21
1 HOTUBA YA MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMWIA JAKAYA MRISHO KIKWETE WAKATI WA KUFUNGA SEMINA YA MAKATIBU WA CCM MIKOA NA WILAYA NA WENYEVITI WA CCM WA WILAYA, INAYOFANYIKA DODOMA TAREHE 24 OKTOBA, 2013 Ndugu Phillip Mangula, Makamu Mwenyakiti wa CCM; Ndugu Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM; Ndugu Manaibu wa Katibu Mkuu; Ndugu Makatibu wa Sekretariat Mliopo; Ndugu Wanasemina; Ndugu Watoa Mada; Mabibi na Mabwana; Nakushukuru na kukupongeza sana Katibu Mkuu kwa uamuzi wa busara wa kuwa na mafunzo haya kwa Wenyeviti wa Wilaya, Makatibu wa Wilaya na Makatibu wa Mikoa wa Chama chetu. Nafurahi kwamba mafunzo haya yamefanyika wakati muhimu katika safari yetu ya kuelekea

Nakushukuru na kukupongeza sana Katibu Mkuu kwa uamuzi …...2 mwaka 2015. Hivi sasa tupo takriban katikati ya safari hiyo. Naamini mafunzo haya yatasaidia kujiweka sawa katika ngwe

  • Upload
    others

  • View
    0

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Nakushukuru na kukupongeza sana Katibu Mkuu kwa uamuzi …...2 mwaka 2015. Hivi sasa tupo takriban katikati ya safari hiyo. Naamini mafunzo haya yatasaidia kujiweka sawa katika ngwe

1

HOTUBA YA MWENYEKITI WA CHAMA CHA

MAPINDUZI NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA

TANZANIA, MHESHIMWIA JAKAYA MRISHO KIKWETE

WAKATI WA KUFUNGA SEMINA YA MAKATIBU WA

CCM MIKOA NA WILAYA NA WENYEVITI WA CCM WA

WILAYA, INAYOFANYIKA DODOMA

TAREHE 24 OKTOBA, 2013

Ndugu Phillip Mangula, Makamu Mwenyakiti wa CCM;

Ndugu Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM;

Ndugu Manaibu wa Katibu Mkuu;

Ndugu Makatibu wa Sekretariat Mliopo;

Ndugu Wanasemina;

Ndugu Watoa Mada;

Mabibi na Mabwana;

Nakushukuru na kukupongeza sana Katibu Mkuu kwa

uamuzi wa busara wa kuwa na mafunzo haya kwa

Wenyeviti wa Wilaya, Makatibu wa Wilaya na Makatibu wa

Mikoa wa Chama chetu. Nafurahi kwamba mafunzo haya

yamefanyika wakati muhimu katika safari yetu ya kuelekea

Page 2: Nakushukuru na kukupongeza sana Katibu Mkuu kwa uamuzi …...2 mwaka 2015. Hivi sasa tupo takriban katikati ya safari hiyo. Naamini mafunzo haya yatasaidia kujiweka sawa katika ngwe

2

mwaka 2015. Hivi sasa tupo takriban katikati ya safari hiyo.

Naamini mafunzo haya yatasaidia kujiweka sawa katika

ngwe ya pili ya kipindi cha pili cha uongozi wa Awamu ya

Nne ya uongozi wa CCM katika nchi yetu. Awamu ambayo

mimi ndiye kiongozi wake kwa niaba ya Chama chetu.

Ni mategemeo yangu kuwa baada ya mafunzo haya,

mijadala iliyofuatia na mapendekezo mliyoyatoa

mnaondoka hapa mkiwa manahodha bora zaidi wa

kuongoza vyema Chama cha Mapinduzi kwenda na kufika

salama katika safari yetu ya kuelekea 2015. Mnatoka kwenye

mafunzo haya mkiwa na kauli mbiu moja tu kwamba

“Ushindi ni Hakika mwaka 2014 na 2015”.

