2
AFYA, MABADILIKO YA MAZINGIRA NA UWEZO WA KUREKEBISHA: KUCHUNGUZA NA KUTAZAMIA HATARI ZA SIKU ZA BAADAYE KUTOKANA NA MAGONJWA YA VEKTA YANAYOHUSIANA NA MAJI AFRIKA MASHARIKI WASHIRIKI WASHIRIKI WALIYO AFRIKA MASHARIKI • Chuo kikuu cha Nairobi, Kenya • Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo, Kenya • Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Rwanda, Rwanda • Taasisi ya Mazingira ya Stockholm, Tanzania • Wizara ya Afya, Uganda • Tasisi ya Utafiti wa Matibabu, Kenya • Wizara ya Afya, Rwanda WASHIRIKI WALIYO ULAYA • Chuo Kikuu cha Trinity, Dublin Ireland – Mratibu • Kituo cha kimataifa cha Fizikia Nadharia cha Abdus Salam, Italy • Chuo Kikuu Paris Lodron cha Salzburg, Austria • Tasisi ya metorolojia na Hydrolojia, Sweden • AquaTT, Ireland • Chuo Kikuu cha Durham, United Kingdom • Chuo Kikuu cha Liverpool, United Kingdom WASHIRIKI WA AFRIKA KUSINI • Chuo Kikuu cha Cape Town, South Africa WASHIRIKI WA KUSINI MASHARIKI MWA ASIA • Chuo Kikuu cha Singapore, Singapore WASILIANA NASI Mratibu wa kisayansi wa mradi Prof David Taylor Idara ya Geografia Chuo Kikuu cha Singapore, Singapore Anwani ya barua pepe: [email protected] Nambari ya Simu: +65 65 16 7394 Msimamizi wa mradi Paul Lowen AquaTT P.O. Box 8989 Dublin 2 Ireland Anwani ya barua pepe: [email protected] Nambari ya simu: +353 1 475 8713 Ama tembelea tovuti ya mradi wetu www.healthyfutures.eu Kanusho Utafiti wa mradi huu umefadhiliwa na programu ya ‘Seventh Framework’ (FP7/2007-2013), chini ya makubaliano ya hazina nambari 266327. Chapisho hili linawakilisha maoni ya mwandishi pekee na Muungano wa Ulaya hauwezi kulaumiwa kutokana na matumizi ya taarifa zilizomo. Limebuniwa na kuendelezwa na AquaTT ENEO LINALOFANYIWA UTAFITI

healthy futures...• Wizara ya Afya, Uganda • Tasisi ya Utafiti wa Matibabu, Kenya • Wizara ya Afya, Rwanda ... dau na jumuia ya watunga sera na wanasayansi ulimwenguni ... Tofauti

  • Upload
    others

  • View
    16

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

AFYA, MABADILIKO YA MAZINGIRA NA UWEZO WA KUREKEBISHA: KUCHUNGUZA NA KUTAZAMIA HATARI ZA SIKU ZA BAADAYE KUTOKANA NA MAGONJWA YA VEKTA YANAYOHUSIANA NA MAJI AFRIKA MASHARIKI

WASHIRIKI WASHIRIKI WALIYO AFRIKA MASHARIKI • Chuo kikuu cha Nairobi, Kenya • Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo, Kenya• Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Rwanda, Rwanda• Taasisi ya Mazingira ya Stockholm, Tanzania • Wizara ya Afya, Uganda• Tasisi ya Utafiti wa Matibabu, Kenya • Wizara ya Afya, RwandaWASHIRIKI WALIYO ULAYA • Chuo Kikuu cha Trinity, Dublin Ireland – Mratibu• Kituo cha kimataifa cha Fizikia Nadharia cha

Abdus Salam, Italy • Chuo Kikuu Paris Lodron cha Salzburg, Austria • Tasisi ya metorolojia na Hydrolojia, Sweden • AquaTT, Ireland • Chuo Kikuu cha Durham, United Kingdom• Chuo Kikuu cha Liverpool, United Kingdom

