Mem Bulletin 23 WIZARA YA NISHATI NA MADINI

Embed Size (px)

DESCRIPTION

HONGERA WATENDAJI WOTE WA WIZARA

Citation preview

  • Mkakati uboreshaji umeme wakamilika Uk8 Maonesho sabasaba Uk4-5

    Toleo No.23 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe Julai 4-10, 2014

    BulletinNews

    Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini

    Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

    http://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI &MADINI

    Bei PoaWAWEKEZAJI NISHATI KUIUZIA TANESCO UMEME

    Waziri wa Nishati na madini Prof. Sospeter Muhongo (kulia) akizungumza na wawekezaji wa umeme wa upepo Wind East Africa unaotarajiwa kujegwa mjini Singida.

  • 2 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzNISHATI/MADINIWawekezaji nishati kuiuzia Tanesco umeme bei nafuu

    Veronica Simba na Nuru mwasampeta

    Serikali imewataka wawekezaji wote katika sekta ya nishati nchini kuhakikisha bei zao za umeme zinakuwa nafuu ili Watanzania wanufaike ipasavyo na vyanzo vya nishati hiyo.

    Agizo hilo lilitolewa hivi karibuni na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alipokuwa akizungumza na wawekezaji wazawa kutoka Kampuni ya GeoWind Limited, walio-wasilisha maombi ya kuzalisha umeme wa upepo mkoani Singida.

    Waziri Muhongo alisema Serikali inapaswa kutimiza ahadi yake iliyoweka kwa Watanzania ya kuhakikisha wananufaika na vyanzo mbalim-bali vya nishati vilivyopo nchini, hivyo lengo lake ni kuhakikisha umeme wa kutosha na wa uhakika unapatikana na pia bei yake iwe nafuu ili wananchi waweze kuimudu.

    Kampuni yoyote inayodhamiria kuzalisha umeme kutokana na chanzo chochote hapa nchini, lazima ihakikishe inapanga bei iliyo chini ya bei ya Tanesco ya sasa ambayo ni Senti 12.6 vinginevyo haitapewa nafasi kufanya shughuli za uzalishaji kwani tutakuwa tunawadanganya Watanzania, alisisitiza Profesa Muhongo.

    Alisema kuwa Tanzania inavyo vyanzo vingi vya nishati vikiwa ni pamoja na makaa ya mawe, gesi asilia, jotoardhi, jua, upepo, nishati jadidifu na maji hivyo hakuna sababu ya kulazimika kuzalisha umeme wa gharama kubwa kama ilivyo kwa nchi nyingine ambazo zina vyanzo vichache vya nishati.

    Akifafanua kuhusu faida za kuzalisha umeme wa kutosha, wa uhakika na wenye bei nafuu, Wa-ziri Muhongo alisema itasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana kwani viwanda vitazalisha zaidi na hivyo kuongeza ajira na pia wengine wataweza kujiajiri kupitia miradi mbalimbali.

    Aidha, Profesa Muhongo alisema lengo la Seri-

    kali ni kuhakikisha Tanesco inaacha-na na utamaduni wa kupata ruzuku kutoka serikalini ili fedha hizo ziende kusaidia wananchi kwenye sekta za elimu, afya na kilimo.

    Kwa upande wake, Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk Parseko Konne aliafiki msimamo wa Waziri Muhon-go na kusisitiza kuwa Serikali haiwezi kukubaliana na wawekezaji wanao-taka kuzalisha umeme na kuuza kwa bei zaidi ya ile ya sasa ya Tanesco. Mnaotaka kuzalisha, hakikisheni bei yenu inakuwa chini ili Watanza-nia wanufaike, alisisitiza.

    Wawekezaji hao wazawa wali-kubaliana na maelekezo ya Waziri Muhongo na Mkuu wa Mkoa Dk

    Konne na kuahidi kuyafanyia kazi am-bapo watawasilisha tena mapendeke-zo yao ya uwekezaji wizarani, tarehe 23 Julai mwaka huu.

    Pamoja na kukutana na wawekeza-ji wazawa, Profesa Muhongo aliku-tana na wawekezaji wa kampuni ya Wind East Africa kujadili namna ya kutekeleza mradi huo wa umeme wa upepo kwa wakati kutokana na tara-tibu za kukamilisha mradi huo ku-suasua.

    Akizungumza wakati wa kikao hicho Muhongo alisema wahusika wanaopaswa kukamilisha mradi huo (Tanesco, Wind East Africa, na Ewura) wawe na ufanisi kwa kuwapa

    watanzania kile wanachokihitaji, yani umeme wa kutosha na unaopatikana kwa gharama nafuu.

    Aidha Kamishna Msaidizi wa Ni-shati. Injinia Inocent Luoga alisema mradi huo wa umeme utakaotekele-zwa na kampuni ya Wind East Afrika Utagharimu kiasi cha Dola za kimare-kani 285 milioni ili kuzalisha umeme wa kiasi cha Megawati 100.

    Kufanyika kwa kikao hicho kume-pelekea kupatikana kwa ratiba ya awali itakayofuatwa na Wizara,Taasisi pamoja na wawekezaji ili kuhakikisha kuanza kwa utekelezaji wa mradi huo ambao utakamilika ifikapo Oktoba 2016.