Lengo Kuu la Chama cha Siasa

Ndugu viongozi wenzangu;

Sote tunafahamu kwamba lengo kuu la Chama cha

Mapinduzi kama ilivyo kwa vyama vyote vya siasa nchini

na duniani ni kushika dola. Hivyo ndivyo Katiba ya CCM

inavyotamka wazi katika Ibara ya 5 kwamba malengo na

Page 3: Nakushukuru na kukupongeza sana Katibu Mkuu kwa uamuzi …...2 mwaka 2015. Hivi sasa tupo takriban katikati ya safari hiyo. Naamini mafunzo haya yatasaidia kujiweka sawa katika ngwe

3

madhumuni ya CCM ni; Nanukuu “Kushinda katika

uchaguzi wa Serikali Kuu na Mitaa, Tanzania Bara

na Zanzibar ili kuunda na kushika Serikali Kuu na Mitaa

katika Jamhuri ya Muungano kwa upande mmoja na

Zanzibar kwa upande wa pili”. Katika mazingira ya nchi

yetu ni kushinda uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya

Muungano wa Tanzania, Rais wa Zanzibar, Wabunge,

Wawakilishi, Madiwani na ule wa viongozi wa Serikali za

Mitaa, Vijiji na Vitongoji. Hivyo pamoja na majukumu

mengine mengi mliyonayo lazima mtambue kwamba

hatimaye shabaha yetu kuu ni kuhakikisha kuwa wagombea

wa Chama chetu wanashinda katika chaguzi hizo.

Nyie kama viongozi na watendaji wakuu wa maeneo

yenu lazima mtambue kuwa chombo cha kutuongoza,

kutuimarisha na kutufikisha kwenye ushindi ni Chama cha

Mapinduzi. Hivyo basi, lazima Chama kiwe na nguvu ya

kutosha ya kutufikisha kwenye lengo letu kuu. Hamna budi

kila mnapofanya jambo mpime kama jambo hilo linakisaidia

Page 4: Nakushukuru na kukupongeza sana Katibu Mkuu kwa uamuzi …...2 mwaka 2015. Hivi sasa tupo takriban katikati ya safari hiyo. Naamini mafunzo haya yatasaidia kujiweka sawa katika ngwe

4

Chama chetu kuwa na nguvu za kushinda uchaguzi au la.

Msifanye mambo yatakayoipunguzia CCM nguvu na

yanayojenga mazingira yatakayosababisha wagombea wa

CCM kushindwa na hivyo Chama chetu kushindwa.

Mkifanya hivyo mtakuwa hamkisaidii Chama chetu. Wakati

wote kila mmoja wetu ajiulize je hili nilifanyalo linasaidia

CCM kushinda? Au kwa lugha nyingine tujiulize ni kitu

gani nikifanya kinasaidia Chama cha Mapinduzi kushinda.

Uhai na Uimara wa Chama

Ndugu viongozi wenzangu;

Kwa maoni yangu kuna mambo matatu muhimu

ambayo yakifanyika yatasaidia Chama cha Mapinduzi

kushinda:-

(1) Uimara wa Chama;

(2) Tabia na mwenendo wa viongozi na wanachama wa

CCM; na,

(3) Utendaji wa Serikali ya CCM.

Page 5: Nakushukuru na kukupongeza sana Katibu Mkuu kwa uamuzi …...2 mwaka 2015. Hivi sasa tupo takriban katikati ya safari hiyo. Naamini mafunzo haya yatasaidia kujiweka sawa katika ngwe

5

Inatupasa kuhakikisha kuwa Chama chetu kinashiriki

katika uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi

Mkuu kikiwa na nguvu kubwa, hai na imara kwa kila hali

toka ngazi ya shina, tawi, kata, jimbo, wilaya, mkoa hadi

taifa. Siku za nyuma nilishasema kuwa Chama ni kama

ulivyo mwili wa mwanadamu, uimara wake unategemea

sana ukamilifu na uzima wa viungo vyake. Kikipungua

kiungo kimojawapo Chama kina ulemavu na kikidhoofika

chochote kinakuwa na afya mbaya. Kwa ajili hiyo basi

uimara wa Chama cha Mapinduzi unategemea kuwepo kwa

wanachama, viongozi, watendaji, vikao, rasilimali na

jumuiya za Chama na vyote vikiwa vinafanya kazi zake

ipasavyo.

