626
Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari

Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

  • Upload
    others

  • View
    7

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari

Page 2: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

Kitabu cha MormoniMwongozo wa Mwalimu wa Seminari

Kimechapishwa na Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho Mjini Salt Lake, Utah

Page 3: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

Maoni na masahihisho insert period after yanakubaliwa. Tafadhali yatume, pamoja na makosa, kwa:

Seminaries and Institutes of Religion Curriculum Services 50 E. North Temple St., Floor 8 Salt Lake City, Utah 84150- 0008

USA Barua pepe: ces - manuals@ ldschurch. org

Tafadhali orodhesha jina lako kamili, anwani, kata, na kigingi. Hakikisha unatoa jina la kitabu cha mwongozo. Kisha toa maoni yako.

© 2012 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa Kimechapishwa Marekani

Kiingereza Kiliidhinishwa: 10/09 Idhinisho la Tafsiri: 10/09.

Tafsiri ya Book of Mormon Seminary Teacher Manual Swahili

09411 743

Page 4: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

iii

Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . vi

Dhamira Yetu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . viMatayarisho ya Somo . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . viKutumia Mwongozo wa Kila Siku wa Mwalimu . . . . . . . . .viiProgramu za Seminari za Kila Siku (Muda wa Ruhusa

na Mapema- Asubuhi) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ixKwa Kutumia Masomo ya Mafunzo- Nyumbani . . . . . . . . . xiMpango wa Seminari wa Mafunzo- Nyumbani . . . . . . . . . . xiiNyenzo Zingine . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . xiii

Masomo ya Kila Siku ya Mafunzo NyumbaniSomo la 1 Wajibu wa Mwanafunzi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .1Somo la 2 Kujifunza Maandiko matakatifu.. . . . . . . . . . . . .5Somo la 3 Mpango wa Wokovu. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .8Somo la 4 Ukurasa wa Kwanza, Utangulizi, na

Shuhuda za Mashahidi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .11Somo la 5 Maelezo ya Jumla ya Kitabu cha Mormoni . . .14Somo la mafunzo ya Nyumbani Kujifunza Maandiko

Matakatifu–Maelezo ya Jumla ya Kitabu cha Mormoni (Kitengo cha 1) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .18

Utangulizi wa Kitabu cha Kwanza cha Nefi . . . . . . . . . . . . .20Somo la 6 1 Nefi 1 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .21Somo la 7 1 Nefi 2 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .24Somo la 8 1 Nefi 3–4 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .27Somo la 9 1 Nefi 5 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .30Somo la 10 1 Nefi 6 and 9 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .33Somo la Mafunzo ya Nyumbani 1 Nefi 1–6; 9

(Kitengo 2). . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .36

Somo la 11 1 Nefi 7 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .38Somo la 12 1 Nefi 8 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .41Somo la 13 1 Nefi 10–11 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .44Somo la 4 1 Nefi 12–13 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .47Somo la 15 1 Nefi 14 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .50Somo la Mafunzo ya Nyumbani 1–Nefi 7–14

(Kitengo cha 3) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .53

Somo 16 1 Nefi 15 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .55Somo la 17 1 Nefi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .58Somo la 18 1 Nefi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .61Somo la 19 1 Nefi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .64Somo la 20 1 Nefi 19 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .67Somo la mafunzo ya Nyumbani 1 Nefi 15–19

(Kitengo cha 4) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .71

Somo la 21 1 Nefi 20–22 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .73Utangulizi wa Kitabu cha Pili cha Nefi . . . . . . . . . . . . . . . . .76Somo la 22 2 Nefi 1 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .77Somo la 23 2 Nefi 2 (Sehemu ya 1). . . . . . . . . . . . . . . . . . .80Somo la 24 2 Nefi 2 (Sehemu ya 2). . . . . . . . . . . . . . . . . . .83Somo la 25 2 Nefi 32:3 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .86

Somo la Mafunzo ya nyumbani 1 Nefi 20–2 Nefi 3 (Kitengo cha 5) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .89

Somo 26 2 Nefi 4 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .91Somo 27 2 Nefi5 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .94Somo 28 2 Nefi 6–8 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .97Somo 29 2 Nefi 9:1–26 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .100Somo 30 2 Nefi 9:27–54 na 2 Nefi 10 . . . . . . . . . . . . . . . .103Somo la Mafunzo ya Nyumbani 2 Nefi 4–10

(Kitengo cha 6) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .106

Somo la 31 2 Nefi 11 na 16 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .108Somo la 32 2 Nefi 12–15 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .111Somo la 33 2 Nefi 17–20 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .114Somo la 34 2 Nefi 21–24 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .118Somo la 35 2 Nefi 25 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .121Somo la Mafunzo ya Nyumbani 2 Nefi 11–25

(Kitengo cha 7) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .124

Somo la 36 2 Nefi 26 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .126Somo la 37 2 Nefi 27 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .129Somo la 38 2 Nefi 28 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .132Somo la 39 2 Nefi 29–30 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .136Somo la 40 2 Nefi 31 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .139Somo la Mafunzo ya Nyumbani. 2 Nefi 26–31 (Kitengo

cha 8) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .142

Somo la 41 2 Nefi 32 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .144Somo la 42 2 Nefi 33 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .147Utangulizi wa Kitabu cha Yakobo. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .150Somo la 43 Yakobo 1–2:11 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .151Somo la 44 Yokobo 2:12–35 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .154Somo la 45 Yakobo 3–4 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .157Somo la Mafunzo ya Nyumbani 2 Nefi 32–Yakobo 4

(Kitengo 9). . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .160

Somo la 46 Yakobo 5:1–51 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .162Somo la 47 Yakobo 5:52–77; Yakobo 6 . . . . . . . . . . . . . . .166Somo la 48 Yakobo 7 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .169Utangulizi wa Kitabu cha Enos . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .172Somo la 49 Enos . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .173Utangulizi wa Kitabu cha Yaromu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .177Utangulizi wa Kitabu cha Omni. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .178Somo la 50 Yaromu na Omni . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .179Somo la Mafunzo ya Nyumbani Yakobo 5–Omni (Kitengo

cha 10) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .182

Utangulizi katika Maneno ya Mormoni . . . . . . . . . . . . . . .184Utangulizi wa Kitabu cha Mosia . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .185Somo la 51 Maneno ya Mormoni –Mosia 1 . . . . . . . . . . .186Somo la 52 Mosia 2 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .190Somo la 53 Mosia 3 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .193Somo la 54 Mosia 4 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .196Somo la 55 Mosia 5–6 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .200

Maudhui

Page 5: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

iv

Somo la Mafunzo ya Nyumbani Maneno ya Mormoni–Mosiah 6 (Kitengo cha 11) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .204

Somo la 56 Mosia 7–8 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .206Somo la 57 Mosia 9–10. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .210Somo la 58 Mosia 11–12:17 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .213Somo la 59 Mosia 12:18–14:12 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .216Somo la 60 Mosia 15–17 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .219Somo la Mafunzo ya Nyumbani Mosia 7–17

(Kitengo cha 12) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .222

Somo la 61 Mosia 18 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .224Somo la 62 Mosia 19–20 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .227Somo la 63 Mosia 21–22 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .230Somo la 64 Mosia 23–24 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .234Somo la 65 Mosia 25 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .237Somo la Mafunzo ya Nyumbani Mosia 18–25

(Kitengo cha 13) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .240

Somo la 66 Mosia 26 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .242Somo la 67 Mosia 27 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .245Somo la 68 Mosia 28–29 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .249Utangulizi wa Kitabu cha Alma . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .252Somo la 69 Alma 1–2 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .253Somo la 70 Alma 3–4 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .256Somo la Mafunzo ya Nyumbani Mosia 26–Alma 4

(Kitengo cha 14) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .259

Somo la 71 Alma 5:1–36. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .262Somo la 72 Alma 5:37–62 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .265Somo la 73 Alma 6–7 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .268Somo la 74 Alma 8 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .271Somo la 75 Alma 9–10 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .274Somo la Mafunzo ya Nyumbani Alma 5–10

(Kitengo cha 15) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .277

Somo la 76 Alma 11 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .279Somo la 77 Alma 12 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .282Somo la 78 Alma 13 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .286Somo la 79 Alma 14 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .289Somo la 80 Alma 15–16 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .292Somo la Mafunzo ya Nyumbani Alma 11–16

(Kitengo cha 16) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .295

Somo la 81 Alma 17 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .297Somo la 82 Alma 18 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .300Somo la 83 Alma 19–20 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .303Somo la 84 Alma 21–22 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .306Somo la 85 Alma 23–24 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .309Somo la Mafunzo ya Nyumbani Alma 17–24

(Kitengo cha 17) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .312

Somo la 86 Alma 25–26 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .314Somo la 87 Alma 27–29 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .317Somo la 88 Alma 30 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .321Somo la 89 Alma 31 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .325Somo la 90 Alma 32 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .328Somo la Mafunzo ya Nyumbani Alma 25–32

(Kitengo cha 18) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .332

Somo la 91 Alma 33 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .334Somo la 92 Alma 34–35 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .338Somo la 93 Alma 36 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .342Somo la 94 Alma 37 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .346Somo la 95 Alma 38 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .349Somo la Mafunzo ya Nyumbani Alma 33–38

(Kitengo cha 19) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .352

Somo la 96 Alma 39 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .354Somo la 97 Alma 40 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .358Somo la 98 Alma 41 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .361Somo la 99 Alma 42 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .364Somo la 100 Alma 43–44 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .368Somo la Mafunzo ya Nyumbani Alma 39–44

(Kitengo cha 20) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .371

Somo la 101 Alma 45–48 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .373Somo la 102 Alma 49–51 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .377Somo la 103 Alma 52–55 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .380Somo la 104 Alma 56–58 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .383Somo la 105 Alma 59–63 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .386Somo la Mafunzo ya Nyumbani Alma 45–63

(Kitengo cha 21) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .389

Utangulizi wa Kitabu cha Helamani . . . . . . . . . . . . . . . . . .391Somo la 106 Helaman 1–2 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .392Somo la 107 Helaman 3–4. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .395Somo la 108 Helamani 5 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .398Somo la 109 Helamani 6–7 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .401Somo la 110 Helamani 8–9 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .404Somo la Mafunzo ya Nyumbani Helamani 1–9

(Kitengo cha 22) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .407

Somo la 111 Helamani 10 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .409Lesson 112 Helamani 11–12 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .412Somo la 113 Helamani 13 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .415Somo la 114 Helamani 14 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .418Somo la 115 Helamani 15–16 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .421Somo la Mafunzo ya Nyumbani Helamani 10–16 (Kitengo

cha 23) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .424

Utangulizi kwa Nefi wa Tatu: Kitabu cha Nefi . . . . . . . . . .426Somo la 116 3 Nefi 1 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .427Somo la 117 3 Nefi 2–5 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .430Somo la 118 3 Nefi 6–7 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .433Somo la 119 3 Nefi 8–10 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .436Somo la 120 3 Nefi 11:1–17 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .439Somo la Mafunzo ya Nyumbani 3 Nefi 1–11:17 (Kitengo

cha 24) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .442

Somo la 121 3 Nefi 11:18–41. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .444Somo la 122 3 Nefi 12 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .447Somo la 123 3 Nefi 13 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .451Somo la 124 3 Nefi 14 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .454Somo la 125 3 Nefi 15–16 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .457Somo la Mafunzo ya Nyumbani 3 Nefi 11:18–16:20

(Kitengo cha 25) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .460

Somo la 126 3 Nefi 17 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .462Somo la 127 3 Nefi 18 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .465

Page 6: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

v

Somo la 128 3 Nefi 19 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .469Somo la 129 3 Nefi 20 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .472Somo la 130 3 Nefi 21–22 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .475Somo la Mafunzo Ya Nyumbani 3 Nefi 17–22

(Kitengo cha 26) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .478

Somo la 131 3 Nefi 23 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .480Somo la 132 3 Nefi 24–26 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .483Somo la 133 3 Nefi 27 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .487Somo la 134 3 Nefi 28 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .490Somo la 135 3 Nefi 29–30 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .493Somo la Mafunzo ya Nyumbani 3 Nefi 23–30

(Kitengo cha 27) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .496

Utangulizi wa Nephi ya Nne: Kitabu cha Nefi . . . . . . . . . .498Somo la 136 4 Nefi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .499Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni . . . . . . . . . . . . . . . . . . .502Somo la 137 Mormoni 1–7 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .503Somo la 138 Mormoni 3–4 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .506Somo la 139 Mormoni 5–6 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .509Somo la 140 Mormoni 7–8:11 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .512Somo la Mafunzo ya Nyumbani 4 Nefi 1–Mormoni 8:11

(Kitengo cha 28) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .515

Somo la 141 Mormoni 8:12–41 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .517Somo la 142 Mormoni 9 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .520Utangulizi wa Kitabu cha Etheri . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .523Somo la 143 Etheri 1 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .524Somo la 144 Etheri 2 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .527Somo la 145 Etheri 3 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .530Somo la Mafunzo ya Nyumbani Mormoni 8:12–Etheri 3

(Kitengo cha 29) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .533

Somo la 146 Etheri 4–5 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .535Somo la 147 Etheri 6 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .538Somo la 148 Etheri 7–11 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .541Somo la 149 Etheri 12:1–22 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .544Somo la 150 Etheri 12:23–41 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .547Somo la Mafunzo ya Nyumbani Etheri 4–12

(Kitengo cha 30) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .550

Somo la 151 Etheri 13–15 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .552Utangulizi wa Kitabu cha Moroni . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .556Somo la 152 Moroni 1–3 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .557Somo la 153 Moroni 4–5 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .560Somo la 154 Moroni 6 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .563Somo la 155 Moroni 7:1–19 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .566Somo la Mafunzo ya Nyumbani Etheri 13–Moroni 7:19

(Kitengo cha 31) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .569

Somo la 156 Moroni 7:20–48 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .571Somo la 157 Moroni 8 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .575Somo la 158 Moroni 9 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .578Somo la 159 Moroni 10:1–7, 27–29 . . . . . . . . . . . . . . . . . .581Somo la 160 Moroni 10:8–26, 30–34 . . . . . . . . . . . . . . . . .585Somo la Mafunzo ya Nyumbani Moroni 7:20–10:34

(Kitengo cha 32) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .588

Kielelezo . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .590Jedwari la Maandiko ya Kusoma . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .590Mwongozo wa Ratiba kwa Walimu wa Kila Siku . . . . . . . .591

Mapendekezo ya Siku Rahisi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .593Mwongozo wa Ratiba wa Walimu wa Mafunzo ya

Nyumbani . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .594Utangulizi wa Umahiri wa Maandiko . . . . . . . . . . . . . . . . .595Shughuli za Umahiri wa Maandiko . . . . . . . . . . . . . . . . . . .596Vifungu 100 vya Umahiri wa Maandiko . . . . . . . . . . . . . . .601Utangulizi katika Mafundisho ya Msingi . . . . . . . . . . . . . .602Kanuni za Kimsingi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .603Mabamba na Uhusiano wake na Kitabu cha Mormoni

Kilichochapishwa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .608Rejeo la Safari Mosia 7–24 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .609Ramani ya Maeneo yanayotajwa katika Kitabu cha

Mormoni . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .610

Page 7: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

vi

Dhamira yetuLengo la Seminari na Vyuo vya Dini linasema: “Dhamira yetu ni kuwasaidia vijana, na vijana wakubwa kuelewa na kutegemea mafundisho na Upatanisho wa Yesu Kristo, kuhitimu kwa ajili ya baraka za he-kalu, na kujiandaa wenyewe, familia zao, na wengine kwa ajili ya uzima wa milele pamoja na Baba yao wa Mbinguni. Ili kutimiza lengo letu, tunawafundisha wanafunzi mafundisho na kanuni za injili kama ipatikanavyo katika maandiko mata-katifu na maneno ya manabii. Mafundisho haya na kanuni hizi zinafundishwa kwa njia ambayo inaelekeza kwa ufahamu na kujengeka. Tunawasaidia wanafunzi kutimiza wajibu wao katika mchakato wa kujifunza na kuwaandaa kufundisha injili kwa watu wengine. Ili kuwasaidia kutimiza malengo haya, wewe pamoja na wanafunzi unaowafundi-sha mna himizwa kushirikisha Misingi ya Mafundisho ya injili ifuatayo na kujifunza unaposoma maandiko matakatifu pamoja: • Fundisha na Jifunze kwa Roho.• Kuza mazingira ya masomo ya upendo,

heshima, na dhamira.• Jifunze maandiko matakatifu kila siku,

na usome vifungu vifupi vya kozi. (Je-dwali la kufuatilia maandiko ya kusoma linaweza kupatikana katika kiambatani-sho mwishoni mwa mwongozo huu)

• Elewa muktadha na maudhui ya maa-ndiko na maneno ya manabii.

• Tambua, elewa, hisi ukweli na umu-himu wa, na utumie mafundisho na kanuni za injili.

• Elezea, shiriki, na shuhudia mafundisho na kanuni za injili.

• Yashike mafungu muhimu ya maandiko matakatifu na Mafundisho ya Msingi.

Mwongozo huu wa mwalimu umeanda-liwa kukusaidia kuwa mwenye mafanikio katika kutimiza malengo haya.

Matayarisho ya SomoBwana amewaamuru wale wanaofu-ndisha injili yake “kufundisha kanuni

za injili, ambazo ziko kwenye Biblia na Kitabu cha Mormoni, ambamo kuna utimilifu wa Injili” (M&M 42:12). Zaidi aliamuru kwamba kweli hizi zifundishwe “kama roho atakavyoamuru,” ambaye “ atapewa . . .katika sala ya imani” (M&M 42:13–14). Unapoandaa kila somo, katika maombi tafuta mwongozo wa Roho ku-kusaidia kuelewa maandiko na mafundi-sho na kanuni zilizomo. Vivyo hivyo, fuata vichocheo vya Roho wakati unapopanga jinsi ya kuwasaidia wanafunzi wako ku-elewa maandiko, wafundishwe na Roho Mtakatifu, na kuwa na hamu ya kuyate-nda yale waliyojifunza. Katika kozi hii, Kitabu cha Mormoni ni nakala yako ya msingi unapojiandaa na ku-fundisha. Kwa maombi jifunze vifungu au mistari utakayokuwa unafundisha. Tafuta kuelewa muktadha na maudhui ya kifungu cha maandiko, ikijumuisha mstari wa hadithi, watu, sehemu, na matukio. Una-pozoweya muktadha na maudhui ya kila kifungu cha maandiko, tafuta kugundua mafundisho na kanuni zilizomo, na amua ni kweli zipi za umuhimu mno kwa wa-nafunzi wako kuelewa na kuzifanyia kazi. Mara unapogundua lengo lako litakuwa nini, unaweza kuamua njia gani, mwele-keo, na shughuli ambazo zitawasaidia sana wanafunzi wako kujifunza na kuifanyia kazi ukweli uliopo katika maandiko.

Mwongozo huu umebuniwa kukusai-dia katika mchakato huu. Kwa umakini tathmini nyenzo za somo zinazoendana na kifungu cha maandiko utakayofundisha. Unaweza kuchagua kutumia yote au baa-dhi ya mapendekezo kwa ajili ya kifungu cha maandiko, au unaweza kubadilisha mawazo yaliyopendekezwa katika mahitaji na mazingira ya wanafunzi unaowafundi-sha. Unavyofikiria jinsi ya kubadilisha nye-nzo za somo, hakikisha unafuata ushauri huu kutoka kwa Mzee Dallin H. Oaks wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili: “Raisi Packer mara nyingi amefundisha, katika kusikia kwangu, kwamba kwa-nza tunapitisha, baadaye tunakabiliana. Kama tumeshindwa kabisa katika somo lililoelezewa ambalo inabidi tulitoe, basi tunaweza kumfuata Roho ili alibadilishe”. (“Kundi la majadiliano na Mzee Dallin H. Oaks” [Seminaries and Institutes of Reli-gion Satellite Broadcast, Aug. 7, 2012], 6, si. lds. org).Unapojiandaa kufundisha, kuwa makini na wanafunzi ambao wana mahitaji muhimu. Rekebisha shughuli na matarajio kuwasaidia wafanikiwe. Mawasiliano na wazazi na viongozi yatakusaidia kuwa makini na mahitaji ya wanafunzi na kuku-saidia kufanikiwa katika kuleta ujuzi wa maana na unaowainua wao.

Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari

Page 8: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

vii

UTANGULIZ I

20

UTANGULIZI WA

Kitabu cha Kwanza cha NefiKwa nini ujifunze kitabu hiki?Wanafunzi wanapojifunza 1 Nefi, wata-gundua kwamba “huruma nyororo [ya Bwana] iko juu ya wale ambao ame-wachagua, kwa sababu ya imani yao, kuwatia nguvu hata kwenye uwezo wa ukombozi”(1 Nefi 1:20). Pia watajifunza kwamba Mungu ana hamu ya kubariki watoto Wake. Lehi na watu wake wali-pata uzoefu wa huruma na baraka za Mu-ngu walipofuata amri Zake. Lehi na Nefi walitafuta mwongozo kutoka kwa Mungu na kuupokea kupitia ndoto, maono, Lia-hona, na mwongozo wa Roho Mtakatifu. Nefi alipokea na kuandika ono pana la historia ya ulimwengu ambalo lilimwo-nyesha maarifa yote ya Mungu; ubatizo, huduma, na kusulubiwa kwa Yesu Kristo; maangamizo ya Nefi; na siku za mwisho. Mungu alimsaidia Nefi na ndugu zake ku-pata mabamba ya shaba ili wapate kuwa na maandiko. Yeye pia alimuokoa Lehi na watu wake kutokana na baa la njaa huko nyikani na maangamizi huko baharini, kawapeleka salama kwenye nchi ya ahadi. Wanafunzi wanapojifunza uzoefu wa Nefi na Lehi katika kitabu hiki, wanaweza kujifundisha jinsi ya kutafuta na kupokea baraka za mbinguni.

Nani aliandika kitabu hiki?Nefi mwana wa Lehi aliandika kitabu hiki kama jibu la amri ya Bwana kwamba yeye aweke kumbukumbu ya watu wake. Nefi kuna uwezekano alizaliwa Yerusalemu au karibu na hapo. Aliishi huko wakati wa huduma ya nabii Yeremia na enzi ya Mfalme Zedekia. Nefi alitafuta ushuhuda wake mwenyewe kuhusu maneno ya baba yake kuhusu maangamizo ya Yerusa-lemu na haja ya familia yao ya kuondoka. Alipoendelea kutafuta na kufuata ushauri wa Bwana, Nefi akawa chombo katika mikono ya Mungu. Yeye kwa utiifu alirudi Yerusalemu na ndugu zake mara mbili—kwanza kutafuta mabamba ya shaba na baadaye kushawishi familia ya Ishmaili iji-unge na familia ya Lehi huko nyikani. Kwa usaidizi wa Bwana, Nefi alijenga merikebu ambayo ilibeba familia yake na wengine kuvuka bahari hadi nchi ya ahadi. Lehi alipokufa, Bwana alimchagua Nefi kuwa kiongozi wa watu wake.

Hiki kitabu kimeandikiwa kina nani na kwa nini?Nefi aliandika akiwa na makundi matatu akilini; uzao wa baba yake, watu wa agano wa Bwana katika siku za mwisho, na watu wote katika ulimwengu (ona 2 Nefi 33:3, 13). Aliandika ili kuwashawi-shi watu wote waje kwa Yesu Kristo na kuokolewa (ona 1 Nefi 6:4).

Kiliandikwa lini na wapi?Nefi aliandika taarifa ambayo ilikuja kuwa 1 Nefi karibu na mwaka wa 570Kabla Kristo Kuzaliwa—miaka 30 baada ya yeye na familia kuondoka Yerusalemu (ona 2 Nefi 5:30). Alikiandika alipokuwa katika nchi ya Nefi.

Ni zipi kati ya sifa bainishi za kitabu hiki?1 Nefi ina taarifa kadhaa za maonyesho ya matakatifu katika ndoto, maono, na funuo za moja kwa moja. Maonyesho haya yanaonyesha kwamba Mungu hufu-nza, uongoza, na kulinda wale wanaom-tafuta Yeye:

• Lehi alipokuwa akiomba, nguzo ya moto ilitokeza, na yeye aliona na kusi-kia mambo mengi ambayo yalimfanya yeye kutetemeka (ona 1 Nefi 1:6–7).

• Lehi alipokea ono ambalo kwalo alimwona Mungu na kusoma kutoka ki-tabu ambacho unabii wa maangamizo ya Yerusalemu na kutekwa kwa wakazi wake (ona 1 Nefi 1:8–14).

• Bwana alimwamuru Lehi aondoke pamoja na familia yake kwenda nyikani (ona 1 Nefi 2:1–2).

• Bwana alimwelekeza Lehi kuwatuma wanawe kurudi Yerusalemu kwa yale mabamba ya shaba (ona 1 Nefi 3:2–4).

• Malaika aliingillia kati wakati Lamani na Lemueli walipokuwa wakimpiga Nefi na Samu (ona 1 Nefi 3:29).

• Bwana alimwamuru Nefi na nduguze kurudi Yerusalemu kuwachukua Ishmaili na familia yake (ona 1 Nefi 7:1–2).

• Lehi na Nefi walipokea ono ambalo lilikuwa na mti wa uzima; kuzaliwa, hu-duma, na Upatanisho wa Yesu Kristo;

historia ya nchi ya ahadi; Urejesho wa injili; na mapambano kati ya majeshi wa shetani na kanisa la Mwana Kondoo wa Mungu (ona 1 Nefi 8;11–14).

• Nefi alionyeshwa jinsi ya kujenga meri-kebu ambayo ingewabeba watu wake hadi nchi ya ahadi (ona 1 Nefi 18:1).

1 Nefi ina taarifa za kibinafsi za watu ambao walisafiri hadi nchi ya ahadi. Kitabu cha Mormoni baadaye kinataja makundi mawili mengine ambayo yalisafiri hadi nchi ya ahadi; Wamuleki (ona Omni 1:14–17) na Wayaredi (see Etheri 6:4–12).Kitabu cha 1 Nefi pia kinatambulisha vitu viwili muhimu: upanga wa Labani na dira, au kielekezi, kinachoitwa Liahona (ona 1 Nefi 18:12; Alma 37:38). Kupitia kwa Liahona, Bwana aliongoza familia ya Lehi kote nyikani na kuvuka bahari. Upanga wa Labani ulikabithiwa kupitia vizazi hadi mwisho wa ustaarabu wa Wanefi. Liahona na upanga wa Labani vyote vilizikwa pamoja na mabamba ya dhahabu, na vilionyeshwa Joseph Smith na Mashahidi Watatu (ona M&M 17:1–2).

Muhtasari1 Nefi 1–7 Lehi anaongoza familia yake kuingia nyikani. Wanawe wanatii amri za Bwana za kurudi Yerusalemu na kuchukua maba-mba na kurudi tena kumshawishi Ishmaili na familia yake ajiunge na wao huko nyikani.

1 Nefi 8–15 Lehi na Nefi kila mmoja alipokea ono la mti wa uzima. Nefi anarejelea ono lake la huduma na matukio ya kihis-toria ya Mwokozi hata kufikia Urejesho wa injili katika siku za mwisho.

1 Nefi 16–18 Bwana anaongoza Lehi na familia yake katika safari yao kupitia nyikani na kuvuka bahari hadi nchi ya ahadi.

1 Nefi 19–22 Nefi anatoa nabii juu ya Yesu Kristo na kutawanyika na kukusanyika kwa Israeli.

527

UtanguliziBaada ya kuondoka kutoka Mnara wa Babeli, Yaredi na ndugu yake na familia zao na marafiki zao walio-ngozwa na Bwana kupita nyikani. Bwana alimwelekeza ndugu ya Yaredi kujenga mashua nane ili kuwabeba

watu wake kuvuka bahari hadi nchi ya ahadi. Ndugu ya Yaredi na watu wake walipomtii Bwana kwa imani, Bwana aliwapa mwongozo na maelekezo yaliyohitajika ili kufanikiwa katika safari yao.

SOMO LA 144

Etheri 2

Mapendekezo ya Kufundisha

Etheri 2:1–12Wayaredi wanaanza safari yao kwenda nchi ya ahadiIli kuwasaidia wanafunzi kuona jinsi tunavyofuata maelekezo tunayopokea kutoka kwa Mungu yanaweza kututayarisha sisi kupokea mwongozo zaidi na maelekezo kutoka Kwake, endesha shughuli ifuatayo:Kabla darasa kuanza, ficha kitu kinachowakilisha hazina katika chumba mnachokutania. Tayarisha msururu wa vidokezo vitatu au vinne ambavyo vinawaongoza wanafunzi hadi kwenye hazina. Wewe utatoa kidokezo cha kwanza kwa wanafunzi. Hicho kidokezo kita-waalekeza kwenye kile kinachofuata, ambacho kitaelekeza kwa kile kingine, na vivyo hivyo hadi wanafunzi wafikie hazina. Baada ya wao kupata hazina, waulize:• Ni nini kingetokea kama ungepuuza kidokezo cha kwanza? (Hawangepata kidokezo

cha pili.)Waalike wanafunzi kurejelea Etheri 1:41–42 kimya, wakitafuta seti ya kwanza ya maelekezo ya kuwaongoza Wayaredi hadi nchi ya ahadi.Ili kuwasidia wanafunzi kuona jinsi Wayaredi walivyojibu maelekezo haya, mwalike mwa-nafunzi asome Etheri 2:1–3 kwa sauti.• Wayaredi walijibu vipi kwa ile seti ya kwanza ya maelekezo ya Bwana?Alika mwanafunzi asomeEtheri 2:4–6kwa sauti. Uliza darasa lifuatilie, likitafuta baraka ambazo Wayaredi walipokea baada ya kufuata seti ya kwanza ya maelekezo.• Ni nini kilitokea baada ya Wayaredi kufuata seti ya kwanza ya maelekezo ya Bwana?

(Bwana aliwapa maelekezo ya ziada kupitia kwa ndugu ya Yaredi.)• Tunaweza kujifunza nini kutoka kwenye tukio hili kuhusu jinsi ya kupokea mwongozo

kutoka kwa Bwana? (Wanafunzi wanaweza kutumia maneno tofauti, lakini majibu yao yanafaa kuonyesha kufuata kanuni: Tunapotenda kwa imani juu ya maelekezo aliyo-tupa Bwana, tunaweza kupokea mwongozo zaidi kutoka Kwake. Unaweza kutaka kupendekeza kwamba waandike ukweli huu katika maandiko yao karibu na Etheri 2:6.)

Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa vyema na kutumia kanuni hii, waalike wao kufikiria juu ya onyesho au msukumo waliopokea hivi majuzi kutoka kwa Bwana. Kisha soma taarifa ifuatayo ya Mzee Richard G. Scott wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili kuhusu jinsi tu-nvyopokea ufunuo kila mara:

“Utakuja sehemu kwa wakati, katika pakiti, ili kwamba ukue katika uwezo. Kila sehemu itafuatiwa na imani, utaongozwa hadi sehemu nyingine mpaka utakapopata jibu lote. Utaratibu ule unahitaji ufanye imani katika uwezo wa kujibu wa Baba yetu. Hali wakati mwingine ni vigumu sana, huleta ukuaji muhimu wa kibinafsi” (“Using the Supernal Gift of Prayer,” Ensign or Liahona, May 2007, 9).

Waalike wanafunzi kujibu maswali yafuatayo kwenye daftari au shajara za kujifunza ma-andiko. Unaweza kutaka kuyaandika kwenye ubao au kuyasoma pole pole ili wanafunzi waweze kuyaandika.

Kujenga hamu na lengoPanga shughuli ambazo zitajenga hamu na kuwasaidia wanafunzi kulenga usikivu wao kwenye maandiko katika somo. Hizi shughuli zinakuwa zinafana zaidi wakati zinakuwa fupi na wakati wanafunzi wana-polenga kanuni muhimu za somo.

Kutumia Mwongozo wa Kila siku wa MwalimuUtangulizi wa KitabuUtangulizi wa Kitabu huleta ma-elezo ya kila kitabu katika Kitabu cha Mormoni. Kati ya mambo Mengine, walielezea nani ame-andika kila kitabu, wameelezea sababu za mwandishi katika ma-andishi, na wametoa muhtasari wa maudhui ya kila kitabu.

Utangulizi wa Fungu la MaandikoTangulizi za fungu la maandiko zinatoa maelezo mafupi ya muk-tadha na maudhui ya fungu la maandiko kwa kila somo.

Kukusanya fungu la Maneno na Muhtasari wa Muktadha Mafungu ya maandiko mara nyingi yamegawanyika katika sehemu ndogo au makundi ya maandiko ambapo mabadiliko ya mada au kitendo hutokea. Kielelezo kwa kila mkusanyiko wa kundi la maandiko kinafua-tiwa na ufupisho wa matukio au mafundisho katika kundi lile la vifungu vya maandiko.

Visaidizi vya KufundishiaVisaidizi vya kufundishia vinaele-zea kanuni na njia za kufundisha injili. Vinaweza kukusaidia katika juhudi zako za kujiboresha kama mwalimu.

Umbo la SomoUmbo la somo linakuwa na mwo-ngozo kwa ajili yako unapojifunza na kufundisha. Kinapendekeza mawazo ya kufundisha. kikijumu-isha maswali, shughuli, nukuu, michoro, na majedwali.

Mafundisho na kanuniKwa vile mafundisho na kanuni vinatokea kwa kawaidia kutoka kwenye mafunzo ya maneno ya maandiko, yameoneshwa katika mkazo ili kukusaidia kugundua na kuzisisitizia katika majadiliano yako pamoja na wanafunzi.

PichaPicha za Viongozi wa Kanisa na matukio kutoka katika maandiko zinawakilisha visaidizi vya kuona ambavyo unaweza kuvionesha, kama vipo, unapofundisha.

Page 9: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

viii

UTANGULIZ I

514

Somo la 140

Hitimisha kwa kushiriki uzoefu wa wakati Bwana alipokubariki kwa kuwa mwaminifu katika hali ya upweke au ngumu.

Rejeo la Umahiri wa MaandikoAndika sihi ubaoni. Eleza kuwa neno sihi linamaanisha kuwahimiza wengine kwa nguvu kutenda jambo kwa njia fulani.. Eleza kwamba maneno ya mwisho ya Mormoni katika Mormoni. ni mfano mzuri mahubiri. Wape vipande vya karatasi wanafunzi na kuwaambia wataandika mahubiri yenye msingi wa mojawapo wa vifungu vya umahiri wa maandiko wanavyopenda zaidi katika Kitabu cha Mormoni Juu ya kipande cha karatasi acha wana-funzi waandike. “Nitanena kwa namna fulani na vijana wa siku za mwisho.” Alika kila mwanafunzi kuchagua vifungu vya umahiri wa maandiko anavyopenda sana kisha aandike mahubiri kwa vijana wa siku za mwisho kwa msingi ya vifungu walivyochagua Mahubiri yao yanaweza kujumuisha mukhtasari wa kweli muhimu zinazopatikana katika taarifa ya umahiri wa maandiko, elezo la kwa nini kweli hizi ni muhimu kwa vijana hivi leo, na mwa-liko kutenda kulingana na kweli hizi. Mahubiri yana weza kuhitimishwa na ahadi kama ile inayopatikana katika Mormoni 7:7 au Mormoni 7:10. Ungeweza kuwauliza wanafunzi wachache kushiriki mahubiri yaliyo kamilika pamoja na darasa. Unaweza kutaka kukusa-nya mahubiri haya yatumike kama vidokezo kwa shughuli za umahiri wa maandiko za siku za usoni au kuyaonesha darasani.Chunga: Unaweza kutaka kutumia shughuli hii wakati wowote katika somo hilo. Kwa mfano, unaweza kuitumia katika mwisho wa somo au unaweza kutumia baada ya kuja-dili Mormoni 7.

Tangazo na Habari za UsuliMormoni 7. Ombi la mwisho la Mormoni la kuamini katika Kristo

Mzee Jeffrey R. Holland wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili alieleza kuhusu ombi la mwisho la Mormoni kuamini katika Kristo, ombi aliloandika kwa watu katika siku zetu baada ya kuona maangamizo ya taifa lake zima”

“Katika mazungumzo ya nafsi juu ya mauti, Mormoni alifikia wakati na upeo kwa wote, hasa kwa. salio la nyumba ya Israeli” ambao siku moja wangesoma kumbukumbu yake tukufu. Wale walio wa wakati na upeo mwingine ni lazima wajifunze kile wale wanao-lala mbele zake walikuwa wamesahau— kuwa wote ni sharti “kuamini katika Yesu Kristo, kwamba yeye

ni mwana wa Mungu,” kwamba kufuatia kusulubiwa kwake Yerusalemu alikuwa na “uwezo wa Baba akafu-fuka tena, hivyo, kupata ushindi juu ya kaburi; na pia katika yeye uchungu wa mauti unamezwa.

“Na alitimiza ufufuo wa wafu [na] ukombozi wa ulimwengu.’ Wale waliokombolewa wanaweza basi, kwa sababu ya Kristo, kufurahia ‘hali ya furaha isiyo na mwisho.’ [Mormoni 7:2, 5–7.] . . .

“Kuamini katika Kristo,’ hasa kukipimwa dhidi ya mato-keo kama hayo yanayoweza kuepukika, lilikuwa ombi la mwisho la Mormoni na tumaini lake tu. Ni kusudi kuu la kitabu kizima ambacho kingekuja duniani katika siku za mwisho kikiwa na jina lake.. (Kristo na agano jipya: Ujumbe wa kimasiya wa kitabu cha mormoni [1997], 321–22).

Wazo la Ziada la KufundishiaMormoni 7:8–9. Biblia na Kitabu cha Mormoni

Onyesha nakala ya Kitabu cha Mormoni kilichobandi-kwa “hiki” Kisha onyesha nakala ya Biblia kilichoba-ndikwa “hicho” Waalike wanafunzi kusoma Mormoni 7:8–9 kimya wakitafuta nini Mormoni alisema kuhusu

uhusiano kati ya “hiki”(Kitabu cha Mormoni) na “hi-cho” (Biblia).

• Kujifunza kwako Kitabu cha Mormoni kumeimarisha vipi ushuhuda wako wa kweli katika Biblia? Kujifu-nza kwako Biblia kumeimarisha vipi ushuhuda wako wa kweli katika Kitabu cha Mormoni ?

Umahiri wa MaandikoMistari 25 ya vifungu vya umahiri wa maandiko vina-vyopatikana katika Kitabu cha Mormoni vimeonyeshwa katika muktadha katika masomo ambayo yametokea. Kila moja wapo ya masomo haya pia kuna wazo la kufundishia kwa kila kifungu cha maneno. Ili kukusaidia kuwa dhabiti katika kufundisha umahiri wa maa-ndiko, kuna shughuli za kurudia Umahiri wa Maandiko zilizo-zagaa kote katika mwongozo. Kwa nyongeza ya mawazo ya kufundishia umahiri wa maa-ndiko, ona kielelezo mwishoni mwa mwongozo huu.

Nafasi ya MhimiliNafasi ya Mhimili inaweza ku-tumika kwa ajili ya maandalizi ya somo, ikijumuisha kuandika mwendelezo, kanuni, ujuzi, au mawazo mengine, kama unavyohisi vichochezi vya Roho Mtakatifu

Tangazo na Habari za UsuliNukuu za ziada na maelezo yameelezewa mwishoni mwa baadhi ya masomo kukupa uelewa wa ziada wa wazo sahihi au kifungu cha maa-ndiko. Tumia maelezo katika sehemu hii ili kujiandaa kujibu maswali au kutoa dondoo zaidi unapofundisha

Mawazo ya Ziada ya KufundishiaMawazo ya ziada ya kufundi-shia yanajitokeza mwishoni mwa baadhi ya masomo. Haya yanatoa mapendekezo ya kufundishia mafundisho na kanuni ambayo hayawezi ku-tambulika au kusisitizwa katika kiini cha somo. Yanaweza pia kuleta mapendekezo katika kutumia vifaa vya kuoneshea, kama vile maonesho ya DVD.

Page 10: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

ixix

UTANGULIZ I

Programu za Seminari za Kila Siku (Muda wa Ruhusa na Mapema Asubuhi)Mwongozo huu umejumuisha Mihutasari ifuatayo kwa ajili ya walimu wa kila siku wa Seminari. Masomo 160 ya walimu kila siku, visaidizi vya kufundishia, na nyenzo za kufundishia umahiri wa maandiko na mafundisho ya Msingi.

Masomo ya Kila siku ya MwalimuMfumo wa SomoKila somo katika mwongozo huu hulenga katika fungu la maandiko badala ya dhana fulani, mafundisho au kanuni. Mfumo huu utakusaidia wewe na wanafunzi wako kujifunza mwendelezo wa maandiko na kujadiliana mafundisho na kanuni zina-vyojitokeza kiasilia kutoka katika vifungu vya maandiko. Wanafunzi wanapojifu-nza muktadha ambamo mafundisho au kanuni zinapatikana, uelewo wao katika ukweli huo unakuwa mkubwa. Kwa kuongezea, wanafunzi wanaweza kuona vyema na kuelewa lengo nzima la ujumbe ambao waandishi wa maandiko ya kuinua walilenga kuuleta. Kufundisha maandiko katika njia hii kutawasaidia pia wanafunzi kujifunza jinsi ya kugundua na kuzifanyia kazi kweli za milele katika mafunzo yao ya maandiko matakatifu.Katika kila somo, siyo kila vipengele vya mafungu ya maandiko vimesisitizwa. Baadhi ya vipengele hupata mvuto mdogo kwa sababu havijalenga katika kiini cha ujumbe mzima wa mwandishi mwenye maongozi au kwa sababu vinaweza kuwa na vinahusika kidogo kwa vijana. Una jukumu la kugeuza nyenzo hizi kulingana na mahitaji na hamu ya kila mwanafu-nzi unayemfundisha. Unaweza kugeuza wazo la somo katika mwongozo huu kwa kuchagua kutoa msisitizo mkubwa kwa mafundisho fulani au kanuni mbali na ili-vyotolewa katika nyenzo za somo au kwa kuchagua kutoa msisitizo mdogo kwa kifungu cha maandiko ambacho kimeku-zwa kwa undani zaidi katika mwongozo. Tafuta mwongozo wa Roho Mtakatifu kukusaidi kufanya mabadiliko haya una-pojiandaa kufundisha.

Mafundisho na KanuniKatika kiini cha kila somo, utaona kwa-mba baadhi ya mafundisho ya msingi na kanuni zimeoneshwa kwa msisitizo.

Mafundisho haya na kanuni zimegu-nduliwa katika mtaala kwa sababu (1) zinahakisi kiini cha ujumbe katika fungu la maandiko, (2) zimelenga katika mahitaji na hali ya wanafunzi, au (3) ni kweli za msingi ambazo zinaweza kuwasaidia wanafunzi kukuza uhusiano wao na Bwana. Kuwa makini kwamba Kitabu cha Mormoni kinafundisha kweli tofauti tofauti zaidi ya hizo zilizoonyeshwa katika mtaala. Raisi Boyd K Packer alifundisha kwamba maandiko yana “Muungano usio na mwisho wa ukweli ambao utatimiza mahitaji ya kila mtu katika kila hali” (“The Great Plan of Happiness” [CES Symposium on the Doctrine and Covenants/Church History, Aug. 10, 1993], 2, si. lds. org).Unapofundisha, mara zote wape wa-nafunzi fursa ya kugundua mafundisho na kanuni katika maandiko. Wanafunzi wanapoelezea ukweli wanaougundua, mara nyingi wanaweza kutumia maneno ambayo yanatofautiana kutokana na jinsi ambavyo mafundisho au kanuni imeelezea katika mwongozo. Vile vile wanaweza kugundua kweli ambazo hazijatambulika katika mpango wa somo. Kuwa makini kutopendekeza kwamba jibu la wana-funzi siyo sahihi kwa sababu tu maneno wanayoyatumia kujielezea yanatofautiana na yale yaliyotumika katika mwongozo au kwa sababu wamegundua ukweli ambao haujatajwa katika mtaala. Hata hivyo, kama kauli ya mwanafunzi haiko sawa-sawa kikanuni, ni jukumu lako kumsaidia kiutaratibu mwanafunzi kusahihisha kauli yake wakati ukiendelea kutunza hali ya upendo na imani. Kwa kufanya hivyo kunaweza kuleta ujuzi mzuri wa kujifunzia kwa wanafunzi katika darasa lako.

KuthibitiKitabu hiki kidogo kimejumuisha masomo ya seminari 160 ambayo yanaweza kuru-husu mwingiliano katika shule ya mwa-nafunzi na ratiba ya familia na pia kuacha idadi ya kila siku, kurudia muktadha wa maandiko matakatifu au kazi katika uma-hiri wa maandiko matakatifu. Unaweza kubadilisha masomo na kuyatenga kama inavyotakiwa kwa urefu wa muda ulionao kufundisha mafunzo haya. (Ona Kielelezo mwishoni mwa kitabu hiki cha mwongozo kwa mfano wa mwongozo wa kutenga.)

Kazi za kurejeaMwongozo wa Masomo wa Kitabu cha Mormoni kwa ajili ya Mafunzo ya Nyumbani ya Wanafunzi wa Seminari kinaweza kutumika katika mipango ya

seminari ya kila siku kama nyenzo ya ku-wapa wanafunzi kufanyia marekebisho ya kazi. Masomo katika mwongozo wa ma-funzo kwa ajili ya mafunzo ya nyumbani kwa wanafunzi yanaambatana na yale yaliyotolewa katika mwongozo huu. Wa-nafunzi ambao ni watoro sana wanaweza kupangiwa kazi ya kumalizia kazi katika mwongozo wa mafunzo ambao unae-ndana na masomo waliyo kosa darasani. Kazi zinaweza kuchapishwa kutoka katika mtandao wa S&I, kwa hiyo huhitaji kutoa mwongozo wote kwa wanafunzi ambao wanahitaji kufanya malipizo ya viporo vya kazi zao. Maelezo zaidi kuhusu Mwo-ngozo wa Kitabu cha Mormoni kwa ajili ya Mafunzo ya Nyumbani kwa wanafunzi wa Seminari yametolewa katika sehemu yenye kichwa “mpango wa mafunzo ya nyumbani ya Seminari”

Visaidizi vya KufundishiaVisaidizi vya kufundishia vimejitokeza ka-tika kingo za mwongozo huu. Mafundisho haya yanasaidia kuelezea na kufafanua jinsi wewe na wanafunzi unaowafundisha mnaweza kuyafanyia kazi Mafundisho ya misingi ya Injili na kujifunza katika mafunzo yako ya Kitabu cha Mormoni. Pia yanatoa mapendekezo ya jinsi ya kutumia kikamilifu njia mbali mbali za kufundi-shia, ujuzi, na mwenendo. Unapofikia kuelewa kanuni zilizomo katika visaidizi vya kufundishia, tafuta njia za kufanyia mazoezi na kuyafanyia kazi kila mara yale unayoyafundisha.

Umahiri wa Maandiko na Mafundisho ya MsingiIli kuwasaidia wanafunzi kuthamini ukweli wa milele na kuongeza ujasiri wao katika kujifunza na kufundisha kutoka kwenye maandiko, Seminari na Vyuo vya Dini (S&V) vimechagua idadi kadhaa ya vifu-ngu vya maandiko kwa ajili ya wanafunzi kuwa mahiri wakati wa mafunzo ya kila kozi. Kwa Nyongeza, orodha ya Mafundi-sho ya Msingi yamejumuishwa kuonesha mafundisho ya msingi ambayo wanafunzi inabidi waweze kuyaelewa, wayaamini, na kuyaishi wakati wote wa miaka minne ya Seminari na kwa maisha yao yote. Mwongozo kwa kila mafunzo uliandaliwa kuonesha Mafundisho ya Msingi yanapo-tokea wakati wa mafunzo ya mwendelezo ya maandiko kwa mwanafunzi. Vingi vya vifungu vya umahiri wa maandiko vilicha-guliwa pamoja na misingi ya mafundisho akilini, kwa hiyo unapofundisha umahiri wa vifungu vya maandiko kwa wanafunzi, utafundisha mafundisho ya msingi vilevile.

Page 11: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

xx

UTANGULIZ I

Wakati watu binafsi wanapothamini kweli za milele katika akili zao na mioyo, Roho Mtakatifu ataleta kweli hizi katika kumbukumbu zao katika wakati wa haja na kuwapa ujasiri wa kutenda kwa imani. (ona Yohana 14:26). Rais Howard W. Hunter alifundisha:“Nawahimiza sana kutumia maandiko katika ufundishaji wenu na kufanya kila linalowezekana katika uwezo wenu kuwa-saidia wanafunzi kuyatumia na kuridhika

nayo. Ningependa vijana wetu wawe na imani katika maandiko. . . .“. . .  Tunataka wanafunzi wawe na imani katika uwezo na kweli za maandiko, imani kwamba Baba yao wa Mbinguni ama kweli anaongea nao kupitia maandiko, na imani kwamba wanaweza kugeukia maandiko na kupata majibu ya matatizo yao na maombi. . . .“. . . Tungetumaini hakuna hata mmoja wa wanafunzi wako wangeacha darasa lako kwa uwoga au kwa kuona haya au

kuaibika kwamba hawawezi kupata msa-ada wanaohitaji kwa sababu hawajui ma-andiko vizuri kuweza kutambua vifungu sahihi” (“Eternal Investments” [address to CES religious educators, Feb. 10, 1989], 2, si. lds. org).Ona kielelezo mwishoni mwa mwongozo huu kwa maelezo zaidi kuhusu umahiri wa maandiko na Mafundisho ya Msingi.

Page 12: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

xi

UTANGULIZ I

205

Somo la mafunzo ya nyumbani

Mormoni zilizopotea. Ona kitengo cha 6, siku ya 1 katika mwongozo wa kujifunza wa mwanafunzi.)

• Uelewa wako kwamba Bwana anajua vitu vyote katika siku za usoni unaweza kukupatia imani ya kutii msukumo wa kiroho unaopokea?

Ikiwa unahisi kuhitaji kutumia muda zaidi katika sehemu hii ya somo, waulize wanafunzi ikiwa wanaweza kushiriki uzoefu wa wakati walihisi kusukumwa na Roho kufanya kitu na hawakujua madhumuni ya msukumo huu mpaka hapo baadaye.

Mosia 1Mfalme Benyamini anawaita watu kukusanyika pamojaElezea kwamba mabamba madogo ya Nefi yalikuwa na historia ya Wanefi kutoka kwa huduma ya Lehi hadi wakati ambapo Mfalme Mosia aliunganisha watu wa Nefi na Zarahemla na wakati Benyamini mwana wa Mosia alitawala ufalme kwa haki. Mfalme Benyamini alikabidhiwa kumbukumbu takatifu. (Ona Omni 1:23, 25.)

Karibu na mwisho wa maisha ya Mfalme Benyamini, alimuomba mwanawe Mosia kukusanya watu pamoja. Waalike wanafunzi kusoma Mosia 1:10–11 na watafute sababu za Mfalme Benya-mini za kutaka kunena na watu. (Alitaka kutangaza kwamba Mosia atakuwa mfalme mtarajiwa na kuwapatia watu jina.)

Mosia 2–6Mfalme Benyamini anawafunza watu wake kuhusu Upatanisho wa MwokoziWaonyeshe wanafunzi picha ya Mfalme Benyamini Akihutubia Watu Wake(62298; Gospel Art Book [2009], no. 74). Soma Mosia 2:12–19 kwa darasa. Alika wanafunzi kuinua mikono yao wanapotambua vishazi ambayo vinaonyesha hulka ya Mfalme Benyamini. Wanafunzi wanapoinua mikono yao, sitisha kusoma na uwaulize kuelezea kile wametambua na jinsi linafunua hulka ya Mfalme Benyamini.

Unaweza kutaka kuwauliza wanafunzi kile wamejifunza kuhusu huduma katika Mosia 2:17. (Majibu ya wanafunzi yanafaa kuakisi uelewa wa kwamba tunapowahudumia wengine, tu-namtumikia Mungu.) Unaweza pia kutaka darasa lirudie Mosia 2:17, kifungu cha umahiri wa maandiko, kwa kukariri. Fikiria kuwaalika wanafunzi kushiriki jinsi hivi majuzi wamemtumikia Mungu kwa kuwahudumia wengine.

Andika vifungu vya maandiko vifuatavyo kwenye ubao au kwe-nye kipande cha karatasi. Usijumuishe majibu yalioko kwenye mabano. Mpatie kila mwanafunzi kazi ya kurejelea mojawapo wa vifungu vya maandiko. Wakumbushe kwamba mahubiri ya Mfalme Benyamini yalilenga kwenye mada hii: “Wokovu utawa-shukia watoto wa watu, ila katika na kupitia jina la Kristo pekee, Bwana Mwenyezi. (Mosiah 3:17). Kila kifungu cha maandiko hufunza kitu kuhusu mada hii.

1. Mosia 2:20–25, 34. (Tunapotambua tu wadeni kwa Mu-ngu, shukrani zetu huongezeka.)

2. Mosia 3:7–11, 17–18 (Yesu Kristo aliteseka ili sisi tuweze kuokolewa kutoka kwa dhambi zetu. Ikiwa tutafanya imani katika Yesu Kristo kupitia toba, tunaweza kuokolewa kutoka kwa dhambi zetu.)

3. Mosia 3:12–16, 19–21. (Ikiwa tutakubali ushawishi wa Roho Mtakatifu, kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo tuna-weza kumvua mtu wa kawaida na kuwa mtakatifu.)

4. Mosia 4:5–8, 19–21, 26. (Ikiwa tutajinyenyekeza wenyewe mbele za Mungu na kujitahidi kukuza sifa kama za Kristo, tunaweza kuhifadhi ondoleo la dhambi.)

Baada ya kuwapatia wanafunzi muda wa kutosha, waruhusu wao waripoti kile walichojifunza kwa darasa au katika vikundi vidogo. Kisha waulize wanafunzi kadhaa kuchagua mojawapo wa kanuni hizi na waelezee jinsi wanaweza kuzitumia katika maisha yao.

Alika mwanafunzi asome Mosia 4:5–8, 19–21, 26. Uliza darasa kufuatilia, likitafuta jinsi watu walijibu kwa maneno ya Mfalme Benyamini. Kisha alika mwanafunzi mwengine kusoma Mosia 5:1–2, 5–8 kwa sauti. Uliza darasa kutafuta jinsi tunaweza ku-jichukulia juu yetu jina la Bwana. Hakikisha wanafunzi wamee-lewa kanuni hii: Sisi tunajichukulia juu yetu wenyewe jina la Yesu Kristo tunapofanya na kuweka maagano mata-katifu. Unaweza kutaka kuwakumbusha wanafunzi kwamba mojawapo wa sababu za Mfalme Benyamini kukusanya watu pamoja ilikuwa ni kuwafundisha wao kuhusu kufanya maagano. Yeye pia alimweka wakfu mwanawe Mosia kuwa mfalme juu ya watu (ona Mosia 6:3).

Kuhitimisha, waulize wanafunzi ikiwa yeyote kati yao ange-penda kushiriki jinsi wanahisi kuhusu kujichukulia juu yao wenyewe jina la Yesu Kristo katika ubatizo. Waulize kutafakari maswali yafuatayo:

• Je! Wewe binafsi unaweza kutumia kanuni kutoka kwa ho-tuba ya Mfalme Benyamini vipi?

• Inamaanisha nini kwako kujichukulia juu yako mwenyewe jina la Yesu Kristo?

Unaweza pia kushuhudia juu ya shangwe ambayo inakuja kupi-tia kuamini katika jina la Yesu Kristo na kutegemea Upatanisho Wake.

Kitengo Kijacho (Mosia 7–17)Waulize wanafunzi: Je! Utasimama imara kwa Yesu Kristo hata kama kufanya hivyo inamaanisha utauawa? Waelezee wanafu-nzi kwamba wiki ijayo watajifunza mafundisho ya nabii Abinadi. Wahimize kutafuta ujumbe wa Abinadi aliokuwa anapendekeza kuuwasilisha kwa Wanefi, hata ingawa alijua atauawa.

204

Somo la Mafunzo ya NyumbaniManeno ya Mormoni–Mosia 6 (Kitengo cha 11)

Vifaa vya Matayarisho kwa Mwalimu wa Mafunzo ya NyumbaniMuhtasari wa Mafunzo ya Nyumbani ya Kila sikuUfuatao ni muhtasari wa mafundisho na kanuni ambazo wa-nafunzi wamejifunza walipojifunza Mosia 6 (kitengo cha 11) Haikusudiwi kufunzwa kama sehemu ya somo lako. Somo unalofundisha linazingatia machache tu ya mafundisho na kanuni hizi. Fuata maelekezo ya Roho Mtakatifu unapofikiria mahitaji ya wanafunzi wako.

Siku ya 1 (Maneno ya Mormoni–Mosia 2)Kwa kujifunza uzoefu wa Mormoni katika kufuata Roho na ikijumuisha mabamba madogo ya Nefi pamoja na kumbu-kumbu zake, wanafunzi walijifunza kwamba Bwana anajua vitu vyote. Mfalme Benyamini alifunza kwamba kama Wa-nefi hawakuwa na maandiko, wangefifia katika kutokuamini na kwamba kupekua maandiko hutusaidia kujua na kuweka amri. Aliwafundisha watu wake umuhimu wa kanuni kama hizo: Tunapowahudumia wengine, tunamtumikia Mungu. Tunapohisi kuwa na deni na Mungu, tunataka kuwahudumia wengine na shukrani zetu huongezeka. Ikiwa tutaweka amri, tutabarikiwa yote kimwili na kiroho.

Siku ya 2 (Mosia 3)Mfalme Benyamini alisimulia maneno ya malaika, ambaye alileta “habari njema ya shangwe kuu” kuhusu kuja wa Bwana katika maisha ya muda. Wanafunzi walijifunza kwamba ilitabiriwa zaidi ya miaka 100 kabla ya matukio yalitokea ambapo Yesu Kristo angeteseka ili tuweze kuoko-lewa kutoka kwa dhambi zetu. Tunaweza kuokolewa kutoka kwa dhambi zetu tunapofanya imani katika Yesu Kristo na kutubu. Kama tutakubali ushawishi wa Roho Mtakatifu, tunaweza kushinda mtu wa kawaida kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo.

Siku ya 3 (Mosia 4)Ujumbe wa Mfalme Benyamini ulijaza watu wake na Roho wa Bwana. Wanafunzi walijifunza kwamba tunapofanya imani katika Yesu Kristo na kutubu kwa uaminifu, tunapokea ondoleo la dhambi zetu. Mfalme Benyamini alifundisha watu wake kwamba wakijinyenyekeza wenyewe mbele za Mungu na kujitahidi kukuza sifa kama Kristo, tunaweza kulinda ondoleo la dhambi zetu.

Siku ya 4 (Mosia 5–6)Walipokuwa wakisoma kuhusu mabadiliko ambayo yalikuja juu ya watu wa Mfalme Benyamini, wanafunzi walijifunza kwamba tunapofanya imani katika Yesu Kristo na kupokea Roho Mtakatifu, tutapata uzoefu wa mabadiliko makubwa ya moyo. Watu wa Mfalme Benyamini walishika maagano kufanya mapenzi ya Bwana na kushika amri Zake, kuonyesha kwamba tunaweza kujichukulia wenyewe jina la Yesu Kristo tunapofanya na kushika maagano matakatifu.

UtanguliziSomo hili litawasaidia wanafunzi kuelewa mafundisho ya Mfalme Benyamini kwa wanawe na watu wake miaka mitatu kabla ya kifo chake. Mfalme Benyamini alifundisha watu wake jinsi ya kupokea na kuhifadhi ondoleo la dhambi zetu kwa kufa-nya imani katika Yesu Kristo.

Mapendekezo ya Kufundisha

Maneno ya MormoniNefi na Mormoni wanaonyesha imani yao katika MunguAlika mwanafunzi asome 1 Nefi 9:2–3 ili kuwakumbusha kwamba Nefi aliamuriwa kutendeneza seti mbili za mabamba. Wasaidie wao kuelewa kwamba katika kifungu hiki, kishazi “haya mabamba” humaanisha mabamba madogo ya Nefi, ambayo yana kumbukumbu kimsingi mambo matakatifu. Uliza mwanafunzi asome 1 Nefi 9:4 kwa sauti. Uliza darasa kutafuta madhumuni ya mabamba makubwa (usimulizi wa utawala wa wafalme na vita vya watu)

Wakumbushe wanafunzi kwamba Mormoni alipokuwa akifupi-sha mabamba makubwa ya Nefi, aligundua mabamba madogo miongoni mwa kumbukumbu zingine. Alikuwa ameongozwa na Roho Mtakatifu kujumuisha kile alipata kwenye mabamba madogo pamoja na ufupisho wake, hata ingawa hakujua kwa nini (ona Maneno ya Mormoni 1:7).

Alika nusu ya darasa kupekua 1 Nefi 9:5–6 ili kujua kwa nini Nefi aliamriwa kutengeneza mabamba madogo. Acha ile nusu ingine ya darasa kupekua Maneno ya Mormoni 1:6–7 ili kujua kwa nini Mormoni aliamua kujumuisha mabamba madogo pa-moja na ufupisho wake. Baada ya washiriki wa darasa, waulize ni nini hivi vifungu kutoka kwa Nefi na Mormoni vinawafundisha kuhusu Bwana. (Wanafunzi wanaweza kutumia maneno tofauti, hakikisha wanaonyesha wanaelewa kwamba Bwana anajua vitu vyote.)

• Ni nini ilikuwa” madhumuni ya hekima” ya siku za usoni ambayo wote Nefi na Mormoni walimaanisha? (Bwana alijua kwamba katika mwaka wa 1828 mabamba madogo yata-chukua nafasi ya kurasa 116 za mswaada wa Kitabu cha

Kwa Kutumia Masomo ya Mafunzo- NyumbaniMuhtasari wa Masomo ya MwanafunziMuhtasari utakusaidia kuuzoea muktadha na mafundisho na kanuni ambazo wanafunzi wamejifunza katikati ya wiki katika mwongozo wa kujifu-nzia wa mwanafunzi.

Utangulizi wa SomoUtangulizi wa somo utakusai-dia kujua sehemu gani ya vifu-ngu vya maandiko vitasisitizwa katika somo.

Kiini cha SomoKiini cha somo huleta mwo-ngozo kwako unaposoma na kufundisha. Kinapendekeza mawazo ya kufundishia, ikijumuisha maswali, shughuli, nukuu, michoro, na majedwali.

Kukusanya fungu la Maneno na Muhtasari wa MuktadhaMistari inawekwa kwenye makundi kulingana na wapi mabadiliko katika muktadhi au yaliyomo hutokea kote katika fungu la maandiko. Rejeo la kila kundi la mistari inafuatiwa na muhtasari mfupi wa matu-kio au mafundisho katika kundi lile la mistari.

Mafundisho na KanuniWakati mafundisho na kanuni kiasilia hutokea kutoka katika mafunzo ya maandiko, yanao-neshwa kwa uzito kukusaidia kugundua na kuyasisitiza ka-tika majadiliano na wanafunzi.

Utangulizi kwa Kitengo KinachofuataMgawanyiko wa mwisho wa kila somo hutoa mwa-nya mdogo wa kuchungulia kitengo kinachofuata. Jadili mgawanyiko huu pamoja na waanafunzi wako katika hiti-misho la kila somo kuwasaidia kutazamia kujifunza maandiko katika wiki inayofuata.

Page 13: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

xiixii

UTANGULIZ I

Mpango wa Seminari wa mafunzo- NyumbaniMpango wa mafunzo ya nyumbani una-ruhusu wanafunzi kupokea pointi katika seminari kwa kumalizia masomo binafsi nyumbani badala ya kuhudhuria madarasa ya kila wiki. Masomo haya yanapatikana katika mwongozo tofauti unaoitwa Mwongozo wa Kitabu cha Mormoni kwa wanafunzi wa Seminari wa Mafunzo ya Nyumbani. Mara moja kwa wiki, wana-funzi wanakutana na mwalimu wao wa seminari kupeleka kazi zao na kushiriki katika masomo ya darasani. Mwongozo wa kujifunzia wa mwanafunzi na masomo ya madarasa ya kila wiki yanaelezwa zaidi hapo chini.

Mwongozo wa mafunzo kwa wanafunzi wa Mafunzo ya nyumbaniMwongozo wa Kitabu cha Mormoni wa mafunzo kwa wanafunzi wa Seminari wa mafunzo Nyumbani  umebuniwa kuwasai-dia wanafunzi wa mafunzo- Nyumbani ku-pokea na kupata uzoefu katika kujifunza Kitabu cha Mormoni sawa sawa na ule wa mwanafunzi wa seminari anayehudhuria madarasa ya kila wiki. Hivyo, mwendo wa mwongozo wa kujifunzia wa mwanafunzi vile vile mafundisho na kanuni unasisitiza sambamba na nyenzo za mwongozo huu. Mwongozo wa kujifunzia wa wanafunzi umejumuisha pia maelekezo ya maandiko kariri Mistari ya maandiko kariri imeele-zewa katika muktadha kama inavyoone-kana nakala ya maandiko. Shughuli za ziada zimetolewa mwishoni mwa masomo ambamo vifungu vimeelezewa. Kila wiki, wanafunzi wa Seminari kwa mafunzo ya nyumbani wanalazimika kumaliza masomo manne kutoka katika mwongozo wa mwanafunzi na kushiriki katika somo la wiki lililotolewa na walimu wa seminari. Wanafunzi wanamalizia zoezi lililopewa namba kutoka katika mwongozo wa kujifunza katika majarida ya maandiko ya kujifunzia. Wanafunzi

wawe na madaftari mawili ya kujifunzia maandiko ili waweze kuacha moja na mwalimu wao na waendelee kufanyia kazi kwenye lingine. Wanafunzi wanapoku-tana na walimu wao kila wiki, jarida moja linarejeshwa kwa mwalimu wa mafunzo ya nyumbani na lingine linarudishwa kwa mwanafunzi ili litumike kwa ajili ya somo la wiki inayofuata. (Kwa mfano, katikati ya wiki, mwanafunzi anamalizia zoezi katika jarida la 1. Mwanafunzi baadaye huleta jarida hili darasani na kumpa mwalimu. Wiki inayofuata, mwanafunzi anamalizia mazoezi katika jarida la 2. Wakati mwanafunzi anapokabidhi jarida la 2, mwalimu atamrudishia jarida la 1. Mwanafunzi baadaye anatumia jarida la 1 kumalizia mazoezi ya wiki inayofuata.)Wanafunzi wote wa Seminari wanahi-mizwa kujifunza maandiko kila siku na kusoma nakala kwa ajili ya kozi, lakini wanafunzi wanaojifunzi nyumbani lazima waelewe kwamba wanategemewa kutu-mia dakika 30 mpaka 40 za ziada katika kila moja ya masomo manne ya nyumbani katika kila kitengo na kuhudhuria ma-somo ya nyumbani ya kila wiki.

Masomo ya kila wiki ya Kujifunzia NyumbaniKila kitengo katika Mwongozo wa Kujifunzia wa Kitabu cha Mormoni kwa ajili ya Seminari ya Wanafunzi ya Kujifu-nzia Nyumbani inarandana na masomo matano katika mwongozo wa mwalimu wa kila siku. Mwishoni mwa kila masomo matano katika mwongozo huu, utakuta somo moja la kila wiki la mwalimu la kujifunzia nyumbani. Masomo ya kujifu-nza nyumbani yatawasaidia wanafunzi kupitia tena, kuboresha uelewo wao, na kuyafanyia kazi mafundisho na kanuni walizojifunza wanapomaliza masomo katika mwongozo wa kujifunzia katikati ya wiki. Masomo haya yanaweza pia kuchunguza ukweli wa ziada ambao hau-jagusiwa katika mwongozo wa kujifunzia wa mwanafunzi. (Kwa msaada katika ku-pangilia ratiba ya somo lako, angalia kasi ya mwongozo kwa walimu wa mafunzo

ya nyumbani katika kiambatisho mwishoni mwa mwongozo huu)Kama mwalimu wa kujifunzia nyumbani, inatakiwa uwe na uelewa mkubwa kile wanafunzi wako wanasoma nyumbani kila wiki ili uweze kujibu maswali na kuje-nga majadiliano ya maana unapokutana nao. Waeleze wanafunzi kuleta maandiko yao, majarida ya kujifunza maandiko, na mwongozo wa kujifunzia wa mwanafu-nzi katika darasa la kila wiki ili waweze kuyarejea wakati wa somo. Linganisha masomo kulingana na mahitaji ya wana-funzi unaowafundisha na kulingana na mwongozo wa Roho Mtakatifu. Unaweza pia kutaka kurejea katika masomo ya mwalimu ya kila siku katika kitabu kidogo unapojiandaa na kufundisha. Kujifunza kuhusu visaidizi na njia za kufundisha zinazotumika katika masomo ya kila siku inaweza kukusaidia kukuza mafundisho yako ya wiki. Weka vyema kila aina ya hitaji la wanafunzi unaowafundisha. Kwa Mfano, kama mwanafunzi ana wakati mgumu kuandika, mruhusu kutumia vifaa vya kurekodia au aelezee mawazo yake kwa mwanachama wa familia au rafiki ambaye anaweza kuandika majibu yao. Mwishoni mwa kila somo la wiki, kusanya vijitabu vya kujifunzia maandiko vya wa-nafunzi na wahimize kuendelea kujifunza. Wapatie vijitabu vya kujifunzia maandiko kwa ajili ya mazoezi ya wiki inayofuata. Kwa Sababu ya vizuizi, huitaji kuongeza msisitizo kwenye maandiko kariri katika masomo yako ya wiki. Unavyosoma kwe-nye mazoezi katika vijitabu vya maandiko ya kujifunzia ya wanafunzi, jibu mara kwa mara kwenye kazi zao kwa kuandika wa-raka au kuwaelezea mara nyingine una-pokutana nao. Ungependa pia kutafuta njia nyingine za kutoa msaada na maoni yenye maana. Hii itawasaidia wanafunzi kujua kwamba unajali kuhusu kazi zao na itasaidia kuwapa moyo wawe na uhakika katika majibu yao.

Page 14: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

xiiixiii

UTANGULIZ I

Nyenzo nyingineWalimu wanaweza kutembelea tovuti ya Seminari na Chuo cha Dini ( si. lds. org) kwa ajili ya msaada katika kuandaa ma-somo na kupokea mawazo ya mafundisho mengine. Nyenzo zifuatazo ziko kwenye mtandao, kupitia msimamizi wako, kupitia vituo vya kanisa vya usambazaji, na kupi-tia duka la mtandaoni la stoo ya Kanisa. (store. lds. org):

Nyenzo za kuonea za DVD za Seminari

Kitabu cha Sanaa za Injili

“Maarifa yanayorekodiwa kwa uangalifu ni maarifa yanayopatikana katika wakati wa mahitaji. Habari nyeti ya kiroho inapaswa kuhifadhiwa katika mahali patakatifu ambapo panamuonyesha Bwana jinsi unaidhamini. Mazoea haya yanaongeza uwezekano wako wa kupokea nuru zaidi.”

Richard G. Scott, “Acquiring Spiritual Knowledge,” Ensign, Nov. 1993, 88.

Jarida la Masomo ya MaandikoMambo Yote Yanamshuhudia Yeye

09591_743_Journal.indd 1 2/11/13 12:32 PM

Majarida ya Masomo ya Maandiko

Alama za Seminari (ambazo zinajumuisha mida na orodha ya kielelezo cha maandiko kariri na kiini cha maneno)

A N D I K OU M A H I R I

A N D I K OU M A H I R I

A N D I K OU M A H I R I

A N D I K OU M A H I R I

A N D I K OU M A H I R I

A N D I K OU M A H I R I

A N D I K OU M A H I R I

A N D I K OU M A H I R I

A N D I K OU M A H I R I

A N D I K OU M A H I R I

A N D I K OU M A H I R I

A N D I K OU M A H I R I

A N D I K OU M A H I R I

A N D I K OU M A H I R I

A N D I K OU M A H I R I

A N D I K OU M A H I R I

A N D I K OU M A H I R I

A N D I K OU M A H I R I

A N D I K OU M A H I R I

1 Nefi 3:7Nitaenda na kutenda.

MuktadhaBwana anamwamuru Nefi na nduguze kurejea hadi Yerusalemu kuleta bamba za shaba.

Mafundisho au KanuniBwana hutayarisha njia kwetu ya kuweka amri Zake.

MatumiziNi nini ambacho Bwana amewaamuru kutenda ambacho wengine wanaweza kukiona kuwa kigumu? Je! Yeye alita-yarisha njia vipi kwako kukitimiza?

2 Nefi 2:27Tuna uhuru wa kuchagua.

MuktadhaLehi aliwafunza wanawe kuhusu nafasi ya wakala katika mpango wa wokovu.

Mafundisho au KanuniTuko huru kumfuata Yesu Kristo, ambavyo itatuletea uhuru na uzima wa milele, au ibilisi, ambavyo itatuele-keza kwenye utumwa na kifo.

MatumiziFikiria wakati wewe ulipochagua kutii amri. Je! Unahisi vipi kwamba utii wako umekupelekea au utakupelekea uhuru mkuu?

2 Nefi 2:25Adamu alianguka ili wanadamu wawe.

MuktadhaLehi aliwafunza wanawe kuhusu haja ya Anguko na matokeo yake.

Mafundisho au KanuniAnguko lilikuwa ni sehemu muhimu ya mpango wa Baba wa Mbinguni na liliwezesha kuwepo kwetu katika maisha ya muda.

MatumiziJe! Kujua kuhusu Anguko na maisha ya muda kunakusaidia vipi kufahamu vyema madhumuni yako maishani?

2 Nefi 9:28–29Kujifunza ni kwema kama tunafuata ushauri wa Mungu.

MuktadhaYakobo alitofautisha kati ya ukuu wa mpango wa wokovu wa Baba wa Mbinguni na mpango wa ulaghai wa ibilisi.

Mafundisho au KanuniWasomi mara nyingi huwa na kiburi kwa sababu ya hekima zao wenyewe na kupuuza ushauri wa Mungu. Kupo-kea elimu ni vyema kama tutaendelea kumtii Mungu.

MatumiziJe! Utii wa ushauri wa Mungu unaku-saidia vipi kuwa na mtazamo mzuri kuhusu hekima ya ulimwengu?

2 Nefi 25:23, 26Kwa neema tunaokolewa.

MuktadhaNefi alielezea kati ya sababu za kwa nini ni tu kupitia Yesu Kristo ndio mtu anaweza kuokolewa.

Mafundisho au KanuniKupitia kwa Yesu Kristo, tunaweza kupokea ondoleo la dhambi na kuoko-lewa kwa neema baada ya yote ya yale tunayoweza kufanya.

MatumiziNi hisia gani za kibinafsi na ushuhuda ambao unaweza kushiriki na mtu ambaye ana shaka kama Watakatifu wa Siku za Mwisho wanaamini katika Yesu Kristo?

2 Nefi 28:7–9Hatuwezi kutetea dhambi yoyote.

MuktadhaNabii Nefi aliwafunza watu wake juu ya uovu mkuu ambao ungezangaa katika siku za mwisho.

Mafundisho au KanuniKatika siku za mwisho, wengi watafundisha mafundisho ya uongo, yasiyofaa na ya upumbavu.

MatumiziJe! Unawezaje kutambua mafundisho ya upumbavu ya ulimwengu?

2 Nefi 31:19–20Vumilia hadi mwisho.

MuktadhaKaribu na mwisho wa huduma yake, Nefi aliandika kwamba watu wote sharti wafuate mfano wa Yesu Kristo ili kurithi uzima wa milele.

Mafundisho au KanuniBaada ya kufanya imani, kutubu dhambi zetu, tunabatizwa, na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu, ni lazima tusonge mbele katika wema na kuvu-milia hadi mwisho ili kupokea uzima wa milele.

MatumiziJe! Ni ushauri gani ambao unaweza kumpatia mshiriki wa Kanisa aliye-batizwa majuzi? Je! Unafanya nini ili “kusonga mbele kwa udhabiti katika Kristo”?

2 Nefi 32:3Sherehekea katika maneno ya Kristo.

MuktadhaKaribu na mwisho wa huduma yake, Nefi aliandika kile watu wote sharti wafanye ili kuelewa na kuishi mafu-ndisho ya Yesu Kristo.

Mafundisho au KanuniKama tutajifunza maneno ya Kristo na ya watumishi Wake wenye maongozi, tutapokea maelekezo tunayohitaji kufanya uchaguzi sahihi.

MatumiziJe! Maneno ya Kristo yamekusaidia vipi kujua kile cha kufanya? Je! Utafa-nya nini ili “kusherekea” maneno ya Kristo?

2 Nefi 32:8–9Ni lazima uombe daima.

MuktadhaKaribu na mwisho wa huduma yake, Nefi aliandika kile watu wote sharti wafanye ili kuelewa na kuishi mafu-ndisho ya Yesu Kristo.

Mafundisho au KanuniRoho hutufundisha kuomba.

MatumiziJe! Unawezaje kukumbuka kuomba usiku na mchana? Je! Unawezaje kutafuta ushawishi wa Roho Mtakatifu katika maombi yako?

Mosia 2:17Kuwahudumia wengine unamhudu-mia Mungu.

MuktadhaMfalme Benyamini aliwahutubia watu wake, kuwatayarisha wao kujichukulia juu yao jina la Yesu Kristo.

Mafundisho au KanuniTunapowahudumia watu wenzetu, tunamhudumia Mungu.

MatumiziJe! Ni vitu gani mahususi unavyoweza kuwafanyia wale walio karibu nawe ambavyo Mwokozi angefanya kama Yeye angekuwa hapa?

Mosia 3:19Mtu wa kawaida ni adui kwa Mungu.

MuktadhaMfalme Benyamini aliwahutubia watu wake, kuwatayarisha wao kujichukulia juu yao jina la Yesu Kristo.

Mafundisho au KanuniTunaweza kumshinda mtu wa kawa-ida kwa kumkubali Roho Mtakatifu na kuwa Mtakatifu kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo.

MatumiziJe! Inamaanisha nini “kukubali usha-wishi wa Roho Mtakatifu”? Je! Ni mi-nong’ono hipi ambayo Roho Mtakatifu amekuwa akikupatia wewe?

Mosia 4:30Chunga mawazo yako, maneno yako na matendo yako.

MuktadhaMfalme Benyamini aliwahutubia watu wake, kuwatayarisha wao kujichukulia juu yao jina la Yesu Kristo.

Mafundisho au KanuniTutahukumiwa na kuwajibika juu ya mawazo yetu, maneno yetu, na matendo yetu.

MatumiziJe! Ni matendo gani mahususi ambayo umefanya ili kudumisha mawazo, maneno, na matendo safi na mema mchana kutwa?

Alma 7:11–13Yesu Kristo alishinda dhambi na kifo.

MuktadhaAlma alitoa unabii kwa watu wa Gidioni kwamba Mwokozi atakuja katika ulimwengu na kwamba lazima wajitayarishe wenyewe.

Mafundisho au KanuniYesu Kristo alijichukulia juu yake mwenyewe maumivu, magonjwa, na udhaifu wa watu Wake; Yeye aliwako-mboa wanadamu kutokana na kifo na kupatia njia ya kushinda dhambi.

MatumiziJe! Ni wakati gani umepata kuhisi nguvu za uponyaji za Upatanisho? Andika katika shajara yako au shiriki ushuhuda wako kwa rafiki yako juu ya nguvu za uponyaji za Upatanisho.

Alma 32:21Imani si kujua kikamilifu.

MuktadhaAlma alifunza wanyenyekevu mio-ngoni mwa Wazoramu kuhusu ibada na imani

Mafundisho au KanuniImani inahitaji mtu kuamini vitu ambavyo ni vya kweli bali haviwezi kuonekana.

MatumiziJe! Unawezaje kumwelezea rafiki jinsi kitu ambacho hakionekani na bado ni cha kweli?

Alma 37:35Jifunze katika ujana wako kuziweka amri.

MuktadhaAlma alimshauri Helamani ili kumta-yarisha kwa majukumu ya uongozi.

Mafundisho au KanuniNi hekima kujifunza katika ujana wetu kuziweka amri za Mungu.

MatumiziJe! Ni uzoefu gani umeshapata ambao umeimarisha hamu yako ya kutii amri?

Alma 39:9Usiende tena kupendeza tamaa ya macho yako.

MuktadhaAlma alikosoa tabia ya Koriantoni, ambaye alikuwa ametenda dhambi mbaya sana.

Mafundisho au KanuniWale ambao wanajiingiza kwenye ta-ama na ukosefu wa maadili hawawezi kuokolewa katika ufalme wa Mungu pasipo wao kutubu.

MatumiziJe! Utafanya nini ili kushinda mawazo ya taama na kuziacha dhambi zako?

Alma 41:10Uovu haujapata kuwa furaha kamwe.

MuktadhaAlma alimfunza mwanawe Koriantoni kuhusu matokeo ya milele ya uovu na wema.

Mafundisho au KanuniDhambi haiwezi kuleta furaha ya kudumu.

MatumiziJe! Furaha yako imeongezeka kiasi gani kwa kufuata mfano na mafundi-sho ya Yesu Kristo?

Helamani 5:12Jenga msingi wako katika Kristo.

MuktadhaNefi na Lehi wanakumbuka ushauri wa baba yao Helamani na wakajitolea wenyewe kuhubiri kwa wale Wanefi waovu.

Mafundisho au KanuniNi tu kwa kuweka maisha yetu chini ya msingi wa Yesu Krsito ndio tuna-weza kustahimili majaribu ya Shetani.

MatumiziJe! Injili ya Yesu Kristo imekuimarisha vipi dhidi ya majaribu? Je! Unawezaje kuweka msingi wa uchaguzi wako vipi kwenye maisha na mafundisho ya Mwokozi?

3 Nefi 12:48 Ninyi mnapaswa kuwa wakamilifu.

MuktadhaYesu Kristo aliwafunza Wanefi sheria ya juu na kuwatayarisha wao kuwa washiriki wa ufalme wa Mungu.

Mafundisho au KanuniTumeamriwa kuwa kama Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo, ambao ni wakamilifu.

MatumiziJe! Unaweza kufanya nini sasa hivi ili kuwa zaidi kama Yesu Kristo?

3 Nefi 18:15, 20–21Chunga na uombe daima.

MuktadhaYesu aliwafunza Wanefi jinsi ya kusta-himili majaribu ya ibilisi.

Mafundisho au KanuniKupitia maombi tunaweza kupatiwa nguvu za kukinza majaribu, kupokea hamu zetu njema, na kubarikiwa katika familia zetu.

MatumiziJe! Unaweza kufanya nini ili kuwa dhabiti katika maombi yako ya kibi-nafsi na ya familia yako?

A N D I K OU M A H I R I Kadi za umahiri wa maandiko

(True to the Faith: A Gospel Reference [2004], 103–4)

Kwa Nguvu ya Vijana

bango la kalenda ya matukio

Page 15: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 16: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

1

SOMO LA 1

Wajibu wa Mwanafunzi

Mapendekezo ya Kufundisha

Majukumu ya kibinafsi ya kujifunza kwa kusoma na kwa imaniAlika mwanafunzi kuja mbele ya darasa. Elezea kwamba unataka kumsaidia mwanafunzi kuwa na nguvu kimwili. Kisha muulize mwanafunzi wa pili kuja mbele na kufanya zoezi la pushiapu tano.Baada ya mwanafunzi wa pili kumaliza pushiapu, muulize mwanafunzi wa kwanza:• Je! Hizo pushiapu zinakufanya wewe kuwa na nguvu?Uliza darasa:• Je! Mfano huu wa mazoezi ya kimwili yana uhusiano na majukumu yenu ya kujifunza

injili? Je! Ni nani aliye na majukumu ya kujifunza kwako injili?Mwalike mwanafunzi asome Mafundisho na Maagano 88:118 kwa sauti.• Je! Unafikiria inamaanisha nini “kutafuta kujifunza kwa kusoma na pia kwa imani”?

(Unaweza kuhitajika kusema wazi kwamba kujifunza kwa kusoma kunahitaji juhudi za kibinafsi)

Mzee David A. Bednar wa Akidi ya wale Mitume Kumi na Wawili kuhusu kile kinachomaanishwa na kujifunza kwa imani. Waagize wanafunzi waandike kauli hii mahali fulani (labda katika shajara zao za kujifunza maandiko au katika daftari za darasani) ili waweze kurejea kila mara katika mwaka wote wa seminari:“Kujifunza kwa imani kunahitaji jitihada za kiroho, akili, na kimwili na sio

kwa upokeaji baridi tu. Mwanafunzi sharti afanye imani na kutenda ili kupokea elimu mwenyewe” (“Seek Learning by Faith” [hotuba kwa waalimu wa dini wa CES , Feb. 3, 2006], 1, si.lds.org).

Kujifunza maandiko kwa kibinafsi kila sikuElezea kwamba kujifunza maandiko kibinafsi kila siku ni sehemu muhimu ya kutafuta kujifunza kwa kusoma na kwa imani.Mualike mwanafunzi kusoma Helamani 3:29–30 kwa sauti.• Je! Ni nini unachofikiria kuwa tofauti katika kusoma kijuujuu maandiko na “kulishikilia

neno la Mungu”?

UtanguliziMadhumuni ya somo hili ni kuwasaidia wanafunzi kutimiza wajibu wao katika kujifunza injili. Wakati mwengine wanafunzi hufikiria kwamba majukumu ya kujifunza kwao yanamtegemea mwalimu tu. Rais He-nry B. Eyring wa Urais wa Kwanza aliongea kuhusu haja ya wote mwanafunzi na mwalimu kutafuta mwongozo wa Roho Mtakatifu:

“Shida na majaribu yaliyowakabili wanafunzi wetu miaka mitano tu yanafifia katika kulinganishwa na kile tunachoona hapa sasa, na hata nyakati ngumu zaidi zilizopo mbele. Nimehisi kwamba kile tumefanya na kile tunachofanya hakitakuwa cha kutosha. Tunahitaji

uwezo mkubwa ili tuweze kufikisha injili katika mioyo na maisha ya wanafunzi wetu. . . .

Ni sharti muwe na Roho kama mwenzi wa kila mara ili kufundisha kwa uwezo, na wanafunzi wenu hawatafaulu kiroho pasipokuwa na Roho kama mwenzi wao” (“The Spirit Must Be Our Constant Companion” [hotuba kwa waalimu wa dini wa CES , Feb. 7, 2003], 1, si.lds.org).

Mnapofundisha kwa uwezo wa Roho Mtakatifu na kuwasaidia wanafunzi kujifunza kwa uwezo huo huo, mnaweza kuwasaidia wao kuongoka kikweli katika injili ya urejesho ya Yesu Kristo. Mnaweza kuhitaji kurejea kanuni zilizofunzwa katika somo hili kila mara ili kuwa-kubusha wanafunzi majukumu yao katika darasa.

Shajara ya kujifunza maandiko au daftari za darasaniShajara ya kujifunza maandiko au daftari za darasani zinaweza kuwa shajara ya kujalidi, daftari, au kurasa katika jadala. Katika shajara ya kujifunza maandiko mwanafunzi anaweza kuandika mambo na kurekodi maono wakati wa masomo, wakati wa kujifunza maandiko kwa kibinafsi, na katika mi-kutano mingine ya Ka-nisa. Wanaporekodi na kupanga mawazo yao na maono, watakuwa tayari kushiriki katika darasa, kuboresha ufahamu wao wa injili, na kupokea ufunuo wa kibinafsi.

Page 17: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

2

SoMo la 1

• Kulingana na mistari tuliyosoma, ni baraka gani zinazopatikana kutokana na “kulishiki-lia neno la Mungu”?

• Ni baraka gani zingine zinazopatikana kupitia kutokana na kujifunza maandiko kila siku?• Ni lini ulipopokea baraka kutokana na kujifunza maandiko kibinafsi kila siku?Wanafunzi wanapojibu maswali haya, hakikisha kwamba wanafahamu kwamba kujifunza maandiko kila siku huimarisha ushuhuda wetu, humwalika Roho Mtakatifu katika maisha yetu, na hutusaidia kujifunza injili.Waalike wanafunzi kujibu mojawapo ya maswali yafuatayo katika shajara zao za kujifunza maandiko:• Je! Unawezaje kuboresha kujifunza kwako Kitabu cha Mormoni mwaka huu?• Je! Ni kwa njia gani kusoma Kitabu cha Mormoni kinaathiri hisia zako kuhusu Yesu

Kristo?Waalike wanafunzi kuweka lengo la kujifunza Kitabu cha Mormoni kila siku mwaka huu. Waalike wao pia kuweka lengo la kusoma Kitabu cha Mormoni chote wakati wa mwaka wa seminari. Unaweza kushawishi kwamba waandike haya malengo katika sharaja zao za kujifunza maandiko. Wakumbushe wao kwamba malengo yanaweza kuwasaidia wao na mahitaji yao katika Wajibu Wangu kwa Mungu na Maendeleo ya Kibinafsi.

Kujifundisha kwa RohoNakili mchoro ufuatao kwanye ubao. Usiandike maneno katika mchoro. Utayaandika somo linapoendelea mbele.

Alika wanafunzi asome Mafundisho na Maagano 50:17–18 kwa sauti.• Kulingana na mistari hii, ni nini Bwana anachohitaji kutoka kwa mwalimu wa injili?

(Kufunza kweli kwa uwezo wa Roho.)Andika Roho Mtakatifu na Mwalimu kwenye mchoro, kama inavyoonyeshwa hapa. Elezea mawazo yako kuhusu kutafuta maongozi ya Roho Mtakatifu unapofundisha. Wasaidie wanafunzi kufahamu kwamba matayarisho yako na kujifunza kwako, unafanya juhudi za halisi za kuongozwa na Roho.Waeleze wanafunzi kuweka alama katika Mafundisho na Maagano 50 (kwa vile watarudi kwenye hii haya katika muda mfupi). Muulize mwanafunzi kusoma 2 Nefi 33:1 kwa sauti.• Je! Roho Mtakatifu hufanya nini kwa mwenye kujifunza wakati injili inapofundishwa?Elezea kwamba kujifunza injili kwa njia ya Bwana, ni sharti tukubali jukumu la kujifunza kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Waalike wanafunzi kusoma Mafundisho na Maagano 50:19–21 kimya.• Je! Ni nini tunachopaswa kuandika katika pembe ya kulia ya pembe tatu? (Andika

Mwanafunzi.• Je! Unafikiria inamaanisha nini kupokea ukweli kwa Roho?Unaweza kufunza kanuni fulani kuhusu kutambua ushawishi wa Roho Mtakatifu. Wasaidie wanafunzi kufahamu kwamba Roho kwa kawaida huwasiliana nasi kimya kimya kupitia hisia zetu na katika akili zetu (ona 1 Nefi 17:45; M&M 8:2). Roho Mtakatifu pia huleta hisia za upendo, furaha, amani, subira, upole, staha, imani na matumaini (ona Wagalatia 5:22–23 M&M 11:12).• Je! Unaweza kufanya nini katika seminari ili kujitayarisha kujifunza kwa Roho?

Kujifunza maandiko kila sikuMzee Dallin H. Oaks wa Jamii ya wale Mitume Kumi na Wawili alifunza:“Kusoma maandiko utuweka katika uwiano na Roho wa Bwana. Kwa sababu tunaamini kwa-mba kusoma maandiko kunaweza kutusaidia kupokea ufunuo, tuna-pata moyo wa kusoma maandiko tena na tena. Kwa njia hii, tunapata kile Baba yetu Mbinguni angependa sisi tujue na kufanya katika maisha yetu ya kibinafsi leo. Hii ndio sababu moja Watakatifu wa Siku za Mwisho wanaamini katika kila siku kujifunza maandiko” Scripture Re-ading and Revelation,” Ensign, Jan. 1995, 8).

Roho Mtakatifu

Mwalimu Wanafunzi

Page 18: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

3

WajibU Wa MWanafUnzi

Kama sehemu ya mazungumzo, wasaidie wanafunzi kufahamu kwamba njia moja mu-himu ya kujifunza kwa Roho ni kuwa tayari kutoa shuhuda zetu kwa kila mmoja. Soma taarifa ifuatayo ya Mzee Richard G. Scott wa Akidi ya wale Mitume Kumi na Wawili:

Wanafunzi wanapotenda juu ya kweli, [hizi kweli] zinatbibitishwa katika nafsi zao na kuimarisha shuhuda zao binafsi” (“To Understand and Live Truth” [hutoba kwa walimu wa dini wa MEC, Feb. 4, 2005], 3, si.lds.org).Wakumbushe wanafunzi kwamba mipango ya Wajibu Wangu kwa Mungu na Maendeleo ya Kibinafsi inajumuisha mapendekezo ya kushiriki kweli za injili na wengine. Watie moyo wao kushiriki uzoefu wao katika madarasa ya se-

minari, katika akidi au madarasa ya mikutano, na katika mazungumzo na wanafamilia wao na marafiki. Tilia mkazo kwamba wanapofanya juhudi za kuelezea, kushiriki, na kushuhu-dia kweli za injili, Mungu ataongezea uwezo wao wa kujadili injili na wengine.Rejea tena kwenye mchoro ubaoni. Muulize mwanafunzi asome Mafundisho na Maagano 50:12, 22 kwa sauti.• Je! Mistari hii inaelezeaje kwa kifupi kazi za Roho Mtakatifu, mwalimu, na mwanafunzi

katika kujifunza injili? (Unaweza kuelezea kwamba Roho Mtakatifu, pia anayeitwa Roho na Mfariji katika aya hii hufunza kweli. Mwalimu anapaswa kufundisha kwa Uwezo wa Roho, na mwanafunzi anapaswa kujifunza kwa uwezo huo huo.)

• Je! Ni nini kinachotendeka mwanafunzi anapojifunza kwa Roho na mwalimu kufunza kwa Roho? (Unaweza kuwa na haja ya kuelezea kwamba adilisha humaanisha kujenga, kuimarisha, kuelimisha, au kuboresha.)

Katika Kitabu cha Mormoni, Enoshi na Alma ni mifano ya watu waliojifunza kwa Roho. Waulize wanafunzi kusoma Enoshi 1:4–10 Alma 5:45–47 kimya kimya. (Unaweza kuandika haya marejeo kwenye ubao.) Kisha uulize:• Je! Ni nini Enoshi (au Alma) alijifunza kwa Roho?• Je! Roho alimfanyia nini Enoshi (au Alma)?Mwalike mwanafunzi kusoma taarifa ifuatayo ya Mzee Bednar:“Tunapaswa daima kukumbuka kwamba Roho Mtakatifu ni mwalimu ambaye, kupitia mwaliko sahihi anaweza kuingia katika moyo wa mwenye kujifunza” (“Seek Learning by Faith,” 4).• Je! Kile tulichojifunza kinafaa vipi katika majukumu yako ya kibinafsi kama mshiriki wa

darasa hili? Wanafunzi wanapojibu, hakikisha wamefahamu kwamba tunapofungua mioyo yetu na kumuuliza Mungu kwa imani, Roho Mtakatifu atatusaidia kue-lewa kweli za injili.).

Ili kuwasaidia wanafunzi fikiria juu ya njia wanazoweza kusaidiana kujifunza kwa Roho, uliza:• Je! Ni vitendo gani tunavyoweza kufanya ambavyo vitasaidia kumwalika Roho ka-

tika darasa letu? (Majibu yanaweza kujumuisha kuimba wimbo wa kufungua, kuja na maandiko darasani na kuyatumia kila siku, kuwa tayari kujibu maswali na kushirikiana uzoefu, kuombeana, na kuomba mwongozo wa Roho Mtakatifu.)

Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa kwamba vitendo vibaya pia vinaweza kuathiri darasa lote, uliza:• Je! Ni mitazamo au tabia gani zinazo mhudhi Roho katika darasa la seminari?Waalike wanafunzi ili kufikiria juu ya thamani ya kuwa na Roho Mtakatifu kama mwa-limu wao.• Je! Ni lini ulipopata uzoefu wa Roho akitenda katika nafasi Yake kama mwalimu?Hitimisha kwa kuwaalika wanafunzi kujifunza kwa kusoma na imani wanapojifunza Kitabu cha Mormoni katika seminari mwaka huu. Unaweza kufuatilia wanafunzi mwaka wote ili kuwatia moyo ili waendelee katika juhudi hizi.

Page 19: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

4

SoMo la 1

Tangazo na Habari za Usuli 2 Nefi 33:1. Kufungua mioyo yetu kwa Roho MtakatifuKama sehemu ya mazungumzo yako ya 2 Nefi 33:1, fikiria kusoma maandiko ya taarifa ifuatayo ya Mzee Da-vid A. Bednar wa Akidi ya wale Mitume Kumi na Wawili:

“Nefi anatufundisha, mwanadamu anapozungumza kwa uwezo wa Roho Mtakatifu uwezo wa Roho Mta-katifu huyapeleka katika mioyo ya watoto wa watu’ (2 Nefi 33:1). Tafadhali tazama jinsi uwezo wa Roho hubeba ujumbe hata lakini sio lazima ndani ya moyo.

Mwalimu anaweza kuelezea, kuonyesha, kushawishi, na kushuhudia, na kufanya hivyo kwa uwezo mkuu wa ki-roho na kupendeza. Hatimaye, hata hivyo, yaliyomo ka-tika ujumbe na ushuhuda wa Roho Mtakatifu hupenya ndani ya moyo tu kama msikiaji anayakubali yaingie. . . .

“Mwenye kujifunza akitumia haki yake ya kujiamulia kwa kutenda kulingana na kanuni sahihi hufungua moyo wake kwa Roho Mtakatifu— na kualika mafu-ndisho Yake, uwezo wa kushuhudia, na ushahidi wa kuthibitisha” (“Seek Learning by Faith” [address to CES Religious Educators, Feb. 3, 2006], 1, 3, si.lds.org).

Page 20: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

5

Mapendekezo ya Kufundisha

Je! Tunapaswa kujifunza maandiko katika seminari kwa njia gani? Kabla darasa kuanza, andika taarifa ifuatayo ya Rais Thomas S. Monson kwenye ubao. (Hii taarifa inapatikana katika ukurasa wa 107 wa Ripoti ya Mkutano Mkuu wa Ocktoba 1970.)

“Lengo la ufundishaji wa injili si ‘kumwaga habari’ kwenye akili za wanadarasa. Dhamira ni kumpatia mtu maongozi ya kufikiria kuhusu, kuhisi juu ya, na kisha kufanya kitu kuhusu kuishi kanuni za injili” (Rais Thomas S. Monson).

Mwombe mwanafunzi kusoma taarifa hii kwa sauti.• Kulingana na taarifa hii, lengo langu linapaswa kuwa nini kama mwalimu wako wa

seminari? Lengo lako linapaswa kuwa nini kama mwanafunzi wa seminari?Waambie wanafunzi kwamba katika somo hili, watagundua njia za “kufikiria kuhusu, kuhisi juu ya, na kisha kufanya kitu juu ya kuishi kanuni za injili” zilizofundishwa katika maandiko.

Kuelewa usuli na mazingira ya maandikoElezea kwamba kitu kimoja wanafunzi wanaweza kufanya kuboresha mafunzo yao ya maandiko ni kujifunza kuhusu usuli na mazingira ya matukio na ufunuo katika maandiko. Usuli na mazingira mara nyingi huitwa muktadha.Mwalike mwanafunzi kusoma ushauri ufuatao kutoka kwa Rais Thomas S. Monson

“Jifahamishe na masomo yanayofunzwa na maandiko. Jifunze usuli na mazingira ya mafumbo ya Bwana na maonyo ya mitume. Jifunze juu yake kama vile wanaongea na wewe, kwani hivyo ni kweli” (“Be Your Best Self,” Ensign au Liahona, Mei 2009, 68).Taja kwamba uelewa wa usuli na mazingira unaweza kutusaidia sisi kuelewa mafundisho katika maandiko. Hutupa habari ambazo zinafafanua na kuleta

ufahamu wa kina wa matukio, mafundisho, na kanuni katika maandishi.Andika maswali yafuatayo kwenye ubao:

Ni nani anayeongea katika vifungu hivi?Na anasema na nani?Ni nini kinafanyika katika tukio hili?

Elezea kwamba maswali haya yanaweza kutusaidia kufahamu muktadha wa ufundishaji au tukio katika maandiko.Waulize wanafunzi waelezee kile wamefanya ili kupata uelewa bora wa usuli na mazingira ya aya za maandiko. Unaweza kuorodhesha kati ya mawazo haya katika ubao.Wanafunzi wanaweza kutaja tabia kama vile kutafuta maana ya maneno magumu au yasiyo ya kawaida, kukagua maandishi husika, kusoma muhtasari wa sura mwanzoni wa sura, au kupekua tanbihi za maelezo na marejeo. Hakikisha umetaja huu ujuzi kama wanafunzi hawatautaja.

UtanguliziHili somo litawasaidia wanafunzi kukuza uelewa wao wa madhumuni ya maandiko. Pia litawasaidia wao kujifunza maandiko katika njia ya maana sana. Inajumuisha shu-ghuli za kujifunza zinazohusu kuelewa usuli na mazingira ya maandiko, kutambua na kuelewa mafundisho na

kanuni, na kutumia mafundisho na kanuni katika maisha yao. Wanafunzi wanapoimarika katika uwezo wao wa kujifunza maandiko, upendo wao wa maandiko utaonge-zeka, vile vile uelewa wao wa injili. Fikiria njia za kurejea kwenye vifaa katika somo hili katika mwaka wote.

SOMO LA 2

Kujifunza Maandiko

Page 21: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

6

SoMo la 2

Ili kufanya utaratibu mmoja kwa ufahamu wa muktadha wa maandiko, alika mwanafunzi asome 3 Nefi 17:1–10 kwa sauti. Uliza darasa kufuatilia, wakitafuta majibu ya maswali ambayo umeandika kwenye ubao. Unaweza pia kuwahimiza wao kutazama muhtasari wa sura kwa maelezo ya jumla ya upesi ya sura.• Ni nani anayesimulia hadithi hii katika vifungu vya 1, 5–6, na 9–10? (Mormoni.)• Katika hadithi hii, ni nani anayeongea? Ni nani anayepokea huu ujumbe?• Ni nini kilichotokea kabla ya matukio katika hii hadithi? (Ona muhtasari wa sura kwa

3 Nefi 8–16.) Je! Ni kwa jinsi gani elimu yako ya usuli huu inaathiri uelewa wako wa kwa nini watu walimtaka Mwokozi kukaa kidogo zaidi? (Ona 3 Nefi 17:5–6.) Ni miujiza gani ilitokea baada ya Yeye kusema kwamba atakaa? (Ona 3 Nefi 17:7–10.)

Kutambua na kuelewa mafundisho na kanuniTia mkazo kwamba wanafunzi wanapoelewa usuli na mazingira ya hadithi za maandiko, wanakuwa wamejitayarisha vema kutambua na kuelewa mafundisho na kanuni zilizomo. Alika mwanafunzi asome maelezo yafuatayo ya kanuni za injili, zilizotolewa na Mzee Richard G. Scott wa Akidi ya Wale Mitume Kumi na Wawili:“Kanuni za ukolezi wa kweli, zilizo unganishwa kwa matumizi ya hali mbali mbali” (“Acquiring Spiritual Knowledge,” Ensign, Nov. 1993, 86).Elezea kwamba mafundisho na kanuni ni za milele, kweli zisizobadilika za injili ya Yesu Kristo ambazo hutoa mwelekeo wa maisha yetu. Ni masomo ambayo manabii wa kale walidhamiria sisi tujifunze kutokana na matukio, hadithi, na mahubiri yaliyoandikwa ka-tika maandiko. Sema kwamba waandishi fulani katika maandiko walitumia maneno kama vile “basi tunaona” (ona Helamani 3:27–29 au maneno kama vile kwa hivyo (ona Alma 32:14) yenye kulenga moja kwa moja katika mafundisho na kanuni. Mafundisho na kanuni nyingi, hata hivyo, hazitajwi wazi kabisa katika maandiko. Badala yake, kweli hizi zinado-kezwa na zinaonyeshwa kupitia maisha ya wale walio katika maandiko.Ili kuwasaidia wanafunzi kujifunza kutambua mafundisho na kanuni ambayo haijasemwa wazi, pendekeza kwamba wanaposoma, wajiulize wenyewe maswali kama hivi: Je! Ujumbe wa hadithi hii ni nini? Mwandishi alidhamiria sisi tujifunze nini kutoka kwenye hadithi? Ni kweli gani zinazofunzwa katika aya hii ya maandiko? Unaweza kuorodhesha maswali haya kwenye ubao.Ili kuwasaidia wanafunzi kutambua mafundisho na kanuni, acha wao warudi kwenye 3 Nefi 17:1–10. Uliza:• Kutoka katika mafundisho ya Mwokozi katika 3 Nefi 17:2–3, ni nini tunachoweza kujifu-

nza kuhusu kuelewa neno Lake?• Ni kweli gani tunazoweza kujifunza kuhusu Mwokozi kutoka 3 Nefi 17:5--7?• Kama jibu kwa imani kuu ya watu, Mwokozi alijitolea kuwaponya. Katika 3 Nefi 17:8–9},

ni kanuni gani unazoona kuhusu kutafuta baraka kutoka kwa Bwana? (Kanuni moja ambayo wanafunzi wanaweza kutambua ni kwamba Bwana hujibu hamu zetu za haki za kujongea karibu Naye.)

Kama kuna muda wa kuwapatia wanafunzi mazoezi zaidi katika kutambua mafundisho na kanuni, waalike wao kutafuta hadithi zao za maandiko wazipendazo. Waulize wao ku-tambua kanuni walizojifundisha kutoka kwenye hadithi hizo. Kisha waalike wao kuelezea hadithi zao na kanuni walizojifunza.

Kutumia mafundisho na kanuniRais Boyd K. Packer, Rais wa Akidi ya Wale Mitume Kumi na wawili alisema:“Mafundisho ya kweli, yakieleweka, hubadilisha mitazamo na tabia. Mafunzo ya mafu-ndisho ya injili yataweza kuboresha tabia kwa upesi kuliko mafunzo ya tabia yanavyoweza kuboresha tabia. Hii ndio maana tunasisitiza kwa nguvu sana mafunzo ya mafundisho ya injili “ (“Little Children,” Ensign, Nov. 1986. 17).Eleza kwamba tunapoelewa mafundisho au kanuni, tunajua zaidi ya maelezo ya maneno. Tunajua kile mafundisho au kanuni inamaanisha katika maisha yetu. Tunapotambua ma-fundisho au kanuni na tunapata kuielewa, tunaweza kuitumia katika maisha yetu. Elezea kwamba matumizi yanafanyika tunapofanya kitu kuhusu kanuni tulizojifunza. Wanafunzi

Page 22: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

7

KUjifUnza MaandiKo

wanaotenda juu ya kanuni walizojifunza watakuwa na nafasi kubwa ya kuhisi Roho Mta-katifu akithibitisha ukweli wa hizi kanuni (ona 2 Nefi 32:5; Moroni 10:5). Hii ndio thamani halisi ya elimu inayopatikana kutokana na kujifunza maandiko. Wasaidie wanafunzi kuona kwamba wanapojifunza maandiko—hata kama wapo nyumbani, kanisani, katika seminari, wanashughulikia Maendeleo ya Kibinafsi au Wajibu kwa Mungu, au katika mazingira—yo-yote mengine mojawapo wa malengo muhimu yapaswa kuwa ni kuboresha juhudi zao za kuishi injili na kujongea karibu na Mungu.Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa na kutumia kanuni walizogundua katika maandiko, wa-tie moyo waombe usaidizi wa Roho Mtakatifu katika kujifunza wao binafsi. Pia watie moto kuuliza maswali kama yafuatayo wanapojifunza: Je! Bwana anataka mimi nifanye nini na elimu hii? Hii inaweza kuleta tofauti gani katika maisha yangu? Ninaweza kuanzisha au kusitisha nini sana ili kuishi maisha bora zaidi? Je! Maisha yangu yatakuwaje bora kama nikifanya hivyo? (Unaweza kuandika maswali fulani au yote kwenye ubao. Pia kama uki-penda shauri kwamba wanafunzi waandike haya maswali katika shajaraa zao za kujifunza maandiko ili waweze kuyarejea kila mara.)Katika kumaliza, gawa wanafunzi wawili wawili. Waombe wao waelezane kila mmoja kanuni walizojifunza leo kutoka 3 Nefi 17:1–10. Watie moyo waongee kuhusu kile wamefa-nya ili kukuza uelewa wao wa hizi kanuni na kile watafanya kutumia kile walichojifunza na kuhisi. Waulize waongee kuhusu jinsi matumizi ya kanuni hizi yanavyoweza kuleta tofauti katika maisha yao.

Mawazo ya Ziada ya KufunzaUjuzi na mbimu za kujifunza maandikoUjuzi ufuatao utawasaidia wanafunzi katika kujifunza kwao maandiko. Umejumuishwa kama kumbusho kote katika hiki kijitabu cha mwongozo.

Maelezo ya maneno: Baadhi ya maneno ambayo manabii hutumia si ya kawaida kwetu. Kamusi ya Biblia, tanbihi katika maandiko, na kamusi ya kawaida inaweza kutu-saidia sisi kujifunza maelezo ya maneno na kutambua visawe vya maneno haya. Mfano: neno Masiya katika 1 Nefi 10:4–17,

Jina badala: Ili kujisaidia mwenyewe kutumia maandiko katika maisha yenu, badili jina lako na jina katika maa-ndiko. Mfano: 1 Nefi 1:1,

Marejeo- mtajo: Unganisha aya za maandiko kwa kila moja ili kufafanua na kufumbua uelewa. Mfano: Katika pambizo karibu na 3 Nefi 12:28, unaweza kuandika muhtasari ya ona Mafundisho na Maagano 42:23,

Sababu na athari: Angalia uhusiano wa kama- kisha na sababu- kwa hivyo. Mfano: 2 Nefi 1:9,

Maneno muhimu: Maneno na vifungu kama tazama, kwa hivyo, kwa sababu, hata hivyo, au hivyo tunaona ni mwaliko wa kutua na kutafuta jumbe mahususi. Mfano: Helamani 6:35–36,

Orodha ya maandiko: Manabii kila mara walitoa orodha ya maonyo na changamoto. Tunapopata hii orodha, fikiria kuweka namba kwa kila kitu. Mfano: Alma 26:22.

Mazingira: Katika taarifa za maandiko, tambua ni nani anaongea, mtu, au watu yeye anaongea nao, ni nini yeye anaongee kuhusu, na lini na wapi hili tukio lina-tokea. Mfano: Mazingira ya Alma 32:21–43 yanayopati-kana katika Alma 31:1, 6–11 na 32:1–6.

Utofautishaji: Haya maandishi ya manabii kila mara huonyesha utofautishaji katika mawazo, matukio, na watu. Utofautishaji huu husisitiza kanuni za injili. Tafuta utofautishaji katika kila kifungu, katika sura, na sura zote na vitabu. Mfano: 2 Nefi 2:27; Alma 48:1–17,

Piga Twasira: Tafuta maelezo ya kina ambayo yanaweza kukusaidia kujenga picha akilini unaposoma. Fikiria ukiwa hapo katika matukio hayo. Mfano: Enos 1:1–8,

Uashiriaji: Maneno kama vile kama, vile, au fananisha na husaidia kutambua ishara. Tazama zaidi ya ishara kwa kukagua uhasili wake na kutafakari juu ya sifa zake. Tanbihi, Kamusi ya Biblia, na Mada ya Mwongozo ina-weza kuwasaidia katika kufafanua ishara fulani. Mfano: Helamani 8:14–15, ikijumuisha tanbihi za vifungu hivi.

Kutafakari: Kutafakari hujumuisha kufikiri, kutaamali, kuuliza maswali, na kupima kile unachojua na kile umejifunza. Kutafakari kila mara utusaidia kuelewa kile tunachohitaji kufanya ili kutumia kanuni za injili.

Page 23: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

8

Mapendekezo ya Kufundisha

Mpango wa wokovu katika Kitabu cha MormoniElezea kwamba katika ulimwengu wa roho kabla ya kuzaliwa, tunajifunza kuhusu Baba yetu wa Mbinguni kwa wokovu wetu (ona Musa 4:1–2; Ibrahimu 3:22–28 ). Kupitia mpa-ngo huu, tutaweza kuwa kama yeye na kuishi katika uwepo Wake.Katika ubao, andika Mpango wa wokovu unajumuisha . . . Waulize wanafunzi wamalize hili wazo katika shajara zao za kujifunza maandiko au vitabu vya darasani.Baada ya wanafunzi kupata nafasi ya kuandika, toa maelezo ya mpango wa wokovu yafua-tayo. Unaweza kuandika kwenye ubao au bango kabla ya darasa kuanza.Mpango wa wokovu ni “utimilifu wa injili ya Yesu Kristo, uliopangiwa kuleta kutokufa kwa binadamu na uzima wa milele. Unajumuisha Uumbaji, Anguko, na Upatanisho, pamoja na sheria, ibada, na kanuni zote zilizotolewa na Mungu. Mpango huu unawezesha watu wote kuinuliwa na kuishi milele na Mungu” (Guide to the Scriptures, “Plan of Redemption,” scriptures.lds.org).Waulize wanafunzi wainue mikono yao kama maneno walioandika yanayofanana na haya maelezo kwa njia yoyote. Kisha elekeza maswali yafuatayo kwa wanafunzi fulani walioinua mikono yao:• Je! Maelezo yako yanafananaje na haya? Kwa nini ulijumuisha hili jambo katika mae-

lezo yako?Wapange wanafunzi kufanya kazi wawili wawili. Muulize mmoja wa wanafunzi katika jozi asome Alma 22:12–14 na yule mwanafunzi mwingine asome 2 Nefi 2:25–28 (Unaweza kuandika haya marejeo kwenye ubao.) Waulize wanafunzi watafute sehemu za mpango wa wokovu zilizotajwa katika msitari waliyopatiwa. Baada ya wanafunzi kusoma, waulize wenzi wao wachukue zamu kuelezea kile walichopata.Andika mrejeo wa maandiko kwenye ubao: 2 Nefi 9:6;2 Nefi 11:5; Alma 12:25; Alma 24:14; Alma 42:8; Alma 42:15. (Unaweza kuyaandika kwenye ubao kabla darasa kuanza.)

UtanguliziRais Boyd K. Packer wa Akidi ya wale Mitume Kumi na Wawili aliwafunza walimu wa seminari kuwasilisha ma-elezo ya jumla ya mpango wa wokovu kwa ufupi hapo mwazoni mwa kila mwaka wa shule:

“Maelezo ya jumla ya ‘mpango wa furaha’ kwa ufupi . . . kama yakitolewa hapo mwanzo kabisa na kurudi-liwa mara kwa mara, yatakuwa na thamani kubwa kwa wanafunzi wako. . . .

“Vijana hushangaa ‘kwa nini?’ —Kwa nini tumeam-riwa kufanya vitu fulani, na kwa nini tumeamriwa tusifanye  vitu vingine? Elimu ya mpango wa furaha, hata katika umbo la muhtasari, inaweza kupatia akili changa ‘kwa nini.’ . . .

“ Hutupatia hisia za msingi kwa mpango wote, hata kama kwa muhtasari. Acha wao wajue yote yahusuyo, kisha watapata kujua ‘kwa nini.’ . . .

“ Kama unajaribu kuwapatia wao kujua ‘kwa nini,’ wafu-ate [huu] mpangilio: ‘Mungu aliwapatia wao amri, baada ya kuzifanya zijulikane kwa mpango wa ukombozi. ’Alma 12:32; italiki imeongezewa.]” (“The Great Plan of Happi-ness” [Kongamano la MEK kuhusu Mafundisho na Maa-gano/Historia ya Kanisa, Aug. 10, 1993], 2–3, si.lds.org).

Kama jibu kwa ushauri wa Rais Packer, hili somo linatoa maelezo ya jumla mafupi ya mpango wa wokovu kama inavyofunzwa katika maandiko. Somo hili linalenga Upatanisho wa Yesu Kristo, ambao ni “jambo la msingi, msingi muhimu, na fundisho kuu la mpango mkuu na wa milele”(Jeffrey R. Holland, “Missionary Work and the Atonement,” Ensign, Mar. 2001, 8). Wanafunzi wana-pokuja kuelewa mpango wa wokovu, imani yao katika Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo itaongezeka. Watakua katika azimio lao la kushika amri, kupokea ibada za wo-kovu, na kuwa wakweli katika maagano yao.

Maelezo ya jumla kwa ufupiWakati Rais Packer alipowashauri walimu kufundisha somo kuhusu mpango wa wokovu, yeye pia aliwapatia wao kazi ya kibinafsi “kutaya-risha kidokezo kifupi au maelezo ya jumla mafupi ya mpango wa furaha” kama sehemu yao ya ku-jifunza maandiko. Yeye aliwashauri: “Uyapange kama umbo ambalo wa-nafunzi wako wanaweza kupanga kweli ulizo shirikiana nao” (“The Great Plan of Happiness” [Kongamano la MEK kuhusu Mafundisho na Maagano/Historia ya Ka-nisa, Aug. 10, 1993], 2–3, si.lds.org). Tumia huu ushauri kama mwongozo unapojitayarisha kufunza hili somo. Haupaswi ku-jaribu kufunza kila kweli ya injili, hata kama kweli zote zimejumhishwa katika mpango.

SOMO LA 3

Mpango wa Wokovu

Page 24: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

9

Mpango Wa WoKovU

Elezea kwamba katika Kitabu cha Mormoni, manabii hutumia vichwa mbali mbali vya mpango wa Baba wa Mbinguni. Waalike wanafunzi kwenda katika 2 Nefi 9:6, na mwombe mwanafunzi asome mstari huu kwa sauti.• Katika mstari huu, ni kifungu gani cha maneno kinachotaja mpango wa Mungu? (Mpa-

ngo wa rehema wa Muumba mkuu.” Andika haya katika ubao karibu na 2 Nefi 9:6.)Waombe wanafunzi kusoma kimya kimya aya zingine za maandiko zilizoorodheshwa kwe-nye ubao, wakitafuta vifungu ambavyo vinataja mpango wa Baba wa Mbinguni. Mwanafu-nzi anapopata kifungu cha maneno kinachotaja mpango wa Baba wa Mbinguni, mwalike yeye aandike kwenye ubao karibu na mtajo wa maandiko pale yanapopatikana. Orodha kamili kwenye ubao inapaswa kuonekana kitu kama hiki:

2 Nefi 9:6—Mpango wa rehema wa Muumba mkuu2 Nefi 11:5—Mpango mkuu na wa milele wa ukombozi kutokana na kifoAlma 12:25}—Mpango wa ukomboziAlma 24:14—Mpango wa wokovuAlma 42:8—Mpango mkuu wa furahaAlma 42:15—Mpango wa rehema

(Ili kuwasaidia wanafunzi kuongeza tathmini yao kwa ufundishaji katika Kitabu cha Mor-moni, unaweza kutaja vifungu kama vile “mpango wa wokovu,” na “mpango wa uko-mbozi” vimetajwa mara kadha katika Kitabu cha Mormoni lakini sio katika Biblia.)• Je! Majina haya yanasisitiza nini kuhusu mpango wa Baba wa Mbinguni? (Hakikisha

kwamba wanafunzi wanaelewa kwamba Mpango wa Baba wa Mbinguni umeundwa ili kuleta wokovu na furaha ya milele kwa watoto Wake. )

Shuhudia kwamba hatuwezi kurudi kwenye uwepo wa Mungu na kupokea wokovu wa milele bila usaidizi wa Mungu. Waalike wanafunzi wasome Mosia 3:17 kibinafsi, wakitafuta kitu muhimu katika mpango wa wokovu. Baada ya wao kuripoti kile walichopata, acha mwanafunzi asome 2 Nefi 2:8 kwa sauti. Sisitiza kwamba Yesu Kristo ni kielezo kikuu katika mpango wa wokovu, na Upatanisho Wake ndio unaofanya mpango huu uwezekane kwa watoto wote wa Mungu. Muulize mwanafunzi asome taarifa ifuatayo ya Nabii Joseph Smith:

“Kanuni za msingi za dini yetu ni ushuhuda wa Mitume na Manabii, kuhusu Yesu Kristo, kwamba alikufa, akazikwa, na akafufuka tena siku ya tatu, na kupaa mbinguni; na mambo yote mengine ambayo yanahusiana na dini yetu ni viambatisho” Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith [2007], 49).Unaweza kueleza kwamba neno kiambatisho linamaanisha kitu au wazo linaloungana na kitu cha umuhimu mkuu, kama vile tawi ambalo ni sehemu

ya mti. Mti unaweza kuishi bila tawi, lakini tawi haliwezi kuishi kama likitenganishwa na mizizi na shina la mti. Rais Boyd K. Packer wa Akidi ya wale Mitume Kumi na Wawili anafunza kwamba fundisho la Upatanisho wa Yesu Kristo ni “mzizi halisi wa fundisho la Kikristo. Unaweza kujua sana kuhusu injili kama matawi yake yanavyochomoka, lakini kama unajua tu matawi na yale matawi ambayo hayashiki mzizi, kama yatakatwa kutoka kwa kweli hiyo, hayatakuwa na uhai wala dutu wala ukombozi ndani yake” (“The Media-tor,” Ensign, May 1977, 56).Elezea kwamba mpango wa Baba wa Mbinguni mara nyingi unaitwa mpango wa wokovu kwa sababu huhusiana na kutuokoa sisi. Kama mtu ambaye amewezesha wokovu wetu kupatikana kupitia Upatanisho, Yesu Kristo anaitwa Mwokozi.Kwenye ubao, andika Tunahitaji kuokolewa kutokana na . . .Muulize mwanafunzi asome 2 Nefi 9:6–10 kwa sauti, na kisha umuulize mwengine asome 3 Nefi 9:21–22 kwa sauti. Waulize wanafunzi wengine wote wafuatie pamoja, wakitafuta njia za kukamilisha taarifa iliopo kwenye ubao. Unaweza kushauri kwamba watie alama kwenye ugunduzi wao kwenye maandiko yao.Waulize wanafunzi washiriki kile walichopata, na waandike majibu yao ubao. Hakikisha kwamba wameelewa kwamba kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo, watu wote wataoko-lewa kutokana na kifo cha mwili. Pia sema wazi kwamba kupitia Upatanisho, tunaweza

Page 25: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

10

SoMo la 3

kuokolewa kutokana na dhambi zetu, ambapo vinginevyo ingekuwa vigumu kwetu kuishi katika uwepo wa Mungu.Soma maneno yafatayo kutoka kwa nabii Yakobo: “Ee jinsi gani ulivyo mkuu wema wa Mu-ngu wetu” (2 Nefi 9:10). “Ee jinsi gani ulivyo mkuu mpango wa Mungu wetu” 2 Nefi 9:13• Ni kwa jinsi gani maneno ya Yakobo katika 2 Nefi 9:6–10 yanaweza kutusaidia kuelewa

kwa nini yeye aliweza kufanya mshangao kama huu?• Kulingana na 2 Nefi 9:7, 9, ni nini kingefanyika kama pasingekuwa na Upatanisho?

(Miili yetu ingekufa na kamwe isifufuke tena, na roho zetu zingekuwa chini ya shetani.)Rejea sentensi ya mwisho katika maelezo ya mpango wa wokovu ambayo ulielezea hapo mapema katika somo: “Mpango huu unawezesha watu wote kuinuliwa na kuishi milele na Mungu.”• Kwa nini ni muhimu kuelewa kwamba mpango huu hufanya kuinuliwa kwetu kuweze-

kana bali si hakika? (Wakati wanafunzi wanapojibu swali hili, hakikisha kwamba wame-elewa kwamba wana haki ya kujiamulia, na uwezo wa kuchagua na kutenda wenyewe. (Kuinuliwa kwetu kunategemea kwa sehemu jinsi tutajibu kwa baraka Mungu alizotu-patia sisi.)

Andika marejeo ya maandiko yafuatayo kwenye ubao: 2 Nefi 2:25–28; 2 Nefi 31:17–20; Alma 34:15–16. Waombe wanafunzi wajifunze aya hizi kimya kimya na waorodheshe ka-tika shajara zao za kujifunza maandiko mambo haya, maandiko yanasema sharti tufanye ili tupokee yale yote Mungu anayotoa kupitia mpango Wake wa wokovu.Wanafunzi wanapokwisha pata muda wa kutosha kumaliza kazi hii, waalike waelezane majibu ya mmoja kwa mwengine. Wanapofanya hivyo, taja mifano ya utiifu kwa “Sheria, ibada, na mafundisho yaliyotolewa na Mungu” yaliyotajwa katika maelezo uliyoshiriki hapo mapema. (Mifano kutoka kwenye aya hizi inajumuisha kuwa na imani hata toba, kubatizwa, na kupokea Roho Mtakatifu.) Baada ya ripoti ya wanafunzi, fikiria kuwauliza maswali yafuatayo:• Je! Matendo yetu yanaathiri vipi uwezo wetu wa kupokea baraka za Upatanisho? (Wa-

kati wanapojibu, tafuta nafasi za kushuhudia kwamba tunapochagua kuishi injili ya Yesu Kristo na kufuata mpango wa Mungu, tunajitayarisha kupokea uzima wa milele kupitia Upatanisho wa Mwokozi.)

• Je! Kuelewa mpango wa wokovu kunaweza kutusaidia vipi kuzishika amri?Mwombe mwanafunzi asome 2 Nefi 2:25 kwa sauti.• Je! Ni kwa njia gani kufuata mpango wa wokovu kumelete shangwe kwako ?Kuhitimisha somo hili, elezea kwamba wanafunzi wanapojifunza Kitabu cha Mormoni, wataelewa mafundisho mengi sana yanayohusiana na mpango wa wokovu; somo hili limewasilisha maelezo ya jumla mafupi. Watie moyo wanapojifunza waangalie yote yale ambayo Mungu amewafanyia wao kama sehemu ya mpango Wake wa wokovu na waanga-lie yote yale wanayohitaji kufanya hili wapokee baraka kamili Mungu alizowapangia. Toa ushuhuda wako wa kweli ambazo zimezungumziwa katika somo hili.

Page 26: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

11

SOMO LA 4

Ukurasa wa jina, Utangulizi, na Ushuhuda wa Mashahidi

Mapendekezo ya KufundishaMapendekezo ya Kufundisha somo hili yanaweza kuchukua muda mrefu kufundisha kuliko muda uliopangiwa somo lako. Kwa maombi fikiria ni sehemu gani ya somo darasa lako linahitaji sana.

Ukurasa wa JinaWaalike wanafunzi kwenda kwenye Ukurasa wa jina wa Kitabu cha Mormoni. Ukurasa huu unaanza na maneno “Kitabu cha Mormoni, taarifa iliyoandikwa kwa mkono wa Mormoni juu bamba zilizotwaliwa kutoka mabamba ya Nefi.” Nabii Joseph Smith alielezea chimbuko la Ukurasa wa jina:“Ukurasa wa jina la Kitabu cha Mormoni ni tafsiri halisi, iliyotwaliwa kutoka kwa jani la mwisho kabisa, katika mkono wa kushoto wa kitabu cha mabamba, kilichokuwemo na kumbukumbu ambayo imetafsiriwa, na ukurasa huu wa jina kwa njia yoyote ile si utunzi wa kisasa, wala wangu au mtu yeyote yule ambaye ameishi au anaishi katika kizazi hiki” (katika History of the Church, 1:71).Alika wanafunzi wasome ukurasa wa jina la Kitabu cha Mormoni kimya kimya. Waulize watafute vifungu ambavyo vinatamka madhumuni ya Kitabu cha Mormoni. (Unaweza ku-wapatia wanafunzi dokezo kwamba haya madhumuni yameelezwa kama ambavyo Kitabu cha Mormoni “kitawaonyesha” wale ambao watakisoma.) Waalike wanafunzi kadha waa-ndike ugunduzi wao kwenye ubao. Wanapomaliza, waulize wanafunzi wasome tena aya ya pili wenyewe, wakiweka majina yao badala ya “sazo la Nyumba ya Israeli.”• Uliposoma Kitabu cha Mormoni, ni madhumuni gani ya kitabu hicho yametimizika

katika maisha yako? Je! Ni kwa namna gani yametimia kwako?• Je! Inasaidiaje kujua kwamba wale wanaofanya maagano na Bwana “hawatatupwa

milele”?Waambie wanafunzi kwamba kunaweza kuwa nyakati ambapo wanahisi kuwa wapweke au kuwa “wametupwa”• Kwa nini ni muhimu kujua katika nyakati hizi kwamba wewe “haujatupwa milele”?• Je! Ni kwa namna gani ahadi hii ni onyesho la upendo wa Mungu kwako?Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa madhumuni ya msingi ya Kitabu cha Mormoni, uliza mwanafunzi asome taarifa ifuatayo ya Rais Ezra Taft Benson:

“Madhumuni makuu ya Kitabu cha Mormoni, kama ilivyoandikwa katika ukurasa wake wa jina, ni ‘kuwathibitishia Myahudi na Myunani kwamba Yesu ndiye Kristo, Mungu wa milele, anayejidhihirisha kwa mataifa yote’“Mtafutaji kweli mwaminifu anaweza kupata ushuhuda kwamba Yesu ndiye Kristo kama kwa maombi atatafakari maneno ya maongozi yaliyomo katika Kitabu cha Mormoni.

UtanguliziUnapofunza Kitabu cha Mormoni, utawasaidia wana-funzi kugundua kweli ambazo zitawaleta karibu na Mungu. Kutoka mwanzo wa kitabu, ni wazi kwamba wa-andishi wa Kitabu cha Mormoni walidhamiria kushuhudia kwamba Yesu ndiye Kristo. Kitabu hiki pia kinathibitisha maagano ya Mungu na nyumba ya Israeli na kuonyesha

haja ya watoto wote wa Mungu kufanya na kushika maagano matakatifu. Wanafunzi wanapojifunza Kitabu cha Mormoni kwa maombi, watapata ushuhuda mkuu wa injili ya Yesu Kristo na Urejesho wa Kanisa Lake katika siku za mwisho. Pia watajifunza kuifanyia kazi imani kuu katika Yesu Kristo na Upatanisho Wake

Kubadili jinaKuwaalika wanafunzi wabadili majina yao we-nyewe na lile ambalo li-naonekana katika mstari wa maandiko husaidia kufanya ufundishaji wa maandiko kuwa wa ki-binafsi zaidi. Wanafunzi wanaposoma majina yao wenyewe kama sehemu ya maandiko, wanaweza kufikiria kwa urahisi sana vile fundisho na kanuni katika mstari ina-wahusu wao wenyewe.

Page 27: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

12

SoMo la 4

“Zaidi ya nusu ya aya zote katika Kitabu cha Mormoni zinamtaja Bwana wetu. Umbo fulani la jina la Kristo limetajwa sana zaidi katika mstari katika Kitabu cha Mormoni kuliko hata katika Agano Jipya.“Yeye amepatiwa zaidi ya majina mia moja tofauti katika Kitabu cha Mormoni. Majina hayo yana umuhimu maalumu katika kuelezea asili Yake takatifu” (“Come unto Christ,” Ensign, Nov. 1987, 83).Toa ushuhuda wako kwamba Kitabu cha Mormoni ni ushahidi kwamba Yesu ndiye Kristo.

Utangulizi wa Kitabu cha MormoniChora kwenye ubao picha ya tao (ona kielelezo kilichoambatishwa), au tengeneza mfano wa tao kutokana na mbao au vifaa vingine.

