Upload
others
View
6
Download
0
Embed Size (px)
Citation preview
i
Dondoo Kuhusu Dhambi
© 2016 Daudi Lubeleje
VIJANA NA UTUMISHI
ii
I Wathesalonike 4: 2 – 5
“2 Kwa kuwa mnajua ni maagizo gani tuliyowapa kwa Bwana Yesu. 3
Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane
na uasherati; 4 kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika
utakatifu na heshima; 5 si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa
wasiomjua Mungu.”
…………… Kitabu hiki ni kwa mwamini yeyote”.
iii
#UTANGULIZI
Bwana Yesu asifiwe,
Si kwa bahati mbaya kitabu hiki kimekufikia. DONDOO KUHUSU DHAMBI ni
kitabu kwa kila mwamini kukisoma. Baada ya kusoma kitabu hiki ni matumaini
yangu kupitia dondoo hizi, utapata majibu ya swali hili “Kwanini yatupasa
kutunza utakatifu?” Hivyo utaongeza bidii yako kumpendeza Mungu katika
mwenendo wako wote.
Kuokoka ni hatua ya kwanza kuliishi kusudi lako. Dhambi ni kikwazo cha
kwanza kuharibu kusudi la Mungu katika maisha yako. Basi, kitabu hiki kiwe
msaada kwako kuongeza chachu ya wewe kutunza kusudi la Mungu kwa
kuepuka kuchafuliwa na dhambi, Kumbuka Neno la Mungu lasema “Msishike, msionje, msiguse” [Wakolosai 2:21]
Asante Pastor Raphael, JL wa YKM.
“Unajua tatizo ni kwamba kitabu ni kitamu sana………kila kijana anatakiwa
akipate hiki” [Raphael Joachim Lyela, Mchungaji wa Vijana na Mwanzilishi wa
Youth Kingdom Ministries, YKM]
Daudi Lubeleje.
iv
#YALIYOMO
#UTANGULIZI ............................................................................................................. iii
#YALIYOMO ................................................................................................................ iv
#DONDOO YA KWANZA. ....................................................................................... 1
#DONDOO YA PILI ..................................................................................................... 3
#DONDOO YA TATU. ................................................................................................. 6
#DONDOO YA NNE ................................................................................................... 8
#DONDOO YA TANO .............................................................................................. 12
#DONDOO YA SITA ................................................................................................. 13
#DONDOO YA SABA ............................................................................................... 16
#MAOMBI YA TOBA ................................................................................................ 18
#IJUE VIJANA NA UTUMISHI .............................................................................. 19
1
#DONDOO YA KWANZA.
Dondoo ya kwanza inasema “dhambi inaotea mlangoni”. Neno la Mungu
linasema katika Mwanzo 4:7 ".......Usipotenda vyema dhambi iko,
inakuotea mlangoni,..........". Nataka nifafanue mstari huu kwa mapana kama
ifuatavyo;
Mlango ni nafasi ya kuruhusu au kutoruhusu
kilicho nje/ndani kuingia/kutoka ndani/nje.
Wakati Bwana Yesu anasema "....nasimama
mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti
yangu, na kuufungua mlango, nitaingia
kwake,............" (Ufunuo wa Yohana 3:20),
HALI KADHALIKA, dhambi haiji kupitia
dirishani au wapi, bali iko mlangoni na yenyewe
ikiotea!. Kama dhambi inaotea mlangoni, lazima
iwe imejificha maana ikija kwa wazi utaiona na
huwezi kufungua mlango ikapita. Tofauti na
Bwana Yesu hapohapo mlangoni anabisha ili
kuingia, haotei kama ilivyo dhambi. Dhambi
inaotea mlangoni kwa sababu hapo ndio sehemu
pekee inaweza fanya maigizo kama yenyewe si
dhambi vile, bali ni jambo zuri, ni uzima,
kwamba ukiruhusu utapata faida na si hasara ila
kumbe ni hila za kukuotea!. Kumbuka 2
Wakorintho 11:14 inasema "........Maana
shetani mwenyewe hujigeuza awe
mfano wa malaika wa nuru". Kujigeuza
huku kwa shetani kuwa malaika wa nuru ni
kukushawishi ili ufungue mlango, maana dhambi
inaotea hapo mlangoni.