    Kampuni yoyote inayodhamiria kuzalisha umeme kutokana na chanzo chochote hapa nchini, lazima ihakikishe inapanga bei iliyo chini ya bei ya Tanesco ya sasa ambayo ni Senti 12.6 vinginevyo haitapewa nafasi kufanya shughuli za uzalishaji kwani tutakuwa tunawadanganya Watanzania, Profesa Muhongo.

    Muhongo: Fuatilieni mapato ya madini

    Waziri wa Nishati na Madini akiwa na watendaji wa wizara ya Nishati na Madini pamoja na wawekezaji wa mradi wa Wind East Africa walipokuwa wanapanga mkakati wa namna ya kufanya mradi huo utekelezeke kwa wakati kutokana na wahusika kupiga danadana katika kuanza utekelezaji wa mradi huo.

    Veronica Simba, Dodoma Viongozi wa dini nchini wamehama-sishwa kufuatilia kwa ukaribu matumi-zi ya fedha zinazotolewa na makampu-ni ya madini kama ushuru wa huduma (service levy) kwa halmashauri husika ili kuhakikisha zinatumika kwa manu-faa ya wananchi.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ametoa hamasa hiyo Julai 3 mwaka huu mji-ni Dodoma, wakati akitoa Mada ya Manufaa ya Rasilimali za Madini na Gesi Asilia kwa sasa na kipindi kija-cho kwa Maaskofu wa Makanisa ya Kipentekoste nchini, katika mkutano wao wa mwaka.

    Akiwasilisha mada hiyo, Profesa Muhongo alisema Halmashauri mbal-imbali nchini zimekwishaanza kupokea ushuru wa huduma kutoka makampu-ni ya madini yaliyoko katika maeneo yao hivyo ni vema mapato hayo pamoja na matumizi yake yawekwe wazi kwa wananchi ili waweze kuelewa manufaa yake kwao.

    Alizitaja Halmashauri hizo kuwa ni pamoja na Geita ambayo mpaka sasa imekwishapokea jumla ya Dola

    za Marekani 1.6 milioni ambazo ni sawa na shilingi za kitanzania bil-ioni 2.62. Nyingine ni Kahama am-bayo imeshapokea Dola za Mare-kani 2.53 milioni sawa na shilingi bilioni 4.15 za Tanzania.

    Halmashauri nyingine ni Ta-rime ambayo imeshapokea Dola

    za Marekani 2.4 milioni sawa na shilingi za Tanzania 3.94 bilioni, Nzega (Dola 3.04 milioni) sawa na shilingi za Tanzania bilioni 4.99 na Kishapu ambayo imekwishapokea Dola za Marekani 202,469 sawa na shilingi milioni 332.05 za Tan-zania.

    Sasa utasikia watu mbalim-bali wakilalamika kuwa makam-puni ya madini hayalipi chochote jambo ambalo siyo la kweli. Ma-pato na matumizi yawekwe wazi kwa wananchi ili waelewe, ali-sisitiza Waziri Muhongo.

    Akifafanua zaidi kuhusu ma-pato yanayotokana na kodi mbal-imbali zinazolipwa na makampu-ni ya madini hapa nchini, Profesa Muhongo alisema kwa sasa ma-pato ya kodi yameongezeka kuto-kana na serikali kuweka usimam-izi na kuhakikisha makampuni yote kwa sasa yanalipa kodi ya kampuni (corporate tax).

    Kwa upande wa wachim-baji wadogo wa madini, Waziri Muhongo alisema serikali im-echukua hatua za makusudi ku-wasaidia ili kuinua kipato chao ili waweze kuchangia katika kukuza uchumi wa nchi.

    Alisema, kwa mwaka wa fedha ulioisha Juni 2014, jumla ya shilingi milioni 880.68 za Tanzania zilitolewa na serikali kwa wachimbaji wadogo kama ruzuku. Aidha, aliongeza kuwa mwezi huu serikali inatarajia ku-toa jumla ya shilingi za Tanzania

    bilioni 2.3 kama mikopo kwa vikundi mbalimbali vya wachim-baji wadogo kupitia Benki ya TIB (Tanzania Investment Bank).

    Profesa Muhongo alisema kuwa kwa mwaka wa fedha 2014/15, serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini inatarajia kutoa mikopo kwa wachimbaji wadogo yenye jumla ya shilingi za Tanzania bilioni 2.5 na kwam-ba jumla ya shilingi bilioni 5.74 kutoka Benki ya Dunia zitatole-wa kwa wachimbaji hao kama ruzuku.

    Mbali na fedha hizo nilizoz-itaja, wachimbaji wadogo wata-patiwa mitambo ya kuchoronga miamba yenye thamani ya jumla ya shilingi za Tanzania bilioni 1.80, alisema Waziri Muhongo.

    Waziri Muhongo alialikwa kama Mgeni Rasmi na pia kama mtoa mada katika Mkutano wa mwaka wa Maaskofu wa Ma-kanisa ya Kipentekoste Tanza-nia (CCT). Katibu Mkuu Kion-gozi, Balozi Ombeni Sefue pia alialikwa kutoa mada iliyohusu masuala ya Matokeo Makubwa Sasa maarufu kama Big Re-sults Now.

    Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akiwasilisha mada kuhusu Manufaa ya Rasilimali za Madini na Gesi Asilia kwa sasa na kipindi kijacho katika Mkutano wa Mwaka wa Maaskofu wa Makanisa ya Kipentekoste nchini (CCT), uliofanyika mjini Dodoma Julai 3, mwaka huu.