Mwambie mwanafunzi asome kwa sauti taarifa ya Joseph Smith katika utangulizi wa Kitabu cha Mormoni (ona aya ya sita). Unaweza kushauri kwamba wanafunzi watie alama maneno haya katika maandiko yao.• Madhumuni ya jiwe la kiungo la tao nini?Elezea kwamba jiwe la kiungo la tao ni jiwe muhimu juu ya tao. Tao linapojengwa, pande mbili hujengwa kwa mihimili ya kuzishikilia. Nafasi juu ya tao hupimwa kwa makini, na jiwe la kiungo la tao hukatwa ili lilingie barabara. Jiwe la kiungo la tao likiwekwa, tao husi-mama bila mihimili.• Je! Ni nini kitafanyika kama jiwe la kiungo la tao likitolewa? (Kama unatumia mfano,

onyesha kwa kutoa jiwe la kiungo la tao.)• Je! Kitabu cha Mormoni kinasimama vipi kama jiwe la kiungo la tao katika urejesho

wa injili?Mwalike mwanafunzi asome kwa sauti taarifa ifuatayo ya Rais Ezra Taft Benson. (Unaweza kutayarisha taarifa iliyotayarishwa na wanafunzi ili kuwekwa kwenye maandiko yao. Vingi-nevyo, unaweza kuwaalika wanafunzi kuandika taarifa ya Rais Benson kwenye maandiko yao, hapo juu au chini ya ukurasa wa kwanza wa utangulizi.)“Kuna njia tatu ambazo kwazo Kitabu cha Mormoni ni jiwe la kiungo la tao la dini yetu. Ndio jiwe la kiungo la tao katika ushahidi wetu wa Kristo. Ndio jiwe la kiungo la tao la mafundisho yetu. Ndio jiwe la kiungo la tao la ushuhuda” (“The Book of Mormon—Keys-tone of Our Religion,” Ensign, Nov. 1986, 5).Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa jinsi gani Kitabu cha Mormoni ni jiwe la kiungo la tao la ushahidi, mwalike mwanafunzi asome taarifa ifuatayo ya Rais Benson:“Kitabu cha Mormoni ni jiwe la kiungo la tao la ushuhuda. Kama vile tao itabomoka kama jiwe la kiungo la tao likiondolewa, vivyo hivyo Kanisa lote litasimama au kuanguka na ukweli wa Kitabu cha Mormoni. Kama Kitabu cha Mormoni ni kweli basi mtu sharti akubali madai ya Urejesho na yale yote yanayoambatana nacho” (“The Book of Mormon—Keystone of Our Religion,” 6).• Je! Ni kwa namna gani ushuhuda wako wa Kitabu cha Mormoni umeathiri ushuhuda

wako juu ya mafundisho na kanuni za injili?• Je! Ni kwa namna gani Kitabu cha Mormoni kimekuleta karibu na Mungu?Unaweza kuwaambia kuhusu jinsi kujifunza kwako Kitabu cha Mormoni kumeimarisha ushuhuda wako na kukuleta karibu na Mungu.

jiwe la kiungo

kwenye tao

Page 28: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

13

UKURaSa Wa j ina, UtangUliz i , na UShUhUda Wa MaShahidi

Waalike wanafunzi washiriki katika nafasi ya uigizaji. Waulize wafikirie wanampatia mtu nakala ya Kitabu cha Mormoni ambaye si muumini wa Kanisa. Wasaidie wao kutayarisha nafasi za uigizaji kwa kuwagawa katika vikundi viwili. Uliza kundi la kwanza lisome aya ya 2–4 ya utangulizi wa Kitabu cha Mormoni. Uliza kundi la pili lisome aya ya 5–8. Acha makundi yote yatafute maelezo wanayohisi yatakuwa muhimu kuelezea wanapofundisha kuhusu Kitabu cha Mormoni.Baada ya kuwapatia wanafunzi muda kujifunza na kujitayarisha, mwalike mwanafunzi aje mbele ya darasa ili kuigiza nafasi ya mtu ambaye si muumini wa Kanisa. Pia uliza mwa-nafunzi kutoka kila kikundi aje mbele ya darasa. Elezea kwamba hawa wanafunzi wawili watatenda kama wamisionari wenzi. Watatumia vifaa ambavyo vikundi viligundua katika utangulizi wa kufunza mwanafunzi wa kwanza kuhusu Kitabu cha Mormoni.Wanafunzi wanapomaliza uigizaji nafasi, unaweza kuwauliza wale wengine wa darasa kama kuna kitu cha ziada kutoka katika utangulizi ambacho wangeelezea kama wange-chaguliwa kufunza.Unaweza kutaja kwamba Kitabu cha Mormoni hakidai kutoa historia yote ya watu wa kale walioishi katika Amerika Kaskazini na Kusini. Ni kumbukumbu ya nasaba ya Lehi pekee (Wanefi na Walamani) na watu wa Yaredi. Yawezekana kuwa kulikuwa na watu wengine walioishi katika bara la Amerika Kaskazini Kusini kabla ya nyakati, na baada ya matukio katika Kitabu cha Mormoni.Waalike wanafunzi wasome Moroni 10:3–5 kimya kimya.• Kulingana na Moroni, tunaweza kujua vipi kwamba Kitabu cha Mormoni ni cha kweli?Waalike wanafunzi wasome aya ya 8–9 katika utangulizi wa Kitabu cha Mormoni. Wau-lize watambue kweli tatu za ziada ambazo kwa hizo watapata ushahidi kama watakubali changamoto ya Moroni.Washuhudie wanafunzi kwamba tunaposoma, tunapotafakari na kuomba kuhusu Kitabu cha Mormoni, Roho Mtakatifu atashuhudia kwamba ni cha kweli, kwa-mba Yesu ndiye Kristo, kwamba Joseph Smith alikuwa nabii wa Mungu, na kwa-mba Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho ni ufalme wa Bwana ulimwenguni.

Ushuhuda wa Mashahidi Watatu na Mashahidi WananeWaulize wanafunzi wafikirie kwamba wameshuhudia mtu akichukua kitu cha thamani kutoka nyumba ya jirani.• Katika kutatua jinai, kwa nini ni muhimu kuwa na shahidi?• Kwa nini itakuwa vyema kuwa na zaidi ya shahidi mmoja?Waulize wanafunzi wasome “Ushuhuda wa Mashahidi Watatu” kimya kimya. Waalike wao watafute vifungu ambavyo hasa vina maana kwao. Unaweza kushauri kwamba waweke alama kwenye vifungu hivi.• Ni vifungu gani mlitia alama? Kwa nini vina maana kwako? (Unaweza kusema kwamba

sauti ya Mungu alitangaza kwa Mashahidi Watatu kwamba mabamba haya yalitafsiriwa kwa kipawa na uwezo wa Mungu.)

Muulize mwanafunzi asome “Ushuhuda wa Mashahidi Wanane” kwa sauti. Waulize wale wengine walio darasani kusikiliza tofauti baina ya ushuhuda wa Mashahidi Watatu na Mashahidi Wanane.• Umegundua tofauti gani?Waalike wanafunzi waandike ushahidi wao wenyewe au hisia kuhusu Kitabu cha Mor-moni. Wanaweza kuandika katika shajara zao za kujifunza maandiko au kwenye ukurasa mtupu katika maandiko yao. Wanafunzi wengine wanaweza kuhisi hawajui kwamba Kitabu cha Mormoni ni kweli. Watie moyo watafute kupata ushuhuda mwaka huu.

Uigizaji- nafasiUigizaji- nafasi usaidia wanafunzi kujizoeza kutumia suluhu za injili kwa hali za kimaisha halisi. Uigizaji- nafasi utaweza kufanikiwa sana kama utawapatia washiriki maelezo na muda wa kutosha wa kujitayarisha. Wanafunzi wanapoigiza –nafasi, wanaweza kufanya makosa. Kuwa msikivu kwa hisia na mitazamo yao, na uwe mwangalifu usikashifu makosa yao. Mwisho wa uigizaji na-fasi, itasaidia kuwauliza watazamaji kama kuna mawazo mengine wa-nayoweza kuleta kama wengekuwa washiriki.

Wasaidie wanafunzi kupata ushuhuda.Njia moja ya kuwasai-dia wanafunzi kupata ushuhuda ni kuwatia moyo kuelezea hisia zao kuhusu injili kwa we-ngine, ikijumuisha wana-familia na marafiki, nje ya darasa. Rais Boyd K. Packer wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alifunza: “Ee, kama mimi ningewafunza kanuni hii moja. Ushuhuda una-weza kupatikana katika kushuhudia . . .“Ni kitu kimoja kupokea ushahidi kutoka kwa kile umesoma au kile mwengine amesema; na huu ni mwanzo muhimu. Ni kitu kingine kabisa kupata Roho kukuthibi-tishia katika moyo wako kwamba kile wewe umeshuhudia ni kweli” (“The Candle of the Lord,” Ensign, Jan. 1983, 54–55).

Page 29: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

14

Mapendekezo ya Kufundisha

Ushuhuda wa Nabii Joseph Smith Kabla ya darasa, weka Kitabu cha Mormoni katika kijisaduku na ukifunge kama zawadi. Weka zawadi hii kwenye meza mbele ya darasa, na uwaambie wanafunzi kwamba ni zawadi ya thamani.• Je! Ni zawadi gani za thamani sana ambazo umeshapokea?• Je! Ni nini kinachofanya zawadi kuwa na thamani?• Je! Unahisi vipi wakati inapotolewa zawadi unayoifikiria kuwa ya thamani na mpokeaji

kuikubali kwa shangwe?Alika mwanafunzi afungue zawadi hii na kuwaonyesha wanafunzi wengine kuna nini ndani yake.• Je! Ni nani alitupatia hii zawadi?• Je! Kwa nini unahisi hii zawadi ni ya thamani?Onyesha picha ya Moroni Akimtokezea Joseph Smith katika Chumba Chake (62492; Go-spel Art Book [2009], no. 91).• Je! Ni tukio gani linaloonyeshwa katika picha hii?• Je! Tukio hili lilichangia vipi kwa Urejesho wa injili?Waelezee wanafunzi kwamba sasa watasoma maneno ya Nabii Joseph Smith mwenyewe kuhusu kuja kwa Kitabu cha Mormoni. Waambie kwamba ushuhuda wa Nabii Joseph Smith ambao unaonekana hapo mwanzoni mwa Kitabu cha Mormoni ulitwaliwa kutoka katika Historia ya—Joseph Smith katika Lulu ya Thamani Kuu. Wanafunzi wanapokamili-sha shughuli ifuatayo, acha wasome kutoka katika Lulu ya Thamani Kuu.Wapange wanafunzi kufanya kazi kwa jozi. Alika mwanafunzi mmoja katika kila jozi asome Historia ya—Joseph Smith 1:30, 32–35, 42 kimya. Muulize mwanafunzi katika kila jozi asome Historia ya—Joseph Smith 1:51–54, 59–60 kimya kimya. Elezea kwamba wanapoma-liza kusoma, kila mwenzi anapaswa kufundisha mwenziwe kuhusu kile walichosoma.Baada ya wanafunzi kuwa na muda wa kutosha wa kusoma na kujadiliana, waulize.• Je! Unadhani ni kwa namna gani Joseph Smith alisaidiwa kwa kusubiri miaka minne

kabla ya kutwaa mabamba ya dhahabu nyumbani? (Muda huu Joseph Smith alipokuwa akifundishwa na Moroni, ndio wakati ambao yeye aliimarishwa katika njia nyingi. Ona Historia ya—Joseph Smith 1:14- - 19.)

• Katika maelezo ya Joseph Smith, ni ushahidi gani unaona kwamba Bwana alikihifadhi Kitabu cha Mormoni kije kutokeza katika siku za mwisho?

• Katika maelezo ya Joseph Smith, ni ushahidi gani unaona kwamba Kitabu cha Mor-moni kimekuja kwa uwezo wa Mungu?

UtanguliziSomo linatoa maelezo ya jumla ya Kitabu cha Mor-moni. Wanafunzi watajifunza ushuhuda wa Joseph Smith kuhusu kutokeza kwa Kitabu cha Mormoni. Pia watajifunza jinsi kitabu kilivyotungwa na kufupishwa

chini ya maelekezo matakatifu. Waandishi wa Kitabu cha Mormoni waliona siku za mwisho, na wakajumui-sha matukio na mafunzo waliyojua kuwa yatakuwa na manufaa mengi kwetu sisi.

Toa maelezo ya jumlaRais Boyd K. Packer wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alisema: “Kuna thamani kubwa katika kuwasilisha muhtasari lakini maelezo yaliyotengenezwa kwa makini sana ya kozi yote hapo mwanzo kabisa. . . .“. . . [Wanafunzi] huku-mbuka mambo mengi wanapojua ni jinsi gani vipande vyote vinaunga-nika pamoja, na nuru ya kujifunza huangaza kwa uangavu sana. Uchambuzi hujenga muundo na una thamani kushinda muda na kazi inayotendeka” (“The Great Plan of Happiness” [Kongamano la MEK juu ya Mafundisho na Maagano/Historia ya Kanisa, Aug. 10, 1993], 2, si.lds.org).

SOMO LA 5

Maelezo ya jumla ya Kitabu cha Mormoni

Page 30: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

15

Maelezo ya jUMla ya KitabU cha MoRMoni

Maelezo Mafupi kuhusu Kitabu cha MormoniIli kuwasaidia wanafunzi kuelewa jinsi Kitabu cha Mormoni kilivyotungwa, acha waende kwenye “Maelezo Mafupi kuhusu Kitabu cha Mormoni” katika kurasa za utangulizi wa Kitabu cha Mormoni. Waalike wanafunzi wanne wachukue zamu kusoma sehemu ya 1–4 kwa sauti. Wanaposoma, acha wengine wasikilize njia ambazo kila fungu la mabamba ni muhimu kwa Kitabu cha Mormoni. Kiambatisho cha kitabu cha mwongozo hiki kina mchoro kwa jina “Mabamba na Uhusiano Wake katika Uchapishaji wa Kitabu cha Mor-moni.” Mchoro huu unaweza kuwasaidia wanafunzi kupata taswira ya mabamba yajadili-wayo katika “Maelezo Mafupi kuhusu Kitabu cha Mormoni.” (Kama unahisi kutakuwa na usaidizi kama sehemu ya majadiliano haya, taja aya ya mwisho ya maelezo mafupi, kuanzia na maneno “Kuhusu hili toleo.” Elezea kwamba katika toleo la Kitabu cha Mormoni ku-mekuwa na marekebisho kidogo ya makosa ya tahajia za maneno na chapa.)Onyesha picha ya Mormoni akifupisha Mabamba (62520; Gospel Art Book, no. 73). Elezea kwamba watu wengi wamehifadhi kumbukumbu ambazo hatimaye zikawa Kitabu cha Mormoni. Andika mitajo ya maandiko ifuatayo kwenye ubao. Waulize wanafunzi waisome kimya; wakitafuta kati ya kanuni ambazo zilisaidia waandishi wa Kitabu cha Mormoni kuamua kile watajumuisha katika hizi kumbukumbu zao. Waalike wanafunzi waeleze kile walichokipata. (Unaweza kuandika majibu yao kwenye ubao,)

1 Nefi 1:201 Nefi 6:4–62 Nefi 4:15 2 Nefi 25:23, 26.

2 Nefi 29:11–13Maneno ya Mormoni 1:4–83 Nefi 16:4Moroni 1:4

• Je! Kuelewa hizi kanuni za mwongozo zinawezaje kukusaidia unapojifunza Kitabu cha Mormoni?

Toa ushuhuda wako kwamba waandishi wa Kitabu cha Mormoni waliona siku zetu na wakaandika kile ambacho kingekuwa cha msaada kwetu. Alika mwanafunzi asome Mormoni 8:35–38 kwa sauti.• Je! Ni shida gani Moroni aliona miongoni mwa watu wa siku zetu?• Kwa nini ni muhimu kujua kwamba Moroni na waandishi wengine wa Kitabu cha Mor-

moni walijua shida ambazo zitatukabili?Alika mwanafunzi asome taarifa ifuatayo ya Rais Ezra Taft Benson kuhusu jinsi ya kujifunza Kitabu cha Mormoni

“Kama waliona siku zetu, na wakachagua mambo yale ambayo yangekuwa ya thamani kuu kwetu, je, hiyo siyo sababu sisi tunapaswa kujifunza Kitabu cha Mormoni? Tunapaswa kujuliza wenyewe kila mara, Kwa nini Bwana alimpatia maongozi Mormoni (au Moroni au Alma) kujumuisha hayo katika kumbukumbu zake? Ni somo gani nimejifunza kutokana na hayo ambacho chaweza kunisaidia kuishi siku hii na nyakati hizi?” (“The Book of Mor-

mon—Keystone of Our Religion,” Ensign, Nov. 1986, 6).Waambie wanafunzi kwamba watu walioandikwa katika Kitabu cha Mormoni walikabiliwa na shida sawa sawa na zetu. Ingawa Kitabu cha Mormoni ni nyaraka za kale, mafundisho yake, historia yake na hadithi zake ni vya thamani kuu leo.Mwombe mwanafunzi asome kwa sauti taarifa ifuatayo ya Rais Ezra Taft Benson. (Unaweza kumpatia kila mwanfunzi nakala ya hii taarifa.) Acha darasa lisikilize baraka ambazo Rais Benson aliahidi kwa wale ambao wataanza kujifunza Kitabu cha Mormoni kwa bidii.“Sio tu kwamba Kitabu cha Mormoni hutufunza sisi kweli, ingawaje kwa kweli hufanya hivyo. Sio tu kwamba Kitabu cha Mormoni hushuhudia juu ya Kristo, ingawaje kwa kweli hufanya hivyo, pia. Lakini kuna kitu zaidi ya hivyo. Kuna uwezo katika kitabu hiki ambao utatiririka katika maisha yako wakati utakapoanza kujifunza kitabu hiki kwa bidii. Utapata uwezo mkuu wa kushinda majaribu. Utapata uwezo wa kuepuka kudanganywa. Utapata uwezo wa kukaa katika njia iliyosonga na nyembamba. Maandiko yanaitwa ‘maneno ya uzima’(ona M&M 84:85), na hakuna popote palipo na kweli nyingi kuliko ilivyo katika Kitabu cha Mormoni. Utakapoanza kuwa na njaa na kiu ya maneno haya, utapata uzima kwa wingi zaidi” (“The Book of Mormon—Keystone of Our Religion,” 7).

Page 31: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

16

SoMo la 5

• Je! Ni kwa jinsi gani ulipata baraka kutokana na kujifunza Kitabu cha Mormoni?Toa ushuhuda wako kwamba Kitabu cha Mormoni hutupatia uwezo mkuu wa kushi-nda majaribu, kuepuka kudanganywa, na kukaa katika njia iliyosonga na nyemba-mba. Waambie wanafunzi kuhusu wakati wewe ulipopokea hizi baraka kama matokeo ya kujifunza Kitabu cha Mormoni.Kabla ya darasa, andika orodha ifuatayo ya maswali na maandiko kwenye ubao:

Je! Kuna Mungu? (Ona Alma 30:37–44.) Je! Naweza kumjua Mungu? (Ona Alma 22:18.) Je! Mungu ananijali mimi? (Ona 3 Nefi 13:26–32.)Je! Nawezaje kushinda majaribu na dhambi? (Ona Helamani 5:12.)Je! Madhumuni ya maisha ni nini? (Ona Alma 34:32–34.)Je! Kuna maisha baada ya kifo? (Ona Alma 40:11–12, 21–23.)Je! Ninawezaje kupata amani na shangwe na niwe na furaha? (Ona Mosia 2:41; 4:2–3; Alma 41:10.)Je! Familia inawezaje kuwa na furaha zaidi na kuwa imeungana? (Ona Mosia 4:14–15.)Je! Naweza vipi kuhukumu kati ya kosa na sahihi? (Ona Moroni 7:16–17.)Je! Kwa nini Mungu hukubali uovu na mateso yatokee? (Ona 2 Nefi 2:1–2, 11–16, 22–27; Alma 14:9–11; 60:13.)

Elezea kwamba kama ziada ya baraka zilizotajwa tayari, Kitabu cha Mormoni kina majibu ya maswali muhimu sana ya maisha. Alika wanafunzi kila mmoja achague swali moja au mawili na wapekue mistari ya maandiko inayoambatana na majibu. Wa-patie dakika chache watafute majibu. Unaweza kuzunguka darasani, ukitoa usaidizi jinsi unavyohitajika.• Je! Ni kwa namna gani Kitabu cha Mormoni kinajibu maswali uliyochagua?Soma taarifa ifuatayo ya Rais Boyd K Packer wa Akidi ya wale Mitume Kumi na Wawili. Wakati akitoa hii taarifa, alikuwa anaongea na walimu wa seminari na chuo kuhusu uwezo wa maandiko katika majibu ya maswali muhimu ya maisha.“Kadiri wanafunzi wako wanavyozidi kujielimisha na ufunuo, hakuna swali—la kibinasfi au kijamii au kisiasa au ajira—ambalo linakosa kujibiwa. Hapa kuna utimilivu wa injili ya milele. Hapa tutapata kanuni za kweli ambazo zitatatua kila mkanganyiko na kila shida na kila utata ambao unaikabili familia ya binadamu au mtu binafsi” (“Teach the Scriptures” [hotuba kwa wanaelimu wa dini wa MEK, Oct. 14, 1977], 3–4, si.lds.org).Elezea jinsi Kitabu cha Mormoni kimebariki maisha yako. Kumbuka wanafunzi wana malengo ya kusoma Kitabu cha Mormoni kila siku na kusoma Kitabu cha Mormoni chote angalau mara moja mwaka huu.

Kabla ya darasa kuanzaKama inawezekana, chukua muda utayarishe chumba kabla ya darasa kuanza. Onyesha mstari wa maandiko, maswali, na shughuli zingine kwe-nye ubao kabla darasa kuanza. Hii itakusaidia kuokoa muda muhimu wa kufunza na kuondoa vivutio ambavyo vina-weza kuharibu mcha-kato wa kufundisha na kujifunza.

Page 32: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

17

Maelezo ya jUMla ya KitabU cha MoRMoni

Tangazo na Habari za UsuliMaelezo Mafupi kuhusu Kitabu cha Mormoni. “Kuhusu hili toleo”Kuna miswada miwili ya Kitabu cha Mormoni: mswada wa asili na mswada wa mpiga chapa. Sehemu ndogo ya chapa kwa toleo la 1830 la Kitabu cha Mormoni ilitolewa kutoka katika mswada wa asili, na mwingine ulitolewa kutoka katika mswada wa mpiga chapa, ambao ulikuwa nakala ya mswada wa asili. Wakati Joseph Smith akita-yarisha toleo la 1840 la Kitabu cha Mormoni, alitumia mswada wa asili ili kurekebisha makosa na ufutaji kwa bahati mbaya katika toleo la 1830. Kwa toleo la 1981, mswada wa asili ulitumika tena kurejesha maneno ya asili katika karibu sehemu 20. Makosa yoyote katika Kitabu cha Mormoni ni makosa ya binadamu, na maba-diliko yalifanywa tu ili kurejesha Kitabu cha Mormoni katika maana na dhamira yake ya asili. (Ona Book of Mormon Reference Companion, ed. Dennis Largey [2003], 124–25.)

Rais Joseph Fielding Smith aliandika:

Kuna uwezakano wa kuwa na makosa ya chapa katika toleo la kwanza [la Kitabu cha Mormoni], na labda

kuondolewa kwa neno moja au mawili. Wale ambao wamechapisha vitabu katika mazingira makini na ya kufana, wamepata, cha kuhuzinisha, makosa, ya chapa na ya mitambo, mengine ambayo hutokea baada ya ukaguzi na masahihisho ya mwisho vimeshafanyika.

 Ukaguzi makini wa orodha ya mabadiliko huonyesha hakuna mabadiliko moja au la ziada ambalo halina uwiano na maandishi ya asili. Mabadiliko yamefanywa ya kuweka vituo na mambo mengine madogo machache ambayo yalihitaji masahihisho, lakini kamwe hamna ma-geuzi wala nyongeza yoyote inayobadilisha wazo. Kama inavyoonekana kwetu, mabadiliko yapo vile kwamba yanafanya maandishi kuwa wazi kabisa na huonyesha kwamba yalikuwa yamesahaulika. Ni hakika kwamba makosa au yaliyorukwa katika toleo la kwanza yalikuwa kwa kiasi kikubwa makosa ya mpanga herufi au mpiga chapa. Mengi ya makosa haya ambayo yalikuwa katika uhakiki wa kwanza yaligunduliwa na Nabii Joseph Smith mwenyewe, na yeye akafanya masahihisho hayo” (Answers to Gospel Questions, comp. Joseph Fielding Smith Jr., 5 vols. [1957–66], 2:199–200; mlazo katika asili).

Page 33: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

18

Somo la Kujifunza NyumbaniKujifunza Maandiko–Maelezo ya Jumla ya Kitabu cha Mormoni

(Kitengo cha 1)

Vifaa vya Matayarisho kwa Mwalimu wa Kujifunza NyumbaniMuhtasari wa Masomo ya Kujifunza Nyumbani Kila SikuUfuatao ni muhtasari wa matukio, mafundisho, na kanuni wanafunzi walijifunza walipomaliza masomo manne ya kujifunza- nyumbani ya mwanafunzi ya kitengo cha 1. Kujua kile wanafunzi wamekuwa wakijifunza kutakusaidia kujitaya-risha kwa ajili ya darasa lako. Muhtasari si sehemu ya somo na haitarajiwi kutolewa kwa wanafunzi. Kwa sababu somo unalofundisha kwa kitengo 1 linaelezea tu mafundisho na ka-nuni hizi chache, unaweza wakati mwingine kuhisi kuvutiwa kurejea au kujadili mengine kulingana na msukumo wa Roho na mahitaji ya wanafunzi wako.

Siku ya 1 (Kujifunza Maandiko)Wanafunzi walijifunza ujuzi wa kuwasaidia kuelewa usuli na mazingira ya maandiko, jinsi ya kujifunza na kutambua kweli za injili, na jinsi ya matumizi ya mafundisho na kanuni za injili katika maisha yao.

Siku ya 2 (Mpango wa Wokovu)Somo hili lilikuwa ni maelezo mafupi ya mpango wa wo-kovu. Kitabu cha Mormoni hufunza kwamba mpango wa Baba wa Mbinguni umeundwa ili kuwaletea watoto Wake wokovu wa milele na furaha. Yesu Kristo ni mtu muhimu katika mpango wa wokovu, na Upatanisho Wake ndio unaofanya mpango utendeke kwa watoto wote wa Mungu. Tunapochagua kufuata mpango wa Mungu, tunajitayarisha kupokea uzima wa milele.

Siku ya 3 (Ukurasa wa Jina, Utangulizi, na Ushuhuda wa Mashahidi)Vifaa vya utangulizi kwa Kitabu cha Mormoni husaidia kuti-miza madhumuni yake na kuelezea ukweli wake na asili yake takatifu. Ukurasa wa jina hufunza kwamba Kitabu cha Mor-moni ni ushahidi kwamba Yesu ndiye Kristo. Tunaposoma, tunapotafakari, na kuomba juu ya Kitabu cha Maandiko, Roho Mtakatifu atashuhudia kwamba ni kweli, kwamba Yesu ndiye Kristo, kwamba Joseph Smith alikuwa nabii wa Mungu, na kwamba Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho ni ufalme wa Bwana ulimwenguni.

Siku ya 4 (Maelezo ya Jumla ya Kitabu cha Mormoni)Ushuhuda wa Nabii Joseph Smith uliwasaidia wanafunzi kuimarisha ushuhuda wao kwamba Kitabu cha Mormoni kimekuja kwa nguvu na uwezo wa Mungu. Bwana alihifadhi Kitabu cha Mormoni ili kije katika siku za mwisho. Waandishi wa Kitabu cha Mormoni waliona siku zetu na kuandika kile kingekuwa cha msaada kwetu. Wanafunzi walitiwa moyo kufikiria maswali waliyonayo na watafute majibu wanapoji-funza Kitabu cha Mormoni.

UtanguliziHili somo la wiki hii linatilia mkazo jukumu la kila mwanafunzi alilonalo la kujifunza injili. Pia linatia mkazo nafasi muhimu ya Kitabu cha Mormoni katika kuwasaidia wanafunzi kujenga ushuhuda wa Yesu Kristo na Kanisa Lake. Unapofunza, wasaidie wanafunzi kuelewa umuhimu wa kujifunza kitabu cha maandiko hiki kitakatifu kwa bidii na baraka ambazo zitajaza maisha yao wanapofanya hivyo.

Mapendekezo ya Kufundisha

Kujifunza MaandikoUnaweza kuanza kwa kuuliza wanafunzi maswali yafuatayo:

• Ni nini tofauti kati ya mtu ambaye husoma Kitabu cha Mor-moni na kupokea ushuhuda na mtu ambaye hukisoma na hapokei ushuhuda? (Watu fulani husoma maneno; wengine husoma kwa imani, kwa dhamira halisi, na kwa moyo wao mkunjufu na kwa Roho Mtakatifu.)

• Je! Mtu hujifunza vipi kweli za kiroho? (Fikiria kuorodhesha majibu ya wanafunzi katika ubao. Rejea tena kwenye orodha hii baada ya kusoma taarifa ya Mzee David A. Bednar hapo chini.)

Andika taarifa ifuatayo kwenye ubao, ukiacha maneno yaliyopi-gwa mstari: “Tafuta kuelimika, hata kwa kujifunza na pia kwa imani.”

Rejea yale ambayo wanafunzi wamejifunza wiki hii kwa kuwaa-lika wao wajaze mianya. Kama unahitaji usaidizi, acha wasome Mafundisho na Maagano 88:118. Waulize wao inamaanisha nini kutafuta kuelimika kwa kujifunza na kwa imani. Mnapojadiliana haya, hakikisha wanaelewa kwamba kuelimika kwa kujifunza na kwa imani kunahitaji juhudi za kibinafsi.

Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa kwa nini juhudi na matendo yanahitajika katika kujifunza injili, acha mwanafunzi asome ma-elezo yafuatayo ya Mzee David A. Bednar wa Akidi ya Mitume

Page 34: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

19

SoMo la KUj ifUnza nyUMbani

Kumi na Wawili. Waalike wanafunzi wasikilize kile kinachote-ndeka wakati tunaweka juhudi katika kujifunza kiroho.

“Mwanafunzi anayetumia haki ya kujiamulia kwa kutenda kulingana na kanuni sahihi huufungua moyo wake kwa Roho Mtakatifu na hualika mafundisho Yake, uwezo ushuhudiao, na ushahidi uthibitishao. Kujifunza kwa imani kunahitaji kujikaza kiroho, kiakili, na kimwili na sio upokeaji baridi’ (“Seek Learning by Faith,” Ensign, Sept. 2007, 64).

Waulize wanafunzi: Ni nini alichosema Mzee Bednar kitatendeka kwa mwanafunzi ambaye hufanya juhudi katika kujifunza kiroho?

Waalike wanafunzi waelezee uzoefu waliopata wakati walipofa-nya juhudi maalum za kiroho na walivyohisi ongezeko la uwenzi wa Roho Mtakatifu kama matokeo. Unaweza kuongezea ushu-huda wako kwamba juhudi zetu katika kujifunza injili kwa maombi zitamwalika Roho Mtakatifu katika mchakato wa kujifunza.

Waulize wanafunzi: “Ni mambo gani maalum unayoweza kufanya mwaka huu ili “kutafuta kuelimika kwa kujifunza na pia kwa imani”?

Mpango wa WokovuRejea majina tofauti ya mpango wa wokovu kwa kuwauliza wanafunzi waandike kwenye ubao majina yaliyoandikwa katika shajara zao za kujifunza maandiko kwa kazi ya 1 ya somo la siku ya 2. Kama wanahitaji usaidizi, acha waende kwenye ukurasa sahihi katika vitabu vyao vya mwongozo wa kujifunza.

Unaweza kuuliza: Majina haya yanakufunza nini kuhusu madhumuni ya mpango wa wokovu? (Mpango wa Baba wa Mbinguni umeundwa ili kuleta wokovu na furaha ya milele kwa watoto Wake.)

Elezea kwamba kutakuwa na nafasi nyingi mwaka wote za kujifunza kweli tulizojifunza kutoka katika Kitabu cha Mormoni kuingiana na mpango wa furaha wa Baba wa Mbinguni. Una-weza kuwauliza wanafunzi watafute na kutia alama maandiko yao kanuni zinazohusiana na mpango wa wokovu wanapo-jifunza mwaka huu. Fikiria kutoa mifano michache ya kile wanachoweza kupata wanapojifunza. Watie moyo wanafunzi washirikiane ugunduzi wao na darasa mwaka huu.

Ukurasa wa Jina, Utangulizi, na Ushuhuda wa MashahidiWaalike wanafunzi washiriki katika uigizaji nafasi kwa kufikiria wanampatia mtu nakala ya Kitabu cha Mormoni ambaye si muumini wa Kanisa.

Gawa darasa katika makundi mawili, na acha kila kundi lijitaya-rishe kwa uigizaji nafasi kwa kujadiliana maswali yaliyotolewa kwa kundi lao. Inaweza kusaidia kuandika maswali kwenye ubao kabla ya darasa au umpatie kila mwanafunzi nakala ya maswali. Watie moyo wanafunzi watafute na kutia alama maelezo wana-yohisi yanaweza kuwa muhimu kushirikiana wakati wa kujifunza kuhusu Kitabu cha Mormoni.

Maswali kwa Kundi la 1: 1. Kitabu cha Mormoni ni nini? (Ona Utangulizi, aya ya 1–3.) 2. Madhumuni ya Kitabu cha Mormoni ni nini? (Ona ukurasa

wa jina, aya ya 2.) 3. Je! Ni baraka gani zinazokuja kutokana na kuishi kwa maa-

dili au kanuni ambazo Kitabu cha Mormoni hufunza? (Ona utangulizi, aya ya 6.)

Maswali ya Kundi la 2: 1. Je! Kitabu cha Mormoni kilitokea vipi? (Ona utangulizi, aya

ya 4–5.) 2. Je! Unawezaje kujua kama Kitabu cha Mormoni ni cha

kweli? (Ona Utangulizi, aya ya 8.) 3. Je! Ni nini kingine tunachoweza kujua kwa uwezo wa

Roho Mtakatifu? (Ona utangulizi, aya ya mwisho.)Baada ya kuwapatia wanafunzi muda wa kutayarisha, chagua mwanafunzi mmoja kumwakilisha mtu mmoja ambaye sio muumini wa Kanisa. Uliza mtu wa kujitolea kutoka katika kila kundi kumzawadia mtu yule na Kitabu cha Mormoni. Watie moyo wanafunzi watumie majibu ya maswali ya makundi yao waliojifunza ili kumfundisha mwanafunzi wa kwanza kuhusu Kitabu cha Mormoni.

Wanapomaliza uigizaji nafasi, fikiria kuuliza wengine walio darasani ni maelezo gani ya ziada wangeweza kueleza kama wao wangekuwa ndio mtu anayezawadiana nakala ya Kitabu cha Mormoni. Unaweza pia kuuliza: Ni nini walichojifunza au kukumbuka kuhusu Kitabu cha Mormoni katika shughuli hii?

Wanafunzi wanapojibu, hakikisha wameelewa kwamba Kitabu cha Mormoni ni ushuhuda kwamba Yesu ndiye Kristo. Tilia mkazo umuhimu wa kuzingatia jinsi Kitabu cha Mormoni hum-shuhudia Yesu Kristo. Kwa ziada, elezea kwamba kujifunza Kitabu cha Mormoni kitawasaidia kuelewa mafundisho na kanuni za injili ya Yesu Kristo na kuimarisha ushuhuda wao juu ya Kanisa Lake.

Wakumbushe wanafunzi kwamba waandishi wa Kitabu cha Mormoni waliona siku zetu na wakaandika kile ambacho kingekuwa na usaidizi mwingi kwetu (ona Mormoni 8:35).

Waulize wanafunzi: Ni nini mlichojifunza wiki hii ambacho kitaa-thiri jinsi unavyojifunza Kitabu cha Mormoni?

Waalike wanafunzi fulani waelezee jinsi wanavyopanga kukamili-sha jukumu lao la kusoma Kitabu cha Mormoni wakati wa shule mwaka huu. Hitimisha kwa kuelezea hisia zako na ushuhuda wako kuhusu Kitabu cha Mormoni na jinsi gani kukisoma huko kimeathiri maisha yako.

Kitengo kifuatacho (1 Nefi 1–6, 9)Waulize wanafunzi kama wameshapata kujua kitu ni sahihi lakini kukifanya kionekane ni vigumu au hata hakiwezekani. Elezea kwamba katika wiki ifuatayo watagundua kwamba Nefi alikabiliana na changamoto ya aina hii, na watajifunza jinsi yeye alivyo mtegemea Mungu na kukamilisha kile kilichoonekana hakiwezekani.

Page 35: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

20

UtangUlizi Wa

Kitabu cha Kwanza cha nefiKwa nini ujifunze kitabu hiki?Wanafunzi wanapojifunza 1 Nefi, wata-gundua kwamba “huruma nyororo [ya Bwana] iko juu ya wale ambao ame-wachagua, kwa sababu ya imani yao, kuwatia nguvu hata kwenye uwezo wa ukombozi”(1 Nefi 1:20). Pia watajifunza kwamba Mungu ana hamu ya kuba-riki watoto Wake. Lehi na watu wake walipata uzoefu wa huruma na baraka za Mungu walipofuata amri Zake. Lehi na Nefi walitafuta mwongozo kutoka kwa Mungu na kuupokea kupitia ndoto, maono, Liahona, na mwongozo wa Roho Mtakatifu. Nefi alipokea na kuandika ono pana la historia ya ulimwengu ambalo lili-mwonyesha maarifa yote ya Mungu; uba-tizo, huduma, na kusulubiwa kwa Yesu Kristo; maangamizo ya Nefi; na siku za mwisho. Mungu alimsaidia Nefi na ndugu zake kupata mabamba ya shaba ili wapate kuwa na maandiko. Yeye pia alimuokoa Lehi na watu wake kutokana na baa la njaa huko nyikani na maangamizi huko baharini, akawapeleka salama kwenye nchi ya ahadi. Wanafunzi wanapojifunza uzoefu wa Nefi na Lehi katika kitabu hiki, wanaweza kujifundisha jinsi ya kutafuta na kupokea baraka za mbinguni.

Nani aliandika kitabu hiki?Nefi mwana wa Lehi aliandika kitabu hiki kama jibu la amri ya Bwana kwamba yeye aweke kumbukumbu ya watu wake. Nefi kuna uwezekano alizaliwa Yerusalemu au karibu na hapo. Aliishi huko wakati wa huduma ya nabii Yeremia na enzi ya Mfalme Zedekia. Nefi alitafuta ushuhuda wake mwenyewe kuhusu maneno ya baba yake kuhusu maangamizo ya Yerusa-lemu na haja ya familia yao ya kuondoka. Alipoendelea kutafuta na kufuata ushauri wa Bwana, Nefi akawa chombo katika mikono ya Mungu. Yeye kwa utiifu alirudi Yerusalemu na ndugu zake mara mbili—kwanza kutafuta mabamba ya shaba na baadaye kushawishi familia ya Ishmaili iji-unge na familia ya Lehi huko nyikani. Kwa usaidizi wa Bwana, Nefi alijenga merikebu ambayo ilibeba familia yake na wengine kuvuka bahari hadi nchi ya ahadi. Lehi alipokufa, Bwana alimchagua Nefi kuwa kiongozi wa watu wake.

Hiki kitabu wameandikiwa kina nani na kwa nini?Nefi aliandika akiwa na makundi matatu akilini; uzao wa baba yake, watu wa agano wa Bwana katika siku za mwisho, na watu wote katika ulimwengu (ona 2 Nefi 33:3, 13). Aliandika ili kuwashawi-shi watu wote waje kwa Yesu Kristo na kuokolewa (ona 1 Nefi 6:4).

Kiliandikwa lini na wapi?Nefi aliandika taarifa ambayo ilikuja kuwa 1 Nefi karibu na mwaka wa 570 K.K.—miaka 30 baada ya yeye na familia kuondoka Yerusalemu (ona 2 Nefi 5:30). Alikiandika alipokuwa katika nchi ya Nefi.

Ni zipi kati ya sifa bainishi za kitabu hiki?1 Nefi ina taarifa kadhaa za maonyesho matakatifu katika ndoto, maono, na funuo za moja kwa moja. Maonyesho haya yanaonyesha kwamba Mungu hufunza, huongoza, na kulinda wale wanaomtafuta Yeye:

• Lehi alipokuwa akiomba, nguzo ya moto ilitokeza, na yeye aliona na kusi-kia mambo mengi ambayo yalimfanya yeye kutetemeka (ona 1 Nefi 1:6–7).

• Lehi alipokea ono ambalo kwalo alimwona Mungu na kusoma kutoka ki-tabu ambacho unabii wa maangamizo ya Yerusalemu na kutekwa kwa wakazi wake (ona 1 Nefi 1:8–14).

• Bwana alimwamuru Lehi aondoke pamoja na familia yake kwenda nyikani (ona 1 Nefi 2:1–2).

• Bwana alimwelekeza Lehi kuwatuma wanawe kurudi Yerusalemu kwa ajili ya yale mabamba ya shaba (ona 1 Nefi 3:2–4).

• Malaika aliingillia kati wakati Lamani na Lemueli walipokuwa wakimpiga Nefi na Samu (ona 1 Nefi 3:29).

• Bwana alimwamuru Nefi na nduguze kurudi Yerusalemu kuwachukua Ishmaili na familia yake (ona 1 Nefi 7:1–2).

• Lehi na Nefi walipokea ono ambalo lilikuwa na mti wa uzima; kuzaliwa, hu-duma, na Upatanisho wa Yesu Kristo;

historia ya nchi ya ahadi; Urejesho wa injili; na mapambano kati ya majeshi ya shetani na kanisa la Mwana Kondoo wa Mungu (ona 1 Nefi 8;11–14).

• Nefi alionyeshwa jinsi ya kujenga meri-kebu ambayo ingewabeba watu wake hadi nchi ya ahadi (ona 1 Nefi 18:1).

1 Nefi ina taarifa za kibinafsi za watu ambao walisafiri hadi nchi ya ahadi. Kitabu cha Mormoni baadaye kinataja makundi mawili mengine ambayo yalisafiri hadi nchi ya ahadi; Wamuleki (ona Omni 1:14–17) na Wayaredi (see Etheri 6:4–12).Kitabu cha 1 Nefi pia kinatambulisha vitu viwili muhimu: upanga wa Labani na dira, au kielekezi, kinachoitwa Liahona (ona 1 Nefi 18:12; Alma 37:38). Kupitia Liahona, Bwana aliongoza familia ya Lehi kote nyikani na kuvuka bahari. Upanga wa Labani ulikabidhiwa kupitia vizazi hadi mwisho wa ustaarabu wa Wanefi. Liahona na upanga wa Labani vyote vilizikwa pamoja na mabamba ya dhahabu, na vilionyeshwa kwa Joseph Smith na wale Mashahidi Watatu (ona M&M 17:1–2).

Muhtasari1 Nefi 1–7 Lehi anaongoza familia yake kuingia nyikani. Wanawe wanatii amri za Bwana za kurudi Yerusalemu na kuchukua maba-mba na kurudi tena kumshawishi Ishmaili na familia yake ajiunge na wao huko nyikani.

1 Nefi 8–15 Lehi na Nefi kila mmoja alipokea ono la mti wa uzima. Nefi ana rejea ono lake la huduma na matukio ya kihis-toria ya Mwokozi hata kufikia Urejesho wa injili katika siku za mwisho.

1 Nefi 16–18 Bwana anamwo-ngoza Lehi na familia yake katika safari yao kupitia nyikani na ku-vuka bahari hadi nchi ya ahadi.

1 Nefi 19–22 Nefi anatoa unabii juu ya Yesu Kristo na kutawa-nyika na kukusanyika kwa Israeli.

Page 36: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

21

SOMO LA 6

1 nefi 1

Mapendekezo ya Kufundisha

1 Nefi 1:1–3Nefi anaanza kumbukumbu yakeWaalike wanafunzi wasome 1 Nefi 1:1–3 kimya kimya. Waulize wao kutambua ni kwa nini Nefi aliandika kumbukumbu yake.• Ni sababu zipi Nefi alizotoa za kutengeneza kumbukumbu ya uzoefu wake?• Unafikiria Nefi alihisi kuwa alikuwa “amependelewa na Bwana” hata kama yeye alikuwa

na uzoefu wa “mateso mengi”?

1 Nefi 1:4–2Lehi alipokea ono na anawaonya watu kwamba Yerusalemu itaangamizwaWaulize wanafunzi kufikiria wakati wazazi wao walipowaonya wao juu ya hatari.• Kwa nini wazazi wenu waliwaonya juu ya hatari?• Ni kwa njia gani Baba wa Mbinguni huwaonya watoto Wake?Elezea kwamba taarifa ya kwanza katika Kitabu cha Mormoni ilianza wakati watu wengi katika Yerusalemu walipokuwa waovu. Alika mwanafunzi asome 1 Nefi 1:4. Uliza darasa litafute njia ambayo kwayo Bwana aliwaonya watu katika Yerusalemu.Elezea kwamba baba ya Nefi, Lehi, alijiunga na “manabii wengi” waliotajwa katika mstari huu. Aliwaonya watu kwamba sharti watubu. Ili kuwasaidia wanafunzi kugundua mao-nyo na mafundisho ya Lehi, wapange wanafunzi katika jozi na acha kila jozi isome 1 Nefi 1:5–13. Waulize wao watambue kile Lehi aliona katika ono, aidha kwa kuweka alama maandiko yao au kutengeneza orodha katika karatasi. Toa kwa kila jozi muda mchache wa kujadili swali lifuatalo. (Unaweza kuandika swali hili kwenye ubao.)• Wewe ungehisi vipi kama wewe ungeona katika ono kwamba mji wako utaangamizwa?Kufuatia shughuli hii, waalike wanafunzi kimya kimya kupitia kwa haraka 1 Nefi 1:15, wakitafuta hisia za Lehi baada ya ono hili.• Lehi alifanya nini juu ya vitu alivyoona?Muulize mwanafunzi asome 1 Nefi 1:14–15 kwa sauti. Tia darasa moyo litafute sababu za kwa nini Lehi alifurahia. (Unaweza kuhitaji kuelezea kwamba hata kama Lehi alijua kwamba Yerusalemu itaangamizwa, yeye pia aliona kwamba wale wanaomwamini Mungu hawataangamia.)• Ni lini umeweza kutoa sifa kwa Mungu, hata katika nyakati ngumu za maisha yako?• Ni zipi baadhi ya baraka za kutambua “wema na huruma” ya Bwana hata wakati wa

nyakati ngumu?Acha mwanafunzi asome taarifa ifuatayo kwa sauti: “Kama manabii wa kale, manabii wa sasa hushuhudia juu ya Yesu Kristo na kufunza injili Yake. Wanajulisha mapenzi na hulka halisi ya Mungu. Wanaongea kwa ujasiri na wazi,

UtanguliziKitabu cha Mormoni kinaanza na Lehi akitimiza kwa uaminifu kazi yake kama nabii. Lehi alikuwa mmoja wa “manabii wengi, wakitoa unabii na kuwaambia watu kwamba lazima watubu”(1 Nefi 1:4) Alipotoa unabii kuhusu maangamizo ya Yerusalemu na kushuhudia juu ya ukombozi kupitia Masiya, watu wengi walimkejeli

na wakataka kumuua. Hata hivyo, Lehi alifurahia katika huruma na nguvu za ukombozi za Bwana. Wanafunzi wanapojifunza kuhusu huduma ya Lehi, wanaweza ku-kua katika uelewa wao wa kazi za manabii leo. Wana-potafuta ushahidi wa huruma na upendeleo wa Mungu katika maisha yao, uhusiano wao na Yeye utaongezeka.

Kujifunza maandiko kila sikuUnaweza kuwasaidia wanafunzi kutimiza kazi yao katika mchakato wa kujifunza kwa kuwatia moyo kujifunza Kitabu cha Mormoni kila siku. Mwaka wote, kwa maombi fikiria njia za kuwasaidia wao kukuza tabia ya kujifunza ma-andiko kila siku. Mara kwa mara, unaweza kushirikiana nao ushu-huda wako wa baraka za kujifunza Kitabu cha Mormoni kila siku.

Page 37: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

22

SoMo la 6

wakishutumu dhambi na kuonya juu ya matokeo yake. Nyakati fulani, wanaweza kupatiwa maongozi kutoa unabii wa matukio ya siku zijazo kwa manufaa yetu” (True to the Faith: A Gospel Reference [2004], 129).Tia mkazo kwamba Lehi ni mfano wa kweli kwamba manabii huonya dhidi ya dhambi na kufunza wokovu kupitia Yesu Kristo. (Unaweza kuandika kweli hii kwenye ubao.)Waalike wanafunzi wasome 1 Nefi 1:19–20• Lehi alifunza nini?• Watu walifanya nini juu ya mafundisho ya Lehi?• Kwa nini watu fulani katika siku zetu wanakataa jumbe kutoka kwa manabii wa Bwana?• Wewe ulibarikiwa au kulindwa wakati gani kwa sababu ya kumfuata nabii?

1 Nefi 1:20Nefi hushuhudia juu ya huruma nyororo za BwanaTaja kwamba katika sentensi ya pili ya 1 Nefi 1:20, Nefi anakatiza simulizi zake ili kueleza ujumbe wale wanaosoma maneno yake. Acha wanafunzi wasome 1 Nefi 1:20 kibinafsi, wakitafuta ujumbe ambao Nefi anataka sisi tuuone. Kama inavyohitajika, elekeza usikivu wao kwa maneno aliyotumia Nefi kutambulisha ujumbe huu (“Mimi, Nefi nitawaonyesha ninyi ”).• Kuwa makini sana kwa maneno kama haya kunaweza kukusaidia vipi katika kujifunza

kwako kibinafsi Kitabu cha Mormoni?• Nefi alitaka kutuonyesha sisi nini?Muulize mwanafunzi asome 1 Nefi 1:20 kwa sauti. Muulize mwanafunzi mwingine asome Moroni 10:3. Uliza darasa litafute mambo yanayofanana katika mistari yote miwili.• Ni wazo gani linalofanana ambalo Nefi na Moroni walitaka wasomaji wa Kitabu cha

Mormoni wagundue?Wasaidie wanafunzi kugundua kanuni hii: Huruma nyororo ya Bwana hutolewa kwa wale wanaofanya imani katika Yeye. (Unaweza kuandika hii kanuni kwenye ubao.)Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa huruma nyororo ya Bwana ni nini na jinsi ya kuzitambua katika maisha yao, elezea taarifa ifuatayo ya Mzee David A. Bednar wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili:

“Huruma nyororo za Bwana ni baraka za kibinafsi kabisa na za kipekee, nguvu, ulinzi, hakikisho, maongozi, ukarimu wa upendo, faraja, uhimili, na vipawa vya kiroho ambavyo sisi hupokea kutokana na kwa sababu ya na kupitia Bwana Yesu Kristo. . . .“. . . Huruma nyororo za Bwana hazitokei hivi hivi au kwa sababu ya bahati. Uaminifu na utii hutuwezesha sisi kupokea hivi vipawa muhimu na, kila

mara, wakati wa Bwana hutusaidia sisi kuvitambua.“Tusidharau au tusipuuze nguvu za huruma nyororo ya Bwana(“The Tender Mercies of the Lord,” Ensign or Liahona, May 2005, 99–100).• Mzee Bednar aliezea vipi maneno “huruma nyororo ya Bwana”?• Ni mifano gani ya huruma nyororo ya Bwana ambayo umeona zikiletwa kwako au mtu

mwingine unayemjua?Baada ya wanafunzi kuwa na muda wa kujibu maswali haya, waalike wao kufikiria jinsi wanavyoweza kutambua vyema huruma nyororo ya Bwana katika maisha yao. Wahimize wao kutambua huruma nyororo ambazo Bwana amewapatia wao. Unaweza kutaka kuwa-shauri kwamba waandike uzoefu wao wa huruma nyororo katika shajara zao za kibinafsi. Fikiria juu ya kuwapatia wao muda wa kuandika katika shajara zao za kujifunza maandiko au vitabu vya darasani kuhusu njia moja au mbili ambazo majuzi Bwana ametoa huruma nyororo kwao.Hitimisha kwa kurejea ushuhuda wa Nefi katika 1 Nefi 1:20 kuhusu huruma nyororo za Bwana. Toa ushuhuda wako wa uhalisi wa baraka na utunzi wa kibinafsi wa Bwana. Wahi-mize wanafunzi kutafuta mifano ya huruma nyororo za Bwana katika maisha yao na kote katika Kitabu cha Mormoni.

Tafuta maneno muhimuNjia moja ya kuwasidia wanafunzi kuwa na uzoefu bora na kusoma kwao kwa maandiko kibinafsi kila siku ni kuwafundisha wao ku-tafuta maneno muhimu. Waandishi wa Kitabu cha Mormoni kila mara walitumia maneno mu-himu kusisita masomo waliokuwa wanajaribu kuleta au kufanya muh-tasari kanuni walizofu-nza—maneno kama vile “Mimi nitawaonyesha ninyi,” “basi tunaona,” na “Mimi nanena nanyi.” Wahimize wanafunzi kuwa makini kwa ma-somo ambayo yanaa-mbatana na maneno kama haya.

Page 38: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

23

1 nefi 1

Tangazo na Habari za Usuli1 Nefi 1:2 “Lugha ya Wamisri”Nefi alisema kwamba alitengeneza kumbukumbu yake katika “lugha ya Wamisri” (1 Nefi 1:2). Karibu miaka 470 baadaye, Mfalme Benyamini aliwafunza wanawe “lugha ya Wamisri” (Mosia 1:1–4). Neno “Kimisri kilichorekebishwa” linatokea katika Mormoni 9:32. Moroni alitaja kwamba katika siku zake, karibu miaka 1,000 tangu nyakati za Lehi na Nefi, watu wamegeuza Kimisri na Kiebrania kile kilichotumika na Lehi na Nefi.

1 Nefi 1:4. “Manabii wengi”Nefi alisema kwamba “manabii wengi” watakuja miongoni mwa watu katika Yerusalemu. Sisi tunawajua Yeremia, Obadia, Nahumu, Habakuku, na Zefania wote walikuwa manabii wa hirimu ambao walishuhudia

katika Ufalme wa Yuda. Yeremia 35:15 Ikijumuisha usemi unaofanana kuhusu manabii wengi watakaotu-mwa na Bwana kuwaonya watu (ona pia 2 Mambo ya Nyakati 36:15–16).

Yeremia alikuwa nabii shupavu katika siku za Lehi na Nefi na imetajwa katika 1 Nefi 5:13 na 7:14. Alihudumu kwa Wayahudi kutoka miaka 626 K.K. hadi miaka 586 K.K. Tofauti na Lehi, Yeremia alikaa katika Yerusalemu na kuendelea kuwaambia watu watubu (ona Bible Dictionary, “Jeremiah”). Baada ya Lehi kuondoka Ye-rusalemu, Yeremia alitupwa gerezani. Akiwa gerezani, aliandika kitabu cha Maombolezo, ambapo aliombo-leza maangamizo ya Yerusalemu na hakika kwamba hawakutubu.

Mawazo ya Ziada ya Kufunza1 Nefi 1:2–3, 20. Kuweka kumbukumbu ya huruma nyororo katika maisha yetu• Thamani ya kuweka kumbukumbu ya uzoefu wako

katika shajara ni nini?

Nefi alishuhudia juu ya huruma nyororo za Bwana katika maisha yake. Alifunza kwamba wale wote walio na imani katika Yesu Kristo wanaweza kupata uzoefu wa baraka kama hizo. Rais Henry B. Eyring wa Urais wa Kwanza alielezea juu ya nyakati ambapo alipata msukumo kuandika ushahidi wa wema wa Mungu kwa familia yake.

“Nilikuja nyumbani usiku kutoka katika shughuli za Kanisa. Ilikuwa ni baada ya jua kuzama. Baba mkwe wangu, aliishi karibu nasi, alinishangaza mimi nili-pokuwa nikitembea kuelekea mlango wa mbele wa nyumba yangu. Alikuwa amebeba mzigo wa mabomba mabegani mwake, akitembea kwa kasi akiwa amevalia mavazi yake ya kazi. Nilijua kwamba amekuwa akije-nga mfumo wa kupiga maji kutoka kwenye kijito hadi kwenye shamba letu.

“Alitabasamu, akaongea kwa upole, na kisha kunipita kasi kwenda gizani hata kwenye kazi yake. Nilichu-kua hatua chache kuelekea nyumbani, nikifikiria kile alichokuwa akitufanyia, na vile nilipofika mlangoni, nilisikia kwenye akili zangu—sio kwa sauti yangu—ma-neno haya: ‘Mimi sikupatii huu uzoefu kwa ajili yako mwenyewe. Uandike chini.’

“Nikaingia ndani. Sikuenda kulala. Ingawa nilikuwa nimechoka, nikatwaa karatasi na kuanza kuandika.

Nilipofanya hivyo, nilifahamu ujumbe huu niliosikia katika akili yangu. Nilihitajika kuandika kwa ajili ya watoto wangu wasome, wakati fulani katika siku za usoni, vile nilivyoona mkono wa Mungu ukibariki fami-lia yangu. . . .

“Niliandika mistari michache kila siku kwa miaka mingi. Kamwe sikukosa hata siku moja bila kujali vile nilivyo-choka au jinsi nitakavyoamuka mapema siku inayofu-ata. Kabla ya sijaandika, ningetafakari swali hili: ‘Je! Nimeona mkono wa Mungu ukinyooshwa ili kutugusa sisi au watoto wetu au familia yetu leo?’ Nilivyoendelea hivyo, kitu kikaanza kutendeka. Nilipokuwa nikipiga taswira juu ya siku, ningeona ushahidi wa kile Mungu alichomfanyia mmoja wetu ambacho sikutambua kwa sababu ya shughuli nyingi za siku” (“O Remember, Remember,” Ensign or Liahona, Nov. 2007, 66–67).

1 Nefi 1:4–20. Kufanana kati ya Lehi na Joseph SmithWaalike wanafunzi wasome 1 Nefi 1:4–20, wakitafuta matukio muhimu kutoka hiki kipindi cha maisha ya Lehi. Kisha waombe wao warejee Historia ya —Joseph Smith 1:1–35, wakitafuta matukio muhimu katika maisha ya Nabii Joseph Smith. Waulize wanafunzi watafute kufanana kati ya maisha ya Lehi na maisha ya Joseph Smith. (Majibu yanaweza kujumuisha kwa-mba wote walimtafuta Mungu kwa maombi ya dhati, walimwona Baba na Mwana, waliwaambia wengine maono yao, walikataliwa na watu wengi, walipata maisha yao kutishiwa, walihitaji kuhamia sehemu mpya, na wakamweka Mungu juu ya vitu vyote vya kilimwengu na sifa za ulimwengu.)

Page 39: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

24

SOMO LA 7

1 nefi 2

Mapendekezo ya Kufundisha

1 Nefi 2:1–7Mungu alimwamuru Lehi aondoke kwenda nyikaniWaulize wanafunzi wafikirie kwamba wazazi wao wamewaambia kwamba familia zao lazima ziondoke nyumbani kwao kesho, waache karibu mali yao yote. Wataenda nyikani, wakichukua tu vitu vinavyohitajika ili wao kuwa hai.• Je! Wewe unaweza kufanya nini?• Je! Ungebadili vipi utakavyofanya kama ungejua kwamba amri hii ya kuondoka hadi

nyikani imetoka kwa Bwana?Alika mwanafunzi asome 1 Nefi 2:1–6 kwa sauti. Uliza darasa kutafuta sababu za kwa nini Lehi aliongoza familia yake hadi nyikani• Ni amri gani ile Lehi alipokea kutoka kwa Bwana? (Ona 1 Nefi 2:2.)• Unaweza kujifunza nini kutokana na uamuzi wa Lehi kuhusu kile ambacho angechukua

na kile cha kuuacha?Mwombe mwanafunzi asome 1 Nefi 2:7 kwa sauti.• Lehi alitoa shukrani kwa Bwana baada tu ya kuacha nyumba yake na vitu vyake. Tuna-

weza kujifunza nini kutokana na haya?• Lehi alikuwa na shukrani?Andika taarifa ifuatayo kwenye ubao: Tunapokuwa waaminifu na watiifu, Bwana ata-tusaidia sisi katika nyakati za majaribu.• Je! Ni lini umepata kuhisi Bwana akikusaidia nyakati za majaribu? (Watie moyo wanafu-

nzi watafute maongozi ya Roho katika kujibu swali hili. Wasaidie wao kuelewa kwamba hawahitaji kuelezea uzoefu ambao ni wa kibinasfi au siri sana.)

1 Nefi 2:8–15Lamani na Lemueli walinung’unika dhidi ya baba yaoWaombe wanafunzi kujiuliza wenyewe kimya kimya kama wameshanung’unika aidha kwa sauti au kindani, kuhusu amri kutoka kwa Bwana au kuhusu chochote wameombwa kuki-fanya na mzazi au kiongozi wa Kanisa. Wapatie muda wa kufikiria juu ya uzoefu wao.• Kwa nini wakati mwengine tunanung’unika tunapopatiwa maagizo?Andika Mto na Bonde kwenye ubao. Alika mwanafunzi asome 1 Nefi 2:8–10 kwa sauti.• Ni kwa njia gani Lehi alimtaka Lamani awe kama mto? Ni kwa njia gani alimtaka Le-

mueli awe kama bonde? (Unaweza kuwauliza wanafunzi waandike majibu yao pembeni karibu na maneno haya Mto na Bonde.)

• Ni nini Lehi alikuwa anajaribu kuwafundisha Lamani na Lemueli?Acha wanafunzi wasome 1 Nefi 2:11–14 kimya kimya.• Ni zipi baadhi ya sababu ambazo Lamani na Lemueli walinung’unika dhidi ya baba yao?• Katika 1 Nefi 2:11, neno ukaidi linamaanisha kiburi au usugu. Kwa nini hisia za kiburi

wakati mwengine husababisha watu kunung’unika?

UtanguliziTaarifa katika 1 Nefi 2 inaonyesha jibu tofauti kwa amri kutoka kwa Bwana. Lehi alitii amri ya Bwana na kuongoza familia yake hata nyikani. Wakikabiliwa na

ugumu wa amri hii, Lamani na Lemueli waliasi. Tofauti na hivyo, Nefi alitafuta ushahidi thibitishi.

Page 40: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

25

1 nefi 2

• Unafikria ni kwa nini kunung’unika wakati mwengine hutokea wakati watu hawafa-hamu mambo ya Mungu?

Elezea kwamba sababu moja Shetani anataka sisi tunung’unike ni kwamba kunatuzuia sisi kufuata manabii hai, na wale viongozi wenye maongozi na wazazi. Kama sehemu ya majadiliano, unaweza kuelezea yafuatayo, kuhusu taarifa ya Mzee H. Ross Workman wa wale Sabini:“Kunung’unika kuna hatua tatu, kila moja ikielekeza kwenye ile ifuatayo katika mapito ya mteremko hadi kutotii.” Kwanza, watu huanza kwa kutilia shaka. Wanatilia shaka “kwa-nza katika akili zao wenyewe,” na kisha wanapanda maswali “katika akili za wengine.” Pili, wale wanaonung’unika huanza “kufanya urazini na kujiondoa kwa kuto kufanya kile wameelekezwa kufanya. Basi, wanatoa kisingizio cha kutotii.” Visingizio vyao huwaelekeza kwenye sehemu ya tatu: “ Uzembe katika kufuata amri ya Bwana. . . .“Nawaalika mlenge juu ya amri kutoka kwa manabii walio hai ambao wanakukera sana. Je! Unatilia shaka kama amri inafaa kwako? Je! Unapata visingizio tayari kwa nini hauwezi kufuata amri hii. Je! Unahisi kusumbuliwa au kuudhiwa na wale wanaokumbusha juu ya amri hii? Je! Wewe ni mzembe katika kuishika? Jihadhari na udanganyifu wa adui. Jiha-dhari na kunung’unika” (“Beware of Murmuring,” Ensign, Nov. 2001, 85–86).Waulize wanafunzi kujibu maswali yafuatayo katika shajara zao za kujifunza maandiko au katika vitabu vya darasani:• Je! Unaweza kufanya nini kama unajipata ukinung’unika kuhusu manabii na amri za

Bwana?

1 Nefi 2:16–19Nefi anatafuta uelewa kutoka kwa BwanaAcha wanafunzi wasome na kutafakari 1 Nefi 2:16, 19 kimya kimya.• Nefi alifanya vipi kuhusu ujumbe wa baba yake?• Je! Umeshamwomba Mungu na kuhisi moyo wako ukilainika?Wape wanafunzi nafasi ya kueleza kuhusu nyakati ambazo Bwana alilainisha mioyo yao (lakini wakumbushe kwamba si lazima kueleza uzoefu ambao ni wa kibinasfi au siri sana). Kwa ziada, unaweza kutaka kuelezea kuhusu wakati ambapo Bwana alilainisha moyo wako. Wahakikishie wanafunzi kwamba tunapomwomba Mungu, Yeye atalainisha mioyo yetu hata kuamini katika maneno Yake. Soma 1 Nefi 2:19 kwa sauti. Acha wanafunzi waeleze kwa maneno yao wenyewe maana ya maneno “bidii” na “unyenyekevu wa moyo.” Wahimize wao kumtafuta Bwana kama vile Nefi alivyofanya.Alika mwanafunzi asome 1 Nefi 2:17–18 kwa sauti.• Ni kanuni gani tunazoweza kujifunza kutoka katika majibu tofauti ya Nefi, Samu, La-

mani, na Lemueli?• Ni lini maneno ya mwanafamilia au rafiki yaliimarisha imani yako, kama vile maneno ya

Nefi yalivyoimarisha imani ya Samu?

1 Nefi 2:20–24Wale ambao watashika amri watastawiAcha wanafunzi wasome 1 Nefi 2:20–21. Waalike kutambua au kuweka alama ahadi ambazo “kadiri utakavyo shika amri zangu, wewe utafanikiwa.” Elezea kwamba wanapoji-funza Kitabu cha Mormoni, mara nyingi watasoma juu ya kutimizwa kwa ahadi hii.Fikiria kutoa taarifa ifuatayo ya Mzee Bruce R. McConkie wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili:“Utiifu ni sheria ya kwanza ya mbinguni. Maendeleo kote, ukamilisho wote, wokovu wote, uungu wote, yale yote yaliyo sahihi na haki na kweli, mambo yote mazuri huja kwa wale wanaoishi sheria Zake Yeye ambaye ni wa Milele. Hakuna chochote katika milele yote kilicho muhimu sana kuliko kushika amri za Mungu” (The Promised Messiah: The First Coming of Christ [1978], 126).Toa ushuhuda wako kwamba Mungu hubariki wale ambao ni watiifu na waaminifu. Kama Nefi, wanafunzi wanaweza kukuza imani katika kupokea maelekezo kutoka kwa

Maswali ambayo yanaalika maongoziRais Henry B. Eyring wa Urais wa Kwanza alifu-nza kwamba maswali fulani hualika mao-ngozi. Alishauri walimu kuuliza maswali “ambayo yataalika watu kupekua kumbukumbu zao kwa hisia.” Kuuliza maswali ambayo huwapa wana-funzi kufikiria juu ya ma-tukio yaliyopita, badala ya kukumbuka habari, unaweza kuwatayari-sha wao kufunzwa kwa Roho. Rais Eyring alisema: “Ngojea kwa hekima kwa muda kabla kumwita mtu kujibu. Hata wale ambao hawaongei watakuwa wakifikiria matukio ya ki-roho. Yale yatakayomwa-lika Roho Mtakatifu” (“The Lord Will Multiply the Harvest” [hotuba kwa walimu wa dini wa MEK, Feb. 6, 1998], 6, si.lds.org).

Page 41: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

26

SoMo la 7

Bwana. Wahimize wao kujitahidi kuwa watiifu zaidi na kufuata maongozi wanayopokea kutoka kwa Roho Mtakatifu.

Tangazo na Habari za Usuli1 Nefi 2:2–6. Labda njia iliyochukuliwa na familia ya LehiLehi labda aliongoza familia yake hata katika Bahari ya Shamu karibu na Ghuba ya Akaba, karibu maili 180 (kilometa 290) kutoka Yerusalemu. Hii ingehitaji kusafiri kupitia kwenye nchi ya joto na ukame, iliyo-julikana kwa wezi ambao walivizia kuwaibia wasafiri wasio na tahadhari. Baada ya kufika Bahari ya Shamu, familia ilisafiri kwa siku tatu zaidi kabla ya kupiga ka-mbi katika bonde la mto. Safari ya kutoka Yerusalemu hadi kwenye bonde la mto inaweza kuwa ilichukua siku 14. Ungependa kuwakumbusha wanafunzi juu ya huu umbali na wakati wanaposoma kuhusu Nefi na nduguze wakisafiri kurudi Yerusalemu.

1 Nefi 2:7. Kuonyesha shukrani kwa BwanaShukrani za Lehi kwa maongozi na ulinzi wa Bwana zinaonyeshwa katika 1 Nefi 2:7: “Alijenga madhabahu ya mawe, na akamtolea Bwana dhabihu, na kumshu-kuru Bwana Mungu wetu.” Hii ni ya kwanza kati ya mara kadha katika Kitabu cha Mormoni wakati wafuasi wa Kristo walitoa dhabihu na matoleo ya kuteketezwa kuonyesha shukrani zao kwa Mungu (ona, kwa mfano, 1 Nefi 7:22; Mosia 2:3–4). Maonyesho ya shukrani na utiifu wa kweli kwa Baba wa Mbinguni ni muhimu kwa watoto Wake wote kama watampendeza Yeye (ona M&M 59:21).

KaskaziniBahari Kuu Bahari ya Galilaya

Bahari ya Chumvi

Ghuba la Wajemi

Bahari Hindi

Yerusalemu

Jangwa la Arabia

Bahari ya Shamu

Neema (?)

“Kwenye mipaka karibu na ufuoni wa Bahari ya Shamu” (1 Nefi 2:5)

“Karibu na upande wa kusini- kusini mashariki” (1 Nefi 16:13)

“Katika mpika karibu na Bahari ya Shamu” ( 1 Nefi 16:14)

“Tulisafiri tukielekea mashariki tangu ule wakati” (1 Nefi 17:1‎)‎

Ishmaili alifariki katika mahali “ambapo paliitwa Nahumu” (1 Nefi 16:34)

Wazo la Ziada la Kufunza1 Nefi 2:1–3, 16–19. Mioyo laini na ufunuoWakumbushe wanafunzi kwamba katika 1 Nefi 1, Nefi alielezea ufunuo aliopokea Lehi alipokuwa “amelewa na Roho” (1 Nefi 1:7). Katika ono hilo, Lehi alisoma kutoka kitabu kilicho na unabii na akawa “amejazwa na Roho” (1 Nefi 1:12). Katika 1 Nefi 2, mada ya ufunuo inaende-lea jinsi Nefi anavyoongea juu ya baba yake akipokea onyo kutoka kwa Bwana katika ndoto (ona 1 Nefi 2:1–3). Nefi pia anaongea kuhusu uzoefu wake mwenyewe katika kupokea ufunuo na kufuatia sauti ya Bwana.

Onyesha vitu viwili—kimoja ambacho ni laini na kinaweza kunyonya (kama vile kitambaa au sponji) na kingine ambacho ni kigumu (kama vile jiwe). Kisha mu-ulize mwanafunzi asome 1 Nefi 2:16–19 kwa sauti.

• Ni kwa njia gani mioyo ya Lehi, Nefi, na Samu ilikuwa kama hiki kitu laini?

• Ni kwa njia gani mioyo ya Lamani na Lemueli ilikuwa kama hiki kitu kigumu?

• Hali ya kiroho ya mioyo yetu inaweza kuathiri vipi uwezo wetu wa kupokea ufunuo?

Wasaidie wanafunzi kuelewa kwamba Bwana anafunua elimu kwetu kadiri sisi tunavyotia bidii ya kumtafuta Yeye. Kama sehemu ya majadiliano, unaweza kugawa wana-funzi wawili wawili na uwaache wao wasome mada ya jina “Revelation” katika Bible Dictionary. Waulize wao kujadili swali lifuatalo:

• Tunaweza kufanya nini ili kujitayarisha kupokea ufunuo kutoka kwa Bwana?

Page 42: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

27

SOMO LA 8

1 nefi 3–4

Mapendekezo ya Kufundisha

1 Nefi 3:1–9, 19–20Wana wa Lehi wanarudi Yerusalemu ili kuchukua mabambaAndika taarifa zifuatazo kwenye ubao kabla ya darasa kuanza. Waulize wanafunzi ku-chagua taarifa ambayo inaeleza vyema jinsi wanaamini Bwana hutusaidia wakati Yeye anapotu agiza kufanya vitu vigumu.Unapojitahidi kutimiza amri au kazi ngumu kutoka kwa Bwana, Yeye:

a. Atabadilisha amri ili iwe nyepesi na rahisi kwako kuitimiza. b. Atabariki juhudi zako kwa kutoa njia kwako ya kutimiza hii amri, hata kama inaweza kuwa

bado ni ngumu. c. Ataingilia kati na kufanya kazi yote kwa ajili yako. d. Atakuhitaji kuifanya yote wewe mwenyewe bila usaidizi wowote.

Waalike wanafunzi wachache waeleze jibu walilochagua na sababu ya kulichugua.Elezea kwamba kuna njia nyingi ambazo kwazo Bwana anaweza kuwabariki wale wanaoji-tahidi kutimiza amri Zake. Wanafunzi wanapojifunza taarifa ya Nefi katika 1 Nefi 3–4, wa-alike watafute mifano ya kanuni hii. Pia wahimize wanafunzi kuona jinsi Nefi na nduguze walivyofanya tofauti katika hizi changamoto.Wateue wanafunzi kadha kuchukua zamu kusoma kwa sauti 1 Nefi 3:1–9. Alika wengine wa darasa kusikiliza sababu za kwa nini Nefi alikuwa radhi kufanya kile baba yake alicho-mwagiza kufanya.Lamani na Lemueli walihisi kwamba amri ya kurudi Yerusalemu kuchukua mabamba ilikuwa “mambo magumu ambayo [Lehi] alihitaji kutoka kwao” (1 Nefi 3:5). Ili kuwasa-idia wanafunzi kuelewa sababu kadha za kwa nini Lamani na Lemueli waliweza kuhisi hivi, unaweza kuwakumbusha wao kwamba walikuwa wamesafiri mwendo mrefu kutoka Yerusalemu.• Unafikiria ni kwa nini Nefi alikuwa radhi kufanya kama vile baba yake alivyomwagiza

bila kunung’unika?Waalike wanafunzi kusema tena kanuni ambayo Nefi alishuhudia juu yake katika 1 Nefi 3:7 kama taarifa ya “kama-basi." Kwa mfano, wanafunzi wanaweza kusema kwamba kama tunatafuta kufanya kile ambacho Bwana ameamuru, basi Yeye atatayarisha njia ambayo kwayo sisi tuitimize. Taja kwamba 1 Nefi 3:7 ni fungu la umahiri wa maa-ndiko. Elezea kwamba wanafunzi watalenga juu ya vifungu 25 vya umahiri wa maandiko katika mwaka wote (kwa habari zaidi, ona kiambatisho katika kitabu hiki). Mafungu 25 ya umahiri wa maandiko yameorodheshwa hapo nyuma ya alamisho ya seminari. Unaweza kuwahimiza wanafunzi kuweka alama vifungu vya umahiri wa maandiko kwa njia ya kipe-kee ili waweze kupata hivi vifungu kwa urahisi.• Ni lini ulihisi kwamba Bwana “ametayarisha njia” kwako ya kushika mojawapo ya

amri Zake?Alika mwanfunzi asome 1 Nefi 3:3, 19–20 kwa sauti. Uliza wengine walio darasani kusi-kiliza maneno ambayo yanasema kwa nini mabamba ya shaba yalikuwa na thamani sana

UtanguliziBwana alimwamuru Lehi kuwatuma wanawe kurudi Ye-rusalemu kuchukua mabamba ya shaba kutoka kwa La-bani. Lamani na Lemueli hawakuona jinsi wangeweza kutimiza hii amri, lakini Nefi alikuwa na imani kwamba Bwana angewapatia njia ambayo kwayo wangetimiza

kile Yeye alihitaji. Licha ya kukabiliana na mfululizo wa ugumu, Nefi kwa uaminifu alijizatiti katika kufanya kile Bwana aliagiza kutoka kwake. Kama matokeo, aliongozwa na Roho Mtakatifu na kufanikiwa kupata mabamba.

1 Nefi 3:7 ni fungu la umahiri wa maandiko. Rejea wazo la kufundisha umahiri wa maandiko mwishoni mwa somo ili kuwasaidia wanafunzi na umahiri wao wa hili fungu.

Page 43: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

28

SoMo la 8

kwa familia ya Lehi na uzao wao. (Unaweza kushauri kwamba wanafunzi waweke alama maneno haya katika maandiko yao.) Baada ya wanafunzi kuelezea kile ambacho wame-pata, elezea kwamba mabamba ya shaba yalikuwa ni juzuu ya maandiko ya kale yaliyo-kuwa na wingi wa maandishi na habari sawa na Agano la Kale.• Kwa nini unafikiria maudhui ya mabamba ya shaba yalikuwa muhimu sana kwa Nefi na

nduguze kurudi Yerusalemu kuyachukua?• Maandiko yana nini siku hizi kilicho cha thamani kwako? Kwa nini kina thamani

kwako?

1 Nefi 3:10–31Labani anaiba mali ya Lehi na kujaribu kumua Nefi na nduguzeAlika nusu ya darasa kujifunza kuhusu jaribio la kwanza la Nefi na nduguze la kuchukua mabamba ya shaba (ona 1 Nefi 3:10–18). Alika ile nusu ingine ijifunze kuhusu jaribio la pili (ona 1 Nefi 3:21–31). Acha kila mwanafunzi afanye kazi peke yake na kujibu maswali yafua-tayo. Unaweza kutaka wao wafanye kazi hii katika shajara za kujifunza maandiko au vitabu vya darasani. Onyesha maswali kwenye ubao au mtayarishie kitini kwa kila mwanafunzi.

1. Ni nani alienda? 2. Walifanya nini? 3. Walifanya nini baada ya jaribio kushindikana? 4. Kwa wanafunzi wanaojifunza jaribio la kwanza: Nefi na nduguze walikuwa na “huzuni

kubwa sana’ baada ya kushindwa kupata mabamba ya shaba (ona 1 Nefi 3:14). Nefi alifanya nini kuhusu kushindwa huku tofauti na ndugu zake? (Ona 1 Nefi 3:15–16.)Kwa wale wanaojifunza jaribio la pili: Lamani na Lemueli walimkasirikia Nefi baada ya jaribio lao la pili kushindikana. Wakampiga na kumkaripia kwa hasira. Hata baada ya malaika kuahidi kwamba Bwana atamweka Labani katika mikono yao, waliendelea kunung’unika na kutilia shaka uwezo wao wa kufanikiwa. Ghadhabu ya Lamani na Lemueli iliathiri vipi uwezo wao wa kuwa na imani na ahadi ya malaika? Ghadhabu, ubishi, kunung’unika, na kutoamini hutuzuia vipi sisi kuelewa ujumbe wa Mungu kwetu? (Ona 1 Nefi 3:28–31; 3 Nefi 11:29.)

5. Je! Umepata mawazo gani kutoka katika mistari uliyojifunza?Baada ya wanafunzi kuwa na muda wa kutosha wa kujibu maswali, waalike wachache kutoa majibu yao.

1 Nefi 4:1–38Nefi alipata mabamba ya shabaWaulize wanafunzi kutambua maswali ambayo Lamani na Lemueli waliuliza katika 1 Nefi 3:31.Alika mwanafunzi asome 1 Nefi 4:1–3 kwa sauti. Uliza darasa lisikilize majibu ya Nefi ya maswali ya ndugu zake.• Hadithi ya Musa inalingana vipi na maswali ya Lamani na Lemueli?Kama wanafunzi wanahitaji usaidizi wa kujibu swali hili, elezea kwamba Musa aliku-mbwa na changamoto kama hiyo wakati alipoamriwa kuwatoa wana wa Israeli kutoka Misri. Licha ya majaribu mengi, Musa hakuweza kumshawishi Farao awaachilie wana wa Israeli kutoka utumwani. Hata hivyo, Musa alisisitiza katika kufanya kile ambacho Bwana alikuwa amemwamuru yeye, na Bwana alitengeneza njia ambayo kwayo yeye aliwafanya huru wana wa Israeli. Nefi alitumia mfano wa Musa katika hali ya familia yake. Alikuwa na imani kwamba Mungu pia angetayarisha njia kwao.• Ni kanuni gani uliyojifunza kutokana na majibu ya Nefi kwa ndugu zake?Ingawa wanafunzi wanaweza kujenga majibu tofauti kidogo, wanapaswa kuonyesha kwamba kama tukisisitiza kwa uaminifu katika kufanya kile Bwana anahitaji, licha ya ugumu, Yeye atatutayarishia njia ya kutimiza kile Yeye anachoamuru. (Unaweza kuandika kanuni hii kwenye ubao.)

Page 44: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

29

1 nefi 3– 4

Rejea taarifa ulizoonyesha kwenye ubao hapo mwanzoni mwa somo.• Sasa kwamba mmejifunza uzoefu wa Nefi, ni taarifa gani unazofikiria zinafanya muhta-

sari vyema wa kanuni uliyotambua?Wanafunzi wanapojifunza sazo la tukio la Nefi, wahimize watafute uthibitisho wa kanuni hii katika matokeo ya uvumilivu wa Nefi.Acha mwanafunzi asome 1 Nefi 4:4–6 kwa sauti. Unaweza kushauri kwamba wanafunzi waiwekee alama 1 Nefi 4:6 katika maandiko yao.Wasaidie wanafunzi kuelewa kwamba Bwana anaweza kutupatia maongozi sisi kufanya ja-mbo bila kutoa ufunuo wa jinsi, lini, au kwa nini tunapaswa kulifanya. Nefi alijua jinsi, lini, na kwa nini Bwana angemsaidia tu baada ya yeye kukubali Roho Mtakatifu amwelekeze na baada ya yeye kuamua kusonga mbele kwa imani.Waambie wanafunzi kwamba Rais Harold B. Lee alisema kwamba sisi kila mara tunataka kuona “mwisho kuanzia mwanzoni,” au matokeo, kabla ya sisi kufuata maelekezo ya Bwana. Alishauri:“Ni sharti wewe utembee kandoni mwa nuru, na labda hatua chache katika giza [kusiko-julikana], na wewe utagundua ile nuru ikitokeza na kwenda mbele yako” (katika Lucile C. Tate, Boyd K. Packer: A Watchman on the Tower [1995], 137–38).Alika mwanafunzi asome 1 Nefi 4:7 kwa sauti.• Katika 1 Nefi 4:7, ni nini cha muhimu katika maneno “Walakini niliendelea mbele”?• Uzoefu wa Nefi unafunza nini kuhusu uhusiano kati ya kuwa radhi kwetu kwa “kwenda

na kutenda” na uwezo wetu wa kuongozwa na Bwana?Waalike wanafunzi kadha kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka 1 Nefi 4:8–18.• Ni sababu gani ambazo Roho alimpatia Nefi za amri ya Bwana ya kumuua Labani?Fanya muhtasari wa tukio lote la Nefi la ufanisi wa kupata mabamba (ona Nefi 4:19–38), Waulize wanafunzi watambue kanuni wanazoona zimeonyeshwa katika hii juhudi ya kupata mabamba. Baada ya wao kutoa mawazo yao, ongezea ushuhuda wako kwamba tu-napofanya imani katika Mungu na kutafuta kufanya kile Yeye ameamuru, hata kama hatuwezi kuona matokeo yake, Yeye atatuongoza kwa ushawishi wa Roho Mtakatifu.Ili kuwasaidia wanafunzi kukuza zaidi shuhuda zao juu ya kanuni hii, waalike wao wasi-mulie uzoefu wao juu ya wakati walipotenda kwa imani bila kujua mapema jinsi au wakati Mungu atakapo wasaidia wao.Waalike wanafunzi kutafakari juu ya hali wanayokabiliana nayo ambayo kwayo mahitaji ya Bwana ni magumu kwao. Waulize wao kuandika katika shajara zao za kujifunza maandiko kile watakachofanya ili kumwonyesha Bwana utayari wao wa “kwenda na kutenda” kile ambacho Yeye ameamuru. Wanapomaliza kuandika, elezea imani yako kwamba tunapoonye-sha imani yetu, Bwana atatusaidia kutimiza chochote kile ambacho yeye ametuamuru sisi.

Umahiri wa Maandiko—1 Nef 3:7Andika kwenye ubao utiifu, imani, na amini. Uliza:• Ni ushahidi gani wa utiifu wa Nefi, imani, na uaminifu unaoona katika 1 Nefi 3?• Hizi sifa zinaweza kumsaidia vipi mtu ambaye ameitwa kuhudumu misheni?Alika kila mwanafunzi kumwandikia barua mmisionari, akimwuliza mmisionari jinsi ambavyo yeye ameona 1 Nefi 3:7 katika vitendo. Wahimize wanafunzi kutoa majibu yoyote wanayopokea kwa barua zao.Tazama: Hapo mwishoni wa kila somo ambalo lina kifungu cha umahiri wa maandiko, utapata shughuli za ziada zinazodhamiriwa kuwasaidia wanafunzi kupata umahiri wa hiki kifungu. Unaweza kutumia hizi shughuli wakati wowote (kwa habari zaidi, ona faharasa na Kitabu cha Mwongozo wa Kufundisha na Kujifunza Injili ). Kwa sababu ya asili na urefu wa somo la leo, unaweza kutumia shughuli hii siku ingine, wakati una muda mwingi.

Kusoma maandiko katika darasaKusoma maandiko katika darasa kunaweza kuwasaidia wanafunzi kuelewa vyema mistari wanayojifunza. Pia inaweza kuwasaidia wao kuwa na imani sana na uwezo wa kusoma ma-andiko wao wenyewe. Hata hivyo, mwalimu kamwe kuwaaibisha wanafunzi kwa kuwa-lazimisha wao kusoma kwa sauti kama wao hawajisikii kufanya hivyo. Baadhi ya njia za kusoma maandiko pamoja katika darasa hujumuisha: 1. Wanafunzi wana-

weza kuchukua zamu kusoma kwa sauti.

2. Mwalimu akisoma kwa sauti wanafunzi nao wakifuatia katika maandiko yao.

3. Kuwauliza wanafu-nzi kadha kusoma ambamo watu wengi wanaongea katika ki-fungu cha maandiko.

4. Wanafunzi wawili wakisomeana kwa sauti katika vikundi vidogo au katika jozi.

Page 45: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

30

SOMO LA 9

1 nefi 5

Mapendekezo ya Kufundisha

1 Nefi 5:1–9Wana wa Lehi walirudi salama kwa familia yao huko nyikaniAlika mwanafunzi asome 1 Nefi 5:1–3 kwa sauti. Uliza darasa litafute sababu za kwa nini Saria alianza kunung’unika.• Manung'uniko ya Saria yalikuwa juu ya nini? (Majibu yanaweza kujumuisha kwamba

Lehi alikuwa mtu wa maono, kwamba alikuwa ameitoa familia kutoka nchi yao ya urithi wao, na kwamba yeye alifanya maamuzi ambayo yangeweza kusababisha kupotea kwa wana wao na kwamba yangeleta vifo vyao wenyewe huko nyikani.)

Waulize wanafunzi kufikiria kuhusu wakati ambao yawezekana walinung’unika kuhusu hali fulani hata kama hawakuwa na taarifa kamili kuhusu hali hiyo.Alika mwanafunzi asome 1 Nefi 5:4–6 kwa sauti. Uliza darasa liwe na usikivu kuhusu njia ambayo kwayo Lehi alifanya kuhusu kunung’unika kwa Saria.• Una msukumo gani kuhusu jinsi Lehi alivyofanya kuhusu kunung’unika kwa Saria?

(Unaweza kutaja kwamba Lehi alijibu kwa ushuhuda na imani katika Bwana badala ya hofu au shaka. Hakujibu kwa hasira au bila subira.)

• Tunaweza kujifunza nini kutokana na majibu ya Lehi kwa Saria?Acha mwanafunzi asome 1 Nefi 5:7–9 kwa sauti.• Ni nini alichopata kutokana na uzoefu wa Saria?

1 Nefi 5:10–22Lehi anapekua mabamba ya shabaWaulize wanafunzi kufikiria kuhusu kitu chochote wanachofikiria kujitolea maisha yao ili kupokea au kushika.Alika mwanafunzi kufanya muhtasari 1 Nefi 3–4 na aseme dhabihu ambazo familia ya Lehi ilifanya ili kupokea mabamba ya shaba. (Nefi na nduguze walihatarishi maisha yao, wakajitolea mali yao, na kusafiri mwendo mrefu.)• Kwa nini unafikiria dhabihu kama hiyo ilikuwa inahitajika?Elezea kwamba baada ya familia kutoa dhabihu na kutoa shukrani kwa Bwana, Lehi mara moja alianza kusoma yaliyomo ndani ya mabamba. Waalike wanafunzi kadha kuchukua zamu kusoma 1 Nefi 5:11–16 kwa sauti. Uliza darasa kutafuta kile ambacho Lehi aligundua kwenye mabamba ya shaba. Unaweza kutaka orodha fupi na majibu yao kwenye ubao.Waalike wanafunzi wasome 1 Nefi 5:10 kimya kimya. Waulize wao kutafuta neno ambalo linaeleza Lehi akisoma maandiko. (Yeye “aliyapekua.”) Waalike wanafunzi kujipanga we-nyewe katika jozi ili kujadili maswali yafuatayo:• Kuna tofauti gani kati ya kupekua maandiko na kuyasoma tu? (Unaweza kuwahimiza

wanafunzi kuongea kuhusu nyakati ambapo walipekua maandiko.)

UtanguliziWakati mke wa Lehi, Saria, alipokuwa akiwangojea wanawe kurudi kutoka Yerusalemu, alikuwa na hofu kwamba walikuwa wameangamia katika juhudi zao za kupata mabamba ya shaba. Wakati waliporudi salama wakiwa na mabamba, alipata ushahidi imara kwamba Mungu alikuwa anaelekeza na kuilinda familia yake.

Lehi alipekua mabamba ya shaba na kugundua kuwa yalikuwa na umuhimu mkubwa kwa familia yake. Ali-poyasoma, alijazwa na Roho Mtakatifu, na alitoa unabii kwamba maandiko waliyokuwa nayo yatahifadhiwa kwa ajili ya uzao wao.

Page 46: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

31

1 nefi 5

Soma kutoka katika taarifa ya Mzee Elder D. Todd Christofferson wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili:“Ninaposema “jifunze,’ ninamaanisha ni zaidi ya kusoma. Ni jambo jema wakati mwe-ngine kusoma maandiko katika kipindi cha muda uliowekwa ili kupata hisia ya jumla ya ujumbe huu, lakini kwa uongofu, unapaswa kuwa makini sana kuhusu muda unaotumia katika maandiko kuliko kuhusu kiasi unachosoma katika huo muda. Nawaona wakati fu-lani mkisoma mistari michache, na kutulia ili kuitafakari, kusoma kwa makini mistari tena, na mnafikiria kuhusu inachomaanisha, kuomba kupata ufahamu, kuuliza maswali katika akili yenu, mkingojea maongozi ya kiroho, na kuandika misukumo na mawazo ambayo yanakuja ili muweze kukumbuka na kujifunza zaidi. Kujifunza katika njia hii, unaweza kutosoma sura nyingi au mistari katika nusu saa, lakini utakuwa ukitoa nafasi ndani moyo wako kwa neno la Mungu, na Yeye ataongea nawe. Kumbuka maelezo ya Alma ya kile mtu huhisi: ‘inaanza kukua ndani ya nafsi yangu; ndio, inaanza kuangaza kuelewa kwangu, ndio, inaanza kunipendeza mimi’ [Alma 32:28]” (“When Thou Art Converted,” Ensign or Liahona, May 2004, 11–12).Wapatie wanafunzi muda wa kufikiria juu ya kujifunza maandiko wao wenyewe. Waagize wao kuandika katika shajara zao za kujifunza maandiko au vitabu vya darasani kuhusu njia zenye maana za kupekua maandiko. Baada ya wao kuandika, waalike wao kufikiria jinsi wanavyoweza kuboresha kujifunza kwao maandiko. Waulize wao wachague njia moja ya kuboresha upekuaji wao wa maandiko kibinafsi. Wahimize wao kuandika lengo lao katika shajara zao za kujifunza maandiko. Unaweza kuwashawishi kwamba wanafunzi waelezane malengo yao (kwa mfano, na wewe, na mzazi, au mwanafunzi mwingine) ambaye atawa-kumbusha wao lengo lile na kuwatia moyo ili kulitimiza.Elezea kwamba Bwana alimbariki Lehi kwa kupekua maandiko. Ili kuwasaidia wanafunzi kugundua hizi baraka, waalike wao kusoma 1 Nefi 5:16–20 kimya kimya.• Kupekua mabamba ya shaba kulimwathiri vipi Lehi?Sisitiza kwamba wakati Lehi alipopekua maandiko, yeye alijawa na Roho Mtakatifu na kupokea ufunuo “kuhusu mbegu yake” (uzao wake). Wahakikishie wanafunzi kwamba tunapopekua maandiko, tunaweza kujazwa na Roho Mtakatifu na kupokea ufu-nuo. Vivyo hivyo, tunapojitolea wakati wetu na nguvu zetu kupekua maandiko kama Lehi alivyofanya, tunaweza kupokea nguvu za kushika amri za Mungu.• Ni kwa njia gani tumeweza kubarikiwa kwa kupekua maandiko?• Ni lini ulihisi Roho Mtakatifu wakati ukijifundisha maandiko?Alika mwanafunzi kusoma taarifa ifuatayo, ambayo Mzee Robert D. Hales wa Akidi ya Wale Mitume Kumi na Wawili anashuhudia juu ya Baraka ya kupekua maandiko:

“Tunapotaka kusema na Mungu, tunaomba. Na wakati tunapotaka Yeye kuongea nasi, tunayapekua maandiko; kwani maneno Yake husemwa kupitia manabii Wake. Kisha Yeye atatufunza sisi tunaposikiliza mnong’ono wa Roho Mtakatifu.Kama haujasikia sauti Yake ikiongea nawe hivi karibuni, rudi kwa macho ma-pya na masikio mapya kwenye maandiko. Ni tegemeo kuu la kiroho” (“Holy

Scriptures: The Power of God unto Our Salvation,” Ensign or Liahona, Nov. 2006, 26–27).Soma 1 Nefi 5:21–22 kwa sauti, na uwaulize wanafunzi kufuatia katika maandiko yao. Unaposoma, sisitiza maneno: “Ni hekima katika Bwana kwamba sisi tunapaswa kuyabeba pamoja nasi, tunaposafiri huko nyikani.”• Kwa nini ni hekima kwetu sisi kubeba maandiko pamoja nasi katika safari yetu?• Ni kwa njia gani tunaweza kubeba maandiko pamoja nasi?Taja kwamba Lehi na familia yake walipata mabamba ya shaba kupitia dhabihu kuu. Pasipo maandiko, Lehi na familia yake wasingefanikiwa katika safari yao. Wahimize wanafunzi kuweka maandiko pamoja nao wanaposafiri katika maisha ya duniani.Waalike wanafunzi kutafakari juu ya kujifunza kwao maandiko kibinafsi. Fikiria kumwalika mwanafunzi ambaye husoma maandiko kila mara ili kuwahimiza na kutoa ushuhuda kwa rika lake. Wahimize wanafunzi kujenga tabia ya kutumia muda kila siku kupekua maandiko.Tazama: Urefu wa somo hili unaweza kuwapatia muda wa shughuli za umahiri wa maa-ndiko kutoka katika somo lililopita.

Page 47: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

32

SoMo la 9

Tangazo na Habari za Usuli1 Nefi 5:10–22. Thamani ya maandikoIli kufundisha jinsi ya kupokea maongozi kupitia kuji-funza maandiko kwetu, Mzee Robert D. Hales wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alielezea juu ya tukio la Lehi akipekua mabamba ya shaba:

“Nefi na nduguze waliporudi [kutoka Yesusalemu na yale mabamba], Lehi, baba yao, alifurahia. Alianza kupekua maandiko matakafitu “kutoka mwanzo,’ na kugundua kwamba yalikuwa ya kutamanika; hata ya thamani kuu alimradi kwamba [Lehi na uzao wake] waliweza kuhifadhi amri za Bwana hata kwa watoto [wao].’

“Hakika, mabamba ya shaba yalikuwa ni kumbukumbu ya wahenga wa Lehi, ikijumuisha lugha yao, nasaba yao, na cha muhimu zaidi, injili iliyofunzwa na manabii watakatifu wa Mungu. Lehi alipokuwa anapekua ma-bamba haya, alijifunza kwamba sisi sote tunajifundisha kwa kujifunza maandiko:

“• Sisi ni kina nani.

“• Kile tunachoweza kuwa.

“• Unabii kwetu sisi na kwa uzao wetu.

“• Amri, sheria, ibada, na maagano ambayo sharti tuya-ishi ili kupokea uzima wa milele.

“• Na jinsi sharti tuishi ili tuweze kuvumilia hadi mwisho na kurudi kwa Baba yetu wa Mbinguni kwa heshima.

“Hizi kweli ni muhimu sana kwamba Baba wa Mbi-nguni aliwapatia wote Lehi na Nefi maono wazi kabisa

yakiashiria neno la Mungu kama fimbo ya chuma. Wote baba na mwana walijifunza kwamba kwa kushikilia huu mwongozo imara, usiopinda, wa kuaminika kabisa ndiyo njia pekee ya kukaa katika ile njia iliyosonga na nyembamba ielekeayo hadi kwa Mwokozi wetu” (“Holy Scriptures: The Power of God unto Our Salva-tion,” Ensign or Liahona, Nov. 2006, 25).

1 Nefi 5:18–19. Mabamba ya shabaMzee Bruce R. McConkie wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alishuhudia umuhimu wa familia ya Lehi kupata mabamba ya shaba:

“Thamani ya Mabamba ya Shaba kwa Wanefi haiwezi kukadiriwa kupita kiasi. Kwa sababu yake waliweza kuhifadhi lugha 1 Nefi 3:19), wingi wa ustarabu, na elimu ya kidini ya watu wa kutoka kule walikotoka. 1 Nefi 22:30.) Kwa njia ya utofautishaji, Wamuleki, wale waliongozwa kutoka Yerusalemu miaka 11 baada ya kuondoka kwa Lehi, na ambao hawakuwa na kumbu-kumbu ya kulinganishwa na Mabamba ya Shaba, punde walififia katika uasi na kutoamini na kupoteza lugha, ustarabu, na dini yao. (Omni 14–18.)

“Kutoka nabii hata nabii na kizazi hata kizazi Ma-bamba ya Shaba yalikuwa yakikabidhiwana na ku-hifadhiwa na Wanefi. (Mosia 1:16; 28:20; 3 Nefi 1:2.) Katika wakati fulani katika siku za usoni Bwana aliahidi kuyaleta tena, bila kufifishwa na nyakati na kubakiza mng’ao wake wa asili, na matukio ya kimaandiko yaliyoandikwa juu yake ili ‘yasonge mbele hata kwa kila taifa, ukoo, ndimi, na watu.’ (Alma 37:3–5; 1 Nefi 5:18–19.)” (Mormon Doctrine, 2nd ed. [1966], 103).

Mawazo ya Ziada ya Kufunza1 Nefi 5:21. Pekua maandikoUliza darasa, liimbe au kusoma maneno ya “As I Search the Holy Scriptures” (Wimbo, nambari. 277). Waalike wanafunzi kutafuta maneno katika wimbo ambayo yanaelezea baraka ambayo inayotokana na kupekua maandiko. Waulize wanafunzi watambue maneno ambayo yana maana kwao na waelezee kwa nini wana-yapenda hayo maneno.

Unaweza kutaka kusoma na kufuatia taarifa ya Rais Marion G. Romney wa Urais wa Kwanza:

“Ni hakika kwamba kama, katika nyumba zetu, wazazi watasoma kutoka katika Kitabu cha Mormoni

kwa maombi na kila mara, wote peke yako na pamoja na watoto wao, roho ya hicho kitabu kikuu itakuja kuenea nyumbani mwetu na kwa wale wanaoishi ndani yake. Roho ya staha itaongezeka; heshima kwa wote na kufikiriana kutaongezeka. Roho ya ubishi itaondoka. Wazazi watawashauri watoto wao kwa upendo na hekima kuu. Watoto watakuwa wasikivu zaidi na wenye kukubali ushauri huo. Wema utaonge-zeka imani, matumaini, na hisani—upendo kamili wa Kristo—utazagaa katika nyumba zetu na maisha yetu, kusababisha kuzinduka kwao, amani, shangwe, na furaha (katika Conference Report, Apr. 1960, 112–13; quoted by Ezra Taft Benson, “Cleansing the Inner Vessel,” Ensign, May 1986, 6).

Page 48: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

33

SOMO LA 10

1 nefi 6 na 9

Mapendekezo ya Kufundisha

1 Nefi 6Nefi aliandika ili kuwashawishi wote kuja kwa Yesu KristoOnyesha vitabu au sinema kadha zilizo nzuri ambazo zinapendwa na vijana leo. Waulize wanafunzi kile wanahisi kilikuwa madhumuni ya mwandishi au mtunzi kwa kila kitabu au sinema. Shikilia juu nakala ya Kitabu cha Mormoni. Waambie wanafunzi kwamba katika 1 Nefi 6, Nefi alielezea madhumuni yake ya kuandika kumbukumbu yake ambayo hati-maye ilikuja kuwa sehemu ya Kitabu cha Mormoni.Acha wanafunzi wasome 1 Nefi 6:3–6 na watafute maneno na misemo ambayo inaonyesha dhamira ya Nefi ya kuweka kumbukumbu zake. (Unaweza kushauri kwamba wanafunzi waweke alama haya maneno.)• Kwa nini ni muhimu kwamba Nefi aandike mambo “ambayo yanapendeza kwa Mungu”

na sio mambo “ambayo yanapendeza kwa ulimwengu”?• Unaweza kusemaje juu ya dhamira ya Nefi kwa maneno yako mwenyewe? (Inaweza ku-

saidia kueleza kwamba maneno “Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo” inamaanisha Yesu Kristo. Unaweza kuwatia moyo wanafunzi kuandika Yesu Kristo katika maandiko yao karibu na 1 Nefi 6:4. Unaweza pia kuelezea kwamba jina la Yehova pia humaanisha Yesu Kristo. (Ona 1 Nefi 19:10; 2 Nefi 11:4, 6–7; ona pia Bible Dictionary, “Christ,” “Christ, Names of.”)

Ili kuwasaidia wanafunzi kutathimini kwamba Kitabu cha Mormoni ni ushuhuda mwi-ngine wa Yesu Kristo, waalike waende kwenye faharasa na wapitie haraka vichwa vyote vinavyohusiana na Yesu Kristo. Waulize wao kutambua njia chache ambazo kwazo Kitabu cha Mormoni hufunza kuhusu huduma ya Mwokozi.Alika mwanafunzi aandike kweli ifuatayo kwenye ubao: Dhumuni moja la Kitabu cha Mormoni ni kuwashawishi watu kuja kwa Yesu Kristo.• Kuelewa madhumuni ya Nefi ya kuandika kunaweza vipi kuathiri vile unavyopanga

kujifunza Kitabu cha Mormoni mwaka huu?Elezea jinsi Kitabu cha Mormoni kimekusaidia wewe kuwa karibu na Baba wa Mbinguni na Mwokozi. Waalike wanafunzi kuelezea jinsi Kitabu cha Mormoni kimeathiri maisha yao na kuwaleta wao karibu na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Watie moyo ili waelezee hisia zao kwa rafiki au mwanafamilia kuhusu Kitabu cha Mormoni na ushuhuda wao juu ya Yesu Kristo katika siku kadhaa zifuatazo.

1 Nefi 9Nefi aliweka seti mbili za mabambaOnyesha darasa kitabu cha historia, na onyesha kila kipindi ambapo kitabu kinahusisha. Kisha onyesha darasa historia ya kibinafsi, shajara, au kitabu cha kumbukumbu ambacho ni cha kipindi hicho hicho. (Kama inavyofaa, soma uzoefu wa kiroho kutoka kwa shajara.)

UtanguliziNefi alitangaza, “Kwani lengo langu kamili ni ku-washawishi watu waje kwa Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo ili waokolewe” (1 Nephi 6:4). Aliweka seti mbili za kumbukumbu: ma-bamba madogo ya Nefi na mabamba makubwa ya Nefi. Bwana alimwamuru yeye kufanya ufupisho wa taarifa

ya Lehi kwenye mabamba madogo (ona 2 Nefi 5:28–31). Baadaye, Mormoni alipata maongozi kujumuisha mabamba madogo katika kufanya mkusanyo wa Kitabu cha Mormoni (ona Maneno ya Mormoni 1: 6–7). Si Nefi wala Mormoni aliyejua kwa nini, lakini wote walifuata maelekezo ya Bwana.

Elezea, toa, au shuhudia nje ya darasaWanafunzi wanapotoa shuhuda zao nje ya da-rasa, ufahamu wao wa kweli wanazojifunza ka-tika darasa huota mizizi. Watie moyo watafute nafasi za kufundisha na kushuhudia kanuni za injili wanaposhiriki-ana na wanafamilia na marafiki.

Page 49: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

34

SoMo la 10

• Je! Haya maandishi mawili yana tofautiana vipi katika mpangilio wao wa kuandika historia?

• Je! Andiko moja lina thamani kushinda lingine? Kivipi? (Kila moja lina thamani kwa sababu tofauti.)

• Je! Haya maandishi yanalingana vipi na Kitabu cha Mormoni?Elezea kwamba katika 1 Nefi 9:1–5, Nefi alielezea kuhusu juhudi zake za kuweka kumbu-kumbu katika seti mbili za mabamba.Seti moja ya mabamba, ambayo sasa inajulikana kama mabamba ya Nefi, aliandika “his-toria ya watu [wake]” (1 Nefi 9:2). Historia hii ina “taarifa za enzi ya wafalme, na vita na mabishano ya watu [wake]” (1 Nefi 9:4). Ilikuwa ni kumbukumbu ya kwanza ambayo Nefi alifanya, lakini haikujumishwa katika kile tulicho nacho sasa kama Kitabu cha Mormoni.Katika seti ingine ya mabamba, ambayo sasa inajulikana kama mabamba madogo ya Nefi, aliandika “huduma ya watu [wake]” (1 Nefi 9:3). Unaweza kuhitaji kuelezea kwamba neno huduma linalenga ufundishaji na shughuli za dini. Kumbukumbu ya Nefi katika mabamba madogo sasa inapatikana katika kitabu cha 1 Nefi na 2 Nefi. Ili kuwasaidia wanafunzi kutofautisha kati ya mabamba madogo na mabamba makubwa wanaposoma {1 Nephi 9, andika yafuatayo kwenye ubao: “haya mabamba”=mabamba madogo na “yale mabamba mengine”=mabamba makubwa. (Unaweza kushauri kwamba wa-nafunzi waandike maneno haya katika maandiko yao mkabala na mistari husika.) Katika 1 Nefi 9, maneno “mabamba haya” kila mara humaanisha mabamba madogo. Maneno “yale mabamba mengine” humaanisha mabamba makubwa.Muulize mwanafunzi asome 1 Nefi 9:3, 5–6 kwa sauti.• Ni sababu gani Nefi alizotoa za kutengeneza mabamba madogo kama ziada ya maba-

mba makubwa? Je! Maelezo haya yanaonyesha vipi imani ya Nefi katika Bwana?Elezea kwamba kwa karibu miaka 1,000 baadaye, nabii Mormoni alitengeneza muhtasari, au toleo lililofupishwa, la kumbukumbu zote ambazo zimeandikwa kwa watu wake. Hii imekuja kujulikana leo kama Kitabu cha Mormoni. Alivyotengeneza muhtasari, alipata mabamba madogo ya Nefi na kuyaingiza katika kumbukumbu zake.Alika mwanafunzi kusoma Maneno ya Mormoni 1:3–7 kwa sauti. Elezea kwamba Mor-moni aliandika haya maneno karibu miaka 385 K.K wakati wa vita vya mwisho kati ya Wa-nefi na Walamani. Wanafunzi wanaposoma hii mistari, acha wao watafute sababu ambazo Mormoni alitoa kwa kujumuisha mabamba ya Nefi katika ufupisho.Soma taarifa ifuatayo ya Mzee Marvin J. Ashton wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili:

“Wakati mwingine tunapoamriwa kuwa watiifu, hatujui kwa nini, bali Bwana ameamuru. Nefi alifuata maelekezo hata ingawa hakujua kikamilifu madhu-muni ya hekima. Utiifu wake ulileta baraka kwa wanadamu wote ulimwe-nguni kote” Mzee Marvin J. Ashton Ensign, Nov. 1978, 51).Taja kwamba kutokana na mfano wa Nefi na Mormoni, tunajifunza kwamba tunafaa kutii amri za Mungu na kufuata maongozi ya Roho hata wakati

hatuelewi kikamilifu sababu zake.• Ni kwa nini ni muhimu kutii amri za Bwana na kufuata msukumo kutoka kwa Roho

hata kama hatuelewi kikamilifu sababu zake?• Ni wakati gani wewe ulikuwa mtiifu kwa Bwana au kufuata msukumo fulani bila ya

kuelewa kikamilifu sababu zake?• Tunawezaje kukuza imani kuu na ujasiri wa kuwa mwaminifu kwa maelekezo ya

Mungu?Shuhudia kwamba tunapotii amri za Mungu na maongozi ya Roho Mtakatifu, uelewa wetu wa madhumuni husika utakua, na Bwana atatubariki sisi kwa utiifu wetu.Acha mwanafunzi asome maelezo yafuatayo kwa sauti. (Unaweza kumpatia kila mwana-funzi nakala ndogo ili waweze kufuatia na kuiweka katika maandiko yao kwa marejeo ya wakati ujao.) Angalau sehemu ya “madhumuni ya hekima” ya Bwana (1 Nefi 9:5; Maneno ya Mormoni 1:7) ya kumfanya Nefi kuweka seti mbili za kumbukumbu ikawa wazi wakati Joseph Smith alipotafsiri Kitabu cha Mormoni. Joseph awali alitafsiri ufupisho wa Mormoni wa mabamba makubwa ya Nefi. Martin Harris, ambaye alikuwa anamsaidia Joseph, alitaka kuonyesha

Page 50: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

35

1 nefi 6 na 9

tafsiri kwa mke wake na familia yake. Kwa shingo upande, Nabii alikubali Martin aazime kurasa 116 za mswaada ambazo zilikuwa zimemalizika wakati huo. Hizi kurasa 116 zilii-biwa kutoka kwa Martin, na, matokeo yake, mabamba, Urimu na Thamimu, na kipawa cha kutafsiri kwa muda kilitwaliwa kutoka kwa Joseph Smith (ona M&M 3:14).Baada ya Joseph Smith kupitia kipindi cha toba (ona D&C 3:10), Bwana alimwambia asitafsiri sehemu iliyopotea (ona M&M 10:30). Badala yake Yeye alimwamuru kutafsiri mabamba madogo ya Nefi (ona M&M 10:41), ambayo yalichukua kipindi cha muda ule ule. Yeye alimweleza Joseph kwamba wale ambao waliochukua zile kurasa 116 walikuwa wamezibadilisha na kupanga kuzitumia kukashifu kazi hii (ona M&M 10:10–19). Bwana alikuwa ameona haya matukio mamia ya miaka mapema na akatoa kumbukumbu ya pili ili kushinda mpango wa Shetani. (Ona History of the Church, 1:20–23; M&M 10:38–46.)Waalike wanafunzi kusoma 1 Nefi 9:6 kibinafsi. Waulize wao kutambua fundisho ambalo Nefi anafunza katika mstari huu. Acha mwanafunzi aandike kanuni ifuatayo kwenye ubao: Mungu anajua mambo yote na hutayarisha njia ya kutimiza kazi Yake yote.• Kwa nini inasaidia kujua kwamba “Bwana anajua mambo yote kutoka mwanzoni”?

1 Nefi 9:6; ona pia 2 Nefi 9:20; Maneno ya Mormoni 1:7.)• Je! Hili fundisho linaweza kushawishi vipi jinsi unavyoishi? (Wanafunzi wanapojibu

swali hili, unaweza kueleza mawazo yako kuhusu jinsi hili fundisho limeongezea imani yako, matumaini, na kuamini katika Mungu.)

• Je! Hili fundisho linaweza kukusaidia vipi unapokabiliana na majaribu? (Jibu kwa kawa-ida linaweza kuwa kwamba tunaweza kupata faraja katika hakikisho kwamba Mungu anaweza kuona matokeo ya majaribu na changamoto zetu, hata kama hatuwezi. Na kupitia Roho Mtakatifu, Yeye anaweza kutupatia nguvu, faraja, na maelekezo ya kushi-nda au kuvumilia shida za maisha.)

Onyesha uthibitisho wako kwamba Mungu anajua mambo yote, ikijumuisha kile kilicho chema kwa kila mtoto Wake. Wasaidie wanafunzi kuona kwamba kote katika maisha yao, watapata amri na kupokea maongozi kutoka kwa Mungu ambayo hawaelewi kikamilifu hapo mwanzoni. Utiifu wao kwa amri za Bwana na msukumo wa Roho Mtakatifu utabariki maisha yao wenyewe na maisha ya wengine.

Tangazo na Habari za Usuli1 Nefi 6:4. “Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo”Rais Ezra Taft Benson alieleza kwamba wakati maa-ndiko yakitaja Mungu wa Ibahimu, Isaka, na Yakobo, yalikuwa yanamtaja Yesu Kristo: “Sisi ni sharti tuelewe Yesu alikuwa nani kabla Yeye hajazaliwa. Yeye alikuwa Muumba wa vitu vyote, Yehova mkuu, Mwanakondoo aliyechinjwa kabla msingi wa ulimwengu, Mungu wa Ibrahimu, Isaka, na Yakobo. Yeye alikuwa na ndiye Mta-katifu wa Pekee wa Israeli” (“Five Marks of the Divinity of Jesus Christ,” Ensign, Dec. 2001, 10).

1 Nefi 9:6. Mungu anajua mambo yote kutoka mwanzoTunaweza kuwa na imani kwamba Mungu anajua mambo yote. “Bila elimu ya mambo yote Mungu hangeweza kuokoa sehemu yoyote ya viumbe vyake; kwani ndiyo sababu ya elimu aliyonayo ya mambo yote, kutoka mwanzo hadi mwisho, ambayo inamwezesha kuwapatia viumbe vyake huu uelewa ambao kwao wanafanywa washiriki wa uzima wa milele; na kama haingekuwa dhana iliyopo ndani mwa akili za bina-damu kwamba Mungu alikuwa na elimu yote ingekuwa vigumu kwao kuwa na imani katika yeye” (Lectures on Faith [1985], 51–52).

Page 51: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

36

Somo la Mafunzo ya Nyumbani1 Nefi 1–6; 9 (Kitengo cha 2)

Vifaa vya Matayarisho kwa Mwalimu wa Mafunzo ya NyumbaniMuhtasari wa Masomo ya Kila Siku ya Mafu-nzo ya NyumbaniMuhtasari ufuatao wa mafundisho na kanuni wanafunzi wa-lijifunza walipokuwa wakisoma 1 Nefi 1–6; 9 (Kitengo cha 2) haikupangiwa kufunzwa kama sehemu ya somo lako. Somo unalofunza linazingatia tu machache ya haya mafundisho na kanuni. Fuata msukumo wa Roho Mtakatifu unapofikiria mahitaji ya wanafunzi.

Siku ya 1 (1 Nefi 1)Wanafunzi wanapojifunza kuhusu unabii wa Lehi kwa watu na onyo kwao la kutubu, walijifunza kwamba manabii huonya dhidi ya kutenda dhambi na hufunza wokovu kupitia Yesu Kristo. Kwa ziada, walijifunza kwamba neema nyororo za Bwana huwafikia wale ambao wanafanya imani katika Yeye.

Siku ya 2 (1 Nefi 2)Lehi alijibu amri ya Bwana kwa kuondoka Yerusalemu. Alionyesha kwa mfano kanuni kwamba kama tukiwa waaminifu na watiifu, Bwana atatusaidia katika nyakati za majaribu. Nefi alionyesha roho wa utii na kujifunza mwe-nyewe kwamba wakati tunamuomba Mungu, Yeye anaweza kulainisha mioyo yetu kuamini maneno Yake. Wanafunzi walijifunza kwamba Mungu hubariki wale ambao ni watiifu na waaminifu.

Siku ya 3 (1 Nefi 3–4)Wakati Lehi alimwambia Nefi na nduguze juu ya amri ya Mungu ya wao warudi Yesusalemu na kuchukua mabamba ya shaba, Nefi alijibu kwa kushuhudia kwamba kama wata-fanya kile ambacho Bwana ameamuru, basi Yeye angetaya-risha njia kwa wao kuitimiza. Nefi na ndugu zake waliona kuwa ilikuwa ni vigumu kutimiza amri ya Bwana. Azimio la Nefi la kurudi Yerusalemu liliwasaidia wanafunzi kuona kwamba wakati tunafanya imani katika Mungu na kutafuta kufanya kile ametuamuru, hata wakati hatuwezi kuona matokeo yake, Yeye atatuongoza kwa Roho Mtakatifu.

Siku ya 41 Nefi 5–6; 9)Wanafunzi walipojifunza kuhusu uzoefu wa Lehi wa kutafuta mabamba ya shaba, waligundua kanuni ifuatayo: Tunapopekua maandiko, tutajawa na Roho Mtakatifu na kupokea ufunuo. Walipojifunza juu ya madhumuni ya Nefi ya kuandika kumbukumbu yake, wanafunzi pia walijifunza kwamba madhumuni ya Kitabu cha Mormoni ni kuwashawi-shi watu wote kuja kwa Yesu Kristo.

UtanguliziSomo la wiki hii litawapatia wanafunzi nafasi ya kurejea na kujadiliana kile walichojifunza kutoka katika mfano wa familia ya Lehi na matendo yao ya imani. Unapofundisha somo hili, sisitiza utiifu na uaminifu wa Nefi kwa amri za Bwana na bidii yake katika kutafuta kujua ukweli wa “maneno yote ambayo baba [yake] alikuwa amezungumza”(1 Nefi 2:16). Wanafunzi wanapofuata mfano wa Nefi wa utiifu, watajenga shuhuda zao wenyewe za injili.

Katika ufunzaji wako, fuata wasia wa Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili:

“Ni sharti sisi tuchangamshe na kuinua ufunzaji bora katika Kanisa—huko nyumbani, kutoka kwenye mimbari, na katika mikutano yetu ya usimamizi, na hasa katika darasa. Ufunzaji wenye maongozi sharti usiwe sanaa iliyopotea katika Kanisa, na ni lazima tuhakikishe utafutaji wetu wa huu ufunzaji hautakuwa desturi iliyopotea. . . .

“. . . Na tuinue uzoefu wa ufunzaji katika nyumba na katika Kanisa na tuimarishe juhudi zetu zote ili kuelimisha na kufunza” (“ A Teacher Come from God,” Ensign, May 1998, 25, 27).

Mapendekezo ya Kufundisha

1 Nephi 1Bwana hutoa neema Zake nyororo kwa mwaminifuAndika kanuni ifuatayo kwenye ubao: Neema nyororo za Bwana zinatolewa kwa wale wanaofanya imani katika Yeye. Waalike wanafunzi kupitia 1 Nefi 1 na kutambua mstari ambao hii kweli inafundishwa (mstari wa 20).

Uliza maswali yafuatayo ili kuwasaidia wanafunzi kukumbuka na kufanya muhtasari wa kile wamejifunza walipokuwa wakisoma 1 Nefi 1–6; 9 wakati wa wiki:

• Kutokana na kile umejifunza katika sura ulizosoma wiki hii, Bwana alitoa vipi neema Zake nyororo kwa Lehi na familia yake?

• Ni mifano gani ya utiifu na imani iliyoonyeshwa na Lehi na familia yake?

• Ni lini uliona Bwana akitoa neema Zake nyororo kwako au kwa mtu unayemjua?

Unaweza kutaka kusema kuhusu wakati ambao Bwana alitoa neema kwako na familia yako ulipofanya kwa imani, au elezea uzoefu uliopata katika machapisho ya Kanisa. Watie moyo wana-funzi kutafuta mifano ya Bwana akitoa neema Zake kwa waami-nifu wanaposoma Kitabu cha Mormoni katika mwaka wote.

1 Nefi 2Bwana anaweza kulainisha mioyo yetu ili kuamini maneno YakeWakumbushe wanafunzi kwamba Lehi aliamriwa kuondoka Ye-rusalemu pamoja na familia yake, mwanawe Nefi alifanya juhudi

Page 52: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

37

SoMo la MafUnzo ya nyUMbani

za kibinafsi ili kujua na kuelewa ukweli wa maono ya Baba yake. Alika mwanafunzi asome 1 Nefi 2:16, 19 kwa sauti.

Waulize wanafunzi: Ingawa Nefi hakunung’unika, kuna ushihidi gani uliopo katika 1 Nefi 2:16 kwamba kuondoka Yesusalemu kungekuwa na ugumu kwake? (Nefi aliandika kwamba yeye aliomba apate ufahamu na Bwana alainishe moyo wake. Hii ina-dokeza kwamba kuondoka Yesusalemu haikuwa rahisi kwake, kwa hivyo Bwana alimsaidia kukubali.)

Uliza: Ni ushahidi gani unaoona ambao ingawa Lehi na familia yake walikuwa watiifu kwa Bwana, maisha hayakuwa rahisi kwao? (Ona 1 Nefi 2:4, 11.)

Waulize wanafunzi waeleze mawazo waliyonayo kuhusu hamu ya Nefi na kuhusu kile alichofanya ambacho kilimfanya kukubali amri za Bwana zilizotolewa kupitia baba yake.

Waalike wanafunzi wachache waelezee kile walichoandika katika shajara zao za kujifunza maandiko kwa siku ya 2; kazi ya 4: Toa mfano wa wakati ambapo, kama vile Nefi, ulimwomba Baba wa Mbinguni na kupata uzoefu wa kulainisha moyo wako kupitia Roho au wakati ulipopokea ushuhuda wa kitu ambacho Bwana alisema.

Toa ushuhuda wako mwenyewe kwamba wakati tunapo-mwomba Mungu, Yeye anaweza kulainisha mioyo yetu ili tuamini maneno Yake.

Waulize wanafunzi kufikiria kile wanachoweza kufanya ili kui-marisha ushuhuda wao na kupokea hakikisho la kibinafsi, kama Nefi alivyofanya. Wapatie nafasi ya kutoa mawazo yao kama wanataka kufanya hivyo. Watie moyo kutenda juu ya fikra zao na mawazo yao.

1 Nefi 3–4Bwana atatayarisha njia tunapotii amri Zake kwa uaminifu.Mpatie kila mwanafunzi kazi pamoja na mwenziwe. Andika marejeo ya maandiko yafuatayo kwenye ubao: 1 Nefi 3:6–7 na 1 Nefi 4:6–13. Waalike wanafunzi wasome vifungu na kujadili maswali yafuatayo na wenzi wao:

• Unafikiria kwa nini ni muhimu kuhusu kauli ya Nefi “Walakini niliendelea mbele”? (1 Nefi 4:7).

• Je! Imani ya Nefi ilimwezesha kupata mabamba ya shaba?

Baada ya wanafunzi kujadili mawazo yao na wenzi wao, elezea kwamba Bwana anaweza kutuamuru sisi kufanya kitu, kama vile Yeye alivyofanya kwa Nefi na nduguze, bila kufunua mara moja kwa nini, lini, au kwa jinsi gani tunaweza kufanya. Nefi alijifunza kwa nini, lini, na jinsi Bwana alimsaidia yeye baada tu yeye kuku-bali Roho amwelekeze yeye na baada ya yeye kuamua kusonga mbele katika imani. Toa ushuhuda wako kwamba wakati tuna-fanya imani katika Mungu na kutafuta kufanya kile Yeye ametuamuru, hata wakati hatuwezi kuona matokeo, Yeye atatuongoza sisi kwa ushawishi wa Roho Mtakatifu.

Kama wakati unaruhusu, unaweza kuwauliza wanafunzi kama wana maswali au wanataka kutoa mawazo kutokana na masomo yao ya siku ya 4 1 Nefi 5–6; 9. Kwa mfano, unaweza kuwaalika wao kuelezea jinsi wanavyoweza kufanya katika kazi ya 4, ambayo kwayo waliulizwa kuandika kuhusu wakati walipo-kuwa wanapekua maandiko na kuhisi Roho wa Bwana.

Hitimisha kwa kuuliza mwanafunzi kusoma kwa sauti (au kuka-riri kutoka akilini) kifungu cha umahiri wa maandiko 1 Nefi 3:7 Kisha uliza maswali yafuatayo:

• Ni kanuni gani 1 Nefi 3:7 inafunza kuhusu utiifu kwa amri za Bwana? (Mwanafunzi anapaswa kuweza kuonyesha kanuni kwamba ikiwa tutatafuta kufanya kile Bwana anaamuru, Yeye atatayarisha njia ili tuweze kukikamilisha.)

• Kulingana na kile mmesoma katika 1 Nefi 1–6 na 9 , ni nini ili-kuwa matokeo ya utiifu wa Lehi na Nefi kwa amri za Mungu?

• Ni wakati gani Bwana alitayarisha njia ya kukusaidia kutii amri?

Waalike wanafunzi kutafakari sehemu moja ambayo kwayo wanaweza kuonyesha kikamilifu zaidi utiifu wao kwa Mungu. Unaweza kutaka kumaliza somo kwa kushuhudia juu ya baraka ambazo zimekuja katika maisha yako kupitia juhudi zako za kutii amri za Bwana.

Kitengo Kifuatacho (1 Nefi 7–14)Katika kitengo kifuatacho, wanafunzi wanaweza kujifunza maono ya Lehi na Nefi. Maono ya Lehi na Nefi ya mti wa uzima yanatumika katika maisha yetu leo. Taarifa ya Nefi ya ono lake inajumuisha maelezo ya kuzaliwa, huduma, na Upatanisho wa Yesu Kristo; uvumbuzi na kutawaliwa kwa Amerika na Wayu-nani; na kupotea kwa kweli muhimu kutoka kwenye Biblia na urejesho wake kupitia Kitabu cha Mormoni. Taarifa ya Nefi ya ono lake ilikuwa na maelezo ya Urejesho wa injili.

Page 53: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

38

Mapendekezo ya Kufundisha

1 Nefi 7:1–5Bwana alimwanuru Nefi kurudi Yerusalemu kwa Ishmaeli na familia yakeOnyesha picha ya wenzi waliooana na watoto wao. (Unaweza kutumia picha ya familia yako mwenyewe.)Alika mwanafunzi asome 1 Nefi 7:1–2 kwa sauti.• Je! Bwana aliwaamuru wana wa Lehi kufanya nini? Je! Ni kweli gani tunajifunza kutoka

katika amri hii? (Hakikisha wanafunzi wanaelewa kwamba Bwana hutuamuru sisi kuoa na kulea watoto kwa njia Yake.)

Wakumbushe wanafunzi kwamba ingechukua siku kadhaa za safari ngumu kupitia nyikani kwa Nefi na ndugu zake kurudi Yerusalemu.• Je! Kwa nini ndoa na familia vina umuhimu wa kutosha kwa Nefi na ndugu zake kusafiri

tena kurudi Yerusalemu kukutana na Ishmaeli na familia yake?Kabla ya kuendelea, unaweza kumpatia kila mwanafunzi nakala ya “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu” au acha waende kwenye nakala ya tangazo katika shajara zao za kujifunza maandiko.Muulize mwanafunzi kusoma kwa sauti kauli ifuatayo kutoka katika “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu.” Waalike wanafunzi kusikiliza kwa makini na kutambua kile ambacho mana-bii wa siku za mwisho wametangaza kuhusu umuhimu wa ndoa.Sisi, Urais wa Kwanza na Baraza la Mitume Kumi na Wawili wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, tunatangaza kwa heshima kwamba ndoa kati ya mwa-naume na mwanamke imetakaswa na Mungu, na kwamba familia ni ya muhimu katika mpango wa Muumba kwa maisha ya milele ya watoto Wake. (“Familia: Tangazo kwa Ulimwengu.”Ensign, Nov. 2010, 129). Waalike wanafunzi wachache waelezee kile wamejifunza kutoka katika taarifa hii. Hakiki-sha kwamba wanaelewa kuwa familia ni kitovu cha mpango wa Muumba kwa hatima yetu ya milele. Sisitiza kwamba hii ndio sababu Bwana alimwamuru Nefi na ndugu zake kualika familia ya Ishmaeli kuenda kuungana nao. Elezea pia kwamba mojawapo ya sababu mu-himu ya ndoa ni kuleta watoto katika ulimwengu.• Je! Unafikiria inamaanisha nini kulea watoto “kwa Bwana”? (1 Nefi 7:1).Baada ya wanafunzi kujibu swali hili, watie moyo kusikiliza mawazo ya ziada wanapo-soma taarifa ifuatayo kutoka katika tangazo la familia. Kama wana nakala zao wenyewe za tangazo, unaweza kutaka kushawishi kwamba waweke alama maneno na vishazi ambavyo ni muhimu kwao.Tunatangaza kwamba amri ya Mungu kwa watoto Wake ya kuzaana na kujaza dunia ime-baki ikizingatiwa. . . .“. . . Wazazi wana jukumu takatifu la kulea watoto wao katika upendo na utakatifu, ku-kimu mahitaji yao ya kimwili na kiroho, na kuwafundisha kupenda na kutumikiana mmoja na mwingine, kutii amri za Mungu, na kuwa raia wenye kutii sheria popote wanapoishi. Wanaume na wanawake—kina mama na kina baba—watawajibika mbele za Mungu kwa kutofanya majukumu haya” (“The Family: A Proclamation to the World,” 129)

Utangulizi1 Nefi 7 inajumuisha mifano ya kujitolea kwa Nefi kwa Mungu. Nefi alitii wakati Bwana alipomwamuru yeye na ndugu zake kurudi na kumwomba Ishmaeli na familia yake kujiunga nao huko nyikani ili waweze

kuoana na kulea watoto. Hata wakati Lamani na Lemu-eli walipoasi dhidi ya Nefi na wakajaribu kumuua, yeye alibakia mwaminifu na kujaribu kuwasaidia wao kuwa waaminfu pia.

Kutumia tangazo la familiaDada Julie B. Beck, Rais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, aliwatia moyo walimu wa seminari na chuo ku-funza kuhusu umuhimu wa familia na kutumia tangazo la familia katika masomo yao.“Katika Kanisa, jambo la msingi ni kufundi-sha kanuni za familia, kanuni ambazo zitawa-fundisha [wanafunzi] kuunda familia, na kufunza familia hiyo, na kuitayarisha hiyo familia kwa kwa ajili ya ibada na maagano. . . .“. . . Wakati unawafunza wao, unaweza kuu-nganisha mafundisho na kauli muhimu na vipengele ambavyo vimo katika tangazo juu ya fa-milia. Tangazo sio somo pekee” (“Teaching the Doctrine of the Family” [Seminaries and Institu-tes of Religion satellite broadcast, Aug. 4, 2009], 5, si.lds.org).

