Upload
lamlien
View
232
Download
0
Embed Size (px)
Citation preview
Jarida la SikikaToleo 19: Septemba, 2015Namba ya Usajili - 00005809
Huduma bora za afya kwa watanzania wote
Utangulizi
Toleo hili la 19 linaelezea kwa ufupi baadhi ya
shughuli zilizotekelezwa na Sikika katika robo ya
tatu ya mwaka 2015.
Sikika ilishiriki katika mafunzo yaliyotolewa na Ofisi
ya Mdihibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
(CAG) kwa Asasi za Kiraia (AZAKI) kutoka katika
mikoa ya Dodoma, Morogoro na Iringa. Mafunzo
hayo yalilenga kuongeza uelewa wa ripoti ya ukaguzi
ya CAG na jinsi ya kuitafsiri.
Shirika pia limeendela kuitaka serikali ijayo kutatua
changamoto za dawa na vifaa tiba nchini ili kuokoa
maisha ya watanzania. Ukosefu wa dawa na vifaa
tiba muhimu umeendela kuwa tatizo sugu nchini na
suluhu ya kudumu bado haijapatikana.
NDANICAG atoa mafunzo kwa AZAKI ........................................................................................................................2
Viongozi wajao watatue changamoto za dawa na vifaa tiba .............................................................................3
Mabadiliko ya mara kwa mara ARVs yawa kero ................................................................................................3
Afya: Kipaumbele muhimu kabla, baada ya Uchaguzi Mkuu .............................................................................4
Ziara ya shirika katika baadhi ya vituo pia ilibaini
kuwa baadhi ya watumia huduma za VVU na
UKIMWI wamekuwa wakibadilishiwa dawa za ARVs
mara kwa mara. Hali hiyo imejitokeza katika vituo
mbalimbali vya afya jijini Dar es Salaam.
Sikika pia ilifanya tathmini ya ilani za baadhi ya vyama
vya siasa na kuvishauri kujumuisha masuala ya afya,
hususan kwenye maeneo manne ambayo shirika
linayafanyia utetezi.
Kwa taarifa zaidi kuhusu kazi za Sikika, tafadhali
peruzi tovuti yetu; www.sikika.or.tz, twitter - @
sikika1, facebook - Sikika Tanzania na blogspot -
www.sikika-tz.blogspot.com. Kwa maoni tafadhali
wasiliana nasi kupitia [email protected] au sms 0688-
493-882.
Mkuu wa Idara ya Dawa na Vifaa tiba, Sikika Bi. Alice Monyo akitoa ufafanuzi juu ya changamoto za mfumo wa
usambazaji dawa na vifaa tiba katika mkutano uliojumuisha wadau mbalimbali nchini. Kushoto kwake ni Afisa
Program wa Idara hiyo, Scholastica Lucas na washiriki wengine.
Sikika Newsletter Q3, 2015 - Toleo 19.indd 1 11/9/15 8:33 AM
Jarida la Sikika - Toleo 19: Septemba, 2015
2
Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG) ilitoa mafunzo kwa wawakilishi wa
Asasi za Kiraia (AZAKI) kutoka katika mikoa ya Dodoma,
Morogoro na Iringa. Sikika ilikuwa ni miongoni mwa
washiriki wa mafunzo hayo yaliyolenga kuongeza
uelewa wa ripoti ya ukaguzi ya CAG na jinsi ya kuitafsiri.
Mafunzo yalifanyika mkoani Morogoro kuanzia Juni 15
hadi 16, 2015.
Sambamba na mafunzo hayo, wawakilishi wa AZAKI
walijadiliana na kuuliza maswali mbalimbali, kupata
ufafanuzi na kutoa michango yao ili ofisi ya CAG iweze
kuifanyia kazi. Baada ya mafunzo na majadiliano AZAKI
na ofisi ya CAG walifikia makubaliano na kuazimia
mambo kadhaa.
Mosi, iliazimiwa kuwa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (CAG)
iishauri serikali kutunga sheria inayowalazimisha
wakaguliwa (mfano Wizara, Idara na Mashirika ya
Umma) kutekeleza mapendekezo ndani ya muda utakao
ainishwa na sheria. Pia kuwepo kitengo maalumu cha
kufuatilia mapendekezo ya CAG na kutoa taarifa ya
hatua gani zichukuliwe endapo hakuna utekelezaji.
Pili, washiriki pia walipendekeza kuimarisha kitengo
cha sheria ili kuisaidia ofisi ya Mdhibiti katika masuala
mbalimbali ya kisheria hasa ukaguzi na katika
kushughulikia masuala mbalimbali yatokanayo na ripoti
za ukaguzi.
Tatu, ofisi ya CAG iimarishe ushirikiano na AZAKI
katika kupanga shughuli za ukaguzi na katika kufuatilia
utekelezaji wa mapendekezo ya ukaguzi. Mfano,
ofisi iangalie namna ya kutumia tafiti mbalimbali
zinazofanywa na asasi za kiraia wakati wa ukaguzi. Pia
ilipendekezwa kuwa ofisi ya Mdhibiti iangalie uwezekano
wa kuwaelimisha wawakilishi zaidi wa AZAKI juu ya
mamlaka ya CAG na masuala ya ripoti. Pia wawakilishi
hao wafuatiliwe na kuwezeshwa kuelimisha watu wengi
zaidi.
