43
VITABU VYA KISWAHILI African Books Collective Katalogi ya 2021

African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

  • Upload
    others

  • View
    34

  • Download
    19

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

VITABU VYA KISWAHILI African Books Collective

Katalogi ya 2021

Page 2: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

African Books Collective LtdPO Box 721, Oxford OX1 9EN, UK

[email protected]

Karibu ABC na karibu upitie katalogi ya Vitabu vya Kiswahili kutoka kwa wachapishaji wa vitabu kutoka Afrika ya Mashariki, na mmoja kutoka Afrika ya Kusini, jambo la kushangaza na kuvutia. Kiswahili kinaenea kote Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Katalogi hii isikudanganye ukafikri kuwa hivi ndivyo vitabu pekee vya Kiswahili kutoka kwa wachapishaji wa Afrika. Orodha hii ni ya vile vitabu visivyo vya shule vilivyochaguliwa kwa kuwa vinawafaa wasomaji nje ya Afrika Mashariki (wanafunzi wa lugha ya Kiswahili na waafrika wanaozungumza Kiswahili walio katika diaspora). Lakini hata kwa kigezo hicho vipo vitabu vya Kiswahili vingi zaidi ambavyo havikuletwa ABC na wachapishaji kwa sababu mbalimbali; hivyo vinapatikana kwa kupitia tovuti za wachapishaji mmoja mmoja.

ABC imedhamiria kuwahudumia wateja wanaohitaji vitabu vya Kiswahili. Tunakaribisha maoni na ushauri ili tuweze kukidhi matarajio yenu. Lengo lake ni ABC kuwa kituo kimoja katika nchi za Kaskazini chenye kukidhi mahitaji ya vitabu kutoka barani Afrika vilivyoachapishwa katika lugha za asili.

Mimi, mwandishi wa utangulizi huu ni mmoja wa wachapishaji waanzilishi wa ABC na Mwenyekiti wake kwa zaidi ya miaka kumi na tano tangu kuanzishwa kwake hadi mwaka 2016. Nakushauri utakapo kitabu cha ABC ukiagize moja kwa moja kutoka kwao kwa sababu kwa njia hiyo ABC inapata faida zaidi na hatimaye faida hiyo inakwenda kwa wachapishaji Afrika na kwa waandishi wao.

Nakutakia usomaji mwema wa vitabu vya Kiswahili.

Walter BgoyaMkuki na Nyota Publishers

Page 3: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

Wachapishaji Wanaoshiriki 1

Vitabu vya watoto 1

Vitabu vilivyoshinda na Kupewa Tuzo ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika 8

Shaaban Robert 50

Tafasiri za riwaya 53

Riwaya 53

Ushairi 25

Tamthiliya 29

Vitabu vya Lugha 31

Historia 33

Wasifu 36

Siasa 39

Page 4: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

BOTSWANALightbooks Publishers, Gaborone

CAMEROONLangaa Research and Publishing Common

Initiative Group, BamendaSpears Media Press, BamendaMuntu Institute Press. Yaounde

ETHIOPIAForum for Social Studies, Addis AbabaOrganisation for Social Science Research in

Eastern and Southern Africa (OSSREA)Shama Books, Addis Ababa

THE GAMBIAEducational Services, Serekunda

GHANAAfram Publications (Ghana) Ltd, AccraAmanza, AccraEducatioanal Logistics, AccraFreedom Publications, AccraGhana Universities Press, AccraSmartline Limted, AccraSub-Saharan Publishers, AccraUnited Nations University Institute for

Natural Resources, AccraWoeli Publishing Services, Accra

KENYABookmark Africa, NairobiEast African Educational Publishers, NairobiFocus Publications, NairobiUniversity of Nairobi Press, NairobiLawAfrica, NairobiLonghorn Publishers, NairobiMau Mau Research Centre (MMRC), NairobiMarimba Publications, NairobiMdahalo Bridging Divides, NairobiMystery Publishers, Nakuru Syokimau Cultural Centre, NairobiTwaweza Communications, NairobiVita Books, NairobiZand Graphics, NairobiZapf Chancery Publications Africa, Limuru

LIBERIACotton Tree Press, Monrovia

MALAWIKachere Series, ZombaLogos – Open Culture, LilongweLivingstonia Press, MzuzuLuviri Press, MzuzuMzuni Press, Mzuzu

MAURITIUSUniversity of Mauritius Press, Réduit

MOROCCOEditions du Sirocco, CasablancaSenso Unico Editions, Mohammedia

MOZAMBIQUEEditora Trinta Zero Nove,

NAMIBIAThe Basler Afrika BibliographienUniversity of Namibia Press, Windhoek

NIGERIAAfrican Heritage Press, LagosAlpha Crownes Publishing, LagosThe Book Company Ltd., LagosBookbuilders: Editions Africa, IbadanCSS Ltd, LagosFourth Dimension Publishing Co. Ltd., EnuguFrontPage Media, LagosHandel Books, Eastern NigeriaHEBN (Nigeria) plc, IbadanIbadan University Press, IbadanKraft Publications, Lagos

Kwara State University Press, MaleteMaiyati Chambers, LagosMalthouse Press Ltd., LagosM & J Grand Orbit Communications, Port

HarcourtOnyoma Research Publications, Port

HarcourtReamsworth Publishing, IbadanSafari Books, IbadanSaros International Publishers, Port HarcourtSCRIBIO Publications, IbadanSpectrum Books Ltd., IbadanUniversity of Lagos Press, LagosUniversity Press Ltd., IbadanUrhobo Historical Society, New York & Lagos

SENEGALCouncil for the Development of Social

Science Research in Africa (CODESRIA), Dakar

SOMALILANDPonte Invisible (Redsea Cultural Foundation),

Hargeisa

SOUTH AFRICAAfrican Minds Publishers, Cape TownAfrican Perspectives, JohannesburgThe African Public Policy and Research

Institute, PretoriaAfro-Middle East Centre, JohannesburgAgency for Social Reconstruction,

JohannesburgBhiyoza Publishers, EnnerdaleBotsotso Publishing, BraamfonteinCover2Cover Books, MuizenbergCrane River, Cape TownDeep South, MakhandaDryad Press, Cape Townimpepho press, TshwaneHands-On Books, Cape TownInstitute for Preservation and Development,

PretoriaMaThoko’s Books, JohannesburgModjaji Books, Cape TownThe Mapungubwe Institute for Strategic

Reflection (MISTRA), JohannesburgMvusi Books, MakhandaNatal Society Foundation TrustNISC (Pty) Ltd, GrahamstownSouthern African Migration Program, Cape

TownUmsinsi Press, Cape TownuHanga Poetry Press, Cape Town

TANZANIADar es Salaam University PressE & D Ltd., Dar es SalaamMkuki na Nyota Publishers,

Dar es SalaamTanzania Educational Publishers, BukobaTanzania Publishing House,

Dar es Salaam

UGANDAAsante Capital Hub, KampalaFountain Publishers Ltd., KampalaFEMRITE (Uganda Women Writers’

Association), KampalaPelican Publishers, KampalaProgressive Publishing House, KampalaStrategic Initiative for Women in the Horn of

Africa, Kampala

ZAMBIABookworld Publishers, LusakaGadsden Publishers, LusakaImage Publishers, LusakaThe Lembani Trust, Zambia, Lusaka

ZIMBABWEAfrica Talent Publishers, Masvingoamabooks, BulawayoAmagugu Publishers, BulawayoBooklove Publishers, GweruGALZ, HarareMambo Press, GweruMwanaka Media and Publishing Pvt Ltd,

ChitungwizaWeaver Press Ltd, HarareZimbabwe Publishing House, Harare

African Books Collective Participating Publishers

Page 5: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

1

www.africanb

ookscollective.c

om

Vitabu vya watoto

��������������������������������������Antoine de Saint-ExuperyMfasiri: Philipp Kruse na Walter Bgoya

������������������������������������������������������ ���������������� ���������������������������������������������������������������������� �������������� ����������������������������������������������������������������������������������� ���� ���������������������������­������������������������������ ������������� ������������� ��­����������������� ������������ ������������

Mwandishi, Antoine de Saint-Exupery, alitumia uzoefu wake kama rubani wa ndege katika jangwa la Sahara. Ndege ya msimulizi inaanguka jangwani Sahara ambapo anakutana na Mwana wa Mfalme (Prince) na kumuonyesha michoro yake, kama njia ya kuanzisha mazungumzo. Hadithi hiyo inahamia kwenye Sayari (Asteroid) ya Mwana Mdogo wa Mfalme, na kutoka huko hutembelea Asteroid zingine na kila moja inakaliwa na mtu mzima mjinga, na mwishowe anatembelea Dunia. Kupitia mazungumzo, uchunguzi wa jumla ya binadamu, wanyama na ulimwengu wa mazingira ya asili, hekima isiyo na kifani inajitokeza: mtu akutanaye na kijana wa ajabu na kujifunza upya maana ya kuwa mtoto; na mvulana mdogo anayejifunza maajabu na kejeli za maisha wakati wa safari ndefu mbinguni. Pamoja na vielelezo vizuri asilia, kito kisicho na wakati kinafungua mlango kwa watu wa kila kizazi kupata ufahamu mpya na wa kina wa falsafa ya maisha.

105 pages | 203 × 133 mm | 2010 | vielelelezovya rangiPublisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaPaperback: 9789987080359 $20/£12/€14

Vitabu vya watoto

Page 6: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

2

www.africanb

ookscollective.c

omVitabu vya watoto

��������� ������������� Bazille Masayo

������������������ �­����������������� ���������������������������������������������������������������

Kitabu cha kuhesabu cha kupendeza cha watoto wadogo, chenye vielelezo vizuri vya rangi. Ni mchezo wa maandishi na muziki kwa Kiswahili na Kiingereza, uliobuniwa kwa ustadi kuzingatia mawazo ya vijana. Kila nambari imepewa sura, ikiwa na ukurasa uliokunjwa ili kuonyesha jinsi ya kutengeneza nambari kwa kutumia mwili wako. Kina CD pia.

45 pages | 229 × 152 mm | 2011 | vielelezo vya rangiPublisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaPaperback: 9789987081158 $22/£17/€20

Page 7: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

3

www.africanb

ookscollective.c

om

Vitabu vya watoto

������ �������Chisato Kubo na Ito Hayato

��������������������­���������� ���­�� ������������������������������ ��� ��������� �����

Kama mtoto angekuwa ndege, angeweza kuruka juu na kunyunyiza kila kitu rangi nzuri, kujengea ndege wengi viota, kubeba rafiki kwenye mabawa yake na kusafiri kwenda maeneo ya mbali. Angekuwa mchawi, mtoto angeweza kuponya wagonjwa, kukua haraka, kuwa mzuri na kuvaa vizuri, kubadilisha rangi za wanyama wote; angekuwa Rais, mtoto huyo angejenga nyumba juu ya Mlima Kilimanjaro, kufanya siku zote kuwa sikukuu za umma, kupanua Tanzania na kufanya maktaba zote kuwa huru. Kuna mawazo mengi ya kusisimua na ya kuvutia akili ya mtoto. Waandishi wawili wa Kijapani na wachoraji walifanya kazi na kuishi nchini Tanzania.

32 pages | 140 × 270 mm | 2011 | vielelezo vya rangiPublisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaPaperback: 9789987081196 $22/£17/€20

Page 8: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

4

www.africanb

ookscollective.c

omVitabu vilivyoshinda na Kupewa Tuzo ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika

�������������� ��Mohammed Khelef Ghassani

����������Ali Hilal

Mateso, maumivu na siasa ni mambo yaliyojaa uchochezi mkali unaomsukuma mshairi kuzungumza waziwazi na kinagaubaga na hatimaye kumfanya mwandishi apandwe na jazba zinazofanya kazi fulani itoke nje ya kingo za ulingo wa kisanaa. Katika hali kama hii mshairi lazima atunge wimbo unaoimbika ndani ya nafsi yake mwenyewe kwanza, wimbo utakaomwezesha kunyanyuka kitandani asubuhi huku akijua hayuko pweke, ana wenzake wenye maumivu kama au kuliko yake. Mohammed Khelef Ghassani ana weledi huu wa kubaki ndani ya kingo za ulingo wa kisanaa, weledi wa kuichenga siasa kwa namna ya kuipa nguvu kubwa zinazoficha na kuzimua unagaubaga na hata ukali wake.