SOMO LA 11

1 nefi 7

Page 54: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

39

1 nefi 7

Alika mwanafunzi asome 1 Nefi 7:3–5 kwa sauti.• Ni kwa namna gani taarifa katika 1 Nefi 7:3–5 ni mfano wa kweli katika 1 Nefi 3:7? (Wa-

saidie wanafunzi kuona kwamba Bwana ametayarisha njia kwa Nefi na ndugu zake kutii amri ya kuoa na kuwa na watoto.)

• Je! Vijana wanaweza vipi kujitayarisha kuoa na “kulea” watoto katika injili?

1 Nefi 7:6–15Akikabiliwa na uasi wa Lamani na Lemueli, Nefi alishuhudia uwezo wa Bwana wa kuwaongoza wao hata nchi ya ahadiAlika mwanafunzi asome 1 Nefi 7:6–7 kwa sauti.• Kwa nini Lamani na Lemueli, na baadhi ya watoto wa Ishmaeli waliasi wakati wa safari

yao nyikani?Watie moyo wanafunzi kufikiria kuhusu wanachoweza kusema kwa Lamani, Lemueli, na wana waasi na mabinti wa Ishmaeli kuwashawishi wao kuendelea na safari yao hata nchi ya ahadi. Kisha waulize wanafunzi wasome 1 Nefi 7:8–12 kimya kimya na kutambua maswali ambayo Nefi aliwauliza Lamani na Lemueli.• Ni kweli gani ambazo Nefi alizitoa alipouliza maswali haya? (Yeye aliwakumbusha

ndugu zake baraka walizokuwa tayari wamepokea kutoka kwa Bwana na uwezo wa Bwana wa kuendelea kuwabariki wao kulingana na imani yao.)

• Kwa nini ni muhimu kwetu kukumbuka kweli hizi?Alika wanafunzi wasome 1 Nefi 7:13–15 na kutambua matokeo kama Lamani, Lemueli na wana waasi na mabinti wa Ishmaeli wangerudi Yerusalemu.

1 Nefi 7:16–22Nefi alikombolewa na BwanaElezea kwamba baada ya Nefi kuwakumbusha Lamani na Lemueli kuhusu maangamizo ambayo yangekuja kwa wale waliokuwa Yesusalemu, walimkasirikia.Alika mwanafunzi asome 1 Nefi 7:16 kwa sauti. Uliza darasa kufikiria kuwa katika hali ya Nefi.• Je! Ungehisi vipi kama ungekuwa katika hali ya Nefi? Ungefanya nini?Sema kwamba Nefi alijibu hali hii kwa maombi ya usaidizi. Muulize mwanafunzi asome maombi ya Nefi katika 1 Nefi 7:17–18 kwa sauti.• Nefi aliombea nini? Umegundua nini kuwa cha muhimu kuhusu maombi yake?Wanafunzi wanapotoa majibu yao, hakikisha wanaona kwamba Nefi aliomba kukombo-lewa “kulingana na imani [yake].” Pia taja kwamba alipoomba ukombozi kutoka kwa ndugu zake, alimwomba Mungu kumuimarisha yeye ili aweze kushughulia shida hizo. Ele-zea kwamba kuomba kwa imani humaanisha kwamba tuombe kwa imani katika Bwana na kwa hiari ya kutenda. Alika mwanafunzi asome taarifa ifuatayo ya Mzee David A. Bednar wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili:

“Nefi alikuwa mfano wa mtu ambaye alijua na kuelewa na kutegemea uwezo unaowezesha wa Mwokozi. Tafadhali tazama maombi ya Nefi katika mstari wa 17: ‘Ewe Bwana, kulingana na imani yangu kwako, unikomboe kutoka mikononi mwa ndugu zangu; ndio, hata unipatie nguvu ili nizikate kamba ambazo nimefungwa nazo. (mkazo umeongezewa). Inapendeza hasa kwangu kwamba Nefi hakuomba kupata hali yake iba-

dilishwe. Badala yake, aliomba apate nguvu za kubadilisha hali yake. Na acha nishauri kwamba aliomba kwa njia hii kwa sababu alijua na kuelewa na kupata uzoefu wa uwezo za kuwezesha wa Upatanisho wa Mwokozi” (“In the Strength of the Lord” [Brigham Young University devotional address, Oct. 23, 2001], 4, speeches.byu.edu).Toa ushuhuda wako kwamba Mungu hujibu maombi kulingana na imani yetu. Taja kwamba katika hali hii, Mungu alijibu maombi ya Nefi mara moja kabisa. Hata hivyo, maombi hayajibiwi kwa njia hii kila mara. Baba wa Mbinguni hujibu maombi katika wakati

Page 55: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

40

SoMo la 11

Wake mwenyewe, katika njia Yake mwenyewe, na kulingana na mapenzi Yake. Wapatie wanafunzi nafasi ya kushuhudia uwezo wa maombi kwa kuwauliza swali lifuatalo:• Uliomba lini kwa imani na kupokea nguvu au usaidizi kutoka kwa Bwana, mara moja au

baada ya muda fulani? (Unaweza kuelezea uzoefu ambao umeupata juu ya kanuni hii.)Waambie wanafunzi kwamba Nefi alipokombolewa kutoka katika kamba zake, ndugu zake walijaribu kumshambulia tena. Alika mwanafunzi asome 1 Nefi 7:19–20 kwa sauti.• Ni nani aliwashauri Lamani na Lemueli kusitisha kumuua Nefi?Taja kwamba maombi yetu mara nyingi hujibiwa na mahitaji yetu mara nyingi hutimizwa kwa vitendo vya wengine. Darasa lako linapojifunza mistari iliyobakia ya 1 Nefi 7, waalike wanafunzi kuona jinsi Nefi alivyowajibu ndugu zake, hata baada ya yale waliyomtendea. Waulize wao kufikiria kuhusu swali lifutalo bila kujibu kwa sauti:• Je! Ulijibu vipi wakati watu wengine walipojaribu kukuumiza?Muulize mwanafunzi asome 1 Nephi 7:21 kwa sauti. Unaweza kushawishi kwamba wana-funzi waweke alama taarifa ya Nefi kuhusu msamaha.• Inamaanisha nini kusamehe wazi kabisa? (Kama wanafunzi hawana hakika, elezea kwa-

mba neno wazi humaanisha kwa uaminifu na moja kwa moja.)• Nefi aliwahimiza ndugu zake wafanye nini? Kwa nini ushauri ulikuwa muhimu?Shuhudia kwamba kutafuta msamaha na kuwasamehe wengine huleta umoja na imani. Alika wanafunzi kufikiria juu ya hali katika familia zao ambazo zilihitaji msamaha.• Kwa nini msamaha hasa ni muhimu kwa familia zetu?• Fikiria kuhusu wakati ambapo ulimsamehe mwanafamilia au wakati mwanafamilia

alikusamehe. Hii iliathiri vipi uhusiano wako na roho katika nyumba yao?Hitimisha kwa kuwakumbusha wanafunzi kwamba Bwana alimwamuru Nefi na ndugu zake kuwaoa na kuwa na familia na kwamba Bwana huhitaji hivyo leo. Pia shuhudia kwamba Bwana hujibu maombi yetu na hutupatia nguvu za kushinda shida zetu kulingana na imani yetu katika Yeye. Waalike wao kufikiria jinsi wanavyoweza kutumia mojawapo ya kanuni hizi katika somo la leo ili kusaidia familia zao.

Rejeo la Umahiri wa MaandikoTazama: Rejeo la umahiri wa maandiko linapatikana kote katika kijitabu hili. Tanguliza baadhi ya mbinu unazoweza kutumia kuwasaidia wanafunzi kurejea vifungu vya umahiri wa maandiko kila mara.Urefu wa somo hili unaweza kukupatia muda wa shughuli ifuatayo ya rejeo la umahiri wa maandiko. Unaweza kufanya shughuli hii hapo mwanzo wa darasa, kama pumziko katika sehemu za somo au mwisho wa darasa. Hakikisha imekuwa kwa muda mfupi ili kutoa muda wa somo. Kwa shughuli zingine za marejeo mengine, ona kiambatisho.Wanafunzi wanapoweza kupata vifungu vya umahiri wa maandiko kwa urahisi na kuelewa maana yake, maudhui, na matumizi yake, wataweza kujiamini sana katika kujifunza kwao kibinafsi, uwezo wao wa kutumia kanuni za injili, na katika nafasi zao za kufunza kutoka katika maandiko. Fikiria tamko lifuatalo la Rais Howard W. Hunter: “Tuna tumaini hakuna yeyote katika wanafunzi wenu atatoka darasani mwenu akiwa na hofu au akidhalilika ua ameaibika kwamba hawezi kupata usaidizi wanaohitaji kwa sababu hawaelewi maandiko vya kutosha kupata vifungu vifaavyo” (“Eternal Investments” [address to CES religious educators, Feb. 10, 1989], 2, si.lds.org).Ili kuwasaidia wanafunzi kujielimisha na kupata vifungu vya umahiri wa maandiko, waa-like wao kurejea alamisho la umahiri wa maandiko, wapate vifungu vitano vya kwanza vya umahiri katika maandiko yao, na wavisome. Unaweza kutaka kuwatia moyo wanafunzi kuweka alama kwenye vifungu vya umahiri wa maandiko kwa njia ya kipekee ili waweze kupata vifungu hivyo kwa urahisi.

Page 56: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

41

Mapendekezo ya Kufundisha

1 Nefi 8:1–18Lehi anapata ono ambalo kwalo yeye anakula tunda la mti wa uzima na kualika familia yake kufanya vivyo hivyoWaalike wanafunzi kufikiria kuhusu nyakati ambapo wamehisi upendo wa Baba wa Mbi-nguni kwao. Waulize wao wafikirie kimya kimya jinsi chaguzi zinavyoweza kuathiri kuwa kwetu karibu na Mungu na uwezo wa kuhisi upendo Wake. Baada ya kuwapatia wao muda wa kutafakari, toa ushuhuda wako kwamba Baba wa Mbinguni humpenda kila mmoja wao. Darasa linapojifunza 1 Nefi 8, watie moyo wanafunzi kutafuta mambo wanayoweza kufanya na vitu wanavyopaswa kuepukana navyo ikiwa wanataka kuwa karibu na Mungu na kuhisi upendo Wake kwa wingi sana katika maisha yao. (Ili kuwatayarisha wanafunzi kwa somo hili, unaweza kuwaalika wao kuimba “The Iron Rod” [Hymns, no. 274] hapo mwanzo wa darasa.)Alika mwanafunzi asome 1 Nefi 8:2 kwa sauti. Uliza darasa kutambua kile Lehi aliona muda mfupi baada ya wanawe kurudi kutoka Yerusalemu na mabamba ya shaba. Acha wanafunzi wachache kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka katika 1 Nefi 8:5–12.• Ni vyombo gani vilivyolengwa katika ono la Lehi? (Mti wa uzima na tunda lake.)• Ni maneno na vishazi gani Lehi alitumia kuelezea tunda ? (Ona 1 Nefi 8:10–11; unaweza

pia kutaka wanafunzi kusoma 1 Nefi 11:8–9 ili kuona jinsi Nefi alivyoelezea juu ya mti.)Elezea kwamba Bwana kila mara hutumia vyombo vya kawaida kama ishara za kutusai-dia kuelewa kweli za milele. Ili kuwasaidia wanafunzi kutambua kile mti na tunda ka-tika ndoto ya Lehi viliashiria, alika mwanafunzi asome taarifa ifuatayo ya Mzee Neal A. Maxwell wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili. Uliza darasa kusikiliza kwa makini na kutambua kile mti na tunda iliashiria.

“Mti wa uzima ni upendo wa Mungu (ona 1 Nefi 11:25). Upendo wa Mungu kwa watoto Wake unaonyeshwa kwa kina katika zawadi Yake ya Yesu kama Mkombozi wetu: ‘Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee’(Yohana 3:16). Kupata upendo wa Mungu ni kupata Upatanisho na ukombozi wa Yesu na shangwe inayopatikana” (“Lessons from Laman and Lemuel,” Ensign, Nov. 1999, 8).

• Kulingana na Mzee Maxwell, mti wa uzima huashiria upendo wa Mungu unaotolewa kwetu hasa kupitia zawadi gani? (Wasaidie wanafunzi kuelewa kwamba Upatanisho wa Yesu Kristo ni onyesho kuu la upendo wa Mungu kwa watoto Wake. Wakati watu katika ono la Lehi walikula tunda la mti wa uzima, ilimaanisha kwamba walikuwa wanapokea baraka za Upatanisho.)

• Ukombozi humaanisha kukomboa au kufanya huru. Je! Upatanisho wa Yesu Kristo hutu-weka huru vipi kutoka na utumwa na kutuletea sisi shangwe?

Ili kuwasaidia wanafunzi kutambua mojawapo ya kanuni zilizoonyeshwa katika 1 Nefi 8:10–12, waulize wao kutambua katika 1 Nefi 8:11 maneno ambayo yanaelezea kile Lehi alichokifanya (“Mimi nilisonga mbele na kula tunda”). Kisha wacha wao watafute mato-keo ya matendo yao katika 1 Nefi 8:12 (lilijaza nafsi yangu na shangwe tele” Unaweza pia

UtanguliziKatika1 Nefi 8, Lehi anasimulia ono lake la mti wa uzima. Katika ono, Lehi anakula tunda la mti, ambalo linaashiria upendo wa Mungu na baraka tunazoweza kupokea kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo. Lehi anaonyeshwa baadhi ya makundi ya watu. Wengine wanapotea na hawafikii mti huu. Wengine wanaona

aibu baada ya kula tunda la mti wa uzima, na wa-naanguka katika mapito yaliyokatazwa na kupotea. Wengine wanashikilia fimbo ya chuma kwa nguvu, wakalila tunda, na kubakia wakweli na waaminifu. Kundi lingine lilichagua kutotafuta njia iendayo kwe-nye mti wa uzima kabisa.

SOMO LA 12

1 nefi 8

Page 57: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

42

SoMo la 12

kuwaambia wanafunzi kwamba, katika 1 Nefi 8:10, Lehi alielezea tunda kama “lilitama-nika kumfurahisha mwanadamu.” (Unaweza kushauri kwamba wanafunzi waweke alama hivi vishazi katika maandiko yao.)• Ni hisia gani Lehi alipata baada ya kula lile tunda?• Tunawezaje “kushiriki” Upatanisho? (Kupitia mchakato wa toba.)• Kwa nini kushiriki Upatanisho hujaza nafsi zetu kwa “shangwe tele”?Toa ushuhuda wako kwamba kuja kwa Yesu Kristo na kushiriki Upatanisho huleta furaha na shangwe. (Unaweza kuandika kanuni hii kwenye ubao.)• Ni lini Upatanisho wa Mwokozi ulikuletea furaha na shangwe katika maisha yako?

(Wakumbushe wanafunzi kwamba hawahitaji kuelezea uzoefu ambao ni wa kibinasfi au siri sana.)

1 Nefi 8:19–35Katika ono lake, Lehi anaona baadhi ya makundi ya watu na ufanisi wao au kushindwa kwao katika kufikia mti wa uzimaOnyesha picha ya ndoto ya Lehi (62620; Kitabu cha Sanaa za Injili [2009], no. 69), na taja ishara ambazo darasa limejadili tayari: mti na tunda. Elezea kwamba katika ono hili, Bwana pia alitumia ishara zingine ili kumfundisha Lehi jinsi ya kwenda kwa Yesu Kristo na kushiriki Upatanisho Wake. Waulize wanafunzi ni ishara gani zingine wameona katika picha hii. (Majibu yanaweza kujumuisha mto, fimbo ya chuma, ukungu wa giza, na jengo kubwa na pana.)Wakumbushe wanafunzi kwamba Bwana alimwonyesha Nefi ono hilo hilo. Nefi baadaye aliandika maana ya baadhi ya ishara na picha katika ono hilo (ona1 Nephi 11,12, na 15).Tayarisha chati ifuatayo kama kitini, au ionyeshe kwenye ubao kabla ya darasa kuanza. (Weka safu ya mkono wa kulia bila maandishi isipokuwa marejeo ya maandiko.) Waalike wanafunzi watumie marejeo yaliyotolewa kutambua ufafanuzi wa kila kitu katika ono la Lehi. Rejea ishara ya kwanza, mti ulio na tunda jeupe, kwa pamoja kama darasa. Acha wanafunzi wachukue dakika chache peke yao kutambua maana ya ishara nne zilizobakia. (Unaweza kushauri kwamba waandike majibu yao katika maandiko yao karibu na mistari inayolingana katika 1 Nefi 8.)

ishara katika ono la lehi Ufafanuzi Uliotolewa na nefi

1 nefi 8:10–12—Mti ulio na tunda jeupe 1 nefi 11:21–25 (Upendo wa Mungu; baraka za Upatanisho wa yesu Kristo)

1 nefi 8:13—Mto wa maji chafu 1 nefi 12:16;15:26–29 (Uchafu; kina cha jehanamu)

1 nefi 8:19—fimbo ya chuma 1 nefi 11:25 (neno la Mungu)

1 nefi 8:23—Ukungu wa giza 1 nefi 12:17 (Majaribu ya ibilisi)

1 nefi 8:26—jengo kubwa na pana 1 nefi 11:35–36;12:18 (Kiburi na fikira tupu za ulimwengu)

Waalike wanafunzi kuelezea ufafanuzi waliogundua. Ili kuwasaidia wao kuona uhusi-ano wa 1 Nefi 8 katika maisha yao, muulize mwanafuzni kusoma taarifa ifuatayo ya Rais Boyd K. Packer wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili. Alika darasa kusikiliza kwa nini ni muhimu kwao kujifunza ono la Lehi:“Unaweza kufikiria kwamba ndoto ya Lehi au ono halina maana maalumu kwako, lakini inayo. Wewe upo ndani yake; sisi sote tupo ndani yake. . . .“Ndoto au ono la Lehi lina kila kitu ndani yake kwa Mtakatifu wa Siku za Mwisho anahitaji kuelewa majaribu ya maisha” (“Finding Ourselves in Lehi’s Dream,” Ensign, Aug. 2010, 22).Wanafunzi wanapojifunza salio la ono, wahimize wao kutafuta watu katika ono ambao wana-weza kuwawakilisha wao. Wahakikishie wao kwamba haijalishi wanajiona wapi katika ono, kila mmoja wao ana nguvu na uwezo wa kuchagua kuhusu kufuzu baraka za Upatanisho.

Kuweka alama na kuandika maneno katika maandikoWanafunzi wanaweza kufaidika kutokana na kuandika marejeo, ufafanuzi wa ishara, na habari zingine pembeni mwa maandiko yao. Pia wanaweza kufaidika kutokana na kuakisi marejeo katika tanbihi. Muhtasari kama huo unaweza kuwa kama ukumbusho wa kuwasai-dia kuelewa na kuwa-fundisha kutoka katika maandiko katika siku za usoni. Huu muhtasari unaweza kupatikana zaidi na kudumu kuliko habari zilizoandikwa katika shajara au kwe-nye kipande cha karatasi kando. Hata hivyo, una-paswa kila mara kuhe-shimu haki ya kujiamulia ya wanafunzi na kamwe usiwalazimishe kuandika katika maandiko yao. Badala yake, fanya usha-uri na uwapatie nafasi wanafunzi kuamua kile kinachofaa.

Page 58: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

43

1 nefi 8

Gawa wanafunzi katika makundi mawili. Elezea kwamba kila kikundi kitatafuta vitu tofauti darasa linaposoma 1 Nefi 8:21–33 kwa pamoja.Uliza kundi la kwanza kutafuta majibu ya maswali yafutayo. (Kabla ya darasa, andika ma-swali haya kwenye ubao au kitini.)• Ni vikwazo gani viliwakabili watu katika Ono la Lehi?• Hivi vikwazo vinaashiria nini?• Hivi vikwazo vina umbo gani leo?• Ni kanuni gani unaona katika hii mistari?Alika kikundi cha 2 kutafuta majibu ya maswali yafuatayo. (Kabla ya darasa, andika ma-swali haya kwenye ubao au kwenye kitini.)• Ni nini kiliwasaidia watu kufikia mti na kula tunda?• Ni kwa njia gani fimbo ya chuma inafanana na neno la Mungu?• Ni kwa jinsi gani neno la Mungu hutusaidia kushinda vikwazo kwenye mapito ya uzima

wa milele?• Ni kanuni gani mnazoziona katika mistari hii?Waalike wanafunzi kadhaa kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka katika 1 Nefi 8:21–33. Kisha waalike wanafunzi katika kundi la 1 ili watoe majibu yao ya maswali wali-yopangiwa. Pia waulize wao kuelezea kanuni wanazoziona katika vifungu hivi. Hakikisha wanafunzi wanaelewa kwamba kiburi, malimwengu, na kuingia katika majaribu kunaweza kutuzuia kupokea baraka za Upatanisho. Waalike wanafunzi kutafakari jinsi hivi vikwazo vinavyoweza kuzuia maendeleo yao ya kiroho.Acha wanafunzi katika kundi la 2 watoe majibu yao kwa maswali waliyopangiwa. Baada ya kujadili mawazo yao, waalike wao waelezee kanuni wanazoziona katika 1 Nefi 8:21–33. Kanuni wanazotambua zinaweza kujumuisha yafuatayo:Kama tutashikilia kwa nguvu neno la Mungu, itatusaidia sisi kushinda majaribu na ushawishi wa malimwengu. Kushikilia kwa nguvu neno la Mungu, hutusaidia kuwa karibu na Bwana na kupo-kea baraka za Upatanisho. • Katika 1 Nefi 8:24 na 30, ni maneno gani yanayoelezea juhudi za watu za kushikilia

fimbo ya chuma na kufikia mti?• Unafikiria inamaanisha nini “kusonga mbele”?• Unafikiria inamaanisha nini kung‘ang‘ania na kuendelea kushikilia kabisa neno la

Mungu? (Unaweza kuhitajika kuelezea kwamba katika 1 Nefi 8:30, neno kwa nguvu humaanisha kung‘ang‘ania kabisa.)

• Kwa nini yatupasa kujifunza maandiko kila siku?Baada ya kujadili maswali haya, unaweza kutaja kwamba katika ono, watu fulani, kama vile Lamani na Lemueli, hawakutaka kula tunda (ona 1 Nephi 8:22–23, 35–38). Hii inaashiria kukataa kwao kutubu na kushiriki baraka za Upatanisho wa Yesu Kristo. Watu fulani wali-anguka hata baada ya kula lile tunda (ona 1 Nefi 8:25, 2). Hii inatukumbusha sisi kwamba baada ya sisi kuanza kupokea baraka za Upatanisho, tunahitaji kuwa na bidii na waami-nifu, kutubu dhambi zetu na kujitahidi kushika maagano yetu. Watie moyo wanafunzi kufuata mfano wa watu waliokula tunda na kubakia katika mti (ona 1 Nefi 8:33).Kusaidia wanafunzi kuona jinsi kanuni katika ono la Lehi zilivyobariki maisha yao, waalike kujibu mojawapo ya maswali yafuatayo katika daftari zao za darasani au shajara zao za kujifunza maandiko:• Ni wakati gani neno la Mungu lilikuongoza wewe au lilikusaidia kushinda majaribu,

kiburi, au malimwengu?• Ni lini ulihisi upendo wa Mungu kwako ulipokuwa ukisoma au kusikiliza neno Lake?Waalike wanafunzi wachache kutoa majibu yao darasani.Wahimize wanafunzi kutenda juu ya kile ambacho wamejifunza na kuhisi walipokuwa wakijifunza 1 Nefi 8 kwa kuweka lengo halisi la kuanza au kukuza tabia ya kujifunza ma-andiko kila siku. Waelezee wanafunzi baraka ambazo zimekuja maishani mwako kupitia kujifunza maandiko kila mara.

Himiza kujifunza maandiko kila sikuVitu vichache vina usha-wishi wa kudumu wa mema kuliko kuwasaidia wanafunzi kukuza tabia ya kujifunza maandiko kila siku. Wahimize wanafunzi kutenga muda kila siku kujifunza maandiko. Pia wapatie wanafunzi nafasi za kila mara katika darasa kuelezea kile ambacho wamejifunza na kuhisi katika kujifunza maa-ndiko kibinafsi.

Page 59: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

44

SOMO LA 13

1 nefi 10–11

Mapendekezo ya Kufundisha

1 Nefi 10:1–16Lehi anatoa unabii kuhusu MasiyaKwa kifupi fanya muhtasari wa 1 Nephi 10:1–16 kwa kuwaambia wanafunzi kwamba baada ya kusimulia ono la mti wa uzima, Lehi pia alitoa mfululizo wa unabii. Huu unajumuisha maelezo ya kina juu ya wakati ambapo Yesu Kristo angekuja ulimwenguni (ona 1 Nefi 10:4), kubatizwa Kwake na Yohana Mbatizaji (ona 1 Nefi 10:7–10), kusulubiwa na ufufuo Wake (ona 1 Nefi 10:11), na kukaribia kwa kutawanyika na kukusanyika kwa Israeli (ona 1 Nefi 10:12–14).Alika mwanafunzi asome 1 Nefi 10:4–6 kwa sauti. (Unaweza kuelezea kwamba Masiya ni “umbo la neno la Kiaramaiki na Kiebrania linalo maanisha “mpakwa mafuta.” Katika Agano Jipya Yesu anaitwa Kristo, ambayo kwa Kigiriki linamaanisha Masiya. Inamaanisha Nabii aliye pakwa mafuta, Kuhani, Mfalme, na Mkombozi ambaye kuja kwake Wayahudi walikuwa wakikungojea kwa hamu" [Guide to the Scriptures, “Messiah,” scriptures.lds.org; ona pia Bible Dictionary, “Messiah”].)• Kulingana na unabii wa Lehi, Mwokozi angekuja lini? (Ona 1 Nefi 10:4.)• Ni nini kingewatokea wanadamu kama hawangemtegemea Mwokozi? (Ona 1 Nefi 10:6.)

1 Nefi 10:17–22; 11:1–6Nefi anatafuta kuona, kusikia, na kujua kweli ambazo baba yake alijifunzaWaulize wanafunzi kufikiria juu ya mfano ufuatao: Vijana watatu wanahudhuria mkutano mmoja wa Kanisa. Baada ya kurudi nyumbani, kijana mmoja anahisi kwamba mkutano ulikuwa wa kuchosha na kupoteza wakati. Mwingine anafikiria mkutano ulikuwa mzuri lakini haukumuathiri. Wa tatu anarudi nyumbani akiwa ameinuliwa na Roho Mtakatifu na kupokea maongozi na maelekezo kwa ajili yake maisha yake, hata zaidi ya kile kilichofu-ndishwa katika mkutano.• Inawezekanaje kwamba hawa vijana watatu walio hudhuria mkutano mmoja lakini

wawe na uzoefu tofauti?Elezea kwamba mfano huu unafanana na uzoefu wa Lamani, Lemueli na Nefi wakati waliposikia unabii wa baba yao na taarifa ya ono lake. Lamani na Lemueli hawakuelewa maneno ya baba yao na walibishana kuhusu kile walichokisikia (ona 1 Nefi 15:2). Nefi, kwa upande mwengine, alimwelekea Bwana kwa uelewa. Alitoa mfano mwema zaidi wa jinsi ya kutafuta na kupokea ufunuo.Waambie wanafunzi kwamba wanapojifunza uzoefu wa Nefi, watapata kanuni ambazo zitawasaidia wao kutafuta na kupokea ufunuo wao wenyewe. Watie moyo kutambua mambo ambayo Nefi alifanya ambayo yalimwezesha kupokea ufunuo sawa na ule ambao Lehi alipokea.Gawa darasa katika vikundi vitatu. Wape kila kikundi mojawapo ya namna na seti ya ma-swali katika chati ifuatayo. (Unaweza kuweka chati kwenye ubao kabla ya darasa kuanza.)

UtanguliziBaada ya kusikia taarifa ya ono la Lehi baba yake, Nefi alikuwa na hamu ya kuona, kusikia, na kujua mwe-nyewe mambo ambayo Lehi alikuwa ameona na kusikia (ona 1 Nefi 10:17). Wakati akiwa anatafakari juu ya ma-fundisho ya baba yake, Nefi “alinyakuliwa na Roho wa Bwana” (1 Nefi 11:1) na akapokea ono lake mwenyewe.

Hili ono limesimuliwa katika 1 Nefi 11–14. Katika 1 Nefi 11 tunasoma kuhusu mti wa uzima, fimbo ya chuma, na jengo kubwa na pana, vile vile kuzaliwa kwa Mwokozi, ubatizo, huduma, na kusulubiwa. Nefi alipokuwa aki-shuhudia mambo haya, aligundua upendo wa Mungu alionao kwa watoto Wake.

Kishiriki bila kujulisha jinaUnaweza kuwaalika wanafunzi kuripoti bila kujulisha jina katika maandishi kile ambacho wamepata uzoefu juu yake wakati wa kujifu-nza maandiko kila siku. Kusanya majibu yao na usome machache katika darasa. Kusikia shuhuda za wanafunzi wenzao kunaweza kuwatia moyo wanafunzi wengine katika kujifunza kwao kibinafsi. Wanafunzi wengine husitasita ku-toa shuhuda na uzoefu wa kiroho wazi wazi kwa sababu hawataki kuonekana wanajivuna au wanaogopa wengine watawahukumu au wa-tachukulia uzoefu wao kijuujuu. Kuripoti bila kujulisha jina kunawa-wezesha wanafunzi ku-eleza uzoefu wa kiroho bila hofu.

Page 60: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

45

1 nefi 10 –11

Waalike wanafunzi wasome 1 Nefi 10:17 na 11:1–6 kimya kimya na watayarishe majibu kwa maswali yao waliopangiwa.

hamu ni nini ambacho nefi alikuwa na hamu kuona, kusikia, na kujua?hamu zetu zinaathiri vipi uwezo wetu wa kupokea ufunuo?ni nini nilicho na hamu ya kujua kutoka kwa bwana?

imani ni imani gani nefi alionyesha alipokuwa anatafuta ufunuo?hii imani inaweza kuathiri vipi uwezo wetu wa kupokea ufunuo?ninawezaje kuongeza ushuhuda wangu na imani katika yesu Kristo?

Kutafakari ni nini kilitendeka wakati nefi akiwaza na akatafakari?Kwa nini kutafakari hutuelekeza kwenye ufunuo?ninaweza kufanya nini ili kuwa na bidii ya kutafakari maneno ya manabii?

Waalike wanafunzi wachache kutoka katika kila kikundi waelezee majibu ya maswali yao mawili ya kwanza waliopangiwa. (Unaweza pia kuwaalika wanafunzi kujibu swali la tatu, lakini wahakikishie wao kwamba hawahitajiki kutoa majibu ambayo ni ya kibinasfi au siri sana.)Alika mwanafunzi asome 1 Nephi 10:19 kwa sauti.• Ni nani anayeweza kujua siri za Mungu?• Ni kwa uwezo gani siri za Mungu ufunuliwa?• Ni sharti tufanye nini ili tupokee ufunuo kwa uwezo wa Roho Mtakatifu?• Unafikiria inamaanisha nini kutafuta kwa bidii?• Nefi alifanya kitu gani ambacho kinaonyesha alikuwa na bidii kutafuta kuona, kusikia,

na kujua mambo ambayo baba yake alikuwa amefunza?Andika taarifa ifuatayo kwenye ubao:Mungu hufunua kweli kwa . . .Waulize wanafunzi wafanye muhtasari kile walichojifunza kutokana na uzoefu wa Nefi kwa kukamilisha taarifa kwenye ubao. Hali wanafunzi wanaweza kuchagua maneno tofauti, majibu yao yanafaa kuonyesha kweli kwamba Mungu hufunua kweli kwa wale wote wanaomtafuta Yeye kwa bidii. (Unaweza kuandika kanuni hii kwenye ubao.)Watie moyo wanafunzi kufikiria wakati kumfuata Mungu kwa bidii kumewasababisha wao kuhisi Roho Yake na kupokea ufunuo. (Inaweza kusaidia kutaja kwamba ufunuo unaweza kujumuisha kupokea mwongozo wakati unafanya uamuzi, kupata ongezeko la uelewa, kupokea faraja, au kupokea hakikisho kuwa jambo ni kweli.) Waalike wanafunzi washiriki uzoefu wao na darasa. Unaweza pia kushuhudia juu ya kile ambacho umepata uzoefu juu yake kupitia juhudi zako za kumtafuta Bwana kwa bidii.

1 Nefi 11:7–36Nefi alishuhudia ufadhili wa MunguElezea wanafunzi kwamba Nefi aliendelea kutafakari na kutafuta mwongozo mtakatifu wa-kati wa ono lake. Wakati Nefi aliomba kujifunza ufafanuzi wa mti ambao yeye na baba yake walikuwa wameona, malaika alimtokea na kumsaidia. Malaika aliuliza, “Je!, Unajua maana ya ule mti ambao baba yako aliuona? (1 Nefi 11:21). Rejea maana ya mti kwa kuwaacha wanafunzi wachache kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka katika 1 Nefi 11:18–23.• Nefi alisema maana ya mti ilikuwa ni nini? (Baada ya wanafunzi kujibu, unaweza kutaja

kwamba Nefi aliona Mariamu akimshika mwana mchanga Yesu, na malaika akamta-mbulisha yule mtoto kama “Mwana wa Baba wa Milele.” Malaika kisha alimuuliza Nefi maana ya mti ili kumsaidia yeye kuona kwamba uliashiria Yesu Kristo. Wakati Nefi aki-jibu kwamba iliashiria “upendo wa Mungu,” alikuwa anamaanisha upendo wa Mungu kama inavyoonyeshwa kupitia zawadi ya Mwanawe. Tunapata uzoefu wa upendo wa Mungu kwa kushiriki baraka za Upatanisho wa Yesu Kristo.)

• Nefi na Malaika walielezea vipi upendo wa Mungu?

Page 61: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

46

SoMo la 13

Alika mwanafunzi asome 1 Nefi 11:16. (Elezea kwamba neno ufadhili linamaanisha kuji-shusha kwa hiari kutoka katika cheo au hadhi. Unaweza kuwaalika wanafunzi waandike maelezo haya katika maandiko yao karibu na 1 Nefi 11:16.)Acha wanafunzi watambue jibu la Nefi kwa swali la malaika kwa kusoma 1 Nefi 11:17 kwa sauti.• Nefi alijua nini?• Hakujua nini?Baada ya Nefi kujibu, malaika alimuonyesha yeye mifano kadhaa ya ufadhili wa Mungu ili kumsaidia kukuza uelewa wake wa upendo wa Mungu. Elezea wanafunzi kwamba “ufa-dhili wa Mungu” huwalenga wote Mungu Baba na Yesu Kristo.Elezea taarifa ifuatayo ya Mzee Bruce R. McConkie wa Akidi ya wale Mitume Kumi na Wawili, ambaye alielezea ufadhili wa Mungu, Baba yetu wa Mbinguni:“Ufadhili wa Mungu ni kwamba Yeye, Kiumbe kilichoinuliwa, hujishusha kutoka kwe-nye kiti cha enzi cha milele na kuwa Baba wa Mwana mwanadamu” (The Mortal Messiah [1979], 1:314).Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa jinsi “ufadhili wa Mungu” pia hulenga Yesu Kristo, onye-sha picha ya Kuzaliwa kwa Yesu (62116; Kitabu cha Sanaa za Injili [2009], no. 30). Muulize mwanafunzi asome 1 Nefi 11:13–21 kwa sauti. Alika mwanafunzi mwingine kutambua ni mistari gani inayolingana na picha. Acha mwanafunzi asome taarifa ifuatayo ya Mzee Gerald N. Lund, aliyekuwa wa wale Sabini. Alika darasa kusikiliza njia ambazo Mwokozi anaonyesha upendo Wake kwetu.Hapa alikuwa Yesu—mshiriki wa Uungu, Mzaliwa wa kwanza wa Baba, Muumba, Yehova wa Agano la Kale—sasa akiacha sehemu Yake tukufu na takatifu; akivua Mwenyewe utukufu na ufahari wote na kuingia katika mwili wa mtoto mchanga; asiyejiweza, mwenye kutegemea kabisa mama na baba yake wa ulimwenguni. Kwani Yeye hakuja kwenye kasri za kifahari za ulimwenguni na kupatiwa johari bali akaja kwenye hori la chini inashangaza. Cha kushangaza zaidi ni kwamba malaika alimwambia Nefi, ‘Tazama ufadhili wa Mu-ngu!’” (Jesus Christ, Key to the Plan of Salvation [1991], 16).• Ni kwa jinsi gani kuzaliwa kwa Mwokozi kunaonyesha upendo Wake kwetu?Hakikisha ni wazi kwamba upendeleo wa Mwokozi wa kuishi maisha ya duniani kulionye-sha upendo Wake kwetu.Onyesha picha ya Yesu akimfufua Binti wa Yairo (62231; Kitabu cha Picha za Injili, no. 41) na Kristo Anaponya Mgonjwa huko Bethesaida (Kitabu cha Sanaa za Injili, no. 42). Alika mwanafunzi asome 1 Nefi 11:28 and 31 kwa sauti. Tia darasa moyo litambue njia ambazo picha hizi zinafanana na mistari.• Nefi alimwona Mwokozi akihudumia na kuponya nani?• Ni kwa namna matendo ya Mwokozi yanaonyesha upendo Wake?Acha mwanafunzi asome 1 Nefi 11:32–33 kwa sauti. Alika darasa lisikilize mfano kamili wa upendo wa Mwokozi.Baada ya wanafunzi kuelezea kile walichokitambua, onyesha picha Kusulubiwa (62505; Kitabu cha Sanaa za Injili, no. 57).Shuhudia kwamba ufadhili wa Yesu Kristo unaonyesha upendo wa Mungu kwetu. Mwokozi ameshuka na kuishi maisha ya duniani, kuhudumia na kuponya wagonjwa na walioathiriwa na kufa kwa ajili ya dhambi zetu ili sisi tuweze kurudi nyumbani katika uwepo wa Baba wa Mbinguni.• Je! Kujua kuhusu ufadhili na upendo wa Mwokozi kunaweza kuathiri hisia zetu

kumhusuYeye?Hitimisha kwa kuwaalika wanafunzi waelezee jinsi upendo wa Mungu “unatamaniwa sana” na unafurahisha sana (ona 1 Nefi 11:22–23). Shuhudia kwamba tunapofuata mfano wa Nefi na kumtafuta Mungu kwa bidii, tutahisi upendo Wake na kupata uzoefu wa sha-ngwe ya kushiriki baraka zilizoletwa na Upatanisho wa Kristo.Waalike wanafunzi kufuata mfano wa Nefi katika juhudi wanazofanya wakitafuta ufunuo. Wakumbushe wao juu ya nafasi yao kama wanafunzi katika darasa la seminari na kwamba imani na juhudi wanazoweka katika kujifunza maandiko kibinafsi kila siku na ushiriki wa darasani unaathiri vyema uwezo wa kujifunza kwa Roho.

Page 62: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

47

Mapendekezo ya Kufundisha

1 Nefi 12Nefi anaona siku zijazo za mataifa ya Wanefi na WalamaniFanya muhtasari wa 1 Nefi 12 kwa kueleza kwamba sura hii endelezo la ono la Nefi. Ndani yake, malaika alimwonyesha Nefi jinsi ishara katika ono la mti wa uzima litatumika kwa uzao wake. Alionyesha kwamba baadhi ya uzao wake watapokea baraka zote za Upatani-sho. Hata hivyo, Nefi pia aliona kwamba uzao wake hatimaye utaangamizwa na uzao wa ndugu zake (Walamani). Waalike wanafunzi wasome 1 Nefi 12:16–19. Acha watafute kwa nini Wanefi wangeangamiza (ona 1 Nefi 12:19). Wakumbushe wanafunzi kwamba wana-pofanya imani katika Yesu Kristo, wanaweza kushinda kiburi na majaribu.

1 Nefi 13:1–9Nefi anaona kanisa kuu na la machukizoUliza wanafunzi wainue mikono yao kana kwamba wanacheza mchezo wowote. Waulize wanafunzi wachache kushiriki mchezo wanaocheza. Elezea kwamba katika michezo, timu mara nyingi hujitayarisha kwa michezo kwa kuchunguza michezo iliyopita na mikakati ya timu pinzani.• Kwa nini kunaweza kuwa na usaidizi kwa timu kujifunza mikakati ya wapinzani wao

kabla hawajashindana?Elezea kwamba Nefi aliona katika ono hamu na mikakati ya wale ambao wangepinga Kanisa la Yesu Kristo katika siku za mwisho. Watie moyo wanafunzi kutafuta hii mikakati wanapojifunza sura hii, ili waweze kujitayarisha kuitambua na wasidanganyike nayo.Waalike wanafunzi wachache kuchukua zamu kusoma 1 Nefi 13:1–4, 6 kwa sauti. Muulize mwanafunzi kutambua kikundi ambacho Nefi aliona kikiundwa miongoni kwa Wayunani wa siku za mwisho.Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa maudhui ya mistari hii, elezea tangazo lifuatalo la Mzee Bruce R. McConkie wa Akidi ya wale Mitume Kumi na Wawili. Waulize wanafunzi kusiki-liza kwa makini na kutambua maelezo ya kanisa kuu na la machukizo.“Majina kanisa la ibilisi na kanisa kuu na la machukizo yanatumika kutambulisha yote . . . mashirika ya jina au hali yoyote ile —iwe ni ya kisiasa, falsafa, elimu, uchumi, jamii, kidugu, kiraia, au kidini—ambayo yameundwa kuwapeleka watu kwenye njia ambayo inawae-lekeza mbali na Mungu na sheria zake na basi kuondoka kutoka kwenye wokovu katika ufalme wa Mungu” (Mormon Doctrine, 2nd ed. [1966], 137–38).

UtanguliziBaada ya Nefi kuona huduma na Upatanisho wa Mwo-kozi katika ono, aliona kwamba baada ya vizazi vinne vya haki, uzao wake utakuwa na kiburi na kwamba wataangushwa na majaribu ya ibilisi na kuangamizwa. Alionyeshwa pia uovu wa wale waliomfuata Shetani katika lile kanisa kubwa na la machukizo. Aliona kwamba wataondoa kweli halisi na za thamani kutoka kwenye Biblia, kuwasababisha wengi kujikwaa kiroho. Licha ya haya madhara ya kuhuzinisha, ono la Nefi pia lilimpatia sababu ya kuwa na matumaini. Aliona kwamba Mungu angetayarisha njia ya Urejesho wa injili katika siku za mwisho. Pia alishuhudia kwamba

kumbukumbu za watu (Kitabu cha Mormoni) kingeto-keza katika siku za mwisho ili kurejesha kweli halisi na za thamani ambazo zilipotea ulimwenguni.

Tazama: Unaweza kukosa wakati wa kutosha wa ku-maliza vifaa vyote katika somo hili. Katika matayarisho yako, tafuta mwongozo wa Roho Mtakatifu ili kujua ni sehemu gani za somo hili zilizo muhimu sana na zinazofaa sana kwa wanafunzi wako. Unaweza kuwa na haja ya kufanya muhtasari sehemu za somo hili ili kutoa muda wa kufundisha mafundisho na kanuni muhimu vyema.

Fanya MuhtasariHautakuwa na muda wa kufundisha kila kitu ka-tika umbo la maandiko kwa msisitizo sawa. Wakati fulani, unaweza kuwa na haja ya kufanya muhtasari wa umbo la hadithi au kufundisha sehemu moja ya umbo la maandiko ili kuwa na muda wa kutosha wa kukamilisha maudhui, mafundisho, au kanuni muhimu sana katika sehemu ingine ya umbo. Kufanya muhtasari, ba-dala ya kuondoa sehemu za umbo la maandiko, husaidia wanafunzi kuelewa vyema umbo la hadithi kwa ujumla na ujumbe wa umbo.

SOMO LA 14

1 nefi 12–13

Page 63: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

48

SoMo la 14

Kuwa wazi kwamba kishazi “kanisa kuu na la machukizo” hakilengi hasa dhehebu au kanisa fulani. Hulenga shirika lolote na yote ambayo yametengenezwa kuwaelekeza watu mbali na Mungu na sheria Zake.Unaweza kuwatia moyo wanafunzi kuandika kishazi mashirika yote ambayo yametengenezwa kuwaelekeza watu mbali na Mungu na sheria Zake pembeni karibu na 1 Nephi 13:6.• Unafikiria kwa nini ni muhimu kujua kwamba Shetani amepanga majeshi yake kutuele-

keza mbali na Mungu na sheria Zake?Elezea kwamba Nefi alielezea kanisa kuu na la machukizo. Alika mwanafunzi asome 1 Nefi 13:5–9 kwa sauti.• Ni vitu gani wale walio katika lile kanisa kuu na la machukizo wanatamani? (Ona 1 Nefi

13:7–8.)• Kulingana na 1 Nefi 13:5, 9, Ni vitu gani wale walio katika lile kanisa kuu na la machu-

kizo wanatafuta kutimiza? Kwa nini?” (Unaweza kuandika kweli ifuatayo kwenye ubao: Shetani na wafuasi wake wanataka kuangamiza Watakatifu wa Mungu na kuwa-leta katika utumwa)

• Kujua hamu na dhamira ya Shetani na wafuasi wake kunatusaidia vipi kupambana na wao?

Wajulishe wanafunzi kwamba baadaye katika sura hii watajifunza kuhusu mojawapo ya njia ambazo kanisa kuu na la machukizo limejaribu kuangamiza wale wanaomtafuta Mungu.

1 Nefi 13:10–19Nefi anaona mkono wa Mungu katika kuanzishwa kwa nchi huru ambapo injili ingerejeshwaShuhudia kwamba Bwana huhakikisha kwamba kazi Yake inasonga mbele licha juhudi za kanisa kuu na la machukizo za kuwafanya watu wajikwae kiroho. Alifanya hivyo kwa kutayarisha njia ya Urejesho wa injili Yake.Taarifa zilizoorodheshwa chini zinafupisha matukio muhimu ambayo Nefi aliona katika ono lake. Acha wanafunzi wasome 1 Nefi 13:10–19 na kulinganisha kila rejeo la maa-ndiko lililoorodheshwa chini na tukio lililoelezwa. (Unaweza kuonyesha marejeo haya ya maandiko na taarifa kwenye ubao kabla ya darasa kuanza. Au unaweza kutengeneza kitini kilicho na marejeo ya maandiko na taarifa. Chini, marejeo ya maandiko yanalinganishwa kwa ushahihi na taarifa. Ili shughuli hii ifanikiwe, unahitaji kubadili mpangilio wa taarifa kama ulivyopanga kwenye ubao au ziongeze kwenye kitini.)

1 Nefi 13:12 Columbus alisafiri kwenda Amerika1 Nefi 13:13 Wahamiaji walisafiri hadi Amerika, wakitafuta uhuru wa kidini1 Nefi 13:14 Wamarekani wenyeji wafukuzwa kutoka kwenye nchi yao1 Nefi 13:15 Wayunani wanastawi katika Amerika1 Nefi 13:16–19 Ingawa walishindwa kwa idadi, jeshi la mapinduzi la Amerika

lilipata ushindi.

Wanafunzi wanapoeleza majibu yao, unaweza kuwatia moyo kuandika maneno au vishazi muhimu katika maandiko yao karibu na kila kifungu. Kwa mfano, wanaweza kuandika Columbus kando ya 1 Nefi 13:12.• Kulingana na 1 Nefi 13:12, kwa nini Columbus alisafiri kwenda Amerika?• Kulingana na 1 Nefi 13:13, kwa nini Wahamiaji walienda Amerika?• Kulingana na 1 Nefi 13:15–19, kwa nini Wayunani walistawi na kupata uhuru kutoka

kwa “mataifa mengine yote”?Alika mwanafunzi asome kwa sauti taarifa ifuatayo ya Rais Joseph F. Smith:“Hili taifa kuu la Amerika Mwenyezi aliliinua kwa uwezo wa mkono wake Wenye Enzi, ili iwezekane katika siku za mwisho ufalme wa Mungu kuazishwa ulimwenguni. Kama Bwana hakuwa ametayarisha njia kwa kuweka msingi wa hili taifa tukufu, haingewezekana (chini ya sheria kali na ulokole wa serikali za kifalme za duniani) ili kuweka misingi ya kuja kwa ufalme mkuu. Bwana amefanya hivi” (Gospel Doctrine, 5th ed. [1939], 409).

Page 64: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

49

1 nefi 12–13

Shuhudia kwamba Bwana alitayarisha njia ya Urejesho kwa kuanzisha nchi yenye uhuru wa dini pale ambapo Yeye angerejesha Kanisa Lake. Shuhudia kwamba Bwana ame-tayarisha, na anaendelea kutayarisha, njia ya urejesho wa injili Yake kwa kila taifa.Kama unafunza somo hili katika nchi iliyo nje ya Marekani, uliza:• Ni kwa namna gani Bwana alitayarisha njia ya kuhubiri injili ya urejesho katika nchi yako?

1 Nefi 13:20–42Nefi anawaona Wayunani wa siku zijazo wakiwa na Biblia, Kitabu cha Mormoni, na maandiko ya siku za mwisho Alika mwanafunzi asome 1 Nefi 13:20–24. Muulize ni chombo gani ambacho Nefi aliona wakoloni wa mwanzo wa Amerika “wakibeba miongoni mwao.” Shikilia nakala ya Biblia, na ueleze kwamba hiki ni kitabu katika ono la Nefi. Unaweza kuwaalika wanafunzi kua-ndika Biblia pembeni karibu na 1 Nefi 13:20.Elezea kwamba malaika alimfunza Nefi kwamba Biblia ni kumbukumbu “ya thamani kuu” (1 Nefi 13:23). Wakati mafunuo yakiandikwa katika Biblia katika lugha ya asili, “ilikuwa na utimilifu wa injili ya Bwana” (1 Nefi 13:24). Acha mwanafunzi asome 1 Nefi 13:26–27 kwa sauti.• Ni nini kanisa kuu na la machukizo lilikiondoa kutoka katika Biblia? Kwa nini vitu hivi

viliondolewa ?Acha mwanafunzi mwingine kusoma 1 Nefi 13:29 kwa sauti.• Ni nini kilifanyika kama matokeo ya kuondolewa kwa vitu halisi na vya thamani na

maagano mengi ya Bwana kutoka kwenye Biblia?Acha wanafunzi wanne wachukue zamu kusoma kwa sauti 1 Nefi 13:34–36, 39. Uliza darasa litafute kile ambacho Bwana atafanya kuwasaidia watu kushinda juhudi za kanisa kuu na la machukizo.• Kulingana na 1 Nefi 13:34, ni nini Bwana ataleta kwa sababu ya neema Zake?• Kulingana na 1 Nefi 13:35–36, ni nini "kitakachofichwa" ili kije kutokea kwa Wayunani?

(Unaweza kushawishi wanafunzi waandike karibu na 1 Nefi 13:35 kwamba “vitu hivi” hulenga Kitabu cha Mormoni.)

• Kulingana na 1 Nefi 13:39, ni nini kingine ambacho Bwana ataleta katika siku za mwi-sho, kama ziada ya Kitabu cha Mormoni? Ni “vitabu vingine” gani Bwana alivyoleta kama sehemu ya Urejesho? (Mafundisho na Maagano, Lulu ya Thamani Kuu, na Tafsiri ya Biblia ya Joseph Smith.)

Waalike wanafunzi kusoma 1 Nefi 13:40–41. Acha wao watafute maelezo ya kile maandiko ya urejesho yanawajulisha watu wote. Baada ya wanafunzi kulezea kile walichopata, inua nakala ya Biblia na utoe ushuhuda wako juu ya ukweli wake. Inua nakala ya Kitabu cha Mor-moni na uviweke pamoja na Biblia. Shuhudia kwamba Kitabu cha Mormoni na maandiko ya siku za mwisho hurejesha kweli halisi na za thamani ambazo hutusaidia kujua kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu na hutusaidia kujua jinsi ya kuja Kwake.Waulize wanafunzi watafute vishazi hapo mwisho wa 1 Nefi 13:41 ambavyo vinaelezea kile ambacho Bwana atafanya na kumbukumbu za Wayahudi (Biblia) na kumbukumbu za uzao wa Wanefi (Kitabu cha Mormoni). Shuhudia kwamba hizi kumbukumbu “zitaunganishwa kuwa moja” (1 Nefi 13:41) na “zitakua pamoja” (2 Nefi 3:12) ili kutusaidia kujua wazi jinsi ya kuja kwa Mwokozi.Ili kuwasidia wanafunzi kutathmini jinsi urejesho wa kweli halisi na za thamani ulivyoa-thiri maisha yao, waalike kutafakari juu ya maswali yafuatayo:• Je, Ni kwa namna gani Kitabu cha Mormoni kumeathiri ushuhuda wako kuhusu Yesu

Kristo na kimekusaidia vipi kusogea karibu na Yeye?Baada ya kuwapatia wanafunzi muda wa kutafakari, alika wachache wao kutoa majibu yao. Unaweza pia kutaka kutoa ushuhuda wako mwenyewe juu ya Kitabu cha Mormoni na jinsi kimeimarisha ushuhuda wako juu ya Yesu Kristo na kukusaidia kujua jinsi ya kuja Kwake. Unapohitimisha darasa, wahimize wanafunzi kujifunza Kitabu cha Mormoni kwa makini mwaka wote, wakitafuta mafundisho na matukio ambayo yanaimarisha shuhuda zao juu ya Yesu Kristo na uwafundishe jinsi ya kuja Kwake.

Page 65: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

50

Mapendekezo ya Kufundisha

1 Nefi 14:1–7Nefi anaona matokeo ya kumtii au kutomtii Bwana kwa vizazi vijavyo Waalike wanafunzi wafungue maandiko yao kwenye 1 Nefi 14. Elezea kwamba leo watae-ndelea kujifunza juu ya ono la Nefi. Wanafunzi watafakari jinsi wanavyoweza kukamilisha sentensi zifuatazo:

Kama nikimfuata Bwana, basi . . .Kama nitakataa kumfuata Bwana, basi . . .

Mara baada ya wanafunzi kutoa majibu yao, taja kwamba neno kama linashauri chaguo. Inategemea juu ya kile tutakacho chagua, tutapata uzoefu wa matokeo tofauti. Elezea kwamba Nefi aliona vizazi vijavyo na kugundua kwamba kama vitakuwa vya wenye haki, vitabarikiwa; au kama vitakuwa vya waovu, vitalaaniwa. Alika darasa kufikiria kote katika somo jinsi kuchagua kuwa mtiifu kwa Bwana kumewaletea wao baraka.Chora mchoro ufuatao kwenye ubao:

Acha mwanafunzi asome 1 Nefi 14:1–2 kwa sauti. Uliza darasa kutambua (1) chaguo Nefi aliloonyesha kama Wayunani wangeweza kufanya, na (2) baraka ambazo Nefi aliona zingekuja kwa Wayunani kama wangefanya hili chaguo. Wanafunzi wanapoeleza kile wa-mekigundua, jaza mapengo kwenye ubao ili ionekane kitu kama ifutavyo:

Kama watamsikia Mwana-kondoo wa Mungu na wasisikilize mioyo yao wenyewe,

basi wao wata . . .hesabiwa miongoni mwa nyumba ya israeli.Watakuwa watu waliobarikiwa milele.hawatakuwa chini ya kifungo.

Unaweza kuwa na haja ya kuelezea kwamba katika maandiko, kishazi cha “vikwazo” (1 Nefi 14:1) mara hukusudia vizuizi ambavyo vinawazuia watu kumfuata Bwana. Kuwa “unahesabiwa miongoni mwa nyumba ya Israeli” (1 Nefi 14:2) humaanisha kuhesabiwa miongoni mwa watu wa agano wa Bwana.• Kwa nini ni muhimu kuwa miongoni mwa watu wa agano wa Bwana? (Ili kupokea

baraka za agano la Ibrahimu [ona M&M 132:30–31].)• Inamaanisha nini “kumsikiliza Mwanakondoo wa Bwana”?• Juu ya zawadi za utiifu zilizoorodheshwa kwenye ubao, ni zipi zilizo na maana sana

kwako? Kwa nini?”• Ni wakati gani wewe ulimsikiliza Bwana na kupata baraka Zake katika maisha yako?

(Wakumbushe wanafunzi kwamba hawahitajiki kushiriki uzefu ambao ni wa kibinasfi au siri sana.)

Utangulizi1 Nefi 14 huhitimisha taarifa ya ono la Nefi. Katika se-hemu hii ya ono, Nefi aliambiwa kuhusu baraka zilizoa-hidiwa kwa wale ambao hutubu na kumsikia Bwana, na laana ambayo huja kwa waovu ambao hufanya mioyo kuwa migumu dhidi ya Bwana. Nefi pia alionyeshwa

pia kwamba Bwana atawasaidia na kuwalinda wale ambao wanaishi kwa haki na kushika maagano yao na kwamba Yeye ataangamiza lile kanisa kuu na la machu-kizo la ibilisi.

Vifaa vya pichaWanafunzi wengi watajifunza vyema na kukumbuka kwa muda mrefu wakati wame-tumia vifaa vya picha kuwasilisha mawazo. Michoro rahisi kama ile ilioonyeshwa katika hili wazo la kufundisha inaweza kuchorwa kwa urahisi ubaoni. Michoro kama hio inaweza kuwa-sidia wanafunzi kulenga mawazo muhimu katika maandiko.

Kama basi

SOMO LA 15

1 nefi 14

Page 66: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

51

1 nefi 14

Kwenye sehemu nyingine ya ubao chora mchoro ufuatao:

Acha mwanafunzi asome 1 Nefi 14:5–7 kwa sauti. Uliza darasa kutafuta (1) baraka ambazo zitakuja kwa wale wanaotubu na (2) matokeo mabaya yakayokuja kwa wale wanaofanya mioyo yao kuwa migumu. Kamilisha mchoro, kama ulivyofanya katika zoezi la awali. (Ikiwa watu watatubu, “itakuwa vyema kwao” [1 Nefi 14:5] na watapokea “amani na uzima wa milele” [1 Nefi 14:7]. Ikiwa watu watafanya mioyo kuwa migumu “wataanga-mia” [1 Nephi 14:5] na “watatiwa utumwani” na “maangamizo” [1 Nephi 14:7].)Wanafunzi wanapojibu, unaweza kuwa na haja ya kuelezea kwamba “kazi kuu na ya ajabu” iliyotajwa katika 1 Nefi 14:7 inalenga urejesho wa ukuhani, injili, na Kanisa la Bwana katika siku za mwisho.• Ni kwa jinsi gani Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho ni “kuu na la

ajabu” kwako? Je! Linaleta vipi amani kwako? Je! Linaleta vipi matumaini ya uzima wa milele kwako?

Fikiria kuwapatia wanafunzi muda wa kutafakari kimya kimya ni njia gani iliyoonyeshwa ubaoni wanayofuata kwa wakati wa sasa. Shuhudia kwamba kumtii Bwana na kutubu dhambi zetu huelekeza kwenye baraka kuu. Unaweza pia kushuhudia kwamba kufanya mioyo yetu kuwa migumu dhidi ya Bwana na Kanisa Lake hutupeleka kwenye utumwa wa kiroho na maangamizo.

1 Nefi 14:8–17Nefi aliona vita kati ya Kanisa la Mwanakondoo wa Mungu na lile kanisa kuu na la machukizoWaalike wanafunzi kufikiria kuwa wamesajiliwa kupigana katika vita.• Mngefanya nini ili kujitayarisha kwa ajili ya vita?Elezea kwamba malaika alimfunza Nefi kuhusu vita vikubwa ambavyo vingefanyika katika siku za mwisho.Waalike wanafunzi watatu kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka katika 1 Nefi 14:9–11. Uliza darasa kutambua vikundi viwili kwenye mapigano. (Unaweza kuwakumbusha wanafunzi kwamba kanisa kuu na la machukizo humaanisha mtu au kundi lolote ambalo linawaelekeza watu kuwa mbali na Mungu na sheria Zake.• Ni maneno na vishazi gani vilivyotumika kuelezea lile “kanisa kuu na la machukizo”?• Kulingana na ono la Nefi, litapatikana wapi lile “kanisa kuu na la machukizo” katika

siku za mwisho?Waulize wanafunzi watatu zaidi kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka katika 1 Nefi 14:12–14. Alika darasa kutafuta sababu za kwa nini tunaweza kuwa na matumaini kuhusu siku za usoni.• Kulingana na 1 Nefi 14:12, ni kanisa gani ambalo litakuwa na watu wengi?• Kwa nini Kanisa la Mwanakondoo litakuwa na watu wachache kuliko kanisa kuu na la

machukizo?• Kulingana na 1 Nefi 14:13, ni kwa madhumuni gani lile kanisa kuu na la machukizo

litakusanya pamoja umati mkubwa?Shuhudia kwamba tuko katika vita ambavyo Nefi alielezea —vita vya kiroho vya siku za mwisho dhidi ya uovu. Kama waumini wa Kanisa la Mwanakondoo, sisi idadi yetu ni ndogo, na tunahitaji usaidizi kama tunataka kuwa washindi dhidi ya jeshi la ibilisi.• Ni nini unachosoma katika 1 Nefi 14:14 ambacho kinakupatia matumaini?Sisitiza kwamba ahadi zilizotolewa katika maandiko haya hasa zinatumika kwa wale wanaofanya na kushika maagano na Bwana. Wakumbushe wanafunzi kwamba waliingia katika agano la ubatizo na Bwana. Vuta usikivu wa wanafunzi kwenye kishazi “wamejiki-nga kwa utakatifu na kwa nguvu za Mungu” 1 Nefi 14:14.

tubu

Kamafanya moyo kuwa mgumu

Page 67: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

52

SoMo la 15

• Kishazi “wamejikinga kwa utakatifu na kwa nguvu za Mungu” kinamaanisha nini kwako?• Ni kwa njia gani kuwa “umejikinga kwa utakatifu na kwa nguvu za Mungu” kunaweza

kuwa kama ngao na silaha katika vita vyetu dhidi ya uovu?• Ni wakati gani ulihisi kwamba wewe “umejikinga kwa utakatifu na kwa nguvu za Mu-

ngu”? Je! Ulihisi vipi?Waulize wanafunzi jinsi wanavyoweza kufanya muhtasari wa ujumbe katika 1 Nefi 14:1–14. Hakikisha wanaelewa kwamba ikiwa tutaishi kwa haki na kushika maagano yetu, nguvu za Mungu zitatusaidia sisi kushinda uovu. Waulize wanafunzi kutathimini maisha yao na kufikiria kile wanachoweza kufanya ili kujiami vyema katika utakatifu. Wahimize wao kutenda juu ya mvuvio wanaopokea. Wa-hakikishie wao kwamba wanapoendelea kuwa waaminifu, watakuwa na nafasi ya kuingia katika mahekalu matakatifu na kufanya maagano ya ziada na Bwana. Ahadi na maagano wanayofanya hapo yatawaletea uwezo na ulinzi mkuu katika maisha yao.Alika mwanafunzi asome 1 Nefi 14:3–4 kwa sauti. Muulize mwanafunzi mwingine kusoma 1 Nefi 14:15–17 kwa sauti.• Ni nini kitafanyika kwa kanisa kuu na la machukizo?• Matokeo ya mwisho yatakuwa nini katika vita kati ya Kanisa la Mwanakondoo (ufalme

wa Mungu) na majeshi ya ibilisi?• Kujua matokeo ya mapambano haya kunaweza kukusaidia vipi?Soma kwa darasa taarifa ifuatayo ya Boyd K. Packer wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili:“Sisi [waumini wa Kanisa] ni sehemu ndogo ukilinganisha na mabilioni ya watu hapa duniani. Lakini sisi ni wale tulio, na tunaojua kile tunachojua, na tutasonga mbele na kuhubiri injili.

“Kitabu cha Mormoni kinasema wazi kwamba kamwe hatutatawaliwa na umati. Bali tuna uwezo wa ukuhani [ona 1 Nefi 14:14]. . . .“Tunaweza na katika wakati ufaao kwa kweli tutawashawishi wanadamu wote. Itajulikana sisi ni kina nani na kwa nini tuko hivyo. Inaweza kuone-kana kama haiwezekani; vigumu sana; lakini sio tu inawezekana bali hakika kwamba tutashinda vita dhidi ya Shetani” (“The Power of the Priesthood,”

Ensign au Liahona, May 2010, 7).Wahakikishie wanafunzi kwamba ufalme wa Mungu utashinda katika siku za mwisho. Onyesha imani kwamba wao wanaweza kuwa na imani katika Mungu na uwezo Wake uta-shinda uovu wote. Watie moyo wao ili wawe jeshi la wema katika kuwashawishi wengine.

1 Nefi 14:18–27Nefi anamwona Yohana MfunuajiAndika maswali yafuatayo kwenye ubao:

Ni nani kati ya Mitume Kumi na Wawili Nefi alimwona katika ono?Huyu Mtume angeandika kuhusu nini?Kwa nini Nefi aliamriwa asiandike ono lote?

Waalike wanafunzi kusoma 1 Nefi 14:18–27 kimya kimya. Kisha jadili kwa kifupi majibu ya maswali yaliyopo ubaoni.Elezea kwamba hii mistari inalenga angalao sehemu ya maandishi ya Yohana katika kitabu cha Ufunuo. Mada kuu ya kitabu hicho ni kwamba Mungu atayashinda majeshi ya ibilisi. Kama vile Yohana, Nefi pia aliona ono la mwisho wa ulimwengu, lakini aliamriwa asiandike kwa sababu Yohana alikuwa amepatiwa jukumu la kufanya hivyo. Kama muda unaruhusu, unaweza kuhitimisha somo kwa mjadala mfupi kuhusu jinsi Biblia na Kitabu cha Mormoni vinavyofanya kazi pamoja ili “kuthibitisha ukweli” wa kila kimoja na kuwa “kimoja” (1 Nefi 13:40–41).

Page 68: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

53

Somo la Mafunzo ya Nyumbani1 Nefi 7–14 (Kitengo cha 3)

Vifaa vya Matayarisho kwa Mwalimu wa Mafunzo ya NyumbaniMuhtasari wa Masomo ya Kila Siku ya Mafu-nzo ya NyumbaniMuhtasari ufuatao wa mafundisho na kanuni ambazo wanafunzi walijifunza walipokuwa wakisoma1 Nefi 7–14 (Kitengo 3) haikusudiwi kufundishwa kama sehemu ya somo lako. Somo unalofunza linazingatia machache tu ya haya mafundisho na kanuni. Fuata msukumo wa Roho Mtakatifu unapofikiria mahitaji ya wanafunzi.

Siku ya 1 (1 Nefi 7)Wanafunzi walivyojifunza jinsi wana wa Lehi walivyorudi Yerusalemu kuchukua familia ya Ishmaeli pamoja nao hata nchi ya ahadi, walijifunza kwamba Bwana aliwaamuru wao kuwaoa na kukuza watoto Kwake na kwamba Mungu hujibu maombi kulingana na imani yetu.

Siku ya 2 (1 Nefi 8)Wanafunzi walijifunza ono la Lehi la mti wa uzima. Wa-lijifunza kwamba kwenda kwa Yesu Kristo na kupokea Upatanisho Wake huleta furaha na shangwe. Waliposoma kuhusu baadhi ya makundi ya watu katika ndoto na ufanisi wao na kushindwa kwao katika mti wa uzima na kula tunda, pia walijifunza kanuni zifuatazo: Kiburi, malimwengu, na kujitia kwenye majaribu hutuzuia kutoka kupokea baraka za Upatanisho. Kama tutashikilia kwa nguvu neno la Mungu, itatusaidia sisi kushinda majaribu na ushawishi wa malimwe-ngu. Kushikilia kwa nguvu neno la Mungu, hutusaidia kuwa karibu na Bwana na kupokea baraka za Upatanisho.

Siku 3 (1 Nefi 10–11)Wanafunzi walijifunza kilichofanyika wakati Nefi alipotaka “kuona, na kusikia, na kujua” (1 Nefi 10:17) mwenyewe vitu ambavyo baba yake aliviona. Kupitia mfano wa Nefi, waliona kwamba Mungu hufunua kweli kwa wale walio na bidii ya kumtafuta Yeye. Nefi alipokea ono ambalo lilifunza upendo wa Mungu kwetu, ulioonyeshwa kupitia zawadi ya Mwanawe. Wanafunzi walipata nafasi ya kuandika maana yake kwao.

Siku ya 4 (1 Nefi 12–14)Katika ukumbusho wa ono lake, Nefi aliona jinsi Bwana alivyotayarisha njia kwa ajili ya Urejesho. Alijifunza kwamba kweli halisi na za thamani zingeondolewa kutoka katika Bi-blia lakini kwamba Kitabu cha Mormoni na maandiko ya siku za mwisho yangerejesha kweli halisi na za thamani ambazo hutusaidia sisi kujua kwamba Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu na kutusaidia kuja Kwake. Nefi pia aliona siku za mwisho. Wanafunzi walitafakari kanuni kwamba kama tuta-ishi kwa utakatifu na kuweka maagano matakatifu, uwezo wa Mungu utatusaidia kushinda uovu.

UtanguliziLengo la somo la wiki ni ono la Lehi katika 1 Nefi 8. Unapofu-ndisha hili somo, sisitiza juu ya shangwe ambayo Upatanisho wa Yesu Kristo unaweza kuleta katika maisha yetu na jinsi tuna-vyopata uzoefu wa baraka za Upatanisho kupitia kuishi neno la Mungu. Wanafunzi watatumia maandiko yao, mwongozo wa kujifunza wa mwanafunzi, na shajara za kujifunza maandiko kote katika somo.

Mapendekezo ya Kufundisha

1 Nefi 7Bwana aliamuru wana wa Lehi kurudi Yerusalemu kumchukua Ishmaeli na familia yakeWeka picha ya wenzi walioana na watoto wao—labda picha yako mwenyewe au yule wanafunzi ambaye ulimwomba kuleta picha.

Waulize wanafunzi: Kwa nini familia ni muhimu katika mpango wa Mungu kwa wokovu wao.

Waalike wanafunzi kurejea na kufanya muhtasari wa 1 Nefi 7:1–5. Uliza ni kanuni gani wamejifunza kutoka katika mistari hii. (Wanafunzi wanaweza kuelezea kanuni mbali mbali. Kanuni iliyotiliwa mkazo katika kitabu cha mwanafunzi ilikuwa kwamba Bwana alituamuru sisi kuoa na kukuza watoto Kwake.)

Katika somo lao la siku ya 1, wanafunzi walipatiwa kazi ya kumuuliza mzazi, kiongozi wa Kanisa, au mwalimu awashauri njia tatu ambazo vijana wanaweza kujitayarisha kwa ajili ya ndoa na kuelea watoto “kwa Bwana.” Waalike wanafunzi wachache kuelezea kile walichojifunza.

1 Nefi 8Lehi anapata ono la mti wa uzimaWakumbushe wanafunzi baada ya Nefi na ndugu zake kuwa-leta Ishmaeli na familia yake katika nyika, Lehi alipata ndoto. Mwanafunzi anapokuwa akisoma 1 Nefi 8:10–13 kwa sauti, acha mwanafunzi mwingine achore kwenye ubao au kipande cha karatasi kile mistari inaeleza. Kama unahisi inafaa sana kwa darasa lako, unaweza kuonyesha picha ya Ndoto ya Lehi (62620; Kitabu cha Sanaa za Injili [2009], no. 69) na baada ya wanafunzi kutambua twasira kadhaa katika hii mistari.

Waulize wanafunzi: Ni nini katika maelezo ya Lehi hufanya tunda na mti kutamanika kwako?

Wakumbushe wao kwamba tunda la mti linaashiria “karama kuu zaidi ya karama zote za Mungu” (1 Nefi 15:36)—baraka ya Upatanisho wa Yesu Kristo. Kama ulipata mwanafunzi kuchora picha, unaweza kuitia nembo kile ambacho tunda linaashiria kwenye mchoro.

Waulize wanafunzi: Kile ambacho wamejifunza kutoka katika 1 Nefi 8:10–13 kuhusu kupokea baraka za Upatanisho? (Ingawa

Page 69: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

54

SoMo la MafUnzo ya nyUMbani

wanafunzi wanaweza kutumia maneno tofauti kuelezea, hakiki-sha kanuni ifuatayo iko wazi Kuja kwa Yesu Kristo na kushi-riki Upatanisho Wake huleta furaha na shangwe. Unaweza kuandika kanuni hii kwenye ubao.)

Katika somo la siku ya 2, wanafunzi waliulizwa kujibu swali “Upatanisho wa Mwokozi ulikuletea furaha na shangwe katika maisha yako wakati gani? Waalike wanafunzi kwenda katika shajara zao za kujifunza maandiko na kimya kimya wasome majibu yao.

Wasaidie wanafunzi kuelezea vyema kweli na shuhuda mmoja kwa mwingine, watie moyo baadhi yao wasome au waongee kuhusu kile walichoandika Unaweza pia kusimulia kuhusu wakati ambapo Upatanisho ulileta furaha na shangwe katika maisha yako.

Elezea kwamba ono la Lehi halifunzi tu kwamba Upatanisho huleta furaha kuu; pia huonyesha kile tunachohitajika kufanya ili kupokea baraka za Upatanisho. Waalike wanafunzi kurejea 1 Nefi 8:19–26 na wachore ishara zingine kutoka katika ono la Lehi, au acha watambue ishara zingine katika picha ya Ndoto ya Lehi. Wanapochora au kutambua ishara, waalike wao kueleza kile ambacho ishara tofauti zinamaanisha. (Kama wanahitaji usaidizi, watie moyo kutumia chati waliokamilisha katika mwo-ngozo wa mafunzo ya mwanafunzi.)

Acha mwanafunzi asome 1 Nefi 8:30 kwa sauti. Kisha uliza maswali yafuatayo:

• Kazi ya fimbo ya chuma ni nini—neno la Mungu—katika ono la Lehi?

• Ulivyosoma1 Nefi 8,ulijifunza nini kuhusu umuhimu wa neno la Mungu?

• Ni vishazi gani katika 1 Nefi 8:30 vinaelezea tunachohitajika kufanya ili kupokea baraka za Upatanisho?

• Unafikiri inamaanisha nini “kusonga mbele, daima kushikilia fimbo ya chuma”?

Andika ubaoni kanuni mbili nyengine walizojifunza katika mwo-ngozo wa kujifunza wa mwanafunzi: Kama tutashikilia kwa nguvu neno la Mungu, itatusaidia sisi kushinda majaribu na ushawishi wa malimwengu. Kushikilia kwa nguvu neno la Mungu, hutusaidia kuwa karibu na Bwana na kupokea baraka za Upatanisho.

Waulize wanafunzi kufikiria kama wangekuwa wamisionari na wakapata nafasi ya kushuhudia kuhusu umuhimu wa kujifu-nza neno la Mungu na kuishi kulingana na kanuni zake. Acha wao waelezee kile ambacho wangesema, kulingana na uzoefu wao wenyewe. Fikiria kuelezea hisia zako kuhusu uwezo wa maandiko na maneno ya manabii katika kukusaidia kuja karibu na Mwokozi.

1 Nefi 10–14Kwa sababu ya imani na bidii yake, Nefi alipokea ufunuo wa kibinafsi kuhusu vitu ambavyo baba yao alifunza na mambo mengine mengiWaulize wanafunzi wasome 1 Nefi 10:17, 19 kwa sauti. Acha darasa kutambua baraka ambazo huja wakati tunatafuta kwa bidii mwongozo wa Bwana. Acha mwanafunzi mmoja au wawili waelezee kile wanachofikiria “tafuta kwa bidii” inamaanisha. (Wakati wa somo lao la siku ya 3, waliulizwa kuandika kile kina-chomaanisha katika mwongozo wa kujifunza wa mwanafunzi.

Fanya muhtasari wa 1 Nefi 11–14 kwa kusema kwamba Nefi alipokea ufunuo wa kibinafsi kwa sababu alimtafuta Bwana kwa bidii. Aliona huduma na Upatanisho wa Yesu Kristo (1 Nefi 11), maangamizo ya siku za usoni ya watu wake kwa sababu ya kiburi na uovu (1 Nefi 12), wakoloni Wayunani wa nchi ya ahadi na urejesho wa kweli halisi na za thamani (1 Nefi 13), na watu wema wakipigana dhidi ya kazi za kanisa kuu na la machukizo katika siku za mwisho (1 Nefi 14).

Tazama: Ili kutayarisha shughuli ifuatayo, unaweza kurejea masomo ambayo yanaambatana katika hiki kitabu na vifaa katika mwongozo wa kujifunza wa mwanafunzi wa siku ya 4 ya kitengo hiki.

Waulize wanafunzi kuchagua mojawapo ya sura hizi katika 1 Nefi 11–14 na kufanya yafuatayo. (Unaweza kuwaambia wafa-nye hivi kwenye ubao au kipande cha karatasi.)

• Andika muhtasari wa sura iliyochaguliwa.• Andika mojawapo ya kanuni za injili zilizofunzwa katika sura

hii. (Unaweza kutumia kanuni iliyoangaziwa katika mwongozo wa kujifunza au kutambua moja wao wenyewe.)

• Andika jinsi kanuni hii inavyohusiana nasi leo.

Baada ya wao kuwa na muda wa kutosha wa kujitayarisha, waalike wanafunzi waelezee kile walichoandika. Alika mwanafu-nzi mmoja au wawili kutoa shuhuda zao za kanuni walizojifunza walipokuwa wakisoma 1 Nefi 7–14 wiki hii.

Kabla ya kumaliza darasa lako, kumbuka kukusanya shajara zao za kujifunza maandiko na kufuatia kazi zote.

Kitengo Kifuatacho (1 Nefi 15–19)Katika kitengo kifuatacho, wanafunzi watajifunza zaidi kuhusu majaribu ya Lehi na watu wake walipokuwa wanaendelea na safari yao katika nyika na kusafiri hadi nchi ya ahadi. Fikiria ku-shangaa kwao wakati walipoamka asubuhi moja na kugundua “kitufe cha wa ufundi maalumu” — Liahona. Liahona ilifanya kazi vipi, na iliwaongoza vipi? Kwa nini Nefi aliwakemea ndugu zake ndani ya meli? Nefi alieleza nini juu ya nchi ya ahadi?

Page 70: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

55

Mapendekezo ya Kufundisha

1 Nefi 15:1–11Ndugu za Nefi walilalamika kwamba hawakuweza kuelewa ono la LehiWaulize wanafunzi kuorodhesha shughuli kadhaa ambazo zinahitaji juhudi katika upande wetu kabla ya kupata matokeo. Unaweza kuorodhesha majibu yao kwenye ubao. (Majibu yao yanaweza kujumuisha kazi za shule, kulima shamba, kucheza chombo cha muziki, kucheza michezo, na mazoezi ya mwili. Waalike wanafunzi kufikiria mifano ya uzoefu waliopata.)• Kwa shughuli unazofikiria juu yake, ni uhusiano gani uliona kati ya juhudi unazofanya

na matokeo ambayo yatafuata?Baada ya wanafunzi kujibu swali hili, watie moyo wao kutafuta mfumo sawa katika somo ili wanapojifunza 1 Nefi 15.Waambie wanafunzi kwamba 1 Nefi 15 inaanza na Nefi akirudi kwenye hema la baba yake baada ya kupokea ono sawa na la Lehi. Alika mwanafunzi asome 1 Nefi 15:1–2, 7 kwa sauti. Uliza darasa kutafuta kile Nefi alipata aliporudi kwenye hema la baba yake.• Nefi alipata nini wakati aliporudi kwenye hema la baba yake?• Ndugu za Nefi walikuwa wanabishania kuhusu nini? Kwa nini?”Alika mwanafunzi asome 1 Nefi 15:3 kwa sauti. Uliza darasa kutambua sababu ya kwa nini ndugu za Nefi walikuwa wanasumbuka kuelewa mambo ambayo Lehi alikuwa amewafunza.• Kulingana na 1 Nefi 15:3, kwa nini ndugu za Nefi walikuwa na shida ya kuelewa mambo

ambayo Lehi alikuwa amewafunza?• Nefi alifanya nini kuwasaidia wao kujifunza kweli za kiroho? (Ili kuwasaidia wanafunzi

kujibu swali hili, unaweza kuwaacha wasome 1 Nefi 10:17.)Alika mwanafunzi asome 1 Nefi 15:8 kwa sauti.• Ukifikiria kwamba Nefi alikuwa amepokea maono ya mbinguni katika jibu la maswali

yake (ona 1 Nefi 11–14), kwa nini ilikuwa ni kawaida kwake kuwauliza ndugu zake kama watamuuliza Bwana?

Uliza mwanafunzi asome 1 Nefi 15:9 kwa sauti. Kisha muulize mwanafunzi mwengine kuandika jibu la ndugu za Nefi kwenye ubao:

Hapana; kwani Bwana hatujulishi vitu hivi.Kwenye ubao, piga mstari chini ya kishazi “hapana”• Ni kitu gani ambacho ndugu za Nefi walikuwa hawajafanya?Weka jibu (kumuuliza Bwana, kuomba, au kuuliza Bwana) katika sentensi kwenye ubao ili sasa isomeke hivi:

Sisi hatujamuuliza Bwana; kwani Bwana hatujulishi vitu hivi.(Kwa maneno mengine, “Sisi hatujauliza, kwa sababu Bwana haongei nasi.”)• Kulikuwa na shida gani katika fikra za Lamani na Lenueli?Hakikisha wanafunzi wanatambua kosa katika fikra za ndugu za Nefi. Waalike wao kupa-nga tena au kugueza sentensi kwenye ubao ili iwe wazi kuelezea kwa nini ndugu za Nefi

UtanguliziBaada ya Nefi kupokea ono sawa na lile ono baba yake alipokea, alirudi kwenye hema la baba yake. Hapo aliwakuta ndugu zake wakibishana kuhusu mafundi-sho ya Lehi. Nefi aliwarudi ndugu zake kwa ugumu wa mioyo yao na kuwakumbusha wao jinsi ya kupokea

ufunuo wao wenyewe. Kisha alielezea baadhi ya mafu-ndisho ya Lehi kuhusu matawi halisi ya mti wa mzietuni na maana ya ono la Lehi la mti wa uzima. 1 Nefi 15 hutofautisha bidii ya Nefi za kutafuta kweli na juhudi za kijuujuu za ndugu zake (ona 1 Nefi 15:9–11).

Maswali ya kufuatiliaMaswali ya kufuatilia yafaayo uwaalika wana-funzi kupekua maandiko kwa kina kuhusu umbo la hadithi na kujenga ue-lewa wao wa msingi wa umbo la maandiko. Haya maswali mara nyingi yanajumuisha maneno kama vile nani, nini, lini,vipi,wapi, na kwa nini. Kwa sababu ma-swali ya kufuatilia huhi-taji wanafunzi kutafuta habari katika maandiko, itasaidia kuuliza maswali kama vile hayo kabla kuwapatia wanafunzi aya za kusoma ambazo kwazo majibu yanapa-tikana. Hii huzingatia usikivu wa wanafunzi juu ya maswali katika kifungu cha maandiko kama inavyosomwa.

SOMO LA 16

1 nefi 15

Page 71: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

56

SoMo la 16

hawakuwa wanapokea usaidizi wa Bwana katika kuelewa mafundisho ya Lehi. Jibu lina-weza kujumuisha “Bwana hatujulishi mambo kama hayo kwetu kwa sababu sisi hatujamu-uliza Yeye” na “Kwa sababu hatujamuuliza Bwana, Yeye hajatujulisha mambo haya.”Muulize mwanafunzi asome 1 Nefi 15:10–11 kwa sauti. Acha darasa litafute kweli ambazo Nefi aliwafunza ndugu zake ili kuwasaidia wao kujifunza jinsi ya kupokea majibu kutoka kwa Mungu.• Ni ushauri gani Nefi aliwapatia ndugu zake ili kuwasaidia wao kuelewa maneno ya

baba yao na kupokea majibu kutoka kwa Mungu? (Nefi aliwashauri ndugu zake kuwa wasifanye mioyo yao kuwa migumu, waombe kwa imani, waamini kwamba watapokea jibu, na wawe na bidii katika kushika amri. Wasaidie wanafunzi kuona kwamba Nefi ali-kuwa anajua thamani ya kanuni hizi kwa sababu alizifuata yeye mwenyewe na kupokea ufunuo kama matokeo yake.)

Ili kuwasidia wanafunzi kutambua kanuni kutoka katika hii mistari, andika yafuatayo kwenye ubao:

Kama . . . , basi . . .• Kulingana na kile tumesoma katika 1 Nefi 15:10–11, tunawezaje kukamilisha taarifa hii?Wanafunzi wanaweza kutumia maneno tofauti, lakini inawapasa kuonyesha uelewa wa kwa-mba kama tutamuuliza Bwana kwa imani na kutii amri Zake, basi tutakuwa tayari ku-pokea ufunuo na mwongozo kutoka Kwake. (Unaweza kuandika kanuni hii kwenye ubao.)Tayarisha maswali yafuatayo kabla ya darasa, kwenye ubao au kama kitini:

1. Ni kwa namna gani kuelezea kanuni ili kumsaidia mtu kuelewa jinsi ya kufunzwa na Bwana na kuelewa kweli za kiroho?

2. Juhudi zako za kibinafsi zimeathiri vipi uwezo wako wa kupokea mwongozo wa Bwana na kuelewa injili?

Panga wanafunzi katika jozi. Katika kila jozi, acha mwenzi atafakari swali la kwanza na yule mwenzi mwingine atafakati swali la pili. Acha wao waelezane majibu yao mmoja kwa mwingine. Baada ya wanafunzi kuwa na muda wa kutosha wa kujadili majibu yao, alika wachache kushiriki mawazo ya pamoja na darasa. Sisitiza kwamba juhudi zetu na hamu yetu ya kutafuta maelekezo ya Roho inaweza kuathiri kwa ushuhuda wetu na ukaribu wetu na Bwana.

1 Nefi 15:12–20Nefi alielezea kutawanyika na kukusanyika kwa IsraeliFanya muhtasari mfupi wa 1 Nefi 15:12–20. Elezea kwamba ili kuwasaidia ndugu zake katika ubishi wao, Nefi aliwafunza maana ya unabii wa Lehi kuhusu “matawi halisi ya mti wa mzeituni” na Wayunani (ona 1 Nefi 10:12–14; 15:7). Yeye alielezea kwamba mti wa mzeituni uliashiria nyumba ya Israeli. Kwa sababu nyumba ya Lehi ilikuwa imeondoka Yesusalemu na wakatengana na nyumba ya Israeli, ilikuwa ni kama tawi ambalo lilikuwa limevunjika kutoka katika mti wa mzeituni (ona 1 Nefi 15:12). Alielezea zaidi kwamba katika siku za mwisho, miaka mingi baada ya uzao wa Lehi utapata kuwa “umefifia katika kutoamini” (1 Nefi 15:13), utimilifu wa injili utatolewa kwa Wayunani. Wayunani kisha wataleta injili kwa uzao wa Lehi, wakiwarejesha kwenye elimu ya Mkombozi wao na kwenye baraka za agano la baba zao. Hii ingekuwa kama kukusanyika na kupandikizwa matawi tena kwenye mti wa mzeituni (ona 1 Nefi 15:13–17). Huu urejesho hautatendeka tu kwa uzao wa Lehi bali kwa wote wa nyumba ya Israeli (ona 1 Nefi 15:18–20; ona pia 1 Nefi 10:12–14).Shuhudia kwamba Bwana atatunza ahadi Zake na kukumbuka maagano Yake na watoto Wake. Ana hamu ya wote kupokea baraka za injili.

1 Nefi 15:21–36Nefi anajibu maswali ya ndugu zake kuhusu ono la LehiElezea kwamba katika masazo ya 1 Nefi 15, tunasoma majibu ya Nefi kwa ndugu zake kuhusu ono la Lehi. Nefi alitumia kile alichojifunza katika ono lake kuwafunza wao.Weka taarifa zifuatazo za Rais Ezra Taft Benson kwenye ubao au katika kitini. Waalike wa-nafunzi kubahatisha neno au kipengele ambacho kinafaa kuwekwa katika kila sentensi.

1. “Katika tunaweza kupata uwezo wa kushinda majaribu.”

Page 72: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

57

1 nefi 15

2. “Ile ina uwezo wa kuwaimarisha watakatifu na kuwahami kwa Roho.” 3. “Yake ni mojawapo ya karama za thamani kuu Yeye ametupatia sisi.”

Mara wanafunzi wachache wakisha toa majibu yao, uliza mwanafunzi kusoma 1 Nefi 15:23–24 kwa sauti. Waalike wanafunzi kutafuta kishazi katika kifungu hiki ambacho kitawasaidia kukamilisha kwa usahihi taarifa za Rais Benson. Baada ya mistari kusomwa, waulize wanafunzi kubahatisha tena neno au kishazi ambacho kitakamilisha kila taarifa. Rejea maswali sahihi pamoja na darasa. Majibu: 1—neno la Mungu; 2—neno la Mungu; 3—neno. [Ona “The Power of the Word,” Ensign, May 1986, 80, 82.])Acha wanafunzi wapekue 1 Nefi 15:24–25 kimya kimya. Alika nusu ya wanafunzi kuta-mbua katika hii mistari baadhi ya baraka za kufuata neno la Mungu. Uliza ile nusu ingine ya darasa kutambua maneno au vishazi ambavyo vinashawishi jinsi ya kufuata neno la Mungu ili kupokea hizo baraka. Acha kila kikundi kielezee kile walichopata.• Tunahitaji kufanya nini ili “kusikia,” kushika kwa nguvu,” na “kutii” neno la Mungu?

(Majibu yanaweza kujumuisha kujifunza maandiko kila siku, kusikia na kutii ushauri wa viongozi wa Kanisa wenye maongozi, na kutafuta na kufuata ufunuo wa kibinafsi kupitia maombi.)

Waalike wanafunzi kusema kwa maneno yao wenyewe kanuni ambayo inafanya muhtasari kile hii mistari inafunza kuhusu kujifunza maandiko na baraka inazoleta kwa maisha yetu. Jibu moja linaweza kuwa ni kwamba kujifunza na kufuata neno la Mungu kila siku hutuimarisha dhidi ya majaribu ya Shetani. Ili kuwapatia wanafunzi nafasi ya kushu-hudia kanuni hii, uliza:• Ni wakati gani kujifunza maandiko kibinafsi kulikuimarisha dhidi ya majaribu? (Wakumbu-

she wanafunzi kwamba hawahitajiki kushiriki uzoefu ambao ni wa kibinasfi au siri sana.)Soma taarifa ifuatayo ya Mzee Robert D. Hales wa Akidi ya wale Mitume Kumi na Wawili:“Muhimu sana ni kweli hizi ambazo Baba wa Mbinguni aliwapatia Lehi na Nefi maono wazi sana yakiashiria neno la Mungu kama fimbo ya chuma. Wote baba na mwana waliji-funza kwamba kushikilia huu mwongozo imara, usiopinda, wakutegemewa sana ndio njia pekee ya kuwa kwenye njia iliyosonga na nyembamba ambayo huelekea kwa Mwokozi wetu” (“Holy Scriptures: The Power of God unto Our Salvation,” Ensign au Liahona, Nov. 2006, 25).Wakumbushe wanafunzi kwamba katika ono la Lehi, wale walioshikilia kwa nguvu ile fimbo waliongozwa salama kupitia ukungu wa giza, ambao uliashiria majaribu ya ibilisi (ona 1 Nefi 12:17).Fanya muhtasari mfupi wa 1 Nefi 15:26–29. Waambie wanafunzi kwamba ndugu za Nefi walimuuliza yeye aelezee maana ya mto baba yao aliona katika ono lake. Alielezea kwa-mba iliashiria jehanamu mbaya waliyotayarishiwa waovu, kuwatenganisha wao na Mungu na watu Wake.• Nefi alitambua nini kuhusu maji ya ule mto ambacho baba yake hakutambua? (Yale maji

yalikuwa machafu.)Elezea kwamba katika 1 Nefi 15:33–36, Nefi hufunza kuhusu haki ya Mungu na kwa nini waovu watatenganishwa mbali na watakatifu. Waalike wanafunzi kadhaa kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka kwa 1 Nefi 15:33–36.• Kwa nini waovu watatenganisha mbali na watakatifu?• Kujua kwamba hakuna mtu mchafu anaweza kuingia katika ufalme wa Mungu kuliwa-

saidiaje Lamani na Lemueli?Watie moyo wanafunzi kufikiria kanuni walizojifunza katika 1 Nefi 15 kwa kutafakari maswali yafuatayo kimya:• Ni kwa njia gani maono ya Lehi na Nefi yanaonyesha upendeleo wa Mungu kwa La-

mani na Lemueli? Ni kwa njia gani yanaonyesha upendeleo wa Mungu kwetu?• Tunaweza kufanya nini ili kutumia kanuni hizi mlizojifunza mlipokuwa mkisoma sura

hii? (Unaweza kuwaalika wanafunzi kuandika majibu yao ya swali hili katika shajara zao za kujifunza maandiko au vitabu vya darasani.)

Fikiria kuhitimisha somo hili kwa kusoma tena 1 Nefi 15:25 kwa darasa. Toa ushuhuda wako juu ya baraka ambazo huja tunapotii neno la Mungu na kushika amri Zake. Wahaki-kishie wao juu ya upendo mkuu Mungu alionao kwao na kwamba Yeye atawabariki katika juhudi zao za wema.

Page 73: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

58

Mapendekezo ya Kufundisha

1 Nefi 16:1−6Nefi alijibu kunung’unika kwa ndugu zakeWaulize wanafunzi kufikiria kuhusu wakati wamekemewa kwa kufanya kitu kimakosa na kuhusu jinsi walijibu. Kisha muulize mwanafunzi asome 1 Nefi 16:1 kwa sauti. Kabla yeye kusoma, alika darasa lisikilize majibu ya Lamani na Lemueli kwa mafundisho ya Nefi. Wakumbushe wanafunzi kwamba Nefi alifunza kwamba waovu watatengwa mbali na watakatifu na kutupwa nje kutoka uwepo wa Mungu (ona 1 Nefi 15:33–36).Waalike wanafunzi kusoma 1 Nefi 16:2 kimya. Unaweza kushauri kwamba waweke alama kishazi Nefi alitumia kuelezea jinsi watu fulani wanafanya baada ya kusikia kweli wakati wao hawaiishi.• Unafikiria inamaanisha kwamba “wenye hatia huchukua ukweli kuwa mgumu”? Unafi-

kiria maana ya kishazi “huwakata hadi sehemu zao za ndani” ni nini?• Ni zipi kati ya njia tunazoweza kujibu kama ukweli ni mgumu kuuvumilia?Waalike wanafunzi kusoma 1 Nefi 16:3–4 kimya kimya. Unaweza kushauri kwamba waweke alama kwenye maneno kama na basi katika mstari wa 3. Watie moyo wao kuta-futa ushauri ambao Nefi aliwapatia ndugu zake kuhusu jinsi wanafaa kufanya juu ya “vitu vigumu” alivyokuwa amesema. Alika mwanafunzi aelezee kwa maneno yake mwenyewe kile Nefi aliwafunza ndugu zake.• Kulingana na 1 Nefi 16:5, ndugu za Nefi walijibu vipi maelekezo yake?• Ni nini 1 Nefi 16:5 inashauri kuhusu jinsi tunavyopaswa kujibu wakati ukweli “unatu-

kata [sisi] hadi sehemu za ndani”?

1 Nefi 16:7−33Bwana anaongoza familia ya Lehi kupitia kwa LiahonaAlika mwanafunzi asome 1 Nefi 16:9–10 kwa sauti. Onyesha picha ya Liahona (62041; Ki-tabu cha Sanaa za Injili [2009], no. 68). Taja kwamba mchoro wa msanii unaashiria Liahona.• Ni kwa njia gani unafikiria kipawa kama hicho kingekuwa usaidizi kwa Lehi na familia

yake katika hali yao?Waalike wanafunzi wachache kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka katika 1 Nefi 16:16–19.• Liahona iliwasaidia vipi familia ya Lehi?• Baada ya familia ya Lehi kupokea Liahona, safari yao ilikuwa rahisi au ngumu? Ni nini

Nefi anasimulia katika 1 Nefi 16:17–19 kuhimili majibu yako?• Kwa nini unafikiri watu wema, kama vile Lehi na Nefi, wakati mwengine hukabiliwa na

majaribu? (Unaweza kuelezea kwamba majaribu mengi tunayokabiliana nayo sio kuwa ni matokeo ya chaguzi mbaya. Bali, ni nafasi za kujifunza na kukua kama sehemu ya safari yetu katika maisha ya muda.)

UtanguliziBaada ya kuchomwa katika mioyo yao na maneno ya Nefi, Lamani na Lemueli walijinyenyekeza mbele za Bwana. Familia iliendelea na safari yao hata nyikani, na Bwana aliwabariki wao kwa Liahona, kupitia kwayo Yeye aliwaongoza katika safari yao. Walipokuwa wakisafiri, walipatwa na shida, ikijumuisha kuvunjika

kwa upinde wa Nefi, ambao ndio ulikuwa njia yao kuu ya kupata chakula. Wengi wa familia—hata Lehi—wa-lianza kunung’unika dhidi ya Bwana. Nefi aliwarudi ndugu zake kwa ajili ya kulalamika, akatengeneza upi-nde mpya, na akatafuta ushauri wa baba yake kuhusu kule anakopaswa kwenda kuwinda.

SOMO LA 17

1 nephi 16

Page 74: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

59

1 nephi 16

Alika nusu darasa kupekua 1 Nefi 16:20–22 kimya kimya, wakitafuta jinsi baadhi ya familia ya Lehi walivyofanya kuhusu majaribu ya kuvunjika kwa upinde wa Nefi. Alika nusu ile ingine ya darasa kupekua 1 Nefi 16:23–25, 30–32, wakitafuta majibu ya Nefi kwa haya majaribu na jinsi majibu yake yalivyoathiri familia yake. Baada ya kila kikundi kutoa ripoti ya kile wamegundua, uliza:• Tunaweza kujifunza nini kwa kulinganisha haya majibu mawili ya majaribu sawa?• Kwa nini ni muhimu kwamba Nefi alienda kwa baba yake ili apate maelekezo, hata

ingawa Lehi alikuwa amenung’unika? Ni kanuni gani tunajifunza kutokana na haya ili kutumia katika maisha yetu? (Unaweza kuelezea kwamba kwa kumwendea Lehi kwa maelekezo, Nefi alionyesha heshima kwake yeye na kulimsaidia kumkumbusha yeye kumgeukia Bwana. Kutafuta ushauri kutoka kwa wazazi na viongozi wa ukuhani, licha ya upungufu wao, ni njia ya kuwaheshimu na kuonyesha imani katika Bwana.)

• Ni kanuni zipi za ziada tunazoweza kujifunza kutoka katika majibu ya Nefi kwa dhiki ya familia yake? (Wanafunzi wanapotoa mawazo yao, hakikisha umesisitiza kwamba kama tutafanya yote tuwezayo na kutafuta maelekezo ya Bwana, basi Yeye atatusaidia sisi kupitia shida zetu)

Uliza mwanafunzi asome 1 Nefi 16:26–29 kwa sauti. Alika darasa kutafuta maelezo ya kina kuhusu jinsi Bwana alivyotumia Liahona kuongoza familia ya Lehi. Ili kuwasaidia wana-funzi kuelewa na kutumia mistari hii kuwafunza kuhusu kupokea mwongozo wa Bwana, uliza maswali yafuatayo:• Ni nini tofauti kati ya kufuata maelekezo ya Bwana kijuujuu na kufuata maelekezo ya

Bwana kwa imani na bidii?Waalike wanafunzi kusoma 1 Nefi 16:29, Alma 37:6–7, na Alma 37:38–41 kimya kimya, wakitafuta kanuni ambazo zinafunzwa katika mafungu yote matatu.• Ni kanuni gani inayofunzwa katika haya mafungu matatu? (Hakikisha kwamba wanafu-

nzi wanaelewa kwamba kwa vitu vidogo, Bwana anaweza kuleta mambo makubwa. Unaweza kuandika kanuni hii kwenye ubao.)

• Kulingana na mistari hii, ni “vitu vidogo” gani Bwana ametupatia ili kutupatia sisi mwongozo?

Andika maswali yafuatayo kwenye ubao, ukisema wazi kwamba katika kila swali kuna neno au kishazi kilichokosekana. (Unaweza kufanya hivi kabla ya darasa.)

1. Ni vitu gani viwili au vitatu ambavyo . . .ni kama Liahona? 2. Ni nini baadhi ya vitu ambavyo vinaweza kutufanya sisi kukosa ujumbe muhimu

kutoka . . . ? 3. Ni wakati gani ulibarikiwa kwa kufuata mwongozo wa . . . ?

Gawa darasa katika vikundi vitatu, kukiwa na kiongozi katika kila kikundi. Mpatie kila kio-ngozi nakala ya mojawapo ya kazi zifuatazo, ambazo kwazo kikundi chao kitajifunza “vitu vidogo” ambavyo Bwana hutumia kutuongoza sisi. (Kama darasa lako ni kubwa, unaweza kugawa wanafunzi katika vikundi zaidi ya vitatu ili kupunguza ukubwa wa kikundi. Kama ukifanya hivyo, utahitajika kupatia kikundi kimoja au zaidi vyenye kazi sawa.)

Kikundi cha 1: Baraka za KipatriakiKisomee kundi taarifa ifuatayo ya Rais Thomas S. Monson:“Bwana yule yule ambaye alitoa Liahona kwa Lehi hutoa kwako na kwangu kipawa nadra na cha thamani ili kutupatia maelekezo ya maisha yetu, na kuweka alama hatari kwa usalama wetu, na kupanga njia, hata mapito salama—sio tu hadi nchi ya ahadi, lakini hadi kwenye nyumba yetu ya mbinguni. Kipawa ambacho nimetaja kinajulikana kama baraka zako za kipatriaki. . . .“. . . Baraka zako hazipaswi kukunjwa kimaridadi na kuwekwa kando. Hazifai kuwekwa kwenye fremu au kuchapishwa. Bali, zinafaa kusomwa. Zinafaa kupendwa. Zinafaa kufu-atwa. Baraka zako za kipatriaki zitakuwezesha kupitia katika usiku wa giza. Zitakuelekeza wewe kupitia hatari za maisha. . . . Baraka zako za kipatriaki ni Liahona ya kibinafsi kwako ya kupanga njia yako na kuongoza njia yako” (“Your Patriarchal Blessing: A Liahona of Light,” Ensign, Nov. 1986, 65–66).Geuza maswali yaliyopo ubaoni ili yawe yanahusu baraka za kipatriaki. Kama kikundi, jadilini maswali hayo. Mpatie kazi mtu mmoja katika kikundi chako kuelezea pamoja na

Page 75: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

60

SoMo la 17

wengine wa darasa kile ambacho kikundi chake kimejifunza. Pia alika mtu mmoja kutoka katika kikundi chake kuelezea uzoefu wake kutokana na swali la 3

Kikundi cha 2: Maandiko na Maneno ya Manabii wa Siku za MwishoKisomee kikundi kufuatana na taarifa ya Mzee W. Rolfe Kerr wa Sabini:“Maneno ya Kristo yanaweza kuwa Liahona ya kibinafsi kwa kila mmoja wetu, kutuo-nyesha njia. Acha tusiwe wazembe kwa sababu ya urahisi wa njia. Acha sisi kwa imani tuchukue maneno ya Kristo katika akili zetu na katika mioyo yetu kama yalivyoandikwa katika maandiko matakatifu na yanavyotamkwa na manabii, waonaji, na wafunuzi walio hai. Acha sisi kwa imani na bidii tusherekee maneno ya Kristo, kwani maneno ya Kristo yatakuwa Liahona ya kiroho ya kutueleza sisi vitu vyote ambavyo tunapaswa kufanya” (“The Words of Christ—Our Spiritual Liahona,” Ensign au Liahona, May 2004, 37).Geuza maswali yaliyopo ubaoni ili yawe yanahusu maandiko na maneno ya manabii wa siku za mwisho. Kama kikundi, jadilini maswali hayo. Mpatie kazi mtu mmoja katika kiku-ndi chako kuelezea pamoja na wengine wa darasa kile ambacho kikundi chake kimejifu-nza. Pia alika mtu mmoja kutoka katika kikundi chake kuelezea uzoefu wake kutokana na swali la 3

Kikundi cha 3: Roho MtakatifuSoma kwa kundi kufuata taarifa ya Mzee David A. Bednar wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili:“Tunajaribu kuwianisha mitazamo yetu na matendo yetu na utakatifu, basi Roho Mtakatifu hufanyika kwetu leo kile ambacho Liahona ilikifanya kwa Lehi na familia yake katika siku zao. Mambo hayo hayo ambayo yalisababisha Liahona kufanya kazi kwa Lehi vile vile hu-alika Roho Mtakatifu katika maisha yako. Na mambo hayo hayo ambayo yalisababisha Lia-hona isifanye kazi wakati wa kale vivyo hivyo yatatufanya sisi kujiondoa wenyewe kutoka kwa Roho Mtakatifu leo” (“That We May Always Have His Spirit to Be with Us,” Ensign au Liahona, May 2006, 30).Geuza maswali yaliyopo ubaoni ili yawe yanahusu Roho Mtakatifu. Kama kikundi, jadilini maswali hayo. Mpatie kazi mtu mmoja katika kikundi chake kuelezea pamoja na wengine wa darasa kile ambacho kikundi chake kimejifunza. Pia alika mtu mmoja kutoka katika kikundi chake kuelezea uzoefu wake kutokana na swali la 3Muhtasari kwa mwalimu: Baada ya dakika sita hadi nane, uliza kila kikundi kufunza darasa kile walichojifunza kutokana na majidiliano yao. Unaweza pia kuwaalika wanafunzi kuandika katika shajara zao za kujifunza maandiko au vitabu vya darasani kuhusu wakati Bwana aliwaongoza wao kupitia vitu vidogo. Fikiria kuwaambia kuhusu wakati wewe ulipopokea mwongozo kutoka kwa Bwana kupitia vitu vidogo.

Tangazo na Habari za Usuli1 Nefi 16:10. Liahona ya kibinafsiRais Spencer W. Kimball alifananisha dhamiri yetu na Liahona:

“Wewe sharti ufahamu kwamba wewe una kitu kama dira, kama Liahona, katika mwili wako. Kila mtoto amepatiwa. Anapofika umri wa miaka minane, anajua wema na uovu, kama wazazi wake wamemfundisha

yeye vyema. Kama yeye akipuuza Liahona ambayo yeye yuko nayo katika maungo yake yeye mwenyewe, hatimaye haitaweza kumnong'onezea. Lakini kama sisi tutakumbuka kwamba kila mmoja wetu ana kitu ambacho humwongoza vyema, chombo chetu hakita-enda mrama na mateso hayatakuja na pinde hazitavu-njika na familia hazitalilia chakula—kama tutasikiliza msukumo wa Liahona yetu wenyewe, ambayo tunaita dhamiri” (“Our Own Liahona,” Ensign, Nov. 1976, 79).

Page 76: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

61

Mapendekezo ya Kufundisha

1 Nefi 17:1−51Safari ya familia ya Lehi hadi Neema, pale Nefi alipoamriwa kujenga chomboChora mchoro ufuatao kwenye ubao.

Waulize wanafunzi kufikiria kama wanaweza kuelezea maisha yao sasa kama rahisi au magumu, na kwa nini. (Unaweza kuwatia moyo wanafunzi kujadili majibu yao na wenzi wao. Au waalike wanafunzi kadhaa kuelezea fikra zao pamoja na darasa lote. Wakumbushe wao kwamba hawahitajiki kushiriki uzefu ambao ni wa kibinasfi au siri sana.)Alika mwanafunzi kusoma 1 Nefi 17:1, 4, 6 kwa sauti. Anaposoma, acha darasa litafute maneno na vishazi ambavyo vinaonyesha kama wakati Nefi na familia yake walikuwa na wakati rahisi au mgumu huko nyikani.• Nefi alifananisha wakati wao nyikani kama rahisi au mgumu? Ni maneno gani yanayoo-

nyesha ulikuwa mgumu?Elezea kwamba Nefi na familia yake walibarikiwa sana wakati huu. Waalike wanafunzi kupitia 1 Nefi 17:2, 5, 12−13 ili kutambua baadhi ya njia Nefi na familia yake ilibarikiwa wakati wa safari yao. Waulize wanafunzi wachache kuelezea kile ambacho wamegundua.Waambie wanafunzi kwamba Nefi alifunza kanuni ambayo inaelezea kwa nini familia yake iliweza kubarikiwa katika wakati huu mgumu. Waalike wanafunzi kusoma 1 Nefi 17:3 kimya kimya na kutambua kanuni ambayo huanza kwa neno kama. Elezea kwa kifupi kwamba katika maandiko, kanuni mara ingine husemwa kwa mbinu ya “kama- basi” Neno kama hutangulia kitendo , na neno basi hutangulia matokeo (mazuri au mabaya) tutakayo-pata kama matokeo ya kitendo hicho.Ingawa 1 Nefi 17:3 haina neno basi, inaelezea kitendo, pamoja na baraka chache ambazo zitakuwa matokeo. Waulize wanafunzi kusema sehemu ya “kama- basi” ya kanuni wali-zotambua. Wanapaswa kusema kitu kama ifuatavyo: Kama tutaweka amri, basi Bwana atatuimarisha na kutupatia njia ya kukamilisha kile ambacho Yeye ameamuru. (Unaweza kuandika kanuni hii kwenye ubao.) Waalike wanafunzi kutafuta ushahidi wa hii kanuni wanapojifunza uzoefu wa Nefi na wanapotafakari juu ya maisha yao wenyewe.Sambaza kitini kilicho na maswali yafuatayo (au andika maswali kwenye ubao kabla ya darasa):

1. Bwana alimwamuru Nefi kufanya nini? (1 Nefi 17:7−8) Nefi alijibu vipi? (1 Nefi 17:9−11, 15−16) Ndugu zake walijibu vipi? (1 Nefi 17:17−21)

2. Bwana alimsaidia vipi Musa kutimiza kazi aliyokuwa ameamriwa kufanya? (1 Nefi 17:23−29)

3. Ndugu za Nefi walikuwa kama watoto wa Israeli kwa njia gani? (1 Nefi 17:30, 42)

UtanguliziBaada ya kusafiri nyikani kwa miaka minane, familia ya Lehi aliwasili katika eneo la pwani ambalo waliita Neema. Baada ya wao kujiandaa katika Neema, Bwana alimwamuru Nefi kujenga chombo. Wakati ndugu zake walipojua kile alikuwa anajaribu kufanya, walimkejeli

na kisha kunung’unika na kukataa kumsaidia. Nefi ali-wafunza ndugu zake kwamba ingawa Bwana alitafuta kuongea nao kupitia ile sauti tulivu, na ndogo ya Roho, uovu wao uliwazuia wao kuhisi maneno Yake. Aliwake-mea wao kwa ajili ya uovu wao na kuwasihi kutubu.

Rahisi Ugumu

Wasaidie wanafunzi kujifunza jinsi ya kutambua mafundisho na kanuniUnapowasaidia wana-funzi kujifunza jinsi ya kutambua mafundi-sho na kanuni katika maandiko, wataweza kujifunza maandiko kwa ufanisi zaidi wenyewe. Wafundishe wanafunzi kutafuta vishazi kama vile “na hivyo,” “kwa hivyo,” “ikawa kwa-mba,” “tazama,” au “kama . . . , basi . . . ,” ambavyo utanguliza kila kanuni au taarifa ya mafundisho.

SOMO LA 18

1 nefi 17

Page 77: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

62

SoMo la 18

4. Ni nini Bwana ameamuru ambacho kinaweza kuwa kigumu kwangu? 5. Ninawezaje kufanya kama Nefi na Musa? Ninawezaje kuepukana na makosa ya

Ndugu za Nefi na watoto wa Israeli?Tanguliza maswali yaliyopo hapa juu kwa kuelezea kwamba itawasaidia wanafunzi kuona jinsi ambavyo Nefi aliendelea kuishi kanuni hii katika 1 Nefi 17:3 baada ya kufika nchi ya Neema. Maswali pia yatawasaidia wanafunzi kutumia kanuni hii wenyewe. Waalike wana-funzi kusoma 1 Nefi 17:7−8 kwa sauti. Uliza wengine walio darasani kutambua kile Nefi alikuwa ameamriwa kufanya. Acha wanafunzi waandike majibu chini ya swali la 1 kwenye kitini au katika shajara zao za kujifunza maandiko.• Ni kwa namna gani amri hii inaweza kuwa ilikuwa ngumu kwa Nefi?Alika mwanafunzi kusoma 1 Nefi 17:9−11 na mwanafunzi mwingine kusoma 1 Nefi 17:15–16 kwa sauti. Kabla ya kusoma, uliza darasa lisikilize majibu ya Nefi ya amri ya kujenga chombo.• Ni nini kinachokupendeza katika majibu ya Nefi?Acha wanafunzi waandike muhtasari wa majibu ya Nefi chini ya swali la 1 kwenye kitini au katika shajara zao za kujifunza maandiko.Waaulize wanafunzi kadhaa kuchukua zamu kusoma kwa sauti 1 Nefi 17:17−21. Acha darasa litafute maneno na vishazi ambavyo vinaonyesha mitazamo ya Lamani na Lemueli. Acha wanafunzi waandike muhtasari wa majibu ya Lamani na Lemueli juu ya amri ya kujenga chombo. Alika mwanafunzi mmoja au wawili kushiriki muhtasari wao pamoja na darasa.Elezea kwamba Nefi alijibu malalamishi ya ndugu zake kwa kuwakumbusha wao kwamba Bwana alimsaidia Musa kutimiza jambo gumu la kuwafanya huru watoto wa Israeli kutoka utumwani. Nefi pia alifananisha ugumu wa moyo wa ndugu zake na ule wa watoto wa Israeli. Waalike wanafunzi kujifunza mafungu ya maandiko na kuandika majibu yao kwa swali la 2 na la 3. Kutegemea mahitaji ya wanafunzi wako, unaweza kuwaacha wafanye haya peke yao au pamoja na wenzi wao.Baada ya wanafunzi kutimiza swali la 2 na la 3, uliza:• Bwana alimsaidia vipi Musa kutimiza kazi aliyokuwa ameamriwa kufanya?• Unafikiria mfano wa Musa uliwezaje kumsaidia Nefi?• Ni kwa njia gani ndugu za Nefi walikuwa kama watoto wa Israeli?Taja kwamba wakati Bwana anatupatia sisi kazi au amri yenye changamoto, tunaweza kuchagua kufanya kama Nefi alivyofanya, au tunaweza kufanya kama Lamani na Lemueli walivyofanya. Elezea kwamba ingawa Mungu hajatuamuru sisi kutimiza kazi kama vile kujenga chombo au kutawanya Bahari ya Shamu, Yeye ametupatia amri na kutuamuru sisi tutimize mambo ambayo watu fulani watayaona kuwa magumu. Kwa mfano, Yeye ame-tuamuru sisi kuwa na fikra safi na kuishika kitakatifu siku za Sabato. Yeye anatutarajia sisi kutimiza miito ya Kanisa (kama vile rais wa akidi au wa darasa) na kuwahudumia wengine. Yeye pia anatarajia sisi kushika maagano yetu na kuwa hai katika Kanisa, hata tunapokabi-liana na changamoto. Wapatie muda wanafunzi kuandika majibu ya swali la 4 na la 5. Wa-tie moyo wao kujibu swali la 4 kwa kuandika kuhusu kila kitu Bwana ameamuru ambacho kinaweza kuwa kigumu kwao.Baada ya wanafunzi kuwa na muda wa kutosha wa kuandika, soma onyesho la imani la Nefi katika 1 Nefi 17:50 kwa sauti. Kisha waulize wanafunzi kusoma 1 Nefi 17:51 kimya kimya na kufikiria jinsi inavyoweza kutumika katika maisha yao. Watie moyo kuongeza majina yao baada ya neno mimi na wabadilishe kishazi cha kujenga chombo na kazi au amri wanayoona kuwa ngumu. Fikiria kuwaalika wanafunzi ambao wako radhi kufanya hivyo kusoma 1 Nefi 17:51 kwa sauti kwa mabadilisho waliyofanya. Rejea tena kwenye kanuni zilizoandikwa ubaoni.• Ni uzoefu gani Nefi alikuwa nao tayari na hii kanuni ambayo ilimpatia imani kwamba

Bwana angemsaidia yeye kutimiza amri yoyote?• Ni nini ambacho umepata uzoefu wake ambacho kinakupatia imani kwamba Mungu

atakusaidia wewe kutimiza chochote Yeye atakacho kuamuru?Toa ushuhuda wako kwamba tunapo shika amri, Bwana hutuimarisha na hutupatia njia za sisi kutimiza mambo ambayo Yeye ametuamuru.

Fikiria mahitaji ya wanafunzi wako unapofunzaNi hekima kugeuza mbinu za ufunzaji ili kuwasidia wanafunzi kufanikiwa kutimiza nafasi zao kama wana-funzi. Kwa mfano, kama wanafunzi wanaone-kana kuchoka, fikiria vile wao wanaweza kufanya pamoja na wenzi wao ili kuwasidia wao kujihu-sisha katika kujifunza. Kama wanafunzi wa hari, unaweza kuwau-liza wao kujifunza peke yao ili kuwasaidia wao kushikilia kazi.

Page 78: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

63

1 nefi 17

1 Nefi 17:45−55Nefi aliwakemea Lamani na Lemueli kwa ajili ya uovu waoOnyesha picha ya Nefi Akiwadhibiti Nduguze Waasi (62044; Kitabu cha Sanaa za Injili [2009], no. 70). Waalike wanafunzi wafanye muhtasari wa kile kinachotokea katika picha hii. Kama wanafunzi hawana jibu, waalike wao watafute jibu katika 1 Nefi 17:48, 53–54.• Kulingana na 1 Nefi 17:53, kwa nini Bwana aliwashtua ndugu za Nefi? (Unaweza ku-

vutia usikivu wa wanafunzi kwenye tanbihi ya 53a ili kuwasaidia wao kuelewa kwamba neno shtua katika muktadha huu linamaanisha “kutikisika au kutetemeka.”)

Elezea kwamba kushtua Bwana alikowapatia Lamani na Lemueli ilikuwa ni mojawapo ya njia nyingi Bwana aliwasiliana nao. Waalike wanafunzi kusoma 1 Nefi 17:45 na watambue njia chache Bwana alitumia kuwasiliana na Lamani na Lemueli katika wakati uliopita.• Ni zipi baadhi ya njia Bwana alikuwa amewasiliana na Lamani na Lemueli? Ni zipi kati

hizi zinazoonekana kuwa njia ambazo Bwana hutumia kuwasiliana nasi?Unaweza kushauri kwamba wanafunzi waweke alama taarifa ifuatayo katika 1 Nefi 17:45: “Amewazungumzia kwa sauti ndogo tulivu.” Muulize mwanafunzi kusoma taarifa ifuatayo ya Boyd K. Packer wa Akidi ya wale Mitume Kumi na Wawili:“Roho Mtakatifu husema kwa sauti ambayo wewe utahisi zaidi ya wewe kusikia. Ina-semekana kama ‘sauti ndogo tulivu’ [M&M 85:6]. Na hali tunaongea juu ya ‘kusikiliza’ mnong’ono wa Roho, mara nyingi mtu huelezea msukumo wa kiroho kwa kusema, ‘mimi nilipata hisia . . .’” (“Personal Revelation: The Gift, the Test, and the Promise,” Ensign, Nov. 1994, 60).Unaweza kuwaalika wanafunzi kuandika kweli ifuatayo katika maandiko yao karibu na 1 Nefi 17:45: Roho Mtakatifu huongea kwa sauti tulivu, ndogo ambayo tunahisi ku-liko kusikia. (Ili kusisitiza hii kanuni, unaweza kuwaacha wanafunzi wasome Mafundisho na Maagano 8:2–3.)• Ni wakati gani ulihisi sauti tulivu, ndogo ya Roho Mtakatifu ikiongea na wewe?• Unaweza kufanya nini ambacho kinaweza kukusaidia kuhisi na kutambua sauti tulivu,

ndogo ya Roho Mtakatifu?Baada ya wanafunzi kujibu, unaweza kuwahimiza wao kuweka alama kwenye kishazi katika 1 Nefi 17:45: “Lakini mlikuwa mmekufa ganzi, kwamba hamkupata yale ma-neno yake.” Acha wanafunzi wasome sentensi ya kwanza ya 1 Nefi 17:45 na watambue kwa nini Lamani na Lemueli walikuwa “wamekufa ganzi.” Waalike wao waelezee kile walichogundua.• Kwa nini kuwa “wepesi kwa kutenda maovu” kuliwafanya Lamani na Lemueli kuwa

“wamekufa ganzi”?• Dhambi zinaweza kuathiri vipi uwezo wetu wa kuhisi ushawishi wa Roho Mtakatifu?Baada ya wanafunzi kujibu, soma taarifa ifuatayo ya Rais James E. Faust, ambaye alihu-dumu kama mshiriki wa Urais wa Kwanza:“Simu za rununu zinatumika kwa mawasiliano mengi katika nyakati zetu. Mara kwa mara, hata hivyo, tunajikuta sehemu ambapo mtandao haupo. Hii inaweza kufanyika wakati mtumiaji wa simu ya rununu yuko ndani ya upenyo chini ya ardhi au korongo kuu au pale ambapo kuna ukinzani wa siginali.“Hivyo ndivyo ilivyo na mawasiliano matakatifu. Sisi mara nyingi tunajiweka kwenye sehemu tupu kiroho—sehemu na hali ambazo zinazuia ujumbe mtakatifu. Kati ya hizi sehemu tupu hujumuisha ghadhabu, picha za ngono, kutenda dhambi, uchoyo, na hali zinazo mhuzunisha Roho” (“Did You Get the Right Message?” Ensign au Liahona, May 2004, 67).Kuhitimisha, waalike wanafunzi kufikiria ujumbe ambao Bwana amejaribu kuwasili-sha kwao hivi majuzi. Watie moyo wao kutafakari kama kuna “sehemu tupu za kiroho” ambazo zinaweza kuwazuia wao kupokea mawasiliano kama hayo. (Unaweza kuwaacha wanafunzi waandike kuhusu haya katika shajara zao za kujifunza maandiko.) Shuhudia kwamba Roho Mtakatifu huongea kwa sauti tulivu, ndogo ambayo tunahisi zaidi ya kusi-kia. Pia shuhudia kwamba tunaweza kupata mawasiliano haya tunapojaribu kuwa wasta-hiki wa huu mvuvio ororo.

Page 79: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

64

Mapendekezo ya Kufundisha

1 Nefi 18:1–8Familia ya Lehi inajiandaa kusafiri hadi nchi ya ahadiAndika uwezo wa Bwana na juhudi zangu kwenye ubao. Waulize wanafunzi kufikiria juu ya shida wanayopata. Waalike wao kuchagua kati ya (uwezo wa Bwana au juhudi zangu) ina-weza kufaa katika kusuluisha shida hiyo, na uwaulize waelezee kwa nini. Baada ya mjadala mfupi, waalike wanafunzi kutafuta njia kwa mfano wa Nefi katika 1 Nefi 18 zinazoweza kuwasaidia kukabili changamoto walizonazo. Onyesha picha ya Lehi na Watu Wake Wakiwasili katika Nchi ya Ahadi (62045; Kitabu cha Sanaa za Injili [2009], no. 71).Waalike wanafunzi kusoma 1 Nefi 18:1–8 kimya. Waulize wao kutafuta (1) kile Nefi na fa-milia yake walifanya kujiandaa kwa safari yao hadi nchi ya ahadi na (2) kile Bwana alifanya kuwasidia wao.• Unafikiria ni kwa nini ilikuwa ni muhimu kwamba Nefi apokee ufunuo “mara kwa mara”?• Katika 1 Nefi 18:2–3, unaona uhusiano gani kati ya matendo ya Nefi na usaidizi aliopo-

kea kutoka kwa Bwana?• Ni kwa jinsi gani mwongozo wa Bwana na juhudi za Nefi mwenyewe zilikuwa muhimu

katika kukalimilisha chombo na kufanya safari hadi nchi ya ahadi?Waulize wanafunzi kufanya muhtasari wa kanuni chache walizojifunza kutoka kwa mfano wa Nefi. Mara wanafunzi wamepata nafasi ya kutambua kweli walizojifunza, andika ka-nuni ifuatayo kwenye ubao: Ili kukamilisha kile Bwana ameamuru, tunahitaji kuta-futa usaidizi Wake na kufanya bidii zetu wenyewe. • Ni wakati gani wewe ulipokea mwongozo au maelekezo kutoka kwa Bwana na pia ulihi-

tajika kuweka bidii yako mwenyewe ili kuweka mojawapo wa amri Zake?Waalike wanafunzi waandike majibu ya mmoja kwa mwingine kwa swali hili katika shajara zao za kujifunza maandiko au vitabu vya darasani.Taja kwamba sisi sote tunahitaji usaidizi katika kutii amri Zake na kufuata viwango vya injili vilivyoorodheshwa katika For the Strength of Youth. (Unaweza kupata na kure-jea nakala ya kitabu For the Strength of Youth, kabla ya darasa.) Watie moyo wanafunzi kutambua amri au viwango vya injili wanavyohitaji usaidizi wa Mungu kuvitii. Wapatie wakati wa kuandika katika shajara zao za kujifunza maandiko kuhusu (1) ) kile wana-weza kufanya ili watafute usaidizi wa Bwana ili kuitii na (2) ni juhudi gani za kibinafsi wanazohitaji kufanya ili kuitii.

UtanguliziKufuatia maelekezo ya Bwana, Nefi na wengine walimaliza kujenga chombo na kusafiri kwenda nchi ya ahadi. Wakati wa safari yao, Lamani na Lemueli na wana wa Ishmaeli na wake wao waliasi dhidi ya Bwana. Wakati Nefi aliwarudi, Lamani na Lemueli walimfunga kwa kamba. Kama matokeo, Liahona ilisita kufanya

kazi na walikuwa hawawezi kujua njia ya kwenda kwa kuelekeza chombo. Wakati dhoruba kali ilitishia maisha ya kila mmoja kwenye chombo, walitubu na kumfu-ngua Nefi. Nefi aliomba na dhoruba ikatulia, na Bwana tena akaelekeza safari yao kuelekea nchi ya ahadi.

SOMO LA 19

1 nefi 18

Page 80: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

65

1 nefi 18

1 Nefi 18:9–2Lamani na Lemueli waliongoza uasi ambao ulitatiza safari kwenda nchi ya ahadiUliza swali lifuatalo:• Unafikiria ni sababu gani tunapatwa na matatizo?Baada ya mjadala, alika mwanafunzi kusoma taarifa ifuatayo ya Mzee L. Whitney Cla-yton wa Sabini. Uliza darasa kusikiliza sababu tatu Mzee Clayton alitoa kwa matatizo tanayoyapata:“Katika hali ya kawaida, mizigo yetu huja kutoka vyanzo vitatu. [1] Mizigo fulani ni ma-tokeo ya asili ya hali za ulimwengu tunamoishi. Ugonjwa, ulemavu wa kimwili, tufani, na matetemeko ya nchi huja mara kwa mara kupitia makosa ambayo siyo yetu wenyewe. . . .“[2] Mizigo mingine inawekwa juu yetu kwa sababu ya makosa ya wengine. Udhalimu na uteja unaweza kuifanya nyumba kuwa chochote bali si mbinguni hapa ulimwenguni kwa wanafamilia wasio na hatia. Dhambi, desturi potovu, ugandamizaji, na jinai inatapakaza waathiriwa walio na mizigo katika mapito ya maisha. . . .“[3] Makosa na upungufu wetu wenyewe huzaa shida zetu nyingi na kuweka mizigo mzito kwenye mabega yetu wenyewe. Mzigo mzito sana tunaojitweka wenyewe ni mzigo wa dhambi” (“That Your Burdens May Be Light,” Ensign au Liahona, Nov. 2009, 12–13).Andika kwenye ubao (1) hali za dunia, (2) makosa ya wengine, na (3) makosa na upungufu wetu wenyewe.Elezea kwamba baada ya familia ya Lehi kuanza safari yao ya baharini, Lamani, Lemu-eli, na wengine walifanya chaguzi duni ambazo zilileta matatizo kwa kila mtu kwenye chombo. Waalike wanafunzi kusoma 1 Nefi 18:9 kwa sauti. Watie moyo wanafunzi kuinua mikono yao wanaposikia mfano wa mtu akifanya chaguo baya.• Ni chaguo gani baya Lamani, Lemueli, wana wa Ishmaeli, na wake wao walifanya? Kwa

nini ni makosa?Wasaidie wanafunzi waelewe kwamba sio makosa kucheza densi, kusikiliza muziki, au kufurahia, lakini huu mstari unaonyesha kwamba Lamani, Lemueli, na wengine walifanya vitu hivi “kwa ujeuri mwingi”(1 Nefi 18:9). Elezea kwamba katika huu muktadha neno ujeuri humaanisha lugha chafu, upotovu. Adui anaweza kutumia kucheza densi, muziki, na njia tunayoongea ili kupotosha mioyo na akili zetu na kutufanya sisi kupoteza wenzi wa Roho Mtakatifu.Alika mwanafunzi asome 1 Nefi 18:10 kwa sauti.• Kulingana na 1 Nefi 18:10, Nefi alihofia ni nini kingefanyika kama wale walioasi

hawangetubu?• Nefi alifanya nini kuwasaidia wao? (Inaweza kuwasaidia wanafunzi kujua kwamba neno

busara humaanisha umakini.)Waalike wanafunzi kutafakari juu ya vile watafanya kama mwanafamilia au kiongozi wa Kanisa atawauliza wao kubadilisha muziki wanaosikiliza, njia wanayocheza densi, au njia wanayoongea. Watie moyo wao kutafakari kama watakuwa tayari kusikia na kubadilika.Alika mwanafunzi asome 1 Nefi 18:11 kwa sauti.• Kulingana na 1 Nefi 18:10–11, Lamani na Lemueli walifanya nini baada ya ushauri wa Nefi?• Kwa nini Bwana alikubali Lamani na Lemueli wamfunge Nefi?Waalike wanafunzi kadhaa kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka 1 Nefi 18:12–14, 17–19. Waulize wanafunzi watafute maneno na vishazi ambavyo vinaonyesha matokeo ya tabia ya Lamani na Lemueli. Waalike wanafunzi kutambua kanuni za injili walizojifunza kutoka kwa tukio hili. Jibu moja linaweza kuwa dhambi huelekeza kwa mateso yetu wenyewe na wakati mwingine kwa wengine pia. Ili kuwasaidia wanafunzi kutumia kanuni hii, unaweza kuuliza maswali kama:• Matendo ya uasi ya wachache yanawezaje kuathiri kundi lote?• Chaguzi zisizo busara au za uasi zinaathiri vipi uwezo wetu wa kupokea ufunuo?Kama sehemu ya majadiliano haya, fikiria kusoma taarifa ifuatayo ya Rais Boyd K. Packer wa Jamii ya wale Mitume Kumi na Wawili:

Page 81: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

66

SoMo la 19

“Tumeshuhudia hali za staha na ukosefu wa staha katika Kanisa. Ingawa wengi ni wa kupongezwa sana, tunaelea. Tuna sababu za kuwa na hofu sana.“Ulimwengu unaendelea kuwa na kelele sana. Mavazi na mapambo na tabia zimelegea na kuzembea na sio nadhifu kabisa. Muziki wa fujo maneno machafu yanavuma kupitia vipaza sauti. Mitindo mbali mbali ya mambo haya yanaendelea kukubalika sana na kuwa na ushawishi juu ya vijana wetu. . . .“Huu mtindo wa kelele nyingi, mhemko mwingi, ubishi mwingi, kutojizui, ukosefu wa nidhamu, ukosefu busara sio jambo la kutokeza kwa bahati, wala maasumu, wala lisilo na madhara.“Amri ya kwanza ya kamanda akiandaa uvamizi wa kijeshi ni kukwamisha mitambo ya mawasiliano ya wale wanataka kuteka.Uholela unaingiana sana na madhumuni ya adui kwa kufunga mitandao ya ufunuo ya kote kwa akili na roho” (“Reverence Invites Revelation,” Ensign, Nov. 1991, 22).• Kama unakuwa muasi na mtovu, unawezaje kuathiri familia yako? Inaweza kuathiri vipi

marafiki zako? Inaweza kuathiri vipi darasa au familia yako?Rejea tena kwenye vyanzo vitatu vilivyoorodhesha kwenye ubao. Elezea kwamba sehemu iliyobakia ya sura hii inaweza kutusaidia kujifunza jinsi tunaweza kufanya wakati matatizo yanapokuja, hata yatatokea kutokana na chaguzi zetu wenyewe au chaguzi za wengine. Waalike wanafunzi kusoma 1 Nefi 18:15–16, 20–23 kibinafsi. Watie moyo wao kutafuta kweli ambazo zinaweza kutimika kwa hali zote. Acha wao washiriki kwa maneno yao wenyewe kile wamejifunza. Majibu yao yanaweza kujumuisha yafuatayo:

Tunaweza kumtegemea Mungu na kubakia waaminifu wakati wa majaribu yetu.Maombi yanaweza kutusaidia kupata imani wakati wa majaribu yetu.

