67
1 HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA, MAJI NA NISHATI MHESHIMIWA SALAMA ABOUD TALIB (MBM) KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA WA FEDHA 2020/2021 KATIKA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR UTANGULIZI 1. Mheshimiwa Spika, kwa ruhusa yako, naomba kutoa hoja kwamba Baraza lako Tukufu sasa likae kama Kamati ya Matumizi ili niweze kutoa maelezo kuhusu shabaha na malengo yaliomo katika Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021. 2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote, naomba nichukuwe nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu (S.W) kwa kutujaalia afya njema na uzima na kwa kuniwezesha kuwasilisha hotuba ya Wizara hii mbele ya Baraza lako Tukufu. 3. Mheshimiwa Spika, vilevile, naomba kuchukuwa fursa hii kutoa shukurani za dhati kwa Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dokta Ali Mohamed Shein pamoja na Mheshimiwa Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi kwa kuendelea kutupa miongozo, ushauri na nasaha katika kuhakikisha kwamba Wizara ninayoiongoza inatoa huduma za msingi kwa Wananchi kwa ufanisi na wakati muafaka. 4. Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee napenda kukupongeza kwa dhati wewe binafsi pamoja na wasaidizi wako kwa busara na hekima unayotumia kwa kuliongoza Baraza hili, namuomba Mwenyezi Mungu akuzidishie moyo huo. 5. Mheshimiwa Spika, naomba pia nimshukuru Mheshimiwa Hamza Hassan Juma Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano pamoja na Wajumbe wake kwa mashirikiano ya pamoja katika kufanikisha kazi za Wizara yangu.

HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA, MAJI NA NISHATI ......HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA, MAJI NA NISHATI MHESHIMIWA SALAMA ABOUD TALIB (MBM) KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI

  • Upload
    others

  • View
    10

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

  • 1

    HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA, MAJI NA NISHATI

    MHESHIMIWA SALAMA ABOUD TALIB (MBM) KUHUSU MAKADIRIO

    YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA WA FEDHA 2020/2021

    KATIKA BARAZA LA WAWAKILISHI

    ZANZIBAR

    UTANGULIZI

    1. Mheshimiwa Spika, kwa ruhusa yako, naomba kutoa hoja kwamba Baraza lako Tukufu sasa

    likae kama Kamati ya Matumizi ili niweze kutoa maelezo kuhusu shabaha na malengo

    yaliomo katika Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na

    Nishati kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021.

    2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote, naomba nichukuwe nafasi hii kumshukuru Mwenyezi

    Mungu (S.W) kwa kutujaalia afya njema na uzima na kwa kuniwezesha kuwasilisha hotuba

    ya Wizara hii mbele ya Baraza lako Tukufu.

    3. Mheshimiwa Spika, vilevile, naomba kuchukuwa fursa hii kutoa shukurani za dhati kwa

    Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dokta Ali Mohamed

    Shein pamoja na Mheshimiwa Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi kwa kuendelea

    kutupa miongozo, ushauri na nasaha katika kuhakikisha kwamba Wizara ninayoiongoza

    inatoa huduma za msingi kwa Wananchi kwa ufanisi na wakati muafaka.

    4. Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee napenda kukupongeza kwa dhati wewe binafsi

    pamoja na wasaidizi wako kwa busara na hekima unayotumia kwa kuliongoza Baraza hili,

    namuomba Mwenyezi Mungu akuzidishie moyo huo.

    5. Mheshimiwa Spika, naomba pia nimshukuru Mheshimiwa Hamza Hassan Juma

    Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano pamoja na Wajumbe wake kwa

    mashirikiano ya pamoja katika kufanikisha kazi za Wizara yangu.

  • 2

    6. Mheshimiwa Spika, naomba sasa uniruhusu kuelezea utekelezaji wa kazi za Kawaida na za

    Maendeleo kwa kipindi cha Mwaka wa Fedha 2019/2020 na muelekeo kwa Mwaka wa

    Fedha 2020/2021.

    MAPATO NA MATUMIZI

    7. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu katika Mwaka wa Fedha 2019/2020 ilipangiwa

    kukusanya jumla ya TZS Bilioni 9.445 kutokana na vyanzo mbali mbali vya Taasisi zake.

    Hadi kufikia tarehe 31 Machi 2020 jumla ya TZS Bilioni 6.735 zimekusanywa. Kiwango

    hichi ni sawa na asilimia 71.3 ya makadirio.

    Kwa ufafanuzi zaidi naomba angalia kiambatisho “A”.

    8. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa matumizi ya Mwaka wa Fedha 2019/2020, Wizara

    yangu imepangiwa kutumia jumla ya TZS Bilioni 156.582. Kati ya Fedha hizo, TZS Bilioni

    12.505 ni kwa ajili ya kazi za kawaida na mishahara na TZS Bilioni 144.077 kwa kazi za

    maendeleo. Hadi kufikia tarehe 31 Machi 2020 Wizara yangu ilikwishapatiwa TZS Bilioni

    9.334 kwa kazi za kawaida na mishahara ambazo ni sawa na asilimia 74 na TZS Bilioni

    19.592 kwa kazi za Maendeleo sawa na asilimia 13.6 ya makadirio. Hivyo kufanya jumla ya

    fedha zote tulizozipata kuwa ni TZS Bilioni 28.927 sawa na asilimia 18 ya makadirio.

    Kwa ufafanuzi zaidi angalia kiambatisho“B1 na B2 ”

    9. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa utekelezaji wa shughuli za Wizara, kwa Mwaka wa

    Fedha 2019/2020 Wizara yangu ilifanikiwa kutekeleza majukumu yake kupitia Programu kuu

    tatu zifuatazo:

    Programu PN0101: Uendeshaji na Uratibu wa Wizara ya Ardhi.

    Programu PN0102: Usimamizi wa Ardhi na Makaazi

    Programu PN0105: Usimamizi wa Huduma za Maji na Nishati.

    PROGRAMU KUU PN0101: UENDESHAJI NA URATIBU WA WIZARA YA ARDHI

    10. Mheshimiwa Spika, Programu hii ina jukumu la uratibu katika utekelezaji wa kazi za

    Wizara na inajumuisha Programu ndogo tatu ambazo zinatekelezwa na Idara ya Mipango,

  • 3

    Sera na Utafiti, Idara ya Utumishi na Uendeshaji, na Afisi Kuu Pemba ambapo kwa kipindi

    cha Mwaka wa Fedha 2019/ 2020 utekelezaji wa huduma za Programu hii ulikuwa kama

    ifuatavyo: -

    PROGRAMU NDOGO YA URATIBU WA MIPANGO, SERA NA TAFITI ZA

    WIZARA.

    11. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2019/2020 utekelezaji wa Programu hii ndogo

    ulilenga kutekeleza shughuli za kuratibu/ kuandaa Mipango na Miongozo ya Kisera ya

    utekelezaji wa kazi za Wizara, kuratibu uandaaji na mapitio ya Sheria zilizochini ya Wizara,

    kuratibu, kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa Programu na miradi ya Wizara pamoja na

    kuendeleza tafiti kwa ajili ya kuimarisha utoaji wa huduma katika Sekta za Wizara.

    12. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi wa Machi 2020 Idara ya Mipango, Sera na Utafiti

    imefanikiwa kutekeleza mambo yafuatayo:

    i. Ufuatiliaji na Kutathmini Miradi ya Maendeleo

    Idara imesimamia Uratibu na Utekelezaji wa Miradi ya maendeleo ya Wizara kwa kufanya

    kazi za Ufuatiliaji na Tathmini ya Utekelezaji (Monitoring and Evaluation) kwa lengo la

    kuhakikisha kwamba miradi hiyo inatekelezwa kwa ufanisi na kufikia malengo

    yaliyokusudiwa. Miradi iliyosimamiwa Kiuratibu na Ufuatiliaji na Idara hii ni kama

    ifuatavyo:

    a) Usambazaji Umeme Vijijini.

    b) Uimarishaji wa Miundombinu ya Umeme na Kulijengea Uwezo Shirika

    (NORAD)

    c) Uendelezaji wa visima vya Ras al- khaimah

    d) Maji Safi na Usafi wa Mazingira wa Mkoa wa Mjini Magharibi (ADF 12).

    e) Uimarishaji wa Miundombinu ya Maji Mkoa wa Mjini Magharibi (JICA)

    f) Uhuishaji wa Mfumo wa Usambazaji Maji Zanzibar (INDIA)

    g) Uhuishaji wa Huduma za Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira – Miji 25

    (INDIA)

    h) Uchimbaji wa Visima na Usambazaji Maji - Bandamaji (CHINA).

  • 4

    i) Utekelezaji wa Sera ya Nishati (SIDA)

    ii. Kusimamia Maandalizi na Utekelezaji Wa Sera za Wizara na Kuratibu Mapitio

    ya Sheria Mbalimbali za Wizara

    13. Mheshimiwa Spika, katika uandaaji wa miongozo ya Kisera na Kisheria, Wizara

    imekamilisha rasimu ya Sera ya Nishati na Sera ya Ujenzi. Sera hizo zimewasilishwa kwa

    Kamati ya Makatibu Wakuu kwa ajili ya kupatiwa maoni na Wizara kwa inakamilisha

    marekebisho kwa mujibu wa maoni na michango ya Wajumbe wa Kamati ya Makatibu

    Wakuu. Wizara pia imeanza kuandaa Sera ya Mipango Miji na Sera ya Madini ambapo kazi

    inayondelea ni ukusanyaji wa taarifa muhimu (situation analysis) zitakazotumika katika

    utayarishaji wa Sera hizo.

    iii. Kuimarisha Mahusiano na Washirika wa Maendeleo

    14. Mheshimiwa Spika, Idara imeendeleza mashirikiano na Shirika la Misaada la Kimatifa la

    Japan (JICA) katika maandilizi ya utekelezaji wa Mradi wa Uimarishaji wa Miundobinu ya

    Maji Mjini Magharibi. Kupitia Mshauri wa Wizara wa Sekta ya Maji kutoka JICA, Idara

    imeendesha Warsha sita (6) za usimamizi wa rasilimali maji na warsha nane (8) za ufuatiliaji

    wa miradi ya maji. Warsha hizo zimewashirikisha watendaji wa Idara ya Mipango, ZAWA,

    ZURA, ZEMA, Wizara ya Fedha na Tume ya Mipango.

    Kwa upande mwengine Idara imeendelea kuimarisha uhusiano baina ya Wizara yetu na

    Wizara ya Nishati; Wazara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makaazi na Wizara ya

    Madini za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo miongoni mwa mambo

    yaliyojadiliwa ni Mkataba wa Mauziano ya Umeme baina ya ZECO na TANESCO pamoja

    na kubalidilishana uzoefu na utaalamu katika utekelezaji wa majukumu yanayofanana kwa

    Wizara hizi.

    15. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2019/2020, katika kutekeleza Programu ndogo

    ya Uratibu wa Mipango, Sera na Tafiti za Wizara jumla ya TZS Milioni 305.351

    ziliidhinishwa kutumika. Hadi kufikia Machi 2020, fedha zilizoingizwa ni TZS Milioni

    200.174 sawa na asilimia 65.6 ya makadirio.

  • 5

    PROGRAMU NDOGO YA UTAWALA NA UENDESHAJI

    16. Mheshimiwa Spika, Programu hii inajukumu la kusimamia uendeshaji wa shughuli za kila

    siku za Wizara pamoja na uendelezaji wa Rasilimali Watu kwa kuandaa mipango ya kujenga

    uwezo wa Watumishi, kushughulikia haki na stahiki za Watumishi waliopo na

    waliohitimisha Utumishi wao kwa sababu mbalimbali, kuhakikisha kuwepo kwa watendaji

    wa kutosha na wenye sifa na kusimamia nidhamu ya Watumishi

    17. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Machi 2020, Idara ya Uendeshaji na Utumishi ilitekeleza

    mambo yafuatayo:

    i. Kufanya malipo kwa kazi za uendeshaji wa Afisi kwa kulipa huduma za umeme,

    mtandao, vifaa vya kuandikia, ununuzi wa samani, matengenezo ya vifaa vya afisi,

    matengenezo ya kawaida kwa vipando 9 pamoja na kulipia bima gari 3 za Wizara.

    ii. Kuratibu mafunzo ya muda mfupi kwa wafanyakazi 564 na muda mrefu kwa

    wafanyakazi 32. Mafunzo hayo yalifanyika ndani na nje ya nchi kwa gaharama za

    Serikali na Washirika wa Maendeleo. Kwa ufafanuzi zaidi naomba angalia

    kiambatisho “C1 na C2”.

    iii. Kulipa stahiki kwa wafanyakazi ikiwemo malipo ya baada ya saa za kazi kwa

    wafanyakazi 34, posho la likizo kwa wafanyakazi 13 ambao walistahiki kwa mujibu

    wa sheria, ubani wa kufiwa kwa wafanyakazi watano (5).

    iv. Idara iliandaa na kuratibu mpango wa Rasilimali watu wa Mwaka wa Fedha

    2019/2020, kuratibu uajiri wa wafanyakazi 103 kwa ajili ya kujaza nafasi tupu na

    mpya zilizokuwepo kwa sababu mbalimbali na pia ilikabidhi majukumu ya kazi (job

    description) kwa wafanyakazi ili kurahisisha kujua majukumu yao na kujiandaa na

    tathmini ya utekelezaji.

    18. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2019/2020, Programu hii iliidhinishiwa jumla

    ya TZS Bilioni 1.727 kwa ajili ya kufanikisha shughuli za Uendeshaji na Utumishi. Hadi

    kufikia Machi, 2020, fedha zilizoingizwa ni TZS Bilioni 1.419 ambazo sawa na asilimia 82

    ya makadirio.