  • 3BulletinNewshttp://www.mem.go.tz MAONI

    Nuru Mwasampeta Dar es Salaam

    Wanafunzi wana-osomea lugha ya Kireno wametakiwa k u o n g e z a

    juhudi katika masomo yao ili kukidhi mahitaji ya kudahiliwa katika vyuo bora nchini Brazil.

    Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo alipokuwa akizungumza na wawekezaji wa kampuni ya mafuta ya Petrobras walipofika katika ofisi yake ili kuzungumzia masuala mtambuka katika sekta ya gesi na mafuta na maendeleo ya uwekezaji wao nchini na bara la Afrika kwa ujumla.

    Muhongo alieleza kuwa mwezi wa nane mwaka huu atatembelea nchi ya Brazili na kueleza kuwa kati ya vitu atakavyopenda kutembelea na kuona vifaa vinavyotumika na kampuni hiyo katika kufanya shughuli za utafiti pamoja na kutembelea vyuo vikuu vinne bora katika kutoa taaluma ya mafuta na gesi ili kuweza ku-waombea watanzania nafasi ya kudahiliwa katika vyuo hivyo.

    Akizungumzia hoja hiyo Samuel Bastos De Miranda Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo alisema wanafunzi wa-takao kuwa na sifa za kuda-hiliwa katika vyuo bora nchini Brazil watapata nafasi.

    Aidha Samuel amezungum-zia nia yao ya kurejesha kitalu namba 5 walichokifanyia utafiti na kubaini kuwa gharama iliyo-tumika katika kuchimba kitalu hicho ni kubwa na hakuna dalili

    yeyote ya kupata kile walicho-tegemea kukipata na hivyo kue-ndelea na utafiti katika kitalu namba 6 na namba 8.

    Aidha alieleza kwamba wa-nafanyakazi katika nchi sita ba-rani Africa ikiwepo Namibia, Benin, Angola, Nigeria, Tan-

    zania na Gabon na kwamba makao makuu ya uendeshaji wa biashara yao yapo katika mji wa Roterdam nchini Uholanzi kutokana na mji huo kuwa ni kitovu cha biashara.

    TahaririMEM

    Na Badra Masoud

    FIVE PILLARS OF REFORMS

    KWA HABARI PIGA SIMU KITENGO CHA MAWASILIANO

    BODI YA UHARIRI MHARIRI MKUU: Badra Masoud

    MSANIFU: Essy OgundeWAANDISHI: Veronica Simba, Asteria Muhozya, Greyson Mwase

    Teresia Mhagama, Nuru Mwasampeta

    INCREASE EFFICIENCYQUALITY DELIVERY

    OF GOODS/SERVICESATISFACTION OF

    THE CLIENTSATISFACTION OF

    BUSINESS PARTNERS

    SATISFACTION OF SHAREHOLDERS

    TEL-2110490FAX-2110389

    MOB-0732999263

    Wiki hii katika gazeti letu ukurasa wa kwanza tuna habari kwamba Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Prof. Sospeter Muhongo ame-wataka wawezaji wote wa umeme wa ndani na nje ya nchi kuiuzia TANESCO umeme wa gharama nafuu ambayo ni ya chini ya bei ya umeme unaouzwa na Shirika hilo kwa wateja wake.

    Prof. Muhongo alienda mbali zaidi kwa kuwataka EWURA kuandaa kanuni zinazoonyesha bei za umeme kwa kila chanzo cha umeme utakaouzwa na wazalishaji binafsi wa umeme kwa TANESCO. Alisema iwapo mwekezaji atamuuzia TANESCO umeme wa bei ya juu ya bei ya TANESCO, shirika hilo litauza Shilingi ngapi kwa wateja wake.

    Vyanzo hivyo ni kama umeme wa gesi, jua, jotoardhi, upepo, mafuta, maji, makaa ya mawe n.k kwamba kila chanzo kitakuwa na bei yake na iwapo wawekezaji wa-takaotaka kuwekeza kwenye sekta hiyo itakuwa ni rahisi kwa wao kuchagua vyanzo wanavyotaka kuwekeza bada-la ya kutumia muda mrefu wa kujadiliana hasa kwenye kipengele cha bei ya umeme.

    Ninaamini kauli hiyo ya Prof. Muhongo kwa namna moja ama nyingine imekuja kutokana na baadhi ya miradi kuchukua muda mrefu kuanza utekelezaji wake na min-gine imeshindikana kutekelezeka au hata mazungumzo (negotiation) kuchukua muda mrefu.

    Aidha, kuna wengine waliodiriki hata kusema kwam-ba Serikali, Wizara ya Nishati na Madini au TANESCO inawakimbiza wawekezaji bila kujua kwamba miongoni mwa vigezo vikuu vya wawekezaji wa makampuni ya kuzalisha umeme wanaruhusiwa kufanya biashara hiyo na TANESCO ni wale wenye gharama nafuu na si vingi-nevyo.

    Kwa hakika, uamuzi huo pamoja na maelekezo ya Prof. Muhongo lazima tuyaunge mkono juu ya bei hizi za umeme kutoka kwa wawekezaji binafsi kwa maslahi ya watanzania na kama tunavyofahamu kwamba iwapo bei za umeme zitakuwa kubwa kuliko bei ya umeme unauzwa na TANESCO kwa wateja wake hakuna watakaoumia zaidi ya Watanzania.

