24

Click here to load reader

Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2016 · PDF fileyao kulingana na maagizo ya Mungu, na kuteketeza juu ya madhabahu. Walifanya hivyo kuonyesha kuwa walikuwa tayari kutii maagizo

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2016 · PDF fileyao kulingana na maagizo ya Mungu, na kuteketeza juu ya madhabahu. Walifanya hivyo kuonyesha kuwa walikuwa tayari kutii maagizo
Page 2: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2016 · PDF fileyao kulingana na maagizo ya Mungu, na kuteketeza juu ya madhabahu. Walifanya hivyo kuonyesha kuwa walikuwa tayari kutii maagizo

Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2016

Mwandishi: Pip Reid Mchoraji: Thomas Barnett

Mkurugenzi Mbunifu: Curtis Reid Mtafsiri: Susan Koech

Njia ya Uhuru Mara ya kwanza kuchapishwa 2015

Shukrani kwa kukisoma kitabu hiki na kuunga mkono Safari ya Kufana Kwa Njia ya Hadithi za Biblia (Bible Pathway Adventures). Shirika letu ni shirika lisilo la faida ambalo huwasaidia wazazi na walimu duniani kote kuwafunza watoto zaidi kuhusu Biblia kwa njia ya kufana na yenye ubunifu. Wadhamini na mashabiki kama wewe ndio hutewezesha kutengeneza app, kufadhili mradi wa utafsiri na utunzi

wa hadithi na vifaa vya elimu vya jamii zote.

Haki zote zimehifadhiwa. Hakuna sehemu ya kitabu hiki kinachoweza kuchapishwa tena, kusambazwa, au kupitishwa kwa njia yoyote, ikiwa ni pamoja na kurekodi au njia nyingine za

kielektroniki bila idhini iliyoandikwa ya Bible Pathway Adventures, isipokuwa katika matumizi ya nukuu inayoweza kutumika wakati wa kudurusu na vilevile matumizi yasiyo ya kibiashara iliyoruhusiwa na sheria ya hati miliki. Kwa maombi ya ruhusa, wasiliana na Bible Pathway

Adventures' katika tovuti iliyoko hapo chini:

www.biblepathwayadventures.com

Page 3: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2016 · PDF fileyao kulingana na maagizo ya Mungu, na kuteketeza juu ya madhabahu. Walifanya hivyo kuonyesha kuwa walikuwa tayari kutii maagizo

1.

Njia ya Uhuru“Njia yako ilikuwa katika bahari. Na mapito yako yalikuwa

katika maji makuu; hatua zako hazikujulikana.” (Zaburi 77:19)

Waebrania walikuwa mateka nchini Misri kwa muda mrefu, hadi wakati Mungu alipomtumia mtu aliyeitwa Musa kuwaokoa kutokana na mfalme wa Misri, Farao.

Huku akiwa na fimbo ya Mungu, Musa aliwaongoza Waebrania kutoka Misri Walipitia katika mabonde ya jangwa na kuelekea palipokuwa na Bahari ya Shamu.

Licha ya hali mbaya ya jangwa, Mungu alikuwa na mpango wa kuwalinda. Mungu aliwatangulia mchana ndani ya wingu wa nguzo ambao ulipunguza miyale ya jua na pia kuwapa mwanga. Usiku, Mungu aliwaongoza kwa nguzo ya moto na kuwatia joto.

Nguzo ya wingu na moto ziliwaongoza Waebrania popote ambapo Mungu aliwaelekeza.

Farao alijawa na hasira Waebrania walipoenda. Moyo wake ukawa mgumu si haba. Alikuwa ameshasahau mapigo ambayo Mungu alikuwa amewaletea juu ya nchi ya Misri. Farao aliwakusanya farasi, magari na wanajeshi kisha akawaamuru waelekee jangwani kuwafuata Waebrania.

Page 4: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2016 · PDF fileyao kulingana na maagizo ya Mungu, na kuteketeza juu ya madhabahu. Walifanya hivyo kuonyesha kuwa walikuwa tayari kutii maagizo

2.

