wako, nakujalia kila la kheri katika maisha.

Akhy: Asante sana, nawe pia ufanikiwe, ukifanikiwa nijulishe tafadhali.

Jina: Amina AliEneo la kuzaliwa: MtwaraCheo au kazi: Mwanafunzi wa Education Chuo kikiuu cha Dar es salaam

Nilikutana na dada huyu katika mojawapo ya compound za chuo kikuu cha Dar

65

Page 66: Vyanzo vya woga, kakitabu

Eugene kawau

es salaaa, Darajani karibu na Cafteria yao. Alikuwa anajisomea History akijiandaa kwa mitihani. Baad ya kusalimiana na kuambulishana, katika mazungumzo nilimgusia maswala ya woga na kumuomba anipe mchango wake. Alikuwa na haya ya kuongea juu ya woga;

Woga ni hali ya mtu ya kumshtua. Hamna aina za woga bali woga ni woga tu na hamna woga mkubwa au mdogo. Hamna chanzo chochote cha woga bali kila mtu ana woga tangia kuzaliwa. Hakuna madhara yoyote ya woga katika maisha maana woga huja na kuisha na wala sioni kama woga ni mbaya au ni mzuri. Upo upo tu. Hakuna namna yoyote ya kuoondokana na tatizo la woga maana hamna mtu anayependa kuwa na woga. Hata mimi nateseka sana maana kila ninaposikia mtihani naogopa au ninapopata jambo nisilolitegemea au kuongea mbele za watu. Lakini nitafanyaje ilihali woga hauna dawa? Kwanza hauonekani na Siamini na wala sidhani kama woga unaweza kudhibitiwa, labda sijui lakini. Mimi nawashauri watu watambue kuwa woga upo na hamna namna ya kuondokana nao ila tu kujiandaa kuupokea.

Jina: Edita Thomas

66

Page 67: Vyanzo vya woga, kakitabu

[ ]

Eneo la kuzaliwa: Rombo - KilimanjaroCheo au kazi: Muuguzi, Hospitali ya

Mkoa, Mara

Jina:Eneo la kuzaliwa:Cheo au kazi:

NB.to be accomplished

67

Page 68: Vyanzo vya woga, kakitabu

Eugene kawau

SURA YA SITA

MAKUNDI MATATU YA WATU NA JINSI WATAKAVYOKUFANYA

UOGOPE AU USIOGOPE KUKAMILISHA MIPANGO YAKO

6.1 Kundi la kwanza – Early adoptersHili ni kundi la watu ambao watakupokea

na kukupa ushirikiano wa moja kwa moja katika mipango yako. Endapo utafanikiwa katika mipango yako, watu hawa hufurahi na endapo hautafanikiwa hawakasiriki wala kuchukia bali watakusifu kwa kujaribu huku wakijaribu njia nyingine ya kufanikiwa. Watu hawa ni wachache sana katika maisha, yawezekana wakawa ni ndugu au watu wengine tofauti kabisa. Ni mara chache sana utakutana na watu wa namna hii, walio na moyo wa kukupa ushirikiano katika mawazo yako na mipango yako kwa namna yoyote ile. Kundi hili humsaidia mtu kutambua kuwa,

68

Page 69: Vyanzo vya woga, kakitabu

[ ]

katika maisha kuna kupanda na kushuka na hivyo hamna sababu ya kuogopa maisha bali jambo la msingi ni kuyakabili kwa kutumia njia sahihi. Watu hawa humjengea mtu mazingira ya kujiamini, na hawachoki kutoa ushauri pale inapotatikana.

6.2 Kundi la pili – Late adoptersHili ni kundi la watu ambao hujiweka

pembeni unapoanza mipango yako na kufuatilia nyendo zako taratibu. Watu hawa hawaoneshi namna yoyote ya kukusaidia au kutokukusaidia. Hutoa sababu mbalimbali kuonyesha kuwa walitaka kukusaidia ila tu wameshindwa au wanajiandaa. Watu hawa hawatoi jibu la moja kwa moja kukupa au kutokupa ushirikiano. Endapo utafanikiwa katika mipango yako, watu hawa wataanza kukusifu huku wakisema maneno kama, ‘nilijua tu atafanikiwa,’ au ‘tangia mwanzo tuliona atafanikiwa tu maana alikuwa anajitahidi sana.’ Na kama imetokea ukashindwa katika mipango uliyopanga basi maneno kama haya hutawala katika midomo yao, ‘nilijua tu hapa hakuna kitu na kweli ameshindwa na ndo maana sikuhangaika kumsaidia tangia mwanzo maana nililifahamu hataenda mbali’ au ‘kwa kweli kwa jinsi tulivyomwona asingeweza