  • 6

    PROGRAMU NDOGO YA URATIBU NA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA

    WIZARA PEMBA

    19. Mheshimiwa Spika, Programu hii ndogo inatekelezwa na Afisi Kuu Pemba na inajukumu la

    uratibu na usimamizi wa kazi za Wizara zinatekelezwa Pemba ikiwemo Programu na Miradi

    ya Maendeleo. Hadi kufika Machi 2020 programu hii imetekeleza kazi zifuatazo:-

    i. Kusimamia shughuli za uendeshaji za kila siku kwa kulipa gharama za ununuzi wa

    gari moja ya ufuatiliaji wa kazi za Wizara Pemba, ununuzi wa vifaa, malipo ya

    huduma za umeme, mtandao, simu, gharama za posta na matengenezo ya vyombo

    vya usafiri.

    ii. Kusimamia maslahi ya wafanyakazi kwa kuwapatia malipo ya baada ya saa kazi

    (Overtime) wafanyakazi kumi na nane (18) na stahiki za likizo wafanyakazi kumi na

    mbili (12).

    iii. Kuwajengea uwezo wafanyakazi ambapo wafanyakazi wawili (2) wamepatiwa

    masomo ya muda mrefu na wafanyakazi watano (5) mafunzo ya muda mfupi

    (Induction Course).

    iv. Kusimamia utekelezaji wa kazi za kawaida zikiwemo upimaji wa viwanja,

    utayarishaji na utoaji wa Hati za Matumizi ya Ardhi, utambuzi na usajili wa Ardhi,

    utatuzi wa migogoro ya ardhi, usambazaji wa huduma za maji safi na salama na

    usambazaji na uimarishaji wa huduma ya umeme.

    v. Kufuatilia utekekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ambayo ni miradi ya maji katika

    maeneo ya Wambaa, Chanjaani, Gombani-Mchuya, Matuleni, Kilindi, Ukutini,

    Kilindini, Kwale Gongo Micheweni Fundo na Uvinje ni miradi ya Umeme katika

    vijiji vya Mteng’ombe, Chozi Minyenyeni, Mtambwe-Uondwe, na Kwale Mpona.

    20. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2019/2020, Programu hii ilipangiwa matumizi

    ya TZS Milioni 724.664 kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wake. Hadi kufikia Machi,

    2020, fedha zilizoingizwa ni TZS Milioni 614.700 ambazo sawa na asilimia 84 ya

    makadirio.

  • 7

    PROGRAMU KUU PN0102: USIMAMIZI WA ARDHI NA MAKAAZI

    21. Mheshimiwa Spika, Programu hii inajukumu la kuhakikisha usalama wa matumizi ya ardhi

    na huduma za makaazi bora kwa Wananchi na inajumuisha Programu ndogo tatu kama

    ifuatavyo:-

    PROGRAMU NDOGO YA UTATUZI WA MIGOGORO YA ARDHI

    22. Mheshimiwa Spika, Mahakama ya Ardhi ina jukumu la kupokea, kusikiliza na kuamua kesi

    za migogoro ya ardhi zinazowasilishwa na wananchi pamoja na Taasisi mbali mbali. Katika

    Mwaka wa Fedha 2019/2020 Mahakama ya Ardhi kupitia Programu hii ndogo ya utatuzi wa

    migogoro ya ardhi imetekeleza shughuli zifuatazo:-

    i. Kutatua migogoro ya ardhi:

    23. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2019/2020 Mahakama ya Ardhi ilipanga

    kuzitolea maamuzi kesi 260. Kwa kipindi hicho, kesi mpya 124 zimefunguliwa Unguja na

    Pemba. Mahakama imeendelea kuendesha kesi mbali mbali ziliopo Mahakamani ambapo

    jumla ya kesi 157 zimetolewa uamuzi sawa na asilimia 60 ya lengo la mwaka kwa

    mchanganuo ufuatao:-

    Jaduweli nambari 1: Mchanganuo wa Migogoro ya Ardhi iliyopokelewa

    sn MKOA KESI MPYA

    ZILIZOFUNGULIWA

    KESI

    ZILITOLEWA

    MAAMUZI

    KESI

    ZINAZOENDELEA

    1 Kaskazini Unguja 28 13 47

    2 Mjini Magharibi 34 69 74

    3 Kusini Unguja 16 21 24

    4 Kaskazini Pemba 21 22 22

    5 Kusini Pemba 25 32 22

  • 8

    24. Mheshimiwa Spika, Hadi kufikia tarehe 31 Machi, 2020 Mahakama ya Ardhi ina jumla ya

    kesi 189 zilizopo katika Mahakama zetu Unguja na Pemba ambapo Unguja ina jumla ya kesi

    145 na Pemba ina jumla ya kesi 44.

    ii. Matengenezo ya majengo ya Mahkama za Ardhi:

    25. Mheshimiwa Spika, Mahakama ya Ardhi imeweza kuifanyia matengenezo Mahakama ya

    Ardhi Mkoa wa Kusini Pemba kwa kufanya utanuzi wa jengo (extension), ujenzi huo

    umekamilika na kupunguza ufinyu wa nafasi kwa wafanyakazi.

    iii. Kutoa elimu kwa jamii:

    26. Mheshimiwa Spika, Mahakama ya Ardhi imeendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya

    umuhimu wa kufuata Sheria mbali mbali za ardhi, ujenzi na mazingira kwa kushiriki katika

    maonesho ya maadhimisho ya Siku ya Sheria Duniani (Law Day).

    27. Mheshimiwa Spika, kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, katika kutekeleza Programu ndogo

    ya Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi jumla ya TZS Milioni 594.732 ziliidhinishwa kutumika.

    Hadi kufikia Machi 2020, fedha zilizoingizwa ni TZS Milioni 344.007 sawa na asilimia 57.8

    ya makadirio.

    PROGRAMU NDOGO YA UTHAMINI WA RASILIMALI

    28. Mheshimiwa Spika, Programu hii inatekelezwa na Ofisi ya Mthamini Mkuu wa Serikali

    ambapo dhumuni lake ni kuhakikisha usimamizi mzuri wa kazi za uthamini kwa Serikali,

    Sekta binafsi na wananchi kwa ujumla. Kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 Ofisi ya Mthamini

    Mkuu wa Serikali ilitekeleza kazi zifuatazo:-

    i. Kupitisha na kuthibitisha ripoti za uthamini wa rasilimali kwa madhumuni

    mbalimbali.

    29. Mheshimiwa Spika, jumla ya ripoti 205 zimethibitishwa kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020

    ambapo kati ya hizo 179 ni ripoti za uthamini kwa ajili mikopo (Morgage purpose), 4 ripoti

    za uthamini kwa ajili ya thamani (Book value), 10 ripoti za uthamini kwa ajili ya mirathi

  • 9

    (Inheritance purpose) na 12 ripoti ya uthamini kwa ajili ya fidia (Compensation purpose).

    Utekelezaji wa Shughuli hii hutegemea maombi yanayowasilishwa.

    ii. Kutayarisha Ripoti ya Shughuli za Uthamini Kwa Kila Robo Mwaka.

    30. Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Mthamini Mkuu wa Serikali imetoa Ripoti ya Shughuli zote za

    uthamini kwa kila robo Mwaka. Ripoti hiyo inaonyesha kazi ambazo Ofisi ya Mthamini

    Mkuu wa Serikali imezifanya kwa kipindi cha robo husika pamoja na Changamoto zake.

    iii. Kutayarisha na Kuingiza Taarifa za Mali Zilizofanyiwa Uthamini Katika

    Mfumo wa Kieletroniki.

    31. Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Mthamini Mkuu wa Serikali tayari imeandaa mfumo wa

    kieletronik unaotumika kuweka taarifa za mali zinazofanyiwa uthamini. Mfumo huo bado

    upo katika majaribio ya uingizaji taarifa kwa sasa.

    iv. Kufanya Mikutano na Taasisi za Serikali.

    32. Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Mthamini Mkuu wa Serikali imejitambulisha uwepo wake na

    majukumu yake kwa Taasisi za Umma ambapo kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 imekutana

    na Wizara 7 za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Taasisi zake ambapo ilitoa

    elimu kwa taasisi hizo kuhusu kazi za uthamini inazozifanya kwa mujibu wa Sheria.

    v. Kutoa Elimu Kuhusu Kazi ya Uthamini kwa Masheha na Wakuu wa Wilaya

    33. Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Mthamini Mkuu wa Serikali imefanya Semina kwa Wakuu wa

    Wilaya na Masheha katika Ofisi za Wakuu wa Wilaya husika kuwapa uelewa kuhusu

    uthamini na kazi ambazo Ofisi inazifanya kwa mujibu wa Sheria, Aidha Ofisi imekutana na

    Wakurugenzi wa Halmashauri na Manispaa za Unguja pamoja na watendaji wao kwa lengo

    hilo la kutoa elimu kuhusu Ofisi ya Mthamini Mkuu wa Serikali na Kazi zake inazozifanya.

    34. Mheshimiwa Spika, kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, katika kutekeleza Programu ndogo

    ya Uthamini wa Rasilimali jumla ya TZS Milioni 135.00 ziliidhinishwa kutumika. Hadi

    kufikia Machi 2020, fedha zilizoingizwa ni TZS Milioni 53.318 sawa na asilimia 39 ya

    makadirio.

  • 10

    PROGRAMU NDOGO YA UTAWALA WA ARDHI NYUMBA NA MAKAAZI

    35. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2019/2020 utekelezaji wa Programu hii ndogo

    ulilenga katika kuhakikisha usalama wa umiliki wa Ardhi na uimarishaji wa huduma za

    makaazi kupitia upimaji wa ardhi, utambuzi na usajili wa ardhi, mipango ya miji na matumizi

    ya ardhi, ukarabati wa nyumba za maendeleo na majengo ya kihistoria.

    KAMISHENI YA ARDHI

    36. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Machi 2020, Kamisheni ya Ardhi imetekeleza kazi

    zifuatazo:-

    i. Utawala na Uendeshaji

    a) Kuwajengea uwezo wafanyakazi ambapo jumla ya wafanyakazi 22 wamepatiwa

    mafunzo ya ndani yanayohusu utayarishaji wa Hati za Ardhi na wafanyakazi 26

    wamepatiwa mafunzo tofauti ya utendaji wa majukumu yao.

    b) Kusimamia maslahi ya Wafanyakazi ambapo stahiki zimetolewa kwa

    wafanyakazi 35 ikiwemo likizo na malipo baada ya saa za kazi.

    ii. Ugawaji na Usimamizi wa Ardhi

    a) Kutayarisha Hati 1,188 ambapo Hati 1,004 kwa Unguja na Hati 184 Kwa Pemba.

    b) Kutayarisha Mikataba ya Ukodishaji Ardhi 74 ambapo Mikataba 41 kwa Unguja

    na Mikataba 5 kwa Pemba.

    c) Kufanya ukaguzi wa maeneo 52 ya Ardhi za Eka Tatu na maeneo 38 ya Ardhi za

    Ukodishwaji.

    d) Kutayarisha Vitambulisho 20 vya Matumizi ya Ardhi ya Eka Tatu.

    e) Jumla ya kazi za uthamini 167 zilifanywa, 146 kwa Unguja na 21 Kwa Pemba.

    Kazi hii hutegemea idadi ya maombi yaliyowasilishwa ya kutaka kufanyiwa kazi

    kwa madhumuni mbalimbali yakiwemo ya mirathi, kujua thamani ya mali na

    ulipaji fidia.

    f) Kufanya utambuzi wa maeneo 472, maeneo 26 Unguja na 446 kwa upande wa

    Pemba. Kazi hii iliendelea kwa kufanya zoezi la uhakiki wa taarifa za maeneo 6

    yaliyokwisha tambuliwa.

  • 11

    iii. Kuratibu na kusimamia Usajili wa Ardhi

    a) kuhakiki maeneo 395 ambapo kwa Unguja ni maeneo 206 na kwa Pemba maeneo

    189. Maeneo hayo ni kwa Wilaya za Mjini, Magharibi B, Chake Chake, Wete na

    Mkoani.

    b) Kusajili maeneo (parcels) 269 ambapo maeneo 123 kwa Unguja na 146 kwa

    Pemba. Maeneo hayo yaliyosajiliwa ni kwa Wilaya za Mjini, Magharibi B, Chake

    Chake, Wete, Mkoani na Micheweni.

    c) Kuweka taarifa za mabadiliko ya umiliki wa matumizi ya ardhi kwa ardhi

    zilizosajiliwa. Afisi ya Mrajis wa Ardhi imeweza kusajili maeneo 14 kati ya

    maeneo 25 iliyojipangia. Kwa Unguja ni maeneo 13 na kwa Pemba ni eneo 1.

    Maeneo hayo ni Mchangani, Kikwajuni Bondeni, Mlandege, Vikokotoni,

    Funguni, Kajificheni, Mwembeladu, Vikokotoni, Mwembetanga, Gulioni,

    Malindi, Kiponda, Mkunazini (Unguja) na Selem (Pemba).

    d) Jumla ya kadi za usajili wa ardhi 416 zimetengezwa ambapo kwa Unguja ni kadi

    349 na Pemba ni kadi 67.

    e) Kutayarisha Marejista 4 katika maeneo yaliyosajiliwa katika Shehia Jang’ombe

    (Unguja), Selem, Limbani na Kiungoni (Pemba).

    f) Kutoa elimu ya uhamasishaji wa Usajili wa Ardhi. Jumla ya mikutano 11

    imefanyika ambapo 9 ni kwa Unguja na 2 ni Pemba. Uhamasishaji umefanyika

    katika vituo vya Kikwajuni Juu, Kikwajuni Bondeni, Mchangani, Kidutani,

    Matarumbeta, Jang'ombe, Mpendae, Wete, Selem na Limbani.

    g) Semina 13 za mafunzo kwa wafanyakazi zimeendeshwa. Mafunzo hayo ni kuhusu

    usajili wa ardhi kwa kutumia njia za elektroniki, Sera ya Miji, utawala wa sheria,

    utambuzi, utayarishaji wa hati, usajili wa nje ya mpangilio (sporadic), fedha,

    hifadhi ya Mji Mkongwe.

    h) Kusajili ardhi kwa ajili ya mirathi ambapo maeneo 13 yamesajiliwa.

    i) Makala 12 zimetayarishwa kwa ajili ya kuchapishwa katika Jarida la ARDHI

    toleo la tano.

  • 12

    iv. Upimaji na Utoaji wa Ramani za Ardhi

    a) Jumla ya viwanja 1,171 vimepimwa kwa upande wa Unguja na 441 Kwa upande

    wa Pemba kwa ajili ya matumizi mbalimbali.

    b) Kuweka alama za Upimaji (control points) 472 katika mfumo wa komputa.

    c) Jumla ya ramani za ardhi 839 zimetayarishwa kwa Unguja na140 kwa Pemba.

    v. Upangaji wa Miji na Matumizi ya Ardhi

    a) Kutekeleza Mpango wa Maendeleo wa kitovu cha Mji wa Zanzibar (Zanzibar

    City Centre-Local Area Plan) kwa kusimamia mradi wa “Green-Corridor”.

    b) Kupanga maeneo ya wazi (Open space) manne (4) ambayo ni Kibanda Maiti,

    Daraja Bovu, na eneo la Kiembe samaki kwa Unguja na Madungu

    (Mwanamashungi) kwa Pemba.

    c) Kuendelea na hatua za utayarishaji wa Sera, Sheria na Kanuni mpya za Mipango

    Miji na Maendeleo ya Ardhi ambapo Idara imekutana na wananchi katika ngazi

    za Halmashauri na Mikoa ili kupata maoni yao.