Waebrania walipofika karibu na Bahari ya Shamu, Mungu akamwambia Musa, “Waambie watu wapige kambi hapa. Nimeufanya moyo wa Farao kuwa Mgumu naye atawajia. Nitajipatia utukufu kwa Farao na kwa jeshi lake na Wamisri watajua kuwa mimi ndimi Mungu.”

Punde si punde, jeshi la Wamisri likakaribia. Wana wa Israeli walijawa wa hofu walipoona kuwa jeshi la Farao lilikuwa likikaribia. Wakamwambia Musa, “Mbona umetutoa Misri ili tufe jangwani?”

Waebrania walikuwa katika hali ya kutatanisha; Walikabiliana na jeshi la Faro na pia Bahari ya Shamu. Walianza kulalamika, “Neno hili silo tulilokwambia huko Misri? Tukisema, tuache tuwatumikie Wamisri? Maana ni afadhali kuwatumiakia Wamisri kulikom kufa jangwani!”

“Msiogope,” Musa akawaambia. “Mungu atawapigania ninyi, nanyi mtanyamza kimya. Hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele.”

Musa alipokuwa akizungumza, wingu likatanda katikati ya Waebrania na jeshi la Wamisri. Upande wa Wamisri ukawa na giza totoro! Lakini kwa Waebrania, kukawa na mwanga. Farao na wanajeshi wake hawakuona lolote!

Page 5: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2016 · PDF fileyao kulingana na maagizo ya Mungu, na kuteketeza juu ya madhabahu. Walifanya hivyo kuonyesha kuwa walikuwa tayari kutii maagizo

3.

Mungu alimpa Musa maagizo, “Inua fimbo yako ukanyoshe mkono juu ya bahari na kuigawanya, nao wana wa Israeli watapita katikati ya bahari katika nchi kavu, lakini Wamisri wataangamia humo.”

Musa alifuata maagizo. Aliinua fimbo yake juu ya bahari. Usiku huo, upepo mkali ulivuma na kuigawanya bahari na kufanya njia katikati. Maji yalikuwa ukuta kwao. Kuta zile zilikuwa ndefu sana.

Waebrania walizitazama nguzo zile kwa mshangao kwani zilikua ndefu kuliko piramidi za Misri. Hawakuamin i macho yao . Mungu a l i kuwa amewafanyia njia katika bahari.

Huku akishikilia fimbo, Musa alinyosha mkono wake baharini. “Wachukueni mifugo wenyu na muifuate njia hii,” aliwaambia Waebrania.

Waebrania walijua wazi kuwa Wamisri hawakuwa mbali nao, hivyo waliogopa sana. Waliwakusanya mifugo na kuanza safari.

Page 6: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2016 · PDF fileyao kulingana na maagizo ya Mungu, na kuteketeza juu ya madhabahu. Walifanya hivyo kuonyesha kuwa walikuwa tayari kutii maagizo

4.

Kuta za maji zilionekana kuwa refu kama milima. Upepo ulivuma na bahari kuvuma kwa sauti. Nyoyo zao zilipapa kwa hofu walipokuwa wakitembea katika barabara ile.

Farao alipoona vile, alituma wanajeshi wake wawafuate Waebrania.

Lakini Mungu alikuwa akiwaongoza Waebrania, aliwahangaisha wanajeshi wa Farao. Farasi waliogopa sana. Aliyaondoa magurudumu ya magari yakaenda kwa uzito, hata wanajeshi waka kwama mchangani. Mambo yalikwenda mrama kwa Wamisri!

“Mungu wao anawapigania.” Wamisri wakajadiliana. “Tutoke hapa!” Lakini walikuwa wamechelewa. Musa na wana wa Israeli walipovuka bahari salama, Mungu akamwambia Musa, “Nyosha mkono wako juu ya bahari ili maji yarudi tena juu ya Wamisri.”

Musa alifanya kama alivyoagizwa na Mungu, na maji yakarudi na kufunikia magari na wanajeshi wa Misri. Jeshi la Farao liliangamizwa kabisa.

Page 7: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2016 · PDF fileyao kulingana na maagizo ya Mungu, na kuteketeza juu ya madhabahu. Walifanya hivyo kuonyesha kuwa walikuwa tayari kutii maagizo

5.

