32
Maana Halisi ya Utumishi Uliotukuka MWAKA MMOJA WA SHUGHULI ZA UTENDAJI JIJINI ARUSHA JULAI 2016 - JUNI 2017

MWAKA MMOJA WA SHUGHULI ZA UTENDAJI JIJINI ARUSHA … · gharama ya Tsh Mil 177. ... huduma ya upimaji kwa bei nafuu ili kila Mwananchi aweze kumudu na zaidi kuwawezesha wananchi

  • Upload
    others

  • View
    15

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: MWAKA MMOJA WA SHUGHULI ZA UTENDAJI JIJINI ARUSHA … · gharama ya Tsh Mil 177. ... huduma ya upimaji kwa bei nafuu ili kila Mwananchi aweze kumudu na zaidi kuwawezesha wananchi

Maana Halisi ya Utumishi Uliotukuka

MWAKA MMOJA WA SHUGHULI ZAUTENDAJI JIJINI ARUSHA JULAI 2016 - JUNI 2017

Page 2: MWAKA MMOJA WA SHUGHULI ZA UTENDAJI JIJINI ARUSHA … · gharama ya Tsh Mil 177. ... huduma ya upimaji kwa bei nafuu ili kila Mwananchi aweze kumudu na zaidi kuwawezesha wananchi

UtanguliziHalmashauri ya Jiji la Arusha imeendelea kutekeleza majukumu yake kwakuzingatia Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2015,

Malengo ya Millenia (Millenium Goals 2015; Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Mwaka 2025 pamoja Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa miaka mitano.

Katika kufanikisha hayo Halmashauri ya Jiji imetekeleza shughuli zinazokuza uchumi na kuondoa umasikini,kutatua changamoto za ukosefu wa ajira na kuendeleza vita dhidi ya adui rushwa na ubadhirifu wa mali ya ummaJiji la Arusha limetekelezayote hayo ili kuhakikisha maisha bora kwa kila mwananchi yanapatikana.

Katika kuwezesha na kusimamia utekelezaji wa kazi za idara mbalimbali kwa kipindi cha Julai 2016 – Juni, 2017 Halmashauri ya Jiji imetekeleza kazi zifuatazo:

Page 3: MWAKA MMOJA WA SHUGHULI ZA UTENDAJI JIJINI ARUSHA … · gharama ya Tsh Mil 177. ... huduma ya upimaji kwa bei nafuu ili kila Mwananchi aweze kumudu na zaidi kuwawezesha wananchi

Ofisi ya MkurugenziMkurugenzi kama mtendaji mkuu amesimamia Sheria, Kanuni na Miongozo ili kuhakikisha Jiji la Arusha linaendelea kuwa bora katika utoaji wa huduma stahiki kwa wananchi na kwa ubora wa hali ya juu.

Mkurugenzi amefanikiwa kusimamia, kuitisha na kuongoza vikao vya Kisheria vya Kamati, Baraza pamoja na vikao vya Menejimenti. Vikao hivi vilisimamiwa kwa ufanisi mkubwa kwani vimeleta matokea chanya katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.Wakati huo huo Mkurugenzi ameiwakilisha Halmashauri katika vikao vya nje ya Halmashauri, Mikutano ya kitaifa na kimataifa pamoja na ziara za mafunzo ambazo kwa kiasi kikubwa zimesaidia kupata uelewa mpana zaidi ya namna na kuleta wepesi katika kusimamia shughuli za Jiji. Pia Mkurugenzi amefanikiwa katika kusimamia watumishi 3450 wafanye kazi kwa Uaminifu, Uadilifu na Weledi wa hali ya juu unaoendeana na kazi ya Serikali ya Awamu ya Tano. Pia amehakikiasha watumishi hao wanapata stahili zao kwa wakati, utii wa sheria mahala pa kazi, huku akiwaunganisha pamoja na kuwajengea uwezo wa kufanya kazi kama Timu (Team work spirit).

Kwa kasi hiyo hiyo Mkurugenzi amehakikisha Halmashauri inajizatiti nakujiimarisha katika ukusanyaji wa mapato na kubana matumiziyasiyokuwa ya lazima.

Page 4: MWAKA MMOJA WA SHUGHULI ZA UTENDAJI JIJINI ARUSHA … · gharama ya Tsh Mil 177. ... huduma ya upimaji kwa bei nafuu ili kila Mwananchi aweze kumudu na zaidi kuwawezesha wananchi

Hadi kufikia mwezi Juni, 2017 Halmashauri imevuka malengo kwa kukusanya jumla ya Sh.13,826,488,518 kutoka katika vyanzo vya ndani sawa na asilimia 112% ya lengo la kukusanya Sh.12,299,585,000.

Mafanikio haya katika ukusanyaji wa mapato yamewezeshwa na uboreshaji wa mfumo ya kielektroniki katika ukusanyaji mapato na usimamizi wa vyanzo vyote vya Halmashauri.