“Dhambi inaotea
mlangoni kwa
sababu hapo
ndio sehemu
pekee inaweza
fanya maigizo
kama yenyewe si
dhambi vile, bali
ni jambo zuri, ni
uzima, kwamba
ukiruhusu
utapata faida na
si hasara ila
kumbe ni hila za
kukuotea!.”
2
Sababu kubwa inayofanya dhambi kuotea mlangoni tunaipata tukisoma
Yohana 10:2 "Aingiaye mlangoni ni mchungaji wa kondoo" na
mchungaji wa kondoo si mwingine ni Yesu Kristo (Yohana 10:11-14). Kama
Yesu Kristo huingia mlangoni, na dhambi kwa kuotea hutaka kupitia hapohapo
ila ikiisha kujigeuza na kuonekana kama ni jambo la faida.
Kuna baadhi ya mambo katika maisha yetu hususani yale
yanayowakumba vijana yanapokuja huonekana ni mema
kumbe ni dhambi inaotea mlangoni. Mfano masuala ya
mahusiano ni eneo ambalo shetani hufanya mambo
yaonekane kama ni ya Mungu kumbe hapana. Mambo
kama kufanya tendo la ndoa kabla ya ndoa na wakati si
wanandoa ni dhambi, kwa bahati mbaya dhambi huotea
hapo, inafanya tendo la ndoa hata kama hamjaingia
kwenye ndoa lionekane ni sawa tu.
Tunapaswa kujua si yote yanakuja kwetu ni mema tu! bali mengine ni dhambi
inaotea mlangoni. Kwa sababu Yesu Kristo anabisha hapo mlangoni na dhambi
inaotea hapo mlangoni ni vema kupima kila jambo kwanza kwa chujio la Neno
la Mungu.
“Tunapaswa
kujua si yote
yanakuja kwetu
ni mema tu!
bali mengine ni
dhambi
inaotea
mlangoni”
3
#DONDOO YA PILI
Dondoo ya pili inasema, “Dhambi inakutamani wewe uliyempa Yesu Kristo
maisha yako”. Tukisoma katika Mwanzo 4:7 "..........Usipotenda vyema
dhambi iko,.............nayo inakutamani wewe.......". Nitafafanua kwa
mapana kama ifuatavyo;
Kutamani kwa lugha rahisi humaanisha "kutaka sana".
Kila mwamini anapaswa kujua dhambi inamtaka sana na
haiwezi kutulia mpaka imempata. Kutamani kwa dhambi
huambatana na ushawishi unaoletwa na dhambi
yenyewe. Ushawishi huu huficha ubaya wa dhambi.
Nitatumia mfano ufuatao kuelezea kutamani kwa
dhambi kulivyo;
Tukisoma Mwanzo 3: 1-6, hasa mstari wa 6 inasema "Mwanamke
alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho,
nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi akatwaa matunda
yake akala, akampa na mumewe, naye akala". Angalia! Kwa sababu
dhambi iliwatamani Adamu na mkewe, kwa kutumia ushawishi wake, ilifanya
mwanamke akaona matunda ya mti waliokatazwa wasile kuwa WAFAA KWA
CHAKULA na tena WAPENDEZA MACHO (Mwanzo 2:17).
Hata leo, kwa yeyote aliyeokoka, dhambi inamtamani,
hata kumshawishi kwa kumwonyesha mambo mengi
Mungu aliyokataza kuonekana ni mazuri. Vijana wengi
leo, kwa kutotambua hilo, wamefanya dhambi na
kuanguka huko. Mtume Paulo alisema
"lakini katika viungo vyangu naona sheria iliyo mbali, inapiga vita
na ile sheria ya akili zangu, na kunifanya mateka ya ile sheria ya
dhambi iliyo katika viungo vyangu" (Warumi 7:23).
“Kutamani
kwa dhambi
huambatana
na ushawishi
unaoletwa na
dhambi
yenyewe.”
