33
Septemba 2014 Mpangilio: [email protected] Hakijamii Economic and Social Rights Centre (Hakijamii) 53 Park Building, kwenye barabara ya Ring Rd, tawi la Ngong Rd Sanduku la Posta 11356 - 00100, Nairobi Kenya Simu: +254 020 2589054/2593141 Rununu: +254 726 527876 Barua pepe: [email protected] Tovuti: www.hakijamii.com © Septemba 2014. Haki zote zimehifadhiwa Hakijamii KUFANIKISHA MAGEUZI YA SHERIA ZA KUMILIKI ARDHI NCHINI KENYA TOLEO MAARUFU LA MSWADA WA KUMILIKI ARDHI YA JAMII Utafiti na uchapishaji wa kitabu hiki umefanikishwa na ubalozi wa Sweden Kupitia mpango wa maendeleo ya mashirika yasio ya kiserikali (CSUDP), KIOS – Hazina ya Finland ya kutetea haki za binadamu, AJWS na MISEROR.

Hakijamii Economic and Social Rights Centre (Hakijamii ... · TOLEO MAARUFU LA MSWADA WA KUMILIKI ARDHI YA JAMII Utafiti na uchapishaji wa kitabu hiki umefanikishwa na ubalozi wa

  • Upload
    others

  • View
    1

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Hakijamii Economic and Social Rights Centre (Hakijamii ... · TOLEO MAARUFU LA MSWADA WA KUMILIKI ARDHI YA JAMII Utafiti na uchapishaji wa kitabu hiki umefanikishwa na ubalozi wa

Septemba 2014

Mpa

ngilio

: pew

ambu

@yah

oo.co

m

Hakijamii

Economic and Social Rights Centre (Hakijamii)53 Park Building, kwenye barabara ya Ring Rd, tawi la Ngong Rd

Sanduku la Posta 11356 - 00100, Nairobi Kenya Simu: +254 020 2589054/2593141

Rununu: +254 726 527876 Barua pepe: [email protected]

Tovuti: www.hakijamii.com

© Septemba 2014. Haki zote zimehifadhiwa

Hakijamii

KUFANIKISHA MAGEUZI YA SHERIA ZA KUMILIKI ARDHI NCHINI KENYA

TOLEO MAARUFU LA MSWADA WA KUMILIKI ARDHI YA JAMII

Utafiti na uchapishaji wa kitabu hiki umefanikishwa na ubalozi wa Sweden Kupitia mpango wa maendeleo ya mashirika yasio ya kiserikali (CSUDP), KIOS – Hazina ya Finland ya kutetea haki za

binadamu, AJWS na MISEROR.

Page 2: Hakijamii Economic and Social Rights Centre (Hakijamii ... · TOLEO MAARUFU LA MSWADA WA KUMILIKI ARDHI YA JAMII Utafiti na uchapishaji wa kitabu hiki umefanikishwa na ubalozi wa

KUFANIKISHA MAGEUZI YA SHERIA ZA KUMILIKI ARDHI NCHINI KENYA

TOLEO MAARUFU LA MSWADA WA KUMILIKI ARDHI YA JAMII

Septemba 2014

Page 3: Hakijamii Economic and Social Rights Centre (Hakijamii ... · TOLEO MAARUFU LA MSWADA WA KUMILIKI ARDHI YA JAMII Utafiti na uchapishaji wa kitabu hiki umefanikishwa na ubalozi wa

Hakijamii

Economic and Social Rights Centre (Hakijamii) 53 Park Building, Along Ring Rd, off Ngong Rd

S.L.P. 11356 - 00100, Nairobi Kenya Simu: +254 020 2589054/2593141

Rununu: +254 726 527876 Barua pepe: [email protected]

Tovuti: www.hakijamii.com

© Septemba 2014. Haki zote zimehifadhiwa.

ISBN No: 978-9966-1688-5-6

Utafiti na uchapishaji wa kitabu hiki umefanikishwa na ubalozi wa Sweden Kupitia mpango wa maendeleo ya mashirika yasio ya kiserikali

(CSUDP), KIOS – Hazina ya Finland ya kutetea haki za binadamu, AJWS na MISEROR.

Wachapishaji watakubali ombi la kuchapisha sehemu ya mwongozo huu kwa nia ya kuhakikisha nakala hii imesambazwa kwa wale wanaohitaji.

Ili kuwasilisha ombi lako wasiliana na:

Mkurugenzi, Economic and Social Rights Centre (Hakijamii)

53 Park Building, Ring rd, off Ngong rd, S.L.P. 11356, 00100 Nairobi Kenya

Page 4: Hakijamii Economic and Social Rights Centre (Hakijamii ... · TOLEO MAARUFU LA MSWADA WA KUMILIKI ARDHI YA JAMII Utafiti na uchapishaji wa kitabu hiki umefanikishwa na ubalozi wa

YALIOMO

ORODHA YA VIFUPISHO ......................................................................... iv

SHUKURANI ................................................................................................ v

1.0 Utangulizi ......................................................................................... 1

2.0 HISTORIA YA KIKATIBA,SHERIA NA SERA

ZA MAPENDEKEZO YA MSWADA WA

KUMILIKI ARDHI ZA KIJAMII ....................................................... 5

3.0 MADHUMUNI YA MSWADA HUU ............................................. 8

4.0 UFAFANUZI WA NENO “JAMII” .................................................... 10

5.0 USAJILI WA ARDHI YA JAMII ....................................................... 12

6.0 MASWALI YANAYOULIZWA KILA WAKATI .............................. 16

7.0 MBINU ZA KUTATUA MIZOZO.................................................... 22

8.0 MAMBO YANAYOFAA KUANGAZIWA KATIKA

KATIBA YA KILA JAMII ................................................................. 23

9.0 KIAMBATISHO ................................................................................. 25

Page 5: Hakijamii Economic and Social Rights Centre (Hakijamii ... · TOLEO MAARUFU LA MSWADA WA KUMILIKI ARDHI YA JAMII Utafiti na uchapishaji wa kitabu hiki umefanikishwa na ubalozi wa

