806
ى س و م صا ع ون ك ف أ مأ ي ف ق ل يFIMBO YA MUSA INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA JUZUU YA KWANZA 1

xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

  • Upload
    lycong

  • View
    947

  • Download
    41

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

عصاموسى

يأفكون ما تلقف

FIMBO YA MUSAINAYAMEZA WANAYOYAZUSHA

JUZUU YA KWANZA

1

Page 2: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Juma Muhammad Rashid Al-MazruiYALIYOMO

Maudhui…………...…………………………………………………UkurasaUTANGILIZI……………………………………Kitabu cha Kasim Mafuta……………………………………………….Kuwacha fursa ya dhahabu………………………………………Utanabahisho…………………………………………………………SURA YA KWANZA……………………………….Kuyajadili maneno ya Sheikh Seif Al-Ghafri………………………..Jawabu kwa maelezo ya Al-Ghafri…………………………………Makosa ya Al-Albani, Imamu wa Hadithi wa Kiwahabi……………Al-Albani hazijui Hadithi zilizomo katika Sahihu Al-Bukhari na Sahihu Muslim!...............................................................................Vifungu vyengine vya kujadiliwa katika maneno ya Seif Al-Ghafri…Mukhtasari na nukta muhimu…………………………………SURA YA PILI…………………………………………Fikra na itikadi za Kiwahabi…………………………………………Mungu ni kiwiliwili si kama viwiliwili!...................................................Kiwiliwili cha Mungu kina viungo!......................................................Naturudi katika riwaya za mungu mwenye mikono……………………Maelezo zaidi kuhusu Aya za mkono wa Mungu…………………………Madai yasio na msingi ……………………………………………Hadithi nyengine za mkono wa Mungu……………………………Mikono miwili haitumiki ila kwa mwenye mikono ya kweli!.......................Mukhtasari……………………………………………………Viungo vyengine vya Mungu……………………………………..Mukhtasari na nukta muhimu………………………………………SURA YA TATU……………………………………Falsafa ya balkafa………………………………………….Mukhtasari na nukta muhimu……………………………………SURA YA NNE………………………………………Natija mbili za hatari……………………………………………….Mjadala wa Diamond Jubilee……………………………..Mungu ana sura ya Adam!............................................

2

Page 3: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

SURA YA TANO…………………………………..Tashbihi ni nini?..........................................................................................Mukhtasari na nukta muhimu…………………………………………SURA YA SITA………………………………………..Mjadala juu ya kuwepo kwa majazi…………………………………………Jawabu niliopata kutoka kwa Sh. Kasim Mafuta na mjadala juu ya jawabu hio………………………………..Tafsiri ya Qur-ani kwa Qur-ani………………………………..Aya za kuja kwa Mwenyezi Mungu kimajazi……………………..Mjadala na Al-Darimi……………………………………………Aya zenye kuonesha kuondoshwa kwa neno amru (jambo)………………Tunarudi katika mjadala wa majazi……………………………Makusudio ya majazu mursal…………………………………Kuichezea lugha na Qur-ani…………………………………….Maelezo zaidi juu ya kuwepo kwa majazi……………………….Jawabu ya Badru Al-din Al-Khalili…………………………………Majazi katika Qur-ani…………………………………………………Majazi katika Hadithi…………………………………………………Majazi katika lugha ya Kiarabu…………………………………Mawahabi hawajui wakisemacho!............................................................Kujigonga kwa Ibn Al-Qayyim……………………………………Kuyatumia kwake majazi……………………………………Kukaribia kwake kuyataja majazi………………………………Kuyataja kwake majazi kwa jina lake la kifani……………………Ibn Taymiyya na majazi…………………………………………Kasim Mafuta naye ajigonga……………………………………Mukhtasari na nukta muhimu………………………………………SURA YA SABA………………………………Kuhusu ta-awil…………………………………………….Ta-awil kilugha……………………………………………….Maneno ya Sheikh Al-Khalili……………………………………Maneno ya Dr. Muhammad Na’iim……………………………………Maneno ya Dr. Al-Buti……………………………………….Kujigonga katika suala la ta-awil…………………………….SURA YA NANE………………………………………Msimamo wa madhehebu za Kisunni juu ya itikadi hizo……………Mukhtasari na nukta muhimu………………………………SURA YA TISA……………………………………..Kuwakafirisha na kuwatukana Waislamu…………………..Matusi na ukafirishaji wa Ibn Al-Qayyim………………………………

3

Page 4: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Tanbihi………………………………………………………Matusi ya Ibn Taymiyya………………………………………….Ukafirishaji wa Al-Rustumi…………………………………….Ukafirishaji wa Ibn Baz………………………………….Ukafirishaji wa Sulaiman Bin Sihmaan……………………….Ukafirishaji wa Abdullahi bin Abdil-Rahmaan Al-Jibrin…………..Ukafirishaji wa Maimamu waasisi………………………………..Hata atayekikataa kitabu cha Imamu wa Kiwahabi pia ni kafiri………Baadhi ya mtu mmoja mmoja waliokafirishwa na viongozi wa Kiwahabi zamani na leo…………………………………………….Kuwafanyia uadui Maimamu wakubwa………………………Kuwakimbiza wafuasi wao wasiitafute haki…………………………SURA YA KUMI………………………………………..Kujigonga……………………………………………………………..Hadithi Ahadi………………………………………………….Makubaliano ya Umma………………………………………….Kufuata Al-Salaf………………………………………………..Qiyas baina ya Allah na viumbe……………………………….Qiyas chengine cha Muumba na kiumbe…………………….Kufuata kundi…………………………………………….Masahaba………………………………………………………..Kuwadhoofisha wapokezi na kuwasahihisha wawatakao………………Wapokezi dhaifu ambao Mawahabi na Maimamu wao wanawakumbatia………….Majazi………………………………………………………….Natija ya kujigonga katika minhaj (methodology)…………………………Mungu ni/si kiwiliwili…………………………………………Mungu yuko juu lakini………………………………………..Mungu ana mpaka lakini hana!............................................SURA YA KUMI NA MOJAKuhusu Ibn Taymiyya na Ibn Al-Qayyim……………………………..Jawabu niliopata…………………………………………………………..Jawabu na maelezo……………………………………………………….Natuingie kwenye maudhui…………………………………………………..Wanavyuoni waliolizungumzia jambo hilo la itikadi ya Ibn Taymiyya ya kutangulia kwa aina ya ulimwengu………………………………….Yaliosemwa na Wanavyuoni kuhusu Ibn Taymiyya……………………Maulamaa waliomjadili au waliomjibu Ibn Taymiyya…………………Kuhusu Ibn Al-Qayyim……………………………………………Jawabu niliopata……………………………………………………

4

Page 5: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Jawabu na Maelezo………………………………………………..Tanbihi………………………………………………………SURA YA KUMI NA MBILI ………………………Tuhuma za uwongo dhidi ya Maimamu wa Ahlu Al-Haqqi Wa Al-Istqaama na majibu Yetu……………………………………………………..Utangulizi Wa Sehemu Hii…………………………………………..Walioitwa Khawarij hawana tabia ya kusema uwongo……………………Tuhuma ya kwanza: tuhuma dhidi ya Al-Imamu Badru Al-Din Al-Khalili Al-Mufassir………………………………………………………………..Jawabu……………………….Mukhtasari na nukta muhimu………………………………………Yaliosemwa na waadilifu wa Kisuni kuhusu Sheikh Al-Khalili………………Tuhuma ya pili: tuhuma dhidi ya Imamu Al-Sunna wal usuli wal furu’i Al-Qannubi………………………………………….Jawabu na Maelezo……………………………………..Je Aliyoyanukuu Al-Qannubi kutoka kwa Al-Albani ni kweli au uwongo?.......................................................................................................Mfumo huo unamtumbukiza Al-Albani na Kasim Mafuta katika dimbwi!..Bali na Kasim Mafuta naye yumo kwenye mezani yake mwenyewe………Mukhtasari na nukta muhimu……………………………SURA YA KUMI NA TATU……………………Sheikh Al-Khalili amtaka Ibn Baz wafanye mjadala wa wazi au wamuombe Allah ateremshe laana yake kwa mwenye itikadi potofu……Kukimbia mjadala ni sera ya Kiwahabi……………………Naturudi tena kwa Al-Khalili na Ibn Baz………………………Nyongeza kuhusu mualiko wa mjadala……………………………

هد اهد وش�� أهلها من ش�� “Na akashuhudia shahidi katika watu wake mwenyewe”………SURA YA KUMI NA NNE……………………..Mawahabi na Maimamu wao ndio wasiosema kweli…………Utangulizi wa sehemu hii……………………..Abu ‘Izz Ibn Kaadish………………………………Abu Talib Al-‘Ushaari…………………………………………Abu Ali Al-Ahwazi………………………………………..Abdul-Aziz bin Al-Harith Al-Tamimi……………………..Al-Hakkaari…………………………………………….Ibn Batta Al-’Ukbari……………………………..Maneno yasio na ukweli ya ‘Uthman Al-Darimi………………Maneno yasio na ukweli ya Ibn Taymiyya………………………Maneno yasio na ukweli ya Ibn Al-Qayyim………………………….

5

Page 6: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Sulaiman bin Sihmaan awazulia Waislamu……….Dr. ‘Ali Al-Faqihi amzulia Sheikh Al-Khalili……………………….Ibn Baz na Al-Fawzaan nao washiriki katika kumzulia uwongo Al-Khalili….Dr. Bakr Abu Zaid atuhumiwa kwa kuzuwa uwongo…………………Dr. ‘Umar Al-Ashqar apotoa maandiko…………………………Yalioandikwa Katika Gazeti La Dustur………………………………Vitabu vya uzushi………………………………………..Al-Radu Alaa Al-Jahmiyya………………………………..Kitabu Al-Sunna Kilichonasibiswakwa Abdullah bin Ahmad……………Kitabu Al-Ru’uya Kilichonasibiswa Na Al-Daraqutni………………Baadhi Ya Mifano Ya Hadithi Zilizotungwa Na Mujassima…………Riwaya za kutungiwa Al-Imamu Ahmad……………………………Mukhtasari Wa Ujumla………………………………………………Hatima………………………………………………………………Vitabu vyengine vya muandishi……………………..Baadhi ya scanned copies nilizoahidi kuziweka mwishoni mwa kitabu…511

6

Page 7: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

الرحيم الرحمن الله بسم

ىلع الإ انودع الو نيقتملل ةباقعالو نيمالعال بر لله دمحالالصالحين نأ دهشأو, نيمالالظ ولي له شرك ال وحده الله إال إله ال

ع دمحم نأ دهشأو غلب هليلخو هقلخ نم هيفصو هلوسرو هدبااأل دأو ةالسالر الله لص ةمالغ هب الله فشكو ةماأل حصنو ةانمى ىآل لعو هيلع ملسو هبحصو هى

UTANGULIZI

Baada ya kumuhimidi Allah na kumtakia rehema Mtume wake (s.a.w.) pamoja na Masahaba wake na waliowema katika watu wa nyumba yake, elewa ndugu msomaji kwamba kabla ya Uislamu, binaadamu walikuwa katika upotovu wa wazi. Hakuna kitu bora chenye kuweza kutoa picha ya wazi juu ya upotovu huo, kuliko ibara fupi ya Qur-ani inayosema:

يين في بعث الذي هو األم ويزكيهم آياته عليهم يتلو منهم رسوال كمة�والح الكتاب ويعلمهم

مبين ضالل لفي قبل من كانوا وإن

Yeye (Allah) ndiye aliyetuma katika ummiyyin (wasiojua kusoma wala kuandika) Mtume miongoni mwao, (akawa) anawasomea Aya zake na kuwatakasa na kuwafunza Kitabu na hekima, pamoja na kuwa hapo mwanzo walikuwa katika upotovu wa wazi.1

Upotovu huo ulidhihiri katika nyanja zote za maisha ya binaadamu: nyanja za kiitikadi, nyanja za kisiasa, nyanja za kijamii na nyanja za kiuchumi. Itikadi katika sehemu kubwa au yote ya Bara Arabu ilikuwa msingi wake mkuu ni ibada ya masanamu. Utawala ulikuwa, katika sehemu nyingi za Waarabu, ni wa mabavu ambao mara nyingi ulikuwa ukidhihiri kwa njia za kivita na kidikteta. Jamii zilikosa maadili hata ikafika katika baadhi ya sehemu za dunia mtu kumuoa dada yake au mama yake. Uchumi ulichukua muundo wa dhulma na ukandamizaji uliodhihiri mara nyingi katika kuhodhi njia za kiuchumi, unyang’anyi na mifumo ya riba. Lakini hakuna shaka

1 - Sura 62, Aya 2.

7

Page 8: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

yoyote ile kwamba msukumo wa upotovu huo wa aina tafauti uliodhihiri katika nyanja hizo tafauti za maisha ya binaadamu, chimbuko lake ni upotovu katika itikadi. Itikadi potofu ndio msingi wa upotovu wote – itikadi mbovu hutoa matunda mabovu. Kwa picha iliowazi zaidi, tazama, kwa mfano, kitendo cha kumuua mtu asiyestahiki kuuliwa; huo ni upotovu wa kijamii au ukipenda kiite kitendo hicho kuwa ni ufisadi katika jamii; kutawala kidikteta ni upotovu wa kisiasa au ni ufisadi wa kisiasa; kuhodhi njia za uchumi na kunyang’anya ni upotovu wa kiuchumi. Mambo hayo yote yalikuwepo katika jamii za Waarabu na wasiokuwa Waarabu kabla ya Uislamu bila ya kuwepo adiolojia tetezi yenye kutetea haki za wanyonge.2 Chimbuko la upotovu wa anayeyatenda hayo yote au baadhi ya hayo, ni kutokuamini kwake kuwepo kwa malipo baada ya kufa – upotovu wa kiitikadi chimbuko la ufisadi wote. Huo ni mtazamo wa ujumla. Ama kwa mtazamo mahususi, ni kuwa hata wale wanaodai kuwa na imani ya siku ya malipo, bado wanafanya mambo ya upotovu kama huo. Hilo linatoa picha ya kuwa matendo yao hayo ndio tafsiri sahihi ya imani yao – hawana ukweli katika imani yao hio.

Kama umelielewa hilo, basi utakuwa umeelewa umuhimu wa itikadi ya dini ya Kiislamu katika maisha ya binaadamu ya kidunia ukiachilia mbali umuhimu wake katika maisha ya kiakhera. Na kwa hivyo, utaona kwamba Mitume wote wanaotumwa na Allah basi wito wao wa kwanza ni kufunza itikadi na tauhidi kama Allah alivyosema:

رسول من قبلك من أرسلنا وما إله ال أنه إليه نوحي إال أنا إالفاعبدون

Na hatukumtuma Mtume yoyote kabla yako, isipokuwa tunamfunulia kwamba hakuna Mola isipokuwa Mimi basi niabuduni.3

Halkadhalika Mtume (s.a.w.) alipomtuma Sahaba wake Mu’adh bin Jabal kwenda Al-Yaman alimwambia:

ل أن شهادة إلى فادعهم كتاب أهل قوما تأتي إل اإنك وأني اإله اللهالله رسول

2 - Political economy (uchumi wa kisiasa) uliosemwa kuwepo hapo zamani ambao uliweza kuhakikisha maslahi ya jamii ni ule ulioitwa primitive communalism. Nao ni mfumo wa kubuni uliotetewa na wanafalsafa wa kijamaa wa Mashariki na kukataliwa na wanafalsafa wa kibepari wa kimagharibi. 3 - Sura 21, Aya 25.

8

Page 9: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Hakika wewe unawaendea watu wa Kitabu, basi (jambo la mwanzo) walinganie katika shahada ya kwamba: ‘Hakuna mola wa haki isipokuwa Allah na kwamba mimi ni Mjumbe wa Allah’.4

Na kwa sababu hio, basi Mtume (s.a.w.) alipigania – kwa muda wa miaka 23 – kuwaonesha watu njia sahihi. Na katika kufanya hivyo, alifunza mambo mawili makuu:

1) Uhusiano wa mtu na mtu. Huu unachukua muundo wa:a) Siasa ya dola.b) Mfumo wa kiuchumi.c) Maadili ya kijamii.

Kwa maana hio, utakuwa umeelewa vyema kwamba Uislamu ni aidiolojia (ideology) yenye kudhamini mfumo kamili wa maisha ya binaadamu, kwani Uislamu unatoa mafunzo ya namna gani dola iendeshwe; vipi na namna gani uchumi uundwe; na vipi na namna gani jamii ijengwe. Na hio ndio maana ya aidiolojia (ideology) – nadharia za kijamii, kisiasa na kiuchumi (social, political and economic theories). Lakini, tena kwa mara ya pili, elewa kwamba tafauti iliopo baina ya aidiolojia za kidunia na aidiolojia ya Kiislamu, ni kuwa aidiolojia za kidunia ni za kibinaadamu (purely human) na kwa hivyo ni nadharia (theories); wakati aidiolojia ya Kiislamu ni ya Allah (Divine ideology) na kwa hivyo, aidiolojia ya Kiislamu haifafanuliwi kwamba ni nadharia za kijamii, kisiasa, na kiuchumi kama zinavyofafanuliwa aidiolojia za kidunia, bali aidiolojia ya Kiislamu inaweza ikafafanuliwa kuwa ni mafunzo ya kijamii, kisiasa, na kiuchumi (social, political and economic teachings), kwani kinachofunzwa na Allah si nadharia: bali ni mafunzo; nadharia leo inaundwa kesho inarekebishwa na kesho kutwa inabomolewa kabisa,5 wakati mafunzo ya Allah ni ya hakika:

حميد حكيم من تنزيل خلفه من وال يديه بين من الباطل يأتيه ال

(Kitabu hiki) Hakiingiwi na batili kutoka mbele yake wala kutoka nyuma yake, ni uteremsho unaotoka kwa (Allah) Mwenye hekima, Mwenye kuhimidiwa.6

Baada ya hayo, basi elewa kwamba kuuita Uislamu kuwa ni aidiolojia (ideology) ni kwa kuizingatia maana ya kiistilahi (technical meaning) ya neno hilo kwani kiistilahi neno hilo linabeba au linaingiza mafunzo ya kisiasa, kijamii na kiuchumi, na hivyo ndivyo Uislamu ulivyo katika upande

4 - Ibn Maja Al-Sunan Hadithi na. 1783. 5 - Kama tunavyoshuhudia mifumo tafauti ya kisiasa na kiuchumi inavyopanda na kuporomoka. 6 - Sura 41, Aya 42.

9

Page 10: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

wake mmoja – upande wa kidunia.7 Ama ukizingatia asili ya kilugha ya neno ideology, basi Uislamu huwezi kuuita kuwa ni ideology kwani neno ideology ama litakuwa linatokana na neno idea na neno ology au linatokana na neno ideo na neno logy. Neno la mwanzo linamaanisha fikra na neno la pili linamaanisha elimu, na kwa hivyo, kilugha neno ideology linamaanisha elimu ya fikra. Uislamu si elimu ya fikra; bali ni mafunzo matakatifu yanayotoka kwa Allah. Lakini – kama tulivyonena – tafauti hio ni kwa kuizingatia maana ya kilugha ya neno hilo: si kwa kuizingatia maana yake ya kiistilahi (technically). Ama utapoizingatia maana ya kiistilahi, basi Uislamu utaukuta kwamba – kwa upande mmoja wa mafunzo yake nayo ni yale mafunzo yanayohusiana na maisha ya Muislamu ya kidunia – ni aidiolojia (ideology), kwani unafunza vipi serikali iwe, vipi uchumi uwe na vipi jamii iwe. Na hili ndilo wanalolikimbia Wamagharibi, ambapo mara zote wanataka kuuonesha ulimwengu kwamba Uislam ni (merely a form of worship) njia ya ibada tu: hauna haki ya utawala!

2) Mafunzo ya pili yaliotolewa na Mtume (s.a.w.), ni kuwafunza watu vipi wajenge uhusiano wao na Muumba wao. Hili – japo kuwa kimpangilio nimeliweka la pili, lakini – ndilo la msingi na ndio injini inayoendesha mafunzo ya kwanza. Bila ya hili, basi hayo ya kwanza hayawezi kupatikana kamwe. Na hili linachukua njia mbili:

a) Mafunzo ya tawhidi na itikadi. Hii ndio nguzo kuu.b) Matendo ya ibada na akhlaq, nayo ni tafsiri sahihi ya mtu ana

imani gani.

Mafunzo yote ya Uislamu yaliobakia yanaingia katika misingi hio. Mtume (s.a.w.), akatoa mafunzo na akafaulu kutoa Masahaba walioufahamu vyema Uislamu. Akaondoka duniani ilhali jamii ya Masahaba wake ndio jamii safi kuliko jamii zote kwa itikadi na matendo mema yenye kujenga jamii na yenye maadili ya hali ya juu.

Eneo la Uislamu likatanuka, na watu wa jamii mbali mbali wakaanza kuingia katika Uislamu. Waislamu wapya walikuwa ni watu waliotoka katika dini mbali mbali na zilizotafauti kabisa na dini ya Kiislamu. Waliingia katika Uislamu watu ambao awali walikuwa wakifuata dini ya kiyahudi, dini ya kikiristo, dini ya kisaabii, dini ya kimajusi; dini ya kibuda na dini na mila nyengine nyingi. Kilichotokea katika harakati hizi za mabadiliko ya kiitikadi, ni kuwa wengine miongoni mwa Waislamu wapya hawa walishindwa kuzivua kikamilifu itikadi zao za asili na badala yake walijaribu kuufahamu Uislamu kwa njia za dini zao za asili. Na hapa ikawa

7 - Ama upande wa pili ni yale mambo ya kiroho, nayo ndio msingi mkuu.

10

Page 11: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

ndio mwanzo wa kutokea mchanganyiko wa itikadi sahihi za Kiislamu na itikadi batili zilizotokea katika mila nyengine.

Kilicho wazi kabisa, ni kwamba itikadi hizo zilizoletwa katika Uislamu, baada ya kukumbatiwa na kupata waumini na watetezi, hazikuweza wala haziwezi kupata ushahidi wa wazi katika Qur-ani wala katika Sunna sahihi ya Mtume (s.a.w.), ingawa inawezekana baadhi ya wakati, si wakati wote, zikapata shubuhat8 na zikajiegemeza hapo katika shubuhati hizo. Lakini kukosekana kwa ushahidi wa wazi katika Qur-ani na Sunna, na ili kuweza kuzihalalisha itikadi hizo, kulizipelekea itikadi hizo mpya zichume nguvu zake kupitia katika mambo mawili:

1) Kutungiwa riwaya za uwongo.2) Kupotoshwa kwa maana za Aya za Qur-ani.

Ikiwa baadhi ya wakati unahitaji uwe Ibn Hajar au Ibn Jarir ili uweze kuligundua hilo, basi mara nyengine huhitaji kuwa chochote isipokuwa uwe ni binaadamu mwenye akili timamu tu ili uweze kuligundua hilo. Huhitaji kuwa Ibn Jarir Al-Tabari ili ujue ubatili wa walioifasiri Aya ya Qur-ani inayosema: الحسنى األسماء 9((Na Allah ana majina mazuri)) وللهkuwa maana ya majina mazuri hayo ni Maimamu wa Kishia;10 kama vile ambavyo huhitaji kuwa Ibn ‘Abbaas ili ujue ubatili wa tafsiri ya Aya ya Qur-ani isemayo راط اهدنا المستقيم الص ((Tuongoze njia ilionyooka)11 kuwa maana yake ni njia ya Sunna wal Jamaa’a.12 Na hii ni pale ambapo itakusudiwa kwa maneno Sunna wal Jamaa’a maana yake ya kiistilahi ya maneno hayo ambapo yakitajwa huwa inaeleweka kwamba wanaokusudiwa ni Waislamu wa madhehebu maalumu. Ama ikiwa itakusudiwa Sunna katika maana yake ya Kisharia, yaani Sunna ya Mtume (s.a.w.) iliomo katika kila madhehebu, basi tafsiri hio itakuwa na muelekeo mzuri, kwani madhehebu zilizojiita hivyo zilikuja baadae na walikwisha kutangulia Maimamu wakubwa sana waliokuwa wakifuata Sunna wala hawakuwa wakifuata madhehebu yoyote katika madhehebu hizo. Halkadhalika huhitaji kuwa Ibn Hajar ili ukubainikie ubatili uliomo katika riwaya kama:

Jahannam ina daraja saba, na sirat iko juu yake na Mwenyezi Mungu atakuwa katika daraja ya nne viumbe watapita juu yake na kwamba hio ndio maana ya Aya: “ مرصادا كانت جهنم Hakika ya jahannam) ”إن

8 - Shubuhat maana yake ni kuwa kitu kinaelekea lakini sio makusudio kamwe. 9 - Sura 7, Aya 180. 10 - Al-Kuleini Al-Kafi j. 1, uk. 192, Hadithi na. 4, babu Al-Nawadir. 11 - Sura 1, Aya 6. 12 - Tazama Al-Baghawi Ma’alimu Al-Tanzil j. 1, uk. 76.

11

Page 12: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

ni yenye kuwangoja (waovu)”,13 na Aya “ لبالمرصاد ربك إن ” (Hakika ya Mola wako yuko katika madoezi),14 na riwaya nyengine zilizo mfano wa hizo.15

Migawanyiko ya kisiasa ilipopamba moto, utunzi zaidi wa riwaya ulishamiri na kuzidi kujitokeza ili kuipa nguvu misimamo ya Kisiasa. Hadithi zenye kuhusiana na suala la Khawaarij, kwa mfano, zimesimuliwa kutoka kwa wapokezi wa Al-Kufa, mji wa Kishia, kuliko sehemu nyengine yoyote ile. Sababu iko wazi, nayo ni kuwa walioitwa Khawaarij walijitenga na Ali baada ya kukubali kwake sulhu katika vita vya Siffin; wakati Al-Kufa ni mji wa Kishia. Kwa hivyo, kuzuka Hadithi hizo zenye kuwatia kasoro walioitwa Khawaarij katika mji huo ni jambo la kimaumbile! Wakati kwa upande wa pili, Hadithi za ubora wa miji zilipokewa kutoka Sham kwa wingi mno. Sh. Hasan Al-Maaliki anaona kwamba sababu iliopelekea kuwepo kwa wingi wa riwaya hizo za ubora wa miji ni utunzi wa riwaya uliosimamiwa na mrengu wa Bani Umayya baada ya kujua kwamba Mu’awiya hakuwa na sifa alizokuwa nazo ‘Ali. Na kwa hivyo, ili kutaka kumpa nguvu Mu’awiya, basi ilibidi zitungwe riwaya kama “Sham ndio mji wa hijra itapotokea fitna”, na “Imani iko Sham itapotokea fitna” na kwamba “Huko (Sham) ndiko kutakokuwa na kundi lenye kunusuriwa (na Allah) ambalo litabakia halidhuriwi na atayelikhalifu mpaka kiama” na “Iraki kuna shari kumi na tisa” na “Uthman atauliwa na wanafiki”.16 Halkadhalika riwaya zenye kukataza kumpinga mtawala! Riwaya za namna hii zilipokewa katika mji wa Sham ya Mu’awiya kuliko sehemu nyengine yoyote ile!

Kwa sabubu hii, utakuta kwamba wanavyuoni tangu enzi ya Masahaba, wamekuwa na tabia ya kuzipima mutun (texts) za riwaya kwa mezani ya Qur-ani. Na hii ni kwa zile riwaya ambazo zimekuja kuleta tafsiri ya Aya au zina uhusiano wa moja kwa moja au japo wa mbali na Qur-ani.

Naturudi katika Waislamu wapya walioingia katika Uislamu baada ya kufa kwa Mtume (s.a.w.) na kupanuka kwa eneo la Waislamu. Watu hao, kama tulivyonena, hawakuweza kuziwacha itikadi zao za mwanzo kikamilifu. Ukweli huu, unakubaliwa na Waislamu wote wa madhehebu zote, lakini tafauti ipo katika je ni ipi itikadi iliopandikizwa katika Uislamu hususun pale ambapo itikadi husika zinapokuwa na shubuhat katika Qur-ani na Sunna. Kwa sababu hii, basi husomi kitabu katika vitabu vya itikadi au vya majibizano ya kiitikadi ila utakuta watu wanatupiana tuhuma kwamba

13 - Sura 80, Aya 21. 14 - Sura 89, Aya 14. 15 - Ibn Ahmad Al-Sunna j. 2, uk. 525-526, riwaya na. 1208. 16 - Al-Maaliki, Hasan bin Farahan Qiraa-a Fii Kutubi Al-’Aqaaid uk. 74.

12

Page 13: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

wapinzani wao wamejichukulia itikadi zao kutoka kwa Mayahudi au Manasara au kutoka katika mila nyengine zisizo za Kiislamu! Jambo hili ni mashuhuri sana ambapo ukisoma vitabu vilivyoandikwa dhidi ya Shia utakuta humo kwamba Shia wamechukua itikadi zao kutoka kwa Yahudi aitwaye Abdullah bin Saba-a. Wakati hakuna riwaya sahihi kamwe juu ya kuwepo mtu anayeitwa Abdullah bin Saba-a: riwaya zote zilizopo juu ya mtu huyu ni riwaya za kufinyanga Wallahu Al-Musta’aan! Sitaki kukwambia kwamba ninakubaliana na kila itikadi ya Kishia, lakini sikubaliani na hii minhaj (methodology) inayotumika katika kushutumiana: ni lazima tuwe na ushahidi madhubuti.

Dr. ‘Abdul-Rahman Al-Tahhaan – katika muhadhara wake aliouweka ili kujibu hoja za Kiibadhi juu ya suala la kuonekana au kutoonekana kwa Allah – aliikataa riwaya ya Mujahid ya kutoonekana kwa Allah kwa madai kwamba Mujahid alikuwa akichukua riwaya kutoka kwa watu wa Kitab – Mayahudi na Makristo. Dr. ‘Ali Al-Faqihi naye, katika kitabu chake Al-Raddu Al-Qawiim, ameelezea jinsi Mayahudi na maadui wengine wa Kiislamu walivyokuwa wanafanya harakati za kueneza fikra zao. Kisha akasema kwamba Waislamu wengine wameghururika wakazifuata itikadi hizo za Mayahudi. Kisha akasema:

وجد لها، وانتصر الحاضر، عصرنا في المنحرفة األفكار هذه تلقف وممنعن المدافعة ها�في

.» الخليلي» حمد بن أحمد

Na miongoni mwa waliozimeza fikra hizo potofu katika zama hizi na kuzitetea na kujitahidi katika kuzihami ni ((Ahmad bin Hamad Al-Khalili)).17

Na anasema Al-Faqihi:

عجزوا ) ولما اليهود( لج أي بالسيف، اإلسالم مواجهة بأن ؤواعن له، للكيدفي بعضهم دخل

فعل كما نفاقا الله (( اإلسالم ) عبد اإلمامية، عقائد أسس الذي سبأ بنوتك الرفض فير���������في

الجهمية بعقائد عقائدهم ختموا ثم القرآن، تحريف ودعوى الصحابة،ومن ����تواالع ها����زال،

القيام يوم ربهم المؤمنين رؤية ة.......إنكار

17 - ‘Ali Al-Faqihi Al-Raddu Al-Qawiim Al-Baaligh uk. 9. Bwana huyu kaandika kitabu hicho ambacho lau alikiandika mwanafuzi basi dahari ingelimcheka! Si hivyo tu, bali hakujilazimisha kusema ukweli hata kidogo katika nukulu zake. Tutakunukulia baadhi ya ghushi zake na baadhi ya yale aliomzulia Sheikh Al-Khalili katika sehemu maalumu tulioiweka ili kunukuu maneno ya Mawahabi yasio na ukweli.

13

Page 14: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Waliposhindwa (Mayahudi) kuukabili uislamu kwa vita basi walikimbilia katika kuufanyia vitimbi, wengine wakajitia katika Uislamu kwa unafiki kama alivyofanya ‘Abdullah bin Saba-a ambaye kaanzisha itikadi za Kishia Imamiyya katika kuwakataa na kuwakafirisha Masahaba na madai kwamba Qur-ani imepotolewa, kisha wakaishia kwa itikadi za Jahmiyya na Mu’utazila, na miongoni mwa hizo ni kukanusha kuwa Waumini watamuona Mola wao siku ya kiama! 18

Hayo ndio maneno ya Dr. Al-Tahhan na Dr. Al-Faqihi. Lakini tukirudi katika maneno ya Dr. Al-Tahhan, utakuta kwamba maneno yake hayo ni kinyume na alivyosema Imamu wake mkuu Ibn Taymiyya, ambapo alisema kuhusu Mujahid:

Kama hukukuta tafsiri (ya Aya ya Qur-ani) katika Qur-ani wala katika Sunna wala kutoka kwa Masahaba, basi Maimamu wengi wamerejea katika hilo kwa kauli za Taabi’iin kama Mujahid bin Jabr hakika yake alikuwa ni muujiza katika (elimu ya) tafsir.19

Anaendelea Ibn Taymiyya kwa kusema: “Ama tafsiri, basi wajuzi wao ni watu wa Makka kwani ni wanafunzi wa Ibn Abbaas kama vile Mujahid”.20

Bali – kama alivyoeleza Ibn Taymiyya katika vitabu tafauti pia Ibn Al-Qayyim – Mujahid tafsiri yake baada ya kuiandika alimuonesha Ibn Abbaas mara tatu akawa anamuonesha Aya moja moja mwanzo hadi mwisho.21 Kwa hivyo, tafsiri yake ni tafsiri ya Ibn Abbaas kwa mazingatio hayo.

Ama tukirudi katika suala la kuchukua riwaya kutoka kwa Ahlil Kitaab kama alivyodai Dr. Al-Tahhaan, na yale alioyasema Dr. ‘Ali Al-Faqihi kwamba Ibadhi wana itikadi za Kiyahudi, utaona kwamba Dr. huyo kayasema hayo alipokuwa akijibu hoja za Ibadhi kuhusu:

1) Kutoonekana kwa Allah.2) Kutotoka motoni.3) Qur-ani ni kiumbe.

Wakati kwa upande mwengine, na sisi katika Ibadhi tunaona kuwa itikadi za wanaoitwa Mawahabi ndizo zenye mkono wa Kiyahudi. Bali hata hizi itikadi ambazo kazitetea Dr. Al-Faqihi utakuta kwamba kuzihusisha na Mayahudi ni sahihi zaidi kuliko hizi itikadi alizozipinga. Wapi kasikia Al-Faqihi na wenzake kwamba Mayahudi walikuwa wakikanusha kuonekana

18 - Al-Faqihi Al-Raddu Al-Qawiim Al-Baaligh uk. 60-61. 19 - Ibn Taymiyya Al-Nukatu Al-Mutammima uk. 96 kwa tahqiq ya ‘Abdil-Mun’im Ibrahim. 20 - K.h.j. uk. 64. 21 - Ibn Taymiyya Majmu’a Al-Fatawa j. 3, uk. 37, j. 13, 209-210.

14

Page 15: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kwa Allah hata akaziita itikadi za Kiibadhi za kukanusha kuonekana kwa Allah kuwa ni itikadi za Kiyahudi? Je si ndio Mayahudi ambao Allah kazisimulia habari zao na Musa kwa kusema:

جهرة الله نرى حتى لك نؤمن لن موسى يا قلتم وإذNa (kumbukeni) muliposema (enyi Mayahudi kumwambia

Musa): E Musa! Sisi hatutokuamini wewe kamwe hadi tumuone Allah wazi wazi.22

Na anasema Allah kuhusu Mayahudi:

جهرة الله أرنا فقالواWakasema (Mayahudi kumwambia Musa)

tuoneshe Allah wazi wazi. 23

Sasa je, kwa mujibu wa Aya hizi, itikadi ya Kiyahudi inakataa kumuona Allah au inatilia mkazo juu ya suala hilo? Na – bila shaka – aliyekubali kuonekana kwa Allah duniani basi kulikubali hilo huko akhera ni rahisi zaidi.

Kwa hivyo, kwa mujibu wa Aya hizo, sisi tunaona kwamba chimbuko la itikadi hii ya kuonekana kwa Allah ni fikra zilizopandwa na Mayahudi. Wakati wenzetu nao wanaona kwamba itikadi ya kukataa kumuona Allah ni itikadi iliopandwa na Mayahudi ili kupotoa Uislamu. Lakini – kama ulivyoona – itikadi ya Mayahudi ni kuonekana kwa Allah: si kukataa kuonekana kwa Allah. Cha kusikitisha ni kuwa wenzetu hawakutupa ushahidi wowote ule ulioweza kuthibitisha madai yao. Ama sisi, mbali na kuwepo kwa Aya hizo, tunasema kwamba ushahidi mwengine juu ya kuwa Mayahudi ndio walioipandikiza itikadi hio, ni ukweli kwamba hakuna riwaya yoyote ile yenye sanad sahihi katika riwaya zenye kuzungumzia kuonekana kwa Allah isipokuwa, inavyosemekana, riwaya moja. Riwaya moja hio ni riwaya iliosimuliwa kutoka kwa Ka’abu Al-Ahbar naye ni Myahudi aliyesilimu katika zama za ‘Umar na akawa anasimulia israailiyyaat (riwaya za Kiyahudi) hadi ‘Umar akamzuia kusimulia riwaya na akamtishia kumfukuza.24 Baadhi ya Masahaba na baadhi ya Tabi’iin wakawa wanazipokea riwaya hizo na – kwa kughafilika – wakawa wakati mwengine wanazihusisha na Mtume (s.a.w.)! Anasema Al-Sayyid Al-Saqqaaf:22 - Sura 2, Aya 55. 23 - Sura 4, Aya 153. 24 - Tutamuelezea zaidi na kunukuu baadhi ya riwaya zake zenye itikadi kama ya Kiwahabi katika juzuu ya mwisho.

15

Page 16: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Katika Siyaru Al-A’alaam25 na Al-Bidaaya wa Al-Nihaaya26 kutoka kwa Busr bin Sa’iid (naye ni katika Matabiina wakubwa na ni katika msimulizi wa wapokezi sita), alisema: ‘Muogopeni Allah, na chukueni hadhari katika masimulizi ya Hadithi, Wallaahi naona tunakaa na Abu Huraira, basi anatusimulia kutoka kwa Mtume (s.a.w.) na anatusimulia kutoka kwa Ka’abu Al-Ahbaar, kisha anaondoka, basi ninawasikia baadhi ya waliokuwa pamoja na sisi wanaifanya Hadithi ya Mtume (s.a.w.) kuwa inatoka kwa Ka’abu na Hadithi ya Ka’abu kuwa inatoka kwa Mtume (s.a.w.).27

Na namna hivyo ziliweza kupenya itikadi za Kiyahudi na Kinasara hata katika zama za mwanzo kabisa za Uislamu. Na utapojua kwamba riwaya pekee yenye sanad sahihi kuhusu kuonekana kwa Allah ni riwaya ya Ka’abu Al-Ahbar, Yahudi aliyesilimu, basi utakuwa umeelewa kwamba riwaya hizo za kuonekana kwa Allah ni mazigazi hususan utapojua kwamba riwaya hizo zinagongana na Aya ya Qur-ani; zinagongana na Hadithi sahihi yenye sanad kama dhahabu alioipokea Muslim; na zinagongana na riwaya nyengine za baadhi ya Tabi’iin. Jambo la pili ambalo limo katika kitabu cha Sheikh Al-Khalili, na ambalo Dr. Al-Faqihi anaona kuwa ni fikra ya Kiyahudi – ni suala la kuwa wenye kufanya maasi makubwa na wakafa bila ya kutubia basi makazi yao ni motoni watakaa humo milele. Dr. Al-Faqihi anaona kwamba hii ni itikadi ya Kiyahudi. Lakini kasahau Al-Faqihi kwamba itikadi ya kuwa watu watatoka motoni ndio ambayo Allah kaisimulia katika kitabu chake kutoka kwa Mayahudi. Anasema Allah:

نا لن وقالوا النار تمس إال الله عند أتخذتم قل معدودة أياما فلن عهدا أم هده�ع الله لف�يخ

به وأحاطت سيئة كسب من ( بلى80) تعلمون ال ما الله على تقولونك���فأولئ خطيئتهخالدون فيها هم النار أصحاب

Na wakasema (Mayahudi): moto hautotugusa ila siku chache. Sema: je mumechukua ahadi kwa Allah, kwani Allah hatokwenda kinyume na ahadi yake au munamsemea Allah mambo musioyajua? Hapana!

25 - J. 2, uk. 606. 26 - J. 8, uk. 109. 27 - Nukulu kutoka kwa Al-Sayyid Al-Saqqaaf Mas-alatu Al-Ru-uya uk. 73. Ninasema: na Hadithi za kuonekana kwa Allah ni katika jumla ya masimulizi ya Ka’ab na Mayahudi wenzake ambazo watu wamezinasibisha na Mtume (s.a.w.).

16

Page 17: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

wataochuma uovu na makosa yao yakawazunguka, basi hao ni watu wa motoni watakaa humo milele.28

Na anasema Allah kuhusu Mayahudi:

أوتوا الذين إلى تر ألم ليحكم الله كتاب إلى يدعون الكتاب من نصيباق�فري يتولى ثم بينهمنا لن قالوا بأنهم ( ذلك23) معرضون وهم منهم النار تمس إال أياما

هم معدودات ي��ف وغريفترون كانوا ما دينهم

Huoni wale waliopewa sehemu ya Kitabu wanalinganiwa kuja katika Kitabu cha Allah ili kiwahukumu baina yao kisha kikundi miongoni mwao wanakengeuka na huku wanapuuza**Hayo ni kwa sababu wao wamesema kwamba moto sisi hautotugusa isipokuwa siku chache, na yakawatia ghururi katika dini yao yale waliokuwa wakiyazua. 29

Utaona kwa uwazi kabisa kwamba itikadi ya Kiyahudi ni kutoka motoni: si kubakia humo milele. Kwa hivyo, maneno ya Dr. Al-Faqihi kwamba itikadi alizozitetea Sh. Al-Khalili ni itikadi za kiyahudi, si maneno madhubuti, bali kinyume chake ndio sahihi – itikadi alizozitetea Al-Faqihi ndio za Kiyahudi kama Qur-ani inavyotongoa.

Lakini kuna kitu kimoja muhimu cha kuzinduana, nacho ni kuwa yalionenwa na Mayahudi na Manasara yanagawika katika sehemu tatu:

1) Yale ambayo yako sawa na mafunzo yaliomo katika Uislamu, yaani Qur-ani au Sunna imeyakubali. Haya yanakuwa sahihi.

2) Yale ambayo yanagongana na Qur-ani au Sunna. Haya ni batili.3) Yale ambayo hayana ushahidi kwamba ni sahihi au ni batili. Haya

tunatakiwa tusiyakubali wala tusiyakatae.Itikadi ya kuonekana kwa Allah pamoja na itikadi ya kutoka motoni zinaingia katika kifungu nambari mbili – zinagongana na Qur-ani na Sunna, kama tutavyobainisha in shaa Allah.

Halkadhalika ukija katika itikadi za tajsim,30utakuta kwamba katika kitabu cha mwanzo cha Taurati iliopotoshwa (yaani hii Bibilia ya leo), kuna maandiko yanayosema: “Tutamuumba mtu kwa sura yetu: anafanana na sisi”. Itikadi hii ya kwamba Adam kaumbwa kwa sura ya Allah inathibitishwa na watu wa skuli ya wanaoitwa Mawahabi pamoja na

28 - Sura 2, Aya 80-81. 29 - Sura 3, Aya 23-24. 30 - Tajsiim maana yake ni kumuitakidi Allah kuwa ni kiwiliwili, au kuwa ni mwenye viungo.

17

Page 18: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Maimamu wao watangulizi, ingawa kipengele “Anafanana na sisi” kimeonekana kudhihiri katika utunzi wa Mawahabi wa mwisho mwisho tu.31

Kwa ujumla ni kuwa, itikadi ambazo wapekuzi wamezikuta kuwemo katika dini nyengine na ambazo baadae zimekutikana katika baadhi ya madhehebu za Kiislamu kwa sababu ya kuchanganyika kwa Waislamu Waarabu na Waislamu wapya kutoka mataifa mengine ni:

1) Itikadi ya kuonekana kwa Mungu.2) Itikadi ya kupita katika Sirat.3) Itikadi ya kuwa Allah yuko mbinguni.4) Itikadi ya kuwa Allah ana sura.5) Itikadi ya kuwa Allah ni kiwiliwili. 6) Itikadi ya kuwa Allah anakaa juu ya ‘Arshi.7) Itikadi ya kuwa kiti ndio sehemu ya Allah ya kuwekea miguu.8) Itikadi ya kulitukuza jiwe lililoko katika Al-Masjid Al-Aqsaa.9) Itikadi kwamba Allah kaweka miguu yake juu ya jiwe hilo.10) Itikadi kwamba Allah ana miguu.11) Itikadi kwamba Allah ana mikono.12) Kupanda na kushuka kwa Allah. 13) Itikadi ya kuwa kuna muokozi anayengojewa (Al-Muntadhar),

ambapo mtaalamu wa Kishia Al-Ustaadh Muhammad Ridhaa Al-Hakimi anathibitisha itikadi ya kuja kwa mgojewa huyo, si katika Qur-ani na Sunna tu,32 bali pia katika mila zilizopita kama vile dini ya Zaraadashtiyya, dini ya Kiyahudi, dini ya Kikiristo, dini ya Kihindu na dini ya Kibuda.33 Ni wazi, kwa mujibu wa madai hayo ya mtaalamu huyo, kwamba itikadi hii ya kumg’ojea muokozi chimbuko lake ni mila zisizo za Kiislamu hasa hasa zile zilizotokea Fursi kama vile Zaraadashtiyya.

14) Na itikadi nyengine nyingi zenye kufanana na hizo.

Anasema Dr. Zakariyya Al-Muharmi:

Katika nchi ya Furs (Iran) walikuwa wakiabudu vitu vya kimaumbile – jua, mwezi, muangaza n.k. Akadhihiri mtu aliyeitwa Zardasht (583 B.C.),34 akaja na kitabu chake kilichoitwa Avesta. Huyu alikuja na itikadi tafauti

31 - Tutanukuu maneno yao kamili tukifika sehemu yake na tutatoa marejeo. 32 - Hili lina maelezo marefu hapa si mahala pake. 33 - Muhammad Ridhaa Al-Hakimi Al-Imamu Al-Mahdi Fii Kutubi Al-Umami Al-Saabiqa Wa Al-Muslimiin uk. 51-58. 34 - Tazama habari za Zardasht kwa urefu katika kitabu Al-Milal Wa Al-Nihal cha Al-Shahrastani j. 1, uk. 263-270.

18

Page 19: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

miongoni mwa hizo ni itikadi kwamba roho ya binaadamu ikifika siku ya hesabu basi itapita katika siraat iliopo juu ya jahannam, nayo hio siraat kwa Mu-umini ni pana na ni rahisi kuipita, na asiyekuwa Mu-umini basi siraat ni nyembamba kuliko unywele. Atayeamini na kutenda mema basi atavuuka katika siraat kwa salama na atakutana na Ahuur (mungu wa kheri), naye atampokea kwa wema na kumkirimu; na asiyekuwa mwema basi ataanguka katika jahannam na atakuwa mtumwa wa Ahraman (mungu wa shari).35

Sasa leo ukitazama itikadi hizi, utaziona zimo katika baadhi ya madhehebu za Kiislamu. Na suala hili lina tafauti kwa wanavyuoni wa Umma.36

Anaendelea Dr. Zakariyya:

Na alidhihiri katika miji ya Furs, mtu aliyeitwa Mani (215-216 M.).37 Madhehebu ya huyu ilienea Asia na Ulaya. Miongoni mwa itikadi zake ni kuingia katika utawa na kuitupilia mbali dunia. Akaweka sharia ya kusali sana na kufunga sana na akaharamisha ndoa ili ulimwengu upate kumalizika haraka haraka. Rai hizi utazikuta zimo katika baadhi ya Masufi.38

Anasema Dr:

Kama ambavyo Wafursi wa Saasaan walikuwa wakiwatazama wafalme wao kwamba ni viumbe wa Kiungu ambao Allah kawachagua na kuwapa nguvu kwa roho kutoka kwake na kwamba damu zao ni za Kiungu. Na wakati watu hawa walipoingia katika Uislamu walikuwa katika kundi la Ali wakaanzisha fikra ya urafidha ya kumkataa Abu Bakr na ‘Umar na kumfuata Ali na watoto wake na wakamtazama ‘Ali na watoto wake kama

35 - Nimeinukuu kwa kuisarifu kidogo na kwa mukhtasari. Tazama Dr. Zakariyya bin Khalifa Al-Muharmi Qiraa-atun Fii Jadaliyyati Al-Riwaya Wa Al-Diraaya uk. 7. Tanbihi: Kitabu hiki ni miongoni mwa vitabu ambavyo havikukubalika kabisa. Mtunzi ni mtu wa fikra ya ‘Aqlaaniyya nao ni watu wanaopinga Hadithi Ahadi hata katika matendo na wanapinga karama za Mawalii na wanapinga miraji na ndoto na mambo kadha wa kadhaa ambayo yamethibiti katika Qur-ani, Hadithi na kukubaliwa na jumhur ya Maimamu wakubwa wa Umma. Kwa hivyo, kwa ujumla hatuwategemei isipokuwa tunaweza kuchagua moja moja lililo sahihi au lenye muelekeo. 36 - Nakusudia kulielezea in shaa Allah katika kazi nyengine, hapa natoa mifano tu. 37 - Mani kaelezewa kwa ufupi na Al-Shahrastani katika Al-Milal Wa Al-Nihal j. 1, uk. 271-72. 38 - Tazama Dr. Zakariyya bin Khalifa Al-Muharmi Qiraa-atun Fii Jadaliyyati Al-Riwaya Wa Al-Diraaya uk. 7. Naye kainukuu kutoka katika kitabu Fajru Al-Islam cha Ahmad Amin uk. 99-104, kwa kuisarifu.

19

Page 20: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

vile walivyokuwa wakiwatazama wafalme wao – mtazamo wa Kiungu!.39

……….

……………Na miongoni mwa itikadi zilizonukuliwa kutoka kwa Ahlu Al-Kitab hususan wale walioingia katika Uislamu ni itikadi ya kuwa Allah yuko mbinguni. Ambapo utaona watu wengine hutoa hoja kwa maandiko ya Bibilia. Anasema Ibn Taymiyya: “Na katika Injili (tunapata) kwamba Masihi (Isa bin Mar-yam) alisema: ‘Musiape kwa mbingu kwani mbingu ni kiti cha Mungu …..mukiwasamehe watu basi Baba yenu ALIYE MBINGUNI atakusameheni…….na Baba yenu ALIYE MBINGUNI ndiye anayewaruzuku. 40

Anasema Al-Imamu Badru Al-Din Al-Khalili Al-Mufassir katika kipindi chake cha T.V. Sualu Ahli Al-Dhikr baada ya kuyanukuu maneno hayo kutoka katika vitabu vya wajiitao Al-Salafiyya: “Lakini hili limebatilishwa na Qur-ani, kwani maandiko hayo ya Bibilia yanadai kuwepo kwa ubaba na umwana baina ya Allah na viumbe, wakati Allah Anasema:

مد ( الله1) أحد الله هو قل له يكن ( ولم3) يولد ولم يلد ( لم2) الص كفواأحد

Sema: Yeye ni Allah aliye pweke. Allah ndiye mkusudiwa (katika kukidhi haja za viumbe wake). Hakuzaa wala hakuzaliwa. Wala hakuna yoyote yule aliye mfano wake.41

Ninasema: wala usiniambie kwamba Bibilia haijakusudia watoto wa kuzaa, bali ni watoto wa kiroho, kwani tunasema kwamba hio ndio ta-awil munayoikimbia. Bali kwa kufuata udhahiri wa lugha kama hizi za kimajazi ndiko kulikowapoteza Wakiristo wakashindwa kuyafahamu makusudio ya maandiko yao. Walipoambiwa: “watoto wa Mungu”, wakadhani kwamba Allah ana watoto; walipoambiwa “Mungu ni roho” wakadhania kuwa Mungu ana roho! Tatizo hili pia limekuwepo kwa wanaojiita Al-Salafiyya ambapo wameshindwa kuzifahamu lugha kama hizo! Iliposemwa “Allah kamuumba Adam kwa sura yake” wakasema “Allah ana sura ya Adam anafanana naye”. Subhaana Allah, hadhaa buhtaanun ‘adhiim!

Naturudi katika nukulu za Dr. Zakariyya. Anasema Dr:

39 - Tazama Dr. Zakariyya bin Khalifa Al-Muharmi Qiraa-atun Fii Jadaliyyati Al-Riwaya Wa Al-Diraaya uk. 8. Naye kainukuu kutoka katika Al-Tashayyu’u Al-’Alawi wa Al-Tashayyu’u Al-Safawi uk. 124. 40 - Tazama Dr. Zakariyya bin Khalifa Al-Muharmi Qiraa-atun Fii Jadaliyyati Al-Riwaya Wa Al-Diraaya uk. 8. 41 - Sura 112, Aya 1-4.

20

Page 21: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Na wengine wanaona kwamba fikra ya kupinga qadar ilienezwa na Yohana Mkiristo……42

….Na dola ya Bani Umayya kuanzia na Mu’awiya bin Abi Sufyaan nao pia ni wenye kutuhumiwa kuzipitisha itikadi nyingi batili katika kukabiliana na itikadi sahihi za wenye kuupinga utawala wao wa kurithi usio wa shura. Walitegemea Bani Umayya ‘aqidatul jabr (itikadi ya ulazimisho). Maana ya itikadi hii ni kuwa walidai kwamba utawala wao umekuwa kwa chaguo la Allah na kwa hivyo Waislamu hawakuwa na mamlaka ya kuupinga isipokuwa kusalimu amri tu; wala haijuzu kwao kuupinga kwani kufanya hivyo ni kuipinga amri ya Allah na maamuzi yake.43

Ninasema: Hapa ilikuwa ndio chanzo cha itikadi hio ya jabr yaani itikadi kwamba mtu hana khiyari katika matendo yake bali kalazimishwa na Allah. Na kilichosahihi ni kuwa Allah kaumba kheri na shari; mazuri na mabaya kisha akampa mtu khiyari ya kufanya anavyotaka – Allah kaumba; binaadamu anachuma atakacho. Vyenginevyo itakuwaje Allah aliyemuadilifu amuadhibu kiumbe dhaifu kwa kitu alichomlazimisha? Lakini Bani Umayya walianzisha itikadi hio ili kuwanyamazisha watu wasiupinge utawala wao.

Anaendelea Dr. Zakaria:

Na wakajisahau (Bani Umayya) kwa kuzua itikadi ya Irjaa. Nayo maana yake ni kuwa mtu naafanye maasi atakayo madamu yeye anasema La ilaha illa Allah basi atakwenda peponi tu? Ama hatoingia motoni kabisa kwa sababu ya maombezi ya Mtume (s.a.w.) au ataingia kisha atatoka…..44

Ninasema: Na Fir’awna naye pia alisema La ilaha illa Allah! Lakini tatizo lake ni lile lile la kuwa alikosa matendo. Bali walisahau Banii Umayya kwamba riwaya zenye kusema: “Atayesema La ilaha illa Allah kwa ikhlasi ataingia peponi” ni riwaya mutlaqa45 ambazo ni lazima zifungamanishwe na

42 - Al-Maaliki, Hasan bin Farahaan Qira-atu Fii Kutubi Al-’Aqaaid 85-88. Katika kopi nilionayo ni uk. 79. 43 - Tazama Dr. Zakariyya bin Khalifa Al-Muharmi Qiraa-atun Fii Jadaliyyati Al-Riwaya Wa Al-Diraaya uk. 9. 44 - Tazama Dr. Zakariyya bin Khalifa Al-Muharmi Qiraa-atun Fii Jadaliyyati Al-Riwaya Wa Al-Diraaya uk. 9. 45 - Andiko mutlaq ni lile ambalo halikufungika na sifa maalumu ambayo inaifanya lafdhi ya andiko hilo kuwa isikiingize kila kile ambacho kinaihusu lafdhi hio. Kwa mfano neno “mtu”. Kila ambaye lafdhi hii inamuingiza basi huyo yumo ndani yake, kwa hivyo neno hilo hapo ni mutlaq (lisilofungamanishwa na kitu chochote). Lakini nikiweka sifa fulani

21

Page 22: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

riwaya nyengine yenye kusema “Atayesema La ilaha illa Allah ataingia peponi madamu anatenda matendo (mema)”.

Anaendelea Dr. Zakaria:

Bali baadhi yao walishiriki katika kutunga riwaya ambazo zinajenga itikadi za Kitaurati (iliopotoshwa). Miongoni mwa hizo, ni riwaya iliosimuliwa na Ibn Khuzaima kutoka kwa ‘Ur-wa bin Zubair kwamba alisema: “Nilikwenda kwa ‘Abdul-Malik nikataja mbele yake jiwe lililoko katika Baitu Al-Maqdis, basi akasema ‘Abdul-Malik: “Hili ni jiwe la Allah mwingi wa rehema ambalo aliweka miguu yake juu yake….’Ur-wa akampinga”.46 Na itikadi hii ambayo ‘Abdul-Malik bin Mar-waan alikuwa akiilingania ni miongoni mwa alioyanukuu kutoka kwa Mayahudi. Imepokelewa kwamba ‘Abdullahi bin Mas’ud alipita kwa mzee ambaye alikuwa anawasimulia watu yaliomo katika Taurat. Alipomuona Ibn Mas’ud akanyamaza. Akasema Ibn Mas’ud: ‘Sahibu yenu anakusimulieni nini?’ Wakasema: ‘Kasema kwamba Allah alipoziumba mbingu na ardhi, alipanda mbinguni47 kutokea Bait Al-Maqdis na akaweka mguu wake juu ya jiwe lililoko katika Bait Al-Maqdis. Ibn Mas’ud akastarjii48 kisha akasema: ‘E Allah! hakuna kukufuru baada ya imani. 49……….…………..Na akasimulia Al-Dhahabi katika kitabu Al-‘Uluwwi kwamba Jarir bin Al-Khatafi alikuja kwa ‘Abdil-Malik ili kumsifu. Akamwambia: ‘Ewe Jarir! Ni kitu gani kilichokuleta hapa? Akasema (Jarir):

*** دليل عليك وإسالم ونور عرشه فوق الذي الله بي 50أتاك

nikasema: “mtu mrefu”, basi hili linaitwa muqayyad na kwa hivyo mtu mfupi anakuwa hayumo. Halkadhalika nikisema “mtu muumini” basi “mtu kafiri” anakuwa hakuingia hapo. 46 - Ibn Khuzaima Al-Tauhid uk. 241, kwa tahqiq ya Samir Al-Zuhairi. 47 - Kwani alikuwa chini hata akasema alipanda? Na hio chini ilikueko wapi kabla ya kuumbwa?! 48 - Akasema: Innaa Lillahi wa innaa ilahi raaji’un (Sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tu ndiko tutakorejea). 49 - Tazama Dr. Zakariyya bin Khalifa Al-Muharmi Qiraa-atun Fii Jadaliyyati Al-Riwaya Wa Al-Diraaya uk. 9. Anasema Dr. Zakaria: “Tazama pia Al-Rabi’u bin Habib Al-Jaami’u Al-Sahih riwaya na. 879. ‘Abdul-Jawaad Yaasin katika Al-Sulta Fii Al-Islam uk. 274, anasema kwamba Ka’abu Al-Ahbaar ndiye aliyekuwa akisimulia riwaya za kuwa Allah kaweka mguu wake katika jiwe la Bait Al-Maqdi pamoja na riwaya nyengine nyingi za kulitukuza jiwe hilo, na katika kuzifanyia tahqiq riwaya hizo akatoa marejeo ya kitabu Nihaayatu Al-Irhaab cha Al-Nuwairi j. 1, uk. 332”.

50 �- مختصر في القيم ابن اإلمام عند ومثله زكريا الدكتور كتاب في جاء كذاص " 359الصواعق عطف " دون دليل عليك إسالم ونور غيرهما عند رأيته والذي ،

." " " نور" على إسالم

22

Page 23: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Kanileta kwako Allah ambaye yuko juu ya ‘Arshi**Na nuru na Uslamu ndio dalili juu yako.51

Kasimulia Abu Sheikh katika kitabu Al-’Adhama52 riwaya…..kutoka kwa Ka’abu Al-Ahbar akisema: ‘Kasema Allah katika Taurat: ‘Mimi ndio Allah niko juu ya viumbe wangu; na ‘Arshi yangu iko juu ya viumbe wangu wote na mimi niko juu ya ‘Arshi naendesha mambo ya waja wangu….53

Hayo ndio alioyasema Dr. Zakariyya.54 Na mengine alioyaeleza ni kuwa katika kipindi cha utawala wa Banii Umayya palitokea mabadiliko katika mfumo wa elimu ambapo walivifasiri vitabu vya elimu vya mataifa mengine ambavyo vilitumika kwa kusomeshewa katika madaris. Na hilo lilianzia na Khaalid bin Yazid bin Mu’awiya. Wasiriani nao wakafanya bidii ya kuvifasiri vitabu vya Kiyunani na kuvieneza kwa Waislamu. Kama vile ambavyo riwaya za Kiisraili (israailiyyaat) zilipamba moto katika kipindi hiki.

Kabla ya hapo, Ka’abu Al-Ahbaar (Yahudi aliyesilimu), alimshauru ‘Umar kuujenga Al-Masjid Al-Aqsaa nyuma ya jiwe ili watu wakisali walielekee jiwe hilo. ‘Umar akamkaripia, lakini hata hivyo Ka’abu aliweza kuwaghururisha baadhi yao. Mutarrif bin Malik alikuwa anasali hali ya kuwa jiwe limemzinga baina yake na Al-Ka’aba. Kama ambavyo Ka’abu huyu alidai kwamba Al-Dhabiih (Mchinjwa) mwana wa Ibrahim ni Is-haaq: si Isma’iil! Na kauli hii walighururika nayo baadhi ya Masahaba na baadhi ya Wafuasi wao.55 Halkadhalika Ka’abu huyu ndiye aliyedai kwamba Mtume (s.a.w.) kamuona Allah! Al-Sayyida ‘Aisha (r.a.) aliposikia akasema: “Atayedai kuwa Muhammad kamuona Mola wake basi huyo kazua uwongo mkubwa”.56 Na Ka’abu huyu ndiye aliyesema: “Allah yuko mbinguni kakaa juu ya Arshi na Arshi iko juu ya viumbe wote”.57 Ni wazi kwamba fikra ya kuwa Allah yuko juu kweli kweli na kwamba anakaa kitako kweli ni fikra ya Kiyahudi iliopandwa katika Uislamu na Ka’abu na wenzake kama riwaya hio inavyojionesha.58

51 - Katika vitabu vyengine imeandikwa: “Na nuru ya Uislamu.”… 52 - Abu Sheikh Al-’Adhama uk. 95-96, nambari. 246. 53 - Tazama Dr. Zakariyya bin Khalifa Al-Muharmi Qiraa-atun Fii Jadaliyyati Al-Riwaya Wa Al-Diraaya uk. 9-10. 54 - Katika sehemu nyengine nimeyanukuu kimaana pamoja na kufupisha. 55 - Tazama pia Ibn Kathir Tafsiru Al-Qur-ani Al-‘Adhim j. 2, uk. 427, tafsiri ya Aya ya 6, ya Surat Yusuf. Kwa maelezo zaidi tazama pia uk. 411, katika maelezo yake ya Aya ya 69-73 za Surat Huud.56 - Tazama Al-Tirmidhi Al-Sunan Hadithi na. 3278. 57 - Ibn Al-Qayyim Mukhtasaru Al-Sawaaiqi Al-Mursala uk. 358-59. 58 - Na Ibn Al-Qayyim anasema kuwa hio ni riwaya sahihi. Tazama marejeo yaliotangulia.

23

Page 24: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Na Myahudi mwengine aliyeingia katika Uislamu na kusimulia riwaya za Kiisraaili katika Uislamu ni Wahb bin Munabbih. Miongoni mwa riwaya zake ni: “Mbingu na bahari ziko katika jengo kubwa (haykal) na jengo hilo liko katika kursiy (kiti) na miguu ya Allah Mtukufu iko juu ya kiti”. Hii ni itikadi ya Kiyahudi ilioenezwa na Mayahudi walioingia katika Uislamu, na ambayo leo tunaona wanaojiita Al-Salafiyya au wanaoitwa Mawahabi wana itikadi hio hio, ambapo Ibn Al-Qayyim na wengine wanasema: “Kiti ndio sehemu ya (kuwekea) miguu yake miwili”59 yaani miguu miwili ya Mungu! Lakini ili itikadi hizi na zilizo mfano wa hizi, ambazo zimeletwa katika Uislamu na Mayahudi waliosilimu, zipate nguvu basi kwanza ilibidi watakaswe wale waliozileta. Wahb bin Munabbih huyu katungiwa riwaya iliompa cheo kikubwa kuliko yeye mwenyewe! Wamesimulia wapambe wake kwamba Mtume (s.a.w.) kasema: “Katika umma wangu kutakuwa na mtu anayeitwa Wahb bin Munabbih huyo Allah atampa hekima…”. Yote haya yamenenwa ili kuziweka akili tayari kupokea mafunzo yake ya Kiisraili. Nayo Hadithi hio ni Hadithi ya kutunga kama alivyosema Ibn Al-Jawzi pamoja na kubainisha sanad yake.60

Halkadhalika ukirudi katika maelezo ya Ibn Al-Qayyim, utamkuta anamtetea Ka’abu Al-Ahbar na kuwaita wale waliomkadhibisha kuwa ni Mu’attila! Anasema Ibn Al-Qayyim:

Tujaaliye kwamba mu’attil anamkadhibisha Ka’abu na anamtuhumu kuwa (ana itikadi) za tajsim (za kumfanya Allah kuwa ni kiwiliwili), basi vipi hawa wanavyuoni wamesimulia kutoka kwake wakimthibitisha pasina kumpinga….61

Bila shaka Ibn Al-Qayyim kayanena hayo ili kuisafisha njia inayotupeleka kwenye riwaya za Kiisraili zilizosimuliwa na bwana Ka’abu. Lakini kasahau Ibn Al-Qayyim kwamba ikiwa kuna mwanachuoni aliyezikubali riwaya za Kiisraili za Ka’abu Al-Ahbar ambaye, kwa mujibu wa maelezo yake, ndiye muthbit lisifaati Allahi (mwenye kuzikubali sifa za Allah), basi kuna wanavyoni wengi zaidi wakiwemo baadhi ya Masahaba ambao

59 - Ibn Al-Qayyim Hadi Al-Arwah uk. 42,299. ‘Uthman Al-Darimi Al-Raddu ‘Alaa Al-Marisi j. 2, uk. 67. Na hii ndiyo iliyokuwa nyimbo ya Ibn Taymiya kama ilivyo katika kitabu chake Majmu’a Fatawa j. 5, uk. 51. Naam! Hapa Ibn Taymiyya ananukuu lakini ananukuu kwa kuyakubali maneno hayo bali kwa kuyatolea hoja. Tazama pia Ibn Ahmad Al-Sunna j. 1, uk. 301, riwaya na. 585. Dr. Ali Muhammad Al-Sallabi Min ‘Aqitadati Al-Muslimin uk. 80.60 - Ibn Al-Jawzi Al-Maudhu’aat j. 2, uk. 47. 61 - Ibn Al-Qayyim Mukhtasaru Al-Sawaaiqi Al-Mursala uk. 358-59.

24

Page 25: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

walizikanusha riwaya za Ka’abu.62 Sijui kwamba Masahaba hao nao watakuwa katika orodha ya Mu’attila ya Ibn Al-Qayyim, au mu’attila tutakuwa mimi na fulani?

Myahudi mwengine aliyesilimu na akawa anasimulia riwaya za Kiisraili ni ‘Abdullahi bin Salam. Huyu inasemwa kuwa aliifasiri Aya ya Qur-ani isemayo: ربك يبعثك أن عسى مقاما محم��ودا (Huenda Mola wako akakuinua cheo cha kuhimidiwa)63 kwa kusema: “Ikifika siku ya kiama basi ataletwa Mtume (s.a.w.) atawekwa mbele ya Allah juu ya kiti chake (kiti cha Allah)”. Na itikadi hii tayari imepata soko hasa hasa katika ulimwengu wa Kiwahabi na Maimamu wao watangulizi.64 Anasema Ibn Taymiyya:

: أن المقبولون وأولياؤه المرضيون العلماء حدث فقد هذا تبين إذاصلى الله رسول محمدا

. بن محمد ذلك روى معه العرش على ربه يجلسه وسلم عليه اللهع ليث عن ن������فضيل

محمودا : } { مجاهد مقاما ربك يبعثك أن عسى تفسير ……في

Basi litapobainika hili, (elewa kwamba) wanavyuoni wema na mawalii waliokubalika wamesema kwamba Muhammad Mjumbe wa Allah, Mola wake atamuweka kitako juu ya Arshi. Na Muhammad bin Fudhail akayasimulia hayo kutoka kwa Laith kutoka kwa Mujahid katika tafsiri ya Aya isemayo: ربك يبعثك أن عسى مقاما محمودا (Huenda Mola wako akakuinua cheo cha kuhimidiwa)……65

Anasema Al-Sayyid Al-Saqqaaf:

Na hizi ni katika jumla ya riwaya za Kiisraili ambazo Ibn Salam kazinukuu na kujaribu kuzipandikiza katika Umma wa Kiislamu, na maneno yake haya ndio asili ya Hadithi refu ya uombezi na Hadithi refu ya kuonekana kwa Allah ambayo ndani yake kumetajwa siraat na mengineo ambayo tumeihukumu kuwa ni shaadh (dhaifu) katika zaidi ya kitabu katika vitabu vyetu. Na riwaya hii inathibitisha kwamba fikra hizi zimechukuliwa kutoka katika riwaya za Kiisraili. Na ‘Abdillahi bin Salaam ni miongoni mwa wanavyuoni wakubwa wa Kiyahudi kabla hajasilimu na kutoka kwake na walio mfano wake zimetoka hizi fikra chafu za kumfaya (Allah) kuwa ni kiwiliwili na zikaingia katika Umma huu. Na kuthibiti riwaya hii kutoka

62 - Juzuu ya nne in shaa Allah itazungumzia suala hili kwa urefu. 63 - Sura 17, Aya 79. 64 - Al-Khallal kapokea riwaya nyingi kutoka kwa Maimamu wao juu ya mas-ala haya katika kitabu chake Al-Sunna. 65 - Ibn Taymiyya Majumu’a Al-Fatawa j. 4, uk. 238, babu: fii tafdhili baina Al-Malaaika.

25

Page 26: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kwa ‘Abdillahi bin Salaam, kunamaanisha kwamba itikadi hizi na fikra hizi chanzo chake ni za Kiyahudi wala si za Kiislamu kamwe.66

Baada ya maelezo hayo, inatubainikia:1) Kwamba kuna mambo mengi ya itikadi ambayo yameingizwa

katika Uislamu.2) Itikadi zile zile za Mayahudi, Manasara na watu wa mila

nyengine, utazikuta zimefuatwa na baadhi ya Waislamu!3) Itikadi ya kuonekana kwa Allah, kutoka motoni, Allah kuwa na

viungo, na kuwa yuko juu, na nyengine tulizozitaja katika utangulizi huu, asili yake ni riwaya za Ahlu Al-Kitaab waliosilimu.

4) Riwaya hizo wengine walikuwa wakizinasibisha na Mtume (s.a.w.), na haya yako kwa wingi kama tutavyoelezea katika juzuu ya nne ya kitabu hiki.

5) Ni lazima kuzipima riwaya kwa mezani ya Qur-ani, baada ya kuifahamu Qur-ani ufahamu sahihi uliojengeka katika kanuni za lugha ya Kiarabu na misingi myengine ya tafsiri, ili tuweze kuijua riwaya je ni ya kweli au si ya kweli. Wala haitoshi kutazama sanad tu ikawa ndio basi. Tutalieleza hili kwa urefu katika juzuu ya nne ya kitabu hiki in shaa Allah.

Huu ni mukhtasari utaokuwezesha kujua kwamba itikadi nyingi zilizopo leo ni natija ya riwaya za Kiisraili na mafunzo ya watu wa mila nyengine tafauti baada ya kuingia katika Uislamu ambapo walishindwa kuzivua itikadi zao za asili kikamilifu. Bali ukweli huu hadi leo hii utauona bado upo ambapo, watu wengi wanaoingia katika Uislamu wanabaki na baadhi ya mila zao na wanajaribu kuufahamu Uislamu kwa kupitia katika zile dini zao za asili. Kwa mantiki hii, ni lazima marejeo ya kwanza wakati wa kuzijadili itikadi yawe ni Qur-ani, na yaliobaki yapimwe kwa Qur-ani.

Sasa kabla ya kuingia katika maudhui za kitabu hiki, ni vyema tutazame kidogo hali ya kitabu cha Al-Akh Sheikh Kasim Mafuta, halafu tutoe utanabahisho na baada ya hapo tuingie katika maudhui za juzuu hii ya kwanza ya kitabu hiki.

Juma Muhammad Rashid Al-Mazrui24/12/2009

66 - Al-Saqqaaf, Hasan bin ‘Ali Al-Ta’aliq ‘Alaa Al-’Uluwwi uk. 307. Kwa maelezo zaidi tazama Dr. Zakariyya Qiraa-atu Fii Al-Jadaliyya Al-Riwaaya uk. 5-22.

26

Page 27: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

KITABU CHA SH. KASIM MAFUTA

Katika miezi ya karibu tumepata kitabu kilichoandikwa na ndugu yetu Sheikh Kasim Mafuta wa Pongwe Tanga alichokiita Hoja Zenye Nguvu Katika Kuthibitisha Kuonekana Allah (Sub’haana Wata’alaa) Kwa Macho Huko Akhera: Majibu Na Maelezo. Kitabu hicho kakiandika ili kujibu kitabu changu nilichokiita Hoja Zenye Nguvu Juu Ya Kutoonekana Allah Kwa Macho nilichokiandika kuthibitisha itikadi sahihi ya Mitume (a.s.) na Masahaba na Al-Salafu Al-Salih ya kutoonekana kwa Allah kwa mujibu wa Qur-ani na Sunna thabiti za Mtume (s.a.w.). Kawaida yangu ninapoandika kitabu au kupata kitabu cha namna hio, huwa nawauliza wasomaji mbali mbali kuhusu fikra zao juu ya kitabu hicho. Ninachoweza kusema ni kuwa Al-Hamdu Lilahi Rabil Al-’Alamin. Watu wote niliowauliza au walioniambia wenyewe kuhusu fikra zao juu ya kitabu hicho cha Sheikh Kasim Mafuta ni kuwa “Hamuna kitu: matusi matupu”. Ninasema na ninakariri kumshukuru Allah Al-Hamdu Lillahi: hii ni neema kubwa kwani matusi ni alama ya mtu asiye na hoja: mwenye hoja huwa hatukani. Kwa hivyo, namwambia ndugu yetu Sheikh Kasim Mafuta kwamba kitabu changu Hoja Zenye Nguvu bado hakijajibiwa kwa hoja sahihi na kwa hivyo bado ni hoja yangu mbele ya Allah siku ya Kiama NA ANAYETAKA MJADALA WA WAZI JUU YA MAUDHUI HII MIMI NIKO TAYARI NA ANAYETAKA MUBAHALA KWAMBA ALLAH ATEREMSHE LAANA YAKE JUU MWENYE ITIKADI MBOVU KATIKA SUALA HILI AU JUU NANI NI MWENYE ITIKADI MBOVU BAINA YETU SISI NA WANAOITWA MAWAHABI MIMI NIKO TAYARI.

27

Page 28: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Kwa ufupi ni kuwa katika kitabu hicho hakuna isipokuwa makosa matupu ya kiminhaj (methodological errors). Sheikh Kasim Mafuta hakujilazimisha kuifuata minhaj inayofuatwa na wanavyuoni katika kuyafasiri maandiko. Kwa hivyo, mimi baada ya kukisoma kitabu cha Sh. Kasim Mafuta, na vilivyo mfano wake kama kitabu cha Dr. Al-Faqihi, moyo wangu ulizidi kutulia juu itikadi ya Ahlu Al-Haqqi Wa Al-Istiqama; na kwa hivyo ninakwambia ewe Sheikh Kasim bin Mafuta mimi sikujuta kwa kitabu changu hicho bali sasa – si kwamba ninakitayarisha kwa chapa ya pili tu, bali – nimekianza kukiweka katika lugha ya Kiingereza ili wenye akili zao timamu waweze kufaidika. Na nashuhudia na namshudisha Allah kwamba Yeye haonekani na kiumbe chochote duniani wala akhera. Allahumma nihuishe juu ya itikadi hii sahihi na nifeshe juu ya itikadi hii na nifufue juu ya itikadi hii. Amin!

Hata hivyo, sitaki kuwa mwizi wa fadhila na kuwa mwenye kuisahau ihsani, Sheikh Kasim Mafuta kaniweka sawa katika baadhi ya sehemu kuhusu suala la kuyaandika majina ya wapokezi kimakosa. Yako baadhi ya majina ambayo niliyaandika sivyo. Ali nilimwita Alei n.k. Sababu kubwa ni kuwa katika kitabu changu hicho – Hoja Zenye Nguvu – mbali na kuwa kilikuwa ni kitabu changu cha mwanzo67 ambacho asili yake ni makala tu: si kitabu; mbali na hayo ni kuwa katika kitabu hicho nilikuwa nikifanya umuhimu zaidi juu ya suala la je mpokezi huyu ni dhaifu au ni sahihi: sikuwa nikitazama sana suala la vipi anatamkwa. Sitaki kusema kuwa hili ni jambo zuri, lakini nataka kusema kwamba wakati Sheikh Kasim Mafuta kachukua bidii kubwa ya kunikosoa juu ya hilo, nalo ni jambo jepesi ambalo halibadilishi hukumu ya Hadithi madamu mlengwa ni yule yule; yeye mwenyewe Sh. Kasim Mafuta kafanya makosa ya kielimu katika fani ya Hadithi, lugha ya Kiarabu, minhaj ya tafsiri na Usulil-Fiq-hi, nayo ni mambo ambayo kuyakosea kwake kunabadilisha hukumu ya Aya au Hadithi! Halkadhalika kafanya tadlis (ghushi) – kama kawaida ya watu wa skuli ya wanaoitwa Mawahabi – ambazo sijapata kuona muandishi yoyote akifanya ghushi za namna hio!

Pamoja na hayo utaona kwamba hata yeye Sheikh Kasim Mafuta naye kamwita Abu Is-haaq Al-Asfaraayiini kwa jina la Abu Is’haaq Al-Isfraayiiniy na sahihi ni Al-Asfaraayiini. Wala hakuna mazingatio kwa makosa yaliomo katika baadhi ya vitabu, kwani Abu Is-haaq huyu ni mtu wa mji uitwao Asfaraayiin si Isfaraayiin.68 Bali Kasim Mafuta kamwita 67 - Na ni katika jumla ya vitabu vyangu vitatu vya mwanzo. 68 - Tazama Yaqut Al-Rumi Mu’ujamu Al-Buldan j. 1, uk. 145-146. Na Al-Asfarayini ndivyo nilivyoliona katika Taarikh Ibn Ma’iin jalada la 2, j. 10, uk. 264, na ndivyo ilivyo katika kopi nilionayo ya kitabu Al-Muqaddima cha Ibn Al-Salah, uk. 25.

28

Page 29: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Imamu wake mwenyewe kwa jina la “Ibnul Qayyim al Jawziyya”69 na sahihi ima ni kumwita “Ibnul Qayyim” au “Ibnu Qayyimi Al-Jawziyya”. Hili linathibitisha kile kilichosemwa na Al-Imamu Ahmad kwamba hakuna mtu yoyote asiyekosea katika majina. Kwa hali yoyote ile, hilo kwangu halina umuhimu mkubwa sana.

Jengine ni kuwa Sheikh Kasim Mafuta pamoja na Sh. Al-Ghafiri wamelichukulia suala la kukosea kwa majina kuwa ni dalili tosha kwamba mtu si mtaalamu. Mimi kwa upande wangu ningependa kushauru fikra nyengine kwamba kukosea kwa jina au majina kunatokana na sababu mbili:

1) Mpekuzi hakurejea kuhakikisha jina linavyotamkwa.2) Jina linakuwa halidhibitiki kwa kutokuwa na mezani ya sarfu.

Na kwa hivyo, kulitamka jina sawa sawa si mara zote inakuwa ni dalili ya utaalam, kwani mwenye kuliandika au kulitamka jina sawa sawa huwa kafanya hivyo baada ya kurejea katika vitabu tu, pamoja na kuwa hayo yalioandikwa katika vitabu si mara zote yanakuwa ni mambo qat’iya (ya yakini).70 Pengine mtu huyo huyo ukimuuliza majina mengine kwa maelfu atashindwa kuwa na hakika. Na huu pia hauitwi utaalamu katika fani ya wapokezi wa riwaya.

Pia, kama tutavyothibitisha humu kwamba, wakuu wetu wamekosea mno katika maudhui hii ya kuyatamka majina ya namna hio (yasiodhibitika). Al-Bukhari – kwa mfano, naye ni Imamu wa dunia – katolewa makosa 74 na Al-Khatib juu ya kuyatamka majina, ingawa na Al-Khatib naye hakukubaliwa juu ya ukosowaji wake wa majina yote hayo, ikimaanisha kwamba na Al-Khatib naye pia kakosea juu ya hilo.71 Al-Dhahabi naye anamwita Al-Imamu Jabir bin Zaid Al-Azdi Al-Jaufi kuwa ni Al-Khaufi badala ya Al-Jaufi;72 nalo ni kosa kwani Jabir anatoka Oman katika sehemu inayoitwa Jauf ndipo aliponasibishwa napo; na wengine wanamnasibisha na Jauf ya Iraki ambako aliishi.73

Tukirudi katika kitabu cha Sh. Kasim Mafuta ni kuwa tatizo moja kuu na la wazi la kitabu cha Sheikh huyo kama kinavyojionesha chenyewe kitabu hicho, ni kuwa hakikuandikwa kwa moyo wa kutaka kuwafahamisha watu

69 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 42. 70 - Kama unavyoona kwamba baadhi ya vitabu vinamwita Al-Asfaraayiini kwa jina la Al-Isfraayiini; Al-Isfahaani vinamwita Al-Asfahaani na sahihi ni ya mwanzo. 71 - Tutatoa mifano tukifika sehemu yake. 72 - Tazama Al-Dhahabi Al-Siyar j. 5 uk. 398, tarjama na. 551. 73 - Salih bin Ahmad Al-Busaidi Riwaayatul Hadithi ‘Inda Al-Ibadhiyya uk. 183. Al-Qannubi Al-Imamu Al-Rabi’u Makanatuhu Wa Musnaduh uk. 23. Yaqut Al-Rumi Mu’ujamu Al-Buldan j. 3, uk. 94.

29

Page 30: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

dini yao, bali kimeandikwa kwa hamasa na chuki na ushabiki. Jambo hili kimekifanya kitabu chake kijae matusi na lugha mbaya sana ambazo mtu mwenye kutafuta dini yake kinamfanya aone kwamba hawezi kujipatia faida katika kitabu hicho. Sijui ni mtu gani anayejinasibu na Sunna za Mtume (s.a.w.) akajiita Ahlu Sunna halafu akaweza kuwatukana Waislamu bila ya kuwa na hoja sahihi, wakati Sunna inasema: “Kumtukana Muislamu ni ufasiki na kumpiga ni ukafiri”, sasa wewe ni Ahlu Sunna vipi, ilhali suna umeiweka pembeni na ukafuata matamanio yako ya nafsi?74

Ninachotaka kumwambia ndugu yangu Sheikh Kasim Mafuta ni kuwa Umma huu uko katika hali mbaya sana. Maadui wake wanauandama kila upande wala hawajui Ibadhi, Shia, Sunni wala Wahabi – wote hawa kwao ni sawa tu. Wakati tuko katika hali hii, basi utaona kwamba wanaojiita Al-Salafiyya au Ansaru Sunna yaani wanaoitwa Mawahabi ndio waliovaa njuga za kuusambaratisha Umma huu kwa kutumia lugha mbaya na hata kwa kuingiana mwilini na wale wasiokubaliana nao katika itikadi. Lugha kama “Kafiri, bidaa dhalala, mwongo, adui wa Allah, n.k” ni kitu cha kawaida tu katika mihadhara na maandishi ya wanaoitwa Mawahabi, kiasi cha kwamba hata wale wasiopenda mtafaruku inawabidi nao wajibu kwa lugha kali. Tukumbuke kwamba kuyajadili mambo ya dini yetu ni kitu kizuri sana na chenye faida, lakini ikiwa tutayajadili kwa uslubu huo uliokwenda nao wewe ndugu yetu, basi hatutofika popote: hakuna yoyote atayefaidika. Sisi kutukana pia tunajua tena kwa point, kwani kutukana si kazi na aibu kwenu ziko nyingi mno, lakini je ni nani anayetaka kusoma matusi: je tunamuandikia nani? Je baada ya kutukana kile tunachokiitakidi na ambacho tunawataka watu kiwafike kinakuwa tayari ndio kimewafika? Kwa hali hii, mimi katika kitabu hiki nitajaribu kujibu hoja na kueleza kwanini siafikiani na Sheikh Kasim Mafuta na madhehebu yake; na kuthibitisha kwanini nakubaliana na Ahlu Al-Haqqi Wa Al-Istiqaama (Ibadhi). Yaani ninakusudia kutoa risala ya kuwajuvya watu hoja za madhehebu ninayoifuata na kwanini nimeikubali. Cha kufahamu ni kuwa hoja zinapothibiti kwa dalili sahihi, basi zinakuwa si hoja za madhehebu tena, bali ni hoja za Uislamu juu ya watu wote – ni wajibu kuzifuata kwa kila mtu.

Leo ukirudi kuutazama ulimwengu mzima utakuta kwamba kila yalipoingia madhehebu hayo ya wanaoitwa Mawahabi basi kuna michafuko na

74 - Sikusudii Ahlu Sunna kama vile Mashafi. Hawa ni watu na ustaarabu wao, na elimu zao, na ucha Mungu wao na wanawaheshimu Waislamu wote. Nakusudia hawa wanaojiita kuwa wao ndio Ahlu Sunna yaani Mawahabi ambao wanawaita wengine kuwa ni watu wa bidaa. Tunasema ni suna gani ilioruhusu kumwita Muislamu mwongo bila ya ushahidi unaofaa Kisharia?! Utaona humu kwamba tuhuma zote za Bwana Mafuta kuwaita wanavyuoni wacha Mungu wa Kiibadhi kuwa ni waongo hazina msingi wowote.

30

Page 31: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kutokuelewana baina ya Waislamu, jambo ambalo zamani halikuwepo. Hata hivi karibuni nilisoma maelezo ya chini katika T.V fulani, nikaona Rais wa Chechnia anawataka Waislamu wote wakubaliane juu ya kuwapiga vita Mawahabi kwa kitendo chao cha kuwakafirisha Waislamu. Huko Somalia Mawahabi wameyafukua makaburi ya Waislamu eti kwa sababu watu wanakwenda kuomba! Sasa dhambi anaifanya huyu anayeomba; yule maiti kule kaburini ana kosa gani hata ukamfukue?

Mmoja wa wanafunzi wa Afrika Magharibi aliyepo hapa Oman anayeitwa Muhammad Munir maarufu (Baba), aliniambia kwamba kwao kulitokea fujo lililosababishwa na Mawahabi wakafa watu wasiopungua thamanini (80).75

Siku za karibu nilitembelewa na kijana wa Tanga mwenye asili ya Kihadharami (Yemen) naye anaishi Uingereza, naye ni Shafi. Aliniambia: “Sisi sasa tumeamua tutafute vitabu kutoka huku kwani vitabu vya Suudia vinatia chuki na kusababisha mifarakano”.76

Akielezea tabia hio ya Mawahabi ya kufanya fitna baina ya Waislamu, Al-Sayyid Al-Saqqaf anasema:

...Nao (Mawahabi) hutumia irhab (terrorism yaani kuwatia watu hofu) kwa njia mbili – ya kifikra na ya kimatendo…..kama vile kumfanyia uadui mtu awapingae kwa kumtukana na kumsema kwa ubaya au kumpiga na kufanya ugomvi Misikitini na kukata umeme katika Msikiti na katika klabu ambayo mwanachuoni au mlinganiaji anataka kuweka muhadhara77 au mkutano wa elimu ambao unapinga fikra yao na misingi yao. Na hayo wakati mwengine huendelea yakageuka kuwa vita vya silaha kama ilivyotokea Pakistan, Afghanistan na miji mengine kama Al-Yaman na Algeria..Na mifano ya hayo ni:1) Muqbil bin Hadi Al-Wadi’i katika Al-Yaman naye ni mmoja wa

walinganiaji wenye kupewa pesa katika sehemu ya Sa’ada huko Al-Yaman. Alikuwa yeye na wenzake wakibeba silaha na kueneza ufisadi huko Al-Yaman…

75 - Al-Hamdu Lillahi! Sasa Ahlu Al-Haqqi Wa Al-Istiqaama (Ibadhi) wamefika huko na watu wamewapokea kwa mikono miwili na wamezipenda tabia zao. 76 - Au meneno yenye maana hio. 77 - Mimi binafsi alinisimulia kijana mmoja wa Mombasa ambaye ni mtu katika ukoo wangu wa Mazrui naye ni Wahabi. Aliniambia kwamba siku moja alikuja Abdillahi Nassir akataka kuweka muhadhara basi sisi tukasimama Msikiti mzima ikawa tunafanya zogo na kuweka ghasia na kuruka huku na kule, alishindwa kusema kitu! Nikamwambia kwani nyinyi hamuna hoja za kumjibu?! Sasa si mungelimsikiliza tu halafu aliposema sivyo mukamjibu?! Hivi ndivyo watu wa batili walivyo!

31

Page 32: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

2) Harakati za Al-Salafiyya huko Algeria na tabu inayowakabili watu huko. Na kila mmoja anajua nini kinachofanyika huko Algeria na anasikia katika taarifa za habari mauaji na kuwachinja watu wasio na hatia.78 Na miongoni mwa hayo ni kuwa kikundi cha Al-Salafiyya cha jihad huko Algeria kilitafautiana na kikundi chenye kukafirisha…basi Al-Salafiyya wakawavamia na kuwaua watu wao.

3) Yale walioyafanya Al-Salafiyya huko Pakistan na Afghanistan, katika kuvipiga vita vikundi vyengine vya Kiislamu.79

Hayo ni machache katika mengi yaliojiri au yanayojiri katika ulimwengu wa Kiislamu tangu kudhihiri kwa madhehebu hio. Na kwa hivyo, Dr. Muhammad Na’iim, baada ya kutaja tabia za Mawahabi za kuwapachika Waislamu majina mabaya, alisema: “Hakika huu walionao hawa (Mawahabi) ukiwa unaonesha jambo lolote lile, basi unaonesha ujinga mkubwa”.80 Mwisho wa kunukuu. Hapa inakubidini musimame na kutafakari sana kuhusu mwenendo munaokwenda nao.

Naturudi katika kukijadili – kwa ufupi – kitabu cha Sh. Kasim Mafuta. Tunasema: ama kuhusu kitabu chenyewe cha Sheikh Kasim Mafuta, chambilecho Waarabu, fas-al wala haraj! Kitabu hicho ingawa mwenyewe kajikaza kwamba anajibu kielimu na kikarejewa na watu mbali mbali – wengine wakafika hadi kusema kwamba Al-Qannubi hajui Lugha ya Kiarabu wala Usuli! –; na yeye mwenyewe Sh. Kasim Mafuta akajikaza kuwa yeye ni mtu wa elimu; lakini pamoja na hayo kitabu chake kina makosa mazito ya kifani – lugha ya Kiarabu, Usulul-Fiq-hi, Usulul-Hadithi, kujigonga na juu ya yote hayo kitabu chake hicho kimejaa tadlis (ghushi). Nakupa mifano inayofuata ya kila maudhui moja katika hizo na mengine utayakuta humu katika jawabu hii:

Mosi: Tadlis (Gushi). Hili lina mifano mingi mno. Nataja miwili:a) Alipokuwa akizungumzia Aya: ***إلى ناضرة ذئموي هوجو

ناظرة ربها “Nyuso siku hio zitangaa. Kwa Mola wake (tu zitakuwa ni) zenye kutazama”81 alikariri yale yale ambayo tumeshayajibu katika kitabu chetu Hoja Zenye Nguvu bila ya

78 - Sitaki kukubaliana na Al-Sayyid Al-Saqqafi 100% juu ya hili. Ni kweli kwamba Mawahabi wamekuwa na tabia ya kutumia nguvu nguvu, kuwakafirisha na kuwapiga Waislamu katika baadhi ya sehemu. Lakini suala la mauaji ya Algeria halikuwa likitokana na wao mara zote bali hata mara nyingi. Ulikuwa ni mchezo wa kisiasa ili kutaka kuipaka matope harakati yao. Kwa hivyo, kwa ujumla ni kuwa kweli nguvu nguvu ndio tabia ya watu hawa, lakini tusiwapachike makosa ya watu. 79 - Al-Saqqaf Al-Salafiyya Al-Wahabiyya uk. 116-117. 80 - Dr. Muhammad Na’iim Al-Qaanun uk. 415. 81 - Al-Qiyama 22- 23.

32

Page 33: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kutoa jawabu juu ya yale nilioyasema. Kisha akataja kanuni dhaifu inayosema kwamba neno nadharu likifuatana na herufi ilaa basi kiasili linakuwa na maana ya kuona. Kisha akadai kwamba wenye kuitakidi kumuona Allah na wenye kupinga kuonekena kwa Allah wamekubaliana juu ya hilo, kisha akatoa ushahidi kwa maneno yangu. Katika kufanya hivyo, alinukuu kipande kidogo na akayawacha maelezo yote ambayo niliyaeleza kuipinga kanuni hio dhaifu! Na zaidi ya hayo, ni kuwa mimi sikusema kwamba neno nadharu likifuatana na herufi ilaa basi kiasili linakuwa na maana ya kuona, hata akadai kwamba sisi tumekubaliana juu ya hilo, bali nimesema kwamba neno hilo maana yake ya asili ni kuona yaani bila kuzingatia kufuatana na herufi ilaa au kutokufuatana na herufi hio. Na bila shaka hii ni ghushi ya wazi ya mtu ajiitaye Ahlu Sunna!

b) Anapozungumzia mpokezi ambaye anataka watu wamuone kuwa ni mpokezi sahihi, basi hanukuu maneno yote yaliosemwa na Wanavyuoni wa wapokezi: yale maneno yenye kumjeruhi mpokezi yeye huyawacha.82 Kwa mfano, alipokuwa akimzungumzia Hammad bin Salama – naye ni mpokezi dhaifu kama tutavyokuthibitishia kwa urefu – basi kaishia kunukuu kutoka kwa Al-Imamu Ahmad na wengine maneno kama: “Hammad ni Thiqa (mwenye kuaminika)”. Kisha akawa anayafasiri maneno hayo na yalio mfano wa hayo: “Ni mwenye kuaminika, mwenye hifadhi nzuri..”. Ilhali mpokezi anaweza kuitwa thiqa (mwenye kuaminika) na Hadithi zake ikawa si hoja kwa sababu ya kuwepo ‘ilal (kasoro) kama vile ghushi, awhaam (kusahau sana) n.k. Na ukiyarejea maneno ya Al-Imamu Ahmad na wengine utaona kwa uwazi kwamba Hadithi za Hammad alizopwekeka nazo, si hoja, basi vipi akiwa atakwenda kinyume na waliowengi zaidi kama ilivyo katika riwaya hio ya Hammad? Tutabainisha hilo kwa urefu na upana tukifika katika sehemu yake in shaa Allah.

Pili: Ubovu wa lugha ya Kiarabu: Sheikh Mafuta pamoja na kuwa anaonekana kuwa ni mtu mwenye kujigamba na kitabu chake kikarejewa na watu wenye kujigamba, lakini yeye na wenzake wanaonekana kwamba kanuni nyepesi za kinahau na kibalagha hawazijui: wanasukuma tu! Tazama ukweli kwamba katika kitabu

82 - Na kuyanukuu maelezo yenye kumjeruhi mpokezi ni muhimu zaidi kwani kujeruhi kunatangulizwa hususan ikiwa kujeruhi huko kumefafanuliwa.

33

Page 34: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

changu Hoja Zenye Nguvu nilizungumzia kanuni ya83. الحصر Na hii ni pale nilipokuwa nikizungumzia tafsiri sahihi ya Aya ya Qur-ani yenye kusema: ناظرة ربها ***إلى ناضرة ذئموي هوجو “Nyuso siku hio zitangaa. Kwa Mola wake (tu zitakuwa ni) zenye kutazama.”84 Nikaeleza kwamba kwa mujibu wa kanuni za lugha ya Kiarabu basi ikiwa tutaifasiri Aya hio kwa maana ya kuona basi itakuwa si sahihi kwani Aya itamaanisha kwamba watu hawamuoni isipokuwa Allah ilhali maandiko na akili zinathibitisha kwamba watu wataonana na pia watakuwa wanaona mambo mengine. Haya – kwa ufupi – ndio nilioyasema na kwa urefu nitaeleza nikifika katika kuielezea Aya hio tena. Lakini Sheikh Mafuta katika kutaka kuipindua hoja hio sahihi, akanijibu kwa kutoa mifano aliochanganya changanya na kuvuruga vuruga lugha ya Kiarabu – hata lugha ya Kiarabu maskini imempita halafu anakimbilia kujibu tu! Tazama mifano aliotoa. Katoa mfano wa Aya: الهدى على العمى فاستحبوا فهديناهم ثمود ا Na ama) وأمThamudi tuliwaongoza, wakapenda upofu kuliko uwongofu).85 Na Aya iliomo katika Surat Al-Dhuha isemayo: تقهر فال اليتيم ا فأم(Basi Yatima usimwonee).86 Na Aya ilio katika Surat Al-Nahl isemayo:

خلقها Na wanyama kawaumba”.87 Katika Aya hizi“ واألنعامwatendwa (Thamud, Yatima na Wanyama) wametangulizwa. Kwa hivyo, Sheikh Mafuta anauliza je hii ina maana kwamba ni Thamud peke yao ndio waliopewa muongozo; na je ni yatima peke yake ndiye tuliyekatazwa kumdhulumu; na je ni wanyama peke yao ndio walioumbwa na Allah? Na bila shaka – ikiwa sisi kwa kuidhoofisha kwetu Hadithi yenye sanad dhaifu na matn munkar – tumekuwa ni wajinga au wenye nia mbaya kama anavyosema Sheikh Kasim Mafuta katika kitabu chake, sijui yeye atajiweka wapi kwa kutoa kwake mifano ya Aya hizo kama ni hoja yake ya kilugha ya على المعمول تقديم Kumtanguliza mtendwa badala ya mtenda”. Ninachotaka“ العاملkumwambia ndugu yetu Sheikh Kasim Mafuta ni kuwa Aya hizi hazihusiani kabisa na mlango wa العامل على المعمول تقديم“Kumtanguliza mtendwa badala ya mtenda” unaozungumzwa katika balagha ya Kiarabu. Hapa katika Aya hizo kumtanguliza mtendwa ni wajibu kama nitavyobainisha nikifika katika sehemu ya kuielezea Aya

83 - Al-Hasr الحصر ni kutumia lugha ambayo inaonesha kuwa kitu fulani au vitu fulani vimefungamanishwa na kitu kimoja tu au na baadhi ya vitu tu ikawa havitoki kwenda kwengine. Kwa mfano “Hakuna ajuaye wakati wa Kiama isipokuwa Allah”. Yaani wote waliobakia hawaujui. Au “Mimi sili isipokuwa mchana”. 84 - Al-Qiyama 22- 23. 85 - Surat Fussilat (41) aya ya 17. 86 - Suratul-Dhuhaa (93) aya ya 9. 87 - Suratu-Nahl (16) aya 5.

34

Page 35: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

hio ya Surat Al-Qiyama; hapa ninataka kukuonesha jinsi huyu mtu alivyofanya haraka ya kutaka kujibu bila ya kuwa na ujuzi wa anayoyasema. “Kumtanguliza mtendwa badala ya mtenda” kunakozungumziwa na wanavyuoni wa balagha ni pale ambapo yote mawili yanajuzu – kumtanguliza mtenda au kumtanguliza mtendwa: sio sehemu ambayo ni lazima kumtanguliza mtendwa kama Aya alizotoa Sheikh Kasim Mafuta.88

Tatu: Kutokujua kuzifuata kanuni za elimu ya Hadithi: Hili lina mifano mingi kwa hapa natutosheke na mfano wa hayo alioyasema kuhusu Hammad bin Salama, na kutokutafautisha kwake baina ya mpokezi thiqa (mwenye kuaminika au reliable) na mpokezi ambaye Hadithi zake ni sahihi! Thiqa ni sharti moja tu katika masharti ya usahihi; si kwamba mpokezi akiitwa thiqa tayari anakuwa Hadithi zake ni sahihi. Hayo yameelezwa hata na Imamu wake Ibn Al-Qayyim kama tutavyomnukuu katika sehemu inayohusika.

Nne: Sheikh Kasim Mafuta sijui kama kasoma Usulil-Fiq-hi au kasoma mu’attila, bidaa, kufru n.k! Tazama wakati alipozungumzia mas-ala ya kuwepo kwa kauli mbili za wanavyuoni watangulizi juu ya mas-ala fulani, alisema kuwa haifai kuzua kauli ya tatu!89 Lau Sh. Mafuta alirejea vitabu vya usuli na vyengine – kama kitabu Maratibu Al-Ijma’i cha Ibn Hazm na Al-Naqdu na Bayanu Talbisi Al-Jahmiyya na Minhaju Al-Sunna vya Imamu wake Ibn Taymiyya – basi angeliona kwamba hili ni suala lenye khilafu baina ya wanavyuoni. Bali suala la wanavyuoni wanapotafautiana katika kauli mbili: je inafaa kuleta kauli ya tatu, ni suala lenye khilafu na kwa hivyo ijma’a yenyewe hapa imekosekana katika msingi wa jambo lenyewe.90

88 - Maelezo ya kilugha ya Aya mbili za mwanzo ni marefu, yatakuja in shaa Allah katika juzuu ya nne. Ama kuhusu Aya: خلقها elewa Sheikh Kasim mwana wa Mafuta , واألنعامkwamba utaratibu huu hapa ni lazima kwani lau mtendwa hapa aliwekwa mwisho ikasemwa: األنعام basi وخلقها hilo lingelipelekea kurejea kwa dhamiri kunako kitu kilichotajwa mwisho kimpangilio na kimatamshi na hilo halijuzu kilugha.

(( )) عود إلى ذلك ألدى األنعام وخلقها فقيل المفعول على الفاعل قدم لو! جائز غير وذلك ورتبة لفظا المتأخر إلى الضمير

Nitakuelezea zaidi in shaa Allah katika juzuu ya nne, nawe kutoa kwako hoja zako kwa Aya hizi ni ushahidi wa wazi kwamba una haraka ya mambo. Bora kwanza ungelitulia ukazisoma hizi fani. Halkadhalika waliokipitia kitabu chako na wakakipasisha wanaonekana pia bado si watu wa fani hii wala ile Wallahu Al-Musta’aan. 89 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 4-5. 90 - Tazama Dr. Al-Zuhaili Usulu Al-Fiq-hi j. 1, 471, اإلجماع ركن أو األول . الضابط

35

Page 36: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Hio ni mifano miwili mitatu na mengi mengineyo mutayaona humu katika jawabu hii. Ninachotaka kusema hapa ni kuwa mtu asistaajabishwe na kusukuma kwa Sh. Kasim Mafuta; hili la kusukuma ndivyo walivyo watu wote wa madhehebu hio; wao kwao lugha kama Umma umekubaliana au Al-Salaf wamekubaliana – katika jambo lenye khilafu – ni kitu mashuhuri. Halkadhalika jambo wasilolijua wao utawasikia wakisema hili halipo kabisa kama Ibn Taymiyya, Imamu wao, alivyosema kuhusu mas-ala ya majazi; na Muhammad Khalil Haraas alivyodai katika mas-ala ya Allah kuwa na mikono na mengineo mengi mno hayahesabiki. Kwa hivyo, musistaajabu kwa mtu kama Sh. Kasim Mafuta kusema hayo na wakati mwengine kutoa chalenj kwa kitu asichokijua ufafanuzi wake ukoje! Yote hayo nitakubainishieni tukifika katika sehemu zake in shaa Allah.

KUWACHA FURSA YA DHAHABU

Sheikh Kasim Mafuta alikuwa achukue fursa ya kitabu chake kwa kutueleza kwanini hakubaliani na Ibadhi ambao kawatukana kwa matusi mbali mbali kama vile kuwaita khawarij, na akatuhusisha wengine kwa kutuita waongo, wajinga na wenye nia mbaya! Lakini kwa bahati mbaya hakutueleza kwa ushahidi sahihi wala dhaifu nini maana ya ukhawarij ili tukaweza kujua nini ukhawarij wa Kiibadhi. Tungelifurahi sana lau Sh. Kasim Mafuta – naye ni mwanachuoni aliyezama katika fani mbali mbali – angetutolea taarifu (definition) ya ukhawarij ili tuweze kuona je wanaoitwa Mawahabi nao wanaingia katika taarifu (definition) hio ya ukhawarij au hawaingii; je nao ni Khawarij au si Khawarij. Unajua Sheikh Kasim Mafuta! Watu wengi wana hamu kubwa ya kuujua uhakika wa Uibadhi na uhakika wa Uwahabi, kwani hizi ni madhehebu ndogo zenye wafuasi wachache kana kwamba ni madhehebu mpya. Sasa utapotulia katika mada na ukakieleza kila kitu kitaalamu na kwa dalili sahihi zisizo na mashaka, basi utawafanya wasomaji wakuelewe vizuri, wala hutohitajia kutoa matusi au maneno ya kulengalenga. Unaweza kuwaonesha watu kwa ushahidi sahihi kuwa fulani ni mwongo bila ya kumwita mwongo, na kwa kufanya hivyo unakuwa umekamilisha ustaarabu wako na umekwenda na adabu za Qur-ani na Sunna.91 Lakini unapopandisha jazba na hamasa basi unakuwa umepoteza fursa kwani lazima utaingia katika makosa.

Na ajabu ya watu hawa! Wanapozirudi au kuzijadili itikadi za Makafiri – Wakiristo, Mayahudi n.k., - basi wanakuwa wanatumia lugha nzuri, nyepesi

91 - Lakini kwa sababu “Allah hapendi kujahirisha kauli ambaya isipokuwa kwa yule aliyedhulumiwa” na kwa kuwa “Atayejitetea basi huyo hakuna njia (ya kulaumiwa)” na “Malipo ya ubaya ni ubaya ulio sawa na ubaya”, basi na sisi tusilaumiwe ikiwa tutatumia lugha nzito. Pamoja na hayo, chochote kile tutachokisema kama ni uwongo wa Kasim Mafuta au wa Kiwahabi au jenginelo basi tutatoa ushahidi wa wazi usio na mashaka.

36

Page 37: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

na laini, na wanatoa hoja tu bila ya kumtukana au kumshambulia mtu. Lakini wanapojadiliana na Waislamu basi wanawatukana, kuwashambulia bali hata kuwapiga au kuwatemea mate! Kwa mfano ukisoma kitabu Talbisun Mardud kilichoandikwa na Sheikh Salih bin ‘Abdillah Al-Humaid, ambacho kakiandika kuwajibu wasiokuwa Waislamu kuhusu mambo ya usawa, uhuru, utumwa, mwanamke, kuifuata Sharia na jihad, utaona anatoa hoja. Ama wakijadiliana na madhehebu ya Kiislamu utaona kiama cha matusi kitavyosimama! Jambo hili hatuwezi kulifasiri isipokuwa ni kwamba katika uwanja huu wamefilisika kwa hoja, na kwa hivyo wamepigwa na

نفسية uqdatu nafsiyya (psychological complex) yaani‘ عقدةwamechanganyikiwa katika nafsi zao, na kwa hivyo wanaishia kutukana kwani itikadi yao wanaitaka na hawana hoja sahihi za kuitetea kwa hivyo wanaishia matusi! Wallahu Al-Musta’aan!

Ama mimi kwa upande wangu, nitajaribu nikujibu kila suala utaloniuliza au unalojiuliza na nitakujibu kila nukta ulioileta katika kitabu chako kizuri sana. Na kwa hivyo, katika juzuu ya pili ya kitabu hiki nitakujibu kwa ushahidi utakaoupoza moyo wako kwamba Ibadhi si Khawarij na kwamba walioitwa Mawahabi ndio Khawarij. Na wewe katika jawabu yako inayofuata, tafadhali chukua fursa hio kwa kuwaonesha watu nini maana ya ukhawarij na wapi umekaa ukhawarij wa Kiibadhi na vipi Mawahabi wametoka katika ukhawarij. Tukifanya hivyo, tutaweza kuendeleza mjadala wenye lengo, wenye elimu na utaoweza kuzaa matunda mazuri in shaa Allah. Ama kutupiana maneno ya sokoni, hilo si kazi, kwani mtu yoyote anaweza kulifanya hilo, hata ukimuokota muhuni barabarani ukimwambia atoe matusi na tuhuma basi hilo halitomshinda: kitachomshinda ni kutoa hoja za kielimu zenye kukubalika kwa watu wenye ujuzi na akili.

Ama suala la uwongo uliounasibisha kwangu na kwa Mashekhe wawili, mimi nitakujibu kwa dalili kwamba hakuna hata moja la uwongo katika yaliosemwa na Sheikh Al-Mufassirin Badru Al-Din Al-Khalili, Imamu Al-Sunna wa Al-Usul wa Al-Furu’i Al-Hujja Al-Qannubi wala katika yale yaliosemwa na Al-Faqiir Juma Al-Mazrui. Lakini tatizo unalo wewe mwenyewe kwa sababu nia yako – kama ilivyo wazi katika kitabu chako – haikuwa kufanya insaf, bali ulikuwa unatafuta shubha ili upate kutoa dukuduku lako! Na hii si tabia ya wasomi wacha Mungu, wala si tabia ya mwenye kudai kuwa yeye anafuata Sunna. Lakini hayo yote si ajabu, kwani Sheikh Kasim wewe unaonekana kwamba hukukusudia kutafuta ukweli kamwe bali ulikusudia kuitetea itikadi yako vyovyote vile iwavyo. Na kwa sababu hio, umeweza kuyakanusha hata mambo yaliowazi kabisa, ambayo kuyajua kwake hakuhitaji kujua hata kitabu kimoja. Tazama mambo mawili tu halafu irejee nafsi yako tena na tena:

37

Page 38: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

1) Kukanusha kwako ukweli kwamba Sheikh Al-Khalili alimtaka Sh. Ibn Baz wafanye mjadala wa wazi na wamuelekee Allah kwa mubahala. Jambo hili hakuna mtu yoyote au msomi yoyote wa hapa Ghuba asiyelijua. Lau ilikuwa ni Hadithi basi ingelipewa hukumu ya mutawaatir. Nami sitaki kuamini kwamba Sheikh Kasim bin Mafuta halijui jambo hili; lakini labda anadhania kwamba watu hawana ushahidi wowote ule juu ya tukio hili isipokuwa kutegemea “Ushahidi wa wenyewe kwa wenyewe katika jambo lililojiri ndani ya chumba”, na kwa hivyo Kasim Mafuta akadhani kwamba kapata njia ya kuwadanganya watu. Nitakupa ushahidi wa kutosha utaoupoza moyo wako juu ya tukio hilo nikifika sehemu yake.92

2) Tulitoa ushahidi wa kutoonekana kwa Allah huko akhera kwa Hadithi isemayo: “Hakuna kitakachozuia baina ya watu na baina ya kumtazama Mola wao katika pepo ya Aden (ya kukaa milele) isipokuwa vazi la kibri (ukuu na utukufu) lililopo katika Dhati Yake.” Wewe ukanijibu kwa kusema:

Hadithi hii ni kama zilivyo dalili zao nyingine zilizotangulia, si hoja ya kukataa kuonekana Allah huko akhera kwa macho. Bali hadithi hii inazungumzia kwamba baina ya waja na Mola wao kuna pazia na kizuizi ambacho kinawazuia wao kumuona yeye hapa duniani.

Sasa ebu itazame hio Hadithi inavyosema kisha tazama jawabu yako ulionijibu. Hadithi inasema kwamba utukufu wa Allah ndio uliowazuia watu wa peponi wasimuone Allah katika pepo ya Aden; wewe unanijibu kwa kusema kwamba Hadithi hii inazungumzia kwamba baina ya waja na Mola wao kuna pazia na kizuizi ambacho kinawazuia wao kumuona yeye hapa duniani. Sasa hio pepo ya Aden iko wapi: iko hapa duniani na nani hao walioingia katika pepo hio hapa duniani? Huoni Sheikh Kasim kwamba unayapotoa maandiko wazi wazi na kwa kukusudia?

Jambo jengine ambalo Sheikh Kasim Mafuta alitarajiwa alifanye katika kitabu chake ni kuwa atueleze kwa nini anakubaliana na wanaoitwa Mawahabi ambao kawaita Ahlu Sunna wa Al-Jama’a. Yaani watu wanahitaji kujua vipi wanaoitwa Mawahabi wamekuwa wao ndio Ahlu Sunna pasina madhehebu nyengine – ni kwa kitu gani hasa. Na haya yote yawe mbali na ile maudhui yake ya msingi ya kuonekana au kutoonekana kwa Allah. Lakini kwa bahati mbaya, Sheikh kaipoteza fursa hii na badala yake kalichafua jina lake kwa kuwatukana bila haki watu waliojulikana kwa

92 - Kumbukumbu yangu ni kuwa hata Marehemu Sh. Qasim bin Juma alilizungumzia suala hili wakati Sheikh Al-Khalili alipofanya ziara ya Tanzania miaka ya nyuma.

38

Page 39: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

sifa njema za elimu na ucha Mungu, jambo ambalo si kwamba litamtia katika jukumu huko akhera tu bali tayari limeshamchafulia jina lake hapa duniani. Lakini kwa kuwa Sh. Kasim Mafuta mwenyewe anajiona kuwa kafanya kazi nzuri ya kuwajibu watu wa bidaa na Makhawarij – kama mwenyewe anavyosema – basi tumuombee Allah amlipe yale anayostahiki hapa duniani kabla ya huko akhera, Amin!

Kwa kweli, mimi nilipoambiwa kwamba kitabu changu kimejibiwa nilifurahi nikitarajia kwamba nitapata kujifunza mengi ya kheri nisioyajua. Lakini baada ya kukipekuwa kitabu hicho nikaona matusi na maneno makali matupu. Amesahau Sheikh huyu kwamba Ahlu Sunna wa kweli huwa wanajadili mambo kama Qur-ani na Sunna zilivyoamrisha: haendi kinyume na andiko. Hio ndio Sunna ya kweli: Ahlu Sunna ni tabia na matendo: sio jina.

Ama mimi, mbali na kutumia fursa hii kwa kuzijibu hoja za Bwana Kasim Mafuta; pia nitachukua fursa hii kwa kuonesha kwanini sisi hatukubaliani na wanaoitwa Mawahabi na kwa nini tunaona kwamba wale walioitwa Ibadhi ndio Ahlu Sunna wa kweli: si wa jina. Na lau sisi hatuna ushahidi wowote juu ya hilo isipokuwa hizi tabia zenu za kutukana watu basi ingelitosha kubainisha kwamba nyinyi muko mbali mno na Sunna. Na lau hatukuwa na ushahidi juu ya kuwa Ibadhi ndio Ahlu Sunna wa kweli isipokuwa tabia zao tu zilivyo, basi hilo lingelitosha kubainisha ukweli huo.

Kwa hali yoyote ile, napenda kuchukua fursa hii kukukaribisha ewe Sheikh Kasim bin Mafuta katika uwanja huu wa mijadala hii ya kiitikadi, karibu sana katika maidatul ‘ilm (meza ya elimu): si katika taawilatul sibaab (si katika meza ya matusi). Kama vile ambavyo, tunakualika katika mjadala wa wazi juu ya maudhui hii ya kuonekana kwa Allah na nyengine ambazo zimekupa mashaka sana juu ya Ibadhi. Kama vile tunavyokukaribisha katika mubahala wa wazi ili tumuache Mjuzi wa yote ahukumu baina yetu na nyinyi kwa haki, karibu sana na tunasubiri kusikia kutoka kwako.

Nitakigawa kitabu hiki katika juzuu nne. Katika juzuu hii ya kwanza nitatoa jawabu juu ya shubuhati tafauti zilizoletwa na Sheikh Kasim Mafuta na wenzake. Pia nitaonesha kwanini sisi hatukubaliani na Mawahabi wanaojiita Ahlu Sunna, ilhali Sunna iko mbali mno na wao. Na hili nitalifanya kwa kuzinukuu itikadi zao za tashbihi (kumshabihisha Allah na viumbe) ambazo kwazo wametoka nje ya makubaliano ya Umma huu. Pia tutabainisha tabia zao na za Maimamu wao zilizo nje ya mafunzo ya Uislamu. Na kwa ufupi ni kuwa sisi hatukubaliani na Mawahabi si kwamba tunawachukia, bali ni kwa sababu zifuatazo:

39

Page 40: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

1) Kumshabihisha kwao Allah na viumbe wake. Na hii ndio sababu kubwa kuliko zote.

2) Tabia za kutukana watu, kinyume na Uislamu unavyofundisha.3) Kuwakafirisha Waislamu.4) Tabia za Maimamu wao za kutunga Hadithi za uwongo katika zama

za riwaya; na kuzikubali Hadithi hizo katika zama za baadae.5) Kushikana kwao na Hadithi Ahadi katika kuthibitisha itikadi.6) Kukanusha kwao majazi. 7) Msisitizo wa Sh. Kasim Mafuta na waliompongeza kuhusu suala la

ukhawarij wa Kiibadhi.8) Suala la kuwaita wafuasi wa madhehebu nyengine kuwa ni watu wa

bidaa. Sisi tunasema kwamba Mawahabi ndio watu wa bidaa, na kwamba wao hata hio bidaa ni nini hawajui: wanapiga kelele tu. Tutalijadili suala hili kwa urefu inshaa Allah.

Ama masuala mengine tuliotafautina na Mawahabi pamoja na Waislamu wengine ni:

1) Kuonekana au kutoonekana kwa Allah.2) Je mwenye kuikubali tauhidi akiingia motoni atatoka au atakaa

humo milele.3) Je Qur-ani ni kiumbe au si kiumbe.93

Katika kitabu hiki – katika juzuu zake tafauti – tutayazungumzia masuala yote hayo kwa kadiri tutavyojaaliwa na kubainisha hoja zetu na za wenzetu, isipokuwa suala la “Je Qur-ani ni kiumbe au si kiumbe” hili hatutolizungumzia humu kwani mahala pake ni katika utangulizi wa maelezo yetu juu ya tafsiri ya Mwanachuoni, Al-Qadhi, Al-‘Allaam Sheikh Abdullah Salih Al-Farisi. Wallahu Al-Musta’aan.

UTANABAHISHO

Hapa ningependa kutoa utanabahisho ule ule nilioutoa katika kitabu Jawabu Yetu nilichokiandika kuwajibu ndugu zetu wa Masjid Sunna. Nayo ni kwamba majibizano ya kidini, si kama ushabiki wa mpira au vyama vya siasa ya kidunia. Tunapojadili mambo ya kidini ya Allah huwa tunajadili kitu adhim kuliko yote yaliopo duniani. Wala si lengo kuwa mtu aambiwe kuwa yeye anajua au aambiwe kuwa kajibu. Bali hilo linaweza kumuangamiza mtu na kumuweka mahala pabaya sana wal’iyaadhu bi-Lahi! Bali hata hapa duniani, mtu mwenye tabia hio, basi elimu yake Allah

93 - Bila ya kusahau kwamba tafauti ya Ibadhi na Ahlu Sunna (Ashaa’ira) katika maudhui hii ni tafauti ya kilafdhi tu: si tafauti ya hakika.

40

Page 41: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

anaiondoshea baraka hata akiwa na elimu kubwa kiasi gani. Kwa hivyo, lengo ni kuifikisha haki kwa watu kwa kutarajia thawabu za Allah. Hii ni kusema kwamba taq-wa na ikhlas ni masharti ya lazima katika mijadala kama hii.

Kwa hivyo, ni wajibu wetu wa lazima – nasi tumo katika mijadala hii ya kiitikadi – kwamba itayembainikia kuwa hoja zake ni dhaifu basi asione tabu wala aibu kutangaza msimamo sahihi. Kufanya hivyo, sio kushindwa bali ni kushinda kwani – mwanzo na mwisho – huko ni kumridhia na kumridhisha Bwana wa ulimwengu ambaye mikononi mwake kuna rehema na thawabu kwa wenye ikhlas, kama vile ambavyo kufanya hivyo ni kuwafanya wajuzi wenye ikhlas wazidi kuwa na imani na wewe kwa kuiona ikhlas yako hata kama wajinga watakucheka.

Jambo la pili ninalotaka kulitolea utanabahisho ni kuwa mimi katika jawabu zangu zinazofuata huko mbele in shaa Allah nitakwenda kwa mujibu wa kanuni za mjadala – sitokariri kitu ambacho nimeshakijibu bila ya kupata jawabu sahihi kutoka upande wa pili. Ikitokea Sheikh Kasim kukariri kitu hicho kwa hicho, kama alivyofanya katika kitabu chake, bila ya kutoa jawabu, basi nikiandika jawabu nyengine nitataja nukta (points) zake tu alizozizungumzia kisha nitawataka watu warejee katika jawabu yangu iliotangulia ili walinganishe. Na kitachofuata ni kuyajadili yale yalio mapya tu. Nitafanya hivyo in shaa Allah mpaka nitakapoona kwamba hatuna jipya tena – ni yayo kwa yao – na hapo nitakuwa nimemaliza na tutawaachia watu walinganishe jawabu hizi.

Jambo la tatu ninalopenda kutoa utanabahisho ni kuwa kitabu hiki in shaa Allah kitakuwa katika juzuu nne. Na nimekusudia kukizungumzia kila kitu ambacho Sheikh Kasim Mafuta kakisema au kakigusia. Kwa hivyo, katika jawabu hii sikujilazimisha kumjibu kwa mujibu wa mpangilio wa kitabu chake. Bali unaweza ukalikuta jambo aliloliweka mwanzo yeye, ikawa mimi nimelizungunzia katika juzuu ya pili au ya tatu. Kwa mfano, kitabu chake kimeanza na maudhui: VIPI TUTAMFAHAMU MOLA WETU NA WAPI TUICHUKUE IMANI YA DINI YETU? Hapa alieleza mambo yenye nukta (points) saba kama inavyofuata:

1) Wao ( Sh. Kasim bin Mafuta na madhehebu yake) ndio Ahlu Sunna wal Jama’a.

2) Watu wengi hawajui vipi watamjua Mola wao: wanaomjua Mola wao ni Yeye Kasim Mafuta na watu wa madhehebu yake inayoitwa ya Kiwahabi! Na kwamba njia sahihi ya kumjua Allah ni kujua vile alivyojielezea Yeye mwenyewe katika kitabu chake (Qur’an tukufu)

41

Page 42: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

na vile alivyotuelezea mjumbe wake mtukufu katika mafundisho yake yaliyo sahihi.

3) Tuzingatie ufahamu wa Al-Salaf Al-Saalih (wema waliotangulia) kama vile; Maswahaba na Taabi’ina (wanafunzi wa Maswahaba) na maulamaa waliokuja baada yao.

4) Tufuate Masahaba.5) Katika suala la kuonekana kwa Allah Masahaba wamekubaliana

kwamba ataonekana.6) Jah’miyyah, Mu’tazila na wajukuu zao kama vile Shia, Ibadhi na

wengineo miongoni mwa watu wa bid’a 94 ndio wanaopinga kuonekana kwa Allah huko akhera.

7) Haifai kuzusha kauli ya tatu ikiwa kuna kauli mbili tafauti katika Al-Salaf.

Mimi nukta hizi nitazichawanya katika juzuu mbali mbali kwa mujibu wa maudhui ninayoizungumzia katika juzuu hio. Kwa hivyo, hapa katika juzuu hii, nitaanza kwa kuyajadili maneno ya Al-Akh Sheikh Seif Al-Ghafri alioyasema katika kutoa pongezi zake kwa Sheikh Kasim mwanangwa wa Mafuta.

Juma Al-Mazrui

94 - Huyu Kasim Mafuta anasukuma tu: hata anachokisema hakijui. Mjukuu bwana Kasim anakuja baada ya babu: babu anakuja mwanzo. Jahmiyya na Mu’utazila wamekuja kwa miaka baada ya Ibadhi na Shia. Ibadhi ndio madhehebu ya kwanza katika madhehebu zote zilizopo leo duniani, ikifuatiwa na Zaidia na Shia Imamiyya. Ama madhehebu ya kisiasa, basi Shia ndio madhehebu ya mwanzo kuliko zote. Inaonesha huyu Kasim Mafuta hata historia haijui, basi kake kanena na miye nanena!

42

Page 43: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

SURA YA KWANZAKUYAJADILI MANENO YA SHEIKH SEIF AL-GHAFRI

Katika kitabu cha Sheikh Qassim Mafuta, ndugu yetu Sheikh Seif Al-Ghafri ametoa pongezi zake juu ya kitabu hicho na kusema mambo mengi kuhusu Imamu Al-Sunna wal Usul wal Furu’i Sheikh Said bin Mabruk Al-Qannubi. Binafsi, naelewa vyema nini msimamo wa Sheikh Seif kwa Maibadhi na wasiokuwa Maibadhi miongoni mwa wale ambao si wafuasi wa skuli anayoifuata yeye, lakini sikudhania kwamba msimamo wake kwa madhehebu nyengine ungemuwezesha kufikia hadi kusema maneno alioyasema. Miongoni mwa maneno yasiopendeza – hasa hasa kwa mtu wa elimu kama yeye – ni haya yafuatayo:

Ama baada ya kukipitia kitabu cha ndugu yetu Abul fadhli Kassim Mafuta, kitabu chenye anuani ya kitabu HOJA ZENYE NGUVU katika kuthibitisha kuonekena Allah kwa macho huko akhera, majibu na maelezo, kitabu hiki nimekipitia chote kwa uwangalifu na insaafu, 95 ni kitabu madhubuti kinacholingana na jina lake kwani makusudio yake makubwa ni kutetea itikadi sahihi ya Manabii na Mitume wote,96 itikadi ya AHLI SUNNATI WAL-JAMAA dhidi ya waandishi wa uwongo, walio dhidi ya itikadi hii safi, kwani kitabu hiki kimebainisha waziwazi kwa hoja sahihi juu ya upotovu wa mtunzi wa kitabu kiitwacho HOJA ZENYE NGUVU JUU YA KUTOONEKANA MWENYEZI MUNGU KWA MACHO cha ndugu JUMA AL-MAZRUI ambae ni miongoni mwa wafuasi wa mapote ya matamanio kwani ndugu Juma ndani ya kitabu chake hicho amemsingizia uwongo Mwenyezi Mungu na Mtume wake97 kama kawaida ya watu wa matamanio kumsifu Allah sub’haanahu wata’alaa kwa

95 - Baada ya kuwa umekipitia chote na kwa uangalifu, sasa tazama makosa kwa kapu na magunia yaliomo katika kitabu hicho kama itakavyokubainikia katika juzuu tafauti hasa hasa juzuu ya nne ya jawabu yetu hii. 96 - Hili si ajabu kwao Sheikh Seif kulisema, kwani nyinyi lugha kama: “Umma umekubaliana juu ya kitu kadha”, ilhali ni makubaliano ya Ibn Taymiyya na Ibn Batta, ni kitu chepesi kwenu. Ni Nabii gani huyo aliyesema kuwa Mungu ataonekana hata ukadai kuwa kumuona Allah ni itikadi ya Mitume. 97 - Wewe uliyedai kuwa itikadi yako ni itikadi ya Mitume umemsingizia uwongo nani?

43

Page 44: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

sifa ambazo ametakasika nazo za kutoonekana, ilhali Mwenyezi Mungu Sub’haanahu wata’alaa amejisifu yeye mwenyewe nafsi yake kwa sifa ya kuonekana huko akhera na pia akasifiwa na Mtume wake Muhammad swalla llaahu alaihi wasallam kwa sifa hiyo hiyo ya kuonekana na hii ndio itikadi ya Maswahaba wa Mtume Muhammad swalla llaahu alaihi wasallam na ndio itikadi ya Taabiina na wema waliofuata baada yao itikadi ya Ahli-Sunnat Wal-Jamaa.

Ndugu Juma Al-Mazrui ameandika kitabu hicho ili atetee itikadi yake ya kikhawarij kama ilivyo kawaida ya watu wa matamanio kabla ya kusoma na kufahamu jambo, wao kwanza ni kutetea itikadi zao vyovyote iwavyo kama vile walivyoipokea toka kwa mababu zao, lakini kwa rehema za Mwenyezi Mungu sub’haanahu wata’alaa amejaalia katika umma huu kama anavyosema Mtume katika hadithi sahihi kwamba: HALITAACHA KUWEPO KUNDI KATIKA UMMA WANGU LENYE KUPIGANIA HAKI HAWATADHURIWA NA WASIOWASAIDIA NA WALA HATADHURIWA NA WANAOWAPINGA MPAKA KITAKAPO SIMAMA KIYAMA na watu hawa ni AHLISUNNAT WAL-JAMAA.98

Ama ndugu Juma Mazrui mimi namlaumu sana kwa kufanya haraka kuandika kitabu hicho bila ujuzi wa dini,99 lakini baada ya lawama namuomba Mwenyezi Mungu amuongoze ndugu Juma na ampe maarifa na amtoe katika hali ya itikadi potofu, kwani kubwa la Juma ni kumuamini sana Said Mabruk Al-Qanuubi100 bila kumuelewa elimu yake na uwadilifu wake kwani inaonyesha bwana Juma hamfahamu bwana huyu Qannubi na ndio maana akampachika majina makubwa ya kielimu ambayo hastahiki jinsi alivyo, kwani Said Qannubi si mwengine zaidi ya kuwa ni mwanakasumba wa kikhawariji si mkweli,101 angelikuwa ni mkweli asingelifikia hali ya kunukuu hoja hai za ndani ya vitabu vya wanakasumba na watu wa matamanio na yeye kuzifanya hoja za kuwarudi Ahli-Sunnat wal-Jamaa.

98 - Kundi lenyewe ni nani: wewe na Kasim Mafuta mwenye kumuabudu Mungu mwenye sura ya binaadamu?! 99 - Na mimi nakulaumu wewe kwa kusema maneno mabaya ambayo hapaswi mtu anayejiita Ahlu Sunna kuyatamka, licha kuyaandika katika kitabu. 100 - Unataka ni muamini nani: Ibn Taymiyya au Al-Albani?! Utaona mwenyewe hali zao humu, kisha utaniambia je watu kama wao wanastahiki kufuatwa, au kipofu kaona jogoo! 101 - Tazameni akili ya mtu huyu! Anasema Sheikh Al-Qannubi si mkweli. Nini ushahidi wake? Ushahidi wake ni kuwa “Angelikuwa ni mkweli asingelifikia hali ya kunukuu hoja hai za ndani ya vitabu vya wanakasumba na watu wa matamanio na yeye kuzifanya hoja za kuwarudi Ahli-Sunnat wal-Jamaa”. Sasa huu ndio unaoitwa uwongo? Ungelikuwa wongo lau alinukuu kitu ambacho hakipo. Lakini tusistaajabu na Huyu Seif Al-Ghafri kwani yeye – kwa habari tulioletewa – anafika kusema kuwa Ibadhi ni mbwa wa motoni! Tunamuomba Seif katika jawabu yao inayofuata atuthibitishie hili au alikanushe. Na hao Ahlu-Suuna unaowakusudia ni nani? Ni Ibn Taymiyya na Ibn Batta? Na hao watu wa kasumba na matamanio ni akina nani? Ni Al-Imamu Ibn Al-Jawzi, Ibn Hajar na walio mfano wa hao?

44

Page 45: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Ama marudio anayorudiwa ndugu Juma ndani ya kitabu hiki ni malipo yatokanayo na chumo la mikono yake iliyoandika maandiko ya Qannubi ambaye ni mwanakasumba wa kikhawariji aliyeiajiri mikono yake juu ya kunukuu maneno ya watu wa matamanio wenye chuki dhidi ya wanasunnah, na maimamu wa Ahli-Sunnat. Miongoni mwa watu anaowaiga Qannubi maandiko yao ni kama Alkauthari, na Abuu Ghudah na Jamal-din Af’ghani ambaye si Muaf’ghani bali ni Muirani, na Butwi na Al-Maliki katika watu wa hivi karibu na pia miongoni mwao hao ni pote la Muutazilah kwani wao ndio wanaopinga sana kuonekana kwa Mwenyezi Mungu sub’haanahu wata’alaa kwani pote hili elimu yao yote imejengeka juu ya misingi ya mijadala ambayo asili yake ni vipimo vilivyo juu ya kufananisha kisichopo kwa kilicho kuwepo na miongoni mwa maigizo ya Qannubi ni pote la Jahmiyyah, Baatiniyya, Mashia Imamiyyah ndio maana utayakuta maandishi yao yote juu ya kutoonekana Mwenyezi Mungu sub’haanahu wata’alaa wanayanukuu kwa mwana matamanio mkubwa adui wa Mwenyezi Mungu sub’haanahu wata’alaa Abdul Jabbar al-Muutazili kwenye kitabu chake almughni, hasa katika zile hoja za kiakili alizozitaja Alkhalili kama alivyomnukuu Juma Mazrui katika kitabu chake Al-Haqu Addamigh ukurasa 67, kwamba kuona kwa macho ni kuingia sura102 …., na kadhalika amefananisha kuonekana Mwenyezi Mungu sub’haanahu wata’alaa na kuonekana viumbe, ametakasika Mwenyezi Mungu na dhana zao.

Na vilevile Qannubi si mwenye elimu ya vitendea kazi (Qawaid) vya elimu za waislamu kama somo la hadithi na ala zake na usuli na misingi ya fiqhi na lugha ya waarabu, lakini ni shujaa asiye na uwoga wala aibu na ndio maana utakuta mara nyingi hutoa hukumu juu ya hadithi kutokana na ushujaa wake mfano;- anasema kwamba hadithi ambazo zimepokewa zenye kuifasiri aya ya 22 na ya 23 za surat Al-Qiyamah ni dhaifu na za uwongo, na Juma Al-Mazrui akamfuata kiongozi wake Qannubi na ilhali hadithi hizo zote zilizokuja kutafsiri aya hizo ni Mutawatir103 kwa mujibu wa majio yake na kwa mujibu wa ushuhuda wa wanazuoni wa somo la hadithi,104 pia Qannubi kutokana na kutoelewa somo hili utakuta anamtia ila (dosari) mpokezi wa hadithi pasi na kuielewa ila ile kwamba haiwi hadithi ya mpokezi yule ni dhaifu, mfano amemwita imamu Zuhri kwamba ni Mudalis105 ili aidhoofishe hadithi zake bila kubainisha ni tadlis ipi ili

102 - Nitakujibu yote hayo nikifika mahala pake in shaa Allah. 103 - Nakuchalenj unioneshe utawatir wa Hadithi hizo na sisi tuko tayari kuikubali haki popote itapokuja. 104 - Hao wanazuoni wao ni Ma’asumin? Wao wana itikadi gani hata kauli zao ziwe hoja dhidi ya wengine? 105 - Wapi Al-Qannubi kazidhoofisha Hadithi za Al-Zuhri kwa dai kwamba yeye ni mudallis. Naam! Al-Zuhri ni Mudallis na ni darraj (mwenye kuchomeka na kuzidisha katika Hadithi) na habari zake ni refu na alipingwa na zaidi ya Wanavyuoni mia wa zama zake. Na aliyesema kwamba yeye ni mudallis ni Al-Dhahabi katika Al-Mizan. Pamoja na

45

Page 46: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

muradi atetee matamanio yake. Haya nimeyataja machache, lakini makosa ya namna hii ni mengi juu ya Qannubi106 na mfano wa hayo, na yote haya yanatokana na kasumba za kimadhehebu zinazompelekea Qannubi na mfano wake kuandika mambo wasioyajua ili watetee madhehebu yao kwa hali na mali, mfano Juma Mazrui, nikisema kwamba hana ujuzi katika somo la hadithi sitakosea,107 lakini hebu tumsikilize yeye mwenyewe anavyojieleza katika kitabu chake “Hoja zenye nguvu” katika ukurasa wa 194 anamwita mpokezi wa hadithi kwa jina ambalo sio lake, mpokezi huyu jina lake ni Ibn Halbas yeye akamwita Abu Halbas,108 mfano mwingine katika kitabu chake hicho katika ukurasa wa 69 amemwita Al-Duuriy, Al-Dauri109 na haya ni mengi mno kwenye maandiko ya Juma na haya ni kwa kuwa haja wahi kukaa na watu wa elimu hizi,110 labda aliwahi kukaa na Qannubi111 kisha akamuiga porojo zake na ndio maana akasema Ibnu-Halbas ni majhulil-ayn bila ya kubainisha ni majhul wa vipi, lakini yeye katika uibadhi wake Imamu wake aitwae Abuu Ubaidah Muslim Ibni Abi Karimah yeye ndiye Majhuli tena ni Majhulil-Ayn, mtu huyu ni kigano, 112 lakini kwa kutojua kwao wanadhania yupo, sitaeleza mengi bali mengi yameshaelezwa ndani ya kitabu hiki na mwenye kutaka haya arudi kuangalia vitabu vya watu wa Sunnah kama kitabu Assunnah, Arrisalatu

hayo, si kwamba alikuwa hana uwezo, lakini ikiwa riwaya imebainika kwamba ni mbovu katika matn na hakuna mwenye ila katika sanad isipokuwa yeye basi bila shaka Hadithi hio itakuwa ni katika tadlis (ghushi) zake. 106 - Ninukulie makosa ya Al-Qannubi na jawabu yako nami niko tayari kukujibu. Na mimi humu nitakunukulia makosa ya Imamu wako Al-Albani nawe nipe jawabu yako. 107 - Umesema kweli, lakini wewe unaonekana uko mbali zaidi na kila fani ndio maana ukakipongeza kitabu cha Kasim Mafuta pamoja na utumbo mtupu aliouandika ambao hauna kima katika uwanja wa elimu. 108 - Mimi nilikufuateni nyinyi nikikuaminini kwamba ni wajuzi wa fani hii, kumbe munapoteza watu. Hivyo nilivyomwita ndivyo ilivyo katika kitabu chenu. Lakini Sheikh Seif ukifungua mlango huu, basi mutajiumiza sana, kwani Masheikh wenu hasa hasa Al-Albani ana makosa kama hayo kwa kapu na magunia. Kwa mfano, Hadithi isemayo: “Kwayo utapata ngamia mia saba wenye kuvishwa hatamu katika pepo”. Anasema Al-Albani kuhusu Hadithi hii: “Kaipokea Abu Nu’aim katika Al-Hilya j. 8, uk. 116, kutoka kwa Ibn Mas’uud”.? Hivyo ndivyo alivyosema Al-Albani wakati kilicho sahihi ni kuwa Hadithi hii imepokewa na KWA NJIA YA ABU MAS’UD SI IBN MAS’UD KAMA ALIVYODAI. Utaona maelezo zaidi juu ya hilo baadae. 109 - Al-Albani ana makosa kama haya kwa magunia. Bali hata wakuu wake wana makosa haya kwa wingi kama utavyoona humu. 110 - Wewe umekaa na mwanachuoni gani wa Hadithi? Huyo Muqbl Al-Waadi’i alikuwa ni mwanafunzi tu: hata daraja ya ‘ilmu hajafika. Ikiwa Sheikh wake Al-Albani alikuwa taabani, basi yeye alikuwaje. Tena Al-Albani hakuwa hata na maadili ya wanavyuoni kama walivyoshuhudia wanafunzi wake waliokuwa karibu naye kwa miaka kama tutavyonukuu humu maneno yao. 111 - Yaa leit nilikaa na Al-Qannubi ningekuwa mjuzi kama wewe! 112 - Nitakubainishia vya kutosha kwamba huu ni uwongo. Abu ‘Ubaida anajulikana na Ibn Ma’in kasema kuwa ni thiqa. Nitakupa maelezo ya kutosha nikifika sehemu yake, nayo ni katika juzuu ya pili ya kitabu hiki.

46

Page 47: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

alhamawiyyatu alkubraa, Al-Aqidatu Atwahawiyah, na Minhaju Assunnah na vinginevyo.113 Ama kitabu hiki cha ndugu yetu Abul-Fadhli ni kitabu kilichokusanya faida nyingi sana haswa katika somo azizi la hadithi na pia katika somo la lugha ya waarabu, faida ambazo hazipatikani katika vitabu vingi vilivyokwisha andikwa kwa lugha ya waswahili. Mwenyezi Mungu sub’haanahu wata’alaa amlipe ndugu yetu huyu kheri na amzidishie elimu na uongofu na kulingania dini ya Mwenyezi Mungu sub’hanahu wata’alaa kwa hekima na elimu, kwani Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kutakabali dua za watu wake na rehema na amani zimfikie Mtume wetu Muhammad swalla llaahu alaihi wasallam na Aali zake na Maswahaba zake.114

JAWABU KWA MAELEZO YA AL-GHAFRI

Hayo ndio maneno ya ndugu yetu Sheikh Seif Al-Ghafri. Sikudhania kuwa Seif anaweza kusema maneno ambayo yatayowajuilisha watu kuwa yeye ni mwenye kupinga kitu kwa chuki, kasumba na kwamba hana insaf. Nilidhania kwamba ta’asubi yake ni kama ile ya viongozi wake kule Suudia, kumbe hata wao kawazidi. Wenzake kule Suudia wanapomsikiliza Al-Imamu Al-Qannubi husema: “Huyu mtu ana elimu sana lakini itikadi yake ni batili”. Hawa wao unaweza kuwapa udhuru kwa kusema kuwa “Itikadi yake ni batili” kwani walivyofahamu wao ni kuwa kumshabihisha Allah na viumbe na kusema balkafa basi ndio itikadi sahihi; kwa hivyo, anayemtakasa Allah na sifa pungufu za kufanana na viumbe kwao ni mpotovu. Ama elimu ni jambo lililio wazi; kwa hivyo hata wao hawakulipinga. Lakini Sheikh Seif Al-Ghafri kwa kutokuwa kwake na uadilifu, basi anasema:

Na vilevile Qannubi si mwenye elimu ya vitendea kazi (Qawaid) vya elimu za waislamu kama somo la hadithi na ala zake na usuli na misingi ya fiqhi na lugha ya waarabu.

Jambo hili Sheikh Seif utakhitalifiana hata na hao Mawahabi wenzako wenye elimu kuliko wewe. Nami ninamwambia Sheikh Seif kwamba kama ni hivyo unavyodai wewe, basi elewa kwamba wakulaumiwa na kubeba jukumu siku ya Qiyama utakuwa ni wewe: si mimi wala si Al-Qannubi. Sababu ya kuyasema haya ni kuwa wewe unajua kwamba Al-Qannubi anapotosha watu au anasema bila ya elimu na wewe upo na una elimu ya kutosha ya vitendea kazi (Qawaid) vya elimu za waislamu kama somo la hadithi na ala zake na usuli na misingi ya fiqhi na lugha ya waarabu,

113 - Hivi ndio vitabu vya Sunna?!!! Vitabu hivi vimejaa matusi na uwongo wewe unaviita vitabu vya Sunna! Nitakubainishia baadhi ya yaliomo katika vitabu hivi nikifika mahala pake. 114 - Tazama maneno hayo katika Hoja Zenye Nguvu cha Kasim Mafuta uk. 9-12.

47

Page 48: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

naye katangaza kwa uwazi kwamba yuko tayari kujadiliana na nyinyi kwa uwazi, lakini wewe umenyamaza kimya tu na uwezo unao, unatuacha tunapotoshwa, sasa jukumu ni la nani? Tafadhali mualike Al-Qannubi au itika wito wake katika mjadala na sisi tutakusikilizeni. Al-Qannubi anasema:

ه دحتن نحنو ي نأ ةيوشحال ءالؤى ل وتأ ب نا اهيف ةح�����يحص ةايوراوأ اررقتساإلب حير��صت

ع ورهظتسيلو يسحال اءوتساإل ذ لا نيلقالثب ولو اءشي نمب كلىك عيمج أ ما ن ننا ىدح�����تاف ملل ةلحالن هذه اببرأ م هريغ وأ ةلأسمال هذه يناظرة نا

ةيادقتعاإل لائسمال

Na sisi tunawachalenj hawa Mahashwiya (Mawahabi) watuletee riwaya sahihi ambayo ndani yake kumesemwa kwa uwazi kuwa (Mwenyezi Mungu) anakaa kitako kweli kweli, na wamuombe msaada yoyote wanayetaka hata binaadamu wote na majini wote. Kama vile ambavyo tunawachalenj kufanya mjadala katika mas-ala haya au mas-ala mengine yoyote yale ya itikadi.115

Na anasema:

ف ��نملل ماكنوعد دقو نحانهو متيبأف ةرم نم رثكأ كلذ ياظرة نإف كلذ مكل رر������كن ءالوأاس لع متنك ال ملهف كلذل اددعتى ب مإلى لقنت نأ طرشناظرة م����لعيسو , ةيمالعاإل لائسوالبأ هنيح س دهأو نماألب قحأ نيقيرفال يا اليبى

Na tumekuiteni kwenye mjadala zaidi ya mara moja mukakataa, basi na hapa sisi tunakurudieni tena katika hilo: kama muko tayari kwa hilo na twende katika mjadala kwa masharti kwamba uchukuliwe na vyombo vya habari, basi hapo litajulikana lipi katika makundi mawili linastahiki amani na liloongoka.116

Na Al-Imamu Badru-Din Al-Khalili anasema:

ح اي����ضقال هذه يف فال���خال مسح الإ نوري ال نيذلل نلعوأ ىتاع هيف قفتت ، ةماأل ةدي���قاال فادهال يادهال يعوضومال اروحال نم فكنتسأ ال يننأب ال يذ،،ق���������حال الإ هب دشني

115 - Al-Qannubi Al-Saif Al-Had uk. 12. 116 - Al-Qannubi Al-Tufan Al-Jarif j. 3, sehemu ya 1 uk. 57.

48

Page 49: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

ت الإ يضفي وال ال لجإلى ث هانهرب روهظو ةقيقحي الإ يدؤي ال ما،األ ن���يب ةدومالو ةفلإلى

نيملسمال

Na ninawatangazia wale (wote) ambao hawaoni (kitu bora) isipokuwa kuziondoa tofauti katika mas-ala haya ili itikadi ya umma ikubaliane (iwe moja), kwamba mimi sikatai mjadala wa kielimu, wa utulivu na wenye lengo, ambao haitafutwi kwa mjadala huo isipokuwa haki, na wala haupelekei isipokuwa kwenye uwazi wa uhakika na kudhihiri hoja zake, kisha haupelekei isipokuwa kwenye mshikamano na mapenzi baina ya Waislamu.117

Sasa baada ya matangazo hayo, tunasubiri kusikia kutoka kwako ili usituache tukapotea, vyenginevyo jukumu liko shingoni kwako hususan kwa vile wewe ni mjuzi wa elimu ya Hadithi, Usulul-Fiq-hi na lugha ya Waarabu na mengineo.

Ama Maulamaa wako – Ibn Baz, Al-Albani, Al-Waadi’i na Ibn ‘Uthaimin – wao wameishi zaidi ya miaka kumi baada ya kutolewa kitabu Al-Haqqu Al-Damigh lakini wameshindwa kunyanyua vichwa vyao wakatoa jawabu ya kielimu. Ama Sheikh Al-Qannubi ambaye hana elimu ya Hadithi wala elimu nyengine ameukata ulimi wenu kwa kitabu Al-Tufan na hadi leo kimekushindeni kukijibu. Sasa sijui angelikuwa na elimu hali ingekuwaje: hana elimu anakuporomosheni! Kwa hivyo, tunasubiri kusikia kutoka kwako kuhusu chalenj aliotoa Al-Qannubi ili musituache akina sisi pangu pakavu tukapotea na Maulamaa mupo.

Anasema Sheikh Seif Al-Ghafri:

Mfano Juma Mazrui, nikisema kwamba hana ujuzi katika somo la hadithi sitakosea, lakini hebu tumsikilize yeye mwenyewe anavyojieleza katika kitabu chake “Hoja zenye nguvu” katika ukurasa wa 194 anamwita mpokezi wa hadithi kwa jina ambalo sio lake, mpokezi huyu jina lake ni Ibn Halbas yeye akamwita Abu Halbas.

Mfano mwingine katika kitabu chake hicho katika ukurasa wa 69 amemwita Al-Duuriy, Al-Dauri na haya ni mengi mno kwenye maandiko ya Juma na haya ni kwa kuwa haja wahi kukaa na watu wa elimu hizi, labda aliwahi kukaa na Qannubi kisha akamuiga ‘Ujyaan porojo zake na ndio maana akasema Ibnu-Halbas ni majhulil-ayn bila ya kubainisha ni majhul wa vipi, lakini yeye katika uibadhi wake Imamu wake aitwae Abuu Ubaidah Muslim Ibni Abi Karimah yeye ndiye Majhuli tena ni Majhulil-

117 - Al-Khalili Al-Haqu Al-Damigh uk. 229.

49

Page 50: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Ayn, mtu huyu ni kigano, lakini kwa kutojua kwao wanadhania yupo, sitaeleza mengi bali mengi yameshaelezwa ndani ya kitabu hiki na mwenye kutaka haya arudi kuangalia vitabu vya watu wa Sunnah kama kitabu Assunnah, Arrisalatu alhamawiyyatu alkubraa, Al-Aqidatu Atwahawiyah, na Minhaju Assunnah na vinginevyo.

Ninasema: Ama Abu Halbas, bila shaka ndilo jina lililoandikwa katika kopi nilioitumia ya Ibn Al-Qayyim. Naam! Inawezekana ikawa ni makosa ya chapa au makosa ya Ibn Al-Qayyim mwenyewe. Nasi hatuwezi kusema kuwa ni kosa la chapa hadi tuwe na ushahidi katika kopi kongwe: mimi sina ushahidi huo. Kwa hivyo, ujinga huu ima kauanza Imamu wenu aliyemwita Ibn Halbas kuwa ni Abu Halbas au wameuanza wafuasi wake kwa kubadilisha jina hilo. Kwa hali yoyote ile, cha msingi hapa ni hukumu ya Hadithi hio yenye sanad hio ya Ibn Halbas: je Hadithi hio inafaa kuwa hoja juu suala la kuonekana kwa Allah au si hoja. Mimi nadai kuwa Hadithi hio si hoja ikiwa mpokezi ni Abu Halbas au ni Ibn Halbas kama nitavyotoa maelezo nikifika katika sehemu hio.

Lakini suali la kuzingatia hapa ni kuwa ikiwa mutatoa hoja kama hizo hamuoni kwamba mutawabomoa Maimamu wenu ambao wameyafanya makosa kama hayo kwa kapu na magunia kama nitavyokuelezeni baadae? Kwa hapa natuonje mfano mmoja tu wa maneno ya Ibn Al-Qayyim na mfano mmoja wa maneno ya Al-Albani na mifano mingine itakuja baadae. Ama Ibn Al-Qayyim – pamoja na kuwa kafanya makosa mengi mno118 katika elimu ya Hadithi – kwa hapa natunukuu mfano mmoja unaofanana na huo uliomuuma Sheikh Seif Al-Ghafri. Anasema Ibn Al-Qayyim kuhusu Abu Sheikh Al-Hunaai:

ال شيخ شيخ به ي وأبو .…..حتج مجهول وهوNa Abu Sheikh ni Sheikh ambaye Hadithi zake si hoja…naye ni majhuul (hajulikani)!119

Hayo ni madai ya Ibn Al-Qayyum, lakini mwanafunzi wake, Sheikh Al-Albani akamrudi kwa kusema:

118 - Usidhanie kwamba nazidisha kwa kusema “mengi mno”, ukweli uko hivyo, na anayependa naasome vitabu vyake vilivyohakikiwa na wataalamu wa sasa. Kama vile Tuhfatu Al-Maudud kilichohakikiwa na Hasan ‘Abdil-Mannaan; na Ijtimaa’i Al-Juyush kilichofanyiwa Takhriij kwa kutegemea maelezo ya Al-Albani na vyengine vingi. Utaona huko jinsi gani Jua la Dini (Ibn Al-Qayyim) alivyokuwa na tabia ya kutoa hoja kwa Hadithi dhaifu na za kutunga. 119 - Ibn Al-Qayyim, Zaadu Al-Ma’aad j. 2, uk. 112.

50

Page 51: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

ابن وثقه وقد هذا، شيخ أبي غير مسلم؛ رجال ثقات رجاله إسناد وهذاوالعج حبان وابن لي، ��سعد

في الحافظ جزم ولذلك الثقات، من جمع عنه : وروى بأنه" " التقريب." ثقة"

الزاد ( في القيم ابن قول وفي) 1/264وأما السنن ، به،" مختصر يحتج ال!" مجهول فليس وهو

عنده من اجتهادا ذلك قال وإنما والتعديل؛ الجرح أئمة من سلف …….له

Na isnad hii wapokezi wake ni wenye kuaminika nao ni wapokezi wa Muslim isipokuwa huyu Abu Sheikh, naye Ibn Sa’ad, Ibn Hibbaan na Al-‘Ijli wamesema kuwa ni mwenye kuaminika, na kwa hivyo Al-Hafidh (Ibn Hajar) kasema kwa mkato kabisa katika Taqriib kwamba “Ni mwenye kuaminika”.

Ama maneno ya Ibn Al-Qayyim katika Al-Zaad j. 1, uk, 264,120 na katika Mukhtasaru Al-Sunan (aliposema kwamba Abu Sheikh) Hadithi zake hazifanywi kuwa ni hoja na yeye mwenyewe (Abu Sheikh) hajulikani, basi hakika yake katika hilo hana yoyote aliyemtangulia katika wanavyuoni wa wapokezi; bali yeye kalisema hilo kwa ijtihad yake tu……121

Kwa hivyo, baada ya hayo utaona kwamba tuliojieleza wenyewe katika uwanja huu tuko wengi; wengine ni ‘Awaam kama sisi, na wengine ni Maimamu Shumusu Al-Din kama Ibn Al-Qayyim, na pia tutaona jinsi nyinyi Maimamu wa Tanga mulivyojieleza katika sehemu mbali mbali za kitabu chenu. Basi ajabu iko wapi?

Ama Al-Albani, yeye anasema kuhusu njia moja ya Hadithi ya Al-Khawaarij, nayo ni njia ya Jaabir bin ‘Abdi-Lahi:

ي أنه إال ثقات، كلهم رجاله إسناد سق �������وهذا فيه أن لي ف�إن �بدو ط�ا،واسمه – المغ��يرة أب�ا

- وهو رفاعة بن معاذ يدرك لم الحمصي الخوالني الحجاج بن عبدالقدوسسنة مات فإنه تابعي

من) 212( سقطت واسطة بينهما يكون أن بد فال عنه، بالتحديث صرح وقدالطابع، أو الناسخ

تعالى الله بإذن به نحظى أن فعسى اآلن، شيء لي يتبين لم هو؟ فمن

Na sanad hii wapokezi wake wote ni thiqat (wenye kuaminika) isipokuwa inanibainikia kwamba kuna mpokezi (mmoja) kaanguka (hakutajwa), kwani Abu Al-Mughira – jina lake ni ‘Abdul-Quddus bin Al-Hajjaaj Al-

120 - Katika kopi niliotumia mimi, juzuu na ukurasa ni kama ilivyo katika maelezo hayo yaliotangulia. 121 - Al-Albani Sahihu Abi Daud j. 6, uk. 46.

51

Page 52: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Khawlani Al-Himsi – hakumuwahi Mu’adh bin Rifaa’a naye ni mfuasi wa Masahaba aliyekufa mwaka wa (212) naye (hapa) kasimulia kutoka kwake kwa uwazi (kasema kanihadithia), kwa hivyo hakuna budi kwamba baina ya watu wawili hao kuna mpokezi kaanguka (hakutajwa) ama kutokana na mwenye kunakili au mwenye kupiga chapa, basi ni nani huyo (mpokezi ambaye hakutajwa)? Hadi sasa hakuna kilichonibainikia. Labda Allah akipenda tukabahatika (kumjua baadae). 122

Hayo ni maneno ya Al-Albani, Imamu wa Kasim Mafuta, Seif Al-Ghafri na madhehebu yao ya Kiwahabi. Nayo ni maneno yaliokosolewa na Sheikh Nasir Al-Sabi’. Anasema Al-Sabi’i:

": كلهم إسناده رجال عن قوله أما نظر، فيه كله هذا األلباني وكالمرفاع" بن معاذ فإن ة�����ثقات

األنص رافع ابن : "�����وهو ص حجر ابن عنه قال وإن رقي الز دوق،������اريالرابعة قد������ف 123)من

معين ابن حبان ������ول 125واألزدي )124(ضعفه ابن سوى يوثقه وذكره 126مح أبي ول ����ابن م�����اتم

تعديال ر���يذك وال جرحا " )127(فيه ": يوهم. ثقات كلهم األلباني قول أن علىعن أب �����صحة ي ���عنة.������الزبي بالسماع نطقه إال منه يقبل ال مدلس أنه ومضى ر،

Na maneno haya ya Al-Albani yote ni ya kufikiriwa! Ama kusema kwake kwamba wapokezi wa sanad hio “wote ni wenye kuaminika”, kwa hakika Mu’aadh bin Rifaa’a naye ni Ibn Rafi’i Al-Ansaari Al-Zuraqi, pamoja na kuwa Ibn Hajar kasema kuhusu yeye kwamba “Ni mkweli katika tabaka ya nne”, lakini Ibn Ma’iin na Al-Azdi wamesema kuwa ni dhaifu. Na hakuna aliyesema kwamba ni mwenye kuaminika isipokuwa Ibn Hibbaan na Ibn Abi Hatim akamtaja bila ya kutaja kuwa ni dhaifu au ni mwenye kuaminika. Bali kauli ya Al-Albani (aliposema): ‘wote ni wenye kuaminika’, inawafanya watu wadhanie kuwa Hadithi (hio) mu’an’an128 ya Abu Zubair ni sahihi, na yametangulia maelezo kwamba yeye ni mudallis (mwenye kughushi), haikubaliki isipokia riwaya yake aliosema kwa uwazi kwamba kaisikia. Ama kile chenye kuhusiana na pengo lililopo baina ya Mu’adh na Abu Al-Mughira, kilichodhahiri zaidi ni kuwa jina Mu’adh bin

122 - Maelezo ya Al-Albani katika Al-Sunna cha Ibn Abi ‘Asim uk. 446. 123 - Ibn Hajar Al-Taqrib uk. 536, tarjama na. 6730. 124 - Ibn Ma’iin Al-Taarikh j. 4, uk. 230, tarjama na. 5134. 125 - Ibn Hajar Al-Tahdhib j. 10, uk. 173, tarjama na. 7044. 126 - Ibn Hibbaan Al-Thiqaat j. 5, uk. 421. 127 - Ibn Abi Hatim Al-Jarhu Wa Al-Ta’adil j. 8, uk. 247, tarjama na. 1119. 128 - Hadithu mu'an'an (معنعن) ni Hadithi ambayo msimulizi wake anatumia lafdhi: ((عن

فالن(( A'n Fulan (Kutoka kwa fulani), Hadithi kama hii ni dhaifu ikiwa itasimuliwa na mpokezi mudallis (mwenye kughushi). Abu Zubair ni mudallis (mwenye kughushi) na Hadithi yake iko hivyo, lakini Imamu wa Kiwahabi Al-Albani anafanya jaribio la kuisahihisha!

52

Page 53: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Rifaa’a ni kupotolewa kwa jina Mu’aan bin Rifaa’a, kwani Mu’aan bin Rifaa’a kapokea Hadithi kutoka kwa Abu Al-Zubair na kutoka kwake kapokea Abu Al-Mughira, na uwezekano wa kulipotosha jina uko karibu zaidi kuliko uwezekano wa kutokutajwa mpokezi.129

Ninasema: bali Al-Albani huyu ambaye hapa katafuta njia ya kuisahihisha au – kwa uchache – katawaqqaf130 kutokana Hadithi mu’an’an ya Abu Zubair, ndiye aliyeidhoofisha Hadithi mu’an’an ya Abu Zubair huyo huyo katika kitabu chake chengine! Anasema:

وهو: مسلم بن المغيرة غير مسلم رجال كلهم ثقات ورجاله قلتأبا لكن ثقة وهو القسملي

بصحته . لقلنا ذلك ولوال عنعنه وقد مدلس الزبير

Ninasema: wapokezi wake wote ni wenye kuaminika, ni wapokezi wa Muslim isipokuwa Al-Mughiira bin Muslim naye ni Al-Qasmali naye ni mwenye kuaminika lakini Abu Al-Zubair ni mwenye kughushi na Hadithi yake hapa ni mu’an’an, na lau si hivyo, basi tungelisema kwamba (Hadithi hii) ni sahihi!131

Tazama mtu huyu! Kule ‘an’ana ya Abu Al-Zubair hakuidhoofisha; huku ‘an’ana ya Abu Al-Zubair kaidhoofisha. Na juu ya yote hayo, kule hakujua kwamba kumetendeka tas-hif (upotoshaji wa jina), yeye akadhani kuwa kuna mpokezi mmoja kaanguka (hakutajwa).

Wala usidhanie kwamba hicho kwa Al-Albani ni kitu cha kutokezea, kallaa thumma kallaa! Makosa kama hayo yako kwake kwa mamia kama si kwa maelfu. Chukua mfano wa pili wa yale aliyoyanena katika Ir-waau Al-Ghalil kuhusu Hadithi isemayo: القرآن أبهمه ما Yale ambayo) أبهمواQur-ani hayakuyaweka wazi nanyi musiyaweke wazi). Anasema Al-Albani:

البيهقي ( وصله قد عن ) 160 / 7وهذا سعيد ثنا بكر بن الله عبد طريق منع ع ���قتادة كرمة �ن

عباس ابن أدري . : …..عن فال البخاري شرط على صحيح سند وهذا قلتابن ��������وج إشارة ه

تضعيفه . إلى كثير

129 - Nassir Al-Sabi’i Al-Khawaarij Wa Al-Haqiqatu Al-Ghaaiba uk. 233. 130 - Hakuidhoofisha wala hakuisahihisha. 131 - Al-Abani Al-Ir-waau j. 4, uk.382.

53

Page 54: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Na (Hadithi hii) Al-Bayhaqi132 kaisimulia kwa sanad yenye kushikana (hadi kwa mpokezi wa mwisho). Ninasema: ‘Sanad hii ni sahihi kwa mujibu wa masharti ya Al-Bukhari, sijui ni kwa kitu gani Ibn Kathir akaashiria kwamba ni dhaifu!133

Ninasema: Al-Albani hapa kasahau kwamba:1) Yeye mwenyewe kainukuu hapa sanad hii ambayo ndani yake kuna

‘an’ana ya Qatada, halafu anauliza: “Sijui ni kwa kitu gani Ibn Kathir akaashiria kwamba ni dhaifu”.

2) Yeye mwenyewe katika sehemu kadha wa kadha za vitabu vyake huidhoofisha sanad yenye ‘an’ana ya Qatada, lakini hapa haijui sababu ya Ibn Kathir kuidhoofisha sanad hio!

3) Kwa hivyo, ‘an’ana ya Qatada, katika vitabu vyengine ni dhaifu; ‘an’ana ya Qatada katika kitabu hiki au katika sehemu hii ya kitabu hiki ni sahihi!

Sasa, baada ya hayo, ukipenda kuthibitisha sehemu ambazo Al-Albani kazidhoofisha sanad kwa sababu ya ‘an’ana ya Qatada, tazama: Ir-waau Al-Ghalil hio hio.134 Tazama na kitabu Al-Thamaru Al-Mustataab135 ambapo anasema: قتادة عنعنة لوال أيضا مسلم شرط على صيحح سند وهذا“Na hii ni sanad sahihi kwa mujibu wa masharti ya Muslim vile vile lau si ‘an’ana ya Qatada”. Tazama na katika Tamamu Al-Minna ambapo anasema:

: له فإن منهم خطأ أو تساهل صححه من وتصحيح ضعيف الحديث قلتالح تمنع عليه �����علة كم

مدلس بالصحة فإنه قتادة عنعنة …..وهي

Ninasema: Hadithi hii ni dhaifu na wale walioisahihisha ni kulegeza kamba au kukosea, kwani ina kasoro inayoitoa katika usahihi nayo ni ‘an’ana ya Qatada, kwani yeye alikuwa ni mwenye kughushi….136

Anaendelea Al-Albani kwa kusema katika Al-Dha’iifa:

بالتدليس : رمي فإنه ، قتادة عنعنة من فالعلة منه سلم فإن ….قلت

132 - Ninasema: bali sanad ya Al-Bayhaqi pia ina dhaifu na wenye kughushi wengine mbali na Qatada. 133 - Al-Albani Ir-waau Al-Ghalil j. 6, uk. 285, Hadithi na. 1878. 134 - J. 7, uk. 237, Hadithi na. 2187. 135 - J. 1, uk. 99. 136 - J. 1, uk. 61.

54

Page 55: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Ninasema: (Sanad hii) ikiwa imesalimika na kasoro basi (elewa kwamba) kasoro iko katika ‘an’ana ya Qatada, kwani yeye katuhumiwa kufanya ghushi…137

Na katika Sahihu Abi Dawud baada ya kumjibu Ibn Al-Qayyim maneno hayo ambayo tumeyanukuu kabla, anasema: قتادة عنعنة العلة وإنما(Bali kasoro yake Hadithi hii ni ‘an’ana ya Qatada).138

Na mfano wa hayo, ni kile alichokinukuu Al-Imamu Al-Qannubi kutoka kwa Al-Albani katika kitabu chake Ir-waau Al-Ghalil139 kwamba Said bin Zaid Hadithi zake hazikushuka daraja ya kuwa ni Hasan (sahihi). Haya kayasema kwa Hadithi anayoitaka. Alipofika Hadithi asioitaka140 katika kitabu chake chengine Mukhtasaru Al-‘Uluuwi Said bin Zaid huyo huyo kawa dhaifu.

Sasa, baada ya hayo sijui hawa Mawahabi wanastaajabu nini kwa ‘Aammiy kukosea jina ilhali Maimamu wao wanakosea majina na hukumu za Hadithi! Bali, Sheikh Seif, utakumbuka kwamba Al-Bukhari katolewa makosa mengi kama hayo, nitakutajia baadae, kwa hapa natutazame mifano miwili katika yale yaliosemwa kwa ujumla kuhusu Al-Bukhari. Katika Tadhkiratu Al-Huffadh cha Al-Dhahabi kumekuja maelezo haya:

البخ أحفظ أيهما عقدة بن سألت حمدان بن عمرو أبو أو ����قال اري : عال محمد كان فقال ما�مسلم

: لمح يقع فقال مرارا عليه فأعدت عالما، أهل ����ومسلم في الغلط مدكت أخذ ألنه وذلك بهم���الشام

يظنهما باسمه آخر موضع في ويذكر بكنيته الرجل ذكر فربما فيها ونظر….اثنين

Kasema Abu ‘Amri bin Hamdaan: ‘Nimemuuliza Ibn ‘Uqda: ‘nani aliyehifadhi zaidi – Al-Bukhari au Muslim?’ Akasema: ‘Muhammad (Al-Bukhari) alikuwa mjuzi na Muslim alikuwa mjuzi’. Basi nikamrejeshea suali langu mara nyingi, akasema: ‘Muhammad (Al-Bukhari) hukosea katika (majina ya) watu wa Shaam, na hilo linatokana na ukweli kwamba yeye alichukua vitabu vyao na kuvitazama; basi wakati mwengine humtaja mtu kwa kun-ya141 yake, kisha akamtaja sehemu nyengine kwa jina lake akidhania kwamba hao ni watu wawili tafauti….142

137 - Al-Dha’iifa j. 5, uk. 475, Hadithi na. 2458. 138 - Al-Albani Sahihu Abi Daud j. 6, uk. 46. 139 - J. 5, uk. 338, maelezo ya Hadithi na. 1507. 140 - Nayo ni Hadithi ya kijakazi aliyesema “Allah yuko mbinguni” ambayo lafdhi ya pili inasema kuwa Mtume (s.a.w.) alimuuliza: “Yuko mbinguni?” Lafdhi hii kaikataa Al-Albani kwa hoja ya udhaifu wa Said bin Zaid ambaye kule kamsahihisha! 141 - Kama vile kusema: “Abu ‘Umar” (Baba Omari). 142 - Tazama Al-Dhahabi, Tadhkiratul huffaadh j. 2, tarjama ya Muslim na. 613.

55

Page 56: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Na Abu Zur’a naye kanukuliwa akisema:

يعن …. الرجال أسماء هذا إسماعيل بن محمد كتاب في ي����نظرتفقلت كثير خطأ فيه فإذا التاريخ

بخ له أهل من العراق من عليه يقدم من كل رجل أنه نظر ��������بلية ارياس رأى فإذا كتبهم ما���في

يضبطون ال وهم كتبه عنده وليس يعرفه خطأ .......ال كتابه في فيضعه

Nimekitazama kitabu cha Muhammad bin Isma’iil huyu (Al-Bukhari) Asmaau Al-Rijaal yaani Al-Taarikh basi kutahamaki humo muna makosa mengi. Nikamwambia (Abu Zur’a): ‘Janga ni kuwa yeye (Al-Bukhari) ni mtu ambaye kila anayemjia kutoka Iraki miongoni mwa watu wa Bukhari basi yeye huvisoma vitabu vyao, akiona jina ambalo halijui wala hana vitabu vyake (mtu mwenye jina hilo) nao (watu hao) majina yao hayakudhibitiwa (kwa kutiwa irabu)…….basi yeye (Al-Bukhari) huliweka kwenye kitabu chake kwa makosa.143

Kwa hivyo, tukirudi katika criticism (نقد) ya Sheikh Seif, tunamsubiri labda kesho atatwambia kwamba Al-Bukhari hakuwa na elimu ya Hadithi kwa sababu ya makosa yake katika majina ya wapokezi. Labda na kesho kutwa Sheikh Seif atatwambia Shu’uba hakuwa na elimu ya Hadithi kwani Khalid bin ‘Alqama kamwita Malik bin ‘Urfuta kama ilivyo katika kitabu cha Al-Hakim,144 na katika kitabu cha Ibn Al-Salah.145 Pia Hujru bin Qais Al-Madari yeye kamwita Ibn Mandali au Ibn Abi Mandali,146 au Al-Qindali kama ilivyo katika Al-Taarikh cha Ibn Ma’iin na Al-Taarikh Al-Kabir cha Al-Bukhari.147 Na riwaya kutoka kwa Abu Al-Thawrain, Shu’uba anasema “kutoka kwa Abu Al-Sawwaar”.148

Ama Ayyub (labda ni Ayyub Al-Sakhtiyani),149 yeye kamwita mpokezi huyo kwa jina la Hujru Al-Mandali. Kwa hivyo, Ayyub si mjuzi wa fani hii ya Hadithi.

143 - Ibn Hajar Tahdhibu Al-Tahdhib j. 9, uk. 47, tarjama na. 53. 144 - Al-Hakim Ma’arifatu ‘Ulumi Al-Hadith uk. 149. 145 - Ibn Al-Salah Al-Muqaddima uk. 176. Lakini katika baadhi ya chapa za Al-Muqaddima cha Ibn Al-Salah kuna kosa la chapa, ambapo imeandikwa “Malik bin ‘Arafa”. 146 - Al-Hakim Ma’arifatu ‘Ulumi Al-Hadith uk. 149. 147 - Ibn Ma’iin Taarikh Ibn Ma’iin j. 9, uk. 262, tarjama na. 4691. Al-Bukhari Al-Taarikh Al-Kabir j. 3, uk. 69, tarjama na. 3154. 148 - Ibn Ma’iin Taarikh Ibn Ma’iin j. 9, uk. 262, tarjama na. 4692. 149 - Wametafautiana kuhusu inavyotamkwa nasaba yake: je ni Al-Sakhtiyaani au Al-Sikhtiyaani au Al-Sukhtiyaani. Lakini Ibn Hajar anaona kwamba sahihi ni Al-Sakhtiyaani. Tazama Fat-hu Al-Bari j. 1, uk. 84, katika sherehe ya Hadithi na. 16, babu halaawatul iimaan.

56

Page 57: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Ama Qatada yeye – kwa mezani ya Sheikh Seif Al-Ghafiri – atakuwa kazidi ujinga kwani yeye kamwita mpokezi huyo kwa jina la Al-Hujur bin Hujr Al-Badri.150

Ama Abu Hanifa yeye Al-Rabi’u bin Sabra kamwita Sabra bin Al-Rabi’i.151 Kwa hivyo, kwa mezani ya Sheikh Seif Al-Ghafri, Abu Hanifa ni mjinga!

Anasema Al-Imamu Al-Shafi: “Malik kalibadilisha jina: kamwita ‘Umar bin ‘Uthman, naye ni ‘Amru bin ‘Uthman”.152 Kwa hivyo, Al-Imamu Malik kajieleza mwenyewe kwamba hana ujuzi wowote kwa mujibu wa mezani ya Sheikh Seif Al-Ghafri.

Halkadhalika wapokezi ambao walimwita Abdul-Aziz bin Qurair kwa jina la ‘Abdul-Malik bin Quraib ni wajinga.153

Wanavyuoni wa Hadithi wa Al-Ahwaaz wamemwita Bukair bin ‘Aamir kwa jina la Ukail.154 Kwa mezani ya Sheikh Seif Al-Ghafri hawa wote ni wajinga! Kwa hivyo, Sheikh Seif, hata wanavyuoni wakubwa wamefanya tas-hif nyingi hususan katika majina yasiodhibitika nayo ni majina yasio mushtaq au yenye muundo mmoja wa muandiko lakini ishtiqaqat tafauti au nasaba tafauti. Ndio maana mara nyingi utakuta wanavyuoni wakubwa husema – kuhusu majina ya namna hio – huyu ima “Jina lake litakuwa ni fulani au fulani”.155 Kwa mfano, Ma’amar bin Yahya bin Sam, anasema Ibn Hajar “Na pia huitwa Mu’ammar”. Na anasema Al-Bukhari kuhusu Zaid bin Buraid: “Zaid bin Buraid au bin Yazid”156 – hana hakika jinsi gani jina la baba yake linatamkwa. Kasema hivyo kwani majina hayo yakiandikwa kwa Kiarabu na ikawa hayakutiwa nukta basi yanasomeka sawa sawa, yote kwa Kiarabu yanaandikwa namna moja. Ama majina yenye ishtiqaq lau mtu atayasahhif (atayabadilisha), hicho ndicho kipimo cha kutokuwa na maarifa. Lau mtu atamwita ‘Aadil kwa jina la ‘Iidil, tutajua kwamba mas-ala mepesi ya sarfu yamemshinda. Lakini Dauri na Duuri, uwezekano wa kufanya tas-hif upo sana ikiwa mtu hajajua nasaba ya Al-Duuri kwa vile majina yote mawili ni yenye kunasibishwa na majina yalioko katika lugha ya Kiarabu

150 - Al-Hakim Ma’arifatu ‘Ulumi Al-Hadith uk. 150. 151 - Al-Hakim Ma’arifatu ‘Ulumi Al-Hadith uk. 150. 152 - Al-Hakim Ma’arifatu ‘Ulumi Al-Hadith uk. 150. 153 - Al-Hakim Ma’arifatu ‘Ulumi Al-Hadith uk. 150. 154 - Al-Hakim Ma’arifatu ‘Ulumi Al-Hadith uk. 151. 155 - Ibn Hajar Taqrib uk. 541, tarjama na. 6814. 156 - Al-Bukhari Al-Taarikh Al-Kabir j. 3, uk. 325, tarjama na. 4188.

57

Page 58: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

nayo ni Duur na Daur, na yote yanawezekana madamu hayakudhibitiwa kwa harakati (hayakutiwa irabu). Bali kwa mezani yako hio Sheikh Seif, tunakusubiri kesho atwambie kwamba Ibn Al-Salah na wenzake ni wajinga: hawajui elimu ya Hadithi, kwani kwa muda yeye – na wenzake – hawakujua kwamba katika jina la Ahmad bin ‘Ujyaan, jimu haina fat-ha na yee haina shadda (shede). Yeye alikuwa akimwita mtu huyo kwa jina la Ahmad bin ‘Ujayyaan. Anasema Ibn Al-Salah “Tulikuwa tukimjua kwa (jina lenye) shadda (shede) kama lilivyo jina la ‘Ulayyaan, kisha nikamkuta (jina lake limeandikwa) kwa maandiko ya Ibn Al-Furaat..(kamuandika kwa jina la) ‘Ujyaan”.157 Kwa hivyo, natarajia si mbali Ibn Al-Salah atakuwa mjinga katika mezani ya Sheikh Seif Al-Ghafri. Na Ibn Al-Salah huyu ndiye aliyesema: “Umaara na ‘Imaara – kwa kasr (kisra) – na hatuna jina ‘Imara lenye ‘ain yenye kisra isipokuwa Abu ‘Imaara naye ni katika Masahaba na wengine wanalitia dhamm (dhamme) na (majina ya) wengine wote waliobakia ni kwa dhamm (‘Umaara), Wa Allahu A’alam”. 158 Hivyo ndivyo alivyosema, lakini akajibiwa kwamba pia “Ammaara” wako wengi kike kwa kiume kama: ‘Ammara bint ‘Abdil-Wahhaab; ‘Ammara bint Naafi’i bin ‘Umar Al-Jumahi; ‘Ammaara bibi yake Abu Yuusuf. Na katika wanaume kuna watu kama: ‘Ammara Al-Balawi; ‘Ammara Al-Harbi na wengine wengi. Kwa hivyo, Ibn Al-Salah naye karibuni atakuwa si mtaalamu tena wa elimu ya Hadithi!

Pia wanavyuoni waliomwita Tadum bin Subaih kwa jina la Yadum159 ni wajinga katika Al-Mawazinu Al-Ghaafiriyya! Pia tunamsubiri Sheikh Seif Al-Ghafri kesho atwambie kwamba Sunaabih bin Al-A’asar sahaba, waliomwita Sunaabihiy ni wajinga. Anasema Ibn Al-Salah: “Waliomwita Sunabihiy wamekosea”.160 Na akanukuu Ibn Hajar maneno ya baadhi ya wanavyuoni wakisema kwamba hao ni watu wawili tafauti.161

Ama Al-Hakim, yeye anasema kuhusu Hadithi isemayo: “Hana sala yule asiye na udhu..” anasema “Hadithi hii isnad yake ni sahihi, Muslim ametoa hoja kwa (Hadithi za) Ya’aqub bin Abi Salama Al-Maajishun, na jina la Abi Salama ni Dinar”.162 Hivyo ndivyo alivyosema Al-Hakim, lakini wanavyuoni wakampinga katika kumwita Ya’aqub bin Abi Salama kuwa ni wa kabila la Al-Maajishun na wakasema kuwa kabila yake ni Al-Laithi si Al-Maajshun. Anasema Al-Dhahabi katika Al-Talkhis: “Sahihi ni Ya’aqub

157 - Tazama Ibn Al-Salah Al-Muqaddima uk. 200. 158 - Tazama Ibn Al-Salah Al-Muqaddima uk. 211, Aina ya 53. 159 - Tazama Ibn Al-Salah Al-Muqaddima uk. 200. 160 - Tazama Ibn Al-Salah Al-Muqaddima uk. 201. 161 - Ibn Hajar Al-Isaba j. 3, uk. 447-448, tarjama na. 4105.162 - Al-Hakim Al-Mustadrak j. 1, uk. 246, Hadithi na. 519.

58

Page 59: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

bin Salama Al-Laithi”. Anasema Ibn Hajar katika Talkhisu Al-Habir: “Al-Hakim kadai kwamba yeye ni Al-Maajishun,…..na sahihi ni kuwa yeye ni Al-Laithi”.163 Labda Sheikh Seif Al-Ghafri siku zijazo atatwambia kwamba Al-Hakim alikuwa ni mjinga: hana elimu ya Hadithi.

Na labda Ibn Ma’in, Imamu Al-Jarhi wa Al-Ta’adil, baada ya siku chache atakuwa hana maana tena katika ulimwengu wa elimu ya Hadithi, kwani Al-’Awwam bin Murajim kamwita Al-’Awwam bin Muzahim.164

Ama Ibn Jarir Al-Tabari, yeye kamwita ‘Utbat bin Al-Nnuddar kwa jina la ‘Utbat bin Al-Nnudhar.165 Ibn Jarir kapewa laqabu ya Imamul-Mufassirin, na katajwa kuwa ni miongoni mwa watu nadra katika zama zote kwa jinsi alivyokusanya fani tafauti za elimu. Labda sasa tukimueka katika Al-Mawazinu Al-Ghafiriyya, Ibn Jarir atakuwa ni miongoni mwa watu wasio na elimu tena!

Na labda baada ya siku chache zijazo, Al-Imamu Al-Bukhari atakuwa si Imamu tena wa Hadithi katika vipimo vya Sheikh Seif Al-Ghafri, kwani Al-Khatib Al-Baghdadi kamtoa makosa sabiini na nne mfululizo166 kuhusu wapokezi tafauti.167 Makosa hayo yako mengine kayafanya Al-Bukhari, lakini mengine bila shaka – kama Muhaqqiq wa kitabu alivyoonesha – ni makosa ya Al-Khatib, na wote – Al-Bukhari na Al-Khatib – ni Maimamu wakubwa mabingwa wa fani ya Hadithi. Lakini katika mezani ya Sheikh Seif, labda Maimamu hawa kesho watakuwa ni katika wajinga wasiojua kitu! Tazama, kwa mfano, Al-Bukhari kamtaja katika Taarikh yake Sumait bin ‘Ajlaan,168 kisha akamtaja katika kitabu hicho hicho, Shumait bin ‘Ajlaan,169 na akawafanya kuwa ni wapokezi wawili tafauti. Lakini Al-Khatib akamjibu kwamba huyo ni mpokezi mmoja na akasema:

Na amekosea (Al-Bukhari) katika sehemu mbili: 1) Moja ni katika kuzitafautisha kwake tarjama (biographies) mbili akidhania kuwa kila mmoja katika watu wawili aliowataja ni tafauti na mwenzake, na wala mambo hayako hivyo bali huyo ni mtu mmoja. 2) Pili ni kumtaja kwake

163 - Tazama maelezo ya chini yaliotiwa na Mustafa ‘Abdul-Qadir katika Al-Mustadrak cha Al-Hakim j. 1, uk. 246, Hadithi na. 519. 164 - Ibn Al-Salah Al-Muqaddima uk. 175. Al-Nawawi Taqribu Al-Nawawi na Sherehe yake Tadribu Al-Rawi cha Al-Suyuti uk. 473. 165 - Al-Nawawi Taqribu Al-Nawawi na Sherehe yake Tadribu Al-Rawi cha Al-Suyuti uk. 473. 166 - Mbali makosa alioyatoa katika sehemu nyengine tafauti. 167 - Tazama Al-Khatib Maudhihu Al-Awham j. 1, uk. 3-211. 168 - Al-Bukhari Al-Taarikh j. 4, uk. 175, tarjama na. 5396. 169 - Al-Bukhari Al-Taarikh j. 4, uk. 216, tarjama na. 5639.

59

Page 60: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kwanza katika mlango wa (herufi za) Sini (S), na hio ni tas-hif haina shaka ndani yake kwani yeye (jina lake ni) kwa Shin (Sh.).

Anaendelea Al-Khatib kwa kusema:

Kosa la thalathini na sita, kasema Al-Bukhari: “Shabbak bin Khulaid Al-Azdi kasikia (Hadithi) kutoka kwake Hudba bin Khalid….kisha akasema (Al-Bukhari): ‘Shibak bin ‘Aidh bin Al-Munakkhal Al-Azdi’…..Basi akakosea (Al-Bukhari) katika kuzifarikisha kwake tarjama (biographies) mbili hizo na akafanya tas-hif kwa jina la mwanzo na akabadilisha nasaba (kabila) zilizotajwa katika tarjama mbili hizo.170

Labda – Al-Bukhari na ukuu wake na uimamu wake – naye atawekwa katika nafasi ya waliojieleza wenyewe kwa vile kakosea katika wapokezi fulani fulani.171

Ama kuhusu makosa ya Al-Albani, chambilecho Waarabu fas-al wala haraj. Makosa yake ya namna tafauti ni mengi kupita kiasi. Na makosa ya Al-Albani ndio hasa ya kuzungumzwa kwani ni mengi kupita kiasi na ni makosa katika hukumu za Hadithi na sanad zake: si makosa ya tas-hif tu. Lakini hapa kwa kuanzia nakupa mfano mmoja unaofanana na huo ambao Sheikh Seif ulimuuma, na mmoja mwengine umetangulia katika maelezo ya Sheikh Nassir Al-Sabi’i aliomrudi Al-Albani, na myengine niliiongezea huko katika kuyatia kwangu sherehe maneno ya Al-Sabi’i, na mifano myengine itakuja in shaa Allah. Anasema (Al-Albani) katika Sahiha yake baada ya maelezo kuhusu Hadithi isemayo “Kila mwenye kufanya khiyana atakuwa na bendera siku ya kiama ambayo kwayo atajulikana iko makalioni kwake”, anasema Al-Abani baada ya maelezo:

Kaipokea Ahmad j. 2, uk. 49, katusimulia Ibrahim bin Wahb bin Al-Shahid….na Ibrahim huyu na baba yake sikuwajua, wala Al-Hafidh hakuwatarajimu172 katika Al-Ta’ajil.173

Hivyo ndivyo alivyosema (Al-Albani). Lakini akajibiwa na Al-Imamu Al-Qannubi kwamba:

170 - Al-Khatib Al-Maudhih j. 1, uk. 122, Al-Wahmu Al-Sadis Wa Thalathun. 171 - Lakini katika kopi nilionayo, sikuona majina Shabbak bin Khulaid Al-Azdi aliyemtaja Al-Bukhari kuwa kasikia (Hadithi) kutoka kwake Hudba bin Khalid; na Shabbak bin ‘Aidh bin Al-Munakkhal Al-Azdi’ alioyataja Al-Khatib. Bali nimeona Shabbak bin Khalid Al-Azdi kasikia (Hadithi) kutoka kwake Mu’awiya; na Shabbak bin ‘Aidh Al-Qaisi. Tazama Al-Bukhari Al-Taarikh Al-Kabir j. 4, uk. 220, tarjama na. 5663-5665. 172 - Hakuwaelezea. 173 -Al-Albani Al-Sahiha j. 4, uk. 261-262.

60

Page 61: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Isnad imekuwa musahhaf basi kashindwa kuijua, na usahihi wake ni Ibrahim bin Habib bin Shahid, nao ni wenye kuaminika katika wapokezi (waliotajwa katika) Tahdhibu Al-Kamal na vitabu vyake vilivyokifanyia mukhtasari. Na baba mtu ni katika wapokezi wa Al-Bukhari na Muslim.174

Kwa hivyo, si haba kwamba Imamu wa Kiwahabi naye ni mjinga kama ‘Ammiy wa Kiibadhi! Na lau Sheikh Seif alijiongoza kwa kauli ya Al-Imamu Ahmad aliposema: “Kwani ni nani aliyetakasika na kukosea na kufanya tas-hif”175 basi angelitazama zaidi yale yanayohusu hukumu za Hadithi, bali angelitazama makosa ya wazi na ya kielimu yaliofanywa na mtunzi wa kitabu hicho alichokipitia yeye hususan naye Sheikh Seif “Ni mwenye elimu ya vitendea kazi (Qawaid) vya elimu za waislamu kama somo la hadithi na ala zake na usuli na misingi ya fiqhi na lugha ya waarabu”!!!!!!!!!

Halkadhalika akadai Al-Albani katika Ir-waauGhalil yake, 20, kwamba Rauh bin Al-Faraj Abu Al-Zinba’i ni “Katika wapokezi wa Al-Bukhari”.176 Lakini akajibiwa na Al-Imamu Al-Qannubi:

Na wala hali haiko kama alivyodai yeye (Al-Albani), na ukipenda kuhakikisha hilo, tazama Al-Taqrib uk. 211,177 kasema (Ibn Hajar) baada ya kumtaja: “Tamyiz”,178 basi yeye si katika mpokezi wa wapokezi sita kamwe.179

Baada ya yote haya, elewa kwamba mimi sikusudii kukwambia kuwa mimi ni mjuzi wa elimu ya Hadithi wala wa elimu nyengine yoyote ile: laa! Si hivyo, ukweli ni kuwa mimi ni katika wanafunzi. Lakini kinachonistaajabisha ni:

1) Mezani uliotumia! Mezani hio itawabomoa wanavyuoni wengi wakubwa sana ambao sisi hatulioni hata vumbi lao. Na itayembomowa kuliko wote ulimwenguni ni Imamu wenu Al-Albani na kwa hivyo itakuboweni nyinyi kwani ikiwa hali ya Imamu wenu iko hivyo tutavyoielezea katika sehemu inyofuata, je nyinyi

174 - Al-Qannubi Al-Imamu Al-Rabi’u Makaanatuhu Wa Musnaduh uk. 96. 175 - Ibn Al-Salah Al-Muqaddima uk. 175. 176 - Al-Albani Ir-waau Al-Ghalil j. 5, uk. 31. 177 - Tarjama na. 1967. 178 - Yaani kataja hivi ili kutafautisha msimulizi wa wapokezi sita na yule ambaye si msimulizi wao ingawa wote wana majina sawa. 179 - Al-Qannubi Al-Imamu Al-Rabi’u Makaanatuhu Wa Musnaduh uk. 91.

61

Page 62: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

munayemfuata yeye hali zenu zikoje? Mimi sikuiteni wajinga, lakini mutachagua wenyewe pa kujiweka.

2) Hukutazama mambo ya msingi, nayo ni kwamba ikiwa Hadithi hio mpokezi wake ni Abu Halbas au ni Ibn Halbas: je inafaa kuwa hoja katika maudhui yetu? Hili ndilo muhimu zaidi la kujadiliwa.

3) Hukutazama kwamba mtu ambaye nyinyi kwenu munamzingatia kuwa ni Imamu na mwanachuoni mkubwa wa Hadithi kafanya makosa fahisha katika vitabu vyake, na badala yake unastaajabishwa na mtu ambaye katika madhehebu yake hazingatiwi hata kuwa ni mwanachuoni muqallid; sikwambii kuwa ni Imamu Mujtahid. Makosa hayo ya Imamu wenu yamo katika sanad na katika Hadithi zenyewe. Tena makosa hayo si mawili matatu ambayo hakuna binaadamu aliyesalimika nayo, bali makosa yake ni mengi mno kwa kapu na magunia!!!!!!

Ama kosa la Al-Duuri kumwita Al-Dauri bila shaka ni kosa lenye kusameheka madamu mtu aliyekusudiwa ni yule yule. Lakini sisi tulikuwa tunamtaraji Sheikh Seif Al-Ghafri – kwa uadilifu wake na ucha Mungu wake – atwambie kwamba Imamu wake Sheikh Al-Albani amejieleza mwenyewe kwa vile kawa jasiri wa kusahihisha na kudhoofisha bila ya elimu! Na juu ya yote Sheikh Seif kamridhia Al-Albani kuwa ni Imamu, jambo ambalo linajieleza kwamba Sheikh Seif Al-Ghafri ni mtu wa aina gani? Kwa hivyo, tulitarajia kwamba Sheikh Seif aseme Al-Albani ni mjinga wa fani hii kama vile alivyothubutu – kwa taasub na bila ya insaf – kumwita mtu aliyekubaliwa na ulimwengu juu ya ujuzi wake kuwa si mwenye ujuzi! Tunakusubiri ewe Sheikh Seif, kusikia maelezo kutoka kwako juu ya baadhi ya makosa yanayofuata na yaliotangulia ambayo yamefanywa na Al-Albani katika vitabu vyake.

Nakunukulia makosa hayo ya Imamu wenu pamoja na jawabu aliojibiwa na Al-Imamu Al-Qannubi. Labda nyinyi mutakuwa na jawabu kwani yeye Al-Albani mpaka kafa hakutoa jawabu.

MAKOSA YA AL-ALBANI IMAMU WA HADITHI WA KIWAHABI

Nimekuwa nikidokoadokoa huko nyuma kuhusu baadhi ya makosa yaliomo katika vitabu vya Al-Albani. Makosa hayo ni mengi mno kiasi cha kwamba wengine wamemtungia majalada ya vitabu. Sasa hapa kidogo natuihusishe sehemu hii kwa kuyatazama baadhi ya makosa yake ambayo kakosolewa na Imamu Sunna, Al-Qannubi.

1) Sulaiman bin Shurahbil

62

Page 63: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Al-Albani kawataja wapokezi kadha wa kadha kwamba ni Majhul (hawajulikani) au hakuwaona walipotajwa nao wamo wametajwa katika vitabu mashuhuri. Na akajibiwa na Sheikh Al-Qannubi kama ifuatavyo. Anasema Al-Albani: “Na Sulaiman bin Shurahbil…..sikukuta katika tabaka hii mwenye jina Sulaiman bin Shurahbil”.180 Anasema Al-Qannubi: “Hivyo ndivyo alivyosema, wakati Sulaiman huyu jina lake kamili ni Sulaiman bin Abdil-Rahman bin ‘Issa bin Maimun bin Bint Shurahbil, na hufupishwa (jina lake) wakati mwengine kama ulivyoona (Sulaiman bin Shurahbil). Naye kaelezewa (katika vitabu tafauti vya wapokezi, kama ilivyo hapo chini)”.181

2) ‘Abdul-A’ala bin ‘Abdillah bin Abi Far-wa

Anasema Al-Albani (kuhusu mpokezi huyu): “..Sikumuona aliyemuelezea”.182 Anasema Al-Qannubi: “Hivyo ndivyo alivyosema (Al-Albani) na hali haiko hivyo, kwani ‘Abdul-A’ala huyu kaelezewa katika vitabu vingi mno.183 Na Ibn Ma’in kasema: ‘Abdul-Hakim bin ‘Abdillah bin Abi Far-wa na Salih bin ‘Abdillah bin Abi Far-wa na Abdul-A’ala bin ‘Abdillah bin Abi Far-wa wote ni wenye kuaminika.’ Na mfano wa hayo kayasema Ya’aqub bin Abi Suf-yan, na akasema Al-Daraqutni: ‘Is-haq bin Abi Far-wa ni mwenye kuachwa; ana ndugu watatu ni wenye kuaminika”.

3) Said bin Ash-wa’i

180 - Al-Albani Al-Dhaifa j. 4, uk. 200. 181 - Kaelezewa katika Rijalu Al-Bukhari cha Al-Kalaabaadhi j. 1, uk. 314; Al-Taarikh Al-Kabir j. 4, uk. 24; Al-Jarhu Wa Al-Ta’adil cha Ibn Abi Hatim j. 4, uk. 29 na pia katika kitabu chake Al-’Ilal; Sualatu Al-Ajurri cha Abi Dawud; Al-Dhu’afaa cha Abu Zur’a Al-Dimashqi; Al-Ma’arifa cha Al-Fasawi; Tahdhibu Al-Kamal j. 8, uk. 79 chapa ya Darul Fikr; Tahdhibu Al-Tahdhib j. 4, uk. 181; Al-Kashif j. 1, uk. 462; Taarikhul Islam; Siyaru Al-A’alam j. 11, uk. 136; Al-Mizan j. 2, uk. 212; Tadhkiratul Huffadh j. 2, uk. 438; Al-’Ibar vya Al-Dhahabi j.1, uk. 413, Al-Bidaya Wa Al-Nihaya j. 10, uk. 312; Al-Taqrib na. 2588; Khulasat Al-Tahdhib cha Al-Khazraji; Shadharat Al-Dhahab j. 2, uk. 78; Al-Jami’u Fii Al-Jarhi Wa Al-Ta’adil j. 1, uk. 340; Al-Jam’u Baina Rijali Al-Sahihain j. 1, uk. 183; Hadyu Al-Sari uk. 408; Al-Thiqat cha Ibn Shahin. Naye (mpokezi huyo) ni mpokezi wa Al-Bukhari na (Maimamu) wanne (Abu Dau, Al-Tirmidhi, Al-Nasai na Ibn Maja). 182 - Al-Albani Al-Dhaifa j. 1, uk. 213. 183 - Miongoni mwa hivyo ni: Al-Taarikh Al-Kabir cha Al-Bukhari j. 6, uk. 71; Taarikh Ibn Ma’in; Al-Jarhu Wa Al-Ta’adil cha Ibn Abi Hatim j. 6, uk. 27; Al-Thiqat cha Ibn Hibbaan, j. 7, uk. 130; Al-Dhu’afaa cha Al-Daraqutni uk. 94; Al-Ma’arifa Wa Al-Taarikh cha Ya’aqub bin Sufyaan Al-Fasawi j. 3, uk. 55; Tabaqat Ibn Sa’ad; Tahdhibul Kamal cha Al-Mizzi j. 11, uk. 8-9, tarjama na. 3669 chapa Daru Al-Fikr; Tahdhibu Al-Tahdhib j. 6, uk. 87; Taqribu Al-Tahdhib uk. 331 na akasema Al-Hafidh kuhusu mpokezi huyo: “Ni mwenye kuaminika; Faqihi”; Al-Jarhu Wa Al-Ta’adil j. 2, uk. 47.