Wanafunzi wanaposhiriki mawazo yao, hakikisha umesisitiza mfano wa Nefi wa wema wa-kati wake wa majaribu. Alika mwanafunzi asome ushuhuda ufuatao wa Mzee L. Whitney Clayton. Acha darasa litambue kile Mzee Clayton alitushauri kufanya wakati tunakumbwa na majaribu:“Bila kujali mizigo yetu tunayokabiliana nayo katika maisha kama matokeo ya hali za asili, makosa ya wengine, au makosa na upungufu wetu wenyewe, sisi sote ni watoto wa Baba wa Mbinguni wenye upendo, ambaye alitutuma hapa ulimwenguni kama sehemu ya mpa-ngo Wake wa milele kwa ukuaji na maendeleo yetu. Uzoefu wetu wa kibinafsi na kipekee unaweza kutusaidia sisi kujitayarisha kurudi Kwake. Ni sharti tufanye kila kitu tunaweza kubeba mizigo yetu ‘vyema’[ona M&M 121:7–8]. . . .“ Najua kwamba kama tutashika amri za Mungu na maagano yetu, Yeye atatusaidia na mizigo yetu. Yeye hutuimarisha. Wakati sisi tunatubu, Yeye hutusamehe na hutubariki kwa imani ya dhamiri na shangwe” (“That Your Burdens May Be Light,” 13–14).Waalike wanafunzi kufikiria kuhusu mojawapo ya kweli walizojifunza kutoka katika somo hili.• Ni lini uliona kweli hii katika maisha yako au maisha ya mtu unayemjua?Unaweza kuogezea ushuhuda wako kwamba Mungu anaweza kutusaidia kupitia majaribu yetu kama sisi ni waaminifu na tunapotubu na kurudi Kwake.Kuhitimisha, wakumbushe wanafunzi kwamba licha ya matatizo yaliyowakabili Nefi na familia yake, wao hatimaye walifika nchi ya ahadi. Shuhudia kwamba tunapotafuta maele-kezo ya Bwana na kufanya bidii kuyafuata, sisi pia tunaweza kufanikiwa kukamilisha safari Bwana alitutuma sisi hapa ulimwenguni kupata uzoefu.

Page 82: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

67

Mapendekezo ya Kufundisha

1 Nefi 19:1–19Nefi anaandika unabii wa Yesu Kristo kuwasaidia watu kumkumbuka Mkombozi waoInua nakala ya Kitabu cha Mormoni. Fanya muhtasari wa 1 Nefi 19:1–4 kwa kuelezea kwa-mba Nefi aliamriwa kutengeneza seti mbili za mabamba—moja kuandika historia takatifu (kidini) na ingine kwa historia ya kilimwengu kwa watu wake. Alika mwanafunzi asome 1 Nefi 19:3, 5–6 kwa sauti. Uliza wengine wa darasa kutafuta kile Nefi alisema kuhusu vitu “vitakatifu.”• Ni kwa nini Nefi aliweka kumbukumbu ya vitu vitakatifu?Alika mwanafunzi asome 1 Nefi 19:7 kwa sauti. Kabla hajasoma, elezea kwamba katika mstari huu, kishazi “Mungu wa Israeli” humaanisha Yesu Kristo. Mstari huu pia unajumui-sha neno bure, humaanisha “hakuna kitu.” Kumweka mtu kuwa bure ni kumchukulia mtu kama vile yeye hana maana.• Baada ya kusema ataandika tu kuhusu kile kilicho kitakatifu, ni nini Nefi alianza kua-

ndika kuhusu nini?• Kulingana na 1 Nefi 19:7, watu fulani wanamkanyangia chini ya miguu yao Mwokozi

vipi au “kumfanya kuwa bure”?• Kukataa kusikia ushauri wa Bwana kunafanana vipi na kumfanya Yeye kuwa bure au

kumkanyagia chini ya miguu ya mtu?Muulize mwanafunzi asome 1 Nefi 19:8–10 kwa sauti. Uliza darasa litafute njia ambazo kwazo watu wanaweza kumfanya Mwokozi kama kitu bure wakati wa huduma Yake du-niani. (Unaweza kushauri kwamba wanafunzi waweke alama kwenye maneno na vishazi walivyopata.)• Ni kwa njia gani watu waliweza kumfanya Mwokozi kama kitu bure wakati wa huduma

Yake duniani?• Ni maelezo gani katika mistari hii yanaonyesha kwamba Mwokozi hatuchukulii kama

“kitu bure”? (Wanafunzi wanafaa kuelewa kwamba Mwokozi aliteseka yote yale Yeye alifanya “kwa sababu ya upendo wake mkarimu na subira yake kwa watoto wa watu.”)

• Unapofikiria kuhusu hii mistari, una hisia zipi kuhusu Mwokozi?Alika mwanafunzi asome 1 Nefi 19:13−14, na uache darasa kutafuta kile nabii Zeno ali-sema kitakuwa sababu za wale waliomsulubisha Mwokozi (na uzao wao) “watapigwa kwa mjeledi na watu wote.”• Ni sababu gani Zeno alitoa kwa nini wale walimsulubu Mwokozi (na uzao wao) “wata-

pingwa kwa mjeledi na watu wote”?Andika taarifa ifuatayo kwenye ubao: Wanageuza mioyo yao upande.• Unafikiria inamaanisha nini kugeuza moyo wa mtu upande kutoka kwa Bwana?

UtanguliziKatika hii sura, Nefi alielezea kwamba watu fulani hawata mheshimu Mungu wa Israeli, Yesu Kristo. Kitamathali, watamkanyagia Yesu Kristo chini ya miguu yao kwa kumfanya Yeye kuwa bure na kukataa kutii ushauri Wake. Nefi pia alisimulia mafundisho ya manabii wa kale ambao walitabiri kwamba wale waliohusika na kumchapa na kumsulubisha Mwokozi, vile vile uzao wao, watatawanywa na kuteswa mpaka

watakapogeuza mioyo kwa Bwana. Wakati huo, Bwana “atakumbuka maagano aliyofanya na baba zao” (ona 1 Nefi 19:15). Nefi alielezea kwamba yeye aliandika vitu hivi ili kuwashawishi watu wake kumkumbuka Bwana na kumwamini Yeye. Yeye pia aliwafunza watu wake kufananisha maandiko na wao wenyewe ili kuwasidia wao kuamini katika Bwana.

SOMO LA 20

1 nefi 19

Page 83: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

68

SoMo la 20

Baada ya wanafunzi kujibu, liambie darasa ugependa wanafunzi kadhaa waonyeshe jinsi kishazi hiki kinavyoeleza hutumika kwetu leo. Waalike wanafunzi kadhaa kuja ubaoni. Mu-ulize kila mmoja wao kuandika mfano wa tendo ambalo linaweza kuonyesha kwamba mtu amegeuza moyo wake upande kutoka kwa Bwana. Kisha waulize wao kuelezea baadhi ya matokeo yanaweza kuwa mtu anapogeuza moyo wake upande katika njia zilizoorodheshwa. (Kwa mfano, mwanafunzi anaweza kuandika kusitisha kujifunza maandiko na kisha kuelezea kwamba mojawapo ya matokeo ya kitendo hiki ni kufifia kwa uwezo wa kupokea ufunuo.)Baada ya wanafunzi kadhaa kuelezea mifano yao, liambie darasa kwamba bila kujali kwa nini tuligeuza mioyo yetu upande kutoka kwa Bwana, tunaweza kuchagua kugeuza mioyo yetu Kwake tena. Waalike wanafunzi kusoma 1 Nefi 19:14−17 kimya kimya, wakitafuta ahadi za Bwana kwa wale wanaogeuza mioyo yao Kwake tena.• Bwana alitawanya Israeli wakati gani? (Wakati walipogeuza mioyo yao upande kutoka

Kwake.)• Bwana atakusanya Israeli wakati gani? (Wakati wao watakapogeuza mioyo yao Kwake.)• Bwana alisema atafanya nini kwa wale ambao hawatageuza mioyo yao upande tena

dhidi Yake?• Unafikiria inamaanisha nini kwamba Bwana atawakumbuka watu hawa na maagano

Yeye alifanya na baba zao?Wasaidie wanafunzi kuelewa kwamba Bwana hakuwasahau watu hawa. Walikuwa wame-ishi katika njia ambayo Yeye hangeweza kuwapatia wote baraka zote za injili. Uzao wao ulipogeuza mioyo yao Kwake, Bwana huahidi kuwakumbuka wao, kuwakusanya wao katika Kanisa Lake, na kupeana baraka za injili zote kwao.• Unafikiria ahadi zilizopo katika mistari ya 15–17 zinamaanisha nini kwetu? (Wazo moja

ambalo linafaa kujitokeza katika huu mjadala ni kwamba tunapogeuza mioyo yetu kwa Bwana, Yeye ataheshimu maagano tuliofanya na Yeye. )

Waulize wanafunzi kutafakari maswali yafuatayo na kuandika majibu katika shajara zao za kujifunza maandiko au vitabu vya darasani. (Unaweza kuandika maswali haya kwenye ubao.)• Ni aina gani za matendo ambayo huonyesha kwamba wewe na familia yako mmegeuza

mioyo yenu kwa Bwana?• Ni wakati gani matendo kama hayo yalikusaidia wewe au familia yako kupokea baraka

za Bwana?Fikiria kuwaalika wanafunzi wachache kushiriki majibu yao pamoja na darasa. Wakumbu-she wao kwamba hawahitajiki kushiriki uzoefu ambao ni wa kibinasfi au siri sana.Elezea kwa kifupi kwamba Nefi alidhamiria kumbukumbu yake kwa washiriki wote wa nyumba ya Israeli—ikijumuisha sisi. Alika mwanafunzi asome 1 Nefi 19:18−19, na uulize darasa kutambua kile Nefi alikuwa anataka kutushauri sisi tufanye. Shuhudia kwamba sisi tunapomkumbuka Bwana na kugeuza mioyo yetu Kwake, Yeye hutoa kwetu baraka za injili Yake.

1 Nefi 19:20–24Nefi anaelezea kwa nini alitumia maandiko ya kale kufundisha watu wakeShiriki taarifa ifuatayo ya Rais Henry B. Eyring wa Urais wa Kwanza, iliyotengenezwa ku-toka kwa hotuba kwa waalimu wa dini wa Mpango wa Elimu ya Kanisa:“Nitawapeni ahadi hii kuhusu kusoma Kitabu cha Mormoni: Mtavutwa kwacho mnapoe-lewa kwamba Bwana ametia ndani ujumbe Wake kwenu. Nefi, Mormoni, na Moroni wa-lijua kwamba, na wale waliokipanga waliweka ndani yake ujumbe wenu. Natumaini mna imani kwamba kitabu hiki kiliandikwa kwa sababu ya wanafunzi wenu. Ni ujumbe rahisi, wa moja kwa moja kwao ambao utawaambia jinsi ya kubadilika. Hayo ndio kile kitabu kinahusu. Ni ushuhuda wa Bwana Yesu Kristo na Upatanisho na jinsi unaweza kufanya kazi katika maisha yao. Ninyi mtapata uzoefu mwaka huu wa hisia ya mabadiliko ambayo yanakuja kwa uwezo wa Upatanisho kwa sababu ya kujifunza kitabu hiki” (“The Book of Mormon Will Change Your Life,” Ensign, Feb. 2004, 11).• Unapojifunza Kitabu cha Mormoni, inasaidia vipi kujua kwamba Nefi, Mormoni, na

Moroni walijumuisha ujumbe kwa ajili yetu?Shiriki taarifa zifuatazo za Rais Ezra Taft Benson:

Page 84: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

69

1 nefi 19

Kitabu cha Mormoni kiliandikwa kwa ajili yetu leo. Mungu ndiye mtunzi wa kitabu hiki. Ni kumbukumbu ya watu walioenda zao, kikapangwa na watu wenye mvuvio kwa baraka zetu. Watu hao kamwe hawakuwa na kitabu hiki—kilidhamiriwa sisi. Mormoni, alikuwa nabii wa kale ambaye kitabu hiki kimeitwa jina lake, alifanya ufupisho wa kumbukumbu za karne nyingi. Mungu, ambaye anajua mwisho kutoka mwanzo, alimwambia yeye kile cha kujumuisha katika ufupisho wake ambacho tungehitaji katika siku yetu” (“The Book of Mormon Is the Word of God,” Ensign, Jan. 1988, 3).“Kama wao waliona siku yetu, na wakachagua yale mambo ambayo yangekuwa ya thamani kuu kwetu, si hivyo ndio tunapaswa kujifunza Kitabu cha Mormoni? Tunapaswa kujiuliza wenyewe kila mara, ‘Kwa nini Bwana alimvuvia Mormoni (au Moroni au Alma) kujumuisha haya katika kumbukumbu yake? Ni somo gani ninaweza kujifunza kutoka kwa haya litakalonisaidia mimi kuishi katika siku hii na nyakati hizi? (“Kitabu cha Mor-moni—Jiwe la Tao la Dini Yetu,” Ensign, Nov. 1986, 6).Alika darasa kusoma 1 Nefi 19:22−23 kimya, likitafuta maelezo ya Nefi ya jinsi yeye aliwa-saidia ndugu zake kupata jumbe wenyewe katika maandiko.• Ni matokeo gani Nefi alitarajia kutokana kufananisha maandiko na yeye mwenyewe na

watu wake?• Neno faida linamaanisha nini? (Fadhila, manufaa, pato la thamani.)Tayarisha chati ifuatayo kama kitini, au uionyeshe kwenye ubao na wanafunzi wainakili katika shajara zao za kujifunza maandiko.

Kufananisha Maandiko na Sisi Wenyewe Kutumia Kweli za Kimaandiko

ni hali au mazingira gani yaliyoelezewa katika kifungu cha maandiko?

hii inafanana vipi na hali katika maisha ya-ngu au katika ulimwe-ngu unaonizunguka?

ni kweli au ujumbe gani uliofunzwa ka-tika hiki kifungu cha maandiko?

ninaweza kutenda vipi juu ya hii kweli au ujumbe huu katika hali yangu?

Tanguliza chati kwa kuelezea kwamba kufananisha humaanisha kulinganisha. Kufanani-sha maandiko na sisi wenyewe humaanisha kwamba sisi tulinganishe mazingira katika maandiko na hali katika maisha yetu wenyewe au katika ulimwengu unaotuzunguka. Ku-tambua mfanano kati ya mazingira katika maandiko na hali katika maisha yetu wenyewe hututayarisha sisi kupata na kutumia kweli za kimaandiko. Kweli hizo hizo ambazo zili-tumika kwa watu tunaosoma juu yao katika maandiko zinaweza kutumika kwetu wakati tunakuwa katika mazingira sawa.Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa jinsi ya kufananisha uelekeza kwenye matumizi, waalike wao kujaza chati zao unaporejelea pamoja nao kifungu cha kwanza cha umahiri wa maa-ndiko cha Kitabu cha Mormoni, 1 Nefi 3:7. Alika mwanafunzi asome 1 Nefi 3:7 kwa sauti.• Ni mazingira gani Nefi alikuwa anajibu aliposema maneno haya? (Yeye alikuwa ame-

ulizwa na nabii—Lehi, baba yake—kurudi Yerusalemu kuchukua mabamba ya shaba. Ndugu zake walikuwa wamenung’unika kuhusu vile hili jukumu lilikuwa gumu.)

• Mazingira ya Nefi yanafanana vipi na hali katika maisha yako? Ni wakati gani Bwana alikutarajia kufanya kitu kigumu?

• Ni kweli gani ilimsaidia Nefi katika hali yake? (Nefi alijua kwamba Bwana anapotoa amri kwa watoto Wake, Yeye hupatiana njia kwao ya kuitimiza.)

• Unaweza kufanya nini kutenda juu ya kweli hii katika hali yako?Waalike wanafunzi wachache kushiriki jinsi wanafananisha 1 Nefi 3:7 na wao wenyewe na jinsi wanavyoweza kuitumia katika maisha yao wenyewe. (Wakumbushe wao kwamba hawahitaji kuelezea habari ambazo ni za kibinasfi au siri sana.)Kuhitimisha somo, inua nakala ya Kitabu cha Mormoni tena. Wakumbushe wanafunzi kwamba Nefi alichukulia maandishi yake kuhusu Mwokozi kuwa matakatifu na yenye tha-mani kuu kwake wa wengine. Watie moyo wanafunzi kujifunza maandiko na kutafuta uju-mbe ambao Bwana na manabii Wake wametuwekea ndani yake kwa ajili yetu. Shuhudia

Kufananisha maandiko na sisi wenyeweLengo muhimu la wa-limu wa injili ni kuwasai-dia wanafunzi kujifunza kufananisha maandiko na wao wenyewe. Waalimu wanaweza kuwasaidia wanafunzi kufanya hivyo kwa kuwauliza maswali kama vile yale ambayo yanatokeza kwenye chati na katika somo hili. Unapofundisha, tafuta nafasi za kuwasaidia wanafunzi kujifunza kufananisha maandiko na wao wenyewe.

Page 85: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

70

SoMo la 20

kwamba tunapofananisha maandiko na sisi wenyewe, tunajifunza na kufaidika kutoka kwayo.Watie moyo wanafunzi kujifunza maandiko peke yao na kutafuta vifungu wanavyoweza kufananisha na wao wenyewe. Wanaweza kujaribu kuweka majina yao kwenye mistari fulani na kusoma mistari kama vile Bwana au manabii Wake wanaongea moja kwa moja na wao. Kwa mfano, wanaweza kusoma sehemu ya kwanza ya 2 Nefi 31:20 kama hivi: “Kwa hivyo, [weka jina] lazima msonge mbele mkiwa na imani imara katika Kristo.”Unaweza kupatiana nakala za chati ambazo hazijaandikwa kwa wanafunzi kutumia nyumbani. Waalike wao kuja darasa lijalo wakiwa tayari kushiriki jinsi walivyofananisha maandiko na wao wenyewe na jinsi wamejifunza na kufaidika kutokana uzoefu huu.

Page 86: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

71

Somo la Mafunzo ya Nyumbani1 Nefi 15–19 (Kitengo cha 4)

Vifaa vya Matayarisho kwa Mwalimu wa Mafunzo ya NyumbaniMuhtasari wa Masomo ya Kila Siku ya Mafu-nzo ya NyumbaniMuhtasari ufuatao wa mafundisho na kanuni wanafunzi walijifunza walipokuwa wakisoma 1 Nefi 15–19 (Kitengo cha 4) haidhamiriwi kufunzwa kama sehemu ya somo. Somo unalofunza linazingatia tu machache ya haya mafundisho na kanuni. Fuata msukumo wa Roho Mtakatifu unapofikiria mahitaji ya wanafunzi.

Siku ya 1 (1 Nefi 15)Nefi na ndugu zake walifanya nini tofauti kwa unabii wa Lehi. Kwa kujifunza matendo ya Nefi, wanafunzi wanaweza kugundua kwamba kama tunamuuliza Bwana kwa imani na kutii amri Zake, tutatayarishwa kupokea ufunuo na mwongozo kutoka Kwake. Nefi alielezea maana ya fimbo ya chuma, kuonyesha kwamba kujifunza na kufuata neno la Mungu kila siku hutuimarisha sisi dhidi ya majaribu ya Shetani.

Siku ya 2 (1 Nefi 16)Kutokana na utendaji wa Lamani na Lemueli kwa mafundi-sho ya Nefi, wanafunzi waliona kwamba “wenye hati huchu-kulia kweli kuwa ngumu” (1 Nefi 16:2). Wakati Nefi alivunja upinde wake, alionyesha kwamba kama tunafanya yote tuna-yoweza na kutafuta maelekezo ya Bwana, Bwana atatusaidia kupitia matatizo yetu. Kwa kujifunza jinsi Liahona ilielekeza familia Lehi, wanafunzi walijifunza kwamba “kwa vitu vidogo Bwana anaweza kuleta vitu vikubwa” (1 Nefi 16:29).

Siku ya 3 (1 Nefi 17)Nefi alisimulia kukaa kwa muda kwa familia yake huko nyikani na kuwasili katika nchi ya Neema. Wakati aliamriwa kujenga chombo, yeye alionyesha kwamba kama tunashika amri, basi Bwana atatuimarisha na kutupatia njia za sisi kutimiza kile ameamuru. Bwana aliwaambia ndugu za Nefi kutubu katika njia kadhaa. Wanafunzi walijifunza kwamba Roho Mtakatifu kwa kawaida huongea nasi kwa sauti tulivu, ndogo ambayo sisi tunahisi zaidi ya sisi kusikia. Waliorodhe-sha hali na sehemu ambazo zinaweza kutuzuia sisi kukosa kutambua sauti tulivu, ndogo.

Siku ya 4 (1 Nefi 18–19)Mfano wa Nefi katika kujenga chombo ulionyesha wana-funzi kwamba ili kutimiza kile Bwana ameamuru, tunahitaji kutafuta usaidizi Wake na kufanya bidii yetu wenyewe. Ku-jifunza safari ya familia ya Lehi hadi nchi ya ahadi kulifunza kwamba dhambi huleta kuteseka kwetu wenyewe na wakati mwingine kwa wengine. Mfano wa Nefi wakati alipokuwa akiteswa na ndugu zake kulifunza kwamba tunapomtege-mea Mungu na kubakia waaminifu wakati wa majaribu yetu na kwamba maombi yanaweza kutusaidia kupata amani wakati wa majaribu yetu.

UtanguliziWiki hii wanafunzi walijifunza matukio muhimu ambayo yali-tokea wakati familia ya Lehi alipokuwa ikisafiri kupitia nyikani na kuvuka bahari hadi nchi ya ahadi. Somo hili litawasaidia wanafunzi kurejea matukio hayo na kujadili na kushuhudia juu ya kanuni walizojifunza. Wasaidie wanafunzi kugudua jinsi Nefi walibakia waaminifu katika mazingira magumu. Watie moyo wao kufuatia mfano wake wa utiifu na kuwa na imani katika Bwana wakati wa nyakati ngumu.

Mapendekezo ya Kufundisha

1 Nefi 15–18Nefi alitoa mfano wa utiifu na imani katika Bwana wakati wa majaribuKama picha zifuatazo zipo, zitayarishe kuzionyesha:

• Liahona (62041; Kitabu cha Sanaa za Injili [2009], no. 68)• Nephi Akiwadhibiti Ndugu Zake Waasi (62044; Kitabu cha

Sanaa za Injili, no. 70)• Lehi na Watu Wake Wakiwasili katika Nchi ya Ahadi (62045;

Kitabu cha Sanaa za Injili, no. 71)

Ili kuwasaidia wanafunzi kurejea na kuelewa usuli wa kile wa-lichojifunza wiki hii, onyesha picha bila utaratibu maalumu na uwaambie wanafunzi kuziweka katika mpangilio wa mfululizo. Waalike wao kufikiria kuwa wao ni wahariri wa habari na wana-hitaji kichwa cha maneno matatu au sita cha kila picha. Onyesha picha kwa utaratibu, na uliza darasa kujibu wakiwa na kichwa. Unaweza kusoma kwa sauti muhtasari wa sura hii 1 Nefi 15–18 ili kuwapatia mawazo fulani.

Page 87: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

72

SoMo la MafUnzo ya nyUMbani

Ili kuwatayarisha wanafunzi kujadili 1 Nefi 15, acha wao wao-ngee kuhusu shughuli walizoshiriki ambazo zinahitaji juhudi upa-nde wao kabla ya wao kupata matokeo. Hii inaweza kujumuisha shughuli kama vile kazi ya shule, kucheza chombo cha muziki, au riadha.

Andika 1 Nefi 15:2–3, 7–11 kwenye ubao, na uwapatie wana-funzi muda wa kusoma hii mistari. Waulize wao kwa nini ndugu za Nefi hawakupokea uelewa sawa na ule Nefi alipokea kuhusu ufunuo wa Lehi.

Baada ya kusikiliza majibu yao, wasaidie kutambua kwamba kupokea maongozi na maelekezo kutoka kwa Bwana kwanza huhitaji kuishi kwa wema, juhudi, na imani katika upande wetu. Unaweza kuangazia kanuni hii kwa kuiandika kwenye ubao.

Waulize wanafunzi kutafakari na kujibu swali lifuatalo: Ni uzoefu gani wewe ulipata ambao umekusaidia wewe kujua hii kanuni ni kweli?

Andika thabiti kwenye ubao. Waulize wanafunzi inamaanisha nini kuwa thabiti. Kufuatia majibu yao, andika kwenye ubao: imara na kutovunjika moyo katika hali ya ugumu au shinikizo.

Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa jinsi neno thabiti linahusiana na Nefi, mpatie mmoja kufuatia sura kwa kila wanafunzi: 1 Nefi 16, 17, au 18. Kama una darasa kubwa, inaweza kusaidia kuwapanga wanafunzi katika vikundi na uwapatie kazi pamoja kwenye sura moja.

Andika maswali yafuatayo kwenye ubao. Watie moyo wanafunzi kutumia sura zao walizopangiwa na vifaa vya kitabu cha mwa-nafunzi husika kujibu maswali haya.

• Ni majaribu gani yalimkabili Nefi katika sura iliyo rejewa?• Nefi alifanya imani kwa njia gani katika yale mazingira? Ni

mistari au vishazi gani vinavyoonyesha ushahidi kwamba imani ya Nefi ilikuwa thabiti?

• Ni kanuni gani za injili zilizoonyeshwa katika sura hii? Umeshapata uzoefu gani na hizi kanuni ambao umeongeza ushuhuda wako?

Toa muda wa kutosha kwa wanafunzi kukamilisha zoezi hili. Kisha muulize angalao mwanafunzi mmoja aliyepangiwa kila sura kueleza majibu yake. (Kama una wanafunzi wa kutosha,

unaweza kuwa na mwanafunzi tofauti kutoa ripoti juu ya kila swali kwa kila sura.)

Alika mwanafunzi asome kwa sauti taarifa ifuatayo ya Mzee Russell M. Nelson wa Akidi ya wale Mitume Kumi na Wawili:

Kwa nini tunahitaji imani thabiti kama hiyo? Kwa sababu ya siku ngumu zilizo mbele. Ni nadra katika siku za usoni kuwa na urahisi au kupendeza kuwa Mtakatifu wa Siku za Mwisho mwaminifu. Kila mmoja wetu atajaribiwa. Mateso yanaweza aitha kukuvunja hata kwenye udhaifu kimya au kukutia motisha wewe kuwa mfano mwema na kuwa jasiri katika maisha yako ya kila siku.

“Jinsi unavyokabiliana na majaribu ya maisha ni sehemu ya ukuaji wa imani yako. Nguvu huja wakati wewe unakumbuka kwamba wewe una asili takatifu, urithi wa thamani usio na kipimo” (“Face the Future with Faith,” Ensign au Liahona, May 2011, 35–36).

Waalike wanafunzi kushiriki mawazo kuhusu jinsi wanavyoweza kukabiliana na changamoto na majaribu ya kibinafsi kama alivyofanya Nefi.

1 Nefi 19Nefi anaandika unabii kuhusu Yesu Kristo kutushawishi sisi kumkumbuka YeyeKama muda unaruhusu, waulize wanafunzi kurejea kile wao waliandika katika shajara zao za kujifunza maandiko kwa siku ya 4, kazi ya 5. Uliza kama yeyote wao yuko tayari kushiriki kile wao waliandika kuhusu upendo wao kwa Mwokozi. Kisha shiriki hisia zako kuhusu Mwokozi.

Nefi alimpenda Mwokozi na kumkumbuka Yeye katika majaribu yake. Shuhudia kwamba tunapompenda na kumkumbuka Mwo-kozi, Yeye atatusaidia na kutuhimili sisi katika majaribu yetu.

Kitengo kifuatacho (1 Nefi 20–2 Nefi 3)Katika kitengo kifuatacho, wanafunzi watajifunza baadhi ya maneno ya mwisho ya Lehi kwa familia yake kabla ya kufariki. Pia watasoma unabii wa siku ya kale sana, kitambo sana kabla ya Kristo, kuhusu Nabii Joseph Smith.

Page 88: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

73

Mapendekezo ya Kufundisha

1 Nefi 20Bwana huwarudi watu Wake na kuwaalika wao kurudi KwakeOnyesha wanafunzi picha ya Isaya Anaandika kuhusu Kuzaliwa kwa Kristo (62339; Kitabu cha Sanaa za Injili [2009], no. 22). Elezea kwamba huu mchoro huonyesha nabii Isaya aki-aandika unabii kuhusu kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Waulize ni wangapi wao wameshasikia kuhusu Isaya.Elezea kwamba Isaya alikuwa nabii ambaye aliishi katika Yerusalemu na alitoa unabii kwa watu kati ya miaka 740 K.K. na miaka 701 K.K. Nefi alifurahia katika maneno ya Isaya na alitumia unabii wa Isaya kufundisha familia yake (ona 1 Nefi 19:23; 2 Nefi 25:5). Kwa sababu ya maneno ya Isaya ni ya kishairi na yamejaa ishara, watu wakati mwingine huona kuwa magumu kuyaelewa. Hata hivyo, tunaweza kupokea baraka tunapojifunza maneno yake na kutafuta kuyaelewa.Elezea kwamba kama Nefi alifunza familia yake, yeye alisoma maneno ya Isaya ambayo yamejumuishwa katika mabamba ya shaba. Alifanya hivi ili kwamba yeye “awashawishi kabisa wamwamini Bwana Mkombozi wao” (1 Nefi 19:23; ona pia mstari wa 24).Alika mwanafunzi asome 1 Nefi 20:1–2 kwa sauti. Kabla hajasoma, elezea kwamba katika kifungu hiki, Isaya huongea na watu waliobatizwa ambao walikuwa sio waaminifu kwa maagano yao. Unaweza kuelezea kishazi “nyumba ya Israeli” kwa kuhusisha yafuatayo: Agano la Kale lina historia ya Yakobo, ambaye akikuwa mwana wa Isaka na mjukuu wa Ibrahimu. Bwana alimpatia Yakobo jina Israeli (ona Mwanzo 32:28). Neno “nyumba ya Israeli’ humaanisha uzao wa Yakobo na watu wa agano wa Bwana (ona Bible Dictionary, “Israel,” and “Israel, Kingdom of”). Waalike wanafunzi kusoma 1 Nefi 20:3–4, 8 kimya. Waulize kutafuta maneno na vishazi vinavyoonyesha nyumba ya Israeli ambao hawakuwa waaminifu kwa Bwana. Watie moyo wanafunzi kushiriki kile wamepata.Onyesha vipande vya chuma ambavyo ni vigumu kupinda. Waulize wanafunzi kile wanafi-kiria inamaanisha na shingo ya mtu kuwa “msuli wa chuma” (1 Nefi 20:4). Elezea kwamba msuli ni kano. Kama vile chuma hakipindi kwa urahisi, mtu wenye kiburi hawezi kuinami-sha shingo yake kwa unyenyekevu. Kishazi “msuli wa chuma” humaanisha kwamba watu wengi katika nyumba ya Israeli wamejawa na kiburi.Acha mwanafunzi asome 1 Nefi 20:22 kwa sauti.• Kwa nini unafikiria waovu hawana amani?Wakumbushe wanafunzi kwamba wakati Nefi alishiriki unabii wa Isaya, alibishana na ndugu zake, “na myalinganishe nanyi” (1 Nefi 19:24).• Wanafamilia wa Nefi fulani walifanana vipi na watu Isaya aliwasihi watubu?Uliza mwanafunzi asome 1 Nefi 20:14, 16, 20 kwa sauti.• Bwana alitaka watu Wake wa Agano kufanya nini na kusema nini? (Unaweza kuelezea

kwamba kuacha Babeli na Wakaldayo ni istairi ya kuacha malimwengu nyuma na ku-mwendea Bwana.)

UtanguliziNefi aliwafunza wanafamilia yake, yeye alisoma kutoka kwenye mabamba ya shaba, akizingatia unabii wa Isaya kuhusu kutawanyika na kukusanyika kwa Israeli. Kisha akajibu maswali ya ndugu zake kuhusu unabii huu. Alielezea kwamba unabii huu ulihusu moja kwa moja

familia zao. Kupiga mwangwi maneno ya Isaya, Nefi alishuhudia kwamba Bwana atakusanya watu Wake wa agano—kwamba hata wakati watu hawakuishi ku-lingana na maagano yao, Bwana aliwapenda na aliwaa-lika wao kutubu na kurudi Kwake.

SOMO LA 21

1 nefi 20–22

Page 89: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

74

SoMo la 21

Waalike wanafunzi kushiriki mifano waliyoona ya watu wakimwendea Bwana na kuacha malimwengu nyuma. Acha wanafunzi wapekue 1 Nefi 20:18, wakitafuta baraka ambazo Bwana hutoa kwa wale ambao huja Kwake na kusikia amri Zake.• Amani inaweza kuwa kama mto vipi? Wema unaweza kuwa kama mavimbi ya bahari vipi?Waalike wanafunzi kufanya muhtasari kweli walizojifunza kutoka 1 Nefi 20. Ingawa wao wanaweza kutumia maneno tofauti, hakikisha wanaelewa kwamba Bwana huwaalika wale ambao wamekuwa si watiifu kutubu na kurudi Kwake.Acha mwanafunzi asome taarifa ifuatayo ya Rais Dieter F. Uchtdorf wa Urais wa Kwanza. Waalike wanafunzi kutafakari jinsi haya yanavyo husiana na 1 Nefi 20.“Shetani . . . anataka sisi tuhisi kwamba tumepita msamaha (ona Ufunuo wa Yohana 12:10). Shetani anataka sisi tufikirie kwamba tumefanya dhambi na tukapita ‘eneo la kuto-weza kurudi” —kwamba tumechelewa sana kubadilisha mwelekeo. . . .“. . . Upatanisho wa Yesu Kristo ni kipawa cha Mungu kwa watoto Wake ili kurekebisha na kushinda matokeo ya dhambi. Mungu huwapenda watoto Wake wote, na Yeye hatasita kamwe kutupenda na kuwa na matumaini juu yetu. . . .“Kristo alikuja kutuokoa. Kama tumechukua mwelekeo mbaya, Upatanisho wa Yesu Kristo unaweza kutupatia sisi hakikisho kwamba dhambi sio eneo la kutoweza kurudi. Kurudi salama inawezekana kama sisi tutafuata mpango wa Mungu kwa wokovu wetu. . . .“. . . Kuna daima eneo la kurudi salama; kuna daima tumaini ” (“Point of Safe Return,” Ensign au Liahona, May 2007, 99, 101).• Ujumbe wa Rais Uchtdorf unafanana vipi na ujumbe wa Isaya?Shuhudia kwamba Bwana huwaalika wale ambao wamekuwa si watiifu kutubu na kurudi Kwake. Wahakikishie wanafunzi kwamba Bwana huwapenda wao kibinafsi na da-ima huwaalika kuja Kwake. Waalike wao kutafakari kile Bwana angependa wao kukiacha nyuma ili waweze kuja Kwake kikamilifu zaidi.

1 Nefi 21:1–17Isaya anatoa unabii kwamba Yesu Kristo hatawasahau watu Wake wa aganoFanya muhtasari mfupi wa 1 Nefi 21:1–13 kwa kuvuta usikivu wa wanafunzi kwa taarifa mbili za kwanza katika muhtasari wa sura: “Masiya atakuwa nuru kwa Wayunani na ku-wafanya huru wafungwa” na “Israeli itakusanywa tena kwa uwezo katika siku za mwisho.” Elezea kwamba katika mistari ya 1–13, maneno ya Bwana yanafunua upendo Wake kwa watu Wake—hata kwa wale ambao wamepotoka na kumsahau Yeye.Kwenye ubao, andika Bwana anatupenda, na Yeye hatatusahau kamwe. Alika mwana-funzi asome 1 Nefi 21:14 kwa sauti.• Kwa nini unafikiria watu wakati mwingine wanahisi kwamba Bwana amewasahau?Waalike wanafunzi kusoma 1 Nefi 21:15–16 kwa sauti. Kisha uulize baadhi ya au maswali yote yafuatayo:• Ni nini Isaya alifundisha kwa kulinganisha Mwokozi na mama na mtoto mchanga?• Neno chongwa linamaanisha nini? (Unaweza kutaja kwamba kwa kawaida tunafikiria

kuchonga jiwe au chuma katika njia ambayo itadumu.)• Inamaanisha nini kwako kuchongwa “juu ya viganja vya mikono ya [Mwokozi]”?• Ni uzoefu gani unaoweza kukusaidia wewe kujua kwamba Bwana hajakusahau wewe?Wanafunzi wanapofikiria kuhusu maswali haya na kusikiliza majibu ya mmoja kwa mwi-ngine, watatayarishwa kuhisi Roho Mtakatifu kutoa ushuhuda wa Mwokozi. Shiriki ushu-huda wako kuhusu upendo wa Mwokozi. Wakumbushe wanafunzi kwamba Nefi alishiriki unabii wa kutushauri sisi kuamini katika Mkombozi na kutusaidia sisi kuwa na tumaini.

1 Nefi 21:18–26; 22:1–22Nefi anaelezea unabii wa Isaya wa kutawanywa na kukusanywa kwa IsraeliWeka vvombo kadhaa (kama vikombe) pamoja kwenye meza au kiti. Waambie wanafunzi kwamba hivi vyombo vinaashiria makundi ya watu. Elezea kwamba Nefi alifunza kwamba Israeli ingetawanywa kwa mataifa yote kwa sababu walifanya mioyo yao kuwa migumu

Wape wanafunzi muda wa kufikiriaUnapouliza maswali, wa-patie wanafunzi muda wa kufikiria kuhusu majibu yao. Maswali yanayofaa mara nyingi uelekeza kwenye wazo na tafakuri, na wanafu-nzi wanaweza kuhitaji muda wa kupata majibu katika maandiko yao au kubuni majibu yenye maana. Hata kama majibu ya wanafunzi si kamili, wanafunzi wata-jifunza masomo muhimu wanapotafakari kweli za injili na kushiriki mawazo yao.

Page 90: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

75

1 nefi 20 –22

dhidi ya Mwokozi (ona 1 Nefi 22:1–5). Unapoongea, hamisha hivi vyombo hadi sehemu tofauti za chumba. Elezea kwamba hii ilikuwa mada muhimu ya Nefi. Familia yake ilikuwa sehemu ya kutawanyika. Imetawanyika kutoka Yerusalemu, nyumbani kwao, kwa sababu ya uovu wa watu walioishi katika eneo hili.Waalike wanafunzi 1 Nefi 21:22–23 na 22:6–8 kimya. Kabla ya wao kusoma, elezea kwa-mba 1 Nefi 21 inajumuisha unabii wa Isaya kuhusu kukusanyika kwa Israeli na kwamba 1 Nephi 22 inajumuisha mafundisho ya Nefi kuhusu unabii wa Isaya.• Ni nini hii “kazi ya ajabu” iliyosemwa katika 1 Nefi 22:7–8? (Urejesho wa Injili.)• Kushiriki injili kunaweza kuwa kama kuwabeba wengine katika mikono yetu au mabega

yetu vipi?Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa kutawanyika na kukusanyika kwa Israeli, unaweza ku-soma taarifa ifuatayo ya Mzee Bruce R. McConkie wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili:“Kwa nini Israeli ilitawanywa? Jibu ni wazi; ni halisi; hamna shaka. Waisraeli wetu wa kale walitawanywa kwa sababu walikataa injili, wakachafua ukuhani, wakatelekeza kanisa, na wakaondoka kutoka kwa ufalme.“Basi, ni nini, kinachohusiana na kukusanyika kwa Israeli? Kukusanyika kwa Israeli kuna-husisha kuamini na kupokea na kuishi katika uwiano na yale yote Bwana aliwapatia watu wateule Wake wa kale. Inahusisha kuamini injili, kujiunga na Kanisa na kuja katika ufalme. . . . Pia inaweza kuhusisha makusanyiko katika sehemu iliyoteuliwa au nchi ya ibada” (A New Witness for the Articles of Faith [1985], 515).Soma 1 Nefi 22:9–12. Elezea kwamba wakati maandiko yanataja Bwana “kuweka mkono wake wazi,” yanamaanisha Bwana akionyesha uwezo Wake.• Katika 1 Nefi 22:11, Nefi anasema Bwana atafanya nini katika siku za mwisho kuonye-

sha uwezo Wake?• Kukusanyika kwa watu katika Kanisa kunawatoaje utumwani na gizani?Waalize wanafunzi kuchukua vile vyombo kutoka chumbani na kuvileta pamoja katika sehemu moja. Elezea kwamba kukusanyika kunaweza kuwa kiroho pia kimwili. Tunapo-shiriki injili na wengine na wanabatizwa na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu, wana-kusanywa kiroho katika Kanisa la Bwana. Wakati wa siku za mapema za Kanisa, waongofu wapya waliulizwa kukusanyika kimwili katika sehemu moja (kwa mfano, Kirtland, Ohio; Nauvoo, Illinois; na Mjini Salt Lake, Utah). Siku hizi waongofu wahimizwa kujenga Kanisa popote pale walipo na kukusanyika katika matawi, kata, na vigingi.• Kulingana na 1 Nefi 22:25, ni baraka gani zinazokuja kwa wale wanaokusanywa na Bwana?

Unafikiria “zizi moja” inamaanisha nini? (Unaweza kuelezea kwamba zizi ni sehemu ambapo kundi la kondoo hulindwa.) Unafikiria “kupata malisho” inamaanisha nini?

Katika siku zetu, Mungu ameomba washiriki wote wa Kanisa kusaidia katika kukusanya “watoto Wake kutoka pembe nne za dunia” (1 Nefi 22:25). Shuhudia kwamba Bwana aliahidi kurejesha injili na kukusanya Israeli katika siku za mwisho.• Unafikiria wale watakaokusanywa (waongofu) watahisi vipi kuhusu wale waliowakusa-

nya wao (wale ambao walishiriki injili nao)?• Unaweza kufanya nini kushiriki injili ya Yesu Kristo na wengine?Wakumbushe wanafunzi kwamba Nefi alimnukuu Isaya ili kuwasaidia wanafamilia wake kuwa na imani kubwa na tumaini katika Yesu Kristo. Unabii wa Isaya na ushuhuda wa Nefi unaweza kutusaidia katika njia hiyo hiyo. Shuhudia kwamba Yesu Kristo hatatusahau na kwamba Yeye anashughulika kwa hari kutukusanya.

Rejeo la 1 NefiChukua muda kurejelea 1 Nefi kwa kuuliza wanafunzi maswali ili wakumbuke kile wame-jifunza katika seminari na mafunzo ya kibinafsi kufikia hapa mwaka huu. Unaweza kuwa-tia moyo wao kurejea muhtasari wa sura katika 1 Nefi. Waulize wao kujitayarisha kushiriki kitu kutoka katika kitabu cha 1 Nefi ambacho kumewapatia mvuvio au kuimarisha imani yao katika Yesu Kristo. Baada ya muda wa kutosha, waulize wanafunzi kuelezea mawazo na hisia zao. Fikiria kuelezea mojawapo ya uzoefu wa kibinafsi kuhusu jinsi mafundisho katika 1 Nefi yamebarikia maisha yako.

Kutoa ushuhudaUnafaa kutoa ushuhuda wa mafundisho ma-hususi unayofundisha katika kila somo, si tu jumla kuhusu kweli za injili. Unaposhuhudia, kumbuka ushauri kutoka kwa Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili: “Toa ushuhuda wako kutoka ndani ya nafsi yako. Itakuwa kitu cha muhimu ambacho utasema katika saa lote zima. . . . Kama tuta-shuhudia kweli ambazo tumefunza, Mungu ata-thibitisha kwenye mioyo yetu na kwa mioyo ya wanafunzi wetu ujumbe wa injili wa Yesu Kristo” (“Teaching and Learning in the Church,” Ensign, June 2007, 104–5).

Page 91: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

76

UtangUlizi Wa

Kitabu cha pili cha nefiKwa nini kusoma kitabu hiki?Kitabu cha 2 Nefi kitawasaidia wanafu-nzi kuelewa mafundisho ya msingi ya Injili, kama vile Kuanguka kwa Adamu na Hawa, Upatanisho wa Yesu Kristo, na wakala. Zaidi ya hayo, kitabu hiki kimejaa na unabii kutoka kwa Nefi na Yakobo, na Isaya, ambao walikuwa mashahidi maalum wa Mwokozi. Walitabiri juu ya Urejesho ya injili katika siku za mwisho, kutawanyika na mkusanyiko wa watu wa Mungu wa agano, Ujio wa Pili wa Yesu Kristo, kuja kwa Kitabu cha Mormoni, na Milenia. Kitabu cha 2 Nefi pia kina maelezo ya Nefi ya fundisho la Kristo na kinamalizika kwa ushahidi wa Nefi juu ya Mwokozi.

Ni nani aliandika kitabu hiki?Mwana wa Lehi, Nefi alikiandika kitabu hiki. Nefi alikuwa nabii na kiongozi wa kwanza mkuu wa watu wa Nefi baada ya kujitenga kwao kutoka kwa Walamani. Maandiko yake yanaonyesha kwamba ali-ona uwezo wa Bwana wa ukombozi (ona 2 Nefi 4:15–35; 33:6) na kutaka kwa roho yake yote kuleta wokovu kwa watu wake (ona 2 Nefi 33:3–4). Ili kutimiza lengo hili, aliwafundisha watu wake kuamini katika Yesu Kristo na kujenga hekalu.

Kitabu hiki kiliandikiwa nani na kwa nini?Nephi aliandika akiwa na dhamira tatu mawazoni: uzao wa baba yake, watu wa agano wa Mungu katika siku za mwisho, na watu wote duniani (ona 2 Nefi 33:3, 13). Kitabu cha 2 Nefi kiliandikwa kwenye mabamba madogo ya Nefi, ambayo yaliteuliwa na Bwana kuwa rekodi ya “hu-duma na unabii” wa Nefi na uzao wake.(1 Nefi 19:3–5). Kwenye bamba hizi, Nefi aliandika “mambo ya nafsi [yake], na ma-andiko mengi ambayo yamechorwa kwe-nye bamba za shaba.” Alieleza kwamba aliandika “kwa elimu na faida ya watoto [wake]”(2 Nefi 4:15). Alitangaza, “Tu-nazungumza kuhusu Kristo, tunafurahia

katika Kristo, tunahubiri kuhusu Kristo, tunatoa unabii kumhusu Kristo, na tunaa-ndika kulingana na unabii wetu, ili watoto wetu wajue asili ya kutegemea msamaha wa dhambi zao” (2 Nefi 25:26). Alihitimi-sha rekodi yake kwa kuwaalika watu wote “kusikiliza maneno [yake] na kuamini katika Kristo” (2 Nefi 33:10).

Ni lini na ni wapi kiliandikwa?Nefi alianza kuandika historia iliyojulikana kama 2 Nefi takribani 570 K.K, miaka 30 baada ya yeye na familia yake kuondoka Yerusalemu. Alikiandika alipokuwa katika nchi ya Nefi (ona 2 Nefi 5:8, 28–34).

Ni nini baadhi ya sifa bainifu za kitabu hiki?Ingawa Nefi ndiye mwandishi wa 2 Nefi, kitabu ambacho ni mkusanyiko wa mafu-ndisho kutoka vyanzo mbalimbali. Kama inavyooneshwa katika orodha ifuatayo, sura nyingi katika kitabu zinajumuisha do-ndoo kutoka kwa manabii wengine. Kwa sababu Lehi, Yakobo, na Isaya walimwona Yesu Kristo na walikuwa mashahidi Wake, Nefi alijumuisha baadhi ya mafundisho yao katika jitihada za kuwashawishi wasomaji kuamini katika Yesu Kristo. Lehi na Yakobo pia waliwanukuu manabii wengine katika hotuba zao.

• Mafundisho ya Lehi yamerekodiwa katika 2 Nefi 1–4. Katika 2 Nefi 3:6–21, Lehi anamnukuu Yusufu wa Misri.

• Mafundisho ya Nefi yamerekodiwa katika 2 Nefi 4–5 and 2 Nefi 11–33. Nefi anamnukuu Isaya kwa kiwango kikubwa katika 2 Nefi 12–24 and 2 Nefi 27.

• Mafundisho ya Yakobo yamerekodiwa katika 2 Nefi 6–10. Katika 2 Nefi 6:6–7 and 2 Nefi 7–8, Yakobo ananukuu Isaya.

Kitabu cha 2 Nefi pia kinataja kifo cha Lehi (ona 2 Nefi 4:12) na mgawanyiko wa kizazi cha Lehi kuwa mataifa mawili—Wa-lamani na Wanefi (ona 2 Nefi 5).

Muhtasari2 Nefi 1–4 Muda mfupi kabla ya kifo chake, Lehi anashauri na kubariki uzao wake.

2 Nefi 4–8 Nefi anafurahia katika Bwana. Anawaongoza wafu-asi wake katika nchi wanaoiita Nefi. Anaandika mafundisho ya Yakobo juu ya kutawanyika na mkusanyiko wa Israeli.

2 Nefi 9–10 Yakobo anafundisha juu ya Upatanisho wa Yesu Kristo. Pia anatabiri juu ya kukataliwa kwa Yesu Kristo na Wayahudi na kukusanyika baadaye kwa Waya-hudi na Wayunani katika nchi ya ahadi.

2 Nefi 11–24 Nefi anaonyesha fu-raha yake katika kutoa ushuhuda wa Yesu Kristo. Ananukuu unabii wa Isaya kuhusu kutawanyika na kukusanyika kwa Israeli, kunye-nyekeza wenye kiburi na waovu kabla ya Ujio wa Pili, na kuzaliwa, na lengo, na utawala wa milenia wa Masiya.

2 Nefi 25–27 Nefi anatabiri juu ya kusulubiwa kwa Mwokozi, Ufu-fuko, na ziara yake kwa Wanefi; kutawanyika na kukusanyika kwa Wayahudi; uharibifu wa Wanefi; Uasi; Kuja kwa Kitabu cha Mor-moni, na Urejesho.

2 Nefi 28–30 Nefi anaonya dhidi ya uovu wa siku za mwisho, anaelezea wajibu wa baadaye wa Kitabu cha Mormoni, na kutabiri juu ya kukusanyiko kwa watu katika agano.

2 Nefi 31–33 Nefi anatusihi kum-fuata Kristo, kula karamu neno Lake, na kuvumilia hadi mwisho. Anashuhudia kwamba ameandika maneno ya Kristo.

76

Page 92: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

77

SOMO LA 22

2 nefi 1UtanguliziKweli katika 2 Nefi 1 zilinenwa na mzazi mwenye upendo na kiongozi ambaye alikuwa mahututi. Lehi aliwasihi wanawe, wana wa Ishmaeli, na Zoramu kutii

amri za Mungu. Aliwaahidi kwamba kama wangetii amri za Mungu, wangeweza kufanikiwa katika nchi. Aliwahimiza pia kufuata uongozi wa kinabii wa Nefi.

Mapendekezo ya Kufundisha

2 Nefi 1:1–23Lehi anawashawishi watu wake kuishi kwa hakiWaulize wanafunzi kufikiria kwamba wanapaswa kuacha familia zao kwa ghafla na kamwe wasiweze kuwaona tena.• Kama ingekuwa uwaachie familia yako maneno ya ushauri wa mwisho, ungesema nini?

Kwa nini?”Baada ya kusikia kutoka kwa wanafunzi wachache, elezea kuwa sura ya 1–4 ya 2 Nefi yana rekodi ya Nefi juu ya ushauri wa mwisho wa baba yake. Somo hili linazingatia 2 Nefi 1, ambayo ina ushauri ambao Lehi alishiriki pamoja na wanawe, wana wa Ishmaeli, na Zoramu.• Kwa nini ushauri wa mwisho wa mzazi au nabii uwe na umuhimu sana? Alika mwanafunzi kusoma 2 Nefi 1:1–5 kwa sauti. Uliza darasa kutambua “mambo makuu ambayo Bwana alifanya” kwa ajili ya familia ya Lehi.• Ni jinsi gani mambo haya makuu yanaonyesha rehema ya Bwana?• Ni mfano upi wa kitu kikuu ambacho Bwana amekufanyia wewe ama familia yako?• Je, hisia zako ni zipi unapofikiri juu ya huruma ya Mungu kwa ajili yako na familia yako?Katika upande mmoja wa ubao, andika Vitendo. Kwa upande mwingine wa ubao, andika Matokeo. Gawanya darasa katika makundi mawili. Karibisha kundi la kwanza kusoma 2 Nefi 1:6–9 na kundi la pili kusoma 2 Nefi 1:10–12. Uliza makundi yote mawili yatafute vitendo ambavyo Lehi alisema watoto wake wanaweza kuchukua. Pia waulize kuangalia matokeo ya matendo hayo. Kwa mfano, Lehi alisema kwamba kama watu watamtumikia Bwana kulingana na amri zake, nchi itakuwa nchi ya uhuru kwa ajili yao (ona 2 Nefi 1:7). Wanafunzi wanaposhiriki majibu yao, acha mwanafunzi ayaandike kwenye ubao.• Unapochunguza majibu hayo kwenye ubao, ni jinsi gani unaweza kufupisha ujumbe wa

Lehi kwa familia yake? (Wanafunzi wanaweza kujibu kwa maneno tofauti, lakini haki-kisha ujumbe ufuatao ni wazi: Bwana hutubariki tunaposhika amri Zake, na Yeye huzuia baraka wakati hatutii amri zake.)

• Katika 2 Nefi 1:9, kifungu “nchi hii” inahusu Marekani. Je Bwana aliahidi nini kwa mtiifu ambaye angeishi katika “nchi hii”?

Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa maana ya istiara ambayo Lehi alitumia kuhimiza wa-nawe kushika amri za Bwana, onyesha saa ya kengele, mnyororo, na kitu fulani chenye mavumbi juu yake (kuwa na uhakika kusisitiza vumbi, sio kitu).Alika wanafunzi kusoma 2 Nefi 1:13–14 kimoyomoyo, wakiangalia maneno na vishazi ambavyo vinahusiana na mambo haya matatu. Baada ya wao kusoma, shikilia kila kitu kimoja na waulize wanafunzi kuelezea maneno na vishazi walivyogundua. (Majibu yana-weza kujumuisha “amka,” “usingizi wa Jehanamu," “kung’uta minyororo mikubwa,” “mi-nyororo ambayo hufunga,” na “kuinuka kutoka mavumbini.") Waulize wanafunzi inaweza kumaanisha nini kuwa katika “usingizi mzito,” kwa kufungwa kwa “minyororo mikubwa,” au haja ya "kuinuka kutoka mavumbini."• Wakati Lehi alipotumia maneno na vishazi hivi, alikuwa akiwahimiza wanawe kufanya

nini? (Kutubu, kubadili njia zao.)

Kuzingatia wanafunziMzee Richard G. Scott wa Jamii ya Mitume Kumina wawili alieleza kuwa kuwasaidia wana-funzi kupata ufahamu ni muhimu zaidi kuliko kupitia nyenzo zote ka-tika mpango wa somo: “Kumbuka, kipaumbele chako siokupitia nyenzo zote kama hiyo ina maana kwamba haiwezi kufyonzwavizuri. Fanya kile unaweza kufanya kwa kuelewa. . . . Ikiwa kanuni muhimu zime-eleweka [na] kutumika . . . basi kanuni muhimu zaidi zimetimizwa” [address to CES religious educators, Feb. 4, 2005], 2–3, si. lds. org).

Page 93: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

78

SoMo la 22

• Ni nini Lehi alionya kingetokea kama wanawe "hawakukung'ota minyororo [yao]”? (Ona 2 Nefi 1:13.)

Alika wanafunzi kusoma 2 Nefi 1:14–18 kimya kimya. Eleza kwamba Lehi alitoa ushauri huu kwa wema na upendo na kwa wasiwasi mkubwa (“wasiwasi”) kwa ajili ya wema wa watoto wake. Waulize wanafunzi kutafuta sababu Lehi alitaka familia yake kutii amri za Bwana.• Kwa nini Lehi alikuwa na wasiwasi kwa ajili ya uzao wake? (Alikuwa na wasiwasi ku-

husu matokeo ambayo wangepata kwa sababu ya matendo yao, naye aliwataka waone upendo wa Mungu, kama alivyokuwa ameona.)

Waache wanafunzi kusoma peke yao 2 Nefi 1:15 tena.• Ni baraka gani ambayo Lehi alipokea kwa sababu ya uaminifu wake?• Ni wakati gani umehisi kuzungukwa katika mikono ya upendo wa Mungu?Gawanya darasa katika majozi. Uliza mwanafunzi mmoja katika kila jozi kutafuta 2 Nefi 1:19–22 kwa ajili ya ahadi ambazo zingewaongoza wana wa Lehi kutubu. Uliza mwana-funzi yule mwengine katika kila jozi kutafuta katika mistari hiyo matokeo ambayo Lehi alisema yatakuja kama wanawe wangechagua kukataa ushauri wake. (Unaweza kutaka kuandika kazi hii ubaoni.) Wape wanafunzi muda wa dakika tatu au nne kukamilisha kazi na kushiriki matokeo ya utafiti wao kwa wao. Unaweza kutaka kuzunguka darasani wana-potoa taarifa zao ili uweze kusaidia kuongoza majadiliano yao.Soma changamoto ya Lehi katika 2 Nefi 1:23 kwa sauti kwa wanafunzi. Unaweza kutaka kuwahimiza wanafunzi kuweka alama kwenye aya hii. Unaweza pia kuwahimiza kuandika katika shajara zao za kujifunza maandiko au daftari za darasa juu ya kitu kimoja wanaweza kufanya ili “kuamka” au “kukung’uta minyororo” au “kuinuka kutoka mavumbini” ili waweze kupokea baraka ambazo Lehi alizungumzia.• Ina maanisha nini kwako “kujitwalia deraya za haki”? (Ona pia M&M 27:15–18.)

2 Nefi 1:24–32Lehi anawausia wanawe kufuata uongozi wa kinabii wa NefiEleza kwamba Lehi alifunza kuhusu chanzo cha nguvu na mwongozo ambao Bwana alipeana kwa ajili ya familia yake. Alika wanafunzi kupata chanzo hicho katika 2 Nefi 1:24. (Chanzo kilikuwa Nefi, ambaye angetumika kama nabii wao baada ya Lehi kufa.)Uliza mwanafunzi kusoma 2 Nefi 1:25–28 kwa sauti. Uliza darasa kuangalia sababu alizo-toa Lehi kwa watu kumfuata Nefi.• Ni sifa zipi ambazo Lehi alisisitiza alipozungumza juu ya uongozi wa Nefi? Kwa nini

ungeamwamini kiongozi mwenye sifa hizi?• Wakati gani umeona viongozi wa Kanisa wakionyesha sifa hizi?Alika wanafunzi kusoma 2 Nefi 1:30–32 kimoyomoyo. Waulize kuangalia ahadi ambazo Lehi alimpa Zoramu.• Ni ahadi zipi ulizopata?• Ahadi hizi zinawezaje kutuhusu pamoja na familia zetu tunapofuata nabii?Baada ya mjadala huu, hakikisha kwamba wanafunzi wanaelewa kwamba tunapofuata wale ambao Mungu amewaita kutuongoza, tunabarikiwa kwa mafanikio ya kiroho na usalama. Ili kusaidia kanuni hii, shiriki ushuhuda wako wa baraka unaokuja wakati tunapofuata viongozi wetu wa Kanisa.

Istiara katika maandikoIstiara ni aina ya hotuba ambayo neno au kifu-ngu kinaeleza kitu au tendo bila ya kuwa na uhusiano halisi na kifaa hicho au tendo. Kwa mfano, wana wa Lehi hawakufunikwa kweli na vumbi wakati Lehi ali-powaambia, “muinuke kutoka mavumbini” (2 Nefi 1:14). Bwana na manabii wake mara nyi-ngi wametumia istiara katika mafundisho yao ili kutusaidia kuhusiana na kanuni za injili. Hizi istiari zinaweza kutu-mika kama vikumbusho vya nguvu. Mnapojadili istiara, wasaidie wanafu-nzi kuzingatia maana ya kiroho inayowasilishwa na maneno.

Page 94: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

79

2 nefi 1

Tangazo na Habari za usuli2 Nefi 1:22. “Uharibifu wa milele”Katika 2 Nefi 1:22, Lehi anaongea kuhusu“kuangami-zwa milele kwa roho na mwili.” Taarifa ifuatayo na Rais Joseph Fielding Smith inaweza kukusaidia kueleza maneno ya Lehi:

“Uharibifu haimaanishi maangamizi. Tunajua, kwa sa-babu tumefundishwa katika funuo za Bwana, kwamba nafsi haiwezi kuharibiwa.

“Kila nafsi iliozaliwa katika dunia hii itapata ufufuo na kutokufa na itadumu milele. Uharibifu haimaanishi, basi, maangamizi. Wakati Bwana anasema zitaanga-mizwa, anamaanisha kwamba zitatengwa mbali na uwepo wake, ya kuwa zitakatiliwa mbali kutokana na uso wa nuru na ukweli, na wala hazitakuwa na haki ya kupata furaha hii; na hiyo ni uharibifu”(Doctrines of Salvation, comp. Bruce R. McConkie, 3 vols. [1954–56], 2:227–28).

2 Nefi 1:28. “Kama mtasikiliza sauti ya Nefi hamtaangamia”Lehi aliahidi kwamba wale ambao “watasikiliza sauti ya Nefi” wangebarikiwa (ona 2 Nefi 1:28). Ili kusoma kuhusu ahadi ambazo Bwana amefanya kwa wale wa-naofuata manabii wanaoishi katika siku zetu, tazama Mafundisho na Maagano 21:5–6.

Rais Wilford Woodruff alisema: “Natumaini sisi sote tu-tafuata mfumo tuliowekewa na watumishi wa Bwana, kwa kuwa tukifanya hivyo ninajua ya kuwa tutakuwa salama katika dunia hii, na kupata furaha na kutu-kuzwa katika dunia ijayo. . . . Kama sisi ni waaminifu watatuongoza katika njia ya maisha, na kadri tulivyo na imani ya kuamini katika maelekezo yao, katika ma-fundisho ya Roho Mtakatifu kwa njia yao, tuko daima katika njia salama, na tutakuwa na uhakika wa malipo yetu” (Teachings of Presidents of the Church: Wilford Woodruff [2004], 199).

Page 95: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

80

Utangulizi2 Nefi 2 kina muendelezo wa mafundisho ya Lehi kabla tu ya kufa kwake. Akizungumza moja kwa moja na mwanawe Yakobo, Lehi, alishuhudia juu ya uwezo wa Bwana wa kuweka wakfu masumbuko yetu kwa faida yetu. Akizungumza na wanawe wote, alifundisha

kuhusu Kuanguka kwa Adamu —kwa nini kulikuwa muhimu na jinsi kunavyo waathiri binadamu—na juu ya haja ya Upatanisho wa Yesu Kristo. (Lehi pia alifundisha kuhusu mafundisho ya haki ya kujiamulia. Mafundisho haya yatashughulikiwa katika kipindi kinachofuata.)

SOMO 23

2 nefi 2 (Sehemu 1)

Mapendekezo ya Kufundisha

2 Nefi 2:1–4Lehi anazungumza na Yakobo juu ya majaribio na barakaKusaidia wanafunzi kuona kuwa 2 Nefi 2 ni muhimu katika maisha yao, waulize kufikiria juu ya mtu waliyemjua ambaye amekabiliwa na matatizo makubwa au mateso. Wakaribi-she kutafakari kile wanachoweza kusema ili kuhamasisha mtu huyo. Waulize wajiandae kushiriki mawazo yao nadarasa.Eleza kwamba 2 Nefi 2 ina rekodi ya Lehi akizungumza na mwana ambaye alikuwa na matatizo. Alika wanafunzi kusoma 2 Nefi 2:1 kimya. Waulize watambue mwana ambaye Lehi alifundisha (Yakobo) na kile kilichosababisha mateso ya mwana huyu (ujeuri wa ndugu zake). Kisha wezesha wanafunzi kusoma 2 Nefi 2:2–3 kimya kimya. Unaweza kupendekeza kwamba waweke alama kwenye maneno na vishazi ambavyo vinaeleza kile Bwana angemfanyia Yakobo.Waulize wanafunzi kushiriki vishazi walivyopata. Kisha waulize maswali yafuatayo ili kuwasaidia kuelewa kwamba Bwana anaweza kuweka wakfu masumbuko yetu kwa faida yetu:• Je, maneno “kuweka wakfu masumbuko yako kwa faida yako” inamaanisha nini? (Una-

weza kuhitaji kueleza kwamba kuweka wakfu inamaanisha kujitolea au kufanya takatifu.)• Ni wakati gani umeona kwamba Bwana anaweza kuweka wakfu masumbuko yetu?

2 Nefi 2:5–25Lehi anafundisha wanawe juu ya Kuanguka na juu ya Upatanisho wa Yesu KristoEleza kwamba Lehi alifundisha Yakobo na wanawe wengine kuhusu Kuanguka kwa Adamu na Hawa. Unaweza kuhitaji kueleza kwamba neno “Kuanguka” inahusu hali ilio-wapata Adamu na Hawa na watoto wao kwa sababu ya uchaguzi wa Adamu na Hawa wa kula tunda lililokatazwa katika bustani ya Edeni.• Ni uchaguzi gani ambao Bwana aliwapa Adamu na Hawa katika bustani la Edeni? (Ali-

waruhusu kuchagua kama watalila au kutoila tunda lililokatazwa.)• Kulingana na 2 Nefi 2:15, kwa nini Bwana aliwapa uchaguzi huu? (“Kutimiza makusudi

yake ya milele katika kikomo cha mwanadamu.” Unaweza kutaka kuhimiza wanafunzi kutia alama kwenye kishazi hiki.)

• Je, nini madhumuni ya milele ya Mungu kwetu sisi? (Ili kutupa nafasi ya kupokea uzima wa milele na kuwa kama Yeye. Unaweza kutaka kuwahimiza wanafunzi kutilia mkazo hili katika maandiko yao karibu na maneno “makusudi ya milele.” Unaweza pia kuwa-taka wasome Musa 1:39.)

Nakili chati ifuatayo ubaoni, ukiacha masanduku mawili za chini tupu. (Unaweza kutaka kupendekeza kwamba wanafunzi wanakili chati hii katika jarida zao ya masomo ya maa-ndiko au daftari za darasa.)

Wasaidie wanafunzi kuona kwamba maandiko ni muhimu kwaoMojawapo ya njia bora ya kusaidia wanafunzi kujiandaa kujifunza ni kuwauliza kutafakari swali au hali ambayo ni muhimu kwao na ambayo itashughulikiwa katika maandiko kwa ambayo unafundisha. Hii itasaidia wanafunzi kusoma maandiko na kusudi.

Page 96: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

81

2 nefi 2 (SeheMU 1)

bila Kuanguka Kwa Sababu ya Kuanguka

vitu vyote vingebaki vivyo hivyo vilivyoumbwa (ona 2 nefi 2:22).adamu na hawa hawangezaa watoto (ona 2 nefi 2:23).adamu na hawa wangeishi katika hali ya kitoto, bila kufahamu furaha wala dhiki, mema au dhambi (ona 2 nefi 2:23).

adamu na hawa walifukuzwa kutoka bustani ili walime ardhi (ona 2 nefi 2:19).adamu na hawa walizaa watoto —jamii ya ulimwengu wote (ona2 nefi 2:20).adamu na hawa na uzao wao wangepitia mai-sha ya dunia, ikiwemo taabu, furaha, na uwezo wa kutenda mema na kutenda dhambi (ona 2 nefi 2:23, 25).tumo chini ya kifo cha kimwili na kiroho (ona 2 nefi 9:6; helamani 14:16).

Alika mwanafunzi kuja kwenye ubao na kuwa mwandishi kwa darasa. Waulize wanafunzi kutafuta 2 Nefi 2:19–25 kimya kimya, wakitambua (1) madhara ambayo yangetokea kama Adamu na Hawa hawangekula tunda lililokatazwa na kuanguka na (2) matokeo ambayo yalitokana na Kuanguka. Uliza mwandishi kuandika majibu ya wanafunzi kwenye chati. Majibu yanapaswa kujumuisha yale yaliooredheshwa hapo juu (isipokuwa kwa habari juu ya kifo cha kimwili na kiroho, ambayo itaongezwa baadaye).Alika wanafunzi kukagua majibu yao chini ya kichwa “Bila Kuanguka.”• Ni vipi hali katika Bustani ya Edeni imewazuia Adamu na Hawa kuendelea katika mpa-

ngo wa wokovu wa Baba wa Mbinguni? (Ona 2 Nefi 2:22–23.)Alika wanafunzi kukagua orodha ya chini ya kichwa “Kwa sababu ya Kuanguka.” Ha-kikisha kwamba wanatambua kwamba kwa sababu sisi ni watoto wa Adamu na Hawa, tunaathiriwa na hali iliyowafikia baada Kuanguka (ona 2 Nefi 2:21).• Kishazi “kulima ardhi” kinamaanisha kwamba baada ya Adamu na Hawa kufukuzwa

kutoka bustanini, walilazimika kufanya kazi ili wapate chakula. Unafikiria kazi inatusai-dia vipi kuendelea katika mpango wa Baba wa Mbinguni?

• Kupata watoto kunawasaidia vipi Adamu na Hawa kuwa zaidi kama Baba wa Mbinguni? Ni kwa njia gani familia ni muhimu katika mpango wa Baba wa Mbinguni?

• Ni Jinsi gani fursa ya kuona furaha na taabu inatusaidia kuendelea katika mpango wa Baba wa Mbinguni?

Baada ya kujadili maswali haya, sisitiza kwamba kuanguka kwa Adamu na Hawa ni sehemu muhimu katika mpango wa Baba wa Mbinguni wa furaha.Onyesha kwamba 2 Nefi 2:25 ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Unaweza kuhimiza wanafunzi kukiweka alama. Kwa sababu ni kifupi, unaweza kutaka kuchukua muda ili kuwasaidia wanafunzi kukikariri.Eleza kwamba ingawa Kuanguka kulitufungulia njia ili kuendelea, pia kulileta maumivu, mateso, dhambi na kifo duniani. Ili kuwasaidia wanafunzi kupanua ufahamu wao wa ukweli huu, uliza mwanafunzi kusoma 2 Nefi 9:6 kwa sauti. Kisha uliza mwanafunzi mwi-ngine kusoma Helamani 14:15–17 kwa sauti. Uliza darasa kuangalia matokeo ya Kuanguka yalivyoelezwa katika mistari hii.• Je, mistari hii inafundisha nini kuhusu Kuanguka? (Kulileta kifo cha kawaida, ambayo

ni kifo ya mwili, na kifo cha kiroho, ambacho ni hali ya kuondolewa mbali na uwepo wa Mungu. Andika Tumo chini ya kifo cha kimwili na kiroho kwenye ubao chini ya “Kwa sababu ya Kuanguka.”)

Ili kuwasaidia wanafunzi kufikiria juu ya jinsi wamepata matokeo ya Kuanguka ambayo yameorodheshwa ubaoni, wahimize kutafakari kimoyomoyo maswali yafuatayo. (Soma maswali polepole na utue katikati yao ili kuwapa wanafunzi muda wa kutosha ili kufikiri.)• Je, ni nini sababu za mateso katika maisha haya?• Kwa nini kifo ni sehemu muhimu ya mpango wa wokovu?• Ni jinsi gani mateso na huzuni unaweza kutusaidia kujifunza na kukua?Eleza kwamba tunapoelewa jinsi Kunguka kunavyotuathiri sisi, tunatambua kwamba tuna-hitaji Upatanisho wa Yesu Kristo. Soma kauli ifuatayo ya Rais Ezra Taft Benson:

2 Nefi 2:25 Rejea wazo la mafundisho wa umahiri wa maandiko kwenye mwisho wa somo ili kuwasaidia wanafunzi na umahiri wao wa kifungu hiki.

Page 97: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

82

SoMo 23

“Kama vile mtu hana hamu ya chakula mpaka awena njaa, hivyo, hana hamu ya wokovu wa Kristo mpaka atakapojua kwa nini anahitaji Kristo.“Hakuna anayejua kikamilifu na ipasavyo kwa nini anahitaji Kristo mpaka atakapoelewa na kukubali mafundisho ya Kuanguka na madhara yake juu ya watu wote. Na hakuna kitabu kingine duniani kinachoelezea mafundisho haya muhimu karibu kama vile Kitabu cha Mormoni”(“The Book of Mormon

and the Doctrine and Covenants,” Ensign, Mei 1987, 85).Baada ya wanafunzi kupata muda wa kutosha kutafakari maswali haya, onyesha picha ya Mwokozi. Shiriki ushuhuda wako kwamba kupitia kwa Upatanisho, Yesu Kristo anatukomboa kutokana na madhara ya Kuanguka na anatoa ukombozi kutokana na dhambi zetu.Alika wanafunzi wachache kuchukua zamu kwa kusoma kwa sauti kutoka 2 Nefi 2:5–10, 21 na Alma 7:11–13. Uliza darasa kutambua vishazi katika vifungu hivi ili kuonyesha kile Mwo-kozi amefanya ili kutukomboa kutokana na madhara ya Kuanguka na kutokana na dhambi zetu binafsi. (Katika uhusiano na mstari 9, unaweza kuhitajika kueleza kwamba kishazi “kuwaombea” kinamaanisha kusihi kwa niaba ya mtu mwingine au kutenda katika nafasi ya mtu mwingine.) Ili kuwasaidia wanafunzi kuchambua vishazi walivyogundua, uuliza:• Ni vishazi gani katika mistari hii vinaonyesha kuwa kupitia Upatanisho, Mwokozi atatu-

komboa kutokana na kifo cha kimwili?• Ni vishazi gani vinavyoonyesha kuwa Mwokozi atatukomboa kutokana na kifo cha

kiroho (kuondolewa kutoka kwa uwepo wa Mungu)?• Ni vishazi gani vinavyoonyesha kuwa Mwokozi anaweza kutukomboa kutokana na

dhambi zetu?• Ni vishazi gani vinavyoonyesha kuwa Mwokozi anaweza kutusaidia katika nyakati za

majaribio kama vile ugonjwa na maumivu?Kulingana na 2 Nefi 2:7–9, 21, tunapaswa kufanya nini ili kupokea baraka zote zinazopa-tikana kwa njia ya Upatanisho? (Kwa mujibu wa mstari wa 7, unaweza kuhitajika kueleza kwamba mtu ambaye ana “moyo uliopondeka na roho iliovunjika” ni mnyenyekevu na tayari kufuata mapenzi ya Mungu. Mtu kama huyo anahisi huzuni wa kina kwa ajili ya dhambi, na kwa dhati anataka kutubu.)Baada ya kujadili maswali haya, wawezeshe wanafunzi kuchunguza mistari iliyotolewa kimoyomoyo, wakiangalia vishazi ambavyo hasa vina maana kwao. Waulize wanafunzi ku-jigawa katika majozi na kushiriki vishazi walivyochagua na kila mmoja. Waalike kushiriki kwa nini vishazi hivi ni vya maana kwao.Alika mwanafunzi moja au wawili kufupisha kwa darasa kwa nini Kuanguka ni sehemu muhimu ya mpango wa wokovu wa Baba wa Mbinguni. Kisha waulize kuelezea hisia zao juu ya jinsi Upatanisho wa Yesu Kristo unatukomboa kutokana na Kuanguka.

Umahiri wa Maandiko—2 Nefi 2:25Fahamu: Fikiria kutumia shughuli zifuatazo ili kuwasaidia wanafunzi kutumia 2 Nefi 2:25 wanapofundisha injili. Kwa sababu ya hali na urefu wa mafundisho ya leo, unaweza kutaka kutumia shughuli hii katika siku nyingine, wakati una muda zaidi.Alika wanafunzi kuandaa somo kuhusu mafundisho ya Kuanguka, kwa kutumia 2 Nefi 2:25. Wanaweza kufundisha somo hili katika jioni ya familia nyumbani au katika mazingira mengine. Waulize wanafunzi wachache ikiwa watakubali kutoa taarifa juu ya uzoefu wao baada ya kufundisha. Ruhusu wanafunzi kuanza maandalizi yao wakati wa darasa, kama muda upo.

Page 98: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

83

UtanguliziSomo lililopita juu ya 2 Nefi 2 lilizingatia Kuanguka kwa Adamu na Hawa na Upatanisho wa Yesu Kristo. Somo hili linazingatia mafundisho ya Lehi kuhusu mafundisho ya wakala, ikiwemo ukweli kwamba tuko huru kucha-gua uhuru na uzima wa milele kupitia kwa Yesu Kristo.

Katika somo hili, wanafunzi watakuwa na fursa ya kufundisha mtu mwingine. Kabla ya darasa, tayarisha brosha zenye maelekezo katika somo hili. Jifahamishe kila seti ya maelekezo ili uweze kuwasaidia wanafunzi wanapojianda kufundisha.

SOMO 24

2 nefi 2 (Sehemu 2)

Mapendekezo ya Kufundisha

2 Nefi 2:11–18, 25–30Lehi anafundisha kuhusu wakala na matokeo ya uchaguzi wetuKwa kifupi wakumbushe wanafunzi kwamba katika somo lililopita, walisoma mafundisho ya Lehi katika 2 Nefi 2 kuhusu Kuanguka kwa Adamu na Hawa na baraka za Upatanisho wa Yesu Kristo. Uchaguzi wa Adamu na Hawa ulituruhusu kuja duniani (ona 2 Nefi 2:25), ambapo tunahisi huzuni, maumivu, na mauti. Kupitia kwa Upatanisho, Yesu Kristo anatukomboa kutokana na Kuanguka na anatoa ukombozi kutokana na dhambi zetu (ona 2 Nefi 2:26). Kwa sababu ya Upatanisho, tuko huru kuchagua uhuru na uzima wa milele au utumwa na kifo (ona 2 Nefi 2:27).Eleza kwamba kadri wanafunzi wanapoendelea na masomo yao ya 2 Nefi 2 katika somo hili, watakuwa na nafasi ya kufundishana kanuni za wakala ambazo Lehi alielezea mwa-nawe Yakobo. Gawanya wanafunzi katika makundi manne. Kipe kila kikundi moja ya seti ifuatayo ya maelekezo ili kuwasaidia kufundisha (kabla ya darasa, kutayarisha brosha ze-nye maelekezo hayo). Kama darasa lina wanafunzi chini ya nne, kutoa seti ya maagizo kwa kila mwanafunzi na kufundisha nyenzo zilizomo katika seti kukaa mwenyewe.Kila seti za maagizo zina kazi tano. Wahimize wanafunzi wote kushiriki kwa kuhakikisha kuwa kila mtu katika kikundi anapata kazi. Katika vikundi vyenye zaidi ya watu watano, wanafunzi wanaweza kugawa kazi. Katika vikundi vilivyo na wanafunzi wasiofika watano, baadhi ya watu binafsi watahitajika kufanya kazi zaidi ya moja. Waarifu wanafunzi kwamba watakuwa na karibu dakika tatu ili kujiandaa na kwamba kila kikundi kitakuwa na karibu dakika tano za kufundisha.

Kundi 1: Mungu alituumba ili kutenda A. Inua jiwe mbele ya darasa. Alika mwanafunzi kusoma 2 Nefi 2:14 kwa sauti. Kabla yeye

kusoma, uliza darasa kutafuta maelezo ya Lehi ya aina mbili ya vitu ambavyo Mungu ameumba katika mbingu na ardhi. (“Vitu vya kutenda na vitu vya kutendewa.”) Uliza: Mstari huu unatuhusisha vipi na jiwe? (Tuliumbwa kutenda, ilihali jiwe liliumbwa kute-ndewa. Jiwe, kama vile maumbile mengine mengi, haliwezi kutenda lenyewe.)

B. Uliza mwanafunzi kusoma sentensi ya kwanza katika 2 Nefi 2:16. Uliza darasa: Katika mpango wa Baba wa Mbinguni wa wokovu, kwa nini unafikiri ni muhimu kwamba tujitendee wenyewe? Baada ya wanafunzi ya kuitikia, uliza: Jinsi gani wakati mwingine sisi husubiri kutendewa badala ya kujitendea wenyewe?

C. Andika M&M 58:26–28 kwenye ubao. Alika darasa kurejea kwa fungu hili. Waongoze katika kulisoma pamoja kwa sauti.

D. Uliza: Je, tunaweza kujifunza nini kutoka Mafundisho na Maagano 58:26–28 kuhusu kujitendea wenyewe? Ni baadhi ya njia gani tunazoweza kujihusha kwa bidii katika kuleta kupatikana kwa haki? Ni lini umeona bidii yako ikileta kupatikana kwa haki? (Baada ya mwanafunzi mmoja au wawili kujibu, unaweza kutaka pia kushiriki uzoefu.)

E. Toa ushuhuda wako kuhusu umuhimu wa kujitendea wenyewe na kutafuta kupatikana kwa haki.

2 Nefi 2:27 ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Rejea wazo la mafundisho wa umahiri wa maandiko kwenye mwisho wa somo ili kuwasaidia wanafunzi na umahiri wao wa kifungu hiki.

Page 99: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

84

SoMo 24

Kundi 2: Ushawishi mwema na ushawishi mbaya A. Alika mwanafunzi kusoma sentensi ya pili katika 2 Nefi 2:16. Uliza darasa: Ni nini ma-

ana ya neno kushawishi? (kukaribisha, kushawishi, au kuvutia.) B. Uliza darasa: Ni zipi baadhi ya njia ambazo Baba wetu wa Mbinguni hutushawishi

kufanya vizuri? (Wanafunzi wanaweza kutaja ushawishi kutoka kwa Roho Mtakatifu, baraka zilizoahidiwa kwa ajili ya kutii amri, na mafundisho ya manabii wa siku za mwisho.)

C. Soma 2 Nefi 2:17–18 kwa sauti, na ukaribishe wanafunzi kufuata pamoja katika maa-ndiko yao. Waulize kubainisha kile shetani anatafuta kwa sisi wote. (Anataka tuwe na taabu.)

D. Uliza: Unawezaje kujua ni ushawishi gani umetoka kwa Mungu na gani ambao ume-toka kwa shetani? (Kama sehemu ya mjadala huu, unaweza kutaka kurejea Moroni 7:16–17.) Baada ya darasa kujibu, uliza: Ni mifano gani ya vitu vinavyoshawishi watu kufanya maovu na vinavyoelekeza kwa taabu?

E. Toa ushuhuda wako juu ya ushawishi wa Mungu unaoelekeza kwa wema na furaha na ushawishi wa shetani unaolekeza kwa uovu na taabu. Kama sehemu ya ushuhuda wako, unaweza kutaka kushiriki uzoefu ili kuonyesha jinsi unajua hii ni kweli.

Kundi 3: Tunawajibika kwa ajili ya uchaguzi wetu A. Soma taarifa hii kwa darasa:

“Uko huru kuchagua na kutenda, lakini hauna huru kuchagua matokeo ya matendo yako. Matokeo huenda yasiwe mara moja, lakini yatakufuata kila mara”(True to the Faith: A Gospel Reference [2004], 12).Uliza: Ni mifano gani ya madhara ambayo hayawezi kuwa mara moja lakini ambayo ya-naweza kuja? (Jibu moja liwezekanalo ni kwamba saratani mara nyingi huletwa sigara.)

B. Alika wanafunzi kusoma 2 Nefi 2:26–27 kimya kimya, wakiangalia maneno na vishazi vinavyoonyesha matokeo ya baadaye ya chaguzi tunazofanya sasa. Waulize wanafunzi kuripoti juu ya kile walichopata. (Majibu yanaweza kujumuisha "adhabu ya sheria katika siku kuu na ya mwisho,” “uhuru”, “uzima wa milele,” “ufungwa,” “kifo,” na “taabu.”) Andika majibu ya wanafunzi ubaoni.

C. Uliza: Kwa nini unafikiri ni muhimu kwetu kuelewa matokeo ya chaguzi zetu katika maisha haya? Baada ya wanafunzi kujibu, uliza:kujua matokeo haya kunawezaje kuna-tuhimize kufanya chaguzi za haki?

D. Onyesha kwamba katika 2 Nefi 2:27, Lehi anasema kwamba tuna “haki ya kuchagua uhuru.” Uliza: Kwa uzoefu wako, uchaguzi wa haki unatusaidia kwa jinsi gani kubakia huru kuchagua? Unaweza kutoa mifano ya hili? (Kuwa tayari kushiriki mfano wako mwenyewe.)

E. Toa ushuhuda wako tunawajibika kwa Mungu kwa ajili ya uchaguzi wetu na kwamba matokeo daima hufuata uchaguzi wetu.

Kundi 4: Kuchagua sehemu nzuri A. Wezesha mwanafunzi kusoma 2 Nefi 2:28 kwa sauti. Uliza darasa kuangalia vitu vinne

ambavyo Lehi alitamani kwa ajili ya wanawe. Baada ya mstari kusomwa, alika wanafu-nzi kushiriki kile walichopata.

B. Uliza: Ni njia gani tunaweza kutazamia kwa Mpatanishi mkuu, Yesu Kristo, ili kutusai-dia kufanya uchaguzi za haki?

C. Alika mwanafunzi kusoma 2 Nefi 2:29 kwa sauti. Uliza darasa: chaguzi zetu zinaweza-kwa jinsi gani kumpa Shetani nguvu ya kutuweka mateka? Kama sehemu ya mjadala huu, onyesha kwamba mengi ya majaribu ya Shetani yanalenga “mapenzi ya mwili,” au tamaa zetu za kimwili. Wakati watu wanapoanguka kwa majaribu haya, wanaweza kutawaliwa na vitu na tabia hatari. Soma kauli ifuatayo ya Mzee Russell M. Nelson wa Akidi ya Wale Mitume na Kumi na Wawili:“Kutokana na jaribio la awali lililodhaniwa kuwa dogo, mzunguko wa matatizo una-weza kufuata. Kutokana na majaribu huja tabia. Kutokana na tabia huja kutegemea. Kutokana na kutegemea huja uraibu. Kushika kwake ni taratibu. Pingu za utumwa za tabia ni ndogo mno kutambulika mpaka zinapokuwa kali mno kuvunjika. . . . Uraibu

Page 100: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

85

2 nefi 2 (SeheMU 2)

hujisalimisha hatimaye uhuru wa kuchagua (“Addiction or Freedom,” Ensign, Nov. 1988, 6–7).Toa ushuhuda wako juu ya haki inayoelekeza kwa uhuru kutokana na tabia hatari na uraibu.

D. Soma 2 Nefi 2:30 kwa darasa. Wanapofuata pamoja, waalike kuzingatia maneno haya: “nimechagua sehemu nzuri.” Uliza: Kauli hii inafundisha nini kuhusu Lehi?

E. Waulize wanafunzi kutafakari maswali yafuatayo: Ni nani unayemjua ambaye “ame-chagua sehemu nzuri” kama Lehi? Ni kwa njia gani ungependa kufuata mfano wa mtu huyu? Baada ya wanafunzi kupata muda wa kutafakari, uliza mmoja au wawili kushiriki mawazo yao. Kisha shiriki wazo lako mwenyewe.

Wazo kwa mwalimu: Kwa kuhitimisha, alika wanafunzi kutafakari kama chaguzi zao zinawaongoza kwa uhuru na uzima wa milele au kwa utumwa, kifo cha kiroho, na taabu. Wahakikishie wanafunzi kwamba chaguzi zozote mbaya ambazo wamefanya tayari zina-weza kushindwa kwa njia ya imani katika Yesu Kristo na toba. Shuhudia juu ya Mwokozi, Upatanisho Wake, na uwezo Wake wa kutuimarisha katika juhudi zetu za kufanya maa-muzi ambayo yataelekeza kwa furaha na uzima wa milele.

Umahiri wa Maandiko—2 Nefi 2:27Ili kuwasaidia wanafunzi kukariri 2 Nefi 2:27, andika herufi ya kwanza kwenye ubao, kama ifuatavyo:Kh, wwuw; nwvvanmkm. Nwhkunuwm, Kymmwww, akunk, knunzi; kawwndky.(Unaweza pia kutaka kuwahimiza wanafunzi kuonyesha kifungu hiki katika njia tofauti ili waweze kukipata kwa haraka.)Wezesha wanafunzi kukariri 2 Nefi 2:27 pamoja (wakitumia maandiko yao ipasavyo) mpaka watakapoweza kukariri mstari mzima kwa kutumia tu herufi za kwanza ili kuwasa-idia. Kisha futa herufi kadhaa na wawezeshe kukariri maandiko pamoja tena. Endelea na utaratibu huu mpaka herufi zote zifutike na darasa linaweza kukariri mstari mzima kutoka katika kumbukumbu. Kama sehemu ya shughuli hii, unaweza kutaka kuelezea kauli ifuatayo ya Mzee Richard G. Scott wa Akidi ya Mitume kumi na Wawili: “Andiko lilioka-ririwa linakuwa rafiki wa kudumu ambalo halilegei kwa mpito wa muda” (“The Power of Scripture,” Ensign or Liahona, Nov. 2011, 6).Fahamu: Unaweza kuwa na muda wa kutumia shughuli hii wakati fulani katika somo hili. Kama hauna muda, fikiria kuitumia katika somo jingine.

Tangazo na Habari za usuli2 Nefi 2:29. “Nia ya mwili na uovu ulio ndani yake”Mstari huu haumaanishi kwamba miili yetu ni mibaya. Badala yake, inaelezea upande wa hali yetu ilioanguka. True to the Faith inajumuisha maelezo haya: “Katika hali hii ya kuanguka, tuna migogoro ndani yetu. Sisi ni watoto wa kiroho wa Mungu, wenye uwezo wa

kuwa ‘washirika wa tabia ya Mungu’ (2 Petro 1:4). Hata hivyo, ‘sisi hatufai mbele ya [Mungu]; kwa sababu ya mwanguko maumbile yetu yamekuwa maovu siku zote (Etheri 3:2). Tunahitaji kujitahidi siku zote kushinda tamaa mbaya na matarajio”(True to the Faith: A Gospel Reference [2004], 57).

Page 101: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

86

Utangulizi2 Nefi 3 ina maneno ya Lehi kwa mwanawe mdogo, Yu-sufu. Lehi alielezea unabii wa Yusufu wa Misri kuhusu

wajibu wa Nabii Joseph Smith, ujio wa Kitabu cha Mormoni, na urejesho ya injili.

SOMO 25

2 nefi 3

Mapendekezo ya Kufundisha

2 Nefi 3:1–25Lehi anaeleza unabii wa Yusufu wa Misri kuhusu Nabii Joseph SmithKabla ya darasa, chora mchoro ufuatao ubaoni.

Ili kuandaa wanafunzi kuelewa mafundisho katika 2 Nefi 3, waambie kwamba sura hii inajumuisha habari kuhusu watu wanne wenye jina moja ya kwanza. Waalike wanafunzi kutafuta kwa haraka marejeo ya maandiko chini ya kila mchoro kwenye ubao ili kuamua ni nani aliyewakilishwa na kila mchoro. Mwanafunzi anapopata majibu, mwezeshe kuandika katika ubao (Mchoro wa kwanza unawakilisha Yusufu, mwana wa Lehi. Wa pili inawakili-sha nabii Joseph ambaye aliuzwa utumwani Misri takribani miaka 1700 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Wa tatu inawakilisha Nabii Joseph Smith. Wa nne inawakilisha Mzee Joseph Smith)Onyesha picha ya Nabii Joseph Smith, kama vile Brother Joseph (62,161, Gospel Art Book [2009], no. 87). Wajulishe wanafunzi kwamba sehemu kubwa ya 2 Nefi 3 inazingatia unabii na Yusufu wa Misri kuhusu Nabii Joseph Smith.Wakaribishe wanafunzi watatu ili kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka 2 Nefi 3:6–8. Uliza darasa kutambua maneno na vishazi kwamba Yusufu wa Misri alikuwa akieleza kuhusu Joseph Smith na kazi ambayo angetimiza. (Unaweza kuhitajika kueleza kwamba wakati Yusufu wa Misri alipotumia kishazi “uzao wa viuno vyangu,” alikuwa akimaani-sha uzao wake.) Kwenye ubao chini ya mchoro inayowakilisha Joseph Smith, orodhesha maneno na vishazi ambavyo wanafunzi wamepata. Wanapaswa kutambua vishazi kama vile “nabii bora nitakayemwinua kutoka matunda ya viuno vyako,” “ataheshimiwa zaidi,” “kuwafahamisha ufahamu wa maagano,” na “nitamuinua juu machoni mwangu.”• Kama tulivyojifunza 2 Nefi 3:6–8, ni nini umejifunza kuhusu Nabii Joseph Smith? (Wa-

saidie wanafunzi kuelewa kwamba Bwana alimwinua Nabii Joseph Smith kusaidia kuleta Urejesho wa Injili.)

Alika wanafunzi kusoma 2 Nefi 3:11–15 kimya kimya. Waulize kutafuta vishazi vya ziada juu ya kile Mungu angekamilisha kupitia Nabii Joseph Smith. Wakati wamekuwa na muda wa kutosha kusoma mistari hii, waulize kile walichokipata. Ongeza majibu yao katika orodha kwenye bodi chini ya mchoro ambao unamwakilisha Nabii Joseph Smith. (Majibu yanaweza kujumuisha “kuleta neno langu,” “kutoka katika unyonge atapewa nguvu,” “wale ambao wanataka kumwangamiza watateketezwa,” na “jina lake lita-kuwa. . . sawa na jina la baba yake.”)

1 2 3 4

2 nefi 3:3 2 nefi 3:4 2 nefi 3:14 2 nefi 3:15

Page 102: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

87

2 nefi 3

Ili kuwasaidia wanafunzi zaidi kuelewa na kutafakari wajibu wa Nabii Joseph Smith katika Urejesho wa injili, soma 2 Nefi 3:11 kwa sauti, ukitilia mkazo maalum kwa kishazi “nguvu za kuleta neno langu.”• Je, ni mifano gani ya neno la Mungu ambayo Joseph Smith alitoa? (Majibu yanaweza

kujumuisha Kitabu cha Mormoni, Mafundisho na Maagano, Lulu ya Thamani Kuu, tafsiri ya Joseph Smith, na mahubiri ya Nabii mwenyewe.)

Katika mwendo wa majadiliano haya, hakikisha umeelezea kwamba Yusufu wa Misri, alitabiri kwamba Nabii Joseph Smith angeleta Kitabu cha Mormoni. Unaweza kuhitajika kueleza kwamba 2 Nefi 3:12 inataja vitabu viwili: kitabu kilichoandikwa na wana wa Yusufu wa Misri kilikuwa Kitabu cha Mormoni; kitabu kilichoandikwa na wana wa Yuda kilikuwa Biblia. Unaweza pendekeza kwamba wanafunzi waandike maelezo haya katika maandiko yao.Alika wanafunzi kutafuta 2 Nefi 3:12 kwa vishazi vinavyoelezea athari itakayoletwa na Kitabu cha Mormoni na Biblia ulimwenguni “itakapokua pamoja.” (Kwa mfano, wanafunzi wanaweza kutambua “kufadhaisha mafundisho ya uwongo,” “kutatua mabishano,” na “kuimarisha amani”.)Ili kuwasaidia wanafunzi kutafakari juu ya jinsi ya Kitabu cha Mormoni kimeshawishi maisha yao, uliza:• Ni lini umeona nguvu ya Kitabu cha Mormoni katika maisha yako au kuona ushawishi

wake katika maisha ya marafiki au familia?Alika mwanafunzi kusoma 2 Nefi 3:15 kwa sauti. Uliza darasa kutilia maanani kishazi “ata-waleta watu wangu kwenye wokovu.”• Ni kwa njia gani Kitabu cha Mormoni kinasaidia kuleta watu kwa wokovu?• Ni tofauti gani ambayo Kitabu cha Mormoni kimefanya katika maisha yako?Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa na kufahamu kazi iliyo takaswa mbele ya Nabii Joseph

Smith, uliza mwanafunzi kusoma kwa sauti kauli ifuatayo ya Rais Brigham Young:“Ilitangazwa katika baraza la milele, muda mrefu kabla ya misingi ya dunia kuwekwa, kwamba yeye, Joseph Smith, anapaswa kuwa ndiye mtu, katika kipindi cha mwisho cha dunia hii, wa kuleta neno la Mungu kwa watu, na kupokea utimilifu wa funguo na nguvu ya ukuhani wa Mwana wa Mungu.

Bwana aliweka macho yake juu yake, na juu ya baba yake, na juu ya baba wa baba yake, na juu ya uzao wao huko nyuma . . . hadi kwa Adamu. Ametazama familia hiyo na damu hiyo kama ilivyosambaa kutoka kwenye chemchemi yake mapaka kuzaliwa kwa mtu huyo. Ali-takaswa mbele katika milele ili kuongoza kipindi hiki cha mwisho”(Discourses of Brigham Young, sel. John A. Widtsoe [1954], 108).Fupisha 2 Nefi 3:16–24 kwa kueleza kwamba Yusufu wa Misri alilinganisha Joseph Smith na Musa. Wezesha wanafunzi kuangalia maneno na vishazi ambavyo vinaelezea Nabii Jo-seph Smith katika 2 Nefi 3:24. Wanaposhiriki maneno na vishazi walivyogundua, ongezea majibu yao kwenye orodha ubaoni.Soma kauli ifuatayo ya Rais Gordon B. Hinckley. Waulize wanafunzi kusikiliza kweli zilizo-funuliwa kupitia kwa Nabii Joseph Smith:”Niruhusu mimi kutaja machache ya mafundisho mengi na matendo ambayo yanatutofa-utisha sisi na makanisa mengine yote, ambayo yote yamekuja kama ufunuo kwa Mtume kijana [Joseph Smith]. . . .“Maarifa ya Uungu. . . .“Kitabu cha Mormoni . . .“. . . Ukuhani uliorejeshwa . . .“. . . Mpango wa uzima wa milele wa familia. . . .“Utakatifu wa watoto. . . .“. . . Fundisho kuu wa wokovu kwa ajili ya wafu. . . .“Asili ya milele ya mwanadamu. . . .“. . . Kanuni ya ufunuo wa kisasa. . . .

Page 103: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

88

SoMo 25

“. . . Wakati mfupi wa miaka 38 na nusu wa maisha yake, ukaja kupitia kwake umwagiko usiopimika wa elimu, karama, na mafundisho”(“The Great Things Which God Has Revea-led,” Ensign or Liahona, Mei 2005, 80–83).Alika mwanafunzi kuongeza orodha ya Rais Hinckley katika orodha ubaoni.Weka mwanafunzi asome Mafundisho na Maagano 135:3 kwa sauti. Eleza kwamba Mzee John Taylor wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, ambaye baadaye alikuwa Rais wa tatu wa Kanisa, aliandika maneno haya mara tu baada ya kifo cha Nabii Joseph Smith. Waulize wanafunzi kuangalia vitu katika aya hii ambavyo wanaweza kuongeza kwenye orodha ubaoni. Jumuisha majibu yao kwenye orodha.Wape wanafunzi muda wa kukagua orodha kwenye ubao. Waalike kutafakari kile wali-chojifunza kuhusu kazi ya Nabii Joseph Smith. Waalike kutafakari wanachojua na kuhisi kuhusu Nabii kwa kuandika majibu kwa moja ya maswali yafuatayo katika jarida zao ya kujifunza maandiko au daftari za darasa:• Umejifunza au kuhisi nini leo ambacho kimeimarisha ushuhuda wako wa Nabii Joseph

Smith?• Ni nini ambacho Joseph Smith alifanya, kufundisha, au kurejesha ambacho unahisi ni

cha “thamani kuu” (2 Nefi 3:7) kwako?Gawanya wanafunzi katika majozi. Watie moyo ili kushiriki shuhuda zao za Nabii Joseph Smith na kila mmoja. Kama una muda, unaweza kuwahimiza baadhi ya wanafunzi kushi-riki na darasa nzima. Toa ushuhuda wako mwenyewe kwamba Mungu alimwinua Joseph Smith kuleta Urejesho. Alika wanafunzi wako kutafuta kwa maombi njia za kushiriki shu-huda zao za Nabii Joseph Smith na Kitabu cha Mormoni pamoja na watu wengine, hasa marafiki zao na familia.

Tangazo na Habari za usuli2 Nefi 3:12. Jinsi Kitabu cha Mormoni na Biblia “vitakua pamoja”Muda tu baada ya uchapishaji wa toleo la Biblia la King James la Watakatifu wa Siku za Mwisho, pamoja na Mwongozo wake wa Mada na tanbihi zake zikire-jea maandiko yote, ya kiwango, Rais Boyd K. Packer wa Akidi ya Mitume kumi na alieleza: “Agano la Kale na Agano Jipya . . . na . . . Kitabu cha Mormoni . . . sasa imesukwa pamoja kwa namna ambayo kwamba unapochunguza moja unavutiwa kwa nyingine; una-pojifunza kutoka kwa moja unaangaziwa na nyingine. Hakika ni kimoja katika mikono yetu” (“Scriptures,” Ensign, Nov. 1982, 53).

2 Nefi 3:18. Ni nani ndiye msemaji?Mzee Bruce R. McConkie wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alidokezea kuhusu utambulisho wa watu wali-osemwa katika 2 Nefi 3:18. Maneno kwenye mabano ni nyongeza za Mzee McConkie. Alisema: “Kumbuka maneno haya ya Bwana: ‘Na mimi, tazama, nitamwe-zesha [Mormoni] kwamba aandike maandishi ya uzao wa viuno vyako [Wanefi], kwa uzao wa viuno vyako [Walamani]; na mnenaji wa viuno vyako ataitangaza.’ Hiyo ni, Mormoni aliandika Kitabu cha Mormoni, lakini kile aliandika kilichukuliwa kutoka katika maandishi ya manabii Wanefi; na maandishi haya, yakiwa yameu-nganishwa katika kitabu kimoja, yalitafsiriwa na Joseph Smith na kutumwa kwa njia yake kwa Walamani” (A New Witness for the Articles of Faith [1985], 426).

Maswali kuhusu hisiaRais Henry B. Eyring wa Urais wa Kwanza aliwa-shauri walimu kuuliza maswali ambayo yana “karibisha watu binafsi kutafuta kumbukumbu zao kwa ajili ya hisia.” Ali-sema, “Baada ya kuuliza, tunaweza kusubiri kwa busara kwa muda kabla ya kumwita mtu kujibu. Hata wale ambao ha-wazungumzi watakuwa wakifikiri juu ya uzoefu wa kiroho. Hiyo itaalika Roho Mtakatifu” (“The Lord Will Multiply the Harvest” [address to CES religious educators, Feb. 6, 1998], 6, si.lds.org).

Page 104: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

89

Mafunzo ya Masomo ya Nyumbani1 Nefi 20–2 Nefi 3 (Kitengo cha 5)

Kifaa cha Maandalizi kwa Mwalimu wa Masomo ya NyumbaniMuhtasari wa Mafunzo ya Masomo ya Kila siku- NyumbaniMuhtasari ufuatao wa mafundisho na kanuni ambao wanafunzi walijifunza waliposoma 1 Nefi 20 kupitia 2 Nefi 3 (kitengo 5) hainuiwi kufundishwa kama sehemu ya somo lako. Somo unalofundisha kwa ajili ya kitengo 5 unazingatia tu kwa mafundisho na kanuni hizi chache. Fuata ushawishi wa Roho Mtakatifu unapofikiria mahitaji ya wanafunzi wako.

Siku 1 (1 Nefi 20–22)Wakati Nefi aliponukuu baadhi ya maneno ya unabii wa Isaya kwa ndugu zake, wanafunzi walijifunza kwamba Bwana anawaalika wale ambao wamekuwa waasi kutubu na kurudi Kwake. Hii inatuonyesha kwamba Bwana anatupenda na ka-mwe hatatusahau. Wanafunzi pia walijifunza kwamba ingawa Israeli itatawanyika kwa kutokutii kwao, Bwana aliahidi kure-jesha Injili na kuwakusanya Israeli katika siku za mwisho.

Siku 2 (2 Nefi 1)Wanafunzi walisoma mafundisho ya mwisho ya Lehi kwa familia yake kabla ya kufa. Lehi alisisitiza kuwa Bwana hutu-bariki tunapotii amri Zake na kwamba anazuia baraka wakati hatutii amri Zake. Wakati Lehi alijua kwamba angekufa hivi karibuni, aliwausia familia yake kufuata Nefi. Wanafunzi walioona ya kwamba tunapowafuata wale ambao Mungu amewaita kutuongoza, tunabarikiwa na mafanikio ya kiroho na usalama.

Siku 3 (2 Nefi 2)Lehi alimweleza mwanawe Yakobo kweli mbili za kimsingi: (1) kwamba Kuanguka kwa Adamu na Hawa ni sehemu muhimu ya mpango wa Baba wa Mbinguni wa furaha na (2) kwamba kupitia kwa Upatanisho, Yesu Kristo ametukumboa kutokana na madhara ya Anguko na anatoa ukombozi kutokana na dhambi zetu. Lehi alieleza kwamba kutokana na Anguko na Upatanisho, tuko huru kuchagua uhuru na uzima wa milele au kufungwa, na kifo (ona 2 Nefi 2:27).

Siku 4 (2 Nefi 3)Akizungumzia mwanawe Yusufu, Lehi alihusisha unabii wa Yusufu wa Misri unaopatikana kwenye mabamba ya shaba. Unabii huu ulitabiri kwamba Bwana alimuinua Nabii Joseph Smith ili kusaidia kuleta Urejesho wa Injili. Wanafunzi wali-ulizwa kuandika katika jarida zao za kujifunza ya maandiko kuhusu jinsi michango ya Nabii Joseph Smith imekuwa ya thamani kubwa kwao.

UtanguliziSomo hili linanuiwa kusaidia wanafunzi kuelewa madhumuni ya milele ya Mungu. Lehi alijua kwamba uzao wake ungeweza kufanya maamuzi ambayo yangewaongoza katika furaha, uhuru, na uzima wa milele tu kama wataelewa na kuamini mafundisho muhimu—kama vile Anguko, Upatanisho wa Yesu Kristo, haki ya kujiamulia, na utii (ona 2 Nefi 2:25, 27). Wahimize wanafu-nzi kuchagua uzima wa milele ili hatimaye waweze “kuzingirwa milele katika mikono ya upendo [wa Mungu]” (2 Nefi 1:15), kama alivyokuwa Lehi.

Mapendekezo ya Kufundisha

2 Nefi 1–2Kabla ya kufa kwake, Lehi ana wausia watoto wake kushika amri za Mungu na anawafundisha mafundisho ya msingi juu ya mpango wa wokovuAnza kwa kuwawezesha wanafunzi kusoma sentensi ya mwisho ya 2 Nefi 3:25 (“Kumbuka maneno ya baba yako anayekufa”). Waulize jinsi nadhari yao kwa ushauri kwa mwana familia ina-weza kubadilika ikiwa wanajua mtu huyo anakaribia kufa.

Shughuli ifuatayo inaweza kuwasaidia wanafunzi kuelewa vyema kweli ambazo Lehi alielezea katika maneno yake ya mwi-sho kwa familia yake. Itawawezesha kushiriki pamoja jinsi kweli hizi zinaweza kuwasaidia kufuata mpango wa Baba kwa ajili ya wokovu wao.

1. Toa kila moja ya vifungu vifuatavyo vya maandiko kwa mwana-funzi binafsi au majozi: 2 Nefi 1:16–20; 2 Nefi 2:6–10; 2 Nefi 2:19–20, 22–25; and 2 Nefi 2:11–13, 27–29. (Ikiwa una wanafunzi wachache kuliko wanne, unaweza kukabiliana na shughuli hii kwa kupatia, wanafunzi zaidi ya kifungu kimoja cha maandiko au kwa kuchagua vifungu vichache vya kujadili.)

2. Wanafunzi wanaposoma vifungu hivi, wawezeshe kujibu maswali yafuatayo katika jarida zao za kujifunza maandiko. (Unaweza kufikiria kuandika maswali ubaoni.)

a. Ni kweli zipi za kimsingi ambazo Lehi alifundisha?b. Kwa nini kweli hizi ni muhimu kwa maslahi yetu ya milele? 3. Baada ya kuwapa wanafunzi muda wa kukamilisha kazi zao,

alika kila mwanafunzi au jozi kuripoti kile wamegundua. Wa-himize wanafunzi wengi iwezekanavyo kushiriki kile wamegu-ndua na kwa nini kilikuwa cha maana kwao.

Baada ya shughuli, andika ukweli ufuatao ubaoni: Kuanguka kwa Adamu na Hawa ni sehemu muhimu ya mpango wa Baba wa Mbinguni wa furaha.

Elezea taarifa ifuatayo ya Rais Joseph Fielding Smith:

“Adamu alifanya tu kile ambacho alipaswa kufanya. Alishiriki tunda hilo kwa sababu moja nzuri, na hiyo ilikuwa ni kufungua mlango ili kukuleta wewe na mimi na kila mtu mwingine katika dunia hii. . . .

Page 105: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

90

MafUnzo ya MaSoMo ya nyUMbani

“. . . Kama isingekuwa kwa ajili ya Adamu, mimi singekuwa hapa; wewe hungekuwa hapa; tungekuwa tunasubiri katika mbingu kama roho” (in Conference Report, Oct. 1967, 121–22).

Waulize wanafunzi maswali yafuatayo:

• Je, ni gani baadhi ya matokeo ya Kuanguka ambayo Lehi alieleza katika 2 Nefi 2:21–24?

• Jinsi gani madhara haya yanaifanya kuwa vigumu kuendelea kulingana na mpango wa Baba wa Mbinguni kwa ajili ya wokovu wetu?

Ongeza ukweli zifuatazo kwa bodi: Kupitia Upatanisho, Yesu Kristo anatukomboa sisi kutokana na Anguko na anatoa ukombozi kutokana na dhambi zetu.

Ili kuwasaidia wanafunzi kupata uelewa zaidi wa ukweli huu, weka mwanafunzi kusoma kwa sauti taarifa ifuatayo ya Mzee Joseph B. Wirthlin wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili:

“Upatanisho wa Kristo Yesu, tendo la upendo msafi, ulishinda madhara ya Kuanguka na kutoa njia kwa wanadamu wote kurudi katika uwepo wa Mungu. Kama sehemu ya Upatanisho, Mwokozi alishinda kifo cha mwili na kuleta maisha ya kutokufa kwa kila mmoja wa watoto wa Mungu kupitia Ufufuko. Pia Yeye alishinda mauti ya kiroho na kuleta uwezekano wa uzima wa milele, maisha ambayo Mungu anaishi na zawadi kuu kuliko za-wadi zote za Mungu” (“Christians in Belief and Action,” Ensign, Nov. 1996, 71).

Waulize wanafunzi: Ni zipi baadhi ya baraka za Upatanisho?

Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa umuhimu wa wakala katika mpango wa Baba wa Mbinguni, soma taarifa ifuatayo ya Mzee Neal A. Maxwell wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili:

“Bila ya kuwepo kwa chaguzi, bila ya uhuru wetu wa kuchagua na bila upinzani, hakutakuwa na kuwepo halisi. . . . Ni ukweli kwamba hatuwezi kukua kiroho wala hatimaye kuwa na furaha ya kweli labda na hadi tutakapo tumia kwa hekima haki yetu ya kujiamulia” (One More Strain of Praise [1999], 80).

Andika kanuni zifuatazo kwenye ubaoi. Tuko huru kuchagua uhuru na uzima wa milele au kufungwa, na kifo.

Wezesha wanafunzi kugeukia zoezi 4 ya siku 3 katika majarida ya masomo ya maandiko yao. Alika wachache wao kueleza kile wamejifunza kuhusu wakala kutoka 2 Nefi 2:26–29.

Soma kwa sauti kauli ifuatayo ya Nabii Joseph Smith:

“Ili kupata wokovu ni lazima siyo tu kufanya mambo mengine, bali kila kitu ambacho Mungu aliamuru”

Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa umuhimu wa utii, unaweza kuuliza maswali yafuatayo:

• Kwa nini unafikiri Lehi alisisitiza utiifu katika ushauri wake wa mwisho kwa familia yake kabla ya kufa?

• Ni uzoefu gani umekuwa nao ambao umekusaidia kujua kwamba Bwana hutubariki tunaposhika sheria Yake, na kuzuia baraka wakati hatutii amri zake? (Ongeza ukweli huu katika orodha kwenye ubao.)

Ili kuhitimisha somo hili, soma kauli ifuatayo ya Rais Boyd K. Packer, Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili:

“Utii ni dawa yenye nguvu ya kiroho. Hukaribia kuwa tiba kwa yote”(“Balm of Gilead,” Ensign, Nov. 1987, 18).

Shiriki ushuhuda wako wa upendo wa Mungu kwa ajili ya wana-funzi wako na upendo Wake wa kuwasaidia kushinda madhara ya Kuanguka na kupokea uzima wa milele.

Kitengo Kifuatacho (2 Nefi 4–10)Baada ya Lehi kufa, Lamani na Lemueli walitaka tena kuchukua maisha ya Nefi. Ni onyo gani ambalo Bwana alitoa liliokoa mai-sha ya Nefi? Pia, ni nini kingetokea kwa miili yetu na roho ikiwa hapangekuwa na Upatanisho? Wanafunzi watapata majibu kwa swali hili katika 2 Nefi 9:7–9.

Page 106: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

91

UtanguliziBaada ya kifo cha Lehi, Lamani na Lemueli walimkasi-rikia Nefi “kwa sababu walirudiwa na Bwana” kama vile Nefi alivyokuwa amewaambia (ona 2 Nefi 4:13–14). Akisumbuliwa na mitazamo ya ndugu zake na mate-ndo na kwa udhaifu wake mwenyewe na dhambi, Nefi

aliandika hisia zake kwa lugha ya uwazi na ushairi. Ali-elezea upendo wake kwa maandiko na shukrani yake kwa ajili ya baraka na nguvu alizopokea kutoka kwa Bwana (ona 2 Nefi 4:15–35).

SOMO 26

2 nefi 4

Mapendekezo ya kufundisha

2 Nefi 4:1–11Lehi anashauri na kubariki familia yakeKabla ya darasa kuanza, andika swali hili ubaoni:

Kama ungekuwa mzazi mkuu mwaminifu na watoto wako walikuwa hawaishi kulingana na kanuni za injili, ni shauri gani ungewapa wajukuu wako?

Anza darasa kwa kualika wanafunzi kujibu swali ubaoni. Baada ya wanafunzi kujibu, uliza:• Ni majukumu gani ambayo wazazi na mababu wanayo katika kufundisha na kushauri

watoto wao na wajukuu?Kama sehemu ya mjadala huu, unaweza kutaka kusoma au kuuliza mwanafunzi kusoma maelezo yafuatayo:“Wazazi wanajukumu takatifu wa kulea watoto wao katika upendo na utakatifu, kukimu mahitaji yao ya kimwili na kiroho, na kuwafundisha kupenda na kutumikiana mmoja na mwingine, kutii amri za Mungu, na kuwa wananchi wenye kutii sheria popote wanapoishi. Waume na wake—akina mama na kina baba—watapasishwa mbele ya Mungu kwa utimi-zaji wa majukumu haya. . . . Familia za ukoo lazima zipeane msaada panapohitajika”(“The Family: A Proclamation to the World,” Ensign, Nov. 2010, 129).Anzisha 2 Nefi 4 kwa kuelezea kwamba kabla ya Lehi kufa, alishauri uzao wake kutii amri. Alika wanafunzi kusoma 2 Nefi 4:3–11, ili kutambua watu ambao Lehi alifundisha na ushauri aliowapa.• Ni nani ambaye Lehi alimfundisha? (Ona 2 Nefi 4:3, 8, 10–11.)• Ni ahadi gani ambayo Lehi aliwapa watoto wa Lamani na Lemueli? (Ona 2 Nefi 4:7, 9.)• Kulingana na 2 Nefi 4:5, ni nini unachoweza kusema ni wajibu ambao Bwana amewapa

wazazi? (Wanafunzi wanaweza kutumia maneno tofauti ili kujibu swali hili, lakini haki-kisha wameelewa kwamba wazazi wana wajibu waliopewa na Mungu wa kuwafu-ndisha watoto wao injili.

• Je, ni kweli zipi umejifunza kutoka kwa wazazi wako au mababu?Wahimize wanafunzi kuweza kuwa miungo vya nguvu katika minyororo ya familia zao —ili kuishi injili na kujiandaa kuwa wazazi wema. Unaweza kuonyesha bango lenye jina la“Be a Strong Link” (see http://lds.org/liahona/2003/09/poster?lang=eng).

2 Nefi 4:12–35Nefi anatambua udhaifu wake na kuonyesha imani yake katika BwanaKwenye ubao, andika Moyo wangu unafurahia . . .Waulizie wanafunzi kuandika kishazi hiki katika shajara zao za kujifunza maandiko au daftari za darasa na kumalizia kauli, wakiorodhesha mambo ambayo yanafurahisha mioyo yao.Uliza mwanafunzi kusoma 2 Nefi 4:15–16 kwa sauti ili kujifunza jinsi Nefi alivyomaliza kishazi hiki.

Kuandika ubaoniDondoo linalocho-chea mawazo au swali kwenye ubao linaweza kuwasaidia wanafunzi kufurahia katika somo na kudumisha nadhari yao. Unaweza pia ku-pata kuwa kuna msaada kuweka nyenzo za somo kama vile marejeo ya maandiko, chati, na michoro kwenye ubao. Kulingana na urefu na matumizi ya kifaa, una-weza kutaka kukiweka kwenye ubao kabla ya darasa kuanza. Hii ina-weza kukusaidia kuokoa muda wakati wa darasa na kuepuka usumbufu usio wa lazima.

Page 107: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

92

SoMo 26

• Je, ni baadhi ya mambo gani tunayoweza kufanya kama nafsi zetu zinafurahia katika maandiko?

• Ina maanisha nini kwako kufurahia katika mambo ya Bwana?• Nefi alisema kuwa moyo wake unatafakari mambo ambayo aliona na kusikia. Hii ina

maana gani kwako?Elezea kwamba Nefi aliona furaha kubwa katika maisha yake. Hata hivyo, pia alikumbana na matatizo. Wezesha wanafunzi kusoma 2 Nefi 4:12–13 kimya kimya ili kuona baadhi ya changamoto ambazo Nefi aliona wakati huu katika maisha yake. (Kifo cha Lehi na hasira ya Lamani, Lemueli, na wana wa Ishmaeli.)Mengi ya majaribio ya Nefi yalitokana na vitendo na tabia ya ndugu zake wakubwa. Lakini Nefi pia aliona huzuni kwa sababu ya udhaifu wake mwenyewe. Andika kwenye ubao Moyo wangu unahuzunishwa kwa sababu . . .Waalike wanafunzi kusoma 2 Nefi 4:17–18 na kupata sababu za Nefi kuhuzunishwa.Wakati wanafunzi wamepata muda wa kusoma mistari hii, waulize kile walichopata. Ele-keza nadhari yao kwa maneno mwovu, mwili, na kunasa katika mistari hii. Eleza kwamba neno mwovu linamaanisha ya kuhuzunika au yenye ubora wa hali ya chini. Katika maa-ndiko, neno mwili mara nyingi inahusu udhaifu tulionao kwa sababu tunaishi katika hali ya kuanguka. Neno kunasa linamaanisha kuzingira au kufinya kutoka pande zote.• Je, ni baadhi ya mifano gani ya matatizo ambayo yanaweza kutunasa? (Majibu yanaweza

kujumuisha matatizo ya nyumbani, shinikizo la rika, kazi ngumu ya shule, na majaribu.)Wawezeshe wanafunzi kusoma 2 Nefi 4:19. Unaweza kutaka kuwahimiza wanafunzi kuweka alama kwenye taarifa “Walakini, ninajua ninayemwamini.” Elezea kwamba katika 2 Nefi 4:19, maneno ya Nefi yanabadilika kutoka kwa huzuni na kuwa matumaini.• Unafikiri Nefi alimaanisha nini aliposema “Ninajua ninayemwamini.”?• Kumkumbuka Bwana na wema Wake kunawezaje kutusaidia wakati wa kufa moyo?Soma 2 Nefi 4:20–25 kwa sauti. Waulize wanafunzi kufuata pamoja katika maandiko yao. Waalike kutazama maneno na vishazi vinavyoonyesha kwamba Mungu huwasaidia wale wanaoweka matumaini yao kwake.• Ni maneno au vishazi vipi katika 2 Nefi 4:20–25 unavyoweza kupata yenye maana?

Kwa nini?”• Fikiria juu ya wakati ambapo Bwana alikusaidia au kukunusuru wakati wa ugumu. Ali-

kusaidia kwa jinsi gani? Ni vipi uzoefu huo umekuvutia?Inaweza kusaidia kuwapa wanafunzi muda wa kufikiri kuhusu uzoefu huo na kuurekodi katika shajara zao za kujifunza maandiko. Wanafunzi wanaweza pia kufaidika ukieleza kuhusu wakati ambapo Mungu alikusaidia au kukuendeleza.Wasaidie wanafunzi kuelewa kwamba uwezo wa Nefi wa kukumbuka na kufahamu kile Bwana amemfanyia katika siku za zilizopita kulimpatia matumaini na kumhimiza kuwa bora zaidi. Waalike wanafunzi kusoma 2 Nefi 4:26–30 kimoyomoyo, wakitafuta jinsi uzoefu wa Nefi ulivyoathiri hamu yake ya kuwa mwenye haki. Waulize wanafunzi wachache ku-shiriki kile wamegundua.Waulize wanafunzi wachache kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka 2 Nefi 4:30–35. Kama darasa, tambua ahadi ambazo Nefi alifanya kwa Bwana na baraka aliyoomba.• Tunaweza kujifunza nini kutokana na ombi hili ambacho kinaweza kutusaidia katika

maombi yetu binafsi? (Wanafunzi wanaweza kutumia maneno tofauti kwa kujibu swali hili, lakini hakikisha wameelewa kwamba sala ya dhati inaweza kuimarisha dhamira yetu ya kushinda dhambi na maudhiko.)

Waalike wanafunzi kufikiria kuhusu wakati ambapo maombi yaliwasaidia kushinda dhambi au maudhiko. Unaweza kutaka kupendekeza kwamba washiriki uzoefu wao au kuuandika katika jarida zao ya masomo ya maandiko.Wape wanafunzi muda wa kuangalia kifungu katika 2 Nefi 4 ambacho kinaonyesha shauku waliyo nayo. Baada ya muda wa kutosha, soma kauli ifuatayo ya Mzee David A. Bednar wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili juu ya vile maombi yanaweza kuendeleza ukuaji wa kiroho:“Yawezekana kuwa kuna vitu katika hulka zetu, katika tabia zetu, au kuhusu ukuaji wetu wa kiroho ambavyo tunahitaji kushauriana na Baba yetu wa Mbinguni katika sala ya asubuhi. Baada ya kuonyesha shukrani ipasavyo kwa baraka zilizopokelewa, tunasihi kwa

Kusoma maandiko kwa sautiMara kwa mara, soma vifungu vya maandiko kwa sauti kwa wana-funzi wako. Hii inatoa nafasi kwao kusikia na kuhisi upendo wako kwa maandiko, na inaweza kuwahamasisha kusoma maandiko wao wenyewe. Inaweza pia kutoa fursa ya kuhakikisha kuwa hatua fulani, kweli, au matumizi yamesisitizwa. Wanafunzi pia wana-faidika kutokana na kusoma maandiko kwa sauti kwa mtu mwingine na hata katika masomo yao binafsi.

Page 108: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

93

2 nefi 4

ajili ya kuelewa mwelekeo, na usaidizi wa kufanya mambo ambayo hatuwezi kufanya kwa nguvu zetu wenyewe. Kwa mfano, tunapoomba, tunaweza:“• Kutafakari juu ya nyakati zile, tulipoongea vibaya au visivyo kwa wale tunaowapenda zaidi.“• Kutambua kwamba tunajua bora zaidi kuliko haya, lakini daima hatutendi kulingana na kile tunajua.“• Kuonyesha majuto kwa udhaifu wetu na kwa kutokuweka mbali mtu wa asili kwa bidii zaidi.“• Kuamua kupangilia maisha yetu kwa mfano wa Mwokozi kikamilifu zaidi.“• Kusihi kwa uwezo mkubwa ili kufanya na kuwa bora zaidi”(“Pray Always,” Ensign or Liahona, Nov. 2008, 41).Kamilisha kwa kurejea katika vishazi ulivyoandika kwenye ubao mapema katika somo (“Moyo wangu unafurahia . . .” na “Moyo wangu unahuzunishwa kwa sababu . . .”). Dhi-hirisha ujasiri wako kwamba hata tukipitia hali ngumu, tutapata furaha na amani tunapo-tafuta msaada wa Bwana.

Ukaguzi wa Umahiri wa MaandikoFahamu: Urefu wa somo hili unaweza kuruhusu muda kwa shughuli ifuatayo ya ukaguzi wa maandiko. Unaweza kufanya shughuli mwanzoni mwa darasa, kama mapumziko kati-kati mwa sehemu ya somo, au katika mwisho wa darasa. Hakikisha umelifanya kuwa fupi ili kuruhusu muda kwa ajili ya somo. Kwa shughuli nyingine ya ukaguzi, angalia kiambati-sho mwishoni mwa mwongozo huu.Maswali yanaweza kuwasaidia wanafunzi kukumbuka yale waliyojifunza na kupima kujifunza kwao. Chagua vifungu vichache vipya vya umahiri wa maandiko, na waalike wanafunzi kusoma na kutia alama katika maandiko yao. Kisha wape maswali ya maneno kwa vifungu hivyo na vifungu vingine vya umahiri wa maandiko walivyojifunza. Kwa kila kifungu, soma neno muhimu au kipengele kutoka katika alamisho la kitabu cha seminari. Kisha waulize wanafunzi kupata kifungu sahihi katika maandiko yao.

Tangazona Habari za usuli2 Nefi 4:16–35. Kushinda dhambi na udhaifu wetuTunapojifunza ombi la dhati la Nefi kwa Bwana kumsa-idia kushinda dhambi zake na udhaifu, tunaona kwa-mba tunaweza kwenda kwa Bwana kwa msaada sawa na huo. Maneno ya Nefi yanarejewa katika maneno ya manabii wa siku za mwisho.

Nabii Joseph Smith alifundisha;

“Kadri mtu anavyokaribia ukamilifu, ndivyo maoni yake yanavyokuwa wazi, na ndivyo starehe zake zinakuwa kubwa, hadi atakaposhinda maovu ya maisha yake na kupoteza kila tamaa ya dhambi” (Teachings of Presi-dents of the Church: Joseph Smith [2007], 210–11).

Mzee Richard G. Scott wa Akidi ya Mitume Kumi na Wa-wili alishuhudia juu ya baraka tunazopokea tunapotubu:

“Kwa nini Baba yetu na Mwanawe wametuamuru kutubu? Kwa sababu wanatupenda. Wanajua sote tuta-kiuka sheria za milele. Kama ni kidogo au kubwa, haki inahitaji ya kwamba kila sheria iliovunjwa kuridhishwa ili kuhifadhi ahadi ya furaha katika maisha haya na

fursa ya kurudi kwa Baba wa Mbinguni. Kama haija-ridhishwa, katika Siku ya Hukumu haki itasababisha kuwa tutupwe nje ya uwepo wa Mungu kuwa chini ya udhibiti wa Shetani [ona 2 Nefi 9:8–10; 2 Nefi 2:5].

“Ni Bwana wetu na tendo Lake la ukombozi linalo-tuwezesha kuepuka hukumu hiyo. Inafanyika kupitia imani katika Yesu Kristo, utiifu kwa amri Zake, na kudumu katika haki hadi mwisho.

“Je, unachukua ufanisi kamili wa nguvu za ukombozi wa toba katika maisha yako ili uweze kuwa na amani zaidi na furaha? Hisia za mtikisiko na huzuni mara nyi-ngi huashiria haja ya kutubu. Pia ukosefu wa mwelekeo wa kiroho unaotafuta katika maisha yako unaweza ku-tokana na sheria zilizovunjwa. Kama inahitajika, toba kamili itaweka maisha yako pamoja. Itatatua maumivu yote tata ya kiroho yanayotoka kwa dhambi. Lakini ka-tika maisha haya haiwezi kukabiliana na baadhi ya ma-dhara ya kimwili ambayo yanaweza kutokea kutokana na dhambi kubwa. Uwe na hekima na uishi vizuri kila mara kwa mipaka ya haki ilivyoelezwa na Bwana”(“The Path to Peace and Joy,” Ensign, Nov. 2000, 25).

Page 109: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

94

UtanguliziAkitii onyo kutoka kwa Bwana, Nefi na wafuasi wake walijitenga na Lamani, Lemueli, na wana wa Ishmaeli.

Waliishi katika haki na furaha, wakati wafuasi wa La-mani na Lemueli walijiweka mbali na Bwana.