ORODHA YA VIFUPISHO

ADR Alternative Dispute Resolution

ESRC Economic and Social Rights Centre

NLC National Land Commission

NRM Natural Resource Management

Page 6: Hakijamii Economic and Social Rights Centre (Hakijamii ... · TOLEO MAARUFU LA MSWADA WA KUMILIKI ARDHI YA JAMII Utafiti na uchapishaji wa kitabu hiki umefanikishwa na ubalozi wa

v

Toleo maarufu la m

swada w

a kumiliki ardhi ya jam

ii

SHUKURANI

Uchapishaji wa kitabu hiki umefanikishwa na juhudi za wafanyikazi wa Hakijamii wakiongozwa na mkurugenzi mtendaji, Marehemu Odindo Opiata. Shukurani za dhati kwa juhudi za Lucy Baraza, Peter Karachu, Irene Mutheu, Collins Liko, Lewis Wandaka, Sylvia Mbataru, Marcy Kadenyeka na Pauline Musangi waliosahihisha rasimu ya mswada huu. Hakijamii inawashukuru Okeyo Isaya na Benedict Omondi, wakufunzi wa shirika hili kwa mchango wao. Twamshukuru pia bi Betty Rabar kwa kuhariri toleo hili na Peter Wambu kwa kukiandaa kitabu kwa uchapishaji.

Hakijamii inawashukuru washirika wa mashirika ya kijamii waliotoa mchango wao kukamilisha rasimu ya mswada wa kumiliki ardhi za jamii. .

Hakijamii inatoa shukurani kwa mchango wa mashirika ya KIOS, SIDA, AJWS na MISEROR kwa mchango wao na kuunga mkono uchapishaji wa toleo hili.

Page 7: Hakijamii Economic and Social Rights Centre (Hakijamii ... · TOLEO MAARUFU LA MSWADA WA KUMILIKI ARDHI YA JAMII Utafiti na uchapishaji wa kitabu hiki umefanikishwa na ubalozi wa

vi

Tole

o m

aaru

fu la

msw

ada

wa

kum

iliki

ard

hi y

a ja

mii

Page 8: Hakijamii Economic and Social Rights Centre (Hakijamii ... · TOLEO MAARUFU LA MSWADA WA KUMILIKI ARDHI YA JAMII Utafiti na uchapishaji wa kitabu hiki umefanikishwa na ubalozi wa

1

Toleo maarufu la m

swada w

a kumiliki ardhi ya jam

ii

1.0 UTANGULIZI

Tarehe 21 Desemba 2012 waziri wa ardhi, James Orengo aliteua jopo la kubuni mswada wa ardhi za jamii, uhamisho na kuwapa watu makazi1. Baada ya majadiliano ya kina,jopo hilo lilikamilisha majukumu yake mwezi Februari 2014,rasimu hiyo inasubiri kuwasilishwa kwa waziri wa ardhi,makazi na maendeleo ya miji kabla kuwasilishwa bungeni ijadiliwe na kupitishwa kama sheria. Toleo hili linaegemea rasimu ya mwisho iliyobuniwa na jopo na ambalo limechapishwa na kusambazwa kwa umma. Mswada huu una athari kuu katika kulinda haki za ardhi ya umma na kufafanua haki za mshirika wa tatu, wakiwemo kampuni zilizo na nia ya kutumia maliasili katika ardhi ya jamii. Hatua iliyosalia ni ya bunge kuidhinisha na kutekeleza sheria hizo.

Licha ya kuwepo sheria za kitamaduni, haki za kumiliki ardhi za jamii hazijalindwa. Kutambua ardhi ya jamii katika katiba ndiyo msingi mkubwa katika mageuzi ya sheria za kumiliki ardhi Kenya. La kutia moyo ni kwamba nchi zengine barani Afrika kama vile Liberia, Namibia na Cameroon wamechukua hatua za kutambua ardhi za jamii

1 Hakijamii ilikuwa mwananchama wa jopo hilo

Page 9: Hakijamii Economic and Social Rights Centre (Hakijamii ... · TOLEO MAARUFU LA MSWADA WA KUMILIKI ARDHI YA JAMII Utafiti na uchapishaji wa kitabu hiki umefanikishwa na ubalozi wa

2

Tole

o m

aaru

fu la

msw

ada

wa

kum

iliki

ard

hi y

a ja

mii

na kuheshimu haki ya asilimali katika ardhi hizo.

Hatahivyo katika nchi nyingi, jamii zinazoishi katika ardhi ya jamii hukumbwa na tisho la kuhamishwa, au mali asili huchukuliwa bila idhini,na hata hunyimwa mapato au fidia.

Madhumuni ya kitabu hiki ni:

°° Kuelewa maswala muhimu kuhusu mswada wa ardhi ya umma

°° Kushirikisha jamii na raia kujadili mswada huu na kutoa mapendekezo ya kuuboresha.