63

Page 64: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Anasema (Al-Albani) katika Irwaau Al-Ghalil alipoitaja riwaya fulani:

“Sanad yake ni hasan lau si (kuwemo ndani yake) mtu ambaye hakutajwa, na Al-Daraqutni katika riwaya yake kamwita Said bin Ash-wa’i, na sikuiona tarjama (biography) yake”.184 Hivyo ndivyo alivyosema maskini huyu (Al-Albani) kwa sababu yeye alitazama baadhi ya vitabu vya wapokezi asimkute Said bin Ash-wa’i, wala hakujua kwamba baba yake jina lake ni ‘Amru bin Ash-wa’i, na wengine wakamnasibisha na babu yake wakasema: ‘Said bin Ash-wa’i’.185

4) ‘Abbadu bin Salim

Anasema (Al-Albani) katika Sahiha186 yake: “Na wapokezi wake ni wenye kuaminika isipokuwa ‘Abbaad bin Salim sikumuona alimtarajimu (aliyemtaja)”. Hivyo ndivyo alivyosema (Al-Albani), na lau alitazama: Al-Tarikh Al-Kabir cha Al-Bukhari;187 Al-Jarhu Wa Al-Ta’adil cha Ibn Abi Hatim;188 Al-Thiqat cha Ibn Hibbaan,189 basi angelijua kwamba (mpokezi huyo) ni mwenye kutarajimiwa.

5) Yahya bin Malik

Anasema (Al-Albani) katika maelezo yake ya kitabu Al-Mishkaat: “Watu wake ni wenye kuaminika isipokuwa Yahya bin Malik naye ni Al-Azdi Al-‘Ataki kamtaja Ibn Abi Hatim bila ya kutaja kujeruhi wala kuwa ni muadilifu”.190 Hivyo ndivyo alivyosema (Al-Albani) wala hakujua kwamba Yahya bin Malik huyu ni mwenye kuaminika kama walivyoeleza kundi (kubwa la wanavyuoni).191 184 - Al-Albani Ir-waau Al-Ghalil j. 3, uk. 121.185 - Na hivi baadhi ya vitabu ambavyo vimetaja tarjama yake: Rijalu Al-Bukhari cha Al-Kalabadhi; Rijalu Muslim cha Ibn Manjuyah j. 1, uk. 247; Al-Ta’arikh Al-Kabir j. 2, uk. 500, Taarikh Ibn Ma’in; ‘Ilalu Al-Tirmidhi; Al-Jarhu wa Al-Ta’adil j. 4, uk. 50; Tabaqat Ibn Sa’ad j. 6, uk. 327; Al-Thiqat cha Ibn Hibbaan; Al-Thiqat cha Al-’Ijli; Tahdhibu Al-Kamal; Tahdhibu Al-Tahdhib; Mizanu Al-I’itidal; Al-Mughni Fii Al-Dhu’afai tarjama na. 2356; Al-Kashif j. 1, uk. 441; Taqribu Al-Tahdhib uk. 239; Khulasat Al-Tahdhib; Al-Jami’u Fii Al-Jarhu wa Al-Ta’adil j. 1, uk. 305; Al-Jam’u baina Rijali Al-Sahihain j. 1, uk. 116; Hadyu Al-Sari uk. 406. 186 - J. 3, uk. 191. 187 -J. 6, uk. 38. 188 - J. 6, uk. 80. 189 - J. 7, uk. 159 190 - Al-Albani Maelezo juu ya Al-Mishkaat j. 1, uk. 438. 191 - Miongoni mwao ni Ibn Sa’ad, Al-Nasai, Ibn Hibbaan, Al-’Ijli, Al-Daraqutni. Naye katarajimiwa katika vitabu vingi mno; miongoni mwa hivyo ni: Rijalu Al-Bukhari j. 2, uk.

64

Page 65: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Na kwa haya yanaporomoka yale alioyasema (Al-Albani) katika Sahihi yake kwamba Yahya huyu hakumtarajimu yoyote miongoni mwa wale walioandika (habari za) wapokezi wa (vitabu) sita; wala (hayumo) katika Al-Tahdhib, wala Al-Tadh-hib wala Al-Taqrib.192

6) Abu Rifa’a, ‘Abdullahi bin Muhammad bin ‘Umar Al-’Adawi

Anasema (Al-Albani) katika Sahiha yake: “Isnad hii wapokezi wake ni wenye kuaminika wenye kujulikana isipokuwa Abu Rifa’a sikumuona alipotarajimiwa”.193 Hivyo ndivyo alivyosema, wakati Abu Rifa’a huyu katarjimiwa katika Taarikh Baghdad cha Al-Khatib194 na akasema: “Ni mwenye kuaminika”.195

7) Al-Harith bin Muhammad Al-Makfuf

799; Rijalu Muslim j. 2, uk. 372, Tabaqat Ibn Sa’ad; Al-Thiqat cha Ibn Hibbaan; Al-Thiqat cha Al-’Ijli; Tabaqat Khalifat Ibn Khayyat na Sualat Al-Barqani uk. 544; Al-Taarikh Al-Kabir cha Al-Bukhari j. 4, uk. 303; Tahdhibu Al-Kamal j. 21, uk. 44; Tadh-hibu Al-Tahdhib cha Al-Dhahabi; Tahdhibu Al-Tahdhib j. 12, uk. 9; Taqribu Al-Tahdhib uk. 620; Khulasat Al-Tahdhib cha Al-Khazraji; Al-Jami’u Fii Al-Jarhi Wa Al-Ta’adil; Al-Jam’u Baina Rijali Al-Sahihain. 192 - Kayasema hayo katika Al-Sahiha j. 1, sehemu ya pili, uk. 705, katika maelezo ya Hadithi na. 365, lakini ibara ya Al-Albani ni: “si katika Al-Tahdhib, wala katika Al-Taqrib wala katika Al-Tadh-hib”. Jambo hili linathibitisha kwamba Al-Imamu Al-Qannubi kaziandika sehemu nyingi za kitabu chake hicho kwa kichwa, na hili linaonesha uwezo wake mkubwa wa kuhifadhi (Allah amzidishie nuru) Amin! 193 - Al-Albani Sahiha j. 5, uk. 368. 194 - J. 10, uk. 83 195 - Ninasema lakini usistaajabu kwani Al-Albani husoma table of contents (yaliyomo) tu kama vile wanavyofanya wapekuzi wengine ambao hawakujihusisha na elimu ya Hadithi. Tazama – kwa mfano – alivyosema kwamba “Hadithi ya Anas sikuiona katika yaliyomo ya kitabu Al-Hilya. Silsila Al-Dhaifa j. 4, uk. 90. Na katika ukurasa 94 anasema: “Wala sikuiona katika yaliyomo ya kitabu Taa-rikh Baghdaad. Pamoja na hayo Hadithi hio ambayo yeye anasema kwamba hakuiona katika table of contents (yaliyomo) ya kitabu Taarikh Baghdad, Hadithi hio imo katika kitabu hicho Taarikh Baghdaad j. 13, uk. 276, tarjama ya Mubaadir bin ‘Ubaidi-Lahi na. 7240. Hii ina maana kwamba Al-Albani anasukuma tu: anadhoofisha Hadithi bila ya kuhakikisha kwamba kuna sanad nyengine sahihi au hakuna. Huyu ndiye mtu ambaye Kasim Mafuta anatwambia “Ni mwanachuoni mkubwa anayekubalika sana!”. Na vipi mwanachuoni mkubwa hasomi vitabu: anasoma table of content (yaliyomo) tu kisha anasahihisha na kudhoofisha! Kiufupi mifano kama hii iko mingi katika vitabu vya Al-Albani.

65

Page 66: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Anasema (Al-Albani) katika Dhaifa yake: “Sikuona tarjama (biography) yake”.196 Hivyo ndivyo alivyosema, na imempita (Al-Albani) kwamba Al-Harith huyu katarjamiwa katika Al-Mizan,197 na Lisanu Al-Mizan.198

8) Ummu Yunus bint ‘Ubaid

Kasema Al-Albani katika kumjibu kwake Al-Habashi: “Katika sanad kufikia kwake kuna Ummu Yunus bint ‘Ubaid, wala hakutajwa katika vitabu vya Tarajim (biographies)”.

Hivyo ndivyo alivyosema, ilhali Ummu Yunus huyu katajwa katika Al-Taarikh Al-Kabir,199 Al-Munfaridat cha Al-Imamu Muslim;200 Al-Jarhu Wa Al-Ta’adil cha Ibn Abi Hatim.201

9 ‘Amru bin Abi ‘Amri Al-’Abdi

Anasema Al-Albani katika Dha’ifa yake: “Na ‘Amru bin Abi ‘Amri Al-’Abdi sikumjua (ni nani).”202 Hivyo ndivyo alivyosema, ilhali ‘Amru huyu ni maarufu katarajimiwa katika vitabu vingi.203

Naye (mpokezi huyu) ni katika wapokezi wa Al-Bukhari na Muslim; na Al-’Abdi ni kunasibishwa na maula (bwana) wake Al-Muttalib bin ‘Abdillah Al-Makhzumi.

10) ‘Isa bin Hilal Al-Sadafi

196 - Al-Albani Dhaifa j.4, uk. 397. Katika chapa ya pili ni uk. 395. 197 - J. 1, uk. 443. 198 - J. 2, uk. 150. 199 - J. 9, uk. 44. 200 - Uk. 19. Yaani riwaya zake alizopwekeka nazo pasina Al-Bukhari. 201 - J. 8, uk. 333. 202 - Al-Albani Al-Dhaifa j. 4, uk. 404. 203 - Miongoni mwa hivyo ni: Rijalu Al-Bukhari cha Al-Kalabadhi j. 2, uk.549; Rijalu Muslim cha Ibn Manjuyah j. 2, uk. 76; Al-Taarikh Al-Kabir j. 3, uk. 2, tarjama na. 359; Al-Jarhu Wa Al-Ta’adil cha Ibn Abi Hatim j. 6, uk. 252; Sunanu Al-Nasai j. 2, uk. 302; Tabaqat Ibn Sa’ad; Al-Thiqat cha Ibn Hibbaan; Al-Kamil cha Ibn ‘Adey; Al-Thiqat cha Al-‘Ijli; Mukhtasar Al-Kamil uk. 540; Tahdhibu Al-Kamal j. 14, uk. 300; Tadh-hibu Al-Tahdhib; Al-Kashif j. 2, uk. 84; Mizanu Al-I’itidal j. 3, uk. 281; Al-Mughni Fii Al-Dhu’afai tarjama na. 4685; Tahdhibu Al-Tahdhib j. 8, uk. 73; Taqribu Al-Tahdhib uk. 425; Khulasatu Al-Tahdhib; Al-Jami’u Fii Al-Jarhi Wa Al-Ta’adil j. 2, uk. 302; Al-Jam’u Baina Rijali Al-Sahihain j. 1, uk. 116.

66

Page 67: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Anasema (Al-Albani) katika maelezo yake juu ya kitabu Al-Mishkaa204 Kuhusu Isa bin Hilal Al-Sadafi: “Naye ninavyoona ni kuwa hajulikani, kwani Ibn Abi Hatim kamtaja katika kitabu Al-Jarhu Wa Al-Ta’adil na wala hakutaja kujeruhiwa (kwa mpokezi huyu) wala kwamba ni mwenye kuaminika, bali aliyesema kuwa ni mwenye kuaminika ni Ibn Hibbaan naye ni maarufu kwa tasahul”. Hivyo ndivyo alivyosema (Al-Albani) wala hakujua kwamba Ya’aqub bin Sufyaan Al-Fasawi amesema kuwa ni mwenye kuaminika kwa kumtaja kwake katika Tabi’ina wenye kuaminika.205

11) Muhammad bin ‘Abdil-Rahman Al-Yahsabi

Anasema (Al-Albani) katika Sahiha206 yake kuhusu sanad ya Hadithi fulani:207 “Ninasema: na hii isnad ni hasan wapokezi wake ni wenye kujulikana isipokuwa Al-Yahsabi huyu, naye ni Muhammad bin ‘Abdil-Rahman bin ‘Irq; Ibn Abi Hatim amemtarajimu208 kwa riwaya ya kundi (kubwa la wapokezi), wala hakutaja ndani yake kujeruhiwa (kwa mpokezi huyu) wala kwamba ni mwenye kuaminika. Na dhahir ni kuwa Ibn Hibbaan kasema kuwa ni mwenye kuaminika kama maneno ya Al-Haithami yaliotangulia yanavyoonesha.

Hayo ndio maneno yake, wala hakujua kwamba Al-Yahsabi huyu katarajimiwa (katika vitabu vingi).209

12) Abu Salih Al-Khawlani

Anasema (Al-Albani) katika takhrij yake ya fadhila za Al-Sham kuhusu Abu Salih Al-Khawlani: “Na sikumjua”. Hivyo ndivyo alivyosema, wala hakujua kwamba Al-Khawlani huyu ni mwenye kutarajimiwa katika Al-Jarhu Wa Al-Ta’adil210 cha Ibn Abi Hatim na akanukuu kutoka kwa baba yake akisema “Hana ubaya”.

13) Ahmad bin Muhammad bin Ghalib bin Mirdas Al-Basri204 - J. 1, uk. 466. 205 - Kama ilivyo katika Al-Ma’arifa wa Al-Taarikh j. 2, uk. 515. 206 - Al-Albani Al-Sahiha j. 3, uk. 253. 207 - Hadithi yenyewe inasema: رآني لمن .(..…kabarikiwa yule aliyeniona) .......طوبى208 - J. 3/2 uk. 316.209 - Kama vile Tahdhibu Al-Kamal na vitabu vya mukhtasari wake….Ametarajimiwa na Al-Mizzi katika Tahdhibu Al-Kamal j. 16, uk. 493 chapa Darul-Fikr; na akamtarajimu Al-Hafidh Ibn Hajar katika Tahdhibu Al-Tahdhib j. 9, uk. 267 na katika Al-Taqrib uk. 492; Al-Dhahabi Al-Kashif j. 2, uk. 193 na katika Al-Tadh-hib; na Al-Khazraji katika Al-Khulasat. 210 -Ibn Abi Hatima Al-Jarhu Wa Al-Ta’adil j. 9, uk. 392.

67

Page 68: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Anasema (Al-Albani) katika Dhaifa211 yake kuhusu njia ya Hadithi fulani alioitaja huko: “Ndani yake yumo (mpokezi) sikumjua”.212 Hivyo ndivyo alivyosema, na katika njia hio kuna Ahmad bin Muhammad bin Ghalib bin Mirdas Al-Basri ajulikanaye kwa jina la Ghulamu Khalil213 naye ni mwongo mkubwa naye ni mwenye kukiri kutunga kwake Hadithi. Na miongoni mwa waliosema kuwa ni mwongo ni Abu Bakr Ibn Is-haq na Isma’il Al-Qadhi, na akasema Abu Dawud: “Hadithi zake ni uwongo”, kama utavyoyakuta hayo katika Lisanu Al-Mizan214 na (vitabu) vyengine. Na Sheikh wake ni Muhammad bin Ibrahim bin Al-’Alaa, anasema Al-Daraqutni kuhusu yeye: “Ni mwongo mkubwa”. Na anasema Ibn Hibbaan: “Anatunga Hadithi”. Na akasema Al-Hakim Abu Ahmad na Abu Nu’aim: “Kasimulia Hadithi za kutunga”.14) Al-Mu’alla bin Ru-ba

Anasema (Al-Albani) katika Sahiha yake: “Na Al-Mu’alla bin Ru-ba sikuiona tarjama yake”.215 Hivyo ndivyo alivyosema, wala hakujua kwamba Al-Mu’alla bin Ru-ba huyu anayo tarjama katika Al-Ma’arifa Wa Al-Taarikh cha Ya’aqub bin Sufyaan Al-Fasawi.216

15) ‘Amru bin Ghalib

Anasema (Al-Albani) katika Irwaau Al-Ghalil217 kuhusu Hadithi fulani ilioko huko: “Wapokezi wake ni wenye kuaminika isipokuwa ‘Amru bin Ghalib, Ibn Hibbaan kasema kuwa ni mwenye kuaminika, na wala hakuipokea kutoka kwake isipokuwa Abu Is-haq naye ni Al-Sabi’i”. Hivyo ndivyo alivyosema na imemfichikia (Al-Albani) kwamba Al-Nasai kasema kuwa ni mwenye kuaminika.218

211 - Al-Albani Al-Dhaifa j. 3, uk. 442. 212 - Ibara ya Al-Albani ni: “Katika (njia ya) kwanza kuna yule ambaye sikumjua”. 213 - Ninasema: Al-Albani mwenyewe kasema katika Dhaifa yake kwamba Ghulam Khalil anatunga Hadithi. Tazama j. 13, uk. 398, maelezo ya Hadithi na. 6179, kisha hapa katika kitabu Makaarimu Al-Akhlaaq cha Al-Kharaaiti Hadithi na. 39, mpokezi huyo huyo alipotajwa kwa jina lake “Ahmad bin Muhammad bin Ghalib” hakujua kwamba huyo ndiye yule mwenye kujulikana kwa jina la “Ghulam Khalil”, yeye akasema: “Katika njia ya kwanza kuna mtu sikumjua”! 214 - J, 1, uk. 272, tarjma na. 832.215 - Al-Albani Al-Sahiha j. 4, uk. 55. 216 - Tazama Ya’aqub bin Sufyaan Al-Fasawi Al-Ma’arifa Wa Al-Taarikh j. 1, uk. 403, na Al-Bukhari Al-Taarikh Al-Kabir. 217 - Al-Albani Ir-waau Al-Ghalil j. 7, uk. 254. 218 - Ninasema: labda Al-Albani kamqallid (kamuiga) Ibn Al-Barqi! Tazama Tahdhib Al-Tahdhib j. 8, uk. 77, tarjama na. 132.

68

Page 69: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

16) Al-Nadharu bin Muhammad Al-Shaibani

Anasema (Al-Albani) katika Dhaifa219 yake: “Na Sheikh wake Al-Nadharu bin Muhammad Al-Shaibani sikumjua”. Hivyo ndivyo alivyosema, na Al-Nadhar bin Muhammad ni mashuhuri katarajimiwa katika vitabu vingi mno.220

17) Imra-atu Ibni ‘Umar

Anasema (Al-Albani) katika Sahiha221 yake: “Na wapokezi wake ni wenye kuaminika isipokuwa Imra’atu Ibni ‘Umar (mke wa Ibn ‘Umar) sikumjua”.

Na Imra’atu Ibni ‘Umar (mke wa Ibn ‘Umar) huyu ni maarufu mashuhuri, na jina lake ni Safiyya bint Abi ‘Ubaid Al-Thaqafiyya. Al-Imamu Muslim na Al-Imamu Al-Bukhari wamepokea (riwaya zake) katika Al-Ta’aaliq. Na hivi ni vitabu vilivyomtarajimu:222

18) Miskin bin Bukair Al-Hadhaai

Anasema (Al-Albani) katika Sahiha223 yake kuhusu Miskin bin Bukair Al-Hadhaai kwamba ni katika wapokezi wa Al-Bukhari”. Na kilicho sahihi ni kuwa yeye ni mpokezi Al-Bukhari na Muslim, kama utavyokuta hayo katika Al-Tahdhib na vitabu vilivyokifanyia mukhtasari na vitabu vilivyoandikwa kuhusu wapokezi wa Mashekhe wawili (Al-Bukhari na Muslim)”.

19) Rauh bin Al-Faraj Abu Al-Zinba’i

219 - Al-Albani Al-Dhaifa j. 3, uk. 469-470. 220 - Al-Taarikh Al-Kabir j.4/2 79; Al-Dhu’afau Al-Saghir uk. 377; Al-Kuna cha Al-Imamu Muslim; Asami Al-Dhu’afai cha Abu Zur’a Al-Razi uk. 339; Al-Jarhu Wa Al-Ta’adil; Al-Thiqat cha Ibn Hibbaan; Tahdhibu Al-Kamal j. 19, uk. 94 Darul Fikr; Tahdhibu Al-Tahdhib; Al-Kashif j. 2, uk. 321; Diwanu Al-Dhu’afai j. 2, uk. 404; Mizanu Al-I’itidal j. 4, uk. 262; Al-Mughni Fii Al-Dhu’afai tarjama na. 6643; Tahdhibu Al-Tahdhib j. 10 , uk. 397; Taqribu Al-Tahdhib uk. 563; Khulasatu Al-Tahdhib; Al-Jami’u Baina Al-Jahi Wa Al-Ta’adil j. 3, uk. 207. 221 - Al-Albani Al-Sahiha j. 4, uk. 269. 222 - Rijalu Muslim j. 2, uk. 423; Al-Thhiqat cha Ibn Hibbaan; Al-Sunan cha Al-Daraqutni; Al-Thiqat cha Al-’Ijli uk. 1875; Al-Isti’aab cha Ibn ‘Abdil-Barr; Tahdhibu Al-Kamal j. 22, uk. 361 chapa Darul-Fikr; Tadh-hibu Al-Tahdhib; Al-Kashif j. 2, uk. 152; Tahdhibu Al-Tahdhib j. 12, uk. 459; Al-Taqrib uk. 749; Al-Isaba cha Al-Hafidh Ibn Hajar; Khulasatu Al-Tahdhib cha Al-Khazraji; Al-Jami’u Fii Al-Jarhi Wa Al-Ta’adil cha 3, uk. 472. 223 - Al-Albani Al-Sahiha j. 1, uk. 42. Katika chapa ya pili ni uk. 75.

69

Page 70: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Anasema (Al-Albani) katika Ir-waauGhalil yake, Rauh bin Al-Faraj Abu Al-Zinba’i ni “Katika wapokezi wa Al-Bukhari”.224 Na wala hali haiko kama alivyodai yeye (Al-Albani), na ukipenda kuhakikisha hilo, tazama Al-Taqrib,225 kasema (Ibn Hajar) baada ya kumtaja: “Tamyiz”, basi yeye si katika mpokezi wa wapokezi sita kamwe.

20) Jarir bin Kulaib

Anasema (Al-Albani) katika maelezo yake juu ya Al-Mishkaa226 kuhusu Jarir bin Kulaib: “Hakupokea (Hadithi) kutoka kwake isipokuwa Abu Is-haq Al-Sabi’i”. Hivyo ndivyo alivyosema (Al-Albani) na lau alitazama Tahdhibu Al-Kamal227 basi angeliona kwamba ‘Aasim bin Abi Al-Najud pia kapokea kutoka kwake.

21) Isa bin ‘Umar

Anasema (Al-Albani) katika maelezo yake juu ya Al-Mishkaa228 kuhusu Isa bin ‘Umar: “Hajulikani”. Lakini kauli ya Al-Daraqutni “Ni mtu wa madina anajulikana”229 inamrudi (Al-Albani).

22) ‘Abdul-Wahid bin Qais

Anasema (Al-Albani) katika Sahiha yake kuhusu Hadithi fulani ilioko huko: “Na isnad yake ni hasan; wapokezi wake ni wenye kuaminika, na kuhusu hifadhi ya ‘Abdul-Wahid bin Qais kuna udhaifu mdogo….”.230 Hivyo ndivyo alivyosema (Al-Albani) wala hakujua kwamba ‘Abdul-Wahid huyu hakusikia (Hadithi) kutoka kwa Abu Huraira kama alivyosema Salih Jazara. Na akasema Ibn Hibbaan: “Anasimulia kutoka kwa Abu Huraira wala hakumuona”.

23) Al-Qasim

Anasema (Al-Albani) katika Sahiha yake: “Ninasema: sanad hii ni sahihi; wapokezi wake ni wapokezi wa Muslim isipokuwa Al-Qasim huyu naye ni

224 - Al-Albani Ir-waau Al-Ghalil j. 5, uk. 31. 225 - Uk. 211, tarjama na. 1967.. 226 - J. 1, uk. 97. 227 - J. 3, uk. 367. 228 - J. 1, uk. 213. 229 - Ibn Hajar Tahdhibu Al-Tahdhib j. 8, uk. 201, tarjama na. 417. 230 - Al-Albani Al-Sahiha j. 4, uk. 397.

70

Page 71: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

mwenye kuaminika, na Muslim amesimulia riwaya zake katika utangulizi”.231 Hivyo ndivyo alivyosema, na imemfichikia (Al-Albani) kwamba Al-Imamu Muslim amesimulia riwaya zake (Al-Qasim) katika Al-Sahih (yake) katika sehemu nyingi.232

24) Al-’Adawi

Anasema (Al-Albani) katika Sahiha yake: “Basi isnad yake ni sahihi kwa (mujibu wa) masharti ya Muslim ikiwa Al-’Adawi alihifadhi”.233 Hivyo ndivyo alivyosema (Al-Albani), wala hakujua kwamba Al-’Adawi huyu si katika wapokezi wa Muslim kama utavyoliona hilo katika Al-Tahdhib na vitabu vyengine. Bali hakuna yoyote aliyesimulia (Hadithi) kutoka kwake katika wapokezi sita isipokuwa Ibn Maja peke yake.

25) Al-Muttalib bin ‘Abdillahi bin Hantab

Anasema (Al-Albani) katika maelezo yake juu ya kitabu Al-Mishkaa234 kuhusu Hadithi fulani ilioko huko: “Isnad yake ni sahihi”. Hivyo ndivyo alivyosema, wala hakujua kwamba riwaya za Al-Muttalib bin ‘Abdillahi bin Hantab aliyeipokea (Hadithi hio) kutoka kwa ‘Aisha ni riwaya mursala kama alivyosema Abu Hatim kwa uwazi.

26) Ahmad bin Al-Miqdaam

231 - Al-Albani Al-Sahiha j. 1, uk. 191. Utanabahisho: maelezo haya Al-Albani kayarekebisha katika chapa ya pili, na akasema: “Ninasema: na sanad hii ni sahihi; wapokezi wake ni wenye kuaminika”. Tazama chapa ya pili j. 1, uk. 241, maelezo ya Hadithi na. 122.232 - Tazama Hadithi na. 1064 (150), 1995 (37). 233 - Al-Albani Al-Sahiha j. 1, uk. 739. Utanabahisho: katika chapa ya zamani ambayo ndio anayotunukulia Al-Qannubi, Al-Albani alijigonga katika sentensi moja. Alisema:

كان إن مسلم شرط على صحيح فاإلسناد العدوي ال الليثي هو هذا أسامةقد شيئا العدوي حفظه في فإن ، حفظ

Usama huyu ni Al-Laithi si Al-‘Adawi, basi isnad yake ni sahihi kwa mujibu wa masharti ya Muslim, ikiwa Al-‘Adawi kahifadhi kwani katika hifadhi yake kuna kitu (kasoro). Na ilivyo, kwa mujibu wa maelezo yake, ni kusema “Ikiwa Al-Laithi amehifadhi”. Marekebisho haya baadae kayafanya mwenyewe katika chapa ya pili j. 1, uk. 817. Kwa hali yoyote ile, Usama bin Zaid Al-‘Adawi hakupokea kutoka kwake, katika wapokezi sita, isipokuwa Ibn Maja, na hapa ndipo Al-Qannubi alipompinga Al-Albani kwa kuifanya kwake sanad hio ya Al-‘Adawi kuwa ni kwa mujibu wa masharti ya Muslim; na Usama bin Zaid Al-Laithi wamepokea kutoka kwake wapokezi wane pamoja na Muslim, na Al-Bukhari katika ta’aaliiq. Tahdhibu Al-Tahdhib j. 1, uk. 181-183. 234 - J. 3, uk. 1409.

71

Page 72: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Anasema (Al-Albani) katika maelezo yake juu ya Sahihu Ibn Khuzaima: “Na sanad yake ni sahihi kwa (mujibu wa) masharti ya Mashekhe wawili (Al-Bukhari na Muslim)”.235 Pamoja na kuwa katika sanad hii kuna Ahmad bin Al-Miqdaam, naye ni mpokezi wa Al-Bukhari tu pasina Muslim236 (kama ilivyo) katika Al-Tahdhib na Al-Taqrib na vitabu vyengine vilivyotungwa katika jambo hili.

27) Yahya bin Al-Mughira Al-Makhzumi

Anasema (Al-Albani) katika Sahiha yake kuhusu Hadithi ilioko huko:

Kaipokea Al-Hakim j. 2, uk. 90, na akasema: ‘Ni sahihi kwa (mujibu wa) masharti ya Mashekhe wawili (Al-Bukhari na Muslim)’. Na Al-Dhahabi akakubaliana naye. Na hivyo ndivyo (ilivyo) kama alivyosema.237

Hivyo ndivyo alivyosema, wakati katika isnad ya Hadithi hii kuna Yahya bin Al-Mughira Al-Makhzumi naye ni katika wapokezi wa Al-Tirmidhi wala Al-Bukhari na Muslim hawakupokea kitu kutoka kwake.238 Na pia ndani yake kuna Muhammad bin Ayyub naye si katika mpokezi wao (Al-Bukhari na Muslim).

28) Hadithi ya Abu Ayyub

Anasema (Al-Albani) katika Ir-waau Ghalil yake: “Ama Hadithi ya Abu Ayyub – yaani ile inayohusu kutenguka udhu kwa kugusa uchi – sikuiona sanad yake, na ameitaja Al-Hafidh (Ibn Hajar) katika Al-Talkhis Hadithi hii – Hadithi ya kutenguka udhu kwa kugusa uchi – kutoka kwa kundi kubwa la Masahaba wala ndani yake hakuna Abu Ayyub, kisha akawataja”.239 Ninasema:240 “Hadithi ya Abu Ayyub imo katika vitabu vingi mashuhuri vyenye kupatikana, vimo mikononi mwa Al-Albani. Kaipokea Ibn Maja241, Al-Tabarani242 Ibn Shaahin,243 Ibn Al-Jawzi”.244

235 - J. 1, uk. 119. 236 - Yaani katika Masheikh wawili hawa (Al-Bukhari na Muslim), basi yeye ni mpokezi wa Al-Bukhari tu. Ama wengine – ukimtoa Muslim – pia wamesimulia riwaya kutoka kwake. 237 - Al-Albani Al-Sahiha j. 2, uk. 277. 238 - Tazama Al-Taqrib uk. 597. 239 - Al-Albani Ir-waau Al-Ghalil j. 1, uk. 151. 240 - Msemaji ni Al-Imamu Al-Rabbani Sheikh Al-’Allama Al-Kabir Said bin Mabruk Al-Qannubi. 241 - Ibn Maja Al-Sunan j. 1, uk. 99 Hadithi na. 482. 242 - Al-Tabarani Al-Kabir Hadithi na. 3928. 243 - Ibn Shaahin Al-Nasikh Wa Al-Mansukh uk. 114. 244 - Ibn Al-Jawzi Al-Tahqiq uk. 1.

72

Page 73: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

29) Hadithi: Tende ni daku jema lilioje kwa Mu-umini

Anasema (Al-Albani) katika Sahiha yake kuhusu Hadithi inayosema: التمر المؤمن سحور :”Tende ni daku jema lilioje kwa Mu-umini“ نعم

Tanbih! Hadithi hii Al-Mundhiri katika Al-Targhib wa Al-Tarhib j. 2, uk. 94 – akifuatiwa na Al-Khatib Al-Tabrizi katika Al-Mishkaa uk. 988245 – kainasibisha kwa Abu Dawud, nao ni wahm (kosa) sijui limewatokea wapi?”246

Hivyo ndivyo alivyosema (Al-Albani) na Hadithi hio imo katika Sunan Abi Dawud.247

30) Hadithi ya Al-Hakim katika Al-Mustadrak

Anasema (Al-Albani) katika Ir-waau Ghalil yake:

…Na akaisahihisha Ibn Daqiiq Al-’Id katika Al-Iqtirah kama ilivyo katika Al-Talkhis na akainasibisha na Al-Hakim vile vile, wala sikuiona katika kitabu chake Al-Mustadrak na vivyo hivyo sikuiona kwa Ahmad na mtunzi – yaani mtunzi wa Manaru Al-Sabil – ameinasibisha kwake.248

Hivyo ndivyo alivyosema (Al-Albani), ilhali Hadithi hio imo katika Al-Musnad249 na katika Al-Mustadrak.250

31) Hadithi: Fuateni kundi kubwa

Anasema (Al-Albani) katika maelezo yake juu ya kitabu Mishkaatul Masaabiih, kuhusu Hadithi “Fuateni kundi kubwa atayepwekeka basi atapwekeka motoni”. Anasema (Al-Albani): “Sikuiona katika chochote miongoni mwa vitabu sita maarufu, hata Al-Amali na Al-Fawaaid na Al-Ajzaa nilivyovipitia navyo vinafika mamia”.251 Hivyo ndivyo alivyosema, na Hadithi imo katika Al-Mustadrak.252

245 - Katika kopi ya Al-Sahiha nilionayo imeandikwa (1998), yaani ukurasa huo wa 1998 wa kitabu Al-Mishkaa. Na maneno hayo katika kopi nilionayo nayo ni chapa ya pili yamo katika uk. 106, ya kitabu hicho Al-Sahiha. 246 -Al-Albani Al-Sahiha j. 2, uk. 99-100. 247 - J. 1, uk. 543, Hadithi na. 2345. 248 - Al-Albani Ir-waau Al-Ghalil j. 8, uk. 222. 249 - Ahmad Al-Musnad j. 3, uk. 363. 250 - Al-Hakim Al-Mustadrak j. 4, uk. 304-305. 251 - J. 1, uk. 62. 252 - Al-Hakim Al-Mustadrak j. 1, uk. 115.

73

Page 74: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

32) ‘An’anatu Abi Is-haq Al-Sabi’i

Anasema (Al-Albani) katika maelezo yake juu ya Sahihu Ibn Khuzaima: “Isnad yake ni dhaifu kwa sababu ya ‘an’anatu Abi Is-haq, naye ni Al-Sabi’i”.253 Hivyo ndivyo alivyosema (Al-Albani), wakati Abu Is-haq amesarrih bisima’i (kasema kwa uwazi kuwa kaisikia Hadithi hio) katika mapokezi ya Al-Tayaalisi254 na Ahmad.255

33) Hadithi: Akisinzia mmoja wenu

Anasema (Al-Albani) katika Sahiha yake (kuhusu Hadithi isemayo): “Mmoja wenu akisinzia katika msikiti siku ya ijumaa basi na-aondoke katika sehemu hile aliokaa ende sehemu nyengine”. Anasema (Al-Albani):

Kasema Al-Tirmidhi: ni Hadithi hasan sahihi. Na akasema Al-Hakim: Sahihi kwa (mujibu wa) masharti ya Muslim. Na Al-Dhahabi akawafikiana naye. Hivyo ndivyo alivyosema, lakini Ibn Is-haq ni mudallis (mwenye kughushi) naye ame’an’an256 katika njia zote kutoka kwake.257

Hivyo ndivyo alivyosema (Al-Albani), na wala habari haikuwa kama alivyodai yeye, kwani Ibn Is-haq amesarihi (amesema kwa uwazi) kwa kuisikia (Hadithi hio) katika mapokezi ya Ahmad.258

34) Lafdhi “Anzeni”

Anasema (Al-Albani) katika Ir-waau Ghalil yake:

…Ama lafdhi ya tatu “Ibdau anzeni” mtunzi – yaani mtunzi wa Manaru Al-Sabil – ameinasibisha (kwa Al-Nasai), naye katika hilo kawafuata Mahuffadh zaidi ya mmoja, kama Al-Zaila’i katika Nasbu Al-Raya,259 Ibn Al-Mulaqqin katika Al-Khulasa,260 na Ibn Hajar katika Al-Talkhis,261 wote wameinasibisha (lafdhi hio) kwa Al-Nasai, na hio kiistilahi ina maana ni

253 - J. 2, uk. 143. 254 - Uk. 15. 255 - Ahmad Al-Musnad j. 1, uk. 105, Hadithi na. 825. 256 - Yaani katika masimulizi yake katumia neno عن ‘An (kutoka kwa….), akasema “An fulani (kutoka kwa fulani)”.257 - Al-Albani Al-Sahiha j. 1, uk. 760, Hadithi na. 468. 258 - Ahmad Al-Musnad j. 2, uk. 135. 259 - J. 3, uk. 54. 260 - J. 2, uk. 108 261 - Uk. 114.

74

Page 75: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

katika Al-Sunan Al-Sughra, na wala haimo humo (katika Al-Sunan Al-Sughra ya Al-Nasai) lafdhi hii kamwe…...262

Hivyo ndivyo alivyosema huyu ajifanyae kuwa ana elimu (ya Hadithi, Al-Albani), ilhali Hadithi hio ipo kwa lafdhi hio katika Al-Sunan Al-Sughra cha Al-Nasai.263

35) Riwaya ya Al-Imamu ‘Ali

Anasema (Al-Albani) katika Ir-waau Ghalil yake kuhusu riwaya ilioko huko kutoka kwa Ali: “Sikuiona isnad yake”.264 Hivyo ndivyo alivyosema (Al-Albani), na riwaya hio imo katika Sunan Al-Bayhaqi. Na hii ndio sanad yake: kasema Al-Bayhaqi: “Katupa habari Abu Said bin Abi ‘Amri, katusimulia Abu ‘Abbaas Muhammad bin Ya’aqub katusimulia Ahmad bin ‘Abdil-Hamid katusimulia Abu Usama kutoka kwa Sufyan kutoka kwa Salamat bin Kuhail kutoka kwa Mu’awiya bin Suwaid kasema: ‘Nimekuta katika kitabu cha ‘Ali’, akaitaja (riwaya)”. 265

36) Sanad Al-Albani hakuiona

Anasema (Al-Albani) katika Ir-waau Ghalil yake kuhusu Hadithi fulani ilioko huko: “Sikuiona isnad yake”.266 Hivyo ndivyo alivyosema (Al-Albani), ilhali Hadithi hio kaipokea Al-Nasai katika Al-Sunan Al-Kubra kama ilivyo katika Tuhfatul Ashraf cha Al-Mizzi267 kwa njia ya ‘Ubaidi-Lahi kutoka kwa Khalid bin Ma’adaan kutoka kwa ‘Abdillahi bin Busr kutoka kwa dada yake Al-Samaa kutoka kwa ‘Aisha. 37) Ibrahim na baba yake

Anasema (Al-Albani) katika Sahiha yake baada ya maelezo:

Kaipokea Ahmad j. 2, uk. 49, katusimulia Ibrahim bin Wahb bin Al-Shahid….na Ibrahim huyu na baba yake sikuwajua, wala Al-Hafidh hakuwatarajimu katika Al-Ta’ajil.268

Hivyo ndivyo alivyosema (Al-Albani), isnad imemgeukia basi kashindwa kuijua, na usahihi wake ni Ibrahim bin Habib bin Shahid, nao ni wenye kuaminika katika wapokezi (waliotajwa katika) Tahdhibu Al-Kamal na 262 - Al-Albani Ir-waau Al-Ghalil j. 4, uk. 317. 263 - Tazama j. 5, uk. 236. 264 - Al-Albani Ir-waau Al-Ghalil j. 6, uk. 251-252. 265 - Al-Bayhaqi Al-Kubra j. 7, uk. 121. 266 - Al-Albani Ir-waau Al-Ghalil j. 4, uk. 120. 267 - Al-Mizzi Tuhfatul Ashraf j. 12, uk. 401. 268 -Al-Albani Al-Sahiha j. 4, uk. 262.

75

Page 76: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

vitabu vyake vilivyokifanyia mukhtasari. Na baba mtu ni katika wapokezi wa Al-Bukhari na Muslim……………………….

Kisha hakika ya Al-Albani kasema katika uk. 432 wa juzuu hio hio tulioitaja kuhusu sanad ya Hadithi ilioko huko:

Ninasema:269 ‘Na sanad hii wapokezi wake ni wenye kuaminika nao ni wenye kujulikana isipokuwa Abu Ya’aqub, na Abdul-Wahid bin Ziyad kamwita “Abdallah” na akataja kwamba yeye ni babu yake kama unavyoona, nami sikumjua.270

Hayo ndio maneno yake, na kasahau kwamba kabla kidogo alisema kwamba hio ni tas-hif. Kisha kauli yake (Al-Albani aliposema) “Katika isnad yake kuna ‘Abdullah, ni tas-hif nyengine, na sahihi ni kuwa (jina lake ni) “Abdul-Rahman” ikiwa hana majina mawili.

38) Hadithi: Watu watatu sala zao hazikubaliwi

Ameitaja Al-Albani katika Sahiha yake Hadithi fulani na lafdhi yake – kwa mujibu wa alivyoitaja Al-Albani -:

“ ... تويز ولم جنازة صلى ورجل صالة منهم تقبل ال ثالثةThalatun laa tuqbalu minhum salat….wa

rajulun salla jinaza walam tuuyiz”.

Na akatia maelezo (Al-Albani) ya neno tuuyiz, akasema: “Na wala haukunibainikia usahihi (wa neno hilo)”.271 Hivyo ndivyo alivyosema maskini huyu ambaye hajui kinachotoka kichwani mwake. Na lau alirejea kitabu chake (mwenyewe) Sahihu Al-Targhib wa Al-Tarhib272 angeliona kwamba yeye mwenyewe kaitaja huko kwa lafdhi yu-umar يؤمر, Fallahu Al-Musta’aan.273

39) Hadithi: Qur-ani imeteremshwa kwa herufi saba

269 - Msemaji ni Al-Albani. 270 -Al-Albani Al-Sahiha j. 1, uk. 427-428. 271 -Al-Albani Al-Sahiha j. 2, uk. 254. 272 - J. 1, uk. 195. 273 - Elewa kwamba Al-Albani alijirekebisha baadae katika baadhi ya makosa haya. Anasema ‘Asili ilikuwa ni tuuyiz, nalo ni (neno) lisilo na maana, na marekebisho ni kutoka katika Al-Targhib cha Al-Mundhiri, j. 1, uk. 171. Tazama Al-Sahiha j. 2, uk. 250, maelezo ya Hadithi na. 650, chapa ya pili 1995-1415 A.H., Daru Al-Ma’aarif.

76

Page 77: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Anasema (Al-Albani) katika maelezo yake juu ya kitabu Mishkaatul Masaabiih kuhusu Hadithi na. 238 nayo ni Hadithi: “Imeteremshwa Qur-ani kwa herufi saba; kila Aya ina nje na ndani; na kila moja ina mpaka na mwanzo” ambayo mwenye kitabu Al-Mishkaat kainasibisha kwa Al-Baghawi katika Sharhu Al-Sunna. Kasema (Al-Albani):

Na itazamwe ni sehemu gani kaipokea katika Sharhu Al-Sunna, hakika ya mimi nimeirejea katika (mlango wa) elimu na katika (mlango wa) fadhila za Qur-ani, wala sikuiona ndani yake.274

Hivyo ndivyo alivyosema (Al-Albani), ilhali Hadithi imo katika Sharhu Al-Sunna.275 Na Hadithi hio kaipokea pia Abu Ya’ala, katika musnad276 wake na Al-Bazzar na Al-Tabarani katika Al-Awsat kama ilivyo katika Al-Majma’u.277

40) Hadithi: Milango ya mbingu hufunguliwa nusu ya usiku

Anasema (Al-Albani) katika Sahiha yake kuhusu Hadithi: “Inafunguliwa milango ya mbingu nusu ya usiku, basi hunadi mwenye kunadi: je kuna mwenye kuomba ili apokelewe (maombi yake)”. Baada ya maelezo (alisema Al-Albani):

Tanbih! Al-Suyuti kainasibisha (Hadithi hii) – katika Al-Jami’u Al-Saghir na Al-Kabir na akaifuatisha katika Al-Fat-hu Al-Kabir – kwa Al-Tabarani katika Al-Mu’ujamu Al-Kabir, nalo ni kosa…. 278.

Hivyo ndivyo alivyosema (Al-Albani), ilhali Hadithi imo katika Al-Mu’ujamu Al-Kabir.279

Hii ni mifano arubaini katika jumla ya mifano khamsini iliotajwa na Al-Imamu Al-Qannubi katika makosa ya Sheikh Al-Albani. Ama kuhusu 274 - Al-Albani maelezo ya Hadithi na. 238 katika Al-Mishkaa. Tazama jinsi mtu anavyojieleza mwenyewe kwamba yeye si mtu wa elimu hii. Vipi mtu mutakhassis (specialist) wa fani fulani anasoma mlango tu ilhali wakati mwengine wasimulizi huisimulia riwaya si katika milango yake. Tena analifanya hilo katika vitabu mashuhuri, alau ingelikuwa ni vile vitabu visivyo mashuhuri! Alipojieleza zaidi ni pale alipotwambia kwamba yeye karejea “Yaliyomo” (table of contents) ili kujua kwamba riwaya fulani imo katika kitabu au Haimo!275 - Al-Baghawi Sharhu Al-Sunna j. 1, uk. 262, katika mlango wa Al-Khusuma Fii Al-Qur-ani. 276 - Hadithi na. 5147, 5403. 277 - J. 7, uk. 152. 278 - Al-Albani Al-Sahiha j. 3, uk. 62. 279 - Al-Tabarani Al-Kabir j. 9, uk. 51.

77

Page 78: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

tanaqudhat (kujigonga) kwa Sheikh Al-Albani katika kusahihisha Hadithi na kudhoofisha, basi fas-al walaa haraj! Sheikh Hasan bin Ali Al-Saqqaf kazikusanya sehemu hizo ambazo Al-Albani kajigonga huku akisema hivi na kule akisema vile katika majalada makubwa. Ama wafuasi wa Al-Albani wanamtetea kwamba hizo ni Taraju’at (kuwacha rai ya kwanza na kuchukua rai nyengine) za Al-Albani: si tanaqudhat (kujigonga). Na’am! Kweli inawezekana sehemu nyengine zikawa hivyo, lakini sehemu nyengine haiwezekani kuwa hivyo. Na hata ikiwa ni Taraju’at (kuwacha rai ya kwanza na kuchukua rai nyengine) kama wanavyodai wao, basi pia hilo linaonesha uchache wake wa maarifa katika elimu hii ya Hadithi, kwani mtu kufika hadi ya kusahihisha Hadithi au kudhoofisha Hadithi kwa mamia bila ya kuhakikisha kwanza sanad zake, huo ni udhaifu mkubwa, unaomfanya mtu kauli yake isizingatiwe katika uwanja huu.

Katika kitabu alichokiita Taraju’at Al-’Allama Al-Albani, Abu Hasan Al-Sheikh kakusanya idadi ya Hadithi 621 katika juzuu mbili ambapo Sheikh Al-Albani kaipa Hadithi moja hukumu tafauti. Tunasema hata kama ni taraju’at basi kwa idadi ya Hadithi hizo ni dosari kubwa kwa mtu anayejiita muhaddith na madhehebu yake ikamzingatia kuwa ni Imamu wa fani hio!

Lakini, kama tulivyosema, nyengine katika Hadithi hizi ni tanaqudhat (kujigonga). Soma mifano miwili mitatu:

1) Hadithi isemayo: “Majirani wangapi watawaning’inia majirani zao siku ya kiama watasema: ‘E Mola wangu huyu kaufunga mlango wake akaninyima wema wake”. Anasema Al-Albani kuhusu Hadithi hii: “Dhaifu”.280 Kisha kuhusu Hadithi hii Al-Albani akasema: “Hasan lighayrih”.281

2) Hadithi isemayo: “Mama yangu kafa, je ni sadaka gani ilio bora?” Akasema (Mtume s.a.w.): “Maji”. Basi akamchimbia kisima”. Anasema Al-Albani katika Al-Mishkaa: “Isnad yake ni dhaifu”. Na Al-Albani huyo huyo anasema katika Sahih Al-Targhib kwamba ni Hasan lighayrih”282 na akaitaja pia katika Sahih Ibn Maja na Sahih Al-Nasai.

280 - Al-Albani Dhaifu Al-Jaami’i na. 4268, imenukuliwa na Abu Hasan Al-Sheikh Taraju’at Al-Albani j. 2, uk. 246. na. 411. 281 - Al-Albani Sahihu Al-Targhib na. 2564; Sahihu Al-Adab Al-Mufrad na. 81, imenukuliwa na Abu Hasan Al-Sheikh Taraju’at Al-Albani j. 2, uk. 246. na. 412. 282 - Yamenukuliwa na Abu Hasan Al-Sheikh Taraju’at Al-Albani j. 2, uk. 248. na. 412.

78

Page 79: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

3) Hadithi isemayo: “Hija ni jihadi ya kila dhaifu”. Hadithi hii ni “Dhaifu” katika baadhi ya vitabu vya Al-Abani na ni sahihi katika vitabu vyengine.283

4) Hadithi isemayo: “ بالنية إال عمل وال حسبة عن إال أجر ”ال(Hakuna malipo isipokuwa (kitendo kifanywe) kutokana na ikhlas wala hakuna (kusihi au kukubaliwa kwa) matendo ila kwa nia”. Anasema Al-Albani kuhusu Hadithi kwamba ni “Dhaifu”.284 Kisha Al-Albani akamjibu Al-Albani akasema katika kitabu chake chengine: “Lakini Hadithi (hii) ni sahihi yenyewe”.285 Na bora lau alisema “Sahihu lighairihi” au “Hasanun lighairihi” tungelisema labda njia ya pili yenye kuipa nguvu ya kwanza alikuwa hajaitafuta katika faharis (yaliyomo au table of contents) ya vitabu vya Hadithi. Lakini kusema kuwa “yenyewe ni sahihi” halafu sehemu nyengine ikawa “ni dhaifu”, huku ni kujigonga kwa wazi!

5) Hadithi isemayo: “Jino la kafiri siku ya kiama ni kama (mlima wa) Uhud”. Anasema Al-Albani “Isnad yake ni dhaifu”.286 Lakini anasema kuhusu Hadithi hio hio: “Ni hasan”.287

6) Hadithi isemayo: “Mmoja wenu akitawadha kisha akatoka kwenda Msikitini, basi asitie vidole vyake chini ya vidole vyengine (asivifungamamishe), kwani yeye (wakati huo) anakuwa tayari yumo katika Sala”. Anasema Al-Albani kuhusu Hadithi hii: “Ni dhaifu, kwani Abu Thumama hajulikani”.288 Lakini Hadithi hio hio ni sahihi katika Sahihu Abi Dawud289 na katika Sahihu Al-Jaami’i,290 anasema Al-Albani: “Ni Hadithi sahihi”.291

7) Hadithi isemayo: “Mimi ni Muhammad bin ‘Abdil-Muttalib. Hakika ya Allah kaumba viumbe akanifanya mimi katika bora wao………”. Anasema Al-Albani katika Al-Mishkaa: “Ni Hadithi sahihi”.292 Lakini katika Dha’ifu Al-Tirmidhi293 na katika Al-Silsila Al-Dha’ifa,294 anasema kuhusu Hadithi hio kwamba ni “Dhaifu”.295

283 - Al-Taraju’at j. 2, uk. 249. 284 - Al-Albani Dhaifu Al-Jaami’i Hadithi na. 6170. Nukulu kutoka kwa Abu Al-Hasan Taraju’at Al-Albani j. 2, uk. 250. 285 - Al-Albani Al-Sahiha j. 5, uk. 538, Hadithi na. 2415. 286 - Al-Albani Al-Mishkaa Hadithi na. 5674. 287 - Al-Albani Al-Sahiha j. 3, uk. 94-96, Hadithi na. 1105. 288 - Al-Albani Sahihu Ibn Khuzaima Hadithi na. 441, na ikanukuliwa na Abu Al-Hasan katika Taraju’atu Al-Albani j. 2, uk. 257, Hadithi na. 425. 289 - Hadithi na. 562. 290 - Hadithi na. 442. 291 - Rejea Abu Al-Hasan Taraju’at Al-Albani j. 2, uk. 257, Hadithi na. 425. 292 - Al-Albani Al-Mishkaa Hadithi na. 5757. 293 - Al-Albani Dhaifu Al-Tirmidhi Hadithi na. 3608. 294 - Al-Albani Al-Dhaifa Hadithi na. 3073. 295 - Rejea Taraju’atu Al-Albani j. 2, uk. 202.

79

Page 80: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Kwa ufupi, ni kuwa Al-Albani si mwanachuoni wa Hadithi kamwe tafauti na wanavyodanganywa walala hoi! Al-Albani hajui hata kitu alichokisema mwenyewe: husema kitu kisha ama akajipinga au akakanusha kuwa hajakifanya naye kakifanya kimo katika maandiko yake. Kilichompa jina mtu huyu ni kuweko kwake katika Madhehebu yenye pesa na iliopo katika sehemu nyeti – anatangazwa. Al-Albani hajui hata Hadithi zilizomo katika Al-Bukhari na Muslim296 kama utavyoona mifano miwili mitatu inayofuata. Na hii mifano saba nilioinukuu hapa ni mifano michache tu: nina mifano 621 ya Hadithi walizozikusanya wenyewe Mawahabi ambapo Al-Albani huku anasema vyengine na kule anasema vyengine. Rejea Taraju’atu Al-Albani cha Abu Al-Hasan Muhammad bin Hasan Al-Sheikh ujionee mwenyewe. Na kwa ziada rejea Tanaqudhaatu Al-Albani cha Al-’Allama Al-Sayyid Al-Saqqaf.

Baada ya haya, tunakuulizeni enyi mujiitao Salafiyya, ivo inajuzu mtu huyu kuitwa Imamu wa Hadithi? Na je inajuzu kutegemea udhoofishaji na usahihishaji wa Hadithi unaofanywa na mtu kama huyu? Nasi tunawachalenj Mawahabi watutolee makosa kwa makapu kama haya kutoka katika vitabu vya Al-Imamu Al-Qannubi.

AL-ALBANI HAZIJUI HADITHI ZILIZOMO KATIKA SAHIHU AL-BUKHARI NA SAHIHU MUSLIM!

Kwa kuanzia ni vyema ukajua ewe ndugu msomaji kwamba Sheikh Al-Albani, ambaye waitwao Mawahabi wanadhania kuwa ni mjuzi mkubwa wa elimu ya Hadithi, anaona kwamba haijuzu kunukuu au kwa usahihi zaidi haifai kuinasibisha297 Hadithi na vitabu vyengine vya Hadithi ikiwa Hadithi hio imo katika Sahihu Al-Bukhari au Sahihu Muslim. Na kwa sababu ya uoni wake huo, Sheikh Al-Albani anasema:

296 - Ukiachilia mbali Hadithi zilizomo katika vitabu vyengine vinne na Musnad cha Ahmad na Hadithi zilizomo katika vitabu vyengine visivyotumika sana! 297 - Makusudio ya neno “kuinasibisha” ni kusema kuwa Hadithi hii kaipokea fulani. Kwa mfano, ukisema kaipokea Muslim basi unakuwa umeinasibisha kwake au umeinasibisha naye.

80

Page 81: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Kufanya kasoro katika takhrij 298 ya Hadithi: Na hio ni kuwa Hadithi iwe imo katika Sahihi mbili (Sahihu Al-Bukhari na Sahihu Muslim) au imo katika moja ya hizo, basi mtu ainasibishe Hadithi kwa baadhi ya (wapokezi) wenye vitabu vya Sunna au wengineo katika Maimamu mashuhuri pasina (kuinasibisha Hadithi hio na Sahihi) mbili hizo (ya Al-Bukhari na ya Muslim)…..na yote hayo hayafai kwa watu wa elimu ya Hadithi kwa sababu kuinasibisha Hadithi na Sahihi mbili hizo kunaipa nguvu Hadithi hio….kisha (Sahihi mbili hizo) zinafuatiwa na vitabu vinne vya Sunna299…300

Anaendelea Al-Albani kwa kusema:

Watu wengi wamefanya makosa katika haki ya Hadithi hii….wa pili: Al-Suyuti, hakika yake alipoitaja (Hadithi hio) katika Al-Jaami’u Al-Saghir na Al-Kabir pia, basi kainasibisha kwa Al-Tabarani tu, na huku ni kufanya upungufu uliopindukia, kwani anawafanya (watu) wadhanie kuwa (Hadithi hio) haimo katika Sahihi mbili, vyenginevyo angeliinasibisha kwa hizo (Sahihi mbili).301

Anaendelea Al-Albani:

Wa tatu: Al-Munaawi: hakika yake kasema katika Sherehe yake Faydhu Al-Taqdir: ‘kaashiria mtunzi (Al-Suyuti) kwamba (Hadithi hio) ni sahihi, lakini ukweli hauko hivyo.’….na hili ni kosa kubwa nililoliona kwa Al-Munaawi, na hili limetokana na uchache wa hifadhi yake302 au kutokukumbuka kwamba Hadithi hio imo katika Sahihi mbili.303

Anaendelea Al-Albani kusema kuhusu Sheikh Al-Jaylani aliyekisherehesha kitabu Al-Adabu Al-Mufrad:304

Hususan kuhusu yale yanayohusiana na takhrij ya Hadithi, kama inavyokuja katika maelezo juu yake, kwa hakika yametokea kutoka kwake makosa ya ajabu yanaonesha kwamba hakuwa mwenye kuhifadhi mwenye ujuzi wa elimu hii na misingi yake….kwa hakika umetokea kutoka kwake

298 - Takhrij ya Hadithi maana yake ni kuwataja wapokezi walipokea Hadithi hio, kama Al-Bukhari, Muslim, Ibn Maja n.k. Lihifadhi neno hilo kwani huenda likatumika sana humu. 299 - Sunan Al-Tirmidhi, Sunan Ibn Majah, Sunan Al-Nasai, Sunan Abi Daud. 300 - Al-Albani Sahihu Al-Targhib j, 1, uk. 6.301 - Al-Albani Al-Sahiha j. 5, uk. 292. 302 - Subhana Allah! Ivo mtu kama Al-Albani ambaye hajui alichokitaja mwenyewe katika ukurasa mmoja: juu anasema vyengine chini anasema vyengine, bado anawambia watu kwamba hawana hifadhi! 303 - K.h.j. 304 - Cha Al-Bukhari.

81

Page 82: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

awhaamu (makosa) mazito…..chukua baadhi ya mifano kutoka katika aina tafauti:

Mosi: Hadithi nambari yake ya asili ni 196, yeye kainasibisha kwa Al-Bukhari wala kwake yeye305 hakuna (maneno yanayosema): “Anasema mkeo: ‘Nipe matumizi au niache”. Ilhali (maneno hayo) yamo katika Al-Bukhari yamepokewa kutoka kwa Abu Huraira.

Pili: Hadithi na. 352. Hii kainasibisha kwa wengine pasina Mashekhe wawili (Al-Bukhari na Muslim), nayo imo katika hizo (Sahihi mbili), basi imemfanya kuwa katika makosa (awhamu) makubwa kama munavyoona.306

Anasema Al-Albani akiwajibu baadhi yao:

Kwa hakika kainasibisha (Hadithi hii) kwa Abu Dawud tu, ilhali imo katika Sahihu Al-Bukhari nalo ni kosa lisilosameheka katika fani ya takhrij.307

Hio ni mifano miwili mitatu miongoni mwa mingi yenye kuthibitisha kwamba Al-Albani anaona kwamba haifai kabisa mtu kuinasibisha Hadithi na vitabu vyengine pasina kuinasibisha na Sahihu Al-Bukhari au Sahihu Muslim ikiwa Hadithi hio imo katika Sahihu Al-Bukhari au Sahihu Muslim. Sasa baada ya hayo, soma aliyoyatenda mwenyewe kuhusu baadhi ya Hadithi, jambo ambalo linathibitisha kwamba hata Hadithi zilizomo katika Al-Bukhari hazijui:

1) Anasema katika maelezo yake juu ya Sahihu Al-Jaami’i Al-Saghir kuhusu Hadithi isemayo: “Ummul Kitabi (Alhamdu) ndio (Aya) saba zenye kukaririwa na (ndio) Qur-ani Tukufu”.308 Anasema Al-Albani: “Kwa hakika (Hadithi hio) ina asili kutoka kwa wengine pasina Al-Bukhari kutoka kwa Abu Huraira”.309 Hivyo ndivyo alivyosema Al-Albani, ilhali Hadithi imo katika Al-Bukhari.310

2) Anasema kuhusu Hadithi isemayo: “Hakika ya dunia ni nzuri, tamu basi waogopeni wanawake kwani fitna ya mwanzo ya wana wa Israili ilikuwa katika wanawake”. Anasema Al-Albani kuhusu

305 - Kwa Sheikh Al-Jaylani, yaani katika sherehe yake maneno yasemayo: “Anasema mkeo: ‘Nipe matumizi au niache”, hakuyatia ilhali ni sehemu ya Hadithi. 306 - Al-Albani Sahihu Al-Adabi Al-Mufrad uk. 11. 307 - Al-Albani Sahihu Al-Targhib uk. 24. 308 - Yaani Alhamdu ndio iliokusudiwa katika Aya ya 87 ya Sura ya15, inayosema: “Na kwa hakika tumekupa (Aya) saba zenye kukaririwa na Qur-ani Tukufu”. 309 - Maelezo ya Al-Albani katika Sahihu Al-Jaami’i Al-Saghir j. 1, uk. 440. 310 - Tazama Al-Bukhari Al-Sahih Hadithi na. 4704.

82

Page 83: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Hadithi hio: “Kaipokea Ahmad katika Al-Musnad311 kwa njia ya Abu Nadhra kutoka kwa Abu Said Al-Khudri kutoka kwa Mtume (s.a.w.) kisha akaitaja (Hadithi hio). Ninasema:312 “Na isnad yake ni sahihi kwa mujibu wa masharti ya Muslim”.313 Hivyo ndivyo alivyosema Al-Albani, ilhali Hadithi hio ya Abu Said imo katika Sahihu Muslim kwa njia ya Abu Said.314

3) Kuhusu Hadithi isemayo: “Kwayo utapata ngamia mia saba wenye kuvishwa hatamu katika pepo”. Anasema Al-Albani kuhusu Hadithi hii: “Kaipokea Abu Nu’aim katika Al-Hilya315 kutoka kwa Ibn Mas’uud”.316 Hivyo ndivyo alivyosema Al-Albani pamoja na kuwa Hadithi hio imo katika Sahihu Muslim317 na wakaipokea wengine miongoni mwa Maimamu wa Hadithi. TENA HADITHI YENYEWE NI KWA NJIA YA ABU MAS’UD: SI IBN MAS’UD KAMA ALIVYODAI, wala hakuna mazingatio kwamba katika Hilya iko namna hio kwani hilo ni kosa kabisa.

4) Hadithi inayosema: “Musifunge siku ya Ijumaa, isipokuwa muwe mumefunga siku kabla yake au siku baada yake”. Anasema Al-Albani kuhusu Hadithi hii kwamba kaipokea: Al-Tirmidhi, Ibn Maja, Ahmad na Al-Tahawi.318 Ilhali Hadithi hio imesimuliwa na Al-Imamu Al-Bukhari katika Sahihu319 yake na lafdhi yake ni: “Asifunge mmoja wenu siku ya Ijumaa ila siku kabla yake au baada yake”. Na pia akaipokea Al-Imamu Muslim.320

5) Hadithi isemayo: “Nimeamrishwa nipigane na watu mpaka wataposhuhudia kwamba hakuna Mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah….”. Anasema Al-Albani kuhusu Hadithi hii: “Muttafaqun ‘alaih (imepokewa na Al-Bukhari na Muslim) kutoka kwa Ibn Abbaas”.321 Hivyo ndivyo alivyosema Al-Albani, na wala hali haiko hivyo alivyodai yeye Al-Albani, kwani Hadithi hii hawakuipokea Al-Bukhari na Muslim wala mmoja wao kutoka kwa

311 - J. 3, uk. 22. 312 - Msemaji ni Al-Albani. 313 - Al-Albani Al-Sahiha j. 2, uk. 613. 314 - Tazama Muslim Sahihu Muslim Hadithi na. 2742. 315 - J. 8, uk. 116. 316 - Al-Albani Al-Sahiha j. 2, uk. 227. 317 - Tazama Muslim Sahihu Muslim Hadithi na. 1892. 318 - Al-Albani Al-Sahiha j. 2, uk. 713. Utanabahisho: katika chapa ya pili j. 2, uk. 675, Al-Albani kafanya marekebisho ya takhrij ya Hadithi hii na akasema: “Kaipokea Al-Bukhari na Muslim pia…”.319 - Al-Bukhari Al-Sahihu Hadithi na. 1985. 320 - Muslim Al-Sahih Hadithi na. 1144.321 - Maelezo ya Al-Albani katika Sharhu ‘Aqiidati Al-Tahaawiyya alipokuwa akiizungumzia Hadithi hio.

83

Page 84: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Ibn Abbaas kamwe,322 bali kutoka kwake (Ibn ‘Abbaas) kaipokea Al-Tabarani katika Al-Kabir.323

6) Hadithi isemayo: “Allah akuongezee hima, wala usirejee (kufanya tena)”. Anasema Al-Albani kuhusu Hadithi hii: “Na isnad yake ni sahihi kwa mujibu wa masharti ya Al-Bukhari na Muslim, na asili yake ni katika Al-Bukhari”.324 Hivyo ndivyo alivyosema Al-Albani ilhali Hadithi hio kwa matamshi hayo hayo kamili imo katika Sahihu Al-Bukhari.325

7) Hadithi inayosema: “Allah kamuumba Adam kwa sura yake urefu wake ni dhiraa sitini”. Anasema Al-Albani326 kuhusu Hadithi hii: “Kaipokea Ahmad327 …na akaipokea ‘Abdullah bin Al-Imami Ahmad katika Kitabu Sunna.328 Hivyo ndivyo alivyosema Al-Albani ilhali Hadithi hio imo katika Sahihu Al-Bukhari329 na pia ikapokewa na Muslim.330

8) Hadithi isemayo: “Atayeniona mimi usingizini basi kana kwamba kaniona akiwa macho, hakika ya shetani hawezi kujifananisha na mimi”. Al-Albani kainasibisha Hadithi hii kwa Ibn Maja331 na Ibn Hibbaan332 kutoka kwa Abu Juhaifa kutoka kwa baba yake kutoka kwa Mtume (s.a.w.).333 Kisha akasema Al-Albani: “Kaitaja mwenye kitabu Mukhtasaru Al-Mishkaa nambari 118, kutoka kwa Abu Huraira”. Hivyo ndivyo alivyosema Al-Albani, ilhali kwake yeye (mwenye kitabu Mukhtasaru Al-Mishkaa) Hadithi hio si kutoka kwa Abu Huraira bali ni kutoka kwa Abu Juhaifa……... Na Hadithi hio ina Shaahid kwa njia ya ‘Abdullahi bin ‘Amri kutoka kwa Mtume (s.a.w.) kaipokea Al-Tabarani katika Al-Kabir kwa isnad ambayo wapokezi wake ni thiqaat (wenye kuaminika) kama alivyosema Al-

322 - Yaani Hadithi hii wameipokea Al-Bukhari na Muslim lakini si kutoka kwa Ibn Abbaas, bali aliyeipokea kutoka kwa Ibn Abbaas ni Al-Tabarani. 323 - Al-Tabarani Al-Kabir Hadithi na. 11487. 324 - Al-Albani Al-Sahiha j. 1, uk. 404. Katika chapa ya pili ni uk. 457. 325 - Al-Bukhari Al-Sahihu Hadithi na. 783. 326 - Al-Albani Al-Sahiha j. 3, uk. 64. 327 - J. 2, uk. 232. 328 - Uk. 186. 329 - Al-Bukhari Al-Sahihu Hadithi na. 6227. 330 - Muslim Sahihu Muslim Hadithi na. 2841. 331 - Al-Sunan j. 4, uk. 390. 332 - Al-Sahih Hadithi na. 1801. 333 - Al-Albani Al-Sahiha j. 3, uk. 277. Katika chapa ya pili ni uk. 5.

84

Page 85: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Haithami.334 Wala hakutaja (Al-Albani) kwamba Hadithi hio kaipokea Al-Bukhari katika Sahihu yake katika sehemu tafauti kutoka kwa Abu Huraira; iliokaribu zaidi na lafdhi hio ni Hadithi na. 6993, lakini hakuna ndani yake neno “فكأنما” (Kana kwamba) bali ni kwa lafdhi: “فسيراني” (Ataniona). Na akaipokea Muslim kwa lafdhi isemayo: “Ataniona akiwa macho au kana kwamba kaniona akiwa macho”.

9) Hadithi isemayo: “Siku za tashriq335 ni siku za kula…”. Kasema Al-Albani kuhusu Hadithi hio: “Kaipokea Al-Tabarani336….Ibn Hibbaan….Ahmad…..na Al-Tahawi kutoka kwa ‘Umar bin Abi Salama kutoka kwa baba yake kutoka kwa Abu Huraira…..na akaipokea Al-Tahaawi kutoka kwa ‘Ali bin Abi Talib na Sa’ad bin Abi Waqaas…nayo pia ni kutoka kwa Nubaisha Al-Hudhali”.337 Hivyo ndivyo alivyosema Al-Albani wala hakusema kwamba Al-Imamu Muslim kaipokea katika Sahihu yake kutoka kwa Nubaisha.338

10) Anasema Al-Albani katika Ir-waau Al-Ghalil: “Nayo ina ushahidi wa Hadithi ya Ibn ‘Umar kutoka kwa Mtume (s.a.w.) kwa lafdhi isemayo: ‘Maumbile ni kukata kucha, kutoa masharubu, na kunyoa sehemu za siri.’ Kaipokea Al-Nasai kwa sanad sahihi kwa mujibu wa masharti ya Muslim, na Ibn Hibbaan akaisahihisha….”339 Hivyo, ndivyo alivyosema Al-Albani wala hakutaja kwamba Hadithi hio imepokewa na Al-Imamu Al-Bukhari.340

Baada ya haya sijui kwamba Sheikh Seif Al-Ghafri na kikundi chake wataendelea kudai kwamba Al-Albani ni Imamu wa Hadithi! Mtu huyu hajui hata Hadithi zilizomo katika vitabu muhimu vyao – Al-Bukhari na Muslim: Hadithi isiokuwemo humo yeye anadai imo; na iliokuwemo humo yeye hajui kama imo na juu ya yote anakosea katika Hadithi na wapokezi ukoseaji ambao hakuufanya yoyote katika wanaojishughulisha na elimu ya Hadithi! Hili linathibitisha ukweli kwamba Al-Albani si mwanachuoni kamwe wa fani hii wala ile kama vitabu vyake vinavyojionesha. Mara ngapi 334 - J. 7, uk. 181. 335 - Siku za tashriq ni tarehe 11-13 za mwezi wa mfunguo tatu. Siku hizi haitakiwi kufunga bali ni siku za kula. 336 - Katika chapa ya pili kasema “Al-Tabari” badala ya Al-Tabarani. Uk. 277, maelezo ya Hadithi na. 1282. 337 - Al-Albani Al-Sahiha j. 3, uk. 5. 338 - Muslim Sahihu Muslim Hadithi na. 1141. 339 - Al-Albani Ir-waau Al-Ghalil j. 1, uk. 112.340 - Al-Bukhari Al-Sahih Hadithi na. 5890.

85

Page 86: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

utaona katika vitabu vyake akisema: “Mpokezi huyu nimetazama katika fahras (yaliyomo au table of contents) sikumuona”. Sasa sijui ni mwanachuoni gani wa Hadithi ambaye anatazama mpokezi katika fahras tu? Mara nyengine utaona katika vitabu vyake akisema: “Nimeirejea Sahihi Muslim au Ibn Maja n.k.” ili kuhakikisha kuwepo kwa Hadithi hio. Ni wazi kwamba huyu mtu alikuwa ni researcher (mpekuzi tu) kama walivyo wanafunzi wengi, vyenginevyo mwanachuoni wa Hadithi hana kawaida hio ya kuwa alazimike kurejea vitabu mashuhuri kama vile vitabu sita! Wangapi katika watu ambao hawajafika daraja ya kuhesabiwa kuwa miongoni mwa wanavyuoni wa Hadithi wamezihifadhi Hadithi za vitabu sita.

Pili: ni kuwa Al-Imamu Al-Qannubi kaweza kututolea makosa hayo machache ya Al-Albani katika makosa yake mengi mno ambayo yametungiwa juzuu kwa juzuu, sasa kilichobaki tukuachieni nyinyi uwanja, Sheikh Seif Al-Ghafri pamoja na Kasim Mafuta, na Abu Hashim Al-Musawi na Abdullah Muhsin, tunakuachieni uwanja mututolee makosa kama hayo katika vitabu vya Al-Qannubi. Hususan ukizingatia maneno ya Sheikh Seif aliposema:

Na vilevile Qannubi si mwenye elimu ya vitendea kazi (Qawaid) vya elimu za waislamu kama somo la hadithi na ala zake na usuli na misingi ya fiqhi na lugha ya waarabu, lakini ni shujaa asiye na uwoga wala aibu na ndio maana utakuta mara nyingi hutoa hukumu juu ya hadithi kutokana na ushujaa wake mfano;- anasema kwamba hadithi ambazo zimepokewa zenye kuifasiri aya ya 22 na ya 23 za surat Al-Qiyamah ni dhaifu na za uwongo na Juma Al-Mazrui akamfuata kiongozi wake Qannubi na ilhali hadithi hizo zote zilizokuja kutafsiri aya hizo ni Mutawatir341 kwa mujibu wa majio yake na kwa mujibu wa ushuhuda wa wanazuoni wa somo la hadithi,342 pia Qannubi kutokana na kutoelewa somo hili utakuta anamtia ila (dosari) mpokezi wa hadithi pasina kuielewa ila ile kwamba haiwi hadithi ya mpokezi yule ni dhaifu, mfano amemwita imamu Zuhri kwamba ni Mudalis….

Sasa, baada ya hayo, nakuachia kazi ewe Sheikh Seif ututhibitishie:1) Ni katika kitabu gani Al-Qannubi kenda kinyume na kanuni za

kiusuli, ili maneno yako uliposema: “Na vilevile Qannubi si mwenye elimu ya vitendea kazi (Qawaid) vya elimu za waislamu kama somo la hadithi na ala zake na usuli” yawe sahihi. Tafadhali tupe ushahidi juu ya hilo.

341 - Tuoneshe utawatir wa Hadithi hizo na sisi tuko tayari kuifuata haki popote pale ilipo. 342 - Wanazuoni gani hao? Si wale wale wenye itikadi ya kumuona Mungu?! Sasa itikadi yao wao itakuwa hoja kwa walimwengu?

86

Page 87: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

2) Ni katika kitabu gani Al-Qannubi kenda kinyume na misingi ya fiqhi (Al-Qawaa’idu Al-Fiqhiyya) iliokubalika. Tafadhali tunukulie alioyasema, utupe jina la kitabu na ukurasa na utupe maelezo yako yatayoweza kutubainishia kosa liko wapi, ili usijiweke katika jumla ya wale wenye kusema kitu tu kama vile watu wa mitaani; nawe ni mtu wa elimu.

3) Wapi Al-Qannubi kenda kinyume na lugha ya Kiarabu katika vitabu vyake? Tafadhali tupe nukulu ili tupate kuujua ukweli wako na kujua makosa ya Al-Qannubi ili tuyaepuke.

4) Unasema: “Qannubi kutokana na kutoelewa somo hili utakuta anamtia ila (dosari) mpokezi wa hadithi pasina kuielewa ila ile kwamba haiwi hadithi ya mpokezi yule ni dhaifu, mfano amemwita imamu Zuhri kwamba ni Mudalis”. Mwisho wa kunukuu. Ninasema: Tafadhali tusaidie kutupatia nukulu ya alioyasema Al-Qannubi juu ya haya ulioyasema hapa, utunukulie hoja zake na utupe jawabu yako ili tupate kuujua ukweli wako.

5) Tunakusubiri ututhibitishie madai yako kwamba Hadithi zilizokuja kuifasiri Aya ya Suratul Qiyaama si za uwongo bali ni mutawaatir. Tafadhali tuthibitishie utawaatir wa Hadithi hizo nasi tupo tayari kuikubali haki popote pale tutapoikuta. Ama waliyoyasema fulani na fulani, hio si hoja kwani fulani na fulani hao si ma’asumin, hususan nawe na Kasim Mafuta munaona kuwa mimi nawafuata Mashekhe wangu tu: sifanyi tahqiq. Sasa nanyi nipeni tahqiq zenu juu ya riwaya hizo ili musije mukawa kama mimi – mukawafuata Mashekhe wenu tu. Ama fulani na fulani hapa si mahala pao, kwani Hadithi ngapi za uwongo hadi leo hii munazitolea hoja kwa kufuata matamanio ya nafsi zenu. Hii riwaya ya Ibn Saba-a haina sanad yoyote ile iliothibiti: sanad zake zote ni za waongo, na hadi leo hii munaitumia kuwadanganyia watu! Kwa hivyo, hoja – hususan katika uwanja wa mjadala – si fulani kanena bali ni ushahidi sahihi. Kwa hivyo, nakuomba utupatie ushahidi wa kielimu ili mioyo yetu itulie kwamba Hadithi hio ni mutawaatir. Vyenginevyo, nakwambia kwamba riwaya zenye sanad sahihi kutoka kwa Al-Salafu Al-Salih zimesema kwa uwazi kwamba maana ya Aya hio ni kungojea rehema ya Allah. Tutakuthibitishia hilo tukifika mahala pake.

Baada ya hayo, sasa ni vyema kukujuvya vifungu vyengine ambavyo vinastahiki kujadiliwa katika maneno ya Sh. Seif Al-Ghafri. Nakutajia hapa kama ni kumbukumbu yako ili uweze kuviweka alama katika akili yako.

VIFUNGU VYENGINE VYA KUJADILIWA KATIKA MANENO YA SEIF AL-GHAFRI

87

Page 88: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

KIFUNGU CHA KWANZA

Sheikh Seif Al-Ghafri – kama mulivyoona – kasema maneno mengi, lakini kama ulivyojionea mwenyewe kwamba mengi ya hayo hayastahiki kujibiwa kwani maneno yenyewe yanatosha kuonesha yeye ni mtu wa aina gani. Nilikuwa najiuliza huyu mtu alikuwa hadhiri alipoandika maneno haya au alikuwa na matatizo ya nafsi? Kwa hivyo, mengine ni bora tumuachie Allah mwenyewe atahukumu baina ya waja wake, naye ni mbora wa wenye kuhukumu. Lakini ningependa kukuwekea hapa vifungu viwili ambavyo tutavijadili katika sehemu zake:

Anasema Sheikh Seif:

….Lakini yeye katika uibadhi wake Imamu wake aitwae Abuu Ubaidah Muslim Ibni Abi Karimah yeye ndiye Majhuli tena ni Majhulil-Ayn, mtu huyu ni kigano.

Hayo ndio maneno yake! Sasa sijui huyu mtu hasomi isipokuwa Minhaju Al-Sunna cha Ibn Taymiyya na Kitabu Al-Sunna kilichozuliwa na kubandikwa nacho Ibn Ahmad! Sheikh Seif! Mumethibitishiwa vya kutosha nani na nani katika wanavyuoni wa Kisunni, Kishia, Kimu’utazila na wengineo ambao wamemtaja Al-Imamu Abu ‘Ubaida (r.a.). Sasa sijui maandiko hayo hayakukufika au unasema kitu kwa chuki na kasumba? Chuki haitokufikisha mahala, bali hata usiyempenda mpe haki yake huo ndio ucha Mungu na huko ndiko kufuata Sunna na ndio kufuata Al-Salafu Al-Salih. Katika juzuu ya pili ya kitabu hiki in shaa Allah nitakupa ushahidi wa kutosha wa wanavyuoni wa Kiibadhi waliomtaja Abu ‘Ubaida katika kila karne hadi kufikia leo. Kama nitavyokutajia Maimamu wa Kisunni ambao wamemtaja Al-Imamu Abu ‘Ubaida.

KIFUNGU CHA PILIAnasema Sheikh Seif:

..Na pia miongoni mwao hao ni pote la Muutazilah kwani wao ndio wanaopinga sana kuonekana kwa Mwenyezi Mungu sub’haanahu wata’alaa kwani pote hili elimu yao yote imejengeka juu ya misingi ya mijadala ambayo asili yake ni vipimo vilivyo juu ya kufananisha kisichopo kwa kilicho kuwepo na miongoni mwa maigizo ya Qannubi ni pote la Jahmiyyah, Baatiniyya, Mashia Imamiyyah ndio maana utayakuta maandishi yao yote juu ya kutoonekana Mwenyezi Mungu sub’haanahu wata’alaa wanayanukuu kwa mwana matamanio mkubwa adui wa Mwenyezi Mungu sub’haanahu wata’alaa Abdul Jabbar al-Muutazili kwenye kitabu chake almughni, hasa

88

Page 89: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

katika zile hoja za kiakili alizozitaja Alkhalili kama alivyomnukuu Juma Mazrui katika kitabu chake Al-Haqu Addamigh ukurasa 67, kwamba kuona kwa macho ni kuingia sura.

Ninasema: Hebu tueleze vipi Mu’utazila wamekuwa na vipimo vilivyo juu ya kufananisha kisichopo kwa kilicho kuwepo? Sheikh Seif mlango huu ukiufungua ubaya wake utakurudieni nyinyi kwani lau tutakukusanyieni kauli za wanavyuoni wenu juu ya kufanya kwao Qiyas cha Allah na viumbe, basi unaweza kuandika vitabu. Kwa hali yoyote ile, maudhui hii sehemu yake ni juzuu ya nne ya kitabu hiki. Nitayanukuu maneno yako haya na kukubainishia kile ambacho hujakifahamu au ambacho hukitaki.

MUKHTASARI NA NUKTA MUHIMU

1) Tulichokijadili hapa ni maneno ya ndugu yetu Sheikh Seif Al-Ghafri.

2) Katika maelezo yake kataja mambo kadha wa kadha ambayo aghlabu yake hayastahiki kujadiliwa kamwe.

3) Miongoni mwa aliodai ni:a) Suala la kukosea kwangu katika kuyatamka baadhi ya majina

ya baadhi ya wapokezi.343

b) Nimemthibitishia kwamba tatizo hili lilikuwa kwa wakuu wetu zaidi hata kuliko kwangu mimi. Al-Bukhari – kama ulivyoona – katolewa makosa 74 mfululizo juu ya maudhui hii. Na vivyo hivyo, Maimamu wengine wakubwa sana ambao mimi na Sheikh Seif Al-Ghafri hatuwaoni hata vumbi lao.

343 - Elewa kwamba aghlabu ya majina haya nilikuwa tayari nimeyaona na nakusudia kuyarekebisha katika chapa ya pili na mengine nilikwishakuoneshwa na baadhi ya Sahibu zangu.

89

Page 90: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

c) Ibadhi ni Khawarij. Hili tutalieleza katika juzuu yake ambapo na mimi nitadai kwamba Mawahabi ndio Khawaarij.

d) Wao (yaani Mawahabi) ndio Ahlu Sunna. Na hili ni dai ambalo kila mmoja analidai, hata Kadiani wanasema kwamba wao ni Sunni.

4) Mwanachuoni wa Kiibadhi, Al-Qannubi, hajui:a) Lugha ya Kiarabu. Lakini Sheikh Seif hakutupa hata mfano

mmoja wa wapi Al-Qannubi kenda kinyume na kanuni za lugha. Wakati Yeye mwenyewe Sh. Seif Al-Ghafiri kakibariki kitabu cha Kasim Mafuta kilichojaa makosa yakiwemo makosa ya lugha ya Kiarabu kama nilivyoashiria katika utangulizi na nitavyokubainishia kwa ufafanuzi nikifika sehemu zake. Ni wazi kwamba huyu aliyewatoa watu makosa bila ya hoja yeye ndiye asiyejua lugha ya Kiarabu, vyenginevyo asingelikibariki kitabu hicho chenye makosa.

b) Al-Qawaaidu Al-Fiqhiyya (misingi ya fiqhi). Lakini Sheikh Seif hakutupa hata mfano mmoja wa wapi Al-Qannubi kafanya makosa katika misingi hio iliokubalika ili akaweza kumkinaisha msomaji.

c) Usulul-Fiqhi. 344 Pia Sheikh Seif hakutupa hata mfano mmoja wa wapi Al-Qannubi kafanya makosa katika fani hio.

d) Elimu ya Hadithi! Pia Sh. Seif hakutunukulia kauli yoyote ya Al-Qannubi kutoka katika vitabu vyake kisha akatubainishia kosa liko wapi.

5) Imamu wa Kiibadhi, Abu ‘Ubaida Muslim ni kigano (hajulikani). Hili linaonesha kwamba huyu Seif kenda kule Al-Yaman kusoma ta’assub (kasumba), na kwamba yeye hasomi ila yalioandikwa na Ibn Taymiyya na Ibn Al-Qayyim! Nitakuthibitishieni kwa urefu nani na nani kamtaja Imamu huyo ili mupate kumjua huyu Seif Al-Ghafri ni mtu wa aina gani.

6) Jengine tulilolijadili kwa urefu zaidi ni suala la baadhi ya makosa ya yule munayemwita kuwa ni Imamu wa Hadithi, yaani Al-Albani, katika elimu hii ya Hadithi. Sisi tumemthibitishia vya kutosha kwamba Al-Albani hajui hata Hadithi zilizomo katika Al-Bukhari na Muslim, wala hawajui wapokezi hata waliomo katika Tahdhibu Al-Tahdhib. Bali kitu alichokiandika mwenyewe katika ukurasa mmoja basi alichokiandika juu ya ukurasa huo chini hakikumbuki tena! Na kajigonga katika Hadithi hazipungui mia sita au zaidi!

344 - Na lau Seif angelijua jinsi Al-Qannubi alivyozama katika fani hii, basi asingelimfananisha na kiumbe yoyote miongoni mwa wale waliosifika kwa fani hii kama vile Al-Amidi na waliomfano wake. Bali angelimwita Al-Qannubi kuwa ni Imamu wa wana usuli.

90

Page 91: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Baada ya haya, itakubainikia kwamba mtu huyu, Seif Al-Ghafri, hakusema lolote la maana, basi kasumba yake na chuki zake zimemfanya aropokwe tu! Wallahu Al-Musta’aa.

SURA YA PILIFIKRA NA ITIKADI ZA KIWAHABI

MUNGU NI KIWILIWILI SI KAMA VIWILIWILI!

Wanaoitwa Mawahabi au wanaojiita Salafiyya au Ansaru Sunna kwa asili ni sehemu ya madhehebu ya Hanbal. Wanavyuoni wa madhehebu hii ya Hanbal wamegawika makundi mawili makubwa kuhusu mambo ya itikadi:

1) Kundi moja lina itikadi sawa na Waislamu wengine, yaani ni Ash’ariyya. Hawa wao hawakubaliani na itikadi za kumshabihisha Allah na kiumbe chini ya falsafa ya balkafa.345 Miongoni mwa hawa ni Ibn Al-Jawzi na Ibn Tamimi.

2) Kundi la pili ni lile lililojulikana kwa kumshabihisha Allah na viumbe, wakasema kuwa Allah ana viungo (mkono, miguu, uso, macho n.k.) kisha wakijifurahisha kwa falsafa ya balkafa wakasema: “Lakini si kama tunavyovijua sisi.” Yaani viungo hivyo anavyo

345 - Bila ya mfano!

91

Page 92: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

lakini havifanani na kitu. Kundi hili pia limekuwa maarufu sana kwa kuwatukana, kuwashambulia na kuwakafirisha Waislamu wengine346

kama utavyoona nukulu zao humu. Miongoni mwa hawa ni Ibn Taymiyya na Ibn Al-Qayyim. Mawahabi wao wametokana na hili kundi la pili.

Kabla ya fikra zao hizo za tajsim347 na tashbih348 kuingia katika madhehebu ya Hanbal na baadae kuingia katika Madhehebu ya Kiwahabi, waasisi wakuu wa fikra hizo walikuwa ni baadhi ya wanavyuoni wa Hadithi walioitwa kuwa ni Hashwiyya.349 Wameitwa hivyo kwa sababu walikuwa wakizichukua lafdhi za Hadithi na Aya kwa udhahiri wake tu bila kutazama maana halisi iliokusudiwa.350 Na chimbuko lake, kama alivyoeleze Al-’Allama Muhammad Zahid Al-Kawthari, ni kuwa:

Kikundi cha watu hao (wenye kumuabudu Mungu mwenye viungo na sura ya mtu) walihudhuria katika kikao cha Al-Hasan Al-Basri, na wakazungumza makosa basi (Al-Imamu Al-Hasan) akasema warejesheni hao huko kwenye Hashaa (pembeni) ya majlisi. Basi wakaitwa Hashawiyya.351

Anasema Dr. Al-Zuhaili:

Na inasemwa kwamba wameitwa hivyo, kwa sababu wao ni mujassima kwa kusema kwao: ‘kiwiliwili ni hasho’, kwa maana hii basi wao ni Hashwiyya (si Hashawiyya).352

Jambo jengine ambalo liliwatumbukiza watu hao katika kuwa na itikadi hizo, ni kuzitegemea kwao Hadithi Ahadi353 katika kuthibitisha mambo ya 346 - Na hii ni moja ya bidaa yao kubwa, kisha wanasema kuwa wao wanapiga vita bidaa. Bidaa wanayoipiga vita ni maulidi na khitma, lakini kumwita Muislamu kuwa ni mtu wa bidaa dhalala, kwa kuwa anasoma dua kwa sauti au kwa pamoja baada ya Sala, hio si bidaa dhalala! 347 - Tajsim maana yake ni kumfanya Allah kuwa ni kiwiliwili chenye viungo. 348 - Tashbihi maana yake ni kumfananisha Allah na viumbe. 349 - Kama ‘Uthman bin Said Al-Darimi, Ibn Khuzaima, Ibn Manda, Al-Ajurri, Ibn Batta na wengine. 350 - Kama alivyosema Al-Sha’abi: “Sisi si mafakihi bali ni wapokezi wa Hadithi”. Tazama ‘Uthmaan Al-Daarimi Al-Raddu ‘Alaa Al-Marisi j. 3, uk. 143. 351 - Na pia inajuzu kuita Hashwiyya na ndio aghlabu kwa Waarabu wa leo. Tazama maelezo ya Al-Kawthari katika Al-Saifu Al-Saqiil cha Al-Imamu Al-Subki uk. 14. 352 - Dr. Wahbat Al-Zuhaili Usulu Al-Fiqhi j. 2, 403, maelezo ya chini, chapa ya 3 1426 A.H. 353 - Hadithi ambayo si mutawatir. Na mutawatir ni ile ambayo imepokewa na kundi kubwa katika tabaka zake tatu za awali – Masahaba, wafuasi wao, wafuasi wa wafuasi wa Masahaba. Baada ya hapa Hadithi zilitegemea maandishi. Na kuna masharti mengine

92

Page 93: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

itikadi hata kama Hadithi hizo ni kinyume na akili ya binaadamu wote na ni kinyume na dhahiri au maana ya Qur-ani. Wakati jumhur ya Umma hawazitumii Hadithi kama hizo isipokuwa katika matendo tu: si katika itikadi. Kwani itikadi ni kitu cha yakini wakati Hadith Ahadi hakuna uhakika juu ya kuthibiti kwake, bali kuthibiti kwake ni dhannun raajih (dhana yenye uzito) tu.

Kisha fikra hizo za tajsim zikaingia zaidi katika madhehebu ya Hanbal kwa sababu madhehebu ya Hanbal imeelemea zaidi katika kuchukua elimu kutoka kwa wale wanavyuoni wa Hadithi ambao aghlabu yao hawakuwa mafakihi: bali ni wenye kunukuu lafdhi bila ya kuzifahamu makusudio yake! Na labda mwanachuoni wa mwanzo wa Kihanbal, ambaye ni katika Maimamu adhimu wa Kiwahabi, kuzikumbatia na kuzilingania itikadi hizo ni Abu Ya’ala hata kama tayari walitangulia kabla yake wengine, lakini inaonesha kwamba mchango wake katika kuzilingania itikadi hizo za tajsim ni mkubwa zaidi. Na hii ni kwa sababu ya yale yalionenwa na Ibn Al-Athir kuhusu matokeo ya mwaka 429. Anasema Ibn Al-Athir:

عل العلماء أنكر من ىوفيها كتابه ضمن ما الحنبلي الفراء بن يعلى أبيتعالى �������صف الله ات

بجامع الزاهد القزويني الحسن أبو وحضر التجسم، يعتقد بأنه المشعرةوتك في ��المنصور، لم

كبيرا علوا الظالمون يقول عما الله تعالى ذلك،

Na katika mwaka huo (wa 429) Wanavyuoni walimpinga Abu Ya’ala bin Al-Faraa Al-Hanbali kwa yale alioyatia katika kitabu chake miongoni mwa sifa za Allah Mtukufu zenye kuonesha kwamba yeye anamuitakidi Allah kuwa ni kiwiliwili.354 Na Abu Al-Hasan Al-Qaz-wini alihudhuria hapo katika Jami’u Al-Mansur355 na akazungumza kuhusu hayo. Basi Allah ametakasika mtakasiko mkubwa kutokana na wanayoyasema madhalimu hao.356

Anaendelea Ibn Al-Athir:

الفراء بن الحسين بن محمد يعلى أبو توفي منها رمضان شهر وفيمصنف ... وهو الحنبلي

ambayo yamesemwa na wajuzi kuhusu Hadithi mutawatir. 354 - Na huu ni ushahidi kwamba wanavyuoni walikuwa wakiliona jambo hilo kuwa ni jambo jipya ambalo halikuwepo kabla (bidaa). Ni wazi kwamba fikra za tajsim ni bidaa iliozushwa: haina uhusiano na Al-Salafu Al-Salih wa Umma huu. 355 - Msikiti wa ijumaa unaitwa hivyo Jami’u Al-Mansur. 356 - Ibn Athir Al-Kamil j. 7, uk. 786. Madhalimu wenyewe anaowakusudia Ibn Al-Athir ni Maimamu watangulizi wa Kiwahabi.

93

Page 94: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

التجسيم” “كتاب على يدل أبوابه ترتيب و ، عجيبة بكل فيه أتى الصفاتالله تعالى المحض،

الف : يعلى أبو خري لقد يقول الحنبلي تميمي ابن وكان ذلك، راء��عنالحن خ ��على رية ����ابلة

. الماء يغسلها ال

Na katika mwezi wa Ramadhani katika mwaka huo (wa 458), alikufa Abu Ya’alaa Muhammad bin Al-Husain bin Al-Faraa Al-Hanbali…naye ni mtunzi wa Kitabu Al-Sifat, kila ajabu kaileta humo na (akakipangilia kitabu hicho) mpangilo wa milango yake (ambao) unaonesha kumfanya Allah kuwa na kiwiliwili safi kabisa. Allah katakasika kutokana na hayo. Na alikuwa Ibn Tamimi Al-Hanbali anasema: ‘Abu Ya’alaa Al-Faraa kawaharia Mahanbali uharo ambao maji (yote ya dunia) hayauoshi. 357

Na miongoni mwa mambo aliolaumiwa kwayo kiongozi huyu wa Kihanbali/Kiwahabi ni ibara yake mashuhuri ilionukuliwa na wanavyuoni tafauti ambayo imeonekana kuwa imetokana na kujingikiwa kwake na uhakika na utukufu wa Mwenyezi Mungu. Anasema Al-Sayyid Al-Saqqaf akinukuu kutoka katika kitabu cha Abu Bakr Bin Al-Arabi kiitwacho Al-’Awaasim358 kwamba Abu Ya’ala alikuwa akitajwa Allah, yeye husema:

والعورة اللحية إال ألتزمه فإني شئتم ما ألزموني(Kiungo chochote) munachotaka nilazimisheni (nikiitakidi kuwa Allah anacho, basi) mimi niko tayari kukikubali hicho, isipokuwa ndevu na uchi!359

Ninasema: na maneno hayo pia yamenukuliwa kutoka kwa Dawud Al-Jawaaribi akisema:

ذلك وراء عما واسألوني واللحية الفرج عن اعفونيNisameheni kutokana na uchi na ndevu, yaliobakia yote niulizeni!360

Anasema Al-Shahrastani akimnukuu Al-Jawaaribi huyo:

: ورج يد من وأعضاء جوارح وله ودم ولحم جسم معبوده إن ل���وقالوعي ولسان نين�����ورأس

كالدماء ال ودم كاللحوم ال ولحم كاألجسام ال جسم ذلك ومع وأذنينالص سائر وهو �������وكذلك فات

357 - Ibn Al-Athir Al-Kamil j. 8, uk. 208, katika matokeo ya mwaka 458. Kweli Sheikh! Kwani hadi sasa wengine wanasema Mungu ana sura ya mtu kama utavyoona humu nukulu zao!358 - Ibn Al-’Arabi Al-‘Awaasim j. 2, uk. 283. 359 - Al-Saqqaf Al-Salafiyya Al-Wahaabiyya uk. 60. 360 - Al-Shahrastani Al-Milal j. 1, uk. 117.

94

Page 95: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

: هو قال أنه عنه وحكي شيء يشبهه وال المخلوقات من شيئا يشبه الصدره إلى أعاله من أجوف

قطط شعر وله سوداء وفرة له وأن ذلك سوى ما مصمت

Na akasema (Al-Jawaaribi) kwamba mola wao wanayemuabudu ni kiwiliwili na damu, na ana viungo kuanzia mkono, mguu, kichwa, ulimi, macho mawili, masikio mawili, lakini pamoja na hayo yeye ni kiwiliwili si kama viwiliwili (vyengine) na ni nyama si kama nyama (nyengine) na ni damu si kama damu (nyengine), na halkadhalika sifa nyengine naye hafanani na chochote katika viumbe wala hakuna kitu chenye kufanana naye. Na ikasimuliwa kutoka kwake akisema: ‘yeye (Mungu) ana uwazi kuanzia juu hadi kifuani kwake, na sehemu zilizobakia hazina uwazi na ana mjazo wa nywele nyeusi na ana nywele fupi na za mviringo (curl).361

Naturudi katika maneno ya Abu Ya’ala. Al-Sayyid Al-Saqqaf, baada ya kuyanukuu maneno hayo ya Abu Ya’ala, akasema:

Wamesema baadhi ya Maimamu wa Ahlu Al-haqq: ‘Na hii ni kufuru mbaya na ni kumfanyia Allah Mtukufu mzaha. Na mwenye kuyasema hayo ni mjinga hamjui Allah. Basi huyo hafuatwi wala hatazamwi kamwe…..362

Ama moja ya sababu zilizowapelekea watu hawa kuwa na itikadi hizi ni kile tulichokigusia kabla cha kuchukua maana za juu juu tu za Aya na Hadithi. Na kwa mfumo wao huo wa kuzifasiri Aya na Hadithi kwa namna hio ya kutazama lafdhi bila kutazama maana sahihi inayopatikana kutokana na utaratibu wa lugha ya Kiarabu, wameweza kuthibitisha kwamba Allah ni kiwiliwili chenye viungo na sura ya binaadamu.363 Na kwa sababu hio, utawakuta wanawatetea mujassima (ambao wanamfanya Allah kuwa ni kiwiliwili) na kuwapiga vita wale wawapingao mujassima. Anasema Ibn Taymiyya:

Na hakuna yoyote katika Al-Salaf (watangulizi) aliyemlaumu mtu yoyote kwamba yeye (mtu huyo) ni mujassim (mwenye kusema kuwa Allah ni kiwiliwili). Wala (hakuna) aliyewalaumu mujasima (wenye kusema kuwa Allah ni kiwiliwili). Bali (Al-Salaf) waliwalaumu Al-Jahmiyya ambao waliyakanusha hayo (ya kuwa Allah ni kiwiliwili)”!364……..

Hayo ni maneno ya Ibn Taymiyya! Sasa jiulizeni:

361 - Al-Shahrastani Al-Milal j. 1, uk. 117. 362 - Al-Saqqaf Al-Salafiyya Al-Wahaabiyya uk. 60. 363 - Usistaajabu juu ya hili wala usifanye haraka ushahidi nitakupa humu. 364 - Ibn Taymiyya Bayaanu Talbisi Al-Jahmiyya j. 1, uk. 100.

95

Page 96: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

1) Ni Al-Salaf gani waliomlaumu mtu kwa sababu ya kukataa kuwa Allah ni kiwiliwili?

2) Ni Al-Salaf wa Umma au ni Al-Salaf wa Ibn Taymiyya? 3) Je Al-Salaf walikuwa wakisema kuwa Allah ni kiwiliwili hata

isemwe kuwa waliwalaumu Al-Jahmiyya kwa kuikanusha kwao itikadi hio ya kuwa Allah ni kiwiliwili.

4) Ni wazi kwamba Ibn Taymiyya anatafuta njia ya kutaka kutupandia itikadi hio ya tajsim kwa kuwapachika mzigo huo Al-Salaf!

Anaendelea Ibn Taymiyya kusema:

Bali wanasema (Al-Imamu Ahmad na Maimamu wengine wa Sunna, kwamba) kuzithibitisha maana hizi ni haki zaidi kwa maana ya tajsim (kwa maana ya kumfanya Allah kuwa ni mwenye kiwiliwili) kuliko kuzithibitisha lafdhi zake bila ya (kuthibitisha maana yake).365

Anachokisema Ibn Taymiyya ni kuwa kauli kwamba Allah ni kiwiliwili kwa mujibu wa kile kinachooneshwa na maandiko yenye kusema kuwa Allah ana viungo (mkono, mguu n.k.), ni kauli ilio bora zaidi au ilio karibu zaidi na haki kuliko kukanusha kwamba Allah ni kiwiliwili! Na hayo – kwa mujibu wake – ndio mafunzo ya Al-Imamu Ahmad na wengine katika Maimamu wa Sunna. Kisha akanukuu – kwa kuyakubali – maneno ya baadhi yao, akasema:

Kisha mutakallimun (wenye kuzungumzia mambo ya tauhid kwa hoja za kiakili) miongoni mwa wale wenye kuthibitisha366 (sifa za Mungu, kama mikono, uso n.k.)……wakasema: ‘hakika ya mkono na uso haiwezekani ila itakuwa ni kiwiliwili, basi na mkono wa Allah na uso wake ni hivyo hivyo. Na mwenye kusifika kwa sifa hizi hawi isipokuwa ni kiwiliwili. Basi Mungu ni kiwiliwili si kama viwiliwili (vyengine).367

Anaendelea Ibn Taymiyya kwa kusema:

Na inaeleweka kwamba (kusema) kuwa Allah si kiwiliwili si jambo ambalo maumbile yanalifahamu kwa mantiki (yaani kiakili), wala halifahamiki kwa vitangulizi (hoja) vilivyokaribu na maumbile…..wala hakuna vitangulizi vya wazi walivyoafikiana kuvikubali wale wenye akili

365 - Ibn Taymiyya Bayanu Talbis Al-Jahmiyya j. 1, uk. 93. 366 - Al-Muthbitun au Ahlu Al-Ithbat ni kinyume cha Mu’attila. Jina la kwanza ndilo wanalojipa wale wenye kusema kuwa Allah ana viungo; na jina la pili ndilo wanalowapa wale wenye kupinga itikadi hio.367 - Ibn Taymiyya Bayaanu Talbisi Al-Jahmiyya j. 1, uk. 100-101.

96

Page 97: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

(wanafalsafa);…..na asilimia kubwa ya watu wa ‘ilmul kalam wanayaponda hayo yote na wanasema (kwamba) dalili za uhakika za kiakili zimesimama kinyume na hivyo, na (wanasema) kwamba mwenye kuisimamia nafsi yake hawi isipokuwa ni kiwiliwili. Na inaeleweka kwamba (kauli) hii iko karibi zaidi na maumbile na akili 368 kuliko (kauli) ya mwanzo. 369

Anaendelea Mzee wa Uislamu, Ibn Taymiyya kwa kunena:

Ikiwa itasemwa je unasemaje kuhusu sifa ya kiwiliwili, ni sifa ambayo Sharia imeitaja kwa uwazi au ni sifa ambayo Sharia imeinyamazia? Basi tutasema: hakika yake ni sifa370 ilionyamaziwa. Nayo katika kuithibitisha kwa uwazi katika sharia ipo karibu zaidi kuliko kuikataa, kwani Sharia imetaja kwa uwazi (kuwa Allah ana) uso na (ana) mikono (yake) miwili”.371

Anaendelea kusema:

Na kwa hivyo, wengi katika Waislamu wamemuitakidi Muumba kwamba ni kiwiliwili ambacho hakifanani na kiwiliwili, na Mahanbali na wengi waliowafuata wao wanafuata (kauli) hii.372

Anaendelea:

Ama sababu ya tatu ni kuwa ikiwa (itikadi ya) kiwiliwili itakataliwa kwa uwazi, basi itatokea shaka nyingi katika sharia miongoni mwa yale yaliosemwa kuhusu kiama na yasiokuwa hayo. Miongoni mwa hizo (shaka zitazotokea) ni kile kitachotokea kuhusu kuonekana (kwa Allah) ambako riwaya thabiti373 zimekuelezea. Na hii ni kwa sababu wale waliokanusha kwa uwazi – yaani kukanusha kiwiliwili – ni makundi mawili: 1) Mu’atazila. 2) Ash’ariyya (Masuni wote taqriban, ukiwatoa baadhi ya Hanbali). Ama Mu’atazila wao jambo hilo (la kukataa kuwa Allah ni kiwiliwili), liliwapelekea kukataa kuwa Allah ataonekana. Ama Ash’ariyya wakataka kuyajumuisha mambo yote mawili yakawawiya tabu hayo juu yao, wakakimbilia kwenye kauli za kuikataa haki na kuipamba batili…..374

368 - Yaani kauli kwamba Allah ni kiwiliwili iko karibu zaidi na akili kuliko kauli ya kukataa hivyo! 369 - Ibn Taymiyya Bayaanu Talbisi Al-Jahmiyya j. 1, uk. 93-94. 370 - Nasi tunasema: hakuna hasa kwa Mungu sifa ya kiwiliwili. 371 - Ibn Taymiyya Bayaanu Talbisi Al-Jahmiyya. j. 1, uk. 24-25. 372 - Ibn Taymiyya Bayaanu Talbisi Al-Jahmiyya j. 1, uk. 25. 373 - Tunasema: hakuna riwaya thabiti juu ya suala hili; bali zote hizo ni riwaya za kutunga kama tutavyobainisha tukifika sehemu yake in shaa Allah. 374 - Ibn Taymiyya Bayaanu Talbisi Al-Jahmiyya j. 1, uk. 26.

97

Page 98: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Na miongoni mwa (sababu) hizo, ni kwamba ikiwa (itikadi ya) kiwiliwili itakataliwa kwa uwazi, basi italazimu kuzikataa harakati, kwa hivyo, ikiwa (harakati) zitakataliwa kwa uwazi, itakuwa vigumu (kuithibitisha) ile sifa ya mkusanyiko (wa siku ya kiama) iliokuja kwamba Allah atawachomozea (atawajia) watu wa siku ya kiama. 375

Lakini, pamoja na maelezo yote hayo, Mzee wa Uislamu, Al-Imamu Ibn Taymiyya Al-Harraani mwenyewe anasema: “Na wajibu ninavyoona mimi ni kuwa sifa hii (ya kuwa Allah ni kiwiliwili) ipitishwe mpito wa Sharia: isithibitishwe wala isikataliwe”.376

Huo ni uoni binafsi wa Ibn Taymiyya. Lakini pamoja na kusema hivyo, ni wazi kwamba hata yeye mwenyewe Ibn Taymiyya anamili zaidi katika itikadi ya kuwa Allah ni kiwiliwili kuliko kuikataa itikadi hio. Na kwa sababu hio, ndio maana akanena:

1) Nayo (itikadi hio ya kuwa Allah ni kiwiliwili) katika kuithibitisha kwa uwazi katika Sharia ipo karibu zaidi kuliko kuikataa, kwani Sharia imetaja kwa uwazi uso (wa Allah) na mikono (yake) miwili.377

Na akasema:

2) Na hakuna yoyote katika Al-Salaf (watangulizi) aliyemlaumu mtu yoyote kwamba yeye (mtu huyo) ni mujassim (mwenye kusema kuwa Allah ni kiwiliwili). Wala (hakuna) aliyewalaumu mujasima (wenye kusema kuwa Allah ni kiwiliwili). Bali (Al-Salaf) waliwalaumu Al-Jahmiyya ambao waliyakanusha hayo (ya kuwa Allah ni kiwiliwili)”!378

Na akasema: “Na mwenye kusifika kwa sifa hizi hawi isipokuwa ni kiwiliwili. Basi Mungu ni kiwiliwili si kama viwiliwili (vyengine)”.379

Lakini tukirudi katika hoja ya Ibn Taymiyya kwamba “Na hakuna yoyote katika Al-Salaf (watangulizi) aliyemlaumu yoyote kwamba yeye (mtu huyo)

375 - Ibn Taymiyya Bayaanu Talbisi Al-Jahmiyya j. 1, uk. 27. 376 - Ibn Taymiyya Bayaanu Talbisi Al-Jahmiyya j. 1, uk. 25. Nasi tunasema kwamba hio si sifa ya Allah kamwe, na kwa hivyo ikataliwe tu, kwani kiwiliwili kinajulikana ni kitu gani na Allah hayuko hivyo. 377 - Ibn Taymiyya Bayaanu Talbisi Al-Jahmiyya j. 1, uk. 24-25. 378 - Ibn Taymiyya Bayaanu Talbisi Al-Jahmiyya j. 1, uk. 100. 379 - Ibn Taymiyya Bayaanu Talbisi Al-Jahmiyya j. 1, uk. 100. Maneno haya kwa mujibu wa alivyoyaeleza Ibn Taymiyya, yanawezekana yakawa ni yake au ni maneno ya hao Mahanbali wenzake anaowaita Ahlu Al-Ithbat.

98

Page 99: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

ni mujassim (mwenye kusema kuwa Allah ni kiwiliwili)”. Tunakuta kwamba hio ni hoja dhaifu, kwani:

a) Ili Al-Salaf wampinge mtu kwa kusema hivyo, ni lazima awe yuko mtu aliyesema hivyo. Na Al-Salaf, tukichukulia kuwa ni Masahaba, basi enzi yao hakukuwa na itikadi hio na ikawa ni kitu kilichoenea na kujulikana na wote – itikadi hio ni bidaa dhalala.

b) Hayo alioyasema ni kutoa hoja kwa kitu kisichokuwepo, na ilivyo ni kutoa hoja kwa kitu kilichokuwepo. Tazama lau leo atatokea mtu akasema kuwa “Mungu ni jiwe si kama mawe”. Je itajuzu kuitetea itikadi hii kwa msingi kwamba hakuna yoyote katika Al-Salaf aliyemlaumu mtu kwa kusema hivyo? Ilivyo kwanza awepo yule mtu aliyesema kuwa “Mungu ni jiwe si kama mawe” katika zama za Al-Salaf, kisha iwe Al-Salaf walimsikia akisema hivyo lakini wakamnyamazia ilhali wanao uwezo wa kumpinga, hapo ndio hoja itanyooka kwamba Al-Salaf hawakumlaumu aliyesema hivyo. Lakini ikawa hakukuwa na mtu aliyesema hivyo, vipi mtu ataweza kudai kwamba “Mungu ni jiwe si kama mawe” kwa msingi kwamba hakuna katika Al-Salaf aliyemlaumu mtu kwa kusema hivyo? Halkadhalika kudai kwamba hakuna katika Al-Salaf aliyemlaumu mtu kwa kusema kwamba “Mungu ni kiwiliwili si kama viwiliwili” kungefaa lau alikuwepo mtu aliyesema hivyo katika zama zao nao wakamnyamazia. Lakini kwa sababu jiwe katika lugha linajulikana ni nini; na Sharia imeshasema kwamba Allah hafanani na kitu, basi elewa kwamba hilo halitojuzu. Halkadhalika kiwiliwili kinaeleweka ni kitu gani, na kwa hivyo huwezi kusema au kuitetea itikadi ya kuwa Allah ni kiwiliwili.

c) Hatimae utaona kwamba hayo yote tulioyasema ya kwamba katika enzi ya Al-Salaf hakukuwa na watu waliosema: “Mungu ni kiwiliwili si kama viwiliwili” ni pale itapokuwa Ibn Taymiyya anakusudia kwamba katika zama zao hakukuwa na waliolitamka neno “kiwiliwili” yaani kiwiliwili cha Mungu. Ama ikiwa anakusudia kuwepo katika enzi hizo kwa watu waliomfananisha Allah na viumbe kwa kutumia lafdhi yoyote ile, basi katika zama za Ali walikuwepo watu hao naye aliwakaripia sana. Anasimulia Al-Imamu Al-Rabi’u bin Habib (r.a.) kwamba baadhi ya watu walikuwa wakisema kuwa “Allah kamuumba Adam kwa sura yake”. Akasimama Al-

99

Page 100: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Imamu Ali akatoa hutuba kali na akawakaripia sana.380 Bali hata katika utangulizi uliomo katika Bayaanu Al-Talbis cha Ibn Taymiyya, imeelezwa kwamba kulikuwa na watu miongoni mwa Mashia ambao walikuwa wakisema kwamba Ali ndiye Mungu na kwamba watu hao Ali aliwachoma moto.381

Baada ya hayo, utaona kwamba katika itikadi za mabwana hao wa Kihanbali, ambao ndio Maimamu watangulizi wa Kiwahabi, tunapata katika maelezo yao hayo kwamba Allah ni kiwiliwili. Na hilo si ajabu kuwa limo katika itikadi yao hata lau hawakulisema kwa uwazi kwani moja ya riwaya zao, inasema:

Hakika ya Allah anakuwa mzito mno juu ya (Malaika) walioibeba Arshi mwanzoni mwa mchana wanaposimama washirikina; hata wakisimama wenye kumsabihi (Allah) basi uzito wake hupungua kwa waliobeba Arshi.382

Jamani ndugu zangu! Tazameni ajabu hii! Hiki ni kiwiliwili cha Mungu kimebebwa na Malaika juu ya kiti nacho – kiwiliwili hicho – kinazidi uzito na kupungua! Astaghfiru Allah! Hii ni akili gani enyi walimwengu! Hio ni moja ya riwaya za Kitabu Al-Sunna cha Ibn Ahmad ambacho Sheikh Seif Al-Ghafri kausia sana kuwa tukisome ili tupate kuongoka!

Ama ‘Uthman bin Said Al-Darimi, yeye anasimulia riwaya ifuatayo:

Na imetufikia kwamba wao (malaika wenye kuibeba ‘Arshi) wakati watapoibeba ‘Arshi (kiti cha enzi) na juu yake yuko (Allah aliye) Jabar katika nguvu zake na utukufu wake, basi watadhoofika383 (hawatoweza) kumbeba na watalegea na watapiga magoti mpaka watafundishwa (kusema) “La hawla wala quwwata illa bi-Llah”.384

Kwa hivyo, tunapata kutoka katika itikadi hizo kwamba Allah ni kiwiliwili. Nacho kiwiliwili hicho ni kizito mno kiasi cha kwamba Malaika hawakiwezi kukibeba ila kwa kufanya dhikr! Lakini cha ajabu tutachokipata hapa, ni kuwa ‘Arshi – kwa maana hio – itakuwa ni kubwa kuliko Mungu

380 - Al-Rabiu’u bin Habib Al-Jaami’u Al-Sahih j. 3, uk. 314, Hadithi na. 836. 381 - Tazama utangulizi wa Muhammad bin ‘Abdil-Rahman katika Bayaanu Talbisi Al-Jahmiyya cha Ibn Taymiyya j. 1, uk. 6. Tazama Dr. Salih Fauzaan Al-Fawzaan Kitabu Al-Tauhiid uk. 121. Na haya pia yameelezwa na Ahmad Al-Katib katika Tatawwuru Al-Fikr. 382 - Ibn Ahmad Al-Sunna uk. j. 2, uk. 455, riwaya na 1026. Na hii ikiwa bado haijawa tashbihi na tajsim basi hakuna tena duniani kitu tashbihi wala tajsim! 383 - Watadhoofika Malaika kwa jinsi Allah alivyokuwa mzito! 384 - ‘Uthman bin Said Al-Darimi Al-Radu ‘Alaa Bishri Al-Marisi uk. 85.

100

Page 101: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kwani Yeye Allah kakaa kitako juu yake na imemtosha, bali katika riwaya nyengine za mabwana hawa ni kuwa baada ya Allah kukaa kitako juu ya ‘Arshi, basi itabakia sehemu kiasi cha vidole vine.385

KIWILIWILI CHA MUNGU KINA VIUNGO!

Baada ya hayo, sasa tazama ukweli kwamba kiwiliwili hicho cha Mungu ni kiwiliwili chenye:

1) Mikono miwili. Anasema mtaalamu wa Kiwahabi: “Na Aya zenye

kuthibitisha kuwa Allah ana mikono miwili ziko wazi’.386….. “Je unaonaje, lau Allah alikuwa hana mikono miwili ingefaa ibara hii ya kukunjua (kwake) mikono miwili.”387

385 - Sijui kadiri hii ya vidole vine iliobakia ni vidole vya Mungu au vya binaadamu? Kwani itikadi ya wenzetu ni kuwa Mungu ana vidole. 386 - Dr. Ali Muhammad Al-Sallabi Min ‘Aqitadati Al-Muslimin uk. 77. Muhammad Khalil Haraas Sharhu ‘Aqiidati Al-Wasatiyya uk. 58. Muhammad bin ‘Abdil-’Aziz bin Mani’i Al-Hashiya ‘Alaa Al-’Aqiidati Al-Wasatiyya uk. 35. Ibn Qayyim Al-Jawziyya Mukhtasar Al-Sawaa’iqi Al-Mursala uk. 322. Ibn ‘Uthaimin ‘Aqiidatu Ahli Sunna Wa Al-Jama’a uk. 12. Ibn Taymiyya Bayaanu Talbisi Al-Jahmiyya j. 1, uk. 100. 387 - Muhammad Khalil Haraas Sharhu ‘Aqiidati Al-Wasatiyya uk. 58. Tazama pia Muhammad bin ‘Abdil-’Aziz bin Mani’i Al-Hashiya ‘Alaa Al-’Aqiidati Al-Wasatiyya uk.

101

Page 102: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Ninasema: lakini jambo muhimu kwa anayeyafasiri maandiko si kutazama nini kimetamkwa tu, bali ni kutazama nini mtamkaji anakikusudia. Yamenifurahisha mno maneno ya Al-Imamu Ibn Al-Qayyim aliyoyanukuu Prof. Muhammad Bakr Isma’il, aliposema:

قال ماذا يقول واللفظي أراد ماذا يقول والعارف

“Mwenye kujua au mwenye kufahamu yeye huwa anasema: ‘Je kakusudia nini? Na mwenye kutazama matamshi tu yeye huuliza: ‘Je kasema nini?”388

Hayo ni maneno ya Ibn Al-Qayyim nayo ni maneno mazuri yalioje, ya lait Ibn Al-Qayyim aliyatendea kazi asingeliingia katika vuli389 la itikadi za kumshabihisha Allah.

Ama njia za kujua nini kimekusudiwa katika andiko fulani, ni kutazama:a) Maandiko mengine. Kwani kama ilivyonenwa kwamba

maandiko yanafasiriana yenyewe kwa yenyewe. b) Maana ya kilugha ya neno. Je neno unalotaka kulifasiri lina

maana gani ya mwanzo na ya msingi ya kilugha kabla ya kuwa katika sentensi na baada ya kuwa katika sentensi limeleta maana gani. Nikisema mguu je mguu katika lugha ni kitu gani? Na kama ibara inayosema: “Ali mguu wake unamuuma” inaonesha mguu wa kweli, je ibara inayosema: “Hakika Al-Imamu Al-Nawawi ana mguu uliozama katika elimu ya fiq-hi na Hadithi” pia inaonesha mguu wa kweli?

c) Je neno kadha limetumika katika maana yake ya asili kama neno mguu wa Ali unaomuuma; au neno hilo limetoka katika maana yake ya asili na kupelekwa katika maana nyengine kama ule mguu wa Al-Imamu Al-Nawawi uliozama katika elimu?

Hayo ni baadhi ya mambo muhimu ya kuyatazama kwa mwenye kuyafasiri maandiko. Sasa tukirudi kuyatazama maandiko mengine, tunakuta Aya kama:

ماء بأييد بنيناها والس

35. Ibn Qayyim Al-Jawziyya Mukhtasar Al-Sawaa’iqi Al-Mursala uk. 322. Ibn ‘Uthaimin ‘Aqiidatu Ahli Sunna Wa Al-Jama’a uk. 12. Ibn Taymiyya Bayaanu Talbisi Al-Jahmiyya j. 1, uk. 100. 388 - Kainukuu Prof. Muhammad Bakr Isma’il katika Al-Qawaaidu Al-Fiqhiya uk. 35, kutoka kwa Ibn Al-Qayyim I’ilaamu Al-Muwaqqa’iin j. 1, uk. 219. 389 - Vuli kwa Kipemba ni sehemu yenye matope ambayo ukiingia basi unaweza kuzama.

102

Page 103: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Na mbingu tumeziumba kwa mikono yetu (mingi zaidi ya miwili).

Na Aya kama:ا لهم خلقنا أنا يروا أولم أيدينا عملت مم ...

Na hawaoni wao kwamba tumewaumbia yale yaliofanywa na mikono yetu (mingi zaidi ya miwili).

Na Aya kama:مبسوطتان يداه بل

Bali mikono yake miwili ni yenye kukunjuliwa.

Na Aya kama:أيديهم فوق الله يد

Mkono (mmoja) wa Allah uko juu ya mikono yao.

Hapa utaona kwamba Aya za Qur-ani zimetaja kuwa Allah ana mikono mingi zaidi ya miwili, na nyengine zikataja mikono miwili na nyengine ikataja mkono mmoja. Sasa ili kuufikia ukweli je Allah ana mikono au hana, ni lazima tukubaliane juu ya msingi gani ulio sahihi katika kuyafasiri maandiko. Je msingi sahihi ni kuyakataa majazi na badala yake kuzichukua lafdhi za Aya kama zilivyo bila ya kuziletea ta-awil iliojengeka juu ya msingi wa kimajazi, au ta-awil inafaa ikiwa kuna qarina ya lafdhi au ya hali au ya kiakili ilioonesha hivyo? Tukichukua msingi wa kukataa majazi na ta-awil, basi natija ni moja katika mbili. Ama tuseme:

1) Allah ana mikono mingi zaidi ya miwili. Na Aya zilizotaja mikono miwili basi zimetaja mikono miwili katika mingi hio, halkadhalika Aya iliotaja mkono mmoja. Lakini natija hii itakuwa na mgongano wa nguvu baina yake na itikadi kwamba Mungu ana mikono miwili – itikadi iliokumbatiwa na wanaoitwa Mawahabi na Maimamu wao watangulizi. Bila kusahau kwamba msingi huo wa kukataa majazi, utatupeleka katika kuemewa mbele ya Hadithi isemayo: “Allah ana mikono miwili (wa kulia na wakushoto), na mikono yake yote ni yakulia”.390 Tazama mgongano uliomo katika Hadithi hizi pindipo tutakataa majazi na ta-awil! Mikono ni miwili wa kulia na wakushoto, lakini yote ni ya kulia! Hapa itakubidi ama uikatae Hadithi hii au ukimbilie kule kule ulikokimbia – kwenye majazi na ta-awil.

390 - Mkono wa kushoto umetajwa katika riwaya ya Muslim katika Sahihu yake Hadithi na. 2788, na mokono wa kulia umetajwa katika riwaya hio na nyengine tutazozinukuu baadae.

103

Page 104: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

2) Kwamba Qur-ani inagongana: mwengine imetaja kuwa Allah ana mkono mmoja na mwengine imetaja kuwa Allah ana mikono miwili na mwengine Allah kasema kuwa ana mikono mingi! Ukisema hivi, basi umekufuru.

Hizo ndio natija za lazima ikiwa tutachukua msingi kwamba haijuzu kuifasiri Qur-ani kimajazi na kwamba haijuzu kuiletea ta-awili: bali ni lazima tuifasiri neno kwa neno (literally). Na kama ulivyojionea mwenyewe ndugu msomaji kwamba natija zote hizo ni natija ambazo ubatili wake uko wazi. Wala usiniambie kwamba: “Aaa! Unajua lugha ya Kiarabu ni pana: inatumika moja kwa maana ya nyingi na nyingi kwa maana ya moja na mbili kwa maana ya nyingi, n.k.”. Ukiniambia hivyo, nitakujibu kwamba hayo ndio majazi yenyewe unayoyakataa. Majazi ni “Kutumika kwa neno kinyume na maana yake ya asili”, vyenginevyo wapi umepata kusikia wewe kwamba uhakika wa moja unakuwa tatu na uhakika wa tatu unakuwa moja n.k.? Lau uhakika wa tatu ulikuwa ni moja basi ikitajwa tatu mtu asingelifahamu isipokuwa moja na ili ifahamike tatu basi kungehitajika qarina! Kwa hivyo, ikiwa unakubali kwamba moja inatumika kumaanisha nyingi na nyingi kumaanisha moja, kipi kinakufanya ukanushe kwamba neno mkono linatumika kwa maana ya uwezo, nguvu, neema, nafsi n.k., ilhali maana zote hizo zimepokewa kutoka kwa Waarabu wa awali nazo zinawiyana zaidi na utukufu wa Allah kuliko maana ya mkono-kiungo? Ni wazi kwamba hakuna njia sahihi ya kuzifasiri Aya hizo zilizotaja mkono mmoja, miwili na mingi ya Allah ila njia ya kimajazi, vyenginevyo dhahiri yake si makusudio yake kama Aya zenyewe zinavyojionesha.

Tukirejea tena katika Aya ماء بأيي��د بنيناها والس�� Wa ssamaa-a banaynaahaa biaydin “Na mbingu tumeziumba kwa mikono yetu” (mingi zaidi ya miwili), tunakuta kwamba watetezi wa itikadi ya tajsim wananukuu kutoka kwa Al-Imamu Abu Al-Hasan Al-Ash’ari akisema:

نعمة هي التي اليد وجمع أيدي يد جمع ألن لليد جمع ليس األيد ) بيدي خلقت لما تعالى قال وإنما يكون (أيادي أن بذلك فبطل

( بيدي : ( قوله ) معنى بأيد : ( بنيناها قوله معنى

(Neno) Aydi (mikono) si wingi wa (neno) yad (mkono); kwani wingi wa (neno) yad ni Aydiy391 na wingi wa (neno) yad (mkono) ambao una maana ya neema ni Ayaadiy; na kwa hakika Allah Mtukufu Yeye kasema: “(E Ibilisi kwanini umekataa kumsujudia) yule niliyemuumba bi-yadayya

391 - Ayadi أيدna Aydiy أيديni neno moja linapoingia tanwin (dhummatain au kasratain) basi al-yaa (yee) yake huondoshwa.

104

Page 105: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

(kwa mikono yangu miwili), basi ikabatilika kuwa maana ya kauli yake Allah aliposema: “bi-yadayya” (kwa mikono yangu miwili) kuwa (ni sawa na) maana ya kauli yake aliposema: “bi-aydin” (kwa mikono mingi zaidi ya miwili).392

Maneno haya ya Abu Al-Hasan ni maneno ya kustaajabisha! Kwa kuanzia ni kuwa kuna mgongano wa maneno haya: kwanza anakataa kuwa wingi wa neno yad ni aydi kisha anathibitisha kuwa wingi wa neno yad ni aydi! Kisha anadai kwamba neno yad linapokuwa na maana ya neema basi wingi wake ni ayaadi: si aydi. Kisha anatafautisha baina ya Aydi na Ayaadi na kwamba mkono ukitumika kwa maana ya neema basi wingi wake unakuwa Ayaadi: si Aydi! Sasa kama ni hivyo, basi kwanini tena atafautishe baina ya Aya “bi-yadayya” (kwa mikono yangu miwili) na Aya: “bi-aydin” (kwa mikono mingi zaidi ya miwili), ilhali mwote zimetumika lafdhi zilizoonesha mikono ya kweli: si kwa maana ya neema! Hii ni ajabu ilioje! Kwa ufafanuzi zaidi ni kuwa:

1) Neno aydi bila shaka ni wingi wa neno yad katika matumizi ya Kiarabu. Na mara ngapi limetumika neno hilo katika Qur-ani kwa muundiko huo likimaanisha wingi wa neno yad. Anasema Allah katika Qur-ani: مبأيديك الله يعذبهم قاتلوهم (Wapigeni, Allah awaadhibu kwa (kupitia katika) mikono yeno).393 Na anasema Mwenyezi Mungu: ون أرج����ل ألهم أيد لهم أم بها يمش����

بها يبطشون (Kwani wao wana miguu wanakwenda kwayo; au wana mikono ambayo wanashikia kwayo?). 394 Mwote humu limetumika neno aydi likiwa ni wingi wa neno yad kwa maana ya mikono.

2) Ama dai kwamba neno yad linapokuwa na maana ya neema basi wingi wake ni ayaadi, ikumbukwe kwamba neno ayaadi ni sigha ya muntaha al-jumu’i (muundo wa wingi uliokomea hapo huwezi kuunda wingi mwengine). Yaani neno yad maana yake ni mkono mmoja; na aydi ni mikono mingi, kisha unaweza kuunda tena sigha (form) ya wingi ukasema ayaadi nayo pia ina maana ya mikono mingi. Anasema mshairi:

األنجل حصحان بالص ل ***كأنه غز بأيادي سخام قطنKana kwamba yeye ni pamba jeusi lililoko mikononi kwa wafumaji huko

(katika sehemu iitwayo) Sahsahaan Al-Anjali.395

392 - Ali Al-Faqihi katika maelezo yake katika Kitabu Al-Tauhid cha Ibn Manda j. 3, uk. 108. 393 - Sura 9, Aya 14. 394 - Sura 7, Aya 195. 395 - Ibn Mandhur Lisanu Al-‘Arab j. 15, uk. 437.

105

Page 106: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Utaona hapa kwamba limetumika neno Ayaadi kwa maana ya mikono ya kweli. Bali kilicho sahihi ni kuwa inapokusudiwa neema basi aghlabu – si mara zote wala si lazima – wingi wa neno yad unakuwa ni ayaadi, kama alivyosema Ibn Jinni.396

Tumebakiwa na suali: je neno aydi halitumiki kumaanisha neema kama ilivyodaiwa katika maelezo ya Abu Al-Hasan? Bila ya kujikalifisha bahth (upekuzi) juu ya dai hili, basi inafaa na sisi tujiulize suali moja tu ili iwe ndio jawabu ya suala hilo, nalo ni kuwa ikiwa neno Aydi (mikono) mingi halitumiki kumaanisha neema, je neno hilo halitumiki kumaanisha maana nyengine kama nguvu, uwezo n.k.? Na kwa hivyo, neno mikono lililomo katika Aya: ماء بأييد بنيناها والس Na mbingu tumeziumba kwa mikono yetu (mingi zaidi ya miwili), na Aya ا لهم خلقنا أنا يروا أولم مم

أيدينا عملت ...Na hawaoni wao kwamba tumewaumbia yale yaliofanywa na mikono yetu (mingi zaidi ya miwili), na zilizo mfano wa hizo, je neno mikono lililomo katika Aya hizo haliwezi kufasirika kwa maana ya “uwezo,” au maana nyengine ya kimajazi ilio mfano wa hio? Vyenginevyo, basi Mungu ana mikono mingi: zaidi ya miwili!

Ama kuhusu Aya isemayo: وطتان ي��داه بل مبس�� ((Bali mikono yake miwili ni yenye kukunjuliwa)) ambayo wengi miongoni mwa watetezi wa itikadi ya tajsim wanadai kuwa haifasiriki ila kwa maana ya mikono ya kweli, ni kinyume na wanavyodhani. Wao hoja yao kubwa ni kuwa lau tutalifasiri neno mkono lililomo katika Aya hio kwa maana ya neema basi maana itakuwa: “bali neema zake mbili zimekunjuliwa” kwani Aya inasema: “Bali mikono yake miwili imekunjuliwa”. Nayo si maneno madhubuti kwani:

1) Hakuna ulazima wa kulifasiri neno mkono katika Aya hio kwa maana ya neema. Bali makusudio ya neno hilo ni kufanya tashbihi ya kibalagha ya kuishabihisha hali ya utoaji wa Allah wa riziki kwa kuishabihisha na hali ya kiumbe anavyotoa mali kuwapa watu. Kama vile unavyoweza kumwita mtu aliyekarimu sana kuwa “Mikono yake anaikunjua” au “Mikono yake yote kaikunjua” na mtu aliyebakhili kuwa “Mikono yake kaikunja”397 kama ilivyo katika Surat Al-Tauba,398 basi lugha hizi ndizo ziliotumika hapa

396 - K. h. j. 397 - Kama ilivyo Aya inayosema: كل تبسطها وال عنقك إلى مغلولة يدك تجعل والyaani usifanye ubakhili (Wala usiufunge mkono wako na shingo yako) البسط (Wala usiukunjue wote) yaani usifanye israfu. Sura 17, Aya 30.398 - Yaani Aya inayosema: أيديهم .(Na (wanafiki) wanaizuia mikono yao) ويقبضونSura 9, Aya 67.

106

Page 107: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kumaanisha ukarimu wa Allah kwa waja wake, ikasemwa: “Bali mikono yake miwili imekunjuliwa”.

2) Pili ni kuwa qarina zilizopo hapa zote zinaonesha kuwa mikono hii si mikono ya kweli. qarina hizo ni:

a. Waliojibiwa jawabu hio ni Mayahudi walipodai kuwa Allah mikono yake imefungwa. Nao hawakukusudia kuwa mikono ya Allah imefungwa kwa kamba au minyororo bali walikusudia kwamba Allah ni bakhili.

b. Jawabu iliokuja ikawa imewajibu kwa mujibu wa itikadi yao hio mbovu. Kwa hivyo, ikiwa Yahudi katumia lugha “kufungwa kwa mkono” kumaanisha ubakhili, basi elewa kwamba jawabu ya Allah ya “kukunjuliwa kwa mkono” ni kinyume na madai ya Mayahudi, yaani maana ya ibara hio ni ukarimu.

c. Aya imeanza kwa kuwajibu Mayahudi kwa maneno yasemayo: أي��ديهم غلت مغلول��ة الله ي��د اليهود وقالت (Na wakasema Mayahudi kwamba mkono wa Allah umefungwa; mikono yao ndio iliofungwa). Lau uliokusudiwa ni mkono wa kweli, basi jawabu isingelikuwa “Mikono yao ndio iliofungwa”, kwani hakuna Myahudi ambaye mkono wake umefungwa, bali tunachokishuhudia ni ubakhili uliopindikia mipaka wa Mayahudi. Kwa hivyo, ni wazi kwamba neno mikono katika sehemu ya kwanza ya Aya isemayo: مغلولة الله يد (mkono wa Allah umefungwa), Mayahudi kwa kauli yao hio walikusudia ubakhili yaani walikusudia kusema kwamba Allah ni bakhili! Na maneno ya sehemu ya pili ya Aya hio yasemayo: مبسوطتان يداه بل ((Bali mikono yake miwili ni yenye kukunjuliwa)), yameletwa ili kuyakanusha maneno ya sehemu ya kwanza

المقابلة سبيل kwa namna ya muqabala (opposite) علىwa kimaana. Na kwa hivyo, maana ni: “Mayahudi wamesema kwamba Allah ni bakhili; naye ni mkarimu. Vyenginevyo, maneno أي��ديهم غلت “mikono yao ndio iliofungwa” basi yasingelikuwa na maana kwani hakuna mkono wa kweli wa Mayahudi uliofungwa kweli kweli, bali kilichopo kwa Mayahudi ni ubakhili wa kweli kweli.

Kwa ufupi ni kuwa, ninachotaka kukisema hapa ni kuwa madai ya watu wa skuli ya tajsim kudai kwamba Abu Al-Hasan Al-Ash’ari alikuwa na itikadi kama zao si madai sahihi. Na tatizo la watu hao ni kuwa wanapenda kufanya tadlis (ghushi) katika nukulu zao: hawanukuu kitu ila watakighushi japo kidogo. Tazama maelezo ya Abu Al-Hasan katika kitabu chake hicho Al-

107

Page 108: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Ibana halafu tazama itikadi za Mawahabi na Maimamu wao. Abu Al-Hasan anasema:

( ) : إثبات ذلك معنى يكون أن بيدي خلقت لما تعالى قوله يخلو وليسمعنى يكون أو نعمتين يدين

جارحتين يدين إثبات ذلك ذلك عن الله إثبات تعالى ذلك معنى يكون أومعنى يكون أو قدرتين يدين

توص ال قدرتين وال جارحتين وال نعمتين ليستا يدين إثبات إال ���ذلك فانوص فال ���كما تعالى الله ف

يقول أن اللسان أهل عند يجوز ال ألنه نعمتين ذلك معنى يكون أن يجوزبي : عملت دي��������القائل

نعمتي وهو

جارحتين نعني أن خصومنا عند وال عندنا يجوز ي وال خصومنا �وال عند جوزقدرتي يعني ،ن����أن

قوله معنى أن وهو الرابع القسم صح الثالثة األقسام فسدت وإذا ( ليستا :( يدين إثبات بيدي تعالى

: يدان إنهما يقال بأن إال يوصفان ال نعمتين وال قدرتين وال جارحتينعن خارجتان كاأليدي ليستا

سلفت التي الثالثة الوجوه ع …سائر المأثور الخبر في النبي ����وجاء نسل و عليه الله م ����صلى

بيده( التوراة وكتب بيده عدن جنة وخلق بيده آدم خلق تعالى الله أن( بيده طوبى شجرة وغرس

سبحانه قدرته بيد أي

Na kauli yake (Allah aliposema): “Kwa yule niliyemuumba kwa mikono yangu miwili”, haiachi kuwa maana yake ni kuthibitisha mikono miwili (kwa maana ya) neema mbili; au mikono miwili (kwa maana ya) viungo viwili, hilo Allah katakasika nalo; au iwe maana ya hayo ni kuthibitisha mikono miwili (kwa maana ya) kuweza kuwili; au iwe maana ya hayo ni kuthibitisha mikono miwili ambayo si neema mbili, wala si viungo viwili, wala si kuweza kuwili, wala haisifiwi isipokuwa vile alivyoisifu Allah Mtukufu; basi haifai kuwa maana ya hayo ni neema mbili kwani kwa watu wa lugha haifai mtu kusema: “Nimekifanya kitu kadha kwa mikono yangu miwili” yaani “Kwa neema zangu mbili”.

Wala haifai kwetu wala kwa wapinzani wetu kwamba tuifasiri (hio mikono miwili ya Allah) kuwa ni viungo viwili; wala haifai kwa wapinzani wetu kuwa (maana ya mikono miwili) iwe ni kuweza kuwili. Basi ikiwa migawanyiko mitatu hio yote haikubaliki, basi kilichobakia ni mgawanyiko wa nne, nao ni kuwa maana ya “kwa mikono yangu miwili” ni kuthibitisha mikono miwili ambayo si viungo viwili wala si kuweza kuwili wala si neema mbili; haisifiwi isipokuwa isemwe: hakika yake ni mikono miwili si kama mikono imetoka katika namna tatu zilizotangulia

108

Page 109: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

(kutajwa) 399…. Na katika riwaya, kumepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.) akisema: “Hakika ya Allah kamuumba Adam kwa mkono wake na akaiumba pepo kwa mkono wake na akaandika Taurati kwa mkono wake, na akaupanda mti tuba kwa mkono wake, yaani mkono wa uwezo wake (Allah) Aliyetakasika. 400

Hayo ndio maneno ya Al-Imamu Abu Al-Hasan Al-Ash’ari, tukijaalia kwamba kitabu Al-Ibaana kweli ni katika utunzi wake. Lakini pamoja na hayo, tunaona kwamba wafuasi wa skuli yake wamekuwa na maelezo tafauti juu ya kitabu chake hicho. Sheikh Muhammad Zaahid Al-Kawthari, katika maelezo yake ya kitabu Al-Saifu Al-Saqiil cha Al-Imamu Al-Subki, anasema kwamba waliodhania kwamba kitabu hicho ni kitabu cha mwisho cha Al-Imamu Abu Al-Hasan Al-Ash’ari wamekosea, bali hicho ni kitabu chake cha mwanzo baada ya kuwacha madhehebu ya Mu’utazila. Na hio ndio sababu ya kuyasema hayo – itikadi yake ilikuwa bado haijatulia.

Ama Sheikh Abdullah Al-Harari, katika Al-Maqaalatu Al-Sunniyya, yeye anaona kwamba kitabu hicho Al-Ibaana hakikuthibiti kamwe kuwa ni kitabu cha Abu Al-Hasan Al-Ash’ari. Sababu yake ni kuwa, As-habu zake (wanavyuoni wafuasi wake) na wanafunzi wake ambao wamechukua itikadi na elimu kutoka kwake moja kwa moja kisha wakarithishana tabaka moja baada ya nyengine, hakuna yoyote miongoni mwao mwenye itikadi hizo. Ninasema: nami nilikuwa nimetoa hoja kama hii katika kitabu changu Hoja Zenye Nguvu, lakini mwanachuoni Sheikh Kasim Mafuta akanijibu kama ifuatavyo:

Kwa maneno haya ya ndugu Juma anatuwekea wazi zaidi namna asivyokuwa mtafiti mzuri wa mambo na huwa hukumu zake ni za kubuni. Tangu lini mtu akahukumiwa kwa matendo ya watu wengine? Kuwa wafuasi wa Abul-Hasan al-Ash’ari wako kinyume na itikadi yake, basi hiyo ndiyo hoja ya kwamba hakusema maneno hayo? Kwanini usiwashangae watu wanaodai kuwa ni wafuasi wa Imamu Shaafiy katika mambo ya twahara na swala lakini katika mambo ya itikadi wamemfuata Abul-Hasan na wako kinyume na Imamu wao? Kwanini wamemkwepa Imamu Shaafiy aliyefariki mwaka 205 H na kumfuata Abul-Hasan al-Ash’ariy aliyezaliwa mwaka 260 H na kufariki mwaka 324 H? Abul-Hasan yeye amezaliwa nusu karne baada ya Imamu Shaafiy kufariki, je Imamu Shaafiy hakuwa na itikadi yoyote? Na je yeye alikuwa akimfuata nani?401

399 - Abu Al-Hasan Al-Ash’ari Al-Ibana uk. 133. 400 - K. h. j. uk. 125. 401 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 19.

109

Page 110: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Hayo ndio maneno ya Kasim Mafuta, nayo si maneno madhubuti, kwani kwanza ili maneno hayo yamfae yeye kama ni hoja yake basi ni lazima akubali kwamba Mashafi ni wafuasi wa Abu Al-Hasan katika itikadi. Hivyo ndivyo yanavyomaanisha maneno yake kama: “Kwanini wamemkwepa Imamu Shaafiy aliyefariki mwaka 205 H na kumfuata Abul-Hasan al-Ash’ariy aliyezaliwa mwaka 260 H na kufariki mwaka 324 H?” Kwa bahati mbaya, maelezo yake mengine yanaonesha kwamba Mashafi hawakumfuata Al-Imamu Abu Al-Hasan katika itikadi, kwani – kwa mujibu wa Kasim Mafuta – Abu Al-Hasan alikuwa na itikadi kama ya Kiwahabi leo ya mungu mwenye mikono, miguu na sura kama ya Adam. Anasema Kasim Mafuta:

Na wanavyuoni walio lithibitisha suala hili la kutubia kwake (Abu Al-Hasan), kuacha misimamo hiyo potofu na kushikamana na msimamo wa Salaf Swalih na kuandika kitabu “al-Ibana”, ni hawa wafuatao….402

Bila shaka misimamo ya Al-Salafu Al-Salih kwa mujibu wa Mawahabi ni kuamini hayo tulioyataja na yalio mfano wa hayo, wakati Mashafi hilo hawalikubali. Kwa hivyo, natija ni kuwa Mashafi hawakumfuata Al-Imamu Abu Al-Hasan Al-Ash’ari. Na kwa maana hiyo, maneno ya Kasim Mafuta yasemayo: “Kwanini wamemkwepa Imamu Shaafiy…na kumfuata Abul-Hasan al-Ash’ariy” yatakuwa hayana maana.

Ama kumpima Imamu kwa mezani ya wafuasi wake, ni minhaj sahihi kabisa ikiwa wafuasi wake ni wanavyuoni waliochukua elimu kutoka kwake tabaka baada ya tabaka na ikawa wanavyuoni hao ni waaminifu. Kauli ngapi utazikuta katika vitabu kuwa ni kauli za Imamu fulani na Imamu fulani, lakini mara zikapingwa kwa sababu wanafunzi wao wamewanukuu Maimamu hao kinyume na kauli hizo. Abu ‘Ali Al-Faarisi, kwa mfano, kasemwa kuwa ni miongoni mwa wenye kukataa majazi, wakati Al-Qannubi anasema:

Na hili halikuthibiti kutoka kwa Abu ‘Ali, kwani mwanafunzi wake Ibn Jinni amesimulia kutoka kwake akiyakubali majazi, naye ni mwenye kumjua zaidi Sheikh wake.403

Kwa hivyo, wanavyosema wanafunzi kuhusu mwalimu wao ni kipimo kizuri zaidi cha kuijua itikadi ya mwalimu. Wanavyuoni wa Al-Ash’ariyya (Sunni) wamechukua elimu hio kutoka kwake na wakapokezana tabaka 402 - Tumetaja marejeo chini katika nukulu inayofuata. 403 - Al-Qannubi Al-Saifu Al-Haad uk. 56. Na kauli hio ya Abu Ali Al-Faarisi iliyonukuliwa na mwanafunzi wake Ibn Jinni iko katika kitabu Al-Khasaais j. 2, uk. 309, ambapo Abu Ali Al-Faarisi anasema hivi: مجازا الواحد على الجماعة لفظ Nikalitumia nenoفوضعتla wingi kumaanisha mmoja kimajazi.

110

Page 111: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

moja baada ya nyengine. Na kama wao ni waongo katika madai yao ya kumfuata Abu Al-Hasan katika itikadi, basi kwanini tena wawe wakweli katika madai yao ya kumfuata Al-Shafi katika fiq-hi?

Na sijui je Sheikh wenu Al-Fawzaan alikuwa katika haki au katika batili alipoikataa riwaya ya Al-Bayhaqi kutoka kwa Al-Imamu Ahmad, na akadai:

اإلمام كتب من يوثقه ولم عنه يثبت لم أحمد اإلمام إلى نسبه كتب ما أوالبيهقي أصحابه، وذكر

الصفات - - تأويل من شيء عنده الله رحمه البيهقي ألن ؛ يعتمد ال لذلكهذا في بنقله يوثق فال

النقل في يتساهل ربما ألنه الباب

Na yale ambayo (Al-Bayhaqi) kayahusisha na Al-Imamu Ahmad hayakuthibiti kutoka kwake wala hakuyathibitisha kutoka katika vitabu vyake Al-Imamu (Ahmad) au vitabu vya wafuasi wake. Ama Al-Bayhaqi kuyataja hayo hilo si la kutegemea kwani Al-Bayhaqi (r.a.) ana kitu kuziletea ta-awil sifa (za Allah), basi katika mlango huu nukulu zake haziaminiki, kwani huenda akapuuza katika kunukuu.404

Je yeye Al-Fawzaan atakuwa yuko sawa kwa kutoa hoja hio ya kutokuwepo kauli hio katika vitabu vya wafuasi wa Al-Imamu Ahmad; na Juma Al-Mazrui atakuwa hayuko sawa – bidhaa moja itapimwa kwa mezani mbili! Au tutakuwa sote tumetoa hoja batili? Na pamoja na yote hayo, kauli ya Al-Fawzaan ni batili kwani yeye kamdhoofisha Al-Bayhaqi katika mlango mzima huu wa Sifaat. Kafanya hivyo ili kuitetea itikadi yake ya tajsim na tashbih. Bali ikiwa Al-Fawzaan anatoa hoja kwa kitu ambacho “hakipo katika vitabu vya wafuasi wa Ahmad” vipi isiwe sahihi kwa Juma Al-Mazrui kutoa hoja kwa kitu ambacho kipo katika vitabu vya wafuasi wa Abu Al-Hasan Al-Ash’ari?

Ama kuhusishwa Mashafi na Al-Imamu Al-Shafi katika fiq-hi na wakahusishwa na Abu Al-Hasan katika itikadi, sababu yake ni kuwa Abu Al-Hasan alikuwa katika zama ambazo mivutano ya kiitikadi ilipamba moto zaidi na kwa hivyo yeye akawa ni mmoja wa viranja wenye kujadiliana na watu juu ya jambo hilo. Hapo wafuasi wake waliokubaliana naye ndio wakahusishwa naye. Wakati Al-Imamu Al-Shafi, yeye katika zama zake, japo kuwa mambo ya tafauti za itikadi yalikuwepo, lakini, fiq-hi ilipamba moto zaidi. Na sijui wewe Kasim Mafuta hapa unastaajbu nini kuhusishwa Mashafi na Al-Imamu Al-Shafi katika fiq-hi na wakahusishwa na Al-Ash’ari katika itikadi na tauhid? Unastaajabu nini, nanyi munawahusisha

404 - Al-Fawzaan Ta’aliqaatu ‘Alaa Kitaabi Al-Salafiyya Laysat Madhaban uk. 33.

111

Page 112: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Ibadhi na watu Nahrawaan (r.a.) au wale munaowaiita Khawaarij katika fikra za kisiasa na – kimakosa – munawahusisha na Abdullah bin Ibadhi (r.a.) katika fiq-hi.405 Na wengine – nao ndio walio sahihi – wanawahusisha Ibadhi na watu Nahrawaan katika fikra za kisiasa na wanawahusisha na Al-Imamu Jabir (r.a.) katika fiq-hi. Mahanafi nao wanahusishwa na Abu Hanifa katika fiq-hi na wanahusishwa na Abu Mansur Al-Maaturidi katika itikadi.406 Na katika Sunni kuna fikra nyingi tafauti, ambapo utakuta fiq-hi ni ya Kishafi au Kimaliki au Kihanafi lakini itikadi ni za Kisufi.

Kisha, baada ya hayo yaliotangulia, Kasim Mafuta akanena:

Na wanavyuoni walio lithibitisha suala hili la kutubia kwake,407 kuacha misimamo hiyo potofu na kushikamana na msimamo wa Salaf Swalih na kuandika kitabu “al-Ibana”, ni hawa wafuatao:1- Abul-Qasim Aliy bin al-Hasan bin Hibatu-llaahi Ibn Asaakir aliyefariki mwaka 571 H, katika kitabu chake “al-Tabyiin” ukurasa wa 28.2- Imamu al-Baihaqiy al-Shaafiy aliyefariki mwaka 458 katika kitabu chake al-I’tikad ukurasa wa 31na 32.3- Imamu al-Dhah’biy aliyefariki mwaka 748 H katika kitabu chake “al-Uluwu” ukurasa wa 160.4- Imamu Ibn al-Imadi aliyefariki mwaka 1098 H katika kitabu chake “Shadharaatul-Dha’hbi” ukurasa wa 303.5- Imamu Abul-Hasan al-Sayyid Murtaza al-Zabidiy katika kitabu chake “It’hafu Saadatil- Mutaqina” juzuu ya 2 ukurasa 2.6- Imamu Ibn Kathir al-Qurashiy al-Shaafiy aliyefariki mwaka 774H, katika kitabu chake “al-Bidayatu wal-Nihayah” juzuu ya 11 ukurasa wa 187.7- Imamu Taaju-Din Abu Nasri Abdul-wahab bin Taqiyu-Din al-Subkiy al-Shaafiy aliyefariki mwaka 771 H, katika kitabu chake “Twabaqaatu al-Shaafi’iya al-Kubraa” juzuu ya 2 ukurasa 246. Na wengi katika maulama ambao hatukuwataja, wote hao wamekiri na kuthibitisha katika vitabu vyao tulivyo vitaja kuwa Abul-Hasan aliziwacha itikadi zote hizo potofu na kushikamana na itikadi sahihiya Salaf Swalih na akatunga kitabu “al-Ibana”.408

Hayo ndio maelezo ya Sh. Kasim Mafuta, nayo mantiki yake haitafautiani na mantiki ya maelezo yake yaliotangulia kabla kidogo. Nami, kwa kuanzia, ninasema kwamba kubadilika kwa Al-Imamu Abu Hasan kutoka katika madhehebu ya Mu’utazila na akawa Sunni, hilo halina khilafu. Ingawa hali

405 - Nayo ni makosa ya wazi, kwani hakuna mas-ala hata moja katika fiq-hi nzima ya Kiibadhi ilio rai ya Abdullah bin Ibadhi. 406 - Dr. Wahbat Al-Zuhaili Usulu Al-Fiq-hi j. 1, uk. 123. 407 - Yaani Al-Imamu Abu Al-Hasan Al-Ash’ari. 408 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 21.

112

Page 113: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

hio haithibitishi usahihi wa madhehebu moja dhidi ya mengine, kwani kuacha madhehebu moja na kwenda katika madhehebu mengine mara nyingi kunatokana na ufahamu wa mtu: si kutokana na uhakika wa jambo ulivyo wala si kutokana na wahyi. Na ufahamu unaweza ukawa sahihi na unaweza ukawa si sahihi. Vyenginevyo, Masuni kila leo wanamiminika katika Ushia, wengine kwa pesa na wengine kwa imani, nawe huamini kwamba Shia ni madhehebu sahihi. Kuna watu wametoka Ibadhi wakaingia Suni na wengine wametoka Suni wakaingia Ibadhi, kila mmoja kwa mujibu wa alivyofahamu. Lakini khilafu iko katika masuali haya:

a) Je Abu Al-Hasan alikuwa na itikadi kama za Kiwahabi, ambazo munaziita kuwa ni itikadi za Al-Salaf, nao si uwongo: kweli ni itikadi za Al-Salaf, lakini Al-Salaf wenyewe ni akina Ibn Batta na Al-Sijzi – si Masahaba.

b) Je kitabu Al-Ibana ni katika utunzi wake.Ninasema: kuhusu nukta ya kwanza, hata hicho kitabu Al-Ibana kikiwa kweli ni chake, basi Abu Al-Hasan hakukubaliana na nyinyi 100% kama ulivyoona baadhi ya nilioyanukuu kabla; na kukubaliana kwa baadhi ya mambo kuko katika madhehebu zote hata zile zilizo mbali mbali zaidi. Bali Sheikh Al-Harari kamnukuu Al-Imamu Abu Al-Hasan akisema katika kitabu chake Al-Nawaadir: “Atayeitakidi kwamba Allah ni kiwiliwili, basi huyo hakumjua Mola wake, naye ni kafiri”.409 Na hili – kama unavyoona – ni tafauti kabisa na yale yalionukuliwa na Ibn Taymiyya, kwa kuyakubali, kutoka kwa Salaf wake wa Kihanbal. Bali ukirudi katika kitabu Tabyiinu Kadhibi Al-Muftari cha Ibn ‘Asaakir, utaona katika sehemu kadha wa kadha anasema: “Mahashwiyya Mujassima wakasema kadha wa kadha, na Mu’utazila na Jahmiyya wakasema kadha wa kadha; Al-Imamu Abu Al-Hasan Al-Ash’ari akashika njia ya kati na kati, akasema kauli kadha” yaani akasema kauli iliotafauti na ile ya “Mahashwiyya Mujassima, Mu’utazila na Jahmiyya”.

Na kuhusu nukta ya pili, ninasema kwamba ikiwa wako waliothibitisha kwamba kitabu hicho ni cha Abu Al-Hasan, basi pia wako waliokanusha kama tulivyonukuu maneno ya Al-Harari na hoja yake ni madhubuti sana japo kuwa Sh. Kasim bin Mafuta hakuipenda. Lakini hatima, natukubaliane kwamba kweli wanavyuoni hao wamekitaja kitabu hicho kuwa ni kitabu cha Al-Imamu Al-Ash’ari, je kukitaja kwao huko tayari kumekifanya kitabu hicho kuwa kimethibiti kutoka kwake? Basi kwanini tena Mawahabi wakikanushe kitabu Al-Fawaaidu Al-Mushawwiq ilaa ‘Uluumi Al-Qur-aan cha Ibn Al-Qayyim ambacho ndani yake kajikanganya kwa kuzungumzia majazi ambayo kayakanusha katika kitabu chake chengine alichokiita Al-

409 - Al-Harari Al-Maqaalaatu Al-Sunniyya uk. 90.

113

Page 114: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Sawaa’iqu Al-Mursala! Utakumbuka kwamba kitabu hicho Al-Fawaaidu Al-Mushawwaq nacho pia kimetajwa na kundi la wanavyuoni kama:

1) Ibn Hajar katika Al-Dururu Al-Kaamina.410

2) Abu Al-Mahaasin katika Al-Nujumu Al-Zahira.411

3) Al-Safadi katika Al-Wafi.412

4) Al-Suyuti katika Bughyatul Wu’aat.413

5) Al-Shaukani katika Al-Badru Al-Taali’u.414

6) Haji Khalifa katika Kashfu Al-Dhunun.415

Kayaeleza hayo Imamu Al-Sunna Wal Usul Al-Qannubi katika Al-Saifu Al-Haad.416 Ninasema: Halkadhalika kitabu cha Al-Dhahabi Zaghlu Al-‘Ilmi, Mawahabi hawakikubali kwamba kweli ni kitabu cha Al-Dhahabi nacho kimetajwa na wanavyuoni wengi akiwemo Al-Sakhaawi. Na sababu zao zilizowapelekea kukikataa kitabu hicho zinafanana na zile alizozitoa Sh. Abdullah Al-Harari katika kukanusha kuhusishwa kitabu Al-Ibaana na Abu Al-Hasan. Ingawa sababu nyengine walizozitoa Mawahabi katika kukataa kwao kuhusishwa kitabu hicho na Al-Dhahabi si sababu sahihi. Wanasema, kwa mfano, Al-Dhahabi hawezi kusema maneno hayo kwa Sheikh wake Ibn Taymiyya kwani alikuwa akimuheshimu sana hususan ukizingatia ukweli kwamba katika vitabu vyengine alimsifu. Lakini hilo linawabomokea katika matukio kadha wa kadha ya kihistoria ambapo wanavyuoni kadha wa kadha walikuwa vipenzi mara wakatafautiana katika kitu na mapenzi yakageuka kuwa uadui. Kwa leo tunashuhudia kwamba Al-Shawish na Al-Istambuli nao ni wanafunzi wa Al-Albani si chini ya miaka arubaini, nao walikuwa wakimsifu naye akiwahimidi, lakini pamoja na hayo, hatimae alichafukiana na wanafunzi hao na wakamshambulia vikali mwalimu wao katika vitabu na barua za wazi. Na watu wangapi walikuwa marafiki vipenzi wa Al-Imamu Ahmad, kama vile Al-Imamu Al-Husain Al-Karabisi, na hatimae wakachafukiana na kukafirishana. Bali tazama yale ulioyaandika wewe mwenyewe kuhusu Al-Imamu Abu Al-Hasan Al-Ash’ari ambaye alikuwa Mu’utazili. Ninasema: huyu alikuwa katika madhehebu hio kwa kipindi kisichopungua miaka arubaini, kisha akageuka kuwa ni adui wao mkubwa. Kwa hivyo, utaona kwamba sababu hiohaina nguvu za kihistoria.

La mwisho tulililobakiwa nalo katika madai ya Kasim Mafuta na watu wa skuli yake ni suala la kuwa Al-Imamu Al-Ash’ari alirudi katika itikadi zao!

410 - Ibn Hajar Al-Dururu Al-Kaamina j. 3, uk. 400. 411 - Abu Al-Mahaasin Al-Nujumu Al-Zahiraj. 10, 249. 412 - Al-Safadi Al-Wafi j. 2, uk. 270. 413 - Al-Suyuti Bughyatul Wu’aat. 414 - Al-Shaukani Al-Badru Al-Taali’u. 415 - Haji Khalifa Kashfu Al-Dhunun. 416 - Al-Qannubi Al-Saifu Al-Haad uk. 56.

114

Page 115: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Ninasema kwamba hii ndio propaganda yenu kwa kila mwanachuoni kiongozi aliyekinyume nanyi, tangu zamani katika zama za watangulizi wenu Banii Umayya hadi leo:

1) Al-Imamu Jabir bin Zaid katungiwa riwaya417 kwamba si Ibadhi, lakini Imamu wenu wenyewe Ibn Ma’iin akazirudi riwaya hizo na kubainisha kwamba Jabir bin Zaid ni Ibadhi.

2) Al-Imamu Al-Ghazali katubia na karejea katika itikadi za mungu mwenye sura ya Adam! Nayo ni madai yaliobomolewa hoja moja moja na Al-Imamu Badru Al-Din Al-Khalili.418

3) Sheikh Sulaiman bin ‘Abdil-Wahhaab, karejea katika itikadi yenu!419

NATURUDI KATIKA RIWAYA ZA MUNGU MWENYE MIKONO

Baada ya kuyatazama maneno ya Sh. Kasim Mafuta na kubainisha udhaifu wake, sasa naturudi katika riwaya zenu za mungu mwenye viungo! Ninasema: jambo jengine la kuzingatia hapa ni lile lenye kuthibitishwa na riwaya za mabwana wa skuli hio ya tajsim, nazo ni riwaya zinazotongoa kinagaubaga kwamba Allah hakumuumba kwa mkono wake yaani kwa kumshika – kama riwaya nyengine zinavyosisitiza – isipokuwa Adam, na riwaya nyengine zimezidisha, Taurati na Pepo; na nyengine zimezidisha lulu na mengineo. Anasimulia aliyekizua kitabu kiitwacho Al-Sunna alichobandikwa nacho Ibn Ahmad:

: وغرس بيده التوراة وكتب بيده آدم خلق بيده أشياء ثالثة خلق الله إنبيده عدن جنة

Hakika ya Allah kaumba vitu vitatu kwa mkono wake: kamuumba Adam kwa mkono wake, na akaandika Taurati kwa mkono wake na akaipanda (miti ya) Pepo ya Adeni kwa mkono wake!!!420

Anasema Dr. Muhammad Khalili Harras:

بال ����فتخ الثالثة هذه في ����صيص المخلوقات لبقية مشاركتها مع ذكربال دال ��وقوعها ى����عل قدرة

. زائد بأمر اختصاصها

417 - Riwaya hizo zote zina sanad dhaifu. Kazijadili Sh. Ali Al-Hijri katika kitabu chake Al-Ibaadhiyya Wa Manhajiyyatul Bahth. Nitazinukuu katika juzuu maalumu ya kitabu hiki inshaa Allah. 418 - Rejea katika Jawaahiru Al-Tafsir Juz’u Khaas cha Sheikh Al-Khalili uk. 343-402. 419 - Muhammed Bashir Al-Sahsawaani Al-Hindi Siyaanatu Al-Insan uk. 496. 420 - Ibn Ahmad Al-Sunna j. 1, uk. 296, Hadithi na. 573.

115

Page 116: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Kuvihusisha vitu vitatu hivi kwa kuvitaja pamoja na kuwa viumbe vyengine vinashirikiana na hivi katika kuumbwa kwake kwa uweza (wa Allah) kunabainisha kwamba (vitu vitatu hivyo) vimehusishwa kwa jambo la ziada.421

Ninasema: lakini riwaya hio ni dhaifu hatuna haja ya kuitegemea katika kuthibitisha itikadi. Anasema muhakiki wa kitabu hicho: “Sanad yake ni dhaifu”. Hivyo ndivyo alivyosema, navyo ndivyo ilivyo kwani katika sanad yake kuna Ibrahim bin Al-Hakam bin Abaan naye ni dhaifu.422

Bali, mbali na udhaifu wa sanad yake, riwaya hio katika kuvihusisha kwake vitu vitatu hivyo, inagongana na riwaya nyengine. Kama riwaya iliotaja vitu vitatu hivyo kisha ikazidisha cha nne kwa kusema:

وأخرجي : أرضي حتى امتدي فقال قضيبا فيها فغرس بيده لؤلؤ ودملجفأخرج بإذني فيك ت�����ما

والثمار األنهار

Na (Allah) alichanganya lulu kwa mkono wake basi alikipanda kigongo kisha akasema: ‘Kua mpaka ufike katika ardhi yangu na yatoe yalio ndani yako kwa idhini yangu, basi ikatoa mito na matunda.423

Anasema muhakiki wa kitabu kuhusu riwaya hii:بن عبدة إسناده ترجمة تفي على لها أقف ولم خالد

Katika sanad yake kuna ‘Abda bint Khalid wala sikuona alipotarajimiwa.

Ninasema: bali riwaya hio ni mursala haina hoja ndani yake. Nayo pamoja na iliotangulia kabla yake zinagongana na riwaya nyengine inayosema:

بيده القلم وخلق بيده عرشه وخلق بيده جبريل وخلق بيده آدم الله خلقبيده التوراة وكتب

بيده غيره عليه يطلع ال عنده الذي الكتاب وكتب421 - Dr. Muhammad Khalil Haraas Shar-hu Al-’Aqiidati Al-Wasatiyya uk. 57. 422 - Anasema Ibn Ma’in: “Si mwenye kuaminika”. Na akasema tena: “Ni dhaifu; si chochote (hana maana)”. Anasema Al-Nasai: “Si mwenye kuaminika wala haandiki Hadithi zake”. Anasema Abu Zur’a: “Si madhubuti, naye ni dhaifu”. Al-Juzajaani na Al-Azdi wanasema: “Ni mwenye kuporomoka (dhaifu sana)”. Kasema Muhammad bin Asad Al-Khushuni: “…naye kwa wanavyuoni wetu ni dhaifu”. Anasema Ibn ‘Adeiy: “Na balaa yake ni kwamba Hadithi mursal kutoka kwa baba yake yeye alikuwa akiziwasilisha, na yote alioyasimulia yeye basi hafuatiwi na (mpokezi mwengine)”. Anasema Al-Daraqutni: “Dhaifu”. Anasema Al-Fasawi: “Hawatafautiani juu ya udhaifu wake”. Anasema Al-Hakim: “Si madhubuti kwao”. Anasema Al-’Uqaili: “si chochote: si mwenye kuaminika”. Ibn Hajar Tahdhibu Al-Tahdhib j. 1, uk. 100, tarjama na. 205. 423 - Ibn Ahmad Al-Sunna j. 1, uk. 297, Hadithi na. 574. Tazama hii lugha yenyewe inavyofana mno na lugha ya Bibilia. Wallahu Al-Musta’aan!

116

Page 117: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Allah kamuumba Adam kwa mkono wake na akamuumba Jibrilu kwa mkono wake na akaiumba Arshi yake kwa mkono wake na akaiumba kalamu kwa mkono wake na akaiandika Taurati kwa mkono wake na akakiandika kitabu, ambacho kiko kwake hakuna yoyote aliyekiona ila Yeye mwenyewe tu, kwa mkono wake. 424

Anasema muhakiki: وردان وهو ترجمة على له أقف لم من إسناده في

Katika isnad yake kuna mtu ambaye sikuona alipotarajimiwa, naye ni Wardaan.

Ninasema: pia yumo ndani yake Haudha bin Khalifa naye wametafautiana. Wakati Al-Imamu Ahmad anasema: “Hadithi zake ni zenye kufaa sana, natarajia ni mkweli”, Ibn Ma’in anasema: “Dhaifu: hakuwa mwenye kuhimidiwa”.425 Na pamoja na yote hayo matn ya riwaya hio inagongana na mutun zilizotangulia.

Kwa hali yoyote ile ninachotaka kukieleza hapa ni kuwa, ikiwa riwaya hizi zinayahusisha mambo hayo yaliotajwa kwamba ndio mambo mahususi alioyaumba Allah kwa mkono wake kama alivyotoa hoja Dr. Muhammad Khalil Haraas,426 na wengine, basi ni wazi kwamba neno mikono katika Aya kama: ماء بأييد بنيناها والس Na mbingu tumeziumba kwa mikono yetu (mingi zaidi ya miwili), na Aya kama: ا لهم خلقنا أنا ي��روا أولم مم

أي���دينا عملت ... Na hawaoni wao kwamba tumewaumbia yale yaliofanywa na mikono yetu (mingi zaidi ya miwili), halina maana ya mikono ya kweli. Sitaki kusema kwamba hii ni hoja sahihi kwa mujibu wetu, lakini ninataka kudai kwamba kwa misingi yenu ewe Sheikh Kasim Mafuta na kwa mujibu wa riwaya zenu hizo, basi hali itakuwa hivyyo. Vyenginevyo hakuna maana ya kuhusishwa vitu hivyo kwamba ndio tu vilivyoumbwa kwa mkono! Jambo la tatu la kuzingatia katika Aya hizo na zilizo mfano wa hizo ni kuwa Aya hizo zimetaja neno mkono. Bila shaka Allah alipozungumza na sisi alizungumza kwa lugha tunayoijua nayo ni lugha ya Kiarabu ilio fasihi. Sasa lugha ya Kiarabu haitumiki ila kwa njia mbili tu: hakuna ziada:

1) Njia ya hakika. Yaani kutumika kwa neno fulani katika maana yake ya uhakika. Na maana ya uhakika wa neno ni ile ambayo likitajwa tu

424 - Ibn Ahmad Al-Sunna j. 1, uk 300 , Hadithi na. 583. 425 - Ibn Hajar Tahdhibu Al-Tahdhib j. 11, uk. 65-66, tarjama na. 116. 426 - Na kitabu chake hicho kimerejewa na ‘Abdul-Razzaaq ‘Afifi mkuu wa Ansaaru Al-Sunna na kupitiwa na kusahihishwa na Sh. Ismaa’il Al-Ansaari.

117

Page 118: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

neno hilo basi watu hawaifahamu ila maana hio. Na linapotajwa neno hilo lakini ikakusudiwa maana nyengine basi maana nyengine hio au hizo huwa hazifahamiki ila kwa kuwepo kwa vifuatanishi vya maneno (qarina) vilivyolitoa neno hilo katika maana yake ya uhakika. Ile maana inayofahamika papohapo ( إلى يتبادر الذيbaada ya kutajwa kwa neno bila (الذهن kuhitajika kuwepo kwa vifuatanishi vya maneno ndio maana ya uhakika. Kwa mfano nikitamka neno gari. Hapa tayari nimeshafahamika kwamba ninakikusudia chombo maalumu kilichoundwa kutokana na vyuma na kutiwa maringi na usukani kinachotumika kwa shughuli za usafiri. Kwa maana hii, jina “gari” ni uhakika wa chombo hicho. Ama ikiwa nitasema “Saidi! A! Yule ni gari moshi bwana!” Nasi tunaelewa vyema kwamba Said si gari moshi, lakini nimemwita hivyo ili kumfananisha na gari moshi kwa sababu anavuta sigara sana, kila wakati anatoa moshi tu kama treni! Au Omari ni gari. Yaani anakwenda sana: hatulii: mara huku mara kule. Katika lugha kama hizi, neno gari linakuwa halikutumika katika maana yake ya uhakika.

2) Njia ya majazi. Njia hii ni kulitumia neno kinyume na ile maana yake ya asili ambayo inafahamika papohapo kwa kulitamka tu neno hilo. Kama tulivyolitumia neno gari au gari moshi kumwita Said. Waarabu wanaitumia sana njia hii ya pili, na imetumika sana katika Qur-ani na Hadithi kama tutavyobainisha katika mlango wake maalumu unaohusu suala la majazi.

Sasa kama umeyaelewa hayo, basi elewa kwamba maana ya uhakika – katika lugha ya Kiarabu na lugha nyengine – ya neno mkono ni hiki kiungo chenye mfupa na nyama. Huu ndio mkono wa hakika. Na dalili ya hayo, ni kuwa haikupokewa kamwe kutoka kwa Waarabu kwamba kuna mkono wa hakika ila huo, na kwa hivyo ukitajwa mkono bila ya kuwepo qarina basi Mwarabu yoyote – wa zamani na wa leo – hafahamu ila kiungo hicho. Sasa suala la kujiuliza ni kuwa je kweli Mungu ana mkono huo wenye mfupa na nyama ili mkono wake uweze kuwa mkono wa hakika? Ukinambia: “Ana mkono unaolingana na utukufu wake, haufanani na kitu”. Nitakujibu kwamba wewe sasa unaleta ta-awil ambayo umeikataa hapo mwanzo. Ukiniuliza: “Vipi nimeleta ta-awil?” Nitakujibu kwamba ta-awil maana yake ni kulitoa neno katika maana yake ya asili au ya uhakika na kulipeleka katika maana nyengine kwa sababu ya kuwepo dalili zilizoonesha hivyo. Sasa ikiwa maana ya asili au ya hakika ya neno mkono ni hiki kiungo chenye mfupa na nyama, je katika maneno yako: “Ana mkono unaolingana na utukufu wake, haufanani na kitu” iko wapi maana ya mkono wa

118

Page 119: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

uhakika? Ukiniambia: “Tafsiri hio imekuwa haina budi kwani Allah anasema: شيء كمثله Hana) ليس mfano wa kitu). Kwa hivyo, ukizifungamanisha Aya zilizosema kuwa Allah ana mikono na Aya hii, natija ni kuwa Allah ana mikono lakini haifanani na kitu”. Ukiniambia hivyo, nitakujibu kwamba:

a) Kitu kimoja kikipewa jina la kitu chengine lakini ikawa vitu viwili hivyo havifanani, basi bila shaka kimoja ndio hakika na cha pili kimetumika kama ni mithali tu ili kufananishiwa na cha kwanza. Vipi hiki kiwe ni kile ilhali kile na hiki havifanani – ni tafauti? Ni wazi kwamba kimoja ni hakika na cha pili ni mithali. Ikiwa Allah ana mkono wa uhakika lakini haufanani na kitu chochote wakati katika lugha aliotuumbia sisi na akazungumza nasi kwayo mkono tunaujua ukoje, basi ni wazi kwamba huo wake si mkono wa uhakika. Hili ni suala la wazi liman kaana lahu qalbun au alqa ssam’a wahuwa shahiid kwa mwenye moyo au atayetega sikio naye yuko hadhiri! Ukiniambia “Aaa! Mkono wake ni hakika kwake na wetu ni hakika kwetu: kila mmoja kwa mujibu wa alivyo”. Nitakujibu basi ni kitu gani kinachozuia Qur-ani isiambiwe kuwa ina mikono miwili ya hakika kwa mujibu wa ilivyo hali yake, ilhali Allah katika Aya kadha wa kadha kasema kuwa Qur-ani ina mikono miwili? Halkadhalika rehema ya Mwenyezi Mungu pia imetajwa katika Qur-ani kuwa ina mikono miwili; halkadhalika mazungumzo yametajwa hivyo hivyo kuwa yana mikono miwili?427

b) La pili ni kuwa, hicho kitendo cha kuzifungamanisha Aya na kuitoa moja katika maana yake ya dhahiri au ya asili ndiko kufanya ta-awil ambako munakuuita tahrif (kupotosha) kwa Aya. Sasa vipi munakikimbilia huku kitu ambacho kule munakikimbia?

c) Tatu ni – kama tulivyosema kwamba – Aya zimeonesha kwamba mikono hio ni mingi na nyinyi hamukubali kwamba mikono hio ni mingi: munasema kwamba ni miwili tu, sasa vipi “Munaamini baadhi ya Kitabu na munakikataa baadhi ya Kitabu?” Ukiniambia: “Aaa! Katika lugha ya Kiarabu hutumika tatu kumaanisha moja na moja kumaanisha nyingi na kumaanisha mbili”. Hili nimeshakujibu kwamba hayo ndio majazi wenyewe, vyenginevyo wapi umepata kusikia kwamba uhakika wa moja ni tatu na uhakika wa tatu ni mbili?

427 - Nitakunukulia Aya hizo baadae kidogo.

119

Page 120: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

MAELEZO ZAIDI KUHUSU AYA ZA MKONO WA MUNGU

Baada ya maelezo hayo na mjadala huo wa kubuni, ndugu msomaji, sasa niruhusu nikueleze machache kuhusu Aya hizo na zilizo mfano wa hizo. Hapa kuna mambo mengi ambayo ni lazima uyazingatie ili uweze kujua nini maana ya mkono katika Aya hizo na zilizo mfano wa hizo:

Mosi: neno mkono katika lugha ya Kiarabu limekuja kwa maana nyingi sana kama ifuatavyo:1) “Kiungo cha mwili nacho kinaanzia katika mabega hadi nchani kwenye

vidole”.428 Na hii ndio maana ya msingi, ya uhakika na ya asili ya neno hilo, kwa hivyo unapodai kuwa Allah ana mkono wa kweli basi ni lazima udai kuwa ana mkono ulio hivyo kama uliotajwa hapo, na kama unadai kuwa mkono wake hauko hivyo, basi elewa kwamba huo si mkono wa hakika na wa kweli.

2) Kitu cha kukamatia kama kikamatio cha begi, kisu au mlango. Waarabu wanasema: “ والفأس والسكين السيف ,Mkono wa upanga) ”يدwa kisu na wa shoka)429 yaani mipini ya vitu hivyo. Mipini imeitwa mikono kimajazi kwa sababu mkono wa binaadamu ndio unaoshika sehemu hizo wakati anapovihitajia kuvitumia.

3) Mkono wa nguo.430 Nao si mkono hakika lakini umepewa jina hilo kwa sababu mtu anaweka mkono wake humo.

4) Neema na ihsani.431 Kama alivyosema mshairi Bishr bin Abi Khaazim: يشكرونها يد قومي في لك Kwa) تكن jamaa zangu, wewe

utakuwa na mkono ambao wanaushukuru),432 yaani unawafanyia ihsani.

5) Utawala. 433 6) Uwezo.434 7) Nguvu. Waarabu wanasema: “ به لي يدان ذما األمر ا ” (Sina mikono

miwili kwa jambo hili),435 yaani siliwezi. 8) Kundi.436 Waarabu wanasema: “ يد على: هم يد وهم أنصاره،

Wao) ”غيرهم ni mkono, yaani watetezi wake…….na wao ni

428 - Al-Mu’ujamu Al-Wasiit j. 2, uk. 1076. Lisanu Al-’Arab j. 15, uk. 437. 429 - K.h.j. 430 - K.h.j. 431 - K.h.j. Lisanu Al-’Arab j. 15, uk. 440.432 - Lisanu Al-’Arab j. 15, uk. 439. 433 - K.h.j. Lisanu Al-’Arab j. 15, uk. 440.434 - K.h.j. Lisanu Al-’Arab j. 15, uk. 440.435 - K.h.j. Lisanu Al-’Arab j. 15, uk. 440-441.436 - Lisanu Al-’Arab j. 15, uk. 440.

120

Page 121: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

mkono juu ya wengine, yaani wameungana na kuwa kitu kimoja dhidi ya wengine”. 437

9) Kumiliki. Waarabu wanasema: “ يدي في ملكي هو في أي ” (Kiko mikononi mwangu, yaani katika milki yangu”, 438 wala si lazima kwamba uwe umekishika kitu chako hicho, bali pengine wewe uko Chokocho na mali yako iko Pongwe.

10) Dhamana katika rehani.439 11) Kutii na kusalimu amri. Waarabu wanasema: “ لك يدي وأعطى هذه

Huu) ”يده mkono wangu kwako na katoa mkono wake, yaani kasalimu amri na kunyenyekea).440 Na katika Hadithi, imesemwa katika dua: “ لك يدي لك وهذه وانقدت لك استسلمت أي ” (Na huu mkono wangu kwako, yaani nimesalimu amri kwako na nimekufuata wewe”. 441 Pia wanasema Waarabu “ عن الجزية أعطى

واستسالم: يد ذل عن ” (Katoa jiz-ya kutokana na mkono, yaani katoa jiz-ya hio kwa udhalili na unyenyekevu). 442

12) Kula. Waarabu husema: “ كل أي يدك ,Weka mkono wako) ”ضعyaani kula).443

13) Majuto. Waarabu wanasema: ندم إذا يده في Imeanguka) سقطmkononi mwake, yaani kajuta). 444

14) Bei. Waarabu wanasema: باليدين ا أو اليدين بتعته (Nimeinunua mikono miwili au kwa mikono miwili) yaani غالي بثمنين kwa bei mbili ya ghali na ya rahisi. 445 ورخيص

15) Na miongoni mwa majazi ya neno mkono ni kusema: في يده ضربفيه كذا شرع أي (Kapiga mkono wake katika jambo fulani, yaani

kalianza jambo hilo). 446 16) Na Mtume (s.a.w.) anasema: السفلى اليد من خير العليا اليد

(Mkono wa juu ni bora kuliko mkono wa chini).447 Yaani mwenye kutoa ni bora kuliko mwenye kupokea.

17) Waarabu wanasema: وعلمه خرجه أي يده تحت من ورباهخرج (Katoka chini ya mkono wake, yaani kamfunza na kumlea). 448

437 - K.h.j. Lisanu Al-’Arab j. 15, uk. 440. 438 - K.h.j. Lisanu Al-’Arab j. 15, uk. 440.439 - K.h.j. 440 - K.h.j. 441 - Lisanu Al-’Arab j. 15, uk. 440. 442 - K.h.j. 443 - K.h.j. 444 - Lisanu Al-’Arab j. 15, uk. 440. 445 - K.h.j. 446 - K.h.j. 447 - K.h.j. 448 - K.h.j.

121

Page 122: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

18) Halkadhalika husema Waarabu: : سخي أي اليد طويل Ana) هوmkono mrefu, yaani ni karimu).449

Na labda lau Sheikh Kasim Mafuta aliyasoma maneno ya Imamu wake, Mu’awiya bin Abi Sufyaan, basi angelisema kuwa Al-Imamu Ali bin Abi Talib alikuwa ana mikono miwili ya kuume mmoja unaitwa Ammar na wa pili unaitwa Al-Ashtar! Kwani Mu’awiwa anasema:

Ali alikuwa na mikono miwili ya kuume mmoja nimeukata siku ya (vita vya) Siffin, Yaani Ammar bin Yasir, na mmoja nimeukata leo, yaani Al-Ashtar”.450

Au vyenginevyo, itambidi Sh. Kasim Mafuta aseme kwamba Mu’awiya hajui lugha ya Kiarabu! Vipi anawaita watu kuwa ni mikono ya mtu mwengine?

Hio ni mifano michache katika mifano mingi iliotajwa na wanavyuoni wa lugha katika vitabu vyao kuhusu matumizi ya neno mkono kinyume na maana yake ya asili.451 Baada ya hayo, utaona kwamba matumizi yote hayo ni matumizi ya kimajazi; na matumizi ya uhakika ni yale tulioyaweka katika kifungu nambari moja. Sasa suala la kujiuliza ni kuwa je ile maana ya hakika ya neno mkono (yaani maana kwamba uhakika wa mkono ni kiungo chenye mfupa na nyama), je maana hio inamfaa Allah ili tuweze kudai kwamba Allah ana mkono wa hakika? Bila shaka jawabu iko wazi kwamba Allah hana mfupa na nyama. Au na hapa utaniambia kwamba “Mfupa anao lakini mfupa wake si kama mfupa wetu; na nyama anayo lakini nyama yake si kama nyama yetu” ili uwe ni mwenye kuthibitisha lafdhi za maneno pasina kuthibitisha maana zilizomo katika lafdhi hizo?

Ama maana hizo za kimajazi, bila shaka nyengine huwezi kuzinasibisha kwa Allah, lakini nyengine kama vile: uwezo, ihsani, neema, nguvu, utawala, kusapoti, na zilizo mfano wa hizo, ni maana zenye kulingana na utukufu wa Allah. Kilicho wajibu kwetu, ni kuitafuta maana inayokubaliana na utukufu wa Allah na kumsifu kwayo, sio kuchukua kiungo tukambandika nacho kisha tukajidanganya kwa falsafa ya “Bila mfano au bila tujuavyo”. Wapi katika lugha ya Kiarabu tumesikia kwamba kuna “Mkono lakini si kama tuujuavyo au kuna mkono lakini hauna mfano?” Hii si lugha ya Kiarabu bali wala si lugha yoyote ya walimwengu.

449 - K.h.j. 450 - Al-Tabari Al-Taarikh j. 3, 133. Ibn Al-Athir Al-Kamil j. 2, uk. 705. Maana ya mikono miwili ya kuume ni ((Wasaidizi wawili wa nguvu)). 451 - Rejea Lisanu Al-’Arab uone mifano myengine mingi.

122

Page 123: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Ama qiyas kinachofanywa na wengi wao akiwemo Sheikh Kasim Mafuta wakasema kwamba huu mfano wake ni kama sifa ya wujud (kuwepo). Ubainifu wake ni kuwa kama vile ambavyo Allah yupo na sisi tupo lakini kuwepo kwake ni tafauti na kuwepo kwetu; halkadhalika Allah ana mkono lakini mkono wake si kama mikono yetu! Halkadhalika Allah ana elimu na sisi tuna elimu lakini elimu yetu si kama elimu yake, nk. Ninasema: watu hawa hawajui yanayotoka vichwani mwao pamoja na kuwa wengine miongoni mwao wamehifadhi maelfu ya Hadithi na mengineo. Cha kufahamu ni kuwa kuna tafauti kubwa baina ya kushabihiana kwa dhati na kushabihiana kwa sifa, au kuzishabihisha dhati na kuzishabihisha sifa za dhati. Sisi viumbe tuna mikono ya uhakika yaani hivyo ndivyo dhati zetu zilivyo. Na ukisema kwamba Allah ana mikono ya uhakika, basi ina maana kuwa hivyo ndivyo dhati yake ilivyo. Kwa hivyo, utachokipata ni kuwa dhati mbili hizo zinashabihiana – dhati ya Allah imefanana na dhati ya binaadamu. Hususan ukizingatia ukweli kwamba mkono wa hakika ni huu tunaoujua: hakuna mkono mwengine wa hakika katika lugha ya Waarabu ila huo. Na hii ni tafauti na kuwa na sifa moja baina ya vitu viwili – hata baina ya viumbe wenyewe – ambazo si sifa za kihisia (pyhsical). Kwani sifa zisizo za kihisia hazipelekei kufanana kwa wasifiwa, tafauti na sifa za kihisia. Inawezekana sana tukasema kwamba Sheikh Kasim Mafuta ana elimu na tukasema kwamba Jibril ana elimu, lakini watajwa wawili hao wasifanane katika dhati wala katika sifa za elimu zao kwani elimu si sifa ya kihisia. Ama ukisema kwamba ndege ana mbawa na malaika wana mbawa, basi kila mtu tayari ameshazifikiria mbawa za malaika kwamba zinashabihiana na mbawa za ndege hata kama mbawa hizo hazifanani 100%. Kwani mbawa ni sifa ya kihisia; wenye nayo sifa hio basi lazima watakuwa wameshabihiana katika sifa hio japo kidogo: tafauti na sifa ya elimu au kuwepo.

Jengine ni kuwa sifa ya elimu na uwezo na kuwepo na zilizo mfano wa hizo, ni sifa za ukamilifu ambazo Allah huwezi kumfikiria bila ya sifa hizo. Na hii ni tafauti na sifa ya kiungo ambacho kwa uwazi kabisa ni sifa ya upungufu kwani mwenye nacho anakuwa anakihitajia katika kufanya mambo yake ya kihisia, wakati Allah Yeye ni العالمين عن غني(Katosheka kutokana na kila kilimwengu na kila mlimwengu: hana haja ya kitu).

Jambo la pili: la kulifahamu ni kuwa vilivyopewa sifa ya kuwa na mkono si lazima kwamba viwe na mkono kweli. Na kwa ukweli huu, kama

123

Page 124: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

alivyosema Bishr Al-Marisi,452 ndio maana unaweza kuwakuta Waarabu wanasema kuhusu mtu aliyekatwa mikono yote miwili kwamba “ كذا فعل

هدبي ” (Kafanya jambo kadha kwa mkono wake” ilhali yeye hana hata mkono mmoja. Kama vile ambavyo Waarabu wanatumia ibara zenye kuonesha kwamba hata kile chenye mikono, basi wakati mwengine hakikufanya kitu kwa mikono hata ikiwa itatajwa kuwa kitu hicho kimefanywa kwa mikono, kama kauli yao: “ ك السعودي جيش الملك ون

بيده Mfalme wa Suudia kaliunda jeshi la nchi yake kwa mkono) ”بالدهwake). Na bila shaka – japo kuwa mfalme wa Suudia anayo mikono lakini – katika ibara kama hii haijakusudiwa kwamba alilifinyanga jeshi hilo kwa mikono yake. Na hii ni ibara sahihi na ni Kiarabu fasihi. Na kwa hivyo, utaona kwamba Allah kavisifu vitu visivyo na mikono kwa kuvipa sifa za mikono. Anasema Allah:

ياح يرسل الذي وهو الر رحمته يدي بين بشراNaye (Allah) ndiye mwenye kutuma upepo kuwa ni habari

njema baina ya mikono miwili ya rehema yake. 453

Hio ni tafsiri ya neno kwa neno. Suala ni kuwa je rehema ya Mungu ina mikono ili misingi waliojijengea wale walioitwa Mawahabi na Maimamu wao ya kuzifasiri lafdhi za Qur-ani kama zilivyo bila ya kuzipotoa kama wanavyosema, iweze kuwa sawa?

Anasema Allah: ............... من وال يديه بين من الباطل يأتيه ( ال41) عزيز لكتاب وإنه

خلفه

Na hakika yake (Qur-ani hii) ni Kitabu kitukufu**Hakijiwi na batili kutoka katika mikono yake miwili wala kutoka nyuma yake…454

Aya hii ikiwa utaifasiri neno kwa neno kama nilivyofanya hapo, basi utapata kwamba Qur-ani ina mikono miwili. Sasa je hili ni kweli: Qur-ani ina mikono? Au tutalazimika kuifasiri Aya hii kwa mujibu wa maana nyengine zilizomo katika neno mikono ambazo ni maana za kimajazi za neno hilo na kwa hivyo – baada ya kutazama qarina iliopo katika al-mutaabaqa (muwiyano) na kwa hapa ni neno nyuma yake – tutalazimika kulitoa neno mikono katika maana yake ya uhakika na kulifasiri kwa maana ya mbele ili iwe kumepatikana al-mutaabaqa baina ya neno (nyume yake) خلفه na

452 - Bishr Al-Marisi ni mwanachuoni wa Kihanafi ambaye alitukanwa sana na ‘Uthman bin Said Al-Darimi kwa sababu ya itikidi yake ya kumtakasa Allah kutokana na viungo. 453 - Sura 25, Aya 48. 454 - Sura 41, Aya 41-42.

124

Page 125: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

neno mikono) يدي��ه yake miwili yaani kwa hapa ni mbele yake)? Vyenginevyo ikiwa tunakataa kuwepo kwa majazi na tunajilazimisha kuzifasiri Aya tafsiri ya neno kwa neno (literally) bila ya kuleta ta-awil (interpretation) basi natuseme kwamba Qur-ani ina mikono miwili ili dunia ipate kutucheka bali ipate kutuzomea? Na mfano wa Aya hio, ni Aya isemayo:

بالحق الكتاب إليك وأنزلنا الكتاب من يديه بين لما مصدقا

Na tumekuteremshia Kitabu (Qur-ani) kwa haki, hali ya kuwa (Qur-ani hio) ni yenye kukisadikisha kile kilicho baina ya mikono yake miwili katika Kitabu. 455

Na Aya isemayo:

يديه بين الذي مصدق مبارك أنزلناه كتاب وهذا

Na hiki ni Kitabu tulichokiteremsha (kwako wewe), chenye kubarikiwa (na) ni chenye kukisadikisha kile kilicho baina ya mikono yake miwili. 456

Na Aya isemayo:

سمعنا إنا قومنا يا قالوا موسى بعد من أنزل كتابا بين لما مصدقا يديه

(Majini) Wakasema: ‘Enyi kaumu yetu! Sisi tumekisikia Kitabu kimeteremshwa baada ya Musa, kinakisadikisha kile kilicho baina ya mikono yake miwili. 457

Hizo zote ni tafsiri za neno kwa neno (literally), ambazo kwa mujibu wake tunapata kwamba Qur-ani ina mikono miwili! Baada ya hayo, elewa ndugu msomaji kwamba neno mikono miwili lililotumika katika Aya hizo halikutumika kumaanisha maana yake ya asili ya mikono. Kwani Qur-ani hii imeteremka kwa lugha ya Waarabu ilio fasihi. Na maneno ya lugha ya Waarabu wakati mwengine yanatumika katika maana yake ya uhakika kama wanapolitumia neno mkono nao wanakusudia kiungo; na wakati mwengine yanatumika kimajazi (metaphorically) kama wanapolitumia neno hilo wakimaanisha maana tafauti ambazo baadhi yake tumezielezea hapo nyuma. 455 - Sura 5, Aya 48. 456 - Sura 6, Aya 92. 457 - Sura 46, Aya 30.

125

Page 126: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Neno mikono miwili katika Aya hizo tulizozinukuu limetumika kumaanisha mbele, na kwa hivyo, maana ya Aya hizo – Aya ya pili kwa mfano – ni “Na hakika yake (Qur-ani hii) ni Kitabu kitukufu**Hakijiwi na batili kutoka mbele yake wala kutoka nyuma yake”. Na hii ni maana ya kimajazi tu, vyenginevyo wapi umesikia kwamba mkono wa uhakika unaitwa mbele au mbele kwa hakika kunaitwa mkono?

Mifano myengine ni Aya kama:صدقات نجواكم يدي بين تقدموا أن أأشفقتم

Nyinyi munaogopa (ufakiri) kutanguliza sadaka baina ya mikono miwili ya kunong’ona kwenu.458

Na Aya kama::

هو إن شديد عذاب يدي بين لكم نذير إالHakuwa yeye isipokuwa ni muonyaji kwenu baina ya mikono miwili ya adhabu kali.459

Hizo zote ni tafsiri za neno kwa neno (literally). Aya ya mwanzo inazungumzia kile kipindi ambacho Waislamu walitakiwa kwamba wakitaka kuzungumza na Mtume (s.a.w.), basi watoe sadaka kwanza. Baadae hilo likafutwa. Sasa ukiwa utaifasiri Aya hio neno kwa neno, basi utapata kwamba Al-Najwaa (kunong’ona au kuzungumza kwa siri) basi kuna mikono miwili! Je kweli kunong’ona nako kuna mikono?

Hatimae ninasema kwamba tafsiri hizo zote hazitulazimu sisi, bali zinawalazimu wale wenye kusema kwamba “Allah alivyosema nasi tuseme hivyo hivyo bila ya kuleta ta-awil (interpretation au tafsiri ya ndani) yaani bila kulitoa neno katika maana yake ya asili”. Ama sisi tunasema kwamba kusifika kwa kitu fulani kwamba kina mikono – kwa mujibu wa matumizi ya lugha ya Kiarabu – si lazima kiwe kina mikono kweli au mikono ya uhakika, bali hizo ni ibara za kimajazi wanazozitumia Waarabu katika lugha yao. Waarabu wana kawaida ya kuyatumia majina ya viungo katika kumaanisha maana za kimajazi kama vile linavyotumika neno pua ikasemwa “ فالن أنف رغم Hata ikiwa pua ya fulani) ”وإن itagusa udongo (yaani itadhalilika). Na makusudio si pua bali makusudio ni kusema: “Hata ikiwa fulani atadhalilika”. Halkadhalika Waarabu husema: “ يداك Mikono yako miwili) ”تربت imegusa udongo” (yaani imebarikiwa), yaani wewe mwenyewe umebarikiwa. Na wanasema:

458 - Sura 58, Aya 13. 459 - Sura 34, Aya 46.