Ninyi mliopo hapa yaani Wenyeviti wa Wilaya,

Makatibu wa Wilaya na Makatibu wa Mikoa ndiyo

mnaotegemewa zaidi kuliko mtu mwingine yeyote

kuhakikisha kuwa viungo vya Chama vinakamilika na

kwamba viko hai kwa maana ya kufanya kazi kama

Page 6: Nakushukuru na kukupongeza sana Katibu Mkuu kwa uamuzi …...2 mwaka 2015. Hivi sasa tupo takriban katikati ya safari hiyo. Naamini mafunzo haya yatasaidia kujiweka sawa katika ngwe

6

inavyotarajiwa kwa mujibu wa Katiba ya Chama cha

Mapinduzi, sera na maamuzi mbalimbali.

Ndugu viongozi;

Ni matumaini yangu na nimehakikishiwa hivyo

kwamba katika mafunzo haya mmepewa maarifa ya

kuhakikisha kuwa Chama cha Mapinduzi kinakuwa hivyo.

Mmejifunza juu ya nini mnachowajibika kufanya ili Chama

chetu kiwe imara, hai na chenye nguvu. Nimeambiwa pia

kuwa katika majadiliano mlipata nafasi ya kubadilishana

uzoefu kutoka kwa wale waliofanikiwa na hata wale

walioshindwa. Ndugu zangu mpate nini zaidi ya hayo.

Mfanyiwe nini tena lililo bora zaidi kuliko hilo. Ndiyo

maana sipati kigugumizi kusema kuwa sasa ninyi

mmekuwa wapiganaji bora zaidi. Haya nendeni mkaoneshe

umahiri wenu kwenye medani ya kujenga Chama. Nendeni

mkaoneshe mtindo bora wa uongozi na utendaji. Nendeni

mkakipe Chama chetu sura mpya, uhai mpya na kasi mpya

ya maendeleo.

Page 7: Nakushukuru na kukupongeza sana Katibu Mkuu kwa uamuzi …...2 mwaka 2015. Hivi sasa tupo takriban katikati ya safari hiyo. Naamini mafunzo haya yatasaidia kujiweka sawa katika ngwe

7

Kuingiza Wanachama

Ndugu Viongozi;

Hatuna budi kwanza kabisa kuhakikisha kwamba

Chama chetu kinapata wanachama wapya wengi na

kuwaimarisha waliopo. Wanachama ndiyo kielelezo cha

awali cha kuwepo kwa Chama. Wingi wa wanachama ndio

nguvu ya kufanya kazi ya Chama na mtaji wa uhakika wa

kuanzia katika kutafuta ushindi. Hivyo basi, lazima wakati

wote Chama chetu kiendelee kuingiza wanachama wapya.

Tusisubiri mpaka karibu au wakati wa uchaguzi ndipo

tuongeze nguvu ya kusajili wanachama wapya. Twende

tukafanye kazi ndani ya umma kuwashawishi na

kuwahamasisha wananchi, hususan vijana, kujiunga na

Chama cha Mapinduzi. Mnapaswa kuwa na mikakati

madhubuti ya kupata wanachama wapya katika maeneo

yenu. Kupata wanachama wapya ni kazi ya kudumu ya

Chama.

