36
Nakala Maalum Dunia Yako INAPOBADILIKA

Dunia Yako INAPOBADILIKAdownloads.biblica.com/free-resources/Swahili... · machozi yako na yatiririke kama mto usiku na mchana; usijipe nafuu, macho yako yasipumzike. Inuka, lia usiku,

  • Upload
    others

  • View
    6

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Dunia Yako INAPOBADILIKAdownloads.biblica.com/free-resources/Swahili... · machozi yako na yatiririke kama mto usiku na mchana; usijipe nafuu, macho yako yasipumzike. Inuka, lia usiku,

Nakala Maalum

Dunia YakoI N A P O B A D I L I K A

SWAHILI: WYWWC-SE

Page 2: Dunia Yako INAPOBADILIKAdownloads.biblica.com/free-resources/Swahili... · machozi yako na yatiririke kama mto usiku na mchana; usijipe nafuu, macho yako yasipumzike. Inuka, lia usiku,

Dunia Yako I N A P O B A D I L I K A

Kujenga Nguvu Zako za Kiroho katika Nyakati za Mashaka

Nakala Maalum

Page 3: Dunia Yako INAPOBADILIKAdownloads.biblica.com/free-resources/Swahili... · machozi yako na yatiririke kama mto usiku na mchana; usijipe nafuu, macho yako yasipumzike. Inuka, lia usiku,

YaliyomoUtangulizi: Kutaendaje sasa?Siku ya 1 Nisaidie!Siku ya 2 Kujihisi Kukosa UsalamaSiku ya 3 Yatosha!Siku ya 4 Je, Mungu Anatuadhibu?Siku ya 5 Machozi YasiokomeshwaSiku ya 6 Nani Anaelewa?Siku ya 7 Je, Mungu Kweli ni Mwema?Siku ya 8 Pweke katika HuzuniSiku ya 9 Usalama katika VuruguSiku ya 10 Kutamani UshirikianoSiku ya 11 HasiraSiku ya 12 Je, Umetenganishwa na Mungu?Siku ya 13 Kutotengeka!Siku ya 14 Thubutu Kutumaini!Siku ya 15 Kuhisi Kukwama

Siku ya 16 Kuthibitishiwa Kukosa UhakikaSiku ya 17 Huzuni KuondokaSiku ya 18 Sio Mtu Yule wa AwaliSiku ya 19 Kupata Furaha MaishaniSiku ya 20 Kusonga MbeleSiku ya 21 KuridhikaSiku ya 22 Upendo MkarimuSiku ya 23 Kushiriki FarajaSiku ya 24 Karama ya KusaidiaSiku ya 25 Pendaneni Mmoja na MwingineSiku ya 26 Kuchagua KusameheSiku ya 27 Kuishi Maisha KamiliSiku ya 28 Tumaini LinarejeshwaSiku ya 29 Kuishi VyemaSiku ya 30 Nguvu za Kuishi KeshoHitimisho: Janga la COVID-19 limebadilisha dunia yetu yote.

Page 4: Dunia Yako INAPOBADILIKAdownloads.biblica.com/free-resources/Swahili... · machozi yako na yatiririke kama mto usiku na mchana; usijipe nafuu, macho yako yasipumzike. Inuka, lia usiku,

Kutaendaje sasa?Janga kama ugonjwa huu wa COVID-19 unaoenea kila mahali linapotokea na kushinda kuthibitika, uwezo wetu wa kukabiliana nalo unazidiwa ghafla. Muungano huu wa mahitaji makuu na kukosa muda wa maandalizi unalemaza uwezo wa serikali na mashirika ya afya kuweza kuthibiti janga, na pia hali hii inashinda uwezo wa miundo msingi inayotoa huduma muhimu.

Kwa hali ya kibinafsi, tunapambana kupata njia katika kiwewe, hofu, na uchungu wa kupoteza wapendwa au mali unaoletwa na janga hili.

Ni watu wachache sana kati yetu wamekumbana na hali ya hatari kama hii, hata wale walio mstari wa mbele katika kukumbana na hali ya hatari ya ugonjwa au maafa. Wengi wetu hatujawahi kuvumilia mabadiliko makubwa ya ghafla kama haya katika maisha yetu ya kila siku. Hatujawahi kukumbana na hali ya kutatanisha ya mabidikilo ya mambo kwa kiasi kikubwa hivi.

Janga la COVID-19 linaathiri kila kitu maishani mwetu, ikiwemo kila wazo, kila uamuzi, kila tendo la kila dakika mchana kutwa. Hatuwezi kujua kesho itatuletea hali gani. Tunajiuliza kana kwamba matukio tunayoyaona katika runinga au kuyasikia yatakuwa matukio yetu kesho.

Katikati ya misukosuko hii, tunaomba faraja, utulivu, na tumaini. Biblia ambayo ni Neno la Mungu kwa walimwengu ni hadithi ya upendo wa kuaminika wa Mungu kwa kila mmoja wetu katika kila hali ya maisha. Hili Neno linaweza kututia moyo sana nyakati kama hizi. Linatusaidia kunena hisia zetu za hasira, huzuni kubwa, hofu, na hata matumaini. Linatufariji leo na kututia nguvu kwa ajili ya siku za usoni. Linatusaidia kuona mbele ya shida za hivi sasa na kuona tumaini la milele ambalo Mungu analeta katika kila hali ya maisha.

Masomo haya ya kila siku yanachunguza mawazo yetu na hisia zingine za kawaida tunazopitia katika janga hili la ugonjwa wa COVID-19. Kila somo linahusisha swali au wazo lililotokana na manusura wa majanga na misukosuko, pia lina kifungu cha kusoma kutoka kwa Biblia, na maneno ya kutia moyo ya kukusaidia kustahimili changamoto mpya za maisha ya kila siku. Masomo yanamalizia kwa wazo au swali lako wewe kutafakari unapoendelea na shughuli zako za siku, au wazo la kukusaidia kuomba au kuweka kumbukumbu.

Mungu akubariki na kukuhifadhi kila wakati, siku baada ya nyingine, unapojaribu kumfuata Yesu kwa uaminifu hata wakati dunia yako nzima inapobadilika.

Page 5: Dunia Yako INAPOBADILIKAdownloads.biblica.com/free-resources/Swahili... · machozi yako na yatiririke kama mto usiku na mchana; usijipe nafuu, macho yako yasipumzike. Inuka, lia usiku,

Nisaidie!Nashangaa!

Nilikuwa nimesikia kwamba ugonjwa wa COVID-19 ungekuwa mbaya, lakini sikudhania janga la ulimwengu wote lingekuwa hivi kwangu, kwa jamaa wangu, na kwa jumuia yangu.

Ni mbaya kuliko nilivyotarajia.

Hata tukifanya yote yanayotakikana, kukaa nyumbani, na kuwa mbali na wenzetu, sina uhakika kwamba niwapendao zaidi watakuwa salama.

Nifanyeje sasa?

Nitapata msaada wapi?

Sote tumepata habari kuhusu majanga. Picha na sauti za maeneo ya mtetemeko wa ardhi, mafuriko, vita, njaa, na magonjwa zinatupa picha kama ya watalii walio mbali na utata huo. Lakini hazianzi kamwe kutuletea mashaka, hasara na uchungu ambao matukio haya yanawaletea watu walioathiriwa.

Na sasa kwa sababu tumepatwa na janga la ugonjwa wa ulimwengu wote, maisha ni magumu zaidi kwa kila mtu. Inatubidi sote tufanye mabadiliko ili kukumbana na uwezekano wa hasara chungu. Kustahimili yaliyo mbele zetu kunaweza kuchukua nguvu zetu zote na uwezo wetu, na hata mengi zaidi.

Hatuko peke yetu wakati tunahisi kuchoka, kukosa nguvu, au kupungukiwa. Kunao wengine ambao wamehitaji msaada nyakati ngumu maishani pia. Vifungu vifuatavyo kutoka kwa kitabu cha Zaburi vilitungwa na Mfalme Daudi, mtu aliyefahamu vizuri hali za kutaabika na uchungu wa moyo. Pengine anaelezea baadhi ya hisia ambazo unapitia.

Ee Bwana unihurumie, kwa kuwa niko kwenye shida;macho yangu yanafifia kwa huzuni,nafsi yangu na mwili wangu kwa sikitiko.Maisha yangu yamedhoofika kwa majonzi,naam, miaka yangu kwa kulia kwa maumivu makali;nguvu zangu zinaisha kwa ajili ya mateso,na mifupa yangu inachakaa.

Atukuzwe Bwana,kwa kuwa amenionyesha upendo wake wa ajabunilipokuwa katika mji uliozingirwa.Katika hofu yangu nilisema,“Nimekatiliwa mbali na macho yako!”Hata hivyo ulisikia kilio changuukanihurumia nilipokuita unisaidie.Zaburi 31:9-10, 21-22

Je, ungependa kumwambia Mungu nini kuhusu janga linalokukumba, na pia athari linazokuletea leo hii?

SIKU YA 1 •••••••••••••••••••••••••••••••

Page 6: Dunia Yako INAPOBADILIKAdownloads.biblica.com/free-resources/Swahili... · machozi yako na yatiririke kama mto usiku na mchana; usijipe nafuu, macho yako yasipumzike. Inuka, lia usiku,

Kujihisi Kukosa UsalamaNi mengi sana yametendeka, na mambo yanaendelea kutendeka.

Siwezi kuzuia uvamizi wa habari mbaya. Siwezi hata kulinda na kutegemeza nyumba yangu na jamaa.

Najihisi kukosa nguvu na kukosa usalama.

Ulimwengu hauna usalama tena.

Sababu moja inayoyafanya majanga ya magonjwa kuhofisha ni kwamba yanatushinda uwezo wa kuyathibiti. Tunaweza kufahamu yanayotukia, lakini hatuwezi kujua athari zake zitatukumba kwa kiasi gani, au zitadumu kwa muda gani.

Hatujui ni lini, au hata kama maisha yetu yatarejea kwa hali ya kawaida. Kwa wengi wetu, wasiwasi huo si mzuri.

Tunapozoea kutumia uwezo wetu na nguvu zetu kwa usalama, tunaweza kujihisi kupungukiwa sana wakati janga linatunyang’anya kujithibiti kwetu. Lakini wakati hatuna uwezo wa kujisaidia, Mungu, aliye Muumba wa mbingu na nchi, bado ni mwenye nguvu na ni mwema.

Tunapata nguvu tunapojiunganisha na Mungu, aliye nguvu za uhai kwa ulimwengu wote.

Bwana hupenda uadilifu na haki;dunia imejaa upendo wake usiokoma.

Kwa neno la Bwana mbingu ziliumbwa,jeshi lao la angani kwa pumzi ya kinywa chake.Ameyakusanya maji ya baharikama kwenye chungu;vilindi vya bahariameviweka katika ghala.Dunia yote na imwogope Bwana,watu wote wa dunia wamche.Kwa maana Mungu alisema, na ikawa,aliamuru na ikasimama imara.

Sisi tunamngojea Bwana kwa matumaini,yeye ni msaada wetu na ngao yetu.Mioyo yetu humshangilia,kwa maana tunalitumainia jina lake takatifu.Upendo wako usio na mwisho ukae juu yetu, Ee Bwana,tunapoliweka tumaini letu kwako.Zaburi 33:5-9, 20-22

Nguvu na wema za Mungu wetu mwenye uwezo wote haziwezi kupunguzwa na janga lolote linalotukumba.

Je, utamtumaini Mungu kuwa msaada na ngao yako katika sehemu gani za kupungukiwa kwako?

•SIKU YA 2 ••

••••••••••••••••••••••••••••

Page 7: Dunia Yako INAPOBADILIKAdownloads.biblica.com/free-resources/Swahili... · machozi yako na yatiririke kama mto usiku na mchana; usijipe nafuu, macho yako yasipumzike. Inuka, lia usiku,

Yatosha!Nimeshindwa! Siwezi kumakinika kwa lolote.

Ni vigumu sana kukumbuka yale watu wanajaribu kuniambia. Nimechoka kabisa, lakini siwezi kupata usingizi. Nahisi kuchafuka roho hadi siwezi kula.

Nakerwa na kila mtu, na nakosa uvumilivu kwa mambo yote. Nataka yote yaniondokee!