126

Page 127: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

“ يده في imeangushwa mkononi mwake” yaani “kajuta” kama) ”سقطilivyo katika Aya inayosema: ا أيديهم في سقط ولم .460 Tafsiri ya neno kwa neno ni: “Mpaka ilipoangushwa mikononi mwao” na tafsiri kwa mujibu wa lugha ya kimajazi ni “Na walipojuta”. Na wanasema Waarabu: “ عقبيه على فالن Fulani“ ”انقلب kageuka au kabirukia juu ya visigino vyake viwili” yaani “Karudi nyuma”. Anasema Allah: ومن

عقبيه على ينقلب .461 Tafsiri ya neno kwa neno ni: “Na atayegeuka juu ya visigino vyake viwili” yaani “Atayerejea nyuma (ukafirini)”. Basi ufasaha huu ndugu zetu wanaoitwa Mawahabi umewapita! Na kwa sababu hio, utaona kwamba Allah – subhaanahu wa ta’aala – aliposema: إبليس يا

جد أن منع��ك ما بي��دي خلقت لما تس�� (..Ewe Ibilisi! Ni nini hasa kilichokuzuia wewe kumsujudia yule niliyemuumba kwa mikono yangu miwili) wao wakasema Allah ana mikono miwili! Basi kwanini tena wasiseme kwamba Qur-ani ina mikono miwili ilhali Allah pia kayasema hayo tulioyanukuu kabla kuhusu Qur-ani? Bali Allah kasema kuwa mchana una uso – kama tutavyoeleza baadae katika mlango wa majazi -, sasa je kweli mchana una uso wa hakika? Na akasema Allah kwamba ukweli una mguu, je ukweli una mguu wa hakika? Na akasema kwamba ardhi ina mabega, je kweli ardhi ina mabega? Hizi zote ni ibara zinazotumika katika lugha hii pana na refu na yenye ufasaha ambao hauko katika lugha yoyote miongoni mwa lugha za binaadamu. Wala haina maana kwamba vitu hivyo vina viungo hivyo (mkono, mguu, uso na mabega) kweli kweli.462

Halkadhalika kule Allah kutaja kwake kwa mikono miwili na kujinasibisha nayo Yeye, haina maana kuwa ana mikono ya kweli. Na lau watu hawa walijiongozea kwa Aya ya Qur-ani Tukufu inayosema: بين تقدموا ال

ورسوله الله يدي (Musijitangulize baina ya mikono miwili ya Allah na mtume wake), na wakaitafakari vyema Aya hii, basi ingeliwatosha kuwaongoza na kuwafikisha katika nchi kavu kwa salama. Jiulize wewe vipi tusijitangulize baina ya mikono miwili ya Allah? Tukijaalia kuwa Allah anayo kweli hio mikono miwili, je sisi tunaiona hata tukakatazwa kujitanguliza baina ya mikono miwili hio ya Allah? Au kuna sehemu ambayo kisharia ukiivuuka unakuwa ndio umeitangulia mikono ya Allah? Au Allah anatukataza kutokana na kitu kisichokuwepo ili maneno yake yawe hayana maana? Na hata Mtume (s.a.w.) ambaye anayo mikono miwili, je makusudio ya Aya hio ni kuwa tusitangulie baina ya mikono yake miwili?

460 - Sura 7, Aya 149. 461 - Sura 2, Aya 143. 462 - Vyenginevyo, basi natuseme: “Mchana una uso, lakini uso wake si kama wetu wala si kama tuujuavyo sisi…na ukweli una mguu wa kweli lakini si kama wetu wala si kama tuujuavyo….na ardhi ina mabega lakini si kama yetu wala si kama tuyajuavyo” ili msingi wenu munaokwenda nao upate kusalimika.

127

Page 128: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

MADAI YASIO NA MSINGI

Ama madai ya watu hawa kwamba lau neno mikono miwili katika Aya inayosema: بيدي خلقت لما تسجد أن منعك ما إبليس يا (..Ewe Ibilisi! Ni nini hasa kilichokuzuia wewe kumsujudia yule niliyemuumba kwa mikono yangu miwili), lilikuwa na maana ya neema au nguvu, basi ingelikuwa hakuna kilichomboresha Adam zaidi kuliko Ibilisi kwani Ibilisi naye pia kaumbwa kwa uwezo wa Allah sawa na Adam na viumbe wengine wote. Ikaeleweka kwamba makusudio ya mikono miwili ni mikono ya kweli.463 Mukhtasari wa dai hilo ni kuwa:

1) Neno mikono miwili katika Aya hio halina maana ya uwezo.2) Kuamini kuwa Allah kamuumba Adam kwa mikono yake miwili ni

kwa sababu ya kumpa Adam maziyya (sifa maalum) pasina Ibilisi, kwani mengineo yanayohusu kuumbwa kwao wameshirikiana ndani yake.

3) Na kwa hivyo, kuumbwa kwa Adam ni lazima itakuwa ni kwa mikono miwili hakika, ili ipatikane tafauti baina ya maumbile ya Ibilisi na maumbile ya Adam – Adam kaumbwa kwa kushikwa kwa mikono miwili ya Allah na Ibilisi kaumbwa kwa kun fayakun tu.

Ninasema: tukirudi katika kifungu cha kwanza, jawabu ni kuwa si lazima kwamba neno mikono miwili katika Aya hio lifasiriwe kwa maana ya uwezo au neema kama wanavyolazimisha wale wenye kudai kwamba Allah ana mikono ya kweli. Bali neno hilo lina maana nyingi sana katika lugha ya Waarabu. Kilichowajibu ni kutafuta maana inayowiyana na utukufu wa Allah na ambayo inanasibiana na mtiririko wa maneno (siyaaq). Na miongoni mwa maana za neno mikono miwili zilizosimuliwa kutoka kwa Waarabu zenye kunasibiana na utukufu wa Allah na zenye kunasibiana na siyaaq ya Aya hio, ni kumaanisha ta-akid (kutilia mkazo au emphasis) kwa maana ya nafsi. Kama unavyosema نفسه kakifanya kitu kadha) فعلهyeye mwenyewe), ambapo neno (nafsuhu) نفسه linakuwa limemaanisha ta-akid (kutilia mkazo) yaani kwa kuliweka neno hilo maana inakuwa “kakifanya kitu hicho yeye mwenyewe”, maneno yeye mwenyewe ni ta-akid (kutilia mkazo), basi vivyo hivyo inasemwa katika lugha ya Waarabu فعله na maana yake ,(kakifanya kitu kadhaa kwa mikono yake miwili) بيديهni sawa na kusema نفسه .(kakifanya yeye mwenyewe) فعله Na hapa neno kwa) بيديه mikono yake miwili) – sawa na kule neno نفسه (nafsuhu) – linakuwa limetumika kumaanisha ta-akid (kutilia mkazo) yaani “kakifanya kitu hicho yeye mwenyewe”. Mfano wa Aya ambayo

463 - Tazama Dr. ‘Ali Al-Faqihi katika maelezo yake juu ya Kitabu Al-Tauhid j. 3, uk. 107.

128

Page 129: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

limetumika ndani yake neno mikono miwili kwa maana ya ta-akid yaani kwa maana ya “nafsi” ni Aya kama:

يداه قدمت ما المرء ينظر يومSiku ambayo mtu ataona yale yaliotangulizwa

(yaliotendwa) na mikono yake miwili.464

Maana ya yaliotangulizwa na mikono yake miwili ni yaliotendwa na yeye mwenyewe. Vyenginevyo, Aya hii inamuhubiri mwenye mikono na asiye na mkono hata mmoja; anayeweza kuitumia mikono yake au aliyepooza mikono; atayetenda dhambi kwa mikono au kwa miguu; atayefanya jarima kwa mikono au kwa ulimi au kwa uchi n.k. Bali inawahubiri watenda dhambi wote ikiwa dhambi hizo ni za kuchumwa kwa mikono au kwa moyo nazo ndio dhambi kubwa zao – dhambi za itikadi. Bila kusahau kwamba aghlabu ya dhambi ni za ulimi au zinaanzia na ulimi. Na aghlabu ya wanaofanya majarima makubwa duniani ni watawala na aghlabu ya majarima yao wanayafanya kwa ulimi ambapo wanakuwa wanaamrisha: “fungua baa, muueni fulani, mfungeni fulani, mpigeni fulani n.k. “. Na wote hawa Aya hio inawahusu.

Na mfano wa Aya hio ni Aya isemayo: …..يداك قدمت بما ( ذلك9) الحريق عذاب القيامة يوم ونذيقه

“Na tutamuonjesha siku ya kiama adhabu ya moto uwakao kwa nguvu**Hayo ni kwa sababu ya yale yaliotangulizwa na mikono yako miwili…..”.465

Maelezo juu ya Aya hii ni sawa na maelezo juu ya Aya iliotangulia: mwote limetumika neno mikono miwili kwa ajili ya kutilia mkazo (ta-akid). Wala haina maana kwamba watu hao wataadhibiwa kwa sababu ya dhambi zao zilizochumwa na mikono yao tu, bali wataadhibiwa kwa dhambi zote – za mkono, za mguu, za macho, za masikio, za uchi, za ulimi na za moyo – itikadi mbovu za kuukataa Uislamu.

Halkadhalika katika Hadithi, kama tulivyonukuu kabla kidogo, utakuta kuna kauli ya Mtume (s.a.w.) isemayo: يداك Mikono) تربت yako miwili itabarikiwa) yaani wewe mwenyewe utabarikiwa: si mikono miwili tu.

Kama umelielewa hilo, basi elewa kwamba maneno kwa mikono yangu miwili yaliomo katika Aya “……Nini kilichokuzuia kumsujudia yule niliyemuumba kwa mikono yangu miwili” ni taukid (kutilia mkazo) na

464 - Sura 78, Aya 40. 465 - Sura 22, Aya 10.

129

Page 130: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

maana ni “……Nini kilichokuzuia kumsujudia yule niliyemuumba mimi mwenyewe”. Kama vile ambavyo maana ya Aya isemayo: “Hayo ni kwa sababu ya yale yaliotangulizwa na mikono yako miwili…..” ni kutilia mkazo (taukid), kwa maana ya: “Hayo ni kwa sababu ya yale ulioyatenda wewe mwenywe”.

Njia ya pili ya kulielezea hilo ni kusema kwamba neno mikono miwili katika Aya: “……Nini kilichokuzuia kumsujudia yule niliyemuumba kwa mikono yangu miwili” ni tashbih.466 Yaani kama vile ambavyo mtu hakifanyi kitu kwa mikono yake miwili ila mtu huyo anakuwa kakifanya yeye mwenyewe kwa uhakika bila ya kuwa kamuamuru mtu mwengine, basi hali hii imefananishwa mfananisho wa kilugha wa kibalagha, ikasemwa kuwa Allah kamuumba Adam kwa mikono yake miwili yaani kamuumba Yeye mwenyewe. Ukiniuliza “kwani viumbe wengine Allah hakuwaumba Yeye mwenyewe, hata ukaifasiri Aya hio kuwa maana yake ni kamuumba Adam Yeye mwenyewe?”. Nitakujibu kwamba wote wameumbwa na Allah mwenyewe, lakini hapa ilikuwa kuna munasaba maalumu uliopelekea kuileta taukid hio kwa sababu ya kile kitendo cha Ibilisi cha kukataa kuitii amri ya Allah. Kana kwamba Allah anamkumbusha Ibilisi nafsi yake kwamba Mimi Mungu ndiye niliyemuumba huyu sasa vipi wewe unakataa kumsujudia baada ya kukuamuru ufanye hivyo? Kumsujudia huyu si jengine bali ni kunitukuza mimi tu kwa kuitii amri yangu. Na kwa hivyo, tunasema kwamba: يقتضيه بما هو وإنما الحصر به يقصد لم هنا التخصيص kuhusishwa kuumbwa kwa Adam na Allah si kwa ajili ya kuwa ni) المقامyeye peke yake ndiye aliyeumbwa na Allah, lakini hayo ni kwa kuzingatia muktadha wa hali ilivyo; hilo ndilo liliopelekea kusemwa hivyo). Na hayo yote ni kwa ajili ya kumkumbusha Ibilisi utukufu wa Allah na uweza wake.

Jambo la tatu – ambalo linaweka wazi hayo yaliotangulia – ni kutazama kwamba Aya hio: بيدي خلقت لما تسجد أن منعك ما إبليس يا (..Ewe Ibilisi! Ni nini hasa kilichokuzuia wewe kumsujudia yule niliyemuumba kwa mikono yangu miwili), ni Aya ambayo ndani yake imetumika herufi maa Herufi hio hapo bila ya shaka inamaanisha .(ما) إنكاريا استفهاما(kuuliza kwa maana ya kupinga). Yaani Aya hio inauliza lakini maana yake ni kuwa inapinga. Na bila shaka kumpinga Ibilisi kwa matendo yake hayo kwa kuzingatia kwamba Adam kaumbwa na Allah mwenyewe kunatoa hoja nzito zaidi dhidi ya Ibilisi kuliko kumkatalia Ibilisi matendo yake hayo kwa sababu Adam kaumbwa kwa mikono miwili ya Allah. Unaonaje lau ilisemwa: (..Ewe Ibilisi! Ni nini hasa kilichokuzuia wewe kumsujudia yule niliyemuumba kwa uwezo wangu), au “Niliyemuumba

466 - Yaani البالغي . التشبيه

130

Page 131: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Mimi mwenyewe” au “Kwa elimu yangu”, je Ibilisi asingelistahiki lawama hio? Kwa hivyo, ni wazi kwamba neno mikono miwili hapo halina mafhumu, bali limetumika kama ni kinaya467 ambacho kwacho imekusudiwa maana nyengine.

Ama madai kwamba:

Kuamini kuwa Allah kamuumba Adam kwa mikono yake miwili ni kwa sababu ya kumpa Adam maziyya (sifa maalum) pasina Ibilisi, kwani mengineo yanayohusu kuumbwa kwao wameshirikiana ndani yake” pamoja na dai la tatu linalotoa natija kwamba: “Na kwa hivyo, kuumbwa kwa Adam ni lazima itakuwa ni kwa mikono miwili hakika, ili ipatikane tafauti baina ya maumbile ya Ibilisi na maumbile ya Adam – Adam kaumbwa kwa kushikwa kwa mikono miwili ya Allah na Ibilisi kaumbwa kwa kun fayakun tu.

Tunasema: madai haya hayatoi hoja sahihi. Kwani lau kuumbwa kwa mikono miwili ya Mungu – kama wanavyosema Mawahabi – kunatoa ubora zaidi kuliko kuumbwa kwa amri ya kun fayakuu tu, basi Adam atakuwa ni bora kuliko Muhammad! Bali lulu, Taurati, Jibril na mengine yaliotajwa katika riwaya za kufinyanga za Kihanbali/Kiwahabi, yote hayo yatakuwa ni bora kuliko Mtume (s.a.w.). Halkadhalika Adam asingelikuwa na maziyya (sifa maalum) katika suala la kuumbwa kuizidi Taurati, Jibril, Arshi na kalamu; bali hata lulu asingeleishinda kwa utukufu wa kimaumbile, kwani riwaya zenu zinasema kwamba yote hayo yameumbwa kwa mikono ya Allah!

HADITHI NYENGINE ZA MKONO WA MUNGU

Ama Hadithi wanazozitolea hoja watu hawa kuonesha kwamba Allah ana mikono miwili, utaona kwamba Hadithi hizo, kama zitasihi basi, ni hoja dhidi yao. Tazama kwa mfano Hadithi alizozinukuu Ibn Manda katika Kitabu Al-Tauhid, kama vile Hadithi isemayo:

أحدكم يربي كما فيربيها بيمينه الرحمن أخذه إال بصدقة أحد تصدق مافتربو 468فلوه فصيله أو

الجبل من أعظم تكون حتى الرحمن كف في467 - Kinaya ni kama majazi bali ni aina ya majazi kwa kauli iliosahihi ya wanavyuoni, na unaweza kulifasiri neno hilo kwa maana ya fumbo. Isipokuwa kinaya baadhi ya wakati kinakuwa kinafasirika katika uhakika wake kama kinavyofasirika katika namna yake ya kimafumbo. 468 - Inatamkwa kabla ya kuwa mtendwa: filwun, au faluwwun au fuluwwun. Na kwa hapa ni: filwan, au faluwwan au fuluwwan.

131

Page 132: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Hakuna yoyote yule atayetoa sadaka isipokuwa Allah Mwingi wa rehema anaichukua (sadaka hio) kwa (mkono wake wa) kulia, basi anailea (sadaka hio) kama mmoja wenu anavyomlea mtoto wa farasi wake au ndama wa ngamia wake. Basi (sadaka hio) inakua katika kiganja cha Allah Mwingi wa rehema mpaka inakuwa kubwa kuliko mlima.469

Hii ni moja ya Hadithi ambazo wanazitolea ushahidi wale wenye kusema kwamba Allah ana mikono! Lakini ebu itazame je dhahiri ya Hadithi hii ndio makusudio yake? Hadithi inasema kwamba mtu akitoa sadaka – yaani ya halali na kwa ikhlas kama yanavyosema maandiko mengine – basi Allah anaichukua kwa mkono wake wa kulia na kuilea mpaka sadaka hio inakuwa kubwa kuliko mlima. Wakati sisi sadaka hio tunaiona imetoka kwa fulani kwenda kwa fulani; kama ni pesa basi fulani huyo aliyepewa sadaka hio ya pesa tunaona anazo mfukoni mwake; kama ni nyumba basi tunaiona imekaa juu ya ardhi; kama ni chakula basi kakila na kukitoa kwa njia nyengine; sasa vipi sadaka hii iambiwe kwamba iko mikononi kwa Allah na kwa hivyo Allah ana mikono? Jamani! Akili ziko wapi enyi binaadamu! Bila shaka Hadithi hii, kama ni sahihi basi, ni kinaya chenye kumaanisha jinsi Allah anavyoipokea sadaka hio na kuitakabalia kama vile ilivyo kawaida ya viumbe kwamba kitu wakikipokea hukipokea kwa mikono yao ya kulia na kukienzi.

Na mfano wa Hadithi hio ni Hadithi isemayo:

منابر على القيامة يوم الله عند المقسطين يمين إن عن نور من......الرحمن يمين يديه وكلتا

Hakika ya waadilifu wako mbele ya Allah siku ya kiama juu ya membari za nuru kuliani kwa Allah, na mikono yake yote miwili ni ya kulia. 470

Sasa jiulize:1) Vipi mikono yake yote ni kulia, na kwamba hilo ni hakika si majazi?2) Kuna faida gani ya kuhusishwa mkono wa kulia ikiwa mikono yake

yote ni ya kulia.3) Vipi waadilifu watakuwa kuliani kwa Allah naye kakaa kitako juu ya

kiti chake (‘Arsh) ambacho ndio kiumbe kikubwa chao kilichozunguka kila kitu. Sasa iko wapi sehemu ya kulia ya kukaa hao waadilifu, ilhali watu walioko katika uwanja wa kiama na kila kiumbe, wote hao wamezungukwa na ‘Arshi alioikalia Allah!

469 - Ibn Manda Al-Tauhid j. 3, uk. 100, Hadithi na. 498. 470 - Ibn Manda Al-Tauhid j. 3, uk. 101, Hadithi na. 501.

132

Page 133: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Hadithi nyengine inasema:

ربي يمين اخترت فقال اختر آلدم فقال ظهره ومسح آدم الله خلق لمايديه مباركة وكلتا يمين

Allah alipomuumba Adam alimpangusa mgongo wake kisha akamwambia: ‘Ewe Adam! Chagua. Akasema: ‘Nimechagua mkono wa kulia wa Mola wangu; na mikono yake yote miwili ni ya kulia yenye kubarikiwa.471

Tafsiri ya Hadithi hio utaipata katika Hadithi isemayo:

مقبوضتان وهما بيديه له قال روحه من فيه ونف������خ آدم الله خلق لماآدم يا ش��ئت أيهما قال خذ

آدم فيهما فإذا بسطهما ثم مباركة يمين يديه وكلتا ربي يمين أخذتكلهم..... وذريته

Allah alipomuumba Adam na kumpulizia roho yake alimwambia kwa mikono yake miwili nayo ilikuwa imefumbatwa (imefungwa): ‘Chagua utakao ewe Adam’. Akasema: ‘Nachagua mkono wa kulia wa Mola wangu’ na mikono yake yote miwili ni ya kulia imebarikiwa. Kisha (Allah) akaikunjua mikono miwili hio, kutahamaki ndani yake yumo Adam na kizazi chake chote…472

Tazama jinsi Hadithi hii inavyounda dhana (concept) ya tajsim safi! Mungu ana mikono miwili kaifumbata konzi kisha akamwambia Adam achague anataka konzi gani! Kwa kweli huku ni kufanya maskhara na Allah Mtukufu! Ule mchezo wa watoto wa kufunga konzi kisha wakaambiana: “Agua iko wapi” ndio ambao Hadithi hii inaunasibisha nao kwa Allah! Mchezo huo hata watu wazima katika binaadamu hawaufanyi, leo Hadithi hii inatwambia kuwa Mungu kafanya hivyo na Adam! Hadithi gani hii?

Kisha tazama – kwa mujibu wa Hadithi hii – Adam naye alikuwa kafumbatwa473 na Mungu, lakini wakati huo huo yuko nje ya mkono wa Mungu anaambiwa achague mkono autakao, kufumbuliwa mkono huo naye yumo pamoja na watoto wake!

Kisha Hadithi hii ni kuwa Adam kaiona mikono ya Mungu na kwa hivyo kamuona Mungu au sehemu ya Mungu474 wakati Qur-ani inasema: “Jicho halimfikii” na inasema kuhusu Musa “Hutoniona”. Na Hadithi inasema:

471 - Ibn Manda Al-Tauhid j. 3, uk. 102, Hadithi na. 502. 472 - Ibn Manda Al-Tauhid j. 3, uk. 105, Hadithi na. 508. 473 - Kakunjwa kwenye kiganja cha Mungu.

133

Page 134: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

“Lau atafunua pazia lake basi kitaungua kila ambacho jicho lake litaishia kwake” yaani kila atayemtazama basi ataungua. Kwa kweli sijui kama kuna anayeitumia akili yake vizuri akazikubali mutun (texts) za Hadithi hii na ilio mfano wa hii.

MIKONO MIWILI HAITUMIKI ILA KWA MWENYE MIKONO YA KWELI!

Ama madai ya wengine kwamba kitu hakisemwi kuwa kina mikono miwili ila kiwe kina mikono ya kweli, kama alivyosema Sheikh Muhammad Khalil Haraas, si madai sahihi. Anasema Sheikh huyo:

اليد فلفظ ولم يوأيضا الحقيقية اليد في إال استعماله يعرف لم بالتثنية نبمعن قط أو �����يرد القدرة ى

ال أنه على بنعمتين، أو بقدرتين الله خلقه يقال أن يسوغ ال فإنه النعمةبمعنى اليدين إطالق يجوز

الحقيقة على باليدين اتصف من حق في إال غيرهما أو القدرة أو النعمةلل يقال ال يد ���ولذلك ريح

. يد للماء وال

Vile vile neno mikono miwili (katika matumizi ya uwili) halikupata kutumika isipokuwa kwa kumaanisha mkono wa kweli kweli, wala haikupokewa kamwe (kutumika neno mikono miwili) kwa maana ya uwezo au neema, kwani haiwi kwamba isemwe kwamba ‘Allah kamuumba kwa kuweza kwake kuwili au kwa neema zake mbili; bali haifai kulitumia neno mikono miwili kwa kumaanisha neema au uwezo wala mengineo isipokuwa kwa yule ambaye ana mikono miwili kweli kweli na kwa hivyo, haisemwi kwamba upepo una mkono wala haisemwi kwamba maji yana mkono.475

Hayo ndio maneno ya Sheikh huyo, nayo ni maneno ya kustaajabisha! Kana kwamba Sheikh huyo hajui kilichomo katika Qur-ani wala kilichomo katika vitabu vya lugha ya Kiarabu, bali Sheikh huyo hakijui hata kitu alichokisema yeye mwenyewe alipokuwa akikisherehesha kitabu Nuniyya cha Al-Imamu Ibn Al-Qayyim. Maneno yake hayo yana nukta hizi:

1) Neno mikono miwili halijulikani kamwe kutumika isipokuwa katika kumaanisha mkono wa kweli.

2) Haikupokewa kwa maana ya uwezo au neema.

474 - Kwa wale wenye kuamini kuwa Allah ana sehemu!!! Sisi hatuna itikadi hio, na tunamuomba Allah atulinde nayo. 475 - Sheikh Muhammad Khalil Harras Shar-hu ‘Aqiidati Al-Wasatiyya 57.

134

Page 135: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

3) Haiwi kwamba mtu aseme: “Allah kamuumba fulani kwa kuweza kwake kuwili au neema zake mbili”.

4) Bali haiwezekani kulitumia neno mikono miwili kwa maana ya neema au uwezo au mengineo isipokuwa kwa yule ambaye ana mikono miwili kweli kweli.

5) Haisemwi katika lugha ya Kiarabu: “mkono wa upepo au mkono wa maji”.

Ama tukirudi katika nukta ya kwanza kwamba “Neno mikono miwili halijulikani kamwe kutumika isipokuwa katika kumaanisha mkono wa kweli”, utaona kwamba nukta hio inajibiwa na Aya tulizozikuu kabla. Aya kama: ياح يرسل الذي وهو الر رحمت��ه ي��دي بين بشرا Naye (Allah) ndiye mwenye kutuma upepo kuwa ni habari njema baina ya mikono miwili ya rehema yake. Na Aya isemayo: مبارك أنزلناه كتاب وهذا

دق يدي��ه بين الذي مص�� Na hiki ni Kitabu tumekiteremsha, chenye kubarikiwa (na) ni chenye kukisadikisha kile kilicho baina ya mikono yake miwili. Na Aya kama: نج��واكم يدي بين تقدموا أن أأشفقتم Munaogopa nyinyi kutangulizi sadaka baina ya mikono miwili صدقاتya kunong’ona kwenu. Katika Aya zote hizi, Allah kavitaja vitu fulani kuwa vina mikono miwili ilhali vitu hivyo havina hata mkono mmoja – Qur-ani haina mkono wala mazungumzo hayana mkono wala rehema ya Allah haina mkono.

Ama nukta ya pili kwamba “Haikupokewa kwa maana ya uwezo au neema” yaani neno mikono miwili pindipo litatumika katika mfumo huo wa uwili,476

basi halimaanishi uwezo wala neema. Suala hili na tumuache Sheikhe huyo, Haraas, ajijibu mwenyewe – Haraas amjibu Haraas. Anasema Sheikh huyo alipokuwa akiusherehesha ubeti wa Ibn Al-Qayyim usemao:

** يدان ذاك بفسخ للصدود ما األركان ثابت المحبة حكمHukumu ya mapenzi, nguzo zake ni imara**Upingaji477

hauna mikono miwili ya kubomoa hilo.478

Anasema mshereheshaji, naye ni Sh. Haraas huyo huyo: القدرة بمعنى يد تثنية يدان

Mikono miwili ni uwili wa (neno) mkono, kwa maana ya uwezo.479

476 - Ikasemwa mikono miwili. 477 - Maana ya neno kwa neno ni “uzuiaji”, lakini ufasaha wa Kiswahili ni kusema “upingaji”. 478 - Ibn Al-Qayyim Al-Nuniyya j. 1, uk. 16. 479 - Muhammad Khalil Harras Sha-hu Al-Nuniyya j. 1, uk. 16.

135

Page 136: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Huo ndio ubeti wa Ibn Al-Qayyim anayekataa kuwepo kwa majazi, na hio ndio sherehe ya Sh. Muhammad Haraas anayesema kuwa neno mkono likitumika katika uwili (mikono miwili) halimaanishi uwezo wala neema wala mengineo, bali limaanisha mikono ya kweli tu! Utaona kwamba Sheikh huyo anakikanusha katika kitabu kimoja kile anachokithibitisha katika kitabu cha pili!

Ama nukta ya tatu yenye kusema kwamba: “Haiwi kuwa mtu aseme kwamba Allah kamuumba fulani kwa kuweza kwake kuwili au neema zake mbili”. Ninasema: na huu pia si upinzani sahihi, kwani:

1) Mikono miwili ilipotolewa katika maana yake ya asili na kupelekwa katika maana nyengine, basi ina maana kwamba imeletewa ta-awil na kwa hivyo hakuna tena ulazima wa kuwa lazima useme neema mbili kama ulivyoitaja mikono miwili.

2) Ubeti huo wa Ibn Al-Qayyim umetaja mikono miwili na mshereheshaji hakusema “kuweza kuwili” bali kasema “uwezo”. Na mshereheshaji ni yeye mwenyewe, Sh. Haraas.

3) Dai lake kwamba haikupokewa katika lugha ya Kiarabu kulitumia neno mkono katika uwili yaani ukasema mikono miwili na likamaanisha neema au uwezo. Dai hilo linabomolewa na kile kilichoelezwa katika makamusi ya lugha. Amenukuu Ibn Mandhur Hadithi: “ ال أي يقاتلهم أن ألحد يدان ال لي عبادا أخرجت قد

طاقة وال ق�درة ..” “Nimewatoa waja wangu (juji-wa-majuji) hakuna mwenye mikono miwili ya kupambana nao, yaani hakuna uwezo wala nguvu”.480

4) Hakuna ulazima wa kuwa maneno “mikono miwili” yafasiriwe “neema mbili” au “kuweza kuwili”, bali yanaweza kumaanisha taukid kama tulivyoeleza.

Nukta ya nne inasema: “Bali haiwezekani kulitumia neno mikono miwili kwa maana ya neema au uwezo au mengineo isipokuwa kwa yule ambaye ana mikono miwili kweli kweli”. Ninasema: dai hili linajibiwa na Aya tulizozinukuu kuhusu Qur-ani, rehema ya Mungu na kunong’ona. Yote hayo yametajwa kuwa ya mikono miwili. Halkadhalika Hadithi tulioinukuu kutoka kwa Ibn Mandhur na maneno ya Waarabu yasiohisabika, yote hayo yanabomoa dai hili. Ama nukta ya tano ni kuwa: “Haisemwi katika lugha ya Kiarabu kwamba mkono wa upepo au mkono wa maji”. Nayo pia si kauli sahihi! Anasema Ibn Mandhur akiwanukuu Waarabu wakisema:

480 - Ibn Mandhur Lisanu Al-’Arab j. 15, uk. 441.

136

Page 137: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

)) : أمر : . : نطاف لبيد قال سلطانها الريح ويد زمانه مد الدهر هايد(( الشمال بيد

Mkono wa dahari, yaani upeo wa zama zake; na mkono wa upepo, yaani nguvu zake; kasema Labid: matone (ya maji) ninayapitisha kwa mkono wa kaskazini. 481 Na sote tunajua kwamba kaskazini haina mkono, bali vitu hivyo vilivyotajwa hapo vyote havina mikono.

MUKHTASARI

Mukhtasari wa haya ni kuwa:

1) Neno mkono katika uhakika wake wa kilugha ni hiki kiungo chenye mfupa na nyama.

2) Maana hii haiwiyani na utukufu wa Allah kwani yeye hana mfano.3) Ukidai kuwa mkono wa Mungu si kama tunavyoujua sisi au hauna

mfano, basi huo si mkono wa uhakika unaofahamika katika lugha ya Kiarabu.

4) Ukidai hivyo au ukidai kuwa mkono ni kwa maana ya neema, nguvu, n.k, basi elewa kwamba umeleta ta-awil, kwani tayari umelitoa neno mkono katika maana yake ya asili.

5) Vitu kadha wa kadha vimetajwa katika Qur-ani, Hadithi na lugha ya Kiarabu kwamba vina mkono wala vitu hivyo havina mkono wa hakika.

6) Hii ina maana kwamba kutajwa kwa mkono wa Allah si lazima iwe mkono wa kweli.

7) Maana nyengine za neno mkono kama vile neema, nguvu, utawala, ihsani, sapoti n.k., zinawiyana zaidi na utukufu na ukamilifu wa Allah kuliko mkono kwa maana ya kiungo.

8) Kwa mujibu wa Qur-ani mikono ya Mungu ni mingi. Kwa hivyo, ni wazi kwamba neno mikono katika Aya hizo halikutumika kwa maana ya uhakika, hususan ukizingatia kwamba mwahala mwengine umetajwa mkono mmoja na mwahala mwengine imetajwa mikono miwili.

VIUNGO VYENGINE VYA MUNGU

481 - Ibn Mandhur Lisanu Al-’Arab j. 15, uk. 441.

137

Page 138: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Kwa hali yoyote ile, hayo ndio maelezo yetu kuhusiana na neno mikono ya Allah, vyenginevyo tumepata katika itikadi za Kihanbali/Kiwahabi kuwa Mungu ni kiwiwili chenye:

1) Mikono miwili. 482

2) Macho mawili. “..Bali Allah Mtukufu ana jicho la kweli kweli..”.483

…. “Kuthibitisha kuwa Allah ana macho mawili”.484…….“Na tunaamini kwamba Allah ana macho mawili”.485 Hivyo ndivyo alivyosema Sheikh Muhammad bin ‘Abdil-’Aziz bin Mani’i na Sh. Ibn ‘Uthaimin, lakini cha ajabu ni kuwa Aya zote walizozitolea ushahidi katika kuithibitisha itikadi yao hio, zinasema kuwa Allah ana macho mengi: zaidi ya mawili! Sasa sijui haya mawili wameyapata wapi? Lakini Imamu wa Ibn Taymiyya, ‘Uthman bin Said Al-Darimi, anatoa hoja ya kwamba Allah ana macho mawili kwa riwaya isemayo kwamba Allah si chongo. Anasema Al-Darimi: “Katika ta-awili486 ya kauli ya Mtume (s.a.w.) aliposema: ‘Mola wenu si chongo’ kuna ubainifu kwamba Yeye (Allah) ni mwenye kuona kwa macho mawili”. Hadithi hii pia ndio dalili ya Sh. Ibn ‘Uthaimin487 na Al-Sallaabi488 katika kuthibitisha kwamba Allah ana macho mawili. Sasa sijui hayo macho mawili yametajwa wapi katika Hadithi hio na wao wanasema: “Tunakithibitisha Allah alichokithibisha na tunakikataa Allah alichokikataa?” Ni wazi kwamba itikadi ya mungu mwenye macho mawili inatokana na qiyas cha Muumba na kiumbe. Ubainifu wake ni kuwa watu hao walitazama wakaona kuwa viumbe vyote vina macho mawili, na ikitokea kuweko kwa kiumbe chenye macho zaidi ya mawili au kuwa na jicho moja, basi kiumbe hicho kinakuwa na umbo lenye kutisha, kwa hivyo na Allah naye wakamuitakidi kuwa ana macho mawili, ilhali hakuna andiko lililosema hivyo!

482 - Tumetoa marejeo kabla. 483 - Dr. Ali Muhammad Al-Sallabi Min ‘Aqitadati Al-Muslimin uk. 78. Muhammad Khalil Haraas Sharhu ‘Aqiidati Al-Wasatiyya uk. 58. Na katika Al-’Aqiidatu Al-Wasatiyya, Ibn Taymiyya kaiweka dalili ya hayo katika uk. 6. Muhammad bin ‘Abdil-’Aziz bin Mani’i Al-Hashiya ‘Alaa Al-’Aqiidati Al-Wasatiyya uk. 34. Ibn ‘Uthaimin ‘Aqiidatu Ahli Sunna Wa Al-Jama’a uk. 12.484 - Tazama yaliomo katika kitabu Hashiyatu Al-‘Aqiidatu Al-Wasatiyya cha Muhammad bin ‘Abdil-‘Aziz bin Maani’i uk. 146. 485 - Ibn ‘Uthaimin ‘Aqiidatu Ahli Sunna Wal Jama’a uk. 12. 486 - Katika kuifasiri. 487 - ‘Uthman bin Said Al-Darimi Al-Radu ‘Alaa Bishri Al-Marisi j. 1, uk. 48. 488 - Dr. ‘Ali Al-Sallaabi Min ‘Aqiidati Al-Muslimiin uk. 79.

138

Page 139: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

2) Masikio. “..Na kwamba yeye anasikia kwa sikio”.489…. “….Basi utaifanyaje ndani yake kwa kutumia Hadithi baada ya kuwepo kauli ya Allah (isemayo): ‘Hakika yake (Allah) ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona) kwa sababu kitu hakiambiwi kuwa kinaona na kinasikia ila kinakuwa ni chenye macho na masikio”.490 Mwisho wa kunukuu. Tazama mtu huyu anavyofanya qiyas cha kumlinganisha Allah na kiumbe! Yaani kama vile ambavyo kiumbe hawezi kusikia ila awe na masikio japo yale ya tundu tu kama vile kuku, basi na Mungu ni hivyo hivyo hawezi kusikia ila awe na masikio!

3) Miguu. “Na mguu (pamoja na muundi wake: leg au رجل) na mguu (wenye kubeba nyayo: foot au قدم) umethibiti kwa Mola wetu (kwamba anao). Na ushahidi ni Hadithi (isemayo)… ‘Jahannam itasema: ‘Je kuna ziada’ mpaka Mola Mtukufu atatia mguu wake, hapo (jahannam) itasema: ‘inatosha inatosha’ na (hapo jahannam) itakunjana’.491 Mwisho wa kunukuu. Ninasema: kesho labda mutatwambia kwamba ukweli nao pia una mguu kwani Allah anasema: ر ربهم عند صدق قدم لهم أن آمنوا الذين وبش (Wabashirie wale walioamini kwamba wao wana mguu wa ukweli kwa Mola wao).492 Simsahau mmoja wa Mashekhe wa Kiwahabi aliposema kuhusu mmoja wa wanasiasa wa Ulaya: له

راسخة قدم السياسة في عندهم (Yeye kwao ana mguu uliozama katika siasa).493 Sijui ni mguu gani huu wa kweli uliozama kwenye siasa!

4) Muundi. “Dalili ya kuthibiti (kuwa Allah) ana muundi”….kasema Mtume (s.a.w.): ‘Allah Mtukufu atafunua muundi wake basi kila Muumini atasujudu”.494 Mwisho wa kunukuu. Ninasema: Hadithi hii ni sehemu ya Hadithi iliosimuliwa na Al-Bukhari495 nayo ni Hadithi

489 - ‘Uthman bin Said Al-Darimi Al-Radu ‘Alaa Bishri Al-Marisi j. 1, uk. 44. Tazama pia Muhammad Khalil Haraas Sharhu ‘Aqiidati Al-Wasatiyya uk. 43. 490 - ‘Uthman bin Said Al-Darimi Al-Radu ‘Alaa Bishri Al-Marisi j. 1, uk. 50. 491 - Dr. Ali Muhammad Al-Sallabi Min ‘Aqitadati Al-Muslimin uk. 79-80. Abu Mu’adh Al-Muntaqa min Sharhi Usuli I’itiqadi Ahli Al-Sunna. uk. 396. Tazama pia ‘Uthman bin Said Al-Darimi Al-Radu ‘Alaa Bishri Al-Marisi uk. 66-67. Muhammad Khalil Haraas Sharhu ‘Aqiidati Al-Wasatiyya uk. 58. Muhammad bin ‘Abdil-’Aziz bin Mani’i Al-Hashiya ‘Alaa Al-’Aqiidati Al-Wasatiyya uk. 51. Ibn Qayyim Al-Jawziyya Mukhtasar Al-Sawaa’iqi Al-Mursala 492 - Sura 10, Aya 2. 493 - Sh. Salih bin ‘Abdillahi Al-Humaid Talbisun Mardud uk. 88. 494 - Dr. Ali Muhammad Al-Sallabi Min ‘Aqitadati Al-Muslimin uk. 79. 495 - Al-Bukhari Al-Sahih Hadithi na. 7439.

139

Page 140: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

refu ya uwongo496 ulio wazi. Na sijui Muislamu ana akili gani hata akaiamini Hadithi hio. Katika Hadithi hio kuna mambo yafuatayo:

a) Allah atawajia watu wote waliokuwa wakimuabudu Yeye – wema na wabaya watamuona! Sasa vipi wabaya nao watamuona Mwenyezi Mungu na kumuona ndio malipo bora kuliko yote kwa waja wema, kisha watu waovu nao wayapate malipo hayo? Nini kitachowazuia waovu hao wasiyapate malipo madogo ya pepo?

b) Allah atawajia kwa sura tafauti na ile waliomuona nayo mara ya kwanza! Tunauliza hio mara ya kwanza walimuona wapi ilhali hiki ndio kisimamo cha kwanza cha Kiama! Na je Allah anabadilika sura hii na ile?

c) Allah atasema mimi ndiye Mola wenu….atasema (Allah kuwambia Manabii): ‘Je muna alama yoyote ile ambayo mukiiona (Mola wenu) mutamjua? Watajibu: (Ndio, alama yake ni) ‘Muundi wa mguu’. Basi atafunua muundi wake watasujudu wote! Ninasema: Mimi nilidhani kwamba alama yake itakuwa laysa kamithlihi shay-un (Hana mfano wa kitu) kumbe alama yake ni muundi wa mguu! Sasa twambieni enyi munaojiita Al-Salafiyya au Ansaru Al-Sunna (Mawahabi) huu muundi wa Mungu ukoje kwani ndio alama yenu ya kumjua Mungu wa kweli huko akhera!

d) Mungu ana miguu miwili497 lakini muundi mmoja! Yote haya yanaonesha kwamba ndugu zetu lugha ya Kiarabu imewapiga chenga: wameshindwa kuziweka Aya na Hadithi mwahala mwake! Bali inaonesha wazi kwamba Hadithi hii ni utunzi wa mazindiki. Lakini Ibn Al-Qayyim anathibitisha itikadi ya muundi wa pili wa Mungu kwa kusema:

في أين فمن صفة هي واحدة ساق عن يكشف أنه أخبر سبحانه أنه هبأنه �ظ اآلية اهرعن ����لي كشفت يقول قائال سمعت لو وأنت الواحدة الصفة تلك إال له س

وأبدي ت���عينيساقي �ع وعن ركبتي إال ن له ليس أنه منه يفهم هل يدي أو قدمي أو

فقط الواحد ذلك

Haya! Natujaalie kwamba Allah ataufunua muundi mmoja wa mguu ambao ni sifa (yake), haya iko wapi katika udhahiri wa Aya hio kwamba yeye (Allah) hana isipokuwa sifa hio moja (ya muundi mmoja)? Nawe ukimsikia mtu anasema: ‘Nimelifunua

496 - Mwongo si Al-Bukhari: yeye kaisimulia hakutanabahi, kwani naye ni binaadamu. 497 - Kama inavyosema riwaya yao “Kiti ndio sehemu ya kuwekea miguu yake miwili”.

140

Page 141: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

jicho langu na nimedhihirisha goti langu na muundi wangu na mguu wangu au mkono wangu, je kinachofahamika kutokana na maneno hayo ni kuwa yeye hana isipokuwa kiungo kimoja hicho?498

Ninasema: asante sana Imamu Shamsu Al-Din, Ibn Al-Qayyim kwa kufanya kwako qiyas hiki cha maajabu baina ya Allah na kiumbe! Lakini Sheikh mimi nina suali moja tu ninataka nikuulize: je nyinyi si munasema kwamba “Munakithibitisha kile ambacho Allah na Mtume wake wamekithibitisha na munakikanusha kile walichokikanusha?” Sasa huu muundi wa pili wa mguu wa mungu mumeutoa katika Aya gani au Hadithi gani? Wapi Allah au Mtume wake wameuthibitisha? Ibn Al-Qayyim ameshakwenda mbele ya haki, lakini mfuasi wake Kasim bin Mafuta yupo atatuletea muundi wa pili wa mguu wa mungu wao, ili tujue kwamba kweli “Wanakithibitisha kile ambacho Allah na Mtume wake wamekithibitisha na wanakikanusha kile walichokikanusha”, vyenginevyo hapa qiyas si mahala pake, na mungu wenu atakuwa anatisha kwani – kwa mujibu wa Aya na riwaya zenu zilivyo, basi – atakuwa ana macho mengi, mikono mingi,499 ubavu mmoja, miguu miwili lakini muundi mmoja!

Utaona kwa uwazi kwamba watu hawa wameijenga itikadi yao katika kumshabihisha Allah na binaadamu. Kwanini ninasema hivyo? Kwa sababu – mbali ya kumpachika Allah viungo hivyo – utaona kwamba:

a) Hadithi na Aya zimeteja muundi mmoja. Lakini wao walitazama wakaona kwamba jambo hili haliwezekani kwani madamu miguu yake ni miwili basi ni lazima atakuwa na miundi miwili. Lakini kwanini wasiseme kwamba ana miundi mitatu au kumi n.k.? Ni kwa sababu wao wamemfananisha Mungu na mtu kwamba kwa vile mtu ana miundi miwili basi na Mungu naye atakuwa ana miundi miwili, vyenginevyo maandiko yametaja muundi mmoja tu?

b) Aya imetaja ubavu mmoja. Wa pili umetoka wapi? Wametazama wakaona kwamba viumbe wote wana mbavu mbili, basi itakuaje Allah awe na ubavu mmoja? Wakamthibitishia ubavu wa pili kwa kumlinganisha na binaadamu (‘Imran bin Al-Husain).

c) Tutaona baadae kwamba kumbe mungu wao ana sura ya Adam!

498 - Ibn Al-Qayyim Al-Sawaaiqu Al-Mursala j. 1, uk. 245. 499 - Kama au kuliko mungu wa Baniani!

141

Page 142: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

5) Uso. Anasema Ibn Al-Qayyim: “Uso wa Mola Mtukufu popote ambapo umetajwa katika Qur-ani basi ni hakika: si majazi”.500 Ninasema: kama ni hivyo kwamba popote palipotajwa uso wa Allah maana yake ni kuwa Allah ana uso kweli kweli basi Aya ya Qur-ani inasema: الله وجه فثم تولوا فأينما (Popote mutapoelekea uko uso wa Allah).501 Na nyinyi munasema kuwa Allah yuko mbinguni kakaa kitako kweli kweli juu ya Kiti chake cha enzi (‘Arsh) hali ya kuwa kaziwacha mbali mbingu na viumbe vyengine. Sasa, kama ni hivyo, je huu uso wake unaning’inia pande zote? Na yeye kabirukia kwenye Arshi miguu juu kichwa chini kachomoza kwenye mbingu ya kwanza? Akili ziko wapi? Na pia Allah anasema: هالك شيء كل وجهه إال (kila kitu kitaangamia isipokuwa uso wake).502 Kwa hivyo, kama Allah ana viungo tafauti ukiwemo uso na kwamba uso ulipotajwa katika Qur-ani ni hakika si majazi yaani ni uso kweli kweli, basi Aya inasema kwamba vyote hivyo vitaangamia na utabakia uso tu – miguu ya Mungu na mikono yake na mgongo na kidakatonge: vyote hivi vitateketea! Akili gani hii enyi binaadamu! Bali hata huo uso nao pia utakuwa haupo kwani Allah anasema: الله لوجه نطعمكم إنما “Kwa hakika tunakulisheni kwa ajili (tuupate) uso wa Allah”.503 Na anasema: إال

األعلى ربه وجه ابتغاء (Hatoi mali yake kwa jengine lolote) “Isipokuwa kwa kutaka uso wa Mola wake Mtukufu”.504 Kwa hivyo, watu wema kesho akhera watakwenda kuupigania uso wa Allah: kila mmoja anautaka yeye auchukue. Hii ndio natija ya tafsiri inayopatikana katika minhaj (methodology) yenu ewe Sheikh Kasim Mafuta! Na kwa fahamu zenu hizo, labda kesho mutatwambia kwamba Hadithi inayosema kwamba katika watu waovu kabisa ni وجهين mwenye) ذوnyuso mbili), kwamba kuna watu wengine wana nyuso mbili hakika lakini si kama tujuavyo! 5) Viganja. Kuthibitisha kuwa Allah ana viganja, ‘Uthman Al-Darimi

ananuku riwaya isemayo: “Hakika ya Mola wangu kaniahidi kuwaingiza watu elfu sabiini katika Umma wangu katika pepo…..kisha atanimwagia konzi tatu kwa kiganja chake”.505 Na riwaya isemayo: “Atayelishika Al-Hajar Al-As-wad (jiwe jeusi), basi

500 - Ibn Qayyim Al-Jawziyya Mukhtasar Al-Sawaa’iqi Al-Mursala uk. 335. Tazama pia Ibn ‘Uthaimin Al-Qawlu Al-Mufid ‘Alaa Kitabi Al-Tawhid uk. 90. Ibn Taymiyya Bayaanu Talbisi Al-Jahmiyya j. I, uk. 100.501 - Sura 2, Aya 115. 502 - Sura 28, Aya 88. 503 - Sura 76, Aya 9. 504 - Sura 92, Aya 20. 505 - ‘Uthman bin Said Al-Darimi Al-Raddu ‘Alaa Bishr Al-Marisi j 1, uk. 37.

142

Page 143: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

huyo kakishika kiganja cha Allah”.506 Ninasema: Enyi walimwengu! Fahamu ziko wapi? Je Hadithi hii si ushahidi tosha kwamba vinapotajwa viungo vya Allah haikusudiwi dhahiri yake? Je Al-Hajar Al-As-wad (jiwe jeusi) ndio kiganja cha Allah? Na je Al-Hajar Al-As-wad halifanani na kitu? العقل نعمة على لله الحمد (Tunamshukuru Allah kwa neema ya akili).

6) Vidole.

Kuthibitisha vidole viwili katika vidole vya Allah Mwingi wa rehema….nayo (sifa hio) imethibiti kwa Hadithi ya ‘Abdullahi bin ‘Amri. Mtume (s.a.w.) kasema: ‘Hakika ya mioyo ya wanaadamu yote iko katika vidole viwili katika vidole vya Allah Mwingi wa rehema, kama moyo wa mtu mmoja tu anausarifu atakavyo.507

Ninasema: Hadithi hii kama ni sahihi basi tafsiri imo ndani ya Hadithi yenyewe. Sehemu ya Hadithi hio isemayo: “Anausarifu atakavyo” inafasiri na kubainisha nini maana ya kuwa mioyo iko katika vidole vya Allah, yaani hiki ni kinaya na maana yake ni kuwa Allah anawasarifu waja wake atakavyo. Na ndio maana Hadithi nyengine ikasema: “Hakuna moyo wowote ila uko baina ya vidole viwili katika vidole vya Allah Mwingi wa rehema: akipenda kuunyoosha anaunyoosha na akipenda kuupotoa basi anaupotoa….na alikuwa (Mtume s.a.w.) akisema: ‘Ewe Mwenye kuigeuza mioyo, uthibitishe moyo wangu katika dini yako”.508 Hii ndio tafsiri inayowezekana kupewa Hadithi hio, vyenginevyo, basi huu ni uzushi wa Kiyahudi. Tazameni jamani:

a) Muungu ana mikono miwili.b) Mkono mmoja una kiganja (labda mmoja ni butu).509

c) Kiganja kina vidole.d) Vidole hivyo ni vitano.510

e) Mkono huo unashika.f) Unapanda miti.g) Unachanganya lulu.

506 - K.h.j.

507 - Dr. Ali Muhammad Al-Sallabi Min ‘Aqitadati Al-Muslimin uk. 78. ‘Uthman bin Said Al-Darimi Raddu Al-Darimi’Alaa Bishri Al-Marisi j. 1, uk. 59. 508 - Kainukuu Dr. ‘Ali Al-Faqihi katika maelezo yake juu ya Kitabu Tawhid cha Ibn Manda j. 3, uk. 110. 509 - Sikuona dalili yao kwamba Allah ana viganja viwili. 510 - Kama inavyosema Hadithi ya Ibn Mas’ud kuhusu Yahudi aliyekuja kumuhoji Mtume (s.a.w.). Tazama ‘Uthman bin Said Al-Darimi Raddu Al-Darimi’Alaa Bishri Al-Marisi j. 1, uk. 60.

143

Page 144: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

h) Basi vipi tena utadai kuwa Mungu hana mfano? Akili gani hii mulionayo nyinyi? Halafu munawaita watu kuwa ni watu wa bidaa kwa kuwa wanasoma maulidi: hii bidaa yenu nyinyi mbingu na ardhi zinakaribia kupasuka? Nyinyi Wallahi aliyeumba mbingu na ardhi ndio watu wa bidaa dhalala safi!

i) Kisha itazameni tena Hadithi: “Hakuna moyo wowote ila uko bina ya vidole viwili katika vidole vya Allah Mwingi wa rehema..”. Je mioyo yetu iko kwenye vidole vya Mungu kweli kweli? Na kama Mungu yuko mbinguni kaachana kabisa na viumbe wake – kama wanavyosema Mawahabi – basi vipi hivi vidole vyake viko chini kwenye mioyo yetu? Je huku ndio kuachana na viumbe? Ni wazi kwamba Hadithi hii – ikiwa ni sahihi – basi njia yake ya kuifasiri ni njia ya kimajazi tu. Na maana yake ni kuwa Allah anawasarifu viumbe wake anavyotaka kama vile ambavyo kitu ambacho mtu kakiweka katika vidole vyake akawa anakisarifu anavyotaka.

7) Mbavu . Anasema Mansur Al-Samawi katika maelezo yake juu ya

kitabu cha ‘Uthman Al-Darimi:

Imekuja kutoka kwa baadhi ya wanavyuoni kuthibitisha kwamba (Allah) ana mbavu..lau kama Allah hakuwa na mbavu (mbili) basi maneno haya yasingelifaa kwake.511

Tuwaulize: wapi wamepata kuwa Allah ana mbavu mbili? Aya walioitegemea wao kuthibitisha kuwa Allah ana mbavu imetaja ubavu mmoja: sasa huu ubavu wa pili umetokea wapi? Al-Sayyid Al-Saqqaf anatwambia kwamba kumbe ubavu wa pili umepatikana kutoka katika kufanya Qiyas cha kumlinganisha Allah na ‘Imraan bin Husain! Anasema:

Amesema mwenye kitabu (kiitwacho) Al-Sawaa’iqu Al-Mursala,512 Ibn Qayyim Al-Jawziyya baada ya kutaja Aya (isemayo): طت ما على حسرتا يا الله جنب في فر (E majuto

511 - Mansur Al-Samawi Ta’aliqihi ‘Ala Raddi Al-Darimi uk. 517. 512 - Ibn Al-Qayyim Al-Sawaaiq Al-Mursala j. 1, uk. 250.

144

Page 145: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

yangu kwa yale nilioyapunguza katika upande513 (ubavu)514 wa Allah). (Amesema Ibn Al-Qayyim baada ya kuinukuu Aya hio): ‘Ya saba: isemwe kwamba dhahiri ya Qur-ani imeonesha kuthibitisha upande (ubavu wa Allah) ambayo ni sifa, lakini je ni wapi imeonesha (kwa) dhahiri yake au (kwa) undani wake kwamba ubavu huo ni mmoja na upande huo ni mmoja? Na inaeleweka kwamba matumizi kama haya hayaoneshi kwamba ni upande mmoja kama Mtume (s.a.w.) alivyosema kumwambia ‘Imraan bin Husain: ‘Sali kwa kusimama; kama huwezi basi sali kitako; kama huwezi basi Sali ubavu’. Na hii haina maana kwamba ‘Imraan bin Husain hana isipokuwa ubavu mmoja………..515

Anachokisema Ibn Al-Qayyim ni kuwa, kama vile ambavyo Mtume (s.a.w.) alimwambia ‘Imraan bin Husain: “Sali kwa kulala upande (ubavu) mmoja” ilhali ‘Imran bin Husain ana mbavu mbili, basi vivyohivyo kutajwa kwa upande (ubavu) mmoja wa Allah hakuna maana kwamba ubavu wa pili haupo: ubavu wa pili anao tu! Kwa hivyo, utaona hapa kwamba Maimamu hawa wa Kiwahabi wamethibitisha ubavu wa pili wa Allah kwa njia ya Qiyas, pamoja na kuwa ngoma yao ni: “Tunathibitisha kile Allah alichokithibitisha katika Qur-ani au alichokithibitisha Mtume wake katika Sunna; na tunakikanusha kile walichokikanusha”. Kwa hivyo, Bwana Kasim Mafuta una deni: uniletee ubavu au upande wa pili wa Allah mumeutoa wapi? Ama Qiyas hapa si mahala pake.

8) Meno/magego. “..Basi Allah Mtukufu atawadhihirikia mpaka atacheka..mpaka kitatokeza kidaka tonge chake na magego yake!”.516

Anasema Ibn Batta517 na Abu Ya’ala:

513 - Elewa ndugu msomaji kwamba neno upande lililomo katika Aya hii halijakusudiwa upande wa kihisia (ubavu) tafauti na zilivyofahamu akili za watu hawa, bali upande ni sawa na mtu kusema “Kwa upande wangu naona kadha wa kadha” yaani “kwangu mimi jambo hili liko kadha wa kadha”. Au ni kama mtu kusema kwa Kiarabu “Janban ilaa janb” (upande kwa upande) au (ubavu kwa ubavu), na hii si maana yake kwamba Juma aliugandanisha ubavu wake na ubavu wa Sh. Kasim Mafuta, bali maana yake ni mshikamano. 514 - Ubavu ni tafsiri ya hao wanaosema kuwa Allah ana ubavu! 515 - Al-Saqqaf Al-Salafiyya Al-Wahabiya uk. 83. 516 - Kaipokea Ibn Manda na kunukuliwa na Mansur Al-Samaari katika maelezo yake ya kitabu Raddu Al-Darimi ‘Alaa Al-Marisi uk. 483. Anasema Al-Samaari: “Na Hadithi hio ni sahihi”. 517 - Imamu wa Mawahabi, lakini kajeruhiwa vibaya na katajwa kuwa miongoni mwa watunzi wa riwaya za uzushi! Wallahu Al-Musta’aan.

145

Page 146: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Basi vivyo hivyo wanaambiwa hawa Jahmiyya wanaozikataa (sifa za Allah),518 munasemaje kuhusu kauli ya Mtume (s.a.w.): “Mpaka kinatokeza kidakatonge chake na magego yake?519

Ninasema: tunasema kuwa huu ni uwongo wa Kiyahudi?

9) Kidakatonge. Tumenukuu na kutoa marejeo katika sehemu iliotangulia (na. 8). Sijui kidakatonge hicho kinadaka tonge gani na Allah hali chakula! Jamani! Ivo kweli hizi ni itikadi za Kiislamu ukiwachilia mbali kuwa itikadi za Al-Salafu Al-Salih?

10) Dhiraa mbili. “Allah kawaumba Malaika kwa nuru ya dhiraa mbili na kifua”.520

11) Kifua. Tumenukuu na kutoa marejeo katika sehemu iliotangulia (na. 10).

12) Kiuno. “Hakika Allah Mtukufu aliumba viumbe alipomaliza basi rahim (tumbo la uzazi)521 lilisimama likamshika Allah kiunoni kwake….”.522 Naam! Walioikubali riwaya katika wanavyuoni wa jumhur – kama Al-Bayhaqi – wameiletea ta-awil, lakini kwa kuwa kwa Mawahabi na Maimamu wao kuleta ta-awil ni kupotoa maandiko, basi mungu wao ni lazima atakuwa na kiuno.

13) Magoti .

Atasema Dawud siku ya Kiama (Ya Rabi) nikurubishe (kwako). Basi itaambiwa: ‘Mkaribie (Allah), basi atasogea mpaka ataligusa goti lake (goti la Mungu).523

Ninasema: Bishr Al-Marisi aliiletea tafsiri riwaya hii kwamba goti hili si la Allah bali ni la viumbe. Basi Al-Darimi akamjibu kwa ukali kabisa:

518 - Ukisikia Wahabi anakwambia kukataa sifa maana yake ni kutokuyakubali haya tulioyanukuu hapa: kidakatonge, mbavu, miguu n.k. Basi sisi hatuabudu Mungu mwenye kidaka tonge! 519 - Ibn Batta Al-Raddu ‘Alaa Al-Jahmiyya j. 3, uk. 111; Abu Ya’alaa Ibtalu Al-Ta-awil uk. 217-218. 520 - ‘Abdullah bin Ahmad Al-Sunna j. 2, uk. 475, riwaya na. 1084. 521 - Yaani jamaa wa mtu hasa hasa wa kukeni. 522 - Al-Bayhaqi Al-Asmaau Wa Al-Sifaat jalada la 2, uk. 222, riwaya namba. 786. 523 - ‘Uthman bin Said Al-Darimi Raddu Al-Darimi’Alaa Bishri Al-Marisi uk. 167.

146

Page 147: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Lau kungelikuwa na mtu akamkata ulimi mpinzani huyu (Bishr Al-Marisi) basi angelikuwa kamfanyia kheri. Wele wako! Kutoka kwa mnafiki gani umeipata tafsiri hii….?524

14) Mgongo.

Mwenyezi Mungu ameiandika Taurati kwa mkono wake na huku ameegemeza mgongo wake kwenye jabali…..sauti ya kalamu inasikika, hakuna baina yake (Mwenyezi Mungu) na baina yake (Nabii Mussa) isipokuwa pazia!525

15) Anakaa juu ya Kiti cha enzi . “Kukaa kwa Allah juu ya kiti chake cha enzi (Arsh)……nako ni kukaa kwa uhakika na maana yake ni kuwa juu (ya kiti) na kutulia..”.526… “Mola Mtukufu akikaa kitako juu ya kiti basi husikika sauti kama sauti ya matandiko ya ngamia”.527 Ninasema: mungu huyu bado hafanani na kitu?

16) Anakwenda kwa miguu . “….Kisha (Mwenyezi Mungu) atatujia baada ya hapo hali ya kuwa anakwenda kwa miguu!”528…… “Basi akawa Mola wako anazunguka katika ardhi, na miji yote imemuinamia (yaani yuko peke yake: katika miji kutupu)”.529 Anasema Ibn Al-Qayyim katika Zadu Al-Ma’ad: ‘‘Hadithi hii ni tukufu, kubwa unatangaza utukufu wake na ukuu wake kwamba inatokana na Mtume (s.a.w.)”.530 Hivyo ndivyo alivyosema, nami ninamwambia: Hadithi hii ni mbaya, mbovu, ya uwongo inaonesha wazi kwamba imetungwa na Mayahudi, maadui wa Allah.531

17) Anashuka wakati wa sehemu ya tatu ya usiku. “Katika kuthibitisha kuteremka kwa Allah kuja katika mbingu ya dunia (mbingu ya kwanza)……Anateremka Mola wetu kuja katika mbingu

524 - K.h.j. Kwa maelezo zaidi. 525 - K.h.j. uk. 67, riwaya na. 568. 526 - Dr. Ali Muhammad Al-Sallabi Min ‘Aqitadati Al-Muslimin uk. 81-82. Tazama pia Muhammad Khalil Haraas Sharhu ‘Aqiidati Al-Wasatiyya uk. 73-74. Muhammad bin ‘Abdil-’Aziz bin Mani’i Al-Hashiya ‘Alaa Al-’Aqiidati Al-Wasatiyya uk. 40-442. Ibn Ahmad Al-Sunna j. 1, uk. 301, riwaya na. 585. 527 - Ibn Ahmad Al-Sunna j. 1, uk. 301, riwaya na. 585. Na mfano wake ni na. 594. 528 - K.h.j. uk. 249, riwaya na. 458. 529 - K.h.j. j. 2, uk. 486, riwaya na. 1120. Tanbihi. Riwaya hii kimakosa imetiwa nambari 11120, katika kitabu kilichohakikiwa na Dr. Muhammad Al-Qahtaani.530 - Ibn Al-Qayyim Zaadu Al-Ma’aad j. 3, uk. 444. 531 - Tutatoa maelezo huko mbele juu ya sanad ya Hadithi hii na walivyosema wanavyuoni wa wapokezi kuhusu sanad yake.

147

Page 148: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

ya dunia kila usiku wakati inapobakia thuluthi ya mwisho ya usiku…”.532 Mwisho wa kunukuu. Nasi tunauliza:

a) Thuluthi ya usiku kila wakati ipo duniani, sasa je huyu Allah anashinda katika mbingu ya kwanza? Au anateremka vipande vipande?

b) Akiteremka kuja katika mbingu ya kwanza kile kiti alichokikalia kule juu anakiwacha kitupu au ananyuuka kama mpira wakati akija huku na kule anakuweko?

c) Juu anakotoka ni wapi na chini anakokuja ni wapi? Maana dunia ni duwara na kila utapokuwa basi mbingu utaziona ziko juu. Jamani! Nyie hamuwezi kutumia hizo akili zenu, munabururwa tu kama magogo?

18) Paja. Mungu ana paja! Paja la mungu kalinukuu Ibn Al-Jawzi kutoka kwa baadhi ya watu wa skuli hii ya tajsim.533

19) Anacheka .

Kuthibitisha sifa ya kucheka…..ni katika sifa za Allah zilizothibiti kwa (mujibu wa) Sunna (Hadithi) na makubaliano534 ya Al-Salaf (watangulizi) wa Umma.535

20) Anakwenda mbio . “Kuthibitisha kuwa Allah anakwenda mbio”536…. “Na (mja wangu) akinijia anakwenda (kwa miguu mwendo wa kawaida) mimi namjia huku natroti”.!537

21) Anastaajabu . “Kuthibitisha sifa ya kuwa Allah anastaajabu”!538 ….

532 - Muhammad bin ‘Abdil-’Aziz bin Mani’i Al-Hashiya ‘Alaa Al-’Aqiidati Al-Wasatiyya uk. 49. Abu Mu’adh Al-Muntaqa Min Sharhi Usuli I’itiqad Ahli Al-Sunna Wa Al-Jama’a uk. 396. 533 - Ibn Al-Jawzi Daf’u Shubahi Al-Tashbih uk. 99. 534 - Mawahabi wao kudai makubaliano katika kila kitu wakitacho ni jambo rahisi. Na wasichokitaka ukisema wewe kuwa hiki wanavyuoni wamekubaliana juu yake, wao watakwamba Al-Imamu Ahmad kasema: “Aliyedai makubaliano ni mwongo, unajuaje kwamba watu wamekubaliana”. 535 - Dr. Ali Muhammad Al-Sallabi Min ‘Aqitadati Al-Muslimin uk. 86. Muhammad bin ‘Abdil-’Aziz bin Mani’i Al-Hashiya ‘Alaa Al-’Aqiidati Al-Wasatiyya uk. 49. Abu Mu’adh Al-Muntaqa Min Sharhi Usuli I’itiqad Ahli Al-Sunna Wa Al-Jama’a uk. 395. Baadae tutanukuu in shaa Allah tafsiri ya Al-Bukhari ya riwaya hii. 536 - Abu Mu’adh Al-Muntaqa Min Sharhi Usuli I’itiqad Ahli Al-Sunna Wa Al-Jama’a uk. 396. 537 - Abu Mu’adh Al-Muntaqa Min Sharhi Usuli I’itiqad Ahli Al-Sunna Wa Al-Jama’a uk. 396. Baadae tutatoa maelezo kidigo kuhusu riwaya hii in shaa Allah.

148

Page 149: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Kustaajabu ni katika sifa za Allah zilizothibiti kwa (mujibu wa) Qur-ani, Sunna (Hadithi) na makubaliano539 ya Al-Salaf (watangulizi) wa Umma.540

Ninasema: kustaajabu kunatokana na kuwa kitu ulikuwa hukijui na sasa umekijua; au unakijua lakini si kwa undani sasa kimekubainikia kwa undani; au kwa sababu kitu kimetokea kinyume na ulivyokitarajia. Huku ndiko kustaajabu, na yote haya kuyanasibisha kwa Allah ni kufuru. Ukinambia “Aaa anastaajabu kustaajabu kunakolingana na utukufu wake ambako sisi hatukufahamu”. Nitakwambia kwamba basi huko si kustaajabu bali limetumika neno kinyume na maana yake ya asili; ama kustaajabu katika maana yake ya hakika ni huku tunakokufahamu na kama kuna kustaajabu kwengine tusikokufahamu basi huko kunahitaji ushahidi wake mbali wa neno lake mbali la kilugha. Kwa mfano, ukitumia neno kwenda lakini kitu kikawa kiko pale pale, huko si kwenda bali ni kulitumia neno kinyume na maana yake ya asili kwa mazingatio mengine. Halkadhalika ukiniambia hivyo, nami nitakwambia kwamba basi na Mashia nao musiwalaumu wanapothibitisha Al-Badaa (kutamburikiwa); kwani lafdhi hio imo katika Hadithi ya Al-Bukhari.541 Nao Mashia hawasemi kuwa Allah alikuwa hajui sasa anajua. Kwa hivyo, itikadi ya Al-Badaa nayo na iwe kama munavyosema nyinyi kuhusu itikadi zenu, na-iwe: “Allah ana Al-Badaa (anatamburikiwa) lakini Al-Badaa yake (kutamburikiwa kwake) si kama Al-Badaa yetu (kutamburikiwa kwetu). Munawalaumu watu kwa kitu mukitendacho?!!

22) Anachoka . Ibn ‘Uthaimin aliulizwa: “Je tunafahamu kutoka katika Hadithi (inayosema kwamba) “Hakika ya Mwenyezi Mungu hachoki mpaka muchoke” kwamba Mwenyezi Mungu anajisifu kwamba (Yeye) anachoka?” Akajibu: “Inajulikana kwamba kawaida ya Ahlu-Sunna Wal-Jama’a kuwa sisi tunamsifu Mwenyezi Mungu kwa (sifa) aliyojisifu Mwenyewe bila ya kummithilisha wala kumfananisha. Ikiwa Hadithi hii inaonesha kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anachoka basi (jua) kwamba kuchoka kwake si kama kuchoka kwetu sisi; bali huko (kuchoka kwake ni kuchoka ambako) ndani yake hakuna upungufu wa namna yoyote!”542

538 - Abu Mu’adh Al-Muntaqa Min Sharhi Usuli I’itiqad Ahli Al-Sunna Wa Al-Jama’a uk. 398. 539 - Jamani makubaliano ya Al-Salaf yananukuliwa ayo! Kunukuu makubaliano wao kwao ni kama kufyetua kumbi! Sijui ni Al-Salaf gani waliokubaliana kuwa Mwenyezi Mungu anastaajabu! 540 - Dr. Ali Muhammad Al-Sallabi Min ‘Aqitadati Al-Muslimin uk. 87. 541 - Al-Bukhari Al-Sahih Hadithi na. 3464. 542 - Ibn Uthaimin Fatawa Al-’Aqida uk. 51-52.

149

Page 150: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

23) Anavuta pumzi: “Musiutukane upepo, kwani upepo ni pumzi za Allah Mwingi wa rehema”543…..…. “Imani ni ya Kiyaman, na hekima ni ya Kiyaman nami naiona pumzi ya Mola wenu kutoka upande wa Al-Yaman”.544

24) Anatoa sauti kama ya chuma. “Allah akisema kwa (kutoa) wahyi, basi viumbe wa mbinguni husikia sauti kama sauti ya chuma (kikibururwa) juu ya jiwe”.545

25) Ana mpaka (mwisho). “…..Katika yale yenye kuonesha kwamba Allah Mtukufu ana mpaka anaopambanuka kwa huo kutokana na viumbe”546……. “….Yeye ana mpaka ambao anaujua Yeye tu haujui mwengine (asiyekuwa Yeye)”. 547

26) Angelitaka angekaa juu ya bawa la mbu. “(Allah) angetaka basi angelikaa juu ya bawa la mbu na likambeba, basi vipi juu ya Arshi tukufu”.548 Mwisho wa kunukuu. Tunasema: labda kesho mutatwambia kwamba Allah angelitaka angelikaa chooni! Angelitaka angelizaa mtoto! Maana munatoa hoja kwa “Angelitaka” mukimaanisha kuwa yeye ana uwezo wa kufanya atakalo wala hakuna wa kumzuia. Basi na haya na mengine pia angelitaka hakuna wa kumzuia. Ukinambia “Aaa! Haya hayawiyani na sifa zake na utukufu wake”. Nitakujibu kwamba pia na kukaa juu ya bawa la mbu hakuwiyani na sifa zake na utukufu wake. Lakini kama ilivyosemwa: “Liman taqrau Zaburak yaa Dawud?” (E Dawud we! Hio Zaburio wansomea nani?).

27) Atakuja siku ya kiama naye kabebwa na kiwingu. “Mungu atashuka katika vivuli vya mawingu kutoka katika Arshi, atajimithilisha (atajigeuza) atawajia………na Mola yuko mbele

543 -Ibn Ahmad Al-Sunna j. 2, uk. 510, Hadithi na. 1195. 544 - Al-Nasai Al-Kubra j. 6, uk. 232. ‘Uthman Al-Darimi Al-Raddu ‘Alaa Al-Marisi j. 3, uk. 151-152. Tanbihi: lakini Hadithi hii Mawahabi wengi au – pengine – wote pamoja na baadhi ya Maimamu wao kama Ibn Taymiyya hawaiamini; na wako wengine katika Maimamu wao wanaikubali kama vile ‘Uthman Al-Darimi lakini wanailetea ta-awil. Na wako wengine wameikubali bila ya kuiletea ta-awil kama alivyosema Ibn Al-Jawzi katika Daf’u Shubahi Al-Tashibih uk. 99. Kwa hali yoyote ile mujassima walioitunga Hadithi hii watakuwa wanaamini kuwa Allah anatoa au anavuta pumzi! 545 - Ibn Ahmad Al-Sunna j. 1, uk. 282, Hadithi na. 537-538. 546 - Ibn Taymiyya Bayanu Talbis Al-Jahmiyya j. 1, uk. 445. 547 - K.h.j. uk. 443. 548 - ‘Uthman Al-Darimi Al-Radu ‘Alaa Bishri Al-Marisi uk. 85.

150

Page 151: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

yao mpaka wavuuke!”549 Mwisho wa kunukuu. Ninasema zingatia mambo haya:

1) Mungu kabebwa na vivuli vya mawingu anateremka chini!2) Atajigeuza: Mungu ageuka au abadilika!3) Mungu yuko mbele na watu wako nyuma wanamfuata! Huyu kweli

ni mungu-mtu au mungu katika kiwiliwili cha mtu (man-god au god-incarnet)!

KWA HIVYO:

Hizo ndio itikadi za Kiwahabi na Maimamu wao watangulizi na ndizo zenye kupambanua kwao baina ya mtu wa Sunna na mtu wa bidaa. Na kwa sababu hio, usione ajabu wewe kuona Mawahabi kuwa wanawashambulia Maulamaa wa madhehebu nyengine za Kiislamu hata Maulamaa wa madhehebu za Kisuni tangu zamani hadi leo. Kwa leo Maulamaa kama Al-Qardhawi, Al-Sha’arawi na wanavyuoni wote wasiokuwa wa Kiwahabi wameshapata mashambulizi ya nguvu kutoka kwa Mawahabi. Wakati watu kama Ibn Batta Al-‘Ukbari na walio mfano wake wanawaita kuwa ndio Ahlu Sunna au Maimamu wa Ahlu Sunna au Al-Salafu Al-Salih! Lakini je nini itikadi ya Ibn Batta? Ibn Batta huyu ndiye aliyesema:

Nabii Musa (a.s.) alimkuta mtu juu ya mti kavaa vazi la sufi na viatu akasema naye (yaani yule mtu akasema na Nabii Mussa a.s). Nabii Mussa (a.s.) akasema: ‘Ni Muibrania gani huyu anayesema na mimi?’ Yule mtu akajibu: “Mimi ni Mungu. 550

Yaani Nabii Musa kamkuta Mwenyezi Mungu juu ya mti katia suti na viatu. Jamani! Huyu aliyeyasema haya bado anaendelea kuwa Muislamu licha ya kuwa ni Ahlu Al-Sunna? Basi mwenye kusema maneno hayo kwa Mawahabi si mtu wa bidaa; bali ndio Ahlu Sunna na ni Imamu miongoni mwa Maimamu Adhimu wa Kiislamu! Na kwa hivyo, utawaona wanamsifu Ibn Batta na aliye mfano wa Ibn Batta kwa sifa nzito nzito. Anasema Dr. Ridhaa kuhusu Ibn Batta: “Alikuwa ni moja ya nguzo za madhehebu ya Hanbal”.551 Anasema Sayyid ‘Imraan kuhusu Ibn Batta kwamba ni: “Imamu

549 - K.h.j. uk. 77. Yaani haya yatatukia siku ya kiyama. Mwenyezi Mungu: a) Atabebwa na mawingu. Aliyesema hivi hakuufahamu muradi wa Aya. b) Atajigeuza. Lakini kumbuka kwamba kubadilika ni sifa ya viumbe: Mwenyezi Mungu ni Mkamilifu katika dhati yake na sifa zake hazidi wala hapunguwi Yeye ni mkamilifu hana haja ya ziada: kuzidi ni alama ya kasoro.c) Atakuwa mbele na watu wako nyuma yake mpaka awavuushe kwenye daraja ya jahanam!550 - Tazama Lisanu Al-Mizan cha Ibn Hajar j. 4 uk. 112-115. 551 - Al-Sharh wa Al-Ibana uk. 48, utangulizi wa Dr. Ridhaa.

151

Page 152: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

aliye Qud-wa (kigezo), mwenye kuabudu, mwanachuoni wa Hadithi, Sheikh wa Iraki”.552 Anasema Ibn Al-Qayyim: “Al-Imamu, Al-Haafidh (aliyehifadhi sana), Al-Zaahid (aliyeitupilia mbali dunia)”.553 Hayo ndio maneno yao kuhusu Imamu wao huyo, ambaye ndiye kigezo chao, nacho kigezo hicho kinaripoti kuwa Allah kajigeuza mtu na akatia suti na viatu akapanda juu ya mti! Tazama pia kwamba wakati Mawahabi na Maimamu wao wanajilazimisha kumsifu Imamu wao huyo kwa sifa hizo, basi vitabu vyote vya tarajim (biographies) za wapokezi vimesema kuwa Ibn Batta ni dhaifu, mwenye hifadhi mbaya, mwenye kutunga riwaya za uwongo. Sasa sijui huo uqud-wa umetoka wapi kwa mtu anayetunga riwaya za uwongo.554

Mfano wa pili wa watu wapotovu ambao Mawahabi kwao ndio Maimamu, ni Al-Hasan bin Ali Al-Ahwazi. Huyu ni Imamu muhimu ambaye Mawahabi wanamzingatia kuwa ni miongoni mwa Ahlu Sunna wakuigwa. Lakini Al-Dhahabi anasema katika Al-Mizan na Ibn Hajar katika Lisanu Al-Mizan  kuhusu Imamu huyu Adhim wa Kiwahabi:

Ametunga kitabu kuhusu sifa (za Mungu, na) lau hakukitunga basi ingelikuwa kheri kwake, kwani kaleta humo Hadithi za kutunga na fedheha tele na alikuwa akimponda Al-Ash’ari (Imamu wa jumhur ya Masuni katika mambo ya itikadi na tawhidi)555 na akatunga (kitabu) kuhusu aibu zake….(Na miongoni mwa utunzi wake ni dai lake kwamba): “Ikifika siku ya Ijummaa, basi Mungu huteremka baina ya Adhana na Iqama naye ana vazi (kama kanzu au jokho!!!) limeandikwa mimi ndiye Mungu hakuna Mungu ila Mimi; anasimama katika kibla cha kila Muumin (yaani mbele yake); Imamu akitoa Salam basi (Mungu) anapaa mbinguni!!!!” ….. Anasema Ahmad bin Mansur: “Abu ‘Ali (Al-Ahwazi) ulipodhihiri kutoka kwake wingi wa riwaya za visomo (vya Qur-ani) alituhumiwa, basi Rasha-a bin Nadhif na Abu Al-Qasim bin Al-Furat waliwasili Baghdad na wakasoma kwa wale Mashekhe ambao Al-Ahwazi kapokea (riwaya) kutoka kwao, basi wakaja na ijaza,556 basi Al-Ahwazi akawaendea na akawaomba wamuoneshe maandiko hayo, basi akayachukua na akayabadilisha majina ya wale aliowataja (yeye) ili ayasitiri madai yake. Anasema Al-Khatib Al-Baghdadi: “Al-Ahwazi ni mwongo mkubwa”. Anasema: Ibn Asaakir katika kitabu chake Tabyin Kadhibi Al-Muftari kwamba Al-Ahwazi: “Alikuwa mwongo kuliko watu wote katika riwaya na visomo”. Na akasema Ibn Asaakir kwamba Al-Ahwazi huyu ndiye

552 - Al-Ibana ‘An Shari’ati Al-Firqati Al-Najia j. 1, uk. 13, utangulizi wa Sayyid ‘Imran. 553 - Ibn Al-Qayyim Mukhtasaru Al-Sawaa’iq uk. 360. 554 - Jamani! Musijemukasema natukana: hayo siyasemi mimi bali yamesemwa na wakuu wetu kwenye vitabu vyao. 555 - Kama alikuwa na itikadi kama yao tena vipi amponde?! 556 - Yaani kumpa mwanafunzi ruhusa ya kusimulia riwaya za kitabu fulani au za Sheikh muhusika n.k.

152

Page 153: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

aliyetunga Hadithi inayosema: “Nilimuona Mola wangu Mina (sehemu ya haram) juu ya ngamia mwekundu kavaa juba!!!!” Na katika riwaya ya pili anasema: “Ngamia mweupe aliyepiga weusi.” Na miongoni mwa Hadithi zake alizozisimulia katika kitabu chake Sharhu Al-Bayaani Fii ‘Uquudi Ahli Al-Iman ni Hadithi isemayo: “Mungu alipotaka kuiumba nafsi yake aliumba farasi kisha akamuendesha mbio mpaka akatoka jasho na kutoka katika jasho hilo la farasi akaiumba nafsi yake”!557

Sasa tazameni ajabu hii enyi walimwengu! Mtu anayesema:1) Mungu kaonekana Mina.2) Mungu kavaa guo jekundu.3) Mungu kapanda ngamia.4) Mungu anateremka kila siku ya Ijumaa na kukaa mbele ya kila

Muumini.5) Mungu kaiumba nafsi yake kutoka katika jasho la farasi! Sijui huyo

farasi kamuumba nani!558

Huyu Mawahabi wanamzingatia kuwa ni Imamu na ni katika Ahlu Sunna, wakati ni wazi kwamba huyu tayari ameshakufuru kufuru ya ushirikina – si Muislamu kabisa. Wakati anayesoma maulidi au khitma bali hata anayechukua mtasbihi tu basi kiama humshukia kwani yeye tayari ni Ahlu bid’a dhalala! Hii ni akili gani? Hata bidaa dhalala pia mumeshindwa kuijua? Basi hiyo ya Al-Ahwazi ndio bidaa dhalala inayomtia mtu motoni, zindukeni.

MUKHTASARI NA NUKTA MUHIMU

1) Tulichokizungumzia hapa ni hii dhana (concept) ya Mungu kwa mujibu wa skuli ya wanaoitwa Mawahabi pamoja na Maimamu wao watangulizi.

2) Maimamu watangulizi wanatwambia kwamba “Mungu ni kiwiliwili si kama viwiliwili”.

3) Kiwiliwili hicho:a) Kinabebwa na Malaika nacho kiko juu ya kiti chake cha enzi.b) Ni kizito sana wakati wanaposimama washirikina katika

ibada zao.c) Wakisimama Waislamu kinakuwa khafifu (kinapungua

uzito).d) Ni kizito juu ya Malaika waliokibeba mpaka

watapofundishwa kumtaja Allah.

557 - Tazama Al-Dhahabi Al-Mizan j. 2, uk. 35, tarjama ya 1916. Ibn Hajar Lissan Al-Mizan cha Ibn Hajar j. 2, uk. 239 tarjama ya 1005. 558 - Labda nafsi kwake yeye ni sifa ilio mbali na dhati!

153

Page 154: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

e) Kina viungo vyote taqriban alivyonavyo binaadamu isipokuwa ndevu na uchi kama alivyonukuliwa Abu Ya’alaa akisema hivyo!

f) Ni wazi kwamba hii ni itikadi ya tajsim559 safi na ni itikadi ya tashbihi560 safi.

4) Wenye itikadi hizo wanasema kuwa Allah yuko hivyo, yaani ana viungo hivyo kweli kweli, lakini pamoja na hayo hafanani na kitu.

5) Msingi wa itikadi yao hio ni:a) Kukanusha kuwepo kwa majazi.b) Kukanusha ta-awil.

6) Lakini mbele ya haya kumekuwa na matatizo kwani:a) Majazi yamethibiti kwa dalili za yakini katika Qur-ani,

Sunna (Hadithi) na lugha ya Kiarabu, kama tutavyobainisha katika mlango wake.

b) Ta-awil ni jambo lisiloepukika na juu ya yote Al-Salaf wamefanya ta-awil katika Aya na Hadithi kadha wa kadha. Na kwa sababu ta-awil ni jambo lisiloepukika, basi utaona kwamba hata wao wenyewe wenye kupinga ta-awil wameemewa na baadhi ya maandiko na kwa hivyo wamelazimika kuyaletea ta-awili. Mfano wa hayo, ni yale maandiko ambayo yanasema kwamba Allah yuko kila mahala, ambapo walilazimika kuyaletea ta-awil kwamba maana ya maandiko hayo ni kuwepo kila mahala kwa elimu yake: si kuwepo kila mahala yeye mwenyewe kweli kweli (physically). Bali hata kusema: “Allah ana mkono lakini haufanani na kitu” pia ni kuleta ta-awil, vyenginevyo wapi umesikia kwamba katika lugha ya Kiarabu kuna “mkono lakini si kama tuujuao sisi”.

7) Kanuni hio ya: “Mkono lakini si kama tuujuavyo” haina msingi katika lugha ya Kiarabu, kwani:

a) Allah alipozungumza na sisi kazungumza na sisi kwa lugha tunayoijua: si kwa lugha tusioijua.

b) Mkono wa hakika katika lugha tunayoijua ni hiki kiungo chenye mfupa na nyama, wala haikupokewa kutoka kwa Waarabu kwamba kuna mkono mwengine wa kweli kweli isipokuwa huo.

c) Linapotumika neno mkono lakini usikusudiwe huo basi huo si mkono wa kweli bali ni majazi kwani matumizi ya lugha ya Kiarabu hayakupokewa kutoka kwa Waarabu wenyewe

559 - Kumfanya Allah kuwa ni kiwiliwili. 560 - Kumfananisha Allah na viumbe.

154

Page 155: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

isipokuwa kwa njia mbili hizo – njia ya hakika kama kulitumia neno mkono kwa kukusudia kiungo; na njia ya majazi kama kulitumia neno hilo kwa kukusudia nguvu, uwezo, ihsani, thamani n.k.

8) Kusemwa katika lugha ya Waarabu kwamba kitu fulani kina mkono, si lazima kiwe na mkono wa kweli kweli, kama vile ilivyosemwa kwamba:

a) Qur-ani ina mikono miwili, ilhali haina.b) Adhabu ina mikono miwili, ilhali haina.c) Mazungumzo yana mikono miwili, ilhali hayana.d) Upepo una mkono ilhali hauna.e) Upande wa kaskazini una mkono, ilhali hauna. Na mengineo

mengi ambayo yako hivyo.9) Hadithi walizozitegemea mabwana wa madhehebu hio ya tajsim

zinakaribia kuwa ziko wazi kwamba neno mkono wa Allah haujakusudiwa mkono hakika. Kwa mfano:

a) Hadithi isemayo kwamba “Jiwe jeusi (la Al-Kaba) ni kiganja cha Mwenyezi Mungu”. Je jiwe hilo ni kiganja cha Mungu kweli? Je jiwe hilo hatulioni? Je hatulishiki? Je halina mfano?

b) Hadithi isemayo: “Anayetoa sadaka basi Allah anaichukua kwa mkono wake wa kulia na kuilea juu ya kiganja chake mpaka inakuwa kubwa kuliko jabali”. Je uliokusudiwa hapa ni mkono wa kweli? Sadaka hio sisi tunaiona na kama ni ya kuliwa basi inaliwa na kutolewa katika njia nyengine, basi vipi tena isemwe kwamba iko katika mkono wa Mungu hakika, na kwa hivyo hio iwe ni dalili kwamba Allah ana mkono hakika?

Hizi baadhi ya nukta muhmu za kuzifikiri tena na tena ili uweze kufikia uhakika wa jambo hili.

SURA YA TATUFALSAFA YA BALKAFA

Sasa baada ya hayo naturudi katika mas-ala ya viungo vya Mungu! Tunasema: baada ya yote hayo tulioyazungumzia huko nyuma ya kuwa

155

Page 156: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Mungu ana viungo hivyo tulivyovinukuu na ana sifa hizo tulizozinukuu kwa mujibu wa itikadi ya Kiwahabi na Maimamu wao, basi Mawahabi wao huwa wanajitetea kwamba kanuni ni kuwa Allah hana mfano na kwa hivyo viungo hivyo vya Allah si kwa mfano wa kitu chochote bali ni kwa namna inayomstahikia Allah! Hivyo ndivyo wanavyosema, nayo ni kauli ya ajabu! Na lau utamfuata mtu mmoja mmoja duniani asiyekuwa Muislamu au Muislamu asiyejua chochote katika itikadi hizi: akili yake bado iko safi: haijaathiriwa na itikadi ya madhehebu yoyote ile, kisha ukawambia: “Allah ana mikono miwili, macho mawili, masikio, miguu miwili, muundi, uso, viganja, vidole, mbavu (au pande mbili), magoti, dhiraa, kidakatonge, meno, anakaa kitako, anachoka, anakwenda mbio, anacheka, anashuka na kupanda n.k.”, kisha baada ya hayo ukamuuliza je unadhani Mungu anafanana na nini? Basi elewa kwa yakini kwamba hakutokuwa na yoyote yule ambaye hatojibu kuwa “Mungu kafanana na mtu”. Hii ni kusema kwamba human logic (akili ya kibinaadamu) na human nature au fitra (yaani maumbile) hayakubali kamwe kuwa kuna mwenye tarakibu (mijengeko) ya namna hio kisha awe hafanani na mtu hususan ukichukua vile wanavyotwambia mabwana wa itikadi hizo kwamba viungo hivi ni vitu tafauti: “Mguu wa Mungu si mkono wake, na mkono wake si kifua chake n.k”. Bali kuwepo kwa viungo hivyo tafauti: mikono na masikio, na kwamba mikono si masikio; kuwepo kwa macho na miguu na kwamba macho si miguu, n.k.; kunatoa tashbihi ya wazi ya kumfanya Mungu kuwa ni kiumbe kwani huku ni kumfanya Mungu kuwa ni mwenye kuundika kutokana na viungo tafauti (composed of different organs) au kwa lugha nyengine ni kuwa Allah ni: (

أعضاء عدة من مركب ) . Na bila shaka mwenye hali kama hii, huwezi kudai kuwa si kiumbe au kuwa hafanani na kitu.

Kwa kukupa mfano utaoikurubisha akili yako kwenye fahamu au fahamu yake kwenye akili, fikiri lau mtu atadai kwamba kiko chenye mabawa mawili; minqar (mdomo wa ndege); makhalib (makucha ya ndege); na kinaruka, lakini hakifanani na ndege! Au mtu akidai kuwa kuna chenye matawi, majani, kigogo, matunda, lakini hakifanani na mti! Maneno haya lau utawambia walimwengu basi ama watakuona kuwa wewe ni mgonjwa wa akili, au unafanya maskhara au mwongo.

Naturudi katika falsafa ya balkafa. Tunasema: ama falsafa ya balkafa yaani madai kwamba kanuni ni kuwa Allah hana mfano, na kwa hivyo viungo hivyo si kwa mfano wa kitu chochote bali ni kwa namna inayomstahikia Allah! Tunasema kwamba kuitumia falsafa hio katika kuzifasiri Aya hizo na Hadithi hizo, ni kosa la wazi, kwani msingi wa tafsiri ni matumizi ya lugha ya Kiarabu. Yaani tafsiri sahihi ni lazima isitoke nje ya matumizi ya lugha ya Kiarabu au kwa lugha nyengine ni kwamba iwe tafsiri hio ni yenye

156

Page 157: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kuwiyana na lugha ya Kiarabu. Sasa ukirudi katika lugha ya Kiarabu, ambayo ndio msingi mama wa kufasiria maandiko, hukuti kamwe kuwa kuna kanuni yenye kusema: “Mkono lakini si kama tunavyoujua”. Bali kilichoko katika lugha ya Kiarabu ni kuwa huu ni “Mkono hakika”; na huu “Ni mkono si hakika” bali ni kwa maana kadha – yaani lafdhi iliotajwa ni mkono lakini maana iliokusudiwa ni nyengine. Kama ilivyo, katika Hadithi isemayo: “Lau aliiba Fatima bint Muhammad, basi ningeliukata mkono wake”.561 Na kama ilivyo katika Aya isemayo: “Na mwizi mwanamme na mwizi mwanamke wakateni mikono yao”. Hapa – katika Aya na Hadithi – neno mkono limetumika kwa maana yake ya uhakika – ni mkono kweli. Lakini neno hilo hilo mkono limetumika si kwa maana yake ya hakika au ya asili katika Aya kama: األيد ذا داوود عبدنا واذكر “Na mkumbuke mja wetu Dawud mwenye mikono mingi (zaidi ya miwili)”.562 Na katika Hadithi isemayo: يد Waislamu ni mkono mmoja”.563 Na“ المسلمونkatika mashairi ya Labid aliposesema: الش أمر طافن بيد مالها “Matone, nayapitisha kwa mkono wa kaskazini”.564 Nasi tunajua kwamba kaskazini haina mkono. Kwa hivyo, hapa mkono si katika maana yake ya uhakika.

Na hayo yote tumelazimika kuyazingatia, kwani, kama tulivyosema na kukariri, Allah alipozungumza na sisi alizungumza kwa lugha ya Kiarabu tunayoifahamu; na lugha ya Kiarabu tunayoifahamu haikuja ila kwa namna mbili hizo tulizozieleza:

1) Hakika. 2) Majazi.

Basi: ni hivyo: hakuna mgawanyiko wa tatu. Sasa ukisema kuwa kitu hiki ni hakika, basi uhakika wake ni vile kinavyojulikana katika lugha ya Kiarabu: hakuna katika lugha ya Kiarabu: “kiungo hiki ni hakika lakini si kwa namna tunavyojua”. Na ukisema kuwa kitu hiki ni majazi, basi kinakuwa kimetumika kinyume na maana yake ya asili au ya uhakika. Sasa cha kufahamu na kilicho muhimu kwa mpekuzi katika hatua ya kwanza ya kuyafasiri maandiko ni kujua je lafdhi: “Mkono wa Mungu” ilipotajwa ilikusudiwa uhakika wake au ilikusudiwa majazi, kwani hatuna mgawanyiko wa tatu – hatuna mkono lakini si kama tuujuavyo. Hio falsafa ya “mkono lakini si kama tuujuavyo” ni falsafa ilioundwa kwa ajili ya kutaka kuhalalisha itikadi fulani tu. Sasa kama ni mkono hakika, basi mkono hakika katika lugha ya Kiarabu ni huu tuujuao – mfupa na nyama. Kama mkono majazi, basi zinaangaliwa maana za kimajazi za neno 561 - Al-Bukhari Al-Sahih Hadithi na. 43733. 562 - Sura 38, Aya 17. 563 - Ibn Mandhur Lisanu Al-’Arab j. 15, uk. 439. 564 - K.h.j.

157

Page 158: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

“mkono” kisha inachaguliwa ipi inayolingana zaidi na utukufu wa Allah na kukubaliana na siyaq ya Aya au Hadithi. Ama kudai kwamba huu ni mkono wa kweli lakini si kama tuujuavyo (balkafa), basi hivi ni kinyume na utaratibu wa lugha ya Kiarabu kwani Waarabu kwao lugha hii haikupokewa kamwe bali kilichopokewa kutoka kwao ni hakika na majazi.

Jambo lisilo na shaka kabisa, ni kuwa kutumia falsafa hio ya “Si kama tujuavyo sisi”, katika kuhalalisha itikadi fulani, basi kunaweza kufungua mlango kwa kila mwenye itikadi yake – ikiwa ni sahihi au si sahihi – akasema kuwa Allah ana sifa kadha lakini kwa namna inayomstahikia Yeye: si kama tujuavyo sisi. Anayesema kuwa Allah yupo kila mahala na akatoa ushahidi kwa Aya “…yuko pamoja nao popote walipo”565 atahalalisha itikadi yake hio kwa kusema kwamba Yeye yupo kila mahala lakini “kwa namna inavyomstahikia: si kama tujuavyo sisi”. Na anayeitakidi itikadi ya Al-Badaa (kutamburikiwa) na akatoa ushahidi kwa Hadithi iliopokewa na Al-Imamu Al-Bukhari isemayo: “... يبتليهم أن تعالى لله Allah) ”بداilimbainikia au alitamburikiwa kuwa awatie katika mitihani…),566 pia naye anaweza kudai kwamba Mwenyezi Mungu anayo Al-Badaa lakini kwa namna inavyomstahikia Yeye: si kwa namna tunavyofahamu sisi. Na huyu naye atasema kwamba kuikataa Al-Badaa ni ku’atil (kuikataa) sifa ya Allah iliomo katika Hadithi hio! Bali kwa msingi huo mtu anaweza kuthibitisha itikadi yoyote ile anayoitaka, na akitokea mwengine akampinga mtu huyo kwa Aya, Hadithi au hoja ya kiakili, basi naye atamjibu kwamba makusudio ya Aya hio au Hadithi hio ni pale ambapo utakusudia kwa namna unavyoifahamu wewe: si kwa namna inavyomstahikia Allah; ama kwa namna inavyomstahikia Allah basi Allah ana sifa kadha.

Na kwa hivyo, itakubainikia kwamba njia sahihi katika kuzitazama Aya na Hadithi hizo mutashabihat ni kuzitazama kwa kioo cha misingi miwili ya lazima – yote miwili kwa pamoja: huwezi kuangalia mmoja ukautupa wa pili. Ni lazima tutazame:

1) Aya شيء كمثله 567 Na tufahamu.(Hana mfano wa kitu) ليسnini maana ya kuwa na mfano na nini maana ya kutokuwa na mfano. Huwezi kuniambia: “Kina maringi manne; kina usukani lakini hakifanani na gari”. Au “kina mbawa; kinaruka lakini hakifanani na ndege”. Hili halikubaliki kilugha wala kiakili. Na kwa msingi huu, huwezi kudai kuwa Mungu ana viungo vyote alivyo navyo binaadamu kwa uhakika – isipokuwa uchi na ndevu kama alivyonukuliwa Abu Ya’alaa akisema – kisha unambiye kuwa

565 - Sura 58, Aya 7. 566 - Al-Bukhari Al-Sahih Hadithi na. 3464. 567 - Sura 42, Aya 11.

158

Page 159: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

hafanani na binaadamu. Hili mutatafautiana na walimwengu wote, hususan ukizingatia ukweli kwamba viungo hivyo ni vitu vya kihisia,568 tafauti na sifa kama ya elimu na uwezo. Isipokuwa mutaposema kuwa viungo hivyo ni majazi: jicho kwa maana ya hifadhi, mkono kwa maana ya nguvu, n.k., hapo tafsiri itakubalika.

2) Matumizi ya lugha ya Kiarabu: je lafdhi kadha ni hakika au ni majazi. Na pia tujue kwamba tunaposema kuwa kiungo hiki ni hakika, basi uhakika wake ni vile inavyoeleweka na Waarabu katika lugha yao, kwani Allah kazungumza na sisi kwa lugha tunayoifahamu: si kwa lugha ya balkafa au “kwa hakika lakini si kama tunavyofahamu”. Na tujue kwamba majazi ni kulitoa neno katika maana yake ya asili na kulipeleka katika matumizi mengine yaliopo katika lugha ya Kiarabu.

Tukifuata utaratibu huo, basi mashua yetu itafika nchi kavu kwa salama kabisa. Ama wenye itikadi ya kuwa “Allah ana viungo lakini havifanani na kitu”, utaona kwamba wao walichukua lafdhi za Aya hizo na Hadithi hizo kisha wakazifungamanisha na Aya شيء كمثله Hana mfano wa) ليسkitu), na – bila ya kufahamu maana ya kuwa Allah hana mfano – wakatoa natija kwamba Allah ana viungo lakini havifanani na kitu!569 Lakini – hata kama msingi huo wa kwanza wameutazama – hawakutazama msingi wa pili wa matumizi ya lugha ya Kiarabu: je lafdhi hizo zimetumika kwa hakika au kwa majazi? Na hatimae hilo liliwapelekea katika kuyakanusha majazi ili wapate kuilazimisha itikadi yao. Tumeona huko nyuma kwamba maandiko yao mengi walioyatumia hayakuwasaidia katika kuthibitisha itikadi yao. Tumebakiwa na suali: je lugha ya Kiarabu, Qur-ani na Hadithi zina majazi ndani yake au hazina? Hilo ni jambo muhimu na la lazima kulifahamu ili kuweza kuufikia uhakika na ukweli. Tutakuwa na maelezo zaidi tukifika sehemu ya kuelezea majazi in shaa Allah. Kwa sasa – baada ya kufanya mukhtasari – natutazame natija mbili za hatari zilizojitokeza kutoka katika itikadi hizo za Kiwahabi.

MUKHTASARI NA NUKTA MUHIMU

568 - Ndio maana Maimamu watangulizi wa Kiwahabi wakasema: “Allah ni kiwiliwili si kama viwiliwili”. 569 - Lakini hata hivyo, tunasema kuwa Mungu waliyemuelezea wao haiwezekani kamwe kuwa hafanani na kitu; bali ana sura ya mtu, na kwa hivyo, wao wenyewe wameshindwa kujizuia kutokana na kusema hivyo kama tutavyobainisha.

159

Page 160: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

1) Tulichokizungumzia hapa ni hii falsafa ya balkafa. Yaani kusema kwamba Allah ana viungo (mikono, miguu n.k.) lakini si kwa namna tunayoijua sisi.

2) Tumesema, na kukariri sana, kwamba Allah kazungumza na sisi kwa lugha tunayoijua: si kwa lugha tusioijua. Kwa hivyo, hakuna kitu mkono lakini si kama tuujuao. Bali kuna mkono wa kweli na mkono majazi, au kwa maneno mengine ni kuwa, kilichoko ni:

a) Neno hili ni hakika.b) Neno hili ni majazi.

3) Aya isemayo: شيء كمثله haikuja ,(Hana mfano wa kitu) ليسkuthibitisha kuwa Allah ana viungo, bali imekuja kuthibitisha kuwa Allah hafanani na kitu chochote. Wala Aya hio haikuja kuondoa utaratibu wa lugha ya Kiarabu uliomo katika Qur-ani, Hadithi na lugha ya Kiarabu, yaani haikuja kuondoa utaratibu wa kuwepo kwa majazi.

4) Ili kufikia natija sahihi ni lazima:a) Tuitazame Aya hio, na tutoe ndani yake natija ya kuwa Allah

hana mfano wa chochote kile. Wala haitoshi kusema “Lakini si kama tujuavyo” kwani kwa kusema hivyo tu bado hujamuondoshea Allah mifano, bali umejidanganya tu kwamba si kwa namna unavyojua wewe: ama maana ya mfano bado ipo pale pale.

b) Lazima tutazame utaratibu wa lugha: je neno kadha katika Aya kadha limetumika kiuhakika au limetumika kimajazi. Kama ni hakika, basi tulipe neno hilo maana yake ya uhakika kwa mujibu wa inavyofahamika katika lugha ya Waarabu; kama ni majazi, basi tulipe maana sahihi ya kimajazi.

c) Tujue kwamba hakuna katika ulimwengu wa Waarabu – ambao lugha yao ndio msingi wa kufasiria maandiko – falsafa ya “neno hili ni hakika lakini si kama tujuavyo sisi”. Na mwenye nao ushahidi juu falsafa hii na-atuletee.

SURA YA NNENATIJA MBILI ZA HATARI

MJADALA WA DIAMOND JUBILEE

160

Page 161: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Kwa kuwa akili ya kibinaadamu haikubali kwamba mwenye viungo kama hivyo tulivyovinukuu kabla kwa uhakika wake, awe hana sura ya binaadamu, basi natija mbili za hatari zimedhihiri katika uwanja wa itikadi za kidini:

Mosi: Kipindi cha nyuma – sikumbuki ni lini hasa – palifanyika mjadala wa kidini baina ya Waislamu na Wakiristo katika ukumbi wa Diamond Jubilee huko Dar-es-Salam. Kukatolewa fursa ya kuuliza masuali: Waislamu wawaulize Wakiristo masuali wayatakayo na Wakiristo wawaulize Waislamu masuali wayatakayo. Mmoja wa Wakiristo akauliza kwamba katika Sahihu Al-Bukhari kuna Hadithi inasema: “Allah ataiuliza jahannam je umeshajaa? Nayo itajibu: Je kuna ziada? Hapo Allah atatia mguu wake kwenye moto na hapo jahannam itakunjana na kusema: qat qat (inatosha inatosha)”.570 Wakiristo wakauliza:

a) Hadithi inasema kuwa Allah atatia mguu katika moto , kwa hivyo, Allah Mwenyewe kumbe atakwenda motoni! Sasa tuonesheni andiko jengine lenye kusema kuwa Allah atatoka humo.

b) Munasema kwamba Allah hana mfano kumbe mfano anao: si huu mguu anao? Kwa hivyo, anafana na mtu!

Masuala haya Waislamu walioshiriki katika mjadala huo hawakuweza kuyajibu kwa jawabu sahihi, bali walibabaika tu huku na kule! Hii ndio natija ya kuzikumbatia Hadithi za kutunga na kuzifanya kuwa ndio dini na Sunna yenyewe! Na ndio natija ya kuyafasiri maandiko kinyume na njia zake sahihi za lugha ya Kiarabu ilivyo!

Lakini, kwa mukhtasari hapa, tunasema kuwambia Wakiristo kwamba:1) Qur-ani ndio msingi571 mama wa itikadi ya Kiislamu, kwani haingii

batili nyuma yake wale mbele yake. Na kwa hivyo, Hadithi inapimwa kwa Qur-ani wala si kwamba Qur-ani inapimwa kwa Hadithi. Sasa kama Qur-ani inasema kwamba Allah “Hana mfano wa kitu”572 na inasema: “Hakuna yoyote aliye kama Yeye”,573 basi elewa kwamba Hadithi yoyote ile itayokuja kuhusu maudhui hii, basi inapimwa na Aya hizo, ikiwa imekubaliana nazo basi Hadithi

570 - Al-Bukhari Sahihu Al-Bukhari Hadithi na. 4849-4850. 571 - Kasim Mafuta yeye niliposema kuwa Qur-ani ndio msingi akanijibu kuwa hata Sunna ni msingi! Namwambia kwamba makusudio ya kuwa Qur-ani ndio msingi ni kuwa usahihi wa Hadithi unapimwa kwa Qur-ani wakati Qur-ani haipimwi kwa Hadithi. Na Qur-ani hatuna shaka juu ya kuthibiti, ama Hadithi hatuna hakika 100% ila iwe ni Hadith mutawaatir.572 - Sura 42, Aya 11. 573 - Sura 112, Aya 4.

161

Page 162: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

hio inazingatiwa; kama haikukubaliana nazo hata kwa tafsiri ya ndani (ta-awil au interpretation), basi hio ni Hadithi ya uwongo: haitoki kwa Mtume (s.a.w.).

2) Hadithi ziko sahihi na ziko dhaifu na ziko za kutunga (za uwongo).3) Maandiko – kama yalivyo maneno ya binaadamu – si mara zote

huwa yanachukuliwa katika udhahiri wake: wakati mwengine kunakuwa na ta-awil (interpretation). Kama nikisema “Yule ana ulimi sana au ana ulimi mrefu”. Yaani yeye ni msemaji sana au ni mtukanaji sana: wala si kwamba ninaukusudia ulimi-kiungo. Halkadhalika ukitajwa mkono au mguu wa Mungu si kwamba Mungu ana mguu, bali inakusudiwa maana ya undani ya kimajazi (metaphorical meaning). Kwani mguu katika maana yake ya uhakika ni kiungo cha kihisia (phyisical organ) na Allah hayuko hivyo.

4) Itikadi ya kuwa Allah ana viungo haiwakilishi itikadi ya Umma wa Kiislamu. Hio ni itikadi ya kikundi fulani kiitwacho Wahabi, ambao hawaundi hata 5% katika jumla ya Waislamu wote duniani. Bali wao wana Hadithi kwamba Mungu (wao) atakuwa katika tabaka ya nne ya jahanam! Kwa hivyo, kwa mujibu wao si kwamba mguu wa Mungu tu ndio utaingia motoni, bali Mungu wote ataingia humo. Sasa ushahidi wa kuwa Mungu atatoka humo tafadhalini waombeni wao tu wakupeni, kwani wao ndio wenye itikadi hio. Kwa hivyo, itikadi hio musiinasibishe na Uislamu na hayo masuali itakubidini muwaulize wao tu. Kama vile ambavyo mfuasi wa madhehebu moja ya Kikiristo halazimiki kujibu masuali yenye kuhusiana na itikadi ya mfuasi wa madhehu mengine kwani yeye hayaamini.

5) Hadithi hio mulioitolea ushahidi, wanavyuoni wa Kiislamu hawakukubaliana kuwa ni sahihi. Wengine wameikanusha na wengine wakaikubali lakini wakaitolea ta-awil (interpretation au tafsiri ya ndani). Cha kufahamu ni kuwa risala ya Kiislamu imekuja kwa lugha ya Kiarab, na lugha hii – kama kilivyo Kiswahili – mara nyengine inatumika katika uhakika wake na mara nyengine inatumika kimajazi (metaphorically). Mswahili akisema “Nilikuwa nipate nafasi ya kwenda masomoni, lakini wizara ya elimu imeiwekea mguu,” hii haina maana kwamba wizara ina mguu, bali maana yake ni kuwa wizara imeizuia nafasi hio. Na uhusiano uliopo baina ya ibara hio ya kimajazi (metaphorical expression) na maana ya uhakika ya kuizuia nafasi ni kuwa kitu ukikiwekea mguu unakuwa umekizuia hakipati kutikisika, halkadhalika kuekewa mguu kwa nafasi ya masomo ni kuzuiwa nafasi hio. Basi vivyo hivyo, iliposemwa kuwa Allah atatia mguu wake, tukijaalia kuwa hio ni riwaya sahihi, basi maana ni kuwa Allah ataudhalilisha moto huo. Na uhusiano baina ya ibara hio ya kimajazi (kutia mguu) na maana

162

Page 163: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

ya uhakika (kudhalilisha) ni kuwa kukiwekea kitu mguu ni kukidharau au kukidhalilisha. Anasema mwanachuoni mkubwa wa lugha Al-Imamu Al-Zamakhshari:

“Na miongoni mwa majazi (metaphor) ni kusema:عنه اعف أي قدميك تحت ذلك اجعل

“iweke hiyo chini ya miguu yako, yaani isamehe”.

Na pia ni kusema: : أهدرها قدميه تحت دماءهم جعل

“kaziweka damu zao chini ya miguu yake, yaani kazimwaga bure”.574

Na “katika Hadithi (imepokewa):

: قدمه فيضع ربها يأتيها حتى مزيد من هل وتقول أهلها النار في يلقىويكس���ر فيسكنها أي

فيسكنه مضطرب شيء على قدمه الرجل يضع كما سوتها

Watatupwa motoni watu wake (watu wa motoni) na moto utasema je kuna ziada mpaka Allah ataujia na atatia mguu wake humo. Yaani atautuliza na kuuvunja nguvu zake kama mtu anavyoweka mguu katika kitu chenye kupapatika akakituliza.575

6) Vyenginevyo, ikiwa Allah atatia mguu kwenye jahannam kweli kweli kama wanavyodai wanaoitwa Mawahabi, basi Mawahabi wana deni kwa Wakiristo waeleze au walete ushahidi wa riwaya nyengine kuonesha wapi pamesemwa kuwa mguu huo atautoa, bali wapi imesemwa kuwa atatoka humo kwa vile atakuwa katika tabaka ya nne ya jahannam? Hili si suala linalowahusu Waislamu wote bali ni suala linalowahusu wanaoitwa Mawahabi tu,576 na Sheikh Mafuta, mmoja wa viranja wao, anaweza kukujibuni - muulizeni.

MUNGU ANA SURA YA ADAM!Jambo la pili: baya lililojitokeza ni kuwa kwa sababu hio ya kuwa akili ya binaadamu yoyote yule haikubali kuwa mwenye viungo hivyo hafanani na binaadamu, basi utakuta kwamba pamoja na kuwa Mawahabi wanatangaza

574 - Au kaiwachia ipite bure bure bila ya kisasi wala dia nayo ni malipo wapewayo jamaa wa mtu aliyeuliwa. 575 - Tazama Al-Zamakhshari Asasu Al-Balagha uk. 592. 576 - Tazama Ibn Al-Qayyim Haadi Al-Ar-waah uk. 299. ‘Uthmaan Al-Darimi Al-Raddu ‘Alaa Al-Marisi uk. 68. Dr. Ali Muhammad Al-Sallabi Min ‘Aqitadati Al-Muslimin uk. 79-80.

163

Page 164: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

usiku na mchana kwamba Allah ana viungo si kwa mfano tuujuao sisi, lakini hata hivyo wao wenyewe hawakuweza kujimiliki – katika baadhi ya maandishi yao – kusema kwa uwazi kuwa Allah kafanana na mtu! Na vipi wasiseme hivyo, na mwenye viungo hivyo lazima atakuwa na sura ya kibinaadamu? Al-Tuwaijri – katika kitabu chake ‘Aqidatu Ahli Al-Iman fii Khalqi Adam ‘Alaa Surati Al-Rahman577 (Itikadi Ya Watu Wa Imani578 Katika Kuumbwa Adam Kwa Sura Ya Allah) ambacho Ibn Baz kakipitia na kukisifu – anasema:

قوله في الضمير يعيد من لقول مبطلة أنها مع كلها الوجوه على( وهذهفه صورته) آدم، ي��إلى

)).... أدلة أن إلى نفسه صورة على آدم خلق الله بأن اإلخبار في مستقلةف: (( وأيضا هذا��������قال

) المعنى فإن( األنبياء عن المؤثورة الكتب من الكتاب أهل عند موجودمن األول السفر ها ������في

يشبهها سنخلق(( صورتنا على . ((بشرا

Na njia hizi zote – pamoja na kuwa zinaibatilisha kauli ya mwenye kuirejesha dhamiri (pronoun) kwa Adam – basi hizi ni habari zenye kujitegemea katika kutoa habari kwamba Allah kamuumba Adam kwa sura yake mwenyewe…….Na maana hii pia ipo kwa Watu wa Kitabu Mayahudi na Manasara katika vitabu vilivyopokewa kutoka kwa Manabii, hakika katika kitabu cha mwanzo (cha Bibilia, imeandikwa kwamba): “Tutamuumba mtu kwa sura kama yetu anafana nayo”.579

Anachokisema Sheikh huyo ni kuwa kuna Hadithi inayosema:

ذراعا ستون طوله صورته على آدم الله وخلقNa (Allah) kamuumba Adam kwa sura yake

urefu wake ni dhiraa sitini.580

Sasa suali lililopo hapa ni kuwa je dhamiri (yaani neno yake katika jumla ya maneno yanayosema sura yake) inarejea kwa nani – kwa Allah au kwa Adam? Sheikh wa Kiwahabi anasema kwamba dhamiri inarejea kwa Allah, na kwa hivyo maana ni: “Adam kaumbwa kwa sura ya Allah,” na kwa hivyo natija ni kuwa sura ya Adam ndio sura ya Allah! Na kwa sababu hio, ndio

577 - Uk. 76. 578 - Watu wa Imani yaani ni Mawahabi na wale wote wenye kusema kuwa Mungu kamuumba Adam kwa sura yake! Na pia anaingia katika sifa hio yule aliyesema kwamba Allah kaumba nafsi yake kutoka katika jasho la farasi! 579 - Humud Al-Tuwaijri ‘Aqiidatu Ahli Al-Iman fii Khalqi Adam ‘Alaa Surati Al-Rahman uk. 76. 580 - Al-Bukhari Al-Sahih Hadithi na. 3326. Muslim Al-Sahih Hadithi na. 2183. Ibn Ahmad Al-Sunna j. 2, uk. 470, riwaya na. 1068.

164

Page 165: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

maana ikaja riwaya nyengine ikibainisha kwa uwazi kwamba binaadamu kaumbwa kwa sura ya Mungu! Inasema riwaya hio:

الرحمن صورة على خلق آدم ابن فإن الوجه تقبحوا الMusiuumbue uso, kwani mwanaadamu kaumbwa

kwa sura ya Allah Mwingi wa rehema!581

Hadithi hii haibebi tafsiri ila moja: Mungu ana sura ya mtu! Kwa hivyo, Mungu kafanana na sisi? Na hii – mbali na kuwa iko wazi katika ibara yenyewe – ni kwa sababu, herufi Al-Faau (fee) katika Hadithi hio ina maana ya ta’alil (kuonesha sababu); na neno inna ni hivyo hivyo – yaani illa ya pili itakuwa inatoa taukid (mkazo) ya illa ya kwanza. Na maana ya yote hayo ni kuwa tumekatazwa kuuchokoza au kuupiga582 uso; je sababu ni nini? Sababu ni kuwa uso wa binaadamu una sura sawa na sura ya Mungu!

Hayo ndio maana ya maelezo ya Sheikh huyo wa Kiwahabi, na kitabu chake hicho kimepitiwa na kusifiwa na Ibn Baz.583 Ni wazi kwamba itikadi ya Kiwahabi ni kuwa Allah ana sura ya binaadamu. Na kwa sababu hio ndio maana Abu Mu’adh, dhahir ni kuwa huyu ni mwanafunzi wa Ibn ‘Uthaimin, anasema:

مند(( ابن هذا : هوعلى .... (( بأن القول يعني قلت اه� التوحيد كتاب فيعائ الله ��������الضمير إلى د

مند ابن قول هو آدم، كصورة صورة لله أن كتاب هبمعنى في أيضا. له التوحيد

Na Ibn Manda anaifuata kauli hii”.584 Ninasema: (yaani kusema kwamba dhamiri inarudi kwa Allah kwa maana kwamba Adam kaumbwa kwa sura ya Mungu ndio kauli ya Ibn Manda katika kitabu chake Kitabu Al-Tauhid).

581 - Ibn Ahmad Al-Sunna j. 1, uk. 268, riwaya na. 498. J. 2, uk 472, riwaya na. 1076. Al-Bayhaqi Al-Asmaau Wa Al-Sifaat j. 2, uk. 63-64, riwaya na. 639-640. Anasema muhakiki naye ni Abdullah bin Muhammad Al-Hashidi: “Ni Hadithi sahihi”. 582 - Kama ilivyo katika riwaya nyengine. 583 - Na Al-Tuwaijri huyo alikuwa mpenzi mkubwa wa Ibn Baz. Anasema mtunzi wa kitabu Jawaanibu Min Siirati Ibn Baaz, uk. 164:

حمود الشيخ العالمة الفضيلة صاحب سماحته؛ عند منزلة لهم الذين العلماء ومنويكتب يقرضها، وكان لكتبه، قارئا له، محبا عبدالعزيز الشيخ كان حيث التويجري

. المقدمات عليهاNa miongoni mwa wanavyuoni ambao walikuwa na nafasi kwake (Ibn Baz), ni Fadhilatu Al-Sheikh Humud Al-Tuwaijri, ambapo Sheikh ‘Abdul-‘Aziz (Ibn Baz) alikuwa akivisoma vitabu vyake na kuvisifu na kuvitia utangulizi. 584 - Abu Mu’adh Al-Muntaqa Min Sharhi Usuli I’itiqad Ahli Al-Sunna Wa Al-Jama’a uk. 413.

165

Page 166: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Kisha Abu Mu’adh akanukuu maneno ya Ibn Manda akasema:

Na (Ibn Manda) kaipinga tafsiri hii ya Ibn Khuzaima (kwamba dhamiri inarejea kwa mtu mwenye kupigwa: (si kwa Mungu)585 na (Ibn Manda) akaizingatia (kauli hio ya Ibn Khuzaima) kuwa ni katika sehemu alizoteleza (Ibn Khuzaima) na kwamba hakufuatiwa na Imamu yoyote yule katika tafsiri hio.586

Hayo ndio aliyoyasema Abu Mu’adh kuhusu msimamo wa Ibn Manda. Lakini dhahir ni kuwa Abu Mu’adh alitaka kuipalilia itikadi yake ya Kiwahabi! Kwani, ukirejea Kitabu Al-Tawhid cha Ibn Manda utakuta ni kinyume na hivyo alivyoeleza Abu Mu’adh.587 Maneno ya Ibn Manda ni haya:

: وتك الحديث هذا معنى في التأويل أهل ض ���اختلف على روب����لمواواألحس من �����شتى، ها:�������ن

الس – عليه آدم خلق تعالى الله ص – ������أن على لم . ��������الم معناه ورتهص ثم طفال ا�بي������يخلقه

.. ...(( اه� شيخا ثم كهال في. ..........ثم آخر �����م وقال (( وضع أراد: وإنماعلي النبي الله ه ��������صلى

آدم وسلم صورة على آدم بني خلق الله أن الكالم اه� .بهذا

Wametafautiana watu wa ta-awil kuhusu maana ya Hadithi hii na wakazungumzia aina tafauti, na bora yao katika hizo ni kuwa: Allah kamuumba Adam (a.s.) kwa sura yake kwa maana kwamba hakumuumba mtoto kisha mtu mzima kisha mzee”.Mwisho wa kunukuu.588 Kisha akasema Ibn Manda katika sehemu nyengine: ‘Na kwa hakika Mtume (s.a.w.) kakusudia kwa maneno haya kwamba Allah kawaumba watoto wa Adam kwa sura ya (baba yao) Adam’.589

Hayo ndio maneno ya Ibn Manda nayo – kama unavyoona – ni tafauti na alivyonukuliwa na Sheikh wa Kiwahabi, Abu Mu’adh. Labda siku zijazo

585 - Yaani Hadithi kwa ukamilifu wake inasema kuwa Mtume (s.a.w.) kakataza kuupiga uso, akasema: “Mmoja wenu akimpiga nduguye na-aepuke (kuupiga) uso kwani Allah kamuumba Adam kwa sura yake”. Tazama Muslim Al-Sahih Hadithi na. 2612. Ninasema: kwa mujibu wa illa hii iliotajwa hapa, huwezi kusema kuwa dhamiri inarejea kwa mtu. Wallahu Al-Musta’aan. 586 - Abu Mu’adh Al-Muntaqa Min Sharhi Usuli I’itiqad Ahli Al-Sunna Wa Al-Jama’a uk. 413. 587 - Lakini kitachomuombea Abu Mu’adh ni kuwa yeye kayanukuu maneno hayo kutoka kwa Humud Al-Tuwaijri. 588 - Ibn Manda Kitabu Al-Tawhid kilichotiwa maelezo na Dr. Ali Al-Faqihi uk. 222-223, Hadithi na. 83. 589 - Ibn Manda Kitabu Al-Tawhid kilichotiwa maelezo na Dr. Ali Al-Faqihi uk. 223-224, Hadithi na. 84.

166

Page 167: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Abu Mu’adh naye atakuwa katika urodha ya waongo ya Sh. Kasim Mafuta na wenzake!

Kwa hali yoyote ile, Sheikh huyo wa Kiwahabi anamkosoa Ibn Khuzaima kwa kusema kwake kwamba dhamiri katika Hadithi hio inarudi kwa kiumbe si kwa Muumba. Ukichanganya na yalionenwa na Humud Al-Tuwaijri na Ibn Baz kuyakubali basi maana ni kwamba wao wanamthibitishia Allah sura kama ya Adam! Basi vipi tena watasema kuwa wao hawamshabihishi Allah na viumbe ilhali sura yake ni kama ya Adam! Bali hicho ndicho alichokinukuu Abu Mu’adh kutoka kwa Imamu Mkuu Ibn Taymiya. Anasema Ibn Taymiyya – katika nukulu hiyo ya Abu Mu’adh -:

السل بين يكن لم ن ���������وأنه الثالثة القرون من أن �ف في زاعتعال ����الض الله إلى عائد ى ���������مير

. اه� ذلك على تدل كلها األحاديث سياق وأن

Na kwamba hakukuwa na tafauti baina ya Al-Salaf katika karne tatu (za mwanzo) kwamba dhamir inarejea kwa Allah Mtukufu na kwamba Siyaaq (context) ya Hadithi inaonesha hivyo.590

Na akasema:

في الجهمية انتشرت لما ولكن وتصديقه تبليغه على اتفقت األمة إنطائ�������فة جعل الثالثة المائة

.... تعالى الله غير إلى عائدا فيه الضمير

Hakika ya Umma wa Kiislamu umekubaliana kuifikisha (Hadithi hio) na kuiamini, lakini Jahmiyya walipoenea katika karne ya tatu, basi baadhi ya watu wakaifanya dhamiri kuwa inarejea kwa asiyekuwa Allah Mtukufu.591

Hayo ndio maneno ya Ibn Taymiyya, na lau aliyasema Sheikh wa Kiibadhi basi tayari angelikuwa katika orodha ya waongo ya Kasim Mafuta. Vyenginevyo, kwa vile Mzee wa Uislamu Ibn Taymiyya hayupo tena, tunamuachia chalenj hii Al-’Allama Kasim Mafuta atuthibitishie kwamba hakukuwa na khilafu katika karne tatu za mwanzo kwamba dhamiri inarudi kwa Allah kama alivyodai Ibn Taymiyya.

Kwa hivyo, ni wazi kwamba Sheikh Al-Islam – sijui ni Uislamu gani – naye pia anamthibitishia Allah sura kama ya Adam! Sasa vipi munadai kuwa hamumfananishi Allah na viumbe? Kama huku si kumfananisha Allah na

590 - Abu Mu’adh Al-Muntaqa Min Sharhi Usuli I’atiqaadi Ahli Al-Sunna uk. 416. 591 - Abu Mu’adh K.h.j. uk. 416-417.

167

Page 168: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kiumbe, basi hakuna tena duniani kitu kumfananisha Allah na kiumbe! Wallahu Al-Musta’aan.

Pia ni vyema kukumbusha kwamba itikadi hio hakupwekeka nayo Ibn Taymiyya na wafuasi wake wa leo, bali hata wale wafuasi wake wa kale walikuwa na itikadi hio hio, ambapo Ibn Al-Qayyim kanena: “Mungu kamuumba Adam kwa mkono wake kwa Sura yake.”592 Kwa hivyo, hio ndio:

1) Itikadi ya Al-Salaf!2) Itikadi ya Masahaba!3) Itikadi ya Mitume! – Mungu kafanana na Adam – god-incarnate

indeed!Kwa hivyo, mukhtasari wa haya ni kuwa itikadi ya Al-Salafu Al-Salih (Watangulizi wema) kuhusu Mwenyezi Mungu, ni kuwa Mwenyezi Mungu ana sura ya mtu! Hio ndio maana inayopatikana katika maandiko ya Kiwahabi! Lakini sijui ni Al-Salaf (watangulizi) gani hao waliokuwa na itikadi hio: je ni Abu Bakr, ‘Umar, ‘Uthman na ‘Ali na walio mfano wa hao; au ni Ibn Batta, Al-Sijzi, ‘Uthman bin Said Al-Darimi na walio mfano wa hao? Ikiwa ni wanne wa mwanzo, basi tutaendelea kutafautina sana na wanaojiita Al-Salafiyya (Mawahabi) na ninaapa kwa jina la Allah aliye Jabbaari wa mbingu na ardhi hakuna yoyote katika hao aliyekuwa na itikadi kwamba “Adam kaumbwa kwa sura ya Mungu”.

Lakini baada ya yote hayo, tunamkuta Sheikh Al-Albani baada ya kuinukuu Hadithi hio ya “Allah kamuumba Adam kwa sura yake” na kusema kuwa ni sahihi, hakukubaliana na Al-Tuwaijri na Mawahabi wengine kwamba dhamiri inarudi kwa Allah. Anasema:

ألنه : : : ف السالم عليه آدم إلى صورته على قوله في الضمير يرجع ائدةمذكور و أقرب ه������ألن،

: آدم الله خلق بلفظ هريرة أبي عن للبخاري آخر رواية في به مصرحطوله صورته ون��ست على

في : ... ……ذراعا حققته كما منكر فهو الرحمن صورة على حديث وأمااآلخر مع.......الكتاب

وغيره الله رحمه التويجري كالشيخ المعاصرين من صححه من على الرد

Faida: katika maneno ya Mtume (s.a.w.) yasemayo: “Kwa sura yake”, basi dhamiri inarejea kwa Adam (a.s.), kwani ndiye aliyetajwa karibu zaidi na kwa sababu ndiye aliyetajwa kwa uwazi katika riwaya nyengine ya Al-Bukhari isemayo: “(Allah) kamuumba Adam kwa sura yake urefu

592 - Ibn Al-Qayyim Hadi Al-Arwah uk. 299.

168

Page 169: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

wake ni dhiraa sitini”.593 Ama Hadithi isemayo: “Kwa sura ya Allah Mwingi wa rehema” hio ni riwaya munkar kama nilivyoielezea katika kitabu chengine….pamoja na kuwarudi wale waliosema kuwa hio ni riwaya sahihi miongoni mwa wanavyuoni wa sasa kama vile Sheikh Al-Tuwaijri – Allah amrehemu – na wengine.594

Hayo ndio maneno ya Al-Albani, lakini kama unavyoona kwamba kipengele kinachosema: “…Waliosema kuwa hio ni riwaya sahihi miongoni mwa wanavyuoni wa sasa…”, ni kinyume na yale tulioyanukuu kutoka kwa Mzee wa Uislamu, Ibn Taymiyya kwamba katika karne tatu za mwanzo hakukuwa na tafauti kwamba dhamiri inarudi kwa Allah; na kwamba waliodai kwamba dhamiri inarudi kwa kiumbe ni Jahmiyya au ilisemwa hivyo baada ya kuenea kwa Jahmiyya.

Ama dhamiri kurudi katika kilichotajwa karibu zaidi, hio ni aghlabu tu: si mara zote. Na kwa hivyo, dhamiri imerejeshwa katika kilichotajwa mbali zaidi katika Aya:

به يعظكم والحكمة الكتاب من عليكم أنزل وما….Na kile alichokuteremshieni katika kitabu na hekima, anakuaidhini kwacho….595

Dhamir (bihi) ama inarudi katika neno “kitabu” au katika maneno “maa anzala”, na zote ziko mbali kuliko neno hikma, kwani kama dhamiri ilirudi katika kilichotajwa karibu zaidi basi ingelikuwa “Ya’idhukum bihaa” si “Ya’idhukum bihi”.. Na haya yote ni pale kwenye qarina zilizoonesha hivyo. Na bila shaka ikiwa kinachofahamika katika Hadithi “(Allah) kamuumba Adam kwa sura yake urefu wake ni dhiraa sitini” ni sura ya Adam, basi kinachofahamika katika Hadithi isemayo: “Mmoja wenu akipiga na-aepuke (kupiga) uso kwani Allah kamuumba Adam kwa sura yake” 596ni sura ya Allah. Kwa sababu maneno ( صورته على آدم خلق الله Kwani“ (فإنAllah kamuumba Adam kwa sura yake” ni السابق للكالم kutoa) تعليلsababu ya maneno yaliotangulia). Na bila shaka illa (sababu) hii hapa haiwi sawa isipokuwa isemwe kwamba tumekatazwa kuupiga uso kwa sababu Adam kaumbwa kwa sura ya Allah; ama kusema kwa sababu “Allah kamuumba Adam kwa sura ya Adam” hiyo si mantiki sahihi.

593 - Al-Bukhari Al-Sahih Hadithi na. 3326. Muslim Al-Sahih Hadithi na. 2183. Ibn Ahmad Al-Sunna j. 2, uk. 470, riwaya na. 1068. 594 - Al-Albani Al-Sahiha j. 2, uk. 519, Hadithi na. 862. 595 - Sura 2, Aya 231. 596 - Nayo ni Hadithi ambayo Al-Albani mwenyewe kaisahihisha. Tazama Al-Sahiha j. 2, uk. 519, Hadithi na. 862.

169

Page 170: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Kwa hali yoyote ile, itikadi ya Al-Albani kuhusu Hadithi hizi ni sahihi; na itikadi ya Ibn Taymiyya, Ibn Al-Qayyim, Abu Mu’adh, Al-Tuwaijri na – dhahir – Ibn Baz na wengine, ni itikadi potofu kabisa haifai hata kutajwa wal’iyaadhi bi-Lahi. Lakini ninachotaka kukisema ni kuwa:

1) Uchambuzi wa Sheikh Al-Albani hapa una mashaka sana. 2) Tayari Mawahabi au baadhi ya Mawahabi pamoja na Maimamu wao

watangulizi au baadhi ya Maimamu wao wameshajenga itikadi kwamba “Adam kaumbwa kwa sura ya Allah”! Na huku ni kumfananisha Muumba na kiumbe wazi wazi!

170

Page 171: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

SURA YA TANOTASHBIHI NI NINI?

Sasa baada ya hayo, ni vyema kutazama kitu chengine ambacho wamekuwa wakikidai mabwana wa itikadi za tashbih, nacho ni madai ya baadhi yao kwamba tashbihi (kumfananisha Allah) ni kusema: “Allah ana mkono kama mkono wangu”. Anasema Dr. ‘Ali Al-Faqihi:

: سمع لله تقول أن وغيره، حنبل بن أحمد اإلمام قال كما التشبيه وإنماكبصري وبصر كسمعي،

. كيدي ويد

Na kwa hakika kumfananisha (Allah na viumbe) – kama alivyosema Al-Imamu Ahmad na wengineo – ni kusema Allah ana sikio kama langu; na jicho kama langu na mkono kama wangu.597

Hayo ndio madai ya Al-Faqihi na wenzake, nayo si madai barabara kwani tashbihi (kufananisha) inakuwa sarih (ya wazi) kama hio alioitaja yeye na inakuwa dhimniy (yenye kuwemo ndani ya maneno) bila ya kutajwa kwa uwazi. Na kwa hivyo, yamehisabiwa kuwa ni katika tashbihi maneno kama:

** إيالم بميت لجرح ما عليه الهوان يسهل يهن من

Anayedharauliwa basi kudharauliwa kunakuwa kwepesi juu yake***Maiti haumii kwa kumjeruhi kwake.

Hii ni tashbihi dhimniy (yenye kuwemo ndani ya maneno). Yaani mshairi anamfananisha mtu ambaye watu wanamdharau na maiti, ambapo mtu huyo mwenye kudharauliwa basi hatima yake anakuwa hajali tena kudharauliwa. Kisha akamshabihisha (akamfananisha) mtu huyo na kitendo cha kumpiga maiti ambapo hasikii maumivu hata ukimpiga vipi. Kwa hivyo, tashbihi ya kitu na kitu katika lugha ya Kiarabu na nyengine si wakati wote inakuwa lazima ulete herufi ya kufananishia kwa uwazi, tafauti na madai ya Al-Faqihi.

Bali kile kinachoitwa tashbihun baligh katika lugha ya Kiarabu, kinatosha kuyarudi madai hayo ya Al-Faqihi. Ukisema (( حمار Fulani ni) ((فالنpunda), basi unakuwa umemfananisha fulani huyo na punda, na hicho ni Kiarabu fasihi. Halkadhalika ukiwa utasema: (( أسد أو جبل أو حجر فالن597 - ‘Ali Al-Faqihi Al-Raddu Al-Qawiim uk. 31. Pia tazama maelezo yake katika Kitabu Al-Tauhid cha Ibn Manda j. 3, uk. 109.

171

Page 172: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

بحر Zote hizi ni .(Fulani ni jiwe, au ni jabali au ni simba au ni bahari) ((أوtashbihi nazo haziko nje ya ufasaha wa lugha ya Kiarabu. Kwa hivyo, kudai kwamba tashbihi ni kusema: كيدي tu, si dai (mkono kama wangu) يدsahihi.

Ukiniambia:

Aaa! Hio mifano uliotoa wewe ni yenye kufananisha sifa na sifa au hali na hali, kwani kauli yako unaposema fulani ni bahari hukusudii kwamba ana sura kama ya bahari, bali unakusudia kwamba ni karimu sana au ana elimu sana, na huku ni kufananisha sifa na sifa. Halkadhalika ukisema fulani ni punda yaani hafahamu au anafanya kazi sana. Na hii ni tafauti na kusema kwamba mkono kama wangu ambapo unakuwa umefananisha dhati na dhati na hii ndio maudhui yetu.

Ukiniambia hivyo nitakujibu kwa kile kilichomo katika Nuniyya ya Ibn Al-Qayyim ambapo katumia hoja yenye kubainisha kuwepo kwa tashbihi dhimniy (yenye kuwemo ndani ya maneno). Tazama ukweli kwamba Ibn Al-Qayyim kasema kuhusu wale aliowaita kuwa ni mu’attila kwamba watu hao ni mushabbiha (wenye kumfananisha Allah na viumbe), ilhali watu hao hawakutumia herufi kafu au neno mathal au mithl au kamaa katika kumsifu kwao Allah. Nasi tunakubaliana sana na Al-Imamu Ibn Al-Qayyim kwamba tashbihi inakuwa dhimniy, lakini kuwaita watu ambao wamekataa kuwa Allah ana mkono, mguu n.k. kuwa ndio wenye kumfananisha Mungu na viumbe ni jambo lisilo sahihi. Ukweli ni kuwa waliosema kuwa ana viungo hivyo, ndio waliomfananisha Allah na viumbe kwani viumbe ndio wenye viungo hivyo.

Hebu natumsikilize Al-Imamu Ibn Al-Qayyim anavyosema kuhusu watu hao, ili tujue kwamba Ibn Al-Qayyim kategemea ukweli huo wa kuwepo kwa tashbihi dhimniy (yenye kuwemo ndani ya maneno), katika kuthibitisha dai lake, japo kuwa natija yake si sahihi – msingi ni sahihi; natija si sahihi. Anasema Al-Imamu Ibn Al-Qayyim:

*** اإليمان على أنتم ما شبيه الت أمة يا لكم مقاالت هذيHaya ndio maneno yenu enyi**Watu wa tashbihi hamuna imani kitu.

لكونه الجاحدين أن وبيان م ** أفصح بحقيقة تكلماAmeweka wazi kabisa kwamba wapingao kuwa**Yeye (Allah) ni mwenye kusema kweli kweli na kutoa ubainifu.

172

Page 173: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

بالجامدات*** والتشبيه التعطيل أهل هم عظيمة معاالنقصان

Hao ndio watu wa ta’atil pamoja na tashbih **(Waliomfananisha Allah) na vitu visivyo na uhai vyenye upungufu mkubwa.598

Anasema mshereheshaji:

: ........ )) قال أن إلى الكفران و التشبيه أمة يا لكم مقاالت فهذه : و تعطيل أهل هم متكلما لكونه المنكرين أن ظهر فهل وبعد

(( معا اه� تشبيه

Basi haya ndio maneno yenu enyi wenye kumfananisha (Allah) na wenye kukufuru………baada ya hayo imebainika kwamba wale wenye kukataa kwamba Allah anasema kweli kweli ndio watu wa ta’atil (wenye kuzikataa sifa za Allah) na ndio watu wa tashbihi (wenye kumfananisha Allah na viumbe).599

Na kwa hivyo, Ibn Al-Qayyim anawafananisha watu hao wenye kukataa kuwa Allah anasema kweli kweli na watu wenye kuabudu masanamu na mungu-hewa (mungu asiyekuwepo), akasema:

الرحمن ... ... عبادة متيقنين هما ما والممثل المعطل إناألوثان ... ... عابد وهذا أبدا سبحانه ال المعدوم عابد ذا

Kwani mu’attil na mwenye kummithilisha (Allah)**Hawana yakini ya kumuabudu Allah.***Yule (wa mwanzo) anaabudu kitu kisichokuwepo (mungu hewa)600**Na huyu (wa pili) anaabudu masanamu.601

Anasema mshereheshaji:

وج�ود ... ي�عقل ال ما الصفات من ربه عن نفى حيث عدما يعبد األول بلووص�فه ب�دونه الموصوف

. والثاني المعدوم الممثل –بصفات ......–وهو صنما يعبد

…Bali wa mwanzo anaabudu kitu kisichokuwepo (mungu-hewa) kwani kamuondoshea Mola wake sifa ambazo haiwezekani kuwepo kwa kitu bila ya (kuwepo kwa sifa) hizo na akamsifu kwa sifa za kitu kisichokuwepo.

598 - Ibn Al-Qayyim Sharhu Al-Nuniyya j. 2, uk. 299. 599 - Ibn Al-Qayyim Sharhu Al-Nuniyya j. 2, uk. 300. 600 - Tazama akili yake mtu huyu! Anaona kuwa Mungu wa kweli haiwezekani kuwepo ila awe na viungo (miguu na mikono), na kwa hivyo, anaona kuwa wasiokubaliana na hayo basi wanaabudu mungu-hewa! 601 - Ibn Al-Qayyim Sharhu Al-Nuniyya j. 1, uk. 419..

173

Page 174: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Na wa pili – naye ni mwenye kummithilisha Mungu – anaabudu sanamu….602

Naye Ibn Al-Qayyim – kwa maneno yake hayo – anamuiga mtangulizi wake, Harun bin Ma’aruf ambaye imepokelewa kutoka kwake akisema:

األصنام ….. يعبد فهو يتكلم ال جل و عز الله أن زعم من

“Atayedai kwamba Allah hasemi kweli kweli basi huyo anaabudu sanamu”!603

Sasa – baada ya hayo – natujiulize suali moja muhimu: kama tashbihi ni kusema kwamba “Allah ana mkono kama mkono wangu”, na ukisema Allah ana mkono tu unakuwa hujamfananisha Allah na kiumbe, je hawa ambao Ibn Al-Qayyim kawaita kuwa ni mushabbiha (wenye kumfananisha Allah) kwa sababu ya kukataa kwao kwamba Allah anasema kweli kweli: je watu hao walisema: يتكلم ال الله واألحجار كماإن األصنام تتكلم ال Allah hasemi kama masanamu na mawe yalivyokuwa hayasemi, hata ikajuzu kuwaita watu hao kuwa ni mushabbiha na ili hoja ya Al-Faqihi alioinukuu kutoka kwa Al-Imamu Ahmad na wengineo iwe sawa?

Utaona kwa uwazi udhaifu wa dai kwamba tashbihi ni kusema kuwa Allah ana mkono kama wangu tu au ibara ilio mfano wa hio. Lakini – chambilecho Wazungu for the sake of argument (kwa ajili ya mjadala) – natukubali kwamba kumfananisha Allah na viumbe ni kusema mkono kama wangu, yaani kuweka التشبيه .herufi ya kufananishia أداة Je riwaya za wanaoitwa Mawahabi hazikufanya hivyo? Soma badhi ya riwaya zao muhimu kutoka katika kitabu tulichousiwa na Sheikh Seif Al-Ghafri kukisoma. Inasema riwaya:

الله تكلم بالوحي إذا وجل صلصلة سمع عز له السماء كصلصلةأهلص الحديد وفي ا ف����������علىالحديد(( رواية صف كصلصلة صفا)) ((على كلمة من بدال .))وان

Allah Mtukufu akisema kwa wahyi basi viumbe wa mbinguni huisikia sauti yake (Allah) kama sauti ya chuma (kikibururwa) juu ya jiwe.604

Haya ndugu zangu! Haya Sheikh Mafuta: 602 - Tazama maelezo ya Dr. Muhammad Khalil Harras katika Sharhu Al-Nuniyya cha Ibn Al-Qayyim j. 1, uk. 420.. 603 - Ibn Ahmad Al-Sunna j. 1, uk. 172, riwaya na. 209. 604 - Ibn Ahmad Al-Sunna j. 1, uk. 281-282, Hadithi na. 537-538. ‘Uthman Al-Darimi Al-Rddu ‘Alaa Al-Marisi uk. 14.

174

Page 175: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

صراحة، التشبيه بأداة جئتم قد أوالء أنتم الله حيث ها صفة هيوشبهتمالكالم ح���د –صفة على

ومكان بزمان المقيد الله كالم أن يرى صفاته صفة من وت�بص –منعلى سلسلة جر من خارج

ستقول !!! ماذا !!!ون؟الصخرة ؟ بالتشبيه هذا أليس

Hapa tayari mumekuja na herufi ya kufananishia (kama) wazi wazi: mumeifananisha sifa ya Allah ya maneno yake – kwa wale wenye kuona kuwa maneno yaliofungamanishwa na wakati na sehemu ni katika sifa za Allah – na sauti itokayo katika chuma kinachobururwa juu ya jiwe!

Inasema riwaya yenu:

أطيط له سمع الكرسي على الرب جلس الحديد كأطيطإذا الرحل

Allah akikaa kitako juu ya kiti basi husikika sauti yake kama sauti ya matandiko ya chuma ya ngamia.605

Na mfano wake ni riwaya:

( ) قيد إال منه يفضل فما وعز جل الكرسي على أي عليه ليقعد أربع إنهكأطيط أطيطا له وإن أصابع

ركب إذا الرحل

Hakika yake Allah Mtukufu anakaa juu yake (juu ya kiti) basi haibakii isipokuwa kiasi cha vidole vinne, na hakika yake ana sauti kama ya matandiko ya ngamia anapopandwa.606

Wala usiniambie kwamba: “Aaa hapa kinachofananishwa ni sauti ya kiti cha Mungu na soji za ngamia: si sauti ya Mungu na sauti ya soji ya ngamia”, kwani tunasema kwamba hata ingelikuwa hivyo, basi sauti hio imeundika kwa ukaaji wa Allah na kuwepo kwa kiti.

Kisha tujiulize je huyu Mungu anakaa juu ya kiti na kuondoka, hata isemwe: “Allah akikaa kitako juu ya kiti”. Au alikaa mara moja baada ya kuiumba hio ‘Arshi? Tazama migongano hii! Hii ndio natija ya kushikamana na Aya mutashabihat, na kukumbatia mahadithi ya kutunga na Hadithi Ahadi katika mambo ya itikad! 605 - Ibn Ahmad Al-Sunna j. 1, uk. 585. 606 - Ibn Ahmad Al-Sunna j. 1, uk. 305, riwaya na 593. Anasema Al-Kawthari kwamba Ibn ‘Asakir katunga kitabu alichokiita Bayaanu Wujuhi Al-Takhlit fii Hadithi Al-Atit ambapo kabainisha udhaifu wa Hadithi hizi. Tazama Takmila ya Al-Kawthari katika Al-Saifu Al-Saqil cha Al-Subki uk.17.

175

Page 176: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Na mfano wa riwaya hizo ni riwaya isemayo:

باأل كلمه موسى الله كلم يقول للما موسى فطفق لسانه، قبل كلها سنةحتى: هذا أفقه ما والله رب يا

بلسانه ذلك آخر : مثلكلمه رب يا هذا السالم عليه موسى فقال صوتهل وجل عز الله فقال و ��كالمك

من : فهل رب أي قال له، تستقم لم قال أو شيئا تكن لم كالمي كلمتكيش شيء قال �خلقك ؟ كالمك به

خلقي وأقرب الصواعق شبهاال، من الناس يسمع ما أشد بكالميWakati Allah alipozungumza na Musa, alizungumza naye kwa lugha zote kabla ya lugha yake, basi Musa akaanza kusema: E Mola wangu! Wallahi miye siyafahamu haya mpaka mwishoni akazungumza naye kwa lugha yake mfano wa sauti yake. Musa (a.s.) akasema: ‘E Mola wangu! Haya (sasa) ni maneno yako. Allah akasema: ‘Lau nilikusemesha maneno yangu (hasa) basi usingelikuwa kitu (ungeangamia) au usingeliyakalia sawa (usingeliyaweza)’. Akasema (Musa): ‘E Mola wangu! Ivo kuna kiumbe chako ambacho kinafanana na maneno yako. (Allah) akasema: ‘Hapana’, na kitu kilichokaribu zaidi kufanana na maneno yangu ni ile radi kali yao wanayoisikia watu. 607

Zingatia:

1) Mfano wa sauti yake. Je hii si tashbih? 2) Kitu kilichokaribu zaidi kufanana na maneno yangu ni ile radi kali

yao. Je hii si tashbih?

Na miongoni mwa hizo ni Hadithi isemayo:

.... فيأتيهم الرب فيتمثل الغمام من ظلل في الله …..ينزل

Allah anateremka katika vivuli vya mawingu…Basi Mola (Mtukufu) atajimithilisha (atajifananisha) atawajia.608

Je maneno atajimithilisha (atajigeuza), si tashbihi ya wazi? Na riwaya kama hizi munazo kwa kapu na magunia katika kitabu chenu hicho ambacho Sheikh Seif Al-Ghafri katuusia tukisome, yaani Al-Sunna cha Ibn Ahmad!

Bali imeelezwa katika Al-Dururu Al-Kaamina cha Ibn Hajar na Al-Rahla cha Ibn Batuta kwamba Imamu wenu Ibn Taymiyya alikuwa akiitaja Hadithi

607 - Ibn Ahmad Al-Sunna j. 1, uk. 383, riwaya na 541.. 608 - Ibn Ahmad Al-Sunna j. 2, uk. 521, riwaya na. 1203.

176

Page 177: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

inayosema kuwa Allah anateremka thuluthi ya tatu ya usiku, alikuwa naye akiteremka vidaraja viwili vya membari kisha anasema kwamba Allah anateremka “Kama hivi ninavyoteremka mimi”.609 Anasema Ibn Batuta kuhusu Ibn Taymiyya:

على الناس يعظ وهو الجمعة يوم فحضرته بدمشق، ذاك إذ وكنتالج .���منبر ويذكرهم امع

: الدنيا سماء إلى ينزل الله إن قال أن كالمه جملة من فكانون هذا درج �����كنزولي ة����زل

ما وأنكر الزهراء، بابن يعرف مالكي فقيه فعارضه المنبر درج من. ����تك فقام به ت ������لم

حتى كثيرا ضربا والنعال باأليدي وضربوه الفقيه هذا إلى العامةعمامته ……سقطت

Na wakati huo mimi nilikuwa niko Damascus (Syria), basi nikamuhudhuria (Ibn Taymiyya) siku ya Ijumaa naye anawaaidhi watu juu ya membari ya Msikiti wa Ijumaa na kuwakumbusha. Basi ikawa katika jumla ya maneno yake ni kuwa alisema: ‘Hakika ya Allah anateremka kuja katika mbingu ya kwanza kama hivi ninavyoteremka mimi’ basi (Ibn Taymiyya) akateremka katika kidaraja kimoja cha membari. Mwanachuoni wa madhehebu ya Maliki ajulikanaye kwa jina la Ibn Al-Zahraa akampinga na kuyakanusha hayo aliyoyasema. Basi wote (waliokuwepo) walimsimamia mwanachuoni huyo na wakampiga kwa mikono na viatu kipigo kikali mpaka kilemba chake kikaanguka….610

Na kwa sababu hio, kama Al-Fakhru Al-Razi anavyomuona Ibn Khuzaima kuwa hana akili, Ibn Batuta naye anamuona Ibn Taymiyya kuwa ni mtu mwenye elimu kubwa lakini hana akili timamu. Anasema:

الح الفقهاء كبار من بدمشق تي �������كان بن الدين تقي كبير ��نابلة ميةيت الفن �����الشام في ون.�����كلم

أن . إال شيئا عقله في

(Wakati huo) Damascus kulikuwa na Ibn Taymiyya ndiye mkuu wa wanavyuoni wa Kihanbali na mkuu wa Sham, anazungumza katika fani (tafauti), lakini katika akili yake kulikuwa na kitu (kasoro).611

609 - Tazama Ibn Hajar Al-Dururu Al-Kamina j. 1, uk. 159. Tumeyanukuu huko mbele maneno ya Ibn Batuta ambaye anasema kwamba alihudhuria muhadhara wa Ibn Taymiyya akamsikia akisema maneno hayo. 610 - Ibn Batuta Al-Rahla uk. 89. Na hili la kutumia nguvu baada ya kutumia hoja ndio siasa ya Mawahabi leo, kumbe latoka mbali! 611 - K.h.j., uk. 89.

177

Page 178: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Hayo ni maneno ya Ibn Batuta kuhusu Ibn Taymiyya. Na mfano wake ni maneno ya Al-Haafidh Al-‘Iraaqi katika kitabu chake Al-Ajwiba Al-Mardhiyya aliposema kuhusu Ibn Taymiyya kwamba: “Elimu yake ni kubwa kuliko akili yake”.612 Kwa hali yoyote ile, ninachotaka kukithibitisha hapa ni kauli ya Ibn Taymiyya aliposema: “Hakika ya Allah anateremka kuja katika mbingu ya kwanza kama hivi ninavyoteremka mimi”. Tunasema: ikiwa kumfananisha Allah ni kusema: “Allah ana sifa kadha kama hii yangu” basi huyu Ibn Taymiyya kasema hivyo. Je Ibn Taymiyya – kwa maneno yake hayo, na kwa mujibu wa kanuni yenu hio – atakuwa ni mushabbih (mwenye kumfananisha Allah na kiumbe) au hatokuwa mushabbih? Jawabu ya Kasim Mafuta inajulikana, lakini tunayoitaka ni jawabu ya kanuni hio. Ewe kanuni toa jawabu. Kanuni yatongoa: “Ibn Taymiyya ni mushabbih.”

MUKHTASARI NA NUKTA MUHIMU

1) Tulichokizungumzia hapa ni hii dhana (concept) ya kumfananisha Mwenyezi Mungu na viumbe: je kumfananisha Mwenyezi Mungu na viumbe ni vipi?

2) Watu wa skuli ya Kihanbali/Kiwahabi wanaona kwamba kumfananisha Allah na viumbe ni kusema: “Mkono kama wangu n.k.”. Ama kusema kuwa Allah ana mikono tu huko si kumfananisha Allah.

3) Tumesema kwamba dai hilo ni kinyume na lugha ya Kiarabu ilivyo ambapo:

a) Tashbihun baligh ni kukifananisha kitu kimoja na chengine, ilhali katika tashbihi hii hakuna ndani yake herufi ya kufananishia (kama).

b) Al-Tashbihu Al-Dhimni pia ni kukifananisha kitu kimoja na chengine ilhali katika tashbihi hii pia hakuna ndani yake herufi ya kufananishia (kama).

c) Mfano mzuri ni kitendo cha Ibn Al-Qayyim – na wengine – kuwaita watu wenye kusema kuwa Allah hasemi kwa hakika kwamba watu hao ni mushabbiha (wenye kumfananisha Allah na viumbe) ilhali watu hao hawakusema kwamba “Allah hasemi kama vile ambavyo masanamu na mawe hayasemi”. Lakini kwa mujibu wa ufahamu wa Ibn Al-Qayyim ni kuwa kitendo cha watu hao cha kumfanya Allah kuwa hasemi kweli kweli basi wamemfanya yeye kuwa ni kama jiwe au sanamu!613

612 - Tazama Al-Maqaalaatu Al-Sunniyya uk. 13. 613 - Huu ni mtazamo wa Ibn Al-Qayyim nao si mtazamo sahihi kwani umejengeka juu ya msingi mbovu sana! Unaonaje kwamba anayekataa kuwa Mungu anasema hakika akijibu kwamba “Na wenye kusema kuwa Mungu anasema hakika basi wamemfananisha na mtu

178

Page 179: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

4) Hatimae tumebainisha kwamba hata ikiwa kweli kumfananisha Allah na viumbe ni kusema: “Mkono kama wangu n.k.”, basi hilo limejaa katika vitabu vya watu hao.

5) Tumebainisha pia kwamba Ibn Taymiyya kanukuliwa akisema: “Allah anateremka kama hivi ninavyoteremka mimi katika membari hii” kama tulivyonukuu maneno ya Ibn Batuta614 hapo nyuma.

6) Na kwa hivyo, Mawahabi na Maimamu wao wamemshabihisha Allah na viumbe kwa hali yoyote ile iwayo.

SURA YA SITAMJADALA JUU YA KUWEPO KWA MAJAZI

Katika sehemu zilizotangulia tumenukuu itikadi za wanaoitwa Mawahabi au wanaojiita Al-Salafiyya au Ansaru Sunna na Maimamu wao watangulizi juu ya itikadi ya tajsim (kumfanya Allah kuwa ana kiwiliwili na viungo). Katika kitabu changu Hoja Zenye Nguvu615 nilinukuu kiasi fulani baadhi ya itikadi hizo kisha nikasema:

Sababu kubwa na chanzo cha Mawahabi kuwa na itikadi hizi za kumfananisha Mwenyezi Mungu na viumbe, wakasema kuwa Mwenyezi Mungu ana mikono, miguu, uso, macho, anakwenda kwenye ardhi, anacheka, anakaa kitako kweli kweli, aliegemeza mgongo wake kwenye jabali huku akiandika Taurati n.k., ni kukanusha kwao kuwepo kwa majazi katika lugha ya Kiarabu na hasa hasa katika Qur-ani. Miongoni mwa walioandika kwa urefu na kukataa jambo hili ni Ibn Qayyim Al-Jawziyya.616

Sasa tazama ajabu! Sheikh Kasim Mafuta kayapindua maneno yangu na badala yake akaninukuu sivyo!617 Anasema:

au kasuku n.k.”. Ilivyo ni kuwa itazamwe kusema katika lugha ni nini? Baada ya kupatikana huko kusema, ndio kutazamwe je inawezekana kumsifu Allah kwa sifa hio? 614 - Na Ibn Hajar. 615 - Uk. 32. 616 - Kama ilivyo katika kitabu chake Mukhtasar Al-Sawaaiq Al-Mursala j. 2 inaanzia uk. 231. Na kichwa cha habari “Heading” cha sehemu hio ni Sehemu Ya Kumvunja Taghuti (Shetani) Wa Tatu…Naye Ni Taghuti Wa Majazi. Lakini kitabu hiki sasa kimejibiwa kwa urefu na Sheikh Al-Khalili katika tafsiri yake Jawahiru Al-Tafsir: Juz-u Khaas. Katika tafsiri hio Sheikh Al-Khalili kaielezea Aya moja tu ya 7 ya Sura ya 3, ambayo imechukua karatasi 403, ambapo alichukua sehemu kubwa kwa kuzijadili hoja za Ibn Al-Qayyim juu ya suala la majazi. 617 - Kama utavyoona katika jawabu hii, kitabu chote cha Kasim Mafuta ni tadlis (ghushi) tupu!

179

Page 180: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Ndugu msomaji kama utakuwa ni mfuatiliaji mzuri wa mambo ya dini yetu hii ya kiislamu na ukawa unashughulishwa na kufuatilia matatizo yanayo usibu umma huu mtukufu, bila shaka utaziona athari za wazi wazi za tofauti za wafuasi wa dini hii tukufu, tena baadhi ya tofauti ni zile tofauti nzito ambazo huwezi kutoa hukumu kwamba wote hao waliotofautiana wako katika haki. Na pengine unaweza kujiuliza ni nini sababu zilizowaingiza watu hawa katika tofauti hizi na itikadi potofu na batili? Ndugu Juma M. Al-Mazrui yeye anadai kwamba chanzo cha watu kutumbukia katika itikadi za batili: “Ni kukanusha kwao kuwepo kwa MAJAZI katika lugha ya kiarabu na hasa katika Qur’an”. Tazama kitabu chake “Hoja zenye Nguvu” ukurasa wa 32.618

Anaendelea Sh. Kasim kwa kusema:

Juma hakusema kwamba vyanzo vya upotevu ni:Kutoshikamana na Qur’an na Sunna, Kumtii shetani na askari wake, Kufuata matamanio ya nafsi,Ujinga, Kiburi, Kufanya is’rafu katika matumizi ya majazi ndani ya Qur’an, na kuzipotosha tafsiri za baadhi ya aya kwa madai kuwa kuna majazi. Na nyinginezo miongoni mwa sababu zilizotajwa na Qur’an au Sunna. Bali yeye ameamua kutaja mambo hayo kuwa ndiyo vyanzo vya upotovu, na hali ya kuwa yeye mwenyewe ana yakini kwamba hawezi kututhibitishia kielimu kwamba itikadi hizo ni vyanzo vya upotevu kivipi?619

Anaendelea Sheikh Kasim Mafuta kwa kusema:

Tumebainisha katika kitabu hiki kwamba, chanzo na chimbuko kubwa la watu kutumbukia katika itikadi za batili ni kuiacha njia sahihi aliyotuwekea bwana Mtume Muhammad swalla llaahu alayhi wasallam, njia ya Qur’an na Sunna kwa ufahamu wa wema waliotangulia (maswahaba na wafuasi wao na maimamu waliokuja baada yao). Na si kama alivyodai mwandishi wa kiibadhi Juma Al-Mazrui, kwamba chanzo cha upotevu ni kupinga kuwepo kwa Majazi katika Qur’an. 620

Hayo ndio alioyasema Sheikh Kasim Mafuta katika kuyajibu yale nilioyasema mimi. Nami namwambia bwana Kasim Mafuta kwamba mimi sikusema “Chanzo cha upotovu ni kukataa majazi,” kama alivyodai yeye, bali nilichokisema ni hiki: “Chanzo cha Mawahabi kutumbukia katika itikadi HIZI ni kukanusha kwao kuwepo kwa majazi”. Sasa kama nilisema itikadi HIZI, suala ni kuwa je ni itikadi zipi hizo nilizozitaja na

618 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 35. 619 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 37-38. Tulia tuli! Nitakuthibitishia kila kitu kwa hoja zitazoupozo moyo wako. 620 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 173.

180

Page 181: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kuziashiria kwa neno HIZI? Utakumbuka kwamba mimi niliyasema hayo baada ya kunukuu zile itikadi za kudai kwamba Mungu ana mkono, mguu, macho n.k. Wewe, Sh. Kasim, umebadilisha na kusema Juma kasema kuwa asili ya upotovu ni kukataa majazi. Je huoni Sheikh kwamba unatumbukia katika kile kile ulichowatia aibu wenzako kwacho? Umedai kuwa Sheikh Al-Khalili kaubadilisha ubeti wa Ibn Al-Qayyim nao ubeti huo upo kama nitavyokuthibitishia nikifika mahala pake. Tena hata kama kweli ubeti huo mjengeko wake umebadilishwa, bado maana ya ubeti huo ni sawa sawa na maana iliomo katika ubeti uliomo katika Nuniyya ya Ibn Al-Qayyim. Wewe hapo ukaona umepata mwanya wa kuweza kutoa dukuduku lako ukimuiga Ali Al-Faqihi. Leo wewe umebadilisha maneno kwa mfumo ambao umeleta maana tafauti kabisa. Huoni kwamba unabeba jukumu na kujitwika mizigo?

Kwa hivyo ni wazi, kwa aliyeyatazama maneno yangu, kwamba mimi nauzungumzia upotovu maalumu, nao ni upotovu wa kumpachika Mungu viungo vya hakika; huo ndio ambao nimedai kwamba chimbuko lake ni kuyakanusha majazi, wala mimi sizungumzii upotovu kama vile ulevi na uzinifu. Ni akili ya mtu gani itayofikiria kwamba mtu anazini – kwa mfano – kwa sababu haamini majazi, au analewa kwa sababu haamini majazi?

Sasa narudia tena kuliweka wazi jambo hilo, labda kule hukulifahamu vizuri au umetaka kupotosha kwa kukusudia. Ninachokisema ni kuwa asili ya kuwepo itikadi za “Mungu ana mkono; mguu; macho n.k”, ni kuwa wenye itikadi hizi wanakanusha majazi, na kwa hivyo ulipotajwa mkono, basi wao wakaufasiri kuwa ni mkono kweli kweli; ulipotajwa mguu wakaufasiri kuwa ni mguu, n.k. Sasa je wewe hili unalipinga? Kama unalipinga tupe tafsiri ya maneno yako uliposema:

Kufanya is’rafu katika matumizi ya majazi ndani ya Qur’an, na kuzipotosha tafsiri za baadhi ya aya kwa madai kuwa kuna majazi…….621

……Na wengine wameona wauite “Usluubun min Asaalibil-Lugha” (utaratibu/mfumo katika taratibu za lugha) na njia hii ndiyo iliyokaribu na usahihi, ili kuwazuia watu wa batili wasiyapotoshe maandiko kwa kuupitia mlango huu. 622

Sasa kabla sijazungumza nilioyakusudia katika sura hii, ni vyema kwanza nikakunukulia nilioyasema katika kitabu changu kisha tuinukuu jawabu kamili ya Sh. Kasim Mafuta aliyonijibu ili tuweze kufikia natija sahihi. Katika kitabu changu Hoja Zenye Nguvu nilisema:

621 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 37-38. 622 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 51.

181

Page 182: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Sababu kubwa na chanzo cha Mawahabi kuwa na itikadi hizi za kumfananisha Mwenyezi Mungu na viumbe, wakasema kuwa Mwenyezi Mungu ana mikono, miguu, uso, macho, anakwenda kwenye ardhi, anacheka, anakaa kitako kweli kweli, aliegemeza mgongo wake kwenye jabali huku akiandika Taurati, n.k., ni tatu:623

1) Kuzikubali Hadithi Ahadi katika mambo ya itikadi.2) Kuchukua Hadithi za kutunga.3) Kukanusha kwao kuwepo kwa majazi katika lugha ya Kiarabu

na hasa hasa katika Qur-ani. Miongoni mwa walioandika kwa urefu na kukataa jambo hili ni Ibn Qayyim Al-Jawziyya.

Katika kitabu hiki tutazungumzia sula la tatu la kukataa majazi. Maana ya “Majazi” ni kutumika kwa neno tafauti na maana yake ya asili. Kwa mfano neno: “Simba”. Neno hili linamaanisha aina maalumu ya mnyama wa porini. Na hii ndio maana yake ya asili. Lakini nikisema kuwa Ali ndio simba wa kijiji hiki, makusudio huwa sio yule mnyama wa porini, bali ni kuwa Ali ni shujaa wa kijiji hiki. Na hii ndio maana ya “Majazi”: kutumika neno kinyume na maana yake ya asili. Sasa wao Mawahabi wanakataa kuwa katika Qur-ani kuna majazi. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu aliposema:

أيديهم فوق الله يد

Mkono wa Mwenyezi Mungu uko juu ya mikono yao 624

wao wakasema kuwa Mwenyezi Mungu ana mkono. Masikini hawa hawakuifahamu Qur-ani wala lugha ya Kiarabu iliotumika kuteremshiwa Qur-ani. Sasa kwanini basi wakasema kuwa Mwenyezi Mungu ana mikono miwili tu na Aya ziko ziliozoonesha kuwa mikono yake ni mingi zaidi ya miwili? Anasema Mwenyezi Mungu:

ماء بأييد بنيناها والسNa mbingu tumezijenga kwa mikono

(yetu, mingi zaidi ya miwili).625

Sasa tafsiri na iwe hivi “Mwenyezi Mungu ana mikono mingi zaidi ya miwili” kama Aya hii inavyosema. Na alipotaja mkono mmoja basi iwe kataja mmoja katika hio mingi na halkadhalika alipotaja miwili awe kataja miwili katika hio mingi. Lakini kwa mujibu wa Aya hii mikono yake ni

623 - Tazama ukweli kwamba haya mengine katika kitabu changu hayamo kwani kitabu hicho nilikuwa tayari ninakitayarisha kwa ajili ya chapa ya pili. Kwa hivyo, kipengele (1-2) ni ziada ambayo katika kitabu Hoja Zenye Nguvu chapa ya kwanza havimo. 624 - Sura ya 48 Aya ya 10. 625 - Sura ya 51 Aya ya 47.

182

Page 183: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

mingi zaidi ya miwili. Sasa kama ni hivi kwanini tena waseme ana mikono miwili tu? Ukiniambia: “Lugha ya Kiarabu inatumika katika wingi (tatu na kuendelea) kumaanisha mbili, na mbili kumaanisha wingi (tatu na kuendelea) na moja kumaanisha wingi vile vile.” Nitakujibu kwamba:

a) Katika lugha ya Kiarabu pia unatumika mkono kumaanisha nguvu, neema, uwezo n.k., kama utavyoona humu.

b) Kama unakubali kwamba wakati mwengine moja hutumika kumaanisha nyingi, basi umejijibu mwenyewe kwani haya ndio majazi yenyewe unayoyakataa: kutumika neno kinyume na maana yake ya asili. Kwani kwa asili moja ni moja; ikitumika kumaanisha tatu basi imetumika kinyume na maana yake ya asili.

Lakini haya yote yanatujuilisha kwamba hawa watu Mwenyezi Mungu hakuwapa nuru hata kidogo ya kukifahamu Kitabu chake. Sasa ukitaka kujua kwamba neno mkono katika lugha ya Qur-ani hutumika si kwa maana ya mkono wa kweli, soma Aya hizi zinazofuata kisha tia akilini, utafakari, uzingatie na kujiuliza je mkono uliotajwa katika Aya hizi ni mkono wa kweli. Anasema Mwenyezi Mungu:

البسط كل تبسطها وال عنقك إلى مغلولة يدك تجعل وال Wala usiufanye mkono wako kuwa wenye kufungwa

kwenye shingo yako wala usiukunjue wote.626

Je neno mkono hapa ni mkono wa kweli au maana yake ni kuwa usifanye ubakhili wala usifanye israfu? Kama ni mkono kweli kweli ndio uliokusudiwa hapa, basi mbona wenye kukataa majazi hawaendi na huku mikono yao ipo kati na kati tu baina ya shingo na kuikunjua yote?

Na anasema Mwenyezi Mungu:

األيد ذا داوود عبدنا واذكر Na mkumbuke mja wetu Dawud mwenye

mikono (mingi, yaani mwenye nguvu).627

Sasa je neno mikono hapa maana yake ni mikono hii ya viungo? Kama ndio basi Nabii Dawud alikuwa na mikono zaidi ya miwili kwa sababu Aya inasema األيد ذا (mwenye mikono mingi zaidi ya miwili). Bali hapa mikono maana yake ni nguvu.

Na akasema Mwenyezi Mungu katika Qur-ani:

626 - Sura ya 17 Aya ya 29. 627 - Sura ya 38 Aya ya 18.

183

Page 184: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

واألبصار األيدي أولي ويعقوب وإسحق إبراهيم عبادنا واذكر

Na wakumbuke waja wetu Ibrahim, na Is-haq na Ya’aqub wenye mikono na macho.628

Katika Aya hii Mwenyezi Mungu anamtaka Mtume wake (s.a.w.) awazingatie Mitume hao kwa sababu Mwenyezi Mungu kawapa mikono na macho. Sasa kwani sisi hatuna mikono na macho? Kwa hivyo, ni wazi kwamba mikono hapa maana yake ni nguvu; na macho maana yake ni busara na uwezo mkubwa wa kutazama mambo, kuyatafakari na kuyafahamu mambo hayo pamoja na hekima.

Kwa hivyo, mkono wa Mwenyezi Mungu maana yake ni nguvu za Mwenyezi Mungu: si kiungo kama wanavyosema baadhi ya watu. Na hivi ndivyo lugha ya Kiarabu inavyosema. Anasema babu yake Mtume (s.a.w.) wakati Mtume (s.a.w.) alipopotea katika mji wa Makka alipokuwa mdogo. Babu yake Mtume aliimba mashairi haya :

*** يدا لي اجعله و ربي اردده محمدا ولدي علي ردNirejeshee (é Mwenyezi Mungu) Muhammad

mwanangu**Mrejeshe é Mola wangu na umfanye kuwa mkono wangu.629

Sasa jiulize wewe vipi Mtume (s.a.w.) afanywe kuwa mkono wa babu yake? Ni wazi kwamba hapa babu yake Mtume anamuomba Mwenyezi Mungu amfanye Muhammad (s.a.w.) kuwa ni sababu ya yeye kupata nguvu au awe ni neema kwake.

Kwa kufahamu zaidi kuwepo kwa majazi katika Qurani soma Aya hii:

األسود الخيط من األبيض الخيط لكم يتبين حتى واشربوا وكلوا Aya hii inahusu mwezi wa Ramadhani, anasema Mwenyezi Mungu katika Aya hii:

Na kuleni na kunyweni mpaka ukubainikieni uzi mweupe kutokana na uzi mweusi. 630

Sasa tunawauliza wanaokataa majazi je nyuzi hizi mbili nyeupe na nyeusi zilizotajwa katika Aya hii ni nyuzi za kweli? Jawabu ni kuwa hizi si nyuzi za kweli kama za kushonea nguo, bali uzi mweupe ni kuchomoza kwa alfajiri sahihi ambayo huanza weupe katika upeo wa mashariki na uzi mweusi ni kiza cha usiku. Na kwa maana hio neno nyuzi katika Aya hii si

628 - Sura ya 38 Aya ya 45. 629 - Tumetaja marejeo huko mbele. 630 - Sura ya 2 Aya ya 187.

184

Page 185: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

hakika bali ni majazi (mithali). Hii ni Aya ambayo mmoja wa sahibu zangu alimtolea mtu mmoja anayekanusha majazi, na ikawa hana jawabu.

Al-Imamu Nur Al-Din Al-Salimi (r.a.) alipokuwa akizungumzia habari ya majazi, alisema kwamba Abu Tammam katika washairi wa zamani alitoa ushairi wake akasema: ةبآكال اءم ينقست ال (usininyweshe maji ya huzuni). Ikawa kuna mtu pale katika wanaopinga majazi. Akasema yule mtu kumwambia Abu Tammam: “Haya nipe hio gilasi yako nikutilie maji ya huzuni”. Yaani anakusudia kumwambia “Tangu lini wewe umesikia kwamba huzuni inanywewa?” Abu Tammam akamjibu yule mtu akamwambia: “Haya huu mkasi nikatie bawa lako la udhalili”. Abu Tammam naye anakusudia kumjengea hoja kwa kutumia Aya inayosema: “Na wainamishie (wazazi wako wawili) bawa la udhalili.”631 Yaani je bawa hapa ni bawa la kweli, na tangu lini na wapi umesikia kwamba mtu ana bawa? Kama si bawa basi elewa kwamba haya yote ni katika majazi ya lugha ya Kiarabu.

Na mimi siku moja nilijadiliana na hao wenye kukataa majazi. Nikamwambia yule bwana kama wewe unakataa majazi hebu soma Aya hii:

الله بحبل واعتصموا جميعاNa kamataneni na kamba ya Mwenyezi

Mungu kwa pamoja632

Nikamwambia haya niletee hio kamba ya kweli kweli ya Mwenyezi Mungu tukamatane nayo. Ikawa hana jawabu isipokuwa kuniambia: “Maudhui hii inahitaji utafiti”. Sasa tazama je kamba hapa katika Aya hii ni kamba ya kweli? Kila mtu anajua kuwa kamba hapa maana yake ni dini: si kamba ya kufungia ng’ombe. Sasa ikiwa umeyafahamu haya basi elewa kuwa makusudio ya mkono wa Mwenyezi Mungu ni nguvu zake. uso ni Dhati Yake, au katika sehemu nyengine limetumika neno uso kwa maana ya radhi zake. Macho kwa maana ya hifadhi yake. Na hivyo hivyo kila kitu kinafasiriwa tafsiri inayokubaliana na sifa za Mwenyezi Mungu.633

Hayo ndio nilioyasema katika kitabu changu Hoja Zenye Nguvu. Sasa natusome maelezo ya Sheikh Kasim Mafuta katika jawabu alionijibu.

631 - Al-Imamu Al-Salimi: Tal’atu Al-Shams j.1 uk. 206. 632 - Sura ya 3 Aya ya 103. 633 - Juma Al-Mazrui Hoja Zenye Nguvu uk. 32-36.

185

Page 186: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

JAWABU NILIOPATA KUTOKA KWA SH. KASIM MAFUTA

Anasema Sheikh Kasim bin Mafuta:

UCHAMBUZI YAKINIFU JUU YA SUALA LA MAJAZI

Ama madai ya kwamba umma umeingia katika upotevu kwa sababu ya kuitakidi kuonekana Allah kwa macho huko akhera ni madai batili kwa hoja tutakazo zitoa katika kitabu chetu hiki Inshaallaah. Na ama kuitakidi kwamba kuna waislamu ambao wataingia motoni kisha watatoka kwa sababu ya shafaa (uombezi):

Suala hili limethibiti kwa hoja zenye nguvu katika kitabu (Qur’an) na sunna sahihi za bwana Mtume -swalla llaahu alayhi wasallam-.

Ama madai yake ya uwongo kuwa suala la kupinga kuwepo kwa majazi ndani ya Qur’an kuwa ndiyo chanzo cha kupotea watu, 634 ufafanuzi wake ni kama ufuatavyo:

Suala la kuwepo majazi na kutokuwepo kwake katika Qur’an na lugha ya kiarabu ni jambo ambalo maulamaa wametofautiana tangu zamani kama walivyotofautiana katika mambo mengine.

Ndugu Juma Al-Mazrui katika kitabu chake “Hoja zenye Nguvu” ukurasa wa 32 amefanya jaribio la kutaka kuuficha ukweli huo ambao uko wazi tena mbele ya macho yake na akafanya upotoshaji kwa makusudi dhidi ya watu anaowaita Mawahabi (akiwa ana wakusudia Ahlu sunna wal Jamaa) kwa kudai kwamba watu hao wamepotea, na chanzo cha upotevu wao huo ni kukanusha kuwepo kwa majazi katika lugha na Qur’an. Amesema ndugu Juma al Mazrui baada ya kichwa cha habari kisemacho:

CHANZO CHA KUTUMBUKIA KATIKA ITIKADI BATILI

Kisha akasema:

634 - Tazama mtu anavyopotoa maudhui huyo! Mimi ninasema kitu chengine na yeye anasema kitu chengine!

186

Page 187: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

“Sababu kubwa na chanzo cha Mawahabi kuwa na itikadi hizi za kumfananisha Mwenyezi Mungu na viumbe, wakasema kuwa Mwenyezi Mungu ana mikono, miguu, uso, macho…ni kukanusha kwao kuwepo kwa majazi katika lugha ya kiarabu na hasa hasa katika Qur’an. Miongoni mwa walioandika kwa urefu na kukataa jambo hili ni Ibn Qayyim Al-Jawziyya katika kitabu chake Mukhtasar Al-Sawaaiq Al Mursala….

Na maana ya “majazi” ni kutumika neno tafauti na maana yake ya asili…

Sasa wao Mawahabi wanakataa kuwa katika Qur’an kuna majazi”. Mwisho wa kunukuu.635

Kisha baada ya Sheikh Kasim kuyanukuu hayo, akajibu kwa kusema:

Majibu yetu yatakuwa katika nukta tatu:Nukta ya kwanza:Ni kuhusu maelezo yake kuhusu neno “Majazi”, kwa ufupi ni kwamba maelezo ya Juma kuhusu majazi yana upungufu alitakiwa aseme hivi: “Majazi ni kutumia neno katika isiyokuwa maana yake ya asili pamoja na kuwepo dalili inayozuia kukusudiwa maana yake ya asili kwa mafungamano ambayo yapo baina ya neno la asili na neno ambalo si la asili”. Kwa sababu ili maneno yawe ni majazi, ni lazima masharti matatu makuu yatimie, nayo ni:1-Kutumika neno katika isiyo kuwa maana yake ya asili.2-Lazima kuwepo na “QARINATUN MAANI’ATUN MIN IRADATI MA’ANAL ASLIY” dalili yenye kuzuia kukusudiwa maana ya asili.3-Lazima kuwepo na “ALAAQAH” mafungamano baina ya neno la asili na neno lisilo la asili.

Na likikosekana sharti moja kati ya haya matatu tuliyoyataja basi hakutakuwa na majazi na atakayedai kuwa ni majazi basi huyo ni mwongo mkubwa na hajui lugha ya kiarabu.636 Kwa mfano nikisema: “Nimemuona Simba anamla Swala”. Kwa mujibu wa misingi ya lugha ya kiarabu neno “Simba” hapa limetumika katika maana yake ya asili. Kwa sababu katika maneno haya hakuna: “QARINATUN MAANI’ATUN MIN IRADATI MA’ANAL ASLIY” dalili yenye kuzuia kuikusudia maana ya asili.

Na yanapotamkwa maneno hayo kila mwenye kusikia atakuwa ameelewa moja kwa moja kwamba simba aliyekusudiwa hapo ni simba mnyama mkali wa porini na wala si vinginevyo. Lakini mtu akisema; “nimemuona simba kwenye uwanja wa mapambano ameshika upanga”. Bila shaka

635 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 38-39. 636 - Kumbe wewe lugha unaijua na majazi umeyaelezea vizuri na ukatoa natija kwamba asiyesema hivyo huyo ni mwongo mkubwa: hajui lugha. Kisha wewe ukageuka ukayapinga majazi! Hii ni ajabu ilioje!

187

Page 188: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

hakuna atakayedhania kwamba simba aliyekusudiwa hapa ni yule mnyama pori, na sababu iliyozuia mtu asidhanie hivyo ni kauli ya msemaji; “ameshika upanga” maana simba asili hawezi kushika upanga, bali huyo ni mtu shujaa aliyefananishwa na simba kwa sababu ya ushajaa wake. Kwa hiyo kusema tu; kwamba majazi ni kutumia neno tafauti na maana yake ya asili, ni makosa kwa sababu tulizozitaja.637

JAWABU

Kwa kuanzia natutazame maneno yako uliposema:

Ama madai ya kwamba umma umeingia katika upotevu kwa sababu ya kuitakidi kuonekana Allah kwa macho huko akhera ni madai batili kwa hoja tutakazo zitoa katika kitabu chetu hiki Inshaallaah.

Na ama kuitakidi kwamba kuna waislamu ambao wataingia motoni kisha watatoka kwa sababu ya shafaa (uombezi):

Suala hili limethibiti kwa hoja zenye nguvu katika kitabu (Qur’an) na sunna sahihi za bwana Mtume -swalla llaahu alayhi wasallam-.

Ninasema: kwamba maelezo juu ya vipengele hivi yatakuja in shaa Allah katika juzuu zenye kuzungumzia mas-ala ya kuonekana au kutoonekana kwa Allah; kama vile ambavyo maelezo juu ya suala la pili mahala pake ni juzuu inayohusu mas-ala ya kutoka au kutotoka motoni ambayo umedai kwamba Qur-ani imesema kwamba watu watatoka motoni. Lakini mukhtasari ninaotaka kukwambia hapa ni kuwa hii Qur-ani ipo kuanzia Suratu Al-Fatiha hadi Suratu Al-Nasi tuoneshe Aya moja tu iliosema kuwa watu watatoka motoni. Na ukituonesha basi mimi ni wa mwanzo kuwa Wahabi! Maelezo kwa urefu yatakuja katika sehemu yake in shaa Allah.

Ama maneno yako yasemayo:

Ama madai yake ya uwongo kuwa suala la kupinga kuwepo kwa majazi ndani ya Qur’an kuwa ndiyo chanzo cha kupotea watu, 638 ufafanuzi wake ni kama ufuatavyo:

637 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 40-41. Tena Sheikh wewe majazi unayajua vyema, na umeyaelezea hapa kwa ulimi wa kalamu yako, halafu ukageuka na kuisapoti kauli ya wanaokanusha majazi! 638 - Tazama mtu anavyopotoa maudhui huyo! Mimi nasema kitu chengine na yeye anasema kitu chengine!

188

Page 189: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Suala kuwepo majazi na kutokuwepo kwake katika Qur’an na lugha ya kiarabu ni jambo ambalo maulamaa wametofautiana tangu zamani kama walivyotofautiana katika mambo mengine.

Ninasema: maelezo juu ya kipengele cha kwanza nimeshayatoa kwamba hivyo sivyo nilivyosema. Ama kuhusu kipengele cha pili jawabu ni kuwa mazingatio hayapo katika kutafautiana kwa Maulamaa, bali mazingatio yapo katika usahihi wa dalili zilizotolewa. Ama lau kama Maulamaa wakitafautiana ndio jambo linazingatiwa basi kwanini tena tujibizane? Hayo yote, lau tafauti hio ilikuwa ni katika kauli zenye Maulamaa wengi, lakini leo kauli ya kukataa majazi ni kauli shaadh walioisema ni watu wachache hata wengine wakafika kusema:

Majazi yapo katika lugha ya Waarabu kwa mujibu wa jumhur ya wanavyuoni, na akapinga Abu Is-haaq Al-Isfaraaini,639 na kupinga kwake huku kunatoa dalili tosha kwamba hakuichungulia lugha ya Waarabu, na kunatoa tangazo kwa sauti ya juu kabisa kwamba sababu ya tafauti (yake) hii ni kupitwa kwake na kuyasoma yale ambayo yanatakiwa ayasome katika lugha hii tukufu na yale yaliomo ndani yake miongoni mwa hakika na majazi ambayo hayajifichi hata kwa mwenye maarifa machache kabisa. Na (Abu Is-haaq huyo) ametoa ushahidi kwa (hoja) ambazo ni dhaifu kuliko nyumba ya buibui.640

Anasema Al-Qannubi:

Na miongoni mwa dalili za wazi juu ya udhaifu wa fahamu za watu hawa na uchache wa maarifa yao kwa Kitabu cha Allah Mtukufu na Sunna za Mtume wake (s.a.w.) na lugha ya Waarabu, ni kuyakanusha kwao majazi katika Kitabu (cha Allah) na Sunna za Mtume wake (s.a.w.) na lugha ya Kiarabu, pamoja na kuwa Umma umekaribia kukubaliana katika kuyathibitisha na wala hakuna aliyepinga isipokuwa wale walio shaadh (wachache waliopwekeka na kauli hio).641

Anasema Al-Suyuti: “Anayejingikiwa na majazi basi huyo yuko mbali na daraja ya (wenye) kufahamu; na upumbavu umemmaliza”.642 Kwa hivyo, 639 - Sahihi ni “Al-Asfarayiini”. 640 - Al-Shaukani Irshaadu Al-Fuhuul uk . 35. Lakini pamoja na hayo, Al-Imamu Al-Qannubi kanukuu maneno ya Imamu Al-Haramain katika kitabu chake Al-Talkhis akisema: “Kinachodhaniwa kwa Al-Ustaadh (Abu Is-haaq) ni kuwa hilo (la kukanusha majazi) halikuthibiti kutoka kwake”. Anasema Al-Qannubi: “Na vivyohivyo Al-Imamu Al-Ghazali kakanusha kunasibishwa kauli hio kwa Al-Ustaadh (Abu Is-haaq)”. Tazama Al-Qannubi Al-Saifu Al-Haad uk. 55. 641 - Tazama Al-Qannubi Al-Saifu Al-Haad uk. 55. 642 - Al-Suyuti Tarzu Al-’Imama nukulu kutoka katika kwa Al-Qannubi Al-Saifu Al-Haad uk. 56.

189

Page 190: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kinachozingatiwa ni dalili: si ikhtilafu. Na dalili za kuwepo kwa majazi hazihitaji kusoma hata nusu kitabu; bali mtu yoyote, mwanachuoni na mtu wa kawaida, anazijua.

Ama tukirudi katika mas-ala ya taarifu (definition) nilioitoa. Ninamwambia Sheikh wetu Kasim bin Mafuta kwamba mwenye kutoa taarifu (definition) anapokusudia kuonesha mahiyya (kiini) ya kitu basi mara nyingi huwa anachukua kile kitu cha msingi tu. Na anapotoa Al-Ta’arifu bil-haddi (normative definition) ndio anakuwa anataja kiini na masharti yake.643 Na mimi katika kitabu changu sikukusudia kusomesha watu somo la balagha; bali nilikusudia kuonesha kiini cha maudhui tu. Taarifu (definition) yangu niliposema “..na maana ya majazi ni kutumika neno tafauti na maana yake ya asili…” tayari imeshatoa kiini cha kile ninachotaka kukielezea. Ama mas-ala ya qarina na ‘Alaqa, hayo ni masharti ya majazi: si kiini cha majazi. Na kwa hivyo, usistaajabu wewe kuona kwamba hata wale wakuu wetu wanapotaka kuonesha kiini tu cha majazi nao hutoa taarifu (definition) kama hio nilioitoa mimi. Anasema Al-Imamu Al-Suyuti: “…Kwani majazi ni kulitumia neno kinyume na maahala pake”.644 Na anasema: “..Na majazi ni kuwa (mtu) akusudie kwayo kinyume cha maudhui yake (maana yake ya asili) kwa matumizi na kuleta maana”.645 Anasema: “Majazi katika neno pweke,646 na pia huitwa majazi ya kilugha, nayo ni kuitumia lafdhi pasina pale ilipowekwa mwanzo (kinyume na matumizi ya asili)”.647 Anasema Al-Imamu Al-Shaukani baada ya kutaja taarifu (definition) kama alioitaja Sheikh Kasim Mafuta: “Na ikasemwa kwamba (majazi) ni lafdhi iliotumika kinyume na mueko wake wa mwanzo kwa namna inayofaa”. 648 Na wengine wakasema kwamba majazi “Ni yalio kinyume cha hakika”.649 Anasema Al-

643 - Lakini ikiwa unataka lazima nitoe hio taarifu ulioitoa wewe, basi ungerudia kitabu changu Hali Sahihi Ya Kimaumbile uk. 14, ungeipata hio taarifu unayoitaka wewe. Huko nilisema kwamba majazi ni: المعنى و الحقيقي المعنى بين رابطة لعالقة له وضع ما غير في استعمل لفظ

الحقيقي المعنى إرادة من مانعة قرينة مع المجازي“(Majazi ni) neno ambalo limetumiwa kinyume na maana yake ya uhakika kwa kuwepo uhusiano wenye kufungamanisha baina ya maana ya uhakika na maana ya kimajazi, pamoja na kuwepo kifuatanishi cha maneno (context) chenye kuizuia maana ya uhakika”. Sheikh Kasim bin Mafuta ikiwa unataka lazima usome maelezo haya kutoka kwangu, basi rejea hicho kitabu changu nilichokutajia utayapata maelezo hayo. Lakini mimi sioni kwamba kuna ulazima wa kusema hivyo wakati wowote kama vile ambavyo wanavyuoni hawaoni ulazima huo wakati wowote. 644 - Al-Suyuti Al-Itqan j. 3, uk. 84. 645 - Al-Suyuti Al-Itqan j. 3, uk. 86. 646 - Al-Mufrad yaani neno lilopekeyake ambalo halikutegemezwa na jengine. 647 - Al-Suyuti Al-Itqan j. 3, uk.72. 648 - Al-Shaukani Irshaadu Al-Fuhuul uk . 33.649 - Al-Shaukani K.h.j.

190

Page 191: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Imamu Abu Is-haaq Al-Shirazi: “Ama Majazi, taarifu (definition) yake ni lile (neno) lililoondolewa kutoka katika ile (maana) ilioekewa”.650 Anasema Al-Amidi: “Na ukiwa unataka taarifu (definition) kwa njia yenye kuzikusanya zote (hizo) basi utasema: ‘Ni lafdhi yenye kujiweka katika matumizi yake au yenye kutumika kinyume na vile ilivyowekewa mwanzo katika fani ambayo kwayo kuna kusemezana kwa sababu ya ule uhusiano uliopo baina yake”. Utaona kwamba taarifu (definition) hii imelitoa neno qarina wakati taarifu (definitions) zilizotangulia zimelitoa neno qarina pamoja na neno ‘alaaqa. Anasema Al-Mamu Nuru Al-Din Al-Salim (r.a.):

** المتسع المجاز فهو مستعمال وضع له ما غير في يكن وإنNa ikiwa (lafdhi) kinyume na ilivyoekwa**Hayo ni

majazi yenye kutoa nafasi, hivyo ikitumika.

*** وعل أصله عن تصرفه قرينة تكشفه قوشرطه ةNa sharti yake ni qarina yenye kuitoa**kutoka Asili yake; na mfungamano unaiweka wazi.651

Anasema katika Sherehe:

Majazi ni lafdhi iliotumika kinyume na ile maana ilioekewa kwa ajili ya kuwepo alaqa na qarina…..na alaqa na qarina ni masharti mawili ya majazi.652

Sasa baada ya haya, ninachotaka kumueleza Sheikh wangu Bwana Kasim bin Mafuta ni kuwa:

1) Unapotaka kuwasomesha watu somo la balagha basi ni lazima utoe hio taarifu ulioitoa wewe.

2) Ukitaka kutoa Al-Taarifu bil-haddi (normative definition) basi ni lazima utoe hio taarifu ulioitoa wewe.

3) Ikiwa lengo lako ni kuonesha msingi tu wa kitu na kiini chake, basi unatoa taarifu kama nilioitoa mimi.

4) Wakuu wetu kadha wa kadha wametoa taarifu kama hio nilioitoa mimi, kwa sababu hio niliokueleza.

5) Maneno qarina na ‘alaaqa si nguzo za taarifu ya majazi, bali ni masharti ya majazi. Na ndio maana ukaona kwamba wakati mwengine – kama nilivyokunukulia kauli tafauti – wanavyuoni huwa hawayataji maneno hayo kamwe.

6) Tafautisha baina ya kiini au nguzo za kitu na masharti yake.

650 - Abu Is-haaq Al-Shirazi Al-Luma’a uk. 37. 651 - Al-Salimi Shamsu Al-Usul uk. 23. 652 - Al-Salimi Tal’atu Al-Shamsi j. 1, uk. 199.

191

Page 192: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Baada ya hayo, utaona makosa aliyoyatenda Sheikh Kasim mwana wa Mafuta aliposema: “Kwa hiyo kusema tu; kwamba majazi ni kutumia neno tafauti na maana yake ya asili, ni makosa kwa sababu tulizozitaja”.653 Tunasema: kusema hivyo si makosa, isipokuwa ukiongeza unakuwa umetaja masharti ya majazi: si kiini na msingi wa majazi. Kwa lugha nyengi ukiongeza unakuwa umeweka wazi zaidi. Ama ibara “Majazi ni kulitumia neno kinyume na maana yake ya asili” ni ibara ambayo tayari imeshajuilisha majazi ni nini, na kwahivyo mara nyingi wajuzi wanaitaja hio tu kama ulivyoona nukulu zao, isipokuwa ukiwa unataka kuwasomesha watu somo la balagha basi hapo utalazimika kusema kama hivyo ulivyosema wewe – kitabu changu Hoja Zenye Nguvu hakikuwa kitabu cha somo la balagh.

Na kwa ujumla ni kuwa kweli taarifu (definition) ulioitaja wewe ni sahihi. Lakini nayo pia ina kosa dogo katika kipengele cha tatu kisemacho: Lazima kuwepo na “ALAAQAH” mafungamano baina ya neno la asili na neno lisilo la asili. Nawe ulitakiwa useme: “Lazima kuwepo na “ALAAQAH” mafungamano baina ya maana ya asili ya neno lililotumika na maana isio ya asili, au useme “Lazima kuwepo na “ALAAQAH” mafungamano baina ya maana ya asili na maana isio ya asili. Ama neno ni moja lile lile: hakuna katika majazi neno la asili lililopelekwa katika neno lisilo la asili: neno ni moja lile lile limepelekwa katika maana nyengine isio ya asili.654

Pia kuna makosa ya kinahau katika kipengele cha pili kisemacho: “QARINATUN MAANI’ATUN MIN IRADATI MA’ANAL ASLIY”, nawe ulitakiwa useme: “QARINATUN MAANI’ATUN MIN IRADATI Al-MA’ANA AL-ASLIY”, au kwa njia yako ya uandishi useme: “……AL-MA’ANAL ASLIY”.

Ama mfano ulioutoa wa kusema: “Nimemuona Simba anamla Swala” pia si mfano unaozungumziwa na wanavyuoni wa kubainisha maana ya uhakika wa neno. Bali kinachozungumzwa ni kuwa neno “Simba” peke yake bila ya kuwa katika sentensi, basi maana yake ya asili ni mnyama wa pori. Na kwa hivyo, nikilitamka neno “Simba” peke yake, basi mtu asidai kwamba “Nakusudia shujaa” kwani maana ya asili ya simba si shujaa, bali ushujaa ni sifa yake tu. Ama nikisema “Ali ni simba”, basi hapa inaeleweka kwamba nimelitumia neno hilo kimajazi kwa njia ya tashbihun baligh kwani simba anaeleweka ni nani na Ali anaeleweka ni nani; kumwita huyu kwa jina la yule ni kulitumia neno kinyume na maana yake ya asili nayo ndio majazi 653 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 41. 654 - Lakini haya hayana umuhimu mkubwa kwani hayana athari katika tafsiri. Umuhimu uko katika suala je majazi yapo au hayapo? Hili ndio muhimu.