Page 8: Nakushukuru na kukupongeza sana Katibu Mkuu kwa uamuzi …...2 mwaka 2015. Hivi sasa tupo takriban katikati ya safari hiyo. Naamini mafunzo haya yatasaidia kujiweka sawa katika ngwe

8

Ndugu viongozi;

Kimsingi uimara wa Chama chetu unategemea uhai wa

wanachama wake. Mwanachama hai wa CCM ni yule

anayelipa ada na kushiriki kwa ukamilifu katika shughuli za

Chama, mojawapo ikiwa kuwashawishi watu wasiokuwa

wanachama kuunga mkono CCM. Ili wanachama wawe

hivyo ni wajibu wa viongozi kuwa na mikakati maalum ya

kuwawezesha kufanya hivyo. Kuwatembelea mara kwa

mara kuzungumza nao na kuwaelimisha mambo

mbalimbali yanayohusu Chama na nchi kwa ujumla ni

mbinu muhimu sana kwa ajili hiyo. Tukifanya hivyo

Chama chetu kitakuwa na wanachama wengi wanaojua

mambo na wenye moyo wa kukitumikia. CCM itakuwa na

uwezo mkubwa wa kujiendesha na kufanya mambo yake.

Kitakuwa kimeimarika zaidi. Viongozi wa Chama lazima

tujenge mazoea ya kuwatembelea wanachama na

kuzungumza nao. Hili ndilo jukumu la msingi na asiyefanya

hivyo ameshindwa kutimiza wajibu wake.

Page 9: Nakushukuru na kukupongeza sana Katibu Mkuu kwa uamuzi …...2 mwaka 2015. Hivi sasa tupo takriban katikati ya safari hiyo. Naamini mafunzo haya yatasaidia kujiweka sawa katika ngwe

9

Ndugu zangu;

Ni ukweli ulio wazi kuwa si viongozi na watendaji

wengi wanaofanya hivyo. Lazima mjisahihishe. Zamani

mlidai hamna magari sasa mnayo. Kwa kweli

kutowatembelea wanachama ni jambo lisilokuwa na

maelezo. Nilishaagiza siku za nyuma na narudia kusisitiza

tena leo kuwa katika Taarifa ya kazi za Chama ya kila

mwezi kila Wilaya itoe taarifa ya kuhusu viongozi

kutembelea matawi na kuzungumza na wanachama. Hivyo

hivyo kwa Mikoa, nao watoe taarifa ya kutembelea Wilaya

zao na kuzungumza na viongozi wa Wilaya, Kata, Matawi

na Mashina pamoja na kuzungumza na wanachama. Ndugu

Katibu Mkuu naomba hili lazima tulidai lifanyike kwani

manufaa yake kwa uhai wa Chama cha Mapinduzi hayana

mfano wake.

Page 10: Nakushukuru na kukupongeza sana Katibu Mkuu kwa uamuzi …...2 mwaka 2015. Hivi sasa tupo takriban katikati ya safari hiyo. Naamini mafunzo haya yatasaidia kujiweka sawa katika ngwe

10

Ndugu viongozi;

Jambo la pili muhimu kwa uhai na maendeleo ya

Chama chetu ni kuwatembelea wananchi na kuzungumza

nao. Ni vyema mkatambua kuwa tunapotaka kuongoza dola

kwa mfumo wa vyama vingi kazi yetu kubwa ni ile ya

kuwavutia watu upande wetu. Tushinde mioyo na akili zao.

Tuwafanye watu waelewe sera na siasa ya Chama cha

Mapinduzi, wazikubali na kutuunga mkono. Tufute maneno

hasi na uongo wa wapinzani dhidi ya CCM na serikali yake.

Lazima viongozi mtoke muwatembelee wananchi,

mzungumze nao kuhusu Chama chetu na taifa kwa ujumla.

Tumekuwa wazito sana kufanya hivyo, lazima tujirekebishe.

Utendaji wa Serikali

Ndugu viongozi na Watendaji;

Kwa vile hivi sasa CCM ndicho Chama tawala,

viongozi wa Chama wanaowajibu wa namna mbili. Kwanza,

kuhakikisha kuwa serikali yao inatekeleza Ilani ya Uchaguzi

Page 11: Nakushukuru na kukupongeza sana Katibu Mkuu kwa uamuzi …...2 mwaka 2015. Hivi sasa tupo takriban katikati ya safari hiyo. Naamini mafunzo haya yatasaidia kujiweka sawa katika ngwe

11

na pili, kuwaelezea wananchi masuala mbalimbali ya

utendaji wa serikali. Viongozi wa Chama mmepewa

dhamana ya kuyasimamia hayo katika maeneo yenu.

