333
Namna Ya Swala Ya Mtume عليه وسلم ا ص IKIELEZWA Kuanzia Takbira Mpaka Kutoa Salamu Kana Kwamba Unaiona عليه وسلم ا ص هاأنك تراتسليم ك ال إ من التكبKimetungwa Na: SHEIKH MUHAMMAD NÂSIR-UD-DÎN AL-ALBÂNI ( رحمه ا) Kimefasiriwa Na: ABU FARIDA MUHAMMAD AWADH SALIM BASAWAD

Ya Mtume - QSSEA Ya Swala Ya Mtume.pdf · 2019-05-25 · Namna Ya Swala Ya Mtume ملسو هيلع للها لىص IKIELEZWA Kuanzia Takbira Mpaka Kutoa Salamu Kana Kwamba Unaiona

  • Upload
    others

  • View
    96

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Namna Ya Swala Ya Mtume

صىل اهلل عليه وسلم

IKIELEZWA

Kuanzia Takbira Mpaka Kutoa Salamu Kana Kwamba

Unaiona

صىل اهلل عليه وسلم

من التكبري إىل التسليم كأنك تراها

Kimetungwa Na:

SHEIKH MUHAMMAD NÂSIR-UD-DÎN AL-ALBÂNI (رحمه اهلل)

Kimefasiriwa Na:

ABU FARIDA MUHAMMAD AWADH SALIM BASAWAD

© HAKI YA UCHAPISHAJI Uchapishaji wa kitabu hiki ni milki ya kiufundi ya “THE QURAN AND SUNNAH SOCIETY OF EAST AFRICA”. Kila kilichomo ndani, kwa ujumla, ni hifadhi ya qssea. Hairuhusiwi kuiga kwa njia yoyote iwayo kutoka kwa wachapishaji asili; hivyobasi uchapishaji wa kitabu hiki utahitaji ridhâ kutoka kwa muandishi. Iwapo chochote kutoka kwenye kitabu hiki kitatumiwa kama sehemu ya shirika jengine la kiufundi ama isokuwa hivyo, basi ruhusa kutoka QSSEA itahitajika. Ruhusa inaweza kuombwa kutoka kwa: The Qur‘ân and Sunnah Society of East Africa, P. O. Box 85477, Mombasa, Kenya. Nambari ya Simu ni 1.647.632.3863 Ama kwa Barua Pepe (e-mail)- [email protected] web-site – www.qssea.net Chapa ya Pili: Nakala 1000 [2017 / 1438] ISBN 978-9966-1824-0-1

JUMUIYA YA QUR’ÂN NA SUNNAH YA AFRIKA YA MASHARIKI

I

YALIYOMO

MAISHA YA SHEIKH AL-ALBÂNI (رحمه اهلل) ....................................... I

KUHAMA KWAKE HADI SYRIA ................................................ III

MWANZO WA KIU YAKE YA ‗ILMU ........................................... IV

WATOTO WAKE ............................................................... VI

KIPA-UMBELE IWE NI HAKI KULIKO MILA ZA WAZEE ..................... VII

SHEIKH AL-ALBÂNI NA BABAKE ............................................. VII

MWANZO WA KAZI YAKE .................................................... VIII

KUMLINGANIA ALLÂH, ALIYE JUU ZAIDI.................................... IX

KUENEA KWA DA‘WAH NJE YA DAMASCUS ................................ IX

BAADHI YA UGOMVI ULIOMKABILI SHEIKH .................................. X

SHEIKH UL-ISLÂM NA SHEIKH AL-ALBÂNI WAFUNGWA KWENYE GEREZA MOJA ........................................................................... XI

KIFUNGO CHA NDANI ........................................................ XII

SHEIKH ACHAGULIWA KAMA MHADHIRI KATIKA CHUO KIKUU CHA MADINAH ...................................................................... XII

MASHEIKH ZAKE WAKIFAIDIKA KUTOKA KWAKE ......................... XIII

ALIYOKUWA AKIYASEMA PINDI ANAPOSIFIWA ............................ XIII

KUHAMA KWAKE KUTOKA DAMASCUS HADI KATIKA MJI WA AMMAN, JORDAN ....................................................................... XIII

II

KURUDI KWAKE KWA GHAFULA KUTOKA AMMAN HADI DAMASCUS NA KISHA KUELEKEA LEBANON ................................................. XV

MIKASA, MMOJA BAADA YA MWENGINE, ILIYOMKUMBA SHEIKH AKIWA LEBANON ..................................................................... XVI

KUKIMBIA KWAKE KUTOKA KWENYE NJAMA ZA KUULIWA NCHINI BEIRUT ...................................................................... XVIII

KUHAMA KUTOKA BEIRUT HADI EMIRATES ............................. XVIII

UADILIFU NA MSIMAMO WAKE WA HAKI ................................. XVIII

MFUMO WAKE KUHUSIANA NA KUZIORODHESHA HADÎTH .............. XIX

UMUHIMU WA WAKATI ...................................................... XIX

MFUMO WAKE KATIKA KUZIORODHESHA HADÎTH KATIKA UKUSANYAJI WAKE WA HADÎTH KWA JINA LA AS-SILSILAH NA ADH-DHA‟ÎFAH ..... XIX

MIFANO YA SUBIRA ZAKE ................................................... XX

SHEIKH AL-ALBÂNI AULIZWA KUHUSU HADÎTH NA BABAKE ............ XX

SHEIKH MUSTAFÂ AZ-ZARQÂ AMUULIZA KUHUSU HADÎTH .............. XX

SAFARI ZAKE KATIKA KUTAFUTA ‗ILMU ................................... XXI EGYPT [MISRI] ............................................................. XXI ALEPPO..................................................................... XXI

SAFARI YAKE YA KUELEKEA BAITAL-MAQDIS [JERUSALEM] ............ XXII SPAIN ...................................................................... XXII MOROCCO ................................................................. XXII QATAR ..................................................................... XXII SAFARI YAKE YA PILI KUELEKEA EMIRATES ........................... XXII

KUVUMILIA KWAKE KATIKA KUTAFUTA ‗ILMU ........................... XXII

III

MRADI ALIOJITOLEA MAISHA YAKE KWA DHATI, ‗KATIKA KUIKURUBISHA SUNNAH KWA UMMAH‘ .................................................... XXIV

LENGO LAKE KATIKA MAISHA .............................................. XXV

NASWIHA YAKE KWA UMMAH ............................................. XXVI

SHEIKH AL-ALBÂNI HAKUWA NI KIONGOZI WA POTE WALA KUNDI LOLOTE ..................................................................... XXVI

KATIKA KUSOMA BAADHI YA VITABU VYA MUSNAD ................... XXVII MUSNAD YA ABU YA‘LÂ ............................................... XXVII MUSNAD YA IBN ABÎ SHAYBAH........................................ XXVII

KUSWALI ISTIKHÂRAH NINAPOHUKUMU JUU YA HADÎTH ............ XXVII

KUFUATA KWAKE KITÂB NA SUNNAH NA KUTUPILIA MBALI KUFUATA KI-UPOFU ..................................................................... XXVIII

KUVIFANYA VITABU KUWA NI MSHIRIKA WAKE NA MARAFIKI ZAKE .. XXIX

KISA CHA KARATASI ILIYOPOTEA ......................................... XXX

AL-ALBÂNI NA ABDUL-FATTÂH ABU GHUDDAH ....................... XXXIV

AL-ALBÂNI NA MUHUBIRI [KHATÎB] ..................................... XXXV

AL-ALBÂNI NA WALE WALIOKUWA NA WIVU NAYE .................. XXXVII

KUTOJALI KWAKE JUU YA WAYASEMAYO WATU WAKATI ANPOJUA ............................................................................ XXXVIII

MKOSI ULIOMPATA AKIWA AMMAN.................................... XXXVIII

ULINGANIZI WAKE ...................................................... XXXVIII

UTAKASO NA MALEZI ..................................................... XXXIX

HAMU YAKE YA KUITEKELEZA SUNNAH ................................... XLI

IV

BAADHI YA SUNNAH ALIZOZIHUISHA ...................................... XLI KHUTBA YA HAJA (KHUTBATUL-HÂJAH) ............................... XLI KUSWALI SWALA YA ‗IDD KATIKA MUSWALLÂ ......................... XLI

KISA CHA KUCHEKESHA NA KUHUZUNISHA WAKATI HUOHUO ......... XLI

MUKHTASAR WA MWISHO .................................................. XLII

DIBAJI ............................................................................ I

UTANGULIZI ................................................................... III

SABABU ZILIZOCHANGIA KATIKA UTUNGAJI WA KITABU HIKI NA BAADHI YA MIPANGILIO YAKE ........................................................ VIII

MFUMO WA KITABU HIKI .................................................... XIII

MISEMO YA MA-IMAAM KUHUSU KUFUATA SUNNAH NA KUWACHANA NA RAI ZAO ZENYE KWENDA KINYUME NA SUNNAH ......................... XVI

ABU HANEEFAH (رحمه اهلل) ................................................... XVIII

MAALIK IBN ANAS (رحمه اهلل).................................................. XXII

SHAAFI‘EE (رحمه اهلل) ......................................................... XXIV

AHMAD IBN HANBAL (رحمه اهلل) .............................................. XXX

WAFUASI WA MA-IMAAM WAKIJIEPUSHA NA MAONI YA MA-IMAAM IWAPO YANAKHALIFU SUNNAH .......................................... XXXVI

UTATUZI WA TASHWISHI ZILIZOKO ......................................... XL

SHUB‘HA YA KWANZA ........................................................ XL

V

SHUB‘HA YA PILI ............................................................ XLII

SHUB‘HA YA TATU ............................................................ LI

SHUB‘HA YA NNE ............................................................ LIII

KUELEKEA AL-KA‘BAH ......................................................... 0

KUSIMAMA NDANI YA SWALA ................................................. 3

SWALA YA MTU MGONJWA AKIWA AMEKETI ................................ 4

KUSWALI NDANI YA JAHAZI ................................................... 6

KIKAO NA KISIMAMO NDANI YA SWALA YA USIKU (TAHAJJUD) ........... 6

KUSWALI NA VIATU NA AMRI YA KUFANYA HIVYO ......................... 7

KUSWALI JUU YA MINBAR ..................................................... 9

SUTRAH (KIZUWIZI) NA UWAJIBU WAKE (WA KUIWEKA MBELE YAKE) . 10

MAMBO YENYE KUHARIBU SWALA .......................................... 14

MAKATAZO YA KUSWALI UKIWA UMEELEKEA KABURI .................... 14

NIYA ............................................................................ 14

TAKBEER ....................................................................... 15

KUINUA MIKONO MIWILI ...................................................... 16

KUWEKA MKONO WA KULIA JUU YA MKONO WA KUSHOTO NA KUAMRISHA KUFANYA HIVYO ................................................ 17

KUWEKA MIKONO MIWILI JUU YA KIFUA ................................... 18

VI

KUTIZAMA MAHALI PA KUSUJUDU NA UNYENYEKEVU .................... 19

DUA‘ ZA KUANZA SWALA .................................................... 22

KUSOMA ........................................................................ 31

KUSOMA AYA MOJA BAADA YA NYENGINE ................................. 32

NGUZO YA FAATIHAH NA FADHLA ZA SOORAH AL-FAATIHAH ........... 33

KUFUTWA HUKMU YA KUSOMA NYUMA YA IMAAM KATIKA SWALA ZA KUDHIHIRISHA SAUTI ......................................................... 37

Uwajibu Wa Kusoma Katika Swala Za Kutodhihirisha Sauti (Swala Za Siri) ............................................................................. 39

KUITIKIA IMAAM ―AAMEEN‖ KAMA WANAVYOITIKIA MA‘MOOM KWA SAUTI ........................................................................... 41

KISOMO CHAKE ( سلمصىل اهلل عليه و ) BAADA YA FAATIHAH ....................... 43

KUKUSANYA SOORAH ZILIZOFANANA NA NYENGINE KATIKA RAKAA‘AH MOJA ........................................................................... 46

KURUHUSIWA KUSOMA AL-FAATIHAH PEKE YAKE ........................ 48

KUSOMA KWA SIRI NA KWA SAUTI KATIKA SWALA TANO NA NYENGINEZO .................................................................. 50

KUSOMA KWA SIRI NA KWA SAUTI KATIKA SWALA YA USIKU (TAHAJJUD) .................................................................................. 51

SURA ALIZOKUWA AKISOMA (صىل اهلل عليه وسلم) KATIKA SWALA TAFAUTI .... 52

Swala Ya Fajr ................................................................. 52

VII

Kusoma Katika Swala Ya Sunnah Ya Kabla ya Fajr ....................... 55

Swala Ya Dhuhr ............................................................... 57

KUSOMA KWA MTUME (صىل اهلل عليه وسلم), AAYAAT BAADA YA SOORAH AL-

FAATIHAH KATIKA RAKAA‘AH MBILI ZA MWISHO. ......................... 58

Swala Ya ‗Asr ................................................................. 60

Swala Ya Maghrib ............................................................. 61

Kisomo Katika Swala Ya Sunnah Ya Ba‘dal Maghrib ..................... 62

SWALA YA ‗ISH‘ ............................................................. 62

Swala Ya Usiku (Tahajjud) .................................................. 64

Swala Ya Witr ................................................................. 70

Swala Ya Jumu‘ah ............................................................ 71

Swala Ya ‗Eid ................................................................. 72

Swala Ya Janaazah ........................................................... 73

Tarteel (Kuisoma Kwa Utulivu, Na Sauti Nzuri), Na Kuifanya Sauti Iwe Ni Ya Kuvutia Wakati Wa Kuisoma ......................................... 73

KUMKUMBUSHA IMAAM ....................................................... 77

KUTAKA HIFADHA NA KUTEMA MATE (KWA KUVUVIA) KATIKA SWALA KWA AJILI YA KUONDOSHA WASIWASI ..................................... 77

KU-RUKUU ..................................................................... 78

Namna Ya Ku-Rukuu ......................................................... 79

VIII

Waajib Wa Kutulizana Katika Rukuu ....................................... 80

Adhkaar Zinazoletwa Katika Rukuu ........................................ 82

Kurefusha Rukuu ............................................................. 85

Makatazo Ya Kuisoma Qur‘aan Katika Ku-Rukuu ......................... 86

KUSIMAMA WIMA KUTOKA KATIKA RUKUU NA LINALOTAKIWA KUSEMWA BAADA YA HAPO .............................................................. 86

KUREFUSHA KISIMAMO HIKI NA WAAJIB WA KUTULIZANA NDANI YAKE 93

KU-SUJUDU .................................................................... 95

Kupomoka hali ya kwenda kwenye Sajdah Kwa Mikono ................ 96

Namna Ya ku-Sujudu ......................................................... 97

Waajib Wa Kutulizana Katika ku-Sujudu ................................ 101

Dhikr Za Kusujudu. ......................................................... 101

Makatazo Ya Kuisoma Qur‘aan Katika Kusujudu. ...................... 106

Kurefusha Kusujudu. ....................................................... 106

Fadhla Za Kusujudu ........................................................ 108

Kusujudu Juu ya Ardhi na Juu ya Zuliya ................................ 109

KUINUKA KUTOKA KWENYE SAJDAH ...................................... 110

Kukaa muftarishan Baina Ya Sijda Mbili ................................. 111

Kikao Cha Iq‘aa‘ Baina Ya Sijda Mbili ................................... 112

Waajib Wa Kutulizana Baina Ya Sijda Mbili ............................. 112

IX

Kurefusha Kikao Baina Ya Sijda Mbili .................................... 113

Adhkaar Baina Ya Sijda Mbili ............................................ 113

SIJDA YA PILI ................................................................ 115

KIKAO CHA KUPUMZIKA .................................................... 116

KUJISAIDIA KWA MIKONO KATIKA HALI YA KUINUKA KWA RAKAA‘AH NYENGINE.................................................................... 116

RAKAA‘AH YA PILI .......................................................... 117

WAAJIB WA KUSOMA FAATIHAH KATIKA KILA RAKAA‘AH .............. 117

TASHAHHUD YA KWANZA .................................................. 118

KUTINGISHA KIDOLE KATIKA TASHAHHUD ............................... 119

WAAJIB WA TASHAHHUD YA KWANZA NA SUNNAH YA KUOMBA KATIKA WAKATI HUO ................................................................ 122

MATAMSHI YA TASHAHHUD ................................................ 123

AS-SWALAATU ‗ALAN-NABIYY (KUMSWALIA MTUME) – MAHALI PAKE NA MATAMSHI YAKE ............................................................ 130

NUKTA MUHIMU KUHUSU AS-SWALAATU ‗ALAN-NABIYY - KUMSWALIA MTUME WA UMMAH ......................................................... 135

DUA‘ KATIKA TASHAHHUD YA KWANZA .................................. 151

KUSIMAMA KWENDA KATIKA RAKAA‘AH YA TATU KISHA YA NNE ..... 152

QUNOOT KATIKA SWALA TANO KUTOKANA NA BALAA ITOKEAPO .... 153

X

QUNOOT KATIKA SWALA YA WITR ........................................ 154

TASHAHHUD YA MWISHO .................................................. 156

Uwajibu Wa Tashahhud Hii ............................................... 156

UWAJIBU WA KUMSWALIA MTUME (صىل اهلل عليه وسلم) KATIKA TASHAHHUD HII

................................................................................ 157

UWAJIBU WA KUTAFUTA HIFADHA KUTOKANA NA MAMBO MANNE KABLA YA DUA‘ ............................................................. 158

DUA‘ ZINAZOLETWA KABLA YA SALAAM NA SAMPULI ZAKE MBALI-MBALI ................................................................................ 159

TASLEEM (MAAMKUZI YA AMANI) ......................................... 167

UWAJIBU WA KUTOA SALAAM ............................................. 169

NYONGEZA ................................................................... 171

KIAMBATISHO 1 ............................................................. 172

Udhaifu Wa Ahaadeeth Zenye Kujuzisha Ikhtilaaf (Kupingana) ...... 172

Ikhtilafu Miongoni Mwa Ummah Wangu Ni Rehma.‖ .................. 172

Maswahaba Zangu Ni Kama Nyota: Yoyote Miongoni Mwao Utakaemfuata, Utaongozwa Katika Njia Ya Sawa.‖ ................... 173

KIAMBATISHO 2 ............................................................. 181

HADEETH SAHEEH: ......................................................... 181

Umepata Sawa Katika Baadhi Yake Na Umekosea Katika Baadhi Yake.‖ ................................................................................ 181

XI

KIAMBATISHO 3 ............................................................. 183

Yule mwenye kuharibu swala yake‖ (رضي اهلل عنه) ........................ 183

KIAMBATISHO 4 ............................................................. 184

Udhaifu wa hadeeth kuhusu kuweka mikono chini ya kitovu. ....... 184

Udhaifu wa ‗Abdur-Rahmaan Ibn Ishaaq al-Koofi katika mtizamo wa ma-Imaam wa Hadeeth .................................................... 185

KIAMBATISHO 5 ............................................................. 188

Udhaifu wa hadeeth zenye kushutumu Usomaji nyuma ya Imaam .. 188

TANBEEH ..................................................................... 191

KIAMBATISHO 6 ............................................................. 194

Uchambuzi wa Ahaadeeth kuhusu kusema ‗aameen kwa Imaam na Jamaa‘ah .................................................................... 194

KIAMBATISHO 7 ............................................................. 199

Rakaa‘ah Mbili za Baada Ya Witr ......................................... 199

KIAMBATISHO 8 ............................................................. 201

Udhaifu Wa Ahaadeeth Zenye Kutaja Kufuta (Upangusaji Wa) Uso Kwa Mikono Baada Ya Du‘aa‘ (Maombi) ....................................... 201

Alipokuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) Akiinua Mikono Yake Anapo Omba

Dua‘, Hayashukishi Chini Mpaka Apangusie Nayo Uso Wake.\ ....... 201

Unapomuomba Allaah, Basi Muombe Kwa Vitanga Vyako Vya Mikono, Na Wala Usiombe Kwa Migongoni Mwake, Na Unapomaliza, Jipangusie Nayo Uso Wako.\ ........................................................... 203

XII

KUMBUKUMBU ZA MUANDISHI ............................................. 206

QUR‘AAN ..................................................................... 206

TAFSEER ..................................................................... 206

SUNNAH ...................................................................... 206

FIQH .......................................................................... 211

SEERAH [Taareekh ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)) na TARAAJUM ........... 213

(Taareekh za wapokezi wa Hadeeth) .................................... 213

Lugha Ya Kiarabu ........................................................... 214

USOOL AL-FIQH (MISINGI YA FIQH) ....................................... 214

ADHKAAR .................................................................... 214

MCHANGANYIKO ............................................................ 215

I

Maisha Ya Sheikh Al-Albâni (رحمه اهلل) Kwa Maneno Yake Mwenyewe

Muandishi: „Iswâm Musa Hâdi:

Kila sifa njema zinamstahiki Allâh‎, tunamsifu yeye, na tunatafuta msaada wake na msamaha. Tunajilinda kwa Allâh‎, aliye juu zaidi, kutokamana na uovu wa nafsi zetu na kutokamana na matendo yetu maovu. Yoyote ambaye aliyeongozwa na Allâh‎, hapana awezae kumpotoa, na yoyote ambaye aliyepotoshwa na Allâh‎, hapana awezaye kumuongoza. Nashuhudia yakwamba hapana mola wa kweli apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allâh‎, peke yake, pasi na mshirika au mwenzake. Na nashuhudia yakwamba Muhammad ni mtumwa wake wa kweli na Mtume.

ة حأ ي ي ا ٱلذ ءا ا ي ٱتذ ن ۦظوذ تيةد ٱللذ ص ذ

ذ إلذ وأ ت ١٠٢ول ت

“Enyi mlioamini! Mcheni Allâh‎ kama ipasavyo kumcha; wala

msife isipokuwa mmekwishakuwa Waislamu kamili.”1

ة حأ ٱجلذةس ي ا ي ٱتذ يربذس جذهس وظدة وخو ٱلذ خيس

ا سريا ة رصةلا ة وبرذ ة زوص و ونصةءا ا ي ٱتذ ي ٱللذ ۦتصةءلن ث ٱلذ و رظةم

إنذ ٱل ر ٱللذ س ـ ١ رجاةكن

“Enyi watu! Mcheni Mola wenu ambaye amekuumbeni katika nafsi (asili) moja. Na akamuumba mkewe katika nafsi ileile. Na akaeneza wanaume wengi na wanawake kutoka

katika wawili hao. Na mcheni Allâh‎ ambae kwaye

1 Âli-‗Imrân 3:102

II

mnaombana. Na (mwatazame) jamaa. Hakika Allâh‎ ni mlinzi

juu yenu (anayaona kila mnayoyafanya).”2

لا ا ى وىل ا ٱللذ ي ا ٱتذ ءا ي ة ٱلذ حأ يص ٧٠ اشديدا ي ط س

ة ؾ ـ زا ورشلۥ ذيد نةز ن يػؿ ٱللذ و ذبس ويلهر س س ؿ ـأ

٧١ “Enyi mlioamini! Muogopeni Allâh‎ na mseme maneno

ya haki. Atakutengenezeeni vizuri vitendo vyenu na

atakusameheni madhambi yenu; Anayemtwii Allâh‎ na Mtume

wake, bila shaka amefanikiwa mafanikio makubwa.3

Ama kwa yafuatayo: Allâh‎ alinibariki mimi kwa kupata usuhuba na

mmojawapo wa washika bendera wa Sunnah wa zama hizi zetu,

Sheikh wetu, Allâmah‎‎, Mwanachuoni wa Hadîth, Muhammad Nâsir ud-

Dîn al-Albâni, twamuomba Allâh‎, aliye juu zaidi, amrehemu.

Miongoni mwa haki za Imâm huyu juu yangu mimi ni kwamba mimi nimfanye yeye, ulinganizi wake na kitu kinachotokamana na juhudi zake na uvumilivu, yote hayo, yawe yanajulikana, pamoja na matunda yaliyovunwa na Waislamu kutokamana na aliyopanda (aliyomeza), isitoshe nikaona yakwamba wanafunzi wengi wa sheikh

walikuwa tayari wameshanitangulia mimi kwa hayo, namuomba Allâh‎ awalipe mazuri. Kwahiyo, mambo ambayo na mimi sitoyakosa kwenye malipo

watakayolipwa wao, Inshâ- Allâh‎, nilitaka nifuate nyayo zao na

2 an-Nisâ‘ 4:1 3 Al-Ahzâb 33:70-71

III

ninywe kutoka kwenye kisima hicho-hicho walichokunwiya wao, kama ilivyokuwa, kwa kuandika wasifu wa sheikh wetu lakini kitu ambacho kitakachokuwa mbali kabisa na marudio yale kwa yale.

Kwahiyo nikatafuta usaidizi wa Allâh‎, nikajitayarisha kuianza kazi kwa

hima, na ikanidhihirikia yakwamba nitakayoandika yatakuwa ni maneno ya sheikh mwenyewe, kwani wasifu (habari za maisha ya mtu) ni sampuli bora zaidi ya tawasifu (habari za maisha ya mtu zilizoandikwa na yeye mwenyewe). Nikaanza kukusanya niliyoweza

kupata ambapo sheikh, Allâh‎ amrehemu, alizungumza kujihusu yeye

mwenyewe katika vitabu vyake vilivyoenea kila mahali. Alipozungumza [kujihusu yeye mwenyewe kama hivyo] ilikuwa ni kwa

njia ya kuzungumza kuhusu baraka za Allâh‎ juu yake.

Kisha nikaipanga orodha ya niliyoyakusanya kama inavyostahili, na

namuomba Allâh‎ atakase kitendo hicho changu kuwa ni kwa ajili ya

uso wake peke yake, aliye juu zaidi, na kwamba amrehemu sheikh wetu na ainyanyue daraja yake kwenye makao yake na kwamba aturehemu na sisi tutakapoishi katika maisha kama alivyokuwa yeye, yeye ni mwenye kusikia, mwenye kuyajibu maombi.

Na twaomba amani ya Allâh‎ na baraka zake zimshukie Muhammad na

maswahaba zake‖. KUHAMA KWAKE HADI SYRIA: Amesema Sheikh al-Albâni, ―Kwa

hakika baraka za Allâh‎ juu yangu ni nyingi kiasi cha kwamba siwezi

kuzihesabu. Labda miongoni mwa zilizokuwa muhimu zaidi ni mbili zifuatazo:

a) Kuhama kwa babangu na kuelekea katika nchi ya Syria.

b) Yakwamba alinifundisha kazi yake ya ufundi wa saa.

IV

[Baraka] ya kwanza ilinifanyia wepesi wa kusoma lugha ya kiarabu, kwani lau kama tungelibaki nchini nilikozaliwa, Albania, mimi siamini yakwamba ningelisoma hata herufi moja ya kiarabu, na hakuna njia

itakayokuelekeza kwenye Kitâb cha Allâh‎ au Sunnah za Mtume wake

isipokuwa kwa kupitia kwenye njia ya kiarabu. [Baraka] ,(صىل اهلل عليه وسلم)

ya pili nayo, kujifunza ilimu ya kutengeneza saa kulinipa muda wa ziyada nilioupatiliza na kutafuta ‗ilmu. Uliniongezea fursa ya kuhudhuria maktaba ya Dhâhiriyyah na maktaba nyenginezo kwa masaa mengi kila siku. Lau kama ningelibaki na kazi ya useremala, ambayo niliyojaribu kujifunza mwanzo, basi ningeliuteketeza wakati wangu wote, na matokeo yake njia za ‗ilmu zingelifungika mbele ya uso wangu, [njia] ambazo wanafunzi wake ni lazima wawe na wakati wa mapumziko.‖ MWANZO WA KIU YAKE YA „ILMU: ―Kitu cha kwanza nilichokuwa na shauku nacho kukisoma kilikuwa ni visa vya kiarabu, kama vile vya Dhâhir na Antara [Ibn Shadâd – mshairi maarufu wa kiarabu], Mfalme Sayf [Ibn Dhi Yazan] na mfano wake, kisha mas‘ala ya uhalifu au visa vya upelelezi kama vile Arsen Luprin na wengineo. Ndipo baadae nikajikuta kwenye mteremko wa kupenda kusoma vitabu vya historia. Kisha siku moja nilipokuwa kwa mwenye kuuza vitabu, niliona mas‘ala katika Jarida liitwalo al-Manâr miongoni mwa vitabu vyengine vilivyokuwa vikiuzwa, basi nikalinunua Jarida hilo. Ndani yake nikasoma sehemu fulani ya utafiti iliyoandikwa na as-Sayyid Rashîd [Ridha] ambamo alikuwa akielezea kuhusu kitabu cha Al-Ihyâ‟ cha al-Ghazâli, akitaja sehemu zake zenye nguvu na zilizo dhaifu. Kwahivyo, kwa mara ya kwanza nikakumbana na sampuli hii ya ukosoaji wa ki-ilimu na hayo yakanipelekea mimi kuyasoma mas‘ala hayo mazima. Nikaendelea kuifuatilia madda ya Ihyâ‟ katika [kitabu cha] Ihyâ‟ chenyewe, na chapa ambamo hadîth zake ziliswahihishwa na al-Hâfidh al-Irâqi, na mara nikajikuta ni mwenye kukiazima kwa sababu sikuwa na pesa za kukinunua. Matokeo yake yakawa ni kuanza kukisoma kitabu [kizima] kwani uswahihishaji wa kina ulinivutia mno, kiasi cha kwamba nikaamua

V

kukiiga kitabu au kukifanyia mukhtasari, baada ya kuvumbua taswira ya ki-akili ya kuiga ukaguzi [wa hadîth] uliochapishwa katika maandishi ya chini ya al-Ihyâ‘. Nikaanza kuiandika hadîth, “Kwa hakika kusifiwa kwa mja kunaweza kusambaa kwa umbali na kwa mapana kama kiasi kilichoko baina ya mashariki na magharibi na

wala asifike kiwango cha uzani wa mbu mbele ya Allâh‎...” hivi ndivyo

jinsi ilivyoandikwa katika Al-Ihyâ‟. Amesema al-Hâfidh al-Irâqi, ―Na mimi nimeinukuu kutoka kwake lakini nikashindwa kuiona kwa matamshi kama hayo. Katika swahîh mbili kutoka katika hadîth ya Abû Hurairah, kunapatikana, “Kwa hakika atakuja mtu mnene mwenye uzito siku ya kufufuliwa na hatofika uzani wa uzito wa

ubawa wa mbu mbele ya mtazamo wa Allâh‎.”

Lakini mimi nimefanya nini? Niliandika kistari ungio (-) na nikaikamilisha hadîth kama ipatikanavyo kwenye swahih mbili na nikaendelea hivyo ili nisije nikamnasibisha al-Hâfidh al-Irâqi na jambo ambalo hakulisema, na vilevile nikaweka nyongeza ambayo niliyoiandika kutoka katika asili aliyoinasibisha na hadîth, baina ya vistari ungio viwili [=]. Siku hizo nilikuwa ni mpya katika mambo ya utafiti na lau kama ningelijua wakati huo ninayoyajua sasa basi ningelitumia alama za mabano kama yale niliyoyatumia kwenye vitabu vyangu baada ya hapo, badala ya vistari ungio viwili. Nikaanza kunakili kisha nikafika nusu njia ya juzuu ya kwanza liliponidhihirikia wazo la kufanya hivyo, ambalo ni wakati wa shughuli zangu katika hadîth, nikapitia baadhi ya sehemu zake ambazo maneno yake sikuwa nikiyafahamu na matokeo yake yakawa maana ya makusudio ya hadîth haikuwa wazi kwangu. Kwahivyo nikajiambia nafsi yangu, ―Kwanini nisiyafafanue maneno yote haya kwenye ukingo wa kitabu yakawa ni marudio kwangu na usaidizi wa kuifahamu hadîth?‖ kwahivyo baada ya kufikia nusu njia ya juzuu ya kwanza niliiwacha na nikaanza kuinakili tena yote juu ya wazo hili jipya. Kila nilipokuwa nikiipata hadîth yenye neno ambalo nisiloweza kulielewa vyema nilikuwa nikitumia kitabu cha Ibn al-Athir Gharîb al-

VI

Hadîth [kitabu kinachofahamisha maneno adimu na magumu yanayopatikana kwenye hadîth] na makamusi, kisha nilikuwa nikiandika maana zake kwenye ukingo, mpaka maandishi niliyojiandikia nafsi yangu yakageuka na kuwa mengi zaidi hata kuliko maandishi yenyewe ya kitabu, na nikaendelea kufanya hivyo mpaka nikamaliza kitabu kizima. Niling‘ang‘ana kufanya hivyo mpaka mfano mzuri ukaasisiwa uliosaidia kuthibitisha nukta zote hizo mpya. Baada ya kufikiri juhudi hii niliyoitumia kwenye ‗ilmu hiyo ndilo jambo lililonipa mimi hima na kupendekeza kwangu kutamani kuendelea juu ya njia hiyo, kwani nilijikuta nikitafuta usaidizi wa vitabu vingi tafauti vya lugha ya kiarabu, Balagha, na vitabu vyenye kueleza maneno adimu na magumu yanayopatikana kwenye hadîth ili maandishi yapate kufahamika yakiwa pamoja na uswahihishaji wake. Na hili ndilo jambo lililonifaidisha mimi pakubwa, na kwa hakika

nasema: Nimeshangazwa na ukarimu wa Allâh‎ kwa waja wake, na

nahisi yakwamba Allâh‎ alikuwa akinisongeza mimi kutoka daraja moja

hadi nyengine. Sasa navuna faida za niliyokuwa nikiandika na kunakili, [wakati huo] mimi sikujua yaliyokuwa nyuma ya kuandika kule au kunakili kule, sasa navuna faida za baadhi ya kazi hizo. Nitakuta maandishi kutoka katika utafiti wangu wa zamani wa ki-ilimu ambao ni maridhawa tele ambao ulikuwa ni kutokana na msimamo wa kutamani kufuatilia utafiti kama huo na kwa sababu nilikuta riwaya za hadîth kuwa ni kitu cha kupendeza. Na mpaka sasa mimi naendelea, walilLaahil-Hamd, kuwa na juhudi na kupenda kufanya utafiti, ingawa utu uzima nao una haki zake.‖

WATOTO WAKE: ―Kwa hakika kutokamana na baraka za Allâh‎ ( سبحانه juu yangu mimi ni kwamba alinifanya moyo wangu kupendelea (وتعىل

kuwaita wanangu wote wa kiume kwa majina ya waja wake, nao ni: ‗Abdur-Rahmân, ‗Abdul-Latîf na ‗Abdur-Razzâq kutoka kwa mke

wangu wa kwanza ( الله رحمها ); na ‗Abdul-Muswawwir, ‗Abdul-Muhaymin

VII

na ‗Abdul- A‘Laa kutoka kwa mke wangu mwengine, na sidhani kuwa mtu yoyote amenishinda mimi katika kuwaita watoto wao jina hili la ‗Abdul-Muswawwir kwani katika majina yote ya wapokezi wa riwaya niliowahi kuyaona kwenye vitabu vya watu wa hadîth na wasimulizi

wao [sijawahi kuliona jina hili]. Na namuomba Allâh‎ ( وتعىل سبحانهه ), anizidishie kufuzu na kwamba anibariki katika jamii yangu.

خي و ة أ ة ىرذ ذ ة وذريذ زوص

أ ت جلة ة ةربذ ة ٱصف ة ذذيي إ ٧٤ل

“Mola wetu! Tupe sisi kutokamana na wake zetu na watoto wetu na utuja‟aliye kuwa ni kiongozi miongoni mwa wacha Mungu.”4

Kisha katika mwaka wa 1383 Hijriyyah [1963 CE] nilipokuwa bado niko

Madinah, Allâh‎ alinibariki na mtoto wa kiume niliyemwita kwa jina la

Muhammad, kama kumkumbuka Mtume wake ( لمصىل اهلل عليه وس ), mji na

utekelezaji wa maneno yake, “Jiiteni kwa jina langu, lakini musitumie kunyaa yangu.”” [al-Bukhâri na Muslim] KIPA-UMBELE IWE NI HAKI KULIKO MILA ZA WAZEE: ―Nikaendelea

kufuata nyayo za babangu kwenye njia hii mpaka pale Allâh‎ aliponiongoza kwenye Sunnah, kwahivyo nikayawacha mengi katika niliyokuwa nimeyasoma kutoka kwake, mambo ambayo yeye alikuwa

akiyazingatia kuwa ni njia za kujikurubisha kwa Allâh‎ na ‗Ibâdah.‖

SHEIKH AL-ALBÂNI NA BABAKE: ―Mimi nilijiendeleza kuisoma Sunnah kwa hamu kubwa na shauku, mpaka babangu alipoliona hilo kwangu alianza kunionya na akaniamabia, ―‘Ilmu ya hadîth ni ta‘luma ya waliofilisika!‖ Lakini licha ya kutafautiana huko kulivyoleta baina yetu kulingana na mtazamo wa ki-itikadi, karibuni na mwisho wa maisha yake tulikuwa na mkuruba zaidi, na alikuwa akisema katika kila hatima ya mahojiano yetu, ‗Mimi sikatai yakwamba wewe umenifunza faida za ki-ilimu kuhusiana na mas‘ala ambayo mimi

4 Al-Furqân (25):74

VIII

sikuwa na ujuzi nayo hapo awali, kama kutoruhusiwa ki-sheriya kukusudia kwenda kuswali katika makaburi ya watu wema.‘‖ MWANZO WA KAZI YAKE: ―Na ukweli ni kwamba, mas‘ala haya [yaani; kuswali katika makaburi ya watu wema] ni miongoni mwa sababu za mwanzo zilizonipelekea mimi kujitenga na Mashekhe wengi, kwa vile katika mas‘ala haya walikuwa kwenye njia aliyokuwa nayo babangu. Kwahiyo, kutokamana na mambo ya awali niliyoanza nayo yenye kufanana na utafiti wa ki-ilimu ni kwamba nilifuatilia Madda hii kwenye kumbukumbu za vitabu vya Fiqh na Hadîth vilivyokuwa vikipatikana kwenye maktaba ya babangu. Nikaandika kurasa chache ambazo ndani yake nilichukuwa rai yakwamba swala kama hizo ni makuruhu kiasi cha kwamba zimeharamishwa katika sehemu hizo. Hususan, swala kwenye misikiti ambayo iliyojengwa juu

ya makaburi ya mitume na ma-walii wa Allâh‎, wakitumia dalili

maneno ya wanavyuoni niliowapata kwenye kumbukumbu hizo. Kisha nikawasilisha utafiti wangu kwa sheikh wangu, al-Burhân, mwishoni mwa mwezi wa Ramadhân na akaniahidi kuyajibu baada ya ‗Eid. Nilipomjia [baada ya ‗Eid], alinipokea kwa kutabasamu, kisha akaniambia, ‗Wewe hujafanya chochote. Kwa vile zile sehemu ambazo wewe ulipochukulia kumbukumbu zako, hazikuzidi hata Hâshiyah Ibn Âbidîn na Marâqi al-FaLaah, na hizo hazikuwa ni katika kumbukumbu za ki-Fiqh. Nilipigwa na butwaa kwa jawabu hilo na nikatambua yakwamba Sheikh hakuyaelewa yote niliyoyaandika, kwani kwa hakika mimi nilinukuu kutoka katika „Umdatul-Qâri, Mirqâh al-Mafâtîh, Mubâraq al-Azhâr na Hâshiyah at-Tahtâwî, na zote hizo ni katika kumbukumbu zinazoheshimiwa na wanavyuoni. Ni kutokana na hayo ndipo nilipo-onelea yakwamba ni bora niendeleze katika kuyatafiti zaidi mas‘ala haya. Katika mfumo huo nikaendelea kupekuwa na kutafiti mpaka ikakamilika nukta kwa dalili kutoka kwenye Kitâb, Sunnah na maneno ya wanavyuoni. Na kwahivyo, matokeo ya utafiti huu ndiwo uliokuja ukawa ni kitabu

IX

changu kiitwacho ―Tahdhîr as-Sâjid min intikhâdh il-Qubûril Masâjid – [Maana yake: Onyo kwa mwenye kusujudu kwa kuyafanya makaburi kuwa ni mahali pa ‗Ibâdah].‖

KUMLINGANIA ALLÂH‎, ALIYE JUU ZAIDI: Mawasiliano yakaanza baina

ya watu waliozoeyana, marafiki na marafiki zao na nikatenga sehemu kwenye duka ambapo tulipoweza kukutana ili nipate nafasi ya kuanza kufundisha. Kisha tukaonelea ni bora kuhamia kwenye nyumba ya ndugu mmoja, na mara tukahamia tena kwenye nyumba iliyokuwa kubwa zaidi mpaka hatimae ikatubidi kukodisha ghorofa moja kwa ajili hiyo ya mafunzo. Waliohudhuria wakaanza kuzidi idadi yao mpaka mahali hapo pakafurika na wasomi na juhudi na bidii za usomaji wa hadîth, ufafanuzi wake na upokezi wa riwaya ukafikia kiwango cha juu. Tukaendelea hivyo mpaka juhudi za waliokuwa wakitupinga sisi zikaelekezwa juu yetu, ndio mambo yakafanywa kuwa magumu kiasi cha kwamba masomo yakawa ni yenye kuakhirishwa na vikao vya masomo vikafungwa. Na hapa tukafikia, mpaka sasa hivi [bado], hatuko huru katika vikwazo hivyo, kwahivyo tunakusanyika kila ikibidi kufanya hivyo, na linapotokea jambo la kutuzuiya kuonana baina yetu, mimi hugeukia kuandika na kuswahihisha badala yake. Hayo ni mambo mawili nisiyoweza kuwachana nayo kabisa. KUENEA KWA DA‟WAH NJE YA DAMASCUS: ―Kutokana na matokeo haya ya mageuzi yenye muelekeo ambayo da‘wah imejipatia ni kwamba tulipanga utaratibu wa kufanya ziyara katika sehemu tafauti, kwa mfano Aleppo, Latakia, Idlib, Salamiyah, Homs, Hama na ar-Raqqah, na licha ya wakati mchache nilioipangia miji hii, misafara ilikutana na natija nzuri. Kutokana na idadi kubwa ya waliokuwa na hamu ya kusoma ta‘luma ya hadîth walikuwa wakikusanyika kwenye mihadhara inayofanana na semina, vitabu vya Sunnah vikisomwa hapo, masuali yakiulizwa na mahojiano yenye kufaidisha yakilipuka.

X

Isipokuwa kwa uhakika yakwamba usafiri huu [wa kusambaza da‘wah] ulizidisha maradufu nguvu za hasira kutoka kwa wengine [kuelekezwa kwetu sisi]. Kwahivyo walizidisha juhudi zao [kusababisha matatizo] mbele ya wenye mamlaka na matokeo yake tukawa kati-kati ya mashaka, haya baada ya yale.‖ BAADHI YA UGOMVI ULIOMKABILI SHEIKH: ―La kwanza miongoni mwa mambo haya ni pale baadhi ya mashekhe, akiwemo mmoja ambaye aliyedhaniwa kuwa angelikuwa ni usaidizi kwa da‘wah ya Salafi, aliyeongoza ulalamishi akadai yakwamba mimi nilikuwa nikiisambaza Da‘wah ya Uwahabi kwa malengo ya kusababisha matatizo miongoni mwa Wasialamu. Kwahivyo wakaanza kukusanya sahihi za ulalamishi kutoka kwa watu, kisha wakaziwasilisha kwa Mufti wa Syria. Kisha, na yeye, akaziwasilisha kwa kiongozi wa Polisi aliyenifungulia mashtaka na kunidadisi kuhusiana na mas‘ala hayo, mpaka mwishoe yakamalizikia patupu. Siku moja rafiki yangu ambaye niliyekuwa nikisoma pamoja naye aliniuliza kuhusu hadîth fulani inayohusu malipo mema ya kufunga swaum, basi nikamueleza yakwamba [hadîth hiyo] ilikuwa ni dhaifu. Rafiki yangu huyu aliwahi kuisikiya hadîth hiyo kutoka kwa Imâm aliyekuwa akitoa khutbah ya Ijumaa akiinukuu kama dalili juu ya minbar, na akashindwa kujizuiya ikambidi arudi kwa Imâm huyo aliyetoa khutbah na kumueleza aliyokuja kuyajua kuhusu udhaifu wa hadîth na marejeo ambayo hadîth hiyo inapopatikana. Kwahivyo matokeo yake, katika Khutbah ya Ijumaa iliyofuata ikawa ni mashambulizi dhidi ya njia ya Salaf na akaanza kuwashutumu wale wenye kuifuata kuwa ni ma-Wahâbi, akionyesha njia hii kuwa ni ya upotofu, akawatahadharisha watu dhidi ya kuwakurubia na akawalingania wawachunge watoto wao dhidi ya walinganizi wake. Miongoni mwa watu waliokuwa wakisikiliza khutbah hiyo [ya pili] hawakuwa sawa wote katika kukubali au kukataa yaliyosemwa, na matokeo yake pakatokea fujo na mchafuko.‖

XI

SHEIKH UL-ISLAAM NA SHEIKH AL-ALBÂNI WAFUNGWA KWENYE GEREZA MOJA

―Ilikwisha kukadiriwa yakwamba nitafungwa katika mwaka wa 1389 Hijriyyah –inayoafikiyana na mwaka wa 1969, pamoja na idadi ya wanavyuoni, si kwa uhalifu wowote isipokuwa tu ni kuwalingania watu katika Uislamu na kuufunza kwa watu. Kwahivyo nikafungwa kwenye ‗Jela ya Ngomeni‘ na wengine wakafungwa Damascus, kisha nikawachwa huru baada ya muda, na mara tena nikafungwa mara ya pili na kisha nikatolewa nje ya mji kwenye visiwa kuhudumu huko kwa idadi ya miezi kadhaa kwenye jela ya huko, jambo amablo mimi

nimelizingatia kuwa ni kwa njia ya Allâh‎, mwenye nguvu na aliye

mtukufu.

[Na hii ndiyo Jela ile-ile ambayo aliyofungwa Sheikh ul-IsLaam Ibn Taymiyyah, kwa miaka mengi iliyopita!] Tizama makala ya kiarabu hapa kwenye mtandao: http://www.alalbany.net/albany_serah.php.

Akakadiria Allâh‎ yakwamba mimi nisiwe na chochote [pindi

nilipowekwa gerezani] isipokuwa kitabu changu cha tunu Swahih Muslim, pencil (kalamu ya risasi), na rubber (kifutio). Hapo ndipo ambapo nilipojishughulisha na kutimiza ndoto yangu ya kuiandika kwa mukhtasari na kuifupisha [yaani Swahih Muslim], kazi ambayo niliyoikamilisha kwa muda wa miezi mitatu, nikajikokota usiku na mchana, bila ya kuhisi machofu wala usumbufu. Na kwahivyo, matokeo yake ambayo maadui wa Ummah waliyokusudia kuwa ni adhabu kwangu yakageuzwa kichwa chini na yakawa ni baraka kwetu, pamoja na wanafunzi wa ki-ilimu kutokamana na Wasilamu wakifaidika nacho katika ulimwengu mzima. Kwahivyo, kila sifa

njema zinamstahiki Allâh‎ ambaye kwa kupitia kwenye baraka zake,

mambo mema hukamilika.‖

XII

KIFUNGO CHA NDANI

―Allâh‎, aliye juu zaidi, akarahisisha ukamilishaji wa vitabu vyingi

vyangu vya ki-ilimu. Nisingelikuwa na fursa ya kuvipa wakati uliohitajika lau kama maisha yangu yangeliendelea kuwa kwenye njia niliyokuwa nikiishi. [Na hii ilikuwa] Ni kwa sababu baadhi ya uongozi mmoja baada ya mwengine uliotangulia ulinizuiya mimi nisisafiri kuelekea kwenye miji ya Syria kwa ajili ya mihadhara ya kila mwezi ambayo ningelikuwa nikiwalingania watu kwenye Qur‘ân na Sunnah, na jambo hili linajulikana mno kwa jina maarufu kama ‗kifungo cha ndani.‘

Vilevile katika zama hizo za uongozi mmoja baada ya mwengine uliotangulia, nilizuiwa kutowa muhadhara wowote miongoni mwa mihadhara mengi ya ki-ilimu niliyokuwa nikitoa, matayarisho ambayo nilikuwa nikitumia sehemu kubwa ya wakati wangu. Jambo hili lilichukuwa kazi nyingi niliyokuwa nikiifanya na ikawa ni baina ya nafsi yangu na kukutana na watu wengi waliokuwa wakichukuwa muda mwingi wa wakati wangu.‖ [Yote hayo yalimpa Sheikh wakati wa ziyada ajishughulishe na utafiti

wake na kuandika, twamuombea Allâh‎ amrehemu]

SHEIKH ACHAGULIWA KAMA MHADHIRI KATIKA CHUO KIKUU CHA

MADINAH

―Mimi nilikuwa ni mhadhiri katika ta‘luma ya hadîth katika Chuo Kikuu Cha al-Madinah, kuanzia mwaka wa 1381 Hijriyyah [1961 CE] hadi mwishoni mwa 1383 Hijriyyah [1963 CE]. Kwenye gari langu nilikuwa nikiwabeba wanafunzi wowote niliokuwa nikiwapata njiani kuelekea katika Chuo na vilevile kurudi Madinah. Kwahivyo wakati wowote, gari langu lilikuwa likijaa wanafunzi, wenda na kurudi.‖

XIII

MASHEIKH ZAKE WAKIFAIDIKA KUTOKA KWAKE ―Ama kuhusu mashekhe zetu siku hizi, pindi wanapokuwa hawajali kuhusu hukmu hii ya kisheriya. Wengi wao watakusudia kwenda kuswali kwenye misikiti kama hii [yaani; misikiti yenye makaburi ndani yake au iliyojengwa juu ya makaburi n.k (na kadhaalika)]. Nilikuwa na mazoweya ya kwenda na baadhi yao tukiswali pamoja katika kaburi la Sheikh Ibn Arabi – nilipokuwa na umri mdogo na nilipokuwa bado sijakuwa na fahamu njema za kutambua Sunnah! Kisha niliposoma kuhusu makatazo yake, nilijadiliana na huyu sheikh

[niliyekuwa nikenda naye pamoja] kwa mara nyingi mpaka pale Allâh‎, aliye juu zaidi, alipomuongoza naye akawacha kwenda kuswali mahali hapo. Baadae alilithibitisha jambo hilo na akanishukuru kwa kusema yakwamba mimi ndiye niliyekuwa sababu ya kuongozwa kwake.

Namuombea Allâh‎, aliye juu zaidi, amrehemu na amswamehe. Na kila

aina ya sifa njema zinamstahiki Allâh‎ aliyetuongoza na

hatungeongoka sisi lau kama si ukweli wa kuongozwa na Allâh‎.‖

ALIYOKUWA AKIYASEMA PINDI ANAPOSIFIWA

―Alikuwa akiyakariri maombi ya Abu Bakr, as-Swiddîq, ‗Yaa Allâh‎! Usinichukulie mimi kwa wanayoyasema wao. Na unifanye mimi kuwa ni mtu bora kuliko wanavyonidhania. Na uniswamehe kwa yale ambayo wao hawayajui.‖

KUHAMA KWAKE KUTOKA DAMASCUS HADI KATIKA MJI WA AMMAN,

JORDAN

―Kwa hakika Allâh‎, kwa hikma zake, amekifanyia kila kitu sababu na

kupanga muda maalum kwa kila jambo, na akakadiria kila kitu kwa njia iliyokuwa bora zaidi. Katika sehemu yake ambayo ilikuwa ni kusafiri mimi pamoja na jamii yangu kutoka Damascus nchini Syria hadi mjini Amman, nchini Jordan, mwanzoni mwa mwezi wa Ramadhân katika mwaka wa 1400 Hijriyyah [1980 CE]. Basi nikaanza kuchukuwa hatua za kujenga nyumba mahali hapo ambayo

XIV

nitakayoweza kuja kuishi kwa muda ambao nitakaokuwa hai na Allâh‎, kwa fadhla zake kubwa na rehma zake, akarahisisha ukamilifu wake. Nikaanza kuishi mahali pale baada ya kazi kubwa sana mpaka nikaathirika kwa maradhi kama matokeo ya juhudi niliyofanya katika kununua kipande hicho cha ardhi, nikajenga msingi na [hatimae] kuijenga nyumba yenyewe, na mpaka hivi sasa athari za ugonjwa huo

hunipa thakili kidogo, na kila sifa njema zinamstahiki Allâh‎ katika kila

hali na kila sifa njema zinamstahiki Allâh‎ ambaye kwaa fadhla zake

matendo mema hukamilika. Kwahivyo ni jambo la kawaida yakwamba shughuli hizi zilinielekeza kwengine kutoka katika yale niliyokuwa nimeyazoweya kuyafanya nilipokuwa mjini Damascus [nilipokuwa nikiishi] nilipokuwa nikijifungamanisha na ‗ilmu kwa njia zote mbili, kusoma na kufundisha, kuandika na kuswahihisha – hususan kwa vile maktaba yangu binafsi bado ilikuwa mjini Damascus kwani sikuwa na uwezo wa kuihamisha mjini Amman kutokana na matatizo yanayojulikana na vikwazo. Kila siku nilikuwa nikijipoza moyo wangu na kubaki na matumaini, nikijiambia [nafsi yangu] yakwamba hivi karibuni maji yataregea kwenye mkondo wake, lakini ni mara ngapi unakuta upepo ukivuma [kwa mielekeo] tafauti na mielekeo ambayo mabaharia hutarajia. Muda mchache tu baada ya baadhi ya ndugu mjini Jordan kuona yakwamba nimeshapata makaazi wakaanza kuniswihi yakwamba nianzishe mihadhara [au darasa] niliyokuwa nikiifanya katika miaka iliyopita kabla ya kuhamia Amman – kwani nilikuwa nikija kwa misafara kila baada ya mwezi au miezi miwili, nikiweka drasa moja au mbili katika kila safari. Wakaendelea kung‘ang‘ania kunisisitiza, kwahivyo hata kama nilikuwa sijaamua kuweka darasa zozote ili nami nipate kutumia nilichobakisha katika nguvu zangu na maisha yangu kukamilisha baadhi ya miradi yangu ya misingi ya ki-ilimu – na ni ngapi hizo – nikaonelea yakwamba sina budi nitekeleze maombi yao na matamaniwa yao mazuri. Kwahivyo, nikawaahidi mazuri na nikawaambia kuwa nitatoa darasa katika kila siku ya Al-Khâmis baada ya swala ya Maghrib nyumbani kwa ndugu mwema fulani ambaye nyumba yake iko karibu na nyumba yangu.

XV

Hilo likatambulika, kwa rukhsah ya Allâh‎, na nikawapa masomo, la

kwanza na la pili kutoka katika kitabu cha RIyâdh as-Swâlihîn cha Imâm an-Nawawi, na nikayajibu baadhi ya muswali yao mengi baada ya darasa, maswali yenye kuonyesha shauku yao kubwa ya ‗ilmu na kutaka kujifungamanisha na Sunnah.‖ KURUDI KWAKE KWA GHAFULA KUTOKA AMMAN HADI DAMASCUS NA

KISHA KUELEKEA LEBANON

―Ilitokea wakati nilipokuwa nikijitayarisha kwa darasa langu la tatu ambapo niliposhangaa kusikiya habari hizo zilizonilazimisha – kwa njia ambayo sikuwa na chaguo lolote – lakini ni kuondoka mjini Amman pamoja na jamii yangu kwani hapakuwa tena na uwezekano wa mimi kuendelea kuishi hapo. Kwahiyo, nikasafiri na kurudi pale nilipohamia mara ya kwanza, Damascus, na hiyo ilikuwa ni siku ya Jumatano wakati wa mchana, 19th mwezi wa Shawwal, 1401 Hijriyyah [August 1981 CE]. Niliwasili hapo wakati wa usiku uliokuwa na baridi ambayo hata sikuwa na nguo za kujikinga nikiwa na huzuni tele na majonzi,

nikimuomba na kumlilia Allâh‎, aliye juu zaidi, aniepushie mabaya

niliyokusudiwa na pia njama za maadui.

Nilibaki hapo kwa nyusiku mbili na katika usiku wa tatu, baada ya kutaka usaidizi na kuomba uongofu [Istikhârah], nikasafiri na kuelekea Beirut kwa tahadhari kubwa na khofu kutokana na yanayojulikana ya misukosuko mikubwa na mitihani kwenye sehemu hizo na mauaji ya kikorofi. Njia ya kuelekea Beirut ilikuwa ni njia

iliyozingirwa na hatari tupu lakini Allâh‎, mwenye baraka na aliye juu

zaidi, aliniokoa mimi na akanirahisishia. Niliwasili Beirut wakati wa thuluthi ya kwanza ya usiku, nikielekea kwenye nyumba ya ndugu yangu mmoja mpendwa, muaminifu, rafiki yangu wa karibu aliyenikaribisha kwa ukarimu wake ujulikanao, mwenye tabia njema na roho nzuri, na aliyenipokea mimi kama mgeni muheshimiwa,

namuombea Allâh‎ amlipe mema.

Nilipoishi kwenye nyumba yake na fahamu zangu hazikuwa zimetawaliwa tena na mashaka ya safari, ilikuwa ni kawaida tu

XVI

yakwamba mimi [ningelihitajika] kuitumia fursa hii ya upweke wa ghafula, kwahivyo nikageuza mazingatio yangu yote kwenye kutaalamika na kusoma katika maktaba yake iliyojaa vitabu na makaratasi adimu ambayo hayajachapishwa, ilikuwa imejaa rasilmali nyingi nilizokuwa nahitaji na nyengine nyingi ambazo sikuwa nazo kwenye maktaba yangu, Damascus. Nilimuomba anonyeshe orodha yake ya makaratasi adimu ambayo hayajachapishwa na makaratasi ya kopi aliyokuwa nayo mikononi mwake na ambayo aliyoyaandika kwenye kadi za kuandikia. Alinijibu hayo kwa moyo uliokuwa wazi na adabu njema za Uislamu zilizokuwa

zikijulikana kumuhusu yeye. Namuombea Allâh‎ amlipe wema.‖

[Ilikuwa ndio matokeo ya safari yake hiyo ambapo Sheikh alipoweza kukamilisha kitabu chake, Raf‟ul-Astâr]

MIKASA, MMOJA BAADA YA MWENGINE, ILIYOMKUMBA SHEIKH

AKIWA LEBANON

―Licha ya ukweli yakwamba wakati huo [yaani; alipokuwa akikifanyia upekuzi kitabu cha BIDÂYATUL USÛL], mara ghafula nilipokea habari za huzuni za kifo cha ndugu yangu mkubwa, Nâji, Abû Ahmad katika msimu wa Hajj, niliendelea katika kukikamilisha kitabu hicho

haliyakuwa nikimuomba Allâh‎ amrehemu, nikiomba anipe subira

katika kukikamilisha. Kwani hakika yeye alikufa akiwa ndiye mbora wa ndugu zangu, alikuwa akinipenda sana mimi, alikuwa ni mwepesi wa kuitikia mwito wangu, akiushughulikia sana na shauku kubwa

katika kuulingania [mwito wangu]. Namuombea Allâh‎ amrehemu

yeye, na atupe nasi, na ndugu zangu wote, watoto wake, wajukuu zake, na wakweze subra wakati huu wa msiba uliowafika wote, na

namuomba Allâh‎ atuja‘aliye na sisi kuwa ni wafuasi wazuri kwa

mtangulizi bora, na atufufue nasi sote pamoja naye chini ya bendera

ya kiongozi wa watoto wa Âdam (صىل اهلل عليه وسلم);

XVII

ت أ إلذ ت شم ٱللذ ٨٩ثي

„Isipokuwa mwenye kuja kwa Allâh‎ na moyo safi (huyu ndiye

atakaepata ya kumfaa).‟5

Sisi sote ni wa Allâh‎ na kwake yeye ndipo tutakaporudi. Yaa Allâh‎! Nifidie mimi kwa msiba huu na unipe badala yake kwa lililo bora. Yaa

Allâh‎! Msamehe Abû Ahmad na umuinue daraja yake miongoni mwa

waongofu, uwaja‘aliye kizazi chake katika watu wema, tuswamehe sisi na yeye, Ewe mola wa walimwengu, mpanulie kaburi lake na ulijaze miangaza! Katika kitabu chake Talkhîs Ahkâm al-Janâiz, Uk.24, Sheikh wetu amesema, ‗Ndugu yangu mkubwa Muhammad Nâji Abû Ahmad ameaga dunia katika msimu wa Hajj wa mwaka uliopita (1401 Hijriyyah / 1980

CE) akiwa kwenye tendo jema insha- Allâh‎, alipokuwa jamarât

amekaa na baadhi ya wenzake ambao nao pia walikuwa wakitekeleza Hajj. Kisha baadae mmoja wao akanisimulia yakwamba mtu mmoja alikuwa amekaa naye alimkaribisha kwa kikombe cha chai, kwa mkono wake wa kushoto, basi yeye akamwambia, Ewe ndugu yangu, nipe kwa mkono wako wa kulia na usiipinge Sunnah,‘ au maneno yenye athari kama hiyo – na mara tu baada ya kusema maneno hayo

akaaga dunia. Namuombea Allâh‎ amrehemu na atukusanye sisi

pamoja naye;

ييي ٱو جلذجي ٱ د ٱو لص عي ٱو داء لظ ة صذ رذيا وله أ ٦٩وظص

„…manabii na Masidiki na mashahidi na masâlih (watu wema). Na uzuri ulioje (kwa mtu) watu hao kuwa rafiki (zake).‟”6

5 ash-Shu‘arâ‘ (26):89 6 an-Nisâ‘ 4:69

XVIII

KUKIMBIA KWAKE KUTOKA KWENYE NJAMA ZA KUULIWA NCHINI BEIRUT

―Mikasa, maafa na mauaji yasiyokuwa na sababu zozote yalikuwa bado yakiendelea (yaani; nchini Lebanon) mpaka mimi na jamii yangu tukawa karibu tuwe ni katika wahasiriwa wake kwa risasi ambazo tulizofyetuliwa nazo na walenga shabaha kutoka kwenye maporomoko ya majengo ya kivita mnamo tarehe 2nd Safar, 1399 Hijriyyah [January 1979 CE]. Gari langu lilidenguliwa kwenye sehemu tatu, na mashambulio yenyewe yalikuwa yamelengwa kwenye ukingo wa

majeruhi mabaya sana lakini Allâh‎ alitunusuru kiasi cha kwamba

hatukupata hata jaraha moja kwenye miili yetu, na kila sifa njema

zinamstahiki Allâh‎ ambaye kwa baraka zake matendo mema

hukamilika.‖

KUHAMA KUTOKA BEIRUT HADI EMIRATES

―Allâh‎ alinikadiria kusafiri kutoka Beirut hadi kule Sharjah kwa ndugu

yetu mmoja, naye akanipokea mimi kama mgeni kwenye nyumba

yake, namuombea Allâh‎ amlipe kheri nyingi kwa ukarimu wake.‖

UADILIFU NA MSIMAMO WAKE WA HAKI

―Basi namuomba Allâh‎ amrehemu mja mwenye kunionyesha makosa

yangu na kuniongoza mimi kwenye kukosea kwangu, kwani ni rahisi

kwangu – kwa uwezo wa Allâh‎ na kukufanya ufaulu – kupokea makosa

yoyote ambayo niliyodhihirishiwa, na vitabu vyangu ambavyo vilivyochapishwa kwa mara ya kwanza na marekebisho yaliyowahi kufanywa ndani mwake [katika chapa za baadae] ndio ushahidi mkubwa wa hayo. Na lau kama watu wenye kutukosoa sisi wangetupasha kuhusu faida kama hizo [yaani; marekebisho] ili tupate kurudi kwenye rai za sawa [katika mas‘ala yoyote ambayo tulipokosea], haliyakuwa tunathibitisha fadhla zake na kuwapa

XIX

shukrani. Na asiyekuwa na madhambi ni yule aliye pewa utakatifu na

Allâh‎ ( وتعاىل سبحانهه )

MFUMO WAKE KUHUSIANA NA KUZIORODHESHA HADÎTH

―Inanistahiki nieleze yakwamba mimi simfuati yoyote ki-Upofu ninapotoa hukmu kuhusiana na hadîth hizo. Bali mimi hufuata sheriya zenye misingi ya ki-ilimu ambazo zilizowekwa na watu wa hadîth [AHLUL HADÎTH], na ambazo wao huzipitia juu yake wanapotoa hukmu zenye kuhusiana na hadîth, iwapo kama ni swahîh au dha‘îf, na huo ndiwo uliokuwa wakati ambapo njia ya ki-maisha ya Uislamu

ilipokuwa kwenye ufanisi. Natumai kutoka kwa Allâh‎, aliye epukana

na kila upungufu na aliye juu zaidi, yakwamba na mimi nimepewa tawfîq ya kufuata mkondo huo, na kuidhihirisha, au hata sehemu yake, kwa Waislamu kwa njia ya utendaji, nikitumai yakwamba kutoka kwa vijana wa ki-Islamu kutakuwa na wenye kuihuisha upya misingi hiyo, misingi iliyotokamana na mifumo ya fikra za kitaalamu zilizo swahîh zilivyowahi kushuhudiwa kupitia kwenye zama tafauti za wana-adamu, kama walivyoyashuhudia kundi la wataalamu wa mambo ya nchi za mashariki na wengine kama wao miongoni mwa wapinzani. Na wahenga walisema, ‗Kufaulu ndilo jambo analolishuhudia adui.‘‖

UMUHIMU WA WAKATI

―Niliwachana na ukosoaji kwa mara ya pili, nikitazamia kuokoa wakati hapo.‖

MFUMO WAKE KATIKA KUZIORODHESHA HADÎTH KATIKA

UKUSANYAJI WAKE WA HADÎTH KWA JINA LA AS-SILSILAH NA ADH-DHA’ÎFAH

―Mimi sikuwa na mfumo makhsusi nilipokuwa nikizikusanya hadîth, bali [niliziorodhesha] kila nilipokuwa nikizipata.‖

XX

MIFANO YA SUBIRA ZAKE

―Nilijinyima chakula mwishoni mwa mwaka wa 1379 Hijriyyah [1959 CE] kwa muda wa siku arubaini mtawalia – sikula chakula chochote katika masiku hayo, hakuna kilichoingia tumboni mwangu isipokuwa maji tu. Nilifanya hayo kwa kutarajia kupata ponyo ya maradhi fulani, na [mwishoni mwake] kwa hakika nilitibika kutokana na baadhi [ya maradhi] lakini sio mengine. Kabla ya kufanya hivi nilitafuta utabibu kwa baadhi ya madaktari kwa takriban miaka kumi bila ya kudhihirika faida yoyote. Nilijipatia faida aina mbili za wazi kabisa kutokamana na njaa hii ya kujilazimisha:‖

“KWANZA: Uwezo wa mtu kuhimili njaa kwa muda wa wakati mrefu kiyasi hicho kinyume cha wanavyodhania watu wengi.‖ NYENGINE: Yakwamba kukaa na njaa kunaweza kusaidia kutibu maradhi yenye kuhusiana na unene wa kupita kiyasi, kama alivyoeleza

Ibn al-Qayyim, Allâh‎ amrehemu, kama ambavyo inavyoweza kusaidia

katika maradhi mengine, kama [walivyojaribu] walivyopata uzoefu watu wengi katika maisha yao. Ingawaje haisaidii kwa maradhi yote kulingana na sampuli tafauti za miili ya watu, kinyume cha madai ya mtunzi (Muingereza) wa kitabu, ‗Kutafuta tiba kutokana na kufunga

Swaum,‘ na Allâh‎ ndiye mjuzi wa yote.‖

SHEIKH AL-ALBÂNI AULIZWA KUHUSU HADÎTH NA BABAKE

―Kwahivyo, nikaonelea yakwamba nimewajibika kulizungumzia suala fulani, na kubainisha makosa yake – hususan pale wakuruba wangu zaidi walipokuwa wakiniulizia kuhusiana nalo, naye si mwengine

asiyekuwa babangu, namuombea Allâh‎ amrehemu, na amlipe kwa

niyaba yangu kwa malipo yaliyo bora.‖

SHEIKH MUSTAFÂ AZ-ZARQÂ AMUULIZA KUHUSU HADÎTH

―Na hadîth hii ni miongoni mwa zile ambazo alizoniletea mwalimu mkarimu Mustafâ az-Zarqâ, aliponitaka niziswahihishe na

XXI

kuzichunguza, na hili lilitokea mnamo tarehe 15th Jumâda ath-Thâni, 1371 [sawa na 12th March, 1952].

SAFARI ZAKE KATIKA KUTAFUTA „ILMU

EGYPT [MISRI]: Katika muda mfupi nilioutumia katika miji ya Cairo na Alexandria nilikuwa na uwezo mdogo tu wa kuonana na wanavyuoni na watu wenye ubora, kwa mfano mtunzi wa vitabu vya ki-Islamu Muhibbud-Dîn al-Khatwîb, Ustadh Muhammad al-Ghazâli [ambaye baadae sheikh alikuja kumkosoa], sheikh ‗Abdur-Razzâq ‗Afîfi na sheikh ‗Abdul-‗Azîz ar-Râshid.

Pindi nilipokuwa niko Cairo, nilikuwa nikenda – kila wakati fursa inapojitokeza – kwenye Dâr al-Kutub al-Misriyyah kuzisoma kurasa za vitabu vya hadîth mahali hapo. Niliendelea kufanya hivyohivyo nilipo ondoka hapo na kuelekea Alexandria, nikenda kwenye Maktaba yake iitwayo al-Maktabah al-Baladiyyah, na nikajipatia faida muhimu na nyingi kocho-kocho kutoka kwenye maktaba zote hizo mbili. Kutoka katika maktaba hii ya pili, nilinakili kwa mkono wangu mwenyewe kitabu cha al-Hâfidh Ibn Hajar al-Asqalâni ambamo ndani yake alizichunguza na kuziswahihisha ahâdîth ambazo al-Hâfidh al-Qizwîni alizozileta kwenye kitabu Maswâbih as-Sunnah na akazihukumu kwenye kitabu hicho kuwa zilikuwa ni za kuzua. ALEPPO: Mojawapo ya tabia zangu kwa miaka mingi ilikuwa ni kusafiri kuelekea mjini Aleppo kwa wiki moja kila mwezi, nikitumia muda huo nikiwa huko au muda wake mwingi, kwenye Maktaba ya kipekee pale iliyojaa kurasa zilizonukuliwa, ikiitwa Maktabah al-Awqâf al-Islâmiyyah. Kwahivyo, kila siku nilikuwa nikitumia masaa mahali hapo nikizisoma kurasa zake, nikinukuu yaliyokuwa muhimu kwa miradi yangu ya misingi ya ki-Ilimu. Zaidi ya hayo, nilikuwa nikisoma Sunnah na ta‘luma zake pamoja na waliokuwa wakipendezwa na mas‘ala ya ki-ilimu, nikitoa fursa ya kuwafunza kila wiki niliyokuwepo hapo.

XXII

SAFARI YAKE YA KUELEKEA BAITAL-MAQDIS [JERUSALEM]

―Na nikasafiri kuelekea Jerusalem kwa mara ya kwanza mnamo 23rd Jumâda al-Awwal, 1385 Hijriyyah [September, 1965], wakati ambapo nchi za Jordan na Syria walipokubaliana kuwaruhusu raiya wao wawe huru kusafiri baina ya nchi hizo bila ya kuwa na hati ya kusafiria (Passport). Basi na mimi nikaitumia fursa hiyo nikasafiri na kuswali katika Msikiti wa Aqswa. Nikalitembelea Jabali, ili nami nilione tu, kwani halina fadhla yoyote [iliyo makhsusi] na [iliyotajwa] katika muangaza wa ki-Sheriya, kinyume cha wengi wa watu wanavyodhania na serikali inavyotangaza.‖

SPAIN: ―Katika mwezi wa Rajab, 1392 Hijriyyah sawiya na August, 1972 CE, sheikh alisafiri kuelekea Andalus alipoitwa kuhudhuria mkutano wa Umoja wa wanafunzi wa ki-Islamu uliofanyika Granada.‖ MOROCCO: ―Safari yangu ya kwanza kuelekea Morocco ilikuwa ni mwishoni mwa mwezi wa nne [Rabî‟uth Thâni 1396 Hijriyyah – 1976 CE].‖ QATAR: ―Katika mwezi mtukufu wa Ramadhân, mwaka wa 1392 Hijriyyah [1972 CE, nilisafiri kuelekea Qatar] na mwanzoni mwa Rabî‟ul Awwal katika mwaka wa 1402 Hijriyyah, sawiya na [1982 CE].‖ SAFARI YAKE YA PILI KUELEKEA EMIRATES ―Nilirudi hapo mnamo 29th March, 1985 kwa ruhusa rasmi ya ki-Serikali yenye nambari 1094/i, kisha nikaondoka mnamo 5th April, 1985 kama ilivyonukuliwa katika hati yangu ya usafiri (Passport) yenye nambari 284024 sr/77. KUVUMILIA KWAKE KATIKA KUTAFUTA „ILMU: ―Kwa hakika miongoni

mwa Baraka za Allâh‎ juu yangu ni kwamba kwa vile zaidi ya miaka

kumi iliyopita nilikuwa nimeshakusanya maelfu ya ahâdîth katika mijalada zaidi ya arubaini, na yote hiyo ikiwa imehusisha asili zake chungu nzima. Nikaziandika kwa khati zangu mwenyewe kwenye mamiya ya kurasa zilizohifadhiwa kwenye idadi ya Maktaba tafauti tafauti zilizo maarufu, kama vile Maktabatu adh-Dhwâhiriyyah iliyoko

XXIII

Damascus, Maktaba ya Al-Awqâf al-IsLaamiyyah iliyoko Aleppo, Maktaba al-Mahmûdiyyah katika mskiti wa Mtume, Madinah, Maktaba ya Aarif Hikmah iliyoko Madînatul Munawwarah, na maktaba nyenginezo zilizojaa vitabu vya rahisi kabisa vya hadîth, na vya faida, seerah, historia, na vitabu vinavyoelezea kuhusu maisha ya watu (wasifu) – mambo ambayo mpaka leo hii hayajachapishwa. Kwahivyo kila mara ninapohitaji kutafiti kuhusu silisili za upokezi za hadîth katika kitabu Al-Jâmi‟ as-Swaghîr au nyongeza zake, nilikuwa nikirudia kwenye mijeledi hii, ambayo iliyopangwa kwa taratibu za abjadi (alphabetically), na huikuta hadîth ndani mwake ikiwa na silisili yake ya upokezi ikihusishwa huku nyuma kwenye asili yake ileile ambayo Imâm Suyûti na wengine wasiokuwa yeye walipoichukuwa kutoka hapo. Na ni kutoka mahali hapa, ambapo siri inapobainika kwa yoyote miongoni mwa wanavyuoni atakae vipitia baadhi ya vitabu vyangu katika masomo mbalimbali ya ‗ilmu za kimsingi – wanapo yaona hayo, licha ya kiasi chake, kitabu kimoja tu kama vile Swifat us-SwaLaatun

Nabî‟ (صىل اهلل عليه وسلم)kimetumia mirundiko ya kurasa za vitabu ambazo

watu wengi hata hawajawahi kuweza kuvumbua majina yake, licha ya kuvisoma na kupata ufahamu wa hadîth zilizomo ndani yake, silisili za riwaya zake, matamshi yake, na riwaya zilizomo zenye kuziunga mkono!

Kwa njia kama hiyo, Allâh‎ akanirahisishia mimi nikakusanya faharasa

kwa utendeti,iliyokuwa na kila kitu kinachopatikana kwenye Maktaba hii iliyoimarishwa madhubuti, kutokamana na vitabu vya hadîth katika mitindo tafauti-tafauti, kama vile vitabu vya hadîth katika Musnad, vitabu vya hadîth vya ukusanyaji, vitabu vya hadîth vya faida, zilizopokewa na Mwanachuoni makhsusi, vitabu vya wasifu na vyenginevyo. Nikiashiriya hapo ndani yake mambo ambayo hayajawahi kutajwa kwenye faharasa [zilizo rasmi] za Maktaba hadi siku ya leo, na mimi nikazipanga faharasa hizo kwa kutegemea majina ya watunzi, kulingana na orodha ya alfabeti. Nikafanya kama hivyo katika vitabu vyao haswa, kwa kuvipanga kulingana na orodha hiyo chini ya jina la kila mtungaji, kwa kuandika humo wasifu kwa

XXIV

mukhtasari nikataja ndani yake tarehe yake ya kuzaliwa, ya kufa, na iwapo alikuwa ni mpokezi muadilifu au dhaifu kama mpokezi na kadhaalika. Hatimae, mwishoe nikaweka faharasa ya ujumla tu pakiwemo vitabu vyote vilevile kwa mpangilio wa orodha ya alfabeti.

MRADI ALIOJITOLEA MAISHA YAKE KWA DHATI, „KATIKA KUIKURUBISHA SUNNAH KWA UMMAH‟

―Mradi uliokuwa muhimu zaidi wa msingi wa ki-ilimu niliokuwa nao ni ule nilouita, ‗Kuikurubisha Sunnah kwa Ummah.‟ Nilikusudia humo kukusanya pamoja yote niliyoweza ambayo ni swahîh kutoka katika

hadîth za Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), kwenye kitabu kimoja, juu ya mfumo

wa Wanavyuoni wa hadîth na misingi yao ya ki-ilimu katika kupambanua baina ya riwaya zilizo swahîh na zilizo dha‘îf.

Namuomba Allâh‎, mtukufu, aliye juu, yakwamba anirahisishie katika

ufahamu wake.

Kwani, kwa hakika nimeutumikia ujana wangu kwa kazi hiyo, kama nilivyofanya katika miaka yangu ya kati na kati, na sasa ndio nakamilisha, hata katika muda huu, katika umri wangu wa uzeeni,

nikiwa katika muda wote huo namuomba Allâh‎ (سبحانه وتعىل), anifanye

mimi niwe miongoni mwa wale ambao Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), aliyesema

kuwahusu, “Wabora miongoni mwenu ni wale watakaoishi umri mrefu na wakawazidi wengine katika kutenda mema.” Nikitarajia kutoka

Kwake ( ه عزه وجل ), yakwamba anija‘aliye mwisho mwema, na anifishe juu

ya Îmân.7

7 Nukta ya Mfasiri: Ibara ifuatayo ni katika ukamilifu wa hiyo iliyo juu yake ambayo haikuingizwa kwenye ukusanyaji wa asili: ―Na hatimae [kwenye mjalada aliokuwa akiandika kuhusiana nao], halijanihadai mimi jambo la kutoa shukrani zangu na furaha kwa binti yangu mkubwa, Umm ‗Abdillaah, aliyenirahisishia usomaji swahîh wa mjalada huu, na akazipeleka fahamu za mtu kwenye mas‘ala ambayo muandishi yoyote anaweza kupitikiwa, licha ya aliyetimia umri wa miaka thamanini; mambo kama kulisahau au kulikosea

XXV

LENGO LAKE KATIKA MAISHA

―Kwa hakika, lengo langu zima katika maisha haya – baada [ya

kukusudia] kutekeleza vitendo na haki ambazo Allâh‎ alizonifaradhishia mimi, hakuna isipokuwa ni kujaribu kuwafahamisha Waislamu kwa njia ya ‗ilmu, madarasa na vitabu ambavyo ninavyoandika, pamoja na wasifu swahîh wa kutoka katika kila kipembe kiasi cha uwezo wangu. Na kuwahimiza wamchukulie Mtume

( وسلم عليه اهلل صىل )kuwa ni mfano wa kipekee wa kuigwa, kama ambavyo

Allâh‎ alivyowahimiza wafanye katika maneno yake,

ف رشل ذيد كن س ا ٱللذ كن يرص ح ل ة ظص ش أ م و ٱللذ ٱألخر ٱحل

ر وذ ا ٱللذ سريا ٢١ “Bila shaka mnao mfano mwema (ruwaza nzuri) kwa Mtume wa

Allâh‎, kwa mwenye kumuogopa Allâh‎ na siku ya mwisho, na

kumtaja Allâh‎ sana.”8

Na hapo ndipo palipo na ufunguo wa furaha katika maisha ya hapa duniani na ya kesho akhera.

neno au ibara, au kupeleka fahamu za mtu kwenye sehemu ambazo upekuzi wa hadîth umerudiwa, au mahali ambapo sikukamilisha majadiliano kuhusiana na hadîth na kadhaalika, kwahiyo namuomba Allaah amjazi kheri kwa niyaba yangu kwa malipo yaliyo mazuri zaidi. Vilevile, Ndugu ‗Ali [Hasan] al-Halabi, mimi nimefaidika mno kutokana na nukta alizoziandika kwenye nyaraka zangu za asili nilizonukuu maandishi yangu, na baadhi nyengine aliandika miaka mingi iliyopita, nyengine aliziandika juu ya nyaraka ambazo alizowahi kuziona. Kwahivyo, yeye na mwengine yoyote aliyechangia katika kuchapishwa kwa mjalada huu chini ya usimamizi wa shemegi yangu, Nidhâm Sakjahâ, mwenye Aal-Maktabah al-Islaamiyyah katika nchi ya Jordan, wana shukrani zangu za dhati.‖ 8 al-Ahzâb 33:21

XXVI

NASWIHA YAKE KWA UMMAH ―Mimi naunaswihi Ummah warudi katika kushikamana madhubuti kwenye Dini yao, Kitabu cha Mola wao, na Sunnah swahih za Mtume wao, waitendee kazi katika nyanja zote za maisha yao, wajivike nafsi zao ndani ya ubora wake na tabia zake njema, na kwamba wajihukumu juu ya kila kitu wanachoitakidi kuwa ni Dini dhidi ya

Kitâb cha Allâh‎ na Sunnah za Mtume wake, washikamane imara na

kila chenye kuafikiana navyo vyote viwili na kuwachana na chochote chenye kwenda kinyume chake. Kwa vile hali ni kama alivyosema Imâm mkubwa Anas ibn Mâlik, Imâm wa mahali pa Hijrah (yaani; Madinah), ―Yoyote mwenye kuanzisha uzushi ndani ya Uislamu akiitakidi kuwa ni mzuri, atakuwa ameswadikisha yakwamba

Muhammad ( وسلم عليه اهلل صىل )amefanya khiyana katika [kuufikiliza]

ujumbe wake. Soma maneno ya Allâh‎ ( وتعىل سبحانهه ):

م ٱ حل دي خ س ز أ ت ورطخ س ف س ـ خ ت

وأ ٱس شؾ ل

ة ا ٣دي“... Leo nimeikamilisha Dini yenu na kuitimiza neema yangu kwenu (kwa kuwaongoza katika Uislamu). Na nimewachagulia

Uislamu kuwa ni Dini yenu...”9 Na sehemu ya mwisho ya taifa hili haitoweza kurekebishika isipokuwa kwa kile ambacho kilichourekebisha sehemu yake ya mwanzo.‖

SHEIKH AL-ALBÂNI HAKUWA NI KIONGOZI WA POTE WALA KUNDI LOLOTE

―Makala hayo10 hayakutoshelezana na madai haya [Pekee], bali yalijiongezea mengine juu ya hayo, ambayo yaliyohusiana na mimi

9 Al-Mâ‘idah 5:3 10 Nukta ya mkusanyaji: Makala yaliyoandikwa na Waziri katika mojawapo ya Ma-Amiri, na kisha yakasambazwa kwenye magazeti mengi kama vile al-Bayân na ambalo lililopeperusha madai mengi ya urongo dhidi ya ma-Salafi.

XXVII

mwenyewe binafsi na tena yaliyobainika zaidi kwenye urongo wake kuliko kwenye madai yake yaliotangulia, kwahiyo yalieleza, ―Na huyu mtu , kwa jina la Nâsir ud-Dîn al-Albâni ndiye kiongozi wake.‖ Kwahivyo huu ni urongo na udanganyifu kamili, na mtu yoyote mwenye kunijua mimi binafsi anashuhudia ukweli huo. Kwahivyo, ukweli ni kwamba juhudi zangu katika uandishi wa vitabu na kuvipitia na kuviswahihisha kwa zaidi ya nusu ya Qarne zinaingia baina yangu na haya madai ya urongo ya uongozi. Na hili lingekuwa lau kama roho yangu ingelikuwa imeinamia upande huo, haya basi itakuwaje hivyo haliyakuwa inapingana moja kwa moja na tabia yangu ya kimaumbile iliyoinamia kunako mkuruba wa msingi wa ki-ilimu?!

KATIKA KUSOMA BAADHI YA VITABU VYA MUSNAD

MUSNAD YA ABU YA‟LAA: ―Hili ndilo litakalodhihirika baada ya

kumaliza kusoma Musnad nzima ya Abû Ya‘Laa inshâ-Allâh‎.‖ ―...

Kisha nikamaliza kuisoma yote kwa ukamilifu.‖

MUSNAD YA IBN ABÎ SHAYBAH: ―Niliupata mjalada wake wa pili kwenye Maktaba Kuu katika mji wa Ribat, niliisoma na nikafaidika kwayo na hiyo ilikuwa ni kwenye msafara wangu wa kwanza katika nchi ya Morocco, mwishoni mwa mwezi wa nne katika mwaka wa 1396 Hijriyyah [sawiya na 1976 CE]

KUSWALI ISTIKHÂRAH NINAPOHUKUMU JUU YA HADÎTH

―Kwahivyo [kuhusiana na hadîth husika], nilikuwa nikimuomba Allâh‎ uongofu [Istikhârah] kisha nikiiweka hapa [yaani; kwenye kitabu chake as-Swahîhah] kutokana na kutiliwa kwake nguvu, pindi njia zake mbali-mbali zote za riwaya zinapozingatiwa.

XXVIII

KUFUATA KWAKE KITÂB NA SUNNAH NA KUTUPILIA MBALI KUFUATA KI-UPOFU

―Nilipojenga na kujiekea mfumo huu, yaani; kushikamana na Sunnah iliyo swahîh, na kuitekeleza kwenye kitabu hiki na vyenginevyo

ambavyo hivi karibuni vitasambaa miongoni mwa watu, inshâ-Allâh‎, nilijua kwa uhakika yakwamba hilo halitowafurahisha makundi na mapote yote. Bali ni kwamba baadhi yao kama si wengi wao watakuwa ni wenye kunivurumizia mimi mashambulizi ya maneno makali pamoja na njia ya maandishi. Na hakuna matatizo kwa hilo, kwa vile najua yakwamba kuwaridhisha watu ni lengo lisiloweza kupatikana, na kwamba,

بصخع اجلذةس رىض اتلس و » اللذ وك «اجلذةس إل اللذ

―Yoyote mwenye kuwaridhisha watu kutokana na kumuudhi Allâh‎, Allâh‎ atawawakilishia watu.‖

Ni msemo mzuri ulioje huu wa aliyesema; ―Na wala sitosalimika na matusi mabaya, hata kama ningelikuwa ndani ya pango juu ya mlima wa kuparuza; na ni nani huyo awezae kuwakimbia watu akiwa salama na uzima wake, hata kama akijipoteza baina ya mbawa za mwewe.‖ Kwahivyo inanitosheleza mimi yakwamba nishikilie msimamo huu

kuwa ndiwo wa sawa ambao Allâh‎ ( وتعىل سبحانهه ), aliowaamrisha nao

waumini, na ambao Muhammad, kiongozi wa Mitume alioubainisha, na ambao watu wema waliotutangulia kutoka kwa Maswahaba, wanafunzi wao na wale waliowafuata wao waliopitia juu ya njia hiyo. Wakiwemo miongoni mwao ni Ma-Imâm wanne ambao madh-hab zao wengi wa Waislamu wanajinasibisha nao leo hii. Wote hao waliafikiana juu ya uwajibikaji wa kushikamana na Sunnah na kufanya marudio yao hapo [kwenye Sunnah] na kutupilia mbali matamshi yoyote yenye kwenda kinyume nayo, pasi na kujali ukubwa wa mwenye kuyasema [matamshi hayo] ulikuwa vipi kwani utukufu wake

Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل )ni mkubwa zaidi, njia yake ndiyo iliyo nyo-oka

XXIX

zaidi. Kwahiyo, mimi nafuata uongofu wao na nyayo zao, nikitekeleza

amri zao kushikamana na matamshi ya Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل )hata kama

hadîth inapinga waliyoyasema wao [wenyewe]. Maamrisho haya yana mshindo mkubwa zaidi katika darasa zangu za hii njia iliyo nyo-oka na

kuwachana kwangu na kufuata ki-upofu. Kwahivyo namuomba Allâh‎ kwa niyaba yangu awalipe mema [kutokana na faida (سبحانه وتعىل)

nilizopata kutoka kwao].

