11
www.habari.go.tz www.habari.go.tz WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO Toleo Na.06 // | Julai, 2020

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO · 2020/2021 kama kuongeza usajili wa kazi na wabunifu husika, kusi-mamia kesi za hakimiliki, kuongeza mashirikiano na Taasisi za Hakimiliki

  • Upload
    others

  • View
    13

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO · 2020/2021 kama kuongeza usajili wa kazi na wabunifu husika, kusi-mamia kesi za hakimiliki, kuongeza mashirikiano na Taasisi za Hakimiliki

www.habari.go.tz

www.habari.go.tz

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Toleo Na.06 // | Julai, 2020

Page 2: WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO · 2020/2021 kama kuongeza usajili wa kazi na wabunifu husika, kusi-mamia kesi za hakimiliki, kuongeza mashirikiano na Taasisi za Hakimiliki

Dkt. Hassan AbbasiKatibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali

Maoni ya MhaririUsiku wa kuamkia Julai 24, 2020 Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli akiwa Ikulu Chamwino Jijini Dodoma alilitangazia Taifa kuhusu kifo cha Rais wa Awamu ya Tatu, Mzee Benjamin William Mkapa aliyefariki hospitalini Jijini Dar es Salaam.

Hakika Taifa limempoteza mwanadiplomasia nguli aliyewahi kutokea Afrika na duniani, ambaye atakumbukwa kwa kusulu-hisha migogoro mbalimbali ya kisiasa katika nchi za Kenya na Burundi pamoja na mchango wake katika kuhimiza na kulinda amani barani Afrika.

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo itamkumbuka kwa mchango wake alipohudumu kwa nafasi ya Waziri wa Habari na Utangazaji mwaka 1990 hadi 1992, na alipokuwa Mhariri wa The Nationalist (Baadae Daily News) na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Habari Tanzania (SHIHATA) mwaka 1974.Aidha, Mzee Mkapa alikuwa mwanahabari mkongwe na kiongozi aliyeleta mabadiliko makubwa katika kuiendeleza tasnia ya habari na michezo katika kipindi chake cha uongozi.

Wakati wa uhai wake akiwa Rais wa Awamu ya Tatu alianzisha Vitengo vya Habari na Mawasiliano Serikalini ambao ndiyo wasimamizi wa masuala ya habari Serikalini. Kwa upande wa tasnia ya michezo alijenga Uwanja wa Michezo wa Kimataifa jijini Dar es Salaam ujulikanao kama Uwanja wa Taifa.Buriani Baba Yetu Benjamin Wiliam Mkapa, Tutakukumbuka Daima kwa alama uliyoicha hususan kwenye Tasnia ya Habari na Michezo.

Page 3: WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO · 2020/2021 kama kuongeza usajili wa kazi na wabunifu husika, kusi-mamia kesi za hakimiliki, kuongeza mashirikiano na Taasisi za Hakimiliki

www.habari.go.tz

Mhariri MkuuDkt. Hassan Abbasi

WajumbeLorietha Laurence Anitha JonasShamimu NyakiEliuteri MangiAdeldaus Kazimbaya

Msanifu JaridaKelvin KanjeAnitha Jonas

COSOTA Yaainisha Mikakatiya kusaidia Wasanii. 01

05

02Dkt.Temu:Warithisheni Utamaduni Watoto na Vijana

Dkt. Makoye : Tumeboresha Mitaala ili kuongeza Tija katika Sekta ya Sanaa.

Page 4: WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO · 2020/2021 kama kuongeza usajili wa kazi na wabunifu husika, kusi-mamia kesi za hakimiliki, kuongeza mashirikiano na Taasisi za Hakimiliki

Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) imeainisha mikakati ambayo itasaidia wadau wa shughuli za ubunifu wanapa-ta haki zao kwa wakati hususani Haki-miliki na Hakishiriki ili kunufaika na kazi zao.Hayo yamesemwa leo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo Bi. Doreen Sinare ambaye ameeleza kuwa taasisi hiyo imepokea kwa furaha maamuzi ya Mh. Rais Dkt. John Pombe Magufuli wa kuhamisha COSOTA kuja Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na hivyo tayari imejipanga kuhakikisha kazi za ubunifu zinasajiliwa.“Kwa hakika tumejipanga kuhakikisha kuwa wadau wote wa ubunifu wanapa-ta haki zao za msingi ikiwemo kuongeza mapato kupitia utoaji leseni na ugawaji mirabaha” amesema Bi. Doreen.

01 www.habari.go.tz

COSOTA Yaainisha Mikakati ya kusaidia Wasanii.