Mifumo hii pia imesaidia kudhibiti udanganyifu, usalama wa fedha pia imerahisisha utunzaji wa kumbukumbu za walipa kodi, kutambua wadaiwa na kusaidia kuongeza mapato.Ukusanyaji wa mapato kwa ufanisi umewezesha

Halmashauri ya Jiji chini ya Ofisi ya Mkurugenzi kutumia asilimia 60% ya mapato yake ya ndani kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kutoa mikopo yenye masharti na riba nafuu kwa vikundi vya wanawake na vijana na 40% ya mapato yametumika kutoa huduma kwa wannachi.

Kati ya makisio hayo kiasi cha Sh.12,299,585,000 zinatokana na vyanzo vya ndani na Sh.52,587,460,000 zinatokana na ruzuku kutoka serikali kuu, mifuko ya pamoja na wafadhili mbalimbali. Kwa kipindi cha mwezi Julai 2016 hadi mwezi Juni 2017 Halmashauri imeweza kukusanya na kupokea jumla ya Tsh .54,771,627,042 kiasi hiki ni sawa na asilimia 84 ya makadirio ya TSh.64,887,045,000 kwa mwaka 2016/17. Hata hivyo hadi kufikia mwezi Juni, 2017 jumla ya Tsh.13,826,488,518 zimekusanywa kutoka katika vyanzo vya ndani sawa na asilimia 112 ya lengo la kukusanya Tsh.12,299,585,000. Aidha mapato kutoka katika vyanzo vya nje ni Tsh. 40,945,138,525 sawa na asilimi 78 ya Lengo la Tsh 52,587,460,000.

Matumizi ya Halmashauri katika maeneo ya mishahara, matumizi ya kawaida, na miradi ya maendeleo imetumia Tsh. 54,771,627,042 sawa na asilimi 84 ya bajeti iliyopangwa ya Tsh.64,887,045,000.

FedhaKatika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/17 Halmashauri imekadiria kukusanya na kutumia jumla ya Sh.64,887,045,000.

Kazi zote hizo zimefanyika kupitia Idara zifuatazo:

Page 5: MWAKA MMOJA WA SHUGHULI ZA UTENDAJI JIJINI ARUSHA … · gharama ya Tsh Mil 177. ... huduma ya upimaji kwa bei nafuu ili kila Mwananchi aweze kumudu na zaidi kuwawezesha wananchi

Aidha Halmashauri ya jiji inatekeleza agizo la Serikali la kuchangia asilimia 10 ya mapato ya ndani na kutoa mikopo kwa wanawake na vijana.

Hadi Juni 2017 Halmashauri imetoa Sh.1,350,000,000 kutoka Sh.1,077,975,152 ya bajeti iliyopangwa hivyo kuvuka malengo kwa asilimia 13.

Page 6: MWAKA MMOJA WA SHUGHULI ZA UTENDAJI JIJINI ARUSHA … · gharama ya Tsh Mil 177. ... huduma ya upimaji kwa bei nafuu ili kila Mwananchi aweze kumudu na zaidi kuwawezesha wananchi

Usafi na MazingiraSuala ya Usafi limeendelea kuwa agenda ya kudumu katika Jiji la Arusha ili kuwakinga wananchi na maradhi yanayoweza kusababishwa na uchafu:

Zaidi ya hapo kuweka Jiji katika hali ya usafi ili kuvutia wageni wanaokuja kutembea na kwenye Mikutano ya Kimataifa.

Jiji limeendelea kusimamia uendelezaji wa Dampo la Kisasa lililopo Murriet. Kupitia Mradi wa Mpango Mji Mkakati (TSCP) uliopo chini ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI vilipokelewa vifaa 30(vifaa, magari na mitambo) kwa ajili ya uendeshaji wa Dampo hilo.

Kutaja kwa uchache vifaa hivyo ni wheel loader, bulldozer, Hydraulic Excavator, Landfill compactor Side loader, Tipper Truck, skip loader bukets nk.Upatikanaji wa vifaa hivi vimewezesha Dampo hilo kuanza kufanya kazi kisasa kwa kusindilia taka zinazomwagwa kila siku katika eneo hilo kwenye Jaa (Cell) maalum; Hali hii imeondoa mlundikano wa taka na kumaliza kabisa harufu katika eneo lile na zaidi inatunza mazingira.

Mradi huu pia umewezesha kujenga Jaa la tatu (Cell no 3) - Hapo awali ilikua moja, mizani, karakana ya Magari pamoja na eneo la kuoshea magari katika Jaa la Kisasa

la kuhifadhia Taka Muriet.Kutoka katika Mapato ya ndani tumefanikiwa kununua Gari Maalum la kufagia barabara nyakati za usiku kwa

Page 7: MWAKA MMOJA WA SHUGHULI ZA UTENDAJI JIJINI ARUSHA … · gharama ya Tsh Mil 177. ... huduma ya upimaji kwa bei nafuu ili kila Mwananchi aweze kumudu na zaidi kuwawezesha wananchi

gharama ya Tsh Mil 177. Gari linasaidia kufanya mji kuwa katika hali ya Usafi kwa kuwa lina uwezo mkubwa wa kufagia barabara nyingi za lami zilizopo katikati ya Mji.