KUVIFANYA VITABU KUWA NI MSHIRIKA WAKE NA MARAFIKI ZAKE

―Kwahivyo, mimi nasema: Abadan! Hukmu hizi hazikuwa bila ya maandalizi, kwa hakika zilikuwa ni matunda ya jitihada zangu kwenye kitengo hiki kitukufu cha ilimu na kubobea katika utaalamu wake kwa

zaidi ya nusu karne kwa ajili ya Allâh‎ ( وتعىل سبحانهه ) – moyo iliojaa mapenzi

tele na tamaa na jitihada za uangalifu katika kuipata kwake, Allâh‎ ( وتعىل سبحانهه ) akaziafiki kufuzu kwa ruhusa yake. Nikajikokota usiku na

mchana, kwa masafa mapana kabisa, katika kufuatilia maandiko adimu na swahih ya hadîth, matamshi yake na njia mbali mbali kutoka katika vitabu vingi ambapo ahâdîth hizo zilipotajwa pamoja na silsila za riwaya zake; kama vile Kitabu cha tafsiri ya Qur‘ân, wasifu, tarekh, riwaya za kulainisha nyoyo na kuupa nyongo ulimwengu, pasi na kuvitaja vitabu makhsusi vya hadîth, ema ni katika kurasa au njia nyenginezo. Na hakuna chenye kuthibitisha hayo kuliko ‗kisa cha kurasa iliyopotea‘ ambayo niliyoitaja katika utangulizi wa kwenye kitabu changu, ‗Faharasa ya kurasa za Maktaba Dhâhiriyyah,‘ ambacho kilichochapishwa na Chuo cha ilimu ya Juu cha kiarabu cha Damascus, kwahivyo rudia katika kitabu hicho [kwa kisa hiki] (Uk. 4-7), kwani ndani yake kuna ushuhuda na mazingatio kwa mwenye kujihadhari.

Katika sehemu ya haya ni kwamba Allâh‎ amenipa mimi fursa, kwa

rehma zake na fadhla zake, kuongozana na ma-mia, bali hata ma-elfu ya wenye ilimu na fadhla kubwa kwenye nyanja tafauti tafauti;

XXX

nikiwa ni mwenye furaha kukutana nao kwa muda wa miaka yote hiyo iliyobarikiwa [kwa kupitia kwenye vitabu vyao], mikusanyiko sampuli hiyo ambayo thamani yake na furaha zake hakuna awezae kuzijua isipokuwa wale waliowahi kupata uzoefu wake. Na aliyeyasema [mistari ya mashairi] yafuatayo kuwahusu watu hao, amesema ukweli:

―Tuko nao wenzetu ambao maneno yao hayatuchoshi; ni wenye busara, waadilifu, wakiwepo au wasiwepo; wanatufaidisha sisi kwa ilimu zao, ilimu za yaliyopita; Akili timamu, na adabu zenye rai za uelekevu; zisizokuwa na uwoga wa vurugu lolote wala usuhuba mbaya; pasi ya kuziogopa ndimi [chafu] kutoka kwao au mkono wa [kupiga]; kwahivyo, ukisema, ‗[Lakini hao] washakufa!‘ Utakuwa hujasema urongo; na ikiwa utasema, ‗[Lakini hao] wako hai!‘ Hutokanushwa.‖

Bado mimi sijakoma kuchukuwa kutoka kwenye ilimu zao na kujichagulia kutoka kwenye matunda yao – hususan wanavyuoni wa hadîth na upokezi wa riwaya [Ahlul Hadîth wal-Athar] kutoka kwao

kiyasi cha kwamba, kwa fadhla za Allâh‎ na taufiki yake, niliweza

kukusanya maelfu ya hadîth na riwaya, [pamoja na] njia zake na silisili za upokezi, minyororo iliyo dhaifu na dhaifu mno, [na haya yalikuwa] ni jambo lililoleta msaada mkubwa katika kuzitambua kasoro zake na kutafautisha baina ya swahîh na dhaifu miongoni mwazo. Kwahivyo matokeo ya yote haya ndio vile vitabu nilivyoandika kwa kutumia miaka mengi juu yake.

KISA CHA KARATASI ILIYOPOTEA

―Niliwahi kuuguwa maradhi ya jicho kwa zaidi ya miaka kumi na mbili, ikabidi daktari mwenye utaalamu wa macho akaninasihi niyape macho yangu mapumziko kwa kuwacha kusoma, kuandika na kufanya kazi (ya kutengeza saa) kwa muda wa miezi sita.

Nikachukuwa ushauri wake hapo awali, kwa kuwacha mambo yote hayo kwa takriban wiki mbili – kisha mara roho yangu ikaanza kunishawishi, ikanipelekea kufanya mambo katika wakati huu wa

XXXI

mapumziko, jambo ambalo lisilowezekana, kwa rai yangu, kwenda kinyume cha alivyoninaswihi daktari. Mara nikaikumbuka nakala fulani niliyoiona katika Maktaba kwa jina la ‗Dhammul-MaLaahi‟ ya Ibn Abid-Dunyâ ambayo kulingana na ilmu yangu ilikuwa haijawahi kuchapishwa wakati huo. Basi nikajiambia nafsi yangu, ‗Kwani kuna ubaya gani ikiwa nitampata mtu aniandikie? Na pindi itakapokuwa nakala hiyo ishakamilika kuandikwa na wakati utakapofika wa kuichunguza nakala hii dhidi ya nakala asili iwapo iko sawa, basi muda wa wakati wa kiasi cha mapumziko ya macho yangu utapita. Na jambo hili halitonikalifisha katika kuichunga hali ya afya yangu, kisha naweza baadae kuichunguza mimi mwenyewe kadiri ya uweza wangu, nikaziswahihisha hadîth zake na kisha tukaweza kuzichapisha, zote kwa mpangilio maalum ili nisijikalifishe nafsi yangu!‘ Huyu mtu alipofika katikati ya kazi hii ya kunakili kurasa hizo alinijulisha yakwamba palikuwa na sehemu fulani iliyokosekana. Mimi nikamwambia aendelee kunakili mpaka aimalize, kisha tutailinganisha na nakala ya asili. [Alipomaliza kazi hiyo] Nikaichunguza na kuhakikisha yakwamba ni kweli palikuwa na sehemu iliyokosekana kama alivyoniashiriya. Nikaikadiria kuwa kiyasi cha takriban kurasa nne. Nikaanza kutafakari juu yake na jinsi nitakavyopambana nalo. Nakala hii imewekwa kwa mjalada mmoja miongoni mwa mengi yaliyowekwa na kuhifadhiwa kwenye Maktaba katika sehemu iitwayo Majâmî‟. Kila moja katika mijalada yote yalikuwa na mikataba mbalimbali na vitabu ndani yake, kwa khati za maandishi tafauti tafauti, milango na kurasa tafauti kwa rangi na vipimo. Basi nikasema na nafsi yangu, ‗Labda, kwa ajali tu, huyu aliyekusanya nakala hii aliigandisha kwenye mojawapo ya mijalada haya mengine.‘ Kwahiyo nikajitupa nafsi yangu kwenye kuipekuwa kwa mlolongo nikiwa na shauku isiyo kifani na nishati. Na nikasahau – au nikajisahaulisha – maradhi katika macho yangu! Kwahivyo kila nilipoyakumbuka sikukosa mbinu ya kujiendeleza, kama

XXXII

vile yakwamba utafiti huu hautoathiri vibaya [mapumziko ya jicho] kwa vile hapakuwa na uandishi wala usomaji wa njia ya kujipinda! Nimewahi kupitia nakala chache pekee wakati uangalifu wangu ulipovutiwa kwenye vichwa vya baadhi ya vitabu na nakala za wanavyuoni maarufu na mahâfidh waliokuwa mashuhuri mno. Kwahivyo, mimi nitawatilia kikomo, niwapekuwe, niwatalii, nikitumai yakwamba zingelinakiliwa na kuchunguzwa na kisha kuchapishwa. Lakini, kwa mara nyingi nimezikuta kuwa ni sehemu zilizokosekana na sura, kwahivyo, kwa mfano nitazikuta za kwanza na sio za pili, na kwa ajili hiyo sitozinakili kwenye faharisi yangu. Nikaendelea kuipekuwa kurasa iliyopotea, bila ya kufaulu, mpaka hatimae nikakamilisha kuyapitia mijalada yote yaliyokuwa kwenye sehemu ya Majâmî‟ yenye jumla ya 152. Aidha, katika wakati huu wa upekuzi nikaanza kuziandika sura za baadhi ya vitabu zilizonivutia na kilichonitia moyo zaidi katika jambo hilo ni ukweli yakwamba nilipokuwa nikifanya upekuzi wangu nilikuta baadhi ya sehemu zilizokosekana za nakala ambazo sikuwahi kuzinukuu hapo awali [kutokana na upungufu uliokuwa nao, na kwa vile sasa zimepatikana sehemu zilizokuwa zimekosekana, na nakala yenyewe ikakamilika ataweza kuyahifadhi majina yake]. Kwa vile nilishindwa kuipata kurasa iliyokosekana miongoni mwa mijalada iliyotajwa, nilijiambia nafsi yangu, ‗Labda ilibandikwa kimakosa kwenye mojawapo ya mijalada ya vitabu vya mkusanyiko wa hadîth, kwenye mrundu wa vitabu katika maktaba chini ya sehemu ya Hadîth!‘ Kwahiyo, nikaanza kupekuwa katika sehemu hii, mjalada baada ya mjalada, mpaka nikayapitia yote bila ya kuipata kurasa iliyopotea. Sikukoma hapo, bali nikaanza kurikodi [kwenye faharasa yangu] majina mengi ya makala na vitabu kiyasi cha alivyoniwezesha

Allâh‎. Kwa njia hii niliendelea kujipa moyo na kujitia nafsi yangu ushawishi mkubwa kwa kusema yakwamba nitaipata karatasi iliyopotea. Basi,

XXXIII

nilipokuwa nikiendelea kuitafuta, nilikwenda kutafuta kwenye mijalada na makala ya kitagaa kimoja cha ‗ilmu hadi nyengine – mpaka nikamaliza kuzipitia nyaraka zoye ziliozkuwa zimewekwa kwenye maktaba ambazo zilizofikia takriban elfu kumi, lakini ikawa bado sijaipata karatasi iliyopotea. Lakini juu ya yote hayo, sikuwa ni mwenye kukata tamaa. Kwani palikuwa na sehemu katika maktaba kulipowekwa mirundiko na milima ya makaratasi na vitabu mbalimbali vya kuchakaa, ambavyo asili zake hazijulikani – basi nikaanza kuvipitia, kwa makini na uswahihi, lakini [kwa mara nyengine tena] bila ya kufaulu. Hapo tena ndipo nilipoanza kuamini yakwamba huwenda nisiweze kuipata kurasa iliyopotea. Lakini ikawa bado baada ya kufikiria kuhusu hali hii nikatambua

yakwamba Allâh‎, mwenye rehma na aliye juu zaidi, ameshanifungulia

kinara cha lango la ‗ilmu, ambayo sikuwa nikiyajua kama ambavyo walivyokuwa wengine kama mimi. [Na huu ni ukweli ambao] maktaba ya Dhâhiriyyah [katika mji wa damascus] iliyo na hazina ya vitabu na makala kwenye vitagaa mbalimbali vya ‗ilmu yenye manufaa ambayo

vizazi vyetu, twamuomba Allâh‎, aliye juu zaidi, awarehemu,

waliyotuachia, na kwamba yenye kurasa chache ambazo inawezekana kuwa hazipatikani kwenye maktaba nyengine katika ulimwengu mzima na ambazo mpaka leo hii hazijachapishwa. Kwahivyo jambo hili [uhakika wa thamani ya vifaa kwenye maktaba] lilipodhihirika kwangu na likathibitika kwenye moyo wangu, nikaanza kurudia tena utafiti wa nakala zote za maktaba, kuanzia mwanzo hadi mwisho. Kwa mara ya pili. [Wakati huu wote nikafanya namna hii] juu ya muangaza wa tajriba niliyoipata kutokana na utafiti wangu wa hapo awali ambapo nilipozinukuu [peke yake] sehemu [nilizochagua] kutoka kwenye vitabu – sasa nikaanza kunukuu kila kitu [nilichokiona ambacho] kilichohusiana na ‗ilmu ya utaalamu wa hadîth. Sikuwahi kuipitia

XXXIV

nukta ya kina chochote isipokuwa nilikinukuu, hata kama kimetoka kwa [aliyepotoka] kurasa ya karatasi ya kitabu au mjalada ambao asili yake isiyojulikana.

Ilikuwa ni kana kwamba Allâh‎, mwenye rehema na aliye juu zaidi,

alikuwa akinitayarisha kwa kuyapitia yote hayo kwa mara ya tatu na ya mwisho ambayo ndiyo ‗ilmu yenyewe ya vitabu hivi, ‗ilmu ya kina, [ili nipate kuweza] kuzichukuwa kutoka humo hadîth za Mtume pamoja na silisili zake za upokezi na njia zake, na faida nyengine [zozote]. Faharasa hii ilitokamana na juhudi za mtu binafsi, msukumo wa kibinafsi, kutoka kwa mtu ambaye hakuajiriwa katika maktaba wala hakupangiwa kuifanya kazi hiyo, na kama hivyo usaidizi ulio muhimu katika kuzipitia nakala hizo, aweze kuzisoma na kuzifanyia utafiti sehemu zake ambazo zilizokuwa hazijulikani hazikuweko kama ambavyo ingelikuwa hali ya mtu ambaye angelikuwa ameajiriwa na maktaba hiyo au akapangiwa kufanya shughuli hiyo na muajiri wa maktaba. Kwa hivyo ni jambo la kawaida tu kwangu mimi kupambana na uzito wakati wa utafiti huo – na kukaja masiku yaliyonipita mpaka ikanibidi kuikweza ngazi, kisha niipande juu na kubakia huko kwa masaa ili nipate kusoma nikiwa huko [kwa] haraka [kama ilivyowezekana]. Kwahivyo pindi nilipokuwa nahitaji kitu chochote kutoka hapo nilichokuwa napendelea kukisoma na kukichunguza kwa undani, ningelikuwa nikimuuliza muhudumu wa maktaba aniteremshie kwenye dawati ...

AL-ALBÂNI NA ABDUL-FATTÂH ABU GHUDDAH

―Mwanzo wangu nilikutana na Sheikh Abdul-Fattâh Abu Ghuddah katika mji wake, Aleppo, takriban zaidi ya miaka ishirini iliyopita. Nilitambua yakwamba yeye alikuwa ni mtu mpindanifu juu ya madh-hab ya ki-Hanafi kiyasi cha kwamba alikuwa akiandama madh-hab hiyo ki-Upofu, aliporuhusu kwenye msikiti wake wa Aleppo kutibiwa

XXXV

mtu kwa tembo (mvinyo) chini ya usimamizi wa tabibu (daktari) aliyekuwa Muislamu.

Basi nikamwambia, ‗Hili halitoshi. Inamlazimu tabibu awe na ufahamu swahîh wa Sunnah. Kwani katika Sunnah, kwa mfano, tembo limesifiwa kuwa ni maradhi na wala sio tiba. Sasa tabibu aliye Muislamu mwenye kujua Sharî‟ah atatoaje maagizo ya kutibu ambayo

yaliyosifiwa na Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) kuwa ni maradhi?!‘ Akanijibu,

‗Penginepo hadîth hiyo ni dhaîf au si swahîh!‘ Nikamjibu, ‗Itakuwaje hivyo kama hadîth yenyewe iko katika swahîh Muslim?‘ Akasema, ‗Wacha twende tukahakikishe.‘ Palikuwa na mtu mmoja kwenye mahojiano hayo ambaye alikuwa na usuhuba pande zote mbili, akasema, ‗Sasa utakapochunguza na kukuta yakwamba ni swahîh, utaifuata kulingana na isemavyo au kulingana na yasemavyo madh-hab?‘ Akajibu Abu Ghuddah, ‗Nitafuata madh-hab!‘

AL-ALBÂNI NA MUHUBIRI [KHATÎB]

―Kisa cha kumuhusu Khatîb ni cha kuchekesha, lakini hapohapo huwenda kikamliza mtu, kinastahiki kusimuliwa kutokana na mafunzo yanayoweza kupatikana ndani yake.

Miaka michache iliyopita mmojawapo wa makhatibu kutoka katika msikiti mmoja wa Damascus alikuja kwangu, naye alikuwa ni muhubiri mwenye ushawishi aliyekuwa akisafiri sehemu mbalimbali [kwa ajili ya kuwaonya na kuwakumbusha watu]. Aliniambia mimi yakwamba aliandika kitabu ambacho alichozikusanya hadîth ndani yake, hadîth alizozinukuu kutoka katika vitabu vya Sunnah na kwamba alimuomba ndugu mwenye ukwasi amsaidie ili kitabu hicho kichapishwe. Huyo ndugu akamwambia ―Iwapo Ustâdh Nâsir ud-Dîn al-Albâni atakubali kitabu hiki kichapishwe, basi nitakusaidia.‖ Kisha muhubiri huyu akaniomba ridhâ yangu lakini mimi nikamkatalia na nikamwambia

XXXVI

sitofanya hivyo mpaka nikione kitabu chenyewe. Akaniletea kitabu hicho. Nilipokisoma kitabu hicho nilikuta mambo ndani yake yaliyokuwa ni ya kushangaza na kusikitisha. Katika kitabu hicho aliyanasibisha

maneno ya Issa (عليه السالم), ambayo Mâlik aliyoyataja katika swahîh

Muslim akisema yakwamba yamepokewa kutoka kwenye riwaya ya

Abu Hurairah na kunasibishwa kutoka kwa Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ), yakwamba yeye Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) amesema, amesema Issa ( عليه !‖... (السالم

Nilipoyaona haya nilishtuka sana kwani nilikuwa nina hakika yakwamba hakujawahi kuwepo hadîth ya sampuli hiyo kwenye Swahîh ya Imâm Muslim wala kwenye kitabu chochote katika vitabu sita vyengine vya hadîth – isipokuwa kwa ibara yake ya kwanza ambayo imepokewa kwenye Sunan at-Tirmidhî kutoka katika hadîth ya Ibn ‗Umar kwa silsila ya riwaya dhaîf, kama nilivyoibainisha katika Silsilah al-Ahâdîth adh-Dha‘îfah, no. 924 au baada ya hiyo. Basi nikampigia simu na nikamwambia rai yangu kuhusu kitabu pamoja na tahkiki na makosa yaliyokuwemo ndani yake, yenye nguvu miongoni mwayo

ikiwemo kunasibishwa kwa riwaya ya Issa ( السالم عليه ), kwa Mtume ( اهلل صىل

وسلم عليه ) Kisha nikamuuliza, ―Uliipata kutoka wapi hii?‖ Basi

akanyamaza kwa muda kidogo, kisha akasema, ―Hebu nisubiri kidogo nikuletee kitabu.‖ Kisha akaniambia, na hayo aliyoyasema yalinishtua na kunitamausha, ―Aliyeinasibisha hadîth hiyo kwenye Swahîh Muslim ni Imâm Mâlik katika Kitabu cha Fadhla na Kuunga kizazi ...‖ na kuendelea. Kwahivyo nikamwambia, ―Ni kitu gani hiki, Ewe Sheikh! Kwani wewe hujui yakwamba kuna pengo kubwa baina ya Muslim na Mâlik? Na kwamba Muslim alikuja baada ya Mâlik; na kwamba miongoni mwa ma-Sheikh wa Muslim ni Imâm Ahmad, na miongoni mwa ma-Sheikh wa Imâm Ahmad ni Imâm ash-Shâfi‘î na miongoni mwa ma-Sheikh wa Imâm ash-Shâfi‘î ni Mâlik? Sasa atawezaje Mâlik

XXXVII

kuinasibisha hadîth hii kwa Muslim haliyakuwa alikufa zamani kwa miaka mengi kabla yake?!‖ Basi alinyamaza katika kutatizika kisha akasema maneno ambayo nilikuja kufahamu yakwamba alikuwa akisema kuwa Mâlik ndiye aliyeizua kauli hii katika kitabu chake al-Muwatta‟! Nikamwambia, hili ni jambo lisilowezekana na mimi nitalichunguza suala hilo na

kukubainishia wewe Insha-Allâh‎.‖

Nikenda katika Al-Maktabah adh-Dhâhiriyyah na kukikagua [Kitabu cha Imâm Mâlik] Al-Muwatta‟ cha tahkiki ya Muhammad Fu‘âd Abdul-Bâqi. Na hapo ndipo ilipofika sababu ya kuyafichua makosa yenye kuzalisha makosa makubwa kuliko hayo! Yote hayo ni kutokana na ujinga wa watu kuhusiana na hadîth na uchache wa bidii walio nao na tahadhari hata kwenye vyuo vya kiislamu vya Sharî‟ah.‖

AL-ALBÂNI NA WALE WALIOKUWA NA WIVU NAYE

―Kwahivyo mimi sikuwa na la zaidi la kufanya isipokuwa kumuomba

Allâh‎ anihifadhi dhidi ya uovu wao, kama alivyotuamrisha Allâh‎ katika

Kitâb chake;

ذ ثرب ى ـة خو ١ هو ٱأ غشو إذا وىت ٢ ش ش ٣و و

ثخ ٱش ٤ فيد ٱف جلذػذ ظةشد إذا ظصد و ٥ش“Sema: Najikinga kwa Mola wa walimwengu wote. Na shari ya

alivyoviumba. Na shari ya giza la usiku liingiapo. Na shari ya wale wanaopulizia (vivia) mafundoni, (wakavunja mashikamano yaliyo

baina ya watu, yaani shari ya mafatani). Na shari ya hasidi anapohusudu.”11

Na mimi natarajia malipo yangu kutoka kwa Allâh‎ kwa msiba huu

walioniletea hawa madhalimu waliopindukia mipaka katika njia

11 Surah al-Falaq 113:(1-5)

XXXVIII

yangu. Namuomba Allâh‎ anisahilishie, Allâh‎ul Musta‟ân, waLaa hawla

waLaa quwwata ilLaa biLaah, na yeye ndiye mtegemewa wa mambo yote. KUTOJALI KWAKE JUU YA WAYASEMAYO WATU WAKATI ANPOJUA

HAKI ILIKUWA UPANDE WAKE

―Uwajibikaji wa kuifundisha ‗ilmu na makatazo ya kuificha ndiyo mambo yaliyonipelekea mimi kutojali iwapo watu wameridhika au kughadhibika.‖

MKOSI ULIOMPATA AKIWA AMMAN

―Nyumba yangu ilivamiwa na kitengo cha upelelezi na kuchakurwa kila kipembe kwa zaidi ya masaa saba. Wakazishika takriban barua sitini zilizotoka kwa nchi tafauti za kiislamu na nyenginezo. Vilevile wakashika kanda za tepu zangu na za wanafunzi wengine wa ki‘ilmu

kwa kisingizio ati yakwamba wanatafuta silaha na vilipuzi! Allâh‎ atusaidie – Allâh‎ul Musta‟ân.”

ULINGANIZI WAKE

1. ―Ni kurudi kwenye Kitâb na Sunnah zilizo swahîh, na kuzifahamu

kulingana na mfumo wa wema waliotutangulia, Allâh‎ awe radhi

nao wote.

2. Kuwajuza na kuwafanya Waislamu waifahamu vizuri dini yao ya

Haki, kuwalingania katika kuyatendea kazi maelekezo na

maamrisho yake, wajipambe nafsi zao kwa wema na tabia njema

zitakazowahakikishia yakwamba watajipatia radhi za Allâh‎, na

kupata uhakika wa furaha na utukufu kwao.

3. Kuwaonya Waislamu kutokamana na kumshirikisha Allâh‎ (shirk)

katika nyanja zake zote, kutokamana na mambo ya uzushi na

mifumo ya kuigwa, kutokamana na hadîth munkar na za kuzuliwa

XXXIX

ambazo zilizouharibu uzuri wa Uislamu na kuwazuiya Waislamu

wasiendelee mbele.

4. Kuhuisha fikra huru za Uislamu zikiwa ndani ya mipaka ya misingi

ya Uislamu, na kuondoa zile fikra zilizoganda na ambazo

zilizoenea na kuzuiya fahamu za Waislamu wengi na

kuwatenganisha mbali na asili zilizotakasika za Uislamu.

5. Kupambana katika kuhuisha njia ya maisha ya Kiislamu,

kuimarisha mujtama‘ wa ki-Islamu waitekeleze Sharî‘ah ya Allâh‎ katika ardhi hii. Huu ndio ulinganizi wetu, na tunawalingania

Waislamu wote waiunge mkono amana hii itakayowainua daraja

zao na waueneze ujumbe wa kudumu wa Uislamu.‖

UTAKASO NA MALEZI

―Kutokana na mtazamo wa kiitikadi na msingi wa kiilimu, mimi naona hali ya Waislamu kuwa ni bora kuliko ilivyokuwa miaka thalathini au arubaini iliyopita. Robo karne iliyopita tulikuwa tukilalamika kuhusu ukosefu wa Waislamu katika taaluma ya sayansi za kisasa, hayo ndiyo waliyokuwa wakiyazungumza wana-Mageuzi.

Kisha matokeo ya vuguvugu hili ulimalizikia kizazi kilichofuata kikageukia kwenye hizo sayansi za kisasa, lakini wakati huohuo kikakurubia kupotea kutoka upande mwengine, na hapa namaanisha yakwamba utaalamu wa sayansi za ki-Islamu, na hatari zake ni nyingi juu ya hatima ya kizazi hicho.

Ama kuhusu tiba ya tatizo hili, basi mimi naamini yakwamba imetulia juu ya nukta mbili; Utakaso na Malezi. Kuhusu ‗Utakaso‘ namaanisha yakwamba ni kuutakasa Uislamu kutokamana na jambo lolote lililo geni na kasoro zote. Njia ya kutekeleza hilo ni kwanza kuitakasa Sunnah kutokamana na mambo ya uzushi na dha‘îf yaliyopenya na

XL

kuingia ndani yake, na kisha ni kuifasiri Qur‘ân juu ya Sunnah hii iliyo swahîh na ufahamu na fikira za wema waliotutangulia. Kwa hayo, simaanishi yakwamba tukome kuhusiana na tafsiri katika kikomo walipokoma Salaf, lakini badala yake, tujifungamanishe na mfumo wao katika tafsîr, na katika kufanya hivyo kuna mafungamano ya muelekeo na kizuizi kutenganishwa. Utakaso huu ninaoukusudia mimi unahusisha yale yaliyotufikia sisi kuhusu taaluma za Uislamu na itikadi, ili tupate kutupilia mbali kila kitu kilichomo ndani chenye kupinga mfumo ulio swahîh. Vilevile inahusisha kutakasa itikadi za Uislamu kutokamana na kasoro zote zilizo geni zikatambaa na kuingia ndani ya itikadi ya Waislamu wa leo kwa njia ya ‗ilmu za ki-Magharibi, hususan filosofia na mafunzo ya ki-ufundi na ki-ilimu, maeneo ambayo yenye uwezekano wa kudunga sindano iliyo na kiwango kikubwa cha sumu ndani ya itikadi ya ki-Islamu. Ama kuhusu malezi, namaanisha kulea kizazi juu ya itikadi ya ki-Islamu iliyo sawa, na swahîh, iliyochukuliwa kutoka katika Kitâb na Sunnah. Nataja hususan suala la malezi kwa watoto wadogo juu ya kuabudu bila ya maneno ya ziada kuhusu faida za vifaa vyenye kutumika kwa ibada kama wafanyavyo wengine. Kwahivyo iwapo faida za vifaa kama hivyo ni lazima zitajwe basi yatakikaniwa ziwe ni kitu cha mwisho kinachostahili kutajwa. Na hapa sisahau kutaja sharî‘ah ya Uislamu, ninaloona lenye kufaa ni kwamba suala hili linatakiwa kusomwa juu ya msingi wa unyenyekevu

kamili katika amri za Allâh‎ na imani kamili katika Hikmah zake bila ya

kuzidisha katika kutaja faida za vifaa vyake, na kwa kufanya hivyo mwanafunzi hupewa hifadha ya nguvu kutokamana na njama zote na kinga ya sumu zote. Kuhusu hili, nakumbuka kisa cha mkataba wa Hudaybiyyah na

umuhimu wa kujisalimisha kwa hukumu ya Allâh‎ na Mtume wake.

XLI

HAMU YAKE YA KUITEKELEZA SUNNAH

―Nilipofanya ‗Umrah wakati wa Ramadhân ya mwaka jana nilikwenda juu kwenye sakafu ya nyumba Madînah nilipokwenda kumtembelea mmojawapo wa marafiki zangu kuhakikisha wakati wa kuzama kwa jua kwa vile nilikuwa nimefunga! Ikawa adhân ya Maghrib imecheleweshwa kwa zaidi ya dakika kumi na tatu baada ya kuzama kwa jua! Ama kuhusu Jeddah, nilipanda juu ya sakafu ya nyumba aliyokuwa mmojawapo wa wakwe zangu akiishi, ikawa jua halijamaliza kuzama na mara [saa hiyohiyo] nikasikiya muadhini, basi

nikamshukuru Allâh‎ kwa hilo.

BAADHI YA SUNNAH ALIZOZIHUISHA

KHUTBA YA HAJA (KHUTBATUL-HÂJAH): ―Kisha Allâh‎, aliye juu

zaidi, akanipa uwezo kiyasi cha kwamba nikaanza kuitumia khutba hii katika darasa zangu na vitabu vyangu, na nikaweza kuisambaza kwenye ulimwengu wa ki-Islamu kwa kupitia vitabu nilivyoandika kuhusiana nayo.

Wengi wa waliokuwa wakiipenda Sunnah wakaiitikia vyema, na kila

sifa njema zinamstahiki Allâh‎, hususan ma-Khatîb misikitini, kwani

kabla ya hapo ilikuwa imetelekezwa.‖

KUSWALI SWALA YA „IDD KATIKA MUSWALLAA: ―Kutokana na hayo ilikuwa yakwamba swala mbili za ‗Idd zilianza kuswaliwa kwenye viwanja vya nje [muswalLaa] katika mji wa Damascus, kisha ndugu zetu walioko Aleppo nao wakaihuisha, na kisha kwenye miji mengine nchini Syria, na Sunnah hii ikaendelea kusambaa mpaka baadhi ya ndugu zetu katika mji wa Ammân, Jordan nao pia wakaihuisha.‖

KISA CHA KUCHEKESHA NA KUHUZUNISHA WAKATI HUOHUO

―Siku moja niliwaswalisha watu katika swala ya al-Fajr siku ya Ijumaa kwenye kijiji kimoja cha az-Zubdâni. Baada ya kusoma Suratil Fâtihah nikasoma nilichoweza katika Surat al-Kahf, kwa vile hifdhi

XLII

yangu ya Surat as-Sajdah haikuwa barâbarâ. Basi niliposema takbir

[yaani Allâh‎u Akbar] kwa ku-Rukû‘, watu wote walipomoka moja kwa

moja mpaka kwenye Sijdah! Sasa kwa vile wao walidhania yakwamba mimi nimeitamka takbir ya kusujudu kwa ajili ya kisomo kinachotokea katika Surat as-Sajdah [na kwa vile Imâm wa kawaida alikuwa akiisoma sura hiyo na hilo ndilo walilokuwa wamezoweya kufanya]. Lakini wale waliokuwa karibu na mimi, nyuma yangu, walitambua yakwamba mimi nime-rukû‘, basi wao wakainuka na kuniunga mimi katika rukû‘. Ama wale waliokuwa nyuma ya minbar na ambao hawakuwa wakiniona, wao walibaki kwenye sijdah mpaka

waliponisikiya nikisema, “Allâh‎ amemsikiya mwenye kumuhimidi ...”

[Sami‟Allâh‎u liman hamidah] wao wakavunja swala zao, mara

kukaanza kelele na majibizano. Baada ya kutoa saLaam [yaani; kutoa saLaam ya kumaliza swala] Nikawageukia kuwapa mawaidha, nikawakumbusha juu ya uwajibu juu yao wa kuwa na khushû‘ [utulivu] kwenye swala na kuwa makini juu ya wanachosomewa

kutoka katika Ayât za [Kitâb cha Allâh‎] na kwamba umakinifu wao

usipate ushawishi wa [mambo yao ya kilimwengu, kama vile] ukulima au kuwakama wanyama maziwa!

MUKHTASAR WA MWISHO

Mtunzi wa kitabu, Essâm Mûsa Hâdi, amesema, ―Nimeuona wasifu wa

Sheikh wetu al-Albâni, Allâh‎ amrehemu, kwa mukhtasar ambao

aliouandika yeye mwenyewe kwa mkono wake katika swahîh, no. 3203 katika kurasa [zilikuwa ni kurasa wakati ambapo Essâm alipokuwa akiandika maneno haya], kwahivyo nilitaka kumaliza

kijitabu hiki kidogo kwa kukinukuu hapa. Sheikh, Allâh‎ amrehemu,

akasema:

―Na kuhusu hili nastahiki kusema kwa ajili ya kumbukumbu na vilevile

kuwa ni shukrani kwa babangu, Allâh‎ aliye juu zaidi, amrehemu: Na

XLIII

vilevile katika hadîth12 kuna bishara njema kwetu, jamii ya babangu, [kwani yeye] alihama pamoja na jamii yake kutoka Ashkodera, iliyokuwa kwa wakati huo Mji mkuu wa Albânia; Akakimbia na dini yake kutoka kwenye mapinduzi ya Ahmad Zogo ambaye moyo wake

Allâh‎ ameusababisha kupotoka, aliyeanza kuwafanyia Waislamu wa

Albânia mambo yaleyale aliyoyafanya mtangulizi wake Ataturk katika nchi ya Turkey. Kutokana na kuhama kwake huku kuelekea Damascus nchini Syria,

nimevuna [baraka hizo], kwa rehma na huruma za Allâh‎, yakwamba

siwezi kumshukuru Mola wangu kiyasi ambacho kinachomstahiki yeye

hata kama ningelija‘aliwa kuishi muda mrefu kama wa Huh ( السالم عليه ).

Kwani hapo ndipo mahali pa kwanza niliposoma kiarabu cha lafdhi ya ki-Syria na baada ya hapo kiarabu fasaha ambacho ndicho kilichoniwezesha kuelewa tawhid ya sawa ambayo waarabu wengi wanaoishi na mimi hawaijui, licha ya jamii yangu na watu wangu isipokuwa wachache miongoni mwao.

Kisha Allâh‎ akanipa mimi uwezo, kwa fadhla zake na baraka zake

tena bila ya maelekezo ya mtu yoyote, nisome hadîth na Sunnah, misingi yake na fiqh [ufahamu], na haya ni baada ya kumaliza kusoma shule na baada ya kusomea sehemu ya fiqh ya ki-Hanafi pamoja na vyombo vya ‗ilmu kama vile sarufi, balagha na nahwu kwa babangu na mashekhe wengine. Kisha nikaanza kuwalingania ndugu zangu na marafiki zangu kwenye urekebishaji wa ‗Aqîdah, na kisha kuwachana na ushupavu wa kung‘ang‘ana juu ya mambo ya madh-hab, nikawatahadharisha dhidi ya hadîth dhaîf na za kuzua, nikawahimiza kuhuisha Sunnah zilizo swahîh ambazo walio wasomi miongoni mwao waliziuwa kabisa. Matokeo ya hayo yote ni kustawisha swala mbili za ‗Idd katika

12 Hadîth: Kutakuwa na kuhama baada ya kuhama. Kwahivyo walio bora miongoni mwa watu ulimwenguni ni wale watakaodumu mahali ambapo alipohamia Ibrâhim.‖ Imepokewa na Abu Dâwûd, no. 2482.

XLIV

MuswalLaa mjini Damascus, kisha ndugu zetu wanaoishi Aleppo nao wakaihuisha, kisha [vilevile ikahuishwa] kwenye miji mengine katika nchi ya Syria na ikaendelea Sunnah hii kuenea mpaka baadhi ya ndugu zetu wanaoishi Ammân nchini Jordan nao wakaihuisha pia.13 Vilevile nikawaonya watu kutokana na kujenga misikiti juu ya makaburi kisha wakaswali humo ndani, nikaandika kitabu changu kuhusiana na hayo, nikakiita, Tahadhari kwa mwenye Kusujudu kutokamana na kuyafanya Makaburi kuwa ni Misikiti.‘ Na nikawagutusha watu wa Taifa langu na nyumba mpya kwa jambo ambalo hawajawahi kulisikia: Niliwacha kuswali kwenye miskiti wa Amawi katika wakati ambao baadhi ya jamaa zangu walikuwa na mazoweya ya kwenda hapo hususan wakiamini yakwamba Kaburi ya Yahya lilikuwa hapo ndani! Katika pirika hizo nilikutana nao, wakiwemo jamaa zangu na wengineo, kwa jambo ambalo kila mlinganizi wa Haki analopambana nalo, pasi na khofu kwa ajili ya

Allâh‎ za lawama za wenye kulaumu.

Nikaandika vitabu kuhusu baadhi ya wajinga wenye ushupavu na nikafungwa mara mbili kutokana na uvumi ambao waliousambaza kwa viongozi wa kitaifa na chama cha Ba‘ath na kwa vile niliwahi kutangaza pindi nilipoulizwa, ―Mimi siungi mkono utawala ulioko kwa vile unapinga Uislamu ...‖ na hayo yakageuka na kuwa mazuri kwangu na kwa kusambaa kwa ulinganizi wangu.

Na Allâh‎ akanirahisishia kutoka na kuzuru miji mingi ya nchi ya Syria

na ya Kiarabu, kulingania kwenye Tawhîd na Sunnah, na kisha [pia] kwenye miji ya Europe. Nikiwa kwenye lengo la uhakika yakwamba hakuna njia yoyote ya kuokoka kwa Wasilamu kutokana na ukoloni, kudhalilishwa na kufedheheshwa kulikowaathiri, yakwamba hakuna faida yoyote katika makundi ya ki-Islamu na mapote ya ki-Siyasa –

13 Tafsiri kwa lugha ya ki-Ingereza ya kitabu cha Sheikh al-Albâni juu ya kuswali swala ya ‗Idd katika Muswallaa, kinapatikana hapa: http://www.islamhouse.com/p/54235

XLV

isipokuwa kwa kushikamana na Sunnah iliyo swahîh juu ya mfumo wa

wema waliotutangulia, twamuomba Allâh‎ awe radhi nao wote. Na sio

kwa kufuata ambayo watu waliyosimama nayo leo yawapo ni katika mas‘ala ya ‗Aqîdah, fiqh au mtazamo ulivyo.

Kwahivyo Allâh‎ amesababisha kufaidika kwa jambo lolote na mtu

yoyote kutokamana na waja wake wema ambao aliowapendelea yeye. Jambo hili likadhihiri waziwazi katika ‗Aqîdah zao, ibâdah zao, jinsi wanavyojenga misikiti yao, jinsi wanavyo onekana na mavazi yao – jambo ambalo kila mwanachuoni muadilifu atashuhudia na hapana atakaekanusha isipokuwa mwenye chuki au mlaghai.

Kwa haya natumai yakwamba Allâh‎ atanisamehe madhambi yangu

yote na kwamba ataniandikia malipo mema kwa hayo kwa babangu na

mamangu, na kila sifa njema zinamstahiki Allâh‎ ambaye kwa baraka

zake mambo mema hutimia.

“Ewe Mola! Nija‟aliye na uniafikiye juu yangu nguvu na uwezo yakwamba nipate kukushukuru kwa fadhla zako ulizonipa na juu

ya wazazi wangu na kwamba nifanye mambo mema yatakayokuridhisha wewe, na uniingize nami kwa rehma zako miongoni mwa waja wema.” Ewe Mola, “... kija‟aliye kizazi

changu kuwa chema. Kwa hakika, mimi natubia kwako unisamehe, na kwa hakika, mimi ni miongoni mwa Waislamu (mwenye

kujisalimisha chini ya matakwa yako).” Nukta ya mfasiri: Kuna kurasa tano zinazofuata ambazo mkusanyaji ameorodhesha vitabu ambavyo Sheikh alivyovitunga, nimeiwacha hiyo na pengine tunaweza kuitaja orodha mpya zaidi katika siku za usoni kwani baadhi ya vitabu vilivyo orodheshwa vimeshachapishwa haliyakuwa vingali katika hali ya kurasa katika wakati kitabu kilipokuwa kikikusanywa. Baada ya kupanga orodha ya vitabu hivyo, mkusanyaji, Esâm Mûsa Hâdi, akasema:

XLVI

Na hili ndilo la mwisho nililoweza kukusanya kuhusiana na wasifu

wake. Yâ Allâh‎! Mfikilizie swala zako Muhammad na Ahli zake na

Maswahaba zake. Muandishi: Esâm Mûsa Hâdi Ammân, Jordan Jumatano. 1st Jumâdi al-Âkhirah, 1421 AH ambayo ni sawiya na 30th August, 2000 CE. Na tafsiri hii kwa lugha ya ki-Ingereza ilikamilika mnamo: Jumapili. 13th March, 2011. Tafsiri kwa lugha ya Kiswahili imekamilika mnamo: Jumapili. 18th January, 2015. Abu Farida Muhammad Awadh Salim Basawad. Mombasa, Kenya

واحلمد هلل رب العلمني

I

3

DIBAJI

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Aliyeumba Ardhi na Mbingu na Anayesifika kwa kila la ukamilifu, na kuepukana na kila upungufu;

Namshukuru Mwenyezi Mungu ( وتعاىل سبحانه ) kwa kupata kukiona kitabu

hiki ambacho ni tafsiri ya kitabu kifupi kilichoandikwa na mwanachuoni mkubwa wa Sunnah (SHEIKH MUHAMMAD NÂSIR-UD-DÎN AL-ALBÂNI) ambacho ni kidogo kulingana na karatasi zake, na ni kikubwa kutokana na yaliyomo ndani mwake. Kijitabu kilichopata umashuhuri katika ulimwengu wa ki-Islamu kilichopendwa na kila mwenye akili mpenda kheri, kinachomfundisha killa Muislamu namna ya kuitekeleza Ibada Tukufu ya Swala kama namna alivyoswali Bwana

Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) kuanzia Takbîr mpaka SaLaam.

Kijitabu hiki kimesomwa sana na TulLaabul-‗Ilmi na hata wasomi wakubwa-wakubwa wa ki-Islamu, na kufidika nacho kupitia

hadîth za Bwana Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) zilizo swahîh sana. Lakini wengi

wa walofidika ni wale wanaoelewa vizuri na lugha ya Kiarabu. Tafsiri hii ya kijitabu hiki imekuja kuziba pengo iliyokuwako na kuifanya faida ya kitabu hiki imfikie killa Muislamu anayeishi katika Africa ya Mashariki. Ni furaha vilevile kuiona kazi hii ikitekelezwa na watoto wetu tunaowatarajia kuwa watetezi wa Qur‘ân na Sunnah ya Bwana

Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ). Sina ninaloweza kulisema illa kumuombea malipo mema

Sheikh “MUHAMMAD NÂSIR-UD-DÎN AL-ALBÂNI” aliyempenda Bwana

Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) na Qur‘ân na Sunnah, na kuwaombea watoto

wetu, Muhammad Awadh Basawad na Ustadh Athman Na‘mân na

II

wenzao. Na kesho tulione toleo jingine: Mungu Awafanye ni watetezi wa Qur‘ân na Sunnah, awape umri mzuri ili watufanyie mazuri.

وصلذ اللذ ذ خري خي ع وش ذ وش ـ د صلذ اللذ ذ م USTADH MOHAMMAD SHARIFF FAMAU [RahimahulLaah], 8th Oct, 2010 /29th Shawwal 1431H

MALINDI,

KENYA.

III

2

UTANGULIZI Kila aina ya Sifa njema ni zenye kumthubutukia Allâh‎, ambaye ndiye Aliyefaradhisha Swala juu ya waja wake kisha akawaamrisha kuisimamisha na kuitekeleza ipasavyo; ambaye aliyefungamanisha kufaulu na furaha kuu na unyenyekevu katika Swala; ambaye ndiye aliyeifanya kuwa ni kigezo cha kupambanua baina ya Îman na kufr; na ndiye aliyeifanya kuwa ni kizuizi kutokamana na vitendo vya aibu na madhambi.

Swala na salamu zimfikiye Mtume wetu, Muhammad ( وسلم عليه اهلل صىل ), aliyekusudiwa katika maneno ya Allâh‎ ( وتعاىل سبحانه ) Aliposema:

زجلة إحلر ٱوأ رون ل ذ حذه ذ وف ة زل إحل ذةس ل ٤٤تلبي

“Na tumekuteremshia mauidha ili uwabainishie watu yaliyoteremshwa kwao, na ili wapate kufikiri.”14

Nae akalitekeleza jukumu hili kikamilifu. Swala ndiyo iliyokuwa mojawapo ya mambo muhimu sana ambayo aliyowahi kuwafundisha watu, kwa kauli na kwa vitendo, hata wakati fulani ikambidi aswali juu ya mimbar – akisimama, akirukû‘ na akisujudu, na kisha akasema kuwâmbia:

ا صالت » ذ ا ب وتلف تذا تلأ فخ ة ص « إجذ

“Mimi nimefanya haya ili mupate kunifuata na kujifunza Swala yangu.”15

14 Surah an-Nahl (16):44

IV

Akatuwajibisha sisi tumuige katika Swala yake, akisema:

صل »ن أ حذ

ة رأ ا « ص

“Swalini kama mulivyoniona nikiswali.”16 Vilevile akatoa bishara njema kwa yoyote atakaeswali kama yeye yakwamba mtu huyo ana ahadi ya Allâh‎ ya Kumuingiza Peponi, akisema:

ات خس » ذ ص اذتط زذ اللذ ذ ـ وص ظصذ أ ء ذ وط وصالذ ذ ل ىذ

ذ تذ وأ خ ر ل ن حلهر ل و

د أ خ ذ كن ل ع اللذ خ ذ وخظ وشضد

ث ذذ ـ د إن طةء دهر ل إون طةء خ نيس ل ع اللذ «حهف“Kuna Swala tano ambazo Allâh‎ ( ه عزه وجل ) alizozifaradhisha: mwenye

kukamilisha wudhu‟ wake ipasavyo, akaziswali Swala zake katika wakati upasao, akakamilisha rukû‟ zake kisawa-sawa, sijda na unyenyekevu, atakuwa mtu huyu ana ahadi kutoka kwa Allâh‎

yakwamba Atamsamehe; na yule asiyefanya hivyo hatokuwa na dhamana kutoka kwa Allâh‎: Akipenda atamsamehe, au akipenda

atamuadhibu.”17 Vile vile Swala na Salamu ziwe juu ya Ahli zake na maswahaba wake

walio wema na waadilifu, waliotunukulia sisi ibada yake ( وسلم عليه اهلل صىل ), Swala yake, kauli na vitendo vyake, na akayafanya haya, na haya pekee, kuwa ndiyo madh-hab yake na kielelezo cha kuigwa; na pia

15 Bukhâri na Muslim – riwaya hii itakuja baadae kikamilifu. 16 Bukhâri na Muslim 17 MÂLIK, Abu Dâwud, an-Nasâ‘î na Ibn Hibbân. Hadîth swahîh, imebainishwa kuwa ni swahîh na ma-Imâm wengi. Nimetoa takhrîj yake katika swahîh Abî Dâwud (451, 1276)

V

juu ya wale wenye kuandama nyayo zao na kufuata njia zao mpaka siku ya Malipo.

********

Nilipomaliza kusoma mlango wa ―Kitâbus-SwaLaah‖ katika Targhîb

wat-Tahdhîb cha al-Hâfidh al-Mundhiri (رحمه اهلل) na kukifundisha kwa

ndugu zetu wa ki-Salafi, takriban miaka minne iliyopita, ikatudhihirikia sisi sote, daraja muhimu ya Swala katika Uislamu; na uzuri wake unaotokana na malipo, fadhila na ta‘adhima kubwa zenye kuwasubiri wale waliokuwa wakiisimamisha na kuitekeleza ipasavyo, na kwamba yote hayo yanatafautiana – imma huzidi au hupungua –

kulingana na ukaribu au umbali na Swala ya Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) kama

alivyoashiria jambo hilo kwa maneno yake:

الة » ة إنذ افجد حلصل الصذ ة شجف ة ث ة تصف ش ـ ة إلذ ة يسذت ل

ة ة صه ة زس ة ربف ة خص « شدش“Hakika mja huswali Swala ambayo haandikiwi chochote (kutokana

na Swala hiyo) isipokuwa ( 1/10) „Usheri, (1/9) tus‟u, (1/8) thumun, (1/7) sub‟û, (1/6) sudus, (1/5) khumus, (1/4) rubu‟, (1/3) thuluth

au (1/2) nusu yake.”18 Kwahivyo, mimi nikawakumbusha ndugu zangu yakwamba hatutoweza kuitekeleza Swala kama inavyostahiki kuswaliwa, au hata angalau kujaribu kuikurubia, mpaka tujue maelezo kwa ukamilifu,

ilivyokuwa Swala ya Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ): yakiwemo mambo ya

Waajib, adabu zake, jinsi ya Swala zenyewe, (du‘â zake) na utajo (adhkâr), kisha baada ya hapo tufanye juhudi kwa tahadhari ya

18 Swahîh, imepokewa na Ibn al-Mubârak katika ―az-Zuhd‖ (10/21/1-2), Abu Dâwud na an-Nasâ‘î ikiwa na isnâd nzuri; nimetoa takhrîj yake kwenye Swahîh Abî Dâwud (761).

VI

kuifanyia kazi ilimu hiyo kwa vitendo, basi hapo tena ndio huenda tukatarajia yakwamba Swala zetu zitatuepusha na vitendo vya aibu na madhambi, na kwamba tutastahiki kuandikiwa thawabu na malipo mema yaliyotajwa kwenye mapokezi mbalimbali. Hata hivyo, kujizoezesha kikamilifu na vipengele vyote hivi vya Swala ni mambo yasiyoweza kutekelezwa na watu wengi siku hizi, hata wakiwemo Wanavyuoni wengi, kwa sababu ya kujiwekea nafsi zao mipaka ya Madh-hab maalum. Lakini, kwa yoyote mwenye kujihusisha na usaidizi katika ukusanyaji na usomaji wa Sunnah iliyotwahirika anajua yakwamba, katika kila Madh-hab kunapatikana Sunnah ambazo zisizopatikana kwenye Madh-hab nyengine; zaidi ya hayo, katika kila madh-hab kuna maneno na vitendo visivyoweza kuthibitishwa uswahîh

wake kutoka kwa Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) – mengi ya mambo haya

hupatikana katika maneno ya Wanavyuoni waliokuja baada e19, wengi

19 Abul Hasanât Al-Lucknowi asema katika an-Nâfi al-Kabîr liman yutâli‘ al-Jâmi‘ as-Swaghîr (Uk. 122-3), baada ya kuvikagua vitabu vya fiqh ya Hanafi na kutaja vipi miongoni mwao ni vyenye kutegemewa na ni vipi visivyofâ: ―Yote ambayo tulowahi kuyasema kuhusu daraja zinazohusika katika vitabu hivi inahusiana na yaliyomo kwenye mas‘ala ya ki-fiqh; lakini, ama yale

yaliyomo yanayohusu ahâdîth za Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), basi hayo hayahusiki,

kwani vitabu vingi vinavyotegemewa na vigogo vya ma-fuqahâ vimejâ ahâdîth za kuzua, licha ya hukmu ya Wanavyuoni. Ni wazi kwetu kwa mtazamo mpana wa utafiti yakwamba hata kama wândishi wao pengine walikuwa na uhodari, lakini walizembea katika kunukuu kwao riwaya.‖ Miongoni mwa ahâdîth hizo za urongo, na kuzua zinazopatikana katika baadhi ya vitabu bora ni: ―Mwenye kuswali Swala ya faradhi katika siku ya Ijumâ ya mwisho ya Ramadhân, (Swala) hiyo itafidia kila Swala aliyoikosa

katika maisha yake mpaka ifikapo miaka sabiini!‖ Amesema Lucknowi ( رحمه katika Al-Âthâr al-Marfû‘ah fil Akhbâr al-Mawdhû‘ah (Uk. 315), baada ya (اهلل

kuisimulia hadîth hii, ―Ali al-Qâri amesema katika kitabu chake, al-mawdhû‘ât as-Sughra na al-Kubra: haya ni maneno ya urongo kabisa, kwani yanakwenda kinyume na Ijmâ‘ (rai iliyoafikiwa) yakwamba kitendo kimoja cha Ibada hakiwezi kuzifidia (‗ibaadah) zilizopita kwa miaka mingi. Mwanzo kabisa, hakuna haja ya kumnukuu mwandishi wa an-Nihâyah wala

VII

wao twawaona wakiyanasibisha madai hayo kwa Mtume ( عليه اهلل صىل – kwa ushupavu tu! Hii ndiyo sababu Wanavyuoni wa hadîth 20(وسلم

washereheshaji waliobaki wa al-Hidâyah, kwa sababu wao si Wanavyuoni wa hadîth, wala wao hawakuinasibisha hadîth hii kwa Mwanachuoni yoyote wa hadîth.‖ Imâm ash-Shawkâni nae pia akaitaja hadîth hii katika kitabu chake cha Al-Fawâ‘id al-Majmû‘ah fil-Ahâdîth al-Mawdhû‘ah kwa maneno kama hayo kisha akasema (Uk. 54), ―Hapana shaka yakwamba hadîth hii ni ya Uzushi – sijawahi kuiona hata kwenye vitabu vyovyote vya hadîth za Uzushi! Hata hivyo, imekuwa ni mashuhuri mno miongoni mwa baadhi ya wanafunzi wa ki-Fiqh katika mji wa San‘â kwenye hizi zama zetu, na wengi wao wameanza kuitekeleza kwa vitendo. Hata sijui ni nani aliyewazuliya hadîth hii – Tunamuomba Allaah Awafedhehi watu warongo.‖ Lucknowi akaendelea kusema, ―Ili kuithibitisha hadîth hii, ipatikanayo kwenye vitabu vya Ibada na maombi, kuwa ni ya Uzushi, nimeandika insha kwa mukhtasar, iliyo na ushahidi wa kitâlamu na upokezi wa riwaya, kiitwacho ―Kuwatahadharisha Ndugu Kutokana na Uzushi wa Ijumâ ya Mwisho ya Ramadhân‖, ambamo nimeratibu nukta zenye kuangazia fahamu zitakazoyazibua masikio, ningekushauri ukipate, kwani kina thamani kubwa katika maudhui haya na uzuri wake ni wa hali ya juu.‖ Kuwepo kwa ahâdîth za urongo katika vitabu vya fiqh kumeharibu uaminifu wa ahâdîth nyengine ambazo wao hawakuzinukuu kutoka kwenye vitabu vya kutegemewa vya Hadîth. Maneno ya ‗Ali al-Qâri yana ishara ya kutujulisha haya: Muislamu hana budi kuchukua Hadîth kutoka kwa watu wenye ujuzi katika tâluma hiyo, chembelecho methali ya zamani ya kiarabu isemayo, ―Wakâzi wa Makka ni bora katika kuzijua njia za Milima yao‖ na ―Mwenye nyumba ndiye mbora wa kujua kila kilichomo nyumbani mwake.‖ 20 Kwa ujumla, maneno ya Imâm an-Nawawî (رحمه اهلل) katika Al-Majmû‘ Sharh

al-Muhadh-dhab (1/60) ni kama yafuatayo. ―Wanavyuoni wa mambo ya utafiti wa Watu wa Hadîth na wengineo wanasema yakwamba iwapo hadîth

ni dha‘îf, hakutosemwa kuihusu hadîth hiyo, ‗Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

VIII

Allâh‎ awajazi kheri nyingi – wakaanza kuandika vitabu vya Takhrîj kuhusu vitabu mashuhuri vya Wanavyuoni waliokuja baada e, wakibainisha hali ya kila hadîth iliyomo kwenye vitabu hivyo: iwapo kwa mfano ni Swahîh, dha‘îf, au maudhû‘. Mfano wa vitabu hivi vya Takhrîj ni: Al-‗Inâyah fi Ma‘rifah Ahâdîth al-Hidâyah na At-Turuq wal-Wasâil fi Takhrîj Ahâdîth Khulâsah‎ ad-DaLaail cha Sheikh ‗Abdul Qâdir ibn Muhammad al-Qurashi al-Hanafi; Nasb ar-Râyah li Ahâdîth al-Hidâyah cha Hâfidh Zayla‘i, na toleo lake kwa Mukhtasar ad-Dirayah cha Hâfidh Ibn Hajar al-AsqaLaani, ambae pia aliyeandika Talkhîs al-Habîr fi Takhrîj Ahâdîth ar-Râfi‘i al-Kabir; kuna vitabu vyengine vingi, ambavyo kwa kuvitaja kutazidi kurefusha majadiliano haya.21

SABABU ZILIZOCHANGIA KATIKA UTUNGAJI WA KITABU HIKI NA BAADHI YA MIPANGILIO YAKE

amesema/amefanya/ameamrisha/amekataza ...‘ au ibara yoyote nyengine yenye kudhihirisha uhakika, lakini badala yake itasemwa, ‗Imesimuliwa/imenukuliwa/imepokewa kutoka kwake ...‘ au ibara nyengine zinazoashiria shaka. Wanasema yakwamba ibara za uhakika ni za ahâdîth zilizo Swahîh au Hasan, na ibara za shaka ni za chochote kinyume cha hayo. Hii ni kwa sababu ibara zenye kudhihirisha uhakika inamânisha yakwamba kinachofuata ni Swahîh, kwa hivyo zitatumika kuhusiana na yaliyo swahîh

peke yake, na lau si hivyo, matokeo yake yatakuwa ni kumzulia (صىل اهلل عليه وسلم).

Mapatano haya yamepuuzwa sana na ma-fuqahâ wengi wa zama zetu, bali, na Wanavyuoni wengi walio kwenye fani mbali mbali, isipokuwa muhaddithîn wenye ujuzi. Haya ni maudhi ya kutojali, kwani wao husema kila mara kuihusu hadîth iliyo swahîh, ‗Imepokewa kutoka kwake yakwamba...‘, na kuihusu hadîth iliyo dha‘îf, ‗amesema‘, na ‗amepokea fulani na fulani...‘, na haya si ya ukweli.‖ 21 Uzundusho wa Mchapishaji: Pia katika mlango huu kuna vitabu vya mwalimu wetu, muandishi wa (k.m kwa mfano) Irwâ‘ al Ghalîl fi takhrîj Manâr as-Sabîl katika Mijalada 8, na Ghâyah al-Marâm fi takhrîj ahâdîth al-Halaal wal-Harâm, hii ni takhrîj ya ahâdîth katika kitabu cha Dr. Yûsuf al-Qardhâwi kiitwacho, al-Halaal wal-Harâm fil Islaam, (kilichojâ ahâdîth zilizo Dha‘îf).

IX

Kwa vile sijawahi kuona kitabu chenye kufahamika kuhusu maudhui haya, nilihisi kuwajibika kukiandika kitabu kitakachokusanya pamoja maelezo mengi kama iwezekanavyo ya mpangilio wa Swala ya Mtume

( وسلم عليه اهلل صىل ) kuanzia takbîr hadi taslîm, kwa faida ya ndugu zangu

Waislamu wenye kutamani kufuata uongofu wa Mtume wao ( عليه اهلل صىل katika ‗Ibada zao, ili iwe rahisi kwa yoyote anayempenda Mtume (وسلم

( وسلم عليه اهلل صىل ) atumie kitabu hiki apate kuitekeleza amri yake, ―Swalini

kama mulivyoniona mimi nikiswali.‖

Hivyo-basi, nikaianza kazi hii nzito, na kuzifanyia utafiti ahâdîth zenye kuhusika kutoka katika asili mbali-mbali za Hadîth , matokeo ya yote hayo ikawa ni kupatikana kitabu kilichoko kwenye mikono yako. Nikajiwekea masharti juu ya nafsi yangu yakwamba nitatumia ahâdîth zilizo na sanad swahîh peke yake kulingana na misingi (Qawâ‘id) na kanuni (usûl ) za ‗Ilmu ya Hadîth . Niliwachana na hadîth yoyote iliyotegemea mpokezi asiyejulikana au mpokezi dha‘îf, sawa iwapo imehusu sifa ya nje ya Swala, adhkâr, fadhla zake na yasiyokuwa hayo. Hii ni kwa sababu mimi naitakidi yakwamba ahâdîth22 zilizo swahîh zinatosha, bila ya kubakisha mahitaji ya chochote dha‘îf, kwani hayo hayazidishi chochote isipokuwa dhana (makisio, shaka), na ukosefu wa kukisia katika hayo, kama alivyosema

Allâh‎ (سبحانه وتعاىل) :

ذ ٱإونذ ؾذ ٢٨ة ا طي لو ٱل حلن “Na kwa hakika dhana haisaidii chochote mbele ya haki.”23

Na Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) akasema:

22 Tamko hili ―Hadîth swahîh‖ linahusu Swahîh na Hasan kulingana na maoni ya Muhaddithîn, iwapo Hadîth ni Swahîh li dhâtihi au Swahîh li ghairihi, au Hasan li dhâtihi au hasan li ghairihi. 23 Surah an-Najm (53): 28

X

زذب الدير »ذ أ ذ نإنذ اؾذ واؾذ « إيذةز

“Jiepusheni na dhana, kwa hakika, dhana ni maneno ya urongo.”24. Kwa hivyo, hatuwezi kumuabudu Allâh‎ kwa vitendo kulingana na

hadîth dha‘îf; kwa hakika, Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) ametukataza sisi

kufanya mambo hayo akasema:

« ذ ـ ة ا الدير خن إلذ ي « اتذ“Jiepusheni na kusema kunihusu mimi, isipokuwa yale muyajuayo.”25 Kwa vile ametukataza sisi tusipokee riwaya dhaifu, inafahamika moja kwa moja yakwamba haifai kuyatekeleza maamrisho yanayolingana na riwaya hizo. Nimekitunga kitabu hiki kwa mândiko aina mbili: Maandishi makubwa na Mândishi tanzu/madogo. Katika maandishi makubwa kunapatikana matamshi halisi ya ahâdîth au ―Matn‖, na vile vile maneno yanayofâ ili yaunganishwe pamoja kupatikane ufasaha kwenye kitabu kuanzia mwanzo hadi mwisho. Nimekuwa muangalifu katika kuhifadhi ‗matn‘ ya kila hadîth kama

24 Bukhâri na Muslim 25 Swahîh – imepokewa na at-Tirmidhî, Ahmad, na Ibn Abî Shaybah. Baadae, niligundua yakwamba hadîth hii kumbe ni dha‘îf: Mimi nilitegemea kitabu cha Manâwi katika kuisahihisha isnâd ya Ibn Abî Shaybah, lakini mara nikaja nikaiona mimi binafsi, kumbe ilikuwa wazi ni dha‘îf, ikiwa na isnâd kama ile ya at-Tirmidhî na wengineo – Tazama kitabu changu Silsilah al-Ahâdîth adh-Dha‘îfah (1783). Hata hivyo, mahali pake pamechukuliwa na

maneno ya Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ),

« ث ذ يرى بدير خن ظدذظد اكذبي أ

أ ذب ذ »

―Yoyote mwenye kusimulia kutoka kwangu hadîth ambayo anaijua yakwamba ni ya urongo basi naye ni mmojawapo wa warongo.‖ [Imepokewa na Muslim na wengineo].

XI

ipatikanavyo kwenye vitabu vya Sunnah; kila nionapo hadîth yenye maneno yaliyotafautiana, mimi nimechagua matamshi yenye kukubaliana na ufasaha nk. (na kadhaalika), lakini nimeyakusanya pamoja matamshi mengine, kwa hivyo: ―(katika lafdhi kadhaa na kadhaa)‖ au ―(katika riwaya kadhaa na kadhaa)‖. Ni mara chache tu nilipomtaja Swahaba aliyepokea hadîth , au kuibainisha hadîth yenyewe, ni Imâm gani wa hadîth aliyeipokea kila hadîth , ili kupatikane wepesi katika usomaji na utafiti wa marejeo. Amma kuhusu maandishi tanzu au Maandishi madogo, hayo ni yenye kuyasherehesha maandishi makubwa. Ndani yake nimeziandamanisha ahâdîth na dalili zake, na kuzifanyia utafiti katika mapokezi yake mbali mbali na njia zake za isnâd. Pamoja na hayo, nimesherehesha kuhusu isnâd zake na riwaya zenye kuunga mkono, na maoni kuhusu uadilifu na ukosoaji wa wapokezi, imma swahîh au dha‘îf, zilizo hukumiwa kulingana na sheriya za Uta‘alamu wa Hadîth . Mara kwa mara, njia moja ya riwaya ina maneno ya ziyada ambayo hayapatikani kwenye njia nyengine, kwahivyo nimeyaingiza haya ndani ya Asili ya Hadîth yenyewe kwenye maandishi makubwa kila ipatikanapo nafasi ya kufanya hivyo bila ya kuharibu ufaswaha, nikiyafunga hayo maneno ya ziyada ndani ya vibano vya mraba: [...] , kwa kawaida (aghlabu) bila ya kueleza ni asili zipi zilikuwa pekee katika kupatikana ziyada hiyo. Jambo hili limefanywa tu, ikiwa asili ya hadîth imepokewa na Swahaba huyo huyo, laa si hivyo, nimeitaja kando, k.m, kwenye Dua za Ufunguzi (Ad‟eya tul istiftah) n.k. Huku kujaliza maneno ya ziyada ni katika manufaa mazuri mno ambayo hutoyapata katika vitabu vingi – Kila Sifa njema ni zenye Kumthubutukia Allâh‎, ambaye kwa Ne‘ema Zake hutimia mambo mema. Kisha, nimetaja kwenye maandishi tanzu, madh-hab ya Wanavyuoni kuhusu hadîth ambayo tuliyoileta na dalili zake pamoja na hoja za kila dalili kwa ubainifu, pamoja na uzito na udhaifu wa kila hoja. Kisha tukachagua kutokana na hayo maoni yaliyo sawa ambayo tuliyoyaona kwenye Maandishi Makuu. Vile vile, katika maandishi tanzu, tumeeleza baadhi ya mas‘ala ambayo yasiyokuwa na ushahidi

XII

katika Sunnah, lakini yakawa yanahitaji kufanyiwa Ijtihâd, na wala hayakuja katika maudhui ya kitabu hiki. Kwa vile uchapishaji wa kitabu hiki katika hali ya maandishi makuu na maandishi tanzu haiwezekani kwa sasa kutokana na sababu nyingi, tumeamua kuchapisha maandishi makubwa ya kitabu peke yake (pamoja na uzindushi mfupi chini ya ukurasa) Insha-Allâh‎ na nikakiita

kwa jina, ―Sifa tus—SwaLaah tun-Nabî ( وسلم عليه اهلل صىل ) minat-Takbîr ilat-

Taslîm Ka‘annaka Tarâhâ (Namna Ya Swala Ya Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) Ikielezwa Kuanzia mwanzo hadi mwisho wake kana kwamba unaiona)‖.

Namuomba Allâh‎ ( وتعاىل سبحانه ) aija‘alie kazi hii iwe ni kwa IkhLaas na

kwa Uso Wake Mtukufu na iwanufaishe ndugu zangu waumini. Hakika Yeye ni Mwenye Kusikiya na Mwenye Kujibu.

XIII

MFUMO WA KITABU HIKI

Kwa vile maudhui ya kitabu hiki ni kuubainisha muongozo wa Mtume

( وسلم عليه اهلل صىل ) katika Swala, ilikuwa ni jambo la msingi yakwamba

nisijifunge nafsi yangu na madh-hab fulani, kwa sababu tulizozitaja hapo awali. Kwahivyo, mimi nitaleta kila lilothibitishwa uswahîh wa

kutoka kwake ( وسلم عليه اهلل صىل ) kama ambavyo yalivyokuwa daima madh-

hab ya Ma‘ulamâ wa hadîth (Muhaddithîn)1, wakiwa ni waliotangulia zamani au ni waliotangulia hivi karibuni2, kama ulivyo msemo mzuri kwamba:

1 Amesema ‗Abdul Hayy Al-Lucknowi katika Imâm al-Kalaam fiy mâ yata‘allaqa bil-Qirâ‘ah Khalfal Imâm (Uk. 156), kama ifuatavyo: ―Yoyote mwenye kujitosa kwenye Bahari za fiqh na misingi ya kisheriya akiwa na fahamu zake kisawa sawa, na wala asijidhalilishe na kuathirika, atajua kwa yakini yakwamba katika mas‘ala mengi ya kimisingi na vipengele vyake, ambavyo Wanavyuoni wamekhitilafiana, misimamo ya madh-hab ya Wanavyuoni wa Hadîth ni Imara kuliko ya madh-hab nyenginezo. Kila ninapoingilia kwenye vitagâ vya ikhtilafu za maoni, mimi hukuta yakwamba Rai za Muhaddithîn ziko karibu zaidi na Ukweli – Allaah Awajazi Kheri, Nae Atawapongeza. Itakuwaje kinyume cha hivyo, ikiwa wao ndiwo warathi wa

kihakika wa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), na mawakala wa Sheriya Zake wenye

ikhlaas.; Namuomba Allaah atuja‘alie nasi kuwa ni miongoni mwao, na asitufishe isipokuwa tuwe na mapenzi nao.‖ 2 Amesema as-Subki katika al-fatâwa (1/148): ―Jambo muhimu mno kwa Waislamu ni Swala, ambayo kila Muislamu ni lazima aijali na ahakikishe utekelezaji wake na kudumisha nguzo zake. Kuhusiana na Swala kuna mas‘ala ambayo yaliyokwisha kuafikiwa ikawa hakuna kuuchenga ukweli, na mas‘ala mengine ambayo Wanavyuoni wamekhitilafiana. Msimamo wa sawa ni imma kujiepusha na mabishano iwapo uwezekano wa kufanya hivyo upo, au kutafuta jambo swahîh

lililothibitishwa kutoka kwa Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) na kushikamana nalo. Mtu

afanyapo hivyo, Swala yake itakuwa nzuri na njema, na itakuwa

XIV

« الدير أ أ الرذشل إون ه أج ص ه ا ج ج ع ص ي ل «ا صعج ةش

“Watu wa Hadîth ndiwo watu wa Mtume, hata kama Hawana usuhuba nae, lakini wamejisuhubisha na kila jambo lake.”1

Kwa hivyo kitabu hiki, Insha-Allâh‎, kitakusanya chochote kinachofaa kwenye kila mas‘ala kutoka katika maudhui mbali mbali ya vitabu vya Hadîth na vitabu vya kuhusu ikhtilafu za madh-hab, ili hukumu ya sawa itakayopatikana kwenye kitabu hiki haitopatikana kabisa kwenye madh-hab yoyote iwayo. Kwahiyo, yoyote atakaetenda kulingana na maelezo yake, Insha-Allâh‎, atakuwa ni miongoni mwa wale walio

ongozwa na Allâh‎ ( وتعاىل سبحانه ):

دى ٱذ ٱ للذ ي ة لذ ا ل ٱءا ا خذه ٱو ۦ بإذ لو ٱذ يظةء للذ دي حصذيم ٢١٣إل صرط

imejumuishwa kwenye maneno ya Allaah (سبحانه وتعاىل) katika Surah Kahf (18),

Aya ya 110:

كن يرصا يةء رب ة ۦذ عا الا ص خ ف ١١٠ن―Anayependa kukutana na Mola wake nâfanye vitendo vizuri.‖

Mimi nasema: Msimamo ulio bora ni huo wa pili, laa – hasha, ni Wâjib; hii ni kwa sababu msimamo wa kwanza, pamoja na kwamba ni jambo

lisilowezekana katika mas‘ala mengi, hayatekelezi amri zake ( وسلم عليه اهلل صىل ):

―Swalini kama munavyoniona mimi nikiswali‖, lakini badala yake husababisha Swala ya mtu bila ya shaka yoyote kuwa tafauti na Swala ya

Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ).

1 Kutoka kwenye mashairi ya Hassan Ibn Muhammad an-Nasawi, kama ilivyopokewa na Hâfidh Diyâ‘ ad-Dîn al-Maqdisi katika makala yake ya kuhusu Ubora wa Hadîth na Watu wake.

XV

“Ndipo Allâh‎ Akawaongoza walioamini kwenye Haki katika yale waliyokhitalifiana, kwa idhini Yake. Na Allâh‎ humwongoza

amtakaye kwenye njia iliyonyooka.”1 Nilipojichagulia nafsi yangu mifumo hii, yaani kushikamana na Sunnah Swahîh, na kuyatekeleza kwenye kitabu hiki na vile vile vitabu vyengine, nilijua kwa yakini yakwamba jambo hili halitowaridhisha kila kundi au pote la watu; kwa hakika matokeo yake yatawapelekea baadhi ya watu, ikiwa si wote, kunitukana na kunilaumu mimi. Mimi siyajali hayo, kwani ninajua pia yakwamba kumridhisha kila mtu ni

jambo lisilowezekana na ndio Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل )akasema:

إل اجلذةس » اللذ ثرطة اجلذةس وك شخع اللذ أ »

“Mwenye kuwaridhisha watu kwa kumuudhi Allâh‎, Allâh‎ Atamsalitisha kwa watu.”2

Allâh‎ Amjazi kheri muandishi wa mistari ifuatayo aliposema:

ية » ةج ولصخ ث ـ ح غةر ... ـ و صج

خ ف غر ع ول اجلذةس شةة ي حض ذا الذ بي خةذت نس ...و غب خ

« ول ―Wala nisingeweza kuyakimbia matusi,

Hata kama lau ningelikuwa pangoni mwa mlima wenye mawe-mawe; Kwani ni nani awezae kuwakimbia waja bila ya kudhuriwa;

Hata akajificha chini ya mbawa za Mwewe?‖3 Inatosha kwangu mimi kuitakidi yakwamba hii ndiyo njia iliyo nyooka

aliyoiamrisha Allâh‎ (سبحانه وتعاىل) kwa waumini waifuate, na ambayo

1 Surah al-Baqarah (2): 213 2 At-Tirmidhî, Qudâ‘i, Ibn Bushrân na wengineo. 3 Al-Khawâfî: Ni manyoya. Ndege anapokusanya mbawa zake manyoya yake hujificha na kuwa nyuma ya miguu yake.

XVI

Mtume wetu, kiongozi wa Mitume ( وسلم عليه اهلل صىل )ameifundisha. Hii ndiyo

njia iliyopitiwa na wema waliotutangulia: Maswahaba, na waliowafuata wao na wale waliowafuata hao, wakiwemo ma-Imâm wanne ambao madh-hab zao Waislamu wengi leo wanajinasibisha nazo. Wote waliafikiana juu ya uwajibu wa kushikamana na Sunnah na kurejea kwake; kupuuza kila rai inayokwenda kinyume nayo, bila ya kujali utukufu wa huyo mwenye rai hiyo, kwani daraja ya Mtume

( وسلم عليه اهلل صىل ) ni tafauti kubwa zaidi, na mfano wake ni wa kweli

kupita kiasi. Kwa sababu hii, mimi nimeandama uongofu wao, nikafuata nyayo zao, na nikatekeleza maamrisho yao kushikamana na Hadîth zilizo swahîh, hata kama zitakwenda kinyume na rai zao. Maamrisho yao haya, yameniathiri sana katika kudurusu kwangu kwa makini katika njia hii, na kukataa kwangu kuandama ufuasi wa upofu

―taqlîd‖ (kufuata rai). Namuomba Allâh‎ ( وتعاىلهسبحانه ) Awajazi Kheri

nyingi.

MISEMO YA MA-IMÂM KUHUSU KUFUATA SUNNAH NA KUWACHANA NA RAI ZAO ZENYE KWENDA KINYUME NA

SUNNAH Ni katika faida iwapo tutaleta baadhi ya kauli zao hapa, kwani huwenda ikawa ni mawaidha au ni ukumbusho kwa wale wenye kufuata rai za ma-Imâm – [na si za ma-Imâm hao tu, bali hata], za wale walio katika daraja ya chini zaidi ya ma-Imâm kwa umbali – tena Ki-Upofu1, wakiyashikilia madh-hab yao au rai zao utadhani

yakwamba hayo yameteremshwa kutoka mbinguni! Lakini Allâh‎ ( سبحانه :amekwisha sema (وتعاىل

1 Hii ni aina ya taqlîd (kufuata ki-Upofu) ambayo Imâm at-Twahâwi aliyoikusudia aliposema, ―Hapana mtu isipokuwa aliye na Ghera za Uanachama au mtu mpumbavu atakaefuata rai ya ki-Upofu‖ – yamenukuliwa na Ibn ‗Âbidîn katika Rasm al-Mufti (vol. 1, Uk. 32 kutoka katika ukusanyaji wa insha zake).

XVII

ٱ ا دو دذجف ا ول دتذجف بس رذ زل إحلس ة أ ة ۦ ذ ىالا وحلةء

أ

رون ذ ٣دذ “Fuateni (Enyi watu!) mliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wenu, wala msifuate (hao mnaowaitakidi kuwa) walinzi badala yake. Ni

machache mnayoyakumbuka.”1

1 Surah al-A‘râf (7): 3

XVIII

1) ABU HANÎFAH (رحمه اهلل): Wa kwanza wao ni Imâm Abu Hanîfah an-Nu‘mân Ibn Thâbit ( رحمه ambaye wafuasi wake wamepokea kutoka kwake, kauli nyingi ,(اهلل

na maonyo mbalimbali, yote hayo yakiwa na shabaha moja: Kuwajibika kuikubali Hadîth, na kukoma kufuata rai za ma-Imâm zenye kukhalifu hadîth : 1)

ذيب » « إذا صطذ الدير ذ“Ikiswihi hadîth basi hayo ndiyo madh-hab yangu.”1

2)

ظد » ل خذ ل ي

ن يأ

جلة أ ثي حف ة ل ح

أ خذةه

« أ

1 Ibn ‗Âbidîn katika al-Hâshiyah (1/63), na katika Insha yake Rasm al-Mufti (1/4 kutoka katika ukusanyaji wa insha za Ibn ‗Âbidîn). Sheikh Sâlih al-Fulaani katika Îqâdh al-Himam (Uk.62) na wengineo. Ibn ‗Âbidîn amenukuu kutoka katika Sharh al-Hidâyah cha Ibn al-Shahnah al-Kabîr, mwalimu wa Ibn al-Humâm, maneno yafuatayo: ―Ipatikanapo hadîth inayokhalifu madh-hab kuwa ni swahîh, inampasa mtu aifuate hadîth, na aifanye hiyo kuwa ndiyo madh-hab yake. Kuifuata hadîth hakutombatilisha mtu kuwa Hanafi, kwani imethubutu kupokewa yakwamba Abu Hanîfah amesema, ‗Ikisihi hadîth basi hayo ndiyo madh-hab yangu‘, na haya yamesimuliwa na Imâm Ibn ‗Abdul Barr kutoka kwa Abu Hanîfah na kutoka kwa maimamu wengine.‖ Hii ni sehemu ya ukamilifu wa ilimu na uchaji Mungu walio nayo ma-Imâm, kwani wao waliashiria kwa kuyasema haya yakwamba wao hawakutopea katika Sunnah yote kamili, na Imâm ash-Shâfi‘î ameyafafanua haya kwa undani (yatakuja baadae). Hutokea mara nyengine wao huikhalifu Sunnah kwa sababu walikuwa hawaijui, kwa hivyo wakatuamrisha sisi tujigandishe na Sunnah na kuifanya ni kama sehemu ya madh-hab yao. Namuomba Allaah Awanyeshî wote Rehma zake.

XIX

“Haifai1 kwa mtu yoyote kuyachukuwa maneno yetu ikiwa hajui tulipoyapata.”2

Katika riwaya nyengine:

3)

حفرف ظرام ع » ل ن حهت دحلل « ثسالم أ

“Haifai3 kwa mtu asiyejua dalili zangu kutoa Hukmu4 kwa kutumia maneno yangu”.

Riwaya nyengine inaongezea kusema:

1 Kwa Kiarabu: Si halali 2 Ibn ‗Abdul Barr katika kitabu chake, Al-Intiqâ fî fadhâ‘il ath-Thalaathah al-A‘immah al-Fuqahâ‘ (Uk. 145), Ibn al-Qayyim katika kitabu chake, I‘laam al-Muwâqi‘în (2/309), Ibn ‗Âbidîn katika uzindushi wake kuhusu Al-Bahr ar-Râ‘q (6/293) na katika Rasm al-Mufti (Uk. 29, 32) na Sha‘râni katika kitabu chake al-Mîzân (1/55) pamoja na riwaya ya pili. Riwaya ya mwisho ilipokelewa na ‗Abbâs ad-Dawri katika kitabu cha at-Târîkh na Ibn Ma‘în (6/77/1) kwa isnâd swahîh kutoka kwa Zafar, mwanafunzi wa Imâm Abu Hanîfah. Kuna riwaya mfano wa hizo zilizopokewa na wanafunzi wa Abu Hanîfah, Zafar, Abu Yûsuf na ‗Âfiyah ibn Yazîd; angalia katika Îqâdh (Uk. 52). Ibn al-Qayyim amekuwa Imara katika kuuthibitisha uswahîh wake kutoka kwa Abu Yûsuf katika I‘laam al-Muwâqi‘în (2/344). Mhariri wa Îqâdh (Uk. 65) ameihusisha nyongeza ya kwenye riwaya ya pili na ibn ‗Abdul Barr, ibn al-Qayyim na wengineo. Ikiwa hivi ndivyo wanavyosema kumuhusu mtu asiyejua dalili zao, jibu lao litakuwaje kwa yule mwenye kujua yakwamba dalili hizo zinakhalifiana na maneno yao, na ikawa wao wanakaidi na kutoa uamuzi wenye kwenda kinyume na dalili za wazi?. Kwa hivyo, hebu yatafakari maneno haya, kwani hayo peke yake yatosha kuporomosha mbinu za ufuasi wa rai ki-Upofu; hii ndiyo sababu ya mmojawapo wa mashekhe Muqallid, nilipolaumu hukmu aliyoitoa kwa kutumia maneno ya Abu Hanîfah bila ya kujua dalili, alikatâ kuamini yakwamba huu ni msemo wa Abu Hanîfah! 3 Kwa kiarabu: harâm 4 Kwa kiarabu: fatwâ

XX

4)

ة » ل نإجذ م ورصؿ بش جيل اي كدا احل « خ“Hakika sisi ni wanadamu, twatamka jambo leo, na twaliwacha

jambo hilo siku ifuatayo.” Katika riwaya nyengine:

5)

ية حفيب » شم) ويع ث ي أ نإين ىد ، ة تصؿ نك ل دسذت (

درك كداأي احلم وأ رى الرذ

أي كدا وأدرك ثفد كد ، أ رى الرذ

« وأ

―Ole wako, Ewe Ya‘qûb1! (ambae ni Abu Yûsuf) Usiandike kila unalosikia kutoka kwangu, kwani hakika yangu mimi huwa na rai leo na kesho nikaitupilia mbali, na kesho nikawa na rai nyengine na nikaitupilia mbali siku inayofuata.‖2

1 Yaani: Mwanafunzi maarufu wa Imâm Abu Hanîfah, Abu Yûsuf ( اهلل رحمه ). 2 Hii ni kwa sababu Imâm mara nyingi alikuwa akitegemeza maoni yake juu ya Qiyâs (makisio), kisha mara humdhihirikia yeye jambo jengine lenye kushabihiana na hilo tena lenye nguvu zaidi kuliko lile la kwanza, au hadîth

ya Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) itamfikia yeye, basi huikubali hiyo na huwachana na

rai yake ya hapo awali. Maneno ya Sha‘râni katika Al-Mîzân ni kama yafuatayo kwa mukhtasar: ―Imani yetu, pamoja na ile ya kila mwenye kufanya utafiti kumuhusu Imâm

Abu Hanîfah ( عنه اهلل رضي ), ni kwamba, lau angeliishi hadi wakati wa

kuhifadhiwa kwa Sharî‘ah, na misafara ya wenye kuzihifadhi Hadîth wakielekea kwenye mipaka na miji mbali mbali kwa ajili ya kuzikusanya na kuzipata, angeliyakubali na kupuuza kila ushabihishaji alokuwa akiutumia. Kiwango cha qiyâs katika Madh-hab yake kingelikuwa kichache kama mfano wa madh-hab nyenginezo, lakini kwa vile dalili za Sharî‘ah zimetapakâ sehemu mbali mbali na warathi wake na wale walokuja kuwarithi wao, ikawa hazikuwahi kukusanywa katika wakati wa uhai wake, ndipo ikabidi kupatikane idadi kubwa ya qiyâs katika madh-hab yake ukilinganisha na yale

XXI

ya ma-Imâm wengine. Kisha wanavyuoni walokuja baadae, wakânza misafara yao ya kutafuta Ahâdîth kutoka sehemu mbali mbali za miji na vitongoji na wakânza kuziandika; kwa hiyo, baadhi ya ahâdîth za Sharî‘ah ni zenye kusherehesha baadhi nyengine. Hii ndiyo sababu ya kupatikana kiwango kikubwa cha qiyâs kwenye madh-hab yake, hali yakuwa katika madh-hab nyenginezo kunapatikana idadi ndogo.‖ Abul-Hasanat Al-Lucknowi ameyanukuu maneno yake kwa ukamilifu katika An-nâfi‘ al-kabîr (Uk. 135), akiunga mkono na kuyafafanua katika tanbîh yake, kwa hivyo, yoyote mwenye kutaka muelekeo wake na afanye hivyo hapo.

Kwa vile hizi ni sababu zinazothibitisha ilikuwaje kwa Abu Hanîfah mara nyengine kukhalifu ahâdîth zilizo swahîh bila ya kukusudia – na ni

sababu zinazokubalika kabisa, kwani Allaah (وتعاىل سبحانه) haikalifishi

nafsi yoyote zaidi ya uwezo wake – haifai kumkashifu kwa hayo, kama walivyofanya baadhi ya watu wajinga. Kwa hakika, ni wâjib kumuheshimu, kwani yeye ni mmojawapo wa ma-Imâm wa Waislamu ambaye, kwa kupitia kwake, Dini hii imehifadhiwa na kufikilizwa kwetu, katika vitagâ vyake vyote; na pia, kwani yeye ni mwenye kupata malipo katika hali yoyote iwayo, iwapo amepata au amekosa. Wala hairuhusiwi kwa wafuasi wake kuendelea kuyashikilia yale maneno yake yanayokwenda kinyume na Ahâdîth zilizo Swahîh, kwani maneno hayo hayana nafasi ya kukubalika katika sehemu ya Madh-hab yake, chembelecho hiyo qauli iliyotangulia. Kwa hiyo, haya ni makundi mawili yaliyopita kiyasi, na ukweli unapatikana kati-kati yake.

