3
1 SHEIKH ‘ABDUL-MĀLIK AR-RAMADHĀNI (hafidhahullâh) Suali: Dada huyu anauliza: “Tunamuhukumu vipi mtu kuwa ‘Ni Salafi’ au ‘Si Salafi’? ni nini hukmu kuhusiana na suala hilo?” Baadhi yao wanasema: “Muhammad Qutb ni Salafi kwa mfano, kuna dalili gani yakwamba yeye ‘Si Salafi’?” Jawabu kutoka kwa Sheikh ‘Abdul-Mâlik ar-Ramadhâni (hafidhahullâh): Mtu huwa ni Salafi iwapo ‘Aqîdah yake mke/mume ni Salafi, huu ndio ufafanuzi wa kimsingi usioweza kukataliwa. Hatuna haja ya kusema, “fulani ana ‘Aqîdah ya ki-Salafi na Manhaj ya ki-Salafi”, kama ambavyo mimi sipendelei kutafautisha baina ya ‘Aqîdah na Manhaj, na wala sijaona hilo kwa yoyote miongoni mwa wanavyuoni aliyeshikilia [tafauti hii] wala kupatikana vitabu vyovyote au ta’aluma yoyote kuhusiana na hili. Bali lilikuwa ni jambo lililozuliwa na baadhi ya Ma-Qutubi, kisha likaigwa na baadhi ya ma-Salafi, kwa vile Manhaj inatokamana na ‘Aqîdah kwahivyo haina haja kuzitafautisha. Lengo la Manhaj ni [kwa mfano] kujihusisha na viongozi na kujiepusha na kuwafanyia u’asi, hili linatokamana na ‘Aqîdah na walillâhil hamd hili linapatikana kwenye vitabu. Iwapo lengo ni Da’wah na kupambana na wazushi katika Da’wah, basi hilo pia ni katika sehemu ya Manhaj na yanapatikana hayo [kwenye vitabu] alhamdulillâh. Kwahiyo, sisi hatuna haja ya kusema, ‘fulani na fulani wana ‘Aqîdah ya Salaf Manhaj ya Salafi. Aqîdah na Manhaj hazitafautishi, kwani kila mwenye ‘Aqîdah ya Salaf ni Salaf.

TUNAMUHUKUMU VIPI MTU KUWA NI SALAFI AU SI · PDF fileSHEIKH ‘ABDUL-MĀLIK AR-RAMADHĀNI (hafidhahullâh) Suali: ... vitabu vya nduguye Sayyid Qutb ambavyo ni vitabu vya wazi vya

  • Upload
    vodien

  • View
    272

  • Download
    9

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: TUNAMUHUKUMU VIPI MTU KUWA NI SALAFI AU SI · PDF fileSHEIKH ‘ABDUL-MĀLIK AR-RAMADHĀNI (hafidhahullâh) Suali: ... vitabu vya nduguye Sayyid Qutb ambavyo ni vitabu vya wazi vya

TUNAMUHUKUMU VIPI MTU KUWA NI SALAFI AU SI SALAFI?

1

SHEIKH ‘ABDUL-MĀLIK AR-RAMADHĀNI (hafidhahullâh)

Suali:

Dada huyu anauliza: “Tunamuhukumu vipi mtu kuwa ‘Ni Salafi’ au ‘Si Salafi’? ni nini hukmu kuhusiana na suala hilo?” Baadhi yao wanasema: “Muhammad Qutb ni Salafi kwa mfano, kuna dalili gani yakwamba yeye ‘Si Salafi’?”

Jawabu kutoka kwa Sheikh ‘Abdul-Mâlik ar-Ramadhâni (hafidhahullâh):

Mtu huwa ni Salafi iwapo ‘Aqîdah yake mke/mume ni Salafi, huu ndio ufafanuzi wa kimsingi usioweza kukataliwa. Hatuna haja ya kusema, “fulani ana ‘Aqîdah ya ki-Salafi na Manhaj ya ki-Salafi”, kama ambavyo mimi sipendelei kutafautisha baina ya ‘Aqîdah na Manhaj, na wala sijaona hilo kwa yoyote miongoni mwa wanavyuoni aliyeshikilia [tafauti hii] wala kupatikana vitabu vyovyote au ta’aluma yoyote kuhusiana na hili. Bali lilikuwa ni jambo lililozuliwa na baadhi ya Ma-Qutubi, kisha likaigwa na baadhi ya ma-Salafi, kwa vile Manhaj inatokamana na ‘Aqîdah kwahivyo haina haja kuzitafautisha.

Lengo la Manhaj ni [kwa mfano] kujihusisha na viongozi na kujiepusha na kuwafanyia u’asi, hili linatokamana na ‘Aqîdah na walillâhil hamd hili linapatikana kwenye vitabu. Iwapo lengo ni Da’wah na kupambana na wazushi katika Da’wah, basi hilo pia ni katika sehemu ya Manhaj na yanapatikana hayo [kwenye vitabu] alhamdulillâh. Kwahiyo, sisi hatuna haja ya kusema, ‘fulani na fulani wana ‘Aqîdah ya Salaf Manhaj ya Salafi. Aqîdah na Manhaj hazitafautishi, kwani kila mwenye ‘Aqîdah ya Salaf ni Salaf.