WASHIRIKI WA AFRIKA KUSINI • Chuo Kikuu cha Cape Town, South Africa

WASHIRIKI WA KUSINI MASHARIKI MWA ASIA• Chuo Kikuu cha Singapore, Singapore

WASILIANA NASI Mratibu wa kisayansi wa mradiProf David TaylorIdara ya GeografiaChuo Kikuu cha Singapore,SingaporeAnwani ya barua pepe: [email protected] ya Simu: +65 65 16 7394

Msimamizi wa mradiPaul LowenAquaTTP.O. Box 8989 Dublin 2 IrelandAnwani ya barua pepe: [email protected] Nambari ya simu: +353 1 475 8713

Ama tembelea tovuti ya mradi wetu

www.healthyfutures.euKanushoUtafiti wa mradi huu umefadhiliwa na programu ya ‘Seventh Framework’ (FP7/2007-2013), chini ya makubaliano ya hazina nambari 266327. Chapisho hili linawakilisha maoni ya mwandishi pekee na Muungano wa Ulaya hauwezi kulaumiwa kutokana na matumizi ya taarifa zilizomo.

Lim

ebun

iwa

na k

uend

elez

wa

na A

quaT

T

ENEO LINALOFANYIWA UTAFITI

MRADI WA AFYA BORA YA BAADAYE ni mradi wa kimataifa wa ushirikiano katika utafiti unaokusudia kuchangia katika kupunguza madhara ya siku zijazo yanayosababishwa na magonjwa matatu ya maji, VBDs (Malaria, homa ya bonde la ufa na kichocho) katika Afrika mashariki (Burundi, Kenya, Rwanda, Uganda na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania). Mradi huu umefadhiliwa kupitia sehemu ya mazingira na afya ya jumuia ya Ulaya, programu ya ‘Seventh Framework’ na unahusisha washiriki kadhaa katika Afrika mashariki.NI NINI HASA MOTISHA WA MRADI WA AFYA BORA YA BAADAYE?Hali ya mazingira inavyoendelea kubadilika, ikiwewemo hali katika tabia ya nchi, ndivyo inaweza kusababisha kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza katika sehemu mbalimbali. Jambo hili linaweza kusababisha magonjwa katika watu wenye kinga ndogo na kwa wale ambao hawana kinga yeyote. Hali hii huweza kuwa tatizo kubwa sana kwa afya ya jamii au afya ya mifugo. Matokeo ya magonjwa yatalingana na sababu kadhaa ambazo zinauhusiano, kama vile:• viwango vya kinga mwilini,• programu za kufaa za kuzuia magonjwa,• uwezo wa huduma za afya ya jamii na ile ya

wanyama kuitikia maonyo ya mlipuko wa magonjwa,• mitindo ya wakati ujao ya uongezeko wa watu na

uamaji wa watu kutoka sehemu za mashabani hadi mijini.

Azimio likiwa kwamba kila mwaka karibu vifo milioni 2.4 vinavyotokana na hali ya mazingira vinaweza kuepukwa, na kwamba athari za mabadiliko ya mazingira, kama vile mabadiliko ya tabia ya nchi, yataathiri zaidi wale waliokumbwa vikali na umaskini katika jamii, MRADI WA AFYA BORA YA BAADAYE unajitahidi kuelewa zaidi uhusiano ulioko kati ya mazingira na afya Afrika mashariki. Kueleweka kwa uhusiano ulioko kati ya tabia ya nchi, mabadiliko katika jamii na afya kunaweza kuwezesha ubashiri wa athari kwa afya na gharama inayotokana na mabadiliko ya tabia ya nchi na pia kuchangia katika kutambua hasa athari zitakazotokana na mabadiliko ya mazingira.