ة » ة جلة اكهر ربذ ا ولخ ي ةن شجية الذ ي ول ثةل ة ف تف ب كال ى ي ا لذ ة آ ربذ

رؤوف إذ « رذظ

“Mola wetu! Tusamehe sisi na ndugu zetu waliotutangulia (kufa) katika Uislamu. Wala usija‟alie katika nyoyo zetu mifundo

kuwafanyia Waislamu (wenzetu). Mola wetu! Hakika Wewe ni Mpole sana, Mwenye rehema mno.” [Al-Hashr (59): 10]

XXII

6)

صل الل ـ الرشل وخرب دفةل الل ذةب خيةم ىل ىخ إذا »ا ىيل وش « نةدرك

“Ninaposema kauli yenye kukhalifu kitabu cha Allâh‎ (سبحانه وتعاىل ) au

yaliyopokewa kutoka kwa Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) iwacheni kauli

yangu.”1

2) MÂLIK IBN ANAS ( اهلل رحمه ): Ama kuhusu Imâm Mâlik ibn Anas ( اهلل رحمه ):

1 Al-Fulaani katika Îqâdh al-Himam (Uk.50), akiifuatiliza kwa Imâm Muhammad na kisha akasema, ―Hii haimuhusu mujtahid, kwani, tangu hapo, yeye hafungamani na maoni yao, lakini inamuhusu Muqallid.‖ Sha‘râni akatoa ufafanuzi wake juu ya hayo katika al-Mîzân (1/26): ―Iwapo itasemwa: ‗Nifanyeje na ahâdîth ambazo Imâm wangu hakuzitumia, na ambazo zilizopatikana kuwa swahîh baada ya kufa kwake?‘ Jawabu la kukutosha wewe ni kwamba zitekeleze, kwani lau kama Imâm wako angeliziona na kuzikuta kuwa ni swahîh, angelikuamrisha wewe uzifuate, kwa sababu ma-Imâm wote ni mateka walio mikononi mwa Sharî‘ah.‘ Yule mwenye kufanya hivyo, atakuwa amekusanya mazuri matupu kwa mikono yake miwili, lakini yule mwenye kusema, ‗Mimi sitotekeleza kulingana na hadîth hii mpaka Imâm wangu afanye hivyo‘, atakuwa amepoteza kiwango kikubwa cha kheri, kama ilivyo hali ya wafuasi wengi wa ma-Imâm wa Madh-hab. Itakuwa ni bora kwao wao kutekeleza kila hadîth ipatikanayo kuwa swahîh baada ya wakati wa Imâm, kwa hiyo watakuwa wanatekeleza misimamo ya ma-Imâm wao; kwani sisi tunâmini kwa dhati kuwahusu ma-Imâm yakwamba lau kama wangelikuwa na maisha marefu wakaja kugundua baadae kuhusu hizo ahâdîth zilizokuwa ni swahîh baada ya wakati wao, basi bila ya shaka yoyote wangelizikubali na kuzitekeleza kama zinavyoamrisha, na kutupilia mbali ukisiaji wowote waliowahi kutumia hapo awali, na maoni yoyote waliokuwa nayo awali.‖

XXIII

1)

الذةب وانو ة نلك رأيي ف نةؾروا وأصت أخػئ بش أة إة »ه والصح الذةب يانو ل ة ولك نخذوه والصح « نةدرك

―Hakika mimi ni mwanadamu: (mara nyengine) hukosea na (mara nyengine) hupata. Kwahivyo, angalieni kwa upelelezi kuhusiana na rai zangu, kila lenye kuafikiana na Kitâb na Sunnah, kubalianeni nayo; na

kila kisichoafikiana na Kitâb na Sunnah, wachaneni nacho.‖1

2)

إل ويؤخذ ىل ويتك إل صل الل ـ وش اجليب ثفد أظد يس » « صل الل ـ وشاجليب

―Hapana yoyote baada ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)isipokuwa maneno yake

yatakubaliwa au yatakataliwa.‖2

1 Ibn ‗Abdul Barr katika Jâmi‘ Bayân al-‗Ilm (2/32), Ibn Hazm, akinukuu kutoka kwa alotajwa awali kwenye kitabu Usûl al-Ahkâm (6/149), na vile vile Al-Fulaani (Uk. 72). 2 Jambo hili ni maarufu sana miongoni mwa wanavyuoni walokuja baadae yakuwa ni msemo wa MÂLIK. Ibn ‗Abdul Hâdi ameithibitisha kuwa swahîh katika Irshâd as-Sâlik (227/1); Ibn ‗Abdul Barr katika Jâmi‘ Bayân al-‗Ilm (2/91) na Ibn Hazm katika Usûl al-Ahkâm (6/145, 179) ameyapokea kuwa ni maneno ya Al-Hakam ibn ‗Utaibah na Mujâhid; Taqi-Ud-Dîn as-Subki ameinukuu, akapendezwa na uzuri wake, katika al-Fatâwâ (1/148) kuwa ni maneno ya Ibn ‗Abbâs na kisha akasema: ―Asili ya maneno haya yalikuwa ni

ya Ibn ‗Abbâs na Mujâhid, na Mâlik (عنهم اهلل يرضه) aliyachukuwa kutoka kwao,

nae akapata umaarufu kwa maneno hayo.‖ Yaonekana kwamba Imâm Ahmad nae akayachukuwa maneno hayo kutoka kwao, kama alivyosema Abu Dâwud katika Masâ‘il ya Imâm Ahmad (Uk. 276): ―Nilimsikiya Ahmad akisema, ‗Kila mmoja ni mwenye kukubaliwa au kukataliwa katika rai zake, isipokuwa

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)‘.‖

XXIV

3) Ibn Wahb amesema: ―Nilimsikiya Mâlik akiulizwa kuhusu kuosha baina ya vidole vya miguu wakati wa kutawadha. Akasema, ‗Watu hawana haja ya kufanya hivyo.‘ Mimi sikumkurubia mpaka kundi la watu likamalizika, ndipo nikamwambia, ‗Sisi twajua kuhusu Sunnah hiyo.‘ Akasema, ‗Na ni nini hiyo?‘ Nikasema, ‗al-Layth ibn Sa‘ad na ibn Lahay‘ah na ‗Amr ibn al-Hârith wametuhadithia kutoka kwa Yazîd ibn ‗Amr al-Ma‘âfiri nae kutoka kwa Abu ‗Abdur-Rahmân al-Hanbalî nae kutoka kwa al-Mustawrid ibn Shadâd al-

Qurashî aliyesema, ‗Nilimuona Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) akipangusa

baina ya vidole vyake vya miguu kwa kidole chake cha mwisho.‘ Akasema, Hadîth hii ni hasan; sijawahi mimi kuisikiya isipokuwa sasa hivi.‘ baada e nilimsikiya akiulizwa kuhusu suala hilo hilo tena, nae akaamrisha kuosha baina ya vidole vya miguu.‖1

3) SHÂFI‟Î ( اهلل رحمه ):

Ama kuhusu Imâm ash-Shâfi‘î, yaliyonukuliwa kutoka kwake kuhusu mas‘ala haya ni mengi na yenye kupendeza mno2, na wafuasi wake walikuwa ni bora wa kushikamana nayo na kuyatekeleza:

1 Kutoka katika utangulizi wa Al-Jarh wat-Ta‘dîl cha Ibn Abî Hâtim, (Uk. 31-2). 2 Amesema Ibn Hazm katika Usûl al-Ahkâm (6/118): ―Kwa hakika, mafuqahâ‘ wote ambao rai zao hufuatwa wanapinga taqlîd, na wakawakataza wafuasi wao wasifuate rai zao ki-Upofu. Aliyekuwa mkali

katika mas‘ala haya miongoni mwao ni ash-Shâfi‘î ( اهلل رحمه ), kwani mara kwa

mara alikuwa akisisitiza, zaidi ya wote, kufuatâ riwaya zilizo swahîh na kukubali lolote lenye kuthibitishwa kwa dalili; pia akajieka mbali na hatia ya yoyote mwenye kumuandama yeye kwa kila jambo, na akawatangazia wale waliokuwa naye kila wakati.. Jambo hilo na limfaidishe mbele ya Allaah

(وتعاىل سبحانه) , na malipo yake yawe ni ya juu kabisa, kwani yeye alikuwa ni

sababu ya kheri nyingi.‖

XXV

1)

ودفزب صل الل ـ وش الل لرشل شح ـ ودذت إل أظد ة »صل الل ـ نة ىخ ىل أو أصخ أص ن ـ رشل الل

صل الل ـ وشخلالف ة ىخ نةيل ة ىةل رشل الل ـ وش ىيل «و

―Hapana mtu yoyote isipokuwa itamfikia Sunnah ya Mtume ( عليه اهلل صىل au itakuwa mbali nae. Kwahivyo, kila nikitoa rai yangu, au (وسلم

nikianzisha msingi wowote, na kukapokewa kinyume cha maoni yangu

kutoka kwa Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ), basi maneno aloyasema Mtume ( اهلل صىلوسلم عليه ) ndiyo maneno yangu.‖1

2)

صل الل ـ الل رشل ـ شح ل اشتجةن أن ع اصن أمجؿ » «ل ي ل أن يدـة يل أظد وش

―Wameafikiana Waislamu kwa Qauli moja yakwamba yoyote

atakaedhihirishiwa Sunnah kutoka kwa Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ), haifai2

kwake kuiwacha kwa ajili ya Qauli ya yoyote.‖3 3)

1 Imepokewa na Hâkim kwa sanad yenye kushikana hadi kufikia Shâfi‘î, kama ilivyo katika Târîkh Dimashq cha Ibn ‗Asâkir (15/1/3), I‘laam al-Muwâqi‘în (2/363, 364) na Îqâdh (Uk. 100) 2 Kwa kiarabu: si halaal. 3 Ibn al-Qayyim (2/361) na Fulaani (Uk. 68)

XXVI

ا صل الل ـ وش الل رشل شح خالف ذةب ف وصدد إذا » نيلا ة ىخ صل الل ـ وشبصح رشل الل ة )ويف روايح ) ودـ نةدجف

ا ول « ( أظد ىل إل دذهذ―Utakapo ona katika kitabu changu chochote chenye kwenda kinyume

na Sunnah ya Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ), basi wewe sema kulingana na

misingi ya Sunnah za Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) na uwachane na yale

niloyasema mimi.‖ Katika riwaya nyengine: ―...basi ifuate (hiyo Sunnah), na wala usiangalie huku na huku kutafuta maneno ya mtu yoyote.‖1 4)

« ذيب ن الدير صط إذا »―Ikiswihi hadîth, basi hayo ndiyo madhehebu yangu.‖2

1 Harawi katika Dhamm al-Kalaam (3/47/1), Khatîb katika Al-Ihtijâj bi ash-Shâfi‘î (8/2), Ibn Asâkir (15/9/10), an-Nawawî katika Al-Majmû‘ (1/63), Ibn al-Qayyim (2/361) na Fulaani (Uk. 100); Riwaya ya pili ni kutoka katika Hilyah al-Awliyâ‘ cha Abu Nu‘aim. 2 An-Nawawî katika Al-Majmû‘ (1/63), Sha‘râni (1/57), akitoa asili zake kutoka kwa Hâkim na Baihaqî, na Fulaani (Uk. 107). Akasema Sha‘râni, ―Ibn Hazm amesema, ‗Na hiyo, ... ameiona yeye au Imâm mwengine yoyote kuwa ni swahîh‘.‖ Kauli yake ijayo inathibitisha ufahamu huu. An-Nawawî amesema: ―Wenzetu wametekeleza kulingana na haya kuhusiana na mas‘ala ya tathwîb (nyongeza katika adhân ya kuwalingania watu kuja kuswali), hukmu ya kujitoa katika ihrâm kwa ajili ya ugonjwa, na mas‘ala mengine maarufu katika vitabu vya Madh-hab. Miongoni mwa wale wenzetu ambao kwa mujibu wa târifa walitoa hukmu juu ya misingi ya hadîth (yaani: badala ya maneno ya ash-Shâfi‘î) ni Abu Ya‘qûb al-Buwîti na Abul-Qâsim ad-Dâriki. Miongoni mwa wenzetu katika Muhaddithîn, Imâm Abu Bakr Al-Baihaqî na wengineo wametumia utaratibu huu. Wenzetu wengi

XXVII

waliotangulia mwanzo, walipokuwa wakikabiliana na mas‘ala ambayo inapatikana hadîth, na madh-hab ya ash-Shâfi‘î yanakhalifiana nayo, wao walikuwa wakitekeleza kulingana na hadîth na kutoa hukmu juu ya msingi huo, wakisema, ‗Madh-hab ya Shâfi‘î ni chochote chenye kukubaliana na hadîth.‘ Sheikh Abu ‗Amr (Ibn as-Salaah) amesema: ‗Yoyote miongoni mwa ma-Shâfi‘î akiona hadîth ikikhalifiana na madh-hab yake, atazingatia iwapo ametimiza hukmu za ijtihâd kwa ujumla, au katika madda hiyo makhsusi au mas‘ala, kwenye hali yoyote iwayo atakuwa na uhuru wa kutekeleza kwa mujibu wa hadîth; na lau si hivyo, lakini kwa sura yoyote iwayo anaona ni vigumu kwake kukhalifu hadîth baada ya utafiti wa ziyada, hatoweza kupata uthibitisho wenye kuridhisha wa kuipinga hadîth. Kwa hiyo, itakuwa ni juu yake atekeleze kulingana na hadîth ikiwa Imâm mwengine mwenye kujitegemea asiyekuwa Shâfi‘î ametekeleza kulingana na hadîth hiyo, na huu utakuwa ndio uthibitisho kamili wa kuiwacha madh-hab ya Imâm wake kwenye mas‘ala hayo.‘ Hayo ambayo aloyasema (Abu ‗Amr) ni ya sawa na yamethibitishwa. Allaah ni Mjuzi zaidi.‖ Kuna uwezekano mwengine ambao Ibn Salaah amesahau kuutaja. Atafanyaje mtu ikiwa hakupata mtu yoyote mwengine aliyetekeleza kulingana na hadîth? Suala hili limejibiwa na Taqi-Ud-Dîn as-Subki kwenye makala yake, Maana ya msemo wa ash-Shâfi‘î, ―Ikisihi hadîth, basi hayo ndiyo madhehebu yangu.‖ (Uk. 102, Vol 3): ―Kivyangu mimi, lililo bora ni kufuata hadîth. Na

ajikisie mtu mwenyewe binafsi akiwa mbele ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم),

ameanza kuyasikiya kutoka kwake: Je, atakuwa na uhuru wowote wa kuwa na fikra ili acheleweshe kuitekeleza? Laa, Wallaahi ...na kila mmoja ana jukumu kulingana na ufahamu alo nao.‖ Majadiliano mengine ya mas‘ala haya yametolewa na kuchambuliwa katika I‘laam al-Muwâqi‘în (2/302, 370) na kwenye kitabu cha Fulaani, (Jina kamili): Îqâdh Himam ulu l-Absâr, lil-Iqtidâ‘ bi Sayyid al-Muhâjirîn wal Answâr, wa Tahdhîruhum ‗an al-Ibtidâ‘ ash-Shâ‘i‘ fi l-Qurâ wal-Amsâr, min Taqlîd al-Madhâhib ma‘a l-Hamiyyah wal-‗Asabiyyah bain al-Fuqahâ‘ al-A‘sâr. (Kuziamsha fahamu za wenye busara, katika kuwândama viongozi wa Muhâjirîn na Answâr, na kuwatahadharisha dhidi ya uzushi ulioenea miongoni mwa wasomi wa kisasa mijini na vijijini, wa kufuata madh-hab kwa ghera na ushupavu wa uwanachama). Hicho ni kitabu cha kipekî katika madda yake, ambacho kila mwenye kupenda haki na ukweli na akisome kwa ufahamu na mazingatio..

XXVIII

5)

ث نأـن الصعط الدير كن نإذا ن والرصةل ثةلدير أـ أذ »ثرصية أو طةة ظت أذت إحل إذا كن صععة أو نة : يسن يشء أي

» ―Nyinyi1ni wajuzi zaidi wa Hadîth na wapokezi wake kuliko mimi, iwapo hadîth ni swahîh, basi nielimisheni na mimi kuhusiana nayo;

iwapo imetoka Kufah, au Basrah, au Shâm ili nipate kuchukuwa muelekeo wa hadîth mâdamu ni swahîh .‖2

6)

ـد أ صل الل ـ وش الل رشل ـ رباخل نة صط مصأح ك » «خبالف ة ىخ نأة راصؿ ـة ف ظةت وبفد ميت اجلي

1 Akimwambia maneno hayo Imâm Ahmad ( اهلل رحمه ) 2 Imepokewa na Ibn Abî Hâtim katika Âdâb ash-Shâfi‘î (Uk. 94-5), Abu Nu‘aim katika Hulyah al-Awaliyâ‘ (9/106), al-Khatîb katika Al-Ihtijâj bish-Shâfi‘î (8/1) na kutoka kwake Ibn ‗Asâkir (15/9/1), Ibn ‗Abdul Barr katika Al-Intiqâ‘ (Uk. 75), Ibn al-Jawzî Manâqib al-Imâm Ahmad (Uk. 499) na Harawi (2/47/2) kwa njia tatu kutoka kwa ‗Abdullaah Ibn Ahmad Ibn Hanbal kutoka kwa babake yakwamba Shâfi‘î amesema kumwambia yeye: ...n.k; kwa hiyo, ni swahîh iliyopokewa kutoka kwa Shâfi‘î. Hii ndiyo sababu ya Ibn al-Qayyim kuihusisha wazi wazi na yeye katika I‘laam (2/ 325), kama alivyofanya Fulaani katika Îqâdh (Uk. 152) na kisha akasema: ―Amesema Baihaqî, ‗Hii ndiyo sababu yeye – yaani: ash-Shâfi‘î – alitumia sana hadîth, kwa sababu alikusanya ilimu kutoka kwa watu wa Hijâz, , Syria, Yemen na Irâq, na kwa hivyo akakubali kila alichopata kuwa ni swahîh, bila ya kulemea au kuangalia yale aliyodhania kutoka kwenye madh-hab ya watu wa mji wake alipoangaziwa na ukweli kwenye sehemu nyengine. Baadhi ya wale walokuwa kabla yake walijiekea nafsi zao mipaka kwa yale waliyoyaona kwenye Madh-hab ya watu wa mijini mwao, bila ya hata kujaribu kuhakikisha uswahîh wa yenye kupinga hayo. Allaah na Atusamehe sote‘.‖

XXIX

―Katika kila mas‘ala ambapo wapokezi wa riwaya wanapopata hadîth

kutoka kwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)ambayo ni swahîh na ikawa ni

kinyume cha yale ninayosema mimi, basi mimi nachukuwa mwenyewe maneno yangu, iwe ni katika uhai wangu au baada ya kufa kwangu.‖1

1 Abu Nu‘aim (9/107), Harawi (47/1), Ibn al-Qayyim katika I‘laam al-Muwâqi‘în.(2/363) na Fulaani (Uk. 104).

XXX

7)

خالن صل الل ـ وش اجليب ـ صط وىد ىل أىل رأيذن إذا »ا أن ـيل ىد ذت «نةـ

―Mutakaponiona mimi nikisema kauli, na kinyume chake imepokewa

kutoka kwa Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ), basi jueni yakwamba akili yangu

imenitoweka.‖1 8)

خالف ىيل ة يصط صل الل ـ وش اجليب ـ نكن ىخ ة ك » «نعدير اجليب أويل نال ديدلون

―Kwa kila ninachosema, ikiwa kuna jambo lililo swahîh kutoka kwa

Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) lenye kwenda kinyume na maneno yangu, basi

hadîth ya Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) ni awla, kwa hivyo musifuate rai

yangu.‖2 9)

«ن ىيل وإن ل تصفه ن صل الل ـ وش اجليب ـ ظدير ك »―Kila hadîth iliyopokewa kutoka kwa Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) ndiyo kauli

yangu pia, hata kama hamukuisikiya kutoka kwangu.‖3

4) AHMAD IBN HANBAL ( اهلل رحمه ):

1 Ibn Abî Hatim katika Al-Âdâb (Uk. 93), Abul Qâsim Samarqandi katika al-Amâli, kama ilivyo kwenye dondû kutoka hapo na Abu Hafs al-Mu‘addab (234/1), Abu Nu‘aim (9/106) na Ibn ‗Asâkir (15/10/1) na sanad iliyo swahîh. 2 Ibn Abî Hâtim, Abu Nu‘aim na Ibn ‗Asâkir (15/9/2). 3 Ibn Abî Hâtim (Uk. 93-4)

XXXI

Imâm Ahmad ndiye aliyekuwa wa kwanza miongoni mwa ma-Imâm katika kuzikusanya Sunnah na kushikamana nazo, kiasi cha kwamba hata akawa ―anachukia kuandikwa kitabu chenye mambo ya makisio na maoni1.‖ Kwa sababu hii akasema: 1)

يع ول الوزايع ول اثلري وخذ الظةن ول ةلك ديدل ول ديدلين ل » «ظر أخذوا

―Musifuate rai yangu; wala rai ya Mâlik, wala ya Shâfi‘î, wala ya Awzâ‘i, wala ya Thawrî, lakini chukuweni kutoka pale walipochukuwa

wao.‖2 Katika riwaya nyengine: 2)

صل الل ـ وش اجليب ـ صةء ة ؤلء أظدا دي ديدل ل » «وأصعةث نخذ ث ز اتلةثفي ثفد الرص ن خمري

―Usiige Dini yako kutoka kwa yoyote katika hawa, lakini chochote

kilichowajia kutoka kwa Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) na Maswahaba zake,

chukuweni; kisha wanafuata at-Tâbi‘în, ambapo mtu ana khiyari [katika kufuata].‖

Alisema wakati mmoja: 3)

أصعةث صل الل ـ وش اجليب ـ صةء ة الرص يتجؿ أن الدجةع » ـو «ز ثفد اتلةثفي خمري

1 Ibn al-Jawzî katika al-Manâqib (Uk. 192) 2 Fulaani (Uk. 113) na Ibn al-Qayyim katika I‘laam (2/302).

XXXII

―Kufuata1 ni mtu kufuata yaliyokuja kutoka kwa Mtume ( صىل اهلل عليه na Maswahaba zake; kisha kwa at-Tâbi‘în, [mtu] ana khiyari.‖2(وسلم

4)

رأي لك ظهح أب ورأي ةل ورأي الوزايع رأي » اء يـد و وإة ش « ازةر ف الضح

―Rai ya al-Awzâ‘î, na rai ya Mâlik, na rai ya Abu Hanîfah, zote hizo ni rai, na kwangu mimi zote hizo ziko sawa. Amma hoja kwetu sisi ni

katika Âthâr (kutoka kwa Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) na Maswahaba zake.)‖3

5)

«ن ع طهة ح صل الل ـ وش الل رشل ظدير رد »―Yoyote mwenye kuikataa Hadîth ya Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ), basi huyo

yuko katika ukingo wa maangamivu.‖4

************* Haya ni maneno yenye kufahamika kwa urahisi, na yaliyo wazi wazi

kutoka kwa ma-Imâm (عنهم اهلل رضي) kuhusu maamrisho ya kushikamana

na hadîth na makatazo ya kufuata rai zao bila ya dalili za wazi, kiasi cha kwamba rai tupu na maelezo mengi hayaruhusiwi. Kwahiyo, yoyote mwenye kushikamana na chochote katika Sunnah kilichothibitishwa kuwa swahîh , hata kama kinapingana na baadhi ya rai za ma-Imâm, hatokuwa akikhalifu madh-hab zao, wala kupotoka kutoka kwenye njia zao; bali mtu aina hiyo atakuwa akifuata zote na atakuwa ameshika kwa nguvu kishikizi cha kuaminika, kisicho-vunjika. Hatahivyo, hii haitokuwa hali ya yule mwenye kuwacha Sunnah yoyote

1 Kwa kiarabu: al-Ittibâ‘ 2 Abu Dâwud katika Masâ‘il ya Imâm Ahmad (Uk. 276-7) 3 Ibn ‗Abdul Barr katika Jâmi‘ al-Bayân al-‗Ilm (2/149). 4 Ibn al-Jawzî katika Manâqib (Uk. 182)

XXXIII

iliyo swahîh kwa sababu tu yakwamba inakhalifiana na rai zao; Laa! [sivyo hivyo] mtu wa aina hiyo atakuwa amewakaidi ma-Imâm na kuwapinga katika maneno yao yaliotangulia hapo juu, ambapo Allâh‎

( وتعاىل سبحانه ) amesema:

نال هصذ ل يدوا ف أ ث ة طضر ثي ك ذ ي ن ظتذ ل يؤ ورب

ة ا ا تص خ ويص ة ىظ ذ ة م ٦٥ظرصا“Naapa kwa (haki ya) Mola wako. Wao hawawi wenye kuamini

(kweli kweli) mpaka wakufanye (wewe ndiye) hakimu (mwamuzi) katika yale wanayokhitilafiana, kisha wasione uzito nyoyoni mwao

juu ya hukumu uliyotoa, na wanyenyekee kabisa.”1 Na pia Akasema:

عذر ٱن ي لذ مره أ ۦ خيةهن خ ن دصج

أ حل

ذاب أ ـ و يصج

ح أ ٦٣نذ

“Basi wajihadhari wale wanaokaidi amri yake, usije ukawapata msiba au ikawafika adhabu iumizayo.”2

Amesema al-Hâfidh Ibn Rajab al-Hanbalî (اهلل رحمه) : ―Kwahivyo, ni

Waajib juu ya kila mmoja atakaesikiya kuhusu amri ya Mtume ( اهلل صىلوسلم عليه ) au akawa anaijua, awabainishie ummah, na awausie kwa njia

nzuri, na awaamrishe wafuate amri zake, hata kama zinakhalifiana na

rai ya mtu yoyote mkubwa. Hii ni kwa sababu amri ya Mtume ( عليه اهلل صىل ina haki zaidi ya kuheshimiwa na kufuatwa kuliko rai ya mtu (وسلم

yoyote mkubwa aliyekhalifu, kwa kupitikiwa na amri ya Mtume ( اهلل صىلوسلم عليه ) katika mas‘ala yoyote. Hii ndiyo sababu ya Maswahaba na

wale walokuja baada yao walimkosoa yoyote mwenye kukhalifu

1 Surah an-Nisâ‘ (4): 65 2 Surah an-Nûr (24): 63

XXXIV

Sunnah swahîh, mara nyengine wakiwa wakali sana katika kukosoa kwao1, na wala sio kwa chuki juu ya yule mtu, kwani wanampenda na

1 Hata dhidi ya baba zao na walio wasomi, kama alivyosema Imâm at-Tahâwî katika kitabu chake Sherh Ma‘âni al-Âthâr (1/372) na Abu Ya‘laa katika Musnad yake (3/1317) alivyopokea, kwa isnâd ya watu wâminifu, kutoka kwa Sâlim Ibn ‗Abdullaah ibn ‗Umar, aliyesema:

―Siku moja nilikuwa nimekâ na Ibn ‗Umar ( عنه اهلل ضير ) msikitini, mara akaja

mtu mmoja kutoka katika watu wa Syria na akamuuliza kuhusu kuendelea kufanya ‗Umrah juu ya Hajj (ijulikanayo kama Hajj Tamattu‘). Akamjibu Ibn ‗Umar, ‗Ni jambo zuri na lenye kupendeza.‘ Akasema yule mtu, ‗Lakini babako (yaani: ‗Umar ibn al-Khattâb) alikuwa akikataza jambo hilo!‘ Basi akasema, ‗Ole wako! Ikiwa babangu alikuwa akikataza jambo ambalo

alilolifanya Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) na kuliamrisha, wewe utaikubali rai ya

babangu, au amri ya Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل )?‘ Akajibu yule mtu, ‗Amri ya

Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) .‘ Akasema (Ibn ‗Umar), ‗Hebu niondokî hapa.‘

Imepokewa na Ahmad (No. 5700), vile vile akapokea at-Tirmidhî (2/82) na akaitangaza kuwa swahîh.. Pia, Ibn ‗Asâkir (7/51/1) akapokea kutoka kwa Ibn Abi Dhi‘b, aliyesema: ―Sa‘d ibn Ibrâhîm (yaani: mwanae ‗Abdur-RAHMÂN ibn ‗Awf) alimuhukumu mtu kulingana na rai ya Rabî‘ah ibn Abu ‗Abdur-RAHMÂN, kwa hivyo,

nikampasha habari kuhusu hadîth ya Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) amabyo

inakhalifiana na hukmu yake aliyoitoa. Kwa hivyo, Sa‘d akamwambia Rabî‘ah, ‗Tunae hapa Ibn Abi Dhi‘b, ambae mimi namuamini kuwa ni mtu

muaminifu, atuhadithia kutoka kwa Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ), kinyume cha

nilivyohukumu mimi.‘ Rabî‘ah akamwambia, ‗Umejitahidi kwa bidii zako, na hukmu yako imepita.‘ Sa‘d akasema, ‗Nimepigwa na mshangao! Nimepitisha

hukmu ya Sa‘d, na wala sio hukmu ya Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل )! Haiwezekani,

mimi nitaibatilisha hukmu ya Sa‘d, mtoto wa mamake Sa‘d, na niipitishe

hukmu ya Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) .‘ Basi Sa‘d akaiitisha ile hati ya hukmu

aliyoitoa, akaichana vipande vipande na akatoa hukmu mpya.‖

XXXV

kumuheshimu, lakini kwa sababu Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) alikuwa

akipendeza zaidi kwao, na amri zake zilikuwa bora kuliko amri za

kiumbe yoyote mwengine. Kwa hiyo, amri ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) ikikhalifiana na amri ya mtu mwengine, amri ya Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) inastahiki zaidi kutekelezwa na kufuatwa. Hapana jambo lolote litakalowazuiya wao wasimuheshimu yule waliyemukhalifu kwa sababu wanajua wao yakuwa atasamehewa1; kwa hakika huyo mtu

hatojali kupingwa amri zake anapo-onyeshwa amri za Mtume ( عليه اهلل صىل kuwa waziwazi ziko kinyume na amri zake.‖2 (وسلم

Kwa kweli, hawatojali wao, iwapo waliwaamrisha wafuasi wao watekeleze hivyo, kama tulivyo ona, na wakahimiza juu yao watupilie mbali rai zao zozote zenye kukhalifu Sunnah. Kwa hakika, Imâm

Shâfi‘î (اهلل رحمه) aliwaambia wafuasi wake wamnasibishie yeye Sunnah

zilizo swahîh, hata kama yeye hakuchukuwa msimamo huo au amechukuwa msimamo uliokhalifiana na huo. Na kwahivyo, pindi

mtafiti Ibn Daqîq al-‗Eid (اهلل رحمه) alipokusanya pamoja kitabu

kikubwa, mas‘ala ambayo Madh-hab ya Imâm mmoja au zaidi katika ma-Imâm wanne amekhalifu hadîth zilizo swahîh, aliandika mwanzoni mwake, ―Haifai kuzinasibisha jawabu hizi na ma-Imâm wenye kujitahidi, na inawapasa ma-fuqahâ‘ wenye kuwafuata wao ki-Upofu

1 Kwa hakika, atapata thawabu, kwa sababu ya hadîth ya Mtume ( عليه اهلل صىل :isemayo (وسلم

إذا » ظس د الةز ذ نةصذ صةب ث أ صران ن

صر أ

أ ن

خػأ

ذ أ د ث نةصذ «إوذا ظس

―Hakimu anapotoa hukumu juu ya jambo, akifanya juhudi zake (Ijtihâd) na kuhukumu sawa, atapata malipo mara mbili, na akifanya juhudi zake (ijtihâd) na kuhukumu kwa makosa, atapata malipo mara moja.‖ (Imepokewa na Bukhârî na Muslim na wengineo). 2 Yamenukuliwa kutoka kwenye nukta za Îqâdh al-Himam (Uk. 93)

XXXVI

kuyajua hayo ili wasije wakawanukuu kuhusu haya wakawa wanawazulia wao.‖1

Wafuasi wa ma-Imâm wakijiepusha na rai za ma-Imâm iwapo zinakhalifu Sunnah.

Kutokana na yote tuloyataja, wanafunzi wa ma-Imâm, sehemu kubwa (katika hawa) ni miongoni mwa (watu) wa mwanzo (huko), na sehemu ndogo ni miongoni mwa (watu) wa mwisho2, hawatokubali maoni yote ya ma-Imâm wao, kwa kweli wameyapuuza mengi wanapoyaona kuwa yanakwenda kinyume na Sunnah iliyo dhahiri. Hata ma-Imâm

wawili, Muhammad ibn al-Hasan na Abu Yûsuf ( اهلل رحمهم )

wamemukhalifu sheikh wao Abu Hanîfah ―kiasi cha thuluthi nzima ya Madh-hab‖3, kama vitabu vya masâ‘il vinavyothibitisha. Vile vile imesemwa kumuhusu Imâm îi4 na wafuasi wengine wa Shâfi‘î na ma-Imâm wengine; Lau tutaanza kutoa mifano, mjadala utazidi kuwa mkubwa, mrefu, na tutatoka nje ya mada tuloikusudia kwenye utangulizi huu, kwa hivyo, tutakoma kwenye mifano miwili:

1) Amesema Imâm Muhammad katika kitabu chake Muwatta‘5(Uk.

158), ―Ama kuhusu Imâm Abu Hanîfah, yeye alikuwa haonelei

1 Fulaani (Uk. 99) 2 Surah al-Wâqi‘ah (56): 13-14 3 Ibn ‗Âbidîn katika Hâshiyah (1/62), na Lucknowi akatoa asili yake katika an-Nâfi‘ al-Kabîr (Uk. 93) kama alivyofanya Ghazâli. 4 Yeye mwenyewe asema katika mwanzo wa Fiqh ya Shâfi‘î kwa Mukhtasar (iliyochapishwa pambizoni mwa kitabu cha al-Umm cha Imâm Shâfi‘î): ―Kitabu hiki ni ―Kitabu Mama‖ kutoka katika ilimu ya Muhammad ibn Idrîs

ash-Shâfi‘î ( اهلل رحمه ) na kutoka kwenye maana ya misemo yake, katika

kuusaidia ufahamu wa yoyote atakae 5 Ambapo amîleza upinzani alokuwa nao dhidi ya Imâm wake katika takriban mas‘ala ishirini (nambari 42, 44, 103, 120, 158, 169, 172, 173, 228, 230, 240, 244, 274, 275, 284, 314, 331, 338, 355, 356 – kutoka katika Ta‘lîq al-

XXXVII

yakwamba kuwe na Swala ya kuomba mvua, lakini msimamo wetu ni kwamba Imâm anaswali rak‘âh mbili kisha anaomba na kuigeuza nguo yake ya juu ...‖

2) Na huyu ‘IsLaam ibn Yûsuf al-Balkhi, mmojawapo wa wafuasi wa

Imâm Muhammad1 na mtumishi wa Imâm Abu Yûsuf2, ambae aliyekuwa ―akitoa fatwâ kinyume cha Imâm Abu Hanîfah kwa sababu alikuwa hajui dalili zake, na badala yake dalili nyengine zilikuwa zikimdhihirikia yeye, kwa hivyo alikuwa akitoa fatwâ kulingana na dalili hizo.‖3 Kwahiyo, ―alikuwa akiinua mikono yake anaporukû‘ (kwenye Swala) na anapoinuka kutoka hapo (kwenye

rukû‘).‖4 Kama ilivyo Sunnah Mutawâtir ya Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل );

Mumajjid ‗alaa Muwatta‘ Muhammad) (Nukta muhimu juu ya Muwatta‘ cha Muhammad) 1 Ibn ‗Âbidîn amemtaja miongoni mwao katika Hâshiyah (1/74) na katika Rasmi al-Muftî (1/17). Qurashi amemtaja katika Al-Jawâhir al-Madiyyah fî Tabaqât al-Hanafiyyah (Uk. 347) na akasema, ―Alikuwa ni mpokezi muaminifu wa Hadîth. Yeye na ndugu yake, Ibrâhîm, walikuwa ndiwo mashekhe wawili wa Balakh katika enzi zao.‖ 2 Al-Fawâ‘id al-Bahiyyah fî Tarâjum al-Hanafiyyah (Uk. 116) 3 Al-Bahr ar-Râ‘iq (6/93) na Rasm al-Muftî (1/28) 4 Al-Fawâ‘id ... (Uk. 116), kisha muandishi akaongezea nukta muhimu: ―Kutokana na haya inadhihirika hatima iliyo bâtil ya riwaya ya Makhûl kutoka kwa Abu Hanîfah: ‗yakwamba, mwenye kuinua mikono yake katika Swala, basi Swala yake imebatilika‘, ambayo ‗Âmir, muandishi wa ‗Itqâni, alidanganyika, kama ilivyosimuliwa chini ya wasifu wake. ‗Islaam ibn Yûsuf, mfuasi wa Abu Yûsuf, alikuwa akiinua mikono yake, sasa ikiwa riwaya hiyo ya hapo juu ingelikuwa na msingi wowote, basi Abu Yûsuf na ‗Islaam wangelikuwa wanaijua khabari hiyo ... ingelidhihirika pia iwapo mfuasi wa Hanafî ameipuuza madh-hab ya Imâm wake katika mas‘ala kwa ajili ya dalili yenye nguvu dhidi yake, jambo hilo halitomtoa yeye kwenye safu za wafuasi wa Imâm, lakini kwa kweli, hii ingelikuwa ndiyo taqlîd ya sawa katika mtindo wa kuwachana na taqlîd; kwani wewe huoni yakwamba ‗Islaam ibn Yûsuf aliyawacha madh-hab ya Abu Hanîfah ya kutoinua mikono, lakini akawa bado anahesabiwa kuwa miongoni mwa ma-Hanafî? ...Namshtakia Allaah kuhusu

XXXVIII

Ukweli kuwahusu ma-Imâm wake watatu (yaani: Abu Hanîfah , Abu Yûsuf, na Muhammad) waliokuwa na misimamo tafauti, hakukumzuiya yeye kuitekeleza Sunnah hii. Huu ndio msimamo anaowajibika kila Muislamu kuwa nao, kama tulivyo-ona kutoka katika ushahidi wa ma-Imâm wanne, na wengineo.

Kwa ujumla: Mimi natarajia kwa moyo safi yakwamba hapana mfuasi yoyote wa Imâm atakaekimbilia kukashifu misingi ya kitabu hiki na

kuwacha kufaidika kutokana na Sunnah zilizomo za Mtume ( عليه اهلل صىل kwa madai yakwamba ati yanakwenda kinyume na madh-hab ,(وسلم

yake. Natumai yakwamba mtu kama huyo badala yake atazingatia yale tuliyoyatanguliza katika naswiha za ma-Imâm kuhusu uwajibu wa kutekeleza Sunnah na kuwachana na maneno yao yenye kuzikhalifu Sunnah hizo. Pia nina matumaini yakwamba atazinduka na kutambua yakwamba kulaumu mtindo wa kitabu hiki ni kumlaumu Imâm yoyote anayemfuata, kwani sisi tumechukuwa misingi hii kutoka kwa hao ma-Imâm, kama tulivyoyaeleza. Kwahivyo, yoyote mwenye kukataa kuongozwa nao katika njia hii yuko kwenye hatari kubwa, kwani kukataa huko kunasababisha kuipa Sunnah mgongo, Sunnah ambayo tuliyoamrishwa kuiregelea itokeapo ikhtilafu ya maoni na ambayo tuliyoamrishwa kuitegemea.

Akasema Allâh‎ ( ه عزه وجل ):

هصذ ل يدوا ف أ ث ة طضر ثي ك ذ ي ن ظتذ ل يؤ نال ورب

ة ا ا تص خ ويص ة ىظ ذ ة م ٦٥ظرصا

ujinga ulioko katika zama zetu, wanapomshambulia yoyote anayekhalifiana na Imâm wake kwenye mas‘ala, kwa sababu ya dalili yenye nguvu dhidi yake, na wakamfukuza kutoka kwenye duara la wafuasi wa Imâm huyo! Si jambo la kushangaza ikiwa wanaofanya hivyo ni katika watu wa kawaida tu, lakini linashangaza ikiwa linatoka kwa wale wenye kuwaiga watu wasomi lakini wakijikokota kwenye njia hiyo kama ng‘ombe!‖

XXXIX

“Naapa kwa (haki ya) Mola wako. Wao hawawi wenye kuamini (kweli kweli) mpaka wakufanye (wewe ndiye) hakimu (mwamuzi) katika yale wanayokhitilafiana, kisha wasione uzito nyoyoni mwao

juu ya hukumu uliyotoa, na wanyenyekee kabisa.”1 Namuomba Allâh‎ atuja‘alie tuwe ni miongoni mwa wale ambao Aliowasema:

ل ة كن ى ي ٱ إجذ ؤ ا إل ل ـ ٱإذا د ا ۦورشل للذ ن حيل أ ثي حلعس

ه ول وأ ة غف

ة وأ ف هعن ٱش يػؿ ٥١ ل ٱو ٱويخض ۥورشل للذ للذ

ه ول ٥٢ هةنزون ٱويذذي نأ

“Haiwi kauli ya Waislamu wanapoitwa kwa Allâh‎ na Mtume wake ili Ahukumu baina yao, ila kusema: “Tunasikiya na tunakubali,” na

hao ndiwo watakaofuzu. Na wenye kumtwi‟i Allâh‎ na Mtume wake na kumhishimu Allâh‎ na kumuogopa, hao ndiwo wenye kufuzu,

(kufaulu).”2

خرة شح 31دمظو 3131مجةدى ا

1 Surah an-Nisâ‘ (4): 65 2 Surah an-Nûr (24): 51-52

XL

UTATUZI WA TASHWISHI ZILIZOKO

Utangulizi wa mwanzo uliandikwa miaka kumi iliyopita, wakati ambao imetudhihirikia waziwazi yakwamba maneno yetu yamekuwa na athari nzuri juu ya vijana wa Kiislamu katika kuwaongoza kwenye kuwajibika katika mas‘ala ya Dini na ‗ibaadah zao ili waweze kurudi katika asili iliyotakasika ya Uislamu: Kitabu na Sunnah. Miongoni mwao, kuliongezeka idadi katika safu za wenye kutekeleza Sunnah na kujitolea nafsi zao kikamilifu, AlhamdulilLaah, mpaka wakawa hawana uoga wa kuidhihirisha Sunnah. Hatahivyo, mimi bado naona miongoni mwa baadhi yao kuna uthabiti wa kukosa kuifuata Sunnah: Wala sio kwa ajili ya shaka yoyote kuhusu uwajibu wake baada ya kusoma aya za Qur‘ân na kauli za ma-Imâm zinazohimiza kurudi kwenye Sunnah, lakini ni kwa sababu za pingamizi na kueleweka vibaya walivyowahi kuyasikiya kutoka kwa baadhi ya mashekhe waliokuwa Muqallid. Kwa hivyo, nimeamua kuzitaja fikra hizi za kimakosa na kuzirudi, ili pengine jambo hili litawahimiza watu wengi kutekeleza Sunnah ili nao wapate kuwa miongoni mwa pote litakalo okolewa, Akipenda Allâh‎.

SHUB‟HA YA KWANZA: Wanasema baadhi yao, ―Hapana shaka

yakwamba ni Waajib kurudi kwenye uongofu wa Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) katika mas‘ala ya Dini yetu, hususan katika vitendo vya ‗ibaadah vilivyokokotezwa kama vile Swala, ambapo hapana nafasi ya rai wala ijtihâd, kutokana na hali yake ya kutobadilika. Hata hivyo, sisi huwa hatumsikii sheikh yoyote aliye Muqallid akiamrisha jambo hili. Kwa hakika, twawaona wakishikilia ikhtilafu ya maoni, ambayo wao wanaichukulia kuwa ni jambo la urahisi na wepesi katika Ummah. Ushahidi wao katika madai hayo ni hadîth ambayo wanapenda kuikariri katika hali kama hizo, wanapowakosoa watetezi wa Sunnah, ‗Ikhtilafu ya maoni miongoni mwa Ummah wangu ni rehma‘. Inaonekana kwetu sisi yakwamba hadîth hii inakhalifu msingi ambao wewe unaulingania na uliotegemezwa juu ya yale uliyoyatungia kitabu hiki na vitabu vyengine. Sasa wasemaje kuhusu hadîth hii?‖

XLI

Jawabu: Jawabu inapatikana katika sehemu mbili:

A) Kwanza: Hadîth hii si swahîh ; Kwa hakika, ni bâtil, tena isiyokuwa na asili. ‗Allâmah‎‎ Subki amesema, ―Sijawahi kuona upokezi wake ulio swahîh, wala dha‘îf, wala maudhû‘‖, yaani hakuna sanad (upokezi) ya ―hadîth ‖ hii!

Vile vile imepokewa kwa maneno yasemayo:

« رمحح س أصعةب اخذالف . . . »―...Ikhtilafu ya maoni miongoni mwa maswahaba zangu ni Rehma juu yenu.‖

Na:

م نجأي اىذديذ اذديذ أصعةب » «كجلض―Maswahaba zangu ni kama nyota, kwa hivyo yoyote miongoni mwao

mutakaemfuata, mutaongoka.‖

Hadîth zote hizi si swahîh : Ya kwanza ni dha‘îf sana, na ya pili ni maudhû‘ (Soma Kiambatisho 1)1

B) Yakwamba hadîth hizi, pamoja na udhaifu wake zinakhalifu Qur‘ân al-Karim, kwani Âyât zilizomo ndani yake (hiyo Qur‘ân) zenye kukataza kuwepo ikhtilafu katika Dini na kuhimiza kupatikana umoja na mashikamano ni maarufu mno kuhitaji ukumbushaji. Lakini hapana ubaya katika kuzitolea baadhi yake

mifano. Allâh‎ ( وتعاىل سبحانه ) akasema:

ت ريعس ا ودذ ا ذذهظ ـ ٤٦ول دجز“...Wala msizozane (msigombane), msije mkaharibikiwa na

kupoteza nguvu.”2

1 Silsilat al-Ahâdîeth adh-Dha‘îfah wal maudhû‘ah Uk. 58, 59, na 61. 2 Surah al-Anfâl (8):46

XLII

ا شكي ٱول دس ٣١ ل ٱ ي لذ ة فا ا ط وك ا دي ى ة نرذ ظزب ثك

نرظن ي ٣٢ل“...Wala msiwe katika washirikina. Katika wale waliofarikisha dini yao na wakawa makundi makundi; kila kikundi kinafurahia kilicho

nacho!”1

إلذ ١١٨ول يزالن خمذهي رب رذظ ١١٩ “...Kwa hivyo wataendelea tu kuhitilafiana, isipokuwa wale ambao

Mola wako amewarehemu”2

Kwa hivyo, iwapo wale waliorehemewa na Mola wako hawahitilafiani, na watu wa bâtil ndiwo wenye kuhitilafiana, itaingiaje akilini yakwamba ati kuhitilafiana ni rehma?! Kwahiyo, imethubutu yakwamba hadîth hii si swahîh katika isnadi yake wala katika matn, na wala katika maana; Kwa hivyo, imebainika wazi yakwamba haijuzu kutumika katika kuhalalisha upinzani dhidi ya Kitâb na Sunnah, ambavyo ndivyo tulivyoamrishwa na ma-Imâm wetu tangu hapo. SHUB‟HA YA PILI: Wengine wanasema, ―Ikiwa kukhitilafiana kwenye dini kumekatazwa, wasemaje kuhusu ikhtilafu miongoni mwa maswahaba na miongoni mwa ma-Imâm baada yao? Kuna tafauti yoyote baina ya ikhtilafu zao na za kizazi kilichokuja baada e? Jawabu: Na‘am, kuna tafauti kubwa sana baina ya mifano hii miwili ya kutafautiana, na imedhihirika katika njia mbili: kwanza, sababu yake, na pili, athari yake.

A) Ama kuhusu ikhtilafu miongoni mwa maswahaba, hakika hayo yalikuwa ni ya ki-dharura, yasioepukika, ikhtilafu ya asliya ya

1 Surah ar-Rum (30):31-32 2 Surah Hud (11):118-9

XLIII

kufahamikiana: Kutafautiana kwao hakukuwa ni kwa hiyari yao. Hali nyengine za zama zao ndizo zilizochangia jambo hili, zikasababisha ikhtilafu za maoni, lakini hayo yakapotea baada ya zama zao.1 Aina hii ya ikhtilafu haiwezekani kuondoshwa kabisa na watu aina hiyo hawawezi kulaumiwa kwenye muangaza wa Âyât zilizotangulia kwa sababu ya kukosekana kwa hali za kisawasawa, Yaani; ikhtilafu ya kukusudia na kufanya ukaidi katika upinzani huo. Ama kuhusu Ikhtilafu miongoni mwa Muqallidîn wa leo, hapana udhuru wa hilo. Mmoja miongoni mwao, ataonyeshwa dalili kutoka kwenye Kitâb na Sunnah, inayokuwa ni yenye kuunga mkono madh-hab mojawapo isiyokuwa aliyojifungamanisha nayo, utamkuta akiitenga kando dalili na si kwa sababu yoyote isipokuwa inakwenda kinyume na madh-hab yake. Utadhani yakwamba madh-hab yake

ndiyo asli, au ndiyo Dini ambayo Muhammad ( وسلم عليه اهلل صىل ) aliyotuletea, na zile madh-hab nyengine ni Dini tafauti zilizofutwa! Wengine wamepindukia mipaka upande mwengine, kuhusiana na madh-hab – kwa ikhtilafu zao zote – kama vifungu vya Sheriya vilivyo sambamba, kulingana na walivyoeleza2 wafuasi wao waliokuja baadae: Hapana madhara yoyote kwa Muislamu kuchukuwa ayatakayo kutokana na hayo na kuyawacha atakayo, kwa sababu yote ni katika vifungu vya Sheriya vinavyofaa! Aina hizi zote za watu wanajuzisha kubakia kwao juu ya mgawanyiko kutokana na hadîth hii ya bâtil,

« رمحح أت اخذالف»―Ikhtilafu miongoni mwa Ummah wangu ni rehma‖ Kwa hivyo, tunawasikiya wengi wao wakitumia hadîth hii kama ni ushahidi! baadhi yao wanajuzisha na kuitolea hadîth hii hoja na

1 Al-Ahkâm fi Usûl al-Ahkâm cha Ibn Hazm, Hujjatullaah al Bâlighah cha al-Dehlawi, na Insha ya aliyefuata iliyohusu mas-ala haya hususan, ‗Iqd Jîd fi Ahkâm al-Ijtihâd wat-Taqlîd. 2 Angalia Faid al-Qadîr cha al-Manâwi (1/209) au Silsilah al-Ahâdîth ad-Dha‘îfa (1/76, 77)

XLIV

malengo yake na kudai yakwamba inahakikisha kupatikana wepesi wa mabadiliko katika Ummah! Mbali na ukweli wa kwamba ―ijaza‖ hiyo inakwenda kinyume na Aya za Qur‘ân zilizo waziwazi na kwenye maana ya maneno ya ma-Imâm yaliyotangulia , vilevile kuna maandishi kutoka kwa baadhi ya ma-Imâm kuyakemea hayo. Amesema Imâm Ibn al-Qâsim: ―Nimemsikiya Mâlik na Layth wakizungumzia kuhusu kukhitilafiana

kwa Maswahaba wa Mtume Muhammad ( وسلم عليه اهلل صىل ): ‗Si kama

wasemavyo watu: ―Ndani yake kuna mapindo yenye maana pana zaidi‖; Laa! Sio hivyo, lakini hakika ni mas‘ala ambayo baadhi yao kuwa kwenye makosa na baadhi nyengine kuwa katika usawa."1 Na Ash-Sha‘b nae akasema, ―Aliulizwa Imâm Mâlik kuhusu mtu aliyeikubali hadîth iliyonukuliwa

na watu wenye kutegemewa kutoka kwa Maswahaba wa Mtume ( اهلل صىل

وسلم عليه ): ―Je unayaona mapindo yoyote ndani yake?‖ Akasema, ―Laa

WAllâh‎i, ili yeye awe kwenye haki. Njia ya haki ni moja tu. Itawezekanaje rai mbili zenye kutafautiana, kuwa zote ziwe katika usawa?! Haki na usawa zote ni kitu kimoja.‖2 Imâm Muzani, ambaye ni swâhib yake Imâm Ash-Shâfi‘î amesema;

―Kwa hakika wamekhitilafiana Maswahaba wa Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ), na

baadhi yao wakawarekebisha baadhi nyengine. baadhi yao wakachunguza rai za wengine mpaka wakapata makosa ndani yake. Lau kama rai zao zote zingelikuwa ni sawa, hawangeliyafanya hayo.‖ ―Alikasirika ‗Umar ibn al-Khattâb kwenye ugomvi baina ya Ubayy ibn Ka‘b na ibn Mas‘ûd kuhusu kuswali na nguo moja. Akasema Ubayy,

1 Ibn ‗Abdul Barr katika Jâmi‘ Bayân al-‗Ilm (2/81-2). 2 Ibid. (2/82, 88-9)

XLV

‗Hakika, kuswali na nguo moja ni jambo zuri lipendezalo‘ na ibn Mas‘ûd nae akasema, ‗Amri hiyo ni kwa mtu aliye na nguo chache.‘ Basi ‗Umar akatoka akiwa na hasira na akasema, ‗Watu wawili

miongoni mwa Maswahaba wa Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ), nao wote hao ni

wenye kufuatwa kwa ajili ya mafunzo ya dini, wamekuwa wanazozana? Ubayy amesema ukweli na hakujali kuhusu ibn Mas‘ûd. Lakini nikimsikiya yoyote atakaepinga hilo baadae nitamuadhibu hivi na hivi‘.‖1 Imâm Muzani pia akasema; ―Kuna yule mwenye kujuzisha ikhtilafu na akadhania yakwamba iwapo Wanavyuoni wawili watafanya ijtihâd katika mas‘ala fulani na mmoja akasema, ‗HaLaal‘, na mwengine akasema, ‗Harâm‘, kisha wote wakawa katika haki kutokana na ijtihâd zao! Husemwa kuambiwa mtu kama huyo, ‗Je, rai yako hii imetegemezwa na Asli (Qur‘ân na Sunnah) au Qiyâs (ukisiaji)?‘ Iwapo atasema, ‗Juu ya Asili‘, ataambiwa, ‗Itategemezwaje juu ya Asli ikiwa Qur‘ân inapinga ikhtilafu?‘ Na iwapo atasema, ‗Juu ya Qiyâs (ukisiaji)‘, ataambiwa, ‗Vipi asli inapinga kukhitilafiana, na iruhusiwe (hiyo ikhtilafu) kwako wewe kutueleza kutokana na rai ya ukisiaji yakwamba ikhtilafu yajuzu?! Jambo hili halikubaliki kwa mtu yoyote mwenye akili, licha kwa mtu msomi.‖2 Iwapo itaendelea kusemwa: Yale uloyanukuu kutoka kwa Imâm Mâlik yakwamba njia ya Haki ni moja pekee, wala si nyingi, yamekosolewa hayo na yale yaliyopatikana kwenye kitabu cha ―al-Madkhal al-Fiqhiyyah” cha al-Ustâdh az-Zarqâ‘ (1/89). Alipendekeza Abû Ja‘ffar pamoja na ar-Rashîd baada yake yakwamba madh-hab ya Imâm Mâlik kupitia katika kitabu chake [cha al-Muwatta‘] iwe ndiyo sheriya ya kutawala Dola ya ‗Abbâsiyyah. Imâm Mâlik akawazuiya kufanya hivyo

na akawaambia; ―Hakika Maswahaba wa Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل )

1 Ibid. (2/83-4) 2 Ibid. (2/89)

XLVI

walikhitilafiana juu ya mas‘ala yasiyokuwa ya kimsingi na wakatawanyika katika miji mbali-mbali, lakini kila mmoja wao alikuwa sawa.‖ Mimi nasema: Hakika kisa hiki cha Imâm Mâlik ni maarufu sana na ni

mashuhuri kutoka kwa Imâm Mâlik ( اهلل رحمه ), lakini mwishoni mwa

maneno yake yakwamba, ―lakini kila mmoja wao alikuwa sawa‖ ni jambo lisilo na msingi wowote kutoka katika asli au riwaya zote nilizowahi kuzipitia mimi1, WAllâh‎i, isipokuwa riwaya nyengine tu iliyopokewa na Abu Nu‘aym katika Hilyah al-Awliyâ‘ (6/332), lakini ilikuwa na msururu wa wapokezi ndani yake akiwemo al-Miqdâm ibn Dâwud aliyetabakishwa miongoni mwa wapokezi dhaifu na adh-Dhahabi katika kitabu chake adh-Dhu‘afâ‘; na si hayo tu, lakini maneno yenyewe yalivyo ni, ―... lakini kila mmoja wao alikuwa sawa kulingana na maoni yake.‖ Kwahivyo, matamshi yasemayo ―kulingana na maoni yake‖ yaonyesha yakwamba riwaya katika Madkhal ni ya kuzua; kwa hakika, itakuwaje vyengine, ikiwa inakhalifu yaliyopokewa kutoka kwa wapokezi wa kutegemewa kutoka kwa Imâm Mâlik yakwamba Haki ni Moja Pekee na wala si nyingi, kama tulivyotangulia kusema, na haya yameafikiwa na ma-Imâm wote wa Maswahaba na waliokuja baada yao pamoja na ma-Imâm wenye kujitahidi wanne na wengineo. Ibn ‗Abdul Barr‘ amesema, ―Iwapo rai zenye kukhalifiana zaweza kuwa sawa zote, basi ma-Salaf hawangeweza kurekebishana ijtihâd zao, hukmu, na uamuzi. Hoja rahisi inakataa yakwamba kitu na kilicho kinyume chake, vyote vinaweza kuwa sawa; kama msemo mzuri unavyoelekeza,

إزجةت طدي فة ف ظةل أىجط ة يأت اعةل―Kuthibitisha vinyume viwili pamoja ni katika uovu usiowezekana.‖2 Iwapo itaendelea tena kusemwa: ―Tukichukulia yakwamba riwaya hii kutoka kwa Imâm Mâlik ni ya urongo, basi ni kwa nini alimkataza al-

1 Cf. Al-Intiqâ‘ cha Imâm ibn ‗Abdul Barr (41), Kashf al-Mughatta fî fadhl al-Muwatta‘ (Uk. 6-7) cha ibn ‗Asâkir, na Tadhkirah cha Imâm Adh-Dhahabi (1/195) 2 Jâmi‘ Bayan al-‗Ilm (2/88)

XLVII

Mansûr kuwaleta watu pamoja juu ya kitabu chake al-Muwatta‘ badala ya kutekeleza matakwa ya Khalifa?‖ Mimi nasema: Nilichokiona kuwa ni bora katika kulijibu suala hili ni alichokizungumza Hâfidh ibn Kathîr katika kitabu chake Sharh Ikhtisâr ‗Ulûm al-Hadîth (Uk. 31), yakwamba Imâm Mâlik alisema, ―Kwa hakika watu wamekusanyika pamoja juu ya, na kuyaelewa, mambo ambayo sisi hatukuyajua.‖ Hii ilikuwa ni sehemu ya ubora ya hikma

aliyokuwa nayo na uadilifu, kama alivyosema ibn Kathîr ( اهلل رحمه ).

Kwa hiyo, imethubutu yakwamba ikhtilafu ni kitu kibaya, wala si rehma! Hata hivyo, aina moja ya ikhtilafu ndio yenye kulaumika, nayo ni ile ya wafuasi wakaidi wa madh-hab, na aina nyengine si ya kulaumika, kama ikhtilafu ya maswahaba na ma-Imâm waliokuja baada yao (warathi wao) – Twamuomba Allâh‎ atufufue pamoja nao tukiwa washirika wao, na atupe uwezo kuandama njia zao. Kwa hivyo, imedhihiri yakwamba ikhtilafu ya Maswahaba haikuwa sawa na ikhtilafu ya muqallidîn. Kwa mukhtasar: Maswahaba walikhitilafiana kwa kukosa budi, lakini walikuwa wakichukia sana ikhtilafu, na walikuwa wakijiepusha nayo kadiri ya uwezo wao; Amma kuhusu hawa muqallidîn, hata kama inawezekana kwa njia nyingi kujiepusha na ikhtilafu, wao walikuwa hawakubali wala hawajitahidi katika kuleta umoja; kwa hakika, wao wanaunga mkono ikhtilafu. Kwa hiyo, kuna tafauti kubwa baina ya hizi aina mbili za watu kuhusiana na ikhtilafu ya rai zao. Hii ilikuwa ni ikhtilafu kutokana na upande wa Sababu.

B) Amma ikhtilafu kutokana na upande wa kuathirika iko wazi zaidi.

Maswahaba , (عنهم اهلل رضي) , licha ya umaarufu wao juu ya ikhtilafu

katika mas‘ala yasiyokuwa ya kimsingi, walikuwa na tahadhari kubwa katika kuhifadhi umoja wa kujidhihirisha, na wakijiepusha mbali kabisa na kitu chochote kiwezacho kuleta mgawanyiko na kuzua

XLVIII

mtafaruku baina yao. Kwa mfano, kulikuwepo na baadhi yao, wale wenye kujuzisha kuitamka basmalah kwa sauti (kwenye Swala) na wale waliopinga hilo; kulikuwepo na wale wenye kushikilia msimamo yakwamba kunyanyua mikono (kwenye Swala) ni jambo lililo pendekezwa na wengine waliopinga hilo; kuna wale wenye msimamo yakwamba kumgusa mwanamke kunatangua wudhu‘; na wengine hawakuwa na msimamo huwo; - lakini juu ya yote hayo, wote walikuwa wakiswali kwa pamoja nyuma ya Imâm mmoja, na hapana miongoni mwao atakaedharau kuswali nyuma ya Imâm kutokana na ikhtilafu ya maoni. Amma kwa muqallidîn, ikhtilafu zao ni tafauti kabisa, kwani imesababisha Waislamu kugawanyika kwenye nguzo kubwa kabisa baada ya shahada mbili za Imani: hakuna isiyokuwa Swala. Wanakatâ kuswali pamoja nyuma ya Imâm mmoja, wakitoa hoja yakwamba Swala ya Imâm imebatilika (bâtil), au kwa uchache ni Makuruhu, kwa mtu aliye kwenye madh-hab tafauti. Haya ni mambo tuliyoyashuhudia na kuyasikiya, kama wenzetu wasiokuwa sisi walivyo ona1; itakosaje kuwa hivyo, ikiwa siku hizi baadhi ya vitabu mashuhuri vya ki-madh-hab vinatoa hukmu kama hizo za ubatilifu au ikirahi. Matokeo ya hayo utakuta yakwamba kunapatikana Mihrâb nne katika misikiti yenye Jamâ‘a kubwa, ambayo ma-Imâm wanne huongoza Swala mmoja baada ya mwengine katika msikiti mmoja, na utakuta watu wakimungoja Imâm wao haliyakuwa Imâm mwengine tayari amesimama kuwaswalisha watu!!! Kwa hakika, baadhi ya hawa muqallidîn, ikhtilafu ya ki-madh-hab imefikiya hali mbaya kuliko hiyo, kama vile marufuku ya kuowana baina ya ma-Hanafî na ma-Shâfi‘î; Mwanachuoni mmoja mashuhuri sana wa ki-Hanafî, aliyejulikana baada e kwa lakabu ya Mufti ath-Thaqalayn (Mufti wa wanadamu na majini), alitoa fatwâ ya kumruhusu mtu aliye kwenye madh-hab ya Hanafî kumuowa

1 Tazama Mlango wa Nane katika kitabu Mâ Laa Yajûz min al-Khilaaf (Uk. 65-72), ambapo utaona mifano chungu nzima ya yale tuliyoyagusia, baadhi yao yakiwahusu Wanavyuoni wa Al-Azhar.

XLIX

mwanamke aliye kwenye madh-hab ya Shâfi‘î, kwa sababu ―nafasi yake ni kama ile ya watu wa kitabu (Ahlul Kitâb)‖1! Hii inamânisha – na maana zilizodokezwa ni zenye kukubalika kwao – yakwamba hali kinyume cha hivyo hairuhusiwi, Yaani, mwanamke wa ki-Hanafî kuolewa na mwanamume wa ki-Shâfi‘î, kama vile mwanamke Muislamu hawezi kuolewa na Myahudi au Mnaswara?!! Mifano hii miwili, kutokana na mengine mingi, yanatosha kutoa ufafanuzi kwa mtu yoyote mwenye fahamu njema athari mbaya za ikhtilafu za kizazi cha baada e na ukaidi walokuwa nao juu ya mambo hayo, kinyume cha ikhtilafu za kizazi cha awali (Salaf), ambacho hakikuwa na athari yoyote mbaya juu ya Ummah. Kwa sababu ya hayo, Salaf (waliokuja baada e) wameokolewa kutokana na Aya zenye kukataza ikhtilafu katika Dini, tafauti na vizazi vya baada e. Twamuomba Allâh‎ atuongoze sote kwenye njia iliyo nyoka. Zaidi, tutatamani vipi sisi yakwamba madhara yaliyosababishwa na ikhtilafu kama hizo zibakie miongoni mwao tu na wala zisiwafikie watu wengine wanaolinganiwa katika njia za da‘wah, kwani hapo haitokuwa na ubaya hivyo, lakini ni ya kuhuzunisha sana wanapoyaruhusu kuwafikiya makafiri kwenye sehemu mbali mbali za Ulimwenguni, na ikhtilafu zao hizo zikawa ni vikwazo kwa watu wengi kuingia katika Dini ya Allâh‎! Kitabu DhwaLaam min al-Gharb cha Muhammad al-Ghazâli (Uk. 200) kimenukuu matukio yafuatayo, ―Kisa kilichotokea wakati wa mkutano uliofanyika katika University of Princeton nchini Marekani ambapo mmojawapo wa wazungumzaji alipouliza suali, ambalo ndilo linalowapendeza mno al-Mustashriqîn (Orientalists) na mâdui wa Uislamu. Ni mafunzo gani ambayo Waislamu waliyo nayo kuwaletea walimwengu ili kuubainisha Uislamu ambao wanaoulingania? Je, ni mafunzo ya ki-Islamu kulingana na ma-Sunni? Au ni kulingana na Imâm iyyah au U-Shî‘ah Zaydiyyah? Imma, mapote haya yote yamegawanyika zaidi, tena juu ya hayo, baadhi yao wanâmini kuwa chini ya mipaka ya kifikra, au wengine ni wakaidi katika imani zao zenye mipangilio mâlum.‘

1Al-Bahr ar-Râ‘iq

L

Matokeo ya mkutano huwo ni kwamba walinganizi wa Uislamu wakawawacha wale waliolinganiwa katika hali ya mtafaruku, kwani wao wenyewe walikuwa wamechanganyikiwa.‖1

1 Na mimi sasa nasema: Hiki kitabu cha hivi karibuni cha Muhammad al-Ghazâlî kiitwacho As-Sunnah an-Nabawiyyah bayna Ahl al-Hadîth wa Ahl al-Fiqh (Sunnah za Mtume baina ya watu wa Hadîth na watu wa Fiqh) kimethibitisha yakwamba yeye mwenyewe ni mmojawapo wa wale walinganizi wa Uislamu ambao wao wenyewe ―wamechanganyikiwa‖! Vitabu vyake vimefichua siri kitambo ya kuchanganyikiwa kwake, upotoshaji wake wa Sunnah, na matumizi ya akili yake katika kuihukumu hadîth – imma ni swahîh au dha‘îf, wala sio kuielekea misingi na uta‘alamu wa Hadîth, wala wata‘alamu wa fanni hiyo; Badala yake, lolote lenye kumvutia, yeye hulisahihisha, hata kama ni dha‘îf, na huthibitisha kuwa jambo si la kuaminika lolote lenye kwenda kinyume na matakwa yake, hata kama limeafikiwa kuwa ni swahîh! Msimamo wake wa hapo juu unaonyesha waziwazi katika maelezo yake ya hadîth katika kitabu chake cha awali Fiqh as-Sîrah, ambapo alieleza mfumo wake wa kuzikubali ahâdîth dha‘îf na kuzitupilia mbali zilizo swahîh juu ya msingi wa matamshi ya hadîth peke yake, ili kutokana na hayo msomaji ajionî malengo ya uchambuzi wa hadîth hayana muelekeo wowote katika maoni yake iwapo yatakwenda kinyume na ―uchanganuzi wa hoja‖, ambayo yanabadilika kimakosa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwengine, kwani lililo la ukweli kwa mmoja ni la urongo kwa mwengine! Hivyo basi, Uislamu wote unakuwa ni wenye kutegemea vituko vya ki-ubinafsi, visivyokuwa na misingi wala nukta za kumbukumbu isipokuwa rai za watu binafsi; Huku ni kukhitilafiana kabisa na msimamo wa ma-‗Ulamâ waliotangulia wa ki-Islaam, ―yakwamba isnâd ni sehemu ya Dini; Lau kama si isnâd, watu wangelisema chochote wapendacho.‖ Kitabu hicho chake kipya kilichotajwa hapo juu kimefichua kwa watu mfumo alokuwa nao wa Mu‘tazila, kujitokeza kwake kwa majivuno ya kuwatweza ma-Imâm wa hadîth na juhudi zao kubwa kwa miaka yote hiyo ya kuihudumikia Sunnah, na upambanuzi wa mafunzo halisi kutokana na yasiyotegemewa, na ukosefu wake wa shukrani kwa juhudi walizofanya ma-Imâm wa Fiqh katika kuweka misingi, na mas‘ala ya kimaendeleo waliyoiweka, kwani yeye huchukuwa atakacho kutoka kwenye hukmu hizo na

LI

Katika Muqaddimah (utangulizi) wa kitabu kiitwacho Hadiyyah as-Sultân iLaa Muslimî biLaad jâbân kilichotungwa na ‗Allâmah‎‎ Sultân al-

Ma‘sûmi ( اهلل رحمه ), mtungaji amesema:

―Niliulizwa suali na Waislamu wa Japan, kutoka kwenye miji ya Tokyo na Osaka huko Mashariki ya Mbali, ‗Ni ipi Dini ya kihakika ya Uislamu? Madh-hab ni nini? Je, inamlazimu mtu aliyepewa hadhi na Dini ya Uislamu ajinasibishe na mojawapo ya madh-hab nne? Yaani, awe Mâlik, Hanafî, Shâfi‘î au Hanbalî, au hilo si jambo la lazima?‘ Hii ni kwa sababu mtafaruku mkubwa, mabishano ya kuchukiza, yametokea hapa, wakati idadi kubwa ya makundi ya wasomi wa ki-Japani walipotaka kuingia kwenye Dini ya Uislamu, ili nao wapate hadhi ya utukufu wa Imani. Walipowasilisha ombi hili kwa baadhi ya Waislamu waliokuwepo mjini Tokyo, baadhi ya watu kutoka India wakasema, ―Ni bora wangelichagua madh-hab ya Imâm Abu Hanîfah , kwani yeye alikuwa ndiye tâ yenye kung‘ara ya Ummah ―; baadhi ya watu kutoka Indonesia (Java) wakasema, ―Laa wangelichagua madh-hab ya Imâm ash-Shâfi‘î!‖ Basi wale wa-Japani walipoyasikiya maneno hayo, kwa hakika walitatizika sana mpaka wakajikuta wametupwa mbali na malengo yao ya asli waliyoyakusudia. Kwa hiyo mas‘ala haya ya madh-hab yakawa ni kizingiti katika njia yao ya kuukubali Uislamu!! SHUB‟HA YA TATU: Wengine wanadhania yakwamba tunayolingania sisi, ya kufuata Sunnah na kushikilia rai za ma-Imâm zenye kwenda kinyume na Sunnah, maana yake ni kujiepusha kabisa kufuata maoni yao na kufaidika kutokana na rai zao na ijtihâd walizofanya. Jawabu: Fikra hii ni mbali kabisa na ukweli – Ni urongo ulio wazi wenye dosari, kama ilivyo-onekana kudhihiri kwake kutoka kwenye mazungumzo yetu yaliyotangulia, yote yakiwa ni yenye kuashiria

kuwacha atakayo, bila ya misimamo iliyo thabiti katika hukmu zozote au misingi yoyote ya kisheriya!

LII

kinyume chake. Ulinganizi wetu sisi ni kuwacha kuyafanya haya madh-hab kuwa ndiyo Dini, kuyaweka mahali pa Qur‘ân na Sunnah, mpaka ikawa ndipo mahali pa marejeo yetu pindi yatokeapo mabishano au inapobuniwa hukmu mpya kwa ajili ya matukio ya ghafula, kama wafanyavyo ma-Faqîh wa zama zetu wanapobuni hukmu mpya kuhusiana na hali za watu, ndoa, talaka, n.k; badala ya kurejea kwenye Qur‘ân na Sunnah katika kupambanua usawa kutokamana na yaliyo na makosa, haki kutoka kwenye bâtil – yote haya juu ya msingi wa fahamu zao yakwamba ―ikhtilafu ni Rehma‖ na kufuata kila ruhusa, yenye tahfifu na maslaha. Ni maneno mazuri

yaliyoje aliyoyasema Sulaiman at-Taymî ( اهلل رحمه ):

«اصذؿ ن الش لك، إن أخذت ثرخصح ك اعل »―Ungelikuwa ni mwenye kukubali anachoruhusu kila Mwanachuoni, Ingekusanyika kwako kila aina ya shari.‖ Yamenukuliwa hayo na Ibn ‗Abdul Barr katika Jâmi‘ BaYân al-‗Ilm (2/91-92), aliyesema baada ya hayo, ―Kuna ijmâ‘ (kuafikiana kwa rai) juu ya hayo: Mimi sijui rai nyengine iliyo kinyume cha hayo.‖ Haya yote ya kujitafutia urahisi kwa ajili hiyo tu ndiyo tunayoyapinga sisi, na yameafikiwa na ijmâ‘, kama uonavyo. Amma kuhusu kurejea kwenye rai za ma-Imâm , kufaidika nazo na kusaidiwa nazo katika kufahamu ukweli mahali penye ikhtilafu na ikawa hakuna maandishi ya Qur‘ân wala Sunnah, au kama kuna haja ya ufafanuzi, sisi hatukatai hayo. Kwa hakika, sisi twayaunga mkono hayo na twayahimiza, kwani kuna faida nyingi sana zinazotarajiwa hapo kwa mtu yoyote mwenye kuandama njia ya uongofu wa Qur‘ân

na Sunnah. ‗Allâmah‎‎ Ibn ‗Abdul Barr ( اهلل رحمه ) amesema (2/172):

―Shikamana, ewe ndugu yangu, na kuihifadhi misingi na kuyatilia umuhimu. Inakupasa ujuwe yakwamba yoyote mwenye kuzihifadhi Sunnah na maamrisho yaliyomo kwenye Qur‘ân, akazingatia rai za ma-Fuqahâ ili zimuongoze kwenye ijtihâd yake,

LIII

akafungua kila pembe ya maelewano na kuzifahamisha Sunnah zenye kufahamika kwa njia nyingi tafauti, akawa hafuati ki-Upofu rai ya yoyote miongoni mwao jinsi ya kufuata Sunnah bila ya utafiti, wala kudharau yale ambayo wanavyuoni wenyewe waliyojitahidi nayo katika kuzihifadhi na kuzizingatia Sunnah, lakini akaziandama kwa kuzijadili, kuzifahamu na kuzitafiti, akawa ni mwenye kuwashukuru kwa jitihada zao ambazo kwa kuzipitia zimemfaidisha na kumtanabahisha kuhusu mas‘ala mengi, akawasifu kwa kusibu hatima zao, kama ilivyo kwenye mas‘ala mengi, lakini akawa hawatakasi na makosa kama ambavyo wao wenyewe hawakujitakasa: huyo ndiye mwenye kutafuta ilimu ambaye aliyejishikamanisha na njia ya Salafu-us-Sâlih (wema waliotangulia); huyo ndiye aliyebahatikiwa na aliyeongozwa kihakika; huyo ndiye mfuasi wa Sunnah za Mtume wake

( وسلم عليه اهلل صىل ), na uongofu wa Maswahaba (عنهم اهلل رضي) .

Lakini yule asiyetaka kujishughulisha na utafiti wa ki-ilimu, akaitupilia mbali mipangilio tuliyoitaja, akazipinga Sunnah kwa rai zake na mapendeleo ya nafsi yake na kuzitumia tu iwapo zitakubaliana na rai zake: mtu kama huyo ni yule aliyepotoka na kuwapotosha wengine. La zaidi ni kwamba, yule asiyeyajua yote hayo tuloyataja, na akajitumbukiza kipumbavu kwenye ukumbi wa kutoa fatwâ bila ya Ilimu: mtu kama huyo ndiye aliyepofuka zaidi, na aliye katika njia iliyopotoka zaidi.‖ SHUB‟HA YA NNE: Kuna shubuhât (tashwishi) nyengine miongoni mwa muqallidîn inayowazuwiya wasitekeleze Sunnah ambayo imedhihiri kwao yakwamba madh-hab yao imetafautiana nayo kwenye mas‘ala hayo: wanadhania yakwamba utekelezaji wa Sunnah hiyo unalazimisha kumkosoa muanzilishi wa madh-hab. Kwao wao, ukosoaji una maana ya ukosefu wa adabu kwa Imâm ; ikiwa haifai kumkosea adabu mtu yoyote Muislamu, watamkoseaje adabu mmojawapo wa ma-Imâm wao?

LIV

Jawabu: Hii ni hoja ya uwongo kabisa, na husababisha kuzipa nyongo Sunnah; au kwa maana nyengine, atawezaje Muislamu muerevu kuleta hoja kama hiyo?!

Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) mwenyewe alisema:

« خػأ

د نأ نةصذ صران إوذا ظس

أ صةب ن

د نأ نةصذ الةز إذا ظس

صر واظد أ « ن

―Hakimu anapojitahidi na kuhukumu jambo akasibu, atapata thawabu mara mbili; lakini atakapojitahidi na kuhukumu jambo akakosea, atapata thawabu mara moja.‖1 Hadîth hii inakanusha mjadala wa hapo juu na kubainisha kwa uwazi kabisa bila ya utata wowote yakwamba ikiwa mtu atasema, ―fulani ibn fulani amekosea‖, maana yake chini ya kifungu cha Sharî‘ah ni kwamba, ―fulani ibn fulani amepata thawabu mara moja.‖ Sasa ikiwa atapata thawabu kulingana na mtazamo wa mkosoaji, wewe utamlaumu vipi huyo alokosa kwa kumtuhumu? Kuna shaka yakwamba lawama za aina hii hazina msingi wowote na mtu yoyote mwenye kujenga hoja zake juu ya msingi huu itamlazimu awachane nao: Au vinginevyo yeye ndiye atakaekuwa ni mwenye kuwatuhumu Waislamu, wala si watu tu wa kawaida miongoni mwa Waislamu, lakini ni katika ma-Imâm wakubwa miongoni mwa Maswahaba, ma-Tâbi‘î, na waliowafuata wao miongoni mwa ma-Imâm walio Mujtahidîn na wengineo. Hii ni kwa sababu sisi twajua kwa yakini yakwamba hawa watu mashuhuri walikuwa wakikosea na kukosoana wao kwa wao2; Je, husemwa na mwenye akili, ―Walikuwa wakishambuliana wao kwa wao‖? Laa! Kwa hakika, imepokewa kwa njia iliyo swahîh yakwamba

Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) yeye binafsi alimkosoa Abu Bakr (عنه اهلل رضي)

katika tafsiri yake ya ndoto ya mtu, akamwambia:

1 Bukhâri na Muslim 2 Tizama maneno yaliyotangulia ya Imâm Muzani na Hâfidh Ibn Rajab al-Hanbalî.

LV

صجخ »ت بفظة أ

خػأ

« بفظة وأ

―Umeipata baadhi yake na baadhi nyengine umeikosa‖1

Je, kwa maneno haya utasema kuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

amemshambulia au kumtukana Abu Bakr?! Mojawapo ya athari ya kushangaza iliyo katika mashikio ya tashwishi hii ni kwamba inawazuiya wao kufuata Sunnah ikiwa ni tafauti na madh-hab zao, kwani kulingana na mtazamo wao, kuitekeleza Sunnah ni kumkosea Imâm , na kumfuata Imâm , hata kama ni kwenda kinyume na Sunnah, maana yake ni kumuheshimu nakumpenda yeye! Kwa hiyo, wanasisitiza kufuata rai zake ili waepukane na hili jambo la ukosefu na adabu. Hawa watu wamesahau – Mimi sisemi: ... wamejifanya kusahau – yakwamba kwa sababu ya muelekeo huu, wamejikuta mahali pabaya zaidi kuliko pale walipopakimbia. Yataka wâmbiwe, ―Ikiwa kumfuata mtu maana yake ni kwamba unamuheshimu, na kumpinga maana yake ni kwamba unamtukana, basi vipi nyinyi munajiruhusu nafsi zenu

kwenda kinyume na Sunnah ya Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) na kutozifuata,

mukafadhilisha kumfuata Imâm wa madh-hab katika njia iliyo kinyume cha Sunnah, haliyakuwa Imâm hakuhifadhiwa na madhambi na kumtukana si ukafiri? Ikiwa utaifasiri kumpinga (kumkosoa) Imâm

kuwa ni kumtukana, basi kumpinga (au kumkosoa) Mtume ( عليه اهلل صىل ,ni dhahiri bila ya shaka yakwamba huko ni kumtusi. Kwa hakika (وسلم

ni ukafiri ulio dhahiri, ambao tunaomuomba Allâh‎ ( وتعاىل سبحانه ) atuilinde

nao!‖ Ikiwa haya watâmbiwa wao, WAllâh‎i, hawatoweza kujibu chochote, isipokuwa jawabu moja tu la kisuluhifu tulisikialo mara kwa mara kutoka kwa baadhi yao: ―Sisi tumeiwacha Sunnah hii tukiwa na Imani kubwa juu ya Imâm wa madh-hab, naye alikuwa na Ilimu zaidi kuhusu Sunnah kuliko sisi.‖

1 Bukhâri na Muslim; Angalia Kiambatisho Cha Pili kwa hadîth kamili.

LVI

Jawabu letu kuhusu suala hili limetoka kwenye pembe nyingi, na lishajadiliwa kwa urefu sana katika utangulizi huu. Hii ndiyo sababu, kwa mukhtasar, mimi nitajiwekea mipaka juu ya mtazamo mmoja,

jawabu iliyo bayana kwa idhni ya Allâh‎ ( وتعاىل سبحانه ). Mimi nasema:

―Imâm wa madh-hab yako si yeye peke yake aliyesoma zaidi Sunnah kuliko wewe: Kwa hakika, kuna madarzeni, Laa ma-miya (100), ya ma-Imâm ambao pia wamesoma sana Sunnah kuliko wewe. Kwa hivyo, iwapo Sunnah iliyo swahîh imetokea kukhalifiana na madh-hab yako, na ikachukuliwa na kufuatwa na mmojawapo wa hawa ma-Imâm wengine, hapana shaka yoyote yakwamba itakulazimu wewe kuikubali Sunnah hiyo katika hali hii. Hii ni kwa sababu hoja yako iliyotajwa hapo juu haifai hapa, kwani mwenye kukupinga wewe atajibu, ‗Sisi tumeikubali Sunnah hii kwa kumuamini Imâm wetu, ambaye aliyeikubali‘ – katika mfano huu, kumfuata Imâm aliyekuja baada ye ni aula kuliko kumfuata Imâm aliyekhalifu Sunnah.‖ Huu ni ubainifu usiokuwa na utata kwa mtu yoyote, akipenda Allâh‎

( وتعاىل سبحانه ).

Kwa sababu ya yote yaliyotangulia, mimi naweza kusema: ―Kwa vile kitabu chetu hiki kimekusanya Sunnah zilizo swahîh

zilizopokewa kutoka kwa Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) kuhusu maelezo ya

Swala yake, hakuna msamaha kwa yoyote atakayekatâ kuyatekeleza mafunzo hayo kulingana na vile yalivyo, kwani hakuna chochote ndani yake ambacho wanavyuoni wameafikiana kukikatâ, nao hawatolifanya hilo. Kwa hakika, katika kila mfano unaoangaziwa, wengi wao wamechukuwa mfumo wa Sunnah zilizo swahîh , yoyote miongoni mwao ambae hakufuata mfumo huo husamehewa na hupata thawabu mara moja, kwa sababu mândiko hayakuwahi kuwasilishwa kwake kabisa, au yamewasilishwa kwake lakini kwa aina fulani ya njia ambayo kwake yeye haikusimamisha hoja, au kwa sababu nyengine maarufu miongoni mwa nyudhuru zijulikanazo na Wanavyuoni. Amma kwa wale watakaokuja baada yake na wakathibitishiwa mândiko

LVII

waziwazi hawatosamehewa kwa kufuata rai yake; bali, ni Waajib kufuata Mândiko Matakatifu. Na hayo ndiyo yaliyokusudiwa kutoka katika utangulizi huu. Amesema

Allâh‎ ( وتعاىل سبحانه ):

ة حأ ٱ ي ي ا لذ ٱءا ا و شذضج ة يس ل ولرذشل إذا داعز ٱللذ ا ـ

نذ ٱأ رء ٱيل بي للذ ج ل ۦوى ذ

ون ۥ وأ ٢٤إحل تش

“Enyi mlioamini! Muitikieni Allâh‎ na Mtume wake anapokuiteni katika yale yatakayokupeni uhai mzuri (wa dunia na Akhera.

Fuateni amri zake Allâh‎ na makatazo yake). Na jueni kuwa Allâh‎ huingia kati ya mtu na moyo wake (mara akafa. Basi

asiakhirisheakhirishe kwa kutumaini uhai ; na jueni), kuwa kwake Yeye mtakusanywa (mulipwe kwa kila mlilolifanya).”1

Allâh‎ ( وتعاىل سبحانه ) Amesema kweli; nae ndiye anayetuongoza kwenye

njia ya sawa; na ndiye Mlinzi bora na Mbora wa wenye kunusuru. Twamuomba Allâh‎ azifikishe Swala na salamu juu ya Muhammad, na juu ya ahli zake na Maswahaba zake. Na Kila Sifa njema ni za Allâh‎, Mfalme wa walimwengu wote. Muhammad Nâsir ad-Dîn al-Albâni Damascus 20/5/1381 AH

1 Surah al-Anfâl (8):24

0

KUELEKEA AL-KA‟BAH

Alipokuwa akisimama Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) kwa ajili ya kuswali,

alikuwa akilielekea al-Ka‘bah katika Swala zote za faradhi na za

Sunnah1 na yeye ( وسلم عليه اهلل صىل ) akâmrisha itekelezwe hivyo, kwa

kumwambia ―mwenye kuharibu Swala yake‖2:

ء ز اشذيج ا » «يجح نربإذا ىخ إل الصالة نأشجق الط―Unaposimama kwa ajili ya kuswali, tekeleza wudhu‘ wako kisawasawa, kisha uelekî qiblah na useme Allâh‎u Akbar.‖3

―Alikuwa Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) katika safari akiswali Sunnah akiwa

juu ya kipando chake, na vilevile akiswali witr juu yake kokote alikoelekea nae (mashariki au magharibi).‖4

Maneno yake Allâh‎ ( وتعاىل سبحانه ):

الل » ذ وص ا ذس ة د ح « نأ

“Kokote muelekeapo, mutaukuta Uso wa Allâh‎.”5 Na alikuwa (mara nyengine) anapoazimia kuswali Swala isiyokuwa ya faradhi akiwa juu ya ngamia wake, kwanza humuelekeza qiblah, kisha huitamka takbîr, na huanza kuswali kokote kipando chake kitakako elekeza uso wake.‖6

1 Huu ni ukweli ulio mutawâtir, kwa hivyo hakuhitajiki uchambuzi wa kina, ingawaje baadhi ya ushahidi unaothibitisha utafuata. 2 Tizama kiambatisho cha tatu (3) 3 Imepokewa na Bukhâri, Muslim na Sirâj 4 Imepokewa na Bukhâri, Muslim na Sirâj. Takhrîj yake inapatikana kwenye Irwâ‘ al-Ghalîl (289 na 588) 5 Imepokewa na Muslim, at-Tirmidhî ameithibitisha kuwa swahîh. 6 Imepokewa na Abu Dâwud, Ibn Hibbân katika Thiqât (1/12), Diyâ‘ katika Mukhtârah kwa sanad iliyo hassan; Ibn as-Sukn ameithibitisha

1

―Na alikuwa akirukû‘ na akisujudu akiwa juu ya mnyama wake hali ya kuashiria kwa kichwa chake, na alikuwa akija‘aliya kule kusujudu anainama zaidi kuliko kurukû‘.‖1

―Na alipokuwa Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) akitaka kuswali Swala ya

faradhi, hushuka juu ya mnyama wake na akaelekea qiblah.‖2

Amma katika Swala ya khofu kubwa, Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) amesunisha kwa umati wake waswali ―hali ya kwenda kwa miguu, hali ya kusimama juu ya miguu yao, au hali ya kupanda vipando; hali ya kuelekea qiblah au isiwe hali ya kuelekea qiblah‖3, na pia akasema:

ا إذا » « ثةلرأس والطةرة اتلجري نإة اخذػ“Watu (majeshi) watakapopambana, basi (Swala) hapo itakuwa

ni Takbîr na kuashiria kwa kichwa.”4

Alikuwa pia Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) akisema:

« ة ثي اشق والرب ىجح »―Upande ulio baina ya mashariki na magharibi ni qiblah.‖5

kuwa ni swahîh, kama alivyoithibitisha Ibn Al-Mulaqqin katika Khulasah Badr al-Munîr (22/1) na kabla yao, ‗Abdul Haqq al-Ishbîli katika kitabu chake kiitwacho Ahkâm (No. 1394 chenye usahihishaji wangu). Ahmad ameitumia kama dalili, kama alivyopokea Ibn Hâni kutoka kwake katika kitabu chake, Masâ‘il (1/67) 1 Imepokewa na Ahmad na at-Tirmidhî, aliyeithibitisha kuwa swahîh. 2 Imepokewa na Bukhâri na Ahmad. 3 Imepokewa na Bukhâri na Muslim. 4 Imepokewa na Baihaqî kwa sanad yenye kuafiki mahitaji ya Bukhâri na Muslim. 5 Imepokewa na at-Tirmidhî na Hâkim, aliyeithibitisha kuwa ni swahîh, na mimi nimeieleza katika Irwâ‘ al-Ghalîl (292), uchapishaji wake

umerahisishwa na Allaah (وتعاىل سبحانه)

2

Amesema Jâbir (عنه اهلل رضي) :

―Siku moja, tulipokuwa na Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) katika

mwendo au kikosi fulani (alichokipeleka Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) bila

ya kushiriki yeye mwenyewe), wingu la mvua likatanda, basi tukajaribu kutafuta Qiblah lakini tukakhitilafiana, kwa hivyo kila mmoja wetu akaswali akiwa amîlekea upande tafauti, na kila mmoja wetu akachora alama mbele yake ili tuhifadhi alama za kule tulikoelekea. Asubuhi kulipopambazuka, tuliziangalia alama zetu na tukakuta yakwamba hatukuswali kuelekea qiblah. Kwa

hivyo tukamsimulia hayo Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) [lakini

hakutuamrisha kuiregelea (Swala hiyo)] na akasema: ―Swala zenu zimewatosheleza.‖1

Alikuwa Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) akiswali hali ya kuelekea Bait al-

Muqaddas [na Al-Ka‘bah ikiwa mbele yake] kabla ya kuteremshwa aya ifuatayo:

ف ىد ت وص ةء ٱرى تي لصذ ذ حل ن ل وص ن ة ىجحا درطى

صضد ٱطػر ١٤٤ لرام ٱ ل “Kwa yakini tukiona unavyogeuzageuza uso wako mbinguni. Basi tutakugeuza kwenye Kiblah ukipendacho. Basi geuza uso

wako upande wa Msikiti Mtakatifu (Al-Ka‟bah).”2

Ilipoteremshwa aya hiyo, Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) alikuwa amîlekea

al-Ka‘bah. Kulikuwa na watu Qubâ‘ wakiswali Swala ya Alfajiri, mara wakajiliwa na mtu mmoja na akawâmbia, ‗Hakika Mtume

( وسلم عليه اهلل صىل ) ameteremshiwa sehemu ya Qur‘ân usiku wa jana na

1 Amepokea Dâraqutnî, Hâkim, Baihaqî, at-Tirmidhî, Ibn Mâjah na Tabarâni; inapatikana kwenye Irwâ‘ (296) 2 Surah al-Baqarah (2):144

3

akâmrishwa kulielekea Al-Ka‘bah, (Ehe!) kwa hiyo elekîni Al-Ka‘bah‘. Nyuso zao zilikuwa zimîlekea Shâm, kwa hivyo wakazunguka. [na Imâm wao akazunguka kuelekea qiblah pamoja nao].‖1

KUSIMAMA NDANI YA SWALA

Na alikuwa Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) akisimama ndani ya Swala za

Faradhi na Sunnah, akitekeleza amri ya Allâh‎ (سبحانه وتعالى):

تي ق ا للذ ٢٣٨وىم“Na simameni kwa unyenyekevu katika kumwabudu Allâh‎.”2

Amma akiwa safarini, alikuwa akiswali Swala za Sunnah akiwa juu ya mnyama wake. Aliwâchia Sunnah Ummah wake waswali wakati wa khofu kubwa wakiwa juu ya miguu yao au wakiwa wamepanda, kama

ilivyotajwa, na hilo ndilo kusudio la Neno la Allâh‎ ( وتعاىل سبحانه ):

ا ت ٱع حهؾ ـ ة ٱو لصذ شػ ٱ لصذ تي ى ل ق نإن ٢٣٨وىما للذ خهذ ن ذ

نإذا أ ة جةجا و ر

ٱنرصةل أ روا ٱ ذ ا للذ دس ة ل ذ س ذ ـ ة

ن ٢٣٩تف“Angalieni sana Swala (zote kuziswali, khasa Jamâ‟ah ) na

(khasa) ile Swala ya kati na kati.3 Na simameni kwa unyenyekevu katika kumwabudu Allâh‎. Na kama mkiwa na

1 Imepokewa na Bukhâri , Muslim, Ahmad, Sirâj, at-Twabarâni (3/108/2) na Ibn Sa‘d (1/234). Pia inapatikana kwenye Irwâ‘ (290) 2 Surah al-Baqarah (2):238 3 Yaani...,ni Swala ya ‗Asr kulingana na kauli iliyosihi ya wanavyuoni wengi, miongoni mwao ni Abu Hanîfah na wanafunzi wake wawili. Kuna ahâdîth kuhusu suala hili ambazo Ibn Kathîr ameziangazia katika tafsîr yake.ya Qur‘an.