Halmashauri imewajengea uwezo na hulka wananchi kufanya usafi katika maeneo yanayowazunguka pamoja na kushirikisha wakala wa usafi ambao ni vikundi vya Jamii vya wanawake na vijana pamoja na makampuni. Lengo ni kutoa ajira kwa makundi yote. Aidha jiji lina vikundi 6 vya vijana, kikundi kimoja cha wakinamama na vijana pamoja na Kampuni 9.

Page 8: MWAKA MMOJA WA SHUGHULI ZA UTENDAJI JIJINI ARUSHA … · gharama ya Tsh Mil 177. ... huduma ya upimaji kwa bei nafuu ili kila Mwananchi aweze kumudu na zaidi kuwawezesha wananchi

Mipango MijiKupitia Idara hii usimamizi na uendelezaji wa Mji kwa kuzingatia Sheria ya Mipango Miji ya mwaka 2007 imezingatiwa na kwa kuwa Mji wa Arusha unakuwa kwa kasi Serikali kupitia Wizara ya Ardhi ilisimamia uandaaji wa Mpango Kabambe wa Jiji la Arusha na kuridhia rasimu ya mwisho ya mpango Kabambe wa Jiji pamoja na viunga vyake unaohusisha eneo lote la Jiji la Arusha pamoja na baadhi ya maeneo ya Halmashauri za Wilaya ya Meru na Arusha.

Mpango huu umehakikisha kwamba kunakuwa na matumizi bora ya Ardhi, Mji unapangwa kwa ufanisi na kunakuwa na eneo la kutosha kwa ajili ya Ukanda wa Kijani.

Pia umeainisha Arusha kuwa Mji Mkuu wa Kijani na Utalii Afrika Mashariki huku dhima ikiwa ni kuwa na Jamii yenye uchumi mpana na unaoshirikishwa, Mawasiliano bila vikwazo, Arusha yenye Teknolojia, Ukanda wa Kijani na yenye utambulisho wa kipekee.

Page 9: MWAKA MMOJA WA SHUGHULI ZA UTENDAJI JIJINI ARUSHA … · gharama ya Tsh Mil 177. ... huduma ya upimaji kwa bei nafuu ili kila Mwananchi aweze kumudu na zaidi kuwawezesha wananchi

Mpango huu pia umekwishawasilishwa kwa wananchi kupitia mikutano ya hadhara kwa kila kata kwa ajili ya kukusanya Maoni (Public hearing).

Wakati huo huo Halmashauri ya Jiji la Arusha imefanyia kazi Malalamiko ya wananchi yaliyokuwa yakielekezwa kwenye gharama kubwa za upimaji wa Ardhi hivyo kwa sasa Jiji limeweza kununua Kifaa kimoja na kukarabati vifaa vitatu kwa ajili ya kupima Ardhi.

Vifaa hivyo vimegharimu Tsh Mil 60 (Mapato ya ndani) lengo nikutoa huduma ya upimaji kwa bei nafuu ili kila Mwananchi aweze kumudu na zaidi kuwawezesha wananchi kufanya shughuli zao katika mji salama na uliopangika.

Page 10: MWAKA MMOJA WA SHUGHULI ZA UTENDAJI JIJINI ARUSHA … · gharama ya Tsh Mil 177. ... huduma ya upimaji kwa bei nafuu ili kila Mwananchi aweze kumudu na zaidi kuwawezesha wananchi

Ardhi Ili kupunguza migogoro ya Ardhi jumla ya Hati 96 zimeandaliwa na kuwasilishwa kwa Ofisi ya Ardhi Kanda ili kukamilisha taratibu za umiliki.

Wakati huo huo Halmashauri imepokea malalamiko ya migogoro ya ardhi 221 ambapo 131 yamepatiwa ufumbuzi kwa kupewa maeneo mbadala eneo la oljoro lenye Ukubwa wa Ekari 100 lililotolewa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Malalamiko 44 yapo Mahakamani wakati 46 yanaendelea kutafutiwa ufumbuzi.

Halikadhalika Jiji limefanikiwa kurejesha Kiwanja cha Hospitali ya Wilaya No. 523 kilichopo eneo la Njiro chenye Ukubwa wa Ekari 7 ambacho kilitolewa kwa mtu binafsi kinyume cha utaratibu.