Madhumuni ya mswada wa ardhi ya umma

Mjadala wa mfumo ulio bora wa kumiliki ardhi utakaolinda haki za ardhi ya jamii umejadiliwa tangu siku za ukoloni. Ilitarajiwa kwamba Kenya itakapojitawala, dhulma za kihistoria dhidi ya kumiliki ardhi zitatatuliwa, lakini hakuna mabadiliko. Miaka 40 baadaye ndipo hatua ya kwanza ilipochukuliwa kutatua tatizo la kumiliki ardhi. Mafanikio haya yalitokana na majadiliano na kubuniwa kwa sera ya kitaifa ya ardhi 2009. Si rahisi kupuuza swala hili hasaa kufuatia idadi ya 67% ya wakenya wanaoishi katika ardhi ya jamii.

La kusikitisha ni kwamba sheria imedhulumu haki ya

Page 10: Hakijamii Economic and Social Rights Centre (Hakijamii ... · TOLEO MAARUFU LA MSWADA WA KUMILIKI ARDHI YA JAMII Utafiti na uchapishaji wa kitabu hiki umefanikishwa na ubalozi wa

3

Toleo maarufu la m

swada w

a kumiliki ardhi ya jam

ii

kumiliki ardhi za jamii, tofauti na haki ya kumiliki ardhi binafsi. Mswada wa ardhi ya jamii ni dhihirisho la hatua ya ujasiri kukomesha dhulma za kihistoria zilizowasababisha wakaazi wengi kutengwa, kufurushwa ovyo na kusalia maskini.

Ardhi ya jamii iliitwa ardhi ya wakfuu chini ya sheria za ukoloni na hata katika katiba baada ya ukoloni,iliwanyima wenyeji asili haki ya kuisimamia.

Haya ndiyo matatizo sera ya kitaifa ya ardhi 2009 na katiba 2010 inalenga kutatua. Mswada wa ardhi ya jamii 2013 in mbinu ya kisheria inayolenga kutambua na kulinda haki ya ardhi za kijamii na kubuniwa kwa taasisi za kuzisimamia. Mswada huo pia unatoa mbinu za kusimamia mali asili, na utatuzi wa mizozo. Katika historia, ardhi ya jamii imedhaniwa kwamba haimilikiwi na mtu yeyote, hata katika maeneo ambapo tamaduni za kijamii zimewezesha watu kumiliki ardhi,kwa mfano katika jamii za wafugaji. Serikali ilimiliki ardhi za jamii na wenyeji kupokonywa makazi na hata kunyimwa fidia.

Mageuzi ya sheria za kumiliki ardhi ya umma yanakabiliwa na changamoto licha ya kuwepo kwa mswada wa kutetea haki ya ardhi ya jamii. Kando na Kenya, mataifa mengine yanayohujumu mfumo wa kitamaduni wa kumiliki ardhi ni kama Africa Kusini, Uganda na Tanzania. Mfano mkuu

Page 11: Hakijamii Economic and Social Rights Centre (Hakijamii ... · TOLEO MAARUFU LA MSWADA WA KUMILIKI ARDHI YA JAMII Utafiti na uchapishaji wa kitabu hiki umefanikishwa na ubalozi wa

4

Tole

o m

aaru

fu la

msw

ada

wa

kum

iliki

ard

hi y

a ja

mii

ukiwa Uganda ambapo kufikia mwaka 1975, walioshi kwenye ardhi ya jamii walitajwa kama “wamiliki wa hiari” waliokabiliwa na tisho la kufurushwa na serikali au watu waliokuwa na idhini ya serikali kusimamia ardhi ya jamii. Na licha ya kwamba Uganda walibuni sheria ya ardhi ya mwaka 1998, ilipendelea wamiliki wa kukodi ardhi tofauti na kutetea wenyeji wa ardhi za jamii. Nchini Kenya, kuna ushahidi wa kutosha wa dhulma dhidi ya kumiliki ardhi ya umma. Kabla mwaka 1954 Swynnerton Plan alibuni jinsi ya kubadilisha umiliki wa ardhi kutoka umiliki wa kitamaduni hadi umiliki wa kukodi. Hatahivyo, katiba ya 2010 ilitoa sheria za kumiliki ardhi ya umma.

Page 12: Hakijamii Economic and Social Rights Centre (Hakijamii ... · TOLEO MAARUFU LA MSWADA WA KUMILIKI ARDHI YA JAMII Utafiti na uchapishaji wa kitabu hiki umefanikishwa na ubalozi wa

5

Toleo maarufu la m

swada w

a kumiliki ardhi ya jam

ii

2.0 HISTORIA YA KIKATIBA,SHERIA NA SERA ZA MAPENDEKEZO YA MSWADA WA KUMILIKI ARDHI ZA KIJAMII

Sera ya kitaifa ya ardhi 2009 ilikuwa hatua ya kwanza kupendekeza umiliki wa ardhi ya umma na katiba ya 2010 kutoa ufafanuzi wa kisheria na kuweka ardhi ya umma katika kitengo kipya cha sheria.Kipengee cha 63 cha katiba kinaelekeza ardhi ya umma isimamiwe na jamii zilizotambuliwa ka misingi ya kabila, tamaduni au jamii zilizo na malengo yanayofanana.Ardhi ya umma inahusisha.

a) Ardhi iliyosajiliwa kisheria katika jina la kundi;

b) Ardhi iliyohamishwa kwa njia halali na ya kisheria kwa jamii.

c) Ardhi yeyote iliyotangazwa kuwa ya jamii kupitia sheria ya bunge; na

d) Ardhi ambayo—

i) Inayosimamiwa kisheria,au kutumiwa na jamii kama msitu,maeneo ya malisho au ya maeneo takatifu;

Page 13: Hakijamii Economic and Social Rights Centre (Hakijamii ... · TOLEO MAARUFU LA MSWADA WA KUMILIKI ARDHI YA JAMII Utafiti na uchapishaji wa kitabu hiki umefanikishwa na ubalozi wa

6

Tole

o m

aaru

fu la

msw

ada

wa

kum

iliki

ard

hi y

a ja

mii

ii) Ardhi ya tangu jadi na ardhi zilizomilikiwa na jamii za wawindaji; au

iii) Ardhi ya wakfu inayosimamiwa na serikali ya kaunti kihalali, wala siyo ardhi ya umma inayodhaminiwa na serikali ya kaunti chini ya kipengeee cha 62 (2).