4

khofu (kuswali kidesturi; mmo katika kupigana; basi swalini) na hali ya kuwa mnakwenda kwa miguu au mmepanda

(wanyama). Na mtakapokuwa katika amani, basi mkumbukeni Allâh‎ (swalini) kama alivyokufunzeni yale mliyokuwa

hamyajui.”1

Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) aliswali hali ya kuketi wakati wa ugonjwa

ambao alokufia nao.2 Vile vile aliswali hali ya kuwa ameketi kwenye tukio jengine kabla ya hapo, alipopata maradhi, na watu nyuma yake wakaswali hali ya kuwa wamesimama; basi akawâshiria wakae, nao wakaketi (na kuswali). Alipomaliza akasema:

مك ع ييمن والروم نةرس نف تلهفن آهة دد إن» وا وإذا رنؿ ا إة صف الةم حلؤد ث نإذا ركؿ نةركف ىفد نال دهف

ا وإذا صل شة نةرنف ا ص «صةلصة نص

“Mumekurubia hapo nyuma kufanya vitendo vya Wafursi na Warumi: wanawasimamia wafalme wao na hali wafalme wao ni wenye kukaa. Musifanye hivyo, kwani Imâm amewekwa ili afuatwe, akirukû‟ (Imâm ) na nyinyi rukû‟uni, na akiinuka na nyinyi inukeni. Na akiswali hali ya kuwa ameketi, na nyinyi swalini kwa kuketi (nyote).”3

SWALA YA MTU MGONJWA AKIWA AMEKETI

1 Surah al- Baqarah (2):238-9 2 At-Tirmidhî, aliyeithibitisha kuwa ni swahîh, na Ahmad 3 Imepokewa na Muslim na Bukhâri, na inapatikana katika kitabu changu, Irwâ‘ al-Ghalîl chini ya hadîth 394

5

‗Imrân ibn Huswein (عنه اهلل رضي) amesema, ―Niliuguwa maradhi ya

bawasili, kwa hivyo nikamuuliza Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) kuhusu

Swala yangu nae akasema, “Swali hali ya kuwa umesimama, na iwapo huwezi, basi swali hali ya kukaa, na iwapo hata hivyo huwezi, basi swali ukiwa umelala kwa ubavu.”1

Akasema tena ‗Imrân Ibn Huswein, ―Nilimuuliza Mtume ( صىل اهلل عليه kuhusu Swala ya mtu akiwa amekaa, basi alisema: Yule (وسلم

mwenye kuswali hali ya kuwa amesimama, hilo ni jambo bora; mwenye kuswali hali ya kuwa amekaa, thawabu zake ni nusu ya thawabu za mwenye kusimama. Na yule mwenye kuswali hali ya kuwa amelala (na kwenye riwaya nyengine: hali ya kujilaza ubavu), ana nusu ya thawabu za mwenye kukaa.2

Hukmu hii inamuhusu mtu mgonjwa, kwani Anas (رضي اهلل عنه)

amesema, ―Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) aliwatokezea watu akawakuta

wakiswali kwa kukaa kwa sababu ya maradhi, kwa hivyo akasema: Kwa hakika, Swala ya mwenye kukaa ina (malipo) nusu ya Swala ya mwenye kusimama.3

Siku moja, Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alimzuru mgonjwa fulani na

akamkuta akiswali (kwa kutegemea) kwenye mto, Mtume ( صىل اهلل

1 Imepokewa na Bukhâri, Abu Dâwud, na Ahmad 2 Ibid. Amesema Khattâbi, ―Maana ya hadîth ya ‗Imrân imemkusudia mtu mgonjwa mwenye hali ya dhiki na kusimama kwa tabu. Kwa hiyo, malipo ya mwenye kuswali kwa kukâ yamefanywa nusu ya malipo ya mwenye kuswali kwa kusimama: akimuhimiza kuswali kwa kusimama huku akimruhusu kukâ.‖ Ibn Hajar amesema katika Fath al-Bâri (2/468): ―Uamuzi huu unakubalika‖. 3 Imepokewa na Ahmad na Ibn Mâjah kwa sanad iliyo swahîh.

6

ه وسلمعلي ) akauchukuwa ule mto, akautupa, yule mtu akachukuwa

ubao ili aswali juu yake, Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akauchukuwa ule

ubao, akautupa, kisha Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akasema: Swali juu ya

ardhi ukiweza, na usipoweza ashiriya kwa kichwa chako, kwa kuashiriya sijdah chini zaidi kuliko rukû‘.‖1

KUSWALI NDANI YA JAHAZI

Aliulizwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) kuhusu kuswali ndani ya jahazi, nae

akasema, Swali (katika jahazi) hali ya kusimama, isipokuwa ukiogopa kughariki.2

Alipokuwa mtu mzima, Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), alijisaidia kwa

kuilemea fimbo katika mahali pake pa kuswali.3

KIKAO NA KISIMAMO NDANI YA SWALA YA USIKU (TAHAJJUD)

Alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), akiswali usiku mrefu hali ya

kusimama, na usiku mrefu wakati mwengine hali ya kukaa, na alikuwa akisoma hali ya kusimama, hurukû‘ hali ya kusimama, na

akisoma hali ya kukaa, hurukû‘ hali ya kukaa.4

1 At-Twabarâni, Bazzâr, Ibn as-Samâk katika kitabu chake cha hadîth (67/2) na Baihaqî. Ina isnâd swahîh kama nilivyoieleza katika Silsilah al-Ahâdîth as-Swahîhah (323). 2 Bazzâr (68), Dâraqutnî. ‗Abdul Ghani al-Maqdisi katika Sunan yake (82/2) na Hâkim akaithibitisha kuwa ni swahîh na Adh-Dhahabi nae akâfiki. 3 Abu Dâwud na Hâkim, aliyeithibitisha kuwa swahîh, kama alivyofanya Adh-Dhahabi. Nimeiweka katika as-Swahîhah (319) na Irwâ‘ (383). 4 Imepokewa na Muslim na Abu Dâwud.

7

Mara nyengine, ―Alikuwa akiswali hali ya kukaa, basi alikuwa akisoma hali amekaa mpaka zikibakia takriban aya thalathini au arubaini za visomo alivyokuwa akisoma, husimama na kuzisoma (hizo aya) hali akiwa amesimama, kisha hurukû‘ na kusujudu kisha hufanya katika Rak‘âh ya pili mfano wa hivyo.‖1 Kwa hakika, aliswali Swala ya as-Subhah2 hali ya kuwa amekaa katika mwisho wa uhai wake alipokuwa mtu mzima, na hilo ni kabla ya kufa kwake kwa mwaka mmoja.3 Na alikuwa akikaa kikao cha tarabbu‘i (kikao cha kimarufâ).4

KUSWALI NA VIATU NA AMRI YA KUFANYA HIVYO

―Na alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akisimama (kwa ajili ya kuswali)

bila ya viatu mara nyengine, na hali ya kuvâ viatu mara nyengine.‖5

Amejuzisha hilo kwa Ummati wake, akasema:

يؤذي ول رص ثي حلخفة أو ف نبس أظدز صل إذا » « كريه ثة

―Akiswali mmoja wenu Na avae viatu vyake au na avivue na kuvieka baina ya miguu yake, Na asimuudhi Kwa viatu hivyo, mtu

mwengine.‖1

1 Imepokewa na Bukhâri na Muslim 2 Yaani; Swala ya Sunnah (usiku au majira ya mchana), jina hilo limetokana na yaliyomo ndani ya Swala hiyo ya tasbîh (kumtukuza Allaah) 3 Imepokewa na Muslim na Ahmad 4 An-Nasâ‘î, Ibn Khuzaymah katika swahîh yake (1/107/2), Abdul Ghani al-Maqdisi katika sunan yake (80/1) na Hâkim, aliyeithibitisha kuwa ni swahîh na Adh-Dhahabi akâfiki. 5 Abu Dâwud na Ibn Mâjah. Ni hadîth mutawâtir kama alivyosema Tahâwi

8

Na Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alilisisitiza suala hili la kuvâ viatu mara

nyengine, aliposema: Jitafautisheni na Mayahudi, kwani wao hawaswali na viatu vyao wala khoff (viatu vya ngozi).2 Alikuwa akivivua viatu vyake kutoka miguuni mwake mara chache hali yakuwa ndani ya Swala na kisha akiendelea na Swala

yake, akasema Abu Sa‘îd al-Khudhrî‘ (رضي اهلل عنه) :

―Siku moja Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) aliswali na sisi. Alipokuwa

akishughulika na Swala alivua viatu vyake na akavieka upande wake wa kushoto. Watu walipoyaona hayo, nao wakavua viatu vyao. Alipomaliza Swala yake akasema, Mbona mumevua viatu vyenu? Wakasema, ‗Tulikuona wewe ukivua viatu vyako, kwa hivyo na sisi tukavua viatu vyetu.‘ Akasema, Kwa hakika amenijilia Jibrîl na akanijulisha yakwamba kulikuwa na uchafu – au alisema: Kitu chenye madhara – (katika riwaya nyengine: Khabathan) kwenye viatu vyangu, kwa hivyo nikavivua. Kwa hivyo, anapokwenda msikitini mmoja wenu, na ângalie viatu vyake: akiona yakwamba vina uchafu – au alisema: kitu chenye madhara - (katika riwaya nyengine: Khabathan) na avipanguse na aswali navyo.3 ―Alipovivua, aliviweka upande wake wa kushoto‖4, na vile vile alikuwa akisema: Anaposwali mmoja wenu, na asiviweke viatu vyake upande wake wa kulia wala upande wake wa kushoto, ambapo vitakuwa ni upande wa kulia kwa mwenzake, isipokuwa

1 Abu Dâwud, na Bazzâr (53 az-Zawâ‘id) na Hâkim akaithibitisha kuwa ni swahîh na Adh-Dhahabi nae akâfiki. 2 Ibid. 3 Abu Dâwud, Ibn Khuzaymah na Hâkim, aliyeithibitisha kuwa swahîh, Adh-Dhahabi na Nawawî wakâfikiana juu yake. Ya kwanza imetolewa katika Irwâ‘ (284) 4 ibid

9

ikiwa hakutokuwa na mtu yoyote katika upande wake wa kushoto, lakini na aviweke baina ya miguu yake.1

KUSWALI JUU YA MINBAR

―Siku moja Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) aliswali juu ya minbar (katika

riwaya nyengine: ... yenye daraja tatu)2. Kwa hiyo, [alipanda juu yake na akasema ‗Allâh‎u Akbar‘ na watu waliokuwa nyuma yake nao wakasema ‗Allâh‎u Akbar‘ haliyakuwa yuko juu ya minbar], [Kisha akarukû‘ akiwa juu ya minbar,] Kisha akasimama wima na akânza kushuka kinyumenyume ili asujudu chini ya minbar. Kisha akarudi, [na akarudia kuyafanya yale aliyoyafanya katika Rak‘âh ya kwanza], mpaka akaikamilisha Swala yake. Kisha akawageukia watu akasema: Enyi watu! Nimeyafanya haya ili muniandame mimi na kujifundisha Swala yangu.3

1 Abu Dâwud, an-Nasâ‘î na Ibn Khuzaymah (1/110/2) kwa isnâd iliyo swahîh. 2 Hii ndiyo sunnah kuhusu minbar: yakwamba iwe na daraja tatu, bila ya kuzidisha, kuwa na ziyada ni bid‘ah, kuanzia zama za Banî Umayyah, mara nyingi inasababisha ukatikaji wa swafu, na kutoka nje ya hapo kwa kuiweka upande wa kipembe cha magharibi ya msikiti au ndani ya mihrâb ni bid‘ah nyengine hiyo, kama ilivyo kuhusiana na kuinyanyua kwenye ukuta mfano wa roshani ambayo mtu huipanda kwa kutumia daraja zake kwenye ukuta! Haliyakuwa uongofu ulio bora ni uongofu wa

Muhammad (صىل اهلل عليه وسلم). Tazama Fath al-Bâri (2/331). 3 Bukhâri, Muslim (aliyepokea riwaya nyengine) na Ibn Sa‘d (1/253). Inapatikana katika Irwâ‘ (545)

10

SUTRAH (KIZUWIZI) NA UWAJIBU WAKE (WA KUIWEKA MBELE YAKE)

―Alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akisimama karibu na kizuwizi

kikawa (umbali) baina yake na hicho kizuizi ni kiyasi cha dhirâ‘ tatu‖1 na ―baina ya mahali anaposujudu na ukuta, (palikuwa na) sehemu kiyasi cha kondoo kupita.‖2

Alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akisema: ―Usiswali isipokuwa uwe

ume-elekea sutrah, wala usimuache mtu yoyote kupita mbele yako, lakini akishindana (na kutaka kupita), basi mpige, kwani yuko pamoja nae, rafiki (Yaani Shetani).‖3

Pia alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akisema: ―Anaposwali mmoja

wenu akielekea sutrah, na aikurubie ile sutrah ili Shetani asiikate Swala yake.‖4

Na alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) mara nyengine akikusudia kuswali

nyuma ya nguzo iliyokuwa ndani ya msikiti wake.5

1 Bukhâri na Ahmad 2 Bukhâri na Muslim 3 Ibn Khuzaymah katika swahîh yake (1/93/1) kwa isnâd iliyo na nguvu. 4Abu Dâwud, Bazzâr (Uk. 24 – Zawâ‘id) na Hâkim aliyeithibitisha kuwa ni swahîh na kuafikiwa na Adh-Dhahabi na an-Nawawî 5 Bukhâri. Sutrah ni lazima kwa Imâm au kwa mtu anayeswali peke yake, hata kama ni ndani ya msikiti mkubwa. Alisema Ibn Hâni kwenye Masâ‘il kutoka kwa Imâm Ahmad (1/66): ―Abu ‗Abdullah (yaani; Imâm Ahmad ibn Hanbal) aliniona mimi siku moja nilipokuwa nikiswali bila ya kuweka sutrah mbele yangu, na nilikuwa ndani ya msikiti wa Jâmi‘ (mkubwa), basi aliniambia: ―Chukuwa kitu kiwe ni sutrah yako‘, hapo nilimfanya mtu aliyekuwa mbele yangu kuwa ni sutrah yangu.‖ Hii inâshiriya yakwamba Imâm Ahmad hakutafautisha baina ya msikiti mkubwa na msikiti mdogo katika mas‘ala ya kuwa na sutrah – na jambo hilo kwa hakika ni la sawa, lakini hili ni jambo lililopuuzwa na watu wengi, wakiwemo ma-Imâm wa misikitini, katika kila nchi niliyowahi

11

Alipokuwa akiswali [katika sehemu iliyokuwa wazi ambapo hakukuwa na chochote kukitumia kama sutrah] alikuwa akikita mbele yake mti au fimbo halafu anaswali nyuma ya mti huo au fimbo hiyo na watu wakiwa nyuma yake.1 Mara nyengine, Mtume

,alikuwa akimuweka mbele mnyama wake ki-ubavu (صىل اهلل عليه وسلم)

halafu humuelekeya akiwa anaswali2; lakini hukmu hii si sawa na Swala katika mabanda ya ngamia3, ambapo alipotukataza4, na mara nyengine huchukuwa shogi lake (tandiko la farasi), akaliweka kwa marefu na kuswali kuelekea pambizoni mwake.5 Alikuwa akisema: Akiweka mmoja wenu mbele yake kitu mfano wa fimbo katika pambizo ya shogi, na aswali bila ya kujali mtu yoyote anaepita nyuma ya kitu hicho.6 Siku moja ―aliswali kwa kuuelekea mti‖7 na mara nyengine ―aliswali kwa kukielekea kitanda ambacho alichokilalia (akiwa

amejifunika) ‗Âishah (رضي اهلل عنها) ‖8

Na alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) hawachi kitu chochote kipite

baina yake na sutrah aliyoiweka mbele yake, kwa ghafula

alipokuwa akiswali Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), alikuja kondoo na

kuazimia kupita mbele yake, kwa hiyo akamtangulia mpaka

kuizuru, hata nchi ya Arabuni nilipofanya ziyara katika mwezi wa Rajab, mwaka huu (1410), kwa hivyo, ma‘Ulamâ na wawaeleze watu na wawanasihi kuhusiana na jambo hili, wawafafanuliye hukmu zake na kwamba inahitajika pia ndani ya misikiti miwili Mitukufu. 1 Bukhâri, Muslim na Ibn Mâjah 2 Bukhâri na Ahmad 3 Yaani; mahali wanapopiga magoti,. 4 Bukhâri na Ahmad 5 Muslim, Ibn Khuzaymah (92/2) na Ahmad 6 Muslim na Abu Dâwud 7 An-Nasâ‘î na Ahmad kwa isnâd iliyo swahîh. 8 Bukhâri, Muslim, na Abu Ya‘laa (3/1107)

12

akambana tumbo lake (kondoo) na ukuta [kisha, huyo kondoo akapita nyuma yake].‖1 Pia siku moja, ―alipokuwa akiswali Swala ya faradhi, alikunja ngumi yake (alipokuwa kwenye Swala), basi alipomaliza, watu wakasema: ‗Ewe Mtume wa Allâh‎, kulizuka kitu chochote wakati tulipokuwa kwenye Swala?‘ Akasema: ‗Laa, isipokuwa shetani alitaka kupita mbele yangu, basi nikamshika kabari (nikamkaba) mpaka nikahisi mzizimo wa ulimi wake (yule shetani) katika mikono yangu. Wallâh‎i! Lau kama si kunitangulia ndugu yangu Suleiman2, ningelimfunga (Shetani huyo) katika mojawapo ya nguzo za msikiti ili watoto wa Madinah wamzunguke. [Kwahivyo,

1 Ibn Khuzaymah katika swahîh yake (1/95/1), at-Twabarâni (3/140/3) na Hâkim aliyeithibitisha uswahîh wake na kuafikiwa na adh-Dhahabi 2 Akikusudia maombi yafuatayo ya Suleiman (مالسالهعليه) ambayo

yaliyokubaliwa na Allaah (وتعاىلهسبحانه) , kama yalivyoelezwa katika Qur‘an:

خ كهر ٱرب ىةل أ بفدي إذ ظد

كا لذ ينجغ ل ت ل م ل و

ةب ٱ ذ رة ٣٥ ل لريط ٱل نصخذ مرهصةب رخةء ظ ۦتري ثأ

٣٦ر أ

حػي ٱو ذاص لظذ ذةء وك جي ف ٣٧كذ ب يرذ صهةد ٱوءاخري ٣٨ ل

“Akasema: „Mola wangu! Nisamehe na unipe Ufalme, asiupate yoyote baada yangu (ya kunipa mimi mpaka niondoke

ulimwenguni). Bila shaka Wewe ndiwe Mpaji (Usiyenyima).” Basi tukamtiisha upepo unaokwenda polepole kwa amri yake,

anakotaka kufika (unamfikisha. Na sasa sisi tumeonyeshwa kidogo haya kwa kupanda eropleni). Pia (tukamtiishia) mashetani, kila

ajengaye na azamiaye (lulu). Na wengine wafungwao minyororoni (wanapokhalifu amri zake).”

[Sûrah as-Swâd (38):35-38]

13

yoyote awezaye kuzuiya kitu kisipite baina yake na qiblah, ni lazima afanye hivyo].‖1 Pia alikuwa akisema: ―Akiwa mmoja wenu anaswali kuelekea kitu ambacho ni sutrah (kinamstiri) baina yake na watu, na mwengine akataka kupita mbele yake, basi na amzuiye kwenye shingo yake [na amzuiye, kadiri ya uwezo wake], (katika riwaya nyengine: na amzuiye, mara mbili) lakini akikatâ basi na apigane nae, kwani kwa hakika huyo ni Shetani.‖2 Pia alikuwa akisema: ―Lau angelijua mwenye kupita mbele ya mwenye kuswali madhambi yaliyo juu yake ingekuwa kusimama arubaini ni bora kwake kuliko kupita mbele ya mwenye kuswali.

1 Ahmad, Dâraqutnî, na at-Tabarî kwa isnâd iliyo swahîh, na hadîth yenye maana iliyofanana na hii iliyopokewa na Maswahaba wengi, yapatikana kwenye Bukhâri, Muslim na wengineo. Ni mojawapo ya ahâdîth nyingi waliyoikatâ pote la ma-Qadiyani, kwani wao hawâmini kuwepo kwa ulimwengu wa ma-Jini ambao umetajwa na Qur‘an na Sunnah. Njiya yao ya kuachana na maandiko ni maarufu: ikiwa inatoka kwenye Qur‘an, wao hubadilisha maana yake, k.m (kwa mfano), maneno ya Aliyetukuka:

ى ذوح إلذ أ

ؿ ٱأ شذ ٱجهر ضجاة ل ـ ة ىرءاة ف ا إذة ش ١ذيةل

“Sema: Imefunuliwa kwangu ya kuwa kundi la majini lilisikiya

(Qur‟an) likasema: „Hakika tumesikiya Qur‟an ya ajabu."

Wao wanasema, ―yaani ni kundi la watu‖! wakalifanya neno ―jinn‖ linahusiana kimaana na ―watu‖! kwa hiyo wanacheza na lugha na Dini; ikiwa inatoka kwenye Sunnah, ikiwa ina uwezekano wa kubadilishwa kwa kuifasiri kimakosa wanafanya hivyo, laa si hivyo, wanaona urahisi wake ni kuithibitisha kuwa ni ya uwongo, hata kama ma-Imâm wa Hadîth wakifuatwa na Ummah mzima wameafikiyana katika kuswihi kwake, licha ya hivyo, hata ikawa mutawâtir. Twamuomba Allaah awaongoze. 2 Bukhâri na Muslim, na riwaya ya ziyada yatoka kwa Ibn Khuzaymah (1/94/1).

14

(Abu an-Nadr asema, ―sikumbuki vizuri iwapo alisema siku arubaini, miezi au miaka.‖)1

MAMBO YENYE KUHARIBU SWALA

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alikuwa akisema: Swala ya mtu hukatika

isipopatikana mbele yake mfano wa pembeni mwa kibao kile anachokalia mpanda farasi; hukatwa Swala yake na mwanamke mwenye heidh2, punda au mbwa mweusi. Akasema Abu Dharr,

‗Nikasema: ―Ewe Mtume wa Allâh‎ (صىل اهلل عليه وسلم), ni kwanini awe ni

mbwa mweusi wala sio mbwa mwekundu?‖ Akasema, Mbwa mweusi ni Shetani.3

MAKATAZO YA KUSWALI UKIWA UMÎLEKEA KABURI

Alikuwa akikataza kuswaliwa hali ya kulielekea kaburi, akisema: Musiswali mukiwa mumîlekea makaburi, na musikae juu ya makaburi.4

NIYA5

1 Ibid. 2 Yaani; aliyebaleghe, na maana ya neno ‗hukatika‘ ni kwamba ‗kukosa malipo‘. Amma kuhusu hadîth: ―Hakuna chenye kukata Swala‖, hiyo ni hadîth dha‘îf kama nilivyo ionyesha kwenye Tamâm al-Minnah (Uk. 306) 3 Muslim, Abu Dâwud na Ibn Khuzaymah (1 / 95 / 2) 4 ibid 5 An-Nawawî asema katika kitabu chake kiitwacho Rawdhwah at-Tâlibîn (1/224 kilichochapishwa na Maktab al-Islaami): Niya ni kukusudia jambo, kwa hivyo mtu anapotaka kuanza kuswali huikusudia katika fahamu yake ile Swala yenyewe na kila jambo lenye kuhusiana na kawaida za Swala hiyo, kama vile ni Swala gani hiyo, au iwapo ni Swala ya faradhi n.k; na huyaleta yote haya kwa pamoja kwenye niya yake yakiandamana na takbîr ya kwanza.‖

15

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), alikuwa akisema: Hakika amali zote

huzingatiwa kwa niya na hakika ana kila mtu jambo analolinuilia.1

TAKBÎR

Kisha Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alikuwa akianza Swala kwa kusema:

«أرب الل »―Allâh‎ ni Mkubwa‖2

Na akamuamrisha ―mwenye kuharibu Swala yake‖ afanye hivyo kama ilivyotangulia, na akamwambia:

اطف دلظ صالة دذ ل إ » ء م اجلةس ظت يذطأ نظؿ الط « أرب الل :ز ييل

―Kwa hakika haitotimia Swala ya mtu yoyote miongoni mwa watu, mpaka atawadhe, aweke wudhu‘ mahali pake, kisha

aseme ‗Allâh‎u Akbar‘‖.3 Pia alikuwa akisema:

1 Bukhâri, Muslim, na wengineo. Inapatikana katika Irwâ‘ (No. 22) 2 Muslim na Ibn Mâjah. Hadîth hii inaonyesha ishara yakwamba hakuanza Swala yake na maneno ya baadhi ya watu: ―Nanuiya kuswali... n.k‖. Jambo ambalo kwa hakika lililoafikiwa yakwamba ni la uzushi. Lakini wana ugomvi kuhusu iwapo ni katika uzushi mzuri au mbaya, jambo ambalo sisi twasema: ―Kwa hakika kila uzushi katika

‗ibaadah ni upotofu, kutoka kwenye jumla ya matamshi yake (الصالة عليه (والسالم ,‘

‗... na kila uzushi ni upotofu, na kila upotofu mwisho wake ni motoni‘.‖ Lakini hapa si mahali pa kuyajadili hayo kwa maelezo ya kikamilifu. 3 At-Twabarâni kwa isnâd iliyo swahîh.

16

«ة اتص وت اتلجري وترية اػر الصالة هذةح»―Ufunguo wa Swala ni wudhu‘, huingiwa kwa takbîr na hutokewa

kwa taslîm.‖1 Vilevile ―alikuwa akipandisha sauti yake kwa takbîr mpaka humsikilizisha aliyekuwa nyuma yake.‖2 Lakini alipokuwa mgonjwa Abu Bakr alikuwa akipandisha sauti yake kuifikisha

takbîr ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) kwa watu.‖ 3

Alikuwa pia akisema:

« أكرب اهلل: فقولوا أكرب اهلل: اإلمام قال إذا »―Imâm anaposema: Allâh‎u Akbar, na nyinyi semeni: Allâh‎u

Akbar.‖4

KUINUA MIKONO MIWILI

Na alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akiinua mikono yake mara

nyengine pamoja na takbîr5, na mara nyengine akiinua baada ya takbîr1, na mara nyengine akiinua kabla ya takbîr2.‖

1 Abu Dâwud, at-Tirmidhî na Hâkim aliyeithibitisha kuwa ni swahîh na ikâfikiwa na adh-Dhahabi. Inapatikana katika Irwâ‘ (No.301). Kwa ufasaha ‗tahrîm yake ni takbîr‘, yaani vitendo ambavyo Allaah alivyovifanya kuwa ni harâm wakati inapotekelezwa (hiyo Swala). Na ‗tahlîl yake ni taslîm‘, yaani mambo yenye kuruhusiwa ukiwa nje ya Swala. Kama ambavyo hadîth inavyothibitisha yakuwa mlango wa Swala umefungwa, hapana mfanya ibada yoyote awezae kuufungua isipokuwa mwenye wodhû‘, vilevile inathibitisha yakwamba huwezi kuingia kwenye Swala bila ya takbîr, na kwamba huwezi kuitoka isipokuwa kwa taslîm. Hii ni rai ya Wanavyuoni wengi. 2Ahmad na Hâkim aliyeithibitisha kuwa ni swahîh na ikâfikiwa na adh-Dhahabi. 3 Muslim na an-Nasâ‘î 4 Ahmad na al-Baihaqî kwa isnâd iliyo swahîh. 5 Bukhâri na an-Nasâ‘î

17

―Alikuwa akiinua mikono yake hali ya kuvinyûsha vidole vyake [bila ya kuvikusanya wala kuvitawanya]‖3, na alikuwa akija‘aliya mikono yake muqâbala na mabega yake4 na huwenda alikuwa akiinua ile mikono mpaka ielekî asli ya (au ndewe za) masikio yake.‖5

KUWEKA MKONO WA KULIA JUU YA MKONO WA KUSHOTO NA KUAMRISHA KUFANYA HIVYO

Alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) AKIWEKA mkono wake wa kulia juu

ya wa kushoto‖6, na alikuwa akisema:

ظؿ وأن شعرة ودأخري نػرة ثذفض أمرة البةء فش إة» « الصالة ف طةاة ع أيةة

―Sisi Mitume tumeamrishwa kuharakisha kufungua (saumu zetu) na kuchelewesha kula Daku na tuweke mikono yetu ya kulia juu

ya mikono ya kushoto katika swala.‖7

Pia Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alimpitia mtu mmoja aliyekuwa akiswali,

haliyakuwa ameweka mkono wake wa kushoto juu ya mkono

wake wa kulia, Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akaivuta (mikono yake hiyo

kwa kuiachanisha) na akaweka mkono wa kulia juu ya wa kushoto.‖8

1 ibid 2 Bukhâri na Abu Dâwud 3 Abu Dâwud, Ibn Khuzaymah(1/62/2, 64/1), Tammâm na Hâkim aliyeithibitisha kuwa ni swahîh na ikâfikiwa na adh-Dhahabi. 4 Bukhâri na an-Nasâ‘î 5 Bukhâri na Abu Dâwud 6 Muslim na Abu Dâwud. Vile vile inapatikana katika Irwâ‘ (352) 7 Ibn Hibbân na Diyâ‘, kwa isnâd iliyo swahîh. 8 Ahmad na Abu Dâwud kwa isnâd iliyo swahîh.

18

KUWEKA MIKONO MIWILI JUU YA KIFUA

―Na alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) AKIWEKA kitanga cha mkono wa

kulia juu ya mgongo wa kitanga, kifundo na kigasha (forearm) chake cha mkono wa kushoto1, na akawâmrisha Maswahaba zake jambo hilo2, na mara nyengine alikuwa AKIUSHIKA mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto.‖3

―Alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akiiweka (mikono yake) juu ya kifua

chake.‖4

1 Abu Dâwud, an-Nasâ‘î na Ibn Khuzaymah (1/54/2) kwa isnâd iliyo swahîh. Na Ibn Hibbân akaithibitisha kuwa swahîh (485) 2 Mâlik, Bukhâri na Abu ‗Awânah 3 An-Nasâ‘î na Dâraqutnî‘ kwa isnâd iliyo swahîh. Katika hadîth hii kuna ushahidi yakwamba kushika ni katika Sunnah, na katika hadîth iliyotangulia yakwamba hata kuweka pia ni katika Sunnah, kwa hivyo zote hizo ni miongoni mwa Sunnah. Amma kuhusu kuchanganya kushika na kuweka, zote mbili wakati mmoja, jambo lililo shikiliwa na ma-Hanafî waliokuja baadae kuwa ni jambo zuri, basi huwo ni uzushi; Aina yake, kama wasemavyo wenyewe, ni kuweka mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto, kwa kukishika kiganja kwa kidole cha mwisho na kidole cha Gumba, na kuvilaza vidole vitatu vilivyo baki, juu ya mgongo wa mkono wa kushoto, kama yalivyoelezwa katika tanbihi ya Ibn ‗Âbidîn juu ya Durr al-Mukhtâr (1/454). Kwa hivyo usibabaishwe juu ya wasemayo. 4 Abu Dâwud, Ibn Khuzaymah katika swahîh yake (1/54/2), Ahmad na Abu Shaykh katika Târîkh Isbahân (Uk. 125); at-Tirmidhî akaithibitisha mojawapo ya isnâd zake kuwa hasan, na maana yake yapatikana katika Al-Muwatta‘ na Swahîh al-Bukhâri ikiwa itazingatiwa kwa hadhari. Nimezinukuu isnâd za hadîth hii kikamilifu katika kitabu changu Ahkâm al-Janâ‘iz (Uk. 118). TANBÎH: Kuiweka juu ya kifua ndilo jambo lililothibitishwa katika Sunnah, na chochote kinyume chake ni imma dha‘îf au kisichokuwa na msingi wowote. Kwa hakika, Imâm Is-hâq ibn Râhawaih aliitekeleza Sunnah hii, kama alivyosema Marwazî katika Masâ‘il (Uk. 222): ―Is-hâq alikuwa akiswali witr na sisi ... alikuwa akiinua mikono yake katika

19

Pia ―alikuwa akikataza mtu asiweke mikono yake katika kiuno chake akiwa katika swala [akaweka mkono wake juu ya kiuno chake (kuonyesha)]‖1. Na huo ndio ―mfupa‖ aliokuwa akiukataza kuushika.2

KUTIZAMA MAHALI PA KUSUJUDU NA UNYENYEKEVU

Na ―alipokuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akiswali huinamisha kichwa

chake na huangalia kwa macho yake kuielekea ardhi‖3 - ―alipoingia ndani ya Al-Ka‘bah macho yake hayakuacha kuangalia anaposujudu mpaka akatoka nje yake‖4; na akasema:

«لاص يظل يشء ابلخ ف يسن أن ينجغ ل »

qunût, na akifanya qunût kabla ya kuruku‘‘, na alikuwa akiweka mikono yake juu ya kifua au chini kidogo ya kifua.‖ Vilevile ndio kauli ya Qâdhi ‗Iyâdh al-MÂLIKi katika Mustahabbât as-Salaah kwenye kitabu chake al-I‘laam (Uk. 15, Chapa ya tatu, Rabat): ―Mkono wa kulia na uwekwe kwenye mgongo wa mkono wa kushoto, katika sehemu ya juu ya kifua.‖ Yenye mkuruba na haya ni aliyosimulia ‗Abdullaah ibn Ahmad ibn Hanbal katika Masâ‘il (Uk. 62): ―Niliona yakwamba tunaposwali, babangu aliiweka mikono yake, mmoja juu ya mwengine, juu ya kitovu.‖ Tizama Kiambatisho 4. 1 Bukhâri na Muslim. Imetolewa katika Irwâ‘ (374) na vilevile hiyo ifuatayo. 2 Abu Dâwud, an-Nasâ‘î na wengineo. 3 Al-Baihaqî na Hâkim, aliyeithibitisha kuwa swahîh na ni kama alivyosema. Vilevile ilikuwa na hadîth yenye kuipa nguvu, iliyopokewa na wenzake kumi: yamesimuliwa na Ibn ‗Asâkir (17/202/2). Tizama Irwâ‘ (354). TANBÎH: Ahâdîth hizi mbili zaonyesha yakwamba sunnah ni kuelekeza macho yake mahali pa kusujudu kwake katika ardhi, kwa hivyo kitendo cha baadhi ya wenye kuswali kufunga macho yao wakati wanaposwali ni kujilinda kusiko takikana, kwani uongofu ulio bora ni uongofu wa

Muhammad (صىل اهلل عليه وسلم). 4 Ibid.

20

―Haitakikani kuwa katika nyumba kitu kinachomshughulisha mwenye kuswali.‖1

―Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alikuwa akikataza kuinua macho juu

mbinguni‖2, na alikuwa akisisitiza kukataza mpaka akasema: Naapa kwamba watakoma watu wanaoinua macho yao juu mbinguni katika swala au hayatawarudia macho yao na katika riwaya nyengine, au yataporwa macho yao.3 Katika hadîth nyengine: Mukiswali musizungushe nyuso, kwani Allâh‎ huuelekeza Uso wake kwenye Uso wa mja wake aliye kwenye swala mâdamu haugeuzi uso wake‖4, na pia alisema kuhusu kuzungusha uso: ―ni kupora anakompora Shetani mja pindi anaposwali‖.5

Na amesema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم): Hatâcha kuwa Allâh‎ (سبحانه وتعاىل) ni mwenye kumuelekea mja wake akiwa katika swala yake muda wa kuwa hatazungusha uso wake, akizungusha uso wake yule mja, Allâh‎ nae huugeuza Uso wake;6 na ―akatukataza mambo matatu: kudona kama kudona kwa Jogoo, na kikao (Iq‟â‟) kama kikao cha mbwa na kuzunguka kama kuzunguka kwa mbweha.‖7.

Pia Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alikuwa akisema:

« يراك نإ دراه ل خ نإن دراه أ مدع صالة ص» 1 Abu Dâwud na Ahmad kwa isnâd iliyo swahîh (Irwâ‘, 1771); Lililokusudiwa hapa na ―nyumba‖ ni Ka‘bah, kama ilivyo onyesha muktadha (context) ya hadîth hii. 2 Bukhâri na Abu Dâwud 3 Bukhâri, Muslim na Sirâj 4 Tirmidhî na Hâkim, aliyeithibitisha kuwa ni swahîh, Tizama Swahîh at-Targhîb (No. 353) 5 Bukhâri na Abu Dâwud 6 Imepokewa na Abu Dâwud na wengineo. Ibn Khuzaymah na Ibn Hibbân wameithibitisha kuwa ni swahîh. Angalia katika Swahîh at-Targhîb (555) 7 Ahmad na Abu Ya‘laa. Angalia Swahîh at-Targhîb (556)

21

―Swali swala ya mwenye kuaga kana kwamba unamuona Allâh‎, ukiwa humuoni, hakika Yeye anakuona."1

Na akasema: Hakuna mtu yoyote ambaye anafikiwa na Swala ya Faradhi, halafu akaufanya uzuri wudhu‘ wake, na unyenyekevu wake ukawa kamili, na Ku-rukû‘ kwake kukawa kamili, isipokuwa (swala ile) inakuwa ni yenye kufuta madhambi yaliyo kabla yake, mâdamu hakufanya madhambi makubwa, na hilo ni mwaka mzima.2

Siku moja Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) aliswali na Khamîsah3 na (wakati

alipokuwa kwenye swala) akângalia ile michoro yake. Basi alipomaliza, akasema: ipelekeni nguo hii kwa Abu Jahm na muniletî (anbijâniyyah)4 nguo nyengine ya Abu Jahm, kwani nguo hiyo yenye michoro imenishughulisha kwenye swala yangu hivi punde (katika riwaya nyengine: ... kwani nimeiangalia michoro yake nilipokuwa ndani ya swala na imekurubia kunifitini .5)

Na ilikuwa kwa Bibi ‗Âishah, nguo yenye mapicha iliyotandazwa hadi kwenye sahwah6, ambapo ndipo alipokuwa akielekea Mtume

anaposwali, akamwambia: Niondolee (kwani (صىل اهلل عليه وسلم)

mapicha yake yanaendelea kunipinga mimi katika swala yangu).7

1 Mukhlis katika Ahâdîth Muntaqâh, at-Twabarâni, Rûyaani, Diyâ‘ katika al-Mukhtârah. Ibn Mâjah, Ahmad na Ibn ‗Asâkir. Akaithibitisha Haithami kuwa ni swahîh katika Asnâ al-Matâlib 2 Muslim 3 Nguo ya sufi yenye michoro. 4 Nguo hafifu isiyo na michoro. 5 Bukhâri, Muslim, na Mâlik. Inapatikana katika Irwâ‘ (376) 6 ―chumba kidogo kilichozama kiyasi kidogo chini ya ardhi, kama mfano wa nafasi ndogo au sanduku‖ (Nihâyah). 7 Bukhâri, Muslim, na Abu ‗Awânah. Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) hakuamrisha

kuharibiwa au kuraruliwa kwa picha hizo lakini aliamuru ziondoshwe tu kwa sababu – na Allaah yanamueleya zaidi – hizo hazikuwa ni picha

22

Pia alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akisema: ―Hakuna swala wakati

chakula kinapoandaliwa, wala wakati mtu akiwa ameshikwa sana na haja ya mikojo au choo.‖1

DUA‟ ZA KUANZA SWALA:

Kisha alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akianza kusoma kwa Dua‘

nyingi mbalimbali ambapo humuhimidi Allâh‎ katika dua‘ hizo, na anamtukuza Allâh‎, na anamsifu. Na amemuamrisha ―mwenye kuharibu swala yake‖ afanye hivyo, kwa kumwambia: ―Haitimii swala ya mtu yoyote mpaka aseme ‗Allâh‎u Akbar‘, na amuhimidi Allâh‎ Mtukufu, na amsifu, na asome kinachosahilika katika Qur‘ân ...‖2

Alikuwa akisoma mojawapo ya Dua‘ zifuatazo:-

1.

والرب اشق ثي ثةـدت ة خػةيةي وبي ثين ثةـد ال » ال النس الثض اثلب يىق ة خػةيةي ين ال

« واربد واثلش ثةةء خػةيةي اكصن

―Ewe Allâh‎! Niweke mbali mimi na madhambi yangu kama ulivyoweka mbali baina ya Mashariki na Magharibi. Ewe Allâh‎! Nitakase na madhambi yangu kama vile inavyotakaswa nguo

zenye roho. Ushahidi wa hayo ni kwamba yeye, ( وسلم عليه اهلل صىل ) alizirarua

baadhi ya picha nyengine kama ilivyothibitishwa na riwaya nyingi katika Bukhâri na Muslim, na yoyote mwenye kutaka kuyafuatilia zaidi mas‘ala haya na ayatafute kwenye Fat-h al-Bâry (10/321) na Ghâyah al-Marâm fî Takhrîj Ahâdîth al-Halaal wal-Harâm.(Nambari 131-145). 1 Bukhâri na Muslim 2 Bukhâri, Muslim na Ibn Abî Shaybah (12/110/2). Inapatikana katika Irwâ‘ (No.8)

23

nyeupe na uchafu. Ewe Allâh‎! Nisafishe na madhambi yangu kwa maji na barafu na theluji.‖

Alikuwa akisoma dua‘ hii wakati wa swala ya faradhi.1

2.

وة [مصة ]لرض ظهة وا الصةوات نػر للي وصيه وصخ »أة اشكي إن صالت ونصيك ومةي وةت لل رب افةي ل شي ل وبذل أمرت وأة أول اصي ال أخ ا ل إل

أخ ريب وأة ـجدك ؽخ هيس [شجعة وبعدك ]إل أخ لهر الب إل أخ واـتنخ ثذيب نةكهر ل ذيب مجفة إ ل ي

وادين لظص الخالق ل يدي لظصة إل أخ وارصف ـن شيبة ل يرصف ـن شيبة إل أخ بل وشفدي واخلري لك ف

ل ] وإحل ث أة [ ديخ وادي ]يدي والش يس إحل وأدب أشذلهرك ودفةحلخ دجةركخ [ إحل إل مضأ ول ضة

« إحل

―Nimeuelekeza uso wangu kwa yule ambae ameumba Mbingu na ardhi hali ya kumtakasia yeye dini yangu, na sikuwa mimi katika

washirikina, hakika swala yangu na kuchinja kwangu na uhai wangu, na kufa kwangu ni kwa Allâh‎, Bwana wa viumbe vyote,

1 Abu Dâwud na Hâkim, aliyeithibitisha kuwa swahîh na kuafikiwa na adh-Dhahabi.

24

hana mshirika, na kwa hilo nimeamrishwa. Nami ni wa kwanza katika Waislamu (wenye kujisalimisha Kwake) 1, Ewe Allâh‎ wewe

ndiye mfalme, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila wewe, wewe ndiye Bwana wangu na mimi ni mtumwa (mja)

wako2, nimeidhulumu nafsi yangu, na nimekiri madhambi yangu kwa hivyo nisamehe madhambi yangu yote, hakika hasamehe

madhambi, ila Wewe. Na niongoze kwenye tabia njema (nzuri), kwani haongozi kwenye tabia nzuri, ila Wewe, niepushe na tabia mbaya, kwani hakuna mwenye uwezo wa kuniepusha na tabia mbaya ila Wewe, naitikia mwito wako, nina furaha kukuitikia3,

1 Hivyo ndivyo ipatikanavyo katika riwaya nyingi; katika baadhi ya riwaya, ni ―...wa ana min al-muslimîn.‖ (―Nami ni katika Waislamu‖). Inaonekana kama kwamba hii ni kwa sababu ya makosa ya mmojawapo wa wapokezi, na ushahidi mwengine unagusia nukta hiyo, kwa hivyo mwenye kuswali na aseme: ―...wa ana awwal-ul-muslimîn.‖ (―Nami ni wa kwanza katika Waislamu‖). Hapana makosa kwa hilo, kinyume na baadhi ya watu wasemao kwa kuleta maana yakwamba hii inamânisha ―Mimi ni mtu wa kwanza mwenye sifa hii, haliyakuwa watu wengine waliobaki hawana sifa hiyo.‖ Lakini sivyo hivyo; kwa hakika, maneno haya yanamânisha kushindana katika kutekeleza mâmrisho – mfano wake ni:

ل إن كن لرذنمح ول ى وذة أ ٱنأ ٨١ عجدي

“Sema: “(Allaah) Mwingi wa rehema angalikuwa na mtoto ningekuwa wa kwanza wa kumuabudu (mtoto huyo kwa kuwa

ni mtoto wa Mungu wangu).” [Zukhruf 43:81]

... na alivyosema Musa (السالم عليه) :

ل وذة أؤي ٱوأ ١٤٣ ل

“... na mimi ni wa kwanza wa wanaoamini.” [al A‘râf 7:143]

2 Azhari amesema: yaani, ‗Mimi siabudu chochote kisichokuwa Wewe.‘ 3 Labbaik: mimi niko imara, na nitaendelea kuwa chini ya twa‘a yako; sa‘daik: nafurahikiya kujisalimisha chini ya amri zako na kuwa mnyenyekevu katika kuifuata Dini uliyoichagua Wewe.

25

na kheri zote ziko mikononi mwako, na shari haitoki kwako1, mimi nimepatikana kwa ajili yako, na nitarudi kwako,

umetakasika na umetukuka, nakutaka msamaha na ninarejea kwako (kwa kutubia).‖

Alikuwa akisoma dua‘ hii wakati wa swala ya faradhi na Sunnah.2

3. Dua‘h inayofanana na hiyo iliyotangulia, lakini bila ya maneno

«أخ ريب وأة ـجدك »Wewe ndiye Bwana wangu na mimi ni mtumwa (mja) wako ...

mpaka mwisho wake, na nyongeza ifuatayo:

1 Yaani: shari haiwezi kusifiwa nayo Allaah kwa sababu hakuna kitu kibaya katika vitendo Vyake, kwani vyote ni vizuri, kuanzia Uadilifu hadi Rehma mpaka Hikma, yote hayo ambayo ni mazuri yasiyokuwa na ubaya wowote. Lakini shari ni shari kwa sababu haiwezi kusifiwa nayo

Allaah. Ibn al-Qayyim (اهلل رحمه) amesema: ―Yeye ndiye Muumba wa kheri

na shari, lakini shari inapatikana kwa baadhi ya viumbe vyake, na sio katika tendo lake la Uumbaji wala katika vitendo Vyake. Kwa hivyo, Allaah ameepukana na dhulma za aina yoyote, ambazo kimsingi ni kuweka kitu mahali pasipostahiki. Yeye haweki chochote, isipokuwa katika mahali panapostahiki, kwa hivyo hayo yote ni mazuri.. Lakini shari ni kuweka kitu mahali pasipostahiki: kikiwekwa mahali panapostahiki, basi si shari hiyo, kwa hivyo hakikisha yakwamba shari haitokani na Yeye …, lakini ikisemwa: Ni kwanini basi ameumba kitu kibaya? Mimi nitasema: Aliumba, na kitendo chake hicho ni kizuri wala si kibaya, kwani kuumba na kutenda yanatokamana na Allaah, na haiwezekani ubaya kutokamana na Allaah, au Allaah kusifiwa kwa sifa hiyo, kwa hivyo hizo ni sifa nzuri.‖ Mazungumzo mengine kama haya muhimu pamoja na hatima yake yanapatikana katika kitabu chake Shifâ‘ al-‗Alîl fî Masâ‘il al-Qadhâ‘ wal-Qadr wat-Ta‘lîl (Uk. 178-206). 2 Muslim, Abu ‗Awânah, Abu Dâwud, an-Nasâ‘î, ibn Hibbân, Ahmad, ash-Shâfi‘î na at-Twabarâni; wale ambao walioiorodhesha kwenye swala za Sunnah wamekosea.

26

«ا ل إل إل أخ شجعة وبعدك ال أخ »―Ewe Allâh‎! Wewe ndiye Mfalme, hapana mola (anaestahiki kuabudiwa kwa haki) isipokuwa Wewe, kutakasika ni kwako

na kila Sifa njema ni zako.‖1

4. Dua‘ inayofanana na No.2 mpaka ufike...

«اصي أول وأة»―…nami ni wa kwanza katika Waislamu, kisha uzidishe...‖

ةل وأظص الخالق لظص ادين ال» لظصة - يدي ل اـلةل الخالق شئ وىن أخ إل « أخ إل شيبة يىق ل واـل

―Ewe Allâh‎! niongoze kwenye tabia njema (nzuri) na matendo mema, kwani haongozi katika chochote ila Wewe, niepushe na tabia mbaya na matendo mabaya, kwani hakuna

mwenye uwezo wa kuniepusha na chochote kibaya ila Wewe.‖2

5.

« كريك إل ول صدك ودفةل اش ودجةرك وبعدك ال شجعة»―Kutakasika ni kwako3, Ewe Allâh‎, na sifa njema zote ni zako4; na limetukuka Jina lako5; na Utukufu ni wako6, na hapana

anaestahiki kuabudiwa kwa haki asiekuwa Wewe‖1.

1 An-Nasâ‘î kwa isnâd iliyo swahîh. 2 An-Nasâ‘î na Dâraqutnî‘ kwa isnâd iliyo swahîh. 3 Yaani: Mimi nakutukuza Wewe, kwa maana yakwamba mimi nakutambua Wewe kuwa Umîpukana kabisa na kila aina ya upungufu. 4 Yaani: Sisi tunapomoka hali ya kukusifu 5 Yaani: Baraka za Jina lako ni Tukufu mno, kwani kheri nyingi zinapatikana kutokana na Utajo wa jina lako 6 Utukufu na Uwezo wako.

27

Pia Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)amesema:

« . . . ال شجعة : افجد ييل -إن أظت الالكم إل الل أن »―Kwa hakika, maneno yenye kupendeza zaidi kwa Allâh‎ ni yale anayoyasema mja wake: Kutakasika ni kwako, Ewe Allâh‎ ..‖2.

6. Kama iliyotangulia hapo juu, na kuzidisha katika swala ya usiku:

«ل إل إل الل »

―Hapana mola anaepasa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allâh‎‖, mara tatu, na

«الل أرب جريا »―Allâh‎ ni Mkubwa, tena sana‖, mara tatu.

7.

«الل أرب جريا والد لل سريا وشجعةن الل ثسرة وأصال »―Allâh‎ ni mkubwa, tena sana, na kila sifa njema ni za Allâh‎, kwa

wingi, na Ametakasika Allâh‎, asubuhi na jioni‖.

1 Abu Dâwud na Hâkim, aliyeithibitisha kuwa swahîh na kuafikiwa na adh-Dhahabi. ‗Uqaili amesema (Uk. 103): ―haya yamepokewa kwa kupitia njia nyingi kwa isnâd nzuri.‖ Inapatikana katika Irwâ‘ (No. 341) Yamepokewa na Ibn Mandah katika at-Tawhîd (123/2) kwa isnâd iliyo swahîh na an-Nasâ‘î katika al-Yawm wal-Laylah kama mawqûf na marfû‘, kama ilivyo katika Jâmi‘ al-Masânîd cha Ibn Kathîr (Vol. 3; sehemu ya 2; Uk. 235/2) 2 Abu Dâwud na Tahâwi kwa isnâd iliyo hasan

28

Mmoja miongoni mwa Maswahaba alianzia kwa Dua‘ hii, na

alipoisikiya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akasema: ―Nimeishangaa (Dua‘

hii) na sababu ni kwamba milango ya Mbingu imefunguliwa kwa ajili yake.1

8.

« الد لل محدا سريا غجة جةرك ن »―Kila Sifa njema ni za Allâh‎, Sifa zilizo nyingi, nzuri na zenye

Baraka.‖

Swahaba mwengine alianza kwa Dua‘ hii, na alipoisikiya Mtume

akasema: ―Nimewaona Malaika kumi na mbili (صىل اهلل عليه وسلم)

wakiinyangarikiya, yupi miongoni mwao atakaepanda nayo juu kwa haraka.2

9.

الد ول ن و الرضو الصةوات ر أخ الد ل ال»ول الد أخ م ]خ ى الصةوات والرض و ن أ

دك الو [الصةوات والرض و ن ول الد أخ الو وـووىل ظو ويةؤك ظو والح ظو واجلةر ظو والصةـح ظو دكخ وب واجلبن ظو ومد ظو ال ل أشخ ـو

1 Muslim na Abu ‗Awânah; imethibitishwa uswahîh wake na at-Tirmidhî. Vilevile imepokewa na Abu Nu‘aim katika Akhbâr Isbahân (1/210)

kutoka kwa Jubair ibn Mut‘am aliyemsikiya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

akiisoma katika swala ya Sunnah. 2 Muslim na Abu ‗Awânah.

29

خ وإحل أجخ و أخ ربة وإحل ]ب خةصخ وإحل ظةخ آ ] [اصري نةكهر ل ة ىدخ وة أخرت وة أرسرت وة أـخ

ل [ إيه أخ ] اؤخر وأخ ايدم أخ [ ن ث أـ أخ وةة ول ظل ول ] أخ إل إل «[ ث إل ى

―Ewe Allâh‎, ni Zako Sifa njema. Wewe ndiye Nuru1 ya Mbingu na Ardhi na vilivyomo ndani yake; na ni Zako Sifa njema;

Wewe ndiye Muendeshaji2 wa Mbingu na Ardhi na vilivyomo ndani yake; [ni Zako Sifa njema; Wewe ndiye Mfalme wa Mbingu na Ardhi na vilivyomo ndani yake]; na ni Zako Sifa

njema Wewe ndiye Haqq3, na Ahadi yako ni haqq, na Maneno Yako ni haqq, na Kukutana na Wewe ni haqq, na Pepo ni haqq, na Moto ni haqq, na Qiyâmah ni haqq, na Mitume ni

haqq, na Muhammad (صىل اهلل عليه وسلم) ni haqq. Ewe Allâh‎, kwako

nimejisalimisha, na kwako nimetegemea, na Wewe nimekuamini, na kwako nimeregea. Kwa ajili yako nimeteta, na kwako nimehukumu,[Wewe ni Mola wetu, na marejeo ni

kwako, kwa hivyo nisamehe niliyoyatanguliza, na niliyoyachelewesha, na niliyoyaficha na niliyoyatangaza]. [ Na Wewe unayajua hayo kuliko mimi]. Wewe ndiye mwenye kutanguliza na Wewe ndiye mwenye kuchelewesha, [Wewe

ndiye Mola wangu], hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe4; [Hapana uwezo wala nguvu ila za Allâh‎].‖

1 Wewe ndiye Mwenye kuwapa Muangaza, na Wewe ndiye ulowaongoza wale walio kwenye Nuru hiyo. 2 Mlinzi na Muangalizi wa kudumu. 3 Haqq: Haki, ukweli 4 Bukhâri, Muslim, Abu ‗Awânah, Abu Dâwud, ibn Nasr na ad-Dârimi.

30

Alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akisoma hii akiswali katika

nyakati za usiku, kama alivyokuwa akisoma Dua‘ hiyo ifuatayo1:

10.

اعل والرض الصةوات نةغر وإرسان وكا صرباا رب ال»ا نة ـجةدك ثي تس أخ والظةدة الت ادين خيذهن ن ك

و ثإذ إ ددي تظةء إل رصاط مصذي ال ن اخذم ة»

―Ewe Allâh‎, Mola wa Jibrâ‘îl na Mîkâ‘îl na Isrâfîl, Muumba wa Mbingu na Ardhi, Mjuzi wa mambo yaliyojificha na yaliyo wazi! Wewe unahukumu baina ya waja wako katika mambo ambayo

walikuwa wakitafautiana, niongoze mimi kwenye haki katika yale waliyotafautiana kwa ruhusa yako, hakika Wewe unamuongoza

umtakae kwenye njia iliyonyoka.‖2

11. Alikuwa akisema ―Takbîr, tahmîd, tasbîh, tahlîl na istighfâr‖, mara kumi kila moja, kisha husema:

« [واعنن ]وادين وارزىن ال اكهر ل »―Ewe Allâh‎, nisamehe na uniongoze, na uniruzuku [na unipe afya

njema].‖

م الصةب » ـشا « ال إين أـذ ث الظو ي

1 Hata kama hiyo waziwazi haikatazi kusomwa katika swala za faradhi, (yaani inaruhusiwa), isipokuwa kwa Imâm tu, asije akawarefushia swala wenye kumfuata. 2 Muslim na Abu ‗Awânah

31

―Ewe Allâh‎, najilinda kwako na dhiki katika siku ya hisabu (mara kumi).‖1

12.

«فؾح وا والربيةء والربوت تا ذو [ زالزة ] أرب الل »―Allâh‎ ni Mkubwa (mara tatu), Mwenye Utawala, na Ufalme, na

Ukubwa, na Utukufu.‖2

KUSOMA:

Kisha Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alikuwa akitaka hifadha kwa Allâh‎

:kwa kusema (سبحانه وتعالى)

«زه وهخ وهس الرص الظػةن للثة أـذ»―Najilinda kwa Allâh‎ na Shetani mwenye kuwekwa mbali na rehma, kutokana na wazimu3 wake na kibri chake na ushairi4

wake‖. Na mara nyengine alikuwa akizidisha kwa kusema:

« . . .أـذ ثةلل الصؿ اف الظػةن »

1 Ahmad, ibn Abî Shaybah (12/119/2), Abu Dâwud na at-Twabarâni katika Mu‘jam al-Awsat (62/2) kwa isnâd moja iliyo swahîh na nyengine iliyo hasan 2 Tayâlisi na Abu Dâwud, kwa isnâd iliyo swahîh. 3 Maneno matatu ya Kiarabu, hamz, nafkh, na nafth, yamefasiriwa hivyo na mpokezi; na tafsiri zote hizo zimehifadhiwa kutoka kwa Mtume

Muhammad ( اهلل عليه وسلمصىل ) kwa isnâd swahîh iliyo Mursal. Maana ya

―Ushairi‖ wake hapa ni ule Ushairi usiofâ, kwani Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

amesema: ―Hakika baadhi ya Mashairi ni Hikma‖ (Bukhâri). 4 Abu Dâwud, Ibn Mâjah, Dâraqutni na Hâkim ambae, pamoja na ibn Hibbân na adh-Dhahabi, wameithibitisha kuwa ni swahîh. Inapatikana pamoja na ifuatayo katika Irwâ‘ al-Ghalîl (342).

32

―Najilinda kwa Allâh‎, Mwenye kusikiya, aliye Mjuzi na Shetani ...‖1

Kisha anaisoma:

ٱ مسب ٱ لرذنمحٱ للذ ١ لرذظ ―Kwa Jina la Allâh‎, Mwingi wa Rehma, Mwenye kurehemu.‖

Wala haisomi kwa sauti ya juu.2

KUSOMA AYA MOJA BAADA YA NYENGINE:

Kisha alikuwa akisoma Sûrah al-Fâtihah na kukigawa kisomo chake, kwa kusoma aya moja. Alikuwa akisema:

ٱ مسب ٱ لرذنمحٱ للذ ١ لرذظ [Hapa anatulia kidogo, kisha anaendelea kusoma:]

د ل ٱ رب ي ٱللذ ٢ ع [Kisha atatulia kidogo, halafu aendelî kusoma:]

ٱ لرذنمحٱ ٣ لرذظ [Kisha atatulia kidogo, halafu aendelee kusoma:]

م ي ٱم ٤ لي

1 Abu Dâwud na at-Tirmidhî kwa isnâd iliyo hasan. Ahmad akaiidhinisha katika (Masâ‘il ya Ibn Hâni 1/50). 2 Bukhâri, Muslim, Abu ‗Awânah, at-Twahâwi na Ahmad.

33

… na kama hivyo mpaka mwisho wa Sûrah. Kisomo chake kilichobaki pia kilikuwa namna hiyo: anasimama mwisho wa aya,

wala hakuwa akiziunganisha aya na zilizo baada yake.1

Mara nyengine alikuwa akisoma:

م ي ٱم ٤ لي(Mfalme wa Siku ya Malipo) badala ya:

م ي ٱم ٤ لي (Mwenye kumiliki Siku ya Malipo).2

NGUZO YA FÂTIHAH NA FADHLA ZA SÛRAH AL-FÂTIHAH

Na alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)akiadhimisha jambo la Sûrah al-

Fâtihah, na alikuwa akisema:

1 Abu Dâwud na Sahmi (64-65); Hâkim aliithibitisha kuwa swahîh na akâfikiwa na adh-Dhahabi. Inapatikana katika Irwâ‘ (343). Abu ‗Amr ad-Dâni aliisimulia katika al-Muktafâ (5/2) , na akasema: ―Hadîth hii ina njia nyingi, na ndiyo yenye kutegemewa katika mas‘ala haya, na ma-Imâm wengi waliotangulia na wasomi wa Qur‘an wanapendelea kusimama (kutulia kidogo) katika kila aya, hata kama baadhi yake zilikuwa zimeshikana (katika maana) na inayofuata.‖ Mimi nasema: Hii ni Sunnah ambayo wasomaji wengi wa Qur‘an wameiacha katika zama zetu hizi, licha ya wasiokuwa wasomi wa Qur‘an. 2 Tammâm ar-Râzi katika al-Fawâ‘id, Ibn Abî Dâwud katika al-Masâhif (7/2), Abu Nu‘aim katika Akhbâr Isbahân (1/104) na Hâkim aliyeithibitisha kuwa swahîh na akâfikiwa na adh-Dhahabi. Visomo vyote hivi ni mutawâtir.

34

« [ نصةـدا ] لذةبا ثهةتح [ نة ] ييرأ ل صالة ل »―Hakuna swala kwa asiyeisoma (akiwa kwenye swala) Sûrah ya

al-Fâtihah (kwa uchache).‖1

na katika hadîth nyengine:

« الذةب ثهةتح نة الرص ييرأ ل صالة تزئ ل »"Haitoshelezi swala ambayo mtu hakusoma ndani yake Sûrah al-

Fâtihah."2

Na mara nyengine alikuwa akisema:

يه خداج يه خداج نيه الذةب ثهةتح نة ييرأ ل صالة صل » « دةم كري خداج

―Mwenye kuswali swala, na asisome ndani yake sûrat al-Fâtihah, basi swala hiyo ni pungufu, swala hiyo ni pungufu, swala hiyo ni

pungufu, haikukamilika.‖3

Pia alikuwa akisema:

وبي ثين - اهةتح يفن - الصالة ىصخ :ىةل الل دجةرك ودفةل » « شأل ة وفجدي فجدي وصهة ل نصهة : صهي ـجدي

1 Bukhâri, Muslim, Abu ‗Awânah na al-Baihaqî. Inapatikana katika Irwâ‘ (302) 2 Dâraqutnî‘, aliyeithibitisha kuwa swahîh, na ibn Hibbân katika swahîh yake. Vilevile inapatikana katika Irwâ‘ (302) 3 Muslim na Abu ‗Awânah

35

Aemsema Allâh‎ Aliyetukuka: ―Nimeigawanya swala1 – Yaani Sûrah al-Fâtihah - baina yangu na baina ya mja wangu, nusu mbili.

Nusu moja ni yangu na nusu nyengine ni ya mja wangu. Na ana mja wangu lolote aliloliomba.‖

Kisha akasema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم): ―Soma:

Mja anaposema:

د ٱ رب ل ي ٱللذ ٢ ع

Allâh‎ ( وتعاىل سبحانه ) Anasema: ―Amenihimidi mja wangu‖

na mja anaposema;

ٱ لرذنمحٱ ٣ لرذظ

Allâh‎ (سبحانه وتعاىل) Anasema: ―Amenisifu mja wangu‖

na mja anaposema;

م ي ٱم ٤ لي

Allâh‎ (سبحانه وتعاىل) Anasema: ―Amenisifu mja wangu‖

Na mja anaposema;

٥نصذفي جفجد إويذةك إيذةك

1 Yaani: Sûrah al-Fâtihah; huu ni mfano wa jina katika kuihusu swala yote, lakini ikawa inakusudiwa sehemu tu, kama njia ya kutilia mkazo kwenye sehemu hiyo.

36

Allâh‎ (سبحانه وتعاىل) Anasema: Hii ni baina yangu Mimi na mja wangu,

na ana mja wangu analoliomba; Na mja anaposema;

دةٱ رط ٱ ٱ لص صذي ٱ صرط ٦ ل ي دري لذ ـ خ جف

لظب ٱأ ل

ول اٱـ ٧ ي لظذ

Allâh‎ (سبحانه وتعاىل) Anasema: "Haya yote ni ya mja wangu na ana

mja wangu analoliomba.‖1

Kisha Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alikuwa akisema:

ة أزل الل ـز وص ف اتلراة ول ف الجن س أم ايرآن ويه » « [ أوديذ الي افؾ وايرآين ]الصجؿ اسةين

―Hakuteremsha Allâh‎ ( وجل عز ), katika Taurât wala katika InJîl

mfano wa Ummul-Qur‘ân. Nayo ni aya saba zinazorudiwa-rudiwa kila mara2 [na Qur‘ân Tukufu ambayo nimepewa].‖1

1 Muslim, Abu ‗Awânah na MÂLIK, na Sahmi ana hadîth yenye kutilia nguvu ya Jâbir katika Târîkh Jurjân (144) 2 Amesema Bâji: ―Anakusudia maneno yake Aliyetukuka:

ويد ة شجفا ج سةين ٱءات ٱ يرءان ٱو ل ٨٧ فؾ“Na tumekupa (hizi Aya) saba (Tukufu za Al-Fâtihah – za

Alhamdu) zisomwazo mara kwa mara, na (tumekupa) Qur‟an

(yote nzima hii) tukufu.” [Sûrah al-Hijr 15:87]

Imeitwa ―saba‖ kwa sababu ina Aya saba, na ni ―yenye kurudiwa-rudiwa‖ kwa sababu inarudiwa mara kwa mara katika swala. Imeitwa kwa jina la ―Qur‘an Tukufu‖ kwa ajili ya kulidhihirisha jina hili, ingawaje kila sehemu ya Qur‘an ni Tukufu, vilevile mfano wa Ka‘bah ni

37

Na Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) amemuamrisha yule ―mwenye kuharibu

swala yake‖ kuisoma sura hii katika swala yake, lakini akamwambia asiyeweza kuihifadhi Sûrah al-Fâtiha aseme:

ة إل » شجعةن الل والد لل ول إل إل الل والل أرب ول ظل ول ى « ثةلل

―Nakiri yakwamba Allâh‎ Ametakasika na kila aina ya upungufu, na kila Sifa njema ni za Allâh‎, na hapana mola apasae kuabudiwa

kwa haki ila Allâh‎, na Allâh‎ ni Mkubwa, na hapana hila wala nguvu isipokuwa kwa uwezo wa Allâh‎.‖2

Pia, Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) amesema kumwambia yule ―mwenye

kuharibu swala yake‖: ―Ikiwa unajua sehemu ya Qur‘ân isome, (na kama huna chochote ujuacho katika Qur‘ân), basi muhimidi Allâh‎ (sema: AlhamdulilLaah), ulete Takbîr (sema: Allâh‎u Akbar), na ulete Tahlîl (sema: Laa iLaaha illa-LLaah).3

KUFUTWA HUKMU YA KUSOMA NYUMA YA IMÂM KATIKA SWALA ZA KUDHIHIRISHA SAUTI

Na alikuwa amewajuzishia wenye kumfuata Imâm waisome Sûrah al-Fâtihah nyuma ya Imâm katika swala ambazo Imâm anazosoma kwa kudhihirisha sauti wakati fulani alipokuwa:

―nyumba ya Allaah‖ ingawaje nyumba zote ni zake Yeye Allaah; hii ni njia ya kuidhihirisha na kusisitiza umuhimu wake.‖ 1 An-Nasâ‘î na Hâkim, aliyeithibitisha kuwa swahîh na kuafikiwa na adh-Dhahabi. 2 Abu Dâwud, Ibn Khuzaymah (1/80/2), Hâkim, at-Twabarâni, na Ibn Hibbân, ambaye pamoja na Hâkim wameithibitisha kuwa swahîh, na kuafikiwa na adh-Dhahabi. Inapatikana katika Irwâ‘ (303). 3 Abu Dâwud na at-Tirmidhî, aliyeithibitisha kuwa hasan; isnâd yake ni swahîh. (Swahîh Abi Dâwud No. 807).

38

―akiswali swala ya Alfajiri, Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akawa anasoma,

mara ikawa uzito kwake kusoma. Alipomaliza swala akasema: Huwenda nyinyi munasoma nyuma ya Imâm wenu. Tukasema: ―Nâm, kwa haraka haraka1, Ewe Mtume wa Allâh‎.‖ Akasema: Musifanye hivyo, ila kwa (kila mmoja wenu na asome) Sûrah al-Fâtihah, kwani hakuna swala kwa asiyeisoma Sûrah al-Fâtihah.2

baada e, aliwakataza kabisa kusoma katika swala ambayo Imâm anasoma kwa kudhihirisha sauti, wakati...

―Alipomaliza kuswali katika swala aliyokuwa akisoma kwa kudhihirisha sauti (katika riwaya nyengine: ilikuwa ni swala ya Alfajiri) na akasema: Je kuna yoyote miongoni mwenu aliyekuwa akisoma pamoja na mimi hivi sasa?! Akasema mtu mmoja: ―Ndio, nilikuwa ni mimi, Ewe Mjumbe wa Allâh‎.‖ Akasema: (Ndio maana) nikasema mimi, kwanini mimi natatizika hivi? [Abu Hurairah akasema:] Kwa hivyo watu wakakoma kusoma pamoja

na Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) akiwa anasoma kwa kuidhihirisha sauti

yake baada ya kusikiya hayo kutoka kwake [lakini walikuwa wakijisomea wenyewe kwa kuficha sauti zao alipokuwa Imâm hadhihirishi sauti yake].‖3

Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) ameja‘alia kunyamaza kwa ajili ya kusikiliza

kisomo cha Imâm ni katika ukamilifu wa kumfuata Imâm , akasema:

1 Hadhdhan: kusoma upesi upesi, kumânisha mashindano au kuharakisha. 2 Bukhâri katika waraka wake, Abu Dâwud, Ahmad, at-Tirmidhî, na Dâraqutnî‘ akaithibitisha kuwa hasan 3 MÂLIK, Humaidi, Bukhâri katika waraka wake, Abu Dâwud na Mahâmali (6/139/1). At-Tirmidhî akaithibitisha kuwa hasan; Abu Hâtim ar-Râzi, Ibn Hibbân, na Ibn al-Qayyim akaithibitisha kuwa swahîh.

39

ا إة صف الةم حلؤد ث نإ» «ذا رب نربوا وإذا ىرأ نأصذ

―Hakika ameja‘aliwa Imâm Ili afuatwe, Kwa hivyo anapoitamka takbîr, Na nyinyi semeni takbîr, Na anaposoma (Imâm ), (nyinyi –

ma‘muma) nyamazeni.‖1

Kama ambavyo Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alivyoja‘alia kumsikiliza

Imâm kunatosheleza kisomo chake nyuma yake, akasema:

« كن ل إةم نيراءة الةم ل ىراءة »―Ambae ana Imâm basi kile kisomo cha Imâm ndio kisomo

chake‖2.

Hii ni katika swala ambayo Imâm anasoma kwa kudhihirisha sauti yake.

UWAJIBU WA KUSOMA KATIKA SWALA ZA KUTODHIHIRISHA SAUTI (SWALA ZA SIRI)

Ama katika swala ya siri, Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) amewatuza

maswahaba kusoma katika swala ile; Jâbir akasema, ―Tulikuwa tukisoma nyuma ya Imâm katika swala ya Dhuhr na ‗Asr: Sûrah

1 Ibn Abî Shaybah (1/97/1), Abu Dâwud, Muslim, Abu ‗Awânah na Ruwayaani katika musnad yake (24/119/1) Inapatikana katika Irwâ‘ (332, 394). 2 Ibn Abî Shaybah (1/97/1), Dâraqutnî‘, Ibn Mâjah, at-Twahâwi na Ahmad kwa kupitia njia nyingi, musnad na mursal. Shaykh-ul-Islaam ibn Taymiyyah ameithibitisha kuwa ni yenye nguvu, kama ilivyo kwenye al-Furû‘ cha ibn ‗Abdul Hâdi (48/2). Bûsayri amezithibitisha baadhi ya isnâd zake kuwa ni swahîh. Nimeieleza kwa upana zaidi na nikachunguza mapito ya riwaya zake katika nyaraka ambazo hazijachapishwa, na kisha katika Irwâ‘ al-Ghalîl (No. 500)

40

al-Fâtihah na Sûrah nyengine kwenye Rak‘âh mbili za mwanzo, na Sûrah al-Fâtihah kwenye Rak‘âh mbili za mwisho.‖1

Hata hivyo, Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) amewakataza wasimshawishi

kwa kusoma kwao, siku moja... ―aliposwali Dhuhr na maswahaba zake, kisha akasema (baada ya kumaliza): Nnani katika nyinyi aliyekuwa akisoma:

ٱشجط ش ع ٱرب ١ ل

―Litukuze Jina la Mola wako aliye Mtukufu.‖ [Sûrah al-A‘Laa]?

Mtu mmoja akasema: Nilikuwa ni mimi [lakini sikukusudia chochote isipokuwa kheri kwa kufanya hivyo]. Basi akasema: Nilikuwa najua tu yakwamba kuna mtu ananitatiza2. Katika

hadîth nyengine: ―Walikuwa wakisoma nyuma ya Mtume ( اهلل صىلوسلم عليه ) [kwa kudhihirisha sauti zao], kwa hivyo akasema:

Mumenitatiza (katika kisomo changu cha) Qur‘ân.3

Pia Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alisema: ―Hakika mwenye kuswali

anazungumza na Mola wake, kwa hivyo mtu na ângalie vile anavyozungumza na Bwana wake, wala wasidhihirishe baadhi yenu (kupâza sauti zao) juu ya baadhi nyengine kwa Qur‘ân‖4.

1 Ibn Mâjah kwa isnâd iliyo swahîh. Inapatikana katika Irwâ‘ (506) 2 Muslim, Abu ‗Awânah, na Sirâj 3 Bukhâri katika waraka wake, Ahmad na Sirâj kwa isnâd iliyo hasan 4 Mâlik na Bukhâri katika Af‘âl al-‗Ibâd kwa isnâd iliyo swahîh. TANBÎH! Rai hii ya kuruhusiwa kusoma nyuma ya Imâm katika swala za ‗Siri‘ na wala sio swala za ‗Sauti‘ ilikuwa mwanzoni ni rai ya Imâm Ash-Shâfi‘î, na pia ni rai ya Muhammad, mwanafunzi wa Abu Hanîfah katika riwaya yake iliyopendekezwa na Sheikh ‗Ali al-Qâri, na ma-Shekhe wengine wa madh-hab; pia ulikuwa ndiwo msimamo wa,

41

Na Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alikuwa vilevile akisema:

ىرأ ظرنة ذةب الل ن ث ظصح والصح ثفش أسةة ل » ( ) و ظرف ( لم ) و ظرف ( أم ) وس ظرف ال :أىل

« ظرف

―Mwenye kusoma herufi moja tu katika Kitâb cha Allâh‎, ana yeye kwa herufi hiyo, jema moja. Na jema moja linalipwa kwa mema

kumi mfano wake. Sisemi kwamba mtu akisoma ―Alif- Laam- mîm‖ ni jema moja, lakini ‗Alif‘ ni herufi (moja); ‗Laam‘ ni

herufi (nyengine); na ‗Mîm‘ ni herufi (nyengine).‖1

KUITIKIA IMÂM “ÂMÎN” KAMA WANAVYOITIKIA MA‟MÛM KWA SAUTI

Alipokuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akimaliza kusoma al-Fâtihah,

alikuwa akisema:

ي » «آ―Âmîn‖ (Anasoma kwa nguvu na anainua sauti yake).2

miongoni mwao, Imâm az-Zuhri, MÂLIK, Ibn al-Mubârak, Ahmad ibn Hanbal, muhaddithîn wengi, na vilevile ni katika mapendekezo ya Sheikh ul-Islaam Ibn Taymiyyah 1 At-Tirmidhî, Ibn Mâjah kwa isnâd iliyo swahîh. Imepokewa pia na Âjur-rî katika Âdâb Haml al-Qur‘an. Ama kuhusu hadîth isemayo: ―Mwenye kusoma nyuma ya Imâm, mdomo wake hujazwa moto‖, hiyo ni hadîth ya Urongo (mawdhû‘) na haya yamechambuliwa katika Silsilat al-Ahâdîth adh-Dha‘îfah (no. 569) – angalia katika ‗Kiambatisho 5‘ 2 Bukhâri, katika Juz‘ al-Qirâ‘ah na Abu Dâwud kwa isnâd iliyo swahîh.

42

Na pia Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alikuwa akiwaamrisha wenye

kumfuata (ma‘muma) waseme âmîn, pindi Imâm anapomaliza kusoma:

ي كري » ة ول الظذ ـ لظب ا ، ال ي :نيل نإن االاسح ]آ

ي وإن الةم يي :ديل ي :ل آ إذا أ الةم نأا :ويف هؼ ) [آإذا ىةل أظدز :ويف هؼ آخر )ن وانو دأ دأي االاسح (

ي واالاسح ف الصةء :ف الصالة خر :آ ي نانو إظداة ا (آ « ذج ديدم ة ل كهر

―Na nyinyi semeni ―âmîn‖ [kwani Malaika husema ―âmîn‖ pindi Imâm anaposema âmîn‖] (katika riwaya nyengine: Imâm anaposema ―Âmîn‖ na nyinyi semeni ―Âmîn‖), kwa hivyo, yule ambaye âmîn yake itâfikiana na âmîn ya MaLaaika (katika riwaya nyengine: pindi asemapo mmoja wenu ―Âmîn‖ katika swala na MaLaaika mbinguni husema ―Âmîn‖ na zikâfikiana), husamehewa madhambi yake yaliyopita.‖1

1 Bukhâri, Muslim, an-Nasâ‘î, ad-Dârimi; matamshi ya nyongeza yamepokewa na wawili wa mwisho na inathibitisha yakwamba hadîth hii haiwezi kukubali yakwamba Imâm hasemi ‗Âmîn‘, kama ilivyopokewa na MÂLIK; kwa sababu hiyo, Ibn Hajar akasema katika Fat-hul-Bâri, ―Inaonyesha waziwazi yakwamba Imâm husema ‗Âmîn‘.‖ Ibn ‗Abdul Barr amesema katika Tamhîd (7/13), ―Ndiyo rai ya Waislamu wengi, akiwemo Mâlik kwa vile watu wa Madînah wamepokea kutoka

kwake, kwani imeswihi kutoka kwa Mtume ( وسلم عليه اهللصلى ) kwa njia ya

ahâdîth za Abu Hurairah (yaani hadîth hii) na ile ya Wâ‘il ibn Hujr (yaani ile iliyotangulia).‖

43

Katika hadîth nyengine: ... semeni Âmîn; Allâh‎ atakupendeni1.

Pia alikuwa akisema: Mayahudi hawawaonei nyinyi uhasidi juu ya kitu chochote zaidi ya kuwahusudu juu ya (kutoleana) SaLaam na (kuitikia) Âmîn. [nyuma ya Imâm ].2

KISOMO CHAKE (صىل اهلل عليه وسلم) BAADA YA FÂTIHAH.

Kisha Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alikuwa akisoma Sûrah nyengine baada

ya al-Fâtihah, mara nyengine akiirefusha, na mara nyengine alikuwa akiifupisha kwa ajili ya safari, kikohozi, maradhi au vilio vya watoto wachanga.

Anas Ibn Mâlik )هنع هللا يضر( amesema: ―Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alikifupisha

(Yaani kisomo chake) siku moja katika swala ya alfajiri.‖ (Katika hadîth nyengine: aliswali swala ya alfajiri na akazisoma Sûrah mbili zilizo fupi zaidi katika Qur‘ân). Basi ikasemwa hapo: ―Ewe Mjumbe wa Allâh‎, mbona umeifanya (swala) kuwa fupi?‖ Akasema: Nimesikiya kilio cha mtoto, na nataraji yakwamba

1 Muslim na Abu ‗Awânah 2 Bukhâri katika al-Adab al-Mufrad, Ibn Mâjah, Ibn Khuzaymah, Ahmad na Sirâj kwa isnâd mbili zilizo swahîh.. TANBÎH! Mwitiko huu wa mkusanyiko wa watu nyuma ya Imâm wa ―Âmîn‖ na uletwe kwa sauti ya juu na uafikiane na mwitiko wa Imâm, na usiwe kabla yake kama wanavyofanya wengi wa wanaofanya ‗ibaadah, na wala usiwe baada yake. Hatimae, hili ndilo jambo lililoniridhisha zaidi, kama nilivyokwisha kuyaeleza hayo katika baadhi ya vitabu vyangu, vikiwa miongoni mwao Silsilat al-Ahâdîth adh-Dha‘îfah (no. 952, vol. 2) ambacho kimeshachapishwa kwa uwezo wake Allaah, na Swahîh at-Targhîb wat-Tarhîb (1/205). Tazama Kiambatisho 6.

44

mamake alikuwa akiswali nasi, kwa hivyo nikakusudia kumpa nafasi yule mamake.1

Na pia alikuwa akisema: Hakika mimi ninaingia katika swala, na hali mimi hukusudia kuirefusha swala, lakini mara husikiya kilio cha mtoto, kwa hivyo inanibidi kuifupisha swala yangu kwa vile ninavyojua huzuni kubwa inayompata mamake kwa kilio cha mwanae.2

Na Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alikuwa akianza mwanzo wa Sûrah, na

katika hali zake nyingi alikuwa akikamilisha.3

Alikuwa akisema: Ipeni kila Sûrah hadhi yake ya rukû‘ na Sujûd.4

Na lafdhi nyengine katika hadîth hiyo: Kila Sûrah Rak‘âh yake.5 Mara nyengine alikuwa akiigawanya Sûrah moja kwa Rak‘âh mbili1 na mara nyengine alikuwa akiirudia tena Sûrah nzima katika Rak‘âh ya pili.2

1 Ahmad na isnâd iliyo swahîh; Hadîth nyengine ilipokewa na Ibn Abî Dâwud katika al-Masâhif (4/14/2). Hadîth hii na nyengine mfano wake zinaruhusu watoto wachanga kuingia misikitini. Ama hadîth zitokazo kwenye vinywa vingi: ―Waepusheni watoto wenu wachanga na misikiti ...‖ , hiyo ni dha‘îf na haiwezekani kabisa kutumiwa kama dalili; miongoni mwa waliosema kuwa hiyo ni dha‘îf ni kina Ibn al-Jawzi, Mundhiri, Haitami, Ibn Hajar al-Asqalaani na Bûsayri. ‗Abdul Haqq al-Ishbîli amesema, ―Haina msingi wowote.‖ 2 Bukhâri na Muslim. 3 Kuna Ahâdîth nyingi zilizotajwa kwengineko zenye kuthibitisha haya. 4 Ibn Abî Shaybah (1/100/1) Ahmad na ‗Abdul Ghani al-Maqdisi katika Sunan yake (9/2) kwa isnâd iliyo swahîh. 5 Ibn Nasr na at-Twahâwi kwa isnâd iliyo swahîh. Mimi nachukulia maana ya hadîth kwamba: Ifanye kila rakâ‘ah iwe na sûrah kamili. Mpangilio wake ni mojawapo ya , isiyolazimishwa, kutokana na ushahidi ufuatao.

45

Mara nyengine alikuwa akizichanganya Sûrah mbili au zaidi katika Rak‘âh moja.3

Mmojawapo wa ma-Answâr alikuwa akiwaongoza watu katika msikiti wa Qubâ‘, na kila wakati alipokuwa akiwasomea Sûrah4, alikuwa akianza na:

ٱى ظد للذ ١أ

“Sema: Yeye ni Allâh‎, Mmoja wa Pekee ...” [Sûrah al-IkhLaas, 112]

hadi mwisho wake, na kisha alikuwa akiisoma na Sûrah nyengine akiiandamiza nayo, na alikuwa akifanya hivyo katika kila Rak‘âh . Kwa sababu hiyo, watu wake wakazungumza nae, wakisema: ―Hakika wewe wânza kwa Sûrah hii, kisha huichukulii kuwa inatosha mpaka usome Sûrah nyengine: Imma uisome (hiyo peke yake) au uiwache na usome nyengine. Akasema: ―Mimi sitowacha kuisoma: Ikiwa hamuna neno mimi niwaongoze kama Imâm kwa Sûrah hiyo, nitakuwa ni mwenye kuendelea, lakini ikiwa hamupendi hivyo, mimi nitawawacha.‖ Wao walikuwa wanaelewa yakwamba alikuwa ni mmojawapo wa wabora wao, na hawakupendezwa kuongozwa na mwengine yoyote, basi

alipowajilia Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), wakamuelezea khabari hiyo.