Lazima mfuatilie utekelezaji wa Ilani kupitia vikao vyenu

hususan Kamati za Siasa na Halmashauri Kuu za Wilaya na

Mikoa. Ndiyo maana Wakuu wa Wilaya na Mikoa ni

wajumbe wa vikao hivyo na hutoa taarifa ya kazi nyakati

mbalimbali.

Ili muweze kufanya hivyo, lazima ninyi wenyewe

mfahamu vizuri Ilani ya CCM inasema nini kuhusu Mikoa

na Wilaya zenu. Pili, lazima mfahamu ahadi za wagombea

wa Chama chetu na za viongozi wa Chama katika ngazi

mbalimbali. Lengo ni kujua na kufuatilia utekelezaji wa

ahadi hizo ili zisije zikageuka kuwa tatizo katika uchaguzi

ujao. Tujue zipi zimetekelezwa, zipi hazijatekelezwa na

zilizotekelezwa zimetekelezwa kwa kiwango gani. Tujue

mipango iliyopo na nini kinapaswa kufanyika ili kutekeleza

au kukamilisha ahadi hizo. Tukumbushane mambo ambayo

Page 12: Nakushukuru na kukupongeza sana Katibu Mkuu kwa uamuzi …...2 mwaka 2015. Hivi sasa tupo takriban katikati ya safari hiyo. Naamini mafunzo haya yatasaidia kujiweka sawa katika ngwe

12

hayajatekelezwa. Wakumbusheni Marais, Mawaziri,

Wabunge, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Madiwani

na viongozi wa Serikali za Mitaa juu ya ahadi zao

walizozitoa ambazo hazijatekelezwa ili wazitekeleze au

wawe na mipango thabiti ya kutekeleza.

Pia, ziambieni serikai katika ngazi zote husika kuhusu

masuala mapya yaliyojitokeza ambayo wananchi wanataka

tuyatekeleze. Tukiweza kuyafanya na hayo pia

yatatuongezea kuaminika, kupendwa na kutuongezea

uhakika wa kuchaguliwa tena. Naomba mshirikiane na

viongozi wa Serikali katika maeneo yenu kutengeneza

utaratibu mzuri ili masuala hayo yajulikane na

kutengenezwa mkakati maalum wa kuyatekeleza.

Ndugu viongozi;

Tumieni vikao vyenu au njia nyingine za mawasiliano

kuyafikisha masuala hayo na mengine. Katika vikao hivyo

pia, Wakuu wa Wilaya na Mikoa wanao wajibu wa kuelezea

na kufafanua masuala mbalimbali yahusuyo Serikali au

Page 13: Nakushukuru na kukupongeza sana Katibu Mkuu kwa uamuzi …...2 mwaka 2015. Hivi sasa tupo takriban katikati ya safari hiyo. Naamini mafunzo haya yatasaidia kujiweka sawa katika ngwe

13

Mkoa au Wilaya husika. Wajumbe waulize ili wapate

maelezo ya kusaidia kujibu hoja za wananchi au

wapotoshaji kwa kazi nzuri za serikali ya CCM.

Vikao

Ndugu Viongozi;

Hatuna budi kuhakikisha kuwa vikao vya Chama

vinafanyika na vinaendeshwa vizuri ili viweze kutekeleza

ipasavyo jukumu lake la kufuatilia utendaji wa serikali ya

CCM na uendeshaji wa Chama. Lazima vikao vya Kikatiba

vifanyike bila kukosa na pawepo na kalenda maalum kwa

ajili hiyo. Kuwa na kalenda inayojulikana ni muhimu kwa

wajumbe kwani wanashughuli zao zinazowapatia riziki

hivyo wakijua mapema vikao vya Chama watajua namna

bora ya kujipanga. Si vizuri taarifa ya vikao vya Kikatiba

ikatolewa kwa muda mfupi kana kwamba ni vikao vya

dharura.

