62
Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10:18:44 AM

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

  • Upload
    others

  • View
    5

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10:18:44 AM

Page 2: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 2 7/26/2016 10:18:45 AM

Page 3: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

i

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini

Kitini hiki kimeandaliwa na PELUM Tanzania kwa msaada wa watu wa Marekani kupitia Shirika la Maendeleo la Msaada la Watu wa Marekani (USAID). PELUM Tanzania inawajibika kwa maudhui yaliyomo ndani ya kitini hiki na maudhui hayo hayawakilishi msimamo wa USAID au Serikali ya Marekani.

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10:18:47 AM

Page 4: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

ii

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini

© PELUM Tanzania 2016

ISBN 978-9987-8956-7-0

Mchora Katuni: Godwin J. Chipenya

Kwa mawasiliano zaidi:

Mratibu,PELU M TanzaniaS.L.P 390, Morogoro-TanzaniaSimu/Nukushi: +255 23 2613677Barua pepe: [email protected]: www.pelumtanzania.org

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 2 7/26/2016 10:18:50 AM

Page 5: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

iii

YALIYOMO

Ufafanuzi 1

Shukrani 3

Sura ya Kwanza 5 1.0. Utangulizi 5

1.1. Mipango ya Matumizi ya Ardhi Vijijni 5

1.2. Historia 5 1.2.1. Utaratibu wa Mipango ya Vijiji Nchini Tanzania 5 1.2.2. Mipango ya Vijiji Wakati wa Operesheni Vijiji 6 1.2.3. Mipango ya Vijiji Kabla ya Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na. 5 ya 1999 7

1.3. Mfumo wa Sera, Sheria na Miongozo 8 1.3.1. Mfumo wa Sera 8 1.3.2. Mfumo wa Sheria 8 1.3.3. Mwongozo wa Mpango wa Matumizi ya Ardhi wa 1998 9

1.4. Malengo ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi 9

1.5. Dhana ya Mpango wa Matumizi ya Ardhi Vijijini 9

1.6. Faida za Kuwa na Mipango ya Matumizi ya Ardhi 10

1.7. Athari za Kukosa Mipango ya Matumizi ya Ardhi 11

Sura ya Pili 13 2.0. Mchakato wa Utayarishaji na Utekelezaji wa Mpango 13

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 3 7/26/2016 10:18:50 AM

Page 6: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

iv

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini

2.1. Utayarishaji wa Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini 13

2.2. Mamlaka za Uandaaji wa Mpango wa Matumizi ya Ardhi 13 2.2.1. Ngazi ya Taifa 13 2.2.2. Ngazi ya Wilaya 15 i. Timu Shirikishi ya Matumizi ya Ardhi ya Wilaya 15 ii. Asasi za kiraia 16 2.2.3. Ngazi ya Kijiji 16 i. Halmashauri ya Kijiji 17 ii. Mkutano Mkuu wa Kijiji 17 i. Kamati ya Usimamizi wa Matumizi ya Ardhi ya Kijiji 17 ii. Timu ya Uandaaji Mipango Kijijini 18

2.3. Maelezo ya Awali ya Uandaaji Mpango wa Matumizi 19

Sura ya Tatu 20 3.0. Mchakato wa Uandaaji wa Matumizi ya Ardhi ya Kijiji 20

3.1. Maana ya Mpango wa Matumizi ya Ardhi wa Kijiji 20

3.2. Hatua Sita za Upangaji wa Mpango wa Matumizi ya Ardhi ya Kijiji 20 3.2.1. Hatua ya Kwanza: Maandalizi Wilayani 20 i. Mamlaka ya Upangaji ya Matumizi ya Ardhi ya Wilaya 20 ii. Timu ya PLUM ya Wilaya na Mpango Kazi wa Utekelezaji 20

3.2.2. Hatua ya Pili: Tathmini ya Matumizi ya Ardhi Vijijini 21 i. Elimu kwa Umma kuhusu Sera na Sheria za Matumizi ya Ardhi 22

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 4 7/26/2016 10:18:50 AM

Page 7: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

v

ii. Tathmini Shirikishi ya Kijiji 23 iii. Kuandaa Mpango Kazi wa Jamii 24 iv. Ujenzi na Uimarishaji wa Taasisi za Kijiji 25

3.2.3. Hatua ya Tatu: Kuhakiki Mipaka Ardhi ya Kijiji 26 i. Kukubaliana kuhusu Mipaka ya Vijiji 26 ii. Utatuzi wa Migogoro ya Mipaka ya Vijiji 27 iii. Cheti cha Ardhi ya Kijiji 28 a. Maana ya Cheti cha Ardhi ya Kijiji 28 b. Utoaji wa Cheti cha Ardhi ya Kijiji 29

3.2.4. Hatua ya Nne: Upangaji wa Matumizi ya Ardhi ya Kijiji 30 i. Mgawanyo wa Ardhi ya Kijiji 30 ii. Utaratibu wa Kutengeneza Mpango 30 iii. Ushiriki wa Walengwa Katika Mipango ya Matumizi ya Ardhi 31 iv. Matokeo ya Ushirikishwaji katika Mipango 32 v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji 33 vi. Kukamilisha Mpango wa Matumizi ya Ardhi ya Kijiji 34 vii. Sheria Ndogo za Matumizi ya Ardhi Vijijini 35 viii. Utaratibu wa Kutunga Sheria Ndogo za Kijiji 36

3.2.5. Hatua ya Tano: Utawala wa Ardhi ya Kijiji 38 i. Hati ya Hakimiliki za Kimila 38 ii. Taratibu za Kutoa Hati za Hakimiliki za Kimila 40 iii. Masijala ya Ardhi ya Kijiji 41

3.2.6. Hatua ya Sita: Usimamizi wa Ardhi ya Kijiji 41 i. Usimamizi 41 ii. Uimarishaji wa Vyombo vya Usimamizi wa Ardhi Kijijini 42

4.0. Hitimisho 44

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 5 7/26/2016 10:18:50 AM

Page 8: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

vi

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini

5.0. Viambatisho 45

5.1. Cheti cha Ardhi ya Kijiji 45

5.2. Fomu ya Maombi ya Hati ya Kimila 47

5.3. Hati ya Hakimiliki ya Kimila 50 6.0. Marejeo 53

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 6 7/26/2016 10:18:52 AM

Page 9: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

1

Katika kitabu hiki, isipokuwa pale ambapo muktadha utahitaji vinginevyo: -Waziri: Maana yake ni Waziri anayewajibika na Mipango ya Matumizi ya Ardhi kama ilivyofafanuliwa katika Sheria ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Na 6 ya mwaka 2007; Mkurugenzi Mkuu: Maana yake ni Mkurugenzi Mkuu aliyeteuliwa kwa mujibu wa kifungu cha 10 cha Sheria ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Na.6 ya mwaka 2007; Hakimiliki ya Kimila: Maana yake ni haki ya kumiliki ardhi ya kijiji kwa mtu mmoja, familia, taasisi, au kampuni chini ya kifungu cha 25 cha Sheria ya Ardhi ya Kijiji Na. 5 ya mwaka ya mwaka 1999; Mpango wa Matumizi ya Ardhi: Maana yake ni mpango wowote uliotayarishwa au uliochukuliwa na mamlaka ya upangaji mipango na hujumuisha mpango wa sekta wa usimamizi wa rasilimali kama ilivyofafanuliwa katika Sheria ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Na 6 ya mwaka 2007; Kupanga Matumizi ya Ardhi: Maana yake ni taratibu na michakato ambayo kwa mujibu wake matumizi ya ardhi katika eneo au kanda ya mipango huelekezwa, husimamiwa, hufuatiliwa na kutathminiwa chini ya Sheria ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Na. 6 ya mwaka 2007; Masijala ya ardhi: Maana yake sehemu salama zaidi ya kuhifadhia nyaraka kama vile Cheti cha Ardhi cha Kijiji, Hati za Hakimiliki ya Kimila na daftari la usimamizi wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi ya Kijiji; Eneo la Mipango: Maana yake ni eneo lilitangazwa kuwa eneo la mipango kwa mujibu wa kifungu cha 25 cha Sheria Na. 6 ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi ya mwaka 2007; Mamlaka za Mipango: Maana yake ni mamlaka za Mipango zilizofafanuliwa chini ya kifungu cha 18 cha Sheria ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Na. 6 ya mwaka 2007; Timu ya Mipango: Maana yake ni timu iliyoteuliwa na Halmashauri ya

UFAFANUZI

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10:18:55 AM

Page 10: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

2

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini

Kijiji kushughulikia mipango ya kina ya matumizi ya ardhi ya kijiji; Kijiji: Maana yake ni kijiji kilichosajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Na.7 ya mwaka 1982; Halmashauri ya Kijiji: Maana yake ni Halmashauri ya Kijiji kama ilivyofafanuliwa kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa Na.7 ya mwaka 1982; Mkutano wa Kijiji: Maana yake ni mkutano wa kijiji kama ilivyofafanuliwa na Sheria ya Serikali za Mitaa Na.7 ya mwaka 1982; Ardhi ya Kijiji: Maana yake ni ardhi iliyotangazwa kuwa ni ardhi ya kijiji chini ya na kwa mujibu wa kifungu cha 7 cha Sheria ya Ardhi ya Kijiji Na.5 ya mwaka 1999

Cheti cha Ardhi cha Kijiji: Maana yake ni nyaraka inayotolewa kwa jina la Rais, kwa kijiji ili kuonesha mipaka na ukubwa wa ardhi ya kijiji, kwa mujibu wa kifungu cha 7 (6) cha Sheria ya Ardhi ya Vijiji, Na, 5. 1999.

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 2 7/26/2016 10:18:55 AM

Page 11: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

3

Kitini cha MPANGO WA MATUMIZI YA ARDHI, kimeandaliwa na shirika la PELUM Tanzania kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Msaada la Watu wa Marekani (USAID) kupitia Mradi wa Ushiriki wa wananchi katika kusimamia sekta ya Kilimo (Citizens Engaging in Government Oversight in Agriculture) unaolenga kuhusisha ushiriki wa wananchi kusimamia utekelezaji wa shughuli za serikali pamoja na uwajibikaji wa serikali kwa ujumla katika masuala ya ardhi.

Kitini hiki pia kinalenga kujenga mtazamo chanya kwa wananchi kuhusiana na ushirikishwaji, kujenga, kutambua na kuhakikisha uwajibikaji katika maeneo yao; kwa kuwa wanakijiji huona kuwa mpango ni wao na huwezesha kushughulikia matatizo yao bila kutegemea sana msaada kutoka nje. Wataalamu (maafisa ugani) na wadau wa maendeleo wawe tayari kusikiliza na kujifunza kwa wenyeji, bila kushinikiza na kuweka mawazo yao mbele katika mpango mzima wa matumizi ya ardhi ya kijiji. Watu wa nje, kazi yao iwe kuwezesha utaratibu wa upangaji na utekelezaji, badala ya kuwafanyia au kuchukua maamuzi kwa niaba yao. Mipango iwe matokeo ya majadiliano na makubaliano ya wahusika wote, iliyojengwa katika vipaumbele, uwezo, utamaduni na maarifa ya wenyeji wenyewe, kwa kuzingatia ushauri wa wataalamu. Ushirikishwaji, usiwe ‘njia’ ya kushawishi walengwa kushiriki katika shughuli ambazo maudhui ya msingi yameamuliwa na watu wa nje. Bali ushirikishwaji uwawezeshe wananchi kuwa na mamlaka zaidi katika utaratibu wa upangaji wa matumizi ya rasilimali ili kuboresha hali ya maisha yao, hivyo kuwa tayari kutekeleza na kuiendeleza mipango yao.

PELUM Tanzania inapenda kutoa shukrani za dhati kwa timu ya wafanyakazi wake wote kwa kukisadifu kitini hiki. Pia, inapenda

SHUKRANI

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 3 7/26/2016 10:18:55 AM

Page 12: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

4

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini

kuwashukuru Wanachama wa PELUM Tanzania; Tanzania Grass Roots Oriented Development (TAGRODE), Uluguru Mountains Agricultural Development Project (UMADEP) na Institut Africain pour le Développement Economique et Social (INADES Information Tanzania) na Wadau mbalimbali ambao walisoma kitini hiki na kutoa maoni yao katika kuboresha kitini. Pia, shukrani za pekee, ziende kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Halmashauri zote za Kilolo, Mufindi, Bahi, Kongwa, Mvomero na Morogoro Vijijini, bila kusahau wataalamu wa lugha ya Kiswahili, Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) kwa mchango wao wa usanifu wa lugha katika kitini hiki. Mwisho kabisa na kwa namna ya pekee PELUM Tanzania inapenda kulishukuru Shirika la Misaada ya Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID) kwa kutoa ufadhili kwa mradi wa Ushiriki wa Wananchi katika Kusimamia Sekta ya Kilimo unaotekelezwa na PELUM Tanzania ambao umefanikisha kuandikwa na kuchapishwa kwa kitini hiki.

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 4 7/26/2016 10:18:55 AM

Page 13: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

5

1.0. UTANGULIZI

1.1. MIPANGO YA MATUMIZI YA ARDHI VIJIJINIMipango ya Kina ya Ardhi Vijijini inahusu na kujumuisha mpangilio wa sehemu ya makazi ya kijiji ambayo hujumuisha matumizi mbalimbali ya ardhi kama ya makazi, miundombinu na huduma za jamii. Eneo la Makazi la kijiji limetokana na mpango wa jumla wa matumizi ya ardhi ya kijiji ambao unaainisha maeneo mbalimbali kwa ajili ya kilimo, misitu, malisho ya mifugo, makazi, huduma za jamii, miundombinu, n.k. Ili kusimamia na kudhibiti uendelezaji wa eneo la makazi ya Kijiji kunahitajika kuwepo mwongozo ambao utasaidia kuongoza mamlaka za uandaaji Mipango katika kupanga, kutekeleza, kuperemba, kutathmini na kuhuisha mipango ya kina ya makazi.