“Kutamani
kwa dhambi
hufanya hata
vita na
wewe!,”
4
Kutamani kwa dhambi hufanya hata vita na wewe!, Yale uliyoyaacha baada ya
kuokoka, unashangaa dhambi inakutamanisha tena, Sikiliza mtoto wa Mungu!,
hiyo ni vita imekuja kwako. Kumbuka hata katika maisha ya kawaida,
unapotamani kufanya mambo fulani uliyojiwekea, hutakaa utulie mpaka
umefanikiwa. Hata dhambi inatamani, ina kiu ya kumwangusha mtoto wa
Mungu, atoke kwenye kusudi la Mungu. 1 Petro 2:11 inasema
"...........ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho", Umeona! tamaa
za mwili ni matamanio ya dhambi kutimiza lengo lake la kukutamanisha ili
umwache Mungu.
Sasa, dhambi inapokutamani, inataka upoteze nafasi
yako kwa Mungu uliyopewa. Leo watoto wa Mungu
wengi wamepoteza huduma, utakatifu, baraka na mambo
mengi lukuki kutoka kwa Mungu, kwa kuifuata dhambi
ilipowatamanisha.
Nimalizie kwa kusema hivi, kwa nafasi kubwa dhambi inapomtamani mtoto wa
Mungu, hutumia mwili kwake. Tukisoma Warumi 8: 5-11, Wagalatia 5:16-
17, 1 Petro 2:11 twapata kujua hili.
Hebu tuamue kujitoa kwa Mungu ki-sawasawa, tunapotembea tujue si yote
yanayokuja ni ya Mungu, mengine ni ushawishi wa dhambi hata kama
yanapambwa vipi kwa kupendeza. Tafakari mistari ifuatayo na Mungu
atusaidie kwa neema yake, kumbuka mimi na wewe ni zaidi ya washindi;
Warumi 6:13 "Wala msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha
za dhuluma kwa dhambi; bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama
walio hai baada ya kufa, na viungo vyenu kuwa silaha za haki”.
Warumi 12:1-2 "...........itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu
ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. Wala
msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa
“Dhambi
inapokutamani,
inataka
upoteze nafasi
yako kwa
Mungu
uliyopewa”
5
upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo
mema, ya kumpendezam na ukamilifu"
6
#DONDOO YA TATU.
Dondoo ya tatu inasema, “Dhambi hufanya mtu kupungukiwa na utukufu
wa Mungu”. Neno la Mungu linasema ".......wote wamefanya dhambi, na
kupungukiwa na utukufu wa Mungu" (Warumi 3:23). Kufanya dhambi
kunapunguza ule utukufu wa Mungu tuliokuwa nao kabla ya kufanya dhambi.
Twende pamoja, ninapofafanua kama ifuatavyo;
Hapa nataka niongee sana na waliompa Yesu Kristo maisha yao [Wameokoka
tayari]. Nitaenda taratibu ili udake kile ninachotaka uone hapa;
Katika Yohana 1:12 "Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa
kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake".
Ukishampokea Yesu Kristo katika maisha yako, twajua kuwa umefanyika
mtoto wa Mungu tayari; dhambi ulizofanya zinafutwa na unakuwa mpya ndani
ya Kristo. Angalia! Baada tu ya kumpokea Kristo, Bwana Yesu anasema
"Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao............" (Yohana 17:22).
Sikiliza! utukufu wa Mungu uliokuwa kwa Kristo, unakuwa kwako tu,
ukimpokea Kristo. Hivyo yeyote aliyeokoka utukufu wa Mungu upo kwake.
Ukisoma Matendo ya Mitume 6:15 Neno la Mungu linasema "Watu wote
walioketi katika ile baraza wakamkazia macho yao, wakamwona
uso wake kuwa kama uso wa malaika". Mtumishi wa Mungu Stefano
kama tunavyoona hapa, uso wake ulionekana kama uso wa malaika katika lile
baraza; Sasa kilichofanya uso wa Stefano kuonekana hivyo, ni ule utukufu wa
Mungu uliokuwa kwake. Utukufu wa Mungu unabadilisha hata muonekano
wako mbele ya watu, Utaonekana mwenye heshima, akili, mvuto mzuri kuliko
kawaida. Kwa nyongeza, soma tena 2 Wakorintho 3:18.
Mtoto wa Mungu anapofanya dhambi tu, dosari inaingia kwenye maisha yake,
Utukufu wa Mungu alionao unapungua, Hasa asipotubu!. Kumbuka
tulivyosoma Warumi 3:23, tumeona kwa wazi kuwa dhambi hufanya utukufu
wa Mungu kupungua na huzidi kupungua kama aliyefanya dhambi asipotubu.