Mapendekezo ya Kufundisha

2 Nefi 5:1–8Bwana hutenganisha wafuasi wa Nefi kutoka kwa wafuasi wa Lamani na LemueliAlika wanafunzi kutafakari baadhi ya matatizo magumu na maamuzi yanayowakabili. Wa-himize kuweka changamoto hizi za kibinafsi akilini wanapojifunza jinsi Nefi alivyozipokea changamoto. Wakumbushe kuwa wakati Lehi alipokufa, Nefi alibakia kuwa kiongozi wa kiroho wa familia. Waulize wanafunzi kusoma 2 Nefi 5:1–4 kimya kimya ili kuona changa-moto ambayo Nefi alikabiliana nayo.• Kulingana na 2 Nefi 5:1, ni nini ambacho Nefi alifanya ili kusaidia kujua suluhu kwa

changamoto yake?• Hata baada ya Nefi kuomba msaada, Lamani na Lemueli walitafuta kufanya nini?Wanafunzi wanaporipoti majibu yao, unaweza kutaka kueleza kwamba maombi yetu haya-wezi kujibiwa kila wakati mara moja au kwa njia tunatamani.Alika mwanafunzi kusoma 2 Nefi 5:5–8 kwa sauti. Uliza darasa kufuata pamoja, wakitafuta kile Bwana alifanya ili kusaidia Nefi na wafuasi wake.Waulize wanafunzi kufupisha yale waliyojifunza kutoka 2 Nefi 5:1–8. Kweli moja unayo-weza kusisitiza ni kwamba Bwana huwaongoza wale wanaomfuata kwa uaminifu katika maombi. Kuhusiana na mistari hii, uliza maswali yafuatayo:• Kwa nini ni muhimu kuendelea kuwa mwaaminifu wakati maombi yetu hayajajibiwa

mara moja au kwa njia tunatamani?• Kwa njia gani ambapo Bwana anaweza kutupa tahadhari?Wanafunzi wanapojibu swali hili, fikiri kusoma taarifa ifuatayo na Rais Boyd K. Packer wa Akidi ya Mitume kumina Wawili:“Hatuwezi kuanza kwa mwendo mbaya bila kwanza kwa kuepuka onyo” (quoted in Ken-neth Johnson, “Yielding to the Enticings of the Holy Spirit,” Ensign, Nov. 2002, 90).• Kwa njia gani tunaweza kufuata mfano wa Nefi tunapokabiliwa na changamoto?Kama sehemu ya majadiliano ya wanafunzi ya 2 Nefi 5:1–8, elezea kuwa mgawanyiko wa Wanefi kutoka kwa Walamani ulikuwa ni kwa ajili ya chuki ya Lamani na Lemueli kwa Nefi. Mgawanyiko huu uliendelea kwa karne, na kwa uzao wa Lamani na Lemueli waki-wafundisha watoto wao kuchukia uzao wa Nefi (ona Mosia 10:12–17).

2 Nefi 5:9–18, 26–27Wanefi waliishi kwa furahaWaelekeze wanafunzi katika kusoma 2 Nefi 5:27 kwa sauti kwa pamoja. Unaweza kutaka ku-shauri kwamba wanafunzi watie alama kwenye mstari huu. Andika neno furaha kwenye ubao.• Unafikiri inamaanisha nini kuishi “kwa furaha”?Uliza mwanafunzi kusoma kwa sauti taarifa ifuatayo na Mzee Marlin K. Jensen wa Wale Sabini:“Baadhi ya kanuni zisizobadilika na kweli huleta furaha kwa maisha yetu. Mada hii ime-kuwa ya kuvutia kwangu kwa miaka mingi kwa sababu ingawa mimi nimebarikiwa sana na nina kila sababu ya kuwa na furaha, wakati mwingine mimi hupambana na kila mara

Waite wanafunzi kwa jinaUnapomwomba mwana-funzi kusoma au kushi-riki katika majadiliano, mwite kwa jina. Hii ita-saidia kukuza mazingira ya kujifunza ya upendo na heshima.

SOMO 27

2 nefi 5

Page 110: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

95

2 nefi 5

sina upendeleo asili kwa furaha na moyo mkunjufu ambayo baadhi ya watu wanaonekana kufurahia.

“Kwa sababu hiyo, miaka kadhaa iliyopita kifungu cha Kitabu cha Mormoni kilishika mawazo yangu. . . . Nefi alianzisha jamii iliyojengwa juu ya kweli za injili; na kuhusu jamii hiyo alisema, ‘Na ikawa kwamba tuliishi kwa furaha’ (2 Ne. 5:27). Kifungu hicho kilinivutia sana. . . . Nilishangazwa . . . kile chembe muhimu cha jamii yenye furaha halisi na maisha kinaweza kuwa, na nikaanza kutafuta maandiko ya Nefi kwa vidokezo. Mimi . . . nawaalika ku-

fanya utafiti wenu wa binafsi. Inaweza kuwa harakati ya maisha yote na yenye thamani. . . .“. . . Mwelekeo huo huo na mambo ya maisha ya kila siku yaliyowezesha Nefi na watu wake kuwa na furaha miaka 560 kabla ya Kristo hutumika vivyo hivyo leo” (“Living after the Manner of Happiness,” Ensign, Dec. 2002, 56, 61).Wahimize wanafunzi kukubali mwaliko wa Mzee Jensen. Waulize kusoma 2 Nefi 5: 6, 10–18, 26–27 kimya kimya, wakitafuta “mambo ya jamii yenye furaha ya kweli na uzima.” Unaweza kutaka kupendekeza kwamba watie alama kanuni ambazo zilichangia kwa fu-raha ya Wanefi. Baada ya dakika chache, alika wanafunzi wachache kuandika matokeo yao ubaoni. (Majibu yanaweza kujumuisha kwamba Nefi na wafuasi wake walienda na familia zao [ona mstari wa 6]; walitii Bwana [ona mstari wa 10]; walifanya kazi kwa bidii ili kujisai-dia wenyewe [ona mistari ya 11, 15 –17], walichukua maandiko pamoja nao [ona mstari wa 12]; walijenga hekalu [ona mstari wa 16];. na wakafuata haki [ona mistari ya 18, 26])Alika wanafunzi kuchagua moja au mbili ya kanuni kwenye ubao na kushiriki jinsi kanuni hizo, zimewasaidia “kuishi kwa furaha.”Kulingana na kile wanafunzi wanasisitiza, unaweza kutaka kufuatilia kwa maswali kadhaa kama haya yafuatayo:• Kulingana na 2 Nefi 5:10–11, 16, ni baraka gani watu walipokea kwa sababu ya kutii amri

za Bwana? Ni wakati gani umehisi kwamba Bwana amekuwa na wewe? Ni jinsi gani ushawishi Bwana umechangia katika furaha yako?

• Ni Jinsi gani hekalu linaweza kuwa limewasaidia watu “kuishi kwa furaha”? Ni jinsi gani hekalu limeleta furaha kubwa kwako au kwa mtu unayemjua?

• Ni kwa njia gani kazi ngumu huchangia kwa furaha?Waalike wanafunzi kufupisha yale waliyojifunza kuhusu jinsi ya kuongeza furaha yao. Ingawa wanafunzi wanaweza kushiriki kanuni mbalimbali, hakikisha wanaelewa kwamba kama vile injili ya Yesu Kristo inakuwa njia yetu ya maisha yetu, tunaongezeka katika furaha. Unaweza kuandika kanuni hii ubaoni.Alika wanafunzi kuchunguza maisha yao na kuamua kitu watakachofanya ili kuishi kikamilifu zaidi “kwa furaha.” Wahimize kuandika hatua hii katika jarida zao ya masomo ya maandiko au daftari za darasa. Toa ushuhuda wako juu ya kanuni na desturi ambazo zimesababisha furaha katika maisha yako.

2 Nefi 5:19–25Walamani walilaaniwa kwa sababu ya kutotii kwaoWaalike wanafunzi kusoma 2 Nefi 5:19–24 Kimoyomoyo, wakiangalia kwa tofauti kati ya njia ya kuishi kwa Walamani na njia kuishi kwa Wanefi.• Kulingana na 2 Nefi 5:20, ni nini ilikuwa matokeo ya uasi wa Walamani’?Hakikisha wanafunzi wanaelewa kwamba laana iliyotajwa katika sura hii ilikuwa ni utengano kutoka kwa Mungu. Kubadilika kwa ngozi yao ilikuwa tu alama au ishara ya laana. Ili kufafa-nua hatua hii, wezesha mwanafunzi kusoma kauli ifuatayo ya Rais Joseph Fielding Smith:

“Ngozi nyeusi iliwekwa juu ya Walamani ili waweze kutofautishwa na Wanefi na kuzuia watu hao wawili kuchanganyika. Ngozi nyeusi ilikuwa ni ishara ya laana. Laana ilikuwa ni uondoaji wa Roho wa Bwana. . . .“Ngozi nyeusi ya wale ambao wameingia Kanisa haipaswi tena kuchukuliwa kama ishara ya laana. Wengi waongofu ni wa kupendeza na wana Roho ya Bwana “(Answers to Gospel Questions, comp. Joseph Fielding Smith Jr.,

5 vols. [1957–66], 3:122–23).

Kueleza mawazo na hisiaWakati vijana wanapo-toa mawazo na hisia zao juu ya kanuni za injili, wanaalika Roho Mtaka-tifu kuzidisha ufahamu wao na kuimarisha shuhuda zao. Unaweza kusaidia hilo kufanyika katika darasa kwa kuwahimiza wanafunzi kueleza kanuni za injili kwa maneno yao we-nyewe. Unaweza pia ku-wakaribisha wanafunzi kushiriki uzoefu muhimu na sahihi na kushuhudia juu ya kile waliyoweza kujua kwa sababu ya uzoefu huu.

Page 111: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

96

SoMo 27

• Jinsi gani 2 Nefi 5:21 inakusaidia kuelewa kwa nini Walamani walitengwa kutoka kwa Bwana? (Unaweza kueleza kwamba gumegume ni jiwe ngumu. Katika kusema kwamba Walamani “walikuwa kama gumegume,” Nefi alielezea ugumu wa mioyo ya Walamani’.)

• Ni onyo gani Bwana alitoa kuhusu Wanefi kwa kuoa Walamani ambao walikataa injili? (Ona 2 Nefi 5:23.)

• Kwa nini ni muhimu kuepuka kutongoza na kuoa wale wasiomsikia Bwana? Unafikirije watu unaotongoza na hatimaye kuowa watabadili juhudi zako za kuishi injili? (Inaweza kusaidia kuwakumbusha wanafunzi kuwa Urais wa Kwanza umeshauri, “Chagua ku-tongoza wale tu ambao wana viwango vya juu vya maadili na ambao kwa ushirika wao unaweza kudumisha viwango vyako” [For the Strength of Youth (booklet, 2011), 4].)

• Je, ni baadhi ya kanuni gani tunayoweza kujifunza kutoka 2 Nefi 5:20–24? (Wanafunzi wanaposhiriki kanuni, hakikisha kwamba wanaelewa kuwa wakati watu wanapoga-ndamiza mioyo yao dhidi ya Bwana, wanajitenga wenyewe kutoka Kwake.)

Sisitiza kwamba 2 Nefi 5 inatoa tofauti kubwa kati ya Wanefi na Walamani. Tunaweza kuchagua mfano wa kufuata. Wahimize wanafunzi kukumbuka kile wameamua kufanya ili kuishi kikamilifu zaidi “kwa furaha.” Dhihirisha matumaini yako kwamba wanaweza kufuata mfano wa Wanefi na kuwa na furaha ya kweli.

Tangazo na Habari za usuli2 Nefi 5:16. “Na mimi, Nefi, nilijenga hekalu”Mzee Marlin K. Jensen Wa Wale Sabini alielezea jinsi kuhudhuria hekalu kunaelekeza kwa furaha:

“Nefi anaandika, ‘Na mimi, Nefi, nilijenga hekalu’ (2 Ne. 5:16). Hekalu la Nefi linaweza kuwa tofauti kwa njia fulani na mahekalu yetu ya siku za mwisho, lakini lengo lake kuu lilikuwa ni sawa: kuwafundisha na kuelekeza watoto wa Mungu juu ya mpango Wake kwa ajili ya furaha yao na kutoa maagizo na maagano muhimu kwa utimizaji wa furaha hiyo.

“Baada ya kuishi katika dunia hii nzuri kwa zaidi ya mi-ongo mitano, naweza kusema kwa uaminifu kwamba

watu wengi waliokomaa kiroho na wenye furaha nina-owajua ni wapenzi wa kwenda hekaluni. Kuna sababu nzuri ya hilo. Ni katika hekalu ambapo mpango kamili wa Mungu kwetu huelezwa na kurudiwa tena, kila kueleza kukileta ufahamu mkubwa na ahadi ya kuishi maisha kwa njia Yake. . . .

“Mtihani mzuri wa jinsi tunavyofanya katika harakati zetu za kuja kwa Kristo inaweza kuwa jinsi tunahisi kuhusu hekalu na uzoefu wetu huko. Hekalu linaweza kufanana na furaha na shangwe. Ilikuwa hivyo kwa Nefi na watu wake” (“Kuishi kwa Furaha,” Ensign, Dec. 2002, 60).

Page 112: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

97

UtanguliziWakati Nefi aliporekodi huduma ya watu wake, aliju-muisha mahubiri ya siku mbili na ndugu yake, Yakobo. Mahubiri yanapatikana katika 2 Nefi 6–10, na hili ni somo la kwanza kati ya masomo yake matatu. Katika

mwanzo wa mahubiri, Yakobo anasoma unabii wa Isaya kuhusu kutawanyika na kukusanyika wa Israeli, ukio-nyesha kwamba “Bwana Mungu atatimiza maagano yake aliyoagana na watoto Wake (2 Nefi 6:12).

Mapendekezo ya Kufundisha

2 Nefi 6Yakobo anashuhudia kwamba Bwana atawakumbuka watu Wake wa agano.Ili kuwasaidia wanafunzi kuona kwamba mafundisho ya Yakobo yanahusiana na maisha yao, waombe kutafakari jinsi ambavyo wangefanya kama rafiki au mwanafamilia angewa-tendea vibaya, kukataa kuamini maneno waliyosema, au kuonyesha kwa njia ya matendo yao au tabia ya kuwa uhusiano haukuwa tena muhimu kwao.Waagize wanafunzi kutafakari swali lifuatalo:• Je, umewahi kuonyesha vitendo au mitazamo sawa na hiyo kwa Bwana?Eleza kwamba katika 2 Nefi 6–8, tunaona jinsi Bwana anawajibu wale ambao wamekimbia kutoka kwake. Sura hizi zina rekodi ya Nefi ya sehemu ya mahubiri ya ndugu yake Yakobo. Mahubiri yaliyosalia ya Yakobo yameandikwa katika 2 Nefi 9–10. Sura hizi zitapitiwa katika masomo mawili yajayo.Alika mwanafunzi kusoma 2 Nefi 6:3–4 and 9:1, 3 kwa sauti. Uliza darasa kubaini sababu ya kwa nini Yakobo alitoa mahubiri.Alika mwanafunzi kuigiza kama mwandishi. Mwulize aandike mada Hotuba ya Yakobo kwenye ubao. Kisha waulize wanafunzi waelezee kile wamejifunza katika mistari ambayo imesomwa. Wezesha mwandishi kuandika majibu yao chini ya kichwa cha habari. Wasaidie wanafunzi kuona kwamba Yakobo alifundisha watu wake kwa ajili ya “masilahi ya nafsi [zao]” (2 Nefi 6:3). Alitaka kuwasaidia “kulitukuza jina la Mungu [wao]” (2 Nefi 6:4), “ku-fahamu kuhusu yale maagano ya Bwana” (2 Nefi 9:1), na “washangilie na wainue vichwa [vyao] juu milele” (2 Nefi 9:3). Hakikisha kwamba madhumuni haya yamejumuishwa katika orodha ya wanafunzi. Shauri kwamba wanafunzi wanaposoma mahubiri ya Yakobo, wanaweza kuangalia mafundisho yanayosaidia kutimiza madhumuni haya.Nakili kipindi kifuatacho kwenye ubao. (Unaweza kutaka kukinakili kabla ya darasa kua-nza.) Alika mwanafunzi kusoma 2 Nefi 6:4. Onyesha kwamba Yakobo alianza hotuba yake kwa kusema kwamba alikuwa anaenda kuzungumza kuhusu hali ilivyokuwa katika siku zake itakavyokuwa katika siku za baadaye (“vitu vilivyo, na vile vitakavyokuja ambavyo ni").

Onyesha namba 1 kwenye kipindi.

• Katika 2 Nefi 6:8, ni nini Yakobo alisema kilichotokea kwa Wayahudi kule Yerusalemu kwa sababu waligeuka kutoka kwa Bwana? (Wengine waliuawa, wengine walipelekwa utumwani. Unaweza kutaka kuwakumbusha wanafunzi kwamba Lehi, Yeremia, na manabii wengine walitoa unabii kuwa mambo haya yangetokea. Unabii wao ulitimizwa

SOMO 28

2 nefi 6–8

Miaka 600 K.K

Miaka 500 K.K

Miaka 400 K.K

Miaka 300 K.K

Miaka 200 K.K

Miaka 100 K.K

Mwaka 1 b.K

Miaka 100 b.K

1 2 3

Page 113: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

98

SoMo 28

karibu 587 K.K, wakati Wababeli waliteka Yerusalemu na kupeleka Wayahudi wengi utumwani. Ona “Chronology” katika Kamusi ya Biblia kwa tarehe hii na mengine.)

Elekeza katika nambari 2.• Kulingana na sentensi ya kwanza ya 2 Nefi 6:9, ni nini hatimaye kitatokea kwa wazao wa

Wayahudi ambao walipelekwa utumwani katika Babeli? (Watarudi Yerusalemu. Unabii huu ulitimia katika mwaka karibu ya 537 K.K, wakati Mfalme Koreshi alipowaruhusu Wayahudi kurudi katika nchi yao.)

Elekeza kwenye nambari 3, na elezea kwamba Yakobo alitabiri ya kwamba Mwokozi ataishi maisha yake ya dunia miongoni mwa Wayahudi.• Katika 2 Nefi 6:9–10, ni vishazi vipi vinavyoelezea jinsi baadhi ya Wayahudi wangefanya

na kuhisi juu ya Mwokozi wakati wa huduma Yake ya dunia? (Majibu yanaweza kuju-muisha “kumpiga,” “kumsulubisha,” na “kushupaza mioyo yao na kukaza shingo zao dhidi” Yake.)

• Kulingana na 2 Nefi 6:10–11, ni nini kingefanyika kwa Wayahudi watakaomkataa Ma-siya? (Watasumbuka sana mwilini, watatawanywa, kupigwa, na kuchukiwa.)

Alika wanafunzi kusoma kimya kimya 2 Nefi 6:6–7, 11–12, 14, 17. Unaweza kutaka kueleza kwamba katika mistari 6 –7, Yakobo anasoma unabii wa Isaya kuhusu Urejesho wa injili na mkusanyiko wa nyumba ya Israeli. Waulize wanafunzi kutambua vishazi vinavyoeleza jinsi Bwana Atakavyofanya kwa nyumba ya Israeli, watu wa Mungu wa agano, hata kama watamkataa. Waulize wanafunzi kushiriki vishazi walivyogundua. Wasaidie kuelewa maana ya vipengele hivi vichache kwa kuuliza maswali yafuatayo:• Katika 2 Nefi 6:7, unafikiri inamaanisha nini “kumsubiri” Bwana? • Yakobo aliahidi kwamba “Bwana atarehemu” Israeli (2 Nefi 6:11). Katika njia zipi baadhi

ya vishazi ulivyovitambua vinahusu rehema ya Bwana?• Yakobo pia aliahidi kwamba Bwana angeweza “kukomboa” Israeli (2 Nefi 6:14). Unafi-

kiri inamaanisha nini kwa Mwokozi kumkomboa mtu?• Kulingana na 2 Nefi 6:11–12, 14, tunapaswa kufanya nini ili kupokea rehema ya Bwana?Wanafunzi wanapo elezea ufahamu wao, hakikisha kuwa wanatambua kwamba Bwana ni mwenye huruma kwa wale ambao watarejea Kwake.Elezea kwamba katika 2 Nefi 6, Yakobo anaelezea juu ya Bwana kuwa na huruma kwa watu Wake wa agano hata baada ya wao kuwa waovu. Hakikishia wanafunzi kwamba kama Bwana angekuwa na huruma kwa watu hawa, hakika atakuwa na huruma kwetu binafsi tunapokuja Kwake na kutii maagano yetu na Yeye. Alika wanafunzi kutafakari njia ambazo Bwana amekuwa na huruma kwao. Waulize waandike kishazi kifuatacho katika jarida zao ya masomo ya maandiko au daftari za darasa: Najua kuwa Bwana ni mwenye huruma kwa sababu. . . . Kisha waalike kuandika mawazo yao na hisia ili kukamilisha taarifa. Baada ya wao kupata muda wa kutosha wa kuandika, unaweza kuwaalika kueleza kile ambacho wameandika.

2 Nefi 7–8Yakobo anaelezea juu ya unabii wa Isaya juu ya uwezo wa Mwokozi wa kuwako-mboa watu wake wa aganoEleza kwamba katika 2 Nefi 7 and 8, Yakobo anasoma unabii kutoka kwa maandiko ya Isaya. Sura ya 7 ina neno la Bwana kwa washiriki wa nyumba ya Israeli waliotawanyika na kupelekwa utumwani kwa ajili ya dhambi zao. Uliza mwanafunzi kusoma 2 Nefi 7:1. Unaweza kutaka kualika darasa kutia alama maswali ambayo Bwana anauliza.Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa maswali katika mstari wa 1, eleza kwamba vishazi “nimekuweka kando,” “cheti cha talaka cha mama yako,” na “nimekuuza” inahusu wazo la kuvunja au kukata maagano. Wasaidie wanafunzi kuelewa kwamba maswali ya Bwana yanaweza kusemwa upya kama ifuatavyo: “Je, nimeondoka mbali na wewe? Je, nimeweka kando ahadi ambayo tumefanya?”

Kuandika kunaboresha ushirikiUnapoalika wanafunzi kujibu swali kwa kua-ndika kabla ya kuelezea mawazo yao kwa darasa, unawapa muda wa kuunda mawazo yao na kupokea maongozi kutoka kwa Roho Mtaka-tifu. Wanafunzi wana-weza kupendelea kutoa mawazo yao wakiwa wa-meyaandika kwanza, na yale ambayo wameyatoa mara nyingi yatakuwa na maana zaidi.

Page 114: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

99

2 nefi 6 – 8

• Ni nini majibu kwa maswali haya? (Jibu ni hapana. Kamwe Bwana hatatuacha au kusa-hau maagano Aliyoyafanya.).

• Kulingana na mwisho wa 2 Nefi 7:1, kwa nini watu hawa walitengwa kutoka kwa Bwana na kuteseka utumwani? (Kwa sababu walitenda dhambi, na kuondolewa mbali na Bwana.)

Elezea kwamba katika 2 Nefi 7:2, Bwana anauliza swali lingine ambalo linaweza kutusaidia kuona kwamba anataka kutusaidia, na kwamba ana uwezo wa kufanya hivyo. Alika wana-funzi kupata na kuweka alama kwenye swali. (“Je, mkono wangu umefupishwa kwamba siwezi kukomboa, au sina uwezo wa kukomboa?”)Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa swali hili, waulize jinsi wanaweza kusema upya swali hilo kwa maneno yao wenyewe. (Kama wana wakati mgumu wa kuelewa kishazi “je, mkono wangu umefupishwa,” alika mwanafunzi kunyoosha mkono wake kwa mwanafu-nzi mwingine kama kwamba anapeana msaada. Kisha mwulize mwanafunzi wa kwanza “kufupisha” mkono wake, kwa ishara ya wazo la kuondoa msaada au kunyima.) Wanafu-nzi wanaweza kurudia swali la Bwana kwa kusema kitu kama hiki: “Je, Mimi nawanyima au nakataa kuwafikia ili niwakomboe? Je, mnaamini nina uwezo wa kuwaokoa?”Waeleze wanafunzi kwamba kwa majibu kwa swali hili, sura zote za 2 Nefi 7 na 8 zina mifano kadhaa inayoonyesha mapenzi ya Mwokozi ya kuwakomboa watu wake wa agano na mifano inaonyesha kwamba Yeye ana uwezo wa kufanya hivyo.Ili kuwasaidia wanafunzi kugundua ushahidi kwamba Mwokozi anataka kuwakomboa watu Wake wa agano na ana uwezo wa kufanya hivyo, gawanya vifungu sita vifuatavyo vya maandiko kutoka 2 Nefi 8 miongoni mwa vikundi vya wanafunzi: mistari 1–3, 4–6, 7–8, 10–11, 12–13, na 14–16. (Ikiwa una wanafunzi 12 au zaidi katika darasa lako, gawanya vifungu kwa jozi au makundi mengine madogo madogo. Kama una wanafunzi wachache zaidi ya 12, gawanya zaidi ya kifungu kimoja kwa baadhi ya vikundi.) Uliza kila kikundi kutafuta kishazi katika kifungu au vifungu vyao walivyopatiwa ambavyo vinaonyesha mapenzi ya Bwana ya kutukomboa na uwezo Wake wa kufanya hivyo. Baada ya muda wa kutosha, alika kila kikundi kisomee darasa kishazi walichochaguliwa. Waulize kushiriki kile walichojifunza kutokana na kifungu. Unaweza kutaka kualika wanafunzi kutia alama vishazi ambavyo wanafunzi wenzao wanashiriki.Kuhitimisha, rejea orodha ya dhamira za Yakobo iliyoandikwa kwenye ubao. Alika wa-nafunzi kufikiria kuhusu ahadi walizofanya na Bwana, na baraka alizowaahidi wanapotii maagano hayo. Shiriki ushuhuda wako wa uaminifu wa Bwana kwetu na maagano Yake nasi, na shuhudia juu ya huruma na ukombozi tunaoweza kupokea kama sisi ni waaminifu kwa maagano yetu na yeye.

Tangazo na Habari za usuli2 Nefi 6:2. Ni ukuhani gani ulioshikiliwa na Lehi, Nefi, na Yakobo?Yakobo alisema kwamba “aliitwa na Mungu, na kuta-wazwa katika ukuhani wake mtakatifu” na kwamba alikuwa “ametawazwa na kaka [yake] Nefi” (2 Nefi 6:2). Alipozungumza kuhusu “ukuhani mtakatifu,” ali-maanisha Ukuhani wa Melkizedeki. Rais Joseph Fielding Smith aliandika kwamba“Wanefi walihudumu kwa mujibu wa Ukuhani wa Melkizedeki kutoka siku za Lehi mpaka katika siku ya kuonekana kwa Mwokozi wetu kati yao” [1957–66], 1:124).

2 Nefi 8. Mkusanyiko wa siku za mwishoUnabii wa Isaya ulinukuliwa katika 2 Nefi 8 unazungu-mzia mkusanyiko wa siku za mwisho wa Israeli. Mzee

Bruce R. McConkie wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alifundisha juu ya asili ya kiroho ya mkusanyiko huu:

“Ni nini, basi, inahitajika katika mkusanyiko wa Israeli? Mkutano wa Israeli inahusu kuamini na kukubali na kuishi kwa ulinganifu na yote ambayo Bwana aliwahi kutoa kwa watu Wake waliochaguliwa wa kale. Ina-husu kuwa na imani katika Bwana Yesu Kristo, kutubu, kubatizwa na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu, na kushika amri za Mungu. Inahusu kuamini injili, kujiunga na Kanisa, na kuingia katika Ufalme. Inahusu kupokea ukuhani mtakatifu, kubarikiwa katika maeneo matakatifu na nguvu kutoka juu, na kupokea baraka zote za Ibrahimu, Isaka na Yakobo, kupitia agizo la ndoa ya selestia” (A New Witness for the Articles of Faith [1985], 515).

Page 115: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

100

UtanguliziKatika mahubiri kwa Wanefi, Yakobo alianza kwa ku-nukuu baadhi ya unabii wa Isaya juu ya Bwana kuwa-komboa watu wake wa agano. Sehemu hii ya hotuba ya Yakobo hupatikana katika 2 Nefi 6–8 (angalia somo la 28 katika mwongozo huu). Muendelezo wa hotuba hii ya siku mbili unapatikana katika 2 Nefi 9–10. Baada ya kunukuu Isaya, Yakobo alishiriki ushuhuda wake mwenyewe wa Upatanisho wa Yesu Kristo —wa nguvu

za Mwokozi wa kutuokoa kutokana na madhara ya Kuanguka na matokeo ya dhambi zetu. Rais Joseph Fielding Smith alifundisha kwamba 2 Nefi 9 ina “moja ya mahubiri ya kuelimisha zaidi iliowahi kutolewa ku-husiana na upatanisho.” Alisema, “Inapaswa kusomwa kwa makini na kila mtu anayetafuta wokovu”(Answers to Gospel Questions, comp. Joseph Fielding Smith Jr., 5 vols. [1957–66], 4:57).

SOMO 29

2 nefi 9:1–26

Mapendekezo ya Kufundisha

2 Nefi 9:1–9Yakobo anaelezea madhara ya AngukoKabla ya darasa kuanza, andika mnyama mwovu katikati ya ubao.Anza somo kwa kueleza kwamba 2 Nefi 9 ina muendelezo wa mahubiri ambayo wanafunzi walianza kusoma katika somo lililopita. Wakumbushe wanafunzi kuwa katika sehemu ya kwanza ya mahubiri, inayopatikana katika 2 Nefi 6–8,Yakobo alimnukuu Isaya ili kufundisha kuhusu rehema ya Mwokozi na uwezo Wake wa kuwakomboa watu Wake wa agano kutoka katika hali yao ya upotevu na mtawanyiko. Akiendeleza hotuba yake, Yakobo alifundisha jinsi Mwokozi anatukomboa sote kutokana na hali yetu ya kuanguka na dhambi.Elekeza mawazo ya wanafunzi katika kishazi ulichoandika kwenye ubao.• Nini kinakuja akilini wakati unafikiri juu ya mnyama mwovu?Katika kujibu swali hili, wanafunzi wanaweza kutaja viumbe wa kufikirika. Ikiwa watataja, elezea kwamba, baadhi ya vitu vya kweli vinaweza kutisha kuliko viumbe vya kufikirika kwa sababu vinaweza kuleta madhara ya kudumu. Waeleze wanafunzi kwamba Yakobo alitumia kishazi“mnyama mwovu”ili kuelezea hali ambayo sote tunapitia na madhara ya milele yana-yoweza kutokana na humo. Waulize wanafunzi kusoma 2 Nefi 9:10 kimoyomoyo, wakianga-lia hoja mbili ya mnyama mwovu ambaye Yakobo alimwelezea. Wakati wanafunzi wakielezea kile walichokipata, ongezea majibu kwenye ubao kama inavyoonyeshwa hapa chini:

Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa matumizi ya maneno ya Yakobo kifo na kuzimu, elezea kwamba maneno yote yanahusu aina ya utengano. Wakati Yakobo alipotumia neno kifo katika mahubiri haya, alimaanisha “kifo cha mwili”, ambacho ni mgawanyo wa mwili na roho. Wakati yeye alitumia neno kuzimu, alimaanisha “kifo cha kiroho,” ambacho ni utengano wa mtu kutoka katika uwepo wa Mungu. Katika maandiko, mgawanyo huu mara nyingi hujulikana kama “kifo cha kiroho.”Alika wanafunzi kusoma 2 Nefi 9:6 kimya kimya. Waulize kutafuta chanzo cha kifo cha kimwili na kifo cha kiroho.• Tukio gani lilileta kifo cha kimwili na kifo cha kiroho kwa sisi sote? (Unaweza kutaka

kueleza kwamba kutokana na Anguko, watu wote wametolewa nje ya uwepo wa Mungu na watu wote hatimaye watakufa kimwili.)

Mnyama Mwovu

kifo kuzimu“kifo cha mwili” “kifo cha roho”

Page 116: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

101

2 nefi 9 :1–26

Eleza kwamba katika 2 Nefi 9:7–9, Yakobo anafundisha kile kitakachotokea kwetu kama hakungekuwa na Upatanisho na madhara ya Anguko kubaki milele. Ili kuandaa wanafunzi kusoma mistari hii, unaweza kutaka kufafanua mambo machache katika mstari wa 7: Wa-kati Yakobo alipoongea kuhusu hukumu ya kwanza iliyompata mwanadamu,” alimaanisha madhara ya Anguko la Adamu na Hawa. Alipoongea juu ya “uharibifu,” alimaanisha miili yetu ya duniani, ambayo itakufa. Alipoongea juu ya “kutoharibika,”alimaanisha miili yetu iliyofufuka, ambayo itaishi milele.Uliza mwanafunzi kusoma 2 Nefi 9:7–9 kwa sauti. Alika darasa kuangalia vishazi vina-vyoeleze kile kitakachofanyika katika miili na roho zetu ikiwa kifo cha kimwili na kiroho vingebakia milele.• Kama hakungekuwa na Upatanisho, ni nini kingefanyika kwa miili yetu?• Ikiwa hakungekuwa na Upatanisho, ni nini kingefanyika kwa roho zetu?Ili kusisitiza hatma yetu itakuwaje bila ya Upatanisho wa Yesu Kristo, uliza mwanafunzi kusoma kwa sauti maneno yafuatayo ya Mzee D. Todd Christofferson wa Akidi ya Mitume

Kumi na Wawili.“Kama kujitenga kwetu na Mungu kwa kifo chetu cha kimwili kungekuwa kwa kudumu, uhuru wa kimaadili haungekuwa na maana. Ndiyo, tunge-kuwa huru kuchagua, lakini ingekuwa na maana gani? Matokeo ya mwisho ingekuwa sawa daima bila kujali matendo yetu: kifo bila matumaini ya ufufuo na hakuna matumaini ya mbinguni. Kama vizuri au vibaya kama

tunavyoweza kuchagua kuwa, sote tungeishia kuwa ‘malaika kwa ibilisii.’ [2 Nefi 9:9.]” (“Moral Agency,” Ensign, June 2009, 50).

2 Nefi 9:10–26Yakobo anafundisha kuwa kupitia kwa Upatanisho, Mwokozi anatukomboa kuto-kana na madhara ya Anguko na kutupatia msamaha wa dhambi zetuWaulize wanafunzi kusoma 2 Nefi 9:10.• Kulingana na aya hii, ni nini Mungu ametayarisha kwa ajili yetu?Sisitiza kwamba ujumbe mkuu wa Yakobo katika mahubiri haya ni kwamba Mungu ame-tayarisha “njia ya kuepuka kunaswa na . . . kifo na kuzimu.” Kuepuka huku—kutokana na kifo cha kimwili na kiroho kilicholetwa na Anguko — umehakikishwa kwa sababu ya dhabihu ya upatanisho wa Yesu Kristo.Gawanya darasa katika makundi mawili. Alika kundi la kwanza kusoma 2 Nefi 9:5, 19–21 kimya kimya, wakiangalia maelezo ya dhabihu ya Mwokozi kwa ajili yetu. Alika kundi la pili kusoma 2 Nefi 9:11–12, 15, 22 kimya kimya, wakitafuta vishazi juu ya Yesu Kristo kutu-okoa kutokana na kifo cha kimwili. (Inaweza kusaidia kuandika marejeo haya ubaoni.)Wanafunzi wakishapata muda wa kusoma, uliza kundi la kwanza maswali yafuatayo:• Ni nini ambacho Mwokozi alikuwa tayari kuteseka ili aweze kutuokoa kutokana na kifo

cha kimwili na kiroho? Ni maelezo gani uliyopata ambayo yana maana kwako?• Yakobo alisisitiza kuwa Yesu Kristo aliteseka maumivu ya watu wote. Hii ina maana gani

kwako? Ufahamu huu unashawishi kwa njia gani hisia zako juu ya Mwokozi? (Ili kuwa-saidia wanafunzi kutafakari uwezo wa dhabihu wa Mwokozi, unaweza kutaka kukatiza majadiliano na kusisitiza kwamba Mwokozi aliteseka maumivu ya wote ambao wamei-shi na watakaoishi duniani. Ili kuwasaidia wanafunzi kutafakari hali binafsi ya dhabihu ya Mwokozi, fikiria kuwaalika kuandika majina yao katika ukingo karibu na 2 Nefi 9:21, kama ukumbusho kwamba Mwokozi alitese kwa ajili ya maumivu yao.)

Uliza kundi la pili maswali yafuatayo:• Ni vishazi vipi ulivyopata vinaelezea Yesu Kristo kutuokoa kutokana na kifo cha kimwili?• Kulingana na 2 Nefi 9:22, ni nani atakayefufuliwa na kurudishwa katika uwepo wa Mungu?Rejea nyuma kwa kishazi “mnyama mwovu” kwenye ubao. Alika wanafunzi kueleza, kwa maneno yao wenyewe, kile ambacho Yakobo alifundisha juu ya jinsi tunavyoweza kuokolewa kutokana na “mnyama” huyu. Hakikisha kwamba wanafunzi wanaelewa kwamba kupitia Upatanisho, Yesu Kristo anakomboa watu wote kutokana na kifo cha kimwili na ki-roho vilivyoletwa na Anguko. Mwalike mwanafunzi kuandika ukweli huu kwenye ubao.

Page 117: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

102

SoMo 29

Wakumbushe wanafunzi kwamba zaidi ya kuwakomboa wanadamu wote kutokana na kifo cha kimwili na kiroho uliosababishwa na Anguko, Yesu Kristo anaweza kutuokoa kutokana na kifo cha kiroho kinachosababishwa na dhambi zetu wenyewe.Eleza kwamba Yakobo alielezea hali ya watu wanaoenda mbele za Mungu katika dhambi zao. Alika wanafunzi kuangalia maelezo haya wakati mwanafunzi anasoma 2 Nefi 9:15–16, 27 kwa sauti.• Yakobo alielezea vipi hali ya watu ambao wataenda mbele za Mungu katika dhambi zao?Eleza kwamba Yakobo alielezea pia hali ya watu walioenda mbele za Mungu katika usafi. Alika wanafunzi kuangalia maelezo haya wakati wanafunzi wanaposoma 2 Nefi 9:14, 18 kwa sauti.• Yakobo alielezeaje hali ya watu ambao wataonekana mbele ya Mungu katika usafi?Elezea kwamba wakati ukombozi kutokana na Anguko ni zawadi kwa watu wote, uko-mbozi wetu kutokana na matokeo ya dhambi zetu kwa sehemu unategemea tamaa na matendo yetu. Andika yafuatayo ubaoni: Kwa njia ya Upatanisho wa Yesu Kristo, tunaweza kushinda matokeo ya dhambi zetu tunapokuwa na . . .Alika mwanafunzi kusoma 2 Nefi 9:21, 23–24 kwa sauti. Uliza darasa kuangalia vishazi ili kukamilisha sentensi kwenye ubao.• Kulingana na mistari hii, unawezaje kukamilisha sentensi hii? (Majibu ya wanafunzi

lazima yaangazie kukamilisha sentensi ifuatayo: Kwa njia ya Upatanisho wa Yesu Kristo, tunaweza kushinda matokeo ya dhambi zetu tunapokuwa na imani katika Yesu Kristo, kutubu, kubatizwa, na kuvumilia hadi mwisho. Wanapotoa majibu yao, kamilisha taarifa kwenye ubao.)

Kamilisha somo hili kwa kuchagua moja ya shughuli zifuatazo. Shughuli zote mbili zina-nuiwa kusaidia wanafunzi kutafakari juu ya maana ya Upatanisho wa Mwokozi kwao na kushiriki hisia zao juu Yake. 1. Waulize wanafunzi kupitia 2 Nefi 9:1–22 na kupata mistari yote inayoanza na neno

O.Waalike wanafunzi kusoma sentensi za kwanza ya mistari hiyo kwa sauti.Alika wanafunzi kuandika sentensi kama hizo katika jarida zao ya masomo ya maandiko au daftari za darasa, zinazoelezea hisia zao binafsi za shukrani kwa ajili ya Mwokozi na dhabihu Yake kwa ajili yao. Waulize kufuata mfano wa Yakobo, kwa kuanza kila sentensi-kwa neno O na kumalizia kwa alama ya mshangao. Waulize wanafunzi wachache kushi-riki sentensi zao ifaavyo. Hakikisha kwamba wanaelewa kwamba hawapaswi kujisikia kuwajibika kushiriki hisia au uzoefu ambao ni wa siri mno au binafsi.

2. Kama darasa, imbeni au someni maneno ya “I Stand All Amazed” (Hymns, no. 193) au wimbo mwingine kuhusu Upatanisho wa Yesu Kristo. Alika wanafunzi kuchagua mistari kutoka katika wimbo unaoangazia hisia zao juu ya Mwokozi na dhabihu Yake ya upata-nisho. Waruhusu kuliambia darasa kuhusu mistari waliyochagua na kueleza sababu yao ya kufahamu mistari hizo.

Tangazo na Habari za usuli2 Nefi 9:7. Ni nini ingekuwa athari za Anguka bila Upatanisho?Mzee D. Todd Christofferson wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alieleza kile hatima yetu itakuwa bila ya Upatanisho wa Yesu Kristo:

“Kama vile kifo kingetuadhibu na kupoteza maana ya wakala wetu, lakini kwa ajili ya ukombozi wa Kristo, vivyo hivyo, bila ya neema Yake, dhambi zetu na maamuzi yetu mabaya yatatufanya kupotea milele.

Hakungekuwa na njia ya kurekebika kikamilifu kuto-kana na makosa yetu, na kwa kuwa wachafu, hatunge-weza kuishi tena katika uwepo wa [Mungu].

“. . . Tunahitaji Mwokozi, Mpatanishi ambaye anaweza kushinda madhara ya dhambi na makosa yetu ili kwa-mba yasiweze kutuangamiza. Ni kwa sababu ya Upa-tanisho wa Kristo ambapo tunaweza kupona kutokana na maamuzi mabaya na kuwa waadilifu chini ya sheria kama kwamba hatujatenda dhambi (“Moral Agency,” Ensign, June 2009, 50).

Page 118: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

103

UtanguliziBaada ya kushuhudia kwamba Yesu Kristo anawako-mboa watu wote kutokana na madhara ya Anguko na anatupatia msamaha kwa dhambi zetu, Yakobo alihitimisha hotuba yake. Alionya dhidi ya mitazamo na vitendo vinavyoelekeza utengano na Bwana, na aka-shuhudia juu ya mitazamo na vitendo vinavyoruhusu watu kuja kwa Kristo na kuokolewa. Siku ya pili, Ya-kobo alielezea kuwa ingawa nyumba ya Israeli ingeta-wanyika kwa sababu ya dhambi, Bwana angekumbuka

maagano Yake nao na kuwakusanya watakapotubu na kurejea Kwake. Yakobo alitoa unabii juu ya Kusu-lubiwa kwa Yesu Kristo. Pia alitabiri ya kwamba nchi ya ahadi ya watu wake itakuwa ni mahali pa uhuru, iliyoimarishwa dhidi ya mataifa yote na huru kutokana na utawala wa wafalme. Yakobo aliwahimiza watu wake kujipatanisha wenyewe kwa mapenzi ya Mungu na kukumbuka kwamba wangeweza kuokolewa tu kwa njia ya neema ya Mungu.

Mapendekezo ya Kufundisha

2 Nefi 9:27–54Yakobo anawaalika wote kuja kwa Kristo na anaonya juu ya tabia na matendo yanayotutenganisha na BwanaUbaoni, andika vishazi kwa nini ninahitaji msaada na kile lazima nifanye. Wawezeshe darasa kufikiria juu ya mtu ambaye ana ugonjwa wa kutisha.• Kwa nini ni muhimu kwamba mtu huyu aelewe haja ya kutafuta msaada?• Kwa nini ni muhimu kwamba mtu huyu pia aelewe cha kufanya ili apate msaada?• Ni nini kitakachotokea kama mtu huyo anaelewa umuhimu wa msaada lakini haelewi

cha kufanya ili kuupokea?Wakumbushe wanafunzi kwamba katika somo lililopita, walisoma kuhusu madhara ya Anguko na matokeo ya dhambi zetu, kujifunza juu ya kwa nini tunahitaji Mkombozi. Shuhudia kwamba anataka kutusaidia na kutukomboa kutokana na dhambi zetu. Waulize wanafunzi kufikiria kama wanajua kile wanapaswa kufanya ili kupokea baraka zote za Upatanisho.Eleza kwamba Yakobo alitaka kuwasaidia watu wake kuchagua “Njia ya uzima wa milele” (2 Nefi 10:23). Aliwasaidia kuelewa kwamba watapokea uzima wa milele tu ikiwa “wange-kuja kwa Bwana” (2 Nefi 9:41). Alika mwanafunzi kusoma 2 Nephi 9:41 kwa sauti. Uliza darasa kuangalia maelezo ya Yakobo ya “njia” tunayopaswa kufuata.• Ina maanisha nini kuja kwa Bwana? (Unaweza kutaka kuwahimiza wanafunzi kufikiria

maisha yao kama njia. Wawezeshe kutafakari kimoyomoyo kule njia yao inaelekea. Je, chaguzi zao zinawaleta karibu na Mwokozi?)

• Yakobo alitumia maneno gani ili kuelezea “njia”? Je, maneno nyembamba na kunyooka yanafundisha nini kuhusu jinsi tunavyopaswa kuishi?

Elezea kwamba kwa uhusiano na njia nyembamba na ilionyooka,Yakobo alitumia mfano wa mlango. Alitoa mfano wa Mwokozi kama mlinzi wa lango lile. Shiriki ushuhuda wako kwamba tunaweza kusamehewa dhambi zetu na kupokea uzima wa milele tu kupitia kwa Yesu Kristo na Upatanisho Wake. Kila kitu tunayofanya ambacho kinaelekeza kwa uzima wa milele —ikiwemo maagizo tunayopokea, sala tunazotoa, shuhuda tunazoshiriki, na kwa njia tunayoishi —lazima ifanyike kwa jina la Yesu Kristo.• Kwa nini ni muhimu kwako kwamba Mwokozi “haajiri mtumishi yeyote pale”? (Una-

weza kutaka kusema kwamba Bwana huwaita watumishi, kama vile maaskofu na marais wa vigingi, kutenda kwa niaba Yake kama waamuzi wa watu. Hata hivyo, atakuwa Ha-kimu wetu wa mwisho na atatoa idhini ya mwisho kulingana na jinsi tulivyoishi.)

• Jinsi gani maarifa kwamba Bwana “hawezi kudanganywa” yanashawishi juhudi zetu za kuja Kwake?

Kufundisha kwa njia ya RohoKama mwalimu wa injili, unapaswa kutafuta uongozi wa Roho Mta-katifu katika maandalizi yako na mafundisho. “Na Roho atatolewa kwenu kwa sala ya imani; na msipompokea Roho msifundishe.” (M&M 42:14).

SOMO 30

2 nefi 9:27–54 na 2 nefi 10

Page 119: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

104

SoMo 30

Eleza kwamba kote katika salio la 2 Nefi 9, mafundisho ya Yakobo yanatusaidia kuelewa jinsi mitazamo yetu na vitendo vinaathiri uwezo wetu wa kuja kwa Mwokozi. Baadhi ya mitazamo na vitendo hutusaidia kuja kwa Kristo, wakati vingine hutuzuia kuja Kwake.Ili kuwasaidia wanafunzi kugundua baadhi ya tabia hizi na vitendo, chora mstari wima chini katikati ya bodi. Kwenye upande mmoja wa mstari, andika Kujiweka mbali na Kristo. Chini yake, andika:

1. 2 Nefi 9:27–332. 2 Nefi 9:34–39

Kwa upande mwingine wa mstari, andika Kuja kwa Kristo. Chini yake, andika:3. 2 Nefi 9:23, 39, 42, 45–464. 2 Nefi 9:49–52

Mpe kila mwanafunzi namba kati ya 1 na 4. Alika wanafunzi kusoma kimoyomoyo aya zinazohusishwa na nambari zao zilizopewa. Waulize wanafunzi waliopewa vikundi vya 1 na 2 kutambua mitazamo na vitendo vinavyoweza kutuweka mbali na Mwokozi. Waulize wanafunzi waliopewa vikundi vya 3 na 4 kutambua mitazamo na vitendo vinavyoweza kutusaidia kuja kwa Mwokozi na kupokea baraka ya Upatanisho Wake. Unaweza kutaka kuwahimiza wanafunzi kutia alama katika matokeo yao katika maandiko yao.Baada ya dakika kadhaa, alika wenye kujitolea kutoka vikundi vya 1 na 2 ili waje kwenye ubao na kuorodhesha mitazamo na vitendo walivyogundua ambavyo vinatutenganisha na Mwokozi. Jadili baadhi ya maonyo ya Yakobo kwa kuwauliza baadhi au yote ya maswali yafuatayo:• Yakobo alitaja kujifunza na fedha, yote ambayo yanaweza kuwa mazuri. Chaguzi zetu

juu ya kujifunza na fedha zinawezaje kutuzuia kuja kwa Bwana? (Elezea kwamba 2 Nefi 9:28–29 ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Unaweza kuwahimiza wanafunzi kutia alama kwenye kifungu hiki.)

• Unafikiri inamaanisha nini kuwa kiziwi au kipofu kiroho? (Ona 2 Nefi 9:31–32.)• Kishazi “wasiotairiwa moyoni” (2 Nefi 9:33) kina wahusu wale wenye mioyo migumu

kwa Mungu na wasiokubali kutii maagano naye. Hali hii inatuzuia vipi kupokea baraka kamili za Upatanisho?

• Ni yapi baadhi ya aina za kuabudu sanamu hivi leo? (Ona 2 Nefi 9:37.)Alika wanafunzi kutoka vikundi ya 3 na 4 ili waje kwenye ubao na kuorodhesha mitazamo na vitendo walivyogundua ambavyo vitatuleta kwa Mwokozi na kutusaidia kupokea ba-raka ya Upatanisho. Ili kuwasaidia wanafunzi kuchambua yale wamejifunza, uliza baadhi au yote ya maswali yafuatayo:• Katika 2 Nefi 9:23,Yakobo anatukumbusha amri ya Bwana ya kutubu na kubatizwa.

kufanywa upya maagano ya ubatizo kwa njia ya Sakramenti kunatusaidiaje kuja kwa Bwana na kupokea baraka ya Upatanisho wake?

• Unafikiri inamaanisha nini “kufikiri kiroho”? (2 Nefi 9:39). Ni shughuli gani ambazo zinaweza kutusaidia kufikiri Kiroho?

• Ina maanisha nini “kuacha dhambi zenu” (2 Nefi 9:45).• Unafikiri Yakobo alimaanisha nini aliposema kunywa, kula, na “kufurahia unono”? (Ona

2 Nefi 9:50–51. Unaweza kutaka kueleza kwamba mistari hii inahusu malisho ya kiroho.)Shuhudia kuwa tunavyokuja kwa Bwana na kuishi kulingana na mapenzi Yake, tutapokea baraka kamili ya Upatanisho. Andika kanuni hii kwenye ubao juu ya orodha ambayo wanafunzi wametengeneza.Wahimize wanafunzi kutafakari ushahidi walioona kuhusu kanuni hii katika maisha yao. Waalike kuandika katika jarida zao ya masomo ya maandiko au daftari za darasa kuhusu ji-nsi wamesogea karibu na Mwokozi kupitia kwa mitazamo moja au zaidi na vitendo katika orodha ya pili kwenye ubao. Alika wanafunzi wachache kushiriki kile wameandika (lakini wasaidie kuelewa kwamba hawapaswi kuhisi kulazimishwa kuelezea uzoefu ambazo ni za siri mno au binafsi).

Kuandika majukumu kwenye ubaoWakati wanafunzi wamewekwa kusoma makundi ya aya, inaweza kuwa muhimu kuandika marejeo kwenye ubao. Hii husaidia wanafu-nzi kukumbuka kile wametakiwa kufanya na husaidia kuzuia mkanga-nyiko kuhusu kazi.

2 Nefi 9:28–29 ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Rejea wazo katika mwisho wa somo ili kuwasaidia wanafunzi kwa umahiri wao wa kifungu hiki.

Page 120: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

105

2 nefi 9 : 27– 54 na 2 nefi 10

2 Nefi 10Yakobo anawahimiza watu wake kushangilia na kuja kwa BwanaWaulize wanafunzi ikiwa wamewahi kupokea zawadi iliyokuwa ya maana kwa sababu mtu alijitahidi au kujitolea ili kutoa zawadi hii. Fikiria kualika mwanafunzi mmoja au wawili kushiriki uzoefu wao.• tunawezaje kutoa shukrani kwa ajili ya zawadi hizo?• tunawezaje kutoa shukrani kwa ajili ya zawadi ya Upatanisho wa Mwokozi?Eleza kwamba siku baada ya Yakobo kutoa hotuba yake juu ya Upatanisho wa Yesu Kristo, alishuhudia tena juu ya ukombozi wa Bwana kutokana na matokeo ya dhambi. Aliwafu-ndisha watu wake kuhusu jinsi wanavyopaswa kufanya kuhusu zawadi ya Upatanisho.Fupisha 2 Nefi 10:1–19 kwa kueleza kwamba Yakobo alielezea kwamba ingawa nyumba ya Israeli ingetawanyika kwa sababu ya dhambi, Bwana angekumbuka maagano Yake pamoja nao na kuwakusanya wakati wangetubu na kurejea Kwake. Unaweza kusema kuwa 2 Nefi 10:3 ni mstari wa kwanza katika Kitabu cha Mormoni ambao unatumia kichwa Kristo katika kumtaja Mwokozi.Uliza mwanafunzi kusoma 2 Nefi 10:20, 23–25 kwa sauti. Alika darasa kutambua kile Yakobo anatusihi kufanya kulingana na zawadi ya Upatanisho. Unaweza kutaka kushauri kwamba wanafunzi watie kile kile walichopata katika mistari hizi. Waalike kushiriki kile walichopata.Tayarisha kijitabu cha mwongozo chenye maswali yafuatayo (au andika maswali hayo kwenye ubao kabla ya darasa kuanza). Alika wanafunzi kuchagua swali moja na kushiriki mawazo yao na hisia kuhusu swali hilo na mwenzake.• Kulingana na kile tumejifunza kuhusu Mwokozi, ni nini unataka kukumbuka daima

juu Yake?• Kwa nini toba ni njia muhimu ya kuonyesha shukrani zetu kwa yale ambayo Bwana

ametutendea?• Umejifunza nini kuhusu Mwokozi ambacho kinatusaidia kuhisi tumaini?Hitimisha kwa kuelezea kwamba neno kupatanisha katika 2 Nefi 10:24 ina maanisha kuleta watu au mambo katika mapatano au makubaliano na kila mmoja. Kwa mfano, marafiki wawili wanapaswa kupatanishwa pamoja baada ya kukosana.• Unafikiri inamaanisha nini kujipatanisha na nia ya Mungu?Waalike wanafunzi kutafakari kile wamejifunza na kuona walipojifunza na kujadili 2 Nefi 9–10. Waalike kutafuta ushauri kutoka kwa Roho Mtakatifu ili kuwasaidia kuamua kile watakachofanya ili kujipatanisha na nia ya Mungu na kushiriki kikamilifu zaidi baraka ya Upatanisho. Kwa mfano, mwanafunzi anaweza kuamua kutii mawaidha fulani kutoka kwa Mungu (angalia2 Nefi 9:29), kuachana na dhambi fulani (ona 2 Nefi 9:45), au kutambua njia ya kukumbuka Mwokozi mara nyingi siku zote (angalia 2 Nefi 10:20). Wahimize wana-funzi kufanya chochote kiwezekanacho ili “kujipatanisha na nia ya Mungu”(2 Nefi 10:24). Shuhudia juu ya baraka ya kufanya hivyo.

Umahiri wa maandiko—2 Nefi 9:28–29Fahamu: Shughuli ifuatayo imeundwa ili kuwasaidia wanafunzi na umahiri wao wa 2 Nefi 9:28–29. Kwa sababu ya urefu wa mafundisho ya leo, unaweza kutaka kutumia shughuli katika siku nyingine, wakati una muda zaidi.Ongoza darasa katika kusoma 2 Nefi 9:28–29 pamoja kwa sauti .• Ni hatari gani zinazoweza kututega sisi tunapotafuta kujifunza? Tunawezaje kutafuta

kujifunza lakini tuepuka mitego hii?• Ni nini kinaweza kutusaidia “kusikia mawaidha ya Mungu”tunapotafuta kuelimika?Wahimize wanafunzi kuendelea kushiriki katika seminari sasa na kupanga kuhudhuria chuo baada ya kuhitimu kutoka seminari.

Page 121: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

106

Mafunzo ya Masomo ya Nyumbani2 Nefi 4–10 (Kitengo cha 6)

Nyenzo za Maandalizi kwa Mwalimu wa Mafunzo ya Masomo ya NyumbaniMuhtasari wa Mafunzo ya Masomo ya Kila Siku ya NyumbaniMuhtasari ufuatao wa mafundisho na kanuni ambayo wanafunzi walijifunza waliposoma 2 Nefi 4–10 (kitengo cha 6)haipaswi kufundishwa kama sehemu ya somo lako. Somo unayofundisha huzingatia tu machache ya mafundisho haya na kanuni. Fuata ushawishi wa Roho Mtakatifu unapofikiria juu ya mahitaji ya wanafunzi wako.

Siku 1 (2 Nefi 4–5)Wanafunzi wanaposoma 2 Nefi 4, walitilia maanani kanuni kwamba Mungu huwasaidia wale wanaomtumainia Yeye (ona 2 Nefi 4:12–35) na kuandika katika jarida yao ya ma-somo ya maandiko kuhusu njia moja ambayo wangependa kuongeza imani yao kwa Mungu. Katika 2 Nefi 5 waliona mifano ifuatayo ya ukweli: Usalama huja kutokana na kutii ufunuo za Mungu (ona 2 Nefi 5:1–8). Jinsi Injili ya Yesu Kristo inavyokuwa njia ya maisha yetu, tutaongezeka katika furaha (ona 2 Nefi 5:9–18, 26–27). Wanafunzi walichunguza maisha yao na kutambua kitu watakachofanya ili kuishi kikamilifu zaidi “kwa furaha.”

Siku ya 2 (2 Nefi 6–8)Katika somo hili wanafunzi walijifunza kwamba Bwana ni mwenye huruma kwa wale wanaorudi Kwake (ona 2 Nefi 6). Walitafakari jinsi Bwana amekuwa na huruma kwao. Pia tumejifunza kwamba Mwokozi anatamani kuwakomboa watu Wake wa agano na ana uwezo wote wa kufanya hivyo (ona 2 Nefi 7–8).

Siku ya 3 (2 Nefi 9)Wanafunzi walipoanza masomo yao ya 2 Nefi 9, walijifunza kile kingetokea kama hakungekuwa na Upatanisho. Pia alisoma kweli zifuatazo: Upatanisho wa Yesu Kristo huwa-komboa watu wote kutoka katika kifo cha kimwili na kiroho kilicholetwa na Kuanguka (ona 2 Nefi 9:1–22). Kupitia kwa Upatanisho wa Yesu Kristo, tunaweza kushinda matokeo ya dhambi zetu ikiwa tuna imani ya Kristo Yesu, kutubu, kubatizwa, na kuvumilia hadi mwisho (ona 2 Nefi 9:14–27). Wanafunzi waliandika aya ya kuonyesha hisia zao juu ya dhabihu ya Mwokozi kwa ajili yao.

Siku ya 4 (2 Nefi 9–10)Wanafunzi waliposoma salio la 2 Nefi 9 na kusoma 2 Nefi 10, walitafakari zipi kati ya chaguzi zao zinaweza kuwatenganisha kutoka kwa Bwana na ambayo inawasaidia kuja karibu Naye. Walijifunza kwamba tunapochagua kuja kwa Bwana na kuishi kulingana na mapenzi Yake, tutapokea baraka kamili ya Upatanisho.

UtanguliziMiongoni mwa kweli nyingi muhimu ambazo wanafunzi wame-soma wiki hii, sisitiza umuhimu wa Upatanisho wa Yesu Kristo. Omba mwongozo kuhusu jinsi unavyoweza kuwasaidia vyema kuelewa na kutegemea Upatanisho. Unapofundisha, wahimize wanafunzi kutafakari kile wanahitaji kufanya ili kupokea baraka ya Upatanisho wa Mwokozi.

Fahamu: Unapoandaa masomo yako kwa maombi, zingatia mahitaji ya wanafunzi wako —hasa mahitaji ya wale ambao wanaweza kuwa na ugumu. Unapoomba kwa ajili ya wanafu-nzi binafsi na kwa ajili ya mwongozo wa jinsi ya kuwafundisha vyema mafundisho na kanuni zinazopatikana katika maandiko, Roho Mtakatifu atakuongoza wewe kujua jinsi ya kukidhi mahi-taji ya wanafunzi.

Mapendekezo ya Kufundisha

2 Nefi 4–5Nefi anaonyesha matumaini Yake katika Bwana, Bwana anawatenganisha Wanefi kutoka kwa Walamani; Wanefi wanaishi kwa furahaAndika habari katika chati ifuatayo kwenye ubao, au itayarishe kama kijitabu cha taarifa.

2 nefi 4 2 nefi 5

1. Soma utangulizi wa sura, na jiandae kufupisha sura kwa maneno yako mwenyewe.

2. Soma 2 nefi 4:19 na ueleze unafikiri inamaanisha “ninajua ninaye mwamini.”

3. Soma kote maandishi yako ya jarida ya masomo ya ma-andiko ya siku 1, kazi 4, na ujitayarishe kuelezea njia moja ambayo ungependa kuongeza imani yako katika bwana.

1. Soma utangulizi wa sura, na ujiandae kufupisha sura kwa maneno yako mwenyewe.

2. Soma 2 nefi 5:27 na ueleze unafikiri inamaanisha kuishi “kwa furaha.”

3. Soma maandishi yako ya jarida ya masomo ya maandiko la siku 1, kazi 6. jiandae kuelezea moja ya matendo ya Wanefi au mitazamo na jinsi kufanya hivyo au kuwa na mtazamo kama huo kumeathiri furaha yako.

Page 122: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

107

MafUnzo ya MaSoMo ya nyUMbani

Gawa darasa nusu. Kuwa na moja ya nusu ya wanafunzi wajia-ndae kufundisha nyenzo kulingana na 2 Nefi 4 na nusu nyingine wajiandae kufundisha nyenzo kulingana na 2 Nefi 5.

Weka kila mwanafunzi aliyepangiwa 2 Nefi 4 pamoja na mwa-nafunzi aliyepangiwa 2 Nefi 5. Waalike wanafunzi kuelezea kwa pamoja na wenzao nyenzo walizotayarisha kwa kazi zao.

2 Nefi 6–8Yakobo anatoa unabii juu ya kutawanyika na kukusanyika kwa Israeli na ananukuu unabii wa Isaya wa uaminifu wa Mwokozi kwa watu wa aganoWakumbushe wanafunzi kwamba 2 Nefi 6–9 ni siku ya kwanza ya mahubiri ambayo Yakobo alitoa kwa watu wake. Siku ya pili ya mafundisho yake inaendelea katika 2 Nefi 10. Katika 2 Nefi 6, Yakobo alitabiri ya kwamba Wayahudi wangemkataa Bwana na watatawanyika. Wawezeshe wanafunzi kusoma 2 Nefi 7:1–2, na wakaribishe waelezee tena maana yake kwa maneno yao wenyewe.

2 Nefi 9Yakobo anafundisha jinsi Upatanisho wa Mwokozi hutukomboa kutokana na madhara ya Anguko na matokeo ya dhambiElezea kauli ifuatayo ya Rais Ezra Taft Benson:

“Kama vile mtu hawezi kuwa na hamu ya chakula mpaka awe na njaa, hivyo ndivyo hatamani wokovu wa Kristo mpaka ajue kwa nini anamhitaji Kristo.

“Hakuna mtu anajua vya kutosha na vizuri kwa nini anamhi-taji Kristo hadi atakapoelewa na kukubali mafundisho juu ya Anguko na madhara yake juu ya watu wote. Na hakuna kitabu kingine duniani kinachoelezea mafundisho haya muhimu kwa ukaribu kama vile Kitabu cha Mormoni (“The Book of Mormon and the Doctrine and Covenants,” Ensign, May1987, 85).

Wezesha mwanafunzi kufikiria kama rafiki angeuliza, “Kwa nini tunamhitaji Mkombozi?” Alika darasa kuandaa kujibu swali hili kulingana na kile wamejifunza katika 2 Nefi 9. Wawezeshe kupitia 2 Nefi 9:7–10, 19–22 kwa ajili ya jibu. Waulize wanafunzi kuelezea majibu yao kwa swali hilo.

Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa jinsi Yesu Kristo anaweza ku-tuokoa kutokana na matokeo ya Kuanguka, soma mlinganisho na Rais Joseph Fielding Smith katika kifaa cha masomo 2 Nefi 9:10–27, katika Kitengo cha 6: Siku ya 3, katika mwongozo wa mwanafunzi. Unaweza kufikiria kualika mwanafunzi kuchora ubaoni au kwenye karatasi kile Rais Smith alieleza. Ukichagua kuwezesha mwanafunzi kuchora kwenye ubao au kipande cha karatasi, unaweza kutaka kualika mwanafunzi kueleza kuhusu mchoro.

Alika wanafunzi kufikiria kuhusu hisia zao wenyewe za kushi-kwa katika shimo refu na kutengwa na Mungu kwa sababu ya changuzi walizofanya. Eleza kwamba kama si kwa ajili ya Upatanisho wa Yesu Kristo, hakungekuwa na fursa ya toba, ha-kungekuwa na matumaini, na hakuna mtu ambaye angeepuka matokeo haya ya dhambi.

Wezesha mwanafunzi kusoma 2 Nefi 9:21–23, na uliza wana-funzi wachache kuelezea kwa maneno yao wenyewe. Ingawa wanaweza kusema tofauti, hakikisha kwamba ukweli ufuatao ni wazi: Kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo, tunaweza kushi-nda matokeo ya dhambi zetu.

Eleza kwamba moja ya fursa kubwa inayopatikana kwa kuku-tana kama kikundi ni kuwa na uwezo wa kushirikiana hisia na shuhuda. Alika wanafunzi kueleza hisia na shuhuda zao kuhusu Yesu Kristo na Upatanisho Wake. Wakiwa na ugumu wa kushi-riki, unaweza kuwawezesha kusoma kile walichoandika katika shajara zao za kujifunza maandiko kwa kazi 4 ya siku ya 3. Una-weza kutaka kuongeza ushuhuda wako katika shuhuda zao.

Fanya darasa kufikiria kwamba mtu alikumbwa na ugonjwa wa kutisha. Kisha jadili maswali yafuatayo:

• Kwa nini ni muhimu mtu aelewe haja ya kutafuta msaada?• Kwa nini ni muhimu mtu pia aelewe cha kufanya ili kupata

msaada?• Nini kitatokea ikiwa mtu anaelewa umuhimu wa msaada

lakini haelewi cha kufanya ili kupata msaada huo?

Waulize wanafunzi kama wanajua kile lazima wafanye ili ku-pokea baraka ya Upatanisho. Wakumbushe kwamba walisoma 2 Nefi 9:23, 42–52 na kutambua vitendo kadhaa na mitazamo inayo tusaidia kuja kwa Kristo na kualika nguvu ya dhabihu ya upatanisho Wake katika maisha yetu. Wawezeshe kupitia maandiko waliyotia alama na orodha waliotengeneza katika majarida yao ya masomo ya maandiko ambayo inatuongoza kwa Mwokozi (siku 4, kazi 1). Alika wanafunzi kuelezea aina moja au zaidi ya matendo haya na mitazamo ambayo imewaleta karibu na Mwokozi. Toa ushuhuda wako kwamba kufuata kanuni zilizofundishwa katika mistari hii kutatusaidia kupokea baraka kamili ya Upatanisho.

2 Nefi 10Yakobo anawatia moyo watu wake kushangilia na kuja kwa BwanaSoma 2 Nefi 10:23–24 pamoja na wanafunzi. Wakumbushe wa-nafunzi kuwa katika siku ya 3, kazi ya 6, walialikwa kuamua kitu watakachofanya ili kujipatanisha na nia ya Mungu. Wahimize kufuatilia kwa mwaliko huu.

Waulize wanafunzi kuelezea ufahamu wa ziada waliopata ku-toka katika sura walizosoma wiki hii. Muda ukiruhusu, hitimisha somo la wiki hii kwa kuimba au kusoma pamoja maneno ya wimbo “I Stand All Amazed”(Wimbo, namba. 193) au wimbo mwingine kuhusu Upatanisho wa Yesu Kristo. Toa ushuhuda wako juu ya umuhimu wa kuja kwa Mwokozi na hali halisi ya baraka ya Upatanisho.

Kitengo Kijacho (2 Nefi 11–25)Wanafunzi wanaposoma 2 Nefi 11–25 wiki hii ijayo, watatambua baadhi ya maneno ya Isaya na jinsi alivyoona siku zetu na kutuonya kulingana na yale aliyoyaona. Baadhi ya maonyo yake yanahusiana na vyombo vyetu vya habari, nguo zetu, maisha yetu, na mitazamo yetu. Wahimize wanafunzi kusoma na kukusanya wanachokiweza kutoka 2 Nefi 11–25, hata kama hawaelewi kila neno.

Page 123: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

108

UtanguliziKatika 2 Nefi 11, Nefi alionyesha upendo wake kwa maneno ya Isaya. Pia alishuhudia waziwazi kwamba Yakobo na Isaya walimwona “Mkombozi, hata vile nili-vyomwona” (2 Nefi 11:2). 2 Nefi 16 ina hadithi ya Isaya ya kutakaswa kwa dhambi zake na kuitwa kama nabii “alipomwona. . .Bwana akikalia kiti cha enzi” (ona 2 Nefi 16:1, 5–8). Wote Nefi na Yakobo walifundisha thamani ya kufananisha maandiko ya Isaya nasi (ona 1 Nefi 19:23;

2 Nefi 6:5; 11:2), na Bwana alitangaza, “maneno ya Isaya ni makuu” (3 Nefi 23:1). 2 Nefi 11 ina baadhi ya mae-lezo ya Nefi kwa ajili ya kuingizwa kwa unabii wa Isaya katika rekodi yake, na hivyo kutumika kama utangulizi kwa maneno ya Isaya katika 2 Nefi 12–24. 2 Nefi 25 inatumika kama hitimisho kwa sura hizi, zenye ushauri wa Nefi juu ya namna ya kuelewa maneno ya Isaya (ona somo la 35 katika mwongozo huu).

Mapendekezo ya Kufundisha

2 Nefi 11Nefi alionyesha furaha yake katika kushuhudia kwamba wokovu huja kupitia kwa Yesu KristoAlika wanafunzi watatu kuandika kimya sentensi moja kila mmoja kuhusu kile kilicho-tokea wakati wa mwisho darasa lilipokutana. Usiwaruhusu kulinganisha au kujadili kile wanachoandika. Ili kuonyesha faida ya kuwa na zaidi ya shahidi mmoja, wezesha wana-funzi watatu kusoma sentensi zao kwa sauti. Baada ya mwanafunzi wa kwanza kusoma sentensi yake, uliza darasa kama ni onyesho kamili ya kile kilichotokea katika darasa lao la mwisho. Kisha kuwa na mwanafunzi wa pili kushiriki sentensi yake, kisha uliza kama ni onyesho kamili ya darasa lao la mwisho. Baada ya mwanafunzi wa tatu kusoma, uliza swali kama hili.• Ni faida gani zilizopo kuwa na mashahidi wengi?Eleza kwamba Bwana huwaita manabii ili wawe mashahidi wake kwa ulimwengu. Wahi-mize wanafunzi kutafakari kinachomaanisha kwao kusikia manabii wakishuhudia juu ya Yesu Kristo.Andika taarifa ifuatayo ubaoni: Kwa kujifunza ushuhuda wa manabii wa Yesu Kristo, tunaweza kuimarisha imani yetu katika Yesu Kristo na kufurahi Kwake.Alika mwanafunzi kusoma 2 Nefi 11:2–3.• Kulingana na mistari hii, Nefi, Isaya, na Yakobo waliona nini ambacho kiliwawezesha

kuwa mashahidi maalum wa Yesu Kristo?• Kwa nini unafikiri ni muhimu kuwa na ushuhuda wa Yesu Kristo kutoka kwa manabii

wengi? (Ona pia Mosia 13:33–35.)Alika wanafunzi kukagua mstari wa kwanza wa kila aya katika 2 Nefi 11:4–6, wakiangalia vishazi ambavyo Nefi alirudia katika kila mstari.• Inamaanisha nini “kufurahia katika” kitu? (Unaweza kueleza kwamba neno kufurahia

linaonyesha hisia ambayo ni zaidi kuliko kupenda tu au kuvutiwa katika kitu fulani. Inamaanisha jambo la furaha na kuridhika.)

Wezesha wanafunzi kusoma 2 Nefi 11:4–7 kimya kimya, wakitambua vitu ambavyo Nefi alifurahia. Kisha ligawe darasa katika jozi. Waulize wanafunzi kushiriki vishazi vinavyo-wavutia sana na kwa nini. Pia wakaribishe kuelezea kinacho wafurahisha au kuwaongoza kufurahia kuhusu Yesu Kristo.Soma 2 Nefi 11:8 kwa sauti, kisha wafanye wanafunzi kuangalia sababu za kwa nini Nefi alijumuisha maandiko ya Isaya katika rekodi yake.• Nini Nefi alitarajia watu wake na wasomaji wa baadaye wa Kitabu cha Mormoni wange-

ona watakapo soma maneno ya Isaya?

Kuelewa IsayaWalimu na wanafunzi wanaweza kuipata kuwa vigumu kuelewa maneno ya Isaya katika Kitabu cha Mormoni. Rais Boyd K. Packer wa Akidi ya Wale Mitume na Kumi na Wawili alita-mbua kuwa tunaposoma Kitabu cha Mormoni, sura hizi zinaweza kuonekana kama vikwazo. Kisha aka-sema: “Usiache kusoma! Songa mbele kupitia sura hizo zilizo ngumu- kuelewa . . . hata kama unaelewa kidogo sana. Songa mbele, kama yote ufanyayo ni kupitia na kukusanya hisia hapa na pale”(“The Things of My Soul,” Ensign, May 1986, 61).

SOMO LA 31

2 nefi 11 na 16

Page 124: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

109

2 nefi 11 na 16

Orodha ifuatayo inatoa baadhi ya mifano ya sababu ambazo Nefi alijumuisha maandiko ya Isaya katika rekodi yake: 1. Isaya alikuwa amemwona Mwokozi, kama vile Nefi na Yakobo walivyomwona (anga-

lia2 Nefi 11:2–3; ona pia 2 Nefi 16:1–5, ambayo inajumuisha maelezo ya Isaya ambayo yanaeleza alimwona Mwokozi).

2. Nefi alifuraha katika kumshuhudia Kristo, na Isaya pia alishuhudia kuhusu Kristo (ona 2 Nefi 11:4, 6; ona pia 2 Nefi 17:14 na 19:6–7, mifano miwili ya unabii wa Isaya juu ya Mwokozi).

3. Nefi alifurahia katika maagano ya Bwana (ona 2 Nefi 11:5). Unabii wa Isaya ulihusiana na maagano ya Bwana. Kwa mfano, alitoa unabii wa kazi ya hekalu ya siku za mwisho (ona 2 Nefi 12:1–3).

Eleza kuwa katika somo hili na matatu yajayo wanafunzi watasoma na kujadili maneno ya Isaya katika 2 Nefi 12–24. Wahimize kutafuta kweli katika sura hizi zinazoimarisha shu-huda zao za Mwokozi na kuwasaidia kufurahia Kwake. Alika wanafunzi kushiriki baadhi ya mistari wanayoipenda kutoka katika sura hizi pamoja na wanafamilia wao na marafiki.

2 Nefi 16Isaya anaitwa kuhudumu kama nabiiEleza kwamba darasa litajifunza 2 Nefi 16 baada ya hiyo kwa sababu ina maelezo ya Isaya ya maono ambayo alipokea wito wa kuwa nabii. Ili kuwasaidia wanafunzi kujiandaa kuelewa mtazamo huu, elezea kwamba maandishi ya Isaya yanajumuisha lugha ya ishara. Maandiko yamejawa na ishara, vielelezo, na maneno ya mafumbo. Eleza kwamba katika moja ya mistari waliosoma awali, Nefi alisema, “Vitu vyote vilivyotolewa na Mungu tangu mwanzo wa dunia, kwa mwanadamu, ni kielelezo cha [Yesu Kristo]” (2 Nefi 11:4). Matu-mizi ya alama na kielelezo ni njia moja ambayo maandiko hutufundisha juu ya huduma ya Bwana ya wokovu.Andika maneno yafuatayo na vishazi katika ubao: pindo, maserafi (Malaika) na mabawa sita kila moja, moshi, kaa la motoWaulize wanafunzi ni mawazo gani huja akilini mwao wanapoona au kusikia maneno haya. Baada ya majadiliano mafupi, eleza kwamba Isaya alitumia maneno haya katika ma-elezo yake ya wito wake wa kuwa nabii wa Mungu. (Jaribu kuwasaidia wanafunzi kuelewa maana ambayo Isaya alinuia. Kuwa makini usije ukafafanua kupita kiasi maana ya lugha ya ishara. Badala yake, wasaidie wanafunzi kuona jinsi ujumbe wa Isaya unavyotumika katika maisha yao.)Uliza mwanafunzi kusoma 2 Nefi 16:1. (Kama wanafunzi wanaweza kupata toleo la Biblia la King James itumiwayo na Watakatifu wa Siku za Mwisho, unaweza kutaka kurejea katika Isaya 6, ambayo ina tanbihi na vielelezo vya kusoma ambayo itaongeza ufahamu wa vifungu vya maandiko vilivyosomwa katika somo hili.)Eleza kwamba katika aya hii, neno pindo lina maana ya mshono au pindo za joho.Alika mwanafunzi kusoma 2 Nefi 16:2–3 kwa sauti. Eleza kwamba “maserafi” ni malaika ambao wanaishi katika uwepo wa Mungu (ona Bible Dictionary, “Seraphim”).• Mabawa sita ya maserafi yana wakilisha nini? (Unaweza kushauri kwamba wanafunzi

wasome Mafundisho na Maagano 77:4 kwa kidokezo. Sura ya mabawa ni ishara ya nguvu ya kusonga na kutenda.)

• Ni maneno gani yanaonyesha mtazamo wa maserafi kwa Bwana?• Ni wakati gani umehisi mtazamo sawa mbele ya Mungu?Wezesha mwanafunzi kusoma 2 Nefi 16:4 na Ufunuo15:8 kwa sauti. Uliza darasa kuangalia maana ya kishazi “ilijaa moshi.” (Unaweza kuwasaidia wanafunzi kuelewa kwamba moshi inawakilisha uwepo, nguvu, na utukufu wa Bwana.) Fikiria kupendekeza kwamba wanafu-nzi waandike Ufunuo 15:8 katika ukingo wa maandiko yao karibu na 2 Nefi 16:4.Alika mwanafunzi kusoma 2 Nefi 16:5 kwa sauti. Uliza darasa kuangalia vishazi vinavyo-eleza jinsi Isaya alivyohisi mbele ya Bwana. (Kama toleo la tafsiri ya Biblia ya King James ya Watakatifu wa Siku za Mwisho inapatikana, wezesha wanafunzi kuangalia Isaya 6:5, tanbihi a na b.)

Page 125: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

110

SoMo la 31

• Unafikiri Isaya alimaanisha nini aliposema, “Nimepotea; kwa sababu mimi ni mtu mwenye midomo michafu”? (Unaweza kutaka kueleza kwamba, katika Isaya 6:5, neno nimepotea limetafsriwa kutoka kwa neno la Kihibrania lenye maana“kuondolewa,” na kishazi midomo michafu inahusu ufahamu wa Isaya wa dhambi zake na dhambi za watu wake. Isaya alikuwa akionyesha kwamba hastahili kuwa katika uwepo wa Bwana.)

Wape wanafunzi muda wa kutafakari kwa nini Isaya aliweza kuhisi hivyo. Eleza kwamba manabii kadhaa wameonyesha jinsi wao walivyohisi kuwa duni walipopokea wito wao. Rais Spencer W. Kimball alieleza mwito wa simu ambayo Rais J. Reuben Clark Jr wa Urais wa Kwanza alimwambia kuwa aliitwa katika Akidi yaMitume Kumi na Wawili:“ ‘Eeh, Ndugu Clark! Si mimi? Humaanishi mimi? Lazima kuna makosa kidogo. Hakika sidhani kama nimekusikia vyema.’ Hivi nilipozama kutoka kwenye kiti hadi sakafuni. . . .“ ‘Eeh, Ndugu Clark! Inaonekana kutowezekana kabisa. Mimi ni mdhaifu na mdogo na mwenye uwezo mdogo na asiyeweza’”(Edward L. Kimball and Andrew E. Kimball Jr., Spencer W. Kimball: Twelfth President of The Church of Jesus Christ of Latter- day Saints [1977], 189).Wasaidie wanafunzi kuelewa kwamba Isaya, mtu mwenye haki, alijihisi “kupotea” na “mchafu” mbele ya Bwana. Ni nani kati yetu asiyeweza kuhisi asiyestahili mbele ya Mungu?Andika ukweli ufuatao ubaoni: Tunaweza kutakaswa kutokana na uchafu wetu kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo.Kama inawezekana, onyesha wanafunzi kipande cha makaa au kipande cha kuni kilicho-chomwa. Waulize ingefananaje kama ingetolewa kutoka motoni.• Nini kingetokea kwa mtu ambaye angegusa makaa ya moto?Soma 2 Nefi 16:6–7 kwa sauti. Waulize wanafunzi kusoma pamoja kimya kimya, wakianga-lia uzoefu wa Isaya unaohusu kaa la moto. (Kama toleo la tafsiri ya Biblia ya King James ya Watakatifu wa Siku za Mwisho linapatikana, wezesha wanafunzi kuangalia Isaya 6:6, tanbihi a, and Isaya 6:7, tanbihi a na b.)• Kulingana na 2 Nefi 16:7, ilimaanisha nini wakati malaika kwa ishara alipogusa midomo

ya Isaya kwa kaa la moto? (Unaweza kutaka kuhitaji kueleza kuwa kaa la moto ni ishara ya utakaso. Wakati malaika katika maono ya Isaya alipogusa midomo yake kwa kaa, iliwakilisha Bwana akitakasa uchafu wa Isaya kumsamehe dhambi zake.)

Wape wanafunzi muda mfupi ili kufikiria juu ya wakati walipohisi nguvu ya utakaso wa Upatanisho wa Yesu Kristo.Alika wanafunzi kusoma 2 Nefi 16:8–13 kimya kimya. Alika mwanafunzi kufupisha kile Bwana alichosema kuhusu huduma ya Isaya miongoni mwa watu. (Unaweza kuhitaji kue-leza kwamba Bwana alishauri Isaya kuwa mahubiri yake kwa Waisraeli waasi, ingepuuzwa pa kubwa bali kwamba anapaswa kuendelea kuhubiri mpaka “nchi itakapokuwa ganjo.” Kwa maneno mengine, Bwana kwa neema ataendeleza ujumbe Wake wa wokovu kupitia kwa watumishi wake “kadiri muda utakapokuwepo au dunia itakapokuwepo, au kutakuwa na mtu mmoja juu ya uso wake kuokolewa” [Moroni 7:36].)Eleza kwamba Isaya alikuwa shahidi wa nguvu wa Bwana Yesu Kristo na injili Yake. Shuhudia kwamba Mwokozi ni halisi na anaweza kutusamehe dhambi zetu, na kwamba tunapoona nguvu ya Upatanisho katika maisha yetu, sisi pia tunaweza kuwa mashahidi wa Mwokozi.

Tangazo na Habari za usuli2 Nefi 16:2–3. Je, malaika wana mabawa?“Malaika wa Mungu kamwe hana mabawa”(Joseph Smith, in History of the Church, 3:392). Basi kwa nini Isaya alielezea malaika kama alikuwa na mabawa? Mzee Bruce R. McConkie alielezea kwamba maelezo

ni mfano: “Ukweli kwamba hawa viumbe watakatifu walionyeshwa kwake kama wenye kuwa na mabawa ili-kuwa tu mfano wa ‘nguvu zao, kwenda kwao, kutenda, nk’ kama ilivyokuwa pia katika maono ambayo wengine walipokea. (M&M 77:4.)” (Mormon Doctrine, 2nd ed. [1966], 703).

Page 126: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

111

UtanguliziIsaya alikashifu uovu wa watu wa siku zake vile vile uovu wa watu wengi katika siku za mwisho. Alionya dhidi ya kuita mabaya mema na mazuri mabaya. Pia ali-sisitiza juu ya Urejesho wa injili katika siku za mwisho,

ikiwemo umuhimu wa hekalu na umuhimu wa kuwa wasafi kutokana na dhambi za ulimwengu. Kwa habari zaidi kuhusu Isaya, angalia somo la 21 katika mwo-ngozo huu.

Mapendekezo ya kufundisha

2 Nefi 12–15Isaya anatofautisha Israeli ovu na Israeli ya hakiIli kuwasaidia wanafunzi kuelewa muktadha wa mafundisho ya leo, anza darasa kwa ku-wakumbusha kwamba katika somo lililopita walijifunza juu ya mwito wa Isaya kuwa nabii. Leo watajifunza kuhusu watu aliowafundisha.Wasaidie wanafunzi kuelewa kwamba wakati Isaya alipoeleza matendo ya watu wa Bwana wa agano katika siku zake, pia alielezea baadhi ya watu katika siku zetu. Mzee Dallin H. Oaks wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alieleza: “Kitabu cha Isaya kina unabii mwingi unaoonekana kutimia kwingi. . . . Ukweli kwamba wingi wa unabii huu unaweza kuwa na maana nyingi inasisitiza umuhimu wa haja yetu ya ufunuo kutoka kwa Roho Mtakatifu kuweza kutusaidia kuyatafsiri” (“Scripture Reading and Revelation,” Ensign, Jan. 1995, 8).Kabla ya darasa, nakili chati ifuatayo ubaoni au kitayarishe kama kijitabu cha taarifa. Acha nafasi ya kutosha ili wanafunzi waandike katika kila safu.

2 nefi 12:5–12, 17–19; 13:8–9 2 nefi 13:16–26

ni mitazamo na mate-ndo gani yanaonyesha dhambi za watu hawa?

ni nini kitafanyika kwa watu hawa kama mato-keo ya dhambi zao?

Eleza kwamba chati hii itasaidia darasa kuchunguza matokeo ya matendo ya watu walioi-shi kinyume na ahadi zao.Gawanya darasa pande mbili. Waulize wanafunzi kusoma 2 Nefi 12:5–12, 17–19; 13:8–9. Uliza nusu nyingine kujifunza 2 Nefi 13:16–26. Alika wanafunzi kusoma mistari yao wa-liyopewa na kutambua majibu kwa maswali mawili katika safu ya kushoto ya chati. Ikiwa chati imeonyeshwa kwenye ubao, alika mwanafunzi kutoka katika kila kundi kuandika majibu yao katika safu muafaka. Ikiwa chati ilisambazwa kama kijitabu cha taarifa, weze-sha wanafunzi kurekodi majibu yao katika vijitabu vyao vya taarifa.Elezea kwa kundi la pili kwamba Isaya alitabiri madhara ya mavazi ya kupita kiasi na mate-ndo ya wanawake wa kidunia katika siku zake mwenyewe, na katika siku zijazo. 2 Nefi 13:16–26 anaelezea yale aliyoyaona. Ingawa Isaya alihutubia hasa “mabinti wa Sayuni,” maneno yake pia yanahusu wanaume. (Unaweza kutaka kueleza kuwa unabii katika 2 Nefi 14:1 si juu ya ndoa ya mitala. Ni juu ya watu wanaokufa katika vita ilivyoelezwa katika 2 Nefi 13:25–26, na kuacha wanawake wengi kama wajane.)Baada ya wanafunzi kupata muda wa kujibu maswali katika chati, uliza:

Kuweka nadhari ya wanafunziMapendekezo yafuatayo yanaweza kukusaidia kuimarisha mawazo ya wanafunzi katika darasa:(1) Wasaidie wa-nafunzi kuona jinsi somo linavyotumika katika maisha yao. (2) Tofa-utisha nguvu ya sauti yako unapofundisha. (3) Dumisha mawasiliano ya macho na wanafu-nzi. (4) Ikiwezekana, zunguka darasani unapofundisha.

SOMO LA 32

2 nefi 12–15

Page 127: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

112

SoMo la 32

• Ni dhambi gani watu hawa walikuwa wametenda? (Majibu yanaweza kujumuisha ki-buri, kuabudu sanamu, kuipenda dunia, na ubatili.) Ni vishazi vipi vinavyoonyesha kuwa watu walikuwa na hatia ya dhambi hizi? Ni nini matokeo ya dhambi hizi?

• Isaya alizungumza kuhusu nchi kuwa “imejaa sanamu”(2 Nefi 12:8). Ni baadhi gani ya aina ya ibada ya sanamu leo?

Kama sehemu ya mjadala huu, soma ushauri ufuatazo kutoka kwa Rais Spencer W. Kimball:“Sanamu za kisasa au miungu ya uongo inaweza kuwa kwa mfano kama vile nguo, nyumba, biashara, mashine, magari, boti za starehe, na vifaa vingine ambavyo hutupotosha kutoka katika njia ya Mungu. . . . Vijana wengi huamua kuhudhuria chuo wakati wanapaswa kuwa kwenye misheni kwanza. Shahada, na utajiri na usalama unaokuja kwa njia hiyo, huonekana kuvutia sana kiasi kwamba misheni inachukua nafasi ya pili. . . . Wengi huabudu uwindaji, safari ya uvuvi, likizo, pikiniki ya mwisho wa wiki na matembezi. Wengine wanazo kama sanamu zao michezo, baseball, soka,vita ya mafahali, au gofu. . . . Na sanamu nyingine watu huabudu ni ile ya nguvu na ufahari”(The Miracle of Forgiveness [1969], 40–41).• Isaya alitabiri juu ya watu ambao wataonyesha kiburi chao na vitu vya dunia kwa njia

wanavyovaa. Tunawezaje kujilinda dhidi ya mitazamo na mwelekeo wa dunia?Ubaoni, andika neno ole. Eleza kwamba neno ole inahusu huzuni na mateso. Manabii wa kale wakati mwingine walitumia neno hili kusisitiza madhara ya dhambi. (Wanafu-nzi wanaweza kukumbuka kuona neno hili mara kwa mara katika 2 Nefi 9:27–38.) Alika wanafunzi kusikiliza unaposoma 2 Nefi 15:18–23 kwa sauti. (Unaweza kutaka kuwahimiza wanafunzi kuweka alama kwenye neno ole na vishazi vinavyoelezea hatua na mitazamo itakayoleta huzuni na mateso. Unaweza pia kushauri kwamba waandike ufafanuzi wa ole  ukingoni karibu na mistari hii.)• Ni nini 2 Nefi 15:20 inamaanisha kwako?• Ni kwa njia gani umeona watu wakiita“mabaya mema, na mema mabaya” katika siku

zetu?Waeleze wanafunzi kwamba sasa watasoma kuhusu kundi la watu ambao walitii ahadi zao. Alika mwanafunzi kusoma 2 Nefi 14:2–4 kwa sauti. Acha wengine wote wa darasa kuangalia maelezo ya Isaya ya kundi hili la watu.• Ni maneno gani au vishazi vinavyoonyesha kuwa kundi hili lilikuwa tofauti na makundi

mengine tuliyochunguza? (Fikiria kuandika majibu ya wanafunzi ubaoni.)Waulize wanafunzi kusoma 2 Nefi 14:5–6 kimya kimya, wakiangalia sehemu tatu ambazo Isaya alieleza ambazo zingetoa ulinzi wa kiroho. Hakikisha wanafunzi wanabaini na ku-elewa maneno makao (nyumba au boma), makanisa (sehemu ya kukutania, kama vile ma-tawi, kata, au vigingi), na tabernakulo (hekalu). Eleza kwamba “nguzo ya wingu na nguzo ya moto na kuwapa nuru wapate kusafiri mchana na usiku” rejea ulinzi na uongozi ambao Musa na watu wake walipokea kutoka kwa Bwana katika jangwa (ona Kutoka 13:21–22). Maneno haya yanatukumbusha juu ya ulinzi na uongozi tunaoweza kupokea kutoka kwa Bwana. Pia elezea kwamba Isaya alifananisha hekalu na makazi ya kinga dhidi ya joto na “maficho,” au makazi, dhidi ya dhoruba na mvua.• Ni lini umehisi ulinzi wa Bwana au mwongozo katika nyumba yako au katika kanisa?• Ni lini umewahi kupata msaada wa kiroho au kinga katika hekalu?• Ni aina gani ya watu wataishi katika nyumba na kuabudu katika makanisa na hekalu

yaliyoelezwa katika vifungu 5–6?• Tunaweza kufanya nini ili kufanya nyumba zetu na matawi au kata maeneo ya ulinzi

dhidi ya ulimwengu?Fupisha sura ya 12–15 kwa kueleza kuwa katika sura hizi tunajifunza kwamba kutii ma-agano yetu huleta baraka za ulinzi wa kiroho, wakati kuvunja maagano hutuacha bila ya ulinzi wa Bwana. Wahakikishie wanafunzi kwamba wanaweza kujenga katika maisha yao wenyewe mazingira kama ilivyoelezwa katika 2 Nefi 14:5–6.

2 Nefi 12:1–5; 15:26Isaya anatabiri kuhusu hekalu na Kanisa ya Bwana kujengwa katika siku za mwishoChora mchoro ufuatao wa mlima na hekalu ubaoni:

Page 128: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

113

2 nefi 12–15

• Kuna mifano gani kati ya mlima na hekalu? (Majibu yafaayo ni pamoja na kwamba yote ni mema na makuu na kwamba yote yanatuvutia kuangalia mbinguni.)

Alika wanafunzi kusoma 2 Nefi 12:2–5 kimya kimya, wakiangalia kile Mungu aliahidi kua-nzisha katika siku za mwisho na jinsi itakavyobariki maisha ya watu.• Je, neno “mlima wa Bwana” inahusu nini? (Ina marejeo maalum kwa Hekalu la Salt

Lake, lakini inaweza pia kuhusu mahekalu mengine ambayo Bwana ameanzisha katika siku za mwisho.)

• Ni baraka gani hutoka katika “nyumba ya Bwana katika siku za mwisho? (Kanuni moja ambayo wanafunzi wanaweza kutambua ni kwamba Mungu ameanzisha mahekalu ili kutufundisha njia zake na kutusaidia kutembea katika njia Zake [ona 2 Nefi 12:3].)

• Mahekalu hutusaidia kwa njia gani kutembea katika njia ya Bwana?Soma taarifa ifuatayo ambayo Rais Gordon B. Hinckley anazungumzia umuhimu wa mahekalu:“Haya majengo ya kipekee na ya ajabu, na ibada zinaziofanywa humo ndani, yanawakilisha umuhimu katika ibada zetu. Ibada hizi zinakuwa dhihirisho kubwa la teolojia yetu. Nawa-himiza watu wetu kila mahali, kwa uvutio wote ambao ninaweza, kuishi wakistahili kuwa na kibali cha hekalu, kupata kimoja na kukijali kama mali ya thamani, na kufanya juhudi kubwa zaidi kwenda katika nyumba ya Bwana na kushiriki katika roho na baraka zinazopa-tikana ndani yake” (“Of Missions, Temples, and Stewardship,” Ensign, Nov. 1995, 53).• Mahekalu yanawezaje kutusaidia kuepuka matokeo ya uovu kama ilivyoelezwa katika

2 Nefi 12–15? (Majibu yanaweza kujumuisha yafuatayo: Kufanya na kushika maagano ya hekalu hutuimarisha na familia zetu dhidi ya uovu. Ibada ya mara kwa mara ya hekalu inatukumbusha juu ya Mwokozi wetu, dhabihu Yake ya upatanisho, na ahadi tulizofanya. Tunaishi tukiwa wenye kustahili kushikilia kibali cha hekalu, tuna matumaini ya baraka ya uzima wa milele. Hilo tumaini hutuhimiza kuendelea kuishi kwa haki.)

• Hekalu limekuvutiaje na kukubariki?Wezesha mwanafunzi kusoma 2 Nefi 15:26 kwa sauti. Uliza darasa kutambua kishazi kina-chonyesha kile Bwana “atainua” ili kuwakusanya watu wa siku za mwisho. Eleza kwamba neno bendera inahusu kiwango, bendera, au bango linalotumika kama kituo cha mkutano au kama ishara ya kukusanyika, hasa katika vita.• Ni nini ndiyo “bendera kwa mataifa” ambayo Isaya alitabiri kuhusu?Soma kauli ifuatayo ya Rais Joseph Fielding Smith:“Hiyo bendera [ni] Kanisa la Yesu Kristo wa Watakatifu wa Siku za Mwisho, ambalo lilianzishwa kwa mara ya mwisho, kamwe haitaharibiwa au kupewa kwa watu wengine. Ilikuwa ni tukio kubwa zaidi ambalo ulimwengu uliwahi kuona tangu siku ambayo Mkombozi aliinuliwa juu kwa msalaba na kutoa upatanisho usio na mwisho na wa milele. Ilikuwa na maana zaidi kwa wanadamu kuliko kitu kingine chochote kilichowahi kutokea tangu siku ile” (Doctrines of Salvation, 3 vols. [1954–56], 3:254–55).• Ni kwa njia zipi Kanisa la Yesu Kristo wa Watakatifu wa Siku za Mwisho ni “bendera kwa

mataifa”?• Ni baraka gani zimekuja katika maisha yako kwa sababu ya ushiriki wako katika Kanisa?• Fikiria juu ya baraka zote ulizopokea na kweli ulizojifunza kama muumini wa Kanisa.

Ni kweli gani moja unaweza kushiriki na wengine ambayo inaweza kuwasaidia kukusa-nyika kwenye “bendera ya mataifa”?

Shuhudia kwamba Bwana ametubariki na msaada mkubwa kuishi kwa mafanikio katika siku za mwisho. Atabariki na kutakasa wale ambao wamechagua kuja Kwake. Tunapofanya na kuheshimu maagano na Yeye, Atatusaidia kutembea katika njia Zake.

Page 129: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

114

UtanguliziKatika 2 Nefi 17–20, Nefi anaandika matukio ya Isaya akijaribu kumshawishi mfalme wa Yuda na watu wake kuaamini katika Bwana badala ya ushirikiano wa dunia.

Kwa kutumia aina na vivuli, Isaya alitabiri kuhusu matu-kio ya siku yake mwenyewe, kuzaliwa kwa Yesu Kristo, na uharibifu wa waovu katika Ujio wa Pili wa Bwana.

Mapendekezo ya Kufundisha

2 Nefi 17–18; 19:1–7Watu wa ufalme wa Yuda wanashindwa kuweka matumaini yao kwa Yesu KristoAnza darasa kwa kuwauliza wanafunzi kuorodhesha majina mengi yenye maelezo ya Yesu Kristo kadiri wawezavyo. Andika majibu yao ubaoni. Kisha waalike kusoma 2 Nefi 17:14. Ongeza jina Imanueli  katika orodha kwenye ubao, au lizungushie kama lipo tayari. Alika wanafunzi kupata maana ya jina hili katika Mathayo 1:23 au katika Kamusi ya Biblia.• Ni nini maana ya jina Imanueli? (“Mungu pamoja nasi.”)Eleza kwamba umuhimu zaidi wa unabii wa Isaya kuhusu Imanueli unapatikana katika Mathayo 1:18–25. Alika mwanafunzi kusoma kifungu hiki kwa sauti.• Unabii wa Isaya kuhusu Imanueli ulitimia kwa njia gani?• Ni wakati gani umeona hali halisi ya Bwana kama Imanueli, au “Mungu pamoja nasi,”

katika maisha yako?Eleza kwamba 2 Nefi 19:6–7 ni mmoja wa unabii unaojulikana vyema juu ya Mwokozi. Soma kifungu hiki kwa sauti. Eleza kwamba kifungu hiki kina majina kadhaa ya Yesu Kristo. (Kama yoyote ya majina haya tayari hayamo kwenye ubao, yaongeze kwenye orodha.)• Ni yapi kati ya majina haya yanaeleza vyema jinsi unavyojisikia kuhusu Mwokozi? Kwa

nini?”Kabla ya kufundisha somo hili lote, wape wanafunzi usuli wa kihistoria kwa ajili ya 2 Nefi 17–18. Eleza kwamba sura hizi mara kwa mara humaanisha mataifa matatu madogo —Yuda, na Israeli, na Shamu—na wafalme wao, vile vile Himaya ya Ashuru, ambayo ilitaka kushinda mataifa matatu madogo. Ikiwa wanafunzi wanaweza kupata toleo la Biblia ya Watakatifu wa Siku za Mwisho, inaweza kuwa na manufaa kuwawezesha kurejea katika ramani 1, 3, na 5, ambazo zinaoyesha maeneo ya kijiografia yaliyo tajwa katika sura hizi. Unaweza pia kutaka kuwasaidia wanafunzi kuelewa muktadha wa sura hizi kwa kuo-nyesha picha ifuatayo (ilichukuliwa kutoka Victor L. Ludlow, Isaya: Mtume, Mwonaji, na Mshairi [1982], 140). Irejee kama inavyohitajika kote katika somo.

Nchi yuda Shamu israeli

Mji Mkuu yerusalemu dameski Samaria

Wilaya au kabila kuu

yuda aramu efraimu

Kiongozi ahazi (mfalme), wa nyumba ya daudi

Resini (mfalme) peka (mfalme), mwana wa Remalia

Andika muungano ubaoni.• Muungano ni nini? (Majibu yanayowezekana ni pamoja na chama, umoja, mkataba au

makubaliano.)• Ni sababu zipi zinazoweza kufanya taifa kutafuta muungano na mataifa mengine?

SOMO LA 33

2 nefi 17–20

Page 130: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

115

2 nefi 17–20

Eleza kwamba wakati wa huduma ya nabii Isaya katika Ufalme wa Yuda, wafalme wa Israeli na Shamu walitaka Mfalme Ahazi wa Yuda kujiunga nao katika muungano dhidi ya himaya yenye nguvu ya Ashuru. Wakati Mfalme Ahazi alipokataa, Israeli na Shamu walishambu-lia Yuda katika jitihada za kulazimisha muungano na kuweka mfalme mwingine kwenye enzi ya Yuda (ona 2 Nefi 17:1, 6). 2 Nefi 17–18 anaeleza ushauri ambao nabii Isaya alimpa Mfalme Ahazi wakati mfalme alipojaribu jinsi ya kulinda Yuda dhidi ya vitisho vitoleavyo na Israeli, Shamu, na Ashuru.Alika mwanafunzi kusoma 2 Nefi 17:1–2.• Unafikiri ina maanisha nini kwamba “moyo wa Ahazi ulitetemeka, na moyo wa watu

wake, jinsi vile miti ya kichaka hupeperushwa na upepo?” (Ahazi na watu wake wali-kuwa waoga na hawakuwa na uhakika juu ya kile ambacho wangefanya baada ya kusha-mbuliwa na Israeli na Shamu.)

Eleza kwamba kwa sababu Ahazi aliogopa Israeli na Shamu, alifikiria kutengeneza muu-ngano na Ashuru ili kulinda ufalme wake (ona 2 Mfalme 16:7). Isaya alimwambia Ahazi kwamba kama yeye (Ahazi) angeweza kuweka imani yake katika Bwana badala ya kufanya muungano wa kisiasa, Bwana angeulinda ufalme wa Yuda.Mkaribishe mwanafunzi kusoma 2 Nefi 17:3–8 kwa sauti. (Kama toleo la tafsiri ya Biblia ya King James linapatikana, alika wanafunzi kusoma Isaya 7:4, tanbihi a. Kama halipatikani, elezea kwamba vijinga vitoavyo moshi inahusu tochi inayoteketea. Bwana alikuwa akima-anisha, “Msitishike na shambulio hilo. Wafalme hao wawili wamebakiza moto kidogo.” Israeli na Shamu walikuwa wamemaliza nguvu zao. Hivi karibuni wangeangamizwa na Ashuru na hawangekuwa tishio tena kwa Yuda.)Weka wanafunzi kusoma kwa zamu kwa sauti kutoka 2 Nefi 17:9, 17–25. Wanaposoma, weka darasa kutambua kile ambacho Bwana alifunua kingetokea kwa watu wa Yuda kama watategemea muungano wa kisiasa badala ya kumtegemea Bwana.• Kulingana na mistari hii, ni nini kingetokea ikiwa Ahazi hangeamini katika Bwana?

(Yuda ingeangamizwa.)Alika mwanafunzi kusoma 2 Nefi 17:10–12 kwa sauti. (Unaweza kutaka kueleza kwamba wakati Isaya alipomwelekeza Ahazi kuuliza ishara, kwa kweli alikuwa akishawishi Ahazi kutafuta ushauri wa Bwana kuhusu tatizo lake. Wakati Ahazi alipokataa, alikuwa akisema kuwa hakuhitaji msaada wa Mungu, na kwamba alikusudia kutegemea uamuzi wake mwenyewe.)Alika mwanafunzi kusoma 2 Nefi 17:13–14. Elekeza wanafunzi mara nyingine kutambua neno Imanueli katika 2 Nefi 17:14 na maana yake, “Mungu pamoja nasi.”• Kwa nini ilikuwa ni muhimu kwa Ahazi kutaka Mungu awe pamoja naye wakati wa

shida ya taifa lake?• Kwa nini ni muhimu kwetu kumgeukia Bwana badala ya kutegemea tu maarifa yetu?Soma 2 Nefi 18:5–8 kwa sauti kwa wanafunzi. Unaposoma mstari wa 6, elezea kwamba neno Shiloa wakati mwingine inamaanisha Yesu Kristo. Unaposoma aya ya 8, elezea kishazi “atafika hata shingoni” kwa kusema kuwa kichwa, au mji mkuu, wa Yuda ulikuwa Yerusa-lemu. Isaya alitabiri ya kwamba watu wa Ashuru wangefika mpaka kuta za Yerusalemu—kwa maneno mengine, shingo ya mji. Unabii huu ulitimia wakati askari 185,000 wa Ashuru walipokwenda kushambulia Yerusalemu, wakisimamia kwenye kuta za mji. Bwana alitetea watu Wake kwa kutuma malaika kuharibu jeshi la adui. (Ona 2 Wafalme 19:32–35.)Alika wanafunzi kusoma 2 Nefi 18:9–10 kimya kimya, wakitafuta maonyo ya Bwana kwa wale ambao watashirikiana pamoja kupigana dhidi ya Yuda.• Nini ingekuwa matokeo kwa wale ambao wangepigana dhidi ya Yuda?• Kulingana na 2 Nefi 18:10, kwa nini mataifa haya yaharibiwe?Wakumbushe wanafunzi kuwa Mfalme Ahazi aliogopa tishio la Israeli na Shamu, na alikuwa anafikiri kuhusu kujiunga na vikosi vya Ashuru. Alika wanafunzi kusoma 2 Nefi 18:11–13 kimoyomoyo.• Ni nini Bwana alisema kuhusu iwapoYuda ilipaswa kuunda muungano (kujiunga na

Ashuru)?• Ni kwa nani ambaye Isaya aliwaambia watu waweke imani yao?Ili kuwasaidia wanafunzi kutumia sura hizi katika maisha yao, uliza:

Page 131: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

116

SoMo la 33

• Je, ni hatari gani zilizoko kwa kuweka imani yetu katika nguvu za ulimwengu na visha-wishi badala ya Bwana? (Wahimize wanafunzi kufikiria juu ya hali zinazoweza kuwaja-ribu kufanya maamuzi kwa ajili ya hofu.)

• Ni wakati gani umemgeukia Mungu kwa nguvu wakati awali ulikuwa ukigeukia vyanzo vingine? Mungu alikusaidiaje? Umejifunza nini kutokana na uzoefu huo?

Shuhudia kuwa Mungu atakuwa pamoja na sisi tunapomtumaini, hata wakati wa shida na hofu. (Unaweza kutaka kuandika kanuni hii ubaoni.)

2 Nefi 19:8–21; 20:1–22Isaya anaeleza uharibifu wa waovu katika Ujio wa PiliFupisha muktadha wa kihistoria wa 2 Nefi 19–20 kwa kuelezea kuwa Ahazi alikataa mpa-ngo wa Isaya na kuamua kufanya muungano na Ashuru (ona 2 Wafalme 16:7–20). Yuda ikawa nchi ya kibaraka, ikilipa kodi kwa Ashuru kwa ajili ya ulinzi dhidi ya tishio la Shamu na Israeli. Kama Isaya alivyotabiri, Ashuru hatimaye ilishinda falme hizi ndogo —Dama-eski (Shamu) mnamo 732 K.K. na Samaria (Israeli) mnamo 722 K.K. Ashuru pia ilikuwa imetawala kote Yuda, isipokuwa Yerusalemu, kufikia 701 K.K.Eleza kwamba wakati Ashuru iliteka Shamu na Israeli na kuzingira mji mkuu wa Yuda, Yerusalemu, Ahazi hakuwa tena mfalme wa Yuda. Mfalme mwenye haki, Hezekia, alikuwa katika kiti cha enzi wakati huo. Kwa sababu Hezekia aliweka tumaini lake kwa Bwana, Bwana alilinda mji wa Yerusalemu dhidi ya kuzingirwa na jeshi la Ashuru. Wakati wa usiku, malaika wa Bwana alipiga kambi ya Waashuri. Asubuhi, maaskari 185,000 katika jeshi la Waashuri walipatikana wamekufa (ona 2 Wafalme 19:34–35; 2 Mambo ya Nyakati 32:21; Isaya 37:36).Unabii wa Isaya katika 2 Nefi 19–20 unazingatia adhabu zitakazokuja juu ya Israeli na Yuda kwa mkono wa Waashuri. Isaya alionya Israeli kwamba uharibifu na uhamisho karibu ungewajia, kisha alitabiri mashambulizi ya baadaye kwa Yuda. Unabii wa Masiya wa 2 Nefi 17–18 umeendelezwa zaidi katika 2 Nefi 19–20. Unabii wa Immanuel umefafanuliwa katika 2 Nefi 19 wakati Isaya anapoahidi mwanga mpya na kiongozi mpya: Hezekia kihistoria, na Masiya kinabii. Huu ni mfano wa unabii na utimizaji kwa njia mbili. Pia ni mfano wa kiele-lezo, maana ya kwamba tukio moja linatumika kama unabii wa tukio la siku zijazo. Unabii wa Isaya wa uharibifu Waashuri katika 2 Nefi 20 ni aina ya uharibifu wa waovu wakati wa Ujio wa Pili.Andika marejeo ya maandiko yafuatayo ubaoni: 2 Nefi 19:12, 17, 21; 20:4. Wezesha wana-funzi kutambua kishazi kinachorudiwa katika mafungu haya. Andika kishazi hicho ubaoni. “Hata baada ya haya hasira yake haitapunguka, lakini bado amenyosha mkono wake.” Eleza kwamba mistari hii inahusu madhara yanayowajia watu ambao wanamwasi Bwana, na kukataa kutubu. Kinaeleza hasira ya Bwana kwa watu wanaoendelea katika dhambi.Eleza kwamba katika mafungu mengine ya maandiko, maneno sawa na hayo hutumika kueleza huruma ya Bwana kwa wale watakaotubu. Ingawa Yeye ni Mungu wa haki, Yeye pia ni mwenye huruma kwa wale watakao kuja Kwake. Alika mwanafunzi kusoma 2 Nefi 28:32 kwa sauti. Kisha soma taarifa ifuatayo na Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Mi-tume Kumi na Wawili:“Kwenu wote mnaofikiri kwamba mmepotea au hamna matumaini, au mnaofikiri kuwa umefanya mengi sana yenye makosa zaidi na kwa muda mrefu sana, kwa kila mmoja wenu ambaye ana wasiwasi kwamba amekwama mahali fulani katika nyanda baridi ya maisha na kuvunja mkokoteni wako katika harakati, mkutano huu mkuu unatoa mwito thabiti wa Yehova, ‘Mkono[wangu] umenyoshwa bado’[ona Isaya 5:25; 9:17, 21]. ‘Nitawa-nyoshea mkono wangu,’Alisema, ‘[na ingawa] watanikana, walakini, Nitawarehemu, . . . kama watatubu na kunijia mimi; kwani mkono wangu umenyooshwa siku yote, asema Bwana, Mungu wa Majeshi’ [2 Nefi 28:32]. Rehema yake inadumu hata milele, na mkono Wake umenyoshwa hata sasa. Wake ni upendo msafi wa Kristo, hisani isiyokosa kufaulu kamwe, hiyo huruma inayodumu hata wakati nguvu zingine zote zimetoweka [ona Moroni 7:46–47]” (“Prophets in the Land Again,” Ensign, Nov. 2006, 106–7).

MuhtasariWakati mwingine hauta-weza kufundisha kichwa chote cha maandiko yaliyopangwa kwa ajili ya siku. Usife moyo. Ambapo kichwa kiku-bwa cha maandiko kina-jumuisha sura kadhaa, unaweza kuhitajika ku-fupisha matukio, kichwa cha hadithi, na, mara kwa mara, mafundisho. Vichwa vya sura, vifaa kutoka kwa mwongozo wa somo, na ufahamu kutoka kwa mafunzo yako mwenyewe vitaku-ongoza katika maanda-lizi yako kwa kufupisha kwa ufanisi.

Page 132: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

117

2 nefi 17–20

Waalike wanafunzi kueleza kwa maneno yao wenyewe ukweli waliojifunza kutoka katika mistari hii. (Hakikisha wanafunzi wanaelewa kwamba Yesu Kristo ni Mungu wa hukumu na huruma. Rehema yake imeenezwa kwa wale wanaotubu na kushika amri Zake.)• unawezaje kutumia kanuni hii katika maisha yako?Isaya alitabiri kwamba katika siku za mwisho watu wa Bwana watarudi Kwake na kusitisha kutegemea mahusiano maovu kwa ajili ya usalama na amani. Ikiwa wanafunzi wanaweza kupata toleo la Biblia ya King James ya Watakatifu wa siku za Mwisho, waalike kusoma Isaya 10:20, tanbihi c, na ueleze maana ya neno kukaa. Unaweza kutaka kueleza kwamba, kwa muktadha huu, neno kukaa ina maana ya kuegemea, kutegemea juu ya, au kuweka matumaini katika kitu fulani au mtu fulani. Wahakikishie wanafunzi kwamba tunapoweka matumaini yetu katika Bwana, hatuhitaji kuhofia hukumu itakayokuja kwa watu wa dunia itakayotangulia Ujio wa Pili.

Page 133: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

118

UtanguliziWingi wa unabii wa Isaya katika Kitabu cha Mormoni unahusu siku za mwisho. Alitabiri kuhusu Urejesho wa injili, Nabii Joseph Smith, Ujio wa Pili, na uharibifu wa waovu. Alitabiri kwamba Bwana “atawatwekea

mataifa bendera" ili kuwakusanya watu Wake katika siku za mwisho (ona 2 Nefi 21:11–12). Isaya pia alishu-hudia kwamba Bwana angepata ushindi juu ya Shetani na kukaribisha Milenia, kipindi cha amani na furaha.

Mapendekezo ya Kufundisha

2 Nefi 21:1–5, 10–12Isaya anatabiri Urejesho wa injili ya Yesu Kristo katika siku za mwishoOnyesha picha ya Moroni akimtokea Joseph Smith katika chumba chake (62492; Go-spel Art Book [2009], no. 91). Eleza kwamba wakati Moroni alimtokea Joseph Smith kwa mara ya kwanza, “alinukuu sura ya kumi na moja ya Isaya, akisema kuwa ilikuwa karibu kutimizwa”(Joseph Smith—History 1:40). Unabii katika Isaya 11 unapatikana pia katika 2 Nefi 21.Alika wanafunzi kusoma 2 Nefi 21:1 kimya. Elekeza mawazo yao katika maneno “fimbo kutoka Shina la Yese.” Kisha waalike kusoma 2 Nefi 21:10 kimya kimya. Elekeza mawazo yao katika kishazi cha “mzizi wa Yese.” Unaweza kutaka kupendekeza kwamba wana-funzi waweke alama kwenye vishazi hivi. Eleza kwamba Nabii Joseph Smith alipokea ufunuo kuhusu vishazi hivi. Waalike wanafunzi kugeukia Mafundisho na Maagano 113:1–6. Soma fungu hili kwa sauti. Kabla ya kusoma, uliza wanafunzi kusoma pamoja na kuangalia maana ya hivi vishazi. Unaweza kutaka kuandika maana hii ubaoni, kama inavyoonekana hapa chini. Unaweza kutaka kuwahimiza wanafunzi kuandika maana hii katika maandiko yao.

Shina la Yese—Yesu KristoFimbo—mtumishi wa Kristo “ambaye juu yake umewekwa uwezo mwingi”Mzizi wa Yese—mtu katika siku za mwisho ambaye atashikilia ukuhani na “funguo za ufalme”

Uliza mwanafunzi kusoma kauli ifuatayo na Mzee Bruce R. McConkie wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili. Uliza darasa kusikiliza utambulisho wa “fimbo” na “mzizi wa Yese.”“Je tumekosea kwa kusema kwamba nabii anayetajwa hapa ni Joseph Smith, ambaye kwake ukuhani ulitokea, ambaye alipokea funguo za ufalme, na aliyeinua bendera kwa mkusanyiko wa watu wa Mungu katika kipindi chetu? Na yeye si pia ni ‘mtumishi katika mikono ya Kristo, ambaye ni wa sehemu ya uzao wa Yese na vile vile ni wa Efraimu, au wa nyumba ya Yusufu, ambaye juu yake umewekwa uwezo mwingi’?” (The Millennial Messiah: The Second Coming of the Son of Man [1982], 339–40).Alika mwanafunzi kusoma 2 Nefi 21:10, 12 kwa sauti. Uliza darasa kutafuta maneno na vishazi vinavyohusiana na Joseph Smith na Urejesho wa injili na Kanisa la Bwana. Kabla ya mwanafunzi kusoma, unaweza kutaka kuwakumbusha kwamba neno bendera inahusu kanuni, bendera, au bendera ambayo inatumika kama kituo cha mkutano au kama ishara ya kukusanyika (angalia somo la 32).• kazi ya Joseph Smith inatimizaje unabii kuhusu ukoo wa Yese?• tunakusanyika kwa njia gani leo kama waumini wa Kanisa? tunainua bendera kwa njia

gani ili kuwasaidia wengine kujua pa kukusanyika?Shuhudia kwamba Bwana amerejesha injili Yake na Kanisa Lake kupitia kwa Nabii Joseph Smith na sasa anawakusanya watu Wake katika siku za mwisho.

Kutoa ushuhudaUshuhuda ni tangazo rahisi, la moja kwa moja la imani. Unapojiandaa kufundisha kila somo, omba kwa ajili ya Roho kukusaidia kujua wakati wa kushuhudia kweli unazojadili. Unaweza kushawishiwa kutoa ushuhuda mara kadhaa wakati wa somo, si tu katika hitimisho.

SOMO LA 34

2 nefi 21–24

Page 134: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

119

2 nefi 21–24

2 Nefi 21:6–9; 22Isaya anaelezea MileniaWaulize wanafunzi kufikiria rafiki ambaye ni muumini wa kanisa jingine amewauliza kile wanachoamini juu ya Milenia. Wawezeshe kusoma 2 Nefi 21:6–9 na 22:1–6 kimya kimya, wakiangalia kweli wanazoweza kueleza katika mazungumzo hayo. Waalike kuandika mawazo yao katika shajara zao za kujifunza maandiko au daftari za darasani. Ili kuwasaidia kujadili walichopata, uliza baadhi au wote maswali yafuatayo:• Maelezo katika 2 Nefi 21:6–8 yanaonyesha nini kuhusu hali ya nchi wakati wa Milenia?• Kulingana na 2 Nefi 21:9, kwa nini dunia itakuwa mahali pa amani wakati wa Milenia?

(Wasaidie wanafunzi kuelewa kwamba wakati wa Milenia, dunia itakuwa mahali pa amani kwa sababu itakuwa na utimilifu wa maarifa ya Bwana.)

• Kumfahamu Bwana kutatusaidia vipi kuishi kwa amani zaidi sasa?• Katika 2 Nefi 22:1–6, Isaya anaelezea roho ya ibada ambayo watu watapata wakati wa

Milenia. Tunawezaje kuendeleza mtazamo huo hivi leo?• Je, ni vipengele vipi vya Milenia ambavyo ungependa kuweka katika maisha yako sasa

hivi? (Wahimize wanafunzi kutafakari kile wanaweza kufanya ili kupokea baadhi ya baraka hizi katika maisha yao.)

2 Nefi 23–24Isaya anafundisha kwamba waovu wataangamia na kwamba Bwana atakuwa na huruma juu ya watu WakeEleza kwamba katika 2 Nefi 23, Isaya anatabiri juu ya uharibifu wa Babeli na kuulingani-sha na uharibifu wa waovu wakati wa Ujio wa Pili wa Mwokozi. Alika wanafunzi kusoma utangulizi wa “Babeli” katika Kamusi ya Biblia. Eleza kwamba katika vifungu kadhaa vya maandiko, neno Babeli kwa kawaida linamaanisha uovu wa ulimwengu. Isaya alitabiri ya kwamba uharibifu mkuu ungewafika waovu katika Babeli, na katika siku za mwisho.Ili kuwasaidia wanafunzi kutambua matokeo kwa waovu katika siku za mwisho, waweze-she kusoma 2 Nefi 23:1, 5–9, 11, 15, 19, na 22 kimya kimya.Elezea kwamba Isaya alielezea kuanguka kwa Ibilisi, au Shetani, kama mfano mwingine wa jinsi waovu watakavyoangamia. Alika mwanafunzi kusoma 2 Nefi 24:12–16 kwa sauti.• Ni vishazi vipi katika mistari hii vinavyoonyesha kiburi cha Shetani?• Je, 2 Nefi 24:16 inaelezaje jinsi tutahisi kuhusu Shetani kama tungeweza kumwona jinsi

alivyo?Alika mwanafunzi kusoma kauli ifuatayo ya Rais Ezra Taft Benson:“Katika baraza kabla ya hapa duniani, kilikuwa ni kiburi ambacho kilimwangusha Lusiferi, ‘mwana wa asubuhi.’ (2 Ne. 24:12–15; ona pia M&M 76:25–27; Musa 4:3.) . . . Katika baraza kabla ya hapa duniani, Lusiferi alitoa pendekezo lake kwa ushindani na mpango wa Baba kama ulivyotetewa na Yesu Kristo. (Ona Musa 4:1–3.) Alitaka kuheshimiwa juu ya wengine wote. (Ona 2 Ne. 24:13.) Kwa ufupi, nia yake yenye kiburi ilikuwa kumwondoa Mungu kwenye ufalme (Ona M&M 29:36; 76:28.)” (“Beware of Pride,” Ensign, Mei 1989, 4–5).Elekeza mawazo ya wanafunzi katika neno la Bwana wakati wa kuhitimisha 2 Nefi 23:22 : “Kwani nitawarehemu watu wangu, lakini waovu wataangamia.” Unaweza kutaka kuwa-himiza wanafunzi kutia alama kwenye tamko hili katika maandiko yao. (Kumbuka kwa-mba sentensi ya mwisho katika aya hii haionekani katika mstari sambamba katika kitabu cha Isaya katika tafsiri ya Biblia ya King James. Hii inaonyesha kwamba mabamba ya shaba yalikuwa na baadhi ya habari isiyopatikana katika Biblia.)• Unafikiri ina maanisha nini kuwa miongoni mwa watu wa Mungu?Waulize wanafunzi kadhaa kusoma 2 Nefi 24:1–7, 24–27 kwa sauti, wakichukua zamu kusoma kifungu kimoja au viwili. Alika darasa kutafuta ahadi za Bwana kwa watu Wake. Wahimize kuelezea maoni yao kila mmoja kwa mwingine. Unaweza kufikiria kuwa na mwanafunzi ambaye ataandika mitazamo hiyo ubaoni.• aya hizi zinashirikisha ujumbe gani kwa wale ambao wanateseka kwa sababu ya uovu

wa watu wengine?

Page 135: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

120

SoMo la 34

• Ni ushahidi gani wa furaha na matumaini unaoweza kuona katika mafungu haya?Hakikisha kuwa wanafunzi wanaelewa kwamba Bwana atakuwa na huruma kwa watu wake, lakini waovu wataangamia. Wasaidie wanafunzi kuelewa kwamba unabii wa Isaya katika 2 Nefi 21–24 unaangazia moja ya jumbe kuu ya Kitabu cha Mormoni —kuwa watiifu watafanikiwa na wasiotii wataangamia. Shuhudia kwamba tunaweza kuishi katika haki na kufanikiwa hivi leo tunapotazamia Milenia

Tangazo na Habari za usili2 Nefi 21:1. “Na tawi litamea kutoka mizizi yake”Mzee Bruce R. McConkie wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alielezea tawi lililotajwa katika 2 Nefi 21:1:

“‘Tazama siku zinakuja, asema Bwana, nitakapomchi-pushia Daudi Chipukizi la haki, naye atamiliki Mfalme atafanya hukumu Mfalme atatawala na kufanikiwa . . .’ (Yer. 23:5–6). Hiyo ni kusema, Mfalme atakayetawala binafsi juu ya nchi wakati wa Milenia atakuwa chipukizi

aliyekua kutoka kwa nyumba ya Daudi. Atafanya hukumu na haki katika nchi yote kwa sababu yeye ni Bwana Yehova, hata yule tunayemwita Kristo. Kwamba Chipukizi la Daudi ni Kristo ni wazi kabisa. Tutaona sasa kwamba anaitwa Daudi, kwamba ni Daudi mpya, Daudi wa milele, ambaye atatawala milele katika kiti cha enzi cha baba yake wa kale (ona Yeremia 30:8–9)” (The Pro-mised Messiah: The First Coming of Christ [1978], 193).

Mawazo ya Ziada ya Kufundisha2 Nefi 21:9. “Dunia yote itajaa elimu ya Bwana”Wezesha mwanafunzi kusoma 2 Nefi 21:9 kimya kimya. Elezea taarifa ifuatayo ya Mzee Dallin H. Oaks wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili:

“Katika siku zetu tunapitia mlipuko wa elimu juu ya uli-mwengu na watu wake. Lakini watu wa ulimwengu ha-wapati uzoefu wa upanuzi wa kulinganishwa wa elimu kuhusu Mungu na mpango wake kwa ajili ya watoto

wake. Juu ya swala hilo, kile ulimwengu unahitaji si elimu zaidi na teknolojia lakini haki zaidi na ufunuo. Natamani siku ya unabii wa Isaya wakati ‘dunia yote itajaa elimu ya Bwana’. (Isa. 11:9; 2 Ne. 21:9.)” (“Alter-nate Voices,” Ensign, May 1989, 30).• Kulingana na Mzee Oaks, ulimwengu unahitaji nini?• Tunawezaje kusaidia kuleta utimilifu wa unabii wa

Isaya?

Page 136: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

121

UtanguliziKuendelea kusisitiza umuhimu wa unabii wa Isaya, Nefi alieleza kuwa mtu yeyote ambaye ana roho ya unabii anaweza kuja kuelewa na kufahamu maneno ya Isaya. Ameelezea madhumuni ya uandishi wake: “kuwashawi-shi watoto wetu, na pia ndugu zetu, kumwamini Kristo,

na kupatanishwa na Mungu” (2 Nefi 25:23). Aliwaalika wote kumwamini Yesu Kristo na “kumwabudu kwa uwezo [wao] wote, akili, na nguvu, na nafsi [zao] zote; (2 Nefi 25:29).

Mapendekezo ya Kufundisha

2 Nefi 25:1–8Nefi anafundisha kwamba tunaweza kuelewa maneno ya Isaya tunapokuwa na roho wa unabiiOnyesha kifuli ambalo haliwezi kufunguliwa bila ufunguo (au chora picha ya kufuli na ufunguo ubaoni) Onyesha kwamba wakati watu wanataka kuweka mali yenye thamani salama, mara nyingi wao huyafungia. Wanaweza kuhifadhi ufunguo muhimu tu wa kufuli, au wanaweza kutoa chapa ya ufunguo kwa rafiki anayeaminika au mwanafamilia.

Eleza kwamba Nefi alijua kwamba unabii wa Isaya “utawasaidia sana” (2 Nefi 25:8). Hata hivyo, hakuuweka siri. Hata pia alifunza kuhusu ufunguo kwa mtu yeyote anayetaka kujua maana ya maneno ya Isaya. Alika mwanafunzi kusoma sentensi ya kwanza katika 2 Nefi 25:4. Uliza darasa kutafuta ufunguo wa kuelewa maneno ya Isaya.• Ni ufunguo upi ulioupata? (“Roho ya Unabii.”)Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa maana ya kuwa na “roho ya unabii,” soma taarifa ifua-tayo kutoka katika Mwongozo wa Maandiko:“Unabii una maneno matakatifu au maandiko, ambayo mtu anapata kwa njia ya ufunuo kutoka kwa Roho Mtakatifu. Ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii (Ufunuo. 19:10). Una-bii unaweza kuhusiana na mambo ya zamani, sasa, na yajayo. Wakati mtu anatoa unabii, yeye husema au huandika yale ambayo Mungu anataka yeye ajue, kwa faida yake mwe-nyewe au ya wengine. Watu wanaweza kupokea unabii au ufunuo kwa ajili ya maisha yao wenyewe”(Guide to the Scriptures, “Prophecy, Prophesy,” scriptures.lds.org).Wasaidie wanafunzi kuona kwamba ufahamu wao wa maneno ya Isaya utaongezeka kama wana (1) tafuta uongozi wa Roho Mtakatifu na (2) kuwa na ushuhuda wa Yesu Kristo na hamu ya kujifunza Kwake. Watakapoyakabili maneno Isaya kwa njia hii, siku zote waki-tafuta njia ambayo unabii wake unashuhudia juu ya Mwokozi, wataweza kujifunza kile Mungu anawataka kujua, kwa faida yao wenyewe au kwa faida ya wengine.Eleza kwamba Nefi alishiriki mawazo mengine ambayo yanaweza kuongeza ufahamu wetu wa maneno ya Isaya. Waulize wanafunzi kusoma 2 Nefi 25:1 kimya kimya, wakitafuta kwa nini watu wengi wa Nefi waliuona unabii wa Isaya kuwa vigumu kuelewa.• Ulipata nini? (Hawakujua “kuhusu mtindo wa kutoa unabii miongoni mwa Wayahudi.”)• Kulingana na kile ulichokisoma kuhusu maneno ya Isaya, je ni zipi sifa za unabii wa

Wayahudi wa kale? (Majibu yanaweza kujumuisha kwamba Isaya na manabii wengine walitumia ishara na lugha ya kishairi.)

SOMO LA 35

2 nefi 25

Page 137: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

122

SoMo la 35

• Unaposoma maneno ya Isaya, kwa nini ni muhimu kufahamu mtindo huu wa kutoa unabii?

Eleza kwamba wazo lingine la kusaidia hupatikana katika 2 Nefi 25:5–6. Alika mwanafunzi kusoma mistari hii kwa sauti. Uliza darasa kuangalia uzoefu ambao Nefi alipata uliomsai-dia kuelewa maneno ya Isaya.• Kwa nini unafikiri kuishi Yerusalemu kulimsaidia Nefi? Kulingana na kile ulichokisoma

kuhusu maneno ya Isaya, kwa nini unafikiri ilimsaidia Nefi kuweza “kuona vitu vya Wayahudi” na “kujua kuhusu eneo karibu lote linaloizunguka” Yerusalemu?

• Tufanye nini ili kupata ufahamu wa mambo haya? (Tunaweza kujifunza utamaduni, historia, na jiografia ya Israeli ya kale.)