Wawakilishi hao wa AZAKI walipendekeza kwamba
ofisi ya CAG iongeze uwanda wa ukaguzi wa masuala
ya mapato ya serikali na madeni ya Taifa ili kutunza
rasilimali za nchi kwa maendeleo ya Wananchi.
Mwisho, washiriki walipendekeza Ofisi ya Taifa ya
Ukaguzi iishauri serikali kuendelea na utaratibu wa
kuwaelimisha wananchi na watumishi wake juu ya
maadili na uwajibikaji kwa ujumla. Wawakilishi hao
wa AZAKI walihitimisha kwa kupendekeza uwepo wa
mikutano ya tathmini ya kufuatilia mapendekezo ya
ripoti za ukaguzi.
CAG atoa mafunzo kwa AZAKI Na Wilson Kitinya, Morogoro
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof. Mussa Assad akiendesha moja ya mafunzo kwa taasisi na
wadau wa usimamizi wa sheria. Picha kwa hisani ya mtandao: http://www.nao.go.tz
Sikika Newsletter Q3, 2015 - Toleo 19.indd 2 11/9/15 8:33 AM
Jarida la Sikika - Toleo 19: Septemba, 2015
3
Mabadiliko ya mara kwa mara ARVs yawa kero Na Maria Kalavo
Baadhi ya watumia huduma za VVU na UKIMWI
katika vituo mbalimbali vya afya jijini Dar es Salaam
wamelalamikia ubadilishwaji wa mara kwa mara wa
chapa (brand) ya dawa wanazotumia kukabiliana na
makali ya VVU na UKIMWI. Haya ni malalamiko ambao
yamekuwa yakijitokeza na kujirudia katika mikutano ya
watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi (WAVIU) ambayo
Sikika imehudhuria kwa nyakati tofauti jijini Dar es
Salaam.
Baadhi ya WAVIU wameeleza kuwa dawa kutoka katika
baadhi ya makampuni zimekuwa zikiwasababishia
madhara kama vile kuishiwa nguvu, kulegea viungo na
kuhisi kizunguzungu jambo linalowafanya washindwe
kuendelea na shughuli zao. Kwa maelezo yao, watumia
huduma hawa wamekua wakiomba kupewa dawa
za aina moja au chapa moja lakini imeshindikana.
Maelezo wanayopata ni kwamba vituo havina uwezo
wa kuwabadilishia kwa kuwa hupokea dawa hizo kama
zilivyo kutoka Bohari Kuu ya Dawa (MSD).
Tatizo la kubadilishiwa dawa na kupewa za aina
nyingine ambazo zimeonekana kuwaathiri watumiaji
linasababisha baadhi ya WAVIU kutotumia dawa siku
zote (adherence) au kuacha kunywa siku ambazo mtu
atakuwa amejipangia safari au shughuli zinazohitaji awe
na nguvu. Kitendo cha kuacha kunywa dawa kina athari
kubwa kwa WAVIU kwani huweza kusababisha mwili
kujijengea usugu wa dawa.
Katuni kwa hisani ya Gazeti la Mtanzania Agosti 20, 2015
Changamoto za dawa na vifaa tiba zitatuliwe Na Siri Mtware
Ukosefu wa dawa na vifaa tiba umeendela kuwa
tatizo sugu ambalo suluhu yake bado haijapatikana.
Taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
kwa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) 2014, imebainisha
uwepo wa dawa kwa asilimia 24 tu kwa vituo vya
serikali na 47% kwa vituo binafsi.
Sababu kuu zinazotajwa ni pamoja na kutoshiriki kwa
wananchi katika kusimamia rasilimali na mipango
iliyowekwa katika vituo vyao vya kutolea huduma za
afya, ufinyu wa bajeti zinazopangwa na serikali na
matumizi mabaya ya rasilimali kwa baadhi ya watendaji
katika sekta ya afya.
Wakati nchi inaelekea kwenye uchaguzi mkuu wa
madiwani, wabunge na Rais, ni wakati sasa wa
wananchi kuhakikisha kuwa viongozi wanaowachagua
wanafanyia kazi changamoto hizo. Tuwahoji wagombea;
watafanya nini ili kuhakikisha tatizo la dawa linakuwa
historia nchini? Je, ni jinsi gani watahakikisha bajeti za
dawa muhimu na vifaa tiba zinaongezeka?
Zaidi, wanaoomba kuongoza waeleze; wataweka
mikakati ipi kuhakikisha wananchi wanashiriki kikamilifu
katika mipango ikiwa ni pamoja na kupatiwa taarifa
muhimu ili waweze kufanya ufuatiliaji wa huduma
zinazotolewa katika vituo vya kutolea huduma za
afya? Wananchi wana wajibu mkubwa wa kuhakikisha
changamoto hizi zinatatuliwa ili kuboresha upatikanaji
wa dawa na vifaa tiba nchini.
