Upload
nguyencong
View
237
Download
0
Embed Size (px)
Citation preview
Newsletter Date
Volume 1, Issue 1
Business Name
WARSHA YA WADAU
WA KILIMO NA MKUTANO MKUU WA MWAKA
1. Dkt Sinare Sinare - Mwenyekiti 7. Bibi. Jackline Mkindi– Mjumbe
2. Professa Andrew Temu - M/ Mwenyekiti 8. Bibi. Helen Ainea Usiri– Mjumbe
3. Dr. Salum Diwani - Mwekahazina 9. Bw. Sebastian Sambuo– Mjumbe
4. Bw. Salum Shamte– Mjumbe 10. Bw. Felix Mosha– Mjumbe
5. Bw. Abdul Mwilima– Mjumbe 11. Mhe. Jitu Soni– Mjumbe
6. Bw. Willigis Mbogoro– Mjumbe
YALIYOMO
Jarida la Agricultural Council of Tanzania
Jarida la Agricultural Council of Tanzania
We unite, we dialogue, we advocate
Toleo Na. 16. Oktoba – Disemba 2013
KILIMO KWANZA– AGRICULTURE FIRST
WARSHA YA
WADAU WA
KILIMO NA
MKUTANO MKUU
WA MWAKA
WAJUMBE WA
BODI WA ACT
KUPEANA
TAARIFA NA
KUZITUMIA
KUENDELEZA
VYAMA
MAFUNZO YA
KILIMO–
BIASHARA KWA
WARATIBU WA
TAP
KUBADILISHANA
UZOEFU KUHUSU
UTUNGAJI WA
SERA ZA KILIMO
KUFUFUA ZAO LA
KOROSHO
Tarehe 2 na 3 Desemba 2013, ACT ilifanikisha
matukio muhimu mawili. Siku ya kwanza
ilikutanisha wataalamu wa nyanja mbalimbali
wapatao 80 kujadili masuala matatu:
Ardhi kwa ajili ya kilimo na ufugaji,
Upatikanaji wa mitaji kwa ajili ya kilimo na
ufugaji,
Athari za kodi kwenye sekta ya kilimo.
Siku ya pili ulifanyika Mkutano Mkuu wa
Mwaka. Wanachama walipokea na kujadili
mada ambazo ni za kawaida katika tukio la
aina hii.
Miongoni mwake ni: Kupokea na kujadili
Taarifa ya Mwenyekiti na Hesabu za ACT, na
kuchagua Wakaguzi wa Hesabu. Wakati
huohuo, ACT inaandaa mkutano wa wadau
utakaofanyika Januari 2014, ambao utajadili
suala la Kilimo cha Kibiashara katika nchi za
Afrika Mashariki.
Pia, Bodi ya ACT ilipata viongozi wapya.
Viongozi hao ni; Dkt. Sinare Y. Sinare kama
Mwenyekiti, Profesa Andrew Temu, kutoka
SUA, Morogoro kama Makamu Mwenyekiti,
na Bw. Abdul Mwilima, kutoka Agricomat,
Kigoma, kama Mjumbe.
WAJUMBE WA BODI YA ACT
KUPEANA TAARIFA NA KUZITUMIA KUENDELEZA VYAMA
Tarehe 22 hadi 25 Oktoba 2013, watumishi
wawili wa ACT, Bw. Cleophas Rwechungura na
Khalid Ngassa, walikuwa Bujumbura, Burundi,
ambako walishiriki katika mafunzo kuhusu
utaalamu wa kupeana habari / taarifa kwa lengo
la kuendeleza vyama vya wakulima. Mafunzo
hayo yalifadhiliwa na IFAD na kusimamiwa na
Muungano wa Vyama vya Wakulima Afrika
Mashariki– EAFF.
Mafunzo hayo yalishirikisha baadhi ya vyama vya
wakulima kutoka Kenya, Burundi na Tanzania.
Washiriki walifundishwa jinsi ya kuimarisha
vyama vya wakulima kwa kuelimisha watendaji
pamoja na wanachama, na mbinu za kupeana
taarifa na kwa lengo la kujiendeleza. Hii ni
pamoja na: “Kuimarisha upashanaij wa habari
na utamaduni wa kubadilishana maarifa na
ujuzi”.