Ardhi yeyote ya umma iliyosajiliwa na kudhaminiwa na serikali ya kaunti kwa niaba ya jamii. Ardhi ya umma haitauzwa, ila tuu kukiwa na sheria maalum inayofafanua haki miliki za wanachama wa jamii hiyo aidha kibinafsi au kijumuiya.

Kando na katiba kuna sheria mbalimbali zinazohusiana na ardhi. Sheria ya ardhi 2012 inashughulikia maswalai kadhaa. Hatahivyo imetenga maswala ya mauzo kwa sheria zitakazobuniwa siku za usoni. Inawahakikishia ulinzi wa haki za ardhi ya jamii kati ya vitengo vitatu vya sheria za ardhi. Inatoa msimamo wa sheria hiyo kutumika kwa ardhi zote za umma Inafafanua neno ‘hali za kitamaduni za ardhi’ Sheria ya ardhi iliyobuniwa mwaka 2012 ilianzisha sajili ya ardhi ya jamii inayowekwa katika idara ya sajili za ardhi. Hatahivyo hakuna usajili wa ardhi yeyeote ya umma utafanywa kabla mswada wa ardhi za umma kuwa sheria.

Sheria pia inatambua baadhi ya mambo yanayotakiwa kaundikwa katika sajili ya ardhi ya umma. Sheria inaelekeza

Page 14: Hakijamii Economic and Social Rights Centre (Hakijamii ... · TOLEO MAARUFU LA MSWADA WA KUMILIKI ARDHI YA JAMII Utafiti na uchapishaji wa kitabu hiki umefanikishwa na ubalozi wa

7

Toleo maarufu la m

swada w

a kumiliki ardhi ya jam

ii

msajili kutoa vyeti vya kumiliki ardhi au kukodi. Sheria inamzuia masajili kutoa cheti kwa ardhi ya umma ila tuu kama imeuzwa kuambatana na sheria za ardhi ya umma.

Page 15: Hakijamii Economic and Social Rights Centre (Hakijamii ... · TOLEO MAARUFU LA MSWADA WA KUMILIKI ARDHI YA JAMII Utafiti na uchapishaji wa kitabu hiki umefanikishwa na ubalozi wa

8

Tole

o m

aaru

fu la

msw

ada

wa

kum

iliki

ard

hi y

a ja

mii

3.0 MADHUMUNI YA MSWADA HUU

Madhumuni ya mswada wa kumiliki ardhi za umma ni kulinda haki ya kumiliki ardhi kwa jamii nchini. Hasa,mswada huu unanuia kuweka sheria ya kutambua,kulinda na kusajili haki za ardhi ya umma ; kusimamia na kuweka mbinu za utawala dhidi ya ardhi ya umma;Kubuni na kufafanua mamalaka ya bodi za kusimamia ,kueleza majukumu ya serikali za kaunti kuhusiana na ardhi ambazo hazijasajiliwa.

Mswada huu unalenga kuhifadhi ardhi za jamii katika misingi ya kabila, tamaduni au maazimio yanayofanana katika jamii.

Inaongozwa na kanuni zikiwemo kuhifadhi ardhi katika jamii ;kutoa haki sawa na kutambua cheti kwa ardhi ya jamii au cheti chochote; kuwezesha wanachama wa jamii kuchagua mfumo wa utawala na wa kusimamia ardhi yao;

Kutoa haki sawa kwa wanajamii na kukomesha ubaguzi.

Baadhi ya malengo na kanuni yalijumuishwa katika maamuzi ya mwaka 2010, katika kesi ya Endorois iliyoendeshwa na tume ya Afrika ya kutetea haki za binadamu, ambapo tume hiyo ilisema kuwanyima jamii usalama wa kumiliki ardhi hukiuka haki zao na kuwanyima uwezo wa kuwa na mbinu za mapato. Chini ya sheria za

Page 16: Hakijamii Economic and Social Rights Centre (Hakijamii ... · TOLEO MAARUFU LA MSWADA WA KUMILIKI ARDHI YA JAMII Utafiti na uchapishaji wa kitabu hiki umefanikishwa na ubalozi wa

9

Toleo maarufu la m

swada w

a kumiliki ardhi ya jam

ii

kimataifa umiliki wa wa ardhi katika mfumo wa kitamaduni lazima utambuliwe, uheshimiwe na haki zao zilindwe na serikali. Madhumuni makuu ya mswada wa kumiliki ardhi za umma unalenga kulinda haki za kumiliki ardhi hasa kwa jamii zilizotengwa, jamii za wafugaji na wanawake.