    37. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2019/2020 jumla ya TZS Bilion 2.111

    ziliidhinishwa kutumika ikiwa ni ruzuku ya matumizi ya kawaida na Mishahara. Hadi kufikia

    Machi, 2019 fedha zilizoingizwa ni TZS Bilion 1.707 sawa na asilimia 80.9 ya makadirio.

    SHIRIKA LA NYUMBA

    38. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2019/2020 Shirika limetekeleza kazi

    zifuatazo:

    i. Matengenezo ya Nyumba za Shirika

    a) Matengenezo ya nyumba kumi (10) za Maendeleo Madungu yanaendelea na

    yamefikia asilimia sitini na tano (65%) ya kukamilika kwake.

    b) Matengenezo madogo madogo ya nyumba za Shirika zikiwemo: nyumba namba

    414 Hurumzi, M16 Kikwajuni, K5 Kikwajuni, 293 Kiponda na Bloki namba 2

    Michenzani, nyumba namba T 1, T 14, T 17 na T 31A+B Selemu-Wete, BL.2/22

    Micheweni, T-18 ChakeChake na Ofisi ya Shirika la Nyumba ChakeChake.

  • 13

    c) Kufanya matayarisho ya ujenzi wa jengo jipya la biashara Kilimatinde ikiwemo

    kuandaa michoro na makisio ya ujenzi ‘BOQ’.

    d) Matengenezo ya dharura kwa kuezeka mapaa ya bloki B na N Kikwajuni

    yaliyoezuka kutokana na upepo.

    e) Kufanya mkutano wa hadhara katika uwanja wa Alabama - Miembeni ukiwa na

    lengo kuu la kutoa taarifa rasmi ya matayarisho ya matengenezo ya Nyumba za

    Maendeleo yakianzia na nyumba 36 za bloki namba 1 Michenzani. Tayari

    mkataba wa matengenezo hayo umesainiwa. Mkandarasi wa kazi hiyo ni Kikosi

    Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM) na Msimamizi ni Wakala wa Majengo

    Zanzibar. Kazi ya matengenezo itaanza hivi karibuni.

    f) Kutayarisha michoro (existing drawings) ya nyumba No.1107-1115 Malindi

    (Mabanda ya Papa), kuendelea kupima na kutayarisha michoro ‘Existing

    drawings” ya nyumba No. 300, 301 na 303 Shangani na nyumba No. 366 Beit-el-

    Ras.

    g) Kusafisha na kuifanyia matengenezo mifumo ya maji machafu ya nyumba za

    Mombasa Mchina Mpya, Bloki D Kikwajuni, Bloki namba 3,5,7,8,9 Michenzani,

    Madungu, Mtemani na Mapinduzi Mkoani.

    h) Kujenga shimo (soak pit) jipya kwenye nyumba za Mombasa Mchina Mpya.

    ii. Kuzitambua, Kuzithamini na Kuziorodhesha Milki za Shirika

    a) Shirika linaendelea na Uthamini wa nyumba zake zilizopo Mji Mkongwe.

    b) Kukamilisha uwekaji wa vibati vya nambari za utambuzi kwa nyumba za Mji

    Mkongwe kwenye mitaa ya Shangani, Forodhani, Gizenga, Kiponda, Mkunazini

    na Hurumzi.

    iii. Kuweka Mazingira Mazuri ya Kazi kwa Wafanyakazi

    a) Matengenezo ya jengo la ofisi awamu ya pili yanaendelea.

    b) Shirika limekamilisha zoezi la uajiri kwa wafanyakazi watatu (3) ambao tayari

    wameshapangiwa kazi.

    c) Wafanyakazi kumi na tano (15) wa fani tofauti wamepatiwa mafunzo ya muda

    mfupi ndani ya nchi.

  • 14

    d) Shirika limenunua vespa tatu (3) kwa ajili ya kurahisisha ufanyaji kazi kwa

    watendaji wake.

    iv. Kuongeza Ufanisi Katika Kukusanya Mapato ya Shirika

    a) Shirika linaendelea kuwafuatilia wapangaji wenye madeni makubwa ikiwemo

    kuunda Kamati ya Bodi ya kufuatilia madeni, kuwaita wapangaji wenye madeni

    na kujipanga kwa ajili kuwapeleka wapangaji wasiotaka kulipa kwenye Bodi ya

    Kudhibiti Kodi za Nyumba.

    b) Kuanzisha mfumo wa kutuma ujumbe mfupi wa simu kwa wapangaji ili

    kuwakumbusha kulipa kodi.

    c) Kufanya ukaguzi wa kawaida wa nyumba za Shirika ili kuwatambua wapangaji

    halisi, kufuatilia madeni, mikataba ya upangishwaji na kujua changamoto

    zilizopo.

    d) Kutoa mikataba mipya ya ukodishaji kwa wapangaji wa nyumba za Shirika.

    39. Mheshimiwa Spika, kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 Shirika lilikadiria kukusanya TZS

    Bilioni 3,035. Hadi kufika Machi 2020 jumla ya TZS 1.815 zimekusanywa ambazo ni sawa

    na asilimia 60 ya makadirio. Kwa upande wa matumizi Shirika lilikadiria kutumia jumla ya

    TZS Bilioni 3.011. Hadi kufikia Machi 2020 jumla ya TZS 1.348 zimetumika ambazo ni

    sawa na asilimia 45 makadirio.

    MAMLAKA YA HIFADHI NA UENDELEZAJI MJI MKONGWE

    40. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2019/2020 Mamlaka imeendelea kusimamia

    uhifadhi na uendelezaji wa Mji wetu wa Urithi wa Kimataifa kwa kutoa ushauri wa

    kitaalamu na kusimamia miradi ya Uhifadhi wa Majengo kama ifuatavyo:-

    i. Ukarabati wa Jengo la Beit-El-Ajaib

    41. Mheshimiwa Spika, Mamlaka inaendelea za kusimamia ukarabati wa jengo hili ambapo

    kazi zilizofanyika hadi kufikia Machi 2020 ni kutayarisha ofisi ya muda ya Meneja wa

    mradi na ya Mkandarasi ambayo baadae itatumika kama ofisi ya Beit-El-Ajaib, Ujenzi wa

  • 15

    paa la dharura katika upande ambao jengo lilianguka ili kuzuia uharibifu zaidi wakati wa

    mvua, Kuzungushia jukwaa la mbao mnara na uparaji wa milango na madirisha kwa ajili ya

    kufanyiwa matengenezo, Kufanya uchunguzi wa vyuma (I section beam) vinavyozuia dari

    za nje ili kujua uimara wake, Kutayarisha sampuli za plasta kwa ajili ya kuthibitishwa na

    Meneja mradi kabla ya kuanza kazi pamoja na kuendeleza michoro kwa baadhi ya sehemu

    zinazotakiwa kufanyiwa ukarabati.

    ii. Makumbusho ya Kasri la Wananchi (People’s Palace Museum)

    42. Mheshimiwa Spika, katika jitihada za kuliimarisha jengo hili la kihistoria, Serikali imetenga

    TZS Bilioni 2.552 kwa ajili ya kulifanyia matengenezo. Gharama hizo zimetokana na

    ukaguzi wa kina uliofanywa na wataalamu wa Mji Mkongwe.

    iii. Ukarabati wa jengo la PBZ Malindi

    43. Mheshimiwa Spika, Mamlaka imeendelea na kazi za kusimamia ujenzi mpya na ukarabati

    wa jengo hili ambapo katika jengo jipya kazi inayoendelea ni kutia milango na madirisha.

    Kwa upande wa jengo la zamani kazi zinazoendelea ni ukataji wa kuta za ndani (partitions)

    pamoja na kutia milango na madirisha, kiujumla kazi imefikia wastani wa asilimia 78 ya

    matengenezo. Jengo linatarajiwa kukabidhiwa mwezi Aprili, 2020.

    iv. Ukarabati Mdogo wa Majengo

    44. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Machi, 2020 Mamlaka imetoa vibali 151 kwa

    matengenezo ya kawaida kwa nyumba mbali mbali zilizomo ndani ya eneo la uhifadhi.

    Mamlaka hufanya ufuatiliaji ili kuhakikisha kwamba walopatiwa vibali hivyo hawakiuki

    masharti ya ujenzi husika.

    v. Ukaguzi wa Majengo Yote Yaliyomo Ndani ya Eneo la Mji Mkongwe

    45. Mheshimiwa Spika, kutokana na uchakavu wa Majengo, Mamlaka ya Hifadhi na

    Uendelezaji Mkongwe ilifanya ukaguzi wa majengo yote yaliyomo katika eneo la hifadhi na

    kubaini kuwepo kwa majengo 1,244 yaliyo katika hali nzuri, 1,131 hali ya wastani , 250

    hali mbaya na 86 hali mbaya sana. Aidha baadhi ya wananchi wameelimika baada ya

    kufanyika ukaguzi wa majengo na wameanza kuchukua jitahada za ukarabati wa majengo

  • 16

    yao. Hata hivyo jitahada za makusudi zinachukuliwa na Mamlaka za kuwaita na

    kuwaelimisha zaidi wamiliki wenye majengo yaliyo katika hali mbaya ili wachukue hatua za

    haraka za kufanya ukarabati wa majengo yao kabla ya kutokea athari.

    vi. Utekelezaji wa Mpango wa Uingiaji waVyombovya Moto

    46. Mheshimiwa Spika, Mamlaka ya Hifadhi na Uendelezaji Mji Mkongwe imekamilisha

    utayarishaji wa Mpango wa Uingiaji wa Vyombo vya Moto kwa kushirikiana na taasisi

    nyenginezo (Baraza la Manispaa Mjini, Usalama Barabarani, Shirika la Bandari, Idara ya

    Usafiri na Leseni, Idara ya Ujenzi na Utunzaji wa Barabara). Mpango huo umeshaanza

    kutumika kuanzia tarehe 10/2/2020 na kuonesha mafanikio ya kupunguza msongamano kwa

    kiasi kikubwa.

    vii. Kuwajengea Uwezo Wafanyakazi

    47. Mheshimiwa Spika, Mamlaka imewajengea uwezo wafanyakazi wake ambapo mfanyakazi

    mmoja (1) anaendelea na masomo ya muda mrefu ndani ya nchi ya shahada ya tatu katika

    masuala ya Upangaji wa Miji na wafanyakazi wanne (4) wamepatiwa mafunzo ya muda

    mfupi nje ya nchi katika masuala ya Uhifadhi wa Mambo ya Kale na Mipango ya Miji.

    Aidha wafanyakazi 58 wamepatiwa stahiki za malipo baada ya saa za kazi.

    48. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2019/2020 Mamlaka ya Hifadhi na

    Uendelezaji Mji Mkongwe ilipangiwa kutumia jumla ya TZS Milioni 804.00 ikiwa ni fedha

    za ruzuku ya mishahara na matumizi ya kawaida. Hadi kufikia Machi,2020 jumla ya TZS

    Milioni 531.92 zimetumika ambazo ni sawa na asilimia 66 ya makadirio

    WAKALA WA MAJENGO

    49. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2019/2020 Wakala wa Majengo imeendelea

    kusimamia na kutoa ushauri kwa miradi ya ujenzi ya taasisi za Serikali na kama ifuatavyo:-

    i. Kutoa Ushauri Elekezi (Consultancy)

    a) Mradi wa nyumba za Wananchi zinazoendelea kujengwa Dundua, Bumbwini

    Mkoa wa Kaskazini Unguja.

  • 17

    b) Mradi ya ujenzi wa ghala la akiba ya chakula Bandarini Unguja.

    c) Mradi wa ujenzi wa chuo cha Amali kiliopo Daya Mtambwe - Pemba na

    Makunduchi Unguja.

    d) Kuandaa michoro na gharama za ujenzi wa Kiwanja cha Michezo kiliopo

    Kitogani Mkoa wa Kusini Unguja na Mkokotoni Kaskazini Unguja.

    e) Kuandaa michoro na gharama za ujenzi wa Nyumba ya Sanaa Mwanakwerekwe

    f) Kuandaa michoro ya marekebisho ya utanuzi (Renovations) ya Ukumbi wa

    Mikutano wa Sheikh Idrisa Abdulwakil - Kikwajuni.

    g) Kuandaa michoro na gharama za ujenzi wa jengo la Ofisi ya ZAECA- Tunguu.

    h) Kuandaa michoro na gharama za ujenzi wa jengo la Ofisi ya Shirika la Bima

    Pemba.

    i) Kuandaa ramani na gharama za ujenzi wa jengo la Ofisi za Wakala wa Majengo

    Mazizini.

    ii. Kusimamia Miradi ya Ujenzi (Clerk of Work)

    a) Mradi wa ujenzi wa Maduka (Shopping Mall) Michenzani.

    b) Mradi wa ujenzi wa jengo la Kitega Uchumi Kisonge.

    c) Mradi wa ujenzi wa Mahkama Kuu Tunguu.

    d) Mradi wa ujenzi wa nyumba za mji mpya wa Kwahani.

    e) Mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Rais Ikulu Chake Chake

    f) Ukarabati wa Jengo la Takwimu Mazizini.

    g) Matengenezo ya Afisi ya Idara ya Leseni iliopo Mwanakwerekwe

    iii. Nyumba za Viongozi wa Serikali na Watumishi wa Umma

    a) Kuendelea kutoa ushauri elekezi na kusimamia ujenzi wa nyumba ya Afisi ya

    Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar iliyoko Pagali, Chakechake Pemba

    b) Kukamilisha matengenezo ya nyumba ya Serikali ilioko Migombani, Unguja

    50. Mheshimiwa Spika, kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 Wakala wa Majengo ilipangiwa

    ruzuku ya TZS Milioni 365.00 kwa kazi za kawaida. Hadi kufikia Machi 2020 jumla ya TZS

    192.50 zimetumika ambazo ni sawa na asilima 52.7 ya makadirio.