Huku wakiimba na kucheza, Waebrania walimsujudia na kumshukuru Mungu kwa kuwaokoa. Walikuwa wamewasili katika jangwa la Shuri. Huko jangwani, Mungu aliwapa Waebrania amri na sheria. Aliwaambia watu. “Mkizitii amri zangu, hamtakuwa na matataizo kama yale yaliyowakumba huko Misri.”

Ingawa wana wa Israeli walimsikiliza Mungu kwa makini, waliendelea kumnung’unikia Musa. “Tulikuwa na maisha mazuri kuliko haya kule Misri. Ulitutoa kule na kutuleta jangwani ili tufie huku kwa njaa. Hatuna chochote cha kula.”

Mungu aliyasikia manung’uniko yao. ”Musa, waambie watu kwamba nitawanyeshea ninyi mvua ya mikate kila siku isipokuwa siku moja. Katika siku hiyo ninyi mtapumzika. Siku hiyo itaitwa siku ya Sabato. Nataka kuona iwapo wanaweza kufuata maagizo Yangu.”

Kila walipozifungua hema zao, waliviona vitu vidogo kama sakitu juu ya nchi. Kitu hicho kilichofanana na mkate kiliitwa “mana” na kilikuwa kitamu kama asali. Wakati wa jioni, Mungu aliwatuma ndege waitwao kware huko makambini. Waebrania waliwala. Walikuwa watamu sana.

Waebrani hawakufahamu kwamba waliishi jangwani kwa muda wa miaka arobaini.

Page 8: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2016 · PDF fileyao kulingana na maagizo ya Mungu, na kuteketeza juu ya madhabahu. Walifanya hivyo kuonyesha kuwa walikuwa tayari kutii maagizo

6.

Musa aliwaongoza wana wa Israeli hadi palipokuwa na jangwa l i l i lo i twa Refidimu. Wal ik i ta kambi . Haikuchukua muda mrefu hata watu walipoanza kulalamika. “Musa, ulituleta huku ili tufe? Hatuna maji ya kunywa.” Musa alivuta pumzi. “Mungu, watu hawa wako tayari kunipiga kwa mawe. Je, nifanye nini?”

“lipige jabali kwa fimbo,” Mungu akasema. “Maji yatatoka na watu wote watayanywa.” Musa alimwamini Mungu na kufanya Alichosema, na maji safi yakatoka katika mwamba. Lakini shida za Waebrania hazikufika kikomo kwani Waamaleki wakatokea. Walikuwa wamesikia habari za mapigo ya Wamisri na maafa ya wanajeshi wa Farao. “Ni wakati wa kuwashinda Wamisri!” walisema. Lakini Waebrania walikuwa safarini. Waamaleki walijifunga kimbwembwe tayari kupigana nao.

Musa aliliona jeshi la Waamaleki akamwambia Yoshua, “Tuchagulie watu watakao pigana na watu hawa.” Bila kusita, Yoshua aliwachagua watu wenye nguvu na wenye uwezo. Aliwaongoza vitani.

Musa alisimama juu ya kilima na kuwatazama watu waliokuwa wakipigana mchana kutwa. Musa alipouinua mkono wake, Waebrania walishinda lakini alipoushusha mkono wake, Waamaleki walishinda. Haruni na Huri walikuwapo pamoja na Musa. Mkono wa Musa ulipokuwa mzito, Haruni na Huri waliyashika na kuyainua hewani. Waebrania waliwapiga Waamaleki na kushinda vitani kwa kuwa Mungu alikuwa upande wa Waebrania. Waamaleki walitorokea nyikani.

Page 9: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2016 · PDF fileyao kulingana na maagizo ya Mungu, na kuteketeza juu ya madhabahu. Walifanya hivyo kuonyesha kuwa walikuwa tayari kutii maagizo

7.

Musa alikuwa na hamu ya kuendelea na safari jangwani. Alikuwa ameishi eneo hilo hapo mwanzo kabla hajatumwa kuwaokoa Waisareli, basi alikuwa mwenyeji wa jangwa lile. kufuatia maagizo ya Musa, watu walikita kambi karibu na mlima Sinai.