Page 17: Hakijamii Economic and Social Rights Centre (Hakijamii ... · TOLEO MAARUFU LA MSWADA WA KUMILIKI ARDHI YA JAMII Utafiti na uchapishaji wa kitabu hiki umefanikishwa na ubalozi wa

10

Tole

o m

aaru

fu la

msw

ada

wa

kum

iliki

ard

hi y

a ja

mii

4.0 UFAFANUZI WA NENO “JAMII”

Jamii huafanuliwa kuwa kundi la watu linaloishi katika ardhi ya kijamii, walio na ukoo mmoja, tamaduni moja na lugha inayofanana. Ufafanuzi huu pia upo katika sheria ya usajili wa ardhi. Ufafanuzi huu ni muhimu kwani unatambua tamaduni za jamii katika miji na katika mienendo ya makaazi.

4.1 Ufafanuzi wa “ardhi ya jamii”

Ardhi ya jamii hufafanuliwa kama ifuatavyo:

°° Ardhi yote inayotumiwa kama makaazi,malisho,kulima,uvuvi,makaazi ya wanyama pori,njia wanayopitia wanyama na mifugo;

°° Ardhi yote inayotumiwa na jamii kitamaduni na kihistoria kama eneo takatifu au kaya,la kitamaduni linalotumiwa na jamii yote;

°° Kubadilisha ardhi kuwa ya jamii kwa kufuata sheria mwafaka

°° Ardhi yote iliyoko Pwani imebadilishwa kuwa ya jamii.

Page 18: Hakijamii Economic and Social Rights Centre (Hakijamii ... · TOLEO MAARUFU LA MSWADA WA KUMILIKI ARDHI YA JAMII Utafiti na uchapishaji wa kitabu hiki umefanikishwa na ubalozi wa

11

Toleo maarufu la m

swada w

a kumiliki ardhi ya jam

ii

°° Jamii

°° Ukoo au familia kuambatana na tamaduni

Shirika la jamii linaloambatana na sheria zilizobuni ushirika huo.

Ni hatua zipi zinazofuatwa kusajili ardhi?

Page 19: Hakijamii Economic and Social Rights Centre (Hakijamii ... · TOLEO MAARUFU LA MSWADA WA KUMILIKI ARDHI YA JAMII Utafiti na uchapishaji wa kitabu hiki umefanikishwa na ubalozi wa

12

Tole

o m

aaru

fu la

msw

ada

wa

kum

iliki

ard

hi y

a ja

mii

5.0 USAJILI WA ARDHI YA JAMII

Ardhi ya jamii itasajiliwa kupitia mbinu hizi: Tume ya kitaifa ya ardhi, kupitia notisi ya gazeti la serikali, itateua afisa msimamizi atakayesimamia kila ardhi ya jamii na kuigawanya, pamoja na kurekodi madai ya jamii.

Baada ya kuigawanya ardhi hiyo, cheti cha ardhi kitatolewa na msajili kwa njia ifuatayo.

Ardhi ya jamii inaweza kusajiliwa kwa jina la—

°° Jamii

°° Ukoo au familia, kuambatana na tamaduni zao

°° Jamii kuambatana na stakabadhi zilizotumiwa kubuni ushirika huo

5.1 Ni hatua gani zinazohitaji kufuatwa wakati wa usajili?

Tume ya ardhi ndiyo iliyopewa jukumu la kuhakikisha harakati ya kurekodi na kuimarisha sajili ya ardhi ya jamii, iwe na uwazi na kushirikisha jamii. Itajumuisha hatua zifuatazo-

a) Tangazo litawekwa kwa stesheni ya radio siku 30 kabla ardhi kusajiliwa kuwa ya jamii. Tangazo hilo litawekwa katika ardhi hiyo

b) Kushirikisha jamii kupitia kampeini ya kuwahamasisha

Page 20: Hakijamii Economic and Social Rights Centre (Hakijamii ... · TOLEO MAARUFU LA MSWADA WA KUMILIKI ARDHI YA JAMII Utafiti na uchapishaji wa kitabu hiki umefanikishwa na ubalozi wa

13

Toleo maarufu la m

swada w

a kumiliki ardhi ya jam

ii

kuhusu haki za ardhi ya

c) Kubuni na kupitisha katiba itakayolinda ardhi ya jamii na maliasili

d) Kuanzisha taasisi za jamii

e) Kuthibithisha cheti cha ardhi ya jamii

5.2 Athari za usajili wa ardhi ya jamii ni zipi?

Ardhi inaposajiliwa kama ardhi ya jamii, itakuwa mali yao na haki zote za kumiliki kuwa zao. Cheti cha ardhi kitakachotolewa na msajili wa ardhi, kitakuwa ushahidi katika mahakama zote kwamba jina la aliyetajwa katika cheo hicho ndiye mmiliki wa ardhi, kukabiliana na ulaghai wowote.

5.3 Taasisi za jamii

(a) Jamii “kama shirika”

Kila jamii, kuambatana na sheria, wanapaswa kusajiliwa kama shirika kabla kusajiliwa kama wamiliki wa ardhi. Shirika hilo liwe na muhuri mmoja,watakuwa na uwezo wa kushtaki na kushtakiwa kupata fidia, kuandika kandarasi, kununua,na kuuza mali na uwezo wa kukopesha na kukopa fedha.