  • 18

    BODI YA USAJILI WAKANDARASI

    51. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2019/2020 Bodi ya Usajili Wandarasi

    imetekeleza kazi zifuatazo:-

    i. Jumla ya Wakandarasi wapya thelathini na nne (34) wamesajiliwa ambapo 13 kutoka

    Zanzibar, 19 kutoka Tanzania Bara na wawili (2) kutoka nje ya Tanzania.

    ii. Kufanya ukaguzi kwa wakandarasi wapya ishirini (20) na thelathini na nne (34)

    waliowasilisha maombi ya kusajiliwa.

    iii. Kufanya ziara 83 za ukaguzi kwa Unguja na 32 kwa Pemba pamoja na kufanya vikao

    51 vya kesi zinazohusiana na uvunjaji wa Sheria za ujenzi.

    iv. Kuwapatia wajumbe na watendaji wa Bodi mafunzo ya muda mfupi Tanzania Bara,

    kuhudhuria mikutano ya kitaalamu pamoja na kufanya mikutano ya mashirikiano na

    Bodi ya Wakandarasi ya Tanzania Bara.

    v. Kufanya mafunzo kwa ajili ya usalama kazini kwa wakandarasi na wadau wengine.

    vi. Kufanya Mkutano Mkuu wa Wakandarasi wote na kujadili mafanikio, changamoto na

    fursa kwa Wakandarasi.

    52. Mheshimiwa Spika. katika Mwaka wa Fedha 2019/2020 Bodi ya Usajili wa Wakandarasi

    ilipangiwa kutumia jumla ya TZS Milioni 50.00 ikiwa ni fedha za ruzuku kwa matuymizi ya

    kazi za kawaida. Hadi kufikia Machi 2020 jumla ya TZS Milioni 25.00 zimetumika ambazo

    ni sawa na asilimia 50 ya makadirio.

    BODI YA USAJILI WAHANDISI WASANIFU NA WAKADIRIAJI MAJENGO

    53. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2019/2020 Bodi ya Usajili Wasanifu,

    Wahandisi na Wakadiriaji Majengo imetekeleza kazi zifuatazo:-

    i. Kuendeleza Usajili wa Wataalamu 10 wa fani ya Ujenzi wa Majengo, Wahitimu 44,

    Mafundi Sadifu watatu (3) na Makampuni ya ushauri wa Ujenzi 15 kama

    ilivyoainishwa katika Sheria.

  • 19

    ii. Kuelimisha na kuwaendeleza Wataalamu wa fani ya Ujenzi kuhusu Ujenzi wa

    Viwango kwa kufanya Programu tatu (3) za mafunzo ya muda mfupi (CPD).

    iii. Kuwajengea uwezo wajumbe wa Bodi kwa kuwapatia mafunzo maalum ya uelewa

    wa kazi za Bodi.

    iv. Kufuatilia kazi za Ujenzi wa Majengo zinazofanywa na Wasanifu, Wahandisi na

    Wakadiriaji Majengo katika maeneo yote ya Unguja na Pemba.

    v. Kushirikiana na Taasisi za ndani na nje ya Nchi zinazofanana na Bodi kwa Lengo la

    kujifunza na kubadilishana ujuzi kwa watendaji wa Bodi lengo la kuleta maendeleo

    na ufanisi wa kazi za Bodi.

    vi. Kuendelea na taratibu wa uwanzishwaji wa Mafunzo ya Vitendo (Structure

    Apprenticeship Program) kwa kuwawezesha wahitimu waliotajwa katika Sheria ya

    Bodi waweze kuwa Wataalamu bora wanaozingatia maadili na wenye uweledi katika

    tasnia ya Ujenzi.

    vii. Kuendelea kuhamasisha uwepo wa Jumuiya ya Wasanifu, Wahandisi na Wakadiriaji

    Majengo kwa mustakbali wa Wataalamu wa fani hizo.

    viii. Kuendelea na hatua za marekebisho ya Sheria namba 5 ya mwaka 2008 ya Bodi ya

    Usajili Wasanifu, Wahandisi na Wakadiriaji Majengo ili iendane na wakati kwa

    kujumuisha Wataalamu wengine wa Ujenzi kwa lengo la kudhibiti na kuwaendeleza

    Wataalamu.

    ix. Kutoa Elimu kwa Jamii na wadau wa Ujenzi juu ya ufahamu wa majukumu ya Bodi

    ya Usajili Wasanifu, Wahandisi na Wakadiriaji Majengo kwa kufanya Mikutano

    minne (4) pamoja na vipindi vinne vya Televisheni na Redio.

    54. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2019/2020 Bodi ya Usajili Wasanifu,

    Wahandisi na Wakadiriaji Majengo ilipanga kutumia jumla ya TZS Million 50.00 ikiwa ni

    ruzuku kwa matumizi ya kazi za ziada. Hadi kufikia Machi 2020 jumla ya TZS Milioni 20.8

    zimetumika ambazo ni sawa na asilimia 41.6 ya makadirio

    BODI YA KONDOMINIO

    55. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2019/2020 Bodi ya Kondominio imetekeleza

    kazi zifuatazo:-

  • 20

    i. Kuwajengea uwezo Wajumbe wa Bodi kupitia kongamano la Kimataifa la masuala ya

    Milki za Ardhi Afrika lililoandaliwa na “Africa Real Estate Society” (AfRES) Jijini

    Arusha. Vilevle, Wajumbe walihudhuria Warsha ya siku moja ya Wasanifu,

    Wahandisi na Wakadiriaji Majengo iliojadili Changamoto ya uhaba wa Mchanga

    Zanzibar na Fursa zake.

    ii. Kuandaa muongozo wa Uendeshaji na Usimamizi wa Majengo ya Kondominio

    Zanzibar “Condominium Properties Administration and Management strategy”

    ambao utatoa miongozo katika utendaji wa kazi za Bodi na kuanza kazi rasmi ya

    usajili.

    iii. Kufanya ziara ya kimafunzo katika Taasisi za Wizara ya Ardhi, Nyumba na

    Maendeleo ya Mkaazi Tanzania Bara (Ofisi za Msajili wa Hati Tanzania na Shirika la

    Nyumba la Taifa – NHC) kwa ajili ya kujifunza uendeshaji na uratibu wa shughuli za

    Kondominio kutokana na uzoefu wa Taasisi hizo.

    iv. Kuendelea na ukarabati wa Nyumba namba 130- Shangani ambayo itatumika kama

    ofisi za kudumu za Bodi.

    v. Kuendesha kikao kimoja cha Bodi ya Zabuni (Tender Board) kwa ajili ya ununuzi

    wa Gari itakayotumika kwa shughuli za Bodi.

    56. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2019/2020 Bodi ya Kondominio ilipangiwa

    kutumia TZS Milioni 185.00 kwa utekelezaji wa kazi zake. Hadi kufikia mwezi Machi

    2020, fedha zilizopatikana ni TZS Milioni 100.21 ambazo ni sawa na asilimia 54.2

    BODI YA KUDHIBITI KODI ZA NYUMBA

    57. Mheshimiwa Spika, Bodi ya Kudhibiti Kodi za Nyumba Zanzibar imeendelea na kazi za

    kupokea kusikiliza na kuamua kesi zinazohusiana na migogoro ya kodi za nyumba kama

    ifuatavyo:-

    i. Kutatua Migogoro ya Kodi za Nyumba

    58. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Machi 2020, Bodi ya Kudhibiti Kodi za Nyumba imepokea

    kesi mpya 42 ambazo zimefunguliwa Unguja na Pemba. Bodi imeendesha vikao vya

  • 21

    kusikiliza kesi hizo pamoja na za awali ambapo kesi 17 zimetolewa maamuzi kwa

    mchanganuo ufuatao:-

    Unguja: kesi mpya ni 36 na zilizotolewa maamuzi ni kesi kumi na nne (14).

    Pemba: Kesi Mpya ni 6 na zilizotolewa maamuzi ni kesi tatu (3).

    ii. Kufanya matengenezo ya jengo la Ofisi ya Bodi ya Kudhibiti Kodi za Nyumba

    Unguja, ambapo hadi sasa Bodi hiyo haijapata Ofisi yake ya Kudumu na imepewa

    jengo lakini halikaliki hadi lifanyiwe matengenezo.

    iii. Kutoa Elimu kwa jamii kuhusiana na shughuli za Bodi ya Kudhibiti Kodi za Nyumba

    Zanzibar kwa kushiriki maonesho ya Siku ya Sheria (Law day )

    iv. Kutoa huduma za uendeshaji wa Ofisi ikiwemo Ununuzi wa Vitabu 100 vya Sheria

    kwa matumizi ya Bodi.

    59. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa 2019/2020, Bodi ya Kudhibiti Kodi za

    Nyumba ilipangiwa matumizi ya TZS Milioni 200.00. Hadi kufikia Machi, 2020 Fedha

    zilizoingizwa ni TZS Milioni 109.97 ambazo ni sawa na asilimia 54.98 ya makadirio.

    PROGRAMU KUU PN0105: USIMAMIZI WA HUDUMA ZA MAJI NA NISHATI

    60. Mheshimiwa Spika, Programu hii inajukumu la kusimamia Uzalishaji na Usambazaji

    Endelevu wa Huduma za Maji na Nishati Nchini na inatekelezwa na taasisi zifuatazo:

    Mamlaka ya Maji (ZAWA) Idara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme (ZECO),

    Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (ZURA), Mamlaka ya Udhibiti wa

    Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia (ZPRA) na Kampuni ya Maendeleo ya

    Mafuta na Gesi Asilia (ZPDC).

    MAMLAKA YA MAJI ZANZIBAR

    61. Mheshimiwa Spika, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuwa mstari wa mbele katika

    kuhakikisha wananchi wa Zanzibar wanapata huduma ya msingi ya maji safi na salama kwa

    kuzingatia mifumo na miongozo ya Malengo Endelevu ya Dunia (Sustainable Development

    Goals– SDGs 2015-2030); Dira ya Taifa ya Maendeleo (2020); Mpango wa Kukuza Uchumi

    na Kupunguza Umaskini Zanzibar (MKUZA III 2016-2020), Ilani ya Uchaguzi ya Chama

  • 22

    Cha Mapinduzi (2015-2020), Será ya Maji ya Taifa ya Mwaka 2004. Malengo hayo yote

    yanaweka msisitizo wa upatikanaji wa huduma za maji safi na salama na usafi wa mazingira

    kwa wote.

    62. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2019/2020 Wizara yangu kupitia

    Mamlaka ya Maji ilitekeleza kazi mbalimbali kupitia miradi na kazi za kawaida kama

    ifuatavyo:

    i. Mradi wa Maji na Usafi wa Mazingira wa Mkoa wa Mjini Magharibi – ZUWSP

    (ADF 12).

    63. Mheshimiwa Spika, Mradi huu uliotekelezwa kwa pamoja kati ya Serikali ya Mapinduzi

    Zanzibar na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) umekamilika na kuwanufaisha wananchi

    wa maeneo ya Mji Mkongwe na Ng’ambo ya zamani. Kazi zilizofanyika ni pamoja na:-

    a) Uchimbaji wa visima vipya sita (6) vyenye uwezo wa kuzalisha wastani wa lita

    150,000 kwa saa kwa kila kisima,

    b) Ukarabati wa visima vikongwe ishirini na tatu (23),

    c) Ujenzi wa Matangi mawili (2) yenye ujazo wa lita Milioni Mbili (2,000,000)

    Saateni na Milioni Moja (1,000,000) Mnara wa Mbao,

    d) Ulazaji wa mabomba yenye urefu wa kilomita 75.7, ambapo kilomita 20.6 ni

    mabomba ya usafirishaji maji yaliyolazwa kutoka visimani Bumbwisudi hadi

    Welezo matangini na kutoka visimani Kaburi kikombe hadi tangi la Mnara wa

    mbao. Kilomita 55.1 ni mabomba ya usambazaji ya yaliyolazwa kutoka matangini

    hadi kwa watumiaji.

    64. Mheshimiwa Spika, Fedha zilizopangwa kwa upande wa Serikali ni TZS Bilioni 2.248 na

    Muhisani TZS Bilioni 6.971. Fedha zilizopatikana kwa upande wa Serikali TZS Milioni

    656.731 sawa na 30% na TZS Bilioni 8.851 sawa na 127% kwa upande wa Muhisani.

    ii. Mradi Wa Uimarishaji Wa Mfumo Wa Usambazaji Maji Zanzibar (INDIA)

    65. Mheshimiwa Spika, Mradi huu unagharamiwa kwa mkopo kutoka Serikali ya India kupitia

    Benki ya Uagizaji na Usafirishaji ya India (Export-Import Bank of India – “EXIM Bank

    India”) na mchango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ). Hadi kufikia Machi 2020,

  • 23

    mradi umekamilisha kazi ya kumpata Mshauri Elekezi wa mradi kwa kazi ya usimamizi na

    usanifu wa mradi, tathmini ya kumpata Mkandarasi wa ujenzi na hatua inayoendelea sasa ni

    kusubiri majibu ya ripoti iliyopelekwa kwa muhisani na kupewa ruhusa (no objection) kwa

    ajili ya kumuajiri na kuanza ujenzi wa mradi, Aidha Serikali kupitia mradi huu imefanikiwa

    kulipa fidia katika eneo linalotarajiwa kujengwa tangi Dimani.

    66. Mheshimiwa Spika, Fedha zilizotengwa kwa upande wa Serikali ni TZS milioni 700 na

    TZS Bilioni 88.420 kwa upande wa Muhisani. Fedha zilizopatikana kwa Upande wa

    Serikali ni TZS Milioni 24.400 sawa na asilimia 5 na kwa upande wa Muhisani hakuna

    fedha zilizopatikana kutokana na kuchelewa kuanza kwa kazi za ujenzi wa mradi.

    iii. Mradi wa Uimarishaji wa huduma za Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira

    Zanzibar (INDIA)

    67. Mheshimiwa Spika, Mradi huu unagharamiwa kwa mkopo kutoka Serikali ya India kupitia

    Benki ya Uagizaji na Usafirishaji ya India (Export-Import Bank of India – “EXIM Bank

    India”) na mchango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Kazi zinazotarajiwa kufanyika

    ni ujenzi wa mtambo wa kusafisha maji machafu (Kisakasaka) na ulazaji wa mabomba ya

    kusambazia maji katika shehia za Mji Mkongwe, Kilindi, Nungwi, Fukuchani, Kigunda,

    Kendwa, Pwani Mchangani, Kiwengwa, Machui, Miwani, Kidimni, Kitumba, Kiboje,

    Kwambani, Mgenihaji kwa Unguja na Taifu, Kinyasini, Wambaa, Ali Khamis Camp,

    Vitongoji, Kilindini, Micheweni, Konde, Makangale, Bungumi na Machengwe kwa upande

    wa Pemba.