192

Page 193: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

yenyewe. Ama mfano huu: “Nimemuona Simba anamla Swala”, si mfano pambanuzi kwani:

a) Hata Ali naye anakula swala na inawezekana ikawa mtu kamkusudia yeye kwa sababu ya ushujaa wake kama simba; na akamkusudia Said kuwa ni swala kwa sababu ya udhaifu wake. Lakini kilichozuia hapo isizingatiwe maana hio ya kimajazi ni kukosekana kwa qarina: si muundiko wa ibara hio, ama ibara hio kama inavyobeba uwezekano wa hakika vivyo hivyo ndivyo inavyebeba uwezakano wa majazi; kwani kama inavyojuzu kumwita ‘Ali kuwa ni simba kwa sababu ya ushujaa wake ndivyo inavyowezekana kumwita Said kuwa ni swala kwa sababu ya udhaifu wake, na kwa mantiki hio ibara ulioitoa ewe Sheikh wetu Kasim bin Mafuta si mfano sahihi katika maudhui hii, kwani kama hapo kumekosekana لفظية قرينة(qarina ya matamshi) jambo ambalo limepelekea kuyazingatia maneno hayo katika uhakika wake; basi elewa kwamba inawezekana ikapatikana حالية itayopelekea kuzingatiwa (qarina ya hali) قرينةibara hio hio kuwa ni majazi. Kwa hivyo, elewa kwamba kilichozuia hapo kuileta maana ya kimajazi si maneno “Anakula swala” kama ulivyodhania wewe, bali ni kwa sababu neno simba ni uhakika wa kitu fulani na hakuna kilichoutoa uhakika huo na kuupeleka katika maana nyengine.

b) Pili: ni kuwa tukijaalia kwamba huo mfano wako ni sahihi, na kwamba hivyo ulivyosema wewe ni sahihi, basi hii ina maana kwamba kilichosababisha kuyazingatia maneno “Nimemuona Simba anamla Swala”, kuwa yapo katika uhakika wake itakuwa ni hio qarina ulioitaja “anamla swala”; na sisi maudhui yetu ni qarina iliolitoa neno kutoka katika maana ya uhakika na kulipeleka katika maana ya kimajazi; si kulitoa neno katika maana ya kimajazi na kulipeleka katika maana ya uhakika au qarina iliolibakisha neno katika maana yake ya asili, kwani hakika ndio asili na kwa hivyo haihitaji qarina.

Ama kauli yako uliposema kuhusu qarina:

…..2-Lazima kuwepo na “QARINATUN MAANI’ATUN MIN IRADATI MA’ANAL ASLIY” dalili yenye kuzuia kukusudiwa maana ya asili.…………Lakini mtu akisema; “nimemuona simba kwenye uwanja wa mapambano ameshika upanga”. Bila shaka hakuna atakayedhania kwamba simba aliyekusudiwa hapa ni yule mnyama pori, na sababu iliyozuia mtu asidhanie hivyo ni kauli ya msemaji; “ameshika upanga” maana simba asili hawezi kushika upanga, bali huyo ni mtu shujaa aliyefananishwa na simba

193

Page 194: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kwa sababu ya ushajaa wake.655 Kwa hiyo kusema tu; kwamba majazi ni kutumia neno tafauti na maana yake ya asili, ni makosa kwa sababu tulizozitaja.

Ninasema: dhahiri ya kutaja kwako mfano huo usemao:

..Na sababu iliyozuia mtu asidhanie hivyo ni kauli ya msemaji; “ameshika upanga” maana simba asili hawezi kushika upanga, bali huyo ni mtu shujaa aliyefananishwa na simba kwa sababu ya ushajaa wake.

Maneno hayo ni sahihi kabisa, lakini ningependa kuongeza kitu kimoja, nacho ni kuwa maneno hayo yanamfanya asiyejua adhanie kuwa qarina siku zote inakuwa lafdhiyya tu au maqaaliyya (iliotajwa katika maneno ya msemaji); ilhali si mara zote hali inakuwa hivyo; bali wakati mwengine qarina inakuwa haliyya (inayofahamika tu katika maneno ya msemaji au hali yake pasina kutamkwa) na mara nyengine qarina inakuwa ‘aqliyya (ya kiakili).656 Na hizi zina njia nyingi mno ambazo kuzijua kwake kunategemea zaidi uwezo wa mtu wa kuifahamu lugha. Kwa mfano nikisema “Ali ni punda” hapa hutoona katika maneno haya qarina lafdhiyya iliolitoa neno punda kutoka katika maana yake ya asili au iliopelekea kutokumzingatia Ali kuwa ni punda wa kweli isipokuwa ukweli kwamba Ali na punda ni

ووضعا عرفا متغايراتان ni vitu viwili tafauti kikawaida na) حقيقتانkimuweko wao wa asili ya kilugha). Yaani nikisema “punda” anafahamika mnyama anayepandwa na kupakiwa mizigo, wakati nikisema Ali inajulikana kwamba namkusudia mtu. Na hapa hakuna qarina ya matamshi iliomtoa punda kutoka katika maana ya asili au kumfanya Ali kuwa si punda wa kweli isipokuwa kile kinachojulikana katika kawaida zetu kwamba huyu si yule na yule si huyu – ni hakika mbili tafauti. Sasa vipi tena nidai kuwa huyu ni yule. Hapa inaeleweka kwamba hayo ni madai ya kimajazi kwa njia ya tashbih (kukifananisha kitu kimoja na chengine). Ninasema: na kwa njia hii na ilio mfano wa hii ndio tunakanusha kuwa Allah ana mkono, uso n.k, kwani mkono – kwa mfano – uhakika wake wa kilugha unajulikana. Tulipojua kwa yakini kwamba uhakika wake wa kilugha hauwiyani na utukufu wa Allah, basi tumejua kwamba neno mkono wa Mungu limetumika kinyume na maana yake ya asili na kwa hivyo ni majazi ambayo ni wajibu kupewa maana inayowiyana na utukufu wa Allah.

655 - Jamani! Mtazameni huyu mtu anayekanusha majazi jinsi anavyoyachambua! Japo kuwa hukoseakosea katika vijipengele vidogo vidogo lakini msingi wa majazi kauelezea vizuri! Halafu akageuka kama siye, akayakanusha! 656 - Tazama Dr. Wahbat Al-Zuhaili Usulu Al-Fiqhi j. 1, uk. 288.

194

Page 195: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Na mfano wa majazi ambayo qarina yake ni ‘aqliyya ni kama Aya isemayo: بالغيب ورسله ينصره من الله وليعلم (Na ili Allah amjue yule

atayemnusuru Yeye na Mtume wake katika hali ya ghaibu).657 Hapa kuna majazu hadhfi (majazi ya kuondoshwa kwa neno). Neno hilo lililoondoshwa ni neno dini, na maana ni “Na ili Allah amjue yule atayeinusuru DINI YAKE na Mtume wake katika hali ya ghaibu”, vyenginevyo hakuna mtu anayeweza kumnusuru Allah mwenyewe. Utaona kwamba hapa kuna majazi na wala hakuna qarina lafdhiyya iliotajwa ambayo imetujuilisha sisi kuwepo kwa majazi hayo isipokuwa kile kinachofahamika kiakili kwamba kiumbe hawezi kumnusuru Allah au kwa usahihi zaidi kwamba Allah mwenyewe yaani dhati yake hainusuriwi. Na kwa hivyo, qarina hapa ni ‘aqliyya. Maelezo haya yanakupa picha kwamba si kila mtu anaweza kuyafasiri maandiko ya Kisharia, bali mwenye uwezo huo ni mtu alikusanya mambo mawili: elimu na kipaji – yote mawili kwa pamoja: si moja peke yake.

Kwa hivyo, qarina inaweza kutajwa kama wewe ulivyotoa mfano wa maneno: “simba kashika upanga” na inawezkana isitajwe lakini ikafahamika katika maneno kwa sababu kitu kimoja kimepewa jina la kitu chengine ilhali vitu viwili hivyo katika lugha vina uhakika tafauti kama vile: punda na Ali; Ali na jiwe; mkono na Mungu n.k., au kwa sababu udhahiri wa kilichotajwa ni kinyume na akili ya binaadamu.

Anaendelea Sheikh Kasim bin Mafuta kwa kusema:

Nukta ya pili; Sina shaka kuwa ndugu Juma na wengineo katika watu wa bid’a wanapokuwa wanataja neno; “Mawahabi” huwa wanawakusudia AHLU SUNNA WAL-JAMAA, nao ni wale ambao wanaziunga mkono hoja na dalili na kazi ya daawa alioifanya Sheikhul Islaam 658 Muhammad

657 - Sura 57, Aya 25. 658 - Huyu naye pia ni Sheikhul-Islam! Kaka yake anashuhudia kwamba hakuwa mwanachuoni kamwe. Kamrudi vikali sana na akamwambia: “Ufahamu wenu nyinyi bado hauzingatiwi (kwani hamuna elimu)”. Al-Sawaa’iqu Al-Ilaahiyya uk. 16. …. “Ninyi mumechukua fahamu zenu na mukafarikiana na kundi la waliowengi na mukaukafirisha umma wote wa Muhammad”. Uk. 17. ….. “Lau muliizingatia ibara hii vizuri basi mungelijua kwamba nyinyi mumeifasiri kinyume na maana yake…..kisha munadai kwamba maneno yenu na ufahamu wenu nyinyi ni makubaliano!” Uk. 21. … “…..mfano wa mtu kama nyinyi hawezi kufanya istimbat (hawezi kutoa hukumu kutoka katika Qur-ani na Hadithi) wala hawezi kufanya qiyas..” Uk. 34. …. “Hakika leo watu wamepata mtihani wa mtu anayejinasibisha na kufuata Qur-ani na Sunna (yaani ndugu yake Muhammad Abdil-Wahhab), na anatoa (hukumu) kutoka katika elimu zake wala hajali nani anakwenda kinyume naye. Na lau utamtaka awaoneshe maneno yake wanavyuoni basi hawaoneshi, bali anawalazimisha watu wachukue kauli yake na ufahamu wake na anayempinga yeye humwita kafiri…NAYE HANA HATA SIFA MOJA YA WATU WA IJTIHAD BALI

195

Page 196: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

bin Abdul Wahaab ambaye amezaliwa mwaka 1115 H na kufariki mwaka 1206 H. Swali, Je ni kweli kwamba hao ambao ndugu Juma anawaita mawahabi ndio wanaopinga majazi? Maulamaa ambao wanapinga kuwepo kwa “Majazi” wako katika makundi mawili:a) wanaopinga kuwepo kwa majazi katika lugha na Qur’an.b) wanaopinga kuwepo kwa majazi katika Qur’an tu.a) Hawa wafuatao ni baadhi ya maulamaa waliopinga kuwepo kwa majazi katika lugha ya kiarabu na halikadhalika katika Qur’an:1- Imamu Abu Is’haaq Ibrahim bin Muhammad bin Mih’raan Al- Is’fraayiiniy Al-Shaafiy aliyefariki mwaka 418 H.2- Imamu Abu Aliy Al Hassan bin Ahmad bin Abdil-Ghaffaar Al-Fasawiy aliyefariki mwaka 377 H.3-Sheikhul Islaam Abul Abbaas Ahmad bin Abdul-Haliim Ibn Taymiyyah aliyefariki mwaka 728 H.4-Shamsud Din Abu Abdillahi Muhammad bin Abi Bakar mashuhuri kwa jina la Ibnul Qayyim al Jawziyyah aliyefariki mwaka 751 H.b) Na hawa wafuatao ni maulamaa ambao wamepinga kuwepo kwa majazi ndani ya Qur’an tu, lakini wakathibitisha kuwepo kwake katika lugha ya kiarabu:1-Muhammad bin Ahmad bin Abdillahi mashuhuri kwa Ibn Khuwayz Min’daad katika maulamaa wa madhehbu ya Ki-Maalik.2-Imamu Abul Abbaas Ahmad bin Ahmad Al-Twabariy Al-Shaafiy mashuhuri kwa Ibnul-Qaadhiy aliyefariki mwaka 335 H.

Ndugu msomaji kama ukiutazama kwa makini mwaka aliozaliwa Sheikh Muhammad bin Abdil-Wahab na mwaka waliokufa maulamaa hawa tuliowataja utagundua kwamba ndugu Juma al-Mazrui ni mwongo.

JAWABU

Mosi: sisi tunapotumia neno Wahabi hatukusudii Ahlu Sunna Wal-Jama’a, Ahlu Sunna ni madhehebu tatu na nusu zinazoeleweka – Shafi, Hanafi, Maliki na baadhi ya Hanbali. Hawa ndio watu wanaofuata Sunna. Na zinatosha kubainisha hilo zile adabu zao, uchaji wao na hata mijadala yao ilivyo, basi ni ya kiheshima na utulivu. Hawa wameishi Afrika Mashariki kwa karne nyingi hadi kufikia zama zetu hujasikiapo kumtukana mtu kwa sababu ya madhehebu yake, tafauti na nyinyi mulivyo duniani kote, ambapo hakuna sehemu yoyote ile ya dunia ambayo hamukuitia fitna! Ninatamani –

(HANA HATA SIFA) MOJA KATIKA KUMI..LAKINI HUYAPIGIA DEBE MANENO YAKE KWA WAJINGA WENGI…”. Uk. 9. Hayo ni maneno ya Sheikh Sulaiman bin Abdil-Wahhab anamwambia ndugu yake Muhammed Abdul-Wahhab. Maelezo yake ni mengi, rejea kitabu hicho Al-Sawaaiqu Al-Ilahiyyya. Bali Al-Albani anashuhudia kwamba Muhammed Abdul-Wahab alikuwa hana elimu ya Hadithi kamwe. Bali vitabu vyake vinajishuhudisha hivyo, kwani ni vitabu visivyo na elimu kabisa hata mwanafunzi wa thanawi (sekondari) anaweza kuvitunga! Haya twendeni!

196

Page 197: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

ewe Sheikh Kasim bin Mafuta – lau Sheikh ‘Umar bin Sumait, Sheikh Sulaiman Al-‘Alawi, Sheikh Abdullah Salih Al-Farisi na walio mfano wa hao wangelikuwa hai ukakaa nao japo siku moja tu, kisha ukaona vipi Sunna inavyotekelezwa kimatendo. Lakini mwenzetu umekwenda kukaa na Mashekhe wa Suudia na Mawahabi wa Yemen, Sunna ya kweli utaipata wapi? Utayoipata huko ni Sunna ya kutukana watu na kuwakafirisha kama kitabu chako kinavyojishuhudisha chenyewe!

Kisha elewa kwamba miongoni mwa Ahlu Sunna wa kweli, ukiwachilia mbali jina, basi ni Ibadhi ndio wanaofuata Sunna za kweli wala hawakubadilisha kitu. Haya ninayokuambia ni kwa ushuhuda wa wasiokuwa Ibadhi kama nitavyokunukulia maneno yao katika juzuu nyengine za kitabu hiki, na ushahidi bora ni ule uliotolewa na mpinzani. Nawe kama huniamini kama Ibadhi ndio Ahlu Sunna wa kweli, tokeni kikundi cha Mawahabi na kikundi cha Maibadhi mukaishi katika nchi hata ya kikafiri, kisha tazameni ni nani ambao tabia zao zitapendwa. Ahlu Sunna hujulikana – si kwa kujipachika jina hilo, bali – kwa tabia zao na mwenendo wao mzuri, na hili nyinyi ulimwengu mzima umeshuhudia kwamba hamunalo, munalolijua nyinyi ni kutukana watu na kumshambulia huyu na yule.659

Pili: ni kwamba ikiwa tutakubaliana na madai yenu kwamba Wahabi ni Ahlu Sunna je hio Jamaa yao iko wapi? Je wao ni wangapi duniani hata taarifu (definition) ya Ahlu Sunna Wa Al-Jamaa iwafae? Usiniambie kwamba Al-Jamaa (kundi kubwa) ni aliye katika haki hata akiwa mmoja kama ilivyopokewa kutoka kwa Ibn Mas-uud, kwani Ibadhi, Zaidia na Bohora watakuja kudai kwamba mmoja huyo aliye katika haki ni wao. Kwa hivyo, sisi tunapotaja Wahabi tunakusudia wafuasi wa Muhammad Abdul Wahhab, nao wako mbali mno na Sunna ya Mtume (s.a.w.) katika itikadi na katika akhlaqi, ijapokuwa wamedanganyika kwa kujipachika jina hilo na kuwarushia wenzao majina mabaya. Kwa hali yoyote ile, hili pia si muhimu, kwani sisi tunachokitaka ni nini unasema na una ushahidi gani: sio jina lako zuri la kujipamba au jina la mwenzio baya la kumpambua? Lakini kwa ufupi ni kuwa mimi katika kitabu changu na maandiko yagu yote, ninapotaja Mawahabi nawakusudia wafuasi wa Muhammad ‘Abdil-Wahhab pamoja na

659 - Bali kanihadithia mwanafunzi mmoja wa Afrika Magharibi ambao kwao sasa Ibadhi imeingia kwamba mwanzo walipodhihiri Ibadhi huko watu walikuwa wakiwachukia wakidhania kuwa ndio wale wale Mawahabi wamekuja kwa sura nyengine. Na baada ya watu kujua kwamba kweli wao si Mawahabi na baada ya kuona mwenendo wao mzuri, sasa wamekuwa ni watu wenye kupendwa sana huko. Na haya yote ni kwa sababu Mawahabi huko wamefanya fitna isio na kifani hata ikapeekea kufa kwa watu wasiopungua thamanini katika fujo la siku moja. Hii ndio dini yenu enyi Kasim Mafuta!

197

Page 198: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Maimamu wao wote watangulizi kama Ibn Taymiyya, Ibn Al-Qayyim, Ibn Batta, Al-Barbahari, na walio mfano wa hao.

Ama kuhusu wanavyuoni uliowataja kwamba wanakataa majazi, elewa kwamba hilo ni jambo lenye kuhitaji maelezo. Abu Is-haaq Ibrahim bin Muhammad bin Mih’raan Al-Is’fraayiiniy,660 kwa mfano, ambaye umemtaja kama ni Shafi. Yeye si Shafi katika itikadi; bali ni Shafi katika fiq-hi. Ama itikadi yake ni kama yenu ya kuwa Allah ana viungo. Na kwa sababu hii ndio maana Ibn Al-Qayyim akamtaja katika Ijtimaa’u Al-Juyuush na akasema: “Alikuwa ni katika Maimamu wakubwa wa Sunna wenye kuzithibitisha sifa (za Allah)”.661 Nawe Sheikh Mafuta unaelewa vyema nini Ibn Al-Qayyim anakusudia anaposema: “Alikuwa ni Imamu wa Sunna na ni mwenye kuzithibitisha sifa za Allah” kwamba ni mwenye kuthibitisha kuwa Allah ana uso, mikono n.k. Kwa hivyo, Abu Is-haq huyu kukataa kwake majazi ni jambo la lazima wala hahisabiwi tena kuwa ni katika wanavyuoni wa Kishafi madamu katafautiana nao katika mambo ya misingi ya itikadi.

Hayo nilioyasema kuhusu Abu Is-haaq ni kwa kutegemea kile alichokisema Ibn Al-Qayyim katika kitabu chake hicho Ijtimaa’u Al-Juyuush kwamba Abu Is-haq huyo: “Alikuwa ni katika Maimamu wakubwa wa Sunna wenye kuzithibitisha sifa (za Allah)”. Vyenginevyo Imamu Al-Haramain na Al-Imamu Al-Ghazali – kama tulivyonukuu kabla – wanakanusha madai kwamba Abu Is-haaq alikuwa akikakanusha majazi.

Ama suala lako ulipouliza: “Je ni kweli kwamba hao ambao ndugu Juma anawaita mawahabi ndio wanaopinga majazi?” Suala hili – pamoja na majibu uliotoa – linaonesha kwamba hufahamu unachoambiwa! Ajabu mtu kukimbilia kujibu bila ya kufahamu anaambiwa nini! Nikisema kwamba Kasim Mafuta anaamini kwamba Mungu ana mikono haimaanishi kwamba ninakataa kwamba kuna wengine wenye kusema kwamba Mungu ana mikono. Bali maneno hayo yanathibitisha kwamba Kasim Mafuta anaamini kwamba Mungu ana mikono. Halkadhalika niliposema kwamba Mawahabi wanasema kuwa hakuna majazi, hio ina maana kwamba ninachokidai – kwa maneno yangu hayo – ni kwamba wao wanasema kuwa hakuna majazi: wala sidai kwamba hakuna mwengine yoyote yule aliyesema kuwa hakuna majazi. Sasa wewe unanijibu kwamba wako Maimamu waliokataa majazi kabla ya kuzaliwa Muhammad ‘Abdil-Wahhab. Jawabu hii ingelifaa lau mimi nilisema kwamba Muhammad ‘Abdil-Wahhab ni wa mwanzo kudai

660 - Sahihi ni kumwita “Al-Asfaraayiini”, japo kuwa wanavyuoni wengi wamemwita hivyo. 661 - Tazam Ijtima’u Al-Juyuush uk. 111.

198

Page 199: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kutokuwepo kwa majazi. Kwa hivyo, ili uwe umenijibu jawabu sahihi niambie kwamba Mawahabi wanayakubali majazi. Na hapa itakubidi ufute usemi wako kwamba:

Na wengine wameona wauite “Usluubun min Asaalibil-Lugha” (utaratibu/mfumo katika taratibu za lugha) na njia hii ndiyo iliyokaribu na usahihi, ili kuwazuia watu wa batili wasiyapotoshe maandiko kwa kuupitia mlango huu.

Kwa ufupi, ni kuwa kauli ya kuwepo kwa majazi katika Qur-ani, Sunna na lugha ya Kiarabu, ndio kauli ya jumhur ya wanavyuoni katika madhehebu zote, na ndio yenye ushahidi wa wazi ambao haupingi ila ambaye hataki ukweli, au aliyepotea au mwenye akili finyu na udhaifu wa kufahamu. Tumetoa ushahidi kidogo katika sehemu tulionukuu yale nilioyasema katika kitabu changu Hoja Zenye Nguvu na nitaeleza tena baadae kwa urefu.

Na kwa hivyo, kauli yako uliposema:

Ndugu msomaji kama ukiutazama kwa makini mwaka aliozaliwa Sheikh Muhammad bin Abdil-Wahab na mwaka waliokufa maulamaa hawa tuliowataja utagundua kwamba ndugu Juma al-Mazrui ni mwongo”.

Kauli hii inaonesha jinsi ulivyokuwa jasiri katika kuwatukana watu bila hata ya kuwafahamu wanachokisema; inaonesha kiasi gani ulivyokuwa humuogopi Mola wako. Mimi nilichokisema ni kuwa Mawahabi wanakataa majazi. Wewe unaniambia kwamba wako maulamaa kabla ya kuwepo Mawahabi walikataa majazi kisha unaniita mwongo! Kwani mimi nilisema hakuna maulamaa hao hata nimekuwa mwongo? Na je tuseme kuwa wewe ni mwongo uliposema:

Ndugu Juma Al-Mazrui katika kitabu chake “Hoja zenye Nguvu” ukurasa wa 32 amefanya jaribio la kutaka kuuficha ukweli huo ambao uko wazi tena mbele ya macho yake na akafanya upotoshaji kwa makusudi dhidi ya watu anaowaita Mawahabi . 662

Na umesema:

Hakuna kitu kingine zaidi ya chuki kilichomfanya awaite Ah’lu Sunna kwa jina la Mawahabi, au Hashawiya, au Mujasima.663

662 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 39.663 - K.h.j. uk. 10.

199

Page 200: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Ninasema: je tuseme na wewe ni mwongo uliposema: “dhidi ya watu anaowaita Mawahabi” kwa sababu mimi siye niliyewaita watu hao Mawahabi na pia kwa sababu wako wengi mno duniani wanavyuoni na wasiokuwa wanavyuoni ambao wanawaita na wamewaita watu hao Mawahabi hata kabla ya kuzaliwa mimi kwa miaka mingi? Kama vile ambavyo jina “Hashwiyya” na jina “Mujassima” yametajwa na wanavyuoni wa karne nyingi. Anasema Al-Imamu Al-Subki Al-Ashafi: “Ama Al-Hashwiyya ni kikundi dhalili cha wajinga wanajinasibisha na (Al-Imamu) Ahmad na Ahmad yuko mbali nao”.664 Anasema Sheikh Al-Kawthari: “…..nao ni Al-Hashwiyya”.665 Bali Ibn Al-Qayyim anasema:

** ترايان ما الحشوي أم أنتم ذا بعد الخوارج دين على ذا من

Basi baada ya hayo ni nani aliye katika dini yaKhawaarij*****Munaonaje: ni nyinyi au ni Al-Hashwiy

... اإليمان ** راية حامل ��وي الحش�� لرأيتم أبصرتم لو والله

Wallahi lau mulitazama basi mungelimuona Al-Hashwiy**Kwamba ndiye aliyebeba bendra ya imani.666

Anasema Ibn ‘Assaakir:

العرش في حال سبحانه إنه والمجسمة الحشوية ن وإوقالتعليه جالس وهو له مكان العرش

Na wakasema Al-Hashwiyya na Al-Mujassima, kwamba Yeye Allah Mtukufu yupo katika ‘Arshi, na kwamba ‘Arshi ndio sehemu yake naye kakaa kitako juu yake.667

Anasema Al-Shahrastani:

…Na kundi la watu wa Hadithi Mahashwiyya….wamesema kwamba Mola wao wanayemuabudu ana sura ya mtu mwenye viungo na migawanyiko…na inajuzu kwake kuondoka (sehemu hadi sehemu) na kushuka na kupanda….668

664 - Al-Subki Al-Kabir Al-Saifu Al-Saqil uk. 16. 665 - Al-Kawthari Takmilatu Al-Raddi ‘Alaa Al-Nuniyya kilicho pamoja Al-Saifu Al-Saqil cha Al-Subki Al-Kabir uk. 15. 666 - Ibn Al-Qayyim Al-Nuniyya j. 1, uk. 362. 667 - Ibn ‘Assaakir Tabyiin Kadhibi Al-Muftari uk. 150. 668 - Al-Shahrastani Al-Milal j. 1, uk. 117.

200

Page 201: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Kwa hivyo, ni wazi kwamba jina hilo liko karne nyingi.669 Ama jina la Al-Mujassima na Al-Tajsim wamelizungumzia wanavyuoni wengi akiwemo Ibn Taymiyya kama tulivyomnukuu sana na wala hakuona kuwa hilo ni jina baya kama alivyosema:

Na hakuna yoyote katika Al-Salaf (watangulizi) aliyemlaumu mtu yoyote kwamba yeye (mtu huyo) ni mujassim (mwenye kusema kuwa Allah ni kiwiliwili). Wala (hakuna) aliyewalaumu mujasima (wenye kusema kuwa Allah ni kiwiliwili). Bali (Al-Salaf) waliwalaumu Al-Jahmiyya ambao waliyakanusha hayo (ya kuwa Allah ni kiwiliwili)!670……..…………………….Bali wanasema (Al-Imamu Ahmad na Maimamu wengine wa Sunna, kwamba) kuzithibitisha maana hizi ni haki zaidi kwa maana ya tajsim (kwa maana ya kumfanya Allah kuwa ni mwenye kiwiliwili) kuliko kuzithibitisha lafdhi zake bila ya (kuthibitisha maana yake).671

Halkadhalika ukisoma kitabu Al-Saifu Al-Saqil cha Al-Subki pamoja na Takmila yake cha Al-Kawthari,672 utaona wakilitumia jina hilo kwa wingi, na Al-Subki huyo kafa 756 A.H. Sasa:

1) Vipi unadai kwamba Juma Mazrui ndiye aliyekuiteni nyinyi Mawahabi, Hashwiyya, Mujassima?

2) Vipi utajitoa katika jina “mwongo” kwa mujibu wa misingi yako uliojijengea ya kuwaita watu waongo?

Sikiliza ewe Sheikh Kasim Mafuta! Elimu ni kufahamu: si kuhifadhi Hadithi nyingi. Mtu akisema kuwa “Mawahabi wanakataa kitu fulani” haileti maana kwamba hakuna mwengine anayekikataa kitu hicho. Isipokuwa ukiwa utajenga hoja kwa kutumia MafhubAl-Laqab nayo ni mafhumu dhaifu taqriban kwa makubaliano ya Umma mzima. Sheikh Kasim! Kwani tukisema kuwa Ibadhi hawaamini kuonekana kwa Allah inamaanisha kuwa huo ni uwongo kwa sababu wako wengine wasiokuwa Ibadhi ambao pia hawaamini kuonekana kwa Allah? Nyinyi ndugu zetu muna fahamu gani?

Anaendelea Sh. Kasim Mafuta kwa kusema:

669 - Rejea pia Tafsiri Mafaatihu Al-Ghaib ya Al-Fakhru Al-Razi utaona akilitumia jina hilo katika sehemu tafauti za tafsiri yake. Tazama, kwa mfano, mas-ala ya kumi na mbili mlango wa pili katika tafsiri ya Suratu Al-Fatiha, mlango kuhusu “Sauti, herufi na hukumu zake”. 670 - Ibn Taymiyya Bayaanu Talbisi Al-Jahmiyya j. 1, uk. 100. 671 - Ibn Taymiyya Bayanu Talbis Al-Jahmiyya j. 1, uk. 93. 672 - Tazama Takmila ya Al-Kawthari katika Al-Saifu Al-Saqil cha Al-Subki uk.17, 19.

201

Page 202: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Kwa mfano, baina ya Sheikh Muhammad bin Abdil Wahaab aliyezaliwa mwaka 1115 H na kufariki mwaka 1206 H na baina ya Imamu Abu Is’haaq al Isfraayiiniy aliyefariki mwaka 418 H, ambaye ni miongoni mwa wanaopinga kuwepo kwa “Majazi” utaona kuwa baina yao kuna miaka takriban 697, kabla ya kuzaliwa huyo wanaedai kuwa ndiyo muasisi wa huo uwahabi! Kwa miaka hiyo tayari upingaji wa majazi ulikuwepo duniani.

Sasa utasemaje kwamba Mawahabi wanapinga majazi na hali yakuwa huyo muasisi wa huo mnaouita uwahabi amezaliwa miaka 697 baada ya kauli hiyo ya kupinga majazi ? Au unataka kutuambia kwamba Imamu Abu Is’haaq Al-Isfraayiiniy alifufuka baada ya kuzaliwa Muhammad bin Abdul-wahab kisha akamfuata sheikh Muhammad bin Abdil-wahab? Au mnataka kutuambia kuwa hawa nao pia ni Mawahabi?673

Ninasema: masuali haya yote, jiulize mwenyewe na ujijibu wewe, kwani msingi wake ni kunizulia kitu ambacho sikukisema. Kwa hivyo, hayo masuali jijibu wewe mwenyewe. Kisha baada hayo, Al-’Allama Sheikh Kasim Mafuta akasema:

JE WENYE KUPINGA MAJAZI WANA HOJA ZA KIELIMU?

Jambo muhimu la kulizingatia ni; je hao maulamaa waliopinga kuwepo kwa majazi, wamepinga kwa hoja na dalili za kielimu? Au ni kwa maneno matupu? Jawabu ni kama ifuatavyo:

Ukirejea kauli za maulamaa hao waliopinga kuwepo kwa majazi ima katika lugha ya kiarabu na Qur’an, au katika Qur’an tu, utagundua kwamba kuna hoja za msingi walizozitoa ambazo haitakiwi kuzipuuza, bali inatakiwa zitazamwe kielimu na kwa jicho la insafu. 674

Ninasema: Kuwepo kwa majazi ni kitu ambacho hata mtoto wa sekondari anakubaliana nako. Hakuna lugha yoyote duniani ambayo haina majazi. Na waliopinga kuwepo kwa majazi ni kwa sababu ya kuhofia kwao kuporomoka kwa itikadi zao: si kwa sababu majazi hayapo. Vyenginevyo mbona wao wenyewe wanalazimika kuyatumia? Hata lugha ya Kiswahili imejaa majazi. Nikisema: “Huyu ana mkono mkono” yaani ni mwizi; “Huyu ana ulimi” yaani ni msemaji; “Ana kichwa” yaani ana akili. Vyenginevyo watu wote wana mikono, ulimi na vichwa.

673 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 42-43.674 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 43.

202

Page 203: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Anaendelea Sh. Kasim Mafuta kwa kusema:

Hizi zifuatazo ni baadhi ya hoja zao:

HOJA YAO YA KWANZA

Miongoni mwa hoja zao zinazowafanya kupinga kuwepo majazi katika lugha na halikadhalika katika Qur’an, ni kuwa maana ya maneno hufahamika kwa kuutazama mtiririko au muktadha (context) na dalili za uhalisia. Pia wakadai kuwa neno linapokuwa peke yake halileti maana kamili mpaka liwe katika sentensi, na linapo unganishwa katika sentensi huwa ule mtiririko wa maneno ndio unao ainisha maana husika ya neno hilo. 675

Ninasema: maneno hayo hayana ukweli hata chembe. Ulazima wa kufahamika kwa neno kwa kuutazama mtiririko au muktadha (context), ni katika hali mbili tu:

1) Neno linapotumika kinyume na maana yake ya asili, kama vile kulitumia neno mkono kwa maana ya nguvu. Hapa ndipo ambapo neno linaambiwa kuwa limetumika kimajazi na ndipo linapohitaji qarina lafdhiyya au haliyya au ‘aqliyya itayobainisha kwamba maana yake ya asili sio iliokusudiwa. Na hayo yote au mfano wa hayo umeyanena wewe mwenyewe kwa ulimi wa kalamu yako.

2) Neno linapokuwa ni mushtarak (asili ya neno hilo lina maana nyingi kwa pamoja). Kama – katika Kiswahili – nikitaja neno “mto” kisha nikanyamaza. Katika hali hii huwezi kujua ni mto gani nilioukusudia – je ni mto wa maji au wa kulalia. Na kwa hivyo hapa ni lazima kuwe na qarina itayobainisha makusudio yangu kama vile “nipe mto nilalie” au “ninakwenda mtoni kukoga”. Maneno “nipe…nilalie” na “ninakwenda…kukoga” ni qarina zilizobainishi ni mito gani hio nilioikusudia.

Katika hali mbili hizo, kama ulivyoona mifano nilioipiga, ndipo ambapo kuna ulazima wa kuwepo kwa qarina itayoainisha maana iliokusudiwa. Ama neno likiwa limetumika katika maana yake ya asili au si mushtarak basi hakuna haja ya kutazama mtiririko au muktadha (context). Na lau Sheikh Kasim bin Mafuta aliyarejea maneno yake alioyaandika mwenyewe, basi asingeliyasema maneno haya. Ebu jikumbushe maneno yako ulioyasema kabla kidogo:

675 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 43.

203

Page 204: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Kwa sababu ili maneno yawe ni majazi, ni lazima masharti matatu makuu yatimie, nayo ni:1-Kutumika neno katika isiyo kuwa maana yake ya asili.2-Lazima kuwepo na “QARINATUN MAANI’ATUN MIN IRADATI MA’ANAL ASLIY” dalili yenye kuzuia kukusudiwa maana ya asili.3-Lazima kuwepo na “ALAAQAH” mafungamano baina ya neno la asili na neno lisilo la asili.

Na likikosekana sharti moja kati ya haya matatu tuliyoyataja basi hakutakuwa na majazi na atakayedai kuwa ni majazi basi huyo ni mwongo mkubwa na hajui lugha ya kiarabu676 …..

Hayo ni maneno yako mwenyewe! Ni wazi kwamba ikiwa masharti hayo hayakupatikana basi neno linabakia katika maana yake ya asili. Sasa vipi tena hapa unadai kwamba: “…Maana ya maneno hufahamika kwa kuutazama mtiririko au muktadha (context) na dalili za uhalisia”? Yaani – kwa lugha nyengine – neno halifahamiki mpaka utazame qarina (context).

Ama madai yako uliposema:

Pia wakadai kuwa neno linapokuwa peke yake halileti maana kamili mpaka liwe katika sentensi, na linapounganishwa katika sentensi huwa ule mtiririko wa maneno ndio unao ainisha maana husika ya neno hilo.

Tunasema: ikiwa neno likiwa peke yake halileti maana kamili na kwa hivyo hakuna majazi, basi pia na hakika isiwepo kwani neno peke yake halileti maana kamili; bali ni mtiririko (siyaq au sibaq) ndio inayobainisha maana husika! Na kwa hivyo, hizi lafdhi zote tukiichukua moja moja zinakuwa hazina maana yenye kufahamika!

Nasi tunasema kwamba neno linakuwa na maana yake ya uhakika nayo ni ile ambayo الذهن إلى yaani ni ile (inayokimbilia katika fahamu) يتبادرmaana ambayo mtu akilisikia tu neno hilo basi anaifahamu maana hio. Nikisema mkono, basi unaeleweka ni nini na hii ndio maana yake ya hakika. Ama kuwepo kwa neno katika sentensi, huko kunaweza kuonesha kwamba neno hilo halikutumika katika maana yake ya asili yaani ni majazi; wala haina maana kwamba neno halipewi maana yake ya uhakika linapokuwa peke yake.

Anaendelea Sh. Kasim Mafuta kwa kusema:

676 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 40. Tena Sheikh Kasim kumbe yeye majazi anayajua basi tu!

204

Page 205: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Mfano, neno “ رأس “ “Ra’asun” lina maana nyingi, lakini maana zote zinaainishwa na mtiririko wa maneno, kwa mfano mtu akisema: Ra’asul-Jabali, atakuwa hapa anakusudia kilele cha mlima.

Na kama atasema:

Ra’asul-Maali, atakuwa anakusudia msingi wa mali au rasilimali. Na kama atasema: Ra’asul-Insaani, atakuwa anakusudia kichwa cha binadamu. Na maana zote za neno hili zimeanishwa na mtiririko wa maneno, na wala hakuna binadamu yoyote anaeweza kututhibitishia kwa hoja na dalili kwamba maana ya asili ya neno “Ra’asi” ni kichwa cha binadamu, na katika sehemu nyingine zote ni Majazi. 677

Ninasema: kwa maana hio mtu akisema “gari” wewe hujui kakusudia nini mpaka aseme “ninakwenda kutengeneza gari” au “ninakwenda kuitia petroli gari” au aseme: “nitasafiri kwa gari”? Na akisema “nyumba” wewe hufahamu anakusudia nini mpaka ataposema “ninakwenda kuezeka nyumba”. Akisema “mti” hufahamu kakusudia nini, mpaka ataposema “mti wenye matunda”. Akisema ndevu hujui kakusudia nini mpaka ataposema “ndevu za binaadamu au za mbuzi”. Akisema “tumbo” hufahamu kakusudia nini; mpaka ataposema “tumbo la mtu”. Hii ni akili gani? Hii ndio Al-Taqlid Al-A’amaa (kufuata kama kipofu). Basi ni hivyo: sisi tunapewa fikra nasi tunazichukua tu kwa sababu kazisema Ibn Al-Qayyim kana kwamba Ibn Al-Qayyim ni ma’asum.

Na kwa ufupi, ni kwamba ikiwa neno “kichwa” kwa kulitaja tu halifahamiki nini makusudio yake, basi sababu si kwamba hakuna majazi na hakika, bali sababu itakuwa neno hilo litakuwa ni mushtarak. Neno mushtarak ni neno lenye maana nyingi wakati mmoja na zote ni maana za uhakika: si za kimajazi. Tumetoa mfano wa neno mto katika lugha ya Kiswahili, na tunatoa mfano wa neno عين ‘Ain katika lugha ya Kiarabu. Neno hili lina maana ya jicho, jasusi, chemchem, dhahabu n.k. Na kwa hivyo, nikisema Ain tu, kisha nikanyamaza huwezi kujua ninakusudia nini. Tafauti na‘ عينnikisema ‘Ain linaniuma. Hapa utafahamu kuwa ninakusudia jicho linaniuma. Ama maneno yenye maana moja ya kimsingi, hayo yanapotajwa huwa yanaeleweka wala hayahitaji qarina au kuwepo katika sentensi ili yaeleweke. Ama maana zake za kimajazi, hizo ndizo zinazohitaji kuwepo kwa Qaraain lafdhiyya au haliyya au ‘aqliyya. Na kwa mantiki hii nikisema kisu, mtu anafahamu ninakusudia nini; nikisema jiwe mtu anafahamu ninakusudia nini; nikisema chungwa mtu anafahamu ninakusudia nini n.k. Bali neno kichwa ukilitaja tu linafahamika ni kitu gani, na maana zake

677 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 44.

205

Page 206: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

nyengine kama ra-sul mali (rasilimali) na ra-sul jabal (kichwa cha mlima yaani kileleni kwake), maana hizo ndizo ambazo hazifahamiki ili zitajwe namna hiyo – kwa kuwepo qarina. Hakuna Mwarabu yoyote utayemwambia “Ra-asun” (kichwa) akafikiria kwamba unakusudia juu ya mlima au rasilimali; bali ukilitaja tu neno hilo moja kwa moja Mwarabu anafahamu “kiungo cha mwili”. Kwa hivyo, madai yako hayo yametokana na kufuata kama bendera inavyofuata upepo: hayakutokana na tahqiq za kielimu!

Na kwa ufupi, ewe Sheikh Kasim Mafuta, ni kuwa hoja yako hio ni hoja ya Imamu wako Ibn Al-Qayyim. Naye kajibiwa jawabu ya uwazi na Al-Imamu Badru Al-Din Al-Sheikh Al-Rabbaani Ahmad bin Hamad Al-Khalili Al-Mufassir. Nakunukulia hoja ya Ibn Al-Qayyim halafu nakufatishia jawabu aliojibiwa. Anasema Ibn Al-Qayyim:

Kufarikisha kwenu baina ya hakika na majazi kwa kufuata kuifungamanisha katika moja ya lafdhi mbili kama vile الذل bawa) جناجla udhalili) na حرب na vilivyo mfano wake. Hakika (moto wa vita) نارya Waarabu hawakuzitumia lafdhi hizo ila katika hali ya kufungamanishwa. Na utafautishaji huu ni katika utafautishaji mbovu kabisa kwani lafdhi nyingi ambazo zimetumika katika maudhui yake (maana yake ya asili) basi wamejilazimisha kuzifungamanisha (hawazitumii peke yake) kama vile neno kichwa na bawa na mkono na mguu. Hakika yao (Waarabu) hawakuzitumia lafdhi hizi na zilizo mfano wa hizi isipokuwa kwa kuzifungamanisha na mwahala mwake na mule zinamotegemezwa, kama vile kichwa cha mnyama na kichwa cha maji na kichwa cha mtaji (ra-asul mali au rasilimali) na kichwa cha jambo. Halkadhalika neno جناح bawa. (Waarabu) hawakulitumia (neno hilo) ila katika hali ya kuliunganisha na kile ambacho hutegemezwa nacho kama vile الطائر الذل na ,(bawa la ndege) جناح .(bawa la udhalili) جناحAma mukilichukuwa neno bawa moja kwa moja (peke yake) bila ya kuliunganisha (na kitu) basi huwa halitoi maana yenye kuleta faida ya maana yake peke yake kamwe ukiachilia mbali kuwa ni hakika au majazi. Na ikiwa mutalizingatia katika hali ya kuunganishwa (na neno jengine) basi (neno hilo) linakuwa hakika katika kile kilichounganishwa nacho. Basi vipi kitu kilichotegemezwa na kitu kimoja kinakuwa hakika katika kitu hicho; halafu kinakuwa majazi katika kutegemezwa kwake na kitu chengine, ilhali kukinasibisha kwake na tegemezi hii ni sawa na kukinasibisha kwake na tegemezi nyengine. Bawa la Malaika (kwa mfano) ni hakika kwake. Allah anasema المالئكة جاعل أجنحة أولي رسال

ورباع وثالث مثنى (Ni mwenye kuumba Malaika kuwa ni wajumbe wenye mabawa mawili mawili, matatu matatu na manne manne). Atayesema kwamba Malaika hana bawa la kweli kweli, basi huyo ni

206

Page 207: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

mwongo, mzushi, mwenye kukikataa kile alichokithibisha Allah Mtukufu……….678

Hayo ndio maneno ya Ibn Al-Qayyim, nayo ni maneno ya kustaajabisha. Kwani mwenyewe kataja الذل na kuliingiza ,(bawa la udhalili) جناحbawa hili kuwa ni bawa la uhakika; nasi tunamuomba Ibn Al-Qayyim atuoneshe wapi duniani linapatikana bawa la uhakika la udhalili. Na kama Ibn Al-Qayyim ameshatangulia kwenda kwenye matendo yake alioyatanguliza, basi wafuasi wake wapo mmoja wao ni Sh. Kasim Mafuta. Tunaomba wafuasi watuoneshe wapi kuna bawa la uhakika la udhalili – je udhalili una bawa na linapatikana wapi? Kwa ufupi ni kuwa Ibn Al-Qayyim hapa anasema yale yale yaliosemwa na Al-’Allama Kasim Mafuta, kwamba neno moja tu peke yake huwa halitoi maana hadi pale litapowekwa katika sentensi au litapotegemezwa na neno jengine au kutegemezwa na mwahala mwake! Lakini akajibiwa na Al-Imamu Badru Al-Din Al-Khalili kama ifuatavyo:

Na jawabu yake: ni kuwa hicho alichokisema ni madai yasio na ushahidi, kwani alioyataja kutoka kwa Waarabu kwamba wao hawavitaji (viungo) kama kichwa, na bawa na mkono na muundi na mguu ila kwa kuviunganisha kwa kuvitegemeza (na neno jengine) ni dai batili halina ushahidi wowote, na wapi ataupata ushahidi? Hakika ya kuvihusisha viungo hivi peke yake kwamba havitumiki ila katika hali ya kuviunganisha (na maneno mengine) hakuna yoyote aliyelisema katika walionukuu lugha (ya Kiarabu) kama vile Abu ‘Amri, Al-Khalil, Sibawayh, Al-Asma’iy, Al-Kisaai na wengineo. Na anayedai hivyo na alete ushahidi katika maneno yao. Na ikiwa (Ibn Al-Qayyim) anadai kwamba viungo vyote havitamkwi ila katika hali ya kuviunganisha (na mwahala mwake), basi hilo ni lenye kukataliwa kwa kuwepo ushahidi usiohisabika wenye kuonesha kinyume na hivyo. Na inatosha kauli ya Mtume (s.a.w.) aliposema: “.. ال ما فيها

سمعت أذن وال رأت Humo (Peponi) kuna mambo ambayo) ”عينjicho halijapata kuona wala sikio halijapata kusikia”. Basi kwa hakika ndani yake (Hadithi hii) jicho na sikio yametajwa bila ya kuyategemeza au kuyafungamanisha na (mwahala mwake)……………….......Na kuna pingamizi gani mtu akisema: قدم أو رجل أو يد أو رأس أو وجه لي بدا

األعضاء هذه من شيء أي أو شعر uso umenidhihirikia au) أوkichwa au mkono au mguu au nywele au chochote katika viungo hivi)?............Anasema ‘Umar bin Abi Rabi’a:

** ببنان زينت خضيب وكف جمرت حين معصم منها لي بدا

Ukanidhihirikia kutoka kwake mkono aliporembea Jamra 678 - Ibn Al-Qayyim Al-Sawa’iq Al-Mursala uk. 247.

207

Page 208: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Na kiganja chenye hina kimepambwa kwa ncha za vidole.

Ama mabawa ya Malaika ni hakika kwao, lakini hilo halitoi upinzani kwa waliosema kwamba bawa la udhalili ni majazi. Kwani inajulikana kwamba bawa ni kiungo cha kiumbe vyenye kuishi linafahamika kwa hisia na kulitumia (neno hilo bawa) kwa vitu visivyo vya hisia ni kiasi cha kutaka kuileta picha yake katika akili (kwa kuvifananisha na vitu) vya kihisia.679

Anachokisema Sheikh Al-Khalili, kwa ufupi, ni kuwa madai ya Al-Imam Ibn Al-Qayyim hayana ushahidi katika lugha ya Kiarabu, bali ni kinyume na ushahidi mwingi uliomo katika lugha ya Kiarabu. Na lau hakukuwa na ushahidi mwengine wowote ule isipokuwa Hadithi hio ya Mtume (s.a.w.) inayosema: “.. سمعت أذن وال رأت عين ال ما Humo (Peponi)) ”فيهاkuna mambo ambayo jicho halijapata kuona wala sikio halijapata kusikia”, basi ungelitosha kubainisha ubatili uliomo katika madai ya Ibn Al-Qayyim. Kwani katika Hadithi hii mumetajwa neno jicho na neno sikio bila ya kutegemezwa na mwahala mwake yaani bila ya kusemwa “Jicho la binaadamu na sikio la binaadamu”. Na pamoja na hayo, imefahamika kwamba linalokusudiwa ni jicho la kweli na sikio la kweli. Hio – kwa mukhtasari680 – ndio jawabu aliojibiwa Ibn Al-Qayyim kwa madai yake hayo. Nayo inatosha kwa mwenye kutaka kutafuta ukweli.

Na kwa ziada ningependa kusema kwamba matumizi kama hayo ni mashuhuri kwa Waarabu ambapo wao huyatumia majina ya viungo bila ya kuyategemeza na mwahala mwake sawa ikiwa matumizi hayo ni ya kimajazi au ni ya hakika. Anasema Mtume (s.a.w.): “ يد ”المسلمون(Waislamu ni mkono).681 Utaona kwamba neno mkono hapa limetumika

اإلضافة عن hali ya kuwa halikutegemezwa na kitu nalo مجردةlimetumika kimajazi, na maana ni kuwa Waislamu ni kitu kimoja wanasaidiana. Na anasema Mtume (s.a.w.) katika Hadithi sahihi: العليا اليد

السفلى اليد من .(Mkono wa juu ni bora kuliko mkono wa chini) خيرYaani mwenye kutoa sadaka ni bora kuliko mwenye kupokea. Na Waarabu wa leo na wa kale husema: يد فالنلإن الفقه وقدما طولى افي Hakika fulani kwenye fiq-hi ana mkono mrefu na mguu) راسخةuliozama). Hapa mkono na mguu imetajwa bila ya kutegemezwa na sehemu zake: haikusemwa: “mkono au mguu wa binaadamu” na yote yametumika kimajazi kwa maana ya uwezo yaani mtu huyo ni mwenye uwezo mkubwa katika elimu ya fiq-hi. Wala usiniambie kwamba maana ya “mkono na

679 - Al-Imamu Badru Al-Din Al-Khalili Jawahiru Al-Tafasir: Juz’u Khaas uk. 191-193. 680 - Nimeikatakata jawabu hii kwa ajili ya kufupisha. 681 - Al-Rabi’u bin Habib Al-Jami’u Al-Sahih j. 4, uk. 354, Hadithi na. 903. Anasema mtiaji maelezo: “Kaitaja pia mwenye kitabu Kanzu Al-’Ummal uk. 441,442,443.

208

Page 209: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

mguu wa binaadamu” inafahamika kwa kutajwa kwa maneno “yeye ana mkono na mguu” kwani tunasema kwamba mkono na mguu wa binaadamu hapa sio iliokusudiwa, vyenginevyo isingelisemwa kuwa “ana mkono mrefu kwenye fiq-hi au mguu uliozama kwenye fiq-hi” kwani inaeleweka kwamba mkono haurefuki kwenye fiq-hi wala mguu hauzami kwenye fiq-hi.

Ama mfano mwengine wa kutumika kwa majina ya viungo pasina kutegemezwa na mwahala mwake na ikawa vimekusudiwa viungo vya kweli, ni Aya ya Qur-ani inayosema:

واألنف بالعين والعين بالنفس النفس أن فيها عليهم وكتبنان باألذن واألذن باألنف ن والس بالس

Tuliwaandikia juu yao humo (katika Taurati) kwamba nafsi kwa nafsi; na jicho kwa jicho; na pua kwa pua; na sikio kwa siko; na jino kwa jino.682

Yaani mtu huuliwa kwa kuua mtu; jicho la mtu hutofolewa atapotofoa jicho la mtu mwengine n.k. Pamoja na hayo, lakini utaona kwamba viungo vyote hivyo vimetajwa اإلضافة عن hali ya kuwa havikutegemezwa na مجردةkitu navyo vinafahamika ni kitu gani na nini makusudio yake. Baada ya haya, utaona kwa uwazi udhaifu uliomo katika hoja ya Ibn Al-Qayyim akiigwa na Kasim Mafuta.683

Na mfano wa Aya hio, ni Aya inayosema:

العين رأي مثليهم يرونهم كافرة وأخرىNa (kundi) jengine ni lenye kukufuru (wakawa) wanawaona (Waislamu) kuwa ni mara mbili ya wao kwa uoni wa jicho. 684

Hapa neno jicho halikutegemezwa na sehemu yake: haikusemwa “Uoni wa jicho la binaadamu”, ilhali sote tunajua kwamba hayo ndio makusudio.Na mifano myengine ni Aya kama:

دور تخفي وما األعين خائنة يعلم الص (Allah) anaijua khiyana ya macho na yale

682 - Sura 5, Aya 45. 683 - Cha kusikitisha ni kuwa Kasim Mafuta yeye anawaambia watu kwamba wanawafuata Mashekhe wao tu bila ya kuhakiki: wakikosea nao wanakosea, wakati yeye kitabu chake kizima ni kufuata tu yasemwayo japo kuwa yana makosa ya wazi kama unavyojionea mwenyewe humu. 684 - Sura 3, Aya 13.

209

Page 210: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

ambayo vifua (mioyo) imeyaficha.685

Na Aya:

األعين وتلذ األنفس تشتهيه ما وفيها Na humo (Peponi) kuna kila yale ambayo nafsi

inayapenda na macho yanayafurahia.686

Na Aya:

وم شجرة إن ق البطون في يغلي كالمهل** األثيم طعام** الزHakika ya mti wa zaqqumi**Ni chakula cha waovu**Kama shaba ilioyayushwa inachemka katika matumbo.687

Na Aya:واعية أذن وتعيها تذكرة لكم لنجعلها

Ili tuifanye kuwa ni ukumbusho kwenu na ili sikio lenye kusikia lisikie.688

Na Aya:

األقدام به ويثبت قلوبكم على وليربط…Na ili (Allah) aifunge mioyo yenu (aipe nguvu) na kwayo (maji ya mvua) aithibitishe miguu. 689

Sasa je bwana Kasim Mafuta bado wewe hujafahamu nini makusudio ya maneno: “Macho, vifua, matumbo, sikio, miguu, nyuso na mioyo” yaliotajwa katika Aya hizi kwa sababu haikusemwa: “Macho ya binaadamu au ya majini; vifua vya binaadamu au vya majini; matumbo ya binaadamu au ya majini; sikio la binaadamu au la jini; miguu ya binaadamu au ya majini n.k.?”

685 - Sura 40, Aya 19. 686 - Sura 43, Aya 71.

687 Sura 44, Aya 43-45. 688 - Sura 49, Aya 12.

689 - Sura 8, Aya 11. Aya nyengine ni Aya kama: نطمس أن قبل من......... ة ي�وم وأنذرهم…أدبارها على فنردها وجوها إذ اآلزف�........ الحناجر لدى القلوب

مع إن…..القلوب تطمئن الله بذكر أال...... ر الس ؤاد والبص� ك�ان أولئك ك�ل والف� عنه يخافون……………..مسئوال واألبصار القلوب فيه تتقلب يوما

Aya hizi zimetaja viungo (nyuso, migongo, myoyo, koo, masikio, macho, vifua) bila ya kuvitegemeza mwahala mwake, lakini bila ya shaka kimefahamika vyema nini kilichokusudiwa kwavyo.

210

Page 211: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Na miongoni mwa dalili hizo ni kauli ya Al-Imamu ‘Ali bin Abi Talib (k.w.), aliposema:

** يا تنظري وال اللحظات إحبسي لعيني بالسرقات عينأقولNinaliambia jicho langu jizuie kidogo**Wala

usiangaliye ewe jicho kwa wizi.690

Hapa jicho limetumika katika maana yake ya uhakika. Na lafdhi ya pili ya jicho, haikutegemezwa na mahala pake. Naam! Mtu anaweza kudai kwamba jicho la pili limefahamika kwa qarina ya jicho la kwanza.691 Ninasema: huo sio mjadala wetu: mjadala wetu ni kuwa je maana ya kiungo huwa haifahamiki hadi kitegemezwe na mwenyewe (yaani hadi isemwe jicho la mtu) au kinafahamika?

Na kwa hivyo, utaona kwamba Ibn Al-Qayyim mwenyewe pamoja na kukataa kwake kuwepo kwa majazi lakini vitabu vyake vimejaa majazi tena wakati mwengine huyataja kwa uwazi kama tutavyomnukuu baadae.

Ama kuhusu majazi ya mikono yasiotegemezwa na mwahala mwake, Ibn Al-Qayyim anafungua kitabu chake kwa kusema:

** يدان ذاك بفسخ للصدود ما األركان ثابت المحبة حكم

Hukumu ya mapenzi, nguzo zake ni imara**Upingaji692

hauna mikono miwili ya kubomoa hilo.693

Anasema mshereheshaji: Na mikono miwili ni uwili wa (neno) mkono, kwa maana ya uwezo.694 Sasa vipi tena Ibn Al-Qayyim anapinga majazi? Huku si kujigonga ambako kunaonesha kwamba hana hoja sahihi, bali anakimbia kuanguka kwa itikadi yake?

Anaendelea Sh. Kasim Mafuta kwa kusema:

HOJA YAO YA PILI

690 - Al-Imamu ‘Ali Diwaanu ‘Ali uk. 52. 691 - Halkadhalika mtu anaweza akadai hivyo kuhusu baadhi ya Aya tulizozinukuu hapa. Na jawabu yetu ni moja kama hii tulioitoa hapa. 692 - Maana ya neno kwa neno ni “uzuiaji”, lakini ufasaha wa Kiswahili ni kusema “upingaji”. 693 - Ibn Al-Qayyim Al-Nuniyya j. 1, uk. 16. 694 - Muhammad Khalil Harras Sha-hu Al-Nuniyya j. 1, uk. 16.

211

Page 212: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Itifaki iliyopo baina ya maulamaa wa lugha ya kiarabu kwamba mtu anaweza akayapinga maneno ambayo yanadaiwa kuwa ni majazi. Na kwa wakati huo huo akawa huyo mpingaji ni mkweli na yule mwenye kudai kuwa maneno hayo ni majazi pia akawa ni mkweli. Kwa mfano mtu akisema kwa kutumia majazi:

“Nimemuona simba ameshika upanga” akiwa anamkusudia mtu shujaa, kama akitokea mtu mwingine akisema huo ni uwongo! Huyo uliemuona wewe si simba, bali ni mtu shujaa, anakuwa huyu mwenye kutumia majazi ni mkweli na wakati huo huo huyu aliyepinga naye pia ni mkweli!

Kwa sababu hiyo wakasema wenye kupinga majazi: Kwa mujibu wa itifaki hiyo ni kwamba mtu akisema kwamba ndani ya Qur’an kuna majazi atakuwa moja kwa moja ameshasema kuwa ndani ya Qur’an kuna vitu ambavyo kuna uwezekano wa mtu akasema kuwa ni uwongo na akawa huyo msemaji kwa wakati huo ni mkweli! Na bila shaka hilo si sahihi kwa itifaki ya waislamu wote, kwa sababu wamekubaliana waislamu wote duniani tangu hapo kale hadi sasa kwamba hakuna kitu chochote ambacho kiko ndani ya Qur’an kinachofaa kukipinga bali ukiipinga herufi moja tu utakuwa tayari umekufuru. 695

Ninasema: tazama watu walivyokuwa wachache wa kufahamu hawa! Hoja inasema:

Itifaki iliyopo baina ya maulamaa wa lugha ya kiarabu kwamba mtu anaweza akayapinga maneno ambayo yanadaiwa kuwa ni majazi. Na kwa wakati huo huo akawa huyo mpingaji ni mkweli na yule mwenye kudai kuwa maneno hayo ni majazi pia akawa ni mkweli.

Sasa ikiwa huyu ni mkweli na yule ni mkweli, kwanini tena unakanusha kuwa kuna majazi na huyu ni mkweli? Na kwanini pia usimpinge yule aliyekanusha kama huyu aliyethibitisha ni mkweli? Na ukiwa utampinga huyu aliyekanusha ni kwa nini umpinge naye ni mkweli? Ninasema: haiwezekani mtu mmoja akanushe kuwepo kwa kitu na mwengine adai kuwepo kwa kitu hicho hicho na wote wawe wakweli isipokuwa kutakuwa na hali mbili au moja ya mbili:

1) Mmoja wao atakuwa yuko sahihi na mwengine kakosea.2) Wawe hawajafahamiana: huyu anakusudia kitu kimoja; na yule

anakusudia kitu chengine kama nitavyozidi kukubainishia.

Kwa hivyo, kama umelifahamu hilo basi utakuwa umefahamu kwamba kuwaita watu hao wote kuwa ni wakweli ni kwa sababu aliyesema kwamba

695 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 44-45.

212

Page 213: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

neno simba katika jumla ya maneno isemayo “Nimemuona simba ameshika upanga” si simba, basi makusudio yake ni kuwa huyo si simba wa kweli ambaye ni mnyama; na aliyemwita huyo kuwa ni simba basi makusudio yake pia ni kuwa huyo si simba mnyama bali ni mtu mwenye sifa ya simba ambayo ni sifa ya ushujaa, na kwa hivyo naye anakusudia kuwa huyo si simba wa kweli bali ni simba majazi. Kwa hivyo, hao tafauti zao ni lafdhiy za kimatamshi: si za uhakika. Kwani wote wanakubaliana kwamba huyo aliyeonekana kakamata upanga si simba wa kweli bali ni shujaa. Sasa upinzani uko wapi na nukta na logic (akili) iko wapi? Yaa Nas! Tusiwe wenye kufuata kama bendera: fulani kanena na miye nanena bila ya hata kufikiri vizuri. Madai hayo yote bado hayajabomoa kuwepo kwa majazi madamu uhakika wake upo tunauona.

Anaendelea Sh. Kasim Mafuta kwa kusema:

Na hii itikadi ya kuwepo kwa Majazi ndani ya Qur’an inawafungulia watu mlango wa kuliingia jambo hilo la hatari. Kwa mfano, pale aliposema Allah:

والملك ربك وجاء صفا صفا“Na akaja Mola wako na Malaika safu safu “.696

Baadhi ya watu wakaigeuza maana ya aya hii wakasema hapana, hatakuja Mola Muumba wa kila kitu, bali itakuja amri yake! Kwa madai kwamba eti kuna “Majazul-Hadh’fi” majazi ya kuondosha kwa hiyo kuna kitu kimeondoshwa. Na kitu kilichowapa ujasiri wa kukana kwao kuja kwa Allah siku ya Qiyama ni pale walipofunguliwa mlango huo na hicho kitu kiitwacho “Majazi”. Kwa mfano, ukiwauliza kwa nini mmekimbilia kuitakidi kwamba hapo kuna majazi? Na hali yakuwa majazi si asili na hairuhusiwi kuiwacha asili na kukimbilia kwenye majazi mpaka itakapo shindikana maana ya asili? Wanadai kuwa asili imeshindikana, kwa sababu Allah hawezi kuja, na kitendo cha kuja kinaonyesha kuwa Allah ana mahali na hiyo ni sifa ya kiwiliwili, na kumpa Allah sifa hiyo ni kumfananisha na viumbe na kufanya hivyo ni kufru!!!

Madai haya si sahihi, kwa sababu kwanza, inatakiwa kukithibitisha kile ambacho Allah amejithibitishia nafsi yake kama anavyo stahiki, pamoja na kumtakasa na kufanana na viumbe, kama tutakavyo lifafanua suala hili mahali pake Inshaallah. Mwisho wa kunukuu.697

Ninasema: hilo la kubatilika kwa itikadi yenu ndilo munalolihofia kama ulivyosema mwenyewe: “Na hii itikadi ya kuwepo kwa Majazi ndani ya 696 - Suratul-Fajri (89) aya ya 22. 697 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 45-46.

213

Page 214: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Qur’an inawafungulia watu mlango wa kuliingia jambo hilo la hatari”. Sasa ninachotaka kukwambia hapa ni kuwa batili haiondoshwi na batili; na maradhi hutibiwa kwa dawa sio kutibu maradhi kwa maradhi. Ikiwa kuna Aya watu wameipotoa – kama unavyodai – kwa kutumia majazi, basi hilo la kuyakanusha majazi halijawa dawa, kwani majazi yamethibiti kwa Qur-ani, Sunna na lugha ya Kiarabu. Dawa ni kubainisha tu kwamba katika Aya hio hakuna majazi. Ama kuyakanusha majazi kwa kuhofia kuanguka kwa itikadi yako, basi ni sawa sawa na mtu anayefanya jaribio la kutibu ugonjwa kwa kutumia ugonjwa mwengine; au anayerekebisha batili kwa kutumia batili nyengine?

Ama Aya isemayo:

والملك ربك وجاء صفا صفاNa akaja Mola wako na Malaika safu safu.698

Aya hii ni kweli jumhur ya wanavyuoni hawakusema kwamba Allah atakuja kweli kweli, bali hio ni kauli yenu na Maimamu wenu munaowafuata nyinyi. Hata hivyo, nao pia wamegongana katika kuifasiri Aya hio. Anasema Ibn Taymiyya akiwanukuu Mahanbali wenzake:

Na miongoni mwa (sababu) hizo, ni kwamba ikiwa (itikadi ya kuwa Allah ana) kiwiliwili itakataliwa kwa uwazi, basi italazimu kuikataa (itikadi ya kuwa Allah anafanya) harakati, kwa hivyo, ikiwa (harakati) zitakataliwa kwa uwazi, itakuwa vigumu (kuithibitisha) ile sifa ya mkusanyiko (wa siku ya kiama) iliokuja kwamba Allah atawachomozea (atawajia) watu wa siku ya kiama. Na kwamba Yeye (Allah) mwenyewe ndiye hasa atayewafanyia hisabu zao, kama alivyosema: “Na akaja Mola wako na Malaika safu safu”.699

Hayo ni maelezo ya Ibn Taymiyya akiwanukuu Mahanbali wenzake. Ama Ibn Al-Qayyim, yeye anasema:

Na kuja kwake (Allah siku ya kiama) si kufanya harakati wala si kuondoka (huko aliko) wala kubadilika kwani hayo ni pale ambapo mwenye kuja akiwa ni kiwiliwili au johari (kitu chenye kuchukua nafasi). Ilipothibiti kwamba yeye si kiwiliwili wala si johari wala si kitu chenye kufahamika (kwa akili tu) ambacho hakionekani wala kushikika (عرض);

698 - Suratul-Fajri (89) aya ya 22. 699 - Ibn Taymiyya Bayaanu Talbisi Al-Jahmiyya j. 1, uk. 27.

214

Page 215: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

basi haikulazimika kwamba kuja kwake kuwe kwa harakati wala kuondoka.700

Kisha baada ya kunena hivyo, Ibn Al-Qayyim akapiga mifano inayofuata, akatongoa hivi:

Na lau ulizingatia hayo kwa kauli yao (Waarabu wanaposema) fulani kiama chake kimemjia ( قيامته فالنا جاءه ) na mauti yamemjia ,(جاءت) na maradhi yamemjia ;(الموت المرض na yaliofanana na hayo ,(جاءهkatika yale ambayo yapo, yanaingia kwake wala hayana mjo (wa kweli kweli) basi hilo lingelikubainikia.701

Na bila shaka hili alilolisema Ibn Al-Qayyim hapa ni jambo sahihi kabisa, kwani neno جاء kuja katika lugha ya Kiarabu na katika Qur-ani, kama vile lilivyotumika kwa kitu chenye kuja kweli kweli, pia limetumika likitegemezwa katika mambo ambayo hayaji kweli kweli, yaani mambo ambayo hayana sifa ya kuhama kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyengine. Na wala hakuna qarina isipokuwa ‘aqliyya, yaani yale yanayofahamika kiakili tu, na kwa hivyo, qarina ni haliyya hali halisi ilivyo au inayofahamika tu katika maneno. Mfano wa hayo ni kama Aya inayosema:

الموت أحدهم جاء إذا حتىMpaka mauti yakimjia mmoja wao.702

Na bila shaka mauti hayaji mjo wa uhakika yaani hayatoki sehemu moja kwenda nyengine, bali ni hali ambayo mtu inamfikia katika nafsi yake ambapo kiwiliwili chake kinatengana na roho yake. Ama kutoka sehemu moja kwenda nyengine, hii si sifa ya mauti bali ni sifa ya malaika wa mauti. Na kilichozuia tusiizingatie maana ya asili ya neno jaa (kuja) katika Aya hio Mpaka mauti yakimjia mmoja wao ni kile kinachofahamika kiakili kwamba mauti si kiwiliwili hata ikajuzu kuwa kifanye harakati ya kuhama kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyengine.

Kama umelifahamu hilo, basi utakuwa umeelewa kwamba neno jaa (kuja) lililomo katika Aya: “Na akaja Mola wako na Malaika safu safu” ni lazima lifasiriwe kwa mujibu wa alivyo yule ambaye neno hilo limetegemezwa kwake naye ni Allah; kama vile ambavyo linafasiriwa neno hilo hilo katika Aya Mpaka mauti yakimjia mmoja wao kwa mujibu wa yalivyo yale ambayo neno hilo limetegemezwa kwake nayo ni mauti. Kwa

700 - Ibn Al-Qayyim Ijtima’u Al-Juyush uk. 88. 701 - Ibn Al-Qayyim Ijtima’u Al-Juyush uk. 89. 702 - Sura 23, Aya 99.

215

Page 216: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

maana nyengine ni kuwa, kama vile ambavyo Aya inasema kwamba mauti yanakuja ilhali hayaji mjo wa uhakika bali ni hali inayomfikia mtu tu kwa sababu mauti si kiwiliwili; basi vivyo hivyo neno kuja lililomo katika Aya inayosema: “Na akaja Mola wako na Malaika safu safu” linafasiriwa kuwa kuja huko kwa Allah si mjo wa kweli kweli ambao ni kuhama kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyengine kwani Allah si kiwiliwili. Kwa ubainifu zaidi ni kuwa, maana ya asili, ya uhakika na ya kweli kweli ya neno kuja katika lugha ya Kiarabu – na nyenginezo – ni kufanya harakati za kuondoka kutoka sehemu hadi sehemu. Na hili ni muhali kwa Allah ambaye:

1) Hana mfano katika dhati yake wala katika sifa zake.2) Ambaye hahitaji chochote katika ulimwengu wala hamuhitajii

yoyote katika walimwengu bali amri yake anapotaka jambo husema kua nalo likawa; na ni mwenye uwezo wa moja kwa moja (

مطلقة .(absolute power قدرة

Na wala kuifasiri Qur-ani hivyo si kuyakataa maneno ya Allah alioyasema, bali ni kutafuta nini Allah kakikusudia katika usemi wake. Nasi tumelazimika kufasiri hivyo kwa sababu zile zile tulizozieleza kabla kwamba lugha ya Kiarabu ina migawanyiko miwili tu:

1) Hakika.2) Majazi.

Na kila neno la Kiarabu linakuwa na maana yake ya uhakika inayotumika katika lugha. Sasa mtu anapolifasiri andiko anatakiwa kwanza atazame je nini maana ya uhakika ya neno hilo katika lugha ya Kiarabu. Kisha baada ya kuipata hio maana ya uhakika ya neno hilo, ndio aitazame tena je maana hio ya uhakika inawezekana kusifiwa kwayo yule ambaye neno lenye maana hio limehusishwa naye? Ikiwa haiwezekani bila ya kuliletea neno hilo ta-awil, basi neno hilo huwa limetumika kimajazi na hapo inabidi zitazamwe maana zake za kimajazi. Kwa msingi huu basi, kama maana ya kuja katika lugha ni kuhama kutoka sehemu moja kwenda nyengine, basi kuja ni sifa ya kiwiliwili kama alivyosema Ibn Al-Qayyim. Na kwa vile Allah si kiwiliwili basi huwezi kusema kwamba atakuja yeye mwenyewe kwa uhakika. Ukiniambia: “Atakuja kwa uhakika unaowiyana na utukufu wake”. Nitakujibu kwamba Allah kaiteremsha Qur-ani kwa lugha ya Kiarabu. Na lugha aliotuhubiria sisi kwayo ni lugha ile ile ya Waarabu wenyewe wanaoielewa. Na Waarabu hawana kwao maana ya kuja kwa hakika isipokuwa kuondoka sehemu moja kwenda nyengine. Vyenginevyo inakuwa kuja kwa maana ya kimajazi. Kwa mfano linapokuja jeshi la Zaid, basi Waarabu wanaweza wakasema kimajazi: زيد yaani jeshi ,(Zaid kaja) جاءlake limekuja: si yeye mwenyewe; au imekuja habari yake. Na lugha hii, kama vile ambavyo Waarabu walikuwa wakiitumia hapo kale, basi ndivyo

216

Page 217: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

wanavyoitumia leo hii. Hadi leo hii basi utawasikia Waarabu wakisema: العراق بوش جوج yaani jeshi lake ,(Gorge Bush kaingia Iraki) دخل

limeingia Iraki: si yeye mwenyewe. Au العراق بوش جوج يوم جاء منذ (Tangu siku Gorge Bush aliokuja Iraki), yaani tangu siku jeshi lake lilipokuja. Na mfano wa hili ni kama Hadithi Qudsi inayosema:

هرولة أتيته يمشي أتاني فإن(Allah anasema: Mja wangu) akinijia naye anakwenda kwa miguu

(mwendo wa kawaida) basi mimi ninamjia mbio.

Ni wazi kwamba kuja kwa Mungu kulikotajwa hapa ni majazi, kwa sababu ya kuwepo qarina inayosema “mja wangu akinijia”, kwani hakuna mtu anayefunga safari ya uhakika akaenda kwa Allah kwa miguu; kama vile ambavyo hatujapata kusikia kwamba kuna mtu kajiwa na Allah kwa uhakika.

Baada ya hayo, sasa tazama kauli ya Al-Imamu Ahmad bin Hanbal. Sheikh Abdullah Al-Harari katika kitabu chake Al-Maqalatu Al-Sunniyya ananukuu yafuatayo:

Amesema Al-Bayhaqi katika manaqib703 ya Ahmad: “Katwambia Al-Hakim katuhadithia Abu ‘Amri bin Simak katuhadithi Hanbal bin Is-haaq kasema nimemsikia ami yangu Aba ‘Abdillah yaani (Al-Imamu) Ahmad anasema: ‘walinitolea hoja siku hio, yaani siku aliojadiliwa katika nyumba ya amiril-Mu-uminin, wakasema: ‘Suratul Baqara itakuja siku ya kiama na itakuja Suratu Tabarak. Basi (Mimi Ahmad bin Hanbal)704 nikawambia: ‘Hizo (zitazokuja) ni thawabu (za sura hizo: sio Sura zenyewe)”, Allah amesema: ربك وجاء (Na akaja Mola wako), yaani utakuja uwezo wake, hakika ya Qur-ani ni mithali (mifano) na mawaidha.

Na akasema Al-Bayhaqi:

Katika haya kuna dalili kwamba yeye Ahmad alikuwa haitakidi kuwa kuja (kwa Allah) ambako kumetajwa katika Qur-ani; na kushuka (kwa Allah) kulikotajwa katika Sunna ni kuondoka kutoka katika sehemu moja kwenda nyengine kama dhati za viwiliwili zinavyokuja na kushuka. Bali huko (kuja kwa Allah) maana yake ni kudhihiri ishara zake na uwezo wake, kwani wao (hao waliojadiliana na Al-Imamu Ahmad) walipodai kwamba Qur-ani lau ilikuwa ni maneno ya Allah na ni sifa katika sifa zake basi isingelijuzu kwake kuwa ije. (Hapo ndipo) Abu Abdillah (Al-Imamu Hanbal) alipowajibu kwamba kinachokuja ni thawabu za kisomo ambacho

703 - Habari zake njema. 704 - Al-Imamu Ahmad.

217

Page 218: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

anataka kukidhihirisha siku hio. Basi kule kukidhihirisha kwake akakuita kuwa ni kuja.705

Sasa baada ya hayo, Sheikh Kasim Mafuta anaweza kuchagua kauli anayoitaka na kuiita kuwa ndio kauli ya Al-Salafu Al-Salih au kauli ya Ahlu Sunna:

1) Kauli ya Ibn Taymiyya anayoinukuu kutoka kwa Mahanbali wengine bila ya kuipinga, bali kwa kuipa uzito zaidi. Nayo ni kauli inayosema kwamba Allah atakuja siku hio ya kiama yeye mwenyewe; na kwa hivyo yeye ni kiwiliwili kwani tukikataa kuwa ni kiwiliwili kuna hatari ya kutoweza kuithibitisha sifa hio ya kuja kwa Mwenyezi Mungu!

2) Kauli ya Ibn Al-Aqayyim katika Ijtimaau Jayshihi. Nayo ni kuwa Allah atakuja lakini si kwamba ataondoka huko aliko kwani kuondoka kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyengine ni sifa ya kiwiliwili na Allah si kiwiliwili.

3) Kauli ya Al-Imamu Ahmad, kwamba makusudio ya Aya hio (Na akaja Mola wako), ni kudhihiri kwa uwezo wake kama vile ilivyosemwa kuwa Suratul Baqara itakuja siku ya kiama yaani yatadhihiri malipo ya sura hio.

4) Na labda chaguo la nne linaweza kuwa katika kauli nilioiona na ambayo inastaajabisha kwa jinsi kichwa chake kinavyogongana na miguu yake. Nayo ni kauli nilioisoma katika maelezo ya Dr. Muhammad Khalil Harras katika Sharhu Al-‘Aqidati Al-Wasatiyya. Anasema Dr. Harras:

. فهذه خلقه من بائن عرشه فوق وهو ويدنو وينزل يجيء سبحانه وهوسبحانه كلها له أفعال

الحقيقة على

Naye Allah Mwenye kutakasika na kila upungufu anakuja na anateremka na anakurubia (kuwakurubia viumbe wake); Naye yuko juu ya arshi yake kapambanuka kutokana na viumbe wake. Haya yote ni matendo ya Allah mtukufu (ambayo anayatenda) kwa uhakika (si kwa majazi).706

Tazameni mantiki hii! Mungu anakuja kweli kweli na anashuka kweli kweli, lakini yuko kule kule aliko kakaa juu ya kiti chake hajaondoka! Na anavikurubia viumbe vyake kweli kweli lakini yuko juu mbinguni mbali na viumbe wake! Sasa huku ndiko kuja kweli kweli na ndiko kushuka kweli kweli; na huko ndiko kukurubia kweli kweli. Labda kesho watu wa skuli hii, 705 - Al-Harari, Abdullah Al-Maqalatu Al-Sunniyya Fii Kashfi Dhalati Ibn Taymiyya uk. 115. 706 - Dr. Muhammad Khalil Haraas Sharhu Al-’Aqiidati Al-Wasatiyya uk. 55.

218

Page 219: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kwa ufahamu wao huu, watatwambia kwamba Allah anakaa katika shingo za watu mkao wa kweli kweli, lakini unaomfalia Yeye au unaomstahikia Yeye, kwani Qur-ani inasema:

الوريد حبل من إليه أقرب ونحنNa sisi tupo karibu naye zaidi kuliko mshipa wa shingo (yake).707

Mshipa wa shingo wa mtu uko ndani ya shingo yake. Na Allah anasema yupo karibu zaidi na mtu kuliko mshipa wake mwenyewe uliomo ndani ya shingo yake. Sasa tuseme – kwa msingi wa kukataa majazi na ta-awil au kwa msingi wa kuzifasiri Aya kwa mujibu wa dhahiri yake (literally) – Allah anakaa katika shingo za watu?

Au labda kesho kutwa watu wa skuli hio watatwambia kwamba mtu anapokufa basi Allah anahudhuria na anakuwa yupo karibu zaidi kuliko watu waliohudhuria hapo, kwani Qur-ani inasema:

( ونحن84) تنظ���رون حينئذ ( وأنتم83) الحلق���وم بلغت إذا فل���والتبصرون ال ولكن منكم إليه أقرب

Basi mbona (roho) inapofika katika koo**Nanyi wakati huo munatazama**Nasi tukaribu zaidi naye (huyo anayekufa) kuliko nyinyi lakini hamuoni.708

Sasa baada ya hayo, kwa upande wetu, tunaomuomba Sheikh Mafuta aturuhusu tumueleze kwanini tumeikubali tafsiri ya waliosema kuwa Aya hio: ربك وجاء (Na akaja Mola wako), kwamba haina maana ya kuwa Allah atakuja kweli kweli; bali itayokuja ni amri yake. Na katika kutoa kwetu maelezo hayo, itatubidi kutazama misingi miwili:

1) Kuifasiri Qur-ani kwa Qur-ani. Nayo ndio njia bora ya kumfahamu Allah anakusudia nini katika ujumbe wake.

2) Kuzitazama hoja za kiakili. Nazo zinakubalika ikiwa hazikugongana na andiko la wazi.

TAFSIRI YA QUR-ANI KWA QUR-ANI

Huu ndio msingi mkuu ambao wanavyuoni tangu zama za Masahaba walikuwa wakiutumia katika kuifahamu maana halisi ya Aya. Anasema Al-Imamu Ibn Taymiyya:

707 - Sura 50, Aya 16. 708 - Sura 56, Aya 83-85.

219

Page 220: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Ikiwa mtu atakuuliza, ni njia gani iliobora katika kuifasiri Qur-ani? Basi jawabu ya (suali) hilo ni kuwa njia sahihi zaidi katika hayo, ni kuwa Qur-ani ifasiriwe kwa Qur-ani, kwani kilichotajwa bila ya kufafanuliwa katika sehemu moja, hakika yake hufasiriwa katika sehemu nyengine. Kilichofupishwa katika sehemu moja basi huelezwa kwa urefu katika sehemu nyengine.709

Anasema Al-Imamu Badru Al-Din Al-Khalili Al-Mufassir:

…Ya kwanza ni Qur-ani yenyewe; hakika ya kitu bora kilichotumika katika kuifasiria Qur-ani ni Qur-ani yenyewe. Aya ngapi hazina ufafanuzi kisha ufafanuzi wake ukafunuliwa katika Aya nyengine. Na mara ngapi ujumla wa Aya moja unahusishwa na Aya nyengine….710

Ama mifano ya Aya ambazo huwezi kuufikia usahihi wa tafsiri yake ila kwa kuzifungamanisha na Aya nyengine kwa sababu ya kuondoshwa neno katika Aya moja au kwa kukosekana ubainifu, ziko nyingi. Mfano mmoja katika mifano iliosemwa na baadhi yao ni Aya isemayo:

يعلمها ال الغيب مفاتح وعنده هو إال

Na kwake Yeye Allah kuna funguo za yaliojificha; hakuna azijuaye ila Yeye tu.711

Amepokea Al-Bukhari kutoka kwa Mtume (s.a.w.) kwamba kaifungamanisha Aya hio na Aya isemayo:

وينز اعة الس علم عنده الله تدري إن وما األرحام في ما ويعلم الغيث لم وم نفس غدا تكسب ا ���اذا

خبير عليم الله إن تموت أرض بأي نفس تدري

Hakika ya Allah anao ujuzi wa saa (ya Kiama kitakuwa wakati gani) na anateremsha mvua na anakijua kilichomo katika matumbo ya uzazi; na nafsi haijui (hata) nini itakichuma kesho; wala nafsi haijui itakufa katika ardhi gani; hakika Allah ni Mjuzi, Mwenye habari (ya kila kitu).712

709 - Al-Harrani, Ibn Taymiyya Al-Nukatu Al-Mutammima uk. 89. 710 - Al-Khalili, Ahmad bin Hamad Jawahiru Al-Tafasir j. 1, uk. 20. 711 - Sura 6, Aya 59. 712 - Sura 31, Aya 34.

220

Page 221: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Na kwa hivyo, Mtume (s.a.w.) akasema katika Hadithi hio: “Funguo za yaliojificha ni tano” kisha akasoma Aya hio tulioinukuu.713 Na kwa tafsiri hio iliopokewa katika Hadithi, basi maana ya funguo za yaliojificha ambayo yametajwa katika Aya 59 ya Sura ya 6, ni mambo hayo matano yaliotajwa katika Aya 34 ya Sura ya 31.

Na msingi huu wa kuifasiri Qur-ani kwa Qur-ani, utawakuta wanavyuoni wengi wamekwenda nao katika tafsiri zao. Mara ngapi utakuta katika tafsiri – kama ya Ibn Kathir – ikisemwa: “Aya hii ni kama Aya kadha”. Abu Hayaan, kwa mfano, kawapinga waliodai kuwa maana ya neno طائف taaifu lililotajwa katika Aya ya Qur-ani isemayo: طائف عليها فطاف

ربك من fataafa ‘alaihaa taaifum Rabbik, “Basi (shamba hio) ikatokewa na taaifu (tukio) juu yake litokalo kwa Mola wako,”714 kawapinga Abu Hayyaan waliodai kuwa maana ya neno hilo taaifu ni mahususi kwa tukio la usiku. Abu Hayyaan kawakatalia dai hilo kwa sababu Allah kasema katika Aya nyengine ya Qur-ani: وا الذين إن هم إذا اتق�� من ط��ائف مس�� يطان inna الش�� lladhina ttaqaw idhaa massahum taaifun mina shaytaan…. (Hakika wale wenye kumcha (Allah) basi taaifu (pepesi)715

ya shetani ikiwagusa…….).716 Anasema Abu Hayyaan kwamba hapa neno taaifu limetumika kumaanisha tukio la pepesi za shetani, nazo hazimpati mtu wakati wa usiku tu; bali hata mchana pia humsibu.

Halkadhalika Aya isemayo: حسنات سيئاتهم الله يبدل فأولئك “Basi hao Allah huyabadilisha mabaya yao (na kuyafanya) mema”717

wanavyuoni wengine wa tafsiri wameifungamanisha Aya hio na Aya nyengine yenye kusema: بدل ثم ظلم من إال وء بع��د حسنا ف��إني س��

رحيم غف��ور “Isipokuwa aliyedhulumu (aliyeidhulumu nafsi yake) kisha akabadilisha (na kufanya) mema baada ya maovu, basi Mimi ni Mwenye kusamehe sana; Mwenye kurehemu sana”.718 Wengine wamezifungamanisha Aya mbili hizi na wakasema kwamba makusudio ya kuyabadilisha maovu na kuyafanya kuwa ni mema si kwamba madhambi yake yanageuzwa kuwa thawabu; bali ni kuwafikishwa kwake kufanya mema akawa sasa anafanya mema badala ya mabaya aliokuwa akiyafanya.

713 - Al-Bukhari Al-Sahih Hadithi na. 4778. Kwa maelezo zaidi tazama Fat-hu Al-Bari j. 9 uk.5531, katika sherehe ya Hadthi hio. 714 - Sura 68, Aya 19. 715 - Yaani tukio vile vile; hapa ni tukio lenye kutokana na shetani kwa hivyo wajuzi wa lugha wamelifasiri “pepesi”. 716 - Sura 7, Aya 201. 717 - Sura 25, Aya 70. 718 - Sura 27, Aya 11.

221

Page 222: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Halkadhalika Aya inayosema: شيء بكل الله وكان محيطا (Na Allah kakizunguka kila kitu).719 Na Aya: محيط ورائهم من والله (Na Allah yuko nyuma yao kawazunguka).720 Aya hizi na zilizo mfano wa hizi, ikiwa utazichukua kwa udhahiri wake na ukatumia msingi wa balkafa (bila ya namna), basi utapata natija kwamba Allah kakizunguka kila kitu kweli kweli. Kisha unaweza ukatumia falsafa ya balkafa ukasema:: “lakini mzunguko unaomstahikia Yeye: si kama tunavyozunguka sisi”. Lakini ikiwa utakwenda na msingi wa kuifasiri Qur-ani kwa Qur-ani na ukazifungamanisha Aya hizo na Aya isemayo: بكل أحاط قد الله وأن

شيء علما (Na kwamba Allah kakizunguka kila kitu kwa ujuzi (kwa kukijua)),721 basi utaipata tafsiri au maana ya “Allah kukizunguka kitu” ambayo imetajwa katika Aya nyengine. Na kwa hivyo, maana ya Allah kukizunguka kila kitu – kwa mujibu wa mjumuiko huu wa Aya za Qur-ani – ni kuwa kakizunguka kila kitu kiujuzi yaani anakijua kila kitu kiukamilifu.

Halkadhalika Aya ya Qur-ani inayosema: الله في وجاهدوا (Na fanyeni jihadi katika Mwenyezi Mungu),722 ni Aya ambayo ndani yake kuna neno lililoondoshwa. Na neno hilo lililoondoshwa utalijua kwa kuitazama Aya nyengine inayosema: الله سبيل في وجاهدوا (..Na wakafanya jihadi katika njia ya Allah).723 Kwa hivyo, neno sabil (njia kwa maana ya dini) ndilo lililoondoshwa katika Aya ya mwanzo na limeweza kubainika kwa msada wa Aya hio ya pili. Halkadhalika katika Aya inayosema: “Na akaja Mola wako…”, tumeweza kujua kwamba neno amr (jambo) ndilo lililoondoshwa kwani ndilo lililotajwa katika Aya nyengine za Qur-ani, kama vile Aya inayosema ينظرون هل يأتي أو المالئكة تأتيهم أن إال

ربك أمر Hawana wanachokisubiri isipokuwa kujiwa na Malaika au iwajie amri (jambo) ya Mola wako.724

Na kwa msingi huo wa kulifungamanisha andiko moja na jengine ndio wanavyuoni wa jumhur wameweza kutoa natija kwamba katika Aya hio “Na akaja Mola wako…” kuna majazu hadhfi yaani majazi ya kuondoshwa neno, na kwamba neno lenyewe lililoondoshwa, kama tulivyosema, ni neno amri (jambo). Na hili la kuwepo kwa majazu hadhfi yaani majazi ya kuondoshwa neno katika Aya za Qur-ani si jambo geni: Aya kadha wa kadha zimekuja katika mfumo huo. Kwa mfano, Aya ya Qur-ani isemayo: هافي كنا التي القرية لئوس “Na kiulize kijiji ambacho

719 - Sura 4, Aya 126. 720 - Sura 85, Aya 20. 721 - Sura 65, Aya 12. 722 Sura 22, Aya 78.

723 - Sura 2, Aya 218. 724 - Sura 16, Aya 33. Maelezo kwa urefu juu ya Aya hizi yatakuja baadae in shaa Allah..

222

Page 223: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

tulikuwemo ndani yake”,725 ndani yake kuna majazu hadhfi, na asili yake Aya hio ni kusema: فيها أهل لئوس كنا التي القرية “Na waulize watu wa kijiji ambacho tulikuwemo ndani yake”, vyenginevyo kijiji hakiwezi kuulizwa kwani hakisemi. Halkadhalika, kama tulivyoeleza hapo nyuma kidogo, mfano wa hilo ni Aya isemayo: الله في وجاهدوا (Na fanyeni jihadi katika Mwenyezi Mungu), ambapo utaona kwamba neno njia kwa maana ya dini katika Aya hii limeondoshwa, na asili yake ni: وجاهدوا

الله سبيل في (Na fanyeni jihadi katika njia (yaani Dini) ya Mwenyezi Mungu), kama Aya nyengine ilivyolibainisha hilo kwa kusema:

الله سبيل في وتجاهدون (…Na mufanye jihadi katika njia ya Allah).726

Kilichobaki ni kujua kwanini wanavyuoni wa jumhur wamedai kwamba katika Aya “Na akaja Mola wako…” kuna majazu hadhfi yaani majazi ya kuondoshwa neno na kwa upande mwengine kwanini wao wamelikadiria neno lililoondoshwa kuwa ni amri (jambo). Tunasema: Ama kwanini wanavyuoni wamedai kwamba katika Aya “Na akaja Mola wako…” kuna majazu hadhfi, ni kwa sababu ambazo tumezitaja kabla kwamba maana ya kuja kweli kweli katika lugha ni kuhama kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyengine. Na hili haliwezekani kwa Allah kwani:

a) Yeye si kiwiliwili, wakati kuja kwa namna hio ni sifa ya viwiliwili.

b) Yeye hahitaji kufanya harakati ili aweze kulifanya alitakalo, bali unatosha uwezo wake na elimu yake kufanya alitakalo kun fayakun, bila ya kukurupuka. Kama vile anavyowaruzuku viumbe wote wakati mmoja kwa elimu yake na uwezo wake bila ya kuwajia; ndivyo atavyowahukumu viumbe wake wote siku ya kiama wakati mmoja bila ya kuwajia.

c) Kuhitaji kwenda sehemu ili uweze kufanya kitu ni alama ya udhaifu na ukosefu wa uwezo kamili.

Ama kwanini wanavyuoni hao wamelikadiria neno hilo amri (jambo) na kwamba ndilo lililoondoshwa, ni kwa sababu tatu:

1) Aya nyengine zimetaja kuja kwa Allah wala huwezi kuzifasiri kuwa kuja huko ni kuja kwa uhakika.

2) Aya nyengine zimetaja kuja kwa amri (jambo) ya Mwenyezi Mungu.

3) Tukalazimika kuzifungamanisha hizi na zile ili kufikia maana sahihi.

725 - Sura 12, Aya 82. 726 - Sura 61, Aya 11.

223

Page 224: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

AYA ZA KUJA KWA MUNGU KIMAJAZI

Ama Aya zilizotaja kuja kwa Allah, bila kutaja ndani yake neno amri (jambo) lakini ikawa kulikadiria neno hilo ni lazima, ni Aya kama:

أطرافها من ننقصها األرض نأتي أنا يروا أولمJe hawaoni kwamba tunaijia ardhi tunaipunguza pembeni mwake.727

Lafdhi ya Aya hii inasema kwamba Allah anaijia ardhi ili kuipunguza pembeni (mipaka) mwake. Lakini je ni kweli kwamba Allah anaijia ardhi kwa hakika? Bila shaka kila mwenye akili – licha ya mwenye alimu – anadiriki kwamba kuja huku kwa Allah kulikotajwa hapa ni kuja kwa amri yake – uwezo wake, nguvu zake n.k.

Na mfano mwengine ni Aya isemayo:

عليهم فخر القواعد نم بنيانهم الله فأتى قبلهم من الذين مكر قدقف وأتاهم وقهم�ف من السيشعرون ال حيث من العذاب

Kwa hakika walifanya hila wale waliokuwa kabla yao, basi Allah AKAZIJIA nyumba zao katika misingi, basi mapaa yakawaangukia kutoka juu na adhabu ikawajia kutoka wasikokujua.728

Aya hii inazungumzia adhabu iliowafika baadhi ya makafiri. Miongoni mwa adhabu hizo ni kuwa Allah ALIKUJA AKAINGIA KWENYE MISINGI YA NYUMBA ZAO. Je hapa aliyekuja ni Allah akaingia chini ya misingi ya majumba au iliokuja ni amri yake pamoja na kuwa neno amri halikutajwa katika Aya hio? Ni wazi kwamba kule kuja kwa amri ya Mwenyezi Mungu ndiko kulikoitwa kuwa ni kuja kwa Mwenyezi Mungu. Na ibara za namna hii kwa Waarabu si ngeni. Waarabu husema: علي ilhali ,(Ali kaja) جاءhakuja yeye binafsi bali imekuja barua yake au jeshi lake au amri yake.

Mfano mwengine ni Aya isemayo:

لم حيث من الله فأتاهم الله من حصونهم مانعتهم أنهم وظنوا يحتسبوا

….Na wakadhania kuwa ngome zao zitawakinga kutokana na Allah, basi Allah AKAWAJIA kutokea wasikokufikiria.

727 - Sura 13, Aya 41. 728 - Sura 16, Aya 26.

224

Page 225: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Aya hii inazungumzia vita vya Waislamu na Mayahudi wa Banii Al-Nadhiir. Tunapata katika Aya hii kwamba Allah KAWAJIA Mayahudi hao kutokea katika sehemu ambayo wao hawakuitarajia. Je aliyekuja hapa ni Mwenyezi Mungu mwenyewe au ni adhabu ya Allah kupitia katika mikono ya waja wake?

Ukiniambia: “Lakini katika Aya hizi kuna qarina zenye kuonesha kwamba Allah hakuja mwenyewe”. Ukiniambia hivyo nitakujibu kwamba:

a) Qarina ni katika masharti ya majazi nawe huamini kuwepo kwa majazi. Au utayathibitisha majazi hapa na uyakatae kwengine?

b) Ikiwa unakubali kwamba hapa kuna qarina iliolitoa neno kuja katika maana yake ya asili na kulipeleka katika maana nyengine au kwamba kuna qarina yenye kuonesha kuwepo kwa neno amri (jambo) japo kuwa neno hilo halikutajwa, basi hii inamaanisha kwamba tumekubaliana kwamba majazi yapo. Ukiniambia kwamba “Aa huu ni uslubu tu si majazi”. Nitakujibu kwamba wanavyuoni wa fani za usuli wanasema kwamba ال

ا في إصطالحلمشاحة Hakuna kujadiliana katika maneno ya kitaalamu au ya kifani (technical terms). Yaani kinachozingatiwa ni uhakika wa kitu: si jina lake, na kwa hivyo je tuyaite hayo kuwa ni majazi au tuuite kuwa ni uslubu, hili si muhimu: kilichomuhimu ni je hapo kuna neno lililotumika kinyume na maana yake ya asili au halipo? Au kwa hapa je kuna neno lililoondoshwa au halipo? Ikiwa lipo neno hilo basi hayo ndio majazi yenyewe wanayoyakusudia wanavyuoni nawe unaweza kuyapa jina unalolitaka ikiwa jina majazi hulipendi. Kama halipo neno hilo lililotumika kinyume na maana yake ya asili au lililoondoshwa, basi itabidi utueleze je Aya hio inathibitisha kwamba Allah kazijia nyumba hizo kweli kweli akajitia chini ya misingi au – kama ilivyo katika dhahiri ya Aya nyengine – Allah kawajia Mayahudi na kuijia ardhi kweli kweli?

MJADALA NA AL-DARIMI

Lakini Sheikh ‘Uthman bin Said Al-Darimi, yeye anatafautisha baina ya Aya hizo au kama hizo na Aya isemayo: “Na akaja Mola wako na Malaika safu safu “.729 Anasema:

729 - Suratul-Fajri (89) aya ya 22.

225

Page 226: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Tafauti iliopo baina ya Aya hizo zenye kusema kuwa Allah kawajia Banu Quraidha730 kutoka wasipopajua, na kwamba kazijia nyumba zao na kwamba kaijia ardhi, ni kuwa Aya hizi zinazungumzia adhabu iliowafika watu hao hapa duniani, wakati Waislamu wamekubaliana kwamba Mwenyezi Mungu hateremki isipokuwa siku ya kiama kwani siku hio Yeye anakuja kupitisha hukumu Yeye mwenyewe baina ya viumbe. Kwa hivyo, Siyaaq ya Aya hizo ni tafauti na Siyaaq ya Aya “Na akaja Mola wako na Malaika safu safu”.

Hayo ndio maneno yake.731 Nayo ni maneno ya ajabu kabisa, kwani:1) Kuja kwa Allah ama kuwe ni kwa hakika au ni kwa majazi.

Tukisema kuwa ni hakika basi ni vile maana ya neno kuja linavyomaanisha katika lugha ya Kiarabu. Na kuja kwa uhakika katika lugha ya Kiarabu – sawa na ilivyo katika lugha nyengine – ni kuhama kutoka sehemu moja kwenda nyengine. Na kuja huku kuna masharti yake:

a) Chenye kuja kiwe ni kiwiliwili.b) Kitoke sehemu kwenda nyengine. c) Sehemu kiliotoka ama kiwe bado kiko au kimeondoka. d) Kikiwa kimekuja huku na huko kilikotoka bado pia kipo,

basi chenye kuja hicho kitakuwa ni chenye kunyuuka au chenye kujizongoa.

e) Kikiwa kule hakiko: kimeondoka, basi hio ni alama ya kwamba chenye kuja kina udhaifu na kwamba hakiwezi kufanya kikitakacho ila kwa kuhama sehemu moja kwenda nyengine.

Hizo si kwamba ni hoja za kiakili tu, bali ndivyo ilivyo maana ya kilugha ya neno kuja. Wala usiniambie kwamba “Masharti haya ni sifa za viumbe, nasi hatuwezi kufanya Qiyas baina ya Muumba na kiumbe”. Kwani tunasema kwamba tunachokizungumzia sisi si mas-ala ya Qiyas, bali ni mas-ala ya madlulu lughawi (maana ya kilugha) ya neno kuja, kwamba neno kuja katika lugha ya Kiarabu haliwi ila na maana hio tulioieleza ikiwa neno hilo litatumika katika maana yake ya uhakika. Ama likitumika na kumaanisha maana nyengine zisizokuwa hizo basi linakuwa limetumika kimajazi: si uhakika wake wa kuja. Na hili ndilo kama lile alilolinena Al-Imamu Jua la Dini Ibn Al-Qayyim: “mauti yamekuja” ilhali mauti hayaji. Au kusema 730 - Hivi ndivyo alivyosema Al-Darimi. Lakini kilicho mashuhuri ni kuwa vita hivi vilikuwa baina ya Waislamu na Banii Al-Nadhir kama alivyosema Ibn Kathir, Al-Tabari, Al-Tabaatabaai, Al-Zamakhshari, Abdul-Razzaaq, Al-Sabuni na wengine. Kwa hivyo, alichokisema Al-Darimi ama itakuwa ni riwaya shaadha au kasahau au kosa la chapa. 731 - Maneno hayo sikuyanukuu neno kwa neno kwani ni marefu: nimenukuu nukta (points) zake tu kimaana. Tazama ‘Uthman Al-Darimi Al-Radu ‘Alaa Bishr Al-Marisi 50-51.

226

Page 227: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

“habari imekuja” ilhali habari haiji bali inasimuliwa. Na kwa hivyo, ilipobainika kwamba Allah hawezi kuja kwa namna yoyote katika hizo tulizozieleza, basi elewa kwamba neno kuja lililotumika katika Aya hio ni kuja kimajazi na kwa hivyo ni lazima lifasiriwe kwa maana inayokubaliana na utukufu wa Allah.

Wala huwezi kusema:

Kuja kwake ni kuja ambako hatuwezi kukufahamu, bali ni kuja kunakokubaliana na utukufu wake, wala kuja huko hakuna mfano kwa sababu Yeye “ شيء كمثله .(Hana mfano wa kitu) ”ليس

Huwezi kutoa hoja hio na hoja yako ikanyooka mnyooko wa mtarimbo, kwani tunasema kwamba Aya isemayo: “Hana mfano wa kitu”, haikuja kubomoa maana za kilugha zilizomo katika lafdhi za Aya za Qur-ani, wakati ukisema “Kaja mjo wa uhakika lakini si kwa namna tunavyojua” basi unakuwa umei’attil (umeibomoa) maana ya neno kuja iliomo katika Aya kwani kuja mjo wa kweli kweli katika lugha ya Kiarabu unafahamika na kulitoa neno katika maana yake hio na kulipeleka katika maana nyengine isiojulikana haikupokewa kamwe katika lugha.732 Katika lugha ya Kiarabu hakuna kusema “kaja mjo wa kweli lakini si kama tunavyojua sisi” bali kuna “Kaja kweli kweli” au “Kaja kimajazi”. Kwa maana hii, inakubainikia kwamba kanuni ya kutokumshabihisha Allah na viumbe iliojengeka katika Aya isemayo: “ شيء كمثله inabidi ,(Hana mfano wa kitu) ”ليسifungamanishwe na kanuni za kilugha ili kufikia maana sahihi, vyenginevyo itatubidi tuutendee kazi msingi mmoja na tuutupe msingi mwengine, nalo ni kinyume na kanuni “ إهماله من أولى النص Kulitendea kazi) ”إعمالandiko ni bora kuliko kulipuuza).

Wala haiwezekani kudai kwamba:

Kuja kwake ni kama kuwepo kwake; yaani kama vile ambavyo Yeye yupo na sisi tupo lakini kuwepo kwetu ni tafauti na kuwepo kwake; halkadhalika kuja kwake ni tafauti na kuja kwetu.

Pia hoja hio ni hoja dhaifu, kwani tunasema:a) Hiki ndio Qiyaas (ulinganisho) cha Kiumbe na Muumba

ambacho munakikataa, yaani Qiyaas kilichojengeka juu ya misingi ya uhakika wa kuja na uhakika wa kuwepo.

b) Kuja tunakokuzungumzia ni huku kunakoeleweka katika lugha ya Kiarabu na lugha nyengine: si kuja kwengine. Ama kuja

732 - Bali kufanya hivyo ni majazi na ta-awil.

227

Page 228: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kwengine – ikiwa kupo – basi kunahitaji ushahidi wake mwengine wa kilugha: ibainishwe kilugha kwamba neno kadha lina maana hio. Kwa hivyo, tuleteeni katika lugha ya Kiarabu kwamba kuna kuja kwa uhakika kusikokuwa huku tunakokujua.

c) Uhakika wa kuwepo (existence) unaofahamika katika lugha ya Kiarabu na nyengine hautafautishi baina ya kuwepo kwa kiumbe na kuwepo kwa Muumba. Yaani uhakika wa kuwepo hauna tafauti kwani kuwepo ni kinyume cha kutokuwepoعدم) non-existence) tu. Bali tafauti iko katika namna ya kuwepo huko: si uhakika wa kuwepo kwenyewe.

d) Kuwepo ni sifa ya ukamilifu bila ya sifa hio hakuna Mungu; ama kuja ni sifa ya udhaifu kwani ni sifa yenye kuonesha kuwa mjaji anahitajia na si mwenye uwezo mutlaq (usio mipaka). Bwana Kasim mwana wa Mafuta hawezi kupata chungwa ila atapolijia soko au kumuagiza mtu atayelijia soko; Allah jambo lake ni kun fayakun: hahitaji kuja ili ndio aweze kuwafanyia waja hesabu.

Jambo jengine: alilolidai Al-Darimi na kutafautisha kwalo baina ya Aya inayosema: “basi Allah AKAZIJIA nyumba zao katika misingi” na Aya: “Na akaja Mola wako na Malaika safu safu” ni kuwa katika Aya ya mwanzo inazungumzia kuja hapa duniani ili kuleta adhabu hapa duniani na:

Waislamu wamekubaliana kwamba Allah yuko juu ya ‘Arshi yake juu ya mbingu zake……; na wala hawakuwa na shaka kwamba Yeye atateremka siku ya kiama ili ahukumu baina ya waja wake….733

Nasi tunasema kwamba – kwanza – maneno haya hayana ukweli. Na bila shaka, pamoja na kuwa Ibn Taymiyya kakisifu sana na kukiusia sana kitabu hicho cha Al-Darimi, lakini tunamsubiri Sh. Kasim Mafuta labda kesho atamueka Imamu wake huyu, ‘Uthman Al-Darimi katika urodha ya waongo! Mimi simwiti mwongo, lakini ninazungumza kwa mujibu wa minhaj ya Sheikh Kasim Mafuta. Wapi kapata Al-Darimi kwamba:

Waislamu wamekubaliana kwamba Allah yuko juu ya ‘Arshi yake juu ya mbingu zake?” Na wapi kapata kwamba “Na wala hawakuwa na shaka (Waislamu) kwamba Yeye atateremka siku ya kiama ili ahukumu baina ya waja wake…?

733 - Tazama ‘Uthman Al-Darimi Al-Radu ‘Alaa Bishr Al-Marisi 50.

228

Page 229: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Makubaliano haya yamo katika vitabu gani? Na ni Waislamu wangapi duniani tangu zamani hadi leo wenye itikadi hizo hata akadai kuwa Waislamu wamekubaliana?

Ama tukija katika tafauti hio alioisema Al-Darimi, tunakuta kuwa ni utafautishaji uliombali na tahqiq za kielimu, kwani::

1) Kinachozungumzwa hapa ni kuwa kutajwa kwa maneno “Kuja kwa Allah” haijaleta maana kwamba ni lazima kuja huko kuwe ni kuja kwa hakika. Hio ndio maudhui inayozungumzwa. Kisha kauli hii ikapatiwa ushahidi wa Aya hizo tulizozinukuu ikiwemo Aya isemayo: “basi Allah AKAZIJIA nyumba zao katika misingi.” Nasi tunakubaliana kwamba Allah hakuzijia nyumba hizo kweli kweli (physically). Kwa hivyo:

a) Hii ina maana kwamba neno kuja hapo ni majazi: si hakika.b) Kuja kwa Allah si lazima iwe kuja kweli kweli.c) Nadharia ya kwamba “tumsifu Allah vile alivyojisifu”

haikuweza kufanya kazi katika ulimwengu wa hakika, kwani hapa Allah anasema kaja na kuingia chini ya misingi ya nyumba, wakati hilo nyinyi hamulikubali.

Ukinambia:

Aa! Unajua Allah kasema: ق ويوم ماء تشق ل بالغمام الس ونز المالئكة تنزيال Siku ambayo mbingu zitapasuka na Malaika

watateremka mteremko wa kweli kweli.734 Hapa imepokewa riwaya kwamba mbingu zitapasuka na Allah atakuja katika kipande cha mawingu. Na hili linathibitishwa na Aya inayosema: ينظرون هل إال

والمالئكة الغمام من ظلل في الله يأتيهم أن Hawana wanachokisubiri isipokuwa Allah awajie katika kivuli cha mawingu na Malaika.735 Basi ikaeleweka kwa mujibu wa maandiko haya kwamba Allah haji isipokuwa siku ya Qiyama.

Ukiniambia hivyo, nitakujibu kwamba:a) Aya mbili hizo – tukijaalia kwamba hiyo tafsiri uliozifasiri wewe ni

sahihi basi – hazijathibitisha kwamba Allah haji isipokuwa siku ya Qiama; bali zinathibitisha kwamba atakuja siku ya kiama. Na hii ni kwa mujibu wa tafsiri yako: si tafsiri ya jumhur. Ama kuzichukua Aya hizo na kuthibitisha kwazo kutokuja kwa Allah hapa duniani ni kuthibitisha kitu kwa njia ya Mafhumu Al-Laqab. Ubainifu wake ni kuwa iliposemwa kwamba Allah atakuja huko akhera; wewe ukadai

734 - Sura 25, Aya 25. 735 - Sura 2, 210.

229

Page 230: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kwamba basi duniani hatokuja. Na kwa msingi huu, ukaikataa sifa ya kuja iliomo katika Aya: “basi Allah AKAZIJIA nyumba zao katika misingi” na Aya: “Je hawaoni kwamba tunaijia ardhi tunaipunguza pembeni mwake” na Aya: “….Na wakadhania kuwa ngome zao zitawakinga kutokana na Allah, basi Allah AKAWAJIA kutokea wasikokufikiria”. Na Mafhumu Al-Laqab – kama unavyojua – haikubaliki katika kuthibitisha mas-ala ya dhana ya kifiq-hi, basi vipi itathibitisha mas-ala ya kiitikadi? Kwa hivyo, sisi bado tunasema kwamba kuja kwa Allah si lazima kuwe ni kuja kwa uhakika au kwa usahihi zaidi haiwezekani kuwe ni kuja kwa uhakika bali kuja kwake ni kuja kwa amri (jambo) yake.

b) Riwaya zilizotegemewa kutoa tafsiri hio ni riwaya za kutunga bila

shaka kama mutun zake zinavyojionesha.736 Riwaya moja imesimuliwa kutoka kwa Abu Huraira lakini katika sanad yake kuna Nu’aim bin Hammad. Naye wengine wamemkubali na wengine wamemkata na wakasema kuwa ni dhaifu na anasimulia Hadithi munkar.737 Na wengine wakasema kwamba alikuwa akitunga riwaya za kumtia aibu Abu Hanifa na kutunga riwaya za kuipa nguvu Sunna! Na wengine wakasema ni Imamu au ni mkweli lakini anakosea sana.738 Sanad hii huenda ikawa ina mpokezi asiyejulikana vile vile. Bali matn ya riwaya hii kama tutavyoijadili katika Hadithi za kuonekana kwa Allah ni matn mbovu ilioje. Riwaya ya pili imenasibishwa na Ibn Abbaas lakini katika sanad yake kuna Hammad bin Salama, naye ni dhaifu, tatamuelezea kwa urefu katika juzuu ya nne. Na katika sanad hii pia yumo ‘Ali bin Zaid bin Jud’aan naye ni dhaifu sana.739 Riwaya ya tatu imenasibishwa na Anas bin Malik, lakini katika sanad yake kuna Ibn Lahi’a naye ni dhaifu mwenye kuchanganyikiwa. Naam! ‘Abdul-Ghaniy anasema kwamba Hadithi zilizopokewa na wenye jina la “Abdullah”740 kutoka kwa Ibn Lahi’a ni sahihi. Ninasema: hata ikiwa hivyo basi ni kwa zile sanad zitazotimiza masharti mengine ya usahihi. Ama katika sanad hii, Ibn Lahi’a kaipokea Hadithi hio kutoka kwa Yazid bin Abi Habib kwa sigha ya ‘an’ana, na Ibn Lahi’a – mbali na udhaifu –

736 - Tazama riwaya hizo katika Uthman bin Said Al-Darimi Al-Raddu ‘Alaa Al-Marisi j. 1, uk. 52-53. 737 - Anasema Al-Albani: “(Nu’aim) Bin Hammad mwenyewe ni dhaifu”. Al-Dhaifa j. 3, uk. 469, j. 13, uk. 393.738 - Tazama habari zake kwa urefu katika Tahdhibu Al-Tahdhib j.10, uk. 412, tarjama na. 833. 739 - Ibn Hajar Tahdhibu Al-Tahdhib j. 7, uk. 283-285, tarjama na. 545. 740 - Yaani majina yote yenye kumaanishwa “Waja wa Allah au waja wa Rahman n.k.”.

230

Page 231: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

pia ni mudallis (mwenye kughushi). Kwa hivyo, riwaya yake hapa haikubaliki kwa hali yoyote ile.741 Pili ni kuwa katika sanad hii kuna Sinan bin Sa’ad naye wemetafautiana kuhusu jina lake je ni Sinan bin Sa’ad au Sa’ad bin Sinan. Na kwa hivyo, Al-Imamu Ahmad, kaziwacha Hadithi zake kwani hajulikani jina lake hasa ni nani. Na Al-Juzjaani anasema “Hadithi zake ni wahi (dhaifu sana)”. Anasema Al-Nasai “Hadithi zake ni munkar”. Kisha mbali na hayo mpokezi huyu ni mwenye kuchanganyikiwa.742 Ama Hadithi ya nne na ya mwisho alioitolea ushahidi Al-Darimi imenasibishwa na Ibn Abbaas vile vile. Lakini katika sanad yake kuna Shahru bin Hawshab, naye ni dhaifu kama walivyosema kundi kubwa la wanavyuoni wa wapokezi na Hadithi. Bali mpokezi huyu katuhumiwa hata katika dini yake kwamba aliiba pesa katika beitil-mali na kwamba alifuatana na mtu wa Sham akamfanyia khiyana.743 Bila kusahau kwamba sanad hii ina wapokezi wengine ambao sikuwaona walipotajwa katika marejeo nilionayo, dhahir ni kwamba wapokezi hao hawajulikani. Wa Allahu A’alam!

2) Jambo la pili: ni kuwa ukweli kwamba Allah atahukumu baina ya waja siku ya kiama; hii bado haijawa qarina yenye kulazimisha kulifasiri neno kuja katika maana yake ya uhakika. Kwani:

a) Ulazima wa kuwepo katika sehemu fulani kikweli kweli (physically) wakati wa kufanya kitu haumuhusu Allah, bali huo unamuhusu kiumbe. Bwana Kasim Mafuta, kama tulivyosema kabla, akitaka chungwa pale sokoni Tanga, hawezi kulipata ila ende mwenyewe. Hii ikiwa tutasema kwamba Sh. Kasim Mafuta kaja kweli kweli au kaja hakika kununua chungwa. Vyenginevyo itambidi amuagize mtu mwengine. Na hapa itajuzu kusema kimajazi kwamba “Sh. Kasim Mafuta kaja kununua chungwa” yaani kaja mjumbe wake. Kama tunavyosema Rais wa Zambia kawambia Watanzania kitu kadha, na pengine msemaji kiuhakika ni balozi wake; ama Rais yeye kaamuru tu akiwa nchini kwake. Na hilo utalifahamu zaidi utapoifahamu maana ya:

b) العالمين الله عن غني (Allah katosheka (hahitaji chochote) kutokana na vilimwengu na walimwengu wote).744 Kudai kwamba Allah hapa atakuja kweli kweli kwani anakuja kuhukumu baina ya viumbe, ni kudai kwamba Yeye hawezi kuhukumu ila ahudhurie. Na

741 - Ibn Hajar Tahdhibu Al-Tahdhib j. 5, uk.327-332, tarjama na. 648. 742 - Ibn Hajar Tahdhibu Al-Tahdhib j. 3, uk. 409, tarjama na. 877. 743 - Ibn Hajar Tahdhibu Al-Tahdhib j. 4, uk. 324-326. tarjama na. 635. 744 - Sura 3, Aya 97.

231

Page 232: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

hio si sifa ya Allah bali ni sifa ya hakimu kiumbe kwa sababu ya upungufu wake.

c) أراد إذا أمره إنما ( فيكون كن له يقول أن شيئا Hakika ya amri yake anapotaka kitu ni kusema kuwa nacho kinakuwa).745 Kwa hivyo, Allah anapotaka kitu chochote halazimiki kuwa ajikalifu au atoke sehemu kwenda sehemu ili kukifanya kitu hicho. Na kwa hivyo ndio maana Al-Imamu Al-Shafi akasema: “Allah alikuwepo kabla ya kuwepo sehemu. Akaumba sehemu naye (Allah) yuko katika sifa zake zile zile za tangu na tangu kama alivyokuwa kabla ya kuumba sehemu. Haimjuzikii Yeye kubadilika katika Dhati yake wala kubadilika katika sifa zake”.746

d) Riwaya inayomnukuu Sayyidna ‘Ali bin Abi Talib akisema kwamba “Allah atawahesabia watu (wote) wakati mmoja kama anavyowaruzuku wakati mmoja”. Nayo ndio moja ya maana za Aya isemayo الحساب سريع الله إن (Hakika ya Allah ni mwepesi wa kufanya hesabu),747 kwa mujibu walivyosema wajuzi. Yote haya yanathibitisha kwamba Allah kuwafanyia watu hesabu, hakujamaanisha kwamba ni lazima aje pale uwanjani mwenyewe. Au aje naye kabebwa na kiwingu au kabebwa na Malaika kama wanavyodai Mawahabi na Maimamu wao!

Baada ya hayo, utaona kwamba Aya tulizozinukuu zinathibitisha kwamba kuja kwa Allah si lazima iwe ni kuja kwa uhakika, kama tulivyoona kwamba Qur-ani inasema kwamba Allah:

1) Anaijia ardhi na kuipunguza pembeni.2) Kazijia nyumba na kujitia chini ya misingi.3) Kawajia Mayahudi wa Banii Al-Nadhir.

Na Aya zote hizo hazimaanishi kwamba Allah alikuja kweli kweli, bali ni ibara zenye kuonesha kuja kwa jambo lake. Kwa hivyo, Allah aliposema: “Na akaja Mola wako na Malaika safu safu”, maana yake ni kuja kwa jambo lake. Na kilichowapelekea wanavyuoni wa jumhur kuwa waifasiri Aya hio hivyo, ni:

1) Maana ya kilugha ya neno kuja haiwiyani na utukufu wa Allah pindipo tutasema kuwa kuja huko ni kuja kweli kweli. Kwani kuja kweli kweli hakuwi ila ni kuhama kutoka sehemu kwenda nyengine. Na hili lingekuwa sahihi lau Allah angelikuwa:

745 - Sura 36, Aya 82. 746 - Kikundi cha wapekuzi Ghayatu Al-Bayaan uk. 68.

747 - Sura 3, Aya 199. Aya hii iko katika Sura nyingi. Tazama tafsiri tafauti za wanavyuoni utaona wakiinukuu riwaya hio ya Sayyidna ‘Ali (k.w.), hususan katika Aya 202 ya Sura ya pili.

232

Page 233: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

a) Anahitaji.b) Hawezi kufanya kitu ila akifate. c) Ni kiwiliwili.

2) Ulazima wa kuzifungamanisha Aya za Qur-ani ili zijifasiri zenyewe kwa zenyewe kwani Qur-ani ni wahyi na wahyi haugongani.

Sasa baada ya hayo tumebakiwa na suali moja nalo ni kuwa: ikiwa tumeweza kuthibitisha kwamba kuja kwa Mungu si lazima iwe ni kuja kwa kweli kweli na kwamba kutajwa kwa maneno kuja kwa Mungu kunaashiria kuwepo kwa majazu hadhfi (majazi ya kuondoshwa neno) katika maneno hayo, je ni Aya gani hizo zilizotoa tafsiri yenye kuonesha kwamba neno amri (jambo) ndilo lililoondoshwa katika Aya والملك ربك وجاء صفا .(Na akaja Mola wako na Malaika safu baada ya safu) صفا

AYA ZENYE KUONESHA KUONDOSHWA KWA NENO AMRU (JAMBO)

Tunasema kwamba chenye kubainisha kuondoshwa kwa neno hilo ni Aya zenye kuzungumzia adhabu zilizowafika baadhi ya watu na Aya zenye kuzungumzia yatayowafika watu kwa kutumia ibara kuja kwa jambo au kwa amri ya Allah. Kwa mfano Aya kama:

ا ربك أمر جاء لم Ilipokuja amri ya Mola wako.748

Anasema Allah:أمرنا جاء فإذا

Basi itapokuja amri yetu.749

Anasema Allah:

ا أمرنا جاء ولمIlipokuja amri yetu.750

Anasema Allah:

ا أمرنا جاء فلم

748 - Ilipokuja amri ya mola wako ya kuwaangamiza Fir’awna na wafuasi wake. Sura 11, Aya 101. 749 - Sura 23, Aya 27. Sura 11, Aya 40 أمرنا جاء إذا . حتى750 - Sura 11, Aya 58.

233

Page 234: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Basi ilipokuja amri yetu.751

Anasema Allah:

ينظرون هل ربك أمر يأتي أو المالئكة تأتيهم أن إال

Hawana wanachokisubiri isipokuwa kujiwa na Malaika au iwajie amri ya Mola wako.752

Anasema Allah:

الغرور …… بالله كم وغر الله أمر جاء حتى األماني تكم وغر

….Na yakakudanganyeni matamanio (ya nafsi zenu) mpaka jambo la Allah likaja753 na mdanganyi (Ibilisi) akakudanganyeni na (habari) za Allah.754

Na Aya hizi ziko nyingi: hatuna haja ya kurefusha. Kisha elewa kwamba Aya hizi na zilizo mfano wa hizi, Wanavyuoni huwa wanatafautiana katika kulifasiri neno amr lililomo ndani yake. Al-Imamu Ibn Jarir, kwa mfano, ananukuu kauli ya mmoja wa Wanavyuoni akisema kuhusu Aya inayosema:

أمرن جاء إذا احتى . Anasema: “itapokuja amri yetu ambayo tulimuahidi kuwa itawajia kaumu yake miongoni mwa mafuriko ambayo yatawagharikisha”.755 Ni wazi kwa mujibu wa tafsiri hii kwamba limetumika neno amr kwa maana ya jambo. Ndio maana akasema “itawajia kaumu yake miongoni mwa mafuriko ambayo yatawagharikisha”.

Wengine hulifasiri kwa maana ya amri ambao wingi wake kwa Kiarabu huwa ni awaamir. Na wengine hulifasiri kwa maana hio ya mwanzo yaani jambo, na wingi wake kwa Kiarabu linakuwa umuur. Sh. Al-Sabuni katika tafsiri ya Aya: ا أمرنا جاء فلم , anasema: “Yaani ilipokuja amri yetu ya kuwaangamiza wao, basi tulimuokoa (Nabii) Salih (a.s.)”. Ni wazi kwa tafsiri hii kwamba, neno amri hapa limetumika kwa maana ya kuamuru.

Baada ya hayo, sasa naturudi katika Aya zetu. Tunasema: ukiniambia:

751 - Sura 11, Aya 66. 752 - Sura 16, Aya 33. 753 - Yaani mauti. 754 - Sura 57, Aya 14. 755 - Al-Tabari, Muhammad bin Jarir Jaami’u Al-Bayaan j. 12, uk. 46.

234

Page 235: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Aaa! Unajua kwamba Aya hizo zinasema kwa uwazi kwamba itakuja au imekuja amri yake, na wala hazijakataa kwamba Yeye Allah atakuja. Na kwa hivyo, kuthibitisha kutokuja kwake kwa kutumia Aya hizo ni kuthibitisha kitu kwa kutumia Mafhumu Al-Laqab. Ubainifu wake ni kuwa iliposemwa kuwa amri yake itakuja, wewe ewe Juma Mazrui ukasema kuwa basi Yeye hatokuja. Na hii ni hoja dhaifu.

Ukiniambia hivyo, nitakujibu kwamba msingi wa hapa si Mafhumu Al-Laqab ambao ndio ulizaa natija hio, bali msingi wa hapa ni kuwa maana ya uhakika wa kilugha ya neno جاء kuja haiwezekani kuitumia kwa Allah kwa sababu ambazo tumezieleza sana na kuzikariri. Na kwa hivyo, haikubakia ila maana ya kimajazi ya neno hilo. Na hakuna maana ya kimajazi inayotoa maana sahihi ila tuseme kwamba maana ya “Atakuja Mola wako” ni “Itakuja amri ya Mola wako” kwani mfumo huu ndio uliomo katika Aya nyengine, na tafsiri bora ni ya kuifungamanisha Aya moja na nyengine. Ukiniambia:

Lakini – kama alivyosema Al-Imamu Al-Darimi – kwamba kuna tafauti ya Aya kama hizo ulizozitoa na Aya hio ya Surat Al-Fajr, kwani Aya hizo zinazungumzia adhabu ya dunia, wakati Aya hio ya Surat Al-Fajr inazungumzia kuja kwake huko akhera, naye anakuja ili kufanya hukumu.

Ukiniambia hivyo, nitakujibu kwamba:1) Hii ina maana kwamba wewe umekufahamu kwamba kule

kufanya kwake hukumu baina ya viumbe wake kuwa ndio qarina ambayo inaonesha kwamba Allah atahudhuria pale uwanjani mwenyewe. Nasi tunasema kwamba Allah hahitaji kutoka sehemu moja kwenda nyengine ili ndio aweze kufanya chochote akitakacho kwani yeye ni العالمين عن غني (Kajitosheleza: hahitaji chochote katika vilimwengu na walimwengu).

2) Hakuna tafauti yoyote ile kwa Allah baina ya dunia na akhera, kwani Yeye habadiliki wala haathiriwi na nyakati wala mwahala wala hapitikiwi na hali tafauti. Yeye kakamilika katika Dhati yake: kama alivyokua ndivyo alivyo na ndivyo atavyokua milele na milele; na ni mkamilifu katika sifa zake wala hahitaji sifa za ziada. Na kwa hivyo, ikiwa duniani kawaadhibu watu na akawahukumu watu kwa baadhi ya makosa yao bila ya kuwajia – kama Aya tulizozinukuu na nyenginezo nyingi zinavyothibitisha – bila ya kuja Yeye mwenyewe, basi hakuna ulazima kwamba akhera asiweze kuwahukumu watu ila kwa kuhudhuria Yeye mwenyewe. Na kwa hivyo, kimepokelewa kutoka kwa Al-Imamu Ali (k.w.) kile tulichokinukuu kabla kwamba “Allah atawahukumu watu wakati mmoja kama anavyowaruzuku wakati

235

Page 236: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

mmoja”. Na bila shaka mwenye uwezo huu basi hahitaji kuwepo ili ndio apitishe hukumu.

TUNARUDI KATIKA MJADALA WA MAJAZI

Hayo ndio maelezo yetu kwa ufupi kuhusu Aya hio inayosema: “Na atakuja Mola wako na Malaika safu safu”. Baada ya hayo, sasa naturudi katika mjadala wa majazi pamoja na Sheikh wetu Al-’Allama Kasim bin Mafuta. Anasema Sheikh Mafuta:

HOJA ZA WENYE KUTHIBITISHA MAJAZI

Wakajitetea wenye kuthibitisha kuwepo majazi ndani ya Qur’an kwa kusema: Majazi ni sehemu katika fasihi za lugha ya kiarabu, na hii Qur’an imeshuka kwa lugha ya kiarabu. Na kila ambacho kinafaa kuwepo katika lugha ya kiarabu kinafaa kuwemo ndani ya Qur’an. Na miongoni mwa mambo yaliyomo ndani ya lugha ya kiarabu ni haya majazi. Kwahiyo, tunapata natija kwamba “Majazi” yamo katika Qur’an.

MAJIBU YA WENYE KUPINGA

Wakawajibu wenye kupinga kuwepo majazi ndani ya Qur’an kama ifuatavyo:

Tumewakubalia (AL-MUQADDIMATU AL-SUGH’RAA) kwamba majazi yamo katika lugha ya kiarabu, lakini hatuwakubalii (ALMUQADDIMATUL-KUBRAA) kwamba kila kilichomo katika lugha ya kiarabu kinafaa kuwemo ndani ya Qur’an, bali sisi tunasema kinyume chake, kwamba; kuna baadhi ya vitu vimo katika lugha ya kiarabu, lakini havifai bali ni haramu kuitakidi kuwemo ndani ya Qur’an.

Kwa mfano;Katika elimu ya balagha sehemu ya Badi’i katika sehemu ya “Muhassinaatul-Ma’anawiyyah” (vitu vyenye kupendezesha maana), kuna kitu kinachoitwa “AL-HAZ’LU” (mzaha/utani). Kitu hiki kimo ndani ya lugha ya kiarabu, lakini huwezi kusema kwamba maadamu kimo kwenye lugha, basi kinafaa kuwemo ndani ya Qur’an, kwa sababu Allah anasema kuhusu Qur’an:

بالهزل هو وما *فصل لقول إنه

236

Page 237: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

“Kwa hakika hii (Qur’an) ni kauli kupambanua756 (13) Na wala si mzaha (14)”. 757

Miongoni mwa fani za lugha ya kiarabu ni suala la utani, lakini ndani ya Qur’ani hakuna utani na mwenye kuitakidi kuwa katika Qur’an kuna utani atakuwa tayari amekufuru. Halikadhalika ndani ya lugha ya kiarabu kuna kitu katika milango ya elimu ya balagha kiitwacho “al Ruju’u” kujirudi, msemaji anaweza kusema neno halafu hapo hapo anajikadhibisha mwenyewe kwa kuwa alisema maneno hayo bila ya uhakika, kutokana na kuweweseka, au hofu, au kuzidiwa na mapenzi n.k.

Halikadhalika kuna kitu kitachoitwa “Hus’nu Ta’alili” kutoa sababu ya kitu ambayo si halisia. Mfano mtu akisema: Mvua imenyesha mjini kwetu kwa sababu ya kutuona758 haya. Mambo haya na mengineyo ambayo sikuyataja, yamo katika lugha ya kiarabu lakini hayamo na wala hayafai kuwemo katika Qur’an, bali kuitakidi kuwemo ndani ya Qur’an ni ukafiri. Kwa hiyo madai ya kwamba kila kilichomo kwenye lugha ya kiarabu kinafaa kuwemo ndani ya Qur’an, madai hayo hapa yanaporomoka.759

JAWABU

Kwa kuanzia ni kuwa mimi nastaajabishwa sana na wewe Sheikh Kasim Mafuta! Wewe unatafuta ile hoja unayodhania kuwa ni dhaifu na ambayo haina msingi wowote wewe ndio unaijadili na unawacha kujadili mambo ya msingi! Hujui ewe Sheikh Kasim kwamba tafauti katika juz-iyyaat (vijisehemu vya jambo) haimaanishi kutokuthibiti kwa asasiyyaat (misingi) yake? Kwa mfano, kutafautiana kwa wanavyuoni juu ya Hadith Mursal: kwamba je aina hio ya Hadithi inafaa kutumika kama ni hoja ya Kisharia au haifai, hakubomoi ukweli wa kuwepo kwa Hadithi dhaifu.

756 - Sahihi ni kuifasiri Aya hio: “Kauli pambanuzi” au “kauli yenye kupambanua” kwani masdar hapa imetumika kwa maana ya sifa, kama inavyosemwa: العدل Imamu) اإلمامuadilifu) yaani “Imamu muadilifu” au “Imamu mwenye uadilifu”. Na katika Qur-ani Allah anasema: صالح غير عمل إنه “Yeye (mtoto wa Nabii Nuha) ni matendo yasio mema” Sura 11, Aya 46, yaani “Yeye ni mtendaji wa yasio mema”. Na bila shaka itakuwa ajabu ilioje ikiwa mtu ataifasiri Aya hio kuwa maana yake ni “Yeye (mtoto wa Nabii Nuha) ni matendo yasio mema” badala ya kusema: “Ni mtendaji wa yasio mema”. Kwa hivyo, kutumika kwa masaadir katika sehemu hizi ni kwa ajili ya mubaalagha kana kwamba Qur-ani ndio upambanuzi wenyewe kwa jinsi inavyopambanua mambo; na kana kwamba Imamu ndio uadilifu wenyewe kwa jinsi alivyo muadilifu; na kana kwamba mtoto wa Nabii Nuhu ndio uovu wenyewe kwa jinsi alivyokuwa muovu. Wa Allahu A’alam!757 - Suratul-Twaariq (86) aya ya 13-14.

758 - Dhahir ni kuwa hili ni kosa la chapa na sahihi ni “kutuonea haya.” 759 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 46-47.

237

Page 238: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Halkadhalika – kama tulivyonena na kukariri – cha muhimu kukielewa ni hii tafauti baina ya kuwepo kwa uhakika wa kitu na kuzuka kwa jina lake la kitaalamu. Jina sala ya tarawehe – kwa mfano – limezuka, lakini uhakika wa sala yenyewe ulikuwepo tangu enzi ya Mtume (s.a.w.). Kwa hivyo, kinachotazamwa ni je hao walioita fani hio kuwa ni Hazlu (mzaha/utani) wanakusudia nini? Baada ya kukipata hicho wanachokikusudia wao ndio kinatazamwa je katika Qur-ani kimo au hakimo. Hazlu wanayoikusudia watu wa balagha si ile yenye kufasiriwa “utani au mzaha” kama ulivyodhania wewe. Nimesema na ninakariri kwamba technical terms (maneno ya kifani) huwa hayatazamwi katika maana yake ya kilugha, bali yanatazamwa nini kinakusudiwa kwayo. Nimekupa mfano wa neno sala ya tarawehe, na nakuongezea mfano wa neno tajaahul ambalo ukilifasiri kilugha maana yake ni kujifanya kuwa hujui nawe unajua. Lakini katika fani ya balagha haikusudiwi hivyo, zinazokusudiwa ni zile nukat za kibalagha kama vile kuonesha kulaumu, kugomba, kustaajabu, kudharau n.k.

Mfano mwengine wa nyongeza ni neno makruh. Unaelewa vyema kwamba katika dhana (concept) ya Qur-ani, neno makruh limetumika kwa mambo yalioharamishwa. Kwa mfano, Allah baada ya kutaja mambo kadha wa kadha alioyaharamisha kama vile kuua; kula mali ya yatima; kupunja katika vipimo n.k., aliishia kwa kusema:

ربك عند سيئه كان ذلك كل مكروهاYote hayo ubaya wake ni makruhu (wenye

kuchukiza) kwa Mola wako.760

Wakati Allah anasema hivyo, utakuna neno makruh kwa wanavyuoni wa fiq-hi linatumika kwa kitu ambacho ukikifanya hupati dhambi na ukikiwacha unapata thawabu zaidi. Sasa huwezi kudai kwamba “si kweli hakuna kitu makruh” kwa sababu katika dhana ya Qur-ani neno hilo limetumika kumaanisha kitu haramu. Huwezi kudai hivyo na hoja yako ikanyooka, bali unachotakiwa ni kutazama je wale waliozigawa hukumu za kifi-qhi migawanyiko hio ya makruh, haramu n.k., wanakusudia nini? Tena: je kile wanachokikusudia wao kipo au hakipo? Hivi ndivyo unavyofanywa utafiti wa kitaalamu.

Halkadhalika neno مفعول “mtendwa”, ukiwa utalichukulia kilugha basi – katika sentensi fulani fulani – huwezi kusema kuwa Allah ni mtendwa kwani – kilugha – mtendwa ni mwenye kufikiwa na kitendo cha mtenda. Lakini watu wa nahau wanaposema فاعل “mtenda” na مفعول “mtendwa”, huwa hawakusudii maana zake za kilugha. Na kwa hivyo, katika maneno kama علي qawiya ‘Ali (Ali kapata nguvu), Ali قوي

760 - Sura 17, Aya 38.

238

Page 239: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

anaitwa kuwa ni mtenda ilhali hapa hajatenda kitu; na katika maneno kama: الله Allah anaitwa mtendwa ilhali ,(nimemuomba Allah) دعوت

hajatendwa kitu kwani Yeye kamwe hafikiwi na kitendo cha yoyote. Kwa hivyo, tunapozungumzia technical terms (maneno ya kifani) huwa hatutazami maana zake za kilugha tu, bali kinachotazamwa ni nini kinakusudiwa kwayo. Na ndio maana wanavyuoni wakasema yale tulioyanukuu kabla: ا في مشاحة إصطالحلال (Hakuna kujadiliana katika maneno ya kitaalamu au ya kifani).

Ama maneno yako uliposema:

Katika elimu ya balagha sehemu ya Badi’i katika sehemu ya “Muhassinaatul-Ma’anawiyyah” (vitu vyenye kupendezesha maana), kuna kitu kinachoitwa “AL-HAZ’LU” (mzaha/utani). Kitu hiki kimo ndani ya lugha ya kiarabu, lakini huwezi kusema kwamba maadamu kimo kwenye lugha, basi kinafaa kuwemo ndani ya Qur’an, kwa sababu Allah anasema kuhusu Qur’an:

بالهزل هو وما *فصل لقول إنه“Kwa hakika hii (Qur’an) ni kauli kupambanua (13) Na wala si mzaha (14)”.

Ninasema: maneno hayo hayakufai wewe ewe Sheikh Kasim mwana wa Mafuta, kwani kama Qur-ani ilivyosema:

بالهزل هو وما *فصل لقول إنه“Kwa hakika hii (Qur’an) ni kauli kupambanua (13) Na wala si mzaha (14)”

ndivyo ilivyosema: بهم يستهزئ الله

Allah atawacheza shere (atawafanyia mzaha).761

Sasa je neno yastahziu (atawafanyia mzaha), utalitoa katika maana yake ya asili na kuliletea ta-awil? Ukifanya hivyo utakuwa umethibitisha majazi na ta-awil katika sifa za Allah. Jambo hilo kwenu nyinyi ni kuyapotoa maandiko! Ukisema “ndio atafanya mzaha”, basi kwa mujibu wa maelezo yako utakuwa umethibitisha itikadi haramu katika Qur-ani na umekufuru. Sasa hapa nakuachia kazi wewe mwenyewe urekebishe fikra zako na kujichagulia minhaj (methodology) itayokufikisha nchi kavu kwa salama na amani – je ni kuyakubali majazi na ta-awil au ni kuyakanusha?

761 - Sura 2, Aya 15.

239

Page 240: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Naturudi katika kulitazama neno Hazl linalotumika katika fani ya balagha. Tunasema: ukirudi katika neno hilo, utakuta kwamba wao hawakusudii kufanya utani kwa maana ya maskhara yasio na ukweli ndani yake, bali wanakusudia kwamba mjengeko wa ile ibara kana kwamba inakusudiwa utani kumbe ni kitu cha kweli. Anasema Jalalu-Din Abu ‘Abdi-Llah:

ومثاله تفسيره عن تغني فترجمته الجد به يراد الذي الهزل ومنهالشاعر قول

للضب ** أكلك كيف ذا عن عد فقل مفاخرا أتاك تميمي ما إذا

Na katika hayo ni Hazlu (utani) inayokusudiwa Jiddu (seriousness au ukweli), basi tarjama (heading) yake inatosha: hakuna haja ya maelezo. Na mfano wake ni kauli ya mshairi aliposema:

Ikiwa mtu wa kabila la tamimi atakujia akijifakharisha**Mwambiye wachana na hayo; vipi na kula kwako dhabb.762

Maneno “Vipi na kula kwako dhabb”763 yaani wajifakharisha nini nawe wala dhabb? Maneno hayo yanaonekana kama ni utani ndio maana yakaitwa Hazl, lakini makusudio yake si utani bali makusudio yake ni kuonesha kumdharau yule aliyejifakharisha. Hii ndio Hazl wanayoikusudia kwenye elimu ya balagha: si utani kwa maana ya kudanganya au utani usio na maana.

Ama utani au Hazlu kwa maana ya kufanya maskhara, huu hata kama upo katika jamii za Waarabu na katika kila jamii pamoja na kuandikwa katika literature (Adab) zao, lakini huu si katika muundiko wa lugha; tafauti na alivyo faa’il (mtenda) na maf’ul (mtendwa) na majazi ambazo ni sehemu za miundiko ya lugha. Ama utani au Hazlu kwa maana ya kufanya maskhara hayo ni katika utamaduni (tradition) wa Kiarabu bali ni katika utamaduni wa binaadamu wote. Na sisi suala letu ni muundiko wa lugha ya Waarabu: si utamaduni wa Waarabu.

Ama “al Ruju’u”, si maana yake kujirudi kwa maana ya kuwa “msemaji anaweza kusema neno halafu hapo hapo anajikadhibisha mwenyewe” kama ulivyodhani wewe! Bali maana ya fani hii ni kukanusha ukamilifu wa kitu au kuikanusha dhana (mafhum au concept) fulani ya kitu na kuithibitisha dhana hio kwa njia nyengine. Al-‘Allama Al-Tiybi anatoa mfano wa Al-Ruju’u ya kibalagha kwa beti hizi:762 - Jalalu-Din Abu ‘Abdi-Llah Al-Idhaahu Fii ‘Ilmil Balagha j. 1, uk. 351.

763 - Dhabbu ni mdudu kama kenge lakini yeye ni mdogo. Urefu wake ni kama guruguru lakini yeye mpana kidogo. Watu wengine huko kwetu wanamfasiri “kenge” lakini kwa

kweli huyu si kenge kafanana naye tu.

240

Page 241: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

* دروعا حسبتهم لألعادي* *****وإخوان ولكن فكانوها** صائبات سهاما فؤادي *****وخلتهم في ولكن فكانوها

** ودادي من ولكن صدقوا لقد القلوب منا صفت قد وقالوا1) Na ndugu niliwafikiria kuwa ni ngao**Basi nao wakawa hivyo

lakini (ngao zenyewe) ni za (kuwakinga) maadui (si za kunikinga mimi).

2) Na niliwadhania kuwa ni mishare yenye kuisibu (shabaha)**Basi wakawa hivyo lakini (shabaha yenyewe) ni katika kifua changu (wakanipiga mimi).

3) Na wakasema mioyo yetu sasa imesafika**Wamenena kweli lakini (imesafika) kutokana na mapenzi yangu (hainipendi).

Hii ndio Al-Ruju’u inayozungumzwa katika fani ya balagha. Utaona kwamba mshairi kathibitisha kwamba watu hao ni ngao; kisha akakanusha kuwa ngao hizo ni za kumkinga yeye; kisha akathibitisha kwamba ni ngao za kuwakinga maadui. Kwa hivyo, kwa ufupi, ni kuwa yeye hajakataa kwamba hizo ni ngao lakini si ngao za kumkinga yeye bali ni za kuwakinga watu wengine. Hii ndio Al-Ruju’u inayokusudiwa katika balagha.

Halafu Al-‘Allama Al-Tiybi akatoa mfano wa Al-Ruju’u kwa Aya isemayo:

للمؤمنين ويؤمن بالله يؤمن لكم خير أذن قل أذن هو ويقولون

(Makafiri) wakasema kuwa yeye (Mtume) ni sikio (kila aambiwalo alisikiliza tu); sema (kweli) ni sikio lakini ni sikio la kheri kwenu: anamuamini Allah na kuwaamini waumini….764

Utaona katika Aya hii kwamba Allah mwanzo anawapinga makafiri kwa kumwita Mtume sikio kwani maana walioikusudia wao si ya kweli: wao wanakusudia kwamba Mtume (s.a.w.) chochote anachoambiwa, basi yeye anakisikiliza na kukikubali; kisha Allah akathibitisha kuwa kweli yeye ni sikio yaani ni mwenye kusikia kila kitu lakini ni katika mambo ya kheri tu. Kwa hivyo, hapa kuna kukadhibisha na kuthibitisha na hii ndio maana ya Al-Ruju’u inayozungumziwa na watu wa balagha.

Ama “Hus’nu Ta’alili” kutoa sababu ya kitu ambayo si sahihi, pia si mfumo wa lugha bali ni madai tu ya adiib (mtu wa literature) katika kuipamba lugha yake. Kwa lugha nyengine husnu ta’alil ni fikra: si muundiko wa lugha: muundiko wa lugha ni ule ambao Waarabu wote

764 - Sura 9, Aya 61.

241

Page 242: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

wanautumia kama: taqdim na ta’akhir; al-muqaabala; al-mushaakala; majaz n.k.

Kwa hali yoyote ile ikiwa tutasalimu amri kwamba si kila kilichomo katika lugha ya Kiarabu kimo ndani ya Qur-ani; suali ni kuwa je baadhi ya yaliomo ndani ya lugha ya Kiarabu yamo katika Qur-ani au yote hayamo? Bila shaka jawabu yako hapa haitotafautiana na binaadamu yoyote kwamba baadhi ya yaliomo ndani ya lugha ya Kiarabu yamo katika Qur-ani. Sasa je katika hayo baadhi ya yaliomo ndani ya Qur-ani, majazi nayo yamo au hayamo? Nadhani hili ndilo suali la kujiuliza na kulitafutia jawabu ili tuweze kuufikia ukweli.

Sasa ili tukuthibitishie hilo, natuanze kwa kutoa ta’arifu (definition) ya majazi. Natuache majina (majazi au uslub); na twende kwenye uhakika. Wanaoamini majazi wanasema: “Majazi ni neno lililotumika kinyume na maana yake ya asili”.765 Kilichobaki ni kujiuliza: je katika Qur-ani hakuna maneno yaliotumika kinyume na maana yake ya asili. Soma Aya zifuatazo halafu niambie je maneno yaliomo humo yametumika kwa maana gani. Anasema Allah:

النور إلى الظلمات من يخرجهم آمنوا الذين ولي الله

Allah ni Msimamizi wa Waumini: anawatoa katika kiza (na) kuwapeleka kwenye nuru. 766

Tazama neno “kiza” na neno “nuru”. Uhakika wa maneno hayo sio uliokusudiwa hapa, bali maana ni: “Allah anawatoa walioamini kutoka katika upotovu na kuwaingiza katika uongofu”. Upotovu umefananishwa na kiza kwa sababu ya kuwa mpotovu anayumbayumba katika upotovu wake kama vile anavyoyumbayumba mtu aliye katika kiza; na uongofu umefananishwa na nuru kwa sababu mtu katika nuru anaona vizuri na anakwenda sawa sawa. Vyenginevyo hakuna nuru ya kweli ambayo Waumini huingizwa humo au kiza cha kweli ambacho Waumini hutolewa kutoka humo.

Anasema Allah: الله بحبل واعتصموا جميعا

Na kamataneni na kamba ya Allah kwa pamoja.767

765 - Hapa natoa ta’arifu yenye kubainisha uhakika wa kitu: sitoi masharti ya majazi. 766 - Sura 2, Aya 257. 767 - Sura 3, Aya 103.

242

Page 243: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Sheikh Mafuta! Hii kamba ya kweli kweli ya Mwenyezi Mungu inapatikana wapi ili nasiye tupatekushikana nayo? Au utaniambia kwamba kamba hapa ina maana ya dini ili tukubaliane kwamba neno kamba hapa limetumika kinyume na maana yake ya asili?

Allah anasema: ثقفوا ما أين الذلة عليهم ضربت الناس من وحبل الله من بحبل إال

Wamepigwa udhalili popote walipo, isipokuwa (wakishikana) na kamba ya Allah na kamba ya watu. 768

Sijui tunakubaliana kwamba kamba ya Allah ni dini yake; na kamba ya watu ni msaada wao? Kama hatukubaliani hivyo, basi Sh. Kasim tueleze nini maana ya kamba hizi na zinapatikana wapi.

Anasema Allah:والنهار الليل مكر بل

Bali (ni) vitimbi vya usiku na mchana.769

Jamani! Usiku na mchana una vitimbi? Au hapa kuna majaz hadhf (majazi ya kuondosha neno) na maana ni: “Bali vituko vyenu mulivyokuwa mukivifanya usiku na mchana?”

Anasema Allah:راط اهدنا المستقيم الص

Tuongoze njia ilionyooka.770

Hii njia ya kweli kweli ilionyooka tunayomuomba Allah atuongoze iko wapi? Je si maana yake kwamba tuongoze katika dini sahihi? Na kwa hivyo, neno njia hapa limetumika kinyume na maana yake ya asili.

Anasema Allah:األيد ذا داوود عبدنا واذكر

Mkumbuke mja wetu Dawud mwenye mikono mingi (zaidi ya miwili).771

768 - Sura 3, Aya 112.. 769 - Sura 34, Aya 33. 770 - Sura 1, Aya 6. 771 - Sura 38, Aya 17.

243

Page 244: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Jamani! Huyu Nabii Dawud alikuwa na umbo la namna yake peke yake? Aya inasema alikuwa na mikono mingi zaidi ya miwili. Ukinambia: “Aa! Unajua katika lugha ya Kiarabu inatumika nyingi kumaanisha mbili na moja kumaanisha nyingi na mbili kumaanisha nyingi”. Dai hili nimeshakujibu sana kwamba hayo ndio majazi yenyewe yaani kutumika neno kinyume na maana yake ya asili. Vyenginevyo wapi umepata kusikia kwamba moja ni mbili au ni tatu na kuendelea?

Anasema Allah:الغيب مفاتح وعنده

Naye ana funguo za (mambo) ya ghaib.772

Je funguo hizi ni funguo za kweli au ni elimu ya ghaib? Au tuseme ghaib ina kufuli za kweli kweli na funguo zake za kweli kweli anazo Allah?

Anasema Allah: األرض لكم جعل الذي هو مناكبها في فامشوا ذلوال

Yeye (Allah) ndiye aliyekufanyieni ardhi kuwa dhalili, basi nendeni (mutembee) katika mabega yake. 773

Tunasubiri labda Sheikh Mafuta atatujuilisha mabega haya ya ardhi yako sehemu gani. Au atatwambia kwamba mabega hapa ni kwa maana ya pande (sehemu) ili iwe neno hilo hapa limetumika kinyume na maana yake ya asili.774

Anasema Allah:

آمن��وا الذين على أن��زل بالذي آمن��وا الكت�اب أهل من ائفةط وقالت آخره واكفروا النهار وجه

Na wakasema baadhi ya watu wa Kitabu: kiaminini kile walichoteremshiwa walioamini (katika) USO wa mchana na mukufuru mwishoni mwake (mwishoni mwa uso huo). 775

772 - Sura 6, Aya 59. 773 - Sura 67, Aya 15. 774 - Naam! Neno mankib lina maana nyengine, lakini zote hizo ni maana za kimajazi: si za hakika. 775 - Sura 3, Aya 72.

244

Page 245: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Bwana Kasim upo? Ivo huu mchana nao una uso bwana Kasim? Allah anasema النهار وجه (Uso wa mchana). Au utaniambia kwamba uso hapa una maana ya mwanzo; na kwa hivyo maana ni mwanzo wa mchana? Basi kama ni hivyo, ni kipi kinachozuia neno “Uso wa Allah” isiwe dhati yake au radhi zake?

Anasema Allah:

ياح يرسل الذي وهو الر رحمته يدي بين بشرا

Naye ndiye anayetuma upepo hali ya kuwa ni bishara baina ya mikono miwili ya rehema yake.776

Jamani! Ivo hii rehema ya Allah ina mikono miwili? Au maana ni: “Naye ndiye anayetuma upepo hali ya kuwa ni bishara itokayo katika rehema yake”. Na kwa hivyo, neno “mikono miwili” ni majazi: limetumika kinyume na maana yake ya asili.

Anasema Allah:حمة من الذل جناح لهما واخفض الر

Na wainamishie (wazee wako wawili) bawa la udhalili wa huruma. 777

Labda kesho tutaambiwa kwamba udhalili una bawa lakini bawa lake si kama bawa la ndege!

Anasema Allah:} للمؤمنين جناحك }واخفض

Na inamisha bawa lako kwa waumini.778

Hapa Mtume (s.a.w.) anaambiwa ainamishe bawa lake. Tunahofia kwamba lugha hii wenzetu itawashinda na kutwambia kuwa bawa hili ni bawa la kweli! Wallahu Al-Musta’aan!

Anasema Allah:العجل قلوبهم في وأشربوا

776 - Sura 7, Aya 57. 777 - Sura 17, Aya 24. 778 - Sura 15, Aya 88.

245

Page 246: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Na wakanyweshwa ndama katika mioyo yao. 779

Jamani! Ni nani anaweza kumnywa ndama? Na ndama ananywewa? Ni wazi kwamba hapa kuna majazu hadhfi (majazi ya kuondoshwa kwa neno) nalo ni mapenzi na kwa hivyo maana ya Aya hio ni “Walinyweshwa mapenzi ya kupenda ibada ya ndama”. Yaani waliipenda mno ibada yao hio ya kuabudu ndama.

Anasema Allah:ر ربهم عند صدق قدم لهم أن آمنوا الذين وبش

Wabashirie wale walioamini kwamba wana mguu wa ukweli kwa Mola wao. 780

Jamani! Ukweli nao una mguu? Basi hatuachi sisi kufuata kama bendera kwa sababu tu msemaji ni Ibn Al-Qayyim na Ibn Taymiyya!

Anasema Allah:

( أو13) رقبة ( فك12) العقبة ما أدراك ( وما11) العقبة اقتحم فال ( أو15) مقربة ذا ( يتيما14) مسغبة ذي يوم في إطعام ذا مسكينا(16) متربة

Basi je ameshaukata mlima?* Na nini kinachokujuilisha, ni nini mlima huo?* (Ni) kuifungua shingo* Au kumlisha katika siku yenye njaa* Yatima aliye na ukaribu (ujamaa)*Au masikini mwenye dongo. 781

Sasa ebu Bwana Kasim bin Mafuta yahesabu majazi yaliomo katika Aya hizi:

4) Neno ‘Aqaba. Maana yake ni njia yenye mawe mawe kwenye mlima.

5) Allah akauliza: je hio ‘Aqaba (njia yenye mawe mawe kwenye mlima) unaijua ni nini?

6) Kisha akabainisha kwamba ‘Aqaba (njia yenye mawe mawe kwenye mlima) ni:

a) Kumlisha masikini.b) Kuifungua shingo. Hapa jiulize tena: nini maana ya

kuifungua shingo katika Aya hio: ni shingo tu au ni mtu kamili? Shingo hapo ni kwa maana ya mtumwa.

779 - Sura 2, Aya 93. 780 - Sura 10, Aya 2. 781 - Sura 90, Aya 11-16.

246

Page 247: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Kwa hivyo kuyafanya hayo, basi Allah kakuita kuwa ni kuupanda mlima. Je bado tu mtu aliyejifungua pingu za kubururwa atakubaliana na madai kwamba katika Qur-ani hakuna majazi (maneno yaliotumika kinyume na maana yake ya asili)?

Allah anasema:رمى الله ولكن رميت إذ رميت وما

Hukurembea uliporembea, lakini Allah ndiye aliyerembea.782

Anasema Al-Imamu Badru Al-Din, Sheikh Al-Mufassirin Al-Khalili:Nanyi munaona vipi Aya ilivyokusanya baina ya kukataa kwamba Mtume (s.a.w.) karembea katika kauli yake Allah رميت وما (Na hukurembea); na baina ya kuthibitisha kuwa karembea katika kauli yake Allah رميت إذ (Uliporembea). Kisha hatima yake, Aya ikakutegemeza kurembea huko kwa Allah (subhanahu wa ta’aala) ikasema: رمى الله ولكن (Lakini Allah ndiye aliyerembea). Basi ivo inasemwa kuwa kile alichokataliwa Mtume (kuwa hakukifanya katika Aya hii) ndicho alichothibitishiwa (kuwa kakifanya), nacho ndicho hicho hicho ambacho mwishowe kimenasibishwa na Allah (kuwa ndiye aliyekifanya). Hapana! Bali alichokataliwa (Mtume s.a.w. kukifanya) ni kukupa tawfiki kule kurembea kwa kulisibu lengo la kile kinachorembewa, na hili ndilo ambalo kiumbe hana uwezo nalo, kwani hilo ni jambo la Allah……783

Hio ni mifano michache sana katika mingi iliomo katika Qur-ani. Je katika Aya hizo hakuna majazi? Je maneno yaliotumika katika Aya hizo yametumika kumaanisha maana zake za asili? Kwa kweli ndugu zetu haki hawaitaki: wao wana msimamo wao huo, basi ni huo huo tu hata kama unapingana na ushahidi wa wazi. Bwana Kasim Mafuta! Kuna msemo wa kizungu wenye kusema “Unaweza kumchukua farasi hadi kwenye mto; lakini huwezi kumlazimisha kunywa maji”. Mimi nimeshakuonesha majazi katika Qur-ani – na nitazidi kukuonesha baadae – lakini siwezi kukulazimisha kurudi katika haki. Natuendelee na kuzitazama hoja za Sheikh Kasim Mafuta.

KICHANGUZI CHA KULLIYYATUN MUUJIBAH NI “JUZ’IYYATUN SAALIBAH”.

Anasema Sheikh wetu Kasim bin Mafuta:

Na kwa kuzitumia njia za kimantiki (logic) wanasema kwamba;

782 - Sura 8, Aya 17. 783 - Al-Imamu Badru Al-Din Al-Khalili Jawahiru Al-Tafasir, Juz-u Khaas uk. 77-78.

247

Page 248: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

سالبة” جزئية الموجبة الكلية نقض““Kichanguzi cha Kulliyyatun Muujibah” ni “Juz’iyyatun Saalibah” Kwamfano: “Kulliyatun Muujibah” kama vile ukisema: kila ambacho kimo kwenye lugha ya kiarabu kinafaa kuwemo katika Qur’an. Maneno hayo yanavunjwa na “Juz’iyyatun Saalibah” ambayo ni kusema: Kuna vitu vingi vimo katika lugha ya kiarabu lakini havifai kuwemo kwenye Qur’an. Na msingi huu (Juz’iyyatun Saalibah” ukithibiti kwa hoja basi msingi huo wa kwanza (Kulliyyatun Muujibah) unaporomoka. Na hapo nyuma tumekuthibitishia kuwepo katika lugha ya kiarabu vitu vingi ambavyo kudai kwamba vimo ndani ya Qur’an ni haramu. Tazama maelezo hayo kwa urefu zaidi katika kitabu “Man’u Jawazil-Majaazi” cha Imamu wa tafsiri katika zama hizi Sheikh Muhammad al-Amin bin Muhammad al-Shin’qitwiy.

JAWABU

Hapa napenda kutoa pongezi zangu kwamba leo Ahlu Sunna wewe unatumia au unasapoti mantiki (logic) kuunga mkono hoja yako. Siisahau jawabu ya Dr. Bakr Abu Zaid aliomjibu mwanachuoni wa Kishia katika mkutano wa fiq-hi uliofanyika hapa Oman ambapo mwanachuoni huyo alitoa hoja kwa kanuni ya mantiki (logic), Dr. Bakr Abu Zaid akamwambia: “Hio ni kanuni ya mantiki (logic) na wanavyuoni hawakutegemea mantiki (logic) katika kuthibitisha hukumu za kisharia”.784 Sheikh Kasim! Mantiq si elimu inayotegemewa katika uwanja wa Sharia. Bali wengine wanasema – nami nawaunga mkono – kwamba mantiki si elimu kamwe. Qur-ani na Sunna zina fani zake za kuzifasiria muhimu yao ni fani za lugha (Nahau, Sarfu na Balagha).

Kwa ufupi ni kuwa hio ni hoja ya kuunda isio na msingi, kwani kama tulivyoeleza kwamba ikiwa kila kilichomo katika Kiarabu hakimo katika Qur-ani, suali ni kuwa je baadhi ya yaliomo katika Kiarabu yamo katika Qur-ani au hayamo? Kama yamo, je majazi katika hayo baadhi ya yaliomo katika Qur-ani, nayo yamo? Kama hayamo, basi tuletee kamba tulioamrishwa kushikamana nayo katika Aya:

الله بحبل واعتصموا جميعاNa kamataneni na kamba ya Mwenyezi Mungu kwa pamoja.785

Sheikh Mafuta una deni la kamba hii, utuletee au utwambie inapopatikana. Hapa sitaki kurefusha kwani maelezo yakutosha yametangulia na nyongeza nyingi itakuja in shaa Allah.

784 - Au maneno yalio na maana hio. 785 - Sura ya 3 Aya ya 103.

248

Page 249: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Anasema Sheikh Kasim Mafuta:

HOJA YAO YA TATU

Pia ukitazama kwa makini utakuta kuwa hakuna vigezo na vidhibiti vya uhakika katika kuitolea Ta’arif (definition) sahihi “Majaazi al-Mur’sal” (Absolute Metaphor), na matumizi yake, na hilo linasababisha mgongano katika matumizi yake kilugha jambo ambalo ni muhali kuwemo katika Qur’an. Kwa mfano mtu akisema: “Nimeingiza kidole sikioni”. Kwa mujibu wa maelezo ya wenye kudai kuwepo majazi wanasema kuwa hapo kuna “Majaazul-Mursal” (Absolute Metaphor) na maana yake ni kwamba umeingiza baadhi ya kidole, kwa sababu kidole chote hakiingii sikioni, kwa hiyo utakuwa umekitaja kidole lakini makusudio ni baadhi yake.

Wakiwa wanaifanyia kazi “Qaaidah” (kanuni) iliyopo katika “Majaazil Mursali” (Absolute Metaphor) isemayo: “Min It’laaqil-Kulli wa Iraadatil-Ba’adhi” (ni kukitaja kitu kizima lakini makusudio ni baadhi yake)”. Lakini ukifanya utafiti wa kina utagundua kwamba wenye kuitumia “Qaaidah” (kanuni) hii wameshindwa kuidhibiti kitaalamu, kiasi ambacho inafikia kuifanya sehemu kubwa ya lugha ya kiarabu kama si yote kuwa ni Majazi! Jambo ambalo si sahihi.

Kwa sababu wanakubaliana wataalamu wote wa lugha ya kiarabu kwamba matumizi ya maneno katika maana zake za asili ni mengi zaidi kuliko maana za ki-Majazi. Na hilo linapingana na kanuni hiyo na nyinginezo za kimajazi. Kwa kuitumia “Qaaidah” hiyo ya kukitaja kitu kizima lakini makusudio ni baadhi yake, kunavunja itifaki hiyo. Kwamfano, mtu akisema: Nimekula wali, au Nimekunywa maji, au Nimekwenda Makka. Kwa mujibu wa kanuni hiyo yanakuwa maneno yote hayo ni “Majazi” hata kama wenye kuyathibitisha hawasemi hivyo, lakini kanuni hiyo waliyoiweka ndiyo inavyoelekeza, kwa sababu utaambiwa wewe umekula baadhi ya wali na hukula wali wote. Na utaambiwa kuwa umekunywa baadhi ya maji na hukunywa maji yote. Na umefika baadhi ya sehemu za jiji la Makka na hukufika Makka yote, pengine umefika Mina, Aziiziyyah, Ajyaad, Ghaza na katika msikiti mtukufu, lakini hukufika Misfala, wala Hafaair, wala Ka’akiyyah na sehemu nyinginezo katika mitaa ya Makka, kwa hiyo ukisema nimefika Makka ni majazi kwa kuwa umetaja Makka lakini makusudio yako ni baadhi yake.

Halikadhalika ukisema nimekaa msikitini, au nyumbani, au darasani, au ofisini, maneno yote hayo ni majazi kwa sababu kiuhakika kabisa utakuwa hukukaa katika msikiti wote bali umekaa katika baadhi ya eneo la msikiti, au nyumba, au darasa, au ofisi. Hivyo basi, kwa sababu ya

249

Page 250: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kukosekana udhibiti ulio makini wa suala hili ndiyo baadhi ya maulamaa wakasema kuwa maneno yote hayo ni hakika na wala si majazi na mtiririko wa maneno (context) ndiyo ulio ainisha maana ya maneno hayo.

JAWABU

Uchambuzi wako huu unaashiria mambo mawili:1) Huwezi kufanya tahqiq ya yanayosemwa.2) Hukuifahamu vyema “Majaazul-Mursal”.

Na kabla ya yote natuanzie na madai yako uliposema:

Kwa sababu wanakubaliana wataalamu wote wa lugha ya kiarabu kwamba matumizi ya maneno katika maana zake za asili ni mengi zaidi kuliko maana za ki-Majazi. Na hilo linapingana na kanuni hiyo na nyinginezo za kimajazi. Kwa kuitumia “Qaaidah” hiyo ya kukitaja kitu kizima lakini makusudio ni baadhi yake, kunavunja itifaki hiyo.

Tunauliza: makubaliano haya yako wapi? Hili ndilo tatizo lenu: kitu musichokijua au mukitakacho basi munakipamba kwa usemi: “Umma umekubaliana” au “Al-Salafu Al-Salih wamekubaliana” au ‘Hakuna khilafu juu ya hili”. Ilikuwa useme kwamba jumhur ya “wataalamu wa lugha wanasema kwamba matumizi ya maneno katika maana zake za asili ni mengi zaidi kuliko maana za ki-Majazi”. Ama makubaliano ya wote hayapo. Ibn Al-Jinni – kwa mfano – anasema: “Asilimia kubwa ya lugha ni majazi”.786 Anasema Ibn Al-Qayyim: “Na kwa hakika baadhi ya Maimamu wa nahau wamesema kwamba asilimia kubwa zaidi ya lugha ni majazi”.787

…. “Na Jahmu (bin Safwaan) kajipa (kanuni kwamba) asilimia kubwa ya lugha ni majazi”. 788 Anasema Abu Al-Balqaa: “Asilimia kubwa zaidi ya lugha ni majazi”.789

Hivi ndivyo walivyosema Maimamu hao. Lakini ninavyoona mimi ni kuwa hakuna khilafu ya hakika baina ya waliosema kuwa majazi ni mengi zaidi

786 - Ibn Jinni, Al-Khsaais j. 2, uk. 308. Na akainuku pia kauli hii Al-Imamu Al-Shaukani katika Irshaadu Al-Fuhuul uk . 36. 787 - Ibn Al-Qayyim Al-Sawaa’iqu Al-Mursala j. 451. 788 - Ibn Al-Qayyim Al-Sawaa’iqu Al-Mursala j. 456. 789 - Abu Al-Balqaa Al-Kulliyyaat j. 1, uk. 1600.

250

Page 251: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kuliko hakika na waliosema kuwa hakika ndio nyingi zaidi kuliko majazi. Na tahrir ya hayo ni kuwa maneno mengi yanakuwa kiasili yana maana kadha; kisha yanatumiwa kwa maana nyengine ilio karibu na ile ya asili kwa sababu ya kuwepo munasaba au alaaqa (uhusiano) baina ya maana ya asili na ile iliotumiwa baadae. Kisha ile maana ya pili inatumika sana na kuenea hadi inafika kwamba neno hilo likitajwa tu basi huwa haifahamiki ila ile maana ya pili: isio ya asili. Na hapa inakuwa maana ya pili ndio ya uhakika kama walivyosema: حقيقةال لحقالمجاز كثرإذا (Matumizi ya majazi yakikithiri basi huuganishwa na hakika).790 Mfano mmoja mzuri ni neno kitabu. Maana ya asili kabisa ya neno kitabu katika lugha ya Kiarabu ni kitu “chenye kukusanya” au “chenye kuunganisha”. Anasema Al-Imamu Al-Baghawi:

Na asili ya kitabu ni kuunganisha na kukusanya. Na (kikosi cha) jeshi huitwa katiiba kwani (majeshi) wanakusanyika pamoja. Na kitabu kimeitwa kitabu kwa sababu ya kukusanya herufi (na kuziunganisha na) herufi nyengine.791

Hio ndio maana ya asili ya neno hilo. Lakini maana hio imehajiriwa kabisa, na leo ukitaja kitabu, basi kinajulikana papo hapo kuwa unakusudia haya maandishi yaliomo katika karatasi au karatasi zenye maandishi. Maana hii ya pili baadae ilizagaa na ikageuka kuwa sasa ndio maana ya uhakika ya neno hilo; wakati ukitazama asili ya neno basi maana hii ya pili ni majazi. Mfano wa pili ni neno kafiri. Asili ya kilugha ya neno kafiri ni mwenye kufukia au mwenye kufunika. Na kwa sababu hii, mkulima kaitwa kafiri kwa sababu anazifunika mbegu kwa udongo wakati anapopanda mimea, kama ilivyo katika Aya ya Qur-ani inayosema:

} يكون ثم مصفرا فتراه يهيج ثم نباته ار الكف أعجب غيث كمثل }حطاما

Ni kama mvua ambayo mimea yake huwafurahisha wakulima, kisha yakakauka ukayaona yamepiga umanjano, kisha yakawa mabuwa..”.792

Na kwa tahrir hii, ynabainika makusudio ya wale waliosema kwamba asilimia kubwa zaidi ya lugha ni majazi kwani ni kweli kwamba asilimia kubwa ya maneno ya Kiarabu yako hivyo. Na yanabainika makusudio ya 790 - Yaani neno la kimajazi likiwa linatumika sana katika hali hio, basi baadae matumizi yake hayo yanakuwa si majazi tena bali ni hakika. Tazama Ibn Taymiyya Majmu’a Al-Fatawa j. 12, uk. 156, babu ghalat man qaala innahu majaz.Tazama pia kichwa cha habari kilichomo katika kitabu Al-Khasaais cha Ibn Jinni j. 2, uk. 308. Dr. Al-Buti Al-Salafiyya uk. 81-82. 791 - Al-Baghawi Ma’aalimu Al-Tanzil j. 1, uk. 81. 792 - Sura 57, Aya 20.

251

Page 252: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

wale waliosema kwamba asilimia kubwa ya maneno ya Kiarabu ni hakika: si majazi, kwani baada ya yale maneno kuhamishwa kutoka katika maana yake ya asili na kuja katika maana ya pili na maana hio ya pili ikaenea na kuzagaa hadi kufikia kwamba neno hilo linapotajwa haifahamiki ila kwa maana yake hio ya pili basi maana hio ya pili inakuwa sasa ni hakika. Na pia kwa tahriri hii unaondoka mgongano baina ya rai mbili za wataalamu wakuu. Wallahu A’alam.

Tukirudi katika maelezo yako, tunasema: lau tutakubaliana na wewe juu ya hayo ulioyasema, basi hii ina maana kwamba Majaazul-Mursal ni batili: hayakuthibiti. Na kubatilika kwa kuwepo kwa aina moja ya Majazi, hakujabatilisha kuwepo kwa asili ya majazi au kuwepo kwa aina nyengine za majazi. Cha kufahamu ni kuwa sisi hatuzungumzii hizi juz-iyyat (vijisehemu vya kitu), bali tunazungumzia kulliyyat (misingi ya kitu); ama juz-iyyat, watu wanaweza wakatafautiana juu yake ilhali wamekubaliana juu ya kuwepo kwa kulliyyat (misingi). Nimekupa mfano wa tafauti za wanavyuoni juu ya kuitumia Hadithu Mursal kwamba hilo halibomoi uhakika wa kuwepo kwa aina nyengine za Hadithi dhaifu. Kwa hivyo, lau tatasalimu amri mbele ya mantiki yako hii ya kutokuwepo kwa Al-Majazu Al-Mursal je huko kunabomoa kuwepo kwa majazi mengine hususan ukizingatia ukweli kwamba ushahidi wa wazi umesimama juu ya kuwepo kwa majazi hayo?

Ama nukta nyengine ni kuwa kuna tafauti kubwa baina ya majazu mursal na mifano uliotoa. Mfano wa kwanza uliotoa ni: “Nimeingiza kidole sikioni”. Haya kweli ni majazu mursal, lakini itakuwa hivyo pindipo utayazungumzia kwa lugha ya Kiarabu: si kwa lugha ya Kiswahili. Na hii ni kwa sababu katika lugha ya Kiarabu kidole ni kile kiungo kizima. Ama sehemu ya mwisho tu ina jina lake mbali nalo ni banaan (fingertips). Sasa wewe ulipotumia jina la kiungo kizima kwa kumaanisha jina la sehemu ya kiungo hicho, ndipo ilipodhihiri kwamba umetumia neno kinyume na maana yake ya asili, kwani kiungo hicho kamili kina jina tafauti na jina la sehemu yake ya mwanzo ambayo ndio ulioitia wewe masikioni mwako.

Ama mfano wako uliposema: Nimekula wali, huu si mfano sahihi, kwani utaposema hivyo kwa lugha ya Kiarabu ama utatumia alifu na lamu useme:

األرز Ukisema hivi, basi alifu na lamu .(Nimekula wali) أكلتimeshabainisha makusudio kwani alifu na lamu hapa ama zinamaanisha:يدهعال فيرعلتا (1 (Al-taarif Al-‘ahdi) nayo ima ni ذكري au عهد Na hii ina maana kuwa wali ulioula ni wali maalumu, kwa maana .ذهنيya kwamba si wali wote. Na kwa hivyo, maneno haya si majazi bali ni hakika kwani vyombo vya lugha vimeshabainisha makusudio.

252

Page 253: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

2) Au iwe الجنس الماهية pia huitwa لتعريف الحقيقة au لبيان .لبيانKwa maana hii itakuwa lengo lako uliposema األرز Nimekula wali, ni أكلتkubainisha uhakika wa ulichokila tu. Katika hali hizi mbili, inakuwa hakuna األرز :katika maneno (ujumla) عموم Nimekula wali , hata ikafaa أكلتkuuliza “je ulioula ni wali wote au ni baadhi tu” kwani vyombo vya lugha vimeshabainisha makusudio.

Vyenginevyo, ikiwa utasema: أرز اأكلت akaltu urzan (Nimekula wali), bila ya kuweka alifu na lamu katika neno urz, basi sigha (form) hii ni في نكرة

اإلثبات (ujumla) عموم nakira fii siyaaqi al-ithbaat, nayo pia haina سياقndani yake, hata ikafaa kuuliza “je ulioula ni wali wote au ni baadhi tu”. Kwa hivyo, mfano huu si mfano sahihi.

Ama mifano ya: Nimekwenda Makka…nimekaa msikitini, au nyumbani, au darasani, au ofisini, haya yote si majazi, wala si sawa na kusema: أدخلت

األذن في Ubainifu wa .(nimeingizi kidole changu kwenye sikio) إصبعيhaya ni kuwa sehemu ya Makka inaitwa Makka kama vile ambavyo sehemu ya Pemba ni Pemba; sehemu ya msikiti inaitwa msikiti – yote hayo huitwa hivyo kwa uhakika. Ama ncha za vidole (banaan) ambazo ndizo unazozitia katika sikio, katika lugha ya Kiarabu zinaitwa vidole kimajazi.

Hayo ndio maelezo yalionibainikia kuhusu suala hili. Kwa hali yoyote ile itayokuwa, ubainfu wa mwanzo unakutosha kukuongoza kwamba lau tutasalimu amri juu ya maelezo yako ulioyatoa hapa, basi upeo uliomo katika maelezo hayo ni kuwa majazu mursal si sahihi, na kutokuwa sahihi kwa majazu mursal hakumaanishi ubatili wa majazi mengine.

Baada ya hayo tumebakiwa na mambo mawili:1) Tuelewe kwamba waliozungumzia majazu mursal wanakusudia

nini. 2) Je hicho walichokizungumzia kipo au hakipo.

MAKUSUDIO YA MAJAZU MURSAL

Ama suala la mwanzo ni kuwa waliozungumzia kuwepo kwa majazu mursal wanakusudia “Kutumika neno kinyume na maana yake ya asili kwa uhusiano usiokuwa wa kutaka kukifananisha kitu kimoja na chengine; na kwa kuwepo qarina inayoizuia maana ya asili”. Sasa mchambuzi huwa hatazami hii istilahi (techinical term): je tuite majazu mursal au tuite uslub; hili si muhimu katika ulimwengu wa uchambuzi, bali anatazama uhakika wa kile kilichosemwa – kama tutavyoeleza zaidi baadae – je kipo au hakipo?

253

Page 254: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Kwa hivyo, cha kujiuliza hapa ni kuwa je maneno yaliotumika namna hio yaani yaliotumika kinyume na maana yake ya asili bila ya kukusudia kufanya tashbih (kufananisha) yapo au hayapo? Kama hayapo, basi itakuwa kweli hakuna kitu majazu mursal; kama yapo basi hii ina maana kwamba uhakika wa kitu hicho upo ama jina ukipenda kuita majazu mursal ita hivyo; kama hupendi tafuta jina jengine ukiite, sisi hatugombanii majina bali tunazungumzia uhakika wa kitu, kwani kama tulivyonukuu zaidi ya mara moja kwamba wataalamu wanasema: ا في مشاحة إصطالحلال Hakuna kujadiliana katika maneno ya kitaalamu au ya kifani (technical terms). Pia kasoro zilizomo katika vijipengele vya kitu, havibomoi uhakika wa misingi ya kitu hicho.

Sasa ili ujue kwamba kitu hicho (majazu mursal) kipo, soma mfano mmoja ufuatao – na mifano iko mingi imetajwa katika vitabu vya balagha. Anasema Allah:

( تصلى3) ناصبة ( عاملة2) خاشعة يومئذ وجوه (4) حامية ناراNyuso siku hio zitahizika*Zitakuwa ni zenye kufanya kazi ngumu*Zitauingia moto mkali.793

Hapa utaona kwamba kumetajwa nyuso kuwa ndizo zitazoingia motoni, bila ya kutajwa mtu kamili ilhali atayeuingia moto ni mtu kamili: si uso tu. Kwa hivyo, imetajwa sehemu ya kitu na kilichokusudiwa ni kitu kamili. Wala haikukusudiwa kufananishwa kitu kimoja na chengine. Hiki ndicho wataalamu wanachoita Al-Mjazu Al-Mursal. Je kipo au hakipo? Narudia tena: sizungumzii majina: ninazungumzia uhakika wa kitu (facts au .(حقائق

KUICHEZEA LUGHA NA QUR-ANI

Anasema Sheikh Al-‘Allama Kasim bin Mafuta:

Pia maulamaa wanaopinga kuwepo kwa majazi wanapowahoji na kuwapa changamoto (challenge) wenye kuthibitisha kuwepo kwa majazi hawapati majibu yoyote ya kuridhisha ndipo pale wakalipinga suala hili ili:-Lugha ya kiarabu isichezewe.-Ili watu wa batili wasipate nafasi ya kuichezea Qur’an kwa kupotosha maana yake kwa madai ya kwamba kuna majazi, na hili walilolifikiria ndilo lililotokea.

793 - Sura 88, Aya 2-4.

254

Page 255: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Kwa sababu wamejitokeza baadhi ya watu wakazipotosha aya nyingi zinazotaja sifa za Allah kwa madai kwamba kuna majazi kwa madai ya kumtakasa Allah na sifa za viumbe na hatima yake wakaingia katika upotofu.

Mpaka hapo itabainika kwamba;

Kupinga kuwepo kwa Majazi ndani ya Qur’an ili kufunga milango ya kuwaingiza watu kwenye upotofu ndiyo msimamo sahihi na wa haki na unaokubaliana na akili794 zaidi kuliko kudai kinyume chake. Mwisho wa kunukuu.

JAWABU

Hayo ndio maneno ya Sheikh huyo wa Pongwe Tanga, nayo si maneno madhubuti. Kwani wanaopinga kuwepo kwa majazi wanapewa jawabu za wazi kabisa, lakini huwezi kumlazimisha farasi kunywa maji; unachoweza ni kumchukua hadi mtoni. Vyengine, tupeni maana ya kamba iliotajwa katika Aya:

الله بحبل واعتصموا جميعاNa kamataneni na kamba ya Allah kwa pamoja.

Na katika Aya:

ثقفوا ما أين الذلة عليهم ضربت الناس من وحبل الله من بحبل إالWamepigwa udhalili popote walipo, isipokuwa (wakishikana)

na kamba ya Allah na kamba ya watu.

Na mutupe maana mkono uliotajwa katika Hadithi:“ يد ”المسلمون

Waislamu ni mkono.795

Na Hadithi:السفلى اليد من خير العليا اليد

Mkono wa juu ni bora kuliko mkono wa chini.

Na ubeti wa babu yake Mtume (s.a.w.) aliposema:

*** يدا لي واجعله ربي اردده محمدا ولدي علي ردNirejeshee (é Mwenyezi Mungu) Muhammad

794 - Akili ya nani?! 795 - Al-Rabi’u bin Habib Al-Jami’u Al-Sahih j. 4, uk. 354, Hadithi na. 903. Anasema mtiaji maelezo: “Kaitaja pia mwenye kitabu Kanzu Al-’Ummal uk. 441,442,443.

255

Page 256: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

mwanangu Mrejeshe é Mola wangu na umfanye kuwa mkono wangu.796

Na mutupe maana ya neno jua lililotajwa katika ubeti wa mashairi yasemayo:

** الشمس من تظلني شمس عجب ومن تظلني قامتAlisimama akanifunika kivuli, na ni ajabu** Jua linanikinga (linanipa kivuli) dhidi ya jua.

Jamani! Wapi mumepata kuona kwamba jua linamziba (linamzinga) mtu asipigwe na jua? Haya! Twambie Sheikh Kasim bin Mafuta! Haya si majazi ni nini?

Kwa hivyo:1) Ni wazi kwamba nyinyi ndio munaoichezea lugha ya Kiarabu kwani

lugha inathibitisha kuwepo kwa majazi; nyinyi munakanusha. 2) Nyinyi ndio munaochezea Qur-ani, kwani Qur-ani inathibitisha

kuwepo kwa majazi tena kwa wingi sana; nyinyi munakanusha.

Ama kauli yako uliposema:

Ili watu wa batili wasipate nafasi ya kuichezea Qur’an kwa kupotosha maana yake kwa madai ya kwamba kuna majazi, na hili walilolifikiria ndilo lililotokea.

Ninasema: hiki ndicho munachokiogopa. Munachokiogopa katika kuyakanusha majazi ni kuanguka kwa itikadi zenu batili za tashbihi na tajsim. Nami ninakwambia ewe Sheikh Kasim Mafuta, tukijaalia kuwa hizo itikadi zenu za Mungu mwenye viungo na sura ya binaadamu kuwa ndio itikadi sahihi, na itikadi zetu za kumtakasa Allah kutokana na sifa za viumbe ndio batili, basi ilivyo ni kuwa huwezi kutibu batili kwa batili. Huwezi kukataa majazi kwa kukimbia Mungu wako mwenye mikono asije akakatwa mikono yake; majazi yapo yapo tu, na hamuna uwezo wa kuyakanusha kwa hoja hata mukikusanyika Mawahabi wa dunia nzima – binaadamu na majini pamoja.

Ama kauli yako uliposema:

796 - Ubeti huu niliuhifadhi miaka mingi kutoka katika kitabu kiitwacho ‘Uyuunu Al-Taarikh kiasi cha kwamba sikumbuki tena juzuu na ukurasa. Lakini nimeukuta tena katika kitabu Al-Ma’arifa Wa Al-Ta’arikh cha Al-Fasawi j. 3, uk. 281 kwa lafdhi isemayo:

يدا ... عندي واصطنع ربي أردده محمدا راكبي إلي رد

256

Page 257: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Mpaka hapo itabainika kwamba: kupinga kuwepo kwa Majazi ndani ya Qur’an ili kufunga milango ya kuwaingiza watu kwenye upotofu ndiyo msimamo sahihi na wa haki na unaokubaliana na akili zaidi kuliko kudai kinyume chake.

Ninasema: upotofu ni kukikanusha kitu kilichothibiti katika Qur-ani au Sunna. Sisi tumekuthibitishia kwa Aya nyingi za Qur-ani, kwamba kuna majazi, na wewe umetoa hoja za kifalsafa ya Kigiriki. Kilichobaki utwambie je maneno hayo yaliotumika katika Aya hizo na Hadithi hizo na maneno hayo ya Waarabu yametumika katika maana yake ya asili, au yametumika kinyume na maana yake ya asili ili tuweze kutoa hukumu adili juu ya kuwepo kwa majazi na kutokuwepo.

Anaendelea Sheikh Kasim kwa kusema:

Na ama baadhi ya mifano ambayo hutolewa kama ni hoja ya kuwakandamiza wenye kupinga majazi Imamu Ibnul-Qayyim katika kitabu chake “AL-SWAWAAI’QUL-MUR’SALA” ameyajibu kwa ufundi mkubwa mno. Kadhalika Imamu wa Tafsiri na Usuul katika zama hizi sheikh Muhammad al-Amin al-Shanqitwiy pia amezijibu hoja nyingi tena kwa ufanisi wa hali ya juu kwa mwenye kutaka faida na arejee kwenye kitabu chake: “MAN’U JAWAAZIL-MAJAZI” Na ukizitazama kwa makini hoja zao utagundua kwamba tofauti ni ya kimatamshi, hawa wameona utaratibu huo wauite “Majazi”, na kwa hakika hilo lina mapungufu mengi kama tulivyo thibitisha hapo nyuma.

Na wengine wameona wauite “Usluubun min Asaalibil-Lugha” (utaratibu/mfumo katika taratibu za lugha) na njia hii ndiyo iliyokaribu na usahihi, ili kuwazuia watu wa batili wasiyapotoshe maandiko kwa kuupitia mlango huu.

JAWABU

Ama kuhusu kitabu Al-Sawaai’qul-Mur’sala cha Al-Imamu Shamsu Al-Din, Ibn Al-Qayyim Al-Zar’i, nakujuilisha kwamba kitabu hicho kimejibiwa hoja moja moja na Al-Imamu Badru Al-Din, Sheikh Al-Mufassirin, Mujthid Al-’Asr, Al-Allama Al-Jami’u Ahmad bin Hamad Al-Khalili Al-Mufassir. Jawabu hio inaitwa Jawaahiru Al-Tafsir Juz-u Khaas, tafadhali itafute uisome. Utakuta humo yenye kuupoza moyo wako. Ninachotaka kukwambia ni kuwa wakuu wako kule Suudia kimewashinda kukijibu kama walivyoshindwa kutoa jawabu sahihi kwa kitabu Al-Haqqu Al-Damigh. Lakini tatizo lenu wenzetu ni kuwa hamuna munachokijua isipokuwa Ibn Taymiyya na Ibn Al-Qayyim!

257

Page 258: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Bali kitabu hicho cha Ibn Al-Qayyim, hakina hoja isipokuwa shubuhati tupu. Watu wanakwambieni “Haya majazi” nyinyi hamuna jawabu ya kuyakataa; halafu munasema hakuna majazi, sasa kama hakuna majazi hiki ni nini? “Huu nchele” wewe huwezi kuukataa kwani unauona kuwa kweli “ni nchele” lakini unashikilia kauli yako “hakuna nchele”. Basi haya bakieni hivyo hivyo kufuata kama bendera au al-taqlidu al-a’ama.

Ama kauli yako uliposema:

Na wengine wameona wauite “Usluubun min Asaalibil-Lugha” (utaratibu/mfumo katika taratibu za lugha) na njia hii ndiyo iliyokaribu na usahihi, ili kuwazuia watu wa batili wasiyapotoshe maandiko kwa kuupitia mlango huu.

Ninasema: yote haya yanaonesha yale yale tulioyasema na kuyakariri kwamba ima ukweli huutaki au hujui kuhakiki mambo! Sisi bwana hatutafautiani katika majina: bali tunatafautina katika uhakika wa kitu – je kipo au hakipo. Majazi ni “kutumika neno kinyume na maana yake ya asili”. Je uhakika wa matumizi haya upo au haupo? Kama upo basi hayo ndio majazi yenyewe ukiwa utayaita majazi au “Usluubun min Asaalibil-Lugha” (utaratibu/mfumo katika taratibu za lugha). Sheikh Kasim upo? Haya majina ni istilahiyya (technical terms) zilizoekwa na wanavyuoni ili kurahisisha kufahamiana katika uwanja wa elimu; ama uhakika wa kile kitu ndio wa kuzungumziwa.

Hadi hapa tutakuwa tumefika mwisho wa kuzijadili shubuhati za Sheikh Mafuta kuhusu Majazi. Sasa natuchukue fursa hii kwa kulielezea tena suala la majazi kwa ufupi ili tuweze kuwa katika ubainifu juu ya jambo hili.

MAELEZO ZAIDI JUU YA KUWEPO KWA MAJAZI Baada ya mjadala huo sasa natuizungumzie maudhui hii kwa ufupi. Elewa ndugu msomaji kwamba jumhur (majority) ya Wanavyuoni wa Kiislamu katika madhehebu zake tafauti wanasema kuwa majazi ni kitu kilichopo katika Qur-ani, Hadithi za Mtume (s.a.w.) na lugha ya Kiarabu. Kama vile ambavyo Al-Salaf Al-Saalih (watangulizi wema, Masahaba na wanafunzi wao) wote wametumia majazi katika maneno yao ya kawaida (prose) na mashairi yao hata kama jina hilo halikuwepo. Wakati – kwa upande wa pili – wengine wachache sana – aghlabu ya wachache hao ni baadhi ya watu wa madhehebu ya Hanbali – wamekanusha kuwepo kwa majazi! Sababu iliowafanya watu hao wayakanushe majazi, si kwamba majazi hayapo, bali

258

Page 259: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

ni kuwa kukubali kuwepo kwa majazi kutapelekea kuibomoa itikadi yao ya kuwa Allah ana viungo, ambavyo ukweli wake ni kuwa vimetajwa katika Qur-ani na Hadithi kimajazi (figuratively)! Na kwa sababu hio ya kukanusha kwao majazi, basi Allah aliposema: “Mkono wa Allah uko juu ya mikono yao”797 na akasema “Nini kilichokuzuia usimsujudie yule niliyemuumba kwa mikono yangu miwili”,798 wenye kukanusha kuwepo kwa majazi wakasema kuwa Allah ana mikono kweli kweli!

Miongoni mwa waliokuwa mstari wa mbele katika kukanusha kuwepo kwa majazi ni Al-Imamu Ibn Taymiyya na mwanafunzi wake Al-Imamu Ibn Al-Qayyim.799 Lakini hoja walizozitegemea juu ya ukanushaji wao huo ni dhaifu kuliko nyumba ya buibui! Hoja yao kubwa ni kuwa wanavyuoni wa lugha wa mwanzo hawakuigawa lugha ya Kiarabu katika migawanyiko miwili hio ya majazi na hakika, bali hayo yalifanywa na waliokuja baadae!800 Anasema Ibn Taymiyya:

Hakika ya wengi katika hawa (wenye kukubali majazi) wameigawa lugha (sehemu mbili): majazi na hakika….bali Maimamu wa lugha kama Al-Khalil, Sibawayh, Al-Kisaai, Al-Farraau na walio mfano wa hao, na Abu ‘Amri bin Al-’Alaa na Abu Zaid Al-Ansari na Al-Asma’i na Abu Amri Al-Shaibani na wengineo hawakuigawa (lugha) kama walivyoigawa hawa.801

Na hoja hio akaikariri Ibn Al-Qayyim kwa kusema:

Wala hakuna yoyote katika Waarabu kamwe aliyesema kwamba neno hili ni hakika na hili ni majazi; wala hakuna hayo katika maneno ya walionukuu lugha ya Waarabu kwa kuzungumza nao mdomo kwa mdomo au kwa kupitia kwa mtu mwengine; kama vile ambavyo hakuna (suala la kuwepo kwa majazi) katika maneno ya Masahaba, wala Tabiina (wafuasi wao) wala Tabii Tabiina (wafuasi wa wafuasi) wala yoyote katika Maimamu Wanne.802

Na akasema Ibn Al-Qayyim:

797 - Sura ya 48 Aya ya 10.798 - Sura 38, Aya 75.799 - Ibn Qayyim kaandika kitabu maalumu juu ya kukanusha majazi, na akarefusha sana kwa hoja ambazo hazina kichwa wala miguu. Hoja hizo zimejibiwa moja moja na Sheikh Al-Khalili katika tafsiri yake Jawahiru Al-Tafasir Juzuu Khas. Anayetaka kuona jawabu juu ya dai moja moja la Ibn Al-Qayyim na-arejee tafsiri hio. 800 - Hoja zao nyengine ni kama alivyozileta Sheikh Mafuta. Na umejionea mwenyewe udhaifu wa hoja hizo. 801 - Ibn Taymiyya Majmu’u Al Fatawa j. 20 – juzuu inayohusu Usulu Al fiqh – uk. 230, na mfano wake katika j. 8, uk. 65.802 - Ibn Al-Qayyim Mukhtasar Al Sawaiq Al Mursala uk. 231-232.

259

Page 260: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Na itapoeleweka kwamba migawanyiko ya maneno katika hakika na majazi si migawanyiko ya Kisharia, wala ya kiakili wala ya kilugha, basi (utakuwa umeelewa kwamba migawanyiko hio) ni ya kifani tu (kiistilahi). Na fani hii imejitokeza baada ya karne tatu zenye ubora kwa mujibu wa andiko. 803

Hayo ndio maelezo ya Maimamu wawili hao: Ibn Al-Qayyim na Sheikh wake Ibn Taymiyya, nayo si maneno yenye uzito katika mezani ya elimu kwani:

1) Kama vile ambavyo Masahaba na Wafuasi wao hawakusema kuwa haya ni majazi, pia hawakukanusha kuwepo kwa majazi.

2) Ikiwa kutokuigawa kwao lugha katika migawanyiko ya majazi na hakika ni dalili kwamba hakuna majazi, basi inabidi kwamba na hio pia iwe dalili ya kutokuwepo kwa hakika, kwani hawakutaja mgawanyiko huu wala ule!

3) Kinachozingatiwa ni ushahidi wa kitu: si nani kakisema au hakukisema; lini kimesemwa au hakikusenwa.

4) Nne – na ndio muhimu – ni kuwa Maimamu wawili hawa wameshindwa kutafautisha baina ya kuwepo kwa uhakika wa kitu (the existence of a fact) na kuvumbuliwa kwa neno la kifani au la kitaalamu la kitu hicho (the rise of a technical word). Uhakika wa majazi ulikuwepo tangu enzi ya Mtume (s.a.w.) na kabla yake, lakini neno lake la kifani ndilo ambalo limeundwa baada ya kuundwa kwa fani za elimu. Kwa mfano, enzi ya Mtume (s.a.w.) hakukuwa na elimu ya Nahau, wala Sarfu, wala Usulu Al-fiqhi wala Tajwid, wala ‘Ulumu Al-Hadith – yaani majina ya fani hizo zote yalikuwa hayapo. Hizi zote ni fani ambazo zimeundwa baadae lakini uhakika wa fani hizo ulikuwepo tangu zamani. Waarabu husema kwa mfano: “Ali yadh-habu” watu wa Nahau husema kuwa Ali ni “Mubtada (kianzilishi)”. Sasa maneno “Ali yadh-habu” yalikuwepo tangu enzi ya Mtume (s.a.w.), lakini jina la kifani au la kinahau la kuuita muundo huu kuwa ni “Mubtada (kianzilishi)” ndilo lililogunduliwa baadae – uhakika ulikuwepo na jina la kifani limefuata baadae. Halkadhalika nikisema Hadithi hii ni dhaifu au hasan au maudhui au mursal au mu’allaq au mawquf, majina yote haya yamepangwa na wataalamu wa Hadithi: hayakuwepo katika enzi ya Mtume (s.a.w.) wala katika enzi ya Masahaba, lakini uhakika wake ulikuwepo. Kwa kufahamu zaidi tazama ukweli kwamba wanasayansi leo wanagundua vitu vilivyokuwepo miaka nenda miaka rudi ndani ya

803 - Ibn Al-Qayyim Mukhtasar Al Sawaiq Al Mursala uk. 233. Kasahau Ibn Al-Qayyim kwamba kinachozingatiwa si wakati bali ni dalili.

260

Page 261: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

miili yetu na katika ulimwengu, kisha baada ya ugunduzi huo wanavipa majina vitu hivyo – uhakika wa vitu hivyo ulikuwepo lakini majina ni ugunduzi wao. Sasa leo itakuwa ni jambo la ajabu ikiwa atatokea mtu atasema kwamba si kweli: hakuna sayari inayoitwa pluto kwani waliotangulia hawakuitaja! Kwa hivyo, uhakika wa sayari hio upo na ulikuwepo tangu ulipoumbwa ulimwengu; na jina ndilo waliloliunda watu ili kurahisisha kufahamiana katika masomo na mazungumzo yao. Kwa hivyo, halkadhalika majazi: uhakika wake ulikuwepo lakini jina ndilo ambalo limeundwa na watu, na kuchelewa kwa Technical term (jina la kifani) hakumaanishi kutokuwepo kwa uhakika wa kitu.