Page 21: Hakijamii Economic and Social Rights Centre (Hakijamii ... · TOLEO MAARUFU LA MSWADA WA KUMILIKI ARDHI YA JAMII Utafiti na uchapishaji wa kitabu hiki umefanikishwa na ubalozi wa

14

Tole

o m

aaru

fu la

msw

ada

wa

kum

iliki

ard

hi y

a ja

mii

(b) Baraza la jamii

Baraza la jamii hujumuisha wanachama wa jamii hiyo. Baraza hilo litakuwa na mwenyekiti, na katibu walioteuliwa na wanachama wa baraza hilo. Baraza la jamii lina uwezo kuteua kupitia uchaguzi utakaosimamiwa na tume ya kitaifa ya ardhi, wanachama wa kamati ya usimamizi wa ardhi ya jamii pamoja na afisi zinazohusika kuhakikisha usimamizi bora wa ardhi ya jamii kama ilivyopangwa na jamii hiyo. Majukumu ya baraza hilo ni; kushauri na kupitisha maamuzinya kamati ya ardhi ya jamii na kuandika katiba ya jamii na masharti yaliokubalika na jamii.

(c) Kamati za kusimamia ardhi ya umma

Kamati ya ardhi itajumuisha wanachama wasiopungua (7) na wasiodizi wanachama 11, kamati hiyo itatilia maanani usawa wa kijinsia na watu walemavu. Wanachama huchaguliwa na baraza la jamii kwa muda wa miaka (3). Wanachama hao watatakikana kuafikia sheria za sura ya sita ya katiba na hawatakiuka sheria za katiba na masharti yote.

Majukumu ya kamati ya kusimamia ardhi ni pamoja na kusimamia ardhi ya jamii,kushirikisha maendeleo na kutumia mipango kwa ushirikiano na taasisi husika,tume

Page 22: Hakijamii Economic and Social Rights Centre (Hakijamii ... · TOLEO MAARUFU LA MSWADA WA KUMILIKI ARDHI YA JAMII Utafiti na uchapishaji wa kitabu hiki umefanikishwa na ubalozi wa

15

Toleo maarufu la m

swada w

a kumiliki ardhi ya jam

ii

ya ardhi ili kuimarisha kanuni za kushirikisa jamii katika shughuli za ardhi ya jamii kwa madhumuni ya kutoa vyeti vya ardhi.

(d) Bodi ya kusimamia ardhi ya umma

Bodi ya kusimamia ardhi ya jamii huteuliwa katika kila kaunti ambapo kuna ardhi ya jamii. Majukumu ya bodi hiyo ni kusimamia kamati ya ardhi za jamii, kuambatana na mamalaka waliyo nayo ikiwemo:

°° Kupendekeza kwa baraza la umma kukagua upya pendekezo au kulistisha ikiwa kamati haikuwa na nia njema;

°° Kupendekeza kwa baraza la jamii kumondoa uongozini mwanahama yeyote;

°° Kutengeneza sheria za mbinu za kujiendesha katika kamati.

Wanachama wa bodi ya kusimamia ardhi ya jamii hujumuisha wataalamu katika sekta mbalimbali kama mawakili, masoroveya an wanachama waliopendekezwa na tume ya kitaifa ili wasaidie bodi kutekelza majukumu yake kwa njia ya ufasaha.

Page 23: Hakijamii Economic and Social Rights Centre (Hakijamii ... · TOLEO MAARUFU LA MSWADA WA KUMILIKI ARDHI YA JAMII Utafiti na uchapishaji wa kitabu hiki umefanikishwa na ubalozi wa

16

Tole

o m

aaru

fu la

msw

ada

wa

kum

iliki

ard

hi y

a ja

mii

6.0 MASWALI YANAYOULIZWA KILA WAKATI

6.1 Ardhi ya jamii inaweza kubadilishwa kuwa ya umma?

Ndiyo. Ardhi ya umma inaweza kubadilishwa kuwa ya umma kupitia kuuzwa, kuhamisha hati miliki au kuitoa kwa hiari. Kabla ardhi ya jamii kubadilishwa, kamati ya kusimamia ardhi ya umma watatafuta maoni ya baraza la jamii

Ardhi ya jamii inaponunuliwa kwa lazima,kuambatana na sheria za ardhi,itatumika tuu kwa maswala ya ulinzi,usalama wa umma,afya na mipango maalum,ikilipiwa fidia kwa njia ya usawa.

6.2 Ardhi ya jamii inaweza kubadilishwa kuwa ya kibinafsi?

Ndiyo, ardhi ya umma iliyosajiliwa inaweza kubadilishwa baada ya baraza la jamii kuidhinisha. Inaweza kubadilishwa kuwa ardhi ya umma kupitia kuhamisha cheti au katika mkutano ulioandaliwa swala hilo la mauzo. Malitaidhinisha mauzo hayo kuambatana na sheria za ardhi na sheria zengine husika.

Page 24: Hakijamii Economic and Social Rights Centre (Hakijamii ... · TOLEO MAARUFU LA MSWADA WA KUMILIKI ARDHI YA JAMII Utafiti na uchapishaji wa kitabu hiki umefanikishwa na ubalozi wa

17

Toleo maarufu la m

swada w

a kumiliki ardhi ya jam

ii

6.3 Ardhi ya kibinafsi inaweza kubadilishwa kuwa ya jamii?

Ndiyo, ardhi ya kibinafsi inaweza kubadilishwa kuwa ya jamii kupitia kuhamisha cheti,kutoa ardhi hiyo au ikiwa inatumiwa na kumilikiwa kwa njia isiyo halali.

6.4 Ardhi ya umma inaweza kubadilishwa kuwa ya jamii?

Ndiyo, ardhi ya umma inaweza kubadilishwa kuwa ya jamii kupitia tume ya kitaifa ya ardhi. Kadhalika, ardhi ya umma katika kaunti za Mombasa, Kwale, Kilifi, Tana River, Lamu na Taita Taveta zitabadilishwa kuwa ardhi za umma licha ya ibara ya tano.