Kukumbana na janga au hangaiko ni vigumu kwa njia nyingi sana. Kila sehemu ya maisha inaweza kutatanishwa na yale yanayotendeka. Njia zetu za kutenda mambo hazitusaidii tena. Kuweza kufanya lolote ni changamoto, na kuna mengi sana ya kufanya ambayo hatujui tuanzie wapi.

Kuyatatua haya yote ni kazi ngumu mno.

Kuenenda katika shughuli zetu za kila siku kunatukumbusha yale tumeyapoteza, na vile hatuna hakika na matukio ya kesho. Kuomboleza kwa hasara hizi na kukabili hofu zetu kunadhoofisha hisia zetu. Ndiposa tunajihisi kushindwa!

Lakini tunaweza kuwa na hakika katika jambo hili: Kwamba Mungu anasikia kilio chetu na anatupa uwepo wake kuwa nasi.

Ee Mungu, sikiliza maombi yangu,wala usidharau hoja yangu.Nisikie na unijibu.Mawazo yangu yananisumbua na nimehangaishwa …

Moyo wangu umejaa uchungu,hofu ya kifo imenishambulia.Woga na kutetemeka vimenizunguka,hofu kuu imenigharikisha.Nilisema, “Laiti ningekuwa na mbawa za njiwa!Ningeruka niende mbali kupumzika.Ningalitorokea mbali sanana kukaa jangwani,ningaliharakisha kwenda mahali pa salama,mbali na tufani kali na dhoruba.

Lakini ninamwita Mungu,naye Bwana huniokoa.Jioni, asubuhi na adhuhurininalia kwa huzuni,naye husikia sauti yangu.Zaburi 55:1-2, 4-8, 16-17

Je, unamtafuta Mungu kuwa kimbilio na nguvu zako kwa njia gani katika siku hizi za taabu?

••

SIKU YA 3 •••••••••••••••••••••••••••••

Page 8: Dunia Yako INAPOBADILIKAdownloads.biblica.com/free-resources/Swahili... · machozi yako na yatiririke kama mto usiku na mchana; usijipe nafuu, macho yako yasipumzike. Inuka, lia usiku,

Je, Mungu Anatuadhibu?Ninapowaza peke yangu, ninajiuliza kwa nini Mungu ameruhusu janga hili la ugonjwa kutukia.

Je, Mungu ana ghadhabu nasi?

Je, Mungu anatuadhibu?

Watu wengine husema anatuadhibu kweli, na kwamba twastahili kuadhibiwa. Jambo hili lanipa hisia za kuwa mkosaji kwa matukio haya.

Je, Mungu bado anatupenda, au ametuachilia?

Biblia inatupa habari za mtu aliyeitwa Ayubu, ambaya alipatwa na majanga yaliyofuatana ghafla. Aliwapoteza watoto wake wote aliowapenda sana, usalama wake wa kifedha ukafutiwa mbali kabisa, na akawa mgonjwa kabisa. Baadhi ya rafiki zake wakasisitiza kwamba lazima alikuwa ametenda jambo baya sana lililomsababisha Mungu kumwadhibu.

Rafiki ya Ayubu aliyeitwa Elifazi akasema haya:

Ni mtu yupi asiye na hatia ambaye aliwahi kuangamia?Ni wapi wanyofu waliwahi kuangamizwa?Kwa jinsi ambavyo mimi nimechunguza,wale walimao ubayana wale hupanda uovu,huvuna hayo hayo.Kwa pumzi ya Mungu huangamizwa;kwa mshindo wa hasira zake huangamia.Ayubu 4:7-9

Hebu tafakari vile Ayubu alihisi baada ya “kutiwa moyo” hivyo! Lakini Mungu alisema kwamba rafiki yake Ayubu alikosea. Mungu hakutuma majanga kwa Ayubu. Matukio ya majonzi na nyakati za ugumu ambazo huleta mateso makubwa zaweza kumjia mtu yeyote. Lakini nyakati hizi zikija, tunaweza kutegemea upendo wa Mungu kwetu usiokoma.

Nayakumbuka mateso yangu na kutangatanga kwangu,uchungu na nyongo.Ninayakumbuka vyema,nayo nafsi yangu imezimia ndani yangu.Hata hivyo najikumbusha neno hilina kwa hiyo ninalo tumaini.Kwa sababu ya upendo mkuu wa Bwana, hatuangamii,kwa kuwa huruma zake hazikomi kamwe.Ni mpya kila asubuhi,uaminifu wako ni mkuu.Maombolezo 3:19-21

Hofu ya kuwa tumejiletea janga ni mzigo mzito moyoni. Lakini kwa sababu ya upendo mkuu wa Mungu kwetu usiokoma, hatupaswi kubeba mzigo huo. Tunaweza kupata pumziko katika faraja ya upendo wake.

Shiriki na Mungu ukimweleza upendo wake una maana gani kwako wakati huu.

•••

SIKU YA 4 ••••••••••••••••••••••••••••

Page 9: Dunia Yako INAPOBADILIKAdownloads.biblica.com/free-resources/Swahili... · machozi yako na yatiririke kama mto usiku na mchana; usijipe nafuu, macho yako yasipumzike. Inuka, lia usiku,

Machozi YasiokomeshwaNajipata nikilia wakati usiotarajiwa.

Nahisi vibaya sana nikiwa peke yangu, lakini ninapolia mbele ya watu wengine, najihisi mnyonge na ninaaibika. Nahisi kujielezea kwa watu, lakini wakati mwingi siwezi.

Najihisi nikiwa na huzuni nyingi na kuvunjika moyo.

Sio jambo la ajabu kupata hisia kuu za huzuni, uchungu, au hisia zingine wakati wa janga.

Kuelezea hisia hizi kwa njia mbali mbali, hata machozi, yaweza kuwa njia bora ya kustahimili janga na kupona kutokana na yote yanayotukia. Na kwa sababu ya upendo mkuu wa Mungu kwetu, hatupaswi kuficha hisia hizo mioyoni mwetu. Tunaweza kumwelezea Mungu uchungu wetu wote wa moyoni.

Mungu anafahamu kabisa ukweli wa mateso ya wanadamu, na anatuita tumlilie tunapoteseka.

Tunapofadhaika, Mungu anahisi uchungu wetu. Tunapoomboleza, Mungu anaomboleza pamoja nasi.

Hakuna jambo lililo mbali lisiloweza kufikiwa na upendo wake wa ukombozi, liwe ni janga au uchungu wa moyo.

Mioyo ya watuinamlilia Bwana.Ee ukuta wa Binti Sayuni,machozi yako na yatiririke kama mtousiku na mchana;usijipe nafuu,macho yako yasipumzike.Inuka, lia usiku,zamu za usiku zianzapo;mimina moyo wako kama majimbele za Bwana.Mwinulie yeye mikono yakokwa ajili ya maisha ya watoto wako,ambao wanazimia kwa njaakwenye kila mwanzo wa barabara.

Macho yangu yatatiririka machozi bila kukoma,bila kupata nafuu,hadi Bwana atazame chinikutoka mbinguni na kuona.

Nililiitia jina lako, Ee Bwana,kutoka vina vya shimo.Ulisikia ombi langu: “Usikizibie masikio yakokilio changu nikuombapo msaada.”Ulikuja karibu nilipokuita,nawe ukasema, “Usiogope.”Maombolezo 2:18-19; 3:49-50, 55-57

Mungu yuko upande wa wale wanaoteseka. Tunaweza kumtegemea kutukaribia tunapomwelezea uchungu wa mioyo yetu.

Je, ombi lako la shukrani kwa uwepo wa Mungu katikati ya uchungu wako ni lipi?

••••

SIKU YA 5 •••••••••••••••••••••••••••

Page 10: Dunia Yako INAPOBADILIKAdownloads.biblica.com/free-resources/Swahili... · machozi yako na yatiririke kama mto usiku na mchana; usijipe nafuu, macho yako yasipumzike. Inuka, lia usiku,

Nani Anaelewa?Nilidhania mambo yangekuwa shwari kidogo, lakini habari za leo hazikuwa nzuri.

Nimevunjika moyo na kuchoshwa na janga hili.

Sitaki kusikia habari zingine za redio wala kuziona katika runinga.

Sihitaji ukumbusho kwamba mambo yangekuwa mabaya zaidi.

Sitaki kuona uso mwingine ukitabasamu na kuniambia kwamba kupitia haya yote kunatujenga tabia na kutuleta pamoja.

Hawaelewi mambo yalivyo kwangu mimi.

Hiyo ni kweli. Hakuna yeyote kati yetu ajuaye au kufahamu hali ilivyo kwa mtu mwingine kukumbana na janga hili.

Tungependa kusaidiana na kufarijiana mmoja na mwingine, lakini mara nyingi hatujui jinsi ya kufanya hivyo. Kwa hiyo, tusipowasikiliza wengine, tunaweza kupeana kauli za haraka na zisizofaa ambazo zinazidisha mfadhaiko na uchungu kuliko kutoa faraja.

Lakini kuna yule anayekufahamu kabisa na anakupenda zaidi ya vile unaweza kufikiria. Anajua kila jambo kukuhusu, kila hisia na wazo. Anafahamu kwa hakika kila hitaji lako, na anakualika uje kwake:

“Njooni kwangu, ninyi nyote mnaotaabika na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jifungeni nira yangu, mjifunze kutoka kwangu, kwa maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata raha nafsini mwenu. Kwa maana nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi.”Mathayo 11:28-30

Maneno yake na uwepo wake huwapa wote wamtafutao faraja ya kweli:

Ee Bwana, umenichunguzana kunijua.Unajua ninapoketi na ninapoinuka;unatambua mawazo yangu tokea mbali.Unafahamu kutoka kwangu na kulala kwangu;unaelewa njia zangu zote.Kabla neno halijafika katika ulimi wangu,wewe walijua kikamilifu, Ee Bwana.Zaburi 139:1-4

Je, ingekuwa faraja aje kujulikana na kufahamika, na kupata pumziko katika uchovu ulio nao? Haustahili kubeba mzigo huu peke yako.

Je, utamtumainia Mungu kukufahamu na kukupa pumziko?

•••••

SIKU YA 6 ••••••••••••••••••••••••••

Page 11: Dunia Yako INAPOBADILIKAdownloads.biblica.com/free-resources/Swahili... · machozi yako na yatiririke kama mto usiku na mchana; usijipe nafuu, macho yako yasipumzike. Inuka, lia usiku,

Je, Mungu Kweli ni Mwema?Sielewi kwa nini Mungu aliruhusu janga hili kutukia.

Adui ambaye hatuwezi kumwona anatokea ghafla na kuanza kuua watu wasio na hatia kiholelaholela. Hata wauguzi, madaktari na wanaotibu kwa haraka wanaofanya kazi mchana na usiku kuwasaidia wagonjwa wanakuwa wagonjwa na kufa.

Hii si sawa hata kidogo! Je, Mungu anawezaje kuruhusu janga hili?

Tunapoteseka kwa sababu ya tatizo chungu, ni kawaida kuuliza maswali.

Tunataka kujua tutamlaumu nani, kwa nini tatizo lilitukia, jambo lipi lingefanywa ili kulizuia, tunaweza kufanya nini zaidi ili kulisimamisha, na Mungu naye anafanya nini katika tatizo hili.

Kuuliza maswali magumu ni jambo la uchungu, hasa tunapokosa majibu, na kuanza kushuku tabia ya Mungu na jukumu lake katika matukio haya.

Hatuko peke yetu katika kutenda haya. Ayubu alipopoteza watoto wake, mali yake, na afya yake, alikuwa na uchungu kwa yale ambayo yalimpata. Alitetea haki yake, akamshuku Mungu, akamlaumu Mungu, na hata akamtaka Mungu amjibu! La ajabu ni kwamba Mungu alisikiliza maneno yote ya Ayubu. Ayubu alipomaliza kusema, Mungu akamwelezea jinsi ilivyo kuwa Mungu aliyeumba, anayependa na kutunza kwa dhati kila hali ya ulimwengu! Mungu akasema,

“Je, mwenye kushindana na Mwenyezi aweza kumsahihisha?Mwenye kumlaumu Mungu na ajibu.”Ndipo Ayubu akamjibu Bwana: “Mimi sistahili kabisa: ninawezaje kukujibu wewe?Nauweka mkono wangu juu ya kinywa changu.Nimesema mara moja, lakini sina jibu;naam, nimesema mara mbili,lakini sitasema tena.”