Mtume akasema: ―Ewe fuLaan, ni jambo gani linalokuzuiya kufanya hivi wanavyokuamrisha wenzako? Na ni jambo gani linalokulazimisha kuisoma Sûrah hii katika kila Rak‘âh ?‖

Akasema: ―Mimi naipenda Sûrah hii‖ Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

1 Ahmad na Abu Ya‘laa kutokamana na njia mbili za upokezi. Pia tazama ‗Kisomo Cha Swala ya Fajr‘. 2 Kama alivyofanya katika swala ya Fajr, kama itakavyokuja mbeleni. 3 Chanzo na maelezo kwa ukamilifu yatafuata muda mchache ujao. 4 Yaani Sûrah al-Fâtihah

46

akamwambia: "Mapenzi yako juu ya Sûrah hii yatakuingiza

Peponi.‖1

KUKUSANYA SÛRAH ZILIZOFANANA NA NYENGINE KATIKA RAK‟ÂH MOJA

Alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akikutaniza baina ya jozi2 ya Sûrah

zilizo mufassal3, kwa hivyo alikuwa akisoma mojawapo ya jozi ya Sûrah zifuatazo katika Rak‘âh moja4;

Ar-Rahmân (55:78)5 na an-Najm (53:62);

Al-Qamar (54:55) na al-Hâqqah (69:52);

At-Tûr (52:49) na adh-DhâriYât (51:60);

Al-Wâqi‘ah (56:96) na al-Qalam (68:52);

Al-Ma‘ârij (70:44) na an-Nâzi‘ât (79:46);

Al-Mutaffifîn (83:36) na ‗Abasa (80:42);

Al-Muddath-thir (74:56) na al-Muzzammil (73:20);

1 Bukhâri kama ta‘lîq na at-Tirmidhî kama mawsûl, na akaithibitisha kuwa swahîh 2 An-Nadhâ‘ir: Sûrah zilizofanana kimaana, k.m zote zina mawaidha, mâmrisho, au visa. 3 Zimeafikiwa kumalizikia mwishoni mwa Qur‘an; rai iliyo na nguvu ni kwamba zinânzia na Sûrah Qâf (no. 50) 4 Bukhâri na Muslim. 5 Nambari ijayo mwanzo ni ya sûrah, haliyakuwa ya pili ni nambari ya Âyât katika sûrah. Kwa kuzichunguza nambari ya mwanzo baina ya nambari mbili katika kila hali, ni rahisi kuyaona hayo katika

kuchanganya huku; Yeye Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) hakugandama na

kuufuata mpangilio wa sûrah za Qur‘an zilivyo, kwa hivyo huu ni ushahidi wa kuruhusiwa kufanya hivyo, hata kama ni bora kufuata mpangilio wa Qur‘an ulivyo. Mas‘ala mfano wa haya yatapatikana baadae chini ya anwani, ―Swala za Usiku.‖

47

Ad-Dahr (76:31) na al-QiYâmah (75:40);

An-Naba‘ (78:40) na al-MursaLaat (77:50);

Ad-Dukhân (44:59) na at-Takwîr (81:29).

Mara nyengine alikuwa akizichanganya Sûrah kutoka katika tiwâl saba (Sûrah ndefu ndefu), kama vile al-Baqarah, an-Nisâ‘ na âl-‘Imrân katika Rak‘âh moja wakati wa swala ya usiku (hapo chini). Alikuwa akisema:

« ايةم غل الصالة أنظ »―Bora ya swala ni ile yenye kisimamo kirefu.‖1

Na pindi anaposoma aya isemayo:

ن يـى أ ثؼدر ع ل يس ذ

يت ٱأ ٤٠ ل

Je! Hakuwa Huyo ni Muweza wa kuhuisha wafu? [Sûrah al-Qiyâmah 75:40]

Alikuwa akisema:

« نجل شجعة »―Kutakasika ni kwako, hapana shaka‖

Na pindi anaposoma aya isemayo:

ٱشجط ش ع ٱرب ١ ل

―Litukuze Jina la Mola wako aliye Mtukufu.‖ [Sûrah alA‘Laa 87:1]

Alikuwa akisema:

« الع يبر شجعةن » 1 Muslim na at-Twahâwi.

48

―Kutakasika ni kwa Mola wangu Aliye juu zaidi.‖1

KURUHUSIWA KUSOMA AL-FÂTIHAH PEKE YAKE

Na alikuwa Mu‘âdh ibn Jabal akiswali swala ya ‗Ishâ‘ [ya mwisho]

pamoja na Mtume ( وسلم صىل اهلل عليه ), kisha anarudi na kuwaongoza

wenzake katika swala. Katika usiku mmoja aliporudi na kuswali nao, palikuwepo na kijana mmoja [aitwae Sulaim, wa Banu Salamah] katika swala hiyo, lakini swala ilipokuwa ni ndefu mno kwake , [aliondoka na] aliswali [kwenye kipembe cha msikiti], kisha akatoka, akashika kamba ya Ngamia wake na akenda zake. Alipomaliza swala Mu‘âdh, alipashwa khabari hizo, kwa hivyo akasema: ―Hakika kijana huyo ana chembe chembe za unafiki

ndani yake! Kwa hakika, mimi nitamfahamisha Mtume ( اهلل عليه صىل kuhusu yale aliyoyafanya huyo kijana.‖ Yule kijana (وسلم

akasema: ―Na mimi nitamfahamisha Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) kuhusu

aliyoyafanya.‖ Basi ilipofika asubuhi, wote wakaja kwa Mtume

( وسلم عليه اهلل صىل ), na Mu‘âdh akamuelezea Mtume ( kuhusu ( عليه وسلمصىل اهلل

kitendo cha yule kijana. Yule kijana akasema: ―Ewe Mjumbe wa Allâh‎! (Huyu) Mu‘âdh anakâ na wewe kwa muda mrefu, na kisha

anarudi kwetu na kuturefushia sisi (swala).‖ Basi Mtume ( صىل اهلل عليه ,akasema: Wewe ndiye mwenye kusababisha fitnah kubwa (وسلم

ewe Mu‘âdh?! na akamwambia yule kijana2: Kwani unafanya vipi, ewe mtoto wa ndugu yangu, ukiswali? Akasema: ―Mimi husoma sûratil-Fâtihah, kisha humuomba Allâh‎ Pepo katika Dua‘ na

1 Abu Dâwud na al-Bayhaqi kwa isnâd iliyo swahîh. Hadîth hii ni yenye kujumuisha, kwa hivyo inahusu visomo vyote wakati wa swala, iwapo ni swala za sunnah na swala za faradhi, na nje yake. Ibn Abî Shaybah (2/132/2) ameipokea kutoka kwa Abu Musa al-Ash‗ari na al-Mughîra ibn Shu‘bah yakwamba walikuwa wakisema hivyo katika swala za faradhi, na kutoka kwa ‗Umar na ‗Ali bila ya nyakati mâlum. 2 Katika asili yake, ―yule kijana akasema.‖

49

hutaka hifadha kwake na moto. Mimi sijui unayoyasema (dandanah zako1) wewe na anayoyasema (dandanah za) Mu‘âdh!‖

Basi Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akasema: Mimi na Mu‘âdh tuko sawa

katika haya.

Mpokezi (wa hadîth hii) akasema: Yule kijana akasema, ―Lakini Mu‘âdh atakuja kujua (kunihusu mimi) kuhusiana na kuwaendea watu wakati watakapokuwa wameshaelezwa yakwamba adui ashawasili.‖ Akasema mpokezi: kwahivyo adui akaja, na yule

kijana akafa shahidi. Basi baada ya hayo, Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akasema kumwambia Mu‘âdh, amefanya nini yule hasimu wangu na hasimu wako? Akasema, ―Ewe Mjumbe wa Allâh‎, (yule kijana) alikuwa ni mkweli mbele ya Allâh‎, na mimi nilisema urongo – aliu-wawa shahidi.‖2

1 Dandanah: wakati mtu anaposema maneno fulani, kiyasi cha kwamba lafdhi zake husikika sauti tu lakini matamshi hayaeleweki; ni zaidi kidogo ya kunon‘gona. (Nihâyah) 2 Ibn Khuzaymah katika swahîh yake (1634) na al-Bayhaqî kwa isnâd iliyo swahîh. Ina riwaya yenye kuipa nguvu katika Abu Dâwud (no. 758, Swahîh Abi Dâwud) na kisa chenyewe kiko katika Bukhâri na Muslim. Nyongeza ya kwanza inapatikana katika riwaya nyengine ya Muslim, ya pili yapatikana katika Ahmad (5/74), na ya tatu na ya nne katika Bukhâri. Vile vile, chini ya mlango huwo ni hadîth iliyopokewa na ibn

‗Abbâs: ―Yakwamba Mtume ( وسلم ليهع اهلل صىل ), aliswali rakâ‘ah mbili,

ambazo ndani yake alisoma al-Fâtihah peke yake‖, imepokewa na Ahmad (1/282), Hârith ibn Abi Usâmah katika musnad yake (Uk. 38 ya Zawâid yake), na al-Bayhaqî (2/62) kwa isnâd iliyo dha‘îf. Nilikuwa nikiithibitisha hadîth hii hasan katika vitabu vyangu vilivyotangulia, mpaka nikazindukana yakwamba nimekosea, kwa sababu hadîth hii inamtegemea Handhwalah ad-Dawsî, ambae ni dha‘îf, na mimi nashangâ, ilikuwaje kwangu mimi halikujulikana jambo hili; labda huwenda nilimdhania kuwa mtu mwengine. Si kitu, kila Sifa njema ni zenye kumthubutukia Allaah Aliyeniongoza mimi katika kutambua makosa yangu, na hiyo ndiyo sababu niliharakisha kuyarekebisha katika

50

KUSOMA KWA SIRI NA KWA SAUTI KATIKA SWALA TANO NA NYENGINEZO

Na alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akisoma kwa sauti kubwa katika

swala ya asubuhi na katika Rak‘âh mbili za mwanzo za Maghrib na ‗Ishâ‘, na kwa siri katika swala za Dhuhr, ‗Asr, Rak‘âh ya tatu

ya Maghrib, na Rak‘âh mbili za mwisho za ‗Ishâ‘.1

Walikuwa na uwezo wa kuthibitisha yakwamba alikuwa akisoma kwa siri kutokana na kutingishika kwa ndevu zake2, na kwa sababu alikuwa akiwasikilizisha kama aya moja hivi mara nyengine.3

Pia alikuwa akisoma kwa sauti kubwa katika swala ya Ijumâ, na swala za ‗Idd mbili4, na swala ya mvua, na swala ya kupatwa kwa jua au mwezi.5

uchapishaji. Kisha Allaah akanifidiya badala yake na hadîth hii iliyo bora ya Mu‘âdh inayoeleza yanayoashiriwa na hadîth ya ibn ‗Abbâs. Anasifika Allaah ambaye kwa Rehma zake, vitendo vizuri hukamilika. 1 Kuna ‗Ijmâ‘ (maafikiano ya rai) ya Waislamu juu ya mas‘ala haya, huku warathi wakiyafikiliza kutoka kwa waliowatangulia, pamoja na hadîth zilizo swahîh zenye kuyathibitisha haya, kama alivyosema an-Nawawi, na baadhi yao wakafuata. Tizama vile vile Irwâ‘ (345). 2 Bukhâri na Abu Dâwud 3 Bukhâri na Muslim 4 Tazama sehemu zenye kuzungumzia kuhusu ‗Usomaji wake katika swala ya Ijumâ na ‗Idd mbili.‘ 5 Bukhâri na Muslim

51

KUSOMA KWA SIRI NA KWA SAUTI KATIKA SWALA YA USIKU (TAHAJJUD)1

Ama kuhusu swala ya usiku, mara nyengine alikuwa akisoma kwa siri na mara nyengine alikuwa akisoma kwa sauti ya juu2, na ―alikuwa akisoma akiwa nyumbani kwake kiasi cha kwamba

aliweza kusikika ndani ya chumba chake.‖3

Na alikuwa mara nyengine akiinua sauti yake zaidi ya hivyo mpaka mtu aliyelala humsikiya4‖ (Yaani; kutoka nje ya chumba chake).

Aliwaamrisha Abu Bakr na ‗Umar رضي اهلل عنهم() wafanye hivyo,

wakati:

―Alipotoka usiku mmoja na kumuona Abu Bakr (رضي اهلل عنه)

akiswali kwa sauti ya chini, na akapita kando ya ‗Umar (رضي اهلل عنه)

aliyekuwa akisoma kwa sauti ya juu. baada ya muda,

1 Amesema ‗Abdul Haqq katika Tahajjud (90/1): ―Ama kuhusu swala za sunnah katika nyakati za mchana, hakuna

chochote kilicho swahîh kutoka kwake (صىل اهلل عليه وسلم) kuhusu imma ni

kisomo cha siri au cha sauti ya juu, lakini yaonekana kama kwamba alikuwa akisoma kwa siri wakati anaposwali. Imepokewa kutoka kwake

yakwamba, siku moja katika wakati wa mchana, alipita (صىل اهلل عليه وسلم)

kando ya ‗Abdullaah ibn Hudhâfah aliyekuwa akiswali na huku anasoma kwa sauti ya juu, hapo akasema kumwambia: Ewe ‗Abdullaah, msikilizishe Allaah, sio sisi. Lakini hadîth hii haina nguvu.‖ 2 Muslim na Bukhâri katika Af‘âl al-‗Ibâd. 3 Abu Dâwud na at-Tirmidhî katika Shamâ‘il kwa isnâd iliyo hasan.

Maana ya hadîth nikwamba alikuwa yeye ( يه وسلمصىل اهلل عل ) akikisia baina ya

kuficha sauti yake na kuidhihirisha sauti yake. 4 An-Nasâ‘î, at-Tirmidhî katika Shamâ‘il na al-Baihaqî katika Dalaa‘il kwa isnâd iliyo hasan

52

walipokusanyika katika hadhara ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) wote

wawili. Akasema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم): Ewe Abu Bakr, mimi

nilikupitia wakati wewe unaswali kwa sauti ya chini? Akasema: ―Nimemsikilizisha ninaemuomba, ewe Mjumbe wa Allâh‎.‖

Akasema kumwambia ‗Umar )هنع هللا يضر( mimi nilikupitia wakati wewe

unaswali kwa sauti ya juu? Basi akasema: ―Ewe Mjumbe wa Allâh‎, mimi ninamuamsha alielala na kumfukuza Shetani.‖

Akasema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم): Ewe Abu Bakr, inua sauti yako

kidogo na kwa ‗Umar: punguza sauti yako kidogo.1

Alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akisema: Mwenye kusoma Qur‘ân

kwa nguvu ni kama mwenye kudhihirisha sadaka yake, na mwenye kuisoma Qur‘ân kwa sauti ya chini ni kama mwenye kuificha sadaka yake na kuitoa kwa siri.2

SURA ALIZOKUWA AKISOMA (صىل اهلل عليه وسلم) KATIKA SWALA

TAFAUTI

Ama ni sura zipi na âyât zipi alizokuwa akisoma Mtume ( صىل اهلل عليه katika swala, haya yametafautiana kulingana na swala (وسلم

tafauti. Sasa yanafuata maelezo, kuanzia swala ya kwanza katika swala tano:

1. SWALA YA FAJR

1 Abu Dâwud na Hâkim, aliyeithibitisha kuwa swahîh, na adh-Dhahabi akaiafiki. 2 Ibid.

53

Alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akisoma katika swala ya alfajiri zile

sura ndefu1 mufassal2 ―alikuwa mara nyengine akisoma Sûrah al-Wâqi‘ah (56:96) na Sûrah mfano wake katika Rak‘âh mbili3‖.

Alisoma Sûrah at-Tûr (52:49) na hiyo ilikuwa katika Hijjatul Wada‘ah (hijja yake ya kuaga).4 Mara nyengine ―alikuwa akisoma Sûrah Qâf (50:45) au mfano wake [katika Rak‘âh ya kwanza].‖5 Mara nyengine alikuwa akisoma Sûrah mufassal fupi, kama vile:

س ٱ إذا رت لظذ ١ "Jua litakapokunjwakunjwa."

Siku moja alisoma:

رض ٱزلزخ إذاة ل ١زلزال

“Itakapotetemeshwa ardhi mtetemesho wake (huo mkubwa)."

Katika Rak‘âh zote mbili, mpaka akasema mpokezi wa hadîth

hii, ―Sijui mimi iwapo Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alisahau au aliisoma

kwa makusudi.6 Siku moja alipokuwa katika safari, alisoma:

1 An-Nasâ‘î na Ahmad kwa isnâd iliyo swahîh. 2 Ni zile sura saba za mwisho za Qur‘an, kuanzia Sûrah Qâf (no. 50) kulingana na rai yenye nguvu zaidi, kama ilivyotangulia. 3 Ahmad, ibn Khuzaymah (1/69/1) na Hâkim aliyeitangaza kuwa swahîh na adh-Dhahabi akaiunga mkono. 4 Bukhâri na Muslim. 5 Muslim na at-Tirmidhî. Imetolewa pamoja na yenye kuifuata katika Irwâ‘ (345) 6 Abu-Dâwud na al-Bayhaqî kwa isnâd iliyo swahîh. Na lililo dhihirika

hapa ni kwamba, Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alifanya hivyo kwa makusudi ili

kuthibitisha kuruhusiwa jambo hilo.

54

ذ ثرب ـ أ ١ هو ٱى

“Sema: Ninajikinga kwa Mola wa Ulimwengu wote.” Na:

ذ ثرب ى ـ ١ جلذةس ٱأ

“Sema: Ninajikinga kwa Mola wa watu.”

Vilevile alimwambia ‗Uqbah ibn ‗Âmir (رضي اهلل عنه) : Soma katika

swala yako mu‘awwadhatain1, kwani hakutaka hifadha mwenye kutaka hifadha kwa mfano wa sura mbili hizi.2 Mara nyengine alikuwa akisoma zaidi ya hivyo: ―alikuwa akisoma ayât sitini au zaidi‖3 – mmojawapo wa wapokezi akasema, ―Mimi sijui ikiwa hii ilikuwa ni katika kila Rak‘âh au katika Rak‘âh zote kwa jumla.‖ Alikuwa akisoma Sûrah ar-Rûm (30:60)4, na mara nyengine Sûrah Yâ Sîn (36:83)5 Siku moja, ―aliswali subh (swala ya fajr) akiwa Makkah na akânza kusoma Sûrah al-Mu‘minûn (23:118) mpaka alipofika katika sehemu aliyotajwa Mûsa na Hârun au kutajwa ‗Issa6 – mmoja wa

1 Maana yake; ―(Sûrah) mbili ambazo watu hujihifadhi kwazo‖, yaani; sûrah mbili za mwisho za Qur‘an, zote huanza kwa:

ذ ثرب ى ـ ١ ...أ

“Sema: Najikinga kwa Mola…” 2 Abu Dâwud na Ahmad kwa isnâd iliyo swahîh 3 Bukhâri na Muslim 4 An-Nasâ‘î, Ahmad na Bazzâr kwa isnâd iliyo nzuri. 5 Ahmad, kwa isnâd iliyo swahîh. 6 Mûsa ametajwa katika aya ya 45:

ذ خةه هرون ا‍ب ثة مس وأ رش

جي أ ن

ة وش ٤٥يذ

55

wapokezi hakuwa na hakika – Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akânza kukohoa

kwahivyo akarukû‘1 Mara nyengine, ―alikuwa akiwaongoza katika swala ya alfajiri kwa as-Sâffât‖ (77:182)2 ―Katika swala ya Fajr, siku ya Ijumâ, alisoma as-Sajdah (32:30) [katika Rak‘âh ya kwanza, na ya pili], ad-Dahr‖ (76:31)3 Na alikuwa akiifanya Rak‘âh ya kwanza ndefu kuliko Rak‘âh ya pili.4

KUSOMA KATIKA SWALA YA SUNNAH YA KABLA YA FAJR

Kisomo chake katika Rak‘âh mbili za sunnah ya alfajiri kilikuwa

ni kifupi mno5 sana hata kikamfanya ‗Âisha (رضي اهلل عنها) aseme: ―Je

Mtume kweli amesoma sûratil Fâtihah au Laa?‖6

Mara nyengine, baada ya al-Fâtihah, alikuwa akisoma âyah no. 136 ya Sûrah al-Baqarah; isemayo:

“Kisha tulimtuma Mûsa na nduguye Hârûn, pamoja na miujiza

yetu na dalili zilizo dhahiri”[Sûrah al-Mu‘minûn 23:45]

‗Issa akatajwa punde tu baada ya hapo katika aya ya 50:

ة ٱوصف ب ذ وأ في ۥ مري ة ذات ىرار و ة إل رب ٥٠ءايحا وءاويج

“Na tulimfanya mwana wa Mariamu na mama yake kuwa ishara (ya uweza wetu na tukawapa makimbilio (kwenda) mahali

palipoinuka penye utulivu na chemchemi za maji.” [Sûrah al-Mu‘minûn 23:50]

1 Muslim na Bukhâri kwa njia ya ta‘lîq. Imetajwa katika Irwâ‘ (397) 2 Ahmad na Abu Ya‘laa katika Musnad zao, na Maqdisi katika al-Mukhtârah. 3 Bukhâri na Muslim 4 Ibid. 5 Ahmad, kwa isnâd iliyo swahîh 6 Bukhâri na Muslim

56

ا ىل ذة ث ٱءا ه للذ زل إل إثرة أ ة و زل إحل

ة أ إوشو و إوشؿف

شجةط ٱويفيب و ويت ل

ة أ ـييس و ويت مس و

ة أ ن ٱو ل جلذب ب رذ

ل ون ظد ن ۥجهرق بي أ ١٣٦مص

Katika Rak‘âh ya kwanza, na katika Rak‘âh ya pili, alikuwa akisoma âyah no. 64 ya Sûrah âl-‘Imrân isemayo:

أ ي تت ٱى لذ جفجد إلذ

أ س ة وبي ثي اء ح ش ا إل لك ٱتفةل للذ

ا طي ۦول نشك ث ربةباة ة بفظة أ ٱدون ة ول حذذخذ بفظ ا للذ ذ نإن د

ا ٱذيل دوا ط ذةثن أ ٦٤1مص

Na mara nyengine alikuwa akisoma badala ya aya hiyo ya mwisho, aya no. 52 ya Sûrah âl-‘Imrân isemayo:

ـييس ظسذ ة أ ذ صةري إل سهر ٱ۞ن

أ ٱ ىةل ىةل للذ

ارين ٱ صةر ل أ ٱن للذ ذة ث ٱءا د ٱو للذ ن ط ذة مص

٥٢2ثأ

Mara nyengine alikuwa akisoma Sûrah al-Kâfirûn (109:6) katika Rak‘âh ya kwanza, na Sûrah al-IkhLaas (112:4) katika Rak‘âh ya pili;3 pia alikuwa akisema: Bora ya Sûrah ni hizo Sûrah mbili!4

Alimsikiya mtu akisoma hiyo Sûrah ya kwanza katika Rak‘âh ya kwanza, basi akasema, Huyu ni mja aliyemuamini Mola Wake.

1 Muslim, Ibn Khuzaymah na Hâkim

2 Muslim na Abu Dâwud 3 ibid 4 Ibn Mâjah na Ibn Khuzaymah.

57

Kisha yule mtu akasoma Sûrah ya pili katika Rak‘âh ya pili, basi akasema, Huyu ni mja aliyemjua Mola Wake.1

2. SWALA YA DHUHR

―Alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akisoma sûratil Fâtihah na Sûrah

mbili nyengine katika Rak‘âh mbili za kwanza, na alikuwa akirefusha katika Rak‘âh ya kwanza, kuliko katika Rak‘âh ya pili.‖2

Na mara nyengine Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alikuwa akiirefusha swala

ya Dhuhr kiasi cha kwamba ―swala ya Dhuhr inaqimiwa, na mtu anaweza kwenda kwenye uwanja: al-Baqî‘, akidhi haja yake ya kuzuru [kisha arudi mahala pake], atawadhe, na kisha aje

(msikitini), akiwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) bado yuko katika Rak‘âh

ya kwanza, ilikuwa ni ndefu kiyasi hicho.‖3

Vilevile, ―walikuwa wakidhania yakwamba alikuwa anafanya hivyo ili watu waipate Rak‘âh ya kwanza‖4

Alikuwa akisoma katika kila Rak‘âh hizi mbili takriban âyât thalathini, kama vile Sûrah al-Fâtihah ikifuatwa na Sûrah as-Sajdah (32:30).‖5

Mara nyengine ―alikuwa akisoma:

ةء ٱو ةرق ٱو لصذ ةء ٱو ١ ػذ وج ٱذات لصذ ٱو ١ رب ١إذا حلش حلذ 1 At-Twahâwi, Ibn Hibbân katika swahîh yake na Ibn Bushrân, Ibn Hajar akaithibitisha kuwa hasan katika al-Ahâdîth al-Âliyât (no. 16) 2 Bukhâri na Muslim. 3 Muslim na al-Bukhâri katika Juz‘ al-Qirâ‘ah (makala ya kuhusu Usomaji). 4 Abu Dâwud kwa isnâd iliyo swahîh na Ibn Khuzaymah (1/65/1). 5 Ahmad na Muslim

58

Na mfano wa hivyo katika Sûrah.‖1 Na huwenda mara nyengine akisoma:

ةء ٱ إذا خ ٱ لصذ ١ نظيذNa mfano wa Sûrah hiyo.2

―Maswahaba walikuwa wakijua kusoma kwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) katika swala ya Dhuhr na ‗Asr kwa kutingishika ndevu zake.‖3

KUSOMA KWA MTUME (صىل اهلل عليه وسلم) ÂYÂT BAADA YA SÛRAH

AL-FÂTIHAH KATIKA RAK‟ÂH MBILI ZA MWISHO.

―Alikuwa akipenda kuzifanya Rak‘âh mbili za mwisho kuwa fupi kiasi cha nusu ya Rak‘âh mbili za mwanzo, takriban kama âyât

1 Abu Dâwud, at-Tirnidhî na Ibn Khuzaymah (1/67/2); hao wawili wa baadae wameithibitisha kuwa swahîh 2 Ibn Khuzaymah katika swahîh yake (1/67/2). 3 Bukhâri na Abu Dâwud

59

kumi na tano1, na mara nyengine alikuwa akisoma ndani yake al-Fâtihah peke yake.‖ 2

Mara nyengine ―alikuwa akiwasikilizisha Maswahaba zake kama âyah moja hivi.‖3 Walikuwa wakisikiya sauti ya kisomo chake cha:

ٱ شجط ش ع ٱرب na ١ ل ظدير دى

حٱأ ١4 غظ

―Mara nyengine alikuwa akisoma:

ةء ٱو ةرق ٱو لصذ ١ ػذ ةء ٱو , وج ٱذات لصذ ١ رب

na Sûrah nyengine zilizo mfano wake.‖1

1 Ahmad na Muslim. Hadîth ina ushahidi kamili yakwamba kusoma zaidi ya al-Fâtihah katika rakâ‘ah mbili za mwisho ni sunnah, na Maswahaba

wengi walifanya hivyo, miongoni mwao ni Abu Bakr as-Siddîq (هنع هللا يضر).

Vilevile hiyo ilikuwa ndiyo rai ya Imâm ash-Shâfi‘î, imma katika swala ya Dhuhr au yoyote nyengine, na pia wanavyuoni wetu walokuja baadae, Abul Hasanât al-Lucknowi alizinukuu kwa khatti za al-Muwatta cha Muhammad (Uk. 102) kisha akasema: ―Baadhi ya wenzetu wameishikilia rai ya kushangaza kabisa katika kuwajibisha Sijda-tis-Sahw (sijda kwa ajili ya kusahau) kwa ajili ya usomaji wa sûrah katika rakâ‘ah mbili za mwisho, lakini wakuufunzi kuhusu al-Maniyyah, Ibrâhîm al-Halabi, Ibn Amîr Hâjj, na wengineo, wameikosoa rai hii kisawasawa. Hapana shaka yakwamba hawa walioisema hivyo hawakuijua hadîth hii, na lau kama ingeliwafikiya, hawangelisema hivyo.‖ 2 Bukhâri na Muslim. 3 Ibn Khuzaymah katika swahîh yake (1/67/2) na Diyâ‘ al-Maqdisi katika al-Mukhtârah kwa isnâd iliyo swahîh. 4 Bukhâri katika makala ya usomaji na Tirmidhî aliyeithibitisha kuwa ni swahîh.

60

Na mara nyengine alikuwa akisoma:

ٱو ١إذا حلش حلذNa Sûrah nyengine zinazofanana na hiyo.‖2

3. SWALA YA „ASR

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم): ―alikuwa akisoma al-Fâtihah na Sûrah mbili

(nyengine) katika Rak‘âh mbili za mwanzo, akiifanya Rak‘âh ya kwanza ndefu zaidi kuliko Rak‘âh ya pili‖3, na walikuwa wakidhania yakwamba alifanya hivyo ili watu waipate Rak‘âh .‖4

Na alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akisoma katika kila Rak‘âh moja

katika hizo Rak‘âh mbili takriban âyât kumi na tano, kiasi cha nusu ya alivyokuwa akisoma katika Rak‘âh mbili za mwanzo katika swala ya Dhuhr, na alikuwa akija‘aliya Rak‘âh mbili za mwisho ni fupi zaidi kiasi cha nusu ya Rak‘âh mbili za mwanzo.‖5

―Alikuwa akisoma al-Fâtihah katika Rak‘âh mbili za mwisho.‖6

―Na alikuwa mara nyengine akiwasikilizisha Maswahaba zake kama âyah moja hivi.‖7

1 Muslim na Tayâlisi 2 Bukhâri na Muslim. 3 ibid 4 Abu Dâwud kwa isnâd iliyo swahîh, na Ibn Khuzaymah 5 Ahmad na Muslim. 6 Bukhâri na Muslim. 7 Ibid.

61

Na alikuwa akizisoma zilezile Sûrah ambazo tulizotangulia kuzitaja hapo awali katika ―swala ya Dhuhr‖.

4. SWALA YA MAGHRIB

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alikuwa (mara nyengine) akisoma Sûrah fupi

za mufassal‖1, ili ―watakapokuwa wamemaliza kuswali na yeye, wataweza kwenda zao na (kuna uwezekano wa) kutupa mkuki na kuuona unapokita.‖2

Siku moja, ―alipokuwa kwenye safari, katika Rak‘âh ya pili, alisoma:

يذن ٱو تلي ٱو ١3 لزذLakini mara nyengine alikuwa akisoma zile Sûrah ndefu na za kiasi za mufassal, kwa hiyo ―alikuwa akisoma ―Sûrah Muhammad‖:

ٱ ي لذ شب ـ وا ٱزهروا وصد للذ ؿ ـذ أ ط

١4أ

Au Sûrah at-Tûr:

ر ٱو صػر ١ ػ ذ ٢5وكتت Au Sûrah al-MursaLaat:

1 Ibid (Bukhâri na Muslim) 2 An-Nasâ‘î na Ahmad kwa isnâd iliyo swahîh. 3 Tayâlisi na Ahmad kwa isnâd iliyo swahîh. 4 Ibn Khuzaymah (1/166/2), at-Twabarâni na Maqdisi kwa isnâd iliyo swahîh. 5 Bukhâri na Muslim

62

رشؾخ ٱو ة ل رنا ١ـAliisoma sura hiyo katika swala yake ya mwisho kabla ya kufa kwake.1

Mara nyengine alikuwa akiisoma Sûrah ndefu zaidi baina ya Sûrah mbili ndefu2 (Al-A‘râf 7:206) [kwa Rak‘âh mbili].‖3 Au ataisoma al-Anfâl (8:75) kwa Rak‘âh mbili.4

KISOMO KATIKA SWALA YA SUNNAH YA BA‟DAL MAGHRIB

Katika swala hii, ―alikuwa akisoma:

ة ى حأ هروٱي na ١ ن ؽ ى ٱ ظد للذ

١5أ

5. SWALA YA „ISHÂ‟

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alikuwa akisoma katika Rak‘âh mbili za

mwanzo6, Sûrah wasatil Mufassal (zenye urefu wa kiasi), kwa hiyo ―alikuwa akisoma:

1 ibid 2 Inaitwa ―at-tûlayain‖:Imeafikiwa yakwamba A‘râf (7) ni mojawapo; An‘âm (6) ni nyengine, kulingana na msimamo wa sawa, kama ilivyo katika fat-hul-Bâri 3 Bukhâri, Abu Dâwud, Ibn Khuzaymah (1/68/1), Ahmad, Sirâj na Mukhlis 4 At-Twabarâni katika al-Mu‘jamul Kabîr kwa isnâd iliyo swahîh 5 Ahmad, Maqdisi, an-Nasâ‘î, Ibn Nasr na at-Twabarâni. 6 An-Nasâ‘î na Ahmad kwa isnâd iliyo swahîh.

63

س ٱو ة و لظذ ١طعىna Sûrah nyengine mfano wake.‖1 Au ―alikuwa akisoma:

ةء ٱ إذا خ ٱ لصذ ١ نظيذNa alikuwa akisujudu akiwa ndani ya swala.‖2 Vilevile, ―wakati fulani alisoma:

يذن ٱو تلي ٱو ١ لزذ

[katika Rak‘âh ya kwanza], alipokuwa kwenye safari.‖3 Alikataza kurefusha kisomo kwenye swala ya ‗Ishâ‘, na hayo yalitokea wakati: Mu‘âdh ibn Jabal aliwaongoza watu wake katika swala ya ‗Ishâ‘, na aliwafanyia swala hiyo kuwa ndefu sana, mara mmojawapo wa Answâr akajiondoa kwenye swala hiyo na akaswali (peke yake). Pindi Mu‘âdh alipoelezwa kuhusu kitendo hicho, alisema: ―Hakika mtu huyo ni mnafiki‖. Yalipomfikia yule

mtu aliyoyasema Mu‘âdh, alikwenda kwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), akamfahamisha aliyoyasema Mu‘âdh. Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akamwambia Mu‘âdh, ―Je unataka kuwa fattani mwenye kufitinisha watu Ewe Mu‘âdh?!‖. Ukiwaswalisha watu, soma:

س ٱو ة لظذ ١وطعىAu

ٱ شجط ش ع ٱرب١ ل

Au

1 Ahmad na at-Tirmidhî, aliyeithibitisha kuwa hasan. 2 Bukhâri, Muslim, na an-Nasâ‘î 3 ibid

64

ٱ ىرأ ٱث ش يٱرب ١خو لذ

Au

ٱو ١إذا حلش حلذ[Kwa sababu wazee wakongwe, watu madhaifu, na wale wenye kutaka kukidhi haja zao, wote hao wanaswali nyuma yako].‖1

6. SWALA YA USIKU (TAHAJJUD)

Mara nyengine alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akisoma kwa

kuidhihirisha sauti yake katika swala za usiku na mara nyengine

kwa kuificha sauti yake2, alikuwa mara nyengine Mtume ( عليه اهللهصىل akifupisha kisomo chake katika swala hii na mara nyengine (وسلم

alikuwa akirefusha kisomo chake, na anazidisha katika kuirefusha swala ya usiku mara nyengine, mpaka siku moja alisema

‗Abdullâh‎ Ibn Mas‘ûd (رضي اهلل عنه) :

―Niliswali na Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) usiku mmoja, na

aliendelea kusimama kwa muda mrefu mpaka nikakusudia jambo baya.‖Akaulizwa, ―Ulikusudia jambo gani?‖ Akasema,

―Nilikusudia nikae na nimuache Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)!‖3

Pia alisema Hudhaifah Ibn al-Yamân:

―Niliswali na Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) usiku ule alipoanza

Sûrah al-Baqarah (2:286). Nikasema (katika nafsi yangu), ―Atarukû‘ akifika âyah mia moja‖. Lakini aliendelea baada ya hivyo, kisha nikafikiriya, ―Ataimaliza (hiyo Sûrah) kwa Rak‘âh mbili‖. Lakini aliendelea, basi nikafikiri, ―Atarukû‘

1 Ibid. Pia inapatikana katika Irwâ‘ (295) 2 An-Nasâ‘î kwa isnâd iliyo swahîh 3 Bukhâri na Muslim

65

atakapoimaliza (Sûrah hiyo).‖ Kisha akânza Sûrah an-Nisâ‘ (4:176) na akaisoma yote, kisha akânza Sûrah Âl-‘Imrân (3:200)1 na akaisoma yote. Alikuwa akisoma kwa mwendo wa taratibu; na alipofika katika âyah ambayo ina tasbîh, humsabbih Allâh‎, na akipitia âyah ambayo inahitaji kuomba, humuomba Allâh‎, na akipitia âyah ambayo ina Isti‘âdha, hutaka hifadha kwa Allâh‎. Kisha akarukû‘ ...‖ mpaka mwisho wa hadîth .2 Vilevile, katika usiku mmoja alipokuwa mgonjwa alisoma Sûrah saba ndefu.‖3 Pia, (mara nyengine) alikuwa akisoma mojawapo ya Sûrah hizi katika kila Rak‘âh .‖4 ―Haikujulikana (kabisa) kutoka kwake yakuwa alisoma Qur‘ân nzima kwa usiku mmoja.‖5 Kwa hakika, hakuliridhia jambo hilo

kwa ‗Abdullâh‎ Ibn ‗Amr (رضي اهلل عنه) , wakati alipomwambia:

―Isome Qur‘ân kila mwezi‖. Nikasema: ―Mimi nina uwezo wa (kufanya zaidi ya hivyo).‖ Akasema: ―Basi isome (Qur‘ân) kwa siku ishirini‖. Nikasema: ―Mimi nina uwezo wa kufanya zaidi‖. Akasema: ―Basi isome (Qur‘ân) kwa siku saba na wala usizidishe juu ya hapo‖.6 Kisha ―akamruhusu kuisoma kwa siku tano.‖7

1 Riwaya yenyewe ni kama hivi, Nisâ‘ (4) kabla ya âl-‗Imrân (3) na kwahivyo ni ushahidi kwa (kuruhusiwa kwa) kurukiza kutoka katika mpangilio wa sûrah zipatikanazo katika nakala za ‗Uthmâni za Qur‘an katika kisomo. Mfano wa haya ushaonekana kitambo. 2 Muslim na an-Nasâ‘î 3 Abu Ya‘laa na Hâkim, aliyeithibitisha kuwa swahîh na kuafikiwa na adh-Dhahabi. Ibn al-Athîr amesema: ―... sûrah saba ndefu ni al-Baqarah (2), âl-‗Imrân (3), an-Nisâ‘ (4), Mâ‘idah (5), An‘âm (6), A‘râf (7) na at-Tawbah (9).‖ 4 Abu Dâwud na an-Nasâ‘î kwa isnâd iliyo swahîh. 5 Muslim na Abu Dâwud 6 Bukhâri na Muslim 7 An-Nasâ‘î na at-Tirmidhî aliyeithibitisha kuwa swahîh

66

Kisha ―akamruhusu tena kuisoma kwa siku tatu.‖1 Mwisho kabisa akamkataza kuisoma Qur‘ân kwa chini ya siku tatu2, na akalitolea sababu hilo kwa kumwambia ‗Abdullâh‎ ibn

‗Amr (رضي اهلل عنه) : ―Mwenye kuisoma Qur‘ân kwa uchache wa siku

tatu hatoifahamu‖.3 Katika riwaya nyengine: ―Hatoifahamu Qur‘ân anayeisoma kwa uchache wa siku tatu‖4. Pia alipomwambia: ―Kila mwenye kuabudu huwa ana (muda wa) uchangamfu5 na kila (muda wa) uchangamfu una machofu6, imma atakwenda kwenye sunnah au ataelekea kwenye bid‘ah (uzushi); kwahivyo yule ambae machofu yake yametokana na kuelekea kwenye sunnah, huyo ameongoka, na yule ambae

1 Bukhâri na Ahmad 2 Ad-Dârimi na Sa‘îd ibn Mansûr katika sunan yake kwa isnâd iliyo swahîh 3 Ahmad kwa isnâd iliyo swahîh 4 Ad-Dârimi na at-Tirmidhî aliyeithibitisha kuwa swahîh 5 Kiarabu; shirrah: uchangamfu, nashât na hima, nguvu. Shirrah ya vijana ni mwanzoni na kuhamasika / ari. Imâm at-Twahâwi amesema: ―Hii ni ari / hamasa za Waislamu katika vitendo vyao vyenye kuwakurubisha kwa Mola wao. Hata hivyo, havikuepukana na makosa na kuwacha baadhi ya vitendo (walivyofanya kutokana na ari hii), kwa

hivyo vitendo vyao vyenye kumridhisha Mjumbe wa Allaah (صىل اهلل عليه وسلم)

ni vile vilivyofanywa kinyume (na kuendelezwa), basi akawâmrisha wafanye vitendo vizuri ambavyo watakavyoweza kuendelea kuvifanya na kudumu navyo hadi watakapomuona Mola wao, Aliyetukuka.

Imepokewa kutoka kwake (صىل اهلل عليه وسلم) katika kuibainisha hii yakwamba

alisema: ―Vitendo vinavyopendeza zaidi mbele ya Allaah ni vile vyenye kudumu zaidi, hata kama ni vichache.‖ Mimi nasema: Hadîth hii ambayo ameitanguliza kwa maneno ―imepokewa‖ ni swahîh, na kuafikiwa na Bukhâri na Muslim kutoka

katika riwaya ya ‗Âisha (رضي اهلل عنها) . 6 Kiarabu; fatrah: Mapumziko, starehe, kupotoka, hapa inahusu kupunguwa kasi ya hima.

67

udhaifu wake na machofu yake yametokana na isiyokuwa sunnah, huyo ameangamia.‖1

Kwa sababu hii, alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) haisomi Qur‘ân kwa

chini ya siku tatu.‖2

Na alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akisema: Mwenye kuswali katika

usiku mmoja kwa âyah mia mbili, mtu huyo atândikwa kama mmojawapo wa wenye kumtwi‘i Allâh‎ wenye kumtakasia ‗Ibaada h3. Pia, ―alikuwa akisoma Sûrah Banî Isrâ‘îl (17:111) na Sûrah az-Zumar (39:75) katika kila usiku.‖4 Pia alikuwa akisema: Mwenye kuswali usiku mmoja kwa âyah mia moja hândikwi katika wenye kughafilika5. Mara nyengine alikuwa akisoma takriban âyât khamsini au zaidi katika kila Rak‘âh ‖6, au ―alikuwa akisoma kiasi cha kipimo cha Sûrah al-Muzzammil (73:20).‖7

―Na hakuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)akiswali usiku mzima8‖

isipokuwa kwa uchache, kwani siku moja:

1 Ahmad na Ibn Hibbân katika swahîh yake. 2 Ibn Sa‘ad (1 / 376) na Abu ash-Sheikh katika ‗Akhlaaq Nabi (281) 3 Ad-Dârimi na Hâkim, aliyeithibitisha kuwa swahîh na akaiafiki adh-Dhahabi 4 ibid 5 Ahmad na ibn Nasr kwa isnâd iliyo swahîh. 6 Bukhâri na Abu Dâwud 7 Ahmad na Abu Dâwud kwa isnâd iliyo swahîh. 8 Muslim na Abu Dâwud. Hadîth hii na nyenginezo imelifanya kuchukiza (makrûh) jambo la kukesha usiku mzima, imma siku zote au mara

nyingi, kwani ni kinyume cha mfano wa Mtume wa Allaah (صىل اهلل عليه وسلم);

kwani lau kama kukesha ni bora, basi Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) angelifanya

hivyo, na uongofu ulio bora ni uongofu wa Muhammad. Kwa hivyo

usidanganywe na yaliyopokewa kutoka kwa Abu Hanîfah (رحمه اهلل)

yakwamba ati aliswali Fajr kwa wudhû‘ wa ‗Ishâ‘ kwa miaka arubaini!! (Tanbîh ya mfasiri: Tizama Tablighi Nisâb: Utukufu wa Swala cha Maulana Zakariyya Kandhalvi kwa mfano wa madai ya aina hiyo) Kwani

68

― ‗Abdullâh‎ ibn Khabbâb ibn al-Arat – aliyeshiriki

katika (vita vya) Badr pamoja na Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)– alikesha

usiku kucha na Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)(katika riwaya nyengine:

katika usiku ambao aliswali kucha) mpaka kulipopambazuka. Basi alipomaliza kuswali, Khabbâb akamwambia: ―Ewe Mjumbe wa

Allâh‎ (صىل اهلل عليه وسلم): Mimi nakukomboa wewe kwa baba yangu na

mama yangu! Usiku huu wa leo, wewe umeswali swala ambayo sijawahi kuiona mfano wake?‖ Akasema: Ndio, hii ilikuwa ni swala ya kupenda kheri na kuogopa shari, na hakika mimi

nilimuomba Mola wangu (عز وجل) mambo matatu; akanipa mawili,

lakini akanikatalia moja. Nilimuomba Mola wangu yakwamba asituangamize sisi kama alivyoYângamiza mataifa kabla yetu (katika riwaya nyengine: yakwamba asiuangamize Ummah wangu kwa ukame) na Akanikubalia mimi hilo; Nilimuomba Mola wangu

yakwamba Asitudhihirishie adui asiyekuwa sisi, na ,(عز وجل)

Akanikubalia mimi hilo; na nikamuomba Bwana wangu Asitutawanye sisi tukawa makundi makundi, lakini Allâh‎ Akanikatalia hilo.‖1

riwaya hii itokayo kwake haina msingi kabisa; kwa hakika ‗Allaamah al-Fairûzabâdi amesema katika ar-Radd alaa al-Mu‘tarid (44 / 1)): ―Riwaya hii ni urongo wa wazi, na wala haiwezi kunasibishwa na Imâm, kwani hakuna chochote chenye ubora kuhusiana na jambo hilo., haliyakuwa ilikuwa ni katika umbile la mfano wa ma-Imâm kufanya yaliyo bora, hapana shaka yakwamba kurudia upya wudhû‘ kwa kila swala ni bora zaidi, ukamilifu zaidi, na bora. Hii ni hata kama ni sawa kwamba alikesha usiku mzima kwa miaka arubaini! Kisa hiki chaonekana kama hekaya, na ni utunzi wa baadhi ya watu wajinga sana, tena walio wakaidi katika walioyashikilia, wenye kuyasema kumuhusu Abu Hanîfah na wengineo, haliyakuwa yote hayo ni urongo mtupu.‖ 1 An-Nasâ‘î, Ahmad na at-Twabarâni (1/187/2); at-Tirmidhî ameithibitisha kuwa swahîh

69

Pia, alisimama Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)usiku mmoja (akiwa kwenye

swala) akiirudia rudia âyah moja mpaka kukapambazuka:

جةدك إن ـ نإجذ ب خ تفذ أ نإذ ٱ فزيز ٱإون تلهر ل ١١٨ ل

“Ikiwa utawâdhibu, basi bila shaka hao ni waja wako; na ukiwasamehe basi kwa hakika wewe ndiye Mwenye nguvu na Mwenye hikima; (hutaambiwa kuwa wamekushinda kuwatia

adabu).” [Mâidah 5:118]

[Na kwa âyah hii akarukû‘, na kwa âyah hii aka-sujudu, na kwa âyah hii akaomba], [Kwa hivyo, asubuhi kulipopambazuka, Abu

Dharr ( عنه اهلل رضي ) akamwambia: ―Ewe Mjumbe wa Allâh‎,

hukuwacha kuendelea kuisoma âyah hii mpaka ikafika asubuhi, ukarukû‘ kwa âyah hii na ukasujudu kwa âyah hii], [na ukaomba kwa âyah hii,] [Na haliyakuwa Allâh‎ Amekufundisha wewe Qur‘ân yote;] [lau angelifanya hivi mmoja wetu tungemuhuzunikia?]

[Akasema: Kwa hakika nimemuomba Mola wangu (عز وجل) Shufâ‘ah kwa Ummati wangu: Akanipa Shufâ‘ah hiyo, na itakuwa ni yenye kupatikana Apendapo Allâh‎ kwa yoyote asiyeshirikisha chochote na Allâh‎.1

Mtu mmoja alimwambia: ―Ewe mjumbe wa Allâh‎, mimi nina jirani yangu anaesimama usiku (akiwa anaswali), na akawa hasomi chochote isipokuwa:

ٱ ى ظد للذ ١أ

[Anairudia rudia], [hazidishi chochote juu ya Sûrah hiyo], Kana

kwamba anaipunguzia fadhla zake.‖ Basi Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

akasema: ―Naapa kwa ambaye nafsi yangu iko katika mikono

1 An-Nasâ‘î, Ibn Khuzaymah (1/70/1), Ahmad, Ibn Nasr na Hâkim, aliyeithibitisha kuwa swahîh na adh-Dhahabi akaiafiki.

70

yake, hakika Sûrah hiyo, (Sûrah al-IkhLaas), inalingana sawa na thuluthi ya Qur‘ân.‖1

7. SWALA YA WITR

Katika Rak‘âh ya kwanza, alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)akisoma:

ٱ شجط ش ع ٱرب١ ل

Na katika Rak‘âh ya pili alikuwa akisoma:

ة ى حأ ٱي ١ هرون ؽ

Na katika Rak‘âh ya tatu alikuwa akisoma:

ى ٱ ظد للذ ١2أ

Mara nyengine alikuwa akiongeza juu ya Sûrah ya mwisho:

« ذ ثرب ى ـ na ١ هو ٱأ ذ ثرب ى ـ

3 ١ جلذةس ٱأ

Siku moja, ―alisoma âyât mia moja kutoka katika Sûrah an-Nisâ‘ katika Rak‘âh ya tatu.‖4 Amma kuhusu Rak‘âh mbili baada ya witr1, alikuwa akisoma:

1 Ahmad na Bukhâri. 2 An-Nasâ‘î na Hâkim, aliyeithibitisha kuwa ni swahîh 3 At-Tirmidhî, Abul ‗Abbâs al-Asamm katika al-Hadîth chake (vol 2 no. 117) na Hâkim, aliyeithibitisha kuwa ni swahîh na ikâfikiwa na adh-Dhahabi 4 An-Nasâ‘î na Ahmad, kwa isnâd iliyo swahîh.

71

رض ٱزلزخ إذاة ل na ١زلزال ة ى ح

أ هرون ٱي ١2 ؽ

SWALA YA JUMU‟AH

Mara nyengine, alikuwa Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل )akisoma Sûrah al-

Jumu‘ah (62:11) katika Rak‘âh ya kwanza na Sûrah al-Munâfiqûn (63:11)3 katika Rak‘âh ya pili:

جهين ٱصةءك إذا ١ لMara nyengine husoma al-Ghâshiyah (88:26):

ظدير دى ٱأ ١ حغظ

1 Ushahidi wa hizi rakâ‘ah mbili unapatikana katika swahîh Muslim na

nyenginezo kama mafundisho ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), lakini yanapinga

maneno yake: ―Ifanyeni swala yenu ya mwisho wa usiku kuwa ni witr‖ – ikapokewa na Bukhâri na Muslim. Wanavyuoni wakakhitilafiana katika kuzipatanisha ahâdîth hizi mbili, na mimi sikuvutiwa na yoyote katika hizo, kwa hivyo jambo kubwa la kujitahadhari nalo ni kuziwacha

rakâ‘ah mbili hizo kulingana na mâmrisho ya Mtume ( سلمصىل اهلل عليه و ). Na

Allaah ni Mjuzi bora wa yote. Baadae, nikaiona hadîth swahîh inayoamrisha kuswaliwa rakâ‘ah mbili

baada ya witr, kwa hivyo amri ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) inakubaliana na

vitendo vyake, na hizi rakâ‘ah mbili ni zenye kuruhusiwa kwa kila mmoja. Kwahiyo, amri ya kwanza ni mojawapo ya yenye kupendekezwa, kutozikatâ rakâ‘ah mbili. Hadîth ya baadae imetajwa katika Silsilat al-ahâdîth as-swahîha (1993) – Tizama katika Kiambatisho 7. 2 Ahmad, Ibn Nasr, at-Twahâwi (1/202), Ibn Khuzaymah na Ibn Hibbân kwa isnâd iliyo hasan swahîh 3 Muslim na Abu Dâwud. Inapatikana katika Irwâ‘ (345)

72

Badala ya hiyo iliyotangulia katika Rak‘âh ya pili1. ―Au mara nyengine alikuwa akisoma Sûrah al-A‘Laa (87:19):

ٱ شجط ش ع ٱرب١ ل

Katika Rak‘âh ya kwanza na Sûrah al-Ghâshiyah (88:26):

ظدير دىحٱأ ١ غظ

Katika Rak‘âh ya pili.‖2

8. SWALA YA „EID

―Na alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) (mara nyengine) akisoma Sûrah

al-A‘Laa (87:19):

ٱ شجط ش ع ٱرب١ ل

Katika Rak‘âh ya kwanza, na Sûrah al-Ghâshiyah (88:26):

دىحٱظدير أ ١ غظ

Katika Rak‘âh ya pili.‖3 Au mara nyengine alikuwa akisoma katika swala hiyo Sûrah Qâf (50:45) na Sûrah al-Qamar (54:55)‖:

ضد ٱ يرءان ٱو ق بخ ٱ na ٢ ل ح ٱ رت ـ ة ر ٱ نظوذ ٱو لصذ ١1 ي

1 ibid 2 Muslim na Abu Dâwud 3 ibid

73

9. SWALA YA JANÂZAH

―Sunnah ni kusoma al-Fâtihah2 [na Sûrah nyengine] katika swala hiyo.‖3 Pia, ―alikuwa akinyamaza kimya kwa muda mchache, baada ya takbîr ya kwanza.‖4

TARTÎL (KUISOMA KWA UTULIVU, NA SAUTI NZURI), NA KUIFANYA SAUTI IWE NI YA KUVUTIA WAKATI WA

KUISOMA

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)alikuwa akiisoma Qur‘ân kwa utulivu, na

mfuatano wa kimahadhi wenye uzani wastani kama alivyoamrishwa na Allâh‎, sio kuisoma haraka haraka, bali kasi yake ilikuwa ni kisomo chenye kufasiriwa harfu kwa harfu‖, kiyasi cha kwamba ―alikuwa akisoma Sûrah kwa utulivu mpaka Sûrah ile inaonekana kuwa ndefu kuliko ilivyo.‖

Vilevile alikuwa akisema: Atâmbiwa mwenye kusoma Qur‘ân (siku ya QiYâmah), ‗Soma na upande daraja na uisome kwa utulivu kama ulivyokuwa ukiisoma katika dunia kwani daraja yako peponi inakuwa ni mwisho wa âyah unayoisoma.

Alikuwa akirefusha kisomo chake (katika harfu za kuvuta), kama vile katika bismil-Laah, katika ar-Rahmân, na katika ar-rahîm‖, na katika ―nadhîd‖ (Sûrah Qâf 50:10) na mfano wa hizo.

1 ibid 2 Huu ni msemo wa Imâm ash-Shâfi‘î, Ahmad na Is-hâq, na baadhi ya ma-Hanafî waliokuja baadae na kufanya utafiti kisha wakachukuwa msimamo huu. Amma kuhusu kusoma sûrah baada ya hiyo al-Fâtihah, basi hii ni rai ya baadhi ya ma-Shâfi‘î na ni rai ya sawa. 3 Bukhâri, Abu Dâwud, an-Nasâ‘î na ibn al-Jârûd. Hiyo nyongeza hapo si Shâdhdh (ngeni) kama anavyofikiriya at-Tuwayjiri 4 An-Nasâ‘î na at-Twahâwi kwa isnâd iliyo swahîh.

74

Alikuwa akikoma mwishoni mwa aya, kama ilivyofahamishwa hapo awali.

Mara nyengine alikuwa akiirudia rudia sauti yake1, kama alivyofanya katika siku ya ufunguzi wa Makka, haliyakuwa yeye alikuwa juu ya mnyama wake, aliposoma Sûrah al-Fat-h [kwa kisomo cha laini]2, na ‗Abdullâh‎ ibn Mughaffal akaiigiza sauti hii ya kuvutia kama : âa.‖3

Na alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)akiamrisha mtu aifanye nzuri

sauti yake anaposoma Qur‘ân, akasema:

ا » ادس ايرآن زي « [ ظصة ايرآن يزيد الص الصت نإن ] ثأص

―Ipambeni Qur‘ân kwa sauti zenu [kwani sauti nzuri huizidisha Qur‘ân uzuri]‖4

1 Tarjî‘ – imechambuliwa kama 2 Bukhâri na Muslim. 3 Ibid. Ibn Hajar amesema katika utangulizi wake kuhusu ―âa (ااا)‖, ―hii

ni hamzah iliyo na fat-hah, ikifuatwa na alif ya kimya, ikifuatwa tena na hamzah nyengine‖. Sheikh ‗Alî al-Qâri, amenukuu hivyo hivyo kutoka kwa wengine kisha akasema: ―Ni wazi yakwamba hizi ni alif tatu zilizorefushwa.‖ 4 Bukhâri kama ta‘lîq, Abu Dâwud, ad-Dârimi, Hâkim na Tammâm ar-Râzi akiwa na swahîh isnâd mbili. TANBÎH: Hadîth hii imegeuzwa na mmojawapo wa wapokezi, aliyeipokea kama ―Zipambeni sauti zenu kwa Qur‘an‖. Haya ni makosa katika riwaya na ufahamu, na yoyote mwenye kuithibitisha kuwa ni swahîh atakuwa amedidimia ndani ya makosa, kwani imekhalifu maelezo ya riwaya iliyoswihi katika kifungu hiki. Kwa hakika, huu ni mfano bora wa maqbûl hadîth, na maelezo kamili kuhusu mukhtasar huu yanapatikana katika Silsilah al-Ahâdîth adh-Dha‘îfah (no. 5328).

75

Na pia akasema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم):

ه إذا الي ثةيرآن صدة اجلةس أظص إن » ه ييرأ شفذ ظصبذ « الل خيش

―Hakika katika watu wenye sauti nzuri zaidi kwa Qur‘ân ni mtu ambaye mukimsikiya akiisoma Qur‘ân, munamdhania kwamba

anamuogopa Allâh‎.‖1

Pia alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)akiwaamrisha kuisoma Qur‘ân

kwa sauti nzuri, akasema:

ا واىذه ودفةدوه الل ذةب دفا » ثده هيس نالي ث ودل « افي ف اخةض أطد

―Jifundisheni Kitabu cha Allâh‎; na mukisome kila mara; na (mukihifadhi) mukimiliki; na kisomeni kwa sauti nzuri, kwani

nâpa kwa ambaye nafsi yangu iko katika Mkono Wake, Qur‘ân ni nyepesi kuponyoka kuliko ngamia kutoka katika kamba zao.‖2

Na akasema tena Mtume (صىل اهلل عليه وسلم):

« ثةيرآن يذل ل ة سي »

1 Hadîth swahîh iliyopokewa na Ibn al-Mubârak katika az-Zuhd (162/1 kutoka katika al-Kawâkib 575), ad-Dârimi, Ibn Nasr, at-Twabarâni, , Abu Nu‘aim katika Akhbâr Isbahân na Diyâ‘ katika al-Mukhtârah. 2 Ad-Dârimi na Ahmad kwa isnâd iliyo swahîh.

76

―Si katika sisi asiyeisoma vizuri Qur‘ân.‖1

Na akasema:

) الصت ظص ] جليب ( أذ : هؼ ويف ) أذن ة لشء الل أذن ة » « [ ث ير ] ثةيرآن يذلن [ ( ات ظص : هؼ ويف

―Hakuna kitu chochote ambacho Allâh‎ (سبحانه وتعاىل) hukisikiliza sana

kama anavyosikiliza (katika riwaya nyengine: kama anavyomsikiza) Mtume [kwa sauti nzuri, na katika riwaya

nyengine: kwa sauti nyororo] mwenye kuisoma Qur‘ân kwa sauti nzuri2 [kwa nguvu].‖3

Alimwambia Abu Mûsa al-Ash‘ari‘ (رضي اهلل عنه) ,

"Lau ungeliniona mimi nikikisikiliza kisomo chako jana usiku! Hakika umepewa mojawapo ya ala za mziki4 za jamii ya Dâwud! [Kisha Abu Mûsa akasema: ―Lau kama ningelijua yakuwa

1 Abu Dâwud na Hâkim, aliyeithibitisha kuwa swahîh na kuafikiwa na adh-Dhahabi. 2 Amesema Mundhiri maana ya taghannâ ina maana ya kusoma kwa sauti nzuri; Sufyân ibn ‗Uyaynah na wengineo wamechukuwa rai yakwamba inahusu istighnâ (yaani kuiwacha Qur‘an imfanye mtu âchane na anasa za kilimwengu), lakini hilo limekataliwa. 3 Bukhâri, Muslim, at-Twahâwi na Ibn Mandah katika Tawhîd (81/1) 4 Wanavyuoni wamesema yakwamba maana ya vyombo vya mziki hapa ni sauti nzuri na kwamba jamii ya Dâwud inamuhusu Dâwud mwenyewe; jamii ya fulani na fulani inaweza kuwa hususan kwa fulani

na fulani peke yao. Dâwud (عليه السالم) alikuwa na sauti nzuri sana. Hii

imetajwa na an-Nawawi katika utangulizi wake wa swahîh Muslim

77

ulikuwepo hapo, ningelikupambia sauti yangu nikaifanya ni yenye kukugusa hisiya yako].‖ 1

KUMKUMBUSHA IMÂM

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)alitufundisha sunnah ya kumkumbusha Imâm

pindi anapochanganyikiwa na kisomo chake, ―aliposwali swala moja, huku akisoma kwa sauti ya juu, mara kisomo chake kikamchanganya, na alipomaliza, akasema kumwambia ‗Ubayy: Wewe uliswali na sisi? Akajibu ‗Ubayy, ‗Na‘am‘. Akasema, basi ni kitu gani kilichokuzuiya [hata hukuweza kunikumbusha]?‖2

KUTAKA HIFADHA NA KUTEMA MATE (KWA KUVUVIA) KATIKA SWALA KWA AJILI YA KUONDOSHA WASIWASI

‗Uthmân Ibn al-‗Âs (رضي اهلل عنه) alimwambia Mtume (صىل اهلل عليه وسلم),

―Ewe Mjumbe wa Allâh‎! Hakika Shetani anakuja baina yangu mimi na swala yangu na ananitatiza katika kisomo changu.‖ Basi

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akasema, ―Huyo ni Shetani anaeitwa

Khinzab, ukimuhisi, taka hifadha na Allâh‎ kwa Shetani huyo, na tema mate kwa kuvivia3 kushotoni kwako mara tatu‖. Akasema

‗Uthmân Ibn al-‗Âs (رضي اهلل عنه) , ―Basi nikalifanya hilo na Allâh‎

Akaniondoshea Shetani huyo.‖4

1 ‗Abdur Razzâq katika al-Amâli (2/44/1), Bukhâri, Muslim, Ibn Nasr na Hâkim 2 Abu Dâwud, Ibn Hibbân, at-Twabarâni, Ibn Asâkir (2/296/2) na Diyâ‘ katika al-Mukhtârah kwa isnâd iliyo swahîh. 3 Kwa kiarabu; Tafl: Kuvivia kwa kupuliza kiwango kidogo cha mate – Nihâyah. 4 Muslim na Ahmad. Amesema an-Nawawi (رحمه اهلل) , ―Hadîth hii

inahimiza kutafuta hifadha kwa Allaah kutokamana na Shetani

78

Ku-rukû‟

baada ya kukamilisha kisomo chake, Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

hunyamaza kidogo1, kisha huinua mikono yake2 katika zile njia zilizoelezwa hapo awali chini ya anwani ―Takbîr ya Ufunguzi‖, aseme takbîr3, na arukû‘.4

Vilevile amemuamrisha ―yule mwenye kuharibu swala yake‖ afanye hivyo, kwa kumwambia, ―Kwa hakika haitatimia swala ya mmoja wenu mpaka akamilishe wudhu‘ kama alivyomuamrisha

Allâh‎ ..., kisha am-Kabbir Allâh‎ (سبحانه وتعاىل), Amsifu na Amtukuze,

kisha na asome Qur‘ân kiasi cha inayosahilika kwake kutokana na alivyomfundisha Allâh‎ na Akamruhusu, kisha aitamke ‗Allâh‎u

anapokushawishi, pamoja na kupuliza mate mara tatu upande wako wa kushoto.‖ 1 Abu Dâwud na Hâkim, aliyeithibitisha kuwa swahîh na kuafikiwa na adh-Dhahabi 2 Bukhâri na Muslim. Huku kuinua mikono kumepokewa kwa njia ya

Mutawâtir kutoka kwake (صىل اهلل عليه وسلم) kama ilivyopokewa kuinua kwake

mikono anaposimama wima baada ya ku-ruku‘. Haya ni katika madh-hab ya ma-Imâm watatu MÂLIK, Shâfi‘î na Ahmad, na kundi kubwa la

ma-Imâm wa hadîth na fiqh. Imâm Mâlik (رحمه اهلل) aliitekeleza sunnah

hiyo hadi kufa kwake, kama ilivyopokewa na Ibn ‗Asâkir (15/78/2). Baadhi ya mahanafî wakachagua kuitekeleza sunnah hiyo, miongoni mwao ni ‗Isâm Ibn Yussuf Abu ‗Asamah al-Balkhi (aliyekufa 210),

mwanafunzi wa Imâm Abu Yusuf (رحمه اهلل) kama ilivyoelezwa katika

utangulizi. ‗Abdullaah Ibn Ahmad akapokea kutoka kwa babake katika Masâ‘il yake (Uk.60), ―Imepokewa kutoka kwa ‗Uqbah Ibn ‗Âmir yakwamba alisema kumuhusu mtu aliyeinua mikono yake wakati anaposwali, ‗Anapata ujira wa malipo mara kumi kwa kila afanyapo hivyo.‖ Hii inaungwa mkono na hadîth Qudsi, ―... yule mwenye kunuilia kufanya jambo zuri na akalifanya, Allaah humuandikia Yeye Mwenyewe kutoka mema kumi hadi mema mia saba.‖ Imepokewa na Bukhâri na Muslim. Angalia katika Swahîh at-Targhîb, no. 16. 3 ibid 4 ibid

79

Akbar‘ na arukû‘, [na aweke mikono yake juu ya magoti yake] mpaka vitulizane na vilegî viungo vyake ...‖1

Namna Ya Ku-Rukû‟

―Na alikuwa Mtume ( ليه وسلمصىل اهلل ع )akiweka vitanga vyake vya

mikono juu ya magoti yake‖2 na ―alikuwa akiwaamrisha maswahaba kufanya hivyo‖3, kama alivyomuamrisha ―yule mwenye kuharibu swala yake‖ kama ilivyotangulia hapo awali katika hadîth .

Na alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)akimakinisha mikono yake juu ya

magoti yake [kana kwamba ameyafumbata yale magoti yake4], na alikuwa akivitenganisha vidole vyake5, na akamuamrisha kufanya hivyo ―yule mwenye kuharibu swala yake‖ kwa kusema: Ukirukû‘, weka vitanga vyako vya mikono juu ya magoti yako, kisha vitenganishe vidole vyako, kisha ubakiye (hivyo hivyo) mpaka kila kiungo kishike mahali pake (panapostahiki).6

Na alikuwa akijikunjua (Yaani; hakuwa akijibana) na akivitenganisha visukusuku vyake mbali na mbavu zake.‖7

―Alipokuwa akirukû‘ alikuwa akiukunjuwa mgongo wake na kuuweka sawa‖8, kiasi cha kwamba hata lau kama maji yangelimiminwa juu ya mgongo wake, (maji hayo) yangelituliya

1 Abu Dâwud na an-Nasâ‘î. Hâkim aliithibitisha kuwa swahîh na adh-Dhahbi akaiafiki. 2 Bukhâri na Abu Dâwud 3 Bukhâri na Muslim 4 Bukhâri na Abu Dâwud 5 Hâkim, aliyeithibitisha kuwa swahîh; wakâfiki hayo adh-Dhahabi na at-Tayâlisi. Inapatikana katika swahîh Abi Dâwud (809) 6 Ibn Khuzaymah na Ibn Hibbân katika swahîh zao 7 At-Tirmidhî aliyeithibitisha kuwa swahîh na Ibn Khuzaymah 8 Bukhâri na al-Baihaqî kwa isnâd iliyo swahîh

80

hapo (Yaani; hayangelimwagika)1. Na pia alisema kumwambia ―yule mwenye kuharibu swala yake‖, ukirukû‘, wekelea vitanga vyako vya mikono juu ya magoti yako, kunjuwa mgongo wako (kwa kuunyosha) na makinika katika Kurukû‘ kwako.2

―Na alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) anaporukû‘, hainamishi kichwa

chake wala hakiinui (Yaani; juu kuliko mgongo wake)‖3, lakini kilikuwa baina ya hapo.4

WAAJIB WA KUTULIZANA KATIKA RUKÛ‟

Na alikuwa Mtume ( يه وسلمصىل اهلل عل ) akitulizana katika Kurukû‘ kwake

na akamuamrisha ―yule mwenye kuharibu swala yake‖ afanye hivyo, kama ilivyotajwa katika sehemu ya kwanza kuhusu rukû‘.

Alikuwa akisema, Kamilisheni kurukû‘ na kusujudu, kwani nâpa kwa ambaye nafsi yangu iko katika mkono wake, hakika mimi ninakuoneni nyie nyuma ya mgongo wangu5 munaporukû‘ na munapo sujudu. ―Na alimuona mtu mmoja ambaye hakamilishi rukû‘ yake kisawasawa, na anadona katika kusujudu kwake na hali yeye anaswali. Mtume akasema, ―Lau angekufa huyu juu ya hali yake hii, angekufa juu ya isiyokuwa mila ya Muhammad, [anadona katika swala yake kama kurabu anavyodona damu] mfano wa mtu ambaye hakamilishi rukû‘ yake na anadona katika Sujûd

1 At-Twabarâni katika Mu‘jam al- Kabîr na Mu‘jam as- Swaghîr, ‗Abdullaah Ibn Ahmad katika az-Zawâ‘id al-Musnad na Ibn Mâjah 2 Ahmad na Abu Dâwud kwa isnâd iliyo swahîh 3 Abu Dâwud na Bukhâri katika Juz‘ al-Qirâ‘ah kwa isnâd iliyo swahîh 4 Muslim na Abu ‗Awânah. 5 Kuona huku ni kwa hakika yake, na ni miongoni mwa miujiza yake ( صىل na ilikuwa ni khaswa kwa hali ya swala tu, wala hakuna dalili ,(اهلل عليه وسلم

juu ya kuenea, labda barabarani pia akitembea huwa yuwaona kwa nyuma, Laa!

81

yake, ni mfano wa mwenye njâ ambaye anakula tende moja au mbili halafu tende hizo hazimtoshelezi kitu chochote.‖1

Abu Hurairah (رضي اهلل عنه) amesema: ― Amenikataza rafiki yangu

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), kudona katika swala yangu kama kudona

kwa Jogoo, pia amenikataza kuzungusha uso kama anavyozungusha uso mbweha na kukaa kama kitako cha nyani.‖2

Pia Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)alikuwa akisema: ―Muovu zaidi wa watu

kwa kuiba ni yule mtu ambaye anaiba katika swala yake‖. Maswahaba wakasema: ―Ewe Mjumbe wa Allâh‎, vipi mtu ataiba

katika swala yake?‖ Akasema Mtume ( يه وسلمصىل اهلل عل ): ―Hakamilishi

rukû‘ yake na Sujûd yake‖.3

Wakati mmoja Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)alikuwa akiswali, mara

akamuona kwa pembe ya jicho lake, mtu ambaye asiyeutuliza uti wake wa mgongo katika kurukû‘ wala kusujudu. Alipomaliza

kuswali, akasema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), ―Enyi kusanyiko la

Waislamu! Kwa hakika, haifai swala ya yule ambaye hautulizi uti wake wa mgongo katika kurukû‘ na ku-Sujûd‖.4

1 Abu Ya‘laa katika Musnad yake (340/3491/1), al-Âjurrî katika al-Arba‘în, al-Baihaqî, at-Twabarâni (1/192/1), Diyâ katika al-Muntaqâ (276/1), Ibn ‗Asâkir (2/226/2, 414/1, 8/14/1, 76/2) kwa isnâd iliyo hasan, na Ibn Khuzaymah akaithibitisha kuwa swahîh (1/82/1). Ibn Battah ana riwaya mursal yenye kuitilia nguvu katika sehemu ya kwanza ya hadîth hiyo, bila ya nyongeza, al-Ibânah (5/43/1). 2 At-Tayâlisi, Ahmad na Ibn Abi Shaybah; ni hasan hadîth, kama nilivyoieleza katika maelezo ya chini katika ukurasa kwenye al-Ahkâm (1348) cha ‗Abdul Haqq Ishbîli. 3 Ibn Abi Shaybah (1/89/2), at-Twabarâni na Hâkim, aliyeithibitisha na ikâfikiwa na adh-Dhahabi 4 Ibn Abi Shaybah (1/89/1), Ibn Mâjah na Ahmad, kwa isnâd iliyo swahîh.

82

Akasema katika hadîth nyengine: ―Swala ya mtu haihesabiwi (haina malipo) mpaka anyoshe uti wake wa mgongo katika rukû‘ na Sujûd‖.1

ADHKÂR ZINAZOLETWA KATIKA RUKÛ‟

Na alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)anasema katika nguzo hii ya

kurukû‘ sampuli sampuli za adhkâr na dua‘, mara nyengine anasoma hii na mara nyengine anasoma hii:

« افؾ ريب شجعةن »―Kutakasika ni kwa Mola wangu, Mtukufu!‖ (utasema) mara tatu2. Lakini mara nyengine, alikuwa akiikariri zaidi ya idadi hiyo.3

Wakati fulani, katika swala ya usiku, aliirudia mara nyingi sana kiasi cha kwamba muda wake aliochukuwa kurukû‘ ukawa ni kiasi cha kisimamo chake kabla ya kurukû‘, ambapo alikuwa amesoma Sûrah tatu ndefu: al-Baqarah, an-Nisâ‘ na Âli-‘Imrân. Swala hii ilikuwa imejâ dua‘ na kutafuta hifadha, na hadîth ishatajwa chini ya ―Kisomo Katika Swala ya Usiku.‖

« وبعده افؾ ريب شجعةن »

1 Abu ‗Awânah, Abu Dâwud na Sahmi (61); Dâraqutnî‘ akaithibitisha kuwa swahîh. 2 Ahmad, Abu Dâwud, Ibn Mâjah, Dâraqutnî‘, at-Twahâwi, Bazzâr na at-Twabarâni katika al-Mu‘jam al-Kabîr, iliyopokewa na maswahaba saba. Kwa hiyo, riwaya hii inawakosoa wale waliopinga kutajwa kwa Utukuzaji mara tatu, kama vile Ibn al-Qayyim na wengineo. 3 Hii inaweza kufasiriwa kutokana na hadîth inayo onyesha wazi

yakwamba Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), alikuwa akiufanya muda wa kisimamo

chake, kuruku‘‘ kwake, na kusujudu kwake sawasawa, kama ilivyotajwa baada ya mlango huu.

83

―Kutakasika ni kwa Mola wangu, Mtukufu, na kila sifa njema‖, (mara tatu)1

« والروح االاسح رب ىدوس شجح »―Mwingi wa Kutakaswa, Mtakatifu2, Mola wa Malaika na Jibrîl.‖3

« ل اكهر ال وبعدك ال شجعة »―Kutakasika ni kwako, Ewe Allâh‎, na Kila Sifa njema ni zako, Ewe Allâh‎ nisamehe.‖

Alikuwa akikithirisha kusema hivi katika kurukû‘ kwake na kusujudu kwake, akitekeleza (maamrisho ya) tafsiri ya Qur‘ân.4

1.

1 Hadîth iliyo swahîh iliyopokewa na Abu Dâwud, Dâraqutnî‘, Ahmad, at-Twabarâni na al-Baihaqî. 2 Amesema Abu Is-hâq: Maana ya Subbûh ni ―Yule aliyîpukana na kila aina ya upungufu‖, na maana ya Quddûs ni ―mwenye Baraka‖ au ―Aliyetakasika‖. Amesema Ibn Saidah: Utukufu na Kutakasika ni

miongoni mwa Sifa za Allaah (سبحانه وتعاىل) kwa sababu anatukuzwa na

anatakaswa na kila kitu. (Lisân al-‗ Arab) 3 Muslim na Abu ‗Awânah 4 Bukhâri na Muslim, maana ya ―Kuifasiri Qur‘an‖ inahusiana na maneno

ya Allaah (سبحانه وتعاىل) :

و نصجط د رب ٱب شذلهره اثا ۥإذ ذ ٣كن د“Basi hapo mtakase Mola wako pamoja na kumsifu, umuombe

maghufira (msamaha); hakika yeye ndiye Apokeaye toba.” [Sûrah Nasr 110:3]

84

خ وب ركفخ ل ال » ل خظؿ [ ريب أخ ] أشخ ول آؾةم روايح ويف )ؾيم ـو ويخ وبرصي شيع صيب ( ـو وة ] ـو

« [ افةي رب لل ىدم ث اشذيخ―Ewe Allâh‎, kwako nimerukû‘, na Wewe nimekuamini na kwako nimejisalimisha (Wewe ni Mola wangu), umenyenyekea kwako usikizi wangu, na uwoni wangu, na ubongo wangu, na mfupa wangu (katika riwaya nyengine: mifupa yangu), na mishipa yangu, [na ambacho kimesimama juu ya miguu yangu1] (ni vyenye kukunyenyekea) Ewe Allâh‎, Mola wa walimwengu wote.]‖2

2.

خ وب ركفخ ل ال » أشخ ول آ أخ دكخ ـوؾيم وليم ودم وبرصي شيع خظؿ ريب لل رب ـصيبو ـو

«افةي ―Ewe Allâh‎, kwako nimerukû‘, na Wewe nimekuamini na kwako nimejisalimisha; na Kwako Wewe ninajitegemeza;

Wewe ni Mola wangu; usikizi wangu, na uwoni wangu, damu yangu, kiwiliwili changu, mifupa yangu, na mishipa

yangu ni yenye kunyenyekea kwa Allâh‎, Mola wa walimwengu.‖3

1 Huu ni mfano utumikao kwenye matamshi ya kikawaida yanayokuja baada ya kutaja mambo makhsusi. 2 Muslim, Abu ‗Awânah, at-Twahâwi na Daraqutnî‘. 3 An-Nasâ‘î kwa isnâd iliyo swahîh. NUKTA: Jî, kuna dalili yoyote ya kuunganisha hizi adhkâr mbili au zaidi katika rakâ‘ah moja, au Laa? Wanavyuoni wamekhitilafiana kuhusu

85

3.

« وافؾح والربيةء وات الربوت ذي شجعةن »―Ametakasika Mwenye Utawala, na Ufalme, na Ukubwa, na Utukufu.‖ Ambayo alikuwa akiisoma wakati wa swala ya usiku.

KUREFUSHA RUKÛ‟

―Alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)akifanya kurukû‘ kwake,

kusimama kwake baada ya rukû‘, kusujudu kwake, na kikao chake cha baina ya sijda mbili, zikikurubiana muda wake.‖1

suala hili. Ibn al-Qayyim hakuwa na hakika kuhusu jambo hili katika Zâd al-Ma‘âd. An-Nawawi alikhiyari kuchagua uwezekano wa kwanza katika al-Adhkâr, akasema: ―Ni jambo zuri kuzichanganya adhkâr hizi ikiwa inawezekana, na vilevile ni sawa tu na adhkâr katika vikao vyengine.‖Abu at-Tayyib Siddîq Hassan Khan hakukubaliana nae, akasema katika Nuzûl al-Abrâr (84), ―Imepokewa na mmoja wao hapa, na mwengine pale, lakini mimi sioni dalili ya kuzichanganya. Mtume

,hakuzichanganya zote kwa kuzifanya mara moja (صلى اهلل عليه وسلم)

lakini alikuwa akisoma mojawapo katika wakati fulani na nyengine wakati ujao, kuandama ni bora kuliko kuzua.‖ Rai hii ni ya sawa, Insha-Allaah, lakini imethubutu katika Sunnah kurefusha kikao hiki, na pia vikao vyengine, mpaka iwe kiyasi cha muda wa kisimamo: Kwa hiyo,

iwapo mwenye kufanya ‗Ibaadah atapendelea kumfuata Mtume ( صلى اهلل ,katika Sunnah hii, njia ya pekî ni kuchanganya hizi adhkâr (عليه وسلم

kama alivyosema an-Nawawi, na kama Ibn Nasr alivyoeleza katika Qiyâm al-Layl (76) kutoka kwa Ibn Jurayj kama ilivyofanywa na ‗Atâ‘, au kuirudia mojawapo ya adhkâr ambayo kunapatikana maandiko yanayoruhusu kurudiwa, na hii ni karibu na Sunnah. Allaah ni Mjuzi bora zaidi. 1 Bukhâri na Muslim. Inapatikana katika Irwâ‘ al-Ghalîl (331).

86

MAKATAZO YA KUISOMA QUR‟ÂN KATIKA KU-RUKÛ‟

―Na alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)akikataza kuisoma Qur‘ân

katika kurukû‘ na kusujudu.‖1 Na zaidi alikuwa akisema, ―Zindukeni, hakika mimi nimekatazwa kuisoma Qur‘ân nikiwa katika hali ya kurukû‘ au hali ya kusujudu. Kwahivyo, katika

rukû‘, mu‘adhimisheni Allâh‎ (عز وجل) katika Utukufu Wake;

amma kuhusu kusujudu, jitahidini katika dua‘, kwani ni hakika kukubaliwa dua‘ zenu.‖2

KUSIMAMA WIMA KUTOKA KATIKA RUKÛ‟ NA LINALOTAKIWA KUSEMWA BAADA YA HAPO

Kisha alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)akiunyûsha mgongo wake

anapotoka kwenye rukû‘, akisema:

« محده الل شؿ »―Allâh‎ Amemsikiya mwenye kumsifu.‖3

Na akamuamrisha ―yule mwenye kuharibu swala yake‖ afanye hivyo, alipomwambia: ―Haikamiliki swala ya yoyote katika watu mpaka … aseme ‗Allâh‎u Akbar‘ …kisha arukû‘ … kisha aseme ‗sami‘Allâh‎u liman hamidah‘ mpaka alingane sawa

1 Muslim na Abu ‗Awânah. Makatazo hayo ni kwa Ujumla, kwani inahusu swala za faradhi na swala za sunnah. Nyongeza katika Ibn ‗Asâkir (17/299/1), ―amma kuhusu swala za sunnah, basi hapana madhara‖ ni imma Shâdh au Munkar – Ibn ‗Asâkir ameutaja udhaifu uliokuwepo – kwa hivyo hairuhusiwi kutekeleza matendo ya hadîth hiyo. 2 ibid 3 Bukhâri na Muslim

87

akiwa amesimama wima.‖1. Na anapoinua kichwa chake, hulingana sawa mpaka kila kiungo kirudi mahali pake‖.2

Kisha, husema haliyakuwa amesimama:

« الد ل [ و ] ربة »Ewe Bwana wetu, (na) ni zako kila Sifa njema.3

Na akamuamrisha hivyo kila mwenye kuswali, ma‘muma au asiyekuwa ma‘muma, afanye hivyo anapoinuka kutoka kwenye rukû‘, kwa kusema:

« أصل رأيذن ة صا »―Swalini kama mulivyoniona nikiswali.‖4

Pia alikuwa akisema:

محده الل شؿ : ىةل وإذا . . ث حلؤد الةم صف إة »ا : نيل

« الد ول ربة [ ال ] )―Hakika ameja‘aliwa Imâm ili afuatwe … na akisema Imâm ‗Sami‘Allâh‎u liman Hamidah‘, semeni ‗Allâh‎umma Rabbanâ

walakal Hamd‘;

1 Abu Dâwud na Hâkim, aliyeithibitisha kuwa swahîh na adh-Dhahabi akâfiki. 2 Bukhâri na Abu Dâwud; kwa kiarabu faqâr: Uti wa mgongo, ―pingili la uti wa mgongo (kuanzia chini ya shingo hadi kwenye kitokono au kifandugu‖ kulingana na Qâmûs; Tazama vilevile Fat-h ul-Bâri (2/308)) 3 Bukhâri na Ahmad 4 ibid

88

Allâh‎ Atawakubaliyeni dua‘ zenu, kwani Allâh‎ (تبارك هلل وتعىل)

amesema juu ya ulimi wa Mtume wake (صىل اهلل عليه وسلم):

‗Sami‘Allâh‎u liman Hamidah.‖1

Vilevile ametoa sababu kwa amri hiyo katika hadîth nyengine, akasema:

«هر ل ة ديدم ذج ك االاسح ىل ىل وانو نإ »Kwani mtu ambaye maneno yake yameafikiana na maneno ya

Malaika, atasamehewa dhambi zake zilizotangulia.2

Alikuwa akiinua mikono yake wakati anaposimama wima1, kulingana na njia zilizoelezwa chini ya ‗Takbîr ya Ufunguzi‘.

1 Muslim, Abu ‗Awânah, Ahmad na Abu Dâwud. TANBÎH: Hadîth hii si yenye kuthibitisha yakwamba wale wenye kumfuata Imâm hawafai kushirikiana nae katika kusema, ―Samiallaahu liman hamidah‖, kama ambavyo haithibitishi yakwamba wale wenye kumfuata Imâm hawafai kushirikiana nae katika kusema, ―Rabbanâ walakal Hamd. Hii ni kwa sababu lengo la hadîth hii si kuweka mpangilio mâlum, yale yenye kuwapasa Imâm na wafuasi wake kusema katika hali hiyo; bali, inafafanua jinsi tahmîd ya ma‘muma inavyoletwa baada ya tasmî‘ ya Imâm. Hili limeungwa mkono na uhakika yakwamba

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alikuwa akiitamka tahmîd alipokuwa ni Imâm, na

pia kwa sababu ufahamu kwa upana wa maneno yake, ―Swalini kama munavyoniona mimi nikiswali‖, inâmuru yakwamba ma‘muma na waseme yale aliyoyasema Imâm, km. Tasmî‘ nk. Wale ndugu zetu waheshimiwa wenye kutuuliza sisi kuhusu mas-ala hayo na wayazingatie haya, na pengine huwenda tuliyoeleza ni yenye kuwatosheleza. Yoyote atakae majadiliano zaidi kuhusiana na mas-ala haya na afanye marejeo kwenye nakala ya al-Hâfidh Suyûti kuhusu mas-ala haya katika kitabu chake al-Hâwi lil Fatâwi (1/529). 2 Bukhâri na Muslim; at-Tirmidhî akaithibitisha kuwa swahîh.

89

Anaposimama, husema, kama ilivyotajwa hapo awali,

1.

« الد ول ربة »Ewe Bwana wetu, (na) ni zako kila Sifa njema2, au

2.

« الد ل ربة »Ewe Bwana wetu, ni zako kila Sifa njema3

Mara nyengine, huongeza mwanzoni mwa yoyote katika hizo:

3. na 4

« ال »Ewe Allâh‎! …4

Alikuwa akiwaamrisha wengine wafanye hivyo, akasema, ―Imâm anaposema: Sami‘Allâh‎u liman Hamidah, na nyinyi semeni: Allâh‎umma! Rabbana Lakal Hamd, kwani yule

1 Bukhâri na Muslim. Huku kuinua mikono hapa kumepokewa kwa njia

ya mutawâtir kutoka kwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), na Wanavyuoni wengi

wameiunga mkono. Wakiwemo baadhi ya ma-Hanafî. Tazama tanbihi iliyotangulia chini ya ukurasa, chini ya kichwa ‗Ruku‘‘. 2 ibid 3 ibid 4 Bukhâri na Ahmad. Ibn al-Qayyim (رحمه اهلل) alikosea kwenye nukta hii

katika Zâd al-Ma‘âd, kwa kupinga kuunganisha, ―Ewe Allaah‖ na ―na‖, licha ya uhakika yakwamba inapatikana riwaya hiyo katika Swahîh al-Bukhâri, Musnad Ahmad, katika an-Nasâ‘î na Ahmad tena kwa kupitia njia mbili za riwaya kutoka kwa Abu Hurairah, katika ad-Dârimi kama hadîth ya Ibn ‗Umar, katika al-Baihaqî kutoka kwa Abu Sa‘îd al-Khudhrî‘, na katika an-Nasâ‘î tena kama hadîth ya Abu Musa al-Ash‘arî.

90

ambaye maneno yake yameafikiana na maneno ya Malaika, husamehewa madhambi yake yaliyotangulia.‖1 Mara nyengine, imma huongezea: 5.

« ثفد يشء طبخ ة ءوم الرض ومء الصةوات مء »―Zimejaa mbingu, na zimejaa ardhi, na zimejaa Sifa zako

Kwa ulichokitaka baada yake‖2, au

6.

طبخ ة ومء ثية وة الرض[ مء ]و الصةوات مء » « ثفد يشء

―Zimejaa mbingu, (na zimejaa) ardhi, na vilivyomo ndani yake Sifa zako, na zimejaa (sifa zako) Kwa ulichokitaka baada yake.‖3 Na mara nyengine atazidisha juu ya hayo:

7.