1.2. HISTORIA

1.2.1. UTARATIBU WA MIPANGO YA VIJIJI NCHINI TANZANIAKabla ya miaka ya sitini, watu walio wengi waliishi katika vijiji vilivyotawanyika katika vikundi vya kiukoo bila huduma muhimu. Baadhi waliishi katika vijiji vya mkusanyiko wa watu vilivyokuwa kama vituo ambako maduka na huduma za jamii vilikuwa vinapatikana. Hadi mwishoni mwa miaka ya sitini pamoja na miaka ya sabini nchini Tanzania ilipoanzishwa operesheni vijiji ambapo Wananchi wa vijijini waliotawanyika na kupewa makazi mapya katika vijiji vilivyokuwa na makazi ya karibukaribu na baadhi yake vilijulikana sana kama vijiji vya Ujamaa vikiwa na makusudi yafuatayo:-

• Kuwezesha uzalishaji kwa ushirika na kufurahia manufaa ya kiuchumi katika hatua mbalimbali za uzalishaji, upataji wa zana na pembejeo za kilimo, uchukuzi na masoko,

• Kukuza upatikanaji wa huduma za jamii kama afya, elimu, maji safi na salama na umeme panapowezekana,

• Kuiwezesha Serikali kuwa na usimamizi mzuri wa wananchi vijijini.

SURA YA KWANZA

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 5 7/26/2016 10:18:55 AM

Page 14: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

6

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini

1.2.2. MIPANGO YA VIJIJI WAKATI WA OPERESHENI VIJIJISerikali kupitia kwa iliyokuwa Idara ya Mipango Miji katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ilitoa mipango ya vijiji kwa msingi wa makazi kuwa karibukaribu. Idara ilitoa mipango ya vijiji ya mfano ya aina hiyo ambayo ilitumika kama miongozo. Dhana ya vijiji ambapo makazi yapo karibukaribu kwa mujibu wa Sheria ya Vijiji vya Ujamaa ya mwaka 1975 na Sera ya Taifa ya Kilimo ya mwaka 1985 viliruhusu rasilimali kuwekwa pamoja kwa ajili kuendelezwa, kutumiwa na kudhibitiwa kwa pamoja na wanakijiji. Lengo lilikuwa ni kuanzisha maeneo ya mashamba ili kuruhusu matumizi ya kiuchumi ya zana za kilimo kama trekta, plau, matumizi ya mbolea na pembejeo nyingine na kusambaza huduma za ugani. Pia, ilikuwa na lengo la kutenga eneo la umma kwa ajili ya malisho ya mifugo. Vijiji vilikuwa na matumizi makuu ya ardhi yafuatayo:

• Eneo la makazi,

• Ardhi ya kilimo,

• Ardhi ya misitu ya kijiji,

• Ardhi kwa ajili ya malisho,

• Kituo cha huduma za jamii,

• Barabara na njia za miguu.

Eneo la makazi lilipangwa kama vitongoji vya makazi mijini. Kwa kawaida ukubwa wa viwanja vya nyumba ulikuwa kati ya nusu eka na eka moja ili kutoa fursa ya kujenga nyumba za kuishi, mazizi na vibanda vya kuku, bustani, upandaji miti kwa ajili ya kivuli, matunda, mbao na mazao mengine yasiyo ya mbao. Baada ya wanakijiji kuhamia katika vijiji vipya bila kuwapo kwa miundombinu inayofaa kwa lengo la kuwezesha fursa za uzalishaji wa kisasa kwa taratibu za ushirika, uzalishaji wa mazao na hata maendeleo ya kiuchumi vijijini vilishuka.

Hali hii ilisababisha upungufu wa chakula, kupungua kwa mapato ya wananchi na jitihada za wakulima kujaribu kuongeza mapato kwa kufanya shughuli zisizo za kilimo kama vile biashara na uvuvi. Hatimaye, hali hiyo ilisababisha baadhi ya watu kurejea kwenye mashamba yao ya awali. Wengi wa hao waliorejea walikuta ardhi yao imekaliwa na watu wengine. Kwa upande mwingine ongezeko la idadi ya watu liliongeza mahitaji ya matumizi mbalimbali ya ardhi, mabadiliko kutoka umiliki wa ardhi wa pamoja kwenda umiliki wa mtu binafsi, yalileta migogoro ya

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 6 7/26/2016 10:18:55 AM

Page 15: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

7

ardhi. Hali hiyo ilisababisha kutungwa kwa Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995 ambayo ilisababisha kutungwa kwa Sheria ya Ardhi Na. 4 ya mwaka 1999 na Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na.5 ya mwaka 1999.

1.2.3. MIPANGO YA VIJIJI KABLA YA SHERIA YA ARDHI YA VIJIJI NA.5 YA 1999

Kabla ya kutungwa kwa Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na 5 ya 1999 sehemu nyingi nchini zilikumbwa na migogoro iliyosababishwa na ongezeko la idadi ya watu, ongezeko la mahitaji ya matumizi ya ardhi na kubadilika kwa mfumo wa umiliki wa ardhi kutoka ule wa wa jumuiya na kuwa binafsi. Hii ilisababisha kutungwa kwa Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995 na kufanyiwa mabadiliko kidogo 1997 na hatimaye Sheria ya Ardhi Na 4 ya mwaka 1999 na Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na 5 ya mwaka 1999. Kabla ya kutungwa kwa Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na 5 ya mwaka 1999, mipango ya vijiji ilikumbwa na vikwazo vifuatavyo;

• Ushirikishwaji mdogo wa wadau katika maandalizi ya mipango,

• Kupuuza haki za ardhi na maslahi mengine ya ardhi wakati wa maandalizi ya mipango,

• Mipango haikuonyeshwa kwa uwazi katika maeneo husika,

• Kukosekana kwa uelewa kuhusu uwepo wa mipango,

• Mipango haikutayarishwa kwa mtindo ambao ungeonesha mpangilio au mwonekano unaotarajiwa,

• Miradi haiambatani na mipango ya uwekezaji katika miundombinu pamoja na bajeti,

• Ukosefu wa rasilimali kwa ajili ya kufidia maslahi ya upande wa tatu ili kupata ardhi ya umma na kuwezesha upimaji wake,

• Uratibu mbovu miongoni mwa waendelezaji na mashirika ya huduma za jamii,

• Utekelezaji mbovu wa hatua za udhibiti wa maendeleo

Kwa wakati huo, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupitia Tume ya Taifa ya Matumizi ya Ardhi, ilitoa Mwongozo wa Usimamizi Shirikishi wa Matumizi ya Ardhi ya Kijiji (1998). Mwongozo huo ulitoa taratibu shirikishi za upangaji na usimamizi wa ardhi ya kijiji yenye kueleza vizuri matakwa ya jamii kijijini.

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 7 7/26/2016 10:18:55 AM

Page 16: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

8

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini

1.3. MFUMO WA SERA, SHERIA NA MIONGOZO Upangaji wa matumizi ya ardhi una kazi mbili yaani za kiufundi na za kisiasa. Ni huduma ya umma ambayo inatakiwa kutimiza masharti kwa mujibu wa sera mbalimbali na hati za kisheria zinazotawala usimamizi na utumiaji wa rasilimali za ardhi. Ni muhimu kwamba wapangaji wa matumizi ya ardhi na wadau wengine waelewe sera na sheria zinazohusika ambazo huongoza na kuwezesha utayarishaji wa mipango na utekelezaji wake.

1.3.1. MFUMO WA SERA Mwongozo huu, unazingatia Sera za Taifa zikijumuisha Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995, Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Makazi ya Binadamu ya 2000, Sera ya Taifa ya Usimamizi wa Mazingira na Sera za Sekta za Rasilimali nyinginezo. Kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Makazi ya Binadamu (2000) mipango ya vijiji ni zana muhimu ya kuhakikisha yafuatayo:-

• Matumizi ya kiwango cha juu ya rasilimali ardhi katika maeneo ya vijijini,

• Maeneo na urahisi wa kufikika kwa ajili ya kuanzisha vijiji, ili kuhifadhi na kulinda mazingira.

1.3.2. MFUMO WA SHERIA Sheria muhimu za kuzingatia hapa ni Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na.5 ya mwaka 1999, Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004, Sheria ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Na.6 ya mwaka 2007 na Sheria ya Mamlaka za Serikali za Mitaa/Wilaya Na.7 ya mwaka 1982.

Kwa mujibu wa Sheria ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Na. 6 ya mwaka 2007, kila Halmashauri ya Kijiji ni Mamlaka ya Upangaji. Muundo, utaratibu na utendaji wa halmashauri ya kijiji umeelezwa chini ya vifungu vya 25, 26, 56, 57, 104 na 142 ya Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka ya Wilaya) Na. 7 ya mwaka 1982 na 12 na 13 ya Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na.5 ya mwaka 1999.

Halmashauri za Vijiji zina wajibu wa kusimamia ardhi yote ya vijiji na zinatimiza wajibu huo wa usimamizi kwa mujibu wa kanuni zinazotumika kwa wadhamini wanaosimamia mali kwa niaba ya wanufaika chini ya udhamini wa ardhi ya Kijiji (wanakijiji). Mamlaka ya kuandaa miongozo

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 8 7/26/2016 10:18:55 AM

Page 17: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

9

inatolewa chini ya kifungu cha 63(2) (c) cha Sheria ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi ya mwaka 2007.

1.3.3. MWONGOZO WA MPANGO WA MATUMIZI YA ARDHI WA 1998

Mwaka 1998 uliandaliwa Mwongozo wa Ushirikishwaji katika Mipango na Usimamizi wa Matumizi ya Ardhi Vijijini, unaojulikana kwa kifupi kama PLUM (Participatory Land Use Management), ambao umerejewa upya na kutolewa na Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi mwaka 2010. Mchakato wa utekelezaji wa Mwongozo huu, unahamasisha na kuelekeza ufanisi katika matumizi ya ardhi, na kurasimisha umilikaji wa ardhi kama mtaji kupitia utekelezaji wa Sheria ya Ardhi ya Vijiji.

1.4. MALENGO YA MIPANGO YA MATUMIZI YA ARDHIKusudio hasa la kutungwa kwa Sheria ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi ni pamoja na kukidhi malengo yafuatayo:-

• Kuweka mfumo wa kuhuisha misingi ya maendeleo ya taifa iliyoainishwa katika sera za serikali,

• Kuwezesha wamiliki na watumiaji wa ardhi kuzingatia matumizi ya ardhi na uzalishaji wenye tija kwenye ardhi wanayomiliki,

• Kuwezesha usimamizi wenye ufanisi wa matumizi ya ardhi,

• Kuweka mfumo wa kuratibu ujumuishaji wa kisekta katika ngazi mbalimbali ikiwemo miundo ya kisiasa na kiutawala,

• Kuwezesha matumizi endelevu ya ardhi na,

• Kuwezesha uhakika na usawa katika kupata rasilimali za ardhi.

1.5. DHANA YA MPANGO WA MATUMIZI YA ARDHI VIJIJINI Kwanini mpango wa matumizi ya ardhi vijijini, ni swali muhimu sana la kujiuliza kabla ya mpango wenyewe kuanza katika eneo linalokusudiwa. Mpango wa Matumizi ya Ardhi ni muhimu sana kwa sababu zifuatazo:-• Kudhibiti kuongezeka kwa idadi ya migogoro miongoni mwa

watumiaji wa ardhi.

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 9 7/26/2016 10:18:55 AM

Page 18: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

10

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini

• Kutokuwa na uhakika wa miliki na matumizi ya ardhi.

• Maendeleo duni ya soko la ardhi lisilo rasmi.

• Uharibifu wa udongo na vyanzo vya maji.

• Kudhibiti ufyekaji holela wa misitu.

• Kudhibiti ongezeko la kuhamahama kwa watu na mifugo.

• Kuongezeka kwa ukame na tishio la kupanuka kwa jangwa.

1.6. FAIDA ZA KUWA NA MIPANGO YA MATUMIZI YA ARDHIKuna faida nyingi na manufaa kwa wakazi wa vijijini pale mpango wa matumizi ya ardhi katika maeneo yao unapokamilika, zifuatazo ni baadhi tu za faida:-

• Kuweka utaratibu wa matumizi ya rasilimali za ardhi kwa kutatua migogoro.

• Kuimarisha miliki za ardhi na matumizi yake.

• Kugawa ardhi na kuboresha matumizi na hifadhi ya ardhi kulingana na mapendekezo na uwezo wa walengwa

• Ni nyenzo muhimu katika kuboresha hali ya maisha ya watu katika kuondoa umasikini na utunzaji wa mazingira (maliasili).

• Kutilia mkazo na kuangalia uwezekano wa kushughulikia suala la kutokuwepo usawa kwenye mgawanyo wa ardhi kijinsia na kati ya makundi mbalimbali yanayotegemea njia mbalimbali kwa kipato na chakula;

• Kusaidia jamii ifikirie njia mpya au zilizoboreshwa za kutegemea kama njia za kuleta kipato ili kumudu maisha;

• Kupanga shughuli zilizochaguliwa kwenye maeneo ambapo zinafaa zaidi kuwepo, na

• Kuwezesha jamii kukaa pamoja kufikiria hali yao ya baadaye kwa pamoja.