“Ninajua ya kuwa unaweza kufanya mambo yote,wala hakuna mpango wako unaoweza kuzuilika.Uliuliza, ‘Ni nani huyu afichaye mashauri yangu bila maarifa?’Hakika nilisema juu ya mambo niliyokuwa siyaelewi,mambo ya ajabu mno kwangu mimi kuyajua.Ayubu 40:2-5; 42:2-3

Tunaweza kukosa majibu ya matatizo yetu, lakini Mungu ni mwema na anatupenda, na anatenda kazi kwa njia za nguvu ambazo hatuwezi kufikiria hata kamwe.

Je, una mashaka gani na maswali unayohitaji kushiriki na Mungu leo hii?

••••••

SIKU YA 7 •••••••••••••••••••••••••

Page 12: Dunia Yako INAPOBADILIKAdownloads.biblica.com/free-resources/Swahili... · machozi yako na yatiririke kama mto usiku na mchana; usijipe nafuu, macho yako yasipumzike. Inuka, lia usiku,

Pweke katika HuzuniMoyo wangu una uchungu!

Watu wanapoteza kazi zao, na hata wengine makazi yao. Wanafunzi wanakosa masomo ya kuwaendeleza na kuwapa fursa siku za usoni. Baadhi ya wafanya biashara wamepoteza mapato yao na hata akiba zao.

Nao wengi sana wamepoteza maisha yao.

Kuzidisha makali, hatuwezi kusimama na wenzetu walio na uchungu.

Nimekufa moyo kiasi kwamba wakati mwingine sijui niendelee aje na maisha.

Mungu hakutuumba kujihudumia katika huzuni zetu. Alituweka katika jamaa, na marafiki, na katika jumuiya ili tuweze kushiriki na wenzetu katika nyakati za mema na za mabaya maishani.

Biblia inathibitisha umuhimu wa mahusiano yetu na wenzetu; inatufunza kwamba wawili ni bora kuliko mtu mmoja, na inatutia moyo kupendana mmoja na mwingine. Hata majadiliano kati ya wawili au kushiriki chakula pamoja kunaweza kuinua mioyo yetu.

Lakini tufanyeje wakati tatizo linatushurutisha kuwa pweke, wakati tumekufa moyo na kuwa wachofu? Tumaini letu la ushirika, faraja na kutiana moyo liko wapi wakati huu? Biblia inatuelezea kuhusu Eliya, mtu aliyekumbana na matatizo ya kutishia maisha, na akahisi kuachiliwa na kuwa pweke kiasi kwamba alikata tamaa ya kuishi tena.

Akasema, “Yatosha sasa, Bwana, ondoa roho yangu, kwani mimi si bora kuliko baba zangu.” Kisha akajinyoosha chini ya mti, akalala usingizi.

Mara malaika akamgusa na akamwambia, “Inuka na ule.” Akatazama pande zote, napo hapo karibu na kichwa chake palikuwepo mkate uliookwa kwenye makaa ya moto na gudulia la maji. Akala na kunywa, kisha akajinyoosha tena.

Yule malaika wa Bwana akaja tena mara ya pili, akamgusa akamwambia, “Inuka na ule, kwa kuwa safari ni ndefu kwako.” Kwa hiyo akainuka, akala na kunywa. Akiwa ametiwa nguvu na kile chakula, akasafiri siku arobaini usiku na mchana mpaka akafika Horebu, mlima wa Mungu. 1 Wafalme 19:4-8

Mungu alifahamu kiasi ambacho Eliya alikuwa amekufa moyo, naye akamtumia msaada kimuujiza. Mungu anaelewa uchungu wa moyo wako pia.

Omba Mungu akupe moyo ulio tayari kupokea karama za Mungu za kukutia moyo.

•••••••

SIKU YA 8 ••••••••••••••••••••••••

Page 13: Dunia Yako INAPOBADILIKAdownloads.biblica.com/free-resources/Swahili... · machozi yako na yatiririke kama mto usiku na mchana; usijipe nafuu, macho yako yasipumzike. Inuka, lia usiku,

Usalama katika VuruguKila siku huleta mabadiliko mapya maishani.

Hakuna chochote kilicho rahisi kama awali, hata kwenda dukani kununua mkate au maziwa.

Mambo yote yamevurugika.

Naogopa yale yatakayotukia kesho. Je, itakuwaje kama nitakosa chakula au dawa? Je, maisha yatarudia kuwa ya kawaida?

Popote unapoishi duniani, janga la ugonjwa wa COVID-19 linaleta mabadiliko yasiyo ya kawaida, na pia mashaka katika maisha ya kila siku. Hakuna awezaye kuepuka athari za ugonjwa huu wala mabadiliko yanayohitajika ili kupunguza kuenea kwake. Serikali nyingi zinasumbuka kutafuta njia bora za kuweka amri na kugeuza tabia za watu.

Kila mtu anajifunza na kukosea.

Matokeo ni vurugu. Ni jambo linalofadhaisha sana.

Tunapobadilisha mfumo wa maisha ya kila siku na kuingia kwa “ukawaida mpya” hapa duniani, tunaweza kuwa na hakika kwamba hakuna chochote kimebadilika kwake Mungu. Bado anatupenda. Bado anatutunza. Bado yeye ni jiwe letu imara la tumaini na nguvu anayetuahidi kuwa pamoja nasi, licha ya majanga yoyote yanayotukumba.

Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu,msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.Kwa hiyo hatutaogopa, hata kama dunia ikiondolewanayo milima ikiangukia moyoni mwa bahari.Hata kama maji yake yatanguruma na kuumuka,milima nayo ikitetemeka kwa mawimbi yake.Zaburi 46:1-3

Hivyo usiogope, kwa maana niko pamoja nawe;usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako.Nitakutia nguvu na kukusaidia;nitakutegemeza kwa mkono wa kuume wa haki yangu.Isaya 41:10

Bwana yu karibu. Msijisumbue kwa jambo lolote, bali katika kila jambo kwa kuomba na kusihi pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Nayo amani ya Mungu, inayopita fahamu zote, itailinda mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.Wafilipi 4:5-7

Omba Mungu akupe amani ya kukuwezesha kupunguza wasiwasi, na hofu, na kukosa usalama.

Mtegemee Mungu kukupa msaada na nguvu wakati huu.

••••••••

SIKU YA 9 •••••••••••••••••••••••

Page 14: Dunia Yako INAPOBADILIKAdownloads.biblica.com/free-resources/Swahili... · machozi yako na yatiririke kama mto usiku na mchana; usijipe nafuu, macho yako yasipumzike. Inuka, lia usiku,

Kutamani UshirikianoSikuwahi kufikiria kwamba virusi vingenitenganisha na shughuli nilizozipenda na pia watu wa maana kwangu. Lakini sasa tunashiriki masomo ya kanisa kupitia simu za mkono na kompyuta. Nafurahia mafundisho ya mchungaji wetu, lakini nakosa sana ushirika, mazungumzo, maombi ya pamoja, na kutiana moyo.

Nyakati za kutenganishwa na jumuiya zetu zinazotutegemeza ni ngumu mno.

Tunahisi upweke na hatuupendi kamwe, lakini haya ni ya kawaida. Mungu anataka washirika wa mwili wa Kristo kuwa na mahusiano ya upendo na ya maana kati ya mmoja na mwingine; mahusiano tunayotamani wakati tumetenganishwa.

Wakristo wa pale mwanzoni pia walivumilia hali ngumu ya kutenganishwa na jamaa zao za kiroho.

Basi, ndugu zangu, nawasihi kwa Jina la Bwana wetu Yesu Kristo na kwa upendo wa Roho Mtakatifu, kujiunga nami katika taabu zangu mkiniombea kwa Mungu.

… ili kwa mapenzi ya Mungu niweze kuja kwenu kwa furaha, nami niburudishwe pamoja nanyi. Mungu wa amani na awe pamoja nanyi nyote. Amen.Warumi 15:30, 32-33

Siku zote tunamshukuru Mungu kwa ajili yenu ninyi nyote, tukiwataja kwenye maombi yetu daima. Tunaikumbuka daima kazi yenu ya imani mbele za Mungu aliye Baba yetu, taabu yenu katika upendo na saburi yenu ya tumaini katika Bwana wetu Yesu Kristo.

Kwa hiyo farijianeni na kujengana, kama vile mnavyofanya sasa.… Furahini siku zote; ombeni bila kukoma; shukuruni kwa kila jambo, kwa maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu kwa ajili yenu katika Kristo Yesu.1 Wathesalonike 1:2-3; 5:11, 16-18

Ni kweli inahitaji bidii zaidi kuuelezea upendo wetu na kudumisha mahusiano yetu ya kijumuiya tunapotekeleza agizo la kukaa mbali mmoja na mwingine. Lakini hata tukiwa mbali mmoja na mwingine, uhusiano wetu katika Kristo unatuunganisha. Nasi tutafurahia tutakapokutana tena.

Kwa sasa, tuombeane mmoja na mwingine, na tutie bidii katika kudumisha mahusiano yetu ya muhimu ya kiroho wakati huu wa kutenganishwa na kuwa mbali na wenzetu.

•••••••••

SIKU YA 10 ••••••••••••••••••••••

Page 15: Dunia Yako INAPOBADILIKAdownloads.biblica.com/free-resources/Swahili... · machozi yako na yatiririke kama mto usiku na mchana; usijipe nafuu, macho yako yasipumzike. Inuka, lia usiku,

HasiraJe, nimekasirika? Wewe unafikiri aje?

Hatuwezi hata kukimu mahitaji yetu muhimu, na sipati msaada popote. Ni kana kwamba hakuna anayejali.

Ndiyo, nimekasirika! Nimekasirishwa sana na kila kitu!

Inakatisha tamaa sana wakati tunapoteza udhibiti wa maisha yetu wakati tunapitia janga hili la ugonjwa wa Covid-19. Wakati ambao tuna mahitaji ambayo hatujayakimu, na hatuwezi wala hatujui namna ya kuyatatua, hisia za kukosa usalama na za hofu zinazidi. Hali hizi zinaibua hasira zetu, na kuongezeka ndani mwetu hadi kufikia kiwango ambacho kinaweza kusababisha uharibifu.

Hasira si makosa.

Hata Mungu hushikwa na hasira.

Lakini hasira yake ni tofauti na yetu, na anataka tujifunze kutoka kwake.

Bwana ni mwingi wa huruma na mwenye neema;si mwepesi wa hasira, bali amejaa upendo.Yeye hatalaumu siku zote,wala haweki hasira yake milele,yeye hatutendei kulingana na dhambi zetuwala hatupatilizi kwa kadiri ya maovu yetu.Zaburi 103:8-10

Ndugu zangu wapendwa, fahamuni jambo hili: Kila mtu awe mwepesi wa kusikiliza, lakini asiwe mwepesi wa kusema wala wa kukasirika. Kwa maana hasira ya mwanadamu haitendi haki ya Mungu.Yakobo 1:19-20

Mkikasirika, msitende dhambi, wala jua lisichwe mkiwa bado mmekasirika, … Ondoeni kabisa uchungu, ghadhabu, hasira, makelele na masingizio pamoja na kila aina ya uovu. Kuweni wafadhili na wenye kuhurumiana ninyi kwa ninyi, mkisameheana, kama vile naye Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.Waefeso 4:26, 31-32

Mungu anajua uchungu, kukata tamaa, na hasira zetu. Hatupaswi kumficha hisia hizi. Lakini pia anatuambia tutulize hasira yetu ili tusiwaumize wengine na tukose kuyafikia mapenzi ya Mungu kwetu.

Mwelezee Mungu hasira yako na umwombe akusaidie kuwa mwaminifu katika hali zote za maisha.

••••••••••

SIKU YA 11 •••••••••••••••••••••

Page 16: Dunia Yako INAPOBADILIKAdownloads.biblica.com/free-resources/Swahili... · machozi yako na yatiririke kama mto usiku na mchana; usijipe nafuu, macho yako yasipumzike. Inuka, lia usiku,

Je, Umetenganishwa na Mungu?Nahisi kana kwamba Mungu yuko mbali nami; hanisikii wala kunijali.

Je, ananipuuza? Je, ana shughuli zingine nyingi? Je, bado ananijali?

