9
12/8/2013 www.mbuke.blogspot.com | www.facebook.com/mbuketimes MBUKE TIMES TAFAKARI ZETU

Tafakari mbuketimes

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Maalum kwa fans wangu wa MBUKE TIMES. www.facebook.com/mbuketimes

Citation preview

Page 1: Tafakari mbuketimes

12/8/2013

www.mbuke.blogspot.com | www.facebook.com/mbuketimes

MBUKE TIMES TAFAKARI ZETU

Page 2: Tafakari mbuketimes

Tafakari zetu 2013

Tafakari yetu leo:

Inawezekana Suluhu ipo karibu sana ila tatizo wewe unafikiria upande mmoja tuu!

--Jifunze toka ktk hadithi hii fupi: Mmama mmoja aliyekuwa akioga alitoka mkuku

bafuni baada ya kusikia sauti ya picha ya X, toka chumbani kwa watoto wake. Kufika

kweli watoto wake wenye umri wa miaka 6-10 walikuwa wakiangalia picha. Yeye

kwa haraka akatoa khanga aliyokuwa amejifunga na kuifunika TV, yeye akabaki

mtupu huku akiwakemea watoto. Mara baba naye aliyekuwa anajiandaa kuvaa

chumbani akakurupuka akiwa kajifunga taulo tuu, kufika chumbani kwa watoto

akaanza kumkaripia mkewe kuwa si vizuri kukaa mtupu mbele ya watoto hivyo

akavua taulo na kumfunika mkewe, huku akimlaumu.

--Ndio hivyo kuna nyakati waweza kujikuta unadhani suluhu ni moja tuu, kumbe

ukifikiria zaidi waweza pata njia nyingi ya kupata suluhu ya magumu unayokumbana

nayo. Fikiri kabla ya kufanya maamuzi hususani maamuzi mazito kama

Mapenzi,Fedha,ajira, malezi ya watoto n.k

Tafakari Yetu leo:

Umekwisha sikia mara nyingi watu wakisema " Aaah mtu ukishamfahamu, hakupi

shida".

-- Leo nakutaka utumie msemo huo kwako mwenyewe yaani jiambie "

Nikishajifahamu sintojipa shida".

Kisha anza juhudi za kujifahamu kweli kweli, fanya bidii kukumbuka kwa kila wakati

na tukio husika jinsi kujifahamu kwako kunavyoweza kusaidia au kutokukusaidia

katika kutimiza majukumu yako ya msingi. Mfano:

Unajifahamu vipi kuhusu matumizi ya fedha ?-basi ukiwa na mshahara au pato lolote

kuwa makini

Unajifahamu vipi kuhusu mapenzi -wivu na kujali? -basi kuwa makini

Unajifahamu vipi kuhusu kujifunza mambo mapya ? -Badilisha hali isiyokusaidia

kama vile kutokupenda kusoma.

--Usijipe shida, JIFAHAMU, chukua hatua kurekebisha yasiyokusaidia.

Tafakari yetu leo:

Ukiwa darasani haileti maana kunyoosha mkono ili kujibu swali wakati haujui jibu.

Mwalimu akikuchagua ukasimama na kusema haujui jibu, ni kujidhalilisha.

Iweje leo unatafuta kazi wakati hauna ujuzi ulichosomea zaidi ya cheti tuu?

Iweje unatafuta schorlaship wakati matokeo yao shule iliyopita ni ya kuunga unga,

hata lugha mama ya elimu-english inakupiga chenga.

Epuka mawazo ya kila kitu utaweza kwa kuunga unga. Jiwezeshe kuwa bora ktk

mambo ya msingi.

Page 3: Tafakari mbuketimes

Tafakari zetu 2013

Tafakari yetu leo:

Wanasema wanawake TISA hawawezi kushirikiana kubeba ujauzito ili kujifungua

mtoto ndani ya MWEZI MMOJA.

---Sio kila ushirikiano unaoutafuta utakuletea mafanikio. Ushirikiano mwingine (team

work) waweza rudisha nyuma maendeleo au isilete matarajio kabisa. Jifunze wakati

fulani kufanya mambo wewe mwenyewe kwa ufanisi zaidi.