    Aidha, kwa kipindi kinachoripotiwa mradi umekamilisha tathmini na kumpata Mshauri

    Mwelekezi wa mradi na tayari ameshaanza kazi.

    68. Mheshimiwa Spika, Mradi huu unatarajia kutumia TZS bilioni 3.68 kutoka kwa Muhisani.

    Hadi kufikia Mwezi Machi 2020 hakuna fedha zilizopatikana kutokana na kuchelewa kuanza

    kwa kazi za ujenzi wa mradi.

    iv. Mradi wa Kuimarisha Miundombinu ya Maji ya Mkoa Wa Mjini/Magharibi –

    (JICA.)

  • 24

    69. Mheshimiwa Spika, mradi huu unagharamiwa kwa pamoja kati ya Serikali ya Jamuhuri ya

    Muungano wa Tanzania na Serikali ya Japan kupitia Shirika la Misaada la Japan (JICA)

    ambapo jumla ya Dola za Kimarekani (USD) Milioni 100 zitatolewa na Serikali ya Japan.

    Aidha, mradi unaendelea na kazi ya kuandaa na kupelekea taarifa zilizohitajika katika

    kufanikisha uandaaji wa mikataba ya makubaliano ya mradi.

    70. Mheshimiwa Spika, Fedha zilizotengwa kwa mwaka kwa upande wa Muhisani ni TZS

    Bilioni 4.557. Hadi kufikia Machi 2019 mradi huu haujasainiwa, hivyo hakuna fedha

    zilizoingizwa.

    v. Mradi wa Uendelezaji wa Visima Vya Ras- Al- Khaimah

    71. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu kupitia Mamlaka ya Maji imefanikiwa kuviendeleza

    visima 59 vilivyochimbwa kupitia mradi wa Ras-al-khaimah na vinatoa huduma kwa jamii.

    Uendelezaji huo unafanyika kupitia Mfuko wa Miundombinu (Infrustructure Fund ) ambapo

    kazi zilizokamilika ni upelekeaji wa umeme na taratibu za manunuzi ya miundombinu

    mengine kwa ajili ya uendelezaji wa visima vya Ras-al-Khaimah yanaendelea.

    72. Mheshimiwa Spika, Fedha zilizopangwa kwa mwaka ni TZS Bilioni 3.0 na Fedha

    zilizopatikana ni TZS Bilioni 2.015 sawa na asilimia 67 ya makadirio.

    vi. Uchimbaji wa Visima na Usambazaji Maji Vijijini (China).

    73. Mheshimiwa Spika, mradi huu wa Uchimbaji wa Visima na Usambazaji wa huduma ya maji

    safi umekamilisha kazi ya uchimbaji wa visima viwili (2) katika eneo la Donge, Ulazaji wa

    bomba kwa masafa ya kilomita 6 kutoka eneo la visima Donge hadi kwenye matangi

    Bandamaji, ujenzi wa matangi 2 (1 Donge na 1 Bandamaji) pamoja na ulipaji wa fidia za

    mazao ya wananchi wa Donge na Banda maji.

    74. Mheshimiwa Spika, Fedha zilizopangwa kwa mwaka kwa upande wa Serikali ni TZS

    Milioni 863 na Muhisani ni TZS Bilioni. 5.081. Fedha zilizopatikana kwa upande wa

    Serikali ni TZS Milioni 198 sawa na asilimia 23 na TZS 5.106 bilioni sawa na asilimia 100

    kwa upande wa Muhisani.

  • 25

    KAZI ZA KAWAIDA

    i. Mafunzo ya Wafanyakazi

    75. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2019/2020, Wizara yangu kupitia Mamlaka ya

    Maji imeendelea kuwapatia mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu ndani na nje ya nchi

    Wafanyakazi kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa

    majukumu yao ya kazi. Hadi kufikia Machi 2020 jumla ya wafanyakazi 35 wamepatiwa

    mafunzo ya muda mfupi na wafanyakazi 6 mafunzo ya muda mrefu kama inavyoonekana

    katika kiambatisho “C1 na C2”.

    ii. Matumizi ya Nishati ya Jua Katika Visima na Vyanzo vya Maji

    76. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu kupitia Mamlaka ya Maji imefanikiwa kufunga Mitambo

    ya Nishati ya Jua katika kisima cha Chumbuni na Ukongoroni na tayari vinatoa huduma kwa

    wananchi.

    iii. Utanuzi na Ukarabati wa Mtandao wa Maji

    77. Mheshimiwa Spika, Mamlaka ya Maji katika Mwaka wa Fedha 2019/2020 imefanikiwa

    kufanya Utanuzi na Ukarabati wa Mtandao wa Maji kwa masafa ya Kilomita 10.7 katika

    maeneo ya Pangeni 1km, Saateni – Kwaabasi Hussein 1km, Kijichi 5.234 km na Jumbi –

    Mwera 2.0 km kwa Unguja na 1.5 km katika eneo la Mtangani kwa upande wa Pemba.

    iv. Matengenezo ya Mabomba

    78. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu kupitia Mamlaka ya Maji imefanya matengenezo ya

    mabomba katika maeneo 57 kwa Unguja na Pemba kama inavyoonekana katika Jaduweli

    lifuatalo:

    Jaduweli Nambari 2: Matengenezo ya Mabomba Unguja na Pemba

    Unguja Pemba

    1. Michenzani 20 Mombasa 1 Ukutini

    2. Magomeni 21 Meya 2 Wingwi Mapofu

    3. Gulioni 22 Shaurimoyo 3 Mchua

    4. Makadara 23 Jang’ombe 4 Junguni

  • 26

    5. Muungano 24 Darajani 5 Machomane

    6. Mkele 25 Maruhubi 6 Mkoroshoni

    7. Sogea 26 Saateni 7 Gombani

    8. Migombani 27 Vuga 8 Kiwani

    9. Mombasa 28 Amani 9 Jadida

    10. Mpendae 29 Kilimani 10 Vitongoji

    11. Nyerere 30 Raha leo 11 Amani Road

    12 Makadara 31 Kwahani 12 Bogoa

    13 Nyarugusu 32 Forodhani 13 Vikunguni

    14 Kwaalamsha 33 M/Mchomeke 14 Wambaa

    15 M/Makumbi 34 Kianga 15 Masipa

    16 Mpendae 35 Welezo 16 Chokocho

    17 Mikunguni 36 Michungwa Miwili 17 Mtambwe Kusini

    18 Dole 37 Uzi 18 Gombani

    19 Kibele 38 Mchangani 19 Bahanasa

    v. Matengenezo ya Hitilafu za Umeme

    79. Mheshimiwa Spika, Mamlaka ya Maji Zanzibar katika Mwaka wa Fedha 2019/2020,

    ilifanikiwa kufanya marekebisho ya hitilafu za umeme katika vituo 52 kama inavyoonekana

    katika jadweli lifuatalo:

    Jaduweli Nambari 3: Marekebisho ya Hitilafu za Umeme Katika Vituo Vya Maji Unguja

    na Pemba

    Unguja Pemba

    1 Makunduchi RH 19. Kitogani 1. Bimtumwa-1

    2. Mikuuni 20. Muembe Mchomeke 2. Ole Skuli

    3. Kibele 21. Uzini 3. Kwapweza

    4. Jendele 22. Bweleo 4. Chanjaani

    5. Mtende RH 23. Jambiani 5. Amani Road

    6. Chumbuni Sola 24. Makunduchi 6. Sharifuali-1

    7. Mzungu Punda 26. Kijito Upele 7. Kironjo

    8. Dole 27. Donge Mchina 8. Kikunguni

    9. Chunga UO9 28. Mbweni 9. Masipa

    10.K/Samaki Masumbani 29. Mtopepo 10. Ole Skuli

    11. Kaburi Kikombe U158 30. Donge Mchina 11. Mkanyageni

    12. Chumbuni (Mbunge) 31. Jambiani 12. Kilindi-1

    13. Chumbuni Tasaf 32. Kiboje 13. Ole Uhanga

    14. Tomondo 33. Chunga 14. Tosa

    15. Msikiti Mzuri 34. Kianga 15. Chokocho

  • 27

    16. Dimani Cave 35. Kwerekwe C 16. Gombani

    17. BLW 36. Bububu

    18. Mombasa

    vi. Matengenezo ya Pampu na Mota

    80. Mheshimiwa Spika, Mamlaka ya Maji Zanzibar katika mwaka wa fedha 2019/2020,

    ilifanikiwa kufanya marekebisho ya pampu na mota zilizoungua katika vituo 38 kama

    inavyoonekana katika jadweli lifuatalo

    Jaduweli Nambari. 4: Matengenezo ya Pampu na Mota Unguja na Pemba

    Unguja Pemba

    1 Hali ya Hewa 1 Kengeja 15 Shengejuu

    2 Chumbuni Tasaf 2 Kwa Changawe 16 Pujini - Dodo

    3 Basra 3 Manyaga 17 Sharifuali-1

    4 Chwaka 4 Junguni 18 Mkanyageni

    5 Jambiani Mfumbwi 5 Penjewani 19 Kangani

    6 Mfenesini 6 Michenzan, 20 Konde

    7 Chunga U26 7 Ulenge 21 Mlindo

    8 Mtopepo 8 Chokocho Skuli 22 Kilindi-2

    9 Donge Kipange 9 Kifundi 23 Kiwani-

    10 Chumbuni 10 Mahuduthi 24 Shidi

    11 Mbunge 11 Jojo 25 Makombeni-Darajani

    12 Kiuyu - Manda 26 Mbuzini

    13 Darajani 27 Bimtumwa-2

    14 Tosa-1

    vii. Uwekaji wa Pampu na Mota Mpya

    81. Mheshimiwa Spika, Mamlaka ya Maji Zanzibar katika Mwaka wa Fedha 2019/2020,

    imefanikiwa kununua na kufunga Pampu na Mota 35 katika maeneo ya Unguja na Pemba

    kama inavyoonekana katika jadweli lifuatalo

    Jaduweli Nambari 5: Uwekaji wa Pampu na Mota Mpya Katika Visima vya Maji Unguja

    na Pemba

    Unguja Pemba

    1 Donge - Mwanakombo 11 Kinduni 1 Ndagoni- Kilindi 9 Kikunguni

    2 Ukongoroni 12 Kandwi 2 Changuo 10 Junguni

    3 K/Samaki 13 Chaani 3 Shumba Viamboni 11 Masipa

    4 Dimani BH 14 Makunduchi 4 Junguni 2 12 Gombani- Mchua

  • 28

    viii. Kutoa Elimu Kwa Watumiaji wa Maji

    82. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu kupitia Mamlaka ya Maji katika Mwaka wa fedha

    2019/2020, imefanikiwa kutoa elimu na kuhamasisha Jamii kwa njia ya Televisheni, redio na

    mikutano juu ya Mafanikio ya Mamlaka ya Maji katika kipindi cha Miaka 56 ya Mapinduzi

    Matukufu ya Zanzibar, Umuhimu wa kuchangia huduma ya maji na kutunza miundombinu

    na rasilimali maji. Aidha, vipindi 15 vya Televisheni na 17 vya Redio vimefanyika.

    Vilevile, jumla ya Mikutano 64 ya uhamasishaji imefanyika katika maeneo mbali mbali ya

    Unguja na Pemba kama inavyoonekana katika kiambatisho “D”.

    ix. Matengenezo ya Vichwa vya Visima (well–head)

    83. Mheshimiwa Spika, Mamlaka ya Maji Zanzibar katika Mwaka wa Fedha 2019/2020,

    ilifanikiwa kufanya matengenezoo ya wellhead katika maeneo ya Chunga U26, Mtende na

    Fuoni Chunga 08 kwa Unguja na Kilindi, Fundo-Uvinje, Mtangani, Jambangome na

    Kinyasini Kwale – Gongo kwa upande wa Pemba.

    x. Ufungaji wa Mita na Usajili wa Wateja Wapya wa Maji

    84. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Machi 2020 Mamlaka ya Maji imefanikiwa kusajili wateja

    wapya 3,775 (2,181 Unguja na 1,594 Pemba). Aidha, Mamlaka imefanikiwa kufunga mita

    1,542 (1,105 Unguja na 437 Pemba) katika maeneo ya Wilaya ya Kaskazini “A”, Kaskazini

    “B”, Magharibi “A”, Magharibi “B,” Mjini, Wilaya ya Kati na Kusini kwa Unguja na Chake

    Chake, Mkoani, Wete na Micheweni upande wa Pemba kwa Pemba.

    xi. Uhifadhi wa Vianzio vya Maji

    Ulenge

    5 Donge Tinga Tinga 15 Matemwe 5 Makombeni- Mgagadu 13 Kangani 2

    6 Meli nne Masumbani 16 Kibele 6 Mkanyageni-Miembeni 14 Konde-Polisi

    7 Jendele 17 Fuoni Chunga 7 Ngwachani 2 15 Sharifu Ali 1&2

    8 Masingini 18 Mfenesini 8 Bimtumwa 1&2

    9 Kizimbani 19 Kitogani

    10 Jambiani 20 Mgeni Haji

  • 29

    85. Mheshimiwa Spika, Miongoni mwa majukumu ya Mamlaka ya Maji ni usimamizi, utunzaji

    na uhifadhi wa rasilimali maji katika kutekeleza hayo Mamlaka ya Maji kwa mwaka wa

    fedha 2019/2020 imefanikiwa kujenga uzio katika kisima cha Bumbwini Uwandani kwa

    Unguja na Mtangani, Kilindi na Amani Road kwa Pemba.

    xii. Ukusanyaji wa Mapato

    86. Mheshimiwa Spika, Mamlaka ya Maji kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 ilijipangia

    kukusanya jumla ya TZS Bilioni 5.638 kutokana na mauzo ya maji na mapato mengineyo.

    Hadi kufikia Machi 2020, jumla ya TZS Bilioni 2.709 zimekusanywa sawa na asilimia 48 ya

    makadirio.