Page 2: TUNAMUHUKUMU VIPI MTU KUWA NI SALAFI AU SI · PDF fileSHEIKH ‘ABDUL-MĀLIK AR-RAMADHĀNI (hafidhahullâh) Suali: ... vitabu vya nduguye Sayyid Qutb ambavyo ni vitabu vya wazi vya

TUNAMUHUKUMU VIPI MTU KUWA NI SALAFI AU SI SALAFI?

2

Kwahivyo inatupasa kuwa na ta’dhima kubwa kwenye Aqîdah na tunautangaza ufafanuzi huu ili tupate kutilia mkazo katika kinga isije ikabaki wazi kwa kila mtu akajaribu kupenya ndani yake. Kwanini? Kwa sababu kuna nguzo za ki-msingi na haiwezekani, kwa mfano kwa mtu aliye kwenye mfumo wa Ikhwâni kutoka katika pote la Ikhwânul-Muslimîn [Muslim Brotherhood] aingilie katika mas’ala hayo, hata kama anaweza kukubaliana na wewe kuhusiana na Majina ya Allâh na Sifa Zake na itikadi ya Salaf us-Swâlih katika mas’ala hayo, akatetea kufanya Khurûj [u’asi] dhidi ya viongozi. Mtu kama huyo si Salafi, kama ambavyo yoyote mwenye kutekeleza Khurûj anazingatiwa kuwa ni miongoni mwa Ma-Khawârij, kama ilivyo katika nguzo zao maarufu za ki-msingi. Mtu anaweza kuwa nje ya mkunjo wa Salafiyyah iwapo yeye, mke/mume, atashikamana na Madh-hab ambayo ni mashuhuri miongoni mwa Madh-hab za Ahlul Bid’ah.

Katika suali lililoulizwa ime-elezwa yakwamba, “Baadhi yao wanadai yakwamba Muhammad Qutb ni Salafi”. Sisi twasema yakwamba inawapasa wathibitishe hayo, wathibitishe yakwamba mtu huyu ni Salafi. Mtu huyu aliingia kwenye Nchi ya Guba la Uarabuni na akaishi kwa muda katika nchi ya Saudi Arabia, na kwa bahati mbaya akaleta ufisadi humo kwenye kila alichoweza kukifisidi. Mwanafunzi wake aliyekuwa na bidii mno katika kushikamana na mfumo wake na ulinganizi alokuwa nao alikuwa ni Safar al-Hawâlî. Huyu Safar al-Hawâlî alikuwa ni maarufu sana kwa takfîr, Khurûj na Uchochezi kuhusiana na haya. Kasome kitabu chake alichokiandika kiitwacho, Wâqi’unâ al-Mu’âsir [Hali katika zama zetu] ikiwa unataka kufahamu yakwamba mtu huyu si Salafi, bali yeye ni Thawrî [Mwana-harakati wa Mapinduzi]. Kwa hakika ni takfîri mkali sana. Yeye anaonelea yakwamba hakuna faida yoyote leo ya kujadiliana kuhusu siyasa kwenye jamii ya Waislamu kwani wao hata hawajui ‘Lâ ilâha illallâh’ na kwahivyo ni lazima ‘Lâ ilâha illallâh’ ithibitishwe kwanza katika nyoyo.” Twamuomba Allâh atusalimu salama! “Kuthibitisha”!? “Kuthibitisha” jambo ni iwapo jambo lile halipo kabisa asilani, ndio lipate kuthibitishwa. Haya ndiyo ayasemayo kwenye kitabu chake Wâqi’unâ al-Mu’âsir [Hali katika zama zetu]. Vilevile amesema maneno mabaya kuhusu Maswahaba katika kitabu chake juu ya tafsîr au Historia ya Uislamu, maneno ya upotofu. Yeye ndiye aliyeizindua upya irjâ’ na kisha akaihusisha kwa Ahlus-Sunnah, kama alivyosema Imâm Ahmad yakwamba Ma-Khawârij huwabadikizia Ahlus-Sunnah wal-Jamâ’ah sifa ya Irjâ’.