Najihisi mpweke sana. Ingenisaidia sana kujua kwamba Mungu hajaniacha wakati wangu wa hitaji.

Kutoka mwanzo hadi tamati, Biblia ni hadithi ya upendo wa Mungu kwa wanadamu wote. Biblia inatuhakikishia ya kwamba Mungu anataka kuishi na watu wake na pia kuishi kupitia kwao.

Matamanio ya Mungu ya kuwa pamoja nasi katika hali zote za maisha hayabadiliki, licha ya hali zetu za maisha au jinsi tunavyohisi.

Mungu alipowakomboa Waisraeli kutoka Misri na kuwapeleka nchi aliyokuwa amewaahidi, walikutana na adui wa kutisha. Mungu alijua wangejihisi wapweke, walioachwa, na waogope. Kwa hiyo Mose akawapa Waisraeli ujumbe muhimu kutoka kwa Mungu:

“Bwana Mungu wenu, yeye mwenyewe atavuka mbele yenu. Ataangamiza mataifa haya mbele yenu, nanyi mtaimiliki nchi yao. Pia Yoshua atavuka mbele yenu, kama Bwana alivyosema.

… Kuweni imara na moyo wa ushujaa. Msiogope wala msifadhaike kwa sababu yao, kwa kuwa Bwana Mungu wenu anakwenda pamoja nanyi; kamwe hatawaacha wala hatawatupa ninyi.

… Bwana mwenyewe atakutangulia naye atakuwa pamoja nawe; kamwe hatakuacha wala hatakutupa. Usiogope, wala usifadhaike.”Kumbukumbu 31:3, 6, 8

Matamanio ya Mungu ya kuwa nasi hayajawahi kupungua. Yesu alipokuja hapa duniani, alipewa jina la ajabu la Imanueli, maana yake Mungu pamoja nasi. Wakati Yesu alitoka duniani kwenda kuwa na Baba yake mbinguni, aliahidi kwamba Roho wake Mtakatifu angekuja kuishi katika wote watakaomfuata. Kwa sababu Mungu angeendelea kuishi kati yao, Yesu aliwatia moyo wafuasi wake kwa maneno haya:

Amani nawaachia, amani yangu nawapa, amani hii niwapayo si kama ile ulimwengu utoayo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiogope.Yohana 14:27

Hata tunapohisi uchungu na upweke, Mungu hayuko mbali nasi.

Mkaribie kwa sababu yuko karibu nawe.

•••••••••••

SIKU YA 12 ••••••••••••••••••••

Page 17: Dunia Yako INAPOBADILIKAdownloads.biblica.com/free-resources/Swahili... · machozi yako na yatiririke kama mto usiku na mchana; usijipe nafuu, macho yako yasipumzike. Inuka, lia usiku,

Kutotengeka!Inaonekana kwamba matatizo ya janga hili yanaendelea kutothibitika. Punde tu tunapofanya rekebisho moja, tunajikuta ya kwamba tunahitaji kufanya rekebisho lingine.

Kila badiliko linatutenganisha zaidi na kutuweka mbali zaidi na wenzetu. Hiyo inapaswa kuwa zuri kwetu, lakini najihisi kutengwa sana hivi kwamba naanza kuhisi nimetengwa kiroho pia!

Majanga ya kila aina yanaweza kuharibu mahusiano yetu, sio tu na jamaa zetu na marafiki, lakini pia uhusiano wetu na Mungu.

Uchovu kutoka kwa mafadhaiko ya majukumu zaidi, majonzi kutokana na hasara tulizozipata, na hofu inayoletwa na wasiwasi wa yale yaliyo mbele zetu; haya yote yanaweza kutuelekeza kujihisi tuko mbali na tumetengwa. Ni wazi kwamba kuweka umbali na wengine unaotakikana ili kupunguza kuenea kwa COVID-19 kunazidisha hisia za utengano zaidi. Tunaweza kuwa na shaka kama uhusiano wetu na Mungu ni thabiti kama tulivyodhania mbeleni.

Hata tukihisi kutengana kiroho au kukosa uhakika wa upendo na uwepo wa Mungu nyakati hizi za mfadhaiko, bado Mungu anatupa habari njema sana.

Hakuna chochote kinachoweza kututenga na upendo wa Mungu.

Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je, ni shida au taabu au mateso au njaa au uchi au hatari au upanga?

... Lakini katika mambo haya yote tunashinda, naam na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. Kwa maana nimekwisha kujua kwa hakika ya kuwa sio mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuja, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kingine chochote zitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu, Bwana wetu.Warumi 8:35, 37-39

Hiyo ni orodha ndefu ya vikwazo ambavyo havina uwezo wa kututenga na upendo wa Mungu! Zaidi ya haya, mafunzo ya Paulo yanatukumbusha kwamba upendo haushindwi kamwe. Upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu upo upande wetu daima, hata kama tunajitahidi kujihisi tumeshikana na upendo huo.

Nena na Mungu kuhusu chochote kinachoweza kuwa kikwazo ambacho kinakuzuia kuupokea upendo wake kwako.

••••••••••••

SIKU YA 13 •••••••••••••••••••

Page 18: Dunia Yako INAPOBADILIKAdownloads.biblica.com/free-resources/Swahili... · machozi yako na yatiririke kama mto usiku na mchana; usijipe nafuu, macho yako yasipumzike. Inuka, lia usiku,

Thubutu Kutumaini!Janga hili linapoendelea, wakati mwingine tunahisi ni bure na haiwezekani kuendelea.

Mambo niliyoyatazamia yamepotea, na sijui nitumaini nini siku zijazo.

Nafikiria sana msemo wa kitambo usemao hivi: Maisha ni magumu halafu unakufa. Lakini nina mtazamo tofauti sasa na msemo huo. Je, utafanya nini wakati maisha ni magumu halafu unaendelea kuishi?

Hasara, masikitiko, na majaribu ya maisha zinaweza kutunyang’anya tumaini hata tunapotaka sana kuendelea kutumaini.

Mungu anajua udhaifu wetu. Alisikia kilio cha Ayubu katika majaribu yake makuu.

Kama nyumba pekee ninayoitarajia ni kaburi,kama nikikitandika kitanda changu gizani, … liko wapi basi tarajio langu?Ni nani awezaye kuona tarajio lolote kwa ajili yangu?Ayubu 17:13-15

Mungu alifurahi mtumishi wake Daudi alipopata furaha na nguvu katika kumtumainia Bwana.

Ee nafsi yangu, upumzike, kwa Mungu peke yake,tumaini langu latoka kwake.Yeye peke yake ndiye mwamba wangu na wokovu wangu; ndiye ngome yangu, sitatikisika.Zaburi 62:5-6

Mungu anajua ilivyo muhimu kwetu kuwa na tumaini ambalo kamwe halitatupelekea kushindwa. Katika upendo wake mkuu, Mungu anatupa tumaini hilo.

Je wewe, hufahamu?Je wewe, hujasikia?Bwana ni Mungu wa milele,Muumba wa miisho ya dunia.Hatachoka wala kulegea,wala hakuna hata mmojaawezaye kuupima ufahamu wake.Huwapa nguvu waliolegeana huongeza nguvu za wadhaifu.Hata vijana huchoka na kulegea,nao vijana wanaume hujikwaa na kuanguka,bali wale wamtumainio Bwanaatafanya upya nguvu zao.Watapaa juu kwa mbawa kama tai;watapiga mbio wala hawatachoka,watatembea kwa miguu wala hawatazimia.Isaya 40:28-31

Je, unatafuta tumaini wapi? Thubutu kutazama mbele ya shida za leo, na utegemee tumaini la upendo wa Mungu kwako.

•••••••••••••

SIKU YA 14 ••••••••••••••••••

Page 19: Dunia Yako INAPOBADILIKAdownloads.biblica.com/free-resources/Swahili... · machozi yako na yatiririke kama mto usiku na mchana; usijipe nafuu, macho yako yasipumzike. Inuka, lia usiku,

Kuhisi KukwamaNinaendelea kutafakari kuhusu yote yaliyotukia tangu watu waanze kuwa wagonjwa: majonzi ya jamaa ambazo wapendwa wao wamekufa, kujitolea mhanga kwa wafanyakazi wa mashirika ya afya na wengine wanaojaribu kuokoa maisha, watu ambao wamepoteza kazi na biashara zao na hawawezi kununua chakula au kulipia nyumba zao.

Natamani kusaidia, lakini najihisi kwamba nimekwama katika ndoto mbaya.

Uchungu na hasara zilizoletwa na COVID-19 ni dhahiri kabisa, na zitaendelea kuathiri kila mmoja wetu kwa kiwango kikubwa. Ni vyema kuomboleza hasara na kujali mateso na mahitaji ya walio karibu nasi. Lakini tukiruhusu hisia za hasara na kufadhaika kuhusu tunayopitia kutushinda kabisa, tunaweza kujipata tumenaswa mawazo na kujawa na wasiwasi. Tunaweza kupoteza tumaini la siku za usoni kuwa bora.

Yesu anatupa jawabu lingine. Yesu aliwafunza wanafunzi wake jinsi ya kuishi bila kushindwa na wasiwasi wakati wangekuwa katika hali ngumu maishani, na jinsi ya kuelekeza mawazo yao katika njia iliyo bora.

“Kwa hiyo msiwe na wasiwasi, mkisema, ‘Tutakula nini?’ Au ‘Tutakunywa nini?’ Au ‘Tutavaa nini?’ Watu wasiomjua Mungu ndio wanaoshindania hayo, lakini Baba yenu wa mbinguni anafahamu kuwa mnahitaji haya yote. Lakini utafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake, na haya yote atawapa pia.”Mathayo 6:31-33

Kwa mtazamo huo, Yesu aliwafundisha jinsi ya kuomba kuhusu jinsi ya kuishi wanapoutafuta ufalme wa Mungu.

“Hivi basi, ndivyo iwapasavyo kuomba:“ ‘Baba yetu uliye mbinguni,Jina lako litukuzwe.Ufalme wako uje.Mapenzi yako yafanyikehapa duniani kama huko mbinguni.Utupatie riziki yetuya kila siku.Utusamehe deni zetu,kama sisi nasi tulivyokwishakuwasamehe wadeni wetu.Usitutie majaribuni,bali utuokoe kutoka kwa yule mwovu.”Mathayo 6:9-13

Haijalishi hali mbaya tunayopitia maishani, Mungu anataka tushirikiane naye kutenda mapenzi yake duniani.

Fikiria jambo moja ambalo unaweza kulenga leo litakalokusaidia kutoka hali ya kuwa na mawazo ya kukugandamiza na uweze kuishi katika upendo, wema na tumaini za Ufalme wa Mungu hapa duniani.

••••••••••••••

SIKU YA 15 •••••••••••••••••

Page 20: Dunia Yako INAPOBADILIKAdownloads.biblica.com/free-resources/Swahili... · machozi yako na yatiririke kama mto usiku na mchana; usijipe nafuu, macho yako yasipumzike. Inuka, lia usiku,

Kuthibitishiwa Kukosa UhakikaHakuna jambo litakalorudi jinsi lilivyokuwa hapo mbeleni.

Kumekuwa na mabadiliko mengi sana yanayohusu jinsi tunavyofanya kazi, jinsi tunavyonunua chakula, hali ya jamaa, jinsi tunavyoshiriki na jumuia yetu, na hata jinsi tunavyoishi kama jamaa moja nyumbani. Sijui ninaweza kutegemea nini tena.

Ni kweli. Maisha yatakuwa tofauti kwa muda wakati tunapopata afueni kutoka kwa athari za janga hili, na mambo mengine hayatarudi kama yalivyokuwa mbeleni. Lakini mabadiliko, hasara zenye uchungu, na maisha magumu havitadumu.

Kuwa katika hali ngumu ya maisha sio kumaanisha kwamba Mungu ametuacha au kwamba maisha hayatakuwa mazuri tena.

Biblia inatupa hadithi ya Yosefu. Alikuwa mwana aliyependwa na baba yake zaidi, nao ndugu zake wakamwonea wivu. Yosefu alipitia katika hali ngumu ndugu zake walipomuuza utumwani! Licha ya usaliti wao, Yosefu akawa mtumwa mzuri nyumbani mwa kiongozi mkuu. Kiongozi huyo akamtuza Yosefu kwa kumpa mamlaka ya kuitawala nyumba yake. Lakini baadaye Yosefu akatiwa gerezani miaka mingi kwa sababu ya mashtaka ya uongo dhidi yake.

