7
1 Utangulizi Kabila lolote ulimwenguni, hutokana na mambo manne yakiwemo jadi, kazi, mji na sifa za watu. Na upande mwingine nayo lugha hutokamana na mazingira maalum ya watu na tamaduni zao. Ikiwa kabila ni desturi na mila za watu, au ni watu walofungamana na kuwa na tabia na nyendo ambazo zitawatofautisha wao na watu wengine, basi waswahili wana mila zao na desturi zao kama makabila mengine ulimwenguni. Kama kwenye maingiliano ya kibinadamu kwa mfano: ndoa, majina, itikadi za pepo na kadhalika, basi liko kabila ila la waswahili lenye mambo kama hayo. Neno itikadi ni istilahi ya kimsingi katika nyugo za kiutamaduni, za fasihi na taaluma zinazohusu filamu. Maana ya istilahi 'itikadi' kiasilia inatokana na maandishi ya mwanafalsafa wa Kijerumani, Karl Marx na mwenzake Friedrich Engels (Abdulla, Mansur na wenzake, 2014). Katika uchanganuzi wao wa kimsingi wa jamii, walifafanua itikadi kama dhana na imani za tabaka tawala katika kipindi maalumu. Dhana na imani za tabaka tawala ndizo hutamalaki taratibu za kuunda fikra, mawazo na mielekeo ya wanajamii kwa ujumla. Kwa hivyo, mfumo wote wa fikra za tabaka tawala ndio unajenga itikadi ya jamii fulani ndiposa tukaona Waswahili wana itikadi na mila tofauti tofauti.

ITIKADI assigno

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: ITIKADI assigno

1

Utangulizi

Kabila lolote ulimwenguni, hutokana na mambo manne yakiwemo jadi, kazi, mji na sifa za watu.

Na upande mwingine nayo lugha hutokamana na mazingira maalum ya watu na tamaduni

zao. Ikiwa kabila ni desturi na mila za watu, au ni watu walofungamana na kuwa na tabia na

nyendo ambazo zitawatofautisha wao na watu wengine, basi waswahili wana mila zao na desturi

zao kama makabila mengine ulimwenguni. Kama kwenye maingiliano ya kibinadamu kwa

mfano: ndoa, majina, itikadi za pepo na kadhalika, basi liko kabila ila la waswahili lenye mambo

kama hayo.

Neno itikadi ni istilahi ya kimsingi katika nyugo za kiutamaduni, za fasihi na taaluma zinazohusu

filamu. Maana ya istilahi 'itikadi' kiasilia inatokana na maandishi ya mwanafalsafa wa

Kijerumani, Karl Marx na mwenzake Friedrich Engels (Abdulla, Mansur na wenzake, 2014).

Katika uchanganuzi wao wa kimsingi wa jamii, walifafanua itikadi kama dhana na imani za

tabaka tawala katika kipindi maalumu. Dhana na imani za tabaka tawala ndizo hutamalaki

taratibu za kuunda fikra, mawazo na mielekeo ya wanajamii kwa ujumla. Kwa hivyo, mfumo

wote wa fikra za tabaka tawala ndio unajenga itikadi ya jamii fulani ndiposa tukaona Waswahili

wana itikadi na mila tofauti tofauti.

Page 2: ITIKADI assigno

2

Kama tulivyosema hapo awali kuwa itikadi ni taasisi iliyo hai katika tamaduni za jamii zote za

wanadamu huku zikiwa zimegawanyika aina kuu mbili za itikadi: itikadi za kisiasa, na itikadi za

kiepistemolojia (ni sehemu ya falsafa ambayo inahusu utafiti wa jinsi tunavyojua mambo).

Itikadi ya kisiasa ni upangiliaji unaohusu mawazo ya kimaadili na vipi nchi itaendeshwa. Itikadi

za kiepistemolojia ni upangiliaji unaohusu mawazo ya kifalsafa, ulimwengu, na jinsi gani watu

wanapaswa kufanya maamuzi.Kuna aina nyingi za itikadi. Moja kati ya hizo ni pamoja na

Ukomunisti, Usoshalisti, na ubepari ni itikadi kubwa sana za kiuchumi na kisiasa kwa ujumla.

Kwa sasa tutaangalia itikadi za Waswahili pekee yake.

Waswahili wana itikadi nyingi sana na mifano ni kama : kula gizani ni kula na shetani. Hivyo

basi walijiepusha na kula gizani kwani waliamini sana. Mtu yeyote akila gizani basi akaumwa na

tumbo au akawa mgonjwa kisa na maana alikula na shetani yaani alikula gizani.

Mtu hafai kula ovyo ovyo bila kujali mazingira. Waswahili itikadi yao hueleza kuwa kula kitu

kitamu kinjia njia mtu atasibiwa na shetani yaani ni tabia mbaya na chafu kula wakati

unatembea. Ama mwenye kula miguu ya kuku atakuwa daima katika mwendo tu kwa sababu ni

nyama moto inayojaza hisia kama ngisi ndiposa Waswahili wakaeka itikadi mtu kama huyo

atakuwa na tabia ya kurangaranga.