    Ni kweli kabisa Serikali na taifa kwa ujumla hatuna budi kushirikiana na wawekezaji binafsi katika kuongeza kiwango cha uzalishaji umeme lakini lazima kuwepo udhibiti wa bei ili kuepukana na bei holela ya umeme.

    Pamoja na Tanzania kuwa ndiyo nchi yenye bei ndo-go ya umeme katika nchi zote za Afrika Mashariki laki-ni bado Serikali inafanya bidii bei hiyo isiongezeke kwa namna yoyote ile na wawekezaji binafsi katika uzalishaji wa umeme wasiuze umeme kwa bei kubwa.

    Tunampongeza Waziri Muhongo kwa uamuzi wake huo na tutamuunga mkono katika kuhakikisha utekelezaji wa uandaaji wa muongozo utakaotekelezwa na kukami-lika kwa muda aliouelekeza ili Taifa la Tanzania liwe na umeme wa kutosha utakaochochea ukuaji wa uchumi.

    Tumuunge mkono Prof. Muhongo kuendeleza

    sekta ya umeme!!!

    TEL-2110490FAX-2110389

    MOB-0732999263

    Watanzania waaswa kujiendeleza kitaaluma

    Profesa Sospeter Muhon-go kushoto akizungumza na viongozi wa Kampuni ya Petrobrass walipom-tembelea ofisini kwake kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Bw. Samuel Bastos De Miranda akifuatiwa na Bw. Paulo Sergio De Sa Campos Mkurugenzi Mkuu wa Fedha wa kampuni hiyo.

  • 4 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    Maonyesho ya 38 ya Sabasaba - 2014

    Mjiolojia Mkuu kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) Bw. Momburi Philip (kulia) akitoa elimu kwa mwananchi aliyetembelea banda la Wizara ya Nishati na Madini.

    http://www.mem.go.tz

    Mtaalamu kutoka Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Bw. Stephen Nyoni Lowoko akimwonesha Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Wizara ya Nishati na Madini, Bw. Mrimia Mchomvu mfano wa mashine ya kufua umeme kwa nguvu ya maji mara alipotembelea banda hilo.

    Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akifungua maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

    Greyson Mwase na Nuru Mwasampeta, Dar es Salaam

    Wizara, taasisi na mashirika binafsi yametak-iwa kutumia maonesho kutangaza fursa za uwekezaji nchini.

    Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho ya kimataifa ya Sabasaba (38 Dar es

    Salaam International Trade Fair (DITF) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd alisema kuwa idadi ya washiriki wa maonesho ya Sabasaba imeongezeka kutoka 1601 kwa mwaka 2013 hadi 1690 kwa mwaka 2014

    Balozi Idd aliendelea kusema kuwa washiriki ambao ni makampuni kutoka nje ya nchi wameongezeka kutoka 460 kwa mwaka 2013 hadi 490 kwa mwaka 2014.

    Kuongezeka kwa washiriki ndani na nje ya nchi ni udhi-hirisho kuwa maonesho haya yanaitangaza Tanzania na rasili-mali zake ndani na nje ya nchi.

    Alisema kuwa mbali na kuonesha mafanikio katika ongeze-ko la washiriki katika maonesho hayo, washiriki wanatakiwa kuongeza bidii kutangaza fursa za uwekezaji nchini na kufungua milango kwa makampuni ya nje kuwekeza zaidi na hivyo ku-changia katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

    Balozi Idd alisisitiza kuwa ili nchi yoyote iweze kupiga hatua ni lazima iwekeze katika sekta ya viwanda na nyinginezo na ku-karibisha wawekezaji nchini

    Tumieni maonesho kutangaza fursa za uwekezaji

  • 5BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    Tuzo za madini

    Maonyesho ya 38 ya Sabasaba - 2014

    Mtaalam wa Mazingira kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA) Bi. Monica Augustino akitoa maelezo kwa kikundi cha kinamama wajasiriliamali kutoka Simanjiro mara wali-potembelea banda hilo.

    Mtaalam kutoka Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Mhandisi Juliana Palangyo akitoa maelezo kwa Mku-rugenzi Mstaafu wa Shirika la Madini la Taifa Bw. Gray Mwakalukwa mara alipo-tembelea banda hilo.

    Mtaalam kutoka Kitengo cha Uthamini wa Madini ya Almasi na Vito (TANSORT) Bi. Teddy Goliama (kulia) akitoa elimu kwa mwananchi aliyeshika kinyago kinachotokana na miamba jinsi shughuli za uthamini wa madini ya vito zinavyofanywa na Kitengo hicho

    Meneja Masoko kutoka Kampuni ya Steps Solar Limited Bw. Pritesh Chavda (mwenye Flana) akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usi-mamizi wa Rasilimali Watu Wizara ya Nishati na Madini, Bw. Mrimia Mchomvu jinsi pampu ya maji inayotumia umeme jua inavyofanya kazi.

    Mjiolojia Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. Mwara Shoo akitoa maelezo kwa mmoja wa wananchi waliotembelea banda la Wizara ya Nishati na Madini kwenye maonesho ya kima-taifa ya Saba Saba yanayo-endelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam

  • 6 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzNISHATI

    KITWANGAUtunzaji Mazingira wamkuna Kitwanga

    Na Asteria Muhozya, Kidatu/Kihansi

    Naibu Waziri Nishati na Madini anayeshu-ghulikia Nishati Mhe. Charles Kitwanga amesifu utunzaji wa mazingira unaofanywa na watumishi wa ma-bwawa ya uzalishaji umeme ya Ki-hansi na Kidatu kwa kushirikiana na wananchi.