Ama madai ya Ibn Taymiyya aliposema:

..Hakuna shaka kwamba wengi wa hawa wameyagawa (maneno ya Kiarabu) mgawanyiko huo (wa hakika na majazi), lakini hakuna katika wao Imamu wa fani yoyote katika fani za kiislamu wala tafsiri, wala Hadithi wala fiq-hi wala lugha wala nahau, bali Maimamu wa nahau kama Khalil, Sibawayh, Al-Kisaai…………hawakuigawa (lugha) kama walivyoigawa hawa.804

Na madai ya Ibn Al-Qayyim aliposema:

…..Kama vile ambavyo hakuna (suala la kuwepo kwa majazi) katika maneno ya Masahaba, wala Tabiina (wafuasi wao) wala Tabii Tabiina (wafuasi wa wafuasi) wala yoyote katika Maimamu Wanne.805

Utaona kwamba maneno hayo yako mbali mno na tahqiqi za kielimu. Bali maneno hayo yanatokana na ile ile kawaida yao ya kila kitu chao wanachokitaka wao basi inakuwa: “Umma umekubaliana” na inakuwa: “Hii ndio kauli ya Al-Salaf Al-Saalih (watangulizi wema)” japo kuwa ukweli uko kinyume na hivyo!

Naturudi katika madai kwamba hakuna yoyote katika hao ambao Ibn Al-Qayyim na Sheikh wake wamewataja aliyezigawa lafdhi za lugha ya Kiarabu migawinyiko hio ya majazi na hakika. Tunasema: ama iwe Ibn Al-Qayyim na Ibn Taymiyya wanakusudia, kwa maneno hayo, kwamba:

1) Hakuna yoyote aliyelitaja neno majazi.

804 - Ibn Taymiyya Majmu’u Al Fatawa j. 20 – juzuu inayohusu Usulu Al fiqh – uk. 230, na mfano wake katika j. 8, uk. 65.805 - Ibn Al-Qayyim Mukhtasar Al Sawaiq Al Mursala uk. 231-232.

261

Page 262: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

2) Au iwe wanakusudia kwamba hakuna aliyetumia majazi (yaani aliyelitumia neno kinyume na maana yake ya asili) hata kama hakuliita majazi.

Ama nukta ya mwanzo utaona ni kinyume na mengi yaliotajwa na wanavyuoni watangulizi. Miongoni mwa hao ni yule ambaye Ibn Taymiyya mwenyewe katoa wasia wa kuwa kitabu chake kisomwe. Huyu si mwengine bali ni ‘Uthman bin Said Al-Darimi. Anasema ‘Uthman Al-Darimi akimjibu Bishr Al-Marsi:

مجاز على بقلوبهم، الناس يعقله الذي المجاز على يجوز هذا فمثلالعرب كالم

Mfano wa (maneno haya) unajuzu kwa misingi ya majazi wanayoyaelewa watu kwa nyoyo zao; kwa misingi ya majazi ya lugha ya Waarabu.806

Na anasema:

المجاز على جائز المعروف في ههنا هذا

Hili hapa kama inavyojulikakana linafaa kwa misingi ya majazi.807

Na anasema:المجاز على مثل الزرع ضحك

Konde imecheka ni mfano wa kimajazi. 808

Na anasema:

معنى على وتسمع تتراءى والقصور الجبال الكالم مجاز في يقال وقدبعض يقابل بعض ����أنها ا���ها

األصوات وتبلغها

Na huenda ikasemwa katika maneno ya kimajazi kwamba milima na majumba yanaonana na yanasikia kwa maana kwamba yanaelekeana na kufikiwa na sauti. 809

Hayo ni maneno ya ‘Uthman Al-Darimi (280 A.H.), yamo ndani ya kitabu ambacho Ibn Taymiyya alikuwa anausia sana kuwa tukisome ili tupate 806 - ‘Uthmaan bin Said Al-Darimi Al-Raddu ‘Alaa Al-Marisi j. 1, uk. 29. 807 - ‘Uthmaan bin Said Al-Darimi Al-Raddu ‘Alaa Al-Marisi j. 3, uk. 156. 808 - ‘Uthmaan bin Said Al-Darimi Al-Raddu ‘Alaa Al-Marisi j. 3, uk. 176. 809 - ‘Uthmaan bin Said Al-Darimi Al-Raddu ‘Alaa Al-Marisi j. 1, uk. 50.

262

Page 263: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kumjua Mungu mwenye viungo! Sasa vipi tena wanadai kwamba hakuna aliyetaja majazi katika karne tatu za mwanzo wala hakuna Imamu yoyote wa fani za elimu aliyeyataja? Hapa inakubainikia ndugu msomaji ukweli kwamba watu hawa wanapenda kuwasingizia Al-Salaf katika itikadi zao wanazozitaka wao. Halafu wanakuwa mabingwa wakubwa wa kuwaita watu waongo! Sasa sijui Sheikh Kasim Mafuta atawaingiza Maimamu wawili hawa katika orodha ya waongo au vipi?

Ama Al-Jahidh (250 A.H.), yeye anasema kuhusu Aya isemayo:

اليتامى أموال يأكلون الذين إن بطونهم في يأكلون إنما ظلما نارا وسيصلون سعيرا

“Hakika wale wanaokula mali za mayatima kwa dhulma, kwa hakika wanakula moto katika matumbo yao na watauingia moto mkali…….”.810Anasema Al-Jahidh katika kitabu chake Al-Hayawaan811 kuhusu Aya hio: “ آخر مجاز 812.(Na haya ni majazi mengine) ”وهذا

Ama Al-Imamu Al-Shafi (150-204 A.H.), yeye kanukuliwa na Al-Bazdawi (483) akisema:

الطالق بلفظ يقع والعتاق مجازا التحرير بلفظ يقع الطالق إنمجازا

Hakika ya talaka inasibu kwa kutumia lafdhi ya ukombozi813 kimajazi, na kuachia huru mtumwa kunasibu kwa kutumia lafdhi ya talaka kimajazi.814

Na – kama alivyoyataja kwa uwazi – Al-Imamu Al-Shafi pia kaashiria juu ya kuwepo kwa majazi katika kitabu chake Al-Risala hata kama hakuyataja kwa jina, lakini alisema:

... سياقه في يعرف وظاهرا بلسانها العرب بكتابه الله خاطب فإنماظاهره غير يراد أنه

810 - Sura 4, Aya 10. 811 - J. 5, uk. 25. 812 - Nukulu kutoka kwa Dr. Zakariya Qira-atu Jadaliyya uk. 138. Na Al-Imamu Badru Al-Din Al-Khalili Jawaahiru Al-Tafsir Juz-u Khaas uk. 122.813 - Yaani lau mtu atamwambia mkewe “nimekuweka huru au nimekupa uhuru au wewe uko huru”.. 814 - Yaani lau mtu atamwambia mtumwa wake “Anta Taaliq” (nimekuacha), basi mtumwa huyo anakuwa huru. Lakini nijuavyo mimi ni kuwa lafdhi kama hizi ni kinaya kwa hivyo, mke haachiki wala mtumwa hakomboki ila iwe niya ya muachaji na mkomboaji ni kuwacha na kukomboa.

263

Page 264: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Kwa hakika Allah kazungumza na Waarabu katika Kitabu chake kwa lugha yao….na (andiko) dhahir (wakati mwengine) linafahamika katika mtiririko wake (siyaaq yake) kwamba halikukusudiwi udhahiri wake.815

Halkadhalika kasema Al-Imamu Al-Shafi katika Diwani yake:

كليلة عيب كل عن الرضا تبدي ***عين السخط عين ولكنالمساوي

Jicho la kuridhia limechoshwa na kila aibu (halijishughulishi na aibu za watu); na jicho la chuki (kazi yake ni) kudhihirisha maovu (ya watu).816

Sasa tuseme Al-Imamu Al-Shafi anakusudia kusema kwamba neno kuridhia na neno kuchukia yana macho kweli kweli?

Hayo ni maneno ya Al-Imamu Al-Shafi, nayo yako wazi juu ya suala la kuwepo kwa majazi. Kwa hivyo, ni wazi kwamba Al-Imamu Al-Shafi kazungumzia majazi hata kama katika nukulu mbili hizi za mwisho hakuyapa jina hilo, na jina – kama tulivyosema na kukariri – si muhimu: kilicho muhimu ni uhakika wa kitu.

Ama Al-Imamu Al-Ash’ari,817 yeye kanukuliwa na Ibn Al-Qayyim akithibitisha majazi. Anasema Ibn Al-Qayyim:

على العبد وفعل الحقيقة على لله فعل العباد أفعال بل فرقة وقالتاألشعري قولي أحد وهذا المجاز

Na wengine wakasema: ‘Bali vitendo vya waja kiuhakika ni vitendo vya Allah,818 na ni vitendo vya mja kimajazi (tu), na hii ni moja ya kauli mbili za Al-Ash’ari.819

Anasema Ibn Taymiyya:

أحمد . اإلمام كالم في إال األئمة من أحد كالم في المجاز لفظ يعرف ولمكتبه فيما الرد من فإن

والجهمية الزنادقة القرآن )على مجاز من : ((.)هذا ولم.. فتاواه في وقالأحد ب��هذا من ينطق

815 - Al-Imamu Al-Shafi Al-Risala uk. 52. 816 - Al-Shafi Diwaan uk. 131. 817 - Kazaliwa mwaka 260 A.H. 818 - Kwa maana kwamba Allah ndiye aliyeviumba. 819 - Ibn Al-Qayyim Shifaau Al-‘Alil uk. 93.

264

Page 265: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

في إال األئمة من أحد كالم في المجاز لفظ يعرف ولم واألئمة السلفأح اإلمام فإن ��كالم ه ����مد

والجهمية الزنادقة على الرد من كتبه فيما القرآن ((قال مجاز من )).هذا

Na neno majazi halikujulikana kwa yoyote katika Maimamu isipokuwa katika maneno ya Al-Imamu Ahmad. Hakika katika maandiko yake ya kuwajibu mazindiki na Jahmiyya (basi kuna maelezo yasemayo): ‘Haya ni majazi ya Qur-ani’.820 …..na akasema Ibn Taymiyya katika Fatawa zake: ‘Na hakuna yoyote katika Al-Salaf na Maimamu aliyelitamka (neno) hili, wala majazi hayakujulikana katika maneno ya yoyote miongoni mwa Maimamu isipokuwa katika maneno ya Al-Imamu Ahmad hakika yake kasema katika maandiko yake ya kuwarudi Al-Zanaadiqa na Al-Jahmiyya: “Haya ni majazi ya Qur-ani”.821

Na maneno alioyaashiria Ibn Taymiyya katika nukulu hio, ni maneno yalio katika kitabu kilichotungwa na kubandikwa nacho Al-Imamu Ahmad kiitwacho Al-Radu ‘Alaa Al-Zanaadiqa Wa Al-Jahmiya ambacho ndani yake kuna maneno haya:

لموسى ا قوله وأما عشر السابعة أسمع )لمسألة معكما إننيآخ (وأرى موضع في إنا ) ر�����وقوله

مستمعون قال )معكم كيف معكما )وقالوا أخرى (إنني آية في إنا)وقالمستمعون كوا ����فش (معكم

قوله أما ذلك أجل من القرآن معكم )في اللغة (إنا مجاز في فهذا

Mas-ala ya kumi na saba: ama kauli yake Allah aliposema: “Hakika Mimi niko pamoja nanyi ninasikia na ninaona”822 na kauli yake katika sehemu nyengine “Hakika ya sisi tuko pamoja nanyi tunasikiliza”.823 Basi (Al-Jahmiyya) wakasema: ‘Vipi (Allah) aseme: ‘Hakika Mimi niko pamoja nanyi’ na aseme katika Aya nyengine “Hakika Sisi tuko pamoja nanyi tunasikiliza”. Basi wao (Al-Jahmiyya) wakawafanya watu waishuku Qur-ani. (Lakini jawabu ni kuwa) ama kauli yake “Hakika Sisi tuko pamoja nanyi” haya ni katika majazi ya lugha. 824

Sasa kilichobakia ni kuwa Sh. Kasim Mafuta amuweke Imamu wake Ibn Taymiyya katika orodha ya waongo kwani kilichonukuliwa kutoka kwa Al-Imamu Ahmad ni: " معكم " إنا قوله اللغة أما مجاز في فهذا “Ama kauli yake ‘Hakika Sisi tuko pamoja nanyi’ haya ni katika majazi ya 820 - Ibn Taymiyya Iqaamatu Al-Dalil ‘Alaa Ibtali Al-Tahlil j. 3, uk. 392. 821 - Ibn Taymiyya Majmu’a Al-Fatawa j. 12, uk. 156, babu ghalat man qaala innahu majaz. 822 - Sura 20, Aya 46. 823 - Sura 26, Aya 15. 824 - Al-Raddu ‘Alaa Al-Zanaadiqa Wa Al-Jahmiyya kilichonasibishwa na Al-Imamu Ahmad na kuhakikiwa na Daghish Al-‘Ajmi uk. 193.

265

Page 266: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

lugha. Ibn Taymiyya kamnukuu Al-Imamu Ahmad akisema: (( من هذاالقرآن Haya ni majazi ya Qur-ani. Kwa mujibu wa vipimo vya((مجاز

bwana Kasim, huu ni uwongo! Kama vile alivyomwita Sh. Al-Khalili kuwa ni mwongo kwa sababu kama hii au inayofanana na hii. Sikusudii chochote hapa isipokuwa kutaka kuwaonesha walimwengu jinsi Kasim Mafuta alivyokuwa na fahamu finyu, vyenginevyo huu hauitwi kuwa ni uwongo bali ni ama kughafilika au kuyanukuu maneno kimaana.

Anasema Ibn Taymiyya:

الناشي العباس كأبي طائفة وقالت فيهما حقيقة أنه على فالجمهورجل و عز الرب في حقيقة إنها

المخلوق في مجاز

Basi jumhur wanasema kwamba hilo (jina ambalo huitwa Muumba na kiumbe)825 ni hakika kwa wote wawili (Muumba na kiumbe), na wengine kama vile Abu ‘Abbaas Al-Nnashi wanasema kwamba hayo (majina ya namna hio) ni hakika kwa Allah826 na ni majazi kwa viumbe.827

Hayo ni maneno anayoyanukuu Ibn Taymiyya mwenyewe kutoka kwa Abu Abbaas Al-Nnashi. Na Abu Abbaas huyu kafa mwaka 293.828 Baada ya yote hayo yaliosemwa na ‘Uthman Al-Darimi, Al-Jaahidh, Al-Shafi, Ahmad na Abu ‘Abbaas Al-Nnaashi, na mengine katika haya kayanukuu Ibn Taymiyya mwenyewe na Ibn Al-Qayyim mwenyewe, bado kutabakia ukweli katika kudai kwamba:

1) Hakukuwa na Imamu wa fani yoyote ile ambaye kayataja majazi.2) Majazi hayakutajwa na yoyote yule katika karne tatu za mwanzo.

JAWABU YA BADRU AL-DIN AL-KHALILI

Sasa baada ya hayo, natutazame jawabu ya Al-Imamu Badru Al-Din Al-Khalili Al-Mufassir juu ya maneno hayo ya Ibn Al-Qayyim na Sheikh wake, Ibn Taymiyya. Anasema Sheikh Al-Khalili:

825 - Kama vile majina عالم أو قادر أو aliye hai, au mwenye uwezo au mwenye حيelimu.826 - Yaani muweza wa hakika – kwa mfano – ni Allah. 827 - Ibn Taymiyya Al-Jawaabu Al-Sahih j. 3, uk. 294. 828 - Al-Dhahabi Al-Siyar j. 11, uk. 134-135.

266

Page 267: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Ama Maimamu wanne (wa Kisuni) wameyataja majazi kwa uwazi au kwa kuashiria. Na miongoni mwa walioyataja kwa uwazi ni Abu Hanifa aliposema:

في بل الحكم، في ال التكلم في الحقيقة عن خلف المجاز إنأصل الحكم

Hakika ya majazi ni badala ya hakika829 katika kusema: si katika hukumu, ama katika hukumu (majazi) ni asili.830

Na akanukuu ‘Alaau Al-Din Al-Bukhari kutoka kwake (Abu Hanifa akisema) kwamba hakika na majazi ni katika sifa za lafdhi kwa makubaliano ya watu wa lugha.

Na mfano wake ni kauli ya Al-Imamu Ahmad (bin Hanbal aliposema): اللغة: مجاز فهذا معكم إني ,Kauli yake: mimi niko na nyinyi) قوله

haya ni majazi ya lugha);831 hakika yake (maneno hayo ya Al-Imamu Ahmad) yako wazi kabisa katika kuthibitisha majazi pamoja na kuwa Ibn Taymiyya na Ibn Al-Qayyim wamefanya jaribio la kutaka kuleta ta-awil kwamba makusudio yake ni kuwa hilo linajuzu katika lugha.832 Bali miongoni mwa masahibu wa Ahmad wako wale ambao walikuwa karibu naye zaidi kwa zama ambao waliyafasiri maneno hayo ya Ahmad katika udhahiri wake katika kuthibitisha majazi. Na hili wamelikiri Ibn Taymiyya na Ibn Al-Qayyim wenyewe waliposema: ‘Na wameshikana na maneno haya ya Ahmad wale wenye kunasibika na madhehebu yake (wakasema) kwamba katika Qur-ani kuna majazi, kama vile Al-Qadhi Abu Ya’alaa, Ibn ‘Aqil, Abu Al-Khattab.833……

Ama (Al-Imamu) Malik na (Al-Imamu) Al-Shaafi hata kama hawakuyataja majazi kwa jina lake834 lakini wameyathibitisha kwa (ibara) zenye

829 - فرع الحقيقة أي عن (Yaani ni tawi au yanatokana na uhakika) katika kusema si katika hukumu. Kuyafahamu maneno haya inabidi ufahamu hukumu ni nini na kusema ni nini. Kusema ni ile lafdhi ya hakika ulioitumia kwa kukusudia majazi, kama neno simba katika jumla ya maneno inayosema: “Ali ni simba”. Na hukumu ni ile sifa iliomo katika lafdhi hio nayo ni “Ushujaa”. Sasa je hii hukumu, ambayo kwa hapa ni ushujaa, ni asili: si majazi; na majazi ni hili tamko “Simba” tu, au ni kinyume chake? Abu Hanifa anaona kwamba hukumu, ambayo kwa hapa ni ushujaa, ni jambo la asili; na tawi yaani majazi yapo katika lile tamko ambalo kwa hapa ni neno simba. Kwa ufafanuzi zaidi, tazama Dr. Al-Zuhaili Usulu Al-Fiqhi j. 1, uk. 293 830 - Tazama Kashfu Al-Asraari ‘An Usuli Fakhri Al-Islaam Al-Bazdawi cha ‘Alaau Al-Din Al-Bukhari, j. 2, uk. 145-146, chapa ya Daru Al-Kitaab Al-’Arabi. Ninasema: maelezo haya pia kayanukuu Dr. Al-Zuhaili katika Usulu Al-Fiqhi j. 1, uk. 293.831 - Ibn Al-Qayyim Mukhtasar Al-Sawaa’iqi Al-Mursala uk. 232. 832 - Nimeinukuu kauli hii ya Al-Imamu Ahmad kabla, lakini sikunukuu madai haya ya Ibn Taymiyya na Ibn Al-Qayyim, kwani madai hayo nimeyanukuu hapa kutoka kwa Sheikh Al-Khalili. 833 - Ibn Al-Qayyim Mukhtasar Al-Sawaa’iqi Al-Mursala uk. 232. 834 - Anakusudia katika yale yaliomo katika vitabu vyao wenyewe. Vyenginevyo Al-Imamu Al-Shafi kanukuliwa na Al-Bazdawi akiyataja majazi kwa jina lake la kifani kama

267

Page 268: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kuyaonesha (hayo majazi)…Katika tafsiri ya Qur-ani ya (Al-Imamu) Malik kuna tafsiri ya maneno kimajazi. Mfano wa hayo ni kile kilichosimuliwa na Ibn Al-Qaasim kutoka kwake (Al-Imamu Malik) kuhusu Aya isemayo:

تأويله يأتي يوم (Siku itayokuja hatima yake). Kasema: ‘Nimemsikia Malik akisema تأويله (Hatima yake) ni malipo yake.835 Na Ibn Wahb kapokea kutoka kwake (Al-Imamu Maalik) kwamba kasema kuhusu Aya isemayo: رهم الله بأيام وذك (Wakumbushe siku za Allah), (anasema Malik kwamba, Allah) anakusudia (wakumbushe kuhusu) neema zake na ataya zake kwao.

Ama Al-Shafi amethibitisha majazi, aliposema…836 Bali Al-Bayhaqi kamnukuu (Al-Imamu Al-Shaafi) akiyataja majazi kwa uwazi kwa maana yake ya kifani, na hayo ni katika kauli yake Mtume (s.a.w.) aliposema:

عاتقه عن العصا يضع ال فرجل جهم أبو Ama Abu Jahm, yeye ni) أماmtu ambaye mkwaju hauondoi mabegani mwake),837 naye (Al-Bayhaqi) akakubaliana naye.838………..

Ama madai ya Ibn Al-Qayyim akimfuata Sheikh wake Ibn Taymiyya kwamba majazi hayapo katika maneno ya Al-Khalil na Sibawayh na Al-Farraa na Al-Asma’i na mfano wa hao, ni madai yaliosimama juu ya msingi wa kusukuma, kwani wote hawa walikuwa wakifahamu vyema nini tafauti ya hakika na majazi, na hayo yako wazi katika maneno yao: ni sawa tu wakiwa wameyataja majazi kwa uwazi au hawakuyataja kwa uwazi. Na hakuna shaka kwamba Abu ‘Amri bin Al-’Alaa ndiye aliyewatangulia kwa zama wote hao waliowataja, naye kataja Al-Isti’ara kwa uwazi nayo (hio Al-Isti’ara) ni majazi bora yao na ndio majazi yalio bayana zaidi. Na hayo ni katika yale alioyasimulia Ibn Rashiq Al-Qayrawaani kutoka kwake katika kitabu Al-’Umda, kwamba alisema kuhusu ubeti wa Dhu Al-Rumma:

ذو حتى به ** ىأقامت الفجر مالءته الثريا وساق والتوى العودAlikaa huko mpaka kijiti kikakauka na akapinda***Na kizibau839 cha (nyota za) thuraiya kikaendeshwa na alfajiri.

tulivyonukuu kabla na kama Sheikh mwenyewe alivyomnukuu kupitia kwa Al-Bazdawi na Al-Bayhaqi. 835 - Al-Qabsu fii Sharhi Al-Muwattai cha Al-’Allama Ibn Al-’Arabi j. 4, uk. 203. 836 - Maneno ya Al-Imamu Al-Shafi tumeshayanukuu kabla, nayo ni:

... غير يراد أنه سياقه في يعرف وظاهرا بلسانها العرب بكتابه الله خاطب فإنماظاهرهKwa hakika Allah kazungumza na Waarabu katika Kitabu chake kwa lugha yao….na (andiko) dhahir (wakati mwengine) linafahamika katika mtiririko wake (siyaaq yake) kwamba halikukusudiwi udhahiri wake.837 - Yaani anapiga sana. 838 - Al-Bayhaqi Manaqibu Al-Shafi’i j. 2, uk. 239. 839 - Kizibau cha nguo.

268

Page 269: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Akasema baada ya ubeti huo:

اللفظة؟ هذه له استعار وإنما له، مالءة وال مالءة له صير كيف ترى أالHuoni namna alivyoifanya (thureyya kuwa ina) kizibau wala haina kizibau, bali neno hili kaliazima tu (ni isti’aara yaani kalitumia kimajazi).840 …..

Kama vile ambavyo kwamba Abu Zaid Al-Qurashi kayataja majazi kwa uwazi katika kitabu chake Jamharatu Ash’aari Al-’Arab, na akataja ushahidi wake kwa urefu katika Qur-ani na maneno ya Waarabu ya kawaida (prose) na ya utenzi.

Na katika maelezo ya Sibawayh kaashiria majazi ya kuondoshwa (kwa neno) na mengineo, isipokuwa yeye kayaita ittisaa’an (kutoa nafasi kwa lugha ya Kiarabu). Mfano wa hayo ni kauli yake aliposema: ‘Huu ni mlango wa matumizi ya kitendo katika tamko si katika maana kwa sababu ya ittisaa’i yao katika lugha………(Na akasema kuhusu Aya isemayo)فيها كنا التي القرية لئوس ……… (Na kiulize kijiji ambacho tulikuwemo ndani yake)…(kasema Sibawayh): ‘Hakika anakusudia (waulizeni) watu wa kijiji…841

Baada ya hayo utaona kwamba:1) Ibn Al-Qayyim na Ibn Taymiyya wamesukuma tu kuhusu suala la

kuyakataa kwao majazi kutoka kwa watu wa karne tatu za mwanzo. Na hii ni kawaida yao na wafuasi wao wote katika kila kitu wasichokijua au wasichokitaka, basi wao husema “Hakuna yoyote aliyesema” au “Al-Salafu Al-Salih wamekubaliana”.842

2) Wameshindwa kujua baina ya kuwepo kwa kitu na baina ya kuanza kwa jina lake la kitaalamu.843 Majazi yalikuwepo tangu enzi ya

840 - Abu Al-Husain bin Rashiq Al-Qayrawaani Al-’Umda Fii Mahaasini Al-Shi’ir Wa Aadaabih j. 1, uk. 428, chapa Daru wa Maktaba Hilal. 841 - Rejea Al-Imamu Badru Al-Khalili Jawaahiru Al-Tafsir Juz-u Khaas uk. 120-126. Bila kusahau kwamba nimeyabutua maneno yake ili kufupisha. Pia elewa kwamba Ibn Al-Qayyim na Ibn Taymiyya wana shubuhat nyengine nyingi walizozileta juu ya maudhui hii, lau tutazijadili itatubidi tufanye juzuu kamili juu ya maudhui hii. Shubuhati hizo zimejibiwa kiufundi na kwa uwazi na Sheikh Al-Khalili katika Jawaahiru Al-Tafsir Juz-u Khaas anayetaka naa arejee huko, labda tukiona kwamba kuna haja ya kukifasiri kitabu hicho tutafanya hivyo inshaa Allah ili uone kwamba hawa watu hawana hoja bali ni kubabaisha watu tu. 842 - Na hapa watu – hususan wa madhehebu za Kisuni – inawabidi wayahadhari sana maneno ya watu hawa na nukulu zao: wasije wakadanganyika na propaganda zao wanaposema “Ahlu Sunna” au “Al-Salaf” au “Umma”. Ahlu Sunna, na Al-Salaf na Umma kwao ni Ibn Batta, Al-Sijzi, Ibn Zaaghun na walio mfano wa hao. Na watu wa bidaa ni wafuasi wa madhehebu tatu za Kisuni, Ibadhi, Shia na Zaidia! 843 - Wala hawakushindwa kujua, lakini hawakutaka tu!

269

Page 270: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Mtume (s.a.w.) na kabla; na jina lake la kifani ndilo lililokuja baadae.

Sasa baada ya hayo, natutazame ushahidi wa kuwepo kwa majazi katika Qur-ani, Hadithi na lugha ya Kiarabu.

MAJAZI KATIKA QUR-ANI

Majazi kama tulivyosema ni kulitumia neno kinyume na maana yake ya asili. Tumenukuu sana huko nyuma ushahidi wa Qur-ani juu ya kuwepo kwa matumizi ya namna hio. Lakini kwa kuwa mlango huu ndio hasa nilioufanya ili kuthibitisha hilo basi hatuna budi kunukuu ushahidi japo kidogo juu ya kuwepo kwa majazi. Nitatumia neno majazi kumaanisha majazi yenyewe, kinaya, tashbihi, tawria au isti’ara: zote hapa nitazipa jina la majazi kwa kuzingatia kwamba zote zimetumika kinyume na maana yake ya asili.844

Baada ya hayo elewa ndugu msomaji mwenye kutafuta ukweli kwamba Aya nyingi za Qur-ani zina majazi lakini nachukua mifano miwili mitatu: 1) Allah anasema: “ الله وجه فثم تولوا فأينما ” “Popote mutapoelekea basi kuna uso wa Mwenyezi Mungu”.845 Neno lililotumika hapa kumaanisha uso ni neno wajhu. Maana ya msingi ya wajhu – kama nilivyoliweka katika Aya – ni uso. Sasa je hii ndio maana iliokusudiwa hapa? Kama ndio basi maana itakuwa Allah ana uso, na uso huo unapatikana kila sehemu popote utapoelekea. Na hili – kama unavyoona – si kwamba litagongana na akili ya kila Muislamu tu, bali pia – litagongana na itikadi ya skuli hio ya Mawahabi na Maimamu wao kwamba Allah yuko mbinguni hali ya kuwa yuko mbali na viumbe madamu uso wake uko kila sehemu! Kwa hivyo, neno uso hapa limetumika kimajazi na maana ni kuwa popote utapoelekea basi Allah yupo846 kama alivyosema katika Aya nyengine كنتم ما أين معكم وهو (Naye yuko pamoja nanyi popote mulipo). Yaani elimu yake ipo pamoja nanyi: si kuwepo kidhati (physically). Au radhi zake utazipata kwa mujibu wa tafsiri nyengine.

2) Allah anasema: “ وجهه إال هالك شيء Kila kitu kitaangamia) ”كلisipokuwa uso wake (Allah).847 Sasa ikiwa tutalifasiri neno uso kwa maana yake ya asili au ya uhakika na tukaitakidi kuwa Allah ana viungo vyengine (miguu, mikono n.k), ikiwa tutakwenda na tafsiri za namna hii, basi Aya hii 844 - Na hii ndio kauli ya aghlabu ya wajuzi. 845 - Sura 2, Aya 115.846 - Yaani elimu yake ipo na radhi zake zipo utazipata. 847 - Sura 28 Aya 88.

270

Page 271: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

inaonesha kuwa vitu vyote hivyo vitaangamia na utaobaki ni uso wa Allah tu: miguu yake, mikono yake na sisi na vitu vyote hivyo vitaangamia! Hii ndio dhahiri ya Aya inavyosema. Lakini ikiwa tutaifasiri Aya hio kimajazi tukasema kuwa neno uso hapa maana yake ni dhati (the essence or the person of Allah), basi tafsiri haitokupa tabu kwani maana ni kuwa kila kitu kitaangamia isipokuwa Dhati ya Allah yaani isipokuwa Allah mwenyewe. Utakumbuka kwamba njia bora ya kuzifasiri Aya za Qur-ani ni kuitazama Qur-ani yenyewe, kwani Qur-ani inajifasiri yenyewe katika maneno yake, sentensi zake na siyaaq zake. Na matumizi ya neno uso kwa maana ya dhati yamekuja katika Aya nyengine za Qur-ani kama vile Aya isemayo:

حامية * * نارا تصلى ناصبة عاملة خاشعة يومئذ وجوهNyuso siku hio zitadhalilika**zikiwa zimetenda kazi nzito** zitaingia moto mkali.848

Sasa jiulize wewe je zitakazoingia motoni ni nyuso tu? Bila shaka ni watu wenyewe. Kwa hivyo, neno uso hapa ni kwa maana ya dhati yaani mtu mwenyewe mzima, na kwa hivyo haya – kama tulivyoeleza kabla – ni majazi. Halkadhalika katika Aya hio isemayo: وجهه إال هالك شيء كل(Kila kitu kitaangamia isipokuwa uso wake (Allah), maana yake ni kuwa kila kitu kitaangamia isipokuwa Dhati ya Mwenyezi Mungu, yaani Allah mwenyewe ndiye atayebakia, na kwa hivyo neno hilo uso limetumika katika Aya hiyo kimajazi (figuratively). Na utakumbuka – ewe msomaji mwenye kutaka haki – kwamba Waarabu hutumia neno uso kumaanisha dhati. Kama vile wanaposema وجهك (Nimeujia au nimeukusudia uso wako) قصدتyaani nimekujia au nimekukusudia wewe. Na miongoni mwa hayo ni kauli ya mshairi aliposema:

** بالفالح يأتي حمن الر إلى ناظرات بدر يوم 849وجوه

Nyuso siku ya (vita vya) Badri zilimtazamia Mwenyezi Mungu alete ushindi.850

Maana ya neno zilimtazamia lililomo katika ubeti huu ni kuwa nyuso siku hio zilimngojea na kumtarajia Allah alete ushindi. Na inaeleweka kwamba zenye kungojea si nyuso tu: bali ni nyuso na kiwiliwili chote na nyoyo na akili na fikra.

3) Allah anasema:

848 - Sura 88 Aya 2-3-4.849 - (( بالخالص (( أخرى رواية وفي850 - Sheikh Al-Khalili Alhaqu Al-Damigh uk. 46.

271

Page 272: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

سبيال وأضل أعمى اآلخرة في فهو أعمى هذه في كان من

Atayekuwa kipofu katika dunia hii, basi akhera atakuwa kipofu na mwenye kupotea njia zaidi.851

Maana ya asili au ya uhakika au ya msingi ya neno kipofu ni “Asiyeona”. Lakini je hii ndio maana ya Aya hii na kwa hivyo vipofu akhera wataingia motoni!? Bila shaka neno hilo halikutumika hapo kwa maana yake hio ya asili, bali maana ni “Atayekuwa mpotovu katika dunia basi akhera atapotea zaidi”, na kwa hivyo neno hilo limetumika kimajazi (figuratively).

4) Anasema Allah: حمة من الذل جناح لهما واخفض الر

Na wainamishie (wazee wako wawili) bawa la udhalili wa huruma. 852

Jamaa! Hata huu udhalili nao una bawa? Na bawa hili lapatikana wapi?

Anasema Allah:ر ربهم عند صدق قدم لهم أن آمنوا الذين وبش

Wabashirie wale walioamini kwamba wana mguu wa ukweli kwa Mola wao. 853

Jamaa! Ivo ukweli nao una mguu? Na uko wapi mguu huo?

5) Anasema Mwenyezi Mungu:

البسط كل تبسطها وال عنقك إلى مغلولة يدك تجعل وال Wala usiufanye mkono wako kuwa wenye kufungwa

kwenye shingo yako wala usiukunjue wote.854

Je neno mkono hapa ni mkono wa kweli au maana yake ni kuwa usifanye ubakhili wala usifanye israfu? Kama ni mkono kweli kweli ndio uliokusudiwa hapa, basi Waislamu tunatakiwa mikono yetu daima iwepo kati na kati tu baina ya shingo na kuikunjua yote: tusije tukaikunjua yote wala tusiikunje!

6) Anasema Allah:851 - Sura 17, Aya 72. 852 - Sura 17, Aya 24. 853 - Sura 10, Aya 2. 854 - Sura ya 17 Aya ya 29.

272

Page 273: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

م تسمع أفأنت إليك يستمعون من ومنهم ) يعقلون ال كانوا ولو الص يبصرون ال كانوا ولو العمي تهدي أفأنت إليك ينظر من ( ومنهم42

(34(

Na miongoni mwao wako wanaokusikiliza, basi wewe utawasikilizisha viziwi hata kama hawafahamu?**Na miongoni mwao wako wanaokutazama, basi wewe utawaongoza vipofu hata kama hawaoni?855

Basi tuseme kwamba vipofu na viziwi waliotajwa katika Aya hizi ni vipofu na viziwi wa kweli au ni watu waliofananishwa tu na vipofu na viziwi kwa sababu ya kutokusikiliza kwao maamrisho ya Allah na kutokuyafuata?

7) Anasema Allah:يرجعون ال فهم عمي بكم صم

Viziwi, mabubu, vipofu, kwa hivyo wao hawatorejea.856

Na anasema:م الله عند الدواب شر إن يعقلون ال الذين البكم الص

Hakika ya viumbe waovu kabisa kwa Mwenyezi Mungu ni viziwi, vipofu ambao hawafahamu (kwa akili zao).857

Je na haya pia si majazi? Hatuna haja ya maelezo, kwani ikiwa mtu anahitaji kusoma Sharhu Ibn ‘Aqiil ili ajue jaar na majrur basi hahitaji kusoma hata alifu inani ili ajue kwamba maneno haya hayakutumika kwa uhakika wake?

MAJAZI KATIKA HADITHI

Natoa mifano kidogo tu: mifano iko mingi mno. Allah anasema katika Hadithi Qudsi:

إزاري والعظمة ردائي الكبرياءUkuu ndio vazi langu la juu na utukufu

ndio vazi langu la chini.858

Allah anasema katika Hadithi hii Qudsi: “Ukuu ndio vazi langu la juu na utukufu ndio vazi langu la chini”. Kwa hivyo, ikiwa tutakataa kuwepo kwa majazi basi natuseme kuwa Allah anavaa nguo mbili kanzu na seruni, kanzu 855 - Sura 10, Aya 42-43. 856 - Sura 2, Aya 18. 857 - Sura 8, Aya 22. 858 - Ibn Maja Al-Sunan Hadithi na. 4174-4175.

273

Page 274: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

yake inaitwa kibriyaa (ukuu); na seruni yake inaitwa Al-‘Adhama (utukufuu au ukuu)!!!

Katika Hadithi nyengine Qudsi, Allah anasema:

يزال.... وما عليه، افترضت مما إلي أحب بشيء عبدي إلي تقرب ومابالن���وافل إلي يتقرب عبدي

أحبه، به حتى يبصر الذي وبصره به، يسمع الذي سمعه كنت أحببته فإذاب يبطش التي ها �����ويده

بها يمشي التي ورجله

….Na mja wangu hajikurubishi kwangu kwa kitu nikipendacho zaidi kuliko yale niliomfaradhishia. Na mja wangu anaendelea kujikurubisha kwangu kwa (kufanya) nawafil (ibada zisizo za lazima) mpaka ninampenda. Basi nikimpenda ninakuwa (Mimi Mungu ndio) sikio lake analosikia kwalo, na jicho lake analoonea na mkono wake anaoshikia na mguu wake anaoendea.859

Jamani hebu nikuulizeni na nikuombeni tuweke ushabiki na umadhehebu kando japo kwa dakika tano. Ivo kweli inawezekana kukataa majazi (metaphor) na kwa hivyo kuifasiri Hadithi hii literally (neno kwa neno kama ilivyo)? Kama ni hivyo, basi Allah anasema hapa kuwa Yeye ni masikio, macho, mikono na miguu ya mawalii wake, kwa hivyo viungo vya mawalii ndio Mungu mwenyewe au ndio sehemu za Mungu! Bila shaka maana hio haiingi akilini – huhitaji kuwa mwanachuoni; na maana inayofahamika kiakili ni kuwa mawalii wanasikiliza yanayomridhisha Allah, na kwa hivyo Allah kajiita Yeye mwenyewe kuwa ndio masikio yao; wanatazama, wanashika na wanayaendea yanayomridhisha Allah. Kwa hivyo, sikio la Allah, jicho lake, mkono wake na miguu yake iliotajwa katika Hadithi hii ni majazi (metaphor) na maana yake ni kama tulivyoeleza.

Lakini nilipojadiliana na baadhi ya ndugu zetu, mmoja wao aliniambia kwamba hili liko wazi katika Hadithi hio. Baadae – baada ya kupekuwa – nikamkuta Sheikh Al-Khalili akiwanukuu baadhi ya wanavyuoni wao wakisema hivyo hivyo. Kisha Sheikh Al-Khalili akajibu kwamba hilo si sahihi kwani maneno: mkono, miguu, macho na masikio, yote haya yana maana zake za uhakika wa kilugha ambao yanapotajwa tu maneno hayo mtu haufahamu isipokuwa uhakika huo. Unapotaja mguu, kwa mfano, mtu hakufahamu isipokuwa kwamba umekusudia kiungo maalumu ambacho tunakijua sote. Na kwa hivyo, ikiwa uhakika wa viungo hivyo wa kilugha

859 - Kaipokea Al-Bukhari na akainukuu Al-Imamu Al-Nawawi Riyaadhu Al-Saalihin uk. 58, Hadithi na. 95.

274

Page 275: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

sio uliokusudiwa katika Hadithi hio basi ni wazi kwamba maneno hayo yametumika kimajazi – yametumika kinyume na maana yake ya asili.

Hadithi nyengine inasema:

: رب وأنت أعودك كيف رب يا قال تعدني فلم مرضت آدم ابن يا : عل أما قال أن ��العالمين؟ مت

....... عنده لوجدتني عدته لو أنك علمت أما تعده؟ فلم مرض فالنا عبدي

Ewe Binaadamu we! Mimi niliumwa basi wewe hukuja kunijuia!860 Atasema (binaadamu): ‘ewe Mola wangu! Vipi nije kukujuia nawe ni Bwana wa ulimwengu? Atasema (Allah) kwani hujui kwamba mja wangu fulani kaumwa wewe hukwenda kumjuia? Hujui kwamba lau ulikwenda kumjuia basi ungelinikuta mbele yake..861

Hadithi hii bila shaka lau haitofasiriwa kwa misingi ya kimajazi basi itakuwa ni mushkeli mkubwa na yatakuwa maneno ya Kisharia yanagongana ambapo sehemu moja inathibitisha kitu na ya pili inakikanusha kitu hicho hicho. Tazama maneno: “Mimi niliumwa basi wewe hukuja kunijuia” je maneno haya inawezekana kuyanasibisha na Mwenyezi Mungu kwa udhahiri wake? Je inawezekana kusema kuwa Allah anaumwa lakini kuumwa kwake si kama kuumwa kwetu? Sasa tazama ukweli kwamba Allah mwenyewe kayafasiri maneno hayo akasema:

Kwani hujui kwamba mja wangu fulani kaumwa wewe hukwenda kumjuia? Hujui kwamba lau ulikwenda kumjuia yeye basi ungelinikuta mbele yake.

Jambo hili linabainisha kwamba kuumwa kulikotajwa mwanzo si hakika bali ni majazi, na kuumwa kwa pili – kuumwa kwa mja – ndio hakika. Vyenginevyo, ukiwa utakataa majazi basi itakubidi useme:

1) Hadithi hii inajigonga. 2) Au Allah anaumwa kweli.3) Tukienda kumtazama mgonjwa tutamkuta Allah yupo mbele yake,

na hili halijawahi kutokea. Sijui labda wale wenye kukataa majazi – akina Kasim Mafuta na wenzake – wao wakenda kuwatazama wagonjwa humkuta Mungu huko, na kwa hivyo kauli yao ya kuwa Mungu haonekani hapa duniani huko inakuwa haitendi kazi!

860 - Kunijuia ni Kipemba, Kiunguja kunijulia, sijui Kitanga wanasemaje, lakini maana yake ni kwenda kumtazama mgojwa. 861 - Muslim Al-Sahih Hadithi na. 2569.

275

Page 276: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

4) Kwa hivyo, kukataa majazi kunaifanya riwaya hii iwe na mgongano au tuwe na itikadi ya tashbihi ilio wazi bali tuwe na itikadi ambayo haikubaliani na matokeo yalivyo.

Hadithi nyengine inasema:تقربت ذراعا إلي تقرب وإذا ذراعا، إليه تقربت شبرا إلي العبد تقرب إذا

أتاني وإذا باعا، إليههرولة أتيته يمشي

Mja wangu akijikurubisha kwangu shubiri moja basi Mimi najikurubisha kwake dhiraa nzima; na akijikurubisha kwangu dhiraa moja, basi Mimi najikurubisha kwake pima nzima; na anayenijia naye anakwenda (mwendo wa kawaida), basi Mimi namjia hali ya kuwa nakwenda mbio (natroti).862

Katika jambo lenye kuonesha kuwa Mawahabi wanasoma lakini hawafahamu ni kusema kwao kwamba har-wala (mwendo wa mbio au kutroti) ni katika sifa za Mwenyezi Mungu wakitegemea Hadithi hii! Hii inaonesha kuwa hawa watu Allah hakuwapa fahamu hata kidogo hata wakihifadhi maelfu ya Hadithi. Tazama qarina za Hadithi hii halafu jiulize je kweli uliokusudiwa hapo ni mwendo wa kweli? Tazama nukta mbili zifuatazo:

1) Mja – kwa mujibu wa dhahiri ya Hadithi hii – anakwenda kwa

miguu huko aliko Allah. Jamani! Wapi tumepata kusikia kuwa kuna mtu anakwenda kwa miguu kumfuata Allah huko aliko? Bila shaka maana ni kuwa anayefanya wema kidogo kwa ajili ya Allah, Allah anamlipa mengi kuliko ule wema wake.

2) Allah anakuja mbio mbio kwa mja! Wapi tumepata kusikia kwamba kuna mja kajiwa na Allah miongoni mwa Manabii, Masahaba au Mawalii wakubwa, na wote hawa ndio walio mstari wa mbele katika uchaji?

Kwa hivyo, ni wazi kwamba lafdhi zote hizi ni majazi; wala huwezi kuifasiri Hadithi hio katika uhakika wake kwani uhakika wake haukubaliani na akili wala haukubaliani na matokeo yalivyo.

Hadithi nyengine inasema:

: : الدهر وأنا الدهر وأنا وادهراه يقول آدم ابن يشتمني وجل عز الله قال

862 - Kaipokea Al-Bukhari na akainukuu Al-Imamu Al-Nawawi Riyaadhu Al-Saalihin uk. 58, Hadithi na. 96.

276

Page 277: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Kasema Allah Mtukufu (katika Hadithi Qudsi): ‘Binaadamu ananitukana, anasema: ‘E dahari weee! Na Mimi (Mungu) ndio dahari; na Mimi (Mungu) ndio dahari.863

Na lafdhi nyengine ya Hadithi hii ni:

والنهار الليل بيدي الدهر وأنا الدهر آدم ابن يسب

Binaadamu anatukana dahari, na Mimi (Allah) ndio dahari yenyewe; mikononi kwangu kuna usiku na mchana.864

Kwa hivyo, kwa wale wanaokataa majazi basi wasipate tabu ya kumjua Mola wao: Mola wao ni hizi zama (dahari) kama Hadithi inavyosema. Na kwa sababu msingi ni kuwa:

Tunakithibitisha kile ambacho Allah na Mtume wake wamekithibitisha na kukikanusha kile walichokikanusha, bila ya kukiletea ta-awil (kukiletea tafsiri ya ndani) wala tahrif (kukipotoa) wala tashbih (kukifananisha),

basi maana na iwe:1) Allah ni dahari.2) Lakini yeye ni dahari si kama dahari.

Lakini kifungu nambari mbili kitabomolewa na ukweli kwamba Allah kawalaumu watu hao kwa kuitukana dahari na kwamba Yeye ndio dahari, na bila shaka dahari wanayoitukana watu hao ni hii tunayoijua ya mabadiliko ya usiku na mchana: si: “dahari lakini si kwa namna tunayoijua”. Kwa hivyo, natija ya kukataa majazi ni kuwa mabadiliko ya usiku na mchana (dahari) ndio Mungu mwenyewe! Huu ni ujuha wa mwisho duniani?

Anasema Mtume (s.a.w.):

السيوف ظالل تحت الجنةPepo iko chini ya vivuli vya panga.865

Tazama ewe mwenye akili timamu! Je utaichukua Hadithi hii literally (neno kwa neno) au utaifasiri kwamba anayetaka pepo basi akapigane jihadi? Vyenginevyo basi natusema kuwa pepo ziko kwenye vivuli vya panga:

863 - Ibn Abi ‘Aasim Sunna j. 1, uk. 410, Hadithi na. 611. 864 - Al-Bukhari Al-Sahih Hadithi na. 7491. Muslim Al-Sahih Hadithi na. 2246. Lafdhi ni ya Muslim. 865 - Al-Bukhari Al-Sahih Hadithi na. 2818. Muslim Al-Sahih Hadithi na. 1902.

277

Page 278: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

tuziweke panga zetu kwenye jua na zikitoa kivuli basi hapo ndipo kwenye pepo!

Anasema Mtume (s.a.w.):

عاتقه عن عصاه يضع فال جهم أبو ا .......أمAma Abu Jahm ni mtu ambaye mkwaju hauondoi begani kwake.866

Yaani anapiga sana. Au utakataa majazi uniambie kuwa maana yake ni kuwa Abu Jahm alikuwa akitembea na bakora begani kila wakati: haiweki chini.

Bali Hadithi inasema kwamba Allah ana wembe mkali zaidi kuliko wa baba yake Abu Al-Ahwas kama alivyosimulia Al-Bayhaqi katika kitabu Al-Asmaau Wa Al-Sifaat.867

MAJAZI KATIKA LUGHA YA KIARABU

Mashairi ya Waarabu na maneno yao ya kawaida (prose) yamejaa majazi kama vile ambavyo sisi Waswahili lugha yetu imejaa majazi pia. Waswahili huwa tunasema:

1) “Yakhe kijana yule ana mkono mkono”! Yaani ni mwizi.2) “Yakhe yule ana ulimi mrefu au ana mdomo sana”! Yaani ana

maneno mengi au mtukanaji.3) “Yakhe mguu huu ni wako”! Yaani nimekujia wewe. Lakini

inaonekana lau Sharia yetu ilikuwa kwa lugha ya Kiswahili na Sheikh Kasim Mafuta akawa ndiye Kadhi, basi angelitukata miguu na mikono sote kwa ufahamu wake wa lugha. Kwa sababu ungelimwambia “Sheikh huu ni mguu wako” yeye angechukua panga akaukata akauchukua mwenyewe!

4) “Yakhe nakupa mkono”! Yaani nakusapoti: nakubaliana na wewe au nakupongeza

5) “Aaa! Mimi sitii mkono wangu”! Yaani mimi sijitii katika jambo hilo: sijihusishi.

6) “Ama yakhe saa zenda”! Au “Siku zenda”! Na bila shaka saa na siku haziendi, bali zinapita.

7) “Biashara inakwenda vizuri”! Yaani bidhaa zinauzwa kwa wingi, vyenginevyo biashara haiendi.

8) “Yakhe Omari kazi kaiwekea mguu”! Yaani kaizuia.

866 - Muslim Al-Sahih Hadithi na. 1480. 867 - J. 2, uk. 176, Hadithi na. 742.

278

Page 279: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

9) “Aaa Bwana usiniangushe wee”! Yaani usinikoseshe yale niyatakayo.

10) “Omari kamvunjia fulani nyumba”. Hii haina maana kwamba Omari alichukua mtaimbo akaenda kubomowa matufali ya nyumba ya fulani, bali haya ni majazi ya kinaya cha Kiswahili na maana yake ni kuwa “Omari anafanya machafu na mke wa fulani”. Mke katika Kiswahili kaitwa nyumba kwani nyumba inaimarika kwa kuwepo yeye, na akihama mke mara nyumba huanguka868 kwa kukosa kushughulikiwa.

11) “Mazoea kilema”. Ilhali mazoea si kilema cha kweli.12) “Mtu kidole”. Ilhali mtu si kidole.13) Siisahau kauli ya mwalimu wangu wa chuo nilipomsikia akisema

maneno yenye maana kwamba: “Naona juu kushagogwa”.! Hiki ni Kipemba. Kiunguja na kistandard ni: “Naona juu kumenuna”. Lakini mtu huyo aliposema juu kushagogwa anakusudia: “Mawingu yametanda”.

Hio ni baadhi ya mifano ya balagha ya Kiswahili. Sasa kama umeyaelewa hayo, basi elewa kwamba lugha ya Kiarabu ni tajiri zaidi katika balagha ya namna hio. Lakini wale ambao wanadhania kuwa kujua balagha ni kujua yale maneno ya kifani technical terms tu yaliyowekwa na wanavyuoni ili kurahisisha darsa zao, basi siku zote huwa wanataabika katika kuyafasiri maneno ya Allah na Mtume wake. Ndugu wasomaji! Kujua balagha sio kujua Hazl (mzaha) au tauria (kugubuka) au maneno mengine ya kifani, bali kujua balagha ni kuweza kujua maana halisi ya maandiko kwa misingi ya lugha ilivyo, yaani kuweza kujua Allah – katika Aya kadha – na Mtume (s.a.w.) katika Hadithi kadha – wanakusudia nini: sio wametamka nini tu. Vyenginevyo hizi istilaahat zote za balagha, Masahaba hawakuwahi kuzijua, ilhali wao ndio wajuzi wao wa lugha ya Kiarabu.

Baada ya hayo, sasa tazama mifano miwili mitatu ya balagha ya Kiarabu. Anasema Mshairi wa kiarabu:

** أعددها وال منها أعد سابغة علي أياد لهAna mikono (mingi) imenienea juu yangu**Naihisabu

lakini siwezi kuihisabu (kwa wingi).869

868 - Hasa ikiwa ni ya makuti au nyasi. 869 - Katika kitabu Dawaawiinu Al-Shi’iri Al-‘Arabi j. 47, uk. 227, ubeti huo umeandikwa:

سابقة إلي أياد أعددها ** له وال منها أعدAna mikono imenitangulia** Naihisabu lakini siwezi kuihisabu (kwa wingi).

279

Page 280: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Jiulize wewe je huyu mtu alikuwa na mikono mingapi mpaka ikafika hadi kuwa mtu hawezi kuihisabu. Bila shaka mshairi anakusudia kusema kwamba takrima na ataya alizopewa ni nyingi na kwa kuwa mkono ndio unaotoa ataya hizo basi ataya zimepewa jina la mkono.

Anasema mshairi:

*** إليه العباد رب محصيه لست ذنبا الله والعمل الوجهأستغفر

Ninamuomba Allah msamaha kwa dhambi nisizozihesabu***Bwana wa waja kwake yeye unakwenda USO na matendo.

Bila shaka neno uso hapa halikukusudiwa uso-kiungo, bali maana ni القصد (makusudio), yaani ikhlas.

Anasema mshairi:

** غائظة ألعدائها وأخرى يرتجى خيرها يد يداك

Mikono yako miwili; mkono mmoja kheri yake inatarajiwa; na mkono wa pili una hasira kwa maadui wake.

Tazama jinsi Waarabu wanavyoitumia lugha yao! Maneno haya lau yalikuja katika Qur-ani au Hadithi basi Mawahabi wangelishindwa kuyafahamu, na wangelisema: “Allah ana mikono miwili; mkono wake mmoja unatoa kheri; wa pili una hasira kwa maadui wa Allah”. Ilhali inaeleweka hapa kwamba mkono-kiungo si makusudio ya maneno hayo kamwe, vyenginevyo asingelisema kwamba una hasira, kwani mkono-kiungo hauna hasira.

Anasema Al-Imamu ‘Ali bin Abi Talib (k.w.):

** والرسوم المعالم ستخبرك تقضت أمم عن األيام سلZiulize siku kuhusu umma zilizoangamia**Alama na

mabaki yatakupa habari870

Sayyidna ‘Ali (r.a.) anatwambia tuziulize siku, sasa je siku kweli zinaulizwa? Kisha anatwambia kwamba alama na mabaki ya umma zilizopita zitatoa habari. Je haya ni kweli ikiwa tutayafasiri maneno hayo kama yalivyo: ni kweli alama zinasema?

870 - Diwan Al-Imami ‘Ali uk. 99, mashairi nambari 154.

280

Page 281: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Anasema Al-Imamu Al-Shafi:

** القضاء حكم إذا نفسا وطب تشاء ما تفعل األيام دعZiache siku zifanye zitakayo**Na poa moyo

wakati qadhaa871 itapohukumu.872

Sasa je ni kweli siku zinafanya kitu? Siku ni mapinduko ya nyakati: usiku na mchana na anayekadiria matokeo mema na mabaya ni Allah: si siku. Lakini pamoja na hayo, Al-Imamu Al-Shafi anatwambia kwamba tuziwache siku zifanye zitakayo. Haya ndio yale wataalamu wanayoita al-majazu al-’aqliy (majazi ya akili). Kama kusema “dawa hii imeniponesha” ilhali Allah ndiye aliyekuponyesha na dawa ni sababu tu.

Sina haja ya kurefusha kwa vile ushahidi mwengine mwingi nimeunukuu hapa na pale. Kwa haya machache inakubainikia ukweli kwamba majazi yapo katika Qur-ani, Sunna na lugha ya Kiarabu bali katika lugha za binaadamu wote, na wala hayakanushi majazi isipokuwa mtu asiyekuwa na fahamu hata kidogo au mwenye fahamu yake lakini anafanya kibri dhidi ya ukweli. Na kilicho wazi kabisa – kama yanavyofahamika maneno ya Sh. Kasim mwenyewe – ni kuwa wanaokataa kuwepo kwa majazi wanayakataa kwa kuhofia kuanguka kwa itikadi yao batili ya mungu-mtu (man-god or god-incarnate).

MAWAHABI HAWAJUI WAKISEMACHO!

Anasema Sheikh Al-Khalili:

Na miongoni mwa ajabu nilioisikia ni kwamba mimi nilikuwa katika hiwaar (discussion au mjadala) pamoja na mmoja wa Hashwiyya wenye kukanusha majazi, basi ikawa miongoni mwa alioyasema ni kuwa: ‘Ni dalili gani iliosema kwa uwazi kwamba (neno) hili ni hakika na hili ni majazi katika Qur-ani au Sunna au yale yaliopokewa kutoka kwa Salaf wa Umma miongoni mwa Masahaba na wafuasi wao? Nami nikamwambia: ‘Ni dalili gani iliosema kwa uwazi ikaielezea dalili ya kisharia kwamba ni Aam‘ عام (ya ujumla) na nyengine kuwa ni ?Khaas (mahususi) خاص Akasema: ‘Kwa kuwa imepokewa kauli ya Mtume (s.a.w.) akisema kwamba: ‘Sisi Manabii haturithiwi’873 pamoja na kwamba Allah kasema (katika Qur-ani): األنثيين حظ مثل للذكر أوالدكم في الله يوصيكم

871 - Maamuzi ya Allah. 872 - Al-Imamu Al-Shafi Diwaan Al-Shafi uk. 18. 873 - Al-Bukhari Al-Sahih Hadithi na. 4036. Muslim Al-Sahih Hadithi na. (49) 1757-(51) 1758.

281

Page 282: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

(Allah anakuusieni kuhusu watoto wenu mwanamme (katika kurithi) apate sawa na fungu la wanawake wawili),874 tukajua kwamba Hadithi hio imeuhusisha ujumla uliomo katika Aya hii; basi tukajua kwamba andiko khaas (specific au exceptional) linabomoa andiko Aam‘ عام (la ujumla)’.

Na nimestaajabishwa na ufinyu wa upeo wa watu hawa na kufinyika kwa akili zao na kupooza kwa fahamu zao,875 kwa sababu suali lilikuwa ni kuhusu kuwepo kwa nassu (andiko linalotamka kwa uwazi) kwamba hii ni Khaas (mahususi au specific au خاص Aam (ya ujumla) na hii ni‘ عامexceptional): wala halikuwa suali kuhusiana na kuwepo kwa عموم (ujumla) na kuwepo خصوص (uhusishaji) kama vile alivyonilazimisha mimi nimletee nassu (andiko la wazi lenye kusema) kwamba haya ni majazi na hii ni hakika…….876

Basi hivyo unavyoona akili ya mtu huyo aliyejadiliana na Sheikh Al-Khalili, ndivyo zilivyo akili za watu hao hata Maimamu wao wakubwa.877 Wallahi ukisoma kitabu Al-Raddu ‘Alaa Bishr Al-Marisi cha ‘Uthman Al-Darimi ambacho Ibn Taymiyya kakiusia sana, basi utastaajabishwa sana na ‘aqliyya (mentality au fikra) ya kiumbe huyu pamoja na kuwa kahifadhi maelfu ya Hadithi? Bishr Al-Marisi anasema vyengine; yeye anamjibu vyengine!

Sasa baada ya hayo, tazama vichekesho vyengine vyenye kuliza, navyo ni vichekesho vya kujigonga kwa Ibn Al-Qayyim mwenye kukanusha/kuthibitisha majazi للمجاز المثبت .النافي

KUJIGONGA KWA IBN AL-QAYYIMKUYATUMIA KWAKE MAJAZI

Sasa baada ya hayo – ukipenda kucheka au kulia – tazama maajabu ya Ibn Al-Qayyim! Ibn Al-Qayyim pamoja na kuwa kakanusha majazi kwa kututungia kitabu kilichochukua sehemu kubwa juu ya kulielezea suala hilo, lakini yeye na wengine wengi hawakuacha kuyatumia majazi, bali na wakati mwengine kuyataja kwa jina. Tazama ukweli kwamba Ibn Al-Qayyim, kitabu chake ambacho ndani yake anakataa majazi, kakiita Al-Sawaai’qu Al-Mursala (Mapigo ya radi yalioachiwa)! Sasa jamani! Kitabu ni radi, au

874 - Sura 4, Aya 11. 875 - Msemaji ni Sheikh Al-Khalili. 876 - Al-Imamu Badru Al-Din Al-Khalili Jawaahiru Al-Tafsir Juz-u Khaas uk. 111-112. Kisha baada ya hapa Sheikh akanukuu Aya zenye kuonesha kuwepo kwa majazi katika Qur-ani. 877 - Siisahau kauli ya kijana mmoja alieniambia: “Wale ni watu wa kuombewa dua, kwani si watu wa akili na fahamu”.

282

Page 283: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

yaliomo ndani ya kitabu ni radi za kweli? Na akakiita kitabu chake chengine Madaariju Al-Saalikin (Njia za wenye kushika njia au wenye kupita). Na namna hivyo unawakuta katika vitabu vyao mbali mbali wanatumia ibara za kimajazi. Tazama maneno ya Ibn Al-Qayyim kuhusu dunia; anasema:

... عذبتهم بعد سمها كؤوس سقتهم شراب أمر وأذاقتهم العذاب بأنواع بحبها..... فسكروا خمرها وسكؤ

….(Dunia)..imewaadhibu kila namna; na ikawaonjesha kinywaji kichungu chao; imewanywesha gilasi za sumu yake baada ya gilasi za pombe yake, basi wakalewa kwa kuipenda (hio dunia)!878

Sasa hebu tujiulize je Ibn Al-Qayyim kayakusudia maneno haya katika maana yake ya uhakika kwamba dunia inawanywesha watu sumu na pombe na kinywaji kibaya chao na watu wakalewa kweli kweli kwa sababu ya kuipenda! Na vipi mtu analewa kweli kweli kwa kupenda!

Na kabla ya hapo, Ibn Al-Qayyim kasema:

والروح القلب بعين أدرك الذي فذلكHayo ndio aliyoyadiriki kwa jicho la moyo na roho.879

Sasa moyo una jicho la kweli; roho ina jicho la kweli? Au ni uoni kwa maana ya basira (uoni wa moyo) si kwa maana ya basar (uoni wa jicho)? Namna hivi utaona mtu huyu anavyojigonga mwenyewe.

Na katika Nuniyya yake, Ibn Al-Qayyim anafungua kitabu chake kwa kusema:

** يدان ذاك بفسخ للصدود ما األركان ثابت المحبة حكم

Hukumu ya mapenzi, nguzo zake ni imara**Upingaji880

hauna mikono miwili ya kubomoa hilo.881

Anasema mshereheshaji: Na mikono miwili ni uwili wa (neno) mkono, kwa maana ya uwezo.882 Sasa vipi tena Ibn Al-Qayyim anapinga majazi? Huku si

878 - Ibn Al-Qayyim Madariju Al-Saalikin 3, uk. 190-191. 879 - Ibn Al-Qayyim Madariju Al-Saalikin 3, uk. 190. 880 - Maana ya neno kwa neno ni “uzuiaji”, lakini ufasaha wa Kiswahili ni kusema “upingaji”. 881 - Ibn Al-Qayyim Al-Nuniyya j. 1, uk. 16. 882 - Muhammad Khalil Harras Sha-hu Al-Nuniyya j. 1, uk. 16.

283

Page 284: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kujigonga ambako kunaonesha kwamba hana hoja sahihi, bali anakimbia kuanguka kwa itikadi yake ya mungu mtu?

KUKARIBIA KWAKE KUYATAJA MAJAZI

Ama kuyataja kwake majazi kwa kuyaashiria kulikokaribia kuyataja kwa uwazi ni kama alivyosema Al-Imamu Badru Al-Din Al-Khalili Al-Mufassir. Anasema:

Na Ibn Al-Qayyim kayabomoa mwenyewe yale alioyajenga hapa ya kukanusha majazi, kwa kuyakiri kwake majazi bila ya kujua wakati alipoifasiri Hadithi isemayo: “ لسانه عني Ukateni ulimi) ”اقطعواwake kutokana na mimi), kwamba makusudio yake ni kumnyamazisha yule mwenye kusifu kwa kumpa tunza ili iikate ulimi wa maneno yake. Na akaifasiri Hadithi (ya Mtume s.a.w.) isemayo: من سيف خالدا إن

الله ,(Hakika ya Khalid ni upanga katika panga za Allah) سيوفkwamba maana yake ni kuwa anawaua washirikina kama upanga usio na ala (ghala) ambao hauhitaji kuchoolewa; na Hadithi inayosema kwamba Hamza ni ورسوله الله أسد من simba) أسدkatika simba wa Allah na Mtume wake), kwamba maana ni kuwa Hamza anawawinda maadui wa Allah.883

KUYATAJA KWAKE MAJAZI KWA JINA LAKE LA KIFANI

Baada ya kuona jinsi Ibn Al-Qayyim alivyoyatumia majazi, sasa tazama jinsi Ibn Al-Qayyim huyo huyo anavyoyataja majazi kwa uwazi. Anasema:

الظاهر في يدخل وإنما المنصوص في يدخل ال والتأويل المجازالمحتمل

Majazi na ta-awil hayaingii katika maandiko ya wazi, bali yanaingia katika maandiko dhahir yenye uwezekano (huu na ule).884

883 - Na Hadithi nyengine nyingi zenye majazi ambazo Ibn Al-Qayyim kayatoa maneno yake katika maana ya asili na kuyapeleka katika maana hizo za kimajazi. Tazama maelezo hayo katika Jawaahiru Al-Tafsir Juz-u Khaas uk. 288-289. Na maneno ya Ibn Al-Qayyim mwenye kujigonga utayapata katika Mukhtasar Al-Sawaa’iqi Al-Mursala uk. 272-273. 884 - Ibn Al-Qayyim Badaai’u Al-Fawaaid j. 1, uk. 19.

284

Page 285: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Anaendelea Ibn Al-Qayyim:

: .... ألفاظ أكثر قيل الفعل في الضمير استتار معنى ما قيل فإنوا والتشبيه االستعارة على محمول تسامح....لالنحاة

Ikiwa itasemwa nini faida ya kujificha kwa dhamiri (pronoun) katika kitendo?….Basi jawabu ni kuwa asilimia kubwa ya lafdhi za watu wa nahau zinafasiriwa kwa njia ya isti’ara (majazi) na tashbihi na tasamuh.885

Anaendelea Ibn Al-Qayyim:

على واستدالله معا، والمجاز الحقيقة إرادة يمتنع ال أنه على قوله أما : بقولهم أحد “ذلك القلم

مثنى اسم اللسانين ألن فيه حجة فال مق���ام اللسانين، قائم فهوبأحدهما أريد باسمين الن����طق

مجاز وباآلخر الحقيقة

Ama kauli yake (aliposema) kwamba hakuna pingamizi katika kukusudia (matumizi ya) hakika na majazi kwa pamoja (katika neno moja) na kutoa kwake ushahidi kwa msemo wao unaosema: ‘Kalamu ni moja ya ndimi mbili’, hakuna hoja ndani yake kwani neno lissanain (ndimi mbili) ni uwili, kwa hivyo limechukua nafasi ya kuyatamka majina mawili, moja lao limekusudiwa uhakika (wake) na jengine ni majazi. 886

Anasema Ibn Al-Qayyim:

فاألوقات الحقيقة في وأما مجازا المعاني بهذه توصف قد األوقات ألنالفلك فإذا........ هي

جعتها وإذا الزمان، مرور من ألنها حقيقة فاللفظ ظرفا، المرة جعلتمجاز فاللفظ مصدرا

Kwani nyakati huenda zikasifiwa kwa maana hizi kimajazi ama katika uhakika nyakati ni falaki……………………Ikiwa (neno) marra utalijaalia kuwa ni dharfu basi tamko hilo litakuwa ni hakika, kwani linatokana na neno mururi azzamaan (kupita kwa zama); na ukilijaalia kuwa ni masdar (chimbuko) basi tamko hilo litakuwa ni majazi. 887

Anasema Ibn Al-Qayyim:

885 - Ibn Al-Qayyim Badaai’u Al-Fawaaid j. 1, uk. 111. 886 - Ibn Al-Qayyim Badaai’u Al-Fawaaid j. 3, uk. 59. 887 - Ibn Al-Qayyim Badaai’u Al-Fawaaid j. 2, uk. 286.

285

Page 286: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

في له ومثبتا عل�يه داال الل��فظ ج���عل ما باللفظ يقصد إنما فالم���عرضيخرج لم فهو الجملة،

الكالم، حدود عن والمجاز بتعريضه حقيقة فيه الكالم فإن

Mwenye kuashiria,888 kwa hakika anakusudia kwa tamko lake kitu ambacho andiko hilo linakimaanisha (kimo ndani ya lafdhi hio) na ambacho kwa ujumla linakithibitisha, kwa hivyo yeye – kwa kuashiria kwake huko huwa hajatoka katika mipaka ya maneno, kwani maneno ndani yake kuna uhakika na majazi. 889

Anaendelea Ibn Al-Qayyim:

لك مسلمين سمنا أي التسمية بمعنى مجاز الله إلى الجعل هذا ونسبةج أي ��������وكلذلك أئمة علناهم

الحقيقة فمنهم وضالل رشد أئمة أنفسهم جعلوا وهم كذلك سميناهمالمجاز ومنه

Na kulinasibisha (neno) jaala kwa Mwenyezi Mungu ni majazi kwa maana ya kuita jina (na maana yake ni) ‘tuite sisi kuwa ni wenye kujisalimisha kwako’; halkadhalika (Aya isemayo) “Na tukawajaalia (tukawafanya) kuwa Maimamu”890 yaani tuliwaita hivyo, nao wakajifanya wenyewe kuwa ni Maimamu wa uongofu na upotufu, basi kutoka kwao ni hakika na kutoka kwake (Allah) ni majazi.891

Anaendelea Ibn Al-Qayyim, akinukuu maneno ya Sheikh wake Ibn Taymiyya:

معنى..... به فيعني معناه في ظاهرا اللفظ كون التوهم سبب يكون أوين���وي بأن باطنا يحتملهحقيقته دون اللفظ .....مجاز

888 - Maana ya kuashiria huku ni kama mtu kusema maneno kadha na maneno hayo yakawa yana maana mbili: maana ya mbali na maana ya karibu. Mwenye kusikiliza akaifahamu ile maana ya karibu. Na lengo ni kujiepusha na shari ya mtu. Na kwa hivyo, ikapokewa riwaya ikisema kwamba: الكذب عن لمندوحة المعاريض في Hakika kuashiria kunampa) إنmtu nafasi asiingie katika uwongo). Mfano wake ni kama watu wanayemtafuta mke wa fulani ili wamdhuru wakakutana naye wakamuuliza: ‘huyu ni nani?’ Akawajibu: “huyu ni ndugu yangu”. Wao wakafahamu ni ndugu yake katika nasaba, na hio ndio maana ya karibu, kumbe yeye anakusudia kuwa ni ndugu yake katika dini – Muislamu mwenzako, na hii ndio maana ya mbali nayo ndio ulioikusudia. Kwa hali hii, anakuwa hakusema uwongo na kajiepusha na shari zao. 889 - Ibn Al-Qayyim Ighaathatul Lahafaan uk. 413, chapa Al-Maktaba Al-Tawfiqiyya, tahqiq: ‘Abdul-Hakim Muhammad ‘Abdil-Hakim. 890 - Sura 21, Aya 73. 891 - Ibn Al-Qayyim Shifaau Al-’Alil uk. 100. Nayo ni maneno ya Ibn Taymiyya katika Kitabu Iqaamati Al-Dalil j. 1, uk. 145.

286

Page 287: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Au iwe sababu ya kukosea ni kuwa tamko ni dhahiri katika maana yake, yeye akusudie maana (yake nyengine) ambayo inawezekana kuwemo katika undani wake kwa maana kwamba akusudie majazi pasina hakika.892

Anasema Ibn Al-Qayyim:

األكثرين: عند مجازا فقط اثنين في استعماله يصح الجمع اسم أن الثاني..... بعضهم عند وحقيقة

Pili: ni kwamba jina la wingi (plural) linafaa kulitumia kwa wawili (lakini) kimajazi tu kwa mujibu wa (wanavyuoni) walio wengi, (na inafaa kulitumia hivyo) kwa hakika kwa mujibu wa baadhi yao.893

Anasema Ibn Al-Qayyim:

: إال الثالث، وبعض اثنين في الجمع استعمال صح وإن أنه الثاني الجوابوالحقيقة مجاز، أنه

ومجازه، حقيقته بين اللفظ دار وإذا اللفظ، وفق على المعنى يكون أنبه أولى فالحقيقة

Jawabu ya pili: ni kuwa hata kama ni sahihi kutumia wingi katika vitu viwili na sehemu ya kitu cha tatu, lakini hayo ni majazi; ama hakika ni kuwa maana iende kwa mujibu wa tamko; na tamko ikiwa lipo baina ya uhakika wake na majazi yake basi uhakika ndio uliobora zaidi (kuzingatiwa).894

IBN TAYMIYYA NA MAJAZI

Kama ulivyoona kwamba Ibn Al-Qayyim kakanusha majazi kisha akageuka na kuyatumia bali na akayataja kwa jina. Pia tumeona katika nukulu moja ya Ibn Al-Qayyim aliomnukuu Sheikh wake, Ibn Taymiyya, kwamba naye – katika nukulu hio – kayathibitisha majazi. Sasa tazama maneno mengine ya mwalimu mkuu, Ibn Taymiyya, ambaye pia alikuwa mstari wa mbele katika kuyakanusha majazi. Anasema:

بالخلق يليق الذي المعنى على الظاهر أطلق من خطأ لك يبين أن ،والذي : أحدهما نوعان األلفاظ

892 - Ibn Al-Qayyim I’ilaamu Al-Muwaqqi’iin j. 3, uk. 246. Ibn Al-Qayyim kaanza maneno haya kwa kusema: عنه الله رضي شيخنا Kasema Sheikh) قال wetu Allah amuwie radhi), kwa dhahir haya katika nukulu hii ni maneno ya Ibn Taymiyya; yeye anayanukuu tu. 893 - Ibn Al-Qayyim Zaadu Al-Ma’aadi j. 5, uk. 475. 894 - Ibn Al-Qayyim Zaadu Al-Ma’aadi j. 5, uk. 476.

287

Page 288: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

أسد قيل إذا فهذا والكلب والبحر والحمار األسد كلفظ مفرد معناه مارسوله وأسد ق ،الله يل������أو

قيل أو بحر الخيل من الجواد أو السخي أو للعالم قيل أو حمار للبليدث مجاز فهذا كلب إن �لألسد م

المراد تبين قرينة به لفرس كقرنت وسلم عليه الله صلى النبي ،قول : طلحة وج ))أبي دناه �����إن

على ))وقوله: ، ((لبحرا الله سله الله سيوف من سيف خالدا إنلعثم . ((المشركين ان: ��وقوله

قميصا )) قمصك الله : ((إن في الله يمين األسود الحجر عباس ابن وقولاستل , فمن مه �األرض

ربه بايع فكأنما ..…وصافحه

Na chenye kukubainishia kosa la wale wenye kuitumia maana ya dhahiri pasina kuifungamanisha na kitu kwa mujibu wa maana yenye kuwiyana na viumbe, ni kwamba matamshi yako ya aina mbili: Moja yao ni tamko ambalo lina maana pweke (halikuunganishwa na tamko jengine) kama vile tamko: simba, punda, bahari, mbwa. (Tamko la namna) hii pindipo itasemwa: ‘Huyu ni simba wa Allah na Mtume wake’, au ‘akaitwa mtu mwenye fahamu nzito kuwa ni punda’, au ‘mwanachuoni au mkarimu au farasi mwenye mwendo akaitwa kuwa ni bahari’ au ‘simba akaitwa mbwa’ basi haya ni majazi. Kisha ikiwa hayo yataambatana na qarina yenye kubainisha nini makusudio yake kama vile kauli ya Mtume (s.a.w.) aliposema kuhusu farasi wa Abi Talha: ‘Kwa hakika sisi tumemuona kuwa ni bahari’ na kauli yake ‘Hakika Khalid ni upanga katika panga za Allah; kauchooa dhidi ya makafiri” na kauli yake kwa ‘Uthman: ‘Hakika ya Allah kakuvisha kanzu’ na kauli ya Ibn ‘Abbaas: ‘Jiwe jeusi ni mkono wa kuume wa Allah katika ardhi’ atayelishika au kulipa mkono basi ni kana kwamba kambai’i895 Mola wake……….. 896

Anaendelea Ibn Taymiyya:

بل قالوا بما ولعنوا أيديهم غلت مغلولة الله يد اليهود وقالت قوله فيك ينفق مبسوطتان يف���يداه

اللفظ من ظاهرة عرفية حقيقة وهي مشهور يشاء مجاز هي أو

Katika kauli yake Allah: “Na Mayahudi wakasema kuwa mkono wa Allah umefungwa; mikono yao ndio iliofungwa na wakalaaniwa kwa walioyasema; bali mikono yake miwili imekunjuliwa anatoa (riziki) namna apendavyo” nayo (Aya hii) ni uhakika wa kikawaida uliowazi katika tamko au ni majazi yalio mashuhuri.897

895 - Kaekeana ahadi na Allah. 896 - Ibn Taymiyya Iqaamatu Al-Dalili j. 4, uk. 82. 897 - Ibn Taymiyya Iqtidhaau Al-Siraat j. 1, uk. 20.

288

Page 289: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

KASIM MAFUTA NAYE AJIGONGA

Kasim Mafuta naye anena:

Pamoja na kwamba inawezekana likatumika neno katika maana nyingine isiyokuwa ya asili, lakini mpaka ishindikane kutumika maana ya asili, kisha kuweko na dalili itakayotufahamisha kushindikana matumizi hayo ya asili ya neno hilo na kwenda nje ya asili yake.

Suali! Pale inaposhindikana kulitumia neno katika maana ya asili na ikabidi kulitumia katika maana isio ya asili, je ile maana isio ya asili inakuwa ni hakika au majazi? Usiniambie ni uslubu kwani – kama nilivyokueleza sana – hatuzungumzii majina ya kifani: tunazungumzia uhakika wa kitu. Suali ni kuwa je neno hilo linakuwa liko katika matumizi ya asili au limetoka katika maana ya asili?

Bila shaka maneno hayo ya Sheikh Kasim bin Mafuta, yanaashiria bali yanatongoa kwamba majazi ni kitu kilichopo. Na hili linapata nguvu kwa maelezo yake mengine aliposema:

Kwa sababu ili maneno yawe ni majazi, ni lazima masharti matatu makuu yatimie, nayo ni:1-Kutumika neno katika isiyo kuwa maana yake ya asili.2-Lazima kuwepo na “QARINATUN MAANI’ATUN MIN IRADATI MA’ANAL ASLIY” dalili yenye kuzuia kukusudiwa maana ya asili.3-Lazima kuwepo na “ALAAQAH” mafungamano baina ya neno la asili na neno lisilo la asili.

Na likikosekana sharti moja kati ya haya matatu tuliyoyataja basi hakutakuwa na majazi na atakayedai kuwa ni majazi basi huyo ni mwongo mkubwa na hajui lugha ya kiarabu898 …..

Lakini baada ya yote hayo, Sheikh Kasim kajikanganya mwenyewe na kujigonga kwa kuyakanusha kwake majazi katika sehemu nyengine za kitabu chake na kukubaliana na wale wenye kuyakanusha. Na hili linatoa jawabu ya wazi kwamba ndugu yetu hayuko katika haki wala haki haitaki wala hakuyakanusha majazi kwa sababu ya kuwa kakinai kwa hoja na dalili. Tazama maneno yake mengine kisha linganisha na hayo yaliotangulia:

JE WENYE KUPINGA MAJAZI WANA HOJA ZA KIELIMU?

898 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 40. Tena Sheikh Kasim kumbe yeye majazi anayajua basi tu!

289

Page 290: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Jambo muhimu la kulizingatia ni; je hao maulamaa waliopinga kuwepo kwa majazi, wamepinga kwa hoja na dalili za kielimu? Au ni kwa maneno matupu? Jawabu ni kama ifuatavyo:

Ukirejea kauli za maulamaa hao waliopinga kuwepo kwa majazi ima katika lugha ya kiarabu na Qur’an, au katika Qur’an tu, utagundua kwamba kuna hoja za msingi walizozitoa ambazo haitakiwi kuzipuuza, bali inatakiwa zitazamwe kielimu na kwa jicho la insafu. 899

Anaendelea Sheikh Ibn Mafuta kwa kusema:

Pia maulamaa wanaopinga kuwepo kwa majazi wanapowahoji na kuwapa changamoto (challenge) wenye kuthibitisha kuwepo kwa majazi hawapati majibu yoyote ya kuridhisha ndipo pale wakalipinga suala hili ili:-Lugha ya kiarabu isichezewe.-Ili watu wa batili wasipate nafasi ya kuichezea Qur’an kwa kupotosha maana yake kwa madai ya kwamba kuna majazi, na hili walilolifikiria ndilo lililotokea.

Kwa sababu wamejitokeza baadhi ya watu wakazipotosha aya nyingi zinazotaja sifa za Allah kwa madai kwamba kuna majazi kwa madai ya kumtakasa Allah na sifa za viumbe na hatima yake wakaingia katika upotofu.

Mpaka hapo itabainika kwamba;

Kupinga kuwepo kwa Majazi ndani ya Qur’an ili kufunga milango ya kuwaingiza watu kwenye upotofu ndiyo msimamo sahihi na wa haki na unaokubaliana na akili900 zaidi kuliko kudai kinyume chake. 901

Ni wazi kwamba Sheikh Kasim, sawa na Maimamu wake Ibn Taymiyya na Ibn Al-Qayyim, anakikanusha hapa kile ambacho kakithibitisha kule. Na hii ndio natija ya kukamatana na batili. Na lau ungelikuwa ewe Sheikh Kasim mwanangwa wa Mafuta hukuyathibitisha majazi kwa maneno yako yoyote yale isipokuwa kitendo chako cha kumwita Ibn Al-Qayyim kwa jina la “Shamsu Al-Din (Jua la dini)”,902 basi kingelitosha kitendo chako hicho kuonesha kuwa umejigonga, vyenginevyo wapi umesikia kwamba Ibn Al-Qayyim au mwanachuoni mwengine yoyote yule ni jua la kweli kweli la

899 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 43.900 - Akili ya nani?! 901 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 50.902 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 42.

290

Page 291: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

dini? Bali wapi umesikia kwamba dini ina jua (sayari). Wa Allahu Al-Musta’aan!

MUKHTASARI NA NUKTA MUHIMU

Baada ya mzunguko huu mrefu,903 ndugu Muislamu sina budi kusema kwamba imekubainikia kwa uwazi – nawe umo katika kuzipekuwa karatasi za kitabu hiki – kwamba:

1) Majazi ni neno lililotumika kinyume na maana yake ya asili.2) Maneno ya namna hio yamo kwa wingi katika Qur-ani, Sunna

(Hadithi za Mtume s.a.w.) na lugha ya Waarabu, kama vile ambavyo yamo katika lugha nyengine za binaadamu.

3) Waliokataa kuwepo kwa majazi hawakuja na hoja yoyote ilioweza kuthibitisha kwamba yale maneno yaliomo katika Qur-ani kama vile dini ya Kiislamu kuitwa kuwa ni kamba au msaada wa watu pia nao kuitwa kuwa ni kamba na mengineo, yametumika katika maana yake ya uhakika, ili iwezekane kuyakanusha majazi kwa hoja sahihi.

4) Sheikh Kasim Mafuta naye – akiwafuata Maimamu wake, Ibn Taymiyya na Ibn Al-Qayyim – kajitumbukiza katika kitu kitachomfanya dahari nzima achekwe kwa kuandika kitabu akakanusha kuwepo kwa majazi! Lakini kama ulivyoona, Sh. Kasim kashindwa kutoa hoja yoyote ya kimaandiko ilioweza kubomoa hoja za kimaandiko tulizozitoa. Bali hata kuzinukuu zile hoja zetu kikamilifu hakuzinukuu kwani kajua kwamba lau atazinukuu kikamilifu basi kila atayezisoma hawezi kukubaliana naye. Alichotegemea yeye ni falsafa na logic, lakini yote hayo yamefeli kuthibitisha madai yake au kubomoa madai yetu.

5) Ibn Al-Qayyim na Ibn Taymiyya – kama kawaida yao – wakadai kwamba hakuna katika Al-Salaf na wanavyuoni wakuu wa lugha na fani nyengine za elimu walioyataja majazi.

6) Tumethibitisha kimaandiko kwamba:a) Wako ambao hawakuyataja majazi kwa jina lakini

wameyatumia, kama vile maneno ya Al-Imamu ‘Ali katika mashairi yake tulioyanukuu.

b) Wako walioyataja majazi kwa jina jengine, kama vile Sibawayh na Al-Imamu Al-Shafi katika kitabu chake Al-Risala na wengine wengi. Lakini hili la kutaja jina – kama tulivyokariri – si muhimu, kwani kinachotazamwa ni uhakika wa kitu: si jina lake.

903 - Lakini usije ukadhania kwamba nimerefusha kama inavyotakiwa; laa, sio hivyo, mas-ala haya ni marefu yanahitaji juzuu yake peke yake. Tukijaaliwa nitavizungumia vipengele vyengine katika kazi nyengine. Kwa hapa natarajia kwamba maudhui hii imefahamika vya kutosha.

291

Page 292: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

c) Wako walioyataja kwa jina lake la kifani, kama ‘Uthman Al-Darimi, Al-Imamu Ahmad, Al-Imamu Abu Hanifa, Abu ‘Abbaas Al-Nnaashi, Al-Imamu Al-Shafi – kama ilivyo katika nukulu ya Al-Bazdawi – na wengine.

d) Kwa hivyo, madai ya Ibn Taymiyya na Ibn Al-Qayyim kwamba Al-Salaf hawakuyataja majazi hayana ukweli. Watu hawa wamekuwa na kawaida hio ya kila wakitakacho wao, basi wao huwatupia mzigo Al-Salaf ili wapate kuitangaza biashara yao. Na hapa inawapasa watu – hasa hasa huko kwetu Afrika Mashariki – wazinduke na propaganda za Kiwahabi za kwamba wao wanafuata Al-Salaf. Wallahi! Al-Salaf na wao ni umbali wa mashariki na magharibi, labda ikiwa wanakusudia Ibn Batta, Al-Hakkaari na walio mfano wa hao: si Al-Salaf Masahaba.

7) Hata kama kweli Al-Salaf hawakuyataja majazi, basi huo si ushahidi kwamba majazi hayapo kwani:

a. Kinachozingatiwa ni dalili: si chengine. Na dalili Wa-Lillahi Al-Hamdu zipo kwa wingi kama tulivyonukuu baadhi yake.

b. Tunachozungumzia ni uhakika wa kuwepo kwa majazi nalo ni neno lililotumika kinyume na maana yake ya asili: si kuwepo kwa technical term (jina la kifani), vyenginevyo fani zote – nahau, balagha, sarfu, pamoja na majina yanayotajwa ndani yake – zilikuwa hazipo. Lakini uhakika wake ulikuwepo.

8) Kwa haya machache, natarajia ndugu msomaji, imeweza kukubainikia haki ni ipi na batili ni ipi juu ya maudhui hii.

292

Page 293: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

SURA YA SABAKUHUSU TA-AWIL

Katika sehemu iliotangulia tulizungumzia suala la kuwepo kwa majazi katika Qur-ani, Hadithi na lugha ya Kiarabu. Tumeona kwamba kuyakataa majazi ndio msingi mmoja katika misingi mikuu iliowapoteza Mawahabi na Maimamu wao watangulizi hadi kufikia kumfanya Allah kuwa ana sura ya Adam!

Jambo jengine lililowapelekea kuwa na itikadi hizo ni kukanusha kwao ta-awil (tafsiri ya ndani au interpretation). Na ukanushaji wa jambo hili la pili limetokana na ukanushaji wa jambo la kwanza. Na dai lao kwa kukanusha ta-awil ni ngoma yao ile ile kwamba “Al-Salaf walikuwa hawafanyi ta-awil” bali walikuwa wanasema “Zipitisheni Aya za Sifa za Allah kama zilivyo”. Sasa kabla ya kuliweka wazi suala hili, kwanza natuanze kwa kuzungumzia nini maana ya ta-awil.

TA-AWIL KILUGHA

293

Page 294: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Kilugha, neno ta-awil linatokana na neno awwala (kitendo kilichopita) yuawwilu (kitendo kilichopo na kijacho). Na chimbuko hasa – kabla ya kulisarifu neno hilo hivyo – ni kitendo aala (kitendo kilichopita) yauulu (kitendo kilichopo na kijacho), na maana yake ni kuhitimika, yaani hatima ya kitu kilivyoishia na kinakorejea mwishoni. Anasema Allah:

ينظرون هل تأويله يأتي يوم تأويله إالHawana904 wanachokingojea isipokuwa matokeo (natija au hatima)

yake, basi siku yatapokuja matokeo yake…….

Anasema Sheikh Al-Saabuni: إليه...أي يؤول وما أمره عاقبة تأويله إليه صار (Maana ya neno) ta-awiluhu (ta-awili yake) ni hatima yake na

kule inakorejea yaani imekweda huko..905

Anasema Sheikhu Al-Mufassirin, Al-Imamu Badru Al-Din Al-Khalili:

Ta-awil – kilugha – inatokana na neno awlu kwa maana ya marejeo, na hio ni kwamba mwenye kufanya ta-awil huwa analirejesha (neno) kutoka kule linakokwenda (na kulipeleka) kule linakotakiwa (liende) kwa sababu ya kuwepo ushahidi wa qarina ambazo zimefuatana nazo.906

Anasema Al-Imamu Al-Zarkashi akifuatiwa na Sheikh ‘Abdul-Mun’im:

Ama ta-awil asili yake katika lugha inatokana na awlu, na maana ya msemo wao (wanavyuoni au Waarabu) wanaposema: ‘Nini ta-awili ya maneno haya? Yaani: ‘katika nini inarejea hatima ya makusudio yake’. Kama Allah alivyosema: تأويله يأتي يوم ((..Basi siku yatapokuja matokeo yake…….)), yaani itapofunuliwa hatima yake….na asili yake ni maalu nayo ni hatima na maishio.907

Hio – kwa ufupi – ndio maana ya kilugha ya neno ta-awil. Na maana hio imeoneshwa pia na baadhi ya maandiko kama vile Aya zenye kuzungumzia ta-awili za ndoto, kama:

904 - Nimeifasiri hivi kwani istifhaamu (neno la kuulizia) likifuatana na istithnaa (neno lenye kuvua kitu yaani exceptional) basi linamaanisha nafyu (kukataa). Mfano wake ni kama kauli yake Allah aliposema: اإلحسان جزاء هل اإلحسان إال “Je malipo ya wema isipokuwa wema”. Istifhamu (neno la kuulizia nalo hapa ni neno je) haliulizi, bali linakataa, na kwa hivyo tafsiri ya Aya hio ni: “Hakuna malipo ya wema isipokuwa wema”. 905 - Al-Sabuni Al-Safwa j. 1, uk. 308. 906 - Badru Al-Din Al-Khalili Jawaahiru Al-Tfaasir j. 1, uk. 16. 907 - Al-Zarkashi Al-Burhaanu Fii ‘Ulumi Al-Qur-an j. 2, uk. 148. Sh. ‘Abdul-Mun’im katika utangulizi wake alioutia katika Al-Nukatu Al-Mutammima cha Al-Imamu Ibn Taymiyya uk. 8-9.

294

Page 295: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

بتأويله نبئناTwambie ta-awili yake.

Maneno haya Nabii Yusuf aliambiwa na wale vijana wawili aliofungwa pamoja nao gerezani, baada ya kumsimulia ndoto zao walizoota. Wakamwambia tupe ta-awili yake, yaani hatima yake itakuwaje na itaishia vipi?908

Pamoja na hayo wanavyuoni wametafautiana kuhusu ta-awil na tafsiri: je ni kitu kimoja au vipi? Wakasema baadhi yao kuwa ni kitu kimoja. Imenukuliwa kauli hii kutoka kwa Abu ‘Ubaida.909 Anasema Al-Imamu Badru Al-Din Al-Zarkashi: “Na kilicho sahihi ni kuwa (tafsiri na ta-awili ni vitu viwili) tafauti”.910

Lakini kwa hali yoyote ile ikiwa ta-awili na tafsiri kwa asili ni sawa au ni tafauti, hili si muhimu kama tunavyoelezea mara nyingi; kilicho muhimu ni je kile kinachoitwa ta-awili na baadhi ya watu kipo katika uwanja wa Sharia au hakipo? Na kabla ya yote, je wao wanakusudia nini kwa neno ta-awil? Ama jina si muhimu. Anasema Ibn Taymiyya:

Hakika ya ta-awili kwa waliokuja baadae….ni kuliondoa neno kutoka katika maana yake yenye uzito na kulipeleka katika maana iliozidiwa uzito kwa sababu ya kuwepo kwa dalili iliofuatana nayo.911

Kwa ufupi ni kuwa ninachotaka kukizungumzia hapa ni kuwa je Al-Salaf (watangulizi) walikuwa wakiziletea ta-awili Aya za Qur-ani au hawakuwa wakifanya hivyo kama wanavyodai Mawahabi? Elewa ndugu msomaji kwamba wako katika Al-Salaf ambao zimepokewa riwaya kutoka kwao za kutokuzifanyia ta-awili baadhi ya Aya. Lakini si kama hivi wanavyotwambia Mawahabi na Maimamu wao kwamba walikuwa wakisema “Mungu ana mkono wa kweli lakini hatuujui ulivyokaa”. Kauli hii au kama hii haikupokewa kutoka kwa sahaba yoyote. Kilichopo ni kuwa walikuwa wakijizuia kuzifasiri Aya mutashabihat za Qur-ani. Na hii sababu yake si kwamba walikuwa wakiitakidi kwamba dhahiri ya Aya hizo ndio makusudio ya Allah; laa (sio hivyo), bali walifanya hivyo kwa sababu mbili:

1) Tahadhari yao kubwa ili wasije wakakosea. Na hili walilifanya hata katika Hadithi: wengi wao walikuwa hawataki kusimulia Hadithi, na wengine wakisimulia basi jasho huwatoka kwa khofu: wanaogopa wasijewakasimulia tafauti na alivyonena Mtume (s.a.w.).

908 - Al-Baghawi Ma’aalimu Al-Tanzil j. 2, uk. 491. 909 - Badru Al-Din Al-Khalili Jawaahiru Al-Tafasir j. 1, uk. 16. 910 - Al-Zarkashi Al-Burhaanu Fii ‘Ulumi Al-Qur-an j. 2, uk. 149. 911 - Ibn Taymiyya Majmu’a Al-Fatawa j. 13, uk. 164.

295

Page 296: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

2) Kutokufanya ijtihadi ikiwa haikulazimika: yaani ikiwa wakati huo ijtihad haihitajiki.

Vyenginevyo, basi elewa kwamba Masahaba hawakuacha kuzifanyia ta-awil Aya za Sifa za Allah tu, bali hata Aya nyengine pia walikuwa wakijizuia kuzifasiri ikiwa hakuna ulazima.

MANENO YA SHEIKH AL-KHALILI

Baada ya kueleza hivyo, Al-Imamu Badru Al-Din Al-Khalili alisema:

….Na miongoni mwa hayo ni kile kilichopokewa kutoka kwa Abu Bakr alipoulizwa kuhusu maana ya neno األب Al-Abbu lililomo katika Aya isemayo: وفاكهة وأبا (Wa faakihatan wa abban). Akasema (Abu Bakr): “Ni mbingu gani zitazonifunika na ni ardhi gani itayonibeba na wapi nitakwenda na nitafanyaje ikiwa nitasema kitu kuhusu kitabu cha Allah kinyume na makusudio ya Allah? Na yakapokewa kutoka kwa ‘Umar maneno yaliokaribu na hayo.

Hakuna shaka ikiwa watazinyamazia Aya mutashabihat kuhusu sifa za Allah, pamoja na kuwa pamepokewa kutoka kwao kwamba wamezifasiri idadi si ndogo katika hizo kwa mujibu wa kile chenye kukubaliana na misingi iliozama kwao nayo ni tanzihi ya (kumtakasa) Allah Mtukufu ambayo imethibiti kwa maandiko na kwa akili, na kujiongozea kwao katika mpito wa ta-awil kwa lugha ya Waarabu ambayo waliielewa vyema na wakaipima undani wake. Na mfano wa hilo ni kama kuifasiri mikono katika kauli yake Allah (S.W.) isemayo: ماء وإنا بأييد بنيناها والس Na mbingu tumeziumba kwa mikono yetu nasi ni wenye) لموسعونuwezo (wa kila kitu), kwa maana ya nguvu. Na halkadhalika kama ilivyopokewa kulifanyia ta-awili neno yamin (mkono wa kulia) lililomo katika kauli yake Allah (S.W.) isemayo باليمين منه خذناأل (Tungelimshika kwa (mkono) wa kulia), kama ilivyopokewa kutoka kwa Ibn Abbaas, Al-Dhahhak, Al-Hasan na Al-Kalbi. Na akasema Al-Hakam bin ‘Uyaina kuwa maana yake ni “kwa haki”. Na Ibn ‘Umar kailetea ta-awili Aya ya Qur-ani isemayo: حمن استوى العرش على الر (Mwingi wa rehema, katandawaa juu ya Kiti cha enzi), kwamba maana yake ni kutandawaa kwa jambo lake na uwezo wake juu ya viumbe vyake. Na ta-awili ya Ibn Abbaas ya Aya ya Qur-ani isemayo: ذو ربك وجه ويبقى

واإلكرام الجالل (Na utabakia uso wa Mola wako mwenye utukufu na heshima) kuwa maana yake ni kuwa kila kitu kitakwisha na atabakia Allah peke yake. Na mfano wake kutoka kwa Anas bin Malik, Al-Dhahhak na Mujahid…na mfano wa haya yako mengi. 912

912 - Badru Al-Din Al-Khalili Jawaahiru Al-Tafsir Juz-u Khaas, uk. 63-64.

296

Page 297: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Baada ya hayo, ni kuwa cha muhimu hapa ni kutazama je Al-Salaf walifanya ta-awili au hawakufanya? Mawahabi na Maimamu wao wanadai kuwa Al-Salaf hawakufanya ta-awil na kwamba madhehebu yao ndio madhehebu ya Al-Salaf. Wengine wasiokuwa Mawahabi wanadai kuwa Al-Salaf walifanya ta-awil. Je nini ushahidi wa wale wenye kudai kuwa Al-Salaf walifanya ta-awil. Baadhi ya ushahidi wao tayari tumeunukuu katika maelezo ya Sheikh Al-Khalili na kuna wengine wengi sana wamelizungumzia sula hili. Nitawanukuu baadhi yao kama inavyofuata:

MANENO YA DR. MUHAMMAD NA’IIM

Anasema Dr. Muhammad Na’iim Muhammad:

Miongoni mwa hao ni Imamu waliyekubaliana juu ya uimamu wake, Amirul-Mu-uminin katika Hadithi Muhammad bin Isma’il Al-Bukhari mwenye kitabu Sahihu Al-Bukhari kasema (Allah amrehemu) kuhusu kauli ya Mtume (s.a.w.): اللية الله ضحك .(Allah kacheka usiku huu) لقدKasema (Al-Bukhari) kuwa (kucheka kwa Allah) maana yake ni rehema.

Na miongoni mwao ni Al-Imamu Al-Shafi, Allah amrehemu, kasema kuhusu kauli yake Allah: الله وجه فثم (Huko kuna uso wa Allah). (Kasema Al-Shafi’i) kwa mujibu wa alivyonukuliwa na mwanafunzi wake Al-Muzani kuwa maana yake ni: “Huko kuna muelekeo aliokuelekezeni Allah”.

Na miongoni mwao ni Mujahid mmoja wa wafasirina wakuu katika Tabi’in, kasema kuhusu Aya hio iliotangulia913 kuwa: “Maana yake ni (kuwa huko kuna) kibla cha Allah, popote mutapokuwa mashariki au magharibi basi musielekee ila kwenye kibla hicho.914

Na miongoni mwao ni Sufyaan Al-Thauri moja ya nguzo za fiq-hi na Hadithi, kasema kuhusu Aya: هالك شيء كل وجهه إال (Kila kitu kitaangamia isipokuwa uso wake), kasema (kwamba maana yake ni kuwa kila kitu kitaangamia) isipokuwa kilichofanywa kwa kutakiwa radhi zake katika matendo mema. Imenukuliwa kauli hii na Al-Hafidh Ibn Hajar katika Al-Fat-hu, pia kauli hii ikanukuliwa kutoka kwa Mujahid.

Na miongoni mwao ni yule Bwana wao na Imamu wao, bahari (ya elimu), mwanachuoni (wa Umma) Ibn ‘Abbaas (r.a.), kasema kuhusu Aya: ( .kuwa maana yake ni “Kawa juu” (ya kila kitu) ,(Katandawaa) (استوى

913 - Yaani Aya isemayo: الله وجه .(Huko kuna uso wa Allah) فثم914 - Ninasema na tafsiri ya Mujahid kamuonesha Ibn Abbaas. Tazama Al-Nukat Al-Mutammima Limuqaddimat Ibn Taymiyya uk. 96.

297

Page 298: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Kainukuu kauli hio Al-Hafidh Ibn Hajar katika Al-Fat-hu na Al-Imamu Al-Baghawi katika tafsiri (yake).

Na miongoni mwao ni (kauli ya) Al-Imamu Al-Hasan Al-Basri kuhusu Aya isemayo: والملك ربك وجاء صفا صفا (Na akaja Mola wako na Malaika safu baada ya safu), kasema (kuwa maana yake ni): “likaja jambo lake na hukumu yake”. Kaisimulia (kauli hii) kutoka kwake Al-Imamu Al-Qur-tubi katika tafsiri yake.

Na miongoni mwao ni Al-Imamu Ahmad bin Hanbal, amesema kuhusu Aya hio iliotangulia : والملك ربك وجاء صفا صفا (Na akaja Mola wako na Malaika safu baada ya safu), (kuwa maana yake ni) “likaja jambo la Mola wako”.

Anasema Ibn Hajar katika Al-Fat-hu kuhusu Hadithi ساق عن فيكشفFayukshafu ‘an saaq (Ukafunuliwa muundi wa mguu).915 Kasema (Ibn Hajar) Allah amrehemu: Ama (neno) saaq imepokelewa kutoka kwa Ibn Abbaas kuhusu Aya (isemayo): ساق عن يكشف يوم (Yauma yukshafu ‘an saaq), kasema (Ibn Abbaas kuwa maana yake ni), kufunuliwa kwa uzito wa jambo,916 na Waarabu husema: الحرب قامت

ساق Vita vimesimama juu ya“ (Qaamatil harbu ‘alaa saaqin) علىmuundi wa mguu”, yaani (vita) vimepamba moto, na miongoni mwa maana hio ni (kauli ya mshairi isemayo):

** ساق على الحرب بنا وقامت األعناق ضرب أصحابك سن قدWatu wako wameanzisha mtindo wa kupiga shingo**Na vita vikatusimamia kwa saaq (muundi wa mguu).917

Na ikapokewa kutoka kwa Abu Musa Al-Ash’ari kuhusu tafsiri yake (Aya hio ساق عن يكشف يوم kwamba maana yake ni) nuru kubwa. Kasema Ibn Fuurak: ‘Maana yake ni yale yenye kujikariri kwa Muumini miongoni mwa faida na ihsani. Na akasema Al-Muhallab: ‘Kuwafunulia Waumini saaq (muundi) ni rehema na kwa wengineo (wasio kuwa Waumini) ni nakama.

Kasema Al-Khattabi:918 ‘Mashekhe wengi wanaogopa kujitumbukiza katika maana ya saaq (muundi) na maana ya kauli ya Ibn ‘Abbaas kwamba (maana ya Aya hio ni kuwa) Allah atafunua uwezo wake ambao kwawo tabu kubwa itadhihiri, na Al-Bayhaqi akaitegemeza riwaya hio iliotajwa

915 - Hii ni tafsiri ya neno kwa neno (literally). 916 - Yaani uzito wa siku ya kiama: sio kufunuliwa mguu wa Mungu kama wanavyoitakidi Al-Hashwiyya, Mujassima. 917 - Yaani vikashamiri kwani vita havina mguu. 918 - Maneno haya yote bado ni “maneno ya Ibn Hajar,” Dr. Muhammad Na’iim ananukuu tu.

298

Page 299: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kutoka kwa Ibn Abbaas kwa sanad mbili zote ni hasan na akaongeza (yaani Ibn Abbaas kwamba) ikiwa kitu chochote kitajificha juu yenu katika Qur-ani basi kifatilieni katika mashairi kwani ndio diwani ya Waarabu. Na akategemeza Al-Bayhaqi kutoka kwa Ibn Abbaas njia nyengine sahihi, kasema (Ibn Abbaas kwamba Allah kwa Aya hio): ‘Anakusudia siku ya kiama.’919

Baada ya hayo, utaona kwamba madai ya kuwa Al-Salaf (watangulizi) walikuwa hawazifanyi ta-awil Aya za sifa za Allah, si madai sahihi. Bali msingi wa madai haya ni zile zile propaganda za watu wenye itikadi ya Mungu mwenye kiwiliwili chenye viungo kutaka kuipigia debe itikadi yao. Nami nasema kwamba kufanya ta-awil ni jambo la kimaumbile kwani hata binaadamu si kila wakati huwa wanazungumza kwa maneno yalio wazi, bali mara nyengine huzungumza kwa mafumbo na mithali. Na hili lipo katika lugha zote. Na kwa hivyo, ninachotaka kukisema ni kuwa ikiwa ta-awili maana yake ni kuacha dhahiri ya neno au sentensi na kuipeleka katika maana nyengine ambayo pia imo katika neno hilo au sentensi hio kwa sababu ya kuwepo ushahidi mwengine, basi elewa kwamba hata hao wanaokanusha ta-awili katika Aya za sifa za Allah kwamba nao pia wameziletea ta-awili baadhi ya Aya hizo. Kwa mfano, Aya inayosema: وهو

كنتم ما أين معكم (Naye yuko pamoja na nyinyi popote mulipo). Aya hii udhahiri wake ni kuwa Allah yupo popote. Lakini pamoja na hivyo, Mawahabi na viongozi wao wanasema kuwa maana yake ni: “Yupo kila pahala kwa elimu yake” ama Yeye Mwenyewe “yuko mbinguni kakaa kitako juu ya ‘Arshi’. Utaona kwamba dhahiri ya Aya hio wameiwacha kwa sababu ya ushahidi mwengine walioutegemea wao.

Halkadhalika tukirudi katika suala la viungo: suala la kuwa Allah ana mkono, mguu n.k. Utaona kwamba mkono na mguu ni uhakika ambao ukiutaja unafahamika katika lugha ya Kiarabu na nyengine. Al-Munazziha (wenye kumtakasa Allah) wakasema kuwa maana ya mkono – kwa mfano – ni uwezo, nguvu n.k., wakati Mawahabi na Maimamu wao wakasema kuwa “ni mkono kweli lakini si kama tuujuavyo”. Kwa hivyo, utaona kwamba hata wao pia hapa wameleta ta-awil kwani kama si mkono huu tuujuao na ujulikanao katika lugha ya Kiarabu ambayo ndio lugha ya Qur-ani, basi pia nawe umeleta ta-awil. Hatimae nikajikuta kumbe nimetanguliwa katika kutoa maelezo haya na Dr. Al-Buti.

MANENO YA DR. AL-BUTI

919 - Dr. Muhammad Na’iim Muhammad Al-Qaanuun uk. 413-414.

299

Page 300: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Na tumebainisha kwamba sehemu waliokubaliana katika maandikio haya ni kutokuyapa maana yoyote yenye kumaanisha kuwa Allah ana mpinzani au anafanana na viumbe, na kutokuzivunja dalili zake za kilugha zilizothibiti.

Na (kwa hivyo) marejeo yaliothibiti katika hali hii ni kuzifasiri lafdhi hizi kwa udhahiri wake kwa mujibu wa inavyowiyana na kumtakasa Allah kutokana na mfano na mshirika, na hili linamaana ya kujikinga zisifasiriwe (lafdhi hizo) kwa maana ya viungo na kiwiliwili; ikasemwa kwa mfano: “katandawaa juu ya ‘Arshi yake kama alivyosema, kutandawaa kwenye kuwiyana na utukufu wake na upweke wake, naye ana mkono kama alivyosema, (lakini mkono) wenye kuwiyana na uungu wake na utukufu wake…..au kuzifasiri (lafdhi hizo) kwa maana ya kimajazi zenye kukubaliana na kanuni za kilugha na kuafikiana na kawaida ya wanavyosemezana Waarabu na maana inayoletwa na qarain (mtiririko wa maneno au context), kwa maana kwamba lifasiriwe neno االستواء (kutandawaa) kwa maana ya kutawala na neno mkono kwa maana ya nguvu…..

Na kuifuata yoyote katika tafsiri mbili hizi basi hakuachi kuwa ni ta-awil. Isipokuwa ta-awil ya mwanzo ni ijmali (ya ujumla tu, haikufafanuliwa) na ta-awil ya pili ni tafsili (iliofafanuliwa).

Huoni kwamba maana ya kilugha ya mkono, uso, na jicho si nyengine bali ni kiungo hiki kinachoeleweka ambacho viumbe wanakitumia, nacho kimeondolewa kwa Allah katika hali zote na katika tafsiri zote (mbili)...920

Hayo ni maneno ya Al-’Allama Dr. Al-Buti. Kisha baada ya hapo akawanukuu wanavyuoni ambao wamefanya ta-awil katika wanavyuoni wa Al-Salaf. Wengi wao tumeshawataja katika nukulu ya Dr. Muhammad Na’iim iliotangulia, lakini tunaongeza:

Kile kilichosimuliwa na Ibn Taymiyya kutoka kwa Ja’afar Al-Saadiq (r.a.) kwamba kaliletea ta-awil neno wajh (uso wa Allah) lililomo katika Aya:

هالك شيء كل وجهه إال (Kila kitu kitaangamia isipokuwa uso wake), kuwa maana yake ni Dini.921.......

…..(Na) kutoka kwa Ibn Abbaas na wafasirina wengi kwamba wameliletea ta-awil neno االستواء (kutandawaa) lililomo katika Aya ya Qur-ani isemayo: حمن استوى العرش على الر (Mwingi wa rehema, katandawaa juu ya Kiti cha enzi), kuwa maana yake ni kuwa juu (ya

920 - Dr. Muhammad Said Ramadhan Al-Buti Al-Salafiyya Marhala Zamaniyya Mubaaraka: La Madh-habun Islamiyya uk. 132-133. 921 - Dr. Muhammad Said Ramadhan Al-Buti K.h.j. uk. 135.

300

Page 301: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

viumbe wote).922 Na mfano wake ni kile alichokipokea Ibn Hajar kutoka kwa Ibn Al-Battal: ……‘Ama kulifasiri neno االستواء (kutandawaa) kuwa maana yake ni kuwa juu (ya viumbe) ni sahihi, nayo ndio madhehebu ya haki na ndio kauli ya Ahli Sunna’.923

Bali wakati Ibn Taymiyya na wafuasi wake wanawapinga wale wenye kuziletea ta-awili lafdhi hizo zenye kuonesha kuwa Allah ana viungo, yeye mwenyewe kaliletea ta-awil neno uso lililomo katika Aya:

واإلكرام الجالل ذو ربك وجه ( ويبقى26) فان عليها من كلKila kilichopo juu yake kitamalizika; na utabakia uso wa

Mola wako mwenye utukufu na heshima.924

Ibn Taymiyya kalifasiri neno uso lililomo katika Aya hio kwa maana ya jiha (upande yaani sehemu au muelekeo) kama alivyonukuliwa na Dr. Muhammad Al-Buti925 kutoka katika kitabu chake Majmuu’a Al-Fatawa.926

Na kwa mukhtasari ni kuwa:

1) Ta-awil ni kulitoa neno au sentensi katika maana yake ya dhahiri na kulipeleka katika maana nyengine ambayo pia imo ndani ya neno hilo au sentensi hio.

2) Sababu ya kulitoa katika maana hio ya dhahiri ni kuwepo ushahidi mwengine kwamba maana ya dhahiri sio iliokusudiwa. Na hii ni pale ambapo:

a) Bila ya kulifanyia ta-awili andiko moja basi dhahiri ya maandiko mawili yatakuwa yanagongana.

b) Dhahiri yake linagongana na hoja ya yakini ya kiakili. Nikisema hoja ya yakini, basi elewa kwamba ni ile hoja ambayo kwa hakika haikubaliani na akili ya mtu yoyote kabla ya kuwa na itikadi fulani. Kama vile mtu mmoja kuwa yuko Zanzibar na Oman kwa wakati mmoja. Na kwa hoja hii haiwezekani kudai kuwa Allah yuko mbinguni au kakaa kitako juu ya ‘Arshi kwani mbingu zimeumbwa na Allah, wakati Allah yupo kabla ya kiumbe chochote. Kwa hivyo, ukisema kwamba Allah yuko mbinguni suali la kuwa je kabla ya kuumba mbingu alikuwa wapi ni suali la lazima. Wakati

922 - Yaani yuko juu ya viumbe wote kwa utukufu, uweza, elimu na nguvu. 923 - Dr. Muhammad Said Ramadhan Al-Buti K.h.j. uk. 136. 924 - Sura 55 Aya 26-27.925 - Dr. Muhammad Said Ramadhan Al-Buti K.h.j. uk. 135. 926 - J. 2, uk. 428 na kuendelea.

301

Page 302: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

tunakubaliana kwamba Allah habadiliki katika Dhati yake wala katika sifa zake akawa ametoka katika hali moja kwenda hali nyengine – hizo ni dalili za kiumbe.

c) Iwe dhahiri ya andiko linamshabihisha Allah na kiumbe.3) Watu wote wameyafanyia ta-awil baadhi ya maandiko kwa sababu

hizo tulizozitoa. Wajiitao Al-Salafiyya (Mawahabi) kwa mfano wameiletea ta-awil Aya : كنتم ما أين معكم وهو (Naye yuko pamoja na nyinyi popote mulipo),927 ambapo dhahiri ya Aya inaonesha kuwa Allah yupo kila sehemu. Lakini wao – na wengine – wamesema kwamba kuwepo huku ni kuwepo kwa elimu yake tu: si Dhati yake. Pia Ibn Taymiyya kaliletea ta-awil neno uso lililomo katika Aya ربك وجه ويبقى (Na utabaki uso wa Mola wako). Kama vile ambavyo Aya nyingi na Hadithi nyingi zenye majazi pia wameziletea ta-awil kwa kuzifasiri kwa maana ya kimajazi. Kama vile Ibn Manda – mmoja wa Maimamu wa Kiwahabi – kuifasiri Hadithi isemayo: “Allah kamuumba Adam kwa sura yake” kuwa maana yake kamuumba kama alivyokuwa hakupita katika utoto, ujana na uzee.

4) Al-Salaf – kama tulivyoona – pia wameziletea ta-awili Aya za sifa za Allah.

5) Wengine hawakufanya hivyo, lakini pia hawakusema kuwa Allah ana mkono wa kweli kweli kama wanavyosema Mawahabi na Maimamu wao.

Kwa hivyo, madai kwamba Al-Salaf hawakuzifanyia ta-awil Aya hizo si madai sahihi bali ni propaganda za wafuasi wa skuli ya mungu-mtu au god-incarnate!

Kwa haya machache, inatosha kubainisha ukweli kwamba kauli sahihi ni kuwa Aya za Qur-ani na Hadithi za Mtume (s.a.w.) zinafanyiwa ta-awil ikibidi, cha muhimu ni kuwa ta-awili hio iwe imo ndani ya kanuni na misingi inayokubalika. Muhimu wao katika hayo ni kuwa:

1) Ile maana ambayo umeizingatia katika ta-awil iwe imo ndani ya neno, kwa maana kwamba Waarabu wanaitumia maana hio pia. Kwa mfano kulifasiri neno mkono kwa maana ya hoja, nguvu, sapoti (kuunga mkono), neema, uwezo, inakubalika kwani maana zote hizo Waarabu wanazitumia. Kwa hivyo, qarina ya kimaandiko au hoja ya kiakili ya yakini ikionesha kwamba neno mkono katika Aya kadha au katika Hadithi kadha halikutumika katika maana yake ya kiasili

927 - Sikusudii kusema kwamba ni wao tu ndio walioiletea ta-awil Aya hii, bali nakusudia kusema kwamba na wao hapa wameleta ta-awil.

302

Page 303: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

basi itaangaliwa qarina ni maana gani katika hizo na nyenginezo ambayo inalifaa neno hilo hapo.

2) Iwe kuna qarina iliozuia kuileta maana ya asili. Na qarina inaweza ikawa lafdhiyya (iliotamkwa) au haliyya (ya hali ilivyo), na hii ya pili inaingia pia qarinatun ‘aqliyya (karina za kiakili).

KUJIGONGA KATIKA SUALA LA TA-AWIL

Baada ya hayo, ndugu msomaji sasa tazama jinsi watu wa batili walivyokuwa maisha yao yote hawana msimamo! Wakati wao wanapinga ta-awil na wanaiita tahrif (upotoshaji), tazama mmoja wa Maimamu wao wakuu anavyosema. Anasema Ibn Manda:

: ض على وتكلموا الحديث هذا معنى في التأويل أهل شتى، ���اختلف روبمن الله: ���واألحسن أن ها

. – – ثم طفال يخلقه لم معناه صورته على السالم عليه آدم خلق تعالىث ا�صبي كهال ))��ثم شيخا م

... في... وقال آخر اه� (( موضع النبي: أراد علي وإنما الله وسلم ����صلى هخ الله أن الكالم لق �بهذا

آدم صورة على آدم اه� .بني

Wametafautiana watu wa ta-awil kuhusu maana ya Hadithi hii na wakazungumzia aina tafauti, na bora yao katika hizo ni kuwa: Allah kamuumba Adam (a.s.) kwa sura yake kwa maana kwamba hakumuumba mtoto kisha mtu mzima kisha mzee”.Mwisho wa kunukuu.928 Kisha akasema Ibn Manda katika sehemu nyengine: “Na kwa hakika Mtume (s.a.w.) kakusudia kwa maneno haya kwamba Allah kawaumba watoto wa Adam kwa sura ya (baba yao) Adam”.929

Natarajia siku haziko mbali Ibn Manda naye atakuwemo katika orodha ya Muawwila Mu’attila na watu wa bidaa, hususan ukizingatia kwamba katika maana hii alioitegemea yeye hapa kenda kinyume na Mzee wa Uislamu Ibn Taymiyya.

Kama vile ambavyo tumeona hapo nyuma kidogo jinsi Ibn Taymiyya alivyolifanyia ta-awili neno uso lililomo katika Aya:

واإلكرام الجالل ذو ربك وجه ( ويبقى26) فان عليها من كلKila kilichopo juu yake kitamalizika; na utabakia uso wa

928 - Ibn Manda Kitabu Al-Tawhid kilichotiwa maelezo na Dr. Ali Al-Faqihi uk. 222-223, Hadithi na. 83. 929 - Ibn Manda Kitabu Al-Tawhid kilichotiwa maelezo na Dr. Ali Al-Faqihi uk. 223-224, Hadithi na. 84.

303

Page 304: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Mola wako mwenye utukufu na heshima.

Ibn Taymiyya kalifasiri neno uso lililomo katika Aya hio kwa maana ya jiha (upande yaani sehemu au muelekeo) kama alivyonukuliwa na Dr. Muhammad Al-Buti930 kutoka katika kitabu chake Majmuu’a Al-Fatawa.931

Na labda yule Sahaba mtukufu sana anayetetewa kwa hali na mali, basi karibu atawekwa katika orodha ya wasiojua lugha ya Kiarabu. Huyu si mwengine bali ni Sheikh Mu’awiya bin Abi Sufyaan ambaye anasema:

Ali (bin Abi Talib) alikuwa na mikono miwili ya kuume mmoja nimeukata siku ya (vita vya) Siffin, Yaani Ammar bin Yasir, na mmoja nimeukata leo, yaani Al-Ashtar”.932

Bwana Kasimu! Vipi Imamu wako anawaita watu kuwa ni mikono ya mtu mwengine au naye hajui lugha kama hivi mimi?

Na lau Sheikh Kasim Mafuta aliyasoma maneno ya mwanachuoni mkuu wa Umma, Al-Bahru Ibn Abbaas (r.a.), basi angelitwambia kwamba Masahaba hawakuwa watu kamili bali walikuwa ni «meno» tu! Kwanini ? Kwa sababu Ibn Abbaas anasema kuhusu Watu wa Nahrawaan:

Wao Wallahi ni jino la mwanzo katika Masahaba wa Muhammad, Wao Wallahi ni watu wa Baranis (kofia refu)933 na viguzo.934

Ama Al-Bukhari, yeye kasema kuhusu Aya: وجهه إال هالك شيء كل(Kila kitu kitaangamia isipokuwa uso wake), kuwa maana yake ni “Isipokuwa ufalme wake”. Sijui kama Al-Bukhari ataendelea kuwa katika Maimamu wa Ahlu Sunna au atageuka sasa kuwa naye mtu wa bidaa!935

930 - Dr. Muhammad Said Ramadhan Al-Buti K.h.j. uk. 135. 931 - J. 2, uk. 428 na kuendelea. 932 - Al-Tabari Al-Taarikh j. 3, 133. Ibn Al-Athir Al-Kamil j. 2, uk. 705. Maana ya mikono miwili ya kuume ni ((Wasaidizi wawili wa nguvu)). 933 - Neno baranis ni wingi wa neno Burnus, nalo lina maana si chini ya tatu: 1) kofia refu 2), nguo yoyote ile ambayo imeungana na kofia yake 3), nguo za kuvaa baada ya kukoga zenye mikono mipana. Lakini dhahir ni kuwa maana ya mwanzo ndio iliokusudiwa hapa. 934 - Maana ya maneno: “Watu wa ….viguzo”, ni kuwa kila wakati walikuwa wameegemea nguzo za msikiti wanasoma Qur-ani. 935 - Al-Bukhari Al-Sahih katika suratu Al-Qasas kabla ya riwaya na. 4772.

304

Page 305: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

SURA YA NANEMSIMAMO WA MADHEHEBU ZA KISUNNI

JUU YA ITIKADI HIZO: NUKULU KUTOKA KATIKA KITABU “AL-BALSAM AL-SHAFI”

Tumeona madai ya Mawahabi kwamba itikadi zao hizo za Mungu mwenye kiwiliwili chenye viungo ndio itikadi za Ahlu Sunna Wa Al-Jamaa’a. Na kama tunavyoelewa kwamba jina hili Ahlu Sunna Wa Al-Jamaa’a linatumiwa na baadhi ya Waislamu kumaanisha madhehebu nne – Hanafi, Maliki, Shafi na Hanbali.

Sasa ninachotaka watu wakifahamu hapa ni kuwa itikadi hizo kimsingi ziko kwa baadhi ya Wanavyuoni wa Kihanbali: si katika madhehebu nne hizo. Ama katika madhehebu hizo huweza kutokea mwanachuoni wa Kishafi au Kihanafi au Kimaliki akawa na itikadi hizo, lakini hio inabakia kuwa ni rai yake naye huwa kiitikadi si Shafi tena au si Maliki tena au si Hanafi tena. Ama Shafi – kwa mfano – tukiizungumzia kama ni madhehebu, basi haikubaliani na itikadi hizo. Na wapo miongoni mwao ambao waliziita itikadi hizo kuwa ni itikadi za washirikina. Kama vile Al-Fakhru Al-Razi alivyokiita kitabu al-tawhid cha Ibn Khuzaima kuwa ni kitabu al-shirk (kitabu cha ushirikina) na kumwita Ibn Khuzaima kuwa hana akili.936 Kwa

936 - Anasema Al-Fakhru Al-Razi:الكتاب في اآلية بهذه أصحابنا استدالل أورد خزيمة بن إسحاق بن محمد أن اعلم

الشرك ( ) كتاب الحقيقة في وهو بالتوحيد سماه الذي“Jua kwamba Muhammad bin Is-haaq bin Khuzaima kataja kutoa ushahidi kwa wanavyuoni wetu kwa kutumia Aya hii katika kitabu alichokiita “Tauhiid” nacho ukweli wake ni Kitabu Al-Shirk (kitabu cha ukafiri).” Tazama Al-Fakhru Al-Razi, Mafatihu Al-Ghaib j. 27, uk. 133, katika tafsiri ya Aya ya 7 ya Surat Al-Shura (Sura 42).

305

Page 306: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

hivyo, dai la Mawahabi kwamba itikadi zao ni itikadi za Ahlu Sunna Wa Al-Jamaa’a ni dai hewa, kama kawaida yao jambo wanalolitaka hukwambia kuwa hili: “Umma umekubaliana juu yake…hii ndio kauli ya Ahlu Al-Sunna….hii ndio kauli ya Al-Salaf” ilhali ni kitu chenye khilafu mashuhuri, na jumhur ya Ahlu Al-Sunna na Al-Salaf wana rai kinyume na hio.

Sasa, ili kuthibitisha hayo, natutazame baadhi ya yaliosemwa na wanavyuoni wa Kisunni zamani na leo.937 Nakunukulia hayo kutoka katika kitabu Al-Balsam Al-Shaafi cha Dr. Zakariyya Al-Muharmi:938

Al-Hasan Al-Basri Anasema kuhusu Aya حمن استوى العرش على الر (Mwingi wa rehema katandawaa juu ya kiti cha enzi) kuwa maana yake ni:

Umetukuka utajo wake, na sifa zake na utukufu wake juu ya viumbe vyake; wala Allah Mtukufu hasifiwi kwa kuondoka kutoka sehemu kwenda sehemu.939

Yaani anachokisema Imamu huyu ni kuwa Allah alikuwepo kabla ya kuumba ‘Arshi naye yuko vile vile habadiliki kutoka hali kwenda nyengine, kwa hivyo Aya hio haijaleta maana kwamba Allah kakaa juu ya Arshi baada ya kuiumba, bali kinachokusudiwa hapo ni kuwa Allah katangaza utukufu wake. Hayo ni Maneno ya Al-Imamu Al-Hasan naye ni katika Al-Salaf na tafsiri yake hio ni tafauti na tafsiri ya Mawahabi na Maimamu wao walipodai kuwa Allah anakaa kitako kweli kweli wakitoa ushahidi kwa Aya hio.

Ali bin Husain bin ‘Ali bin Abi Talib. Anasema: “Wewe ndiye Allah ambaye humo katika sehemu (huna kitu pahala au sehemu)”.940 Ninasema: lakini Mawahabi na Maimamu wao wanasema “Yuko mbinguni” kwa hivyo dhana (concept) ya Mungu kwao ni changing god (Mungu mwenye

937 - Wanavyuoni na Maimamu wa Kisuni waliozipinga itikadi za Kiwahabi na watangulizi wao ni wengi mno, lau sihofii kurefusha sana ningelikunukulia ziada nyingi. Lakini ukipenda rejea kitabu Al-Maqaalatu Al-Sunniyya cha Sh. Abdullah Al-Harari uone humo maneno ya watu kama Ibn Hajar na walio mfano wake. 938 - Tazama nukulu hizi kutoka katika kitabu Al-Balsam Al-Shafi cha Dr. Zakaria uk. 72-85. Yako mengine nimeyawacha na mengine nimeyaongeza kutoka katika vitabu vyengine nayo ni yale nilioyaweka chini ya heading “SIFA TAFAUTI”. Halkadhalika nimeongeza sherehe katika baadhi ya sehemu na nimeweka marejeo (references) katika baadhi ya sehemu ambazo hakuweka marejeo.939 - Al-Rabi’u bin Habib Al-Jami’u Al-Sahih riwaya na. 873. 940 - Ittihafu Sadati Al-Muttaqin j. 4, uk. 340. Maj’mu’a Al-Baahithin Ghayatul Bayaan uk. 67.

306

Page 307: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kubadilika) kwani yeye yupo kabla ya kuziumba mbingu kisha akaumba mbingu na Arshi akenda akakaa juu ya Arshi huko mbinguni! Sisi tunasema kuwa Mungu habadiliki katika sifa zake wala katika dhati yake: kama alivyokuwa ndivyo alivyo na ndivyo atavyokuwa milele.

Ja’afar bin ‘Ali bin Al-Husain. Anasema:

Atayedai kwamba Allah yumo ndani ya kitu au anatokana na kitu basi amekufuru (kufuru ya ushirikina), kwani lau alikuwa juu ya kitu basi angelikuwa kabebwa (na kitu hicho); na lau alikuwa ndani ya kitu angelikuwa kazungukwa na kitu hicho; na lau alitokana na kitu basi angelikuwa kazuka (alikuwa hayupo baadae akawepo).941

Ninasema: lakini Mawahabi na Maimamu wao wanasema: “Wewe ndiye Allah uliyebebwa mzegamzega juu ya kiti na Malaika wenye sura za wanyama: na uko mbinguni lakini miguu yako ipo kila mahala942 kwani kiti (kursiy) ndio sehemu ya kuweka miguu hio, nacho kimeenea mbingu na ardhi kama Qur-ani ilivyonena!!!”

Al-Imamu Abu Hanifa. Anasema:

Na tunakiri kwamba Allah Mtukufu yuko juu ya ‘Arshi bila ya kuwa Yeye anaihitijia (hio ‘Arshi) wala (bila ya) kukaa (kitako) kweli kweli juu yake. Naye anaihifadhi ‘Arshi na mengineo bila ya kuwa anayahitajia, lau alikuwa ni mwenye kuhitajia basi asingeliweza kuuleta ulimwengu na kuuendesha kama (walivyokuwa hawawezi) viumbe. Na lau alihitaji kukaa kitako na kutulia (juu ya ‘Arshi), basi Allah alikuwepo wapi kabla ya kuumba ‘Arshi. Basi Allah ametakasika mtakasiko mkubwa kutokana na hayo.943

Anaendelea Al-Imamu Abu Hanifa kwa kusema:

Unaonaje lau itasemwa Allah yuko wapi? Alisema – yaani Abu Hanifa –: ‘Ataambiwa Allah alikuwepo wala hakuna sehemu kabla ya kuumba viumbe, na Allah alikuwepo wala hakuna kitu “wapi” wala (hakuna) kiumbe wala kitu (chochote) naye ndiye mwenye kuumba kila kitu.944

941 - Maj’mu’a Al-Baahithin Ghayatul Bayaan uk. 67. 942 - Usijeukasema: “Aaa! Watuzulia uwongo: sisi hatusemi hivyo”. Kwani hivyo ndivyo itikadi yenu inavyomaanisha, kwani ikiwa miguu ya Allah iko juu ya kursiy (kiti) kama munavyosema na Qur-ani inasema kwamba kursiy (kiti) kimenea mbingu na ardhi. Kwa hivyo, natija ni kuwa miguu ya Allah iko kila pahala: mbinguni na ardhini! 943 - Kitabu Al-Wasiyya Majmu’a Rasaail Abi Hanifa Bi-Tahqiq Al-Kawthari uk. 2, tazama: Maj’mu’a Al-Baahithin Ghayatul Bayaan uk. 67.944 - Maj’mu’a Al-Baahithin Ghayatul Bayaan uk. 68, Al-Fiq-hu Al-Absat uk. 20.

307

Page 308: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Ninasema: Lakini ewe Imamu Abu Hanifa we! Kuna watu wanajiita Ahlu Sunna wanadai kwamba Allah kakaa kitako juu ya ‘Arshi huko mbinguni!

Al-Imamu Al-Shafi, Muhammad bin Idris. Anasema:

Hakika yake Allah Mtukufu alikuwepo wala hakuna sehemu, basi akaumba sehemu naye yuko katika sifa yake ya azali kama alivyokuwa kabla ya kuumba sehemu, haimfalii Yeye kubadilika katika Dhati yake wala kubadilika katika sifa zake.945

Dhu Al-Nun Al-Misri (245 A.H.). Aliulizwa Imamu huyu wa Kisufi kuhusu Aya حمن استوى العرش على الر (Mwingi wa rehema katandawaa juu ya ‘Arshi). Akajibu: “Kathibitisha Dhati yake na akajikatalia sehemu. Basi Yeye yupo kwa Dhati yake na vitu vipo kwa hekima kama Allah alivyotaka”.946

Abu Ja’afar Ahmad bin Salaama Al-Tahawi Al-Hanafi (321 A.H.). Anasema katika kitabu chake Al-Tahawiyya:

Na Allah ametakasika kutokana na mipaka na ukomo na nguzo na viungo na visaidizi; haingii katika sehemu sita (juu, chini, kulia, kushoto, mbele na nyuma) kama (vile vinavyoingia) vitu vilivyozuka (katika sehemu sita hizo).947

Imamu Ahli Sunna, Abu Al-Hasan Al-Ash’ari (324 A.H.). Anasema:

Allah alikuwepo wala hakuna sehemu, akaumba ‘Arshi na Kiti (Kursiy) wala hakuwa na haja ya sehemu, naye baada ya kuumba sehemu yuko kama alivyokuwa kabla ya kuziumba. 948

Al-Imamu Abu Mansur Al-Maaturidi (333 A.H.). Anasema katika kitabu chake Kitabu Al-Tawhid:

Hakika ya Allah alikuwepo wala hapakuwa na sehemu. Na sehemu zinajuzu kuondoka naye akabakia vile vile alivyokuwa. Basi Yeye yuko

945 - Ittihaafu Sadatil Muttaqin j. 2, uk. 24. Maj’mu’a Al-Baahithin Ghayatul Bayaan uk. 71-164.946 - Kitabu ninachokinukuu hakikutaja marejeo ya kauli hii. Tazama Dr. Zakaria Al-Muharmi Al-Balsam Al-Shafi uk. 77. 947 - Al-’Aqiidatu Al-Tahaawiyya uk. 26. 948 - Kainukuu Ibn ‘Asaakir katika Tabyiinu Kadhibi Al-Muftari uk. 150.

308

Page 309: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kama alivyokuwa, alivyokuwa ndivyo alivyo sasa hivi. Ametakasika kutokana na kubadilika, kuondoka na kuhama (sehemu hadi sehemu).949

Al-Hafidh Muhammad bin Hibbaan, mwenye Sahih Ibn Hibbaan (354 AH). Anasema katika utangulizi wa kitabu chake Al-Thiqat: “Sifa zote zilizo njema ni za Allah ambaye hana mpaka ikawa ni sababu ya kuangamia….”.950 Ninasema: Ewe Ibn Hibbaan we! Mbona Ibn Taymiyya na wenzake wanasema kuwa Allah ana mipaka? Hili ndilo lililokuchongea wewe mpaka Hashwiyya wakakufukuza na kusema kuwa “una elimu nyingi lakini dini kidogo”!951

Abu Bakr Muhammad Al-Baaqillaani Al-Maliki (403 A.H.). Anasema katika kitabu Al-Insaafu Fii Maa Yajibu I’itiqaaduhu Wala Yajuuzu Al-Jahlu Bih:

Wala hatusemi kwamba ‘Arshi imetulia (mahala) au kwamba ina sehemu, kwani Allah alikuwepo wala hakukuwa na sehemu, alipoumba sehemu Yeye hakubadilika kutokana na alivyokuwa (awali).952

Abu Bakr Muhammad bin Al-Hasan Al-Shafi ajulikanaye kwa jina la Ibn Furak (406 A.H.). Anasema:

Haimfalii Allah kuweko katika sehemu kwani ni muhali Yeye kuwa ana mipaka na kuwa na ukomo, na hio ni kwa sababu ni muhali Yeye kuwa ni mwenye kuzuka. 953

Abu Mansur ‘Abdil-Qahir Al-Baghdadi (429 A.H.). Anasema: “Na wakakubaliana kwamba Yeye hayumo katika sehemu wala zama hazimpitikii”.954

Ibn Hazm. Anasema:

949 - Kitabu Al-Tawhid uk. 69. 950 - Katika kitabu ninachokinukuu mumeandikwa فيحتوي lakini niliporejea kitabu thiqat cha Ibn Hibbaan nimekuta imeandikwa فيتوى. Neno la pili ambalo ndilo nililoliona katika kitabu cha Ibn Hibbaan mwenyewe ndilo nililolitegemea katika tafsiri ya Kiswahili, hususan ukizingatia kwamba qarina zinaonesha kuwa neno la pili ndilo lenye kuwiyana na mtiririko wa maneno. Tazama utangulizi wa kitabu cha Ibn Hibbaan Al-Thiqaat uk. 5 (kwa kopi nilionayo).951 - Al-Dhahabi Tadhkiratu Al-Huffadh j. 3, uk. 921, tarjama na. 879. 952 - Al-Insaafu Fii Maa Yajibu I’itiqaaduh uk. 65.953 - Mushkilu Al-Hadith uk. 75.954 - Al-Farqu Baina Al-Firaq uk. 333.

309

Page 310: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Na Allah Mtukufu hayumo katika sehemu wala katika zama, bali Yeye Allah Mtukufu ndiye aliyeumba zama na sehemu. Na zama na sehemu ni viumbe; Allah alikuwepo kabla ya hizo, na sehemu ni kwa ajili ya viwiliwili.955

Al-Imamu Al-Bayhaqi, Al-Shafi (485 A.H.). Anasema:

Katuhadithia Abu Abdillah Al-Hafidh kasema nimemsikia Abu Muhammad bin Abdillah Al-Muzani anasema: ‘Hadithi kuhusu kuteremka kwa Allah (Hadithu Al-Nuzul) imethibiti kutoka kwa Mtume (s.a.w.) kwa njia sahihi. Na ikaja katika Qur-ani chenye kukiunga mkono nayo ni kauli yake Allah: والملك ربك وجاء صفا صفا (Na akaja Mola wako na Malaika safu baada ya safu). Na kuteremka (kweli kweli) na kuja (kweli kweli) ni sifa mbili ambazo, kwa namna ya kufanya harakati na kuhama kutoka hali moja kwenda hali nyengine, Allah anakataliwa nazo. Bali ni sifa za Allah bila ya kufanana. Basi Allah katakasika kutokana na wanavyosema Al-Mu’attila (wenye kuzikataa) sifa zake, na wanavyosema Al-Mushabbiha (wenye kumshabihisha). Ninasema: 956 ‘Na alikuwa Abu Sulaiman Al-Khattabi – Allah amrehemu – anasema: ‘Kwa hakika anayakataa haya yule mwenye kulinganisha mambo kwa (mezani ya) yale anayoyashuhudia kama vile kuteremka ambako ni kutoka juu kwenda chini; na kuhama kutoka juu kwenda chini, na hii ni sifa ya viwiliwili na roho, ama kuteremka kwa yule ambaye hana sifa za viwiliwili (Allah), basi maana hizi huwezi kuzifikiria kwake, BALI HUKO (KUTEREMKA KWAKE) NI HABARI YA UWEZO WAKE NA REHMA (HURUMA) YAKE KWA WAJA WAKE NA KUWAFANYIA UPOLE NA KUWAPOKELEA MAOMBI YAO NA KUWAGHUFIRI…….. 957

Abu Al-Mudhaffar Al-Asfarayini (471 A.H.). Anasema:

Mlango wa kumi na tano: katika kubainisha itikadi ya Ahlu Sunna Wa Al-Jamaa’a. ‘Na ujue kwamba kila ambacho ni ishara ya kuzuka kwa kitu kama vile mipaka, ukomo, sehemu, muelekeo, kutulia, kutikisika; yote hayo ni mustahili kwa Allah. Kwani yule ambaye si mwenye kuzuka hayamfalii yale ambayo ni dalili ya kuzuka.958

Imamu Al-Haramain, ‘Abdul-Malik bin ‘Abdillah, Abu Al-Ma’ali Al-Juwaini (478 A.H.) Anasema:

955 - ‘Ilmu Al-Kalaam uk. 65.956 - Msemaji ni Al-Bayhaqi. 957 - Al-Sunan Al-Kubra j. 3, uk. 3. 958 - Al-Tabsiru Fii Al-Din uk. 161.

310

Page 311: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Allah Mtukufu ni Mwenye kuwepo kwa Dhati yake; hahitaji sehemu ya kukaa wala sehemu ya kumbeba……Madhehebu ya watu wote wa haki ni kuwa Allah katakasika kutokana na kuchukua nafasi au kujihusisha na upande (fulani). 959

Al-Imamu Al-Ghazali Al-Shafi (505 A.H.). Anasema:

Msingi wa saba: Kujua kwamba Allah kidhati katakasika kutokana na kujihusisha na pande (sehemu maalumu), hakika ya upande ama utakuwa ni juu au chini; au kulia au kushoto; au mbele au nyuma; na pande hizi Yeye ndiye aliyeziumba au kuzizua kupitia katika maumbile ya binaadamu….Ama (kile kitendo cha) kunyanyua mikono mbinguni wakati wa maombi ni kwa sababu huko (juu) ndio kibla (maelekeo) cha dua……960

Abu Bakr bin Al-’Arabi Al-Maliki (543 A.H.). Anasema: “Mwenyezi Mungu katakasika kutokana na kuwekewa mipaka au kuingia kwenye vitongoji”.961

Al-Qadhi ‘Iyaadh bin Musa Al-Maliki (544 A.H.) Anasema:

Jua kwamba kile kilichotokea hapa cha kulitegemeza (neno) kukurubia kwa Allah, si kukurubia kwa sehemu wala kukurubia kwa masafa, kama tulivyoeleza kutoka kwa Ja’afar bin Muhammad Al-Sadiq: ‘Si kukurubia kwa mpaka, bali kukurubia Mtume (s.a.w.) kwa Mola wake ni kubainisha ukuu wa nafasi yake na kukitukuza cheo chake’.962

Ibn ‘Asaakir (571 A.H.) Anasema:

Al-Najjariyya963 wamesema: ‘Hakika ya Muumba Mtukufu yupo kila pahala bila ya kuteremka hapo (bila ya kuwepo hapo physically),’ na wakasema Al-Hashwiyya na Al-Mujassima:964 ‘Hakika ya Allah Mtukufu yupo katika Arshi na kwamba Arshi ndio sehemu yake naye kakaa kitako juu yake’. Basi (Abu Al-Hasan Al-Ash’ari) akashika njia ya Allah baina ya mawili hayo, akasema: ‘(Allah) alikuwepo wala hapakuwa na sehemu,

959 - Al-Irshadu Ilaa Qawaati’u Al-Adillah uk. 53.960 - Al-Ihyaau j. 1, uk. 128. 961 - Al-Qabas Fii Sharhu Al-Muwattai j. 1, uk. 395. 962 - Al-Shifaa j. 1, uk. 205. 963 - Wafuasi wa Al-Husain bin Muhammad Al-Najjar. Tazama Al-Shahrastani Al-Milal wa Al-Nihal j. 1, uk. 98. 964 - Bwana Kasim Mafuta, Abdallah Ali Muhsin, Seif Al-Ghafri na Abu Hashim Al-Musawi mupo? Si Juma Mazrui aliyeanza kukuiteni nyinyi Hashwiyya na Mujassima , bali hilo ni jina lenu – na mumepewa kwa haki – katika ndimi za wanavyuoni tangu wa kale wa Ahlu Sunna.

311

Page 312: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

akaumba ‘Arshi na Kursi na wala hakuhitaji sehemu, naye baada ya kuumba sehemu basi yuko kama alivyokuwa.965

Ibn Al-Jawzi Al-Hanbali (587 A.H.). Anasema:

Kilicho wajibu juu yetu ni kuitakidi kwamba dhati ya Allah Mtukufu haiingii katika kitu sehemu966 wala hasifiwi kwamba anabadilika au anahamahama.967

Saifu Al-Din Al-Aamidi (631 A.H.). Anasema:

Na kile kilichopokewa kutoka kwa Al-Salaf katika lafdhi ambazo dhahiri yake zinathibitisha muelekeo na sehemu……..pamoja na kukubaliana kwao kwa pamoja kwamba Allah hakukaa katika sehemu wala hakuwepo katika upande (fulani).968

Al-Qurtubi Al-Mufassir (671 A.H.):

Na (maana ya Allah kuwa ni) ‘Aliy (aliye juu) ni kuwa juu kwa utukufu na cheo: si kuwa juu katika sehemu, kwani Allah katakasika kutokana na kuwepo katika nafasi.969

Al-Imamu Al-Nawawi (676 A.H.). Anasema:

Hakika ya Allah hana mfano wa kitu, na kwa hakika Yeye ametakasika kutokana na kuwa ni kiwiliwili na kuhama (kutoka sehemu kwenda sehemu) na kuchukua nafasi (akawa yuko sehemu au upande fulani) na (katakasika) na sifa nyengine za viumbe.970

Ahmad bin Idris Al-Qaraafi Al-Maliki (684). Anasema: “Naye – yaani Allah – hayupo katika upande (fulani)”. 971

Ibn Mandhur: (711 A.H.) Anasema:

Na katika Hadithi “Atayejikurubisha kwangu shubiri moja, basi mimi najikurubisha kwake dhiraa”. Makusudio ya mja kuwa karibu na Allah ni

965 - Tabyiinu Kadhibi Al-Muftari uk 150. 966 - Yaani Allah hana sehemu. 967 - Daf’u Shubahi Al-Tashbih uk. 85. 968 - Abkaaru Al-Afkaar uk. 194-195. 969 - Al-Jami’u Li-Ahkaami Al-Qur-ani katika tafsiri ya Aya 255 ya Suratul Baqara, j. 3, uk. 278. 970 - Shar-hu Sahihi Muslim j. 3, uk. 19. 971 - Al-Ajwiba Al-Faakhira uk. 93.

312

Page 313: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kumtaja (Allah) na kutenda mema: si kukurubia kwa dhati na sehemu, kwani hio ni sifa ya viwiliwili; na Allah ametakasika na hayo.972

Muhammad bin Ibrahim ajulikanaye kwa jina la Ibn Jama’a Al-Shafi (733 A.H.). Anasema:

Ikiwa itasemwa kwamba kukataa kwamba kitu kilichopo kina upande (direction) kunapelekea kukataa kutokuwepo kwa (kitu hicho) kilichopo, kwani ni muhali kuwepo kwa chenye kuwepo bila ya kuwa kiko katika upande (maalumu). Basi tutajibu kwamba: vyenye kuwepo ni namna mbili: 1) chenye kuwepo ambacho hakiingii katika fikra, hisia na mpambanuko. 2) Chenye kuwepo ambacho hayo yanakiingia. Basi ya mwanzo ni yenye kuzuilika kwani ni muhali – Allah hayamuingii hayo, kwani Yeye si kiwiliwili wala si ‘ardh (kitu chenye kufahamika kwa akili lakini hakigusiki) wala si johari (matter). Basi ikafaa kiakili kwamba (Allah) awepo bila ya (kuwepo katika) upande (fulani) au kuchukua (to occupy) nafasi kama dalili ya kiakili ilivyoonesha. Basi ikafaa kiakili kumkubali kama zilivyoonesha dalili za kiakili juu ya kuwepo kwake bila ya kuwa ni kiwiliwili wala kuwa ni ‘ardh (kitu chenye kufahamika kwa akili lakini hakigusiki)…. 973

‘Ali bin ‘Abdil-Kaafi Al-Subki Al-Shafi (756 A.H.). Anasema:

Nasi tunasema kwa yakini kwamba wamekubaliana juu ya (kumtakasa Allah); basi haoni haya (Ibn Al-Qayyim) kunukuu makubaliano ya Mitume974 kwa kuthibitisha upande (alioko Allah) na kwamba (yuko) juu kweli kweli? Na wanavyuoni wa Sharia wanalikanusha hilo, basi huwaogopi (ewe Ibn Al-Qayyim) wakajakukwambia kwamba umewazulia uwongo Mitume.975

Abu Is-haaq Ibrahim bin Musa Al-Shaatibi Al-Andalusi (790 A.H.). Anasema:976

Abu Said, Faraj bin Qaasim alimuuliza kuhusu suala la kinahau. Na mwisho wake ni: “Na kwamba Yeye (Allah) hakukaa katika sehemu au kuikurubia.977

Abu Zur’a, Ahmad bin ‘Abdil-Rahim Al-’Iraqi (826 A.H.). Anasema: 972 - Lisanu Al-‘Arab j. 1, uk. 663-664. 973 - Idhahu Al-Dalil uk. 104-105. 974 - Haoni haya kwani hio ndio sera yao. 975 - Al-Saifu Al-Saqil Fii Al-Raddi ‘Alaa Ibn Zafil uk. 105. 976 - Nafupisha na nanukuu kimaana tu. Nafupisha kuhifadhi wakati. Maneno yake ni marefu kidogo kuliko nilivyoeleza hapa. 977 - Al-Ifaadaat wa Al-Inshaadaat uk 93-94.

313

Page 314: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Kauli yake – yaani Mtume s.a.w. – (aliposema): العرش فوق عنده هو(Basi (hicho kitabu) kiko kwake juu ya Arshi), hakuna budi kuiletea ta-awil lafdhi hii عند ‘inda, kwani (lafdhi hii) maana yake ni kuhudhuria kwa kitu, na Allah katakasika kutokana na kuwepo (akawa kakaa sehemu) na kuchukua nafasi na (kuwa yuko katika) upande (fulani)….978

Al-Imamu Al-Hafidh, Ibn Hajar Al-’Asqalani (852 A.H.). Anasema:

Na wala vile kuweko katika upande wa juu na wa chini ni muhali kwa Allah hakumaanishi kwamba Allah asisifiwe kuwa hana sifa ya kuwa ni aliye ujuu, kwani ujuu wake ni ujuu wa kimaana (si wa kihisia: not physically), na ni muhali hilo; ni muhali kuwa hio ni (sifa) ya kihisia979…..Basi chenye kutegemewa katika Salaf (watangulizi) wa Ummah na Maulamaa wa Sunna na Khalaf (waliokuja baadae) ni kuwa Allah katakasika kutokana na kufanya harakati (kutikisika) na kuhama na kukaa katika sehemu.980

Al-Hafidh Muhammad bin ‘Abdil-Rahman Al-Sakhawi (902 A.H.). Anasema:

Kasema Sheikh wetu – yaani Ibn Hajar –: ‘Hakika ya elimu ya Allah ipo katika vitongoji vyote (anajua kila kitu), na Allah (subhaanahu wa ta’aala) ametakasika kutokana na kuwepo katika sehemu kwani Allah (subhaanahu wa ta’aala) alikuwepo kabla ya kuja kwa sehemu.981

Jalalu Al-Din Al-Suyuti (911). Alipokuwa akiisherehesha Hadithi inayosema: “Mja huwa karibu zaidi na Mola wake wakati anaposujudu” anasema (Al-Suyuti):

Kasema Al-Qurtubi: ‘Huyu yupo karibu zaidi (na Allah) kwa cheo na karama: si kwa masafa, kwani Yeye katakasika kutokana na sehemu (hana kitu sehemu).982

Ibn Hajar Al-Haytami (974 A.H.). Anasema:

Itikadi ya Imamu wa Sunna Ahmad bin Hanbal inawafikiana na itikadi ya Ahlu Sunna Wa Al-Jamaa’a katika kumtakasa mno Allah Mtukufu kutokana na yale wanayoyasema madhalimu na wenye kukanusha.983

978 - Tarhu Al-Tathriib j. 8, uk. 84. 979 - Fat-hu Al-Bari j. 6, uk. 136. 980 - Fat-hu Al-Bari j. 7, uk. 124. 981 - Al-Maqaasidu Al-Hasana uk. 342, nambari 886. 982 - Sharhu Sunani Al-Nasaai j. 1, uk. 576. 983 - Al-Fatawa Al-Hadithiyya uk. 144. Bila kusahau kwamba Ibn Hajar ni Ash’ari: hakubaliani na itikadi za tajsim. Kwa hivyo, Ibn Hajar Al-Haytami hapa anadai kuwa Al-

314

Page 315: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Sh. Mulla ‘Ali Al-Qari (1014 A.H.). Anasema:

Ama kuweko juu kwa Allah ambako kunapatikana katika Aya kama هعباد فوق القاهر وهو “ ” (Naye ni mshindi juu ya waja wake), ni kuweko juu kicheo: si kuweko juu kwa sehemu kama ilivyoelezwa na Ahlu Sunna Wa Al-Jamaa’a, bali na (kama wanavyosema) makundi mengine ya Kiislamu miongoni mwa Mu’utazila na Khawarij na makundi mengine ya bidaa, isipokuwa kundi la Mujassima (wenye kumfanya Allah kuwa ni kiwiliwili) na wajinga wa Kihanbali wenye kusema kwamba (Allah yuko katika) upande (maalumu)…984

Mahmud bin Muhammad Al-Subki (1352 A.H.). Anasaema:

Ama madhehebu ya Al-Salaf (watangulizi Masahaba na wafuasi wao) na Al-Khalaf (waliokuja baadae) kuhusiana na Aya na Hadithi Mutashabihat; wamekubaliana wote kwamba Allah hana sifa za vilivyozuka (viumbe), hana sehemu katika ‘Arshi wala katika mbingu wala penginepo; wala hasifiki kwamba yupo kaingia katika kitu chochote katika vilivyozuka (viumbwa) wala kugusana na kitu wala kubadilika na kuhama na zisizokuwa (mfano wa) hizo miongoni mwa sifa za vilivyozuka (viumbe).985

Muhammad Zahid Al-Kawthari (1393 A.H.). Anasema:

Na kumtakasa Allah kutokana na sehemu au sifa za sehemu; na nyakati au sifa za nyakati ndio itikadi ya watu wa haki hata wakikasirika Mujassima wa wazi (wenye kumfanya Allah – kwa uwazi – kuwa ni kiwiliwili).986

Al-Imamu Muhammad Al-Tahir bin ‘Ashur Al-Maliki (1393 A.H.). Anasema:

Kauli yake (Allah aliposema) “ ماء في من الس ” (Aliye mbinguni) ni katika (Aya) mutashabiha ambayo dhahiri yake inapewa maana ya kuweko katika sehemu (kweli kweli), na hilo halimstahikii Allah.987

‘Abdu-Lahi bin Muhammad Al-Ghummari (1413 A.H.). Anasema:

Imamu Ahmad alikuwa na itikadi kama yake, nayo ni ile ya Mungu asiye na viungo wala sehemu, n.k. 984 - Sharhu Al-Fiqhi Al-Akbar uk. 196-197. 985 - Itihafu Al-Kainat uk. 5. 986 - Maqaalatu Al-Kawthari: Maqalu Al-Israa wa Al-Mi’iraaj uk. 452. 987 - Al-Tahriru wa Al-Tanwir j. 29, uk. 33.

315

Page 316: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Allah alikuwepo wala hapakuwa na chochote kabla yake, hapakuwa na wakati wala sehemu wala kitongoji wala nyakati wala ‘Arshi wala Malaika wala sayari wala falaki (orbit), kisha akauleta ulimwengu wala si kwamba anauhitajia, na lau alitaka asingeliuleta. Basi huu ulimwengu wote pamoja na vilivyomo – johari (matter) na ‘ardh (mambo yanayofahamika lakini hayashikiki) – basi yote hayo ni yenye kuzuka kutoka pasipo kitu (from nothing), hakuna ndani yake mchanganyiko wa (sifa ya) kutangulia kwa mujibu wa mambo ya kiakili ambayo yanapewa nguvu na dalili za kimaandiko na wakakubaliana mamilioni isipokuwa wanafalsafa wachache waliopwekeka wakasema kuwa ulimwengu una sifa ya kutangulia, nao ni makafiri bila ya khilafu.988

SIFA TAFAUTI

Kucheka: Anasema Al-Khattabi:

Kucheka ambako kunamuingia binaadamu hakujuzu kwa Allah….(bali kucheka kwa Allah) maana yake ni (kukiridhia) kitendo cha mmoja wao na kukikubali cha mwengine. Na Al-Bukhari amelifasiri neno kucheka (kwa Allah) kuwa maana yake ni kurehemu, lakini kulifasiri (neno hilo) kwa maana ya kuridhia kuko karibu zaidi, kwani kucheka ni alama ya kuridhia na kukubali. Basi maana ya (Hadithi isemayo): “Allah anacheka” ni kuwa anatoa ataya kwa wingi.989

Uso, jicho na mkono: Anasema Al-Raaghib:

Asili ya uso ni kiungo….na Allah katakasika kutokana na viungo kwa hivyo, (viungo) kwa mujibu wa lafdhi zake ni mutashabihat kwani dhahiri yake ni kumfananisha Muumba na kiumbe na halkadhalika jicho katika Aya kama عيني على ولتصنع (Na ili ulelewe juu ya jicho langu),990 (kwamba maana ya jicho katika Aya hio ni) malezi na kuchunga, yaani malezi ya (Nabii) Musa (a.s.) yanatazamwa kwa hifadhi ya Allah…na neno mkono katika Aya: بيدي خلقت لما (Kwa yule niliyemuumba kwa mikono yangu miwili), na kauli yake Mtume (s.a.w.): “ نفسي والذي 991(…Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mikononi mwake) ”...بيدهkwamba maana yake ni nguvu…na kulitumia neno mkono kwa maana ya

988 - Qasasu Al-Anbiyaai uk. 11. 989 - Fat-hu Al-Bari j. 6, uk. 39-40, nukulu kutoka katika kitabu Shar-hu Jawhari Al-Tawhid j. 1, uk. 459. 990 - Maana sahihi ya neno jicho katika Aya hii ni hifadhi. Na maana ya Aya ni: “Ili ulelewe kwenye hifadhi yangu”. Ama ukikataa majazi basi itakubidi useme kwamba Nabii Musa kalelewa juu ya jicho la Allah. Sijui kama kuna mwenye akili yake timamu atayekubaliana na hili.

316

Page 317: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

uwezo ni matumizi ya kimajazi mashuhuri, husemwa: بكذا لي يدين ال(Sina mikono miwili mimi kwa kitu kadha)992 yaani sikiwezi, tukijua kwamba Al-Salaf wanaijuzisha maana iliosemwa na waliokuja baadae……993

Anasema Ibn Al-Tiin: “kuhusu Hadithi: الميزان األخرى Na) وبيدهmkono wake mwengine una mezani) ta-awil ya mkono hapa ni uwezo”.994

Anasema Al-Kashmiri: “Ninasema: أيديهم فوق الله يد (Mkono wa Allah uko juu ya mikono yao) kama alivyosema, wala sisemi kuwa Allah ana mkono”.995 Mwisho wa kunukuu. Anachokisema Sheikh huyu ni kuwa Aya hio anaiamini lakini hasemi kuwa Allah ana mkono wa kweli.

Huu ni mukhtasari mfupi sana juu ya nini Maimamu wa Ahlu Sunna wanasema kuhusu sifa za Allah. Nimewacha maelezo mengi kutoka kwa Maimamu wengi ambao maelezo yao yamenukuliwa katika kitabu Sharhu Jawharati Al-Tawhid, anayetaka ziada na arejee huko.996

Baada ya haya, utaona kwamba madai ya Mawahabi kwamba itikadi zao ndio itikadi za Ahlu Sunna wa Al-Jamaa na Al-Salafu Al-Salih, si madai ya kweli, bali itikadi yao ni itikadi ya Al-Hashwiyya Al-Mujassima ambao aghlabu yao ni baadhi ya Mahanbali ambao hawakuwa ni watu wenye ufahamu sahihi wa maandiko. Kwa kulithibitisha hili zaidi tutaona katika juzuu nyengine za kitabu hiki nini Mawahabi wanakikusudia wanapolitumia jina Ahlu Sunna na jina Al-Salafu Al-Salih.

MUKHTASARI NA NUKTA MUHIMU

991 - Tazama lau Allah alikuwa ana mikono kweli, na Mtume (s.a.w.) anasema: “..yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake”, basi hio ingelimaanisha kwamba Allah kaigusa nafsi ya Mtume (s.a.w.), na hapo dai kwamba Allah “yuko mbinguni kapambanuka na viumbe vyake” lisingelikuwa na muelekeo, madamu kaishika nafsi ya Mtume Muhammad. 992 - Ninasema: hata Ibn Al-Qayyim – kama tulivyomnukuu kabla – pamoja na kukataa kwake majazi na kuizungusha Aya hii huku na kule, basi naye kaanza kitabu chake kwa ubeti usemao: ** يدان ذاك بفسخ للصدود ما األركان ثابت المحبة Hukumu ya حكمmapenzi, nguzo zake ni imara**Upingaji hauna mikono miwili ya kubomoa hilo. Yaani hauna uwezo wa kubomoa hilo kama mshereheshaji alivyosema. Ibn Al-Qayyim Al-Nuniyya j. 1, uk. 16.993 - ‘Abdul-Karim na Muhammad Al-Kaylaani Sharhu Jawharati Al-Tawhid j. 1, uk. 480-481. 994 - ‘Abdul-Karim na Muhammad Al-Kaylaani Sharhu Jawharati Al-Tawhid j. 1, uk. 482. 995 - ‘Abdul-Karim na Muhammad Al-Kaylaani Sharhu Jawharati Al-Tawhid j. 1, uk. 483. 996 - Nafupisha kwa sababu mengi mengine natarajia kuyaweka katika kazi nyengine ambayo nilikwisha kuianza na ambayo Allah akipenda itakuwa pana zaidi.

317

Page 318: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

1) Tulichokizungumzia hapa ni kubainisha kwamba wanavyuoni wa Kisuni tangu enzi za Maimamu wakubwa hadi leo wana itikadi tafauti na itikadi za Kiwahabi leo na viongozi wao wa awali.

2) Halkadhalika Al-Salaf (watangulizi) wa Umma huu walikuwa na itikadi zilizo mbali umbali wa mashariki na magharibi kutokana na itikadi za Kiwahabi.

3) Ni kweli kwamba wako wanavyuoni waliokuwa wakijiita kuwa ni Sunni tangu zamani ambao walikuwa na itikadi kama hizo za Kiwahabi.

4) Lakini wanavyuoni hao ni wachache mno; aghlabu ya wachache hao ni wanavyuoni wa Kihanbali.

5) Maimamu wakuu wanne wa Kisunni hawakuwa na itikadi hizo kamwe kama tulivyoona nukulu zao.997

6) Mawahabi wanataka kuubirua ukweli kwa kudai kwamba itikadi yao ndio ya Ahlu Sunna na ndio itikadi ya Al-Salaf, ili waipigie debe itikadi yao.

7) Masuni amkeni musikubali kudanganywa na propaganda za Mawahabi wakidai “Sisi ndio Ahlu Sunna” au “Sisi tunafuata Al-Salaf” au “Sisi tunapiga vita bidaa” ilhali wao ndio waliozama katika bidaa ya kumfananisha Mungu na viumbe hadi wengine wakasema kuwa Allah ana sura ya Nabii Adam. Basi kuna bidaa gani tena kubwa kuliko hio? Au bidaa kubwa ni kuchukua mtasbihi na kusoma khitma na maulidi na kuomba dua ya pamoja?

997 - Tafauti na madai ya Kasim Mafuta kwamba itikadi ya Imamu wake Ibn Taymiyya ndio itikadi ya Abu Hanifa, Abu Al-Hasan Al-Ash’ari na Maimamu wengine. Basi kwanini tena watunge riwaya kadha wa kadha za kumtukana Abu Hanifa na kumponda Al-Ash’ari kama walikuwa na itikadi kama zao?!

318

Page 319: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

SURA YA TISAKUWAKAFIRISHA NA KUWATUKANA WAISLAMU

MATUSI NA UKAFIRISHAJI WA IBN AL-QAYYIM

Katika kitabu chetu Hoja Zenye Nguvu, tumenukuu matusi mabaya ya Ibn Al-Qayyim dhidi ya wale wasioafikiana naye katika itikadi ya kuonekana kwa Allah. Si vibaya hapa tukakumbushana tena hususan ukizingatia ukweli kwamba sura hii ni mahususi kwa maudhui hio. Anasema Ibn Al-Qayyim kuhusu watu hao ambao hawaikubali itikadi ya kuonekana kwa Allah:

Watu wa bidaa, na wenye kutoka katika dini, na ni Jahmiya, na ni wafuasi wa Fir’awna wenye kuzikataa sifa za Allah, na wametoka katika dini zote, na wamekamatana na kamba ya shetani, na wamekatikiwa na kamba998 ya Allah, na wanazipiga vita Sunna na (kuwapiga vita) watu wenye kuzifuata (Sunna hizo), na wanampa amani kila adui wa Allah na (adui wa) Mtume wake na (adui wa) dini yake, na wote hawa (ambao hawaamini kuwa Allah ataonekana) basi watazuiliwa kutokana na Mola wao, hao ndio wafuasi wa upotovu, na kikundi cha yule aliyelaniwa, ……basi ajabu ilioje! Vipi wamekuwa (hawa) wafuasi wa Saiba (wenye kuabudu nyota) na Majusi (wenye kuabudu moto) na washirikina na wenye kuabudu Masanamu, na wafuasi wa Jahmiya na wafuasi wa Fir’awna, wanamjua Allah zaidi kuliko Nabii Mussa!999

Hayo ndio alioyasema Ibn Al-Qayyim kuhusu wasioamini kuonekana kwa Allah siku ya kiama yaani Maibadhi, Mashia, Jahmiyya, Mu’utazila na baadhi ya Masunni.1000 Ni wazi kwamba Ibn Al-Qayyim anawakafirisha Waislamu. Ama kuhusu itikadi ya kuumbwa kwa Qur-ani, Ibn Al-Qayyim anasema:

كالم القرآن أن زعم ومن كافر جهمي فهو مخلوق القرآن أن زعم فمنووق يق ��الله ولم ل���ف

فهو بمخلوق ال أليس من زع ��خبث ومن األول ألفاظنا �قول أن موالق مخلوقة رآن ����وتالوتنا

998 - Tazameni huyu mtu anayekanusha majazi! 999 - Ibn Al-Qayyim: Hadi Al-Rwah Ila Bladi Al-Afrah uk. 210. Je baada ya haya Kasim Mafuta na kikundi chake watakanusha kwamba Maimamu wao wanawakafirisha Waislamu?! Tena wanawakafirisha ukafiri wa kuwatoa katika Umma! 1000 - Jumhur ya Masunni wanaamini kuonekana kwa Allah; lakini wako wachache ambao itikadi hio hawakuikubali kama tutavyoeleza katika juzuu ya nne in shaa Allah.

319

Page 320: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

جهمي فهو الله كالم

Atayedai kwamba Qur-ani ni kiumbe basi huyo ni Jahmi kafiri; na atayedai kwamba Qur-ani ni maneno ya Allah lakini asiseme kwamba si kiumbe basi huyo ni muovu zaidi kuliko wa mwanzo, na atayedai kwamba matamshi yetu (tunaposoma Qur-ani) na kisomo chetu ni kiumbe basi huyo ni Jahmi.1001

Kauli ya kwanza ni kauli ya Ibadhi, Jahmiyya na Mu’utazila.1002 Hawa wote ni makafiri kwa mujibu wa Ibn Al-Qayyim na watu wa skuli yake.1003 Kauli zinazofuatia ni za baadhi ya wanavyuoni wa Kisuni, na kauli ya mwisho hasa hasa ndio ya wanavyuoni wengi wa Kisuni akiwemo Al-Bukhari na Muslim.1004 Hawa wao ni Jahmiyya, na kwa hivyo ni makafiri vile vile kwani Jahmiyya – kama zinavyosema riwaya za Maimamu wa Kihanbali/Kiwahabi – ni makafiri!

Hilo ni jambo baya ambalo Ibn Al-Qayyim hakuishia kwa madhehebu hizo tu na watu wenye itikadi hizo tu, bali Waislamu wa madhehebu zote kwake ni makafiri washirikina (waliotoka katika mila ya Uislamu) isipokuwa watu wa madhehebu yake wenye kumshabihisha Allah na viumbe. Soma maneno yake mwenyewe aliposema:

*** مصطحبان شك ال هما كانا مذ والتعطيل الشرك بأن واعلم ******** التبيان واضح هذا حتما مشرك هو معطل فكل أبدا

Na elewa kwamba ushirikina (ukafiri) na ta’atil1005 tangu**yalipokuwa (mambo mawili hayo) basi bila shaka ni yenye kuambatana**Daima kila Mu’attili ni mshirikina (kafiri)**Kwa lazima, (na jambo) hili ubainifu wake uko wazi.1006

Mu’atil – katika fiq-hi ya itikadi ya Kiwahabi na Maimamu wao – ni mtu anayezikataa sifa za Mungu. Na sifa zenyewe ni zile tulizozitaja katika

1001 - Ibn Al-Qayyim Haadi Al-Ar-waah uk. 299. 1002 - Bali hata Sunni basi hawakutafautina na Ibadhi juu hili tafauti ya uhakika, bali tafauti yao ni ya kimatamshi tu. Labda tutatoa ufafanuzi huo katika sehemu nyengine in shaa Allah. 1003 - Riwaya za namna hio zimejaa kwa watu wa skuli hii kama ilivyo katika Al-Sunna cha Ibn Ahmad j. 1, uk. 172-74, riwaya na. 207,208,210,211. 1004 - Maelezo kuhusu Al-Bukhari na itikadi hii ya kuwa lafdhi zetu tunaposoma Qur-ani ni kiumbe yatakuja baadae. Ama Muslim yeye unaweza kutazama kwa ufupi katika tarjama hio hio ya Al-Bukhari katika Siyaru Al-A’alaam j. 10, uk. 315. 1005 - Yaani kukataa kuwa Allah hana mkono wa kweli, mguu wa kweli, macho ya kweli. Hio ndio ta’atil katika fiq-hi ya itikadi ya Kiwahabi kama tulivyotoa maelezo. 1006 - Ibn Al-Qayyim Al-Nuniyya j. 2, uk. 307, kwa sherehe ya Harras.

320

Page 321: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

sehemu iliotangulia – Mungu ana mkono, mguu, macho, mgongo, kifua, kamuumba Adamu kwa sura yake na mengineo. Hizo ndio sifa za Mungu ambazo anayezikataa huwa ni Mu’atil au Jahmiy! Sasa hapa Ibn Al-Qayyim anasema kwamba atayeyakataa hayo basi yeye si Muislamu bali ni kafiri mshirikina sawa na Abu Jahl na Yahudi na Mkiristo! Bali anasema kwamba hao washirikina ni bora zaidi kuliko wenye kuzikataa itikadi zake. Sasa jiulize wewe, leo ni Waislamu wangapi duniani wanaoamini kuwepo kwa Mungu mwenye viungo na ni Waislamu wangapi ambao hawaliamini hilo? Au ni madhehebu ngapi zenye itikadi hizo na madhehebu ngapi ambazo hazina itikadi hizo. Ibn Al-Qayyim, kwa maneno yake hayo, kawakafirisha: Mashafi, Maliki, Hanafi, baadhi ya Hanbali, Ibadhi, Shia na Zaidia! Hawa wote kwake ni makafiri zaidi kuliko Abu Jahl, Mayahudi na Wakiristo!

Anaendelea Ibn Al-Qayyim kwa kunasema:

** والبرهان بالمعقول إشراك ال أخي من شر التعطيل أخو لكنLakini mu’attil ni muovu zaidi kuliko**Mshirikina kwa

(hoja za) kiakili na kwa hoja (za kimaandiko)!1007

Anasema Harras, mshereheshaji wa kitabu hicho:

Ikiwa ta’atil kama tulivyobainisha ni ndugu ya ushirikina (yaani zinafuatana) na kuambatana, basi mu’attil ni muovu zaidi kuliko mshirikina na ni mbaya zaidi kuliko yeye kwa itikadi ya Mola wake.1008

Anasema Sh. Hasan bin Farhaan Al-Maaliki akisherehesha beti hio na zinazoifuatia:

Basi huku ni kuikafirisha kwa wazi jumhur ya Waislamu, kwani Mahanbali ni wachache katika zama za Ibn Al-Qayyim au kabla yake au baada yake; na aghlabu ya Waislamu ama ni Asha’ira (kama aghlabu ya madhehebu za kisuni) au Shia au Mu’tazila, nao ndio wanaoziletea ta-awil sifa ambazo Ibn Al-Qayyim anaziita ta’atil nao wana hoja zao katika kufanya hivyo kama vile ambavyo wenye kuzithibitisha (sifa hizo kwa maana kwamba Allah ana viungo) wana hoja zao. Na si muhimu kwangu kuonesha hoja hizi au zile, bali kilicho muhimu kwangu ni kutilia mkazo kwamba kukafirishana kumeharamishwa kisharia; na kukafirisha bila hoja ni alama ya uchache wa elimu na uchache wa uchaji…1009

Anaendelea Ibn Al-Qayyim:1007 - Ibn Al-Qayyim Al-Nuniyya j. 2, uk. 310, kwa sherehe ya Harras. 1008 - Ibn Al-Qayyim Al-Nuniyya j. 2, uk. 310, kwa sherehe ya Harras. 1009 - Al-Maliki, Hasan bin Farahan Qira-atu Fii Kutubi Al-’Aqaaid uk. 109.

321

Page 322: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

** الشيطان شيعة من وكالهما كفرانهم في أخف والمشركون ********* لرحمن التنزيه قالب في قائم بالعداوة العطل إن

Na makafiri washirikina ni wepesi zaidi katika ukafiri wao**Na yote makundi mawili (makafiri washirikina na mu’atila) ni kikundi cha shetani**Hakika ya Mu’attil ni mwenye kuusimamia uadui (ni adui wa Allah)**Katika mfumo wa kumtakasa Allah. 1010

Kisha mshereheshaji akabainisha kwamba maana ya beti hizo ni kuwa makafiri (washirikina kama Mayahudi na Makiristo) wamekuwa bora zaidi kuliko Muislamu mwenye kukataa kuwa Allah ana viungo kwa sababu makafiri washirikina wao wamemkubali Allah kuwa ndiye Mola wa kweli aliyekamilika katika ufalme wake, na wakazithibitisha sifa zake zote. Isipokuwa tatizo lao ni kuwa baada ya hayo wamemfanya Mungu kuwa na wapinzani.

Basi je anakuwa sawa huyu aliyekiri juu ya uungu na akamthibitishia (Allah) yale aliojithibitishia mwenyewe katika sifa za ukamilifu na wala asikanushe kitu chochote katika hizo lakini akamfanya Allah kuwa ana wapinzani katika viumbe wake; (je huyo ni sawa) na yule aliyemvua (Allah) sifa zake za ukamilifu….hakuna shaka kwamba (makafiri) washirikina ni wepesi zaidi katika ukafiri wao kuliko hawa Mu’attila.......basi mu’attil ni adui wa Allah kamsimamishia Mola wake uadui, lakini anajifanya kwamba anakusudia kumtakasa (Allah) kutokana na yale yasiomstahikia katika mambo ya kumshabihisha na kumfanya kuwa ni kiwiliwili.1011

Hayo ndio maelezo ya Ibn Al-Qayyim na mshereheshaji wa Qasida yake. Nayo ni maneno ya hatari kupita kiasi. Huyu mtu sijui ni mgonjwa wa akili au kawa zumbukuku au ni ta’asubi iliopita mipaka? Dini yetu ina nguzo tano za Uislamu na nguzo sita za Imani. Huyu mtu kazikubali nguzo zote za Uislamu na za Imani. Mwengine kazikataa zote. Yule aliyezikataa ndiye bora kuliko huyu aliyezikubali kwa sababu haamini kuwa Mungu ana viungo na ana sura ya binaadamu! Na wapi kasikia kuwa washirikina 1010 - Ibn Al-Qayyim Al-Nuniyya j. 2, uk. 319, kwa sherehe ya Harras. Anasema Al-Subki: “Hakuna kwa yule mwenye kuwaitakidi Waislamu hivi, isipokuwa upanga (auliwe)”. Anasema Al-Kawthari: “Kwani huo ni uzindiki (unafiki) uliowazi na ni kutoka (katika dini) na kuendelea kuiitakidi imani kuwa ndio ukafiri. Basi Allah amdhalilishe (Ibn Al-Qayyim), vipi anaitakidi kwamba makafiri washirikina ni wepesi zaidi katika ukafiri kuliko Waumini?!” Tazama Al-Saifu Al-Saqiil na Takmila yake uk. 208. Scanned copy yake iko mwisho wa kitabu hiki. 1011 - Sifa za ukamilifu yaani: mkono, macho, uso, n.k. Tazama Ibn Al-Qayyim Al-Nuniyya j. 2, uk. 317-320, kwa sherehe ya Harras.

322

Page 323: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

wamemkubali Allah na sifa zake zote za ukamilifu na kwamba hawakukanusha chochote juu ya hayo? Si ndio wao waliosema:

وكنا متنا أئذا ترابا لمدينون أئنا وعظاما1) Ivo tukifa na tukawa udongo na mifupa, ndio kweli (tutafufuliwa) tulipwe? 1012

ا أنفقوا لهم قيل وإذا آمنوا للذين كفروا الذين قال الله رزقكم مم أنتم إن أطعمه الله يشاء لو من أنطعم مبين ضالل في إال

2) Na wakiambiwa kwamba yatoeni yale Allah aliokuruzukuni, basi wale waliokufuru husema kuwambia wale walioami: ivo tuwalishe wale ambao lau Allah alitaka angeliwalisha! Nyinyi hamupo isipokuwa katika upotovu wa wazi.1013

العظيم بالله يؤمن ال كان إنه

3) Hakika yake alikuwa hamuamini Allah Mtukufu.1014

Na Aya nyengine nyingi. Je hawa ndio wamemuamini Allah na sifa zake za ukamilifu? Au ndio kama ilivyosemwa kwamba ta’assub inamfanya mwenye kuona kuwa kipofu? Bali ukweli ni kuwa washirikina – kama Aya nyengine zinavyosema – walikuwa wakijua kuwa Allah yupo, lakini ukidai kuwa walikuwa wakimuamini basi utapingana na Aya kama “Hakika yake alikuwa hamuamini Allah Mtukufu”. Na ukidai kuwa walikuwa wanaziamini sifa zake za ukamilifu utapingana na Aya kama “Na wakiambiwa kwamba yatoeni yale Allah aliokuruzukuni, basi wale waliokufuru husema kuwambia wale walioami: ivo tuwalishe wale ambao lau Allah alitaka angeliwalisha! Nyinyi hamupo isipokuwa katika upotovu wa wazi”. Aya hii inaonesha kwamba washirikina walikuwa wakiipinga itikadi ya kuwa Allah anawapa riziki Waumini, na mwenye itikadi hii haambiwi kwamba anaziamini sifa za Allah za ukamilifu.

Kwa ufupi ni kuwa hawi sawa mtu aliyezikubali nguzo za Uislamu na nguzo za Imani na yule aliyezikanusha. Ikiwa Ahlu Al-Kitabi, nao ni makafiri, wamepewa hakumu maalumu kwa sababu ya kumuamini Mungu japo kuwa mambo mengine ya lazima wameyakanusha, basi vipi atakuwa Abu Jahl ni bora kuliko Shafi, Hanafi, Ibadhi, Shia na wengine kwa sababu hawakubali kuwa Allah ana mkono wa kweli? Hii ni akili gani?1012 - Sura 37, Aya 53. 1013 - Sura 39, Aya 47. 1014 - Sura 69, Aya 33.

323

Page 324: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

TANBIHI

Tumenukuu kabla kidogo beti zisemazo:

** الشيطان شيعة من وكالهما كفرانهم في أخف والمشركونال ********* مإن لرحمن التنزيه قالب في قائم بالعداوة عطل

Na makafiri washirikina ni wepesi zaidi katika ukafiri wao**Na yote makundi mawili (makafiri washirikina na mu’atila) ni kikundi cha shetani**Hakika ya Mu’attil ni mwenye kusimamisha uadui (ni adui wa Allah)**Katika mfumo wa kumtakasa Allah. 1015

Beti hizi pia zimepokewa kwa lafdhi isemayo:

الكفران ** في أخف والمشركون معلن بالعداوة المعطل إنHakika ya mu’attil ni mwenye kutangaza uadui**Na makafiri

washirikina ukafiri wao ni mwepesi zaidi (kuliko mu’attil).

Na hii ni tafauti na dhana ya Sh. Kasim Mafuta aliposema:

Na haya ndiyo maajabu ya makhawariji hawa wa akhiril-zaman! Wanasema uongo wala hawana haya, na vitabu vyao vimejaa uongo. Kwa ushahidi zaidi hebu tukudokolee mfano mmoja wa uongo wao na mingine itafuatia katika sehemu zake, ni pale mufti wao Khalili alipoamua kulipindua shairi la Ibnul-Qayyim kwa makusudi, kisha Juma naye akafuatia vivyo hivyo! Ametaja al-Khalili katika kitabu chake Al-Haqu Damigh, naye Juma katika kitabu chake “Kisimamo” ukurasa wa 93 akasema hivi: “Na akasema katika “NUNIA” kuhusu wote ambao hawana itikadi ya kihashawiya (Kiwahabi) kwamba ni maaduwi ambao ukafiri wao ni mkubwa kuliko mushrikina (wenye kuabudu masanamu) Anasema (Ibnul-Qayyim):

الكفران فى أخف نكووالمشر *** معلن بالعداوة المعطل إنNa muatil ni mwenye kuutangaza uadui *** na Makafiri

washirikina ni wepesi zaidi katika ukafiri.

Juma na mufti wake Khalili wameyapindua maneno haya ya Ibnul-Qayyim kwa makusudi, mimi ninawapa chalenji watuletee maneno haya, na mimi ninasema kwamba maneno haya hayamo katika “NUNIA” ya Ibnul-Qayyim. Maneno yaliyomo katika “NUNIA” ni haya:

للرحمن التنزيه قالب فى** * معلن بالعداوة المعطل إنNa muatila ni wenye kuutangaza uadui *** kwa sura ya kumtakasa

Rah’man (Allah mwingi wa reh’ma).

1015 - Ibn Al-Qayyim Al-Nuniyya j. 2, uk. 319, kwa sherehe ya Harras.

324

Page 325: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Haya ndugu msomaji ni machache kati ya mengi ya uongo1016 yaliyojaa kwenye vitabu vya makhawarij (maibadhi) wa zama hizi, mpaka Mufti wao pia asema uongo! Na inaonekana kuwa Juma hasomi vitabu kwa kuhakiki mambo, bali yeye ananukuu kiupofu kutoka katika vitabu vya masheikh zake Khalili na Qannubi.

Hayo ndio matusi ya Kasim Mafuta, nayo si ajabu kwa mtu aliyekulia katika vitabu vya matusi na uwongo kama hivi tunavyovinukuu hapa na akatiwa kasumba katika vyuo vya kusoma matusi, na akapandikizwa chuki na kupewa mafunzo ya kuwatukana Waislamu! Je itakuaje tabia ya mtu kama huyu, na je nini hali yake huko twendako?

Baada ya hayo tunakwambia ewe Kasimu mwana wa Mafuta, beti hiyo ipo katika vitabu vya wanavyuoni walioishi katika zama za Ibn Al-Qayyim, lakini wewe – pamoja na kughururika kwako ukijidhania kuwa una elimu sana – basi inaonesha husomi isipokuwa vitabu vya Ibn Al-Qayyim na Ibn Taymiyya na wajukuu zao akina Ali Al-Faqihi. Ali Al-Faqihi ndiye aliyedhani kuwa beti hio haipo, basi Kasim Mafuta naye akamuiga bila hata ya kuwa na elimu juu ya suala lenyewe likoje! Na elewa ewe Kasimu bin Mafuta kwamba uwongo sisi sio dini yetu, uwongo ni dini yenu na nitakuthibitisha hayo kwa maandiko yenu wenyewe nikifika sehemu zake. Na ushahidi zaidi kuhusu hio beti ulioiita kuwa ni uwongo wa Juma na Mufti wake nitakupa katika sehemu yake maalumu ili walimwengu waone je ni uwongo wetu au ni uchache wako wa maarifa; hapa ninatoa utanabahisho tu.

TUNAREJEA

Naturudi tena katika beti za Ibn Al-Qayyim alizowakafirisha ndani yake Waislamu wa madhehebu zote isipokuwa madhehebu yake ya kumfananisha Mungu na kiumbe. Baada ya Ibn Al-Qayyim kutamka mwenyewe kwamba wale aliowaita kuwa ni Mu’attila nao ni, Mashafi, Mahanafi, Maliki, Ibadhi, Shia Ithnashariyya, Zaidia na baadhi ya Hanbali, hawa wote kwao ni makafiri waovu zaidi kuliko Mayahudi, Manasara na wenye kuabudu masanamu! Sasa tazama alivyowatukana Waislamu hao kwa matusi ya kihuni ya mitaani! Anasema:

1016 - Na mimi nitakujibu chalenj yako hii, kisha nikuchalenj wewe tena utuletee nukta moja tu ya uwongo wa Kiibadhi. Halafu nawe nichalenj mimi tena nikuletee maneno na riwaya mia moja za uwongo wa Kiwahabi na Maimamu wao nami niko tayari kukujibu katika kitabu kimoja kizima cha maudhui hio tu.

325

Page 326: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

*** النسوان شمائل عليه تبدو سمعه يقرع حين المخنث وترى

Utamuona khanithi wakati inapomgonga masikioni mwake**Hudhihiri juu yake tabia za wanawake.1017

Anaendelea: *** الكفران أخي زنديق ولكل معطل لكل منكوحا ويظل

Na anakuwa ni mwenye kuolewa (au kuingiliwa) na kila mua’attil (Shia, Ibadhi na Suni wa kawaida asiye Wahabi)**Na kila zindiki na kafiri.1018

Anaendelea: *** اإليمان وال ينحازوا الكفران ��ى إل فال الوجود مخانيث ليسوا

Si (kama) makhanithi wa ulimwengu**Hawako katika ukafiri wala hawako katika imani. 1019

Anasema mshereheshaji:

....Hivi ndivyo walivyosema kwa uwazi hawa mafilosofa ambao ndio nguzo za ukafiri (kama Ibn Sina) katika vitabu vyao, hawakufanya kama walivyofanya MAKHANITHI wao miongoni mwa MU’UTAZILA na ASH’ARIA 1020 wa mwisho mwisho. 1021

Anaendelea Ibn Al-Qayyim kutoa matusi yake ya kihuni baada ya kuzielezea itikadi zake za kumshabihisha Allah na viumbe wake, anasema: “..Basi wanadhani makinda (wafuasi) ya Mu’utazila na makhanithi wa Jahmiyya na wafuasi wa Wagiriki…..”.1022

Anaendelea Ibn Al-Qayyim kwa kusema kuhusu watu wanaosema kwamba Allah ataonekana bila ya kuwa na sehemu maalumu nao ni jumhur ya Masunni. Anasema:

: للمرئي مباينة غير من ويرى يبصر بل فقالوا فتناقضوا مخانيثهم وأماله، مقابلة وال المبصر

..... ( العقل ( إلى أقرب الجهمية يعني فحولهم فكانت1017 - Tazama Ibn Al-Qayyim Al-Nuniyya j. 2, uk. 177, kwa sherehe ya Muhammad Khalil Haras. 1018 - K.h.j. 1019 - K.h.j. uk. 47. 1020 - Ash’aria ni Masuni – Shafi, Maliki, Hanafi na baadhi ya Hanbali – Ibn Al-Qayyim na mshereheshaji wake wanasema kwamba wote hawa ni MAKHANITHI! 1021 - Dr. Muhammad Khalil Haraas Sharhu Nuniyya j. 2, uk. 48. 1022 - Ibn Al-Qayyim Ijtima’u Juyushi Al-Hashwiyya alichokiita Ijtima’u Al-Jayshi Al-Islamiyya uk. 197, mwishoni mwa kitabu.

326

Page 327: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

…Ama makhanithi wao (Masuni Al-Asha’ira); wao wamejigonga wakasema anaonekana bila ya kuwa mbali na chenye kuonekana wala kuelekeana nacho, basi madume wao (yaani Jahmiyya) wamekuwa karibu zaidi kwa akili….1023

Anasema Ibn Al-Qayyim:...... العلو وينكرون بالرؤية يقرون ومخانيثهم

Na makhanithi wao1024 wanakubali kuwa Allah ataonekana lakini wanakanusha kuwa yuko juu! 1025

Anasema Ibn Al-Qayyim:

إذا والمبتدعة الجهمية تالميذ مخانيث من كثير وغيرنا نحن شاهدنا وقدآيات من شيئا سمعوا

كأنهم معرضين عنها رأيتهم لبدعتهم المنافية الصفات وأحاديث الصفاتف مستنفرة رت ��حمر

هذا غير شيئا واقرأوا الباب هذا عنا سدوا مخنثهم ويقول قسورة من

Na tumewashuhudia sisi na watu wengine makhanithi wa wanafunzi wa Jahmiyya na watu wa bidaa wakisikia chochote katika Aya za sifa (za Allah)1026 na Hadithi za sifa (za Allah) zenye kugongana na bidaa zao, basi utawaona wanakengeuka kana kwamba ni punda wenye kwenda mbio, wenye kukimbia simba. Na (utaona) khanithi wao anasema: ‘tufungie mlango huu na tusomee kitu chengine kisichokuwa hiki…!1027

Hivyo ndivyo alivyosema Ibn Al-Qayyim! Sikudhania kwamba mtu anayeitwa Imamu anaweza kutukana hivi katika vitabu vyake vitavyomtia doa milele kwa kila atayevisoma! Lakini afanyaje naye hana hoja – ‘uqda nafsiyya ya akhii! Na kama munavyojua kwamba neno ukhanithi si jina la hukumu ya Kisharia, huwezi kumwita mtu hivyo kwa sababu ya itikadi yake; bali unaweza kumwita asi, kafiri, fasiki n.k, ikiwa una dalili za Kisharia juu ya hayo. Ama jina hilo alilolitumia Ibn Al-Qayyim kuwaita wapinzani wake ni jina la kihuni kabisa, na lau sikutaka kutoa ushahidi wa wazi basi nisingelilinukuu kamwe. Ndugu Waislamu haya yanatuthibitishia kwamba huyu si mtu wa kufuatwa; Allah hakumpa nuru hata kidogo, labda kaghururika kwa sababu ya kuhifadhi sana mutun za Hadithi!

1023 - Ibn Al-Qayyim Al-Sawaa’iqu Al-Mursala j. 4, uk. 1334-1335. 1024 - Yaani Masuni wa kawaida wasiokuwa Mawahabi au Hashwiyya Mujassima. 1025 - Ibn Al-Qayyim Al-Sawaa’iqu Al-Mursala j. 4, uk. 1333. 1026 - Yaani Aya zenye kusema – kwa mfano – “Mkono wa Allah uko juu ya mikono yao”, au “Ili tukulee juu ya jicho letu”, na zilizo mfano wa hizo. 1027 - Ibn Al-Qayyim I’ilaamu Al-Muwaqqa’iin j. 1, uk. 151.

327

Page 328: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

MATUSI YA IBN TAYMIYYA

Lakini hayo aliyoyasema Ibn Al-Qayyim kumbe si ajabu: walimu wake walikwisha kumtangulia kuyanena. Anasema Ibn Taymiyya:

Na kwa hivyo, walikuwa wakisema kwamba Mu’utazila ni makhanithi wa wanafalsafa, na Al-Ash’ariyya (Masuni wote taqriban ukiwatoa baadhi ya Hanbali na firanga vyao vya Kiwahabi) ni makhanithi wa Mu’utazila.1028

Huyo ndiye Imamu mkuu, kwa hivyo Maamuma watakuwaje? Wala usiniambie kwamba Ibn Taymiyya hapa alikuwa akinukuu tu, kwani mtu akinukuu kitu kwa kukikubali au kukitolea hoja basi huwa naye kakisema. Maneno yaliomo katika kitabu cha Mafuta si kwamba yote ni yake, lakini madamu kayatolea hoja na kuyakubali basi maneno hayo yanakuwa ni yake. Halkadhalika Ibn Taymiyya naye hapa ananukuu kwa kuyakubali maneno hayo, kwahivyo naye yumo katika matusi hayo. Bali wafuasi wa Ibn Taymiyya wamemnukuu yeye mwenyewe Ibn Taymiyya akisema maneno hayo machafu. Anasema:

تيمية ابن االسالم شيخ قال كما المعتزلة مخانيث والرافضةNa Rafidha (Shia) ni makhanithi wa Mu’utazila kama

alivyosema Sheikh Al-Islam Ibn Taymiyya.1029

Bali yeye mwenyewe Ibn Taymiyya katumia Ibara kama hizo katika Majmu’a Al-Fataawa. Anasema: مخانيث الصفات في فالمعتزلة Kwa hivyo, Mu’utazila katika itikadi ni Makhanithi wa“ الجهمية

Jahmiyya”.1030……... المنكرين الذكور للجهمية مخانيث وصارواالصفات Na. wakawa makhanithi wa Jahmiyya (ambao ndio)“.…لجميع

wanaume (wao) wenye kuzikanusha sifa zote”.1031

Kwa hakika vitabu vya Ibn Al-Qayyim hasa hasa Qasidatu Al-Nuniyya na vitabu vya Ibn Taymiyya vimekuwa mashuhuri kwa kuwatukana watu wa madhehebu nyengine. Wapekuzi wanasema kwamba katika kitabu kimoja tu cha Ibn Taymiyya, Majmu’a Al-Fatawa, basi katumia maneno kama “Watu

1028 - Ibn Taymiyya Al-Risala Al-Madaniyya fii Al-Haqiqat Wal Majaz kilichomo katika Majmu’a Al-Fatawa j. 6, uk. 359. 1029 - Mawsuu’a Shubahi Al-Rafidha Wa Al-Raddu ‘Alaiha j. 66, uk. 4. 1030 - Ibn Taymiyya Majmu’a Al-Fataawa j. 8, uk. 146. Na, j, 14, uk. 196. 1031 - Ibn Taymiyya Majmu’a Al-Fataawa j. 12, uk. 215, sehemu ya “Furuukh Al-Llafdhiyya”.

328

Page 329: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

wa bida’a, makafiri, Mayahudi, maadui wa Allah, wajinga, wapotovu na yalio mfano wa hayo zaidi ya mara mia tisa kuwaita wale Waislamu wasiokubaliana naye. Chukua mfano mdogo. Anasema:

1) Hakika ya hawa wazushi (watu wa bidaa).1032

2) Wakakusanya baina ya ujinga (wa kutokuijua) njia ya Al-Salaf katika kuwazulia uwongo, na baina ya ujinga na upotovu.1033

3) Wameshirikiana na ndugu zao makafiri.1034

4) Basi walipojenga jambo lao juu ya utangulizi wa aina hizi mbili za kufuru na za uwongo.1035

5) Makinda ya wanafalsafa, wafuasi wa Uhindu na Wagiriki, Warathi wa majusi na washirikina na upotovu wa Mayahudi na wakiristo na Saiba na walio mfano wa hao.1036

6) Wale ambao mashetani wameyageza maumbile yao.1037 (Yaani wasiokubali kwamba Mungu kakaa kitako kwenye Arshi).

7) Hizi shubuhati zote ambazo wanaziita dalili, hakika wameziiga kutoka kwa shetani (taghut) miongoni mwa mashetani wa kikafiri (washirikina) ... 1038

8) Asili ya kauli hii, kauli ya kuzikataa sifa (za Mungu kama mkono, mguu, jicho, Allah anakaa kitako kwenye Arshi, n.k) imechukuliwa kutoka kwa wanafuzi wa Mayahudi na washirikina (makafiri). 1039

9) Na kwa hivyo, wakawa wengi katika watu wa elimu ya Hadithi wanaziita kauli za hawa kuwa ndani yake zina unafiki.1040

10) Kisha wao (Mu’utazila na Jahmiyya) waliyakanusha hayo kwa Allah kwa ujumla, basi wakawa ni washirikina mu’attilil. 1041

1032 - Ibn Taymiyya Majmu’a Al-Fatawa j. 5, uk. 9. 1033 - Yaani wale wenye kusema kuwa Mungu hana mguu, hakai kitako nk., nao ni jumhur ya Umma huu. Tazama nukulu hio katika Ibn Taymiyya Majmu’a Al-Fatawa j. 5, uk 10. 1034 - Ibn Taymiyya Majmu’a Al-Fatawa j. 5, uk 10. 1035 - Ibn Taymiyya Majmu’a Al-Fatawa j. 5, uk 10. 1036 - Ibn Taymiyya Majmu’a Al-Fatawa j. 5, uk. 11,15,18,21,24. Tazama mtu huyu anavyokafirisha Waislamu hivi! Halafu tukisema, Mafuta agogwa! 1037 - Ibn Taymiyya Majmu’a Al-Fatawa j. 5, uk. 14. 1038 - Ibn Taymiyya Majmu’a Al-Fatawa j. 5, uk. 16. 1039 - Ibn Taymiyya Majmu’a Al-Fatawa j. 5, uk. 18. Ninasema: Mahlan Sheikh Al-Islam! Mayahudi ndio waliosema kuwa “Mkono wa Allah umefungwa”. Nanyi munaufasiri mkono huo kuwa ni mkono wa kweli. Wakati hawa uliowataja wewe hapa wanakataa kuwa Mungu ana mkono? Mayahudi ndio waliomwambia Musa “Tufanyie miungu (ya sanamu) kama yao”. Ivo wenye kusema hivi watakataa kuwa Mungu ana mkono na miguu na masikio na mengineo?! Ukweli ni kuwa Mayahudi ndio walioanzisha itikadi hizo kwani zinakubaliana na fikra zao. 1040 - Ibn Taymiyya Bayanu Talbis Al-Jahmiyya j. 2, uk. 89. 1041 - Ibn Taymiyya Bayanu Talbis Al-Jahmiyya j. 2, uk. 96.