Lakini hali mbaya maishani hazimzuii Mungu kutimiza kazi yake. Kupitia mateso haya, Mungu alimfunza Yosefu njia zake na akamtayarisha kuwa kiongozi mwenye hekima. Mwishowe Yosefu aliongoza nchi ya Misri katika kujiandaa na kushinda njaa kubwa. Hata jamaa ya Yosefu walikuja Misri kupata chakula!

Je, unafikiri Yosefu alichukulia aje mbadiliko ghafla ya matukio? Angalia jibu lake kwa ndugu zake ambao walidhania angelipiza kisasi kwao kwa kumtesa.

Ndipo ndugu zake wakaja na kujitupa chini mbele yake. Wakasema, “Sisi ni watumwa wako.”Lakini Yosefu akawaambia, “Msiogope. Je, mimi ni badala ya Mungu? Mlikusudia kunidhuru, lakini Mungu alikusudia mema, ili litimie hili linalofanyika sasa, kuokoa maisha ya watu wengi. Hivyo basi, msiogope. Mimi nitawatunza ninyi nyote pamoja na watoto wenu.” Akawahakikishia na kusema nao kwa wema.Mwanzo 50:18-21

Siku zijazo huwa hazina uhakika. Baada ya yote yaliyotokea kwake, Yosefu alitambua kwamba Mungu alikuwa usukani akitimiza kazi yake njema.

Je, hakikisho la wema wa Mungu linakupa tumaini unapokumbana na hali ya kukosa uhakika maishani?

•••••••••••••••

SIKU YA 16 ••••••••••••••••

Page 21: Dunia Yako INAPOBADILIKAdownloads.biblica.com/free-resources/Swahili... · machozi yako na yatiririke kama mto usiku na mchana; usijipe nafuu, macho yako yasipumzike. Inuka, lia usiku,

Huzuni KuondokaHofu na hasara za janga hili bado ziko nami, lakini siku zingine nahisi huzuni ikiondoka.

Mambo madogo madogo ya kufurahia maishani yanarudi.

Ninatazamia umaridadi wa jua likichomoza au likikucha.

Ninatoka nje ili nipunge hewa ya anga iliyosafishwa na mvua kubwa. Nafurahia kuongea na rafiki kwa simu na kucheka na watoto wangu.

Ninafikiria njia salama za kuwasaidia majirani walio na mahitaji.

Tutapitia mathara ya COVID-19 kwa muda. Maisha duniani kamwe hayatakuwa kamili au kukosa uchungu. Hatutaamka ghafla siku moja tupate hali ya maisha imerudi ilivyokuwa kabla ya janga hili kutukia. Pengine tutaomboleza baadhi ya hasara zetu kwa muda mrefu. Lakini tunaweza kupata moyo tunapokubali ishara ndogo za kupata ahueni kwa kutoka janga, na kuukumbatia uponyaji unapokuja. Tumaini hilo litakua tunapochukua wakati wetu kumshukuru Mungu kwa ukarimu wake, uaminifu, na upendo wake kwetu.

Huenda ikawa Zaburi ifuatayo iliyotungwa ili kumshukuru Mungu kwa ukarimu wake wakati wa shida inaelezea hisia zako za shukrani na tumaini kwa siku zijazo.

Ninampenda Bwana kwa maana amesikia sauti yangu;amesikia kilio changu ili anihurumie.Kwa sababu amenitegea sikio lake,nitamwita siku zote za maisha yangu.Bwana ni mwenye neema na haki,Mungu wetu ni mwingi wa huruma.Bwana huwalinda wanyenyekevu,nilipokuwa katika shida kubwa, aliniokoa.Ee nafsi yangu, tulia tena,kwa kuwa Bwana amekuwa mwema kwako.Kwa kuwa wewe, Ee Bwana,umeniokoa nafsi yangu na mauti,macho yangu kutokana na machozi,miguu yangu kutokana na kujikwaa,ili niweze kutembea mbele za Bwana,katika nchi ya walio hai.Zaburi 116:1-2, 5-9

Unapotafuta mtazamo mpya kuhusu majaribu uliyopitia hivi karibuni na kutafuta tumaini unaposonga mbele maishani, je, unaweza kumshukuru Mungu kwa mambo gani? Je, utamwelezeaje shukrani zako?

••••••••••••••••

SIKU YA 17 •••••••••••••••

Page 22: Dunia Yako INAPOBADILIKAdownloads.biblica.com/free-resources/Swahili... · machozi yako na yatiririke kama mto usiku na mchana; usijipe nafuu, macho yako yasipumzike. Inuka, lia usiku,

Sio Mtu Yule wa AwaliSikutarajia mambo yawe tofauti hivi. Ni changamoto sana kujaribu kuyarejesha maisha yangu katika “kawaida mpya” bila rasilimali na fursa tulizokuwa nazo.

Tunawaza kuhusu mambo yaliyo muhimu na kukata kauli kuhusu mambo ambayo hatukuyawaza hapo mbeleni.

Ninatambua kwamba nimebadilika. Siyatazami mambo kwa mtazamo wa hapo mbeleni.

Mimi sio mtu yule nilikuwa.

Wakati hali zetu za maisha yetu zinabadilika, pamoja na kazi za kila siku na mambo tuliyoyapa kipaumbele, mahusiano ya jamii, au mtazamo wetu kwa dunia , ndipo tunaanza kutilia maanani sisi ni nani, mambo ambayo ni muhimu kwetu, na mahali tunapoelekea.

Tashwishi na mabadiliko zilizoletwa na mgogoro au janga zinaweza kuchochea mgeuzo na kufanywa upya maishani mwetu. Tunaweza kupata shauku mpya katika kugundua kilicho cha muhimu kufuatilia na kukishikilia katika dunia inayobadilika.

Mungu aliye Muumba wetu anatupenda. Anataka tupate msingi imara ndani yake yeye na kuupitia mgeuzo wa kweli utakaotupa nguvu mpya, tumaini mpya na kusudi mpya maishani. Biblia ina hadithi nyingi za kuhusu upendo wa Mungu uletao mgeuzo maishani mwa watu ambao wamepitia kiwewe au mabadiliko mapya maishani yasiyokusudiwa. Angalia vile watu wengine wanasema kuhusu kumtumainia Mungu kuwa msingi wao imara:

Ee nafsi yangu, upumzike, kwa Mungu peke yake,tumaini langu latoka kwake.Yeye peke yake ndiye mwamba wangu na wokovu wangu; ndiye ngome yangu, sitatikisika.Wokovu wangu na heshima yangu viko kwa Mungu,ndiye mwamba wangu wenye nguvuna kimbilio langu.Zaburi 62:5-7

Kwa hiyo, hatukati tamaa. Ingawa utu wetu wa nje unachakaa, utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku. Kwa maana dhiki yetu nyepesi iliyo ya kitambo inatutayarisha kwa ajili ya utukufu wa milele unaozidi kuwa mwingi kupita kiasi, kwa sababu hatuangalii yale yanayoweza kuonekana bali yale yasiyoweza kuonekana. Kwa maana yale yanayoweza kuonekana ni ya kitambo tu, bali yale yasiyoweza kuonekana ni ya milele.2 Wakorintho 4:16-18

Je, utamtumainia Mungu kuwa msingi wako na kuwa uwepo wa mgeuzo maishani mwako?

•••••••••••••••••

SIKU YA 18 ••••••••••••••

Page 23: Dunia Yako INAPOBADILIKAdownloads.biblica.com/free-resources/Swahili... · machozi yako na yatiririke kama mto usiku na mchana; usijipe nafuu, macho yako yasipumzike. Inuka, lia usiku,

Kupata Furaha MaishaniKwa nini niliendelea kuishi wakati wengine walikufa?

Janga hili halibagui.

Hakuna mtu angetabiri nani ataambukizwa na nani hataambukizwa.

Hakuna aliyetarajia watu wadhaifu kunusurika wakati vijana wenye afya walikufa.

Maisha yanaonekana kuwa dhaifu sasa.

Tungependa maisha yawe tofauti, lakini maisha ni dhaifu. Maisha hayaji na hakikisho za furaha au maisha marefu.

Wakati Biblia inathibitisha vile maisha yetu duniani yalivyo dhaifu, pia inatuahidi kitu bora zaidi.

Kuhusu mwanadamu, siku zake ni kama majani,anachanua kama ua la shambani;upepo huvuma juu yake nalo hutoweka,mahali pake hapalikumbuki tena.Lakini kutoka milele hata mileleupendo wa Bwana uko kwa wale wamchao,nayo haki yake kwa watoto wa watoto wao:Zaburi 103:15-17

Lakini wote wakimbiliao kwako na wafurahi,waimbe kwa shangwe daima.Ueneze ulinzi wako juu yao,ili wale wapendao jina lako wapate kukushangilia.Zaburi 5:11

Kwa sababu ya upendo mkuu wa Mungu kwetu, uhafifu wa maisha sio mwisho wa hadithi. Tunaweza kupata furaha ya kudumu maishani tunapotafuta usalama katika msamaha wa Mungu na kujitolea kuishi maisha yanayompendeza Mungu.

Nasi tunaomba haya ili mpate kuishi maisha yanayostahili mbele za Bwana, na mpate kumpendeza kwa kila namna: mkizaa matunda kwa kila kazi njema, mkikua katika kumjua Mungu, mkiwa mmetiwa nguvu kwa uwezo wote kwa kadiri ya nguvu yake yenye utukufu, ili mpate kuwa na wingi wa saburi na uvumilivu. Nanyi kwa furaha mkimshukuru Baba, ambaye amewastahilisha kushiriki katika urithi wa watakatifu katika ufalme wa nuru. Kwa maana ametuokoa kutoka ufalme wa giza na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wake mpendwa, ambaye katika yeye tunao ukombozi, yaani msamaha wa dhambi.Wakolosai 1:10-14

Mshukuru Mungu kwa karama yake ya msamaha na uzima!

Unapoenenda katika shughuli zako za siku, tafuta nyakati maalum za kusudi, lengo, na furaha, na umshukuru Mungu kwa uzima wa milele anaokushirikisha.

••••••••••••••••••

SIKU YA 19 •••••••••••••

Page 24: Dunia Yako INAPOBADILIKAdownloads.biblica.com/free-resources/Swahili... · machozi yako na yatiririke kama mto usiku na mchana; usijipe nafuu, macho yako yasipumzike. Inuka, lia usiku,

Kusonga MbeleNahisi kwamba naweza kusonga mbele.

Ninaanza kuhisi kwamba nyakati hizi gumu zitaisha hivi karibuni.

Ninataka kusherehekea na kulenga siku zangu za usoni. Lakini tena nahisi kuwa na hatia, na ni kama nawasaliti wale watu ambao wamekufa.

Maisha yana misimu, nyakati na mifuatano inayotambulika.

Maisha hayasimami kwa muda. Machafuko ya janga hili yatakapopita, shairi lifuatalo kutoka kwenye Biblia litatukumbusha kwamba kutakuwa na wakati wa kuomboleza, uponyaji, kumbukumbu, na mwishowe wakati wa kuchukua hatua kwenda mbele.

Kuna wakati kwa ajili ya kila jambo,nayo majira kwa kila tendo chini ya mbingu:wakati wa kuzaliwa na wakati wa kufa,wakati wa kupanda na wakati wa kungʼoa yaliyopandwa,wakati wa kuua na wakati wa kuponya,wakati wa kubomoa,na wakati wa kujenga,wakati wa kulia na wakati wa kucheka,wakati wa kuomboleza na wakati wa kucheza,wakati wa kutawanya mawe na wakati wa kukusanya mawe,wakati wa kukumbatia na wakati wa kutokumbatia,wakati wa kutafuta na wakati wa kupoteza,wakati wa kuweka na wakati wa kutupa,wakati wa kurarua na wakati wa kushona,wakati wa kunyamaza na wakati wa kuzungumza,wakati wa kupenda na wakati wa kuchukia,wakati wa vita na wakati wa amani.Mhubiri 3:1-8

Ikiwa hisia za hatia au usaliti zinakuzuia kuendelea, jitengenezee ukumbusho. Unaweza kukusaidia kuchukua hatua kwenda mbele. Mungu alianzisha tabia ya kutengeneza kumbukumbu kwa Israeli ya kale. Aliwaamuru Waisraeli kujenga ukumbusho wa mawe ili uwasaidie kukumbuka jinsi alivyowasaidia kuvuka Mto Yordani hadi nchi ambayo Mungu alikuwa amewaahidi.