    Naibu Waziri ameeleza hayo akiwa katika ziara ya kutembelea Mabwawa ya kufua umeme ya Ki-datu na Kihansi ambapo ameleeza kuwa, utunzaji wa mazingira ni muhimu kutokana na kuwa na uhusiano wa moja kwa moja na vyanzo vya maji ambavyo vina mchango mkubwa katika kuzali-

    sha nishati ya umeme inayotokana na maji.

    Kwa kweli nimefurahishwa sana na utunzaji wa mazingira. Tuhakikishe tunaendelea kutunza vyanzo vyetu vya maji. Tushiriki-ane na wananchi kulinda vyanzo hivi. Amesisitiza. Kitwanga.

    Katika hatua nyingine ameeleza kuwa, amefanya ziara katika mabwawa hayo ili kuona namna shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linavyofanya kazi, kutambua changamoto na kuona namna ambavyo Shirika hilo li-taendelea kuzalisha nishati ya ku-tosha.

    Kuhusu uboreshaji wa TANE-SCO ameeleza kuwa, mabadiliko yataendelea kufanywa ndani ya shirika hilo ikiwemo kuboresha mi-undombinu ili kuongeza uzalishaji na kuhakikisha kwamba Tanzania

    inakuwa na nishati umeme ya ku-tosha.

    Aidha, Kitwanga amesisitiza kuwepo kwa vyanzo mbadala vya kuzalisha umeme mbali ya kutegemea nishati ya gesi na maji.

    Lazima tuwe na nishati mchanganyiko inayotokana na vyanzo mbalimbali na mpango uliopo ni kuzalisha megawati za umeme 10,000 ifikapo mwaka 2025.

    Wakati huo huo, Kitwanga amesifu uwajibikaji wa watumishi katika Bwawa la kuzalisha umeme la Kihansi kutokana na jitihada zao za kurejesha faida kwa wananchi wanaozunguka eneo hilo ambapo wananchi wanafaidika moja kwa moja na huduma muhimu zinazo-tolewa na shirika hilo ikiwemo za afya na elimu.

    n Apongeza Uwajibikaji wa Tanesco n Asisitiza nishati mchanganyiko

    Kihansi&Kidatu

    Kihansi

    Kidatu

    Mabadiliko menejiment i TANESCONa Henry Kilasila

    Kufuatia uteuzi wa Mhandisi Boniface S. Njombe kuwa Meneja Mkuu wa Kampuni ya Tan-

    zania Geothermal Development Company (TGDLC) Uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TA-NESCO) umemteua Mhandisi Nazir Kachwamba kuwa Kaimu Naibu Mkurugenzi Mkuu Uzal-ishaji Umeme kuazia tarehe 15/06/2014.

    Mhandisi Kachwamba aliajiri-wa rasmi tarehe 01/04/1987 kama Mhandisi wa Umeme. Imeele-zwa kwamba Kabla ya uteuzi wa sasa, Kachamba alikuwa Meneja Mwandamizi Uzalishaji Umeme wa Maji.

    Mhandisi Nazir Kachwamba ana Shahada ya Uhandisi wa Umeme (Electrical Engineering) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alipohitimu mwaka 1987. Pia ana Stashahada ya Uzamili (Postgraduate Diploma in Scien-tific Computing) kutoka Chuo

    Kikuu cha Dar es Salaam aliyohit-imu mwaka 2007.

    Pamoja na uteuzi wa Mhandisi Kachamba Shirika hilo limem-teua Ndugu Godson Makia kuwa Kaimu Mwanasheria Mkuu na Katibu wa Shirika baada ya aliyekuwepo Ndugu Godwin S. Ngwilimi kuacha kazi, Uongozi wa Shirika la TANESCO umewe-ka wazi kuwa Ndugu Makia ame-kuwa akikaimu nafasi hiyo tangu mwezi Machi, 2014.

    Kabla ya uteuzi huu, Ndugu Godwin alikuwa Mkuu wa Idara ya Sheria akishughulikia masuala ya biashara za Shirika (Legal Man-ager Commercial Affairs)

    Wakili Godson E. Makia ana Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alipo-hitimu mwaka 1992. Licha ya taaluma katika fani ya Sheria, ana stashahada (Diploma) ya Ualimu kutoka Chuo cha Ualimu Korog-we ya mwaka 1985. Hii inamfanya awe mtu makini wa kuweza ku-changanua mambo kwa busara na uadilifu na kusaidia kutoa ushauri madhubuti katika Shirika.

    Makia amelitumikia Shirika la

    Umeme (TANESCO) katika nya-dhifa mbalimbali za uongozi ikiwa ni pamoja na kukaimu nafasi ya Katibu wa Shirika, Mshauri wa Sheria (Legal Counsel), pia am-etumika kama Mtaalam wa sheria (Legal Specialist) katika kilichoku-wa Kitengo cha Ubinafsishaji wa Shirika (Privatization).

    Kutokana na taaluma yake na

    uzoefu wa miaka mingi katika ma-sula ya uzalishaji umeme, Uongozi wa Shirika una imani na uwezo al-ionao katika kufanikisha mipango na malengo kama yalivyoainishwa katika dira ya Shirika.

    Kutokana na taaluma na uzoe-fu wa miaka mingi katika utendaji wa shirika la umeme (TANESCO) Uongozi wa Shirika una imani na uwezo walionao viongozi hawa wapya katika kufanikisha mipango na malengo kama yalivyoainishwa katika dira ya Shirika.