104 pages | 229 × 152 mm | 2019Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaPaperback: 9789987083756 $16/£12/€14

Riwaya ya Mmeza Fupa ni riwaya iliyoshinda na kupewa tuzo ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika kwa mwaka 2017. Katika tangazo la ushindi wa riwaya hii jopo la majaji lilitoa sifa zifuatazo: Si mno mtu kukutana na riwaya ya Kiswahili ambayo mwandishi wake amejidhihirisha kuwa ni mbuji wa lugha fasaha na ya kisanii, inayotiririka kitabia kwa hiari yake, na bila ya kuonesha dalili zozote kwamba imelazimishwa. Wahusika wake wote wamebuniwa kwa ustadi, na kupewa kazi muwafaka za kuziwakilisha tanzu na matabaka mbalimbali ya jamii - pamoja na mikinzano na mazingira yao ya kihistoria, ya kisiasa, ya kisaikolojia, ya kitamaduni, ya kimjini au ya kijijini. Licha ya kwamba matukio ya riwaya hii yanatokea katika kisiwa cha kubuni, maswala yanayojadiliwa humu ni miongoni mwa yale maswala sugu yanayoendelea kulisumbua bara la Afrika kisiasa, kijamii na kiuchumi. Riwaya hii inatudhihirishia mandhari mapya ya utanzu huu wa Fasihi ya Kiswahili.

212 pages | 198 × 129 mm | 2019Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaPaperback: 9789987083794 $16/£12/€14

Page 9: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

5

www.africanb

ookscollective.c

om

Vitabu vilivyoshinda na Kupewa Tuzo ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika

���������������Zainab Alwi Baharoon

��������������� ������Dotto Rangimoto

Riwaya ya Mungu Hakopeshwi inaelezea maisha ya familia moja ya Unguja iliyoingia katika mitafaruku na mikasa mingi. Kila kitu huwa na chanzo na khatima; basi ni nini chanzo cha mitafaruku hiyo na khatima yake ilikuwaje? Simulizi ni juu ya baba, Bw. Ahmed, mwenye hasira kali zisizo na mipaka, aliyeongoza familia yake kwa utashi wa nafsi yake, bila kujali hisia za mkewe wala wanawe. Kumbe moyoni mwake alihifadhi siri, na hiyo siri ndiyo iliyomfanya Bw. Ahmed kuwa mkali bila kiasi, ikimsukuma azuie kurejea kwa yale yaliyomfika zamani. Lakini kivuli cha historia ya maisha yake ya nyuma hakikuacha kumuandama. Riwaya hii i meandikwa kwa lugha nzuri na fasaha, kwa ufundi wa msanii makini na mwelewa wa maisha ya jamii za Kizanzibari na za mwambao kwa jumla.

Wakizingatia historia ndefu ya uandishi katika lugha ya Kiswahili, majaji wa Tuzo ya Kiswahili ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika wameeleza: Mashairi yaliyomo katika diwani hii yametumiliwa lugha iliyojaa taswira na majazanda yanayowakilisha vyema hisia zinazoelezwa katika dhamira mbalimbali. Mshairi amefaulu sana kuzitumia mbinu na miundo kadha wa kadha ili kuyajadili masuala yanayohusu hali na mazingira tafauti tafauti katika maisha ya binadamu. Anayazungumza maswala mazito mazito, lakini kwa namna ambayo hayamuelemei msomaji wake. Bali, badala yake, huwa yanamhimiza aendelee kuyasoma. Hata yale masuala makongwe, kwa mfano uhusiano baina ya wazazi na wana wao, yanajadiliwa kwa namna ya kuvutia na kuyafanya kama kwamba ndiyo mwanzo yanaanza kujadiliwa sasa. Dotto Rangimoto ni mtunzi stadi. Na diwani hii ni mchango mkubwa katika ushairi wa Kiswahili wa zama zetu hizi.

254 pages | 198 × 129 mm | 2017Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaPaperback: 9789987753932 $16/£12/€14

94 pages | 198 × 129 mm | 2018Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaPaperback: 9789987083749 $16/£12/€14

Page 10: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

www.africanb

ookscollective.c

omShaaban Robert

6

Shaaban Robert

���������������������������������������

�������������­��������� ���� ������������������������� � ����������������� ����� �����������

Katika kitabu hiki, Shaaban Robert anaelezea maisha ya umaskini na hali ya chini aliyoishi msanii huyu, katika jamii ya Zanzibar iliyokitwa na tabaka za kijamii miaka ya kwanza ya karne ya ishirini. Licha ya kuwa sura yake ati haikuwa nzuri, alifikia hali ya juu ya nyota wa uimbaji wa taarabu akapendwa na wapenda taarabu si Zanzibar tu na Afrika ya Mashariki, lakini pia alipendwa hadi Misri na India. Kwa wapenzi wa taarab bado ni malkia, sawa na alivyokuwa Om Kulthum wa Misri.

Shaaban Robert is to the Swahili language what Shakespeare was to English. Acclaimed as the national poet, his publications have always been the touchstone of beauty of language, purity of spirit, and deep wisdom informed by African and Swahili culture in particular, but imbued with respect for and understanding of other cultures. Most prominent of his work is Kusadikika (To be believed), an allegorical work of an imaginary country or state in which injustices are perpetrated against all notions of justice, law and humanity. Published at the height of colonial occupation in Tanzania.

198 pages | 203 × 133 mm | 2010 Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaPaperback: 9789976973099 $17/£12/€14

Shaaban Robert kwa lugha ya Kiswahili ni sawa na Shakespeare kwa lugha ya Kiingereza. Akikubalika kama mshairi wa taifa, vitabu vyake daima vimekuwa kipimo cha juu cha uhondo wa lugha, usafi wa nia na hekima kutokana na utamaduni hususan wa Kiafrika na wa Waswahili lakini pia kwa jinsi alivyoelewa na kusheshimu tamaduni nyingine. Katika vitabu vyake Kusadikika ndicho maarufu kushinda vyote. Hii ni hadithi ya kiistara juu ya nchi ambako dhulma inatawala kinyume na haki, sheria na utu. Kitabu kilichapishwa wakati ukoloni umetanda nchini Tanzania.

Page 11: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

7

www.africanb

ookscollective.c

om

Shaaban RobertShaaban Robert

 ���������������Shaaban Robert

­����������������Shaaban Robert

­���������Shaaban Robert

Hadithi liyochapishwa kwa mara ya kwanza mnamo 1980, toleo hili jipya linaelezea juu ya malaika na mashetani na viumbe vingine vya kushangaza. Ni gari la uvumbuzi wa maswala katika kitabu hicho ambayo ni juu ya ardhi na mimea yake, madini na thamani yake, mifugo na kilimo, biashara, safari, utajiri na umaskini, matajiri na utajiri wao na uhusiano kati ya ndugu. Tabia ya kusonga ya watu katika harakati tofauti za utajiri na ustawi.

Katika kazi hii muhimu, Shaaban Robert anatoa miongozo kwa waandishi na washairi juu ya ujanibishaji, lakini pia juu ya mahitaji ya mapema ya uandishi mzuri.

Riwaya hii iliyochapishwa kwanza katika kilele cha enzi ya wakoloni, imejikita katika kuangazia baadhi ya mila na desturi zisizoendana na wakati hii ni kazi ya mfano ya nchi ya kufikiria au serikali ambayo dhuluma hufanywa dhidi ya maoni yote ya haki, sheria na ubinadamu. Kutoka kwa bwana wa lugha ya Kiswahili na utamaduni.

51 pages | 203 × 131 mm | 2010Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, Tanzania | Paperback: 9789976102475 $18/£15/€18

88 pages | 206 × 145 mm | 2004Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, Tanzania | Paperback: 9789976973150 $18/£15/€18

60 pages | 206 × 137 mm | 2019 | Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaPaperback: 9789976973068 $18/£15/€18

Page 12: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

www.africanb

ookscollective.c

omShaaban Robert

8

Shaaban Robert

­����������Shaaban Robert

��������������������� ���������������Shaaban Robert

Iliyochapishwa kwanza katika kilele cha kazi ya wakoloni, hii ni kazi ya mfano ya nchi ya kufikiria au serikali ambayo dhuluma hufanywa dhidi ya maoni yote ya haki, sheria na ubinadamu. Kutoka kwa bwana wa lugha ya Kiswahili na utamaduni.

Maisha Yangu Baada ya Miaka Hamsini ni maelezo ya kihistoria na wasifu wa mwandishi. Kinaeleza mambo yaliyomtokea na changamoto mbalimbali alizozipitia katika maisha yake ya kikazi kama muajiriwa wa Serikali na baadae kama muandishi wa mashairi. Anaeleza ubaguzi wa rangi uliokuwa ukiendeshwa na wakoloni, kwa mfano wa safari aliyofanya kwa treni tarehe 13 Julai 1944, wakati akisafiri kutoka Korogwe, Mkoa wa Tanga kuelekea Mpwapwa. Licha ya kwamba alikuwa ofisa wa serikali na alistahili kusafiri katika daraja la kwanza au la pili, alikataliwa na ikabisi asafiri katika daraja la chini.

67 pages | 206 × 137 mm | 1991Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaPaperback: 9789976973105 $18/£15/€18

124 pages | 203 × 147 mm | 2003Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaPaperback: 9789976973167t $18/£15/€18

Page 13: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

9

www.africanb

ookscollective.c

om

Shaaban RobertShaaban Robert

������������Shaaban Robert

�������������������������Shaaban Robert

Mapenzi Bora ni diwani iliyoandikwa na Shaaban Robert mwaka 1958. Diwani hii yenye beti 700, imedhamiria kuiadilisha jamii juu ya maana, faida na hasara za kukosa mapenzi bora. Kimewalenga watu wenye uwezo wa kuwaza na kuhoji neno, kitu au tendo kwa akili ingawa mtu yeyote japo hajafikia upeo wa juu wa kuhoji mambo atafaidika kwa kukisoma.

Siti binti Saad was the first woman Taarab singer in Zanzibar. In this book Shaaban Robert looks at the background of the singer: poverty and low birth, in a society riven by class and race in early 20th century Zanzibar. Despite her so-called bad looks, she became a star whose voice was recognized and loved by many, not only in Zanzibar and East Africa, but as far as Egypt and India. She was and remains to taarab lovers, the equivalent of Egypt’s Om Kulthoum.

69 pages | 208 × 147 mm | 2010Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaPaperback: 9789976973082 $18/£15/€18

124 pages | 203 × 147 mm | 1991Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaPaperback: 9789976973099 $18/£15/€18

Page 14: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

Tafasiri za riwaya

�����������­�������� �� ���������������� ������������������������Mfasiri: Hassan Adam

�������������������������������������������­����� ���������������������������������������������������������� ��������������������������� ��

Hadithi hizi za Alfu Lela U Lela zimetafsiriwa kutoka kwa matoleo ya Kiingereza na Kijerumani. Lugha hizi za Ulaya zilikuwa za kwanza kutafsiri hadithi hizi kutoka Kiajemi, Kiarabu na Kihindi. Tafsiri ya kwanza ya Kiingereza ilifanywa na Sir Richard Burton ambaye anajulikana sana kama mmoja wa wasafiri wa kwanza wa Uropa kutembelea Afrika na “kugundua” maeneo waliyofika. Tafsiri ya kwanza ya Kiswahili ilifanywa mwaka 1928 na katika kufanya hivyo sehemu nyingi zilikatwa au kuachwa makusudi kwa sababu wamisionari hawakutaka wasomaji wa Kiswahili kusoma sehemu kadhaa kwa sababu zao wenyewe. Matoleo haya kwa kifupi, ndiyo yenye na hadithi kamili kwa hakika; yaani, mtiririko na maana halisi ya hadithi jinsi zilivyotungwa na kufasiriwa na mashujaa wa lugha hizo mbili zaidi ya miaka mia moja iliyopita. Kiswahili kimebahatika kupata mtafsiri, Hassan Adam, Mtanzania ambaye anajua lugha zote tatu zinazohusika katika kuandaa tafsiri hizi. Bwana Hassan Adam ni mhadhiri wa muda mrefu katika Taasisi ya Lugha za Kiafrika katika Chuo Kikuu cha Cologne, Ujerumani.