Jambo lingine muhimu kuhusu vikao ni kuwa na

agenda za maana na zilizoandaliwa vizuri. Kwa mfano,

Page 14: Nakushukuru na kukupongeza sana Katibu Mkuu kwa uamuzi …...2 mwaka 2015. Hivi sasa tupo takriban katikati ya safari hiyo. Naamini mafunzo haya yatasaidia kujiweka sawa katika ngwe

14

mnaweza mkaamua kila kikao kiwe na agenda ipi kuu

katika Wilaya na Mkoa wenu. Mathalani mnaweza kupanga

kuwa kikao cha mwezi fulani kiwe cha kupokea taarifa ya

utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi, cha mwezi fulani kupokea

taarifa ya uhai wa Chama na kadhalika. Mkifanya hivyo

mnajipa muda wa kushughulikia masuala muhimu. Hata

hivyo haizuiliwi kuzungumzia au kushughulikia masuala

mengine muhimu. Ni muhimu pia kuhakikisha kuwa vikao

vinaendeshwa vizuri na wajumbe wanapata nafasi ya kutoa

maoni yao kwa uhuru. Kumbukumbu za vikao ziandikwe

vizuri na kuhifadhiwa vizuri.

Ndugu Katibu Mkuu;

Chama lazima kiwe na utaratibu wa kuwafundisha

Makatibu Tawi, Makatibu Kata, Makatibu Wasaidizi,

Makatibu wa Wilaya na Mikoa kuhusu uandishi wa

kumbukumbu na namna ya kuzihifadhi na kuzifanyia kazi.

Lazima pia kiwe na utaratibu wa mafunzo kwa watumishi

na watendaji wake wa kada mbalimbali katika ngazi zote za

Page 15: Nakushukuru na kukupongeza sana Katibu Mkuu kwa uamuzi …...2 mwaka 2015. Hivi sasa tupo takriban katikati ya safari hiyo. Naamini mafunzo haya yatasaidia kujiweka sawa katika ngwe

15

utumishi na utendaji. Chama kina mifumo yake na taratibu

zake za kuendesha shughuli ambazo lazima zifuatwe. Ni

lazima watu wafundishwe ili wazielewe na kuzifuata. Vile

vile ni muhimu Chama kuwekeza katika kuwaendeleza

watumishi na watendaji wake kielimu na kitaaluma. Aidha,

tuwalipe maslahi mazuri.

Mali za Chama

Ndugu Viongozi na Watendaji;

Jambo lingine muhimu sana katika kuimarisha Chama

ambalo naamini mmelizungumzia kwa undani ni rasilimali

za Chama kwa Chama kuwa na fedha, majengo, vyombo

vya usafiri na vifaa vingine vya kuendeshea shughuli zake

ni jambo la kufa na kupona. Lazima tuwe na fedha za

kutosha, majego mazuri ya kufanyia kazi, magari na

vyombo vingine vya usafiri na vifaa mbalimbali. Lazima

tuwe na mipango na mikakati dhabiti ya kuwa na rasilimali

hizo na hasa fedha. Katika historia ya Chama chetu vyanzo

vikuu vya fedha ni ada za wanachama, uuzaji wa vitabu na

Page 16: Nakushukuru na kukupongeza sana Katibu Mkuu kwa uamuzi …...2 mwaka 2015. Hivi sasa tupo takriban katikati ya safari hiyo. Naamini mafunzo haya yatasaidia kujiweka sawa katika ngwe

16

mali nyingine za Chama na michango ya hiari. Hali ilivyo

sasa ni kwamba wanachama wamekuwa wazito kulipa ada,

vitabu na mali za kuuza hazipo za kutosha. Na michango ya

hiari haibuniwi. Kwa kweli, Chama siku hizi kinaendeshwa

kwa taabu. Wilaya na Mikoa hutegemea Makao Makuu

tofauti na ilivyokuwa zamani. Pale ambapo kuna wafadhili

ambao ni wabunge wajumbe wa NEC wenye uwezo na

wapenzi wa Chama mambo huwa mazuri. Pale ambapo

hawapo kuna shida. Aghalabu baadhi ya wafadhili au

wapenzi wa Chama ni watu wenye agenda zao. Ama wana

tamaa za kugombea uongozi fulani hivyo wananunua

kuungwa mkono au wanatafuta msaada fulani.