7
Kufanya dhambi bila kutubu ni hatari sana kwa mwamini yeyote. Nimeona iko
shida leo, hasa kwa vijana kuwa wagumu kutubu wakifanya dhambi. Madhara
yake ni kuzoelea kufanya dhambi kwani utukufu wa Mungu umepungua.
Jambo la kufanya ni kuwa ukifanya dhambi TUBU! la
sivyo tegemea kuona utukufu wa Mungu kupungua
kwenye maisha yako. Neno la Mungu linasema
"..........Na kama mtu akitenda dhambi tunaye
Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye
haki, naye ndiye kipatanisho kwa dhambi
zetu............" ( 1 Yohana 2:1-2). Yesu Kristo ndiye
kipatanisho kwa dhambi zetu, tubu na mrudie Mungu,
songa mbele na wokovu. Mithali 28:13 "Afichaye
dhambi zake hatafanikiwa, Bali yeye
aziungamaye na kuziacha atapata rehema".
Kupata rehema ni kusamehewa, kutohesabiwa dhambi
(Zaburi 32:1-2).
Ni vizuri zaidi ukatunza utakatifu wako ili utukufu wa Mungu uzidi kuwa na
wewe, badala ya kuanguka na kutubu mara kwa mara!. Kumbuka dhambi
hupunguza utukufu wa Mungu kwako, JITUNZE!.
“Kufanya
dhambi bila
kutubu ni
hatari sana
kwa
mwamini
yeyote”
8
#DONDOO YA NNE
Dondoo ya nne inasema, “Dhambi ikikomaa huzaa mauti”. Neno la Mungu
linasema “………na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti”
(Yakobo 1:15). Kuzoelea kufanya dhambi bila kutubu hufanya ile dhambi
ikomae [full grown/matured]. Kukomaa kwa dhambi ni hatua ya mwisho
kabisa inayozaa mauti/kifo.
Nataka nikuonyeshe mambo kadhaa yanayotokea kabla dhambi haijazaa mauti.
"MAMBO YANAYOWEZA KUTOKEA KABLA DHAMBI HAIJAZAA
MAUTI"
MAONYO______#01
Kufuatana na Ezekieli 18:23,32 inaweka wazi kuwa Mungu hafurahii mwenye
dhambi kufa bila kutubu. Ukisoma utakutana na maneno yafuatayo;
“Je! mimi ninafurahia kufa kwake mtu mwovu? asema Bwana
MUNGU; si afadhali kwamba aghairi na kuiacha njia yake,
akaishi? Maana mimi sikufurahii kufa kwake afaye, asema Bwana
MUNGU; basi ghairini mkaishi”.
Hivyo basi, mtu afanyapo dhambi na kabla haijakomaa kuzaa mauti, hupokea
MAONYO mengi ili atubu. Mungu hutumia MAONYO ili kumrudisha
mwenye dhambi atubu. Kupitia watumishi wa Mungu, atendaye dhambi
hupokea MAONYO ya Mungu ya kumfanya arudi kwenye toba ya kweli ili
apone!. Katika Ezekieli 3:16-21 [soma yote], hasa mstari wa 17 tunaona Mungu
anasema “……….basi, sikia neno hili litokalo katika kinywa changu,
ukawape maonyo haya yatokayo kwangu” Sikiliza! Ukipokea
maonyo usichukie na kukasirika, bali jitathimini. Kuna baadhi ya vijana siku
hizi wakionywa wanageuka mbogo! Kwenye eneo hili usijifanye mjanja, kuwa
mnyenyekevu ikusaidie kujua hali yako mbele za Mungu ili utubu na upone.
9
Yona 1:2 “Ondoka uende ninawi, mji ule mkubwa, ukapige kelele
juu yake; kwa maana uovu wao umepanda juu mbele zangu”.
Kama nilivyosema awali kuwa, Kabla dhambi haijazaa mauti, Mungu hufanya
kila njia kumrudisha mtu ili asife akiwa dhambini. Kabla Mungu hajaiangamiza
ninawi, alimtuma mtumishi wake Yona ili ahubiri kwanza kutoa nafasi kwa
watu wa ninawi kutubu.