KITABU CHA 1 : 9789987083268 $28/£21/€24232 pages | 203 × 133 mm | 2004

KITABU CHA 2 : 9789987417032 $28/£21/€24194 pages | 203 × 133 mm | 2004

KITABU CHA 3 : 9789987417414 $28/£21/€24226 pages | 203 × 133 mm | 2006

KITABU CHA 4 : 9789987449293 $28/£21/€24202 pages | 203 × 133 mm | 2007

KITABU CHA 5 : 9789987449484 $28/£21/€24172 pages | 203 × 133 mm | 2007

KITABU CHA 6 : 9789987449491 $28/£21/€24184 pages | 203 × 133 mm | 2008

KITABU CHA 7 : 9789987080151 $28/£21/€24160 pages | 203 × 133 mm | 2010

KITABU CHA 8 : 9789987080144 $28/£21/€24196 pages | 203 × 133 mm | 2010

KITABU CHA 9 : 9789987753079 $28/£21/€24162 pages | 203 × 133 mm | 2016

Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, Tanzania

Hassan Adam alikuwa mhadhiri kwa miaka mingi katika Taasisi ya Lugha za Kiafrika katika Chuo Kikuu cha Cologne.

10

www.africanb

ookscollective.c

om

Page 15: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

Tafasiri za riwaya

������������­�������Mariama BaMfasiri: Clement Maganga

�����Naguib MahfouzMfasiri: Deogratius Simba

Ramatoulaye, mwanamke Msenegali ameolewa na Mody, mtu mzito serikalini. Baada ya miaka mingi ya ndoa Modu anaoa mke mwingine, msichana mdogo mwenye umri sawa na wa binti yake. Ramatolaye anasahauliwa; pesa na mapenzi vinahamia kwa mke mdogo. Modu anakufa katika ajali ya gari. Nani atakayerithi mali za marehemu? Halafu kuna umati uliokuja kwenye kilio ambao “lazima ulishwe na upewe pesa kwa heshima ya marehemu”. Mariana Ba, mwandishi wa riwaya hii, alikuwa wa kwanza kupewa tuzo ya Noma mwaka 1980. Riwaya hii imetafsiriwa katika lugha kumi na nane na umaarufu wake unazidi kukua.

Shetani Msalabani, iliyochapishwa kwa mara ya kwanza katika lugha ya Gikuyu kama Caitaani Mutharabaini (1980) na hapa kwa Kiswahili kama Shetani Msalabani, ni onyesho la rushwa na jinsi ilivyojiingiza katika jamii. Sherehe ya ufisadi kwa aina zote, inamlazimisha Wariinga, ambaye kukata tamaa kumemfukuza kutoka Nairobi kurudi katika mji wa llmorog, kukiri kwamba maisha yake hayakuwa zaidi ya kukubali ufisadi wenyewe. Katika riwaya hii, miondoko ya zamani ya kusimulia hadithi za jadi hutumiwa kinyume na mitindo iliyoandikwa.

Ngugi huchochewa na vikosi vya Brecht, Bunyan, Swift na Beckett.

122 pages | 200 × 128 mm | 2009Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaPaperback: 9789976973211 $16/£12/€14

212 pages | 198 × 129 mm | 2019Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaPaperback: 9789987083794 $16/£12/€14

11

www.africanb

ookscollective.c

om

Page 16: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

Tafasiri za riwaya

����������������Ngugi wa Thiong’o

�����������������Ayi Kwei Armah

Shetani Msalabani, iliyochapishwa kwa mara ya kwanza katika lugha ya Gikuyu kama Caitaani Mutharabaini (1980) na hapa kwa Kiswahili kama Shetani Msalabani, ni onyesho la rushwa na jinsi ilivyojiingiza katika jamii. Sherehe ya ufisadi kwa aina zote, inamlazimisha Wariinga, ambaye kukata tamaa kumemfukuza kutoka Nairobi kurudi katika mji wa llmorog, kukiri kwamba maisha yake hayakuwa zaidi ya kukubali ufisadi wenyewe. Katika riwaya hii, miondoko ya zamani ya kusimulia hadithi za jadi hutumiwa kinyume na mitindo iliyoandikwa.

Ngugi huchochewa na vikosi vya Brecht, Bunyan, Swift na Beckett.

Wema hawajazaliwa bado ni riwaya ya mwandishi wa Ghana Ayi Kwei Armah. Ilichapishwa kwa Kiingereza mnamo 1968. Kitabu hiki kinasimulia hadithi ya mtu asiye na jina ambaye anajitahidi kujipatanisha na ukweli wa Ghana baada ya uhuru. Mhusika mkuu ambaye hakutajwa jina, anayejulikana kama “mtu huyo” anafanya kazi katika kituo cha reli na anafikiwa na hongo; anapokataa, mkewe hukasirika na hawezi kujizuia kujiona kama mwenye hatia licha ya kuwa hana hatia. Riwaya inaelezea kuchanganyikiwa kwa raia wengi wa nchi mpya huru barani Afrika baada ya kupata uhuru wa kisiasa. Mataifa mengi ya Kiafrika kama Ghana yalifuata njia kama hizo zilizopelekea ufisadi na uchoyo wa wasomi wa Kiafrika kuongezeka. Rushwa ilichujwa kwa jamii yote na ‘uozo’ ambao ulijulikana baada ya uhuru wa Ghana katika miaka ya mwisho ya Nkrumah ni mada kuu katika kitabu hicho.

278 pages | 203 × 127 mm | 1982Publisher: East African Educational Publishers, KenyaPaperback: 9789966461674 $17/£12/€14

180 pages | 203 × 127 mm | 1969Publisher: East African Educational Publishers, KenyaPaperback: 9789966460721 $17/£12/€14

12

www.africanb

ookscollective.c

om

Page 17: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

13

www.africanb

ookscollective.c

om

Riwaya

������� ����������������� ����

Dogoli, kijana shababi kutoka kwenye ukoo maarufu anachumbiwa mke na shangazi yake. Mchumba ni Kijakazi. Taratibu zote zinafuatwa na sherehe kubwa ya harusi inaandaliwa. Kama ilivyo katika mila na desturi za watu wa Pwani, harusi haikamiliki hadi jambo moja muhimu sana kutendeka. Kwa mila na desturi Kwa mila na desturi hizo, bwana harusi anapaswa kumuingilia mchumba wake kimwili mbele ya somo yake huku wageni wakisubiri kwa hamu na shauku kubwa jibu la tendo hilo. Muda unawadia na Dogoli na Kijakazi wanapewa chumba. Baada ya kuhaha na kuhangaika mule chumbani kwa muda huku jasho likimmiminika kama mchoma mabiwi ya mkaa, ama kutokana na kitete, ama kuwa si riziki, jogoo lake linashidwa kuwika. Dogoli anashidwa kutimiza tendo la ndoa; yaani jogoo linashindwa kupanda mtungi.

Sasa kijana akiwa pale chumbani anatweta kwa marefu na mapana. Baada ya muda auonao kama mwaka mzima, taratibu anachukua nguo zake na kuvaa, mgonjwa, kwa aibu isiyo na kifani. Habari zinatapakaa nje kuwa jogoo la Dogoli haliwiki - si matusi, si nyimbo za kejeli, fujo na umbea huku kila mtu akisema lake; yote yalitanda, “Dogoli si riziki; jogoo lake haliwiki, jongoo halipandi mtungi.” Iliyokuwa iwe furaha kubwa kwake na jamaa zake inageuka kuwa huzuni kubwa.

“Ooh! Chaudele wangu, dume langu shababi, baba yangu kuzimu nimekukosea nini? Nimeumbuka mimi jamani; si bure, kuna mkono wa mtu si bure, kuna mkono wa mtu,”

Mama Dogoli amlilia mwanawe kwa uchungu.

Katika muendelezo wa kisa hiki cha kusikitisha Dogoli anakufa katika mazingira ya kutatanisha na anazikwa kwa kufuata mila zao. Baada ya maziko wanakijiji wanaamua kuwatuma wajumbe wawili kwenda ughaibuni kwa waganga wa jadi kubaini sababu ya kifo cha Dogoli.

138 pages | 203 × 133 mm | 2016Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaPaperback: 9789987082827 $20/£15/€18

Athumani Mauya ni mwalimu mstaafu kutoka Bagamoyo, Tanzania.

Page 18: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

www.africanb

ookscollective.c

omRiwaya

14

Riwaya

�����������������������John Rutayisingwa

������James A. Bwana

����Zefania Kalumuna

Riwaya mbili maarufu za marehemu John Rutayisingwa. Ya kwanza inaasa msomaji dhidi ya tabia mbaya katika mahusiano ya wanaume na wanawake. Ya pili inazungumzia matumizi mabaya ya madaraka; lakini katika kula na kulipa pia kupo.

Riwaya ya kusikitisha na kusisimua; ya maisha ya Bahati, mtoto “asiye na baba; mwenye nuksi”. Katika kutetea utu wake anaua. Soma humu kila aina ya mapambano; ufukara, uonevu, UKIMWI na hatima ingojeayo kugunduliwa.

Hii ni hadithi inayochambua jamii ya mjini kwa kina na kuweka bayana matukio na matatizo mbalimbali ya vijana na jamii nzima. Mhusika mkuu katika hadithi hii, Heri, ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi anayeona vigumu kizingatia masomo kwa vishawishi vya mapenzi na kujikuta amebanwa na mahitaji ya mpenzi wake, Pendo, na ukali wa walimu wake na jinsi anavyojitahidi kujikwamua. Baba yake Heri, anamhamasisha kwa kumwambia kuwa jina lake, Heri, lina maana kubwa: Hangaikia Elimu Raha Inakungoja. Ni Hadithi nzuri inayoonya, kufundisha na kuelimisha.

79 pages | 203 × 127 mm | 2004Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, Tanzania | Paperback: 9789987686131 $19/£17/€20

134 pages | 205 × 147 mm | 2004Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, Tanzania | Paperback: 9789987417087 $23/£15/€18

60 pages | 206 × 137 mm | 2019 | Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaPaperback: 9789976973068 $18/£15/€18

Page 19: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

15

www.africanb

ookscollective.c

om

RiwayaRiwaya

­������ ���John ´Habwe

������� ��������C.G. Mung’ong’o

Kovu Moyoni ni hadithi ya kusisimua inayosimulia matukio katika kijiji cha Siloko katika nchi huru ya Tandika. Inahusu mapambano ya mjane mmoja dhidi ya utawala dhalimu unaolinda na kulifadhili genge la wanamgambo la vijana wanaoshambulia na kupora kijiji cha Siloko kwa kisingizio cha kuondoa watu wasio wenyeji. Serikali ambayo Boke anatarajia imlinde na mali yake inafeli katika jukumu lake la kimsingi na badala yake inalinda kundi lenye uwezo mkubwa la wanyakuzi wa ardhi na mibabe wa kivita.