فخ ة فػى ول أـػخ ة ةؿ ل واضد اثلةء أ » « الد الد ذا يهؿ ول

1 Bukhâri na Muslim; at-Tirmidhî akaithibitisha kuwa swahîh. 2 Muslim na Abu ‗Awânah 3 ibid

91

―Mstahiki wa Sifa na Utukufu! hapana anaeweza kukizuiya ulichokitoa, na wala kutoa ulichokizuiya, na wala

haumnufaishi mwenye utajiri, kwako Wewe utajiri‖1.

Au mara nyengine, nyongeza inakuwa: 8.

يشء ثفد أ طبخ ة ومء الرض ومء الصةوات مء »ل ةؿ [ال ]اثلةء واضد أظو ة ىةل افجد وكة ل ـجد

الد الد ذا يهؿ ول [ فخ ة فػى ول ]ة أـػخ »

―Zimejaa mbingu, na zimejaa ardhi, na zimejaa Sifa zako Kwa ulichokitaka baada yake, Mstahiki wa Sifa na Utukufu! Ni kweli aliyoyasema mja wako, na sote ni waja wako, Ewe

Allâh‎ hapana anaeweza kukizuiya ulichokitoa, [na wala kutoa ulichokizuiya], na wala haumnufaishi mwenye

utajiri, kwako Wewe utajiri.‖2 Mara nyengine alikuwa akisema dhikr ifuatayo katika swala za usiku:

9.

« الد لريب الد لريب »

1 Jadd: Utajiri, Uwezo, Nguvu; yaani, Kwa yule mwenye utajiri, watoto wa kiume, uwezo na nguvu hapa ulimwenguni hatofaidika navyo mbele Yako; Umiliki wake hautomsaidia chochote na Wewe:Vitendo vyema peke yake ndivyo vitakavyomsaidia au kumuokoa mtu yoyote. 2 Muslim na Abu ‗Awânah.

92

―Sifa zote njema Ni zenye kumstahiki Mola wangu, kila sifa njema ni zenye kumstahiki Mola wangu,‖ huendelea

kuikariri hiyo mpaka kisimamo chake kinakisiwa kuwa sawa na kurukû‘ kwake, ambapo ilikuwa ni karibu kusimama kwake kwa kwanza, alikuwa amesoma (ndani ya kule

kusimama kwa kwanza) Sûrah al-Baqarah.‖1

10.

ة ـ جةرك ] ن جةرك غجة سريا محدا الد ول ربة » « [ ويرىض ربة يت

―Ewe Mola wetu, ni zako kila Sifa njema, Sifa nyingi, nzuri, na zenye Baraka [zilizojâ Baraka kama apendavyo Bwana

wetu na aridhiavyo].‖2

Swahaba mmoja aliyekuwa akiswali nyuma yake ( صىل اهلل عليه alipoinua(صىل اهلل عليه وسلم) alisema hivyo baada ya Mtume(وسلم

kichwa chake kutoka kwenye kurukû‘ na akasema:

‗Sami‘Allâh‎u liman Hamidah‘. Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)alipomaliza

kuswali, alisema, ―Ni yupi yule aliyekuwa akisema maneno sasa hivi‖? Akasema yule swahaba, ―Nilikuwa ni mimi, Ewe

Mjumbe wa Allâh‎.‖ Kisha Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)akasema,

―Nimewaona Malaika zaidi ya Thalathini wakiikimbilia kuwa wa kwanza kuiandika.‖3

1 Muslim, Abu ‗Awânah na Abu Dâwud 2 Abu Dâwud na an-Nasâ‘î, kwa isnâd iliyo swahîh. Inapatikana katika Irwâ‘ (no. 335). 3 MÂLIK, Bukhâri na Abu Dâwud.

93

KUREFUSHA KISIMAMO HIKI NA WAAJIB WA KUTULIZANA NDANI YAKE

Na alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)akifanya kisimamo chake hiki

ni karibu na kurukû‘ kwake, kama ilivyotangulia; kwa hakika, ―alikuwa akisimama (kwa muda mrefu) mara nyengine mpaka husema msemaji, ‗Amesahau‘, [kutokana na urefu wa anavyosimama].‖1

Na alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)akiamrisha kutulizana katika

I‘tidâl; hapo akamwambia ―yule mwenye kuharibu swala yake‖, ... ―Kisha inua kichwa chako mpaka ulingane sawa haliyakuwa umesimama [na kila kiungo kikae mahali pake] – katika riwaya nyengine, ―Ukiinuka simamisha mgongo wako na inua kichwa chako, mpaka mifupa irudi kwenye sehemu zake‖.2

1 Bukhâri, Muslim na Ahmad. Inapatikana katika Irwâ‘ (307). 2 Bukhâri na Muslim (kifungu cha kwanza cha maneno peke yake), ad-Dârimi, Hâkim, ash-Shâfi‘î na Ahmad. ‗Mifupa‘ hapa inamânisha ile iliyoko kwenye pingili la Uti wa mgongo, kitokono au kifandugu, kama ilivyokuja kwenye mândishi yaliyotangulia. TANBÎH: Maana ya Hadîth hii ni yenye kudhihiri waziwazi: kutulia katika kisimamo hiki. Amma kuhusu matumizi ya hadîth hii kwa ndugu zetu wa kutoka Hijâz na kwengineko kuwa ni dalili kuruhusu kuweka mikono wa kulia juu ya mkono wa kushoto katika kisimamo hiki, hilo ni mbali kabisa kutoka katika maana ya idadi kubwa ya riwaya za Hadîth hii. Kwa kweli, ni ubishi wa kimakosa, kwa vile kuweka huku kulikotajwa hakuhusishwi na kisimamo cha kwanza katika riwaya yoyote au maneno ya hadîth yenyewe; kwa hivyo, itakuwaje ―mifupa irudi kwenye sehemu zake‖ iliyotajwa katika hadîth imânishe mkono wa kulia kuushikilia mkono wa kushoto kabla ya Ruku‘‘?‘ Hii itakubalika iwapo riwaya zote za hadîth zitafasiriwa kumânisha hivi. Sasa jî, ikiwa watadokeza maana nyengine iliyodhihiri kuwa tafauti? Kwa hakika, huku kuweka kwao hakuwezi kufahamika kutokana na hadîth hiyo kabisa, kwani ‗mifupa‘ inayomânishwa hapa ni mifupa ya Uti wa mgongo, kama

94

Na alimtajia ―yule mwenye kuharibu swala yake‖ yakwamba: ―Haitimii swala ya yoyote katika watu asipofanya hivyo‖, na

alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akisema: ―Haiangalii Allâh‎ ( عز ilivyothibitishwa na Sunnah, ―...atasimama wima mpaka mifupa irudi kwenye sehemu zake‖ Mimi, sina shaka yoyote yakwamba kuweka mikono juu ya kifua katika kisimamo hiki ni Bid‘ah na ni jambo lenye kupoteza, kwani halikutajwa hilo katika ahâdîth zozote zinazohusu Swala, licha ya kuwepo idadi kubwa (ya ahâdîth hizo). Lau kama jambo hilo lingelikuwa na msingi wowote, basi lingelitufikiya sisi hata kwa uchache wa riwaya nyengine. Zaidi ya hayo, hakukupatikana hata Salaf mmoja aliyefanya hivyo, wala hata Mwanachuoni mmoja maarufu wa Hadîth aliyelitaja hilo, kulingana na nijuavyo mimi. Hapa hakuna uwiano na yale aliyoyanukuu Sheikh at-Tuwayjiri katika

nakala yake (UK 18-19) kutoka kwa Imâm Ahmad (رحمه اهلل) , ―Mtu

akipenda, anaweza kuiwacha mikono yake ikining‘iniya kwenye sehemu zake (za mbavu), au, akipenda, anaweza kuiweka juu ya kifua

chake‖, Imâm Ahmad hakuyanasibisha haya na Mtume ( وسلمصىل اهلل عليه ),

lakini aliyasema hayo kutokana na Ijtihâd yake na rai, na rai huwenda ikawa ni ya makosa. Ushahidi ulio swahîh unapothibitisha hali ya uzushi wa jambo lolote, kama jambo hili, basi maneno ya Imâm katika kulitetea hayakanushi kuwa hilo ni jambo la uzushi, kama alivyoandika

Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyyah (اهلل رحمه) . Kwa hakika, katika maneno

yake haya, mimi naona ishara yakwamba Imâm Ahmad hakuhusisha huko kuweka kulikotajwa hapo juu, kuwa kumethibitishwa katika Sunnah, kwani aliruhusu kuchaguwa baina ya kulitekeleza jambo hilo na kuliwacha! Jî, Sheikh muheshimiwa, anadhani yakwamba Imâm vilevile ameruhusu chaguo kama hilo kuhusu kuweka mikono kabla ya kuruku‘‘? Kwa hivyo, imethubutu yakwamba kuweka mikono juu ya kifua katika kisimamo cha baada ya kuruku‘ si sehemu ya Sunnah. Huu ni mjadala kwa mukhtasar kuhusiana na mas-ala haya, mjadala ambao unaoweza kushughulikiwa kwa kina na upana zaidi, lakini kutokana na uchache wa nafasi hapa, unaofanyika badala yake katika ukosoaji dhidi ya Sheikh at-Tuwayjiri.

95

swala ya mja ambaye hasimamishi mgongo wake baina ya (وجل

rukû‘ yake na sujûd yake.1

KU-SUJUDU

Kisha ―alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)akitamka ‗Allâh‎u Akbar‘ akiwa

katika hali ya kusujudu‖2 na akamuamrisha ―yule mwenye kuharibu swala yake‖, afanye hivyo, na akamwambia, ―Haitimii swala ya yoyote katika watu mpaka aseme: ‗Sami‘Allâh‎u liman Hamidah‘, mpaka alingane sawa katika hali ya kusimama, kisha aseme, ‗Allâh‎u Akbar‘ kisha asujudu mpaka vitulizane viungo vyake‖.3

Vilevile alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)akitaka kusujudu, hutamka

‗takbîr‘, [na huiweka mbali mikono yake kwa kuiepusha na mbavu zake], kisha husujudu.4

Na ―alikuwa mara nyengine akiinua mikono yake akitaka kusujudu.‖5

1 Ahmad na at-Twabarâni katika Mu‘jam al-Kabîr kwa isnâd iliyo swahîh. 2 Bukhâri na Muslim 3 Abu Dâwud na Hâkim, aliyeithibitisha kuwa swahîh na kuafikiwa na adh-Dhahabi. 4 Abu Ya‘laa katika Musnad yake (284/2) kwa isnâd nzuri na Ibn Khuzaymah (1/79/2) kwa isnâd tafauti iliyo swahîh. 5 An-Nasâ‘î, Dâraqutnî‘ na Mukhlis katika al-Fawâ‘id (1/2/2) kwa isnâd mbili zilizo swahîh. Huku kuinua mikono kumepokewa kutoka kwa Maswahaba kumi, na idadi kubwa ya Salaf wakaionelea kuwa ni sawa, wakiwemo miongoni mwao, Ibn ‗Umar, Ibn ‗Abbâs, Hassan al-Basrî, Twâwûs, mwanae ‗Abdullaah, Nâfi‘n – mtumwa wa Ibn ‗Umar aliyewachwa huru, Sâlim – mwanae Ibn ‗Umar, Qâsim Ibn ‗Umar,

96

KUPOMOKA HALI YA KWENDA KWENYE SAJDAH KWA MIKONO

―Na alikuwa akiweka mikono yake juu ya ardhi kabla ya magoti yake.‖1

Na alikuwa akiamrisha hivyo, kwa kusema, ―Akisujudu mmoja wenu, asikite magoti yake kama anavyokita magoti Ngamia, lakini na aweke mikono yake kwanza kabla ya magoti yake‖.2

‗Abdullaah Ibn Dînâr na ‗Atâ‘. ‗Abdur-Rahman Ibn Mahdi pia alisema, ―Hii ni katika Sunnah‖, ilitekelezwa na Imâm wa Sunnah, Ahmad Ibn Hanbal, na imenukuliwa kutoka kwa Mâlik na ash-Shâfi‘î. 1 Ibn Khuzaymah (1/76/1), Dâraqutnî‘, na Hâkim aliyeithibitisha kuwa swahîh na adh-Dhahabi akâfiki. Ahâdîth zote zinazokwenda kinyume na hii si swahîh. Njia hii imeungwa mkono na MÂLIK, na yakapokewa kama hayo kutoka kwa Ahmad katika kitabu cha Ibn al-Jawzî kiitwacho at-Tahqîq (108/2). Vilevile al-Marwazî amenukuu kwa isnâd iliyo swahîh, Imâm al-Awzâ‘i katika kitabu chake Masâ‘il (1/147/1) akisema, ―Mimi nimewaona watu wakitanguliza kuweka mikono yao kabla ya magoti yao.‖ 2 Abu Dâwud, Tammâm katika al-Fawâ‘id, na an-Nasâ‘î katika as-Sughrâ na Sunan al-Kubrâ (47/1) kwa isnâd iliyo swahîh. ‗Akaithibitisha kuwa swahîh ‗Abdul Haqq katika al-Ahkâm (54/1), na akaendelea kusema katika Kitâb at-Tahajjud (56/1), ―ina isnâd yenye nguvu zaidi kuliko ile iliyotangulia‖, yaani, hadîth ya Wâ‘il ambayo ni kinyume cha hivyo (magoti kabla ya mikono). Kwa hakika, hadîth hiyo iliyokuja, pamoja na kwamba inapingana na hadîth hii iliyo swahîh na ile iliyotangulia, haikuswihi katika isnâd yake wala katika maana yake, kama nilivyoyafafanua katika Silsilah ahâdîth adh-Dha‘îfah (no. 929) na al-Irwâ‘ (357). Inatakiwa ijulikane yakwamba njia ya kutafautiana na Ngamia ni kutanguliza kuweka mikono kabla ya magoti, kwa sababu Ngamia hutanguliza magoti yake kwanza; ―Magoti‖ ya Ngamia yako kwenye miguu yake ya mbele, kama yalivyoelezwa kwenye Lisân al-‗Arab na vitabu vyengine vya lugha ya Kiarabu, na kama alivyotaja at-Twahâwi katika Mushkil al-Âthâr na Sharh Ma‘âni al-Âthâr. Vilevile Imâm Qâsim

al-Saraqusti (اهلل رحمه) akapokea katika Gharîb al-Hadîth (2/70/1-2), kwa

isnâd iliyo swahîh. Qauli ya Abu Hurairah, ―Asipige magoti mtu yoyote

97

Na pia alikuwa akisema, ―Hakika (vitanga viwili vya) mikono vinasujudu kama unavyosujudu uso, kwa hivyo akiweka mmoja wenu uso wake (juu ya ardhi), na aweke mikono yake, na akiuinua (uso wake), na aiinue (mikono yake)‖.1

NAMNA YA KU-SUJUDU

―Na alikuwa akitegemea juu ya vitanga vyake (na akivikunjua)‖2, na ―akikusanya vidole vyake pamoja‖3, na ―akivielekeza upande wa qiblah.‖4

Vilevile alikuwa akiviweka (vitanga vyake) sawa na mabega yake5, na mara nyengine ―sawa na masikio yake‖6. Alikuwa akiweka pua yake na bapa lake la uso juu ya ardhi.‖1

kama afanyavyo Ngamia mtoro‖, kisha akaongezea, ―Hii ni katika Sajdah. Anasema mtu na asijibwage chini, kama afanyavyo Ngamia mtoro (au Ngamia mwitu), mbiombio na bila ya utulivu, lakini na apomoke kwa utaratibu, kwa kutanguliza mikono yake mwanzo, kisha yafuate magoti yake, na imepokewa hadîth marfû‘ yenye kufafanua kuhusu mas-ala haya.‖ Kisha akaitaja hiyo hadîth iliyoko hapo juu. Amma kuhusu maneno ya Ibn al-Qayyim ya kushangaza, ―Maneno haya hayaeleweki, na wala hayaeleweki na hata mabingwa wa lugha‖, hayo yamejibiwa na asili tulizozitaja, na nyengine ambazo zinazohitaji kupekuliwa. Pia nimefafanua kuhusiana na mas-ala haya katika kumkosoa Sheikh at-Tuwayjiri, ambayo huwenda ikachapishwa. 1 Ibn Khuzaymah (1/79/2), Ahmad na Sirâj; Hâkim akaithibitisha kuwa swahîh na adh-Dhahabi akaiafiki. Inapatikana katika Irwâ‘ (313). 2 Abu Dâwud na Hâkim, aliyeithibitisha kuwa swahîh na kuafikiwa na adh-Dhahabi. 3 Ibn Khuzaymah, al-Baihaqî na Hâkim aliyeithibitisha kuwa swahîh na kuafikiwa na adh-Dhahabi. 4 al-Baihaqî kwa isnâd iliyo swahîh. Ibn Abi Shaybah (1/82/2) na Sirâj, wamepokea kuhusu kuvielekeza vidole (vya miguu) katika riwaya nyengine. 5 Abu Dâwud na at-Tirmidhî, aliyeithibitisha kuwa swahîh, kama alivyofanya Ibn al-Mulaqqin (27/2); Inapatikana katika Irwâ‘ (309). 6 Abu Dâwud na an-Nasâ‘î kwa isnâd iliyo swahîh.

98

Na alimwambia ―yule mwenye kuharibu swala yake‖, ―Unaposujudu, basi makinika katika sijda yako‖2; katika riwaya nyengine: ―Unaposujudu, makinisha uso wako na mikono yako juu ya ardhi, mpaka mifupa yako itulizane kwenye mahali pake.‖3

Na alikuwa akisema, ―Hakuna swala kwa mtu ambaye pua yake haiipati ardhi kiyasi ambacho hupata bapa lake la uso.‖4

Alikuwa akimakinisha magoti yake na ncha za vidole vya miguu yake katika ardhi5, na akivielekeza qiblah, ncha za vidole vyake vya miguu yake6, ncha za vidole vyake vya miguu‖, akivishikanisha visigino vyake7, akiistawisha miguu yake sawasawa‖8, na akaamrisha jambo hilo.9‖ Na alikuwa akivipindisha vidole vyake vya miguu ili vielekî qiblah.

Hivi ndivyo viungo saba ambavyo alivyokuwa Mtume ( صىل اهلل عليه akisujudu juu yake, vitengele viwili vya mikono, na magoti(وسلم

mawili, na miguu miwili, na bapa la uso na pua - na Mtume ( صىل 1 Abu Dâwud na at-Tirmidhî, aliyeithibitisha kuwa swahîh, kama alivyofanya Ibn al-Mulaqqin (27/2); Inapatikana katika Irwâ‘ (309). 2 Abu Dâwud na Ahmad kwa isnâd iliyo swahîh. 3 Ibn Khuzaymah (1/10/1) kwa isnâd iliyo hasan 4 Dâraqutnî‘, at-Twabarâni (3/140/1) na Abu Nu‘aim katika Akhbâr isbahân. 5 Al-Baihaqî kwa isnâd iliyo swahîh. Ibn Abi Shaybah (1/82/2) na Sirâj wamepokeya kuhusu kuelekeza vidole upande wa qiblah katika riwaya nyengine. 6 Bukhâri na Abu Dâwud, Ibn Sa‘d (4/157) akapokea kutoka kwa Ibn ‗Umar yakwamba alikuwa akipenda kuelekeza qiblah, kila kiungo cha mwili wake awezacho, anaposwali, hata vidole Gumba vyake. 7 At-Twahâwi, Ibn Khuzaymah (no. 654) na Hâkim, aliyeithibitisha kuwa swahîh na kuungwa mkono na adh-Dhahabi 8 Al-Baihaqî kwa isnâd iliyo swahîh. 9 At-Tirmidhî na Sirâj. Hâkim akaithibitisha kuwa swahîh na kuafikiwa na adh-Dhahabi.

99

akaja‘aliya hivi viungo viwili vya mwisho kuwa ni kama(اهلل عليه وسلم

kiungo kimoja katika kusujudu pindi aliposema: ―Nimeamrishwa kusujudu (na katika riwaya nyengine: ―Tumeamrishwa kusujudu) juu ya viungo saba: juu ya bapa la uso ..., na akâshiriya kwa mkono wake1 katika pua yake, ...na mikono miwili, (na katika riwaya nyengine : na vitanga viwili vya mikono), na magoti mawili, na ncha za vidole vya miguu miwili, na tusikusanye2 nguo na nywele.‖3

Na alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)akisema, ―Anaposujudu mtu,

husujudu nae viungo saba, uso wake, vitanga vyake viwili, na magoti yake na miguu yake.‖4

Alisema kuhusu mtu mmoja aliyekuwa akiswali haliyakuwa nywele zake zimefungwa5 nyuma yake, ―Hakika mfano wa huyu, ni mfano wa mtu ambae anaswali na hali yeye ni mwenye kufungwa mikono yake (nyuma ya mgongo wake)6. Na akasema

1 Huku kuashiriya kwa mkono wake kumetokana na ithbati iliyoko kutoka kwenye Lugha ya ―Kiarabu‖ (Fat-h al-Bârî). 2 Yaani; kuzifungasha na kuzizuiya zisitapakae, kwa maana ya kuzikusanya nguo au nywele kwa mkono kwa ajili ya kuruku‘‘ na kusujudu (Nihâyah). Makatazo haya si makhsusi kwa wakati wa swala tu; Wanavyuoni wengi wameingiza kuzifungasha nywele na nguo kabla ya swala katika makatazo. Yamekokotezwa haya kwa kuwakataza kwake wanaume kuswali haliyakuwa wamezisuka nywele zao, itakayofuata baadae. 3 Bukhâri na Muslim. Inapatikana katika Irwâ‘ (310) 4 Muslim, Abu ‗Awânah na Ibn Hibbân 5 Zilizosukwa au kusongwa. 6 Muslim, Abu ‗Awânah na Ibn Hibbân. Amesema Ibn al-Athîr: ―Maana ya hadîth hii ni kwamba, lau kama nywele zake zingelikuwa hazikufungwa, zingelitulia juu ya ardhi wakati wa kusujudu; kwahivyo, mtu atapata thawabu kwa ajili ya kusujudu kwa nywele zake. Lakini ,ikiwa nywele zimewekewa kibano, matokeo yake ni kama kwamba hazikusujudu, kwani alizifananisha na mtu ambae mikono yake imetiwa pingu, kwa vile zitakuwa hazikutulia juu ya ardhi kwa kusujudu.‖

100

pia, ―hapo ni makaazi ya Shetani‖, Yaani; anapokâ Shetani, akikusudia mafundo katika nywele.1

Na ―alikuwa haiegemezi mikono yake (sehemu ya kuanziya kwenye vitanga vya mikono hadi kwenye visukusuku) juu ya ardhi2‖, lakini ―alikuwa akiiweka mbali na ardhi, na akiiweka (mikono hiyo yake) kando ya mbavu zake, mpaka hudhihiri weupe wa makwapa yake kutoka kwa nyuma yake3‖, na pia ―kiyasi cha kwamba lau mtoto wa mbuzi au mtoto mchanga angelitaka kupita chini ya mikono yake, angeliweza kufanya hivyo.‖4

Na alikuwa akizidisha katika jambo hilo mpaka wakasema baadhi

ya maswahaba zake, ―Tulikuwa tukimuhuzunikiya Mtume ( صىل اهلل عليه kwa jinsi alivyokuwa akiiweka mbali mikono yake kuiepusha(وسلم

na mbavu zake anaposujudu.‖5

Na alikuwa akiamrisha jambo hilo, akisema, ―Ukisujudu, weka vitanga vyako vya mikono (katika ardhi) na uinue tindi zako mbili (visukusuku vyako6), na mulingane sawa katika kusujudu, na wala asitandike mmoja wenu dhirâ zake katika ardhi kama kutandika kwa Mbwa (katika riwaya nyengine ... ―kama

Inaonekana hapa yakuwa mâgizo haya ni yenye kuwahusu wanaume peke yao na wala haiwahusu wanawake, kama alivyonukuu Imâm ash-Shawkâni kutoka kwa Ibn al-‗Arabî. 1 Abu Dâwud, at-Tirmidhî, aliyeithibitisha kuwa hasan; Ibn Khuzaymah na Ibn Hibbân wameithibitisha kuwa swahîh. Tazama Swahîh Abi Dâwud (653) 2 Bukhâri na Abu Dâwud 3 Bukhâri na Muslim. Inapatokana katika Irwâ‘ (359) 4 Muslim, Abu ‗Awânah na Ibn Hibbân. 5 Abu Dâwud na Ibn Mâjah kwa isnâd iliyo hasan. 6 Muslim na Abu ‗Awânah.

101

anavyotandika dhirâ zake, Mbwa)1. Katika hadîth nyengine, ―...na asitandike mmoja wenu dhirâ zake katika ardhi kama anavyotandika Mbwa dhirâ zake.‖2 Na pia alikuwa akisema, ―Usitandike dhirâ zako [kama afanyavyo mnyama mbwa], jitulize juu ya vitanga vyako na uiweke mbali mikono yako, kwani ukiyafanya yote hayo, basi kila kiungo chako kitasujudu pamoja na wewe.‖3

WAAJIB WA KUTULIZANA KATIKA KU-SUJUDU

Alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)akiamrisha kukamilisha na kutimiza

rukû‘ na Sujûd, na alikuwa akimpigia mfano asiyefanya hivyo na mwenye njâ anayekula tende moja au mbili zisizomtosheleza kitu chochote, na pia kusema kuhusu mtu huyo; ―hakika yeye ni katika watu wabaya kwa kuiba.‖

Pia alihukumu yakwamba swala ya mtu ambaye hasimamishi mgongo wake kikamilifu katika kurukû‘ na kusujudu haifai, kama ilivyotajwa chini ya ―kurukû‘‖, na akamuamrisha ―yule mwenye kuharibu swala yake‖, kutulizana katika kusujudu, kama ilivyotangulia katika mwanzo wa mlango huu.

DHIKR ZA KUSUJUDU.

Alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)akisema aina tafauti-tafauti ya

adhkâr na dua‘ alipokuwa kwenye mkao huu wa kusujudu:

1.

1 Bukhâri, Muslim, Abu Dâwud na Ahmad 2 Ahmad, na at-Tirmidhî, aliyeithibitisha kuwa swahîh 3 Ibn Khuzaymah (1/80/2), al-Maqdisi katika al-Mukhtârah na Hâkim aliyeithibitisha kuwa swahîh na kuafikiwa na adh-Dhahabi.

102

« ( مرات زالث ) الع ريب شجعةن »―Ametakasika Mola wangu aliye juu‖ (atasema hivi mara

tatu).1 Mara nyengine ―huirudia hiyo mara nyingi zaidi ya hivyo.‖2 Wakati mmoja aliikariri sana kiyasi cha kwamba muda wa ku-sujudu kwake ukawa karibu na muda wa kisimamo chake, ambacho alichosoma Sûrah tatu zile ndefu: al-Baqarah, an-Nisâ‘, na âl-‘Imrân. Swala hiyo ilijâ dua‘ nyingi sana na kuomba maghfirah, kama ilivyotajwa hapo awali chini ya mlango ―Swala Ya Usiku.‖ 2.

«( زالزة ) وبعده الع ريب شجعةن »―Ametakasika Mola wangu aliye juu na kila Sifa njema ni

Zake.― (atasema hivi mara tatu).‖3 3.

«والروح االاسح رب ىدوس شجح »―Mwingi wa kutakaswa, Mtakatifu, Mola wa Malaika na

Jibrîl.‖4

4.

1 Ahmad, Abu Dâwud, Ibn Mâjah, Dâraqutnî‘, at-Twahâwi, Bazzâr na at-Twabarâni katika al-Mu‘jam al-Kabîr kutoka kwa maswahaba saba tafauti. Angalia pia Hâshiyah (fût-note) kuhusu dhikr hii chini ya mlango wa ―Ruku‘‘. 2 Tazama Hâshiyah (fût-note) iliyotangulia kabla ya hii chini ya mlango wa ―Ruku‘‘‖ pia. 3 Swahîh, imepokewa na Abu Dâwud, Dâraqutnî‘, Ahmad, at-Twabarâni na al-Baihaqî. 4 Muslim na Abu ‗Awânah

103

« ل اكهر ال وبعدك ربة ال شجعة »―Kutakasika ni Kwako, Yâ Allâh‎, Mola wetu, na Sifa njema

zote ni Zako, Yâ Allâh‎ nisamehe‖;

Ambayo huisema kila mara anapo-rukû‘ na kusujudu, akitekeleza maamrisho ya Qur‘ân.1 5.

خ وب شضدت ل ال » شضد [ ريب وأخ ] أشخ ول آ ] وبرصه شف وطو [ صره نأظص ] وصره يخ للي وصيه

« اخلةيي أظص الل دجةرك [ ف―Yâ Allâh‎, kwako nimesujudu, na Wewe nimekuamini, na

kwako nimesilimu, umesujudu uso wangu kumsujudia aliyeuumba na akautia sura na akaupasua usikizi wake na

uwoni wake, ametukuka Allâh‎, Mbora wa waumbaji!‖2

6.

اليذ وآخره وأول وص ودى لك ذيب ل اكهر ال » ورسه ـو»

―Yâ Allâh‎ nisamehe dhambi zangu zote, ndogo na kubwa, za mwanzo na za mwisho, za dhahiri na za siri.‖3

1 Bukhâri na Muslim. 2 Muslim, Abu ‗Awânah, at-Twahâwi na Dâraqutnî‘. 3 Muslim na Abu ‗Awânah

104

7.

ادي ل شضد » وخةل ش ء نؤادي ث وآ ع ثفذ أث « هيس ع صخ وة يدي - ذي

―Vimekusujudia Wewe kiwiliwili changu na kivulivuli changu, na moyo wangu umekuamini Wewe, nakiri nîma zako juu yangu: mikono yangu iko hapa na kila nilichokichuma dhidi ya nafsi yangu.‖1 8.

« وافؾح والربيةء وات الربوت ذي شجعةن »

―Ametakasika Mwenye Utawala, na Ufalme, na Ukubwa, na Utukufu.‖2

Aliyokuwa akiisoma katika swala za usiku, kama alivyokuwa akisoma na zifuatazo: 9.

« أخ إل إل ل وبعدك [ ال ] شجعة »―Kutakasika ni kwako [Yâ Allâh‎] na Sifa njema zote ni zako,

hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Wewe.―3

1 Ibn Nasr, Bazzâr na Hâkim, aliyeithibitisha kuwa swahîh, lakini adh-Dhahabi hakuiafiki, hata hivyo, inayo usaidizi uliotajwa katika makaratasi ambayo hayajachapishwa 2 Abu Dâwud na an-Nasâ‘î kwa isnâd iliyo swahîh. 3 Muslim, Abu ‗Awânah, an-Nasâ‘î na Ibn Nasr.

105

10.

«أرسرت وة أـخ ة ل اكهر ال »―Yâ Allâh‎! Nisamehe yale (madhambi) ambayo

niliyoyaficha na yale (madhambi) ambayo niliyoyafanya dhahiri.‖1

11.

شيع ف واصف [ را ينلصة ويف ] را ىيب ف اصف ال » نيق واصف را تت واصف را ثرصي ف واصف را را يصةري را واصف أةم را ـو واصف -ين را ـو

« را ل وأـؾ [ را هيس ف واصف ] را خيف―Yâ Allâh‎! Weka katika moyo wangu nuru, [na katika ulimi wangu nuru]. Na uja‘aliye katika masikio yangu nuru, na

uja‘aliye katika macho yangu nuru, na uja‘aliye chini yangu nuru, na uja‘aliye juu yangu nuru, na kuliani kwangu nuru, na kushotoni kwangu nuru. Na uja‘aliye mbele yangu nuru –

Na uja‘aliye nyuma yangu nuru, [na weka katika nafsi yangu nuru], na unifanyie kubwa nuru.‖2

12.

1 Ibn Abi Shaybah (62/112/1) na an-Nasâ‘î; Hâkim ameithibitisha kuwa swahîh na adh-Dhahabi akaiafiki 2 Muslim, Abu ‗Awânah na Ibn Abi Shaybah (12/106/2, 112/1)

106

ثفةنةد [ أـذ ]ثرطةك شخػ و أـذ [ إين ] [ ال ] » ة أخ ـ زةء أظيص ل ث وأـذ ـيبذ

« هص ع أزنخ―[Yâ Allâh‎]! [Hakika mimi] najilinda kwa radhi Zako

kutokana na hasira Zako, na [najilinda] kwa msamaha Wako kutokana na adhabu Yako, na najilinda Kwako

unihifadhi na Wewe, mimi siwezi kuzidhibiti sifa Zako, Wewe kama ulivyojisifu Mwenyewe.‖1

MAKATAZO YA KUISOMA QUR‟ÂN KATIKA KUSUJUDU.

Alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akikataza kuisoma Qur‘ân katika

kurukû‘ na kusujudu, na alikuwa akiamrisha kujitahidi na kukithirisha dua‘ katika nguzo hii ya kusujudu kama ilivyopita katika ―rukû‘‖. Pia alikuwa akisema, ―Mahali karibu zaidi anapokuwa mja na Bwana wake ni hapo wakati akisujudu, kwa hiyo kithirisheni dua‘ [mukiwa hapo].‖2

KUREFUSHA KUSUJUDU.

Alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akija‘aliya kusujudu kwake ni karibu

na kurukû‘ katika kurefusha, na huwenda akazidisha katika kurefusha kwa jambo lililozuka kama walivyosema baadhi ya Maswahaba:

―Alitutokea Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)katika mojawapo ya swala

mbili za kuchelewa (Dhuhr au ‗Asr) akiwa amembeba Hasan au

Husein. Kisha Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)akaja mbele na akamshukisha

1 ibid 2 Muslim, Abu ‗Awânah na al-Baihaqî. Inapatikana katika Irwâ‘ (456).

107

chini [kando ya mguu wake wa kulia], akaleta takbîr ya swala na kuanza kuswali. Alipokuwa kwenye swala, alisujudu kwa muda mrefu sana, basi mimi nikainua kichwa changu [miongoni mwa watu], mara nikamkuta yule mtoto ananing‘iniya juu ya mgongo

wa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), aliyekuwa kwenye sijdah. Kisha mimi

nikarudi kwenye sijdah yangu. Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)alipomaliza

kuswali, watu wakasema, ―Ewe Mjumbe wa Allâh‎! Wakati ulipokuwa katikati ya (hii) swala yako, ulisujudu na ukairefusha sana sijda yako mpaka tukadhaniya yakwamba imma kumetokea kitu au labda ulikuwa ukipokea wahyi!‖ Akasema, Yote hayo hayakuwa: Kwa hakika, mtoto wangu (mjukuu wangu) alinifanya mimi ni kipando chake, basi mimi sikutaka kumuharakisha mpaka amalize haja yake.1

Katika hadîth nyengine, Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alikuwa akiswali.

Alipokuwa amesujudu, al-Hasan na al-Husein wakamdandia mgongoni mwake. Watu walipojaribu kuwazuiya, , aliwâshiriya kwa kuwadokeza yakwamba wawachane na hao vijana wawili. baada ya kumaliza kuswali, aliwapakata kwenye mapaja yake na kusema, ―Yoyote mwenye kunipenda mimi na awapende hawa wawili.‖2

1 An-Nasâ‘î, Ibn ‗Asâkir (4/257/1-2) na Hâkim aliyeithibitisha kuwa swahîh na adh-Dhahabi akaiafiki. 2 Ibn Khuzaymah katika swahîh yake, kwa isnâd iliyo hasan kutoka kwa Ibn Mas‘ud (887) na al-Baihaqî kwa njia ya mursal. Ibn Khuzaymah akaitangulizia na, ―Mlango: Dalili yakwamba kuashiriya ukiwa ndani ya swala kunakofahamika, hakubatilishi wala hakuharibu swala‖ – Kitendo hiki ndicho kile ambacho walichokikataza watu wa Rai! Kuhusiana na mas-ala haya, vilevile kuna ahâdîth zinazopatikana kutoka kwa Bukhâri, Muslim na wengineo.

108

FADHLA ZA KUSUJUDU

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)alikuwa akisema, Hakuna yoyote katika

Ummati wangu, isipokuwa mimi nitamjua Siku ya QiYâmah. Wakasema, ―Utawajuaje, Ewe Mjumbe wa Allâh‎, miongoni mwa halaiki ya viumbe siku hiyo?‖. Mtume akasema, ―Waonaje lau kama mmoja wenu angeliingia ndani ya banda ambalo ndani yake kuna farasi aliye shujâ, na rangi yake ni mweusi tititi1 na farasi mwengine mwenye alama nyeupe kwenye kipaji chake na miguu yake2, kweli utashindwa kuwatambua kwa alama zao hizo na kuwatenganisha‖? Wakasema, ―Hapana shaka juu ya hilo‖. Akasema, ―Kwa hiyo,Kwa hakika Ummah wangu siku hiyo watakuwa na nyuso nyeupe3 kwa ajili ya kusujudu, na mikono meupe na miguu meupe4 kwa ajili ya kutawadha.‖5

Vilevile alikuwa akisema, Allâh‎ akimtakia Rehma anaemtaka katika watu wa motoni. Huwâmrisha Malaika wamtoe yoyote aliyekuwa akimuabudu Allâh‎; kwa hiyo watawatoa na watawajua kutokana na athari za kusujudu, kwani Allâh‎ ameharamisha juu ya moto, kula athari za sijdah. Kwa hivyo, watatolewa motoni,

1 Yaani; Rangi yake ni nyeusi iliyozagâ mwili mzima, bila ya mchanganyiko wa rangi nyengine yoyote. (Nihâyah) 2 Weupe ni ule ulio kwenye sehemu ya farasi katika bangili anazofungwa nazo au cheni yake, na sehemu ya chini ya miguu yake, isipokuwa magoti. 3 Yaani; kung‘ara kwa nyuso kwa ajili ya muangaza wa sujûd. 4 Yaani; kung‘ara kwa sehemu zilizoenezwa wudhû‘: Uso, mikono na miguu. Alama za kung‘ara za wudhû‘ katika sehemu za uso, mikono na miguu ya wanâdamu yanalinganishwa na weupe wa uso wa farasi na miguu. 5 Ahmad kwa isnâd iliyo swahîh. At-Tirmidhî ameipokea sahemu yake na akaithibitisha kuwa ni swahîh. Inapatikana katika Silsilah al-Ahâdîth as-Swahîhah.

109

kwani moto utakula kiwiliwili chote cha mwana-adamu isipokuwa ile athari ya kusujudu1

KUSUJUDU JUU YA ARDHI NA JUU YA ZULIYA2

Na alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)akisujudu juu ya ardhi (kavu)

Sana3.―Maswahaba zake walikuwa wakiswali na yeye katika joto kali, asipoweza mmoja wao kumakinisha bapa lake la uso katika ardhi, hukunjua nguo yake na akaitandika, kisha akasujudu juu yake.‖4

Pia alikuwa akisema, ―...Ardhi yote imefanywa kuwa ni mahali pa kufanya ‗ibaada h (masjid) na mahali pa kujitwahirisha kwangu mimi na Ummah wangu; kwa hivyo, popote itakapomdiriki swala, mtu yoyote katika Ummah wangu, basi hapo ni mahali pake pa kuswaliya (masjid) na ni mahali pake pa kujitwahirisha.‖ Na walikuwa waliotangulia kabla yangu wakidhaniya yakwamba hilo limepita kiyasi (ni zito kwao): Kwa hakika wao walikuwa wakiswali kwenye makanisa yao na ma-sinagogi yao peke yake.5

Mara nyengine alikuwa akisujudu kwenye udongo na maji, na lilimtokea hilo katika alfajiri ya usiku mmoja wa tarehe ishirini na moja ya mwezi wa Ramadhân, kuliponyesha mvua, na pâ la msikiti lililotengezwa kwa makuti ya mtende lilipochukuliwa na

1 Bukhâri na Muslim, hadîth hii yaonyesha yakwamba wale ma‘âsi miongoni mwa wenye kuhudhuria swala, hawatobakiya motoni milele; kwa hakika, hata wale wenye kuzikosa swala kutokana na uvivu hawatobaki motoni milele, hii ni swahîh – angalia as-Swahîhah (2054) 2 Kiarabu; hasîr: mkeka uliotengezwa kwa majani ya mtende au ‗Miyâ‘ (au Nyâ), n.k 3 Hii ni kwa sababu msikiti wake haukuwa na mikeka, n.k; imedhihiri hii kutokana na ahâdîth nyingi, mfano wa ifuatayo na baadae ya Abu Sa‘îd. 4 Muslim na Abu ‗Awânah 5 Ahmad, Sirâj na al-Baihaqî, kwa isnâd iliyo swahîh.

110

maji. Kwahivyo, Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)akasujudu kwenye udongo

na maji; Abu Sa‘îd al-Khudhrî akasema: ―Basi nikaona, kwa

macho yangu, Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), akiwa na alama za udongo na

maji katika bapa lake la uso na pua yake.‖1

Pia ―alikuwa akiswali juu ya Khumrah‖2 mara nyengine, au ―juu ya zuliya‖3 mara nyengine, na ―aliswali juu yake wakati mmoja lilipopiga weusi kutokana na kukaa kwake sana.‖4

KUINUKA KUTOKA KWENYE SAJDAH

Kisha, ―alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)akiinua kichwa chake kutoka

kwenye Sujûd na huku akileta takbîr‖5, na akamuamrisha ―yule mwenye kuharibu swala yake‖ afanye hivyo, akasema, Haitimii swala ya yoyote katika watu mpaka ... asujudu mpaka viungo vyake vitulizane, kisha akasema, ‗Allâh‎u Akbar‘ na ainue kichwa

1 Bukhâri na Muslim. 2 Ibid. Khumrah ni kipande cha mkeka, ukuti, au kitandiko fulani chenye ukubwa kiyasi cha mtu kuweka bapa lake la uso ili aweze kusujudu juu yake; neno hili halitumiki kwa pande kubwa la tandiko. 3 ibid 4 Muslim na Abu ‗Awânah. Kiarabu; Labisa kwa kawaida ina maana ya ‗Kuvâ‘, lakini hapa imetumika kumânisha ‗Kutumia‘, yaani; kukâ juu yake; kwa hiyo, ‗kuvâ‘ inahusu pia ‗kukâ juu yake‘, kwa hivyo hii inâshiriya yakwamba imeharamishwa (harâm) kukâ juu ya hariri, kwa sababu ya kuharamishwa kuivâ iliyothubutu katika swahîh al-Bukhâri na Muslim, na wengineo. Kwa kweli, uharamu wa dhahiri wa kuketi juu ya hariri umepokewa katika hadîth hizi, kwa hivyo usibabaishwe kwa ukweli yakwamba baadhi ya Wanavyuoni wakubwa wameliruhusu hilo. 5 Bukhâri na Muslim

111

chake mpaka alingane haliyakuwa amekaa sawa sawa1. Pia, ―mara nyengine huinua mikono yake anapoleta takbîr hii.2

KUKAA MUFTARISHAN BAINA YA SIJDA MBILI

Kisha ―anaulaza mguu wake wa kushoto juu ya ardhi na anakâ juu yake (katika hali ya kutulizana3)‖, na akamuamrisha hayo ―yule mwenye kuharibu swala yake‖ , akasema kumwambia, Unaposujudu, makinika katika sijdah yako, kisha unapoinuka,

keti juu ya paja lako la kushoto.4 Na ―alikuwa Mtume ( صىل اهلل عليه

1 Abu Dâwud na Hâkim, aliyeithibitisha kuwa swahîh na adh-Dhahabi akaiafiki. 2 Bukhâri katika Juz‘ Raf al-Yadayn, Abu Dâwud kwa isnâd iliyo swahîh, Muslim na Abu ‗Awânah. Inapatikana katika Irwâ‘ (316). Kuinua mikono hapa, na pamoja na kila takbîr ni rai iliyoanzishwa na Ahmad, kama ilivyo katika kitabu cha Ibn al-Qayyim, Badâ‘i‘ (3/89): ―Amepokea Athram kutoka kwake (Imâm Ahmad) yakwamba alipoulizwa kuhusu kuinua mikono, alisema: Kwa kila harakati, juu na chini. Athram akasema: Nimemuona Abu ‗Abdullaah (yaani; Imâm Ahmad) akiinua mikono yake kwenye swala katika kila harakati chini na juu.‖ Hii pia ilikuwa ndiyo rai ya Ibn al-Mundhir, na Abu ‗Ali katika madh-hab ya ash-Shâfi‘î, na pia rai ya Mâlik na ash-Shâfi‘î, wao wenyewe, kama ilivyo katika Tarh at-Tathrîb. Kuinua mikono hapa vilevile kumeswihi kupokewa kwake kutoka kwa Anas Ibn MÂLIK, Ibn ‗Umar, an-Nâfi‘î, Twâwûs, Hasan al-Basrî, Ibn Sirîn na Ayyûb as-Sakhtiyaani, kama ilivyo katika Musannaf Ibn Abi Shaybah (1/106) kwa riwaya zilizo swahîh kutoka kwao. 3 Ahmad na Abu Dâwud kwa isnâd iliyo nzuri. 4 Bukhâri na al-Baihaqî

112

,akisimamisha mguu wake wa kulia1‖, na ―akielekeza qiblah (وسلم

vidole vyake vya miguu.‖2

KIKAO CHA IQ‟Â‟ BAINA YA SIJDA MBILI Mara nyengine alikuwa akikaa kitako cha Iq‘â‘ [kuvikalia visigino vyake viwili na vidole vyake (vyote) vya miguu].‖3

WAAJIB WA KUTULIZANA BAINA YA SIJDA MBILI

1 An-Nasâ‘î kwa isnâd iliyo swahîh. 2 Muslim, Abu ‗Awânah, Abu Shaikh, katika Mâ Rawâhu Abu az-Zubair ‗an Ghayr Jâbir (no. 104-6) na al-Baihaqî. 3 Ibid; Ibn al-Qayyim (اهلل رحمه) amepitikiwa katika jambo hili, kwahivyo

baada ya kutaja iftirâsh ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) baina ya sijdah mbili,

alisema, ―hakuna njia yoyote nyengine ya kikao iliyopokewa kutoka kwake‖! Itawezekanaje hii kuwa ni sawa, haliyakuwa iq‘â‘ imetufikia sisi kwa njia ya: Hadîth ya Ibn ‗Abbâs kutoka kwa Muslim, Abu Dâwud, na at-Tirmidhî, aliyeithibitisha kuwa swahîh, na wengineo (angalia katika Silsilah al-Ahâdîth as-Swahîhah 383); Hadîth ya Ibn ‗Umar kwa isnâd iliyo hasan katika al-Baihaqî, ikathibitishwa uswahîh wake na Ibn Hajar. Pia akapokea Abu Is-hâq al-Harbi katika Gharîb al-hadîth (5/12/1) kutoka kwa Twâwûs, aliyewaona Ibn ‗Umar na Ibn ‗Abbâs wakitekeleza kikao cha iq‘â‘; isnâd yake ni swahîh. Twamuomba Allaah Amteremshie Rehma zake Imâm MÂLIK, aliyesema: ―Kila mmoja wetu anaweza kumkosoa mtu na yeye mwenyewe kukosolewa isipokuwa mwenye kaburi hili‖, na akâshiriya kwa kidole chake kwenye kaburi la

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم). Sunnah hii ilitekelezwa na Maswahaba wengi,

Matâbi‘î na wengineo, na mimi nikayaeleza kuhusiana na hayo katika al-Asl. Ndiyo, iq‘â‘ hii ni tafauti na iq‘â‘ ile iliyoharamishwa, ifuatayo chini ya ―Tashahhud‖.

113

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)alikuwa akitulizana mpaka kila mfupa urudi

mahali pake (pa asili)1, na akamuamrisha hivyo ―yule mwenye kuharibu swala yake‖, akamwambia, ―Haitimii swala ya mmoja wenu yoyote mpaka afanye hivyo.‖2

KUREFUSHA KIKAO BAINA YA SIJDA MBILI

Pia ―alikuwa akikirefusha kikao hicho mpaka kikafikiya muda wa sijdah yake3‖, na mara nyengine, alikuwa akibakiya hapo (katika

kikao hicho) mpaka husema mwenye kusema: Amesahau.‖4

ADHKÂR BAINA YA SIJDA MBILI

Na ―alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)akisema akiwa katika kikao hiki:

1 Abu Dâwud na al-Baihaqî kwa isnâd iliyo swahîh 2 Abu Dâwud na Hâkim, aliyeithibitisha kuwa swahîh na adh-Dhahabi akaiafiki. 3 Bukhâri na Muslim 4 Ibid; Amesema Ibn al-Qayyim, ―Sunnah hii imesusiwa na watu baada ya wakati wa Maswahaba. Lakini kwa yule mwenye kushikamana na Sunnah, na akawa hângalii pambizoni, kutazama kitu chochote chenye kuikhalifu sunnah hiyo, yeye hababaishwi na chochote chenye kuupinga uongofu huu.‖

114

1.

] [ واصربن ] وارمحن ل اكهر ( رب : هؼ ويف ) ال » « وارزىن [ واعنن ] - وادين [ وارنفن

―Yâ Allâh‎ [na katika lafdh nyengine: Ewe Mola] Nisamehe na unirehemu, [na uniunge], [na uniinue daraja yangu], na

uniongoze – [na unipe afya], na uniruzuku.‖1

Au mara nyengine alikuwa akisema:

2.

« ل اكهر ل اكهر رب »Mola wangu! Nisamehe, Nisamehe.2

Alikuwa akisema dhikr hizo mbili hapo juu katika swala za usiku vilevile.3

1 Abu Dâwud, at-Tirmidhî, Ibn Mâjah na Hâkim, aliyeithibitisha na adh-Dhahabi akaiafiki. 2 Ibn Mâjah, kwa isnâd iliyo hasan. Imâm Ahmad alichagua kuomba kwa Dua‘ hii; Is-hâq Ibn Râhaway akasema, ―Akipenda, anaweza kusema dhikr hii mara tatu, au aweza kusema ―Yâ Allaah! Nisamehe ...‖, kwa

sababu zote hizo zimepokewa kutoka kwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) baina ya

sijdah mbili.‖ (Masâ‘il ya Imâm Ahmad na Is-hâq Ibn Râhaway, kama ilivyopokewa na Is-hâq al-Marwazî Uk. 19). 3 Hii haikanushi ruhusa ya kutumia matamshi yaliyo katika swala za faradhi kutokana na ukosefu wa chochote chenye kutafautisha baina ya adhkâr hizo na zile za Sunnah. Hii ni rai ya ash-Shâfi‘î, Ahmad na Is-hâq, aliyeshikiliya yakwamba hii yaruhusiwa katika swala ya faradhi na Sunnah, kama alivyopokea at-Tirmidhî. Vilevile Imâm at-Twahâwi amechukuwa msimamo huu katika Mushkil al-Âthâr. Uchambuzi wa kina unaunga mkono hoja hii, kwani hakuna nafasi yoyote kwenye swala

115

SIJDA YA PILI

Kisha, alikuwa akisema ―Allâh‎u Akbar‖ na akisujudu mara ya pili.‖1. Na alimuamrisha kufanya hivyo ―yule mwenye kuharibu swala yake‖, akimwambiya baada ya kumuamrisha kutulizana baina ya sijdah mbili, Kisha sema ‗Allâh‎u Akbar‘ na usujudu mpaka viungo vyako vitulizane [na ufanye hivyo katika swala yako yote]2. Alikuwa akiitekeleza sijdah hiyo, Kama vile alivyoitekeleza sijdah ya kwanza. Pia, alikuwa akiinua mikono yake pamoja na takbîr hii mara nyengine.3

Kisha ―huinua kichwa chake na huku akisema ―Allâh‎u Akbar‖‖4, na akamuamrisha ―yule mwenye kuharibu swala yake‖ afanye hivyo, akamwambia baada ya kumuamrisha asujudu kwa mara ya pili, ―kisha inua kichwa chako na useme ―Allâh‎u Akbar‖‖5. Pia akamwambia, [―kisha fanya hivyo katika kila raka‘ah na kila sijdah,] kwani ukifanya hivyo swala yako itakuwa imekamilika, na lau utapunguza kitu katika hivyo, utakuwa na upungufu katika swala yako.6‖ Na pia, alikuwa akiinua mikono yake7 mara nyengine pamoja na takbîr hii.

ambapo dhikr imekatazwa, kwa hivyo, inatoshea hapa yakwamba hali ndiyo itakuwa hivyo. 1 Bukhâri na Muslim 2 Abu Dâwud na Hâkim, aliyeithibitisha kuwa swahîh na adh-Dhahabi akaiafiki; nyongeza hiyo ni ya Bukhâri na Muslim 3 Abu ‗Awânah na Abu Dâwud, kwa sanad mbili zilizo swahîh. Huku kuinua mikono kumeungwa mkono na Ahmad, MÂLIK, na ash-Shâfi‘î kutoka katika riwaya walizopokea wao. Tizama nukta iliyotangulia chini ya Mlango wa ―Sujûd‖. 4 Bukhâri na Muslim. 5 Abu Dâwud na Hâkim, aliyeithibitisha kuwa swahîh na adh-Dhahabi akaiafiki. 6 Ahmad na at-Tirmidhî, aliyeithibitisha kuwa swahîh. 7 Angalia nukta inayofuata baada ya hii.

116

KIKAO CHA KUPUMZIKA

Kisha, Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)alikuwa akilingana sawa katika hali ya

kukaa [juu ya mguu wake wa kushoto, hali ya kuwa sawasawa, mpaka urudi kila mfupa kwenye mahali pake].‖1

KUJISAIDIA KWA MIKONO KATIKA HALI YA KUINUKA KWA RAK‟ÂH NYENGINE

Kisha, Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)alikuwa akiinuka kwa Rak‘âh ya pili,

kwa kujisaidia juu ya ardhi.‖2 Pia ―alikuwa akikunja ngumi zake3 wakati akiwa kwenye swala: kwa kuilemea mikono yake anapoinuka.‖4

1 Bukhâri na Abu Dâwud. Kikao hiki chajulikana kwa jina la Jalsah al-Istirâhah (kikao cha kupumzika) na Wanavyuoni wa fiqh. Ash-Shâfi‘î akaiunga mkono, kama alivyofanya Ahmad katika Tahqîq (111/1) na kuongeza nguvu zaidi katika kuipendelea, kama inavyojulikana katika sifa zake yakwamba anapenda kusisitiza juu ya kuifuata Sunnah isiyokuwa na chochote cha kupingana nayo.. Akasema Ibn Hâni katika Masâ‘il ya Imâm Ahmad (Uk. 42), ―Nilimuona Abu ‗Abdullaah (yaani; Imâm Ahmad) mara nyengine akijiegemeza juu ya mikono yake anapotaka kusimama kwa rakâ‘ah inayofuata, na mara nyengine akijituliza katika kikao chake na kisha huinuka.‖ Hilo pia lilikuwa ni chaguo la Imâm Is-hâq Ibn Râhaway, aliyesema katika Masâ‘il ya

Marwazi (1/147/2), tuliekewa mfano na Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) wa

alivyokuwa akijisaidia kwa mikono yake anapotaka kusimama, akiwa ni kijana au hata mzî.‖ Pia tizama Irwâ‘ (2/82-3). 2 Bukhâri na ash-Shâfi‘î 3 Maana halisi, ―kama mtu anaekanda unga.‖ 4 Abu Is-hâq al-Harbi kwa sanad isiyo na dosari yoyote na ufafanuzi wake unapatikana katika Baihaqî kwa sanad swahîh. Ama kuhusu hadîth, ―Alikuwa akiinuka kama mshale, bila ya kujisaidia kwa mikono yake‖, hiyo ni mawdhû‘ (imezuliwa), na riwaya zote zenye maana mfano wake ni dha‘îf, si swahîh, na mimi nimeyaeleza hayo katika Silsilah al-Ahâdîth adh-Dha‘îfah (562, 929, 968).

117

RAK‟ÂH YA PILI

Alipokuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)akiinuka kwa Rak‘âh ya pili,

huanza na AlhamdulilLaah (Fâtihah 1:1), bila ya kupumua.‖1

Na alikuwa akifanya katika Rak‘âh ya pili kama alivyofanya katika Rak‘âh ya kwanza, isipokuwa alikuwa akiifanya fupi kuliko ya kwanza, kama ilivyotangulia.

WAAJIB WA KUSOMA FÂTIHAH KATIKA KILA RAK‟ÂH

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)alimuamrisha ―yule mwenye kuharibu swala

yake‖ asome al-Fâtihah katika kila Rak‘âh , alipomwambia baada ya kumuamrisha aisome kwenye Rak‘âh ya kwanza2, ―kisha fanya hivyo katika swala yako yote‖3 (katika riwaya nyengine: katika kila Rak‘âh 4). Pia alikuwa akisema, Katika kila Rak‘âh kuna kusoma (Fâtihah)5.

1 Muslim na Abu ‗Awânah. Kupumua kuliko katazwa katika hadîth hii, hwenda kukawa ni kupumua kwa ajili ya kusoma dua‘ ya ufunguzi, bila ya kuhusisha kupumua kwa ajili ya kusoma isti‘âdhah, au hwenda ikawa na maana pana zaidi kuliko hivyo; Mimi naona uwezekano uliotajwa mwanzo una nguvu zaidi. Kuna maoni mawili miongoni mwa Wanavyuoni kuhusiana na isti‘âdhah, na sisi twaonelea ya sawa kuwa ni ile isemwayo katika kila rakâ‘ah; Masimulizi kwa kina ya yote hayo yametolewa kwenye al-Asl. 2 Abu Dâwud na Ahmad kwa sanad iliyo na nguvu. 3 Bukhâri na Muslim 4 Ahmad kwa isnâd nzuri 5 Ibn Mâjah, Ibn Hibbân katika swahîh yake na Ahmad katika Masâ‘il ya

Ibn Hâni (1/52). Jâbir Ibn ‗Abdillaah ( عنه اهلل رضي ) amesema, ―Mwenye

kuswali rakâ‘ah ambayo ndani yake hakusoma ―Mama wa Qur‘an‖, basi huwa hajaswali, isipokuwa ikiwa alikuwa nyuma ya Imâm‖ – imepokewa na Mâlik katika al-Muwatta‘

118

TASHAHHUD YA KWANZA

Kisha, Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)alikuwa akikaa kwa ajili ya tashahhud

baada ya kumaliza Rak‘âh ya pili. Katika swala ya Rak‘âh mbili kama vile, Fajr, ―alikuwa akikaa muftarishan‖ (kikao cha kukalia miguu)1, kama alivyokuwa akikaa baina ya sijdah mbili, nae ―alikuwa akikaa katika tashahhud ya kwanza kama vile alivyokuwa akikaa2 kwenye swala ya Rak‘âh tatu au nne.

Na amemuamrisha hivyo ―yule mwenye kuharibu swala yake‖, akamwambia, ―Ukikaa katikati ya swala, tulizana, na utandaze paja lako la kushoto, kisha soma tashahhud.‖3

Amesema Abu Hurairah (رضي اهلل عنه) : ―Rafiki yangu ( صىل اهلل عليه amenikataza mimi nisichotame (Iq‘â‘) kama mbwa‖4; katika(وسلم

hadîth nyengine, ―Alikuwa akikataza mchotamo wa (kikao cha) Shetani.‖5 ―Alipokuwa akikaa katika tashahhud, alikuwa akiweka kitanga chake cha kulia juu ya paja lake la kulia (kwenye riwaya nyengine: juu ya goti lake la kulia), na alikuwa akiweka kitanga chake cha kushoto juu ya paja lake la kushoto, (kwenye riwaya nyengine: juu ya goti lake la kushoto, hali ya kuvikunjua (hivyo

1 An-Nasâ‘î (1/173) kwa isnâd iliyo Swahîh. 2 Bukhâri na Abu Dâwud 3 Abu Dâwud na al-Baihaqî kwa sanad iliyo nzuri. 4 Tayâlisi, Ahmad na Ibn Abî Shaybah. Kuhusu iq‘â‘, Amesema Abu ‗Ubaydah na wengineo yakwamba, ―Ni pale mtu anapokalia kwa kitako chake juu ya ardhi, akasimamisha wima miundi yake ya miguu, na akailemea mikono yake aliyojizuiya juu ya ardhi, kama mfano anavyofanya mbwa. Hii ni tafauti na kikao cha iq‘â‘ baina ya sijdah mbili, kikao ambacho kilichoruhusiwa katika Sunnah, kama ilivyotangulia kuelezwa. 5 Muslim, Abu ‗Awânah na wengineo. Imetajwa katika Irwâ‘ (316).

119

vitanga vyake))‖1; na alikuwa akiweka ncha ya kisukusuku chake (tindi) cha kulia juu ya paja lake la kulia.‖2 Pia, ―alimkataza mtu mmoja aliyekuwa amekaa katika swala na huku amejitegemeza juu ya mkono wake wa kushoto na akamwambia: ―Kwa hakika, hiyo ni swala ya Mayahudi‖3; katika riwaya nyengine, ―Usikae namna hii, kwani kwa hakika hiki ni kikao cha wale walioadhibiwa‖4; katika hadîth nyengine, ―ni jinsi ya kikao cha wale waliopata ghadhabu (za Allâh‎).‖5

KUTINGISHA KIDOLE KATIKA TASHAHHUD

Alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)akikunjua kitanga chake cha kushoto

juu ya goti lake la kushoto, na alikuwa akikunja vidole vyake vyote vya kitanga chake cha kulia, huku akielekeza Qiblah kwa kidole chenye kufuata kidole gumba, na macho yake akiwa anakiangalia kidole hicho.6‖

1 Muslim na Abu ‗Awânah 2 Abu Dâwud na an-Nasâ‘î kwa Sanad iliyo Swahîh. Ni kama kwamba maana yake alikuwa hatenganishi baina ya visukusuku vyake na mbavu zake, kama alivyofafanua zaidi Ibn al-Qayyim katika Zâd al-Ma‘âd. 3 Baihaqî na Hâkim, aliyeithibitisha kuwa swahîh na adh-Dhahabi akaiafiki. Inapatikana pamoja na hiyo ifuatayo, katika Irwâ‘ (380). 4 Ahmad na Abu Dâwud kwa isnâd iliyo nzuri. 5 ‗Abdur-Razzâq, ‗Abdul Haqq akaithibitisha kuwa swahîh katika kitabu chake, Ahkâm (no. 1284 – kwa usahihishaji wangu). 6 Muslim, Abu ‗Awânah na Ibn Khuzaymah. Humaidi (13/1) na Abu Ya‘laa (275/2) akaongezea kwa sanad iliyo swahîh kutoka kwa Ibn ‗Umar: ―Na huu ni ushambulizi dhidi ya Shetâni; hapana atakaesahau baada ya kufanya hivi‖, na Humaidi akakiinua kidole chake. Pia Humaidi akasema yakwamba Muslim Ibn Abî Maryam alisema, ―Mtu mmoja alinihadithia mimi yakwamba katika Kanisa huko Syria, aliona picha za Mitume zimechorwa kama hivi‖, na Humaidi akainua kidole chake. Haya ni matamshi ya kushangaza mno, lakini sanad yake mpaka kufikia kwa ―mtu mmoja‖ ni swahîh

120

Pia, ―alipokuwa akionyesha kwa kidole chake, alikuwa akiweka kidole chake cha gumba juu ya kidole chake cha katikati1‖, na mara nyengine ―alikuwa akifanya duara kwa vidole hivyo viwili2‖.

Alipokuwa akiinua kidole chake (cha shahada), alikuwa akikitingisha, akiomba kwa kidole hicho3‖, na alikuwa akisema,

1 Muslim na Abu ‗Awânah 2 Abu Dâwud, an-Nasâ‘î, Ibn al-Jârûd katika al-Mutaqâ (208), Ibn Khuzaymah (1/86/1-2) na Ibn Hibbân katika Swahîh yake (485) kwa sanad iliyo Swahîh. Ibn al-Mulaqqin pia akaithibitisha kuwa ni swahîh (28/2) na ina riwaya yenye kuipa nguvu katika Ibn ‗Adi (287/1). 3 Ibid. Kuhusu ―akiomba kwa kidole hicho‖, , amesema Imâm at-Twahawi, ―Huu ni ushahidi yakwamba ilikuwa ni mwishoni mwa swala.‖ Kwa hiyo, kuna ushahidi hapa yakwamba Sunnah ni kuendelea kukinyosha (kuashiriya) na kukitingisha kidole mpaka taslîm (utoapo salaam), kwani maombi huendelea mpaka hapo. Hii ni rai ya Mâlik na wengineo. Imâm Ahmad aliulizwa, ―Jî, inampasa mtu kuashiriya kwa kidole chake akiwa kwenye swala?‖ Nae akajibu, ―Ndio, tena kwa nguvu.‖ (Yametajwa na ibn Hâni katika Masâ‘il ya Imâm Ahmad yake, 1/80). Kutokana na haya, imedhihiri hapa yakwamba kutingisha kidole

katika tashahhud ni Sunnah iliyothubutu kutoka kwa Mtume ( صىل اهلل عليه na ilitekelezwa na Ahmad na ma-Imâm wengine wa Sunnah. Kwa ,(وسلم

hivyo wale wanaodhania yakwamba jambo hilo halina maana na haliingii akilini na wala halina mafungamano yoyote na swala, na wamche Allaah, kwani kutokana na hayo, wao hawatingishi vidole vyao ingawaje wanajua vyema yakwamba hiyo ni Sunnah iliyothubutu; na pia hujikalifisha kwa kila njia katika kuitolea ta‘wili Sunnah hii ambayo ‗Uslubu wa kiarabu‘ haufahamishi ta‘wili hiyo na kinyume cha ufahamu swahîh wa ma-Imâm kuhusiana na suala hilo. Jambo la kushangaza ni kwamba baadhi yao humtetea Imâm kuhusu mas‘ala mengine, hata kama rai yake inakhalifiana na Sunnah, kwa hoja yakwamba kuyabainisha makosa ya Imâm iwapo hapana budi ni kumânisha yakwamba huko ni kumsuta na kumkosea adabu. Kisha wao husahau haya na huikanusha Sunnah hii iliyothibitishwa, na hapo hapo wakânza kuwafanyia istihzâ‘ wale wanaoitekeleza Sunnah hiyo. Iwapo wao ni wenye kuyazingatia hayo au laa, kuikejeli kwao Sunnah hii vilevile kunawahusu ma-Imâm hao hao ambao wao huwatetea

121

―Kwa hakika (Kidole hicho cha shahada) ni kikali dhidi ya Shetani kuliko chuma‖, akimânisha kidole cha shahada.‖1

Pia ―Maswahaba wa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)walikuwa

wakikumbushana, Yaani, kuhusu kunyosha kidole wakati wa dua‘.‖2 Siku moja, ―alimuona mtu mmoja akiomba huku amenyosha vidole viwili, basi akamwambia, ―Fanya kwa kidole

kimakosa, na ambao wamepata kuihusu Sunnah hii! Kwa hakika wao

wanamkejeli Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) mwenyewe, kwani yeye ndiye

aliyetuletea sisi Sunnah hiyo, na kuizomea (kuizoma) Sunnah hiyo ni

sawa na kumzomea (kumzoma) yeye mwenyewe; Mtume (صىل اهلل عليه وسلم).

« Lakini ni yapi malipo ya wale miongoni mwenu wenye tabia kama hiyo

isipokuwa ... «

Amma kuhusu kuteremsha kidole chini baada ya kukinyosha, au kukinyosha kiasi cha muda fulani wa kukanusha (kusema laa ilaaha: ‗hapana mola ...‘) na kuthibitisha (kusema illallaahu: ‗... isipokuwa Allaah), yote hayo hayana msingi wowote katika Sunnah; kwa hakika, ni kinyume cha Sunnah, kama hadîth hii inavyothibitisha. Zaidi ya hayo, hadîth yakwamba alikuwa hatingishi kidole chake haina isnâd swahîh, kama nilivyoeleza katika Dha‘îfa Abî Dâwud (175). Hata kama lau ingelikuwa ni swahîh, itakuwa imejengwa juu ya msingi wa ukanushaji, haliyakuwa hadîth ya hapo juu imejengewa juu ya uthibitishaji: Uthibitisho hupewa nafasi ya mwanzo kuliko Ukanushaji, kama ilivyo maarufu miongoni mwa Wanavyuoni. 1 Ahmad, Bazzâr, Abu Ja‘far al-Bukhtîri katika al-Amâli (60/1), ‗Abdul Ghani al-Maqdisi katika Sunan yake (12/2) kwa isnâd iliyo hasan, Rûyaani katika Musnad yake (249/2) na Baihaqî. 2 Ibn Abî Shaybah (2/123/2) kwa sanad iliyo hasan.

122

kimoja tu, ―[Fanya kwa kidole kimoja tu]‖ na kumuashiria kwa kidole chake cha shahada.‖1

―Alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)akifanya hivyo katika tashahhud

zote mbili.‖2

WAAJIB WA TASHAHHUD YA KWANZA NA SUNNAH YA KUOMBA KATIKA WAKATI HUO

―Alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akisoma Tahiyyah katika kila

Rak‘âh mbili‖3; kitu cha kwanza ambacho alikuwa akitamka kwenye kikao hicho kilikuwa ni: Attahiyyâtu-LilLaah.‖4

―Aliposahau kutekeleza tashahhud baada ya Rak‘âh mbili za mwanzo, alikuwa akisujudu (sijdah mbili) kwa ajili ya kusahau.‖5 Alikuwa akiwaamrisha watekeleze tashahhud, akasema, ―Mukikaa katika kila Rak‘âh mbili, semeni: Attahiyyât ... mpaka mwisho wake, kisha kila mmoja wenu na achague dua‘ bora

aipendayo, na amuombe Allâh‎ (عز وجل) [kwa hiyo]6; katika riwaya

nyengine: Semeni, Attahiyyâtu … katika kila kikao7, na pia

1 Ibn Abî Shaybah (12/40/1, 2/123/2) na an-Nasâ‘î. Hâkim alithibitisha kuwa ni swahîh na akâfikiwa na adh-Dhahabi, na pia kunapatikana riwaya yenye kuipa nguvu kutoka kwa Ibn Abî Shaybah. 2 An-Nasâ‘î na al-Baihaqî, kwa sanad iliyo swahîh. 3 Muslim na Abu ‗Awânah. 4 Al-Baihaqî aliisimulia kama riwaya kutoka kwa ‗Âisha kwa isnâd iliyo nzuri, kama ilivyothibitishwa na Ibn al-Mulaqqin (28/2). 5 Bukhâri na Muslim. Inapatikana katika Irwâ‘ al-Ghalîl (338). 6 An-Nasâ‘î, Ahmad na at-Twabarâni katika Mu‘jam al-Kabîr (3/25/1) kwa sanad iliyo swahîh. Maana halisi ya hadîth hii inadhihirisha kuruhusiwa kuleta dua‘ katika kila tashahhud, ijapokuwa haifuatii hiyo tashahhud ya taslîm (tashahhud ya kwanza), na hii ndiyo rai ya Ibn

Hazm (اهلل رحمه) 7 An-Nasâ‘î kwa sanad iliyo swahîh.

123

akamuamrisha ―yule aliyeharibu swala yake‖ afanye hivyo, kama ilivyotangulia huko nyuma.

―Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)alikuwa akiwafundisha tashahhud kama

alivyokuwa akiwafundisha Sûrah ya Qur‘ân‖1, na ―Sunnah ni kuisoma kwa sauti ya chini.‖2

MATAMSHI YA TASHAHHUD

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)alifundisha namna nyingi za tashahhud:

1. Tashahhud ya Ibn Mas‘ûd, aliyesema: ―Mtume ( صىل اهلل عليه alinifundisha tashahhud, [na hali] kitanga changu(وسلم

kikiwa baina ya vitanga vyake, kama anavyonifundisha Sûrah katika Qur‘ân:

ات لل اتلعةت » اجليب أية ـ الصالم واػجةت والص نإ ] الصةلي الل ـجةد وع ـة الصالم وبركد الل ورمحح

أن أطد [ والرض الصةء ف صةط ـجد ك أصةب ذل ىةل إذا « ( ورشل ـجده مدا أن وأطد الل إل إل ل

―Kila aina ya Shukrani3, swala4 na maneno yaliyo matakatifu5 ni zake Yeye, Allâh‎. Amani1 ya Allâh‎

1 Bukhâri na Muslim 2 Abu Dâwud na Hâkim akathibitisha kuwa ni swahîh na akâfikiwa na adh-Dhahabi 3 Kwa Kiarabu; tahiyyât, yaani; ―Kila neno lenye kumânisha Amani, Enzi na Milele, ni yenye kumstahiki Allaah.‖ (Nihâyah) 4 Kwa Kiarabu; swalawât, yaani; ―Maombi yote yenye kutumika kusifu Utukufu wa Allaah, kwani Yeye ndiye Mwenye kustahiki zaidi kupewa sifa hizo, na hapana asiyekuwa Yeye anaestahiki yote hayo..‖ (Nihâyah) 5 Kwa Kiarabu; twayyibât, yaani; ―Kila aina ya maneno mazuri na yaliyo matukufu yanayostahiki kumsifu nayo Allaah, wala siyo yale yasiyolingana na sifa Zake, ambayo huamkuliwa kwayo wafalme.‖ (Fat-hul-Bâri)

124

ikuteremkie Ewe Mtume wa Allâh‎ pamoja na rehema na baraka Zake2. Nasi pia itushukie Amani ya Allâh‎ pamoja na

waja Wake wema wote‖. [Kwani mtu akisema hayo, inamuhusu kila mja mwema aliye mbinguni na aliye ardhini.] ―Nashuhudia yakwamba hapana anaestahiki kuabudiwa kwa hakki isipokuwa Allâh‎, na nashuhudia

yakwamba Muhammad ni mja Wake na ni mjumbe Wake.‖

[Amenifundisha hivi wakati alipokuwa miongoni mwetu, lakini baada ya kufa kwake, tulikuwa tukisema]

« اجليب ع الصالم »―[Amani iwe juu ya Mtume].‖3

1 Maana yake ni kutafuta hifadhi kwa Allaah na kuzidishiwa nguvu na Yeye, kwani, ukweli ni kwamba, as-Salaam (Amani) ni miongoni mwa majina ya Allaah. Kwa hiyo, maana ifâyo ya mâmkuzi ni: Allaah ndiye Muangalizi na Mlinzi juu yako. Vile vile, husemwa, ―Allaah awe nawe‖, yaani, katika kukulinda, kukusaidia, na kukufadhili. 2 Ni neno linalohusu uzuri wote wenye kuendelea utokao kwake Allaah 3 Bukhâri, Muslim, Ibn Abî Shaybah (1/90/2), Sirâj na Abu Ya‘laa katika Musnad yake (258/2). Inapatikana katika Irwâ‘ (321) Maneno ya Ibn Mas‘ud, ―Tulisema: Amani iwe juu ya Mtume,

inadhihirisha yakwamba Maswahaba (عنهم اهلل رضي) walikuwa wakisema,

―Amani iwe juu yako, Ewe Mtume‖ katika tashahhud wakati Mtume ( صىل alipokuwa hai, lakini baada ya kufa kwake, waliwacha kufanya (اهلل عليه وسلم

hivyo, na badala yake wakawa wanasema, ―Amani iwe juu ya Mtume‖. Bila ya shaka yoyote, jambo hilo lilikuwa limeandamana na ridhâ ya

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم); limeungwa mkono jambo hilo na uhakika

yakwamba Bibi ‗Âisha (رضي اهلل عنها) alikuwa akiwafundisha watu kuisoma

tashahhud hivyo hivyo katika swala na ―Amani iwe juu ya Mtume‖ kama alivyopokea Sirâj katika Musnad yake (9/1/2) na Mukhlis katika al-Fawâ‘id (11/54/1) kwa isnâd mbili zilizo swahîh kutoka kwake (‗Âisha

(رضي اهلل عنها) ).

125

Akasema Ibn Hajar, ―Nyongeza hii yaonyesha waziwazi yakwamba walikuwa wakisema ‗Amani iwe juu yako, Ewe Mtume‘, wakimkusudia

yeye moja kwa moja katika uhai wake, lakini alipokufa Mtume ( صىل اهلل عليه waliwacha kumkusudia yeye moja kwa moja na badala yake ,(وسلم

wakawa wanamtaja kama mtu asiyekuwepo nao, wakisema, ‗Amani iwe juu ya Mtume‘. Pia akasema mahali pengine, ―Amesema Subki katika Sharh al-Minhâj, baada ya kuitaja riwaya hii kutoka kwa Abu ‗Awânah peke yake, ‗Ikiwa hii imeswihi kuwa imepokewa kutoka kwa Maswahaba, ni dalili yakwamba baada ya wakati wake, si jambo la

lazima kumswalia Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) kama kwamba yupo kwenye

hadhara, kwa hivyo , mtu na aseme, ‗Amani iwe juu ya Mtume‘. (Ibn Hajar aendelea:) Bila ya shaka yoyote hii ni swahîh (yaani; kwa sababu imethubutu katika swahîh al-Bukhâri), na pia mimi nikaipatia riwaya inayoiunga mkono hiyo.: - Amesema ‗Abdur-Razzâk: Amenipasha khabari Ibn Jurayj: ‗Atâ‘ amenipasha khabari yakwamba Maswahaba walikuwa wakisema ‗Amani iwe juu yako, Ewe Mtume‘ wakati Mtume

( وسلم عليه اهلل صىل ) alipokuwa hai, lakini baada ya kufa kwake, walikuwa

wakisema ‗Amani iwe juu ya Mtume‘, na hii ni isnâd iliyo swahîh. Amma kuhusu riwaya ya Sa‘îd ibn Mansûr kutoka kwa Abu ‗Ubaydah ibn ‗Abdullaah ibn Mas‘ud, aliyepokea kutoka kwa babake yakwamba

Mtume ( وسلم صىل اهلل عليه ) aliwafundisha kuisoma tashahhud kisha yeye

(‗Abdullaah Ibn Mas‘ud) akaisoma (tashahhud); Ibn ‗Abbâs akasema:

Tulikuwa tukisema ‗Amani iwe juu yako, Ewe Mtume‘ wakati Mtume ( صىلوسلم اهلل عليه ) alipokuwa hai tu, ambapo Ibn Mas‘ud nae akamjibu, ‗Hivi

ndivyo tulivyofundishwa, na hivyo hivyo ndivyo tunavyoifundisha‘, inaonekana kama kwamba Ibn ‗Abbâs alikuwa amelileta hili suala kwa njia ya kujadiliwa lakini Ibn Mas‘ud hakulikubalia njia hiyo. Hata hivyo, riwaya ya Abu Ma‘mar (yaani: riwaya ya Bukhâri) ni swahîh zaidi, kwani Abu ‗Ubaydah hakusikiya (ahâdîth) kutoka kwa babake, na zaidi ya hayo, hiyo isnâd mpaka kufikia kwa Abu ‗Ubayda ni dha‘îf.‖ [Mwisho wa kunukuu kutoka kwa Ibn Hajar] Maneno haya ya Ibn Hajar yamenukuliwa na Wanavyuoni wengi katika uchambuzi wao, k.m (kwa mfano); Qastalaani, Zarqâni, Lucknowi, n.k (na kadhâlika). Wote walichagua kuyanukuu maneno yake bila ya

126

2. Tashahhud ya Ibn ‗Abbâs: ―Mtume ( ه وسلمصىل اهلل علي )alikuwa

akitufundisha tashahhud kama alivyokuwa akitufundisha [Sûrah za] Qur‘ân; alikuwa akisema,

ات اػجةت لل اتلعةت » ـ شالم [ ال ]اجةركت الص الل ـجةد وع ـة شالم [ ال ] وبركد الل ورمحح اجليب أية

. الل رشل مدا أن [ أطد ] و الل إل إل ل أن أطد الصةلي « ورشل ـجده : روايح ويف

―Kila aina ya Shukrani, maneno yaliyobarikiwa, swala, maneno matakatifu ni yenye kumstahiki Allâh‎. Amani iwe juu yako, Ewe Mtume, na pia rehema za Allâh‎ na baraka Zake. Amani iwe juu yetu na juu ya waja wema wa Allâh‎.

Nakiri yakwamba hapana apasae kuabudiwa kwa hakki isipokuwa Allâh‎, na [nakiri] yakwamba Muhammad ni

Mjumbe wa Allâh‎‖ (katika riwaya nyengine ― ... ni mtumwa wake na Mjumbe).‖1

3. Tashahhud ya Ibn ‗Umar, aliyepokea kutoka kwa Mtume ( صىل :yakwamba katika tashahhud alikuwa akisema (اهلل عليه وسلم

ات [ و ] لل اتلعةت » أية ـ الصالم اػجةت [ و ] الص الصالم - وبركد : نة زدت : ـر اث ىةل - الل ورمحح اجليب اث ىةل - الل إل إل ل أن أطد الصةلي الل ـجةد وع ـة

kuyafafanua zaidi. Mas‘ala haya yamechambuliwa kwa undani zaidi katika al-Asl 1 Muslim, Abu ‗Awânah, ash-Shâfi‘î na an-Nasâ‘î

127

ـجده - مدا أن وأطد - ل شي ل وظده : نة دتوز : ـر « ورشل

―Kila aina ya Shukrani, swala, na maneno mazuri ni yenye kumstahiki Allâh‎. Amani iwe juu yako, Ewe Mtume, na pia

rehema za Allâh‎ – Ibn ‗Umar akasema, ―Nikaongeza:‖1 … na baraka Zake – Amani iwe juu yetu na juu ya waja wema wa

Allâh‎. Nakiri yakwamba hapana apasae kuabudiwa kwa hakki isipokuwa Allâh‎ – Ibn ‗Umar akasema, ―Nikaongeza:‖2

… peke yake, Hana mshirika, - na nakiri yakwamba Muhammad ni mja wake na Mjumbe.‖3

4. Tashahhud ya Abu Mûsa al-Ash‘ari‘, aliyesema yakwamba

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alisema ... ―unapoketi, kitu cha

kwanza atakachosema kila mmoja wenu ni:‖

ات اػجةت اتلعةت » ورمحح اجليب أية ـ الصالم لل الص إل ل أن أطد الصةلي الل ـجةد وع ـة الصالم وبركد الل «ده ورشل ـج مدا أن وأطد [ ل شي ل وظده ] الل إل

―Kila aina ya Shukrani, maneno mazuri na swala ni yenye kumstahiki Allâh‎, Amani iwe juu yako, Ewe Mtume, na pia

1 Angalia nukta ifuatayo. 2 Nyongeza hizi mbili zimethibitishwa kuwa ni katika sehemu ya

tashahhud kutoka kwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم). Ibn ‗Umar hakuzuwa yeye

kwa mapendeleo yake (ameepukana mbali kabisa na kufanya jambo hilo); kwa hakika, yeye alijifunza kutoka kwa Maswahaba wengine

waliozipokea kutoka kwa Mtume ( وسلم صىل اهلل عليه ), ndio nae akaziongezea

kwenye tashahhud aliyoisikiya yeye mwenyewe kutoka kwa Mtume ( صىل (اهلل عليه وسلم3 Abu Dâwud na ad-Dâraqutnî‘ aliyeithibitisha kuwa ni swahîh.

128

rehema za Allâh‎ na baraka Zake. Amani iwe juu yetu, na juu ya waja wema wa Allâh‎. Nakiri yakwamba hapana

apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allâh‎ [peke yake, Hana mshirika], na nakiri yakwamba Muhammad ni mja

wake na mjumbe – matamshi saba, hayo ndiyo tahiyyatus Swala.‖1

5. Tashahhud ya ‗Umar ibn al-Khattâb, aliyowafundishia watu

haliyakuwa yuko juu ya minbar, akisema, ―Semeni:

ات [ لل ] اػجةت لل الزاةت لل اتلعةت » ,لل الصالصالم ـ أية اجليب ورمحح الل وبركد الصالم ـة وع ـجةد الل الصةلي أطد أن ل إل إل الل وأطد أن مدا ـجده

«ورشل ―Kila aina ya Shukrani ni zenye kumstahiki Allâh‎; kila matamshi matakatifu ni yenye kumstahiki Allâh‎; kila

maneno mazuri [ni yenye kumstahiki Allâh‎]; na swala zote ni zenye kumstahiki Allâh‎. Amani iwe juu yako, Ewe

Mtume, Na pia rehema za Allâh‎ Na Baraka Zake. Amani iwe juu yetu na juu ya waja wema wa Allâh‎. Nakiri yakwamba hapana apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allâh‎, na nakiri yakwamba Muhammad ni mja wake na Mtume."2

1 Muslim, Abu ‗Awânah, Abu Dâwud na Ibn Mâjah 2 Mâlik na Baihaqî kwa isnâd zilizo swahîh. Hata kama hadîth hii ni mawqûf, inafâ kuwa marfû‘, kwani inajulikana yakwamba jambo kama hili huwa halisemwi kutokana na rai ya mtu binafsi, kwa vile hivyo ndivyo ilivyokuwa, haitokuwa ni jambo zuri kuliko matamshi yoyote mengine ya dhikr, chembelecho aliyoyasema Ibn ‗Abdul-Barr . *TANBÎH*: Hakuna katika aina zote hizo za tashahhud, hata mahali pamoja nyongeza ya neno: wa maghfiratuhu (... na msamaha Wake), kwa hivyo mtu na asijizoezeshe nyongeza hiyo. Kwa hiyo baadhi ya Salaf walilikemea jambo hilo, kama riwaya ifuatayo inavyo onyesha:

129

6. Tashahhud ya Bibi ‗Âisha (رضي اهلل عنها) : Amesema Qâsim Ibn

Muhammad, ―Alikuwa ‗Âisha akitufundisha tashahhud na huku akiashiriya kwa mkono wake huku akisema:

ات اػجةت اتلعةت » اجليب ع الصالم لل الزاةت الص

أطد . ورمحح الل وبركد الصالم ـة وع ـجةد الل الصةلي «أن ل إل إل الل وأطد أن مدا ـجده ورشل

―Kila aina ya Shukrani, kila maneno yaliyo mazuri, swala zote, kila matamshi matakatifu ni yenye kumstahiki Allâh‎. Amani iwe juu ya Mtume na rehma Zake na Baraka Zake. Amani iwe juu yetu na iwe juu ya kila mja mwema. Nakiri

yakwmba hapana anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allâh‎. Na nakiri yakwamba Muhammad ni mja

Wake na Mtume Wake.‖

At-Twabarâni (3/56/1) amepokea kwa isnâd iliyo swahîh kutoka kwa Talhah Ibn Musarrif, aliyesema: Rabî‘ Ibn Khaitham aliongeza katika tashahhud, ― ... na baraka Zake, na msamaha Wake‖! Basi Alqamah akasema, ―Sisi twakoma pale tulipofundishwa: Amani iwe juu yako, Ewe Mtume, na pia rehema za Allaah na baraka Zake‖, kwa hakika Alqamah alikuwa akiandama mfano wa mwalimu wake, ‗Abdullaah Ibn

Mas‘ud (رضي اهلل عنه), ambae imeswihi kupokewa kutoka kwake yakwamba

alikuwa akimfundisha mtu tashahhud: na alipofika mahali isemapo ―Nakiri yakwamba hapana mola (wa kweli) isipokuwa Allaah …‖, yule bwana akasema: ―peke yake, Yeye hana mshirika‖, na kwa hiyo ‗Abdullaah akamwambia, ―Yeye yuko hivyo, twajua, lakini sisi twakoma pale ambapo tulipofundishwa tukome.‖ (Imepokewa na at-Twabarâni katika Mu‘jam al-Awsat, no. 2848 kwa isnâd iliyo swahîh).

130

AS-SWALAATU „ALAN-NABIYY (KUMSWALIA MTUME) – MAHALI PAKE NA MATAMSHI YAKE

Mtume ( وسلم صىل اهلل عليه )alikuwa akiiswalia nafsi yake katika

tashahhud ya kwanza na pia tashahhud nyengine1. Vile vile amelifanya jambo hilo kuwa ni Sunnah kwa Ummah wake, akawâmrisha ummati wake kumswalia yeye baada ya kumuombea amani2, na akawafundisha aina mbali mbali za kufanya hivyo.