Page 11: MWAKA MMOJA WA SHUGHULI ZA UTENDAJI JIJINI ARUSHA … · gharama ya Tsh Mil 177. ... huduma ya upimaji kwa bei nafuu ili kila Mwananchi aweze kumudu na zaidi kuwawezesha wananchi

Ujenzi / Huduma za Barabara Halmashauri ya Jiji la Arusha iko katika utekelezaji wa miradi ya barabara kwa kutumia pesa za vyanzo vya ndani kiasi cha shilingi 1,953,079,500, fedha za mfuko wa barabara kiasi cha Shilingi 3,655,851,903.2. Kazi zinazofanyika ni:

Ujenzi wa mfereji wa maji ya mvua barabara ya Oljoro – Muriet (1.2Km) na Sekei na Baracuda

Matengenezo(Upgrading), barabara ya Sombetini–Tanesco kwa kiwango cha Lami(2.00Km)

Matengenezo (Rehabilitation), barabara ya Sunflag-Njiro kwa kiwango cha Lami (0.85Km), Matengeneo (Rehabilitation & Periodic Maintenance), barabara ya Kanisa-Haileselasie (2.0Km).

Ujenzi wa Kivuko (Box Culvert), barabara ya Kanisa-Njia ya Ng’ombe (Sombetini)

Matengenezo ya muda maalum kwenye barabara ya Mateves (Olmot) urefu (5Km).

ii.

iii.

iv.

v.

i.

Page 12: MWAKA MMOJA WA SHUGHULI ZA UTENDAJI JIJINI ARUSHA … · gharama ya Tsh Mil 177. ... huduma ya upimaji kwa bei nafuu ili kila Mwananchi aweze kumudu na zaidi kuwawezesha wananchi

Katika mradi uboreshaji miundombinu (TSCP) chini ya Ofisi ya Rais Tamisemi kupitia fedha za nyongeza (additional financing subproject) ziletengwa fedha Tsh. 17,979,985,486 na imetumika kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Unga Ltd- Muriet kwa kiwango cha lami (km 6.5) na ujenzi wa bwawa la kuhifadhi taka ngumu (Dampo) na uongezaji wa mfereji wa maji ya mvua (bondeni storm water drains)wenye urefu wa mita 300.

Matengenezo (Rehabilitation) ya barabara za katikati ya Mji (Ethiopia, Levolosi, Sharif, Clinic/Depot, Polisi-Esso kwa kiwango cha Lami

Matengenezo ya muda maalum na mfereji wa maji ya mvua kwenye barabara ya kijenge-mwanama-ppf (3.5Km), na matengenezo ya kawaida, barabara ya kijenge juu – Ngulelo (3.0Km).

Matengenezo ya muda maalumna ujenzi wa mfereji wa maji ya mvua, barabara za Esso-Longdong (3.0Km), Oljoro-Kisimani (4.0Km), Siara (2.2Km) na barabara ya Olasit (4.0Km).

Matengenezo ya maeneo korofi, barabara ya Moshono-Kwa Mrefu na Relini-Kwa Mrefu (3.5Km), Shamsa-Kibanda maziwa (1.8Km) na Oljoro-Terrat (3.5Km).

Matengenezo ya muda maalum, barabara za Olkeryan-Kanisa (4.0Km) na Tbl-Tanesco (4.5Km).

Matengeneo ya kawaida kwenye barabara za Muriet-Nadosoito (6.0Km), Mkonoo (6.0Km), na matengenezo ya maeneo korofi kwenye barabara za Engosheraton (4.60Km) na Tbl-Unga Ltd (1.30Km) na ujenzi wa Kivuko kwenye barabara ya Engosheraton.

Ujenzi wa Daraja katika Mto Ngarenaro kwenye barabara ya Lolovono na kivuko kwenye barabara ya Esso-Longdong.

vii.

viii.

ix.

x.

xi.

xii.

vi.

Page 13: MWAKA MMOJA WA SHUGHULI ZA UTENDAJI JIJINI ARUSHA … · gharama ya Tsh Mil 177. ... huduma ya upimaji kwa bei nafuu ili kila Mwananchi aweze kumudu na zaidi kuwawezesha wananchi

Maendeleo ya JamiiHalmashauri imeendelea kuwawezesha wananchi kujikwamua kimaisha kwa kuwajengea uwezo wa kukabiliana na changamotoza kiuchumi wa kuwapatia mikopo. Katika kipindi cha mwezi Januari hadi Juni, 2017 Jiji limetoa Jumla ya Sh.1,350,000,000/=kwa vikundi vya wanawake na vijana 270. Ambapo kati ya fedha hiyo jumla ya Shs. 815,000,000/= zimekopeshwa kwa vikundi 163vya wanawake na jumla ya Sh.535,000,000/= zimekopeshwa kwa vikundi vya vijana 107.

Halikadhalika marejesho ya mikopo ya vikundi vya wanawake na vijana kuanzia Julai, 2016 hadi Juni, 2017 ni Sh.309,888,200/=fedha hizi pia zimeendelea kukopesha vikundi vya Wanawake na vijana.