Gusto, kijana mdogo wa shule, hakurithi mali ya marehemu baba yake tu, bali pia amerithi tunguri zake, madaraka yake ya kiwanga na mlolongo mzima wa visa, visasi na vinyongo vya baba yake. Urithi huu unamtia Gusto katika ulimwengu wa wachawi. Hatimaye, baada ya kupambana na vitimbi, hasara na mikasa ya kutisha, inambidi Gusto akate shauri kati ya kuyatekeleza matakwa ya marehemu baba yake na kuyatimiza matakwa ya dhamiri yake binafsi na ya jumuiya yake inayotafuta maendeleo ya kisasa. Mvutano unaotokea unaukiuka uwezo wake alioupata shuleni, na kutisha kumrarua vipande vipande...Hiki ni kisa cha kutisha na kutaharukisha, kinachotuingiza katika undani wa uganga wa uchawi na mazingaombwe, na hatimaye kutuacha tukijiuliza kama kweli mambo hayo yanayo manufaa yoyote kwa jamii yetu au ni doa na mirathi ya hatari tu katika utamaduni wetu.

166 pages | 178 × 127 mm | 2014Publisher: Bookmark Africa, KenyaPaperback: 9789966055354 $22/£15/€19

86 pages | 203 × 127 mm | 1977Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaPaperback: 9789976102451 $20/£15/€18

Page 20: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

www.africanb

ookscollective.c

omRiwaya

16

Riwaya

����E.A. Musiba

­��������­�����E.A. Musiba

Ni nani hasa anayewaua viongozi wa wapigania uhuru? Kwa nini wengi wa viongozi hawa wameuawa jijini Kinshasa kuliko mahali pengine popote Afrika? Ili kukomesha vitendo hivi vya kijahili, Umoja wa Nchi Huru za Kiafrika (OAU) unakata shauri kuwasaka wauwaji hawa na kuwafagilia mbali. Willy Gamba, mpelelezi maarufu wa Afrika, anachaguliwa kuongoza kikosi cha wapelelezi wa Kiafrika kuwasaka. Kinshasa, jiji linalosifika kwa starehe zake linageuka uwanja wa mapambano kati ya vijana wapiganaji shupavu wakiongozwa na Willy Gamba, na wapinga mapinduzi wakiongozwa na Kaburu Pierre Simonard.Willy pamoja na kikosi chake wanalivamia jiji la Kinshasa kuhakikisha wanakomesha mauaji hayo. Ndipo patashika ambalo halijawahi kutokea barani Afrika linapoanza na kuliwasha moto jiji hili…

Mauaji ya kikatili yanafanyika karibu na mji wa Uitenhage nchini Afrika Kusini siku ya kuwakumbuka wazalendo, waliouawa mjini Sharpeville mwaka 1960. Makaburu wanajawa na hofu kwa mauaji hayo, na wanawatilia shaka kikundi cha watu weusi wanaotaka kupindua mfumo wa Serikali yao ya Ubaguzi wa Rangi. Uongozi wa Makaburu wa Afrika Kusini wakiongozwa na Mkurugenzi wa Shirika la Ujajusi, Kamanda wa Jeshi la Kulfut na Mkuu wa Magaidi, na wasaliti wa UNITA, wanakutana ili kukabili juhudi za ukombozi wa Afrika Kusini kwa wimbi la mauaji. Mkutano wa Wapigania Uhuru wa Afrika Kusini unafanyika Arusha, nchini Tanzania. Mpelelezi nguli wa Afrika, Willy Gamba, hakosi panapokuwa na mapambano kati ya upande wenye haki, upande wa umma na ule wa dhuluma. Kwa kushirikiana na wapelelezi mahiri kutoka nchi za Kusini mwa Afrika kwa kutumia medani za kivita, mateke, ngumi, kung fu achilia mbali bastola, visu na silaha nyingine wanapambana dhidi ya Makaburu hao na vikundi mbalimbali vya kigaidi vilivyoshirikiana nao.

162 pages | 198 × 129 mm | 2018Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaPaperback: 9789987083275 $16/£12/€14

234 pages | 198 × 129 mm | 2019Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaPaperback: 9789987083183 $16/£12/€14

Page 21: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

17

www.africanb

ookscollective.c

om

RiwayaRiwaya

­�������­�����E.A. Musiba

�����E.A. Musiba

Nyaraka za siri zimeibiwa kutoka ofisi moja ya wapigania uhuru jijini Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania inaingiwa na hofu kuwa nyaraka hizo zitaishia mikononi mwa adui na kuhatarisha maisha ya watu wengi wasio na hatia. Kutokana na ishara maalumu inasadikiwa kuwa majasusi hao wamekimbilia jijini Nairobi. Mpelelezi nguli, Willy Gamba, anapewa kazi ya kuwatafuta popote walipo, kwa gharama yoyote na kuwapokonya nyaraka hizo. Kazi hiyo lazima ifanyike haraka kabla hawajaziuza kwa adui. Muda unazidi kwenda na mapambano ya kuwasaka majasusi hao yanazidi kuwa makali na hakuna huruma. Pande zote zinapoteza watu muhimu. Wapelelezi, majasusi na raia wengine wasio na hatia wanauawa. Wakati wote huo Willy Gamba anaendelea na upelelezi wake mgumu na ndipo anapokutana na mrembo Lina. Lakini mrembo huyu yuko upande gani? Na Lulu je? Je, Chifu yupo sahihi anapomwonya Willy Gamba asimwamini mwanamke yeyote mrembo? Willy Gamba na wenzake wanabanwa vilivyo lakini hawana ruhusa ya kushindwa. Maisha ya wengi yanawategemea. Ni mapambano ya kufa na kupona, lakini wanawashindaje maadui wakali kama hawa?

Alipoamua kwenda Kigoma, Joram Kiango alitarajia kupumzika, akiburudishwa na mandhari murua ya Ziwa Tanganyika lakini haikuwa hivyo. Likizo yake ilibadilika ghafla huku maisha yake yakiingia katika utata mkubwa. Katika jitihada za kutatua utata huo, Joram Kiango anakabiliana uso kwa uso na mjumbe wa mauti, mwenye kiu kali cha damu na anayesheheni silaha zote. Mjumbe ambaye yuko tayari kwa lolote; tayari kufa, tayari kuua...

118 pages | 198 × 129 mm | 2017Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaPaperback: 9789987083138 $16/£12/€14

194 pages | 198 × 129 mm | 2018Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaPaperback: 9789987083237 $16/£12/€14

Page 22: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

18

www.africanb

ookscollective.c

omRiwaya

1918

www.africanb

ookscollective.c

om

Riwaya

��������������Ben R. Mtobwa

Alipoamua kwenda Kigoma, Joram Kiango alitarajia kupumzika, akiburudishwa na mandhari murua ya Ziwa Tanganyika lakini haikuwa hivyo. Likizo yake ilibadilika ghafla huku maisha yake yakiingia katika utata mkubwa. Katika jitihada za kutatua utata huo, Joram Kiango anakabiliana uso kwa uso na mjumbe wa mauti, mwenye kiu kali cha damu na anayesheheni silaha zote. Mjumbe ambaye yuko tayari kwa lolote; tayari kufa, tayari kuua...

104 pages | 178 × 127 mm | 1984 | Publisher: East African Educational Publishers, KenyaPaperback: 9789966561541 $15/£12/€10 eBook: 9789966565914 $9.99/£6.99/€7.99

���������������Ben R. Mtobwa

Joram Kiango anajikuta katika mkasa mzito na wa kutisha, na ambao hajawahi kukutana nao maishani alipokurupuka usiku wa manane na kumkuta Mona Lisa akiwa maiti, tundu la risasi likivuja damu kifuani mwake. Mkasa unazidi kuwa mzito pale Mona Lisa, aliyekufa anapotokea, tena katika kila maficho ya Joram Kiango. Kila anapotokea maisha ya watu wengi wasiokuwa na hatia yanaangamia. Mona Lisa ni binadamu wa kweli? Ni jini au ni malaika? Ni miongoni mwa maswali ambayo nusura yamtie wazimu Joram Kiango, jeshi zima na vikosi vyote vya usalama.

194 pages | 178 × 127 mm | 2004 | Publisher: East African Educational Publishers, KenyaPaperback: 9789966259974 $15/£12/€10 eBook: 9789966565907 $9.99/£6.99/€7.99

����������­��������Ben R. Mtobwa

“...Inspekta, najisikia kuua tena...” inadai sauti katika sim ambayo imo mikononi mwa shupavu wa polisi. Hii ikiwa simu ya pili, baada ya ile ya awali ambayo ilifuatwa na kifo cha mwandishi maarufu, inamtia Inspekta hasira kali, nusu ya wazimu. Anafanya yote awezayo kufanya ili amtie mwuaju huyu mikononi mwa sheria...hapatikani...Ndipo anajitokeza Joram Kiango. Mbinu zake za pekee, pamoja na kutokwa jasho jingi, kunamwezesha kugundua mengi amabyo yanaitisha dunia na kuitetemesha nchi nzima. lakini kila hatua anayoipiga katika upelelezi wake inamsongeza karibu zaidi na kinywa cha mauti chenye kiu ya damu yake, kilicho wazi kikimsubiri kwa hamu...

114 pages | 178 × 127 mm | 1984 | Publisher: East African Educational Publishers, KenyaPaperback: 9789966469533 $15/£12/€10 eBook: 9789966565976 $9.99/£6.99/€7.99

� ���� ���������Ben R. Mtobwa

Tanzania iliingia katika uchaguzi mkuu ulioshirikisha vyama vingi kwa mara ya kwanza mwaka wa 1995. Yako mengi yaliyokuwa yakiendelea ‘Nyuma ya Mapazia’. Mengi ya kutisha na kuogofya, na ambayo yaliambatana na matumizi makubwa ya pesa, mauaji ya kikatili na ujambazi usio na kifani. Joram Kiango, Inspekta Kombora na kikosi kizima cha polisi wanagonga mwamba katika harakati zao za kutatua kizungumkuti hicho. Kutokweka kwa King Halfan King na maiti ya mpenziwe kupatikana ikielea ufukweni wa Bahari ya Hindi kunazidisha maswali mengi bila majibu. Hata hivyo, kizungumkuti hiki kitatatuliwa?

104 pages | 178 × 127 mm | 1984 | Publisher: East African Educational Publishers, KenyaPaperback: 9789966561541 $15/£12/€10 eBook: 9789966565914 $9.99/£6.99/€7.99

Page 23: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

19

www.africanb

ookscollective.c

om

Riwayawww.africanb

ookscollective.c

omRiwaya

������������������Ben R. Mtobwa

Hii ni riwaya nzito ya kihistoria. Mwandishi anaivulia jamii miwani na kuitazama kwa makini bila uoga, huku akimulika unafiki na ukatili uliofichika katika mioyo ya wengi. Hata anakutana na huyu ambaye anaambiwa: “Umemuua mwanao ... Lazima umle ... ” Ni riwaya ambayo itakutoa machozi!

162 pages | 178 × 127 mm | 1993 | Publisher: East African Educational Publishers, KenyaPaperback: 9789966561572 $15/£12/€10 eBook: 9789966565969 $9.99/£6.99/€7.99

�������­������­�����Ben R. Mtobwa

Kifo kaja duniani. Akikuchekea umekwisha … Akikusalimu umekwisha … Hana mzaha …Lakini yeye anataka watu wakubwa zaidi. Anataka kuifanya Afrika nzima iangue kilio na maombolezo amabayo hayajapata kutokea duniani. Na anataka hilo litokee siku moja, saa moja… “Bendera zote duniani zipepee nusu mlingoti,” anasema akichekelea. “Sijawahi kushindwa …” Jasho linawatoka watu mashuhuri: Damu inamwagika kama mchezo. Inspekta kombaro machozi yanamtoka. Joram Kiango kaduwaa.