329

Page 330: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

11) “Na asili ya kauli za Jahmiyya zimetokana na washirikina…na wazushi wa Ahlil Kitab”. Mwisho wa kunukuu.1042

Tunasema: lakini baadhi ya itikadi za Jahm bin Safwaan ni hizi:

a) “Mungu haonekani duniani wala akhera”. Sasa ukirudi kuitazama itikadi ya Mayahudi utawakuta kwamba wao ndio waliosema kumwambia Musa: “Hatutokuamini mpaka tumuone Allah wazi wazi”. Na wakamwambia: “Tuoneshe Allah wazi wazi”. Na Wakiristo nao wakasema: “Mola kaingia katika kiwiliwili cha Yesu, na kwa hivyo Yesu ni Mungu katika kiwiliwili (God in flesh or God-incarnate). Suala: je itikadi ya Ahlil-Kitabi ni kumuona Mungu au kutokumuona? Na nani kachukua itikadi yake kutoka kwa Mayahudi?

b) Jahm bin Safwaan anaamini kuwa adhabu ya moto ina mwisho. Ibn Taymiyya na Ibn Al-Qayyim wamemuunga mkono katika itikadi hii katika baadhi ya vitabu.1043 Sasa nani kachukua itikadi yake kutoka kwa makafiri?1044

Hayo ni machache katika mengi yaliosemwa na Ibn Taymiyya! Mirathi ya matusi hayo inaendelea, na katika zama hizi tuna mwanachuoni wa Kiwahabi aitwae Dr. Bakr Abu Zaid ambaye walimu wake wamemsifu kwa tabia mbaya na ukhabithi na uchache wa maarifa na fitna na mengineyo. Anasema Abdullahi Al-Ghummari: katika kitabu chake alichokiita Baini Wa Baina Al-Sheikh Bakr:

….Kisha katika udhalimu wa wazi na upuuzi mbaya, ni kule Bakr kulileta kwake neno khanithi kalisema khanithi…..katika kuwaita Mashekhe wawili, Al-Kawthari na Abu Ghudda….basi hayo ndio madai yako ambayo anayowatupia watu ujinga na ukafiri.1045

Na kwa hivyo, usione ajabu ukakuta katika vitabu tafauti vya Kiwahabi ibara hizo zinajikariri, kama ilivyo katika baadhi ya sherehe za Al-‘Aqiidatu Al-Wasatiyya:

المعتزلة مخانيث األشاعرة يسمي السلف أئمة بعض ولذلك

1042 - Mtiaji maelezo katika utangulizi wa kitabu Bayanu Talbis Al-Jahmiyya cha Ibn Taymiyya j. 1, uk. 9. 1043 -Nitakuthibitishia hilo kwa urefu katika juzuu maalumu ya kitabu hiki, in shaa Allah. 1044 - Subiri ewe Kasim Mafuta usifanye pupa; nitakupa ushahidi juu ya haya. 1045 - Sh. Abdullah Al-Ghammari Baini Wa Baina Al-Sheikh Bakr uk. 67, nukulu kutoka Al-Imamu Al-Rabi’u Makanatuhu Wa Musnaduhu cha Imamu Al-Sunna Wa Al-Usul Wa Al-Furu’i, Al-Qannubi, uk. 150.

330

Page 331: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Na kwa hivyo, baadhi ya Maimamu watangulizi wanawaiita Al-Ashaa’ira kuwa ni makhanithi wa Mu’utazila.

Na sherehe ya Kitabu Al-Tawhiid:

الفالسفة مخانيث العلماء بعض يسميهم ولهذا

Na kwa hivyo, baadhi ya Maulamaa huwaita wao kuwa ni makhanithi wa wanafalsafa.

AL-RUSTUMI

Al-Hasan Bin Abas Al-Rustumi anasema kuhusu Masuni wa kawaida, kama Mashafi’i na Malik na Hanafi, kwamba:

*** *** بربهم الالت مع العزى عبدوا من إخوانهم زنادقة ضالل األشعريةوقول �������كف هم��روا

المقاالت*** أسوا تدبرته إذا

Al-Ashariya (Masuni) ni wapotovu mizandiki (wanafiki)***Ndugu zao ni wenye kuabudu Uzza na Lata***Wamemkufuru Mungu wao wazi wazi. Na maneno yao***Ukiyazingatia ndio maneno maovu kabisa.1046

IBN BAZ

Halkadhalika Ibn Baz katoa fat-wa ya wazi ya kuwakafirisha Ibadhi na wengineo wengi wasiokuwa Mawahabi. Lakini katika kitabu chake Hoja Zenye Nguvu, Kasim Mafuta anasema:

Je ni kweli Ibn Baz amewaita maibadhi makafiri? Ni mahali gani hapo? Kitabu gani ? Mbona hukututajia? Vitabu vya Ibn Baz vimejaa tele hapa duniani, hebu tutajie kitabu kimoja ambacho Ibn Baz amesema maneno hayo, na hii ni chalenji nina kupa wewe Juma na masheikh zako Khalili, al-Qannubi, na Ahmad bin Su’ud al-Siyabi mtutajie ni mahali gani Ibn Baz amewaita maibadhi kuwa ni makafiri kwa uwazi kabisa, bila ya kuhitajia taawili.1047

Ama je ni kweli Ibn Baz kawakafirisha Maibadhi au si kweli, hilo utaliona kwa macho yako katika sehemu yake maalumu. Ama kauli yako uliposema: “Bila ya kuhitajia taawili” inaonesha kwamba ukweli unaujua lakini 1046 - Al-Saifu Al-Haadi uk. 39 1047 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 85.

331

Page 332: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

unajiwekea ngao kabisa! Kwani wapi na lini umesikia kwamba ta-awili ikiwa ni sahihi inakataliwa? Tazama, kwa mfano, kwamba katika Qur-ani kuna Aya inasema: “Naye (Allah) yuko pamoja nanyi popote mulipo”. jumhur ya wanavyuoni – wakiwemo wa Kiwahabi – wanasema kwamba maana ya kuwa Allah yupo kila pahali ni kuwepo kwa elimu yake kila pahali: si kuwepo kwake Yeye Mwenyewe. Hii ni ta-awili, je nayo tuikatae? Sasa vipi Ibn Baz kawakafirisha Maibadhi nitakueleza kwa urefu katika sehemu yake maalumu. Ama kwa hapa nakusudia kukuonesha jinsi Ibn Baz alivyowakafirisha walimwengu wote. Anasema Ibn Baz kuhusu wenye kusema kwamba dunia ni duara:

Hakika kusema kwamba jua limetulia na kwamba ardhi ni duara ni kauli mbaya yenye kuchukiza. Na atayesema kwamba ardhi ni duara na kwamba jua haliendi basi kakufuru na kupotea. Na ni wajibu atakiwe kuleta toba, akiwa atatubia (basi), na kama hakutubia basi atauliwa hali ya kuwa yeye ni kafiri na aliyertadi.1048

Kisha Ibn Baz akatoa hoja juu ya kauli yake hio kwa kusema:

Lau ardhi ilikuwa ni yenye kufanya harakati basi lazima mtu angelikuwa mahala pake pale pale: asingelifika anapotaka kwenda.1049

Anaendelea:

Lau ardhi ilikuwa inazunguka kama wanavyodai basi miji na miti na mito isingelitulia, na watu wangeliiona miji ya magharibi iko mashariki na miji ya mashariki iko magharibi, na kibla kingewabadilikia watu kwani kuzunguka kwa ardhi kunapelekea kubadilika kwa mielekeo (directions) ya miji na mabara……lau kama ardhi ilikuwa inazunguka basi watu wangelihisi mtikisiko (wake) kama wanavyohisi mtikisiko wa meli na ndege… 1050

Huo ndio ufahamu wa Ibn Baz! Kwa hivyo, usione ajabu mtu kama huyu kusema kuwa Mungu ana mikono na miguu ya kweli kweli na kwamba ana sura ya Adam!1051 Na kuanzia hapa utaanza kukubainikia ukweli uliosemwa juu ya kwanini uwahabi umeweza kupata nguvu huko Suudia – sababu ni

1048 - Fatwa hii imechapishwa na Al-Riasa Al-‘Amma mwaka 1976. Na ilinukuliwa na magazeti mengi, kama ambavyo pia mwenyewe nilishuhudia katika intaneti ya mtandao wa omani.net ulipofanyika mjadala baina ya Mawahabi na Maibadhi na ikatajwa fat-wa hii bila ya Wahabi yoyote yule kukanusha. Kwa sasa tazama kitabu Al-Khawarij cha Abdullah Al-Qahtani uk. 103-105. Kwa hali yoyote ile, fat-wa hii ni jambo lililoenea katika ndimi na maandiko ya watu wengi wala hakuna Wahabi aliyeikanusha. 1049 - Tazama kitabu Al-Khawarij cha Abdullah Al-Qahtani uk. 104. 1050 - K.h.j. uk. 105.

332

Page 333: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kuwa umewakuta watu ni Mabedui wajinga: hawajui chochote kuhusu dunia wala dini! Na hayo wameyanena wenyewe Mawahabi. Anasema Muhammad Haamid Al-Faqihi:

Njia ya Sheikh Al-Islam Ibn Taymiyya na mwanafunzi wake Ibn Al-Qayyim ndio alioifuata Muhammad bin ‘Abdil-Wahhaab, lakini yeye (Muhammad bin ‘Abdil-Wahhab) hali zilimruhusu tafauti na Mashekhe wawili hao. Kwani miji ya Najd (Suudia) ya Kibedui (ulipoanzia ulinganio wa Muhammad ‘Abdil-Wahhaab) ni tafauti na Misr na Shaam (alikofanya harakati Ibn Taymiyya kisha mwanafunzi wake Ibn Al-Qayyim, ambako) kulikojaa wafalme na maamiri na majeshi na viongozi na vyuo na ustaarabu na sehemu tafauti za kujifungia Masufi (yaani skuli tafauti za kisufi), na Maqadhi na Maulamaa na wasomeshaji wa kila madhehebu.1052

Kwa ufupi, ni kuwa fat-wa hio tulioinukuu kabla imewakafirisha Waislamu mashariki na magharibi kwa sababu ya ufahamu finyu wa mtu ambaye Kasim Mafuta anasema kuwa ni mwanachuoni mkubwa sana Wallahu Al-Musta’aan!1053

SULAIMAN BIN SIHMAAN

Anasema Sheikh huyu wa Kiwahabi, Allah amlipe kile anachostahiki, kuhusu Maibadhi:

سبرت إذا وطريقتهم مذهبهم فحقيقة الزمان هذا أهل أباضية أماقبوري جهمية فهم ون������أحوالهم

إال وضاللهم كفرهم في يشك فال انتسابا األباضية إلى ينتسبون وإنماعل غلب اله ������من وى�����يه

ومباعدته هجره يجب ظالم عاص فهو توالهم فمن بصيرته عين وأعمىيعل حتى منه ن �والتحذير

والمعصية بالظلم أعلن كما بالتوبة

الزمان هذا أهل وأباضية الجهمية كفر يرى ال عمن السؤال في ذكر وماج أن أهل �������ويزعم هاد

يعرف لم فهذا كاللصوص المال ألجل وهو غلوا سابقا لهم اإلسالمرائح شم وال اإلسالم ته�حقيقة

أهله من أنه وزعم إليه انتسب ………………وإن1051 - Kitabu cha Al-Tuwaijri kinasema hivyo, nacho kimepitiwa na Ibn Baz na kusifiwa mno! 1052 - Al-Faqihi Atharu Al-Da’awa Al-Wahhaabiyya chapa 1354 A.H, uk. 22. Nukulu kutoka katika kitabu Al-Khawarij cha Abdullah Al-Qahtani uk. 12. 1053 - Na Ibn Baz nijuavyo – kama vitabu vyake vinavyoonesha – ni muqallid wa Ibn Taymiyya na Ibn Al-Qayyim, wala yeye hakuwa mujtahid kamwe.Wala elimu yake haimruhusu kujitahidi.

333

Page 334: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Ama Maibadhi wa zama hizi, uhakika wa madhehebu yao na njia yao ukiwa utazipima hali zao basi wao ni Jahmiyya wenye kuabudu makaburi. Lakini wao wananasibika na Maibadhi (wa kale kama ni) kunasibika (tu), mtu yoyote yule hatii shaka yoyote kuhusu ukafiri wao na upotovu wao, isipokuwa yule ambaye matamanio ya nafsi yake yamemzidi na yakamtia upofu katika jicho lake la uoni wa moyo, basi atayewapenda (Maibadhi) huyo ni asi dhalimu ni wajibu kumuhama na kujitenga naye na kuwahadharisha watu dhidi yake mpaka atapotangaza toba kama alivyotangaza dhulma na maasi.

Na kile kilichotajwa katika suali kuhusu yule ambaye haoni kuwa (ni sahihi) kuwakafirisha Jahmiyya na Maibadhi wa zama hizi; na akadai kwamba kuwapiga jihadi hao kulikotangulia ni kuchupa mipaka na (jihadi hio)1054 ilikuwa ni kwa kutaka mali kama vile wezi wanyang’anyi. Basi huyu (aliyedai hivi) hakuufahamu uhakika wa Uislamu wala hakunusa hata harufu yake hata akiwa anajinasibisha nao (huo Uislamu) na akawa anadai kwamba naye ni katika wafuasi wake……..1055

Tazama jinsi Sheikh huyu wa Kiwahabi alivyokuwa jasiri si katika kuwakafirisha Waislamu tu bali na kuwazulia watu uwongo! Kapata wapi kusikia au kuona kwamba Ibadhi wanatukuza makaburi licha ya kuyaabudu. Nimeishi Oman si chini ya miaka 15 na Zanzibar katika utoto wangu wote sijapata kumuona Ibadhi yoyote – si Sheikhe wala si mtu wa kawaida – kwenda kuweka nadhiri yake kaburini au kwenda kuomba kaburini. Wanavyuoni na watu wema wanaokwenda makaburini ni kwa kuwasalimia maiti na kuwaombea dua tu, hili ndilo nililolishuhudia nalo ni jambo la Kisharia kama Hadithi sahihi zinavyothibitisha.

Pia kasahau mtu huyu kwamba Salaf (watangulizi) wake ndio waliokuwa wakihimiza kuabudu makaburi kama walivyokuwa wakisema: “Mwenye dhiki akalizuru kaburi la Ahmad siku ya J/tano na akaomba dua, basi Allah atamruzuku nafasi”.1056 Na riwaya hizi ziko nyingi mno, nitazinukuu baadhi yake in shaa Allah katika sehemu ya mwisho ya juzuu hii.

Hayo ndio alioyanena kuhusu Ibadhi, na mwanzo wa suali ni:

األولى المسئلة

1054 - Yaani mauaji liofanywa na Muhammad ‘Abdil-Wahhaab na wafuasi wake ya kuwaua Waislamu kwa dhulma na kuwapora mali zao. 1055 - Sulaiman bin Sihmaan Kashfu Al-Awhaami Wa Al-Iltibaas uk. 156. Publisher: Daru Al-‘Aasima Al-Riyyadh Saudia, chapa ya kwanza 1415 A.H. 1056 - Ibn Al-Jawzi Manaaqibu Ahmad uk. 580.

334

Page 335: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

بلغتهم وهل واإلباضية والقبورية الجهمية تكفير في تنازعا رجلين فيالحجة عليهم وقامت الدعوة

السؤال آخر إلى أوالMas-ala:Kuhusu watu wawili waliotafautiana katika kuwakafirisha Jahmiyya, wenye kuabudu makaburi na Maibadhi, na je ulinganio umewafika na hoja zimewasimamia au hazikuwasimamia….(mpaka mwisho wa suali).

الله رحمه أحمد مذهب من فالمشهور الجهمية أما لله الحمد الجوابتكفي السنة أئمة رهم�����وعامة

الكتب به وأنزلت الرسل به جاءت ما مناقضة في صريح قولهم ألنالص جحود قولهم انع��وحقيقة

الله عبد اإلمام قال ولهذا الرسل وجميع بل نفسه عن به أخبر ما وجحودلنح إنا المبارك كي ���بن

كفروا وبهذا الجهمية كالم نحكي أن نستطيع وال والنصارى اليهود كالمالقرآن يقول وق �مخل من

علم له ليس وأنه العرش على ليس الله وأن اآلخرة في يرى ال الله وأنرح وال قدرة وال ����وال مة

ابن مثل السلف من كثير عند وهم صفاته من ذلك غير وال غضبأسب بن ويوسف اط����المبارك

فرقة وسبعين الثالث من ليسوا أحمد أصحاب من وطائفة

Jawabu: Sifa zote zilizo njema zinamstahikia Allah. Ama Jahmiyya, kilicho mashuhuri katika madhehebu ya (Al-Imamu) Ahmad (bin Hanbal) – Allah amrehemu – na Maimamu wote wa Ahlu Sunna, ni kuwakafirisha kwani kauli yao iko wazi katika kuyapinga yale waliokujanayo Mitume na vitabu (vya Allah) vikateremka nayo. Na uhakika wa kauli yao ni kumpinga Allah Mwenye kuumba na kuyakanusha yale ambayo Yeye (Allah) kayazungumzia kuhusu nafsi yake1057 bali (na yakaelezwa pia na) Mitume wote. Na kwa hivyo, Al-Imamu ‘Abdullahi bin Mubarak kasema: ‘Hakika ya sisi tunasimulia kauli za Mayahudi na Makiristo lakini hatuwezi kusimulia maneno ya Jahmiyya’. Na kwa sababu hii, basi (wanavyuoni hao) wamewakafirisha wale wenye kusema kwamba Qur-ani ni kiumbe na kwamba Allah haonekani huko akhera na kwamba Allah hayuko (hakukaa kitako) juu ya Kiti chake cha enzi (‘Arshi), na kwamba Yeye hana elimu wala uwezo wala rehema wala ghadhabu wala mengineo katika sifa zake. Na hao – kwa mujibu wa Al-Salaf wengi kama Ibn Al-Mubarak na Yusuf bin Asbaat na kundi (kubwa) la wanavyuoni wafuasi wa (Al-Imamu) Ahmad – sio katika jumla ya yale makundi sabiini na tatu (ya Umma huu: wao wametoka katika Umma).

1057 - Anakusudia kukanusha kwamba Mungu ana viungo! Kukanusha haya ndio ukafiri wenyewe! Wallahu Al-Musta’aan!

335

Page 336: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Ninasema: ndugu Waislamu tazameni hatari ya Mawahabi hii jinsi wanavyoukafirisha Umma mzima kwa kutegemea kauli ya fulani na fulani kana kwamba fulani na fulani hao ni ma’asumun! Maneno haya hayakuwakafirisha Maibadhi tu, bali yameukafirisha Umma mzima isipokuwa baadhi tu ya Wafuasi wa madhehebu ya Hanbal na mtu mmoja mmoja katika mujassima. Tazama sababu alizozitoa ambazo kwazo watu hao wameingia katika ukafiri:

1) Wanasema kwamba Qur-ani ni kiumbe.2) Allah haonekani.3) Allah hakukaa kitako kweli kweli juu ya ‘Arshi.

Kifungu cha kwanza na cha pili wanaingia Maibadhi, Jahmiyya na Al-Mu’utazila. Shia na Zaidia wanaingia katika kifungu cha pili. Kifungu cha mwisho Unaingia Umma wote wa Kisuni na madhehebu nyengine zote isipokuwa Mawahabi na watangulizi wao wa Kihanbali au baadhi ya Hanbali na mtu mmoja mmoja katika mujassima.

Isitoshe bwana huyu hakutosheka na jarima lake hilo bali kawazulia uwongo Waislamu! Ni Muislamu gani au ni madhehebu gani – Ash’ariyya, Shia, Ibadhi, Zaidia, Mu’utazila, Jahmiyya – yenye kusema kwamba Allah hana elimu wala uwezo!1058 Huu ni uzushi wa wazi uliofanywa na Sheikh huyu wa Kiwahabi.

Anaendelea Sheikh wa Kiwahabi:

والح العلم أهل من وأمثاله أحمد اإلمام أن مضى فيما لك بينا ديث��وقديخ تك ���ال في فير������تلفون

السن في صنف من ذكر وقد مرتدون زنادقة ضالل وأنهم ة��الجهميةم �تكفيره أه ��م عامة ل�������ن

أح واألثر العلم اإلمام بن الله وعبد أبي �كالاللكائي وابن له السنة في مدوالخ ����مل ف ����يكة ي ����الل

األئمة وإمام له أساطين السنة عن ونقله كفرهم قرر قد خزيمة ابنشمس كفرهم حكى وقد األئمة

رحمه القيم ابن المسلمين الله الدين أئمة من خمسمائة عن كافيته فيانضاف إذا فكيف وعلمائهم

إشك فال طريقتهم وعلى القبور عباد من كونهم ذلك هذه اإلى والحالة لوضاللهم كفرهم في

Na tumebainisha katika hayo yaliotangulia kwamba Al-Imamu Ahmad na walio mfano wake miongoni mwa watu wa elimu na watu wa Hadith hawatafautiani katika kuwakafirisha Jahmiyya na kwamba wao ni

1058 - Watu wanatafautiana kuhusu elimu na uwezo wa Allah ukoje: si kwamba wanatafautiana juu ya kwamba je ana au hana elimu na uwezo?

336

Page 337: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

wapotovu Mazindiki (wanafiki) waliortadi. Na wanavyuoni wote wa elimu na mapokezi waliotunga vitabu vya Sunna wametaja kuwakafirisha kwao (watu hao); kama vile Al-Llaalikai na Abdullahi bin Al-Imam Ahmad katika (kitabu chake) Al-Sunna na Ibn Abi Mulaika na Al-Khallaal katika (kitabu chake) Al-Sunna na kiongozi wa Maimamu Ibn Khuzaima ameikubali (kauli ya) kuwakafirisha na akanukuu kutoka kwa vigogo wa Maimamu. Na Shamsu Al-Din Ibn Al-Qayyim rahimahu Allahu amesimulia katika kitabu chake Al-Kafiya kutoka kwa Maimamu mia tano na wanavyuoni wao, basi vipi ikiwa itaongozeka pamoja na hayo kwamba wao ni katika wenye kuabudu makaburi na wanaifuata njia yao. Hakuna mushkeli wowote ule – wakati hali iko hivi – kuhusu ukafiri wao na upotovu wao.

ABDULLAHI BIN ABDIL-RAHMAAN AL-JIBRIN

Sheikh huyu sijui ana akili gani! Kwa kweli ni mtu wa ajabu sana; ajabu iliotokana na kufungika kwake katika vitabu vya madhehebu moja au kufungika katika fikra ya mtu mmoja alioifanya kuwa ndio dini yenyewe. Sheikh huyu hajui hata kilichoko duniani wala haijui siasa ya dini ya Kiislamu! Utakumbuka wakati Hizbu Allah kule Lebanon walipokuwa wanapigana na Mayahudi, basi yeye alitoa fat-wa kwamba haijuzu kuwaombea dua Hizbu Allah ili Allah awape ushindi katika vita hivyo. Yaani yeye alikuwa anatamani kwamba bora washinde Mayahudi kuliko kushinda Hizbu Allah kwa sababu wao ni Mashia. Hii ni akili gani! Sasa baada ya hayo, soma alioyanena kuhusu Maibadhi baada ya kuulizwa suali linalofuata:

Suali: Maibadhi ni katika madhehebu zilizopo mjini kwetu, nao wanadai kwamba wao si Makhawarij, na wanalingania kuzikurubisha madhehebu (kwamba madhehebu zote ziwe na maelewano), basi nini uhakika wa madai yao? Na nini lengo la wito wao huo? Na vipi yanakuwa maingiliano nao? Na je inajuzu kusali nyuma yao? Na nini hukumu ya kuoana nao?

Hilo ndilo suali aliloulizwa! Na bila shaka suali hili linaonesha kwamba muulizaji tayari alikuwa ameshajengwa fikra mbaya juu ya Maibadhi ndio maana akauliza hivyo. Sasa tazama jawabu ya huyo Sheikh! Anasema:

Jawabu: kikundi hiki cha Maibadhi kipo hapa Bara Arabu na kituo chake ni Oman na asili yao ni Khawarij ambao wanawakafirisha Waislamu kwa sababu ya kutenda dhambi na wanawaua Waislamu kwa sababu ya kufanya dhambi na wanaona kwamba kusamehe ni dhambi na ni ukafiri. Lakini hawa wao hawawezi kuwaua Waislamu kwa sababu ni wachache na hawana uwezo. Kisha hawa tulionao wao wamefuata itikadi za Mu’utazila wakazikanusha sifa za Allah kama kusikia na kuona na kusema na kuwa

337

Page 338: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Allah yuko juu kweli kweli na kukaa kwake kitako kweli kweli. Na wakayakanusha maneno ya Allah na wakadai kwamba Qur-ani ni kiumbe na wakakanusha kuonekana kwa Allah kwenye pepo. Na wakazikataa Hadithi Ahadi hata zikipokewa katika Sahihi mbili (Al-Bukhari na Muslim), na mmoja wao akaandika kitabu kwa jina Al-Saifu Al-Haadi ‘Alaa Al-Muhtajjina Bi-Akhbaari Al-Ahadi. Na kadhalika Mufti wao kaandika kitabu kwa jina la Al-Haqqu Al-Daamigh ambapo ameziletea ta-awili humo dalili za kuonekana kwa Allah na dalili kwamba Qur-ani ni maneno ya Allah na dalili za kuthibiti ujumla wa uwezo wa Allah na yaliofanana na hayo.

Wala hayakubaliwi madai yao kwamba wao si Khawarij, wala haikubaliwi kauli yao ya kuzikurubisha madhehebu (zote za Kiislamu), bali ni lazima waache itikadi zao na waingie katika itikadi za Ahlu Sunna Wa Al-Jamaa’a.1059 Lakini madamu wao hawakulikubali hilo, basi (elewa kwamba) ulinganio wao huo ni kwa ajili ya kuwa (watu) wasameheane nao tu na waache kuwakafirisha (kuwaita makafiri), basi kilicho wajibu kwetu ni kuwadhihirishia wao uadui wala tusisali nyuma yao wala tusioe wanawake wao bali tuwagomee kabisa……1060

Hio ndio fat-wa ya Sheikh Al-Jibrin أقبحه ما الجهل الله Allah !قاتلauangamize ujinga ni jambo baya lililoje! Maneno hayo ndani yake:

1) Yana uzushi.2) Yanaonesha kwamba huyu mtu hana akijuacho, hasomi isipokuwa

“huyu ni kafiri; huyu ni mtu wa bidaa; huyu ni mu’attil”. 3) Yana makosa na kila balaa.

Ama uzushi umo katika madai yake kwamba:

wanawakafirisha Waislamu kwa sababu ya kutenda dhambi na wanawaua Waislamu kwa sababu ya kufanya dhambi na wanaona kwamba kusamehe ni dhambi na ni ukafiri. Lakini hawa wao hawawezi kuwaua Waislamu kwa sababu ni wachache na hawana uwezo.

1059 - Itikadi ya Ahlu Sunna wenyewe ni itikadi za Kiwahabi wenye kusema kuwa Mungu ana kiuno, mguu, macho mkono, na ana sura ya Adam! Hii ndio Sunna wanayotulingania tuingie na kuwacha itikadi zetu! 1060 - Fat-wa hii imo katika web-site rasmi ya Sheikh huyo. Nayo ni fat-wa nambari 3177, na maudhui ni:

: اإلباضية حقيقة الفتوى موضوعMaudhui ya fat-wa: uhakika wa Maibadhi.

Andika maneno yafuatayo yatakupeleka moja kwa moja katika web-site ya Sheikh huyo. Andika:

الجبرين الشيخ موقع

338

Page 339: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Kasikia wapi Sheikh huyu kwamba katika sira ya Ibadhi zamani na leo ni kuua mtu kwa sababu ya kutenda dhambi? Ebu na-asome historia ya Ibadhi hata ilioandikwa na wasio Waislamu; kisha na-asome historia ya Muhammed bin ‘Abdil-Wahhab na wafuasi wake ambayo wameiandika wao wenyewe Mawahabi, kisha alinganishe aone nani kaua watu bila haki?1061

Kisha kasikia wapi Sheikh huyu kwamba Ibadhi wanawakafirisha Waislamu kwa sababu ya kufanya dhambi. Ama kile wanachokiita Maibadhi kuwa ni kufru ni’ima (ukafiri wa neema), elewa kwamba hicho kimo katika Hadithi kadha wa kadha na Aya kadha wa kadha. Soma, kwa mfano, Hadithi kama: “Nimeuona moto na wakazi wake wengi zaidi ni wanawake….. wanaikufuru ihsani” na Hadithi “Musigeuke kuwa makafiri baada yangu mukawa munakatana shingo zenu”…… “Mambo mawili katika umma wangu ni ukafiri kuitukana nasaba na kumuombolezea maiti”…….. “Hakuna baina ya mtu na ukafiri isipokuwa kuacha sala”. Bila kusahau kwamba Mawahabi wao kwao aliyeacha sala si kafiri-neema tu bali ni kafiri aliyetoka katika mila ya Kiislamu: ni sawa na Yahudi na Mkiristo!1062 Sasa nani aliyewakafirisha Waislamu!

Kwa hivyo, watu wenye kutenda dhambi kubwa bila ya kutubia Ibadhi huwaita Makafiri wa neema za Allah yaani ni watu walioacha kuzishukuru neema za Allah, wala hawawaiti watu hao kuwa ni makafiri kwa maana ya kuwa wametoka nje ya Uislamu, bali wao ni Waislamu wana haki zote za Uislamu – kusaliwa wakifa, kuozeshwa n.k., isipokuwa haki za Al-Walaya wa Al-Baraa. Cha kujiuliza ni kuwa: je ni Ibadhi peke yao waliosema hivyo? Katika kitabu Majmu’a Al-Tauhid chenye mafunzo ya Muhammad bin ‘Abdil-Wahhaab na Ibn Taymiyya kuna maelezo haya: “….Na kufuru ndogo ambayo haimtoi (mtu) katika mila (ya Uislamu) nayo ni kufru- ni’ima (kuikufuru neema ya Allah)”. 1063 Mwisho wa kunukuu. Na Al-Imamu Muslim naye – akifuatiwa na Al-Imamu Al-Nawawi – anasema: “…..Kulitumia neno ukafiri kwa usiokuwa ukafiri wa kumkufuru Allah, kama vile kufru-ni’ima (kuikufuru neema ya Allah).” 1064 Sasa baada ya haya sijui zogo hili ni la nini? Kilichosemwa na Ibadhi kimo katika Hadithi na Aya na kimo katika madhehebu nyengine yakiwemo madhehebu ya Kiwahabi?

Kisha tazama maelezo ya Sheikh huyo alivyosema:

1061 - Maelezo juu ya mwenendo wa Kiibadhi yatakuja katika juzuu ya pili in shaa Allah. 1062 - Utaona huko mbele nukulu zao na marejeo ya vitabu vyao. 1063 - Majmu’a Al-Tauhid uk. 10. 1064 - Tazama Muslim Sahihu Muslim kichwa cha habari cha Hadithi na. 79-80. Al-Nawawi Sharhu Sahihi Muslim j. 2, uk. 141.

339

Page 340: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Kisha hawa tulionao wao wamefuata itikadi za Mu’utazila wakazikanusha sifa za Allah kama kusikia na kuona na kusema na kuwa Allah yuko juu kweli kweli na kukaa kwake kitako kweli kweli.

Tazama uzushi wa Al-Jibrin huu! Kwanza kasikia wapi kwamba Ibadhi wamewafuata Mu’atazila ilhali Imamu wa Kiibadhi, Jabir bin Zaid na mwana harakati wao mkuu Abdullahi bin Ibadhi walikuwepo kabla ya kuundika kwa madhehebu ya Mu’utazila. Madhehebu ya Mu’utazila imewakuta Maibadhi wapo tayari na fiq-hi yao na itikadi zao. Kisha kapata wapi kusikia au kuona kwamba Ibadhi wanakataa kwamba Allah anaona na anasikia? Huu ni uzushi mweupe kama jua la mchana. Maibadhi, sawa na Masunni wote na Mashia na Zaidia, wanasema kwamba Allah anasikia wala hana masikio; anaona wala hana macho! Mola mwenye macho na masikio si mola wa Waislamu wote, bali ni mola wa Mawahabi tu. Ama itikadi ya kuwa Allah yuko juu na kwamba kakaa juu ya kiti kweli kweli ni itikadi ya Mawahabi tu na Maimamu wao. Ama itikadi ya kuwa Allah anasema kweli kweli hii ina maelezo marefu hapa si mahala pake.1065

Kisha tazama maneno ya Sheikh wa Kiwahabi aliposema: “Na wakayakanusha maneno ya Allah na wakadai kwamba Qur-ani ni kiumbe na wakakanusha kuonekana kwa Allah kwenye pepo”. Tunasema: ni kweli kwamba Ibadhi wanasema kuwa Allah haonekani; Qur-ani ni kiumbe kwani wao wanasema kwamba chochote kisichokuwa Allah basi hicho ni kiumbe chake na kwamba chochote ambacho kuna siku fulani kimetokea basi hicho ni kuimbe; na Qur-ani si Allah na kuna siku imetokea baada ya kuwa mwanzo haikuwepo. Ukinambia kwamba hio ni sifa ya Allah kwani ni maneno yake, nitakwambia kwamba Allah hana sifa inayoitwa Qur-ani, wala sifa yake haigawanyiki ikawa nyengine ni mansukh (imefutwa) na nyengine ipo imethibiti; nyengine ni mufassal (imefafanuliwa) na nyengine ni mujmal (haikufafanuliwa); nyengine ni bora na nyengine imezidiwa ubora. Huoni kwamba huwezi kudai kwamba elimu ya Allah kwa fulani yaani anavyomjua fulani ni bora kuliko elimu yake kwa mwengine kama unavyoweza kusema kwamba Ayatul Kursiy au Suratul Ikhlaas ni bora kuliko Ayatul Dain. Halkadhalika huwezi kusema kwamba elimu ya Allah ni bora kuliko uwezo wake, wakati Qur-ani uaweza kusema kwamba sura kadha au Aya kadha ni bora zaidi kuliko Aya kadha kama ilivyokuja katika Hadithi kwamba “Qul Huwa Allahu ni sawa sawa na thuluthi moja ya Qur-ani” na “Suratul Baqara ndio nundu la Qur-ani”. Kwa hali yoyote ile mjadala hapa si mfupi na mahala pake ni katika sherehe yetu ya tafsiri ya

1065 - Mahala pake ni maelezo yetu juu ya tafsiri ya Sheikh Abdullah Salih Al-Farisi.

340

Page 341: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Al-Farisi;1066 lakini suali ni kuwa: je ni maneno gani hayo ya Allah walioyakanusha Maibadhi kama alivyodai Sheikh huyo.

Kisha tazama maneno yake yasemayo:

Na wakazikataa Hadithi Ahadi hata zikipokewa katika Sahihi mbili (Al-Bukhari na Muslim), na mmoja wao akaandika kitabu kwa jina Al-Saifu Al-Haadi ‘Alaa Al-Muhtajjina Bi-Akhbaari Al-Ahadi.

Tazama jinsi mtu anavyoghushi huyu! Wapi kasikia au kaona kwamba madhehebu ya kiibadhi inazikataa Hadithi Ahadi kama hivi alivyodai yeye hapa? Hadithi Ahadi zinakataliwa katika itikadi tu, na wenye kusema hivi si Ibadhi tu, bali ni jumhur ya madhehebu za Kiislamu.1067 Kisha kasahau Sheikh huyu kwamba Imamu wake Ibn Taymiyya – kama tutavyomnukuu baadae – pia naye ana msimamo huo huo. Halkadhalika Al-Imamu Ahmad na Maimamu wengine wote hao wana msimamo huo huo. Halkadhalika baadhi ya Hadithi za Al-Bukhari na Muslim zimekataliwa na wanavyuoni zaidi ya mia mbili wa Kisunni akiwemo Ibn Taymiyya, Ibn Al-Qayyim, Al-Albani na wengine. Sasa kosa la Maibadhi liko wapi?

Halafu Sheikh huyo akaendelea na ghushi zake akasema:

Na kadhalika Mufti wao kaandika kitabu kwa jina la Al-Haqqu Al-Daamigh ambapo ameziletea ta-awili humo dalili za kuonekana kwa Allah na dalili kwamba Qur-ani ni maneno ya Allah na dalili za kuthibiti ujumla wa uwezo wa Allah na yaliofanana na hayo.

Maneno haya ni maneno ya kufyatua tu! Je Ibadhi hawaamini kwamba Qur-ani ni maneno ya Allah hata akadai hivi? Je Ibadhi hawaamini uwezo wa hakika wa Allah?

Kisha Sheikh wa Kiwahabi akawakafirisha Maibadhi kwa kusema:

….basi (elewa kwamba) ulinganio wao huo ni kwa ajili ya kuwa (watu) wasameheane nao tu na waache kuwakafirisha (Waache kuwaita makafiri), basi kilicho wajibu kwetu ni kuwadhihirishia wao uadui wala tusisali nyuma yao wala tusioe wanawake wao bali tuwagomee kabisa……

1066 - Kwa wenye kusoma Kiarabu basi maudhui hii imeelezwa kwa ufafanuzi na hoja za wazi katika kitabu Al-Haqqu Al-Damigh cha Al-Imamu Badru Al-Din Al-Khalili. Rejea huko ili ufaidike. Na kwa urefu zaidi sasa Sheikh anatayarisha kitabu Burhanu Al-Haqqi chenye juzuu 15 juu ya itikadi sahihi ya Kiislamu. 1067 - Rejea kitabu Al-Saifu Al-Haad cha Imamu Al-Sunna Al-Qannubi, uone maelezo kwa urefu juu ya maudhui hii.

341

Page 342: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Maneno yasemayo: “Na waache kuwakafirisha (Waache kuwaita makafiri),” yana maana kwamba Maibadhi kwa kitendo chao cha kuwataka watu wa madhehebu tafauti wafahamiane ni kuwa huo ni ujanja tu ili Maibadhi wasalimike na kuitwa makafiri ilhali ni makafiri! Kwa hivyo, kilicho wajibu ni kujenga nao uadui tu! Jamani ivo kweli mtu mwenye akili hii anaweza kuwaongoza Waislamu! Huu ndio uwahabi na hii ndio mentality yao! Ndio maana Sheikh huyu akaona bora Mayahudi kuliko Mashia! Sijui lini watu hawa watakuwa na akili!

UKAFIRISHAJI WA MAIMAMU WAASISI

Hayo tulioyanukuu ni baadhi ya yaliosemwa na baadhi ya Maimamu wa Kiwahabi waliokuja baadae pamoja na Masheikh wafuasi wa madhehebu hio. Na asili ya tatizo hilo – la kupenda kuwatukana na kuwakafirisha wafuasi wa madhehebu mengine – lilioko katika madhehebu ya Kiwahabi na watangulizi wao wa madhehebu ya Hanbali, ni zile riwaya zilizopokewa kutoka kwa Al-Imamu Ahmad bin Hanbali na wenzake. Hata ikafika hadi kuwa madhehebu ya Hanbali ni maarufu kwa kuwashambulia na kuwatukana wasioafikiana nao katika rai. Ndio maana Sh. Kasim Mafuta naye akamnukuu Al-Imamu Ahmad bin Hanbali akisema: “Atayesema kuwa Allah haonekani huyo ni kafiri”!1068 Kasim Mafuta kayanukuu hayo akidhania kuwa hio ni sifa njema ambayo yeye na Al-Imamu Ahmad watahimidiwa kwayo; kumbe hio ni kasoro ya Kisharia na ni ila mbaya ilioje!

Na mfano wa kauli hio, miongoni mwa kauli zilizosimuliwa kutoka kwa Al-Imamu Ahmad na waliokuwa pamoja naye ni riwaya kama:

Atayedai kwamba Qur-ani ni yenye kuumbwa basi huyo ni Jahmiy kafiri, na atayesema kuwa Qur-ani ni maneno ya Allah lakini asiseme kuwa si kiumbe basi huyo ni mchafu zaidi kuliko wa kwanza na atayedai kwamba matamshi yetu ya hio (Qur-ani wakati tunapoisoma) na usomaji (wetu wa hio Qur-ani) ni kiumbe basi huyo ni Jahmi. Na yule ambaye hakusema kuwa hawa wote ni makafiri, basi huyo ni mfano wao.1069

Tunasema: basi kwa maana hio, Al-Bukhari na wengine wengi watakuwa ni makafiri kwani Al-Bukhari naye ni miongoni mwa wenye kusema kuwa matamshi yetu tunapoisoma Qur-ani ni kiumbe. Tazama hatari hii iliokuweko katika Umma huu! Na watu wenye kufuata kama bendera

1068 - Abul Fadhl Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 170. 1069 - Ibn Abi Ya’alaa Tabaqatu Al-Hanabila j. 1, uk. 29. Na mfano wake ni riwa na. 164 katika Al-Sunna cha Ibn Ahmad j. 1, uk. 160.

342

Page 343: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

wakawa wanafuata tu! Sasa mtu kama Al-Bukhari akiwa ni kafiri nini kilichobakia tena ilhali ulimwengu mzima wa Kiislamu unamtegemea yeye katika masimulizi ya Hadithi za Mtume (s.a.w.)?

Riwaya kutoka kwa Al-Imamu Ahmad zinaendelea. Na tunakutana na riwaya isemayo: “Atayesema kuwa matamshi yangu ninapoisoma Qur-ani ni kiumbe basi huyo ni jahmiy atakaa motoni milele”.1070 Anasema Sh. Hasan bin Farahan Al-Maaliki akitia maelezo riwaya hii:

Allah amsamehe Ahmad! Kauli hii ikithibiti kutoka kwake basi inafanana na kumfanyia kibri Mwenyezi Mungu; basi kauli kwamba tamko wakati wa kusoma Qur-ani ni lenye kuumbwa ni kauli ya Al-Karabisi na Al-Imamu Al-Bukhari na wengineo katika Maulamaa wakubwa wa Ahlu Al-Sunna; bali madhehebu zote za Kiislamu taqriban wanafuata (kauli) hio, isipokuwa Mahanbal.1071

Riwaya nyengine za Al-Imamu Ahmad zinasema:

Atayesema kuwa Qur-ani imeumbwa, basi damu yake ni halali; na yule ambaye kawaita watu hao kuwa ni makafiri basi asisikilizwe (riwaya zake zisipokewe) wala asisalimiwe hata akiwa ni katika jamaa wa karibu wala usende katika maziko yao wala wakiumwa usiwajuilie hali.1072

Anasema Ahmad:

Al-Jahmiyya wamegawanyika sehemu tatu….na wote hawa ni makafiri; wanatakiwa watubie, ikiwa watatubia (basi sawa); kama hawakutubia basi watauliwa”.1073

Mtu mmoja alimuuliza Ahmad:

Je nisali nyuma ya anayekunywa pombe, akajibu “Usisali”. Akamuuliza: je nisali nyuma ya mtu anayesema kuwa Qur-ani imeumbwa, akajibu Ahmad: Subhana Allah! Nakukataza (kusali nyuma ya) Muislamu wewe unaniuliza kuhusu kafiri? 1074

Akaulizwa Al-Imamu Ahmad kuhusu mtu anayewatukana Masahaba wa Mtume (s.a.w.). Akajibu: “Sioni kuwa hao wana Uislamu kitu”. Anasema 1070 - Ibn Abi Ya’alaa Tabaqatu Al-Hanabila j. 1, uk. 47. Sasa ile itikadi kwamba atayesema Laa Ilaha Illa Allah hakai motoni mile imekwenda wapi?!1071 - Al-Maliki, Hasan bin Farahan Qira-atun Fii Kutubi Al-’Aqaaid uk. 103. 1072 - Ibn Abi Ya’alaa Tabaqatu Al-Hanabila j. 1, uk. 156-157. 1073 - Ibn Abi Ya’alaa Tabaqatu Al-Hanabila j. 1, uk. 157.1074 - Ibn Abi Ya’alaa Tabaqatu Al-Hanabila j. 1, uk. 326.

343

Page 344: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Sheikh Hasan Al-Maaliki: “Al-Nawasib miongoni mwa Banii Umayya walikuwa wakimlani Ali juu ya membari, je walikuwa makafiri?1075 Ninasema: na hapa ndipo uadilifu ulipowashinda wengi: kitendo kimoja kinapewa hukumu mbili – moja ya Kombo nyengine ya Faki!

Anasema Al-Imamu Ahmad:

…Atayesema kuwa kitu kitokacho kwa Allah, elimu yake au maneno yake, kuwa kimeumbwa basi huyo ni zindiki kafiri; hasaliwi (akifa) wala hapasaliwi nyuma yake (akisalisha) na mali yake inafanywa kama mali ya aliyertadi.1076

Inasema riwaya ya Ibn Batta kutoka kwa Abdullahi bin Idris:

..Nilikuwa mbele ya Abdillahi bin Idris Al-Awdi, akamjia mtu mmoja akasema: ‘Hakika watu wanadai kuwa Qur-ani ni yenye kuumbwa. Akasema: (Hao ni) Mayahudi. Akasema ni Muwahhidun (watu wa tauhidi). Akasema: ‘Atayedai kwamba Qur-ani ni yenye kuumbwa basi kadai kuwa Allah ni mwenye kuumbwa;1077 na atayedai kuwa Allah ni mwenye kuumbwa basi ni kafiri”.1078

Ninasema: Kwani Qur-ani ndio Allah hata iwe hivyo? Na kwanini basi yule aliyesema kuwa: “Allah alipotaka kuumba nafsi yake kwanza alimuumba farasi kisha akamuendesha mbio mpaka akatoka jasho na kutoka katika jasho hilo la farasi Allah akaumba nafsi yake,” kwanini yule awe Ahlu Al-Sunna na awe Al-Salafu Al-Salih: asiwe kafiri naye?

Zinaendelea kauli za Kihanbali/Kiwahabi. Na heading moja – ya kauli hizo – inasema hivi: “Kubaiinisha ukafiri wao na upotovu wao na kutoka kwao katika milla (ya kiislamu: si Waislamu kabisa) na ruhusa ya kuwaua”.1079 (Yaani watu wanaosema kuwa Qur-ani imeumbwa).

Inasema riwaya: “Atayesema kuwa Qur-ani ni yenye kuumbwa basi anauliwa wala hatakiwi toba”!!! 1080

1075 - Al-Maliki, Hasan bin Farahan Qira-atun Fii Kutubi Al-’Aqaaid uk. 106. 1076 - Ibn Ahmad Al-Sunna j. 1, uk. 164, riwaya na. 179. 1077 - Tazama akili hio! Kwani Qur-ani ndio Allah! Mjadala juu ya maudhui hii uko katika kitabu Sherhe ya Tafsiri ya Al-Farisi In shaa Allah. 1078 - Ibn Batta Al-’Ukbari Al-Inaba ‘Ani Al-Shari’a j. 12, jalada la nne uk. 294-95, riwaya na. 2251. 1079 - Tazama heading katika j. 12, jalada la nne uk. 294 wa kitabu Al-Inaba ‘Ani Al-Shari’a.1080 - Ibn Batta Al-’Ukbari Al-Inaba ‘Ani Al-Shari’a j. 12, jalada la nne uk. 295, riwaya na. 2254.

344

Page 345: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Riwaya nyengine yanena:

….Je imekufikia habari ya Ibn ‘Ulayya kuhusu Qur-ani! (Yule aliyepewa habari ya Ibn ‘Ulayya) akasema: Nisikilize! Atayedai kuwa Qur-ani imeumbwa basi huyo kwetu ni kafiri zindiki (mnafiki) adui wa Allah, usikae naye wala usimsemeshe”.1081

Ninasema: lakini Ibn ‘Ulayya huyu ni mpokezi wa Al-Bukhari na Muslim na wengine wanne. Kwa hivyo, Al-Bukhari na Muslim wamepokea Hadithi kutoka kwa makafiri, mazindiki na maadui wa Allah. Hata ikisemwa kwamba katubia – kama ilivyodaiwa katika Tahdhib Al-Tahdib – je zile Hadithi alizozisimulia naye ni kafiri tuzifanyeje? Bali wale wengine ambao hawakutubia kutokana na kauli hio na kauli nyengine – miongoni mwa Mashia, Qadariyya, Khawaarij n.k. – nao riwaya zao zimo katika Sahihu Al-Bukhari na Sahihu Muslim je wao nao tuzifanyeje riwaya zao? Tuzikubali riwaya za makafiri wanafiki au tuzitoe na kuzitupa? Waislamu tazameni hatari hio ya Maimamu wa Kiwahabi!

Riwaya za kuwakafirisha Waislamu zinaendelea, na tunakutana na riwaya isemayo:

Lau jambo (la utawala) lingekuwa kwangu basi ningelikaa kwenye daraja, hapiti yoyote yule mwenye kusema kuwa Qur-ani ni kiumbe ila ningemkata shingo yake. 1082

Zinasema riwaya: “Nimemsikia Ibn Mubarak akisema: Al-Jahmiyya ni makafiri”..1083……..“Wenye kusema kuwa Qur-ani imeumbwa wanauliwa kwa upanga”.1084

Hayo ndio maneno ya Maimamu wa Kiwahabi nayo ni machache mno katika mengi. Anayependa kujua zaidi na arejee vitabu vyao kama Sunna (nacho ni Bida’a) cha Ibn Ahmad, Al-Inaba cha Ibn Batta, Sharhu Al-Sunna cha Al-Barbahari na vyenginevyo vingi.1085 Kwa hivyo, kama umeyajua 1081 - Ibn Batta Al-’Ukbari Al-Inaba ‘Ani Al-Shari’a j. 12, jalada la nne uk. 296, riwaya na. 2256. 1082 - Ibn Batta Al-’Ukbari Al-Inaba ‘Ani Al-Shari’a j. 12, jalada la nne uk. 296, riwaya na. 2257. 1083 - Ibn Batta Al-’Ukbari Al-Inaba ‘Ani Al-Shari’a j. 12, jalada la nne uk. 299, riwaya na. 2268. 1084 - Ibn Batta Al-’Ukbari Al-Inaba ‘Ani Al-Shari’a j. 12, jalada la nne uk. 300, riwaya na. 2272. 1085 - Kwa ufupi ni kuwa riwaya hizi ambazo Ibn Batta anazinukuu kutoka kwa watu wa Hadithi na viongozi wa Kihanbali, ni nyingi mno. Tazama kitabu chake hicho Al-Ibana ‘Ani Al-Shari’a juzuu ya 12 kuanzia ukurasa wa 248 hadi ukurasa wa 314.

345

Page 346: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

hayo, utakuwa umejua kwanini watu hawa wamekuwa wakipenda kukafirisha, kutukana na kufanya chuki na uadui kwa Waislamu wa madhehebu nyengine – vitabu vya Maimamu vimewalea hivyo wa Allahu Al-Musta’aan. Na kwa hivyo, ni wajibu wa Waislamu wote wawajue vyema watu hawa na wawaepuke na kuwaepusha watoto wao kutokana na mafunzo yao mabaya yaliokwenda kinyume kabisa na mafunzo ya Uislamu. Na ni lazima bali ni wajibu kwa Mashekhe hasa hasa wa Ahlu Sunna (Mashafi) washikamane katika kuwajuvya watu uwahabi ni nini na usunni ni nini, kwani si kila anayedai kuwa yeye ni Sunni anakuwa Sunni kweli, vyenginevyo hata Kadiani wanasema kwamba wao ni Sunni. Mawahabi nao – kwa itikadi zao hizo – wametoka nje ya usunni.

HATA ATAYEKIKATAA KITABU CHA IMAMU WA KIWAHABI PIA NI KAFIRI

Mahanbali/Mawahabi si kwamba wamekuwa na riwaya hizo tu kutoka kwa Maimamu wao kuhusu atayesema kuwa Qur-ani ni kiumbe au imeumbwa au atayezipinga itikadi zao nyengine, bali wanaona kuwa kuyakataa au kukikataa kilichomo katika vitabu vyao pia ni sawa na kuikataa Qur-ani! Na kauli hii kwao si bidaa bali ndio Sunna yenyewe! Al-Barbahari, mmoja wa Maimamu Adhimu wa Kiwahabi1086 yeye anakifananisha kitabu chake na Qur-ani na kwamba yoyote atayekipinga chochote kile kilichomo katika kitabu chake basi huyo si Muislamu. Juu ya yote hayo, Mawahabi wanakichapisha kitabu chake hicho kila leo ili kueneza Sunna, jambo ambalo linaonesha kuwa wanaafikiana naye juu ya kauli zake hizo! Anasema Al-Barbahari:

Basi Allah amrehemu mja… atayesoma kitabu hiki na akakieneza na akakifuata na kukilingania na kukitolea hoja, kwani hio ndio dini ya Allah na dini ya Mtume wake; basi hakika ya yule atayehalalisha kitu kinyume na yaliomo katika kitabu hiki, basi yeye haifuati dini ya Allah, na huyo amekikanusha (kitabu) kizima. Kama lau mja aliyaamini yote alioyasema Allah Mtukufu lakini akatia shaka katika herufi moja tu basi huyo ni kafiri.1087

Na anasema:

Atayeyakubali yaliomo katika kitabu hiki na kuyaamini na akakifanya (kitabu hiki) kuwa ndio Imamu wake na asiitilie shaka hata herufi moja katika hicho wala asiikanushe hata herufi moja, basi huyo ni mtu wa Sunna

1086 - Mawahabi wanamwita Imamu wa Ahli Sunna katika zama zake! 1087 -Al-Barbahari Sharhu Al-Sunna uk. 100-101.

346

Page 347: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

na Jama’a, kakamilika na Sunna imekamilika kwake; na atayeikanusha herufi moja katika kitabu hiki au akatia shaka au akasimama (asipinge wala asikiri) basi huyo ni mtu wa matamanio ya nafsi.1088

Tazama mtu huyu alivyoghururika! Anakifananisha kitabu chake kilichojaa uzushi na bidaa na Hadithi za kutunga1089 na Kitabu cha Allah ambacho hakina shaka wala hakiingii batili. Hayo ndio alioyasema, lakini je kitabu chake hicho kina nini? Anasema:

a) “Na (Allah) kakaa juu ya ‘Arshi.”1090 Sasa ni Waislamu wangapi wenye kuamini hivi na ni Waislamu wangapi ambao hawaamini. Wote hawa hawana dini: ni mapagani!

b) “Mbora katika Umma huu baada ya kufa Mtume wake ni Abu Bakr na ‘Umar na ‘Uthman……kisha baada ya hawa ni ‘Ali na Talha na Zubair”.1091 Ninasema: tatizo ni kuwa miongoni mwa Masahaba (r.a.) wako waliokuwa wakimfanya Ali kuwa ndio bora kuliko hao aliowafadhilisha yeye. Je Masahaba hao hawana dini: ni makafiri? Akisema “ndio” atabomoa msingi wake kwamba “Masahaba wote ni waadilifu”; akisema “Sio” atabomoa msingi wake kwamba “Kila kilichomo katika kitabu chake ni sahihi na ni haki tupu”.

c) “Atayetoka dhidi ya Imamu miongoni mwa Maimamu wa Waislamu basi huyo ni Khawarij, na amevunja nguvu za Waislamu na kenda kinyume na athari (Hadithi) na kifo chake ni kifo cha ujahili………..Haifai kumpiga vita mtawala hata akifanya dhulma…”.1092 Suala: vipi kuhusu Talha na Zubair waliompiga vita Ali, Khalifa wa Waislamu? Si ndio hawa ambao kasema kuwa ni katika watu bora? Sasa ubora umetoka wapi nao ni Makhawarij kwa mujibu wa maelezo yake? Na vipi kuhusu Mu’awiya aliyempiga vita ‘Ali na kumuasi? Na kwa leo vipi kuhusu

1088 - K.h.j. uk. 125. 1089 - Kwa mfano Hadithi kama “Masahaba wangu ni kama nyota: yoyote mutayemfuata mutaongoka”. Nayo ni Hadithi dhaifu sana bali maudhui (ya kutunga). Anasema Al-Bazzaar: “Maneno haya hayakuthibiti kutoka kwa Mtume s.a.w.”. Anasema Ibn Hazm: “Ni ya uwongo, ya kutunga, batili”. Anasema Al-Bayhaqi: “Matn yake ni mashuhuri, na sanad zake ni dhaifu: haikuthibiti sanad yoyote katika hili”. Anasema Ibn Kathir: “……Nayo ni dhaifu”. Na akaidhoofisha Al-’Iraqi, Ibn Hajar na Al-Albani. Rejea maelezo ya Khalid Al-Raddadi katika Sharhu Al-Sunna cha Al-Barbahari uk. 69. Sasa baada ya hayo, je bado atayeikanusha herufi moja ya yale yaliomo katika kitabu chake ni mtu wa bida’a, hana dini! Tunasema: hio kauli yake yenyewe ndio bida’a. 1090 - K.h.j., uk. 64. 1091 - K.h.j., uk. 68. 1092 - K.h.j., uk. 70.

347

Page 348: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Muhammad Abdul-Wahhab aliyewavamia na kuwaua Waislamu tafauti bila haki.

d) “Allah anateremka katika mbingu ya kwanza…na anateremka siku ya arafa…na siku ya kiama…na jahannam haiachi kutupwa (watu) humo mpaka (Allah) atatia mguu wake….Allah kamuumba Adam kwa sura yake….Kauli ya Mtume (s.a.w.) aliposema: nimemuona Allah katika sura nzuri..”.1093 Tunauliza: Je ni Waislamu wangapi tangu zamani hadi leo wenye kukubaliana na itikadi hizi?

e) “Atayesema kuwa matamshi yangu (ninaposoma) Qur-ani, ni yenye kuumbwa, basi huyo ni mtu wa bidaa; na atayenyamaza asisema kuwa ni kiumbe au si kiumbe basi huyo ni Jahmiy. Vivyo hivyo kasema Ahmad bin Hanbal”.1094 Ninasema: Lakini Al-Bukhari, Al-Karabisi, Imamu mkubwa wa Mashafi na wengine wengi, kama tulivyosema kabla, wanasema hivyo kwamba mtu anaposoma Qur-ani basi ile lafdhi yake ni kiumbe. Sasa hawa wote ni Ahlul bidaa, kisha munapokea Hadithi zao na kuzikubali kuwa ndio sahihi baada ya Qur-ani?

f) “Sala tano zinafaa kusaliwa nyuma ya utayesali naye, isipokuwa awe jahmi kwani yeye ni mu’attil”.1095 Ninasema: kwa hivyo, haifai kusali nyuma ya Shafi, Hanafi, Maliki kwani hawa wote ni mu’attila!

Hivyo ndivyo, kinavyotongoa kitabu cha Al-Barbahari ambacho anasema kuwa atayekipinga kitabu hicho basi huyo hana dini na ni mtu wa matamanio. Jamani! Kauli hio yenyewe si bidaa katika dini? Huyu ni mtu Adhim na ni nembo ya Sunna ya Kiwahabi!

BAADHI YA MTU MMOJA MMOJA WALIOKAFIRISHWA NA VIONGOZI WA KIWAHABI ZAMANI NA LEO

Hayo tulioyanukuu kabla ni baadhi tu ya mambo yaliosemwa na viongozi wa Kihanbali pamoja na wafuasi wao wa Kiwahabi kuhusu kuwakafirisha watu kwa ujumla. Ama mifano michache ya namna gani waliwakafirisha mtu mmoja mmoja ni riwaya kama:

1) Nilimwambia Ahmad bin Hanbal: ‘Je mtu anapata ujira kwa kumchukia Abu Hanifa? Akasema “Ndio Wallahi”.1096 Nayo ni

1093 - K.h.j., uk. 74-75. 1094 - K.h.j., uk. 92. 1095 - K.h.j., uk. 104. 1096 - Ibn Ahmad Al-Sunna j. 1, uk. 180, riwaya na. 228.

348

Page 349: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

riwaya dhaifu. Likini pamoja na hayo Sufyaan Al-Thauri ilipomfikia kwamba Abu Hanifa kafa alisema:

Al-Hamdu Li-Lahi! Alikuwa (Abu Hanifa) akiubomoa Uislamu kifungo kimoja kimoja (kidogo kidogo); katika Uislamu hajazaliwa mtu nuhusi kama yeye (Abu Hanifa).1097

2) Ananukuliwa Ahmad bin Hanbal akisema: “Al-Husain Al-Karabisi, (mwanachuoni wa Kishafi) kwetu sisi ni kafiri”.1098

3) Anasema ‘Uthman Al-Darimi, Imamu wa Ibn Taymiyya na Mawahabi kwa ujumla, kwamba Bishr Al-Marisi ni kafiri. Anamwambia hivi: “……Ewe Marisi, kwa hakika umekusanya ujinga na ukafiri…..ama ukafiri wako ni……. 1099

4) Al-Tirmidhi. Al-Tirmidhi ni mmoja katika wapokezi sita wa Hadithi wenye kuaminika sana. Lakini Al-Khallal, Imamu mtangulizi wa Kiwahabi, kanukuu riwaya nyingi sana katika kitabu chake alichokiita Al-Sunna zenye kumponda na nyengine kumkafirisha. Tutazinukuu baadhi ya riwaya hizo katika sehemu inayofuata.

5) Ibn Taymiyya kawakafirisha:c) Al-Imamu Al-Ghazali .d) Al-Fakhru Al-Razi.e) Abu Bakr bin Fuurak.f) Abu Al-Wafaa bin ‘Aqi.g) Abu ‘Ali Al-Jubbaai. h) ‘Abdul-Jabbar bin Ahmad Al-Hamdani.i) Abu Al-Husain Al-Busri.1100

1097 - Al-Bukhari Al-Taarikh Al-Saghir j. 2, uk. 93. 1098 - Ibn Abi Ya’alaa Tabaqaatu Al-Hanaabila j. 1, uk. 172. 1099 - ‘Uthman Al-Darimi K.h.j. j. 1, uk. 42. Maneno kamili ya Al-Darimi tumeyanukuu katika sura inayofuata. 1100 - Ibn Taymiyya Majmu’a Al-Fatawa j. 5, uk. 19-20. Tazama maelezo yake vizuri usije ukasema “Aaa yeye hakuwaita makafiri”. Ninasema: alichokisema hapa ni kuwa watu hawa wana itikadi sawa na ile ya Bishr Al-Marisi Al-Hanafi. Kisha akasema katika uk. 20: “Basi ikiwa Maimamu wa uongofu wamekubaliana juu ya kuwatia lawamani Al-Marisiyya (wafuasi wa Bishr Al-Marisi) na wengi wao wamewakafirisha hao au wamewaita wapotovu; na itapojulikana kwamba kauli hii (ya kuwa wao ni makafiri au wapotovu) yenye kwenda miongoni mwa hawa waliokuja baadae (akina Al-Ghazali na wenzake) ndio madhehebu ya Al-Marisi, basi uongofu umebainika kwa yule Allah anayetaka kumuongoa.” Kwa hivyo, Bishr Al-Marisi ni kafiri kwa sababu ya itikadi yake; na hawa nao wamechukua itikadi ya Al-Marisi, kwa hivyo hukumu yao ni kama yake – wote ni makafiri.

349

Page 350: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

6) Anasema Abu Abdillahi: “Na nimemsikia Abu ‘Abdil-Wahhab akisema: “Wafuasi wa Jahm ni makafiri, mazindiki (wanafiki) washirikina. Kasema Sheikh: ‘Fahamuni yale yaliokuja katika riwaya na tulioyapokea kutoka kwa watangulizi wema (Al-Salafu Al-Salih)………..na (fahamuni) uovu wa wale waliojitenga nao (hao Al-Salafu Al-Salih) na wakamfuata Jahm (bin Saf-waan) aliyelaniwa pamoja na wafuasi wake; mfano kama:

i. Dhirar.ii. Abu Bakr Al-Asam.

iii. Bishr Al-Marisi.iv. Ibn Abi Duaad. v. Al-Karabisi. (Huyu ni Imamu mkubwa wa Kishafi).1101

vi. Shu’aib Al-Hajjam.vii. Burghuth.

viii. Al-Nadham.ix. Na walio mfano wa hao miongoni mwa viongozi wa

ukafiri na maimamu wa upotovu ambao wameikanusha Qur-ani na Sunna na wakakikataa kitabu cha Allah na Sunna za Mtume wa Allah, na wakavikufuru kwa uwazi na kwa kukusudia na kwa kufanya inda na hasadi na kwa dhulma na ukafiri!!!1102

Ni wazi kwamba Imamu huyu wa Kihanbali/Kiwahabi, si kwamba kawakafirisha Waislamu kwa ujumla tu, bali pia kawakafirisha Maimamu hawa mmoja mmoja.!

KUWAFANYIA UADUI MAIMAMU WAKUBWA

Jambo jengine baya ambalo halikubaliki katika Sharia yetu Tukufu, ni ile tabia ya wafuasi wa Kihanbali/Kiwahabi kuwafanyia uadui watu wa madhehebu nyengine ambao hawakubaliani nao katika rai. Hali inakuwa yenye kuchukiza zaidi ikiwa uadui huo wanafanyiwa wanavyuoni wa Kiislamu. Sitaki hapa kupekuwa sana ili niweze kukusanyia idadi kubwa ya wanavyuoni wakubwa wa Umma huu waliofanyiwa uadui na watu hao, bali nitakutajia mifano miwili1103 mitatu tu:

1101 - Tazama pia yalionukuliwa kutoka kwa Al-Imamu Ahmad bin Hanbal kuhusu Imamu huyu wa Kishafi. Tazama Al-Sunna cha Ibn Ahmad j. 1, uk. 165-166, riwaya na. 186-188. 1102 - Ibn Batta Al-’Ukbari Al-Ibana j. 12, jalada la nne, uk. 314. 1103 - Haya katika vitabu utayakuta kwa wingi. Na lau nilijua kwamba kuna siku nitayahitaji basi ningeweza kukusanyia mifano mingi mmo ilioandikwa juu ya tabia hii mbaya ya watu hawa.

350

Page 351: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

1) Imamu wa Ulimwengu, Muhammad bin Isma’il Al-Bukhari mwenye kitabu Sahihu Al-Bukhari. Imamu huyu alipata madhila makubwa kwa sababu ya itikadi yake kwamba matamshi ya mtu anaposoma Qur-ani ni kiumbe. Alipata tabu na madhila makubwa na kufukuzwa katika mji huu na ule. Na aghlabu ya waliokuwa wakiwatesa watu kwa itikadi hio ni watu wa Madhehebu ya Hanbali ambao ndio watangulizi wa Mawahabi. Basi wakamuhajiri Al-Bukhari na wakawa wanamwambia: “Ukiwacha kauli yako hii basi tutarejea kwako”, na hayo ni baada ya kumzingira nyumbani kwake na kumfukuza kila anayetaka kwenda kwa Al-Bukhari. Na wengine wakamkafirisha Al-Bukhari, akasema mmoja wao: “Al-Bukhari kaidhihirisha kauli ya Al-Lafdhiyya1104 na Al-Lafdhiyya kwangu mimi ni waovu kuliko Al-Jahmiyya”.1105 Huku ni kumkafirisha Al-Bukhari kwani Al-Jahmiyya kwa mujibu wa Mahanbali na Warithi wao (Mawahabi) ni makafiri. Sasa ikiwa Al-Bukhari ni muovu kuliko kafiri sijui yeye atakuwa nani? Bali wengine walimwita Al-Bukhari kuwa ni kafiri kinagaubaga!1106 Ama Abu Hatim Al-Razi na Abu Zur’a, nao ni Mahanbal, wao waliziwacha Hadithi za Al-Bukhari kwa sababu ya itikadi yake hio.1107 Kwa ufupi, ni kuwa tabu na uadui uliompata Al-Bukhari kwa itikadi yake hio ni mkubwa, kwa maelezo zaidi rejea Siyaru Al-I’ilam cha Al-Dhahabi.1108

2) Imamu Al-Mufassirin, Ibn Jarir Al-Tabari. Mahanbali walikuwa wanawazuia watu wasiingie kwa Imamu huyu.1109 Na kwa hivyo, Ibn Khuzaima anasema: “Simjui yoyote aliye juu ya ardhi hii mjuzi kuliko Ibn Jarir, na Mahanbali wamemdhulumu”.1110 Anasema Al-Dhahabi: “Na baina ya Ibn Jarir na Ibn Abi Dawud paliingia (uadui), na kila mmoja hakumfanyia mwenzake insaaf; na Mahanbali walikuwa ni kundi la Ibn Abi Dawud basi wakawa wengi na wakamfanyia Ibn Jarir fitna na ikampata adha. Basi akabakia nyumbani kwake (akawa hatoki). Allah atulinde na matamanio ya nafsi.1111

3) Ibn Hibbaan. Huyu ni Muhammad bin Hibbaan mwenye kitabu Sahihu Ibn Hibbaan. Ni mmoja katika Maimamu wakubwa wa

1104 - Wenye kusema kuwa matamshi yetu tunaposoma Qur-ani ni kiumbe. 1105 - Al-Dhahabi Al-Siyar 10, uk. 314 tarjama na. 2136. 1106 - Al-Dhahabi Al-Siyar j. 10, uk. 315. Naye akawajibu kwamba Mtume kasema: “Atayemwita nduguye ewe kafiri, basi mmoja wao kastahiki ukafiri”. 1107 - Ibn Abi Hatim Al-Jarhu wa Al-Ta’adil j. 7, uk. 191, tarjama na. 1087. Al-Dhahabi Al-Siyar 10, uk. 316 tarjama na. 2136. 1108 - J. 10, uk. 277-312, tarjama na. 2136. 1109 - Al-Dhahabi Tadhkiratu Al-Huffadh j. 2, uk. 712, tarjama na. 728. 1110 - K.h.j. 1111 - Al-Dhahabi Al-Siyar j. 11, uk. 297, tarjama na. 2696.

351

Page 352: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Hadithi, fiq-hi, lugha ya Kiarabu na mengineo. Lakini kwa kuwa alikuwa na itikadi ya tanzih (kumtakasa Allah) basi hilo lilimchongea sana. Kosa lake ni kusema kuwa Allah hana mpaka. Basi wale wenye itikadi kama ya Ibn Taymiyya kwamba Allah ana mpaka wakamfukuza katika mji wa Sijistaan na wakasema kwamba Ibn Hibbaan ana elimu kubwa lakini dini kidogo. Anasema Abu Ismail Al-Harawi: “Nilimuuliza Yah-ya bin ‘Ammaar kuhusu yeye (kuhusu Ibn Hibbaan) akasema: ‘Sisi tumemfukuza Sijistaan, alikuwa na elimu wala hakuwa na dini kubwa; alikuja kwetu akakanusha kuwa Allah ana mpaka”.1112 Lakini je unajua kwanini hili likawakera? Sababu ni kuwa watangulizi hao wa Mawahabi wanasema kuwa Allah yuko juu kakaa kitako juu ya Arshi. Sasa madamu Arshi ni kiumbe basi itakuwa ina mwisho (mipaka). Na kama ni hivyo, basi Allah, madamu yuko juu ya Arshi kakaa kitako Naye atakuwa ana mipaka! Jamani hii ndio Sunna! Tazama watu walivyomfanya Allah kuwa ni kiwiliwili chenye mipaka kisha wanakereka wakiitwa Mujassima! Kama hii si tajsim basi duniani hakuna tena kitu tajsim!

4) Al-Tirmidhi mwenye kitabu cha Sunan Al-Tirmidhi. Huyu – kama tulivyoashiria kabla – Maimamu watangulizi wa Kiwahabi wamemkafirisha kwa sababu ya kuikanusha kwake riwaya ilionasibishwa na Mujahid pamoja na ‘Abdullahi bin Salam – Yahudi aliyesilimu na kueneza fikra za Kiyahudi katika Uislamu.1113

Riwaya yenyewe alioikanusha Al-Tirmidhi ni ule uwongo wa Kiyahudi, uliopandikizwa na Ibn ‘Abdi Salam na wenzake, unaosema kwamba siku ya kiama ikifika: “Allah atamueka Mtume wake (s.a.w.) kitako pamoja naye katika ‘Arshi”!1114 Yaani ‘Arshi italetwa siku ya kiama, kisha Allah atakaa kitako kisha baada ya Allah kukaa kitako juu ya Arshi yake basi pembeni kutabakia nafasi kidogo ambayo ataikalia Mtume! Subhana Allahi! Huu ni ujuha gani huu? Basi Maimamu wa kiwahabi wanatwambia kwamba atayeukanusha uzushi huu huyo ni zindiki (mnafiki). Na kwa hivyo, Al-Tirmidhi alipoukataa uzushi huo basi alikafirishwa. Anasema Al-Nnajjad:

1112 - Al-Dhahabi Tadhkiratu Al-Huffadh j. 3, uk. 921, tarjama na. 879. 1113 - Fikra hizo za kina Ibn Salam na wenzake ndio chimbuko la itikadi ya tajsim ambayo Mawahabi leo wanaikumbatia na kuitetea kwa hali na mali na kuipamba kwa kuiita itakadi ya Al-Salafu Al-Salih. 1114 - Riwaya hii kaisimulia Al-Khallaal katika kitabu chake alichokiita Sunna kwa sanad nyingi za wasimulizi wa mujassima wa Kihanbal. Tazama juzuu ya kwanza katika maelezo ya Aya: محمودا مقاما ربك يبعثك أن عسى

352

Page 353: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

فض رد الذي الترمذي أمر السلمي إسماعيل أبو لنا النبي -������وذكر يلةعل الله يه����������صلى

: . – م���������وسل الحساب بيوم يؤمن ال وقال أمره وصغر

Na ametutajia Abu Ismaa’iil Al-Sulami habari ya Al-Tirmidhi ambaye kaipinga fadhila (hii) ya Mtume (s.a.w. ya kukaa juu ya Arshi pamoja na Mola wake) na kulidharau jambo lake na akasema: “(Huyo Al-Tirmidhi) haamini siku ya hesabu” 1115 (Haamini kwamba kuna akhera).1116

Ama Al-Khallaal, yeye amesimulia kutoka kwa baadhi yao kwamba atayeipinga Hadithi hio basi huyo ni kafiri.1117 Na akamnukuu ‘Ali bin Dawud akisema kuhusu Al-Tirmidhi kwamba yeye (Al-Tirmidhi) ni mtu wa bidaa na ni Jahmi mchafu! 1118

Anasema Al-Sayyid Al-Saqqaaf katika Al-Salafiyya Al-Wahabiyya:

Na akasema Ibn Kathir katika Taarikh yake kwamba Mahanbali waliwashuhudia1119 watu wengi kuwa wamefanya maovu mwaka 323 katika zama za Al-Barbahari, na walikuwa wakijisaidia kwa watu vipofu katika kuwapiga wapinzani wao misikitini. Na akasema Ibn Al-Athir katika matukio ya mwaka 567 kwamba (Mahanbali) walimtilia sumu Mwanachuoni wa Kishafi aitwaye Al-Buri, basi akapigwa na tumbo la kuendesha mpaka akafa kutokana na haluwa (yenye sumu) ambayo alipewa na Mahanbali naye alikuwa akiwalaumu.

Halkadhalika alikufa Al-Imamu Abu Bakr bin Fuurak kwa sumu aliotiliwa na Al-Karraamiyya nao walikuwa na uhusiano mkubwa na Mahanbali mwaka 546.1120

Baada ya nukulu hizo mbili tatu ndugu msomaji kuhusu mwenendo wa watangulizi wa Mawahabi, basi sina budi kusema kwamba kama

1115 - Kwa hivyo, ni kafiri! Au Bwana Kasim utaniambia wapi kasema kuwa yeye ni kafiri bila ya Ta-awil? Ninakwambia tena kwamba ta-awil ikiwa sahihi, basi inakubalika. Asiyeamini siku ya mwisho au kukanusha nguzo moja ya Uislamu au ya imani huyo ni kafiri. Imamu wenu anasema Al-Tirmidhi haamini siku ya kiama! Je bado atakuwa Muislamu?! Bali tunasema kwamba riwaya nyengine za Al-Khallaal zimenena kinagaubaga kwamba atayeikataa riwaya hio ni: mtu wa bidaa, mpotovu, kafiri n.k.1116 - Tabaqaatu Al-Hanabia j. 2, uk. 9. 1117 - Tazama Al-Khallaal Al-Sunna j. 1, uk. 215, riwaya na. 246-247. 1118 - K.h.j. j. 1, uk. 233, riwaya na. 269. 1119 - Yaani ushahidi wa uwongo. 1120 - Anasema Al-Sayyid Al-Saqqaaf: “paragraph hii nimeinukuu kutoka katika kitabu Qira-atun Fii Kutubi Al-‘Aqaaid: Al-Madh-habu Al-Hanbali Namudhajan. Tazama Al-Saqqaaf Al-Salafiyya Al-Wahaabiyya uk. 112.

353

Page 354: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

umeyaelewa hayo, basi utakuwa umeelewa kwamba kawaida hii mbaya yenye kulaumiwa Kiislamu ambayo imetendwa na Maimamu na watangulizi wa Kiwahabi, hadi leo hii inaendelea. Mashekhe wangapi wa leo wanatukanwa na kupigwa na kudhalilishwa na Mawahabi. Na Waislamu wangapi wanauliwa na Mawahabi! Hakuna nchi yoyote iliofika madhehebu hio ila huingia fitna kubwa hadi kufikia kupoteza roho za watu! Sijui huu ndio Uislamu gani na hii ndio Sunna gani!

Anasema Al-Akh Sheikh Khalfan Al-Tiwani katika Ansaru Al-Sunna Tahta Al-Mijhar:

Amesema Muqbil Al-Waadi’iy maneno mabaya kuhusu viongozi wakuu wa Al-Ashaa’ira kama vile Al-Hakim, Al-Nawawi na Ibn Hajar Al-‘Asqalani. Alipoulizwa kuhusu wao: ‘Je tuwaite watu wa bidaa?’ Akasema kwa mkato: ‘Atayewaita kuwa ni watu wa bidaa hatumpingi, lakini mimi najiepusha kuwaita watu wa bidaa.1121

Na (Muqbil Al-Waadi’iy) akasema kuhusu Al-Sheikh Dr. Al-Qaradhawi:

Yusuf Al-Qaradhawi tangu tulipomjua na kumsikia, naye ni mtu wa kupenda migawanyiko, mtu wa bidaa, na kama ilivyotangulia kwamba yeye anazikata suna za Mtume (s.a.w.) vipande vipande. Basi yeye anazingatiwa kuwa ni mpotovu mtu wa bidaa….mimi siusii kusikiliza kaseti zake wala kuhudhuria mihadhara yake wala kusoma vitabu vyake, (yeye ni) mwehu mwehu!1122

Ama Abu Ghudda, yeye mmoja wa Mawahabi alimtemea mate. Mashaa Allah! Suna ya Mtume hio jamani! Ama kweli nyinyi ni Ahlu Al-Sunna Wal Jamaa! Mtu akipotea husimamishiwa hoja: sio kutemewa mate. Sasa ukimtemea mate ndio tayari wewe umekuwa katika haki na ndio tayari umeshamsimamishia hoja! Kwa kweli hii ni alama ya waliofilisika kihoja.

KUWAKIMBIZA WAFUASI WAO WASIITAFUTE HAKI

Tatizo jengine la Mawahabi pamoja na Maimamu wao waasisi, ni kuwakimbiza wafuasi wao ili wasizijue hoja za wengine. Na kwa sababu hii, utawakuta watu hawa daima wana mawazo finyu: hawajui wengine wana hoja gani wala hawataki kujua kamwe, kwani wanahofia haki ikaja ikawapambanukia ikabidi kuporomoka kwa itikadi zao batili. Na haya hata kwetu Zanzibar tunayashuhudia ambapo tunaona kwamba watu hawa

1121 - Al-Ajwiba Al-Sadida Fii Fatawa Al-‘Aqida uk. 166, nukulu kutoka kwa Al-Tiwani, Khalfaan bin Sulaiman (‘Abdullah) Ansaru Al-Sunna uk. 25. 1122 - K.h.j. uk. 170. Tazama Al-Tiwani, Khalfaan (‘Abdullah) K.h.j.

354

Page 355: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

mambo yao ni peke yao peke yao tu! Si rahisi kumkuta Sheikh wa kikundi hiki kenda msikiti mwengine kutoa mawaidha au hata kusali: kama itatokea basi ni nadra sana. Inasemekana hata wanafunzi wao hawatakiwi waende kusoma kwa mashekhe wengine.

Sababu ya kuwa na msimamo huu, inarejea katika yale yale tulioyanukuu kutoka kwa viongozi wao wakuu ya kuwakafirisha Waislamu wengine na kuwaita kuwa ni watu wa bidaa. Ama njia zilizotumika katika kuwaepusha wafuasi wao na fikra zilizoko katika madhehebu nyengine ni zile njia za kisaikolojia za kuwatia kasumba mbaya kwamba ni bora mlevi fasiki wa Kiwahabi au wa Kihanbali kuliko mtu mcha Mungu wa madhehebu nyengine. Mafunzo kama haya ndio yaliowalea watu hawa katika tashaddud hizi na wakawa wao ni maarufu kwa kukafirisha na kutukana. Anasema Al-Barbahari:

Ukimuona mtu katika Ahlu Al-Sunna1123 ana mwenendo mbaya, fasiki, muovu, mtu wa maasi mpotovu lakini anafuata Sunna, basi fuatana naye na kaa pamoja naye kwani maasi yake hayakudhuru kitu. Na ukimuona mtu anajitahidi katika ibada, hana haja ya dunia, anaabudu sana, lakini ni mtu wa matamanio ya nafsi basi usikae naye wala usisikilize maneno yake wala usifuatane naye njiani, kwani nahofia ukaja ukaipenda njia yake ukaangamia pamoja naye.1124

Kisha baada ya mafunzo hayo, Al-Barbahari akasema:

Yunus bin ‘Ubaid alimuona mwanawe katoka kwa mtu wa matamanio ya nafsi yake,1125 akasema: ‘E mwanangu! Unatoka wapi? Akasema: ‘Natoka kwa fulani’. Akasema: ‘E mwanangu! Bora nikuone unatoka nyumbani kwa khuntha kuliko kukuona unatoka nyumbani kwa fulani. Na kukutana na Mwenyezi Mungu nawe ni mzinifu, fasiki, mwizi ni bora kwangu kuliko kukutana naye na kauli ya fulani na fulani.1126

Na wasia huo ndio uliotekelezwa na Muqbil Al-Waadi’iy aliposema:

Yusuf Al-Qaradhawi tangu tulipomjua na kumsikia, naye ni mtu wa kupenda migawanyiko, mtu wa bidaa, na kama ilivyotangulia kwamba yeye anazikata suna za Mtume (s.a.w.) vipande vipande. Basi yeye anazingatiwa kuwa ni mpotovu mtu wa bidaa….mimi siusii kusikiliza

1123 - Ahlu Sunna anaokusudia yeye si wale Mashafi, Maliki, Mahanafi na baadhi ya Hanbali; bali ni wale wasemao kuwa Mungu ana mkono, mguu, n.k. 1124 - Al-Barbahari Al-Sunna uk. 114-115. 1125 - Mtu wa matamanio yaani ni yule asiyekubali kuwa Allah ana viungo!1126 - Al-Barbahari Al-Sunna uk. 115-116.

355

Page 356: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kaseti zake wala kuhudhuria mihadhara yake wala kusoma vitabu vyake, (yeye ni) mwehu mwehu!1127

MUKHTASARI

Tulichojaribu kukieleza katika sura hii, ni hii tabia mbaya ya Mawahabi na Maimamu wao ya kuwatukana na kuwakafirisha Waislamu. Jambo hili ni kinyume kabisa na mafunzo ya Qur-ani na Sunna. Qur-ani imetufunza kwamba:

هي بالتي وجادلهم الحسنة والموعظة بالحكمة ربك سبيل إلى ادعأحسن

Lingania katika njia ya Mola wako kwa hekima na mawaidha mema na jadiliana nao kwa wema.1128

Na Mtume (s.a.w.) anasema:

وفى بالكفر باء فقد وإال ، قال كما كان فإن رجال كفر رجل أيماوج�����ب كافر يا ألخيه قال اذا أحدهما رواية على وفي …الكفر

ولي رواية: ... الله عدو قال أو بالكفر رجال دعا إال �������ومن كذلك سكفر: …….عليه حار وقتاله فسوق المسلم سباب وقال

Mtu yoyote atayemwita mwenzake kafiri basi akiwa kafiri kama alivyosema (hilo ni sawa) vyenginevyo, basi yeye ndiye aliyestahiki ukafiri…na katika riwaya nyengine “Mtu akimwambia nduguye ewe kafiri, basi mmoja wao kawajibikiwa na ukafiri”. …….na katika riwaya nyengine: ‘Atayemwita mtu kafiri au adui wa Allah naye hayuko hivyo, basi (kukafirisha huko) kunamrudia mwenyewe……..na akasema Mtume (s.a.w.): “kumtukana Muislamu ni ufasiki na kumpiga ni ukafiri”.1129

Ni wazi kwamba wale wajiitao Ahlu Sunna (Mawahabi), bado Qur-ani na Sunna hawajaitekeleza kwani – kama mulivyoona – wao ndio walioshika bendera ya kuwakafirisha na kuwatukana Waislamu. Allah awasaidie wao na sisi katika kukitekeleza Kitabu chake na Sunna za Mtume wake.

1127 - Al-Ajwiba Al-Sadida Fii Fatawa Al-‘Aqida uk. 170. Tazama Al-Tiwani, Sh. Khalfaan (‘Abdullah) bin Sulaiman Ansaru Al-Sunna uk. 25..

1128 - Sura 16, Aya 125. 1129 - Hadithi hizi zimepokewa na wapokezi wengi.

356

Page 357: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

SURA YA KUMIKUJIGONGA

Ikiwa binaadamu yoyote yule hujigonga baadhi ya wakati ikiwa kama ni natija ya udhaifu wa kibinaadamu, jambo ambalo ni lazima lisameheke

357

Page 358: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

ikiwa kujigonga huko ni katika furu’u (matawi) za kitu, basi elewa kwamba kujigonga huko hakuwezi kusameheka kukiwa ni kujigonga katika misingi ya jambo. Hayo yote ikiwa kujigonga huko ni kijigonga kidogo yaani ikiwa ni jambo adimu linalojitokeza baadhi ya nyakati, basi vipi ikiwa ni kijigonga sana na kulikokithiri kila wakati na ikawa ni kujigonga katika misingi ya jambo? Je hio haitokuwa alama ya batili alioshikana nayo yule mwenye kujigonga.

Madhehebu ya Hanbali/Wahabi ni mashuhuri sana kwa kujigonga katika mambo muhimu. Wamejigonga katika misingi, na natija ikawa ni kujigonga katika furu’u (matawi). Mifano michache inayofuata itakupa picha ya wazi ya maudhi hii.

MOSI: HADITHI AHADI

Je Hadithi Ahadi itumike katika itikadi au itumike katika matendo tu? Jumhur inasema kwamba Hadithi Ahadi haitumiki ila katika matendo.1130 Mawahabi – na wachache wengine – wanasema kwamba Hadithi Ahadi inatumika katika itikadi pia.1131 Lakini tazama wanavyogongana na Imamu wao mkuu Ibn Taymiyya bali na Al-Imamu Ahmad. Ama Ibn Taymiyya baada ya kuipinga Hadithi isemayo: “Allah alikuwepo wala hapakuwa na kitu chengine….wala hapakuwa na kitu pamoja naye”. Anasema:

ذكر فيما نصا كان لو الحديث وهذا الله، كتاب في ليس اللفظ فهذامتواترا هو فليس

1130 - Al-Imamu Abu Is-haaq Al-Shirazi Al-Luma’a uk. 154. Al-Imamu Hujjatul Islam Al-Ghazali Al-Mustasfaa uk. 116. Al-Imamu Badru Al-Din Al-Khalili Al-Haqqu Al-Damigh uk. 57 chapa Darul Hikma London 2008. Al-Imamu Al-Qannubi Al-Saifu Al-Haad uk. 7. Na akawanukuu Imamu Al-Sunna wal Usuli wal Furu’i Al-Hujja Al-Qannubi katika kitabu chake hicho Al-Saifu Al-Haad uk. Huo huo, idadi kubwa ya wanavyuoni wenye kauli hii kama: Al-Nawawi katika utangulizi wake wa Sharhu Sahihi Muslim na katika Al-Irshaad na katika Al-Taqrib; Imamu Al-Haramain katika Al-Burhaan; Al-Sa’ad katika Al-Talwih; Al-Ghazali katika Al-Mustasfaa; Ibn ‘Abdil-Barr katika Al-Tamhid; Ibn Al-Athir katika utangulizi wa Jami’u Al-Usul; Safiy Al-Din Al-Baghdadi Al-Hanbali katika Qawaa’idu Al-Usul; Ibn Qudama Al-Hanbali katika Raudhatu Al-Nadhir; ‘Abdul-‘Aziz Al-Bukhari katika Kashfu Al-Asraar; Ibn Al-Subki katika Jam’u Al-Jawami’i; Al-Mahdi katika Sharhu Al-Mi’iyaar; Al-San’aani katika Ijaabatu Al-Sail; Ibn ‘Abdil-Shakur katika Muslim Al-Thubut; Al-Shanqiti katika Maraqi Al-Sa’uud na wengine. Nayo ndio kauli ya Al-Imamu Malik na Al-Imamu Ahmad. 1131 - Rejea kitabu Qudumu Kataaibi Al-Jihaad cha ‘Abdul-‘Aziz Al-Rajihi, Sheikh wa Kiwahabi. Kitabu hicho kakitunga ili kujibu kitabu Al-Saifu Al-Haad cha Imamu Al-Sunna wa Al-Usul wa Al-Furu’i Al-Hujja Al-Qannubi. Naye akajibiwa kwa kitabu kiitwacho Al-Tufaan Al-Jaarif, mpaka leo kaufyata: hakuibuka tena.

358

Page 359: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

“Na lafdhi hii haimo katika Qur-ani; na Hadithi hii hata lau ilikuwa ni andiko la wazi katika kile kilichotajwa, basi si mutawatir..”.1132

Hapa utaona kwamba Ibn Taymiyya kazikataa lafdhi mbili za Hadithi hio kwa hoja mbili:

a) Lafdhi hizo hazimo katika Qur-ani; wakati lafdhi alioisema yeye kuwa ndio sahihi ni kwa sababu imo katika Qur-ani.

b) Hadithi hizo si mutawatir.Ninasema: Hoja hizi hizi wakizitoa watu wengine kuikataa riwaya basi, Mawahabi huwazingatia watu hao kuwa wameikanusha Sunna ya Mtume (s.a.w.) na watu hao wanaitwa “Mazindiki” (wanafiki). Nayo ndio moja ya hoja ambazo Ibadhi wamezitumia kuikataa Hadithi ya Suhaib kuhusu kuonekana kwa Allah. Lakini Maibadhi ni wapotovu; Ibn Taymiyya ni Salafiy, Ahlu Sunna! Natuendelee na nukulu za Ibn Taymiyya. Anasema kuhusu Hadithi zinazosimulia kuja kwa Al-Mahdi Al-Muntadhar:

ال الذي الدين أصل به يثبت فكيف األحآد أخبار من هذا أن الثانيبه إال اإليمان يصح

“Pili ni kuwa hii ni katika Habari Ahadi basi vipi utathibiti kwayo msingi wa dini (itikadi) ambao imani haisihi ila kwa huo”.1133

Hayo ndio maneno ya Ibn Taymiyya. Wakati yeye anena hivyo, basi mmoja wa wafuasi wake, Abdul-‘Aziz Al-Rajhi, hivi karibuni kaandika kitabu kuwaita wenye kuikataa Hadith Ahadi katika mambo ya itikadi kuwa ni mazindiki (wanafiki) na wapotovu. Al-Hamdu Lillah! Na Sheikh Al-Islam naye yumo katika uzindiki na upotovu!

Ama Al-Imamu Ahmad – ambaye Mawahabi wanajinasibisha naye – yeye kanukuliwa na Ibn Abi Ya’ala akisema:

Ama Khabaru Ahadi (Hadith Ahadi) inawajibisha matendo kwa kile kilichomo ndani yake na kuifuata hukumu ya matamshi yake; bila kusema kuwa imethibiti kwa uhakika ( بعينه القطع na imesimuliwa……(دونkutoka kwa baadhi ya wafuasi wake kwamba yeye anasema kwamba (Hadith Ahadi) inatoa yakini; lakini mimi sijapata kuiona (kauli) hio kutoka katika matamshi yake (mwenyewe) na sidhani kuwa anafuata (kauli) hio.1134

Anasema Al-Qannubi:

1132 - Ibn Taymiyya Naqdu Maratibi Al-Ijma’a uk. 304. 1133 - Ibn Taymiyya Minhaju Al-Sunna j. 2, uk. 133. 1134 - Ibn Abi Ya’ala Tabaqatu Al-Hanabila j. 2, 245-246.

359

Page 360: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Al-Imamu Ahmad imethibiti kutoka kwake kwa uwazi kabisa kama lilivyo jua kwamba alikuwa akiona kwamba Hadithi Ahadi haitoi yakini, na dalili juu ya hayo ni nyingi mno kwa hapa natosheka na kutaja dalili mbili.

Kisha baada ya hapo Sheikh Al-Qannubi akataja Hadithi ambazo Ahmad kazikataa kama vile Hadithi inayosema: “Umma wangu utaangamizwa na kabila hili la Kiquraish”, ambapo Abdullah bin Ahmad anaripoti kwamba baba yake (Al-Imamu Ahmad) aliikanusha riwaya hii katika maradhi yake aliokufa na akasema: “Itupilie mbali Hadithi hii, kwa hakika iko kinyume na Hadithi nyengine”. Anasema Al-Qannubi: “Hii ni hoja ya wazi kwamba yeye anaona kwamba Hadithi Ahadi haitoi yakini, vyenginevyo asingeliitupilia mbali Hadithi hii”.1135 Ama Hadithi nyengine ambayo kaitaja Al-Qannubi kama ni dalili ya kuwa Ahmad alikuwa akiona kwamba Hadithi Ahadi haitoi yakini, ni Hadithi isemayo: “Sala inakatwa na mwanamke, punda na mbwa”. Anasema Ahmad kama alivyonukuliwa na Al-Tirmidhi katika Al-Sunan:1136 “Hakuna shaka kwamba mbwa mweusi anakata sala, ama kuhusu punda na mwanamke mimi nina wasi wasi”. Anasema Al-Qannubi kwamba lau Ahmad anaona kwamba Hadithi Ahadi inatoa yakini, basi asingeliikataa Hadithi hii. Na Hadithi ya mwanzo kaipokea yeye Ahmad, Al-Bukhari na Muslim wakati ya pili ni riwaya ya Muslim.1137

Huo ni mgongano mmoja katika minhaj (methodology) ya tafsiri uliopo baina ya Maimamu wakubwa na wafuasi wao! Tatizo ni kuwa Hadithi wanapoitaka watakwambia kuwa hii ni mutawatir kama wanavyodai kuhusu riwaya za kuonekana kwa Mungu; nazo si kwamba ni riwaya Ahadi tu, bali ni riwaya za kutunga 100%: mutun zake zinagongana na Qur-ani kama tutavyobainisha; na sanad zake ni mbovu kabisa na wala hazikupata sifa ya kuitwa kuwa ni mutawatir kama tutavyobainisha. Na Hadithi ikiwa hawazitaki – hata kama ni mutawatir – watatafuta kipengele cha kuipiga chenga. Tazama mfano mmoja wa namna gani Ibn Taymiyya anavyoidhoofisha Hadithi sahihi kwa sababu haitaki. Hadithi ya Mtume (s.a.w.) isemayo مواله فعلي مواله كنت Yule ambaye mimi ni) منMaula1138 wake, basi Ali naye ni Maula wake).1139 Hadithi hii, Al-Amin,

1135 - Kwani hii ni Hadithi sahihi. 1136 - J. 2, uk. 163. 1137 - Tazama maelezo zaidi katika Al-Saifu Al-Haad cha Al-Imamu Al-Qannubi uk. 11-12. 1138 - Neno Maula linakuwa na maana ya rafiki na kipenzi; na linakuwa na maana ya msimamizi wa mambo. Katika Hadithi hii jumhur imechukua maana ya kwanza na Shia wamechukua maana ya pili.1139 - Binafsi nimeipekuwa Hadithi hii nikafika njia ishirini na nane za Masahaba na nyengine sikuzimaliza, na nikazikuta njia nyengine ni sahihi kabisa. Lakini maana ambayo ndugu zetu wa Kishia wameipa Hadithi hii ndio tunayotafautiana. Nikipata nafasi

360

Page 361: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

mwanachuoni wa Kishia, kaikusanya kwa njia za Masahaba mia moja na ishirini (120); Tabiina thamanini na nne (84) na wanavyuoni walioitaja miongoni mwa wapokezi mia tatu na sitini (360).1140 Na hayo yamo katika vitabu vya Kisunni. Hadithi hii Ibn Taymiyya kaipiga chenga kwa dai kwamba haimo katika Al-Sihah – kama Al-Bukhari na Muslim – na kwamba wanavyuoni wamezozana juu ya usahihi wake.1141 Lakini kasahau Ibn Taymiyya kwamba katika kitabu chake Naqdu Maratibi Al-Ijmaa kazikataa lafdhi mbili za Hadithi ya Al-Bukhari yaani Hadithi zilizomo katika Sahih na pia kasahau kwamba mazingatio si kuwepo kwa ikhtilafu bali ni kuwa je Hadithi ni sahihi au si sahihi. Hadithi hio ni sahihi hata Al-Albani kakiri juu ya usahihi wake.1142 Kisha Al-Albani akastaajabishwa na kitendo cha Ibn Taymiyya cha kuikanusha Hadithi hio akasema: “Ni ajabu kweli kwa Sheikh Al-Islami kuthubutu kuikanusha Hadithi hii na kuikadhibisha kwake katika Minhaju Al-Sunna..kama alivyofanya katika Hadithi iliotangulia”.1143 Sasa kama kule kazikataa Hadithi zilizomo katika Al-Sihah vipi tena huku anatoa sababu kwamba Hadith hio (Yule ambaye mimi ni Maula wake, basi Ali naye ni Maula wake) haimo katika Al-Sihah!

Halafu tazama ukweli kwamba Hadithi Al-Thaqalain wanakiri wanavyuoni wa Kiwahabi kwamba Hadithi hio ni sahihi, lakini mbona hawaifuati na maana yake iko wazi kwamba tumeachiwa Kitabu cha Allah na Ahlu Al-Bayt?1144 Hadithi hio kainukuu Ibn Baz katika kitabu chake Tuhfatu Al-Ikhwaan na akasema kuwa ni sahihi.1145 Ama Ibn Taymiyya, yeye kainukuu kipande kidogo tu katika Majmua Al-Fatawa, nacho ni kipande kisemacho “Hakika yangu nimekuachieni kile ambacho mukishikana nacho hamutopotea, Kitabu cha Allah”.1146

MAKUBALIANO YA UMMA

Jambo la pili lenye kuonesha mgongano wa Mawahabi katika manhaj (methodology) yao ni ngoma yao ya kila walitakalo wao basi wao hudai kwamba jambo hili “Al-Salaf wamekubaliana” au “Umma umekubaliana”! Bali wakati mwengine hufika hadi kusema hili “Mitume wamekubaliana”!!!

nitaikamilisha risachi yangu hio na kuitoa. 1140 - Al-Amin Al-Ghadir j. 1, uk. 35-190. 1141 - Ibn Taymiyya Minhaju Al-Sunna j. 4, uk. 86. 1142 - Al-Albani Al-Sahiha j. 4, uk. 330, Hadithi na. 1750. 1143 - Al-Albani Al-Sahiha j. 5, uk. 263, katika maelezo ya Hadithi na. 2223. 1144 - Kwa wale wanaoikataa Hadithi hio, sawa hatuna hoja juu yao, lakini kuikubali halafu usiifuate ni ajabu ilioje! Mimi binafsi siikubali kama nilivyoeleza kwa urefu katika kitabu changu Mezani ya Haki. 1145 - Tazama Ibn Baz Tuhfatu Al-Ikhwaan uk. 41-42. 1146 - Ibn Taymiyya Al-Haraani Majmua Al-Fatawa j. 5, uk. 17.

361

Page 362: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Ndio maana Sh. Kasim Mafuta naye akadai kwamba Masahaba wamekubaliana juu ya itikadi ya kumuona Allah huko akhera, ilhali hakuna chembe ya riwaya sahihi kutoka kwao juu ya maudhui hii. Riwaya iliosemwa kuwa ni sahihi ni moja tu: nayo ni riwaya ya Ka’abu Al-Ahbar, Myahudi aliyesilimu katika zama za ‘Umar akawa anasimulia israiliyyat (riwaya za Kiisraili) hadi ‘Umar akataka kumuhamisha, nayo riwaya hio moja iliothibiti kutoka kwa Ka’abu inazungumzia mas-ala ya Mtume (s.a.w.) kumuona Allah wakati wa miraji. Na kutoka kwake Ka’abu na wenzake ndio zimezaliwa riwaya za kuonekana kwa Allah na riwaya za tajsim na tashbih. Sheikh Seif Al-Ghafri naye akadai kuwa kuonekana kwa Allah ndio itikadi ya Mitume! Hayo ndio madai yao. Sasa mgongano uko wapi? Mgongano ni kuwa wakati wao hutoa hoja kwa “Makubaliano ya Umma au ya Al-Salaf” kwa kile wakitakacho wao, basi wewe ukitoa hoja kama hio kwa kitu wasichokitaka wao husema: “Al-Imamu Ahmad kasema atayedai makubaliano basi kasema uwongo: unajuaje kama wako waliopinga”.1147 Tazama kwa mfano ‘Abdul-Aziz Al-Rajihi, Sheikh wa Kiwahabi, anadai kwamba Umma umekubaliana kwamba Hadithi zote za Al-Bukhari na Muslim ni sahihi. Wakati, Ibn Taymiyya, Ibn Al-Qayyim, Al-Albani wamezidhoofisha baadhi ya Hadithi hizo. Kilichodhoofishwa na Maimamu wao hawakusema kitu, kilichodhoofishwa na wengine basi kiama kimesimama na makubaliano ya Umma yamekuwa ndio msingi wa hoja!

KUFUATA AL-SALAF

Nyimbo nyengine ya Mawahabi ni kuwa “Tufuate Qur-ani na Sunna kwa mujibu wa ufahamu wa Al-Salafu Al-Salih”. Lakini hayo ni kwa yale wayatakayo wao. Ama kwa kitu wasichokitaka wao basi hakuna Salaf wala Khalaf! Ananukuu Al-Sayyid Al-Saqqaf na Al-Imamu Al-Qannubi maneno ya mmoja wao akisema:

Ongezea kwamba sisi hatukuwajibika kuabudu kwa ufahamu wa yoyote yule awaye, akiwa ni Ibn Mas’ud (Sahaba) au mwengineo; bali sisi tumelazimika kuabudu kwa andiko la Mtume (s.a.w.) lililothibiti kutoka kwake.1148

Hapa ufahamu wa Al-Salaf umeekwa pembeni kwani hauwezi kumfikisha anakokutaka kwenda!

1147 - Tazama Ibn Al-Qayyim, Mukhtasaru Al-Sawaa’iqi Al-Mursala uk. 506. 1148 - Al-Insafu Fii Ahkami Al-I’itikaf uk. 35, chapa AL-Maktaba Al-Islamiyya ‘Amman (Jodan) chapa ya mwanzo mwaka 1407 A.H. Nukulu kutoka kwa Al-Saqqaf Al-Salafiyya Al-Wahabiyya uk. 89, maelezo ya chini. Kauli hii pia kainukuu Al-Qannubi katika Al-Tufan j. 3, sehemu ya kwanza.

362

Page 363: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

QIYAS BAINA YA ALLAH NA VIUMBE NI HARAMU LAKINI….

Miongoni mwa propaganda za Kiwahabi na Maimamu wao watangulizi, ni kuwa hoja zinapowashinda basi husema: “Allah halinganishwi (hafanyiwi Qiyaas) na kiumbe”. Na hayo, ni maneno sahihi, lakini wao huyasema kukimbia hoja sahihi zenye kukubaliana na akili na tafsiri zilizojengeka juu ya njia sahihi za tafsiri ya maandiko. Ukitazama katika yaliomo (table of contents) ya kitabu Haashia ‘Alaa Al-‘Aqidati Al-Wasatiyya,1149 cha Sheikh Muhammad bin ‘Abdil-‘Aziz bin Maani’i, basi utamkuta anasema maneno haya: بخلقه الله يقاس Allah hafanyiwi qiyaas (halinganishwi) na) الviumbe vyake). Kisha ndani katika uk. 26, utakuta maelezo yenye maana hio. Nayo, kwa ujumla, ni maneno sahihi, mazuri. Lakini ukirudi katika vitabu vyao, basi unaweza ukakusanya kitabu kizima au zaidi kuhusu walivyomlinganisha Allah na viumbe! Mifano miwili mitatu ni hii inayofuata. Anasema Al-Darimi:

فال يتحرك وال مكانه من يزول ال الذي القيوم تفسير أن دعواك وأمابأثر إال التفسير هذا منك يقبل

أو أصحابه بعض عن أو وسلم عليه الله صلى الله رسول عن مأثور صحيحالح ألن ي������التابعين

ويقبض شاء إذا ويرتفع ويهبط شاء إذا ويتحرك يشاء ما يفعل القيومويجل ويقوم إذا ���ويبسط س

الح شاء بين ما أمارة التح �������� ألن والميت ال ������� ي متحرك حي كل ركغ ميت وكل ير ������� محالةمحالة ال متحرك

Ama madai yako kwamba tafsiri ya neno qayyum (maana yake) ni yule asiyeondoka pale alipo wala hatikisiki, basi (tafsiri) yako hio haikubaliki isipokuwa ikiwa itapata riwaya sahihi iliopokelewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.) au kutoka kwa baadhi ya Masahaba wake au wafuasi wa Masahaba, kwani (Allah) aliyehai na ambaye ni msimamizi wa kila kitu, anafanya akitakacho na anatikisika (anafanya harakati) akitaka na anashuka na kupanda akitaka na anazuia (riziki) na kuzikunjua akitaka na anakaa kitako akitaka, KWANI ALAMA YA ALIYEHAI NA ALIYEKUFA NI KUTIKISIKA, BASI KILA KILICHOHAI KINATIKISIKA HAKUNA SHAKA YOYOTE NA KILA KILICHOKUFA HAKITISIKI HAKUNA SHAKA YOYOTE!1150

1149 - Uk. 145. 1150 - ‘Uthman Al-Darimi Al-Raddu Alaa Bishr Al-Marisi j. 1, uk. 20.

363

Page 364: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Hayo ni maneno ya ‘Uthman bin Said Al-Darimi, Imamu wa Ibn Taymiyya, alipokuwa akimjibu Bishr Al-Marisi! Tazama maneno yake haya anayomjibu Bishr Al-Marisi, mwanachuoni wa Kihanafi: tazama jinsi anavyomkisia (anavyomfanyia Qiyas) Allah kwa kumlinganisha na viumbe wake! Anachokisema Al-Darimi ni kuwa, Allah anatikisika yaani anafanya harakati (movement), kwani Allah yuko hai, na tafauti baina ya waliohai na waliokufa ni kutikisika! Yaani analinganisha uhai na kufa kwa viumbe na hali ya uhai wa Allah – Qiyas cha Allah na viumbe!

Anaendelea Al-Darimi kwa kusema:

! ! ( ) ! بصير سميع الله أن تعالى الله قول في أيضا المريسي وادعىبص( أنه ) ! �والله بالعباد ير

) بصير قوله وأن بصر وال سمع بال األلوان ويعرف األصوات يسمعأنه ) ال بهم عالم يعني بالعباد

ما أي أبصره ما ألعمى يقال فقد بعين إليهم ينظر وال ببصر يبصرهمبعين يبصر ال كان وان .أعلمه

Na akadai Al-Marisi vile vile kuhusu kauli yake Allah: “Allah ni mwenye kusikia, mwenye kuona”1151…. “Allah ni mwenye kuwaona waja (wake)”, 1152 kwamba Yeye (Allah) anasikia sauti na anazijua rangi bila (ya kuwa Yeye ana) sikio na jicho. Na kwamba kauli yake (Allah aliposema): “(Allah) ni mwenye kuwaona waja” maana yake ni kuwa ni mwenye kuwajua: si kwamba anaona kwa uoni au kuwatazama kwa jicho, kwani huenda kipofu akaambiwa “Ni mwenye uoni ulioje” yaani “Ni mjuzi alioje” hata akiwa haoni kwa jicho.1153

Hayo ni maneno ambayo ‘Uthman Al-Darimi anayanukuu kutoka kwa Bishr Al-Marisi, nayo ni maneno sahihi na madhubuti kabisa na ndio itikadi ya Ahlu Sunna na jumhur ya Waislamu, kwamba Allah anaona bila ya kuwa na jicho na anasikia wala hana sikio. Lakini sasa tazama jawabu ambayo ‘Uthmaan Al-Darimi kamjibu Bishr Al-Marisi. Anasema Al-Darimi:

هذه على إله من حاال أحسن والكلب الحمار الضال المريسي لهذا فيقاليسم الحمار ألن ع�الصفة

يسمع ال أصم أعمى بزعمك وإلهك بعين األلوان ويرى بسمع األصواتببص يبصر وال ر ����بسمع

سماع لها ليس التي والجبال الحيطان يدرك كما الصوت يدرك ولكنجم ……. أي ������فقد ها ��عت

1151 - Sura 22, Aya 61. 1152 - Sura 3, Aya 15. 1153 - ‘Uthman Al-Darimi K.h.j. j. 1, uk. 41-42.

364

Page 365: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

الك أما وكفرا جهال هذه دعواك في تعالى ������المريسي الله فتشبيهك فريبص ال الذي ر������باألعمى

أن العرب كالم في يستقيم ال بأنه الناس فمعرفة الجهل وأما يرى والبصير سميع هو لشيء يقال

واألسماع األعين ذوي من والبصر بالسمع موصوف الشيء وذلك إالواألبصار

Tunamwambia huyu Al-Marisi mpotovu kwamba PUNDA NA MBWA BASI NI BORA ZAIDI KULIKO MOLA MWENYE SIFA HIZO, kwani punda anasikia sauti kwa masikio na anaona rangi (tafauti) kwa macho, lakini mola wako – kwa madai yako – ni kipofi, kiziwi: hasikii kwa sikio wala haoni kwa jicho, bali anazifikia sauti kama vile kuta na milima ambazo hazina masikio zinavyozifikia sauti. Ewe Marisi, kwa hakika umekusanya ujinga na ukafiri. Ama ukafiri wako ni kumshabihisha Mola wako mtukufu na kipofu ambaye haoni; ama ujinga wako, NI KUWA WATU WOTE WANAJUA KWAMBA KATIKA LUGHA YA KIARABU HAISEMWI KWAMBA KITU FULANI KINASIKIA NA KINAONA ISIPOKUWA KITU HICHO NI CHENYE KUSIFIKA KWA KUSIKIA NA KUONA, NA NI KATIKA VYENYE MACHO NA MASIKIO. 1154

Tazama jinsi mtu huyu alivyokuwa jasiri kwa maneno yake hayo! Bado Ibn Taymiyya anausia sana kuwa watu wasome kitabu chake hicho ili wapate kuijua itikadi sahihi! Halafu tazama alivyofanya qiyas baina ya viumbe na Allah, na kwamba kiumbe yoyote huwa hasikii sauti ila huwa ana masikio, na hawezi kuona ila anakuwa ni mwenye jicho; na kwa hivyo madamu na Allah naye ni mwenye kusikia sauti basi ni lazima atakuwa ana masikio; na madamu anaona basi ni lazima atakuwa ana macho! Mashaa Allah! Hio ndio itikadi ya Al-Salafu Al-Salih – imejengeka juu ya qiyas baina ya kiumbe na Allah!

Halafu tazama maneno yake aliposema:

…lakini mola wako – kwa madai yako – ni kipofi, kiziwi: hasikii kwa sikio wala haoni kwa jicho, bali anazifikia sauti kama vile kuta na milima ambazo hazina masikio zinavyozifikia sauti.

Hapa Al-Darimi anamlaumu Al-Marisi kwa kusema kwake kwamba Allah anasikia wala hana masikio na kwamba kusema hivyo ni kumfananisha Allah na kuta na milima na kwamba punda na mbwa ni bora kuliko mola mwenye sifa hizo! Suali: je na yeye Al-Darimi alipodai kuwa mola wake anasikia kwa masikio na anaona kwa macho alikuwa akidai kwamba mola

1154 - ‘Uthman Al-Darimi K.h.j. j. 1, uk. 42.

365

Page 366: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

wake kafanana na punda?1155 Tazama mtu huyu alivyokuwa hana akili: hajui hata kuzungumza!

Ama kuhusu kuwa je Allah ana mbavu mbili au sehemu mbili (two sides), hili tumetangulia kulieleza kwamba Ibn Al-Qayyim kaweza kulithibitisha kwa kumfanyia qiyas Allah na ‘Imran bin Husain!1156

Hayo ni machache; yalio vitabuni mwao ni mengi kama vile kukisia kwao kuwa fulani ni kiongozi wa Pemba na Unguja na Bara naye yuko Bara, halkadhalika Allah yupo mbinguni na ardhini lakini anakaa mbinguni!1157

Lakini kwa kuhitimisha naturudi katika kanuni yao isemayo: “Tunathibitisha kile Allah alichokithibitisha katika Qur-ani na Mtume wake katika Sunna; na tunakikanusha kile walichokikanusha bila ya tahrif1158 (upotoshaji) wala tashbih”. Ninasema: si kweli: hamufanyi hivyo, vyenginevyo Allah anasema: وجهه إال هالك شيء Kila kitu) كلkitaangamia isipokuwa uso wake). Je hapa munathibitisha alichokithibitisha Allah bila ya ta-awiil? Au mutalazimika kufanya ta-awil ambayo munaikimbia kwengine?

QIYAS CHENGINE CHA MUUMBA NA KIUMBE

Anasema Ibn Al-Qayyim:

الرحمن ... ... عبادة متيقنين هما ما والممثل المعطل إناألوثان ... ... عابد وهذا أبدا سبحانه ال المعدوم عابد ذا

Kwani mu’attil na mwenye kummithilisha (Allah)**Hawana yakini ya kumuabudu Allah.***Yule (wa mwanzo) anaabudu kitu kisichokuwepo (mungu hewa)1159**Na huyu (wa pili) anaabudu masanamu.1160

Anasema mshereheshaji:

1155 - Huyu si mola wetu sisi; mola wetu sisi Waislamu hafanani na kitu wala hana viungo! 1156 - Rejea sura ya pili kwenye kichwa cha habari kinachosema: “VIUNGO VYENGINE VYA MUNGU”. 1157 - Huu ni mfano wa maneno anayoyanukuu Ibn Taymiyya kutoka kwa mmoja wa Maimamu wao. Tazama Ibn Taymiyya Majmu’a Al-Fataawa j. 5, uk. 50. 1158 - Tahrifu yaani ta-awil. Kufanya ta-awil ndiko ambako wao wanakuita tahrif. 1159 - Tazama akili yake mtu huyu! Anaona kuwa Mungu wa kweli haiwezekani kuwepo ila awe na viungo (miguu na mikono), na kwa hivyo, anaona kuwa wasiokubaliana na hayo basi wanaabudu mungu-hewa! 1160 - Ibn Al-Qayyim Sharhu Al-Nuniyya j. 1, uk. 419..

366

Page 367: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

وج�ود... ي�عقل ال ما الصفات من ربه عن نفى حيث عدما يعبد األول بلووص�فه ب�دونه الموصوف

. والثاني المعدوم الممثل –بصفات ......–وهو صنما يعبد

…Bali wa mwanzo anaabudu kitu kisichokuwepo (mungu-hewa) kwani kamuondoshea Mola wake sifa ambazo haiwezekani kuwepo kwa kitu bila ya hizo na akamsifu kwa sifa za kitu kisichokuwepo. Na wa pili – naye ni mwenye kummithilisha Mungu – anaabudu sanamu….1161

Maneno haya yanaonesha kuwa watu hawa wanaona kwamba haiwezekani kuwa Mwenyezi Mungu awepo ila ikiwa atakuwa na viungo! Na kwa hivyo, kuikataa itikadi hio ya mungu-mwenye-viungo, ni kuabudu mungu-hewa (mungu asiyekuwepo) au chambilecho Sh. Deedat “the god that never was”. Ni wazi kwamba wao waliwatazama viumbe wakaona kwamba viumbe wote wana sifa za namna hio na asiyekuwa na sifa hio huwa hayupo, kwa hivyo na Allah naye wakampachika sifa hizo ili aweze kuwepo – Qiyas safi cha Muumba na kiumbe!

KUFUATA KUNDI

Mawahabi na Maimamu wao huwa wanasema kuwa wao ni Ahlu Sunna wal Jama’a. Sasa hio Jama’a yao iko wapi? Kwani wao ni wachache tangu enzi ya uhanbali hadi leo hii? Anasema mmoja wa Maimamu wao wakuu: “Miongoni mwa Sunna ni kufuata kundi (kubwa); atayelichukia kundi na kufarikiana nalo, basi Uislamu kauvua shingoni mwake na amekuwa mpotovu mwenye kupoteza (watu)”.1162 Na bila shaka hata Al-’Allama Qasim Mafuta hapingi kwamba wao ni wachache hasa hasa katika mambo ya itikadi. Na kwa hivyo, kasema Sh. Mafuta: ….. “Waislamu wengi hawajui vipi watamfahamu mola wao muumba”.1163 Na bila shaka Kasim Mafuta hakusudii kwamba Mawahabi ni katika wengi hao; bali anakusudia kwamba wao ndio wale wachache wenye kumjua Mola wao Muumba! Bora Kasim Mafuta angelitamka yale yaliomo moyoni mwake kwa uwazi kama walivyotamka maimamu wake kwamba mu’attila (Shia, Ibadhi, Mashafi, Maliki, Hanafi, na baadhi ya Hanbali) ni makafiri!

Lakini baada ya yote hayo, ukiwa wewe utawapa hoja kwamba “hii ndio kauli ya ya jumhur” basi wao watakujibu kwamba “Ibn Mas’uud kasema

1161 - Tazama maelezo ya Dr. Muhammad Khalil Harras katika Sharhu Al-Nuniyya cha Ibn Al-Qayyim j. 1, uk. 420.. 1162 - Al-Barbahari Al-Sunna uk. 59, tahqiq Khalid bin Qasim. 1163 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 1.

367

Page 368: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kwamba jamaa (kundi kubwa) ni yule aliye katika haki hata akiwa mtu mmoja”.

MASAHABA

Suala la kuwajeruhi Masahaba kunasababisha pia kuwepo kwa manahij (methodologies) tafauti za tafsiri, kwani inapelekea ama kuiwacha kabisa riwaya ya sahaba uliyemjeruhi au kuipa uzito riwaya ya mwengine dhidi ya riwaya yake. Vitabu vyote vya Kiwahabi taqriban vinasema kwamba tuache kuzizungumzia tafauti za Masahaba mule walimogombana, na tuwapende na kuzungumzia fadhila zao.1164 Anasema Ibn Taymiyya: “Haijuzu kumtukana hata Sahaba mmoja”1165 na ni wajibu “Kuzisalimisha nyoyo na ndimi kwa Masahaba wa Mtume (s.a.w.)”1166 “Na wala hatumchukii yoyote miongoni mwao”1167 “Na kuwachukia wao (Masahaba) ni ukafiri na unafiki na kuasi”.1168 “Waombee (Masahaba) rehema na utaje fadhila zao na ujizuiye kutokana na (kutaja) walimoteleza. Wala hatumtaji yoyote miongoni mwao ila kwa kheri.”1169 “Wacha kuvitaja vita vya Ali na Mu’awiya na ‘Aisha na Talha na Zubair”.1170

Hayo ndio mafunzo tunayopewa. Lakini pamoja na hayo ya kututaka sisi tusiwaseme Masahaba na tuwache kuvitaja vita vya ‘Ali na Mu’awiya, utaona kwamba wao wanamsema ‘Ali bin Abi Talib1171 na wale waliokuwa pamoja naye na kumtetea Mu’awiya ambaye Mtume (s.a.w.) mwenyewe kamjeruhi yeye na kundi lake aliposema kumwambia ‘Ammar bin Yasir: “Ammar atauliwa na kikundi cha waasi”, naye akauliwa na jeshi la Mu’awiya. Na hapa kila mwenye akili anajiuliza: je huyu Mu’awiya asisemwe hata katika kile alichokisema Mtume (s.a.w.)? Yaani je ile Hadithi ya Mtume (s.a.w.) isemayo: “Ammar atauliwa na kikundi cha waasi” nayo

1164 - Tazama Sheikh Ibn Baz Al-Aqidatu Al-Sahiha Wa Nawaqidhu Al-Islam uk. 20. 1165 - Ibn Taymiyya Minhaju Al-Sunna j. 2, uk. 225. 1166 - Ibn Taymiyya Al-’Aqiidatu Al-Wasatiyya uk. 25. Na mfano wake ni maneno ya Abu Zur-a Al-Razi kama alivyomnukuu Sh. Muhammad bin Yusuf katika Hayatu Al-Sahaba uk. 7, kutoka katika Al-Kifaya cha Al-Khatib Al-Baghdadi, uk. 97. 1167 - Ibn Abi Al-‘Izz Sharhu Al-’Aqiidati Al-Tahawiyya uk. 466. 1168 - Sadru Al-Din Al-Hanafi Sharhu Al-’Aqiidati Al-Tahawiyya uk. 466. (Wengine wanasema kwamba huyu si Hanafi, bali ni Hanbali, na ndivyo kitabu chake kinavyojionesha).1169 - Al-Barbahari Sharhu Al-Sunnah uk. 68-69. 1170 - Al-Barbahari Sharhu Al-Sunna uk. 103. 1171 - Katika juzuu ya pili tutakupa nukulu za kutosha juu ya nini Ibn Taymiyya kakisema kuhusu Sayyidna Ali (k.w.), hata wanavyuoni wengine wakamwita Ibn Taymiyya kuwa ni mnafiki kwa sababu ya alioyasema dhidi ya Ali kama alivyoeleza Ibn Hajar katika Al-Dururu Al-Kaamina.

368

Page 369: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

pia tuifukie jaani: tusiizungumzie kamwe kwa kuhofia kumtia doa Bwana Mu’awiya?

Pili ni suala la watu wa Nahrawaan ambao walikuwa ndio Masahaba Qurraa (wanavyuoni).1172 Masahaba hawa Banii Umayya wamewatungia kila uwongo ilimradi watu wasiwakubali. Na wamepachikwa majina mabaya ya kuchukiza na wametukanwa kila aina ya matusi. Na miongoni mwa waliowatukana sana Masahaba hawa ni watu wa madhehebu ya Hanbali akiwemo Ibn Taymiyya pamoja na wafuasi wao wa Kiwahabi. Sasa vipi tusiwatukane Masahaba; na vipi tusiingilie mizozo yao ilhali hawa wanatukanwa. Ni wazi kwamba fikra ya kuwacha kuzungumzia mizozo ya Masahaba haikukusudiwa ila ni kama mbinu ya kisiasa ya kutaka kuyafunika makosa ya Mu’awiya na dola yake.

KUWADHOOFISHA WAPOKEZI NA KUWASAHIHISHA WAWATAKAO

Tatizo hili hujitokeza kila wanapopata riwaya ambayo haikubaliani na fikra yao au mwanachuoni asiyekubaliana nao. Na kwa hivyo, baadhi ya Mahanbali wamedhoofisha watu kama:

1) Al-Bukhari. Ambapo Abu Hatim Al-Razi na Abu Zur’a Al-Razi, nao ni Mahanbali, waliziwacha Hadithi zake kwa sababu ana itikadi mbovu! Anasema Ibn Abi Hatim: “Baba yangu na Abu Zur’a walipokea (Hadithi) kutoka kwake (Al-Bukhari), kisha wakamuacha baada ya Muhammad bin Yahya Al-Naysaburi kuwaandikia kwamba yeye (Al-Bukhari) anadhihirisha kauli kwamba lafdhi yake (anaposoma) Qur-ani ni kiumbe”.1173 Ama Ibn Manda, naye pia ni katika Mahanbali, Maimamu wa Kiwahabi, anasema kuhusu Al-Bukhari: “Alikuwa akighushi”.1174 Na haya yote wameyasema si kwa sababu ya udhaifu wa Al-Bukhari, bali ni kwa sababu ya tafauti zao katika baadhi ya vipengele vya itikadi!

2) Al-Imamu Muslim. Huyu, kama inavyojulikana kwamba, naye alikuwa na itikadi sawa na ya Al-Bukhari katika suala hilo la “Matamshi yetu tunapoisoma Qur-ani”. Kwa hivyo, bila shaka naye anakuwa dhaifu kwa mtazamo wa Abu Hatim Al-Razi na Abu Zur’a

1172 - Suala la kuthibitisha kuwepo kwa Masahaba miongoni mwa watu wa Nahrawaan, hapa si mahala pake. Hapa nakusudia kuonesha huu mgongano tu. Anayetaka kulijua suala hili, naarudie kitabu Al-Khawarij wa Al-Haqiqatu Al-Ghaiba cha Sh. Nasir Al-Sabi’i ikiwa anajua lugha ya Kiarabu, au kitabu Makhawarij Baina Ya Hakika Na Visa Vya Kutunga cha Juma Mazrui ikiwa anasoma Kiswahili. 1173 - Ibn Abi Hatim Al-Jarhu Wa Al-Ta’adil j. 7, uk. 191, tarjama na. 1086. 1174 - Ibn Hajar Tabaqaatu Al-Mudallisin uk. 24.

369

Page 370: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Al-Razi. Na hicho ndicho alichokisisitiza Sheikh Hasan Al-Maaliki katika kitabu chake Qira-atun Fii Kutubi Al-‘Aqaaid.1175 Kwa hali yoyote ile, binafsi sikuona mahali ambapo Abu Hatim katamka kwa uwazi kwamba Muslim ni dhaifu au Hadithi zake zinaachwa. Lakini kama tulivyoona kwamba sababu iliowafanya yeye na Abu Zur’a kuziwacha Hadithi za Al-Bukhari, sababu hio pia iko kwa Muslim. Bali ibara aliotumia Al-Razi inaonesha kutokuridhika kwake moja kwa moja na Muslim kwani alipoulizwa kuhusu Muslim alisema: “Saduuq” (Ni mkweli),1176 na lugha hii kwa mujibu wa maelezo ya Ibn Abi Hatim hutumika kwa wapokezi ambao “Hadithi zao zinaandikwa na kupelelezwa”.1177 Labda mazingato haya na yale ya kuwepo kwa sababu moja ya itikadi ya Al-Bukhari na Muslim, ndio yaliompelekea Sheikh Hasan Al-Maaliki kumtaja Muslim kuwa miongoni mwa wapokezi waliodhoofisha na Abu Hatim na Abu Zur’a. Hayo ni kwa upande wa Abu Hatim. Ama Abu Zur’a, yeye imepokewa na Al-Bardha’i kwamba alikuwa akimponda Muslim kwa sababu ya kupokea kwake riwaya kutoka kwa wapokezi dhaifu kama vile Asbaat bin Nasr, Qatan bin Nusair na Ahmad bin Isa na wengine. Na alikuwa Abu Zur’a anasema kwamba Muslim katunga kitabu hicho wala alikuwa hajafikia bali alitaka aonekane kwamba katunga kitabu ambacho hajatanguliwa na mtu yoyote yule katika utunzi wa aina hio ili apate ukubwa!1178 Inawezekana ikawa Ibara hizi ndizo alizozizingatia Al-Maaliki kwamba Abu Zur’a kamdhoofisha Muslim.

3) Al-Bayhaqi. Ama Al-Bayhaqi hakuna aliyemdhoofisha isipokuwa Sheikh Salih Al-Fawzaan mwanachuoni wa sasa wa Suudia! Anasema Al-Fawzaan:

كتب أو اإلمام كتب من يوثقه ولم عنه يثبت لم أحمد اإلمام إلى نسبه ماالبيهقي وذكر أصحابه،

الصفات - - تأويل من شيء عنده الله رحمه البيهقي ألن ؛ يعتمد ال لذلكهذا في بنقله يوثق فال

النقل في يتساهل ربما ألنه الباب

Na yale ambayo (Al-Bayhaqi) kayahusisha na Al-Imamu Ahmad hayakuthibiti kutoka kwake wala hakuyathibitisha kutoka katika vitabu vyake Al-Imamu (Ahmad) au vitabu vya wafuasi wake. Ama Al-Bayhaqi kuyataja hayo hilo si la kutegemea kwani Al-Bayhaqi (r.a.) ana kitu

1175 - Uk. 121. 1176 - Ibn Abi Hatim Al-Jarhu Wa Al-Ta’adil j. 8, uk. 183, tarjama na. 797. 1177 - Ibn Abi Hatim Al-Jarhu Wa Al-Ta’adil j. 2, uk. 37. 1178 - Al-Bardha’i Al-Dhu’afaau Wa Ajwibatu Abi Zur’a Alaa Sualaati Al-Bardha’i j. 2, uk. 675.

370

Page 371: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kuziletea ta-awil sifa (za Allah), basi katika mlango huu nukulu zake haziaminiki, kwani huenda akapuuza katika kunukuu.1179…….Al-Bayhaqi anaziletea ta-awil sifa (za Allah), huenda akapuuza katika kunukuu… 1180

Lakini baadae nikaona katika baadhi ya maandishi ya Mawahabi kwamba Al-Fawzaan kajitetea kwamba yeye hajamdhoofisha Al-Bayhaqi moja kwa moja, bali kasema “Katika mlango huu wa sifa za Allah” kwani Al-Bayhaqi ana tabia ya kuziletea ta-awili sifa hizo za Allah, yaani sifa za mkono, mguu n.k. Ninasema: kwa hali yoyote ile ewe Al-Fawzaan, umemdhoofisha Al-Bayhaqi kwa kufuata matamanio ya nafsi yako, kwani huwezi kumdhoofisha mtu katika mlango mzima kwa sababu hio ulioitoa wewe kwani yeye Al-Bayhaqi anadai – katika masimulizi yake – kwamba “kutoka kwa fulani kwamba Ahmad bin Hanbal kasema kadha”. Kwa hivyo, hii ni riwaya anayoisimulia kutoka kwa Ahmad, sasa hio ta-awili yake imetoka wapi hapa? Ta-awili hio yeye anaisimulia kutoka kwa Al-Imamu Ahmad kwa sanad sahihi au hasan, kwa hivyo hio si ta-awili yake, bali ni riwaya anayoisimulia kutoka kwa Ahmad. Kinachowezekana ni kusema kuwa riwaya zake alizozipokea kutoka kwa fulani ni dhaifu; au riwaya zake kutoka kwa watu wa mji fulani hazikuthibiti.

WAPOKEZI DHAIFU AMBAO MAWAHABI NAMAIMAMU WAO WANAWAKUMBATIA

Hio iliotangulia ni baadhi ya wale watu waliokubaliwa na Umma ambao Mawahabi na Maimamu wao wamewadhoofisha kwa matamanio yao ya nafsi! Ama watu dhaifu ambao wao ndio wanawakubali ni kama:

1) Ibn Batta. Tumenukuu kabla maneno ya Ibn Al-Qayyim na maneno ya Dr. Ridhaa na maneno ya Sayyid ‘Imran waliomsifu Ibn Batta kwamba ni Imamu mwenye dini sana na mwanachuoni wa Hadithi mkubwa. Na chenye kustaajabisha zaidi ni maneno ya Al-Dhahabi aliposema: “Pamoja na kuwa Ibn Batta ana uwezo mdogo katika riwaya lakini ni Imamu katika Sunna”.1181 Lakini ukirejea vitabu vya wapokezi utaona kwamba Ibn Batta ni dhaifu na kasimulia riwaya za uwongo. Anasema Al-Dhahabi “Ni Imamu ana awham (ana makosa

1179 - Al-Fawzaan Ta’aliqaatu ‘Alaa Kitaabi Al-Salafiyya Laysat Madhaban uk. 33. 1180 - Al-Fawzaan K.h.j. uk. 35. 1181 - Al-Dhahabi Al-Mizaan j. 3, uk. 412, tarjama na. 5394. Ni Sunna gani?! Ni sunna ya kutunga riwaya za uwongo; ni sunna ya kuiba vitabu vya watu; ni sunna ya kumshabihisha Allah na viumbe na kuwakafirisha Waislamu!

371

Page 372: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

mengi).”1182 Anasema Abu Qasim Al-Azhari: “Ibn Batta ni dhaifu; ni dhaifu”. Anasema Ibn Hajar: “Nimelikuta jambo la Ibn Batta, ambalo lilinistaajabisha na mwili ulinisisimka”. Kisha Ibn Hajar akasimulia maneno ya Ibn Batta tulioyanukuu kabla kwamba: “Nabii Musa (a.s.) alimkuta mtu juu ya mti kavaa vazi la sufi na viatu vya ngozi ya punda, basi akasema naye (yaani yule mtu akasema na Nabii Mussa a.s). Nabii Mussa (a.s.) akasema: ‘Ni Muibrania gani huyu anayesema na mimi juu ya mti?’ Yule mtu akajibu: “Mimi ni Mungu”. Kisha Ibn Hajar akasimulia kisa cha Ibn Batta cha kuzibadilisha sanad za riwaya. Ufupisho wake ni kuwa Nasru Al-Andalusi alikwenda ‘Ukbaraa na akaandika Hadithi kutoka kwa Mashekhe wa huko akiwemo Ibn Batta. Aliporudi Baghdad, Al-Daraqutni akamuuliza umeandika nini kutoka kwa Ibn Batta? Akamwambia Kitabu Al-Sunan cha Rajaa bin Murajjaa, kanisimulia hicho kutoka kwa Hafs bin ‘Umar Al-Ardabili kutoka kwa Rajaa bin Murajjaa. Al-Darqutni akasema hili haliwezekani kwani Rajaa bin Murajjaa kaja Baghdad mwaka wa 40, na Hafs bin ‘Umar kaja mwaka wa 70 basi vipi kapokea Hadithi kutoka kwake? Basi baada ya hapo Ibn Batta akawa anazifuata kopi (vitabu) zilizoandikwa kutoka kwake na ikawa anabadilisha riwaya na akaweka badala yake: “Kutoka kwa Abu Al-Baraa, Hibban kutoka kwa Fat-h bin Shakhraf kutoka kwa Rajaa. 1183 Anasema Al-Khatiib: “Kanisimulia Ahmad bin Al-Hasan bin Khayrun kasema: ‘Nimekiona kitabu cha Ibn Batta kuhusu Mu’ujam cha Al-Baghawi, kitabu hicho kilikuwa cha mtu mwengine basi yeye (Ibn Batta) akalifuta jina la mwenyewe akaweka jina lake!1184 Anasema Ibn Asakir: ‘Na Sheikh wetu, Abu Al-Qasim Al-Samarqandi alinionesha baadhi ya kopi za Ibn Batta kuhusu Mu’ujam cha Al-Baghawi nikakuta ndani yake mapokezi yake yamerekebishwa baada ya kufuta kama alivyosimulia Al-Khatiib.1185 Tazameni mtu huyu alivyosemwa kuwa ni mwongo, mtunzi wa Hadithi, mbadilishaji wa sanad, mwizi wa vitabu, lakini juu ya yote hayo Mawahabi na Maimamu wao wanawadanganya watu kwamba ni “Imamu, mcha Mungu, Haafidh n.k.”. Yote hayo wameyasema ili wapate kufaidika

1182 - Na Al-Dhahabi kumwita huyu Imamu ni kwa sababu yumo katika madhehebu yake ya Hanbal. Ama lau mtu kama huyu alikuwa Shia au Ibadhi basi angelimshabulia sana na wala laqab ya uimamu asingelimpa! 1183 - Tazama kazi ya Ibn Batta hii! Halafu Mawahabi wanatwambia kuwa huyu ni Imamu mcha Mungu kwa sababu ana itikadi kama yao ya tajsim. 1184 - Jamaa Imamu aiba kitabungwa! 1185 - Tazama Ibn Hajar Lisanu Al-Mizan j. 4, uk. 112-114, tarjama na. 231.

372

Page 373: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

au kuhasirika kwa riwaya zake za kukafirisha na riwaya zake za mungu-mtu. Wa Allahu Al-Musta’aan.

2) Al-Ahwazi. Huyu tumemuelezea kabla hatuna haja ya kumrejea tena.

3) Hammad bin Salama. Huyu naye ni dhaifu na kasimulia Hadithi munkar kupita kiasi. Tutamuelezea kwa urefu tukifika katika mas-ala ya kuonekana kwa Allah. Hii ni mifano tu ya jinsi gani watu wa skuli hio ya Kihanbali/Kiwahabi wanavyowakubali wapokezi wanaoafikiana nao na kuwakataa wasioafikiana nao hata kama utafiti wa riwaya unathibitisha kwamba wale waliowakubali wao ndio wapokezi dhaifu na wale waliowakataa ndio wapokezi sahihi – hilo kwao si muhimu!

MAJAZI

Kuthibitisha majazi na kuyakanusha kwake kunajenga manahij (methodologies), tafauti zenye kutufikisha katika natija tafauti katika tafsiri za maandiko. Na kwa hivyo, tumekuwa na itikadi ya Mungu mwenye kiwiliwili na viungo; na itikadi ya Mungu asiye na kiwiliwili wala viungo! Wenye kukanusha majazi, kwao ukitajwa mkono huwa ni mkono wa kweli; na wenye kuthibitisha majazi wao mkono huwa wanaupa ta-awil (interpretation).

Chenye kustaajabisha ni kuwa wakati Ibn Al-Qayyim – akimfuata mwalimu wake Ibn Taymiyya – katutungia kitabu chenye mlango mzima kuhusu kukanusha majazi, basi yeye mwenyewe katumia majazi katika sehemu kadha za vitabu vyake. Bali mara nyengine husema kwa uwazi kwamba “Haya ni majazi”. Na bila shaka huu ni mgongano wa wazi kabisa. Tumetoa nukulu zake katika sehemu tuliyozungumzia majazi.

Halkadhalika Ibn Taymiyya, naye hukanusha majazi kwa uwazi mara akayataja na kuyaelezea. Yote haya tumeyabainisha vya kutosha Wa Li-Lahi Al-Hamdu.

373

Page 374: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

NATIJA YA KUJIGONGA KATIKA MINHAJ (METHODOLOGY)

Hayo yaliotangulia ni kuhusu mgongano wao katika minhaj (methodology) yao ya kufasiria maandiko. Je baada ya hayo ni nini chenye kufuata? Bila shaka mgongano katika minhaj unazaa mgongano katika fiq-hi, sawa ikiwa ni fiq-hi ya itikadi au ya ibada au nyengineo. Mifano miwili mitatu inayofuata inaweka wazi maudhui:

Mungu ni/si Kiwiliwili

Ibn Taymiyya amenukuu – kwa kuyakubali au kwa kuyapa uzito zaidi – maneno ya aliowaiita kuwa ni Ahlu Al-Ithbat yaani watu wenye kuthibitisha itikadi ya kuwa Allah ana viungo (mkono, mguu n.k), wakisema: “Mungu ni kiwiliwili”. Anasema Ibn Taymiyya:

Ama sababu ya tatu ni kuwa ikiwa (itikadi ya) kiwiliwili itakataliwa kwa uwazi, basi itatokea shaka nyingi katika sharia miongoni mwa yale yaliosemwa kuhusu kiama yasiokuwa hayo. Miongoni mwa hizo (shaka zitazotokea) ni kile kitachotokea kuhusu kuonekana (kwa Allah) ambako riwaya thabiti1186 zimekuelezea. Na hii ni kwa sababu wale waliokanusha kwa uwazi – yaani kukanusha kiwiliwili – ni makundi mawili: 1) Mu’atazila. 2) Ash’ariyya (Masuni wote taqriban, ukiwatoa baadhi ya Hanbali). Ama Mu’atazila wao jambo hilo (la kukataa kuwa Allah ni kiwiliwili), liliwapelekea kukataa kuwa Allah ataonekana. Ama Ash’ariyya wakataka kuyajumuisha mambo yote mawili yakawawiya tabu hayo juu yao, wakakimbilia kwenye kauli za kuikataa haki na kuipamba batili…..1187

Anaendelea:

Na miongoni mwa (sababu) hizo, ni kwamba ikiwa (itikadi ya) kiwiliwili itakataliwa kwa uwazi, basi italazimu kuzikataa harakati, kwa hivyo, ikiwa (harakati) zitakataliwa kwa uwazi, itakuwa vigumu (kuithibitisha) ile sifa ya mkusanyiko (wa siku ya kiama) iliokuja kwamba Allah atawachomozea (atawajia) watu wa siku ya kiama. 1188

Sasa wakati Ibn Taymiyya ananena hivyo, mwanafunzi wake Ibn Al-Qayyim anatongoa hivi:

1186 - Tunasema: hakuna riwaya thabiti juu ya suala hili; bali ni za kutunga kama tutavyobainisha tukifika sehemu yake in shaa Allah. 1187 - Ibn Taymiyya Bayaanu Talbisi Al-Jahmiyya j. 1, uk. 26. 1188 - Ibn Taymiyya Bayaanu Talbisi Al-Jahmiyya j. 1, uk. 27.

374

Page 375: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Na kuja kwake (Allah siku ya kiama) si kufanya harakati wala si kuondoka (huko aliko) wala si kubadilika kwani hayo ni pale ambapo mwenye kuja akiwa ni kiwiliwili au johari (kitu chenye kuchukua nafasi). Ilipothibiti kwamba yeye si kiwiliwili wala si johari wala si kitu chenye kufahamika (kwa akili tu) ambacho hakionekani wala kushikika (عرض); basi haikulazimika kwamba kuja kwake kuwe kwa harakati wala kuondoka.1189

Sasa tazama hapa wanavyogongana:

a) Huyu kwake Mungu si kiwiliwili; wale kwao ni kiwiliwili, na wote wanasema kuwa wanafuata Al-Salaf! Sasa kauli ya Al-Salaf ni ipi: Mungu ni kiwiliwili au si kiwiliwili?

b) Halafu tazama tena maneno ya Ibn Al-Qayyim kwamba Allah atapokuja siku ya kiama hatofanya harakati wala hatoondoka huko aliko. Sasa je huku ndiko kuja kwa uhakika au ni kuja kwa majazi ambako wanavyuoni wa jumhur ndiko wanakokuzungumzia?

c) Ibn Al-Qayyim hapa anakanusha harakati: wale wanathibitisha harakati!

d) Tazama ukweli kwamba wao wanasema kuwa Mungu hapa atakuja hakika kwani anakuja kufanya hukumu kwa waja. Sasa vipi atakuja hakika naye yuko kule kule! Huu ni mgongano ulio wazi kwa yule mwenye moyo au kutege sikio naye yuko hadhiri!

Mungu yuko juu lakini!!!

Mawahabi na Maimamu wao watangulizi wanaowafuata wanaamini kuwa Allah yuko juu ya mbingu kakaa kitako juu ya ‘Arshi naye kapambanuka kutokana na viumbe. Wakati wao wanaona hivyo, jumhur ya wanavyuoni wa umma wanaona kwamba Allah hana kitu sehemu kwani sehemu zimeumbwa na Allah; na Yeye alikuwepo kabla ya kuziumba sehemu naye habadiliki kutoka hali moja kwenda nyengine kwani kubadilika ni katika sifa za viumbe. Kwa hali yoyote ile hili silo ninalotaka kulizungumzia hapa; ninalotaka kulizungumzia ni huu mgongano uliopo katika itikadi ya kuwa “Mungu yuko juu kakaa juu ya kiti chake cha anzi (‘Arsh) kweli kweli, naye

لخلقه yuko mbali na viumbe vyake (hakuvigusa)”1190 na itikadiمباينkwamba “kiti (kursi) ndio sehemu yake ya kuwekea miguu”.1191 Sasa kama Yeye yuko juu baada ya mbingu saba mbali na viumbe, halafu kiti ndio

1189 - Ibn Al-Qayyim Ijtima’u Al-Juyush uk. 88. 1190 - ‘Uthmaan Al-Darimi Al-Raddu ‘Alaa Al-Marisi j. 2, uk. 67, 71. 1191 - Ibn Al-Qayyim Hadi Al-Ar-waah uk. 299.

375

Page 376: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

sehemu ya kuwekea miguu yake na kiti hiki tunaambiwa – kwa mujibu wa tafsiri za watu hawa – kwamba kimeenea mbingu na ardhi kama Aya inavyosema:

موات كرسيه وسع واألرض السKiti1192 chake kimeenea mbingu na ardhi.1193

Sasa Mungu huyu, kiti ndio sehemu ya kuwekea miguu yake, na kiti hiki kimeenea katika mbingu na ardhi, sasa hii miguu si itakuwa iko mbinguni na ardhini? Basi vipi tena museme kuwa Mungu yuko juu ya ‘Arshi baada ya mbingu saba na yuko mbali na viumbe vyake: hakuvigusa, na kwamba hayupo ardhini? Sijui na hapa mutalazimika kuleta ta-awil ili iwe munapotaka nyinyi ta-awil ni halali na musipoitaka nyinyi iwe ni haramu!

MUNGU ANA MPAKA LAKINI HANA!

Wakati Ibn Taymiyya anasema: “…..Katika yale yenye kuonesha kwamba Allah Mtukufu ana mpaka anaopambanuka nao kutokana na viumbe”1194……. “….Yeye ana mpaka ambao anaujua Yeye tu haujui mwengine (asiyekuwa Yeye)”. 1195 Ibn Al-Qayyim anasema:

مستو وجل عز والله يحملونه حملة وللعرش عرش وجل عز وللهحد له وليس عرشه على

Na Allah Mtukufu ana Kiti cha enzi (‘Arshi), na ‘Arshi hio ina Malaika wabebaji walioibeba na Allah kakaa juu ya ‘Arshi yake Naye hana mpaka! 1196

Utaona hapa kwamba Mungu wa mwalimu ana mpaka; Mungu wa mwanafunzi hana mpaka! Lakini baada ya yote hayo, kichekesho chenye kuliza ni sura za hawa Malaika waliombeba Allah! Malaika hao wanatisha kwani Al-Darimi anasema: ككعوب كعوب لها قرون العرش لحملة Malaika walioibeba ‘Arshi wana pembe zenye vifundo kama“ .…… القناvifundo vya mkuki……….”.1197 Kisha baada ya kuwa Malaika hao wana pembe hizo, basi sura zao ni za wanyama: hakusalimika isipokuwa mmoja

1192 - Elewa kwamba tafsiri ya neno kursiy hapa ni “elimu”. Na maana ni “elimu yake imeenea kila pahala”. Ama tafsiri hio niliotoa hapo ni kwa mujibu wa Mawahabi na Maimamu wao wanaowafuata. 1193 - Sura 2, Aya 255. 1194 - Ibn Taymiyya Bayanu Talbis Al-Jahmiyya j. 1, uk. 445. 1195 - Ibn Taymiyya Bayanu Talbis Al-Jahmiyya j. 1, uk. 443. 1196 - Ibn Al-Qayyim Haadi Al-Ar-waah uk. 299. 1197 - ‘Uthman Al-Darimi Al-Raddu ‘Alaa Bishr Al-Marisi j. 2, uk. 91.

376

Page 377: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

tu. Inasema riwaya kutoka katika kitabu tulichousiwa na Sheikh Seif Al-Ghaafri kuwa tukisome:

تحمله رآه ذهب من كرسي ص أعلى في ملك المالئكة من ورة����ربعةص في وملك سد أورة ���رجل

نسر صورة في وملك ثور صورة في …..وملك

….. (Mtume s.a.w.) kamuona Allah (naye Allah) kakaa juu ya kiti; kimebebwa na malaika wane: malaika mmoja ana sura ya mtu; malaika wa pili ana sura ya simba; Malaika wa tatu ana sura ya ng’ombe dume na malaika mwengine ana sura ya ndege nasr (eagle)….!1198

Hee! Salafiyya nyi! Mbona vitabu vyenu vina tumbaku nno! Nyie ndio mwafuata watangulizi wema! Allah akusaidieni na azitie nuru akili zenu na akujaalieni hio elimu yenu munayoisoma ikuonesheni njia sahihi, na istikhara ndio njia bora kuliko kung’ang’ania kitu ambacho elimu yake ya mwisho iko kwa Allah.

1198 - Ibn Ahmad Al-Sunna j. 1, uk. 175-176, riwaya na. 217. Al-Bayhaqi Al-Asmaau Wa Al-Sifat j. 2, uk. 361-362 Hadithi na. 934.

377

Page 378: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

SURA YA KUMI NA MOJAKUHUSU IBN TAYMIYYA NA IBN AL-QAYYIM

Katika kitabu changu Hoja Zenye Nguvu nilisema yafuatayo kuhusu Ibn Taymiyya:

Falsafa ya Ibn Taymiyya kuhusu maumbile ni kuwa ulimwengu una sifa ya kutangulia, kama alivyosema haya katika kitabu chake Naqdu Maratibi Al-Ijmaa.1199 Nini maana ya ulimwengu kuwa na sifa ya kutangulia? Sisi Waislamu tunaamini kuwa Mwenyezi Mungu tu ndiye mwenye sifa ya kutangulia, yaani kabla yake hapakuwa na kitu chochote: kila kilichopo tunapopajua na tusipopajua tunapopaona na tusipopaona basi ni kiumbe cha Mwenyezi Mungu. Lakini itikadi ya Ibn Taymiyya wanaemwita Sheikh wa Uislamuu, ni kuwa Mwenyezi Mungu alikuwanavyo vitu ambavyo kutokana na vitu hivyo ndio kaanzia kuumba maumbile yote. Sasa suala ni kuwa hivi vitu vya mwanzo ambavyo Mwenyezi Mungu kaanzia kuumba viumbe, kaviumba nani? Je haoni yeye huyu Ibn Taymiyya kuwa falsafa hii inapelekea kurudi kwenye itikadi ya kuwepo kwa Mungu zaidi ya mmoja? Huyu ndiye ambaye Mawahabi wanamwita Sheikh Al-Islam. Kaisahau kauli ya Mwenyezi Mungu kwamba akitaka kitu husema:

فيكون كنKua, nacho kinakua.1200

Na nilikuwa mimi binafsi nafuatilia kusoma Intaneti, akadhihiri mmoja ya wafuasi wake na kutaka mjadala juu ya itikadi hii ya kwamba Mwenyezi Mungu alikuwa na vitu huko mwanzo ambavyo kaanzia kuumba viumbe. Na hoja yake katika itikadi yake hio ni: “From nothing comes nothing” (pasipo na kitu hapatoki kitu). Kwa hivyo kutokana na maneno haya ya mfuasi huyu wa Ibn Taymiyya, Mwenyezi Mungu hawezi kuumba kitu mpaka apate kitu chengine ndio kutoka katika hicho aumbe anachokitaka! Kwa hivyo anaunda sio anaumba! Tazama itikadi za Waislamu zilivyopotolewa mpaka wanatoa hoja kwa falsafa za kimagharibi na wanaacha maneno ya Mwenyezi Mungu ambayo hayabatiliki wala hayana shaka. Lakini wakamjibu watu jawabu ndogo tu akajiona hana maana: wakamwambia: “Wewe tatizo lako ni kuwa huamini kwamba Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.”

1199 - Naqdu Maratibi Al-Ijmaa cha Ibn Taymiyya kilichochapishwa pamoja na kitabu Maratibu Al-Ijmaa cha Ibn Hazm uk. 304. Daru Ibn Hazm, chapa ya kwanza 1419 A.H, 1998 A.C. Pia tazama Minhaj Al-Sunnah cha Ibn Taymiyya kilichochapishwa pamoja na kitabu chake chengine kinachoitwa Baya Nu Muwafaqati Sarihi Al-Maaqul Lisahihi Al-Manquul j. 2 uk. 75. 1200 - Sura ya 36 Aya ya 86.

378

Page 379: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Na akitegemea Hadithi za uwongo, Ibn Taymiyya katika kitabu chake Al-Aqida Al-Wasatiyya,1201 anasema: “Jahanam haiachi kutupwa (waovu) ndani yake nayo inasema ongeza mpaka Mwenyezi Mungu atatia mguu wake ndani yake!”1202 Kisha anasema Ibn Taymiyya kuwa (Mwenyezi Mungu) “Anaendelea kucheka.”1203

JAWABU NILIOPATA

Hayo ndio nilioyasema katika kitabu changu. Sasa je ndugu yetu Sheikh Kasim Mafuta ana jawabu gani? Sheikh Kasim Mafuta akanijibu kama ifuatavyo:

MAJIBU YETU

Maneno yote haya ya ndugu Juma ni maneno ya uwongo yaliyojaa chuki dhidi ya mwanachuoni huyu mkubwa wa kiislamu, si kweli kwamba itikadi ya Ibn Taymiyya ni kuwa ulimwengu una sifa ya kutangulia. Na wala maneno ya Ibn Taymiyya katika suala hili hayapelekei kwenye dhana ya kuwepo Mungu zaidi ya mmoja, lakini huo ni ufahamu mbaya wa ndugu yetu Juma uliosababishwa na chuki binafsi dhidi ya maulamaa wa Ah’li Sunna hasa Ibn Taymiyya.

Katika kubatilisha madai haya ya uwongo ya Juma, hebu tukunukulie kidogo ndugu msomaji maneno ya Ibn Taymiyya yanayohusu masuala haya ya maumbile, amesema Ibn Taymiyya:

المختص – سبحانه- وهو يكن لم أن بعد آئنك حادث الرب سوى ماكل يس�فل, واألزلية بالقدم

يزل لم أنه قدر وإن قديم مفعوالته ىف قديم شيئ معه وليس فاعالالمفعوالت فى ليس بل, بقدمه سواه ما لكل الخالق وحده وهو- سبحانه –هو إال قديم ال بل, ألبته قديم

وق��مخل سواه ما كلو تعارض درء/272 26 الزمر))” شيئ لك خالق الله- ((سبحانه (( –قال ماك

والنقل العقل

“KILA KISICHOKUWA MOLA NI CHENYE KUZUKA KIMEPATIKANA BAADA YA KUTOKUWEPO, na yeye (Allah) –Sub’hanah- ndiye mwenye kuhusishwa na kutangulia na azal, hakuna kitu katika viumbe vyake kilichokuwa ni chenye kutangulia, hata kama ikikadiriwa kuwa yeye (Allah) hakuacha kuwa ni mwenye kutenda, (lakini) hakuna kitu kilichotangulia kwa kutangulia kwake, bali hakuna kabisa

1201 - Uk. 12. 1202 - Naye kategemea Hadithi iliosimuliwa na Al-Bukhari katika Sahih yake, Hadithi na. 4849-4850, lakini kuna tafauti kubwa sana za wanavyuoni juu ya maana ya Hadithi hii kama ilivyoelezwa katika Fat-hu Al-Bari cha Ibn Hajar na vitabu vyengine.1203 - Ibn Taymiyya Al-‘Aqiidatu Al-Wasatiyya uk. 12.

379

Page 380: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

katika viumbe (vyake ambavyo) ni vyenye kutangulia, BALI HAKUNA KILICHOTANGULIA ILA YEYE (ALLAH) – Sub’haanah-. Na yeye pekeyake ndiye mwenye kukiumba kila kisichokuwa yeye, kila kisichokuwa yeye ni chenye kuumbwa kama alivyosema - Sub’ahaanah-: ((Allah ni muumba wa kila kitu))”.1204

Ndugu msomaji, je kwa maneno haya umefahamu kwamba Ibn Taymiyya ana itikadi ya kuwa ulimwengu una sifa ya kutangulia kama anavyodai Juma? Au umefahamu kwamba Ibn Taymiyya anasema kuwa kila kisichokuwa Allah ni chenye kuzuka na kimepatikana baada ya kutokuwepo? Je kwa maneno haya ya Ibn Taymiyya umefahamu kwamba ana itikadi ya kuwepo Mungu zaidi ya mmoja kama anavyodai ndugu Juma kuwa sheikhul islam Ibn Taymiyya ana itikadi hiyo? Au umefahamu kwamba ndugu Juma si mkweli? Hebu yatupie jicho maneno mengine ya Sheikul-Islam Ibn Taymiyya tuone anavyosema:

يكون وأن بالفاعل مسبوقا يكون أن بد ال أفعاله من واحد لك مسبوقاونك������ ويمتنع, بالعدم

الفاعل مع المعين لفعلا أزال من فعل لك على يتقدم فالفاعل...وأبداكل أن يوجب وذلك أفعاله

18 الفتاوى مجموع/ 227-228. .مخلوق” محدث سواه ام

Kila kitu katika vitendo vyake hakuna budi kuwa ni chenye kutanguliwa na mwenye kutenda na ni chenye KUTANGULIWA NA KUTOKUWEPO. NA HAIWEZEKANI KUWA KITENDO FULANI KILIKUWEPO PAMOJA NA MTENDAJI TANGU MWANZO NA AZAL…..Mwenye kutenda (ambaye ni Allah) anakitangulia kila kitendo katika vitendo vyake na hilo linawajibisha kuwa KILA KISICHOKUWA YEYE (ALLAH) NI CHENYE KUZUKA NA NI CHENYE KUUMBWA”.1205

Bila shaka maneno haya yako wazi katika kuufichua uwongo wa ndugu Juma na wala hayahitajii maelezo.1206

JAWABU NA MAELEZO

Hio ndio jawabu alionijibu Sheikh Kasim Mafuta kuhusu yale nilioyasema. Nayo ni jawabu nzuri lau haikutokana na ufahamu wake mbaya wa kuyasoma maandiko hata hayo alioyanukuu yeye mwenyewe kutoka kwa Sheikh Al-Islam. Bila shaka asingelitoa hoja hio lau alikifahamu kile

1204 - Surat Zumar aya ya 26. Tazama kitabu Dar’u Ta’arudh juzuu ya 8 ukurasa wa 272 cha Ibn Taymiyya. 1205 - Tazama Maj’muul-Fatawa juzuu ya 18 ukurasa wa 227-228. 1206 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 13-14.

380

Page 381: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

nilichokisema katika kitabu changu Kisimamo na pia lau aliyafahamu vizuri maneno ya Ibn Taymiyya yasemayo:

يكون وأن بالفاعل مسبوقا يكون أن بد ال أفعاله من واحد لك مسبوقا ون ك������� ويمتنع , بالعدم الفاعل مع المعين الفعل أزال من فعل لك على يتقدم فالفاعل... وأبدا�ل�ك أن يوجب وذلك أفعاله

18 الفتاوى مجموع/ 227-228. .مخلوق” محدث سواه ما

Kila kitu katika vitendo vyake hakuna budi kuwa ni chenye kutanguliwa na mwenye kutenda na ni chenye KUTANGULIWA NA KUTOKUWEPO. NA HAIWEZEKANI KUWA KITENDO FULANI KILIKUWEPO PAMOJA NA MTENDAJI TANGU MWANZO NA AZAL…..Mwenye kutenda (ambaye ni Allah) anakitangulia kila kitendo katika vitendo vyake na hilo linawajibisha kuwa KILA KISICHOKUWA YEYE (ALLAH) NI CHENYE KUZUKA NA NI CHENYE KUUMBWA”.1207

Nitakufahamisha vizuri nini Ibn Taymiyya anakisema katika maneno yake hayo. Ama maneno ya Ibn Taymiyya yasemayo:

المختص – سبحانه- وهو يكن لم أن بعد آئنك حادث الرب سوى ماكل يس�فل, واألزلية بالقدم

يزل لم أنه قدر وإن قديم مفعوالته ىف قديم شيئ معه وليس فاعالالمفعوالت فى ليس بل, بقدمه سواه ما لكل الخالق وحده وهو- سبحانه –هو إال قديم ال بل, ألبته قديم

وق��مخل سواه ما كلو تعارض درء/272 26 الزمر))” شيئ لك خالق الله- ((سبحانه (( –قال ماك

والنقل العقل

“KILA KISICHOKUWA MOLA NI CHENYE KUZUKA KIMEPATIKANA BAADA YA KUTOKUWEPO, na yeye (Allah) –Sub’hanah- ndiye mwenye kuhusishwa na kutangulia na azal, hakuna kitu katika viumbe vyake kilichokuwa ni chenye kutangulia, hata kama ikikadiriwa kuwa yeye (Allah) hakuacha kuwa ni mwenye kutenda, (lakini) hakuna kitu kilichotangulia kwa kutangulia kwake, bali hakuna kabisa katika viumbe (vyake ambavyo) ni vyenye kutangulia, BALI HAKUNA KILICHOTANGULIA ILA YEYE (ALLAH) – Sub’haanah-. Na yeye pekeyake ndiye mwenye kukiumba kila kisichokuwa yeye, kila kisichokuwa yeye ni chenye kuumbwa kama alivyosema - Sub’ahaanah-: ((Allah ni muumba wa kila kitu))”.

Maneno haya, Sheikh Kasim nakuomba uyarejee tena na tena uyatazame vizuri, nahofia kwamba hapa Ibn Taymiyya alikuwa anatoa natija za kauli

1207 - Tazama Maj’muul-Fatawa juzuu ya 18 ukurasa wa 227-228.

381

Page 382: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

za watu wengine, husasan ukizingatia kwamba maneno yake yasemayo: فكل هذا wewe umeyaruka (..…Na kwa msingi huu, basi kila) ...وعلى

maneno hayo, nayo ndio mwanzo wa sentensi hio. Maneno kamili ni haya:

فكل هذا وهو وعلى يكن لم أن بعد كائن حادث الرب سوى ماوإن قديم مفعوالته في فليس واألزلية بالقدم المختص سبحانهفي ليس بل بقدمه قديم شيء معه وليس فاعال يزل لم أنه قدر

الخالق وحده وهو سبحانه هو إال قديم ال بل البتة قديم المفعوالتكل : } خالق الله تعالى قال كما مخلوق سواه ما وكل ماسواه لكل

شيء {

Bali wewe hata ile Al-Faau (fee) ambayo inaonesha بعده بما قبله ما ربطkuyafungamanisha maneno ya mwanzo na ya pili, pia umeiondosha! Utakumbuka kwamba Ibn Taymiya katika sehemu hii alianza na kuzungumzia mambo ya kifalsafa. Akaanza na maneno yenye nukta hizi:

1) Jumhur ya Ahli Al-Haia (wanavyuoni wa maumbile, falaki n.k.) wanasema kwamba chenye kufanya haraka (movement) ni falaki.

2) Harakati (Mitikisiko) za mashariki ni za bahari kuu pamoja na yaliomo.3) Vyovyote vile iwavyo si kweli kwamba harakati ya kila sayari na orbit

inatokana na harakati ya bahari, bali hizo ni harakati tafauti.4) Kama harakati hizi ni tafauti basi haziwezi kutoka kwa mmoja aliye simple

(si murakkab au asiye na mijengeko tafauti).5) Kwa hivyo, kinachotokea kutoka kwa huyu mmoja ni kitu kimoja, sawa

ikiwa kitu kimoja hicho kitatokea kwa kuwepo mwengine katikati au bila ya kuwepo mwengine.

6) Kutokea kwa harakati tafauti kutoka katika kitu ambacho hakitokei kutoka kwake ila kitu kimoja, basi hilo ni kuyakusanya mambo mawili yenye mgongano.

Halafu akaja katika paragraph ya pili akazungumzia maneno yenye nukta hizi:

1) Wa mwanzo huwa anaujua ugunduzi wake na kuijua nafsi yake.2) Kwa kuizingatia akili yake ya mwanzo, basi imetokea akili kutoka kwake.3) Kwa kuzingatia kujifahamu yeye mwenyewe, imetokea kwake nafsi.4) Mambo haya yote hayana dalili bali ni batili.5) Lakini hakuna jawabu juu ya kuwa misingi yake ni batili: misingi yake ni

sahihi.

Halafu akaendelea na falsafa zake na za wengine, hadi akaja katika mas-ala ya علة illa (Sababu) na معلول ma’aluul (kilichosababishwa), na kwamba je kilichosababishwa kinatokea kabla ya kutimia sababu au vipi? Kisha

382

Page 383: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

akalibomoa dai la wale waliosema kwamba chenye kusababishwa kinaambatana na sababu ambao walitoa mfano wa jiwe lenye kuanguka na msafiri anayekata masafa kwenda katika mji. Naye akawajibi kwamba mifano hii inawiyana na fikra ya wale wenye kusema kwamba Allah hajawacha kuwa ni mwenye kuleta vitu kimoja baada ya chengine na kwamba kuleta cha pili hakuwi ila baada ya kumalizika cha kwanza. Na kauli ya waliosema kuwa Allah hajaacha kuwa ni mwenye kusema akitaka; mwenye kuyafanya ayatakayo; na kwamba kumalizika cha pili sharti yake ni kumalizika cha kwanza na cha kwanza kikimalizika basi muathir (illa au sababu) iliopelekea kuwepo cha pili inakuwa imepatikana.

Kisha baada ya falsafa hizo, ndio Ibn Taymiyya akataja hayo maneno ulioyanukuu bila ya kuyakamilisha vizuri. Kwa hivyo, inawezekana ikawa hayo ni maelezo yake na inawezekana ikawa yeye anatoa natija ya kauli mbili hizo za mwisho. Na kwa hivyo, kaanza na maneno: فكل هذا وعلى(Na kwa msingi huu, basi kila…..) .

Lakini baada ya yote hayo, katika kuijadili jawabu hio, ningependa kusimama na Sheikh Kasim bin Mafuta katika visimamo vyengine vifuatavyo:

Mosi: kwa kuanzia natuitazame ibara yako uliposema: “maneno ya uwongo yaliyojaa chuki dhidi ya mwanachuoni huyu mkubwa wa kiislamu, si kweli kwamba itikadi ya Ibn Taymiyya ni kuwa ulimwengu una sifa ya kutangulia”. Mwisho wa kunukuu. Nadhani Sheikh Kasim Mafuta kasoma kitabu changu Kisimamo kwani yeye mwenyewe kakinukuu. Na kwa hivyo, natarajia kwamba atakuwa amejua nini hasa ninachokizungumzia. Kwa ajili ya kuweka wazi, natunukuu nilioyasema katika kitabu hicho kuhusu suala hili. Nilisema:

Anasema Ibn Taymiya:-

وم الحديث أهل أكثر يج �وأما ال فإنهم وافقهم ح � النعلون �ن بل � وع ادثابي �ويف ما � قدي ن���رقون

أفراده حدوث من الفرد وحدوث النوع

Ama waliowengi katika watu wa Hadithi na walioafikiana nao hawaifanyi AINA kuwa ni kitu kilichozuka bali ni kitu kilichotangulia, na wanatafautisha baina ya kuzuka kwa AINA na kuzuka kwa sehemu za AINA .1208

1208 - Ibn Taymiyya Muwaafaqatu Sariihi Al-Ma’aquul Li-Sahihi Al-Manquul kilichochapishwa pamoja na Minhaju Al-Sunna j. 2, uk. 75.

383

Page 384: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Kwa hivyo, lau Sheikh Kasim alilitazama andiko hili muqayyad liliomo katika kitabu changu Kisimamo, asingelipata tabu katika kuyafahamu maandiko yangu mutlaq yaliomo katika kitabu changu Hoja Zenye Nguvu. Kwa ufupi ni kuwa nilichodai ni kuwa Ibn Taymiyya ana itikadi ya kutangulia kwa AINA ya ulimwengu.

Pili: ni kuwa Sheikh Kasim kanizulia kitu ambacho sikukisema. Yeye kasema hivi:

Je kwa maneno haya ya Ibn Taymiyya umefahamu kwamba ana itikadi ya kuwepo Mungu zaidi ya mmoja kama anavyodai ndugu Juma kuwa sheikhul islam Ibn Taymiyya ana itikadi hiyo? Au umefahamu kwamba ndugu Juma si mkweli?

Mimi sikusema kwamba Ibn Taymiyya ana itikadi hio, bali nilichokisema ni hiki: “Je haoni yeye huyu Ibn Taymiyya kuwa falsafa hii inapelekea kurudi kwenye itikadi ya kuwepo kwa Mungu zaidi ya mmoja?”.1209 Sijui maneno haya unayafahamu ewe Sheikh Kasim bin Mafuta? Kama huyafahamu basi mimi sikulaumu kwa kusema kwako kuwa Allah ana viungo, maana utakuwa si mtu mwenye kufahamu.

Tatu: naturudi tena katika nukulu uliotupa ya Ibn Taymiyya akisema:

المختص – سبحانه - و����وه يكن لم أن بعد آئنك حادث الرب سوى ماكل ية�واألزل بالقدم

يزل لم أنه قدر وإن قديم مفعوالته فى فليس , شيئ معه وليس فاعالفى ليس بل, بقدمه قديم

الخالق وحده وهو- سبحانه –هو إال قديم ال بل, ألبته قديم المفعوالت ما كلو سواه ما لكل

26 الزمر))” شيئ لك خالق الله- ((سبحانه (( –قال ماك مخلوق سواه تعارض درء/272

والنقل العقل

“KILA KISICHOKUWA MOLA NI CHENYE KUZUKA KIMEPATIKANA BAADA YA KUTOKUWEPO, na yeye (Allah) –Sub’hanah- ndiye mwenye kuhusishwa na kutangulia na azal, hakuna kitu katika viumbe vyake kilichokuwa ni chenye kutangulia, hata kama ikikadiriwa kuwa yeye (Allah) hakuacha kuwa ni mwenye kutenda, (lakini) hakuna kitu kilichotangulia kwa kutangulia kwake, bali hakuna kabisa katika viumbe (vyake ambavyo ) ni vyenye kutangulia, BALI HAKUNA KILICHOTANGULIA ILA YEYE (ALLAH) – Sub’haanah-. Na yeye pekeyake ndiye mwenye kukiumba kila kisichokuwa yeye, kila

1209 - Juma Al-Mazrui Hoja Zenye Nguvu uk. 23.

384

Page 385: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kisichokuwa yeye ni chenye kuumbwa kama alivyosema - Sub’ahaanah-: ((Allah ni muumba wa kila kitu))”. Surat Zumar aya ya 26.

Maneno haya, hata tukijaalia kuwa ni ya Ibn Taymiyya, hayajaonesha kwamba Ibn Taymiyya anapinga kutangulia kwa AINA ya ulimwengu. Bali maneno haya yanaonesha kwamba yeye anasema kwamba hakukuwa na kitu kilichomtangulia Allah, yaani حادثة النوع sehemu za AINA ni) أفرادzenye kuzuka), قديم Na AINA ya ulimwengu una sifa ya) والنوعkutangulia), kama yeye mwenyewe anavyobainisha katika sehemu nyengine tutazozinukuu.

Nne: Sh. Kasim Mafuta kaeleza kwamba Ibn Taymiyya kasema kwamba kila kitu ambacho si Allah basi hicho si qadim (chenye sifa ya kutangulia) bali ni muhdath, makhluq (kimezuka, kimeumbwa), lakini hakuweza kuthibitisha kwamba yale nilioyasema mimi ya kwamba Ibn Taymiyya kasema kwamba AINA YA ULIMWENGU INA SIFA YA KUTANGULIA, ni ya uwongo: Ibn Taymiyya hakuyasema. Na kwa hivyo, ikiwa Ibn Taymiyya hiki nilichokinukuu mimi kakisema kweli na kile alichokinukuu Kasim Mafuta – japo kuwa kakibutua na hakiko wazi kwamba msemaji ni Ibn Taymiyya – kakisema kweli, je mwongo ni nani? Ni mimi au ni Kasim Mafuta au ni sote wawili? Kwanini mimi niwe mwongo wewe usiwe mwongo na nilichokinukuu mimi kimo katika vitabu vyake, kama nitavyokupa ushahidi wa ziada?

Tano: Sheikh Kasim Mafuta kashindwa kujua kwamba maneno ya binaadamu – kama yalivyo maneno ya Allah na Mtume wake – yana عموم (ujumla) na خصوص (uhusishaji). Mara ngapi utasikia mtu akisema “watu wote wamekweda msikitini”. Halafu utamsikia mtu huyo huyo anakwambia “Kombo hakwenda msikitini”. Maneno kama haya hufasiriwa kuwa yana Na maana ni kuwa watu wote .(uhusishaji) خصوص na (ujumla) عمومwamekwenda msikitini isipokuwa Kombo. Wala atayesema kuwa fulani kasema kuwa Kombo hakwenda msikitini haambiwi kuwa kasema uwongo kwa sababu katika ibara nyengine kasema “Watu wote wamekwenda Msikitini”. Naomba Bwana Mafuta kwanza uufahamu msingi huu. Halkadhalika Allah aliposema: “Allah anakuusieni katika watoto wenu mwanamme apate fungu la wanawake wawili” ni ujumla ambao Mtume (s.a.w.) haumuhusu kwa sababu ya kuwepo andiko خاص (mahususi) lenye kumtoa yeye aliposema “Sisi Manabii haturithiwi….”.

Sita: ni kuwa Maulamaa wengi wa zamani na wa karibuni wamelizungumzia suala hilo na kuonesha kutokukubaliana kwao na Ibn

385

Page 386: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Taymiyya juu ya suala hilo. Kama ilikuwa suala hilo halipo basi wanavyuoni hao wasingelilizungumzia kamwe.

Saba: ni kuwa Wanavyuoni wafuasi wa Ibn Taymiyya hawakupinga kwamba Ibn Taymiyya kweli kasema hivyo, lakini wamedai kuwa kajitahidi na akakosea. Kwa hivyo, kupinga kwa Sh. Kasim Mafuta hakuna uzito wowote ule.

Nane: ni kuwa miongoni mwa wafuasi wake wako waliomrudi Ibn Taymiyya kwa itikadi yake hio. Miongoni mwa hao ni Al-Albani kama tutavyomnukuu baadae.

NATUINGIE KWENYE MAUDHUI

Hizo ni nukta muhimu za kuzizingatia katika mas-ala haya. Baada ya hayo sasa natuingie kwenye maudhui. Tunasema: kwa ufupi, ni kuwa nilichokidai mimi ni kuwa Ibn Taymiyya kasema kuwa AINA ya ulimwengu ina sifa ya kutangulia (qadim). Kilichobaki ni:

a) Kujua nini maana ya AINA ya ulimwengu.b) Kunukuu maandiko ya Ibn Taymiyya ambayo kasema hivyo

kwamba Aina ya ulimwengu ina sifa ya kutangulia.

Ama kuhusu suala la kwanza ni kuwa maana ya AINA (NAW’U) ni kuwa vitu vinagawika katika sehemu tatu:

1) Jinsi. Na katika jinsi kuna:2) Aina. Na katika aina kuna.3) Afraad (sehemu za Aina).

Kwa mfano neno gari. Gari ni jinsi.1210 Na katika jinsi hii kuna aina tafauti kama vile (Toyota, Mazda n.k. au Saloon, Bus n.k). Na katika aina ya Saloon kuna afraad (sehemu za aina). Kwa mfano, Saloon yangu sio yako; na yako si ya Ali.

Sasa anachokizungumzia Sheikh Al-Islaam, Ibn Taymiyya, ni kuwa ikiwa utaizingatia Saloon yangu ambayo ni fard (sehemu ya aina) basi utaikuta kwamba ina siku ilioundwa; lakini ukiwa utazungumzia Naw’u (AINA) za

1210 - Na unaweza kuvizingatia vyombo vya usafiri kwa ujumla kuwa ndio jinsi na gari ikawa ni aina, na toyota ikawa ni afraad (sehemu za aina).

386

Page 387: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

gari hio (Saloon au Toyota) basi utakuta kwamba hazina mwanzo kwani kabla ya kila Saloon kuna Saloon nyengine!

Huo ni mfano wa kuiweka wazi – katika akili – picha ya nini Mzee wa Uislamu anazungumzia. Sasa ondoa neno Saloon na Toyota katika mfano huo na badala yake weka neno viumbe. Utapata kwamba ukichukua kiumbe kimoja kimoja yaani Afraad (sehemu za viumbe) basi utakikuta kwamba kila kiumbe kina mwanzo, lakini ukiwa utazungumzia maumbile kwa ujumla basi utakuta kwamba hayana mwanzo kwani kabla ya kila kiumbe kuna kiumbe, kama Ibn Taymiyya mwenyewe alivyosema: “Kabla ya kila wakati basi kuna wakati mwengine”.1211 Na hii kama unavyoona inakaribia kuwa ni Theory of Evolution, hususan ukiyachukua maelezo yake alioyatoa katika Naqdu Al-Maraatib, kwamba kitu kadha kimetokana na kitu kadha na kitu kadha kimetokana na kitu kadha. 1212

Baada ya hayo, sasa natutazame baadhi ya nukulu za Ibn Taymiyya alizozungumzia kutangulia kwa AINA ya ulimwengu. Anasema Al-Imamu Ibn Taymiyya:

وافقهم ومن الحديث أهل أكثر بل وأما حادثا النوع يجعلون ال فإنهمبي قديما ن �������ويفرقون

أفراده من الفرد وحدوث النوع دوام حدوث بين العقالء جمهور يفرق كماواحد ودوام النوع

.... أعيانه من

Ama waliowengi katika watu wa Hadithi na walioafikiana nao hawaifanyi AINA kuwa ni kitu kilichozuka bali ni QADIM (kitu kilicho tangulia), na wanatafautisha baina ya kuzuka kwa AINA na kuzuka kwa sehemu za AINA kama vile ambavyo jumhur ya watu wa akili (wanafalsafa) wanavyotafautisha baina kudumu kwa AINA na kudumu kwa moja katika sehemu zake.1213

Hayo ndio maelezo ya Ibn Taymiyya katika kitabu chake hicho Bayanu Muwafaqati Sarihi Al-Maaqul. Utaona kwamba:

1) Kawanasibishia watu wa Hadithi kitu ambacho hawakukisema. Vyenginevyo tutajieni wanavyuoni wengi wa Hadithi waliosema hivyo.

1211 - Tutayanukuu maneno yake karibu na kukupa marejeo. 1212 - Naqdu Maratibi Al-Ijmaa cha Ibn Taymiyya kilichochapishwa pamoja na kitabu Maratibu Al-Ijmaa cha Ibn Hazm uk. 304-5. Daru Ibn Hazm, chapa ya kwanza 1419 A.H, 1998 A.C. 1213 - Ibn Taymiyya Bayanu Muwafaqati Sarihi Al-Maaqul Lisahihi Al-Manquul kilichochapishwa pamoja na Minhaju Al-Sunna j. 2, uk. 75.

387

Page 388: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

2) Kasema kwamba AINA ya ulimwengu ina sifa ya kutangulia. 3) Kisha akapiga mfano wa makusudio ya kutangulia huko kwamba ni

kama vile ambavyo watu wa filosofi (aliowaita watu wa akili) wanavyotafautisha baina ya kudumu kwa AINA pasina kudumu kwa kila moja katika sehemu zake. Yaani – kama alivyosema Ibn Taymiyya mwenyewe – neema za peponi – kwa mfano – ni AINA ambayo inadumu milele lakini hii haina maana kwamba kila neema moja iliomo humo itadumu: bali kitachodumu ni aina ya neema, yaani kitachodumu ni neema kwa ujumla, ama sehemu za aina hio ya neema zitakwisha!

Kwa ujumla ni kuwa anachokieleza Ibn Taymiyya hapa ni chain of creation (silsila ya maumbile) kwamba maumbile hayana mwanzo kila kitu kimoja kimetokana na chengine, hivyo hivyo hadi kufikia pasipo ukomo, pamoja na kuwa kitu kimoja kimoja kinaanza na kutoweka. Sasa Muumbaji ni nani? Suali bado lipo pale pale na uwezekano wa itikadi hii kuishia katika polytheism (itikadi ya miungu mingi) upo sana!

Kisha katika kitabu chake Naqdu Maratibi Al-Ijmaa akatoa mifano yenye kuthibitisha itikadi yake ya chain of creation (silsila ya maumbile). Akatoa mfano wa mbingu kuwa zimeumbwa kutokana na moshi na watu na majini kutokana na mada (matter).1214

Na kwa sababu hio ya kuamini kwamba AINA ya ulimwengu ina sifa ya kutangulia, ndio maana akampinga Ibn Hazm katika mambo yafuatayo:

Mosi: Ibn Hazm kasema kwamba Umma umekubaliana kwamba Allah katika enzeli1215 alikuwa peke yake wala hakuna kitu isipokuwa Yeye na kwamba atayesema kinyume na hivyo basi huyo ni kafiri. Ibn Taymiyya akampinga, akasema:

Na ajabu kuliko hilo ni kusimulia kwake makubaliano ya kumkafirisha anayepinga kwamba Allah hajaacha kuwa peke yake wala hakuna kitu isipokuwa Yeye. Kisha akaumba vitu kama alivyotaka. Na inaeleweka kwamba ibara hii haimo katika Kitabu cha Allah, wala hainasibishwi na Mtume.1216

1214 - Ibn Taymiyya Naqudu Maratibi Al-Ijmaa’i kilichochapishwa pamoja na Maratibu Al-Ijmaa’i cha Ibn Hazm uk. 304-305. 1215 - Enzeli ndio lugha tuliowakuta nayo wazee wa Kipemba wakiitumia, wakimaanisha azal (pasina mwanzo). 1216 - K.h.j., uk. 303.

388

Page 389: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Pili: Kisha baada ya hapo, Ibn Taymiyya akanukuu Hadithi iliosimuliwa na Al-Bukhari isemayo:

... ... معه شيء وال غيره شيء وال قبله شيء وال الله كان

Allah alikuwepo wala hakukuwa na kitu chochote kabla yake…wala hakukuwa na kitu chochote kisichokuwa Yeye…..wala hakuna kitu chochote pamoja naye. 1217

Kisha lafdhi mbili hizi, lafdhi isemayo: غيره شيء wala hakukuwa) ...والna kitu chochote kisichokuwa Yeye), na lafdhi isemayo: معه شيء وال(wala hakuna kitu chochote pamoja naye), akazikataa na akaipa nguvu lafdhi inayosema: قبله شيء وال الله Allah alikuwepo wala) كانhakukuwa na kitu chochote kabla yake), kwa hoja kwamba lafdhi hii ndio inayokubaliana na dua ya Mtume (s.a.w.) na kwamba lafdhi nyengine zimepokelewa kimaana tu.1218 Sasa jiulize wewe ni kitu gani kilichomfanya Ibn Taymiya azikatae lafdhi mbili hizo ilhali:

1) Zimekuja kwa sanad sahihi.2) Hazigongani na lafdhi alioisahihisha yeye wala hazigongani na Qur-

ani wala Sunna wala makubaliano ya Umma?Sababu ni kuwa kusema kwamba (Allah alikuwepo wala hakukuwa na kitu chochote kisichokuwa Yeye…..wala hakuna kitu chochote pamoja naye) – kama zinavyosema lafdhi mbili hizo – kunagongana na itikadi yake ya kutangulia kwa العالم yaani maumbile ,(Aina ya ulimwengu) نوعyasiokuwa na mwanzo. Kwa maneno mengine ni kuwa Ibn Taymiyya hakubali kwamba kulikuwa na kitu kabla ya Allah, lakini anakubali au anaitakidi kwamba kulikuwa na kitu pamoja na Allah kama utavyoona moja ya nukulu zake inavyosema kwamba kuweko kwa kitu pamoja na Allah hakujakataliwa na Sharia wala akili bali huo ni katika ukamilifu wake Allah!

Baada ya hayo, sasa soma maneno mengine ya Ibn Taymiyya kama yalivyonukuliwa na Sheikh ‘Abdullah Al-Harari katika kitabu chake Al-Maqalatu Al-Sunniya.1219 Anasema Ibn Taymiyya:

ولم لها أول ال بحوادث مسبوقا اليومي الحادث يكون بل نسلم ال؟ : جائز غير ذلك إن قلتم

1217 - K.h.j., uk. 304. 1218 - K.h.j., uk. 304. 1219 - Elewa kwamba pamoja na kuwa maneno haya nimeyanukuu kutoka kwa Sh. Abdullah Al-Harari, lakini nimevirejea vitabu vyote alivyovitaja ambavyo ninavyo na sikuona tafauti hata ya herufi moja. Vitabu vyengine utaona kuna tafauti ya marejeo kwani baada ya kuvirejea nilitegemea kitabu nilichonacho, na nukulu nyengine nimeongeza kidogo.

389

Page 390: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

…Hatukubaliani (na hayo), bali (ukweli ni kuwa) chenye kuzuka leo, basi kimetanguliwa na vyenye kuzuka visivyo na mwanzo! Na kwanini mukasema kwamba hilo halijuzu?1220

Anaendelea Ibn Taymiyya:لها؟...... أول ال الحوادث امتناع القرآن في وأين

Na kuko wapi katika Qur-ani kupingwa kwa kuwepo vilivyozuka (vitu) ambavyo havina mwanzo?1221

Aasema Ibn Taymiyya:

أزليا العالم من شيء كون فيمتنع من وحينئذ نوع يكون أن جاز وإنف��إن يزل، لم دائما العالم

آخر وقت وقبله إال وقت من ما بل محدد شيء عن عبارة هو ليس األزلدوام من يل������زم فال

بعينه شيء قدم ما ف النوع بل محدد شيء عن عبارة هو ليس األزل إنوقب إال يقدر وقت له ���من

قدم يمتنع قيل وإنما بعينه شيء قدم النوع دوام من يلزم فال آخر وقتبعينه شيء

Basi kwa hivyo, haitowezekana kwa kitu chochote katika ulimwengu kuwa ni cha enzeli (kisichokuwa na mwanzo), pamoja na kuwa inajuzu ikawa AINA ya ulimwengu ni yenye kudumu, yenye enzeli (pasina mwanzo), hakika ya enzeli si maana yake kwamba kitu hakina mipaka, bali HAKUNA WAKATI WOWOTE ULE ISIPOKUWA KABLA YAKE KUNA WAKATI MWENGINE, BASI KUDUMU KWA AINA HAKUMAANISHI KUWA LAZIMA KITU MAALUMU KIWE KIMETANGULIA!!! Kwani enzeli si maana yake kitu chenye mipaka, BALI HAKUNA WAKATI WOWOTE ULE UTAOKADIRIWA ILA KABLA YAKE KUNA WAKATI MWENGINE, BASI KUDUMU KWA AINA 1222 HAINA MAANA KWAMBA KITU MAALUMU (SEHEMU YA AINA) KINA SIFA YA KUTANGULIA, BALI IMESEMWA KWAMBA KISICHOKUBALIKA NI (KUSEMA KWAMBA) KITU MAALUMU KINA SIFA YA KUTANGULIA (SIO KUSEMA KWAMBA AINA YA KITU INA SIFA YA KUTANGULIA). 1223

Sheikh Mafuta upo? Sijui umeyafahamu maneno haya ya Ibn Taymiyya? Kama tulivyosema kwamba itikadi ya Ibn Taymiyya ni kuwa AINA ya

1220 - Ibn Taymiyya Dar-u Al-Ta’aarudh uk. 228. 1221 - Ibn Taymiyya K.h.j. uk. 67. Yaani Ibn Taymiyya anapinga hapa itikadi kwamba viumbe (yaani Aina si Afraad) vina mwanzo.1222 -Yaani kutokuwa na mwanzo kwa aina. 1223 - Ibn Taymiyya Minhaju Al-Sunna j. 1, uk. 109.

390

Page 391: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

ulimwengu ndio yenye sifa ya kutangulia; na sehemu zake ndizo ambazo zina mwanzo na mwisho. Pamoja na kuwa tumepiga mifano huko nyuma lakini huenda ikawa baadhi ya watu hawajafahamu nini hasa anakikusudia Ibn Taymiyya kwa kusema hivyo. Mfano mzuri ni huu alioutoa Ibn Taymiyya mwenyewe hapa aliposema: “HAKUNA WAKATI WOWOTE ULE ISIPOKUWA KABLA YAKE KUNA WAKATI MWENGINE.” Yaani wakati hauna mwanzo, kabla ya saa kulikuwa na saa; kabla ya siku kulikuwa na siku hivyo hivyo hadi kufikia pasipo na ukomo! Na huu bila shaka ni wahmu (makosa) wa Ibn Taymiyya, kwani wakati ni kiumbe kwa hivyo ni lazima kuna siku umeanza tu na kwa hivyo kabla yake hakukuwa na wakati mwengine.

Anaendelea Ibn Taymiyya:

به، متصفا يزل لم لكنه فشيئا شيئا وقدرته بمشيئته يقول من ومنهماآلحاد حادث النوع فهو قديم

أصحاب من وغيرهم الحديث أصحاب أئمة من يقول من ذلك يقول كماوسائ����ر وأحمد الشافعي

الطوائف..

Na miongoni mwao wako wanaosema kwamba (matendo ya Allah yanakuwa) kwa matakwa yake na uwezo wake kitu kimoja baada ya chengine, kwa hivyo Yeye (Allah) tangu enzeli alikuwa akisifika kwayo (matendo),1224 basi hayo (matendo) ni yenye kuzuka ukizingatia (kitendo) kimoja kimoja (lakini) AINA yake ni QADIM (yenye sifa ya kutangulia), kama wanavyosema wenye kusema hivyo, miongoni mwa Maimamu wa watu wa Hadithi na wengineo miongoni mwa wanavyuoni wafuasi wa (Al-Imamu) Al-Shafi na (Al-Imamu) Ahmad na makundi mengine.1225

Hayo ndio maneno ya Ibn Taymiya, nayo kama unavyoona:1) Anathibitisha kwamba AINA ya matendo ya Allah ni Qadim

(yenye sifa ya kutangulia).2) Kama kawaida yake yeye na mwanafunzi wake, kawazulia

wanavyuoni wa Hadithi na wanavyuoni wa Kishafi kuwa wana itikadi hio.

Lakini Sheikh Al-Harari akamjibu kwamba huo ni uzushi. Anasema Sheikh Abdullah Al-Harari baada ya kuyanukuu maneno hayo ya Ibn Taymiyya:

افترى كيف الحديث –كعادته –أننظروا أئمة على الخبيثة المقولة هذهب���ه انفرد شيء وهذا

1224 - Yaani kutenda ni sifa ya Allah ya enzeli (tangu na tangu). 1225 - Ibn Taymiyya Al-Sunna j. 1, uk. 224. Kwa kuifahamu maudhui vizuri anzia ukurasa wa 223.

391

Page 392: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

والفقهاء الحديث أئمة على تقول ولكنه الفالسفة، متأخري به ووافقالشافع��ي أصحاب من

يروج أن أراد لكن ذلك منهم أحد يقل ولم عليهم، وافترى وغيرهم وأحمدبين المفتراة عقيدته

وافق إنه يقال أن عن بنفسه ويربأ األفهام ضعاف على المسلمينالعقيدة هذه في الفالسفة

Tazama namna alivyowazulia Maimamu wa Hadithi – kama kawaida yake – maneno haya machafu; na ilhali jambo hili kapwekeka nalo1226 na kwalo akaafikiana na wanafalsafa wa mwisho mwisho; lakini huo ni uzushi juu ya Maimamu wa Hadithi na Mafakihi miongoni mwa wafuasi wa (Al-Imamu) Al-Shafi na (Al-Imamu) Ahmad na wengineo na akawazulia uwongo, na hakusema hivyo yoyote katika wao, lakini alitaka kuipigia debe itikadi yake ya uzushi kwa Waislamu; kwa wale wenye fahamu dhaifu, na ajiepushe yeye asije akaambiwa kwamba kakubaliana na wanafalsafa katika itikadi hii.1227

Anasema Ibn Taymiyya:

وال شرع ينفها لم المعية فهذه معه يزل لم نوعها أن قدر وإن... كماله من هي بل عقل،

Na ikiwa itakadiriwa kwamba AINA yake – aina ya yaliozuka – haikuacha kuwa pamoja na Allah katika enzeli, basi kuwa pamoja huku hakukukataliwa na Sharia wala akili, bali huko ni katika ukamilifu wake!1228

Sheikh Kasim! Upo? Je Ibn Taymiyya anapinga au anakubali kwamba AINA ya ulimwengu ina sifa ya kutangulia? Hapa itakubainikia ni kwanini Ibn Taymiyya kazikataa lafdhi mbili za Hadithi ya Al-Bukhari: lafdhi inayosema: شيء وال wala hakukuwa na kitu chochote kisichokuwa (Allah alikuwepo) ...غيرهYeye), na lafdhi isemayo: معه شيء wala hakuna kitu chochote) والpamoja naye). Kwani yeye anataka kuthibitisha kuwa mada ya asili (primeval matter), ilikuwa pamoja na Allah ingawa haikuwa kabla ya Allah! Ndio maana hapa akasema:

Na ikiwa itakadiriwa kwamba AINA yake – aina ya yaliozuka – haikuacha kuwa pamoja na Allah katika enzeli, basi kuwa pamoja huku hakukukataliwa na Sharia wala akili, bali huko ni katika ukamilifu wake!

1226 - Kalisema yeye tu. 1227 - Al-Harari Al-Maqaalaatu Al-Sunniya uk. 69-70. 1228 - Ibn Taymiyya Sharhu Hadithi ‘Imraan bin Husain uk. 193, nukulu kutoka katika kitabu Al-Maqaalaatu Al-Sunniya cha Sh. Abdullah Al-Harari uk. 70.

392

Page 393: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Anasema Ibn Taymiyya:

...... النوع الناس من كثير على يشتبه لكن معه يزالون ال والخلقبين....... يفرقوا لم إذ بالعين

معين والحادث الحوادث نوع

Na viumbe hawakuacha katika enzeli kuwa pamoja naye….lakini watu wengi inawatatiza (tafauti baina ya) AINA (ya vitu) na kitu (kimoja) maalamu1229……...kwani hawakutafautisha (watu hao) baina ya AINA ya vyenye kuzuka na (kitu kimoja) maalumu kilichozuka.1230

Anasema Ibn Taymiyya:

يدل فإنما العقلية األدلة من المتفلسفة عند ما أن أيضا يظهر هنا ومنالس������ل�ف مذهب على

(( وأنه (( فاعال، يزل لم الرب أن على العالم قدم في عمدتهم فإن أيض��ا،يص���������ير أن يمتنع

وهذا يكن، لم أن بعد له ممكنا الفعل يصير وأن يكن لم أن بعد فاعالب�������ه احتجوا ما وجميع

على يدل الفعل إنما نوع قدم

Na kuanzia hapa inabainika vile vile kwamba ile (fikra) walionayo wanafalsafa itokanayo na ushahidi wa kiakili, ndio vile vile inayooneshwa na madhehebu ya Al-Salaf (watangulizi), kwani tegemeo lao katika ((kutangulia ulimwengu)) ni kwamba Mwenyezi Mungu hakuwacha kuwa ni mwenye kutenda tangu enzeli na kwamba haiwezekani kwamba (Allah) awe ni mwenye kutenda baada kuwa si mwenye kutenda, na kwamba kitendo (sasa) kiwe ni chenye kuwezekana kwake baada ya kuwa kilikuwa hakiwezekani, na (hoja) hii na hoja zote walizotoa zinaonesha KUTANGULIA KWA AINA YA VITENDO (VYA ALLAH). 1231

Kisha Ibn Taymiyya akaidhoofisha itikadi kwamba AINA ya viumbe ina mwanzo, akasema:

: : يزل لم يكن، لم أن بعد كائن حادث العرش يقال أن الرابع الوجهوج���وده، بعد عليه مستويا

قد لها أول ال حوادث امتناع على ودليله نوعه في فالكالم الخلق وأماضعفه عرف

1229 - Ibn Taymiyya Sharhu Hadithi ‘Imraan bin Husain uk. 193, nukulu kutoka katika kitabu Al-Maqaalaatu Al-Sunniya cha Sh. Abdullah Al-Harari uk. 70. 1230 - Ibn Taymiyya Sharhu Hadithi Nnuzuul uk. 161, nukulu kutoka katika kitabu Al-Maqaalaatu Al-Sunniya cha Sh. Abdullah Al-Harari uk. 70. 1231 - Ibn Taymiyya Majmuu’a Al-Fatawa j. 6, uk. 300. Al-Subki kampinga Ibn Taymiyya kwa kauli yake hii. Tazama Al-Saifu Al-Saqil uk. 18.