Kuna aliyekuwa ameokoka, amerudi nyuma tena kwenye dhambi, Mungu
anataka utubu tena na urejee kwake. Kuna ambae hajaokoka kabisa, Mungu
anataka utubu. Kuna ambae ameokoka ila kazoelea kufanya vidhambi fulani,
Mungu anataka utubu na utembee kwa uaminifu; Kumbuka dhambi ikikomaa
huzaa mauti. Injili ni MAONYO kumrudisha aliyepotea kwa Mungu kabla hiyo
dhambi haijazaa mauti!. Kuna sehemu Mungu anasema “Aonywaye mara
nyingi akishupaza shingo, Atavunjika ghafla, wala hapati dawa”
(Mithali 29:1). Hatua ya kutopata dawa ni mauti, mtu anakufa amebeba furushi
lake la dhambi, USIFIKE HUKU! amua kutubu.
Ukisoma Warumi 6:23 inasema "........mshahara wa dhambi ni
mauti.....". Fahamu kwamba baada ya kazi mtu hulipwa mshahara. Huwezi
kulipwa mshahara mpaka ufike muda wa kulipwa, iwe kwa mwezi/wiki au hata
siku moja. Mtu halipwi mshahara kabla ya ule muda wa kupokea mshahara
haujafika/kutimia.
Nikulete sasa kwa upande wa dhambi, Kile kipindi ambacho mtu hajapokea
mshahara wake wa dhambi, ni kwamba ule muda wa kupokea haujafika au bado
yuko kazini akiizalia dhambi matunda. Kufuatana na Yakobo 1:15, kwa tafsiri
nyingine twaweza sema dhambi inakuwa haijakomaa ili kuzaa mauti, Hivyo
mtu anakuwa anaifanyia kazi dhambi na ikikomaa [yaani ule muda wa kupokea
mshahara ukitimia] hiyo dhambi huzaa mauti [mtu anapokea mshahara wake!].
10
Kabla ya kupokea mshahara wa dhambi, katika kipengele cha kwanza, tuliona
Mungu hutumia MAONYO ili anaefanya dhambi atubu na kurejea kwa Yesu
Kristo.
KUMBUKA: Mungu hafurahii kufa kwake mwenye dhambi. MAUTI kwa
mwenye dhambi ni KUTENGWA na Mungu. Kabla dhambi haijakomaa na
kuzaa hiyo MAUTI, ni vema mtu asifanye moyo mgumu bali akumbuke
KUMPOKEA Yesu Kristo.
ADHABU______#02
Kama huelewi MAONYO basi kinachofuata ni ADHABU ili utubu. Wapo
baadhi ya watu, hata ahubiriweje moyo wake ni mgumu kumpokea Yesu.
Kuna ndugu wengine wameokoka na bado kuna
dhambi hawaachi, wameonywa na Mungu ila
bado hawaelewi. Njia nzuri hapa ni ADHABU!.
Kupitia adhabu wengi huanza kumwelewa
Mungu anataka nini, basi wanarudi na kutubu.
Fungua biblia yako kwenye Waamuzi 2:11-15, Neno la Mungu linasema;
"Wana wa Israeli walifanya yaliyokuwa ni maovu mbele za macho ya
Bwana, nao wakawatumikia Mabaali. Wakamwacha Bwana, Mungu wa
baba zao, aliyewaleta kutoka katika nchi ya Misri, wakafuata miungu
mingine, baadhi ya miungu ya watu wale waliokaa karibu nao pande zote,
wakajiinamisha mbele yao; wakamkasirisha Bwana, akaghadhibika.
Wakamwacha Bwana, wakamtumikia Baali na Maashtorethi. Hasira ya
Bwana ikawaka juu ya Israeli, naye akawatia katika mikono ya watu
waliowateka nyara, akawauza na kuwatia katika mikono ya adui zao
pande zote; hata wasiweze tena kusimama mbele ya adui zao. Kila
walikokwenda mkono wa Bwana ulikuwa juu yao kuwatenda mabaya,
kama Bwana alivyosema, na kama Bwana alivyowaapia; nao
wakafadhaika sana".
“Kupitia adhabu
wengi huanza
kumwelewa Mungu
anataka nini, basi
wanarudi na kutubu.”