194 pages | 178 × 127 mm | 2004 | Publisher: East African Educational Publishers, KenyaPaperback: 9789966469298 $15/£12/€10 eBook: 9789966565952 $9.99/£6.99/€7.99

���������������������Ben R. Mtobwa

Hata hivyo haikupatikana kutokea tishio zito la kutisha kama hili, ambalo linakaribia kutokea. Tukio la kutatanisha ambalo linawatoa machozi wananchi wa nchi mbalimbali. Wanajitokeza mashujaa kwenda Afrika Kusini, lakini kila aendaye huko hurudi na roho yake. Inspekta Kombora anawathamini mashujaa wengi lakini anamtambua shujaa mmoja; Joram Kiango. Jambo la kusikitisha ni kwamba sasa hivi, Joram ni mtumiaji mzuri ambaye anatembea kutoka jiji hadi jiji akiwa na yule msichana mzuri Nuru. Juhudi za Kombora kumsihi hazifui dafu. Badala yake Joram anafanya maajabu mengine ambayo yanalichafua jina lake hapa nchini na kote duniani. Wakati huo siku ambayo utawala huo umeweka ili kuachia pigo lao la mwisho inazidi kukaribia.

114 pages | 178 × 127 mm | 1984 | Publisher: East African Educational Publishers, KenyaPaperback: 9789966469533 $15/£12/€10 eBook: 9789966565976 $9.99/£6.99/€7.99

������� ��������Ben R. Mtobwa

Idd Amini, kiongozi dhalimu kutoka nchi ya Uganda, alipoiteka sehemu ya nchi ya Tanzania na kuangamiza mamia ya watu wasiokuwa na hatia, serikali ya Tanzania iliamua kumkomesha kabla hajatekeleza maafa zaidi. Iliwatuma vijana wake wakapambane naye ili kusalimisha nchi yao. Sikamona akiwa kijana barubaru aliukubali mwito wa serikali na kuingia vitani kukabiliana na Idd Amin na kikosi chake. Maisha ya Sikamona yalibadilika kabisa baada ya vita hivi. Hata ingawa walifaulu kumkomesha Idd Amin, Sikamona alibaki na makovu mengi yaliyoiharibu sura yake asijione kustahili kuitwa binadamu tena.

104 pages | 178 × 127 mm | 1984 | Publisher: East African Educational Publishers, KenyaPaperback: 9789966561541 $15/£12/€10 eBook: 9789966565914 $9.99/£6.99/€7.9919

Page 24: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

Riwaya

� ������������Nkwazi Nkuzi Mhango

��������������Shafi Adam Shafi

Nyuma Ya Pazia inazungumzia ubadhirifu unaomhusisha rais na mawaziri wake katika nchi ya Mafuriko au Abracadabra. Rais akishirikiana na waziri mkuu walileta kampuni ya kigeni ya kuua wadudu ya Richmen kuwekeza kwenye kuzalisha umeme nchini Mafurikoni; Richmen to invest in power generation in Mafuriko. Kupitia rushwa na ushawishi wa wakubwa hawa Richmen ilipata tenda na kutumika kama mrija wa kuibia mabilioni ya fedha za umma toka Benki Kuu. Wananchi walipogundua jinai hii waliiangusha serikali na kuwaaadhibu watawala wao kwa kuwafunga maisha na wengine kuhukumiwa vifo. Kitabu kinaupiga kijembe tawala fisadi barani Afrika.

Shafi Adam Shafi aliyeandika Kasri ya Mwinyi Fuad na Kuli anainua kiwango na hadhi ya fasihi ya Kiswahili katika riwaya hii Vuta N’ kuvute. Kwanza, kuna ndoa ya Yasmin, mtoto wa kihindi kwa Bwana Raza, mzee sawa na babu yake. Yasmin anafukuzwa na wazee wake kwa kumwacha Raza. Katika upweke wake anasitiriwa na Mwajuma, shoga yake anayeishi ili kustarehe katika dansa, taarab na pegi za vikali. Yasmin anaingizwa uswahilini. Kuna wivu unaopelekea kifo cha Shibab, mume wa pili wa Yasmin. Kuna Denge, Yasmin anampenda lakini hapendeki. Kwa Denge ni mapambano na ukoloni tu na makachero wake. Hii ni Vutu N’ kuvute ambayo sherti yeye na wenzake waishinde.

254 pages | 203 × 127 mm | 2015Publisher: Langaa RPCIG, CameroonPaperback: 9789956792184 $22/£15/€19

277 pages | 203 × 130 mm | 1999Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaPaperback: 9789976973297 $22/£16/€19

20

www.africanb

ookscollective.c

om

Page 25: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

21

www.africanb

ookscollective.c

om

UshairiUshairi

��������� ����������­������������������������Ally Yusufu Mugenzi

Vitimbi vya Mama wa Kambo, Wivu, Radhi za Wazazi, Ra ki Maluuni, Mchumba Kaka na Adui Mama ni hadithi zinazosawiri jamii alimochipukia mwandishi, au kuishi na kufanya kazi akiwa polisi, mwandishi wa habari na mtangazaji wa redio katika nchi za Tanzania, Rwanda, Burundi na Uingereza kwa takriban miaka 40. Kitabu hiki ni matokeo ya maombi ya watu wengi waliomsikiliza akizisimulia katika kipindi cha Hadithi na Muziki cha Redio Rwanda katika miaka ya 1980 na 1990. Hadithi hizi pia zimekuwa zikitumiwa na wakuza mitaala wa Kiswahili nchini Rwanda shuleni na zimewafurahisha wapenzi wengine wa fasihi nje ya shule.

162 pages | 198 × 129 mm | 2020Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaPaperback: 9789987084081 $24/£18/€21

Ally Yusufu Mugenzi kwa jina jingine Ally Kayamba alijiunga na Chuo cha Uandishi wa Habari Tanzania mwaka 1978. Alipohitimu mwaka 1980, aliajiriwa na Shirika la Habari Tanzania - SHIHATA. Mwaka 1983 aliacha kazi SHIHATA akajiunga na Idhaa ya Kiswahili ya Redio Rwanda. Mwanzoni mwa mwaka 1994, aliacha kazi Radio Rwanda alipoajiriwa na Idhaa ya Kiswahili ya BBC-London. Akiwa BBC, alianzisha idhaa ya kukutanisha watu waliotenganishwa na mauaji ya kimbari ya Rwanda. Baadaye ilibadilika na kuwa Idhaa ya Maziwa Makuu. Mwaka 2005 aliteuliwa kuwa mhariri wa idhaa hiyo ambako yuko mpaka sasa.

Page 26: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

Ushairi

������� ������� ��������� ���������������� Juzuu la Pili

�������������� ����­���������­��������������������������������������� ����������������������� ���������������������������������������������������­��������� ������������ ������������������������������������� ��������� ��������������� �������������������� ����������� ���������������������

Belkin alifanya kazi bega kwa bega na Profesa Ebrahim Hussein, mwanazuoni maarufu na mwandishi wa tamthilia na mashairi. Kupitia kwa Hussein, Belkin alivutiwa na utamaduni wa Kiswahili, hususani ushairi. Katika wosia wake, kabla ya kufikwa na mauti, aliacha fungu la fedha ili zitumiwe kushindanisha washairi wa Tanzania, na tuzo itolewe kwa washindi watatu wa kwanza. Belkin alianzisha tuzo hii ili kuuenzi mchango wa rafiki yake, Ebrahim Hussein, katika kuijenga fasihi ya Kiswahili.

Ebrahim Hussein ametoa mchango mkubwa katika utunzi, uchambuzi na falsafa ya fasihi. Vitabu vyake, kwa mfano, Kinjeketile, Mashetani, Wakati Ukuta na Kwenye Ukingo wa Thim vimebeba fikra nzito juu ya migogoro ya kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiutamaduni inayotokana na mabadiliko ya kihistoria nchini Tanzania na barani Afrika kabla na baada ya uhuru.

Mashairi haya yametungwa na washairi mchanganyiko – vijana, watu wazima, wazee, wanawake, wanaume, wafanyakazi, wasomi, wakulima, n.k. Kwa pamoja, mashairi haya yanatusawiria hali ya Tanzania na Afrika katika kipindi hiki, na kubainisha mitazamo anuai ya wananchi wa kawaida kuhusu hali hiyo na kuhusu mustakabali wa nchi yao na bara lao la Afrika. Diwani hii inafaa kusomwa na watu wote wanaojali hali na hatima ya Mwafrika.

105 pages | 203 × 133 mm | 2010 | vielelelezovya rangiPublisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaPaperback: 9789987083268 $24/£18/€21

Page 27: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

23

Ushairi

­���� ���������������������������������������Mhariri: Abdilatif Abdala

����������������������������� ���������� ������������������� ��������������������������������� ��� ����������� ����� �������� ����� �� ������ ������� ��� ������� �������������������������������� �����������������������

Kale ya Pemba ni kale ya Waswahili na mazingira yao. Maandiko machache ya Abdulrahman Saggaf Alawy na AliAbdala El Maawy yameonesha mazingira ya watu wa kale na mawazo yao. Kale hiyo si kale ya kabla ya Fumo Liyongo, bali ni kale ya akina Kamange na Sarahani. Kamange na Sarahani waliingia katika karne ya kumi na tisa na kufariki katika karne ya ishirini. Mashairi yao yalivuma pwani yote ya Afrika Mashariki. Mwandishi Abdulrahman Saggaf Alawy amefanikiwa kukusanya baadhi tu ya maandiko ambayo yote yameandikwa katika mtindo wa kale wenye kujali bahari ya vina, mizani na kibwagizo cha wazo moja. Kamange alipenda sana kutunga mashairi ya kujitoma, ya ushaha, ya utendaji na ukali wa mapenzi ya wanawake. Sarahani alipenda elimu na kusomesha, kuingia katika falsafa na kutoa mawaidha.

Mashairi ya washairi hawa ni changamoto kubwa kwa wasomi wa Kiswahili wa ushairi kwa upeo wa juu sana wa sanaa na umahiri wa lugha.

150 pages | 229 × 152 mm | 2012Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaPaperback: 9789987082827 $24/£18/€21eBook: 9789987081608 $11/£8/€10

Abdilatif Abdalla mhariri wa kitabu hiki ni mwandishi wa Kenya na mwanaharakati wa kisiasa. Alifungwa gerezani kwa kuunga mkono Umoja wa Wananchi wa Kenya, na akiwa kifungoni aliandika mashairi yaliyokusanywa katika kitabu, Sauti ya Dhiki, ambayo baadaye yalipewa Tuzo ya Jomo Kenyatta ya Fasihi. Baada ya kuachiliwa kutoka gerezani mnamo 1972 aliondoka Kenya na kufanya kazi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania na baada ya hapo akafanya kazi kwenye idhaaa ya Kiswahili ya BBC, London. Baadaye aliteuliwa kuwa Mwalimu wa Kiswahili katika Idala ya Mafunzo ya Mashariki na Afrika katika Chuo Kikuu cha London na, hivi karibuni, katika Chuo Kikuu cha Leipzig Ujerumani. Alistaafu mwaka 2011. Mwaka 2018 alipewa Tuzo ya Fonlon-Nichols ya Chama cha Fasihi ya Afrika.

Page 28: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

Ushairi

������� �����������Ali Salim Zakwany

������� �������Charles Mloka

������� ���������� ������Khamis Amani Nyamaume

Kitabu hiki kina tungo za mshairi Ali Salim Zakwany. Tungo zake zimesheheni maarifa na hekima maridhawa kwani zagusa nyanja zote ya maisha ya watu: Maadili, Elimu, Siasa, Dini n.k.

Diwani ya Mloka ni mkusanyiko wa mashairi yanayozungumzia masuala mbalimbali ya kijamii na yanayomwandaa msomaji katika misingi bora kimaisha; kuchochea hamasa na juhudi za kuendeleza Kiswahili; na kuhifadhi mashairi yanayoakisi migogoro mbalimbali ya kisiasa, kijamii na kiuchumi iliyokuwepo wakati wa utawala wa chama kimoja nchini Tanzania. “Hatua hii ya Mloka ni ya kufaa kuigwa...”.