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 10 7/26/2016 10:18:55 AM

Page 19: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

11

1.7. ATHARI ZA KUKOSA MIPANGO YA MATUMIZI YA ARDHIKuna athari nyingi tu zinazoweza kutokana na kukosekana kwa mpango wa matumizi ya ardhi,yaani kutumia ardhi kiholela, bila kufuata utaratibu maalum uliowekwa kwa misingi ya kitaalam. Ni vigumu kuonesha athari kwa kila eneo husika lisilo na mpango wa matumizi ya ardhi. Zifuatazo ni baadhi ya athari zitokanazo na kukosekana kwa mipango ya matumizi ya ardhi:-

• Ongezeko la kuhamahama watu na mifugo yao,

• Ufyekaji ovyo wa misitu na mapori,

• Kuongezeka kwa idadi ya migogoro ya ardhi miongoni mwa watumiaji wa ardhi,

• Kutokuwa na uhakika wa umiliki na matumizi ya ardhi,

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 11 7/26/2016 10:18:56 AM

Page 20: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

12

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini

• Ongezeko la soko lisilo rasmi la ardhi,

• Mabadiliko ya hali ya tabia ya nchi na athari zake kama vile ukame, mafuriko, vimbunga na uwezekano kutokea kwa jangwa.

• Uharibifu wa vyanzo vya maji na udongo.

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 12 7/26/2016 10:18:56 AM

Page 21: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

13

SURA YA PILI

2.0. MCHAKATO WA UTAYARISHAJI NA UTEKELEZAJI WA

MPANGO

2.1. UTAYARISHAJI WA MPANGO WA MATUMIZI YA ARDHI KIJIJINI

Maeneo ya vijiji, ndiko mahali pa chimbuko kuu la uchumi wa Tanzania kwa kuwa wakulima wengi wanaishi huko na kuendesha shughuli zao za kiuchumi na kijamii. Ili kuwepo na mwongozo wa uendelezaji mzuri wa ardhi vijijini, wilayani na mkoani, kunahitajika mipango thabiti ya matumizi ya ardhi. Sheria ya mipango ya matumizi ya ardhi inaunda vyombo mbalimbali vyenye mamlaka katika utayarishaji, usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi katika ngazi mbalimbali. Vyombo hivyo ni pamoja na; waziri mwenye dhamana ya masuala ya ardhi, tume ya taifa ya mpango wa matumizi ya ardhi, Halmashauri ya Wilaya na Halmashauri ya Kijiji. Kwa maana hiyo kulingana na mahitaji ya kimaeneo mipango ya matumizi ya ardhi yanaweza kupangwa na kuandaliwa katika ngazi ya kanda na hii imesababisha kuwepo kwa mamlaka za kikanda ambazo zinaweza kuandaa mpango mzima.

2.2. MAMLAKA ZA UANDAAJI WA MPANGO WA MATUMIZI YA ARDHI

Mipango ya matumizi ya ardhi huandaliwa na kutekelezwa katika ngazi mbalimbali ikiwemo:-

• Ngazi ya Taifa: Tume ya Taifa ya Matumizi ya Ardhi

• Ngazi ya Wilaya: Timu Shirikishi ya Usimamizi Matumizi Ardhi ya Wilaya

• Ngazi ya Kijiji: Halmashauri ya Kijiji/Serikali ya Kijiji

2.2.1. NGAZI YA TAIFANgazi ya Taifa ndiko mahali penye chombo cha juu cha mpango wa matumizi ya ardhi hapa nchini Tanzania. Chombo hicho kinaitwa Tume ya Taifa ya Matumizi ya Ardhi (National Land Use Plan Commission-NLUPC). Tume hii kwa kawaida huundwa na wawakilishi kutoka sekta mbalimbali za kijamii ambao huteuliwa na Waziri mwenye dhana ya ardhi. Tume hii huuongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume. Majukumu ya msingi ya Tume hii kwenye mpango wa matumizi ya ardhi ni kama ifuatavyo:-

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 13 7/26/2016 10:18:56 AM

Page 22: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

14

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini

• Kuratibu, kushauri na kukagua sekta zote kuhusu viwango vya pamoja na kumshauri Waziri kuweka viwango vilivyokubalika.

• Kutoa msaada kwenye mamlaka zote za upangaji wa matumizi ya ardhi na kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi, kuratibu utekelezaji wake na kuifanyia tathmini kila wakati.

• Kuratibu shughuli za vyombo vyote vinavyohusika na mambo ya upangaji wa matumizi ya ardhi na kutumika kama njia ya mawasiliano kati ya taasisi hizo na Serikali.

• Kubuni na kuhakikisha uendelezaji wa progamu ambazo zitalinda na kuimarishwa kwa ukamilifu wa ardhi na upangaji wa matumizi ya ardhi

• Kuhamasisha ushiriki wa umma na sekta binafsi katika shughuli zinazohusiana na upangaji wa matumizi ya ardhi yenye uwiano na manufaa.

• Kuendeleza ushirikiano kati ya Serikali, mamlaka za serikali za mitaa na taasisi nyingine zinazojishughulisha na upangaji wa matumizi ya ardhi.

• Kuhuisha maendeleo ya maarifa ya kisayansi katika mambo ya upangaji wa matumizi ya ardhi na kuhimiza maendeleo ya teknolojia yanayolenga kwenye uzuiaji au upunguzaji wa madhara makubwa katika ardhi.

• Kuainisha viwango, desturi na vigezo kwa ajili ya ulinzi wa matumizi yenye manufaa na kudumisha ubora wa ardhi.

• Kuendesha na kuratibu utafiti uchunguzi na upimaji wa ardhi unaohusiana na upangaji wa matumizi ya ardhi na kukusanya taarifa, kuzipanga kwa utaratibu na kuanzisha benki ya taifa ya takwimu ya kueneza taarifa ya matokeo ya utafiti, uchunguzi au tathmini za ardhi.

• Kuanzisha na kuendesha mfumo wa kumbukumbu na uenezaji wa taarifa inayohusiana na upangaji wa matumizi ya ardhi.

• Kwa kushauriana na wizara zozote za kisekta, kutathmini sheria zilizopo na kuishauri Serikali juu ya hatua za kisheria na nyinginezo kwa ajili ya upangaji wa matumizi ya ardhi na kupendekeza utekelezaji wake.

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 14 7/26/2016 10:18:56 AM

Page 23: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

15

• Kuanzisha na kudumisha ushirikiano na nchi nyingine na mashirika ya kimataifa, kwa ajili ya masuala na mambo yanayohusiana na upangaji wa matumizi ya ardhi.

• Kushirikiana na sekta binafsi, taasisi zisizo za kiserikali, wakala wengine katika kuandaa na kutekeleza programu zinazokusudia kuimarisha elimu ya upangaji wa matumizi ya ardhi, na mwamko wa umma kuhusu haja ya usimamizi wa matumizi ya ardhi na kwa ajili ya kushawishi umma kusaidia na kuhimiza jitihada zinazofanywa na vyombo vingine kwa ajili hiyo.

• Kuendesha na kuunga mkono programu za mafunzo katika upangaji wa matumizi ya ardhi kwa ajili ya kuelimisha umma juu ya upangaji wa matumizi ya ardhi unaofaa na wajibu wa umma katika ulinzi, matumizi na uboreshaji wake.

• Kuhakikisha na kuratibu utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi inayoidhinishwa

• Kufanya shughuli nyingine kama itakavyoagizwa chini ya Sheria ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi.

2.2.2. NGAZI YA WILAYAHalmashauri ya Wilaya imetamkwa kisheria kuwa ndiyo yenye mamlaka ya upangaji wa matumizi ya ardhi ya Wilaya. Katika kifungu cha 21 cha Sheria ya Matumizi ya Ardhi Na 6 ya 2007, Halmashauri ya Wilaya kupitia kamati ya kudumu inayohusika na ardhi na mazingira katika kuandaa mpango wa matumizi. Pia, Halmashauri ya Wilaya ina jukumu kuunda timu ya matumizi ya ardhi ya Wilaya inayojulikana kama PLUM yenye wajumbe wasiopungua 6 na wasiozidi 8 kutoka miongoni mwa sekta mbalimbali zinazohusika na masuala ya ardhi, kama vile maliasili, ardhi, maendeleo ya jamii, maji, kilimo na mifugo. Pia, Halmashauri ya Wilaya, inawajibika kuishauri Halmashauri ya Kijiji kuunda Kamati ya Usimamizi wa Ardhi ya Kijiji lakini kama kuna Kamati ya Uamuzi ya Kijiji basi kijiji hakina budi kuitumia kamati hiyo kama kamati ya usimamizi ya mpango wa matumizi ya ardhi ya kijiji.

i. Timu Shirikishi ya Matumizi ya Ardhi ya Wilaya. Majukumu ya timu ni kama yafuatavyo:

• Kuzijengea uwezo Halmashauri za Wilaya na Vijiji katika kutoa maamuzi,

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 15 7/26/2016 10:18:56 AM

Page 24: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

16

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini

• Kuhamasisha na kuelimisha taasisi zilizoko katika ngazi za chini kuhusu uhitaji na umuhimu wa kuwa na mipango ya kina wa makazi vijijini,

• Kuanzisha na kuwezesha kazi za upangaji vijijini.

ii. Asasi za kiraiaHizi ni taasisi zilizoundwa kwa hiari zenye lengo la kukuza na kuboresha hali ya maisha ya kundi linalolengwa. Majukumu yake ni:

• Kuelimisha na kujenga uelewa wa kuboresha hali ya maisha ya watu

• Kukusanya rasilimali zinazohitajika katika utekelezaji wa mipango

• Kusaidia Serikali katika kutoa huduma kwa lengo la kuboresha hali ya maisha ya wananchi.

2.2.3. NGAZI YA KIJIJIHalmashauri ya Kijiji/Serikali ya Kijiji katika ngazi hii ndio mamlaka na chombo chenye mamlaka ya kuandaa mpango wa matumizi wa ardhi ya

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 16 7/26/2016 10:18:57 AM

Page 25: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

17

kijiji, inafanya utekelezaji wake kupitia kamati ya usimamizi na matumizi ya ardhi ya kijiji maarufu kama VLUMC. Suala muhimu na la kuzingatia katika mamlaka hii ni kwamba mpango mzima wa matumizi ya ardhi ya kijiji ni lazima uwe wa matokeo shirikishi wa jamii na kufuata taratibu zote, ili upate uhalali kwa wananchi wa kijiji kinachohusika.

i. Halmashauri ya Kijiji Halmashauri ya kijiji ni mamlaka ya upangaji katika ngazi ya kijiji na imepewa nguvu kisheria ya kusimamia ardhi ya kijiji (kifungu 8 cha Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na 5 ya mwaka 1999). Majukumu ya Halmashauri ya kijiji ni kama yafuatavyo:

• Halmashauri ya kijiji ina nguvu kisheria kupanga na kusimamia ardhi ya kijiji,

• Kuunda kamati pale inapohitajika na kuikasimisha majukumu,

• Kuandaa mikutano ya wanakijiji,

• Kuandaa Sheria Ndogo za Kijiji na kuhakikisha zinafuatwa.

ii. Mkutano Mkuu wa Kijiji Mkutano wa kijiji ndio chombo kikuu cha maamuzi katika ngazi ya kijiji.

Majukumu ya chombo hiki ni kama ifuatavyo:-

• Kuidhinisha mipango ya matumizi ya ardhi ya kijiji,

• Kupendekeza kutungwa kwa sheria ndogondogo pale inapolazimu,

• Kuidhinisha sheria ndogondogo za vijiji,

Mamlaka hizi za uandaaji na upangaji katika ngazi ya kijiji huunda kamati kwa ajili ya kuisaidia kuandaa na kusimamia utekelezaji wa Mpango wa Matumizi ya Ardhi ya Kijiji. Hii ni pamoja na Kamati ya Usimamizi wa Matumizi ya Ardhi ya Kijiji au Kamati ya Uamuzi ya Kijiji na Timu ya Uandaaji Mipango Kijijini

i. Kamati ya Usimamizi wa Matumizi ya Ardhi ya Kijiji Kamati ya usimamizi wa matumizi ya ardhi ya kijiji ina majukumu yafuatayo:

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 17 7/26/2016 10:18:57 AM

Page 26: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

18

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini

• Kushirikiana na timu ya upangaji ya kijiji kuandaa mipango ya kina ya matumizi ya ardhi,

• Kuwasiliana na taasisi nyingine katika masuala ya kiutawala na kiutaalam,

• Kuhamasisha na kuwaandaa wanakijiji katika masuala yanayohusu upangaji matumizi ya ardhi,

• Kuainisha changamoto na masuala ambayo ni vipaumbele vya jamii

ii. Timu ya Uandaaji Mipango Kijijini Timu ya uandaaji wa mipango kijijini itafanya kazi zote zinazohusu mipango ya kina ya matumizi ya ardhi vijijini. Timu ya uandaaji inajumuisha wajumbe wote wa kamati ya usimamizi wa ardhi kijijini, na wajumbe wa halmashauri ya kijiji ikiongezewa timu ya wataalamu kutoka wilayani yaani PLUM, basi timu inakuwa imekamilika na kuwa tayari kwa kuanza maandalizi ya mpango kabambe wa matumizi ya ardhi katika kijiji.

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 18 7/26/2016 10:18:57 AM

Page 27: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

19

2.3. MAELEZO YA AWALI YA UANDAAJI MPANGO WA MATUMIZI

Uandaaji wa mpango wa matumizi ya ardhi unafuata utaratibu maalumu ambao umewekwa na mwongozo shirikishi wa Taifa katika mpango wa matumizi ya ardhi, ili kupata uhalali wa mpango mzima kwa wananchi ni lazima taratibu hizo zifuatwe. Kwa kufuata mchakato huu, wilaya na vijiji vilivyokwishaanza utekelezaji wa mpango; kila wakati viwe katika nafasi ya kujitathmini na kuelewa vyema kuwa vimo katika hatua gani ya mpango kwa kufuata Mpango Kazi wa Jamii waliojiwekea, ambao kimsingi huandaliwa katika Hatua ya 2 ya mpango.