11
Hebu angalia ADHABU hii kwa Wana wa Israeli "..akawatia katika
mikono ya watu waliowateka nyara, akawauza na kuwatia
katika mikono ya adui zao pande zote; hata wasiweze tena
kusimama mbele ya adui zao. Kila walikokwenda mkono wa
Bwana ulikuwa juu yao kuwatenda mabaya, kama Bwana
alivyosema, na kama Bwana alivyowaapia; nao wakafadhaika
sana".
Lengo la Mungu katika adhabu si kumtesa mtu, bali kumfanya afikirie toba
maana amemwacha Mungu. Mungu anakupenda sana ila hapendi dhambi,
Hivyo unapofanya dhambi ni ngumu mkaambatana naye ila kwa ule upendo wa
Mungu kwako, utapata ADHABU ya kukurudisha kwake.
Hebu nikuulize ya nini kung'ang'ania dhambi? Unataka mpaka ubanwe na
Mungu kwenye kona na hilo li-ADHABU amekupa ndipo utubu? Kwanini
ufike mpaka huko, kama unaweza kufanya maamuzi sasa na ukamrudia Mungu
kikamilifu? Mimi nimeokoka na Bwana Yesu ni Mwokozi wa maisha yangu,
wewe je? Neno la Mungu linasema ".......Leo, kama mtaisikia sauti yake,
Msifanye migumu mioyo yenu...." (Waebrania 3:7-8) na tena
"....tazama, wakati uliokubalika ndio sasa; tazama siku ya wokovu
ndiyo sasa" (2 Wakorintho 6 :2). Je unataka kumpokea Yesu Kristo sasa?,
umefanya maamuzi ya busara. Unaweza kuomba maombi ya toba yaliyo
ukurasa wa mwisho wa kitabu hiki.
12
#DONDOO YA TANO
Dondoo ya tano [5] inasema “Dhambi ni kizuizi cha mema Mungu
aliyokuandalia!”. Tunapata uhakika wa hili tunaposoma Yeremia 5:28
“……….dhambi zenu zimewazuilia mema msiyapate”. Mema yako ni
ahadi za Mungu kwako ikijumuisha maeneo yote yanayogusa maisha yako. Ni
mkusanyiko wa baraka zako zote kiroho na kimwili! (3 Yohana 1:2)
Kuzuiliwa kwa mema yako ni sawa na kutolewa
kwenye foleni ya kupokea mema uliyokusudiwa.
Dhambi inakutoa kwenye eneo la kupokea mema
yako.
“Mema yako ni ahadi
za Mungu kwako
ikijumuisha maeneo
yote yanayogusa
maisha yako”
13
#DONDOO YA SITA
Dondoo ya sita [6] inasema “Dhambi inakufanya kuonekana kama KITU
KICHAFU na Wote waliokuheshimu wanakudharau kwa sababu
wameona UCHI WAKO”. Maandiko yanasema “Yerusalemu amefanya
dhambi sana; kwa hiyo amekuwa kama kitu kichafu; Wote
waliomheshimu wanamdharau, kwa sababu wameuona uchi
wake…………..” (Maombolezo 1:8). Nieleze kwa kina kidogo kama
ifuatavyo;
Mstari wa 8 unaweka wazi matokeo mawili ya dhambi; 1). Kuonekana kitu
kichafu 2). Kuonwa uchi wako hivyo waliokuheshimu kukudharau
KUONEKANA KITU KICHAFU_______#01
Maandiko yanaweka wazi kuwa Mungu ametuchagua ili tuwe watakatifu, watu
tusio na hatia mbele zake katika pendo (Waefeso 1:4). Kuwa mtakatifu ni
kutengwa na uchafu wa dhambi, ni kutakaswa na damu ya Yesu na kuwa safi
bila hatia mbele za Mungu. Mtu akiokoka au kwa lugha rahisi kuzaliwa mara
ya pili anaingia kwenye kundi la watakatifu wa Mungu walio hapa duniani.
Maandiko yanasema “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora,
Hao ndio niliopendezwa nao” (Zaburi 16:3).
Sasa, mtu asipotunza utakatifu wake na kufanya
dhambi, Hiyo dhambi inamchafua na
anaonekana kama kitu kichafu. Popote ulipo
uchafu unakaribisha mainzi na magonjwa.
Ukiwa mchafu kwa sababu ya dhambi unakuwa
kituo cha mapepo. Tunza utakatifu wako!