Ni lazima ja ya ibada kwa kila jambo kumtanguliza Maulana. Waswahili waliamini

kutomtanguliza Jalali katika maakuli basi ni kosa adhimu. Wao huamini mtu akila bila ya kupiga

Bismillahi basi baraka itaondoka na mtu hataweza kushiba.Na isitoshe hata mgeni akija ghafla

wakati wa chakula na hakuna aliyepija Bismillahi basi chakula hakitatosha na italeta izara baada

yake.

Page 3: ITIKADI assigno

3

Sote tunaamini ubadhirifu kwa jambo lolote lile halifai. Waswahili walikuwa na itikadi ya

kuukomesha ubadhirifu na israfu kwa kuwa na itikadi ya ukikanyaga chakula makusudi utasibika

na maradhi ya matende (elephantiasis). Ni ada kukataza watoto haswa kula sufuriani kwa sababu

hudhihakiwa kuwa harusi yakoitanyesha. Maneno haya yamesadikishwa na Waswahili na

wakaamini kwamba mwenye kuzowea kula ndani ya chungu basi atapata mvua kubwa siku ya

harusi yake.

Lingine ni kunywa maji msalani mtu huwa mwongo. Iwapo mtu ana mazoea ya kudangaya basi

Waswahili huamini mtu huyo amekunywa maji msalani kwa sababu wakaazi msalani ni ma jini.

Wao majini ndiyo husababisha mtu kudangaya akinywa maji msalani. Eti wamekunywesha maji

hayo ndiposa ukawa na tabia ya kudanganya. Aidha, Kwa mwanadamu kuwa na afya bora ni lazima

achunge usafi. Hii ni kwa sababu maradhi mengi husababishwa na kutotilia maanani usafi wa vyakula na

vinywaji ndiposa Waswahili wakakataza kunywa maji ndani ya kata pasi na kuikung’uta. Hii ni kwa

sababu huenda maji yale yakawa na wadudu na kusababisha maradhi yasiyo na tiba.

Bundi ni ndege mweusi anayeonkana sana sana wakati wa usiku.Waswahili wanaamini bundi

akilia juu ya nyumba anatangaza kifo cha mtu katika nyumba hio. Pindi mtu anapomwona bundi

basi ni bora kujiepusha na pahali hapo ili asije akafa yeye. Aidha watu wazima katika jamii ya

waswahili ni watu wanaopenda mavazi ya kikoi ambamo ndani ya kikoi ni aghalabu kwa mtu kuvaa

suruali ya ndani ndiposa wakatoa ilani kali kwa wenye tabia ya macho makali kwa kuashiria kuwa

kumchungulia mtu mzima aliyekaa uchi kunaleta upofu.Hapa si ule upofu wa macho bali ni kukosa

nuru ya macho kama kuto ona vizuri.

Page 4: ITIKADI assigno

4

Kushona nguo mwilini kunaleta ufukara; tabiahii aidha inajongeza kifo, maana inakuwa kama

mtu anajishonea sanda yake mwenyewe.Na ni kupitia kwa itikadi kama hizi Waswahili

waliepuka sana hata kushona nguo kwa cherehani kwa sababu waliamini hio ndio sababu

mwafaka ya kujitafutia jongomeo.

Ulishuhudia wapi binadamu akitembea kwa kiatu kimoja kama sio kurukwa na akili? Waswahili

katika itikadi zao waliamini kutembea hali ya kuwa mtu amevaa kiatu kimoja tu kunavimbisha

ziwa la mama wake. Je ni nani leo atakaetaka kumwadhibu Mama mlezi wake? Ni jambo adhimu

ambalo ni itikadi ya Waswahili.

Karne hii ya sasa twanywa maji kwa kutumia mageleni huku tukisahau mitungi na vyungu. Basi

kuanzia leo fahamu kuwa mtu akinywa maji usiku pasi na kuufunika mtungi wa maji, usiku roho

yake itaingia ndani ya mtungi na iwapo atatokea mtu akaufunika huo mtungi wakati uo huo, basi

atakufa papo hapo.Hii ni itikadi kali iliyo na msingi wa mtu kuwa mwangilifu wakati wowote

anapotumia kifaa chake.

Wageni ni Baraka kama tujuavyo. Iwapo leo utafikwa na sisimizi wengi nyumbani kwako basi

fahamu kuwa utabahatika na wageni kwako. Waswahili wana itikadi kuwa iwapo mtu ataona

chunguchungu ama sisimizi ukutani basi atafikiwa na wageni wa ghafla.Hii ni ishara kwa

mwanadamu apate kujitayarisha kuwalaki wageni hao.