MAFUNZO YA KILIMO– BIASHARA KWA WARATIBU WA TAP
Ubia wa Kilimo Tanzania - TAP kwa sasa unao waratibu
wa shughuli zake katika wilaya 25. Katika jitihada za
kufanya kilimo kiendeshwe kibiashara, TAP iliomba msaada
wa kifedha na kitaalamu ili kuelimisha Waratibu wake
ustadi wa kilimo cha kibiashara na kanuni za kilimo cha
mkataba.
Mafunzo haya yamekuwa yakifanyika kwa awamu. Zoezi
la karibuni lilifanyika katikati ya Novemba 2013, jijini Dar
es Salaam. FAO kupitia Programu ya Kuendeleza
Mifumo ya Uzalishaji wa Chakula, Nyanda za Juu- SHFSP,
ilifanikisha mafunzo kwa Waratibu wa TAP, ambao
baadae watatoa elimu hiyo kwa wakulima, na kwa wadau
wengine kwenye mlolongo wa thamani.
Utaalamu huu ni muhimu sana, hasa tukizingatia
kwamba TAP II itaanza karibuni, ambayo mkazo wake ni:
“Kukuza kilimo kwakuchochea uwekezaji na
kukiendesha kibiashara”.
Page 2 Jarida la Agricultural Council of Tanzania ACT NEWS
2 Jarida la ACT– Toleo Na. 16
Awamu ya kwanza ilikuwa ya miaka mitatu
2008– 2011 na ilihusisha wilaya 25. Matarajio ni
kwamba awamu ya pili itapanuka kwa
kujumuisha wilaya nyingine 25.
Baadhi ya washiriki kwenye mafunzo wakisikiliza kwa makini mtoa mada.
ACT hufanya shughuli zake kwa kushirikiana na sekta binafsi na ya umma. Huduma zake zinalenga wadau wote, wa ngazi zote kulingana na mahitaji yao halisi.
KUFUFUA ZAO LA KOROSHO
Mwanzoni mwa Oktoba 2013, Bw. Renatus
Mbamilo kutoka ACT alikuwa miongoni mwa
washiriki kwenye warsha iliyojadili uzoefu wa
Vyama vya Wakulima katika michakato ya
kuimarisha hali ya chakula katika ngazi ya taifa na
kanda. Warsha hiyo ilifanyika jijini Nairobi.
Madhumuni ya jumla, ni kuimarisha ushiriki wa
Shirikisho la Vyama vya Wakulima, Afrika
Mashariki - EAFF kwenye mchakato huu.
Washiriki walipanuliwa ufahamu wao kuhusu
utaratibu wa mchakato. Kumewekwa mfumo
wa kupima, kufuatilia na kutathmini athari za sera
za kilimo kwa wazalishaji.
Mfumo huu unatekelezwa na FAO kwa
kushirikiana na wabia wengine kwa lengo kukuza
utendaji katika vyama, na hivyo kuimarisha
ukuaji wa kilimo.
Page 3 Volume 1, Issue 1 ACT NEWS
3 Jarida la ACT– Toleo Na. 16
Tarehe 4 na 5 Novemba 2013, ANSAF na ACT kwa
pamoja waliandaa warsha ya kujadili changamoto
zinazokabili zao la korosho nchini Tanzania.
Wabia wengine kwenye shughuli hii ni; Bodi ya
Korosho Tanzania, Kituo cha Uwekezaji Tanzania,
Taasisi za Kifedha, Wahisani, na wawakilishi wa
wakulima wa korosho. Lengo la warsha lilikuwa
kutafakari jinsi ya kufufua zao la korosho ili tunufaika
nalo.
Hali ya korosho siyo nzuri, kiwango cha uzalishaji wa
korosho na ubora wake, uko chini sana, isitoshe, ni
asilimia 20 tu ndiyo inayosindikwa hapa Tanzania, kiasi
kinachobakia husafirishwa hadi India kubanguliwa.
Katika hali hii, washiriki wa warsha walikubaliana:
Kusaidia wakulima katika jitihada zao za kupata
mazao makubwa yenye ubora wa juu.
Kuhakikisha kwamba korosho zote zinabanguliwa
hapahapa Tanzania, kusudi bei yake iongezeke, pia
wananchi wapate ajira.