Hebu fikiria ingekuwa vipi watu wa jamaa yako wakipiga kambi kwa muda wa miaka arobaini. Je, mngeishi kwa amani siku zote? Basi ndivyo ilivyokuwa kwa Waebrania. Musa alijaribu kushughulikia malalamishi ya kila mmoja. Malalamishi yalikuwa mengi kupindukia hadi masikio yake yakachoka kuyasikiliza. Kwa bahati nzuri, Yethro alikuwa na wazo zuri.

“Musa, utadhoofika kwa kuketi hapa toka asubuhi hadi jioni, na kutatua matatizo ya kila mmoja. Wachague watu wenye hekima tena wamchao Mungu ili kwamba wakusaidie kutekeleza haya.”

Ingawa Musa alikuwa kiongozi mkuu, alitilia maanani ushauri wa Yethro. Aliwachagua watu wenye hekima ili kwamba wamsaidie kutatua matatizo.

Page 10: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2016 · PDF fileyao kulingana na maagizo ya Mungu, na kuteketeza juu ya madhabahu. Walifanya hivyo kuonyesha kuwa walikuwa tayari kutii maagizo

8.

Mwezi watatu baada ya Waebrania kutoka Misri, walifika milimani Sinai. Walipokuwa wakipiga kambi huko, Mungu akamwambia Musa, “Waarifu watu kuwa wazifue nguo zao. Baada ya siku tatu nitashuka mlimani na kuwajia.”

Asubuhi ilipofika katika siku ya tatu, wingu jeusi lilitua mlimani Sinai. Ngurumo za radi zikasikika na umeme ukaonekana mbinguni. Sauti ya baragumu ilisikika jangwani.

Musa aliwaongoza Waebrania kukutana na Mungu wao. Miguu zao zilitetemeka huku wakitazama moshi ukifuka mlimani. “Jamani! Nini kimetutendekea?” walijawa na hofu sana.

Sauti ya baragumu ilizidi kuwa kubwa kisha sauti ya radi ikanena jangwani. “Mimi ndimi Bwana Mungu, niliyewaokoa na kuwatoa kwenye utumwa Misri.”

Waebrania walianguka na kufunika nyuso zao, walitetemeka kwa woga. Mungu alikuwa tayari kuwapa maagizo na amri Zake. Taifa lilikuwa karibu kuzaliwa.

Page 11: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2016 · PDF fileyao kulingana na maagizo ya Mungu, na kuteketeza juu ya madhabahu. Walifanya hivyo kuonyesha kuwa walikuwa tayari kutii maagizo

9.

Kwa umeme na ngurumo za radi, Mungu akawanenea watu maneno haya.

i. “Usiwe na miungu mingine ila mimi.”

ii. “Usijifanyie sanamu wala mfano wa kitu chochote ili kunisujudia.”

iii. “Usilitaje bure jina la bwana”

iv. “Ikumbuke siku ya sabato na kuitakasa”

v. “Waheshimu baba yako na mama yako”

vi. “Usiue”

vii. “Usizini”

viii. “Usiibe”

ix. “Usimshuhudie jirani yako uongo”

x. “Usitamani chochote alicho nacho jirani yako”

Mungu aliwanenea watu wake maneno haya mlimani. Amri za kwanza zilielekeza kila mmoja jinsi ya kumsujudu na kumheshimu Mungu. Amri zilizosalia zilielezea uhusiano kati ya wanadamu na jinsi wanavyopasa kuishi.

Page 12: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2016 · PDF fileyao kulingana na maagizo ya Mungu, na kuteketeza juu ya madhabahu. Walifanya hivyo kuonyesha kuwa walikuwa tayari kutii maagizo

10

Watu walitetemeka na kusonga mbali na mlima huku wakiyazuia masikio yao. “Sema nasi wewe,” wakamwambia Musa. “Mungu akisema nasi tutafa.”

“Msiogope,” Musa akasema. “Mungu amekuja kuwajaribu ili kwamba msifanye dhambi, bali mtii.”