Maandalizi Wilayani: Uhamasishaji, kuunda timu ya PLUM ya wilaya, na kuweka Mpango wa Utekelezaji wa PLUM wa wilaya.

Tathmini ya Matumizi ya Ardhi Vijijini (PRA): Uhamasishaji taasisi za kijiji; Elimu ya Sera na Sheria za Ardhi; Tathmini ya matumizi ya ardhi na raslimali; kubaini matatizo fursa na vikwazo; na kuweka Mpango Kazi wa Jamii CAP).

Kuhakiki Mipaka Ardhi ya Kijiji:. Kubaini, kuweka na kupima mipaka ya ardhi ya kijiji; utatuzi wa migogoro ya mipaka; Masijala ya Ardhi ya Wilaya; Utoaji wa Cheti cha Ardhi ya Kijiji. Kuandaa ramani ya msingi ya Matumizi ya Ardhi ya kijiji.

Upangaji Matumizi ya Ardhi ya Kijiji: Ushirikishwaji katika mipango na usimamizi; kuainisha hatua stahili za usimamizi; na Sheria Ndogo za Usimamizi wa Matumizi ya Ardhi.

Utawala wa Ardhi ya Kijiji: Masijala ya Ardhi ya Kijiji; Utoaji, usajili na Usimamizi wa Hatimiliki za Kimila; na Utatuzi wa Migogoro ya miliki.

Usimamizi na Uimarishaji: Utekelezaji wa Hatua Stahili za Usimamiaji wa Ardhi na Uimarishaji (Mafundi sanifu wa kijiji; Uimarishaji; Tathmini; Ufuatiliaji na Urejeaji Mipango).

MUHIMU: Kwa kufuata mpango kazi wa jamii, Halmashauri ya Kijiji kwa kutumia Kamati ya Usimamizi wa Ardhi ya Kijiji (VLUMC) huandaa rasimu ya mpango wa matumizi ya ardhi ya kijiji, ambayo baadaye huwasilishwa kwenye Mkutano wa Kijiji kujadiliwa ili kuidhinisha na kuwa na mpango kamili wa matumizi ya ardhi ya kijiji.

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 19 7/26/2016 10:18:57 AM

Page 28: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

20

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini

3.0. MCHAKATO WA UANDAAJI MPANGO WA MATUMIZI YA ARDHI YA KIJIJI

3.1. MAANA YA MPANGO WA MATUMIZI YA ARDHI WA KIJIJI

Mpango wa Matumizi ya Ardhi ya Kijiji: Ni utaratibu wa kutathmini na kupendekeza namna mbalimbali ya matumizi ya maliasili/rasilimali ili kuinua hali ya maisha ya wanakijiji na kuondoa umaskini. Utaratibu wa kupanga, kutekeleza na kuhuisha matumizi ya ardhi unafaa zaidi iwapo utafanyika kwa njia ya ushirikishwaji, ikiwa na maana kuwa watumiaji wakubwa wa ardhi ambao ni wanakijiji wanashirikishwa kikamilifu. Ili kuhakikisha kuwa wanakijiji wanashiriki kikamilifu, ni muhimu kuzingatia makundi mbalimbali yaliyopo katika kijiji kama vile; wakulima, wafugaji, wakiwemo wanawake na wanaume na rika, ambayo yanaweza kuwa na utashi na malengo yanayotofautiana. Maana hii ni kwa mujibu wa mwongozo wa Tume ya Taifa ya Mpango wa Matumizi ya Ardhi wa Mwaka 2010.

3.2. HATUA SITA ZA UPANGAJI WA MPANGO WA MATUMIZI YA ARDHI YA KIJIJI

Mwongozo wa Taifa wa Ushirikishwaji Katika Mipango na Usimamizi wa Matumizi ya Ardhi, unabainisha hatua kuu 6 na muhimu, katika mchakato wa upangaji na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi vijijini. Hatua hizi zinapitia mchakato mzima wa maandalizi, upangaji, utawala na usimamizi wa ardhi, tathmini, ufuatiliaji, uimarishaji na urejeaji mipango.

3.2.1. HATUA YA KWANZA: MAANDALIZI WILAYANIi. Mamlaka ya Upangaji ya Matumizi ya Ardhi ya Wilaya

Sheria ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Na. 6 ya 2007 katika kifungu cha 21 inaweka Halmashauri ya Wilaya kuwa Mamlaka ya Upangaji wa Matumizi ya Ardhi ya Wilaya. Halmashauri ya Wilaya inaweza kufanya kazi hii kupitia Kamati inayohusika na Ardhi na Maliasili .

ii. Timu ya PLUM ya Wilaya na Mpango Kazi wa UtekelezajiTimu ya PLUM ya Wilaya huundwa na Halmashauri ya Wilaya inayohusika, ikihusisha wajumbe 6 – 8 kutoka sekta kuu zinazohusika na

SURA YA TATU

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 20 7/26/2016 10:18:58 AM

Page 29: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

21

matumizi ya ardhi ikiwamo kilimo, mifugo, maliasili, Ardhi na Maendeleo ya Jamii. Mtaalamu (wa Mipango Miji na Vijiji) anayehusika na mipango ya matumizi ya ardhi wilayani huwa mratibu wa timu hii.

Timu ya PLUM inawajibika kuratibu na kuwezesha uandaaji, utekelezaji na usimamizi wa mipango ya matumizi ya ardhi wilayani. Ili kufanya hivi, timu hii haina budi iandae mpango wa jumla wa utekelezaji, unaoonesha jinsi gani wilaya inakusudia kuviwezesha vijiji vyake vyote kuandaa na kutekeleza mipango ya matumizi ya ardhi. Kwa kufuata vigezo vilivyoainishwa, hupendekeza kuteua baadhi ya vijiji kuwa vya kuanzia (vya mfano) ambavyo vitawezeshwa katika kipindi cha muda mfupi (miaka 1-3), vijiji vitakavyoongezeka katika muda wa kati (miaka 3-5), na muda mrefu (miaka 5 na kuendelea); kama inavyoshauriwa kwenye mwongozo shirikishi wa Taifa.

Ni muhimu timu hii izingatie uhusishaji wa sekta zote zinazohusika (sectoral intergration) katika upangaji na utekelezaji, ikiwemo miradi na taasisi zisizo za kiserikali (CBOs na NGOs), zinazohusika na matumizi ya ardhi na rasilimali zake. Aghalabu, Tume ya Taifa ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC), huwezesha warsha iliyoandaliwa na wilaya inayohusika, ili kuhakikisha wilaya inajiandaa vyema kutekeleza PLUM katika vijiji vyake. Vijiji ambavyo vina mipango ya matumizi ya ardhi iliyoandaliwa kwa ushirikishwaji ikihusisha sekta kuu za matumizi ya ardhi, vina nafasi kubwa ya kutekeleza kwa ufanisi miradi ya kisekta kama vile DADP na PADEP (Kilimo na Mifugo), WMA na PFM (Maliasili), MACEMP (Mazingira) na Utoaji na Usajili wa Hatimiliki za Kimila (Ardhi). Vilevile miradi hii itumike kugharamia uandaaji na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya Ardhi vijijini.

Baada ya vijiji vitakavyowezeshwa kuandaa na kutekeleza mipango ya matumizi ya ardhi kuteuliwa na kuidhinishwa, Timu ya PLUM huandaa mpango kazi wa utekelezaji unaohusisha kwanza hatua ya 2 – 4. Vilevile timu ihakikishe rasilimali zinazohitajika kwa utekelezaji kama vile fedha, nguvu kazi na vitendea kazi vinapatikana kwa wakati.

3.2.2. HATUA YA PILI: TATHMINI YA MATUMIZI YA ARDHI VIJIJINI

Katika hatua hii, inajumuisha hatua zingine ndogo nne za kufuatwa ili kufanya tathmini shirikishi ya matumizi ya ardhi ya kijiji. Hatua hizo ni kama zifuatazo hapa chini:-

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 21 7/26/2016 10:18:58 AM

Page 30: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

22

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini

i. Elimu kwa Umma kuhusu Sera na Sheria za Matumizi ya Ardhi;

Timu ya PLUM huvitaarifu rasmi kwa barua vijiji vinavyohusika, kuhusu kuanza kwa uandaaji wa mpango wa matumizi ya ardhi ya kijiji. Hupanga na kukubaliana na viongozi wa kijiji siku na wakati wa kukutana na Halmashauri ya Kijiji kuelezea madhumuni, utaratibu na maudhui ya mpango. Mkutano huu hujumuisha pia Baraza la Ardhi la Kijiji. Katika mkutano huu timu ya PLUM hutoa mafunzo yanayo husiana na :-

• Madhumuni, umuhimu, utaratibu na maudhui ya mpango wa matumizi ya ardhi ya kijiji

• Maudhui ya Sera na Sheria zinazohusu matumizi ya ardhi na raslimali zake (kv. Sera na Sheria za Ardhi, Mazingira, Misitu, Maji, Madini, Wanyama pori, Kilimo. Mifugo n.k.)

• Takwimu za kijiji zinazohitajika toka ngazi ya vitongoji kama vile; idadi ya kaya, watu, mifugo na huduma za jamii.

• Pia, kuiongoza Halmashauri ya Kijiji kuteua Kamati ya Usimamizi wa Matumizi ya Ardhi ya Kijiji (maarufu kama VLUMC), kama kamati ya uamuzi ya kijiji itakuwepo basi hiyo pia inaweza kuwa mjarabu katika mpango mzima.

Hata hivyo, timu ya PLUM hupanga na viongozi wa kijiji siku na wakati wa kufanya Mkutano wa Kijiji ili kuelezea madhumuni, utaratibu na maudhui ya mpango wa matumizi ya ardhi ya kijiji. Pia, katika mkutano huu timu ya PLUM hutoa mafunzo (mada) kama zilivyoainishwa hapo juu. Ni vyema Mkutano wa Halmashauri ya Kijiji ufanyike asubuhi na Mkutano wa Kijiji ufanyike jioni, ili kuokoa gharama na muda.

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 22 7/26/2016 10:18:58 AM

Page 31: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

23

ii. Tathmini Shirikishi ya kijiji Kati ya siku 2 hadi 4, Timu ya PLUM huiwezesha Halmashauri ya Kijiji ikijumuika na Kamati ya Usimamizi wa Matumizi ya Ardhi ya Kijiji kufanya Tathmini Shirikishi ya Kijiji (PRA) inayolenga matumizi ya ardhi. Hii hufanyika kwa kukusanya, kuchambua na kuwekea kumbukumbu takwimu muhimu za kijiji kwa kila kitongoji kama vile idadi ya watu, mifugo, vyanzo vya maji, misitu, huduma za kiuchumi, jamii n.k. Pia, Timu ya PLUM huiwezesha Halmashauri ya Kijiji ikijumuika na Kamati ya Usimamizi wa Matumizi ya Ardhi ya Kijiji kuchambua na kutathmini matatizo, vikwazo na fursa za utatuzi katika matumizi ya ardhi.

Uchambuzi wa namna hii ni muhimu na unawasaidia wanakijiji kulinganisha kati ya kushughulikia matatizo ya ufumbuzi wa papo kwa papo na yale yanayohitaji upangaji wa muda wa kati au muda mrefu. Vilevile, ni muhimu kwa wanakijiji kuelewa kuwa uwekezaji unaohitajika kwenye sekta za huduma kama vile elimu na afya, unatoka katika sekta ya uzalishaji kama vile kilimo,ufugaji, misitu, uvuvi n.k. Katika uchambuzi wa fursa, shughuli zinazohitaji msaada wa nje ya kijiji na nje ya majukumu ya timu ya PLUM zinaweza kurejewa kwa taasisi husika ndani na hata nje ya wilaya.

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 23 7/26/2016 10:18:59 AM

Page 32: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

24

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini

iii. Kuandaa Mpango Kazi wa JamiiMatokeo ya kazi ya tathmini shirikishi ya kijiji ni kuwa na mpango kazi wa jamii unaolenga kwenye usimamizi wa matumizi ya ardhi (Community Action Plan – CAP). Huu ni mpango kazi.Vilevile, Mpango kazi huu huandaliwa baada ya kubaini matatizo, fursa na vikwazo katika matumizi ya ardhi kijijini. Mpango huu huweka bayana mambo yafuatayo:-

• Vipaumbele vya fursa za maendeleo (Malengo ya utatuzi wa matatizo ya msingi).

• Shughuli zinazopaswa kufanywa kufikia malengo

• Muda unaohitajika kufanya shughuli hizo

• Mahitaji ya raslimali na nyenzo

• Kazi na majukumu ya watu binafsi na vikundi

• Uhusishaji wa miradi ya kijiji, wilaya na taifa

• Maeneo yanayohitaji msaada kutoka nje

• Matokeo ashiria ya kufikia malengo.

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 24 7/26/2016 10:19:03 AM

Page 33: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

25

iv. Ujenzi na Uimarishaji wa Taasisi za KijijiUfanisi wa kazi zilizoainishwa katika hatua hii, na hatua zote zinazofuatia unategemea sana kuwepo kwa taasisi imara katika ngazi ya kijiji na vitongoji vyake. Taasisi kama vile halmashauri ya kijiji, mkutano mkuu wa kijiji pamoja na kamati zake ni muhimu kuimarishwa kwa lengo la kuziwezesha kumudu majukumu yake katika uandaaji wa mpango wa matumizi ya ardhi ya kijiji.