Tafakari yetu:

Kila kukicha dunia inabadilika, fursa na hatari zinaongezeka. Ni mbaya kama uwezo

wako wa ufahamu haubadiliki. Mfano ajira haitegemei tena aina gani ya elimu

uliyonayo bali uwezo na utayari wako wa kufanya kazi fulani. Lugha za kigeni na

kompyuta hazihitajiki tena kuwa tuu kwenye cheti chako bali ni nyenzo haswa za

'kukutoa'.

--Huu si muda wa kungoja kutafutwa, bali wewe mwenyewe chukua hatua ya

kujiweka mbele ili uonekane.

--Kila mtu sasa ni mzalishaji au mteja wako mtarajiwa, angalia unavyoonekana

mbele ya wazalishaji wenzako na wateja wako watarajiwa. Muonekano wako na

ufahamu wako utatumika kukuhukumu ktk kukupatia 'dili' na kufungua njia ya

mafanikio yako.

Tafakari yetu ni kuwa:

Hauhitaji kujirusha toka ghorofa ya 20 kujua kama unaweza kufa kwa kufanya hivyo.

---Hivyo usiwe mgumu kuchukua tahadhali kuhusu ukimwi kwakuwa bado

haujakukuta.

Tafakari yetu leo:

Fanya likupasalo kwa nguvu zako zote na maarifa yako yote bila kuhofu ni kwa

kiwango gani ufanyacho kitaonekana BORA, kwani ubora wa jambo hautegemei tuu

ufanyacho- mara nyingi hutegemea tafsiri za watu, muda uliopo, vitu vingine

vilivyopo, taarifa ambazo watu wanazo, na zaidi sana uwepo wa watu wengine

wafanyao kitu kama chako.

--Inasikitisha watu hawajadili ubora wa kitu au mtu kwa kuangalia kitu au mtu

mwenyewe bali mambo mengi kama hayo ndio maana leo simu za mche wa sabuni

si mali tena, Messi ni bora zaidi ya Ronaldo, na hatari hata kwa wapenzi

wanafananishwa na waliopita au watu tuu wengine huko mitaani. Hata MBUKE

TIMES ni mbaya, ukilinganisha na blog nyingine uifikiriayo ni bora!

Page 4: Tafakari mbuketimes

Tafakari zetu 2013

Tafakari yetu leo ni:

Ukiota ndoto nzuri unatamani iwe kweli, na hautamani iwe kweli -usingizini, bali

unatamani iwe kweli katika maisha yako halisi-wakati umekwisha amka.

---Ndivyo ilivyo, kama unawaza na kutamani mambo mazuri katika maisha yako -

acha kuendelea kulala kijuhudi, kimawazo, kimbinu, na kimazingira. Mambo

yanabadilika kila siku, amka sasa uanze kutekeleza unayotamani.

Maneno matupu, mipango mitupu bila utekelezaji ni sawa na kuendelea kulala ukiota

ndoto nzuri ambayo haikusaidii chochote huko usingizini hata kama ndoto hiyo

inasema umekwa bilionea namba 1 dunia nzima.

Tafakari yetu leo ni :

Usikubali Teknolojia ichukue nafasi ya ubinadamu wako kwa kujiaminisha kuwa

unaweza kuishi maisha ya namna mbili-moja ya hapa mtandaoni (FB) kwa lugha

mbovu, ukajipa majina yasiyo yako, na kuandika "utakavyo" na nyingine eti wewe ni

mtu mstaarabu na mwenye muelekeo wa maisha , mtu wa kutegemewa.

--Labda tuu uwe na mkakati madhubuti katika kufanya hivyo, ila kujipa maisha

yasiyo yako hapa mtandaoni kuna madhara mengi kwako kuliko faida zake.

Unachoandika(kusema) ndicho kilichomo akilini mwako, na kilichomo akilini ndicho

kinachokufanya uwe hivyo ulivyo, na ndivyo watu watakavyokuelewa.

Tafakari yetu leo:

Kigumu zaidi katika kujiletea mabadiliko sio ugumu wa kutenda unayopaswa kufanya

ili kuleta mabadiliko bali ni Ugumu wa wewe kukubali kuwa mabadiliko

yanawezekana, na kwamba wewe unaweza kubadilika.