Je, ni njia gani ya maana inaweza kukukumbusha wakati huu mgumu maishani mwako au kukumbuka watu ambao unaowakosa maishani?

•••••••••••••••••••

SIKU YA 20 ••••••••••••

Page 25: Dunia Yako INAPOBADILIKAdownloads.biblica.com/free-resources/Swahili... · machozi yako na yatiririke kama mto usiku na mchana; usijipe nafuu, macho yako yasipumzike. Inuka, lia usiku,

KuridhikaNimejipata katika hali nyingi tofauti hivi karibuni. Mawazo yangu yanarudia kila kipindi. Nasikia sauti, naona picha na kukumbuka nyuso za watu.

Sio kwamba nataka kusahau yote yaliotukia. Lakini nataka kupata amani dhidi ya mawazo mengi, na niwe na mtazamo mpya kuhusu janga hili lote.

Tunapowahudumia wengine wakati wa janga kama hili la ugonjwa wa COVI-19, tunaweza kukosa namna ya kuthibiti yale tunayoyapitia. Tunaweza lazimikakufanya kazi muda mrefu bila kupumzika. Tunaweza kukosa maoni kuhusu chakula tunachopata, kama tunakipata. Tunaweza kutakiwa kufanya kazi bila vifaa vya kazi vya kutosha au ambavyo havina ulinzi wa kutosha. Tunaweza kutakiwa kuhudumia watu wengi mno.

Hali hizi zinaweza kuleta hali ya kutoridhika.

Kuridhika katika hali zote huanza na kuwa na mtazamo wa kuamini na kutumaini katika uongozi mwaminifu wa Mungu na kutujali kwa upendo.

Kuridhika kunaweza kuimarishwa na watu tunaokaa nao sana.

Rafiki anaweza kuleta mtazamo mpya, fadhili, au kutusikiliza wakati ufaao. Tukianza kufa moyo au kunung’unika, rafiki anaweza kutusaidia kuwa na mtazamo mpya kwa hali ile.

Paulo aliandika kuhusu yale aliyojifunza kuhusu kuridhika katika hali nyingi tofauti:

Sisemi hivyo kwa vile nina mahitaji, la! Kwa maana nimejifunza kuridhika katika hali yoyote. Ninajua kupungukiwa, pia ninajua kuwa na vingi. Nimejifunza siri ya kuridhika katika kila hali, wakati wa kushiba na wakati wa kuona njaa, wakati wa kuwa na vingi na wakati wa kupungukiwa. Naweza kuyafanya mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.Lakini, mlifanya vyema kushiriki nami katika taabu zangu.Wafilipi 4:11-14

“Lakini, mlifanya vyema kushiriki nami katika taabu zangu.” Kushiriki katika taabu za mtu mwingine ni heshima kubwa. Je, utachukua muda kushiriki katika taabu za mtu mwingine?

Je, unatarajia kujifunza nini kuhusu kuridhika kutokana na ushirika wako na mtu huyo?

••••••••••••••••••••

SIKU YA 21 •••••••••••

Page 26: Dunia Yako INAPOBADILIKAdownloads.biblica.com/free-resources/Swahili... · machozi yako na yatiririke kama mto usiku na mchana; usijipe nafuu, macho yako yasipumzike. Inuka, lia usiku,

Upendo MkarimuWakati wote nimefikiria kuwa mimi ni mtu mkarimu, lakini jambo la kutatanisha lilitukia nilipoenda dukani.

Walikuwa wamepunguza mgawo wa baadhi ya bidhaa tulizohitaji, na wazo la kwanza kwangu lilikuwa kujichukulia bidhaa hizo kwa wingi niwezavyo! Ingawa tulihitaji bidhaa moja tu, nilinunua mbili kwa sababu nilikuwa na pesa. Baadaye, nikajihisi mwenye hatia. Je, na kama mtu ambaye alihitaji bidhaa hizo hakuzipata kamwe?

Kudumisha mtazamo mzuri, wa upendo na ukarimu katika janga ni changamoto, hasa kama hujui kama utakuwa na rasilimali unazohitaji ili uendelee kuishi.

Lakini ukarimu wako unasaidia kuonyesha upendo na haki za Mungu ulimwenguni, na utazawadiwa.

Mema yatamjia mtu yule aliye mkarimu na mwenye kukopesha bila riba, anayefanya mambo yake kwa haki.Zaburi 112:5

Biblia pia inatuambia kwamba ukarimu wetu utapelekea wengine kumshukuru Mungu!

Kila mtu atoe kama anavyokusudia moyoni mwake, si kwa uchoyo au kwa kulazimishwa, kwa maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo mkunjufu. Naye Mungu aweza kuwapa kila baraka kwa wingi, ili katika mambo yote kila wakati, mwe na kila kitu mnachohitaji, ili mweze kushiriki kwa wingi katika kila kazi njema. Kama ilivyoandikwa:

“Ametawanya vipawa vyake kwa ukarimuakawapa maskini;haki yake hudumu milele.”Mtatajirishwa kwa kila namna ili mpate kuwa wakarimu kila wakati, na kupitia kwetu, ukarimu wenu utamletea Mungu shukrani.Huduma hii mnayofanya si tu kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya watakatifu, bali huzidi sana kwa shukrani nyingi apewazo Mungu. Kwa sababu ya huduma ambayo mmejithibitisha wenyewe, watu watamtukuza Mungu kwa ajili ya utiifu ufuatanao na ukiri wenu wa Injili ya Kristo, na kwa ukarimu wenu wa kushiriki pamoja nao na pia wengine wote.2 Wakorintho 9:7-9, 11-13

Je, ina umuhimu gani kwako kuonyesha upendo wa Mungu kwa kuwa mtoaji mkarimu na mwenye furaha? Je, utatimizaje haya?

•••••••••••••••••••••

SIKU YA 22 ••••••••••

Page 27: Dunia Yako INAPOBADILIKAdownloads.biblica.com/free-resources/Swahili... · machozi yako na yatiririke kama mto usiku na mchana; usijipe nafuu, macho yako yasipumzike. Inuka, lia usiku,

Kushiriki FarajaNilipoanza kupanda joto mwilini, ilinibidi kujitenga na watu wengine kwa siku kumi na nne zilizokuwa ndefu sana kwangu. Mimi ni mtu ambaye nina bidii ya kutimiza mambo, kwa hivyo wakati huo peke ulikuwa kama mateso.

Nilikuwa nimechoka kiasi cha kushindwa kula. Nilikuwa peke yangu na nikahofu kwamba naweza kuugua zaidi. Mwishowenilipimwa na kufahamu ya kwamba sikuwa na COVID-19. Lakini hivi kwamba nimepata nafuu, naona kwamba muda wangu wote wa kujitenga ulikuwa bure. Mateso hayo yote na wasiwasi bila sababu!

Mateso kawaida huelekeza mtu kuhisi upweke.

Tunawezakosa mtu yeyote wa kutufariji.

Tunaweza kuhisi kwamba hakuna mtu anayeelewa jinsi mateso yetu yalivyo.

Kwa njia moja, mateso yetu ni ya kipekee, na hakuna mtu mwingine yeyote anayeweza kufahamu tunavyohisi kabisa. Kwa njia ingine, mateso ni jambo ambalo watu wote hupatana nalo. Tunapopata faraja ya uwepo wa Mungu katika mateso yetu, tunaweza kushiriki faraja hiyo na wengine katika uchungu na upweke wao.

Mtume Paulo alipitia mateso makubwa maishani mwake na katika huduma yake, hivi kwamba anasema kwamba hata alikata tamaa ya kuishi! Licha ya haya, anapoandika kuhusu mateso hayo, anayaelezea kama karama anayoweza kushiriki na wengine.

Ahimidiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa huruma na Mungu wa faraja yote. Yeye hutufariji katika taabu zetu, ili tuweze kuwafariji walio katika taabu yoyote kwa faraja ambayo sisi wenyewe tumepokea kutoka kwa Mungu. Kama vile mateso ya Kristo yanavyozidi ndani ya maisha yetu, hivyo ndivyo faraja yetu inavyofurika kwa njia ya Kristo. Kama tunataabika, ni kwa ajili ya faraja na wokovu wenu; kama tukifarijiwa, ni kwa ajili ya faraja yenu, iwaleteayo saburi ya mateso yale yale yanayotupata. Nalo tumaini letu kwenu ni thabiti, kwa sababu tunajua kwamba kama vile mnavyoshiriki mateso yetu, ndivyo pia mnavyoshiriki katika faraja yetu.

2 Wakorintho 1:3-7

Tunaweza kuhesabu nyakati za mateso na hasara kuwa bure au zisizo na maana, lakini kwa mtazamo wa Mungu, nyakati hizo zinatupa fursa isiyo kifani ya kushiriki katika mateso ya wengine.

Je, ni faraja gani umepokea kutoka kwa Mungu ambayo unaweza kushiriki na wengine?

••••••••••••••••••••••

SIKU YA 23 •••••••••

Page 28: Dunia Yako INAPOBADILIKAdownloads.biblica.com/free-resources/Swahili... · machozi yako na yatiririke kama mto usiku na mchana; usijipe nafuu, macho yako yasipumzike. Inuka, lia usiku,

Karama ya KusaidiaMshahara wangu ulipunguzwa wakati wa janga hili, na baada ya kulipa kodi ya nyumba, tulibaki na pesa kidogo sana za kununua chakula. Ilitunyenyekesha sana kukubali usaidizi kwa sababu sisi kwa kawaida hujitegemeza.

Hatukutaka kuhurumiwa, lakini tulishukuru kwa msaada huo.

Kuwasaidia watu wengine wakati wa janga laweza kuonekana kuwa jambo rahisi. Lakini kusaidia kunaweza kuwa na maana na athari tofauti kulingana na vile msaada unapeanwa, na ni nani anayeupokea.

Kwa watu wengine, kusaidia ni jambo rahisi la kupeana bidhaa kwa wale wasioweza kujitegemeza, au kuwafanyia kazi wasioweza kujifanyia. Kwa wengine, kusaidia kunaonyesha upendo na kujali hali ya mtu mwingine.

Kutoa msaada kunaweza kuwa na motisha ya ukarimu, au kunaweza kutiwa doa na huruma na kuhisi hatia. Kuhitaji msaada kunaweza kuchukuliwa kuwa udhaifu au kushindwa. Kupokea msaada kunaweza kuvutia nafuu, shukrani na tumaini.

Kuwasaidia watu wakiwa na mahitaji kunaweza kuwa na athari za kudumu kukifanywa kwa moyo safi wa kuwaelewa wengine, kuwajali na kuwapenda. Kuwasaidia wengine kunaweza kuwaonyesha watu jinsi Mungu alivyo na kiasi anachowapenda. Hebu zingatia jumbe hizi kuhusu kuwasaidia wengine katika maisha na huduma ya Yesu.

Yesu akazunguka katika miji yote na vijiji vyote, akifundisha katika masinagogi yao, akihubiri habari njema za Ufalme, na akiponya kila ugonjwa na kila aina ya maradhi. Alipoona makutano, aliwahurumia kwa sababu walikuwa wanasumbuka bila msaada, kama kondoo wasiokuwa na mchungaji.

Umati mkubwa wa watu ukamjia, wakiwaleta vilema, vipofu, viwete, bubu na wengine wengi, wakawaweka miguuni pake; naye akawaponya. Hao watu wakashangaa walipoona bubu wakisema, vilema wakipona, viwete wakitembea na vipofu wakiona, wakamtukuza Mungu wa Israeli.Mathayo 9:35, 36; 15:30, 31

Unapomsaidia mtu, tafakari maana na athari za matendo yako. Omba Mungu akusaidie kuwaelewa watu walio na mahitaji na kuwashughulikia kama vile Yesu alifanya.

Muulize Mungu aibariki karama yako ya kuwahudumia watu ili watambue upendo wa Mungu kwao na wamsifu kwa wema wake.