    87. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu kupitia Mamlaka haikuweza kufikia lengo iliojipangia

    kutokana baadhi ya maeneo kuwa na upungufu wa maji na hata yale maeneo ambayo

    huduma hii inapatikana vizuri wananchi walio wengi bado hawajaitikia vizuri wito wa

    kuchangia huduma hii. Aidha, nitumie nafasi hii kutoa wito kwa wananchi wanaopata

    huduma ya maji kuendelea kutoa ushirikiano katika kulipa ankara za maji. Ni vyema

    wananchi watambue kuwa michango yao ni muhimu katika kupanua mtandao wa huduma ya

    maji ili wananchi wengi zaidi waunganishwe na kupata huduma.

    IDARA YA NISHATI NA MADINI

    88. Mheshimiwa Spika, kwa Mwaka wa Fedha wa 2019/2020, Idara ya Nishati na Madini

    ilisimamia na kutekeleza yafuatayo:-

    i. Mradi wa Kuijengea Uwezo Sekta ya Nishati (Zanzibar Energy Sector Support

    Project)

    89. Mheshimiwa Spika, Hadi kufikia Machi 2020, mambo yafuatayo yalitekelezwa katika mradi

    huu:

  • 30

    a) Ukamilishaji wa Mfumo Mkuu wa Kuhifadhi Takwimu za Nishati-“Energy

    statistics database”

    90. Mheshimiwa Spika, Idara imeendelea kusajili takwimu za bidhaa za Nishati (mafuta,

    umeme, kuni na mkaa) kwa kuziingiza katika tovuti ya Idara ya Nishati na Madini. Aidha,

    Idara inashirikiana na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali katika utekelezaji wa suala hili

    ili kukidhi matakwa ya kisheria.

    b) Kufanya mapitio ya Sera ya Nishati ya mwaka 2009 na utungaji wa Sheria ya

    Nishati ya Zanzibar “Zanzibar Energy Act”.

    91. Mheshimiwa Spika, Rasimu ya mapitio ya Sera ya Nishati iliwasilishwa kwa Kamati ya

    Makatibu Wakuu mnamo mwezi Disemba 2019 ambapo maoni na maelekezo yao

    yamepelekea Rasimu hiyo kufanyiwa marekebisho zaidi. Hatua inayofuatia ni kuiwasilisha

    tena kwa Kamati ya Makatibu Wakuu ili kupata ridhaa ya kuiwasilisha Baraza la Mapinduzi

    kwa hatua zinazofuata. Sambamba na hilo, Idara inaendelea na matayarisho ya Rasimu ya

    Sheria ya Nishati ambayo inatarajiwa kukamilika baada ya kuridhiwa Sera ya Nishati.

    c) Kuijengea Uwezo Idara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Zanzibar

    (ZECO), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (ZURA) na

    Wizara

    92. Mheshimiwa Spika, kazi ya kuzijengea uwezo taasisi za Nishati imeendelezwa ambapo hadi

    Mwezi Machi 2020, jumla ya maafisa wawili (2) kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na

    Nishati, maafisa wawili (2) kutoka Idara ya Nishati, maafisa (8) kutoka ZURA na maafisa

    (12) kutoka ZECO wamepatiwa mafunzo nje ya Nchi ikiwemo Africa Kusini, Kenya,

    Uganda na Misri. Aidha jumla ya semina tisa (9) za mafunzo ya ndani ya Nchi

    zimeendeshwa kwa maafisa tofauti kutoka katika Taasisi hizo za Nishati. Mafunzo hayo

    yamesaidia kuimarisha utoaji wa huduma za Nishati hapa Zanzibar.

    ii. Utekelezaji wa Kazi za Mradi wa Nishati Mbadala

  • 31

    93. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha Zanzibar inazalisha umeme kwa kutumia nishati ya

    jua na upepo, Serikali imeridhia wazo la kuendesha uwekezaji huu kwa ushirikiano baina ya

    Serikali na Sekta Binafsi (Public Private Partnership – PPP). Hivyo, Kamati Maalum

    imeundwa ambayo inashirikisha Wizara ya Ardhi Nyumba Maji na Nishati, Wizara ya Fedha

    na Mipango, Tume ya Mipango na Shirika la Umeme katika kusimamia suala hili ambapo

    Makampuni kadhaa yameonesha nia ya kutaka kuekeza katika eneo hili la nishati.

    Aidha, Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia (World Bank) imeanza utekelezaji wa

    hatua za awali kwa kuandaa mazingira yatakayowezesha uwekezaji huu ikijimuisha

    utayarishaji wa maeneo ya uwekezaji, utayarishaji wa rasimu ya zabuni na matayarisho ya

    ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji , upokeaji na usambazaji wa umeme kutoka maeneo

    ya uzalishaji.

    iii. Kushiriki Katika Masuala ya Nishati ya Kitaifa, Kikanda, na Kimataifa.

    94. Mheshimiwa Spika, Idara ya Nishati na Madini imeendelea kushiriki katika mikutano ya

    pamoja kati ya Wizara ya Nishati na Wizara ya Madini ya Jamhuri ya Muungano wa

    Tanzania kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika masuala ya Nishati na Madini. Aidha

    Idara imeshiriki katika Mkutano Mkuu wa 18 wa Baraza la IRENA (International Renewable

    Energy Agency) uliofanyika nchini Abu Dhabi, UAE mwezi Novemba 2019.

    SHIRIKA LA UMEME

    95. Mheshimiwa Spika, Shirika la Umeme Zanzibar limeendeleza juhudi za kusambaza na

    kuimarisha upatikanaji wa huduma ya umeme mijini na vijijini. Utekelezaji wa kazi hizo

    unachangia katika kukuza ustawi wa Jamii na pato la Taifa.

    Mapato na Matumizi

    96. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2019/2020, Shirika lilikadiria kukusanya TZS

    Bilioni 146.576 kutokana na biashara ya kuuza umeme na huduma nyenginezo zinazotolewa

    kwa wananchi. Hadi kufikia Machi 2020 Shirika limekusanya jumla ya TZS Bilioni 98.939

    sawa na asilimia 67.5 ya makadirio ya mwaka.

  • 32

    Kwa upande wa matumizi, Shirika lilikadiria kutumia TZS Bilioni 145.655. Hadi kufikia

    Machi 2020 Shirika limetumia TZS Bilioni 90.529 sawa na asilimia 62.1 ya Makadirio.

    i. Uimarishaji wa Miundombinu ya Umeme

    97. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha huduma ya Umeme inapatikana kwa ubora

    unaotakiwa pamoja na kupunguza upotevu wa Umeme, Shirika limeimarisha huduma ya

    umeme katika maeneo 39 yaliyokuwa na umeme mdogo, kubadilisha nguzo mbovu 1,551 na

    kupima transfoma 1,089 kwenye maeneo ya Mijini na Vijijini pamoja na kuzifanyia

    marekebisho Transfoma zilizobainika kuwa na kasoro.

    ii. Usambazaji wa Umeme Vijijini

    98. Mheshimiwa Spika, kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, Shirika lilikadiria kupeleka huduma

    ya umeme katika vijiji 45 Unguja na Pemba. Hadi kufikia Machi 2020, Shirika la Umeme

    limefanikiwa kupeleka huduma hiyo katika vijiji 44 ambayo ni sawa na asilimia 98 ya lengo.

    Orodha ya vijiji hivyo inaonekana katika Kiambatisho “E”.

    Katika ufanikishaji wa kazi hizo, Shirika limetumia jumla ya TZS Bilioni 1.688 kwa ajili ya

    ununuzi wa vifaa vya umeme vikiwemo waya, nguzo, transfoma pamoja na malipo ya fidia

    za mali na mazao ya wananchi yaliyoathiriwa na utekelezaji wa kazi hizo.

    iii. Mradi wa Ufungaji wa Mita za TUKUZA

    99. Mheshimiwa Spika, kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, Shirika lilipanga kubadilisha mita

    11,250 za kawaida na kufunga mita za TUKUZA. Hadi kufikia Machi 2020 Shirika

    limebadilisha mita za 11,751 sawa na asilimia 104 ya utekelezaji. Lengo la mradi huu ni

    kukuza ukusanyaji wa mapato ya Shirika na kupunguza malimbikizo ya madeni.

    MAMLAKA YA UDHIBITI WA HUDUMA ZA MAJI NA NISHATI

    100. Mheshimiwa Spika, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (ZURA)

    katika Mwaka wa Fedha 2019/2020 imetekekeleza kazi zifuatazo;

    i. Ujenzi wa jengo jipya litakalotumiwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati;

    (Taasisi zinazohusika na Nishati pamoja na ZURA).

  • 33

    ii. Kuratibu mradi wa ujenzi wa Bandari na Bohari ya Mafuta Mangapwani ambapo

    Upembuzi Yakinifu (feasibility study) umeshaanza na uhakiki wa kitaalamu wa

    kujiridhisha (due diligence) umefanyika.

    iii. Ununuzi wa Vifaa vya maabara kwa ajili ya kuchunguza ubora wa bidhaa

    zinazodhibitiwa.

    iv. Kukagua vituo 76 vya kuuzia Mafuta na Bohari 5 Unguja na Pemba kwa lengo la

    kuhakikisha ubora wa bidhaa na huduma zinazotelewa. Aidha, ZURA imekagua

    maeneo kumi na saba (17) kufuatia maombi ya ujenzi wa Vituo vipya vya mafuta

    ambapo maeneo saba (7) kwa Unguja na manne (4) kwa Pemba yamekidhi vigezo na

    kuruhusiwa kuendelea na hatua za ujenzi.

    v. Kukamilisha taratibu zote za Udhibiti wa Gesi ya matumizi ya majumbani (Liquified

    Petroleum Gas - LPG) ili kuwapa leseni waingizaji na wasambazaji wa bidhaa hiyo.

    vi. Kukamilisha Taratibu za kudhibiti huduma ya Maji na Umeme ili kuanza kuzipatia

    leseni taasisi za ZECO na ZAWA kwa lengo la Udhibiti.

    vii. Kuajiri Mshauri Elekezi kupitia mradi unaodhaminiwa na AfDB kwa ajili ya kuunda

    Mfumo wa TEHAMA utakaosimamia huduma zinazodhibitiwa kwa njia ya

    elektroniki.

    MAMLAKA YA UDHIBITI WA UTAFUTAJI NA UCHIMBAJI WA MAFUTA GESI

    ASILIA

    101. Mheshimiwa Spika, Mamlaka ya Udhibiti wa Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi

    Asilia ni taasisi yenye jukumu la kusimamia na kudhibiti shughuli zote za Utafutaji na

    Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia hapa Zanzibar.

    102. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2019/2020, Mamlaka ya Udhibiti wa

    Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia imetekeleza kazi zifuatazo:-

    i. Kuandaa Rasimu za Kanuni na Miongozo ya Sheria ya Mafuta na Gesi Asilia

    103. Mheshimiwa Spika, Mamlaka imefanikiwa kuandaa rasimu sita (6) za Kanuni na

    Miongozo kwa ajili ya Kusimamia Shughuli za Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi

    Asilia kati ya rasimu nane (8) zilizokusudiwa. Rasimu zilizoandaliwa ni:

  • 34

    a) Rasimu ya Kanuni ya Mgawanyo wa Vitalu (Graticulation Regulation) ambayo

    imeshakamilika na kuwasilishwa kwa Afisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

    b) Rasimu ya Mpango Mkakati wa Mamlaka (Strategic Plan) ambayo imeshakamilika

    na inasubiri kuwasilishwa katika kikao cha Bodi ya Mamlaka.

    c) Rasimu ya Kanuni ya Fedha (Financial Regulation),

    d) Rasimu ya Kanuni ya Thamani ya Wadau wa ndani (Local Content Regulation)

    ambayo ipo katika hatua ya kuwasilishwa kwa wadau kwa ajili ya kupatiwa maoni.

    e) Rasimu ya Kanuni ya Wafanyakazi (Staff Regulation) ambayo ipo katika hatua ya

    kuwasilishwa kwa wadau kwa ajili ya kupatiwa maoni.

    f) Rasimu ya Kanuni ya Utafiti wa Awali, Mitetemo na Uwasilishaji wa taarifa za

    Utafiti kwa Mamlaka (Reconnaissance, Seismic and Data submission Regulation).

    104. Mheshimiwa Spika, timu ya wataalamu wanane (8) pamoja na wajumbe wanne (4) wa

    Bodi ya Mamlaka kwa pamoja walishiriki katika Warsha mbili tofauti zilizofanyika Mkoani

    Morogoro chini ya Mshauri elekezi kutoka Norway na Wataalamu wa Mamlaka ya Mafuta

    na Gesi Asilia ya Norway (Norwegian Petroleum Directorate Experts) kwa ajili ya

    kuimarisha baadhi ya rasimu za Kanuni zilizoandaliwa na Mamlaka kwa lengo la kupata

    ushauri wa kitaalamu katika rasimu hizo. Aidha, baada ya mashauriano ya pamoja kati ya

    Mshauri Elekezi kutoka Norway na Timu kutoka Mamlaka, iliafikiwa kuwa Rasimu ya

    Utafiti wa Awali wa Mafuta na Gesi Asilia, Rasimu ya Kanuni ya shughuli za Utafiti kwa

    njia ya Mtetemo pamoja na Rasimu ya Kanuni ya Uwasilishaji wa Taarifa za Mafuta na Gesi

    Asilia ziunganishwe pamoja na kuwa rasimu moja itakayojulikana kwa jina la Rasimu ya

    Kanuni ya Utafiti wa Awali, Mitetemo na Uwasilishaji wa taarifa za Utafiti kwa Mamlaka

    “Reconnaissance, Seismic and Data submission Regulation” kwa vile masuala yote matatu

    yanakwenda sambamba.

    ii. Kuendesha Programu za Kujenga Uelewa kwa Makundi na Wananchi

    Katika Masuala mbali mbali Yanayohusiana na Mafuta na Gesi Asilia

    105. Mheshimiwa Spika, Mamlaka imeendesha programu 43 za kujenga uelewa kwa

    wananchi wa Unguja na Pemba kati ya Programu 100 zilizopangwa. Kati ya hizo, programu

    tano (5) zilifanyika Dar es Salaam na Zanzibar kwa njia za Makongamano na Maonesho.