  • 7BulletinNewshttp://www.mem.go.tz NISHATI/MADINI

    TPDC yaibuka kidedea kwenye maonesho ya Sabasaba

    Greyson Mwase na Malik Munisi

    Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) limeibuka kidedea na kukabidhiwa kikombe cha ushindi katika

    kundi la mashirika ya petroli na mafuta nchini baada ya kuyashinda mashirika mengine yaliyokuwa yanawania kikombe hicho katika Maonesho ya 38 ya Kimataifa ya Sabasaba ya-nayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere vilivyopo ji-jini Dar es Salaam.

    Kikombe hicho kilikabidhi-wa na mgeni rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi ambapo aliyataka makampuni mengine kuiga mfa-no wa TPDC katika uwekezaji kwa maendeleo ya nchi.

    Balozi Iddi alisema ili nchi yoyote iweze kukua kiuchumi haina budi kuwekeza kupitia vi-wanda na kusema kuwa serikali imeweka mkakati wa kuhakiki-

    sha kuwa viwanda vinachangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

    Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa kikombe hicho kwa niaba ya TPDC Msemaji wa shirika hilo na Msimamizi wa banda Bw. Sebastian Shana amesema kuwa ushindi huo ni faraja kwa shirika hilo na kuongeza kuwa shirika hilo li-taendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuchangia ukuaji wa uchumi kupitia sekta za gesi na mafuta.

    Akizungumzia siri ya mafan-ikio ya ushindi Shana alisema ni kuanza kwa maandalizi mape-ma na kujituma zaidi.

    Mikakati ya shirika hilo Bw. Shana alisema kuwa shirika hilo limepanga kufanya utafiti zaidi wa gesi na mafuta kwa kush-irikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha nchi inapiga hatua kubwa kiuchumi.

    Unajua nia ya serikali ni kuhakikisha kuwa nchi inakuwa katika kipato cha kati ifikapo mwaka 2025, na katika kuhakik-

    isha serikali inafikia lengo hilo, TPDC ipo tayari kushirikiana na wadau wa ndani na nje ya nchi katika kuendeleza sekta ya gesi na hivyo kuchangia katika ukua-ji wa uchumi wa nchi. Alisema Bw. Shana

    Bwana Shana aliendelea kusema kuwa gesi iliyogunduli-wa inachangia kwa zaidi ya asil-imia 50 katika umeme wa gridi ya taifa na kusisitiza kuwa kama shirika, wako tayari kuweka ngu-vu zaidi katika utafutaji na uzal-ishaji wa gesi ili iweze kuwa na mchango mkubwa zaidi katika uzalishaji wa umeme.

    Bw. Shana alisema kuwa TPDC imekuwa ikishirikiana na wadau wakuu kama Wizara ya Nishati na Madini ambayo imelisaidia shirika hilo kupiga hatua kubwa katika uendelezaji wa shughuli za utafutaji wa gesi na mafuta.

    Hii ni mara ya saba kwa shirika hilo kujinyakulia vikombe kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba tangu lilipoanza kushiriki.

    Washiriki kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) wakiwa katika picha ya pamoja na kikombe cha ushindi mara baada ya kuibuka washindi wa kwanza katika kundi la makampuni ya mafuta na gesi katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam

    Naibu Waziri Nishati kuongoza ujumbe wa Tanzania CanadaTeresia Mhagama

    Dar es SalaamNaibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga, ataongoza ujumbe wa Tanzania kwenda nchini Canada kwa ajili ya ziara ya kikazi ambayo inalenga kuiwezesha serikali na watunga sheria kuongeza uelewa kuhusu namna bora ya uandaaji, usimamizi na na utekelezaji wa miradi ya Nishati na Madini nchini pamoja na kupata uelewa wa namna Serikali inavyoweza kuongeza mapato kupitia miradi ya uziduaji.

    Mhe. Kitwanga ataongozana na wajumbe wa Kamati ya Ku-dumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Naibu katibu Mkuu,Wizara ya Nishati na Madini, Eng.Ngosi Mwihava na wataalam kutoka wizarani ambao kwa pamoja watatembelea miradi mbalimbali ya Nishati na Madini pamoja na Taasisi za elimu ya Juu kuanzia tarehe 7 hadi 22 Julai 2014.

    Kampuni tanzu ya umeme utokanao na jotoardhi kuanzishwa

    Na Henry KilasilaKufuatia uhitaji wa nishati ya umeme nchini Shirika la Umeme Tanzania limeanzisha Kampuni tanzu itakayojishu-ghulisha na utafiti na uzalishaji umeme utokanao na joto ar-dhi, yaani Geothermal Energy. Kampuni hiyo imesajiliwa rasmi kisheria na kutambuliwa na Serikali.

    Kufuatia kuanzishwa kwa Kampuni hiyo Tanzu ya Tan-zania Geothermal Development Company Limited (TG-DLC), Mhandisi Boniface Simon Njombe ameteuliwa kuwa Meneja Mkuu wa kampuni hiyo kuanzia tarehe 1/6/2014. Uteuzi huu unalenga kuendeleza tafiti na uzalishaji umeme wa joto ardhi (Geothermal Energy) nchini kama chanzo kingine kikubwa cha umeme kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu.