6.5 Mwanachama wa jamii anaweza kupewa haki za ardhi ya umma?

Ndiyo na la. Mwananchama au kundi wanachama wa ardhi ya jamii wanaweza kuweka ombi la kupewa na kutumia ardhi hiyo, lakini hakuna cheti kingine hakitatolewa. Wanachama hao wataweka ombi kwa kamati ya ardhi ya jamii baada ya kuidhinishwa na baraza la ardhi ya jamii. Nafasi ya kutumia ardhi hiyo haita dhulumu haki ya jamii dhidi ya ardhi hiyo.

Page 25: Hakijamii Economic and Social Rights Centre (Hakijamii ... · TOLEO MAARUFU LA MSWADA WA KUMILIKI ARDHI YA JAMII Utafiti na uchapishaji wa kitabu hiki umefanikishwa na ubalozi wa

18

Tole

o m

aaru

fu la

msw

ada

wa

kum

iliki

ard

hi y

a ja

mii

6.6 Je, mila na desturi kuhusiana na matumizi ya ardhi na jamii za wafugaji (haki ya kulisha mifugo) zimetambuliwa katika mswada?....

Ndiyo. Mila na destrui zinazohusiana na ardhi inayotumika na jamii za wafugaji zitatiliwa maanani. Ardhi ya jamii iliyoko katika jamii ya wafugaji itaweza kutumiwa na jamii hiyo kuambatana na sheria zilizowekwa na kamati. Hizi ni pamoja na idadi na aina ya wanyama wanaopelekwa malishoni;eneo la ardhi ambapo wanyama hao watakula lishe,kuwalisha wanyama hao kwa kubadilisha maeneo ya ardhi ya malisho na mpangilio wa kuwalisha

6.7 Haki ya malisho ya mwanachama wa jamii inaweza kuondolewa, na katika hali gani?

Haki za malisho hutolewa kwa mtu yeyeote na inaweza kufutiliwa mbali ikiwa kuna ukame au sababu nyengine, na hatua hii ichukuliwe kulinda maslahi ya jamii pekee.

6.8 Je, mtu asiye mwanachama wa jamii anaweza kupewa haki ya malisho?

Kamati hiyo inaweza kutoa ruhusu kumpa mtu ardhi ya malisho, ikiwa atakuwa ametoa ombo hilo, na atatakiwa kufuata masharti ya tume ya ardhi au sheria yeyote husika.

Page 26: Hakijamii Economic and Social Rights Centre (Hakijamii ... · TOLEO MAARUFU LA MSWADA WA KUMILIKI ARDHI YA JAMII Utafiti na uchapishaji wa kitabu hiki umefanikishwa na ubalozi wa

19

Toleo maarufu la m

swada w

a kumiliki ardhi ya jam

ii

6.9 Jee wanajamii hupata haki sawa katika faida ya ardhi ya jamii?

Ndiyo. Kila mtu anayetoka katika jamii ana haki ya kufaidi ardhi ya jamii bila kubaguliwa. Wanawake,walemavu,jamii zilizotengwa na wanaume wana haki ya kuhudumiwa kwa usawa katika maswala ya ardhi.Kamati haitabagua kwa njia yeyote ile mwanachama wa jamii kwa misingi ya jinsia,kabila,rangi,miaka au ulemavu.

6.10 Ni shughuli zipi za kisheria zinaweza kutekelezwa katika ardhi ya jamii?

Maswala ya kisheria yanayoweza kutekelzwa katika ardhi ya jamii ni pamoja na:

°° Kandarasi za ardhi, malipo yote yatashughulikiwa kama ilivyo katika ardhi ya kibinafsi kuambatana na sheria ya ardhi.

°° Umiliki wa muda katika ardhi ya jamii utatekelezwa kuambatana na makubaliano kati ya jamii na anayekodi ardhi hiyo.

°° Ardhi ya jamii haiwezi kupeanwa kwa mtu asiye raia wa Kenya.

Page 27: Hakijamii Economic and Social Rights Centre (Hakijamii ... · TOLEO MAARUFU LA MSWADA WA KUMILIKI ARDHI YA JAMII Utafiti na uchapishaji wa kitabu hiki umefanikishwa na ubalozi wa

20

Tole

o m

aaru

fu la

msw

ada

wa

kum

iliki

ard

hi y

a ja

mii

6.11 Jinsi gani jamii zinaweza kunufaika kutokana na maliasili katika ardhi ya jamii?

Maliasili inayopatikana katika jamii itatumiwa na kusimamiwa kwa njia itakayofaidi jamii,kwa uwazi na uwajibikaji na kwa msingi wa ugavi sawa wa mapato.

Kila jamii itakadiria na kuweka rekodi ya maliasili kwa ushirikiano na taasisi za serikali husika na kutayarisha mpango wa kusimamia maliasili (NRM).

Uwekezaji wowote unaohusiana na matumizi ya maliasili ya jamii utatekelezwa kufuatia mkataba baina ya jamii na wawekezaji. Mkataba huo utatekelezwa baada ya majadiliano yalio wazi, na kuwa na mwongozo unaojumuisha maswala yafuatayo—

f) Utafiti wa kubaini athari za kimazingira,jamii,tamaduni na kiuchumi;

g) Masharti ya kushirikisha jamii;

h) Kufuatilia na kukagua athari za uwekezaji katika jamii;

i) Malipo ya fidia kwa umma kuambatana na mapato yanayotokana na mradi wa uwekezaji;

j) Masharti ya kukarabati ardhi baada ya mradi wa uwekezaji kukamilika;

Page 28: Hakijamii Economic and Social Rights Centre (Hakijamii ... · TOLEO MAARUFU LA MSWADA WA KUMILIKI ARDHI YA JAMII Utafiti na uchapishaji wa kitabu hiki umefanikishwa na ubalozi wa

21

Toleo maarufu la m

swada w

a kumiliki ardhi ya jam

ii

k) Matakwa ya kuweka mikakati ya kukabiliana na athari mbovu za mradi wa uwekezaji;

l) Mwekezaji anatakiwa kuwahamasisha jamii na kuwafundisha teknologia ya mradi huo.