Fedha hizo ni asilimia kumi ya mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji na kwa mwaka 2016/2017 na Halmashauri haina deni kwenye utoaji wa mikopo kwa mwaka husika kwa kuwa fedha zimeendelea kutolewa kwa kila robo kadiri ya makusanyo yaliyopatikana. Mafanikio katika utoaji wa Mikopo umetokana na uongozi wa Jiji chini ya Mkurugenzi kubadili utaratibu wa mazoea uliokuwepo wa kufuata miongozo ya

Page 14: MWAKA MMOJA WA SHUGHULI ZA UTENDAJI JIJINI ARUSHA … · gharama ya Tsh Mil 177. ... huduma ya upimaji kwa bei nafuu ili kila Mwananchi aweze kumudu na zaidi kuwawezesha wananchi

ukopeshaji iliyotolewa na Wizara yenye dhamana ya Wanawake na Vijana, kuunda Kamati za mikopo katika kila kata na ile ya Makao makuu ya halmashauri ya Jiji.Wito kwa vikundi vyote ni kuhakikisha wanafuata taratibu zote na kukamilisha usajili mapema ikiwa ni pamoja kufuata maelekezo yote watakayopewa na Maafisa Maendeleo ya Jamii.

Page 15: MWAKA MMOJA WA SHUGHULI ZA UTENDAJI JIJINI ARUSHA … · gharama ya Tsh Mil 177. ... huduma ya upimaji kwa bei nafuu ili kila Mwananchi aweze kumudu na zaidi kuwawezesha wananchi

Huduma za Tiba zimeendelea kutolewa katika vituo vyote vya Serikali na Binafsi sambamba na Halmashauri kufanikisha kazi ya kununua na kusambaza Dawa na Vifaa Tiba katika vituo hivyo pamoja na Zahanati.

Uhamasishaji wa Jamii kujiunga na Mfuko wa Tika umefanyika na Jumla ya Kaya 18,364 zimejiunga na Bima ya Afya ijulikanayo kama tiba kwa kadi (TIKA) na wateja wanaendelea kupata huduma za Afya katika vituo vya huduma za Afya 7 vilivyoko chini ya Jiji. Watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi 1000 wamelipiwa huduma ya matibabu kwa mfuko wa Tiba kwa Kadi.

Kama tunavyofahamu Lishe ni Mpango wa Kitaifa na Jiji tumeutekeleza kwa kugawa matone ya Vitamin A na Dawa za Minyoo. Jumla ya watoto 60,065 sawa na 87% waliweza kufikiwa. Elimu imetolewa kwa wauguzi 20 na matabibu 10 juu ya upimaji na ushauri wa masuala ya Lishe. Wiki ya Unyonyeshaji imeadhimishwa kwa kutoa Elimu kwa wazazi/walezi 3242 na kufanya thathmini ya Hali ya Ukuaji wa watoto 1303 walio chini ya Umri wa miaka mitano na matokeo ni watoto 1282 (98.4%) hali nzuri ya Lishe, watoto 9 (0.7%) Lishe ya wastani, watoto 3(0.2%) hali mbali ya Lishe na watoto 9(0.7%) waligundulika kuwa na Lishe iliyozidi.

Afya

Page 16: MWAKA MMOJA WA SHUGHULI ZA UTENDAJI JIJINI ARUSHA … · gharama ya Tsh Mil 177. ... huduma ya upimaji kwa bei nafuu ili kila Mwananchi aweze kumudu na zaidi kuwawezesha wananchi

Vituo vya Afya

Zahanati

Ili kuongeza wigo wa utoaji huduma Wilaya inajenga Zahanati mpya 3 katika Kata za Olmoti, Baraa na Kimandolu ambazo tayari zipo katika hatua mbalimbali za ujenzi. Aidha zahanati ya Kimandolu imekamilika na inatoa huduma kwa wananchi.

Katika mwaka huu wa Fedha Halmashauri imeweza kuongea Vituo vya Afya kwa kuanza ujeni wa Kituo cha Afya Moshono, Muriet na kwa hivi sasa wananchi wanahudumiwa na vituo vya Afya 7 na zahanati 7.

Aidha Wilaya kwa kupitia wadau wake, imefanikiwa kufanya ukarabati wa vyumba kwa ajili ya Huduma za uzazi wa mpango na kuwahudumia kinamama walioharibikiwa mimba katika vituo vya afya vinne (Themi, Kaloleni, Mkonoo na Levolosi.Pia Vituo viwili (Kaloleni & Levolosi) vimeweza kufungiwa mfumo wa Kielektroniki wa kukusanya mapato na Utunzaji wa taarifa za huduma za Afya Vituoni.

Halmashauri ya Jiji ina mpango wa kujenga Hospital ya Wilaya katika eneo la Njiro ambapo katika mwaka wa Fedha 2017/2018 imetenga Tsh Bil 1 toka katika mapato ya ndani.