--Busara inaanza na kuweza kuji-amrisha kufanya tofauti na

uliyokwishazoea,kuishinda hofu,na kufuta mengi uliyokwisha jifunza. JISHINDE

WEWE MWENYEWE.

Tafakari Yetu leo:

Ukiacha familia gani umezaliwa, au nchi gani umezaliwa na uwepo wa bahati hapa

na pale, chunguza kwa makini utagundua kushindwa kwako katika mambo mengi ni

kwa sababu yako wewe mwenyewe !

--Hata hivyo una haki ya kushinda, unaweza kubadilika sasa na kuishi maisha ya

ushindi. Fikiria kwa mapana, anza hata ikibidi kidogo kidogo kujiletea mabadiliko.

Page 5: Tafakari mbuketimes

Tafakari zetu 2013

Tafakari yetu leo:

MAMBO YASIPOENDA SAWA LEO,KUMBUKA IPO KESHO PIA!

Kuna utofauti mkubwa kati ya KUTUMAINI na KUTARAJIA kufanyika kwa jambo

fulani.

1. Kutumaini kunakuruhusu kufikiria njia mbadala na kuwa na subira bali kutarajia ni

kuwa na mtazamo wa aina moja na kutojiandaa au kutokuwa tayari kuchagua au

kutafakari njia mbadala.

2.Kutumaini mara nyingi hakuleti maumivu makali kulinganisha na KUTARAJIA

hususani pale mambo yanapoenda sivyo ndivyo. Mfano UNATUMAINI mtu atafanya

kitu fulani ukimpatia kitu fulani, asipofanya sio shida sana, kuliko UKITARAJIA kabisa

kuwa atafanya halafu asifanye,utabaki UNAHUZUNIKA.

Tafakari yetu leo:

Ingawa bahati ipo na pia tunafanya maombi lakini kumbuka maandalizi na juhudi ya

kile unachotamani ni ya msingi, na pengine maandalizi na juhudi zako zinaweza

kuwa SUMAKU ya BAHATI.

--Chukulia mfano una kiingereza cha "kuokoteza" halafu unapata ufadhili wa kusoma

UINGEREZA, ila kwanza unatakiwa ufanye interview ya ana kwa ana masaa mawili

na timu ya wafadhili wako ! Utajikuta hivi hivi unaiacha bahati !

Tafakari yetu leo:

Kumbuka ili kufanikiwa sio lazima ufanye kitu KIKUBWA au kwa USTADI mkubwa

sana bali la msingi ni kufanya toka moyoni na kwa juhudi ya kiwango chako cha juu

kabisa.

--Biashara nyingi kubwa hazikuanza zikiwa kubwa, kuna makosa mengi mengi

yalifanyika kabla ndege ya kwanza haijaanza kuruka hewani, kuna hasara nyingi

katika ugunduzi mbalimbali kama baruti (niliandika hapa MBUKE TIMES) hata hivyo

uduni wa mwanzo wa hayo ni historia tuu, hakuna anayetilia maanani.

-Au basi embu jikumbushe SIMU za mkononi zilipotoka,enzi za "mche wa

sabuni"mpaka Iphone.

--Anza sasa kujishughulisha kwa ajili ya ndoto yako.

Tafakari yetu:

Mambo yafuatayo yanaweza onekana kama msaada katika kuleta furaha kwetu, hata

hivyo kwa baadhi imekuwa kinyume,yanaongeza GHARAMA ya kuwa na FURAHA:

1. Utajiri

2. Marafiki wenye mafanikio

3. Mpenzi /Mke Mzuri

4. Ajira

5.Watoto

--Zaidi ya kutafuta vitu tunavyodhani vitatupatia furaha tutumie muda pia kuboresha

Page 6: Tafakari mbuketimes

Tafakari zetu 2013

UFAHAMU wetu, tujitambue na tufanye akili zetu ziwe huru. Na zaidi sana TUMCHE

MUNGU.

Tafakari yetu leo:

Watoto wanapoanza kujifunza kusoma huanza na A E I O U. Hata hesabu huanzia

kuhesabu 1, 2, n.k. Hata hivyo leo hii wewe uliyeanza na A E I O U, unachat

FB,kama vile sio yule ambaye A E I O U zilikuwa zinamsumbua !