Soma 2 Nefi 25:7–8 kwa wanafunzi. Unaposoma, eleza kwamba unabii wa Isaya ni wa thamani kubwa kwetu tunapoona kwamba umetimia. Ili kuelezea ukweli huu, uliza:• Katika siku chache zilizopita, ni unabii gani tuliosoma ambao tayari umetimia? (Wana-

funzi wanaweza kukumbuka unabii kuhusu Hekalu la Salt Lake [ona 2 Nefi 12:2–3], ku-zaliwa kwa Yesu Kristo (Ona 2 Nefi 19:6], na Joseph Smith [ona 2 Nefi 21:1, 10].) Katika njia zipi utabiri huu unakuwa wa maana zaidi unapoona kwamba umetimia?

Ili kuhimitisha sehemu hii ya somo, eleza matumaini yako kwamba wanafunzi wanaweza kukua katika ufahamu wao wa maneno ya Isaya wanapotafuta roho ya unabii. Eleza kwa-mba wanaweza kuimarisha ufahamu wao kwa kujifunza kuhusu mtindo wa kutoa unabii miongoni mwa Wayahudi wa kale na utamaduni, historia, na jiografia ya Israeli ya zamani.

2 Nefi 25:9–19Nefi anatoa unabii kuhusu kutawanyika na kukusanyika kwa WayahudiFupisha 2 Nefi 25:9–19 kwa kusema kwamba Nefi alitoa unabii kuhusu Wayahudi na nchi yao katika Yerusalemu na maeneo yanayoizingira. Alisema kuwa Wayahudi ambao wali-kuwa wamepelekwa utumwani Babeli baada ya uharibifu wa Yerusalemu watarudishwa “katika nchi yao ya urithi” (ona 2 Nefi 25:9–11). Yesu Kristo, Masiya, ataishi kati yao, lakini wengi watamkataa na kumsulubisha (ona 2 Nefi 25:12–13). Baada ya kifo na Ufufuo wa Mwokozi, Yerusalemu ingeharibiwa tena, na Wayahudi wangetawanywa na kuumizwa na mataifa mengine (ona 2 Nefi 25:14–15). Hatimaye waliamini katika Yesu Kristo na Upatani-sho Wake, na Bwana atawarudisha “kutoka kwenye hali yao ya kupotea na kuanguka”(ona 2 Nefi 25:16–19).

2 Nefi 25:20–30Nefi anashuhudia juu ya Yesu KristoWaulize wanafunzi kufikiria kuhusu namna wanavyoweza kukabiliana na mtu ambaye anadai kuwa Watakatifu wa Siku za Mwisho hawaamini katika Yesu Kristo. Unaweza kuuliza mwanafunzi moja au wawili kuelezea kwa ufupi kuhusu uzoefu walizopata wakati watu wengine wanapowapatia changamoto juu ya imani yao katika Yesu Kristo. Wanafunzi wanaposoma na kujadili 2 Nefi 25:20–30, waalike kuangalia vifungu wanavyoweza kushi-riki katika hali kama hizo.Waulize wanafunzi kutambua“njia iliyo sawa” katika 2 Nefi 25:28–29. Baada ya kugundua kuwa “njia iliyo sawa ni kuamini katika Kristo, kutomkana,” andika kwenye ubao Kwa nini kuamini katika Yesu Kristo ni njia iliyo sawa. Kisha waulize wanafunzi kupekua 2 Nefi 25:20, 23–26, wakitafuta kwa nini kuamini katika Yesu Kristo ni njia iliyo sawa. Waalike kuandika majibu yao ubaoni chini ya kichwa ulichoandika. Majibu yanaweza kujumuisha yafuatayo:Wokovu huja kwa njia ya Yesu Kristo.Kwa sababu ya Yesu Kristo, tunaweza kuokolewa kwa neema baada ya yote tunayo-weza kufanya.Kwa njia ya Upatanisho wa Mwokozi, tunaweza kupokea ondoleo la dhambi zetu.Alika mwanafunzi kusoma 2 Nefi 25:23 and 2 Nefi 10:24 kwa sauti. Eleza kwamba mis-tari hii inajumuisha neno kupatanisha, ambalo linamaanisha kuwaleta watu au vitu katika mapatano au makubaliano kimoja kwa kingine.• Katika ya mistari hizi miwili, manabii wanatuhimiza kujipatanisha wenyewe na Mungu.

Unafikiri hii inamaanisha nini?

2 Nefi 25:23, 26 ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Unaweza kutaka kuwahimiza wanafunzi kuutia alama katika maandiko yao. Rejea wazo la mafundi-sho mwishoni mwa somo ili kuwasaidia wanafunzi na umahiri wao wa kifungu hiki.

Page 138: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

123

2 nefi 25

Eleza kwamba vifungu hivi viwili pia vinajumuisha neno neema. Neema ni zawadi kutoka kwa Baba wa Mbinguni inayotolewa kupitia kwa Mwanawe, Yesu Kristo. Neno neema, kama inavyotumika katika maandiko, inahusu hasa nguvu za kuwezesha na uponyaji wa kiroho inayotolewa kupitia kwa huruma na upendo wa Yesu Kristo.• Ni nini 2 Nefi 10:24 na 25:23 zinafundisha juu ya uhusiano kati ya neema na juhudi zetu?Alika wanafunzi kutumia kile walichojifunza kwa kuandika majibu ya maswali yafuatayo katika jarida zao ya masomo ya maandiko au daftari za darasa. Unaweza kutaka kuandika swali ubaoni.• Ina maanisha nini kwako kuokolewa kwa neema?Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa madai ya Nefi katika 2 Nefi 25:24–25 kwamba sheria ilikuwa imekufa kwa watu wake, eleza kuwa alikuwa akimaanisha sheria ya Musa. Sheria hiyo, pamoja na mfumo wake wa sherehe, matambiko, ishara, na amri, ikiwemo dhabihu za wanyama, ilikuwa bado inatumika wakati wa Nefi. Nefi na wengine walijua kuwa sheria itatimizwa kupitia kwa Upatanisho wa Yesu Kristo. Baada ya Upatanisho, wanafunzi wa Mwokozi hawangehitajika tena kushika sheria ya Musa. Lakini Wanefi waaminifu waliende-lea kutii sheria kwa wakati huu, hata wakijua kwamba sheria ya sasa itabadilishwa siku moja.Wakati Nefi aliposema kuwa sheria ilikuwa imekufa kwake na kwa wengine, alimaanisha kwamba sheria haitawaokoa. Walitii sheria kwa sababu walitaka kuwa watiifu na kwa sababu walijua sheria iliwaelekeza kwa Yesu Kristo, ambaye angewaletea wokovu.• Tunaweza kujifunza nini kutoka 2 Nefi 25:23–26 kuhusu sababu ya kuzishika amri?• Utafanya nini kuweza “kuzungumza kuhusu Kristo” na “kufurahia katika Kristo”?

(2 Nefi 25:26). Utafanya nini ili kuwasaidia wengine kuamini katika Kristo?Waulize wanafunzi kuelezea vufungu walivyogundua ambavyo vitawasaidia kujibu madai kwamba Watakatifu wa Siku za Mwisho hawaamini katika Yesu Kristo. Waulize waeleze kwa nini wanapenda vifungu hivyo.Elezea ushuhuda wako juu ya kweli ulizojadili leo. Unaweza kutaka pia kuwapa wanafunzi nafasi ya kutoa ushuhuda wa kweli hizi.

Umahiri wa maandiko—2 Nefi 25:23, 26{Fahamu: Fikiria kutumia wazo la kufundishia wakati wa sehemu ya mwisho ya somo hili Ikiwa huna muda wa kutumia wazo hili katika somo hili, unaweza kulitumia katika somo jingine kama marekebisho.Il kuwasaidia wanafunzi kukariri 2 Nefi 25:26, moja ya mistari katika kifungu hiki cha uma-hiri wa maandiko, andika yafuatayo ubaoni:

TunazungumzaTunarahiaTunahubiriTunatoa unabiiTunaandikaIli watoto wetu . . .Wajue asili . . .Msamaha wa . . .

Alika wanafunzi kutumia neno ishara kwenye ubao ili kukariri 2 Nefi 25:26. Baada ya ku-rudia mstari mara chache, uliza iwapo yeyote katika darasa yuko tayari kukariri aya kutoka katika kumbu kumbu hii. Kisha alika wengine wa wanafunzi kukariri aya kwa pamoja bila kuangalia kwenye ubao. Kuhitimisha, unaweza kutaka kushauri kwamba kuna thamani katika kusikiliza kwa makini wakati wazazi, viongozi, na walimu wanafanya kazi kutusha-wishi kuangalia kwa Mwokozi.Toa kipande cha karatasi kwa kila mwanafunzi. Alika wanafunzi kuandika barua kwa watoto wao wa baadaye, kuwahimiza kuweka maisha yao kwa Yesu Kristo. Wanafunzi wa-naweza kutaka kuweka barua zao katika maandiko yao ili kuzihifadhi kwa siku zijazo.

Kuwahimiza wanafunzi kutoa ushuhudaWanafunzi wanaposikia kila mmoja akishuhu-dia ukweli wa injili, wanaweza kukua katika ufahamu wao wa kanuni za injili na tamaa yao ya kutumia kanuni hizo katika maisha yao. Unaweza kuwahi-miza wanafunzi kutoa ushuhuda wao darasani kwa kuuliza maswali yanayoanza na vishazi kama vile “Jinsi gani ulipata ushuhuda wako wa . . .” au “Ni lini kwa mara ya kwanza uliweza kujua kwamba . . .” au “Kwa jinsi gani unaweza kueleza au kushuhudia juu ya . . .”Baada ya mwanafunzi mmoja kutoa ushahidi wa kweli, unaweza kuuliza, Nani mwengine anaweza ku-shuhudia ukweli huu?”

Page 139: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

124

Mafunzo ya Masomo ya Nyumbani2 Nefi 11–25 (Kitengo cha 7)

Vifaa vya maandalizi kwa Mwalimu wa Mafunzo- NyumbaniMuhtasari wa Masomo ya Mafunzo ya kila siku- NyumbaniMuhtasari ufuatao wa mafundisho na kanuni ambao wana-funzi walijifunza waliposoma 2 Nefi 11–25 (kitengo cha 7) haidhamiriwi kufundishwa kama sehemu ya somo lako. Somo unalofundisha huzingatia tu machache ya mafundisho haya na kanuni. Fuata ushawishi wa Roho Mtakatifu unapofikiria mahitaji ya wanafunzi wako.

Siku ya 1 (2 Nefi 11–16)Isaya alieleza kiburi cha Israeli ya kale na uovu na hukumu zilizowasuburi. Pia alitabiri kuhusu hekalu litakalojengwa katika siku za mwisho na kufundisha kwamba Mungu huaanzisha hekalu ili kutufundisha njia Zake na kutusaidia kutembea katika njia Zake. Isaya aliona Bwana na akasafi-shwa kutoka kwa dhambi. Kutokana na uzoefu wa Isaya, wanafunzi walijifunza kwamba tunaweza kutakaswa dhambi zetu kupitia kwa Upatanisho wa Yesu Kristo.

Siku ya 2 (2 Nefi 17–20)Isaya anarudi ufalme wa Yuda kwa kushindwa kuweka tumaini lao kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Wana-funzi walijifunza kwamba Mungu atakuwa na sisi wakati tumeweka tumaini Kwake, hata wakati wa shida na hofu. Isaya alieleza uharibifu wa waovu wakati wa Ujio wa Pili na kufundisha kwamba Yesu Kristo ni Mungu wa hukumu na huruma, na rehema Yake inawafikia wote wanaotubu, na kushika amri Zake.

Siku ya 3 (2 Nefi 21–24)Katika somo hili, wanafunzi walijifunza kwamba Yesu Kristo atahukumu kwa haki na kwamba hatimaye, kupitia kwa Na-bii Joseph Smith, Bwana atarejesha Kanisa lake ili kuwaku-sanya watu wake katika siku za mwisho. Nefi pia alifurahia katika unabii wa Isaya kwamba wakati wa Milenia, amani na ufahamu wa Bwana utaijaza dunia. Wanafunzi walihimizwa kufikiri kuhusu ukweli huu na namna wanavyoweza kuwa tayari zaidi kwa wakati huu.

Siku ya 4 (2 Nefi 25)Nefi alipofupisha ujumbe mkuu wa maandiko ya Isaya, alipitia tena kweli rahisi kuhusu kazi ya Mungu kati ya wana wa watu: Yesu Kristo ndio jina pekee chini ya mbingu “ambamo kwamba mwanadamu anaweza kuokolewa” (2 Nefi 25:20), na Yesu Kristo ndiye asili pekee ya kutegemea msamaha wa dhambi zetu. Nefi alitaka kila mmoja kujua kwamba “tuki-tenda yote tunayoweza,” Yesu Kristo atatubariki kwa neema —msaada wa Mungu na nguvu (ona 2 Nefi 25:23).

UtanguliziWiki hii wanafunzi walisoma sura kadhaa za Isaya ambazo Nefi alijumuisha katika maandishi yake. Rais Boyd K. Packer wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alisema kuhusu sura hizi za Isaya: “Usiache kusoma! Songa mbele kupitia sura hizo ngumu kue-lewa za unabii za Agano la Kale, hata kama unaelewa kidogo sana ya hiyo. Songa mbele, kama yote ufanyalo ni kupitia kwa haraka na kukusanya hisia za hapa na pale”(“The Things of My Soul,” Ensign, May 1986, 61).

Unapokutana na wanafunzi wiki hii, wahimize kuwa na subira wanapojifunza maneno ya Isaya. Unaweza pia kuwaalika kuele-zea jinsi maandiko ya Isaya yamewasaidia “kuinua mioyo yao na kufurahia” katika wema wa Mungu (2 Nefi 11:8).

Mapendekezo ya Kufundisha

2 Nefi 11–25Nefi ananukuu unabii wa Isaya kuhusu Yesu KristoOnyesha kiookuzi au chora picha ya kimoja kwenye ubao. Alika mwanafunzi kusoma 2 Nefi 25:13 kwa sauti. Uliza darasa kua-ngalia kile Nefi “alitukuza.” Eleza kwamba sababu moja ya Nefi kuandika maneno ya Isaya, inapatikana katika 2 Nefi 11, ilikuwa ni kulitukuza jina, huduma, na Upatanisho wa Yesu Kristo katika maisha ya wale wanaotaka kusoma maneno ya Nefi.

Acha mwanafunzi asome 2 Nefi 11:4–8 kwa sauti. Uliza darasa kutafuta vishazi vinavyotambua madhumuni ya Nefi kwa kunu-kuu maneno ya Isaya.

Katika masomo yao nyumbani, wanafunzi waliulizwa kuweka alama kwenye jina “Kristo” kila wakati lilipoonekana katika 2 Nefi 25:20–30. Waalike kurejea katika 2 Nefi 25:28–29 na ku-tafuta vishazi ambavyo vimerudiwa katika mafungu haya. (“Njia ya haki ni kuamini katika Kristo na kutomkataa.”)

Waulize wanafunzi: Ni matukio gani katika maisha yako yame-kufundisha kwamba kuamini katika na kumfuata Yesu Kristo ni njia ya haki ya kuishi?

Orodha ifuatayo ina ukweli, mafundisho, na kanuni ambazo wa-nafunzi walisoma katika 2 Nefi 11–25 wiki hii. Andika kauli tisa zifuatazo kwenye ubao au zijumuishe katika kipeperushi kwa kila mwanafunzi. Alika wanafunzi kusoma orodha na kutafuta kweli hizi, mafundisho, na kanuni katika aya zilizotajwa.

Kuelewa Mafundisho ya Isaya katika siku zetu 1. Mungu ameanzisha hekalu ili atufundishe njia Zake na kutusa-

idia kutembea katika njia Zake (ona 2 Nefi 12:2–3). 2. Tunaweza kutakaswa kutokana na uchafu wetu kupitia kwa

Upatanisho wa Yesu Kristo (ona 2 Nefi 16:5–7). 3. Mungu atakuwa pamoja nasi tukimwamini Yeye, hata wakati

wa shida na hofu (ona 2 Nefi 17:4, 7, 14).

Page 140: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

125

MafUnzo ya MaSoMo ya nyUMbani

4. Yesu Kristo ni Mungu wa hukumu na huruma. Huruma yake inafikishwa kwa wale walio tubu, na kushika amri Zake (ona 2 Nefi 19:12, 17, 21; 20:4).

5. Bwana amerejesha injili yake na Kanisa Lake kupitia kwa Nabii Joseph Smith na sasa anawakusanya watu wake katika siku za mwisho (ona 2 Nefi 21:10, 12).

6. Wakati wa Milenia, dunia itakuwa mahali pa amani kwa sababu itajawa na maarifa ya Bwana (2 Nephi 21:6–9).

7. Bwana atakuwa na huruma kwa watu wake, lakini waovu wataangamia (ona 2 Nefi 23:22).

Mafundisho ya Nefi 8. Kwa sababu ya Yesu Kristo, tunaweza kuokolewa kwa neema

baada ya yote tunayoweza kufanya (ona 2 Nefi 25:23). 9. Kupitia kwa Upatanisho wa Mwokozi, tunaweza kupokea

ondoleo la dhambi zetu (ona 2 Nefi 25:26).

Baada ya muda wa kutosha, uliza maswali yafuatayo:

• Ni mada zipi unazoona katika mafundisho haya kutoka kwa Isaya na Nefi? (Mada iwezekanayo ni: Baba wa Mbinguni alimtuma Mwanawe, Yesu Kristo, ili kuleta wokovu na amani kwa watoto Wake. Tunaweza kuamini Mungu katika hali yoyote ile. Hekalu hutufundisha juu ya Mungu.)

• Ni kauli gani kati ya hizi tisa unapata kuwa ya maana zaidi? Kwa nini?

Gawia kila mwanafunzi fundisho au kanuni moja kutoka kwenye orodha hapo juu, na acha wanafunzi wafanye yafuatayo:

1. Soma kifungu cha maandiko ambamo mafundisho au kanuni imetolewa.

2. Jibu swali hili: Mafundisho haya au kanuni imekusaidiaje kuweza “kufurahia”katika Bwana? (Ona 2 Nefi 11:4–6.)

3. Fikiria juu ya hali ambapo kuwa na ufahamu wa fundisho hili au kanuni inaweza kukuletea matumaini na nguvu.

Alika wanafunzi watoe mawazo yao. Wanapofanya hivyo, unaweza kuuliza, “Ni nani mwingine ana ushuhuda au ufahamu

kuhusu kile kimefundishwa?” Kuwaruhusu kushirikiana ufa-hamu na ushuhuda kutathibitisha ukweli katika mioyo yao na mioyo ya wenzao. Washukuru kwa kushirikiana huko.

Alika mwanafunzi kusoma 2 Nefi 25:13 kwa sauti. Uliza darasa kufuatana pamoja, wakitafuta sababu za Nefi za kufurahia kutu-kuza jina la Bwana. Waulize wanafunzi kusema kile walichopata.

Alika mwanafunzi kusoma ushuhuda ufuatao wa Rais Thomas S. Monson:

“Ninaamini kuwa hakuna hata mmoja kati yetu anayeweza kue-lewa umuhimu halisi wa kile Kristo alitufanyia kule Gethsemane, lakini nina shukrani kila siku ya maisha yangu kwa dhabihu Yake ya upatanisho kwa niaba yetu.

“Wakati wa mwisho, Angerudi nyuma. Lakini hakufanya hivyo. Alipitia chini ya vitu vyote ili aweze kuokoa vitu vyote. Kwa kufanya hivyo, alitupatia maisha zaidi ya maisha haya ya muda. Alitukomboa kutokana na Anguko la Adamu.

“Hadi kwenye kina cha moyo wangu, nina shukrani Kwake. Ali-tufunza jinsi ya kuishi. Alitufunza jinsi ya kufa. Alilinda wokovu wetu” (“At Parting,” Ensign, Mei 2011, 114).

Uliza: Ni mifanano gani unaona kati ya maneno Nefi katika 2 Nefi 25:13 na maneno ya Rais Monson?

Hitimisha mafundisho ya leo kwa kuuliza wanafunzi kuelezea njia ambazo vijana Watakatifu wa Siku za Mwisho wanaweza kutukuza jina la Bwana. Baada ya wanafunzi kujibu, wahimize kulitukuza jina la Bwana kila siku.

Kitengo kifuatacho (2 Nefi 26–31)Katika kitengo kifuatacho wanafunzi watasoma baadhi ya unabii wa Nefi kuhusu siku za mwisho. Nefi aliona kwamba makanisa ya uwongo na miungano ya siri ingeongezeka kwa wingi. Pia aliona kwamba Bwana angefanya “kazi ya kushangaza na ya maajabu” (2 Nefi 27:26) na kwamba wengi watakataa Kitabu cha Mormoni kwa sababu tayari wana Biblia. Aidha, Nefi aliele-zea fundisho la Kristo.

Page 141: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

126

UtanguliziNefi alitoa unabii kwamba uzao wake siku moja unge-tembelewa na Yesu Kristo mfufuka na kwamba baada ya tukio hili wataishi kwa vizazi vitatu katika haki. Hata hivyo, Nefi alihuzunika kwamba miongoni mwa kizazi cha nne cha kizazi chake, baadhi wataanguka nje ya

haki, kumkataa Masiya, na hatimaye kuharibiwa. Nefi alionya wale wanaoishi katika siku za mwisho dhidi ya kiburi, miungano ya siri, na ukuhani wa uongo. Alifu-ndisha kwamba Bwana anawapenda watu wote, na anawaalika kuja Kwake.

Mapendekezo ya Kufundisha

2 Nefi 26:1–13Nefi anatabiri kwamba watu wake wangeangamizwa kwa sababu wangemkataa Yesu KristoAndika kwenye ubao Hukumu ya Mungu.• Unapoona au kusikia kishazi hiki, ni mawazo gani huja akilini mwako?Eleza kwamba ingawa watu wengi wana mawazo hasi wanapoona maneno haya, na hukumu ya Mungu, lakini kwa kweli huleta baraka kwa watu wengi. Katika 2 Nefi 26, tunasoma kuhusu madhara ambayo haki huleta kwa waovu na wenye haki.Ili kujenga mazingira ya ujumbe mkubwa wa 2 Nefi 26, eleza kwamba Nefi alisema kwa-mba ishara nyingi zitafuata kuzaliwa, kifo, na Ufufuo wa Yesu Kristo. Alitabiri kwamba watu wengi wangeangamia karibu na baada ya kifo cha Mwokozi kwa sababu watawa-tupa nje manabii na wafuasi waaminifu wa Yesu Kristo ambao waliishi miongoni mwao. Pia alitabiri ya kwamba hata baada ya kupokea ziara ya Mwokozi alipofufuka, wengi wa uzao wake “wangechagua matendo ya giza kuliko mwanga” na wangeangamizwa. (Ona 2 Nefi 26:1–11.)Alika mwanafunzi kusoma 2 Nefi 26:7 kwa sauti. Uliza darasa kutafuta majibu ya Nefi kwa maono ya uharibifu wa watu. Alika wanafunzi kuelezea walichopata. Unaweza kupendekeza kwamba watie alama kwenye tangazo la Nefi mwishoni mwa aya: “Njia zako ni za haki.• Taarifa “Njia zako ni za haki” ina maana gani kwako? (Unaweza kutaka kueleza kwa-

mba mtu ambaye ni wa haki kila mara huwatendea watu haki.)Baada ya kuwasaidia wanafunzi kuelewa kuwa haki ya Mungu inahitaji kwamba waovu waadhibiwe kwa ajili ya matendo yao, eleza kwamba haki ya Mungu pia inahitaji kwamba wenye haki walipwe kwa vitendo vyao. Kama sehemu ya maelezo haya, unaweza kutaka kuwaalika wanafunzi kusoma Mafundisho na Maagano 130:20–21. Wezesha wanafunzi kusoma 2 Nefi 26:8–9, 13, wakitafuta baraka ambazo Nefi alisema zitakuja kwa wazawa wake wema.• Katika mstari wa 8 na13, ni vishazi vipi vinaelezea matendo ya haki?• Ni lini umeshuhudia baraka zilizotajwa katika mstari wa 13? Ni baadhi ya njia gani mba-

limbali ambayo Bwana hujidhihirisha kwetu?Andika kanuni zifuatazo kwenye ubao: tunapotumia imani katika Yesu Kristo, atajidhi-hirisha Mwenyewe kwetu kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.• Jinsi gani kujua ukweli huu huongeza imani yako katika Yesu Kristo?

2 Nefi 26:14–33Nefi alitoa unabii kuhusu siku za mwisho na anawaalika wote kuja kwa KristoFupisha 2 Nefi 26:14–19 kwa kuelezea kuwa Nefi alitabiri ya kwamba Kitabu cha Mormoni kingetokea katika siku za mwisho wakati wa kipindi ambapo watu wengi watajawa na kiburi na kukosa imani.

SOMO LA 36

2 nefi 26

Page 142: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

127

2 nefi 26

Waulize wanafunzi kufikiri kuhusu wakati walipojikwaa kuhusu jambo fulani (au unaweza kuwafanya wafikirie kuwa wamejikwaa gizani). Waalike kupekua 2 Nefi 26:20–21 kimya kimya wakitafuta vikwazo ambavyo watu wanaweza kujikwaa kwavyo katika siku za mwisho.• Kulingana na 2 Nefi 26:20–21, ni vikwazo vipi ambavyo Nefi aliona vinaweza kuwafanya

Wayunani kujikwaa?• Ni ipi mifano mingine ya vikwazo ambavyo Shetani hutumia kuongoza watu kujikwaa?Eleza kwamba zaidi ya kuweka “vikwazo vikuu” katika njia yetu ili kutupotosha mbali na Mungu, Shetani analenga kutufunga. Shikilia juu kipande cha uzi na ualike wanafunzi kupitia 2 Nefi 26:22, wakitafuta kile Nefi aliandika juu ya kitu kama hicho. Alika mwana-funzi kuja mbele ya darasa. Funga mikono ya mwanafunzi pamoja kwa uzi moja uliolegea. Mwulize kukata uzi. Rudia utaratibu, wakati huu ukiunganisha uzi kuzunguka mikono yake mara kadhaa. Endelea kufanya hivyo mpaka mwanafunzi ashindwe kukata uzi—uki-onya mwanafunzi kuwa makini asije akajiumiza. (Ikiwa huna uzi karibu na wewe, unaweza kutaka kuwauliza wanafunzi kuwaza kuhusu onyesho hili.) Waulize wanafunzi kujifunza 2 Nefi 26:22, wakitafuta jinsi aya inavyohusiana na maonyesho.• Katika 2 Nefi 26:22, nini umuhimu wa kishazi “hadi anawafunga”? Aya hii inafundisha

nini jinsi Shetani hufanya kazi?• Ni vipi umeona Shetani akiwaongoza watu na“mkanda wa kitani”? (Kitani ni kifaa

ambacho hutumika kutengeneza nguo.)• Ni zipi kati ya dhambi hizi (mikanda ya kitani) unafikiri ni hatari zaidi kwa watu wa umri

wako?Wakumbushe wanafunzi kwamba Shetani hutushawishi kufanya matendo ya giza ili aweze kutufunga na kutuongoza kutoka kwenye njia ya haki. Eleza kuwa aya za mwisho katika 2 Nefi 26 inaonyesha tofauti kati ya njia za Shetani na njia za Mungu. Waulize wanafunzi kusoma 2 Nefi 26:23–24 kimya kimya.• Kulingana na mistari hii, Bwana anafanya kazi vipi? Nini lengo la kila kitu ambacho

Bwana anafanya? (Unaweza kushauri kwamba wanafunzi waweke alama kwenye se-hemu ya 2 Nefi 26:24 inayofundisha kwamba kila kitu ambacho Bwana anafanya ni kwa manufaa ya ulimwengu.)

Waulize wanafunzi kutafakari kwa muda kwa wakati walipohisi kuvunjika moyo au kuwe-kwa mbali na Bwana. Ili kuwasaidia wanafunzi kuhisi kuwa ujumbe wa Nefi wa upendo wa Bwana unatumika katika maisha yao, waalike kupekua 2 Nefi 26:24–28, 33. Unaweza kutaka kupendekeza kwamba waweke alama kwenye maneno wote, yoyote, na hakuna (isi-pokuwa kwa mara ya kwanza ya neno hakuna katika mstari wa 33). Wawezeshe wanafunzi kuchukua dakika chache ili kusoma tena sentensi ambazo zina maneno haya.Waulize kila mwanafunzi kumgeukia mshiriki moja wa darasa na kujadili kwa ufupi kile tunaweza kuelewa kutokana na mistari hii. Baada ya wanafunzi kushiriki mawazo yao na mwingine, fikiria kualika wanafunzi wachache ili kushirki mawazo makuu kutoka kwa mazungumzo yao. Wazo moja kuu linalopaswa kutokana na mjadala huu ni kwamba Bwana anawapenda watu wote na anawaalika wote kuja Kwake na kushiriki wokovu Wake. Unaweza kutaka kuandika kauli hii kwenye ubao. Unaweza pia taka kualika wanafunzi kuandika majibu kwa maswali yafuatayo katika shajara zao za kujifunza maandiko au daftari za darasani:• Ni wakati gani umetambua wema wa Bwana katika maisha yako?• Inawezeje kukusaidia kujua kwamba Bwana anawapenda watu wote na anawaalika

wote kuja Kwake?Kuhitimisha, alika mwanafunzi kusoma 2 Nefi 26:25, 33 kwa sauti. Kabla hajasoma, pendekeza kwamba wanafunzi watie alama vishazi ambavyo vinawahimiza. Ili kuwasaidia wanafunzi kuona matumizi ya ziada katika mistari hii, soma kauli ifuatayo ya Rais Dieter F. Uchtdorf wa Urais Kwanza:“Natumaini kwamba tunawakaribisha na kuwapenda wana wote wa Mungu, ikiwa ni pamoja na wale ambao wanaweza kuvalia, kuangalia, kusema, au tu

kufanya mambo kwa njia tofauti. Si vizuri kuwafanya watu wengine kuhisi kama kwamba wao wana upungufu. Hebu tuwainue wale walio karibu nasi. Hebu tunyoshe mkono wa

Kuwaalika wanafunzi kutendaMafundisho yenye ufa-nisi kawaida hujumuisha mwaliko wa kutenda juu ya kanuni zilizofu-ndishwa. Ikiwa elimu ya kanuni ya injili imeso-mwa lakini haijatendwa, mafunzo si kamili. Mia-liko ya kutenda inaweza kutokana na mwalimu, na hata kwa nguvu zaidi, kutoka kwa Roho Mtakatifu.

Page 143: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

128

SoMo la 36

kukaribisha. Hebu tutoe juu ya ndugu na dada zetu katika Kanisa utunzaji maalum wa binadamu, huruma, na upendo ili wahisi, hatimaye, kwamba wamepata nyumbani. . . .“Inaonekana kuwa haki na sahihi kwamba tuwape wengine kile ambacho tunahitaji kwetu sisi wenyewe.“Mimi sipendekezi kuwa tukubali dhambi au kupuuza mabaya katika maisha yetu binafsi au katika dunia. Hata hivyo, katika juhudi zetu, wakati mwingine sisi huchanganya dhambi na mwenye dhambi, na tunahukumu kwa haraka na kwa huruma kidogo sana. . . .“. . . Hebu mioyo yetu na mikono inyooshwe kwa huruma kwa wengine, kwa kuwa kila mtu anatembea katika njia ngumu yeye pekee yake” (“You Are My Hands,” Ensign, May 2010, 68–69).• Ni kwa njia gani tunaweza kutumia 2 Nefi 26:33 na mafundisho ya Rais Uchtdorf?Alika wanafunzi kufikiria kile wanaweza kufanya ili kuwafikia wengine wenye shida na kuwasaidia kuhisi upendo wa Bwana.

Wazo la Ziada la Kufundisha2 Nefi 26:29–31. Nefi anaonya juu ya dhambi ya ukuhani wa uongoAndika majina yafuatayo ubaoni: Sherem, Nehor, Korihor. Waulize wanafunzi kile wanajua kuhusu watu hawa. Ikiwa wanafunzi wana ugumu wa kujibu, kwa ufupi eleza kwamba watu hawa walijaribu kuongoza watu mbali na imani katika Yesu Kristo. Walikuwa na hatia ya dhambi ya ukuhani wa uongo.

Nefi alionya watu wake—na wale wetu ambao wanai-shi katika siku za mwisho — juu ya ukuhani wa uongo. Alika mwanafunzi kusoma 2 Nefi 26:29–31 kwa sauti. Uliza darasa kusikiliza ufafanuzi wa ukuhani wa uongo.• Ni nini lengo la watu wanaohusika katika ukuhani

wa uongo?

Mzee M. Russell Ballard wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alionya kwamba ukuhani wa uongo unaweza kutokea katika Kanisa. Uliza mwanafunzi kusoma ushauri:

“Hebu Jihadharini na manabii wa uongo na walimu wa uongo, wanaume kwa wanawake, ambao wamejiteua

wenyewe kama watangazaji wa mafundisho ya Kanisa na ambao wanataka kueneza injili yao ya uongo na kuvutia wafuasi kwa kudhamini makongamano, vitabu, na majarida ambayo maudhui yake yanapinga mafu-ndisho ya msingi ya Kanisa. Jihadharini na wale ambao wanasema na kutangaza kwa upinzani dhidi ya mana-bii wa kweli wa Mungu ambao huhamasisha wengine kwa kupuuza bila kujali ustawi wema wa milele wa wale wanao wapotosha. Kama Nehor na Korihor katika Kitabu cha Mormoni, wanategemea hila ili kudanganya na kuwavuta wengine kwa maoni yao. ‘Wanajiinua wawe nuru ya ulimwengu, ili wafaidike na wapate sifa za ulimwengu; lakini hawajali usitawi wa Sayuni’ (2 Nefi 26:29)” (“Beware of False Prophets and False Teachers,” Ensign, Nov. 1999, 63).

• Waumini wa Kanisa wanawezaje kuanguka katika mtego wa ukuhani wa uongo?

• Kwa mujibu wa 2 Nefi 26:30, nini kinachoweza kuzuia ukuhani wa uongo? (Wasadie wanafunzi kue-lewa kwamba tunaweza kuepuka dhambi ya ukuhani wa uongo kwa kuwa na upendo kwa watu wote.)

Page 144: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

129

UtanguliziAkirejea mara nyingi maneno ya Isaya, Nefi alitabiri ya kwamba Bwana angeweza kufanya “kazi ya kusha-ngaza na ya maajabu” siku za mwisho. Kazi hii ya maa-jabu ingekuwa Urejesho wa injili ya Yesu Kristo. Kitovu cha unabii wa Nefi kilikuwa ni kuja kwa Kitabu cha Mormoni. Nefi alitabiri kwamba mashahidi wakiona Kitabu cha Mormoni na kushuhudia ukweli wake. Pia,

alishuhudia juu ya jukumu la kimsingi ambalo Kitabu cha Mormoni kingefanya katika kazi ya Bwana katika siku za mwisho— kuwa kitakuwa ni zawadi ya miujiza kwa ulimwengu. (Fahamu: 2 Nefi 27 kwa karibu sawa sawa na Isaya 29. Katika toleo la Biblia ya Watakatifu wa Siku za Mwisho, tanbihi katika Isaya 29 inatoa ufa-hamu wa kusaidia kwa masomo ya sura zote mbili.)

Mapendekezo ya Kufundisha

2 Nefi 27:1–5Nefi anatabiri kwamba katika siku za mwisho dunia itajawa na uovuOnyesha vitu vifuatavyo: chombo cha kuondoa harufu, tyubu ya dawa ya meno, na miti au chombo cha sabuni. Eleza kwamba kila kitu kinanuiwa kuwa suluhu kwa tatizo. Waulize wanafunzi kutambua tatizo kila kitu kinanuiwa kutatua. (Unaweza kuchagua kutumia vitu vingine ambavyo vinaweza kuchukuliwa kama suluhu kwa matatizo maalum.)Eleza kwamba unabii wa Nefi katika 2 Nefi 27 unaelezea matatizo ambayo yatakuwepo katika siku zetu. Alifundisha kwamba watu wangejikwaa kiroho kwa sababu ya uovu wao, kwamba wangepata upofu wa kiroho, na kwamba wangeweza kukataa manabii. Nefi pia alitabiri juu ya kile Mungu angefanya ili kutatua matatizo haya.Alika wanafunzi wachache kuchukua zamu ya kusoma 2 Nefi 27:1–5 kwa sauti. Uliza darasa kutafuta maneno na vishazi ambavyo vinaelezea baadhi ya matatizo ya siku za mwisho. Waulize wanafunzi wachache kuelezea vishazi walivyogundua. Ili kuwasaidia wanafunzi kuchambua vishazi hivi, unaweza kuuliza maswali yafuatayo:• Unafikiri nini maana ya “kulewa kwa maovu”?• Katika 2 Nefi 27:3, watu wengine katika siku za mwisho wanafananishwa na mtu mwe-

nye njaa ambaye anaota juu ya kula au mtu mwenye kiu anayeota juu ya kunywa lakini baadaye anaamka na kuhisi nafsi yake imo tupu. Tunaweza kujifunza nini kutokana na hili? (Kula au kunywa katika ndoto haitoi furaha ya kudumu na hakutimizi chochote, kwani njaa au kiu hubakia baada ya ndoto. Vilevile, wale “wapiganao dhidi ya Mlima Sa-yuni” hawatakuwa na furaha ya kudumu, wala hawataweza kukamilisha kitu cha maana.)

• Unafikiri kipengele“mmefunga macho yenu” kinamaanisha nini?Ili kuwasaidia wanafunzi kutambua ukweli wa injili katika 2 Nefi 27:1–5, waalike kufupi-sha yale waliyojifunza kutoka kwenye mistari hii. Andika majibu yao ubaoni. Hakikisha wanafunzi wanaelewa kwamba katika siku za mwisho, watu wengi watajawa na uovu na kukataa manabii.• Kwa nini unafikiri ni muhimu kujua kuhusu unabii huu na utimilifu wake?

2 Nefi 27:6–23Unabii wa Nefi wa kuja kwa Kitabu cha MormoniAlika wanafunzi kusoma 2 Nefi 27:6–7 kimya kimya. Waulize waangalie kitu ambacho Bwana anaweza kutoa ili kusaidia kutatua matatizo ya kiroho ya watu katika siku za mwisho.• Ni nini Bwana angepeana?• Ni nini ingekuwa kwenye kitabu?• Ni kitabu gani unafikiri mistari hii inaelezea nini? (Ili kuwasaidia wanafunzi kujibu swali

hili, unaweza kushauri kwamba waangalia marejeo ya maandiko yaliyotajwa katika 2 Nefi

Maswali yanayoelekeza kwa uchambuziKwa kutumia maswali ya uchambuzi, unaweza kuwahimiza wanafunzi kufikiria juu ya maana ya aya wanazosoma. Kwa Kawaida unapaswa kuuliza maswali haya baada ya wanafunzi kufahamu mistari. Maswali ya uchambuzi mara nyingi huanza kwa vishazi kama “kwa nini unafikiri” au “unafikiri nini.” Kwa mfano, una-weza kuuliza, “Unafikiri hiki (vishazi au neno) humaanisha nini?"

SOMO 37

2 nefi 27

Page 145: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

130

SoMo 37

27:6, tanbihi b. Unaweza pia kutaka kuelezea kwamba kishazi "ya waliokufa" kina maana manabii walikokufa ambao waliohifadhi kumbukumbu zilizokuwa Kitabu cha Mormoni.)

Inua nakala ya Kitabu cha Mormoni. Eleza kwamba Bwana alileta kitabu hiki ili kusaidia kutatua matatizo katika siku za mwisho na kuleta mwanga kwa ulimwengu wenye giza. Bwana alifunulia manabii wa kale maelezo kuhusu kuja kwa Kitabu cha Mormoni. Nefi ali-andika maelezo haya katika 2 Nefi 27. Eleza kwamba unabii sawa unapatikana katika Isaya 29. (Unaweza kueleza kuwa baadhi ya watu wamekabili Kitabu cha Mormoni kwa kuhoji kwa nini Biblia haikitaji. Onyesha kwamba unabii katika Isaya 29 unaonyesha kwamba Biblia kwa kweli inakishuhudia Kitabu cha Mormoni.)Alika mwanafunzi kusoma 2 Nefi 27:12–14 kwa sauti. Uliza darasa kutafuta ni nani ambaye Nefi alisema ataruhusiwa kuona kitabu.• Hawa mashahidi watatu walikuwa akina nani ambao waliruhusiwa kuona Kitabu cha

Mormoni “kwa uwezo wa Mungu”? (Oliver Cowdery, David Whitmer, na Martin Harris. Ona “ushuhuda wa mashahidi watatu,” Kitabu cha Mormoni.)

Elezea kwamba Nefi aliwataja “wachache” wengine ambao pia wataruhusiwa kuona kitabu.• Unafikiri hawa mashahidi wengine walikuwa akina nani? (Unaweza kuhitajika kuwa-

kumbusha wanafunzi wa mashahidi wanane wa ziada wa Kitabu cha Mormoni. Ona “Ushuhuda wa mashahidi wanane,” Kitabu cha Mormoni.)

Elezea kwamba 2 Nefi 27:14 kinatajwa kuwa Bwana, “ataendelea kutoa maneno ya kitabu hicho” katika “vinywa vya mashahidi wengi kama apendavyo.”• Unafikiri Nefi alimaanisha nini aliposema kwamba mashahidi watatoa neno la Mungu?

(Wale wanaopokea na kukubali neno la Mungu kwa njia ya Kitabu cha Mormoni wataki-shiriki pamoja na watu wengine na kushuhudia ukweli wake.)

• Hawa mashahidi wanaweza kuwa akina nani?• Ili kuwasaidia wanafunzi kufahamu kwamba wanaweza pia kuwa mashahidi wa ukweli

wa Kitabu cha Mormoni, unaweza kutaka kuwakaribisha kuandika majina yao kwenye ukingo karibu na 2 Nefi 27:14. Jinsi gani kila muumini wa Kanisa, ukiwemo wewe, ana-weza kusaidia kutoa ukweli wa Kitabu cha Mormoni?

• Ni lini umewahi kushiriki ushuhuda wako wa Kitabu cha Mormoni na wengine?Katika somo la mapema, unaweza kuwa umewahimiza wanafunzi kutoa ushuhuda wao wa Kitabu cha Mormoni na mtu mwingine. Kama ulifanya hivyo, fuatilia zoezi hilo kwa kualika wanafunzi kadhaa kuelezea kile walichofanya. Wahimize wanafunzi kuendelea kutafuta fursa ya kushiriki ushahidi wao wa Kitabu cha Mormoni kwa wengine, ikiwa ni pamoja na wale wa dini nyingine.Nakili chati ifuatayo ubaoni. (Ili kuokoa muda, unaweza kuhitaji kufanya hivyo kabla ya darasa kuanza.)

Unabii wa nefi juu ya nini mtu atafanya

jina la mtu Utimilifu wa unabiijoseph Smith—his-toria 1:63–65

Mtu wa 1 (“si msomi”)2 nefi 27:9, 15, 19

Mtu wa 2 (“mwingine”)2 nefi 27:15, 17

Mtu wa 3 (“msomi”)2 nefi 27:15–18

Gawa wanafunzi katika jozi. Eleza kwamba kila jozi itajifunza unabii kuhusu kuja kwa Ki-tabu cha Mormoni pamoja na kutimia kwa unabii huo. Wezesha wanafunzi kunakili chati katika shajara zao za kujifunza maandiko au daftari za darasani kisha waandike majibu wakitumia marejeo ya maandiko yaliyotolewa. (Unaweza kueleza kuwa, neno michoro, li-nalopatikana katika Joseph Smith —Historia 1:63 –65, inahusu uandishi kwenye mabamba

KufuatiliaMara kwa mara uliza wanafunzi kutoa taarifa ya mialiko ya zamani na kazi. Hii inaruhusu wanafunzi kushiriki uzoefu wa kuhimiza, na inaweza kutoa motisha kwa baadhi ya wana-funzi kufuatilia mialiko ambayo umewapa. Pia inakuruhusu kuvipa kipaumbele mambo mema ambayo yameto-kea wakati wanafunzi wanapotekeleza mialiko na kazi.

Page 146: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

131

2 nefi 27

ya dhahabu ambayo Kitabu cha Mormoni kilitafsiriwa.) Wakati wanafunzi wamemaliza, waalike kueleza majibu yao kwa darasa.• Kwa mujibu wa 2 Nefi 27:15 na Joseph Smith—Historia 1:64, ni msomi gani ambaye

Martin Harris alimpelekea maneno ya kitabu? (Charles Anthon.)• Kwa njia gani mtu asiye kuwa na elimu ya shule, kama Joseph Smith, anaweza kuwa

bora kutafsiri Kitabu cha Mormoni kuliko msomi kama Charles Anthon?Wawezeshe wanafunzi kusoma 2 Nefi 27:20–21 kimya kimya, wakitafuta kishazi kilichoru-diwa katika kila mstari. (“Ninaweza kufanya kazi yangu mwenyewe.”)• Je, kishazi “Ninaweza kufanya kazi yangu mwenyewe" kina maana gani kwako?• Jinsi gani Urejesho wa injili na ujio wa Kitabu cha Mormoni ni uthibitisho kwamba Mu-

ngu anaweza kufanya kazi yake mwenyewe?• Ni zipi baadhi ya kanuni zinazofundishwa na mafungu haya? (Wanafunzi wanaposhiriki

mawazo yao, sisitiza kwamba kuja kwa Kitabu cha Mormoni ni njia moja ambayo Mungu atakamilisha kazi yake katika siku za mwisho.)

• Jinsi gani ya utimizaji wa unabii huu unaimarisha ushuhuda wako wa Kitabu cha Mor-moni na wajibu wake katika Urejesho wa Kanisa ya Bwana?

2 Nefi 27:24–35Nephi anatabiri juu ya matokeo mazuri ya Injili uliorejeshwa wa Yesu Kristo na Kitabu cha MormoniSoma 2 Nefi 27:24–26 kwa sauti wakati wanafunzi wakifuata pamoja katika maandiko yao.• Je, unakumbuka ukisikia haya maneno mbeleni? Kama ni hivyo, ni wapi? (Kama wanafunzi

wanaugumu kujibu, eleza kwamba Bwana alitumia maneno sawa na hayo wakati Alipozu-ngumza na Joseph Smith katika Kichaka Takatifu; ona Joseph Smith—Historia 1:19.)

Shikilia moja ya vitu ulivyoonyeshwa mwanzoni mwa somo hili, na uwakumbushe wana-funzi kwamba viliundwa ili kutatua tatizo fulani.• Katika 2 Nefi 27:25, ni matatizo gani ambayo Bwana alisema yatakuwepo miongoni mwa

watu wa siku za mwisho? (Unaweza kutaka kuandika majibu ya wanafunzi ubaoni.)Wakumbushe wanafunzi juu ya matatizo mengine ya kiroho ya siku za mwisho yaliyotajwa katika 2 Nefi 27:5. (Unaweza kutaka kuongeza uovu, upofu wa kiroho, na kuwakataa manabii katika orodha kwenye bodi.)• Kitabu cha Mormoni na Urejesho wa injili ya Yesu Kristo vinasaidiaje kutatua matatizo

haya?Waulize wanafunzi kusoma 2 Nefi 27:29–30, 34–35 kimya kimya, kutafuta njia ambayo kwayo Bwana alisema injili rejesho na Kitabu cha Mormoni vingebariki watu wa siku za mwisho. Alika wanafunzi kuorodhesha baraka hizi kwenye ubao.• Kwa mujibu wa 2 Nefi 27:29, Kitabu cha Mormoni kitasaidia “macho ya vipofu . . . ku-

ona kutoka fumboni na giza.” Unafikiri hii ina maana gani?Wasaidia wanafunzi kuelewa kwamba Kitabu cha Mormoni na injili rejesho ya Yesu Kristo vinaleta furaha na ufahamu kwa wale wanaosoma na kuvikubali. Wahimize wanafunzi kutafuta suluhisho kwa changamoto zao katika Kitabu cha Mormoni na kutoa ushuhuda wao wa Kitabu cha Mormoni kwa watu wengine.

Page 147: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

132

UtanguliziNefi alitabiri kwamba baadhi ya hali zenye changamoto katika siku za mwisho, zikiwemo mafundisho ya uongo na kiburi cha makanisa mengi ambayo yangejengwa.

Aliwafundisha jinsi ya kutambua mafundisho ya uongo na mitazamo ya kidunia, na alionya dhidi ya njia ambazo Shetani atajaribu kutuvuruga kutoka kwa uadilifu.

SOMO LA 38

2 nefi 28

Mapendekezo ya kufundisha

2 Nefi 28:1–19Nephi anaelezea makanisa ya uongo na mawazo ya uongo ya siku zetuKwenye ubao, chora ishara ya onyo ambayo inajulikana katika utamaduni wenu. Kwa mfano, unaweza kuchora ishara ya trafiki au alama ya mawasiliano ya dutu fulani ina madhara au sumu.• Ni nini lengo la ishara hizi?

Kueleza kwamba Kitabu cha Mormoni kinaweza kutusaidia kuona ishara za maonyo ya kiroho juu ya mvuto wenye kudhuru. Rais Ezra Taft Benson alielezea kuwa moja ya madhumuni ya Kitabu cha Mormoni ni kueleza wazi jinsi adui na maadui wengine wa Kristo watafanya kazi katika siku za mwi-sho. Alika mwanafunzi kusoma taarifa ifuatayo ya Rais Benson:“Kitabu cha Mormoni kinafichua maadui wa Kristo. Kina angamiza mafu-

ndisho ya uongo. . . . Kinaimarisha wafuasi wanyenyekevu wa Kristo dhidi ya mipango ya hila, mikakati, na mafundisho ya shetani katika siku zetu. Aina ya waasi katika Kitabu cha Mormoni ni sawa na aina ya siku zetu leo”(“The Book of Mormon Is the Word of God,” Ensign, Jan. 1988, 3).• Kitabu cha Mormoni kinafichua vipi maadui wa Kristo? (Kinajumuisha historia ya watu

ambao walijaribu kuwaongoza wengine mbali na imani katika Kristo. Kinaturuhusu kuona makosa yao na mawazo ya uongo.)

• Jinsi gani Kitabu cha Mormoni kinatuimarisha dhidi ya adui?Shuhudia kwamba Kitabu cha Mormoni kinafichua mawazo ya uongo ya shetani na kinatuimarisha dhidi ya miundo yake miovu. Eleza kwamba wanafunzi wataona mfano wa hilo katika 2 Nefi 28. Sura hii ina moja ya unabii za Nefi kuhusu siku za mwisho. Katika unabii huu, Nefi alionya dhidi ya mafundisho ya uongo ambayo yangeenea katika siku zetu.Alika wanafunzi kutafuta 2 Nefi 28:3–9 kimya kimya, wakitafuta maonyo ya Nefi kuhusu mafundisho ya uongo. Elezea kwamba 2 Nefi 28:7–9 ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Unaweza kuwahimiza wanafunzi kutia alama kifungu hiki katika njia tofauti ili waweze kuitambua kwa urahisi. Baada ya wanafunzi kupata muda wa kutosha wa kusoma kifungu, waalike wanafunzi kadhaa kuja kwenye ubao. Uliza kila mmoja wao kuandika fundisho moja la uongo au wazo kutoka kwenye kifungu hiki, ikiwemo ni pamoja na aya ambako inapati-kana. Kisha waulize wanafunzi wengine ikiwa wamegundua mafundisho mengine ya uongo au mawazo katika kifungu. Kama walifanya hivyo, waalike kuongeza kwenye orodha ubaoni.Ili kuwasaidia wanafunzi kujadili mafundisho haya machache ya uongo na mawazo, wau-lize maswali yafuatayo:• Je, ni mfano gani wa siku za kisasa wa mojawapo ya mawazo haya ya uongo? (Hakikisha

kwamba darasa halitaji kanisa lo lote wanapojibu swali hili.)• Wazo hili la uongo linazuia watu vipi kutokana na kufuata mpango wa Baba yetu wa

Mbinguni?

2 Nefi 28:7–9 ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Rejelea wazo la mafundisho mwishoni mwa somo ili kuwasaidia wanafunzi na umahiri wao wa kifungu hiki.

Page 148: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

133

2 nefi 28

Uliza mwanafunzi kusoma 2 Nefi 28:12–14 kwa sauti. Alika darasa kutafuta onyo la Nefi kuhusu kile kitakachotokea kwa makanisa mengi na watu katika siku za mwisho kwa sababu ya kiburi na mafundisho ya uongo.• Ni katika njia zipi kiburi na mafundisho ya uongo huwashawishi watu?• Kwa nini “wafuasi wanyenyekevu wa Kristo" hawapotezwi kwa kiburi na uovu? Tuna-

weza kuepuka vipi kudanganywa na “mawaidha ya wanadamu”? (Unaweza kuhitajika kueleza kwamba kishazi “mawaidha ya wanadamu” ina maanisha mafundisho ya watu —tofauti na mafundisho ya Bwana.)

Alika wanafunzi kusoma 2 Nefi 28:15–16, 19 kimoyomoyo, wakitafuta matokeo ya mafu-ndisho ya uongo.• Ni maneno gani au vishazi unavyoona katika mistari hii ambavyo vinaelezea matokeo ya

kiburi na mafundisho ya uongo?

2 Nefi 28:20–32Nefi anaonya juu ya jinsi Shetani anavyojaribu kutudanganyaElezea hadithi zifuatazo kwa wanafunzi:Wakiwa kazini Afrika, Rais Boyd K. Packer alienda kuona wanyama katika hifadhi ya wa-nyama. Aliona kwamba wanyama katika shimo la maji maangavu walikuwa na wasiwasi. Alipomwuliza mwongozaji kwa nini wanyama hawakunywa, mwongozaji alisema ilikuwa ni kwa sababu ya mamba. Rais Packer alikumbuka:“Nilijua ni lazima ilikuwa utani na nikamwuliza kwa makini, ‘Tatizo ni nini?’ Jibu tena: ‘Mamba.’ . . .“Aliweza kuona sikumwamini na nikiwa na uhakika, nadhani, kunifundisha somo. Tulie-lekea kwenye eneo lingine ambapo gari lilikuwa kwenye kimwinuko pembeni yetu kuna

shimo lenye matope ambapo tungeweza kuangalia chini. ‘Pale,’ alisema. ‘Jionee mwenyewe.’“Sikuweza kuona lolote ila matope, maji kidogo, na wanyama waoga kwa umbali. Kisha ghafla kwa mara moja nikamwona!—mamba mkubwa, kalala katika matope, akisubiri mnyama mwengine asiyeshuku kupata kiu ya kuto-sha ili kuja kunywa.

“Mara nikawa mwamini! Alipoona ya kuwa nilikuwa tayari kusikiliza, akaendelea na somo. ‘Kuna mamba kote juu ya mbuga,’ alisema, ‘sio tu katika mito. Hatuna maji yoyote yasiyo na mamba karibu yake, na ni vyema ujue hayo.’ . . .“Katika safari nyingine ya Afrika nilimsimulia tukio hili mhifadhi wa mbuga katika mbuga nyingine. . . .“Kisha akanionyesha mahali ambapo janga lilitokea. Kijana mdogo kutoka Uiingereza alikuwa akifanya kazi katika hoteli kwa msimu. Pamoja na tahadhari ya mara kwa mara, aliruka wigo wa kiwanja ili kuangalia kitu katika maji maangavu ambayo hata hayakufu-nika viatu vyake vya tenisi.“Yeye wala hakupiga hatua mbili ndani,’ mhifadhi alisema, ‘kabla ya kushikwa na mamba, na hatukuweza kufanya chochote kumwokoa”’ (“Spiritual Crocodiles,” Ensign, May 1976, 30–31).• Ni nini kilichosababisha kijana huyu kuwa mwathirika wa mamba? Ni jinsi gani, angee-

puka janga hili? (Kwa kutii maonyo aliyopewa.)Alika mwanafunzi kusoma kwa sauti mashauri yafuatayo kutoka kwa Rais Packer:“Wale walio mbele yenu katika maisha wamechunguza kifupi juu ya mashimo ya maji na kuongeza sauti ya onyo kuhusu mamba. Si tu mijusi mikubwa, yenye rangi ya majivu ambayo inaweza kukukata vipande vipande, bali mamba wa kiroho, ambao ni hatari zaidi, na wenye udanganyifu zaidi na wasioonekana, hata, kuliko wale wanyama watambaao wajifichao vizuri wa Afrika.“Hawa mamba wa kiroho wanaweza kuua au kulemaza nafsi zenu. Wanaweza kuharibu amani yenu ya akili na amani ya akili ya wale wanaowapenda ninyi. Hao ndio wale wa kuonywa dhidi ya, na hakuna pahali pa maji katika maisha haya yote sasa pasipo athiriwa na mamba hao” (“Mamba wa Kiroho,”31).• Ni kwa njia zipi mamba katika hadithi ya Rais Packer ni sawa na majaribu na mbinu za

Shetani? Ni maonyo gani tunapokea ili kutusaidia kuepuka hatari ya kiroho?

Kutumia hadithiHadithi inaweza kusaidia kuhusisha wanafunzi kwa kuweka maslahi na kuwasaidia kushiriki katika mchakato wa kujifunza kwa njia ya kusikia uzoefu wa we-ngine. Hadithi zinaweza pia kusaidia wanafunzi kuona jinsi kanuni za injili zinatumika katika maisha ya watu.

Page 149: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

134

SoMo la 38

Soma 2 Nefi 28:19 kwa sauti wakati wanafunzi wanafuata pamoja. Kisha andika kwenye ubao Shetani analenga kutukamata katika uwezo wake kwa . . .Eleza kwamba kama Nefi aliendeleza unabii wake, alipoongea juu ya mbinu ambazo She-tani hutumia dhidi yetu katika siku za mwisho. Gawa wanafunzi katika jozi. Karibisha kila jozi kusoma 2 Nefi 28:20–29, ukitafuta njia ya kukamilisha sentensi kwenye bodi.Baada ya dakika chache, alika jozi zote kuripoti juu ya jinsi walivyokamilisha taarifa kwenyeubao. Kama sehemu ya mjadala huu, hakikisha wanafunzi wanaelewa kwamba Shetani hutumia mbinu nyingi kujaribu kutushinda, kama vile kwa kutuvuruga kwa hasira, kutuduwaza na kutuliwaza, na kutudanganya.• Je, ni ipi baadhi ya mifano ya Shetani ya kujaribu “kuvuruga [watu] wakasirikie yale

ambayo ni mema”? Jinsi gani hasira huwachanganya watu kuhusu yale yaliyo mema na mabaya?

• Kwa nini unafikiri ni hatari kwa kukaa “starehe Sayuni,” wakifikiri kwamba hakuna ma-boresho yanayohitajika? Kwa nini unafikiri Shetani ana uwezo wa kuongoza watu kama hao “kwa makini hadi jehanamu”?

• Nini maana ya kudanganya mtu? (Kutoa sifa yakupotosha na pongezi.) Kwa nini uda-nganyifu unaweza kuongoza baadhi ya watu mbali na Bwana?

• Kwa nini Shetani hujaribu kuwashawishi watu kwamba hayupo?• Je, ni mambo gani ambayo tunaweza kufanya ili kujilinda dhidi ya hasira? Jinsi gani

tunaweza kujilinda dhidi ya hisia kwamba yote ni sawa? Jinsi gani tunaweza kujilinda dhidi ya udanganyifu?

Kuhitimisha somo, wajulishe wanafunzi kuwa mwisho wa 2 Nefi 28 kuna onyo la mwisho na hakikisho kutoka kwa Bwana. Alika wanafunzi kusoma 2 Nefi 28:30–32 kimya kimya.• Bwana huheshimu haki yetu ya kujiamulia na juhudi zetu za kujifunza juu Yake. Kuli-

ngana na 2 Nefi 28:30, Anatufundisha “mstari juu ya mstari, amri juu ya amri.” Hiyo ina maana gani kwako? Kulingana na aya hii, nini hutokea kwa wale wanaosema, “Tuna ya kutosha”?

• Katika 2 Nefi 28:32, Bwana anaongea na watu waliomkana Yeye. Katika mstari huu, unafikiri Anamaanisha nini wakati Anaposema, “nitawanyoshea mkono wangu siku kwa siku”? (Katika aya hii, Bwana anaelezea kuhusu rehema Yake na nia Yake ya kutusaidia kila siku tunapotaka kufuata mapenzi Yake, hata kama tumemkataa siku za nyuma. Wasaidie wanafunzi kuelewa kwamba Bwana atakuwa na huruma kwa watu wote wanaotubu, na kuja kwake.)

Andika ubaoni: Kwa sababu ya kile nimejifunza leo, Mimi . . . Waalike wanafunzi kumaliza sentensi hii katika jarida zao ya masomo ya maandiko au daftari za darasa kwa kueleza kile watafanya kama matokeo ya kusoma unabii wa Nefi katika 2 Nefi 28. Unaweza kutaka ku-alika wanafunzi wachache kuelezea kile wameaandika kwa darasa. Hata hivyo, hakikisha wanaelewa kwamba hawapaswi kujisikia kuwajibika kushiriki mawazo au uzoefu ambao ni binafsi mno au ya siri.Shuhudia kwamba kwa ushauri na nguvu kutoka kwa Bwana, tunaweza kushinda maja-ribu. Na hata tukifanya dhambi, Bwana atakuwa na huruma kwetu tukitubu kwa dhati.

Umahiri wa Maandiko—2 Nefi 28:7–9Eleza kwamba watu wakati mwingine hudunisha dhambi kwa kujiaambia kwamba kila mtu anaifanya au kwamba wanaweza kutubu baadaye. Gawanya darasa katika makundi madogo. Alika vikundi kusoma 2 Nefi 28:7–9 pamoja, wakitafuta maneno na vishazi amba-vyo vinahusiana na mawazo haya ya uongo. Alika wanafunzi kujadili maswali yafuatayo katika makundi yao (unaweza kutaka kuandika maswali kwenye ubao kabla ya darasa):• Je, ni hatari gani iliyoko kwa kufanya “dhambi kidogo”?• Je, Mungu atahalalisha dhambi zetu ndogo au nadra? (Waulize wanafunzi kusoma Ma-

fundisho na Maagano 1:31 kwa ufahamu wa ziada).• Mtu anawezaje “kutumia wengine kwa sababu ya maneno yao,”? Tunawezaje wakati

mwingine “kumchimbia jirani [yetu] shimo”?

Page 150: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

135

2 nefi 28

Alika kila kundi kuandika upya aya hizo kwa lugha ambayo watu wanaweza kutumia leo ili kuwashawishi vijana kufuata mafundisho haya ya ujinga.Waulize wanafunzi kufikiria kuhusu nyakati ambapo wameiimarisha nguvu yao ya kiroho, licha ya mawazo ya uongo katika shule, katika vyombo vya habari, au kutoka kwa marafiki. Waalike kuandika kuhusu uzoefu huu katika shajara zao za kujifunza maandiko au daftari za darasani. Fikiria kuuliza wanafunzi wachache kushiriki kile wameandika.Fahamu: Unaweza kutumia wazo hili wakati wa somo unapoanzisha kifungu cha umahiri wa maandiko, au unaweza kuutumia katika mwisho wa somo.

Page 151: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

136

UtanguliziNephi alitabiri kuhusu Urejesho wa injili katika wa siku za mwisho, ambao Bwana alisema ungekuwa“kazi ya kushangaza” (2 Nefi 29:1). Nefi alishuhudia kwamba katika siku za mwisho, maandiko yote yatashirikiana pamoja ili kuonyesha kwamba Mungu anakumbuka

watoto Wake. Alitabiri kwamba wengi wangekataa Kitabu cha Mormoni lakini kwamba wale walioamini watakusanywa katika Kanisa. Aidha, alifundisha kwa-mba watu wa Mungu wa agano ni wale walio tubu, na kuamini katika Mwana wa Mungu.

SOMO 39

2 nefi 29–30

Mapendekezo ya Kufundisha

2 Nefi 29Nefi anatabiri kwamba katika siku za mwisho, wengi watakataa Kitabu cha MormoniAlika wanafunzi kudhania kwamba rafiki shuleni anauliza kwa dhati, “Kwa nini Wamor-moni wana Biblia nyingine?” Unaweza kuwauliza wanafunzi kuinua mikono yao ikiwa wameulizwa swali kama hili. Kisha alika wachache kushiriki jinsi walivyojibu swali.Eleza kwamba Nefi alitoa baadhi ya majibu kwa swali hili kwa kuandika maneno ya Bwana juu ya jukumu la Kitabu cha Mormoni katika Urejesho wa injili siku za mwisho, ambayo Bwana aliita “kazi ya kushangaza.” Alika wanafunzi kusoma 2 Nefi 29:1–2 kimya na kuta-mbua kile maneno ya Bwana ingefanya katika siku za mwisho. (Kwamba “utatoka” hadi kwa mbegu, au uzao wa Nefi, na pia “yatapigwa miunzi hadi mwisho wa dunia.”) Rais Ezra Taft Benson alieleza kwamba “sisi, waumini wa Kanisa, na hasa wamisionari, lazima wawe ‘wavumishaji,’ au wasemaji na washahidi, wa Kitabu cha Mormoni hata mwisho wa dunia” (“The Book of Mormon Is the Word of God,” Ensign, May 1975, 65).Eleza kwamba neno bendera katika 2 Nefi 29:2 inahusu kitu kinachotumika kukusanya na kuunganisha watu. Bendera mara nyingi huitwa viwango. (Angalia maelezo ya neno bendera katika somo 32.)• Kulingana na 2 Nefi 29:2, ni “bendera” gani ambayo itaenda “hadi mwisho wa dunia”

ili kuwakusanya watu wa Bwana? (Kitabu cha Mormoni—maneno ya mbegu, au uzao wa Nefi.)

• Kulinga na 2 Nefi 29:1–2, ni nini madhumuni ya Bwana kwa kupeana maandiko ya ziada, kama vile Kitabu cha Mormoni? (Wasaidie wanafunzi kuelewa kwamba Bwana hutoa maandiko kama ushuhuda wa pili na kukusanya watu kwa ahadi Yake.)

Ubaoni, andika taarifa ifuatayo ya Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili (kutoka Christ and the New Covenant: The Messianic Message of the Book of Mormon [1997], 4.):

“Kitabu cha Mormoni ni taarifa kuu ya agano la Mungu kwa na upendo wake kwa watoto wake hapa duniani.” (Mzee Jeffrey R. Holland)

Eleza kwamba katika 2 Nefi 29, neno Wayunani  inahusu watu wasiokuwa wa nyumba ya Israeli. Neno Wayahudi inahusu watu ambao ni wa nyumba ya Israeli, wakiwemo familia ya Lehi na uzao wake. Wawezeshe wanafunzi kusoma 2 Nefi 29:3–6 kimya kimya, wakita-futa athari kwa Wayunani wengine kwa maandiko ya ziada.• Wengine watasemaje kuhusiana na maandiko ya ziada?• Bwana alisema nini juu ya watu wanaosema namna hii?Elezea kwamba Nefi alitabiri kinabii katika maelezo yake ya mwitiko wa watu wa Kitabu cha Mormoni. Watu hivi leo mara nyingi huonyesha shaka juu ya Kitabu cha Mormoni kwa sababu tayari wana Biblia.Wape kazi wanafunzi kujifunza 2 Nefi 29:7–11 katika majozi. Waalike kupata madhumuni ya Bwana ya kutoa maandiko kama nyongeza kwa Biblia. Baada ya dakika chache, waulize

Page 152: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

137

2 nefi 29 – 30

kuelezea walichopata. Majibu yanayowezekana yanajumuisha kwamba (1) ) Bwana anaku-mbuka watu wote na hutuma ujumbe wake kwa mataifa yote (angalia mstari 7); (2) Bwana anaongea ujumbe huo huo kwa mataifa yote, na Kitabu cha Mormoni ni ushuhuda wa pili kwa ukweli katika Biblia (angalia mstari 8); (3) Bwana siku zote ni sawa, na Anasema kulingana na radhi Yake (angalia mstari 9); (4) Kazi ya Mungu haijamalizika, na ataendelea kuongea ili kukamilisha kazi yake (angalia mstari 9); (5) watu hawapaswi kudhania kwa-mba Biblia ina maneno yote ya Bwana au kwamba Bwana haja sababisha maneno zaidi kuandikwa (angalia mstari wa 10); na (6) Bwana anawaamuru watu katika mataifa yote kurekodi maneno Yake (angalia mstari 11). Ili kuwasaidia wanafunzi kufupisha na kutumia kile walichojifunza kutoka sehemu hii ya masomo, wauulize baadhi au yote ya maswali yafuatayo:• Jinsi gani 2 Nefi 29 inaweza kutumika kutatua wasiwasi juu ya Kitabu cha Mormoni

kama kitabu cha ziada kwa Biblia?• Mistari hii imeongezaje upendo wako kwa Kitabu cha Mormoni?Gawa wanafunzi katika jozi tena. Waulize kufanya mazoezi ya kujibu swali “Kwa nini Wamormoni wana Biblia nyingine?” Kualika mtu mmoja kuuliza swali na mwingine kujibu swali. Kisha waulize kubadili majukumu na kurudia majadiliano. Katika mwisho wa shughuli hii, unaweza kuwahimiza wanafunzi kufikiria juu ya watu wanaowajua ambao wanaweza kunufaika kwa majadiliano ya kanuni hizi na kutafuta ushauri kutoka kwa Roho Mtakatifu juu ya jinsi ya kuzungumza na watu hawa.Unapokamilisha sehemu hii ya somo, hakikisha kwamba wanafunzi wanaelewa kwamba Bwana anakumbuka watu wote na atapeleka maneno Yake kwao.

2 Nefi 30:1–8Nefi anatabiri juu ya jukumu la Kitabu cha Mormoni katika siku za mwishoElezea kwamba baada ya kuwafundisha kuwa Mungu angekumbuka nyumba ya Israeli, Nefi alionya watu wake wasifikiri walikuwa na haki kuliko vile Wayunani wangekuwa. Pia aliwakumbusha kwamba watu wote wanaweza kuwa watu wa agano wa Mungu. Uliza mwanafunzi kusoma 2 Nefi 30:2 kwa sauti, na alika darasa kuangalia mambo mawili ambayo lazima tufanye ili kuwa sehemu ya watu wa Mungu wa agano. Alika wanafunzi kushiriki kile walichopata. Hakikisha kwamba wameelewa kwamba tunakuwa sehemu ya watu wa Mungu wa agano tunapotubu na kuamini katika Yesu Kristo.Eleza kwamba katika 2 Nefi 30:3, Nefi anaeleza njia moja ambayo Bwana anawakusanya watu wake wa agano katika siku za mwisho. Alika wanafunzi kusoma 2 Nefi 30:3 kimya kimya na kutambua mchakato huu. (Bwana anatuma Kitabu cha Mormoni. Wengi wa-nakiamini, na kuwaeleza wengine.) Unaweza kutaka kueleza kwamba Nefi hasa alitaja kwamba maneno ya Kitabu cha Mormoni kitapelekewa “sazo la uzao wetu,” maana yake ni wana wa Lehi.Wahimize wanafunzi kusoma 2 Nefi 30:4–8 kimya kimya, wakitafuta vishazi ambavyo vinaonyesha jinsi watu watabarikiwa wanapopokea Kitabu cha Mormoni.• Ni kwa njia gani ambapo wazao wa Lehi watabarikiwa wanapojifunza kuhusu ma-

babu zao?• Je, mistari hii inafundisha nini juu ya athari ambayo Kitabu cha Mormoni kinaweza

kuwa nayo juu ya watu wote?Hakikisha kwamba wanafunzi wanaelewa kwamba Kitabu cha Mormoni kinaweza kusaidia watu wote kuja kumjua Yesu Kristo na kuishi injili Yake. Unaweza kutaka kuandika kauli hii kwenye ubao.• Tunaweza kufanya nini ili kuwasaidia wengine kumjua Yesu Kristo kwa njia ya Kitabu

cha Mormoni?• Kitabu cha Mormoni kimekusaidia vipi kumjua Mwokozi?Alika wanafunzi kueleza uzoefu ambao wamekuwa nao kwa kushiriki Kitabu cha Mor-moni. Wahimize wanafunzi kuomba kwa ajili ya fursa ya kushiriki Kitabu cha Mormoni na watu wengine.

Mazoezi ya MwanafunziUnapowauliza wa-nafunzi kuzoea kue-leza ukweli wa injili, unawapa fursa ya kupata ufahamu mpana zaidi wa kweli hizo na kujiandaa kufundisha injili kwa watu wengine. (Kumbuka kudumisha uwiano katika matumizi yako ya mbinu hii ya mafundisho haya. Wa-limu hawapaswi kuacha wajibu wao na kufanya wanafunzi kuchukua mafundisho ya darasa.)

Page 153: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

138

SoMo 39

2 Nefi 30:9–18Nefi anatoa unabii wa hali ya dunia wakati wa MileniaElezea kwamba Nefi pia alitabiri juu ya Milenia —miaka 1000 kufuatia Ujio wa Pili wa Mwokozi. Fupisha 2 Nefi 30:9–10 kwa kueleza kuwa katika Ujio wa Pili wa Bwana, waovu wataanga-mizwa. Waulize wanafunzi kusoma 2 Nefi 30:12–18 kimya kimya, wakitafuta maelezo ya maisha wakati wa Milenia. Alika wanafunzi kufikiria kuwa wanaandika makala ya habari wakati wa Milenia, inayoelezea hali waliyogundua. Waulize waandike vichwa vya makala na kushiriki vichwa hivyo vya habari na kila mmoja.• Ni hali ipi ya milenia uliosoma katika 2 Nefi, ambayo inatarajiwa zaidi? Kwa nini?Elekeza mawazo ya wanafunzi kwa taarifa ifuatayo katika 2 Nefi 30:18: “Na Shetani hata-kuwa na nguvu juu ya mioyo ya watoto wa watu tena, kwa muda mrefu.” Unaweza kutaka kudokeza kwamba wanafunzi watie alama kwenye taarifa hii katika maandiko yao.• Kwa nini ni muhimu kujua kuwa haki hatimaye itashinda uovu?Baada ya wanafunzi kujibu, shuhudia kwamba Shetani hatakuwa na uwezo juu ya mioyo ya watu wakati wa Milenia, na haki na amani itaendelea. Waalike wanafunzi kusoma kwa sauti taarifa zifuatazo za Rais George Q. Cannon wa Urais wa Kwanza. Uliza darasa kusikiliza kwa nini Shetani hatakuwa na nguvu wakati wa Milenia.“Tunazungumza kuhusu Shetani kufungwa. Shetani atafungwa kwa nguvu za Mungu, lakini atafungwa pia kwa uamuzi wa watu wa Mungu kutomskiliza, kutotawaliwa naye. Bwana hatamfunga na kuchukua nguvu zake kutoka duniani wakati kuna wanaume na wanawake walio tayari kutawaliwa na yeye. Hiyo ni kinyume cha mpango wa wokovu. Kuwanyima watu haki yao ya kujiamulia ni kinyume na madhumuni ya Mungu wetu. Kulikuwa na wakati katika bara hili, ambao sisi tunakumbukumbu, wakati ambapo watu walikuwa wenye haki kiasi kwamba Shetani hakuwa na nguvu kati yao. Karibu vizazi vinne vilipita katika haki. Waliishi katika usafi na kufa bila dhambi. Hiyo ilikuwa ni kupitia kukataa kwao kumwitikia Shetani. Haijaandikwa kwamba Shetani hakuwa na nguvu katika maeneo mengine ya nchi katika kipindi hicho. Kulingana na historia yote tulinayo katika milki yetu, Shetani alikuwa na nguvu sawa juu ya watu ambao walikuwa tayari kumsikiliza. Lakini katika nchi hii hakuwa na nguvu, na alikuwa amefungwa hasa. Naamini kuwa hii itakuwa ndio hali katika milenia; na ninaelezea juu yake kama ninavyoeleza juu ya hali hiyo ya fu-raha ambayo imeelezwa katika rekodi ambayo nasema. Natarajia kwamba kabla ya Shetani kufungwa kikamilifu waovu wataangamizwa” (in Conference Report, Oct. 1897, 65).• Shetani atafungwa vipi katika kipindi cha Milenia?Wahimize wanafunzi kuishi kwa haki ili adui asiwe na nguvu juu yao.

Wazo la Ziada la Kufundisha2 Nefi 29:12–14. Ni zipi baraka za kumbukumbu za ziada za maandiko?Waulize wanafunzi kusoma 2 Nefi 29:12–14 kimya kimya, wakitafuta kile kitakachotokea katika siku za mwisho na maneno yote ambayo Mungu ameamuru kuandikwa katika nchi.

• Unafikiri ni vipi watu tofauti tofauti wa ulimwengu watafaidika kutokana na kuwa na kumbukumbu za kila mmoja?

Mzee Neal A. Maxwell wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alifundisha kwamba rekodi zingine zitatokea ili kushuhudia juu ya Yesu Kristo:

“Vitabu vilivyopotea ni miongoni mwa hazina ambazo bado hazijatokea. Zaidi ya ishirini ya hizi zimetajwa kwenye maandiko yaliyopo. Pengine ya kushangaza zaidi na kwa ukubwa zitakuwa kumbukumbu za ma-kabila yaliyopotea ya Israeli (ona 2 Nefi 29:13). Hatu-ngeweza hata kujua ushuhuda wa tatu unao kuja wa Kristo, ila kwa njia ya thamani ya Kitabu cha Mormoni, ushuhuda wa pili wa Kristo! kundi hili la tatu la ku-mbukumbu takatifu litakamilisha upatanifu wa ukweli. Basi, kama Mchungaji Mkamilifu alivyosema, ‘Neno langu litakusanywa pamoja’ (v. 14). ‘Na kutakuwa na zizi moja na mchungaji mmoja’ (1 Nefi 22:25) katika muunganiko wa pamoja wa vipindi vyote vya Wakristo wa historia ya wanadamu (ona M&M 128:18)” (“God Will Yet Reveal,” Ensign, Nov. 1986, 52).

Page 154: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

139

UtanguliziMiaka mingi kabla ya Yesu Kristo kuzaliwa, Nefi alipokea ufunuo kuhusu ubatizo wa Mwokozi. Wakati Nefi alipo-kuwa akiwaambia watu wake juu ya Ufunuo huo, aliwa-fundisha kile alichokiita “fundisho la Kristo” —kwamba

ili kupata uzima wa milele, ni lazima tufanye imani katika Yesu Kristo, kutubu dhambi zetu, kubatizwa, kupokea Roho Mtakatifu, na kuvumilia hadi mwisho.

SOMO 40

2 nefi 31

Mapendekezo ya Kufundisha

2 Nefi 31:1–13Nefi anafundisha kwamba wakati tunapobatizwa, tunafuata mfano wa MwokoziAnza darasa kwa kuwauliza wanafunzi maswali yafuatayo:• Je, unakumbuka nini juu ya ubatizo wako? Ulihisi vipi ulipobatizwa?Eleza kwamba wakati wanafunzi walipobatizwa, walikuwa wanafuata mfano ambao daima umekuwa ni sehemu ya Injili ya Yesu Kristo. Nefi alitumia kishazi fulani ili kurejea katika mfano huu. Alika wanafunzi kutafuta kishazi kinachopatikana katika 2 Nefi 31:2 na 2 Nefi 31:21. Wakishatambua kishazi “fundisho la Kristo,” uliza:• Ni maneno au vishazi gani katika 2 Nefi 31:2, 21 vinaonyesha umuhimu wa “fundisho

la Kristo”? (Majibu yanaweza kujumuisha “ lazima niongee kuhusu,” “hakuna njia nyi-ngine,” na “mafunzo pekee na ya kweli”.)

Onyesha picha ya Yohana Mbatizaji Akimbatiza Yesu (62133; Kitabu cha Sanaa za Injili [2009], no. 35). Alika wanafunzi kujifunza 2 Nefi 31:5–9 kimya kimya, wakitafuta vishazi vinavyobaini kwa nini Yesu Kristo alibatizwa. (Unaweza kutaka kupendekeza kwamba watie alama kwenye vishazi hivi.) Baada ya dakika chache, waulize wanafunzi kusoma vishazi walivyogundua.• Unafikiri ina maanisha nini “ili kutimiza utakatifu wote”? (Baada ya wanafunzi kujibu,

unaweza kueleza kwamba inamaanisha kutii amri. Rais Joseph F. Smith alisema kwamba “kutimiza utakatifu wote” ni “kutimiza sheria” [in Conference Report, Apr. 1912, 9].)

Uliza mwanafunzi kusoma 2 Nefi 31:10–12 kwa sauti.• Ni vipi mistari hii inaonyesha umuhimu wa ubatizo? (Nefi anafundisha kwamba ubatizo

ni amri kutoka kwa Baba wa Mbinguni, kwamba unahitajika ili kupata kipawa cha Roho Mtakatifu, na kwamba ni muhimu katika juhudi zetu za kumfuata Yesu Kristo.)

Waulize wanafunzi kufupisha mafundisho na kanuni walizojifunza kutoka 2 Nefi 31:5–12. Wanaposhiriki mawazo yao, hakikisha kwamba waelewa kanuni zifuatazo:Yesu Kristo aliweka mfano kamili wa utii kwetu ili kufuata.Ni lazima tumfuate Yesu Kristo, kubatizwa, na kupokea Roho Mtakatifu.Yesu Kristo, ingawa ni mtakatifu, alibatizwa ili kutimiza utakatifu wote.Uliza mwanafunzi kusoma 2 Nefi 31:13 kwa sauti. Elekeza mawazo ya wanafunzi katika vishazi “kwa moyo wa lengo moja,” “bila unafiki na udanganyifu mbele yake Mungu,” na “kwa kusudi kamili.” Unaweza kupendekeza kwamba watie alama vishazi hivi.• Vishazi hivi vinamaanisha nini kwenu? (Unaweza kutaka kuonyesha kwamba visha-

zivyote vitatu vinahusu haja ya kuwa waaminifu katika jitihada zetu za kutumia imani katika Mwokozi, kutubu dhambi zetu, na kufuata mfano wa Mwokozi.)

Ili kuwasaidia wanafunzi kuzidisha uelewa wao wa jinsi ya kufuata mfano wa Mwokozi katika aina mbalimbali za hali, uliza maswali kama yafuatayo:• Ni kwa jinsi gani vishazi hivi vinahusu shughuli kama vile masomo ya kila siku ya maa-

ndiko na mahudhurio ya Kanisa?• Kuna tofauti gani kati ya “kusema maombi” na kuomba “kwa moyo wa lengo moja”?

Page 155: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

140

SoMo 40

• Kuna tofauti gani kati ya kula mkate wa sakramenti na kushiriki mkate wa sakramenti “kwa kusudi kamili.”?

• Kuna tofauti gani kati ya kusema kwamba unasikitika kuhusu kitu fulani ulichofanya na kutubu “kwa moyo wa lengo moja”?

2 Nefi 31:14–21Nefi anafundisha kwamba baada ya ubatizo, tunahitaji kumpokea Roho Mtaka-tifu na kuendelea kufuata mfano wa MwokoziEleza kwamba Nefi alizungumza juu ya mlango unaofunguka kwenye njia. Uliza mwana-funzi kusoma 2 Nefi 31:17–18 kwa sauti. Wakati mwanafunzi amemaliza kusoma, chora mchoro rahisi kama ufuatao ubaoni:

• Kulingana na 2 Nefi 31:17, lango ni nini? (Toba na ubatizo. Andika Toba na Ubatizo chini ya lango.) ubatizo na toba ni sawa na njia na lango gani?

• Kulingana na 2 Nefi 31:18, njia inaelekea wapi? (Uzima wa milele. Andika Uzima wa milele katika mwisho wa njia. Unaweza kuhitajika kuelezea kwamba, kishazi “uzima wa milele” inahusu kutukuzwa katika ufalme wa selestia.)

• Nefi alifundisha kwamba baada ya ubatizo, tunapokea kipawa cha Roho Mtakatifu (ona 2 Nefi 31:13–14). Kulingana na 2 Nefi 31:17–18, Roho Mtakatifu hutufanyia nini? (Wasaidie wanafunzi kuelewa kwamba Roho Mtakatifu hushuhudia juu ya Baba na Mwana na huleta ondoleo la dhambi.)

• Kwa nini ni muhimu kwetu kupokea ushuhuda wa Baba na Mwana kwa njia ya Roho Mtakatifu?

Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa kazi ya Roho Mtakatifu katika ondoleo la dhambi, una-weza kutaka kueleza kishazi “ubatizo wa moto na wa Roho Mtakatifu” (2 Nefi 31:13–14; ona pia mstari wa 17). Alika mwanafunzi kusoma kauli ifuatayo ya Mzee Daudi A. Bednar wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili. Uliza darasa kusikiliza maana ya kubatizwa kwa moto na kwa Roho Mtakatifu.“Lango la ubatizo linatuingiza katika njia nyembamba iliyosonga. . . .“Tumeamriwa na kuelekezwa kuishi ili kwamba asili yetu ya anguko ibadilishwe kupitia kwa nguvu ya utakaso wa Roho Mtakatifu. Rais Marion G. Romney alifundisha kwamba ubatizo wa moto kwa Roho Mtakatifu ‘hutuongoa kutoka katika hali ya kimwili, kuwa hali ya utakatifu. Unatakasa, kuponya, na kutakasa nafsi. . . . Imani katika Bwana Yesu Kristo, toba, na ubatizo wa maji vyote ni sharti la kwanza, ambayo, kisha [ubatizo wa moto] ndio ukamilifu. Ili kupokea [ubatizo huu wa moto] ni lazima kuosha mavazi ya mtu katika damu ya upatanisho wa Yesu Kristo’ (Learning for the Eternities, comp. George J. Romney [1977], 133; ona pia 3 Nefi 27:19–20).“Hivyo, tunapozaliwa mara ya pili na kujitahidi daima kuwa na Roho Wake pamoja nasi, Roho Mtakatifu hutakasa na kusafisha nafsi zetu kama kwa moto (ona 2 Nefi 31:13–14, 17). Hatimaye, tutasimama bila doa mbele ya Mungu” (“Clean Hands and a Pure Heart,” Ensign or Liahona, Nov. 2007, 81).• Ni nini Mzee Bednar na Rais Romney walisema “ubatizo wa moto” unatufanyia?• Ni baraka zipi za ziada tunazoweza kupokea kupitia kwa ushawishi wa Roho Mtakatifu?

VielelezoVielelezo kwenye ubao vinaweza kuwasaidia wanafunzi kuelewa mawazo ya kufikirika. Unapochora kwenye ubao, kumbuka kwamba michoro rahisi kawaida huwa bora kuliko ile ngumu. Kwa kawaida ni wazo nzuri kufanya mazoezi ya maonyesho mara chache kabla ya wanafunzi kuwasili dara-sani. Ikiwa una wasiwasi kuchora kwenye ubao, fikiria kuuliza mwanafu-nzi kukuchorea.

Page 156: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

141

2 nefi 31

• Unawezaje “kujitahidi ili daima kuwa na Roho Wake”pamoja na wewe?• Ni wakati gani umewahi kuhisi Roho Mtakatifu akitenda kazi katika maisha yako?Eleza kwamba katika 2 Nefi 31:18, neno iliyosonga ina maanisha nyembamba, thabiti, kamili, na kuruhusu bila kupotoka. Nephi alitumia neno hili kuelezea njia ambayo lazima tuchukue baada ya ubatizo ili kupokea uzima wa milele. Waulize wanafunzi kutafakari kimoyomoyo swali ifuatayo:• Tunahitaji kufanya nini baada ya ubatizo ili kukaa katika njia ya uzima wa milele?Wakati wanafunzi wanapotafakari swali hili, waalike kutafuta majibu katika 2 Nefi 31:15–16, 19–21. Unaweza kupendekeza kwamba waweke alama kwenye maneno au vishazi vinavyoeleza kile tunachopaswa kufanya ili kupokea uzima wa milele. Baada ya muda wa kutosha, alika wanafunzi wachache kushiriki yale waliyoweka alama. Wanapojibu, andika majibu yao ubaoni. Mfano wako lazima ufanane kitu kama hiki:

Hakikisha kwamba wanafunzi wanaelewa kwamba kama tunaishi kulingana na fundi-sho la Kristo, tutapata uzima wa milele.Kuhitimisha somo, mwulize mwanafunzi kusoma 2 Nefi 31:20 kwa sauti. Onyesha wazi kwamba 2 Nefi 31:19–20 ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Unaweza kuhimiza wa-nafunzi kutia alama kwenye kifungu hiki katika njia tofauti ili waweze kukitambua kwa urahisi. Waalike kujibu moja ya maswali yafuatayo katika jarida zao masomo za maandiko au daftari za darasa:• Kulingana na yale uliyosoma katika somo hili, ni nini kinakupa matumaini kuwa una-

weza kupata uzima wa milele?• Je! Agano ulilofanya katika ubatizo limeathiri vipi maisha yako?

Umahiri wa Maandiko—2 Nefi 31:19–20Shiriki kauli ifuatayo ya Mzee Richard G. Scott wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili:“Uwezo mkubwa unaweza kutokana na kukariri maandiko. Kukariri maandiko ni kujenga urafiki mpya. Ni kama kugundua mtu mpya ambaye anaweza kusaidia wakati wa mahi-taji, kutoa mwongozo na faraja, na kuwa chanzo cha motisha ya mabadiliko unaohitajika” (“The Power of Scripture,” Ensign or Liahona, Nov. 2011, 6).Kwenye bango (au kipande cha karatasi), andika Mimi nimekariri 2 Nefi 31:19–20.  Weka bango mahali ambapo wanafunzi wataweza kuona. Wape wanafunzi changamoto ku-kariri kifungu hiki wao wenyewe au pamoja na familia zao. Waalike kutia saini kwenye bango katika siku zijazo wakati wamekariri kifungu. Kama wamefanya kazi na familia zao kukariri, wanaweza pia kuandika majina ya familia zao kwenye bango. Kumbuka kupima changamoto hii kulingana na uwezo wa watu binafsi na hali ili kila mwanafunzi aweze kuwa na mafanikio.Toa ushuhuda wako juu ya thamani ya kukariri maandiko, kama vile 2 Nefi 31:19–20, ambayo ina maneno ya matumaini.Angalia: Kwa sababu ya hali na urefu wa mafundisho ya leo, unaweza kutaka kutumia shu-ghuli hii katika siku nyingine, wakati una muda zaidi.

Toba na Ubatizo

Uzima wa Milele

endelea kufuata mfano wa Mwokozi, endelea mbele kwa subira katika Kristo, kuwa na imani na tumaini, upendo wa Mungu na watu wote, shiriki

maneno ya Kristo, vumilia hadi mwisho

2 Nefi 31:19–20 ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Rejea wazo la mafundisho mwishoni mwa somo ili kuwasaidia wanafunzi katika umahiri wao wa kifungu hiki.

Page 157: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

142

MafUnzo ya MaSoMo - nyUMbani

Mafunzo ya Masomo - Nyumbani2 Nefi 26–31 (Kitengo cha 8)

Nyenzo za maandalizi kwa Mwalimu wa Mafunzo- Nyumbani Muhtasari wa Mafunzo ya Masomo ya Kila Siku ya NyumbaniMuhtasari ufuatao wa mafundisho na kanuni ambazo wa-nafunzi walijifunza waliposoma 2 Nefi 26–31 (kitengo cha 8) haukusudiwi kufundishwa kama sehemu ya somo lako. Somo unalofundisha huzingatia tu mafundisho na kanuni hizi chache. Fuata ushawishi wa Roho Mtakatifu unapofikiria mahitaji ya wanafunzi wako.

Siku 1 (2 Nefi 26–27)Wanafunzi walisoma unabii wa Nefi kuhusu siku za mwisho. Walijifunza kuwa kila kitu ambacho Bwana hufanya ni kwa manufaa ya dunia na kwamba Bwana anapenda watu wote na anawaalika wote kuja Kwake na kushiriki wokovu Wake. Wanafunzi pia waligundua ukweli kwamba kuja kwa Kitabu cha Mormoni ni njia moja ambayo Mungu atakamilisha kazi Yake katika siku za mwisho. Aidha, waligundua kwamba Kitabu cha Mormoni na injili ya urejesho vitaleta furaha na ufahamu kwa wale wanaosoma na kuvikubali.

Siku 2 (2 Nefi 28)Wakati wa kusoma maonyo ya Nefi kuhusu mafundisho ya uwongo yanayopatikana katika siku za mwisho, wanafu-nzi walijifunza kwamba Kitabu cha Mormoni kinafunua mawazo ya uongo ya shetani na kinatuimarisha dhidi ya miundo yake miovu. Zaidi ya hayo, walijifunza jinsi Shetani anavyotumia mbinu nyingi ili kujaribu kutushinda, kama vile kutuchochea kwa hasira, kututuliza na kutuliwaza, na kujipendekeza kwetu.

Siku 3 (2 Nefi 29–30)Wanafunzi walijifunza kwamba Bwana hutoa maandiko kuleta watu kwa maagano Yake na kwamba Kitabu cha Mormoni kinaweza kusaidia watu wote kumjua Yesu Kristo na kuishi injili yake. Bwana alimwonyesha Nefi kwamba watu wengi katika siku za mwisho watakataa Kitabu cha Mormoni. Wanafunzi walipata fursa ya kufikiria juu ya ma-isha yao wenyewe na jinsi jamii yao itakuwa tofauti wakati wa Milenia kwa sababu Shetani hatakuwa na uwezo juu ya mioyo ya watu, na haki na amani itadumu.

Siku 4 (2 Nefi 31)Kweli zifuatazo kuhusu mafundisho ya Kristo na mfano wa Mwokozi zilisisitizwa: Yesu Kristo alitimiza haki zote kwa kutii amri zote za Baba, na ni lazima tufuate mfano wa Yesu Kristo wa utiifu kwa kubatizwa na kupokea Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu anashuhudia kuhusu Baba na Mwana na analeta ondoleo la dhambi. Kama tunaishi kuli-ngana na mafundisho ya Kristo, tutapata uzima wa milele. Kama tunaishi kulingana na mafundisho ya Kristo, tutapata uzima wa milele.

UtanguliziSomo hili linasisitiza kuwa kila kitu Baba wa Mbinguni anafanya ni kwa faida ya ulimwengu na kinakuzwa kwa upendo kwa watoto Wake. Somo hili pia linagusia jinsi Kitabu cha Mormoni kinaanika mafundisho ya uongo ya Shetani yanayopatikana katika siku zetu na jinsi uzima wa milele huja kwa wale wanao-fuata mafundisho ya Kristo.

Mapendekezo ya KufundishaWaulize wanafunzi kama wana mawazo yoyote au ufahamu kutoka masomo yao ya maandiko ambayo wangependa kushi-riki na wanafunzi kabla ya kuanza somo. Wahimize wanafunzi kuuliza maswali yoyote waliyonayo juu ya kile walisoma. Waalike kuandika hisia za kiroho wanazopokea wanaposoma na kuta-fakari maandiko na kufanya kazi zao. Hii italeta roho ya ufunuo katika maisha yao.

Waulize wanafunzi kukusaidia kuorodhesha ubaoni au kwe-nye kipande cha karatasi baadhi ya majibu kwa swali lifuatalo: Kama ungejua kwamba muda wako duniani unafika mwisho na kwamba ungeweza kuandika barua moja ambayo uzao wako na ulimwengu mzima ungeweza kusoma, ungechagua mada gani ili kujumuisha katika ujumbe wako?

Alika wanafunzi kupitia kwa haraka 2 Nefi 26–31 na shajara zao za kujifunza maandiko ili kuona ni mada zipi Nefi alieleza alipo-karibia mwisho wa maisha yake. Linganisha kile wanachopata na majibu waliyoandika kwenye ubao. Ushauri wa mwisho wa Nefi uliandikwa kwa wale watu wanaoishi katika siku za mwisho na una vidokezo vya kutusaidia kutambua ukweli, kuepuka vizuizi vya Shetani, na kufuata mafundisho ya Yesu Kristo.

Page 158: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

143

MafUnzo ya MaSoMo - nyUMbani

2 Nefi 26Baada ya Nefi kutoa unabii kuhusu kuharibiwa kwa watu wake, anatabiri kuhusu siku za mwisho na kuwaalika wote kuja kwa KristoAlika wanafunzi kusoma 2 Nefi 26:29–31 na kutafuta moja ya mbinu za Shetani ambayo Nefi alituonya juu yake. Baada ya wa-nafunzi wachache kujibu kwa kile walichokiona, uliza maswali yafuatayo:

• Kulingana na 2 Nefi 26:29, ukuhani wa uongo ni gani?• Ni nini kinachoonekana kama motisha kwa wengine kushiriki

katika ukuhani wa uongo?• Bwana anatarajia tutiwe motisha na nini tunapofanya kazi

Kanisani? Unamjua nani ambaye ni mfano mzuri wa hili?

Angalia 2 Nefi 26:23–28, 33 na kazi ya siku 1, 3. Uliza: Ni kitu gani kilichompa Bwana motisha katika kazi Yake?

Baada ya wanafunzi kadhaa kujibu, wezesha darasa kujibu maswali yafuatayo:

• Ni vishazi gani katika 2 Nefi 26:23–28, 33 vina tufundisha kwamba Bwana anawapenda watu wote na ana waalika wote kuja Kwake na kushiriki wokovu Wake na kwamba kila kitu Bwana anachofanya ni kwa manufaa ya dunia?

• Kwa nini ingekuwa muhimu kwetu kujifunza kuwa na moti-sha ya upendo kwa wengine badala ya uchoyo au tamaa ya kupata sifa za watu wengine?

• Unafikiria ni kwa njia gani tunaweza kuwa zaidi na hisani, upendo, na kama Kristo katika kazi zetu za Kanisa?

2 Nefi 28Nefi anaonya dhidi ya udanganyifu wa ShetaniWaeleze wanafunzi kwamba katika 2 Nefi 28, Nefi aliendelea kuweka wazi mawazo ya uongo yanayofundishwa na shetani. Pitia “uwongo na yasiyofaa na mafundisho ya kipumbavu” ilivyoelezwa katika 2 Nefi 28:3–9, na waulize wanafunzi maswali yafuatayo. Yanaweza kujumuisha majibu waliyoandika katika jarida zao ya masomo ya katika wiki iliopita.

• Ni nini maana ya “tumieni wengine kwa sababu ya maneno yao”? (2 Nefi 28:8). (Mifano inaweza kujumuisha kuwadhi-haki wengine na kunukuu vibaya au kuongeza chumvi kile wengine wamesema.)

• Watu wa leo wanawezaje “kuchimba shimo” (2 Nefi 28:8) kwa jirani zao?

• Kuna hatari gani katika kujaribu kumficha Bwana dhambi au kuweka matendo yetu katika giza? (Ona 2 Nefi 28:9.)

• Ni mafundisho gani ya uwongo katika 2 Nefi 28:3–9 una-yofikiri ni potovu zaidi kwa vijana leo? Kwa nini unafikiri ni hatari? Vijana hushawishiwa vipi na fundisho hilo la uongo? (Ona siku 2, kazi 1.)

Pitia 2 Nefi 28:20–23 na hadithi ya Rais Boyd K. Packer juu ya mamba wa kiroho kutoka somo la siku 2. Alika wanafunzi kushiriki na darasa ishara za onyo walizochora katika shajara zao za kujifunza maandiko (siku ya 2, kazi 5) zinazoonyesha hatari za kiroho wanazofikiri vijana wanahitaji kuonywa kuhusu leo.

Uliza: Kati ya mambo yote ambayo Nefi angeweza kuandika alipokamilisha rekodi yake, kwa nini unafikiri aliandika kuhusu udanganyifu na mbinu za Shetani? (Unaweza kutaka kushuhu-dia juu ya msaada na nguvu tunazopokea ili kushinda mbinu za Shetani tunaposoma kwa makini Kitabu cha Mormoni.)

2 Nefi 31Nefi anafundisha jinsi Mwokozi aliweka mfano kamili kwa ajili yetuChora picha rahisi ya njia inayoongoza katika lango. Alika wana-funzi kusoma 2 Nefi 31:17–18 na kutafuta jinsi Nefi alitumia huu mfano wa njia na mlango kusisitiza njia pekee ya kuja kwa Yesu Kristo. Kisha uliza maswali yafuatayo:

• Kulingana na mistari hii, mlango na njia zinawakilisha nini? (Mlango unawakilisha toba, ubatizo, na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu.)

• Kutokana na yale uliyojifunza katika masomo yako binafsi ya 2 Nefi 31, kwa nini kupokea Roho Mtakatifu kunajuli-kana kama “ubatizo wa moto”? (Ona 2 Nefi 31:13; ona pia mstari 17.)

Alika mwanafunzi kusoma 2 Nefi 31:19–21 kwa sauti. Waulize wanafunzi kuangalia kinachohitajika kwetu baada ya kupita katika “njia.” Baada ya wanafunzi kujibu kile walichokiona, uliza maswali yafuatayo:

• Unafikiri Nefi alimaanisha nini alipoandika, “Hili ndilo fundi-sho la Kristo”? (2 Nefi 31:21).

• Kuzingatia yale ulisoma leo, unafikiri Baba wa Mbinguni anakuhitaji kufanya nini ili kukusaidia kuendelea katika njia nyembamba na iliyosonga? (Unaweza kutaka kuhimiza wana-funzi kuweka lengo katika kujibu swali hili.)|

Kitengo Kifuatacho (2 Nefi 32–Yakobo 4)Unapenda kula? Katika kitengo kifuatacho, wanafunzi wata-jifunza kuhusu maana ya “kushiriki maneno ya Kristo” (2 Nefi 32:3). Ni kwa jinsi gani nabii anastahili kusahihisha watu walio-anza kuathiriwa na upendo wa mali au kwa watu wanaovunja sheria ya usafi wa kimwili? Fahamu jinsi Yakobo anavyokabiliana na matatizo haya.

Page 159: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

144

UtanguliziBaada ya kufundisha juu ya “njia nyembamba na iliyosonga” (2 Nefi 31:18), Nefi alidhania kwamba watu wake walihangaika juu ya kile wangefanya baada ya kuingia katika ile njia. Yeye akajibu maswali yao kwa

kuwahimiza “kushiriki maneno ya Kristo” na “kusali kila wakati” (2 Nefi 32:3, 9). Aliwahakikishia kwamba kama wangefanya mambo haya, Roho Mtakatifu ange-wasaidia kujua la kufanya.

SOMO 41

2 nefi 32

Mapendekezo ya Kufundisha

2 Nefi 32:1–7Nephi anatushauri kutafuta mwongozo wa Mungu kupitia maneno ya Yesu Kristo na ushawishi wa Roho MtakatifuAlika wanafunzi kufikiria juu ya wakati ambapo walielezea njia ya kutoka sehemu moja hadi nyingine. Waulize kuelezea kwa nini ilikuwa rahisi au vigumu kutoa maalezo hayo.Wakumbushe wanafunzi kwamba katika somo lililopita, walisoma maelekezo ambayo Nefi aliwapa watu wake. Baada ya kutoa maalekezo hayo, alisema, “Hii ndiyo njia” (2 Nefi 31:21). Ili kuwasaidia wanafunzi kutathmini yale waliojifunza, uliza maswali yafuatayo:• Tukifuata maelekezo ya Nefi, yatatuelekeza wapi? (Katika uzima wa milele; ona 2 Nefi

31:20.)• Kulingana na 2 Nefi 31:17–18, tunaanzaje kwenye njia inayoelekea kwenye uzima wa milele?Eleza kwamba 2 Nefi 32 ni mwendelezo wa mafundisho ya Nefi katika 2 Nefi 31. Waulize wanafunzi kuangalia katika 2 Nefi 32:1 kwa swali ambalo watu wa Nefi walikuwa nalo kuhusu yale aliyowafundisha. Alika wanafunzi wachache kuelezea swali hili kwa maneno yao wenyewe. (Hakikisha kwamba wanafunzi wanaelewa kwamba watu walishangaa kile wangefanya baada ya kuanza katika njia ya uzima wa milele.)Alika mwanafunzi kusoma 2 Nefi 32:2–3 kwa sauti. Uliza darasa kuangalia majibu ya Nefi kwa swali la watu. Elezea wazi kwamba 2 Nefi 32:3 ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Unaweza kuwahimiza wanafunzi kukiweka alama katika njia tofauti ili waweze kukipata kwa urahisi.• Ni maneno gani katika 2 Nefi 32:3 yanaeleza jinsi tunavyopaswa kupokea maneno ya

Kristo? Kushiriki na kunyofoa kunatofautiana kwa njia gani?• Unafikiri inamaanisha nini kushiriki maneno ya Kristo?• Ni nini Nefi alisema itakuwa matokeo tunaposhiriki maneno ya Kristo?• Ni sehemu gani nyingine tunakoweza kupata maneno ya Yesu Kristo? (Majibu yanaweza

kujumuisha maandiko, maneno ya manabii wa kisasa, na mwongozo kutoka kwa Roho Mtakatifu.)

Hakikisha kwamba wanafunzi wanaelewa kwamba tunaposhiriki maneno ya Kristo, maneno ya Kristo yatatuambia mambo yote sisi tunapaswa kufanya.Ili kuwasaidia wanafunzi kufikiri kuhusu jinsi wanavyostahili kushiriki maneno ya Yesu Kristo, soma orodha ifuatayo, ukitua baada ya kila kipengele. Uliza wanafunzi kuandika orodha katika shajara zao za kujifunza maandiko au daftari za darasani au kwenye kipande cha karatasi. 1. Masomo ya maandiko ya binafsi 2. Mkutano wa Sakramenti 3. Mkutano mkuu 4. Masomo ya binafsi ya mandiko 5. Seminari

2 Nefi 32:3 ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Rejelea wazo la mafundisho mwishoni mwa somo ili kuwasaidia wanafunzi kwa umahiri wao wa kifungu hiki.

Page 160: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

145

2 nefi 32

6. Jioni ya familia nyumbani 7. Mkutano wa akidi ya Ukuhani wa Haruni au darasa la Wasichana 8. Maombi binafsiAlika wanafunzi kufikiria kuhusu jinsi wanavyostahili kutafuta maneno ya Yesu Kristo katika kila moja ya mipangilio hii. Kwa kila kitu, wawezeshe kuandika shiriki, nyofoa, au njaa. Kwa mfano, mwanafunzi anaweza kushiriki katika masomo ya binafsi ya maandiko lakini kunyofoza katika mkutano mkuu. Mwanafunzi asiyekuwa makini katika mkutano wa sakramenti anaweza kuandika neno njaa kando ya neno hilo.Waulize wanafunzi kuchagua moja ya shughuli ambayo wao kwa sasa “wananyofoa” au “kujinyima” na waalike kuweka malengo yatakayo wasaidia“kushiriki maneno ya Kristo” zaidi katika mazingira hayo. (Unaweza kuwahimiza kufikiri kuhusu Wajibu wao kwa Mu-ngu au malengo ya Ukuaji Binafsi kwa uhusiano na malengo haya).Ili kuimarisha ufahamu wa wanafunzi wa majukumu yao ya kutafuta uongozi wa binafsi kutoka kwa Roho Mtakatifu, wawezeshe kusoma 2 Nefi 32:4–7 7 kimya. Kisha waombe kujadili maswali yafuatayo pamoja na mwenzi. (Unaweza kutoa maswali haya kwenye kipeperushi au kuyaandika ubaoni kabla ya darasa kuanza.)• Katika mstari wa 4, unafikiri inamaanisha nini “kuuliza” au “kubisha”? Ni nini Nefi

anasema ni matokeo kwa wale ambao hawataomba au kubisha?• Nefi anaahidi kuwa tunaweza kupata baraka zipi tunapompokea Roho Mtakatifu?• Kwa nini Nefi aliomboleza kwa ajili ya watu wake?Dhihirisha matumaini yako kwamba wanafunzi waposhiriki maneno ya Yesu Kristo, Roho Mtakatifu atawasaidia kufuata njia ya uzima wa milele.

2 Nefi 32:8–9Nefi anatushauri kuomba kila sikuEleza kwamba Nefi baadaye alilenga katika jambo moja tunaloweza kufanya ili kupata maneno ya Yesu Kristo. Alika wanafunzi kusoma 2 Nefi 32:8 kimya kimya, wakitafuta kile Nefi alisema tunapaswa kufanya. Baada ya kutambua jibu, waulize maswali yafuatayo ili kuwasaidia kutafakari umuhimu wa sala:• Kwa nini unafikiri Roho Mtakatifu anataka tuombe?• Kwa nini unafikiri Shetani hataki tuombe? Shetani anaweza kwa njia gani kujaribu

kuwashawishi watu wasiombe?Alika mwanafunzi kusoma 2 Nefi 32:9 kwa sauti. Onyesha wazi kwamba 2 Nefi 32:8–9 ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Unaweza kutaka kushauri kwamba wanafunzi waweke alama kwa njia bainifu ili waweze kuitambua kwa urahisi.• Tunapaswa kuomba mara ngapi? Unafikiri inamaanisha nini “kusali kila wakati”?Elezea kauli ifuatayo na Mzee David A. Bednar wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili. (Kama inawezekana, toa nakala ya nukuu hili ili wanafunzi waweze kusoma pamoja na kuzingatia maneno ya Mzee Bednar. Ikiwa umenakili, kumbuka kuwa nukuu imeendele-zwa baadaye katika somo baada ya mjadala mfupi. Jumuisha sehemu hiyo ya taarifa pia.) Alika wanafunzi kusikiliza ushauri wa Mzee Bednar juu ya jinsi ya “kusali kila wakati.”

“Kunaweza kuwa na vitu katika hulka zetu, katika tabia zetu, au kuhusu maendeleo yetu ya kiroho ambavyo tunahitaji kushauriana na Baba wa Mbi-nguni katika sala ya asubuhi. . . .“Wakati wa mkondo wa siku, tunaweka maombi katika mioyo yetu kwa ajili ya misaada na uongozi wa kila mara. . . .“Tunatambua wakati wa siku hii fulani kuwa kuna matukio ambapo kwa

kawaida tunataka kuwa na tabia ya kuzungumza kwa ukali, na haifanyiki; au tunaweza kuelekezwa kwa hasira, lakini hatukubali. Tunahisi msaada wa mbinguni na nguvu na kutambua kwa unyenyekevu majibu ya maombi yetu. Hata katika wakati huo wa kutambua,tunatoa maombi ya shukrani kimya kimya” (“Pray Always,” Ensign or Liahona, Nov. 2008, 41–42).Ili kuwasaidia wanafunzi kutafakari ushauri huu, uliza:

2 Nefi 32:8–9 ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Rejelea wazo la mafundisho kufikia mwisho wa somo ili kuwasaidia wanafunzi kwa umahiri wao wa kifungu hiki.

Page 161: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

146

SoMo 41

• Je, unaweza kufikiria nyakati leo au katika siku za hivi karibuni ambapo ungeweza kufuata haya mapendekezo kutoka kwa Mzee Bednar? (Unaweza kuuliza wanafunzi kutafakari swali hili kimoyomoyo badala ya kujibu kwa sauti.)

Endelea kusoma ushauri wa Mzee Bednar:“Kufikia mwisho wa siku yetu, tunapiga magoti tena na kutoa ripoti kwa Baba yetu. Tunatathmini matukio ya siku na kutoa shukrani za dhati kwa ajili ya baraka na msaada tu-liopokea. Tunatubu na, kwa msaada wa Roho wa Bwana, kubaini njia tunazoweza kufanya na kuwa bora kesho. Hivyo jioni yetu ya sala hujenga juu ya na ni endelezo la sala yetu ya asubuhi. Na jioni yetu ya maombi pia ni maandalizi kwa sala ya maana ya asubuhi.“Sala za asubuhi na jioni —na sala zote zilizo katikati ya —si matukio yaliyo tengana, bali yanahusishwa pamoja kila siku na katika siku, wiki, miezi na hata miaka. Hii ni kwa sehemu jinsi ya kutimiza marudio ya maandiko ya ‘kusali kila wakati’(Luka 21:36; 3 Nefi 18:15, 18; M&M 31:12). Kadiri sala ya maana ni muhimu katika kupata baraka kutoka juu. Mungu ana akiba kwa ajili ya watoto wake waaminifu “(“Salini kila wakati,” 42).Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa sehemu ya mwisho ya 2 Nefi 32:9, elezea kwamba neno kutakasa lina maana “ kweka wakfu, kufanya takatifu, au kuwa na haki” (Guide to the Scriptures, “Consecrate, Law of Consecration,” scriptures.lds.org).• Kwa nini tunapaswa kuomba wakati “tunafanya lolote kwa Bwana”?• Unafikiri inamaanisha nini kwa Bwana kutakasa kile ambacho tunafanya kwa ajili ya

wema wa roho zetu?• Ushauri wa Mzee Bednar unaweza kutusaidia vipi kuishi maisha ya wakfu zaidi?Shuhudia kwamba tunaposali kila wakati, tutaweza kufanya yote ambayo Bwana

angetaka tufanye kwa ajili ya ustawi wa roho zetu.Ili kufupisha kile wanafunzi wamejadili katika somo hili, shiriki kauli ifuatayo ya Mzee Spencer J. Condie wa Wale Sabini:“Unaweza kuwa unakabiliwa na maamuzi kuhusu umisionari, kazi yako ya baadaye, na hatimaye, ndoa. Unaposoma maandiko na kuomba kwa ajili ya mwelekeo, huwezi kuona kiuhalisia jibu katika mfumo wa maneno

yaliyochapishwa kwenye ukurasa, lakini unaposoma utapata hisia tofauti, ushawishi, na, kama alivyoahidi, Roho Mtakatifu ‘atakuonyesha vitu vyote ambavyo mnastahili kutenda.’ [2 Nefi 32:5.]” (“Becoming a Great Benefit to Our Fellow Beings,” Ensign, May 2002, 45).

Umahiri wa Maandiko—2 Nefi 32:3Waulize wanafunzi ni kwa muda gani wanafikiri itawachukua kukariri 2 Nefi 32:3 ikiwa wataisoma kila wakati wanapokula chakula. Wape changamoto kupekua maandiko haya—wakishiriki maneno ya Kristo—kila wakati wanapokula chakula kwa siku chache zijazo. Baada ya wanafunzi kukariri mstari, waalike kuripoti ni muda gani wa chakula ilichukua

Umahiri wa maandiko—2 Nefi 32:8–9Waulize wanafunzi kama wamewahi kujaribu kuwa na maombi katika mioyo yao kwa siku nzima au wiki nzima. Waalike kushiriki uzoefu wao. Alika darasa kufikiria njia ambayo wa-naweza “kusali kila wakati” kwa saa 24 zijazo. Wape changamoto kufanya hivyo na kutoa majibu juu ya uzoefu wao katika mwanzo wa darasa.Fahamu: Kama huna muda wa kutumia mawazo haya ya kufundisha katika somo hili, fikiria kuyatumia kama mapitio katika masomo ya baadaye.

Tangazo na Habari za Usuli2 Nefi 32:2. Nini maana ya kuzungumza kwa lugha ya malaika?Wengine wanaweza kustajabu nini maana ya “kuzu-ngumza kwa lugha ya malaika.” Rais Boyd K. Packer

alifundisha kwamba kuzungumza kwa lugha ya malaika “kwa urahisi inamaanisha kwamba unaweza kuzungumza kwa nguvu ya Roho Mtakatifu” (“The Gift of the Holy Ghost: What Every Member Should Know,” Ensign, Aug. 2006, 50).

Page 162: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

147

UtanguliziNefi alihitimisha rekodi yake kwa kutangaza kwamba maneno yake yalioandikwa yanashuhudia Yesu Kristo na yana washauri watu kutenda mema na kuvumilia hadi mwisho. Alisema kwamba ingawa aliandika “kwa unyonge,” maneno yake yalikuwa “yenye thamani

kuu” na yangeweza “kutiwa nguvu” kwa ajili ya wale ambao wangeyasoma (ona 2 Nefi 33:3–4). Alishuhudia kwamba maandiko yake yalikuwa “maneno ya Kristo” na kwamba watu wange wajibika kwa Mungu kwa majibu yao kwao (ona 2 Nefi 3:10–15).

SOMO 42

2 nefi 33

Mapendekezo ya Kufundisha

2 Nefi 33:1–2Nefi anafundisha juu ya nguvu ya Roho Mtakatifu katika kuweka ukweli kwa mioyo yetuChora picha ifuatayo ubaoni:

• Nini tofauti kati ya ujumbe kwenda kwa moyo wa mtu na ujumbe kwenda ndani  ya moyo wa mtu?

Alika mwanafunzi kusoma 2 Nefi 33:1 kwa sauti. Kisha waulize wanafunzi kutafakari swali llifuatalo kimya kimya.• Kwa nini unafikiri ni muhimu kwamba Roho Mtakatifu huweka ukweli kwa mioyo yetu

wala si ndani  ya mioyo yetu?Wanafunzi wanapotafakari swali hili, soma kwa sauti kauli ifuatayo ya Mzee David A. Bednar wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili. Eleza kwamba katika kauli hii, Mzee Bednar anazungumza juu ya 2 Nefi 33:1.

“Tafadhali angalia jinsi nguvu za Roho huweka ujumbe kwa lakini si lazima ndani  ya moyo. Mwalimu anaweza kueleza, kuonyesha, kushawishi, na kushuhudia, na kufanya hivyo kwa nguvu kubwa za kiroho na ufanisi. Hati-maye, hata hivyo, maudhui ya ujumbe na ushahidi wa Roho Mtakatifu hupenya ndani ya moyo tu kama mpokeaji anayaruhusu kuingia” (“Seek Learning by Faith” [address to CES religious educators, Feb. 3, 2006], 1, si.lds.org).

Alika mwanafunzi kusoma kwa sauti taarifa ifuatayo na Mzee Gerald N. Lund wa Wale Sabini:“Kwa nini tu kwa moyo? Haki ya kujiamulia ya mtu binafsi ni takaifu sana na kwamba Baba wa mbinguni kamwe hatalazimisha moyo wa binadamu, hata kwa nguvu Zake za milele. . . . Mungu anaturuhusu kuwa walezi, au walinda lango, wa mioyo yetu wenyewe. Ni lazima, kwa mapenzi yetu wenyewe, tumfungulie Roho mioyo yetu” (“Opening Our Hearts,” Ensign or Liahona, May 2008, 33).• Nini inaonyesha kama ujumbe unaingia katika moyo wa mtu?• Ni lini umehisi kuwa ujumbe wa injili uliingia moyoni mwako? Je, hii inakuambia nini

juu ya moyo wako wakati huo?Waulize wanafunzi kusoma 2 Nefi 33:2 kimya kimya, wakitambua jinsi watu wanakabiliana na Roho Mtakatifu wakati wanaposhupaza mioyo yao. Unaweza kueleza kwamba neno

kwa ndani

Page 163: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

148

SoMo 42

“visivyofaa” inamaanisha “bure.” “Kutupa vitu vingi ambavyo vimeandikwa na kuvichu-kua kama vitu visivyofaa” ni kufikiri kuwa havina maana.• Ni nini baadhi ya tabia na mitazamo ya watu wenye mioyo migumu?• Kwenu ninyi, kuna ujumbe gani katika 2 Nefi 33:2? (Wanafunzi wanaweza kujibu

kwamba tunachagua kufungua au kufunga mioyo yetu kwa uongozi wa Roho Mtakatifu. Hakikisha kwamba wanatambua kwamba tunapofungua mioyo yetu, ujumbe kutoka kwa Roho Mtakatifu unaweza kuingia mioyoni mwetu.)

Kabla ya kuendelea na masomo, wape wanafunzi muda wa kufikiria kimya kimya hali ya mioyo yao na kuamua kama wanaruhusu ujumbe wa kweli katika mioyo yao.

2 Nefi 33:3–15Nefi anaelezea madhumuni ya rekodi yake na matumaini yake kwamba wasomaji wake wataamini katika KristoAndika yafuatayo ubaoni:

2 Nefi 33:3—Nawaombea siku zote . . .2 Nefi 33:4—Najua . . .2 Nefi 33:6—Natukuza . . .2 Nephi 33:7—Nina . . .

Alika wanafunzi kusoma 2 Nefi 33:3–7 7 kimya kimya, wakitafuta matumaini ya Nefi kwa wale ambao wangesoma maneno yake. Alika wanafunzi wachache kuja kwenye ubao kukamilisha sentensi, kwa kutumia maneno yao wenyewe au maneno ya Nephi. (Vishazi vichache kwenye ubao vinaelekeza kwenye zaidi ya jibu moja.)• Tunawezaje kuimarisha shuhuda zetu za kibinafsi juu ya Yesu Kristo na Upatanisho wake?Wezesha wanafunzi watano kusoma kwa zamu kwa sauti kutoka 2 Nefi 33:10–14. Uliza darasa kufuatilia kwa pamoja, wakitafuta vishazi katika buriani ya Nefi ambavyo vina ma-ana kwao. Unaweza kudokeza kwamba wanafunzi watie alama kwenye vishazi hivi.• Ni vishazi gani vyenye maana kwako? Kwa nini?”• Ikiwa watu wanaamini katika Kristo, je, watahisi vipi kuhusu Kitabu cha Mormoni?

(Ona 2 Nefi 33:10.)• Nefi alionya kuwa nini ingetokea kwa wale ambao wangekataa maneno yake? (Wakati

wanafunzi wanapojibu swali hili, unaweza kushauri kwamba wafikiri pia juu ya namna watakavyohisi katika uwepo wa Bwana kama wameamini, na kufuata maneno ya Nefi na manabii wengine.)

Waulize wanafunzi kusoma 2 Nefi 33:15 kimya kimya na kutafakari maneno ya mwisho ya Nefi: “Ni lazima nitii” Kisha wape dakika chache kuangalia nyuma kupitia Nefi 1 na 2 , wakitambua mifano ya utii wa Nefi. Baada ya dakika chache, waulize wanafunzi kushiriki walichopata. Majibu yanaweza kujumuisha kuondoka Yerusalemu, kurudi Yerusalemu ili kupata mabamba ya shaba, kurudi Yerusalemu tena kuomba familia ya Ishmaeli kujiunga nao, kuweka seti mbili za mabamba, kufuata maelekezo katika Liahona, kujenga meli, sa-fari ya nchi ya ahadi, kujitenga na Lamani na Lemuel, na kuongoza watu wake katika haki. Wakati wanafunzi wanapotoa mifano, unaweza kuyaorodhesha ubaoni.Andika yafuatayo ubaoni: lazima ni . . .Alika wanafunzi kukamilisha sentensi hii katika shajara zao za kujifunza maandiko au daf-tari za darasani. Onyesha matumaini yako kwamba wanaweza kuchagua kutii. Toa mawazo yako kuhusu jinsi maneno ya Nefi yanavyoweza kuwasaidia kuimarisha imani yao katika Yesu Kristo na kuongezeka kwa uwezo wao wa kufanya vizuri.

Page 164: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

149

2 nefi 33

Tathmini ya 2 Nefi Chukua muda fulani ili kuwasaidia wanafunzi kutathmini 2 Nefi. Waulize kufikiri juu ya kile walichojifunza kutokana na hiki kitabu, katika seminari na katika masomo yao binafsi ya maandiko. Kama inahitajika, wahimize kuangalia kwa haraka 2 Nefi ili kuwasaidia ku-kumbuka. Waulize wajiandae kuelezea kitu kutoka 2 Nefi ambacho kiliwaongoza kutenda wema na kuwa na imani katika Yesu Kristo, kama vile Nefi alivyosema (ona 2 Nefi 33:4). Baada ya muda wa kutosha, waulize wanafunzi kadhaa kutoa mawazo na hisia zao.Elezea kauli zifuatazo kuhusu wajibu tulio nao wa kusoma Kitabu cha Mormoni na baraka zinazokuja katika maisha yetu tunapotimiza wajibu huu:Rais Joseph Fielding Smith alisema: “Inaonekana kwangu kwamba muumini yeyote wa kanisa hili kamwe hataridhika mpaka akisome Kitabu cha Mormoni tena na tena, na kukitilia maanani kabisa ili aweze kushuhudia kwamba hakika ni rekodi yenye uongozi wa Mwenyezi ndani yake, na kwamba historia yake ni ya kweli” (in Conference Report, Oct. 1961, 18).Rais Gordon B. Hinckley alifundisha kwamba kama waumini wa Kanisa watasoma Kitabu cha Mormoni, “kutakuja katika maisha [yao] na nyumbani [mwao] kipimo kilichoongeza cha Roho wa Bwana, azimio imara la kutembea katika utiifu kwa amri Zake , na ushuhuda wa nguvu wa hali halisi ya uhai wa Mwana wa Mungu (“A Testimony Vibrant and True,” Ensign, Aug. 2005, 6).Kuhitimisha somo, unaweza kufikiria kushiriki uzoefu wako binafsi kama ushuhuda kwa-mba maneno ya Nefi katika aya hii yametimia katika maisha yako.

Kutia moyo wanafunzi kutamka kweliWanafunzi hunufa-ika kutokana na fursa za mara kwa mara ili kuelezea mawazo na hisia zao, kueleza kanuni za injili, na kushuhudia ukweli. Mzee Richard G. Scott wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alisema, “Wanafunzi wanapo-sema ukweli, unathibiti-shwa katika nafsi zao na kuimarisha shuhuda zao binafsi”(“To Understand and Live Truth” [address to CES religious educa-tors, Feb. 4, 2005], 3, si.lds.org). Hata hivyo, wakati ni muhimu ku-wapa wanafunzi nafasi ya kuelezea, hawapaswi kujisikia kulazimishwa au kushinikizwa kufanya hivyo.

Page 165: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

150

UtangUlizi Wa

Kitabu cha yakoboKwa nini tukisome kitabu hiki?Kwa kusoma kitabu cha Yakobo, wanafu-nzi wanaweza kujifunza masomo kutoka kwa mtu aliyekuwa na imani isiyotiki-sika katika Yesu Kristo. Yakobo alirudia ushuhuda wa Mwokozi na kuwaalika watu wake na wale ambao wangesoma maneno yake kutubu. Alifundisha na ku-dhihirisha umuhimu wa bidii na kutimiza miito kutoka kwa Bwana. Aliwaonya watu wake dhidi ya hatari za kiburi, utajiri na utovu wa maadili. Yakobo pia alinukuu na kuzungumzia mfano wa Zeno wa miti ya mizeituni, inayodhihirisha bidii isiyo na kifani ya Mwokozi ya kuleta wokovu kwa watoto wote wa Mungu na kutoa mtazamo wa matendo ya Mungu katika nyumba ya Israeli. Katika kukutana kwake na Sheremu mpinga Kristo, Yakobo anadhihirisha jinsi ya kujibu kwa haki wale wanaopinga au kukosoa imani yetu.

Ni nani aliyeandika kitabu hiki?Yakobo, mwana wa tano wa Saria na Lehi alikiandika kitabu hiki. Alizaliwa nyikani wakati wa safari ya familia yake kuele-kea nchi ya ahadi. Katika ujana wake, Yakobo “aliteseka kwa masumbuko na huzuni nyingi kwa sababu ya ujeuri wa kaka zake” (2 Nefi 2:1). Hata hivyo, Lehi alimuahidi Yakobo kuwa Mungu “ange-weka wakfu masumbuko [yake] kwa faida [yake]” na kwamba angetumia siku zake “kumhudumia Mungu [wake] ” (2 Nefi 2:2–3). Katika ujana wake Yakobo aliona utukufu wa Mwokozi (ona 2 Nefi 2:3–4). Nefi alimweka wakfu Yakobo kuwa kuhani na mwalimu wa Wanefi (ona 2 f5:26) na baadaye kumkabidhi yale mabamba madogo ya Nefi (ona Yakobo 1:1–4). Kama kiongozi na mwalimu mwaminifu wa ukuhani, Yakobo alifanya kazi kwa bidii kwamba awashawishi watu wake kuamini katika Kristo (ona Yakobo 1:7). Alipokea funuo kuhusu Mwokozi,

akapata uzoefu wa huduma ya malaika, akasikia sauti ya Bwana (ona Yakobo 7:5), na kumwona Mkombozi wake (ona 2 Nefi 11:2–3) Yakobo alikuwa Baba wa Enoshi, ambaye alimkabidhi mabamba kabla ya kifo chake.

Kitabu hiki kiliandikiwa nani, na kwa nini?Nefi alimshauri Yakobo kurekodi mafundi-sho matakatifu, funuo, na unabii “kwa ajili ya Kristo na kwa faida ya watu wetu” (Yakobo 1:4). Yakobo alitii maelekezo haya na kuhifadhi maandishi ambayo aliyaona kuwa “yenye thamani zaidi” (Yakobo 1:2). Aliandika: “Tunatumikia kwa bidii kuchora maneno haya kwenye bamba, tukitumai kwamba ndugu zetu wapendwa na watoto wetu watayapokea kwa mioyo ya shukrani. Kwani, kwa ma-dhumuni haya tumeandika mambo haya, ili wajue kwamba tulijua kuhusu Kristo, na tulikuwa na matumaini ya utukufu wake miaka mia mingi kabla ya kuja kwake” Yakobo 4:3–4 Yakobo alizungumizia juu ya mada muhimu ya maandishi yake aliposema hivi, “Kwa nini isizungumziwe upatanisho wa Kristo, na kupata ufahamu wake kamili?” Yakobo 4:12

Kiliandikwa lini na wapi?Kitabu cha Yakobo kinaanza karibu 544 K.K. wakati Nefi alipokabidhiwa mabamba madogo. Kinahitimishwa karibu mwishoni mwa maisha ya Yakobo, alipoyapasisha mabamba kwa mwanawe Enoshi. Yakobo aliandika rekodi hii alipokuwa akiishi katika nchi ya Nefi

Je! Ni nini baadhi ya sifa tofauti za kitabu hiki?Kitabu cha Yakobo kinatoa habari kuhusu serikali ya Wanefi kufuatia kifo cha Nefi. Nefi alimtawaza mtu kumrithi

kama mfalme na mtawala wa watu huku Yakobo na nduguye Yusufu wakiendelea kuwa viongozi wa kiroho wa Wanefi. Sifa nyingine inayo tofautisha kitabu hiki ni shutuma ya Yakobo kuhusu mazoea yasiyo kubalika ya kuwa na wake wengi. Rejeo la pekee kuhusu suala hili katika Kitabu cha Mormoni linatokea katika Ya-kobo 2. Kitabu cha Yakobo pia kinajumu-isha mlango ulio mrefu zaidi katika Kitabu cha Mormoni, Yakobo 5, ulio na istiari ya Zeno juu ya miti ya mizeituni. Kuongezea, kitabu cha Yakobo kinarekodi kisa cha kwanza cha nabii wa Kitabu cha Mormoni akiwaonya moja kwa moja Wanefi dhidi ya kiburi — dhambi ambayo hatimaye ingesababisha kuangamia kwao (ona Yakobo 2:12–22; Moroni 8:27). Inarekodi pia kutokea kwa mara ya kwanza kwa mpinga Kristo kati ya Wanefi.

MuhtasariYakobo 1 Yakobo atii amri ya Nefi ya kuweka kumbukumbu taka-tifu. Nefi afa Yakobo na Yusufu wahudumu miongoni mwa watu, wakiwafundisha neno la Mungu.

Yakobo 2–3 Akinena hekaluni, Yakobo awaonya Wanefi dhidi ya kiburi, kupenda anasa na utovu wa uadilifu.