Mkataba baina ya jamii na mwekezaji hauna msingi wowote ikiwa haujakubaliwa na kuidhinishwa na thuluthi mbili za baraza la jamii.

Page 29: Hakijamii Economic and Social Rights Centre (Hakijamii ... · TOLEO MAARUFU LA MSWADA WA KUMILIKI ARDHI YA JAMII Utafiti na uchapishaji wa kitabu hiki umefanikishwa na ubalozi wa

22

Tole

o m

aaru

fu la

msw

ada

wa

kum

iliki

ard

hi y

a ja

mii

7.0 MBINU ZA KUTATUA MIZOZO

Bodi ya kusimamia ardhi ya jamii itaunda mbinu ya kutatua mizozo kuambatana na sheria ya mizozo ya jamii hiyo. Harakati ya kutatua mizozo itafuata mkondo wa mbinu mbadala ya kupata suluhisho kabla kuwasilisha malalimishi mahakamani. Mtu anaweza kuenda mahakamani ikiwa hakutosheka na uamuzi wa bodi na anaweza kukata rufaa kwa baraza la jamii.

Page 30: Hakijamii Economic and Social Rights Centre (Hakijamii ... · TOLEO MAARUFU LA MSWADA WA KUMILIKI ARDHI YA JAMII Utafiti na uchapishaji wa kitabu hiki umefanikishwa na ubalozi wa

23

Toleo maarufu la m

swada w

a kumiliki ardhi ya jam

ii

8.0 MAMBO YANAYOFAA KUANGAZIWA KATIKA KATIBA YA KILA JAMII

1) Jina la kamati na maelezo ya eneo la ardhi inayomilikiwa na jamii.

2) Watu ambao ni halisi kutoka jamii hiyo na wanaweza kusajiliwa

3) Stakabadhi za watu walaioko katika ofisi hiyo, muda wa kuhudumu na mbinu na jinsi wanavyochaguliwa, kusimamishwa au kufutwa kazi.

4) Mamlaka na mbinu ya kujaza nafasi za kazi zinazotokea miongoni mwa maafisa wa kamati.

5) Malipo ya marupurupu ya wanachama wa kamati na makundi yao na jinsi wanavyotayarisha mikutano mkuu wa mwaka .

6) Usimamizi wa miradi ya uwekezaji na hazina ya fedha za jamii, uteuzi wa mtu atakayesimamia, na madhumuni ya hazina hiyo na mali ya kamati itakavyotumiwa.

7) Usimamizi wa vitabu vya makadirio ya fedha na ukaguzi wa vitabu vya sajili za fedha hizo.

Page 31: Hakijamii Economic and Social Rights Centre (Hakijamii ... · TOLEO MAARUFU LA MSWADA WA KUMILIKI ARDHI YA JAMII Utafiti na uchapishaji wa kitabu hiki umefanikishwa na ubalozi wa

24

Tole

o m

aaru

fu la

msw

ada

wa

kum

iliki

ard

hi y

a ja

mii

8) Njia ya kubadilisha jina, katiba na sheria za jamii.

9) Njia ya kuvunja kamati na kuuza mali ya jamii.

10) Mbinu za kutatua matatizo.

Page 32: Hakijamii Economic and Social Rights Centre (Hakijamii ... · TOLEO MAARUFU LA MSWADA WA KUMILIKI ARDHI YA JAMII Utafiti na uchapishaji wa kitabu hiki umefanikishwa na ubalozi wa

25

Toleo maarufu la m

swada w

a kumiliki ardhi ya jam

ii

9.0 KIAMBATISHO

Kufikia sasa sheria za kumiliki ardhi zimepitia hatua nyingi ili kukabiliana na matatizo ya kulinda haki za jamii. Mswada wa kumiliki ardhi ya umma ni mojawapo ya mbinu muhimu za mageuzi ya sheria za ardhi. Hatahivyo mwenendo wa kuchelewa kupitisha mswada huu unatia hofu. Mswada huu utashughulikia matatizo ya kumiliki ardhi ya umma inayotajwa kuwa asilimia 60% ya ardhi nchini Kenya. Mashirika mengi yamelezea nia ya kuchimba maliasili katika ardhi hizi na mswada huu ndiyo unaoelezea wawekezaji hatua za kufuata. Mashirika yasio ya kiserikali na jamii yanapaswa kufanya kampeini kushinikiza serikali kupitisha mswada huu. Ni jambo la kusikitisha kwamba malumbano kati ya wizara ya ardhi na tume ya ardhi yanazuia maendeleo katika mageuzi ya sheria za ardhi. Wakati umefika wa taasisi za ardhi kushirikiana na kufanikisha sheria za kumiliki ardhi.

Page 33: Hakijamii Economic and Social Rights Centre (Hakijamii ... · TOLEO MAARUFU LA MSWADA WA KUMILIKI ARDHI YA JAMII Utafiti na uchapishaji wa kitabu hiki umefanikishwa na ubalozi wa

26

Tole

o m

aaru

fu la

msw

ada

wa

kum

iliki

ard

hi y

a ja

mii