Kifungu cha 55 cha Sheria ya Serikali za Mitaa kinaweka utaratibu wa kila kijiji kuwa na Mkutano wa Kijiji ambao ni mkutano wa wanakijiji wote wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea na wenye akili timamu. Sheria ya Ardhi ya Vijiji ya 1999 katika kifungu cha 8(5), inaielekeza Halmashauri ya Kijiji kutogawa ardhi au kutoa hati za hakimiliki za kimila za ardhi bila kwanza kupata kibali cha Mkutano wa Kijiji. Vilevile katika kifungu cha 8(6) (a), Sheria inaielekeza Halmashauri ya Kijiji kutoa taarifa katika Mkutano wa Kijiji na kuzingatia maoni ya Mkutano wa Kijiji kuhusiana na mambo yote ya usimamizi na utawala wa ardhi ya kijiji.

MUHIMU: Hapana budi kusisitiza umuhimu wa kuwepo mikutano, kwani maeneo mengi yenye migogoro ya ardhi, yamechangiwa na kupuuzwa, kutofanyika, na kutofuata taratibu za mikutano. Katika vijiji vingi, maamuzi yanayopaswa kutolewa na Halmashauri ya Kijiji, yanatolewa na mtu mmoja tu (labda Mwenyekiti au Katibu), na kuchukuliwa kama maamuzi ya Halmashauri ya Kijiji.

Kuna watu wanaona mikutano ni kupoteza muda, au kuchelewesha maamuzi.

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 25 7/26/2016 10:19:03 AM

Page 34: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

26

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini

Hii ni mifano michache tu, ambayo inapaswa isaidie kutoa tahadhari wakati taasisi za vijiji zinaposhughulikia masuala nyeti, kama ardhi. Watu wachache wasipewe fursa, kutumia vibaya mamlaka ambayo Sheria inatoa kwa taasisi za kijiji kushughulikia ardhi.

3.2.3. HATUA YA TATU: KUHAKIKI MIPAKA ARDHI YA KIJIJI

Hii ni hatua inayohusisha timu ya PLUM ya wilaya kuhakiki kama mipaka ya kijiji inatambulika au la kupitia Idara ya Ardhi ya Wilaya na kuweka orodha ya vijiji katika makundi yafuatayo;

a. Vijiji ambavyo vimeshapimwa (vina ramani) na havina migogoro ya mipaka na kisha kuviandalia Cheti cha Ardhi ya Kijiji.

b. Vijiji ambavyo mipaka yake inatambulika lakini havijapimwa na havina migogoro ya mipaka. Vijiji hivi vinaweza kuandaliwa ramani ya mipaka kwa njia ya chombo cha upimaji (GPS), na kuandaliwa Cheti cha Ardhi ya Kijiji.

c. Vijiji ambavyo mipaka yake ilishapimwa, lakini kwa sasa vina migogoro ya mipaka kwa mfano, kama vimegawanyika. Migogoro ya mipaka itatuliwe kwanza na kubaini mipaka inayokubalika kwa pande zinazohusika.

d. Vijiji ambavyo havijapimwa na vina migogoro ya mipaka basi ni sharti migogoro hiyo itatuliwe kwanza, na kubaini mipaka inayokubalika kwa pande zinazohusika.

Jukumu la awali na la msingi ili Halmashauri ya Kijiji isimamie ardhi ya kijiji kwa mujibu wa sheria, ni kutambua mipaka ya kijiji na kupata Cheti cha Ardhi ya Kijiji. Katika kufanya hili, Halmashauri ya Kijiji kinachohusika haina budi kuwasiliana na mamlaka za ardhi inayopakana na kijiji; kama vile Mamlaka za Hifadhi, na Halmashauri za Vijiji jirani; ili wakubaliane mpaka wa ardhi yao. Halmashauri ya Kijiji, aghalabu itakasimu shughuli hii kwenye kamati; kama vile Kamati ya kusimamia Matumizi ya Ardhi au Maliasili.

i. Kukubaliana kuhusu Mipaka ya VijijiMamlaka na Halmashauri za Vijiji jirani huombwa na Halmashauri ya Kijiji kinachohakiki mipaka yake kuwakilishwa angalau na watu wawili, katika kujadili na kukubaliana uwandani (kwenye maeneo yanayohusika) kuhusu mipaka yao. Hawa wawe watu ambao wanaheshimika na wanaelewa vizuri kuhusu mipaka ya vijiji vinavyohusika. Ni muhimu pia

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 26 7/26/2016 10:19:04 AM

Page 35: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

27

wawepo wapima ardhi (aghalabu kutoka wilayani) kama washauri ili kuwezesha zoezi hili kufanyika kwa ufanisi.

Timu ya majadiliano ya mipaka itembelee maeneo, kufanya majadiliano na makubaliano kuhusu mahali halisi pa kila kona, ambapo kila kona huwekewa alama ya muda kwa kuchimba shimo au kusimika kigingi. Makubaliano huwekwa kwenye kumbukumbu kama muhtasari, kuonesha maelezo ya mahali penye kona au alama, ikiwa na majina na sahihi za wajumbe wa timu nzima. Baadaye wawasilishe makubaliano haya katika Halmashauri za Vijiji vinavyohusika, ambazo ndizo zenye mamlaka ya kuweka mikataba ya makubaliano.

ii. Utatuzi wa Migogoro ya Mipaka ya Vijiji Kifungu cha 7 (2) cha Sheria ya Ardhi ya Vijiji ya 1999 kinatoa utaratibu wa kutatua migogoro ya mipaka ya kijiji na vijiji au mamlaka nyingine. Halmashauri ya Kijiji inapaswa kufanya kila juhudi kufikia makubaliano ya mipaka na majirani zake ikiwemo kuhusisha na kupata ushauri wa halmashauri ya wilaya inayohusika. Wilaya inaweza kutumia timu ya ‘PLUM’ ya wilaya kama mshauri wa utatuzi wa migogoro ya mipaka ya vijiji. Watendaji wa wilaya wanapofanya kazi kama washauri au wasuluhishi wa migogoro ya mipaka ya vijiji, ni muhimu wakaelewa na kutumia mbinu za usuluhishi ili kuepuka upendeleo, uonevu, upuuzaji,

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 27 7/26/2016 10:19:04 AM

Page 36: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

28

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini

na kutozingatia sheria; hivyo kufukia tu kwa muda au kukuza mgogoro badala ya kusaidia kutatua.

iii. Cheti cha Ardhi ya Kijiji Mipaka ya kijiji ikishawekwa na kupimwa, mamlaka husika (Kamishna wa Ardhi) atatoa Cheti cha Ardhi ya Kijiji kwa Halmashauri ya Kijiji kwa mujibu wa kifungu cha 7 (6) cha Sheria ya Ardhi Vijiji ya 1999. Hii ni hati muhimu inayopaswa kutunzwa na Halmashauri ya Kijiji, inayotumika kumaanisha mamlaka ya Halmashauri ya Kijiji kutawala na kusimamia ardhi ya kijiji.

Cheti cha Ardhi ya Kijiji kinakuwa badala ya Hatimiliki ya Ardhi ya Kijiji zilizotolewa kwa baadhi ya vijiji, ambazo zinapaswa kufutwa kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi Vijiji ya 1999. Usimamizi wa ardhi ya kijiji ni pamoja na uwekaji na upimaji mipaka ya kijiji , upangaji kwa ushirikishwaji wa matumizi ya ardhi ya kijiji, ugawaji na umilikishaji wa maeneo ya ardhi kwa taasisi na watu binafsi (wanakijiji), kutoa Hatimiliki za Haki za Ardhi

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 28 7/26/2016 10:19:08 AM

Page 37: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

29

za Kimila, na kuanzisha na kutunza Masijala ya Ardhi ya Kijiji, ambayo inapaswa kuwa sehemu ya Masijala ya Ardhi ya Wilaya.

a. Maana ya Cheti cha Ardhi ya KijijiCheti cha Ardhi ya Kijiji ni nyaraka inayobainisha usimamizi wa ardhi ya Kijiji (chini ya Halmashauri ya Kijiji) ikionesha mipaka na ukubwa wa eneo lote la kijiji. Sheria ya Ardhi ya Vijiji (1999), inabatilisha Hatimiliki ya Ardhi ya Kijiji, na badala yake Halmashauri ya Kijiji kupewa Cheti cha Ardhi ya Kijiji. Halmashauri ya Kijiji inapokuwa na Hati ya Kumiliki Ardhi ya Kijiji; inamaanisha wanakijiji hawawezi tena kumiliki ardhi ndani ya kijiji hicho. Vinginevyo itamaanisha kumilikisha ardhi hiyohiyo kwa mtu/taasisi mbili yaani hati pandikizi (double allocation) kati ya Halmashauri ya Kijiji na wanakijiji, jambo hili ni kosa kisheria.

Pengine Halmashauri ya Kijiji ikiwa na Hati Miliki ya Ardhi ya Kijiji inaweza kuazimisha (sub-lease) ardhi kwa wanakijiji wake. Kuazimisha huku hakuna hadhi ya dhamana kwa aliyeazimishwa, bali ni haki ya kutumia ardhi tu. Mwenye haki ya dhamana anabakia kuwa mmiliki wa ardhi yaani Halmashauri ya Kijiji. Hata hivyo, Halmashauri ya Kijiji haiwezi kutumia hatimiliki ya ardhi ya kijiji chote kama dhamana katika taasisi za fedha, kama benki. Ikiweza kufanya hivi, inaweza kutoa fursa kwa benki kunadi ardhi yote ya kijiji, kama Halmashauri ya Kijiji itashindwa kutimiza masharti ya dhamana; kama vile kutolipa mkopo n.k.

Kwa kuzingatia matatizo haya, ndiyo maana Sheria ya Ardhi ya Vijiji imebainisha kwamba wanaohitaji kutumia hatimiliki ya ardhi kama dhamana ni wanakijiji na wala si Halmashauri ya Kijiji. Utawala wa kijiji unapaswa kuwa na hadhi ya kuweza kusimamia na kutawala ardhi ya kijiji, kiasi cha kuweza kutoa hatimiliki kwa wanakijiji wake kama anavyofanya Kamishna wa Ardhi kwa Ardhi ya Kawaida. Hivyo Sheria ya Ardhi ya Vijiji ya 1999 inatoa mamlaka kwa Kamishna wa Ardhi kutoa Cheti cha Ardhi ya Kijiji kwa kijiji chochote ambacho mipaka yake imekubalika, imewekwa, na au kupimwa.

b. Utoaji wa Cheti cha Ardhi ya KijijiCheti cha Ardhi ya Kijiji kinatolewa kwa jina la Rais, akikasimu mamlaka yake kwa Halmashauri ya Kijiji kusimamia Ardhi ya Kijiji. Cheti hiki kinahakikisha kukaliwa na kutumiwa kwa ardhi ya kijiji na wanakijiji kwa kuzingatia taratibu na kanuni za kimila zinazotumika katika ardhi, ambako kijiji kipo. Cheti cha Ardhi ya Kijiji kinaandaliwa na Ofisa Ardhi wa Wilaya kwa kutumia Fomu ya Ardhi ya Vijiji Na.16, kuwekewa ramani ya upimaji wa mipaka ya kijiji na ukubwa wa eneo lake, na kisha

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 29 7/26/2016 10:19:09 AM

Page 38: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

30

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini

kusainiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kijiji na Ofisa Mtendaji wa Kijiji, halafu kusajiliwa wilayani na kupewa Na. ya usajili. Hatimaye Cheti hutumwa kwa Kamishna wa Ardhi kusainiwa na kuwekwa lakiri. Ofisi ya Kamishna hubaki na nakala moja kwa ajili ya kumbukumbu, nakala mbili hutumwa katika wilaya inayohusika, ili nakala moja ibaki katika Masijala ya Ardhi ya Wilaya, nakala moja ipelekwe kwenye Masijala ya Ardhi ya Kijiji kinachohusika.

Ni wajibu wa Halmashauri ya Kijiji kuangalia na kutunza kwa usalama Cheti cha Ardhi ya Kijiji. Inapotokea mipaka ya ardhi ya kijiji ikabadilishwa vyovyote vile, ni wajibu wa Halmashauri ya Kijiji kumjulisha mapema Kamishna wa Ardhi mabadiliko hayo. Vilevile, Halmashauri ya Kijiji inapaswa imtumie Kamishna wa Ardhi Cheti cha Ardhi ya Kijiji, ili Kamishna afanye mabadiliko yaliyotokea katika cheti husika. Kwa mintarafu hii; Kamishna wa Ardhi atatunza Daftari ya Ardhi za Vijiji.

3.2.4. HATUA YA NNE: UPANGAJI WA MATUMIZI YA ARDHI YA KIJIJI

Katika kifungu cha 33 cha Sheria ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Na. 6 ya 2007; na kifungu cha 12 na cha 13 katika Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na. 5 ya 1999 vinatoa taratibu na maagizo ya kisheria kuhusu mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji kama ifuatavyo:-

i. Mgawanyo wa Ardhi ya Kijiji • Ardhi inayokaliwa na kutumiwa na mtu, familia au kikundi cha

watu kwa mujibu wa Sheria za Kimila.

• Ardhi ya makazi au matumizi ya jumuiya ambayo inaweza kutolewa kwa njia ya mgao na Halmashauri ya Kijiji.

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 30 7/26/2016 10:19:09 AM

Page 39: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

31

• Ardhi ya pamoja ambayo Halmashauri ya Kijiji itapendekeza katika Mkutano wa Kijiji maeneo na makusudio ya matumizi ya maeneo hayo.

ii. Utaratibu wa Kutengeneza Mpango• Mapendekezo ya Halmashauri ya Kijiji yanaweza kuwasilishwa

kama mpango wa matumizi ya Ardhi ya Kijiji au sehemu ya kijiji.