    Tangu alipoajiriwa mwaka 1986, amelitumikia Shirika la Umeme (TANESCO) katika nyadhifa mbalimbali hadi ku-fikia ngazi za juu za uongozi. Injinia Njombe ameshika na-fasi mbali mbali ndani ya Shirika, kama ifuatavyo;

    Amewahi kuwa Meneja wa vituo vya Kuzalisha Umeme wa Maji - Pangani, Mratibu mkuu wa miradi millennia chini ya ufadhili wa Serikali ya Marekani (Project Coordinator - MCC ), Meneja wa Mkoa wa Arusha, Kaimu Mkurugenzi wa Miradi, Mhandisi Mkuu Miradi na mpaka anateuliwa ali-kuwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia masu-ala ya Uzalishaji Umeme.

    Mhandisi Boniface Njombe ana Shahada ya Uhandisi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alipohitimu mwaka 1987 na ni mwenye upeo mkubwa wa masuala mbalimbali ya kitaifa na kimataifa kuhusiana na masuala ya kiufundi na ki-uongozi. Hii inatokana na kuwa amehudhuria mafunzo, makongamano, warsha na semina mbalimbali ndani na nje ya nchi zilizomfanya kuwa mmoja wa wahandisi mahiri we-nye uwezo wa kusimamia kampuni mpya iliyoundwa.

    Mitambo ya kufua umeme kwa kutumia Methanol nchini Canada

  • 8 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHABARI

    Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wasiliana nasi kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

    WIZARA YA NISHATI NA MADINI

    TANZANIA DAIMA LAIKOSEA WIZARA

    Teresia Mhagama Dar es Salaam

    Serikali imetangaza kukamilika na kuanza kwa utekelezaji wa Mkakati na Mwelekeo wa kubore-sha Sekta Ndogo ya umeme nchini ili kuongeza ufanisi, upatikanaji na

    ubora wa huduma ya umeme.Akitangaza mkakati huo mbele ya

    waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, EliakimMaswi ameeleza kuwa mkakati huo ulioanza kutekelezwa Julai mosi mwaka huu unalenga kulipunguzia mzigo Shirika la Umeme nchini (TANESCO) wa kuwa ndilo lililobeba jukumu kuu la uzal-ishaji, usambazaji na usafirishaji umeme kwani sasa shirika hilo litagawanywa katika awamu mbalimbali na wawekezaji binafsi wataruhusiwa kupeleka huduma hiyo kwa wananchi.

    Alisema kuwa mkakati huo unaainisha kuwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) utabaki kama ulivyo lakini Wakala huo utasadia utekelezaji wa majukumu ya ofisi za kanda za TANESCO ambazo zitaanza kujitegemea.

    Mwongozo wa kutekeleza maboresho ya sekta ndogo ya umeme umeme uko ka-tika awamu nne na kuna mambo ambayo yameanza kutekelezwa ndani ya mwaka mmoja, ambao ni Julai 2014 hadi 2015, mengine yatafanyika ndani ya muda mfupi yani mwaka 2015 hadi 2018, na kuna masu-ala yatakayotekelezwa katika muda wa kati ambao ni 2018-2021 na awamu ya mwisho ya utekelezaji wa mkakati itafanyika mwaka 2021 hadi 2025.Alifafanua Katibu Mkuu

    Amesema kuwa mkakati na mwelekeo wa mwaka mmoja ulioanza kutekelezwa Julai mosi 2014 na unaotarajiwa kufika ukomo mwaka 2015, umeainisha masuala

    muhimu yanayohitaji kutekelezwa ndani ya kipindi hicho ili kuboresha sekta ndogo ya umeme ambayo kuwa ni pamoja na kuima-risha hali ya kifedha ya Tanesco, kufanya tathmini ya mali na madeni ya shirika, ku-fanya tathmini ya mahitaji ya rasilimali watu, kufanya ukaguzi wa mifumo ya taarifa za umeme, na kudhibiti upotevu wa umeme kutoka asilimia 19 hadi 18.

    Katibu Mkuu mefafanua kuwa Mkakati na Mwelekeo huo wa sekta ndogo ya umeme pia umeainisha masuala yatakay-ofanyika katika kipindi cha mwaka 2015 hadi 2018 kwamba ifikapo Desemba 2017 itaanzishwa kampuni mpya inayojitegemea ya uzalishaji umeme, huku shughuli za usafirishaji na usambazaji umeme zikienda pamoja.

    Tunasema kuwa shughuli za uzal-ishaji umeme zitakuwa zikijitegemea ifikapo mkwaka 2017 kwa sababu mpaka mwaka huo tayari Tanzania itakuwa na umeme wa kiasi cha megawati 3000 kiwango ambacho kinaruhusu utenganishaji wa shughuli za uzalishaji umeme kutoka katika usafirishaji na usambazaji.Alisisitiza Katibu Mkuu.

    Katika kipindi hiki alieleza kuwa sheria ya umeme ya mwaka 2008 itarekebishwa hasa kifungu 41 (6) ili kuruhusu wawekezaji binafsi kuuza umeme moja kwa moja kwa watumiaji wakubwa.

    Kuhusu Ofisi za Tanesco mikoani kuwa na maamuzi, Katibu Mkuu alieleza kuwa ifikapo Desemba 2016 maamuzi ya ununuzi na mipango ya Tanesco itagatuliwa kutoka makao makuu hivyo watumishi wa mikoani watakuwa na madaraka kamili ya kufanya mipango na manunuzi lengo likiwa ni kuongeza ufanisi katika kanda na mikoa.