Na Shamimu Nyaki -WHUSM

Bibi Sinare meongeza kuwa COSOTA ina mikakati mbalimbali kwa mwaka 2020/2021 kama kuongeza usajili wa kazi na wabunifu husika, kusi-mamia kesi za hakimiliki, kuongeza mashirikiano na Taasisi za Hakimiliki za nchi nyingine pamoja na zile za

kanda na kimataifa.

Mkakati mwingine aliouanisha Bibi.Doreen ni kuboresha ushirikiano na kuongeza mapato, kufungua ofisi katika Jijini Dodoma, kurekebisha Sheria ili kuweka vifungu vitakavy-onufaisha watu wenye ulemavu wa kuona na kusimamia masuala ya

uharamia (piracy).

Aidha, Afisa Mtendaji huyo ame-ongeza kuwa kwa sasa Taasisi imejipanga kutatua changamoto zilizokua zinaikumba taasisi hiyo ikiwemo suala la watumishi, mifumo ya ICT na muundo wa taasisi kuweza kufanyiwa kazi jambo ambalo litaongeza kasi ya utendaji na kuongeza tija ya kuzali-

sha kazi bora za sanaa.

Taasisi ya Hakimili Tanzania (CO-SOTA) imehamishiwa katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa sababu Zaidi ya asilimi 80% ya wadau wake ni wasanii ambao wako chini ya

Idara ya Maendelo ya Sanaa.

Page 5: WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO · 2020/2021 kama kuongeza usajili wa kazi na wabunifu husika, kusi-mamia kesi za hakimiliki, kuongeza mashirikiano na Taasisi za Hakimiliki

Dkt.Temu:Warithisheni Utamaduni Watoto na VijanaWazee wa jamii za kitanzania wasisitizwa kurithisha mambo ya utamaduni kwa watoto na vijana ili tamaduni hizo ziweze kuendelea kwa vizazi vijavyo.Wito huo umetolewa leo na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Emmanuel Temu alipokuwa katika ziara kutoa Elimu ya Uhifadhi na Uen-delezaji wa Urithi wa Utamaduni alipotem-belea kikundi cha Utamaduni cha Nyati Mchoya, kilichopo katika Kijiji cha Nzali, Kata ya Chilonwa, Dodoma.

“Niwapongeze kwa kazi nzuri mnayofanya ya kuwarithisha watoto na vijana shughuli za utamaduni hii inasaidia mambo haya kuen-delea hata kwa vizazi vijavyo na msipofanya hivi mnahatarisha asili ya utamaduni wenu kupotea,”alisema Dkt.Temu. Akiendeleza kuzungumza katika ziara hiyo Dkt. Temu alisema kuwa serikali inataka kupanua wigo wa utalii na kuifanya sekta ya Utamaduni kuwa ya utalii hivyo nijukumu la kila mtanzania kulinda na kuhifadhi utama-duni wake kwani nchi hii inautajiri mkubwa katika sekta hiyo ambao unaweza kukuza uchumi wa mwananchi kwa urahisi zaidi kutoka na namna ya uendeshaji wake.

Pamoja na hayo Mkurugenzi huyo aliendelea kutoa wito kwa watanzania kuwa wanaji-tokeza kwenda kuangalia burudani za utam-aduni kama wanavyojitokeza kwenda kutazama mpira, na kusema serikali inatara-jia kuanzisha matamasha mbalimbali ya utamaduni kwa lengo la kukuza na kutan-

gaza utamaduni wa mtanzania.

Naye Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Maadili na Urithi wa Taifa Bw.Boniface Kadili alipongeza uongozi wa vikundi vilivyotoa burudani ya ngoma kwa namna walivyonesha sanaa yao kwa kuzingatia kuzingatia uchezaji wa asili ambao hauna kuiga watu wa nje, zana za jadi

walizotumia pamoja na uvaaji wa maleba.

Aidha, naye Kiongozi wa Kikundi cha Nyati Mchoya Bw. John Mchoya alitoa ombi kwa wizara la kusaidia baadhi ya vikundi visivyo na uwezo wa kujisajili BASATA pamoja na kusaidia vikundi hivyo vidogo kupata fursa za kushiriki shughuli mbalimbali ikiwemo mata-

masha na shughuli za serikali.Halikadhalika nae mmoja wa kikundi cha Msamaria Bibi. Rhoda Petro alishukuru uon-gozi wa wizara kwa kuwatembelea na kuwa kutoa elimu ya namna ya kuhifadhi utama-duni wao na kuwaomba kurudi tena wakati

mwingine.