• Uandaaji wa Mpango wa Matumizi ya Ardhi ya Kijiji uzingatie ushiriki wa wanakijiji wote (Wadau mbalimbali kwa kujali jinsia, rika n.k.) na upangaji na utekelezaji wa hatua kwa hatua kama zilivyoainishwa kwenye Mwongozo wa Ushirikishwaji Katika Mipango na Usimamizi wa Matumizi ya Ardhi Vijijini.

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 31 7/26/2016 10:19:11 AM

Page 40: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

32

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini

iii. Ushiriki wa Walengwa Katika Mipango ya Matumizi ya Ardhi

Mwelekeo wa ushirikishwaji katika mipango na usimamizi wa matumizi ya ardhi unazingatia yafuatayo:-

• Kwanza kabisa, umuhimu wa mipango ya matumizi na usimamizi wa ardhi utokane na watumiaji wa ardhi wenyewe, ambao ndio wanaoathirika moja kwa moja na migogoro na uharibifu wa ardhi, na ambao ndiyo watanufaika kutokana na usimamizi wa matumizi ya rasilimali kuboreshwa.

• Wanakijiji wanahusika kikamilifu katika kuandaa utaratibu, ugawaji ardhi na kutawala upangaji katika hatua zote. Uwezo wa wenyeji katika kufanya maamuzi unajengwa kupitia uhamasishaji wa taasisi zilizopo kwenye kijiji.

• Kazi ya kukusanya taarifa na uchambuzi wake, mambo gani yapewe umuhimu, na mipango yenyewe; inatokana na wenyeji, na hivyo kuweza kunyumbulika na kushirikisha taaluma za sekta mbalimbali.

• Jukumu kubwa la wataalamu ni kuasisi, kushauri na kuwezesha mfumo wa ushirikishwaji katika mipango na usimamizi wa matumizi ya ardhi; kuliko kutayarisha mipango yao wenyewe kama ilivyozoeleka katika mipango msonge (juu kwenda chini). Wataalamu wawe makini kuhakikisha viwango na ushauri wa kitaalamu vinazingatiwa.

ANGALIZO: Ni muhimu sana wataalamu wa sekta kuu za matumizi ya ardhi kama ilivyoainishwa katika Hatua ya 1, wakati wa kuunda Timu ya ‘PLUM’ ya wilaya wakawezesha kwa pamoja hatua hii, ili kupata muafaka wa mpango wa matumizi ya ardhi ya kijiji unaozingatia viwango vya utaalamu wa sekta zote, hususan kilimo, maliasili, mifugo, na ardhi. Sekta hizi zikishauri na kufikia maamuzi ya matumizi ya ardhi ya kijiji bila ushirikiano, na kwa nyakati tofauti, hujikanganya, kuwakanganya wanakijiji, na kupoteza muda na raslimali.

iv. Matokeo ya Ushirikishwaji katika MipangoWanakijiji wakishirikishwa kikamilifu katika mipango yao ya matumizi ya ardhi basi yafuatayo yanaweza kujitokeza:-

• Mipango ya matumizi ya ardhi ya kijiji inatekelezwa kwa kuwa inapangwa na wanakijiji wenyewe; inazingatia mahitaji yao na

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 32 7/26/2016 10:19:11 AM

Page 41: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

33

mazingira halisi.

• Migogoro ya ardhi inatatuliwa na matakwa ya wanufaikaji (wanaume, wanawake, vijana, wakulima, wafugaji n.k) yanaweza kuainishwa na kuheshimiwa, kwa kuwa mipango hiyo imeandaliwa kupitia majadiliano na hatimaye makubaliano.

• Uzalishaji kutokana na ardhi utaongezeka na kuwanufaisha watumiaji wa ardhi mbalimbali kwa sababu mipango inatekelezwa na inaakisi matakwa yao.

• Mipango inaweza kurejewa, kurekebishwa na kuendelezwa na wakazi wenyewe bila kutegemea sana misaada ya nje kwa kuwa taasisi za kijiji zimewezeshwa kushughulikia sehemu kubwa ya masuala ya usimamizi wa matumizi ya ardhi wao wenyewe.

v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya KijijiHata hivyo; uandaaji wa mpango wa matumizi ardhi ya kijiji sharti uzingatie ugawaji wa ardhi kwa matumizi mengine yoyote kuendana na mahitaji ya watumiaji kwa kuzingatia viwango vilivyoainishwa na Wizara ya Ardhi kama ifuatavyo;

• Maeneo ya makazi na huduma za jamii. Mfano shule, zahanati, ofisi, masoko, maduka nyumba za ibada barabara na makaburi.

• Maeneo ya kilimo. Maeneo ya kilimo cha mazao ya kudumu, mazao ya misimu, mazao ya kilimo cha umwagiliaji na kilimo cha misitu.

• Maeneo ya kuchungia. Maeneo kwa ajili ya malisho, nyika, njia za mifugo, huduma za mifugo kama vile majosho na maji.

• Maeneo ya misitu. Huhusisha /misitu asilia yenye miti mingi, matumizi ya mbao, majengo, kuni, mkaa, asali, dawa za mitishamba, na uhifadhi wa mimea asilia.

• Maeneo ya uwekezaji

Baada ya mpango wa matumizi ya ardhi kukamilika timu ya PLUM huwezesha Halmashauri ya Kijiji kupitia Kamati ya Matumizi ya Ardhi ya Kijiji kuandaa rasimu ya mpango ya matumizi ya ardhi ya kijiji pamoja na rasimu ya sheria ndogo ambazo huwasilishwa kwenye Mkutano

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 33 7/26/2016 10:19:11 AM

Page 42: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

34

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini

mkuu wa Kijiji na kujadiliwa. Utaratibu wa kutunga sheria ndogo za kijiji umefafanuliwa katika kipengele cha (vii& viii).

vi. Kukamilisha Mpango wa Matumizi ya Ardhi ya Kijiji

Wakati wa kuandaa na kukamilisha mpango wa matumizi ya ardhi, kazi kubwa zaidi ni kazi ya kufanya majadiliano katika ngazi mbalimbali (mashamba, vitongoji, kijiji n.k), na hatimaye kuamua ni eneo lipi litumike kwa matumizi gani ya ardhi; wataalamu watoe ushauri wa

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 34 7/26/2016 10:19:14 AM

Page 43: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

35

msingi ili kuwezesha zoezi hili kufanikiwa. Wataalamu watoe ushauri na athari au ubora wa eneo moja hadi eneo jingine kwa ajili ya matumizi mjarabu . Kwa mfano, wataalamu wanaweza kuelezea athari za kufyeka miti na kulima kwenye vyanzo vya maji, iwapo wanakijiji watapendekeza kufanya hivyo. Wataalamu wanaweza pia, kushauri kuhusu ubora wa udongo kwa matumizi au aina ya mazao yanayokusudiwa kustawishwa. Pia, wataalamu watoe ushauri kuhusu ukubwa wa maeneo dhidi ya mahitaji halisi na uwezo wa mkulima kulima kulingana na nyenzo alizonazo. Kwa mfano, eneo la kilimo dhidi ya mahitaji ya chakula na mazao ya biashara. Eneo la kuchungia dhidi ya idadi ya mifugo. Eneo la misitu dhidi ya mahitaji ya kuni, miti, mbao, hifadhi, n.k.

Mara nyingi msingi huwa ni jinsi gani maeneo yalivyotumika hapo awali au kulingana na umilikaji wa ardhi uliopo na ilivyoainishwa katika ramani ya msingi ya kijiji. Inapotokea wanakijiji wanataka mabadiliko makubwa katika mpango wa ugawaji ardhi, wataalamu wasaidie kuhakikisha taratibu na uhakiki wa maslahi katika ardhi vinazingatiwa kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Ardhi ya Vijiji 1999 kifungu cha 49 – 58. Hii ni pamoja na Halmashauri ya Kijiji kufuata taratibu na kupata kibali cha Mkutano wa Kijiji.

Wakati wa mikutano katika ngazi mbalimbali, mabadiliko yanayopendekezwa hujadiliwa na kupitishwa, na hivyo kuwa sehemu ya Mpango wa Matumizi ya Ardhi ya Kijiji. Makubaliano huwekwa katika kumbukumbu za maandishi, na ikiwezekana kuchorwa kwenye ramani ya kijiji. Timu ya PLUM ya wilaya isaidiane na Kamati ya Ardhi ya Kijiji (k.n.y Halmashauri ya Kijiji) kutayarisha ramani ya matumizi ya ardhi inayoonyesha maeneo halisi ya mpango wa matumizi ya ardhi.

vii. Sheria Ndogo za Matumizi ya Ardhi VijijiniSheria ndogo za vijiji zinahusu taratibu ambazo huwekwa na mamlaka za wenyeji, ambazo hazina budi kufuatwa katika eneo fulani, ambapo Sheria Kuu haifungamani ipasavyo. Sheria ndogo zinaweza kutungwa kwa ngazi ya halmashauri za miji, wilaya na kijiji; na lazima zisipingane na Sheria za Kitaifa. Kwa usimamizi wa ardhi (PLUM), sheria ndogo zinaweka msingi wa usimamizi kisheria, na zinaangaliwa kama nyenzo za kutia nguvu utekelezaji wa makubaliano maalumu ya wenyeji yanayohusu usimamizi wa maliasili na mipango ya matumizi ya ardhi.

Sheria ndogo, zinaweza kutungwa kwa madhumuni ya kugawa ardhi kwa matumizi mbalimbali na kutoa zuio na maagizo kwa usimamizi wa matumizi mbalimbali yaliyoainishwa, ili kulinda maliasili mbalimbali

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 35 7/26/2016 10:19:14 AM

Page 44: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

36

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini

kama vile maji, udongo na mimea (misitu). Sheria ndogo za vijiji ni muhimu katika maeneo yaliyo na migogoro mikubwa ya ardhi, ambapo makubaliano yaliyoidhinishwa na Mkutano wa Kijiji yanaweza kukiukwa na baadhi ya watu.

viii. Utaratibu wa Kutunga Sheria Ndogo za KijijiKulingana na Sheria ya Serikali za Mitaa Na.7 (1982) Kifungu cha 163 – 167 ufuatao ni muhtasari wa taratibu za kutunga Sheria Ndogo za Kijiji:-

• Halmashauri ya Kijiji inaweza kuanzisha utaratibu huu wakati inapoona kuwa kuna haja ya kujadili malengo na maudhui ya Sheria Ndogo. Kwa upande wa Sheria Ndogo zinazohusu matumizi ya ardhi ni vyema kuhusisha Kamati ya Usimamizi wa Ardhi, na Timu ya ‘PLUM’ ya wilaya ili kupata ushauri wa kiufundi.

• Halmashauri ya Kijiji huwaagiza viongozi wa vitongoji (wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji) na wajumbe wa Kamati ya Usimamizi wa Ardhi, kuandaa mikutano ya vitongoji au aina nyingine ya sehemu ya kijiji kwa majadiliano na wanakijiji, juu ya malengo na maudhui ya Sheria Ndogo.

• Viongozi wa vitongoji na/au Kamati ya Usimamizi wa Ardhi, hutoa ripoti ya matokeo ya mikutano midogo kwenye Halmashauri ya Kijiji. Halmashauri ya Kijiji pamoja na Kamati ya Usimamizi wa Ardhi, hutumia matokeo haya kutayarisha Rasimu ya Sheria Ndogo kwa msaada wa timu ya PLUM ya wilaya.

• Timu ya wilaya (PLUM) huwasilisha rasimu kwa Hakimu wa Wilaya au Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ili kuhakikisha kuwa maudhui hayakiuki au kugongana na sheria ndogo za wilaya na pia Sheria na Sera za Kitaifa.

• Hatimaye, Halmashauri ya Kijiji huwasilisha rasimu ya Sheria Ndogo kwenye Mkutano wa Kijiji kwa majadiliano na kuidhinishwa. Ni vyema kumkaribisha Ofisa Mtendaji Kata na Diwani kwenye mkutano huu.

• Sheria Ndogo pamoja na muhtasari wa Mkutano wa Kijiji hupelekwa kwenye Kamati ya Maendeleo ya Kata ambayo huhakikisha kuwa matakwa na masilahi ya vijiji vingine jirani yanalindwa.

• Ofisa Mtendaji wa Kata au Diwani wa Kata huipeleka Sheria Ndogo katika Halmashauri ya Wilaya kuidhinishwa na

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 36 7/26/2016 10:19:14 AM

Page 45: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

37

inapohitajika kusaidia utekelezaji wake. Wilaya hupeleka nakala ya Sheria Ndogo iliyotiwa sahihi na Mkurugenzi na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya kwenye Halmashauri ya Kijiji, ikionyesha tarehe ya kuanza kutumika kwake.

• Ni wajibu wa Halmashauri ya Kijiji kutangaza kwa wanakijiji uamuzi wa Halmashauri ya Wilaya. Hii inaweza kufanyika katika Mikutano ya Kijiji, na au vitongoji, ikisaidiwa na kuitangaza kwenye mikutano ya umma na hadhara nyinginezo.