Mkusanyiko wa mashairi ya mmoja kati ya washairi maarufu na waliopendwa, Khamis Amani Nyamaume. Alifahamika kwa uwezo wake wa kutunga mashairi juu ya mada nyingi na tofauti na katika mapana ya aina za mashairi. Kwa sababu hiyo na nyingine Khamis Nyamaume alipendwa na wasomaji wa rika zote. Washairi wenzake walikuwa akina Shaaban Robert, Mathias Mnyampala, Sheikh Kaluta Amri Abedi, Hassan Mbega, Mdanzi Hanasa na Mahmood Hamdouny na wote hawa walithamini sana ushairi wake.

128 pages | 204 × 145 mm | 2004Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, Tanzania | Paperback: 9789987686780 $24/£18/€21

94 pages | 205 × 147 mm | 2002Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, Tanzania | Paperback: 9789987686445 $24/£18/€21

132 pages | 210 × 148 mm | 2004 | Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaPaperback: 9789987686834 $24/£18/€21

Page 29: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

Ushairi

�� Kithaka wa Mberia

������������������Kithaka wa Mberia

Profesa Kithaka wa Mberia anafundisha na kufanya utafiti katika Idara ya Isimu na Lugha, Chuo Kikuu cha Nairobi, Kenya. Mbali na kufundisha na kufanya utafiti, anajishughulisha na uandishi wa mashairi na tamthilia. Tamthilia yake maarufu iitwayo Kifo Kisimani ilikuwa kitabu cha lazima katika mtihani wa kidato cha nne nchini Kenya kuanzia 2006 hadi 2012. Tamthilia yake nyingine iitwayo Natala ilikuwa kitabu cha kutahiniwa katika vyuo vya walimu, pia nchini Kenya, kuanzia 2005 hadi 2016. Mwandishi amewahi kukariri mashairi yake katika maeneo kadhaa ikiwa ni pamoja na Kenya, Tanzania, Iran, Marekani, US Virgin Islands, United Arab Emirates, Upolanzi, Ujerumani na Italia.

Prof. Kithaka wa Mberia anafundisha na kufanya utafiti katika Idara ya Isimu na Lugha, Chuo Kikuu cha Nairobi, Nairobi, Kenya. Amewahi kufundisha Virginia State University, Marekani, kama Fulbright Scholar-in-Residence; University of Warsaw, Upolanzi; na hivi sasa anafundisha Hankuk University of Foreign Studies, Korea Kusini.

Mbali na Mvumo wa Helikopta, Kifo Kisimani na Natala, Prof. Kithaka wa Mberia amechapisha vitabu vingine ambavyo ni Mchezo wa Karata (mashairi), Bara Jingine (mashairi), Redio na Mwezi (mashairi), Msimu wa Tisa (mashairi), Rangi ya Anga (mashairi), Doa (shairi) na Maua Kwenye Jua la Asubuhi (tamthilia).

130 pages | 178 × 127 mm | 2018Publisher: Marimba Publications, KenyaPaperback: 9789966794420 $16/£12/€13

94 pages | 178 × 127 mm | 2019Publisher: Marimba Publications, KenyaPaperback: 9789789966400 $16/£12/€13

Page 30: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

26

Tamthilia

�������������Ngugi wa Thiong’o

��������������������������������������������������������������������������Masitha Hoeane

Yampasa Remi, wa kwanza wa kabila lake kupata masomo ya chuo kikuu, kurudi kwa watu wake? Yampasa kumrudia Thoni, mjane wa nduguye, ambaye ilimbidi kumwoa kufuatana na mila za kikabila? Au aendelee kuwa mtawa mweusi mjini, akitembelea vilabu vya usiku pamoja na rafiki yake Jeni? Yampasa kukitetea Chama cha Mwafrika hali watu wake wanaona kwamba mahali pa dhuluma za kikoloni, zimeanzishwa tu dhuluma za aina ingine mpya? Haya ndiyo mapingano ya maswali kwenye huu mchezo ambao umekwisha igizwa katika sehemu nyingi Afrika na ng’ambo.

Jumuiya ya Edladleni inajitahidi kujikubali katika Afrika Kusini baada ya uhuru wakati wanapoogelea dhidi ya wimbi la umuhimu wa kuishi na mamilioni ya matarajio yaliyokwamishwa. Safari za wahusika zinajumuisha mzozo na utelezi kutoka kwa kunyimwa, chuki dhidi ya wageni, uhalifu, kusambaratika kwa kitengo cha familia, kujitenga na ubinafsi na jamii, uzembe, na uchungu wa kujiharibu. Walakini hata katika kina cha ukombozi wa kukata tamaa bado kunawezekana katika mapumziko ya maadili ya Ubuntu-binadamu, roho ya jamii na harakati za mazingira.

94 pages | 203 × 127 mm | 2010Publisher: East African Educational Publishers, KenyaPaperback: 9789987083268 $24/£18/€21

104 pages | 210 × 148 mm | 2017Publisher: African Perspectives, South AfricaPaperback: 9780639918730 $57/£45

Page 31: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

27

Tamthilia

������������������­��������Victor Hugo, Jean-Luc Luc Lagarce Mfasiri: Marcel Kalunga Mwela

������Masereka Levi Kahaika

Professor Marcel Kalunga Mwela-Ubi ni raia wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo na tafsiri hizi zilishinda na kupewa tuzo katika mashindano ya kutafsiri tamthilia za Kifaransa katika Kiswahili. Kwa jinsi maandiko yenyewe yalivyo na mvuto mkubwa, baada ya kusoma kurasa chache na kuzoea matumizi ya Kiswahili cha Congo (Kingwana), msomaji atazama katika uhondo wa ucheshi wa tamthilia hizi na kugundua kuwa, kumbe si lazima, waandishi wote watumie Kiswahili sanifu.

Victor Hugo (1802–1855) alikubalika kuwa mshairi bora wa Ufaransa na mwandishi wa pekee kabisa wa tamthilia, riwaya na insha. Anahesabika kuwa mmoja wa waandishi maarufu kabisa kutoka Ufaransa.

Jean-Luc Lagarce (1957–1995) “Kanuni kwa kuishi maisha ya kisasa” ni mmoja wa michezo yake ya kuigiza ambayo imemfanya kuwa msanii anayeongoza katika michezo inayoonyeshwa kwenye majukwaa nchini Ufaransa katika miongo ya mwisho ya karne ya ishirini.

Mkwamo ni tamthilia ya Kiswahili iliyoandikwa na Masereka Levi Kahaika na Iliyochapishwa mwaka 2013. Kwa kiasi kikubwa Mkwamo wa kupendeza umejengwa kwa sehemu juu ya msingi wa falme mbili zilizopo za Kasulenge na Bupomboli, ambazo zinawakilisha falme za Buganda na Bunyoro wakati wa ukoloni nchini Uganda. Mchezo huo pia unaangazia mauaji ya Mashahidi wa Uganda; jinsi na kwa nini yalitokea. Mchezo huo huwapa wasomaji mtazamo wa kuchanganyikiwa kati ya wafalme wa wakati huo na wakoloni, na kutafakari juu ya mbegu za udini katika ya jamii ya Waganda.

150 pages | 198 × 129 mm | 2013Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaPaperback: 9789987083268 $24/£18/€21

94 pages | 210 × 148 mm | 2018Publisher: Fountain Publishers, UgandaPaperback: 9789970252954 $20/£15/€18

Page 32: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

Vitabu vya Lugha

­������ ���������Jordan Nyenyembe

�� ���������������������� �������������� ��� ��� ���� �������������������������������� ������������������������ ����������������������­���

Kamusi ya Ukristo inazo sifa hizi, na za ziada kwani ni kamusi ya kwanza kwa lugha ya Kiswahili ambayo inaweka pamoja, tafsiri ya dhana mbalimbali, majina mbalimbali ya Wakristo na desturi za Makanisa ya Kikristo.

Kamusi ya Ukristo ni kamusi ambamo kwa umahili mkubwa mwandishi amefuatilia na kufanikiwa kukusanya vitomeo vinavyowakilisha madhehebu mbalimbali ya Kikristo. Kuna vidahizo ambavyo hutumiwa zaidi na dhehebu moja kuliko lingine, lakini mwandishi ameviweka pamoja ili kuuondoa umadhehebu na kuujenga umoja wa Ukristo. Ni ukweli usiopingika kuwa waamini wengi hawaelewi misamiati na istilahi nyingi za dini zao. Hivyo basi kwa msaada wa Kamusi hii msomaji atafaidi maarifa ya maana na matumizi ya maneno si tu ya dhehebu moja, dhehebu lake, bali Ukristo kwa ujumla wake.

322 pages | 178 × 127 mm | 2016Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaPaperback: 9789987753178 $34/£24/€28

Jordan Nyenyembe ni mwanatheolojia Mkatoliki na kuhani wa Dayosisi ya Mbinga nchini Tanzania. Amesoma katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino cha Tanzania na Chuo Kikuu cha Vienna mtawaliwa; ambapo alipata jina lake la Udaktari katika Kitivo cha Theolojia Katoliki. Hivi sasa, anafanya kazi ya kichungaji katika Parokia ya Mtakatifu Alois Gonzaga katika Dayosisi ya nyumbani kwake.

Page 33: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

29

Vitabu vya Lugha

­������ ���������������������Ahmed E. Ndalu

­������������ ��­���������­������������

Hii ni kamusi ya Kiswahili inayowalenga wanafunzi wa msingi wa lugha hiyo. Ni zao la utafiti mpana uliofanywa na mwandishi na kukaguliwa sana na waandishi wa kamusi wenye uzoefu kutoka Afrika Mashariki. Baadhi ya huduma muhimu zinazofanya kamusi hii kuwa bora ni pamoja na: zaidi ya vichwa vya maneno 7,000; Maneno 170,000, madarasa ya nomino yaliyofafanuliwa wazi, na faharisi ambayo inajumuisha vielelezo vya rangi ya aina tofauti za wanyama, maumbo, rangi, na ndege.

Kamusi hii ya Kiswahili ni zao la utafiti wa kina uliofanywa na wasomi na waandishi wa kamusi wenye uzoefu. Inalenga wanafunzi wa shule za sekondari, na kwa wasomi wa lugha hiyo, na usomaji wa jumla.

Kurasa 42 za habari ya ziada ni pamoja na:

• Uchanganuzi wa semantik, sintaxical na mofological wa madarasa ya nominoization

• Uainishaji wa maneno k.m. nomino vielezi n.k.

• Istilahi za sarufi ya Kiswahili, Sehemu za hotuba

• Aina za tungo za Kiswahili zinazofundishwa shuleni

• Istilahi zinazotumika katika Fasihi ya Kiswahili -

• Istilahi zinazotumika katika ushairi wa Kiswahili

• Istilahi zinazotumika katika ushairi wa Kiswahili

384 pages | 210 × 148 mm | 2011| vielelelezovya rangiPublisher: East African Educational Publishers, KenyaPaperback: 9789966258083 $61/£46/€53

804 pages | 210 × 148 mm | 2013 | vielelelezovya rangiPublisher: East African Educational Publishers, KenyatPaperback: 9789966259363 $61/£46/ $61/£46/€53

Page 34: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

Historia

��������� ����������������������� �����������������������������������������������Ina Heumann, Holger Stoecker, Mareike Vennen

����������������� �������������� ��������������������������������������������������� ���������������� ��������������������� �������� ��������������������������������� ���������­�������������� ��������� �������������������������������������������������������������������� ��������������������� ���������������������

Mnamo mwaka 1907, habari za uvumbuzi wa kusisimua wa mifupa, katika kilima cha Tendaguru, ziliufikia Ufalme wa Ujerumani. Muda mfupi baadaye, ikafahamika kwamba kilichovumbuliwa ni visukuku vya mifupa ya dinosaria wakubwa ajabu, wenye ukubwa ambao haujawahi kuonekana, walioishi duniani miaka milioni 150 iliyopita na waliokwisha kutoweka. Miaka michache baadaye, msafara ulioongozwa na wanasayansi wa Kijerumani, ulikwenda mahali hapo na kufanikiwa kuchimbua tani 250 za visukuku vya mifupa hiyo ya wanyama wa zama za kale. Mojawapo ya mapato ya uchimbuaji huo ni kiunzi maarufu kiitwacho Graffatitan brancai ambacho kimewekwa kwenye maonesho ya Jumba la Makumbusho ya Historia ya Asili, Berlin.