Ni watu wengi ulimwenguni hukoga kabla ya kulala. Je, ushawahi kujiuliza kwa nini? Kwa

sababu Waswahili wanaamini Kwenda kulala pasi na kuosha miguu, basi hiyo miguu italazwa

katika moto wa Jahannam. Mtu akilala pasipo kuosha miguu, nyayo zake zitarambwa na

shetani.Na hii ni ishara mtu huyo ni mchafu na shetani anapenda uchafu.

Page 5: ITIKADI assigno

5

Pia mtu akifagia usiku ati anafukuza baraka katika nyumba yao. Je kitu cha sukari kikimwagika

hatutasafisha ili tusifukuze baraka? Lakini cha kustaajabisha sana ni kuwa itikadi za Waswahili

hutokea kweli kwa kila anayeamini kwa sababu ni taasisi ilyokokotezwa katika jamii yao.

Kuchanganya mikasa katika jamii ni jambo lianloepukwa sana na Waswahili katika itikadi zao

wakakataza watu kukusanya taka za chumba kimoja na kupeleke chumba kingine hii ni kwa

sababu huko ni miongoni mwa sababu zitakazo changia kuongeza na kuleta matatizo wakati

mmoja. Vilevile, Kuuza chumvi usiku ni nuksi kwa mwenye duka.Hii ni itikadi iliyo nzito

kufahamika katika fahamu zetu za kileo.

Aidha, watoto wamehusishwa sana katika itikadi za Waswahili. Nilipokuwa mdogo nilikanywa

kuchezea moto wa koroboi na wala sikufahamu maana yake na la kustaajabisha usiku wake

nilijipata nimeamka huku nikiwa nimelowa mikojo. Waswahili waliamini katika itikadi zao

kuwa mtoto mwenye kuchezea kivuli chake cha taa atakojoa kitandani na hili mimi nakubaliana

nalo mia kwa mia. Isitoshe, mtoto mchanga akiachwa peke yake, atageuzwa na shetani.

Inaaminika na jamii ya Waswahili kuwa Shetani yupo kila sehemu haswa sehemu ambazo hazina

watu ndiposa tunakanywa tusiwaache watoto wachanga pekee yao. Si ajabu ukaona watoto

wengi wa karne hii na majivuno mengi kwa sababu Waswahili wanaamini itikadi zao kuwa

kumbusu mtoto usingizini kunasabibisha mtoto huyo kuwa na majivuno ukubwani mwake. Hizo

ni baadhi za itikadi zinazohusishwa na watoto.

Aidha, kuna sehemu ya nyumba ijulikanayo kama Kizingiti. Sehemu hii ina athari kubwa katika

itikadi za waswahili kwani wao huamini kwamba Mwenye kufanya mazowea ya kukaa

kizingitini atakawia kuoa. Hii ina maana kuwa mtu huyo anawaza zaidi ya yanayotarajiwa na

atapoteza muda tele hao kizingitini bila kunufaika. Isitoshe ya kuoa, mja mzito pia atakapokukaa

Page 6: ITIKADI assigno

6

kizingitini basi kutasababisha mwanae kuzaliwa kuchelewa kuliko ule muda uliyotarajiwa na

Wauguzi.Mbali na hayo, Kula wima kizingitini, mtu atapigwa dafrau na shetani. Hii ni kwa

sababu kizingiti sio mahali sahihi kupata chakula.

Hitimisho

Waswahili wana itikadi na mila nyingi sana tofauti. Katika kitabu cha Mbaabu anamalizia sura

ya mwisho wa kitabu chake na maneno haya: `Itikadi ... zina mafunzo mengi yanayostahili

kuhifadhiwa na kuzingatiwa ' (uk.49).

Page 7: ITIKADI assigno

7

MAREJELEO

Abeid K.A. 1965. Sheria za Kutunga Mashairi na Diwani ya Amri. Dar

es Salaam: East African Literature Bureau.

Akida H. 1977. Utamaduni,matumizi na misingi ya lugha ya Kiswahili.

MULIKA 11, kur. 9-18.

Chiraghdin S. 1974. Kiswahili na Wenyewe. Kiswahili 44:1, kur. 48-53.

Chum H. Utamaduni wa Watu wa Wilaya ya Kusini-Unguja. (Mswada

unaotayarishwa kutolewa kitabu, Mhariri Dkt. T.S.Y. Sengo).

Mbaabu I. (Mhar.) 1985. Utamaduni wa Waswahili. Nairobi: Kenya

Publishing & Book Marketing Co. Ltd.

Mwinyihaji, Esha Faki (2001). “The Contribution of Islam Towards women Emancipation: A case Study of the Swahili Muslims in Mombasa District”, Unpublished M.Phil Thesis, Moi University,2001.

Ndzovu, Hassan Juma (2001). “The impact of Islam on witchcraft and

sorcery among the Adigo community”, Unpublished M.Phil Thesis, Moi University, pp. 98-99

Sengo T.S.Y. 1985. The Indian Ocean Complex and the Kiswahili folklore: The case of Zanzibarian Tale-Performance. Unpublished Ph.D thesis. Khartoum University