Wana wa Israeli walipokuwa wakitazama mlima ukitoa moshi, Mungu aliendelea kunena na Musa. Kisha Musa akajenga madhabahu kwa mawe kumi na miwili. Kila jiwe liliwakilisha kabila la Israeli. Watu walitoa mifugo yao kulingana na maagizo ya Mungu, na kuteketeza juu ya madhabahu. Walifanya hivyo kuonyesha kuwa walikuwa tayari kutii maagizo yake

Walipomaliza kutoa sadaka, Musa alielekea mlimani palipokuwa na wingu jeusi la Mungu. Alikaa huko siku arobaini. Mungu alimfunza kuhusu agano lake ili kwamba Musa awafunze Israeli sheria na njia za Mungu.

Musa alisikiliza kwa makini yote aliyonenewa na Mungu. Aliyaandika maagizo yale kwenye mbao mbili za mawe ili kuwaonyesha watu.

Page 13: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2016 · PDF fileyao kulingana na maagizo ya Mungu, na kuteketeza juu ya madhabahu. Walifanya hivyo kuonyesha kuwa walikuwa tayari kutii maagizo

11

Kule kambini, watu walianza kulalamika walipoana Musa amekawia ku shuka ku toka m l iman i . “Hatujamuona Musa kwa muda mrefu.” Wasijue la kufanya, waliwaza na kuwazua kisha wakawa na wazo.

“Tujifanyie mungu kwa mfano wetu,” wakamwambia Haruni.

Pasi na ushauri wa nduguye Musa, hakujua la kufanya. Alitaka kufurahisha watu. Aliitazama mlima kwa hofu kisha Haruni akasema, “Zivunjeni pete zenyu za dhahabu mkaniletee.”

Haruni aliyeyusha kwa patasi dhahabu na kuifanya iwe sanamu ya ndama. Akatengeneza dhabahu la jiwe na watu wakatoa sadaka za amani. Walisherehekea usiku mzima na mschana.

Page 14: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2016 · PDF fileyao kulingana na maagizo ya Mungu, na kuteketeza juu ya madhabahu. Walifanya hivyo kuonyesha kuwa walikuwa tayari kutii maagizo

12.

Mungu aliwatazama watu wale kambini. Akamwambia Musa, “Haya! Tazama watu wako wanaiabudu sanamu ya ndama. Niache ili hasira Zangu ziwake juu yao, niwaangamize wote nami nitakufanya wewe uwe taifa kuu.” Musa alimsihi Mungu kwamba asiwaangamize Waisraeli. “Geuka katika hasira yako, ughairi nia yako ya kuwaangamiza watu uliowatoa Misri. Kumbuka ahadi yako kwa Ibrahimu, Isaka na Yakobo, kwamba utawafanya kuwa Taifa kuu.”

Mungu alisikia na kuridhishwa na kilio cha Musa. Alikuwa amekubali watu wale wayatende maovu ili kumjaribu Musa. Alighairi nia yake ya kuwaangamiza wana wa Israeli. Musa alifurahishwa na uamuzi wa Mungu lakini hakufurahishwa na matendo ya wana wa Israeli. Alizichukua mbao zile na kushuka katika mlima hadi kambini.

Musa alipoona watu wakiabudu ile sanamu ya ndama, alichemka nyongo. Alizitupa zile mbao na kuzivunja. “Watu hawa wamekufanyani hata ukaleta dhambi kuu ya kuifanya sanamu ya ndama?” alimuuliza Haruni.

Haruni alipata aibu. “Wewe unawajua watu hawa. Ulikawia sana mlimani. Watu walijawa na hofu basi wakaniamuru niwafanyie sanamu ya ndama…” Musa alijawa na hasira. Aliamrisha sanamu ile kuchomwa na kuwa mavumbi. Kisha akanyunyuzia juu ya maji na kuwanywesha wana wa Israeli ili kuwaadhibu kwa ajili ya kile walichokuwa wamefanya.

Page 15: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2016 · PDF fileyao kulingana na maagizo ya Mungu, na kuteketeza juu ya madhabahu. Walifanya hivyo kuonyesha kuwa walikuwa tayari kutii maagizo

13.