KUBADILISHANA UZOEFU KUHUSU UTUNGAJI WA SERA ZA KILIMO
Baadhi ya wawakilisha wa taasisi
zilizoandaa warsha hii.
Zabibu ni zao linaloweza kutajirisha Wakulima.
Soko lake ni kubwa.
ACT NEWS
Ubia wa Kilimo Tanzania (Tanzania Agricultural Partnership– TAP. Ni muungano wa hiari
baina ya taasisi za umma na binafsi zinazofanya kazi kwa pamoja katika masuala ya kilimo.
Wabia wanochangia katika ushirikiano huu ni pamoja na CNFA/TAGMARK, AGRA, FIPS,
RUDI. Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, NMB na MS-Tanzania. Pamoja na makampuni
ya mbolea na mbegu na mbegu kama Yara, minjingu Mines & Fertilizer Co. Bytrade, Pannar,
Mosanto, Seedco na Kibo Seed. Hadi sasa shughuli za TAP zimeenea kwenye wilaya 25.
Malengo ya TAP
Lengo kuu la Ubia wa Kilimo Tanzania ni kuchangia kupunguza umasikini vijijini. Na lengo
mahususi ni kutoa pembejeo sahihi za kilimo kwa ajili ya kuongeza uzalishaji na kuboresha
masoko ya mazao kwa kutumia mlolongo wa thamani wenye tija ukisaidiwa na sekta ya
umma na binafsi.
Programu inalenga katika:
Upatikanaji nafuu wa pembejeo
Masoko bora ya bidhaa za wazalishaji
Ongezeko la uzalishaji katika kilimo
Uwekezaji kwenye sekta binafsi ya Kilimo
Mbinu za kufanikisha shughuli za maendeleo na biashara
Wasiliana na: Mratibu Kitaifa,
Tanzania Agricultural Partnership,
S. L. P 14130,
Dar es Salaam.
Simu: +255-22-2128032
Barua pepe: [email protected]
1. Ms. Janet Bitegeko—Mwenyekiti
2. Mr. Mark Magila—Mjumbe
3. Mr. Cleophas Rwechungura—Mjumbe
4. Ms. Milly Sanga-Mjumbe
Bodi ya Wahariri
Je, unataka kufahamu zaidi kuhusu ACT?Je, unataka kufahamu zaidi kuhusu ACT?
Wasiiliana na:Wasiiliana na:
Mkurugenzi Mtendaji:Mkurugenzi Mtendaji:
Agricultural Council of Tanzania Agricultural Council of Tanzania
S.L.P 14130,Dar es Salaam S.L.P 14130,Dar es Salaam
Simu:+255 22 2124851, Simu:+255 22 2124851,
Nukushi: +255 22 2128032, Nukushi: +255 22 2128032,
Barua pepe: act@actanzania .or.tzBarua pepe: act@actanzania .or.tz
Tovuti: www.act.anzania. or.tzTovuti: www.act.anzania. or.tz
DIRA YA ACT
DHAMIRA YA ACT
MALENGO YA ACT
1. Kuimarisha uwezo wa ACT wa kushawishi na kutetea masuala
yaliyofanyiwa utafiti na kuhakikiwa, ambavyo yanaathiri sekya ya
Kilimo.
2. Kuimarisha uwezo wa ACT wa kubuni na kutoa huduma katika
maeneo ya kimuundo, kiufundi, kiuongozi na programu za kutoa
huduma, kwa wanachama wake.
3. Kuongeza uelewa kwa wanachama wa ACT kuhusu programu zake,
huduma za kuwaongezea uwezo na kupata mitaji; ili kubaki na
angalau asilimia 85 ya wanachama wake, pamoja na kurudufu idadi
ya wanachama ifikapo 2018.
4. Kupanua uwanja wa kupata rasilimali –fedha, ili ACT iwe na uwezo
wa kujitegemea kwa asilimia 20 ifikapo 2018.
4 Jarida la ACT– Toleo Na. 16
FAHAMU SHUGHULI ZA TAP
Kuwa chombo kilele na kiongozi,
chenye jukumu la kuinua ustawi wa
wadau katika sekta ya Kilimo
nchini Tanzania
Kutetea kuwepo kwa mazingira
muafaka kwa Biashara ya Kilimo,
na kutoa huduma stahiki ili
kuongeza tija na faida kwa jamnii
ya Wakulima