MADHUMUNI YA MRADIMRADI WA AFYA BORA YA BAADAYE unalenga:1) Kujenga uhusiano kati ya watafiti na mashirika

ya Ulaya na Afrika katika nyanja za mabadiliko ya mazingira, afya ya jamii na afya ya wanyama

2) Kupata maelezo ya jumla na maarifa ya kihistoria, hali ya kijamii, kiuchumi na mazingira kuhusu magonjwa yale matatu yanayolengwa na mradi huu (3 VBDs)

3) Kuunda mifumo itakayowezesha kugundua uwezekano wa kuzuka kwa magonjwa na yenye kuonyesha maeneo yanayoweza kukumbwa na magonjwa haya, vikiwemo vyombo vitakavyowezesha kutazamia na kuitikia maonyo dhidi ya kuzuka kwa magonjwa

4) Kuunganisha na kutoa maarifa kwa washika dau na jumuia ya watunga sera na wanasayansi ulimwenguni

KWA NINI ENEO HILI LILICHAGULIWA?Athari na kusambaa kwa magonjwa ya vekta yanayohusiana na maji (VBDs) kuna vuka mipaka ya nchi mbalimbali. Kwa hivyo ili kuweza kukabiliana na athari za kiafya na kiuchumi zinazosababishwa na mabadiliko ya mazingira, mikakati ya kufanya kazi pamoja (nchini na ulimwenguni) inafaa kuweko. Sababu ya kuchagua Afrika Mashariki kama eneo la utafiti kunadhibitisha kwamba maeneo yote katika jamii-yakiwemo mashirika ya kimataifa kama vile Muungano wa Afrika Mashariki (EAC) – yako tayari kuwezesha kutekeleza matokeo ya utafiti na kuongezea kuelewa utafiti wa kisayansi uliofanywa.Baadhi ya maeneo yaliyoinuka (kutoka usawa wa bahari) na yaliyoko mbali au karibu na ikweta yaliyo na uhusiano na mabadiliko ya mazingira, yakiwemo maeneo makubwa ya milimani na ya nyanda za chini za pwani, hata sehemu zenye hali ya unyevunyevu unaotofautiana, zenye unyevunyevu mwingi na zile zenye ukavu, zinashughulikiwa katika eneo la utafiti huu. Tena, maeneo makubwa ya maji baridi pamoja na sehemu kubwa za unyevunyevu, ambazo hivi sasa zinatumiwa kukuza vyakula, pia zinashughulikiwa na mradi huu. Tofauti hii ya mazingira inalingana na tofauti ya watu wenye lugha, dini, utamaduni na makaazi mbalimbali. Aidha utumizi wa ardhi pamoja na maeneo ya ardhi unaendelea kubadilika kutokana na ongezeko la idadi ya watu na maendeleo katika uchumi.

Hata kama MRADI WA AFYA BORA YA BAADAYE unaangazia Afrika Mashariki kama eneo lake la utafiti, mbinu iliyochukuliwa na matokeo ya utafiti yanatarajiwa kuweza kutumika sehemu zisizokuwa katika eneo linalotafitiwa.MRADI WA AFYA BORA YA BAADAYE UNATARAJIWA KUWA NA MATOKEO GANI?MRADI WA AFYA BORA YA BAADAYE unatarajiwa kuwa na matokeo haya yanayohusiana na magonjwa matatu ya vekta (VBDs) katika eneo la utafiti:1) Kuwa na data za mazingira na za magonjwa

zinazoweza kupatikana kwa urahisi, data ambazo zimepangwa kwa utaratibu na zenye kueleweka

2) Kuboresha kuelewa muungano ulioko kati ya mazingira (ikiwemo tabia ya nchi) na magonjwa

3) Kuwezesha kuonyesha mitindo ya magonjwa4) Kuonyesha na kukadiri tofauti iliyoko ya hatari

inayoweza kusababisha magonjwa na athari zingine5) Kuimarisha mifumo ya kutoa onyo mapema

kuhusu magonjwa6) Kuwezesha kutekelezwa, kama ifaavyo, kwa sera

zinazoangazia mabadiliko ya tabia ya nchi na afya katika eneo linalotafitiwa

7) Kuongezea uwezo katika eneo linalofanyiwa utafiti kwa kutoa nafasi zilizofadhiliwa kwa masomo ya uzamili kwa njia ya utafiti

8) Kuwa na machapisho katika majarida ya hali ya juu ya kisayansi