Na Anitha Jonas – WHUSM, Chamwino

02www.habari.go.tz

Page 6: WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO · 2020/2021 kama kuongeza usajili wa kazi na wabunifu husika, kusi-mamia kesi za hakimiliki, kuongeza mashirikiano na Taasisi za Hakimiliki

03 www.habari.go.tz

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Dkt.Emmanuel Temu kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akipongeza Kikundi cha Utamaduni cha Nyati Mchoya (hawapo

pichani) kwa namna wanavyorithisha utamaduni kwa watato na vijana leo katika ziara ya kutoa elimu ya uhifadhi na uendelezaji wa urithi wa utamaduni katika Kijiji cha Nzali,Kata ya Chilonwa,

Dodoma.

Page 7: WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO · 2020/2021 kama kuongeza usajili wa kazi na wabunifu husika, kusi-mamia kesi za hakimiliki, kuongeza mashirikiano na Taasisi za Hakimiliki

04www.habari.go.tz

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Dkt. Emmanuel Temu kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akiwa katika picha ya pamoja na Kikundi cha Msamaria kutoka

Kijiji cha Nzali mara baada ya ziara ya kutoa elimu ya Uhifadhi na Uendelezaji wa Urithi wa Utam-aduni iliyofanyika leo katika Kijiji cha Nzali,Kata ya Chilonwa, Dodoma.

Page 8: WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO · 2020/2021 kama kuongeza usajili wa kazi na wabunifu husika, kusi-mamia kesi za hakimiliki, kuongeza mashirikiano na Taasisi za Hakimiliki

Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Baga-moyo (TaSUBa) imeboresha mitaala ambayo itatoa fursa kwa wanafunzi wengi zaidi kujiunga na Taasisi hiyo pamoja na kuongeza udahili wa wanafunzi jambo ambalo litaleta tija katika ukuaji wa Sanaa, Urithi wa Utamaduni, Utalii na Masoko.

Akizungumza katika mahojiano maalum na AFisa Habari wa Kitengo cha Mawasilino Serikalini cha Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mkuu wa Taasisi hiyo, Dkt. Hurbert Makoye ameeleza kuwa mitaala hiyo mipya itasaidia kuongeza chachu ya ajira nchini.

“Tumekamilisha kuandaa program hizo mpya na hapo baadae tutakuwa na kozi za Astashahada na Stashaha-

da” alisema Dkt. Makoye. Aidha Dkt. Makoye amezitaja Prog-amu hizo ambazo ni pamoja na Uon-gozi wa Sanaa na Masoko na ya pili ni ya Urithi wa Utamaduni na Utalii

ambazo tayari zimeshaandaliwa.

Anazidi kufafanua kuwa Mitaala hiyo ipo kwenye mchakato wa kupata Ithibati tayari kwa ajili ya kutumika mwaka ujao wa masomo ( 2021/2022) ambapo kozi hizo zitaongezeka na Taasisi itazidi kus-onga mbele kwenye eneo la taaluma.

Aidha, Dkt. Makoye , amesema katika kuhakikisha Taasisi hiyo ya Sanaa na Utamaduni inafikia malengo yake na kupanua wigo , ujio wa programu hizo mbili mpya utafungua wigo mpana kwa wasanii na watu mbalimbali

watakaojitokeza kusoma kozi hizo.

Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Baga-moyo ni kituo chenye ubora uliotuku-ka Afrika Mashariki katika kutoa mafunzo ya Sanaa za maonyesho na ufundi ambapo majukumu yake makubwa ni kuhudumia mahitaji ya nchi washirika wa jumuiya ya Afrika Mashariki katika kutunza, kuhamasi-sha na kuendeleza Sanaa za maonye-

sho na ufundi.

05 www.habari.go.tz

Na. Lorietha Laurence

Dkt. Makoye : Tumeboresha Mitaala ili kuongeza Tija katika Sekta ya Sanaa.

Page 9: WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO · 2020/2021 kama kuongeza usajili wa kazi na wabunifu husika, kusi-mamia kesi za hakimiliki, kuongeza mashirikiano na Taasisi za Hakimiliki

06www.habari.go.tz

Kikundi cha Ngoma cha Nyati Mchoya kilichopo katika Kijiji cha Nzali,Kata ya Chilonwa, Dodoma kikicheza ngoma ya asili ya jamii ya Wagogo mbele ya Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya

Utamaduni Dkt.Emmanuel Temu kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (hayupo pichani) leo katika ziara ya kutoa elimu ya uhifadhi na uendelezaji wa urithi wa utamaduni.

Page 10: WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO · 2020/2021 kama kuongeza usajili wa kazi na wabunifu husika, kusi-mamia kesi za hakimiliki, kuongeza mashirikiano na Taasisi za Hakimiliki
Page 11: WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO · 2020/2021 kama kuongeza usajili wa kazi na wabunifu husika, kusi-mamia kesi za hakimiliki, kuongeza mashirikiano na Taasisi za Hakimiliki

www.habari.go.tzWizara_HabariTZWizara_habaritzWizara HabariTz

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI,SANAA NA MICHEZO