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 37 7/26/2016 10:19:16 AM

Page 46: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

38

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini

3.2.5. HATUA YA TANO: UTAWALA WA ARDHI YA KIJIJI

Halmashauri ya Kijiji ni msimamizi wa ardhi ya kijiji kwa niaba ya wanakijiji kwa mujibu ya Sheria ya Ardhi ya Vijiji. Halmashauri ya Kijiji husimamia ujenzi wa Masijala ya Kijiji ambayo hutunza nyaraka zote zikiwemo nakala za Hati ya Hakimiliki za Kimila ambazo hugawiwa kwa kila mwenye ardhi katika kijiji mara baada ya mchakato wa matumizi ya ardhi kufikia mwisho. Utambuzi wa maeneo yaliyopangwa hufanyika katika hatua hii pamoja na kusimikwa kwa mabango yanayoonesha maeneo yaliyotambuliwa kwa ajili ya matumizi mbalimbali.

i. Hati ya Hakimiliki za KimilaKimsingi watu wana haki juu ya ardhi wanayoimiliki (Hakimiliki) na kutumia, ambayo wameipata kutokana na mila na desturi za eneo linalohusika kama vile; kurithi, kugawiwa na Halmashauri ya kijiji n.k. Haki hizi juu ya ardhi sasa zinaweza kurasimishwa kwa mujibu wa sheria kwa kuandaliwa hati ya kumiliki ardhi (Hatimiliki). Sheria ya Ardhi ya Vijiji (1999) vifungu 18-47 vinatoa mamlaka na wajibu kwa Halmashauri ya Kijiji kusimamia na kutoa Hatimiliki za Haki za Ardhi za Kimila na kuanzisha na kutunza Masijala ya Ardhi ya Kijiji.

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 38 7/26/2016 10:19:16 AM

Page 47: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

39

Ni muhimu kuzingatia kutatua migogoro mbalimbali ya ardhi, kabla ya kuanza utoaji na usajili wa Hatimiliki. Kwa mfano, si sahihi Halmashauri ya Kijiji kumilikisha na kutoa hatimiliki, katika eneo ambapo kijiji kina mgogoro wa mipaka na kijiji au mamlaka nyingine. Vilevile si, sahihi kutoa hati katika eneo ambalo linagombewa na watumiaji mbalimbali. Ni vyema migogoro ya namna hii kutatuliwa kwanza kama ilivyoelezwa katika hatua 3 – 4 za ‘PLUM’.

Kijiji chenye Mpango wa Matumizi ya Ardhi, kina fursa zaidi ya kushughulikia utoaji na usajili wa hatimiliki kwa wakazi wake. Kwa

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 39 7/26/2016 10:19:18 AM

Page 48: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

40

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini

mfano, masharti ya matumizi ya ardhi yanayopaswa kuwekwa kwenye hatimiliki, hutolewa kwa kufuata eneo linalohusika na lipo wapi katika mpango wa matumizi ya ardhi ya kijiji, badala ya kubuniwa tu, au kufuata jinsi anavyotaka mwombaji. Vilevile, haja na mahitaji (k.m. Masijala ya Ardhi ya Kijiji) ya utoaji na usajili wa hatimiliki za ardhi huwa tayari imeishabainishwa kama sehemu ya mchakato wa utekelezaji katika mpango kazi wa jamii (CAP), katika hatua ya 2 ya ‘PLUM’

ii. Taratibu za Kutoa Hati za Hakimiliki za KimilaTaratibu za utoaji na usimamizi wa hatimiliki za ardhi za kimila zimefafanuliwa kwa urahisi katika Mwongozo wa Kutoa Elimu ya Sheria ya Ardhi ya Vijiji. Katika Sheria ya Ardhi ya Vijiji, kifungu Na 18 - 20 vinafafanua maana ya Hatimiliki ya Haki ya Ardhi ya Kimila na utumikaji wake kisheria. Kifungu Na. 22 - 47 vinatoa maelezo ya kina kuhusu namna ya kuomba, kufikiria, kutoa na kusimamia Hatimiliki za Haki za Ardhi za Kimila.Kwa muhtasari, Sheria ya Ardhi ya Vijiji inabainisha taratibu zifuatazo katika kutoa hatimiliki za ardhi za kimila:-

• Mtu, familia au kundi la watu wanaweza kuomba hati ya haki ya ardhi ya kimila katika ardhi ya kijiji kwa Halmashauri ya kijiji kwa kujaza Fomu ya Ardhi ya Vijiji Na. 18 (Maombi ya Hatimiliki ya Kimila), ambayo imeambatishwa katika kitabu hiki. Wakati mwingine, inapobidi Halmashauri ya Kijiji inaweza kumtaka mwombaji kutoa maelezo ya ziada, kama vile kumiliki ardhi mahali pengine. Mwombaji anawajibika kulipia Fomu ya Maombi shilingi 500/= kwa Halmashauri ya Kijiji kwa kila hatimiliki (kila shamba/eneo la ardhi) kama ni mtu binafsi au familia, na shilingi 2500/= kama ni ushirika au taasisi.

• Mara maombi yanapoamriwa, mwombaji hupewa Barua Ahadi ya Toleo (Letter of Offer) iliyowekwa sahihi na Mwenyekiti wa Kijiji na Mtendaji wa Kijiji, ikionyesha masharti ya toleo.

• Mwombaji anapaswa, katika muda usiozidi siku tisini (90), akubali au akatae barua ya toleo na masharti (pamoja na malipo) kwa maandishi kwa Halmashauri ya Kijiji. Kukubali kufikiriwe tu baada ya malipo yote yanayohitajika kulipwa, ikiwemo shilingi 750/= za usajili na kodi ya pango la ardhi kama itakuwa imeamriwa hivyo na kijiji kinachohusika. Kwa kurahisisha utekelezaji, Fomu Na.19 ya Barua ya Ahadi ya Toleo imeandaliwa ikiunganishwa na Fomu Na.20 ya kukubali au kukataa ili kuweza kuweka Mkataba baina ya Mwombaji na Halmashauri ya Kijiji.

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 40 7/26/2016 10:19:18 AM

Page 49: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

41

• Halmashauri ya Kijiji, ndani ya siku tisini (90) baada ya kupokea kukubali kwa barua ya ahadi ya toleo; itatoa Hati ya Hakimiliki ya Kimila kwa mwombaji, kwa kutumia Fomu ya Ardhi Na.21, ambayo imeambatishwa katika kitabu hiki. Hati hii isainiwe na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kijiji na Ofisa Mtendaji wa Kijiji na kugongwa muhuri/lakiri wa Halmashauri ya Kijiji; isainiwe na mwombaji/waombaji na kubandikwa picha yake/zao; iwasilishwe na Ofisa Mtendaji wa Kijiji kwa Ofisa Ardhi wa Wilaya ili isainiwe, kuwekewa lakiri ya Wilaya na kusajiliwa; halafu irejeshwe kwa ajili ya kusajiliwa kijijini kabla ya mmiliki kupewa nakala ya hati yake.

iii. Masijala ya Ardhi ya Kijiji Kifungu cha 21 cha Sheria ya Ardhi ya Vijiji (1999), kinaelezea jinsi ya kuanzisha na kusimamia Masijala ya Ardhi ya Kijiji na Wilaya. Ili Halmashauri ya kijiji itoe na kusajili Hatimiliki ya Kimila, ni lazima ianzishe Masijala ya Ardhi ya Kijiji inayosimamiwa na Ofisa Mtendaji wa Kijiji (VEO). Ofisi ya VEO inaweza kupanuliwa au kukarabatiwa ili kuwa na chumba cha Masijala chenye hadhi na sifa ya kudumu. Kwa hiyo, pamoja na kuandaa mpango wa matumizi ya ardhi, ratiba ya utekelezaji wa mpango huo ihusishe na ujenzi wa masijala ya ardhi ya kijiji na wilaya kama sehemu ya mchakato wa utekelezaji wa mpango wa matumizi ya ardhi, ili kuwezesha usajili wa hatimiliki za ardhi kwa wamiliki.

Masijala ya ardhi ya kijiji na wilaya yasitumike kusajili hati ya hakimiliki ya kimila kwa ajili ya watu binafsi pekee, bali pia kusajili maeneo ya matumizi ya pamoja na ya jumuia kama vile;. maeneo ya huduma za jamii, maeneo ya malisho, misitu ya aina mbalimbali, vyanzo vya maji, hifadhi ya wanyama pori (WMAs), kilimo cha umwagiliaji n.k. kwa vikundi husika ili kulinda maeneo hayo yasivamiwe.

3.2.6. HATUA YA SITA: USIMAMIZI WA ARDHI YA KIJIJI

Katika hatua hii Halmashauri ya Kijiji inatakiwa kusimamia sheria ndogo za kijiji kwa kushirikiana na Kamati ya Usimamizi na Matumizi ya Ardhi.

i. UsimamiziBaada ya kupunguza kwa kiasi kikubwa vikwazo vikuu vya uboreshaji wa usimamizi wa matumizi ya ardhi (k.m. migogoro ya mipaka, matumizi, miliki n.k.) kama ilivyoelezwa katika hatua zilizopita; wanakijiji sasa wanakuwa katika nafasi nzuri ya kupanga na kutekeleza hatua stahili za usimamizi wa ardhi ili kuzuia uchakavu na uharibifu wa ardhi, kuongeza uzalishaji wake, na kuboresha hali zao za maisha.

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 41 7/26/2016 10:19:18 AM

Page 50: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

42

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini

Hatua mwafaka zinabainishwa na wanakijiji kwa msaada wa wataalamu (ugani) kwa kila matumizi ya ardhi, kama vile; uanzishaji na uendelezaji wa mashamba darasa ya mazao mbalimbali ya kilimo na mifugo, uboreshaji wa njia za kilimo cha umwagiliaji, uhifadhi wa misitu ya kijiji na vyanzo vya maji, mipango ya miundo mbinu ya msingi ili kuboresha hali katika maeneo ya makazi, n.k. Madhumuni ya kupanga hatua hizi ni:-

• Kubainisha na kubuni hatua kwa ajili ya uboreshaji wa usimamizi wa ardhi katika maeneo yaliyotengwa kwa uzalishaji mazao, ufugaji wa mifugo, misitu, matumizi ya makazi, huduma za jamii, umwagiliaji, wanyamapori n.k.

• Kuwezesha utekelezaji wa hatua zilizochaguliwa.

• Kujenga uwezo wa wanakijiji wa upangaji na utekelezaji wa hatua zilizochaguliwa, pamoja na urejeaji, ufuatiliaji na tathmini kwa kupata na kutoa mafunzo kwa Mafundi Sanifu wa Kijiji.

Katika kila eneo la matumizi ya ardhi, wataalamu huwawezesha wanakijiji kutathmini mbinu au hatua za kutumia katika usimamizi wa ardhi. Katika tathmini hii ni vyema kutambua kwanza tatizo lililopo dhahiri k.m. ukame, rutuba duni mashambani, makorongo n.k. Halafu kuangalia chanzo au sababu ya tatizo kama vile, ufyekaji miti, uhaba wa mvua, kilimo mfululizo, mmomonyoko wa udongo n.k. Baada ya kubaini tatizo na chanzo chake; kuangalia athari zake, yaani jinsi matatizo yanavyoathiri jamii na wakulima binafsi, kama vile, uhaba na uhafifu wa mazao, njaa, hali duni ya maisha n.k.

ii. Uimarishaji wa Vyombo vya Usimamizi wa Ardhi kijijiniKama shughuli za usimamizi shirikishi wa matumizi ya ardhi zitatekelezwa kwa ufanisi kijijini, itafikia hatua ambayo wanakijiji kwa kushirikiana na Timu ya Usimamizi wa Ardhi ya Kijiji/Kamati ya Maamuzi ya Kijiji wataweza kuendelea kwa kujitegemea wenyewe, bila msaada mkubwa wa timu ya PLUM kutoka Wilayani. Wanakijiji wanaweza kurejea na kutekeleza mipango yao, na kutafuta mtaalamu kila inapobidi; kwa kudumisha mawasiliano na timu ya PLUM ya wilaya. Hii inatoa fursa kwa timu ya PLUM kushughulikia vijiji vingine wilayani, na hata kutumia ujuzi na uzoefu wa vijiji ambavyo vimeishaanza utekelezaji, kama mafundi sanifu washauri wa vijiji jirani.

Vilevile ni jukumu la Timu ya ‘PLUM’ ngazi ya Wilaya kuijengea uwezo Halmashauri ya Kijiji na Timu ya Usimamizi wa Ardhi ya Kijiji/Kamati ya

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 42 7/26/2016 10:19:19 AM

Page 51: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

43

Maamuzi ya Kijiji kwa utaratibu wa kutoa mafunzo elekezi ya mara kwa mara kwa ajili ya kuwakumbusha majukumu yao wakati wa kusimamia utekelezaji wa mpango wa matumizi ya ardhi ya Kijiji.

Kimsingi Hatua ya 5-6 za ‘PLUM’, ni za kudumu kijijini, kwani siku zote hatua za utawala wa ardhi na utekelezaji wa hatua stahili za usimamizi wa ardhi zitaendelea. Utoaji na usajili wa hati ya hakimiliki za ardhi utaendelea kwa wamiliki wapya, au yanapotokea mabadiliko ya wamiliki kutokana na kurithi, mauzo, kugawana n.k. Aidha maendeleo ya teknolojia na mbinu mpya za kilimo, ufugaji, misitu, ujenzi wa makazi n.k. unaweza kuanzisha hatua stahili mbadala za usimamizi wa ardhi.

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 43 7/26/2016 10:19:21 AM

Page 52: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

44

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini

4.0. HITIMISHOSura zote ndani ya kitabu hiki zimesisitiza kuwa muhimili mkuu wa uandaaji wa mpango wa matumizi ya ardhi ya kijiji wenye ufanisi ni ushiriki wa wananchi wenyewe hatua kwa hatua. Mpango wa matumizi ya ardhi katika kijiji hautakuwa na tija endapo wananchi hawatakuwa sehemu ya utekelezaji wa mpango wenyewe. Mada imeonesha jinsi ambavyo mpango wa matumizi ya ardhi ya kijiji unavyoweza kutoa suluhu kwa matatizo sugu ya migogoro ya mipaka baina ya wanavijiji, kukabiliana na uharibifu wa mazingira na hata kuchangia katika jitihada za kukabili athari za mabadiliko ya tabia nchi. Ni vema wananchi wakajitokeza kuwa sehemu ya huu uamuzi wa msingi kuhusiana na ardhi wanayoitegemea kwa maisha yao.