Yakobo 4–6 Yakobo ashuhudia Kristo na kunukuu istiari ya Zeno ya miti ya mizeituni. Anawa-himiza watu wake kutubu, kupokea rehema ya Bwana, na kujitayarisha kwa hukumu.

Yakobo 7 Kwa usaidizi wa Bwana, Yakobo ana mshinda Sheremu, mpinga Kristo. Anataja ugomvi kati ya Wanefi na Walamani na kuyapashisha mabamba madogo kwa Enoshi.

150

Page 166: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

151

SOMO LA 43

yakobo 1–yakobo 2:11UtanguliziBaada ya kifo cha Nefi, Wanefi walianza "kujiingiza wenyewe katika desturi za uovu" chini ya utawala wa mfalme mpya (Yakobo 1:15). Yakobo na nduguye Yusufu walikuwa wametengwa rasmi na Nefi kama

makuhani na walimu wa watu, walifanya kazi kwa bidii ili kushawishi watu kutubu na kumjia Kristo. Yakobo alitii anri ya Nefi ya kurekodi mafundisho matakatifu, ufunuo na unabii katika mabamba madogo.

Mapendekezo ya Kufundisha

Yakobo 1:1–8Yakobo arekodi kweli takatifu na kuhudumu kuwasaidia wengi kumjia Yesu KristoWaulize wanafunzi kutoa mifano ya vyeo tofauti vya viongozi wa ukuhani. (Majibu yanaweza kujumuisha manabii na mitume, Viongozi wenye mamlaka, marais wa vigingi, maaskofu, marais wa akidi) Waalike wanafunzi wachache kuelezea kwa ufupi baadhi ya njia ambazo viongozi wa ukuhani wamebariki maisha yao kupitia huduma ya ukuhani. Eleza kuwa Nefi alikuwa amewaweka wakfu ndugu zake wadogo Yakobo na Yusufu kama makuhani na walimu wa watu. (ona 2 Nefi 5:26; Yakobo 1:18). Nefi alipokaribia mwisho wa maisha yake, alimpa Yakobo usimamizi wa mabamba yaliyokuwa na kumbukumbu ya watu wao.Waalike wanafunzi kusoma Yakobo 1:1–4 kimya kimya. Waulize kutambua ni nini Nefi ali-mwamrisha Yakobo kurekodi katika mabamba na kwa nini. (Unaweza kutaka kupendekeza kwa wanafunzi kuweka alama Maelekezo ya Nefi kwa Yakobo.) Baada ya wanafunzi kuwa na nafasi ya kutosha ya kusoma. Waalike wachache kati yao kulieleza darasa kile walichopata.Ikiwa wanafunzi hawatataja, waonyeshe kishazi cha mwisho cha Yakobo 1:4—“kwa faida ya watu wetu.”• Je! kishazi “Kwa faida ya watu wetu” kinamaanisha nini (Kwa faida yao.)Alika mwanafunzi asome Yakobo 1:5–6 kwa sauti. Uliza darasa kutambua ni nini Bwana alimfunulia Yakobo na Yusufu ambacho kingewasaidia kufundisha watu wao. (Unaweza kutaka kueleza kuwa “wasiwasi mwingi’ inamaanisha huruma yao kuu kwa ajili ya watu.)• Ni nini ambacho Bwana aliwafunulia Yakobo na Yusufu? (Aliwaonyesha kile ambacho kinge-

tendeka kwa Wanefi katika siku za usoni, na aliwafunulia mambo kuhusu ujio wa Kristo)• Kujua mambo haya kunaweza kuwa kuliwasaidiaje Yakobo na Yusufu katika kufundisha

watu wao?Andika neno shawishi kwenye ubao. Waulize wanafunzi wasome Yakobo 1:7–8 kimya, wakitafuta kile Yakobo na Yusufu walitaka kuwashawishi watu kufanya. (Unaweza kupe-ndekeza kuwa wanafunzi waweke alama kile walichopata) Waalike wanafunzi kadhaa kuandika ubaoni kitu kimoja walichogundua.Kutoka orodha ubaoni, waalike wanafunzi kutaja kishazi au viwili wanavyotaka kuelewa zaidi. Wanafunzi wanapotaja vishazi hivi, uliza ikiwa wanafunzi wengine wanaweza kusai-dia kuvieleza. Katika mjadala, maelezo yafuatayo yanaweza kuwa yenye usaidizi:“Ingia rahani mwake” — Kuingia rahani mwa Bwana kunamaanisha kufurahia amani katika maisha haya na kupokea “utimilifu wa utukufu wa [Mungu] katika maisha yajayo (M&M 84:24).“Kutafakari kifo cha [Kristo]”— Elezo moja la tafakari ni kuangalia au kuchunguza kwa makini. Wakati Yakobo alipoandika kuwa alitaka kuwashawishi watu “Kumwamini Kristo na kutafakari kifo chake,” anaweza kuwa alimaaanisha aliwataka kuchunguza Upatanisho wa Yesu Kristo kwa makini, kutambua umuhimu wake, na kupata ushuhuda wake wa kibinafsi.“Kubeba msalaba wake ”— Kishazi hiki kinamaanisha hiari yetu ya kujikana uovu na tama za dunia na kushika amri za Mungu (Ona Tafsiri ya Joseph Smith, Mathayo 16:26 [katika

Maneno magumu na vishaziUkiwasaidia wanafu-nzi kuelewa maneno magumu na vishazi kutoka katika maandiko, wataweza kuvitumia vyema katika maisha yao. Wakati wa kujaribu kueleza neno au kishazi, inaweza kuwa usaidizi kutumia kamusi au kusoma neno kama li-navyoonekana kwingine katika maandiko.

Page 167: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

152

SoMo la 43

Mathayo 16:24, tanbihi d]; Luka 9:23; 2 Nefi 9:18). Inamaanisha pia hiari yetu kuvumilia na kujitolea tunapomfuata Mwokozi.“Kuchukua aibu ya ulimwengu”— Kishazi hiki kinamaanisha kushika amri licha ya msu-kumo wa ulimwengu, kudhalilishwa, na upinzani ambao kila mara huja kwa wafuasi wa Yesu Kristo. Waulize wanafunzi kufanya muhtasari wa kile walichojifunza kutoka Yakobo 1:1–8 kuhusu majukumu ya viongozi wa ukuhani. Wanafunzi wanaposhiriki mawazo yao, sisitiza kuwa viongozi wa ukuhani hutumikia kwa bidii ili kutusaidia kuja kwa Kristo. (Unaweza kupenda kuandika kanuni hii ubaoni)• Viongozi wa ukuhani hufanya kazi vipi ili kutusaidi kuja kwa Kristo?Wape wanafunzi dakika chache kuandika katika shajara zao za kujifunza maandiko ku-husu njia ambazo manabii au viongozi wengine wa ukuhani wamewasaidia katika sehemu moja au mbili waliotambua katika Yakobo 1:7–8. Waalike wanafunzi wachache kuelezea walichoandika. (Wakumbushe kuwa hawahitaji kuelezea jambo lolote la kibinafsi au siri)

Yakobo 1:9–2:11Yakobo ana watahadharisha watu kuhusu uovu waoWahimize wanafunzi kutafakari swali lifuatalo katika sehemu iliyosalia ya somo:• Kwa nini viongozi wa kanisa hutuonya dhidi ya dhambi?Yakobo alirekodi kuwa baada ya kifo cha nduguye Nefi, watu walianza kujiingiza katika tabia kadha za uovu. Waalike wanafunzi wasome Yakobo 1:15–16 kimya kimya. Waulize kutambua sehemu tatu ambazo zilimpa wasiwasi Yakobo. (Mara wanafunzi wakijibu, una-weza kutaka kuandika maneno utovu wa maadili, kiulimwengu, na kiburi ubaoni.)Acha wanafunzi wasome Yakobo 1:17–19 kimya kimya, wakitafuta kile Yakobo na Yusufu walifanya kuwasaidia watu wao. Waulize kuripoti walichopata. Alika mwanafunzi kuandika majibu yao ubaoni.• Unafikiri inamaanisha nini kupata “mwito wangu kutoka kwa Bwana”? ( Yakobo 1:17).

(Kujifunza kile Bwana angetaka sisi tufanye.)Alika mwanafunzi kusoma kwa sauti kauli ifuatayo ya Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili. Uliza darasa kusikiliza njia ambapo viongozi wa Kanisa wanata-futa kazi zao kutoka kwa Bwana wanapojitayarisha kufundisha katika Mkutano mkuu.

Pengine tayari mnajua (na kama hamjui mnapaswa kujua) kwamba labda kwa jambo la pekee lililo nadra, hakuna mume au mke anayezungumza [katika Mkutano Mkuu] anaye pangiwa mada. Kila mmoja hufunga na kuomba, hujifunza na kutafuta, na kuanza na kusitisha na kuanza tena hadi awe na hakika kuwa kwa mkutano huu mkuu, wakati huu, mada yake ndiyo mapenzi ya Bwana ya kile mnenaji huyo atawasilisha licha ya upendeleo wa

kibinafsi au mapendeleo ya kibinafsi. . . .Kila mmoja amelia, kuwa na wasiwasi, na kwa dhati kutafuta mwongozo wa Bwana kuongoza mawazo na madhihirisho yake.” (“An Ensign to the Nations,” Ensign or Liahona, Mei 2011, 111).• Wanenaji katika mkutano mkuu hufanya nini ili kutafuta kazi zao kutoka kwa Bwana?• Kwa nini ni muhimu kuelewa kuwa viongozi wa Kanisa hutafuta kutufundisha kile

Bwana anataka tujue? Kukumbuka hili kunaathiri vipi mtazamo wetu tunapowasikiliza wakifundisha?

• Kulingana na Yakobo 1:19, majukumu ya Yakobo na Yusufu yalikuwa nini? Wanafunzi wanapojibu, hakikisha kuwa wanaelewa kuwa viongozi wa ukuhani wana jukumu la kiungu la kufundisha neno la Mungu na kutahadharisha dhidi ya dhambi. Una-weza kutaka kuandika ukweli huu ubaoni.)

• Kwa nini ni baraka kupata wazazi na viongozi wa Kanisa kututahadharisha dhidi ya mitazamo na tabia za dhambi?

• Ni maneno gani ambayo Yakobo alitumia kueleza jinsi wanavyopaswa kufundisha? Ma-tokeo yangekuwaje ikiwa hawangetimiza majukumu yao?

Waulize wanafunzi kufikiri jinsi wangehisi ikiwa, kama Yakobo, wangekuwa katika nafasi ya uongozi na waliongozwa kuwaita watu katika toba na utovu wa maadili, kiulimwengu

Page 168: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

153

yaKobo 1–yaKobo 2:11

na kiburi. Gawa darasa katika jozi. Waalike wenzi kuchukua zamu kusomeana kutoka Yakobo 2:1–3, 6–7, 10–11. Waulize kutambua vishazi vinavyoonyesha hisia za Yakobo ku-husu jukumu lake la kuwaita watu kutubu. Baada ya muda wa kutosha, waalike wanafunzi kadha kuelezea walichopata.• Vishazi hivi vinaonyesha nini kuhusu hisia za Yakobo kuhusu kuwaita watu wake

kwenye toba? (Hakikisha kuwa wanafunzi wanaelewa kuwa ingawa Yakobo aliliona jukumu hili kuwa gumu, alilitekeleza kwa sababu aliwajali watu na kwa sababu alitaka kutii amri za Mungu.)

Kwa kuhitimisha acha wanafunzi waandike katika shajara zao za kujifunza maandiko kuhusu 1) Kile viongozi wa Kanisa wamewafunza hivi karibuni na jinsi wanavyoweza ku-tumia maishani mwao au (2) jinsi wanavyoweza kutumia kile walichojifunza hivi leo katika miito yao darasani au katika urais wa akidi, katika majukumu yao kama walimu wa nyu-mbani, au katika nafasi zingine za uongozi. (Unaweza kutaka kuandika maelekezo haya katika ubao.) Himiza wanafunzi kufuata ushauri wa viongozi wao wa ukuhani. Hitimisha kwa kutoa ushuhuda wako wa kanuni zilizofundishwa katika somo hili.

Tangazo na Habari za UsuliYakobo 1:19. “Tuliadhimisha ofisi yetu kwa Bwana”Rais Thomas S Monson alieleza maana ya kuadhimisha wito.

Inamaanisha nini kuadhimisha wito? Inamaanisha ku-ujenga kwa heshima na umuhimu, kuufanya kuwa wa heshima na wa kutukuzwa katika macho ya watu wote, kuupanua na kuuimarisha, kufanya nuru ya mbinguni kuangaza kupitia mtazamo wa watu wote.

“Na je, mtu anaadhimisha vipi wito? Kwa urahisi, kwa kutimiza huduma inayomhusu. Mzee huadhi-misha wito aliotawazwa kama mzee kwa kujifunza majukumu yake kama mzee na kwa kuyatenda. Kama ilivyo kwa mzee, pia vivyo hivyo na shemasi, mwalimu, kuhani, askofu na kila mmoja anayeshikilia ofisi katika ukuhani.” (“Wito Mtakatifu wa Huduma,” Ensign au Liahona, Mei 2005, 54).

Yakobo 1:19; 2:2. “Kujibu dhambi za watu juu ya vichwa vyetu wenyewe”Wale walio na majukumu ya uongozi Kanisani hubeba jukumu la ajabu. Yakobo alifunbdisha kuwa wakati viongozi wanapopuuza kufundisha neno la Mungu kwa wale ambao wameitwa kuwaongoza, wanawajibika kwa kiwango fulani kwa dhambi za watu. Wakati aki-zungumzia juu ya ndugu wa ukuhani, Rais John Taylor alifafanua kuhusu jukumu lililoelezwa na Yakobo:

“Msipoadhimisha miito yenu, Mungu atawatuhumu kwa wale ambao huenda mgewaokoa kama mnge-fanya jukum lenu” (Teachings of Presidents of the Church: John Taylor [2001], 164).

Rais Hugh B. Brown wa Urais wa Kwanza baadaye alizungumzia kauli ya Rais Taylor:

“Hii ni kauli ya kutia changamoto. Ikiwa kwa sababu ya dhambi ya kutotenda au kutenda nitapoteza kile ambacho ningekuwa nacho baada ya hapa, mimi mwenyewe ni lazima kuumia, na bila shaka, wapendwa wangu pamoja nami. Lakini nikikosa katika ushawishi wangu kama askofu, rais wa kigingi, rais wa misheni au mmoja wa Viongozi Wakuu wenye Mamlaka wa Kanisa — ikiwa yeyote atakosa kufundisha, kuongoza, kuelekeza na kusaidia kuwaokoa wale walio chini ya maelekezo yetu na katika mamlaka yetu, basi Bwana atawatuhumu ikiwa watapotea kutokana na kukosa kwetu” (Katika Ripoti ya Mkutano Mkuu, Okt. 1952, 84)

Yakobo 2:8. “Neno la Mungu linaponya nafsi iliyojeruhiwa”Wakati habari mpya inakanganya au inasumbua kwa wanafunzi wa injili, ni bora kwao kutafuta majibu kutoka kwa Mungu, anayejua mambo yote, badala ya kufanya utafutaji wa jumla kwenye mtandao au kugeu-kia vifaa vya wapinga Mormoni. Kuenda moja kwa moja kwa Mungu kwa majibu huonyesha imani yetu kwake na hutuwezesha kupokea majibu kupitia kwa Roho Mtaka-tifu. Tunapaswa pia kugeukia maandiko na maneno ya manabii na mitume wa siku za mwisho yanayoweza ku-jibu maswali magumu na kuponya majeraha. Maandiko yafuatayo hutufundisha tunakopaswa kugeukia na tuna-chopaswa kufanya wakati tuna maswali au mhangaiko:

Yakobo 2:8— “Neno la Mungu linaponya nafsi iliyojeruhiwa.”

Yakobo 1:5–6— “Lakini kwenu mtu akipungukiwa na hekima na aombe dua kwa Mungu. . .naye atapewa. Ila aombe kwa imani.”

Moroni 10:5— “Na kwa uwezo wa Roho Mtakatifu mtajua ukweli wa vitu vyote.”

Page 169: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

154

SOMO LA 44

yakobo 2:12–35

Mapendekezo ya Kufundisha

Yakobo 2:12–21Yakobo aliwashutumu watu wake kwa kiburi chaoAndika yafuatayo ubaoni: pesa, akili, marafiki, talanta, ujuzi wa injili. Waalike wanafunzi kufikiria kuhusu baraka ambazo Bwana amewapatia katika maeneo haya. Wahimize kuta-fakari jinsi wanavyohisi kuhusu baraka hizi wanapojifunza Yakobo 2.Uliza mwanafunzi asome Yakobo 2:12–13 kwa sauti. Waalike wanafunzi waliosalia kufuati-lia, wakitambua kile wengi wa Wanefi walikuwa wakitafuta. Baada ya wanafunzi kujibu, eleza kuwa Yakobo aliwaambia watu wake kuwa walikuwa wamepata mali kwa nija ya “mkono wa majaliwa” Unaweza kutaka kueleza kuwa neno majaliwa linarejea kwa Mungu.• Kwa nini ni muhimu kwetu kukumbuka kuwa baraka zetu zote zinatoka kwa Baba yetu

wa Mbinguni? • Kulingana na Yakobo 2:13, Kwa nini wengi wa Wanefi walijiinua katika kiburi?Alika mwanafunzi asome kwa sauti kauli ifuatayo ya Rais Dieter F. Uchtdorf wa Urais wa Kwanza. Uliza darasa lisikilize kwa umaizi kinachomaanisha kujiinua katika kiburi.

“Katika kina chake, kiburi ni dhambi ya ulinganisho, kwani, ingawa inaanza na ‘Tazama jinsi nilivyo bora, na vitu vikuu nilivyofanya,’ kila mara inaone-kana kuishia ‘ Kwa hivyo mimi ni bora kukushinda wewe.’ . . .“ Hii ni dhambi ya ‘Shukrani kwa Mungu, mimi ni bora kuliko wewe.’ Na katika kina, ni tamaa ya kutaka kustahiwa au kuhusudiwa. Ni dhambi ya kujitukuza” (“Pride and the Priesthood,” Ensign au Liahona, Nov. 2010, 56).

Wahimize wanafunzi kutafakari kimya kimya ikiwa wamewahi kuwa hatia ya dhambi ya kufikiri wao ni bora kuliko mtu mwingine. Alika mwanafunzi asome Yakobo 2:14–16 kwa sauti. Uliza darasa kutafuta vishazi vinvyoo-nyesha matokeo ya kiburi. Waulize waripoti walichopata.• Kwa nini unafikiri kiburi kina uwezo wa “kuangamiza mioyo [yetu]”? (Yakobo 2:16).Waalike wanafunzi wasome Yakobo 2:17–21 kimya kimya. Waulize kutafuta vishazi vina-vyofundisha jinsi tunavyoweza kushinda kiburi na mitazamo isiyofaa kuhusu mali. Una-weza kupendekeza kuwa waweke alama katika vishazi wanavyopata. Baada ya kujifunza aya hizi, waalike kuchagua kishazi kimoja walichopata. Wape wanafunzi kadha nafasi ya kueleza jinsi vishazi walivyochagua vinaweza kutusaidia kushinda kiburi au mitazamo isi-yofaa ya mali. (Kama sehemu ya shughuli hizi, unaweza kupendekeza pia kuwa wanafunzi wasome aya zifutazo za maandiko: 1 Wafalme 3:11–13; Marko 10:17–27, pamoja na Tafsiri ya Joseph Smith katika tanbihi 27a; 2 Nefi 26:31; Alma 39:14; M&M 6:7.)• Unafikiri inamaanisha nini kutafuta ufalme wa Mungu? Unafikiri inamaanisha nini

kupata tumaini katika Kristo?• Kutafuta ufalme wa Mungu na kupata tumaini katika Kristo kunawezaje kuathiri mita-

zamo yetu kuhusu utajiri na mali?Waulize wanafunzi kutafakari jinsi wangeweza kufupisha mada kuu ya Yakobo 2:12–21 kwa mwanafunzi asiyekuwa darasani hivi leo. Wape nafasi wanafunzi wawili au watatu

UtanguliziMkweli katika jukumu lake kama kiongozi wa ukuhani, Yakobo aliwaita watu wake kwenye toba, akiwaonya dhidi ya dhambi ya kiburi na utovu wa maadili wa

uasherati. Alifundisha kuhusu hatari na matokeo ya dhambi hizi mbili zilizokithiri.

Page 170: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

155

yaKobo 2:12– 35

kuelezea kile ambacho wangesema. Wanafunzi wanaweza kutaja baadhi ya kanuni za kweli. Hakikisha kuwa wanaelewa kuwa tunapaswa kutafuta ufalme wa Mungu juu ya maslahi mengine yote. Wape wanafunzi wakati wa kuandika katika shajara zao za kujifunza maandiko au daftari za darasani kuhusu njia moja ambayo wanaweza kutumia baraka na nafasi ambazo Bwana amewapa kujenga ufalme wa Mungu na kubariki maisha ya wengine.

Yakobo 2:22–35Yakobo awakemea watu waliovunja sheria ya usafi wa kimwiliAndika ubaoni kauli hii ya Rais Ezra Taft Benson:“Dhambi ya kuudhi ya kizazi hiki ni . . .”Waalike wanafunzi kufikiria jinsi Rais Benson angehitimisha sentensi hii. Kisha soma kauli ifuatayo:Dhambi ya kuudhi ya kizazi hiki ni uasherati. Hii, Nabii Joseph alisema itakuwa chanzo cha majaribu mengi, mapigo mengi, na ugumu mwingi kwa wazee wa Israeli kuliko nyi-ngine” (The Teachings of Ezra Taft Benson [1988], 277).Waalike wanafunzi wasome Yakobo 2:22–23, 28 kimya kimya, wakitambua maneno na vishazi ambavyo Yakobo alitumia kueleza uzito wa uasherati. (Unaweza kuhitaji kueleza neno ukahaba inamaanisha dhambi ya uasherati.) Waulize wanafunzi kushiriki maneno na vishazi walivyogundua.Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa amri ya usafi wa kimwili, soma kauli ifuatayo kutoka ka-tika kijitabu cha For the Strength of Youth . Waulize wanafunzi kusikiliza matendo ambayo wanapaswa kuepukana nayo.“Kiwango sanifu cha Bwana kuhusu usafi wa kimwili ni dhahiri na hakibadiliki. Msiwe na uhusiano wowote wa kimwili kabla ya ndoa, na muwe waaminifu kikamilifu kwa mwenzi wako baada ya ndoa. . . .“Usifanye lolote litakaloweza kukuongoza kwenye dhambi ya kimwili. Tendea wengine he-shima, si kama vyombo vinavyotumiwa kutosheleza tamaa za shauku na hamu za uchoyo. Kabla ya ndoa, usishiriki katika kubusu kwa tamaa, kulala juu ya mtu mwingine, au kugusa sehemu za siri za mwili wa mtu mwingine ikiwa amevaa nguo na, au bila nguo. Usifanye jambo lolote litakalo tia ashiki hisia za kimwili. Usiamshe hisia hizo katika mwili wako mwenyewe” (For the Strength of Youth [booklet, 2011], 35–36).Eleza kwamba kulingana na Yakobo 2:23–24, baadhi ya watu katika siku za Yakobo walija-ribu kutoa udhuru dhambi zao za uasherati.• Watu hutoa udhuru vipi kuhusu uasherati hivi leo ?• Ni yapi baadhi ya mambo ambayo vijana huweza kufanya ili kushinda majaribu ya

uasherati? (Majibu yanaweza kujumuisha kuomba nguvu, kushirikiana na marafiki wema, kuchagua burudani zilizo safi, na kuepukana na hali na mahali ambapo majaribu yanaweza kukutokea)

Unaweza kutaka kueleza kuwa mmojawapo ya dhambi za Wanefi inaonekana kuwa ni desturi isiyoidhinishwa ya ndoa ya mitala. Waalike wanafunzi kusoma Yakobo 2:27–30 ki-mya. Kabla hawajasoma, unaweza kuhitaji kueleza kuwa neno suria inamaanisha mwana-mke aliyeolewa kihalali lakini alikuwa na hadhi ya chini kuliko mke.• Kulingana na Yakobo 2:27, Ni nini “neno la Bwana” kuhusu kuwa na mke mmoja?

(Hakikisha kuwa ni bayana kuwa kutoka mwanzo, Bwana aliamuru kuwa mtu anapaswa kuwa na mke mmoja, Ona pia M&M 49:15–16.)

Eleza kuwa desturi isiyo idhinishwa ya ndoa ya mitala ni mfano mbaya. Machoni pa Mu-ngu, dhambi hizi zina uzito mkubwa.• Kulingana na Yakobo 2:30, ni wakati gani ambapo watu wa Bwana huidhinishwa kuwa

na desturi ya ndoa ya mitala? (Wakati Bwana akiamrisha hivyo)Eleza kwamba nyakati fulani katika historia ya ulimwengu, Bwana ameamuru watu wake kuwa na desturi ya ndoa ya mitala. Kwa mfano, ndoa ya mitala ilifanywa katika nyakati za Agano la Kale na Ibrahimu na Sara (ona Mwanzo 16:1–3; M&M 132:34–35, 37) na kwa mjukuu wao Yakobo (ona M&M 132:37), na ilikuwa desturi kwa muda wakati wa siku za kwanza za Kanisa lililorejeshwa, ikianza na Joseph Smith (ona M&M 132:32–33, 53).

Kufundisha kuhusu usafi wa kimwiliUnapofundisha kuhusu usafi wa kimwili, kuwa mwenye heshima, wa kujenga, na muwazi katika maelekezo yako. Unapofuatilia nyenzo za somo kwa uhalisi na kufuata maongozi ya Roho Mtakatifu, utaweza kuwasaidia wanafunzi kuelewa kile wanachihitaji kufanya ili kushika sheria ya usafi wa kimwili.

Page 171: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

156

SoMo la 44

Ili kutilia mkazo kuwa uasherati una athari ya kuangamiza katika familia, soma Yakobo 2:31–35 kwa sauti. Waulize wanafunzi wasome pamoja, wakitafuta baadhi ya matokeo ya utovu wa maadili. Eleza kwamba ingawa Yakobo anawazungumzia wanaume, amri ya usafi wa kimwili ni muhimu vile vile kwa wanawake. • Kulingana na Yakobo ni vipi ambavyo familia inaathiriwa wakati mwanafamilia huvunja

amri ya usafi wa kimwili? Hii inaeleza vipi kuwa kuvunja amri ya usafi wa kimwili ni dhambi kubwa?

• Baadhi ya vijana hutoa udhuru kuwa wanaweza kuvunja amri ya usafi wa kimwili kwa sababu matendo yao hayaumizi mtu mwingine. Je, utovu wa maadili ya mtu unawezaje kuathiri watu wengine?

Ili kuhitimisha mjadala huu kuhusu matokeo ya dhambi za uasherati, fikiria kusoma kauli hii ya Mzee Richard G Scott wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili. Waalike wanafunzi kusi-kiliza matokeo ya utovu wa maadili ya usafi wa kimwili.

“Hivyo vitendo vya undani vimekatazwa na Bwana nje ya sharti linalodumu la ndoa kwa sababu vinahujumu makusudi yake. Katika agano takatifu la ndoa, mahusiano kama haya ni kwa mujibu wa mpango Wake. Wakati yanapofanyika kwa njia nyingine, ni kinyume na nia Yake. Husababisha uharibifu mkubwa wa kihisia na kiroho. Ingawa wanaoshiriki hawatambui kuwa inatendeka sasa, watatambua baadaye. Utovu wa uasherati huweka

kizuizi dhidi ya kazi ya Roho Mtakatifu pamoja na kuinua kwake na kuangaza, na uwezo wa kutia nguvu. Husababisha mhemko wenye nguvu wa kimwili na kihisia. Baada ya muda hujenga hamu isiyovunjwa ambayo humpeleka mkosaji katika dhambi nzito zaidi. Husababisha uchoyo na kuzaa matendo ya uchokozi kama vile ukatili, utoaji mimba, mateso ya ngono, na uhalifu wa kimabavu. Mhemko kama huo huongoza katika vitendo vya mapenzi kati ya jinsia moja, na ni uovu na makosa kabisa.” (“Making the Right Choices,” Ensign, Nov. 1994, 38).Waalike wanafunzi kuhakiki mwanzo wa Yakobo 2:28 na kutambua kile Bwana hufurahia. (Unaweza kupendekeza kuwa wanafunzi watie alama kile wanachopata. Hakikisha wana-elewa kuwa Bwana hufurahia usafi wa kimwili.)• Kutokana na kile tulicho jadili leo, kwa nini unafikiria Bwana hufurahia usafi wa kimwili?Fikiria kuonyesha picha ya familia yako. Shuhudia baraka ambazo zimekujia wewe na familia yako mnapoishi amri ya Bwana ya usafi wa kimwili. Sisitiza kuwa uwezo wa kupata watoto ni karama kuu kutoka kwa Baba yetu wa Mbinguni inapotumiwa katika mipaka aliyoweka. Wahimize wanafunzi kuwa wasafi na nadhifu sana ili Bwana aweze “kufurahia usafi [wao] wa kimwili" ( Yakobo 2:28).Ili kuwasaidia wanafunzi kutoa shuhuda zao kuhusu kuishi amri ya usafi wa kimwili, una-weza kutaka kuwauliza swali lifuatalo:• Je! Ungemwambia nini mtu anayesema kuwa amri ya usafi wa kimwili ni ya zamani

na isiyo na maana? (Wanafunzi wanapojibu swali hili, waulize washuhudie baraka za kushika amri ya usafi wa kimwili, si tu hatari za kutoitii.)

Waambie wanafunzi kuwa una hakika kuwa wanaweza kuwa wasafi kimaadili. Sisitiza kuwa ikiwa wamefanya dhambi dhidi ya amri ya usafi wa kimwili, wanapaswa kutafuta usaidizi kutoka kwa askofu au rais wa tawi lao, ambaye anaweza kuwasaidia kutubu na kuwa wasafi kupitia kwa upatanisho wa Yesu Kristo.

Page 172: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

157

SOMO LA 45

yakobo 3–4

Mapendekezo ya Kufundisha

Yakobo 3Yakobo awafariji na kuwashauri walio wasafi moyoni na kuwahimiza wengine watubuWaalike wanafunzi kufikiri juu ya ushauri ambao wangewapa watu katika hali zifuatazo: 1. Msichana anajibidiisha kuishi kwa haki lakini anaumia kwa sababu baba yake ni wa

pombe. 2. Kijana anafanya anavyoweza kuishi injili lakini anajikuta anapatwa na majaribu kwa

sababu ya talaka ya wazazi wake. 3. Msichana anajaribu kwa bidii kupenda familia yake lakini anasumbuka nyumbani kwa

sababu ya uchoyo wa dadake na matendo yasiyo ya kujali.Waalike wanafunzi kusoma sentensi ya kwanza ya Yakobo 3:1 kimya kimya. Waulize kuta-mbua ni nani Yakobo anamlenga katika mlango wa Kwanza.Eleza kuwa Yakobo alikuwa akizungumza moja kwa moja kwa watu waliokuwa na hatia ya kiburi na usherati. Kisha akageuza nadhari yake kwa watu wenye haki waliokuwa wa-kipata uzoefu wa majaribu kwa sababu ya uovu wa wengine. Waalike wanafunzi kusoma Yakobo 3:1–2 kimya kimya. Waulize kutafuta vitu vinne ambavyo Yakobo aliwauliza wenye moyo safi kufanya. • Ni vitu gani vinne ambavyo Yakobo aliwashauri wenye mioyo safi kufanya. (“Mtegeme-

eni Mungu kwa mawazo yenu yote. . . na mmuombe, kwa imani kuu, . . . inueni vichwa vyenu na kupokea neno la kupendeza la Mungu, na kusherekea upendo wake”) Ni nini Yakobo aliahidi wenye mioyo safi ikiwa wangebaki waaminifu? (Faraja katika mateso na kulindwa dhidi ya maadui)

• Unafikiri tunaweza kufanya nini ili tupokee neno la Mungu?Kuhusiana na swali kuhusu ahadi ya Yakobo kwa walio na mioyo safi, hakikisha kuwa wanafunzi wanaelewa kuwa Mungu atawafariji wenye mioyo safi katika mateso yao. Unaweza kuhitaji kueleza kuwa neno fariji linamaanisha kumtuliza mtu aliye na huzuni au mwenye shida. Ili kuwasaidia wanafunzi kutafakari na kutumia ukweli huu, uliza:• Je Bwana amekufariji vipi?• Kuomba kwa imani kumekusaidia vipi katika wakati wa majaribu?• Ni lini ambapo neno la Mungu limekusaidia kuuhisi upendo Wake?Eleza kuwa baada ya kuzungumza kwa wenye mioyo safi, Yakobo pia alizungumza kwa wale wasio na mioyo safi.Alika mwanafunzi asome Yakobo 3:3–4 kwa sauti. Uliza darasa kutambua ni nini ambacho Yakobo aliwahimiza wasio na mioyo safi kufanya. • Ni nini kingefanyika ikiwa watu wa Yakobo hawangetubu?

UtanguliziKatika Yakobo 3, tunasoma hitimisho la mahubiri ambayo Yakobo aliwatolea watu wake. Yakobo kwa ufupi alitoa maneno ya faraja na ahadi kwa walio safi moyoni. Pia, aliwakemea wenye kiburi na wasio wasafi kimwili kati ya watu wake, akawatahadharisha kuhusu matokeo ambayo yangewapata ikiwa hawangetubu. Yakobo 4 ina maneno ambayo Yakobo aliongozwa

kuwaandikia watu ambao siku moja wangesoma ku-mbukumbu yake. Alishuhudia kuhusu Upatanisho wa Yesu Kristo na kuwausia wasomaji wake kujipatanisha na Mungu Baba kupitia kwa Upatanisho. Kwa sauti ya tahadhari, alizungumza juu ya Wayahudi ambao wa-ngemkataa Yesu na uwazi wa injili Yake.

Page 173: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

158

SoMo la 45

Eleza kuwa Yakobo alisema kwamba Walamani walikuwa wenye haki kuliko Wanefi fulani wakati huu. Waulize wanafunzi wasomeYakobo 3:5–7 kimya, wakitafuta njia ambazo Wala-mani walikuwa wenye haki kuliko Wanefi fulani.• Ni kwa njia gani Walamani walikuwa wenye haki kuliko Wanefi fulani?• Ni kanuni zipi unazojifunza kutoka Yakobo 3:7 kuhusu uhusiano wa Familia? (Waume

na Wake wapendane, na wazazi wanapaswa kuwapenda watoto wao.)• Ni yapi baadhi ya matokeo yanayotokea wakati wanafamilia wakikosa kupendana na

wasipotimiza majukumu yao ya kifamilia?Waulize wanafunzi wasome Yakobo 3:10 kimya kimya, wakitafuta maonyo ambayo Yakobo aliwapa hasa akina baba Wanefi.• Yakobo alitoa maonyo yapi kwa akina baba Wanefi?• Kwa nini unafikiri ni muhimu kwa kila mwana familia kuwa mfano mwema kwa

mwengine?Soma Yakobo 3:11–12 kwa sauti kwa wanafunzi. Unaweza kutaka kueleza kuwa (aya ya 11, kishazi “amsheni fahamu za nafsi zenu” inammanisha haja ya kuamka kiroho. Katika Yakobo 3:12, kishazi “uasherati na tamaa” ina maanisha dhambi za uasherati. Unaposoma aya hizi, sisitiza “matokeo” ya dhambi ya uasherati. Kwa ziada, wakumbushe wanafunzi kuhusu ahadi za Yakobo kwa wenye mioyo safi Yakobo 3:1–2). Wasaidie wanafunzi kuelewa kuwa njia bora zaidi ya kupokea baraka hizo zilizoahidiwa ni kwa kuwa wenye mioyo safi kila wakati. Hata hivyo, watu waliotenda dhambi ya uasherati wanaweza kutafuta usaidizi kutoka kwa askofu au rais wa tawi, ambao watawasaidia kuwa wasafi kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo, na kupokea baraka walizoahidiwa wenye mioyo safi.

Yakobo 4Yakobo alishuhudia kuwa kupitia kwa Upatanisho wa Yesu Kristo, tunaweza kupatanishwa na MunguMbele ya darasa weka picha ndogo ya Yesu Kristo katikati ya ubao. Karibu na picha, andika maneno machache yanayowakilisha vitu ambavyo vinaweza kuwazuia watu kuja kwa Mwokozi na injili Yake. Kwa mfano, unaweza kuongeza vitu vizuri —kama vile elimu, michezo, na marafiki —kwamba ni muhimu lakini havifai kuwa kitovu cha kim-singi katika maisha yetu. Unaweza pia kuorodhesha vitu vingine—kama vile picha za ngono, muziki usiofaa, madawa ya kulevya—ambayo yanadhuru roho zetu na kutuele-keza mbali na Mwokozi.Waulize wanafunzi kugeukia Yakobo 4:14. Eleza kuwa aya hii inajumuisha vishazi “kuanga-lia zaidi ya lengo” Mzee Neal A. Maxwell wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alifundisha kuwa katika aya hii, “lengo ni Kristo” (“Jesus of Nazareth, Savior and King,” Ensign, Des. 2007, 45). Unaweza kutaka kuwahimiza wanafunzi kuandika kauli hii katika maandiko yao karibu na Yakobo 4:14.Baada ya kutoa maelezo haya, alika mwanafunzi asome Yakobo 4:14–15 kwa sauti.• Unafikiri inamaanisha nini kuangalia zaidi ya lengo? (Kuweka maisha yetu katika ma-

mbo mengine isipokuwa Mwokozi na injili yake.)• Kulingana na Yakobo, ni mitazamo ipi na matendo yapi yaliwazuia Wayahudi kumkubali

Yesu Kristo?Eleza kuwa ingawa Yakobo alirejea dhambi za baadhi ya Wayahudi, sehemu za Yakobo 4:14–15 zinaweza kutumika kwetu pia na kutumika kama onyo kwetu. Ili kuwasaidia wa-nafunzi kuona matumizi haya, uliza maswali yafuatayo:• Kwa nini watu wakati mwingine hukataa “maneno yaliyo wazi” na kutafuta badala

yake vitu ambavyo hawawezi kuvielewa? Ni zipi baadhi ya hatari za kupuuza kweli rahisi za injili?

• Tunaweza kuongeza nini ubaoni kama mfano wa vivutio vya kutuondoa kwa Mwokozi na injili Yake? (Ongeza majibu ya wanafunzi kwa maneno ambayo umeandika tayari ubaoni.)

Futa maneno uliyoandika ubaoni na kuandika swali lifuatalo: Tunaweza kufanya nini ili tusiangalie zaidi ya lengo bali tuzingatie Yesu Kristo?

Page 174: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

159

yaKobo 3– 4

Andika marejeo ya maandiko ubaoni: Yakobo 4:4–5; Yakobo 4:6–7; Yakobo 4:8–9; Yakobo 4:10; Yakobo 4:11–13. Eleza kuwa katika Yakobo 4, Yakobo alaelezea kanuni zinazoweza kutusaidia kumzingatia Yesu Kristo. Wape wanafunzi jukumu la kufanya kazi katika jozi na kutafuta kanuni hizi katika maandishi ya maandiko yaliyoorodheshwa ubaoni. (Kulingana na wanafunzi katika darasa lako, unaweza kupatia aya moja kwa zaidi ya jozi moja ya wa-nafunzi. Ama unaweza kuuliza jozi ya wanafunzi kusoma zaidi ya aya moja.)Baada ya dakika chache, waalike wanafunzi kuripoti majibu yao. Wanapofanya hivyo, una-weza kutaka kuuliza maswali kuwasaidi kufikiria zaidi kuhusu kile walichojifunza katika aya hizi. Ili kukusaidia kuongoza mjadala huu, maswali yafuatayo yamebuniwa kulingana na aya husika:• Yakobo 4:4–5. Ni kwa jinsi gani shuhuda za manabii zimekusaidia kumzingatia Yesu

Kristo? Umeimarishwa vipi kwa shuhuda za watu wengine juu ya Mwokozi? Yakobo alisema kuwa utiifu wa watu wake kwa sheria ya Musa ilikuwa na ufanisi katika “kuele-keza mioyo [yao]” kwa Bwana. Ni kwa njia gani bidii zetu za kupokea ibada za ukuhani na kushika amri zinaweza kuelekeza mioyo yetu kwa Bwana?

• Yakobo 4:6–7. Je, ufunuo kwa manabii unatusaidia vipi kupata matumaini na imani katika Yesu Kristo? Ufunuo wa kibinafsi au ushuhuda wa kiroho uliopokea umeimarisha imani yako kwa njia ipi? Kwa nini unafikiri ni muhimu kukumbuka kuwa ni kwa kupitia tu katika rehema ya Bwana ndipo tunapoweza kufanya kazi Yake?

• Yakobo 4:8–9. Kwa nini unafikiri ni muhimu kutambua kuwa kazi ya Bwana ni “kuu na ya ajabu”? Kazi ya Bwana kama Muumba inaathiri vipi ushuhuda wako juu Yake? Inamaanisha nini kwako “kutopuuza mafunuo ya Mungu?” Tunawezaje kumwonyesha Bwana kuwa tunathamini mafunuo anayotupatia?

• Yakobo 4:10. Ni ipi baadhi ya mifano ya jinsi mtu anavyoweza “kutojaribu kumshauri Bwana, lakini akapokea ushauri kutoka mkono wake”?

• Yakobo 4:11–13. Kama ilivyotajwa katika somo la 35, neno patanisha linamaanisha kuleta katika uwiano. Upatanisho unatusaidia vipi kuja katika uwiano na Baba yetu wa Mbinguni? Yakobo alitukumbusha umuhimu wa kufundisha kuhusu Upatanisho akiuliza “Kwa nini tusiongelee juu ya upatanisho wa Kristo . . . ?” Tunawezaje kufuata kanuni hii tunapotoa shuhuda zetu kwa wengine na wakati tuna nafasi ya kufundisha injili? Tunapotoa shuhuda zetu, kwa nini ni muhimu kufanya hivyo kwa njia ambayo watu wataweza kuelewa? Roho Mtakatifu anatusaidia kwa njia gani kutimiza hayo?

Kutokana na mjadala huu, hakikisha kuwa ukweli huu ni bayana: Kupitia kwa Upatanisho wa Yesu Kristo, tunaweza kujazwa na matumaini na kujipatanisha sisi kwa Mungu.Shiriki hisia zako za shukrani kwa Mwokozi na Upatanisho wake. Shuhudia kuwa Yesu Kristo ndiye “lengo” ambalo kwalo tunapaswa kuzingatia maisha yetu. Ili kuhitimisha somo hili, waulize wanafunzi kufikiri kile watakachofanya ili kuzingatia Mwokozi katika siku chache zijazo. Unaweza kutaka kupendekeza kuwa waandike mipango yao katika shajara zao za kujifunza maandiko. Fikiria kuwaalika wachache wao kuliambia darasa kile wanachopanga kufanya.

Rejeo la Umahiri wa MaandikoMarudio huwasaidia wanafunzi kukumbuka mahali pa vifungu vya umahiri wa maandiko. Njia moja ya kuhimiza marudio ni kutumia kadi za umahiri wa maandiko (Nambari 32335; pia inapatikana kama PDF katika si.lds.org). Kama huwezi kupata kadi, wasaidie wanafu-nzi kutengeneza kadi zao, na maneno muhimu kutoka katika kifungu cha upande mmoja wa kadi, na rejeo upande mwingine. Wagawe wanafunzi katika jozi. Wafanye watumie dakika chache kujiuliza maswali kwa kutumia kadi. Kwa mfano, mwanafunzi mmoja anaweza kusoma maneno muhimu, na yule mwingine atafute rejeo la maandiko. Waalike wanafunzi kutumia kadi hizi kila mara kujiuliza maswali.Angalia: Urefu wa somo hili unaweza pia kutoa wakati kwa hii shughuli ya kurejea uma-hiri wa maandiko. Unweza kuendesha shughuli hii katika mwanzo wa darasa, au kama kituo katikati ya sehemu za somo, au katika mwisho wa darasa. Fanya shughuli kuwa fupi ili kutoa muda kwa somo. Kwa shughuli zingine za marejeo ona kiambatisho katika mwongozo huu.

Page 175: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

160

Somo la Mafunzo ya Nyumbani2 Nefi 32–Yakobo 4 (Kitengo cha 9)

Vifaa vya Matayarisho kwa Mwalimu wa Mafunzo ya NyumbaniMuhtasari wa Mafunzo ya Nyumbani ya Kila sikuUfuatao ni muhtasari wa mafundisho na kanuni ambazo wanafunzi wamejifunza waliposoma 2 Nefi 32–Yakobo 4 (Ki-tengo cha 9) Haikusudiwi kuwa sehemu ya somo lako. Somo unalofundisha linazingatia machache tu ya mafundisho na kanuni hizi. Fuata maelekezo ya Roho Mtakatifu unapofikiria mahitaji ya wanafunzi wako.

Siku ya 1 (2 Nefi 32)Wanafunzi walipokuwa wakisoma 2 Nefi 32, walijifunza kuwa tunapojifunza maneno ya Kristo, maneno ya Kristo yatatuambia mambo ambayo tunapaswa kufanya. Walijifu-nza pia kuwa tunapoomba kila mara, tutaweza kufanya yote ambayo Bwana angetaka tufanye kwa ustawi wa mioyo yetu Somo hili liliwaalika wanafunzi kushirikisha katika muda wa masaa 24 kile walichojifunza kuhusu kuomba kila wakati.

Siku ya 2 (2 Nefi 33)Katika somo hili kuhusu ushuhuda wa mwisho wa Nefi, wa-nafunzi walijifunza kuwa tunachagua ikiwa tutafungua au ha-tutafungua mioyo yetu kwa maongozi ya Roho Mtakatifu. Pia waliangalia kwa makini 1 Nefi na 2 Nefi, wakichagua andiko ambalo limewapa ari kutenda wema au kumwamini Kristo.

Siku ya 3 (Yakobo 1–2)Katika somo lao kuhusu Yakobo 1–2, wanafunzi walijifu-nza kuwa viongozi wa ukuhani hufanya kazi kwa bidii ili kutusaidia kumjia Kristo na kwamba wana jukumu la kiungu la kufundisha neno la Mungu na kutahadharisha dhidi ya dhambi. Kwa kujifunza mahubiri ya Yakobo kwa watu wake, wanafunzi walijifunza kuwa tunapaswa kutafuta ufalme wa Mungu badala ya vivutio vingine. Waliandika katika shajara zao za kujifunza maandiko kuhusu njia moja wanayoweza kutumia baraka na nafasi ambazo Bwana amewapa kujenga ufalme wa Mungu na kubariki maisha ya wengine. Pia wa-lizingatia ukweli kwamba Bwana hufurahia usafi wa kimwili wa watu wote, waume kwa wake. Waliulizwa kutafakari jinsi kuishi amri ya usafi wa kimwili kunabariki familia na kumfurahisha Bwana.

Siku ya 4 (Yakobo 3–4)Wanafunzi walipoendelea kujifunza kuhusu mahubiri ya Yakobo, walijifunza kuwa Mungu atawafariji wale walio na mioyo safi katika mateso yao. Somo lilizingatia fundisho hili: Kupitia kwa Upatanisho wa Yesu Kristo, tunaweza kujazwa na matumaini na kujipatanisha kwa Mungu. Wanafunzi wali-andika kuhusu sababu zao za kibinafsi za kutaka kushuhudia juu ya Yesu Kristo na Upatanisho.

UtanguliziSomo hili litawasaidia wanafunzi kuelewa kuwa Nefi alishuhudia misheni ya Yesu Kristo. Wanafunzi watakuwa na nafasi ya kushi-riki jinsi maneno ya Yakobo yanavyoweza kuwasaidia kushinda kiburi na kutumia baraka zao kutoka kwa Mungu kuujenga ufalme Wake. Watakuwa na nafasi ya kutumia kanuni na mafu-ndisho waliojifunza katika Yakobo 2 ili kujadili umuhimu wa kutii amri ya Bwana ya usafi wa kimwili. Watajadili njia za kutafuta nafasi za kuzungumza kuhusu Yesu Kristo na Upatanisho.

Mapendekezo ya Kufundisha

2 Nefi 32–33Nefi anatushauri kutafuta mwongozo wa kiungu kupitia kwa maneno ya Yesu Kristo Anzisha somo hili kwa kuuliza maswali yafuatayo:

• Ni nini moja ya michezo au shughuli unazo zipenda zaidi?• Ni ujuzi gani wa kimsingi unaohitaji kufanya mazoezi ili kufa-

ulu katika mchezo au shughuli hii?• Ni nini kitafanyika ikiwa mtu atapuuza kufanya mazoezi ya

huu ujuzi wa kimsingi?

Liambie darasa kwamba kuna vitendo vya kimsingi ambavyo vinamwalika Roho Mtakatifu kutupa uongozi kutoka kwa Baba yetu wa Mbinguni. Nakili chati ifuatayo ubaoni au itayarishe kama kitini.

Maombi Kupokea Mwo-ngozo kutoka kwa Roho Mtakatifu

Kujifunza Maandiko

2 nefi 32:8–9 2 nefi 32:5; 33:1–2 2 nefi 32:3; 33:4

Uliza kila mwanafunzi kuchagua mojawapo ya matendo haya katika chati na asome maandiko yanayoandamana. Gawanya darasa katika jozi au vikundi vidogo vidogo. Waulize wanafunzi wafanye zamu kuelezea jinsi maombi, kupokea mwongozo wa Roho Mtakatifu na kujifunza maandiko kumewasaidia kupokea maongozi kutoka kwa Mungu.

Unaweza kutaka kuwauliza wanafunzi kueleza jinsi maelekezo ya Mzee David A. Bednar kuhusu amri ya kuomba yamewasaidia kila mara. Unaweza pia kuwauliza jinsi maombi yao yalivyo-boreshwa kwa kazi ya ziada ya kujumuisha kwa masaa 24 kile walichojifunza kuhusu kuomba kila mara. (Hii ilikuwa kazi ya ziada kutoka siku ya 1.)

Page 176: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

161

SoMo la MafUnzo ya nyUMbani

Yakobo 1–2Yakobo anawashutumu watu wake kwa kupenda mali kwao, kiburi na uasheratiAndika sentensi ifuatayo ubaoni: Kwa kuwa watu wengine wana . . . zaidi ya wengine, wanahisi jaribio la kuamini kuwa wao ni bora kuliko wengine.

Waalike wanafunzi kupendekeza baadhi ya maneno ambayo yanaweza kukamilisha kauli hii. Baadhi ya majibu yanajumuisha pesa, mali, uwezo wa muziki, ujuzi wa riadha, talanta, elimu, akili, nafasi za ukuaji, ujuzi wa injili na bidhaa. Waalike wana-funzi kufikiria kimya kimya ikiwa kauli hii, pamoja na baadhi ya maneno waliyopendekeza imewahi kuwa kweli kwao.

Wakumbushe wanafunzi kuwa kwa sababu ya upendo wa Yakobo kwa watu wake na utiifu wake kwa amri za Bwana, aliwaonya watu wake dhidi ya udhaifu na dhambi zao. Waa-like wanafunzi wasome Yakobo 2:12–13 na kupendekeza njia ambazo wanaweza kukamilisha kauli ubaoni ili kueleza kuhusu baadhi ya Wanefi wakati wa huduma ya Yakobo.

Waalike wanafunzi wasome Yakobo 2:17–21 na kutafuta ma-neno ya ushauri ambayo yanaweza kuwasidia kushinda kiburi ( Wanaweza kuwa wameweka alama kwenye maneno haya ya ushauri katika kujifunza kwao maandiko kibinafsi). Waalike wanafunzi kuelezea baadhi ya maneno ya ushauri waliyota-mbua na kueleza jinsi ushauri huu unavyoweza kuwasaidia kushinda kiburi.

Eleza kuwa aya hizi zinafundisha ukweli ufuatao: tunapaswa kutafuta ufalme wa Mungu kabla ya maslahi mengine yote. Waalike wanafunzi kadha kuelezea njia moja ambayo wanaweza kutumia baraka na nafasi ambazo Bwana amewapa kujenga ufalme wa Mungu na kubariki maisha ya wengine.

Kuwatayarisha wanafunzi kuzingatia mafundisho ya Yakobo kuhusu usafi wa kimwili, waalike kufikiria kuwa mtu amewauliza kwa nini wanaamini katika amri ya usafi wa kimwili. Waulize wanafunzi wasome Yakobo 2:28–35 kwa usaidizi katika kujibu swali hili. Inaweza kuwa ni bora kuwakumbusha kuwa walijifu-nza funzo hili kama sehemu ya kujifunza kwao kibinafsi: Bwana hufurahia usafi wa kimwili. Walisoma pia kuhusu matokeo ya uasherati kama ilivyoelezwa katika aya hizi. Waalike wanafunzi kushiriki jinsi wanavyoweza kueleza juu ya Yakobo 2:28–35, jinsi wangejibu swali hili.

Uliza: Kulingana na Yakobo 2:27, Ni nini “neno la Bwana” kuhusiana na kuwa na zaidi ya mke mmoja? (Hakikisha kuwa ni dhahiri kuwa Bwana ameamuru kuwa mtu anapaswa kuoa mke mmoja pekee).

Eleza kuwa katika nyakati fulani katika historia ya ulimwengu, Bwana ameamuru watu wake kuwa na desturi ya ndoa ya mitala. Kwa mfano ndoa ya mitala ilifanyika katika Agano la Kale na Ibrahimu na Sera (Ona Mwanzo 16:1–3; M&M 132:34–35, 37) na mwanawe Isaka na mjukuu wake Yakobo (ona M&M

132:37), na ilifanyika pia kwa muda nyakati za mwanzo za Kanisa la urejesho likianza na Nabii Joseph Smith (ona M&M 132:32–33, 53). Hata hivyo, mnamo 1890, Mungu alimwamuru Nabii wake Wilford Woodruff kusitisha desturi ya ndoa ya mitala (Ona M&M, Tamko Rasmi 1).

Wape wanafunzi wakati wa kutafakari jinsi chaguo wanazofanya kuwa wasafi wa kimwili zingemfurahisha Bwana na wengine. Wa-alike kueleza jinsi kushika amri ya usafi wa kimwili sasa kutawa-bariki wao na familia zao sasa na siku za usoni. Eleza jinsi kushika amri ya usafi wa kimwili kumekubariki wewe na familia yako.

Yakobo 3–4Yakobo anawahimiza watu wake kutubu na kupata matumaini kuwa wanaweza kurejea katika uwepo wa MunguMbele ya darasa weka picha ndogo ya Yesu Kristo katikati ya ubao, kwenye bango au karatasi. Karibu na picha, andika maneno machache yanayowakilisha vitu ambavyo vinaweza kuwazuia watu kutoka kwa Mwokozi na injili yake. Waulize wa-nafunzi warejelee Yakobo 4:14. Eleza kuwa aya hii inajumuisha kishazi “kuangalia zaidi ya lengo” Waulize “lengo” inamanisha nini katika aya hii. (Mzee Neal A. Maxwell wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alifundisha kuwa “lengo ni Kristo” [“Jesus of Nazareth, Savior and King,” Ensign, Des. 2007, 45].) Baada ya kushiriki maelezo haya alika mwanafunzi asome Yakobo 4:14–15 kwa sauti.

Uliza: Unafikiri inamaanisha nini kuangalia zaidi ya lengo? (Kuweka maisha yetu kwenye kitu kingine mbali na Mwokozi na injili Yake.)

Waalike wanafunzi wasome Yakobo 4:4–12 na kutambulisha sababu kadha kwa nini Yakobo alimwamini Yesu Kristo na kwa nini alihisi ni muhimu kuwafanya wengine kufahamu kuhusu Upatanisho. Kama matokeo ya mjadala huu, hakikisha kuwa kufuata ukweli inakuwa dhahiri: Kupitia kwa Upatanisho wa Yesu Kristo, tunaweza kujazwa na matumaini na kujipata-nisha na Mungu.

Elezea hisia zako za shukrani kwa Mwokozi na Upatanisho wake. Shuhudia kuwa Yesu Kristo ndiye “lengo” ambalo tunapaswa kuzingatia maishani mwetu. Ili kuhitimisha somo hili, waulize wanafunzi kufikiri kile watakachofanya ili kumzingatia Mwokozi katika siku chache zifuatazo.

Kitengo Kifuatacho (Yakobo 5 hadi Omni)Waulize wanafunzi: Mpinga Kristo ni nini? Ungemjibu vipi mpinga Kristo? Unaposoma maandiko katika kitengo kifuata-cho, ona kile Yakobo alisema alipokabiliwa na Sheremu, mpinga Kristo. Pia, tafuta baraka ambazo Enoshi alipokea kwa sababu alimtafuta Mungu kwa moyo wake wote, akiomba mchana ku-twa hadi usiku. Angalia sababu za Wanefi kuacha nchi ya urithi wao wa Kwanza na kuungana na Wamuleki.

Page 177: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

162

SOMO LA 46

yakobo 5:1–51

Mapendekezo ya Kufundisha

Yakobo 5:1–14Yakobo alimnukuu Zeno, ambaye alifananisha nyumba ya Israeli na Mzeituni shambaFikiria kuanza somo hili kwa kusoma mifano ifuatayo ya vijana walioshuku upendeleo wa Bwana wa kuwasamehe dhambi zao.• Kijana mwenye ukuhani anakuza tabia ya dhambi. Anaamini kuwa wengine wanaweza

kusamehewa lakini anatia shaka kama Bwana atakubali toba yake.• Msichana anavunja amri. Anahisi hatia, anajisikia vibaya juu ya hilo, na kujiuliza ikiwa

Bwana bado anampenda.Waalike wanafunzi kutafakari swali lifuatalo bila kujibu kwa sauti:• Umewahi kushangaa kuhusu upendeleo wa Bwana wa kukusamehe dhambi zako?Eleza kuwa Yakobo alitabiri kuwa Wayahudi wangemkataa Yesu Kristo (ona Yakobo 4:15). Alifundisha pia kuwa Yesu Kristo angeendelea kutumikia wokovu wa watu Wake hata baada ya wao kumkataa Yeye (ona Jacob 4:17–18). Ili kudhihirisha ukweli huu, Yakobo ali-nukuu fumbo lililotolewa na nabii aliyeitwa Zeno. Fumbo hutumia wahusika kiishara, vitu, na vitendo ili kufundisha kweli. Wanafunzi wanapojifunza fumbo hili, wanaweza kujifunza masomo muhimu kuhusu upendeleo wa Yesu Kristo kusaidia wale ambao wamegeukia mbali kutoka kwake. Waalike wanafunzi wasome Yakobo 5:1–2 kwa sauti na fanya darasa kutafuta ni nani Zeno alikuwa anazungumza nao (nyumba ya Israeli). Unaweza kuhitaji kueleza kuwa wakati Nabii Yakobo wa agano la Kale alipofanya maagano na Bwana, Bwana alibadilisha jina lake kuwa Israeli. Kishazi “nyumba ya Israeli” humaanisha uzao wa Yakobo na watu wote waliobatizwa na kufanya maagano na Bwana.• Ni nani katika darasa hili ambaye ni mshiriki wa nyumba ya Israeli? (Unaweza kuhitaji

kueleza kuwa waumini wote waliobatizwa wa Kanisa ni sehemu ya nyumba ya Israeli. Wao ni sehemu ya fumbo katika Yakobo 5.)

Alika mwanafunzi asome Yakobo 5:3 kwa sauti. Wakati darasa linapotafuta kile Zeno alitumia katika fumbo lake kama kuashiria nyumba ya Israeli. Baada ya wanafunzi kuripoti walichopata, eleza kuwa miti ya mizeituni ilikuwa ya thamani sana katika Israeli ya kale mahali ambapo Zeno aliishi. Mazeituni ilitumiwa kwa chakula, na mafuta ya mazeituni yalitumiwa kupikia na kama dawa na kama mafuta ya taa. Miti ya mizeituni ilihitaji ulinzi mkubwa na kazi ili kuisaidia kuzaa matunda mazuri. Eleza kuwa katika fumbo hili, miti ya mzeituni ipo kwenye shamba la mizabibu, ambayo inaashiria ulimwengu.• Kulingana na Yakobo 5:3, nini kilianza kutendeka kwa miti ya mizeituni shamba? Kuoza

kwa mti kunaashiria nini? (Himiza wanafunzi kutumia tanbihi 3d ili kujibu swali hili.)• Uasi ni nini? (Kugeuka kutoka kwa Mungu na injili Yake.)Waalike wanafunzi wasome Yakobo 5:4–6 kimya kimya. Waulize kufikiria kuhusu ni nani bwana wa shamba la mizabibu, na ni nini matendo yake ya kupogoa, kupalilia na kulisha yanaweza kuashiria. Kisha wafanye waelezee wanachofikiri juu ya viashiria hivi. (Unaweza

UtanguliziKatika kufundisha watu wake, alinukuu fumbo la miti ya mizeituni shamba na mwitu, ambalo mwanzoni lilitolewa na Nabii aliyeitwa Zeno ambaye alijumuishwa katika mabamba ya shaba. Yakobo alitumia fumbo hili

kufundisha kuwa Bwana angetafuta kuleta wokovu kwa watu wote— hata miongoni mwa Watu wake wa Agano waliogeuka kutoka Kwake. Kwa sababu ya urefu wa Yakobo 5, imegawanywa katika masomo mawili.

Page 178: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

163

yaKobo 5:1– 51

kuhitaji kuwaeleza kuwa bwana wa shamba la mizabibu iliashiria Yesu Kristo. Kupogoa, kupalilia na kulisha inawakilisha juhudi za Bwana kutusaidia kupokea baraka za Upatani-sho Wake na juhudi za manabii kuwafundisha na kuwaita watu katika toba.) Alika mwanafunzi mmoja asome kauli hii ya Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili:“ Fumbo hili kama linavyo simuliwa na Yakobo linakusudiwa tangu mwanzo kuwa juu ya Kristo. . . . Hata pale ambapo Bwana wa shamba la mizabibu na wafanyi kazi wake wanapojitahidi kuimarisha, kupogoa, kusafisha na kufanya miti iweze kuzaa kwa kile ki-nachokuwa mlango mmoja wa mchoro wa kihistoria wa kutawanyika na kukusanyika kwa Israeli, maana ya undani wa Upatanisho ndiyo kiini cha kimsingi cha kazi zao” (Christ and the New Covenant: The Messianic Message of the Book of Mormon [1997], 165).Ili kuwasaidia wanafunzi kuona jinsi fumbo hili linavyodhihirisha kujali kwa Bwana juu yao, wafundishe kuwa wanaweza kubadilidha majina yao katika mahali linaporejewa neno miti ya mizeituni. Unaweza kuonyesha hii kwa kutoa mfano ufuatao Yakobo 5:7: “ina nihuzunisha kwamba nitampoteza [jina lako].” Eleza kuwa tunapoweka majina yetu katika Yakobo 5 katika mahali ambapo kuna maana na kunafaa, tunaweza kujifunza zaidi kuhusu fikira za Bwana juu yetu.Onyesha chati ifuatayo. Eleza kuwa inaorodhesha maana ya ishara katika fumbo la Zeno. Unaweza kutaka kufanya nakala za chati kama mwongozo au kufanya wanafunzi kunakili chati katika shajara zao za kujifunza maandiko.

Yakobo 5: Fumbo la miti ya mizeituni shamba na mwitu.

Ishara Maana Inayowezekana

Mti wa mzeituni shamba nyumba ya israeli, watu wa Mungu wa agano

Shamba la Mizabibu Ulimwengu

Kuoza dhambi na uasi

bwana na bwana wa shamba la mizabibu yesu Kristo

Kupogoa, kupalilia na kulisha juhudi za bwana kusaidia watu kupokea baraka za Upatanisho Wake

Mtumishi wa bwana wa shamba la Mizabibu.

Manabii wa bwana

Matawi vikundi vya watu

Mti wa mzeituni mwitu Wayunani —wale ambao hawajafanya maagano na bwana. baadaye katika fumbo hili, miti ya mizeituni asili ikawa mwitu, ikiwakilisha nyumba ya israeli iliyoanguka katika uasi.

Kupandikiza na kupanda matawi Kutawanyika na kukusanyika kwa watu wa bwana wa agano. cha ziada, katika kupandikiza matawi ya mizeituni mwitu kwenye mizeitunishamba kunawaki-lisha kuongoka kwa wale ambao wanakuwa sehemu ya watu wa bwana wa agano.

Kuchoma matawi hukumu ya Mungu juu ya waovu

tunda Maisha au kazi za watu

Mwulize mwanafunzi asome Yakobo 5:7, 9–10 kwa sauti, na kufanya darasa kutafuta kile bwana wa shamba la mizabibu alifanya ili kuokoa mizeituni shamba. Acha wanafunzi kuripoti walichopata ( Unaweza kuhitaji kueleza kuwa kupandikiza ni kuweka tawi la mti mmoja katika mti tofauti. Kupandikiza katika aya hizi kunawakilisha juhudi za Bwana kuwasaidia Wayunani kuwa sehemu ya watu wake wa agano kupitia ubatizo na kuongo-lewa. Kuchomwa kwa baadhi ya matawi kunawakilisha hukumu ya Bwana juu ya washiriki waovu zaidi katika nyumba ya Israeli.)

Page 179: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

164

SoMo la 46

Alika mwanafunzi asome Yakobo 5:11 kwa sauti. Uliza darasa kutafuta ushahidi wa fikira za bwana kwa ajili ya mizizi ya mzeitunishamba. Acha wanafunzi waripoti walichopata.Wakumbushe wanafunzi kuwa Yakobo 5:6 inaeleza kuwa mzeituni shamba ulikuwa umeanza kuzaa matawi machanga na laini. Uliza mwanafunzi asome Yakobo 5:8, 13–14 kwa sauti. Uliza darasa kutambua kile bwana alikifanya kwa matawi haya. Unaweza pia kuwauliza kufikiri jinsi safari ya familia ya Lehi inavyotoa mfano wa matendo ya bwana katika Yakobo 5:8, 13–14.

Yakobo 5:15–40Bwana wa shamba la mizabibu na mtumishi wake wafanya kazi kusaidia shamba kuzaa tunda zuriGawanya darasa katika vikundi viwili. Wape kikundi cha kwanza kusoma Yakobo 5:15–28 na kikundi cha pili kusoma Yakobo 5:29–40. Waulize wanafunzi kufanya yafuatayo wana-pojifunza (unaweza kutaka kuandika , maelekezo haya ubaoni): 1. Fanya muhtasari wa kile kilichofanyika katika shamba la mizabibu na kile kinachoweza

kuwakilisha. 2. Tambua vishazi vinavyoonyesha juhudi za bwana wa shamba la mizabibu za kuhifadhi

mzeitunishamba (au wa asili) na matawi yake.Baada ya wanafunzi kuwa na muda wa kutosha kusoma aya walizopewa, waulize kufa-nya muhtasari wa kile kilichofanyika katika shamba la mizabibu na kueleza kinachoweza kuwakilisha. Anza na wanafunzi waliojifunza Yakobo 5:15–28. Hapa chini ni mifano ya muhtasari na ufafanuzi.Yakobo 5:15–28. Kilichofanyika: Matawi yote ambayo yaliyokuwa yamepandikizwa yalizaa matunda mazuri. Hata hivyo, tawi moja, licha ya kuwa lilipandwa katika sehemu nzuri ya shamba la mizabibu, lilizaa yote matunda shamba na mwitu. Kile hii inaweza kuwakilisha: Tunda zuri au shamba kote katika shamba la mizabibu linawakilisha haki iliyokuwa duni-ani wakati wa Kristo na Mitume Wake. Tawi lililozaa matunda mengine mazuri na matunda mengine mwitu linawakilisha wenye haki na waovu wa uzao wa Lehi.Yakobo 5:29–40. Kilichofanyika: Matunda yote katika shamba la mizabibu yaliharibika. Kile hii inaweza kuwakilisha: Uharibifu wa matunda yote unawakilisha Uasi Mkuu, ambapo utimilifu wa injili ya Yesu Kristo ulipotea kutoka ulimwenguni kufuatia huduma ya Mitume wa Kristo duniani.Baada ya vikundi kushiriki miuhtasari hii, uliza: • Ni vishazi vipi vinavyoonyesha juhudi za bwana za kuhifadhi mti wa mzeitunishamba

pamoja na matawi yake? Hii inadhihirisha nini kuhusu hisia za Bwana kwa watu Wake wa agano?

• Tulipojadili fumbo hili, umejifunza nini kumhusu Yesu Kristo, bwana wa shamba la mi-zabibu? (Baadhi ya kweli zinazofunzwa katika aya hizi, wanafunzi wanapaswa kuelewa kuwa Bwana anatupenda na hufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya wokovu wetu.)

• Fumbo hili linahusiana vipi na mifano katika mwanzo wa somo hili kwa vijana wawili waliouliza kuhusu upendeleo wa Bwana wa kuwasamehe?

Yakobo 5:41–51Bwana anahuzunika kwa ajili ya shamba lake la mizabibuWaalike wanafunzi kadha kuchukua zamu katika kusoma kwa sauti kutoka katika Yakobo 5:41–42, 46–50. (Unaweza kutaka kueleza kuwa kishazi “kiburi cha shamba lako” katika Yakobo 5:48 inaweza kumaanisha kujikweza.) Uliza darasa kutafuta vishazi vinavyoonye-sha upendo wa bwana na kulijali kwake shamba lake la mizabibu na huzuni yake wakati miti inakosa kuzaa matunda mazuri. Waalike wanafunzi kuelezea vishazi kutoka katika aya hizi, ambavyo hasa vina maana kwao na kueleza kwa nini vishazi hivi vina maana. Baada ya wanafunzi kuelezea, uliza darasa:• Je utunzaji wa bwana wa shamba lake la mzabibu inawakilisha kwa njia gani upendo wa

Bwana kwetu?

Page 180: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

165

yaKobo 5:1– 51

• Ni nini baadhi ya mifano, kutoka katika maandiko au kutoka katika maisha yako inayo-onyesha kuwa Bwana anaendelea kuwapenda na kuwatunza watu hata baada ya wao kugeuka kutoka Kwake?

Ili kuhitimisha, wakumbushe wanafunzi kuwa bwana alifikiria kukata miti yote kwa sababu matunda yake yote yalikuwa yameharibika licha ya kazi yote aliyofanya (ona Yakobo 5:49).• Unafikiri bwana ataliacha shamba lake la mizabibu? Kwa nini?Baada ya wanafunzi kutoa majibu yao, soma Yakobo 5:51 kwa darasa. Shuhudia kuwa Bwana anatupenda na hudhihirisha huruma na subira kuu anapofanya kazi kutusaidia kuja Kwake na kuzaa matendo ya haki. Eleza kuwa somo litakalofuata litajumuisha mjadala wa juhudi za mwisho za bwana kuokoa shamba lake la mizeituni.

Page 181: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

166

UtanguliziKatika somo la awali, wanafunzi walianza kujifunza kuhusu fumbo la Zeno la miti ya mizeituni shamba na mwitu. Katika somo hili watajifunza sehemu ya mwisho ya fumbo, ambapo bwana wa shamba la mizabibu

anafanya kazi na watumishi wake kwa mara ya mwisho kuisaidia miti kuzaa matunda mazuri. Watajifunza pia Yakobo 6, ambapo Yakobo anazungumzia fumbo na kuwausia watu wake kutubu.

SOMO LA 47

yakobo 5:52–77; yakobo 6

Mapendekezo ya Kufundisha

Yakobo 5:52–60Katika fumbo la mizeituni shamba na mwitu, bwana wa shamba la mizabibu anaokoa miti na kuisaidia kuzaa matunda mazuriKabla ya darasa, chora ubaoni picha ya miti mitatu.

Wakumbushe wanafunzi kuwa katika somo lililopita, walianza kujifunza fumbo la miti ya mizeitunishamba na mwitu katika Yakobo 5. Katika mwisho wa somo hilo, miti yote katika shamba la mizabibu ilikuwa inazaa matunda mwitu (ona Yakobo 5:30–42). Hii iliwakilisha Uasi Mkuu.Ili kurejea somo lililopita, gawa darasa katika jozi. Acha kila jozi kujadili majibu yao kwa kauli zifuatazo zisizokamilika (unaweza kutaka kuandika kauli hizi ubaoni): 1. Bwana wa shamba la mizabibu anawakilisha . . . 2. Juhudi za bwana wa shamba la mizabibu ili kuokoa miti yake inawakilisha . . . 3. Kitu kimoja nimejifunza kuhusu Yesu Kristo kutoka katika maneno au matendo ya

bwana wa shamba la mizabibu ni . . . 4. Baada ya miti yote na matunda ya shamba la mizabibu kuharibika, bwana aliamua . . .Baada ya wanafunzi kujadili kauli hizi katika jozi zao, chambua kwa ufupi majibu yao kama darasa. Wanafunzi wanaporipoti majibu yao kwa kauli mbili za kwanza hakikisha ni dhahiri kuwa bwana wa shamba la mizabibu anawakilisha Yesu Kristo na juhudi zake kuokoa miti yake zinawakilisha juhudu za Mwokozi kuwasaidia watu wake kurejea kwake. Wanafunzi wanaweza kushiriki mafunzo ya thamani wanapokamilisha kauli ya tatu. Acha wanafunzi kuangalia majibu yao kwa kauli ya mwisho kwa kuangalia Yakobo 5:51, ambayo inasema bwana aliamua kuliacha shamba la mizabibu “kwa muda mdogo zaidi.” Eleza kuwa somo la leo linajumuisha sehemu ya mwisho ya fumbo, ambayo inawakilisha siku za mwisho, pamoja na Urejesho wa injili.Eleza kuwa bwana wa shamba la mizabibu aliamua kuokoa shamba la mizabibu kwa kupandikiza matawi zaidi. Acha wanafunzi kuchukua zamu wakisoma kwa sauti kutoka Yakobo 5:52–58. Alika darasa kutafuta kile bwana alichofanya ili kuimarisha matawi na mizizi. (Wasaidie wanafunzi kuona kuwa bwana wa shamba la mizabibu alipandikiza matawi kutoka kwenye miti halisi na kuyarudisha kwenye mti ya asili — mti unaowakili-sha nyumba ya Israeli. Kisha akapandikiza matawi kutoka kwa mti huo katika miti mingine ya asili. Pia alitupa matawi yaliyokuwa machungu sana ndani ya moto. Unaweza kutumia miti iliyo ubaoni kudhihirisha maelezo haya. Kwa mfano, unaweza kufuta tawi kutoka mti mmoja na kuchora tawi jipya katika mti mwingine)

Wapange wanafunzi kufanya kazi katika joziKufanya kazi katika majozi kunaweza ku-wapa nafasi ya “kufu-ndishana mafundisho ya ufalme” (M& M 88:77). Kuwa mwenye kufikiri katika maamuzi yako kuhusu wanafunzi wapi utawapa kufanya kazi pamoja— wanafunzi wengine wanaweza kusaidiwa au kuvurugwa ikiwa ni wenzi pamoja.

Page 182: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

167

yaKobo 5:52–77; yaKobo 6

Alika mwanafunzi asome Yakobo 5:59 kwa sauti. Uliza darasa kusikiliza kile bwana wa shamba la mizabibu alitumaini matendo haya yangefanya kwa mizizi ya mti.• Bwana alitumaini nini kingefanyika kwa mizizi? (Aliitaka “ ipate nguvu”)Wakumbushe wanafunzi kuwa kwa wakati huu, miti yote ilikuwa inazaa matunda mabaya, ikiwakilisha hali yote ya uasi. Eleza kuwa wakati mizizi ingepata nguvu, matawi kote katika shamba la mizabibu yangebadilika “ili kwamba wema uzidi ubaya” (Yakobo 5:59).Hakikisha kuwa wanafunzi wanaelewa kuwa aya hizi zinafundisha kuwa athari ya ma-agano ya injili huwawezesha watoto wa Baba wa Mbinguni kushinda dhambi na kuleta utakatifu.• Ni kwa njia gani maagano ya injili hutuimarisha? Je, maagano yako yameathiri vipi mai-

sha yako? (Unaweza kutaka kushiriki hisia zako na ushuhuda kuhusu kanuni hii.)

Yakobo 5:61–77Bwana wa shamba la mizabibu anafanya kazi katika shamba la mizabibu na watumishi wakeWaalike wanafunzi wasome Yakobo 5:61–62 kimya, wakitafuta kile bwana wa shamba la mizabibu alichowaagiza watumishi wake kufanya na kwa nini aliwaagiza kufanya hivyo.• Mtumishi mwanzoni mwa fumbo anawakilisha manabii wa Bwana. Ni nani anawa-

kilishwa na watumishi wengi katika Yakobo 5:61? (Wasaidie wanafunzi kuona kuwa watumishi hawa wanaweza kuwakilisha waumini wote wa Kanisa, Manabii na Mitume, viongozi wenye mamlaka na viongozi wakazi, wamisionari, walimu wa nyumbani, wa-limu watembeleaji na kila mtu anayeshiriki katika kazi ya Bwana.)

• Ni nini muhimu kuhusu maneno sisi, yetu, na sisi katika Yakobo 5:61–62? ( Bwana hufa-nya kazi nasi. Hatujaachwa kufanya kazi Yake peke yetu)

• Kulingana na Yakobo 5:62, ni nini tofauti kuhusu wakati ambapo watumishi hawa wa-liitwa kufanya kazi? ( Ilikuwa “wakati wa mwisho” ambapo bwana angepogoa shamba la mizabibu. Manabii wamerejea katika huu “wakati wa mwisho” kama “maongozi ya Mungu ya utimilifu wa wakati." Kwa mfano, ona Waefeso 1:10 na M&M 128:20.)

Ili kuwasaidia wanafunzi kuona kuwa sehemu hii ya fumbo inawahusu, fanya mwanafunzi kusoma kauli ifuatayo ya Mzee Dean L. Larsen wa wale Sabini:“[Sasa] ni wakati ambapo Bwana na watumishi wake watafanya juhudi za mwisho kupeleka ujumbe wa ukweli kwa watu wote ulimwenguni na kudai tena uzao wa Israeli ya kale ambao wamepoteza utambulisho wao wa kweli. . . .“Mmekuja duniani wakati msingi umewekwa wa kazi hii kuu. Injili imereje-

shwa kwa mara ya mwisho. Kanisa limeimarishwa katika karibu kila sehemu ya ulimwe-ngu. Jukwaa limetayarishwa kwa mandhari ya tamthiliya ya mwisho ikichezwa. Ninyi ndio mtakuwa wachezaji wakuu. Ninyi ni baadhi ya watumishi wa mwisho katika shamba la mizabibu. . . . Hii ndiyo huduma ambayo kwayo mlichaguliwa” (“A Royal Generation,” Ensign, May 1983, 33).• Inakuathiri vipi kujua kuwa umeitwa kumtumikia Bwana wakati huu wa mwisho wa

kufanya kazi?• Ni wakati gani umehisi kuwa Bwana amefanya kazi nawe uliposhiriki katika kazi Yake?• Ni zipi baadhi ya nafasi ulizo nazo za kumtumikia Bwana na kusaidia wengine kuzaa

“matunda mema”? (Wanafunzi wanaweza kutaja miito yao na kazi kanisani, majukumu yao kuwasaidia wanafamilia na marafiki na wengine kumkaribia Mwokozi, na fursa watakayopata kumtumikia Bwana kama wamisionari wa wakati wote.)

Andika Yakobo 5:70–75 ubaoni. Tanguliza aya hizi kwa kueleza kuwa zinafundisha kuhusu uhusiano ambao Bwana anao na watumishi Wake. Zinaeleza pia kile Bwana na watumishi Wake wanaweza kutimiza kupitia kwa kazi yao pamoja. Waalike wanafunzi kusoma aya hizi kimoyomoyo na kuchagua aya inayowapa maelezo wanayopenda zaidi kuhusu uhusi-ano wa Bwana na watumishi wake. Baada ya wanafunzi kuwa na muda wa kusoma, alika wachache wao kusema aya waliyochagua, kwa nini wanaipenda, na inavyoweza kuwasai-dia wanapomtumikia Bwana.

Page 183: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

168

SoMo la 47

Wanafunzi wanaposhiriki katika shughuli hii, hakikisha kuwa wanaelewa kuwa Bwana anatuahidi furaha tunapofanya kazi Naye kutimiza kazi Yake. Ili kusaidia wanafunzi kupanua uelewa wao wa Yakobo 5:70–75, fikiria kuuliza baadhi ya maswali haya yafuatayo:• Bwana wa shamba la mizabibu aliwaahidi nini wale waliofanya kazi naye? (ona Yakobo

5:71, 75.) Ni wakati gani umehisi furaha katika kazi ya Bwana?• Kwa nini unafikiri watumishi walifanya kazi “kwa uwezo wao” na “kwa bidii yao yote”?

(Ona Yakobo 5:72, 74.) Ni masomo gani unayoweza kupata kutoka katika vishazi hivi unapomtumikia Bwana?

Hitimisha sehemu hii ya somo kwa kuuliza wanafunzi kujibu maswali yafuatayo katika shajara zao za kujifunza maandiko au katika daftari zao za darasa (unaweza kutaka kua-ndika katika ubao):• Unapofikiria nafasi za kumtumikia Bwana , utatumia kwa jinsi gani kweli tulizojadili

katika Yakobo 5?Baada ya wanafunzi kuwa na wakati wa kutosha kuandika, unaweza kuuliza mmoja au wawili kati yao kusoma majibu yao kwa darasa.

Yakobo 6Yakobo afundisha kuhusu neema za Mungu na kuwaalika watu wake kutubuTanguliza kwa ufupi Yakobo 6 kwa kuelezea kwamba ina muhtasari wa Yakobo wa kweli muhimu kutoka katika fumbo la miti ya mizeituni shamba na mwitu.Alika mwanafunzi asome Yakobo 6:4–6. Uliza nusu ya darasa kutafuta kile Yakobo alitaka watu wake kujifunza kuhusu Bwana. (Kwamba anawakumbuka watu wake. Kwamba Yeye “anawashikilia” na kwamba “mkono wake wa neema umenyoshwa [kwao].” Unaweza kuhitaji kuelezea kuwa katika kifungu hiki , neno kushikilia linamaanisha kukaa karibu sana na kitu au mtu.) Uliza nusu ile nyingine ya darasa kutafuta kile Yakobo aliwahimiza watu wake kufanya kama matokeo ya ufahamu huu. (Kutoshupaza mioyo yao, kutubu na kumjia Bwana kwa “moyo wa lengo moja” na “kumshikilia Mungu kama vile anavyowashikilia [wao].”) Baada ya wanafunzi kuliambia darasa kile walichojifunza, uliza:• Yakobo alielezea vipi kuhusu Bwana? Inamaanisha nini kwako kwamba “mkono wa

Bwana wa neema umenyoshwa kwako”?• Ulijifunza nini kuhusu Bwana kutoka katika fumbo la miti ya mizeituni ambacho kina-

dhihirisha jinsi Yeye anavyokushikilia wewe? Unaweza kufanya nini kuonyesha kuwa unamshikilia Bwana?

Fanya muhtasari Yakobo 6:7–10 kwa kueleza kuwa baada ya “kulishwa kwa neno jema la Mungu,” hatupaswi kuzaa matunda maovu. Tunapaswa kufuata maneno ya manabii. Tu-sipotubu, Yakobo alionya, tutawajibika kwa ajili ya dhambi zetu mbele ya kiti cha hukumu cha Bwana. Wahimize wanafunzi kusoma Yakobo 6:11–13 kimya kimya na kutafuta ushauri wa mwisho wa Yakobo. Baada ya kushiriki walichopata, uliza:• Kwa nini ni hekima kuchagua kutubu na kujitayarisha sasa kusimama mbele ya Bwana

na kuhukumiwa Naye?Thibitisha kwamba tunakuwa wenye hekima kujitayarisha sasa kwa hukumu kwa kutubu na kupokea neema za Bwana.Ili kuhitimisha somo, sisitiza kuwa toba hututayarisha, si tu kwa hatima ya hukumu bali pia kuweza kumtumikia Bwana sasa. Shuhudia kwa wanafunzi kuwa Bwana anawataka watumike pamoja Naye na kupata furaha pamoja Naye, na kwamba waweze kuwa wenye kustahili kufanya hivyo wanapotii amri Zake, kutubu, na kupokea neema Zake.

Mawazo ya Ziada ya KufundishaYakobo 5. Maonyesho ya videoUnapofundisha somo la 47, unaweza kutaka kuonyesha sehemu ya mwisho ya onyesho la video “The Olive Tree

Allegory,” ambalo inapatikana katika DVD inayoitwa Book of Mormon DVD Presentations 1–19. Unaweza kutaka kuonyesha sehemu ya wakati wa mgao wa pili wa somo hili, baada ya kauli ya Mzee Dean L. Larsen.

Page 184: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

169

SOMO LA 48

yakobo 7

Mapendekezo ya Kufundisha

Yakobo 7:1–14Yakobo alimtegemea Bwana alipokabiliana na Sheremu, mpinga KristoKabla ya darasa, andika ubaoni kauli ifuatayo ya Mzee Robert D. Hales wa Akidi ya Mi-tume Kumi na Wawili (imenukuliwa kutoka “Christian Courage: The Price of Discipleship,” Ensign or Liahona, Nov. 2008, 72):

“Mojawapo ya majaribu makubwa ya maisha ya muda huja wakati imani yetu inatiliwa shaka au kukosolewa” ” (Mzee Robert D. Hales).

Waulize wanafunzi kufikiria wakati ambapo mtu alitilia shaka au kukosoa imani yao. Waalike baadhi yao kushiriki jinsi walivyohisi wakati haya yalifanyika. Unaweza pia kutaka kushiriki uzoefu kutoka katika maisha yako.Eleza kuwa Yakobo 7 inarejea tukio la Yakobo na Sheremu, mpinga-Kristo (Unaweza kutaka kueleza kuwa mpinga-Kristo ni “mtu yeyote au kitu chochote kilicho bandia kwa injili au mpango wa wokovu na ambacho kiko kinyume na Kristo kwa siri au uwazi” [Bible Dictionary, “Antichrist”].) Sheremu alimtafuta Yakobo ili kufanyia ubishi imani yake.Waalike wanafunzi kusoma Yakobo 7:1–5 kimya kimya. Waulize kutambua (1) kile Sheremu alikuwa akijaribu kufanya na (2) jinsi alivyotafuta kutimiza shabaha zake. Baada ya wana-funzi kumaliza kusoma, waulize kueleza kile walichojifunza kuhusu Sheremu. Unaweza kutaka kuuliza baadhi yao maswali yafuatayo ili kuboresha mjadala:• Ni athari gani aliyokuwa nayo Sheremu kwa watu? • Ni nini unachoona katika Yakobo 7:1–5 kinacho kukumbusha kuhusu nyakati ambapo

wengine wameshuku au kukosoa imani yako? Mnapojadili swali hili, unaweza kuhitaji kuwasaidia wanafunzi kuelewa kuwa si watu wote wanaoshuku au kukosoa imani yetu wana malengo sawa na yale ya Sheremu. Ingawa watu kama Sheremu wanatafuta kwa makusudi kuangamiza imani, wengine hushuku imani yetu kwa sababu wanataka kujua au wamepewa habari isiyo kweli kuhusu imani yetu.)

• Kwa nini wakati mwingine ni vigumu kulinda imani yetu dhidi ya watu kama Sheremu?Nakili marejeo yafuatao ya maandiko na kauli ubaoni. (Ili kuokoa wakati, unaweza kutaka kunakili hizi ubaoni kabla ya darasa. Unaweza pia kutaka kutayarisha kitini)

1. Yakobo 7:5 a. Alishuhudia maandiko na maneno ya manabii.2. Yakobo 7:8 b. Aliacha matokeo mikononi mwa Bwana.3. Yakobo 7:10–11 c. Alitegemea mwongozo na nguvu kutoka kwa Roho Mtakatifu.4. Yakobo 7:12 d. Alikumbuka uzoefu wa awali ambao ulikuwa umeimarisha imani yake.5. Jacob 7:13–14 e. Alitoa ushuhuda aliokuwa amepokea kupitia kwa Roho Mtakatifu.

Waalike wanafunzi kushiriki uzoefuWanafunzi wanaposhi-riki uzoefu wa kutoa ari, hii hualika Roho wa Bwana katika darasa. Wanafunzi wanaposi-kia uzoefu na shuhuda za wenzao, shuhuda zao zinaimarishwa na wanajifunza njia mpya za kutumia kanuni za injili katika maisha yao. Kwa kawaida inatosha kuwa na wanafunzi watatu kushiriki uzoefu. Epukana na kuwaita wanafunzi walewale wachache kushiriki kila siku; jaribu kuhusisha kila mmoja.

UtanguliziYakobo alimtegemea Bwana na kwa ushuhuda wake thabiti kushinda mawazo potovu na ubishi wa She-remu, mpinga Kristo. Alitoa hasa nguvu kutokana na uzoefu wa awali ambao ulikuwa umeimarisha imani yake katika Yesu Kristo. Alitegemea pia mwongozo wa Roho Mtakatifu, ujuzi wake wa maandiko na maneno ya manabii, na ushuhuda wake wa Yesu Kristo. Wakati

Sheremu alipodai ishara ambayo ingethibitisha maneno ya Yakobo, alipigwa na Mungu. Yakobo alihitimisha kumbukumbu yake kwa kueleza jinsi Wanefi walivyo-mwamini Bwana wakijiimarisha dhidi ya Walamani. Kabla ya Yakobo kufa, alikabidhi mabamba madogo kwa mwanawe Enoshi.

Page 185: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

170

SoMo la 48

Eleza kuwa aya katika orodha hii zinaeleza majibu ya Yakobo wakati Sheremu alipoifanyia ubishi imani yake. Kauli katika sehemu ya kulia inawakilisha majibu ya Yakobo, lakini yameorodheshwa kwa ajili ya mpangilio na hitaji la kuyaweka sare na aya inayoambatana. Waalike wanafunzi kadha kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka Yakobo 7:5–14. Wana-posoma, acha watue baada ya kila kifungu kilichoorodheshwa ubaoni. Waulize wanafunzi kuweka sare kila andiko pamoja na kauli inayoambatana. Unaweza kutaka kumwalika mwanafunzi kuja mbele ubaoni na kuchora mstari kutoka kwenye marejeo ya maandiko hadi kwenye kauli inayofanana nayo. (Majibu: 1-d; 2-c; 3-a; 4-e; 5-b.)Wakati wanafunzi wamekamilisha kazi ya kuweka sare, uliza:• Ni kanuni gani uliyoona ikifundishwa katika aya tuliyosoma?Kama hakuna yeyote anayependekeza, hakikisha kuwa wanafunzi wanaelewa kuwa tunapomtegemea Bwana, tunaweza kushinda changamoto za imani yetu. (Unaweza kutaka kuandika kanuni hii ubaoni.)Eleza kuwa majibu ya Yakobo kwa Sheremu yanatoa mfano kwetu kufuata tunapojibu wale wanaoshuku au kukosoa imani yetu.Maswali yaliyo orodheshwa hapa chini yameundwa kuwasaidia wanafunzi kufikiri kwa kina zaidi kuhusu kile Yakobo alifanya ili kumtegemea Bwana. Kujibu maswali haya kuta-wapa wanafunzi nafasi ya kudhihirisha na kushuhudia jinsi matendo sawa na hayo yalivyo wasaidia wakati wengine walipo pinga imani yao. Itawasaidia pia kujifunza jinsi ya kujibu ipasavyo changamoto za imani yao katika siku za usoni. Kwa kuwa kuna maswali mengi hapo chini kuliko yale ambayo unaweza kuwa na wakati wa kutumia darasani, chagua maswali machache tu ya kutumia katika mjadala wako. Unapofanya hivi, tafuta mwongozo wa Roho Mtakatifu na kufikiria uzoefu wa wanafunzi walioshiriki mwanzoni mwa darasa. Unaweza pia kufikiria kuwauliza wanafunzi ni yapi kati ya matendo ya Yakobo wangepe-nda kujadili zaidi. • Ni nini kilichofanyika kwa Yakobo awali ambacho kilifanya imani yake kuwa isiyo tiki-

sika? (ona Yakobo 7:5.)• Ni nini baadhi ya uzoefu ambao umeimarisha imani yako? (Unaweza kuwapa wanafunzi

wakati kutafakari swali hili kabla ya kuwauliza kujibu. Wahahikikshie kuwa hawahitaji kushiriki uzoefu ulio wa kibinafsi au siri.) Kukumbuka uzoefu huu kunawezaje kukusai-dia wakati mtu anashuku au kukosoa imani yako?

• Ni wakati gani ambapo Roho Mtakatifu amekusaidia kujibu maswali au ukosoaji kuhusu imani yako? (Ona Yakobo 7:8.)

• Mazoea ya kila siku ya kusoma maandiko na maneno ya manabii wa siku za mwisho yana-kusaidia vipi wakati wengine wanaposhuku au kukosoa imani yako? (Ona Yakobo 7:10–11.)

• Ni wakati gani umeshiriki ushuhuda wako na mtu ambaye ameshuku au kukosoa imani yako? (Ona Yakobo 7:12.) Matokeo yalikuwa ni nini?

• Wakati Sheremu alipodai ishara, kwa nini ilikuwa hekima kwa Yakobo kuacha matokeo katika mikono ya Bwana badala ya kuthibitisha ukweli wa ushuhuda wake mwenyewe? (Ona Yakobo 7:14.) Inakusadiaje kujua kuwa si muhimu kwako kuthibitisha ukweli wa ushuhuda wako kwa wale wanaokinza imani yako?

Yakobo 7:15–27Baada ya Sheremu kufanywa kuwa bubu, alitubu dhambi zake, akashuhudia ukweli, kisha akafa, hivyo kuongoza umati wa Wanefi kwake Bwana tenaSoma kauli ifuatayo ya Mzee Robert D. Hales:“Kupitia miaka, tunajifunza kuwa changamoto kwa imani yetu si mpya, na si rahisi kuwa itapotea hivi karibuni. Lakini wafuasi halisi wa Kristo wanaona nafasi katika upinzani. . . .“. . . Kwa bahati njema, Bwana anajua mioyo ya wanaotutuhumu na jinsi tunavyoweza kuwajibu kikamilifu. Kama wafuasi wa kweli wakitafuta mwongozo wa Roho, wanapata ari iliyokusudiwa katika kila mkabiliano. Na katika kila mkabiliano, wafuasi wa kweli hujibu ka-tika njia zinazomkaribisha Roho wa Bwana” (“Christian Courage: The Price of Discipleship,” 72–73; italics in original).

Uliza maswali ya kufuatiliaUnapouliza maswali ya kufuatilia, inawapa wanafunzi nafasi ya kueleza kile walicho-jifunza, na kuimarisha kuelewa wao, na kufikiri jinsi kweli za injili zina-vyo husiana na maisha yao. Angalia usikimbilie kupitia orodha ndefu ya maswali ya kufuatilia. Kwa kawaida ni bora ku-uliza maswali machache na kuwapa wanafunzi muda wa kujibu baada ya kufikiria.

Page 186: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

171

yaKobo 7

• Inamaanisha nini “kuona nafasi katika upinzani”? (Wanafunzi wanapojibu swali hili, wasaidie kuelewa kuwa matokeo mema yanaweza kuja tunapojibu changamoto kwa imani yetu kwa njia zinazokaribisha Roho wa Bwana.)

Wagawe wanafunzi katika jozi. Acha kila jozi lisome Yakobo 7:15–23, wakitafuta chochote chema kinachotokea kutoka katika makabiliano ya Yakobo na Sheremu. Baada ya wanafu-nzi kumaliza kusoma, alika wachache kati yao kueleza walichopata. Fikiria kutumia baadhi ya maswali yafuatayo kuwasaidia wanafunzi kuchanganua aya hizi:• Unaona ushahidi gani kwamba Yakobo alitumaini kwamba makabiliano yake na She-

remu yangesaidia wengine? (Ona Yakobo 7:22. Wasaidie wanafunzi kuona kuwa Yakobo alikuwa ameombea mkusanyiko wa Wanefi walioshuhudia kukiri na kufa kwa Sheremu.)

• Kulingana na Yakobo 7:23, makabiliano ya Yakobo na Sheremu yaliathiri vipi mkusanyiko? • Ni kweli zipi tunazoweza kujifunza kutokana na makabiliano ya Yakobo na Sheremu?

(Wanafunzi wanaweza kutambua majibu mengi kwa swali hili. Wengine wanaweza kupendekeza kanuni zilizoorodheshwa hapa chini.)

Manabii wote hushuhudia kuhusu Yesu Kristo.

Tunapojibu maswali au ukosoaji wa imani yetu kwa njia zinazomkaribisha Roho Mtakatifu, tunaweza kuwasaidia wengine kumgeukia Bwana.

Manabii hutusaidia kutambua na kushinda uongo wa Shetani.

Wale wanaoasi dhidi ya Mungu na kuhubiri dhidi ya ukweli watapata adhabu kali kutoka kwa Bwana.

Kupekua maandiko kunatusaidia kuepukana na kudanganywa.Waulize wanafunzi kutambua kanuni kama hizo zilizoorodheshwa hapo juu, fikiria kuwau-liza maswali ya kufuatilia ili kuwasaidia kutumia kanuni hizi katika maisha yao.• Kuishi kulingana na kanuni hii kutakusaidia vipi?• Kujua kanuni hii kunaweza kukusaidia vipi kuwasaidia wengine?• Unawezaje kutafuta kutumia kanuni hii maishani mwako?Waalike wanafunzi kujibu maswali yafuatayo katika shajara zao za kujifunza maandiko:• Ni kitu gani utakachoanza kufanya (au kuendelea kufanya) ili kikusaidie kujitayarisha

kwa wakati mtu anapokinza imani yako?Shiriki ushuhuda wako kwamba tunaweza kufaulu kushinda changamoto kwa imani yetu tunapofuata mfano wa Yakobo wa kumtegemea Bwana.

Marejeo ya YakoboChukua wakati kuwasaidia wanafunzi kufanya marejeo ya kitabu cha Yakobo. Waulize kile walichojifunza kutoka katika kitabu hiki katika seminari na pia katika masomo yao binafsi ya maandiko. Ikihitajika, waalike kupitia milango saba ya Yakobo ili kuwasaidia kukumbuka. Waulize kutayarisha kitu cha kushiriki kuhusu Yakobo au maandishi yake ambacho kimewa-furahisha. Unaweza kutaka kuwakumbusha kuwa Yakobo alizaliwa katika nyika ya nchi ya Bountiful (karibu na Bahari ya Shamu) na akafa katika nchi ya Nefi. Pia alibarikiwa na Lehi (ona 2 Nefi 2:1–4), na alimwona Mwokozi (ona 2 Nefi 11:3). Ndugu yake mkubwa alijumu-isha baadhi ya mahubiri yake katika mabamba madogo (ona 2 Nefi 6–10). Baada ya muda wa kutosha, waalike wanafunzi kadha kushiriki mawazo na hisia zao. Fikiria kushiriki ushu-huda wako kuhusu jinsi mfano wa Yakobo na mafundisho yake vimebariki maisha yako.

Page 187: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

172

Kwa nini kujifunza kitabu hiki?Kitabu cha Enoshi kinadhihirisha nguvu za Upatanisho wa Yesu Kristo kutakasa watu kutokana na dhambi na kuwafanya wa-zima. Enoshi alipiga mweleka wa maombi ya nguvu mbele za Mungu kabla dhambi zake kusamehewa. Kisha akaombea wema wa kiroho wa Wanefi na Walamani na akatumia salio la maisha yake akitumi-kia wokovu wao. Wanafunzi wanaposoma Kitabu cha Enoshi, wanaweza kugundua masomo muhimu kuhusu maombi, toba na ufunuo. Wanaweza pia kujifunza kuwa kama watu binafsi wanapopokea Upa-tanisho, watakuwa na hamu ya kushiriki baraka hizo na wengine.

Nani alikiandika kitabu hiki?Enoshi mwana wa Yakobo na Mjukuu wake Lehi na Saria, alikiandika Kitabu hiki. Enoshi alirekodi kuwa baba yake alimfundisha “katika malezi na maonyo ya Bwana” (Enoshi 1:1). Karibu mwishoni mwa maisha yake, Enoshi aliandika kuwa alikuwa ametangaza “ukweli ulio katika Kristo” siku zote za maisha yake (Enoshi 1:26). Kabla ya kifo chake, Enoshi aliyatoa mabamba madogo ya Nefi kwa mwanawe Yaromu (ona Yaromu 1:1). Enoshi alihi-timisha rekodi yake kwa kusema kuwa alishangilia siku ambapo angesimama mbele ya Mkombozi wake. Alitangaza, “kisha nitaona uso wake kwa furaha, na ataniambia: Njoo kwangu, heri wewe, umetayarishiwa mahali katika nyumba za Baba yangu” (Enoshi 1:27).

Kitabu hiki kiliandikiwa nani na kwa nini?Wakati Enoshi alipopokea mabamba madogo kutoka kwa baba yake, aliahidi kuandika tu maandishi aliyofikiri kuwa ya thamani zaidi, ambayo ilijumuisha mafundisho matakatifu, ufunuo na unabii (ona Yakobo 1:1–4; 7:27). Enoshi aliwajua watu wake, Wanefi, hatimaye wangea-ngamizwa. Alimwomba Bwana kuhifadhi rekodi ya Wanefi “ili katika siku za usoni yafunuliwe kwa Walamani, ili, pengine, waokolewe” (Enoshi 1:13).

Kiliandikwa lini na wapi?Enoshi alifunga rekodi yake kwa kuta-ngaza kuwa miaka 179 ilikuwa imepita tangu Lehi kuondoka Yerusalemu (ona Enoshi 1:25). Hiyo inaweka tarehe ya maandishi yake ikikadiriwa kuwa kati ya 544 K.K (wakati Yakobo alipofunga rekodi yake) na 421 K.K Enoshi aliandika rekodi hii akiishi katika nchi ya Nefi.

Ni zipi baadhi ya sifa bainifu za kitabu hiki?Kitabu cha Enoshi kinatanguliza mpangilio unaoonyesha jinsi watu binafsi wanavyo-weza kupokea baraka za Upatanisho wa Yesu Kristo na kushiriki baraka hizo na wengine. Kwanza, Enoshi alifundishwa injili ya Yesu Kristo (ona Enoshi 1:1, 3). Kisha, alitambua haja yake ya Mwokozi na kuomba msamaha (ona Enoshi 1:2–4). Kisha, baada ya kupokea ondoleo la dha-mbi yake, aliomba na kufanya kazi kwa bidii kuwaleta wengine katika wokovu.

(ona Enoshi 1:5–27). Mpangilio huu unao-nekana kote katika Kitabu cha Mormoni. Mifano inajumuisha Alma (ona Mosia 17:1–2; 18:1–2), Alma Mdogo na wana wa Mosia (ona Mosia 27–28), na Lamoni na watu wake (ona Alma 18–19).Kwa ziada, kitabu cha Enoshi ni cha kwanza kueleza kwa kina hali ya uasi wa uzao wa Lamani na Lemueli (ona Enoshi 1:20). Kinataja kuwa “kulikuwa na mana-bii wengi sana” miongoni mwa Wanefi, ingawa wengi wa Wanefi walikuwa “shi-ngo ngumu” ambao walihitaji kila mara kuchochewa “ili wamwogope Bwana” (Enoshi 1:22–23).

MuhtasariEnoshi 1:1–8 Enoshi anaomba ondoleo la dhambi na kupokea msamaha kwa sababu ya imani yake katika Yesu Kristo.

Enoshi 1:9–18 Enoshi aombea Wanefi na Walamani na anamwo-mba Bwana kuhifadhi kumbuku-mbu za Wanefi.

Enoshi 1:19–24 Enoshi anaeleza kuhusu uovu wa Walamani na hali ya shingo ngumu ya Wanefi. Yeye na manabii wengine wanae-ndelea kutumikia wokovu wao.

Enoshi 1:25–27 Enoshi anahitimi-sha kumbukumbu yake na kua-ndika kuhusu hakikisho la uzima wa milele alilopokea kupitia kwa Mkombozi wake.

UtangUlizi KWa

Kitabu cha enoshi

Page 188: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

173

SOMO LA 49

enoshi

Mapendekezo ya Kufundisha

Enoshi 1:1–8Baada ya kutafakari maneno ya baba yake, Enoshi aliomba kupokea ondoleo la dhambi zakeAndika nafsi yangu ilipata njaa ubaoni. Waalike wanafunzi kufikiria wakati ambapo walihisi njaa sana.• Ni nini baadhi ya maneno ambayo ungetumia kueleza hisia zako ukiwa na njaa? (Wana-

funzi wanaweza kueleza njaa kama utupu, uchungu, udhaifu, haja ya kujazwa)• Mtu anaweza kumaanisha nini kwa kishazi “nafsi yangu ilipata njaa?” (Hisia za utupu,

uchungu, au udhaifu na haja ya kujazwa kiroho.)Waalike wanafunzi kufikiria wakati ambapo nafsi zao zimepata njaa. Eleza kuwa hivi leo, watajifunza uzoefu wa mtu ambaye nafsi yake ilipata njaa. Onyesha picha ya Enoshi akio-mba (62604; Gospel Art Book [2009], no. 72).• Unafahamu nini kuhusu mtu aliye katika picha? (Kama wanafunzi hawana hakika, eleza

kuwa hii ni picha ya Enoshi, ambaye alikuwa mjukuu wa Lehi na Saria na mwana wa Yakobo. Alikabidhiwa mabamba madogo muda mfupi kabla ya kifo cha Baba yake [ona Yakobo 7:27].)

Alika mwanafunzi kusoma Enoshi 1:1, 3 kwa sauti. Uliza darasa kutafuta jinsi Ya-kobo alivyokuwa amemwathiri Enoshi. Waalike wanafunzi wachache kuliambia darasa walichopata.Onyesha chati ifuatayo ubaoni. (Ili kuokoa wakati, unaweza kuweka chati ubaoni kabla ya darasa.) Chati imetengenezwa kuwasaidia vikundi vya wanafunzi kuzingatia maelezo kamili ya uzoefu wa Enoshi wanapojifunza Enoshi 1:2–8.

Kile enoshi alitamani Kile enoshi alifanya Matokeo ya kile enoshi alifanya

enoshi 1:2enoshi 1:3

enoshi 1:2enoshi 1:4enoshi 1:8

enoshi 1:5enoshi 1:6enoshi 1:8

Eleza kuwa Enoshi alifikiri kuhusu mafunzo ya baba yake na uzoefu wa kiroho uliomwo-ngoza kufanya vitu fulani ambavyo baadaye vilizaa matokeo fulani maishani mwake.Gawanya darasa katika vikundi vitatu. Someni Enoshi 1:2–8 kwa sauti. Mnaposoma, acha kikundi kimoja kutafuta vishazi vinavyoonyesha hamu ya Enoshi. Alika kikundi cha pili kutafuta kile Enoshi alifanya. Uliza kikundi cha tatu kutafuta matokeo ya hamu na mate-ndo ya Enoshi. (Eleza kuwa aya zilizoorodheshwa katika chati zina habari zinazohusiana na kazi ya kila kikundi.)Baada ya kukamilisha kusoma Enoshi 1:2–8, alika wanafunzi katika kikundi cha kwanza kuripoti vishazi walivyopata kuhusiana na hamu ya Enoshi. Waulize wanafunzi kutaja vishazi hivi, acha waviandike ubaoni. Unaweza kutaka wanafunzi kuweka alama katika

Kutafuta maelezo katika maandishi marefu ya maandiko Baadhi ya wanafunzi wanahisi kushindwa wanapoulizwa kutafuta maelezo mengi katika maandishi marefu ya maandiko. Ili kuwasaidia wanafunzi hawa, gawa-nya darasa katika viku-ndi kadha. Ongoza kila kikundi kutafuta elezo tofauti katika maandishi marefu. Hii inaweza kuwasaidia wanafunzi kuzingatia vidokezo muhimu wanaposoma. Pia inawapa nafasi ya kufundishana maelezo muhimu wanayogundua katika maandiko.

UtanguliziBaada ya kutafakari maneno ya baba yake, Enoshi alio-mba kupokea ondoleo la dhambi zake. Kisha akaombea

wema wa kiroho wa Wanefi na Walamani na kutumia maisha yake kutumikia wokovu wao.

Page 189: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

174

SoMo la 49

vishazi hivi katika maandiko yao. Wanafunzi wanaweza kutaja vipengele kama vile “ondo-leo la dhambi zangu,” "uzima wa milele” na “furaha ya Watakatifu.”Baada ya safu ya kwanza kujazwa, alika darasa kupitia haraka mwanzo wa Enoshi 1:4. Wafanye kutambua uzoefu ambao Enoshi alipata kama vile maneno ya baba yake “kuhusu uzima wa milele na shangwe ya watakatifu yalipenya ndani ya moyo [wake]” (Enoshi 1:3). Wanafunzi wanapaswa kuona kishazi “na nafsi yangu ilipata njaa.” (Unaweza kutaka kuwahimiza wanafunzi kuweka alama katika kishazi hiki katika maandiko yao.)• Je, kutafakari mafunzo ya nabii kuhusu uzima wa milele na shangwe ya watakatifu ku-

naweza vipi kusababisha nafsi ya mtu kupata njaa? (Inaweza kumsaidia mtu kutamani kuwa wa kustahili kuwa na Bwana na kutamani furaha inayotokana na kuishi injili.)

Eleza kuwa Enoshi pia alitamani ondoleo la dhambi zake. Eleza kuwa kishazi “nafsi yangu ilipata njaa” inaweza kuonyesha utupu wa kiroho unaotokana na dhambi. Inaweza pia kuonyesha haja ya mtu kusogea karibu na Bwana na kujifunza kutoka Kwake.• Kwa nini dhambi hutufanya kuhisi utupu kiroho? (Dhambi husababisha Roho Mtakatifu

kuondoka na tunahisi kuwa mbali na Bwana.)Ili kusidia wanafunzi kujihusisha na uzoefu wa Enoshi, waulize kufikiri kimya ikiwa wana baadhi ya hisia za njaa ya kiroho ambazo Enoshi alieleza. Ili kusaidia darasa kuona kile Enoshi alifanya kushibisha njaa yake ya kiroho, waalike wanafunzi katika kikundi cha pili kuripoti walichopata na kurekodi majibu yao ubaoni. Majibu yanapaswa kujumuisha yafuatayo: Mweleka ... mbele ya Mungu “kumlilia katika sala kuu,” na “Kutumia imani katika Kristo”• Kishazi “mweleka. . . mbele ya Mungu” kinawezaje kueleza juhudi za mtu kupokea

ondoleo la dhambi? (Eleza kuwa Enoshi hapigani mweleka na Mungu, bali mbele ya Mungu katika maombi. Huku kupigana mweleka kunaonyesha juhudi za Enoshi ku-mwonyesha Baba wa Mbinguni ukweli wa haja yake na hiari yake kutubu kwa kufanya mabadiliko yaliyohitajika maishani mwake.) Kwa nini mweleka ni neno zuri la kueleza juhudi zetu za kutubu?

• Katika Enoshi 1:4, ni ushahidi gani unaona kuwa Enoshi alikuwa mkweli alipotafuta ondoleo la dhambi zake? (Unaweza kuhitaji kuwasaidia wanafunzi kuelewa kuwa kusihi kunamaanisha kuuliza kwa unyenyekevu na hamu kubwa.)

• Ni kwa njia gani tunaweza kuonyesha ukweli tunapotafuta msamaha wa Bwana? (Unaweza kueleza kuwa maombi yetu hayahitaji kuwa marefu kama ya Enoshi, lakini yanahitaji kuwa ya kweli.)

Ili kusaidia darasa kuona matokeo ya kile Enoshi alifanya, waalike wanafunzi katika kikundi cha tatu kuripoti walichopata na kurekodi ubaoni. Majibu yanafaa kujumuisha yafuatayo “ Dhambi zako zimesamehewa,” “hatia yako umetupiliwa mbali,” na "imani yako imekufanya mkamilifu.” (Unaweza kutaka kueleza kuwa kufanywa kuwa mkamilifu kunamaanisha kuponywa au kutakaswa.)• Kulingana na Enoshi 1:7–8, ni nini kilichomwezesha Enoshi kusamehewa na kuwa mka-

milifu? (Imani Yake Katika Yesu Kristo.)• Ni masomo yapi tunayoweza kujifunza kutoka kwa Enoshi kuhusu njia ya kupokea

msamaha wa dhambi zetu? (Zaidi ya kweli zingine ambazo wanafunzi wanaweza kutaja, hakikisha kuwa wanaelewa kuwa tunapofanya imani katika Yesu Kristo, dhambi zetu husamehewa na tunaweza kufanywa wakamilifu.) Kwa nini kutumia imani katika Yesu Kristo ni muhimu kwetu ili kupata baraka hizi? (Yesu Kristo alipatanisha kwa ajili ya dhambi zetu. Ni kwa kupitia tu katika upatanisho wake ndipo tunapoweza kuwa wazima.)

• Kulingana na Enoshi 1:5–6, Enoshi alijuaje kuwa alikuwa amesamehewa? (Unaweza kutaka kuonyesha kuwa sauti iliyotajwa katika Enoshi 1:5 ilikuwa sauti iliyokuja kwenye akili ya Enoshi [Ona Enoshi 1:10].)

• Unaweza kujuaje kuwa umesamehewa dhambi zako?Kama sehemu ya majadiliano ya swali la mwisho hapo juu, soma taarifa ifuatayo ya Rais Dieter F. Uchtdorf wa Urais wa Kwanza:“Tukiisha tubu kwa kweli, Kristo atachukua mzigo wa hatia ya dhambi zetu. Tunaweza kufahamu sisi wenyewe kuwa tumesamehewa na kufanywa kuwa wasafi. Roho Mtakatifu

Page 190: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

175

enoShi

atatuhakikishia; Yeye ndiye Mtakasaji. Hakuna ushuhuda mwingine unaoweza kuwa mkuu” (”Point of Safe Return,” Ensign au Liahona, Mei 2007, 101).• Kwa nini inasaidia kujua kuwa Kristo atachukua mzigo wa hatia ya dhambi zetu baada

ya sisi kutubu kweli?Uliza wanafunzi kutafakari kwa kimya maswali yafuatayo:• Ni wakati gani ulipohisi kuwa Bwana amekusamehe dhambi zako?• Je, Ulifanya imani vipi katika Upatanisho wa Yesu Kristo?• Ulijuaje kuwa ulisamehewa?• Je! Umehisi msamaha wa Bwana hivi karibuni?Shuhudia kuwa tutasamehewa tukiwa na imani katika Yesu Kristo na kutubu kabisa dhambi zetu. Kwa sababu ya Mwokozi, hatia yetu inaweza kufagiliwa na sisi tunaweza kufanywa wakamilifu.

Enoshi 1:9–27Enoshi anaomba kwa ajili ya wema wa kiroho wa Wanefi na Walamani na anafa-nya kazi kwa bidii kwa ajili ya wokovu waoChora mchoro ufatao ubaoni. Eleza kwamba baada ya Enoshi kujiombea, alipanua maombi yake kujumuisha maombi kwa ajili ya wema wa wengine. Waagize wanafunzi kufanya kazi katika jozi. Waalike wanafunzi katika kila jozi kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka kwa Enoshi 1:9–14. Waulize kutambua vikundi viwili vya watu ambao Enoshi aliwaombea na nini alichowaombea katika kila kisa hiki. Wanafunzi wanaporipoti walichojifunza, ongeza maneno Wanefi na Walamani katika mahali penye alama za swali katika mchoro.

• Kulingana na Enoshi 1:14, ni nini yalikuwa makusudi ya Walamani kuhusu Wanefi?• Tunaweza kujifunza nini kuhusu Enoshi kutoka kwa maombi yake kwa Walamani?Soma kauli ifuatayo kutoka kwa Rais Howard W. Hunter. Waulize wanafunzi kusikiliza jinsi inavyohusiana na uzoefu wa Enoshi.“ Wakati wowote tunapopata uzoefu wa baraka za Upatanisho maishani mwetu, hatuwezi kusaidia tu bali kujali wema wa ndugu zetu. . . .“Dalili kubwa ya mabadiliko ya kibinafsi ni hamu ya kushiriki injili na wengine.” (The Teachings of Howard W. Hunter, ed. Clyde J. Williams [1997],• Tamko hili linahusiana vipi na uzoefu wa Enoshi? (Enoshi alionyesha kwamba tuna-

popata uzoefu wa baraka za Upatanisho wa Yesu Kristo, tutatafuta kuwasaidia wengine kupokea wokovu. Unaweza kutaka kuwahimiza wanafunzi kuandika kanuni hii katika maandiko yao.)

Waulize wanafunzi wasome Enoshi 1:12, 15–20 kimya kimya, wakitafuta kile ambacho Enoshi alidhihirisha kuhusu uhusiano kati ya maombi, imani na bidii.• Unafikiri inamaanisha nini kuomba kwa imani?• Kulingana na Enoshi 1:12, 19–20, Enoshi alionyeshaje bidii wakati wa maombi na baadaye?• Tunaweza kujifunza nini kutokana na mfano wa Enoshi? (Wanafunzi wanapaswa ku-

weza kuona kuwa Bwana hujibu maombi yetu kulingana na imani na bidii yetu. )Ili kusaidia wanafunzi kufikiria njia ambazo wanaweza kufuata mfano wa Enoshi, andika taarifa zifuatazo katika ubao au wape kitini. Waalike wanafunzi kuchagua taarifa na kua-ndika katika shajara zao za kujifunza maandiko.

nafsi

??

Page 191: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

176

SoMo la 49

1. Kama vile Enoshi, nina hamu ya kupokea ondoleo la dhambi zangu. Nitamwonyesha Bwana kuwa ni mwaminifu katika hamu hii kwa ... 

2. Kama vile Enoshi, nina hamu ya kuwasaidia wanafamilia yangu kuja kwa Kristo. Mtu mmoja ambaye ninatafuta kumsaidia ni . . . Nitatafuta kumsaidia mtu huyu kwa . . .

3. Enoshi aliwaombea Walamani, ambao walifikiriwa kuwa maadui zake. Kama vile Enoshi, ninataka kuonyesha upendo wa Bwana kwa wale wasio wapole kwangu. Njia moja nitakavyo-fanya hivi ni . . .

Baada ya wanafunzi kumaliza kuandika, acha mwanafunzi asome Enoshi 1:26–27. Alika darasa kutafuta ushahidi wa shangwe ambayo Enoshi alipata uzoefu wake kwa sababu ya bidii yake. Baada ya wanafunzi kuripoti walichopata, watie moyo kutimiza kile walicho-andika katika shajara zao za kujifunza maandiko. Shuhudia kwamba tunapofanya imani katika Yesu Kristo, tunaweza kupata msamaha na shangwe, na hamu yetu ya kuwasidia wengine kuja kwa Kristo itaongezeka.

Page 192: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

177

UtangUlizi Wa Kitabu cha yaromuKwa nini kujifunza kitabu hiki?Wanafunzi wanapojifunza kitabu cha Ya-romu, wataona kwamba Mungu huweka ahadi zake kwa wale wanaotii amri Zake. Pia watajifunza kuhusu juhudi za wafalme, manabii, waalimu, na makuhani Wanefi wa siku za Yaromu za kuwasaidia watu kutubu na kuepukana na maangamizo.

Nani aliandika kitabu hiki?Yaromu mwana wa Enoshi ndiye aliyea-ndika kitabu hiki. Kama baba yake—na kama vile babu yake Yakobo na babu yake mkuu Lehi—Yaromu alikuwa na roho wa unabii na ufunuo (ona Yaromu 1:2). Alipo-maliza kumbukumbu yake, alimkabithi mabamba mwanawe Omni.

Kitabu hiki aliandikiwa nani na kwa nini?Yaromu alisema kwamba aliandika “ku-lingana na amri ya Enoshi, baba [yake] kwamba nasaba [yao] iweze kuwekwa” (Yaromu 1:1). Yeye pia alisema kwamba kumbukumbu yake “iliandikwa kwa . . . faida ya ndugu [Zake] Walamani” (Yaromu 1:2; ona pia Enoshi 1:13–18). Yaromu hakuandika kumbukumbu ya unabii na ufunuo wake mwenyewe, kwa sababu aliamini zile kumbukumbu zilizoandikwa na Baba yake zilifunua “mpango wa

wokovu uliofunuliwa” unatosha. (Yaromu 1:2). Badala yake, alielezea kuhusu kazi za viongozi wa Kinefi wakati wa huduma yake. Viongozi hawa “walikuwa watu wenye nguvu katika imani ya Bwana” Yaromu 1:7 ambao daima waliwasihi watu kutubu na kutii amri (ona Yaromu 1:3–5, 10–12). Yaromu alisema kwamba wakati watu wanachagua kufuata ushauri wa viongozi wema, wanafanikiwa na walikuwa wanaweza kujikinga dhidi ya Walamani. Alishuhudia, “Lakini neno la Bwana lilithibitishwa, ambalo aliwazungu-mzia Baba zetu, akisema kwamba: Kadiri mtakavyo tii amri zangu ndivyo mtaka-vyofanikiwa nchini” (Yaromu 1:9; ona pia 1 Nefi 2:19–20).

Kiliandikwa wakati gani na wapi?Kitabu cha Yaromu kinajumuisha miaka 59, kutoka karibu miaka 420 K.K hadi miaka 361 K.K (ona Enoshi 1:25; Yaromu 1:13). Kiliandikwa katika nchi ya Nefi.

Ni zipi baadhi ya sifa bainifu za kitabu hiki?Kitabu cha Yaromu ni kitabu kifupi sana katika Kitabu cha Mormoni. Kinatoa maelezo kuhusu ukuaji wa ustaraabu wa Wanefi, kusema kwamba walikuwa

“wamezaana sana, na kuenea juu ya uso wa nchi” (Yaromu 1:8). Walikuwa pia wamekuwa matajiri sana kwa raslimali na kuwa wenye ujuzi wa kufanya kazi za mbao na chuma, wakijenga majengo, wa-kiunda mashini, na kutengeneza vyombo na silaha (ona Yaromu 1:8).

MuhtasariYaromu 1:1–2 Yaromu anapokea mabamba na kuelezea madhu-muni yake ya kuandika.

Yaromu 1:3–12 Yaromu anaandika kuhusu kutimia kwa ahadi ya Bwana ya kubariki na kuwafa-nikisha Wanefi wakishika amri Zake. Anashuhudia uwezo wa Mwokozi wa kuokoa watu ku-tokana na dhambi hata kabla ya huduma Yake ya duniani, kuwa-wezesha watu “kuamini katika yeye kama vile alivyokuwa tayari akiamini” (Yaromu 1:11).

Yaromu 1:13–15 Yaromu alisema kwamba tukio la vita kati ya Wanefi na Walamani liliandikwa katika mabamba makubwa ya Nefi. Anayakabidhi mabamba madogo kwa mwanawe Omni.

Page 193: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

178

UtangUlizi Wa Kitabu cha omniKwa nini kujifunza kitabu hiki?Kupitia kujifunza kitabu cha Omni kwao, wanafunzi watajifunza kwamba Bwana aliwalinda Wanefi wema na kuwaelekeza hadi nchi ya Zarahemla (ona Omni 1:7, 12–13). Wao pia watajifunza kuhusu ma-kundi mengine —Waamuleki (au watu wa Zarahemla) na Wayaredi —ambao Bwana aliwaongoza hadi nchi ya ahadi.

Ni nani aliandika kitabu hiki?Kitabu cha Omni kiliandikwa na wanaume watano tofauti: Omni, Amaroni, Kemishi, Abinadomu, na Amaleki. Omni alikuwa mwana wa Yaromu na kitukuu cha Lehi na Saria. Alijieleza mwenyewe kama “mtu mwovu”ambaye hakuwa “anashika amri za Bwana” (Omni 1:2). Amaroni (Mwa-nawe Omni) Kemishi (Kakaye Amaroni) na Abinadomu (mwanawe Kemishi) kila mmoja wao aliongeza nyongeza ndogo. Amaleki mwanawe Abinadomu aliandika mengi ya kitabu cha Omni na alikuwa mtu wa mwisho kuandika kwenye mabamba madogo ya Nefi. Alimkabidhi mabamba hayo Mfalme Benyamini.

Kitabu hiki kiliandikwa kwa ajili ya nani na kwa nini?Omni alisema kwamba yeye aliamriwa na Yaromu, baba [yake], kwamba [yeye] anapaswa kuandika ili kuhifadhi nasaba [yao]” (Omni 1:1). Taarifa hii inashawishi kwamba Omni aliandika kwa manufaa ya uzao wake. Waandishi watatu waliofuata

katika kitabu cha Omni hawakujumuisha hadhira fulani au kutaja madhumuni ya kuandika kwao. Lakini mwaliko wa Amaleki kwa watu wote wa “njooni kwa Kristo. . . na mpate wokovu wake” (Omni 1:26) unaonyesha kwamba yeye alikuwa anajali wokovu wa wale ambao wange-soma maneno yake.

Kiliandikwa wakati gani na wapi?Baadhi ya waandishi wa kitabu cha Omni waliandika kati ya miaka 361 K.K na miaka 130 K.K Waandishi wanne wa kwanza waliandika katika nchi ya Nefi. Amaleki aliandika kumbukumbu yake katika nchi ya Zarahemla.

Ni zipi baadhi ya sifa bainifu za kitabu hiki?Kitabu cha Omni ni kitabu cha mwisho cha mabamba madogo ya Nefi. Omni kinatamba kipindi kirefu kuliko kitabu kingine katika mabamba madogo. Katika Kitabu cha Mormoni chote, ni kitabu cha 4 Nephi na Etheri tu vinavyojumuisha kipi-ndi kirefu cha nyakati kuliko kile kilicho-shughulikiwa na Omni.Kitabu cha Omni pia hutoa maelezo ya kina kuhusu utawala wa Mfalme Mosia wa kwanza, ambaye alikuwa baba yake Mfalme Benyamini na babu wa Mfalme Mosia wa pili. Mfalme Mosia wa kwanza aliwaongoza Wanefi wema kutoka nchi

ya Nefi na kuwaunganisha na watu wa Zarahemla (ona Omni 1:12–23). Kitabu cha Omni kinasema kwamba Bwana aliwaongoza watu wa Zarahemla (pia wa-naojulikana kama Waamuleki ) kutoka Ye-rusalemu hadi nchi ya ahadi muda mfupi baada ya Lehi na familia yake kuondoka Yerusalemu (ona Omni 1:15).Omni ndio kitabu cha kwanza katika Kitabu cha Mormoni kutaja Wayaredi. Pia kinataja kwamba baadhi ya Wanefi waliondoka Zarahemla ili kurudi kwenye nchi ya Nefi, kuonyesha dalili ya matukio yaliyosimuliwa katika Mosia 7–24. Hati-maye, kitabu cha Omni humtambulisha Mfalme Benyamini na kuelezea ni kwa nini Amaleki alimkabidhi yeye kumbuku-mbu takatifu (ona Omni 1:25).

MuhtasariOmni 1:1–3 Omni anaelezea vipindi vya amani na vita kati ya Wanefi na Walamani.

Omni 1:4–11 Amaroni, Kemishi, na Abinadomu wanaandika kwenye mabamba madogo ya Nefi. Wa-kati huu, Wanefi walikuwa katika hali ya uasi.

Omni 1:12–30 Amaleki anaandika matukio muhimu ambayo yalito-kea wakati wa utawala wa Mfalme Mosia na Mfalme Benyamini. Ana-waalika wote kuja kwa Kristo.

Makadirio ya idadi ya Miaka iliyojumuishwa na Kila Kitabu katika Mabamba Madogo.

1 nefi2 nefi

yakoboenoshi

yaromuomni

0 Miaka 50

Miaka 100

Miaka 150

Miaka 200

Miaka 250

Page 194: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

179

UtanguliziVitabu vya Yaromu na Omni vina maandishi ya mwisho katika mabamba madogo ya Nefi. Yaromu anapokea mabamba kutoka kwa Enoshi, baba yake, na akaa-ndika shida na baraka za zaidi ya kipindi cha takriban miaka 60. Kisha akayakabidhi mabamba kwa mwanawe Omni. Kitabu cha Omni kina maandishi ya waweka

kumbukumbu watano tofauti na kinajumuisha takri-bani miaka 230. Amaleki, mwandishi wa mwisho katika kitabu cha Omni, anahitimisha kumbukumbu yake kwa mwaliko wa “njooni kwa Kristo na mtoe nafsi zenu zote kama toleo kwake” (Omni 1:26).

SOMO LA 50

yaromu na omni

Mapendekezo ya Kufundisha

Yaromu 1:1–15Yaromu anaelezea jinsi Wanefi walivyofanikiwa wakati wakishika amri za BwanaSoma taarifa ifuatayo ya Rais Dieter F. Uchtdorf wa Urais wa Kwanza. Kama inawezekana, onyesha picha ya Rais Uchtdorf unaposoma:“Nakumbuka wakati nilipokuwa nikijitayarsiha kufunzwa kuwa rubani wa ndege ya vita. Tulitumia wakati mwingi wa mafunzo yetu tangulizi ya kijeshi kwa mazoezi ya kimwili. Mimi bado sina hakika kabisa kwa nini kukimbia kusiko na mwisho kulichukuliwa kuwa sehemu muhimu ya mayarisho ya kuwa rubani. Hata hivyo, tulikimbia na tukakimbia na tukakimbia sana zaidi.Na nilipokuwa nikikimbia niliona kitu ambacho, hakika, kilinisumbua. Tena na tena nili-kuwa nikipitwa na wanaume ambao walikuwa wanavuta sigara, wanakunywa pombe, na waliokuwa wanafanya mambo yote yaliyo kinyume na injili, na, hasa, Neno la Hekima.“Nakumbuka nikisema, ‘Hebu kidogo! Mimi si ninafaa kuweza kukimbia na nisichoke?’ Lakini mimi nilikuwa nikichoka, na kupitwa na watu ambao bila shaka walikuwa hawafu-atii Neno la Hekima. Nakiri, ilinisumbua mimi wakati huo. Nikajiuliza, hii ahadi ilikuwa ni kweli au si kweli?” (“Continue in Patience,” Ensign au Liahona, May 2010, 58).Waalike wanafunzi kufikiria kama wameshapata kuhisi sawa na hivyo kusumbuka, kushangaa kama au jinsi Bwana angeweza kutimiza ahadi Yake kuwabariki wale wanao-shika amri Zake.Andika neno thibitisha kwenye ubao, na uwaulize wanafunzi kuelezea kile hili neno lina-maanisha (thibitisha au bainisha kwamba kitu ni kweli). Elezea kwamba Yaromu, ambaye alikuwa mwana wa Enoshi, alitumia neno ilithibitishwa alipokuwa akiandika kuhusu ahadi iliyotolewa kwa wahenga wake. Waulize wanafunzi kusoma Yaromu 1:9 kimya, wakitambua ahadi ya Bwana ambayo ilithibitishwa. (Unaweza kupendekeza kwamba wanafunzi watie alama ahadi hii katika maandiko yao.) Hakikisha kwamba wanafunzi wanatambua taarifa hii “Kadiri mtakavyo tii amri zangu ndivyo mtakavyofanikiwa nchini.”Andika marejeo ya maandiko na maswali yafuatayo kwenye ubao. (Ili kuokoa muda, una-weza kuyaandika kwenye ubao kabla ya darasa kuanza.)

yaromu 1:4–5, 8 ni ipi baadhi ya mifano ya jinsi Wanefi walikuwa watiifu na jinsi walibarikiwa?

yaromu 1:7, 10–12

ni vipi viongozi na manabii wanasaidia Wanefi kutii na kufanikiwa?

omni 1:5–7 ni vipi ahadi ya Mungu baadaye ilithibitishwa kwa njia tofauti?