Mwisho, pamoja na changamoto zinazoendelea
kujitokeza, suala la upatikanaji wa dawa na vifaa tiba
lipewe kipaumbele kwa kusimamiwa na kufuatiliwa
kwa karibu ili kuondoa mianya ya ubadhilifu wa
watendaji wasio waaminifu. Kiasi kidogo cha fedha
kinachopatikana kikitumika ipasavyo kitapunguza
pengo la upungufu wa dawa na vifaa tiba katika vituo
vya kutolea huduma za afya vya umma nchini.
WAVIU hao wanaiomba serikali iweke utaratibu wa kupata
mrejesho kutoka kwa watumiaji wa dawa na huduma za
UKIMWI. Kwa sasa hakuna sehemu ambapo WAVIU
wanaweza kupeleka maoni/malalamiko yao moja kwa
moja kwa watunga sera au viongozi wanaohusika na
shughuli za UKIMWI.
Utaratibu wa kubadilishiwa dawa mara kwa mara
umeendelea kuwepo kwa muda sasa lakini watumia
huduma hawajaona serikali ikichukua hatua zozote.
Ushauri kwa serikali ni kushirikiana na wafadhili ili
kuhakikisha kwamba dawa zinazoagizwa ni zile
zinazotoka kwenye makampuni ambayo dawa zake
hazijalalamikiwa na watumiaji kuwa zina madhara.
Sikika Newsletter Q3, 2015 - Toleo 19.indd 3 11/9/15 8:33 AM
Nyumba Na. 69Ada Estate, KinondoniBarabara ya TunisiaMtaa wa WaverleyS.L.P 12183Dar es Salaam, TanzaniaSimu: +255 22 26 663 55/57
Ujumbe mfupi: 0688493882Faksi: +255 22 26 680 15Barua pepe: [email protected]
Blog: www.sikika-tz.blogspot.com
Facebook: Sikika Tanzania
Nyumba Na. 340Mtaa wa KilimaniS.L.P 1970Dodoma, TanzaniaSimu: 026 23 21307Faksi: 026 23 21316
Zaidi, ilipendekezwa kuongeza rasilimali watu katika
afya, kuhakikisha uwepo na upatikanaji wa dawa na
vifaa tiba wa uhakika pamoja na kuboresha huduma za
VVU na UKIMWI.
Shirika limeendela kutoa elimu kwa jamii kuhusu tathmini
hiyo kwa kutumia njia mbalimbali za mawasiliano.
Tunaamini tathmini hiyo itachangia kuboresha Ilani za
vyama mbalimbali vya siasa nchini. Vilevile itakuza uelewa
na ushiriki wa wananchi katika kufuatilia utekelezaji wa
vipaumbele vya afya, kwa wagombea na vyama vyao.
Sikika inatoa rai kwa wananchi wasiishie kuwa
watazamaji katika kipindi cha uchaguzi bali kushiriki kwa
kipindi chote cha miaka 5 kwa kudai utekelezaji wa Ilani
na vipaumbele hata baada ya uchaguzi. Hii itatoa fursa
kwa jamii kuwawajibisha wanaowapa kura kwa lengo la
kupata huduma bora za jamii.
Ilani ya chama ni mkataba au hati ya chama cha
siasa inayotoa muhtasari wa mambo ambayo chama
kinapanga kuyatekeleza endapo wapiga kura watakipa
fursa ya kuunda serikali.
VYAMA vya Siasa nchini vimeshauriwa kutunga ilani
ambazo zitatekelezeka baada ya uchaguzi mkuu
unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2015.
Ni takriban miaka 23 sasa tangu Tanzania ilipoingia rasmi
katika mfumo wa vyama vingi. Vyama mbalimbali vya
siasa nchini vimekuwa vikiandaa Ilani zao na kunadi sera
na vipaumbele kwa wananchi lakini baadhi zimekuwa
hazifahamiki kwa wananchi na hazitekelezwi, mathalan
kwa upande wa afya.
Kwa kutambua hivyo, Sikika ilitathmini ilani za vyama
4 vya siasa kwa miaka mitano iliyopita na hatimaye
kuandaa mapendekezo na matarajio ya wananchi kwa
miaka 5 ijayo, kwa upande wa afya. Shirika lilipata fursa
ya kutoa maoni juu ya vipaumbele vya afya kwa vyama
vya siasa kupitia kituo cha Demokrasia na Maendeleo
(TCD).
Tathmini ya Sikika iliyojikita katika upande wa afya
ilipendekeza kuimarisha utawala bora, uwazi na ushiriki
wa wananchi katika kupanga bajeti za afya na utekelezaji.
Afya: Kipaumbele muhimu kabla, baada ya Uchaguzi MkuuNa Richard Msittu, Dodoma
Baadhi ya akinamama wakisubiri huduma katika kituo cha cha afya Ndago wilayani Iramba.
Sikika Newsletter Q3, 2015 - Toleo 19.indd 4 11/9/15 8:33 AM