Hata Sheria ya Ardhi ya Vijiji (1999) imelenga kutekeleza misingi ya Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995 inayoelekeza, pamoja na mambo mengine, kwamba upangaji wa matumizi ya ardhi ufanyike kwa mfumo wa ushirikishwaji kwa kuwahusisha walengwa. Ndiyo maana basi, kifungu cha 8 cha Sheria ya Ardhi ya Vijiji, kinatoa mamlaka kwa Halmashauri ya Kijiji kusimamia utawala wa ardhi ya kijiji na vifungu vya 12 na 13 vinavyoelekeza jinsi ya kupanga ardhi ya kijiji. Ni makusudi ya kitabu hiki kuweka bayana juu ya mamlaka haya na jinsi gani wanakijiji wayatumie kwa mujibu wa sheria; ili kupunguza au kuepusha migogoro ya ardhi na kuitumia ardhi inavyostahili kuboresha hali ya maisha yetu na vizazi vijavyo.

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 44 7/26/2016 10:19:21 AM

Page 53: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

45

5.0. VIAMBATISHO

5.1. CHETI CHA ARDHI YA KIJIJI

Fomu ya Ardhi ya Vijiji Na.16

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SHERIA YA ARDHI YA VIJIJI,1999

(Na.5 ya 1999)

CHETI CHA ARDHI YA KIJIJI

(Chini ya Kifungu la 7)

Kumb. Na. …………….

Leo tarehe …………………….ya mwezi ………...……….mwaka 20……

Hii ni kuthibitisha kuwa Halmashauri ya Kijiji (humu ikirejewa kama “Halmashauri”) cha …………………katika Wilaya ya …………………… inakabidhiwa kama mdhamini usimamizi wa ardhi yote iliyoelezwa katika jedwali lililoambatishwa (humu) ikielezwa kama “ardhi ya kijiji”) kadri ya nia na maana halisi ya Sheria ya Ardhi ya Vijiji na kwa masharti yafuatayo:-

Halmashauri itasimamia ardhi ya kijiji kadri ya sheria za mila zinazohusu ardhi kwenye eneo husika;

Halmashauri italinda mazingira kwa kuhifadhi rutuba ya ardhi na kuzuia mmomonyoko wa udongo;

Halmashauri italinda haki za njia;

Halmashauri italinda na kutunza mipaka ya kijiji;

Halmashauri itatunza na kuhifadhi kwa usalama cheti hiki;

Endapo mipaka ya kijiji imebadilishwa au kurekebishwa, Halmashauri itatuma cheti kwa Kamishna ili kuidhinisha mabadiliko au marekebisho ya mipaka kwenye cheti;

Halmashauri itatoa hati ya hakimiliki ya kimila na kutunza daftari la ardhi ya kijiji.

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 45 7/26/2016 10:19:21 AM

Page 54: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

46

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini

JEDWALI

(Maelezo kamili ya ardhi na mipaka ya jumla, ikiwemo mchoro wa mipaka)

MCHORO WA MIPAKA

Eneo lote lijulikanalo kama Kijiji cha...............................katika Wilaya ya....................lenye ukubwa wa...................................... kama mipaka inavyooneshwa kwa wino katika ramani/mchoro ulioambatishwa hapa.

IMETOLEWA na Rais na imekabidhiwa kwa MKONO wangu na LAKIRI rasmi kuwekwa siku na mwaka vilivyoandaliwa hapo juu.

………………….……………………………

Kamishna wa Ardhi

IMEWEKEWA LAKIRI halisi ya Halmashauri ya Kijiji cha ……………………mbele yetu:

1. Jina: ………………………………………………………………….

Saini: …………………………………………………………….

Cheo: Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kijiji..

Anwani ………………………………………….………………LAKIRI/MUHURI

2. Jina: ……………………………………………………………………

Saini: ………………………………………………………………………

Cheo: Katibu (VEO) wa Halmashauri ya Kijiji

Anwani: ……………………………………………………………………

ADA (kama ipo)

Nakala: Msajili (Masijala ya Ardhi ya Wilaya).

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 46 7/26/2016 10:19:21 AM

Page 55: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

47

5.2. FOMU YA MAOMBI YA HATI YA KIMILA

Fomu ya Ardhi ya Vijiji Na.18

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SHERIA YA ARDHI YA VIJIJI,1999

(Na.5 ya 1999)

OMBI LA HATIMILIKI YA KIMILA

(Chini ya Kifungu Na 22)

SEHEMU YA 1: (Ijazwe na mwombaji/waombaji)

Jina la Mwombaji*:

Jina/Majina Kamili ya Mwombaji/Waombaji: (Jina la familia kwanza)

.……………………………………………………………………………

Jinsi/Umri:……………………………………………………………………..

Jinsi/Umri: ……………………………………………………………………

(Ongeza itakavyolazimu)

*Je, maombi ni ya wanandoa ? (Ndiyo/Hapana)

Majina kamili ya wanafamilia inayoomba (Jina la familia kwanza).

……………………………………………………………………………

Jinsi/Umri: ………………………………………………………………………

Jinsi/Umri: ………………………………………………………………………

(Ongeza itakavyolazimu)

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 47 7/26/2016 10:19:21 AM

Page 56: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

48

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini

(Angalau wanafamilia wawili wawasilishe maombi).

Jina la chombo au taasisi inayoleta maombi.

……………………………………………………………………………

Jinsi/Umri………………………………………………………………………

Jina la Chombo au Taasisi inayowasilisha maombi: ……………………………………………………………………………………

*Jaza kifungu kinachoendana na ombi lako

Anwani (kama kwa kawaida si mkazi kijijini/mahali ndani ya kijiji).

………………………………………………………………………………

Uraia: …………………………………………………………………………….

Kuoa/kuolewa (inahusika na kifungu A na B hapo juu).

Watoto na miaka (inahusika na kifungu A na B hapo juu)

………………………………………………………………………………………

*Ongeza karatasi zaidi inavyohitajika.

Mahali ilipo ardhi inayoombwa:

Kitongoji: …………………………………………………………………..

Kijiji: ………………………………………………………………………………….

Wilaya: ………………………………………………………………………………..

Wastani wa eneo la ardhi: ………………………………………………………

Matumizi ya ardhi kwa sasa hivi (kama vile kilimo, ufugaji, makazi)

………………………………………………………………………………………

Matumizi yanayopendekezwa au yanayokusudiwa katika ardhi (kama ni tofauti na inavyotumiwa hivi sasa)

………………………………………………………………………………………

Mfumo wa umiliki kwa pamoja

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 48 7/26/2016 10:19:21 AM

Page 57: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

49

Umiliki wa pamoja..........................................................

Umiliki wa pamoja na mgawanyo wa hisa

Jina..............Hisa....................................

Jina..............Hisa....................................

Jina..............Hisa....................................

Saini/kidole gumba cha mwombaji/waombaji

Jina..............................saini/dole gumba...................................

Jina..............................saini/dole gumba....................................

Jina..............................saini dole gumba....................................

Angalau wanafamilia wawili, viongozi wawili wa kijadi, ua maofisa wateule wawili wa chombo, lazima waweke saini kwenye ombi.

Jina..............................saini/dole gumba...................................

Jina..............................saini/dole gumba....................................

Endapo maombi yanawasilishwa na mtu/watu ambao kwa kawaida si wakazi wa kijiji ombi liwekwe saini na WANAKIJIJI WATANO.

Saini/dole gumba za wanakijiji watano (inapolazimu).

Tarehe ya ombi ………………………………………………………………………

SEHEMU YA PILI: (Kwa matumizi ya ofisi tu)

Maoni na mapendekezo ya Halmashauri ya Kijiji*/Halmashauri ya Wilaya*:

(*Futa isiyohusika)

…………………………………………………………………………………………

Majina na Saini za Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji:

……………………………………………………tarehe ………………………

……………………………………………………tarehe ………………………

……………………………………………………tarehe ………………………

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 49 7/26/2016 10:19:21 AM

Page 58: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

50

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini

5.3. HATI YA HAKI MILIKI YA KIMILA

Fomu ya Ardhi ya Vijiji Na.21

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SHERIA YA ARDHI YA VIJIJI,1999

(Na.5 ya 1999)

HATI YA HAKIMILIKI YA KIMILA

(Chini ya Kifungu Na 25)

Hati ya Kijiji Na. ………………………

Leo tarehe ……………………mwezi ………………........… mwaka 20…......

Hii ni kuthibitisha kwamba Halmashauri ya Kijiji cha …………………………… (taja jina na anwani ya Halmashauri ya Kijiji) imetoa kwa …………………………………. (jina la mkazi) (humu ndani akirejewa kama “Mkazi”) hatimiliki ya kimila (itaitwa “hatimiliki”) juu ya ardhi iliyofafanuliwa katika Jedwali (humu ndani itaitwa “ardhi”) kwa kipindi kisicho na kikomo*/99*/ kwa miaka ………… tangu ……………. tarehe…..……… mwezi ………………. mwaka 20……………. kwa madhumuni na tafsiri halisi ya Sheria ya Ardhi ya Vijiji na kwa kuzingatia vipengele vyake na kanuni zozote zinazotungwa chini ya sheria hiyo au sheria mbadala au marekebisho yake na kwa mujibu wa masharti yafuatayo:

*Futa isiyohusika

Mkazi/Wakazi watalipa kodi ya mwaka ya Shs. ……………… kabla ya tarehe ………………… ya mwezi kila mwaka (kama inahusika).

Ardhi itatumika kwa ajili ya ……………………………………………………..

Mkazi/Wakazi watawajibika kuhifadhi mazingira (ardhi na maji).

Mkazi/Wakazi watahakikisha kwamba mipaka ya ardhi inalindwa na kutunzwa na idumu kuwa bayana kwa kipindi chote cha hakimiliki.

Mkazi/Wakazi wataheshimu na kuhifadhi haki za njia zilizopo.

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 50 7/26/2016 10:19:21 AM

Page 59: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

51

Uwakilishi wa hakimiliki kwa mtu au kikundi chochote cha watu ambao kwa kawaida si wakazi wa kijiji lazima uidhinishwe na Halmashauri ya Kijiji.

JEDWALI

(Maelezo kamili ya eneo na mipaka yake)

Mchoro wa mipaka

Jina ……………………………... Lakiri/Muhuri wa Halmashauri ya Kijiji

Saini …………………………….

Anwani.......................................

Wadhifa: Mwenyekiti wa Kijiji

Jina ………………………………….

Saini …………………………………

Anwani.......................................

Wadhifa: Katibu (VEO) wa Kijiji

Mmiliki (Mkazi)

PICHA

Jina Saini /Kidole gumba la mkazi

..................................... ..............................................

..................................... .............................................

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 51 7/26/2016 10:19:22 AM

Page 60: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

52

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini

..................................... ..............................................

Imegongwa lakiri ya halmashauri ya wilaya............. na kusainiwa na leo tarehe.................... mwezi........................ mwaka 20..............

LAKIRI

Jina ................................................................

Saini ..............................................................

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 52 7/26/2016 10:19:22 AM

Page 61: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

53

Wadhifa: Ofisa Ardhi wa Wilaya

6.0. MAREJEO

1. Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995/972. Sera ya Maendeleo ya Makazi ya mwaka 20003. Sheria ya Ardhi Na. 4 ya mwaka 1999 4. Sheria ya Ardhi ya Vijiji (Mipango na Matumizi) Na. 14 ya mwaka

1973 5. Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na. 5 ya mwaka 19996. Kanuni za Ardhi ya Vijiji, 20027. Sheria ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Na. 6 ya mwaka 20078. Sheria ya Misitu Na. 14 ya mwaka 20029. Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Na. 7 ya mwaka

198210. Sheria ya Uanzishwaji wa Milki za Vijiji Na. 22 ya mwaka 1992 11. Sheria ya Vijiji na Vijiji vya Ujamaa (Usajili, Uundwaji na

Usimamizi) Na. 21 ya mwaka 1975.12. NLUPC (2010); Kiongozi cha Mwanakijiji katika Ushirikishwaji wa

Mipango na Usimamizi wa Matumizi bora ya Ardhi Vijijini, Toleo la 2, Dar es Salaam

13. NLUPC (2010); Kiongozi cha Mwanakijiji katika Ushirikishwaji wa Mipango na Usimamizi wa Matumizi bora ya Ardhi Vijijini, Toleo la 3, Dar es Salaam

14. PELUM (2012); Haki ya kupata, kumiliki na kutumia ardhi Tanzania: Kitini cha Mwanakijiji

15. HAKIARDHI (2013); Mwongozo wa Mafunzo Juu ya Sheria za Ardhi na Utawala katika Muundo wa Serikali za Mitaa; Ecoprint Limited, Dar es Salaam

16. Mwongozo wa Usimamizi Shirikishi wa Matumizi ya Ardhi ya Vijiji nchini Tanzania (1998) na mabadiliko yake ya 2010.

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 53 7/26/2016 10:19:22 AM

Page 62: Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 1 7/26/2016 10 ...pelumtanzania.org/wp-content/uploads/2018/06/Mpango-wa-Matumizi-ya... · v. Aina za Matumizi ya Ardhi kwenye Ngazi ya Kijiji

PELUM TanzaniaS.L.P 390, Morogoro-Tanzania

Simu/Nukushi: +255 23 2613677Barua pepe: [email protected]

Tovuti: www.pelumtanzania.org

Mpango wa Matumizi ya Ardhi Kijijini.indd 54 7/26/2016 10:19:22 AM