--Mambo mazuri na makubwa huanza kidogo kidogo

-Tukumbushane kaugonjwa ka kushindwa kuchukua hatua ya kuanza jambo la

msingi! Hatua shuleni, makazini, katika mahusiano, biashara , n.k.

--Kama hamasa umeshapata sana, kama masomo na mbinu hizo ulizonazo unaweza

anza nazo kufanya jambo la msingi. Hata hivyo wengi tunasubiri mpaka tuwe na

uwezo wa kufanya "jambo kubwa".

Usingoje "uwezo mkubwa", anza kidogo kidogo, uzoefu utakaoupata na makosa

utakayofanya yatakusaidia kujiweka vema hapo baadae.

Tafakari yetu leo ni:

"Usiogope kihivyo kuwa dunia itaisha leo hii Jumatano, kumbuka kuna nchi nyingine

Jumatano yako kwao bado ni Jumanne, au ndio Alhamis yao "

--- La msingi katika tafakari hii ni kuwa ingawa woga ni muhimu wakati fulani, ila

angalia pia na vitu vya kuogopa! Vitu vingine unaogopa ni kwakuwa tuu hauna

taarifa sahihi !

Tafakari yetu leo:

Kirahisi rahisi huwa tunawaambia wengine tunawapenda na tupo tayari kufanya

lolote kwa ajili yao.

Tugeuze kibao sasa…

Inaweza kuonekana kama jambo rahisi rahisi hivi, ila embu fikiria WEWE

UNAJIPENDA KWELI KWELI .

1. Je ni kwa kiwango gani unajali afya yako: Ili uweze kuwepo kwa miaka mingi zaidi

2. Je ni kwa kiwango gani una juhudi ya kutafuta mambo ya kuboresha ufahamu

wako, kupata busara zaidi ili uongeze nafasi za kuwa na furaha ( Kwa kuwa FURAHA

kwa kiwango kikubwa ni vile tunavyochukulia mambo –kifikra zetu na fikra zetu

zinaboreshwa au kudhoofishwa na kiwango cha ufahamu, uzoefu na makuzi yetu)

3. Je ni kwa kiwango gani una juhudi katika kufanya bidii ya kazi ya kukupatia kipato

, au una zuga zuga tuu ugange njaa

4. Je ni kwa kiwango gani unafanya mazingira uliyopo yawe masafi na salama ili

wewe ubaki kuwa salama

5. Je ni kwa kiwango gani unawajali wengine ili nao waweze kukujali wewe

--Kujipenda kazi , ni zaidi ya kula bata !

Page 7: Tafakari mbuketimes

Tafakari zetu 2013

Tafakari yetu leo:

Wewe ndie unayejifahamu zaidi kuliko mtu mwingine yeyote yule. Kumbuka hili hasa

unapohisi kukatishwa tamaa na maneno ya wengine.

Hao wanasema maoni yao, kutokana na waliyokumbana nayo, au waliyosikia,

waliyoyaona n.k, hata hivyo wewe ni wa pekee, mazingira yako, uliyopitia, bahati

yako, na pengine hawajajua uwezo wako halisi upo vipi.

Na hata kama wapo sahihi, bado ukweli ni kuwa unayo nafasi ya kubadilika, na

kuwaonyesha HAWAPO SAHIHI !

Wewe una nguvu sana,kuliko ulivyodhani, itumie nguvu yako.

--Siku njema fans.

Tafakari Yetu leo:

Jiulize kwanini wewe unadhani HAUWEZI kufanya mambo makubwa ya kijamii na

kimaendeleo ? Sio lazima kuwa maarufu ila kufanya jambo lenye kugusa na

kuboresha maisha ? Je ni kwa sababu :-

1. Hauna MTAJI wa kutosha: DELL ilianzishwa kwa mtaji mdogo sana kama dola

1000 tuu !

2: Wewe sio Maarufu : Mark Zuckerberg alianzisha FB akiwa chuoni wala hajawa

maarufu kama sasa.