Hospital ya Wilaya

Page 17: MWAKA MMOJA WA SHUGHULI ZA UTENDAJI JIJINI ARUSHA … · gharama ya Tsh Mil 177. ... huduma ya upimaji kwa bei nafuu ili kila Mwananchi aweze kumudu na zaidi kuwawezesha wananchi

Elimu Msingi Katika halmashauri ya Jiji la Arusha kuna shule za msingi 141 ikiwa za Serikali ni48 na93 ni binafsi zenye Jumla ya wanafunzi 91,499. Hali ya uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza imeongezeka na kufikia wanafunzi 16,205 sawa na 190.93% ukilinganisha na maoteo yalikuwa wanafunzi 8,487.

Idara hii inafanya vizuri katika kusimamia utoaji wa Elimu bora kwani na kwa mwaka 2016 kiwango cha Ufaulu kwa wanafunzi waliofanya mtihani wa darasa la saba ni 92.5%.

Page 18: MWAKA MMOJA WA SHUGHULI ZA UTENDAJI JIJINI ARUSHA … · gharama ya Tsh Mil 177. ... huduma ya upimaji kwa bei nafuu ili kila Mwananchi aweze kumudu na zaidi kuwawezesha wananchi

Elimu SekondariElimu ya Sekondari Jiji la Arusha lina jumla ya Shule 50 kati ya hizo 26 ni za Serikali na 24 ni binafsi/ Mashirika ya dini.

Takwimu zinaonyesha kuna ongezeko la Udahili wa wanafunzi wa Kidato cha kwanza kwa mwaka 2016 na 2017 kwa zaidi ya wanafunzi 1617 sawa na 22.33% kulinganisha na miaka ya nyuma.

Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa mwaka 2016/17 imejenga jumla ya madarasa 85 ya shule za Sekondari na Msingi ambayo yamekamilika na yanatumika kama ifuatavyo:

Madarasa yaliyojengwa

Page 19: MWAKA MMOJA WA SHUGHULI ZA UTENDAJI JIJINI ARUSHA … · gharama ya Tsh Mil 177. ... huduma ya upimaji kwa bei nafuu ili kila Mwananchi aweze kumudu na zaidi kuwawezesha wananchi

i. Shule za Msingi 60 kwa thamani ya Sh.1, 265,264,894.00ii. Shule za Sekondari 25 kwa thamani ya Sh. 404,854,127.92Jumla Kuu ya gharama iliyotumika kujenga madarasa yote 85 hadi kukamilika niSh. 1,670,119,021.92.

Aidha, ujenzi wa vyumba vyote vya madarasa ulifanywa na Bodi/Kamati za Shule husika chini ya usimamizi wa Wahandisi na Wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Jiji.

Halkadhalika tulipokea Fedha kutoka Wizara ya Elimu kwa ajili ya Ujenzi wa bweni 1 lenye uwezo wa kubeba wanafunzi 120, madarasa manne na maabara 1 katika shule ya sekondari Arusha Girls na kutoka Tasaf Opec III tulipata fedha za ujenzi wa hostel 2 kwenye shule ya Sekondari Korona, miradi yote imekamilika.

Halmashauri ya Jiji imeweza kupunguza gharama za Ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa Tsh 472,564,434/= na hii imetoka-na na kutumia mafundi wa kienyeji (Local Fundi) badala ya Kutumia Makandarasi.

Katika Shule za Msingi kiasi cha Tsh 395,547,434/= na Sekondari Tsh 77,017,000/=.

Madeni ya waalimu wapatao 569 yanayotokana na Likizo, uhamisho, masomo, matibabu na gharama za mazishi kiasi cha shilingi 110,006,595.05.

Ofisi ya Rais – TAMISEMI mwezi Machi, 2017 ilileta fedha Tshs. 12,573,700/=kwa ajili ya kuwali-pa Walimu wa Shule za Msingi 88 wenye madai ya likizo, masomo, mazishi na uhamisho.

Kupunguza Gharama za Ujenzi

Madeni ya Walimu

Page 20: MWAKA MMOJA WA SHUGHULI ZA UTENDAJI JIJINI ARUSHA … · gharama ya Tsh Mil 177. ... huduma ya upimaji kwa bei nafuu ili kila Mwananchi aweze kumudu na zaidi kuwawezesha wananchi

Malipo haya yalifanywa kwa Walimu tarehe 30/04/2017 na Halmashauri ya Jiji la Arusha tayari imelipa Sh. 169,000,000 kwa walimu mbalimbali na fedha hizo ni za mapato ya ndani.

Katika Jiji laArusha kuna viwanda vikubwa zaidi ya 20 na viwanda vidogo vidogo zaidi ya 200.

Kwa kipindi kirefu viwanda hivi vimekua vikifanya kazi kwa ushindani mkubwa lakini bado vinakabiliwa na changamoto ya Soko na ushindani uliopo katika bidhaa nyingi zinazotoka nje ya Nchi.