Musa alielewa ni kwa nini Mungu alikuwa na hasira juu ya watu hao. Musa alisimama mlango pa marago kisha akasema kwa sauti, “Mtu yeyote aliye upande wa Bwana na aje kwangu.”

Kundi la wana wa Israeli lili mkusanyikia Musa. Akawaambia, “Jifungeni panga zenyu kiunoni,mkapite huku na kule, mlango hadi mlango, mkawaangimize hao wanaozidi kuabudu sanamu.”

Siku hio, watu elfu tatu waliangamia kwa upanga kwani waliendelea kuabudu sanamu na miungu ya uongo badala ya Mungu mkuu, Yawe.

Musa alirudi mlimani na kumwomba Mungu awassmehe watu lakini Mungu aliwarudi kwa kosa la kujifanyia sanamu. Aliwaletea pigo ili kuwakumbusha kuwa Alikuwa na hasira. Kwa mkono wake, Mungu aliandika amri zake katika mawe.

Page 16: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2016 · PDF fileyao kulingana na maagizo ya Mungu, na kuteketeza juu ya madhabahu. Walifanya hivyo kuonyesha kuwa walikuwa tayari kutii maagizo

14.

Wana wa Israeli walipokuwa jangwani, Mungu aliwaagiza wajenge maskani maalum. Maskani hayo yangekuwa mahali pa kufanyia ibada na kusali. Hakuna mtu aliyejua kujenga maskani yale basi Mungu akawapa maelezo.

Wana wa Israeli walisikiliza masharti kwa makini sana. Walitengeneza mbao na kuziweka ndani ya hema. Walitengeneza sanduku la mti wa mshita uliofunikwa kwa dhahabu. Ndani yake kukawekwa ushuhuda wa Mungu, nao ni agano la Mungu kwa watu wake. Sanduku lile lilijulikana kama Sanduku la Agano.

Mungu alimteua Haruni kuwa mkuu wa makazi yale kisha akamfanya kuwa Kuhani Mkuu. Haruni na wanawe walipewa majukumu maalum ya ukuhani. Walivalia nguo zilizokuwa tofauti na waliwasaidia watu kumwabudu Mungu.

Wana wa Israeli walipomaliza kutengeneza ile hema maalum, wingu kuu lilishukia juu ya makazi hayo. Kulikuwa na uwepo wa Mungu. Toka siku hiyo, wingu hilo lilipoondoka, Waebrania walibaini kuwa ilikuwa wakati wa kuchukua mizigo yao na kuendelea na safari.

Page 17: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2016 · PDF fileyao kulingana na maagizo ya Mungu, na kuteketeza juu ya madhabahu. Walifanya hivyo kuonyesha kuwa walikuwa tayari kutii maagizo

15.

Mungu alijua watu wale walijifunza kuabudu sanamu walipokuwa mateka huko Misri, “Msiishi kama waishivyo Wamisri,” Mungu aliwambia. “Maana wameasi na kuabudu miungu mingine, na hili si jambo zuri.”

“Musa, wafunze watu watakavyoshereheka Sikukuu zangu.” Mungu alisema. “Haya ni makutano yangu maalum, na nguo zitakazo valiwa wakati huo.”

Musa aliwaelezea wana wa Israeli kuhusu Mikutano ya Mungu. Aliwaelezea kuhusu sherehe za Pasaka, siku ya mkate usiotiwa chachu, Mazao ya kwanza na Pentekosti. Kisha akawafunza kuhusu Sikukuu za Kinumbi, sikukuu za Upatanisho, kusanyiko takatifu na kisha Sikukuu ya Mwisho.

“Hazi ndizo tarehe na nyakati maalum za Mungu,” Musa alisema. “Yanatufunza kuhusu ahadi na mipango ya Mungu. Mungu anataka tuzifaute na kuzikumbuka hata milele.”

Watu walianza kuzifuata amri za Mungu badala ya kufuata desturi za Wamisri. Mungu alifuarahia jambo lile.

Page 18: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2016 · PDF fileyao kulingana na maagizo ya Mungu, na kuteketeza juu ya madhabahu. Walifanya hivyo kuonyesha kuwa walikuwa tayari kutii maagizo

16.