Kitabu hiki kinafuatilia hatua kwa hatua mwendo wa visukuku hivyo kutoka kilima cha Tendaguru kwenda pote vilikofikishwa, katika kipindi cha karne ya ishirini. Sura za kitabu hiki, kwa kutegemea vyanzo vya habari kutoka hifadhi za nyaraka za Tanzania, Ujerumani na Uingereza, pamoja na mahojiano, zinauliza, ni kwa jinsi gani historia ya msafara huo imekuwa ikisawiriwa hadi wakati wa sasa. Kitabu kinaonesha jinsi historia ya nyara hizo zilizopatikana Tendaguru inavodhihirisha muingiliano baina ya siasa, sayansi na majumba ya makumbusho, ulivyoyapa sura majadiliano na mabishano; mawasilisho na ufahamu uliopo hadi leo kuhusu Giraffatitan brancai.

236 pages | 303 × 220 mm | 2020 | vielelelezovya rangiPublisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaHardback: 9789987084869 $45/£30/€32

Ina Heumann aliongoza mradi wa “Dinosaria huko Berlin”. Anafanya kazi kama mwanahistoria wa sayansi na mweledi wa Historia ya Kipindi Tulichonacho sasa, katika Jumba la Makumbusho ya Historia ya Asili, Berlin. Utafiti wake umejikita katika Siasa ya Historia ya Asili Katika Karne ya Ishirini.

Holger Stoecker ni mwanahistoria na alifanya uchunguzi akiwa Idara ya Masomo ya Kiafrika ya Chuo kikuu cha Humboldt, Berlin, kuhusu historia ya wakati wa ukoloni inayoohusu dinosaria wa Afrika walioko Berlin. Vilevile anashughulika na uchunguzi kuhusu historia ya ukoloni na sayansi kati ya Afrika na Ujerumani na pia utafiti kuhusu asili ya nyara zilizokusanywa kutoka Afrika wakati wa ukoloni.

Page 35: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

31

Historia

��������� ��­�����������������������������������������������������������������Mfasiri: Galasius B. Kamanzi Mhariri: Peter R. Schmidt

�������������������������� �������������������� ���������������������� ���� ����� ������� �����������������������������������������������������������������������������

Utafiti wa Mfalme Mutahangarwa wa Kiziba (aliyetawala 1903–1916) katika mwanzo wa karne ya ishirini ulikusanya mabingwa wa simulizi za mdomo kutoka katika koo za kifalme na zisizo za kifalme na shuhuda zao ziliandikwa na watu waliokwisha kujua kusoma na kuandika, akiwemo F.X. Lwamgira. Miongo mine baadaye matokeo ya utafiti huo yalipigwachapa kikatolea kitabu chenye kurasa 490 katika lugha ya Kihaya ambacho kilibaki bila kujulikana ingawa kilikuwa kitabu muhimu. Tafsiri hii muhimu itafanya historia ya Kaskazini Magharibi mwa Tanzania na Kusini Magharibi mwa Uganda kabla na mwanzoni mwa ukoloni iwafikie kwa mara ya kwanza wasomi wengi.

476 pages | 229 × 152 mm | 2020Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaPaperback: 9789987083695 $45/£35/€37

Mtafsiri Galasius B. Kamanzi ni mwanafunzi wa muda mrefu wa historia ya Kiziba na ngano za Kihaya. Yeye ni mwalimu wa zamani na mtumishi wa serikali aliye na B.A. katika Elimu, inayojihusisha na Uchumi na Isimu, kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Alipata pia diploma ya kuhitimu katika Usimamizi Mkuu kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe. Yeye ni mwandishi mwenza wa Folktales kutoka Buhaya.

Peter R. Schmidt ni Profesa Emeritus wa Anthropolojia katika Chuo Kikuu cha Florida na Profesa Maalum wa Anthropolojia na Akiolojia katika Chuo Kikuu cha Pretoria, Afrika Kusini. Yeye ni mwandishi au mhariri wa vitabu kumi na tano juu ya historia ya Kiafrika, mila ya mdomo, urithi, na akiolojia - nyingi zinalenga Buhaya.

Page 36: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

Historia

��������� �������� ��������������� �����������������������Laura Fair

������ ����������������������� ���Petro Itosi Marealle

Katika kitabu hicho mwandishi anaelezea jinsi watumwa walivyodai uhuru wao kutoka kwa mabwana zao na jinsi walivyojaribu kudai haki zao kutoka kwa watawala wapya, Waingereza. Baadaye alitafiti visiwa na Tanzania Bara kuhusu historia ya sinema na anatarajia kuchapisha kitabu kingine juu ya sinema hivi karibuni. Kama maprofesa wengi wa zamani katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Fair pia ni mfugaji. Huko Merika anafuga kuku na kondoo bila kutumia dawa (asili) na pamoja na mtoto wake Sabri wanapanda karibu chakula chao chote. Njoo Merika, tembelea vijijini.

Mangi Petro Itosi Marealle, aliyekuwa Mangi Mwitori wa Vunjo, amewafanyia kabila la Wachagga na wazao wa baadaye, kazi ya maana sana kwa kuandika kitabu hiki juu ya desturi za Wachagga kabla hazijatoweka na kupotea. Alijitolea miaka mingi kujifunza kwa uangalifu mila na desturi hizi, na alipata mashaka katika kutafuta njia ya kukichapa kitabu hiki. Ninafurahi kusema amekwisha pata njia. Natumaini kitabu hiki hakitapendwa na Mchagga tu, lakini kila mmoja atakaye kujifunza maendeleo ya Wanadamu, na natumaini kitaamsha WaAfrika wa makabila mengine kutunga habari za namna hii za watu wao. Mwandishi wa kitabu hiki Marehemu Mangi Petro Itosi Marealle alikuwa Mangi wa Marangu kuanzia mwaka 1931 hadi 1946, na ‘Mangi Mwitori’ wa Vunjo hadi mwaka 1961. Umangi ulipofutwa mwaka 1962 alishika wadhifa mbalimbali katika Halmashauri ya Wachagga na wadhifa wake wa mwisho ulikuwa kama Mwenyekiti wa Tume ya Serikali za Mitaa. Aliafriki mweai Mei, 1982.

120 pages | 210 × 148 mm | 2015Publisher: Twaweza Communications, KenyaPaperback: 9789966028396 $35/£26/€30

132 pages | 230 × 147 mm | 2002Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaPaperback: 9789976973914 $28/£21/€24

Page 37: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

Wasifu

������������������� �������������Ali Hassan Mwinyi

��������������������������������������� �������������������������������������������� �������������������������������������� �������������� ��� �������� ���������� ����������������������������������

Vitabu hivi vinasaidia kuweka historia sawa; vinaziba baadhi ya mapengo katika kuelewa mambo mbalimbali ya kihistoria. Kitabu kinaitwa “Mzee Rukhsa” kuakisi uongozi wa Rais Mwinyi aliyependa kutumia neno jepesi kama hili kuashiria mambo makubwa aliyokuwa akiyafanya kufungua mipaka ya uchumi na siasa katika Tanzania.

Mojawapo ya mambo yanayowekwa sawa humu, ni kwamba, si kweli kuwa Rais Mwinyi alimkaidi Mwalimu kwa kuanzisha mageuzi kwenye uchumi. Kwa heshima kubwa aliyokuwa nayo kwa Mwalimu, hata akajiona kama ni kichuguu mbele yake aliyemlinganisha na Mlima Kilimanjaro, asingeweza kufanya hivyo. Isitoshe, Rais Mwinyi aliongoza serikali kwa miaka mitano ya mwanzo bila kuvaa kofia ya mwenyekiti wa chama (CCM). Mwalimu asingetaka, yasingewezekana.

Mwalimu alishajaribu kila njia lakini uchumi wa Tanzania uliendelea kudorora. Hazikuwepo fedha za kigeni hata kwa mambo ya msingi kabisa. Mwalimu akampa rukhsa Mwinyi kujaribu maarifa mengine. Baadaye yalikuwapo mambo ambayo Mwalimu hakuyafurahia, akayakemea hadharani. Lakini kimsingi alikubali hoja ya mageuzi, ikiwemo kufungua uchumi kwa sekta binafsi ya ndani na nje ya nchi.

Kadhalika kwenye siasa. Mwalimu aliona umuhimu wa mageuzi kwenye siasa, ikiwemo mabadiliko yaliyoakisiwa kwenye “Maamuzi ya Zanzibar”. Kitabu kinafafanua ilivyotokea, na kwamba wazo la awali lilikuwa la Mwalimu Nyerere, ingawa baadaye kuna mambo hakuyapenda.

Kitabu pia kinazungumzia changamoto nyingi za urais wa Ali Hassan Mwinyi, ikiwemo ile ya muundo wa muungano; migomo; uzawa na chuki baina ya wafanyabiashara; migogoro ya kidini na kadhalika. Yote hayo na mengine yamewekwa vizuri katika lugha nyepesi ya kueleweka na kila mtu.

512 pages | 229 × 152 mm | 2020| vielelelezovya rangiPublisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaHardback: 9789987084364 $55/£40/€42

Page 38: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

34

www.africanb

ookscollective.c

omHistoria

35

���������������� ������ ������� ��������������

Peter D.M. Bwimbo

����������������������� ����������������������������������������������� � ����������������������������������������������������������������������������� ����������� ������������ ����������������­��­�����������������������������

Kikundi kimoja kilikwenda Ikulu kutaka kumlazimisha Rais Nyerere kukubali matakwa yao. Haijulikani ingekuwaje kama kingefanikiwa, na kama Rais Nyerere angeyakataa madai yake. Lolote lingetokea na historia ya Tanzania na ya Afrika ingeathirika vibaya mno. Kwa ujasiri na ubunifu makini, Peter Bwimbo, aliyekuwa mkuu wa kitengo cha ulinzi wa viongozi, (Presidential Securty Unit) na mlinzi mkuu (Bodyguard) wa Rais Nyerere, iliwahamisha Rais Nyerere na Makamo wake Rashis Kawawa, akawapeleka mahali salama, akawaepusha hatari, pengine ya kuuawa. Hiyo ndiyo iliyoitwa Operesheni Magogoni. Katika kitabu hiki, Peter Bwimbo, kwa maelezo yake mwenyewe ametoa siri ambayo ni wachache sana waliyoifahamu; haya ndiyo maelezo sahihi ya mbinu alizotumia kuwaokoa viongozi wa nchi.

Kitabu hiki pia ni historia ya Peter Bwimbo, na ya Kitengo cha ulinzi wa viongozi katika Idara ya Usalama wa Taifa. Historia hiyo inaeleza mambo mengi pia kuhusu Tanganyika na Tanzania katika vipindi mbalimbali; jinsi viongozi wa TANU walivyojaribu kuzuia asiwe mlinzi wa Rais kwa sababu alikuwa “jasusi” wa wakoloni katika Special Branch; jinsi Mwalimu alivyoingia kati na kumaliza fitina hiyo; sifa za kazi ya ulinzi wa Rais (ujasiri, umakini na uwezo wa kufanya uamuzi sahihi na haraka, na uzalendo wa kuwa tayari kujitoa muhanga ili kumlinda) na mengine. Kutokana na matatizo ya kinidhamu na uadilifu yaliyoikumba Idara ya Usalama wa Taifa, mwaka 1975 Mwalimu aliamua kuwastaafisha viongozi wote wa juu katika Idara ya Usalama wa Taifa, licha ya kuwa alifahamu kuwa Peter Bwimbo hakuwa na dosari yoyote, na hasahasa alikuwa mbele katika kufichua madhambi yaliyokuwa yakitendeka Idarani. Mwaka 1978 alipewa kazi katika Shirika la Reli kuanzisha kitengo cha Usalama, kazi iliyokuwa muhimu sana wakati wa Vita ya Kagera. Mwaka 1985 alipewa Nishani ya Ushupavu (Gallantry Medal) kwa ujasiri wake wakati wa Operation Magogoni na uaminifu wake katika kazi ya Bodyguard wa Rais Nyerere.