Katika kukabiliana na hali hiyo elimu imetolewa kwa wananchi kuthamini vya nyumbani kuliko bidhaa na nje.

Pia Halmashauri ya Jiji katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya Tano kwenye mpango Kabambe wa Jiji la Arusha (Master Plan) limeainishwa eneo lenye Ekari 750 lililoko katika kata ya Terrat kwa ajili ya uwekezaji wa Viwanda.

Kumekuwa na ongezekola wanafunzi 1,617 sawa na asilimia 22.33% kulinganisha na udahili wa mwaka 2015 kabla ya Elimu bila malipo na mwaka 2017 baada ya Elimu bila malipo.

Elimu bure

VIWANDA NA UWEKEZAJI

Page 21: MWAKA MMOJA WA SHUGHULI ZA UTENDAJI JIJINI ARUSHA … · gharama ya Tsh Mil 177. ... huduma ya upimaji kwa bei nafuu ili kila Mwananchi aweze kumudu na zaidi kuwawezesha wananchi
Page 22: MWAKA MMOJA WA SHUGHULI ZA UTENDAJI JIJINI ARUSHA … · gharama ya Tsh Mil 177. ... huduma ya upimaji kwa bei nafuu ili kila Mwananchi aweze kumudu na zaidi kuwawezesha wananchi

Utawala

Utumishi uliotukuka

Halmashauri imeendelea kusimamia watumishi wa kudumu 3,450.

Watumishi hao wamepatiwa mafunzo na kujengewa uwezo wa kutoa huduma bora kwa mujibu wa Mkataba wa Huduma kwa Wateja.

Kupitia Idara hii Vikao vya kisheria vimefanyika kuanzia ngazi ya Jiji hadi kwenye Mitaa ambavyo Kwa kiasi kikubwa vimeleta tija na kasi ya maendeleo katika Jiji yetu.

Viongozi waJiji wameweza kukutana na wananchi wao mara kwa mara na kutatua changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika kuimarisha ushirikiano na nguvu ya pamoja ili kuleta maendeleo ya haraka.

Page 23: MWAKA MMOJA WA SHUGHULI ZA UTENDAJI JIJINI ARUSHA … · gharama ya Tsh Mil 177. ... huduma ya upimaji kwa bei nafuu ili kila Mwananchi aweze kumudu na zaidi kuwawezesha wananchi

Kitengo cha sheriaKitengo hiki kimeendelea kutekeleza majukumju yake ya Msingi ya kuishauri Halmashauri kwenye masuala yote ya Kisheria, kuiwakilisha halmashauri kwenye mashauri 53 yaliyoko Mahakamani, kuhakikisha wadaiwa wa majengo wanapelekwa Mahakamani, kuandaa na kutoa mikataba ya upangaji pamoja na kuandaa Sheria ndogo za Jiji pamoja na kuhakiki Mikataba yote ya Halmashauri.

Pia kitengo hiki kiliweza kuiwakilisha vyema Halmashauri kwenye mashauri yote yaliyoko Mahakani na mpaka kufikia Mwezi Machi 2017 Kesi zilizoko Mahakani ni 34, Kesi tulizoshinda ni 9 tulizoshindwa 2 na mashauri mengine bado yanaendelea Mahakani.

Page 24: MWAKA MMOJA WA SHUGHULI ZA UTENDAJI JIJINI ARUSHA … · gharama ya Tsh Mil 177. ... huduma ya upimaji kwa bei nafuu ili kila Mwananchi aweze kumudu na zaidi kuwawezesha wananchi

Mradi wa Tasaf

-

-

Halmashauri ya Jiji la Arusha inanufaika na Mradi wa Uhawilishaji wa kaya maskini sambamba na miradi yenye lengo la kunusuru kaya maskini inayofadhiliwa na Opec – Tasaf III.

Mradi huu umetekelezwa kwenye Mitaa 70 ya Jiji la Arusha yenye Kaya 5149 na kaya zote zimelipwa kwa awamu 11 tangu mradi huu ulivyoanzwa kutekelezwa na Fedha zilizotumika ni Bil 2.5.

Pia tulipokea jumla ya Ths Mil. 357 kwa ajili ya Miradi ya kunusuru kaya Maskini na tuliweza kutekeleza miradi tisa ambayo ni kuku wa kienyeji– Lolovono, Kuku na Mbuzi –Terrati Mlimani, Kuku wa kienyeji – Moivoi, Ushonaji Kambi ya Fisi pamoja na miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa Shule ya Msingi Azimio, Ujenzi wa bweni Shule ya Sekondari Korona, vitalu vya Mitti – Ally nyanya na Osunyai na ujenzi wa kivuko oloresho.

Halikadhalika tumefanikiwa kuunda vikundi 37 vya kuweka akiba na kukopa kwenye ya Jiji la Arusha.