393

Page 394: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Njia ya nne: Ni kuwa isemwe kwamba ‘Arshi ni yenye kuzuka: yenye kuwepo baada ya kuwa haikuwepo, (Naye Allah) hajaacha kuwa mwenye kukaa juu yake baada ya kuwepo kwake (hio ‘Arshi); Ama viumbe maelezo kuhusu AINA yao na dalili yake juu ya kutowezekana (kuwepo kwa) vyenye kuzuka (viumbe) ambavyo havina mwanzo imeonekana udhaifu wake!!! 1232

Baada ya hayo, itakubainikia kwa uwazi kwamba:1) Ibn Taymiyya anasema kwamba kila kisichokuwa Allah ni kiumbe

cha Allah.2) Anajikanganya mwenyewe kwa itikadi yake ya chain of creation

(silsila ya maumbile) – maumbile yasiokuwa na ukomo! 3) Afraad (sehemu) za AINA si qadim (si zenye sifa ya kutangulia).4) AINA ya ulimwengu ni qadim (wenye sifa ya kutangulia). Yaani kila

kiumbe kimetokana na chengine hivyo hivyo bila ya kuwa na mwanzo!

5) Kwa itikadi hii, kapata lawama sana kutoka kwa wanavyuoni wengi wa Umma.

WANAVYUONI WALIOLIZUNGUMZIA JAMBO HILO LA ITIKADI YA IBN TAYMIYYA YA KUTANGULIA

KWA AINA YA ULIMWENGU

Baada ya hayo machache katika mengi yalionenwa juu ya suala hili, sasa natutazame wataalamu wawili watatu waliomrudi Ibn Taymiyya kwa itikadi yake hio:

1) Ibn Daqiq Al-’Iid. Huyu kamjibu Ibn Taymiyya katika suala hilo la kuwa Aina ya ulimwengu una sifa ya kutangulia, kama alivyonukuliwa na Al-Sayyid Al-Saqqaaf.1233 Anasema Ibn Daqiq:

1232 - Ibn Taymiyya Al-Tafsiru Al-Kabir j. 6, uk. 113, katika tafsiri ya Suratu Al-A’alaa. 1233 - Al-Saqqaaf Al-Salafiyya Al-Wahaabiyya uk. 133.

394

Page 395: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

أن هنا وقع فظن الفلسفة إلى ويميل المعقوالت في الحذق يدعي منحدوث ف���ي المخ����الف

.......... يكفر ال العالم

Katokea hapa yule ajidaie ubingwa katika mambo ya kiakili naye anaelemea katika falsafa akadhani kwamba mwenye kupinga kuzuka kwa ulimwengu hakafirishwi…….1234

2) Dr. Muhammad Al-Buti. Kalizungumzia suala hili katika kitabu chake Al-Salafiyya akanukuu kile alichokisema Ibn Hazm katika Maratibu Al-Ij’maa’i, kisha akanukuu upinzani uliotolewa na Ibn Taymiyya kisha akasema:

حزم، ابن كالم في جاء ما على وإنكارا تعليقا بطوله، تيمية ابن كالم هذاق���د اإلجماع أن من

خلق انعقد ثم معه، غيره شيء وال وحده يزل لم تعالى الله أن على. شاء كما كلها األشياء

هذه في والفالسفة الكالم علماء من طوائف يقرره ما بيان في أطال ثمإلى لينت���هي المسألة،

قديمة ولكنها والجزئيات بالعين حادثة األشياء أن من الفالسفة يقرره ماوسلس������لة بالن��وع

التوالدات......

Haya ni maneno ya Ibn Taymiyya akitia maelezo na kuyapinga maneno ya Ibn Hazm kwamba pamekuwa na makubaliano (ya Umma) kwamba Allah alikuwepo hapo enzeli wala hakuna kitu chochote pamoja naye isipokuwa Yeye, kisha akaumba vitu vyote kama alivyotaka.

Kisha akarefusha (Ibn Taymiyya) katika kuyaelezea yale yakubaliwayo na watu wa ‘ilmu al-kalaam na wanafalsafa katika mas-ala haya, na hatimae akaishia kwa kile wanachokikubali wanafalsafa kwamba vitu ni vyenye kuzuka kwa (kuzingatia) kitu kimoja kimoja na sehemu zake; lakini kwa (kuzingatia) AINA na mnyororo wa kuzaana (chain of creation) basi (vitu) ni vyenye sifa ya kutangulia.1235

3) Ibn Hajar Al-Haitami. Anasema kuhusu Ibn Taymiyya na itikadi hio ya kwamba AINA ya ulimwengu ina sifa ya kutangulia:

1234 - Tazama Ibn Hajar Al-Fat-hu j. 12, uk. 202. Nukulu kutoka katika Al-Salafiyya Al-Wahaabiya uk. 133, na Al-Harari Al-Maqaalatu Al-Sunniyya uk. 72. 1235 - Dr. Muhammad Said Ramadhan Al-Buti Al-Salafiyya Marhala Zamaniyya Mubaaraka: La Madh-habun Islamiyya uk. 164-173. Hapa kuna maelezo mengi na muhimu nimeyawacha kwa kuhofia kurefusha.

395

Page 396: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

فجعله ………... ؛ دائما مخلوقا الله مع يزل ولم ، بالنوع قديم العالم وأنبالذات �������موج با

باالختيار فاعال ...ال

Na (kusema kwake Ibn Taymiyya) kwamba: ‘AINA ya ulimwengu ni yenye kutangulia” na haujawacha (ulimwengu) kuwa ni kiumbe daima. Basi (Ibn Taymiya) akamfanya (Mungu) kuwa Dhati yake ni mwenye kuwajibikiwa (mwenye kulazimishwa) si mwenye kufanya (mambo) kwa khiari yake.1236

4) Al-Qannubi. Anasema:

شيء.... (( يكن ولم الله كان حديث رد عندما الحراني الشيخ صنع كمارواه)) ال��������ذي غيره

البخاري ( وقوله) 3191اإلمام العكر لمشربه مخالفا رآه حين وغ������يره : إن القائ�����ل النكر

.... كثير عليه رد وقد ثابتة صحيحة الرواية هذه أن مع بالنوع قديم العالم..... ذلك بسبب العلماء من

….Kama alivyofanya Sheikh Al-Harrani (Ibn Taymiyya) alipoikataa Hadithi isemayo: (( غيره شيء يكن ولم الله Allah alikuwepo“ ((كانwala hakukuwa na kitu chochote isipokuwa Yeye” ambayo kaipokea Al-Imamu Al-Bukhari na wengineo, alipoona (Ibn Taymiyya) kwamba (Hadithi hio) inakwenda kinyume na fikra yake chafu na kauli yake mbaya yenye kusema kwamba: ‘AINA ya ulimwengu ni qadim (ina sifa ya kutangulia).1237

Sh. Abdullah Al-Harari. Huyu tumetaja nukulu zake nyingi kabla, na hapa tunanukuu maneno yake yanayosema:

والح�����ديث للقرآن مخالف العالم نوع بأزلية تيمية ابن فقولاألم����ة وإج�����ماع والص�����ريح

العقل وقضية

Basi kauli ya Ibn Taymiyya kwamba AINA ya ulimwengu ni ya enzeli (haina mwanzo) ni kinyume na Qur-ani, Hadithi ya wazi, makubaliano ya Umma na akili.1238

Al-Subki. Huyu kanukuliwa na Sheikh Al-Harari akiyataja – katika kitabu chake Al-Durra Al-Mudhiyya – mambo ambayo Ibn Taymiyya kenda 1236 - Tazama kitabu Al-Fatawa Al-Haditha  uk. 116. 1237 - Imamu Al-Sunna wa Al-Usuul wa Al-Furu’i, Al-Qannubi Al-Saif Al-Haad uk. 183, chapa ya tatu 1417 A.H. 1238 - Al-Harari Al-Maqaalatu Al-Sunniyaa uk. 73.

396

Page 397: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kinyume na ijmaa (makubaliano); na miongoni mwa hayo ni kauli hio ya kutangulia kwa ulimwengu – yaani Aina ya ulimwengu.1239

Al-Albani: anasema:

محاوال الفالسفة على رده في الكالم الله رحمه تيمية ابن أطال ولقدح ل ����إثبات أول ال ها،���وادث

العقول، فيه تحار بما ذلك أثناء في حت وجاء القلوب، أكثر تقبله ى����والخص �اتهم بأن ���ه ه ���ومه

ال قديمة المخلوقات بأن من يقول ما بأن يصرح و يقول أنه مع لها، أولمسبوق وهو إال مخلوق

لكنه و ، . بالعدم كما له بداية ال ما إلى الحوادث بتسلسل يقول ذلك معبتسلسل غيره و هو يقول

مقبول غير منه القول فذلك نهاية، ال ما إلى الحوادث

Na kwa hakika Ibn Taymiyya – Allah amrehemu – amezungumza kwa urefu akiwarudi wanafalsafa akijaribu kuthibitisha matukio (viumbe) yasiokuwa na mwanzo na katika hayo kaleta mambo ambayo akili zinaemewa, na nyoyo nyingi haziyakubali mpaka wapinzani wake wakamtuhumu kwamba anasema kwamba viumbe vina sifa ya kutangulia havina mwanzo pamoja na kwamba yeye kasema kwa uwazi kwamba hakuna kiumbe chochote isipokuwa kimetanguliwa na kutokuwepo (mwanzo kilikuwa hakipo), lakini pamoja na hayo yeye anaitakidi kuwepo kwa silsila ya viumbe (chain of creation) ambavyo havina mwanzo, kama vile ambavyo yeye na wengine wanaitakidi kuwepo kwa silsila ya viumbe visivyo na mwisho, basi kauli yake hio haikubaliki.1240

Kwa hivyo, tukirudi katika maelezo ya Sheikh Kasim Mafuta aliposema:

Maneno yote haya ya ndugu Juma ni maneno ya uwongo yaliyojaa chuki dhidi ya mwanachuoni huyu mkubwa wa kiislamu, si kweli kwamba itikadi ya Ibn Taymiyya ni kuwa ulimwengu una sifa ya kutangulia.

Ninamwambia kwamba:1) Maneno hayo si uwongo, bali ni ukweli mtupu kama

tulivyomthibitishia vya kutosha. 2) Hakuna kitu chuki kabisa bali kuna kuwahadharisha Waislamu

kutokana na mtu mwenye itikadi batili. Huu ni wajibu wangu wa Kisharia, kwani kuwahadharisha watu kutokana na bidaa na watu wa bidaa ni jambo la lazima, na bila shaka Ibn Taymiyya kaleta bidaa nyingi katika dini, tena bidaa dhalala kabisa!

1239 - Al-Harari Al-Maqaalatu Al-Sunniyaa uk. 13. 1240 - Al-Albani Al-Sahiha j. 1, uk. 258, maelezo ya Hadthi na. 133.

397

Page 398: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

3) Maulamaa wengi mno wa madhehebu zote za Kiislamu wamemjibu Ibn Taymiyya kwa sababu ya itikadi yake hio kama tulivyowanukuu wawili watatu na kama tutavyowataja wengine wengi baadae. Wala si sahihi kwamba wanavyuoni hao wote wamchukie Ibn Taymiyya bure bure.

4) Hayo hayakusemwa na Ibn Taymiyya tu, bali hata wafuasi wengine wa skuli ya tajsim kama vile mshereheshaji wa Al-‘Aqiidatu Al-Tahaawiyya anasema:

: ممتنع، الحوادث دوام إن قالوا فإنهم الجهمية، من الكالم هذا وأصلللحوادث يكون أن يجب وإنه

- - لم وجل عز الباري يكون أن فيمتنع لها، أول ال حوادث المتناع مبدأ؛بمشيئة، متكلما فاعال يزل

ممتن الممتنع على القدرة ألن ذلك، على قادرا يكون أن يمتنع عة !������بلعلى يدل فإنه فاسد، وهذا

يكن امتناع لم أن بعد حدث إذا والحادث حادث، وهو العالم حدوثممكنا، ������مح يكون أن بد فال دثا

فيه، ثابت واإلمكان إال يقدر وقت من وما محدود، وقت له ليس واإلمكانإلم �����فل الفعل ����يس كان

جائزا ممكنا الفعل يزل لم أنه فيجب إليه، ينتهي مبدأ وصحته وجوازهل أنه فيلزم يزل ���صحيحا، م

. ألولها نهاية ال حوادث جواز فيلزم عليه، قادرا الرب

Na asili ya maneno haya ya Al-Jahmiyya ni kuwa wao walisema kwamba kudumu kwa viumbe haiwezekani na kwamba hakuna budi kwamba viumbe lazima vitakuwa na mwanzo kwani ni muhali kuwa viumbe havina awali, kwa hivyo, haiwezekani kuwa Allah alikuwa ni mwenye kutenda na kusema kwa matakwa yake, bali haiwezekani kuwa alikuwa ni mwenye kuweza,1241 kwani haiwezekani kuwa kuwe na uwezo juu ya kisichowezekana.

Na haya yote ni batili, kwani yanaonesha kutokuzuka kwa ulimwengu ilhali ni wenye kuzuka. Na chenye kuzuka kinapozuka baada ya kuwa mwanzo hakikuwepo hakuna budi kwamba kitakuwa ni chenye kuwezekana, na kuwezekana hakuna wakati uliowekewa mipaka, na hakuna wakati wowote ule isipokuwa kuwezekana kuko ndani yake. Kuwezekana kwa kitendo na kujuzu kwake na kusihi kwake hakuna mpaka. Basi ni lazima kwamba kitendo tangu enzeli (pasina ukomo) kilikuwa ni chenye kuwezekana, chenye kujuzu chenye kusihi. Na hii ina maana kwamba Allah alikuwa ni mwenye kuweza. NA HII INA MAANA KWAMBA NI LAZIMA KUNA VIUMBE VISIVYOKUWA NA

1241 - Maneno haya mengine hayaelekei kwamba kweli hao Jahmiyya walikuwa wakiyasema, lakini inaonekana haya yote ni katika kutiliana maneno mdomoni.

398

Page 399: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

UKOMO KATIKA KUANZA KWAKE (HAVINA MWANZO). 1242

Anasema Sheikh huyo:

: والمستقبل،: الماضي في دوامها يمكن يقول من قول والثالثالح أئمة يقوله ديث، ������كما

الكبار المسائل من وهي

Na (kauli) ya tatu ni kauli ya wenye kusema kwamba (viumbe) vinawezekana kuwepo daima huko nyuma na huko mbele (havina mwanzo wala mwisho) kama wanavyosema Maimamu wa Hadithi, 1243 na haya ni katika mas-ala makubwa1244!

1242 - Ibn Abi Al-‘Izz, Sharhu Al-‘Aqiidatu Al-Tahaawiyya uk. 80. 1243 - Tazama mtu huyu anavyowazulia wanavyuoni wa Hadithi! Hizi ni falsafa za Imamu wao Ibn Taymiyya pamoja na wanafalsafa wengine, yeye anazinasibisha na wanavyuoni wa Hadithi! 1244 - Ibn Abi Al-‘Izz, Sharhu Al-‘Aqiidatu Al-Tahaawiyya uk. 80. Rejea kitabu hicho katika sehemu hio yote, uone jinsi Sheikh huyo anavyoyakariri yale yale ya Ibn Taymiyya. Anasema Al-Saqqaaf kwamba Sheikh huyo watu kimakosa wanasema ni Hanafi, lakini ukweli ni kuwa yeye ni Hanbali mujassim.

399

Page 400: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

YALIOSEMWA NA WANAVYUONI KUHUSU IBN TAYMIYYA

Ama kuhusu yaliosemwa kuhusu Ibn Taymiyya, tayari tumeyanukuu baadhi yake katika kitabu chetu Kisimamo Katika Sala. Na kwa vile hii ni jawabu maalumu inayoihusu maudhui hio hasa, basi hapa tutayanukuu tena baadhi ya maelezo hayo pamoja na kuongeza mengine.

Tulimnukuu Al-Imamu Ibn Hajar Al-Haitami Al-Shafi’i akisema kuhusu Ibn Taymiya:

) و إ( فجعله قوله ؛ دائما مخلوقا الله مع يزل ولم بالنوع، قديم العالم نفاع ال بالذات ال�����موجبا

ذلك – باالختيار عن الله وأنه – تعالى ، واإلنتقال والجهة بالجسمية وقولهأصغر ال بقدرالعرش

والكفرالبواح - القبيح الشنيع االفتراء هذا عن الله تعالى ، أكبر والالصريح -

(Na kusema kwake Ibn Taymiyya) kwamba: AINA ya ulimwengu ni yenye kutangulia na haujawacha (ulimwengu katika enzeli) kuwa ni kiumbe daima. Basi (Ibn Taymiya) akamfanya (Mungu) kuwa Dhati yake ni mwenye kuwajibikiwa (mwenye kulazimishwa) si mwenye kufanya (mambo) kwa khiari yake. Na kauli yake (Ibn Taymiyya kuhusu Mungu) kwamba ana kiwiliwili na yuko upande (fulani) na anahama (kutoka sehemu moja kwenda nyengine) na kwamba Yeye (Mungu) ni sawa sawa na kiti chake (kwa ukubwa) si Mkubwa (zaidi ya kiti chake cha enzi) wala si mdogo (kuliko kiti chake). Ametakasika Mungu na uzushi huu mbaya na kufuru hii ya wazi.1245

Anayendelea Ibn Hajar Al-Haytami kwa kusema:

قيم ابن وتلميذه تيمية ابن كتب في ما إلى تصغي أن وإياكوغ ��������الج اتخذ ����وزية ممن ، يرهما

وخ ، علم على الله وأضله هواه، سم ����إلهه على وقلبه، ��������تم عهبص على غش ������وجعل اوة،�ره

! ...... ؟ الله بعد من يهديه فمن

1245 - Tazama kitabu Al-Fatawa Al-Haditha  uk. 116.

400

Page 401: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Tahadhari na kuyasikiliza yaliyomo katika vitabu vya Ibn Taymiya na mwanafunzi wake Ibn Qayyim Al-Jawzia na wengineo katika wale walioyafanya mapendwa moyo yao kuwa ndio mola wao  na Mwenyezi Mungu akawapoteza juu ya elimu yao (walio nayo) na akawapiga mihuri juu ya masikio yao na nyoyo zao na akajaalia vifuniko kwenye macho yao. Basi ni nani atayemuongoa baada ya Mwenyezi Mungu?1246

Na akasema:

فإنه �������واليغ ، وسلم عليه الله صلى زيارته لسن تيمية ابن بإنكار ترقال ؛كما الله أضله عبد

تصنيف في السبكي التقي عليه الرد في وأطال ، جماعة بن العزووقوع ، في ��������مستقل ه

ليس وسلم عليه الله صلى الله رسول في   حق وقع فإنه ؛ بعجيبسبح ��������ح الله انه �������ق

يق ل����������وتعا عما ، ���������ى كبيرا علوا والجاحدون الظالمون ول:�فن كقوله العظائم إليه سب

وعي ورجال ويدا جهة تعالى لله ، ��إن الشنيعة القبائح من ذلك وغير ناكف ���������ولق ره���������د

ما ����������كث نصروا الذين متبعيه وخذل بعدله الله عامله ، العلماء من يرعل �����اف ى ��������تراه

الغراء الشريعة

Wala (mtu) asidanganyike kwa kuikataa Ibn Taymiya Sunna ya kumzuru Mtume (s.a.w.) (yaani kuizuru kaburi yake) hakika yake (Ibn Taymiya) ni mja ambaye Mwenyezi Mungu kampotoa kama alivyosema Al-‘Izz bin Jamaa. Na akamjibu kwa urefu Al-Taqi Al-Subki katika utunzi (vitabu) maalum. Na kuivunja kwake haki ya Mtume (yaani Ibn Taymiyya kuikana haki ya Mtume) si ajabu kwani ameivunja haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu aliyetakasika na wanayoyasema madhalimu mtakasiko mkubwa kabisa. Basi (Ibn Taymiyya huyu) kamnasibisha Mwenyezi Mungu na mambo makubwa kwa mfano aliposema kwamba (Mwenyezi Mungu) yuko upande (maalum); ana mkono; ana mguu ana macho na mengineo katika mambo maovu kabisa. Na (kwahivyo) wanavyuoni wengi wamemwita kafiri. Basi Mwenyezi Mungu amlipe kwa uadilifu wake na awaache mkono wafuasi wake wanaotetea uzushi wake juu ya sharia takatifu.1247

Anasema Al-Dhahabi kuhusu Ibn Taymiyya:

1246 - K.h.j. uk. 203. 1247 - Ibn Hajar Al-Haytami katika maelezo yake juu ya kitabu Manaask Al-Nawawi uk. 489.

401

Page 402: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Na nimepata tabu katika kumpima na kumpekuwa mpaka nikachoka miaka mingi, basi sina nilichokiona ambacho kimemuweka nyuma baina ya watu wa Misr na Shaam na kumchukia kwao katika nafsi zao, na wakadharau na kumwita mwongo na kumwita kafiri isipokuwa kibri chake na kujiona kwake na kung’ang’ania – kupindukia – ukuu wa Mashekhe (kutaka ukubwa wa kuchukua nafasi ya wanavyuoni) na kuwadharau wakuu, tazama basi balaa la (mtu) kujidai na kupenda aonekane…..na mambo ambayo Allah kamlinda yeye na wafuasi wake ni mengi zaidi, na yaliojiri kwao ni baadhi tu ya wanayostahiki, basi usiwe na shaka ya hilo.1248

Kisha baada ya hayo, Al-Dhahabi akatoa nasaha zake kwa Ibn Taymiyya, akisema:

Mpaka lini wewe utakuwa unaona kibanzi kwenye jicho la nduguyo na unasahau gogo lililomo jichoni mwako? Mpaka lini wewe utakuwa unaisifu nafsi yako na zogo lako na ibara zako, na kuwaponda wanavyuoni na kufuatilia aibu za watu nawe unajua kwamba Mtume (s.a.w.) kakataza: ((Musiwataje maiti wenu ila kwa wema, kwani wameshakwenda katika kile walichokitanguliza)). Hapana! Najua kwamba utaniambia – ili ujitetee –: ‘Hakika ya kuwasema kwa ubaya hawa ambao hawakuinusa harufu ya Uislamu wala hawakukijua kile alichokujanacho Muhammad (s.a.w.) ni jihadi. Basi sio hivyo! Wao wamezijua kheri nyingi ambazo lau mja atazitendea kazi basi atafuzu, na walijingikiwa na mambo mengi ambayo hayawahusu na ((Katika Uislamu ulio bora ni mtu kuwacha yale yasiomuhusu)).

Ewe mtu! Nakuapia kwa jina la Allah! Hebu achana na sisi. Hakika ya wewe ni mwenye kupenda kukithirisha mijadala, mjuzi wa ulimi hutulii wala hulali. Jihadharini na dhana zenye kupelekea katika makosa katika dini, Mtume (s.a.w.) kachukia kuhojihoji na akakutia aibu na akakataza kuuliza sana…..

Ewe Mtu we (Ibn Taymiyya)! Wewe umemeza sumu ya watu wa falsafa na vitabu vyao……1249

E! Kupunjika kulioje kwa anayekufuata wewe! Kwa hakika hio ni sababu ya uzindiki na kuporomoka, hasa hasa akiwa na elimu chache, mwenye ushujaa, mwenye kufuata matamanio yake……1250

1248 - Al-Dhahabi Zaghlu Al-’Ilmi uk. 17, nukulu kutoka katika Al-Saifu Al-Haad cha Al-Imamu Al-Qannubi uk. 186. 1249 - Bila shaka anayesoma kitabu Dar-u Al-Ta’aarudh au kwa jina jengine Bayaanu Muwaafaqatil Sariihi Al-Ma’aqul na kitabu Minhaju Al-Sunna anauona ukweli huu kwa uwazi. Ibn Taymiyya bora angeliviita vitabu vyake hivyo kuwa ni Fundamentals of Syrian philosophies (Misingi ya falsafa za Sham). Humo kuna falsafa tupu: Suna ni nadra!

402

Page 403: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Anasema Al-Dhahabi akitoa nasaha zake kwa wanafunzi:

Ikiwa wewe umekuwa bingwa katika usuli na vifuasi vyake kama vile elimu ya mantiki, hekima, falsafa, rai za watangulizi na mule akili zilimoemewa na ukashikana na Kitabu (cha Allah) na Sunna na misingi ya Al-Salaf na ukajikusanyia (mambo ya) akili na ya kimaandiko, basi mimi sikudhanii kwamba unafikia daraja ya Ibn Taymiyya katika hayo, Wallahi wala humkaribii! Nami niliiona hatima yake ya kupondwa na kusemewa ovyo na kufanywa kuwa ni mpotovu na kukafirishwa na kuitwa mwongo kwa haki na kwa batili. Kwa hakika alikuwa kabla hajaingia katika usanii huu (wa kifalsafa) ni mwenye kutoa nuru uso wake unang’ara, alama ya Al-Salaf, kisha akawa ni kiza (kama mwezi) ulioliwa…mwenye kuleta bidaa…...1251

Anasema Al-Sayyid Al-Saqqaaf, baada ya kuyanukuu maneno hayo: “Na maneno haya yamethibiti kuthibiti kwa uhakika kwamba ni maneno ya Al-Dhahabi, na wameyanukuu na kuyathibitisha kundi kubwa la Mahuffadh, miongoni mwao ni Al-Hafidh Al-Sakhaawi katika kitabu chake Al-I’ilaanu Bittawbikh ukurasa wa 136.1252

Hayo ni machache sana katika mengi yaliosemwa na wanavyuoni wengi kuhusu Ibn Taymiyya. Mengi mno nimeyawacha ili kufupisha. Ama Maulamaa walinukuuliwa wakimjadili au kumjibu Ibn Taymiyya ni wengi mno. Baadhi ya hao ni hao tunaowataja hapo chini.

MAULAMAA WALIOMJADILI AU WALIOMJIBU IBN TAYMIYYA

Maulamaa wa Kisuni na wengineo waliomjibu Ibn Taymiyya, kama tulivyosema, ni wengi mno. Kawataja Sh. Abdullah Al-Harari katika Al-Maqaalaatu Al-Sunniyya na Al-Sayyid Al-Saqqaaf katika Al-Salafiyya Al-Wahaabiyya. Nitanukuu waliotajwa na Al-Harari na waliotajwa na Al-Saqqaaf sitowanukuu bali nitataja idadi tu ya wanavyuoni hao, bila kusahau kwamba wengine waliotajwa na Al-Saqqaaf ni wale wale waliotajwa na Al-Harari. Wanavyuoni hao ni:

1250 - Hivyo ni baadhi ya vipande vipande vya maneno ya Al-Imamu Al-Dhahabi aliomwambia Ibn Taymiyya pamoja na kuwa Al-Dhahabi ni mtu aliyeathirika na Ibn Taymiyya. Rejea Al-Qannubi Al-Saifu Al-Haad uk. 186. 1251 - Al-Dhahabi Zaghlu Al-’Ilmi uk. 23, nukulu kutoka katika Al-Salafiyya Al-Wahabiyya cha Al-Sayyid Al-Saqqaf uk. 134. 1252 - Al-Saqqaaf Al-Salafiyya Al-Wahabiyya uk. 134.

403

Page 404: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

1) Al-Qadhi Al-Mufassir Muhammad ibn Ibrahim bin Jama’a Al-Shafi’i (733H).

2) Muhammad bin Al-Hariri Al-Ansari Al-Hanafi. 3) Muhammad bin Abi Bakr Al-Maliki.4) Ahmad bin ‘Umar Al-Maqdisi Al-Hanbali.5) Sheikh Salih bin Abdillah Al-Battaihi (707H). 6) Kamal Al-Diin Muhammad bin Abi Al-Hasan Al-Shafi’i.7) Qadhi Al-Qudhaat Ahmad bin Ibrahim Al-Suruuji (710H). 8) Qadhi Qudhaati Al-Malikiya, Ali bin Makhluf (718H). 9) Sheikh Al-Faqiih Ali bin Ya’aqub Al-Bakri (724H)10) Al-Faqih Shamsu Al-Diin Muhammad bin ‘Adlaan Al-Shafi’i

(749H). 11) Al-Hafidh Taqiyyu Al-Diin Al-Subaki (756H).1253 12) Al-Muhaddith, Al-Mufassir Muhammad bin ‘Umar bin Makki

ajulikanaye kwa jina la Ibn Al-Murahhil Al-Shafi’i (716H). 13) Al-Hafidh Abu Said Salahu Al-Diinn Al-’Alaai (761H).1254 14) Qadhi Qudhaati Al-Madina Abu Abdillahi Muhammad bin

Musallam bin Malik Al-Hanbali (726H). 15) Sheikh Ahmad bin Yahya Al-Kilaabi (733H).1255

16) Al-Qadhi Kamalu Al-Diin Al-Zamlakani (727H). 17) Al-Qadhi Safiyyu Al-Diin Al-Hindi (715H). 18) Al-Faqih Al-Muhaddith Ali bin Muhammad Al-Baaji Al-Shafi’i

(714H).19) Al-Muarrikh Al-Faqih Al-Fakhr bin Mu’allim Al-Qurashi

(725H).1256

20) Al-Faqih Muhammad bin Ali bin Ali Al-Maazini (721H).1257

21) Al-Faqih Abu Al-Qassim Ahmad bin Muhammad bin Muhammad Al-Shirazi (733H).1258

22) Al-Faqih Al-Muhaddith Muhammad Al-Qaz-wini Al-Shafi’i (739H).23) Marsum Al-Sultaan bin Qalaawun (741H).

1253 - 1) Al-I’tibaar bibaqaai Al-Jannatu wa Al-Naar. 2) Al-Duratu Al-Mudhiyya fi Al-Radd Ala Ibni Taymiyya. 3) Shifaau Al-Saqami fi Ziyaratiu Khayri Al-Anaami. 4) Al-Nadharu Al-Muhaqqiqu fi Al-Halfi bi Al-Talaaqi Al-Mu’allaq. 5) Daqdu Al-Ijtima’i wa Al-Iftiraaqu fi Masaaili Al-Ayman wa Al-Talaaq. 6) Al-Tahqiiqu fii Mas-alati Al-Ta’aliq. 7)Raf’u Al-Shiqaaqi ‘an Mas-alati Al-talaaqi. 1254 - Tazma: 1) Dakhaairu Al-Qasri fi Taraajumi Nubalaai Al-‘Asri cha Ibnu Taaluun uk.32-33. 2) Ahaadith Ziyarati Qabri Al-Nabiyi (s.a.w). 1255 - Risaalatu fii Nafyi Al-Jihat. 1256 - Najmu Al-Muhtadi wa Rajmu Al-Mu’tadi. 1257 - Risaalatu fi Raddi ‘Ala Ibni Taymiyya fi Mas’alati Al-Talaaq. 2) Risaalatu fi Raddi ‘Ala Ibni Taymiyya Fi Mas’alat Al-Ziyara. 1258 - Risaalatu fi Raddi ‘Ala Ibni Taymiyya.

404

Page 405: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

24) Al-Hafdh Al-Dhahabi (748H).1259 25) Al-Mufassir Abu Hayyan Al-Andalusi (745H).1260 26) Sheikh ‘Afifu Al-Diin Abdullahi bin As’ad Al-Yaafi’i (768H). 27) Al-Faqih Ibnu Batuta (779).1261 28) Al-Faqih Taaj Al-Diin Al-Subaki (771H).1262 29) Al-Muarrikh Ibnu Shaakir Al-Kutubi (764H).1263 30 Sheikh ‘Umar bin Abi Al-Yumn Al-Maliki (734H).1264 31) Al-Qadhi Muhammad Al-Sa’adi Al-Masri (750H).1265 32) Sheikh Isa Al-Zawawi Al-Maliki (743H).1266

33) Sheikh Ahmad bin ‘Uthman Al-Turkumani Al-Juuzjaani Al-Hanafi (744H).1267 34) Al-Hafidh Abdul Rahman bin Ahmad (Maarufu) Ibnu Rajab Al-Hanbali (795H).1268

35) Al-Hafidh Ibnu Hajar Al-’Asqalani (852H).1269

36) Al-Haafidh Walii Al-Diin Al-’Iraqi.1270

37) Al-Faqihi Al-Muarrikh Ibnu Qaadhi Shuhba Al-Shafi’i (851H).1271 38) Al-Faqihi Abu Bakr Al-Husni (829H).1272

39) Sheikh Ifriqiyya, Abu Abdillah bin Urfa Al-Tuunisi Al-Maliki (803H). 40) Al-’Allamah ‘Alau Al-Diin Al-Bukhari Al-Hanafi (841H). 41) Sheikh Mahammad bin Ahmad Hamiidu Al-Diin Al-Farghani Al-Hanafii (867H).1273

1259 - 1) Bayanu Zaghli Al-’Ilmi wa Al-Talab. 2) Al-Nasiihatu Al-Dhahabiya.1260 - Tafsiru Al-Nahri Al-Maadi mina Al-Bahri Al-Muhiit. 1261 - Rihlatu Ibni Batuta. 1262 - Tabaqaat Al-Shafi’iyyati Al-Kubra. 1263 - ‘Uyuun Al-Tawaarikh. 1264 - Al-Tuhfatu Al-Mukhtara fi ‘Ala Munkiri Al-Ziyara. 1265 - Al-Maqaalatu Al-Marfhiyyatu fi Al-Raddi ‘Ala Man Yunkiru Al-Ziyaarata Al-Muhammadiyyah " للعزامي " الساطعة البراهين ضمن . طبعت1266 - ) Risaalatu Fii Mas-alati Al-Talaaq33) Sheikh Ahmad bin Othman Al-Turkani. 1267 - Al-Abhaathu Al-Jaliyyah Fii Al-Raddi ‘Ala Ibni Taymiyya. 1268 - Bayaana Mushkil Al-Ahaadithi Al- Waarida Fii Anna Al-Talaaqa Al-Thalaath Waahida. 1269 - Katika:

a) Al-Durur Al-Kaamina Fii A’ayaan Al-Ma-ati AL-Thaamina.b) Lisaanu Al-Miizan.c) Fat-hu Al-Baari Sharhu Sahihi Al-Bikhari.d) Al-Ishaara Bituruqi Hadiithi Al-Ziyaara.

1270 - Al-Ajwiba Al-Mardhiyya Fii Al-Raddi ‘Ala As-ilati Al-Makiyya. 1271 - Taarikh Ibni Qaadhi Shuhba. 1272 - Daf’u Shubahi Man Shabbaha Watamarrada wa nasaba dhalika ilaa Al-Imami Ahmad. 1273 - Al-Raadu ‘Ala Ibni Taymiyya Fii Al- I’itiqaadaat.

405

Page 406: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

42) Sheikh Ahmad Zaruuq Al-Faasi Al-Maliki (899H).1274

43) Al-Hafidh Al-Sakhaawi (902H).1275

44) Sheikh Ahmad bin Muhammad (Maarufu) Ibnu Abdi Al-Salaam Al-Misri (931H).1276 45) Ahmad bin Muhammad Al-Khuwaarizmi Al-Dimashqi (Maarufu) Ibnu Qaraa (968H). 46) Al-Qadhi Al-Bayaadhi Al-Hanafi (1098H).1277 47) Sheikh Ahmad bin Muhammad Al-Witri (980H).1278 48) Sheikh Ibnu Hajar Al-Haytami (974H).1279 49) Sheikh Jalaalu Al-Diin Al-Dawwaani ( 928H).1280 50) Sheikh Abdu Al-Naafi’I bin Muhammad bin Ali bin ‘Iraq Al-Dimashqi (962H).1281 51) Al-Qadhi Abu Abdillah Al-Muqri.1282 52) Mulla Ali Al-Qari Al-Hanafi (1014H).1283

53) Sheikh Abdul Rauf Al-Munaawi Al-Shafi’i (1031H).1284 54) Al-Muhaddith Muhammad bin Ali bin ‘Allaan Al-Sadiiqi Al-Makki (1057H).1285

55) Sheikh Ahmad Al-Khafaaji Al-Misri Al-Hanafi (1069H).1286 56) Al-Muarrikh Ahmad Abu Al-Abbas Al-Muqri (1041H).1287 57) Sheikh Muhammad Al-Zarqani Al-Maliki (1122H).1288 58) Sheikh Abdul Al-Ghani Al-Nabulusi (1143H).1289

59) Al-Faqihi Al-Suufi Muhammad Mahdi bin Ali Al-Sayyadi (Maarufu Al-Rawaas) (1287H). 60) Al-Sayyid Muhammad Abu Al-Huda Al-Sayyadi (1328H).1290

1274 - Sharhu Hizbi Al-Bahr.1275 - Al-I’ilaan Bi Al-Tawbiikh Liman Dhamma Al-Taariikh. 1276 - Al-Qawlu Al-Naassir Fi Al-Raddi Khabaat ‘Ali bin Nassir. 1277 - Ishaaraati Al- Maraam Fii ‘Ibaaraati Al-Imaam.1278 - Rawdhatu Al-Naadhiriin Wakhulaassatu Manaaqibi Al- Saalihiin. 1279 - Al-Fataawa Al-Hadithiyyah, b) Al-Jawharu Al-Munadh-dham Fii Ziyaati Al-Qabri Al-Mu’adh-dham, c) Haashiyatu Al-Iidhahi Fii Al-Manaasik. 1280 - Sharhu Al-’Adhudiyya. 1281 - Tizama. Dakhaairu Al-Qasri Fii Taraajimi Nubalaai Al-’Asri cha Ibnu Tuuluun uk. 32-33. 1282 - Nadhmu Al-Laali Fi Suluuki Al-Amaali. 1283 - Sharhu Al-Shafaa cha Al-Qadhi ‘Iyadh. 1284 - Sharhu Al-Shamaail cha AlTirmidhi. 1285 - Al-Mubrad Al-Mubki Fi raddi Al-Saarimi Al-Munki. 1286 - Sharhu Al-Shafaa cha Al-Qadhi ‘Iyadh. 1287 - Azhaaru Al-Riyaadh. 1288 - Sharhu Al-Mawaahibi Al-Laduniyyah. 1289 - Dhammuhu Fii Akthari Min Kitaab. 1290 - Qilaadatu Al-Jawaahir.

406

Page 407: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

61) Al-Mufti Mustafa bin Ahmad Al-Shati Al-Hanbali (1348H).1291

62) Mahmuud Khattab Al-Subki (1352H).1292

63) Mufti wa Madina Sheikh Muhaddith Muhammad Al-Shanqiti (1353H).1293

64) Sheikh Salaamtu Al-’Azzami Al-Shafi’i (1376H).1294

65) Mufti Al-Diyaar Al-Misriyya Sheikh Muhammad Bukhayti (1354H).1295

66) Sheikh Muhammad Zahid Al-Kawthari (1371H).1296 67) Sheikh Ibrahim bin ‘Uthman Al-Samannudi Al-Misri.1297 68) Sheikh Muhammad Al-Arabi Al-Tabbani (1390H).1298 69) Sheikh Muhammad Yusuf Al-Banuri Al-Bakistani.1299

70) Sheikh Mansur Muhammad Uweis.1300

71) Al-Hafidh Sheikh Ahmad bin Siddiq Al-Ghummari (1380H).1301 72) Sheikh Al-Muhaddith Abdullahi Al-Ghummari Al-Maghribi (1413H).1302

73) Sheikh Abu Al-AShbaali Salim bin Jundaani Al-Andonesi.1303

74) Hamdu Allah Al-Baraajuwi.1304

75) Sheikh Mustafa Abu Seif Al-Hamaami.1305

76) Sheikh Muhammad bin Isa bin Badraan Al-Sa’adi.77) Sheikh ‘Alawi bin Tahir Al-Haddaad Al-Hadhrami. 78) Mukhtar bin Ahmad Al-Muayyad (1340H).1306

79) Shekh Ismail Al-Azhari.1307

80) Sheikh Siraaju Al-Diin Abbas Al-Indonesi (1403H).

1291 - Al-Nuquulu Al-Shar’iyyah. 1292 - Al-Diinu Al-Khaalis au Irshaad Al-Khalq Ila Diini Al-Haqq. 1293 - Luzun Al-Talaaqi Al-Thalaathi Duf’a Bimaa Laa Yasta’tii’u Al-‘Aalimu Daf’ah. 1294 - 1) Al-Baraahinu Al-Sati’a Fi Raddi Ba’adhi Al-Bida’ati Al-Shaai’ah. 2) Maqaalatu Fi Jariidati Al-Muslim Al-Misriyya. 1295 - Tat-hiiru Al-Fuadi min Danasi Al-I’itiqaadi. 1296 - 1) Kitabu Maqaalati Al-Kawthari. 2) Al-Ta’aqqubu Al-Hathithi limaa Yanfiihi Ibnu Taymiyya mina Al-Hadithi. 3) Al-Buhuuthu Al-Wafiyya Fii Mufradaatu Ibni Taymiyya. 4) Al-Ishfaaqu ‘Ala Ahkaami Al-Talaaq. 1297 - Nasratu Imami Al-Subki Biraddi Al-Saarimi Al-Munki. 1298 - Baraatu Al-Ash’ariyyiina min Aqaaidi Al-Mukhaalifiina. 1299 - Ma’aarifu Al-Sunani Sharhu Sunani Al-Tirmidhi. 1300 - Ibnu Taymiyya Laysa Salafiyyan. 1301 - 1) Hidaayatu Al-Sughraa. 2) Al-Qaulu Al-Jaliyyu. 1302 - 1) Itqaanu Al-San’ah Fii Tahqiiqi Ma’ana Al-Bid’a. 2) Al-Subhu Al-Saafir Fii Tahqiiqi Salaati Al-Musaafir. 3) Al-Rasaailu Al-Ghammariyya. 1303 - Al-Khulaasatu Al-Kaafiya Fi Al-Asaaniidi Al-’Aaliya. 1304 - Al-Basaairu limunkiri Al-Tawaasuli Bi Ahli Al-Kubuuri. 1305 - Ghawyhu Al-’Ibaadi Bi Bayaani Al-Rashaadi. 1306 - Jalaaau Al-Awhaami ‘An Madhaahibi Al-Aimmah Al-’Udhaam. 1307 - Mir-aatu Al-Najdiyya.

407

Page 408: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Hawa ni baadhi ya wanavyuoni ambao wamemrudi Ibn Taymiyya ambao kawataja Sheikh Al-Harari.1308 Miongoni mwa hawa wako ambao walimkafirisha kabisa Ibn Taymiyya. Ama Al-Sayyid Al-Saqqaf, yeye kataja idadi ya wanavyuoni 105 waliomrudi Ibn Taymiyya na Muhammad ‘Abdil-Wahhaab, baadhi yao ni hao hao aliowataja Sheikh Al-Harari na baadhi yao ni Mashekhe wengine.1309

Baada ya hayo, sidhanii kwamba mtu mwenye akili yake na fikra sahihi atasema kwamba “Juma amesema haya kwa kumchukia Ibn Taymiyya”. Ivo tuseme na wanavyuoni hao wote wanamchukia Ibn Taymiyya; na wanamchukia bure bure? Watu wanachokipinga ni itikadi batili ya Ibn Taymiyya anayojaribu kuipandikiza katika Uislamu: si Ibn Taymiyya mwenyewe. Kwa mukhtasari ni kuwa:

1) Ibn Taymiyya anaitakidi kwamba AINA ya ulimwengu ina sifa ya kutangulia.

2) Aina ya ulimwengu haina mwanzo. Na huu ni upotovu wa wazi kabisa, kwani asiye na mwanzo ni mmoja tu, naye ni Allah.

3) Jambo hili hakulisema Juma Mazrui tu, bali wanavyuoni kadha wa kadha, wakiwemo wanavyuoni wa Kiwahabi, wamelisema.

4) Wanavyuoni wengi wamemrudi Ibn Taymiyya kwa sababu ya itikadi yake hio na wengine hata kufikia hadi ya kumkafirisha.

Baada ya kuyaweka yale nilioyasema kuhusu Ibn Taymiyya wazi na kumjibu Sheikh Kasim Mafuta juu ya madai yake yasio na msingi, sasa natutazame yale nilioyasema kuhusu Ibn Al-Qayyim, kisha tuitazame jawabu alionijibu Sheikh Ibn Mafuta.

1308 - Tazama Abdullah Al-Harari Al-Maqaalatu Al-Sunniyya Fii Kashfi Dhalaalati Ahmd Ibn Taymiyya uk. 444-452. 1309 - Tazama Al-Saqqaf Al-Salafiyya Al-Wahabiyya uk. 133-146.

408

Page 409: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

KUHUSU IBN AL-QAYYIM

Kuhusu Ibn Al-Qayyim nilisema haya yafuatayo:

Anasema Ibn Al-Qayyim akitaja sifa za Mwenyezi Mungu: “Na kwamba yeye (Mwenyezi Mungu) ana mikono miwili bila ya mfano na ana macho mawili na ana uso.”1310 Naye Ibn Al-Qayyim anasema kuwa kayanukuu maneno haya kutoka kwa Abu Al-Hasan Al-Ash’ari, lakini naye ndio yumo katika kuyatolea hoja kuwa ni maneno sahihi. Lakini kudai kwamba haya ni maneno ya Al-Imamu Al-Ash’ari ni kitu cha kutazamwa zaidi kwani wafuasi wa Al-Imamu Al-Ash’ari nao ni Masuni kama Mashafi hawakubaliani na haya.

Na anasema: “Na kwamba Mwenyezi Mungu yuko kwenye ‘Arshi na miguu yake miwili ipo kwenye kiti.”1311 Bali kafikia kuifasiri Aya ya Mwenyezi Mungu inayosema:

فنسيهم الله نسواWamemsahau Mwenyezi Mungu na Yeye akawasahau.1312

Kaifasiri Aya hii kwa maana yake ya dhahiri akasema: “Zingatia kauli yake Mwenyezi Mungu (katika Aya hio na ilio mfano wa hio) namna alivyo fanya uadilifu kamili kwao akawasahau kama walivyomsahau!” 1313

1310 - Hadi Al-Arwaah uk. 13. 1311 - Hadi Al-Arwaah uk. 42 na 299.1312 - Sura ya 9 Aya 67. 1313 - Tazama kitabu chake Mukhtasar Al-Sawaiq Al-Mursala j. 2 uk. 210 chapa Daar Al-Kutub Al-Ilmiya kilicho chapishwa Bairut Lebanon, na kufanyiwa ufupisho na Sheikh Muhammad bin Al-Musala.

409

Page 410: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Na Ibn Al-Qayyim akafikia kusema kuwa moto wa akhera kuna siku adhabu yake itakwisha kwa Waislamu na wasio kuwa Waislamu na utabaki mtupu bila ya mtu yoyote.1314 Na akinasibisha kauli hii kwa Sheikhe wake Ibn Taymiyya na akaisifu kuwa kauli hii ndio inayokubaliana na Qur-ani na suna.1315 Tazama matatizo yetu sisi binaadamu: kabla ya kusema maneno haya, Ibn Al-Qayyim kanukuu Aya zenye kusema kwa uwazi kuwa watakaoingia humo hawatotoka kama Aya inayosema:

النار من بخارجين هم وماNa wala wao hawatokuwa wenye kutoka katika moto. 1316

Na Aya inayosema: بمخرجين منها هم ما و

Na wala wao humo hawatotolewa.1317

Halafu Aya kaziwacha na akafuata maneno ya Shekhe wake Ibn Taymiyya!!!.”1318

Na akasema Ibn Al-Qayyim katika kitabu chake hicho: “Mwenyezi Mungu anacheka na kufurahi! Na nyoyo za waja ziko katika vidole viwili miongoni mwa vidole vyake! Na kamuumba Adam kwa sura yake! (yaani Mwenyezi Mungu ana sura kwa sura hio ndio kaitumia kuchukuwa kigezo cha kuumba sura ya Adam)! Anaendelea kwa kusema: “Na mbingu na ardhi siku ya kiama zitakuwa kiganjani mwake! “Na ataweka mguu wake kwenye moto….na atawatoa watu kwenye moto kwa mkono wake!!!” 1319

Ibn Al-Qayyim na Mashekhe wake na wafuasi wake wanayasema haya kwa uhakika wake, sio kwa kuyaletea tafsiri bali tukisema kwamba Mwenyezi Mungu ana mkono ni kuwa kweli anao mkono lakini hatujui umekaaje wala haufanani na kitu! Sasa tunamuuliza huyu aliyesema maneno haya je yeye ni mfuasi wa nani? Kwa sababu yeye anasema kuwa wenye kusema kuwa Mwenyezi Mungu haonekani basi ni wafuasi wa Fir-

1314 - Ibn Al-Qayyim Hadi Al-A r-wah uk. 258-282. 1315 - Anasema Al-Qannubi kwamba katika vitabu vyengine, Ibn Al-Qayyim kaafikiana na jumhur kwamba adhabu haina mwisho. Tazama Al-Saifu Al-Haad uk. 28. 1316 - Sura ya 2 Aya ya 167. 1317 - Sura ya 15 Aya ya 48. Aya hii Ibn Al-Qayyim kainukuu kimakosa katika uk. 259 wa kitabu chake Hadi Al-Ar-wah, alipokuwa akizungumzia kauli ya tatu kuhusu kumalizika kwa adhabu ya moto. Dhahiri ni kuwa kalamu ilimteleza, kwani Aya hii haizungumzii watu wa motoni; bali inazungumzia watu wa peponi na tafsiri yake ni: “Na wala wao humo (kwenye pepo) hawatotolewa.” Lakini cha ajabu ni kuwa Ibn Al-Qayyim katika uk. 260, kamnukuu mwalimu wake Ibn Taimiyya akiipa Aya hio tafsiri hio hio, nalo ni kosa la wazi.1318 - Tazama Hadi Al-Arwaah uk. 259. Tazama kauli ya saba, na kwa kufahamu zaidi basi isome sehemu hio yote mpaka uk. 282. 1319 - K.h.j., uk. 299.

410

Page 411: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

awna, kama tutakavyonukuu maneno yake baadae Mwenyezi Mungu akipenda.

Hayo ndio nilioyasema katika kitabu changu Hoja Zenye Nguvu1320 katika kuibainisha itikadi batili ya Ibn Al-Qayyim. Sasa je Sheikh Kasim Mafuta ana jawabu gani? Ifuatayo ndio jawabu yake kwangu.

1320 - Juma Mazrui Hoja Zenye Nguvu uk. 24-26.

411

Page 412: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

JAWABU NILIOIPATA

Anasema Sheikh Al-‘Allama Kasim Mafuta:

Miongoni mwa mambo mabaya kabisa katika uislamu ni kumzulia mtu jambo asilolifanya au asilosema, na kama mtu mwenyewe ni mwanachuoni basi ubaya unakuwa maradufu. Vitendo vya ndugu Juma anavyovifanya dhidi ya maulamaa ni hiyana na ni dhulma ambayo inamporomoshea mtu uadilifu wake na kumfanya asikubaliwe maneno yake. Je ni kweli Ibn al-Qayyim anasema kuwa Allah anasahau kweli kweli? Au Juma amekusudia kusema uwongo ili kupotosha? Jawabu ni kwamba, si kweli kuwa Ibn al-Qayyim anaitikadi kwamba Allah anasahau, bali itikadi yake ni itikadi ya Qur’an na Sunna kuwa Allah hasahau, lakini ndugu yetu Juma alikusudia kupotosha kama ilivyo kawaida ya watu wa batili. Na ushahidi wa kuwa Ibn al-Qayyim hana itikadi hiyo chafu ni pale alipokuwa akiitafsiri kauli ya Allah isemayo:

52 طه الله)) عند علمها(( اه���أحص قد لربي معلوم وشركهم وكفرهم رون���الق تلك أعمال أيكتاب فى وأودعه فظه��وح

عليه النسيان خشية تابالك فى يودعه ولم, القيامة يوم فيجازيهمحانه���سب فإنه الل������والض

كتابه !!!!!ينسى” وال يضل ال الكتاب دار مطبعة 141 ص العليل شفاء انظر –بيروت العربي

ه� 1424لعام األولى الطبعة لبنان

“Ujuzi wake (karne hizo) uko kwa Allah”.1321 Makusudio ni kwamba matendo ya karne hizo (zilizopita) kufru zao na shirki zao zote zinajulikana kwa Mola wangu amezidhibiti, amezihifadhi na ameziweka katika kitabu na atawalipa siku ya Qiyama, na hakuziweka katika kitabu kwa sababu ya kuogopea kusahau na kupotea. KWA SABABU YEYE –SUB’HANAH- HAPOTEI WALA HASAHAU!!!!!1322

Swali, kwa mujibu wa maneno haya, je ndugu msomaji umefahamu kwamba Ibn al-Qayyim itikadi yake ni kuwa Allah anasahau au hasahau? Je umegundua kwamba Juma al-Mazrui anaendelea kusema uwongo? Pengine Juma mwenyewe au mtu mwengine katika wapenzi wake anaweza kusema: lakini maneno hayo siyo aliyo yanukuu kutoka kwa Ibn al-Qayyim bali yeye amenukuu maneno mengine kwenye kitabu kingine ambayo Ibn al-Qayyim anaelezea kwa uwazi kuwa Allah anasahau kweli kweli.

1321 - Surat Twaha aya ya 52. 1322 - Tazama kitabu chake “Shifaul-Alili” ukurasa wa 141 chapa ya Darul-kitabil- Arabi Beirut – Lebanon,chapa ya kwanza mwaka 2004.

412

Page 413: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

MAJIBU YETU

Sababu ya kunukuu kauli hiyo ya Imamu Ibn al-Qayyim ni kutaka kukuthibitishia ndugu msomaji kwamba Ibn al-Qayyim hana itikadi hiyo ya kikafiri ambayo ndugu Juma amembabatiza nayo. Kisha ndiyo tutupie macho hayo maneno ya Ibn al-Qayyim aliyo yanukuu Juma, na tutakapoyatazama tunakuta kwamba Ibn al-Qayyim hakutoka nje ya ibara ya Qur’an na Sunna, na wala maneno yake hayamaanishi kuwa Allah anasahau kweli kweli. Na kama maneno hayo yanaleta maana hiyo, basi hata Qur’an yenyewe na Sunna zitakuwa zina maanisha hivyo. Ibn al-Qayyim katika maneno yake ametumia ibara isemayo:

نسوه” كما نسيهم بأن““Bi an-nasiyahum kamaa nasuuhu”

Maana yake Kiswahili ni “kwa kuwa amewaacha (amewapuuza) wao kama walivyomsahau (walivyompuuza)” na ibara hiyo hiyo ndiyo iliyotumika katika Qur’an amesema Allah:

فنسيهم الله نسوا “Wamemsahau Allah naye akawaacha (akawapuuza)”.

Na haya hapa ni maneno ya Ibn al-Qayyim kwa ukamilifu:

((الحق قوله وتأمل )) فنسيهم الله نسوا ((وقوله : كالذين تكونوا وال فأنس�����������������اهم الله نسوا

عدل )) أنفسهم 1323.نسوه” كما نسيهم بأن العدل كل فيهم كيف

“Izingatie kauli yake al-Haq (Allah) “Wamemsahau Allah na yeye kawaacha wao (katika adhabu), na kauli yake “Wala msiwe kama wale ambao wamemsahau Allah na yeye akawasahaulisha nafsi zao” zingatia) namna alivyo wafanyia wao uadilifu kwa kuwa walimsahau na yeye akawaacha (katika adhabu).”1324

Hapa nataka kuelezea kitu kimoja muhimu kwa faida ya wasomaji: Tulipo litafsiri neno “Nasiya hum” kwa maana ya kuacha, lengo si kutaka kuleta taawili na kupotosha. Bali neno hili la kiarabu “Nasiya” ambalo limetasuliwa (limenyambuliwa) kutoka kwenye asili ya neno “Al-Nis’yaanu” lina maana mbili na zote ni za asili. Amesema Imamu Abul-Husain Ah’mad bin Faaris aliyefariki mwaka 395 H, katika kamusi yake “Mu’jamu Maqaaisil-Lugha” ukurasa wa 987:

210/1 المرسلة الصواعق مختصر ? - 1323 . 1324 - Tazama kitabu “Mukh’tasaru Sawaaiqil-Mur’slah” juzuu ya 1 ukurasa wa 210.

413

Page 414: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

إغفال على أحدهما يدل : صحيحان أصالن والياء والسين النون : نسيي����والثان , الشيئ

987 ص اللغة مقاييس معجم. .شيئ” ترك لىع

“Nasiya: Nuni, Siin, na Yaau ni asili mbili zilizo sahihi: moja yao inafahamisha “Kughafilika” na ya pili ni “Kuacha kitu”. Kwa hiyo tumefahamu kuwa neno “Nasiya” lina maana mbili:i) Kughafilika.ii) Kuacha.Na kwa mujibu wa kanuni na misingi ya elimu ya itikadi linapotumika neno lolote lenye zaidi ya maana moja: Maana moja inalingana na utukufu wa Allah, na maana ya nyingine hailingani na utukufu wake Allah, basi neno hili litachukuliwa kwa maana ambayo inalingana na utukufu wake Allah. 1325 Kwamfano hapa limetumika neno “Nasiyahum” ambalo maana yake ima itakuwa: “(Allah) Amewasahau wao” au “(Allah) Amewaacha wao”. Tukitazama baina ya maana mbili hizi, ni ipi inayonasibiana na utukufu wake Allah –Jalla Jalaaluh-?

Bila shaka kulitumia neno hili kwa maana ya “kuacha” ndiyo sahihi bali ni wajibu kufanya hivyo kwa sababu Allah hasahau kama ilivyotuelezea Qur’an na Sunna na alivyotuelezea Ibn al-Qayyim hapo nyuma. Na hakuna shaka kwamba naye Ibn al-Qayyim amelitumia neno hili hapa kwa maana inayolingana na utukufu wake Allah, nayo ni kwa maana ya “kuacha”.

Na mtu akilitumia neno hili na jingine kama hili kwa utaratibu ule ule uliotumika katika Qur’an au katika Sunna hatakuwa na hatia wala hastahiki lawama, na hivyo ndivyo alivyofanya Ibn al-Qayyim, lakini kwa masikitiko makubwa jambo hili halikumfurahisha ndugu Juma na kaumu yake na wakalifanya hilo ni kosa kubwa lisilo na mfano! Na -wali llaahil-hamdu- ukirejea sehemu mbali mbali katika vitabu vya Ibn al-Qayyim utaona anavyosema kwa uwazi kabisa kwamba:

!ينسى وال يضل ال سبحانه فإنه“KWA SABABU YEYE (ALLAH) –SUB’HANAH- HAPOTEI WALA HASAHAU”!1326

Lakini ah! tutazifanya nini sisi nyoyo zilizonyweshwa chuki, husda na uadui mpaka zikawa hazioni kwa waislamu wenzao ila shari tupu! Lakini hii ndiyo sera ya watu wote wa bid’a tangu azal. Ewe Mola wetu usijaalie

1325 - Sasa vipi kuhusu neno “Yad”?! Neno hili lina maana ya kiungo na lina maana ya nguvu na uwezo. Je ni ipi katika maana hizi inayolingana na utukufu wa Allah?! Sheikh Mafuta kanuni hii hamukuitendea kazi! 1326 - Tazama kitabu chake “Shifaul-Alili” ukurasa wa 141 chapa ya Darul-kitabil- Arabi Beirut – Lebanon,chapa ya kwanza mwaka 2004.

414

Page 415: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

ndani ya nyoyo zetu chuki na undani dhidi ya ndugu zetu walio amini, Allaahumma Aamin!

JAWABU NA MAELEZO

Hio ndio jawabu alionijibu Sheikh Kasim Mafuta. Lakini mimi naona Sheikh Kasim:

1) Kafanya tatizo lile lile alilolifanya katika kuyaelezea maneno ya Ibn Taymiyya. Nalo ni kushindwa kujua kuwepo kwa عموم (ujumla) na خصوص (umahususi) katika maneno ya Ibn Al-Qayyim. Ukiyakusanya maneno ya Ibn Al-Qayyim:

ينسى وال يضل ال سبحانه فإنه(Kwani Yeye Allah hapotei wala hasahau)

na maneno yake aliposema:عدل )) ...... كل كيف ))نسوه كما نسيهم بأن العدل فيهم

(Tazama) namna alivyowasahau kama walivyomsahau),ukiwa utayakusanya maneno haya basi utapata natija moja katika mbili:

a) Iwe Ibn Al-Qayyim aliposema kuwa Allah hasahau basi kakusudia kusahau katika uhakika wake: si majazi. Na hivi ndivyo alivyokusudia bila shaka.

b) Aliposema kuwa anawasahau watu wa motoni iwe kakusudia neno kusahau kimajazi kwa maana ya kuwaacha. Angelikusudia hivi ingelikuwa hakuna mushkeli, lakini tunasema kwamba hili sio lengo la Ibn Al-Qayyim kwani yeye anakanusha majazi.

c) Lakini zaidi ya hayo ni kuwa qarina ya maneno yake haioneshi kwamba yeye alikusudia hivyo kama tutavyobainisha.

2) Jambo la pili la msingi la kulijadili ni neno nasia. Sheikh Kasim Mafuta kadai kuwa neno hili lina maana mbili na kwamba zote ni za asili na akanukuu maneno ya Ibn Al-Faris yasemayo:

إغفال على أحدهما يدل : صحيحان أصالن والياء والسين النون : نسيى�عل لثانيوا الشيئ

987 ص اللغة مقاييس معجم. .شيئ ترك

“Nasiya: Nuni, Siin, na Yaau ni asili mbili zilizo sahihi: moja yao inafahamisha “Kughafilika” na ya pili ni “Kuacha kitu”.1327

Ninachotaka kumwambia ndugu yetu Sheikh Kasim ni kuwa, maneno ya Ibn Al-Faaris yasingelikuwa na mashaka lau alisema:1327 - Kasim Mafuta Hoja Zenye Nguvu uk. 27.

415

Page 416: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

والترك الغفلة في حقيقة المشترك معا والنسيان قبيل من فهو وعليهمعن أحد يتعين ييه ����الذي

بالقرائن

Na nisyaan ni hakika (si majazi) kwa maana ya kusahau na kwa maana ya kuwacha, na kwa hivyo ni katika neno mushtarak (neno lenye maana nyingi wakati mmoja) ambalo kujua maana gani ndio ilokusudiwa basi kunahitaji kuwepo kwa qarina (ushahidi).

Lakini yeye kasema: ni asili mbili zilizo sahihi, na hii labda si kwamba kakusudia kwamba zote ni hakika; ingawa dhahir ya mfumo wake katika kamusi yake hio unamaanisha hivyo. Kwa hali yoyote ile, hata akiwa kakusudia hivyo, basi hilo ni kosa kwani ushahidi uko kinyume na hivyo. Nawe Sheikh Kasim umetutaka tufanye tahqiq: sio tufuate tu kama bebdera; kwa bahati mbaya wewe umefuata tu hapa bila ya kutafakari vyema. Cha kufahamu ni kuwa tunaposema kuwa neno hili ni hakika na hili ni majazi basi tunakuwa tunakusudia kwa neno hakika ile maana yake ya asili. Na nini kitatujuilisha sisi maana ya asili. Maana ya asili alama yake – kama wanavyosema wanavyuoni – ni:

األذهان في المعنى تبادرKukikimbilia kwa maana katika fahamu.

Yaani maana ya asili ni ile ambayo neno likitajwa tu basi ndio inayofahamika katika akili bila ya kuhitaji kuwepo kwa qarina. Na maana za kimajazi ni zile ambazo hazifahamiki ila kwa kutowezekana kwa maana ya asili na kwa kuwepo kwa qarina. Sasa ukirudi katika neno nisyaan (kusahau), utaona kwamba neno hilo Mwarabu yoyote wa zamani na wa leo ukimtajia, basi haifahamu isipokuwa maana ya kughafilika tu. Ukisema:

محفظتي atafahamu “Nimekisahau kipochi changu” basi نسيتMwarabu hufahamu maana ya kughafilika. Halkadhalika ukisema: نسيت Mwarabu atakufahamu kuwa unakusudia kusema: “Nimesau مفتاحيufunguo wangu: sio nimeuacha”. Hio ndio maana atayoifahamu Mwarabu yoyote utapolitumia neno hilo. Hii ni kusema kwamba kulitumia neno nisyaan kwa maana ya kusahau au kughafilika ndio asili ya neno hilo. Ama maana ya kuacha, ni maana ambayo kufahamika kwake kunahitaji:

1) Kutowezekana kwa maana ya asili.2) Kuwepo kwa qarina.

Na masharti hayo yote ni kwa msingi wa wale wenye kuthibitisha kuwepo kwa majazi: si kwa wale wenye kuyakanusha majazi. Ibn Al-Qayyim – hata

416

Page 417: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kama kajigonga – lakini kimsingi ni kuwa yeye anakanusha kuwepo kwa majazi.

Kisha elewa kwamba hilo nililokwambia kwamba neno nisyaan ni uhakika kwa maana ya kusahau na ni majazi kwa maana ya kuwacha ndivyo wanavyosema wanavyuoni. Anasema Imamu wa Balagha, Al-Zamakhshari:

)) : : تركته الشيء نسيت المجاز ((فنسيهم الله نسواومنNa katika majazi (ni kusema): ‘Nimesahau kitu’ (yaani) nimekiwacha. (Kama Allah alivyosema): ‘Wamemsahau Allah Naye akawasahau”.1328

Kwa hivyo, neno nisyaan ni hakika kwa maana ya kusahau, ndio maana ikawa maana hio haihitaji qarina ili ifahamike; na ni majazi kwa maana ya kuwacha, na kwa hivyo, maana hio inahitaji qarina ili ifahamike. Na kwa maana hii, basi Sheikh Kasim Mafuta – kwa misingi yao ya kukataa majazi na ta-awil – atakuwa kaipotosha maana ya Aya isemayo: “Wamemsahau Allah Naye akawasahau”, na atakuwa kayapotosha maana ya maneno ya Imamu wake, Ibn Al-Qayyim.

Sasa naturudi katika maneno ya Ibn Al-Qayyim na tutazame ni kwanini tumesema kwamba yeye kaifasiri Aya hio kwa maana ya dhahiri: hakuipa ta-awil. Maneno ya Ibn Al-Qayyim ni haya:

ن�������كالذي تكونوا واله ((وقول ))فنسيهم الله نسواق ((الح قوله وتأملم���فأنساه الله نسوا

عدل )) أنفسهم وأنساهم نسوه كما نسيهم بأن العدل كل فيهم كيف ، ونعيم����ها أنفسهم حظوظ

نسيان على لهم عقوبة وفرحها لذاتها وأسباب وكمال�����������هاالن��عم بصنوف إليهم المحسن

واإلع�����راض ذكره بنسي����ان ذلك فقابلوا بآالئه إلي�������هم المتحببفيهم ف���عدل شك���ره عن

فعطلوها أنفسهم مص����الح أنس���اهم بأن

…Na zingatia kauli yake Allah: ((Wamemsahau Allah Naye akawasahau)) na kauli yake ((Wala musiwe kama wale waliomsahau Allah naye akawasahaulisha nafsi zao)) namna alivyowafanyia uadilifu kamili ya kwamba Naye (Allah) aliwasahau kama walivyomsahau na akasahaulisha hadhi za nafsi zao na neema zake na ukamilifu wake na sababu za ladha zake na furaha yake, yakiwa ni malipo kwao kwa kumsahau kwao yule aliyewafanyia wema wa kuwapa neema za kila aina,

1328 - Al-Zamakhshari Asaasu Al-Balaagha uk. 750. Tazama pia maelezo ya Al-Imamu Badru Al-Din Al-Khalili katika Jawaahiru Al-Tafsir Juz-u Khaas uk. 77, utaona kwamba anakusudia hivyo nilivyokueleza hata kama hakusema hivyo kwa uwazi.

417

Page 418: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

na ambaye kajipendekeza kwao kwa (kuwapa) neema zake. Basi wao wakazijazi (in exchange) kwa kusahau kumkumbuka na wakakengeuka kutokana na kumshukuru. Basi naye (Allah) akawafanyia uadilifu kwa kuwasahalisha maslahi yao wakayavunja.1329

Hayo ndio maneno ya Ibn Al-Qayyim, na sidhani kwamba kuna mtu mwenye kujua lugha ya Kiarabu ambaye atakubaliana na Sheikh Mafuta kwamba Ibn Al-Qayyim hakukusudia maana ya dhahir na ya msingi ya neno nisyaan (kusahau). Zingatia mambo yafuatayo:

1) Ibn Al-Qayyim hapa anazungumzia uadilifu (usawa) wa Allah kwa waja wake, na kwamba kama vile walivyofanya na Allah naye kafanya hivyo hivyo. Na katika kulithibitisha hilo akatoa mifano ya Aya mbili. Aya ya kwanza: ((Wamemsahau Allah Naye akawasahau)). Sasa kusahau ambako makafiri kuliwasibu ni kusahau katika mioyo na akili yaani kughafilika na kuyasahau matendo mema (yaani kuyaacha); na kule kuyafanya mabaya ni natija ya kusahau – katika mioyo na akili zao – ahadi na maonyo ya Allah. Sasa ili maana ya uadilifu alioudai Ibn Al-Qayyim ipatikane katika Aya hii na ili kule Allah kuwafanya wao kama walivyomfanya kupatikane, basi ni lazima Ibn Al-Qayyim awe kaifasiri Aya hii kwa dhahiri yake. Ama ukiwa utalifasiri neno kusahau lililomo katika sehemu ya kwanza kwa maana ya kusahau na neno kusahau lililomo katika sehemu ya pili kwa maana kuacha basi usawa anaoudai Ibn Al-Qayyim hautopatikana. Yaani Ibn Al-Qayyim anadai kwamba Allah kawafanyia usawa au uadilifu watu hao kwa maana kwamba kama walivyomsahau hapa duniani naye kawasahau motoni. Hii ndio maana ya wazi inayofahamika katika maneno yake. Ama tukisema kwamba kawafanyia usawa kama walivyomsahau naye akawawacha katika moto, basi (japo kuwa hivi ni kweli) lakini ibara ya Ibn Al-Qayyim ya kupatikana neno usawa haitopatikana. Kwani usawa wa kusahau ni kusahau; na usawa wa kuacha kitendo ni kuacha kitendo: si kuacha kitendo na kuadhibu. Kwa hivyo, ikiwa Ibn Al-Qayyim kakusudia hivyo alivyodai Sheikh Mafuta, basi ibara zake alizozitumia hazimaanishi hivyo.

2) Pili ni kuwa maana alioieleza Sheikh Kasim Mafuta inawezekana

lakini ni maana ya kimajazi na ni ta-awil, kwani neno kusahau likitumika kwa maana ya kuwacha basi linakuwa limetumika kinyume na maana yake ya asili. Na kwa kuzingatia kwamba – kimsingi – Ibn Al-Qayyim anapinga majazi na ta-awil, basi

1329 - Ibn Al-Qayyim Mukhtasar Al-Sawaa’iqi Al-Mursala uk. 210.

418

Page 419: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kuyapeleka maneno yake huko kunahitaji qaraain. Na hapo tutasema kajigonga kama kawaida yake.

3) Tatu: ikiwa makusudio ya maneno ya Ibn Al-Qayyim yasemayo: “Tazama jinsi alivyowafanyia uadilifu: akawasahau kama walivyomsahau”, ni “Tazama jinsi alivyowafanyia uadilifu: akawaacha kwenye adhabu kama walivyomsahau au kama walivyoacha itikadi na matendo”. Suali: nini faida ya kuuhusisha uadilifu wa Allah na Aya hii pasina Aya nyengine ikiwa kweli Ibn Al-Qayyim kakusudia hivyo? Kwani Aya nyengine pia si zinasema kwamba wataomuasi Allah watakwenda motoni, mbona Ibn Al-Qayyim hakusema kuhusu Aya hizo: “Tazama alivyowafanyia uadilifu?” Bila shaka, kila mwenye ufahamu sahihi, anajua kwamba hapa Ibn Al-Qayyim anazungumzia kitu maalumu ambacho hakiko katika Aya nyengine, nacho ni kuwa Ibn Al-Qayyim kaifasiri Aya hio kwa mujibu wa dhahiri yake kwamba Allah atawasahau watu hao kama walivyomsahau.

Na kwa hivyo, kauli ya Sheikh Kasim bin Mafuta aliposema:

Na mtu akilitumia neno hili na jingine kama hili kwa utaratibu ule ule uliotumika katika Qur’an au katika Sunna hatakuwa na hatia wala hastahiki lawama, na hivyo ndivyo alivyofanya Ibn al-Qayyim.

Tunasema kwamba kosa si kutumia ibara ya Qur-ani yoyote ile iwayo; lakini kosa linaweza likawa katika kuifasiri ibara fulani kwa udhahiri wake. Atayesema “Kila kitu kitaangamia isipokuwa uso wa Allah” atakuwa na kosa ikiwa ataufasiri uso wa kweli ikimaanisha kwamba viungo vyengine vitatoweka; na mtu hatokuwa na kosa ikiwa atakusudia uso kwa maana ya dhati. Ibn Al-Qayyim kaifasiri Aya hio kwa mujibu wa dhahiri yake ndio maana tukamlaumu.

TANBIHI

Miongoni mwa maelezo yangu kama ulivyoona ni kuwa nilisema katika kitabu changu Hoja Zenye Nguvu:

Na Ibn Al-Qayyim akafikia kusema kuwa moto wa akhera kuna siku adhabu yake itakwisha kwa Waislamu na wasio kuwa Waislamu na utabaki mtupu bila ya mtu yoyote.1330 Na akinasibisha kauli hii kwa Sheikhe wake

1330 - Ibn Al-Qayyim Hadi Al-A r-wah uk. 258-282.

419

Page 420: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Ibn Taymiyya na akaisifu kuwa kauli hii ndio inayokubaliana na Qur-ani na suna.

Sheikh Kasim bin Mafuta akanijibu katika ukurasa wa 29-34, wa kitabu chake kwamba hayo si kweli, bali Ibn Al-Qayyim hakuwa na itikadi hio. Mimi nitamthibitishia yale nilioyasema katika juzuu ya tatu ya kitabu hiki in shaa Allah, kwani najaribu kila jawabu yangu kwake ije katika sehemu yenye maudhui inayokwenda sambamba na jawabu hio.

420

Page 421: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

SURA YA KUMI NA MBILI TUHUMA ZA UWONGO DHIDI YA MAIMAMU WA AHLU AL-

HAQQI WA AL-ISTQAAMA NA MAJIBU YETU

UTANGULIZI WA SEHEMU HII

Sheikh Kasim Mafuta mbali na kuwa katika kitabu chake kasema maneno mengi yasio na ukweli na kafanya ghushi nyingi, pia amewatuhumu wanavyuoni wacha Mungu (Sh. Al-Khalili na Sh. Al-Qannubi) kwa jarima baya mno – jarima la uwongo! Sijui kama Sheikh Kasim atafanya akili aandike upya kitabu chake atangaze kosa lake, atubie na kuomba radhi, au atafanya kibri mpaka akutane na Mola wake na kuingia katika hatia.

Sasa kabla ya kulieleza suala hili kwa ufafanuzi na kubainisha kwamba Masheikh hao hawajasema uwongo wala hawajapatapo kusema uwongo, ni vyema kumkumbusha Sheikh Mafuta na wenzake jambo moja. Nalo ni kuwa katika kitabu chao chote tangu mwanzo hadi mwisho mumejaa maneno: “Ibadhi ni Makhawaarij”. Anasema Kasim mwanangwa wa Mafuta:

Katika itikadi ya makhawaarij (maibadhi) ni kwamba mtu akifanya dhambi kubwa kama vile kusema uongo, basi anakua kafiri1331 na huko akhera ataingia motoni milele na hatoki katu.1332

Anasema:

Lakini hadithi hii ni kama hadithi nyingine zilizotangulia, haikuwafurahisha watu wa bid’a wote kuanzia Jah’miyyah, Mu’tazila, Khawaariji (Maibadhi) na wengineo.

Anasema:

1331 - Anakuwa kafiri vipi? Tutakuelezea hili kwa urefu kwani unaonekana unataka kuwapaka watu matope bila ya elimu au kwa chuki. 1332 - Tutakuelezea hili kwa hoja zitazoupoza moyo wako katika kitabu chake in shaa Allah.

421

Page 422: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Na haya ndiyo maajabu ya makhawariji hawa wa akhiril-zaman! Wanasema uongo wala hawana haya, na vitabu vyao vimejaa uongo.1333

Anasema:

Bali kwa mujibu wa itikadi yao ya batili ya kikhawariji (kiibadhi) hiyo ni dhambi ya kumuingiza mtu motoni milele na wala hatoki tena, na hakuna wa kumuombea, na kama ataombewa basi maombi hayo hayatokubaliwa!

Na anasema Seif Al-Ghaafri, katika utangulizi wake wa kitabu hicho: “Said Qannubi si mwengine zaidi ya kuwa ni mwanakasumba wa kikhawariji: si mkweli”.

Anasema Abu Haashim Al-Musawi katika pongezi zake alizotoa juu ya kitabu hicho:

Nimekitalii kitabu cha ndugu mbora Abul-Fadhli Kassim Mafuta Kassim, nikakikuta kuwa ni kitabu kilicho na faida kwa sampuli yake, katika kuwajibu Makhawariji wa Kiibadhi, pale mtunzi alipozileta HOJA ZENYE NGUVU katika kuthibitisha kuonekana Allah huko Akhera kwa macho, na akaufichua uwongo wa ndugu Juma Al-Mazrui na masheikh zake.

Sasa baada ya hayo, utaona kwamba Maibadhi, kwa mujibu wa Mashekhe hao wa Kiwahabi, ni Makhawaarij na ni waongo na hususan Juma Mazrui na Mashekhe wake (Al-Khalili na Al-Qannubi). Sasa kabla ya mimi kuliweka wazi hilo, napenda kuwakumbusha ndugu zangu mambo mawili:

1) Makhawaarij hawakusemwapo kuwa ni waongo wala hakuna Hadithi yoyote ile iliotungwa na walioitwa Khawaarij, kama walivyokiri wanavyuoni wa Kisunni akiwemu Mzee wa Uislamu, Ibn Taymiyya.

2) Maimamu wa Mawahabi ndio waliosemwa kuwa ni waongo na watunzi wa Hadithi, kama tutavyobainisha humu kwa ushahidi.

Nukta ya kwanza tumeielezea vya kutosha katika vitabu vyetu tafauti. Lakini kwa kuwa kazi hii ni mahususi kwa kuwajibu Mawahabi waliotoa

1333 - Tunukulie huo uwongo ulijaa katika vitabu vyao, ili tukujibu. Mimi nitakunukilia uwongo uliojaa katika vitabu vyenu nawe nipe jawabu yako, yaani ubainishe kwamba hayo nitayoyanukuu hayapo au yapo lakini ni ya kweli.

422

Page 423: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

tuhuma hizo zisizo na ukweli, basi si vibaya hapa tukayanukuu baadhi ya tulioyasema katika kazi nyengine.

WALIOITWA KHAWARIJ HAWANA TABIA YA KUSEMA UWONGO

 Katika baadhi ya maandiko yangu nilisema yafuatayo:

Wanavyuoni wakubwa na watafiti wa sasa wamethibitisha kwamba Khawarij hawakutunga Hadithi. Na zifuatazo ni nukulu za baadhi ya wanavyuoni hao: 1) Anasema Abu Dawud (mpokezi wa Hadithi): “Hakuna katika watu wenye kufuata matamanio yao watu ambao Hadithi zao ni sahihi kuliko Khawarij!” 1334

Na maneno hayo kayanukuu vile vile:

2) Ibn Hajar Al-‘Asqalani. 1335

Na kayanukuu pia:

3) Al-Suyuti. 1336

4) Na anasema Ibn Taymiya:

….tafauti na Makhawarij, hakika yao hajulikani yoyote miongoni mwao (Makhawarij) anayesema uwongo”.1337…………Hakuna katika watu wanaofuata matamanio yao watu wakweli na waadilifu kuliko Khawarij.…wao si katika wanaokusudia kuzua

1334 - Tazama Mizan Al-Itidal cha Al-Dhahabi j. 4 uk. wa 156 katika tarjama ya (عمران حطان .Imran bin Hittan (بن

1335 - Ibn Hajar “HADYU AL-SARI: MUQADDIMATU ALAA FAT-HI ALBARI” uk. 611 katika maelezo yake juu ya Imran bin Hittaan. Tazama wapokezi walioanzia na harfu ya Al-ain ( العين .(حرف1336 - Al-suyutiyy: “TADRIB AL-RAWI” katika mlango kuhusu sifa za mpokezi mwenye kukubalika riwaya zake uk. 285, mas-ala ya 7. Juu utayapata maneno ya Al-Nnawawiy na chini kwenye Tanbihaat utayapata maneno ya Al Suyuti. 1337 - Ibn Taymiyya Al-Tafsiru Al-Kabir . 1, uk. 124.

423

Page 424: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

uwongo bali wao ni maarufu kwa ukweli mpaka inasemwa kwamba Hadithi zao ndio Hadithi sahihi kuliko zote.1338

Na maneno hayo ya pili kayanukuu vile vile: 

5) Dr. Mustafaa Al-Sibai.1339

6) Na akasema Dr. Mustafa niliyemtaja hapo nyuma:

Sikugundua Hadithi iliotungwa na Khawarij, na nimefanya upekuzi (research) sana katika vitabu vya Hadithi za kutunga sikuona Khawarij aliyehesabiwa kuwa miongoni mwa waongo na watunzi wa Hadithi.1340

Na akasema katika uk. 100:

Na kwa hakika nimejaribu kutafuta ushahidi wa kielimu unaounga mkono (dai la) kuwanasibisha Khawarij na utunzi (wa Hadithi), lakini nimeona ushahidi wa kielimu uko kinyume chake: (ushahidi wa kielimu) unawaondoshea tuhuma hii. Na walikuwa (Al-Khawarij) katika ibada ni wenye hadhi kubwa, mashujaa wa wazi, hawamlazii mtu wala hawakimbilii katika taqiyya kama wanavyofanya Shia. Na watu wenye sifa hizi ni vigumu sana kuweza kutokea uwongo kwao. Na lau kama walikuwa wanahalalisha (kumzulia) Mtume (s.a.w.) basi wangewazulia (pia) wale waliokuwa chini yake (kwa daraja) miongoni mwa Makhalifa na Maamiri (viongozi) na Waovu kama Ziyad na Al-Hajjaaj. Na maandiko yote ya historia tulionayo yanatoa ushahidi wa wazi kwamba wao (Al-Khawarij) waliwakabili watawala, Makhalifa na viongozi kwa kipeo cha mwisho cha uwazi na ukweli, basi kwanini waseme uwongo baada ya hapo? Bali mimi narejea kusema kwamba kilichomuhimu kwetu ni kutafuta ushahidi wa kielimu wa wazi wenye kuonesha kwamba wao (Al-Khawarij) ni katika waliotunga Hadithi, na hili ni jambo ambalo sikuligundua hadi sasa.

7) Anasema Sheikh Al-Tiwaani akimnukuu Ibn Taymiyya akisema: ‘Dini yao (Makhawaarij) ni sahihi zaidi kwani hawasemi uwongo.1341….Na akasema katika Al-Furqaan: ‘Na Makhawaarij ni wakweli, basi Hadithi zao ni katika Hadithi sahihi kabisa.1342……. Na Makhawaarij hawasemi

1338 - Ibn Taymiyya “MINHAJ AL-SUNNAH” j. 3, uk. 3. 1339 - Dr. Al-sibai “AL-SUNNA WA MAKANATUHA FII AL-TASHRII AL-ISLAMI” uk. 99- 101.  1340 - Tazama kitabu hicho ukurasa huo huo wa 99. 1341 - Ibn Taymiyya Minhaaju Al-Sunna (Mukhtasar) j. 2, uk. 197. 1342 - Ibn Taymiyya Al-Furqaan Baina Al-Haqqi Wa Al-Baatil uk. 227.

424

Page 425: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

uwongo, nao ni wakweli na ni mashujaa kuliko wao, na ndio wenye kutekeleza zaidi ahadi kuliko wao... 1343

 8) Anasema Al-Mubarad: “Na makundi yote ya Khawarij wanajitenga na kila mwongo na kila mwenye kufanya maasi ya wazi.”1344

 9) Anasema Dr. Muhammad ‘Ajaj Al-Khatib: “Hatukugundua katika vitabu

vya marejeo (books of reference) vilivyo karibu yetu (tulivyonavyo) chenye kuonesha kwamba Khawarij wametunga Hadithi au kwamba wao wametegemea hilo (wametegemea Hadithi ya kutunga) katika kuupa nguvu msimamo wao na kuthibitisha madai yao”.1345

Hizo ni shahada za wasiokuwa Maibadhi wala Khawarij kuhusu suala la kutunga Hadithi au kusema uwongo kwamba suala hilo kwa walioitwa Khawarij halikuwepo kamwe.

Sasa baada ya hayo, utaona kwamba kuna mgongano baina ya madai ya Sheikh Kasim Mafuta na wenzake kwamba Ibadhi ni Makhawaarij na maneno ya wanavyuoni hao walioshuhudia kwamba Makhawaarij ndio watu wakweli kuliko watu wote. Kwa hivyo, tumuachie Bwana Mafuta achague, ama awaite Maibadhi kuwa ni Khawaarij, akifanya hivyo awatoe katika tuhuma yake ya kuwaita waongo; au awaite waongo, akisema hivyo basi awatoe katika matusi yake ya kuwaita Makhawaarij. Au awaite kuwa ni Makhawaarij na ni waongo; ili Imamu wake Ibn Taymiyya na wengine nao wawe waongo kwa kusema hivyo. Kisha baada ya hapo tutampa fursa ya kujadiliana nasi kuhusu:

1) Ukhawarij wa Kiibadhi na wa Kiwahabi.2) Uwongo wa Kiibadhi na wa Kiwahabi. Tutoe ushahidi nani ni

Khawaarij na nani ni mwongo. Naam! Sheikh Mafuta ana ushahidi wake ambao kwawo kawaita Mashekhe wa Kiibadhi kuwa ni waongo. Je nini ushahidi wake? Soma yafuatayo:

1343 - Ibn Taymiyya Minhaaju Al-Sunna (Mukhtasar) j. 1, uk. 393. Nukulu kutoka katika kitabu Ansaru Al-Sunna Tahta Al-Mijhar cha Fadhilatu Al-Sheikh Khalfaan Al-Tiwaani uk. 33. 1344 - Al-Mubarrad “AL-KAMIL FII AL-LUGHA WA AL-ADAB” j. 2, uk. 106. 1345 - Dr. Muhammad Ajaj Al-Khatib “AL-SUNA QABLA AL-TADWIN” uk. 204 – 205.

425

Page 426: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

TUHUMA YA KWANZA: TUHUMA DHIDI YA AL-IMAMU BADRU AL-DIN

AL-KHALILI AL-MUFASSIR

Anasema Kasim Mafuta:

Na haya ndiyo maajabu ya makhawariji hawa wa akhiril-zaman! Wanasema uongo wala hawana haya, na vitabu vyao vimejaa uongo. Kwa ushahidi zaidi hebu tukudokolee mfano mmoja wa uongo wao na mingine itafuatia katika sehemu zake, ni pale mufti wao Khalili alipoamua kulipindua shairi la Ibnul-Qayyim kwa makusudi, kisha Juma naye akafuatia vivyo hivyo! Ametaja al-Khalili katika kitabu chake AL-HAQU DAMIGH, naye Juma katika kitabu chake “Kisimamo” ukurasa wa 93 akasema hivi:

“Na akasema katika “NUNIA” kuhusu wote ambao hawana itikadi ya kihashwiya (Kiwahabi) kwamba ni maadui ambao ukafiri wao ni mkubwa kuliko mushrikina (wenye kuabudu masanamu) Anasema (Ibnul-Qayyim):

الكفران فى أخف ونكوالمشر *** معلن بالعداوة المعطل إنNa muatil ni mwenye kuutangaza uadui *** na washirikina

ni wepesi zaidi katika ukafiri.”

Juma na mufti wake Khalili wameyapindua maneno haya ya Ibnul- Qayyim kwa makusudi, mimi ninawapa chalenji watuletee maneno haya, na mimi ninasema kwamba maneno haya hayamo katika “NUNIA” ya Ibnul-Qayyim. Maneno yaliyomo katika “NUNIA” ni haya:

للرحمن التنزيه قالب فى** * معلن بالعداوة المعطل إنNa muatila ni wenye kuutangaza uadui *** kwa sura ya kumtakasa

Rah’man (Allah mwingi wa reh’ma).

Haya ndugu msomaji ni machache kati ya mengi ya uongo yaliyojaa kwenye vitabu vya makhawarij (maibadhi) wa zama hizi, mpaka Mufti wao pia asema uongo! Na inaonekana kuwa Juma hasomi vitabu kwa kuhakiki mambo, bali yeye ananukuu kiupofu kutoka katika vitabu vya masheikh zake Khalili na Qannubi.

426

Page 427: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

JAWABU

Hayo ndio maneno ya Sheikh Kasim bin Mafuta, nayo yanaonesha kwamba ni mtu asiyemuogopa Mungu hata kidogo. Kwanza tazama ibara yake aliposema: “Na vitabu vyao vimejaa uongo”. Mimi namchalenj huyu Kasim Mafuta anikusanyie huo uwongo tele uliomo katika vitabu vya Kiibadhi, bali aniletee uwongo uliomo katika vitabu vya Kiibadhi kama mimi nitavyomletea uwongo uliomo katika vitabu vya Mawahabi na Maimamu wao. Itakubainikia kwamba mtu huyu hasemi chochote kwa ikhlas wala kwa kutarajia rehema ya Mola wake, bali ni mtu wa kasumba na kupenda mijadala tu na chuki alizonyweshwa kule Suudia! Na hii ni hatari kubwa hasa kwa mtu mwenye kusoma. Namuhurumia sana huyu Kasim Mafuta atakuja kufika mbele ya Allah ajikute kamtukana huyu na yule na hatimae ajikute hana jema hata moja: kafilisika.

Sasa kuhusu ubeti huo, mimi ningependa kusimama na Kasim Mafuta visimamo vingi, kisha baada ya hapo ndipo atapoweza kuamua kumwita mtu mwongo au mkweli:

Kisimamo cha kwanza. Sheikh Kasim elewa kwamba mtu anapozua uwongo dhidi ya mtu mwengine lengo lake ni kuleta maana tafauti na ile iliomo katika maneno ya mtu mwengine huyo. Akifanya hivyo, basi hapo ndio huambiwa kuwa kasema uwongo. Ama anayetumia ibara nyengine yenye maana sawa sawa na ile ya msemaji, huyu huwa haitwi mwongo. Vyenginevyo, wapokezi wote wa Hadithi ni waongo, kwani zaidi ya 70% ya Hadithi za Mtume (s.a.w.) zimepokewa kimaana, yaani wapokezi hutumia lugha zao na maneno yao tafauti na yale alioyanena Mtume (s.a.w.) – ibara ni tafauti na maana ni moja. Isipokuwa akiwa Bwana Mafuta anadai kwamba ubeti wa Ibn Al-Qayyim ni mtukufu zaidi kuliko Hadithi za Mtume (s.a.w.). Hapo, itakuwa hoja ya Bwana Mafuta ni sawa. Baada ya hayo, basi elewa kwamba tafauti baina ya beti mbili hizo ni katika ibara si katika maana kama tutavyokuthibitishia.

427

Page 428: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Kisimamo cha pili. Mara nyingi hutokea beti za mashairi zikawa na riwaya mbili au zaidi. Na hii inatokana na sababu tafauti, moja ya hizo ni kuwa mtunzi mwenyewe abadilishe neno au mjengeko (construction) baada ya kuwa utunzi wa kwanza umeshaenea. Na hili lipo hata kwa washairi wa karibu. Al-Imamu Abu Muslim Al-Bahlaani Al-Rawaahi ni mshairi wa hivi karibuni. Imamu huyu ana shairi la nuniyya lenye kumalizikia:

** �ان حس لإلسالم الي���وم فإنني صدرت ل�كم ان حس وصية تلـكم ** اإلحسان يعقب و إنما كتبت فقد نصحي في أحسنت كن�ت إن

إحسان *** إيمان النص�ح بغير وال يص��ح يناصح�ه من إال الدين يصـدق ال

** فرقان الح���ق ضياء من لكم بدا بصائ�ركم من نص�حي تمكن فإن

Ubeti wa kwanza umepokewa kwa neno sadart:

ل�كم ان حس وصية �ان* صدرت*تلـكم حس لإلسالم الي���وم فإنني

na umepokewa kwa neno thabatat:

ل�كم ان حس وصية �ان* * ثبتتتلـكم حس لإلسالم الي���وم فإنني

Halkadhalika washairi wa kale, utakuta sehemu nyingi za vitabu vya lugha zikisema kwamba shairi hili limepokewa hivi na limepokewa hivi. Kwa mfano ubeti usemao:

أعظمه صدع وشيكا رأبت عطبه** واه من أنقذت عطبا وربه

Mwanzo wa ubeti huu umepokewa pia kwa lafdhi:1346

............ أعظمه صدع وهايا رأبت كائنHalkadhalika ubeti usemao:

*** أغص أكاد قبال وكنت الشراب لي الحميم فساغ بالماء

Ibn ‘Aqiil kautaja kwa lafdhi hio,1347 wakati Ibn Hishaam1348 kautaja kwa lafdhi:

*** أغص أكاد قبال وكنت الشراب لي الفرات بالماء فساغ

1346 - Tazama Sharhu Ibn ‘Aqiil j. 2, uk. 15, kilichotiwa maelezo na Muhammad Muhyi-Din. 1347 - Tazama Sharhu Ibn ‘Aqiil j. 2, uk. 69, kilichotiwa maelezo na Muhammad Muhyi-Din. 1348 - Ibn Hishaam Qatru Al-Nada uk. 34.

428

Page 429: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Anasema mtiaji maelezo:.... (( )) (( عقيل (( ابن في كما الفرات بدل الحميم أخرى رواية للبيت

Ubeti huu una mapokezi mengine ya neno Al-Hamim badala ya neno Al-Furaat kama ilivyo katika Shar-hu Ibn ‘Aqiil.1349

Na pia ukapokewa ubeti huo kwa lafdhi nyengine, 1350 nayo ni: أغص........................ القراح أكاد بالماء

Ubeti wa Hassan bin Thaabit, mshairi wa Mtume (s.a.w.), usemao:

** يأتي حمن الر إلى ناظرات بدر يوم بالفالحوجوه

ubeti huo pia umepokewa kwa lafdhi:

** يأتي حمن الر إلى ناظرات بدر يوم بالخالص وجوه

Kwa hivyo, kwa ujumla ni kuwa hiki ni kitu kilichopo, wala haitakiwi mtu kurukia akawaita watu waongo tu kwa sababu anawachukia. Hata unayemchukia basi ni wajibu wako wa Kisharia kwamba umfanyie uadilifu, hio ni kheri kwako. Bora kwanza Sheikh Kasim Mafuta angeliuliza: “Wapi mumeupata ubeti huu kwa muundo huo?” Bora angeuliza hivyo bila ya kutukana na kuchalenj bila ya elimu. Hapo tungeweza kumsaidia ndugu yetu. Lakini kajitumbukiza kwenye dimbwi la tope kwa kumtukana Muislamu tena mwanachuoni mcha Mungu.

Kisimamo cha tatu. Tukijaalia kwamba kweli, Sheikh Al-Khalili kaupindua ubeti huo, kama ulivyodai, suala ni kuwa je kuna tafauti ya maana baina ya beti mbili hizo?1351 Tazama ubeti alioutaja Sheikh Al-Khalili katika Al-Haqqu Al-Damigh akifuatiwa na Juma Al-Mazrui katika Kisimamo:

فى أخف ونكوالمشر *** معلن بالعداوة المعطل إنالكفران

Na muatil ni mwenye kuutangaza uadui *** na makafiri washirikina ni wepesi zaidi katika ukafiri.”

1349 - Marejeo ilio kabla. 1350 - Marejeo ilio kabla, katika maelezo ya chini. 1351 - Basi kwa mantiki hii na Al-Albani kamzulia uwongo Ya’aqub bin Shaiba Al-Sadusi kwani kamnukuu kwa lafdhi tafauti na ile alioinena yeye, pamoja na kuwa maana ni moja. Tazama matamshi ya Ya’aqub bin Shaiba katika Tahdhibu Al-Tahdhib j. 8, uk. 346-347, tarjama na. 691, katika tarjama ya Qais bin Abi Haazim. Kisha tazama maelezo ya Al-Albani katika Al-Sahiha j. 1, sehemu ya pili uk. 847, maelezo ya Hadithi na. 474, utaona kwamba maana ni moja, lakini ibara za Al-Albani zimekatwa na kubadilishwa kidogo. Sijui na huu pia kwako ni uwongo ewe Kasim bin Mafuta?!

429

Page 430: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Halafu tazama beti zilizomo katika Nuniyya, katika chapa hii tulionayo leo:

كفرانهم في أخف الشيطان ***والمشركون شيعة من وكالهماقائم بالعداوة المعطل ل�ل���ر�ح�م�ن� ***إن ا�ل�ت�ن�ز�ي�ه� ق�ا�ل�ب� ف�ي�

Na washirikina ni wepesi zaidi katika ukafiri wao Na wote ni wafuasi wa shetani.

Hakika ya Mu’attil ni wenye kusimamisha uadui Katika mfumo wa kumtakasa Mwingi wa rehema.

Sasa kimsingi hapa, ukitazama beti zote mbili utaona kwamba zina maana moja nayo ni kuwa Mu’attila (yaani jumhur ya Sunni, Ibadhi, Shia, Zaidia na wengine) wote hawa ni makafiri na ukafiri wao ni mkubwa zaidi kuliko ukafiri wa Abu Jahl, Yahudi na Nasara! Haya ndio madhumuni ya beti hizo na mwote madhumuni hayo yamo sawa sawa hakuna ziada inayopatikana katika ubeti ulionukuliwa na Sheikh Al-Khalili hata ikafaa kuambiwa kwamba lafdhi yake kaibadilisha – lafdhi ni tafauti; maana ni moja.

Lakini wewe Sheikh Kasim bin Mafuta, ulipojua kwamba lengo la beti hizo ni kuwa Ibn Al-Qayyim kawakafirisha jumhur ya Waislamu wa madhehebu zote, jambo ambalo ndilo analolizungumzia Sheikh Al-Khalili, basi umefanya tadlis (ghushi) kama kawaida yako katika sehemu kadha wa kadha za kitabu chako – kughushi! Ulipolijua hilo basi ubeti wa kabla hukuutaja, ili watu maana isiwabainikie, na badala yake umetaja ubeti:

للرحمن التنزيه قالب فى** * معلن بالعداوة المعطل إنNa muatila ni wenye kuutangaza uadui *** kwa sura ya

kumtakasa Rah’man (Allah mwingi wa reh’ma).

Ninakwambia kwamba: maudhui ya ubeti huu uliounukuu wewe, kimsingi sio anayoizungumzia Sheikh Al-Khalili, kwani yeye anazungumzia kitendo cha Ibn Al-Qayyim cha kuwakafirisha Waislamu, jambo ambalo linathibiti kwa beti mbili kwa pamoja – ya mwanzo ulioiwacha na ya pili ulioinukuu. Sasa kama ulikuwa unaona kwamba ubeti aliounukuu Sheikh Al-Khalili umepinduliwa – japo kuwa maana ni moja – na kwa kuwa maudhui inayozungumziwa hapa umeshaifahamu, basi ulikuwa ufikishe amana ya elimu, na unukuu beti zote mbili ili maana ikamilike na wenye akili wahukumu kwa haki. Lakini wewe hukufanya hivyo, kwani ulikuwa unajua kwamba:

3) Maudhui anayoizungumzia Sheikh Al-Khalili inathibiti sawa sawa kwa kutumia ubeti wowote katika beti hizo – aliyoinukuu yeye au ulioinukuu wewe.

430

Page 431: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

4) Ibn Al-Qayyim kafanya jarima kubwa kwa maneno alioyasema katika ubeti huo uliouwacha ya kuwakafirisha Waislamu wote isipokuwa wachache ambao wanakubaliana naye. Tena kawakafirisha ukafiri wa kuwatoa kabisa katika mila ya Uislamu kwani kawafanya kuwa ni waovu kuliko makafiri washirikina.

Kisimamo cha nne. Ni kuwa tatizo lako Sheikh Mafuta na watu wengi wa skuli yenu ni kuwa nyinyi hamusomi isipokuwa vitabu vya Ibn Al-Qayyim na Ibn Taymiyya na walio mfano wa hao – hamujui nini kilichoko ulimwenguni! Ndio maana Sheikh Seif Al-Ghafri akatutaka tusome Minhaju Al-Sunna cha Ibn Taymiyya na Al-Sunna cha Ibn Ahmad. Hii ni kuwa yeye hajaona vitabu bora kuliko hivyo, pamoja na kuwa kitabu kiitwacho Al-Sunna kimejaa riwaya za kutunga na itikadi ya tashbihi na kuwakafirisha Maimamu wakubwa kama vile Abu Hanifa na wengine, na Minhaju Al-Sunna watu wamekiita Minhaju Al-Bidaa kwa jinsi kilivyojaa bidaa na falsafa za Kiyunani (Kigiriki). Wallahu Al-Musta’aan! Ninachotaka kukwambia hapa ewe Sheikh Kasim “Ntotongwa wa” Mafuta ni kuwa ubeti huo haukutungwa na Sheikh Al-Khalili wala haukupinduliwa na Sheikh Al-Khalili, bali ubeti huo umo katika kitabu cha mwanachuoni mkubwa aliyeishi katika zama moja na Ibn Al-Qayyim. Na kitabu hicho mwanachuoni huyo kakitunga ili kumjibu Ibn Al-Qayyim kwa upotovu wake uliomo katika Qasidatu Nnuuniyya. Huyu si mwengine bali ni Imamu mkubwa wa Kishafi, Al-Imamu Abu Hasan Taqiyyu-Din Al-Subki aliyefariki mwaka 754 A.H. Ubeti huo uko katika kitabu chake alichokiita Al-Saifu Al-Saqiil Fii Al-Raddi ‘Alaa Ibn Zafil uk. 207 kwa mpangilio wa Sharhu ya Muhammad Zahid Al-Kawthari.1352 Unasema ubeti:

فى أخف ونكوالمشر *** معلن بالعداوة المعطل إنالكفران

Hakika ya mu’attil ni mwenye kuutangaza uadui *** na makafiri washirikina ni wepesi zaidi katika ukafiri.”

Na Al-Subki huyu – kama tulivyosema – kaishi zama moja na Ibn Al-Qayyim na kitabu hiki kakitunga kumjibu Ibn Al-Qayyim, wala hakusema Ibn Al-Qayyim kumwambia Al-Subki kwamba umenizulia uwongo. Hii ina maana kwamba:

1) Ubeti huo ni sahihi. Na kwamba hio ni moja ya riwaya zake hususan ukizingatia ukweli kwamba maana ya beti zote mbili ni sawa sawa.

1352 - Mwisho wa kitabu hiki nitakuwekea scanned copy ya kitabu hicho cha Al-Subki Al-Shafi.

431

Page 432: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

2) Au Ibn Al-Qayyim alibadilisha muundo wa beti zake, lakini maana kaiwacha ile ile.

3) Au Al-Subki kauleta ubeti kimaana, na Ibn Al-Qayyim mwenyewe hakuona kwamba kuna tafauti.

Kwa hali zote zile, hakuna hapa kitu uwongo, bali kuna:1) Uchache wa maarifa ya Kasim Mafuta na yule aliyemuiga kule

Suudia yaani Dr. ‘Ali Al-Faqihi.2) Kutokuyajua yaliomo katika vitabu vya watu wengine.3) Kutokuwa na uadilifu wakati wa kuandika, kwa hivyo kumwita mja

mwema wa Allah aliyesifika kwa elimu, ucha Mungu na karama za wazi kuwa ni mwongo ni jambo rahisi kwa watu wa skuli hio ya Kiwahabi. Hivyo ndivyo walivyolelewa na Mashekhe wao na Maimamu wao kama mulivyojionea. Fawailun lakum min wa’idin shadid!

Wala huwezi kudai kwamba Al-Subki alikuwa adui wa Ibn Al-Qayyim kwa hivyo nukulu zake hazikubaliki, kwani tunasema:

1) Hakuna tafauti ya maana baina ya ubeti aliounukuu Al-Subki na beti zilizomo leo katika Nuniyya ya Ibn Al-Qayyim.

2) Al-Subki ni mwanachuoni mkubwa wala hakuna aliyemtuhumu kwa uwongo. Na ni jambo la kawaida kwa wanavyuoni kunukuliana maneno yao.

3) Al-Subki kaishi zama moja na Ibn Al-Qayyim, na wala Ibn Al-Qayyim hakumpinga kwa hilo.

MUKHTASARI NA NUKTA MUHIMU

1) Tulichokizungumzia hapa ni madai ya Kasim Mafuta kwamba Sheikh Al-Khalili, Mufti Mkuu wa Oman, ni mwongo!!!

2) Uwongo wake – kwa mujibu wa Kasim Mafuta akimuiga ‘Ali Al-Faqihi – ni kwamba Sheikh Al-Khalili kaunukuu ubeti wa shairi la Ibn Al-Qayyim kwa matamshi yalio kinyume na yalivyo matamshi ya ubeti wenyewe.

3) Lafdhi za beti za Ibn Al-Qayyim katika kitabu chake kinachopatikana leo ni:

كفرانهم في أخف الشيطان ***والمشركون شيعة من وكالهماقائم بالعداوة المعطل ل�ل���ر�ح�م�ن� ***إن ا�ل�ت�ن�ز�ي�ه� ق�ا�ل�ب� ف�ي�

Na washirikina ni wepesi zaidi katika ukafiri wao Na wote ni wafuasi wa shetani.

Hakika ya Mu’attil ni wenye kusimamia uadui Katika mfumo wa kumtakasa Mwingi wa rehema.

4) Sheikh Al-Khalili kaunukuu kwa lafdhi isemayo:

432

Page 433: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

فى أخف ونكوالمشر *** معلن بالعداوة المعطل إنالكفران

Hakika ya mu’attil ni mwenye kuutangaza uadui *** na washirikina ni wepesi zaidi katika ukafiri.”

5) Tumebainisha kwamba beti za mashairi zinakuwa na riwaya tafauti, haitakiwi kumwita mtu mwongo mpaka uwe na hakika na kuwe na tafauti ya maana baina ya ubeti alioutaja na ubeti unaodai wewe kwamba ndio sahihi.

6) Tumebainisha kwamba ili mtu aitwe mwongo ni lazima anukuu kitu ambacho maana yake ni tafauti na kilivyosemwa. Wala mtu haitwi mwongo kwa kutumia maneno tafauti akaifikisha maana sawa na ya msemaji au muandishi. Vyenginevyo, asilimia kubwa ya Hadithi lafdhi zake hakuzitamka Mtume (s.a.w.), bali Hadithi nyingi zimepokewa kimaana.

7) Ubeti alioutaja Sheikh Al-Khalili na beti zilizomo katika kitabu Nuniyya cha Ibn Al-Qayyim leo ni sawa sawa kimaana: maana haizidi haipungui. Kwani zote:

a) Zinasema kwamba Muattila (jumhur ya Masuni, Maibadhi, Mashia, Zaidiyya na wengineo), wote hawa ni maadui wa Allah.

b) Wote hao ni makafiri zaidi kuliko washirikina (kama Mayahudi na Manasara). Sasa uwongo uko wapi na una faida gani?

8) La mwisho ni kuwa huo ubeti aliounukuu Sheikh Al-Khalili pia upo katika kitabu cha mwanachuoni mkubwa wa Kishafi, naye ni Al-Subki Al-Kabir, aliyeishi zama moja na Ibn Al-Qayyim. Ubeti huo umo katika kitabu cha mwanachuoni huyo ambacho anamjibu Ibn Al-Qayyim kama tulivyobainisha.

9) Kwa hivyo, kudai kwa Kasim Mafuta – akimuiga ‘Ali Al-Faqihi – kwamba ubeti huo kaupindua Sheikh Al-Khalili, kunaonesha uchache wake wa kutaalii vitabu vya wanavyuoni.

10) Al-Subki ni mwanachuoni aliyesifika kwa elimu na ucha Mungu, kwa hivyo inafaa kunukuu kutoka kwake.

11) Ibn Al-Qayyim hakusema kumwambia Al-Subki kwamba umenizulia uwongo.

Huu ndio mukhtasariwa jawabu yetu kwa Kasim Mafuta juu ya maneno yake munkar alioyasema kwa chuki zake na uadui wake. Akipenda kutangaza kosa lake na toba yake – yeye na waliomuunga mkono kwa kukipitia kitabu chake na kumzuzua – na atubie, akipenda kufanya kibri na afanye, na Mbora wa kuhukumu yupo na siku itafika tu atajulikana mkweli na mwongo.

433

Page 434: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

YALIOSEMWA NA WAADILIFU WA KISUNIKUHUSU SHEIKH AL-KHALILI

Baada ya hayo, sasa wacha nikunukulie baadhi ya yaliosemwa na Masuni waadilifu – si wenye chuki kama Kasim Mafuta na Mashekhe wake – kuhusu Sheikh Al-Khalili. Dr. Abdullah Al-Qatm wa Kuweit aliielezea ziara yake ya Oman katika Gazeti Aqabas la Kuweit 19/11/2008. Na katika maelezo yake marefu alisema:

Madhehebu Rasmi ya Ufalme wa Oman ni Madhehebu ya Kiibadhi, na mufti wa Oman ni Sheikh Ahmad Al-Khalili naye ni mtu mwenye mitazamo iliofunguka anachukua (rai) kutoka katika madhehebu zote na anawashauru wanavyuoni wa Madhehebu nyengine wala hayadharau madhehebu mengine huku akijipa nguvu kwa utawala wa dola, Waomani wote wanamuabudu Allah kila mmoja kwa mujibu wa madhehebu yake na kwa kile alichokikinai. Basi kwanini dola za majilis Al-Ta'awun za Ghuba haziigi siasa ya Ufalme wa Oman katika mshikamano wa madhehebu za Kiislamu badala ya kupigana vita na kupakaziana (majina mabaya), jambo ambalo limeuhujumu msafara wetu kana kwamba madhehebu nyengine zimetoka katika sayari nyengine (isiokuwa dunia). Na baadhi ya wenye kasumba huyachukua madhehebu ya waliowengi ili kuyashambulia madhehebu ya walio wachache; na baadhi ya wengine hukusudia kukiangusha kima cha upande mwengine (madhehebu nyengine).

Ama Dr. ‘Aaidh Al-Qarni wa Suudia, yeye baada ya kutembelea Oman alistaajabishwa na tabia za Waomani, ukarimu wao, tawadhui zao na ufasaha wao. Na akafanya mahojiano na T.V. ya Jazira na katika maelezo yake alisema:

Mufti wao Sheikh Ahmad Al-Khalili ni aya katika ukarimu. Alitupokea nyumbani kwake na akatukirimu kiasi cha kwamba alitukumbusha

434

Page 435: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

(ukarimu wa) Hatim Al-Tai……niliyasikia haya kabla ya safari yangu lakini kusikia si kama kuona..1353

Hayo ni machache katika mengi mno yaliosemwa kuhusu mwanachuoni huyu mcha Mungu. Binafsi nimeyasoma na kuyasikia mengi lakini haikunijia kuwa niyahifadhi kwa vile sikudhania kwamba kuna siku nitayahitaji. Lakini kama utafuatilia kwa watu mbali mbali basi utayasikia mengi yalionenwa na yalioandikwa na wanavyuoni waadilifu wa Kisuni kuhusu Imamu huyu.

Kwa hivyo, baada ya hayo machache, utaona kwamba wanavyuoni waadilifu na Waislamu wengine wanamsifu Sheikh Al-Khalili kwa elimu, ucha Mungu, ukarimu na tabia nzuri; na Kasim Mafuta, kwa dhulma na uzushi, anamwita mwongo! Fartaqibuu inii ma’akum raqiib.

1353 - Ingia katika google au hotmail au youtube kisha andika an-wani ifuatayo utaipata video hio ya mahojiano. Andika:

وأهلها عمان يمدح القرني عائض الشيخ

435

Page 436: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

TUHUMA YA PILI: TUHUMA DHIDI YA IMAMU AL-SUNNA WAL USULI

WAL FURU’I AL-QANNUBI

Anasema Sheikh Mafuta kuhusu Al-Imamu Al-Qannubi:

Hebu ndugu msomaji yasome tena maneno ya ndugu Juma ambayo amemnukuu sheikh wake al Qannubi kwa uangalifu, amesema bwana Juma: “Na akasema Al-Albani (mwanachuoni wa Hadithi wa kiwahabi) katika kitabu chake Al-Dhaifa: “Hakika ya Hamad anakosea sana”1354.!!! Mwisho wa kunukuu.

Ndugu msomaji, hebu linganisha maneno haya ya ndugu Juma na sheikh wake Al-Qannubi wanayodai kuwa ni maneno ya sheikh Al-Albani, na hayo maneno yenyewe ya sheikh Al-Albani ambayo tumeyanukuu hapo juu kutoka kwenye kitabu chake, ukilinganisha utaona yanatofautiana. Sheikh Al-Albani anasema:

“HAMAD BIN SALAMA NI IMAMU MIONGONI MWA MAIMAMU WA KIISLAMU NI THIQA TENA NI HOJA NA HAKUNA SHAKA YOYOTE KATIKA HILO, NA SUALA LA KUKOSEA HALIMTOI KATIKA DARAJA HIYO, KWANI NI NANI ASIEKOSEA?

Juma anadai kwamba sheikh Al-Albani amesema: “HAKIKA HAMAD ANAKOSEA SANA” na maneno hayo ameyanukuu Juma kutoka kwa sheikh wake al-Qannubi! Bali la ajabu zaidi ni kuwa tunaona katika maneno ya sheikh Al-Albani kinyume chake: kwamba HAMAD NI IMAMU MIONGONI MWA MAIMAMU WA KIISLAMU, THIQA, TENA HOJA…? Bali isitoshe sheikh Al-Albani amemtetea sana Hamad dhidi ya wale wenye kudai kwamba anakosea.

1354 - Al-Abani Al-Dhaifa juzuu ya 2 ukurasa wa 333.

436

Page 437: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Bila shaka ndugu msomaji kwa maelezo haya utakuwa umebainikiwa na uongo alioufanya Juma na sheikh wake al-Qannubi.

Wameamua kufanya hivyo kwa makusudi baada kugundua kwamba sheikh Al-Albani mwanachuoni mkubwa wa Hadithi katika zama hizi, anayekubalika na waislamu wengi duniani tena kwa kiwango cha juu mno! Kwa hiyo wakaona wamtumie kama ngazi ili wafikie malengo yao mabaya, ndipo bila haya wala aibu wakaamua kumzulia uongo wa wazi. Wameamua kumzulia uongo sheikh huyo ili msomaji akiyasoma maneno hayo moja kwa moja adhanie kwamba sheikh Al-Albani naye ni miongoni mwa wanaomtia kasoro Hamad bin Salama na kumdhoofisha kwa sababu ya kukosea sana, na hali yakuwa hivyo sivyo kabisa! Bali ni uwongo mweupe kama jua la mchana wa saa sita. Na hapana shaka kuwa kitendo hiki ni kitendo kiovu tena cha kidhalimu, na huo si mwenendo wala sera za maulamaa waliosimama katika njia ya haki ambao lengo lao ni kutaka kuwaelimisha watu haki ili waifuate, bali hivyo ni vitendo vya watu wa batili waliofilisika katika hoja, kwa sababu siku zote mtu mkweli mwenye hoja zenye nguvu hayuko tayari kughushi 1355 wala kusema uongo katika suala lolote, wachilia mbali suala la dini, sasa inakuwaje mtu mwenye kudai uimamu na ijtihadi tena mcha Mungu awafanyie ghushi waislamu katika jambo la itikadi ya dini yao kwa sababu ya kulinda misimamo ya kimadhehebu na ukabila?1356 Bali kwa mujibu wa itikadi yao ya batili ya kikhawariji (kiibadhi) hiyo ni dhambi ya kumuingiza mtu motoni milele na wala hatoki tena, na hakuna wa kumuombea, na kama ataombewa basi maombi hayo hayatokubaliwa!

1355 - Sasa wewe Kasim Mafuta katika kitabu chako umeghushi mara ngapi?! 1356 - Huu ukabila nao umetoka wapi?! Mafuta wee! Weye wajua kwamba madhehebu ya Ibadhi ndio ya mwanzo kuukataa ukabila? Mafuta wee! Wajua weye kwamba watangulizi wa Maibadhi ni watu wa mwanzo kumchagua khalifa asiye Quraishi?! E Mafuta wee! Wajua weye kwamba katika madhehebu ya Ibadhi Imamu wa dola anakuwa mtu wa kabila yoyote tafauti na itikadi ya madhehebu nyengine ambapo wanalazimisha kwamba lazima khalifa awe Quraishi na wengine wakazidisha ulazima wa kuwa Ahlu Al-Bait. Mafuta! Weye wawajua viongozi wa Dola ya Kiibadhi ya Kirustumi iliokuwa Magharibi ya Kiarabu? Je wao walikuwa ni Waarabu ukiachilia mbali uquraishi na uahlu al-bayt? E Mafuta wee! Wajua weye kwamba Abu ‘Ubaida, Imamu wa pili wa Kiibadhi naye si Mwarabu bali ni mtumwa mkombolewa (mawla), aliwaamrisha Maibadhi Mabarbari wa Magharibi ya Kiarabu wamchague Abu Al-Khattab mwarabu wa Yemen kuwa ndiye Imamu wao na wakafanya hivyo? Sasa ikiwa huyajui hayo basi soma yalioandikwa na Dr. mwanamke wa Kimisri aitwaye Al-Ustadha Al-Duktura Sayyida Ismaa’iil Kashif, anasema: “Na kwa kupitia katika hizi sira tunazozisimamia kuzieneza, basi tumeweza kujua kwamba Maibadhi au “Waislamu” walikuwa wakitilia mkazo suala la umoja wa dini wala si umoja kasumba za Kikabila”. Tazama kitabu Al-Siyar chenye mjumuiko wa risala za Maimamu wa Kiomani na wa Kiibadhi wa awali kilichohakikiwa na Dr. huyo uk. 13. Tanbihi: neno “Muslimun (Waislamu)” ndilo walilokuwa wakijiita Maibadhi wa awali. Wao walikuwa wakijiita Waislamu tu, kwa hivyo maneno Maibadhi au “Waislamu” yana maana moja katika istilahi ya Maibadhi wa awali.

437

Page 438: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Na hapa Juma anajinyonga mwenyewe kwa kitanzi chake kwa sababu ya itikadi yao potofu, anasema katika kitabu chake kisimamo katika sala: “Na unajua Sheikh X. ni kitu gani kimewafanya wanazuoni wa kiibadhi wasiseme uwongo? Ni kwa sababu ya itikadi yao kwamba MADHAMBI MAKUBWA YANAMUWEKA MTU MOTONI MILELE NA YANAMPOROMOSHEA MEMA YAKE, NA UWONGO NI KATIKA MADHAMBI MAKUBWA”. Mwisho wa kunukuu. 1357

Tazama hapa namna wanavyojinyonga na kamba yao wenyewe! Je wewe ndugu Juma, na sheikh wako Al-Qannubi hamuogopi kukaa motoni milele kwa kusema uongo? Je hamuogopi kuporomoshewa amali zenu na kuanguka uadilifu wenu?

Hivi ndugu Juma kwa sababu ya uongo wenu kama huu ndiyo mnataka kufanya mijadala na maulamaa wakubwa kama Ibn Baz – kama mnavyodai – na mko tayari kwenda kuapa kwenye Ka’aba? Hamuogopi?

Hivi kweli mnaweza kudai kwamba mwanchuoni mkubwa kama al-Allaama sheikh Abdul-Aziz Ibn Baz awakimbie watu kama nyinyi wenye hoja dhaifu tena za uongo namna hii ?!!

Kama mkiwa mmeweza kupotosha yaliyoandikwa vitabuni ambayo yako dhahiri shahiri, na mkaweza kuwazulia maulamaa mambo ambayo hawakusema, kweli mtashindwa kuzipotosha, na kuzigeuza habari zilizofanyika ndani ya ofisi tena kwa siri, tena mashahidi wa tukio hilo ni nyinyi wenyewe? Eti Ibn Bazi amkimbia Khalili! Kwa hoja gani alizonazo Khalili na wafuasi wake? Hoja zenyewe ni hizi za uwongo anazozitaja Juma kutoka kwa Qannubi na Khalili? Vitabu vya Al-Albani vimejaa ulimwenguni mashariki na magharibi, mmemzulia wazi wazi! Je mtashindwa kuzua yaliyofanyika ofisini kwa siri?

Ndiyo maana ukiyatazama maneno ya Juma kuhusu suala la kukutana Ibn Baz na Khalili utauona uongo unaelea juu juu, kwa mfano pale aliposema:

“Kwa hivyo Al-khalili akamtaka Ibn Baz ambaye kawaita maibadhi MAKAFIRI wende mbele ya Al-kaba Takatifu wakaombe hivi hivi, lakini Ibn Baz akaogopa.

Na hii inatosha kuonesha kuwa hata yeye mwenyewe Sh. Ibn Baz hana hakika na itikadi yake. Na kama si hivyo kipi kimemzuia kumtaka Mwenyezi Mungu aibainishe haki baina yake na watu ambao kawaita makafiri.”!!!! Mwisho wa kunukuu uwongo wa ndugu Juma.

1357 - Juma Mazrui Kisimamo Katika Sala uk. 28.

438

Page 439: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Tazama kitabu chake “Hoja zenye Nguvu” ukurasa wa 42. Je ni kweli Ibn Baz amewaita maibadhi makafiri? Ni mahali gani hapo? Kitabu gani ? Mbona hukututajia? Vitabu vya Ibn Baz vimejaa tele hapa duniani, hebu tutajie kitabu kimoja ambacho Ibn Baz amesema maneno hayo, na hii ni chalenji nina kupa wewe Juma na masheikh zako Khalili, al-Qannubi, na Ahmad bin Su’ud al-Siyabi mtutajie ni mahali gani Ibn Baz amewaita maibadhi kuwa ni makafiri kwa uwazi kabisa, bila ya kuhitajia taawili.

JAWABU NA MAELEZO

Hayo ndio matusi ya mtu ajiitaye Ahlu Sunna. Sujui ni Sunna ya nani anayoifuata, kwani Mtume (s.a.w.) alikuwa hatukani watu, hata mwenye kukosea basi humfahamisha kwa njia nzuri. Kwa ufupi ni kuwa, hapa – katika maneno ya Sheikh Kasim – tuna masuala haya:

1) Suala la kuwa Hammad bin Salama ni thiqa au si thiqa.2) Al-Qannubi kamzulia Al-Albani kitu ambacho hakukisema. Na kitu

chenyewe ni madai ya Al-Qannubi kwamba Al-Albani kasema: “Hakika Hammad anakosea sana”. Sasa je Al-Albani ni kweli kasema hivyo ili Kasim Mafuta awe mwongo; au hakusema ili Al-Qannubi awe mwongo?

3) Je kweli Sheikh Al-Khalili alimtaka Ibn Baz wafanye mjadala na wende mbele ya Al-Kaba wakaapishane au huo ni uwongo?

4) Je Ibn Baz kawakafirisha Maibadhi au hakuwakafirisha?

Hizo ndio nukta muhimu zilizomo katika maelezo ya Sheikh Kasim bin Mafuta. Ama kuhusu je Hammad bin Salama ni thiqa au si thiqa hili nitakujibu kwa urefu katika sehemu tutayozungumzia riwaya yake, nayo ni katika juzuu ya mwisho ya kitabu hiki itayokuwa mahususi kwa suala la kuonekana au kutoonekana kwa Allah.

Ama kuhusu maneno yako mengine nitakujibu katika sehemu hii jawabu ambayo kila mtu atamjua mkweli ni nani na mwongo ni nani. Natuanzie na maneno yako uliposemma:

Wameamua kufanya hivyo kwa makusudi baada kugundua kwamba sheikh Al-Albani mwanachuoni mkubwa wa Hadithi katika zama hizi, anayekubalika na waislamu wengi duniani tena kwa kiwango cha juu mno!

Kwanza nikuulize: ivo wewe huoni haya kumwita Al-Albani kuwa ni mwanachuoni wa Hadithi, licha ya kuongeza sifa ya “mkubwa

439

Page 440: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

anayekubalika duniani”. Rejea katika sehemu tulioyajadili maneno ya Sheikh wako Seif Al-Ghafri uone nukulu za makosa ya Al-Albani katika Hadithi. Na hayo ni machache tu: makosa yake ni kwa maelfu, yametungiwa vitabu kwa majalada! Hebu niambie ni nani aliyekubaliana na Al-Albani duniani isipokuwa baadhi ya watu wa madhehebu yake ya Kiwahabi. Al-Albani:

1) Alikuwa hajui hata mambo alioyaandika mwenyewe. Bali kitu alichokiandika katika ukurasa mmoja anajigonga katika ukurasa huo huo.

2) Alikuwa hajui hata Hadithi zilizomo katika Al-Bukhari na Muslim. Na ushahidi tumetoa.

3) Alikuwa akiisahihisha Hadithi asubuhi na jioni akiidhoofisha.4) Kajigonga katika mamia kama si maelfu ya Hadithi.5) Katolewa makosa ambayo hajawahi kutolewa kiumbe yoyote wa

Allah.6) Hajui tawaadhu’i ilivyokaa: haoni tabu kujisifu! Sijasikia

mwanachuoni mcha Mungu kujisifu. 7) Kasemwa kwa tabia mbaya na wanafunzi wake mwenyewe alioishi

nao miaka nenda miaka rudi. Bila shaka hao wanamjua Al-Albani zaidi kuliko Kasim Mafuta wa Pongwe.

Baada ya hayo, wewe Sheikh Mafuta unamponda Sheikh Said Al-Qannubi, na unamsifu Al-Albani? Ni kweli kabisa kwamba wewe unazungumza kwa msukumo wa umadhehebu na kasumba halafu unawambia watu wana umadhehebu! Ama kuhusu Sheikh Said Al-Qannubi, kasifiwa na idadi kubwa ya wasio kuwa Maibadhi. Nakupa baadhi ya sifa zake:

1) Asilimia sabiini au zaidi ya elimu yake imo kichwani: sio vitabuni.2) Kahifadhi vitabu vya Hadithi na sanad zake na njia zake kwa idadi

ambayo hawakuhifadhi maelfu ya walioitwa kuwa ni mahuffadh. 3) Kahifadhi vitabu vya fani nyengine zote zilizobaki kwa wingi mno.4) Ana hifadhi kali ambayo hata Maimamu wakubwa waliotangulia

basi ni nadra aliyekuwa mfano wake. Tazama kitabu cha Al-Imamu Al-Rabi’u bin Habib kina Hadithi 1005, kakihifadhi usiku mmoja.

5) Ikiwa Ibn Taymiyya kasifiwa kwa kutunga Al-’Aqidatul Al-Wasatiyya bila ya kurejea vitabuni nacho ni kitabu ambacho mwanafunzi yoyote anaweza kukiandika, basi ninakwambia rudi ukisome kitabu Al-Ra-ayu Al-Mu’utabar cha Al-Imamu Al-Qannubi alichokiandika kwa kichwa bila ya kurejea kitabu, utazame elimu iliokuwemo. Pia tazama kitabu Al-Imamu Al-Rabi’u Musnaduhu wa Makanatuh uone elimu iliokuwemo pamoja na kuwa – kama kitabu chenyewe kinavyojieleza – sehemu kubwa ya kitabu hicho kaiandika bila ya kurejea kitabu, pia rejea kitabu Al-Saifu Al-Haadi

440

Page 441: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

uone elimu iliokuwemo, nacho pia baadhi ya sehemu zake kakiandika bila ya kurejea kitabu.

6) Kasifika kwa ucha Mungu na zuhd na wara’a.

Baada ya hayo, elewa ndugu msomaji kwamba mimi sikusudii kumponda Al-Albani kwa sababu ya madhehebu yake na kumsifu Al-Qannubi kwa sababu ya madhehebu yake, lakini nashangazwa na akili ya huyu Sheikh Mafuta! Ivo anadhani Kasim Mafuta kwamba wakati wa leo atamdanganya nani na watu wanamuona Al-Qannubi live katika T.V. anavyojibu masuali; na, kwa upande wa pili, wanasoma vitabu tafauti alivyokosolewa Al-Albani na wanaona makosa yake kwa maelfu alioyafanya. Bali tatizo zaidi la Al-Albani ni pale anapozungumza: sio anapoandika, kwani akiandika alau hutazama fahras (table of contents au yaliyomo) za vitabu, lakini akizungumza ndio kabisa haipati fursa hio, basi mambo yote huyaweka kichwa chini miguu juu! Sisi tunawachalenj Mawahabi akiwemo Kasim Mafuta mutoe makosa katika vitabu vya Al-Qannubi kama alivyotolewa Al-Albani. Sikusudii makosa mawili matatu, kwani hakuna binaadamu asiyekosea, lakini makosa yanapofika kuwa ni kwa kapu na magunia kama yalivyo makosa ya Al-Albani basi tena mtu huyo anakuwa dhaifu. Sina shaka yoyote kwamba Al-Albani angeliishi katika zama za Ibn Ma’in basi tungelimsoma katika diwani za wapokezi dhaifu na mudallisin (wenye kughshi)! Na Al-Qannubi angeishi zama hizo basi tungelisoma ibara kama: “Thiqa, Hafidh, Hujja, na alikuwa Ibadhi au alikuwa na rai za Khawarij!”

Ama tukirudi tena katika maneno yako uliposema:

Wameamua kufanya hivyo kwa makusudi baada kugundua kwamba sheikh Al-Albani mwanachuoni mkubwa wa Hadithi katika zama hizi, anayekubalika na waislamu wengi duniani tena kwa kiwango cha juu mno!

Ninakwambia! Sikiliza ewe Sheikh Mafuta! Tatizo lako ni lile lile husomi isipokuwa vitabu vyenu! Sheikh Al-Qannubi katika vitabu vyake ameeleza kwa uwazi kwamba yeye kumnukuu kwake Al-Albani si kwa sababu usahihishaji wake na udhoofishaji wake wa Hadithi unazingatiwa, bali ni kwa sababu ya kutaka kuwarejeshea Mawahabi hoja zao kwani wao wanadhania kuwa Al-Albani ni mwanachuoni! Al-Albani kadhoofisha Hadithi nyingi sahihi na kasahihisha Hadithi nyingi dhaifu bali maudhui (za kutunga). Na wala hakuwa na akhlaaq kwa ushahidi uliotolewa na wanafunzi wake.

441

Page 442: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Mahmud Al-Istambuli ni mwanafunzi wa Al-Albani aliyeishi naye kwa zaidi ya miaka arubaini kamuandikia mwalimu wake Al-Albani barua ya wazi, na akamwambia:

منذ : الحقد كل علي تحمل إنك له وقال أدبك، وسوء حماقتك ومنالت امتنع ��الساعة ت ��������ي

شخصيا المدرسة بذلك حدثتني ، عنهم األجرة بدفع إال أوالدك قبول منوقل لك، :ت��فاعتذرت

رأسك فهززت ؛ األخيرة األنظمة بسبب شريكات أصبحن المعلمات بأنقص وكل دك �����غضبا،

دون ابنتك األخت بتدريس سنوات لعدة حقوقي أكلت كما حقوقهن أكلشك بكلمة تتلفظ ر، ����أن

وقد ولو عليها، فطر التي بطريقته بالشكر لتقدم هر مع فعلت ما فعلتبسل �������سب وكك �����قت

ضريبة هذا الشاذ لهم طالبهم تبرع يعتبرون الذين الجاحدين الشيوخعين وفرضا يا، ������الزمة

ثم: تقتضي سرقت وقال كما الجماعة إلى تعدها ولم السلفيين أموالالحتكام ورفضت األمانة،

الشرع إلى

Na katika wazimu wako na adabu zako mbovu!.....Na akamwambia: hakika yako wewe unanijengea kila aina ya chuki tangu wakati ambapo madrasa (skulii) ilikataa kuwapokea watoto wako ila kwa kuwalipia ujira. Umenisimulia wewe mwenyewe nikakutaka radhi na nikakwambia kwamba: “Walimu wamekuwa nao sasa ni washirika (wana shea au hisa yao) kwa sababu ya nidhamu (organization) za mwisho. Ukatikisa kichwa chako kwa ghadhabu. Na makusudio yako yote ni kuzila haki zao kama ulivyozila haki zangu kwa muda wa miaka mingi kwa kumsomesha mtoto wako bila ya kutamka neno moja la shukurani. Na lau kama niliyoyafanya niliyafanya na paka basi angeshukuru kwa njia ambayo kaumbwa. Na umewashinda kwa mwenendo wako huu usio wa kawaida (abnormal behaviour) mashekhe wasio na shukurani wanaozingatia kwamba wanafunzi wao kutoa mchango ni kodi ya lazima na ni fardhi ya kila mmoja…..Kisha ukaiba mali ya Salafiyin (Mawahabi) wala hukuirejesha kwa Jamaa (jumuiya yao) kama amana inavyotaka, na ukakataa kupitisha hukumu kwa mujibu wa sharia!!!!

Sheikh Mafuta huyu ndiye mwanachuoni mkubwa wa Hadithi aliyekubalika duniani kote ilhali wanafunzi wake wanatoa ushuhuda huo dhidi yake?

Anaendelea Al-Istambuli kwa kusema:

: تق وقال أدبك، وقلة سلوكك وأحمق أقبح األكل؛ �ومن لقمة تريد إنك ولف أت ����وهل ذلك باع�عل

442

Page 443: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

على بناء مرارا ساعدوك كما فيساعدوك إخوانك إلى شكوت هال الرسل؟الكنود، أيها اقتراحي

األموال في التكاثر ألجل بل الطعام لقمة ألجل ليس عفوا

Na katika mwenendo wako mbaya kabisa na wa kiwazimu na utovu wa adabu wako……….Unasema kwamba wewe unataka tonge ya chakula. Je umewashtakia ndugu zako (Waislamu) wakakusaidia kama walivyokusaidia mara nyingi (tena) kwa ushauri wangu ewe usie na shukurani. Samahani (kidogo) si kwa ajili ya tonge bali ni kwa kutaka kujikithirisha katika mali.

Hii ni barua ya wazi ambayo Al-Istambuli kampelekea Al-Albani. Na Al-Istambuli huyu anamjua Al-Albani vyema kwa sababu – kama tulivyosema – ni mwanafunzi wake na kakaa naye kwa muda usiopungua miaka 40.

Na mwanafunzi mwengine wa Al-Albani ambaye kasoma kwa Al-Albani kwa zaidi ya miaka 40, ni Al-Shawish. Huyu anasema kuhusu mwalimu wake Al-Albani:

أن بلغني فقد ذلك؛ من أشد المشايخ بعض من رأينا أننا العجائب ومنل لمن يقول هم ����أحدهم: مادية حقوق تجادلوا عليه وال تناقشوا وال أقول لما بالتسليم عليكم

به لكم أعترف ما واقبلواأكذب ال ألنني بأنه ،…فقط المغرور هذ يكذب وغفل ال عندهم كان لو.. ينسى أو يهم فقد

Na katika mambo ya ajabu ni kwamba sisi tumeona kutoka kwa baadhi ya Mashekhe (mambo) mazito kuliko hayo. Imenifikia kwamba mmoja wao (yaani Al-Albani) huwambia wale ambao wana haki za mali juu yake (yaani wanaomdai pesa au mali nyengine): ‘Ni juu yenu kusalimu amri kwa ninayoyasema na musilete hoja wala musijadiliane (na mimi, bali) kubalini kile ninachokikiri kwenu kwa sababu mimi sisemi uwongo……na kaghafilika (mtu) huyu mwenye kughururika kwamba hata akiwa kwao yeye hasemi uwongo huenda akakosea au kusahau…….

Bali Al-Shawish huyo kasema maneno mazito kuliko haya katika maelezo yake juu ya kitabu: الثياب اتفضيل لبس ممن كثير على لكالب Tafdhilu Al-Kilaab ‘Alaa Kathiir Mimman Labisa Al-Thiyab, ambapo alimtaja mwalimu wake Al-Albani kwa sifa mbovu sana na mwenendo mbaya kabisa na kwamba anawafanya watu waidhanie Hadithi ya kutunga kuwa ni Hadithi sahihi.

443

Page 444: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Baada ya hayo, sasa naturudi kutazama kwanini Al-Imamu Al-Qannubi anamnukuu Al-Albani. Ama sababu ya Al-Imamu Al-Qannubi, kumnukuu Al-Albani si kwa sababu kwamba Al-Albani ana kauli inayozingatiwa katika uwanja wa Hadithi,1358 bali sababu kaielezea mwenyewe Al-Qannubi kama inavyofuata:

Na miongoni mwa yenye kustahiki kutajwa ni kuwa Muqbil (Al-Waadi’i) huyu si mwanafarasi1359 wa fani hii (ya Hadithi), basi haitakiwi kabisa kunukuu maneno yake wala (maneno yake) hayazingatiwi kamwe, na halkadhalika walio mfano wake kama vile ‘Ali Al-Halabi na Mash-huur na walio mfano wao, halkadhalika Sheikh wao Al-Albani mwenye kuporomoka; bali mimi nataja maneno yao katika kitabu hiki kwa ajili ya kumlazimisha (hoja) Muokotaji wa kuni za usiku (Mwenye kukomba komba kila kitu) 1360 mwenye kitabu Kataaibu Al-Baghyi Al- Mahzuuma na walio mfano wake ambaye anadai kwamba watu wa madhehebu yake wamekubaliana 1361 tangu siku walioanza kuwepo hadi siku alipotunga kitabu chake Al-Kataaibu Al-Mahzuuma. 1362

Na akasema Al-Imamu Al-Qannubi katika kitabu chengine:

Jua kwamba hakika ya mimi nataja maneno ya mtu huyu kwa ajili ya kumlazimisha (maneno yake mwenyewe) yeye na wafuasi wake wanaokaa kusoma vitabu vyake pamoja na makosa mazito yaliomo (ndani ya vitabu vyake) na kujigonga (kwake) kwa wazi…..1363

Na akasema Al-Imamu Al-Qannubi katika kitabu chengine:

….Na sababu ya Al-Albani kutokumjua mpokezi huyo, ni kuwa katika sanad ya Hadithi hii mpokezi mmoja kaanguka (hakutajwa) , na kwa hivyo yeye hakumjua, kwani yeye si mwanafarasi wa fani hii…..1364……...wala hakujua mnyonge huyu (Mash-huur bin Sulaimaan) kwamba Al-Albani ni mjinga wa fani hii ujinga ambao – ukweli wake – unakaribia kuwa wakati

1358 - Lau Al-Albani alikuwa bado yuko hai hatujui hadi leo ni Hadithi ngapi alizozisahihisha angelikwishazigeukia tena na kuzidhoofisha; na Hadithi alizozidhoofisha angelizigeukia tena na kuzisahihisha kama kawaida yake ilivyo. Na kwa maana hii haifai kamwe kutegemea usahihishaji na udhoofishaji wake. 1359 - Yaani si katika mabingwa. 1360 - Asiyejua akisemacho. 1361 - Yaani wamekubaliana kwamba Hadithi zote za Al-Bukhari na Muslim ni sahihi. Hayo ndio madai hewa ya Abdul-Aziz Al-Rajihi. Labda Al-Albani, Ibn Taymiyya na Ibn Al-Qayiim si watu wa madhehebu yake kwani wote hawa wamezidhoofisha baadhi ya Hadithi za Al-Bukhari na Muslim. 1362 - Al-Qannubi Al-Tufan Al-Jaarif j. 3, sehemu ya pili uk. 514. 1363 - Al-Qannubi Al-Saifu Al-Haad uk. 177, chpa ya 3, katika maelezo ya chini. 1364 - Al-Qannubi, Al-Imamu Al-Rabi’u Makaanatuhu Wa Musnaduh uk. 90.

444

Page 445: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

mwengine jahlan murakkaban. Na wala hakuna chenye kuonesha ukweli huo kuliko kutokuwajua kwake wapokezi wengi ambao wengine katika hao ni wapokezi wa Sahihi mbili (Al-Bukhari na Muslim), na kutokujua kwake kuwepo kwa Hadithi nyingi na nyingi ya hizo ni Hadithi za Sahihi mbili (Al-Bukhari na Muslim) ambazo yeye mwenyewe anadai kuwa kazifanyia mukhtasar, na (Hadithi nyengine nyingi zimo) katika vitabu mashuhuri vyenye kutumika. Na mimi nina mifano mingi mno, natosheka hapa kwa kukutajia mifano khamsini…1365(kisha Sheikh Al-Qannubi akaitaja mifano hio ambayo baadhi yake tumeinukuu kabla).

Kwa hivyo, Sheikh Mafuta, elewa kwamba Al-Qannubi hamnukuu Al-Albani ili aipigie debe biashara yake kama ulivyodhania wewe, bali kaeleza kwa uwazi kwamba kauli za Al-Albani anazinukuu ili kuwalazimisha hoja wafuasi wake wanaodhania kuwa Al-Albani ni mwanachuoni wa Hadithi!

JE ALIYOYANUKUU AL-QANNUBI KUTOKA KWA AL-ALBANI NI KWELI AU UWONGO?

Sasa naturudi katika sula lako ambalo kwalo umemwita Al-Imamu Sai’d Al-Qannubi kuwa ni mwongo ili tupate kuuona huo uwongo umekaa wapi! Tazama nukulu alioinukuu Sheikh Al-Qannubi kutoka kwa Al-Albani. Anasema Al-Qannubi akimnukuu Al-Albani kwamba Al-Albani kasema:

أوهام له حمادا 1366أن

Hakika ya Hammad ana makosa (mengi).

Haya ndio alioyanukuu Al-Qannubi katika kitabu chake kutoka kwa Al-Albani.1367 Sasa Bwana Mafuta tukuulize, uwongo uko wapi hapa? Je maneno haya hayamo katika Al-Dha’ifa cha Al-Albani?1368 Hapa ndipo tunapojua hali ya huyu Kasim Mafuta: huyu mtu hajui hata anachokisema wala hafahamu kamwe nini anaambiwa! Vyenginevyo anakusudia kuwadanganya watu, halafu anasema kwamba sisi tunawadanganya watu ilhali kitu kiko wazi!1369

Halafu Kasim Mafuta akamnukuu Al-Albani, akisema:

1365 - Al-Qannubi, Al-Imamu Al-Rabi’u Makaanatuhu Wa Musnaduh uk. 82. 1366 - Katika kitabu cha Al-Albani imeandikwa: أوهاما له حماد Sijui hili ni kosa la . إنchapa au hiki ndio Kiarabu cha Imamu huyu wa Kialbania!1367 - Tazama Al-Qannubi Al-Tufan Al-Jaarif j. 3, sehemu ya kwanza uk.313. 1368 - Tazama Al-Albani Al-Dh’ifa j. 2, uk. 333. 1369 - Nitakufanyia scanned copy wa maneno ya Al-Albani mwisho wa kitabu hiki.

445

Page 446: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

أئمة من إمام سلمة بن حماد فإن قبله الذيك واه التعليل وهذاذلك فى ما جة���ح ثقة المسلمين

له أن ذلك من يخرجه وال ريب وال شك له ليس الذي فمن وإال أوهاماالراوي انكولو أوهام؟

جماهير من القليل إال لنا سلم لما له أوهام لمجرد حديثه يرد الثقةالصحيحين رجال من الثقات

النووي منهم - وخلفا سلفا الحديث علماء جرى ولذلك .غيرهما عن فضال تجاج��اإلح على–

...وهمه ثبت إذا إال سلمة بن حماد بحديث2 والموضوعة الضعيفة األحاديث سلسلة انظر/ 333-332.

Hii ni sababu nyonge kama ilivyo sababu iliyotangulia kabla yake, kwa sababu Hamad bin Salama ni IMAMU miongoni mwa maimamu wa kiislamu ni THIQA (muadilifu mwenye hifdhi nzuri)1370 tena ni HOJA na hakuna shaka yoyote katika hilo, na suala la kukosea halimtoi katika daraja hiyo, kwani ni nani asiyekosea? Lau kama kila mpokezi zitakataliwa hadithi zake kwa sababu ya kuwa anakosea tu, basi wasingesalimika ila wachache miongoni mwa kundi kubwa la watu Thiqaat (waadilifu wenye hifdhi nzuri) tena katika watu waliomo katika sahihi mbili (Sahihi Bukhari na Sahihi Muslim) wachalia mbali vitabu vingine.

Hayo ndio maelezo ya Kasim Mafuta aliomnukuu Sheikh wake Al-Albani. Baada ya hayo, hatuna budi kusema: الفهم نعمة على لله الحمد(Tunamuhimidi Allah kwa neema ya fahamu). Sheikh Mafuta! Je maneno haya yanathibitisha kwamba Hammad ana awhaam (makosa mengi) au yanakanusha? Al-Albani anasema hapa:

له أن ذلك من يخرجه وال أوهاماWala halimtoi hilo (katika kuwa ni mwenye kuaminika) ukweli kwamba

yeye (Hammad) ni mwenye awhaam (makosa mengi).

Je anathibitisha kwamba Hammad ana awhaam (makosa mengi) au anakanusha?

Kwa hivyo, Sheikh Mafuta, Al-Albani kasema kwamba Hammad bin Salama ana awhaam (makosa mengi), lakini kilichobakia ni kuwa yeye baada ya kusema hivyo kamtetea kwamba:

1) Hakuna asiyekuwa na awhaam (makosa mengi). Na hii ni jawabu ya ajabu inayoonesha kwamba huyu Al-Albani anasukuma tu. Sasa kama kila mtu ana awhaam (makosa mengi), wala hakusalimika mtu na hilo, kuna faida gani tena kwa wanavyuoni wa wapokezi

1370 - Hii ulioongeza hapa sio maana ya thiqa. Tutakuwa na maelezo tukifika katika sehemu yake.

446

Page 447: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kuwataja baadhi ya wapokezi kwamba wana awhaam (makosa mengi) pasina kuwataja wengine kwa kasoro hio kama watu wote wana awhaam (makosa mengi)? Kwanini wahusishwe wapokezi maalumu na kasoro ambayo wote wanayo?

2) Hammad ni thiqa. Na Al-Albani kasahau kwamba mpokezi thiqa Hadithi yake haiwi sahihi mpaka pale itapokuwa haina ‘illa. Bali Al-Albani – kama kawaida yake – kayasahau yale aliyoyasema katika vitabu vyake vyengine bali kikiwemo kitabu hicho hicho Al-Dhaifa katika kuwadhoofisha wapokezi wenye awhaam (makosa mengi) kama huyo. Katika Ir-waau Al-Ghalil, kwa mfano, anasema kuhusu mpokezi aitwaye Muhammad bin Mutawakkil: “Naye ni dhaifu na (amesema Ibn Hajar) katika Taqriib: ‘Ni mkweli lakini ana Awhaam (makosa mengi)”.1371 Bila kusahau kwamba wengine – kama Ibn Ma’iin na Ibn Hibbaan – wamesema kwamba Muhammad bin Mutawakkil huyu ni thiqa.1372

Kwa ufupi ni kuwa ibara alioinukuu Sheikh Al-Qannubi kutoka kwa Al-Albani haikuongezeka hata herufi moja isipokuwa marekebisho ya nahau. Kwa hivyo, hii ni kusema kuwa Al-Albani kakiri juu ya ukweli kwamba Hammad bin Salama ana makosa mengi. Sasa kilichobakia ni kuwa je baada ya kukiri huko, kule kumtetea kwake ni sahihi? Sisi tunasema kwamba kumtetea kwake si sahihi kama nitavyobainisha kwa urefu in shaa Allah nikifika katika Hadithi hio ya kuonekana kwa Allah iliopokewa kwa njia ya Hammad bin Salama.

Baada ya hayo, utaona kwamba maneno ya Sh. Kasim Mafuta yametokana na chuki zake na uadui wake kwa Ahlu Al-Haqqi Wa Al-Istiqaama. Vyenginevyo, Al-Qannubi hakunukuu uwongo kama mulivyojionea wenyewe. Bali kamnukuu Al-Albani akisema: أوهام له حمادا Hakika أنya Hammad ana makosa (mengi), na maneno haya yamo katika kitabu cha Al-Albani.

Ama zile hoja nyengine alizozitoa Al-Albani, hoja hizo hazijafuta ule ukweli alioutangaza wa kwamba Hammad anakosea sana au ana makosa mengi, lakini kilichobaki ni kuwa je pamoja na kuwa anakosea sana Hadithi zake tuzichukue? Al-Albani anasema ndio: tuzichukue! Na hii ni akili ya ajabu: vipi mtu anakosea sana halafu zichukuliwe Hadithi zake alizopwekeka nazo. Na kwa hivyo, wale wenye kuijua fani hii ya Hadithi

1371 - Al-Albani Ir-waau Al-Ghalil j. 4, uk. 383. 1372 - Ibn Hajar Tahdhibu Al-Tahdhib j. 9, uk. 376-77, tarjama na. 697.

447

Page 448: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

wamesema tafauti na hivyo, kama alivyosema Al-Albani mwenyewe na akunukuliwa na Sheikh Mafuta. Anasema Al-Abani:

Amesema Imamu Ibn Hajar: Sanad ya hadithi hiyo ni sahihi kwa sababu Atwaa amepokea kutoka kwa Hamad kabla ya Hamad hajachanganyikiwa.

Hayo ndio maneno ya Ibn Hajar. Nayo – kama mulikuwa watu wa kufahamu – basi mungelijua kwamba maana ya maneno hayo ni kuwa baada ya kuchanganyikiwa, Hammad hawezi tena kuwa hoja katika Hadithi zake alizopwekeka nazo.

Kisha akanukuu Al-Albani maneno ya Al-Imamu Al-Nawawi, akasema:

Naye Imamu al-Nawawy akasema; “Hadithi hii ni dhaifu kwa sababu Atwaa amedhoofishwa, na Hamad anakosea…”.

Ni wazi kwa mujibu wa maneno haya ya Al-Imamu Al-Nawawi kwamba hakusudii kudhoofika kwa Hammad bin Salama kwa sababu ya makosa ya binaadamu yoyote kama Al-Albani anavyotaka kuwafanya watu wadhanie, wala hili silo hasa linalotajwa katika elimu ya Hadithi, bali yanayokusudiwa ni makosa mengi ambayo yanamtoa mpokezi katika kanuni ya: ضبط (uwezo kamili wa kudhibiti Hadithi). Lakini Al-Albani anatoa hoja isiokubalika kabisa kwamba kila mtu anakosea kana kwamba kukosea huku ndiko kunakozungumzwa na wanavyuoni!

MFUMO HUO UNAMTUMBUKIZA AL-ALBANI NA KASIM MAFUTA KATIKA DIMBWI!

Baada ya hayo, ningependa kumfahamisha Sheikh Kasim Mafuta kitu kimoja, nacho ni kuwa akiwa atakwenda na mfumo huo aliokwenda nao hapa na akafikia natija – kwa sababu ya mfumo huo – kwamba Al-Qannubi ni mwongo, basi atawaita waongo Maulamaa wote. Kwani kuna tafauti baina ya kunukuu kitu kwa ajili ya kumlazimisha mtu hoja, na kunukuu kwa ajili ya kutoa ushahidi. Vyenginevyo, basi hata Al-Albani naye atakuwa mwongo, kwani ukitazama kitabu chake alichokiita Sifatu Salaati Al-Nabiy utaona kwamba kamnukuu Al-Haafidh Ibn Hajar kipande kidogo na akatolea hoja kwacho. Wakati ukiyasoma maneno ya Ibn Hajar hadi mwisho utayaona yanabatilisha ile sehemu alioinukuu Al-Albani.

448

Page 449: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Ibn Hajar alipokuwa akizungumzia mas-ala ya kuwa je Bismillahi inasomwa wakati wa kusoma Al-Hamdu au haisomwi, au je inasomwa kwa siri au inasomwa kwa uwazi, alisema:

السماع نفي على القراءة نفي حمل األلفاظ هذه بين الجمع فطريقنف����ي على السماع ونفي

بسم (( قراءة يسمعنا فلم زادان بن منصور رواية لفظ أن ويؤيده الجهر، (( الرحيم الرحمن الله

كانوا (( بلفظ خزيمة ابن عند أنس عن الحسن رواية ذلك من وأصرحالرحمن الله بسم يسرون

ألن)) الب���ر، عبد كابن باالض���راب أعله من تعليل ب����هذا فاندفع الرحيمتعين أمكن إذا الجمع

..... إليه المصير

Basi njia ya kuzikusanya lafdhi hizi ni kuzifasiri (riwaya zenye) kukataa kusomwa (kwa Bismillah) kwamba maana yake (ni kuwa Anas) hakuisikia (ikisomwa); na (riwaya zenye) kukataa kusikia kuwa maana yake ni kuwa (Bismillahi) haikudhihirishwa kwa uwazi. Na hili linaungwa mkono na ukweli kwamba lafdhi ya riwaya ya Mansur bin Zaadaan ni ((Hakutusikilizisha kisomo cha Bismillah Al-Rahmaani Al-Rahiim), na ilio wazi zaidi ya hio ni riwaya ya Al-Hasan kutoka kwa Anas iliopokewa na Ibn Khuzaima: (Walikuwa wakiisoma Bismillah Al-Rahmaani Al-Rahiim kwa siri); basi ikaondoka kwa ujumuisho huu kasoro ya mgongano ambayo wengine, kama Ibn ‘Abdil-Barri – wameitia Hadithi hii; na kuyajumuisha (maandiko) ikiwezekana basi ni lazima kufanywe.1373

Maelezo hayo ya Al-Hafidh Ibn Hajar, ameyastaghili Al-Albani ili kuipa nguvu rai yake, lakini alisahau Al-Albani kuwa Ibn Hajar hakusema hayo kwa kuwa anaiunga mkono rai ya kutodhihirisha Bismillahi, bali Ibn Hajar hapa alikuwa akielezea kanuni ya kujumuisha maandiko tu. Ama rai yake Ibn Hajar kaieleza kwa uwazi mwisho wa maelezo ya Hadithi hio hio, lakini Al-Albani hakuyataja maelezo hayo ya Ibn Hajar kwani alijua kwamba yanabomoa rai yake. Tazama maneno ya Ibn Hajar yanavyomalizikia:

على بالبسملة الجهر نفي أنس حديث محصل أن إلى البحث انتهى وإذاطري�������ق من ظهر ما

قدمت الجهر إثبات رواية وجدت فمتى عنه الروايات مختلف بين الجمعلمج���رد ال نفيه، على

النبي يصحب أن جدا يبعد أنسا ألن النافي على المثبت رواية –تقديموسلم عليه الله –صلى

سنة وعشرين خمسا وعثمان وعمر بكر أبا يصحب ثم سنين عشر مدةالج���هر منهم يسمع فلم

1373 - Ibn Hajar Al-Fat-hu j. 2, uk. 1064, maelezo ya Hadithi na. 743-744.

449

Page 450: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

كأنه الحكم هذا يحفظ ال بأنه اعترف أنس لكون بل واحدة، صالة في بها , تذكر ثم به عهده لبعد

فيتعين بالبس���ملة الجهر يستحضر ولم جهرا بالحمد باالفتتاح الجزم منهم���ن بح����ديث األخذ

الجهر أثبت

Na utafiti (research) ukiishia katika natija kwamba Hadithi ya Anas ni kukanusha kusomwa Bismillahi kwa uwazi kwa mujibu wa kile kinachodhihiri kutokana na njia ya kuzijumisha riwaya mbali mbali zitokazo kwake (Anas), basi (elewa kwamba) zitapopatikana riwaya zenye kuthibitisha kuisoma Bismillahi kwa uwazi basi zinatangulizwa pasina riwaya zenye kukanusha. (Na hii) si kwa sababu ya (kanuni ya) kuitanguliza riwaya yenye kuthibitisha tu (positive narrative) pasina kuitanguliza riwaya yenye kukataa (negative narrative), kwani Anas ni vigumu kuwa amuandame Mtume (s.a.w.) kwa muda wa miaka kumi kisha aandamane na Abu Bakr, ‘Umar na ‘Uthmaan kwa muda wa miaka ishirini na tano halafu awe hakusikia kutoka kwao ikisomwa (Bismillahi) kwa uwazi hata katika Sala moja, bali kwa kuwa Anas kakiri kwamba yeye hana kumbukumbu ya hukumu hii kana kwamba ni kwa sababu ya umbali wa zama zake na hayo, kisha akakumbuka uhakika wa kuanza (kuisoma) Al-Hamdu wazi wazi wala hakukumbuka kusomwa kwa Bismillahi kwa uwazi, BASI IKALAZIMU KUICHUKUA HADITHI YA WALIOITHIBITISHA KUSOMWA KWA BISMILLAHI KWA SAUTI YA WAZI. 1374

Hayo ndio maelezo ya Ibn Hajar akizielezea kanuni hizo za kiusuli, nayo yako wazi kwamba kwa mujibu wa fani zilivyo ni kuwa Hadithi za kwamba Bismillahi inasomwa wazi wazi katika Sala ndizo zinazotangulizwa kwani:

مقرر هو كما النافي على المثبت قدم والمثبت النافي تعارض إذااألصول في

Andiko lenye kuthibitisha hukumu likigongana na andiko lenye kuikataa hukumu, basi linalotangulizwa ni lenye kuthibitisha hukumu kama ilivyo katika Usulul-Fiq-hi. Ama yale maelezo ya mwanzo ya Ibn Hajar, ambayo kayastaghili Al-Abani, ni kwamba yeye (Ibn Hajar) alikuwa akiielezea kanuni ya kujumuisha maandiko tu. Kisha natija iliopatikana baada ya mjumuisho huo ni nini? Natija ni kuwa Hadithi ya Anas ni نافي (yenye kukanusha hukumu) nayo inapingana na Hadithi nyengine مثبت (yenye kuthibitisha hukumu). Kwa hivyo, Ibn Hajar anasema kwamba kanuni ni kutanguliza Hadithi مثبت (yenye kuthibitisha hukumu).

Lakini – baada ya hayo – ukirudi kukitazama kitabu Sifa ya Sala ya Al-Albani, utamkuta Al-Albani kanukuu maneno haya:

1374 - Ibn Hajar Al-Fat-hu j. 2, uk. 1065, maelezo ya Hadithi na. 743-744.

450

Page 451: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

السماع نفي على القراءة نفي حمل األلفاظ هذه بين الجمع فطريقنف����ي على السماع ونفي

ويؤيده قراءة ( 1375الجهر، يسمعنا فلم زادان بن منصور رواية لفظ أن ( الرحيم الرحمن الله بسم

كانوا (( بلفظ خزيمة ابن عند أنس عن الحسن رواية ذلك من وأصرحالرحمن الله بسم يسرون

ألن)) الب���ر، عبد كابن باالض���راب أعله من تعليل ب����هذا فاندفع الرحيمتعين أمكن إذا الجمع

..... إليه المصير

Basi njia ya kuzikusanya lafdhi hizi ni kuzifasiri (riwaya zenye) kukataa kusomwa (kwa Bismillah) kuwa maana yake (Anas) hakuisikia (ikisomwa); na (riwaya zenye) kukataa kusikia kuwa maana yake ni kuwa (Bismillahi) haikudhihirishwa kwa uwazi. Na hili linaungwa mkono na ukweli kwamba lafdhi ya riwaya ya Mansur bin Zaadaan ni (Hakutusikilizisha kisomo cha Bismillah Al-Rahmaani Al-Rahiim), na ilio wazi zaidi ya hio ni riwaya ya Al-Hasan kutoka kwa Anas iliopokewa na Ibn Khuzaima: (Walikuwa wakiisoma Bismillah Al-Rahmaani Al-Rahiim kwa siri); basi ikaondoka kwa ujumuisho huu kasoro ya mgongano ambayo wengine, kama Ibn ‘Abdil-Barri – wameitia Hadithi hii; na kuyajumuisha (maandiko) ikiwezekana basi ni lazima kufanywe. 1376

Halafu baada ya hapo, Al-Albani akasema:

( كان ( وسلم عليه الله صلى كونه في حجة أنس حديث أن يتبين وبذلك... بالبسملة يسر

Na kwa hayo, inabainika kwamba Hadithi ya Anas ni hoja kwamba Mtume (s.a.w.) alikuwa akiisoma Bismillahi kwa siri.1377

Utaona hapa kwamba Al-Albani kachukua kipande kidogo cha maneno ya Al-Hafidh Ibn Hajar akayatolea hoja bila ya kuyanukuu maneno yote ambayo – kama ulivyoona – yanabomowa maneno hayo alioyanukuu Al-Albani. Kwa hivyo, kwa mujibu wa mezani ya Sh. Kasim Mafuta, natarajia siku haziko mbali tutamsoma Al-Albani katika urodha ya waongo iliotayarishwa na Kasim Mafuta. Au atawapima watu kwa mezani mbili 1375 - Katika nukulu ya Al-Albani kaandika منصور رواية Na) ....وتؤيده inaungwa mkono na riwaya ya Mansur..). Na maana ni moja, lakini labda Sheikh Mafuta – kwa mujibu wa mezani yake ya kupima uwongo na ukweli – kesho atatwambia kwa Al-Albani kamzulia uwongo Ibn Hajar: kayapindua maneno yake!!!1376 - Al-Albani Sifa ya Sala ya Al-Albani alichokiita Sifa ya Salatu Al-Nabiy j. 1, uk. 282. Maktabatu Al-Ma’aarif - Riyaadh, chapa ya kwanza 1427 A.H. = 2006 M.1377 - Al-Albani Sifa ya Sala ya Al-Albani alichokiita Sifa ya Salatu Al-Nabiy j. 1, uk. 282. Maktabatu Al-Ma’aarif - Riyaadh, chapa ya kwanza 1427 A.H. = 2006 M.

451

Page 452: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

tafauti! Ndugu Muislam! Mimi simwiti Al-Albani kuwa ni mwongo, nakuomba unifahamu vizuri, lakini ninachotaka kukuonesha ni kuwa kwa mujibu wa minhaj (methodology) ya uchambuzi ya Kasim bin Mafuta basi Al-Albani atakuwa naye ni mwongo. Pamoja na yote hayo, alichokifanya Al-Albani ni tafauti na alichokifanya Al-Qannubi, kwani alichokifanya Al-Albani ni kunukuu kitu kilicho kinyume na misingi ya usuli alioielezea Ibn Hajar, wakati alichokifanya Al-Qannubi hakiko hivyo.

BALI NA KASIM MAFUTA NAYE YUMO KWENYE MEZANI YAKE MWENYEWE

Bali ninakwambia ewe Sheikh Kasim bin Mafuta kwamba kwa mujibu wa minhaj (methodology) yako hio ya uchambuzi, basi wewe mwenyewe utajiweka wapi? Tadlis (ghushi) ulizozifanya katika kitabu chako hazina idadi. Nakupa mfano mmoja na mifano myengine utaisoma katika sehemu tafauti za kitabu hiki. Katika kitabu changu Hoja Zenye Nguvu nilizungumzia Aya isemayo:

ناضرة ذئموي هوجو(Kuna) nyuso siku hio zitangaa.1378

ناظرة ربها إلىKwa Mola wake tu ndiko zitakakotazama.1379

Nilizinukuu Aya hizi kisha nikazielezea kilugha, kisha nikatoa hoja ya kilugha wanayoitegemea wale wanaosema kuwa Allah ataonekana, nikasema:

Hoja yao ya kilugha (ya wenye itikadi ya kumuona Allah) inahusu matumizi ya neno hili “النظر” al-nadharu katika lugha ya Kiarabu ambayo ndiyo lugha ya Qur-ani. Wanasema kuwa kweli neno hili النظر al-nadharu lina maana nyingi katika lugha ya Kiarabu, lakini kutokana na lilivyotumika hapa katika Aya hii ya 23 ya Surat Al-qiyama halina tafsiri nyengine isipokuwa ni kuona tu. Na hii ni kwa sababu hili neno hapa limefuatana na herufi “إلى” “ilaa” kama unavyoona lilivyo katika Aya hii: “ ناظرة ربها Kwa Mola wake tu (nyuso hizo) ndiko“ ”إلىzinakotazama”. Na linapotumika namna hii hali ya kuwa limefuatana na herufi hii إلى ilaa basi huwa halina maana nyengine yoyote ile isipokuwa moja tu nayo ni kuona. Hii ndiyo hoja ya kilugha wanayoitegemea watetezi wa itikadi ya kuonekana kwa Mwenyezi Mungu.

1378 - Sura ya 75 Aya ya 22. 1379 - Sura ya 75 Aya ya 23.

452

Page 453: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Lakini wakajibu wale wenye kusema kuwa Mwenyezi Mungu haonekani kwamba madai haya sio sahihi; ukweli ni kuwa neno hili النظر al-nadharu linapofuatana na herufi إلى ilaa si lazima limaanishe kuona kama unavyopatikana ushahidi katika Qur-ani na Hadithi sahihi za Mtume (S.A.W) na katika lugha ya Kiarabu, kinyume na madai hayo ambayo wameyatoa wenye itikadi hii ya kuonekana kwa Mwenyezi Mungu. Ama katika Qur-ani ni pale Mwenyezi Mungu aliposema:

لهم خالق ال أولئك قليال ثمنا وأيمانهم الله بعهد يشترون الذين إنالقيامة يوم إليهم ينظر وال الله يكلمهم وال اآلخرة في

Hakika ya wale wanaouza ahadi ya Mwenyezi Mungu na viapo vyao kwa thamani ndogo, basi hao hawana fungu huko akhera, na wala

Mwenyezi Mungu hatowasemesha, na wala hatowatazama siku ya kiama. 1380

Katika maneno haya yanayosema: “Mwenyezi Mungu hatowatazama” limetumika neno lile lile “ رظين ” yandhuru ambacho ni kitendo kilichopo cha neno “ ظرن “ nadhara. Kisha neno hilo likafuatana na herufi ile ile “ ilaa ambayo watetezi wa itikadi ya kuonekana kwa Mwenyezi ”إلىMungu wamesema kwamba likifuatana nayo halileti maana nyengine ila “kuona,” kama ilivyo katika sehemu hii ya Aya inayosema: “ رظني الو

مهيلإ ” (wala hatowatazama). Na hili neno “ “ مه “hum” katika sehemu inayosema “ مهيلإ ” “ilaihim” lisikubabaishe bure herufi ni ile ile “ إلى” ilaa hapa imechanganyishwa tu kwa kutegemezwa na neno hili: “ مه ” “hum” ambalo hapa ni mtendwa. Yaani Mwenyezi Mungu hawatazami wao. Neno “ مه ” “hum” maana yake ni ‘wao’.

Sasa suala ni kuwa je hapa katika Aya hii neno “النظر” al-nadharu limemaanisha ‘kuona’? Ikiwa ndio basi tafsiri ya Aya hio ni hivi: “Hakika ya wale ambao wanaiuza ahadi ya Mwenyezi Mungu na viapo vyao kwa thamani ndogo, basi hao hawana fungu huko akhera, na wala Mwenyezi Mungu hatowasemesha, na wala hatowaona siku ya kiama!!!” Kwa sababu Aya inasema “wala hatowatazama” kama ilivyo katika sehemu hii ya Aya : “ مهيلإ رظني الو ” kwa hivyo tafsiri iwe “wala hatowaona” badala ya kufasiri “wala hatowatazama” kwa sababu masharti walioyatoa ili neno النظر al-nadharu lilete maana ya kuona tayari yameshapatikana. Sasa Je ni kweli Mwenyezi Mungu hatowaona watu waovu siku ya kiama? Ukisema ndio umekufuru; ukisema sio hoja yako imeporomoka.

Na anasema Mwenyezi Mungu: ميسرة إلى فنظرة عسرة ذو كان إن و

Na akiwa (mwenye kudaiwa) ni mwenye (hali) nzito (hana

1380 - Sura ya 3 Aya ya 77.

453

Page 454: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

uwezo) , basi subirini mpaka awepesike (apate uwezo). 1381

Hapa chimbuko la neno ni lile lile “النظر” al-nadharu na limefuatana na herufi ile ile “إلى” ilaa na hakuna katika ulimwengu wa Kislamu aliyesema kwamba hapa neno hili maana yake ni kuona, bali wote wanalifasiri neno: “النظر” al-nadharu liliomo katika Aya hii kuwa maana yake ni kusubiri (kungojea).

Hii ni kwa upande wa Qur-ani. Ama kwa upande wa kauli ya Mtume (S.A.W) ni Hadithi nyingi; moja katika hizo ni Hadithi inayosema:

ةاميقال موي هيلإ الله رظني مل اءليخ هبوث رج نمMwenye kuburura nguo yake kwa sababu ya kibri (chaketu) basi Mwenyezi Mungu hatomtazama siku ya kiama. 1382

Katika Hadithi hii neno lililotumika ni lilelile “النظر” al-nadharu kisha likafuatana na herufi ile ile إلى ilaa. Sasa je Mwenyezi Mungu hatomuona mtu huyo? Ukisema ndio basi kashahadie upya wewe umeshakuwa kafiri mshirikina; ukisema anamuona basi hoja yako imeporomoka.

Ama katika lugha ya Kiarabu, ni kauli ya mshairi wa Mtume (s.a.w.) ambaye ni Sahaba Hassan bin Thaabit, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi. Anasema mshairi huyo:

** بالفالح يأتي حمن الر إلى ناظرات بدر يوم وجوهNyuso siku ya (vita vya) Badri zilimtazama

Mwenyezi Mungu alete ushindi.” 1383

Katika ubeti huu wa ushairi neno lililotumika ni lilelile النظر al-nadharu na limefuatana na herufi ile ile “إلى” ilaa, suala ni kuwa je nyuso za Masahaba zilimuona Mwenyezi Mungu siku hio ya vita vya Badri? Au maana yake zilisubiri ushindi kutoka kwa Mwenyezi Mungu? Sasa tazama katika Aya, Hadithi na maneno ya Sahaba huyu Hassaan bin Thaabit, mshairi wa Mtume (s.a.w.) utakuta mwote limetumika neno lilelile ““ ilaa na sote ”إلى“ al-nadharu na limefuatana na herufi ile ile النظرtunakubaliana kuwa katika sehemu hizi neno hilo halijamaanisha kuona. Kwa hivyo madai ya wenye kuitakidi kumuona Mwenyezi Mungu kwa kutumia Aya hii na kuichambua kilugha na kwamba neno “النظر” al-nadharu linapofuatana na herufi “إلى” ilaa huwa halileti maana isipokuwa kuona tu, madai haya si sahihi wala hayana msingi wowote.1384

Hayo ni baadhi ya nilioyasema kuhusu Aya hizo na mengi mengine yatakuja katika juzuu mahususi kwa suala hili la kuonekana au kutoonekana kwa

1381 - Sura ya 2 Aya ya 280. 1382 - Al-rabii bin Habib Al-Jamii Al-Sahih uk. 71. Al-nnawawi Riadh Al-Salihin uk. 248. 1383 - Sheikh Al-Khalili Alhaqu Al-Damigh uk. 46. 1384 - Tazama Juma Mazrui Hoja Zenye Nguvu 58-61.

454

Page 455: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Allah. Sasa baada ya kuona hayo nilioyasema, tazama alivyosema Sheikh Kasim mwanangwa wa Mafuta ili uone kwamba huyu mtu si mkweli hata kidogo. Anasema:

HOJA YA KWANZA

Miongoni mwa hoja za wenye kuthibitisha kuonekana Allah huko akhera kwa macho ni pale aliposema Allah;

.ناظرة ربها إلى***ناضرة يومئذ وجوه“Zipo nyuso siku hiyo ni zenye kung’ara* Ni zenye kumwangalia

(kumuona) Mola wake”.1385

Aya hii ni miongoni mwa hoja zilizowazi ambazo Ahlu-Sunna wanazitegemea katika kuthibitisha kwamba watu wema watamuona Mola wao huko akhera kwa macho yao.1386 Na kuna hoja nyingi zinazoipa nguvu hoja hii yenye kuthibitisha kuonekana Allah –Azza wajallah- huko akhera kwa macho: kuna hoja za ndani na hoja za nje. Hoja za aina ya kwanza ni:-Hoja za ndani, ni muweko wa neno hili katika upande wa kilugha, kwa sababu limetumika neno “Naadhirah” ambalo limenyambuliwa kutokana na asili ya neno “Nadharan”, na likawa neno hili limekuja baada ya herufi “ILAA”, na kwa mujibu wa kanuni za lugha ya kiarabu linapokuwa neno hili limekuja baada ya herufi hiyo maana yake ya asili ni kutazama kwa macho.

Na kwa bahati nzuri hata wale wenye kupinga kuonekana Allah huko akhera wanakubaliana na sisi katika hilo, na ushahidi wa madai haya ni kauli ya ndugu Juma M. Al-Mazrui aliposema katika ukurasa wa 53 wa kitabu chake, pale alipokuwa akielezea maana za neno “AL-NADHARU”: “Tukitazama maana ya neno hili: “ (al-nadharu) kupitia kiyoo cha Qur’an tunakuta ni:1)Kutazama kikawaida kwa macho: NA HII NDIO MAANA YA MSINGI YA NENO HILO….”. mwisho wa kunukuu. Kama ndugu Juma anakubaliana na sisi kuwa neno “AL-NADHARU” maana yake ya asili ni kutazama kwa macho, basi anatakiwa pia akubali kwamba kwa mujibu wa kanuni za lugha ya kiarabu ambazo wataalamu wote wa lugha hiyo wamekubaliana ni kuwa: maana ya kwanza inayozingatiwa katika matumizi ya neno ni kulitumia neno katika maana yake ya asili kwanza, kabla hatujakwenda katika maana nyingine.

Pamoja na kwamba inawezekana likatumika neno katika maana nyingine isiyokuwa ya asili, 1387 lakini mpaka ishindikane kutumika maana

1385 - Surat al-Qiyamah aya 22-23. 1386 - Bali hata wanafiki kwa mujibu wa riwaya zenu pia watamuona! Hili peke yake basi linatosha kuonesha kwamba Aya haina maana hio.

455

Page 456: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

ya asili, kisha kuweko na dalili itakayotufahamisha kushindikana matumizi hayo ya asili ya neno hilo na kwenda nje ya asili yake.

Na sisi tukilitazama neno “NAADHIRAH” hapa tunaona kuwa bado haijashindikana kulitumia katika maana yake ya asili ambayo ni kutazama kwa macho, na wala hakuna hoja yoyote ya msingi yenye kutufanya tutoke nje ya asili ya neno hili, bali ni kinyume chake; kuna hoja nyingi zinazolipa nguvu neno hilo libaki katika matumizi yake ya asili ambayo ni (kutazama kwa macho). Kama vile kutajwa neno: “وجوه” “Wujuuhun” (Nyuso) katika aya tunayoijadili.

Hio ndio jawabu ya Kasim Mafuta. Nami hapa sitaki kueleza chochote juu ya hayo alioyasema kwani hayo yatakuja katika juzuu yake maalumu inayohusu suala hilo la kuonekana au kutoonekana kwa Allah. Lakini ninachotaka kukuonesha hapa ni hii tadlis (ghushi) anayoifanya Sheikh huyu kwa kukusudia:

Mosi: Zile hoja zote za kilugha nilizozitoa za kuonesha kwamba neno annadhar likifuatana na herufi ilaa si lazima limaanishe kuona, yeye hakuzinukuu bali kakariri kitu kile kile ambacho kimeshajibiwa bila ya kubainisha ubatili wa jawabu iliotolewa.

Pili: Anasema:

Hoja za ndani, ni muweko wa neno hili katika upande wa kilugha, kwa sababu limetumika neno “Naadhirah” ambalo limenyambuliwa kutokana na asili ya neno “Nadharan”, na likawa neno hili limekuja baada ya herufi “ILAA”, na kwa mujibu wa kanuni za lugha ya kiarabu linapokuwa neno hili limekuja baada ya herufi hiyo maana yake ya asili ni kutazama kwa macho.

Na kwa bahati nzuri hata wale wenye kupinga kuonekana Allah huko akhera wanakubaliana na sisi katika hilo, na ushahidi wa madai haya ni kauli ya ndugu Juma M. Al-Mazrui aliposema katika ukurasa wa 53 wa kitabu chake, pale alipokuwa akielezea maana za neno “AL-NADHARU”: “Tukitazama maana ya neno hili: “ (al-nadharu) kupitia kiyoo cha Qur’an tunakuta ni:1)Kutazama kikawaida kwa macho: NA HII NDIO MAANA YA MSINGI YA NENO HILO….”. mwisho wa kunukuu.

Sasa tazama mtu anavyozua huyu! Kitu anachokizungumzia ni neno annadhar likifuatana na herufi ilaa je ni lazima limaanishe kuona. Halafu 1387 - Tazama Kasim Mafuta hapa anathibitisha majazi aliyoyakanusha yeye na Imamu wake katika sehemu nyengine. Hivi ndivyo batili ilivyo! Lazima ijigonge tu!

456

Page 457: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

akadai kuwa hata wenye kusema kuwa Allah haonekani hilo wanalikubali. Kisha akatoa ushahidi kwa maneno yangu niliosema:

Tukitazama maana ya neno hili: “ (al-nadharu) kupitia kiyoo cha Qur’an tunakuta ni:1)Kutazama kikawaida kwa macho: NA HII NDIO MAANA YA MSINGI YA NENO HILO….”. mwisho wa kunukuu.

Haya! Sasa tukuulize Sheikh Kasim: je maneno haya yanamaanisha kwamba neno annadhar likifuatana na herufi ilaa ni lazima limaanishe kuona? Au yanamaanisha kwamba maana ya msingi ya neno hilo ni kuona kwa maana kwamba ikiwa hakuna qarina basi hapo ndipo itapozingatiwa maana hio ya asili; na pakiwa na qarina litapelekwa katika maana nyengine kwa mujibu wa qarina zinavyoonesha?

Ni wazi kwamba Kasim Mafuta anakusudia kupotosha maneno ya watu ili afikie lengo lake kisha yeye kawa na ulimi mrefu wa kuwatukana watu kwa dhulma. Na mutakumbuka katika nukulu nilioitaja huko nyuma ambayo ndani yake Kasim Mafuta kayabadilisha maneno yangu kuhusu suala la majazi kama vile ambavyo kayapotoa maneno yangu kuhusu falsafa ya Ibn Taymiyya. Wakati mimi nilisema: “Je haoni yeye huyu Ibn Taymiyya kuwa falsafa hii inapelekea kurudi kwenye itikadi ya kuwepo kwa Mungu zaidi ya mmoja?”, yeye akasema:

Je kwa maneno haya ya Ibn Taymiyya umefahamu kwamba ana itikadi ya kuwepo Mungu zaidi ya mmoja kama anavyodai ndugu Juma kuwa sheikhul islam Ibn Taymiyya ana itikadi hiyo? Au umefahamu kwamba ndugu Juma si mkweli?

Namna hivi ndivyo mtu huyu anavyofanya tadlis (ghushi)! Na kitabu chake kimejaa ghushi za aina tafauti kama utavyojionea mwenyewe ndugu msomaji katika juzuu tafauti za kitabu hiki. Wallahu Al-Musta’aan!

Kwa ufupi – ninachotaka kukwambia hapa ewe Sheikh Kasim – ni kuwa, ikiwa kwa mujibu wa minhaj yako Al-Qannubi ni mwongo – naye ni mkweli asiyejua uwongo ulivyokaa – basi jina hili wewe na Al-Albani munastahiki zaidi kama nilivyokuthibitishia hapa na nitavyozidi kukuthibitishia katika sehemu mbali mbali za kitabu hiki in shaa Allah. Narudia tena, hayo ni kwa mujibu wa minhaj (methodology) yako ya uchambuzi.

Na la mwisho ninalotaka kumfahamisha huyu Kasim Mafuta ni kwamba baada ya Al-Imamu Al-Qannubi kuandika kitabu hicho nilichomnukuu, basi Al-Albani alikuwa bado yuko hai na aliishi kipindi cha kutosha. Na katika

457

Page 458: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kitabu hicho, Al-Albani kanukuliwa sana na kujibiwa na kuchalenjiwa, wala hakuweza kunyanyua kichwa chake mpaka kafa, wala hakusemapo: “Al-Qannubi kanizulia uwongo”. Wewe unakuja kudai hivyo leo? Tena wala huna hoja yoyote kwani alichokinukuu Al-Qannubi kutoka katika kitabu cha Al-Albani kimo kweli katika kitabu hicho. Bali hayo ulioyanukuu wewe pia ndani yake yamo yale aliyoyasema Al-Qannubi, lakini wewe, kama ilivyo kawaida ya Mawahabi, si mtu wa kufahamu.

MUKHTASARI NA NUKTA MUHIMU

1) Tulichokizungumzia hapa ni madai ya Kasim Mafuta kwamba Al-Qannubi ni mwongo kamzulia uwongo Al-Albani.

2) Uwongo wenyewe – kwa mujibu wa Kasim Mafuta – ni kuwa Al-Qannubi kanukuu kinyume na alivyosema Al-Albani.

3) Maneno alioyanukuu Al-Qannubi kutoka kwa Al-Albani ni haya:أوهام له حمادا 1388أن

Hakika ya Hammad ana makosa (mengi).

4) Maneno haya yamo katika kitabu cha Al-Albani haikuongezeka hata herufi moja, isipokuwa marekebisho ya nahau.

5) Kasim Mafuta mwenyewe kutunukulia kutoka kwa Al-Albani maneno yasemayo:

له أن ذلك من يخرجه وال ريب وال أوهاماNa bila shaka ukweli kwamba yeye ana makosa (mengi) hakumtoi katika hilo (la kuwa ni mwenye kuaminika).

6) Hii ni kusema kwamba Al-Albani anakiri kwamba Hammad bin Salama anakosea sana au ana makosa mengi.

7) Lakini kilichobakia ni kuwa yeye anamtetea, na katika kufanya hivyo, Al-Albani:

a) Kenda kinyume na mabingwa wengi waliomzidi katika fani hii ya Hadithi kama tutavyobainisha tukifika sehemu yake.

b) Kenda kinyume na mustalah al-hadith kama tutavyobainisha tukifika sehemu yake.

c) Kajigonga, kwani watu wengi thiqa kawadhoofisha ikiwa wana illa fulani kama hio.

8) Al-Albani mwenyewe kayakata maneno ya Ibn Hajar akayatolea hoja kinyume na maelezo ya mwisho ya Ibn Hajar. Tena kuyakata Al-Albani kwa maneno ya Ibn Hajar kunaivunja hoja ya kiusuli alioitoa Ibn Hajar; tafauti na Al-Qannubi alipoyawacha maneno ya

1388 - Katika kitabu cha Al-Albani imeandikwa: أوهاما له حماد Sijui hili ni kosa la . إنchapa au hiki ndio Kiarabu cha Imamu huyu wa Kialbania!

458

Page 459: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Al-Albani: maneno ya Al-Albani yalikuwa ni rai yake tu si kanuni ya Hadithi, ya lugha wala ya kiusuli. Bali ile sehemu aliyoinukuu Al-Qannubi kutoka kwa Al-Albani ndiyo yenye kukubaliana na fani za Hadithi na usuli – mwenye kukosea sana akipwekeka na riwaya basi riwaya yake ni dhaifu.

9) Kwa hivyo, naye Al-Albani kwa alivyoyafanya maneno ya Ibn Hajar basi – kwa kipimo cha Kasim Mafuta – na-awe mwongo!

10) Kasim Mafuta mwenyewe kayaghushi maneno yangu na amewaghushi maulamaa katika sehemu nyingi za kitabu chake. Tutabainisha yote hayo in shaa Allah. Kwa hivyo, na yeye ajitafutiye mwenyewe kwa uadilifu jina linalomfaa.

11) Tunamnasihi Sheikh Kasim Mafuta, asione haya katika kutangaza toba yake na kuomba radhi. Huko ndiko kufuata Sunna ya kweli na ndio kufuata Al-Salaf na huo ndio ucha Mungu wenyewe.

12) Au asubiri hata Allah ahukumu baina yetu Naye ndiye mbora wa kuhukumu!

SURA YA KUMI NA TATU

459

Page 460: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

SHEIKH AL-KHALILI AMTAKA IBN BAZ WAFANYE MJADALA WA WAZI AU WAMUOMBE ALLAH

ATEREMSHE LAANA YAKE KWA MWENYE ITIKADI POTOFU

Jambo jengine ambalo Kasim Mafuta anasema ni la uwongo, ni yale nilioyaandika katika baadhi ya vitabu vyangu kwamba Sh. Al-Khalili alimtaka Sheikh Ibn Baz wafanye mjadala wa wazi na kwamba Sheikh Ibn Baz alikataa. Hapo Sheikh Al-Khalili akamtaka wafanye mubahala mbele ya Al-Kaba ili kumuomba Allah ateremshe laana yake juu ya yule mwenye itikadi potofu. Sheikh Ibn Baz akakataa kwa kuogopa laana ya Allah isije ikamshukia! Sasa kabla sijakunukulia alioyasema Kasim “mwanangwa” wa Mafuta kuhusu tukio hili, ni vyema nikunukulie tena yale yaliojiri baina ya wanavyuoni wawili hao. Nilisema katika kitabu Hoja Zenye Nguvu kuhusu tukio hilo, maneno yafuatayo:

…….Mpaka ilipofika mwezi wa mfunguo sita mwaka wa 1406 A.H. Sh. Al-Khalili akapata mualiko kutoka katika wizara ya mambo ya Dini ya Suudia. Akatoka yeye na kikundi cha wanavyuoni wa Oman. Walipofika Suudia, Mufti wa Suudia Sh. Ibn Baz akawaalika katika ofisi yake. Wakaitikia wito; wakaenda kuonana na Sh. Ibn Baz. Sh. Ibn Baz akamwita Sheikh Al-Khalili pamoja na wenzake ndani, wakaingia watu wawili - Sh. Al-Khalili na Naibu wake, Sh. Said bin Khalef Al-Kharusi. Sh. Ibn Baz akamwambia Sh. Al-Khalili “Nyinyi Maibadhi, na Mashia, na Al-Ashaira (Masuni kama walioko Afrika nzima takriban na sehemu nyengine za dunia) na Maaturidia (Masuni kama waliko India na Pakistan wa madhehebu ya Hanafi), basi nyote nyinyi katika itikadi mumepotea.” Na Sh. Ibn Baz akawa katika upande wa Ibadhi anazungumzia zaidi mas-ala haya ya kuonekana kwa Mwenyezi Mungu. Sh. Al-Khalili akamwambia: “Tafauti hizi hazikuzaliwa leo, bali zipo kwa muda mrefu.” Ikawa Sh. Ibn Baz anaendelea kuwasema Maibadhi kuwa ni wapotovu. Sh. Al-Khalili akamjibu kwamba kama uko tayari basi natufanye mjadala wa wazi karibu na msikiti mtakatifu wa Makka, na mjadala huo uwe kwa ajili ya kutafuta haki tu: uwe mbali na kasumba za kimadhehebu, na redio zote na vyombo vyote vya habari virushe moja kwa moja ikiwemo redio Makka na mjadala huo uwe wazi kwa kila anayetaka kushiriki. Sh. Ibn Baz akakataa. Sh. Al-Khalili akamuuliza: “Unaonaje kama atakujia Mkiristo au Myahudi akakwambia mufanye mjadala wa wazi je utakubali? Akasema Sh. Bib Baz: “Ndio.” Sh. Al-Khalili akauliza: “Kwanini basi hutaki sisi tufanye mjadala?” Sh. Ibn Baz akasema: “Jambo hili linaeneza bidaa.” Sh. Al-Khalili akamwambia: “Laa! Jambo hili linaiuwa bidaa na kuiacha dini safi kwa sababu kila mtu atajua ukweli uko wapi.” Ibn Baz akakataa na

460

Page 461: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kusema: “Watu wa bidaa hawakubali kuwachana na bidaa zao.” Sh. Al-Khalili akamwambia: “Nimelihakikisha hili kutokana na msimamo wako huu.” Na mwisho Sh. Al-Khalili akamwambia Ibn Baz: “Kama wewe unasema uko kwenye haki na sisi tuko kwenye batili, basi twende pale mbele ya Al-Kaaba tukamuombe Mwenyezi Mungu amlani aliyeko kwenye batili.” Sh. Ibn Baz akakataa. Na Sh. Al-Khalili akaondoka hali ya kuwa Sh. Ibn Baz kakasirika.

Hayo ndio nilioyasema katika kitabu changu Hoja Zenye Nguvu kuhusu mkutano huo wa Sheikh Al-Khalili na Sheikh Ibn Baz. Sheikh Kasim Mafuta akanijibu kama inavyofuata:

Hivi ndugu Juma kwa sababu ya uongo wenu kama huu ndiyo mnataka kufanya mijadala na maulamaa wakubwa kama Ibn Baz - kama mnavyodai- na mko tayari kwenda kuapa kwenye Ka’aba? Hamuogopi ?

Hivi kweli mnaweza kudai kwamba mwanchuoni mkubwa kama al- Allaama sheikh Abdul-Aziz Ibn Baz awakimbie watu kama nyinyi wenye hoja dhaifu tena za uongo namna hii?!!

Kama mkiwa mmeweza kupotosha yaliyoandikwa vitabuni ambayo yako dhahiri shahiri, na mkaweza kuwazulia maulamaa mambo ambayo hawakusema, kweli mtashindwa kuzipotosha, na kuzigeuza habari zilizofanyika ndani ya ofisi tena kwa siri, tena mashahidi wa tukio hilo ni nyinyi wenyewe? Eti Ibn Bazi amkimbia Khalili! Kwa hoja gani alizonazo Khalili na wafuasi wake? Hoja zenyewe ni hizi za uwongo anazozitaja Juma kutoka kwa Qannubi na Khalili?

Vitabu vya Al-Albani vimejaa ulimwenguni mashariki na magharibi, mmemzulia wazi wazi ! je mtashindwa kuzua yaliyofanyika ofisini kwa siri? Ndiyo maana ukiyatazama maneno ya Juma kuhusu suala la kukutana Ibn Baz na Khalili utauona uongo unaelea juu juu, kwa mfano pale aliposema: “Kwa hivyo Al-khalili akamtaka Ibn Baz ambaye kawaita maibadhi makafiri wende mbele ya Al-kaba Takatifu wakaombe hivi hivi, lakini Ibn Baz akaogopa.

Na hii inatosha kuonesha kuwa hata yeye mwenyewe sh. Ibn Baz hana hakika na itikadi yake. Na kama si hivyo kipi kimemzuia kumtaka Mwenyezi Mungu aibainishe haki baina yake na watu ambao kawaita makafiri.”!!!! Mwisho wa kunukuu uwongo wa ndugu Juma.1389

Je ni kweli Ibn Baz amewaita maibadhi makafiri? Ni mahali gani hapo? Kitabu gani ? Mbona hukututajia? Vitabu vya Ibn Baz vimejaa tele hapa

1389 - Tazama kitabu chake “Hoja zenye Nguvu” ukurasa wa 42.

461

Page 462: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

duniani, hebu tutajie kitabu kimoja ambacho Ibn Baz amesema maneno hayo, na hii ni chalenji nina kupa wewe Juma na masheikh zako Khalili, al-Qannubi, na Ahmad bin Su’ud al-Siyabi mtutajie ni mahali gani Ibn Baz amewaita maibadhi kuwa ni makafiri kwa uwazi kabisa, bila ya kuhitajia taawili.1390

Kwa hivyo, ushahidi wa Al-’Allama Sheikh Kasim bin Mafuta juu ya kukanusha kwake suala la kwamba Sheikh Al-Khalili alimtaka Ibn Baz wafanye mjadala wa wazi, ni:

1) Kwa sababu ya uwongo aliousema Sheikh Al-Khalili na Sheikh Al-Qannubi, haiwezekani kuwa Sh. Al-Khalili awe kweli alimtaka Sh. Ibn Baz wafanye mjadala.

2) Kwa sababu hoja za Kiibadhi ni dhaifu sana.3) Ibn Baz ni mwanachuoni mkubwa sana! 4) Wapi Sh. Ibn Baz kawakafirisha Maibadhi.

Huo ndio ushahidi wa Sheikh Kasim bin Mafuta katika kulikanusha tukio hilo. Ama suala la kwanza nimeshakujibu kwamba Sheikh Al-Khalili hakusema uwongo kuhusu ubeti huo wa Ibn Al-Qayyim, kwani:

a) Maana ya beti zote ni sawa.b) Kukinukuu kitu kimaana inakubalika ikiwa hukupoteza maana.c) Ubeti huo hakuunukuu Sheikh Al-Khalili, bali wa kwanza kuunukuu

ni Al-Imamu Al-Subki (756 A.H.) katika kitabu chake Al-Saifu Al-Saqiil ambacho kakiandika ili kukijibu kitabu Nuniyya cha Ibn Al-Qayyim.

d) Ibn Al-Qayyim mwenyewe alikuwa hai, angeweza kusema kwamba Al-Subki kanizulia uwongo, lau ubeti huo haukuwepo au ulikuwa na maana tafauti na ile alioikusudia Ibn Al-Qayyim, hususan ukizingatia ukweli kwamba Al-Subki na Ibn Al-Qayyim waliishi zama moja.

Ama kuhusu Al-Qannubi, nimeshakuthibitishia kwamba alichokinukuu katika kitabu chake Al-Tufaan Al-Jarif kimo katika kitabu Al-Dhaifa cha Al-Albani wala hakuongeza hata herufi moja, isipokuwa kufanya marekebisho ya kinahau. Al-Albani katika kitabu chake kasema: ... أوهاما أ له حماد ن na ilivyo ni: .... أوهام له حمادا أن

Ama kuhusu kusema kwako kwamba Ibn Baz ni mwanachuoni mkubwa sana! Nami ninakwambia vivyo: “Ibn Baz ana elimu kubwa sana”, lakini sijapata kumsikia mtu yoyote wa elimu aliyemlinganisha na Sheikh Al-Khalili kwa lolote: si kwa elimu wala uchaji. Na lau Sheikh Al-Sha’arawi 1390 - Kasim Mafuta, Hoja Zenye Nguvu uk. 84-85.

462

Page 463: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

alikuwa hai ningelikwambia kamuulize? Hata hivyo hili si muhimu: kilicho muhimu ni hoja yake. Lakini kwa kitendo chake cha kukimbia mjadala, Ibn Baz katukosesha faida kubwa ya kujua ana nini cha kutueleza. Hata hivyo, tunayoyasoma katika vitabu vyake na vya wenzake tunaona kuwa ni yayo kwa yayo maji ya futi kwa nyayo – hawana jipya!

Sasa kabla ya kukuthibitishia kwamba tukio hilo ni la kweli, tazama ulioyaandika mwenyewe, utajijua kwamba wewe – kama kawaida yako – ni mtu unayependa ushindani tu, huungi mkono kitu kwa kukikinai wala hupingi kitu kwa kutokukikinai. Tama maelezo yako yasemayo:

Hivi ndugu Juma kwa sababu ya uongo wenu kama huu ndiyo mnataka kufanya mijadala na maulamaa wakubwa kama Ibn Baz - kama mnavyodai- na mko tayari kwenda kuapa kwenye Ka’aba? Hamuogopi ?

Tazama maneno yako yasemayo: “Na mko tayari kwenda kuapa kwenye Ka’aba? Hamuogopi ? Je maneno haya yana maana gani ikiwa tukio hilo ni la uwongo? Mimi hapa sina ta’aliiq (maelezo), isipokuwa kukwambia irejee nafsi yako tena na tena!