476 pages | 229 × 152 mm | 2020Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaPaperback: 9789987083695 $45/£35/€37

Mtafsiri Galasius B. Kamanzi ni mwanafunzi wa muda mrefu wa historia ya Kiziba na ngano za Haya. Yeye ni mwalimu wa zamani na mtumishi wa serikali aliye na B.A. katika Elimu, inayojihusisha na Uchumi na Isimu, kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Alipata pia diploma ya kuhitimu katika Usimamizi Mkuu kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe. Yeye ni mwandishi mwenza wa Folktales kutoka Buhaya.

Peter R. Schmidt ni Profesa Emeritus wa Anthropolojia katika Chuo Kikuu cha Florida na Profesa wa Ajabu wa Anthropolojia na Akiolojia katika Chuo Kikuu cha Pretoria, Afrika Kusini. Yeye ni mwandishi au mhariri wa vitabu kumi na tano juu ya historia ya Kiafrika, mila ya mdomo, urithi, na akiolojia - nyingi zinalenga Haya.

Page 39: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

35

www.africanb

ookscollective.c

om

Historia

���� ����� ������­�������������������� � ��������������Nasra Mohamed Hilal

����������������� ��������� ����������������­��������������������������Pat Caplan

Wapenzi wa muziki wa Taarab wana deni kubwa kwa mwinbaji maarufu Siti Binti Saad mzaliwa wa Unguja, ambaye katika uhai wake na baadaye, amejulikana kama Malkia wa Taarab. Malkia huyu aliuchukua muziki wa Taarab akaupa sura mpya, akaubeba na kuufikisha katika ngazi ya kimataifa. Licha ya kuwa waimbaji wengi wa Taarab wamekuja na kuondoka, hakuna ambaye amefikia kilele alichofika Siti Binti Saad. Hayati Shaaban Robert, ambaye nae alikuwa na kipaji cha pekee katika uwanja wa ushairi kwa lugha ya Kiswahili, alihusudu uimbaji na kushangilia maendeleo ya Siti kiasi cha kuandika kitabu juu yake. Kitabut hicho, ‘Wasifu wa Siti Binti Saad’ ndicho kilichochora, kwa mara ya kwanza picha halisi ya Siti Bint Saad kama ilivyojulikana kwa machache waliomuenzi na waliotaka kuweka kumbukumbu yake kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

Wazo la kuandika kitabu hiki limetokana na uhusiano wangu na kisiwa cha Mafia Tanzania, ulioanza takriban miaka arobaini na tano iliyopita. Katika muda huo nimetembelea Mafia mara saba na nimeandika na kuchapisha makala na vitabu vingi. Baadhi ya watu wanaoishi kisiwani wamekuwa rafiki zangu wa karibu; mmoja wao ambaye nilimjua vizuri tangu kukutana kwetu mwaka 1965 akiwa kijana mdogo ni Mikidadi Kichange. Tangu kifo chake cha ghafla mwaka 2002 alipokuwa na umri wa miaka arobaini na tisa tu, nimetafakari jinsi anavyoweza kukumbukwa kwa kuandika kitabu kuhusu maisha yake, na kuonyesha mabadiliko makubwa yaliyotokea kisiwani Mafia na nchini Tanzania kwa jumla tangu ipate uhuru. Kitabu hiki ni wasifu wa kihistoria kwa upande mmoja na historia kwa kupitia wasifu kwa upande mwingine, ambamo maisha ya watu wa kawaida yanaonesha mapambano yao na maisha, changamoto, na katika mfano huu uwezo wa ajabu walio nao wa kuyashinda yote yanayowakabili.

91 pages | 207 × 145 mm | 2007Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaPaperback: 9789987449460 $27/£20/€23

190 pages | 229 × 152 mm | 2014Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaPaperback: 9789987082957 $28/£21/€24

35

Page 40: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

Siasa

����������������������� ������������������������

Julius Kambarage Nyerere alikuwa kiongozi wa kwanza wa serikali wa Tanzania na kabla ya hapo wa Tanganyika, kutoka 1960 hadi kustaafu kwake mnamo 1985.

Kitabu hiki kinaelezea matatizo mazito yanayowakabili Watanzania, na kinalenga hasa masuala yanayohusiana na Muungano, uadilifu na utulivu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia, kinajadili changamoto za muungano ambazo ni matokeo ya mfululizo wa kupinga uhalali wake chini ya Katiba ya Muungano.

Kitabu hiki kinaelezea sababu za uamuzi wa awali wa kuanzisha muundo wa Serikali Mbili na kusisitiza kwamba, tarehe 26 Aprili 1964, nchi mbili huru ziliachilia haki zao za kuwa Jamhuri na kuunda nchi moja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kusaini Mkataba wa umoja huo. Hii ilikuwa kweli kwa Tanganyika, ambayo haikubaki na Serikali yake, ili kuanzia hapo na kuendelea kutokuwa na Serikali yoyote tofauti na ile ya Muungano. Pia, ilikuwa kweli Zanzibar, ambayo ina Serikali tofauti na mamlaka ya kukabiliana na masuala yote yanayohusiana na Zanzibar ambayo hayakuhamishiwa katika Serikali ya Muungano

98 pages | 178 × 127 mm | 2016Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaPaperback: 9789987753420 $24/£18/€21

Julius Kambarage Nyerere alikuwa kiongozi wa serikali wa Tanzania ambaye aliwahi kuwa kiongozi wa Tanzania, na hapo awali Tanganyika, kutoka 1960 hadi kustaafu kwake mnamo 1985.

Page 41: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

Siasa

����������������­��������­��������������������������������������Benjamin W. Mkapa

Hotuba hizo ni ufunguo wa uelewa sahihi wa siasa, uchumi na masuala ya jamii katika nchi yetu katika kipindi hiki cha historia. Umoja wa taifa, mshikamano na juhudi za maendeleo yanahitaji kipaumbele maalum katika dunia ya leo ya utandawazi, na Rais Mkapa anaeleza kwa ufasaha ni nini tunapaswa kufanya ili tuweze kufanikiwa.

138 pages | 205 × 143 mm | 2004 | Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaPaperback: 9789987417421 $30/£22/€26

����������������­���������������������������������������������Benjamin W. Mkapa

Rais Mkapa anaeleza kwa kina maana na athari za utandawazi kwetu kama taifa na kwa watu binafsi. Aidha anaendelea kueleza, kufafanua na kutetea sera ya ubinafsishaji na kuonyesha matunda ya sera hiyo bila kupuuza sokomoko kama lile lililofuatia hatua ya kubinafsisha shirika la TANESCO.

194 pages | 203 × 127 mm | 2002 | Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaPaperback: 9789987686766 $30/£22/€26

����������������­���������������������������������������������Benjamin W. Mkapa

Kitabu hiki kitawafaa Watanzania wote hasa wanapotaka kufuatilia kwa karibu utendaji kazi wa serikali waliyoiweka madarakani. Ni kumbukumbu muhimu kwa maendeleo ya Taifa na Katika Kuelewa masuala ya siasa, jamii na uchumi wa jamii ya Tanzania.

138 pages | 205 × 143 mm | 2004 | Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaPaperback: 9789987417421 $30/£22/€26

����������������­��������������������������������������������Benjamin W. Mkapa

Hiki ni Kitabu cha Tano na cha mwisho katika mfululizo wa vitabu vya Uwazi na Ukweli. Mfululizo huu una malengo makuu matatu: Kwanza ni kufanya mihadhara kuwa moja ya vyanzo vya elimu ya ziada, haswa juu ya maswala anuwai ya kitaifa na kimataifa, sababu na mwelekeo wa maswala hayo.

138 pages | 205 × 143 mm | 2004 | Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaPaperback: 9789987417421 $30/£22/€26

Page 42: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

����������������������������� ����������� ����������������������������������� ����������������� ������� �������� ������ �������� ���������������������������������� �����������

Lilianzishwa, linamilikiwa na kudhibitiwa na kikundi cha wachapishaji wa Kiafrika wanaozingatia maadili ya tamaduni za Kiafrika, na kusisitiza umuhimu wa sauti za waAfrika kusikika ndani ya Afrika na kimataifa. Linajumuisha wasomi, waandishi wa fasihi, na baadhi ya wachapishaji wa vitabu vya watoto, taasisi za utafiti, waandishi katika vyuo vikuu, wafanya biashara kubwa na ndogo, Asasi Zisizo za Serikali (NGOs), na mashirika ya waandishi.

Page 43: African Books Collective VITABU VYA KISWAHILI

`

Sisi ni Nani?African Books Collective ni duka la vitabu linalomilikiwa na Waafrika, linaloshughulikia masoko na usambazaji ulimwenguni kote wa vitabu kutoka Afrika – vitabu vya kitaaluma, fasihi, na vya watoto. ABC ni ushirika unaomilikiwa na wachapishaji waanzilishi wake. Wachapishaji hao huchagua Baraza la Uendeshaji linalokutana mara moja kwa mwaka. Baraza hilo lina wajibu wa kuweka mikakati ya ABC na uwakilishi wake kwenye uigo mpana wa vitabu na dunia ya uchapishaji. ABC imesajiliwa Uingereza kama kampuni isiyo na lengo la faida na yenye kikomo cha dhamana. Lengo la ABC ni kuwatafutia faida wachapishaji wake na siyo kujitafutia faida.

HistoriaMwaka 1985 kikundi cha wachapishaji walikutana kujadili changamoto zilizokuwa zikiwakabili katika kuuza na kusambaza vitabu vyao nje ya masoko yao ya ndani. Walianzisha ABC kama jitihada ya kuijisaidia wao wenyewe, katika kuimarisha biashara zao na kukidhi mahitaji ya maktaba na wanunuzi wengine wa vitabu. Kwa ufadhili wa mashirika ya kimataifa ya misaada mwanzoni, biashara ilianza mwaka 1989. Mwaka 2007, mabadiliko makubwa katika uendeshaji wake yalifanywa na ikaanza kujitegemea kifedha. Fursa mpya zilijitokeza kutokana na maendeleo ya uchapishaji wa kidijitali na vitabu vya kilektronik, zikachangamkiwa, ABC ikiongoza katika kuweka utajiri wa utamaduni wa kiAfrika katika mfumo wa kidijitali. Pamoja na kwenda na mabadiliko na mbinu yanayojitokeza, sababu na malengo ya kuianzisha bado yako palepale na ABC imeendelea kutolenga kutengeneza faida kwa ajili yake yenyewe.

PersonnelOfisa Mtendaji Mkuu Justin Cox | [email protected] wa Wateja, UK David Brooks | [email protected] wa Wateja, USA Carolina Bruno | [email protected]

Council of ManagementKiaire Kamau, East African Educational Publishers, KenyaTapiwa Muchechemera, Mkuki na Nyota Publishers, TanzaniaIbrahim Oanda, Codesria, SenegalAkoss Ofori-Mensah, Sub-Saharan Publishers, GhanaFrancois van Schalwyck, African Minds Publishers, South Africa

Kwa maelezo kuhusu jinsi tunavyofanya kazi, na jinsi ya kuagiza vitabu, tafdhali tembelea tovuti yetu: http://www.africanbookscollective.com/faq