1 Abu ‗Awânah katika swahîh yake (2/324) na an-Nasâ‘î 2 Wao walisema, ―Ewe Mjumbe wa Allaah, sisi tumefundishwa tukuswalie (yaani: katika tashahhud), lakini tukuswalie vipi? Akasema, ―Semeni: Yâ Allaah! Mswalie Muhammad ...‖ n.k (na kadhâlika) Kwa hiyo, hakuainisha tashahhud moja kwa kuiwacha nyengine, kwa hivyo kuna ushahidi hapa unaothibitisha kumswalia katika tashahhud ya kwanza pia. Huu ndio mfumo wa Imâm ash-Shâfi‘î, kama ilivyo kwenye mândishi kwenye kitabu chake Al-Umm, na imeshikiliwa kuwa katika usawa na wafuasi wake, kama alivyofafanua an-Nawawî katika al-Majmû‘ (3/460) na kuipa nguvu katika Rawdhwah Tâlibîn (1/263). Pia hii ni rai ya Wazîr Ibn Hubairah al-Hanbalî katika al-Ifsâh, kama alivyonukuu na kuunga mkono kikamilifu Ibn Rajab katika Dhail Tabaqât

(1/280). Kuna ahâdîth nyingi kuhusiana na kumswalia Mtume ( صىل اهلل عليه katika tashahhud; hakuna katika zote hizo kupatikana kutajwa (وسلم

kipambanuzi kama hicho. Kwa hakika ahâdîth hizi ni za kuzungumzia ki-Ujumla, kwa hiyo inahusu kila tashahhud, na nimeziweka katika Al-Asl kama ta‘lîq, lakini sikuweka kwenye Maandiko yenyewe (Matn), kwani hazitoshelezi masharti yetu ya uswahîh. Hata hivyo, zinasaidiana zenyewe kwa zenyewe ki-maana, na wale wenye kukatâ na kupinga haya hawana ushahidi ulio swahîh kutumia kama dalili, kama nilivyoyachambua katika Al-Asl. Vile vile kusema yakwamba, nyongeza yoyote katika, ―Yâ Allaah! mswalie Muhammad‖ ni makrûh haina msingi wowote kwenye Sunnah, wala haina ushahidi wowote wenye uzito. Kwa hakika, sisi twaona yakwamba yoyote mwenye kusema maneno haya

hatekelezi mâmrisho yaliyotangulia kutoka kwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم),

131

1.

ة وذريذ أزواص وع ثيذ أ وع مد ع ص ال » آل وع مد ع وبةرك جمد محد إ إثرا آل ع صخ محد إ إثرا آل ع ثةركخ ة وذريذ أزواص وع ثيذ

« جمد―Yâ Allâh‎! Mfikilizie amani Muhammad1, Na jamii yake, Na wake zake Na kizazi chake, Kama ulivyowafikilizia jamii ya Ibrâhîm; Kwa hakika Wewe ndiye Mtukufu, unaestahiki kila Sifa njema. Na umfikilizie Baraka Muhammad2, Na jamii yake, Na wake zake Na kizazi chake, Kama ulivyowafikilizia Baraka jamii ya Ibrâhîm. Kwa hakika Wewe ndiye, Mtukufu, unaestahiki kila Sifa njema.‖

Dua‘ hii alikuwa akiitumia yeye mwenyewe.3

―Semeni: Yâ Allaah! Mfikilizie swala Muhammad, na Jamii yake Muhammad ...‖; kuna mjadala zaidi wa haya katika al-Asl. 1 Mojawapo ya rai ya zamani kuhusu maana ya kumswalia Mtume ( صىل اهلل ni ile ya Abu al-‗Âliyah (kuhusiana na surah al-Ahzâb 33:56) (عليه وسلم

―Maana ya Allaah kumswalia Mtume Wake ni kumtukuza Kwake na kumuinua daraja yake; Maana ya Malaika na wengineo kumswalia ni kuomba kwao haya kutoka kwa Allaah, na hapa inamânisha kuomba swala ziongezeke, sio kuomba swala yenyewe halisi.‖ Ameyanukuu haya Ibn Hajar katika Fat-hul-Bâri, na akaendelea kulikosoa hili wazo lililoenea yakwamba swala ya Allaah juu ya mtu ni Rehma Zake; Ibn al-Qayyim pia akayafafanua haya katika Jalaa‘ al-Afhâm, akawacha mwanya mdogo sana kwa maelezo ya zaidi 2 Kutokana na barakah, kukua, kuzidi. Kwa hiyo maombi haya yanamuhifadhia Muhammad ule uzuri ambao Allaah ameihifadhia jamii ya Ibrâhîm, kwa kuendelea, uzuri uliothabiti, pamoja na kuongezeka na kuzâna 3 Ahmad na at-Twahâwi kwa sanad iliyo swahîh.

132

2.

إثرا ] ع صخ ة مد آل وع مد ع ص ال » آل وع مد ع ثةرك ال جمد محد إ إثرا آل [ وع جمد محد إ إثرا آل [ وع إثرا ]خ ع ثةرك ة مد

» ―Yâ Allâh‎! Mfikilizie amani Muhammad, Na jamii ya

Muhammad, Kama ulivyomfikilizia [Ibrâhîm, Na1] jamii ya Ibrâhîm; Wewe ndiye Mtukufu, unaestahiki kilaSifa njema.

Yâ Allâh‎! Mfikilizie Baraka Muhammad, Na jamii ya Muhammad, kama ulivyowafikilizia Baraka [Ibrâhîm, na2] jamii ya Ibrâhîm; Wewe ndiye Mtukufu, unaestahiki kila

Sifa njema.‖3

1 Angalia nukta ifuatayo. 2 Nyongeza hizi mbili hupatikana bila ya shaka yoyote katika Bukhâri, at-Twahâwi, al-Baihaqî, Ahmad na an-Nasâ‘î. Na vile vile zinapatikana kwa kupitia njia tafauti tafauti za riwaya aina nyengine ya dua‘ hii (tizama no. 3, 7), kwa hivyo usibabaishwe na rai ya Ibn al-Qayyim katika Jalaa‘ al-Afhâm (Uk. 198), alipokuwa akiandama nyayo za mwalimu wake Mkubwa Ibn Taymiyyah katika al-Fatâwâ (1/16), ―Hakuna hadîth swahîh iliyo na matamshi ‗Ibrâhîm‘ na ‗Jamii ya Ibrâhîm‘ pamoja‖; hapa, sisi tumekuonyesha ahâdîth zilizo swahîh. Makosa ya Ibn al-Qayyim yamezidi kuthibitishwa juu ya uhakika yakwamba yeye mwenyewe amethibitisha no. 7 kuwa ni swahîh, ambayo iliyokuwa na yale aliyoyakanusha hapo awali! 3 Bukhâri, Muslim, Humaidi (138/1) na Ibn Mandah (68/2), aliyesema, ―hakuna muafaka juu ya kusihi kwa hadîth hii.‖

133

3.

] إثرا ع صخ ة مد آل وع مد ع ص ال » ة مد آل وع مد ع وبةرك جمد محد إ [ إثرا وآل

« جمد محد إ إثرا وآل [ و إثرا ] ع ثةركخ―Yâ Allâh‎! Mfikilizie amani Muhammad, na jamii ya

Muhammad, kama ulivyomfikilizia amani Ibrâhîm, [na jamii ya Ibrâhîm]; Wewe ndiye Mtukufu, unaestahiki kila

Sifa njema. Na umfikilizie Baraka Muhammad, Na jamii ya Muhammad, Kama ulivyomfikilizia Baraka [Ibrâhîm, na] jamii ya Ibrâhîm; Wewe ndiye Mtukufu, unaestahiki kila

Sifa njema.‖1

4.

صخ ة مد آل وع [ الم اجليب ] ص ع مد ال » مد آل وع [ الم اجليب ] مد ع وبةرك إثرا [ آل ] ع

« جمد محد إ افةي ف إثرا [ آل ] ع ثةركخ ة―Yâ Allâh‎! Mfikilizie amani Muhammad [Mtume aliyekuwa

hajui kusoma wala kuandika] na jamii ya Muhammad, kama ulivyomfikilizia [jamii ya] Ibrâhîm. Na uzifikilize baraka kwa Muhammad [Mtume aliyekuwa hajui kusoma wala kuandika] na jamii ya Muhammad kama ulivyofikiliza

baraka kwa [jamii ya] Ibrâhîm miongoni mwa mataifa; Wewe ndiye Mtukufu, unaestahiki kila Sifa njema.‖2

1 Ahmad, an-Nasâ‘î na Abu Ya‘laa katika Musnad yake (44/2) kwa sanad iliyo swahîh. 2 Muslim, Abu ‗Awânah, Ibn Abî Shaybah (2/132/1) na Abu Dâwud; Hâkim aliithibitisha kuwa ni swahîh.

134

5.

[ آل ] ع صخ ة ورشل ـجدك مد ع ص ال » [ مد آل وع ] [ ورشل ـجدك ] مد ع وبةرك إثرا

« [ إثرا آل وع ] إثرا ع ثةركخ ة―Yâ Allâh‎! Mfikilizie amani Muhammad, mja Wako na

mjumbe, kama ulivyomfikilizia amani [jamii ya] Ibrâhîm. Na umfikilizie baraka Muhammad [mja Wako na mjumbe [Na jamii ya Muhammad] kama ulivyomfikilizia baraka

Ibrâhîm [na jamii ya Ibrâhîm]‖.1

6.

] ع صخ ة وذريذ أزواص [ ع ] و مد ع ص ال »ةركخ ث ة وذريذ أزواص [ ع ] و مد ع وبةرك إثرا [ آل

« جمد محد إ إثرا [ آل ] ع -―Yâ Allâh‎! Mfikilizie amani Muhammad, na [kwa] wakeze, na kizazi chake, kama ulivyowafikilizia amani [jamii ya]

Ibrâhîm. Na umfikilizie baraka Muhammad na [kwa] wakeze, na kizazi chake kama ulivyowafikilizia – [jamii ya]

Ibrâhîm. Wewe ndiye Mtukufu, unaestahiki kila Sifa njema.‖2

1 Bukhâri, an-Nasâ‘î, at-Twahâwi, Ahmad na Ismâ‘îl al-Qâdhi katika Fadhl as-Swala ‗alan-Nabiyy Sallallaahu ‗alayhi wasallam (Uk. 28 Chapa ya kwanza, Uk. 62 Chapa ya Pili ikiwa na usahihishaji wangu). 2 Bukhâri, Muslim na an-Nasâ‘î

135

7.

آل وع مد ع وبةرك مد آل وع مد ع ص ال » محد إ إثرا وآل إثرا ع وبةركخ صخ ة مد

« جمد―Yâ Allâh‎! Mfikilizie amani Muhammad na jamii ya

Muhammad na umfikilizie baraka Muhammad na jamii ya Muhammad kama ulivyomfikilizia amani na baraka Ibrâhîm na jamii ya Ibrâhîm. Wewe ndiye Mtukufu, unaestahiki kila

Sifa njema.‖1

NUKTA MUHIMU KUHUSU AS-SWALAATU „ALAN-NABIYY - KUMSWALIA MTUME WA UMMAH

1) Ni jambo la dhahiri yakwamba nyingi katika njia hizi za

kumswalia Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), haionekani kutajwa kwa

Ibrâhîm mbali na jamii yake, maneno yenyewe ni hivi, ―... kama ulivyowafikilizia amani jamii ya Ibrâhîm.‖ Sababu ya hii ni kwamba katika lugha ya kiarabu, jamii ya mtu yoyote huwa inamkusanya mtu mwenyewe pia na vile vile

wanaomtegemea yeye, k.m. katika maneno yake Allâh‎ ( سبحانه :(وتعاىل

1 An-Nasâ‘î, at-Twahâwi, Abu Sa‘îd Ibn al-‗Arabi katika al-Mu‘jam (79/2) kwa sanad iliyo swahîh. Ibn al-Qayyim ameitolea asili yake kama Muhammad Ibn Is-hâq as-Sirâj katika Jalaa‘ al-Afhâm (Uk. 14-15) kisha akaithibitisha kuwa ni swahîh. Neno hili limewahusu wote ‗Ibrâhîm‘ na ‗jamii ya Ibrâhîm‘. Ni jambo lililowapitikia Ibn al-Qayyim na Ibn Taymiyyah, mwalimu na mwanafunzi wake, kama ilivyoelezwa hapo awali.

136

2)

ٱإنذ رن ع صػيف ٱ للذ ـ وءال ة وءال إثر ظا ي ٱءادم و ع٣٣

“Hakika Allâh‎ alimchagua Âdam na Nuhu na kizazi cha Ibrâhîm na kizazi cha „Imrân (Babâke Musa; na „Imrân

mwengine aliye baba yake Maryam) juu ya walimwengu wote (wa zama zao).” [Âl-‘Imrân 3:33].

ة بصعر إجذ ج ذ ءال لط جنذ ظةصجة إلذ

ـ ة رش ٣٤أ

“Hakika Sisi tuliwapelekea vijiwe (vya kuwatoboa tosi zao vikawângamiza wote) isipokuwa wafuasi wa Luti;

Tuliwaokoa karibu na Alfajiri.” [Qamar 54:34]

Pia mfano mwengine ni maneno yake (صىل اهلل عليه وسلم):

« أويف أب آل ع ص ال »―Yâ Allâh‎! Ifikilizie amani jamii ya Abu Awfâ.‖

Neno hili Ahl al-Bayt (watu wa nyumba) pia ni kama hivyo, k.m.(kwa mfano)

ٱرمحخ للذ ۥوبركذ أ س خ ٱـ بل د ۥإذ ٧٣محد جمذ

“Rehema ya Allâh‎ na Baraka Zake ziko juu yenu, enyi watu wa nyumba hii!” [Hud 11:73]

Kwa hiyo, Ibrâhîm anakuwa yumo ndani ya ―jamii ya Ibrâhîm‖

Shaykh ul-IsLaam Ibn Taymiyyah amesema,

―Kwa hiyo, ndio imekuja katika matamshi mengi, ‗kama ulivyowafikilizia amani jamii ya Ibrâhîm‘ na ‗kama

137

ulivyowabariki jamii ya Ibrâhîm‘; baadhi yake inayo ‗Ibrâhîm‘ mwenyewe. Hii ni kwa sababu yeye ndiye mwenye kusababisha hayo maombi yote na kutakasika juu yao; na baki ya jamâ zake inapatikana hilo kwa kufuatia tu. Ili kuonyesha hizi nukta mbili, matamshi yote mawili yametumika mbali mbali.‖

Zaidi ya hayo kuna suali maarufu sana baina ya wanavyuoni kuhusu hali ya ulinganishaji katika matamshi yake, ―kama ulivyofikiliza amani juu ya ...‖ kwani ni kweli yakwamba jinsi ya ulinganishaji kwa kawaida huwa ni kubwa zaidi kuliko ile jinsi nyengine inayolinganishwa; hapa kinyume chake ndiyo hali

yenyewe, kwani Muhammad (صىل اهلل عليه وسلم)ni mtukufu kuliko

Ibrâhîm, na kwa hivyo utukufu wake unaonyesha yakwamba maombi yaliyo ombwa ni matukufu zaidi kuliko maombi yoyote yapatikanayo au yatakayopatikana na mtu yoyote. Ma-‗Ulamâ‘ wamelijibu hilo kwa jawabu nyingi, na yanaweza kupatikana hayo katika Fat-hul Bâri na JaLaa‘ al-Ifhâm. Kuna takriban kiasi cha jawabu kumi, zote zisizothibitika, baadhi yake ni dhaifu zaidi kuliko baadhi nyengine, isipokuwa moja tu, na hakika kauli hiyo ina nguvu, na akaifanya kauli hiyo kuwa nzuri Shaykhul IsLaam Ibn Taymiyyah na mwanafunzi wake Ibn al-Qayyim. Kauli hiyo ni: ―Hakika jamii ya Ibrâhîm, ndani yake kuna Mitume ambao hakuna katika Jamii ya Muhammad mfano wao. Kwa hiyo,

tunapo omba amani afikiliziwe Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)na jamii yake

kama anavyofikiliziwa amani Mtume Ibrâhîm na jamii yake, ambayo wamo ndani yake Mitume, basi jamii ya Muhammad wanapata kutokana na maombi hayo kiasi chao kiwatoshacho. Kwani jamii ya Muhammad haifikilii daraja ya Mitume, faida na baraka za ziada wanazopewa Mitume, akiwemo Ibrâhîm,

amebakishiwa Muhammad (صىل اهلل عليه وسلم). Kwa hiyo anapata nafasi

teule ambayo wengine hawawezi kuifikia.‖

Amesema Ibn al-Qayyim,

138

―Kauli hii ni nzuri zaidi kuliko zilizotangulia: yakwamba

Muhammad (صىل اهلل عليه وسلم)ni katika jamii ya Ibrâhîm; Kwa

hakika, yeye ni mbora zaidi katika jamii ya Ibrâhîm, kama

alivyopokea ‗Ali Ibn Talhah kutoka kwa Ibn ‗Abbâs ( رضي اهلل(عنه kuhusu maneno ya Allâh‎ Mtukufu:

ٱإنذ ة و صػيف ٱ للذ ظا رن ع ءادم و ـ وءال ي ٱءال إثر ع٣٣

“Hakika Allâh‎ alimchagua Âdam na Nuhu na kizazi cha Ibrâhîm na kizazi cha „Imrân (Babâke Musa; na „Imrân

mwengine aliye baba yake Maryam) juu ya walimwengu wote (wa zama zao).” [Âl-‘Imrân 3:33].

Akasema Ibn ‗Abbâs, ―Muhammad ni miongoni mwa jamii ya Ibrâhîm‖. Na hii ni Nass kwa uhakika yakwamba iwapo Mitume wengine ni kizazi kinachotokana na Ibrâhîm wataingizwa katika jamii yake, basi kuingizwa kwa Mtume

ni bora zaidi. Itakuwa neno letu, ―kama(صىل اهلل عليه وسلم)

ulivyowafikilizia amani jamii ya Ibrâhîm, itakuwa ni lenye

kukusanya kumswalia Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)na Mitume

wengine waliotokana na kizazi cha Ibrâhîm. Kwahivyo,

kisha Allâh‎ (سبحانه وتعاىل) ametuamrisha sisi tumswalie Mtume

( هلل عليه وسلمصىل ا )na Jamii yake Khaswa, kwa kiasi cha

tunavyomswalia pamoja na jamâ wote wa Ibrâhîm kwa ujumla, na yeye akiwemo ndani yao. Kwa hivyo, jamii ya Mtume watapata kutokana na hayo kiasi kinacholingana

na wao, wabakishe ile ziyada kwa Mtume ( عليه وسلم صىل اهلل ).

139

Hapana shaka yakwamba jumla ya kiwango cha maombi

inayopatikana na jamii ya Ibrâhîm, akiwemo Mtume ( صىل اهلل miongoni mwao, ni kubwa zaidi kuliko kiwango (عليه وسلم

cha maombi anachopata Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) peke yake.

Kwa hivyo, dua‘ anayo ombewa yeye ni katika fadhla kubwa, bila ya shaka kubwa zaidi kuliko yale maombi anayo ombewa Ibrâhîm.

Kwa hiyo, hali ya asili ya ulinganifu na uzito wake unadhihiri. Dua‘ anayo ombewa kwa kutumia maneno haya ni kubwa zaidi kuliko anayo ombewa kwa njia yoyote nyengine, kwani kinacho ombwa na dua‘ ni kwamba kupatikane malipo yaliyozidi ile jinsi iliyolinganishwa

nayo, na kwamba fungu la Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) liwe ni

kubwa zaidi. Ulinganifu unâmuru yakwamba kilichotakiwa ni zaidi ya alichopewa Ibrâhîm na wengineo.

Vivi hivi, Utukufu na daraja kubwa ya Mtume ( صىل اهلل عليه kuliko Ibrâhîm na jamii yake, wakiwemo Mitume ,(وسلم

wengi, inadhihirika, na ni kama anavyostahiki. Huku

kumswalia Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) kunadhihirika kwa huu

Ubora wake, na hii haikuzidi anavyostahiki. Basi, twamuomba Allâh‎ amfikilizie amani na jamii yake, na awafikilizie amani juu yao, mâmkuzi mengi ya amani, na amlipe yeye kutokana na dua‘ zetu, zilizo bora kuliko

(Allâh‎ (سبحانه وتعاىل)) Alivyowahi kumlipa Mtume yoyote

kutokana na dua‘ za watu wake. Yâ Allâh‎! Mfikilizie amani Muhammad, na jamii ya Muhammad, kama ulivyowafikilizia amani jamii ya Ibrâhîm; Kwa hakika, Wewe ndiye Mtukufu, unaestahiki kila aina ya Sifa njema. Na mfikilizie Baraka Muhammad, na jamii ya Muhammad, kama ulivyowafikilizia baraka jamii ya Ibrâhîm; Kwa

140

hakika, Wewe ndiye Mtukufu, unaestahiki kila aina ya Sifa Njema.‖

3) Msomaji mtukufu ataona yakwamba sehemu hii ya dua‘, pamoja na njia zake zote tafauti, daima ni kuwaombea jamii

ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), wake zake na watoto pamoja na yeye

mwenyewe. Kwa hivyo, si katika Sunnah, wala utekelezaji wa amri ya Mtume, kuifupisha na kukoma katika ―Yâ Allâh‎! Mfikilizie amani Muhammad‖ peke yake. Bali ni lazima mojawapo ya hizi aina za dua‘ zilizokamilika zitumike,

kulingana na yaliyopokewa kutokana na vitendo vyake ( صىل اهلل .imma katika tashahhud ya kwanza au ya mwisho ,(عليه وسلم

Kuna Nass‘ kuhusu haya kutoka kwa Imâm ash-Shâfi‘î katika al-Umm: ―tashahhud ya kwanza na ya pili ni lafdhi moja isiyokuwa na ikhtilafu; maana ya maneno yangu ‗tashahhud‘, namânisha kushuhudia na kufikiliza dua‘ za amani kwa Mtume

haiwezi mojawapo kutosheleza bila ya (صىل اهلل عليه وسلم)

nyengine.‖

Kwa hakika, mojawapo ya mambo yenye kushangaza mno yaliyojitokeza katika mchafuko wa kwenye ‗ilmu ya zama zetu hizi ni kufanya ujasiri baadhi ya watu, mtu mmoja aitwae Muhammad Is‘âf Nashâshîbi, katika kitabu chake al-IsLaam as-Swahîh (―Uislamu ulio Swahîh ‖), alifanya ujasiri wake wa

kukataa kuwaswalia jamâ za Mtume ( اهلل عليه وسلم صىل )pindi

anapomswalia Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), licha ya kuthubutu kwake

imara katika swahîh za Bukhâri na Muslim, na kwengineko, na kupokewa na baadhi ya Maswahaba, k.m; Ka‘b ibn ‗Ujrah, Abu Humaid as-Sâ‘idî, Abu Sa‘îd al-Khudhrî, Abu Mas‘ûd al-Answarî, Abu Hurairah, na Talhah ibn ‗UbaydulLaah! Katika ahâdîth zao,

imepatikana yakwamba wao walimuuliza Mtume (صىل اهلل عليه وسلم),

―Tukuswalie vipi?‖, basi ndio akawafundisha jinsi ya kufanya.

141

Madai ya Nashâshîbi kuhusu maoni yake ni kwamba Allâh‎ ( سبحانهصىل اهلل عليه ) hakumtaja mtu yoyote mwengine pamoja na Mtume (وتعاىل :katika maneno yake (وسلم

ة حأ ٱي ي ة لذ ا تص وش ـ ا ا ص ٥٦ءا

“Enyi Mlioamini! Mswalieni Mtume na mumuombî amani.” [Sûrah al Ahzâb 33:56]

Kisha akaendelea kusema katika ukosoaji wake yakwamba

Maswahaba walimuuliza Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)suali hilo kwa sababu

maana ya ―Swala‖ ilikuwa ikijulikana kwao kuwa ni ―dua‘‖, vipi watamuuliza, ―Tutakuombeaje wewe?‖! Hili ni kosa la wazi, kwani suali lao halikuwa kuhusu maana ya ―kumswalia‖, ili angalau awe na hoja, lakini ilikuwa ni kuhusu jinsi ya utekelezaji wa kumswalia, kama ilivyopatikana katika riwaya ambazo tulizowahi kuziregelea. Kwa hiyo, yote yanaingiliana, kwani walimuuliza kuhusu jinsi ya utekelezaji kulingana na Sharî‘ah, jambo ambalo haiwezekani kwao kutambua isipokuwa kwa kupitia kwenye uongofu wa Mjuzi wa kila jambo, Mwenye Hikmah, Mwenye kuweka Sharî‘ah. Vile vile, walikuwa pia na uwezo wa kumuuliza jinsi ya kutekeleza swala iliyofanywa ni Waajib kutokana na matamshi yake Aliyetukuka kama vile ―Simamisheni swala‖, kwani ujuzi wao wa maana halisi ya ―Swala‖ katika lugha haiwatoshelezi kuulizia kuhusu jinsi ya kuitekeleza kulingana na sharî‘ah, na hili liko wazi halijifichi. Amma kuhusu hoja ya Nashâshîbi iliyoashiriwa, haina kitu chochote, kwani ni jambo maarufu mno kwa Waislamu kwamba

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) ndiye mwenye kubainisha maneno ya Bwana

wa Viumbe, pale aliposema:

زجلة إحلر ٱوأ ل ة زل إحل ذةس ل ٤٤تلبي

142

“Na Tumekuteremshia mauidha ili uwabainishie watu yaliyoteremshwa kwao.” [An-Nahl 16:44]

Kwa hiyo, Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) amebainisha namna ya kumswalia,

na namna yenyewe muna kutaja ―Âl‖ jamâ zake, kwahivyo ni Waajib kukubali hivyo kutoka kwake, kutokana na maneno yake

Allâh‎ (سبحانه وتعاىل): س ة ءادى ٧ نخذوه لرذشل ٱو

“Na anachokupeni Mtume basi pokîni.” [surah Al-Hashr 59:7]

Na maneno yake (صىل اهلل عليه وسلم)katika hadîth mashuhuri iliyo

swahîh isemayo:

« ف وس ايرآن أودخ إين أل »―Ehî! hakika mimi nimepewa Qur‘ân na mfano wa hiyo

Qur‘ân pamoja nayo.‖1 Mimi kwa hakika nashangâ na Nashâshîbi na wale walioghurika na maneno yake yenye jeuri watakavyosema ikiwa mtu huwenda akazikatâ tashahhud zote katika swala, au akatae kujiepusha kuswali na kufunga swaum mwanamke mwenye heidh, yote hayo

kwa hoja yakwamba Allâh‎ (سبحانه وتعاىل) hakuitaja tashahhud katika

Qur‘ân; Ametaja kurukû‘ na kusujudu peke yake, na kwamba

Allâh‎ (سبحانه وتعاىل) hakumuondoshea mwenye heidh katika Qur‘ân,

swala na swaum!! Sasa Je, kwani wao wanakubaliana na hoja kama hizo, zinazokwenda sambamba na msimamo wake asliya, au Laa? Iwapo wanakubali hivyo, na sisi twatarajia kuwa hawayakubali hayo, basi wao watakuwa wamepotoka mbali sana, mbali na uongofu, na wamejitenga na mkondo wa Waislamu;

1 Abu Dâwud na Ahmad kwa isnâd iliyo swahîh.

143

Ikiwa wao hawatokubali hayo, basi watakuwa sawa katika kukubali pamoja nasi, na sababu zao za kuzikanusha hoja hizo ni sawa sawa na sababu zetu za kuyakanusha maneno aliyoyatangaza mwenyewe Nashâshîbi tuliyoyaeleza kwa uwazi kabisa. Kwa hivyo tahadhari, Ewe Muislamu, kujaribu kuifahamu Qur‘ân bila ya kutumia Sunnah, kwani hutoweza kufanya hivyo, hata kama utakuwa wewe ni Sîbawaih1 wa zama zako, bingwa wa zamani katika lugha ya Kiarabu. Hapa chukuwa mfano mbele yako, kwani huyu Nashâshîbi alikuwa ni miongoni mwa wanavyuoni wakubwa wa lugha ya Kiarabu katika karne ya sasa; umeona jinsi alivyopotoka, baada ya kudanganyika kutokana na ilimu yake ya lugha, kwa kutotafuta msâda wa Sunnah katika kuifahamu Qur‘ân; kwa kweli yeye ameukatâ msâda huu, kama ujuavyo. Kuna mifano mengine mingi sana ya haya – hatuna nafasi ya kutosha hapa ya kuyataja hayo, lakini yanatosheleza yale tuliyoyataja, na Allâh‎ ndiye Mwenye kuafikisha.

4) Pia msomaji wa kitabu hiki ataona yakwamba hakuna katika

hizi aina za kumswalia Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), neno ―Sayyid‖

(Bwana). Wanavyuoni waliokuja nyuma wamekhitilafiana kuhusiana na kufâ kuingizwa katika swaLaat al-Ibrâhimiyyah. Kutokana na uchache wa nafasi, hatutokwenda kwenye kuyapambanua ki-Undani maneno hayo, wala kuwataja wale waliokanusha kufâ kwake katika kushikamana na mafunzo ya

Mtume ( ىل اهلل عليه وسلمصه ) kwa Ummah wake alipowâmrisha,

―Semeni: Yâ Allâh‎! Mswalie Muhammad ...‖ alipoulizwa jinsi ya kumswalia yeye, lakini sisi tutamnukuu Al-Hâfidh Ibn-Hajar al-AsqaLaani kuhusu haya, kwa kumzingatia daraja yake kama mmojawapo wa wanavyuoni wa ki-Shâfi‘î katika fanni ya hadîth na fiqh, kwani kukhalifu mafundisho ya

1 Mmalenga maarufu na Mwanachuoni mkubwa wa karne ya Pili (Hijriya) wa lugha ya Kiarabu.

144

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) kumekithiri miongoni mwa wanavyuoni

wa ki-Shâfi‘î! Amesema al-Hâfidh Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad al-Ghurâbîli (790-835 AH), ambaye ni swâhib yake Ibn Hajar, nami nanukuu kutoka katika waraka wake1

―Yeye (Yaani; Ibn Hajar), twamuomba Allâh‎ atunufaishe

na maisha yake, aliulizwa namna ya kumswalia Mtume ( صىل katika swala au nje ya swala, ni waajib au ni (اهلل عليه وسلم

jambo lililopendekezwa: Je, mojawapo ya shuruti zake

yakwamba Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) anasibishwe na hili tamko

la ―Sayyidinâ‖ (bwana wetu), k.m. ‗Yâ Allâh‎! Mfikilizie amani Sayyidinâ (bwana wetu) Muhammad ...‘ au ‗Sayyid al-Khalq‘, au ‗Sayyid walad Âdam‘ n.k? Au mtu na ashikilie ile ile asli ‗Yâ Allâh‎! Mfikilizie amani Muhammad‘? Ni upi kati ya hizi mbili ulio muongozo bora: Kulihusu neno ―Sayyid‖, kutokana na neno hilo kuwa ni

sifa iliyothubutu ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), au kuliwacha

kando neno hilo kutokana na kukosekana kwake katika riwaya?

Akajibu (Ibn Hajar) (رحمه اهلل) :

―Nâm kufuata tamko lililonukuliwa ni jambo lenye nguvu

zaidi. Haiwezekani kusemwa, ―Labda Mtume ( صىل اهلل عليه yeye mwenyewe hakulisema tamko hilo kutokana na ,(وسلم

unyenyekevu wake, kama ambavyo hakusema ( صىل اهلل عليه juu ya kutajwa jina lake, hata kama Ummah wake (وسلم

umehimizwa kufanya hivyo‖ – kwani sisi twasema iwapo

1 Iliyohifadhiwa katika Maktaba ya Zâhiriyyah iliyoko mjini Damascus.

145

jambo hilo lingekuwa kubwa zaidi, lingelinukuliwa kutoka kwa Maswahaba na kisha kufuatia kwa Tâbi‘în, lakini hatuoni hilo katika riwaya zozote kupokewa kutoka kwa Maswahaba wala ma-Tâbi‘în. Pamoja na wingi wa yaliyopokewa kutoka kwao katika hilo la kumswalia

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم). Tunae Imâm Shâfi‘î, Allâh‎ aiweke

juu daraja yake, mmojawapo miongoni mwa watu katika

kumuheshimu Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), asema katika

utangulizi wa kitabu chake ambacho ndicho msingi wa watu wa madh-hab yake: ―Yâ Allâh‎! Mfikilizie amani Muhammad ...‖ n.k. mpaka mwisho wa ilivyompelekea Ijtihadi yake , ―... kila wakati mmojawapo wa wenye kumkumbuka humkumbuka, na kila wakati mmojawapo wa wajinga huwacha kumkumbuka‖, kama kwamba yeye, Imâm Shâfi‘î amechukuwa maneno hayo kutokana na hadîth swahîh ambayo muna ndani yake:

« خي ـدد الل شجعةن »

Imethubutu yakwamba Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)alimwambia

Ummul-Mu‘minîn alipomuona akishughulika na kuleta nyuradi ndefu kwa wingi, basi akamwambia:

« لزذ ىخ ثة وزخ ل لكةت ثفدك ىخ يد »

―Nimesema baada yako matamshi ambayo, lau yangepimwa uzani wake na ulivyosema, yangelikuwa sawa uzani wake.‖

Alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akipenda dua‘ zilizo fupi

zenye kukusanya mambo mengi. Qâdhi ‗Iyâdh alitunga mlango mzima kuhusu kumswalia

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) katika kitabu chake ash-Shifâ‘ (Kitabu

146

cha Pozo), akanukuu ndani yake âthâr zenye kurufaishwa kutokana na kundi la maswahaba na tabi‘în; katika yote hayo haikupokewa hata mahali pamoja neno ―Sayyidinâ‖

A. Hadîth ya‘Ali (رضي اهلل عنه), yakwamba alikuwa akiwafundisha

watu jinsi ya kumswalia Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akisema:

ات ظييدا ال » ا اصف اصكت ييوبةر ادظ ثو شام ثركد وزااد تذ ع مد ـجدك ورشل اد و ص

«اهةدط ة أكو

Vile vile hadîth nyengine ya ‗Ali (رضي اهلل عنه), yakwamba

alikuwa akisema:

ات» واجلبي ايربي واالاسح الرظ ارب الل صرب ية يشء ل شجط وة يوالصةل والظداء والصدييي

...«افةي ع مد ث ـجد الل خةد اجلبي وإةم اذيي الدير

B. Imepokewa kutoka kwa ‗Abdullâh‎ Ibn Mas‘ûd (رضي اهلل عنه), yakwamba alikuwa akisema:

اد ال اصف » وبركد ورمحذ ع مد ـجدك ص الدير... «لرمحح ورشل إةم اخلري ورشل ا

C. Imepokewa kutoka kwa Hassana al-Basrî (رضي اهلل عنه), yakwamba alikuwa akisema, ―Yoyote mwenye kutaka

147

kunywa kutoka kwenye kikombe ambacho hukata kiu, kutoka katika hawdh ya al-Mustafâ, na aseme:

وذريذ وأولده صوأزوا وأصعةث آل وع مد ع ص ال» «ذ وأصةره وأصةره وأطةـ ومج ثي وأ

Haya ndiyo ambayo aliyoyaandika (Qâdhi ‗Iyâdh) katika ash-Shifâ‘, kuhusu jinsi ya kumswalia, yakipokewa kutoka kwa maswahaba na wale waliokuja baada yao, na pia akataja mambo mengine ndani yake.

Ndio, imepokewa katika hadîth ya Ibn Mas‘ûd yakwamba

katika kumswalia kwake Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), alikuwa

akisema:

اد نظةا اصف ال » « ارشي شد ع وبركد ورمحذ ص الدير...

Imepokewa na Ibn Mâjah, lakini isnâd yake ni dha‘îf, kwa hivyo hadîth ya ‗Ali, iliyopokewa na at-Twabarâni kwa isnâd yenye kukubalika, inachukuwa nafasi ya mwanzo. Hadîth hii ina maneno magumu niliyoyapokea na kuyachambua katika kitabu

―fadhl un-Nabî” (fadhla za Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) cha Abul Hasan

Ibn al-Fâris. Baadhi ya ma-Shâfi‘î wamesema yakwamba ikiwa

mtu amekula kiapo cha kumswalia Mtume (صلى اهلل عليه وسلم) bora ya

kumswalia, basi itakuwa njia ya kutimiza kiapo chake ni kusema:

ره لكة مد ع ص ال» ره ـ وشة الارون ذ « الةنن ذ Amesema Imâm an-Nawawî, ―Ile ambayo inayofaa zaidi kuwa ni ya sawa kwamba mtu na aseme:

148

« إثرا ع صخ ة مد آل وع مد ع ص ال » الدير...

Idadi kubwa ya wanavyuoni waliokuja baada e wameyajibu haya kwa kusema yakwamba hakuna katika njia mbili hizo zilizotajwa inayofahamisha juu ya kuthibiti ubora katika matamshi hayo mawili kwa kuzingatia kunakili. Amma kwa kuzingatia maana, matamshi yaliyo bora zaidi ni dhahiri katika lile la kwanza. Mas‘ala haya ni mashuhuri katika vitabu vya fiqh, na makusudio ya mas‘ala haya, kila aliye yataja mas‘ala haya katika wanavyuoni wa fiqh wote haikupatikana kwa yoyote katika hao wanavyuoni wa fiqh tamshi hili ―Sayyid‖. Lau ingelikuwa ziyada hii ni sunnah, isingejificha kwao wote mpaka wakaghafilika nayo.

Na kheri yote hupatikana katika kumfuata Mtume (صىل اهلل عليه وسلم).

Wallahu a‘lam.

Rai aliyokwenda nayo al-Hâfidh, Ibn Hajar (رحمه اهلل) , ya

kutokubaliwa kumsifu Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) kama sayyid katika

wakati wa kumswalia kulingana na amri ya Qur‘ân, pia ni ile ya wanavyuoni wa ki-Hanafî. Nayo ndiyo rai ambayo ipasayo kuambatana nayo, kwani hiyo ni ishara ya ukweli wa mapenzi juu

yake, (صىل اهلل عليه وسلم);

تجن ى ذ ٱإن دذجفن ٱن للذ ٱيججس ٣١ للذ"Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Allâh‎, basi nifuateni;

(hapo) Allâh‎ atakupendeni ...” [Âl-‘Imrân 3:31] Kwa ajili hii, Imâm an-Nawawî akasema katika Rawdhatu-Tâlibîn (1/265), ―Yâ Allâh‎! Mfikilizie amani Muhammad ...‖ n.k. kwa kuafiki namna ya tatu iliyotangulia, pia Imâm an-Nawawî hapa hakutaja neno sayyid!

149

5) Inatakiwa ijulikane hapa yakwamba namna ya kwanza (1) na

namna ya nne (4) ndizo ambazo Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

alizowafundisha maswahaba zake walipomuuliza kuhusu jinsi ya kumswalia, kwahivyo hii imetumiwa kama ushahidi yakwamba hizi ndizo njia bora zaidi za kumswalia yeye, kwani hawezi kuwachagulia maswahaba zake au kujichagulia yeye mwenyewe isipokuwa yaliyo matukufu na bora zaidi. Imâm an-Nawawî amefanya sawa katika kitabu chake (Rawdhatu-Tâlibîn) yakwamba iwapo mtu atakula kiapo

yakwamba atamswalia Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) kwa njia iliyo bora

zaidi, haliwezi kukamilika hilo isipokuwa kwa njia hizi. Subki ametoa sababu nyengine: Yoyote mwenye kumswalia

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) kwa njia hizo atakuwa amemswalia kwa

yakini, na yoyote mwenye kufanya hivyo kwa kutumia matamshi mengine huwa kwenye shaka iwapo amemswalia kama inavyohitajika. Hii ni kwa sababu walimuuliza, ―Sisi tutakuswalia vipi?‖ na akawajibu, ―Semeni: ...‖ kwa hiyo, ameja‘alia kumswalia kutokana na wao, ni kusema kwao kadhaa na kadhaa. Haya yametajwa na Haitami katika ad-Dâr al-Mandhûd (25/2); kisha akasema (27/1) yakwamba lengo linapatikana kwa njia zote zilizopatikana katika ahâdîth zilizo swahîh .

6) Inapasa kujulikana yakwamba haitakiwi kuyaingiza matamshi ya swala moja katika jumla ya matamshi haya ya kumswalia

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), na vile vile husemwa hivyo katika

matamshi ya tashahhud yaliyotangulia. Kwa hakika, huwo ni uzushi katika dini; Sunnah ni kusema matamshi tafauti katika nyakati tafauti, kama alivyoibainisha hivyo Sheikh ul-IsLaam Ibn Taymiyyah katika kuyazungumzia mas‘ala yanayofungamana na takbîr za Idd mbili (Majmû‘ al-Fatâwâ 29/253/1).

150

7) ‗Allâmah‎‎ Siddîq Hasan Khân amesema katika kitabu chake Nuzul al-Abrâr bil ‗Ilm al-Ma‘thûr min al-Ad‘iyah wal-ADHKÂR, baada ya kutoa ahâdîth nyingi za kuhusu fadhla za

kurudia-rudia kumswalia Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) (Uk. 161):

―Hapana shaka yakwamba watu wengi wanaokithirisha

kumswalia Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) ni watu wa hadîth na wapokezi wa

Sunnah zenye kutakaswa, kwani ni katika kazi zao, katika hii

‗ilmu tukufu ya kumswalia Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) mbele ya kila

hadîth , na kwahivyo ndimi zao haziachi kuwa majimaji kwa

kumtaja Mtume (صىل اهلل عليه وسلم). Hakuna kitabu chochote katika

vitabu vya Sunnah, wala mkusanyo wa hadîth , iwe ni Jâmi‘, Musnad, Juz‘, n.k, isipokuwa zimekusanya maelfu ya ahâdîth; hata kijitabu kidogo chao kilichoandikwa na Imâm as-Suyûti, ambacho ni al-Jâmi‘ as-Swaghîr‎‎, kina hadîth Elfu-kumi, sasa

fananisha hapo vitabu vyote vya hadîth za Mtume ( هلل عليه وسلمصىل ا ).

Kikundi hiki chenye kuokoka, na kikundi hiki cha watu wa hadîth

ndio watu bora kwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) siku ya QiYâmah, na

ndio wema wao siku ya QiYâmah kwa kupata Shifâ‘ ya Mtume ( صىل Wala halingani sawa na hao katika fadhila yoyote .(اهلل عليه وسلم

katika watu, ila waliokuja na jambo bora zaidi kuliko na waliokuja nayo, jambo lenye kukurubia kutowezekana. Kwahivyo, ni juu yako ewe mwenye kutaka kheri, mwenye kutafuta uokofu bila ya madhara, usijali chochote, ni imma uwe ni muhaddith, au ujikurubishe na hawa muhaddithîn; usiwe vyenginevyo ... kwani mbali na hivyo hakuna kitakachokufaidisha wewe.‖

Namuomba Allâh‎ (سبحانه وتعاىل) anija‘alie mimi ni mmojawapo wa

watu hawa wa Hadîth , ambao ndio bora wa watu kwa Mtume ( صىل Pengine huwenda kitabu hiki kikawa ndio ushahidi ya ;(اهلل عليه وسلم

151

hayo. Namuomba Allâh‎ (سبحانه وتعاىل) amteremshie Rehma zake Imâm

Ahmad, aliyetunga beti hizi:

ف اػح لهت آزةر دي اجليب مد أخجةر نةلرأي حل والدير ةر ل دركنب ـ الدير وأ

ار ولربة ص اهت أزر ادى والظس ثةزكح ة أDini ya Mtume Muhammad imejengewa katika mapokezi,

Vipando bora kwa kijana ni âthâr;

Usizichukie Hadîth na watu wake, Kwani rai ni usiku, haliyakuwa Hadîth ni mchana,

Huwenda kijana mdogo asizijue athari za uongofu ...

Hata kama Jua lang‘ara kwa miyale yake yote

DUA‟ KATIKA TASHAHHUD YA KWANZA

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) pia aliweka uongofu wa dua‘ katika

tashahhud hii vilevile, kwa kusema, Unapokâ baada ya kila Rak‘âh mbili, sema: Attahiyyâtu LilLaah ... (mpaka mwisho wake, kisha akasema:) ... kisha na ajichagulie miongoni mwa dua‘ yoyote aipendayo.1

1 An-Nasâ‘î, Ahmad na at-Twabarâni kwa idadi kubwa ya isnâd kutoka kwa Ibn Mas‘ud – masimulizi yake zaidi yanapatikana katika as-Swahîhah (878) – na kuna hadîth yenye kuitilia nguvu ya Ibn az-Zubeir katika Majma‘ az-Zawâ‘id (2/142)

152

KUSIMAMA KWENDA KATIKA RAK‟ÂH YA TATU KISHA YA NNE

Kisha Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alikuwa akiinuka kwenda katika Rak‘âh

ya tatu hali ya kuleta takbîr1, na akamuamrisha ―yule mwenye kuiharibu swala yake‖ afanye hivyo: kisha fanya hivyo katika kila Rak‘âh , kama ilivyotangulia.

Alipokuwa akisimama (صىل اهلل عليه وسلم) kutoka katika kikao,

alikuwa akitamka takbîr, kisha husimama‖2; na alikuwa ( صىل اهلل عليه .mara nyengine akiinua mikono yake3 anapoitamka takbîr hii (وسلم

―Alipotaka kuinuka kwa Rak‘âh ya nne, alikuwa akisema: Allâh‎u Akbar‖4, na akamuamrisha ―yule mwenye kuiharibu swala yake‖

afanye hivyo, kama ilivyotangulia, na alikuwa (صىل اهلل عليه وسلم) mara

nyengine akiinua mikono yake5 anapoitamka takbîr hii.

Alikuwa akikaa hali ya kulingana juu ya mguu wake wa kushoto, kwa umakinifu, mpaka kila mfupa urudi mahali pake, kisha anasimama, hali ya kujisaidia juu ya ardhi; na alikuwa akikunja ngumi zake6: Akijisaidia kusimama kwa nguvu za mikono yake.‖7

1 Bukhâri na Muslim 2 Abu Ya‘laa katika Musnad yake (284/2) kwa isnâd iliyo nzuri. Inapatikana katika Silsilah al-Ahâdîth as-Swahîhah (604) 3 Bukhâri na Abu Dâwud 4 Ibid. 5 Abu ‗Awânah na an-Nasâ‘î kwa sanad iliyo swahîh. 6 Maana halisi, ―kama mtu anaekanda unga.‖ 7 Harbi katika Gharîb al-Hadîth; maana yake inapatikana katika Bukhâri na Abu Dâwud. Amma kuhusu hadîth, alikataza mtu asijisaidie kwa mikono yake anaposimama wakati wa swala‖, hii ni munkar wala si swahîh, kama nilivyoeleza katika Silsilah al-Ahâdîth adh-Dha‘îfah (967).

153

Alikuwa akisoma Al-Fâtihah katika Rak‘âh zote hizi, na akamuamrisha ―yule mwenye kuiharibu swala yake‖ afanye hivyo. Katika swala ya Adhuhuri, mara nyengine alikuwa akiongeza Âyât chache juu yake, kama ilivyoelezwa chini ya anwani ya ―Kisomo katika swala ya Adhuhuri.‖

QUNÛT KATIKA SWALA TANO KUTOKANA NA BALAA

ITOKEAPO

Na alikuwa Mtume (صلى اهلل عليه وسلم) akitaka kumuapiza yoyote au

kumuombea yoyote, alikuwa akifanya qunût1 katika Rak‘âh ya mwisho, baada ya rukû‘; baada ya kwisha kusema: Sami‘ Allâh‎u Liman Hamidah Allâh‎umma Rabbanâ Lakal Hamd.2 Alikuwa akiomba kwa sauti3, akiinua mikono yake4, na wale waliokuwa nyuma yake huitikiya: ―Âmîn‖5.

1 Qunût: Ina maana nyingi, kwa mfano, unyenyekevu, utiifu. Linalokusudiwa hapa ni dua‘ mâlum ukiwa katika hali ya kusimama katika swala. 2 Bukhâri na Ahmad 3 Ibid. 4 Ahmad na at-Twabarâni kwa sanad iliyo swahîh. Kuinua mikono katika Qunût ni madh-hab ya Imâm Ahmad na pia Is-hâq Ibn Râhawayh, cf. Kitabu cha Marwazi Masâ‘il (Uk. 23). Amma kuhusu kupangusa uso kwa mikono, hiyo haikupokewa katika hali hii (ya kisimamo), na kwa hivyo inakuwa ni Uzushi; Amma kuhusu nje ya swala, haikuswihi kupokewa: yote yaliyopokewa kuhusiana na suala hili ni imma dha‘îf au dha‘îf kabisa, kama nilivyo onyesha katika Dha‘îf Abu Dâwud (262) na Silsilah al-Ahâdîth as-Swahîhah (597). Hii ndiyo sababu kwanini ‗Izz Ibn ‗Abdus-Salaam akasema katika mojawapo ya Fatâwa zake, ―Jambo hilo hufanywa na mtu mjinga peke yake..‖ Angalia katika Kiambatisho cha 8. 5 Abu Dâwud na Sirâj; Hâkim aliithibitisha kuwa ni swahîh na , na adh-Dhahabi na wengineo wakakubaliana na hayo.

154

Na alikuwa akikunuti katika swala tano zote1, lakini alikuwa hakunuti katika swala hizo isipokuwa akiwaombea watu au akiwâpiza watu2. Kwa mfano, siku moja alisema:

ةش ظةم ث وشح الحلد ث الحلد اش ال » ربفح أب ث ـوشم صن شني واصفة مرض ع وغأد اطدد ال ال ] ي

ال لةن اف ان وـر صح وذ 3« [ ورشل الل ـصخ ـو Kisha, ―alikuwa akisema: ―Allâh‎u Akbar‖ amalizapo qunût, halafu anasujudu.‖4

QUNÛT KATIKA SWALA YA WITR

Alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akifanya qunût katika Rak‘âh (ya

mwisho) ya witr5, mara nyengine6, na alikuwa akiifanya kabla ya rukû‘1.‖

1 Abu Dâwud, Sirâj na Dâraqutnî‘, kwa sanad mbili zilizo hasan 2 Ibn Khuzaymah katika swahîh yake (1/78/2) na Khatîb katika Kitâb al-Qunût, kwa sanad iliyo swahîh. 3 Bukhâri na Ahmad; hiyo nyongeza iko katika Muslim. 4 An-Nasâ‘î, Ahmad na Sirâj (109/1) na Abu Ya‘laa katika Musnad yake kwa isnâd nzuri. 5 Ibn Nasr na Dâraqutnî‘ kwa sanad iliyo swahîh. 6 Tumesema, ―… mara nyengine‖ kwa sababu maswahaba waliopokea kuhusu swala ya Witr hawakutaja qunût ndani yake, na lau kama Mtume

angelikuwa akiifanya hivyo wakati wowote, hao wote (صىل اهلل عليه وسلم)

wangelilitaja hilo. Hata hivyo, ‗Ubayy Ibn Ka‘b peke yake ndiye aliyeipokea kuhusu Witr, kwa hivyo hii yaonyesha yakwamba alikuwa akifanya hivyo mara nyengine. Kwa hiyo, huu ni ushahidi yakwamba qunût katika Witr si Wâjib, na huu ndio msimamo wa wengi wa wanavyuoni. Kwa sababu hii, mwanachuoni-mtafiti wa ki-Hanafî, Ibn al-Humâm, aligunduwa yakwamba katika Fat-hul Qadîr (1/306,359,360) yakwamba rai yake kuwa ni wâjib ni dha‘îf na wala haikuthibitishwa kwa dalili. Hii yaonyesha uadilifu wake na ukosefu wa upendeleo wa

155

Alimfundisha al-Hasan Ibn ‗Ali (رضي اهلل عنه) aseme [baada

amalizapo kisomo chake katika Witr]:

ن ودن اعنخ ن واعنن ديخ ن ادين ال » إ [ ف ] ىظخ ة ش وىن أـػخ نة ل وبةرك دحلخ يفز ول ] واحلخ يذل ل إ [ و ] ـ يييض ول دييض

2 « [ل ضة إل إحل ]دجةركخ ربة ودفةحلخ [ اعديخ

kimadhehebu, kwani rai hii ambayo aliyoiunga mkono ni kinyume cha madh-hab yake! 1 Ibn Abî Shaybah (12/41/1), Abu Dâwud, an-Nasâ‘î katika Sunan al-Kubra (218/1-2), Ahmad, at-Twabarâni, al-Baihaqî na Ibn ‗Asâkir (4/242/2) waliyapokea haya, pamoja na dua‘ baada yake, kwa sanad iliyo swahîh. Ibn Mandah alipokea kuhusu dua‘ peke yake katika Tawhîd (70/2) kwa sanad tafauti iliyo hasan. Takhrîj yake pia inapatikana katika Irwâ‘ (426). 2 Ibn Khuzaymah (1/119/2) na pia Ibn Abî Shaybah n.k, ama kuhusu hadîth ya mwisho. TANBÎH! An-Nasâ‘î ameongeza mwishoni mwa qunût: ―... wa sall-Allaahu ‗ala-n-Nabiyy al-Ummiyy‖, imepokewa kwa isnâd iliyo dha‘îf; Miongoni mwa wale walioithibitisha udhaifu wake ni Ibn Hajar al-‗Asqalaani na Zurqâni. Kwa hivyo, hatukuijumuisha katika mpangilio wetu wa kuunganisha riwaya zinazokubalika. ‗Izz Ibn ‗Abd as-Salaam

amesema katika al-Fatâwa (66/1,1962), ―Kumswalia Mtume ( صىل اهلل عليه katika qunût si swahîh, wala haifai kuongeza katika kumswalia (وسلم

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) kwa njia yoyote. Rai hii yake yaonyesha yakwamba

hakuyakuuza majadiliano kwa kuingiza fikra ya bid‘ah hasan (Bid‘ah ―Nzuri‖), kama wanavyuoni wa baadae walivyo zoea kufanya! Hata hivyo, Imethibitishwa kwenye hadîth kuhusu ‗Ubayy Ibn Ka‘b akiongoza watu kwenye swala ya usiku katika mwezi wa Ramadhân

156

TASHAHHUD YA MWISHO

UWAJIBU WA TASHAHHUD HII

Kisha, baada ya kukamilisha Rak‘âh ya nne, alikuwa Mtume ( صىل akikaa kwa tashahhud ya mwisho. Alikuwa akiamrisha (اهلل عليه وسلم

kuhusiana na tashahhud, na akifanya katika hiyo tashahhud kama vile alivyokuwa akifanya katika tashahhud ya kwanza, isipokuwa alikuwa akikaa kikao cha mutawarrikan‖1, ―kwa kuweka sehemu ya juu ya paja lake la kushoto kwenye ardhi, haliyakuwa miguu yake yote ikijitokeza kutoka upande mmoja2‖ (Yaani; upande wa kulia). Alikuwa akiweka mguu wake wa kushoto chini ya paja lake (la kulia) na muundi‖3, mguu wake wa kulia huuweka sawa‖4 au mara chache ―huulaza kwenye ardhi.‖5 Kitanga chake cha kushoto kilikuwa kikiziba goti lake (la kushoto), ambalo alokuwa akililemea kwa uzito mkubwa juu yake.‖6

yakwamba alikuwa akimswlia Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) mwishoni mwa qunût,

na hiyo ilikuwa wakati wa utawala wa ‗Umar (رضي اهلل عنه) - imepokewa na

Ibn Khuzaymah katika swahîh yake (1097). Vile vile imethibitishwa kutoka kwa Abu Halîmah Mu‘âdh al-Aswâri, ambae pia alikuwa akiwaongoza wakati wa utawala wa ‗Umar – Imepokewa na Ismâ‘îl al-Qâdhi (no.107) na wengineo, kwahivyo nyongeza hii imethibitishwa kwa vitendo vya Salaf, na kwahivyo haifai kukatikiwa kusema yakwamba nyongeza hii ni Uzushi. Allaah Anajua zaidi. 1 Bukhâri 2 Ibid. Amma kwa swala ya rakâ‘ah mbili kama vile Fajr, Sunnah ni kukâ Muftarishan. Tafauti iliyoko imesimuliwa kwa utondoti kutoka kwa Imâm Ahmad, cf. Masâ‘il ya Imâm Ahmad cha Ibn Hâni (Uk. 79) 3 Abu Dâwud na al-Baihaqî kwa sanad iliyo swahîh. 4 Muslim na Abu ‗Awânah 5 Ibid. 6 Ibid.

157

Akaonyesha mfano wa kumswalia yeye (صىل اهلل عليه وسلم) katika

tashahhud hii, kama ilivyokuwa katika tashahhud ya kwanza; njia

za kumswalia yeye (صىل اهلل عليه وسلم) zimekwisha tangulia huko

nyuma.

UWAJIBU WA KUMSWALIA MTUME (صىل اهلل عليه وسلم) KATIKA

TASHAHHUD HII

Siku moja Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alimsikiya mtu mmoja akiomba

dua‘ haliyakuwa yuko kwenye swala, lakini akawa hakumtukuza

Allâh‎ (سبحانه وتعاىل) wala hakumswalia Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), basi

akasema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم): Mtu huyu alikuwa na pupa.‖ Kisha

akamwita na akamwambia yeye pamoja na maswahaba wengine,

―Anaposwali mmoja wenu, na aanze kumsifu Mola wake (عز وجل) na kumtukuza, kisha na amuombî rehma Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

(katika riwaya nyengine, na amswalie Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), kisha

na aombe dua‘ aitakayo.‖1

1 Ahmad, Abu Dâwud, Ibn Khuzaymah (1/83/2) na al-Hâkim, aliyeithibitisha kuwa swahîh na adh-Dhahabi akaiafiki. Inapasa kujulikana yakwamba hadîth hii inathibitisha yakwamba Swala

(kumswalia) Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) katika tashahhud hii ni wâjib,

kutokana na amri iliyowekwa. Rai hii imechukuliwa na Imâm ash-Shâfi‘î na Imâm Ahmad katika ya pili miongoni mwa riwaya mbili zitokazo kwake, na kabla yao kutoka kwa maswahaba, na vilevile wanavyuoni. Kwa ajili hii, Imâm al-Âjurrî akasema katika kitabu chake Sharî‘ah (Uk.

415): ―Yule ambae asomswalia Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) katika tashahhud ya

mwisho, basi ni lazima airudie swala yake.‖ Kwa hiyo, wale wenye kumbandikiza Imâm ash-Shâfi‘î yakwamba yeye ni kituko aliye peke yake na rai yake juu ya jambo hilo, si wâdilifu kabisa, kama alivyoeleza Faqîh Haitami katika Dâr al-Mandûd (Sehemu ya 13-16).

158

Pia, alimsikiya mtu akiswali, akamtukuza Allâh‎ (سبحانه وتعاىل), akamsifu na akamswalia Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), basi Mtume ( صىل اهلل akamwambia: Omba utajibiwa; na omba utapewa.‖1 (عليه وسلم

UWAJIBU WA KUTAFUTA HIFADHA KUTOKANA NA MAMBO MANNE KABLA YA DUA‟

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alikuwa akisema, ―Mmoja wenu amalizapo

tashahhud [ya mwisho], na atake hifadha kwa Allâh‎ kutokana na mambo manne; [aseme:]

ايرب و ـذاب و ص ـذاب [ ث أـذ إين ال » « الصةل اصط [ نذح ]نذح اعة واةت و ش

―Yâ Allâh‎! Kwa hakika mimi naomba hifadha kwako kutokana na adhabu ya Jahannam, na kutokana na adhabu

ya kaburi, na kutokana na mitihani ya uhai na kufa, na kutokana na shari (mitihani) ya Masîh ad-Dajjâl.‖

[Kisha na ajiombî Dua‘ nafsi yake dua‘ inayomdhihirikia.]‖2 –

Alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akiomba kwa dua‘ hii katika

tashahhud yake.‖3

Pia, alikuwa akiwafundisha maswahaba zake (رضي اهلل عنهم) haya

kama alivyokuwa akiwafundisha Sûrah katika Qur‘ân.‖4

1 An-Nasâ‘î kwa sanad iliyo swahîh. 2 Muslim, Abu ‗Awânah, an-Nasâ‘î na Ibn al-Jârûd katika al-Muntaqâ (27). Inapatikana katika Irwâ‘ (350) 3 Abu Dâwud na Ahmad kwa sanad iliyo swahîh. 4 Muslim na Abu ‗Awânah

159

DUA‟ ZINAZOLETWA KABLA YA SALAAM NA SAMPULI ZAKE MBALI-MBALI

Na alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akiomba dua‘ mbali mbali katika

swala yake1, akiomba kwa dua‘ tafauti katika nyakati tafauti; pia amezituza dua‘ nyengine, na ―akamuamrisha mja kukhitari anayoitaka katika dua‘ hizo.‖2 Nazo ni:

1 Hatujasema, ―... katika tashahhud yake‖ kwa sababu nass yenyewe ni, ―... katika swala yake‖, bila ya kueleza bayana iwapo ni tashahhud au ni kitu chochote. Kwa hiyo, inahusu vikao vyote vinavyofâ kwa dua‘, k.m, sijdah na tashahhud; maelezo kamili kuhusu dua‘ katika vikao hivi viwili imetangulia kutajwa huko nyuma. 2 Bukhâri na Muslim. Amesema Athram, ―Nilimuuliza Ahmad: ―Mimi niombe kwa (maneno gani) baada ya tashahhud?‘ Akasema, ‗Kama

ilivyopokewa.‘ Nikasema, ‗Kwani Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) hakusema, ―Kisha

na akhitari dua‘ yoyote aipendayo‖?‘ Akasema, na achague kutokana na yaliyopokewa.‘ Nikarudia tena swali langu: akasema, ‗Kutokana na yaliyopokewa‘.‖ Yamenukuliwa haya na Ibn Taymiyyah (Majmû‘ al-Fatâwa 69/218/1), aliyeiunga mkono, na kuongezea, ―Kwa hiyo, makusudio ya ‗dua‘ yoyote aipendayo‘ ni dua‘ ambayo Allaah anaipenda, na wala sio dua‘ yoyote tu ...‖ kisha akasema, ―Kwa hiyo, ni bora kusema: (mtu na aombe) kwa iliyoidhinishwa, dua‘ iliyothubutu, na haya ndiyo yaliyowahi kupokewa na yenye faida.‖ Hivi ndivyo ilivyo, lakini ukitaka kutambua kwa hakika ni dua‘ gani iliyo na faida inategemea juu ya ‗ilmu iliyo swahîh, na jambo hili ni nadra sana kupatikana miongoni mwa watu, kwa hivyo ni bora kushikamana na dua‘ zilizonukuliwa, hususan ikiwa ndani yake munapatikana yale anayoyataraji kuyaomba mja. Allaah ni Mjuzi zaidi.

160

1.

اصط نذح ث وأـذ ايرب ـذاب ث أـذ إين ال » ث أـذ إين ال واةت اعة نذح ث وأـذ الصةل

«أز والرم ا―Yâ Allâh‎! Hakika yangu mimi nataka hifadha Kwako

kutokana na adhabu ya kaburi, na nataka hifadha Kwako kutokana na fitna za Masîh ad-Dajjâl, nataka hifadha

Kwako kutokana na mitihani ya uhai na kufa. Yâ Allâh‎! nataka hifadha Kwako kutokana na madhambi1 na

majukumu 2.‖3

2.

ثفد ]ـأ ل ة ش و ـخ ة ش ث أـذ إين ال »] »

―Yâ Allâh‎! Hakika yangu mimi nataka hifadha Kwako kutokana na shari ambazo nilizozitenda na kutokana na

shari ambazo [bado].4sijazitenda.‖ 5

1 ma‘tham: yanayomsababisha mtu kufanya madhambi, au madhambi yenyewe. 2 maghram: Jukumu, maana yake hapa ni deni, kama ilivyothibitishwa na baki ya hadîth, ambayo ‗Âisha aliposema, ―Mtu mmoja akamwambia, ‗Ni kwanini mara kwa mara waomba hifadha kutokana na maghram, Ewe Mjumbe wa Allaah?‘ Akamjibu, Kwa hakika mtu anapokuwa na deni, husema urongo, na hutoa ahadi kisha akazivunja ahadi hizo. 3 Bukhâri na Muslim 4 Yaani; Kutokana na shari za vitendo vibaya nilivyovitenda, na kutokana na kutotenda vitendo vizuri. 5 An-Nasâ‘î kwa sanad iliyo swahîh na Ibn Abî ‗Âsim katika kitabu chake As-Sunnah (no.370 – chenye usahihisho wangu); na nyongeza imetoka kwenye iliyofuatia.

161

1.

«صةثة يصريا ظ ظةشبن ال »―Yâ Allâh‎! Nihisabie mimi, kwa hisabu yenye wepesi.‖1

2.

ـخ ة أظن اخلو ع وىدرد الت ثف ال » وأشأل ال ل خريا النةة كخ إذا ودنن ل خريا الةة : روايح ويف ) الو لكح وأشأل والظةدة الت ف خظيذلظت والرىض وأشأل ايصد ف اهير ا ف وافدل ( الس

ل [دهد و ل ]والن وأشأل فة ل يبد وأشأل ىرة ـي ديػؿ وأشأل الرىض ثفض ايظةء وأشأل ثرد افيض ثفد

الظق إل [أشأل ]ات وأشأل لة اجلؾر إل وص و يةا ف كري رضاء مرضة ول نذح مظح ال زية ثزيح

«اليةن واصفة داة ذدي ―Yâ Allâh‎! [nakuomba], kwa ‗Ilmu yako ya yaliyofichamana, na kudura zako juu ya viumbe : nihuishe mâdamu wajua yakwamba uhai ni bora kwangu mimi, na unifishe mâdamu

wajua yakwamba mauti ni bora kwangu mimi. Yâ Allâh‎! Vilevile naomba kutoka kwako uchaji juu yako katika siri na dhahiri. Na nakuomba Neno la Haki‖ [na katika riwaya nyengine: ―Hikma] na uadilifu ninapofikwa na ghadhabu na ninapokuwa radhi. Na nakuomba uongofu katika ufukara

1 Ahmad na Hâkim aliyeithibitisha kuwa swahîh na adh-Dhahabi akaiafiki.

162

na ukwasi; na nakuomba ne‘ema isiyopotea; na nakuomba yenye kunipumbaza‖ [yasiyo ondoka, wala] ―yasiyokwisha;

nakuomba niridhike na Qadar itokayo kwako; nakuomba ubaridi wa maisha baada ya mauti; na nakuomba ladha ya mtazamo wa Uso Wako; na [nakuomba] unipe shauku ya kukuona Wewe; isiwe katika hali ya kudhurika kwa mâfa, wala katika hali ya fitna ya upotofu. Yâ Allâh‎! Tupambe sisi kwa pambo la Imân na utuja‘aliye tuwe ni waongofu

wenye kuongoza.1

3.

ال إين ؽخ هيس ؽة سريا ول يلهر الب إل أخ » «نةكهر ل لهرة ـدك وارمحن إ أخ الهر الرظ

―Yâ Allâh‎! Kwa hakika mimi nimejidhulumu nafsi yangu dhulma nyingi, wala hapana mwenye kusamehe dhambi

isipokuwa Wewe, basi nisamehe nami kutokana na Msamaha Wako, na unirehemu nami, hakika Wewe daima,

ni Mwenye kusamehe na Mwenye huruma.‖2

4.

ـخ ة [ وآص اعص ] لك اخلري أشأل إين ال » ـخ ة [ وآص اعص ] لك الش ث وأـذ ـأ ل وة وة الح ( أشأل إين ال : روايح ويف ) وأشأل أـ ل وة إحلة ىرب وة اجلةر ث وأـذ ـ أو ىل إحلة ىرب

1 An-Nasâ‘î na Hâkim aliyeithibitisha kuwa swahîh na adh-Dhahabi akaiafiki. 2 Bukhâri na Muslim

163

[ال ] (ال إين أشأل :ويف روايح )أشأل و ـ أو ىلمد وأـذ ث ش ة ] خري ة شأل ـجدك ورشل

] [ صل الل ـ وشاشذفةذك ـجدك ورشل مد « رطدا [ ل ] اعىجذ تف أن أمر ل ىظخ ة [وأشأل

―Yâ Allâh‎! Kwa hakika mimi nakuomba kutokana na kila Kheri, [ya karibu na ya mbali] ile ambayo mimi naijua na

ile nisoijua; Na najilinda kwako na kila shari, [ya karibu na ya mbali] ile ambayo mimi naijua na ile nisoijua.

Nakuomba (katika riwaya nyengine: Yâ Allâh‎! Kwa hakika mimi nakuomba) Pepo, na kila chenye kunikurubisha nayo, miongoni mwa maneno au vitendo; Na najilinda kwako na Moto, na kila chenye kunikurubisha nao, (na kutokana na)

miongoni mwa maneno au vitendo; Na nakuomba (Na katika riwaya nyengine: Yâ Allâh‎! Kwa hakika nakuomba) kutokana na [la] kheri aliloliomba mja wako na mtume

wako [Muhammad; na nakuomba hifadha itokayo kwako na shari ambayo aliyoitakia hifadha mja wako na mtume wako

Muhammad (صىل اهلل عليه وسلم)] [Na nakuomba] yote

uliyonikadiriya mimi, matokeo yake yawe ni yenye kunifaidisha [mimi].‖ 1

5. Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)alimuuliza mtu mmoja, ―Unasema nini

wewe wakati unaposwali?‖ Akajibu yule mtu, ―Mimi nashuhudia (Yaani; nasoma tashahhud), kisha namuomba Allâh‎ Pepo, na nataka hifadha kwake na Moto. Hata hivyo,

1 Ahmad, Tayâlisi, Bukhâri katikan al-Adâb al-Mufrad. Ibn Mâjah na Hâkim aliyeithibitisha kuwa swahîh na adh-Dhahabi akaiafiki. Nimeitolea takhrîj yake katika Silsilat al-Ahâdîth as-Swahîhah (1542).

164

WAllâh‎i mimi sina minon‘gono1 mizuri ya dua‘ kama yako wala kama ya Mu‘âdh‖. Basi akasema, ―Minon‘gono yetu ni kama yako tu.‖ 2

6. Alimsikiya mtu akisoma katika tashahhud yake:

اظد ] ( ثةلل : روايح ويف ) الل ية أشأل إين ال » الظد [ الا أظد أن دلهر ل يس ول يل ول يدل ل الي الصد ل ه

«ذيب إ أخ الهر الرظ ―Yâ Allâh‎! Kwa hakika nakuomba, Yâ Allâh‎ (katika riwaya

nyengine: kwa jina la Allâh‎) Mmoja tu, Aliye Pekee, anaestahiki kukusudiwa, ambae Hakuzâ wala Hakuzaliwa,

asiyekuwa na anaefanana nae hata mmoja, yakwamba unisamehe madhambi yangu, , hakika Wewe daima, ni

Mwenye kusamehe na Mwenye huruma.‖

Juu ya hayo, Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)akasema, ―Amesamehewa,

amesamehewa.‖ 3

7. Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)alimsikiya mtu mwengine akisema katika

tashahhud yake pia:

1 Dandanah: kutamka kwa sauti nyororo ikasikika vyema, lakini maneno yenyewe ukashindwa kuyaelewa – katika hali hii, maneno ya kutamkwa kwa siri katika dua‘. Maneno ya mwisho maana yake ni, ―Maneno yetu ni kama yako.‖ 2 Abu Dâwud, Ibn Mâjah, na Ibn Khuzaymah (1/87/1) kwa isnâd iliyo swahîh. 3 Abu Dâwud, an-Nasâ‘î, Ahmad na Ibn Khuzaymah. Hâkim akaithibitisha kuwa swahîh na adh-Dhahabi akaiafiki

165

شي ل وظدك] أخ إل إل ل الد ل ثأن أشأل إين ال » والرام الالل ذا ية والرض الصةوات ثديؿ [ية] [اةن] [ل

م ية ح ية « [الح وأـذ ث اجلةر] [أشأل إين] ى―Yâ Allâh‎! Hakika nakuomba, kwa haki yakwamba Kila sifa njema ni zenye kukustahiki Wewe, Hapana (mola) apasae

kuabudiwa kwa haki isipokuwa Wewe. [Wewe Pekee, usokuwa na mshirika;] Mpaji wa fadhla; [Ewe] muanzilishi wa Mbingu na Ardhi; Ewe wa pweke Uliye na Utukufu na

Ikiramu; Ewe Uliye Hai, Ewe wa Enzi; [Hakika yangu mimi, nakuomba] [Pepo na naomba hifadha kutoka kwako

kutokana na Moto]. [Basi Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)akawâmbia

Maswahaba zake baada ya kumsikiya mtu huyo akiomba kwa dua‘ hiyo, Je munajua alivyo omba? Wakasema, ―Allâh‎ na Mtume wake ni bora ya wanaojua.‖Akasema, Naapa kwa

yule ambae Mkononi mwake ndipo ilipo roho yangu,] amemuomba Allâh‎ kwa Jina lake kubwa (katika riwaya

nyengine: Kubwa zaidi) na jina1 ambalo iwapo huombwa

1 Hii ni tawassul (kutafuta kitakachokuletea mkuruba) kwa Allaah, ambao kwa kupitia Majina Yake mazuri zaidi na sifa Zake, na haya

ndiyo ambayo Allaah (سبحانه وتعاىل) aliyotuamrisha:

ةء ٱ وللذ شه ٱن لصن ٱ ل ـ د ة ١٨٠ث

“Na Allaah ana majina mazuri mazuri; muombeni kwayo.” [Sûrah al-A‘râf 7:180]

Amma kutaka kujikurubisha kwa Allaah kwa kupitia njia nyengine; k.m, kwa ajili ya fulani wa fulani, au kwa haki ya fulani wa fulani, au kwa ajili ya hadhi ya fulani wa fulani, au kwa ajili ya heshima ya fulani wa

fulani, n.k. Kuna dalili kutoka kwa Imâm Abu Hanîfah (اهلل رحمه) na

wenzake yakwamba kitendo kama hicho ni, kwa uchache chenye kuchukiza (makrûh); kwa ujumla imekatazwa (harâm). Kwa hivyo, ni jambo la kusikitisha yakwamba utawaona watu wengi, miongoni mwao

166

kwalo, Yeye hujibu, na jina ambalo iwapo huulizwa kwalo, Yeye hutoa1.

8. Mojawapo ya kitu cha mwisho ambacho hukisema baina ya tashahhud na taslîm ni:

خ وة أخرت وة أرسرت وة أـخ وة ىد ة اكهر ال »أرسنخ وة أخ أـ ث ن أخ ايدم وأخ اؤخر ل إل إل

«أخ

―Yâ Allâh‎! Nisamehe niliyotangulia kuyafanya, na nitakayofanya katika siku zijazo, na niliyoyaficha, na

niliyowahi kuyafanya dhahiri, na niliyopitisha, na Wewe unayajua hayo kuliko mimi, Wewe ndiye Mwenye

kuyatanguliza, na Wewe ndiye Mwenye kuYâkhirisha, hapana mola (wa kweli) isipokuwa Wewe.‖2

mashekhe wengi, wakiipuuza kabisa tawassul iliyothibitishwa, - hutowasikiya wao wakijikurubisha kwa Allaah kwa njia hii – lakini wanazijua mno njia za uzushi za tawassul, ambazo zisizoweza hata kujadiliwa, kama kwamba hakuna njia yoyote nyengine inayokubalika!

Shaikh ul-Islaam Ibn Taymiyyah (اهلل رحمه) ameandika mtungo mzuri sana

kuhusu Madda hii kwa jina la Tawassul na Wasîlah (―Kujikurubisha kwa Allaah, na njia zake.‖), kifâcho kutoa ushauri mwema, kwani ni muhimu sana, na ni vichache mno vya kulinganishwa nacho katika yaliyomo ndani yake. Hata mimi ninao mtungo wangu Tawassul – aina zake na hukmu zake, ambacho pia ni muhimu sana kwenye maudhui yake na ukubwa wa kitabu, na pia kuyakosoa baadhi ya mambo mapya yaliyoeleweka vibaya na kuenezwa na madaktari wa kisasa wa dini. Twamuomba Allaah atulinde sisi na wao. 1 Abu Dâwud, an-Nasâ‘î, Ahmad, Bukhâri katika al-Adab al-Mufrad, at-Twabarâni na Ibn Mandah katika Tawhîd (44/2, 67/1, 70/1-2) kwa isnâd zilizo swahîh. 2 Muslim na Abu ‗Awânah

167

TASLÎM (MÂMKUZI YA AMANI)

Kisha alikuwa Mtume ( وسلم صىل اهلل عليه )akitoa salamu upande wake

wa kulia:

« الل ورمحح ـس الصالم »―Amani na Rehma za Allâh‎ ziwe juu yako‖,

[kiasi cha kwamba weupe wa mashavu yake ya upande wa kulia ulikuwa ukionekana,] na upande wake wa kushoto:

« الل ورمحح ـس الصالم »―Amani na Rehma za Allâh‎ ziwe juu yako‖,

[kiasi cha kwamba weupe wa mashavu yake ya upande wa kushoto ulikuwa ukionekana].‖1

Mara nyengine, alikuwa akiongezea juu ya SaLaam katika upande wa kulia:

« وبركد »―... na baraka Zake (ziwe juu yako).‖ 2

―Anaposema:

«صالم ـس ورمحح الل ال » 1 Abu Dâwud, an-Nasâ‘î na at-Tirmidhî, aliyeithibitisha kuwa swahîh. 2 Abu Dâwud na Ibn Khuzaymah (1/87/2) kwa sanad iliyo swahîh. Vilevile ‗Abdul Haqq ameithibitisha kuwa swahîh katika Ahkâm chake (56/2), kama walivyofanya an-Nawawi na Ibn Hajar. Pia imepokewa kwa kupitia njia nyengine na ‗Abdur-Razzâk katika kitabu chake cha Musannaf (2/219), Abu Ya‘laa katika kitabu chake Musnad (3/1253), at-Twabarâni katika kitabu chake Mu‘jam al-Kabîr (3/67/2) na Mu‘jam al-Awsat (no. 4476 – nambari zangu nilizoziweka mimi) na Dâraqutnî‘.

168

―Amani na Rehma za Allâh‎ ziwe juu yako‖, katika upande wake wa kulia, mara nyengine alikuwa akifupisha SaLaam yake katika upande wake wa kushoto kwa kusema:

« ـس الصالم »―Amani iwe juu yako.‖ 1

Mara nyengine ―alikuwa akitoa SaLaam mara moja tu:

« ـس الصالم »

[―Amani iwe juu yako‖] mbele ya uso wake, akigeuka upande wake wa kulia kidogo,] [au kwa uchache].‖2

―Walikuwa Waislamu hapo awali wakiashiriya kwa mikono yao walipokuwa wakitoa SaLaam upande wao wa kulia na wa

kushoto; Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alipowaona, akawâmbia, ―Muna

nini nyinyi, munâshiriya kwa mikono yenu kama kwamba ni mikiya ya Farasi wanaohangaika?! Anapotoa SaLaam mmoja wenu na azungushe uso kwa mwenzake, wala asiashiriye kwa mikono yake.‖ [Kwa hivyo, waliposwali nae, hawakuashiriya tena.] (katika riwaya nyengine: ―Hakika inamtosheleza mmoja wenu kuweka mkono wake juu ya paja lake kisha atoe SaLaam juu ya ndugu yake ambae yuko katika upande wake wa kulia na upande wake wa kushoto).‖ 3

1 An-Nasâ‘î, Ahmad na Sirâj kwa sanad iliyo swahîh 2 Ibn Khuzaymah, al-Baihaqî, Diyâ‘ katika kitabu chake al-Mukhtârah na ‗Abdul Ghani al-Maqdisi katika Sunan yake (243/1) kwa isnâd iliyo swahîh; Ahmad, at-Twabarâni katika Mu‘jam al-Awsat (32/2), al-Baihaqî, Ibn al-Mulaqqin (29/1) na Hâkim, aliyeithibitisha kuwa ni swahîh na ikâfikiwa na adh-Dhahabi. Takhrîj yake inapatikana katika Irwâ‘ ul-Ghalîl chini ya hadîth nambari 327. 3 Muslim, Abu ‗Awânah, Sirâj, Ibn Khuzaymah na at-Twabarâni. *TANBÎH! ma-‗Ibaadhiyyah wameipotosha hadîth hii: Mwanachuoni wao aitwae Rabî‘ ameisimulia katika kitabu chake cha ‗Musnad‘

169

UWAJIBU WA KUTOA SALAAM

Na alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)akisema:

« اتذص « وت“... na kuhalalisha kwake (swala) ni kutoa SaLaam.” 1

Haya ndiyo ya mwisho katika yale niliyoweza kuyakusanya

kuhusiana na maelezo ya swala ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) kuanzia

takbîr mpaka taslîm: Nataraji yakwamaba Allâh‎ Ataifanya ‗amali hii iwe ni kwa ajili ya Uso wake, uliojaa Heshima kubwa, na uongofu wa kwenye Sunnah ya Mtume Wake aliye mkarimu, na mwenye huruma.

ل إ ل أن أطد وبعدك ال شجعة وبعده الل شجعةن » «حل إل أخ أشذلهرك وأدب إ

آل وع مد ع وبةرك مد آل وع مد ع ص ال» محد إ إثرا آل وع إثرا ع وبةركخ صخ ة مد

« جمد

―Kutakasika ni kwa Allâh‎, na kusifika. Kutakasika ni Kwako, Yâ Allâh‎, na kusifika; Nashuhudia yakwamba hapana mola

kisichotegemewa kwa matamshi tafauti ili wapate kuigeuza haki na kuiafiki rai yao yakwamba kuinua mikono wakati wa takbîr hubatilisha swala! Hilo ni tamshi la urongo, kama nilivyoifafanua katika adh-Dha‘îfah (6044). 1 Hâkim na adh-Dhahabi wameithibitisha kuwa ni swahîh; Tayari imebainishwa kwa urefu chini ya ―Takbîr ya kuhirimiya‖.

170

wa haki isipokuwa Wewe. Naomba msamaha kutoka kwako na kutubia kwako‖.

―Yâ Allâh‎! Mfikilizie amani Muhammad na jamii ya Muhammad na umfikilizie baraka Muhammad na jamii ya Muhammad kama ulivyomfikilizia amani na baraka Ibrâhîm na jamii ya Ibrâhîm. Wewe ndiye Mtukufu, unaestahiki kila Sifa njema.‖ 1

1 Dua‘ ya kwanza ndiyo dua‘ iliyo katika ukamilifu wake, ijulikanayo kwa jina la Kaffârah al-Majlis (kafara ya kikao); ―Yoyote mwenye kuisema katika kikao cha ukumbusho (wa Allaah), itakuwa ni kama muhuri wa kuifungia, na yoyote mwenye kuisema katika kikao cha maneno ya upuzi, itakuwa ni kafara yake.‖ – Imeswihi kupokewa na Hâkim na at-Twabarâni. Dua‘ ya pili ni, kama ijulikanavyo, kutoka

katika Sunnah ya kumuombea Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) amani na rehma.

Kwa hiyo, hizi dua‘ mbili, ndio njia bora za kutekeleza uongofu wa ki-Islamu ufuatao: ―Hapana watu wanaokâ katika mkusanyiko ambao ndani yake hawamtaji Allaah, wala kumswalia Mtume, bila ya kikao hicho kuwa ni chanzo cha majuto juu yao; Akipenda Allaah, atawâdhibu, au akipenda, atawasamehe.‖ – Imeswihi kupokewa na at-Tirmidhî, Hâkim na Ahmad. Tizama katika kitabu cha Sheikh al-Albâni Silsilah al-Ahâdîth as-Swahîhah (74-81) kwa maelezo zaidi.

171

NYONGEZA Kila yaliyotangulia katika namna ya Swala ya Mtume ( صىل اهلل عليه ni sawa ndani yake kwa wanaume na wanawake, kwani ,(وسلم

hakuna kitu chochote katika Sunnah kinacholazimisha kuwatoa wanawake katika njia hizi; kwa hakika, katika kuenea kwa

maneno yake Mtume (صىل اهلل عليه وسلم):

ا» » أصل رأيذن ة ص

"Swalini kama mulivyoniona nikiswali" Neno hili linawakusanya wanawake pia. Na hii ndiyo rai ya Ibrâhîm an-Nakha‘i, aliyesema, ―Mwanamke anafanya katika swala kama anavyofanya mwanamume.‖ – imepokewa hiyo na Ibn Abî Shaybah (1/75/2), kwa sanad iliyo swahîh kutoka kwake. Vilevile akapokea Bukhâri katika Târîkh as-Swaghîr‎‎ (UK. 95) kwa sanad iliyo swahîh kutoka kwa Umm ad-Dardâ‘, yakwamba alikuwa akikaa katika swala yake kama anavyokâ mwanamume, na yeye alikuwa ni mwanamke mwenye ‗ilmu ya fiqh.‖ Hadîth kuhusu indImâm (kujikusanya) kwa mwanamke anaposujudu, na kwamba mwanamke si kama mwanamume katika kusujudu, ni mursal na wala si swahîh . Amepokea Abu Dâwud kwa njia ya al-Marâsîl kutoka kwa Yazîd Ibn Abî Habîb. Amma kuhusu hadîth aliyoipokea Imâm Ahmad, kama ilivyo katika kitabu cha mwanae, Masâ‘il, kutoka kwa Ibn ‗Umar, yakwamba alikuwa akiwaamrisha wake zake wakae ki-marufâ (miguu ipitane) katika swala, sanad yake si swahîh , kwani ndani yake kuna mtu aitwae ‗Abdullâh‎ Ibn ―Umar al-‗Amri, ambae ni mpokezi aliye dha‘îf.

172

KIAMBATISHO 1

UDHAIFU WA AHÂDÎTH ZENYE KUJUZISHA IKHTILAAF‎ (KUPINGANA)

Kutoka: Silsilah Al-Ahâdîth Adh-Dha‘îfah Wal-Mawdhû‘ah (58-62) Na Sheikh Al-Albâni

1) “IKHTILAFU MIONGONI MWA UMMAH WANGU NI REHMA.”

a) Laa Asla Lahu (Haina msingi). Ma‘ulamâ wa Hadîth wamejaribu sana kuitafuta isnâd ya hadîth hii, lakini hawajaona hata moja, ndipo Suyûti alipofikilia kusema katika kitabu chake al-Jâmi‘ as-Swaghîr‎‎, yakwamba, pengine ilipokewa katika mojawapo ya vitabu vya ma-huffâdh ambacho hakikutufikiya sisi‖!

Shauri hili si la kuaminika kabisa, kwani itamânisha yakwamba

baadhi ya maneno ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)yamepotea kwa

Ummah huu milele, jambo ambalo lisilofaa kwa Muislamu kuamini. Manâwi amemnukuu Subki kuwa alisema, ―Haijulikani (Yaani, hadîth ) na Muhaddithîn na mimi siwezi kuipatia isnâd yake, imma swahîh , dha‘îf au mawdhû‘‖, na haya yamethibitishwa na Shaikh Zakariyyah al-Ansâri katika maandishi yake kuhusu TAFSÎR al-Baidhâwi (92/2). Zaidi ya hayo, maana ya hadîth hii vilevile yana kasoro kama ilivyobainishwa na Wanavyuoni wa uhakikishaji, kwa hiyo, amesema Ibn Hazm katika al-Ihkâm fî USÛL al-Ahkâm (5/64) baada ya kutoa ishara yakwamba hiyo si hadîth ,

173

―Hii ni mojawapo ya misemo ya kimakosa iwezekanayo kupatikana, kwani ikiwa ikhtilafu ni rehma, basi maafikiano‎ yatakuwa ni adhabu, jambo ambalo hakuna Muislamu awezae kulisema, kwa sababu ni jambo moja peke yake linaweza kupatikana, imma maafikiano‎ au ikhtilafu, na huwenda kukapatikana rehma au adhabu.‖ Maneno zaidi ya Ibn Hazm yamenukuliwa hapo chini:

b) Inakwenda kinyume na Qur‘ân, ambayo imelaumu Ikhtilaaf‎ mahali pengi sana.

2) “MASWAHABA ZANGU NI KAMA NYOTA: YOYOTE MIONGONI MWAO UTAKAEMFUATA, UTAONGOZWA KATIKA NJIA YA SAWA.”

Mawdhû‘ (hadîth ya urongo). Imepokewa na Ibn ‗Abdul-Barr katika Jâmi‘ al-Bayân al-‗Ilm (2/91) na Ibn Hazm katika al-Ihkâm (6/82) kwa kupitia njia ya:

Sallâm‎ Ibn Sulaim, aliyesema: al-Hârith Ibn Ghissîn alituhadithia sisi kutoka kwa al-A‘mash kutoka kwa Abu Sufyân kutoka kwa

Jâbir kutoka kwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم).