  • 35

    Mamlaka ilipata nafasi ya kuandaa na kushiriki kongamano kubwa hapa Zanzibar

    lililowashirikisha vijana 500 kutoka asasi mbali mbali za kiraia na vyombo vya habari. Kwa

    upande wa Maonesho, Mamlaka ilishiriki Maonesho ya sita ya Maadhimisho ya miaka 56 ya

    Mapinduzi ya Zanzibar yaliyoshirikisha taasisi mbali mbali za Serikali, Asasi za kiraia na

    wajasiriamali wa Bara na Visiwani kuanzia tarehe 02 hadi 17 Januari 2020.

    Vilevile , jumla ya programu 38 ziliendeshwa kupitia vyombo vya habari nchini vikiwemo

    Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC), Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Zanzibar Cable

    Television pamoja na Magazeti ya Zanzibar leo, Uhuru na Mwananchi. Lengo kuu la

    programu zote hizi ni kutoa elimu ya shughuli za Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi

    Asilia hapa Zanzibar sambamba na kuendelea kuitambulisha Mamlaka ya Udhibiti wa

    Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia ikiwa ndio msimamizi mkuu wa shughuli

    za Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asili hapa Zanzibar.

    iii. Kuendelea Kusimamia Zoezi la Utafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia

    106. Mheshimiwa Spika, Mamlaka imeendelea kufuatilia zoezi la Utafutaji wa Mafuta na

    Gesi Asilia katika hatua za usafishaji wa taarifa zilizochukuliwa pamoja na tafsiri zake (data

    processing and interpretation) kwa kitalu cha Pemba- Zanzibar. Kamati ya wataalamu wa

    ZPRA, ZPDC na Kampuni ya Rak Gas imefanikiwa kujadili hatua iliyofikiwa pamoja na

    changamoto zake katika zoezi hilo kufuatia ripoti ya muendelezo wa matokeo ya tafsiri ya

    awali ya taarifa za mtetemo kwa Kitalu cha Pemba –Zanzibar iliyowasilishwa na Kampuni

    ya Rak Gas.

    Pia, Mamlaka ya Udhibiti wa Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia pamoja na

    Kampuni ya Maendeleo ya Mafuta na Gesi Asilia zimeendelea na vikao kupitia Timu ya

    Usimamizi wa Mkataba wa PSA ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kujadiliana hatua

    zilizofikiwa za utekelezaji wa Mkataba wa Mgawanyo (PSA), Mpango wa Ununuzi wa vifaa

    vya kusomea na kutafsiri taarifa za Mafuta na Gesi Asilia pamoja na mafunzo kwa

    wataalamu wa taasisi hizi mbili.

    107. Mheshimiwa Spika, vile vile katika kusimamia zoezi la kusafisha na kutafsiri taarifa

    zilizochukuliwa, Mamlaka imefanya ziara tatu (3) nchini Ras Al Khaimah na moja (1) nchini

    Norway kwa ngazi ya maafisa watendaji. Pia, Mamlaka ilishiriki ziara moja (1)

  • 36

    iliyowakutanisha Timu ya Serikali na Mkandarasi wa Mradi huko Kualar Lumpar nchini

    Malaysia ili kuangalia maendeleo na changamoto katika zoezi la usafishaji na Tafsiri ya

    Taarifa kwa kitalu cha Pemba- Zanzibar.

    iv. Kusimamia Zoezi la Utafiti wa Pamoja (Multi Client) wa Mafuta na Gesi

    Asilia Katika Maeneo ya Kina kirefu cha Bahari ya Zanzibar.

    108. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2019/2020, Mamlaka ilipanga kukamilisha

    hatua za kumpata Mkandarasi wa kufanya zoezi la Utafiti wa Pamoja wa Mafuta na Gesi

    Asilia katika Maeneo ya kina kirefu cha Bahari ya Zanzibar.

    Changamoto kubwa kwa Mradi huu ni kukosekana kwa Kampuni ya kupewa zabuni

    kutokana na kukosa mrejesho wa ununuzi wa zabuni licha ya kujitokeza kwa kampuni saba

    zilizoonesha nia ya kutaka kushiriki ushindani wa zabuni hii.

    Kufuatia matokeo ya zoezi hili, Mamlaka inaendelea na utekelezaji wa agizo la Serikali ya

    Mapinduzi ya Zanzibar kuhusiana na kupatiwa taarifa za Mafuta na Gesi Asilia kutoka

    Shirika la Maendeleo ya Petroli la Tanzania – TPDC ambazo zilichukuliwa miaka ya 2000

    katika eneo la bahari ya Zanzibar ili kufanyiwa usafishaji mwengine (re-processing). Lengo

    la kuzifanyia usafishaji mwengine Taarifa hizi ni kuweza kutumika kwa ajili ya ugawaji wa

    vitalu kupitia kampuni ya shughuli za utafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia kwa masharti

    yatakayoafikiwa baina yao.

    v. Kuendelea Kushirikiana na Washirika wa Maendeleo Katika Kuimarisha

    Taasisi na Kuwapatia Watendaji Nafasi za Mafunzo Yanayohusiana na

    Usimamizi wa Mafuta na Gesi Asilia.

    109. Mheshimiwa Spika, Mamlaka inaendelea kushirikiana na Serikali ya Norway kupitia

    mradi wa Mafuta kwa Maendeleo (Oil for Development - OfD). Kupitia mradi huu, kampuni

    ya Bridge Consultant ambayo ni Mshauri Elekezi imekamilisha ripoti ya mwisho ya Mpango

    wa Uendelezaji wa Mamlaka kiutendaji ikiwa ni sehemu ya kuendeleza na kukuza

    mashirikiano baina ya Mamlaka ya Mafuta na Gesi Asilia ya nchini Norway (Norwegian

    Petroleum Directorate - NPD) na Mamlaka ya Udhibiti wa Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta

  • 37

    na Gesi Asilia. Kufuatia ripoti hiyo Mamlaka imeanza utekelezaji wa mapendekezo

    yaliyowasilishwa katika ripoti hiyo.

    Aidha, kupitia mradi huu, Mamlaka imefanikiwa kuajiri Mshauri Elekezi ambae ni Kampuni

    ya Simonsen VogtWiig (SVW) kutoka Norway ambayo kwa mujibu wa makubaliano

    yaliyofikiwa, atafanya kazi ya kutoa ushauri wa kitaalamu kwa muda wa miezi sita (6) katika

    kuandaa kanuni mbali mbali za kitaalamu za Mafuta na Gesi Asilia.

    110. Mheshimiwa Spika, Vile vile, Bodi ya Mamlaka pamoja na wafanyakazi wa Mamlaka

    wamekuwa wakishiriki mafunzo tofauti ya muda mfupi yaliyofanyika nchini Norway katika

    vipindi tofauti kupitia Mradi wa OfD kwa lengo la kujifunza usimamizi wa taarifa za Mafuta

    na Gesi Asilia, Utawala bora katika masuala ya Mafuta na Gesi Asilia na Mafunzo

    yanayohusiana na Uchumi wa Mafuta na Gesi Asilia.

    Kimsingi, mafunzo hayo yanasaidia kujenga uwezo na kubadilishana uzoefu katika masuala

    ya usimamizi na uendelezaji wa Sekta ya Mafuta na Gesi Asilia, kuitangaza Mamlaka yetu

    nje ya nchi pamoja na kuwashawishi washirika wa maendeleo katika kuisaidia Zanzibar.

    vi. Kushiriki katika Masuala ya Mafuta na Gesi Asilia ya Kitaifa, Kikanda, na

    Kimataifa.

    111. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza kazi hii, Mamlaka imeshiriki mikutano miwili (2)

    ya Jumuiya ya Afrika Mashariki katika masuala ya Mafuta na Gesi Asilia iliyofanyika

    Uganda na Sudani ya Kusini. Aidha, katika mikutano hiyo, washiriki kutoka nchi

    wanachama wamekubaliana kuendelea na mashirikiano katika uendelezaji wa sekta ya

    Mafuta na Gesi Asilia kwa ajili ya ukuaji wa uchumi wa nchi husika.

    Mikutano hiyo imesaidia kubadilishana uzoefu katika masuala ya usimamizi na

    uendelezaji wa sekta ya Mafuta na Gesi Asilia, kuitangaza nchi yetu nje ya nchi pamoja

    na kuwashawishi washirika wa maendeleo katika kuisaidia Zanzibar.

    vii. Kuimarisha Mazingira ya Kazi kwa Watendaji ikiwemo Ubora wa Ofisi,

    Nguvu kazi pamoja na Kuwapatia Mafunzo Wafanyakazi waliopo ili Kuleta

    Ufanisi zaidi wa Mamlaka.

  • 38

    112. Mheshimiwa Spika, Katika jitihada za kuhakikisha kuwa watendaji wa Mamlaka hii

    wanakuwa na mazingira bora zaidi na salama ya kufanyia kazi, Mamlaka imefanikiwa

    kuongeza idadi ya vitendea kazi vikiwemo ununuzi wa gari moja (1) na jenereta la

    dharura. Pia, Mamlaka imefanikisha ushiriki wa wafanyakazi wake mbali mbali katika

    mafunzo ya muda mrefu na mfupi ili kukabiliana na upya wa sekta ya Mafuta na Gesi

    Asilia hapa Zanzibar.

    Vile vile wafanyakazi wanne (4) wameshiriki katika mafunzo ya vitendo yaliyofanyika

    Wilayani Meatu Mkoani Simiyu huko Tanzania Bara Mwezi Novemba 2019 kwa muda

    wa siku 14 katika zoezi la Uchimbaji wa visima vifupi vya kuchukua sampuli. Lengo kuu

    la mafunzo hayo ambayo yamesimamiwa na Kampuni ya Maendeleo ya Mafuta ya

    Tanzania (TPDC) ni kujifunza namna ya uchukuaji wa sampuli za miamba kwa ajili wa

    utafiti wa Mafuta na Gesi Asilia.

    KAMPUNI YA MAENDELEO YA MAFUTA NA GESI ASILIA

    113. Mheshimiwa Spika, Kampuni ya Maendeleo ya Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar ni

    Kampuni ya Serikali yenye jukumu la kushiriki katika Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta,

    kufanya biashara katika Sekta ya Mafuta na Gesi Asilia kwa niaba ya Serikali na kulinda

    maslahi ya Taifa katika Biashara ya Mafuta

    114. Mheshimiwa Spika, Kampuni kwa Mwaka 2019 imetekeleza kazi zifuatazo:

    i. Kuandaa Kanuni ya Wafanyakazi (Staff Regulations) pamoja na Muongozo wa Uajiri

    wa Kampuni (Recruitment Guidelines).

    ii. Kujenga uwezo wa wafanyakazi kwa kuendesha mafunzo ya ndani (in house training)

    kuhusiana na Mafuta na Gesi pamoja na kuwapeleka watendaji wawili (2) mafunzo

    ya muda mfupi nchini Malaysia kuhusiana na uchimbaji na utafutaji wa mafuta.

    Kampuni pia imewapeleka Wahandisi wawili wa Mafuta (Petroleum Engineers)

    Mkoa wa Simiyu Tanzania Bara kujifunza kwa vitendo uchimbaji wa visima vya

    utafiti vya Mafuta na Gesi kupitia Shirika la Maendeleo ya Mafuta Tanzania (TPDC)

    na Mamlaka ya Usimamizi wa Utafutaji Mafuta na Gesi Tanzania (PURA). Vilevile

    Kampuni ilifanya ziara ya kimafunzo Mtwara, Songosongo na Somangafungu kuona

  • 39

    na kujifunza kuhusiana na mitambo ya uchakataji na usafirishaji wa Gesi Asilia.

    Aidha, Kampuni imeshiriki makongamano matatu (3) ya Mafuta na Gesi nchini

    Kenya, Uganda na Dar es Salaam, Tanzania.

    iii. Kampuni imefanya vikao sita (6) na Mkandarasi (Rak Gas) kujadili maendeleo ya

    utafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia.

    iv. Kusimamia utoaji wa huduma za uendeshaji wa ofisi ikiwemo mtandao, umeme,

    ununuzi wa vifaa vya ofisi na vitendeakazi

    115. Mheshimiwa Spika, Kwa Mwaka wa Fedha wa 2019, Kampuni ilipokea mtaji wa hisa

    zenye thamani ya TZS Billioni 2.00 kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambapo

    katika hizo TZS Bilioni 1.8 zilikadiriwa kutumika kwa kazi za maendeleo na uendeshaji

    wa Kampuni. Hadi kufikia Disemba 2019 TZS Milioni 313.808 sawa na asilimia 19

    zimetumika katika kazi za Kawaida.

    MUELEKEO KWA MWAKA WA FEDHA 2020/2021

    116. Mheshimiwa Spika, baada ya kutoa maelezo ya utekelezaji wa bajeti ya Wizara yangu

    kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, sasa naomba kuwasilisha muelekeo wa Bajeti yenye

    kuzingatia Programu ya Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati kwa Mwaka wa

    Fedha 2020/2021.

    a. Programu PN0101: Uendeshaji na Uratibu wa Wizara ya Ardhi.

    b. Programu PN0102: Usimamizi wa Ardhi na Makaazi

    c. Programu PN0105: Usimamizi wa Huduma za Maji na Nishati.

    117. Mheshimiwa Spika, jumla ya TZS Bilioni 110.057 zinatarajiwa kutumika katika

    utekelezaji wa Programu hizi tatu.

    118. Mheshimiwa Spika, Naomba sasa uniruhusu kutoa maelezo kuhusu Programu Kuu na

    Programu ndogo zinazohusiana na Wizara yangu kama ifuatavyo:-

    PROGRAMU KUU PN0101: UENDESHAJI NA URATIBU WA WIZARA YA

    ARDHI

    119. Mheshimiwa Spika, Programu hii inajukumu la kuimarisha uratibu katika utekelezaji wa

  • 40

    Kazi za Wizara ambapo matokeo ya muda mrefu yanayotarajiwa ni Kukuza ufanisi katika

    utawala wa rasilimali pamoja na utoaji huduma za kijamii. Programu hii itasimamiwa na

    Idara ya Mipango, Sera na Utafiti, Idara ya Utumishi na Uendeshaji, na Afisi Kuu Pemba

    ambapo jumla ya TZS Bilioni 3.096 zinatarajiwa kutumika kwa utekelezaji wake.

    Programu hii imegawanyika katika Programu ndogo kama ifuatavyo:-

    PROGRAMU NDOGO YA URATIBU WA MIPANGO, SERA NA TAFITI ZA

    WIZARA.