“Dhambi humfanya atendaye kuonekana kama KITU KICHAFU na uchafu huu huvuta mapepo, magonjwa, umaskini na mengine mengi yafananayo”
14
Kuwa KITU KICHAFU kwa sababu ya dhambi humvuta zaidi shetani na
mnakuwa marafiki bali kwa Mungu unazidi kuwa mbali, ila neema Mungu
itakuvuta utubu!.
KUONWA UCHI WAKO_____#02
Afanyaye dhambi hujiondolea utukufu wa Mungu uliomfunika kama vazi.
Utukufu wa Mungu kwa mwamini huleta heshima na kuficha aibu.
Maandiko katika Mwanzo 3:1-11 [soma yote] yanasema;
“9 Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi? 10
Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa
mimi ni uchi; nikajificha. 11 Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa
u uchi? Je! Umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale?”
Adamu na mkewe walipokula tu matunda ya mti uliokatazwa wakajua wako
UCHI kwa sababu utukufu wa Mungu uliowafunika uliondoka!. Kuwa UCHI
ni kuwa mtupu bila Mungu. Uhusiano uliokuwepo kati ya Adamu na Mungu
uliingia doa. Bwana Yesu alifanya kazi ya kuturejeza tena kwa Mungu alipolipa
fidia ya dhambi zetu pale msalabani. Alitununua kwa damu yake iliyomwagika
msalabani, Hivyo yeyote anayeamua kumpa Yesu maisha yake UCHI wake
Bwana Yesu anaondoa kwa kumpa vazi jipya la wokovu.
Kijana uliyeokoka unapaswa kutunza vazi lako la wokovu lisichafuliwe na
dhambi. Si kuchafua tu peke yake bali dhambi inaweza kukuvua kabisa vazi
lako la wokovu ukabaki uchi. Kurudia kufanya dhambi tena bila kutubu
hufanya UCHI WAKO kuonwa. Yako mambo mengi ulifichiwa na Mungu
kwa sababu wewe ni mtoto wake, aibu yako haikuonekana ulipata heshima na
utukufu wa Mungu ulikufunika. Sasa kufanya dhambi tena inafunua hayo yote
uliyofichiwa na Mungu yanakuwa hadharani na utaanza kudharauliwa.
15
Katika Ufunuo 3:4 maandiko yanasema “4 Lakini unayo majina
machache katika Sardi, watu wasioyatia mavazi yao uchafu. Nao
watakwenda pamoja nami hali wamevaa mavazi meupe, kwa
kuwa wamestahili”. Ukitunza vazi lako la wokovu kuwa jeupe unatembea
na Bwana Yesu katika maisha yako.
Kwahiyo, nimalizie kusema dhambi inafanya
waliokuheshimu kukudharau kwa sababu wameona uchi
wako. Umekuwa mtupu na wazi, yale uliyofanya sirini
kwamba watu hawakuoni yako wazi na heshima yako
imepotea. Kama umerudi nyuma kiroho bado waweza
kusimama tena. Neno la Mungu linasema katika Ayubu
14:7-9 kwamba;
“7 Kwani yako matumaini ya mti, ya kuwa ukikatwa utachipuka
tena, Wala machipukizi yake hayatakoma. 8 Ijapokuwa mizizi
yake huchakaa mchangani, Na shina lake kufa katika udongo; 9
Lakini kwa harufu ya maji utachipuka, Na kutoa matawi kama
mche”.
“Dhambi
inafanya
waliokuheshim
u kukudharau
kwa sababu
wameona uchi
wako.”
16
#DONDOO YA SABA
Dondoo ya saba [7] kuhusu dhambi ambayo ndiyo ya mwisho katika mfululizo
wa dondoo hizi kuhusu dhambi inasema “Dhambi inauficha uso wa Mungu
usiuone, Hata asitake kusikia”. Neno la Mungu katika Isaya 59:2 linasema
“…………dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki
kusikia”.
Katika mstari wa 2 kama tulivyosoma kuna pointi mbili za kujifunza, nami
nitafafanua kama ifuatavyo;
Twende taratibu, nikiurudia mstari wa 2 ili tuone hizo pointi. Maandiko
yanasema “…………dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone [huu
ni upande wa atendaye dhambi-HAWEZI KUUONA USO WA
MUNGU], hata hataki kusikia [huu ni upande wa Mungu-HAWEZI
KUSIKIA MAOMBI/MAHITAJI YA AOMBAYE]”.