Mtakubaliana nami kuwa jambo hili muhimu sana kwa

uhai wa Chama lakini halijapata mwelekeo mzuri. Lazima

tubadilike tena tubadilike haraka vinginevyo mbele ya safari

hali itakuwa mbaya zaidi. Hatuna budi kuwa wabunifu na

kuongeza jitihada za kukijengea Chama uwezo wa kifedha

na rasilimali katika ngazi zote. Tulishatoa maagizo kwa kila

Page 17: Nakushukuru na kukupongeza sana Katibu Mkuu kwa uamuzi …...2 mwaka 2015. Hivi sasa tupo takriban katikati ya safari hiyo. Naamini mafunzo haya yatasaidia kujiweka sawa katika ngwe

17

ngazi kuwa na mfuko wa uchaguzi, sijui ni wangapi wanao

na wana kiasi gani. Na watu hawashtuki. Hali hii

haikubaliki lazima tujirekebishe, hatujachelewa.

Mtakumbuka katika Mkutano Mkuu uliopita niliagiza

majengo na viwanja vyote vya Chama vipatiwe hati. Je,

limekalimika?

Maadili

Ndugu viongozi na Watendaji;

Tabia na mwenendo mwema ni sifa ya msingi ya kuwa

kiongozi na mtendaji wa Chama cha Mapinduzi. Kwa

namna ya pekee kiongozi hutoa taswira ya CCM kwa

wananchi na wanachama. Mkiwa wachapa kazi hodari,

watu wenye nidhamu na waadilifu ni sifa njema kwa Chama

chetu. Mkiwa tofauti na hayo ni sifa mbaya kwa CCM.

Naamini haya ninayoyasema yameelezwa vizuri na

kusisitizwa sana katika mafunzo haya. Naomba

muwayazingatie na kuyatekeleza.

Page 18: Nakushukuru na kukupongeza sana Katibu Mkuu kwa uamuzi …...2 mwaka 2015. Hivi sasa tupo takriban katikati ya safari hiyo. Naamini mafunzo haya yatasaidia kujiweka sawa katika ngwe

18

Nendeni sasa mkadhihirishe kuwa ni mfano bora kwa

wanachama na wananchi tunaowaongoza. Mkifanya hivyo

mtakubalika na kuungwa mkono na wanachama na jamii

kwa ujumla. Na hivyo basi chama chetu kitanufaika.

Ndugu viongozi;

Si jambo jema hata kidogo kwa viongozi au watendaji

wa Chama kuwa na tabia na mwenendo mbaya

wanakiumiza Chama. Jiepusheni kuwa waombaji na

wapokeaji wa rushwa. Epukeni kuwa mawakala na

wasambazaji wa fedha chafu za wagombea wanaotaka

kununua uongozi. Tukifanya hivyo tutaiharibu sana sifa ya

CCM. Mtashindwa kusimamia haki na mtakigawa Chama

chetu. Ninyi mnategemewa kuwa wasimamizi wa

michakato ya uchaguzi lazima mtende haki na muwe

waadilifu. Mkikubali kuhongwa au kuwa wakala wa

mgombea mtawanyima haki baadhi ya wagombea na

itakuwa vigumu kwenu kutatua malalamiko yanayotokea

kwa sababu ninyi wenyewe ni sehemu ya tatizo. Isitoshe

Page 19: Nakushukuru na kukupongeza sana Katibu Mkuu kwa uamuzi …...2 mwaka 2015. Hivi sasa tupo takriban katikati ya safari hiyo. Naamini mafunzo haya yatasaidia kujiweka sawa katika ngwe