Amesema Ibn ‗Abdul-Barr, ―Dalili haiwezi kuthibitishwa kwa isnâd hii kwa sababu huyu al-Hârith Ibn Ghissîn ni majhûl (mtu asojulikana)‖; Ibn Hazm akasema, ―Hii ni riwaya ya kuporomoka. Abu Sufyân ni dha‘îf; al-Hârith Ibn Ghissîn ni Abu Wahb ath-Thaqafî; Sallâm‎ Ibn Suleimân ni mpokezi wa hadîth za kuzua – (Hadîth ) Hii ni mojawapo bila ya shaka yoyote.‖ Kuihukumu hadîth hii juu ya Sallâm‎ Ibn Sulaim – ambae pia anajulikana kwa jina la Sallâm‎ Ibn Suleimân – ni bora, kwani imeafikiwa yakwamba yeye ni dha‘îf; kwa hakika, amesema Ibn Khirâsh kumuhusu yeye, ―mrongo kabisa‖ na Ibn Hibbân akasema, ―amepokea ahâdîth za kuzua.‖

174

Ama kuhusu Abu Sufyân, yeye si dha‘îf kama alivyosema Ibn Hazm , bali yeye ni mwenye kutegemewa kama alivyosema Ibn Hajar katika at-Taqrîb, na Muslim hupokea kutoka kwake katika swahîh yake. Al-Hârith Ibn Ghissîn ni mtu asojulikana kama alivyosema Ibn Hazm, na kama alivyofanya Ibn ‗Abdul-Barr, hata kama Ibn Hibbân amemtaja katika ath-Thiqât (Wapokezi Wanaotegemewa). Kwa hiyo, amesema Ahmad, ―Hadîth hii si swahîh ‖, kama ilivyonukuliwa kutoka katika al-Muntakhab (10/199/2) cha Ibn Qudâmah. Ama kuhusu matamshi ya Sha‘râni katika al-Mîzân (1/28), ―Hadîth hii, hata kama haikuthubutu kulingana na maoni ya Muhaddithîn, lakini hata hivyo, ni swahîh kulingana na watu wa kashf‖, ni urongo mkubwa na ajabu mpya, na wala haifai kuithamini kwa vyovyote! Hii ni kwa sababu kusahihisha ahâdîth kwa njia ya Kashf (―kufunua‖, ukiwa katika hali ya usingizi mzito sana) ni uzushi mbaya wa ma-Sufi , na kujitegemeza juu yake humuelekeza mtu mpaka akasahihisha ahâdîth za kuzua na zisizo na misingi kama hii. Hii ni kwa sababu, hata katika nyakati zilizokuwa ni bora, kashf ni kama rai, ambazo mara nyengine huwa sawa na mara nyengine huwa ni makosa – na hapo ni pale iwapo hakuna mapendeleo ya u-binafsi yaliyoingia kati yake! Twamuomba Allâh‎ atuhifadhi kutokamana na hayo na kutokamana na chochote ambacho kisichomridhisha Yeye. Riwaya zinazofanana na hayo yaliyopita ni kama zifuatazo: 2.1) ―Mfano Wa Maswahaba Zangu Ni Kama Ule Wa Nyota:

Yoyote Utakaemfuata Mmoja Katika Wao, Utaongozwa Katika Njia Ya Sawa.‖

Mawdhû‘ (hadîth ya urongo). Imepokewa na Qudâ‘i (109/2) kutoka kwa:

175

Ja‘far Ibn ‗Abdul Wâhid, aliyesema: Wahb Ibn Jarîr Ibn Hâzim ametupasha habari kutoka kwa babake kutoka kwa al-A‘mash kutoka kwa Abu Salih kutoka kwa Abu Hurairah kutoka kwa

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم).

Mmojawapo katika Muhaddithîn, imma Ibn al-Muhibb, au adh-Dhahabi, aliandika pambizoni mwa kitabu, ―Hadîth hii si swahîh hata chembe‖, Yaani. Imezuliwa: Ila yake ni huyu Ja‘far hapa, ambae aliyesemwa na ad-Dâraqutnî‘ yakuwa, ―Alikuwa akizua ahâdîth‖; Abu Zur‘ah akasema, ―Amepokea ahâdîth zisizokuwa na misingi yoyote‖; adh-Dhahabi akatoa baadhi ya hadîth zilizomsababisha yeye kumshusha hadhi, miongoni mwao ni hadîth hii, kisha akasema, ‗Hii ni mojawapo ya baLaa zake!‖

2.2) Munawajibika kufuata chochote mulichopewa kutoka katika Kitabu cha Allâh‎; haruhusiwi mtu yoyote kuwachana nacho. Iwapo hakuna katika kitabu cha Allâh‎, basi (andameni) mifano (sunnah) yangu iliyotangulia. Na iwapo hakuna mfano (sunnah) wangu uliotangulia, basi (fanyeni) waliyoyasema Maswahaba zangu. Kwa hakika, Maswahaba zangu ni kama nyota zilizo mbinguni, kwa hivyo yoyote miongoni mwao utakae muandama, utapata uongofu, na ikhtilafu za Maswahaba zangu ni rehma kwenu nyinyi.‖

Mawdhû‘ (hadîth ya urongo). Imepokewa na Khatîb katika al-Kifâyah fî ‗Ilm ar-Riwâyah (Uk.48) na vilevile imepokewa na Abul-‘Abbâs al-Asamm katika kitabu chake Hadîth (No.142), na Ibn ‗Asâkir [7/315/2] kwa njia ya:

Suleimân Ibn Abî Karîmah kutoka kwa Juwaibir kutoka kwa adh-

Dhahhâk kutoka kwa Ibn ‗Abbâs kutoka kwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم).

Hadîth hii ni dha‘îf Jiddan (Dhaifu sana).

Kuhusu huyu Suleimân Ibn Abî Karîmah, Ibn Abî Hâtim [2/1/138] amepokea kutoka kwa babake kumuhusu yeye, ―Huyu ni dhaifu katika hadîth .‖

176

Juwaibir ni Ibn Sa‘îd al-Azadî, naye ni matrûk (aliyesusiwa) kama alivyosema ad-Dâraqutnî‘, an-Nasâ‘î na wengineo, na Ibn al-Madîni alimtangaza kuwa ni mtu aliye dhaifu sana.

Dhahhâk ni Ibn Muzâhim al-HiLaalî, nae hakuwahi kukutana na Ibn ‗Abbâs.

Al-Irâqi akanukuu sehemu ya mwisho ya hadîth hii katika kitabu chake Takhrîj ya IhYâ‘ ‗Ulûm ad-Dîn [1/25] cha Imâm al-Ghazâli, kisha akasema, ―Isnâd yake ni dha‘îf.‖

Isnâd hii kwa hakika ni dhaifu sana kutokana na tuliyoyataja kumuhusu Juwaibir, kama alivyosema Sakhâwi katika al-Maqâsid – Hata hivyo, kimaana, hadîth hiyo imezuliwa, kama ilivyodhihiri kutokana na yaliyotangulia na yatakayofuata.

Suyûti ameinukuu hadîth nzima mwanzoni mwa kitabu chake Jazîl al-Mawâhib fî Ikhtilaaf‎ al-Madhâhib kutoka katika riwaya ya al-Baihaqî katika al-Madkhal, na Dailamî akaipokea kutoka katika njia hii, kama ilivyo katika al-Mawdhû‘ât cha ‗Ali Qâri (Uk.19). Pindi ukishayajua haya, basi maneno ya Suyûti katika kitabu chake kilichotangulia ni ya kushangaza mno: ― ... na hadîth hii ina nukta chungu nzima za kufâ kuangaliwa, miongoni mwake ni

kutupasha habari kwake (صىل اهلل عليه وسلم) kuhusu kukhitilafiana baina

ya madhâhib katika mas‘ala yasiyokuwa ya kimsingi, na hilo ni mojawapo ya miujiza yake, kwa vile ni habari zenye kuhusiana na mambo yaliyofichamana; na pia, kuridhika kwake na hayo na kuyajuzisha kwake, kwani aliyapa hayo sifa ya rehma na kwamba mwenye kukalifishwa anaweza kujichagulia atakavyo.‖

Huwenda akâmbiwa: Kwanza imarisha kiti, kisha ndio ukikalie. Aliyoyataja kuhusu kujichagulia ni urongo, ni jambo lisilowezekana kwa Muislamu kujifungamanisha juu ya hilo na kutekeleza juu ya muelekeo huo kwa ujumla, kwani itakuelekeza kujitoa katika mipaka ya Sharî‘ah, kama ambavyo si jambo gumu kujionea. Tizama pia, maelezo chini ya nukta 2.4 hapo chini.

177

2.3) ―Nilimuuliza Mola wangu kuhusu kitu ambacho watakacho khitilafiana Maswahaba zangu baada ya kuondoka kwangu, basi Allâh‎ akanifahamisha: Ewe Muhammad! Maswahaba zako kwangu mimi ni kama nyota zilizo Mbinguni – baadhi nyengine zinan‘gara kuliko baadhi nyengine; kwa hivyo yoyote atakaechukuwa kutoka kwa yoyote miongoni mwao katika mas‘ala yale waliyokhitilafiana, basi kwangu Mimi, huyo atakuwa juu ya uongofu.‖

Mawdhû‘ (Imezuliwa). Imepokewa na Ibn Battah katika al-Ibânah [4/11/2], Khatîb, Nizam al-Mâlik katika al-Amâli [13/2], DiYâ‘ katika al-Mutaqâ ‗an-Masmû‘âtihi bimarû [116/2] na Ibn ‗Asâkir [6/303/1] kwa njia ya:

Nu‘aim Ibn Hammâd, aliyesema: ‗Abdur-Rahmân Ibn Zaid alituhadithia kutoka kwa babake kutoka kwa Sa‘îd Ibn al-Musayyib kutoka kwa ‗Umar Ibn al-Khattâb kutoka kwa Mtume

.(صىل اهلل عليه وسلم)

Isnâd hii ni mawdhû‘.

Nu‘aim Ibn Hammâd ni dha‘îf: Ibn Hajar amesema, ―Anafanya makosa mengi sana.‖

Kuhusu ‗Abdur-Rahmân Ibn Zaid al-‗Ammî, al-Bukhâri amesema, ―Alisusiwa‖; Abu Hâtim akasema, ―Ahâdîth zake zimesusiwa: hakubaliki katika hadîth – alikuwa akimfitini babake kwa kusimulia mâfa kutoka kwake‖; Ibn Ma‘în amesema, ―Alikuwa ni mrongo wa kupindukia.‖

Kumuhusu babake, Zaid al-‗Ammî Ibn al-Hawârî, Ibn Sa‘d amesema, ―Alikuwa ni dha‘îf katika hadîth .‖

Suyûti aliinukuu hadîth hii katika al-Jâmi‘ as-Swaghîr‎‎ kupitia kwenye riwaya ya Sijizzi katika al-Ibânah na Ibn ‗Asâkir kutoka kwa ‗Umar; Manâwi akasema katika sherehe yake ya al-Jâmi‘ as-Swaghîr‎‎:

Ibn al-Jawzi amesema katika kitabu chake al-‗Ilal, ―Hii haikusihi. Nu‘aim ameumbuliwa; Ibn Ma‘în alimkashifu ‗Abdur-Rahîm kuwa

178

ni mrongo mkubwa; Inasema katika al-Mîzân: Hadîth hii ni ya urongo.‖

2.4) ―Kwa Hakika, Maswahaba Zangu Ni Kama Nyota: Kwa Hiyo Utakapokubali Yoyote Katika Watakayoyasema, Utaongoka.‖

Mawdhû‘ (Imezuliwa). Ibn ‗Abdul-Barr ameitaja kwa njia mu‘allaq (Iliyoangikwa, Yaani; silsila ya wapokezi yenye upungufu katika kikomo cha mpokezi) na Ibn Hazm akaitaja kutoka kwake; Silsila iliyokamilika imetolewa na ‗Abd Ibn Humaid katika al-Muntakhab min al-Musnad (86/1):

Ahmad Ibn Yûnus amenipasha mimi: Abu Shihâb al-Hannât ametuhadithia, kutoka kwa Hamzah al-Jazrî, kutoka kwa Nâfî‘,

kutoka kwa Ibn ‗Umar kutoka kwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم).

Pia, Ibn Battah ameipokea katika al-Ibânah [4/11/2] kwa silsila nyengine ya upokezi kutoka kwa Abu Shihâb.

Amesema Ibn ‗Abdul-Barr, ―Isnâd hii si swahîh ; hakuna yoyote anaekubalika kama dalili, aliyeipokea kutoka kwa Nafî‘.‖

Huyu Hamzah ni Ibn Abî Hamzah; Dâraqutnî‘ amesema kumuhusu yeye, ―Matrûk‖ (Aliyetupiliwa mbali); Ibn ‗Adi akasema, ―Riwaya zake nyingi ni za kuzuliwa‖; Ibn Hibbân amesema, ―Hubakia peke yake katika kupokea mambo ya kuzua kutoka kwa wapokezi wanaotegemewa, kiasi cha kwamba ionekane yakuwa alifanya hivyo kwa makusudi – hairuhusiwi kupokea kutoka kwake; adh-Dhahabi amezinukuu baadhi ya ahâdîth zake alizozua katika al-Mîzân, ikiwa hii ni mojawapo.

Akasema Ibn Hazm katika al-Ihkâm (6/83), baada ya kuithibitisha hadîth hii (no. 2, kwa mapokezi yake yote) bila ya shaka yoyote kuwa ni ya urongo kwa vile imekwenda kinyume na Âyât nyingi za Qur‘ân, k.m; Najm (53: 3-4), an-Nisâ‘ (4:82), al-Anfâl (8:46), yafuatayo:

―... kwa hivyo, ni jambo lisilowezekana yakwamba Mtume

atuamrishe sisi tufuate kila rai inayoletwa na (صىل اهلل عليه وسلم)

179

Maswahaba zake (رضي اهلل عنهم) , kwani wako miongoni mwao

walioruhusu jambo na baadhi yao wakalikataza: Iwapo hali ni kama hiyo, biashara ya ulevi ingelikuwa ni halali lau mtu angeamua kumfuata Samurah Ibn Jundub; ingelikuwa yafâ kwa aliyefunga (swaum) kula theluji iwapo mtu atâmua kumfuata Abu Talhah, lakini imeharamishwa kwa kuwafuata wengine wasiokuwa yeye; kujiepusha kuoga janaba kutokana na kukamilika kitendo cha kuingiliana (mke na mume) ingelikuwa ni jambo la Waajib ikiwa mtu angemuandama ‗Ali, ‗Uthmân, Talhah, Abu Ayyûb na ‗Ubayy Ibn Ka‘b, lakini ikaharamishwa iwapo mtu atamuandama ‗Âishah na Ibn ‗Umar; tumeletewa mifano yote hii kwa riwaya za mapokezi yaliyo swahîh .‖

Kisha akaendelea kueleza kwa urefu zaidi baadhi ya rai zilizotolewa na Maswahaba ambazo wao walikuwa wamekosea

kuhusiana na Sunnah, tena katika uhai wake Mtume ( صىل اهلل عليه ,na baada ya kufa kwake. Kisha Akasema (6/86)(وسلم

―Sasa itawezekanaje kuruhusiwa kufuata ki-Upofu rai za watu wanaofanya makosa mara nyengine na wakafanya ya sawa mara nyengine?!‖

Kabla ya hayo, amefafanua, chini ya kichwa ―Kukhitilafiana Kunalaumiwa‖ (5/64), makosa ya wale wenye kusema, ―Kukhitilafiana ni rehma‖, kwa kutumia dalili hadîth isemayo, ―Maswahaba zangu ni kama nyota: yoyote miongoni mwao utakaemfuata, utaongoka‖, kwa kudhihirisha yakwamba hadîth hiyo ni ya urongo kwa sababu nyingi:

(i) Si swahîh kuhusiana na silsila yake ya upokezi;

(ii) Zaidi ya hayo ni kwamba haiwezekani kwa Mtume ( صىل اهلل عليه kutuamrisha sisi kufuata jambo ambalo yeye mwenyewe (وسلم

ashawahi kulithibitisha yakwamba lina makosa; k.m; alitaja

180

makosa aliyoyafanya Abu Bakr katika kuifasiri ndoto, makosa ya ‗Umar katika tafsiri nyengine na kukosea kwa Abus-Sanâbil katika fatwa aliyoitoa; kwa hiyo, haiwezekani kwake yeye kutuamrisha sisi kumfuata mtu aliyekosea;

(iii) Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) hakuwahi kuzungumza mambo ya

urongo; maneno yake daima yalikuwa ni ukweli mtupu: ulinganifu na nyota ni wazi yakwamba una kasoro, kwani kwa mfano, iwapo mtu atakusudia kusafiri kwa kupitia njia fulani inayo-ongozwa na nyota katika kundi la Capricorn, lakini badala yake akândama nyota katika kundi la Cancer, hato-ongozwa kwenye njia ya sawa, lakini atatokomea mbali sana na njia ya sawa na apotî vibaya sana; kwa hivyo, ni makosa yaliyo wazi kusema yakwamba kufuata nyota yoyote kutamuongoza mtu katika njia ya sawa.

Ibn al-Mulaqqin ametoa târifa ya mukhtasar kutoka kwenye maneno ya Ibn Hazm katika al-Khulâsah‎ yake [2/175], akaiidhinisha na kumalizia mazungumzo yake ya hadîth hiyo kwa kusema: Amesema Ibn Hazm, ―Hii ni riwaya iliyotungwa, ya kuzuliwa, tena ya urongo, si swahîh hata kidogo.‖

181

KIAMBATISHO 2

HADÎTH SWAHÎH :

“UMEPATA SAWA KATIKA BAADHI YAKE NA UMEKOSEA KATIKA BAADHI YAKE.” Kutoka katika: Swahîh al-Bukhâri, Kitabu cha Ndoto, Tafsiri ya Ki-Ingereza ya maana zake na Daktari. Muhammad Muhsin Khan.

Imepokewa na Ibn ‗Abbâs (رضي اهلل عنه) :

Alikuja mtu mmoja kwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)akasema,

―Mimi nimeona katika ndoto, kiwingu chenye kivuli. Siyagi na asali zilikuwa zikituruzika kutoka hapo na nikawaona watu wakizikinga mikononi mwao, baadhi yao wakawahi kukinga kwa wingi na baadhi nyengine kwa uchache. Mara kwa ghafula, palikuwepo na kamba yenye urefu wa kutoka ardhini hadi mbinguni, nikakuona kuwa uliishikilia na kupanda juu kwa kamba hiyo; kisha, mtu mwengine akaishikilia na kupanda juu nae, (baada e) mtu mwengine (wa tatu) nae pia akaishikilia na kupanda juu, kisha mtu mwengine (wa nne) akaishikilia, lakini ikakatika na mara ikaunganika tena.‖ Abu Bakr akasema, ―Ewe mjumbe wa Allâh‎! Najitolea babangu kuwa kafara yako! WAllâh‎i, niruhusu mimi

niifasiri ndoto hii.‖ Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)akamwambia,

Haya tufasirie. Abu Bakr akasema, ―Hicho kiwingu chenye kivuli kinâshiria Uislamu, na siyagi na asali zilizokuwa zikituruzika kutoka hapo zilikuwa zikiashiria Qur‘ân, utamu wake na baadhi ya watu kukithirisha kuisoma Qur‘ân na baadhi nyengine kuisoma kwa uchache. Hiyo kamba iliyokuwa na urefu wa kutoka mbinguni hadi

ardhini ndiyo Hakki ambayo uifuatayo wewe (Mtume ( صىل اهلل

182

Wewe ukaifuata hiyo hakki na Allâh‎ atakuinua .((عليه وسلم

juu na hakki hiyo, na kisha mtu mwengine ataifuata hakki hiyo na atainuliwa juu na hakki hiyo na kisha mtu mwengine ataifuata hiyo hakki lakini itakatika kisha ataunganishiwa na atainuka juu na hakki hiyo. Ewe mjumbe wa Allâh‎! Najitolea babangu kuwa kafara yako! Je nimeipatia au nimekosea?‖

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akamjibu, ―Umeipatia katika baadhi

na umekosea katika baadhi nyengine.‖ Akasema Abu Bakr, ―Ewe mjumbe wa Allâh‎! Wallâh‎i, lazima unieleze katika baadhi niliyoikosea.‖

Akasema Mtume: (صىل اهلل عليه وسلم), ―Usiape‖.

(Imepokewa na Bukhâri na Muslim, na pia na Abu Dâwud, at-Tirmidhî, ad-Dârimi, Ibn Mâjah, Ibn Abî Shaybah na Ahmad).

183

KIAMBATISHO 3

“YULE MWENYE KUHARIBU SWALA YAKE” (رضي اهلل عنه)

Katika fanni ya Hadîth na Fiqh, tamko hili linamuhusu yule Swahaba aliyetajwa katika hadîth ifuatayo ya Bukhâri (Kitabu cha Swala, Tafsiri ya ki-Ingereza cha Dr. Muhammad Muhsin Khan); riwaya nyengine nyingi za tukio hili hupatikana katika mikusanyiko mbali mbali ya hadîth , na inaweka wazi msingi

muhimu wa maelezo kutoka kwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) kuhusu njia

ya sawa ya kuswali:

Amepokea Abu Hurairah (رضي اهلل عنه) :

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) aliingia msikitini na mtu mmoja

akamfuata. Yule mtu akaswali kisha akenda kwa Mtume

na akamuamkuwa; akamjibu mâmkuzi yake (صىل اهلل عليه وسلم)

kisha akamwambia (yule mtu), Rudi ukaswali, kwani wewe bado hujaswali. Yule mtu akarudi na akaswali tena kama jinsi alivyotangulia kuswali, na kisha akarudi na akamuamkuwa

tena Mtume ( ,aliyemwambia, ―Rudi ukaswali ,( عليه وسلمصىل اهلل

kwani wewe bado hujaswali‖, mara tatu. Yule mtu akasema, ―Naapa kwa Yule ambae Aliyekuleta wewe kwa Hakki, mimi siwezi kufanya bora zaidi ya hivi, kwahivyo tafadhali nifunze.‖ Akasema, ―Unaposimama kwa ajili ya kuswali, tamka Takbîr kisha usome kilicho sahali kwako kutoka katika Qur‘ân (kutokana na ulichohifadhi kwa moyo); kisha urukû‘ mpaka upate utulivu katika hali ya Kurukû‘, kisha uinue kichwa chako na usimame wima, kisha Usujudu mpaka upate utulivu katika hali ya Kusujudu; kisha ukae kwa utulivu mpaka ujisikie umetulia, na uendelî hivyo katika swala zako zote‖.

184

[Riwaya za ziyada za hadîth hii zinazopatikana katika vitabu vyengine vya Hadîth kama vile Sunan Abî Dâwud, n.k zina maelezo kwa utondoti.]

KIAMBATISHO 4

UDHAIFU WA HADÎTH KUHUSU KUWEKA MIKONO CHINI YA KITOVU. Kutoka katika Irwâ‘ ul-Ghalîl (353) & Ahkâm ul-Janâ‘iz (Uk. 118) cha Sheikh al-Albâni . Abu Dâwud (756), Dâraqutnî‘ (107), Baihaqî (2/310). Ahmad katika Masâ‘il ya mwanae ‗Abdullâh‎ (62/2), na pia katika Zawâ‘id al-Musnad (1/110), na Ibn Abî Shaybah (1/156/1), wote hao wamepokea: ‗an ‗Abdur-Rahmân Ibn Is-hâq ‗an Ziyâd Ibn Zayd as-Siwâ‘i ‗an

Abu Juhaifah ‗an ‗Ali (رضي اهلل عنه) , aliyesema, ―Ni katika Sunnah

wakati wa kuswali kuweka mkono mmoja juu ya mkono mwengine, chini ya kitovu.‖ Hii ni sanad iliyo dha‘îf kutokana na ‗Abdur-Rahmân Ibn Is-hâq (al-Wâsiti al-Kûfi ), ambaye ni mtu dha‘îf (tizama hapo chini). Na juu ya hayo, hadîth hiyo ina idhtirâb (isiyo imara) ndani yake, kwani yeye ameisimulia:

1) Kwa mara moja ‗an Ziyad ‗an Abu Juhaifa ‗an ‗Ali (kama ilivyo hapo juu);

2) Kwa mara nyengine ‗an Nu‘man Ibn Sa‘d ‗an ‗Ali (imepokewa na Dâraqutnî‘ na Bayhaqî); na

3) Kwa mara nyengine ‗an Siyâs Abul Hakam ‗an Abu Wâ‘il, aliyesema, ―Amesema Abu Hurairah: Hiyo ni katika Sunnah ...‖ (imepokewa na Abu Dâwud [758] na Dâraqutnî‘).‖

185

Udhaifu wa ‗Abdur-Rahmân Ibn Is-hâq al-Kûfi katika mtizamo wa ma-Imâm wa Hadîth

1) Amesema Abu Dâwud, ―Mimi nilimsikiya Ahmad Ibn Hanbal akimtangaza ‗Abdur-Rahmân Ibn Is-hâq al-Kûfi kuwa ni dha‘îf. [―Hii ndiyo sababu iliyomfanya Imâm Ahmad kutoikubali hadîth hii yake, kwani mwanae ‗Abdullâh‎ alisema, ―Niliona yakwamba alipokuwa akiswali, babangu alikuwa akiweka mikono yake, mmoja juu ya mwengine, juu ya kitovu.‖]

2) An-Nawawi alisema katika Majmû‘ (3/313), na pia katika Sharh Swahîh Muslim na kwengineko, ―Wao (wanavyuoni wa hadîth ) wameafikiana katika kuithibitisha hadîth hii kuwa ni dha‘îf, kwa sababu ni riwaya ya ‗Abdur-Rahmân Ibn Is-hâq al-Wâsiti, ambaye ni mpokezi aliye dha‘îf, kama ilivyoafikiwa miongoni mwa wanavyuoni wa Jarh wat Ta‘dîl‖.

3) Az-Zayla‘i alisema katika Nasb ar-Râyah (1/314), ―Amesema al-Bayhaqî katika al-Ma‘rifah: ‗Isnâd yake haina nguvu, kwani ni riwaya ya kipekee iliyo dhaifu ya ‗Abdur-Rahmân Ibn Is-hâq al-Wâsiti, ambaye ni matrûk (aliyetupwa na kuachiliwa mbali)‘.‖

4) Amesema Ibn Hajar katika Fat-hul-Bâri (2/186), ―Ni hadîth dha‘îf.‖

Jambo la ziyada lenye kuashiriya udhaifu wake ni kwamba imepokewa kinyume chake kutoka kwa ‗Ali kwa isnâd iliyo bora: Hadîth ya Ibn Jarîr al-Dabbi kutoka kwa babake, aliyesema,

―Mimi nilimuona ‗Ali (رضي اهلل عنه) ameuzuiya mkono wake wa

kushoto kwa mkono wake wa kulia juu ya kitengele, juu ya kitovu‖ – Isnâd hii ni yenye kugombea daraja ya hasan; Baihaqî (1/301) alijikita imara katika kuidhihirisha kuwa ni hasan, na Bukhâri (1/301) nae akaidhihirisha juu ya uhakika mkubwa pindi alipoisimulia kwa njia ya ta‘lîq.

186

Yaliyosihi kutoka kwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)kuhusiana na mahali pa

uwekaji mikono ni kwamba yanatakiwa kuwa juu ya kifua; kuna ahâdîth nyingi kuhusiana na jambo hili, miongoni mwao ni ile

iliyopokewa na Tâwûs, aliyesema, ―Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)alikuwa

akiweka mkono wake wa kulia juu ya mkono wake wa kushoto, kwa kuifumbata vyema juu ya kifua chake wakati wa swala.‖ – Imepokewa na Abu Dâwud (759) kwa isnâd iliyo swahîh . Hata hivyo, hii ni mursal, inatosheleza kama dalili kwa wanavyuoni wote, pamoja na rai zao zote kuhusiana na Hadîth Mursal, kwa vile ni swahîh kama Isnâd iliyo Mursal na pia kuchukuliwa kuwa mawsûl katika riwaya nyingi; Kwa hiyo, inafâ kuwa ni dalili kwa yote hayo. baadhi ya riwaya zenye kuiunga mkono ni kama zifuatazo:

1) Kutoka kwa Wâ‘il ibn Hujr: ―Kuwa alimuona Mtume ( صىل اهلل عليه akiuweka mkono wake wa kulia juu ya mkono wake wa(وسلم

kushoto na kuekeza juu ya kifua chake.‖ Imenakiliwa na Ibn

Khuzaimah katika Swahîh yake (Nasbur-Râyah, 1/314) na

imenakiliwa na Al-Baihaqî katika Sunan yake (2/30) pamoja

na minyororo miwili ya riwaya zenye kusaidiana.

2) Kutoka kwa Qabîsah ibn Hulb, kutoka kwa babake aliyesema:

―Nilimwona Mtume ( لمصىل اهلل عليه وس )akiondoka [baada ya kumaliza

swala] kutoka katika upande wake wa kulia na kushoto, na nilimwona akiyaekeza juu ya kifua chake – YahYâ (Ibn Sa‘îd) akaelezea yakwamba wa kulia (mkono) aliuwekelea juu ya wa kushoto na kupandisha juu ya kiungo.‖ Imepokewa na Ahmad (5/226) kwa mnyororo wa wapokezi ambao wamewekwa katika daraja iliyowekwa na Muslim isipokuwa kwa Qabîsah, lakini huyu amethibitishwa kuwa ni wa kutegemewa na ‗Ijli na Ibn Hibbân; hata hivyo, hakuna mtu anayepokea kutoka kwake isipokuwa Simâk ibn Harb ambaye Ibn al-Madîni na Nasâ‘î wamesema: ‖Hajulikani‖ na Ibn Hajar akasema katika Taqrîb:

187

―Yeye ni ‗Maqbûl‘ [Yaani. Anakubalika tu iwapo ataungwa mkono].‖ Hadîth zenye mtu kama huyu ni hasan kama riwaya zenye kuunga mkono, na kwa hivyo Tirmidhî amesema baada ya kunukuu kipande hiki cha Hadîth kuhusu kuuchukuwa mkono wa kushoto kwa mkono wa kulia, ‖Ni hadîth hasan.‖ Kwahivyo hizi ni ahâdîth tatu zinazo onyesha yakwamba Sunnah ni kuweka mikono juu ya kifua, na yoyote atakaeziona hatokuwa na shaka yakwamba kwa pamoja hizo zinatosheleza kulithibitisha jambo hili.

188

KIAMBATISHO 5

UDHAIFU WA HADÎTH ZENYE KUSHUTUMU USOMAJI NYUMA YA IMÂM

Kutoka katika: Silsilah al-Ahâdîth ad-Dha‘îfah wal- Mawdhû‘ah (568-570) na Shaykh al-Albâni

1) ―Mwenye kusoma nyuma ya Imâm , mdomo wake hujazwa

moto.‖

Mawdhû‘ (Iliyozuliwa). Ibn Tâhir aliinukuu katika Tadhkirah

al-Mawdhû‘ât (Uk.93), kisha akasema, ―Isnâd ina Ma‘mûn Ibn

Ahmad al-Harawi, msema urongo aliyekuwa akisimulia

uzushi.‖ Sifa zake zaidi zimetolewa katika hadîth 2 hapo

chini. Ibn Hibbân ameitaja hadîth hii chini ya jina lake

katika adh-Dhu‘afâ (Wasimulizi Walio Dhaifu) na adh-Dhahabi

ameizingatia sifa hiyo kuwa ni mojawapo ya majanga yake!

baadhi ya ma-Hanafî wamedanganyika na hadîth hii,

wakitegemea juu ya misingi yake yakwamba kisomo chochote

nyuma ya Imâm ni harâm kabisa! Abul Hasanât al-Luknawi

amesema katika at-Ta‘lîq al-Mumajjid ‗aLaa Muwatta‘

Muhammad (Uk. 99), ―Imetajwa na muandishi wa Nihâyah na

wengineo kama marfû‘ kwa maneno, ‗... kuna makâ ya moto

ndani ya mdomo wake‘, na wala haina msingi wowote.‖

Kabla ya hapo aliwahi kusema yakwamba, ―Hakuna katika

hadîth yoyote iliyo swahîh marfû‘ makatazo ya kusoma al-

Fâtihah nyuma ya Imâm ; yote waliyowahi kuyanukuu kama

marfû‘ kuhusiana na haya ni aidha yasiyokuwa na msingi

wowote au ni dha‘îf‖, na kisha akaitaja hadîth hii kwa

kutumia matamshi yote hayo mawili kama mfano.

189

Ma‘ulamâ, wakiwemo wa zama zilizopita na zama zetu,

wamekhitilafiana kuhusiana na kusoma nyuma ya Imâm , kwa

kuchukuwa mojawapo ya rai tatu:

1. Yakwamba kusoma katika Swala ya Sauti na Siri ni

Waajib.

2. Yakwamba kunyamaza katika Swala ya Sauti na Siri ni

Waajib.

3. Yakwamba kuwepo na kisomo katika Swala ya Siri, wala

kusisomwe kitu katika Swala ya Sauti.

Hii rai ya mwisho ndiyo iliyo na uzani wa kati na kati na iliyo

karibu zaidi na ukweli, kwani ndani yake, dalili zote

zinaweza kupewa nafasi kiasi cha kwamba hakuna yoyote

itakayokataliwa kabisa. Ni rai ya Mâlik na Ahmad, na pia

ndiyo iliyofadhilishwa baada ya utafiti wa baadhi ya ma-

Hanafi, akiwemo Abul Hasanât al-Luknawi katika kitabu

chake kilichotajwa hapo awali.

Mfano mwengine aliouzua Ma‘mûn al-Harâwi ni huu ufuatao:

2) ―Mwenye kuinua mikono yake anaposwali, basi huwa hana

swala.‖

Mawdhû‘ (Iliyozuliwa). Imenukuliwa na Ibn Tâhir katika

Tadhkirah al-Mawdhû‘ât (Uk. 87), na kisha akasema, ―Isnâd

yake ina Ma‘mûn Ibn Ahmad al-Harawi, msema urongo

aliyekuwa akizua ahâdîth.‖

Adh-Dhahabi alisema kumuhusu yeye, ―Alileta baLaa na

habari za kufedhehesha. Alizua ahâdîth, na hii ikiwemo ni

mojawapo, na kuzidhihirisha mafungamano yake juu ya idhini

za wapokezi wenye kutegemewa.‖

190

Ni wazi kwangu mimi kutokana na ahâdîth ambazo alizozizua

Ma‘mûn al-Harawi yakwamba yeye ni mkereketwa aliye

mkaidi-shupavu wa madh-hab ya ki-Hanafi, kwani ahâdîth

zote zilizotajwa chini ya wasifu wake (katika vitabu vya

wapokezi) huzunguka kwenye mviringo wa kumshabikia Imâm

Abu Hanîfah na kumtuhumu Imâm ash-Shâfi‘î; miongoni

mwake ni hii: Tuhuma ya waziwazi dhidi ya rai ya Imâm ash-

Shâfi‘î, yenye kujuzisha kuinua mikono katika wakati wa

kwenda kwenye rukû‘ na kuinuka kutoka hapo (kitendo

ambacho ni cha sawa bila ya shaka yoyote), haliyakuwa

waziwazi wakiiunga mkono rai ya Hanafi isemayo yakwamba

jambo hilo ni makrûh. Mtu huyu mwenye ikirahi, hata

hakutosheka na msimamo wa madh-hab yake yakwamba

kuinua mikono ni makrûh: Bali alifikilia kiwango cha kuizua

hadîth hii, ili aeneze miongoni mwa watu yakwamba kwa

hakika kuinua mikono hubatilisha swala!

Pengine alikuwa amekusudia kuiunga mkono rai ya Makhûl

kutoka kwa Abu Hanîfah yakwamba alisema, ―Mwenye

kuinua mikono yake wakati anaposwali, swala yake

huharibika‖, riwaya iliyomdanganya Amîr Khâtib al-Itqâni

aliyeandika kitabu juu ya msingi huwo kwa hoja ya kubatilika

kwa swala kutokana na kuinua mikono! Vilevile aliyehadaiwa

ni aliyeandama njia yake na kuhukumu yakwamba haifai kwa

ma-Hanafî kuswali nyuma ya ma-Shâfi‘î kwa sababu ya kuinua

mikono kwa hao waliotajwa baada e (ma-shafi‘î)! Haliyakuwa

, riwaya hii kutoka kwa Abu Hanîfah ni maneno ya urongo,

kama alivyobainisha ‗Allâmah‎‎ Abul Hasanât al-Luknawi katika

al-Fawâ‘id al-Bahiyyah fî Tarâjum al-Hanafîyyah (Uk. 116,

216-7).

191

Sheikh ‗Ali al-Qâri ameinukuu hadîth hii katika al-Mawdhû‘ât

kisha akasema (Uk. 81), ―Hadîth hii imezuliwa na Muhammad

Ibn ‗Ukâshah al-Kirmâni, Allâh‎ Amfedheheshe.‖ Kisha (Uk.

129), akamnukuu Ibn al-Qayyim akisema, ―Imezuliwa.‖

Haya ni kinyume na yaliyothibitishwa (hapo awali) yakwamba

mzushi alikuwa ni al-Harawi; ikiwa itathibitishwa, basi

pengine mmojawao alimuibia mwenzake!

Tunaona kutokana na yote haya namna ya uchache wa kuwa

na hadhari katika Sunnah, na kupuuza kuzihakiki riwaya

kutoka kwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)na ma-Imâm kunavyoweza

kufanya!

TANBÎH: Kuhusu kuinua mikono wakati wa kwenda kwenye rukû‘ na kuinuka kutoka hapo, ahâdeth nyingi sana zimepokewa kutoka

kwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم): kwa hakika hizo ni mutawâtir katika

mtazamo wa Wanavyuoni; kwa hakika, kuinua mikono wakati wa kila takbîr kumethubutu kutokana na mapokezi yatokayo kwake katika ahâdîth nyingi; haliyakuwa haikusihi kutoka kwake kutoinua mikono isipokuwa mara moja tu kupitia kwa ‗Abdullâh‎

Ibn Mas‘ûd (رضي اهلل عنه), lakini haifai kutekeleza hivyo, kwani hiyo

ni nâfyu (ukanushaji). Ni jambo lililothubutu, kulingana na mtazamo wa ma-Hanafî na wengineo, yakwamba muthbit (muafaka) hupewa kipa-Umbele kuliko nâf (ukanushaji); Hii ndiyo kawaida hata kama muafaka uko peke yake, licha ya hali ikiwa ni riwaya chungu nzima, kama ilivyo kuhusu mas-ala haya! Juu ya msingi huu, na katika ukosefu wa pingamizi yoyote, hii inawalazimu na kuwashurutisha wao watekeleze kitendo cha kuinua mikono, badala ya kujifunga kiudhalilifu kwenye madh-hab baada ya kuthibitishiwa ushahidi. Hatahivyo, ni jambo la kusikitisha kuona yakwamba ni wachache mno wa waliotangulia au waliokuja baada e ndio waliofuata hayo, kiasi cha kwamba kutoinua mikono ndio kumekuwa ni alama yao maarufu !

192

Isitoshe baada ya hapo uzushi mwengine wa mrongo huyu muovu, wakati huu tuhuma dhidi ya Imâm Shâfi‘î (Muhammad Ibn Idrîs), ni huu ufuatao: 3) ―Kutakuwepo na mtu miongoni mwa Ummah wangu aitwae

Muhammad Ibn Idrîs, ambae atakaekuwa na madhara kwa

Ummah wangu kuliko Iblîs, na Kutakuwepo na mtu miongoni

mwa Ummah wangu aitwae Abu Hanîfah , ambae atakaekuwa

ni tâ ya Ummah wangu..‖

Mawdhû‘ (Iliyozuliwa). Ibn al-Jawzi ameinukuu katika al-Mawdhû‘ât (1/457) kutoka kwa: Ma‘mûn Ibn Ahmad as-Salmi, aliyesema: Ahmad Ibn ‗Abdullâh‎ al-Juwaibâri alitusimulia sisi: ‗Abdullâh‎ Ibn Mi‘dân al-Azadi alitupasha khabari kutoka kwa Anas, kwa njia ya marfû‘; Kisha akasema, ―Imezuliwa; Aliyeizua ni Ma‘mûn au JuwaiBâri . Hâkim akaitaja katika Madkhal yakwamba Ma‘mûn aliambiwa, ‗Wewe humtegemei Shâfi‘î na wafuasi wake?‘ Basi akasema, ‗Ahmad al-JuwaiBâri alitusimulia sisi ...‘n.k (na kadhaalika), kwa hivyo hii inakuwa ni dalili tosha yakwamba yeye ndiye aliyeizua hiyo.‖ Nyongeza ifuatayo inapatikana katika Lisân: ―Kisha Hâkim akasema, ‗Mtu yoyote aliyeja‘aliwa kiwango kichache cha ufahamu atajishuhudia yakwamba hadîth kama hii ni uzushi

aliobandikizwa nao Mjumbe wa Allâh‎ (صىل اهلل عليه وسلم).‘‖

Hadîth hiyo ina njia nyengine za riwaya, lakini hizi zategemea warongo na watu wasiojulikana. Kwahivyo, ni kioja kikubwa yakwamba ‗Allâmah‎‎ ‗Ayni yatakiwa aelekî kwenye kuipa nguvu hadîth hiyo kwa hizo njia nyengine, na aungwe mkono na Sheikh Kawthari! Hata hivyo, si jambo la kushangaza kutoka kwa Sheikh Kawthari, kwani yeye alikuwa ni mkaidi kwa kudidimizwa kwenye

ghera juu ya Imâm Abu Hanîfah (رحمه اهلل), hata ikibidi

193

kuwatukana ma-Imâm wengine; lakini ni jambo la kushangaza sana kwa ‗Ayni, kwani yeye alikuwa akijulikana kawaida yake huwa hapinduki mipaka kiasi hicho. Rai za hawa wawili zimekosolewa, kwa uchambuzi wa njia nyengine za riwaya zilizorejelewa, kwa aina ya kipekee katika kitabu chenye kufaidisha mno cha ‗Allâmah‎‎ Yamânî kiitwacho at-Tankîl bi mâ fî Ta‘nîb al-Kawthari min al-Abâtîl (1/20, 446-9).

194

KIAMBATISHO 6

UCHAMBUZI WA AHÂDÎTH KUHUSU KUSEMA “ÂMÎN” KWA IMÂM NA JAMÂ‟AH Kutoka: Silsilah al-Ahâdîth adh-Dha‘îfah (951-2) na Sheikh al-Albâni 1. ―Anaposema Âmîn, na wale walio nyuma yake walikuwa

wakisema âmîn, kiasi cha kwamba kulikuwa na makelele

msikitini.‖

Hakuna msingi wowote katika hadîth hiyo kwa matamshi haya

kulingana na ujuzi wetu. Ibn Hajar amesema katika Talkhîs al-

Habîr (Uk.90), ―Mimi siioni kwa matamshi haya, lakini maana

yake yameelezwa na Ibn Mâjah katika hadîth ya Bishr Ibn Râfi‘‖:

2. ―Alipokuwa akisoma:

لظب دري ول ٱل ي ـ ا ٧ ٱلظذ

Alisema, ‗âmîn‘, kiasi cha kwamba wale waliokuwa karibu

yake katika mstari wa kwanza walikuwa wakimsikiya [na

msikiti ulitetema kwayo (sauti)].‖

Dha‘îf (Nyonge). Imepokewa na Ibn Mâjah (1/281) na Abu Dâwud

bila ya nyongeza (1/148), zote hizo kupitia kwa:

Bishr Ibn Râfi‘ kutoka kwa Abu ‗Abdullâh‎, binamu yake Abu

Hurairah, kutoka kwa Abu Hurairah kutoka kwa Mtume ( ليه صىل اهلل ع .(وسلمIbn Hajar akasema katika Talkhîs (Uk.90), ―Bishr Ibn Râfi‘ ni

dhaifu; binamu yake Abu Hurairah anasemekana kuwa ni mtu

195

asojulikana, lakini Ibn Hibbân amemthibitisha kuwa ni

mtegemewa.‖

Bûsayri amesema katika Zawâ‘id (56/1), Hii ni isnâd dha‘îf; hali

ya Abu ‗Abdullâh‎ haijulikani; Bishr alithibitishwa na Ahmad kuwa

ni dha‘îf na Ibn Hibbân akasema, ‗ni mpokezi wa uzushi‘.‖

Hadîth no. 2 inâshiriya sehemu tu ya hadîth no.1, Yaani; Imâm

peke yake kuitamka âmîn. Ama kuhusu ―âmîn‖ ya walioko

nyuma, huwenda hii ikawa ndiyo sababu ya matamshi ―na msikiti

ulitetema kwayo (sauti).‖ lakini hadîth ki-maana inâshiriya

yakwamba ―âmîn‖ ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) ndiyo sababu ya haya.

3. ―Alipomaliza kuisoma ‗Mama wa Qur‘ân‘, alipâza sauti yake

kwa kusema ‗âmîn‘.‖

Dha‘îf (Nyonge). Imepokewa na Dâraqutniyy, Hâkim na Baihaqî.

Asli zote zilizotajwa hapo juu zina ndani yake Is-hâq Ibn Ibrâhîm

Ibn al-‗ALaa‘ az-Zubaidi, pia akijulikana kama Ibn Zibrîq, ambae

ni dha‘îf: Abu Hâtim akasema, ―Mzee, hana madhara yoyote‖;

Ibn Ma‘în akamsifu kwa sifa njema; an-Nasâ‘î akasema, ―Si mtu

wa kutegemewa‖; Muhammad Ibn ‗Awf akasema, ―Mimi sina

shaka yakwamba Is-hâq Ibn Zibrîq alikuwa akipenda kusema

urongo.‖ Hata hivyo, matamshi haya yako sawa ki-maana, kwani

kuna hadîth yenye kusaidia ya Wâ‘il Ibn Hajar yenye sanad iliyo

swahîh .

(Kwa vile hadîth hii haiashirii ―âmîn‖ ya Jamâ‘ah kabisa,

inakuwa ni makosa kuifanya kuwa ni riwaya nyengine ya hadîth

no.2, kama alivyofanya ash-Shawkâni)

196

Usaidizi wa no.1 pekee ni alivyoeleza ash-Shâfi‘î katika Musnad

yake (1/76) kupitia kwa Muslim Ibn Khâlid kutoka kwa Juraij

kutoka kwa ‗Atâ‘, aliyesema:

4. ―Nilikuwa nimezoea kuwasikiya ma-Imâm : Ibn az-Zubair na

wengine baada yake wakisema ‗âmîn‘, na waliokuwa nyuma

yake nao walikuwa wakisema ‗âmîn‘, mpaka msikiti

ukaviringwa kwa sauti.‖

Hii ina kasoro mbili:

I. Udhaifu wa Muslim Ibn Khâlid az-Zanji; Amesema Ibn Hajar,

―Alikuwa ni mtu mkweli, lakini ana makosa mengi.‖

II. ‗an‘anah ya Ibn Juraij, aliyekuwa ni mudallis; labda huwenda

pengine aliichukuwa kutoka kwa Khâlid Ibn Abi Anûf,

aliyeipokea kutoka kwa ‗Atâ‘ kama ifuatavyo:

―Mimi nilikutana na Maswahaba mia mbili wa Mtume wa Allâh‎

,katika msikiti huu (Yaani Masjid al-Harâm (صىل اهلل عليه وسلم)

Makkah): Pindi Imâm alipokuwa akisema:

ول ا ٧ ي ٱلظذ―Walipaza sauti zao kwa kusema ‗âmîn‘ (katika riwaya nyengine: Nilisikiya sauti ya kunguruma katika ‗âmîn‘

yao).‖

Imepokewa na Baihaqî (2/59) na Ibn Hibbân katika Thiqât (2/74);

riwaya hiyo nyengine ni ya kutoka kwa aliyetangulia (Baihaqî).

Khâlid huyu alisifiwa na Ibn Abî Hâtim (1/2/355-6), lakini

hakuingiza usahihishaji wowote wala ukosoaji. Ibn Hibbân

alimuingiza miongoni mwa msururu wa wapokezi wenye

197

kutegemewa, lakini Ibn Hibbân alikuwa akijulikana sana kwa

kujiepusha na msimamo mkali katika hali kama hizo, kwa hivyo

mimi sikutosheka yakwamba riwaya hii ni swahîh . Hii ni kwa

sababu ikiwa imethubutu yakwamba kwa hakika Ibn Juraij

aliipokea kutoka kwake, jambo hili linaleta hoja moja tu ya

mjadala; na lau si hivyo, basi sisi hatujui mahali alipoipokea

Juraij. Inaonekana yakwamba Imâm ash-Shâfi‘î mwenyewe pia

hakutosheka na uswahîh wa riwaya hii, kwani msimamo wake ni

kinyume chake: Alisema katika al-Umm (1/95), ―Kwahivyo Imâm

anapomaliza kusoma ‗Mama wa Kitabu‘, husema ‗âmîn‘, kwa

kuinua sauti yake ili wale waliokuwa nyuma yake wamfuate

yeye: anapoitamka, na wao huitamka kwa ndani ya nyoyo zao,

lakini mimi sipendelei wao waitamke kwa sauti ya juu‖; lau

kama riwaya hiyo ya hapo juu kutoka kwa Maswahaba ingelikuwa

ni swahîh kulingana na maoni ya ash-Shâfi‘î, hangeliwapinga

kitendo chao hicho.

Kwa hiyo, rai iliyozidi ukweli katika mas‘ala haya inaonekana

kuwa ni madh-hab ya Imâm ash-Shâfi‘î: yakwamba Imâm , wala

sio wafuasi wake, na aseme ‗âmîn‘ kwa sauti ya juu.

Yanamueleya Allâh‎ zaidi.

Lakini kisha nimeona yakwamba Bukhâri amelitaja andiko

(pekee) la riwaya hiyo kumuhusu Ibn az-Zubair katika Swahîh

yake (Yaani kwa njia ya Mu‘allaq) kwa mtindo wa kusadikisha.

Amesema Ibn Hajar katika Fat-hul-Bâri (2/208), ―Isnâd ya kiungo

imetolewa na ‗Abdur-Razzâq kutoka kwa Ibn Juraij kutoka kwa

‗Atâ‘. Yeye (Yaani Ibn Juraij) amesema, ‗Nilimuuliza, ―Je Ibn az-

Zubair alitamka âmîn baada ya mwisho wa ‗Mama wa Qur‘ân‘?‖

Akasema, ―Na‘am, na wale waliokuwa nyuma yake pia nao

wakasema âmîn, mpaka msikiti ukaviringwa kwa sauti.‖ Kisha

198

akasema, ―Kwa hakika ―Âmîn‖ ni maombi (Dua‘)‖.‘‖ Hii

inapatikana katika Musannaf ya ‗Abdur-Razzâq (2640/2), na

kutoka kwenye njia hiyo, katika kitabu cha Ibn Hazm kiitwacho

al-MuhalLaa (3/364).

Katika riwaya hii, Ibn Juraij amedhihirisha yakwamba

amechukuwa riwaya hiyo kutoka kwa ‗Atâ‘ alipokutana nae uso

kwa uso, kwa hivyo tumehakikishiwa kwa kutopatikana tadlîs, na

riwaya ya Ibn az-Zubair imethibitishwa kwa mkazo mkubwa.Na

pia imethibitishwa kutoka kwa Abu Hurairah; Amesema Abu

Râfi‘:

5. ―Abu Hurairah alikuwa akiadhini kwa Marwan Ibn al-Hakam,

akashurutisha kama ni ada yake (Marwan) kabla hajafika

katika ‗Waladh-Dhâllîn‘ isipokuwa ajue yakwamba Abu

Hurairah ameingia katika safu. Kwa hivyo Marwan alipokuwa

akisema ‗Waladh-Dhâllîn‘, Abu Hurairah aliitikia kwa kusema

‗Âmîn‘, kwa kuivuta. Na pia alisema, ‗Âmîn‘ ya wale

waliokuwa katika ardhi ikilingana na ‗âmîn‘ ya walioko

mbinguni, watasamehewa‘.‖

Imepokewa na Imâm al-Baihaqî (2/59); Isnâd yake ni swahîh .

Kwa hiyo, kwa vile hakuna kilichothibitishwa kutoka kwa

swahaba yoyote isipokuwa Abu Hurairah na Ibn az-Zubair

kinyume cha ‗Âmîn‘ yao kwa sauti kubwa, hii hainabudi

kukubaliwa. Kwa muda huu, mimi siijui riwaya yoyote

inayoipinga hii. Allâh‎ yanamuelea zaidi.

199

KIAMBATISHO 7

RAK‟ÂH MBILI ZA BAADA YA WITR

Kutoka katika: Silsilah al-Ahâdîth as-Swahîh ah (1993) Cha Sheikh

al-Albâni

1) Amesema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), ifanyeni swala yenu ya

mwisho ya usiku kuwa Witr (idadi isiyo na mwenzi).

Imepokewa na Bukhâri na Muslim.

2) Abu Salamah alimuuliza ‗Âisha kuhusu swala aliyokuwa

akiiswali Mtume (صىل اهلل عليه وسلم). Akasema, ―Alikuwa akitekeleza

Rak‘âh kumi na tatu (katika swala za usiku): alitekeleza Rak‘âh

nane na kisha akatekeleza Witr na kisha hutekeleza Rak‘âh mbili

hali ya kukaa, na alipokuwa akitaka Kurukû‘, husimama na kisha

hurukû‘, na kisha hutekeleza Rak‘âh mbili baina ya adhân na

iqâmah ya swala ya fajr.‖

Imepokewa na Muslim.

3) Amesema Thawbân, ―Tulikuwa kwenye msafara pamoja na

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), pindi aliposema, Kwa hakika safari hii ni

ugumu na hali ya kulemewa, kwa hivyo iwapo mmoja wenu

amemaliza kuswali Witr, na atekeleze Rak‘âh mbili; iwapo

atâmka (basi ni uzuri), lau si hivyo, hizo mbili ndio zitakazokuwa

(swala ya usiku) kwake.

Imepokewa na ad-Dârimi (1/374), Ibn Khuzaymah katika swahîh

yake (2/159/1103) na Ibn Hibbân (683) kutokana na njia

mbalimbali zote zikielekea kwa: Ibn Wahb, aliyesema:

Mu‘âwiyah Ibn Sâlih alinisimulia mimi kutoka kwa Shuraih Ibn

‗Ubaid kutoka kwa ‗Abdur-Rahmân Ibn Jubair Ibn Nufair kutoka

kwa babake kutoka kwa Thawbân, aliyesema ...

200

Ibn Wahb ameungwa mkono na ‗Abdullâh‎ Ibn Sâlih, aliyesema:

Mu‘âwiyah Ibn Sâlih alitusimulia ... n.k (na kadhaalika),

imepokewa na Dâraqutnî‘ (Uk.177) na Tabarâni katika Mu‘jamul

Kabîr (1410). ‗Abdullâh‎ Ibn Sâlih ni Sheikh wa Bukhâri, kwa hivyo

anaweza kutumika kama ni dalili katika kuunga mkono riwaya

nyenginezo.

Imâm Ibn Khuzaimah ameitumia hadîth hii kama dalili,

―yakwamba swala baada ya Witr inaruhusiwa kwa mtu yoyote

anaetaka kuswali baada yake, na kwamba Rak‘âh mbili ambazo

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alizokuwa akiziswali baada ya Witr

hazikuwa ni makhsusi kwake yeye juu ya Ummah wake, kwani

ametuamrisha sisi kuswali Rak‘âh mbili baada ya Witr, amri ya

mapendekezo na ubora, wala sio (amri) ya uwajibu na

ulazimishaji.‖

Kwa hiyo, ni wazi kwetu sisi kutokamana na hadîth hii (kwa

sababu ya amri yake ya ujumla kwa Ummah wake) yakwamba

Rak‘âh mbili baada ya Witr hazikuwa ni makhsusi kwake yeye;

inaonyesha hapa yakwamba malengo ya amri yake kuifanya swala

ya mwisho ya usiku iwe juu ya idadi isiyoweza kugawanyika kwa

mbili ilikuwa ni kuepuka kuipuza hiyo Rak‘âh moja isiyo na

mwenzi, kwahivyo shauri hili halikupingana na Rak‘âh mbili

baada yake, kama ilivyothubutu katika vitendo vyake na

mafundisho yake. Allâh‎ ndiye Mjuzi aliye bora.

201

KIAMBATISHO 8

UDHAIFU WA AHÂDÎTH ZENYE KUTAJA KUFUTA

(UPANGUSAJI WA) USO KWA MIKONO BAADA YA DU‟A

(MAOMBI)

Kutoka katika: Irwâ‘ al-Ghalîl (2/178-182) Cha Sheikh al-Albâni

1) Alipokuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akiinua mikono yake anapo

omba dua‘, Hayashukishi Chini Mpaka Apangusie Nayo Uso

Wake.‖

Dha‘îf (Nyonge). Imepokewa na Tirmidhî (2/244) na Ibn ‗Asâkir

(7/12/2) kupitia kwa: Hammâd Ibn ‗Isa al-Juhani kutoka kwa

Handhwalah ibn Abi Sufyân al-Jamhi kutoka kwa Sâlim Ibn

‗Abdullâh‎ kutoka kwa babake kutoka kwa ‗Umar ibn al-Khattâb,

aliyesema: ...

Tirmidhî akasema baada yake, ―Hii ni hadîth swahîh gharîb.

Sisi twaijua tu kama ni hadîth ya Hammâd Ibn ‗Isa, kwani yeye

alikuwa peke yake katika kuisimulia; yeye ana ahâdîth chache

tu, lakini watu wamepokea kutoka kwake.‖

Hatahivyo, mpokezi huyu ni dha‘îf, kama ilivyo katika Taqrîb cha

Ibn Hajar, aliyemzungumza katika Tahdhîb:

Amesema Ibn Ma‘în, ―Sheikh mzuri‖1; Abu Hâtim

akasema, ―Dha‘îf katika hadîth ‖; Abu Dâwud akasema,

1 Ibn Ma‘în anapomzungumza mpokezi kwa vizuri, haliyakuwa wanavyuoni wengine wakamthibitisha kuwa dha‘îf, basi matamshi ya Ibn Ma‘în huwa hayazingatiwi, sababu ni kwamba alikuwa akijulikana kwa ukali wake na ukazaji mambo katika kukashifu kwake: wapokezi

202

―Dha‘îf, hupokea munkar ahâdîth‖; Hâkim na Naqqâsh

wakasema, ―Hupokea ahâdîth za kuzuliwa kutoka kwa Ibn

Juraij na Ja‘far as-Sâdiq.‖ Amethibitishwa kuwa dha‘îf na

Dâraqutnî‘. Amesema Ibn Hibbân, ―Hupokea vitu ambavyo

ni ‗kinyume cha ilivyo kutoka kwa Ibn Juraij na ‗Abdul

‗Azîz Ibn ‗Umar Ibn ‗Abdul ‗Azîz, kiasi cha kwamba

ionekane na walio na ujuzi katika ta‘aluma hii yakwamba

alikusudia; hairuhusiwi kumtumia yeye kama ushahidi.‖

Ibn MâkûLaa amesema, ―Wamethibitisha ahâdîth zake

kuwa ni dha‘îf.‖

Kwa hiyo, mfano wa wapokezi kama huyu ni dha‘îf mno, kwa

hivyo ahâdîth zake haziwezi kuinuliwa kwenye daraja ya hasan,

licha ya swahîh !

Hadîth mfano wa hiyo ni:

―Alipokuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)akiomba du‘a na kuinua mikono

yake, alikuwa akifuta uso wake kwa mikono yake.‖

Dha‘îf (Nyonge). Abu Dâwud (1492) kutoka kwa Ibn Lahî‘ah

kutoka kwa Hafs Ibn Hishâm Ibn ‗Utbah Ibn Abi Waqqâs kutoka

kwa Sâ‘ib Ibn Yazîd kutoka kwa babake.

Hii ni sanad dha‘îf kutokana na Hafs Ibn Hishâm yakwamba ni

mtu asojulikana na udhaifu wa huyu Ibn Lahî‘ah (cf. Taqrîb at-

Tahdhîb).

waliodhaifu huwa na tahadhari sana wasijidhihirishe udhaifu wao mbele yake; basi nae hutoa hukumu kulingana na hali ilivyo. Hii inaelezea ni kwanini yeye huwa peke yake katika kumthibitisha mpokezi.

203

Hadîth hii haiwezi kutiwa nguvu kwa njia mbili za riwaya kwa

pamoja kutokana na uzito wa udhaifu wa hadîth ya kwanza,

ambao ushauona.

2) “UNAPOMUOMBA ALLÂH‎, BASI MUOMBE KWA VITANGA

VYAKO VYA MIKONO, NA WALA USIOMBE KWA

MIGONGONI MWAKE, NA UNAPOMALIZA, JIPANGUSIE

NAYO USO WAKO.”

Dha‘îf (Nyonge): Imepokewa na Ibn Mâjah (1181, 3866), Ibn

Nasr katika QiYâm al-Lail (Uk. 137), Tabarâni katika Al-Mu‘jam

al-Kabîr (3/98/1) na Hâkim (1/536), kutoka kwa Sâlih Ibn Hassân

kutoka kwa Muhammad Ibn Ka‘b kwa njia ya marfû‘ kutoka kwa

Ibn ‗Abbâs (رضي اهلل عنه) Hii ni sanad dhaifu mno kutokana na Ibn Hassân, ambaye ni

munkar katika Hadîth , kama alivyosema Bukhâri; Nasâ‘î

akasema, ―Huyu ametupiliwa mbali katika Hadîth ‖; Ibn Hibbân

amesema, ―Alikuwa na waimbaji wanawake na yeye mwenyewe

alikuwa akisikiza nyimbo, na alikuwa akisimulia khabari za kuzua

kutoka kwa wapokezi wâminifu‖; Ibn Abi Hâtim amesema katika

Kitâb al-‗Ilal (2/351), ―Nilimuuliza babangu (Yaani: Abu Hâtim

ar-Râzi) kuihusu hadîth hii, ambayo aliyoisema kuwa ni:

‗Munkar‘.‖

Ibn Hassân ameungwa mkono na ‗Isa Ibn Maimûn, ambaye pia

aliyeipokea kutoka kwa Muhammad Ibn Ka‘b, kama ilivyopokewa

na Ibn Nasr. Lakini hata hivyo, hii haibadilishi chochote, kwa vile

Maimûn mwenyewe pia ni dha‘îf: Ibn Hibbân akasema,

204

―Anapokea ahâdîth, ambazo zote ni za kuzua‖; Nasâ‘î akasema,

―Si muaminifu.‖

Hadîth hii ya Ibn ‗Abbâs pia imepokewa na Abu Dâwud (1485),

na Baihaqî kutoka kwake (2/212), kwa kupitia kwa: ‗Abdul Mâlik

Ibn Muhammad Ibn Aiman kutoka kwa ‗Abdullâh‎ Ibn Ya‘qûb Ibn

Is-hâq kutoka kwa mtu aliyemsimulia yeye kutoka kwa

Muhammad Ibn Ka‘b, maneno yasemayo:

―Musizizibe kuta. Mwenye kusoma barua ya ndugu yake bila ya

ruhusa yake, kwa hakika anautazama moto. Muombeni Allâh‎ kwa

viganja vyenu vya mikono, na wala musimuombe kwa migongo

yake, na mumalizapo, ipanguseni kwayo nyuso zenu.‖

Hii ni sanad dhaifu: ‗Abdul Mâlik amethibitishwa kuwa dhaifu na

Abu Dâwud; vilevile ndani yake yumo Sheikh wa ‗Abdullâh‎ Ibn

Ya‘qûb ambaye jina lake hakutajwa, na kwahivyo, amebakia

kuwa ni mtu asojulikana – pana uwezekano kuwa huwenda akawa

ndiye huyo Ibn Hassân au Ibn Maimûn, wote wakiwa ni miongoni

mwa waliotajwa hapo juu.

Hadîth hiyo vilevile imepokewa na Ibn Hâkim (4/270) kwa njia

ya: Muhammad Ibn Mu‘âwiyah, aliyesema yakwamba Masâdif Ibn

ZiYâd al-Madîni alimsimulia yakwamba aliisikiya kutoka kwa

Muhammad Ibn Ka‘b al-Qurazi. Adh-Dhahabi akaifuatilia kwa

kutaja yakwamba Ibn Mu‘âwiyah amethibitishwa kuwa ni mrongo

na Dâraqutnî‘, kwahivyo hadîth hiyo imeorodheshwa miongoni

mwa hadîth za urongo.

Abu Dâwud amesema kuihusu hadîth hii, ―Hadîth hii imepokewa

kwa kupitia njia zaidi ya moja kutoka kwa Muhammad Ibn Ka‘b;

wote hao ni dhaifu.‖

205

Kunyanyua mikono katika Qunût kwa ajili ya janga fulani

imethubutu kutoka kwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)alipowâpiza

washirikina waliowauwa mahuffâdh (waliohifadhi Qur‘ân) sabiini

– Imepokewa na Imâm Ahmad (3/137) na Tabarâni katika al-

Mu‘jam as-Swaghîr‎‎ (Uk. 111) kama ilivyo katika hadîth ya Anas

kwa sanad iliyo swahîh . Imethubutu mfano wake kutoka kwa

‗Umar na wengineo katika Qunût ya Swala ya Witr. Hatahivyo,

kwa vile kujipangusa uso (au kufuta uso) baada ya du‘a al-Qunût

haikuwahi kupokewa kabisa kutoka kwa Mtume ( ,( عليه وسلمصىل اهلل

wala kutoka kwa Swahaba wake yoyote, linakuwa hilo ni jambo

la kuzua bila ya shaka yoyote.

Ama kuhusu kupangusa uso baada ya du‘a nje ya swala, kuna

ahâdîth hizo mbili pake yake; si sawa kusema yakwamba ahâdîth

hizo zinasaidiana kutia nguvu ili zifikie daraja ya Hasan, kama

alivyofanya Manâwi, kutokana na udhaifu wake wa kupindukia

uliopatikana katika njia za mapokezi. Hii ndiyo sababu Imâm an-

Nawawi akasema katika al-Majmû‘ , ―Haijuzu‖ (Yaani: Haifai

kufuta uso), akathibitisha Ibn ‗Abd as-SaLaam, aliyesema, ―Mtu

mjinga peke yake ndiye mwenye kufanya hivyo.‖

Rai yakwamba kupangusa uso baada ya du‘a haikuthubutu

imetiliwa nguvu na ukweli yakwamba kuna ahâdîth nyingi sana

zilizo swahîh zinazohusu kuinua mikono katika du‘a, na hakuna

hata mojawapo inayotaja kuhusu kupangusa uso, hii yaonyesha

yakwamba, Insha-Allâh‎, ni jambo lisilofaa na halikuthubutu.

206

KUMBUKUMBU ZA MUANDISHI A QUR‟ÂN

1. Qur‘ân B TAFSÎR

2. Qur‘ân Ibn Kathîr (701-774 AH): TAFSÎR al-Qur‘ân al-‗Adhîm, Chapa ya Muhammad Mustafa, 1365.

C SUNNAH

3. Mâlik Ibn Anas (93-179): Al-Muwatta‘, Dâr IhYâ‘ Kutub al-‗Arabiyyah, 1343

4. Ibn al-Mubârak, ‗Abdullâh‎ (118-181): Az-Zuhd, ms.

5. Muhammad Ibn al-Hasan ash-Shaibâni (131-189): Al-Muwatta‘, Al-Mustafâ‘i, 1297

6. Tayâlisi (124-204): AL-Musnad, Dâ‘irah al-Ma‘ârif, Hyderabad Deccan, 1321.

7. ‗Abd ar-Razzâq bin Humâm (126-211): Al-Amâli, ms.

8. Humaidi, ‗Abdullah Ibn az-Zubair (...-219): Musnad, ms

9. Ibn Sa‘d, Muhammad (168-230): at-Tabaqât al-Kubrâ, Uropa.

10. Ibn Ma‘în, YahYâ (...-233): Târîkh ar-Rijâl wal-‗Ilal, ms

11. Ahmad Ibn Hanbal (164-241): Musnad, Al-Matba‘ah al-Maymaniyyah, 313; Matba‘ah al-Ma‘ârif, 1365.

12. Ibn Abi Shaybah, ‗Abdullâh‎ Ibn Muhammad Abu Bakr (...-235): Musannaf, ms.

13. Dârimi (181-255): Sunan, Matba‘ah al-I‘tidâl, Damascus, 1349

14. Bukhâri (194-256):Al-Jâmi‘ as-Swahîh , Al-Matba‘ah al-Bahiyya al-Misriyyah, 1348. Imechapishwa na Sherhe yake, fat-hul-Bârî.

15. ...............: Al-Adab al-Mufrad, Matba‘ah al-Khalili, India 1306.

16. ...............: Khalq Af‘âl al-‗Ibâd, Matba‘ah al-Answâr, India.

17. ...............: At-Tarîkh as-Swaghîr‎‎, India.

18. ...............: Juz‘ al-Qirâ‘ah (―Mândishi kuhusiana na Usomaji‖), imechapishwa.

207

19. Abu Dâwud (202-275): Sunan, Al-Matba‘ah at-Tâziah, 1349.

20. Muslim (204-261): Swahîh , Chapa ya Muhammad ‗Ali.

21. Ibn Mâjah (209-273): Sunan, Al-Matba‘ah at-Tâziah, 1349.

22. Tirmidhî (209-279): Sunan, ed. Ahmad Shâkir, Halab, 1356.

23. ...............: Shamâ‘il Muhammadiyyah, na sherhe yake cha ‗Ali al-Qâri na ‗Abdur-Ra‘ûf al-Manâwi, Al-Matba‘ah al-Adabiyyah, Egypt, 1317.

24. Al-Hârith Ibn Abi Usâmah (176-282): Musnad –zawâ‘iduh, ms.

25. Abu Is-hâq al-Harbi, Ibrâhim Ibn Is-hâq (198-285): Gharîb al-Hadîth (Maneno magumu katika Hadîth ) ms.

26. Bazzâr, Abu Bakr Ahmad Ibn ‗Amr al-Basrî‘ (...-292): Musnad – zawâ‘iduh, kopi ya chapa.

27. Muhammad Ibn Nasr (202-294): QiYâm al-Layl, Matba‘ah Rifâh ‗Âmm, Lahore 1320.

28. Ibn Khuzaymah (223-311): Swahîh , Al-Maktab al-IsLaami.

29. Nasâ‘î (225-303): Sunan – Al-Mujtabâ, Al-Matba‘ah al-Maymaniyyah.

30. ...............: as-Sunan al-Kubrâ, ms.

31. Al-Qâsim al-Sarqasti (255-302): Gharîb al-Hadîth au ad-DaLaa‘il, ms.

32. Ibn al-Jârûd (...-307): Al-Muntaqâ, ms., Egypt.

33. Abu Ya‘Laa al-Mûsîli (...-307): Musnad, ms.

34. RûYaani, Muhammad Ibn Hârun (...-307): Musnad, ms.

35. Sirâj, Abul-‘Abbâs Muhammad Ibn Is-hâq (216-313): Musnad, mijalada mengi yakiwa kama ms., katika maktaba ya Zâhiriyyah, Damascus.

36. Abu ‗Awânah (...-316): Swahîh , Dâ‘irah al-Ma‘ârif, Hyderabad Deccan, 1326.

37. Ibn Abi Dâwud, ‗Abdullâh‎ Ibn Suleimân (230-316): Al-Masâhif, ms.

38. Tahâwi (239-321): Sharh Ma‘âni al-Âthâr (Maelezo kuhusu maana za riwaya), Al-Mustafâ‘i, India, 1300.

39. ...............: Mushkil al-Âthâr (Maneno magumu katika riwaya), Dâr al-Ma‘ârif, India, 1333.

208

40. ‗Uqaili, Muhammad Ibn ‗Amr (...-322): Adh-Dhu‘afâ‘ (Wapokezi dhaifu), ms.

41. Ibn Abi Hâtim (240-327): Al-Jarh wat-Ta‘dîl (Jaraha na Mâdili ya wapokezi).

42. ................: ‗Ilal al-Hadîth (Ila za katika hadîth ), As-salafiyyah, Egypt, 1343.

43. Abu Ja‘far al-Bukhturi, Muhammad Ibn ‗Amr ar-Razâz (...-329): Al-Amâli, ms.

44. Abu Sa‘îd Ibn al-A‘râbi, Ahmad Ibn ZiYâd (246-340): Mu‘jam, ms.

45. Ibn Sammâk, ‗Uthmân Ibn Ahmad (...-344): Hadîth , ms.

46. Abul-‘Abbâs al-Asamm, Muhammad Ibn Ya‘qûb (247-346): Hadîth , ms.

47. Ibn Hibbân (...-354): Swahîh , Dâr al-Ma‘ârif, Egypt.

48. Tabarâni (260-360): Al-Mu‘jam al-Kabîr mijalada mengi yakiwa kama ms., katika maktaba ya Zâhiriyyah, Damascus.

49. ...............: Al-Mu‘jam al-Awsat min al-Jam‘ bainahu wabain as-Swaghîr‎‎, ms.

50. ...............: Al-Mu‘jam as-Swaghîr‎‎, Matba‘ah al-Ansârî, Delhi, 1311.

51. Abu Bakr al-Âjurrî (...-360): Al-Arba‘în (Hadîth arubaini), ms.

52. ...............: Âdâb Hamlah al-Qur‘ân, ms.

53. Ibn As-Sunni (...-364): ‗Amal al-Yawm wal-Laylah, Dâ‘irah al-Ma‘ârif, India, 1315.

54. Abu Ash-Sherikh Ibn HayYân (274-369): Tabaqât al-Isbahâniyyîn, ms.

55. ...............: Mâ rawâhu Abu Az-Zubair ‗an Ghair Jâbir (Aliyoyapokea Abu Az-Zubair kutoka kwa asiyekuwa Jâbir), ms.

56. ...............: AkhLaaq an-Nabî SallAllâh‎u ‗alayhi wasallam (Tabia ya Mtume), Egypt.

57. Dâraqutnî‘ (306-385): Sunan, India.

209

58. Khattâbi (317-388): Ma‘âlim as-Sunan, Ansâr as-Sunnah, Egypt.

59. Mukhlis (305-393): Al-Fawâ‘id, ms., Maktabat az-Zâhiriyyah, Damascus.

60. Ibn Mandah, Abu ‗Abdullâh‎ Muhammad Ibn Is-hâq (316-395): At-Tawhîd wa Ma‘rifah Asmâ‘ Allâh‎ Ta‘âlah, ms.

61. Hâkim (320-405): Al-Mustadrak, Dâ‘irah al-Ma‘ârif, Hyderabad, 1340.

62. Tamâm ar-Râzi (330-414): Al-Fawâ‘id, kopi mbili kamili kama ms., Maktaba az-Zâhiriyyah, Damuscus.

63. Sahmi, Hamzah Ibn Yusuf al-Jurjâni (...-427): Târîkh Jurjân (Historia ya Jurjân), imechapishwa.

64. Abu Nu‘aim al-Isbahâni (336-430): Akhbâr Isbahân (Habari za Isbahân), Imechapishwa Uropa.

65. Ibn Bushrân (339-430): Al-Amâli, milango yake mengi, ms., Maktaba Zâhiriyyah, Damascus.

66. Baihaqî (384-458): as-Sunan al-Kubrâ, Dâ‘irah al-Ma‘ârif, Hyderabad, 1352.

67. ...............: DaLaa‘il an-Nubuwwah, ms.,Maktaba Ahmadiyyah, Halab.

68. Ibn ‗Abd al-Barr (368-463): Jâmi‘ BaYân al-‘Ilm wa fadhlih, Al-Matba‘ah al-Munîriyyah.

69. Ibn Mandah, Abul-Qâsim (381-470): Ar-Radd ‗aLaa man Yunfi al-Harf min al-Qur‘ân, ms., Maktaba az-Zâhiriyyah, Damascus.

70. Bâji (403-477): Shrha al-Muwatta‘, imechapishwa.

71. ‗Abdul haqq al-Ishbîli (510-581): Al-Ahkâm al-kubrâ, ms.

72. ...............: Tahajjud, ms.

73. Ibn al-Jawzi (510-597): At-Tahqîq ‗aLaa Masâ‘il at-Ta‘lîq, ms.

74. Abu Hafs al-Mu‘âdib, ‗Amr Ibn Muhammad (516-607): Al-Muntaqâ min Amâli Abil Qâsim as-Samarqandi, ms.

75. ‗Abdul Ghani Ibn ‗Abd al Wâhid al-Maqdisi (541-600): Sunan, ms.

210

76. DiYâ‘ al-Maqdisi (569-643): Al-Ahâdîth al-Mukhtârah, mijalada mengi yakiwa kama ms., katika maktaba ya Zâhiriyyah, Damascus.

77. ...............: Al-Muntaqâ min al-Ahâdîth as-Sihah wal-Hisân (ukusanyaji wa Ahâdîth zilizo swahîh ), ms.

78. ...............: Juz‘ fi fadhl al-hadîth wa Ahlil (Makala ya kuhusu fadhla za hadîth na watu wake) , ms.

79. Mundhiri (581-656): At-Targhîb wat-Tarhîb, al-Matba‘ah al-Munîriyyah, Egypt.

80. Zayla‘i (...-762): Nasb ar-Râyah, Dâr al-Ma‘mûn, Egypt, 1357.

81. Ibn Kathîr (701-774): Jâmi‘ al-Masânîd, ms .

82. Ibn al-Mulaqqin, Abu Hafs ‗Amr Ibn Abil-Hasan (723-804): Khulâsah‎ al-Badr al-Munîr, ms.

83. ‗Irâqi (725-806): Tarh at-Tathrîb, Jam‘iyyah an-Nashr wat-Ta‘lîf al-Azhariyyah, 1353.

84. ...............: Takhrîj ya IhYâ‘ ‗Ulûm ad-Dîn cha Ghazali, Egypt, 1346.

85. Haithami (735-807): Majma‘ az-Zawâ‘id: Husâm ad-Dîn al-Qudsi, 1352

86. ...............: Mawârid az-Zam‘ân fi Zawâ‘id Ibn Hibbân, Chapa ya Muhibb ad-Dîn.

87. ...............: Zawâ‘id al-Mu‘jam as-Swaghîr‎‎ wal-Awsat lit-Tabarâni, ms.

88. Ibn Hajar al-‗AsqaLaani (773-852): Takhrîj Ahâdîth al-Hidâyah, India.

89. ...............: Talkhîs al-Habîr, Al-Matba‘ah al-Munîriyyah.

90. ...............: Fat-hul-Bâri , Al-Matba‘ah al-Bahiyyah.

91. ...............: Al-Ahâdîth al-‗ÂliYât, ms.

92. Suyûti (889-911): Al-Jâmi‘ al-Kabîr, ms.

93. ‗Ali al-Qâri (...-1014): Al-Ahâdîth al-Mawdhû‘ah, Istanbul.

94. Manâwi (952-1031): Faid al-Qadîr Sharh al-Jâmi‘ as-Swaghîr‎‎, Chapa ya Mustafa Muhammad.

95. Zurqâni (1055-1122): Sharh al-Mawâhib al-Ladunniyyah, Egypt.

211

96. Shawkâni (1171-1250): Al-Fawâ‘id al-Majmû‘ah fil Ahâdîth al-Mawdhû‘ah, India.

97. ‗Abd al-Hayy Lucknowi (1264-1304): At-Ta‘lîq al-Mumajjid ‗aLaa-Muwatta‘, Muhammad, al-Mustafâ‘i, 1297.

98. ...............: Al-Âthâr al-Marfû‘ah fil akhbâr al-Mawdhû‘ah, India.

99. Muhammad Ibn Sa‘îd al-Halbi (...-...): MusalsaLaat, ms.

100. Albâni , Muhammad Nâsir ad-Dîn al-: Takhrîj Sifah SaLaah an-Nabi,ms., shughuli ya asli ya kitabu hiki, ambacho kimehusishwa kama al-Asl.

101. ...............: Irwâ‘ al-Ghalîl fi Takhrîj Ahâdîth Manâr as-Sabîl, mijalada 8., al-Maktab al-IsLaami, kimechapishwa chote, AlhamdulilLaah.

102. ...............: Swahîh Abi Dâwud, Hakijakamilika bado.

103. ...............: Nukta za kuhusu Ahkâm za ‗Abd al-Haqq al-Ishbîli., haijakamilika.

104. ...............: Takhrîj ya ahâdîth za Sharh ‗Aqîdah at-Tahâwiyyah, al-Maktab al-Islami.

105. ...............: Silsilah al-Ahâdîth adh-Dha‘îfah, Vol 4, al-Maktab al-Islami.

D FIQH

106. Mâlik Ibn Anas (93-179): Al-Mudawwanah (Fiqh ya ki- MÂLIK), Matba‘ah as-Sa‘âdah, 1323.

107. Shâfi‘î, Muhammad Ibn Idrîs (150-204): Al-Umm (Shâfi‘î), AlMatba‘ah al-Amîriyyah, 1321.

108. Marwazi, Ishâq Ibn Mansûr (...-251): Masâ‘il al-Imâm Ahmad wa Is-hâq Ibn Râhawaih, ms.

109. Ibn Hâni, Ibrâhim Naisâburi (...-265): Masâ‘il al-Imâm Ahmad, ms.

110. Muzani (175-264): Mukhtasar fiqh ash-Shâfi‘î, imechapishwa pambizoni mwa kitabu cha al-Umm.

111. Abu Dâwud (202-275): Masâ‘il al-Imâm Ahmad (Hanbali), al-Manar, 1353.

212

112. ‗Abdullâh‎ Ibn al-Imâm Ahmad (203-290): Masâil al-Imâm Ahmad, ms.

113. Ibn Hazm (384-456): Al-MuhalLaa (Zâhiri), al-Matba‘ah al-Munîriyyah.

114. ‗Izz Ibn ‗Abd as-SaLaam (578-660): Al-Fatâwâ, ms.

115. Nawawi (631-686): Al-Majmû‘ Sharh al-Muhadh-dhab (Shâfi‘î), al-Matba‘ah al-Munîriyyah.

116. ...............: Rawdhah at-Tâlibîn (Shâfi‘i), al-Maktab al-Islami.

117. Ibn Taymiyyah (661-728): al-Fatâwâ, chapa ya Farj ad-Dîn al-Kurdi.

118. ...............: min kaLaam lahu fit-Takbîr fil-‗Îdain wa ghairuh (mazungumzo kuhusiana na Takbîr za swala mbili za ‗Eid) ms.

119. Ibn al-Qayyim (691-751): I‘Laam al-Muwaqqi‘în.

120. Subki (683-756): fatâwâ, (Shâfi‘î).

121. Ibn al-Humâm (790-869): Fat-hul-Qadîr (Hanafî), chapa ya BûLaaq.

122. Ibn ‗Abd al-Hâdi, Yusuf (840-909): Irshâd as-Sâlik (Hanbalî), ms.

123. ...............: al-Furû‘ (Hanbalî).

124. Suyûti (809-911): al-Hâwi lil-fatâwi (Shâfi‘î) al-Qudsi.

125. Ibn Nujaim al-Misri (...-970): Al-Bahr ar-Râ‘iq (Hanafî), al-Matba‘ah al-‗Ilmiyyah.

126. Sha‘râni (898-973): Al-Mîzân (kulingana na madhâhib Mane).

127. Haitami (909-973): Ad-Dâr al-Mandûd fis-SaLaah was-SaLaam ‗aLaa Sâhib al-Maqâm al-Mahmûd, ms.

128. ...............: Asmâ al-Matâlib, ms.

129. Wali-UlLaah Dehlawi (1110-1176): HujjatulLaah al-Bâlighah, al-Munîrah.

130. Ibn ‗Âbidîn (1151-1203): Nukta za chini kuhusu ad-Darr al-Mukhtâr. (Hanafî).

213

131. ...............: Nukta za chini kuhusu al-Bahr ar-Râ‘iq. (Hanafî).

132. ...............: Rasm al-Mufi. (Hanafî).

133. ‗Abd al-Haqq (1264-1304): Imâm al-KaLaam fî mâ yata‘allaq bil-Qira‘ah Khalf al-Imâm , Al-Baladi, India.

134. ...............: An-Nâfi‘ al-Kabîr liman yuâli‘ al-Jâmi‘ as-Swaghîr‎‎, Al-Yusufi, India 1349.

E SÎRAH [TÂRÎKH YA MTUME (صىل اهلل عليه وسلم)) NA TARÂJUM

(TÂRÎKH ZA WAPOKEZI WA HADÎTH )

135. Ibn Abi Hâtim, ‗Abd ar-Rahmân(240-327): Taqaddamah al-Ma‘rifah li Kitâb al-Jarh wat-Ta‘dîl, India.

136. Ibn Hibbân (...-354): Ath-Thiqât (Wapokezi wanaotegemewa), ms.

137. Ibn ‗Âdiy (277-365): Al-Kâmil, ms.

138. Abu Nu‘aim (336-430): Hilyah al-AwliYâ‘, Matba‘ah as-Sa‘âdah, Egypt, 1349

139. Khatîb Baghdâdi (392-463):Târîkh Baghdâd (Historia ya Baghdâd), Matba‘ah as-Sa‘âdah,Egypt.

140. Ibn ‗Abd al-Barr (368-463): Al-Intiqâ‘ fi fadhâ‘il al-Fuqahâ‘.

141. Ibn ‗Asâkir (499-571): Târîkh Dimashq (Historia ya Damascus), ms.

142. Ibn al-Jawzi (508-597): Manâqib al-Imâm Ahmad, imeshachapishwa.

143. Ibn al-Qayyim (691-751): Zâd al-Ma‘âd, chapa ya Muhammad ‗Ali 1353.

144. ‗Abd al-Qâdir al-Qurashi (696-775): Al-Jawâhir al-Madiyyah, India.

145. Ibn Rajab al-Hanbali (736-795): Dhail at-Tabaqât, Egypt.

146. ‗Abd al-Hayy Lucknowi (1264-1304): Al-Fawâ‘id al-Bahiyyah fi Tarâjum al-Hanafiyyah, Matba‘ah as-Sa‘âdah, Egypt, 1324.

214

F LUGHA YA KIARABU

147. Ibn al-Athîr (544-606): an-Nehâyah fi Gharîb al-Hadîth wal-Athar, Al-Matba‘ah al-‗Uthmâniyyah, Egypt, 1311.

148. Ibn Manzûr al-‗Afrîqi (630-711): Lisân al-‗Arab, Dâr Sâdir, Beirut, 1955 A.C

149. Fairuz Âbâdi (729-817): Al-Qâmûs al-Muhît, Chapa ya Tatu, 1353.

G USÛL AL-FIQH (MISINGI YA FIQH)

150. Ibn Hazm (384-456): Al-Ihkâm fi USÛL al-Ahkâm, Matba‘ah as-Sa‘âdah, Egypt, 1345.

151. Subki (683-856): Ma‘nâ Qawl ash-Shâfi‘î al-Matlabi, ―idhâ sahh al-Hadîth fahuwa madh-habi‖ (Mâna ya Maneno ya ash-Shâfi‘î, ―Ipatikanapo hadîth kuwa ni swahîh , basi hayo ndiyo madh-hab yangu‖), kutoka katika Majmû‘ah ar-Rasâ‘il, al-Munîriyyah.

152. Ibn alQayyim (691-856): Badâ‘i‘ al-Fawâ‘id, al-Matba‘ah al-Munîriyyah.

153. Wali-ulLaah Dehlawi (1110-1176): ‗Iqd al-Jed fi Ahkâm al-ijtihâd wat-Taqlîd, India.

154. FuLaani (1166-1218): Îqâz al-Himam, Al-Matba‘ah al-Munîriyyah.

155. Zurqâ‘, Sheikh Mustafâ ( Mwanachuoni wa zama zetu): Al-Madkhal iLaa ‗Ilm USÛL al-Fiqh, Ishachapishwa.

H ADHKÂR

156. Ismâ‘îl al-Qâdi al-Maqdisi (199-282): Fadhl as-SaLaah ‗aLaa an-Nabi sallAllâh‎u ‗alayhi wa sallam, pamoja na utafiti wangu, Al-Maktab al-IsLaami.

157. Ibn al-Qayyim (691-751): jaLaa‘ al-ifhâm fi as-SaLaah ‗aLaa khair al-Anâm, Al-Matba‘ah al-Munîriyyah.

158. Siddîq Hasan Khân (1248-1307): Nuzul al-Abrâr, al-jawâ‘ib.

215

I MCHANGANYIKO

159. Ibn Battah, ‗Abdullah ibn Muhammad (304-387): Al-Ibânah ‗an Sharî‘ah Al-Firqah An-Nâjiyah (ubainifu wa kanuni za kikundi kilichonusurika), ms.

160. Abu ‗amr Ad-Dâni, ‗Uthmân bin Sa‘îd (371-444): Al-Muktafâ fi Ma‘rifah al-Waqf at-Tâmm, ms.

161. Khatîb Baghdâdi (392-463): Al Ihtijâj bi ash-Shâfi‘î fi mâ asnada ilaih ..., ms.

162. Harawi, ‗Abdullâh‎ Ibn Muhammad al-Ansâri (396-481): Dhamm al-KaLaam wa-Ahlah, ms.

163. Ibn al-Qayyim (691-751): Shifâ‘ al-‗Alîl fi masâ‘il al-Qadhâ‘ wal-Qadr wat-Ta‘lîl, kishachapishwa.

164. Fairuz Âbâdi (729-817): Ar-Radd ‗aLaa al-Mu‘tarid ‗aLaa Ibn ‗Arabi, ms