Page 25: MWAKA MMOJA WA SHUGHULI ZA UTENDAJI JIJINI ARUSHA … · gharama ya Tsh Mil 177. ... huduma ya upimaji kwa bei nafuu ili kila Mwananchi aweze kumudu na zaidi kuwawezesha wananchi

Malalamiko ya wananchi yanaratibiwa kwa kusikilizwa na Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi kila siku ya Jumatano. Pia Mkuu wa Wilaya amefanya mikutano katika mitaa yote ya Jiji la Arusha kuskiliza kero mbalimbali za wananchi.

Zaidi ya hapo malalamiko hupokelewa kwenye sehemu maalumu ya Dawati la Malalamiko ambalo liko wazi kwa siku zote za kazi. Dawati hilo linaratibiwa na maafisa wanne ambao wanasikiliza na kutafuta ufumbuzi wa malalamiko ya Ardhi, Biashara, Barabara,Utumishi n.k.

Jumla ya kero zilizopokelewa kwenye Dawati la Malalamiko ni 161 na zilizopatiwa ufumbuzi ni 149 na kero nyingine zinafanyiwa kazi.

Malalamiko

Page 26: MWAKA MMOJA WA SHUGHULI ZA UTENDAJI JIJINI ARUSHA … · gharama ya Tsh Mil 177. ... huduma ya upimaji kwa bei nafuu ili kila Mwananchi aweze kumudu na zaidi kuwawezesha wananchi

HitimishoKatitka kipindi cha mwaka mmoja wa utekelezaji na usimamizi wa kazi za Halmashaurichini ya Mkurugenzi Athumani Kihamia kumemekuwa na mafanikio makubwa katika utekelezaji wa miradi, utoaji wa huduma na kuwajengea wananchi uwezo wa kujikwamua kiuchumi.

Hata hivyo bado imewekwa mikakati ya kuhakikisha kuwa Jiji hili linaendelea kutoa hudumabora kwa wananchi:

Kuongeza juhudi za ukusanyaji wa mapato ya ndani na fedha zinazopatikana kupelekwa katika utekelezaji wa vipaumbele vya Jiji.

Kuendeleza ujenzi wa vyumba vya madarasa, nyumba za walimu, majengo ya utawala, mabweni na maabara kwenye shule za Msingi na sekondari

Kuhakikisha kila Kata inakuwa na zahanati au Kituo cha afya

Kuendelea kushirikiana na wadau na wafadhili mbalimbali Kujenga masoko ya kisasa, Stendi, Miji ya Kisasa ili kuwawezesha wananchi wengi kukuza kipato chao kwa kujiajiri na kupunguza umasikini wa kipato

Kulinda Amani na kudumisha Ulinzi na Usalama

Kuanza kutekeleza Mpango Kabambewa Jiji la Arusha

Kuboresha usafi wa mji na maeneo ya pembezoni

Kutoa fursa za uwekezaji katika Jiji la Arusha

Jiji la Arusha linatarajia mafanikio makubwa zaidi na ushirikiano toka kwa wananchi ili kukamilisha yale yaliyoainishwa kwenye ilani ya uchaguzi kwa maendeleo ya wananchi wa Arusha.

Page 27: MWAKA MMOJA WA SHUGHULI ZA UTENDAJI JIJINI ARUSHA … · gharama ya Tsh Mil 177. ... huduma ya upimaji kwa bei nafuu ili kila Mwananchi aweze kumudu na zaidi kuwawezesha wananchi
Page 28: MWAKA MMOJA WA SHUGHULI ZA UTENDAJI JIJINI ARUSHA … · gharama ya Tsh Mil 177. ... huduma ya upimaji kwa bei nafuu ili kila Mwananchi aweze kumudu na zaidi kuwawezesha wananchi
Page 29: MWAKA MMOJA WA SHUGHULI ZA UTENDAJI JIJINI ARUSHA … · gharama ya Tsh Mil 177. ... huduma ya upimaji kwa bei nafuu ili kila Mwananchi aweze kumudu na zaidi kuwawezesha wananchi
Page 30: MWAKA MMOJA WA SHUGHULI ZA UTENDAJI JIJINI ARUSHA … · gharama ya Tsh Mil 177. ... huduma ya upimaji kwa bei nafuu ili kila Mwananchi aweze kumudu na zaidi kuwawezesha wananchi
Page 31: MWAKA MMOJA WA SHUGHULI ZA UTENDAJI JIJINI ARUSHA … · gharama ya Tsh Mil 177. ... huduma ya upimaji kwa bei nafuu ili kila Mwananchi aweze kumudu na zaidi kuwawezesha wananchi
Page 32: MWAKA MMOJA WA SHUGHULI ZA UTENDAJI JIJINI ARUSHA … · gharama ya Tsh Mil 177. ... huduma ya upimaji kwa bei nafuu ili kila Mwananchi aweze kumudu na zaidi kuwawezesha wananchi

ATHUMANI J. KIHAMIAMKURUGENZI WA JIJI

ARUSHA