Wana wa Israeli waliendelea na safari yao nyikani. Walipokaribia nchi ya Kanaani, Mungu akamwagiza Musa, “Watume wapelelezi kumi na wawil i wakaipeleleze nchi nliyo waahidi.”

Musa aliwachagua wapelelezi kutoka katika kila kabila la Waebrania wakiwemo Kalebu na Yoshua.

“Nataka sana kujua jinsi Kanaani ilivyo,” Musa aliwaambia wapelelezi. “Je, watu wale ni wenye nguvu? Miji wanaoishi yako vipi? Hata ikiwezekana mchume mizabibu, kisha mje mtupe habari juu ya kila kitu!”

Wapelelezi walitembea huku na kule kwa muda wa siku arobaini Kanaani. Wapelelezi walipigwa na butwaa walipofika Kanaani, waliona miti mirefu zaidi. Pia, hawakuwa wamewaona watu wakubwa hapo awali.

Huku wakitetemeka, walikimbia na kurudi kambini.

Page 19: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2016 · PDF fileyao kulingana na maagizo ya Mungu, na kuteketeza juu ya madhabahu. Walifanya hivyo kuonyesha kuwa walikuwa tayari kutii maagizo

17.

Huko kambini, wapelelezi walimkabithi Musa matunda ya mizabibu. “Pasi na shaka, nchi hiyo inabubujika maziwa na asali. Lakini watu wa kule ni wa kutisha. Isitoshe, tumewaona Waamaleki! Kamwe hatuwezi kuishi huko!”

Kalebu na Yoshua, waliokuwa shujaa kuwapiku wenzao, wakasema. “Mwazungumzia kuhusu nini? Nchi hiyo ni ya kupendeza. Twendeni tukainyakue hivi sasa!”

“Hatuwezi kuwashambulia wale watu,” mmoja wao akasema. “Je, hukuyaona majitu? Watu hao ni wa kubwa na wenye nguvu. Mbele yao, sisi tu kama siafu. Una wazimu?”

Kalebu na Yoshua walimwamini Mungu sana na basi wakawasihi wana wa Israeli. “Hatupaswi kuwa na hofu. Mungu yuko upande wetu. Atatupa nchi hiyo kama alivyotuahidi.”

Page 20: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2016 · PDF fileyao kulingana na maagizo ya Mungu, na kuteketeza juu ya madhabahu. Walifanya hivyo kuonyesha kuwa walikuwa tayari kutii maagizo

18.

Lakini wana Waisraeli hawakuwa wamemwamini Mungu vikamilifu, hivyo basi wakakataa kuwaamini Kalebu na Yoshua. Waliomboleza na kulia usiku kucha.

“Laiti tungalifia jangwani. Mbona Mungu alituleta huku ilia apate kutuua? Ni heri tumchague kiongozi mwingine kisha turudi Misri.”

Mungu alijawa na hasira alipoona kuwa hawakuwa na imani. “Hata lini nitazidi kuvumilia manung’uniko ya watu hawa? Kamwe hawakomi. Hakika hapana mmoja wao atakayeiona nchi hiyo!”

Ili kuwaadhibu, Mungu aliwafanya wana wa Israeli waishi jangwani hadi watu wazima wakafa wote. Ni kizazi kipya tu ambacho kingeweza kuiingia katika nchi hiyo mpya.

Page 21: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2016 · PDF fileyao kulingana na maagizo ya Mungu, na kuteketeza juu ya madhabahu. Walifanya hivyo kuonyesha kuwa walikuwa tayari kutii maagizo

19.

Musa alimwamini Mungu sana hata akaweza kuwaongoza wana wa Israeli kwa muda wa miaka arobaini. Hilo lilikuwa jambo gumu. Musa alichoshwa na ukosefu wa imani wa Waebrania kwani licha ya Mungu kuwapigania vita vingi, walizidi kuasi.

Pia, walizidi kulalamika wakisema, “Hatuna maji ya kunywa.” Musa alikuwa amechoka si haba. Alichukuwa fimbo na kusimama. “Sikieni enyi waasi, je, tuwatokezee maji katika mwamba huu?” Musa aliinua mkono na kugonga mwamba kwa fimbo yake, maji yakatoka.