3: Miundo Mbinu mibovu: Kuna mwafrika mwenzetu yupo Angola ambapo

katengeneza printer kwa kutumia takataka za vifaa vya kielectroniki

4: Hauishi Ulaya: Mwanamke wa kwanza mwana mahesabu (Hypatria) alikuwa

Mwafrika na aliishi Afrika.

5: Hauna elimu ya kutosha kama digrii au Masters: Bill Gates hakuwa hata na

degree alipoanzisha kampuni ya kutengeneza software ya Microsoft.

---Kumbuka la msingi sio nini kimekutokea katika maisha yako, bali ni kwa namna

gani wewe unayachukulia hayo yaliyokutokea. Dunia ni kama kisima kuna kila fursa,

ni wewe tuu jinsi ya kuchota. Je unashindaje mazingira au umekubali mazingira

yakushinde?

Tafakari yetu leo:

Kama una jambo la msingi la kufanya usiache kulifanya kwa kuogopa UTAKOSEA.

Utakosea tuu katika maisha yako, na hata usipofanya hilo unalotaka kufanya vado

watu watatafuta na kuweka wazi makosa (mapungufu) yako mengine.

Makosa yapo kila siku, utastaajabu kujua kuwa kwa wengine hata wewe kuwa hai au

kuwa hivyo na hapo ulipo wanaona ni kosa kubwa. Wanatamani ingekuwa

vinginevyo kabisa.

Page 8: Tafakari mbuketimes

Tafakari zetu 2013

Tafakari yetu leo:

Wala usishangae mtu aliyekuwa tajiri kwa miaka 20, leo hii akafirisika na kuwa

maskini, wakati yule maskini mlalahoi aliyehangaika na kuishi katika ufukara kwa

miaka 30 leo hii akawa tajiri.

Maisha ni safari , maisha ni muda, thamini na mpe heshima yake kila mtu.

Tafakari Yetu Leo:

Ni kweli kuwa tunahitaji watu wa aina tofauti na fani tofauti, hata hivyo SIO LAZIMA

wewe ndio uwe wa kufanya kazi zisizolipa au usiyoipenda. Uchaguzi na Nguvu ni

Yako Kubadilika.

Tafakari Yetu Leo:

Fanya bidii katika mambo ya msingi kwa maisha yako, lakini usiache pia kuwa na

SUBIRA. Kwani kuna wakati, hata juhudi za kipekee haziwezi kuleta utakacho, bali

inakupasa usubiri wakati muafaka.

Tafakari Yetu Leo:

Unahisi Umekosea jambo, au Unaogopa Kujaribu utakosea? Msikie Eistein:-

Anyone who has never made a mistake has never tried anything new.- Eistein.

“Yeyote ambaye hajawahi kukosea basi hajawahi kujaribu jambo”

Fans, ijumaa njema na wikiend njema.

Wakati Tajiri anapomdhulumu maskini inaitwa Biashara, ila Masikini anapojaribu

kuzuia asidhulumiwe/anapodai haki yake, huwa inaitwa Kuwa na Vurugu.

Tafakari Yetu Leo:

Eti unaogopa kutia hasara au kukosea mbele za watu ? Wakati hata kuwa kwako hai

ni KOSA au hasara kwa wengine (Wanaokuchukia). La msingi katika maisha fanya

jambo linaloleta tija, usiogope watu, wala kukosea

Tafakari Yetu Leo:

Vitabu vya dini vinasisitiza tuelimike,na haviweki kikomo cha kuelimika. Je,

unajielimisha mara kwa mara? Unaitafuta elimu au unatafuta cheti/vyeti na vyeo tu?

Tafakari Yetu Leo:

MAISHA MAGUMU, SO WHAT ? Tuendelee Kulalamika na Kulaumu Wengine, Au

Tujibidiishe Katika Kufanya Kazi na Kupata Ufahamu wa Kutukomboa na Hali Hii ?.

Page 9: Tafakari mbuketimes

Tafakari zetu 2013

Tafakari Yetu Leo:

Ukitaka kukumbuka jambo vema, lielewe kwa ufasaha.

Ukitaka kuelewa kwa ufasaha, sikiliza au soma kwa umakini.

Ukitaka kuwa na umakini, jenga hamasa katika jambo husika.