9
USALAMA WA MOTO KATIKA NYUMBA YAKO Toleo 1 – March 2017 - Swahili

USALAMA WA MOTO KATIKA NYUMBA YAKO · . Tunza blanketi za moto katika jiko ambapo zinaweza kuonekana kwa urahisi. Tumia dakika chache ukiwa na familia yako na kuchora mpango wa kuepuka

  • Upload
    others

  • View
    11

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

USALAMA WA MOTO

KATIKA NYUMBA YAKO

Toleo 1 – March 2017 - Swahili

32

Kengele ya moshi inayofanya kazi tu ndiyo inaokoa maisha. Kama ya kwako haifanyi kazi vizuri haiwezi kukuonya wewe na familia yako kama kuna moto nyumbani kwako.

Ili kuhakikisha kengele yako ya moshi inafanya kazi vizuri, fuata hatua hizi rahisi:• Angalia tarehe ya mwisho kutumika kwenye

kengele za moshi na ujaribu kupima kila mwezi.• Ikiwa una kengele za moshi zinazoongezwa

nguvu, angalia kuona kama betri zinahitaji kubadilishwa.

• Kengele zote za moshi lazima zibadilishwe kila baada ya miaka 10, bila kujali aina na chanzo chake cha nguvu.

Je unajua?Nyumba zote zinatakiwa na sheria kuwa na kengele za moshi zinazoongezwa nguvu zilizowekwa kwa kitaaluma kabla ya kuuzwa au kupangishwa.

Usalama wa Moto Katika Nyumba YakoKila mwaka, karibu moto 1,000 hutokea ndani ya nyumba na kusababisha mamilioni ya dola katika uharibifu na watu kupoteza maisha yao. Vifo vingi vinatoka na moshi na mafusho yenye sumu. Kwa kuchukua hatua hizi 10 rahisi, wewe unaweza kuboresha usalama wa nyumba yako na familia yako.

01Kengele ya Moshi

Zima moto na blanketi za moto zinaweza kutumika kuzima moto mdogo katika nyumba.

Kizima moto cha poda kikavu ni aina ya kawaida inayotumiwa katika nyumba. Kutumia aina mbaya ya kizima moto inaweza kuwa hatari. Kabla ya kufunga kizima moto nyumbani kwako, angalia ni kipi kinaweza kuwa bora kwako kwa kuingia kwenye tovuti ya DFES kwenye www.dfes.wa.gov.au.

Tunza blanketi za moto katika jiko ambapo zinaweza kuonekana kwa urahisi.

Tumia dakika chache ukiwa na familia yako na kuchora mpango wa kuepuka. Jifunze mara kwa mara au angalau mara moja kwa mwaka.

Mpango wako wa kuepuka lazima ujumuishe:• zaidi ya njia moja kwa kila chumba, ikiwa ni pamoja na madirisha pale

inapowezekana;• njia salama na rahisi ya kuepuka kwa ndugu zako wa familia wenye

mahitaji maalumu;• njia ya kuepusha wanyama wapenzi wako; na• sehemu ya kukutania kwa kila mmoja nje.

03Zima moto& Blanketi za Moto

02Mpango wa KuepukaMoto Nyumbani

54

Moto mwingi majumbani huanza jikoni. Kaa salama wakati unapika kwa kufuata hatua hizi:

• usiache chakula kwenye jiko bila kuwa na mtu.

• usiweke vitu kama vile taulo za chai karibu na jiko au kwenye vifaa vya kupikia.

76

04 Moto Jikoni

Kama mafuta au mgando ukishika moto wakati unapika:

• zima moto;• kama inawaka kwa juu, usiuhamishe;• funika moto kwa kifuniko, ubao wa kukatia wa mbao, au blanketi ya moto; na• usitumie maji kamwe. Mafuta yanayowaka au

mafuta hupuka juu na kusababisha moto kuenea.

Ikiwa huwezi kuzima moto, piga simu sifuri tatu (000) na anza kutenda mpango wako wa kuepuka.

Kuweka joto majumbani ni sababu kubwa ya moto wa majumbani wakati wa baridi.• Tumia tu vifaa vinavyokubalika kwa viwango vya Australia na

viweze kuwekwa na mtu mwenye sifa zinazostahili.• Angalia vifaa vyako mara moja kwa mwaka. Vipande vya

umeme vya vilivyochakaa au vifurushi vinapaswa kubadilishwa mara moja.

• Daima weka vifaa moja kwa moja kwenye vituo vya nguvu ya umeme vya kudumu na kamwe usiwazike kwenye adapta vifaa zaidi ya nguvu yake.

• Usiache kamwe watoto karibu na vifaa vya moto bila usimamizi.

• Hakikisha vifaa vyote viko angalau mita moja kutoka kwenye hita

Chanzo kingine kikubwa kinachofuata cha moto majumbani ni moshi kutoka kwenye vitu. Hakikisha:

• Huachi sigara inayowaka sehemu isiyostahili;• usivute sigara kwenye kitanda;• kutumia kipulizo na kuzima kabisa cheche za

sigara;• usiwaache watoto peke yao karibu na kiwasha

sigara au viberiti na• Jihadharini wakati unavuta sigara na kunywa

pombe maana uko katika hatari kubwa ya kusinzia.