Vilevile akaandika utangulizi katika kitabu chenye upotofu kilichoandikwa na mwanafunzi wake, Safar al-Hawâlî, kwa jina al-‘Ilmâniyyah [Mlimwengu – asiyeamini Dini]. kitabu hiki, kuanzia mwanzo hadi mwisho, kinawafanyia takfîr pasi na ufafanuzi, viongozi kwa kutohukumu kwa aliyoyateremsha Allâh. Kuanzia mwanzoni mwa kitabu mpaka mwisho wake, muandishi [yaani; Safar al-Hawâlî] hakuieleza kabisa tafsîr ya Ibn ‘Abbâs, ‘Attwâ’, Twâwûs au Ijmâ ya Salaf. Salaf wanaamini yakwamba kuhukumu kwa kisichokuwa hicho alichohukumia Allâh ni Kufr ndogo na si Kufr Kubwa isipokuwa iwapo itaandamana na dalili ya katika hali nyengine kama vile kiongozi anapohukumu kwa kisichokuwa alichokiteremsha Allâh pamoja na kuhalalisha [istihlâl – kuamini yakwamba ni halali] baada ya kubainishiwa dalili. Al-Hawâli hakurejea hata mara moja kwenye tafsîr ya Salaf ya aya kuhusu kuhukumu kwa kisichokuwa alichokiteremsha Allâh, hata ingawa alirudia kuitaja aya mara kwa mara katika kitabu chake, na ni kitabu kilichoandikiwa utangulizi na Muhammad Qutb.

Page 3: TUNAMUHUKUMU VIPI MTU KUWA NI SALAFI AU SI · PDF fileSHEIKH ‘ABDUL-MĀLIK AR-RAMADHĀNI (hafidhahullâh) Suali: ... vitabu vya nduguye Sayyid Qutb ambavyo ni vitabu vya wazi vya

TUNAMUHUKUMU VIPI MTU KUWA NI SALAFI AU SI SALAFI?

3

Vilevile Muhammad Qutb alimuandikia utangulizi mwanafunzi wake Dr. Safar al-Hawâlî kwenye kitabu chake Dhâhirat ul-Irjâ’ fi’l-Fikr il-Islâmî [Kudhihirika Irjâ’ kwenye mfumo wa Uislamu], ambacho asili yake kilikuwa ndicho tasnifu yake ya kupata shahada ya Udaktari [doctoral thesis]. Kitabu hiki kina ulinganizi wa wazi kwenye takfîr na khurûj, katika Manhaj ya mfumo wa muandishi. Zaidi ya hayo, vilevile al-Hawâlî alimtuhumu Sheikh al-Albâni kuwa ni miongoni mwa Murji’ah au kwa kukubaliana na madh-hab yao kwenye mas’ala kadhaa na kadhaa, haya ni pamoja na tuhuma nyenginezo. Vilevile al-Hawâlî amesema yakwamba mas’ala ya khurûj dhidi ya kiongozi aliye dhâlim ni suala la Ijtihâd yenye faida, ambapo hapafai kuwepo tadhlîl [kumtangaza mtu kuwa mpotofu]’. Hebu zingatia! Haya ndiyo aliyoyasema Muhammad Qutb katika utangulizi wake. Kwahivyo ukweli wa mambo ni kwamba, Muhammad Qutb alikuja katika sehemu za Guba la Uarabuni kwa lengo la kusababisha mapinduzi hususan katika sehemu za Guba la Uarabuni, na kwa uhakika alisababisha mfumo wa kimapinduzi miongoni mwa wafuasi wake. Sasa hivi wafuasi wake na wanafunzi wake ndio hao wenye kuchochea mikasa, milipuko ya mabomu na kuchapisha vitabu vya nduguye Sayyid Qutb ambavyo ni vitabu vya wazi vya takfîr, tafjîr na kuwakashifu Maswahaba.

Amesema Sheikh Muhammad Jamî Zeynû: “Nilimpigia simu Muhammad Qutb nikamwambia, ni kwanini wewe bado waendelea kuchapisha vitabu vya nduguyo haliyakuwa yeye amewakashifu Maswahaba kama vile ‘Uthmân na akasema yakwamba wale waliomu’asi yeye walikuwa ni karibu zaidi na dhati ya Dini ya Usilamu kuliko yeye [‘Uthmân]? Kuna Sunni yoyote aliyewahi kusema maneno hayo?” Muhammad Qutb alijibu kwa kusema, “Mimi nachapisha vitabu vya ndugu yangu kama vilivyo! Allâh amesema, ‘Na saidianeni kwenye wema na ucha-Mungu, lakini musisaidiane katika makosa na uadui.” {al-Mâidah 5:2}.”

Siku ya Qiyâmah, stakabadhi hii itasimama na kuthubutu dhidi yako na upotofu ambao wewe unaousambaza miongoni mwa watu. Kwa hali yoyote iwayo, mtu huyu Muhammad Qutb ni hatari kwa Sunnah na Salafiyyah. Allâh Ndiye msimamizi wa kutegemwa.

Mfasiri: Abu Farida Muhammad Awadh Salim Basawad, Mombasa

http://www.qssea.net

Tarehe August 2015, kuanzia kikao cha tatu baina ya Shaykh ‘Abdul-Mâlik na Jukwaa la:

“Mahajjat us-Salafiyyah”.

Tizama katika: http://www.kulalsalafiyeen.com/vb/showthread.php?t=66419

Kwa hisani ya: brixtonmasjid.co.uk

http://brixtonmasjid.co.uk/project/how-do-we-judge-a-person-to-be-salafi-or-not/