69

Page 70: Vyanzo vya woga, kakitabu

Eugene kawau

kufanikiwa na ukweli ameshindwa.’ Lakini ukweli ni kwamba watu hawa hawakujua lolote kwamba utafanikiwa au la. Ndio watu ambao wataaza kukutafuta pale unapofanikiwa au unakaribia kufanikiwa katika maisha yako ingawa mwanzoni walikaa kimya kama hawakufahamu. Kwa namna moja au nyingine watu wa kundi hili wanaweza kukufanya ukate tamaa na kuogopa kuendelea mbele na mipango yako. Ni watu ambao wanapenda kutoa mawazo hasi yaliyochanganyikana na chanya unapohitaji ushauri wako. Wanaweza kukupa mifano ya kutisha kuhusu unalotaka kufanya ingawa hawakupi namna nyingine, au hata kukufanya ushindwe kuendelea mbele kwa vile hawaonyeshi kukuunga mkono katika mipango yako. Watu hawa humfanya mtu awe katika mazingira ya woga kama mtu huyo hatakuwa na uelewa wa kuwepo watu wa aina hii. Hivyo basi, tusiogope watu wa aina hii maana tumeshatambua wapo na ndio wengi zaidi. 6.3 Kundi la tatu – Reluctants

Hili ni kundi la watu ambao hawataki kuonyesha kabisa dalili ya kutoa ushirikiano. Ni watu ambao wapo kama walivyo na hawataki kabisa kujishughulisha na kutoa mchango wao

70

Page 71: Vyanzo vya woga, kakitabu

[ ]

katika maswala ya kimaendeleo. Mara nyingi watu hawa hukubali hali walizo nazo, hawaamini kwamba wanaweza kutoa mchango wao katika maendeleo ya mtu, watu au wao binafsi. Mara nyingi watu hawa humsingizia Mungu mambo mengi kwa kusema kuwa Mungu amewaumba katika hali hiyo. Kwa mfano, Badala ya watu hawa kufanya kazi hukesha kanisani wakisali, huomba Mungu awape chakula bila kufanya kazi, humwomba Mungu wafaulu bila kusoma, humwomba Mungu wapone bila kujitahidi kuwaona wataalam pia, humwomba Mungu wawe matajiri bila kujituma n.k. Katika hali kama hii, usishtuke sana kukutana na watu wa aina hii, kwani wapo na wanastahili kuelimishwa maana wanakuwa nyuma katika maswala mengi ya kimaisha. Watu hawa wasikukatishe tamaa na kukufanya uogope kuendelea na mipango yako mizuri.

Recipes for Knowladge – Mbinu za Maarifa

Keep away from people who try to discourage you. Small people always do that but the greatness within you; will make you great – Jiepushe na watu wanaojaribu kukukarisha

71

Page 72: Vyanzo vya woga, kakitabu

Eugene kawau

tama. Watu wadogo hufanya hivyo lakini ukuu wako utakufanya mkuu. Mark Twain

People know you for what you have done, not for what you plan to do – Watu wanakufahamu kwa kile ulichofanya, sio unachopanga kufanya. Anonymous

What does not destroy me, makes me stronger – Kile ambacho hakiniharibu, kinanifanya niwe na nguvu. Friedrich Nietzsche

Self trust is the secret of success. Kujiamini mwenyewe ni siri ya mafanikio. Ralph Waldo Emerson

Have courage to use your own understanding! – Jipe ujasiri wa kutumia ufahamu wako mwenyewe! Emanuel Kant

The difference between a succesfull person and the others is not luck of strength or knowledge, but rather in luck of will - Tofauti kati ya mtu aliyefanikiwa na wengineo sio kukosa nguvu au maarifa bali ni kutodhamiria/kutotia nia. Vince Lombardi

72

Page 73: Vyanzo vya woga, kakitabu

[ ]

HITIMISHO

73