•••••••••••••••••••••••

SIKU YA 24 ••••••••

Page 29: Dunia Yako INAPOBADILIKAdownloads.biblica.com/free-resources/Swahili... · machozi yako na yatiririke kama mto usiku na mchana; usijipe nafuu, macho yako yasipumzike. Inuka, lia usiku,

Pendaneni Mmoja na MwingineMimi ni mtu mzima. Ninaishi peke yangu bila jamaa karibu. Hivyo ilikuwa tukio la ajabu jumuia yetu iliposhurutishwa kufunga kwa muda wa takriban mwezi moja!

Niliwakosa wafanyakazi wenzangu, kukutana na marafiki, na shughuli zangu za kawaida. Mara kwa mara, kukaa mbali na watu wengine kulinipelekea kuhisi kwamba sikufaa wala sikuwa wa maana kwa mtu yeyote.

Popote tunapoishi, janga la COVID-19 litatuathiri. Utengano wa usalama kama kujitenga na watu, biashara na mawasiliano kufungwa, na pia hali ya kufanya kazi au kusomea nyumbani umetuathiri vibaya kisaikolojia.

Tuliumbwa kuishi na kufanya kazi katika ushirika na Mungu na watu wengine, hivyo utengano unatuathiri visivyotakikana.

Unapojihisi upweke na kukosa usalama wakati kila mahali pamefungwa, usisahau kwamba watu duniani kote wanateseka kwa njia kama hizo. Tunaweza kuwasiliana na jamaa na marafiki kwa ujumbe mfupi, kupiga simu, au barua pepe ili kuonyesha upendo na kuwajali wenzetu.

Kama watu wa imani, sisi pia tuna fursa na tumaini la kuishikanisha mioyo yetu pamoja, na kuwaombea wengine na kuomba pamoja nao.

Zaidi ya maadili haya yote jivikeni upendo, ambao ndio unaofunga kila kitu pamoja katika umoja mkamilifu.Amani ya Kristo na itawale mioyoni mwenu, kwa kuwa ninyi kama viungo vya mwili mmoja mmeitiwa amani. Tena kuweni watu wa shukrani. Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu, mkifundishana na kuonyana katika hekima yote, mkimwimbia Mungu zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni, huku mkiwa na shukrani mioyoni mwenu. Lolote mfanyalo, ikiwa ni kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba katika yeye.Wakolosai 3:14-17

Mungu hakukusudia maisha kuwa jitihada la upweke. Tunapofungamanishwa katika kifungo cha imani, tunaweza kuungana mikono na kutiana moyo mmoja na mwingine kupitia kwa maombi.

Je, una mtu unayeweza kuomba pamoja naye kwa mahitaji yenu wawili, kuombea jamii yenu, kuombea wote wanaoteseka duniani, na pia kutiana moyo katika safari yenu ya imani?

••••••••••••••••••••••••

SIKU YA 25 •••••••

Page 30: Dunia Yako INAPOBADILIKAdownloads.biblica.com/free-resources/Swahili... · machozi yako na yatiririke kama mto usiku na mchana; usijipe nafuu, macho yako yasipumzike. Inuka, lia usiku,

Kuchagua KusameheNinashangaa mara kwa mara ni nani alileta matatizo haya yote.

Mambo yote yamechafuka. Je, ni nani anafanya maamuzi yaliyo sahihi? Na, je, ni nani anaharibu mambo zaidi?

Kujua ni nani wa kulaumu kungeleta amani mawazoni mwangu.

Wakati mambo yanakosa kuthibitika, tunapopitia hali ngumu, tunapopata hasara, tunaweza kujaribiwa kufikiri ya kwamba kwa kupata majibu kuhusu jambo lililoenda mrama na kugundua ni nani wa kulaumiwa yaweza kutufanya tuhisi vyema. Hiyo ndiyo sababu wengi wanakisia njama nyingi wakati wa janga.

Majibu yanaweza kupunguza msukumo wa wasiwasi na kutupa amani katika machafuko kwa muda mfupi. Lakini mashtaka na lawama hayabadilishi hali, wala hayainui nia yetu na uwezo wetu wa kustahimili yaliyotukia.

Ukweli ni kwamba kukabiliana na janga la ugonjwa wa dunia yote ni jambo gumu na tata. Hatuna majibu yote. Mambo yasiyoyotarajiwa hutendeka. Uamuzi wa busara leo unaweza kuonekana kuwa wa upumbavu kesho. Tunaposumbuka mawazo sana, tunaweza kuwalaumu watu vikali.

Baada ya mambo kupita, sote tuna masikitiko kuhusu tulivyotenda. Tunatambua kwamba tungetatua hali zingine vizuri zaidi. Tungefanya maamuzi ya busara zaidi. Lakini hatupaswi kukaa katika hali ya kulaumiana. Kujisamehe na kuwasamehe wenzetu kwa makosa na kushindwa kwaweza kuwa kugumu. Lakini hii ni hatua muhimu inayotuweka huru ili tupate kupona, kukua, na kuendelea na maisha ya baadaye tukiwa na tumaini.

Vumilianeni na kusameheana mtu akiwa na lalamiko lolote dhidi ya mwenzake. Sameheaneni kama vile Bwana alivyowasamehe ninyi.Wakolosai 3:13

Kuweni wafadhili na wenye kuhurumiana ninyi kwa ninyi, mkisameheana, kama vile naye Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.Waefeso 4:32

Mungu anatusamehe kwa ajili ya dhambi zetu zote na makosa yote. Nasi tunaweza kuwatendea wenzetu vivyo hivyo. Je, kuna mtu unayemlaumu bila haki? Ni makosa gani unayowawekea wengine yanayokufungia katika maisha ya kale?

Je, ni nani utakayemtunukia kipawa cha msamaha ambao Mungu amekupa wewe bure?

•••••••••••••••••••••••••

SIKU YA 26 ••••••

Page 31: Dunia Yako INAPOBADILIKAdownloads.biblica.com/free-resources/Swahili... · machozi yako na yatiririke kama mto usiku na mchana; usijipe nafuu, macho yako yasipumzike. Inuka, lia usiku,

Kuishi Maisha KamiliNayakosa maisha yangu ya awali. Laiti mambo yote yangerudi kama kawaida.

Najua shida na hofu za leo zitapita.

Hapa na pale naona ishara za maisha mapya baadaye.

Biashara zingine zinaonekana kutayarishwa kufungua milango tena, lakini sidhani maisha yatakuwa kama mbeleni.

Wakati unapowadia wa kurudia maisha ya kawaida baada ya kupitia janga fulani, mara kwa mara tunaupokea kwa hamu kubwa. Hata hivyo, tunapoendelea kupatana na ukweli wa maisha mapya ya kila siku, tunaweza kuvunjwa moyo na masikitiko na changamoto. Lakini pia hali hizo zinatupa fursa za kuyafuatilia maisha kwa njia ambayo hatukuwahi fikiria mbeleni.

Je, uko tayari kufikiria kuishi maisha mapya? Mabadiliko hutupa fursa ya kuanza tena na kujenga maisha bora zaidi. Tunaweza kufikiria upya vipaumbele na malengo ya maisha yetu. Tunaweza kufanyisha kazi maoni yetu mapya. Tunaweza kujaribu kuponya mahusiano ya awali. Tunaweza kuanzisha tabia bora zaidi. Pia tunaweza kufikiria upya yale tunayoamini kumhusu Mungu, na apasacho kufanya maishani mwetu.

Alipokuwa hapa duniani, Yesu aliwaonyesha na kuwafundisha watu kuhusu maisha makamilifu na tele anayopeana. Watu wengine walimkataa. Nao wengine walipata tumaini katika mafunzo yake na wakapokea makusudi yake. Yesu alisema:

Mwizi huja ili aibe, kuua na kuangamiza. Mimi nimekuja ili wapate uzima kisha wawe nao tele. Yohana 10:10

Mtume Paulo aliyanukuu maneno ya nabii Isaya alipoelezea kuhusu maisha tele ambayo Mungu anapeana:

Lakini ni kama ilivyoandikwa: “Hakuna jicho limepata kuona, wala sikio limepata kusikia, wala hayakuingia moyoni wowote, yale Mungu amewaandalia wale wampendao”: Lakini mambo haya Mungu ametufunulia kwa Roho wake. Roho huchunguza kila kitu, hata mambo ya ndani sana ya Mungu.1 Wakorintho 2:9, 10

Mungu anatupa kila mmoja wetu nafasi ya kuishi maisha mapya, tele na uzima wa milele ambao hauwezi kuibiwa au kuharibiwa na tukio lolote duniani.

Je, maisha tele ambayo Mungu anapeana yako wapi katika mipango yako?

••••••••••••••••••••••••••

SIKU YA 27 •••••

Page 32: Dunia Yako INAPOBADILIKAdownloads.biblica.com/free-resources/Swahili... · machozi yako na yatiririke kama mto usiku na mchana; usijipe nafuu, macho yako yasipumzike. Inuka, lia usiku,

Tumaini LinarejeshwaMaisha yanaweza kuwa na udhalimu sana.

Siku moja una afya na unaendelea na maisha kama kawaida. Ghafla, bila onyo, bila kufanya jambo lolote tofauti, unakuwa mgonjwa na virusi visivyoonekana ambavyo vinaweza kukuua.

Naona ugumu kukubali kwamba maisha yanapaswa kuwa hivyo.

Kwangu mimi, maisha hayaonekani kuwa mazuri tena. Nina shaka maisha yanahusu nini hasa.

Mungu alipoumba ulimwengu, ulikuwa mkamilifu kwa namna zote. Vitu vyote ambavyo Mungu aliumba vilionyesha picha ya taswira yake: tabia yake, maadili yake na kusudi lake. Vitu vyote vilikuwa vya kuvutia na vilitenda kazi pamoja kama vile alivyokusudia kabisa. Lakini uasi na dhambi dhidi ya Mungu viliharibu dunia iliyokuwa kamilifu. Machafuko yakaingia mahali pa mpangilio wa amani wa Mungu, na kutoka hapo ulimwengu umekuwa ukiishi mbali na uhusiano unaofaa kati yake na Mungu.

Hivyo, dunia leo si nzuri kama vile Mungu alivyoiumba iwe. Uchungu, huzuni, mchafuko na wasiwasi tunazohisi kuhusu janga hili la ugonjwa zinaashiria vile maisha yanavyokuwa wakati uhusiano wetu na Muumba wetu umevunjika. Lakini hatupaswi kuishi katika hali hiyo ya uchungu na kukata tamaa. Mungu alimtuma Mwanawe, Yesu, aweze kurejesha uhusiano wetu naye, ili tuweze kuunganishwa naye tena. Na pia ameahidi kwamba siku moja vitu vyote vilivyoumbwa pia vitarejeshwa kwa hali ya ukamilifu.

“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Kwa maana Mungu hakumtuma Mwanawe kuuhukumu ulimwengu, bali kupitia kwake ulimwengu upate kuokolewa.”Yohana 3:16-17

Mungu wa tumaini awajaze ninyi furaha yote na amani katika kumwamini, ili mpate kujawa na tumaini tele kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.Warumi 15:13

Dhambi zetu zinaposamehewa na uhusiano wetu na Mungu kurejeshwa, tunaweza kuishi kwa amani na tumaini. Tunaweza kufanyiwa upya kusudi la maisha yetu: kumjua, kumtumainia, na kumtumikia Mungu katika mambo yote tuyafanyayo.

Je, kumtumainia Mungu kunabadilisha mtazamo wako kuhusu nyakati ngumu maishani kwa njia zipi?

•••••••••••••••••••••••••••

SIKU YA 28 ••••

Page 33: Dunia Yako INAPOBADILIKAdownloads.biblica.com/free-resources/Swahili... · machozi yako na yatiririke kama mto usiku na mchana; usijipe nafuu, macho yako yasipumzike. Inuka, lia usiku,

Kuishi VyemaImekuwa vigumu kuishi vyema wakati huu wa janga la COVID-19. Hata shughuli za kawaida za kila siku za maisha zimebadilika. Wakati tu nafikiri ya kwamba nimeyapambanua, mambo yanabadilika tena.

Wakati wote nimekuwa na uwezo wa kuwafikia na kuwasaidia watu wengine, lakini sasa sijui watu wanahitaji nini wala niwezacho kufanya ili niwasaidie.

Mungu alituumba tuwe watendakazi pamoja naye katika kuwaonyesha watu upendo wake na kuwasaidia wakati wana mahitaji.