98

05Sigara, Washa moto& Viberiti 06

Umeme wa Nyumbani& Vifaa vya Moto

Hizi ni hatua rahisi ambazo zinaweza kutunza familia na nyumba yako salama.

• Angalia sehemu ya moto, kwenye matofali, mirija na mafuta kabla ya kuwasha moto wa kwanza wa mwaka.

• Angalia kama flue ina ngozi mbili au tatu za kinga ili kuzuia joto kali linalowaka moto au mbao kwenye paa.

• Usitumie vimiminika vyenye kuwaka (petroli, maji nyepesi, nk) kuwasha moto wa wazi.

• Muda wote linda mahali pa moto wako wa wazi na skrini nzuri ya meshi.

• Hakikisha unazima moto wote na kuondoa mkaa kabisa kabla ya kwenda kulala au kutoka nyumbani.

• Usiache kamwe watoto peke yao karibu na moto wa wazi.• Hakikisha vitu vyote viko angalau mita moja kutoka

kwenye joto.

Mara nyingi mishumaa na viwasha mafuta vinahusika kwa kuanzisha moto wa nyumbani. Ili kuzuia hili:

• usiweke mishumaa kwenye madirisha. Inaweza kurushwa na kusababisha vitambaa na mapazia ya madirisha kukamata moto;

• zima mishumaa na mafuta ya kuwaka kabla ya kwenda kulala au kutoka nyumbani; na

• kamwe usiache watoto bila kuwa na mtu mzima na mishumaa inayowaka ya mafuta.

10

07Moto wa Wazi,Mafuta & Mirija

08 Mishumaa& Viwasha Mafuta

11

Kama moto ukianza katika nyumba yako na huwezi kuuzima kwa usalama, fuata hatua hizi:• Zima moto na uupunguze kasi ili usieneze kwa kufunga mlango wa

chumba kama ikiwezekana.• Toa taarifa na kusaidia wengine katika nyumba kuweza kuondoka kama

ni salama kufanya hivyo.• Ili kuepuka kuhema moshi, jaribu kuwepo chini na karibu ya sakafu.• Tendea mpango wako wa kuepuka.• Kabla ya kufungua mlango uliofungwa, usikilize kwa nyuma ya mkono

wako. Ikiwa una moto basi tumia njia nyingine ya kutoka.• Toka kwenye nyumba yako na nenda mahali salama panapokubalika

kwenye mpango wako, kama vile boksi yako ya barua.• Piga simu sifuri tatu (000) mara moja na onya jirani zako inavyohitajika.• Kumbuka, usirudi tena katika nyumba inayowaka moto kwa hali yoyote.

Kama nguo ya mtu ikikamata moto, wanalazimika:

1312

10Simama, Anguka, Funika & Zungusha

Ili kumsaidia mtu akiwa na nguo zinazoungua moto, wazungushe nyuma na mbele kwenye sakafu au funika mishale na blanketi ya moto.

mara moja. Kukimbia kutaongeza muwasho.

kwenye sakafu.

nyuso zao na mikono yao ili kuepuka mishale na moshi.

nyuma na mbele kwenye sakafu kuzima mishale ya moto.

09Kuhusika na Moto katika Nyumba yako

SIMAMA ANGUKA FUNIKA ZUNGUSHA

Mpango wa Kuepuka Moto NyumbaniTumia nafasi hii kuchora mpango wako wa kuepuka moto wa nyumbani. Ishara kwenye kulia itakusaidia kuchora mpango wako. Mara baada ya kupangilia mpango wako, jizoeze mara kwa mara na familia yako.

Chora alama hizi

SehemuYa kukutania

Blanketiya moto

Njia yakuepuka

Zima moto

Sehemu yaMlango/funguo

za dirisha

Kengeleya moshi

1514

Government of Western Australia (Serikali ya Australia ya Magharibi )Department of Fire and Emergency Services (Idara ya Moto na Huduma za Dharura )Simu: +61 8 9395 9300 Faksi: +61 8 9395 9384Baruapepe: [email protected] Tovuti: http://www.dfes.wa.gov.auhttp://www.emergency.wa.gov.au

Onyo: Taarifa zilizomo katika chapisho hili hutolewa kwa hiari kama huduma ya umma na Idara ya Moto na Huduma za Dharura (DFES). Chapisho hili limeandaliwa kwa uaminifu na linatokana na vyanzo vilivyoaminika kuwa vinaaminika na sahihi wakati wa kuchapishwa. Hata hivyo, kuaminika na usahihi wa habari hauwezi kuhakikishiwa na DFES haitahusika na dhima au tendo lolote au ukosaji uliofanywa au usiofanywa kwa kutegemea habari na kwa matokeo yoyote yawe ya moja kwa moja au yasiyo ya moja kwa moja, kutokana na tendo kama hilo au ukosefu wa kitu. Chapisho lina lengo la kuwa mwongozo tu na wasomaji wanapaswa kupata ushauri wao wenyewe wa kujitegemea na kufanya maswali yao wenyewe muhimu.

USALAMA WA MOTO KATIKA NYUMBA YAKO

Toleo 1 – March 2017 - Swahili