    Masuala mengine yatakayofanyika katika kipindi cha mwaka 2015 hadi 2018 ni kudhibiti upotevu wa umeme kutoka asilimia 18 hadi asilimia 16 ifikapo mwaka 2016 na kuanzisha dawati linaloshughulikia

    masuala yote yanayohusu umeme.Habari njema kwa wawekezaji binafsi

    zilizoainishwa katika mkakati na mwele-keo wa sekta ndogo ya umeme ni kuwa kuanzia Desemba 2017 wazalishaji bin-afsi wa umeme watakuwa na mamlaka ya kuuza umeme moja kwa moja kwa wa-nanchi badala ya kuiuzia TANESCO tu. Maswi ameeleza kuwa masuala mengine yaliyoainishwa ili kutekelezwa katika katika kipindi cha 2015-2018 ni kuongeza uungan-ishaji umeme kutoka asilimia 30 hadi 33, kuanzisha msimamizi huru wa biashara ya umeme, na kuanzisha msimamizi huru wa mfumo wa umeme.

    Vilevile alitanabaisha kuwa masuala yanayopaswa kutekelezwa katika kipindi cha muda wa kati, mwaka 2018 hadi 2021 ni kutenganisha shughuli usambazaji na usafirishaji umeme hivyo ofisi za kanda zitakuwa zikijitegemea katika kusambaza na kusafirisha umeme kwa ushindani, pia kupunguza upotevu wa umeme kutoka asilimia 16 hadi 14, kuongeza uunganishaji umeme kutoka asilimia 33 hadi 39, na ku-weka kanuni na taratibu za uendeshaji wa biashara ya uuzaji wa umeme moja kwa moja kwa watumiaji wadogo.

    Kuhusu awamu ya mwisho ya Mkaka-ti na Mwelekeo wa kuboresha Sekta Ndogo ya Umeme ambayo itafanyika mwaka 2021 hadi 2025, Katibu Mkuu aliyataja ma-jukumu yanayopaswa kufanyika kuwa ni kuanzisha kampuni za usambazaji umeme zinazojitegemea, kampuni za umeme ku-jisajili katika Soko la Hisa la Dar es Salaam, kupunguza upotevu wa umeme kutoka asilimia 14 hadi 12, kuongeza uunganishaji umeme kutoka asilimia 39 hadi 50 na ku-fanya tathmini ya mahitaji ya rasilimali watu na kuwekeza kwenye rasilimali hiyo.

    Katibu Mkuu alidadafua kuwa ili kutekeleza masuala yote yaliyoainishwa ka-tika mkakati huo, ni lazima serikali ifanyie

    kazi kazi vitu vinavyotishia kukwamisha ukuaji wa sekta ndogo ya umeme.

    Huku akitolea mfano hoja hatarishi ya kuwa na mwitikio mdogo wa wawekezaji katika sekta ya umeme kutokana na nchi kuwa maskini, lakini Katibu Mkuu alieleza kuwa suala hilo linaweza kutatuliwa kwa kubadilisha sheria na taratibu zilizopo ili kurahisisha shughuli za uwekezaji nchini.

    Kihatarishi kingine kinachotia mashaka ni suala la Tanesco kuleta faida kama tunavyotarajia kwani Shirika hili li-natumia fedha nyingi kwa ajili ya kuzalisha umeme, ila serikali inaweza kuondokana na kihatarishi hiki kwa kuondoa mitambo ya dharura ambayo inatumia kiasi kikubwa cha fedha ili kuzalisha umeme, pia serikali kujikita katika ujenzi wa mitambo ya ku-zalisha umeme kwa kutumia gesi ambayo gharama zake ni nafuu na kurekebisha gharama za bili ya umeme.Alisema Ka-tibu Mkuu

    Aliongeza kuwa ili sekta ndogo ya umeme ichangie katika kufanya mageuzi ya kiuchumi, ni lazima nchi iachane na uzalishaji mdogo wa umeme na hili lita-fanyika kuanzia mwaka 2017 ambapo tayari kutakuwa na umeme wa kiasi cha megawati 3000 huku lengo ni kuwa na megawati 10,000 ifikapo mwaka 2025.

    Katibu Mkuu alitoa angalizo kuwa pamoja na serikali kuja na Mkakati na Mwelekeo mzuri wa sekta ndogo ya umeme nchini lakini kama watendaji hawa-tabadilika na kuachana na mawazo mgan-do mkakati huo utakuwa hauna maana, hivyo amewataka watendaji kubadilika na kuwatumikia wananchi kwa ufanisi.

    Utekelezaji wa majukumu yaliyopang-wa kufanyika katika mwaka 2014/15 uta-gharimu kiasi cha shilingi bilioni 565.771 ambapo fedha hizo zitatolewa na Wizara ya Nishati na Madini, TANESCO na wa-shirika wa maendeleo.

    Mkakatiumeme wakamilika

    TUFANYE KAZI KWA UADILIFU, BIDII, WELEDI, NA USHIRIKIANO BILA KUKATA TAMAA

    DAIMA TUSONGE MBELE KURUDI NYUMA NI MWIKO!!

    UJUMBE WA WAZIRI WIKI HII

    nTANESCO kugawanywa kwa awamun2017 wazalishaji binafsi ruksa kuuza umemenKutekelezwa 2014-2025

    Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, EliakimMaswi