Kwa hivyo si ajabu kwamba tunahisi kuridhika wakati tunaweza kuwasaidia watu wengine kukimu mahitaji yao, kwani ndivyo Mungu alituumba tutende.

Bwana yu karibu na waliovunjika moyo,na huwaokoa waliopondeka roho.Zaburi 34:18

Yesu alipokuja duniani, alikuwa mkarimu, mpole na mfariji kwa watu wengi. Alipowahudumia wengine, alituonyesha jinsi ya kuishi vyema kwa kupenda vyema.

Roho wa Bwana Mwenyezi yu juu yangu,kwa sababu Bwana amenitia mafutakuwahubiria maskini habari njema.Amenituma kuwaganga waliovunjika moyo,kuwatangazia mateka uhuru wao,na hao waliofungwahabari za kufunguliwa kwao;kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa,na siku ya kisasi ya Mungu wetu,kuwafariji wote waombolezao,na kuwapa mahitajiwale wanaohuzunika katika Sayuni,ili kuwapa taji ya uzuri badala ya majivu,mafuta ya furaha badala ya maombolezo,vazi la sifa badala ya roho ya kukata tamaa.Nao wataitwa mialoni ya haki,pando la Bwana,ili kuonyesha utukufu wake.Isaya 61:1-3

Je, umepokea uponyaji, wema na faraja gani kutoka kwa Mungu?

Je, ni jinsi gani unayoweza kushiriki upendo huo wa Mungu kwa watu wengine?

••••••••••••••••••••••••••••

SIKU YA 29 •••

Page 34: Dunia Yako INAPOBADILIKAdownloads.biblica.com/free-resources/Swahili... · machozi yako na yatiririke kama mto usiku na mchana; usijipe nafuu, macho yako yasipumzike. Inuka, lia usiku,

Nguvu za Kuishi KeshoKushughulikia COVID-19 limekuwa jambo gumu kwangu. Lakini imekuwa uchungu sana kwa watu ambao wamewapoteza wapendwa wao, na wale ambao wameathirika kifedha.

Sisi sote tunatazamia mwisho wa ugonjwa huu, lakini nahofia kwamba tutachukua muda mrefu kukumbana nao.

Natumai ya kwamba tuna nguvu za kupambana na yaliyo mbele yetu.

Janga la ugonjwa kama huu wa COVID-19 haliishi mara moja. Kuanza maisha tena na kuyajenga upya huchukua muda. Bila matibabu yanayoweza kuponya na chanjo ambazo zinaweza kuzuia COVID-19, tishio la ugonjwa huu linaendelea kutulemea.

Kuishi na huu wasiwasi ni kumbusho la kila wakati la jinsi tulivyo na uthibiti mdogo sana kwa mambo yatakayotukia kesho. Lakini Biblia inatuhakikishia kwamba Mungu ndiye tumaini na nguvu yetu, licha ya lolote litakalotukia. Mtume Paulo alikuwa na ujasiri kwamba Mungu ataliwezesha kanisa kutimiza kusudi lake la kumfanya Mungu ajulikane kote, hata katikati ya mateso makuu. Hivyo akaandika:

Namwomba Mungu awaimarishe kwa kuwatia nguvu mioyo yenu kwa njia ya Roho wake kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, ili kwamba, Kristo apate kukaa mioyoni mwenu kwa njia ya imani. Nami ninaomba kwamba ninyi mkiwa wenye mizizi tena imara katika msingi wa upendo, mwe na uwezo wa kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, urefu, kimo na kina upendo wa Kristo, na kujua upendo huu unaopita fahamu, ili mpate kujazwa na kufikia kipimo cha ukamilifu wote wa Mungu.

Basi kwa yeye awezaye kutenda mambo ya ajabu yasiyopimika kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya uweza wake ule utendao kazi ndani yetu, yeye atukuzwe katika kanisa, na katika Kristo Yesu kwa vizazi vyote, milele na milele. Amen.Waefeso 3:16-21

Hakuna mtu ajuaye raha au hatari zitakazoletwa na kesho . Lakini tunajua kwamba Mungu anatupenda zaidi ya vile tunaweza kufikiria, na kwamba nguvu zake ndizo zitatuwezesha kushinda mambo yoyote yaliyo mbele zetu.

Je, ahadi ya nguvu za Mungu na kusudi lake kwa maisha yako inaathiri aje jinsi unavyokumbana na siku za usoni ambazo hauna uhakika nazo?

•••••••••••••••••••••••••••••

SIKU YA 30 ••

Page 35: Dunia Yako INAPOBADILIKAdownloads.biblica.com/free-resources/Swahili... · machozi yako na yatiririke kama mto usiku na mchana; usijipe nafuu, macho yako yasipumzike. Inuka, lia usiku,

Janga la COVID-19

limebadilisha dunia

yetu yote.

Labda umepitia katika hali ya uchungu na hasara, lakini janga hili limebadilisha maisha yako kwa njia kubwa zaidi. Uchungu na hasara huathiri kila sehemu ya maisha yetu, na kukosa uthibiti wa maisha unaumiza moyo sana. Kwa namna moja au nyingine, tunafahamu kwamba machafuko haya hayakupaswa kuweko.Ulimwengu ulipoanza, uumbaji wa Mungu ulikuwa mahala pa amani. Ulikuwa mahala ambapo wanadamu walifurahia ushirika mzuri na Mungu huku wakiutunza uumbaji wake mzuri.

Lakini wanadamu hao wakaamua kwamba njia yao ilikuwa bora kuliko ya Mungu. Walichagua njia ya dhambi na mauti ambayo iliharibu mahusiano yote ya wanadamu: uhusiano na Mungu, na wenzao, pia na uumbaji wa Mungu. Uchungu, mapambano, uharibifu, na uchungu wa moyo yameathiri mahusiano ya wanadamu tangu hapo.

Lakini Mungu alitaka kurejesha uumbaji wake, kwa hiyo akalichagua kundi la watu, Waisraeli, ili aionyeshe dunia upendo wake. Lakini Waisraeli walisumbuka kuwa suluhisho, na shida ikaendelea kuwa kubwa. Lakini Mungu hakufa moyo.

Mungu alimtuma Mwana wake wa pekee, Yesu, ulimwenguni kuwa Masiya wa Waisraeli, yaani Mfalme wao. Yesu alikuja kuonyesha kusudi la wanadamu kuumbwa. Alikuja kufanya jambo ambalo Waisraeli walishindwa kufanya: kuonyesha upendo wa Mungu kwa wanadamu wote. Pia alikuja kuwa Mfalme na Mwokozi wa ulimwengu.

Badala ya kujipeana kwa dhambi na kufa kama vile kila mwanadamu mbele yake alikuwa amekufa, Yesu alikabiliana na hali hizo na kuzishinda. Je, aliwezaje kutenda haya?

Yesu alitangaza kuja kwa ufame wa Mungu. Hata hivyo, wafalme na waliokuwa katika mamlaka hawakupenda tishio aliloleta kwa utawala wao. Waliimarisha utawala wao kupitia mauti. Ili kumshinda, walitumia nguvu za mauti walipomsulubisha msalabani hadi kufa.

Lakini baada ya siku tatu, nguvu zao zikapoteza uwezo. Yesu alifufuka kutoka mautini na kuonyesha kwamba nguvu za Mungu za kufufua zina uwezo kuliko dhambi na mauti. Upendo na uhai wa Mungu zikashinda nguvu hizi za uovu.

Tunapokumbana na vitisho vya kuogofya kama tishio hili linalotukumba, hatupaswi kupuuza giza yake. Badala ya hivyo, Mungu anatupa hadithi ya tumaini, hadithi ambayo nuru inashinda giza.

Sote tumekuwa sehemu ya giza hili kwa kufuata mawazo yetu na tamaa zetu badala ya kuyafuata mawazo na matamanio ya Mungu. Lakini kama vile Mungu amejitolea kufanya upya uumbaji wake, pia anataka kukurejesha uwe kile alichokusudia tangu mwanzoni, na akusamehe dhambi zako ili nawe upeleke maisha haya mapya kwa dunia yake.

Kusudi la Mungu ni kuufanya upya uumbaji wote, ili ulimwengu usirudi kuathirika na hali ya majanga na uharibifu. Katika uumbaji mpya, makao ya Mungu yatakuwa pamoja na watu wake, na ataishi nao na kuwa Mungu wao: “Atafuta kila chozi kutoka macho yao. Mauti haitakuwepo tena, wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu, kwa maana mambo ya kwanza yamekwisha kupita” (kutoka kwa kitabu cha Ufunuo 21:3).

Hivi sasa, Mungu anataka kukutana nawe hapo ulipo na akufariji. Lakini pia anataka umfuate, utoke gizani na kuwa mnara wake wa nuru duniani. Bado kuna uchungu mwingi sana duniani. Kuna watu wengi sana wanaohitaji tumaini lili hili, na wanahitaji kujua kwamba Yesu anatupa ushindi dhidi ya giza.

Hatuwezi kufanya haya peke yetu. Mungu ametupa Roho wake Mtakatifu kuishi nasi, nalo Neno lake kutupa habari za Mungu, na pia tuna wenzetu ili tushiriki maisha yetu nao. Kwa hiyo tunakushawishi umwalike Roho wake Mungu maishani mwako, utafute kundi la wafuasi wa Yesu ushirikiane nao, na upate nakala yako ya Neno lake ulisome.

Page 36: Dunia Yako INAPOBADILIKAdownloads.biblica.com/free-resources/Swahili... · machozi yako na yatiririke kama mto usiku na mchana; usijipe nafuu, macho yako yasipumzike. Inuka, lia usiku,

Shirika la Biblica, hapo awali International Bible Society, lilianzishwa mnamo mwaka wa 1809 katika mji wa New York. Biblica hutafsiri Neno la Mungu na kupeana taratibu zilizo na msingi katika Neno la Mungu ili kuwasaidia watu kuweza kuelewa Neno la Mungu vizuri zaidi, na kulisoma. Tunasaidia watu kupata nakala zao za Biblia na kuelewa vile Neno la Mungu linaweza kuwafaidi katika maisha yao ya kila siku. Biblica kwa wakati huu inahudumu katika nchi 55, na kufikia zaidi ya watu milioni 100 kila mwaka kwa Neno la Mungu. Ombi letu ni kwamba ushuhudie binafsi uwezo ubadilishao maisha unaopatikana tu katika Neno la Mungu.

Dunia Yako Yote InapobadilikaTM Nakala MaalumHakimiliki © 2020 na Biblica, Inc.

Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.

When Your Whole World ChangesTM Special Edition (Swahili)Copyright © 2020 by Biblica, Inc.

All rights reserved worldwide.

Maandiko ya Biblia yamenakiliwa kutoka kwaNeno: Biblia TakatifuTM

Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015 na Biblica, Inc.Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.

“Biblica”, “Bango la Biblica” na “International Bible Society” ni alama za biashara zilizosajiliwa katika Ofisi ya Hataza na Alama za Biashara Marekani (United States Patent and Trademark Office) na shirika la Biblica, Inc.

Idara ya Humanitarian Disaster Institute (HDI) ni sehemu ya Wheaton College (chuo cha mafunzo ya Biblia), na ilianzishwa mnamo mwaka wa 2011. Idara hii ndiyo ya kwanza nchini Marekani iliyo na misingi ya imani ambayo ni kituo cha utafiti wa mambo yanayohusiana na dhiki. Kusudi letu ni kusaidia kanisa kujiandaa ili kuweza kuhudumia dunia iliyojaa dhiki. Tunatumia utafiti wetu kutayarisha rasilimali na matukio yanayowalenga wanafunzi, manusura, wasaidizi, na watafiti. Mnamo mwaka wa 2018, idara ya HDI ilianzisha mafunzo ya shahada ya pili (yaani MA) katika masomo ya Uhisani na Uongozi wakati wa Dhiki (Humanitarian & Disaster Leadership) katika chuo cha Wheaton. Kusudi ni kuandaa kizazi kijacho cha wafanyakazi waliohitimu katika usaidizi na uongozi wakati wa dhiki ili waweze kuongoza kwa imani na unyenyekevu, wakitumia utafiti unaotumia ushahidi katika utekelezaji wao, na kuwahudumia watu walioadhirika zaidi na Kanisa duniani kote.