Sehemu zilizo katika [ ] ni ufafanuzi kutilia mkazo wa uelewa.Tumeona sasa,
kwamba dhambi inauficha uso wa Mungu kwake atendaye dhambi na
humfanya asiweze kuuona huo uso wa Mungu.
Kufahamu hili vizuri twaweza kurejea habari za mfalme Sauli katika 1
Samweli 28:6 “Lakini Sauli alipouliza kwa BWANA, BWANA
hakumjibu, wala kwa ndoto, wala kwa Urimu, wala kwa
manabii”. Mfalme Sauli hakuwa na tabia ya kutubu alipokosea bali alijenga
hoja za kujitetea aonekane hana kosa, Hakujua kwamba dhambi ingemfanya
kutouona uso wa Mungu. Katika mstari wa 6, Mfalme Sauli yupo kwenye
uhitaji wa kujua vita iliyo mbele yake kama angeshinda au la na alipoutafuta
uso wa Mungu kwa maombi hakupata majibu iwe kwa ndoto au kwa Urimu au
manabii.
17
Tunajifunza hata sisi tukisoma habari hizi, Sikiliza! unapokosea na ukakaa bila
kutubu matokeo yake utayaona siku upo kwenye uhitaji utakapotafuta uso wa
Mungu bila kupata majibu yoyote. Dhambi inauficha uso wa Mungu na huwezi
kuuona, inakuwa kizuizi cha kumwona Mungu.
18
#MAOMBI YA TOBA
Baada ya kusoma dondoo hizi Je! unataka kuokoka? waweza fuatisha maombi
haya;
“Bwana Yesu, ni wewe uliyatoa maisha yako kwa ajili yangu msalabani, ulilipa
deni ya dhambi zangu na kufuta hukumu zote shetani alizonishitaki. Sasa ninakuja
kwako tena kwa upya, ninatubu dhambi zangu zote. Naomba damu ya Yesu Kristo
iliyomwagika msalabani kwa ajili yangu initakase sasa katika roho yangu na nafsi
yangu na mwili wangu. Nimefungua moyo wangu. Bwana Yesu Kristo
nakukaribisha ndani yangu. Ingia kwa uwezo wa Roho wako – uwe Bwana na
Mwokozi wangu kuanzia sasa na siku zote. Ahsante kwa kunisamehe na kwa
kuniokoa. Nimejitoa kwako nikutumikie katika siku zote za maisha yangu. Shetani
hana mamlaka tena juu yangu katika jina la Yesu Kristo. Amina”
Kama umefuatisha maombi haya na unahitaji msaada zaidi tumia namba
0764771298/0652034083 kuwasiliana nasi. Mungu akubariki!
MWISHO
19
# IJUE VIJANA NA UTUMISHI
-Inahusika na nini?
VIJANA NA UTUMISHI inafanya yafuatayo;
1. Kuwajenga VIJANA ki-Utumishi ili KUMTUMIKIA Mungu kwa
huduma mbalimbali ambazo Mungu ame-INVEST kwa VIJANA
[kanisa] kupitia njia zifuatazo;
Jumbe mbalimbali za Neno la Mungu & Masomo ya Utumishi
Kutoa Majibu ya Maswali yaulizwayo na VIJANA [Maswali &
Majibu]
Ushauri kwa VIJANA
2. Katika kutimiza kusudi no. 1 hapo huu, VIJANA NA UTUMISHI
inatengeneza “UWANJA” au PLATFORM kwa VIJANA kutumia
vipawa na nafasi zao kwa utukufu wa Mungu.
Baada ya kukisoma kitabu hiki, je! una ushuhuda, maoni au ungependa
kushirikiana na VIJANA UTUMISHI? Usisite kututumia ushuhuda/maoni
yako kupitia mawasiliano yetu
Cell: +255 764 771 298
Email: [email protected]
20
-Kama hukupata vitabu hivi “JIFUNZE UKUE KIROHO” na “MAMBO
MUHIMU UNAPOANDAA SOMO/UJUMBE WA KUFUNDISHA”
waweza kuwasiliana nasi