Mungu hakufurahishwa na tabia ya Musa. “Je, wewe ndiwe uliyeyafanya maji kutoka mwambani? Maana umeuchukua utakufu wangu hautaingiza kundi hili katika ile nchi nliyowapa.”

Musa hakuyaamini masikio yake. “Nimefanya kosa.” Alikuwa amewaongoza watu nyikani kwa muda wa miaka arobaini, na sasa hakuruhisiwa kuingia katika Nchi ya Ahadi.

Huku akimsihi Mungu, Musa alisema, “Tafadhali, niruhusu nivuke mto Yordani ili kwamba nione Nchi ya Ahadi.” Lakini Mungu hakubadili mawazo Yake. “Na yatoshe hayo! Sitazungumzia haya tena.”

Page 22: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2016 · PDF fileyao kulingana na maagizo ya Mungu, na kuteketeza juu ya madhabahu. Walifanya hivyo kuonyesha kuwa walikuwa tayari kutii maagizo

20.

Musa aliendelea kumtumainia Mungu na kwaongoza watu. Hatimaye alipotimiza miaka mia na ishiri, Mungu akamwambia ampe Yoshua uongozi juu ya wana wa Israeli.

Musa aliwakusanya watu na kuwakumbusha maagizo ya Mungu, akiwaambia, “Mmeshuhudia matendo ya Mungu juu ya maisha yenu. Zitiini amri Zake na maisha yenu yatakuwa bora.”

Musa akashuka kutoka uwanja wa Moabu mpaka mlima Nebo. Alipofika kileleni, Mungu alimwonyesha nchi yote aliyowaahidi watu wake, wakiwemo makabila kumi na miwili ya Israeli. Mungu akasema, “Hii ndiyo nchi Niliyoapa kuwapa Ibrahamu, Isaka, na Yakobo. Nitakipa kizazi chako nchii hii.”

Hata ingawa Musa hakuingia katika nchi hiyo ya ahadi, Mungu alikuwa ameridhishwa na Musa. Alimpenda sana mtumishi wake mnyenyekevu. Musa alipokufa, Mungu mwenyewe alimzika huko Moabu.

Kisha Yoshua akawa kiongozi wa wana wa Israeli. Alichukua fimbo na kuiinua juu kisha akawaambia Waisraeli, “Mungu yu pamoja nasi. Ni wakati wa kuinyakua Nchi yetu ya Ahadi!”

Mwisho

Page 23: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2016 · PDF fileyao kulingana na maagizo ya Mungu, na kuteketeza juu ya madhabahu. Walifanya hivyo kuonyesha kuwa walikuwa tayari kutii maagizo

Je, umefurahia Njia ya Uhuru? Kwa hadithi zaidi za Safari ya Kufana kwa Njia Ya Biblia, agalia vitabu hivi!

Arushwa Katika Tundu la Simba

Auzwa Utumwani

Gharika Kuu

Amezwa Na Samaki

Kutoroka Kutoka Misri

Usaliti wa Mfalme

Kuzaliwa kwa Mfalme

Shukrani kwa kukisoma kitabu hiki na kuunga mkono Safari ya Kufana Kwa Njia ya Hadithi za Biblia (Bible Pathway Adventures). Shirika letu ni shirika lisilo la faida ambalo huwasaidia wazazi na walimu duniani kote kuwafunza watoto zaidi kuhusu Biblia kwa njia ya kufana na yenye ubunifu. Wadhamini na mashabiki kama wewe ndio hutewezesha kutengeneza app, kufadhili mradi wa utafsiri na utunzi

wa hadithi na vifaa vya elimu vya jamii zote.

Unaweza kujifunza mengi zaidi kuhusu matukio na hadithi kupitia:

www.biblepathwayadventures.com

Page 24: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2016 · PDF fileyao kulingana na maagizo ya Mungu, na kuteketeza juu ya madhabahu. Walifanya hivyo kuonyesha kuwa walikuwa tayari kutii maagizo

www.biblepathwayadventures.com