Tumebakiwa na kumthibitishia Sheikh Kasim Mafuta kwamba tukio hilo ni la kweli. Sasa ili ufahamu kwamba tokeo hilo ni la kweli yazingaatie mambo yafuatayo:

Kwa kuanzia: nataka kumjuilisha Sheikh Mafuta kwamba tukio hilo ni mutawaatir (lililoenea na kuzagaa) hata halina haja ya ushahidi kwani hapa Ghuba ya Uarabu hakuna mtu asiyelijua hata mmoja, labda wale ambao hawajishughulishi na dini kabisa. Na kitu kikifika daraja kama hii, basi kinakuwa hakihitaji ushahidi. Wewe Sheikh Kasim Mafuta wa Pongwe Tanga natarajia kwamba ni mtu wa mwanzo kulikanusha tukio hilo! Lakini hio si ajabu kwa kila anayekisoma kitabu chako na kuona ulivyoichafua historia yako kwa kutukana na kughushi vibaya sana. Hii inaonesha kwamba lengo lako ni kuinusuru fikra maalumu vyovyote vile iwavyo. Na mtu mwenye mwenendo kama huu lazima atayakanusha yale yalio ya kweli na kujaribu kuthibitisha yasio na ukweli kwa gharama zote! Tazama ukweli kwamba Hadithi inayosema kwa uwazi kwamba Waumini hawatomuona Allah katika Pepo, wewe unasema kwamba hii ni hapa duniani kana kwamba hio Pepo iko duniani, basi kweli wewe utashindwa kuyakanusha yale ambayo hayamo katika Qur-ani wala Sunna?

463

Page 464: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Pili: Nimeshakueleza kwamba Maimamu wako unaowakubali wamekiri kwamba makundi yote ya Khawaarij hawasemi uwongo bali wanajitenga na kila mwongo. Na Ibadhi kwa mujibu wako – kama ulivyotueleza sana katika kitabu chako – ni katika Khawaarij, kwa hivyo tena ukiwa utawaweka katika makundi ya waongo utakuwa unagongana na Maimamu wako.

Tatu: Tokeo hilo baada ya kutokea lilifuatiwa na matokeo mengine matatu:1) Fat-wa ya Ibn Baz ya kuwakafirisha Maibadhi.2) Suali aliloulizwa huko Saudia kwamba je kweli katoa fat-wa hio?

Pamoja na jawabu aliojibu kulijibu suali hilo. Na yote hayo ni katika barua.1391

3) Jawabu aliojibiwa na Sheikh Al-Khalili juu ya fat-wa yake hio.

Sasa natuingie katika ufafanuzi. Mambo yalivyokuwa ni hivi: Sheikh Ibn Baz na wenzake walitoa fat-wa kwamba Ibadhi ni wapotovu na kwamba haifai kusali nyuma yao, bali katika fat-wa nyengine waliashiria karibu kuwa ni kauli ya uwazi ya kwamba Maibadhi ni makafiri. Hapa tutanukuu fatawa mbili hizo – ya kwanza ni ile fat-wa alioashiria ndani yake ukafiri wa Kiibadhi na ya pili ni ile aliosema ndani yake kwa uwazi juu ya upotovu wao. Fat-wa ya kwanza – pamoja na suali lake – inasema:

الرسول: حديث معنى هو ما وسلم –س عليه الله عليه –صلى المتفق)) : س قال خرج��يحيث

- : األسنان، - حدثاء قال أو أحداث األحالم سفهاء الزمان آخر في قومخ من قول ������يقولون ير

حناجرهم ،بريةال إيمانهم يجاوز من ، ال السهم الدين يمرقون يمرق كماالرمية ف من أين��������ما،

فاقتلو ملقيتموه عظيما أجرا قتلهم في فإن يوم هم، قتلهم لمنالحديث)) هذا قيل فيمن ، القيامة

الرسول إليه أشار زمان ))–وأي وسلم( عليه الله .صلى

Suali: Nini maana ya Hadithi ya Mtume (s.a.w.) ilioafikiwa (na Al-Bukhari na Muslim) ambapo alisema: ‘Watatokea watu katika zama za mwisho wajinga wasio na busara; au akasema ni chipukizi watakuwa wakisema kauli nzuri yao ya viumbe (lakini) imani yao haivuuki kwenye koo zao (hawana imani), wanatoka katika dini kama mshare unavyotoka katika kiwindwa, basi popote munapowakuta wauweni, kwani katika kuwaua

1391 - Barua anayo Sh. Al-Khalili hadi leo.

464

Page 465: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

wao kuna ujira mkubwa siku ya kiama kwa atayewaua’. 1392 Je Hadithi hii imesemwa kwa kuwakusudia nani na ni katika zama gani hizo?

Hilo ndilo suali alililoulizwa Sheikh Ibn Baz na timu yake. Sasa soma jawabu walioitoa:

: الخوارج ب� المسماة الطائفة في النبي قاله معناه في وما الحديث هذاالدي�ن في يغلون ألنهم

وقد مكفرة، اإلسالم يجعلها لم التي بالذنوب المسلمين ويكفرونأبي بن علي زمن في خرجوا

وناظرهم الحق إلى فدعاهم أشياء عليه وأنكروا عنه الله رضي طالبمنهم كثير فرجع ذلك في

علي قاتلهم المسلمين على تعدوا فلما آخرون، وبقي الصواب إلىوقاتل������هم عنه الله رضي

األحاديث، من معناه في جاء وما المذكور بالحديث عمال بعده، األئمةاآلن إلى بقايا ول��������هم

ومكان زمان كل في عقيدتهم اعتقد من كل في عام والحكم

Hadithi hii na zilio na maana moja na (Hadithi) hii, kaitamka Mtume (s.a.w.) kuhusu kikundi kinachoitwa: “Al-Khawaarij”, kwani walikuwa wakipindukia mipaka katika dini na wanawaita Waislamu kuwa ni makafiri kwa sababu ya kutenda kwao madhambi ambayo Uislamu haukuyafanya kuwa ni madhambi yenye kumtia (mtu) katika ukafiri. Nao (watu hao: Makhawaarij) walitoka katika zama za Ali bin Abi Talib wakampinga kwa sababu ya mambo (fulani fulani). Basi akawalingania katika haki na kujadiliana nao kuhusu hilo, basi wengi wao wakarejea katika usawa na wengine wakabakia. Basi walipowafanyia uadui Waislamu, Ali (r.a.) akawapiga vita na Maimamu baada yake pia nao wakawapiga vita1393 kwa kuitendea kazi Hadithi iliotajwa (hapa) na Hadithi nyengine zenye maana kama hio. Na hadi leo hawa (Makhawarij) wamebakia, na hukumu (ya kuuliwa) ni ya ujumla (kwa wote) kwa kila atayekuwa na itikadi kama yao (hao Makhawaarij) katika zama zote na popote pale (watapokuwa). 1394

1392 - Ahmad Abdul-Razzaq Fatawa Al-Lujna Al-Daaima j. 2, uk. 368, chapa Balnasya mwaka 1421 A.H. = 2000 M. Tanbihi: 1) Ahmad Abdul-Razzaq siye mwenye fatawa hizi: yeye kazikusanya tu. Fatawa hizi ni za kamati ya fatawa na Ibn Baz akiwa kama ndiye raisi wa kamati hio. 2) Katika chapa ya siku hizi nasikia fat-wa hio imeondoshwa. Kwa hivyo, nitakufanyia scanned copy ya fat-wa hii na nitakuwekea mwisho wa kitabu hiki. 1393 - Inaonesha Ibn Baz na wenzake suala hili hawakulisoma kamwe, bali wanakariri kile walichokirithi kutoka kwa waliowatangulia. Kwani maneno yote haya ni ya kuqallid (kufuata) tu bila ya kufanya uchambuzi wa kielimu! 1394 - Ahmad Abdul-Razzaq Fatawa Al-Lujna Al-Daaima j. 2, uk. 368-369, chapa ya mwaka 1421 A.H. = 2000 M. Scanned copy yake iko mwishoni mwa kitabu hiki.

465

Page 466: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Hio ndio jawabu ya Sheikh Ibn Baz na wenzake. Sasa tazama mambo yanayofuata:

1) Muulizaji kamuuliza Ibn Baz na wenzake kuhusu maana ya Hadithi: الزمان س آخر في قوم يخرج .. ((Watatokea watu katika zama za

mwisho))……2) Maelezo yaliomo katika Hadithi hii yanaeleza kwamba watu hao

watatoka katika dini. Anayetoka katika dini huyo si Muislamu tena. 3) Kuwaua watu hao ni ujira mkubwa.4) Ibn Baz na wenzake wametoa fat-wa – ya al-taqlid al-a’amaa –

kwamba hao ni wale aliopigana nao Ali yaani ni watu wa Nahrawaan (r.a.).

5) Ibn Baz anasema kwamba watu hao bado wapo. 6) Hukumu yao ni moja yaani hukumu ya kuuliwa ni moja katika zama

zote na mahala popote pale walipo.1395

7) Lakini ikiwa riwaya inanena kwamba watu hao watatokea akheri zamani (zama za mwisho),1396 basi vipi tena Ibn Baz na wengine waihusishe riwaya hio na watu wa zama za mwanzo ambao waliishi katika karne bora yao, karne ya kwanza ambayo ni zama za Masahaba? Na kwanini asiihusishe na Mawahabi ambao ndio:

a) Waliodhihiri zama za mwisho.b) Wakawakafirisha Waislamu. c) Wakawaua Waislamu?1397

Sasa hapa natutazame mambo matano halafu tutoe natija. Jambo la kwanza: ni kuwa watu hao wametoka katika dini kama ilivyosema Hadithi iliomo katika suali. Suali: je baada ya watu hao kutoka katika Uislamu wataendelea kuwa Waislamu? Pili: ni kuwa hukumu yao ni kuuliwa; bila shaka ima ni kwa sababu ya kurtadi kwa uwazi au kwa sababu ya kuitakidi itikadi za kikafiri baada ya Uislamu – na yote ni kurtadi. Tatu: ni kuwa watu hao ni hao walioitwa Khawaarij, bila ya kusahau kwamba – kwa mujibu wa Bwana Mafuta – Ibadhi ni Khawaarij. Nne: ni kuwa Khawaarij wenyewe ni wale aliopigana nao ‘Ali, yaani watu wa Nahrawaan. Tano: ni kuwa hadi leo bado watu hao wapo katika baadhi ya sehemu.

1395 - Na hapa Ibn Baz atagongana na Sayyina ‘Ali aliposema: “Musiwaue tena khawaarij baada yangu, kwani aliyetafuta haki akakosea si kama aliyetafuta batili kwa kukusudia”. Aliyetafuta haki akakosea kwa mujibu wake ni Watu wa Nahrawaan; aliyetafuta batili kwa kukusudia ni Mu’awiya na wafuasi wake ambao ndio maimamu wa Kasim Mafuta na wenzake. 1396 - Bila kusahau kwamba hata Kasim Mafuta kalifasiri neno akheri zamani (zama za mwisho), kuwa ni zama hizi tulizonazo. Anasema: “Na haya ndiyo maajabu ya makhawariji hawa wa akhiril-zaman!” yaani Maibadhi wa sasa. 1397 - Maelezo zaidi juu ya hili ni katika juzuu ya pili.

466

Page 467: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Kifungu namba moja bila ya shaka yoyote na kwa uwazi kabisa kinawakafirisha watu hao, kwani kama wametoka katika Uislamu basi hawana pakwenda isipokuwa ukafirini. Kifungu namba mbili pia kinawakafirisha kwani anayestahiki kuuliwa bila ya kutenda kosa linalopasa kuuliwa isipokuwa kwalo – kama zina au kuua – bali ni kwa sababu ya itikadi yake tu, basi ni lazima itikadi yake hio ni ya kikafiri iliomtoa katika Uislamu – kartadi. Kifungu cha tano kinawahusu Ibadhi. Vyenginevyo Sheikh Kasim tueleze ni nani hao ambao mpaka leo wapo ambao watu wanawaita kuwa ni Khawaarij na ambao wanajihusisha na watu wa Nahrawaan? Tena tukirudi katika kifunga cha pili, tunakuta Ibn Baz na wenzake wanahalalisha damu ya Maibadhi! Wala usiniulize wapi kasema hivyo, kwani tunasema kwamba sifa alizozitaja zote zinafahamisha kwa uwazi nani kawakusudia. Vyenginevyo, na mimi nikisema: “Wanaofunga mikono juu ya kifua wakati wa kusali si Waislamu” basi nitakuwa sijaeleweka nawakusudia nani! Wakati ukweli ni kuwa tayari nimeshaeleweka nani hao ninaowakusudia hata kama sikuwataja kwa jina. Kwa hivyo, Bwana Mafuta usimtetee Sh. Ibn Baz kwa kosa lake; kosa kalifanya bila shaka, na kawakafirisha Maibadhi kama alivyowakafirisha Mashia na kuwaingiza katika upotovu Masuni wa madhehebu nyengine. Bali kama alivyowakafirisha walimwengu kwa fat-wa yake juu ya mwendo wa jua na mzunguko wa ardhi. Sasa baada ya hayo, natutazame fat-wa yake ya pili ambayo ndani yake kawaita Maibadhi kuwa ni wapotovu ambao haijuzu kusali nyuma yao. Fat-wa hio aliosema hivyo – pamoja na suali lake – ni kama inavyofuata:

وهل: الخوارج، فرق من الضالة الفرق من اإلباضية فرقة تعتبر هل سخل��فهم الصالة يجوز

الدليل؟ مع

Je madhehebu ya Kiibadhi ni katika madhehebu zilizopotea miongoni mwa madhehebu za Kikhawaarij? Na je inajuzu kusali nyuma yao? Nitajie ushahidi. 1398

Hilo ndilo suali waliloulizwa Sheikh Ibn Baz na wenzake. Jawabu yao ni:

على والعدوان البغي من فيهم لما الضالة، الفرق من اإلباضية فرقةوعل����ي عفان بن عثمان

... خلفهم الصالة تجوز وال عنهما الله رضي

1398 - Ahmad Abdul-Razzaq Fatawa Al-Lujna Al-Daaima j. 2, uk. 369, chapa ya mwaka 1421 A.H. = 2000 M.

467

Page 468: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Madhehebu ya Ibadhi ni katika madhehebu potovu, kwa sababu ya uasi walionao na uadui (wao) dhidi ya ‘Uthman bin ‘Affaan na Ali1399 Allah awawiye radhi, na haifai kuwafuata1400 katika sala! 1401

Sasa hapa sitaki kumjadili Ibn Baz kwa fatawa zake hizi, kwani suala hili la walioitwa Khawaarij nimeshaliandika kwa urefu katika kitabu chake maalumu na nitalizungumzia kwa mukhtasari katika juzuu maalumu in shaa Allah katika juzuu za kitabu hiki. Lakini ninachotaka kukionesha hapa ni:

1) Ukweli kwamba Ibn Baz kawakafirisha Maibadhi.2) Chanzo cha kutoa kwake barua hio nilioitaja kabla ambayo aliitoa

kujibu suali alilotumiwa na mmoja wa watu wa huko Suudia na ambayo ndani yake alitoa ushahidi – wa kuwakafirisha Maibadhi1402 – kwa kutegemea maneno ya Al-Imamu Ahmad na Al-Imamu Malik na wanavyuoni wengine!1403 Yaani hiyo yote ni baada ya kuulizwa kwamba je kweli katoa fat-wa hii tulioinukuu hapa? Hapo ndipo alipojibu hivyo, na fat-wa yenyewe ndio hio tulioinukuu hapa.

Kwa hivyo, baada ya Sheikh Ibn Baz kutoa fat-wa hio tulioinukuu, hapo mmoja wa watu wa huko Saudi Arabia alipompelekea Sheikh Ibn Baz barua ya kumuuliza je kweli katoa fat-wa hio. Hapo ndipo alipotoa barua kwamba kweli katoa fat-wa hio na akatoa ushahidi kwa kauli za Maimamu kama vile Al-Imamu Ahmad bin Hanbal kwamba kasema: “Anayepinga kuonekana kwa Allah basi huyo ni kafiri”.1404 Na kwamba Al-Imamu Malik alipoulizwa kuhusu wapingao kuonekana kwa Allah, alisema: “Upanga! Upanga!”. Yaani hukumu yao ni kuuliwa.

1399 - Sasa yeye Sh. Ibn Baz atakuaje? Kwani yeye ni mfuasi wa Muawiya naye kamuasi na kumpiga vita ‘Ali. Na wale Masahaba waliomuua ‘Uthman bin ‘Affaan watakuaje, pamoja na kuwa itikadi ya Ahlu Al-Sunna ni kuwa Masahaba wote ni waadilifu? Ufafanuzi wa masuala haya nimeutoa katika kitabu Makhawaarij Baina Ya Ukweli Na Visa Vya Kutunga juzuu ya kwanza. Rejea huko utazame maelezo kwa ufafanuzi. Kitabu hicho pia nimekifasiri kwa lugha ya Kiingereza na kinapatikana katika vitabu vidogo vidogo, kwa sasa zimetoka juzuu mbili ndogo ndogo. 1400 - Yaani haifai kuwa wao wawe Maimamu na Wahabi awe ma-amuma! 1401 - Ahmad Abdul-Razzaq Fatawa Al-Lujna Al-Daaima j. 2, uk. 369, chapa ya mwaka 1421 A.H. = 2000 M. 1402 - Katika barua hakutaja ukafiri wa Kiibadhi, lakini kataja ukafiri wa wasioamini kuwa Allah ataonekana. Lakini suala aliloulizwa lilikuwa ni kuhusu Ibadhi. Kwa hivyo, suala na jawabu yamewatia Ibadhi katika ukafiri. 1403 - Na hii ni ajabu kwa mtu anayeitwa Mufti, kwani ukafiri na Uislamu ni hukumu za Kisharia ambazo hazithibiti ila kwa Qur-ani na Sunna: si kwa maneno ya Maimamu hata wakifikia daraja gani ya kielimu! 1404 - Kauli hii ya Ahmad hata Sheikh Kasim Mafuta kainukuu katika kitabu chake Hoja Zenye Nguvu uk. 170.

468

Page 469: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Sasa ninachotaka kumfahamisha Bwana Kasim bin Mafuta hapa ni mambo haya:

Mosi: Ibn Baz katika barua yake hio aliyomjibu muulizaji, katoa ushahidi wa kuwakafirisha Maibadhi kwa kutegemea:

a) Maneno ya Al-Imamu Ahmad aliposema: “Anayepinga kuonekana kwa Allah basi huyo ni kafiri”. Na kutoa ushahidi kwa andiko – likiwa ni la Mtume (s.a.w.) au la Imamu – basi ni kulikubali kwamba andiko hilo ni sahihi. Ndio maana tukakwambia kwamba Ibn Baz kawakafirisha Maibadhi kwani katoa ushahidi kwa kutegemea fat-wa ya Al-Imamu Ahmad ambayo ndani yake kuna kuwakafirisha wapingao kuonekana kwa Allah. Na jambo hili hata wewe umelitenda katika kitabu chako ambapo umemnukuu Al-Imamu Ahmad akisema hivyo.

b) Pia katoa ushahidi kwa maneno ya Al-Imamu Malik: “Upanga! Upanga!”. Yaani hukumu yao ni kuuliwa. Sasa Bwana Kasim bin Mafuta ni kitu gani kilichohalalisha damu ya Maibadhi au damu ya wenye itikadi ya kutoonekana kwa Allah. Ni wazi kwamba fat-wa hii inawakafirisha Maibadhi, wala hamuna njia yoyote ya kuitetea. Kilichobaki – kama nyinyi ni wakweli – mukiri kosa na muirekebishe hali.

c) Bila ya kusahau kwamba jawabu alioitoa Sh. Ibn Baz juu ya suali aliloulizwa kuhusu Hadithi ya wataotoka katika dini, pia inawakafirisha watu wa Nahrawaan pamoja na Maibadhi kwa mujibu wa suali na jawabu yake ilivyokuja.

Pili: tumebakiwa na suali hili: nini kitachotujuilisha kwamba kweli Sh. Ibn Baz alitoa barua hio yenye fat-wa hio ya kuwa “Wasioamini kuonekana kwa Allah ni makafiri?” na fat-wa ya Al-Imamu Malik isemayo: “Upanga upanga?”. Jawabu ni kuwa:

a) Kama nilivyotangulia kusema kwamba baada ya Sheikh Ibn Baz kutoa fat-wa alioitoa, Sheikh Al-Khalili alimjibu kwa uwazi katika T.V. ya Oman.1405

b) Katika jawabu hio, Sheikh Al-Khalili aliisoma barua yote hio ya Ibn Baz, na barua hio ilivutwa kwa kamera hadi ikawa watazamaji wanaiona.

c) Sheikh Al-Khalili aliuzungumzia mkutano wake na Ibn Baz na yaliojiri baina yao na kwamba alimtaka wafanye mjadala lakini Ibn Baz akakataa.

1405 - Na kaseti za video zipo hadi leo. Mimi kwa mara ya kwanza niliona keseti hio katika Maktaba ya Shia iliopo Kiponda Zanzibar. Natarajia kwamba bado hadi leo ipo.

469

Page 470: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

d) Suala la mubahala limetajwa katika kitabu kilichoandikwa na Sheikh Ahmad Al-Siyabi.

e) Baada ya Sheikh Al-Khalili kusema hayo na kubainisha yaliojiri baina yake na Sheikh Ibn Baz; na Sheikh Al-Siyabi kuandika alioyaandika kuhusu suala la mubahala, basi Ibn Baz na wenzake waliishi si chini ya miaka kumi, na wala hakuna hata siku moja walioyakanusha hayo na kusema: “Ahmad Al-Khalili katuzulia uwongo”.

Baada ya hayo, utaona kwamba kila mwenye akili hawezi kulikanusha suala hilo, kwani Sheikh Ibn Baz kaishi miaka mingi bila ya kulikanusha na jambo hilo limeenea na kuzagaa katika sehemu zote za hapa Ghuba. Bali hata leo hii – ninavyotarajia – hajatokea mtu aliyelikanusha, isipokuwa Kasim Mafuta wa Pongwe!

KUKIMBIA MJADALA NI SERA YA KIWAHABI

Sasa baada ya hayo, ndugu Mafuta nataka uelewe tena mambo haya:1) Kukimbia mijadala ndio sera ya Kiwahabi, kwani wanajijua

kwamba hawana hoja, wanataka watu wawafuate tu katika itikadi zao za kumfananisha Allah na binaadamu, bila hata ya kuzijadili hoja zao. Na ushahidi wa kwamba sera za Mawahabi ni kukimbia mijadala ni mwingi, nakupa mifano michache tu ifuatayo:

2) Yalioandikwa na mmoja wa Mashekhe wenu, naye ni Dr. Sabir Ta’ima. Anasema:

منهج نرد ال لكن اإلباضية ومؤرخي مفكري مع مراء وال جدال نريد ال ونحنكل وقف���وم

المقاالت أصحابNa sisi hatutaki mjadala wala ubishi na wanafikra na wanahistoria wa kiibadhi, lakini hatuirejeshi minhaj (methodology) na msimamo wa kila wenye kuandika vitabu vya makala……1406

2) Sahibu yako aliyekushauri ukichapishe kitabu chako, Abdullah Ali Muhsin alipotoa fat-wa kwamba mwanamme wa Kiibadhi haijuzu kumuoa mwanamke wa Kisunni aliitwa kwenye mjadala, akakimbia. Vyenginevyo, naende akatoe ushahidi wa Kisharia juu ya yale alioyasema. Na miongoni mwa mambo alioyasema ni: “Maibadhi wao wanakimbilia katika mjadala, na wao huwa wanatumia mantiq (logic)”. Sasa hii logic nyinyi hamuna? Kwa ufupi, ni kuwa mjadala

1406 - Dr. Saabir Ta’ima Al-Ibadhiyya ‘Aqiidatan Wa Madhaban uk. 70-71.

470

Page 471: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

alioitiwa si kujadili mantiq (logic): bali ni kuthibitisha madai yake kwa njia zenye kukubalika Kisharia.

3) Maimamu wa Kiwahabi wamekuwa wakiwafundisha wafuasi wao – hata kwa kutumia riwaya za kutunga – kwamba wasikae wala wasichanganyike wala wasiseme na watu wa bidaa, bali wajitenge nao na wawaambie maneno makali ili wapate amani siku ya kiama! Na kama inavyoeleweka kwamba watu wa bidaa katika dhana (concept) ya Kiwahabi ni wale ambao hawakubaliani na itikadi za kumfananisha Allah na binaadamu (hawamkubali mungu mwenye macho, na mikono na miguu na kidakatonge na sura ya Adam)! Sasa soma baadhi ya mifano miwili mitatu yenye kuwasisitiza wafuasi wa skuli ya tajsim kujitenga na Munazziha. Soma mifano hio kutoka katika kitabu Sharhu Sunna cha Al-Barbahari ambapo utakuta maelezo kama:

a) Ukimuona mtu katika Ahlu Al-Sunna1407 ana mwenendo mbaya, fasiki, muovu, mtu wa maasi mpotovu lakini anafuata Sunna,1408 basi fuatana naye na kaa naye kwani maasi yake hayakudhuru kitu. Na ukimuona mtu anajitahidi katika ibada, hana haja ya dunia, anaabudu sana, lakini ni mtu wa matamanio ya nafsi (mtu wa bidaa) basi usikae naye wala usisikilize maneno yake wala usifuatane naye njiani, kwani nahofia ukaja ukaipenda njia yake ukaangamia pamoja naye.1409

b) Yunus bin ‘Ubaid alimuona mwanawe katoka kwa mtu wa matamanio ya nafsi yake,1410 akasema: ‘E mwanangu! Unatoka wapi? Akasema: ‘Natoka kwa fulani’. Akasema: ‘E mwanangu! Bora nikuone unatoka nyumbani kwa khuntha kuliko kukuona unatoka nyumbani kwa fulani. Na kukutana na Mwenyezi Mungu nawe ni mzinifu, fasiki, mwizi ni bora kwangu kuliko kukutana naye na kauli ya fulani na fulani.1411

1407 - Ahlu Sunna anaokusudia yeye si wale Mashafi, Maliki, Mahanafi na baadhi ya Hanbali; bali ni wale wasemao kuwa Mungu ana mkono, mguu, n.k. 1408 - Jamani huyu mtu ni timamu?! Mtu muovu, fasiki ana mwendo mbaya anafata Sunna vipi? Sunna gani iliokuja kufundisha uovu na ufasiki?! Kuanzia hapa utaanza kuelewa yale niliokwambia kwamba dhana (concept) ya Sunna kwa Mawahabi na Maimamu wao watangulizi ni vile kusema Allah ana viungo na sura ya Adam. Ukiamini hivyo wewe ni mtu wa Sunna hata kama ni mlevi, mzinifu, mwizi, n.k! Hii ni hatari ilioje iliowakabili Waislamu. 1409 - Al-Barbahari Al-Sunna uk. 114-115. 1410 - Mtu wa matamanio yaani ni yule asiyekubali kuwa Allah ana viungo!1411 - Al-Barbahari Al-Sunna uk. 115-116. Tazama watu wanavyowalea wafuasi wao vibaya.

471

Page 472: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

c) Atayesikiliza kwa sikio lake (kusikiliza maneno ya) mtu wa bidaa, basi katoka katika hifadhi ya Allah.1412

d) Allah alimpa wahyi Musa bin ‘Imraan: ‘Usikae na watu wa bidaa, kisijekikakuingia katika moyo wako kitu katika yale wanayoyasema, nikakutia katika moto wa jahannam.1413

e) Atayekaa na mtu wa bidaa basi hapewi hekima. 1414

f) Usikae na mtu wa bidaa, kwani nahofia laana itakushukia!1415

g) Atayekaa na mtu wa bidaa katika njia moja, basi wewe pita njia nyengine. 1416

h) Atayemtukuza mtu wa bidaa, basi kasaidia katika kuubomoa Uislamu; na atayetabasamu mbele ya uso wa mtu wa bidaa, basi kayadharau yale Allah alioyateremsha kwa Muhammad (s.a.w.); na atayemuozesha kipenzi chake mtu wa bidaa basi huyo ameukata uhusiano wake;1417 na atayefuata jeneza la mtu wa bidaa basi haachi kuwa katika ghadhabu za Allah mpaka arejee. 1418

i) Mimi nakula na Yahudi na Nasara lakini sili pamoja na mtu wa bidaa,1419 na natamani lau baina yangu na mtu wa bidaa kuwe kuna ngome ya chuma! 1420

j) Allah akijua kwamba mtu anamchukia mtu wa bidaa basi humsamehe (madhambi yake), na mtu wa Sunna hakumpunja mtu wa bidaa isipokuwa unafiki; na anayeugeuza uso wake kutokana na mtu wa bidaa, basi Allah huujaza moyo wake imani; na atayemkaripia mtu wa bidaa basi Allah atamuweka katika amani siku ya mfazaiko mkuu (siku ya Kiama);1421 na atayemdharau mtu wa bidaa basi Allah atamnyanyulia daraja mia katika pepo…”.1422

1412 - Tazama Al-Barbahari Sharhu Al-Sunna uk. 127.1413 - Tazama Al-Barbahari Sharhu Al-Sunna uk. 127. Jamani! Hebu tazameni uzushi huu wanamzulia Allah! Sasa Mitume kama hawakukaa na watu wabaya wakafundisha dini ni nani atayekaa nao. Pili mitume ni ma’asumun hakuna anayeweza kuwapotoa. 1414 - Tazama Al-Barbahari Sharhu Al-Sunna uk. 128.1415 - Tazama Al-Barbahari Sharhu Al-Sunna uk. 128.1416 - Tazama Al-Barbahari Sharhu Al-Sunna uk. 128.1417 - Labda hili ndio tegemeo la Abdallah Muhsin katika kutokujuzisha ndoa ya Ibadhi na Sunni! 1418 - Tazama Al-Barbahari Sharhu Al-Sunna uk. 128-129.1419 - Sheikh kula nao hao ndio ndugu zako! 1420 - Tazama Al-Barbahari Sharhu Al-Sunna uk. 129.1421 - Mafunzo kama haya ndio yanayowafanya Mawahabi siku zote kuwa ni watu wa kusema maneno mabaya kwa watu wengine, kama mulivyoona kilivyo kitabu cha Kasim Mafuta. 1422 - Tazama Al-Barbahari Sharhu Al-Sunna uk. 129.

472

Page 473: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Hio ni mifano miwili mitatu ambayo inaonesha kwamba sera ya Mawahabi na Maimamu wao ni kukimbia mijadala. Na kwa hivyo, usione ajabu kwamba Al-Harawi (396-481 A.H.) katunga kitabu chenye juzuu sita alichokiita Dhammu Al-Kalaam ili kupinga kufanya mijadala. Utakuta humo ananukuu Hadithi kama vile inayosema: المراء Wacheni) ..ذرواushindani….) na Hadithi kama: … صادق أنك تعلم وأنت المراء وترك(….Na kuwacha ushindani ilhali unajijua kwamba wewe ndiye mkweli (ndiye mwenye hoja ya haki).1423

Lakini kwa hali yoyote ile kinachokatazwa katika Hadithi hizo ni ushindani ambao mtu hakusudii kutafuta haki. Ama kujadiliana kwa ajili ya kutafuta haki, huko kumehimidiwa sana bali kumeamrishwa na Allah aliposema katika Kitabu chake: صادقين كنتم إن برهانكم هاتوا قل (Sema: leteni hoja zenu ikiwa nyinyi ni wakweli).1424 Na anasema: وجادلهم

أحسن هي بالتي (Na jadiliana nao kwa wema).1425 Kwa hivyo, mkusanyiko wa Aya hizi na Hadithi hizo unaleta maana kwamba mijadala ambayo si kwa ajili ya kutafuta haki basi hio ni haramu. Hio ndio maana inayopatikana katika Hadithi hizo; na mijadala inayofanyika kwa ajili ya kutafuta haki, hiyo ni yenye kuhimidiwa, na hii ndio maana ya Aya hizo. Na hivi ndivyo Al-Salafu Al-Salih walivyofahamu ambapo Masahaba walikuwa wakijadiliana kwa ajili ya kutafuta haki kama mijadala iliofanyika baina ya ‘Ali (k.w.) na Mu’awiya; na Ibn ‘Abbaas (r.a.) pamoja na Watu wa Nahrawaan (r.a.). Sasa wewe leo ukiwa umeshatiwa kasumba kwamba fulani ni mtu wa bidaa, halafu ukatiwa kasumba kwamba mtu huyo usizungumze naye wala usimkaribie kamwe, natija ni kuwa ukiwa wewe ndiye uliyepotea, basi utaganda katika upotovu wako, na kama yeye ndiye aliyepotea, basi ataendelea kuganda katika upotovu wake. Kwa hali hii, ufumbuzi ni kujadiliana kwa ikhlas na kwa namna nzuri.

Ama hilo wanalolifanya Mawahabi la kutoa mihadhara na kuandika vitabu wakatoa maneno makali na kumshambulia huyu na yule na kumtukana huyu na yule haliwafanyi watu wakubaliane nao; bali watu wenye akili wanazidi kuwaona kuwa ni watu walio mbali na muongozo sahihi wa Uislamu, bali wanawaona kuwa ni watu waliofilisika kihoja. Wenye akili wanakuwa wanasikiliza hoja na kujichagulia ilio na nguvu.

NATURUDI TENA KWA AL-KHALILI NA IBN BAZ

1423 - Al-Harawi Dahmmu Al-Kalaam j. 1, uk. 171, chapa ya kwanza 1416 A.H. (1995 M.) Maktaba Al-’Uluumi wal Hikam, Al-Madinatu Al-Nabawiyya, Suudiyya. 1424 - Sura 2, Aya 111. 1425 - Sura 16, Aya 125.

473

Page 474: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Baada ya hayo, sasa nikupe ushahidi mwengine wa kwamba, kweli Sheikh Al-Khalili alimtaka Ibn Baz wafanye mjadala na akakataa! Baada ya sheikh Ibn Baz kutoa fat-wa yake hio ya kwamba Maibadhi ni wapotovu, kilichotokea huko Suudia – kama tulivyosema – ni kuwa baadhi ya watu wa huko walimuandikia Sheikh Ibn Baz barua ya kutaka kuhakikisha kwamba kweli katoa fat-wa hio. Hapo Ibn Baz – kama tulivyotanguliza maelezo – ndipo alipotoa barua ya kuwakafirisha Maibadhi akitegemea maneno ya Al-Imamu Ahmad na Al-Imamu Malik. Ama kwa upande wa Oman, kilichotokea baada ya hapo ni mambo mawili:

1) Sheikh Al-Khalili kumjibu Ibn Baz live katika T.V. ya Oman na kuyaeleza yote yaliojiri baina yake na Ibn Baz. Na kama tulivyosema kwamba Sheikh Ibn Baz baada ya hapo aliishi zaidi ya miaka kumi wala hakukanusha hata herufi moja katika yale alioyaeleza Sheikh Al-Khalili.

2) Sheikh Al-Khalili alitunga kitabu alichokiita Al-Haqqu Al-Damigh akaelezea ndani yake hoja zake juu ya lile suala ambalo Sheikh Ibn Baz lilimpa mashaka kwa upande wa Maibadhi – suala la kuonekana kwa Allah.1426 Pia akaongeza masuala mengine mawili – suala la kuwa je Qur-ani ni kiumbe au si kiumbe na suala la kutoka motoni. Na mwishoni mwa kitabu hicho Sheikh Al-Khalili katangaza kwa uwazi kwamba yuko tayari kujadiliana na mtu yoyote yule juu ya masuala hayo. Tumeyanukuu maneno yake kabla, na hapa nitakukumbusha. Anasema Sheikh Al-Khalili:

ااي������ضقال هذه يف فالخال مس����ح الإ نوري ال نيذلل نلعوأع ه��يف قفتت ىتح ،ةماأل ةديقاال فادهال ياد�����هال يعوضومال اروحال نم فكنتسأ ال يننأب يذ،

، ق�����حال الإ هب دشني الت الإ يضفي الو ال لجإلى ث هانهرب روه��ظو ةقيق�����حي يدؤي ال ما،األ الإ ةدو�����مالو ةفلإلى نيملسمال نيب

Na ninawatangazia wale (wote) ambao hawaoni (kitu bora) isipokuwa kuziondoa tofauti katika mas-ala haya ili itikadi ya uma ikubaliane (iwe moja), kwamba mimi sikatai mjadala wa kielimu, wa utulivu na wenye lengo, ambao haitafutwi kwa mjadala huo isipokuwa haki, na wala haupelekei isipokuwa kwenye uwazi wa uhakika na kudhihiri hoja zake,

1426 - Suala hili sasa Sheikh Al-Khalili kaliandika kwa urefu katika kitabu cha tauhidi chenye juzuu kumi na nne kubwa. Kwa mara ya mwisho, alinipa habari kwamba yuko juzuu ya nane na alinionesha juzuu inayohusu kuonekana kwa Allah nayo ni juzuu kubwa. Kwa hivyo, masuala haya in shaa Allah yataelezwa na Sheikh kwa ufafanuzi wa hali ya juu na wengi wataweza kujipatia faida.

474

Page 475: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kisha haupelekei isipokuwa kwenye mshikamano na mapenzi baina ya Waislamu.1427

Sheikh Al-Khalili aliyasema maneno haya baada ya kutokea hayo yaliotokea baina yake na Sh. Ibn Baz. Sasa wewe Kasim Mafuta unachokipinga ni nini na tangazo hili liko wazi kwa watu wote duniani: si Sh. Ibn Baz peke yake? Hata wewe – kwa vile ni katika Maulamaa wakubwa – unaweza kuitika wito huo.

Kisha baada ya hayo, Sheikh Al-Qannubi akatunga vitabu mbali mbali, na katika baadhi ya vitabu vyake akazielezea Hadithi muhimu zao wanazozitegemea wale wenye imani ya kuonekana kwa Allah na akawachalenj akina Al-Albani na wafuasi wake juu ya itikadi zao. Anasema Al-Qannubi:

ه دحتن نحنو ي نأ ةيو���شحال ءالؤى ل وتأ ب نا اهيف ةحي����حص ةايوراوأ اررقتساإلب حيرصت

ع ورهظتسيلو يسحال اءوتساإل ذ لا ولو اءشي نمب كلىك عيمج ني�����لقالثب أ ما ن ننا ىدحتاف ملل ةلحالن هذه اببرأ م هريغ وأ ةلأسمال هذه يناظرة نا

ةيادقتعاإل لائسمال

Na sisi tunawachalenj hawa Mahashwiya (Mawahabi) watuletee riwaya sahihi ambayo ndani yake kumesemwa kwa uwazi kuwa (Mwenyezi Mungu) anakaa kitako kweli kweli, na wamuombe msaada yoyote wanayetaka hata binaadamu wote na majini wote. Kama vile ambavyo tunawachalenj kufanya mjadala katika mas-ala hii au mas-ala nyengine yoyote ile ya itikadi.1428

Na anasema:

ف ملل ماكنوعد دقو نحانه و متيبأف ةرم نم رثكأ كلذ يناظرة نإف كلذ مك������ل رركن ءالوأاس لع متنك ال ملهف كلذل اددعتى ب مإلى لقنت نأ طرشناظرةملع���يسو , ةيمالعاإل لائسوالبأ هنيح س دهأ و نماألب قحأ نيقيرفال يا اليبى

Na tumekuiteni kwenye mjadala zaidi ya mara moja mukakataa, basi na hapa sisi tunakurudieni tena katika hilo: kama muko tayari kwa hilo na twende katika mjadala kwa sharuti kwamba uchukuliwe na vyombo vya

1427 - Al-Khalili Al-Haqu Al-Damigh uk. 229. 1428 - Al-Qannubi Al-Saif Al-Had uk. 12.

475

Page 476: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

habari, basi hapo litajulikana lipi katika makundi mawili linastahiki amani na liloongoka.1429

Tazama maneno yake yanayosema: “Na tumekuiteni kwenye mjadala zaidi ya mara moja mukakataa” utaona kwamba yanamaanisha kwamba huko nyuma walikwishawahi kualikwa katika mjadala wakakimbia! Na vipi wasikimbie na wanasoma hoja za Ahlu Al-Haqqi Wa Al-Istiqaama (Maibadhi) na kuzilinganisha na hoja zao, na wanaona udhaifu walio nao. Kama unavyojua hoja zao ni “Sheikh Al-Islam kasema; Shamsu Al-Din kasema!”. Basi hali ni hio, hakuna Aya iliojengeka katika minhaj (methodology) sahihi ya tafsiri wala hakuna Hadithi sahihi!

NYONGEZA KUHUSU MUALIKO WA MJADALA Sasa baada ya hayo, nakuongeza tena sehemu mbili ambazo Al-Imamu Badru Al-Din Al-Khalili na Imamu Al-Sunna Al-Qannubi waliwataka Mawahabi wafanye mjadala wa wazi, lakini wakanyweya!

Mosi: Katika ibada za hija, Al-Qannubi alikuwa akitoa muhadhara kule Mina. Mmoja wa waliohudhuria akamwambia: “Lakini Masheikh hapa hawatoi fat-wa hio”. Naye akamjibu: “Kawaite hao Masheikh waje hapa”, waje watoe ushahidi wao! Bwana muulizaji akanywea! Hili la kwanza unaweza kulikataa, kwa vile “Mashahidi ni wenyewe kwa wenyewe”.

Pili: ni tukio lililotokea baina ya Sheikh Al-Khalili na Mawahabi katika mkutano uliofanyika huko Bahrain. Mkutano huo ulirushwa na T.V. live watu wote wanauona.1430 Maudhui za mkutano huo zilikuwa ni za kifi-qhi tu. Basi alisimama Sheikh wa Kiwahabi akasema: “Nyinyi Maibadhi munajifanya kwamba munamfuata Al-Imamu Jabir bin Zaid, si kweli: nyinyi munamfuata Al-Imamu Al-Salimi kipofu wa macho na moyo”. Tazama mtu huyu alivyokuwa hana mwenendo wa watu wa ‘ilmu! Hata wale wanavyuoni wote waliokusanyika pale kashindwa kuwapa heshima yao. Basi hizi ndio lugha za watu hawa kama munavyokiona kitabu cha Sheikh Kasim Mafuta. Tena anajisemea tu: wapi kasikia kwamba

1429 - Al-Qannubi Al-Tufan Al-Jarif j. 3, sehemu ya 1 uk. 57. 1430 - Mimi sikuuona, kwani sikutazama T.V., lakini watu waliotazama wote waliuona na baadae suala hili likawa linajadiliwa katika internet, ambapo niliweza kuyasoma yote yaliotokea.

476

Page 477: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

madhehebu ya Kiibadhi imeanza na Al-Imamu Al-Salimi aliyekufa karne moja na kidogo iliopita? Kasumba yake imemfanya asijue kwamba hata huyo Abdullah bin Ibadhi – ambaye madhehebu kimakosa imenasibishwa kwake – ni mkubwa kwa umri kuliko Al-Imamu Jaabir bin Zaid.

Cha muhimu ni kuwa baada ya bwana huyo kuyasema hayo – na yote hayo – ni katika mkutano wa Bahrain uliorushwa na T.V.: si katika chumba cha siri ambapo mashahidi ni wenyewe kwa wenyewe. Hapo walisimama watu watatu kwa pamoja kutaka kumjibu – Sheikh Al-Khalili, Sheikh Nassir Al-Sabi’i, na Sheikh Zahir Al-’Abri. Lakini bila shaka akisimama Sheikh Al-Khalili inabidi wengine warudi. Sheikh Al-Khalili hapo alikwenda kuwasomea matatizo yao yote wanayomfanyia yeye binafsi katika mikutano inayofanyika kujadili mambo ya dini. Mifano miwili ya hayo ni kuwa:

a) Kanuni ni kwamba ikiwa mtu kaandika bahth (utafiti) yake basi mwenye jawabu juu ya bahth hio anatakiwa amjibu kwa muda wa wiki mbili kabla ya siku ya mkutano ili akiwa naye ana jawabu aitayarishe. Basi Mawahabi wanachokifanya – wakiongozwa na Dr. Bakr Abu Zaid mkuu wa vikao hivyo – ni kuwa Sheikh Al-Khalili akiandika bahth yake, wao wanaijibu halafu wanampelekea hotelini usiku wa kuamkia siku ya mkutano, ili asiwahi kuandika jawabu, pengine – kama kachoka – hata kuisoma hawahi. Sasa watu hawa ndio kweli wanatafuta haki au wanataka kulazimisha fikra zao tu?

b) Jawabu isiwe kubwa kuliko bahth. Basi wao huandika jawabu kubwa mara tatu ya bahth! Kisha jawabu hio wanampelekea mtu usiku wa kuamkia siku ya mkutano!

Hayo ni baadhi ya mambo wanayoyafanya kuwafanyia Waislamu wengine; mengi wanayatenda hata ikafikia Dr. Bakr Abu Zaid, Wahabi mwenye kasumba mbaya ambaye ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa vikao hivyo, kutaka kushtakiwa! Sasa baada ya Sheikh Al-Khalili kuwasomea makosa yao wanayoyafanya katika mikutano ya kifi-qhi. Aliwataka wafanye mjadala wa wazi hapo hapo Bahrain. Narudia tena, hili lilikuwa Bahrain katika mkutano uliochukuliwa na T.V., na wengine tumelisoma tukio hilo katika intrenet na waliosema hayo si Maibadhi. Sheikh Kasim bin Mafuta upo? Je:

1) Na huu uliorushwa katika vyombo vya habari live pia utasema ni uwongo?

2) Je hayo alioyasema Sheikh Al-Khalili katika kitabu chake kwamba yuko tayari kufanya mjadala na yoyote yule, pia utasema ni uwongo: hajayasema?

477

Page 478: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

3) Je yale alioyatangaza Al-Qannubi nayo yamo katika kitabu chake, pia utasema ni uwongo: hajayasema?

Kwa hivyo, kwa kuhitimisha ni kuwa ninataka kumuhakikishia bwana Kasim Mafuta na wenzake kwamba Sh. Al-Khalili ni kweli kabisa alimtaka Ibn Baz wafanye mjadala wa wazi, na Ibn Baz alikataa. Na baada ya kukataa alimtaka wafanye mubahala pia akakataa. Sasa ninachotaka kukumbusha wewe ewe Bwana Kasim mwana wa Mafuta ni kuwa:

1) Chalenj hii si mahususi kwa Ibn Baz, bali ni kwa Mawahabi wote, hata wewe umo: ukitaka mjadala wa wazi au mubahala tueleze tu; wakati wowote ule sisi tuko tayari.

2) Chalenj hio kama ilivyotolewa katika chumba cha siri, pia imetolewa hadharani huko Bahrain na ikatolewa kwa kuandikwa vitabuni. Sasa wapinga nini ewe Sheikh Kasim bin Mafuta?

3) Masheikh wenu wakubwa, Ibn Baz, Ibn ‘Uthaimin, Al-Albani na wengine, wameishi zaidi ya miaka kumi baada ya chalenj hio kuandikwa vitabuni, nao hawakuweza kujibu kitu.

4) Masheikh wenu hao wameishi miaka hio bila ya kukanusha kile kilichosemwa na Sh. Al-Khalili live katika T.V. ya Oman na kuandikwa kwa ufafanuzi na Sh. Ahmad Al-Siyaabi.

5) Wewe unaona kuwa hoja za Maibadhi ni dhaifu na ni za uwongo. Sasa nawe – kwa vile ni bingwa wa lugha ya Kiarabu – unayo nafasi bado ya kuitika chalenj hio. Waandikie Al-Khalili na Al-Qannubi uwaambie “Mimi Kasim mwana wa Mafuta wa Pongwe Tanga niko tayari kujadiliana na nyinyi, na kufanya mubahala na nyinyi”. Au ukiona ni uzito kwako, basi waombe Mashekhe wako waitike chalenj, ili sisi wanyonge wa elimu tujipatie faida.

أهلها من شاهد وشهدNA AKASHUHUDIA SHAHIDI KATIKA

WATU WAKE MWENYEWEBaada ya maelezo yote hayo niliokupa ambayo kila mwenye akili basi yanamtosha kuujua ukweli wa tukio hilo ukoje, sasa Sheikh Mafuta yasome yalioandikwa na mmoja wa Mawahabi wa Suudia. Kisha baada ya hapo, utajijua nafsi yako ina nini na wewe ni mtu wa aina gani! Anasema muandishi wa kijitabu kiitwacho Al-Ibadhiyya alichokiiandika kuwatukana Maibadhi baada ya kueleza sababu zake za kuandika kitabu hicho:

478

Page 479: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

..(( )) - خليلهم فعل كما السنة، أهل مباهلة وتبجح صلف بكل ويطالبونسماح من طلب ة ��������عندما

المناظرة في لما سماحته، فامتنع المباهلة، باز بن العزيز عبد الشيخالناس بعض إيقاع من المعلنة

- - هالة يعطي ذاته بحد المناظرة وقوع أن كما وشبهات، شكوك فيعليها ويضفي اإلباضية، لفرقة

.م مزيدا ذلك - - دون شك بال وهم والظهور، الشهرة ن

Na (Maibadhi) – kwa maringo kabisa na madaha yote – basi wanataka wafanye mubaahala1431 na Ahlu Sunna1432 kama alivyofanya Khalili wao alipomtaka Samaahatu Al-Sheikh ‘Abdul-‘Aziz bin Baz kuwa wafanye mubaahala. Basi Sheikh (Ibn Baz) akakataa, kwa sababu kufanya mjadala wa wazi kunapelekea kuleta shaka na shubuhat, kama vile ambavyo kufanyika kwa mjadala kunaipa madhehebu ya Kiibadhi umashuhuri na kuiongezea umashuhuri na kudhihiri, nao – bila shaka – ni watu walio chini ya hayo (ni watu duni hawastahiki hayo)!1433

Sheikh Kasim “mwanangwa wa” Mafuta upo! Je umeyasikia maneno ya mwenzenu? Je ni kweli Al-Khalili alimtaka Ibn Baz wafanye mjadala wa wazi na mubahala naye akakataa au ni uwongo wa Kikhawarij wa akeri-zamaan? Je “ushahidi wa wenyewe kwa wenyewe juu ya yaliojiri katika chumba cha siri” ni ushahidi wa kweli au wa uwongo?

Sasa baada ya hayo, tazama sababu za Ibn Baz za kukataa mjadala wa wazi! Sababu ya kweli ni kuwa aliogopa kwani alijijua kwamba hana hoja za

1431 - Kumuomba Allah ateremshe laana yake juu ya mwenye itikadi potofu. 1432 - Yaani Mawahabi ndio anaowaita yeye kuwa ni Ahlu Sunna! 1433 - Al-Ibaadhiyya uk. 6. Kijitabu hiki kwa bahati tu bila ya kutarajia nimekigundua katika intaneti katika Al-Maktaba Al-Shaamila. Hadi sasa sijalijua jina la muandishi. Lakini nadhani sana kimeandikwa na Dr. Saabir Ta’iima kwani nimezikuta ibara zake ambazo nimeziona zikinukuliwa katika vitabu vyengine. Kwa hali yoyote ile, Dr. Sabir Ta’iima ana kitabu kama hiki. Kwa sasa sina kopi yake lakini nimekiagizishia na wakati wowote ule kitafika, na hapo nitaweza kujua kwamba je ni kitabu chake au si chake. Kwa hali yoyote ile kitabu hiki kina maelezo haya:

محفوظة الطبع حقوقاألولى الطبعة

ه� 1412من الكتاب هذا بطبع اإلذن صدر

تبوك - اإلعالم بوزارة للمطبوعات العامة المديريةتاريخ / / 482برقم ت ه� 1412 / 8 / 13م

Haki za uchapishaji zimehifadhiwa.Chapa ya kwanza 1412 A.H.Ruhusa ya kichapisha kitabu hiki imetolewa na:Kurugenzi kuu (directorate-general) ya uchapishaji, Wizara ya Habari, Tabuk.Nambari: 482/ Tarehe 13/8/1412 A.H.

479

Page 480: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kielimu zenye kuunga mkono itikadi yake. Lakini anadai kuwa mjadala unatia shaka na shubuhati na kuipa umashuhuri madhehebu ya Ibadhi! Nami ninasema:

1) Qur-ani imehimiza mijadala ya kutafuta haki. Na anayeogopa mijada ya aina hio basi huyo haifuati Qur-ani wala hayuko katika haki.

2) Masahaba walijadiliana sana tena kwa uwazi. Sasa kama yeye anadai kuwa yeye ni Salafi (anafuata Al-Salaf) kwa nini asifanye kama walivyofanya wao?

3) Kama yeye anaogopa kuwa mjadala wa wazi utawapa Ibadhi umashuhuri, basi – madamu Ibadhi kwa mujibu wake wako katika batili – yeye angeliudhihirisha ubatili wao na kwa hapo mjadala huo ungewapa Ibadhi umashuhuri wa ubatili wao: si wa haki.

4) Mjadala hauleti shaka na shubuhati; vyenginevyo nini njia ya kuijua haki? Na je haki inashindwa na batili.

5) La mwisho ni kuwa ikiwa mjadala unaleta shubuhati na shaka, je mubahala (kumuomba Allah ateremshe laana yake juu ya aliye katika batili) pia nao unaleta shaka na shubuhati? Mbona pia kaogopa kufanya hivyo?

SURA YA KUMI NA NNEMAWAHABI NA MAIMAMU WAO

NDIO WASIOSEMA KWELI

UTANGULIZI WA SEHEMU HII

Katika sura iliotangulia tulijibu tuhuma za Kasim Mafuta dhidi ya Sheikh Al-Islam Al-Imamu Badru Al-Din Al-Khalili na Imamu Al-Sunna wa Al-Usuli wa Al-Furu’i Al-Hujja Al-Qannubi (a’azzahuma Allah). Tumebainisha kwamba:

1) Watu wa skuli hii ya Kiibadhi – kwa ujumla – hawakusemwapo kwa tatizo la uwongo, bali wamesifika kwa ukweli kushinda watu wa madhehebu zote. Na hilo ni kwa kukiri wanavyuoni na watafiti wa Kisunni.

2) Yale ambayo Sh. Kasim Mafuta kayaita kuwa ni uwongo, yote ni ya kweli tupu: hakuna uwongo – nukulu alioitaja Sh. Al-Qannubi kutoka katika kitabu Al-Dhaifa cha Al-Albani imo katika kitabu hicho; na ubeti ambao Kasim Mafuta kadai kwamba umepinduliwa na Sheikh Al-Khalili umo katika kitabu kilichoandikwa karne nane zilizopita – katika zama za Ibn Al-Qayyim mwenyewe. Bali tumesema kwamba beti zote hizo zina maana moja, na katika hali

480

Page 481: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kama hii huwezi kuuita huo kuwa ni uwongo hata lau ilikuwa ni kweli lafdhi za ubeti huo kazipindua Sh. Al-Khalili.

Sasa na sisi tunataka tumthibitishie Kasim Mafuta mambo machache katika mengi mno yaliosemwa na Maimamu wao ambayo hayana ukweli. Kwa kuanzia natuyanukuu baadhi ya yale niliyoyazungumza katika kitabu Kisimamo Katika Sala miongoni mwa yale yaliyosemwa na wanavyuoni wakubwa kuhusu wanavyuoni wa skuli hio ya Sh. Kasim Mafuta. Soma yanayofuata kuhusu Maimamu wa Kihanbali/Kiwahabi.

ABU AL-‘IZZ IBN KAADISH

Huyu alikuwa mtunzi wa Hadithi za kumzulia Mtume (S.A.W.). Anasema Ibn Assakir:

Aliniambia Abu Al-‘Izz Ibn Kaadish kwamba alimsikia mtu katunga Hadithi ya kumsifu Ali (bin Abi Talib) anasema (Ibn Kaadish huyu basi) na mimi nikatunga Hadithi ya kumsifu Abu  Bakar!1434

Anasema Al-Dhahabi: “Hili linaonesha ujinga wake: anaona fakhari kumzulia Mtume (s.a.w.) uwongo!”1435 Na imeelezwa pia katika kitabu Lisanu Al-Mizaan: “Alikuwa ni mwenye kuchanganyikiwa (na)  mwongo sana.”

Anasema Al-Qannubi: “Ama madai ya Al-Dhahabi katika kitabu chake Al-Mizan1436 aliposema kwamba Ibn Kaadish alitunga Hadithi lakini alikiri na kutubia, maneno haya hayana kima kwa sababu riwaya ya mtu mwongo hata akitubia haikubaliki kama walivyosema wanavyuoni wa Hadithi na usuli, miongoni mwao ni: “Ahmad bin Hanbal, Al-Humaidi, Al-Sairafi (يرفي .Al-Sam’ani, Ibn Qattan, Ibn Jamaa, Al-Zarkashi na wengineo ,(الص

1434 - Ibn Hajar Lissan Al-Mizan j.1, uk. 218, tarjama na. 677. 1435 - Al-Dhahabi Siyar Al-Aalaam j. 19 uk. 559. 1436 - J. 1, uk. 78, tarjama ya 461.

481

Page 482: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Na kwa hivyo, anayedai kwamba (Ibn Kaadish) katubia na atupe sanad sahihi ambayo ndani yake kunapatikana toba hii (ya Ibn Kaadish) ….. na Ibn Kaadish alikuwa rafiki kipenzi wa Ibn Batta Al-Ukbari1437 jiongo kubwa lenye kutunga Hadithi mpotovu mujasim.”1438

Cha kufahamu ni kuwa Ibn Kaadish huyu ni katika Maimamu wenye itikadi kama za Kiwahabi – ni mmoja wa Maimamu wao. Na hio ndio hali yake. Jambo la kustaajabisha ni kuwa Al-Albani kama kawaida yake akiwapitia viongozi wa madhehebu yake ya tajsim na tashbih, basi ama hawajeruhi kabisa hata kama ni waongo, au atanukuu kitu kilicho chepesi katika mezani ya elimu ya Hadithi na kile kizito atakiwacha. Na hivyo ndivyo alivyofanya kuhusu Imamu wake huyu. Al-Albani – alipokuwa akimuelezea Imamu wake huyu, basi – kaishia kunukuu maneno ya ‘Abdul-Wahhab Al-Anmaati akisema: “Ni mwenye kuchanganyikiwa”. Hivyo ndivyo alivyosema Al-Albani katika Al-Dhaifa.1439 Dhahiri ni kuwa anachokitaka Al-Albani ni kuwa watu wadhanie kwamba Ibn Kaadish ni thiqa lakini kachanganyikiwa! Vyenginevyo angelizitaja zile kasoro zenye uzito za uwongo na utunzi wa Hadithi ambazo ndizo zenye kuthibitisha kwamba beti za mashairi alizozinukuu hapo zenye kusema kuwa Allah atamuweka Muhammad pamoja naye katika ‘Arshi, ni beti za uwongo.

ABU ALI AL-AHWAZI

Anasema Al-Dhahabi katika kitabu chake Al-Mizan kuhusu Imamu huyu Adhim wa Kiwahabi, kwamba “Ametunga kitabu kuhusu sifa za Mungu akaleta humo Hadithi za kutunga na fedheha tele na alikuwa akimponda Al-Ash’ari (Imamu wa Masuni katika mambo ya itikadi na tawhidi).1440

Anasema Al-Khatib Al-Baghdadi: “Al-Ahwazi ni mwongo mkubwa.”1441

Anasema Ibn Asaakir katika kitabu chake Tabyin Kadh’b Al-Muftari: “(Al-Ahwazi) alikuwa mwongo kuliko watu wote katika riwaya na visomo.” Na akasema Ibn Asaakir kwamba Al-Ahwazi huyu ndiye aliyetunga Hadithi inayosema: “Nilimuona Mola wangu Mina juu ya ngamia mwekundu kavaa juba!” Na katika riwaya ya pili anasema: “Ngamia mweupe aliyepiga

1437 - Tazama kuhusu Ibn Bata kitabu Lisanu Al-Mizan cha Ibn Hajar j. 4, uk. 112-113 tarjama na. 231. Jina la Ibn Bata ni “Ubeid-lah bin Muhammad bin Bata Al-Ukbari” na jina la Abu Al-‘Izz bin Kaadish ni “Ahmad bin Ubaid-llah.” 1438 - Al-Qannubi Al-Saifu Al-Haad uk. 189. 1439 - J. 2, uk. 256, maelezo ya Hadithi na. 865. 1440 - Al-Dhahabi Al-Mizan j.1, uk. 512, tarjama ya 1916. 1441 - K.h.j.

482

Page 483: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

weusi.”

Na alisimulia idadi kubwa ya Hadithi za uwongo miongoni mwa hizo ni Hadithi alioisimulia katika kitabu chake Sharhu Al-Bayaani Fii Uquudi Ahli Al-Iman. Hadithi hiyo inayosema: “Mungu alipotaka kuiumba nafsi yake aliumba farasi kisha akamuendesha mbio mpaka akatoka jasho na kutoka katika jasho hilo la farasi akaiumba nafsi yake”!1442

Na miongoni mwa riwaya zake alizozitaja Al-Dhahabi ni riwaya inayosema:

Ikifika siku ya Ijummaa, basi Mungu huteremka baina ya Adhana na Iqama naye ana vazi (kama kanzu au jokho!!!)1443 limeandikwa mimi ndiye Mungu hakuna Mungu ila Mimi; anasimama katika kibla cha kila Muumin (yaani mbele yake), Imamu akitoa Salam basi (Mungu) anapaa mbinguni!

Hayo ndiyo alioyasema Imamu huyo wa Kiwahabi, naye Sheikh huyo kwa Mawahabi ni miongoni mwa Ahlu Sunna wakubwa na hiyo ndio Sunna yake!

ABDUL-‘AZIZ BIN AL-HARITH AL-TAMIMI

Anasema Al-Dhahabi: “Alikuwa katika viongozi wa Mahanbali na wakuu wa Wanavyuoni wa Baghdad, lakini alijiudhi mwenyewe: na kutia Hadithi mbili tatu katika kitabu cha Hadithi cha Al-Imamu Ahmad bin Hanbal (yaani anatunga Hadithi halafu anaitia katika kitabu hicho anamzulia uwongo Mtume s.a.w. na Al-Imamu Ahmad).1444

Anasema Al-qannubi:

Na Al-Imamu Ahmad amepata mtihani wa wafuasi wajinga wakamzulia uwongo na wakamnasibishia mambo ambayo hakuyasema miongoni mwa itikadi mbovu na rai zenye kudoda (hazina soko) kama walivyosema kundi kubwa la wanavyuoni miongoni mwao ni: Ibn Al-Jawzi, Ibn Al-Salah, Ibn ‘Abdi-Salam, Al-Imamu Al-Subki, Al-Taaj, na Al-Dhahabi na wengineo.

1442 - Tazama “LISSAN AL-MIZAN” cha Ibn Hajar juzuu ya 2 ukurasa wa 239 tarjama ya 1005. 1443 - Sijui ni Ijummaa ya nchi gani? Kwani katika dunia kila wakati iko adhuhuri na kwahivyo ikiwa siku ya Ijummaa kila wakati ipo saa ya Ijummaa katika nchi japo moja au sehemu japo moja katika dunia. Na kwahivyo ni sawa sawa na kusema kwamba siku ya Ijummaa Mungu anashinda ardhini!!! 1444 -Al-Dhahabi Mizanu Al-Iitidaal j. 3, uk. 338 tarjama na. 5092.

483

Page 484: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Na jambo la kufurahisha kuliko yote kuhusu Imamu huyu wa Kiwahabi ni lile aliloliandika Ibn Hajar Katika Lisanu Al-Mizan1445 na Al-Dhahabi katika Al-Mizan1446 kuhusu Hadithi ambayo aliitolea hoja Imamu huyu Abdul-’Aziz bin Al-Harith, akaulizwa na Amru bin Muslim: “Hadithi hii umeipata wapi?” Akamwambia: “Nimeiunda sasa hivi nipate kumbomowa mpinzani wangu?” Yaani anakubali asishindwe kwenye mjadala kwa hali yoyote hata kama kwa kutunga Hadithi ya uwongo ya kumzulia Mtume (s.a.w.)!

AL-HAKKAARI

Anasema Ibn Al-Najjar:

Anatuhumiwa kwamba alikuwa akitunga Hadithi na kuunda sanad……. na aghlabu ya riwaya zake ni ngeni na munkar na katika Hadithi zake kuna mambo ya kutunga.

Amesema Ibn Hajar: “Nimeona maandishi ya baadhi ya Maulamaa wa Hadithi kwamba alikuwa akitunga Hadithi katika (mji wa) Isbahaan.” 1447

IBN BATTA AL-’UKBARI

Huyu pia ni Imamu adhimu wa Kiwahabi, naye tumeshamuelezea kabla na kwamba kasimulia riwaya inayosema:

Nabii Musa (a.s.) alimkuta mtu juu ya mti kavaa vazi la sufi na viatu akasema naye (yaani yule mtu akasema na Nabii Mussa a.s). Nabii Mussa (a.s.) akasema: ‘Ni Muibrania gani huyu anayesema na mimi?’ Yule mtu akajibu: “Mimi ni Mungu.1448

Na bila shaka kwa anayekisoma kitabu Al-Ibana Wa Al-Shari’a cha Ibn Batta huyu, hawezi kumuweka katika kundi la wakweli milele. Bali wanavyuoni wa wapokezi wamemuweka katika kundi la waongo, kwani kama tulivyotangulia kumueleza kabla – alikuwa akitunga sanad za Hadithi

1445 - J. 4 uk.26. 1446 - J.3, uk. 338. 1447 - Na ajabu ya binaadamu tulivyo, baada ya kuwa mtu huyu anatunga Hadithi bado wamembandika sifa kubwa wakamwita “Sheikh Al-Islam!!!” Tazama habari zake katika lisanu al-mizan j. 4, uk. 195, tarjama na. 519. Jina lake kamili ni “Ali bin Ahmad bin Yusuf Abu Al-hasan Al-Hakkaari.” 1448 - Tazama Ibn Hajar Lisanu Al-Mizan j. 4, uk. 112-114, tarjama na. 231.

484

Page 485: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

na akichukua vitabu vya watu akifuta majina yao na kuweka jina lake.1449

Hio ni mifano miwili mitatu ya namna gani Maimamu watangulizi wa Mawahabi walivyokuwa. Bila shaka kwa anayevisoma vitabu vyao vya riwaya kama Al-Sunna cha Ibn Ahmad na Al-Ibana Wa Al-Shari’a cha Ibn Batta na vyengine, anaona kwa uwazi kabisa utunzi wa riwaya za kubuni zilizojaa katika vitabu vya Maimamu watangulizi wa Mawahabi! Wallahu Al-Musta’aan.

Sasa baada ya kuona hayo yalionenwa kuhusu Maimamu watangulizi wa Kiwahabi, na kwa sababu Sheikh Kasim Mafuta kafanya فاشلة محاولةmuhaawala faashila (jaribio lenye kufeli) la kutaka kuonesha kwamba Masheikh wa Kiibadhi ni waongo – na hilo hatolipatia ushahidi hata ngamia akipenya kwenye tundu ya sindano na awaombe msaada binaadamu wote na majini wote – basi na sisi wacha tumthibitishie kwa maandishi maneno yasio na ukweli yaliosemwa na Maimamu wake wengine anaowategemea zaidi. Baada ya hapo itambidi Bwana Mafuta atupe jawabu sahihi au awaite Maimamu wake kuwa nao ni waongo kama alivyowaita Wanavyuoni wema, wacha Mungu. Na ili Kasim Mafuta awe katujibu ni lazima aseme:

1) Nukulu nilizozitaja ni za uwongo: hazipo. 2) Nukulu hizo zipo lakini hawakusema uwongo, bali walioyasema ni

kweli. Kama ni kweli basi itambidi Sheikh Kasim atupe ushahidi juu ya ukweli huo.

MANENO YASIO NA UKWELI YA ‘UTHMAN AL-DARIMI

Al-Darimi katika kutafautisha kwake baina ya Aya inayosema: “basi Allah AKAZIJIA nyumba zao katika misingi” na Aya: “Na akaja Mola wako na Malaika safu safu” alitoa madai haya:

Waislamu wamekubaliana kwamba Allah yuko juu ya ‘Arshi yake juu ya mbingu zake……; na wala hawakuwa na shaka kwamba Yeye atateremka siku ya kiama ili ahukumu baina ya waja wake….1450

Tunauliza: makubaliano hayo ya Waislamu juu ya itikadi hizo yako wapi? Ni wazi kwamba Sheikh huyu hakujilazimisha kusema ukweli hata kidogo,

1449 - Rejea sura ya kumi kwenye kichwa cha habari kinachosema: “WAPOKEZI DHAIFU AMBAO MAWAHABI NA MAIMAMU WAO WANAWAKUMBATIA”. Tazama mpokezi nambari moja uone habari za Ibn Batta. 1450 - Tazama ‘Uthman Al-Darimi Al-Radu ‘Alaa Bishr Al-Marisi 50.

485

Page 486: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

bali anachotaka ni kuipigia debe itikadi yake kwa kutumia nguvu za: “Waislamu wote wamekubaliana”.

MANENO YASIO NA UKWELI YA IBN TAYMIYYA

Anasema Ibn Taymiyya:

Na kwa hivyo, wengi katika Waislamu wamemuitakidi Muumba kwamba ni kiwiliwili ambacho hakifanani na kiwiliwili, na Mahanbali na wengi waliowafuata wao wanafuata (kauli) hii.1451

Bwana Kasim bin Mafuta upo? Tunakuomba ututajie ni Waislamu gani hao walio wengi wenye itikadio hio ya Mungu mwenye kiwiliwili ambacho hakifanani na kiwiliwili?

Anasema Ibn Taymiyya:

يجعلون ال فإنهم وافقهم ومن الحديث أهل أكثر بل وأما حادثا النوعح قديما بين دوث ����ويفرقون

أفراده من الفرد وحدوث النوع

Ama walio wengi katika watu wa Hadithi na walioafikiana nao hawaifanyi AINA kuwa ni kitu kilichozuka bali ni kitu kilichotangulia, na wanatafautisha baina ya kuzuka kwa AINA na kuzuka kwa sehemu za AINA.1452

Sheikh Kasim una deni la kututajia wanavyuoni wengi zaidi wa Hadithi au hata wengi tu wenye itikadi hii ya kwamba AINA ya ulimwengu ni QADIM (ina sifa ya kutangulia). Vyenginevyo, usiwache kumuweka Mzee wa Uislamu, Ibn Taymiyya, katika orodha yako ya wasiosema kweli au wenye kusema uwongo!

Anasema Ibn Taymiyya:

به، متصفا يزل لم لكنه فشيئا شيئا وقدرته بمشيئته يقول من ومنهماآلحاد حادث قدي�����مفهو

من النوع وغيرهم الحديث أصحاب أئمة من يقول من ذلك يقول كماالشافع�������ي أصح����اب

.. الطوائف وسائر وأحمد

1451 - Ibn Taymiyya Bayaanu Talbisi Al-Jahmiyya j. 1, uk. 25. 1452 - Ibn Taymiyya Muwaafaqatu Sariihi Al-Ma’aquul Li-Sahihi Al-Manquul kilichochapishwa pamoja na Minhaju Al-Sunna j. 2, uk. 75.

486

Page 487: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Na miongoni mwao wako wanaosema kwamba (matendo ya Allah yanakuwa) kwa matakwa yake na uwezo wake kitu kimoja baada ya chengine, kwa hivyo Yeye (Allah) tangu enzeli alikuwa akisifika kwayo (matendo),1453 basi hayo (matendo) ni yenye kuzuka ukizingatia (kitendo) kimoja kimoja (lakini) AINA yake ni QADIM (yenye sifa ya kutangulia), kama wanavyosema wenye kusema hivyo, miongoni mwa Maimamu wa watu wa Hadithi na wengineo miongoni mwa wanavyuoni wafuasi wa (Al-Imamu) Al-Shafi na (Al-Imamu) Ahmad na makundi mengine.1454

Hayo ndio maneno ya Ibn Taymiyya, nayo ni maneno yenye mashaka sana. Na kwa hivyo, Sheikh Abdullah Al-Harari baada ya kuyanukuu maneno hayo ya Ibn Taymiyya, alisema hivi:

افترى كيف الحديث –كعادته –أننظروا أئمة على الخبيثة المقولة هذهب��ه انفرد شيء وهذا

والفقهاء الحديث أئمة على تقول ولكنه الفالسفة، متأخري به ووافقالشافع�ي أصحاب من

أن أراد لكن ذلك منهم أحد يقل ولم عليهم، وافترى وغيرهم وأحمدالمفت����راة عقيدته يروج

إنه يقال أن عن بن�����فسه ويربأ األفهام ض������عاف على المسلمين بينالفالس������فة واف�����ق

العقيدة هذه في

Tazama namna alivyowazulia Maimamu wa Hadithi – kama kawaida yake – maneno haya machafu; na ilhali jambo hili kapwekeka nalo1455 na akawawafiki kwalo wanafalsafa wa mwisho mwisho; lakini huo ni uzushi juu ya Maimamu wa Hadithi na Mafakihi miongoni mwa wafuasi wa (Al-Imamu) Al-Shafi na (Al-Imamu) Ahmad na wengineo na akawazulia uwongo, na hakusema hivyo yoyote katika wao, lakini alitaka kuipigia debe itikadi yake ya uzushi miongoni mwa Waislamu; kwa wenye fahamu dhaifu, na ajiepushe yeye asije akaambiwa kwamba kakubaliana na wanafalsafa katika itikadi hii.1456

Anasema Ibn Taymiyya:

عائد(( الضمير أن في نزاع الثالثة القرون من السلف بين يكن لم وأنهسي وأن تعالى الله اق ���إلى

(( اه� ذلك على تدل كلها األحاديث

1453 - Yaani kutenda ni sifa ya Allah ya enzeli (tangu na tangu). 1454 - Ibn Taymiyya Al-Sunna j. 1, uk. 224. Kwa kuifahamu maudhui vizuri anzia ukurasa wa 223. 1455 - Kalisema yeye tu. 1456 - Al-Harari Al-Maqaalaatu Al-Sunniya uk. 69-70.

487

Page 488: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Na kwamba hakukuwa na tafauti baina ya Al-Salaf (watangulizi) katika karne tatu (za mwanzo) kwamba dhamir inarejea kwa Allah Mtukufu na kwamba Siyaaq (context) ya Hadithi inaonesha hivyo.1457

Anayoizungumzia Ibn Taymiyya hapa ni Hadithi inayosema:

ذراعا ستون طوله صورته على آدم الله وخلقNa (Allah) kamuumba Adam kwa sura yake

urefu wake ni dhiraa sitini.1458

Kama tulivyosema kwamba Ibn Taymiyya na Masheikh wengine wanaofuatwa na Mawahabi, wanasema kwamba dhamiri katika Hadithi hio inarejea kwa Allah. Natija ya kauli hii ni kuwa Allah kamuumba Adam kwa sura yake (sura ya Allah), kwa hivyo Allah kafanana na Adam!

Mzee wa Uislamu, Ibn Taymiyya, anasema kuwa katika karne tatu za mwanzo hakukuwa na khilafu yoyote ile baina ya wajuzi kwamba dhamiri inarejea kwa Allah. Tunamuomba Mzee wa Uislamu Ibn Taymiyya atuthibitishie hilo, lakini kwa kuwa Mzee wa Uislamu, Ibn Taymiyya, hayupo tena basi tunamuachia chalenj hii Al-’Allama Kasim Mafuta atuthibitishie kwamba hakukuwa na khilafu katika karne tatu za mwanzo kwamba dhamiri inarudi kwa Allah kama alivyodai Ibn Taymiyya. Vyenginevyo, Sheikh Kasim bin Mafuta usiwache kumuweka Sheikh Al-Islam katika orodha yako ya wasiosema ukweli au ya waongo.

MANENO YASIO NA UKWELI YA IBN AL-QAYYIM

Anasema Ibn Al-Qayyim katika Ijtimaa’u Jayshihi:

ع ابن حديث من أحمد اإلمام مسند الله �������وفي رضي باسالشفاع �������عن قصة ،ة�����هما

على فأجده جل و عز ربي فآتي وفيه مرفوعا بطوله الحديثسريره أو جالسا كرسيه

Na katika Musnad cha Ahmad katika Hadithi ya Ibn Abbaas (r.a.) kuna kisa cha uombezi, Hadithi hio (iko) kwa ukamilifu wake kutoka kwa Mtume (s.a.w.), na ndani yake kuna (maneno haya): ‘Basi nitamjia Mola wangu Mtukufu nitamkuta juu ya kiti kakaa kitako’!1459

1457 - Abu Mu’adh uk. 416. 1458 - Al-Bukhari Al-Sahih Hadithi na. 3326. Muslim Al-Sahih Hadithi na. 2183. Ibn Ahmad Al-Sunna j. 2, uk. 470, riwaya na. 1068. 1459 - Ibn Al-Qayyim Ijtimaa’u Al-Juyuush uk. 56.

488

Page 489: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Anasema Al-Sayyid Al-Saqqaf:

Maneno kakaa kitako, Ibn Al-Qayyim kayaongeza kutoka mfukoni mwake wala hayamo katika Hadithi katika Musnad cha Ahmad.1460 Neno hili ni katika jumla ya ziada zake (Ibn Al-Qayyim) na ni utunzi wake katika Hadithi.1461

Baada ya hayo, hatuna budi kumuuliza Kasim Mafuta: je ni nani aliyetenda dhambi kubwa: ni yule uliyedhania kwamba ubeti wa Ibn Al-Qayyim kaupindua – ilhali maana ni moja: haikubadilika, na ubeti huo upo tangu enzi ya Ibn Al-Qayyim – au ni huyu aliyeongeza kitu katika Hadithi ya Mtume (s.a.w.). Tena kitu hicho kinaongeza maana inayoweza kujenga itikadi mbovu. Je Bwana Kasim mwana wa Mafuta, na Ibn Al-Qayyim naye ni mwongo? Au yeye utampa udhuru usiowapa wengine? Ninamwambia ndugu yetu Kasim mwana wa Mafuta kwamba mlango huu wa kutaka kuwajeruhi watu kuwa ni waongo nyinyi haukufaini: musiufungue kwani kutokusema kweli kwenu ni kwingi mno. Mlango huu utakudhuruni nyinyi wenyewe.

Tukiendelea na tadlis na udanganyifu wa Ibn Al-Qayyim – nakunukulia machache kwani haya ni mengi mno kwa Ibn Al-Qayyim unaweza kuunda kitabu – ni kule kuondoa kwake wapokezi dhaifu katika sanad ili sanad ionekane kuwa ni sahihi1462 na kuzisahihisha sanad zenye wapokezi dhaifu na wasiojulikana kisha akadai kwamba hakuna yoyote katika wanavyuoni wa Hadithi aliyemponda mpokezi yoyote wa sanad hio. Tumenukuu huko nyuma riwaya ya kutunga inayosema: “Basi akawa Mola wako anazunguka katika ardhi, na miji yote imemuinamia (yaani yuko peke yake: katika miji kutupu)”,1463 na kwamba Ibn Al-Qayyim kasema kuhusu Hadithi hii: ‘‘Hadithi hii ni kubwa, tukufu; unatangaza utukufu wake na ukuu wake na adhama yake kwamba inatokana na Mtume (s.a.w.)”.1464 Hayo ni baadhi ya maneno yake, na kwa ukamilifu anasema:

تناد جليل، كبير حديث خرج يهذا قد أنه على وعظمته وفخامته جاللتهالنبوة، مشكاة ……من

1460 - Ahmad Al-Musnad j. 1, uk. 282-296. 1461 - Al-Saqqaaf Al-Salafiyya Al-Wahabiyya uk. 40. 1462 - Nitakunukulia mfano huu katika juzuu ya nne ya kitabu hiki ambayo ni mahususi kwa suala la kuonekana au kutoonekana kwa Allah. 1463 - Ibn Ahmad Al-Sunna j. 2, uk. 486, riwaya na. 1120. Tanbihi. Riwaya hii kimakosa imetiwa nambari 11120, katika kitabu kilichohakikiwa na Dr. Muhammad Al-Qahtaani.1464 - Ibn Al-Qayyim Zaadu Al-Ma’aad j. 3, uk. 444.

489

Page 490: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

بالتسليم …. وقابلوه بالقبول، وه وتلق كتبهم، فى نة الس أهل أئمة ورواهأح يطعن ولم د�واالنقياد،

. رواته من أحد فى وال فيه، منهم

Hadithi hii ni kubwa, tukufu unatangaza utukufu wake na ukuu wake na adhama yake kwamba inatokana na Mtume (s.a.w)………wameipokea Maimamu wa Hadithi katika vitabu vyao na wakaikubali, na wakasalimu amri mbele ya (usahihi) wake na kuifuata; wala hakuna yoyote aliyeiponda wala aliyemponda yoyote katika wapokezi wake (Hadithi hio).1465

Hivyo, ndivyo alivyosema Ibn Al-Qayyim. Pamoja na hayo, watiaji maelezo wa kitabu chake hicho, Dr. ‘Umar Al-Farmaawi, Muhammad Al-Bayyumi na ‘Abdullah Al-Minshaawi, wanasema kwamba ni Hadithi: “Dhaifu…. katika sanad yake Dalham bin Al-As-wad na babu yake ‘Abdullahi bin Haajib, kasema Al-Dhahabi kwamba hawajulikani”.1466 Na akasema aliyetia maelezo Kitabu Sunna cha Ibn Ahmad kuhusu Hadithi hio kwamba ni “Dhaifu”.1467

Baada ya hayo, utaona kwa uwazi kwamba Ibn Al-Qayyim – na kabla yake Imamu wake Ibn Manda – kadai kitu kisicho na ukweli kwamba wapokezi wa riwaya hio wote wamekubalika. Ninasema: hii ni kawaida ya Ibn Al-Qayyim katika Hadithi nyingi za kumshabihisha Allah na viumbe utasikia anasema: ‘‘Hadithi hii ni kubwa, tukufu, unatangaza utukufu wake na ukuu wake na adhama yake kwamba inatokana na Mtume (s.a.w.)”, japo kuwa katika sanad ya Hadithi hio kuna wapokezi dhaifu au kuna mutun (texts au maneno) zilizo munkar! Mfano mmoja ni kama ile Hadithi ya uwongo ya kumuona Allah inayosema:

..Katusimulia Muhammad bin Nadhri Al-Azdi na Abdu-llah bin Ahmad bin Hanbal na Al-Hadhrami wamesema ametusimulia Ismail bin Ubaid bin Abi Karima Al-Harraani ametusimulia Muhammad bin Salama Al-Harraani kutoka kwa Abi Abdi-Rahim kutoka kwa Zaid bin Unaisa kutoka kwa Al-Minhal bin Amri kutoka kwa Abi Ubaida bin Abi Abdillah kutoka kwa Masruq bin Al-Ajda'a ametusimulia Abdullahi bin Mas'ud kutoka kwa Mtume (s.a.w.) kasema: ' Mwenyezi Mungu atawakusanya wa mwanzo na wamwisho katika siku maalum iliowekwa hali ya kuwa wamesimama kwa muda wa miaka arubaini wamekodoa macho yao mbinguni wanasubiri upambanuzi wa hukumu. Akasema (Mtume (s.a.w.) ) 'na atateremka Mwenyezi Mungu katika vivuli vya mawingu kutoka katika Arshi mpaka

1465 - Ibn Al-Qayyim Zaadu Al-Ma’aad j. 3, uk. 444. 1466 - Tazama maelezo hayo katika Zaadu Al-Ma’aad j. 3, uk. 444, maelezo ya chini. 1467 - Dr. Muhammad Al-Qahtaani katika maelezo yake ya Al-Sunna cha Ibn Ahmad j. 2, uk. 485.

490

Page 491: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

juu ya kiti!!! Kisha atanadi mwenye kunadi: ‘enyi watu hamjaridhika na Mola wenu ambaye kakuumbeni na akakuruzukuni na akakuamrisheni mumuabudu Yeye tu na wala musimshirikishe na kitu (leo) akawafanya kila watu kuwa wamfuate yule waliyemfanya kuwa ni kipenzi chao na kumuabudu duniani?’ Watasema "tumeridhika." Basi kila kaumu itaondoka na kukifuata kile walichokuwa wakikiabudu na kukipenda duniani-----basi waliokuwa wakimuabudu (Nabii) Issa watafanyiwa shetani mfano wa (Nabii) Issa na waliokuwa wakimuabude Uzair watafanyiwa shetani mfano wa Uzair. Na atabakia Muhammad na umma wake, atawajia Mola wao Mtukufu atasema: 'mna nini nyinyi mbona hamuondoki kama walivyoondoka watu (wengine)? Basi watasema hakika ya sisi tuna Mola wetu hatujamuona bado!!! Atasema (Mwenyezi Mungu) je mukimuona munamjua? Watasema: 'hakika baina yetu na baina yake kuna alama tukiona tutamjua!!! Atasema ni nini hio? Watasema (alama yake ni kuwa) atafunua MUUNDI (WA MGUU) WAKE!!! Basi hapo atafunua MUUNDI (WA MGUU) na wao wataanguka chini na kusujudu!!!

Riwaya hii ni refu sana, na inaendelea baada ya haya kwa kutaja habari za mtu aliyeokolewa na moto ikasema Hadithi:

Na ataona au itainuliwa nyumba mbele ya hapo---atasema é Mola wangu nipe mimi nyumba ile. Atamwambia labda nikikupa hutoomba tena. Atasema naapa kwa utukufu wako sitokuomba tena kitu chengine. Na nini kilichokuwa kizuri zaidi yake? Basi atapewa na atakaa hapo.

Kisha mtu huyu ataendelea kuomba huku anapewa na hali anavunja viapo alivyoapa na ahadi aliyompa Mwenyezi Mungu. Hadithi ni refu sana; nanukuu vipande vipande tu. Hadithi inaendelea kutoa habari za mtu huyu kwa kusema:

Kisha atanyamaza (kuomba). Basi Mwenyezi Mungu atasema 'una nini mbona huombi tena? Atasema é Mola wangu nimekuomba mpaka ninakuonea haya na nimekuapia mpaka ninakuonea haya . Atasema Mwenyezi Mungu 'je huridhiki wewe nikakupa mfano wa dunia tangu siku niliyoiyumba hadi siku niliyoiyangamiza na zaidi yake mara kumi? Atasema (yule mtu kumwambia Mwenyezi Mungu) UNANIFANYIA MZAHA na Wewe ni mola wa ulimwengu!!!!!!!!! Basi Mwenyezi Mungu ATACHEKA kutokana na maneno yake hayo!!! Atasema Mola Mtukufu omba (unachotaka). Atamwambia nikutanishe na watu (huko peponi), atasema (Mwenyezi Mungu) nenda ukakakutane na watu. Basi ataondoka na huku anakimbilia katika pepo mpaka akiwakaribia watu basi atanyanyuliwa Qasr (jumba kubwa) la lulu. Basi hapo ataanguka na kusujudu. Atasema nyanyuwa kichwa chako una nini wewe? Atasema nimemuona Mola wangu au kajionesha kwangu Mola wangu!!!!!!!! Basi ataambiwa hii ni nyumba tu katika nyumba zako!!! Akasema (Mtume

491

Page 492: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

(s.a.w.) ) 'basi kisha atamuona humo mtu basi atajitayarisha kusujudu, atamwambia suburi una nini wewe? Atamwambia niliona kuwa wewe ni malaika miongoni mwa malaika. Atamwambia mimi ni mlinzi (mtumishi) katika walinzi (watumishi) wako (wa peponi).!!!! Anasema Ibn Al-Qayyim: “ حسن كبير حديث 1468.(Hii ni Hadithi kubwa nzuri) ”هذا

Hayo ndio maneno yake! Jamani ivo kweli Hadithi hii ni sahihi licha ya kuwa ni kuu na njema? Hayo ni kwa mujibu wa mutun zake. Ama sanad yake tumeilezea katika kitabu chetu Hoja Zenye Nguvu kama ifuatavyo. Tumesema:

Baada ya kuona mgongano uliomo katika matn ya Hadithi hii sasa hebu natuitazame sanad yake ili izidi kutubainikia. Hadithi hii imepokewa kutoka kwa Al-Minhal bin Amri naye hakuwa madhubuti. 1469 Pia yumo katika sanad hii Abu Ubaida bin Abdillah naye ni mwenye kughushi. 1470 Pia kuna sanad ya pili ya Hadithi hii 1471 , lakini anayeisimulia Hadithi hio kutoka kwa Ibn Mas'ud ni Abu Ubaida bin Abdillah yule yule aliye katika sanad iliotangulia. Na katika sanad ya tatu ya Hadithi hii 1472 kuna Al-Minhal bin Amri na Abu Ubaida bin Abdillah, ambao wamo katika sanad ya kwanza. Pia yumo katika sanad hii ya tatu Abdul-Salam bin Harb, naye ni mwenye udhaifu: anasimulia Hadithi munkar. 1473 Katika sanad ya nne ya Hadithi hii1474 kuna Al-Minhal bin Amri na Abu Ubaida bin Abdillah

1468 - Ibn Al-Qayyim Hadi Al-Arwaah uk. 224-26. Mifano ya maneno haya katika kuzisifu Hadithi dhaifu iko mingi katika maandiko ya Ibn Al-Qayyim. Tutainukuu mingine katika sehemu nyengine za kitabu hiki in shaa Allah. 1469 - Anasema Abdalla bin Ahmad: "nimemsikia baba yangu akisema kuwa " Shuuba kamuwacha Al-Minhal (kaziwacha Hadithi zake) kwa kukusudia (si kwa bahati mbaya tu)." Na anasema Wahb bin Jarir kutoka kwa Shuuba akisema kuwa "nilikwenda nyumbani kwa Al-Minhal nikasikia sauti ya gita (la muziki)." Na hivyo hivyo akasema Ibn Al-madiniy. Na akasema Al-ghalabi kuwa "Ibn main alikuwa akimuangusha (akimponda) Al-Minhal (akimuona kwamba hafai)." Na akasema Al-jawzjani kuwa "mwenendo wake ni mbaya ." Na akasema Al-mughira "hustaajabu wewe na huyu Al-a’amash mjinga, mimi nimemkataza asipokee Hadithi kutoka kwa Al-Minhal bin ‘Amri na ‘Abaaya tukaafikiana kwamba hatopokea kisha anapokea kutoka kwao. Nakuuliza kwa jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu: je inafaa shahada ya Al-Minhal juu ya dirham mbili? Akasema: "é Mwenyezi Mungu haifai." Na akasema Al-Hakim kuwa " Yahya bin Al-qatan kamtia kasoro Al-Minhal bin ‘Amri." Na akasema Abu Al-hasan bin Al-qatan kuwa "Abu Muhammad bin Hazm alikuwa akimdhoofisha (akisema kuwa ni dhaifu) Al-Minhal." Tazama Tahdhibu Al-Tahdhib j. 10 uk. 283. 1470 - Tazama Ibn Hajar, Tabakat Al-Mudalisin uk. 48. 1471 - Ibn Al-Qayyim Hadi Al-Arwaah uk. 227. 1472 - Ibn Al-Qayyim Hadi Al-Arwaah uk. 227. 1473 - Anasema Ibn Sa’ad "Alikuwa na udhaifu katika Hadithi”. Tahadhib j. 6 uk. 282. Na

anasema Ibn Hajar katika Taqrib uk. 355 tarjama no. 3067: "Ana Hadithi (nyingi) Munkar."

1474 - Ibn Al-Qayyim Hadi Al-Arwaah uk. 227.

492

Page 493: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

ambao wamo katika sanad ya kwanza. Sanad ya tano 1475 ina Abu Ubaida bin Abdillah.1476

Ni wazi kwamba Ibn Al-Qayyim, Imamu wa Mawahabi, haujui ukweli ulivyokaa! Maelezo mengine yasio na ukweli ya Ibn Al-Qayyim ni madai yake – sawa na Imamu wake, ‘Uthman Al-Darimi – kwamba:

Waislamu kuanzia Masahaba na wafuasi wao wamekubaliana kwamba Allah yuko juu ya Arshi yake (yaani kaka huko kwa dhati yake), juu ya mbingu zake hali ya kuwa yuko mbali na viumbe wake!1477

Na dhahir ni kuwa haya ni maneno ya Ibn Batta, lakini na Ibn Al-Qayyim naye ndio anayatolea hoja. Kwa hali yoyote ile, tunauliza makubaliano haya yako wapi? Na kweli inajuzu mtu kuwafunza watu dini yao kwa kutegemea masimulizi ya mtu kama Ibn Batta ambaye wanavyuoni wa wapokezi wameshuhudia kwamba ni mwongo na ni mtunzi wa riwaya na sanad? Huku ni kuufanyi ghushi umma huu!

MANENO YASIO NA UKWELI YA IBN ‘UTHAIMIN

Alipokuwa akiisherehesha Hadithi isemayo: أو بالكفر رجال دعا منالله : عدو :Atayemwita mtu (Muislamu) kafiri au kumwambia“ .....قال

(wewe ni) adui wa Allah”, Sheikh Ibn ‘Uthaimin alisema yafuatayo:

…Na mas-ala ya kukafirisha ni mas-ala ya hatari sana, kwa sababu yake milango mikubwa ya shari ilifunguliwa dhidi ya Umma wa Kiislamu. Kwa hakika wa mwanzo aliyejifanyia madhehebu haya machafu nayo ni kuwakafirisha Waislamu ni Al-Khawarij. Al-Khawarij ambao Mtume (s.a.w.) aliwatabiri kwamba: “Wanatoka katika Uislamu kama mshare unavyotoka katika kiwindwa; na kwamba wanasoma Qur-ani lakini haivuuki koo zao, na kwamba watakuwa wanasali, wanatoa sadaka na wanasoma Qur-ani”. Mpaka akasema (Mtume s.a.w.) kwamba Masahaba watakuwa wanazidharau sala zao mbele ya sala za watu hawa (mbele ya sala za Makhawaarij), lakini wao – Allah atulinde – waliwakafirisha

1475 - Ibn Al-Qayyim Hadi Al-Arwaah uk. 227. 1476 - Na kwa ujumla sanad zote tano njia yake ni moja, nayo ni njia ya Abu Ubaida bin Abdillah.1477 - Ibn Al-Qayyim Mukhtasaru Al-Sawaaiq uk. 361.

493

Page 494: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Waislamu na wakahalalisha damu yao na mali zao na wanawake wao. Allah atuafu! Na hukumu hii hadi leo bado ipo, kwani kuna kikundi kipotovu cha bidaa kichafu kinawakafirisha kwa matamanio yao wale ambao Allah na Mtume wake hawakuwakafirisha, huyu ni kafiri, huyu ni mtu wa bidaa; huyu ni fasiki na yalio mfano wa hayo. Na nini hasa kiliwatokea hawa Khawaarij? Kilichowatokea ni kuwa walikuwa pamoja na ‘Ali bin Abi Talib (r.a.), naye ni Khalifa Muongofu wa nne miongoni mwa Makhalifa Waongofu; walikuwa pamoja naye katika kuwapiga watu wa Sham, na wakakubaliana juu ya hilo na vikatokea vita vikali na umwagikaji mkubwa wa damu. Kisha Ali akakubaliana na watu Sham na akaafikiana nao ili kuzuia umwagikaji wa damu za Waislamu. Makhawaarij wakasema kumwambia ‘Ali wewe ni kafiri, kwanini anafanyiana nao sulhu? Umekufuru kama walivyokufuru wao. Basi wakatoka dhidi yake na wakampiga vita lakini Al-Hamdu Lillahi hatima (njema) ikawa ni yake; aliwaua kama walivyouliwa ‘Aad na Iram. Aliwamaliza wote, lakini hajaacha kati yao: bado madhehebu hii chafu ipo miongoni mwa Waislamu. Wanahalalisha damu ya Waislamu na huku wanaiheshimu; na (wanahalalisha) mali zao na huku wanaziheshimu; na (wanahalalisha kuwateka nyara) wanawake wao pamoja na kuzitukuza heshima, wanasema kwa mfano: atayezini ni kafiri; atayeiba ni kafiri; atayekunywa pombe ni kafiri: kila dhambi kubwa kwao ni ukafiri – Allah atulinde – wenye kumtoa mtu katika mila (ya Uislamu). Basi hawa ambao wanawakafirisha Waislamu bila ya shaka wao ndio makafiri……1478

Hayo ndio maneno ya Sheikh Ibn ‘Uthaimin, nayo, kama unavyoona, ni maneno ambayo yako mbali mno na tahqiq za kielimu. Nitayajadili maneno hayo katika juzuu maalumu itayozungumzia suala la Khawaarij in shaa Allah. Lakini kwa hapa ninataka nizungumzie nukta moja, nayo ni kuwa Sheikh Ibn ‘Uthaimin baada ya kuzungumzia suala la ukafirishaji wa walioitwa kuwa ni Khawaarij, alisema kwamba kikundi chenye hukumu hizo hadi leo bado kipo, kisha akasema je unajua habari za Khawaarij? Kisha akataja habari za ‘Ali (k.w.) na watu wa Nahrawaan. Kwa hivyo, ni wazi kwamba anakusudia kwamba wenye kuwakafirisha watu ni:

1) Watu wa Nahrawaan.2) Maibadhi.

Hili ndilo lililowazi katika maelezo hayo, kwani madhehebu yenye kukubaliana na watu wa Nahrwaan ni madhehebu ya Kiibadhi tu, katika madhehebu zilizopo leo duniani, kwa hivyo maelezo hayo yanawafaa wao na Watu wa Nahrawaan tu. Sasa kama umelielewa hilo, basi utaanza kuona jinsi Sheikh huyu alivyokuwa mzushi kupita kiasi! Tazama alivyozua:

1478 - Ibn ‘Uthaimin Sharhu Riyaadhu Al-Salihin j. 4, uk. 308-309, katika sherehe ya Hadithi na. 1732-1733.

494

Page 495: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

….Wanahalalisha damu ya Waislamu na huku wanaiheshimu; na (wanahalalisha) mali zao na huku wanaziheshimu; na (wanahalalisha kuwateka nyara) wanawake wao pamoja na kuzitukuza heshima, wanasema kwa mfano: atayezini ni kafiri; atayeiba ni kafiri; atayekunywa pombe ni kafiri: kila dhambi kubwa kwao ni ukafiri – Allah atulinde – wenye kumtoa mtu katika mila (ya Uislamu). Basi hawa ambao wanawakafirisha Waislamu bila ya shaka wao ndio makafiri.

Suali: ni nani hao waliobakia hadi leo wenye siasa ya Watu wa Nahrawaan ambao wana itikadi hizo alizozitaja Ibn ‘Uthaimin? Katika hali zote na kwa makadirio yoyote yale Sheikh huyu hapa hakusema kweli. Akiwa anakusudia Maibadhi – nao ndio anaokusudia – basi Ibadhi hawana itikadi hizo na hivi vitabu vya Kiibadhi natuoneshwe kwamba wenye kufanya maasi hayo ni makafiri waliotoka katika mila ya Uislamu! Akiwa anakusudia watu wengine natuelezwe ni nani hao waliopo mpaka leo wenye kukubaliana na watu wa Nahrawaan na ambao wana itikadi hizo. Utaona kwamba kwa makadirio yoyote Sheikh Ibn ‘Uthaimin hakutongoa kweli – na hii ndio sera na dini ya Mawahabi na Maimamu wao wote – kuwazulia watu uwongo!

Cha kustaajabisha ni kuwa, haya alioyataja hapa yote ndio yalio katika vitabu vya Kiwahabi na Maimamu wao watangulizi. Wala hakuna duniani zamani na leo watu ambao wamekuwa na tabiya ya kuwakafirisha watu kama Mawahabi na Maimamu wao watangulizi. Maneno kama: “Watu wa bidaa; mafasiki; makafiri;1479 asiyeamini kadha ni kafiri; anayeamini kadha ni kafiri; ni adui wa Allah”,1480 kwa mfano “Atayesema Allah haonekani ni

1479 - Kama ulivyoona maneno ya Sulaiman bin Sihmaan – ambayo baadhi yake tutayanukuu tena hapo mbele – jinsi alivyowakafirisha Waislamu wote isipokuwa watu wa madhehebu yake. Na kama ulivyoona maneno ya Al-Jibrin jinsi alivyowakafirisha Maibadhi. 1480 - Al-Albani – kwa mfano – anawaita Al-Ashaa’ira, nao ni Masuni kama Shafi, Maliki na wengine, kuwa ni maadui wa Sunna. Na kwa maana hio ni maadui wa Mtume (s.a.w.), na kwa hivyo ni maadui wa Allah! Anasema Al-Albani:

أنا ما األمة " " فإن يدي بين السنة تقريب العظيم بالمشروع االشتغال من فيهيشغلني مجالت الذي و كتب و رسائل في تنشر ردود األحيان من كثير في عنه

السنة أعداء بعض وغيرهم من والمتصوفة واألشاعرة المتمذهبة من

Hakika ya kile ambacho mimi nimo ndani yake cha kuishughulikia kazi (project) kuu (nitayoiita kwa jina la) “Kuikurubisha Sunna mbele ya Umma”, ambayo mara nyingi hunishughulisha kutokana na kazi hio majibizano yenye kuenezwa katika baadhi ya risala na vitabu na magazeti kutoka kwa baadhi ya maadui wa Sunna miongoni mwa watu wa madhehebu na Al-Ashaa’ira (Masunni wasiokuwa Mawahabi) na Masufi na wengineo. Tazama Al-Sahiha j. 6, uk. 676, maelezo ya Hadithi na. 2786. Tazama pia maneno ya Seif Al-Ghafri alivyomwita mmoja wa wanavyuoni wa Kiislamu kuwa ni “adui

495

Page 496: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kafiri; atayesema Qur-ani ni kiumbe huyo ni kafiri; atayetawassal katika dua huyo ni kafiri” na mengineo ni lugha za kawaida katika vitabu vyao kama tulivyonukuu baadhi yake na kama tutavyozidi kunukuu in shaa Allah katika juzuu nyengine.

Bali yeye mwenyewe Ibn ‘Uthaimin kawakafirisha wanaoacha kusali hadi akafika kusema kwamba Yahudi na Nasara ni bora kuliko asiyesali! 1481 Na akasema kwamba:

Akifa naye hasali basi hakoshwi wala havishwi sanda wala hasaliwi wala hazikwi pamoja na Waislamu wala haombewi dua ya kutakiwa arehemewe….lakini tumfanyeje? Je kiwiliwili chake tuwaachie mbwa wakile nasi tunashuhudia? “Sio”: kwa sababu kufanya hivyo ni kuiharibu mioyo ya jamaa zake……na lau si jamaa zake basi tungelisema kuwa (kiwiliwili chake) kiachwe juu ya ardhi mbwa wakile – na watu wanakitazama – lakini kinatupwa (kwenye shimo la kaburi) kwa ajili ya kulinda uoza wake na harufu yake na uchafu wake!

Hio ndio kauli ya Sheikh Ibn ‘Uthaimin na pia hio ndio fat-wa ya Ibn Baz.1482 Wakati hii ni kauli ya wachache: jumhur ya wanavyuoni wa madhehebu zote wanasema kwamba mwenye kuacha sala akiwa kaiwacha kwa kupinga uwajibu wake akasema kwamba sala si wajibu, basi huyo ndio kafiri aliyetoka katika mila ya Uislamu; na akiwa anakubali kwamba sala ni wajibu lakini akawa hasali, basi huyo ni kafir neema au wengine husema kufr duna kufr (ukafiri uliochini ya ukafiri mkubwa wenye kumtoa mtu katika mila), yaani huyo ni fasiki tu: si kafiri mshirikina. Bali fat-wa hio ya Ibn ‘Uthaimin wengine wanaitazama kuwa ni itikadi ya Kikhawaarij safi ya kuwakafirisha watu kwa sababu ya madhambi, halafu yeye anageuka na kuwaita watu Makhawaarij na kuwalaumu kwamba wanawakafirisha watu, kisha naye akawakafirisha!

Kwa kuhitimisha ninasema:1) Alichokisema Ibn ‘Uthaimin kuhusu watu wa Nahrawaan, ni makosa

matupu ya kihistoria. Hili tutalizungumzia katika juzuu yake in shaa Allah.1483

wa Allah” kwa sababu tu yeye ni Mu’utazili: yuko tafauti na yeye kimadhehebu! 1481 - Ibn ‘Uthaimin Sharhu Riyaadhu Al-Salihin j. 3, uk. 280, katika sherehe ya Hadithi na. 1077. Lakini Al-Albani hakukubaliana na kauli hii. Tazama Al-Dhaifa j. 1, uk. 212-213, maelezo ya Hadithi na. 94.1482 - K.h.j. uk. 281. 1483 - Na kwa ufafanuzi zaidi rejea katika kitabu chetu Khawarij Baina ya Ukweli Na Visa Vya Kutunga kitachokuwa katika juzuu tatu au nne. Kwa sasa hivi imetoka juzuu ya kwanza.

496

Page 497: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

2) Alichokisema kuhusu Ibadhi kwamba wanawakafirisha watu ukafiri unaowatoa katika mila kwa sababu ya maasi, ni maneno yasio na ukweli. Na hili pia tutalizungumzia katika sehemu yake in shaa Allah ili watu wajue nini hasa Ibadhi wanachokisema na wana dalili gani.

3) Akiwa hakukusudia Ibadhi – kama mtu anavyoweza kudai – basi natutajiwe hao watu waliobakia hadi leo ambao wanafuata siasa ya Watu wa Nahrawaan, na ambao wanawakafirisha watu ukafiri wa aina hio kwa sababu ya kufanya kwao madhambi makubwa.

4) Utaona kwamba kwa makadirio yoyote yale, basi maneno yake hapa hayana ukweli, bali ni uzushi mtupu kama kawaida yao na hio ndio dini ya Kiwahabi. Wa Allahu Al-Musta’aan!

SULAIMAN BIN SIHMAAN AWAZULIA WAISLAMU

Tumenukuu huko nyuma maneno ya uwongo ya Sheikh huyu aliposema kuhusu Maibadhi:

سبرت إذا وطريقتهم مذهبهم فحقيقة الزمان هذا أهل أباضية أماقبوري جهمية فهم ون������أحوالهم

إال وضاللهم كفرهم في يشك فال انتسابا األباضية إلى ينتسبون وإنماعل غلب اله ������من وى�����يه

ومباعدته هجره يجب ظالم عاص فهو توالهم فمن بصيرته عين وأعمىيعل حتى منه ن �والتحذير

والمعصية بالظلم أعلن كما بالتوبة

Ama Maibadhi wa zama hizi, uhakika wa madhehebu yao na njia yao ukiwa utazipima hali zao basi wao ni Jahmiyya wenye kuabudu makaburi. Lakini wao wananasibika na Maibadhi (wa kale kama ni) kunasibika (tu), mtu yoyote yule hatii shaka yoyote kuhusu ukafiri wao na upotovu wao, isipokuwa yule ambaye matamanio ya nafsi yake yamemzidi na yakamtia upofu katika jicho lake uoni wa moyo, basi atayewapenda (Maibadhi) huyo ni asi dhalimu ni wajibu kumuhama na kujitenga naye na kuwahadharisha watu dhidi yake mpaka atapotangaza toba kama alivyotangaza dhulma na maasi. 1484

Na akasema kuhusu wasiokuwa Ibadhi:

1484 - Sulaiman bin Sihmaan Kashfu Al-Awhaami Wa Al-Iltibaas uk. 156. Publisher: Daru Al-‘Aasima Al-Riyyadh Saudia, chapa ya kwanza 1415 A.H.

497

Page 498: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

رح أحمد مذهب من فالمشهور الجهمية السنة �أما أئمة وعامة الله مهق رهم�����تكفي هم��������لوألن

وحق الكتب به وأنزلت الرسل به جاءت ما مناقضة في يقة����������صريحالص جحود انع�������قولهم

الله عبد اإلمام قال ولهذا الرسل وجميع بل نفسه عن به أخبر ما وجحودلنح إنا المبارك كي ���بن

كفروا وبهذا الجهمية كالم نحكي أن نستطيع وال والنصارى اليهود كالمالقرآن يقول وق �مخل من

على ليس الله وأن اآلخرة في يرى ال الله علم وأن له ليس وأنه العرشرح وال قدرة وال مة ���� وال

ابن مثل السلف من كثير عند وهم صفاته من ذلك غير وال غضبأسب بن ويوسف اط����المبارك

فرقة وسبعين الثالث من ليسوا أحمد أصحاب من وطائفة

Ama Jahmiyya, kilicho mashuhuri katika madhehebu ya (Al-Imamu) Ahmad (bin Hanbal) – Allah amrehemu – na Maimamu wote wa Ahlu Sunna, ni kuwakafirisha kwani kauli yao iko wazi katika kuyapinga yale waliokujanayo Mitume na vitabu (vya Allah) vikateremka nayo. Na uhakika wa kauli yao ni kumpinga Allah Mwenye kuumba na kuyakanusha yale ambayo Yeye (Allah) kayazungumzia kuhusu nafsi yake1485 bali (na yakaelezwa pia na) Mitume wote. Na kwa hivyo, Al-Imamu ‘Abdullahi bin Mubarak kasema: ‘Hakika ya sisi tunasimulia kauli za Mayahudi na Makiristo lakini hatuwezi kusimulia maneno ya Jahmiyya’. Na kwa sababu hii, basi (wanavyuoni hao) wamewakafirisha wale wenye kusema kwamba Qur-ani ni kiumbe na kwamba Allah haonekani huko akhera na kwamba Allah hayuko (hakukaa kitako) juu ya Kiti chake cha enzi (‘Arshi), na kwamba Yeye hana elimu wala uwezo wala rehema wala ghadhabu wala mengineo katika sifa zake. Na hao – kwa mujibu wa Al-Salaf wengi kama Ibn Al-Mubarak na Yusuf bin Asbaat na kundi (kubwa) la wanavyuoni wafuasi wa (Al-Imamu) Ahmad – sio katika jumla ya yale makundi sabiini na tatu (ya Umma huu: wao wametoka katika Umma).

Hayo ndio maneno ya Sheikh huyo nayo si maneno yenye ukweli hata chembe! Ni Muislamu gani au ni madhehebu gani – Ash’ariyya, Shia, Ibadhi, Zaidia, Mu’utazila, Jahmiyya – yenye kusema kwamba Allah hana elimu wala uwezo! Na ni Maibadhi gani wanaoabudu makaburi. Sheikh Mafuta ulikuwa unazungumzia uwongo mweupe kama jua la mchana, basi ndio huu!

1485 - Anakusudia kukanusha kwamba Mungu ana viungo! Kukanusha haya ndio ukafiri wenyewe! Wallahu Al-Musta’aan!

498

Page 499: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

SHEIKH ABDULLAHI BIN ABDIL-RAHMAAN AL-JIBRIN AWAZULIA MAIBADHI

Huyu tumeyanukuu maneno yake aliowazulia Maibadhi na kufyatua kwake kusiko na mpango, na tumeyaelezea hayo kwa urefu katika sura ya tisa. Rejea huko utazame hatuna haja ya kukariri.

DR. ‘ALI AL-FAQIHI AMZULIA SHEIKH AL-KHALILI

Ama Dr. ‘Ali Al-Faqihi yeye kaandika kitabu chake alichokiita Al-Raddu Al-Qawiim eti anajibu kitabu Al-Haqqu Al-Daamigh cha Al-Imamu Badru Al-Din Al-Khalili! Lakini, kwa kupitia katika maandiko yake hayo, Al-Faqihi huyu kaonekana kuwa ni mtu ambaye hamuogopi Mola wake wala hawaonei haya walimwengu! Na, bila shaka, yule ambaye hamuonei haya Allah hawezi kuwaonea haya viumbe. Mbali na kukichafua kitabu chake hicho alichokiita Al-Raddu Al-Qawiim nacho ni Al-Mardudu Al-Mu’wajju kwa matusi ya kila aina, kama ilivyo kawaida ya watu wa madhehebu yake ambao hawajui kujadili kitu ila kwa njia ya matusi mabaya, Dr. Al-Faqihi kamzulia Sheikh Al-Khalili humo mambo mengi ambayo hakuyasema. Soma mifano miwili mitatu. Anasema Al-Faqihi:

:» إن » العدل المسمى الخمسة أصولهم أحد في المعتزلة قال حيث

أفعال يخلق ه��������العبدعقائدهم، في إليه يذهبون ما جميع في بقولهم يقول والخليلي

العباد بخلق القول ذلك ومن أفعالهم

……….Ambapo Mu’utazila wamesema katika mmoja wa misingi yao mitano unaoitwa Al-‘Adlu (usawa) kwamba mja anaumba vitendo vyake…

Na Al-Khalili anakubaliana nao (Mu’atazila) katika madhehebu yao yote ya itikadi na miongoni mwa hizo ni (itikadi hio) ya kuwa waja wanaumba vitendo vyao……1486

Tazameni enyi walimwengu huu uzushi ambao hauna kifuniko kutoka katika kitabu kilichopitiwa na kuhimidiwa na Dr. Al-Fawzaan mmoja wa

1486 - ‘Ali Al-Faqihi Al-Raddu Al-Qawiim uk. 149.

499

Page 500: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

wanavyuoni wakuu wa Suudia! Wapi kapata Al-Faqihi kwamba Sheikh Al-Khalili anasema au Maibadhi wanasema kwamba mja anaumba vitendo vyake?

Suala hili Sheikh Al-Khalili kalizungumzia kwa urefu katika vitabu vyake tafauti kama vile tafsiri yake Jawaahiru Al-Tafsiir na Sharhu Ghaayati Al-Muraad na hata katika hicho kitabu Al-Haqqu Al-Daamigh, ambacho Al-Faqihi anajidai kukirudi, ilhali hata lugha ya Kiarabu maskini haijui bado anasahihishwa nahau na Al-Fawzaan, Sheikh Al-Khalili kaligusia suala hilo. Tazama baadhi ya vipande vipande vya maelezo ya Sheikh Al-Khalili kuhusu suala hilo. Anasema:

سبحانه فهو وإرادته، الله بقدرة صلة لها لربه العبد معصية أن تعلم وبهذاتتجه عندما لها الخالق

....... اكتسابها إلى العبد إرادة

Na kwa haya utajua kwamba (kitendo cha) mja cha kumuasi Mola wake kina uhusiano na uwezo wa Allah na matakwa yake, KWANI YEYE ALLAH NDIYE ALIYEYAUMBA (HAYO MAASI) WAKATI MATAKWA YA MJA YANAPOELEKEA KUTAKA KUYAFANYA….1487

Anaendelea:

... ............ نفوا الذين المعتزلة الطائفة هذه ويمثل طائفتان فيها ضلت وقدوإرادته الله ق���درة تعلق

..... أفعاله بخلق تاما استقالال يستقل العبد أن وزعموا العباد، بأفعال

Na makundi mawili yamepotea (katika suala hili)….(kundi moja) linawakilishwa na Mu’utazila…ambao wamekataa kuwepo kwa mafungamano baina ya uwezo wa Allah na matakwa yeke pamoja na matendo ya mja, na wakadai kwamba mja ana uhuru kamili wa kuumba vitendo vyake…..1488

Anaendelea:

فاعتقدوه البصائر أهل إليه الله هدى الذي الفصل والقولاللتان........... وهما وإرادته الله قدرة دينا

...... الفعل له وتخلقان للعبد الكسب أسباب تهيئان

Na kauli pambanuzi (kauli ya haki) ambayo Allah kawaongoza wenye mitazamo sahihi wakaiitakidi kuwa ndio dini….(ni kauli kwamba) uwezo

1487 -Al-Imamu Badru Al-Din Al-Khalili Jawaahiru Al-Tafsiir j. 2, uk. 205. 1488 - K.h.j.

500

Page 501: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

wa Allah na matakwa yake ndio yenye kumuandalia mja (kule) kuyachuma (matendo yake) na ndio yenye kumuumbia matendo….1489

Sasa baada ya hayo, tazameni aliyoyasema Sheikh Al-Khalili katika hicho hicho kitabu Al-Haqqu Al-Daamigh ambacho Al-Faqihi anajidai kuwa anakijibu. Sheikh kasema hivi:

: أمران لكالمه العبد وإحداث لكالمه الله إحداث بين والفارق

ال: العبد إن حيث من العباد وأفعال الله أفعال بين به يفرق ما أولهمااست����قالال فعله بإيجاد يستقل

... تاما، له الخالق هو والله الكسب جانب منه وإنما

Na tafauti baina ya Allah kuyaleta maneno yake na mja kuyaleta maneno yake ni mambo mawili:

Moja lao: ni kile ambacho kwacho hutafautishwa baina ya vitendo vya Allah na vitendo vya mja ambapo mja hana uhuru kamili wa kuyaleta matendo yake, bali chake yeye ni kuyachuma tu (hayo matendo) na anayeyaumba hayo (matendo) ni Yeye Allah…1490

Haya yamo kwenye kitabu ambacho kwa hakika kabisa Al-Faqihi kakisoma, kisha akazua mambo tafauti kabisa. Je huyu ndiye mkweli na ndiye anayetafuta haki na kuwafikishia watu ukweli? Ni wazi kabisa kwamba Dr. Al-Faqihi ni mzushi wa kukusudia dhidi ya Ahlu Al-Haqqi Wa Al-Istiqaama (Ibadhi).

Kwa nyongeza zaidi juu ya suala hili, rejea katika qasida ya Al-Imamu Nuru Al-Din Al-Salimi (r.a.) iitwayo Ghaayatu Al-Muraad ambapo utakuta beti hizi:

قدره الرحمن وبما حلال **وبالقضا أفعالنا خالق وأنهلنا منه كان بجبر ال جعال **لكنه ما كل في سابق وعلمه

ومكتسب مخلوق الفعل فعال **وإنما لمن والكسب لله فالخلق

Qasida hii natarajia imo katika kitabu chake maalumu, lakini pia imo katika kitabu Talqiinu Al-Sibyaan na pia kaifanyia sherehe Sheikh Al-Khalili. Maana ya beti hizo ni:

1489 - K.h.j., uk. 206. 1490 - Al-Imamu Badru Al-Din Al-Khalili Al-Haqqu Al-Daamigh uk. 111, au uk. 121 kwa chapa ya ya pili ya Darul Hikma London 2008.

501

Page 502: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

1) Na kwa qadhaa na kwa qadari ya Allah**NA KWAMBA YEYE KAYAUMBA MATENDO YETU YOTE.2) Lakini si kwamba katulazimisha**Naye kajua kwa elimu yake ya enzeli kila kitachokuwa.3) BASI MATENDO NI YENYE KUUMBWA na kuchumwa**Na Allah ndiye mwenye kuumba (matendo) na ayatendae huwa kayachuma.

Sheikh Al-Khalili kazisherehesha beti hizo na kutoa maelezo sawa na hayo tulioyanukuu.1491 Je baada ya hayo, unaweza kudai kwamba Mawahabi ni wakweli?

UZUSHI WA PILI

Uzushi wa pili ni mrefu sitaki kuunukuu wote, lakini nataka ninukuu kile alichokisema Sheikh Al-Khalili kisha utazame alivyosema Al-Faqihi kwa ufupi tu. Anasema Sheikh Al-Khalili:

المتلو القرآن هذا عن نتحدث فإنما القرآن خلق عن نتحدث عندما ونحنف�����ي المك���توب باأللسن

يقم لم إذ النفسي الكالم عن نتحدث ولسنا تعريفه، السابق المصاحفوال نف����سه الكتاب من شاهد

... قرآنا تسميته على السنة من

Na sisi tunapozuungumzia kuumbwa kwa Qur-ani, basi tunazungumzia hii Qur-ani inayosomwa kwa ndimi, ikaandikwa kwenye Misahafu ambayo taarifu (definition au ufafanuzi) yake imetangulia huko nyuma, na wala hatuzungumzii kuhusu maneno yaliomo katika nafsi kwani (haya maneno yaliomo ndani ya nafsi) hayana ushahidi wa Qur-ani wala wa Sunna kwamba yameitwa Qur-ani……1492

Basi maneno hayo Al-Faqihi kayapindua na badala yake akasema:

ص ( في بالكالم) 103ولكنه المسمى أن ويثبت كله ذلك ينقض هذا كتابه من

يق لم م�����النفسي

ص ( عليه فيقول السنة من وال الكتاب من ال عندما): ( 103شاهد ونحن

خل عن ق ��������نتحدث

1491 - Al-Imamu Badru Al-Din Al-Khalili Sharhu Ghaayati Al-Muraad uk. 78-82. 1492 - Al-Imamu Badru Al-Din Al-Khalili Al-Haqqu Al-Damigh uk. 103.

502

Page 503: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

فإنما في القرآن المكتوب باأللسن، المتلو القرآن هذا عن نتحدث

نتح ولسنا دث ���المصاحف،

الك ����ع من الم����ن وال نفسه الكتاب من شاهد عليه يقم لم إذ النفسي

السنة).

…..Lakini katika uk. 103 wa kitabu chake hiki (Al-Haqqu Al-Daamigh), basi (Al-Khalili) anayabomoa yote hayo na anathibitisha kwamba kile chenye kuitwa kuwa ni maneno yaliomo katika nafsi hayana ushahidi wa Qur-ani wala wa Sunna, basi anasema (Al-Khalili): “Na sisi tunapozuungumzia kuumbwa kwa Qur-ani, basi tunazungumzia hii Qur-ani inayosomwa kwa ndimi, ikaandikwa kwenye Misahafu ambayo taarifu (definition au ufafanuzi) yake imetangulia huko nyuma, na wala hatuzungumzii kuhusu maneno yaliomo katika nafsi kwani (haya maneno yaliomo ndani ya nafsi) hayana ushahidi wa Qur-ani wala wa Sunna.1493

Sasa ndugu msomaji linganisha alivyosema Sheikh Al-Khalili na alivyozua Dr. Al-Faqihi. Sheikh Al-Khalili anasema kwamba Al-Kalaamu Al-Nafsi (maneno yaliomo ndani ya nafsi) hayana ushahidi “kwamba yameitwa Qur-ani” Al-Faqihi yeye kipengele kisemacho: “kwamba yameitwa Qur-ani……” kakiondoa na badala yake akadai kwamba Al-Khalili anadai kuwa Al-Kalaamu Al-Nafsi (maneno yaliomo ndani ya nafsi) hayana ushahidi wa Qur-ani wala Sunna! Sheikh Kasim Mafuta tafadhali usiwache kumuweka Al-Faqihi katika urodha yako ya wasionena kweli au ya waongo!

Hii ni mifano miwili ambayo Sheikh Al-Khalili mwenyewe kaitaja katika makala yake fupi aliowajibu Mawahabi wa Algeria. Ama mimi binafsi nimekisoma kitabu cha Al-Faqihi na ninayo mifano mingine mingi ya uzushi wake. Kwa mfano katika uk. 11, wa kitabu chake anasema kuhusu Sheikh Al-Khalili:

« في الصواب غرس سماها رسالة في الرؤية لمبحث له ملخص وفي » وهو األحباب دير �ج قلوب

» « : له، كاسيت أشرطة ثم الغافل قلب في الباطل غرس يسمى بأنب تنشر مسلكه يسلك ين ��ولمن

أجالء علماء من السلف منهج ألتباع صريح تكفير وفيها الشباب،

1493 - ‘Ali Al-Faqihi Al-Raddu Al-Qawiim uk. 169.

503

Page 504: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Na katika mukhtasari wa utafiti wake wa mas-ala ya kuonekana kwa Allah katika kitabu alichokiita Gharsu Al-Sawaabi Fii Quluubi Al-Ahbaab ambacho kinastahiki kuitwa Gharsu Al-Baatili Fii Qalbi Al-Ghaafil, kisha katika kaseti zake, pamoja na wanaokwenda katika mwenendo wake, ambazo zinaenezwa kwa vijana, na ndani yake kuna kuwakafirisha kwa uwazi wafuasi wa mwenendo wa Al-Salaf miongoni mwa wanavyuoni watukufu….

Haya kuko wapi huko kuwakafirisha kwa uwazi wafuasi wa mwenendo wa Al-Salaf miongoni mwa wanavyuoni watukufu katika kitabu Gharsu Al-Sawaaab na katika kaseti za Sheikh Al-Khalili? Hata jawabu yake aliomjibu Ibn Baz katika T.V. ya Oman na kurikodiwa katika keseti ilikuwa ni kwa heshima kabisa ambako alikuwa akimwita “Samaahatu Al-Sheikh”.

Hii ni mifano michache ya uzushi wa Dr. Al-Faqihi, ninayo mingi nimeikusanya labda Allah akinijaalia nitaitoa katika munasaba mwengine.

IBN BAZ NA AL-FAWZAAN NAO WASHIRIKI KATIKA KUMZULIA UWONGO AL-KHALILI

Kasim Mafuta alifanya jaribio lenye kufeli la kutaka kuonesha kwamba “Hata Mufti wao, yaani Sheikh Al-Khalili, naye pia anasema uwongo”. Hilo tumeshalijibu kwa ufafanuzi. Na sisi tunasema: “Hata Mufti wao, yaani Ibn Bazi, naye kashiriki katika kuzua uwongo”. Je nini ushahidi wetu?

Kabla ya kuja kwa Ibn Baz, kwanza natuanzie kwa Al-Fawzaan. Tunasema kwamba Al-Fawzaan yeye kakipitia kitabu hicho cha Al-Faqihi na akakisifu. Kwa hivyo, naye anahusika katika uwongo huo aliouzua Al-Faqihi dhidi ya Sheikh Al-Khalili.

Ama Ibn Baz, yeye hakukiwahi kitabu kamili cha Al-Faqihi, lakini aliiwahi juzuu ya kwanza inayohusu suala la kuonekana kwa Allah. Na juzuu hio ya kwanza aliisoma,1494 bila ya kumuhadharisha Al-Faqihi kutokana na uzushi wake na tadlis (ghushi) zake. Na kwa maana hio, naye kashiriki katika uzushi huo na tadlis (ghushi) hizo. Mfano mmoja – mifano ni mingi na nimeikusanya – ya uzushi huo na tadlis (ghushi) hizo iliomo katika juzuu ya kwanza ya kitabu hicho, ni huu unaofuata. Anasema Al-Faqihi, baada ya kutaja maana tafauti za neno Al-Nadhar:

1494 - Tazama ‘Ali Al-Faqihi Al-Raddu Al-Qawiim uk. 145, katika maelezo ya chini.

504

Page 505: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

السنة أهل الشريعة وعلماء اللغة، علماء عند النظر معاني بيان هو فهذا

يري الذين دون ��والجماعة

. إليه ويدعون به ويعملون إال الحق يذكر فلم اإلباضي الخليلي المؤلف أما

يري الذي ده، ��������المعنى

. االنتظار وهو

Basi huu ndio ubainifu wa maana za neno Al-Nadhar kwa wanavyuoni wa lugha na wanavyuoni wa Sharia Ahlu Al-Sunna Wa Al-Jamaa’a ambao haki wanaitaka na wanaitekeleza na kuilingania. Ama Al-Khalili, yeye hakuitaja isipokuwa maana (moja tu) anayoitaka yeye, nayo ni maana ya “kungojea”. 1495

Hayo ndio maneno ya Al-Faqihi yaliopitiwa na Mufti wake Ibn Baz. Sasa je ni kweli Sheikh Al-Khalili hakutaja isipokuwa maana moja tu ya neno hilo Al-Nadhar? Soma alioyaandika Sheikh Al-Khalili akinukuu kutoka katika kamusi la Kiarabu:

والنظر التأمل به ي��راد وقد ورؤيت��ه، الش��يء إلدراك البصيرة تقليب أيضابه يراد وقد والفحص، االنتظار بمعنى النظر شاع وقد………. الفحص بعد الحاصلة المعرفة

Na Al-Nadharu ni kubiruza jicho ili ukifikie kitu na kukiona, na huenda ikakusudiwa kwa neno hilo maana ya kutafakari na kupekuwa; na huenda ikakusudiwa kwa neno hilo maana ya kujua kunakopatikana baada ya kupekuwa…..na (pia) imeenea kulitumia neno hilo Al-Nadhar kwa maana ya kungojea.1496

Suali: je ni kweli kwamba Sheikh Al-Khalili kaitaja maana moja tu ya neno hilo. Au umejua ndugu msomaji kwamba Al-Faqihi na Mufti wake Ibn Baz wamemzulia uwongo Sheikh Al-Khalili ili kutaka kuipigia debe itikadi yao batili? Narudia tena: haya ni machache, mifano iko mingi labda tukijaaliwa tutaitoa katika munasaba mwengine.

DR. BAKR ABU ZAID ATUHUMIWA KWA KUZUWA UWONGO

1495 - Tazama ‘Ali Al-Faqihi Al-Raddu Al-Qawiim uk. 78. 1496 - Al-Imamu Badru Al-Din Al-Khalili Al-Haqqu Al-Damigh uk. 42.

505

Page 506: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Tumenukuu huko nyuma maneno ya Sheikh Abu Abdillahi Al-Ghummari, katika kitabu chake alichokiita Baini Wa Baina Al-Sheikh Bakr, kuhusu vipi Dr. Bakr Abu Zaid alitumia neno chafu kuwaita wanavyuoni wa madhehebu mengine – Abu Ghudda na Al-Kawthari. Sheikh Al-Ghummari anaendelea kusema yafuatayo kuhusu Dr. Bakr Abu Zaid:

Na (Bakar Abu Zaid) kayapotoa maneno yangu alioyanukuu mara mbili….ikanibainikia kwamba hilo (alilolifanya) ni kosa la kukusudia na kwamba alikusudia kutia fitna baina yangu na baina ya ustadh ‘Abdul-Fattaah Abu Ghudda, na si tabia za watu wa elimu kutia fitna baina ya watu na kutafuta kuharibu mapenzi baina yao, na kwa hivyo natangaza mara nyengine kwamba maneno “Mwenye kuunda maandiko” sikuyasema kamwe, wala Sheikh Bakr hakunisikiapo mimi nikiyasema, na kwa kweli kanipachika nayo (tu maneno hayo) kwa kukusudia.1497

Tazama mtu huyu ambaye ni mwenyekiti wa Majma’a Al-Fiqhi ya Kiwahabi anamzulia mtu kitu ambacho hakukisema na anatia chokochoko baina ya Mashekhe wa Kiislamu! Je hivi ndivyo walivyokuwa Al-Salafu Al-Salih? Je huku ndio kufuata sunna?

DR. ‘UMAR AL-ASHQAR APOTOA MAANDIKO

Huyu kanukuliwa na Al-Qannubi1498 na Al-Saqqaaf1499 akisema kuhusu Hadithi inayosema kwamba (kwa amri ya Allah), basi siku ya kiama patanadiwa kwa sauti, basi Dr. ‘Umar Al-Ashqar akaipotoa Hadithi hio kwa kuongeza neno ili iwiyane na itikadi yake. Hadithi inasema:

يأمرك دفينا……. الله إن بصوت …..ىBasi patanadiwa kwa sauti, ya kwamba Allah anakuamuru…1500

Na wengine wakaisimulia riwaya hio kwa matamshi yasemayuo:

يأمرك ديفينا الله إن …..بصوتBasi atanadi kwa sauti, ya kwamba Allah anakuamuru…

1497 - Sh. Abdullah Al-Ghammari Baini Wa Baina Al-Sheikh Bakr uk. 67, nukulu kutoka Al-Imamu Al-Rabi’u Makanatuhu Wa Musnaduhu cha Imamu Al-Sunna Wa Al-Usul Wa Al-Furu’i, Al-Qannubi, uk. 150. 1498 - Al-Qannubi Al-Tufan j. 3, sehemu ya pili uk. 731-32. 1499 - Al-Saqqaf Al-Salafiyya Al-Wahabiyya uk. 80. 1500 - Al-Bukhari Al-Sahih Hadithi na. 7483. Katika Fat-hu Al-Bari Hadithi hio iko katika uk. 9283 chapa mpya al-maktaba al-‘asriyya 2001, na sherehe yake ni uk. 9291. Wengine wameitamka Hadithi hio hivi: بصوت .(Basi patanadiwa kwa sauti) فينادى

506

Page 507: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Basi Dr. Al-Ashqar kaongeza hau (hee) na akainukuu Hadithi hio hivi:

بصوت فيناد…….……. يأمرك هى الله …..إنBasi atanadi kwa sauti YAKE, ya kwamba Allah anakuamuru…

Tafauti baina ya nukulu mbili hizo ni kuwa katika nukulu alioipotoa Dr. Al-Ashqar, lengo ni kuipa nguvu itikadi yake ya kwamba Allah anasema kwa kutoa meneno hasa yanayotoka katika dhati yake;1501 wakati Hadithi kama ilivyo katika usahihi wake haitoi itikadi hio kwani inawezekana ikawa ama Allah ataumba sauti iite au atayeita ni Malaika kwa amri ya Allah. Wala hili la maneno ya Allah kunasibishwa nalo Malaika si geni, kwani Qur-ani ni maneno ya Allah, lakini pamoja na hayo imeitwa kuwa ni kauli ya Jibri katika Aya inayosema:

كريم رسول لقول إنهHakika yake ni kauli ya Mjumbe mwenye kuheshimiwa (Jibril).1502

Yaani ni maneno aliokuja nayo Jibril. Kwa hivyo, kwa kuzingatia kwamba Sheikh wa Kiwahabi anataka lazima itikadi yake ipate hoja za wazi aliamua kuipotosha Hadithi. Hayo, kwa mujibu wa Al-Saqqaaf yalitendeka katika kitabu cha Dr. huyo kiitwacho Al-‘Aqidatu Fii Allahi uk. 175 chapa ya tano maktaba Al-Falah. Ninasema: kisha mimi niliyafuatilia maneno hayo katika chapa nyengine nikakuta yamesharekebishwa, inaonesha Dr. Al-Ashqar alifanya hivyo baada ya kufedheheshwa na Sh. Al-Sayyid Al-Saqqaaf.

Hatimae – baada ya yote hayo – tunamkuta Al-Hafidh Ibn Hajar anabainisha kwamba mwenye kuita kwa sauti ni Malaika: si Mwenyezi Mungu. Anasema:

قوله قرينة يأمرك إ)فان الله على )ن ظاهرا يأمره أتدل ملك المنادي نبذلك ينادي بان الله

Hakika ya qarina ya maneno yake aliposema: ‘Allah anakuamuru’ inaonesha kwa uwazi kabisa kwamba Mwenye kunadi ni Malaika ambaye Allah atamuamuru afanye hivyo.1503

Lakini ikabainika kwamba kumbe tatizo hilo kwa Dr. ‘Umar Al-Ashqar, halikuwa ni kosa la kibinaadamu, bali ilikuwa ni ghushi ya kukusudia. Na 1501 - Kama wanavyoitakidi Mawahabi na Maimamu wao wanaowafuata. Tazama Sherh Nuniyya Ibn Al-Qayyim j. 1, uk. 417, kwa sherehe ya Muhammad Khalil Haraas. 1502 - Sura 69, Aya 40. 1503 - Al-Bukhari Al-Sahih Hadithi na. 7483. Katika Fat-hu Al-Bari Hadithi hio iko katika uk. 9283 chapa mpya al-maktaba al-‘asriyya 2001, na sherehe yake ni katika uk. 9291.

507

Page 508: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kwa hivyo, kanukuliwa pia akipotoa Hadithi alioipokea Al-Bukhari isemayo:

فهو غضبي سبقت رحمتي إن الخلق يخلق أن قبل كتابا كتب الله إنالعرش فوق عنده مكتوب

Hakika Allah aliandika kitabu kabla ya kuumba viumbe kwamba rehema yangu imeishinda ghadhabu yangu, basi hicho kimeandikwa kwake juu ya ‘Arshi yake.1504

Na imekuja kwa matamshi mengine yasemayo:

سبقت رحمتي إن عرشه فوق عنده كتب الخلق قضى ا لم الله إنغضبي

Allah alipohukumu (kuwaumba) viumbe aliandika kwake juu ya ‘Arshi yake kwamba rehema yangu imeishinda ghadhabu yangu.1505

Dr. Al-Ashqar kainukuu Hadithi hio kwa lafdhi isemayo:

نفسه على وتعالى تبارك ربكم ......بيده كتب الخلق يخلق أن قبل

Kaandika Mola wenu Mtukufu kwa mkono wake kabla ya kuumba viumbe…..1506 ….maneno بيده biyadihi (kwa mkono wake), hayamo katika Hadithi za Al-Bukhari, hapa Dr. Al-Ashqar kayaongeza ili kuipalilia itikadi yake ya mungu mwenye mkono.

Hii ni mifano miwili mitatu ya namna gani Mawahabi na Maimamu wao wanawadanganya watu wasiosoma hata kwa kuyapotoa maandiko matukufu au kwa kuyapa tafsiri zisizo sahihi ikiwa ni maandiko yasiopotosheka kama vile Aya za Qur-ani. Hio – kama nilivyosema – ni mifano michache sana, ukitaka kujionea mifano zaidi tazama kitabu Al-‘Uluwwu kilichohakikiwa na Al-Saqqaaf1507 ambapo kataja mifano ya jinsi gani Mawahabi na watangulizi wao wanavyoyapotoa maandiko. Tazama pia kitabu Qamus Al-Hajji Wa Al-‘Umra1508 cha Sheikh Khalfaan Al-Tiwaani uone anavyonukuu maneno yasio na ukweli yaliosemwa na Muqbil Haadi katika kitabu chake 1504 - Al-Bukhari Al-Sahih Hadithi na. 7554. 1505 - Al-Bukhari Al-Sahih Hadithi na. 7422. 1506 - ‘Umar Al-Ashqar, Al-‘Aqiidatu Fii Allahi uk. 162.Kanukuliwa na Al-Qannubi katika Al-Tufaan Al-Jaarif j. 3, sehemu ya 2, uk. 732. 1507 - Uk. 87-90. 1508 - Al-Tiwaani, Khalfaan bin Sulaiman, Qaamus Al-Hajj Wa Al-‘Umra (2009-1430 H.) uk. 148-151.

508

Page 509: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Al-Ajwiba Al-Sadida.1509 Na miongoni mwa maneno ya kufyatua ya watu hawa ni kile kilichojaa katika vitabu vyao vyote taqriban kwamba: “Al-Salaf wamekubaliana kwamba Qur-ani ni maneno ya Allah wala si kiumbe”. Tazama ghushi zao hizi wanazozifanya kwa umma! Al-Salaf kweli wamekubaliana kwamba Qur-ani ni maneno ya Allah, lakini vipi watakubaliana kuwa si kiumbe na mas-ala haya ni ya kuzuka baadae: enzi ya Masahaba hayakuwepo kamwe. Ninasema: jambo la kusikitisha zaidi ni ile kauli ya Raisi wa Jamaa wa Ansari Sunna (Mawahabi) alipokuwa akizipotoa Hadithi. Anasema Ahmad Shaikr kuhusu Raisi huyo ambaye alikuwa ni sahibu yake kwa muda usiopungua miaka 40:

Na ulikuwa baadhi ya wakati ikiwa Hadithi hukuipenda wala hukuweza kuihukumu kuwa ni dhaifu, basi unailetea ta-awil inayokaribia kuitoa maana ya lafdhi zake…kisha mambo yakazidi ulipoandika maelezo maalumu, nami nikajaribu kukukinaisha kwamba hayo ni batili, lakini wewe ukashikilia kuyathibitisha (kuyawacha katika kitabu).1510

Baada ya kukuthibitishia kwa ushahidi kwamba waliotajwa kwa sifa mbaya ya uwongo na ambao hawanukuu ukweli katika vitabu vyao, ni Mashekhe wa Kiwahabi na Maimamu wao watangulizi, sasa natutazame mifano miwili mitatu ya vitabu walivyovitunga watu wa skuli hio kisha wakawazulia watu wengine ili kutaka kuipa nguvu itikadi yao. Lakini kabla ya hapo, natutazame yalioandikwa katika gazeti la Jordan liitwalo Jaridatu Al-Dustur.

YALIOANDIKWA KATIKA GAZETI LA DUSTUR

Mutakumbuka kwamba katika miaka ya nyuma kuna kikundi ambacho kiliuvamia Msikiti Mtukufu wa Makka. Basi Mawahabi ili kutaka kuuficha upinzani wanaopata nchini kwao, walizua kwamba waliovamia Msikiti huo ni Ibadhi! Linasema gazeti la Jordan liitwalo Jaridatu Al-Dustur toleo na. 4412, tarehe 22-2-1979, likinukuu chanzo (Masaadir au Source) cha Suudia kwamba:

Wanachama wa kikundi kilichouvamia Msikiti Mtakatifu alfajiri ya mwanzo wa mwezi, mwaka 1400 A.H, ni kikundi cha Khawarij. Na kikundi hiki ni chenye kasumba na siasa kali…nao ni katika Maibadhi wanakaa Algeria, Maskati, Afrika (ya Mashariki), Tunis, Libya na Oman.1511

1509 - Al-Waadi’i, Muqbil Haadi Al-Ajwiba Al-Sadida uk. 133. Asili yake ni keseti. 1510 - Ahmad Shaakir Al-Maqaalaat j. 1, uk. 300. 1511 - Maskati na Oman kwa matumizi ya sasa ni moja – Maskati ni mji mkuu wa Oman. Zamani Oman ilikuwa sehemu za ndani na Maskati ni sehemu ya pwani ambayo kwa sasa

509

Page 510: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Anasema Sheikh Al-Khalili:

Natuutazame huu uzishi mkuu! Je kuna hata mtu mmoja miongoni mwa Ibadhi katika waliovunja heshima ya Msikiti Mtukufu? Je yumo katika kikundi hiki kilichovamia Msikiti Mtukufu katika zama hizo mtu japo mmoja katika Ibadhi? Hakika hakuna miongoni mwa hawa hata Muomani mmoja wala Mualgeria hata mmoja wala Muafrika Mashariki hata mmoja wala yoyote kutoka Tunis wala yoyote kutoka Libya, bali (walikuwa wavamizi) ni kutoka Suudia yenyewe na walioambatana nao kutoka nje ya Suudia ni Mawahabi wenye siasa kali, basi vipi tuhuma hii wanabandikwa nayo Ibadhi.1512

Ninasema: sisi kule kwetu Zanzibar tulikuwa tunadanganywa kwamba waliouvamia Msikiti ni Mashia wa Iran! Hivi ndivyo, uwongo hadi leo unavyoendelezwa kuzuliwa madhehebu fulani kwa sababu za Kisiasa! Basi elewa kwamba hivi unavyoona leo ndivyo hivyo hivyo ilivyokuwa katika zama hizo za Sheikh Mu’awiya, Al-‘Allama Amru bin Al-’Aas na wafuasi wao.

Jambo la kufurahisha ambalo nimesimuliwa ni kuwa katika miezi ya karibu, mmoja wa wavamizi hao alitoka akihojiwa katika T.V. ya Al-Arabiyya. Huyu yeye alitiwa hatiani kwa kufungwa miaka sita kwa sababu hakuhusika moja kwa moja:

a) Jina la muhusika huyo ni: Nassir Al-Huzaini.b) Kafungwa kwa muda wa miaka 6. c) Kafanya mahojiano hayo siku ya Ijumaa 20, 11,2009.d) T.V. ya Al-Arabiyya.e) Kipindi: Sinaa’atul maut.f) Mkuu wa kikosi chao alikuwa ni: Jahiman Al-‘Utaibi

ambaye aliuliwa.

Alhamdu Lillahi ambaye kaufichua uwongo waliouzua! Watu hao wote ni Wasaudia wenyewe, isipokuwa huyu Al-‘Utaibi ni kutoka Kuweit. Ukiwa utaingia yuotube au arabia.net kisha ukaandika الموت utavipata صناعةvipindi hivyo, kisha andika العتيبي itakuchukua mpaka kwa جهيمانwahusika wa tukio hilo. Huo uliotangulia ni uzushi wa Kiwahabi ambao – bila ya haya – wameuchapisha katika gazeti. Sasa tazama baadhi ya vitabu walivyovitunga na kuwabandika navyo Maimamu wengine ili kutaka kuupa nguvu msimamo wao.

ndio mji mkuu wa Oman. 1512 - Tazama Sheikh Al-Khalili: Nabdhu Al-Ta’assubi Al-Madh-Habi uk. 41-42.

510

Page 511: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

VITABU VYA UZUSHIAL-RADU ALAA AL-JAHMIYYA

Hiki ni kitabu ambacho kimetungwa na watu wa skuli ya tajsim kisha wakakinasibisha na Al-Imamu Ahmad bin Hanbal. Na hadi leo, Mawahabi bado wanakichapisha. Anasema Al-Dhahabi: “….Si kama Rissalatu Al-Istakhri wala si kama Al-Raddu ‘Alaa Al-Jahmiyya alichozuliwa nacho Abu ‘Abdillah (Al-Imamu Ahmad bin Hanbal)…..”.1513 Ninasema: katika sanad ya kitabu hicho kuna mpokezi hajulikani kama alivyosema mtiaji maelezo wa kitabu Al-Siyar cha Al-Dhahabi, kisha mtiaji maelezo huyo akatoa hoja kwamba kitabu hicho hakuna yoyote aliyekitaja katika wale walioishi na Al-Imamu Ahmad au waliokuja moja kwa moja baada yake.

KITABU AL-SUNNA KILICHONASIBISWA KWA ABDULLAH BIN AHMAD

Kitabu hiki ndio moja ya tegemeo kubwa la Kiwahabi katika mapokezi yao ya riwaya za kukafirisha na riwaya za mungu-mtu – mungu mwenye viungo. Na kwa hivyo, Seif Al-Ghafri katuusia sana kuwa tukisome! Mambo yanazidi kuwa mabaya pale Mawahabi wanapofanya khiyana wakaficha ukweli kwa kudai kwamba kitabu hicho kimethibiti kwamba ni cha mtoto 1513 - Al-Dhahabi Al-Siyar j. 9, uk. 503, tarjama na. 1876.

511

Page 512: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

wa Al-Imamu Ahmad bin Hanbal – Abdullah bin Ahmad,1514 ilhali katika sanad ya kitabu hicho hadi kufikia kwa mtoto wa Al-Imamu Ahmad kuna mpokezi asiyejulikana.

KITABU AL-RU’UYA KILICHONASIBISWANA AL-DARAQUTNI

Kitabu hiki kimekusanya riwaya mia mbili na thamanini na saba (287) kuhusu kuonekana kwa Allah! Lakini – mbali na kuwa riwaya hizo zote zimekuja kwa sanad dhaifu – kitabu chenyewe hakikuthibiti kuwa ni kitabu kilichoandikwa na Al-Imamu Al-Daraqutni. Na hili peke yake basi lingetosha kuthibitisha kwamba suala zima la kuonekana kwa Allah huko akhera ni suala la kuundiwa riwaya, vyenginevyo wasingelihitaji kutunga kitabu kizima juu ya suala hilo. Tazama sanad iliotajwa na wahakiki wa kitabu hicho Kitabu Al-Ru’uya kilichonasibiswa kwa Al-Daraqutni! Wanasema kuhusu sanad ya kitabu hicho:

العالء أبي الحافظ عن جماعة رواية من جاءت النسخة وهذهالشيخ على بقراءته محمد العطار بن الله عبيد بن أحمد العز أبي

العكبراوي ( ) كادش بن بن علي بن محمد طالب أبي عن بروايتهالدارقطني الحسن أبي عن الفتح

Na kopi hii imepokewa kutoka katika masimulizi ya wengi kutoka kwa Al-Hafidh Al-’Alaa Al-’Attar kwa kumsomea kwake Sheikh Abu Al-’Izz Ahmad bin ‘Ubaidi-Lahi bin Muhammad bin Kaadish Al-‘Ukbaraawi kwa masimulizi yake kutoka Muhammad bin ‘Ali bin Al-Fat-hi kutoka kwa Abu Al-Hasan Al-Daraqutni.1515

Utaona kwamba katika sanad ya kitabu hicho kilichonasibishwa kwa Al-Imamu Al-Daraqutni kuna Abu Al-’Izz Ahmad bin ‘Ubaidi-Lahi bin Muhammad bin Kaadish Al-‘Ukbarawi. Wamaa adraak: maa Ibn Kaadish Al-‘Ukbarawi (na nini kinachokujuilisha wewe ni nani huyo Ibn Kaadish)? Huyu tumemuelezea kabla, naye alikuwa ni mtunzi wa Hadithi za uwongo.1516

1514 - Soma maelezo yaliotiwa na Dr. Salim bin Muhammad Al-Qahtaani katika ukurasa wa 59 wa juzuu ya kwanza wa kitabu hicho. 1515 - Kitabu Al-Ru-ya uk. 85.1516 - Tazama mwanzoni mwa sura hii.

512

Page 513: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Baada ya haya, utaona kwamba kwa kila atayeihukumu kesi hii kwa uadilifu baina yangu mimi na Sheikh Kasim Mafuta, basi hatotafautiana nami kwamba:

1) Wanavyuoni wa skuli ya Kiwahabi na Maimamu wao watangulizi ndio waliotajwa kwa uwongo na utunzi wa riwaya. Na haya hayakutajwa na Ibadhi au Khawaarij, bali yametajwa na watu kama Al-Dhahabi na walio mfano wake.

2) Wanavyuoni wa Kiwahabi na Maimamu wao watangulizi ndio wanaonukuu mambo yasio na ukweli kama ulivyoona nukulu za ‘Uthaman Al-Darimi, Ibn Taymiyya, Ibn Al-Qayyim, Ibn ‘Uthaimin, Dr. Bakr Abu Zaid na wengine tuliowataja humu na wengi wengine ambao hatukuwataja humu.

3) Wanavyuoni wa Kiwahabi au Maimamu wao watangulizi ndio waliotunga vitabu na kuwapachika navyo Maimamu ili kutaka kuipa nguvu misimamo yao ya kiitikadi. Na hili linaonesha wazi kwamba hawakukamatana na kamba madhubuti, vyenginevyo wasingelihitajia kutunga kitu cha kuzua ili kuupa nguvu msimamo kwani Qur-ani ipo na Sunna sahihi zipo.

Baada ya hayo, sasa natutazame baadhi ya riwaya walizozitunga watu wa skuli hio ya tajsim ambao ndio watangulizi (Salaf) wa Mawahabi.

BAADHI YA MIFANO YA HADITHI ZILIZOTUNGWA NA MUJASSIMA

1) Kutoka kwa Ikrima kwamba Mtume (s.a.w.) kasema: “Nimemuona Mola wangu Mtukufu naye ni kijana amrad,1517 mwenye nywele zilizosokotana (curl)1518 kavaa guo jekundu”.1519.....…… “Nimemuona Mola wangu naye ni kijana amrad, mwenye nywele zilizosokotana kavaa guo la kijani”1520…… “Muhammad kamuona Mola wake katika sura ya kijana hana ndevu, mbele yake kuna pazia la lulu, miguu yake iko katika sehemu yenye rangi ya kijani”.1521

2) Nabii Mussa (a.s.) alimkuta mtu juu ya mti kavaa vazi la sufi na viatu akasema naye (yaani yule mtu akasema na Nabii Mussa a.s). Nabii Mussa (a.s.) akasema: ‘Ni Muibrania gani huyu anayesema na mimi?’ Yule mtu akajibu: “Mimi ni Mwenyezi Mungu.”1522 Haya ni

1517 - Amrad: hana ndevu au hana nywele au manyoya. 1518 - Kusokotana kwa uzuri yaani: si kusokotana kwa ubaya. 1519 - Ibn Abi Ya’ala Tabaqatu Al-Hanabila j. 2, uk. 419. Mashaa Allah! Mubarakun Ya Ahla Sunna Wal Jama’a! 1520 - Al-Bayhaqi Al-Asmaau Wa Al-Sifat j. 2, uk. 363-364 Hadithi na. 938. 1521 - Al-Bayhaqi Al-Asmaau Wa Al-Sifat j. 2, uk. 363-364 Hadithi na. 938. 1522 - Tazama Lisanu Al-Mizan cha Ibn Hajar j. 4 uk. 112-115.

513

Page 514: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

maneno ya Ibn Batta, Imamu Adhimu wa Kiwahabi, na tumeyanukuu maneno yake haya kabla.

3) (Mwenyezi Mungu) kamuumba Adam kwa kumshika!”1523 Huu ni mkono wa Mungu unashika kitu lakini haufanani na mkono!

4) Hakika yake (Mwenyezi Mungu) anakaa kitako juu ya kiti basi haibakii (nafasi) isipokuwa kiasi cha vidole vinne!”1524 Mwisho wa kunukuu. Ninasema: Kwa hivyo, Arshi ni kubwa kuliko kiwiliwili cha Mungu – kiumbe mkubwa kuliko Muumba! Lakini kumbe sehemu hio ya vidole vinne iliobakia haikubakishwa bure bure tu, dhahir – kama inavyoashiria riwaya nyengine – hio ni nafasi ya kukaa Mtume (s.a.w.)! Mtume (s.a.w.) naye atakaa juu ya Arshi Al-Rahman (Kiti cha ufalme wa Allah).!1525 Anasema Abu Bakr Al-Nnajjad: “Dini ya Allah tunayoifuata na kuitakidi ni ile tulioiandika na kuibainisha katika maana za Hadithi zilizotegemezwa kutoka kwa Mtume (s.a.w) na alizozisema Ibn Abbaas na waliokuja baadae katika watu wa elimu…..katika kuifasiri kauli yake Allah: ربك يبعثك أن عسى مقاما محمودا (Huenda Mola wako akakuinua cheo cha kuhimidiwa), kwamba cheo cha kuhimidiwa (chenyewe atachopewa Mtume s.a.w. siku ya kiama) ni kukaa kwake kitako pamoja na Mola wake juu ya Arshi yake!!! Na alikuwa mwenye kukanusha hayo na akayazungumza kwa kuyapinga basi kwa hakika kakusudia kwa maneno yake hayo (kuyasapoti) maneno ya Jahmiyya. Basi huyo anaepukwa na kuwekwa mbali na kuhadharishwa (watu) kutokana na yeye.1526 Na vivyo hivyo, kaniambia Abu Bakr Al-Katib kutoka kwa Abu Dawud Al-Sijistani kwamba kasema atayeipinga Hadithi ya Mujahid1527 basi huyo ni Jahmi…….Kwa hivyo, ninasema: lau mtu aliapa kwa kumuacha mkewe kwamba Allah atamuweka Muhammad (s.a.w.) pamoja naye juu ya Arshi, na akanitaka fat-wa kuhusu kiapo chake, basi ningemwambia: ‘Umesema kweli katika kauli yako na kiapo chako umekitekeleza na mke wako yuko kama alivyokuwa (bado ni mke wako). Basi haya ndio madhehebu yetu na dini yetu na itikadi yetu na juu ya hayo tumechipukia na in shaa Allah tunayafuata hayo mpaka kufa, basi imekuwa lazima kumpinga yule atayeikataa fadhila

1523 - Tazama kitabu Radu Al-Imamu Al-Darimi Alaa Bishri Almarisi uk. 25. Kwa hivyo, kwa mujibu wa Al-Darimi Mwenyezi Mungu kamfinyanga Nabii Adam (a.s.)!1524 - K.h.j. uk. 74. 1525 - Katika utangulizi tumenukuu maneno ya Ibn Taymiyya kuhusu mas-ala haya. Na Al-Khallal kapokea riwaya nyingi kutoka kwa Maimamu wao juu ya mas-ala haya katika kitabu chake . 1526 - Hii ndio sera ya Kiwahabi na maimamu wao watangulizi: kukwepa mijadala ya kutafuta ukweli, na kuwapandikiza wafuasi wao Al-Irhabu Al-Fikri (kuwatisha kifikra)! 1527 - Yaani hio iliotangulia.

514

Page 515: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

hio (ya Mtume s.a.w. ya kukaa kitako pamoja na Allah juu ya Arshi) ambayo Maulamaa wameisema na kuikubali, basi atayeikataa huyo ni katika vikundi vilivyoangamia.1528

5) Na imetufikia kwamba wao (malaika wenye kuibeba Arshi ya Mwenyezi Mungu) walipoibeba (hio Arshi) na juu yake alikuwako (Mwenyezi Mungu) Jabari katika utukufu wake!1529 Jamani! Mungu wa Mawahabi kabebwa mzegamzega! Mimi najitoa, huyu aliyebebwa mimi si Mungu wangu! Mimi Mungu wangu hafanani na kitu, wala haguswi wala habebwi wala haonekani kamwe. Huyu ndiye Mungu ninayemuabudu.

6) …..Kwamba (Mtume s.a.w.) kamuona Allah katika bustani ya kijani mbele yake kuna zulia la dhahabu (Naye Allah) kakaa juu ya kiti; kabebwa na Malaika wane: malaika mmoja ana sura ya mtu; Malaika wa pili ana sura ya ng’ombe dume; Malaika wa tatu ana sura ya ndege nasr (eagle) na Malaika mmoja kwa sura ya simba!1530

Tazama: hapa sio kuwa Mungu kabebwa tu, bali hao waliombeba wana sura za kutisha: sura za wanyama.

7) “Kiti ndio sehemu ya (kuwekea) miguu yake miwili.”1531 Alaa! Kwa hivyo, miguu yake iko mbinguni na ardhini, maana kiti kimeenea mbingu na ardhi. Sijui tuifanyaje itikadi ya Al-Salaf wetu kwamba

لخلقه مباينا عرشه على جالسا السماء فوق Allah yuko) اللهjuu ya mbingu kakaa juu ya ‘Arshi yake yuko mbali na viumbe vyake hakuvigusa).

8) Allah akitaka kuwatisha waja wake basi hujifunua sehemu yake (kuionesha) ardhi, basi ardhi hutetemeka; na akitaka kuwaangamiza watu hujidhihirisha (kamili) kwa hio (ardhi).1532 Jamani: Mungu anagawika sehemu sehemu. Na nyengine – inavyoonesha – kazi yake ni kutisha waja tu!

RIWAYA ZA KUTUNGIWA AL-IMAMU AHMAD

Baada ya kuona machache yenye kuhusu utunzi wa riwaya za watu wa skuli ya tajsim, walizozitunga kumzulia uwongo Allah na Mtume wake (s.a.w.), sasa tazama riwaya mbili tatu walizomtungia Al-Imamu Ahmad. 1528 - Ibn Abi Ya’ala Tabaqatu Al-Hanabila j. 2, uk. 10. Al-Hamdu Lillahi! Al-Albani, Imamu wa Kasim Mafuta, naye atakuwa mwenye kuangamia, kwani naye ni katika wenye kuipinga riwaya hio! Tazama Al-Dhaifa j. 11, uk. 14, Hadithi na. 5008. J. 13, uk. 1043, Hadithi. Na. 6465. J. 2, uk. 255-256, maelezo ya Hadithi na. 865.1529 - K.h.j. uk. 85. Kwa hivyo hapa kiti kimebebwa na Malaika na Mwenyezi Mungu yuko juu kabebwa mzega mzega! 1530 - Al-Bayhaqi Al-Asmaau Wa Al-Sifat j. 2, uk. 361-362 Hadithi na.934. 1531 - K.h.j. uk. 67. Yaani miguu ya Mwenyezi Mungu! 1532 - Ibn Ahmad Al-Sunna j. 2, uk. 470, riwaya na. 1069.

515

Page 516: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Al-Imamu Ahmad bin Hanbal – bila shaka yoyote – ni mmoja katika Maimamu wakubwa wenye elimu nyingi sana. Lakini, Mawahabi1533 na watangulizi wao wa Kihanbali na watu wa skuli ya tajsim walitaka kumfanya Al-Imamu Ahmad kuwa ni bora hata kuliko Mitume! Hilo wamelifanya ili kutaka kuzipigia debe itikadi zao za mungu-mtu. Wamemtungia sifa ambazo hata Mitume hawanazo. Wamesahau hawa watu wa skuli ya tajsim kwamba wamepita watu wazito zaidi kuliko Al-Imamu Ahmad1534 na wamekuja baadae watu wazito kuliko Al-Imamu Ahmad na wala hawakuwa na hizo sifa walizomtungia wao Al-Imamu Ahmad. Soma baadhi ya mifano ya walioyasema kuhusu Al-Imamu Ahmad:

1) “Atayemchukia Ahmad bin Hanbal, basi huyo ni kafiri”.1535 Kauli hii imenasibishwa kwa Al-Imamu Al-Shafi, nao ni uwongo, Al-Imamu Al-Shafi – na akili yake pana na elimu yake kubwa na ucha Mungu wake – hawezi kusema maneno haya.

2) ….Alipokufa Ahmad bin Hanbal, basi kuna mtu mmoja aliona usingizini kana kwamba kuna taa ya kandili katika kaburi, akasema: ‘Nini hiki?’ Akaambiwa: ‘Hujui kwamba watu wa makaburini makaburi yao yameingia nuru kwa kuteremka mtu huyu miongoni mwao? Na walikuwemo miongoni mwao waliokuwa wakiadhibiwa basi wakarehemewa!1536 Ninasema: huyu mtunzi wa uwongo huu labda alikuwa hajui kwamba Allah anasema: “Na iogopeni siku ambayo nafsi haitoifaa nafsi nyengine chochote wala hayatokubaliwa maombezi kutoka kwake…..”.1537 Kama vile ambavyo alisahau Hadithi ya Mtume (s.a.w.) aliposema: “Enyi Maquraish jikomboeni kutokana na moto, enyi Bani Ka’ab jikomboeni kutokana na moto, enyi Banii Hashim jikomboeni kutokana na moto ………..ewe Fatima bint Muhammad ikomboe nafsi yako kutokana na moto hakika yangu Wallahi sina uwezo wowote (wa kukukomboeni) kwa Allah.” Na riwaya nyengine: “Ewe

1533 - Usiniambie kwamba “Aaa wakati huo hakuna Mawahabi, sasa vipi wewe unawashirikisha katika utunzi huu?” Ninasema kwamba nimewashirikisha kwa sababu baadhi ya riwaya hizi nao wamezikubali kwa hivyo nao wamo. Kwa mfano riwaya ya mtu aliyekumbwa na shetani, Al-Imamu Ahmad akapeleka viatu vyake tu akasema “Mwambiye shetani Ahmad bin Hanbal anakuamrisha utoke” na shetani akatoka! Ninasema: sipingi karama lakini Imamu mcha Mungu hawezi kufanya hivi kwani huku ni kujitukuza ambako Maimamu walikuwa hawakufanyi kabisa. 1534 - Kama Jabir bin Zaid, Al-Hasan Al-Basri, Mujahid na wenziwao. 1535 - Ibn Abi Ya’alaa Tabaqaatu Al-Hanaabila j. 1, uk. 13. 1536 - Ibn Al-Jawzi Manaaqibu Ahmad uk. 465. 1537 - Sura 2, Aya 49.

516

Page 517: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Faatma bint Muhammad, ewe Safiyya bint Abdil-Muttalib……sina uwezo wowote (wa kukukomboeni) kwa Allah.” 1538

3) …… “Alikufa mtu khanithi basi akaonekana usingizini akasema: “Nimesamehewa; kazikwa Ahmad bin Hanbal basi watu wa makaburini wamesamehewa!”1539 Ninasema: Basi na wanafiki wa Madina – akina Abdullah bin Ubeiy – watasamehewa kwa kuzikwa Mtume (s.a.w.) na Masahaba watukufu katika ardhi ya Madina! Bwana Kasim bin Mafuta! Je waongo ni Maibadhi au ni watangulizi wenu wa Kihanbali?

4) …..Nilisoma usiku huu – nami niko kaburini kwa Ahmad bin Hanbal – kauli ya Allah (isemayo): “Miongoni mwao kuna waovu na wema”.1540 Basi kilepe kikanichukua nikamsikia mtu anasema: ‘Hakuna muovu kwetu – Alhamdu Li-Lahi – kwa baraka ya Ahmad.1541

5) ……Majini walisikiliza kwa kudoea (basi wakawasikia) Malaika wakipeana mkono wa pole kwa kufa Al-Imamu Ahmad.1542 Ninasema: Haya! Nyiye baadae ni nani aliyekupeni khabari hio? Ama kweli njia ya mwongo fupi!

6) …..Hakuna yoyote katika mava1543 ya Ahmad anayeadhibiwa kwa moto.1544 Ninasema: utunzi wenu wa upotovu huu ndio unaowapa silaha wapinzani wenu wakapata njia ya kukupingeni kwa riwaya zenu. Al-Amini – mtafiti wa Kishia – katika kitabu chake Al-Ghadir1545baada ya kuzinukuu baadhi ya riwaya hizi tulizozitaja hapa alisema: “Hii ni mifano ya maneno ya Mahanbali kuhusu kulizuru kaburi la Imamu wao na baraka za ujirani wake. Na hii ni sira iliokwenda kwa mfululizo katika kuyazuru makaburi ya Mashekhe wao kama tutavyoeleza; basi wapi na wapi baina yake na baina ya anachokiona Ibn Taymiyya na wafuasi wake……”.

7) Kwa (njia ya) Al-Imamu Ahmad basi inawezekana akajulikana Muislamu na zinddik (mnafiki)! 1546

1538 - Al-Rabi’u bin Habib Al-Jami’u Al-Sahih Hadithi na. 890-1005. Al-Bukhari Al-Sahih Hadithi na. 4771. Al-Bukhari Al-Sahih Hadithi na. 4771.1539 - Ibn Al-Jawzi Manaaqibu Ahmad uk 465. Al-Dhahabi Al-Siyar j.9, uk. 544.1540 - Sura 11, Aya 105. 1541 - Ibn Al-Jawzi Manaaqibu Ahmad uk. 466. 1542 - Ibn Al-Jawzi Manaaqibu Ahmad uk. 466. 1543 - Mava ni sehemu ya kuzikia watu (makaburini). 1544 - Ibn Al-Jawzi Manaaqibu Ahmad uk. 466. 1545 - J. 5, uk. 247, chapa ya kwanza 1414 A.H., (1994), Al-A’alami Library (Lebanon). 1546 - Ibn Al-Jawzi Manaaqibu Ahmad uk. 476.

517

Page 518: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

8) …..Nimemsikia Abdallah bin Ahmad anasema: ‘Nimemsikia baba yangu (Al-Imamu Ahmad) akisema: ‘Nimemuona Mola Mtukufu usingizini’.1547

9) Al-Khidhru na Nabii Musa walimsifu (Al-Imamu Ahmad)!1548 10) Kumtazama (Al-Imamu) Ahmad ni bora kuliko ibada ya mwaka!1549

11) Allah anafanya ziara ya kumtembelea (Al-Imamu) Ahmad katika kaburi lake kila mwaka.1550 Maashaa Allah! Leteni vitu Al-Salafiyya; tuburudisheni kwa mafunzo ya Al-Salafu Al-Salih au Al-Salafu Al-Talih!

12) Kaburi la (Al-Imamu) Ahmad ni katika jumla ya makaburi manne ambayo kwayo Baghdaad (Iraki) balaa zote huondoshwa!1551

13) Kutabarruk kwa kaburi la (Al-Imamu) Ahmad ni jambo la Kisharia.1552

14) Kalamu ya Ahmad ilikuwa inawekwa katika mtende usiozaa, basi unazaa kwa baraka yake.1553

15) Mmoja wao aliota kwamba (Al-Imamu) Ahmad aliwaghadhibikia Munkar wa Nakiir akawambia: ‘Ivo mtu kama mimi anaulizwa nani Mola wako’. Basi wakamuomba radhi na wakamwambia kwamba hakuna budi na hilo kwani wao wamelazimishwa.1554

16) Majini walitangaza kifo cha (Al-Imamu) Ahmad kwa muda wa siku arubaini kabla ya kufa kwake.1555

17) Allah anajifakharisha kwa (Al-Imamu Ahmad) mbele ya Malaika wake.1556 Ninasema: haya aliyeyajua ni nani?

18) Mmoja wa Mahanbali, katika usingizi aliwaulizia (Al-Imamu) Ahmad na Ibn Ma’in, akaambiwa wamekwenda kumtembelea Allah Bwana wa Ulimwengu na wamewekewa meza ya chakula.1557

19) Mmoja wa Mahanbali alimuona Allah akamwambia: ‘Atayemukhalifu Ahmad bin Hanbal basi ataadhibiwa’.1558

1547 - Al-Dhahabi Al-Siyar j. 9, uk. 540. 1548 - Manaaqibu Ahmad uk. 188. 1549 - Manaaqibu Ahmad uk. 197. 1550 - Manaaqibu Ahmad uk. 550. 1551 - Manaaqibu Ahmad uk. 189. 1552 - Ibn Abi Ya’alaa Tabaqaatu Al-Hanaabila j. 1, uk. 288, j. 2, uk. 663, 234, 241. Manaaqibu Ahmad uk. 191. Yuko wapi Sulaiman bin Sihmaan aje ajionenee wenye ibada za makaburi ili apate kuwaweka katika orodha yake ya makafiri?! 1553 - Manaaqibu Ahmad uk. 270. 1554 - Manaaqibu Ahmad uk. 549. Haya! Baadae nyinyi ni nani aliyekujuvyeni hayo?!1555 - Manaaqibu Ahmad uk. 513. 1556 - Manaaqibu Ahmad uk. 557. 1557 - Manaaqibu Ahmad uk. 562. 1558 - Manaaqibu Ahmad uk. 563.

518

Page 519: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

20) Allah aliwaamuru viumbe wa mbinguni na Mashahidi wote wahudhurie jeneza ya (Al-Imamu) Ahmad bin Hanbal.1559

21) Malaika wa mbingu ya saba mpaka kufikia mbingu ya kwanza, wameshughulika na kufunga bendera ili kumpokea Ahmad bin Hanbal. 1560

22) Mtu mmoja alimuona Zubaida katika pepo akamuuliza kuhusu (Al-Imamu) Ahmad, akamjibu kwamba karuka katika lulu nyeupe kaelekea kwa Mwenyezi Mungu.1561

23) Mwenye dhiki akalizuru kaburi la Ahmad siku ya J/tano na akaomba dua, basi Allah atamruzuku nafasi.1562

24) Yoyote atayezikwa katika mava aliozikwa (Al-Imamu) Ahmad bin Hanbal, basi huyo kasamehewa kwa baraka za (Al-Imamu) Ahmad bin Hanbal.1563

25) Allah kila siku anautazama udongo wa Ahmad bin Hanbal mara elfu sabiini, na anamsamehe yule mwenye kulitembelea (kaburi lake).1564

26) Anasema Zakariya bin Yahya kwamba alimuota Ahmad bin Hanbal akamwambia…. “Allah kanisamehe, na kanikurubisha katika nafsi yake na kanivisha taji hili kwa mkono wake”.1565 Ninasema: kitendo hiki kitakuwa kimeongeza idadi ya vitu vilivyoshikwa na Allah kwa mkono wake, ambavyo vimetajwa katika riwaya tulizozinukuu huko nyuma!

Nukulu hizi1566 zinaonesha kwa uwazi kabisa, jinsi gani watu hawa wa skuli hii ya Kihanbali – ambao ndio watangulizi wa Mawahabi – walivyokuwa wakijishughulisha na utunzi wa riwaya ili kuipa nguvu misimamo yao na itikadi zao. Jambo hili, kwa sisi Ahlu Al-Haqqi Wa Al-Istiqaama, ndilo linalotufanya tusikubaliane na riwaya zenu zote mulizotukhalifu kwani ukweli kwenu umekuwa ni mchache wakati sisi viongozi wetu Walillahi Alhamdu hawakusifika kwa dosari hilo, bali – kinyume chake – wao walisifika kwa ukweli wa hali ya juu kama walivyoshuhudia wanavyuoni

1559 - Manaaqibu Ahmad uk. 563. 1560 - Manaaqibu Ahmad uk. 564. 1561 - Manaaqibu Ahmad uk. 567. 1562 - Manaaqibu Ahmad uk. 580. 1563 - Manaaqibu Ahmad uk. 584. 1564 - Manaaqibu Ahmad uk. 580. 1565 - Ibn Al-Jawzi Manaaqibu Ahmad uk. 425. 1566 - Nukulu ambazo nimeanza kwa maneno “Ibn Al-Jawzi” basi nimezinukuu katika kitabu hicho katika kopi nilio nayo; nukulu ambazo nimeandika: Manaaqibu Ahmad tu bila ya kutaja Ibn Jawzi, basi nimezinukuu kutoka katika kitabu Al-Qiraa-a Fii Kutubi Al-’Aqiida cha Sh. Hasan bin Farahan Al-Maaliki, uk. 135-137. Sikunafasika kukupitia kitabu chote nilicho nacho na kwa hivyo sehemu nyengine nimetegemea maandiko ya Sheikh huyo Hasan Al-Maliki ili kujirahisisha kazi.

519

Page 520: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

wakubwa wakiwemo wanavyuoni wenu wenyewe. Na hili liko wazi kabisa kwa kila aliyevichungulia vitabu vya Kiibadhi bali vitabu vyote vya riwaya na mapokezi ambapo hagundui kuwepo kwa riwaya zilizotungwa na Maibadhi au walioitwa Khawarij kwa ujumla, na hata ikitokea mtu kutolea hoja kwa riwaya ya kutunga kwa kutokuijua basi utakuta kwamba riwaya hio kainukuu kutoka kwa watu wengine – imetungwa na wengine. Ama kukusudia kutunga riwaya au kuzua uwongo, basi hilo Walillahi Alhamdu halipo kwa Maibadhi wala kwa wote wale walioitwa Khawaarij.

Kitu kibaya zaidi ni kutunga riwaya za kuwa fulani kaotwa yuko motoni kwa sababu fulani huyo alikuwa mpinzani wao katika itikadi. Kwa hivyo, usione ajabu ukakuta katika baadhi ya utunzi wao riwaya ambayo mukhtasari wake ni kuwa:

Mwanamke mmoja aitwaye Zubaida kaotwa na katika uso wake kuna rangi ya njano. Akaulizwa vipi kuhusu huu umanjano? Akajibu: ‘Unajua kuna mtu anaitwa Bishr Al-Marisi kazikwa pamoja na sisi hapa basi jahannam imempuliza mpulizo ambao uliifanya ngozi yangu isisimke’. Ama kuhusu Al-Imamu Ahmad, riwaya inasema kwamba yeye kenda kumtembelea Allah na kwamba hayo ni malipo yake kwa itikadi yake ya kwamba Qur-ani si kiumbe.

Lakini jambo la kushangaza hapa katika nukulu hizo nilizozitaja na nyengine nyingi nisizozitaja, ni kuona kwamba Mawahabi wanawalaumu Mashia kwa sababu ya:

1) Ghuluwwu (kupindukia mipaka) katika riwaya za kuwasifu Maimamu wao na riwaya za kutunga, wakati riwaya za namna hio zimejaa katika vitabu vya Kiwahabi vinavyotegemewa, kama ulivyojionea mifano miwili mitatu katika nukulu hizo kuhusu Al-Imamu Ahmad na riwaya nyengine tulizozinukuu kabla.

2) Kuwakafirisha Waislamu hasa hasa Masahaba. Wakati bendera ya suala hili imeshikwa na Mawahabi na Maimamu wao watangulizi. Ingawa wao, hawawakufurishi Masahaba lakini wako Masahaba waliowajeruhi. Ninasema: bali hata baadhi ya Masahaba wanawakafirisha! Watu wa Nahrawaan ndani yake kulikuwa na Masahaba wengi kuliko makundi yote,1567 lakini pamoja na hayo Mawahabi wanawakafirisha kama ulivyoona maelezo ya Ibn Baz na Ibn ‘Uthaimin.

1567 - Rejea kitabu chetu Khawarij Baina ya Kweli Na Visa Vya Kutunga uone mifano miwili mitatu ya Masahaba waliokuwemo katika watu wa Nahrawaan ambao – kwa dhulma – wameitwa Khawaarij.

520

Page 521: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Sasa jambo la kimantiki la kujiuliza ni kwamba ikiwa Shia wamekuwa wabaya kwa kuwaponda baadhi ya Masahaba, kwanini Mawahabi wasiwe wabaya zaidi kwa itikadi yao ya kumsema Allah kuwa ana sura ya binaadamu – kamuumba Adam kwa sura yake. Nani hapa kenda mbali zaidi?

Baada ya hayo, elewa kwamba riwaya hizo nilizokunukulia hapa, inawezekana ikawa Mawahabi nyengine hawazikubali navyo ndivyo dhahir inavyoonesha; au ikawa zote hawazikubali au ikawa wanazikubali zote. Kwa hali yoyote ile, hilo silo ninalotaka kukuthibitishia hapa: ninalotaka kukuthibitisha hapa ni kuwepo kwa utunzi mkubwa wa riwaya katika skuli hii ya Kihanbali/Kiwahabi pamoja na mujassima kwa ujumla. Kwa hivyo, namwambia bwana Mafuta kwamba ushahidi uliowazi kabisa unathibitisha kwamba:

1) Utunzi wa riwaya za uzushi na uwongo uko katika skuli yenu.2) Mashekhe wenu na Maimamu wenu ndio waliofanya ghushi na

udanganyifu kama tulivyobainisha kwa kuyanukuu maneno yao herufi moja moja.

3) Walioitwa Khawaarij kwa ujumla na Ibadhi hasa hasa hawakuwa na tabia hio.

4) Uliouita wewe kuwa ni uwongo, katika nukulu ya Al-Imamu Badru Al-Din Al-Khalili ya ubeti wa Ibn Al-Qayyim, nimekubainishia kwamba alichokisema kipo: si uwongo. Tatizo unalo wewe mwenye, tafadhali irejee nafsi yako tena na tena na ukumbuke unakokwenda.

5) Nukulu alioitaja Al-Imamu Al-Qannubi kutoka kwa Al-Albani imo katika kitabu cha Al-Albani herufi moja moja.

6) Kwa haya machache, natarajia kwamba mwongo na mkweli wamebainika kwa kila mwenye akili yake timamu.

521

Page 522: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

MUKHTASARI WA UJUMLA

Baada ya kuzunguka pamoja nawe ndugu msomaji katika kuzipekuwa kurasa za kitabu hiki, sina budi kusema kwamba kila muadilifu mwenye kutaka haki na kuutupilia mbali ushabiki na umadhehebu inambainikia kwa uwazi kabisa kwamba muandishi wa kitabu Hoja Zenye Nguvu Katika Kuthibitisha Kuonekana Allah (Sub’haana Wata’alaa) Kwa Macho Huko Akhera, hakuweza kuthibitisha chochote katika yale alioyadai ambayo tumeyajadili humu. Kama utavyoona katika juzuu nyengine za kitabu hiki in shaa Allah kwamba madai yake mengine yote hayakujengeka katika misingi sahihi ya uchambuzi wa kielimu. Kitabu hiki nimekigawa katika utangulizi, sura kumi na nne, mukhtasari wa ujumla na hatima:

Utangulizi: unazungumzia umuhimu wa itikadi katika maisha ya Muislamu na ya binaadaamu kwa ujumla. Pia unazungumzia jinsi gani itikadi batili ambazo ziko kinyume na itikadi sahihi ya Kiislamu ziliweza kupenya katika Umma huu. Sehemu hii pia inazungumzia mukhtasari wa baadhi ya kasoro zilizomo katika kitabu cha Kasim Mafuta. Sura ya kwanza: inajadili suala kuwepo kwa makosa ya majina ya wapokezi katika kitabu changu. Nimewajibu wahusika kwamba:

522

Page 523: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

a) Wakuu wetu, kama Al-Bukhari, Al-Imamu Malik na wengine tuliowataja humu, wamekosea mno kuliko mimi katika suala hili.

b) Maimamu wao kama Al-Albani na Ibn Al-Qayyim pia wamekosea katika suala hili.

c) Al-Albani kazidi kufanya makosa kwa wingi mno, tena makosa yake si katika majina ya wapokezi tu, bali na katika hukumu za Hadithi pia.

d) Al-Albani kajigonga mno kupita kiumbe yoyote yule aliyejishughulisha na elimu ya Hadithi.

e) Al-Albani hazijui hata Hadithi zilizomo katika Al-Bukhari na Muslim.

f) Al-Albani anaonekana si mtu wa kupekuwa vitabu bali anatazama yaliyomo (table of contents) kisha anasahihisha na kudhoofisha!

Sura ya pili: inazungumzia itikadi za Kiwahabi za kumshabihisha Allah na viumbe. Tumeona kwamba Maimamu wao wanasema kwa uwazi kwamba:

a) Mungu ni kiwiliwili si kama viwiliwili.b) Kiwiliwili hicho kinabebwa na Malaika nacho kiko juu ya kiti.c) Kiwiliwili hicho ni kizito wakisimama washirikina katika ibada zao.d) Wakisimama Waislamu katika ibada zao kinakuwa chepesi.e) Malaika hawakiwezi mpaka wafundishwe kumtaja Allah utajo

maalum.f) Kiwiliwili hicho kina viungo vyote alivyonavyo binaadamu

isipokuwa ndevu na uchi.g) Kikitaka kinakaa juu ya bawa la mbu. h) Kina sura ya Adam.i) Kinakwenda kwa miguu.j) Kinapanda na kushuka na kukaa kitako.

Sura ya tatu: inazungumzia falsafa ya balkafa. Yaani wenye itikadi hizo wanasema kwamba pamoja na kuwa Allah yuko hivyo lakini si kama tunavyojua sisi, yaani hafanani na kitu! Nasi tumebainisha kwamba:

a) Huo ni mgongano kwani hakuna katika akili wala lugha kusema: “Kina usukani, na maringi” lakini hakifanani na gari; au “Una majani, kigogo na matunda” lakini haufanani na mti.

b) Wao wenyewe wameshindwa kujizuia kutokana na kumfananisha mungu mwenye sifa hizo na viumbe, na kwa hivyo, wakasema kuwa “Adam kaumbwa kwa sura ya Allah”.

c) Kanuni hio “Mkono si kama tuujuao” haiko katika lugha ya Kiarabu, bali kilichoko ni:

d) Mkono hakika. Nao ni ule unaofahamika katika lugha ambao ni mfupa na nyama.

523

Page 524: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

e) Mkono si hakika (majazi). Nao ni pale linapotumika neno mkono lakini ikawa maana iliokusudiwa ni maana nyengine.

Sura ya nne: inazungumzia natija mbili za hatari zilizojitokeza katika ulimwengu wa itikadi. Moja ni suala mungu atayetia mguu wake kwenye moto wa jahannam! Jambo ambalo Wakiristo waliwajadili Waislamu nao hawakuweza kutoa jawabu ya wazi. Pili ni suala la kwamba itikadi ya mungu mwenye viungo ni lazima itamfanya mtu amfikirie mungu huyo kuwa ana sura ya binaadamu. Na hiki ndicho kilichotokea ambapo Ibn Taymiyya, Ibn Al-Qayyim, Al-Tuwaijri dhahir na Ibn Baz na wengine wamekuwa na itikadi hio. Kuhusu suala la mwanzo tumetoa jawabu ambayo ufupisho wake ni kama ifuatavyo:

a) Qur-ani ndio msingi mama; ama Hadithi inapimwa kwa Qur-ani wala si kwamba Qur-ani inapimwa kwa Hadithi.

b) Hadithi ziko sahihi na ziko dhaifu.c) Hadithi ya kwamba Allah atatia mguu wake kwenye moto ina

khilafu za wanavyuoni katika usahihi wake; kama vile ambavyo wale wenye kuiona kuwa hio ni Hadithi sahihi pia wanatafautiana kuhusu maana yake.

d) Itikadi hio ya kuwa Allah atatia mguu wake kwenye moto kweli kweli ni itikadi ya Mawahabi tu na Maimamu wao: haiwahusu Umma mzima.

Sura ya tano: inazungumzia nini maana ya tashbihi (kumfananisha Mungu na kiumbe). Watu wa itikadi ya tajsim wamedai kwamba tashbihi si kusema kuwa Allah ana mkono, bali ni kusema kuwa Allah ana mkono kama wangu. Tumebainisha kwamba:

d) Tashbihun baliigh – kwa mujibu wa lugha ya Kiarabu – ni tashbihi wala hakuna ndani yake muundo huo.

e) Tashbihi inakuwa sariih (ya wazi) kama hio waliodai wao, na inakuwa dhimni (ambayo imo katika maneno wala haikutamkwa kwa uwazi).

f) Tumethibitisha hilo kwa kutoa mfano wa maneno ya Ibn Al-Qayyim.

g) Tumesema kwamba hata kama kweli ilikuwa tashbihi ni kusema kuwa ana mkono kama wangu, basi mfumo huo uko katika riwaya nyingi za Kiwahabi.

h) Ibn Taymiyya kasema kwa uwazi: “Allah anateremka kama ninavyoteremka mimi”. Na hii bila shaka yoyote ile ni tashbih ya wazi.

i) Ni wazi kwamba madhehebu hii ya Kiwahabi na Maimamu wao ni mushabbiha, mujassima.

524

Page 525: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Sura ya sita: inazungumzia mjadala kuhusu kuwepo au kutokuwepo kwa majazi katika Qur-ani, Hadithi na lugha ya Kiarabu. Tumesema:

a) Majazi ni kulitumia neno kinyume na maana yake ya asili.b) Maneno yaliotumika namna hio yako kwa wingi mno katika

Qur-ani, Hadithi na lugha ya Waarabu. c) Tumetoa mifano mingi kama vile kutumika neno kamba kwa

maana ya dini na kwa maana ya msaada.d) Sheikh Kasim Mafuta hakutoa hoja yoyote ile ya msingi

isipokuwa falsafa za Kiyunani!e) Hao walioyakataa majazi katika baadhi ya vitabu vyao

wamejigonga sana wakayatumia na kuyataja kwa jina lake katika vitabu vyao vyengine.

Sura ya saba: ni kuhusu kuwepo au kutokuwepo kwa ta-awil kwa wanavyuoni watangulizi (Masahaba na wafuasi wao). Tumethibitisha kwamba Al-Salaf (watangulizi) wamezifanyia ta-awil Aya kadha wa kadha. Sura ya nane: inazungumzia kuhusu misimamo ya madhehebu za Kisuni kuhusu itikadi za tajsiim (mungu-mwenye-viungo). Tumeona kwamba:

a) Ahlu Al-Sunna Wal-Jamaa’a hawakubaliani na itikadi hizo.b) Hizo ni itikadi za baadhi ya watu wa madhehebu ya Hanbali na

mmoja mmoja katika watu wa madhehebu nyengine.Sura ya tisa: inazungumzia tatizo lililoko katika madhehebu ya Kiwahabi na Maimamu wao watangulizi la kuwakafirisha Waislamu wote wa Umma isipokuwa wafuasi wa madhehebu yao. Na hii ni moja ya sababu zinazowafanya Waislamu kutokuwakubali Mawahabi, kwani ni jambo ambalo liko kinyume na mafunzo ya Allah na Mtume wake; nalo ni katika majarima makubwa yalioje.

Sura ya kumi: inazungumzia jinsi gani Mawahabi wamejigonga katika minhaj (njia za kufasiria maandiko) na katika itikadi zao. Jambo hili linathibitisha kwamba hawako katika haki kabisa.

Sura ya kumi na moja: inazungumzia kuhusu itikadi ya Ibn Taymiyya ya kutangulia kwa AINA ya ulimwengu; na kosa la Ibn Al-Qayyim la kifasiri Aya “Wamemsahau Allah Naye akawasahau” kwa udhahiri wake.

a) Tumethibitisha vya kutosha kwamba hakuna cha uwongo katika yale tulioyanena kuhusu Ibn Taymiyya.

b) Tumetoa nukulu za kutosha ambazo ziko wazi juu suala hili. c) Tumethibitisha kwamba maneno ya Ibn Al-Qayyim – kwa mujibu

wa qarina yake – haiwezekani kusema kwamba yeye kakusudia

525

Page 526: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

kulitumia neno nisyaan (kusahau) kwa maana ya “kuwacha”, tafauti na alivyodai Kasim Mafuta.

Sura ya kumi na mbili: inazungumzia kuhusu tuhuma za uwongo alizozitoa Kasim Mafuta dhidi ya Wanachuoni wacha Mungu Al-Imamu Badru Al-Din Al-Khalili na Al-Imamu Al-Hujja Al-Qannubi. Tumethibitisha kwamba:

a) Ubeti aliodai Kasim Mafuta kuwa Sheikh Al-Khalili kaupindua, hauna tafauti ya kimaana na ubeti uliomo katika Nuniyya ya Ibn Al-Qayyim.

b) Beti zote mbili zina maana ya kuwakafirisha Waislamu wote, na kwamba bora Mayahudi na Wakiristo kuliko Waislamu wenye itikadi tafauti na ile ya Ibn Al-Qayyim – itikadi ya mungu-mwenye-viungo!

c) Kasim Mafuta alipoyajua hayo, kafanya ghushi akanukuu beti moja na kuiacha ya pili ambapo mjumuiko wa beti hizo ndio unaoleta maana sawa na ile alioielezea Sheikh Al-Khalili.

d) Ubeti huo aliounukuu Sheikh Al-Khalili umo katika kitabu Al-Saif Al-Saqiil cha Al-Subki aliyeishi katika zama moja na Ibn Al-Qayyim, naye kakiandika kitabu hicho ili kumjibu Ibn Al-Qayyim.

e) Ibn Al-Qayyim hakusema kumwambia Al-Subki kwamba umenizulia uwongo. Hii ina maana kwamba:

f) Ubeti huo ni moja kati ya riwaya zake.g) Au Ibn Al-Qayyim hakuona kwamba kuna tafauti ya maana baina

beti mbili hizo.h) Kuhusu nukulu ya Al-Qannubi tumesema kwamba alichokinukuu

kutoka kwa Al-Albani ni “Hammad anakosea sana” au “Ana makosa mengi”. Tumethibitisha kwamba mneno hayo yamo katika kitabu Dhaifa cha Al-Albani: haikuzidi hata herufi moja wala haikupungua, isipokuwa marekebisho ya nahau.

i) Lakini Al-Albani baada ya kukiri hivyo, bado kamtetea Hammad bin Salama.

j) Kilichobaki ni kujua je kumtetea kwake kuna uzito katika uwanja wa elimu ya Hadithi au hakuna uzito wowote ule?

k) Hilo tutalibainisha tukifika sehemu yake in shaa Allah.

Sura ya kumi na tatu: inajadili na kuthibitisha ukweli wa tukio la mkutano wa Ibn Baz na Al-Khalili na kwamba Al-Khalili alimtaka Ibn Baz wafanye mjadala na wafanye mubahala, lakini Ibn Baz akanywea!

Sura ya kumi na nne: inathibitisha kwa ushahidi kwamba Mawahabi na Maimamu wao ndio wasiosema kweli, na kwamba riwaya za kutunga kwao zimekithiri.

526

Page 527: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

HATIMAHadi hapa ndugu msomaji tutakuwa tumefika mwisho wa juzuu ya kwanza ya jawabu yetu hii kwa Kasim Mafuta na hizbu yake. Tunamuomba Allah atupokelee kazi yetu hii na aijaalie kuwa khaalisan liwajhih, na awazindue Waislamu kwayo waione njia ya haki. Na wale waliochukuliwa na mkumbo wa Kiwahabi kwa uchache wa elimu au kwa ufahamu finyu Allah awape nuru na kuiona haki na kuifuata.

Kitabu hiki ni juzuu ya kwanza. Kitafuatiwa na juzuu nyengine tatu. Na juzuu inayohusu kuonekana kwa Allah itakuwa ni juzuu ya mwisho: juzuu ya nne. Lakini huenda nikaitayarisha1568 na kuitoa kabla ya juzuu ya pili na ya tatu, kwani maudhui ya kuonekana au kutoonekana kwa Allah ndio maudhui ya asili ya mjadala huu.

Ninamshukuru Allah kwa kuniwezesha kuimaliza kazi hii. Hiki ni kitabu pekee ambacho nimekiandika katika hali ya tabu kwa sababu ya matatizo ya kifamilia na ya kiafya na pia kwa kutokuwepo katika nchi ninayoishi kwa kipindi si kidogo. Kwa hivyo, sina budi kukariri kumshukuru Allah tena na tena ilhali natambua kwamba hakuna anayeweza kumshukuru Allah kwa neema zake kama anavyopaswa kushukuriwa.

1568 - Na nimeshaianza.

527

Page 528: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

Tunamsalia na kumtakia rehema Mtume wetu Muhammad (s.a.w.) pamoja na Masahaba wake na watu wa nyumba yake. Na tunawaombea ndugu zetu wote wenye itikadi za kumshabihisha Allah kwamba Allah awaongoze na kuwapa nuru katika mioyo yao. Aamin!

Juma Muhammad Rashid Al-MazruiTel: (00968) 92213669.E. Mail: [email protected]@yahoo.comAl-Qurm Muscat Oman.Tarehe 3/7/2010.

VITABU VYENGINE VYA MUANDISHI

1) Hoja Zenye Nguvu Juu Ya Kutoonekana Mwenyezi Mungu Kwa Macho.

2) Kisimamo Katika Sala. (Jawabu kwa waliosema kuwa wasionyanyua mikono wakati wa kusali wanasali kama mipopoo).

3) Hali Sahihi Ya Kimaumbile. (Kubainisha uharamu wa maingiliano ya kindoa kwa njia isio ya kawaida).

4) Mezani Ya Haki. (Kinatoa ufafanuzi juu ya Hadithi Thaqalain na juu ya Ahlu Al-Bait).

5) Ushahidi Uliowekwa Wazi. (Kinazungumzia kuhusu suala la miandamo ya mwezi, na je muandamo mmoja unatosheleza duniani kote au kila eneo fulani na muandamo wake).

6) Jawabu Yetu. (Kinatoa jawabu kwa wale waliotoa kitabu chao ili kukijibu kitabu changu cha mwezi Ushahidi Uliowekwa Wazi).

7) Ukhalifa. (Hakijachapishwa. Kinazungumzia suala la kuwa je Mtume s.a.w. aliacha ujumbe wa kuwa fulani ndio awe khalifa baada yake).

8) Hukumu Za Sala ya Safari. (Hakijachapishwa).9) Fimbo Ya Musa ( موسى .(عصا (Juzuu nne, ndio kitabu hiki

kilichomo mikononi mwako).10) Sherehe Na Maelezo Ya Tafsiri Ya Sheikh Abdullah Salih Al-

Farisi. (Iko Mwanzoni).

528

Page 529: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

11) Al-Khawarij Reality Or Legend. (Juzuu tisa kwa lugha ya kiingereza, nacho ni tafsiri ya kitabu chetu Khawarij Baina Ya Ukweli Na Visa Vya Kutunga. Hadi sasa kimetoka juzuu ya kwanza na yapili).

12) Khawarij Baina Ya Ukweli Na Visa Vya Kutunga. (Juzuu nne, kinahusu suala la wanaoitwa Khawarij, na historia yao na riwaya zilizopokewa juu ya suala hili. Hadi sasa imechapishwa juzuu ya kwanza).

ZINAZOFUATA NI BAADHI YA SCANNED COPIES AMBAZO NILIAHIDI KUZIWEKA MWISHONI MWA KITABU

1) Kopi ya kwanza, ya pili na ya tatu zinatoka katika kitabu cha Al-Albani ambapo alisema kwamba1569 أوهام له حمادا Hammad إنbin Salama ana awham (ana makosa mengi).1570 Kasim Mafuta kadai kuwa huo ni uwongo wangu mimi na Sheikh wangu Al-Qannubi. Sasa tazama kopi hio1571 je maneno hayo yamo au hayamo?

2) Kopi ya nne,1572 ya tano na ya sita ni kopi za fata-wa za Ibn Baz na wenzake ambayo ndani yake waliwakafirisha Maibadhi si kwa matamshi ya wazi kama tulivyoeleza katika kitabu.

3) Kopi ya saba ni maneno ya Al-Jibrin wa Suudia aliyowakafirisha Maibadhi. Fat-wa hio iko katika web site yake rasmi.

4) Kopi ya nane1573 na ya tisa ni kopi za kitabu Al-Saifu Al-Saqiil cha Al-Imamu Al-Subki. Kopi hio ina ubeti wa qasida ambayo Kasim Mafuta kadai kuwa Sheikh Al-Khalili kaupindua na kwa hivyo kasema uwongo. Tumetoa majibu ya kutosha juu ya hilo katika kitabu hiki na hapa tunakunakilia ubeti huo kwa kukufanyia scanned copy.

1569 - Tumesema kwamba Al-Albani yeye kasema أوهاما له حماد nayo ni makosa ya إنkinahau na sahihi ni hivyo tulivyoandika.1570 - Kopi ya kwanza ni kopi ya gamba la kitabu hicho.

1571 - Kopi ya tatu msitari wa pili. 1572 - Kopi ya nne ni kopi ya gamba la kitabu hicho. 1573 - Kopi ya nane ni kopi ya gamba la kitabu hicho.

529

Page 530: xa.yimg.comxa.yimg.com/kq/groups/9596131/1664572042/name/FIMBO+YA... · Web viewتلقف ما يأفكون . FIMBO YA MUSA. INAYAMEZA WANAYOYAZUSHA. JUZUU YA KWANZA. Juma Muhammad

TANBIHI

Scanned copies za vitabu zimenishinda kuziupload kwa hivyo hapa katika makala hii nimezitoa. In shaa Allah tutazisoma katika hard copy.

530