19

wagombea watapoteza imani kwa viongozi na watendaji wa

Chama chao, jambo ambalo ni la hatari. Linalofanya watu

kupata hasira na wengine kufanya uamuzi usiotarajiwa na

kukiathiri Chama. Katika maeneo mengi tuliyopoteza

katika uchaguzi uliopita upendeleo wa viongozi kwa

wagombea ulichangia sana. Hakikisheni kasoro za chaguzi

zilizopita hazijirudii tena siku za usoni. Msije mkakiingiza

Chama kwenye matatizo yanayoweza kuepukika.

Ndugu viongozi na Watendaji;

Kabla ya kumaliza, ningependa kuwakumbusha kuwa

Chama chetu kupitia serikali yake kimefanya mambo mengi

mazuri kwa maendeleo ya nchi yetu na watu wake. Sina

shaka ifikapo 2015 tutakuwa tumefanya vizuri zaidi na

hivyo hatutasutwa kwa kutokuwa wakweli. Kwa ajili hiyo

sioni sababu kwa nini tusifanye vizuri katika chaguzi za

2014 na 2015. Lakini, tutaweza kutokufanya vizuri iwapo

tutafanya makosa katika uteuzi wa wagombea. Tukiteua

watu wasiokubaliwa na jamii kwa sababu ya urafiki, ujamaa

Page 20: Nakushukuru na kukupongeza sana Katibu Mkuu kwa uamuzi …...2 mwaka 2015. Hivi sasa tupo takriban katikati ya safari hiyo. Naamini mafunzo haya yatasaidia kujiweka sawa katika ngwe

20

au kwa kupewa chochote binafsi zetu, jamii itatuadhibu.

Anayedhani kuwa kila aliyeteuliwa na CCM atachaguliwa

anajidanganya. Wakati huo umepita. Tupate wagombea

wazuri tusiendekeze rushwa. Tusiwaonee au kuwadhulumu

watu na kuwafanya wajenge chuki dhidi ya Chama chetu na

hata kususa au kufanya matendo ya kukidhuru Chama.

Tusiwasukume watu ukutani bila ya sababu acheni mambo

yawe wazi, ushindi uwe wa haki ili mtu akishindwa ajue

kuwa haikuwa bahati yake. Mtu mwenye upungufu

aambiwe kasoro zake kama ilivyo mila na desturi ya CCM.

Si vizuri mtu ajione kaonewa au kadhulumiwa na viongozi

wa Chama waliopokea rushwa kutoka kwa wagombea au

wanaomchukia. Nalisema hili kwa sababu habari zimezagaa

za watu wanaojipanga kugombea uongozi kuwa wanahonga

sana viongozi na watendaji wa CCM. Mzee Mangula

analishughulikia hilo. Nawasii mjiepushe nao msije

mkakutwa kuhusika, mtapata matatizo makubwa. Lazima

tulinde na kudumisha heshima ya Chama chetu.

Page 21: Nakushukuru na kukupongeza sana Katibu Mkuu kwa uamuzi …...2 mwaka 2015. Hivi sasa tupo takriban katikati ya safari hiyo. Naamini mafunzo haya yatasaidia kujiweka sawa katika ngwe

21

Ndugu viongozi na watendaji;

Nimalizie kwa kuwapongeza watoa mada kwa kazi

nzuri waliofanya ya kutoa mafunzo kwa viongozi wetu

hawa. Viongozi wenzangu tusiwaangushe wakufunzi wetu

kwa kutoonesha mabadiliko katika uongozi na utendaji

wetu baada ya mafunzo hayo. Nawatakia safari njema na

utendaji ulio bora zaidi.

Baada ya kusema haya, natamka rasmi kwamba,

semina yenu imefungwa. Asanteni kwa kunisikiliza.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.