    120. Mheshimiwa Spika, dhumuni la Programu ndogo hii ni Uratibu wa Shughuli na Kazi

    za Wizara kwa Ufanisi. Kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 Programu hii imepanga

    Kuratibu na kuandaa Mipango na Miongozo ya Kisera ya utekelezaji wa kazi za Wizara,

    Kuratibu uandaaji wa Sheria zilizo chini ya Taasisi za Wizara, Kufuatilia na kutathmini

    utekelezaji wa Programu, Miradi ya Wizara na Kuandaa Tafiti kwa ajili ya kuwezesha

    utoaji wa huduma bora katika sekta za Wizara.

    121. Mheshimiwa Spika, ili kuiwezesha Programu hii kutekeleza majukumu yake kwa mwaka

    wa fedha 2020/2021, naliomba Baraza lako Tukufu kuidhinisha jumla ya TZS Milioni

    328.670

    PROGRAMU NDOGO YA UTAWALA NA UENDESHAJI

    122. Mheshimiwa Spika, lengo la Programu hii ni kusimamia Uendeshaji wa Wizara,

    Usimamizi na Uendelezaji wa Rasilimali watu. Kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021

    Programu hii imepanga kuendeleza kutoa huduma za uendeshaji, kuhakikisha kuwepo

    kwa watendaji wa kutosha na wenye sifa, kujenga uwezo wa wafanyakazi na kuwapatia

    stahiki kwa mujibu wa taratibu za utumishi.

    123. Mheshimiwa Spika, ili kuiwezesha Programu hii kutekeleza majukumu yake kwa

    Mwaka wa Fedha 2020/2021, naliomba Baraza lako Tukufu kuidhinisha jumla ya TZS.

    Bilioni 2.155

    PROGRAMU NDOGO YA URATIBU NA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA

  • 41

    WIZARA PEMBA

    124. Mheshimiwa Spika, dhumuni la Programu hii ni Uratibu na Utekelezaji wa shughuli za

    Wizara Pemba, ambapo kwa mwaka wa fedha 2020/2021 Programu hii imepanga kuratibu

    shughuli za Wizara kwa Pemba, kuimarisha kazi za usimamizi na ufuatiliaji wa Programu

    na miradi ya Maendeleo ya Wizara Pemba na Kuimarisha mazingira bora ya kufanyia

    kazi.

    125. Mheshimiwa Spika, ili kuiwezesha Programu hii kutekeleza majukumu yake kwa mwaka

    wa fedha 2020/2021, naliomba Baraza lako Tukufu kuidhinisha jumla ya TZS Milioni

    612.302

    PROGRAMU KUU PN0102: USIMAMIZI WA ARDHI NA MAKAAZI

    126. Mheshimiwa Spika, Programu hii ina jukumu la kuhakikisha usalama wa matumizi ya

    ardhi (Security of Land Tenure) na huduma za makaazi bora kwa Wananchi. Matokeo ya

    muda mrefu yanayotarajiwa ni kuwa na matumizi ya ardhi yaliyobora na fanisi pamoja na

    Makaazi bora. Programu hii inasimamiwa na Kamisheni ya Ardhi, Bodi ya Uhaulishaji

    Ardhi, Afisi ya Mthamini Mkuu wa Serikali, Mahakama ya Ardhi, Shirika la Nyumba,

    Mamlaka ya Hifadhi na Uendelezaji Mji Mkongwe, Wakala wa Majengo, Bodi ya

    Wakandarasi, Bodi ya Wahandisi, Wasanifu na Wakadiriaji Majengo, Bodi ya Kudhibiti

    Kodi za Nyumba na Bodi ya Kondominio ambapo jumla ya TZS Bilioni 8.138 zinatarajiwa

    kutumika.

    127. Mheshimiwa Spika, Programu hii imegawanyika katika Programu ndogo kama

    ifuatavyo:-

    PROGRAMU NDOGO YA UTAWALA WA ARDHI, NYUMBA NA MAKAAZI

    128. Mheshimiwa Spika, dhumuni la Programu ndogo hii ni kuhakikisha usalama wa umiliki

    wa Ardhi na upatikanaji wa makaazi bora kwa wananchi ambapo matokeo ya muda

    mfupi (output) yanayotarajiwa katika utekelezaji wa Programu hii ni ugawaji na

    usimamizi wa ardhi kwa matumizi mbali mbali, uthamini wa ardhi, usajili wa ardhi,

  • 42

    usimamiaji wa shughuli za upimaji na ramani, upangaji wa miji na matumizi ya ardhi,

    uhifadhi na uendelezaji Mji Mkongwe pamoja na makaazi bora . Jumla ya TZS Bilioni

    7.469 zinatarajiwa kutumika katika Programu ndogo hii.

    KAMISHENI YA ARDHI

    129. Mheshimiwa Spika, kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 Wizara ya Ardhi, Nyumba Maji

    na Nishati kupitia Kamisheni ya Ardhi katika Programu hii ndogo imepanga kutekeleza

    kazi zifuatazo:-

    i. Kuwapatia mafunzo ya muda mfupi wafanyakazi watano (5) na muda mrefu

    wafanyakazi watano (5).

    ii. Kulipa stahiki kwa wafanyakazi 70 ikiwemo likizo na malipo baada ya saa za kazi.

    iii. Matengenezo ya jengo la Kamisheni na Kuendelea kusimamia shughuli za

    uendeshaji.

    iv. Kutayarisha hati za Haki ya Matumizi ya Ardhi 1,900, Mikataba 140 ya Ukodishaji

    Ardhi, na Vitambulisho 100 vya matumizi ya Ardhi za Eka Tatu pamoja na

    kuingiza taarifa zake katika Mfumo wa kompyuta.

    v. Kuendeleza ukaguzi wa maeneo 150 ya uwekezaji na maeneo 150 ya Eka Tatu za

    Ardhi za Kilimo.

    vi. Kufanya kazi za Uthamini wa Ardhi kwa maeneo 350 kwa ajili ya shughuli

    mbalimbali.

    vii. Kuendelea na zoezi la kuwatambua wenye Haki ya Matumizi ya Ardhi kwa viwanja

    2,000.

    viii. Usimamiaji wa shughuli za upimaji wa viwanja 1,625 nchini.

    ix. Utayarishaji wa Ramani 1,000 za Ardhi pamoja na utoaji wa taarifa 12 za kupwa na

    kujaa kwa maji ya bahari.

    x. kufanya uhakiki wa maeneo ya ardhi 1,200 (Unguja maeneo 800 na kwa Pemba

    maeneo 400).

    xi. Kusajili maeneo ya ardhi 1,000 (Unguja ni maeneo 700 na Pemba ni maeneno 300).

    xii. Idadi ya hati zitakazolipiwa na wananchi ni 440 ambapo kwa Unguja ni hati 400 na

    kwa upande wa Pemba ni hati 40.

  • 43

    xiii. Idadi ya maeneo yatakayoendelezwa kiusajili ni 25 ambapo kwa Unguja ni 15 na

    kwa upande wa Pemba ni 10.

    xiv. Idadi ya mikutano ya uhamasishaji wa usajili wa ardhi itakaofanyika ni 20 ambapo

    12 ni kwa upande wa Unguja na Pemba ni 8.

    xv. Kutayarisha Marejista ya Shehia 8 (Unguja ni 4 na Pemba ni 4).

    xvi. Kutayarisha kadi za usajili 1,000 (Unguja 800 na Pemba ni 200).

    xvii. Kufanya semina na mafunzo kwa wafanyakazi 20 (Unguja ni 15 na Pemba 5).

    xviii. Kutayarisha Makala 16 kwa ajili ya Jarida la ARDHI toleo la tano.

    xix. Kuchukuwa taarifa za mji mdogo wa Konde (Pemba) na Makunduchi (Unguja).

    xx. Kutoa miongozo ya ujenzi (Planning Policy Guidelines-PPG) 600 Kwa Unguja na

    Pemba.

    xxi. Kufanya semina na Warsha nane (8) kwa washirika wa Idara na kutoa elimu kwa

    wananchi kwenye vipindi (8) vya Redio na TV.

    xxii. Kuimarisha kitengo cha utafiti na mashirikiano kuendeleza tafiti 4 Unguja na

    Pemba 1 juu ya Mipango Miji.

    xxiii. Kuendelea na hatua za utayarishaji wa Sera, Sheria na Kanuni mpya za Mipango

    Miji na Maendeleo ya Ardhi.

    xxiv. Kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Kitovu cha Mji wa Zanzibar (Zanzibar City

    Cetre- Local Area Plan) katika mradi wa “Green Corridor”.

    xxv. Kupanga miji midogo ya Uroa na Pwani Mchangani.

    xxvi. Kuimarisha maeneo ya miji (Upgrading Schemes) kwa maeneo saba (Unguja 4 na

    Pemba 3).

    130. Mheshimiwa Spika, ili kuiwezesha Kamisheni ya Ardhi kutekeleza majukumu yake kwa

    Mwaka wa Fedha 2020/2021, naliomba Baraza lako Tukufu kuidhinisha jumla ya TZS

    Bilion 2.776 ambazo ni ruzuku kwa kazi za Kawaida na Mishahara.

    BODI YA UHAULISHAJI

    131. Mheshimiwa Spika, Bodi ya Uhaulishaji inajukumu la kusimamia uhaulishaji (Transfer)

    wa umiliki wa Ardhi kutoka kwa mmiliki mmoja kwenda kwa mwengine. Kwa Mwaka

    wa Fedha wa 2020/2021 Bodi imepanga kutekeleza kazi zifuatazo:-

  • 44

    i. Kusimamia Uhalishaji wa ardhi kwa kujadili na kupitisha maombi 3,000 ya

    uhaulishaji yatakayowasilishwa na kuendesha Vikao vya Bodi Unguja na Pemba.

    ii. Kutoa Elimu ya Uhaulishaji wa ardhi kwa wananchi kwa Shehia 20 pamoja na

    Masheha kuhusu Sheria, Kanuni na vigezo vya Uhaulishaji.

    iii. Kuwajengea uwezo Wajumbe na Watendaji wa Bodi kwa kuwapatia mafunzo ya

    muda mfupi ya ndani na nje ya nchi kwa Wajumbe na Watendaji 12 wa Bodi

    Unguja na Pemba.

    iv. Kuimarisha Mfumo wa Uwekaji Kumbukumbu za Uhaulishaji utakaosaidia

    utaratibu bora wa upokeaji na kupitisha maombi ya uhaulishaji wa ardhi.

    v. Kuendelea kufanya mapitio ya Sheria na Kanuni za Bodi ya Uhaulishaji ili ziendane

    na mabadiliko ya kiuchumi na kijamii.

    132. Mheshimiwa Spika, ili kuiwezesha Bodi ya Uhaulishaji kutekeleza majukumu

    yaliyopangwa kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021, naliomba Baraza lako Tukufu kuidhinisha

    jumla ya TZS Bilioni 1.717 ambazo ni ruzuku kwa kazi za kawaida.

    OFISI YA MTHAMINI MKUU WA SERIKALI

    133. Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Mthamini Mkuu wa Serikali inajukumu la kuhakikisha

    usimamizi mzuri wa kazi za uthamini kwa Serikali, Sekta binafsi na wananchi kwa ujumla

    kwa kuhakiki na kuidhinisha kazi zote za uthamini nchini. Kwa Mwaka wa Fedha

    2020/2021 Ofisi ya Mthamini Mkuu wa Serikali imepanga kutekeleza kazi zifuatazo:-

    i. Kuhakiki na kuidhinisha ripoti 280 za uthamini wa rasilimali kwa madhumuni

    mbalimbali.

    ii. Kutayarisha ripoti za shughuli za uthamini kwa kila robo mwaka zinazofanyika

    Zanzibar.

    iii. Kutayarisha kanuni ya viwango vya uthamini wa majengo.

    iv. Kuingiza taarifa za mali zilizofanyiwa uthamini katika mfumo wa kieletroniki.

    v. Kuwajengea uwezo wafanyakazi 5 kwa kuwapatia mafunzo ya muda mfupi.

  • 45

    vi. Kutoa elimu kwa Wananchi kuhusu shughuli za uthamini wa kazi za Ofisi ya

    Mthamini Mkuu wa Serikali kupitia vipindi vya Televisheni (2), Redio (2) pamoja na

    Mikutano kwa Taasisi za Serikali na Sekta Binafsi.

    134. Mheshimiwa wa Spika, ili kuiwezesha Afisi ya Mthamini Mkuu wa Serikali kutekeleza

    majukumu yake kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021, naliomba Baraza lako Tukufu

    kuidhinisha jumla ya TZS Milioni 132.00 ambazo ni ruzuku kwa kazi za kawaida.

    SHIRIKA LA NYUMBA

    135. Mheshimiwa Spika, kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 Shirika la Nyumba katika

    Programu hii ndogo limepanga kutekeleza kazi zifuatazo:-

    i. Kuzifanyia matengenezo nyumba 32 za Maendeleo zinazomilikiwa na Shirika;

    Unguja 24 na Pemba 8.

    ii. Kuanza matengenezo makubwa ya nyumba namba 1699-1705 Mnadani.

    iii. Kuendelea kuzithamini na kuziorodhesha milki za Shirika.

    iv. Kukuza uwezo wa kitaaluma kwa wafanyakazi wa Shirika.

    v. Kuongeza ufanisi katika kukusanya mapato ya Shirika.

    136. Mheshimiwa Spika, kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 Shirika la Nyumba linatarajia

    kukusanya jumla ya TZS Bilioni 3.035 kutokana na kodi za nyumba, mikataba, dhamana,

    adhabu na nyenginezo. Aidha, Shirika linatarajia kutumia jumla ya TZS Bilioni 2.855

    kwa kazi za kawaida na za maendeleo.

    MAMLAKA YA HIFADHI NA UENDELEZAJI MJI MKONGWE

    137. Mheshimiwa Spika, kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 Mamlaka ya Hifadhi na

    Uendelezaji Mji Mkongwe imepanga kutekeleza kazi zifuatazo:-

    i. Kuendelea kutoa ushauri wa kitaalamu na kusimamia miradi ya Uhifadhi wa Majengo

    na maeneo ya Mji Mkongwe.

  • 46

    ii. Kutoa taaluma kwa taasisi za Serikali, binafsi na jamii kwa ujumla kuhusiana na

    umuhimu wa kuhifadhi na kuutunza Mj