Gawa wanafunzi katika vikundi vitatu. Pangia mojawapo wa marejeo ya maadiko yaliyo kwenye ubao kwa mtu mmoja katika kila kikundi. Acha wanafunzi wasome vifungu vyao vya maadiko walivyopangiwa kimya, wakitafuta majibu ya maswali yanayohusiana na maswali. Kisha toa dakika moja au mbili kwa kila mtu katika kikundi kufanya muhtasari

Onyesha picha za viongozi wa KanisaKuonyesha picha za viongozi wa Kanisa unaposoma maneno yao kutasaidia wanafunzi kujifahamishana na wale ambao Bwana ameita kama manabii, waonaji, na wafunuaji. Pia itao-ngezea hamu ya wanafu-nzi katika maneno yao. Kama unapanga kutumia taarifa kutoka kwa ho-tuba ya mkutano mkuu, fikiria kuyawasilisha ukitumia video ya digitali au faili ya sauti, zinapati-kana katika LDS. org.

Page 195: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

180

SoMo la 50

wa kile yeye amesoma na kujibu swali walilopangiwa. Alika mwanafunzi mmoja au wawili wafanye muhtasari kwa darasa wa ukweli waliojifunza kutokana na kujifundisha na kuja-dili maandiko haya. Wanafunzi wanapotoa majibu yao, hakikisha wamefahamu kwamba tunapotii amri za Mungu, tunafanikiwa.• Kulingana na kile umejifunza kutokana na uzoefu wa Wanefi, ni baadhi ya njia gani

Mungu atawabariki wale wanaotii amri Zake?Ili kuimarisha kanuni hii, kumbusha darasa kuhusu uzoefu wa Rais Uchtdorf wakati alipo-shangaa kama ahadi ya Bwana iliyotolewa katika Neno la Hekima ingethibitishwa. Kisha soma taarifa yake iliyobakia:“Jibu halikuja mara moja. Lakini hatimaye nilijifunza kwamba ahadi za Mungu daima hazitatimizwa mara moja au katika njia tunayotarajia; zinakuja kulingana na wakati Wake na katika njia Yake. Miaka mingi baadaye, nimeweza kuona wazi ushahidi wa baraka za muda ambazo huja kwa wale wanaotii Neno la Hekima— kama ziada kwa baraka za kiroho ambazo huja mara moja kutokana na utiifu wa sheria yoyote ya Mungu. Kutazama nyuma, najua kwa hakika kwamba ahadi za Bwana, daima si ghafula, bali ni hakika daima” (“Continue in Patience,” 58).Waalike wanafunzi kutafakari maswali yafuatayo:• Ni wakati gani Bwana alikubariki, au kukufanikisha, kwa sababu ya kushika amri Zake? Ku-

tokana na uzoefu wako, ni ushuhuda gani unaoweza kuutoa kuhusu Bwana na ahadi Zake?

Omni 1:1–30Waweka kumbukumbu wanasimulia historia ya WanefiKwa ufupi tambulisha kitabu cha Omni kwa kuelezea kwamba kiliandikiwa uzao wa Yaromu na kinajumuisha takribani miaka 230. Waalike wanafunzi kupitia kitabu cha Omni kutambua majina ya watu ambao waliweka mabamba madogo baada ya Yaromu. Ili

kusaidia wanafunzi kupata majina mara moja, fikiria kutoa marejeo ya maandiko: Omni 1:1, 4, 8, 10, 12, 25.Elezea kwamba kitabu cha Omni kinaelezea matukio kadhaa muhimu katika historia ya watu katika Kitabu cha Mormoni. Kinataja watu wa Zarahemla (pia wanaojulikana kama Wamuleki) na Koriatumuri (Myaredi wa Mwisho), na pia kwa muhtasari kinasimulia jinsi Wanefi walivyo hama hadi Zarahemla na kuunganishwa na Wamuleki. Una-weza kuwaelekeza wanafunzi kwenye wendo katika alamisho la Kitabu cha Mormoni (nambari 10458) na uwasaidie kutambua muungano wa Wanefi na Wamuleki. Pia acha wanafunzi watafute palipowekwa alama ya jina Koriantumuri chini ya kichwa “Wayeradi.”Kwenye ubao, chora ramani inayoonyeshwa katika ukurasa huu, lakini usijumuishe mishale. Watie moyo wanafunzi kunakili ramani katika shajara zao za kujifunza maandiko au daftari za darasani.Wakumbushe wanafunzi kwamba katika nyakati za Nefi, Wanefi wa-lijitenga na Walamani na wakafanya makazi mahali ambapo walipaita nchi ya Nefi. Kwenye ramani, chora mshale kutoka nchi ya urithi wa kwanza hadi nchi ya Nefi. Waulize wanafunzi kusoma Omni 1:12–13 kimya kimya na kutambua jinsi Wanefi walianza kuishi katika nchi ya Zarahemla. Wanafunzi wanapoonyesha kile walichopata, chora mshale kutoka nchi ya Nefi hadi nchi ya Zarahemla. Taja kwamba Omni 1:12–13 hufundisha kwamba Bwana hutoa mwongozo wa wema.Mwalike mwanafunzi asome Omni 1:14–19 kwa sauti. Uliza darasa litafute mfanano na tofauti kati ya Wanefi na watu waliowapata katika nchi ya Zarahemla. Waalike wanafunzi wachache kuonyesha kile walichojifunza.Fanya muhtasari wa Omni 1:20–22 kwa kuelezea kwamba watu wa Zarahemla walikutana na Koriantumri, ambaye alikuwa mmoja wa ma-nusura wawili wa taifa la Wayaredi (mwengine alikuwa ni nabii Etheri) Kwenye ramani, onyesha nchi ya Ukiwa, na elezea kwamba hapa ni mahali katika nchi iliyo kaskazini mwa pale “mifupa ya Wayaredi

Zingatia mafundisho na kanuniHali ya mambo kuhusu historia na jiografia ya-naweza kuwa muhimu ili kugundua maktadha wa maandiko unayofundi-sha, masomo yanapa-swa kuzingatia kuhusu kusaidia wanafunzi ku-tambua, kufahamu, na kutumia mafundisho na kanuni za injili. Chunga usipuuze mafundisho ya-liyofunzwa katika Omni kwa kutumia muda mwingi kwenye historia na jiografia.

Muhtasari wa Uhamiaji wa Wanefi

nchi ya Ukiwa

nchi ya zarahemla

nchi ya nefi

nchi ya Urithi wa Kwanza

bahari ya Magharibi

Page 196: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

181

yaRoMU na oMni

ilitawanyika” baada ya wao kuangamizwa (Omni 1:22). Waambie wanafunzi kwamba wa-tajifunza kuhusu Wayaredi wanapojifunza kitabu cha Etheri. Unaweza kutaka kuwahimiza wanafunzi kuandika Wayaredi katika maandiko yao karibu na Omni 1:20–22.Chora mshale ambao unaanzia nchi ya Zarahemla hadi nchi ya Nefi na kisha ugeuze kurudi tena hadi Zarahemla. Chora mshale mwingine kutoka nchi ya Zarahemla ambao unaanzia katika upande mmoja hadi nchi ya Nefi. Waulize wanafunzi kama wanaweza kuelezea kile hii mishale miwili inaashiria. Kama wanahitaji usaidizi, fanya muhtasari Omni 1:27–30 kwa kuelezea kwamba makundi mawili kutoka Zarahemla yalijaribu kurudi hadi nchi ya Nefi. Kundi la kwanza lilishindwa na kurudi Zarahemla. Amaleki alivyofunga kumbukumbu yake, alitaja kwamba hakujua kilichowatokea kundi la pili. Waambie wana-funzi kwamba watajifunza kuhusu hili kundi, watoto wa Zenifu, wanapojifunza kitabu cha Mosia. Unaweza kutaka kuwahimiza wanafunzi kuandika watu wa Zenifu katika maandiko yao karibu na Omni 1:29–30.Elezea kwamba Kitabu cha Mormoni hakidai kuwa kumbukumbu ya watu wote ambao waliishi Amerika ya kale. Licha ya Wayaredi, Wamuleki, na kundi la Lehi, kuna uwezekano makundi mengine ya watu ambao walikuja kwenye bara Amerika.Elezea kwamba Amaleki alipokamilisha kumbukumbu yake, aliandika mwaliko muhimu kwa wale ambao watasoma maneno yake. Waulize wanafunzi kusoma mwaliko wa Ama-leki katika Omni 1:25–26 kimya, wakitafuta wazo ambalo alirudia mara tatu. (Unaweza kutaka kuwahimiza wanafunzi kuweka alama kile wanachopata.)• Inamaanisha nini kwako kuja kwa Kristo?Taja kwamba kama sehemu ya mwaliko wa Amaleki wa kuja kwa Kristo, alitushauri sisi kufanya vitu mahususi. Andika yafuatayo kwenye ubao:

Njooni kwa Kristo na . . .Acha wanafunzi warejee tena kwenye Omni 1:25–26. Waalike baadhi yao kukamilisha sentensi kwenye ubao wakitumia vishazi kutoka katika mistari hii.• Kulingana na Omni 1:26, sisi tutabarikiwa vipi kwa kufanya mambo haya? (Wasaidie

wanafunzi kufahamu kwamba kama tunamwendea Kristo na kuvumilia hadi mwi-sho, tutaokolewa. Unaweza kutaka kuandika kanuni hii kwenye ubao.)

Waulize wanafunzi kuchagua kimoja kati ya vishazi vilivyo ubaoni. Waalike wao waandike au wafanye muhtasari katika shajara zao za kujifunza maandiko hotuba fupi wanaweza kutoa katika mkutano wa sakramenti kuhusu jinsi wanaweza kwenda kwa Kristo kwa njia hii. Pendekeza kwamba hotuba zao zinaweza kujumuisha: (1) kusoma Omni 1:25–26 na kuelezea kwa maneno yao wenyewe kishazi walichochagua, (2) kusoma maandiko ya zi-ada ambayo yanafafanua au yanaongeza maana katika kishazi, (3) kushiriki uzoefu husika kutoka kwa maisha yao au kutoka kwa maisha ya watu wanaojua, au (4) kushiriki mawazo, hisia, na ushuhuda wao. (Unaweza kutaka kuandika mapendekezo haya kwenye ubao, wa-patie wao kwenye kitini, au kuyasoma kwa sauti ili wanafunzi waweza kuyaandika katika shajara zao za kujifunza maandiko.)Wapatie wanafunzi dakika sita au saba kutayarisha hotuba zao. Alika wanafunzi kadha kushiriki hotuba zao mbele ya darasa. (Kama hamna muda wa haya, fikiria kuwauliza ba-adhi yao kushiriki hotuba zao hapo mwanzoni wa somo lijalo au kama sehemu ya darasa la ibada wakati ujao. Unaweza pia kuwahimiza wao kushiriki hotuba zao wakati wa jioni ya familia nyumbani au katika mazungumzo na wanafamilia au marafiki.) Ili kuhitimisha, shiriki ushuhuda wako kwamba kama tunaenda kwa Kristo na kuvumilia hadi mwisho, tutaokolewa.

Rejeo la Umahiri wa MaandikoWajulishe wanafunzi vifungu vichache vipya vya umahiri wa maandiko. Ili kufanya hivyo, andika marejeo kadhaa kwenye ubao na uwaulize wanafunzi kutafuta na kusoma vifu-ngu hivi katika maandiko yao. Unaweza pia kuhimiza wanafunzi kuweka alama kwa njia wazi ili waweze kuyapata kwa urahisi. Ili kuwasaidia wanafunzi kukumbuka marejeo na maneno muhimu ya vifungu hivi, fikiria kutumia shughuli ya “Zoezi la Shabaha” katika kiambatisho hapo mwisho wa kitabu hiki cha kiada.Tazama: Unaweza kutaka kutumia shughuli hii katika siku ingine unapokuwa na wakati mwingi.

Page 197: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

182

Somo la Mafunzo ya NyumbaniYakobo 5–Omni (Kitengo cha 10)

Vifaa vya Matayarisho kwa Mwalimu wa Mafunzo ya NyumbaniMuhtasari wa Masomo ya Kila Siku ya Mafu-nzo ya NyumbaniMuhtasari ufuatao wa mafundisho na kanuni wanafunzi wa-lijifunza walipokuwa wakijifunza Yakobo 5–Omni (Kitengo cha 10) haikupangiwa kufunzwa kama sehemu ya somo lako. Somo unalofunza linazingatia tu machache ya haya mafundisho na kanuni. Fuata msukumo wa Roho Mtakatifu unapofikiria mahitaji ya wanafunzi.

Siku ya 1 (Yakobo 5–6)Katika somo lao juu ya istiari ya miti ya mzeituni katika Yakobo 5, wanafunzi walizingatia kanuni kwamba Bwana anatupenda sisi na hufanya kazi kwa wokovu wetu. Wana-funzi waliandika kile walijifunza kutoka Yakobo 5 kuhusu upendo wa Bwana kwao. Katika Yakobo 6, wanafunzi wali-jifunza kwamba tunakuwa na hekima kujitayarisha sasa kwa hukumu kwa kutubu na kupokea neema za Bwana.

Siku ya 2 (Yakobo 7)Wanafunzi walijifunza kukutana kwa Yakobo na Sheremu, mpinga- Kristo. Walijifunza kwamba tunapomtegemea Bwana, tunaweza kushinda changamoto katika imani yetu. Kutokana na mfano wa Yakobo, pia walijifunza kwamba hatuwezi kutetereka katika imani yetu kama shuhuda zetu zina msingi wa ufunuo na uzoefu wa kweli za kiroho. Kama ziada, wanafunzi waliona onyesho la kanuni kwamba kama tutajibu maswali au ukosoaji wa imani yetu katika njia ambazo zinamwalika Roho, tunaweza kuwasaidia wengine kumgeukia Bwana. Wanafunzi waliandika kuhusu jinsi wali-vyotumia kanuni walizotambua katika Yakobo 7:15−23.

Siku ya 3 (Enoshi)Kutoka katika mfano wa Enoshi, wanafunzi walijifunza kwamba tunapofanya imani katika Yesu Kristo, dhambi zetu zinaweza kusamehewa na tunaweza kufanywa upya. Pia walijfunza kwamba tunapopata uzoefu wa baraka za Upatanisho wa Yesu Kristo, tutatafuta kuwabariki wengine kupokea wokovu. Wanafunzi waliandika kuhusu njia moja wanayoweza kutumia hizi kanuni.

Siku ya 4 (Yaromu na Omni)Katika kujifunza kwao kwa Yaromu na Omni, wanafunzi walitambua ukweli ufuatao: Tunapotii amri za Mungu, tuta-fanikiwa. Waliandika jinsi Bwana amewabariki kwa kuweka amri Zake. Wanafunzi pia walijifunza kwa kifupi uhamiaji wa Wanefi hadi nchi ya Zarahemla na kuwafahamu watu wa Zarahemla, Wayaredi, na kikundi cha Wanefi (watu wa Zenifu) ambao walirejea katika nchi ya Wanefi. Wanafunzi wamejifunza kanuni ifuatayo: Kama tutamwendea Kristo na kuvumilia hadi mwisho, tutaokolewa. Walihitimisha somo hili kwa kuandika hotuba ya dakika moja–hadi mbili juu ya mojawapo wa njia Amaleki alituhimiza kuja kwa Kristo.

UtanguliziKatika somo hili, wanafunzi wanakuwa na nafasi ya kufiki-ria upendo wa Bwana kwa kama unavyoonyeshwa katika Yakobo 5. Kama wakati unaruhusu, unaweza pia kupendelea kuwafunza kutoka kwa Yakobo 5 kuhusu nafasi yao kama wa-tumishi wa Bwana. Wanafunzi wataweza kujadili kweli zilizopo katika Yakobo 7 ambazo zinaweza kuwasaidia wakati wengine wanatilia shaka na kukosoa imani yao. Pia watakuwa na nafasi ya kuliambia darasa jinsi walivyotumia kile wamejifunza kutoka kwa kitabu cha Enoshi. Kama ziada, wanafunzi wanaweza kushiriki hotuba walizotayarisha kuhusu jinsi tunaweza kuitika mwaliko uliotolewa katika Omni wa kuja kwa Kristo. Kama ungependa wao kufanya hivyo, inaweza kusaidia kuwasiliana na wanafunzi kadhaa mapema na kuwaalika kujitayarisha kushiriki hotuba zao darasani.

Mapendekezo ya Kufundisha

Yakobo 5–6Yakobo ananukuu istiari ya miti ya mzeituni kuonyesha kwamba Bwana hufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya wokovu wetuWakumbushe wanafunzi kwamba katika istiari ya miti ya mzeituni, matawi kutoka kwa mti wa mzeituni shamba yameta-wanywa kote katika shamba la mzeituni. Hii huashiria kutawa-nyika kwa watu wa agano wa Mungu—washiriki wa nyumba ya Israeli—kote ulimwenguni. Hatimaye, hata hivyo, miti yote ya shamba la mizeituni ikaharibika (ona Yakobo 5:46). Elezea kwamba hii inaashiria kipindi cha Uasi Mkuu.

Page 198: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

183

SoMo la MafUnzo ya nyUMbani

Waalike wanafunzi wasome Yakobo 5:61–62 kimya, wakitafuta kile Bwana alielekeza mtumishi Wake (nabii Wake) kufanya ili kuisaidia miti izae tunda zuri mara ingine tena. Kisha uliza maswali yafuatayo:

• Unadhani hawa “watumishi” inalenga kina nani? (Viongozi wa Kanisa, wamisionari, na waumini wote wa Kanisa.)

• Ni nini cha kipekee kuhusu wakati ambapo watumishi hawa waliitwa kufanya kazi?

Kwa ufupi elezea kwamba juhudi hizi zinaashiria kukusanyika kwa Israeli. Ili kuwasaidia wanafunzi kuona kwamba wao ni sehemu ya kundi la watumishi ambao wameitwa kufanya kazi katika shamba la mizeituni la Bwana, soma taarifa ifuatayo ya Mzee Dean L. Larsen wa wale Sabini. Waulize wanafunzi kusikiliza ni kina nani anaotambua kama “watumishi wa mwisho katika shamba la mizeituni.”

“[Sasa] ndio kipindi ambacho Bwana na watumishi wake wata-fanya juhudi kubwa za mwisho kupeleka ujumbe wa ukweli kwa watu wote wa ulimwenguni na kuwakomboa uzao wa Israeli ya kale ambao wamepoteza utambulisho wao wa kweli. . . .

“Mmekuja ulimwenguni wakati msingi wa kazi hii kuu umewe-kwa. Injili imerejeshwa kwa mara ya mwisho. Kanisa limeanzi-shwa katika karibu kila sehemu ya dunia. Jukwaa limeandaliwa tayari kwa kuchezwa tena. Ninyi mtakuwa wachezaji muhimu. Ninyi ni miongoni mwa watumishi wa mwisho katika shamba la mzeituni . . . Hii ni huduma ambayo kwayo mmeteuliwa” (“A Royal Generation,” Ensign, May 1983, 33).

Uliza maswali yafuatayo:

• Mzee Larsen alisema ni kina nani ndio watumishi, au “watu-mishi wa mwisho,” walioitwa katika shamba la mzeituni.

• Ni nafasi gani ulizonazo za kumtumikia Bwana na kuwasaidia wengine kuzaa “tunda zuri”?

Darasa, linaposoma Yakobo 5:71 kwa sauti. Waalike wanafunzi kutambua kile Bwana ameahidi wale wanaotumika pamoja na Yeye. Waulize wanafunzi ni wakati gani wao walihisi kubarikiwa kwa juhudi zao za kumtumikia Bwana.

Yakobo 7Yakobo humtegemea Bwana anapokabiliana na Sheremu na kuuongoza umati wa Wanefi kumgeukia BwanaTazama: Katika Yakobo 7 wanafunzi walijifunza kuhusu jinsi Ya-kobo alishinda upinzani kwa imani yake katika Yesu Kristo dhidi ya mtu aliyeitwa Sheremu, mpinga- Kristo. Hali somo hili halizi-ngatii juu ya uzoefu wa Yakobo na Sheremu, unaweza kupe-ndelea kuwaalika wanafunzi kufanya muhtasari wa matukio na kutambua ukweli waliojifunza kutokana na mfano wa Yakobo. Hasa, unaweza kutaka kusisitiza ukweli kwamba hatuwezi ku-tindikiwa imani yetu kama shuhuda zetu zina msingi wa ufunuo na uzoefu wa ukweli wa kiroho.

EnoshiBaada ya kupokea ondoleo la dhambi zake, Enoshi anawaombea wengine na kufanya kazi kwa ajili ya wokovu wao

Chora mchoro huu kwenye ubao au kwenye kipande cha karatasi. Waulize wanafunzi kuelezea jinsi inahusiana na uzoefu wa Enoshi.

Gawa wanafunzi katika vikundi vitatu. (Kama darasa lako ni dogo, kikundi kinaweza kuwa ni mtu mmoja.) Uliza kikundi cha kwanza kusoma Enoshi 1:4–6 na kujitayarisha kuelezea ukweli tunaoweza kujifunza kutokana na maombi ya Enoshi kwa niaba yake mwenyewe. Uliza kikundi cha pili kusoma Enoshi 1:9–10 na kujitayarisha kuelezea ukweli tunaoweza kujifunza kutokana na sehemu ya maombi ya Enoshi. Acha wale walio katika kikundi cha tatu kusoma Enoshi 1:11–14 na kujitayarisha kuelezea ukweli tunaoweza kujifunza kutokana na sehemu ya maombi ya Enoshi. Kisha muulize mshiriki wa kila kikundi kuelezea kile wametayari-sha. Waulize wanafunzi warejelee siku ya 3, kazi ya 9 katika sha-jara zao za kujifunza maandiko, na waalike wachache kuelezea jinsi wamechagua kutumia kweli kutoka kwa kitabu cha Enoshi.

Yaromu na OmniWaweka kumbukumbu wanasimulia masumbuko na baraka za WanefiKama wanafunzi wana maswali kuhusu uhamiaji wa makundi tofauti ya watu hadi nchi za Nusu Mzunguko wa Magharibi, unaweza kutaka kujadili pamoja nao kifaa katika kitabu cha kiada cha mwanafunzi kuhusu Omni 1:1−30, ikijumuisha taarifa ya Rais Anthony W. Ivins wa Urais wa Kwanza.

Waalike wanafunzi kurejea hotuba walizotayarisha kuhusu ku-mwendea Kristo (siku ya 4, kazi ya 4). Kama muda unaruhusu, unaweza kuwauliza wanafunzi kadhaa kuwasilisha hotuba zao darasani. Kama ulikuwa umewauliza wanafunzi mapema kutoa hotuba zao, hakikisha kupeana muda wa kutosha kwao kufanya hivyo.

Hakikisha umewashukuru wanafunzi kwa kushiriki kwao. Shuhudia kuhusu upendo Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo walionao kwa kila mwanafunzi wako, na wahakikishie kwamba wanapomwendea Kristo kwa nafsi zao zote, wataokolewa katika ufalme Wake.

Kitengo kifuatacho (Maneno ya Mormoni–Mosia 6)Katika kitengo kifuatacho, wanafunzi watasoma juu ya malaika wa Mungu akimtokea Mfalme Benyamini, akimwelekeza, na kumwambia kile atakachowaambia watu wake (ona Mosia 3). Mfalme Benyamini alisema maneno haya kwa watu wake, ambao walipata uzoefu wa mabadiliko makubwa katika mioyo yao.

nafsi

??

Page 199: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

184

UtangUlizi Wa Maneno ya MormoniKwa nini kujifunza kitabu hiki?Kupitia kujifunza Maneno ya Mormoni, wanafunzi wanaweza kuongeza imani yao kwamba “Bwana anajua vitu vyote” (Maneno ya Mormoni 1:7) Kama simulizi ya kihistoria, kitabu hiki kinatumika kama daraja kati mabamba madogo ya Nefi (1 Nefi–Omni) na ufupisho wa Mor-moni wa mabamba makubwa ya Nefi (Mosia–4 Nefi). Kinaweza kuwasiadia wanafunzi kufahamu vyema ni kumbuku-mbu gani Mormoni alifupisha alipokuwa akitengeneza Kitabu cha Mormoni. Pia kinawatambulisha wanafunzi juu ya imani na mafanikio ya Mfalme Benyamini.

Ni nani aliandika kitabu hiki?Mormoni ndiye aliandika kitabu hiki. Yeye alikuwa nabii, mweka kumbukumbu, na mhariri na mtunzi wa Kitabu cha Mormoni. Yeye alikuwa pia baba mwema na kiongozi wa kijeshi wa Wanefi. Nabii Moroni alikuwa mwanawe.

Ni kina nani waliandikiwa kitabu hiki na kwa nini?Mormoni alihutubia hadhira ya siku zijazo, kwa matumiani kwamba maandishi yake na maandishi ya mwanawe “yaweze kuwasaidia wao”(Maneno ya Mormoni 1:2). Haswa, aliandika kwa manufaa ya Walamani. Juu yao alisema, “Na sala ya-ngu kwa Mungu ni kuhusu ndugu zangu, kwamba wamfahamu Mungu tena, ndio, ukombozi wa Kristo; ili tena wawe watu wema. ( Maneno ya Mormoni 1:8).

Ni lini na wapi kiliandikwa?Mormoni aliandika kitabu hiki karibu na miaka 385 B.K, baada ya “kushuhudia karibu maangamizo yote ya watu wangu, Wanefi” (Maneno ya Mormoni 1:1). Mor-moni hakuandika pale alipokuwa wakati akiandika kitabu hiki.

Ni zipi baadhi ya sifa za kipekee za kitabu hiki?Kitabu hiki kifupi kinakatiza wendo wa utaratibu wa vitabu hapo mwanzoni mwa Kitabu cha Mormoni. Mormoni aliandika zaidi ya miaka 500 baada ya Amaleki kuhitimisha kitabu cha Omni. Katika kitabu hiki, Mormoni anaelezea kwa ufupi utungaji wake na ufupishaji wa kumbuku-mbu za watu wake. Ili kufahamu maelezo yake, itasaidia kukumbuka kwamba Bwana alimwamuru Nefi kutengeneza seti mbili za mabamba kwa madhumuni “maalumu” na “hekima” (ona 1 Nefi 9:3, 5). Seti moja ya mabamba, kwa kawaida inaitwa mabamba makubwa, ina historia kilimwengu ya Wanefi, hali ile seti ingine, kwa kawaida inaitwa mabamba madogo, ina kumbukumbu takatifu ya mahubiri, ufunuo, na unabii wa Nefi (ona 1 Nefi 9:2–4; Yakobo 1:3–4).Mormoni aligundua mabamba madogo ya Nefi baada ya kuwa tayari alikuwa amefanya ufupisho sehemu ya mabamba makubwa (ona Maneno ya Mormoni 1:3). Akiongozwa na Roho wa Bwana, Mormoni alijumuisha mabamba pamoja na ufupisho wake wa mabamba maku-bwa. Alifanya hivyo “kwa madhumuni ya hekima” kulingana na mapenzi ya Bwana (ona Maneno ya Mormoni 1:4–7).Miaka mingi baadaye, sababu moja ya maongozi haya ikajitokeza. Wakati Joseph Smith alipokuwa ameanza kutafsiri Kitabu cha Mormoni, alianza na ufupisho wa Mormoni wa mabamba makubwa ya Nefi—historia ya kilimwengu. Martin Harris, ambaye alikuwa mwandishi wa Nabii kwa sehemu hii ya tafsiri, kurasa 116 za mswada zilipotea. Bwana alifunua kwa Joseph Smith kwamba watu waovu walikuwa wamechukua hizo kurasa na kubadilisha maneno (ona M&M 10:8–10). Kama Joseph angetafsiri kurasa hizo tena, wale watu wangedai kwamba yeye hakuwa nabii kwa sababu angeweza kutafsiri kitabu hicho kwa njia mbili (ona M&M 10:11–19). Bwana alimwambia Joseph hasitafsiri hiyo sehemu tena bali atafsiri mabamba madogo ya Nefi

kwamba Mormoni alikuwa amejumuisha pamoja na ufupisho wake wa mabamba makubwa (ona M&M 10:30–45). Basi, Maneno ya Mormoni hutusaidia kuona jinsi Bwana alitayarisha njia ya kuzima njama za watu waovu na kujumuisha ma-andiko ambayo hayakuhusika na kipindi hicho cha mswaada uliopotea lakini ulitoa “ufahamu mkubwa wa injili [ya Bwana]” (M&M 10:45). Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alifunza: “Ni wazi kabisa itakuwa ya kufurahisha ikiwa mtu siku moja atapata kurasa 116 zilizopotea za mswada wa asili wa Kitabu cha Mormoni. Lakini chochote kile hizi ku-rasa inajumuisha, hakiwezi kuwa muhimu zaidi au cha msingi zaidi kwa madhumuni ya Kitabu cha Mormoni kuliko mafundi-sho yaliyoandikwa kwenye mabamba madogo” (Christ and the New Covenant: The Messianic Message of the Book of Mormon [1997], 35–36).Kama ziada katika kushiriki umaizi kuhusu utunzi wa kumbukumbu takatifu za watu, Mormoni alitoa maelezo mafupi ya huduma ya Mfalme Benyamini (ona Maneno ya Mormoni 1:10–18). Maelezo haya husaidia kuunganisha mabamba madogo ya Nefi na ufupisho wa Mormoni wa mabamba makubwa. Mfalme Benya-mini anatajwa katika tamati ya kitabu cha Omni, ambacho ni kitabu cha mwisho katika mabamba madogo (ona Omni 1:23–25). Kitabu cha Mosia, kitabu cha kwanza katika kile tulichonacho cha ufupi-sho wa mabamba makubwa, huanza kwa kusimulia mwisho wa enzi na huduma ya Mfalme Benyamini (ona Mosia 1:1, 9).

MuhtasariManeno ya Mormoni 1:1–9 Mormoni anagundua mabamba madogo ya Nefi na kuyajumuisha na ufupisho wake wa mabamba makubwa.

Maneno ya Mormoni 1:10–18 Mor-moni anafanya ufupisho wa enzi ya Mfalme Benyamini.

Page 200: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

185

UtangUlizi Wa Kitabu cha MosiaKwa nini kujifunza kitabu hiki?Katika kujifunza kwao kwa kitabu cha Mosia, wanafunzi watasoma shuhuda za nguvu za huduma ya Yesu Kristo. Pia watajifunza kuhusu watu ambao Bwana aliwakomboa kutokana na kifungo cha dhambi au kutokana na ukandamizaji wa kimwili. Zaidi ya hivyo, wanafunzi wata-jifunza jinsi juhudi za haki za watu kama vile Mfalme Benyamini, Abinadi, na Alma zilileta baraka za ajabu kwa wengine. Kinyume chake, wanafunzi wataona jinsi chaguzi duni za watu kama Zenifu na mwanawe Mfalme Nuhu zilileta matokeo mabaya juu yao na watu wao.

Nani aliandika kitabu hiki?Mormoni alitunga na kufupisha kumbu-kumbu za waandishi kadhaa na kute-ngeneza kitabu cha Mosia. Kitabu hiki kinaitwa Mosia, ambaye alikuwa mwana wa Mfalme Benyamini. Mosia alikuwa nabii, muonaji, mfunuzi, na mfalme aliye-tawala karibu miaka 124 K.K hadi 91 K.K Aliitwa kama babu yake Mosia, ambaye alikuwa pia mfalme wa Zarahemla (ona Omni 1:12–13, 19).Mormoni alichukua idadi fulani ya ku-mbukumbu ili kutunga Kitabu cha Mosia. Alifupisha na kudondoa kutoka kwa kumbukumbu zilizowekwa na Mosia kwe-nye mabamba makubwa ya Nefi, ambayo yalikuwa na maelezo ya historia ya Wanefi katika nchi ya Zarahemla (ona Mosia 1–7; 25–29). Pia alichukua kutoka katika kumbukumbu ya Zenifu, ambayo ilisimulia historia ya watu wa Zenifu kutoka wakati waliondoka Zarahemla mpaka waliporudi (ona Mosia 7–22). Kwa ziada, Mormoni alidondoa kutoka katika sehemu za ufupisho za maandishi ya Alma, ambaye alihifadhi maneno ya Abinadi na kuweka kumbukumbu za watu wake mwenyewe (ona Mosia 17:4; 18; 23–24).

Kitabu hiki kiliandikiwa nani na kwa nini?Mormoni hakulenga kitabu cha Mosia kwa hadhira mahususi au hakutaja kwa nini aliandika kitabu hiki. Hata hivyo, kitabu cha Mosia kinachangia pakubwa kwa madhumuni ya jumla ya Kitabu cha Mormoni—kushuhudia kwamba Yesu

ndiye Kristo na kuyajulisha maagano ya Bwana (ona ukurasa wa kichwa cha Ki-tabu cha Mormoni). Kitabu cha Mormoni hujumuisha mahubiri mawili ya ustadi sana kuhusu huduma ya Yesu Kristo: ma-neno ya Mfalme Benyamini katika Mosia 2–5 na maneno ya Abinadi katika Mosia 12–16. Kwa ziada, kitabu cha Mosia kwa kurudia kimeonyesha umuhimu wa kufanya na kushika maagano na Bwana (ona Mosia 5:5–9; 18:5–10; 21:31–32; 24:13–15; 25:16–18; 26:20).

Ni lini na ni wapi kiliandikwa?Kumbukumbu za asili zilitumika kama vyanzo vya kitabu cha Mosia inawezekana ziliandikwa kati miaka 200 K.K na 91 K.K Mormoni alifupisha kumbukumbu hizo karibu na kati ya miaka 345 B.K na miaka 385 B.K. Mormoni hakuandika pale alipo-kuwa wakati akitunga kitabu hiki.

Ni zipi baadhi ya sifa bainifu za kitabu hiki?Mosia ni kitabu cha kwanza katika Kitabu cha Mormoni ambacho kilifupishwa kutokana na mabamba makubwa ya Nefi. Kinatoa mafundisho kuhusu uwezo wa muonaji (ona Mosia 8:13–18; 28:10–17). Kwa ziada, kitabu cha Mosia ni cha kipekee katika simulizi ya matukio na safari za makundi tofauti ya Wanefi— yale yaliyokuwa katika nchi ya Zarahemla; wale waliotawaliwa na Zenifu, Nuhu, na Limhi katika nchi ya Nefi; na wale ambao walitoroka kutoka nchi ya Nefi pamoja na Alma. Kujifunza zaidi kuhusu makundi haya, unaweza kutaka kurejea maelezo ya jumla ya safari katika Mosia 7–24, yanayo-patikana katika kiambatisho hapo mwisho wa kitabu cha kiada hiki.Kitabu cha Mosia kinaelezea muungano wa watu walioongozwa na Limhi na Alma pamoja na Wanefi katika nchi ya Zara-hemla (ona Mosia 25:1–13). Pia kinatoa maelezo kuhusu usimamizi wa Kanisa la Yesu Kristo kote katika nchi ya Zarahemla (ona Mosia 25:14–24; 26). Hatimaye, kitabu cha Mosia hutoa utangulizi kwa enzi ya waamuzi (ona Mosia 29).

MuhtasariMosia 1–5 Mfalme Benyamini anamteua mwanawe Mosia kama mrithi wake na kuwajibika kuhusu enzi yake. Benyamini anafunza kuhusu Yesu Kristo na hualika watu kuingia katika agano na Mungu.

Mosia 6–8 Mosia anaanza enzi yake. Amoni na wengine 15 wa-natafuta uzao wa watu wa Zenifu katika nchi ya Nefi. Amoni ana-kutana na Mfalme Limhi, mjukuu wa Zenifu, na kujifunza jinsi watu walivyoingizwa utumwani.

Mosia 9–17 Historia ya watu wa Zenifu inatolewa. Baada ya kifo cha Zenifu, mwanawe Nuhu alitawala kwa uovu. Abinadi anashuhudia juu ya Yesu Kristo na kumsihi Mfalme Nuhu na watu wake kutubu. Abinadi auawa kwa moto.

Mosia 18–20 Alma, kuhani wa Mfalme Nuhu, anatubu. Anafu-nza injili na kutoroka pamoja na wafuasi wake hadi nyikani. Wa-nefi katika nchi ya Nefi wanasha-mbulia Walamani na kuwaweka chini ya utumwa. Nuhu anauawa na watu wake na anarithiwa na mwanawe Limhi.

Mosia 21–22 Limhi na watu wake wanatubu. Bwana anawakomboa kutoka utumwani, na Amoni anawaongoza kutoka nchi ya Zarahemla.

Mosia 23–24 Alma na wafu-asi wake wanaanzisha mji wa Helamu. Wanawekwa chini ya utumwa na Walamani na kute-swa na Amuloni na ndugu zake, makuhani wa Nuhu wa hapo awali. Bwana anamkomboa Alma na watu wake na kuwaelekeza hadi nchi ya Zarahemla.

Mosia 25–29 Wanefi wanaungana chini ya utawala wa Mosia, na Alma anasimamia Kanisa. Alma mwana wa Alma (anayejulikana kama Alma Mdogo) na wana wa Mosia wanaongoka. Kabla ya kifo chake, Mosia anaanzisha utawala wa waamuzi.

Page 201: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

186

UtanguliziKitabu kinachoitwa Maneno ya Mormoni kinatumika kama daraja kati ya mabamba madogo ya Nefi na ufupisho wa Mormoni wa mabamba makubwa ya Nefi. Katika kitabu hiki, ambacho Mormoni aliandika karibu miaka 400 baada ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo, Mormoni anaelezea kwamba yeye alitafuta maelekezo kutoka kwa Mungu na kuongozwa na Roho Mtakatifu

kuhusu kile atakachojumuisha katika kumbukumbu yake. Pia alitaja Mfalme Benyamini na kutoa umaizi wa thamani kuhusu kwa nini Mfalme Benyamini alikuwa na ushawishi mkubwa juu ya watu wake. Mosia 1 ina baadhi ya mafundisho ya Mfalme Benyamini kwa wanawe. Aliwafunza kwamba maandiko hutusaidia kumkumbuka Mungu na amri Zake.

SOMO LA 51

Maneno ya Mormoni–Mosia 1

Mapendekezo ya Kufundisha

Maneno ya Mormoni 1:1–11Mormoni anashuhudia kwamba Mungu alihifadhi kumbukumbu kadhaa kwa madhumuni ya hekimaWaulize wanafunzi wafikirie kuhusu wakati Roho alipowasukuma kufanya jambo. Una-weza kutaka wao waandike kuhusu uzoefu huu katika shajara zao za kujifunza maandiko au daftari ya darasani. Kuwasaidia wao kufikiria kuhusu uzoefu wao, unaweza kutaka kushiriki uzoefu mfupi wako mwenyewe. Acha wanafunzi wajue kwamba baadaye katika somo, utauliza maswali machache kushiriki uzoefu wao katika darasa.Elezea wanafunzi kwamba leo watajifunza mfano wa mtu ambaye alifuata msukumo hata kama yeye hakufahamu sababu zote kwa nini alihitaji kufanya hivyo.Acha wanafunzi waende kwenye Maneno ya Mormoni na kupata (hapo chini ya ukurasa au katika muhtasari wa sura) tarehe ya kukisiwa wakati Mormoni aliandika kitabu. Waulize walinganishe tarehe hiyo na tarehe za vitabu vya Omni na Mosia.• Tunajifunza nini kuhusu Maneno ya Mormoni kutoka kwa hizi tarehe?Onyesha picha ya Mormoni Akifupisha Mabamba (62520; Gospel Art Book [2009], no. 73). Alika mwanafunzi asome Maneno ya Mormoni 1:1–2 kwa sauti. Wasaidie wanafunzi kufahamu kwamba Mormoni aliandika kitabu kinachoitwa Maneno ya Mormoni baada ya karibu matukio mengi ya Kitabu cha Mormoni kutokea. Elezea kwamba Maneno ya Mor-moni hutusaidia kufahamu kwamba Kitabu cha Mormoni kilitungwa kutokana na kumbu-kumbu kadhaa. Pia kinaonyesha kwamba ufunuo ndio ulioongoza kazi hii.Ili kuwasaidia wanafunzi kupata twasira ya jinsi Maneno ya Mormoni, mabamba madogo ya Nefi na ufupisho wa Mormoni wa mabamba makubwa ya Nefi yanaingiana pamoja katika Kitabu cha Mormoni, fikiria kuwaonyesha chati ilio na jina “Mabamba na Uhusiano Wake na Kitabu cha Mormoni Iliyochapishwa” katika kiambatisho hapo mwisho wa kitabu cha kiada hiki. Unaweza pia kutayarisha kifaa cha picha mbele ya darasa:Weka vitabu viwili na kipande cha karatasi. Kitabu kinoja kinafaa kuwa na unene mara dufu ya kile kingine. Kwenye mgongo wa kitabu chembamba, tia kibandiko cha karatasi kilichoandikwa Mabamba Madogo ya Nefi. Kwenye mgongo wa kitabu kinene, tia kibandiko cha karatasi kilichoandikwa Ufupisho wa Mormoni wa Mabamba Makubwa ya Nefi. Kwenye kipande cha karatasi, andika Maneno ya Mormoni.Kutumia kifaa cha picha hiki katika darasa, inua kitabu kinachowakilisha ufupisho wa Mormoni wa mabamba makubwa ya Nefi. Elezea kwamba kumbukumbu katika maba-mba makubwa ya Nefi yalikuwa chanzo cha msingi kwa Kitabu cha Mormoni. Kutokana na ufupisho wa Mormoni wa kumbukumbu hii, Joseph Smith alitafsiri vitabu vya Mosia, Alma, 3 Nefi, na 4 Nefi.Waalike wanafunzi kusoma Maneno ya Mormoni 1:3 kimya kimya. Waulize watafute kile Mormoni aligundua baada ya kufanya ufupisho wa sehemu ya mabamba makubwa ya

Page 202: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

187

Maneno ya MoRMoni–MoSia 1

Nefi. Wanafunzi wanapoelezea kile walichopata, wasaidie kuelewa kwamba vishazi “haya mabamba” humaanisha mabamba madogo ya Nefi. Inua juu kitabu kinachowakilisha mabamba madogo ya Nefi. Elezea kwamba kutokana na kumbukumbu hii, Joseph Smith alitafsiri vitabu vya 1 Nefi hadi Omni.Acha wanafunzi wasome Maneno ya Mormoni 1:4–6 ili kujifunza jinsi Mormoni alihisi kuhusu mabamba madogo ya Nefi.• Mormoni alipata nini cha kupendeza katika mabamba madogo ya Nefi?• Mormoni alifanya nini na mabamba madogo ya Nefi?Ili kuonyesha kwamba Mormoni alijumuisha mabamba madogo ya Nefi pamoja na ufupi-sho wa mabamba makubwa ya Nefi, wekelea kitabu chembamba juu ya kitabu kinene.Alika mwanafunzi asome Maneno ya Mormoni 1:7 kwa sauti. Uliza darasa kutafuta sababu ya Mormoni ya kujumuisha mabamba madogo ya Nefi pamoja na ufupisho wa mabamba makubwa ya Nefi.• Kwa nini Mormoni alijumuisha mabamba madogo pamoja na ufupisho wake wa maba-

mba makubwa? (Alifuata msukumo kutoka kwa Roho.) Je! Yeye alielewa sababu zote za kwa nini alifanya hivi?

Wasaidie wanafunzi kuona kwamba Mormoni alielewa sababu kadhaa za kwa nini ma-bamba madogo yangeweza kuwa muhimu. Alitambua thamani yake kuu ya kiroho na alipendezwa na unabii juu ya Yesu Kristo uliokuwepo (ona Maneno ya Mormoni 1:4–6). Haya hivyo, hakujua sababu zote za kwa nini yeye alihitajika kuyajumuisha kama ziada ya sehemu ya mabamba makubwa ambayo yalikuwa historia ya kipindi hicho. (Ili kusoma kuhusu sababu moja ambayo Mormoni hakujua wakati huo, ona utangulizi wa Maneno ya Mormoni katika kitabu cha kiada hiki.)Acha wanafunzi warejee katika Maneno ya Mormoni 1:7 kimya kimya wakitafuta mafundi-sho ambayo Mormoni alijifunza kumhusu Bwana. Hakikisha kwamba wanaelewa kwa-mba Bwana alijua vitu vyote na kwamba Bwana anaweza kutenda kupitia kwetu ili kutimiza mapenzi Yake.• Haya mafundisho yaliweza vipi kumsaidia Mormoni kutenda juu ya msukumo aliopokea?• Hizi kweli zinaweza kukusaidia wewe vipi wakati unapokea msukumo wa Roho?Wahimize wanafunzi kurejelea hali walioandika kuhusu au walifikiria kuhusu hapo mwa-nzoni wa darasa. Waalike wachache wao kuelezea kuhusu misukumo wamepokea, jinsi walitenda juu ya hiyo misukumo, na nini kilitendeka kama matokeo. (Hakikisha kwamba wanaelewa kwamba hawahitaji kuhisi kushurutishwa kushiriki uzoefu ambao ni wa kibi-nafsi sana au kisiri.) Wanafunzi wanaposhiriki uzoefu wao, unaweza kutaka kuuliza baadhi ya maswali yafuatayo:• Je! Ulijua jinsi kila kitu kitakuja kuwa kama ukifuata msukumo huu?• Ni nini kilikupatia azimio na imani ya kutenda juu ya msukumo?Inua juu kitabu kinachowakilisha ufupisho wa Mormoni wa mabamba makubwa, pamoja na kitabu kinachowakilisha mabamba madogo ya Nefi kikiwa juu yake. Kisha inua juu kipande cha karatasi ambacho kinawakilisha Maneno ya Mormoni• Ni wapi kitabu cha Maneno ya Mormoni kinapaswa kuwa katika uhusiano wa hizi

kumbukumbu zingine?Wanafunzi wanapojibu, weka kipande cha karatasi kinachowakilisha Maneno ya Mormoni kati ya hivi vitabu viwili. Elezea kwamba Maneno ya Mormoni huwa kama daraja ambayo inaunganisha mfululizo wa hadithi kati ya mabamba madogo ya Nefi na ufupisho wa Mor-moni wa mabamba makubwa.Alika mwanafunzi asome Maneno ya Mormoni 1:8 kwa sauti. Uliza darasa litafute kile Mormoni alitarajia kingekuwa matokeo ya kufuata msukumo wa kujumuisha mabamba madogo ya Nefi katika mtungo wake wa kumbukumbu.Tia mkazo kwamba maandishi yote wanafunzi wamejifunza kufikia hapa kwa mwaka huu katika Kitabu cha Mormoni (1 Nefi–Omni) yanapatikana kwao kwa sababu Mormoni alifuatia msukumo wa kiroho kujumuisha mabamba madogo.• Utiifu wa Mormoni kwa msukumo wa Roho Mtakatifu umebariki maisha yetu vipi?• Ni baadhi ya mafundisho gani katika 1 Nefi hadi Omni ambayo una shukrani kuwa

nayo? Kwa nini una shukrani kwa sababu ya mafundisho haya?

Page 203: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

188

SoMo la 51

• Fikiria kuhusu upendeleo wa Mormoni wa kufuata msukumo wa kiroho. Upendeleo wetu wa kufuata msukumo wa kiroho huathiri vipi maisha yetu? Upendeleo wetu unaweza vipi kuathiri maisha ya wengine? (Elezea kwamba Bwana anaweza kubariki maisha ya wengine kupitia kwetu tunapofuata msukumo wa Roho Mtakatifu.)

Shuhudia kwamba tunapokuwa waaminifu kwa msukumo wa Roho Mtakafitu, Bwana atatenda “katika [sisi] kulingana na mapenzi Yake” (Maneno ya Mormoni 1:7).

Maneno ya Mormoni 1:12–18 Mfalme Benyamini alianzisha amani katika nchiAndika kutoka mabishano hata amani kwenye ubao. Elezea kwamba Maneno ya Mormoni 1:12–18 utangulizi wa enzi ya Mfalme Benyamini. Mtu mwema huyu alikabiliana na vikwazo vingi wakati wa huduma yake kama nabii na mfalme wa watu. Acha wanafunzi wawe katika jozi na wasome Maneno ya Mormoni 1:12–18 pamoja na wenzi wao. Wau-lize kutambua kile Mfalme Benyamini na manabii wengine walifanya kuanzisha amani katika nchi.Baada ya wanafunzi kuwa na wakati wa kusoma, muulize kila mwanafunzi aandike taarifa katika shajara zao za kujifunza maandiko ambazo zinafanya muhtasari kile Mfalme Benya-mini na watu walifanya ili kuendelea kutoka kwa mabishano hadi amani. Waalike wanafu-nzi wachache kuandika taarifa zao kwenye ubao. Muhtasari wa wanafunzi unaweza kuwa sawa sawa na taarifa zifuatazo:Tunapofuata uongozi wenye maongozi ya kinabii, tunaweza kuanzisha amani.Katika nguvu za Bwana, tunaweza kushinda changamoto. Tumeitwa kufanya kazi kwa uwezo wetu wote kuimarisha amani. Elekeza usikivu wa wanafunzi kwa Maneno ya Mormoni 1:17, ambapo Mormoni anasema kwamba Mfalme Benyamini na “watu wengi watakatifu nchini ile . . . na walinena neno la Mungu kwa nguvu na mamlaka. Elezea kwamba katika masomo machache yafuatayo, wanafunzi watajifunza mahubiri ya Mfalme Benyamini yanayoonyesha mfano wa uwezo na mamlaka ya mafundisho yake.

Mosia 1:1–18Mfalme Benyamini anawafunza wanawe umuhimu wa maandikoWaulize wanafunzi kufikiria kwamba hawakujua lolote kamwe kuhusu maandiko.• Je! Maisha yako yangekuwa namna gani kama kamwe haungekuwa na maandiko?• Je! Ni kweli gani bila hayo zingekuwa ngumu kwako kuishi?Kwa kufupi tambulisha kitabu cha Mosia. Elezea kwamba mwanzo wa kitabu hiki una-onyesha hamu ya Mfalme Benyamini kwa wanawe wa kuendelea kujifunza kutoka kwa maandiko (ona Mosia 1:2). Mfalme Benyamini alipokuwa akiwafunza wanawe, alielezea jinsi maisha yao yangekuwa tofauti kama kamwe hawangekuwa wamepokea maandiko.Alika wanafunzi wachache kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka kwa Mosia 1:3–8. Uliza darasa litafute njia ambazo Wanefi walibarikiwa kwa sababu walikuwa na maandiko. Waulize wanafunzi waelezee kile wamejifunza.• Ni kwa njia gani Mfalme Benyamini aliamini maandiko yangeweza kuwasaidia wanawe?• Mfalme Benyamini alipendekeza nini ndicho uhusiano kati ya kupekua maandiko na

kuweka amri za Mungu? (Ingawa wanafunzi wanaweza kutumia maneno tofauti kuele-zea majibu yao, wanapaswa kutambua ukweli ufuatao: Kupekua maandiko hutusaidia kujua na kushika amri. Unaweza kutaka kupendekeza kwamba wanafunzi waandike ukweli huu katika maandiko yao karibu na Mosia 1:3–8.)

• Ni wakati gani maandiko yalikusaidia kushika amri?Toa ushuhuda wako kwamba maandiko ni ya kweli na kwamba yanaweza kutusaidia katika kushika amri.

Waruhusu wanafunzi kutumia maneno yao wenyeweWanafunzi wanapoo-nyesha mafundisho na kanuni walizopata ka-tika maandiko, usionye-she kwamba majibu yao ni si sawa tu kwa sababu wanatofautiana kwa maneno yaliyotumika katika kitabu cha kiada hiki. Hata hivyo, kama taarifa ya mwanafunzi si sawa kimafundisho, ni jukumu lako kwa upole kumsaidia kurekebisha taarifa hiyo. Kufanya hivyo unaweza kupatia uzoefu muhimu wa kuji-funza huku ukidumisha mazingira ya upendo na kuaminiana.

Page 204: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

189

Maneno ya MoRMoni–MoSia 1

Andika maswali yafuatayo kwenye ubao. (Unaweza kutaka kuyaandika kabla ya darasa kuanza.)

Ni tangazo gani ambalo Mfalme Benyamini alipanga kufanya kuhusu mwanawe Mosia?Ni kitu gani ambacho Mfalme Benyamini alisema kuhusu “jina” kilichokuwa tofauti na watu?Ni kwa nini Wanefi hawakuwa wameangamizwa na Walamani?Ni vyombo gani ambavyo Mfalme Benyamini alimuomba Mosia atunze?

Waulize wanafunzi kuchukua dakika moja na kuona mangapi ya maswali haya wanaweza kupata majibu yake katika Mosia 1:10–18.Baada ya wanafunzi kutoa majibu kwa ufupi kwa maswali haya, onyesha kwamba kwenye masomo machache watajifunza mahubiri ambayo kwayo Mfalme Benyamini aliwapatia watu wake “jina ambalo halitafutwa, ila tu kwa dhambi.” (Mosia 1:12).

Page 205: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

190

UtanguliziMfalme Benyamini alipoelekea mwisho wa maisha yake, alikuwa na hamu ya kutoa mahubiri ya mwisho kwa watu. Mahubiri yake, yaliyoandikwa katika Mosia 2–5, ndio mada ya somo hili na masomo ya 53–55. Hapo mwanzoni wa mahubiri, alisumilia juu ya huduma yake

miongoni mwa watu wake, akisisitiza kwamba tunam-tumikia Mungu tunapowatumikia wengine. Yeye pia alishuhudia juu ya hali ya furaha ya wale ambao wana-shika amri za Mungu.

SOMO LA 52

Mosia 2

Mapendekezo ya KufundishaTazama: Muhtasari ufuatao unaweza kuwa wa msaada kama utachagua kutoa maoni ya jumla kuhusu mahubiri ya Mfalme Benyamini hapo mwanzo wa somo hili.Kuelekea mwisho wa maisha yake, Mfalme Benyamini alihutubia watu wa ufalme wake karibu na hekalu katika Zarahemla. Alitoa uwajibikaji wa utumishi wake kwa watu na kwa dhamiri safi mbele za Mungu, na akamwasilisha Mosia mwanawe kama mfalme mpya wa watu. Katika mahubiri haya ya mwisho, yanayopatikana katika Mosia 2–5, Mfalme Benya-mini alishiriki jumbe juu ya mada kadhaa, ikijumuisha umuhimu wa kuwatumikia we-ngine, deni letu la milele kwa Baba yetu wa Mbinguni, huduma ya Yesu Kristo duniani na Upatanisho, haja ya kuvua mtu kawaida, kuamini katika Mungu kwa ajili ya wokovu, kutoa mali kwa fadhila ya maskini, kupata ondoleo la dhambi, na kuwa wana na mabinti wa Kristo kupitia imani na matendo mema daima. Tazama kwa makini, Mosia 3 ina ujumbe ambao Mfalme Benyamini alipokea kutoka kwa malaika.

Mosia 2:1–9Familia zinakusanyika na kujitayarisha kupokea maneno ya Mfalme BenyaminiAndika maswali yafuatayo kwenye ubao juu: Nani? Wapi? Nini? Kwa nini?Waulize wanafunzi wapekue Mosia 2:1–6 kimya, wakitafuta utondoti ambao utajibu maswali yaliyopo ubaoni. Baada ya wao kusoma, alika wanafunzi kadhaa kuandika ubaoni utondoti mwingi wanavyoweza chini ya kila swali. (Unaweza kuhitaji kuelezea kwamba watu walijitayarisha kupokea maneno ya Mfalme Benyamini kwa kutoa dhabihu zilizozi-ngatia sheria ya Musa. Katika kutoa dhabihu hizi, watu walionyesha shukrani kwa Mungu na kujitolea wenyewe Kwake.)Waalike wanafunzi kusoma Mosia 2:9 kimya, wakitafuta maneno na vishazi ambayo vinao-nyesha kile Mfalme Benyamini alitaka watu kufanya walipokuwa wakisikiliza maneno yake.• Kutoka kwa maneno na vishazi ulivyopata, unafikiria Mfalme Benyamini alihisi vipi

kuhusu ujumbe wake?• Kulingana na sehemu ya mwisho ya Mosia 2:9, Mfalme Benyamini aliamini nini kitato-

kea kama watu watafungua masikio yao na mioyo yao kwa ujumbe wake?• Unafikiria inamaanisha nini kufungua masikio na mioyo yetu kwa wale walioitwa

kufunza?Watie moyo wanafunzi kuuweka mwaliko wa Mfalme Benyamini akilini wanapojifunza ujumbe wake na wanaposikiliza maneno ya manabii wa siku za mwisho.

Mosia 2:10–28Mfalme Benyamini anafunza kuhusu umuhimu wa kumtumikia Mungu na kila mmoja na kuhusu deni letu la milele kwa MunguWaonyeshe wanafunzi picha ya Mfalme Benyamini Akiwahutubia Watu Wake (62298; Go-spel Art Book [2009], no. 74). Wakumbushe wanafunzi kwamba Mfalme Benyamini alikuwa amewaita watu wake kukusanyika ili Mosia mwanawe aweze kuchukua nafasi yake kama

Kutoa maoni ya jumla kwa mahubiri marefuHiki kitabu cha kiada cha somo hutoa uangalifu maalum kwa mahubiri marefu ya kinabii kama vile Mosia 2–5. Mahubiri haya mara nyingi huchu-kua zaidi ya somo moja. Inaweza kuwa vyema kutia maoni ya jumla kwa kifupi juu ya mahu-biri haya. Katika hali ya somo la leo, maoni ya jumla yanaweza kuwa-saidia wanafunzi kupata umaizi wa kina wa madhumuni ya mahubiri ya Mfalme Benyamini na “mabadiliko makuu” ambayo watu wali-pata katika mioyo yao walipokuwa wakisikiliza (ona Mosia 5:2).

Page 206: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

191

MoSia 2

mfalme na kuwapa wao “jina, ili waweze kutofautishwa kutokana na watu wote ambao Bwana Mungu aliwatoa kutoka nchi ya Yerusalemu” (ona Mosia 1:9–12).Soma Mosia 2:10–15 kwa sauti kwa darasa. Waulize wanafunzi kutambua vishazi ambavyo vinaonyesha kujali kuhusu kuwahudumia watu kwa Mfalme Benyamini, siyo kuhusu hadhi yake mwenyewe au kusifiwa. Waalike wainue mikono yao wanaposikia mojawapo wa vishazi hivi. Wanapoinua mikono yao, tua kusoma na uwaulize waelezee kile wametambua na kile kinafunua kuhusu Mfalme Benyamini.Kama sehemu ya majadiliano, shiriki taarifa ifuatayo ya Rais Howard W. Hunter:“Usijali sana kuhusu hadhi. Ni muhimu kutambulikana. Lakini lengo letu linapaswa kuwa wema, siyo sifa; juu ya huduma, siyo hadhi” (“To the Women of the Church,” Ensign, Nov. 1992, 96).Waalike wanafunzi wasome Mosia 2:16–17 kimya na watambue kile Mfalme Benyamini alitaka watu wake wajifunze. Wasaidie kuona kwamba tunapowatumikia wengine, tu-namtumikia Mungu. Andika taarifa hii kwenye ubao. Taja kwamba Mosia 2:17 ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Unaweza kutaka kuwahimiza wanafunzi kuweka alama kifungu hiki kwa njia ya kipekee ili waweze kukipata kwa urahisi.Waalike wanafunzi kufikiria nyakati ambapo wamewahudumia watu wengine.• Ulipowahudumia wengine, ulikuwa pia unamtumikia Mungu vipi?• Watu wengine wamebariki maisha yako vipi kupitia huduma? Walipokuhudumia, wali-

mtumikia Mungu pia kwa jinsi gani?Waalike wanafunzi kadhaa kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka kwa Mosia 2:18–24, 34.• Kwa nini Mfalme Benyamini ajiite na kuwaita watu wake “watumishi wasio wa faida”?

(Unaweza kuhitaji kuelezea kwamba watu hupata faida wanapopokea zaidi kuliko wa-navyotoa. Tunakuwa watumishi wasio wa faida kwa Baba yetu wa Mbinguni kwa sababu thamani ya baraka Yeye anazotupatia daima zitakuwa kuu zaidi ya thamani ya utumishi anapokea kutoka kwetu.)

• Ni baraka gani umeshapokea ambazo kwazo unahisi kuwa na deni na Mungu?• Kwa nini ni muhimu kutambua kwanza sisi “tuna deni milele” kwa Mungu? (Jibu

linaweza kujumuisha kwamba tunapotambua kwamba sisi tuna deni kwa Mungu, shukrani zetu zitaongezeka, tunakuwa na hamu ya kushika amri, na tunataka sana kuwahudumia wengine.)

Elezea kwamba katika Mosia 2:34, neno toa humaanisha kupatiana au wasilisha. Waalike wanafunzi kutafakari juu ya jinsi wanaweza “kutoa kwa [Baba wa Mbinguni] yote yale [wao] waliyonayo na waliyo.” Shuhudia kwamba wakati tunaweka amri za Mungu na kutafuta kutoa huduma ya uaminifu, Yeye hutubariki.

Mosia 2:29–41Mfalme Benyamini anawasihi watu wake kuwa watiifu kwa MunguAndika TAHADHARI kwenye ubao. Waulize wanafunzi kueleza kuhusu nyakati ambazo waliona ishara ambayo ilitumia neno hili au iliwasilisha wazo hili. Taja kwamba maonyo yanaweza kutulinda au kuokoa maisha yetu.Waalike wanafunzi kusoma Mosia 2:32–33, 36–38 kimya kimya, wakitafuta kile Mfalme Benyamini aliwaambia watu wake kujitahadhari nacho. Unaweza kuhitajika kuelezea kwa-mba katika Mosia 2:33, neno ole hulenga huzuni na taabu.• Ni maonyo gani Mfalme Benyamini alitoa kwa watu wake?• Tunaweza kujua vipi kama tumeanza kufuata roho ya ukosaji? Kwa nini ni muhimu

kutambua hili mapema?• Kulingana na Mosia 2:38, ni matokeo gani yatakuja kwa wale wanaokufa katika

dhambi zao?Unaweza kutaka kutilia mkazo mafundisho katika Mosia 2:36 kwamba mtu, kupitia kwa tabia yake mwenyewe, anaweza kujiondoa kutoka kwa Roho wa Bwana. Mzee David A. Bednar wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alinena juu ya umuhimu wa kutambua wakati kuna uwezekano tunajiondoa sisi wenyewe kutoka kwa Roho:

Mosia 2:17 ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Rejea kwenye wazo la kufunza hapo mwisho wa somo na wasaidie wanafunzi na umahiri wao wa kifungu hiki.

Page 207: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

192

SoMo la 52

“Tunapaswa . . . kujitahidi kutambua wakati “tunajitenga wenyewe kutoka kwa Roho wa Bwana, kwamba hana nafasi ndani [yetu] ya kutuongoza [sisi] katika njia za hekima ili [sisi] tupate baraka, mafanikio, na ulinzi’ (Mosia 2:36). . . .“. . . Ikiwa kitu tunachodhania, kuona, kusikia, au kufanya kinatupeleka mbali na Roho Mtakatifu, basi tunapaswa kuacha kufikiria, kuona, kusikia, au kufanya kitu hicho. Ikiwa kwamba kile kinachotarajiwa kuburudisha, kwa mfano, kinatutenganisha na Roho Mtaka-tifu, basi hamna budi kwamba aina hiyo ya burudani siyo njema kwetu. Kwa sababu Roho hawezi kukaa kwenye kile kilicho, kisicho na adabu, kisicho adilifu, au kilicho potovu, basi ni wazi vitu kama hivi siyo vyema kwetu. Kwa sababu tunafarakana na Roho wa Bwana tunapojiingiza katika shughuli tunazojua tunapaswa kuziepuka, basi bila shaka vitu kama hivi si vyema kwetu” (“That We May Always Have His Spirit to Be with Us,” Ensign or Liahona, May 2006, 30).• Mzee Bednar alisema ni nini kitatutenganisha mbali na Roho Mtakatifu?• Tunaweza kujua vipi tunapojitenga mbali wenyewe kutoka kwa Roho Mtakatifu?Andika KUMBUKA na FIKIRIA kwenye ubao karibu na TAHADHARI.Waalike wanafunzi kusoma Mosia 2:40–41 kwa sauti. Waulize wanafunzi kutambua kile Mfalme Benyamini alitaka watu wake wafikirie na kile alitaka wao wakumbuke. Wana-funzi wanapojibu, unaweza kutilia mkazo mafundisho ya Mfalme Benyamini kwa kua-ndika ukweli ufuatao kwenye ubao: Kama tutashika amri, tutabarikiwa kwa vitu vya kimwili na kiroho.• Ni wakati gani ulishuhudia au kupata uzoefu wa furaha ambao huja kutokana na kuwa

mtiifu kwa amri za Bwana?Shuhudia ukweli wa vitu ambavyo wanafunzi wamejadili leo. Hitimisha kwa kuwahimiza wanafunzi kuweka malengo mahususi ya kuwa watiifu zaidi katika sehemu ambazo ni ngumu kwao au wajaribu kuboresha sehemu zilizotajwa katika Maendeleo ya Kibinafsi (kwa wasichana) na Wajibu kwa Mungu (kwa wavulana).

Umahiri wa Maandiko—Mosia 2:17Waalike wanafunzi kusoma Mosia 2:17, Mathayo 22:36–40, na Mathayo 25:40. Vifungu ka-tika Mathayo vinasaidia kufafanua mafundisho, kufungua uelewa, na kubainisha maana ya Mosia 2:17. Unaweza kutaka kuwatia moyo wanafunzi kufanya mfulululizo wa maandiko kwa kuandika Mathayo 22:36–40 karibu na Mosia 2:17, Mathayo 25:40 karibu na Mathayo 22:36–40, na Mosia 2:17 karibu na Mathayo 25:40.Waulize wanafunzi wachache kuelezea kuhusu nyakati wamehisi kuwa wanamtumikia Mungu kwa kuwatumikia watu wengine.Waalike wanafunzi kumtumikia mtu fulani kabla ya darasa la seminari lijalo. Wapendeke-zee kwamba wanaweza kujitayarisha kushiriki uzoefu wao kwa shughuli hii (lakini hakiki-sha wameelewa kwamba hawana haja kujisikia kushurutishwa kushiriki uzoefu ambao ni wa kibinafsi sana ua wa siri.)Unaweza pia kuwapatia wanafunzi changamoto ya kukariri Mosia 2:17 kabla ya wakati unaokuja mnapokutana darasani.Shuhudia kwamba tunapowahudumia wengine kwa uaminifu, tunamtumikia Bwana.Tazama: Kwa sababu ya hali ya urefu wa somo hili, unaweza kutaka kutumia shughuli hii katika siku ingine, wakati una muda wa ziada.

Tangazo na Habari za UsuliMosia 2:33, 38–39. “Adhabu isiyo na mwisho,” “moto usiozimika,” na “mateso yasiyo na mwisho”

Katika onyo kuhusu matokeo ya uasi dhidi ya Mungu, Mfalme Benyamini alitumia vishazi “Adhabu isiyo na

mwisho” (Mosia 2:33), “moto usiozimika” (Mosia 2:38), na “mateso yasiyo na mwisho” (Mosia 2:39). Ili kupata uelewa bora wa haya maneno, ona maneno ya Bwana katika Mafundisho na Maagano 19:6–12.

Page 208: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

193

SOMO LA 53

Mosia 3UtanguliziAkiendelea na hotuba yake kwa watu wake, Mfalme Benyamini alitumia maneno ambayo malaika alikuwa amesema kwake kuhusu huduma ya Yesu Kristo. Mfalme Benyamini alishuhudia kwamba kupitia imani katika Yesu Kristo na toba, wale ambao wametenda

dhambi wanaweza kupokea wokovu. Pia alifunza kwa-mba kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo, mtu ambaye anakubali ushawishi wa Roho Mtakatifu, “umvua mtu wa kawaida na kuwa mtakatifu” (Mosia 3:19).

Mapendekezo ya KufundishaTazama: Ikiwa katika somo lililopita uliwatia moyo wanafunzi kukariri na kutumia Mosia 2:17, fikiria kuwapatia wao nafasi ya kushiriki uzoefu wao wakati fulani leo. Kuwa makini usitumie muda mwingi katika rejeo hili. Tenga muda wa kutosha wa kujadili mafundisho na kanuni katika Mosia 3.

Mosia 3:1–10Mfalme Benyamini alisema maneno ya malaika kuhusu Upatanisho wa Yesu KristoOnyesha glasi tupu na chupa ya maji. Mwalike mwanafunzi kuonyesha ni maji kiasi gani yeye anaweze kumimina kwenye glasi kwa mtu anayetaka tu kuonja maji. Kisha acha mwanafunzi aonyeshe ni kiasi gani anaweza kumimina kwa mtu ambaye anataka kujazwa. Waulize wanafunzi kutafakari swali lifuatalo:• Ikiwa maji yanawakilisha shangwe, ungetaka kiasi gani katika glasi yako?Waelezee wanafunzi kwamba mafundisho katika Mosiah 3 yatawasaidia kuona jinsi wana-vyoweza kujazwa na shangwe.Mwalike mwanafunzi asome Mosia 3:2–5 kwa sauti. Uliza darasa kutambua chanzo cha ujumbe wa Mfalme Benyamini katika Mosia 3.Sisitiza kwamba Mosia 3 ina tangazo la malaika la “habari njema za shangwe kuu” (Mosia 3:3). Waalike wanafunzi wachache kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka kwa Mosia 3:5–10. Uliza darasa litafute maneno au vishazi ambavyo vitawasaidia kufahamu vyema huduma ya Yesu Kristo. Unaweza kutaka kupendekeza kwamba waweke alama maneno na vishazi hivi. Waalike wanafunzi wachache kushiriki maneno na vishazi walivyopata.• Ni nini Mosia 3:7 inakusaidia kuelewa kuhusu huduma ya Yesu Kristo?• Unafikiri kwa nini malaika alisema ujumbe huu ungeleta shangwe kuu?Waalike wanafunzi kuandika ufupisho kwa sentensi moja wa Mosia 3:5–10 katika shajara zao za kujifunza maandiko, au katika daftari za darasani. Baada ya wao kuwa na wakati wa kutosha wa kuandika, waalike wanafunzi wachache kushiriki kile wameandika. Muhtasari wa wanafunzi unafaa kuonyesha uelewa wa mafundisho ya malaika kwamba Yesu Kristo aliteswa ili sisi tuweze kuokolewa kutokana na dhambi zetu.Unaweza kutaka kufuatilia majibu ya wanafunzi kwa maswali yafuatayo:• Hisia zako ni zipi unapofikiria kuhusu kile Mwokozi amekufanyia wewe?Ili kuwasaidia wanafunzi kuzidisha uelewa wao wa kuteseka kwa Mwokozi, shiriki taarifa ifuatayo ya Mzee James E. Talmage wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili:"Maumivu ya Kristo katika bustani hayaeleweki na akili zenye kipimo, yote kwa uzito na chanzo. Alitaabika na alipiga kite chini ya mzigo kama ambavyo hajapata mtu mwingine aliyeishi hapa ulimwenguni kuweza kudhania. Hayakuwa maumivu ya kimwili, wala mfadhaiko wa kiakili pekee, ambao ulimfanya Yeye kuteseka mateso hata kutoa mtiririko wa damu kutoka kila kinyweleo; bali maumivu ya kiroho ya nafsi ambayo ni Mungu pekee ndiye alikuwa na uwezo wa kuyapitia. Katika hilo saa ya mfadhaiko Kristo alikutana na kushinda matishio yote ambayo Shetani, “mwanamfalme wa ulimwengu huu,’ angeweza

Waulize maswali ambayo yanaalika wanafunzi kushiriki hisia na ushuhuda.Ili kuwasaidia wanafu-nzi kushiriki hisia zao na shuhuda zao, fikiria kuuliza maswali ambayo yatawasaidia kutafakari juu ya uzoefu waliopata kutoka kwa kanuni au mafundisho yanayojadi-liwa. Unaweza kusema “Umepata kujua vipi kwamba . . . ?” au Ni wakati gani umepata kuhisi . . . ?” Kisha waa-like wanafunzi kushiriki uzoefu wao na hisia zao. Kukubali kwao kwa mwaliko huu kutaruhusu Roho Mtakatifu kuwa-shuhudia ukweli wao na wanadarasa wao.

Page 209: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

194

SoMo la 53

kufanya. Kwa njia fulani, asili ya kweli na ya kuogopa ya mwanadamu isiweze kueleweka, Mwokozi alichukua juu Yake mzigo wa dhambi za mwanadamu kuanzia Adamu hata mwi-sho wa ulimwengu (Jesus the Christ, 3rd ed. [1916], 613).

Mosia 3:11–27Mfalme Benyamini anashuhudia kwamba kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo, tunaweza kumvua mtu wa kawaida na kuwa watakatifuWaambie wanafunzi kwamba Mfalme Benyamini alishiriki maelezo ya malaika ya maku-ndi tofauti ya watu na jinsi Upatanisho wa Yesu Kristo unatumika kwa kila kundi. Andika maswali yafuatayo kwenye ubao. Waulize wanafunzi kusoma Mosia 3:11–13, 16 kimya, wakitafuta majibu kwa maswali yafuatayo:

Upatanisho unatumika vipi:Kwa wale waliokufa bila ufahamu wa injili?Kwa wale ambao wanaasi dhidi ya Mungu na kufanya dhambi kwa makusudi?Kwa watoto ambao walikufa kabla ya kufikia umri wa uwajibikaji?

Baada ya muda wa kutosha, waulize wanafunzi kushiriki majibu ya maswali haya. (Ili kuwasaidia wao kujibu swali la kwanza, unaweza kuwataka wao kusoma Mafundisho na Maagano 137:7–10. Ili kuwasaidia wao na swali la tatu, unaweza kuwataka wao kusoma Moroni 8:8, 17 na Mafundisho na Maagano 29:46–47.)Soma taarifa ifuatayo ya Mzee Dallin H. Oaks wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili kuhusu athari ya Upatanisho kwa watoto wote wa Baba wa Mbinguni:“Sisi tunasoma kwamba ‘damu yake inalipia dhambi za wale ambao walikufa bila kujua mapenzi ya Mungu juu yao, au ambao walitenda dhambi bila kujua’ (Mosia 3:11). Vivyo hi-vyo, ‘damu ya Kristo inawalipia [watoto wadogo]’ (Mosia 3:16). Haya mafundisho kwamba nguvu za kufufuka na kutakasa za Upatanisho ni kwa wote ni kinyume cha madai kwamba neema za Mungu huwaokoa wateule wachache tu. Neema yake ni kwa wote. Mafundisho haya ya Kitabu cha Mormoni hupanua maono yetu na kukuza uelewa wetu wa upendo wa Mungu unaofinika na athari ya kote ya Upatanisho Wake kwa watu wote kila mahali” (“All Men Everywhere,” Ensign or Liahona, May 2006, 77).• Ni kanuni gani tunajifunza kutoka kwa Mosia 3:12 kuhusu jinsi Upatanisho unatumika

kwetu? Sisi tutaokolewa kutokana na dhambi zetu tunapofanya imani katika Yesu Kristo na kutubu.

• Kulingana mstari huu, ni nini kitatendeka kwa wale ambao wanachagua kutofanya imani katika Yesu Kristo?

Taja kwamba Mosia 3:19 ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Unaweza kutaka kuwatia moyo wanafunzi kuweka alama kifungu hiki kwa njia ya kipekee ili waweze kukipata kwa urahisi. Pia weka usikivu katika Mosia 3:19 kwa matumizi ya malaika ya maneno “mtu wa kawaida.” Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa kushazi hiki, soma maelezo yafuatayo kutoka kwa Mwongozo wa Maandiko:Mtu wa kawaida ni “mtu yule anaechagua kushawishiwa na hisia kali, shauku, tamaa, na hisi za mwili badala ya msukumo wa Roho Mtakatifu. Mtu kama huyu anaweza kuelewa vitu vya kimwili bali si vya kiroho. Watu wote ni wa kimwili, au wenye kufa, kwa sababu ya kuanguka kwa Adamu na Hawa. Kila mtu lazima azaliwe tena kupitia upatanisho wa Yesu Kristo” (Guide to the Scriptures, “Natural Man,” scriptures.lds.org).Andika maswali yafuatayo kwenye ubao. Acha wanafunzi watafute majibu ya maswali wanapopekua Mosia 3:19 kimya.

Malaika alielezea vipi uhusiano wa mtu wa kawaida na Mungu?Kulingana na kifungu hiki, tunawezaje kumvua mtu wa kawaida?

Taja kwamba kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo, mtu hufanya mengi kuliko kusitisha kuwa “mtu wa kawaida.” Yeye “kuwa mtakatifu.” Zaidi ya kutuokoa sisi kutoka kwa dhambi zetu, Mwokozi hutubadilisha sisi kuwa watu wema kuliko vile tungefanya wenyewe. Yeye hutusaidia kuwa zaidi kama Yeye. Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa fundisho hili, soma taarifa ifuatayo ya Mzee David A. Bednar wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili.

Mosia 3:19 ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Rejea kwa wazo la kufundisha hapo mwisho wa somo ili kuwasaidia wanafunzi na umahiri wao wa kifungu hiki.

Page 210: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

195

MoSia 3

“Yote mikono safi na moyo mweupe inahitajika kuupanda mlima wa Bwana na kusimama mahali patakatifu pake [ona Zaburi 24:3–4].

“Acha mimi nipendekeze kwamba mikono inafanywa kuwa safi kupitia mfanyiko wa kumvua mtu wa kawaida na kwa kushinda dhambi na ushawi-shi ovu katika maisha yetu kupitia Upatanisho wa Mwokozi. Mioyo hutaka-swa tunapopokea nguvu Zake za kuimarisha za kufanya mema na kuwa bora. Hamu zetu stahiki na kazi njema, kama inavyohitajika, zinaweza kuzaa mikono safi na mioyo safi. Ni Upatanisho wa Yesu Kristo ambao unapatiana

yote nguvu za kusafisha na kukomboa ambazo zitatusaidia kushinda dhambi na nguvu za kutakasa na kuimarisha ambazo hutusaidia kuwa bora kuliko vile tungekuwa tukitegemea nguvu zetu wenyewe. Upatanisho usio na mwisho ni kwa wote mtenda dhambi na mtakatifu katika kila mmoja wetu” (“Clean Hands and a Pure Heart,” Ensign or Liahona, Nov. 2007, 82).Ili kuwasaidia wanafunzi kufanya muhtasari mafundisho waliyojifunza kutoka katika Mosia 3:19, uliza:• Ni zipi baadhi ya kweli za injili ambazo unapata katika Mosia 3:19?Wanafunzi wanaweza kuorodhesha mafundisho kadhaa kutoka kwa kifungu, ikijumuisha yafuatayo:Mwanadamu wa kawaida ni adui kwa Mungu.Tunapoakubali ushawishi wa Roho Mtakatifu, tunamvua mtu wa kawaida. Kupitia Upatanisho wa Kristo, tunamvua mtu wa kawaida na kuwa watakatifu.Waalike wanafunzi kujibu mojawapo wa maswali yafuatayo katika shajara zao za kujifunza maandiko. (Unaweza kutaka kuandika maswali haya kwenye ubao kabla ya darasa, tayari-sha kitini pamoja na maswali, au soma maswali pole pole ili wanafunzi waweze kuandika katika shajara zao za kujifunza maandiko.)• Unaweza kufanya nini ili kukubali kikamilifu “ushawishi wa Roho Mtaktifu? Utafanya

nini katika wiki inayokuja ili kuboresha katika sehemu hii ya maisha yako?• Ni sifa gani za mtoto zilizoorodhesha katika Mosia 3:19 unazohitaji kukuza zaidi? Utafa-

nya nini katika wiki ijayo ili kukusaidia kukuza hiyo sifa?Ili kuwasaidia wanafunzi kupata ufahamu zaidi wa Upatanisho wa Mwokozi, wasomee Mosia 3:23–26. Elezea kwamba kishazi “kikombe cha ghadhabu ya Mungu” katika kifungu cha 26 kinalenga kuteseka mwishowe kwa wale wanaotenda dhambi kwa makusudi na hawatubu. Kisha mwulize mwanafunzi asome Mafundisho na Maagano 19:16–19. Waulize wanafunzi kusikiliza neno kikombe katika mstari wa 18.• Ni nini Yesu Kristo amefanya ili kwamba sisi tusinywe “kutoka kwa kikombe cha gha-

dhabu ya Mungu”? (Yeye amekunywa kikombe hicho Mwenyewe, alikichukua juu Yake Mwenywe kama adhabu ya dhambi zetu. Kama tutatubu kikweli, hatutateseka kwa hiyo adhabu.)

Hitimisha kwa kutoa ushuhuda wako wa kweli zilizojadiliwa katika somo hili.

Umahiri wa Maandiko—Mosia 3:19Ili kuwasaidia wanafunzi kukariri Mosia 3:19, wagawe katika jozi. Waulize wao kusoma Mosia 3:19 kwa sauti, neno moja kwa wakati, ikibadilishana kila neno lifuatalo pamoja na wenzi wao. Waulize kurudia zoezi hili mara kadhaa. Unaweza kutaka kuongezea ladha kwa shughuli hii kwa kuacha kila mwenzi kusoma maneno mawili au matatu kwa wakati.Kurudiarudia hii shughuli kutawasaidia wanafunzi kuelewa maudhui ya kifungu na ita-warahisishia wao kukariri kifungu chote. Wapatie changamoto ya kumaliza kukariri Mosia 3:19 peke yao.Tazama: Kwa sababu ya hali ya urefu wa somo hili, unaweza kutaka kutumia shughuli hii katika siku ingine, wakati una muda wa ziada.

Page 211: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

196

SOMO LA 54

Mosia 4UtanguliziKwa kuvutiwa na mafundisho ya Mfalme Benyamini, watu walitubu na kupokea ondoleo la dhambi zao. Wao “walijawa na shangwe” na walipata “amani na dhamira” (Mosia 4:3). Mfalme Benyamini aliendelea kuwafundisha, kuwasaidia kuelewa kile sharti wafanye

ili "kuhifadhi msamaha wa dhambi [zao]” (Mosia 4:12). Katika kufanya hivyo, aliwalinganisha na waombaji, wanaotegemea Mungu kwa wokovu. Pia aliwaonya wao juu ya hatari ya kuzembea katika kuchunga ma-wazo, maneno, na matendo yao.

Mapendekezo ya Kufundisha

Mosia 4:1–8Watu wa Mfalme Benyamini walipokea ondoleo la dhambi zao na wakajawa na shangwe na imaniWaulize wanafunzi kutafakari maswali yafuatayo:• Je! Tunaweza kujua vipi kwamba tumesamehewa dhambi zetu?Soma taarifa ifuatayo ya Rais Harold B. Lee:

“Ikiwa wakati utakuja ambapo wewe umefanya yote ambayo unaweza kutubu dhambi zako, hata kama wewe ni nani, popote ulipo, na umefanya mabadiliko na kulipia kwa uwezo wako wote; ikiwa itakuwa kitu ambacho kitaathiri hadhi yako katika Kanisa na umeenda kwa mamlaka husika, basi ungependa jibu la uthibitisho kama Bwana amekukubali au la. Katika tafakuri yako, kama unatafuta na kupata amani ya dhamiri, kwa ishara hiyo

unaweza kujua kwamba Bwana amekubali toba yako” (“Stand Ye in Holy Places,” Ensign, July 1973, 122).Wakumbushe wanafunzi kwamba Mfalme Benyamini alishiriki maneno ya malaika kuhusu vile wanaweza kupokea ondoleo la dhambi. Unaweza kuwakumbusha hasa maneno ya malaika kuhusu mtu wa kawaida kuwa adui wa Mungu na kuhusu matokeo ambayo yana-wangojea wale wanaokufa bila kutubu dhambi zao (ona Mosia 3:19, 23–27).Waulize wanafunzi kusoma Mosia 4:1–2 kimya, wakitafuta vishazi ambavyo vinaonyesha jinsi watu wa Mfalme Benyamini walitenda kuhusu maneno ya malaika. Acha wanafunzi wachache kushiriki vishazi walivyopata. Ikiwa wanafunzi wanahitaji usaidizi kuelewa kishazi “hali ya mwili,” elezea kwamba neno mwili ni kinyume cha kiroho. Inalenga tamaa zetu za kimwili badala ya hamu za kiroho zetu ili kujongea karibu na Bwana. Unaweza kuwauliza wanafunzi kusoma Alma 41:11 na kisha kuelezea kishazi “hali ya mwili” kwa maneno yao wenyewe. Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa kishazi “hafifu kuliko mavumbi ya dunia,” Helamani 12:4–8. Kisha waulize waelezee kwa maneno yao wenyewe jinsi mtu ambaye anakataa kufuata ushauri wa Bwana anaweza kuelezewa kama kuwa hafifu kuliko mavumbi ya dunia. Hakikisha kwamba wanaelewa kwamba Baba wa Mbinguni hawezi kuwafikiria watoto Wake kuwa hafifu kuliko mavumbi ya dunia.Taja kwamba kwamba wakati watu walitambua utendaji dhambi wao, walitubu, wakionye-sha imani yao katika Yesu Kristo na Upatanisho Wake. Waalike wanafunzi kusoma Mosia 4:3 kwa sauti. Uliza darasa kuzingatia jinsi watu walijua walikuwa wamesamehewa dhambi zao.• Kulingana na Mosia 4:3, ni hisia gani zinazowajia wale ambao wamesamehewa na Bwana?• Watu walipokea ondoleo la dhambi zao kwa sababu ya “imani nyingi ambayo walikuwa

nayo katika Yesu Kristo.” Ni vitendo gani vilionyesha imani yao? (Ona Mosia 4:1–2.)• Kwa maneno yako mwenyewe, ni nini tunachoweza kujifunza kutoka katika Mosia

4:1–3 kuhusu kupokea ondoleo la dhambi zetu? (Jibu moja linaloweza kujitokeza ni tu-napofanya imani katika Yesu Kristo na kutubu kwa uaminifu, tunapokea ondoleo

Page 212: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

197

MoSia 4

la dhambi zetu. Unaweza kutaka kuwaalika wanafunzi kuweka alama maneno na vishazi muhimu katika Mosia 4:1–3 ambavyo vinasisitiza kanuni hii.)

Soma taarifa ifuatayo ya Mzee Neil L. Andersen wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, ina-yofanya muhtasari wa kile ambacho ni sharti tufanye ili kupokea ondoleo la dhambi:

“Tunapokiri dhambi zetu kwa uaminifu, kurejesha kile tunaweza kwa wakosewa, na kuziacha dhambi zetu kwa kushika amri, tunakuwa katika mfanyiko wa kupokea msamaha. Kwa wakati, tutahisi maumivu ya huzuni wetu yakipoa, yakiondolea ‘mbali hatia kutoka katika mioyo yetu’ (Alma 24:10) na kuleta ‘amani ya dhamiri’ (Mosia 4:3).“Kwa wale ambao wametubu kikweli lakini inaonekana hawawezi kuhisi na-

fuu: endeleeni kushika amri. Nawaahidi ninyi, afueni itakuja kwa ratiba ya Bwana. Kupoa pia huhitaji muda” (“Repent . . . That I May Heal You,” Ensign au Liahona, Nov. 2009, 42).Waalike wanafunzi kuandika katika shajara zao za kujifunza maandiko au daftari za dara-sani kuhusu kile wamejifunza kuhusu toba walipokuwa wakijadili Mosia 4:1–3. Pia waulize wao kuandika kuhusu jinsi wanaweza kufanya imani katika Yesu Kristo wanapotafuta ondoleo la dhambi zao.Elezea kuwa baada ya kushuhudia mtazamo wa toba wa watu, Mfalme Benyamini ali-wakumbusha juu ya kutegemea kwao kwa Bwana. Waulize wanafunzi kadhaa kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka kwa Mosia 4:4–8. Uliza darasa kutafuta kile Mfalme Be-nyamini alitaka watu wake kuelewa baada ya wao kupokea ondoleo la dhambi zao.• Kulingana na mistari hii, ni “masharti gani tu ambayo kwayo [sisi] tunaweza

kuokolewa”?Baada ya wanafunzi kujibu swali hili, waalike warejelee Mosia 4:4–8 kimya, wakitafuta vishazi ambavyo vinaelezea watu ambao hupokea wokovu. Unaweza kutaka kuwashawishi kwamba waweke alama vishazi hivi. Fikiria kuuliza maswali yafuatayo:• Unafikiri inamaanisha nini “kuwa na bidii katika kuweka amri za [Bwana]”?• Ni vipi baadhi ya vitendo ambavyo vinaonyesha kwamba mtu “ameweka matumaini

[yake] katika Bwana”?• Ni katika njia gani umeona “wema wa Mungu” na “nguvu Zake zisizo na kifani”?Taja kwamba toba na utiifu huhitaji kazi nyingi na juhudi kwa sehemu yetu. Hata hivyo, haijalishi tunafanya kazi sana vipi, kamwe hatuwezi kupokea msamaha wa dhambi zetu na kipawa cha wokovu bila Upatanisho wa Yesu Kristo.

Mosia 4:9–30Mfalme Benyamini anafunza jinsi ya kuhifadhi ondoleo la dhambiAndika kuhifadhi ondoleo la dhambi zetu kwenye ubao. Wajulishe wanafunzi kwamba baada ya watu kupokea ondoleo la dhambi zao, Mfalme Benyamini aliwafunza jinsi ya kuhifadhi, au kuweka, ile hali safi na halisi.• Kwa nini hii ni muhimu kwa kila mmoja wetu kujua?Waalike wanafunzi kupekua Mosia 4:9–11 kimya, wakitafuta kile sharti tufanye ili kuhifadhi ondoleo la dhambi zetu. Baada ya muda wa kutosha, acha wanafunzi kushiriki kile wame-pata. Fikiria kuandika majibu yao kwenye ubao. Majibu yanaweza kujumuisha kwamba tunahitaji kukumbuka ukuu wa Mungu, tujinyenyekeze wenyewe, tuombe kila siku, na kusimama imara katika imani.Fikiria kuuliza maswali yafuatayo ili kusaidia wanafunzi kuzidisha uelewa wao na kutumia kile wamesoma:• Mfalme Benyamini alifunza kwamba ni sharti sisi “tuamini katika Mungu”(Mosia 4:9).

Pia alinena juu ya kuonja upendo wa Mungu na daima kukumbuka “ukuu wa Mungu” (Mosia 4:11). Ni uzoefu gani ambao umekusaidia kutambua kwamba Mungu kweli yupo na ana nguvu na kwamba Yeye anakupenda?

• Je! Kukumbuka nguvu, wema, na upendo wa Mungu kunashawishi vipi upendeleo wetu wa kumtii Yeye?

Wasomee wanafunzi Mosia 4:12 kwa sauti. Waulize kutambua katika mstari huu baraka ambazo zitakuja kwa wale wanaotenda kile kimefunzwa katika Mosia 4:5–11.

Page 213: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

198

SoMo la 54

Elezea kwamba Mosia 4:13–16 ina maelezeo ya Mfalme Benyamini ya watu ambao walihi-fadhi ondoleo la dhambi zao. Gawa darasa katika vikundi vitatu. Uliza kikundi cha kwanza kupekua Mosia 4:13, kikundi cha pili kupekua Mosia 4:14–15, na kikundi cha tatu kupekua Mosia 4:16. Acha kila mwanafunzi kusoma mstari au mistari yake aliopangiwa kibinafsi na kutambua mtazamo na sifa ambazo Mfalme Benyamini alielezea katika wale ambao wanatafuta kuhifadhi ondoleo la dhambi zao.Baada ya muda wa kutosha, waalike wanafunzi kuelezea kile walichopata. Wanapofanya hivyo, sisitiza ukweli kwamba ikiwa tutajinyenyekeza wenyewe mbele za Mungu na kujitahidi kukuza mtazamo kama wa Kristo, tunaweza kulinda ondoleo la dhambi zetu. Wasaidie wanafunzi kutumia kile wanachojifunza kwa kuuliza moja au maswali yote yafuatayo kila mtazamo au sifa inapotajwa.• Kwa nini unafikiri mtazamo (au sifa) hii ina usaidizi katika kulinda ondoleo la dhambi zetu?• Ni wakati gani wewe umeona mifano ya mtazamo huu (au sifa hii)?Mfalme Benyamini alitumia analojia ya nguvu sana ambayo inaweza kuwasaidia wana-funzi kuelewa baraka ambazo wamepokea kutoka kwa Mungu na kuwapatia motisha kukuza mitazamo waliyojifunza katika Mosia 4:13–16. Waulize wanafunzi kusoma Mosia 4:16–23 kimya.• Kulingana na Mfalme Benyamini, ni kwa vipi sisi sote ni waombaji?• Je! Uelewa huu unaweza kutusaidia vipi kuwa na fadhila zaidi kwa wengine?• Kwa wale ambao hawawezi kuwapatia waombaji, au kwa wale ambao wana kidogo cha

kutoa, ni ushauri gani Mfalme Benyamini alishiriki katika Mosia 4:24–26?• Katika Kanisa leo, kutoa matoleo ya mfungo kunaweza kutusaidia vipi kufuata ushauri

huu katika Mosia 4:26? Vijana wanaweza kushiriki vipi katika matoleo ya mfungo? (Ma-jibu yanaweza kujumuisha kwamba wanaweza kufunga, wengine wanaweza kuchangia matoleo ya mfungo, wenye Ukuhani wa Haruni katika sehemu fulani za ulimwengu hukusanya matoleo ya mfungo kutoka kwa washiriki wa kata au tawi.)

Taja kwamba katika vitu vyote vizuri tunavyoulizwa kufanya, inaweza kuwa changamoto wakati mwingine kupata mapatano ya haki katika maisha yetu. Acha mwanafunzi asome Mosia 4:27 kwa sauti.• Unafikiria inamaanisha nini kufanya vitu vyote kwa “hekima na utaratibu”?• Je! Ushauri huu utakusaidia vipi?Alika mwanafunzi asome Mosia 4:29–30 kwa sauti. Taja kwamba Mosia 4:30 ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Unaweze kuwahimiza wanafunzi kutia alama kifungu hiki kwa njia ya kipekee ili waweze kukipata kwa urahisi.• Kuna uhusiano gani kati ya mawazo yetu, maneno, na matendo yetu? Tunaweza

kufanya nini kuwatunza wengine? Ni kwa njia gani tunaweza kusaidiana mmoja kwa mwengine?

Fikiria kuwapatia wanafunzi dakika chache za kuandika katika shajara zao za kujifunza maandiko kuhusu jinsi kanuni katika Mosia 4:9–30 zinavyoweza kuwasaidia wao wana-pojitahidi kulinda ondoleo la dhambi zao. Shuhudia juu ya upendo wa Bwana kwa kila mmoja wenu na hamu Yake ya wao kutubu na kuhifadhi ondoleo la dhambi zao.

Umahiri wa Maandiko—Mosia 4:30Ili kuwasaidia wanafunzi kuona uhusiano katika mawazo, maneno, na matendo, kama ilivyoelezwa katika Mosia 4:30, soma taarifa ifuatayo ya Mzee Ezra Taft Benson:“Fikiria mawazo safi. Wale wanaofikiria mawazo safi hawafanyi matendo machafu. Wewe hauna tu jukumu mbele za Mungu kwa matendo yako bali pia kwa kudhibiti mawazo yako. Kwa hivyo ishi hivi kwamba usije ukaona haya kwa aibu ikiwa mawazo na matendo yako yanaweza kuonyeshwa kwenye skrini katika Kanisa lako. Msemo wa kale bado ni kweli kwamba unapanda mawazo na unavuna vitendo, unapanda vitendo na unavuna tabia, unapanda tabia na unavuna hukla, na hulka yako inabainisha hatima yako ya milele. ‘Mtu aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo’” (katika Conference Report, Oct. 1964, 60; quoting Mithali 23:7).

Mosia 4:30 ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Rejelea wazo la kufundisha hapo mwisho wa somo ili kuwasaidia wanafunzi na umahiri wao wa kifungu hiki.

Kuandika misukumoMzee Richard G. Scott wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili ali-wahimiza wanafunzi kuandika misukumo wanayopokea: “Kuza ujuzi wa kujifunza kwa kile unachoona na hasa kwa kile Roho Mtaka-tifu hukusukuma wewe kuhisi. Andika chini katika mahali salama vitu muhimu ulivyo-jifunza kutoka kwa Roho. Utapata kwamba unapoandika misukumo yenye thamani, mara nyingi itakuja zaidi” (“To Acquire Knowledge and the Strength to Use It Wisely,” Ensign, June 2002, 32).

Page 214: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

199

MoSia 4

Elezea kwamba nuru na giza haiwezekani kuwa pamoja katika wakati mmoja. Nuru hu-fukuza giza. Kwa mfano, muziki ufaao, picha za kuinua, shughuli maridhawa, na mawazo safi na maneno safi humwalika Roho katika maisha yetu na kusukuma mawazo yasiyosta-hili nje ya akili zetu. Wasaidie wanafunzi kuelewa kwamba wanaweza kupambana na giza kwa kujaza maisha yao na nuru.• Tunaweza kufanya nini ili kuweka mawazo, maneno, na vitendo vyetu kuwa safi?Wahimize wanafunzi kufanya mpango mahususi wa kujaza maisha yao na nuru. Unaweza kutaka wao waandike mipango yao katika shajara zao za kujifunza maandiko.

Page 215: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

200

UtanguliziMosia 5 ina hitimisho la hotuba ya Mfalme Benyamini kwa watu wake, kumbukumbu ambayo inaanza katika Mosia 2. Kama matokeo ya imani yao katika maneno ya Mfalme Benyamini, watu walipata mabadiliko maku-bwa ya moyo. Waliingia katika agano na Mungu na

wakajichukulia juu yao wenyewe jina la Yesu Kristo. Kama ilivyoandikwa katika Mosia 6, Mfalme Benya-mini aliukabidhi ufalme wake kwa mwanawe Mosia, ambaye alitawala kulingana na mfano ambao baba yake aliweka.

SOMO LA 55

Mosia 5–6

Mapendekezo ya Kufundisha

Mosia 5:1–4Watu wa Mfalme Benyamini walielezea mabadiliko makubwa waliyopata kupitia RohoKabla ya darasa, andika maswali yafuatayo kwenye ubao:

Je! Wewe umewahi kuhisi kwamba unahitaji kubadilika kiroho?Ulifanya nini kuhusu hivyo?Ikiwa unameshapata mabadiliko, umedumusha hayo mabadiliko hadi siku hii?

Waulize wanafunzi kujibu maswali haya katika shajara zao za kujifunza maandiko au daftari za darasani. Kisha soma taarifa ifuatayo ya Mzee w David A. Bednar wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili:“Kiini cha injili ya Yesu Kristo huhitaji mabadiliko ya kimsingi na kudumu katika asili yetu inavyowezesha kupitia kutegemea kwetu kwa ‘fadhili, na rehema, na neema za Masiya Mtakatifu’ (2 Nefi 2:8). Tunapochagua kumfuata Bwana, tunachagua kubadilishwa—kuza-liwa tena kiroho” (“Ye Must Be Born Again,” Ensign au Liahona, May 2007, 20).Unaweza kupendekeza kwamba wanafunzi waandike dondoo katika maandiko yao karibu na Mosia 5:2 au katika shajara zao za kujifunza maandiko: “Tunapochagua kumfuata Bwana, tunachagua kubadilika” (Elder David A. Bednar).• Ni kwa njia gani sisi tunachagua kubadilika tunapochagua kumfuata Yesu Kristo?Wapatie wanafunzi dakika cha za kurejelea Mosia 2–4. Unaweza kupendekeza kwamba wasome muhtasari wa sura. Waulize kile wanachokumbuka kuhusu maudhui ya sura hizi. Kisha waalike wasome Mosia 5:1 kimya.• Ni nini Mfalme Benyamini alikuwa na hamu ya kujua kutoka kwa watu wake?Waulize wanafunzi kusoma Mosia 5:2–5 kimya, wakitafuta majibu ya watu kwa maswali ya Mfalme Benyamini. Kabla ya wanafunzi kusoma, unaweza kutaka kuelezea kwamba katika mstari wa 2, neno silika humaanisha asili ya mtu—hamu yake na mwenendo wake. Baada ya wao kusoma, waulize maswali yafuatayo ili kuwasaidia wao kuchanganua mistari:• Watu walisema nini kuhusu mwenendo wao?• Ni nini kilicholeta haya mabadiliko katika mwenendo wao? (Waliamini mafundisho ya

Mfalme Benyamini kuhusu Yesu Kristo na Upatanisho, na Roho ilibadilisha mioyo yao.)Sisitiza kwamba mabadiliko ya moyo ni zaidi ya mabadiliko ya tabia tu. Tunapata uzoefu wa mabadiliko ya moyo, tunakuwa watu wapya, waliobadilika kupitia nguvu za Upata-nisho wa Mwokozi. Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa ukweli huu, waalike wanafunzi kusoma taarifa ifuatayo ya Mzee David A. Bednar wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili:“Injili ya Yesu Kristo inahusisha zaidi sana kuliko kuepuka, kushinda, na kutakaswa ku-tokana na dhambi na ushawishi mbaya katika maisha yetu; pia kimsingi huhitaji kutenda mema, kuwa mwema, na kuwa bora. Haya mabadiliko makubwa siyo tu matokeo ya kufanya kazi sana au kukuza nidhamu nyingi ya kibinafsi. Badala ya yake, ni matokeo ya mabadiliko ya kimsingi katika hamu yetu, nia yetu, na asili yetu yanayowezeshwa kupitia

Page 216: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

201

MoSia 5 – 6

Upatanisho wa Kristo Bwana. Madhumuni yetu ya kiroho ni kushinda yote dhambi na hamu ya kutenda dhambi, yote mawaa na udhalimu wa dhambi” (“Clean Hands and a Pure Heart,” Ensign au Liahona, Nov. 2007, 81–82).• Kwa nini unafikiria tunahitaji Upatanisho wa Yesu Kristo ili kubadilika kikweli?Elekeza usikivu wa wanafunzi kwenye kishazi “kwa sababu ya Roho wa Bwana Mwe-nyezi” katika Mosia 5:2. Unaweza kuhitaji kubainisha mwenyezi, ambayo humaanisha enye nguvu zote.• Tunaweza kujifunza nini kutoka kwa Mosia 5:2–4 kuhusu jinsi tunaweza kupata maba-

diliko makubwa katika maisha yetu?Wanafunzi wanapojadili swali hili, hakikisha wanaelewa kwamba tunafanya imani katika Yesu Kristo na kupokea Roho Mtakatifu, tunaweza kupata uzoefu wa mabadiliko makubwa ya moyo.Elezea kwamba kupata mabadiliko makubwa ya moyo ni mfanyiko ambao hutokea kote katika maisha yetu, siyo tukio moja. Shiriki taarifa ifuatayo ya Rais Ezra Taft Benson:“Kuwa kama Kristo ni kazi maisha yote na mara nyingi hujumuisha ukuaji na mabadiliko ambayo ni pole pole karibu kabisa pasi kutambulika. . . .“. . . Toba ya kweli inajumlisha mabadiliko ya moyo na siyo tu mabadiliko ya tabia. . . . Toba kwa wingi haijumlishi mabadiliko ya mhemko au kidrama, bali mwendo wa hatua kwa hatua, thabiti, na uaminifu kuelekea uungu” (“A Mighty Change of Heart,” Ensign, Oct. 1989, 5).Ili kuwasaidia wanafunzi kutumia kanuni hii na kutathimini maendeleo yao katika kupata uzoefu wa mabadiliko ya mioyo yao, waulize kujibu katika shajara zao za kujifunza ma-andiko maswali yafuatayo. (Unaweza kutaka kuandika maswali haya kwenye ubao kabla ya darasa, tayarisha kitini pamoja na maswali, au soma maswali pole pole ili wanafunzi wayaandike katika shajara zao za kujifunza maandiko.)• Je! Mwenendo wako umebadilika vipi unapomfuata Mwokozi?• Je! Unahitaji kufanya nini ili Bwana aendelee kukusaidia kupata uzoefu wa mabadi-

liko haya?Mpe mwanafunzi mmoja au wawili nafasi ya kushiri majibu yao kwa maswali haya. Haki-kisha kwamba wanaelewa kwamba hawapaswi kuhisi kushurutishwa kushiriki uzoefu au mawazo ambayo ni ya kibinafsi sana au ya kisiri.

Mosia 5:5–15Watu wa Mfalme Benyamini wanaingia katika agano na Mungu na wakapatiwa jina jipyaAlika mwanafunzi asome Mosia 5:5 kwa sauti. Uliza darasa kutafuta kile watu wa Mfalme Benyamini walikuwa tayari kufanya kwa sababu mioyo yao ilikuwa imebadilika.• Watu walikuwa tayari kufanya nini sasa kwamba mwenendo wao ulikuwa umebadilika

kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo?Ili kuwasaidia wanafunzi kuongezea uelewa wao wa maagano, wapatie dakika chache za kujifunza mada kibinafsi. Unaweza kupendekeza kwamba wajifunze mada hii katika Bible Dictionary au Kweli kwa Imani au kwamba watafute maandiko juu ya mada katika kiele-lezo cha Kitabu cha Mormoni au utatu wa maandiko. Baada ya muda wa kutosha, acha wanafunzi wagawanyike katika jozi na kuelezeana mmoja na mwingine kwa maneno yao wenyewe.• Ni maneno au vishazi gani katika Mosia 5:5 vinavyoonyesha hamu ya watu ya kufanya

na kushika maagano na Mungu? (Majibu yanaweza kujumuisha “kufanya mapenzi yake,” na “katika mambo yote,” na “maisha yetu yaliyosalia.”)

• Ni maneno au vishazi gani katika Mosia 5:5 vinavyokukumbusha ahadi tunazofanya upya tunapopokea sakramenti?

• Unafikiria kufanya na kuweka maagano hutusaidia vipi kuendelea katika mfanyiko wa kupata uzoefu wa mabadiliko ya moyo?

Waalike wanafunzi kusoma Mosia 1:11 kimya. Waulize watafute sababu moja Mfalme Benyamini aliwakusanya watu pamoja. (Kuwapa wao jina.) Elezea kwamba Mosia 5:7–15

Acha wanafunzi waelezeeMara kwa mara, waulize wanafunzi kuelezeana mafundisho na kanuni wawili wawili. Kwa ku-fanya hivyo, utawasaidia wanafunzi kuimarisha imani yao na kuongeza uelewa wao wa injili ya Yesu Kristo. Pia utawa-saidia kujifunza jinsi ya kushiriki kweli za injili na wengine.

Page 217: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

202

SoMo la 55

imeandikwa maelezo ya Mfalme Benyamini ya jina aliloahidi kuwapatia watu wake. Wa-patie wanafunzi dakika chache kupitia Mosia 5:7–14, wakitafuta maneno jina na kuitwa. Unaweza kutaka kupendekeza kwamba wanafunzi waweke maneno haya alama kila mara yanapotokea.Waalike wanafunzi wachache waelezee kwa nini walipatiwa majina yao. Kwa mfano, unaweza kuwauliza waelezee kuhusu jinsi wazazi wao waliamua kuwaita wao au unaweza kuuliza kama majina yao yana maana maalum. Kisha uliza darasa:• Jina lina umuhimu gani? (Kwenye ubao, fanya muhtasari wa majibu ya wanafunzi ya

swali hili. Majibu yanaweza kujumuisha kwamba jina ni jinsi tunavyojulikana, linahu-siana na utambulisho wetu, ni njia moja ya kututofautishana na wengine, na kila mara hubeba sifa na matarajio kwa sababu ya familia inayohusishwa nalo.)

Alika mwanafunzi asome Mosia 5:7–8 kwa sauti. Uliza darasa kutafuta jina ambalo Mfalme Benyamini aliwapatia watu wake. Pia waulize watafute maneno na vishazi ambavyo vina-onyesha umuhimu wa jina hilo. Unaweza kutaka kuwahimiza wao kuweka alama maneno na vishazi hivi.• Ni jina gani Mfalme Benyamini aliwapatia watu wake?• Ni maneno na vishazi gani ulivyotambua? Maneno na vishazi hivi vinakufunza nini

kuhusu jina la Kristo?• Ni wakati gani tunajichukulia juu yetu wenyewe jina la Yesu Kristo? (Hakikisha wa-

nafunzi wanaelewa kwamba tunajichukulia juu yetu wenyewe jina la Yesu Kristo tunapofanya na kuweka maagano matakatifu.)

Wanafunzi wanapojadili mstari hii, wanaweza kuhitaji usaidizi wa kuelewa mafundisho kwamba tunaweza kuwa “watoto wa Kristo” (Mosia 5:7). Unaweza kutaka kutaja kwa-mba baba humpa uzima mtoto. Sisi tu watoto wa kiroho wa Baba wa Mbinguni. Sisi pia tu watoto wa baba zetu wa ulimwenguni, ambao, pamoja na mama zetu, walipatiana nafasi kwetu ya kuishi kwenye ulimwengu huu katika miili yetu ya kimwili. Kurejea Mosia 5:7, Rais Joseph Fielding Smith alifunza kwamba Yesu Kristo pia “huwa Baba yetu” kwa sababu Yeye “hutupatia sisi uzima, uzima wa milele, kupitia upatanisho ambao alifanya kwa ajili yetu. Rais Smith alielezea, “Tunakuwa watoto, wana na mabinti wa Yesu Kristo, kupitia maagano yetu ya utiifu kwake” (Doctrines of Salvation, comp. Bruce R. McConkie, 3 vols. [1954–56], 1:29).Warejeshe wanafunzi kwenye maneno ubaoni ambayo yanaelezea umuhimu wa jina.• Majina yaliyo ubaoni yanaweza kusaidia vipi kuelewa umuhimu wa kujichukulia juu

yetu wenyewe jina la Yesu Kristo?Waulize wanafunzi kusoma Mosia 5:9–13 kimya, wakitafuta ushauri zaidi kutoka kwa Mfalme Benyamini kuhusu kujichukulia juu yetu wenyewe jina la Yesu Kristo. Unaweza kutaka kupendekeza kwamba wanafunzi wasome mistari hii kama vile Mfalme Benyamini alikuwa akinena na wao kibinafsi. Gawa wanafunzi katika majozi, na uwaulize wao kujadili maswali yafuatayo kulingana na vile wamesoma. (Unaweza kutaka kuandika maswali haya kwenye ubao au uwapatie kitini.)• Fikiria kuhusu umuhimu wa kujichukulia juu yetu wenyewe jina la Kristo. Unafikiria

humaanisha nini kuwa na jina la Kristo kuandikwa katika mioyo yetu? Ni baraka gani zinazokuja kwa wale ambao jina la Kristo limeandikwa katika mioyo yao?

• Fikiria juu ya watu unaowajua ambao wanaheshimu jina la Kristo. Watu hawa hufanya nini ili kuonyesha wanastahi na upendo walionao kwa jina la Kristo?

Uliza mwanafunzi asome Mosia 5:15 kwa sauti. Alika darasa litafute matendo ambayo yanawatambulisha wale ambao wanaweka maagano yao.• Ni baadhi ya maswali gani tunayoweza kujiuliza sisi wenyewe ili kutathimini jinsi sisi

tumejichukulia juu yetu wenyewe jina la Kristo?Shiriki hisia zako kuhusu kile inamaanisha kujichukulia juu yako mwenyewe jina la Yesu Kristo. Shuhudia umuhimu wake katika maisha yako.

Page 218: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

203

MoSia 5 – 6

Mosiah 6:1–7Mosia anaanza utawala wake kama mfalmeWaulize wanafunzi kusoma Mosia 6:1–3 kimya, wakitambua kile Mfalme Benyamini alifa-nya kabla ya kuruhusu umati kuondoka.• Kwa nini unafikiria ilikuwa ni muhimu kuandika majina watu wote ambao walikuwa

wameingia katika agano? Kwa nini Mfalme Benyamini aliwateua makuhani miongoni mwa watu?

Elezea kwamba baada ya kunena na watu Mfalme Benyamini aliukabidhi ufalme kwa mwanawe Mosia. Miaka mitatu baadaye, Mfalme Benyamini alifariki. Alika mwanafunzi asome Mosia 6:6–7 kwa sauti. Uliza darasa kutafuta maneno na vishazi ambavyo vinao-nyesha kwamba Mosia alifuata mfano wa baba yake na kuwasaidia watu wake kuendelea kupata uzoefu wa mabadiliko makubwa katika mioyo yao.

Page 219: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

204

Somo la Mafunzo ya NyumbaniManeno ya Mormoni–Mosia 6 (Kitengo cha 11)

Vifaa vya Matayarisho kwa Mwalimu wa Mafunzo ya NyumbaniMuhtasari wa Mafunzo ya Nyumbani ya Kila sikuUfuatao ni muhtasari wa mafundisho na kanuni ambazo wa-nafunzi wamejifunza walipojifunza Mosia 6 (kitengo cha 11) Haikusudiwi kufunzwa kama sehemu ya somo lako. Somo unalofundisha linazingatia machache tu ya mafundisho na kanuni hizi. Fuata maelekezo ya Roho Mtakatifu unapofikiria mahitaji ya wanafunzi wako.

Siku ya 1 (Maneno ya Mormoni–Mosia 2)Kwa kujifunza uzoefu wa Mormoni katika kufuata Roho na ikijumuisha mabamba madogo ya Nefi pamoja na kumbu-kumbu zake, wanafunzi walijifunza kwamba Bwana anajua vitu vyote. Mfalme Benyamini alifunza kwamba kama Wa-nefi hawakuwa na maandiko, wangefifia katika kutokuamini na kwamba kupekua maandiko hutusaidia kujua na kuweka amri. Aliwafundisha watu wake umuhimu wa kanuni kama hizo: Tunapowahudumia wengine, tunamtumikia Mungu. Tunapohisi kuwa na deni na Mungu, tunataka kuwahudumia wengine na shukrani zetu huongezeka. Ikiwa tutaweka amri, tutabarikiwa yote kimwili na kiroho.

Siku ya 2 (Mosia 3)Mfalme Benyamini alisimulia maneno ya malaika, ambaye alileta “habari njema ya shangwe kuu” kuhusu kuja kwa Bwana katika maisha ya muda. Wanafunzi walijifunza kwa-mba ilitabiriwa zaidi ya miaka 100 kabla ya matukio kutokea ambapo Yesu Kristo angeteseka ili tuweze kuokolewa kutoka kwa dhambi zetu. Tunaweza kuokolewa kutoka kwa dhambi zetu tunapofanya imani katika Yesu Kristo na kutubu. Kama tutakubali ushawishi wa Roho Mtakatifu, tunaweza kushinda mtu wa kawaida kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo.

Siku ya 3 (Mosia 4)Ujumbe wa Mfalme Benyamini ulijaza watu wake na Roho wa Bwana. Wanafunzi walijifunza kwamba tunapofanya imani katika Yesu Kristo na kutubu kwa uaminifu, tunapokea ondoleo la dhambi zetu. Mfalme Benyamini alifundisha watu wake kwamba wakijinyenyekeza wenyewe mbele za Mungu na kujitahidi kukuza sifa kama Kristo, tunaweza kulinda ondoleo la dhambi zetu.

Siku ya 4 (Mosia 5–6)Walipokuwa wakisoma kuhusu mabadiliko ambayo yalikuja juu ya watu wa Mfalme Benyamini, wanafunzi walijifunza kwamba tunapofanya imani katika Yesu Kristo na kupokea Roho Mtakatifu, tutapata uzoefu wa mabadiliko makubwa ya moyo. Watu wa Mfalme Benyamini walishika maagano kufanya mapenzi ya Bwana na kushika amri Zake, kuonyesha kwamba tunaweza kujichukulia wenyewe jina la Yesu Kristo tunapofanya na kushika maagano matakatifu.

UtanguliziSomo hili litawasaidia wanafunzi kuelewa mafundisho ya Mfalme Benyamini kwa wanawe na watu wake miaka mitatu kabla ya kifo chake. Mfalme Benyamini alifundisha watu wake jinsi ya kupokea na kuhifadhi ondoleo la dhambi zetu kwa kufa-nya imani katika Yesu Kristo.

Mapendekezo ya Kufundisha

Maneno ya MormoniNefi na Mormoni wanaonyesha imani yao katika MunguAlika mwanafunzi asome 1 Nefi 9:2–3 ili kuwakumbusha kwamba Nefi aliamuriwa kutengeneza seti mbili za mabamba. Wasaidie wao kuelewa kwamba katika kifungu hiki, kishazi “haya mabamba” humaanisha mabamba madogo ya Nefi, ambayo yana kumbukumbu kimsingi mambo matakatifu. Uliza mwanafunzi asome 1 Nefi 9:4 kwa sauti. Uliza darasa kutafuta madhumuni ya mabamba makubwa (usimulizi wa utawala wa wafalme na vita vya watu)

Wakumbushe wanafunzi kwamba Mormoni alipokuwa akifupi-sha mabamba makubwa ya Nefi, aligundua mabamba madogo miongoni mwa kumbukumbu zingine. Alikuwa ameongozwa na Roho Mtakatifu kujumuisha kile alipata kwenye mabamba madogo pamoja na ufupisho wake, hata ingawa hakujua kwa nini (ona Maneno ya Mormoni 1:7).

Alika nusu ya darasa kupekua 1 Nefi 9:5–6 ili kujua kwa nini Nefi aliamriwa kutengeneza mabamba madogo. Acha ile nusu ingine ya darasa kupekua Maneno ya Mormoni 1:6–7 ili kujua kwa nini Mormoni aliamua kujumuisha mabamba madogo pamoja na ufupisho wake. Baada ya washiriki wa darasa kuri-poti, waulize ni nini hivi vifungu kutoka kwa Nefi na Mormoni vinawafundisha kuhusu Bwana. (Wanafunzi wanaweza kutumia maneno tofauti, hakikisha wanaonyesha wanaelewa kwamba Bwana anajua vitu vyote.)

• Ni nini ilikuwa” madhumuni ya hekima” ya siku za usoni ambayo wote Nefi na Mormoni walimaanisha? (Bwana alijua kwamba katika mwaka wa 1828 mabamba madogo yata-chukua nafasi ya kurasa 116 za mswaada wa Kitabu cha

Page 220: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

205

SoMo la MafUnzo ya nyUMbani

Mormoni zilizopotea. Ona kitengo cha 6, siku ya 1 katika mwongozo wa kujifunza wa mwanafunzi.)

• Uelewa wako kwamba Bwana anajua vitu vyote katika siku za usoni unaweza kukupatia imani ya kutii msukumo wa kiroho unaopokea?

Ikiwa unahisi kuhitaji kutumia muda zaidi katika sehemu hii ya somo, waulize wanafunzi ikiwa wanaweza kushiriki uzoefu wa wakati walihisi kusukumwa na Roho kufanya kitu na hawakujua madhumuni ya msukumo huu mpaka hapo baadaye.

Mosia 1Mfalme Benyamini anawaita watu kukusanyika pamojaElezea kwamba mabamba madogo ya Nefi yalikuwa na historia ya Wanefi kutoka kwa huduma ya Lehi hadi wakati ambapo Mfalme Mosia aliunganisha watu wa Nefi na Zarahemla na wakati Benyamini mwana wa Mosia alitawala ufalme kwa haki. Mfalme Benyamini alikabidhiwa kumbukumbu takatifu. (Ona Omni 1:23, 25.)

Karibu na mwisho wa maisha ya Mfalme Benyamini, alimuomba mwanawe Mosia kukusanya watu pamoja. Waalike wanafunzi kusoma Mosia 1:10–11 na watafute sababu za Mfalme Benya-mini za kutaka kunena na watu. (Alitaka kutangaza kwamba Mosia atakuwa mfalme mtarajiwa na kuwapatia watu jina.)

Mosia 2–6Mfalme Benyamini anawafunza watu wake kuhusu Upatanisho wa MwokoziWaonyeshe wanafunzi picha ya Mfalme Benyamini Akihutubia Watu Wake(62298; Gospel Art Book [2009], no. 74). Soma Mosia 2:12–19 kwa darasa. Alika wanafunzi kuinua mikono yao wanapotambua vishazi ambayo vinaonyesha hulka ya Mfalme Benyamini. Wanafunzi wanapoinua mikono yao, sitisha kusoma na uwaulize kuelezea kile wametambua na jinsi kinafunua hulka ya Mfalme Benyamini.

Unaweza kutaka kuwauliza wanafunzi kile wamejifunza kuhusu huduma katika Mosia 2:17. (Majibu ya wanafunzi yanafaa kuakisi uelewa wa kwamba tunapowahudumia wengine, tu-namtumikia Mungu.) Unaweza pia kutaka darasa lirudie Mosia 2:17, kifungu cha umahiri wa maandiko, kwa kukariri. Fikiria kuwaalika wanafunzi kushiriki jinsi hivi majuzi wamemtumikia Mungu kwa kuwahudumia wengine.

Andika vifungu vya maandiko vifuatavyo kwenye ubao au kwe-nye kipande cha karatasi. Usijumuishe majibu yalioko kwenye mabano. Mpatie kila mwanafunzi kazi ya kurejea mojawapo wa vifungu vya maandiko. Wakumbushe kwamba mahubiri ya Mfalme Benyamini yalilenga kwenye mada hii: “Wokovu utawa-shukia watoto wa watu, ila katika na kupitia jina la Kristo pekee, Bwana Mwenyezi. (Mosiah 3:17). Kila kifungu cha maandiko hufunza kitu kuhusu mada hii.

1. Mosia 2:20–25, 34. (Tunapotambua tu wadeni kwa Mu-ngu, shukrani zetu huongezeka.)

2. Mosia 3:7–11, 17–18 (Yesu Kristo aliteseka ili sisi tuweze kuokolewa kutoka kwa dhambi zetu. Ikiwa tutafanya imani katika Yesu Kristo kupitia toba, tunaweza kuokolewa kutoka kwa dhambi zetu.)

3. Mosia 3:12–16, 19–21. (Ikiwa tutakubali ushawishi wa Roho Mtakatifu, kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo tuna-weza kumvua mtu wa kawaida na kuwa mtakatifu.)

4. Mosia 4:5–8, 19–21, 26. (Ikiwa tutajinyenyekeza wenyewe mbele za Mungu na kujitahidi kukuza sifa kama za Kristo, tunaweza kuhifadhi ondoleo la dhambi.)

Baada ya kuwapatia wanafunzi muda wa kutosha, waruhusu wao waripoti kile walichojifunza darasani au katika vikundi vidogo. Kisha waulize wanafunzi kadhaa kuchagua mojawapo wa kanuni hizi na waelezee jinsi wanaweza kuzitumia katika maisha yao.

Alika mwanafunzi asome Mosia 4:5–8, 19–21, 26. Uliza darasa kufuatilia, likitafuta jinsi watu walijibu kwa maneno ya Mfalme Benyamini. Kisha alika mwanafunzi mwengine kusoma Mosia 5:1–2, 5–8 kwa sauti. Uliza darasa kutafuta jinsi tunaweza ku-jichukulia juu yetu jina la Bwana. Hakikisha wanafunzi wamee-lewa kanuni hii: Sisi tunajichukulia juu yetu wenyewe jina la Yesu Kristo tunapofanya na kuweka maagano mata-katifu. Unaweza kutaka kuwakumbusha wanafunzi kwamba mojawapo wa sababu za Mfalme Benyamini kukusanya watu pamoja ilikuwa ni kuwafundisha wao kuhusu kufanya maagano. Yeye pia alimweka wakfu mwanawe Mosia kuwa mfalme juu ya watu (ona Mosia 6:3).

Kuhitimisha, waulize wanafunzi ikiwa yeyote kati yao angependa kushiriki jinsi wanahisi kuhusu kujichukulia juu yao wenyewe jina la Yesu Kristo katika ubatizo. Waulize kutafakari maswali yafuatayo:

• Je! Wewe binafsi unaweza kutumia kanuni kutoka kwa ho-tuba ya Mfalme Benyamini vipi?

• Inamaanisha nini kwako kujichukulia juu yako mwenyewe jina la Yesu Kristo?

Unaweza pia kushuhudia juu ya shangwe ambayo inakuja kupi-tia kuamini katika jina la Yesu Kristo na kutegemea Upatanisho Wake.

Kitengo Kijacho (Mosia 7–17)Waulize wanafunzi: Je! Utasimama imara kwa Yesu Kristo hata kama kufanya hivyo inamaanisha utauawa? Waelezee wanafunzi kwamba wiki ijayo watajifunza mafundisho ya nabii Abinadi. Wahimize kutafuta ujumbe wa Abinadi aliokuwa anapendekeza kuuwasilisha kwa Wanefi, hata ingawa alijua atauawa.

Page 221: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

206

UtanguliziTakribani miaka 80 kabla ya Mosia mwanawe Mfalme Benyamini kuwa mfalme, mtu aliyeitwa Zenifu alio-ngoza kundi la Wanefi kutoka Zarahemla kuishi katika nchi ya Nefi, ambayo waliichukulia kama “nchi yao ya urithi” (ona Omni 1:27–30). Mfalme Mosia alimpatia mtu aliyeitwa Amoni mamlaka ya kuongoza kikundi kidogo kuenda katika nchi ya Nefi ili kujua kichowa-pata kundi la Zenifu. Amoni na wenzake walipata uzao wa kundi la Zenifu likiishi katika utumwa chini ya

Walamani. Zenifu mjukuu wa Limhi alikuwa mfalme wao. Kuwasili kwa Amoni kulimpatia Limhi na watu wake matumaini. Limhi alimuomba Amoni ikiwa ange-weza kutafsiri mchoro iliyokuwa kwenye mabamba 24 ya dhahabu watu wake walikuwa wamegundua. Amoni alieleza kwamba mfalme katika nchi ya Zarahemla, Mfalme Mosia, alikuwa muonaji ambaye angeweza kutafsiri hizi kumbukumbu za kale.

SOMO LA 56

Mosia 7–8

Mapendekezo ya Kufundisha

Mosia 7Amoni anapata nchi ya Lehi- Nefi na kujua jinsi watu wa Mfalme Limhi walikuja-kuwa chini ya utumwa.Andika yafuatayo kwenye ubao: omboleza: kuhisi majuto au huzuni• Ni baadhi ya sababu gani watu wanaweza kuomboleza?Alika mwanafunzi asome Mosia 7:24 kwa sauti, na uulize darasa kufuatilia. Taja kishazi “yote kwa sababu ya dhambi.” Elezea kwamba kifungu hiki kinalenga hali ambayo zilikuja kwa sababu ya chaguzi ovu za kikundi cha watu. Waalike wanafunzi kutafakari kama wameshaomboleza kuhusu hali kama hiyo iliyotendeka “kwa sababu ya dhambi.” Elezea kwamba leo watajifunza Mosia 7–8 ili kujifunza kuhusu mfalme aliyeitwa Limhi na sababu

za kujuta kwa watu wake. Waalike wanafunzi kutafuta kile Limhi aliwahimiza watu kufanya ili kushinda huzuni wao.Alika mwanafunzi asome Mosia 7:1 kwa sauti. Uliza darasa kutambua sehemu mbili zilizotajwa katika kifungu hiki. Nakili mchoro wa kwanza ambao unaambatana na somo hili kwenye ubao, na waalike wanafunzi kufanya vivyo hi-vyo katika shajara zao za kujifunza maandiko au daftari za darasani. Unapotumia mchoro huu, elezea kwamba Kanisa halina msimamo rasmi kuhusu jiografia ya Kitabu cha Mor-moni bali tu kwamba matukio yalitokea katika Amerika.Tazama: Wakati wao wa kujifunza kitabu cha Mosia, wana-funzi wataongeza maelezo zaidi kwenye michoro yao. Ili kuhakikisha kwamba wana nafasi ya kutosha ya kuongeza maelezo haya, nakili mchoro kwenye ubao kama inavyo-onyeshwa. Taja nafasi ya ziada kabla wanafunzi kuanza kuchora. (Kukamilisha mchoro iliopo katika kiambatisho hapo mwisho wa kitabu cha kiada hiki.)Elezea kwamba wakati familia ya Lehi ilipowasili katika nchi ya ahadi, walianzisha katika nchi ya Nefi (wakati mwengine inaitwa nchi ya Lehi- Nefi au nchi ya urithi wa kwanza). Muda mfupi baada ya kifo cha Lehi, Bwana alimwamuru Nefi kutorokea nyikani, akiwachukua wale

wote ambao wangeenda pamoja naye. Watu wa Nefi waliendelea kuishi katika nchi ya Nefi lakini walitenganishwa na wale ambao walimfuata Lamani na Lemueli. Miaka mingi baadaye, Bwana aliamuru kundi la Wanefi kutoroka kutoka nchi ya Nefi. Kundi

Maelezo ya Jumla ya Safari Mosia 7–24

Nchi ya Zarahemla

Nchi ya Nefi (Lehi- Nefi)

Page 222: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

207

MoSia 7– 8

hili hatimaye lilifanya makazi katika nchi iliyoitwa Zarahemla, ambayo ilikuwa kaskazini mwa nchi ya Nefi.Vizazi kadhaa baadaye, mtu anayeitwa Zenifu aliongoza kundi la Wanefi hadi nchi ya Nefi ili “kumilki nchi yao ya urithi” (ona Omni 1:27–30). Zenifu alikuwa amekuwa sehemu ya kundi lingine ambalo lilishindwa kupata ardhi katika eneo hilo (ona Mosia 9:1–2). Waalike wanfunzi kuchora mshale kutoka Zarahemla hadi nchi ya Nefi na upatie jina “Kundi la Wanefi lililoongozwa na Zenifu.” Kundi hili liliondoka Zarahemla karibu miaka 80 kabla Mosia kuwa mfalme.Waalike wanafunzi kupitia Mosia 7:1 tena, wakitafuta kile Mosia alitaka kujua. Baada ya wao kutoa ripoti, waalike kusoma Mosia 7:2–3 ili kupata kile Mosia alifanya ili kupata jibu la swali lake. Waulize wanafunzi kuchora mshale wa pili kutoka Zarahemla hadi nchi ya Nefi, kuashiria safari ya kundi la watafutaji lililoongozwa na Amoni, na uupatie jina vivyo hivyo.Fanya muhtasari wa Mosia 7:4–11 kwa kuelezea kwamba Amoni alipata mji ambamo uzao wa watu Zenifu waliishi chini ya utawala wa Limhi mjukuu wa Zenifu. Limhi aliona kundi la Amoni nje ya kuta za mji. Akifikiria walikuwa baadhi ya makuhani waovu wa baba yake ambaye alikuwa ashafariki, Nuhu, aliwaamuru walinzi wake kuwakamata na kuwatia gerezani (ona Mosiah 21:23). Aliwahoji wao siku mbili baadaye. Waulize wanafunzi kusoma Mosia 7:12–15 kimya, wakitafuta majibu ya Limhi alipojua Amoni alikuwa nani na alitoka wapi.• Kwa nini Limhi alikuwa na furaha jinsi hiyo kugundua Amoni alikuwa anatoka nchi ya

Zarahemla?Rejea tena kwenye neno omboleza kwenye ubao. Fanya muhtasari wa Mosia 7:16–19 kwa kuelezea kwamba Mfalme Limhi alikusanya watu wake pamoja ili kumtambulisha Amoni kwao, kunena nao kuhusu sababu za huzuni wao na majuto yao, na kuwasaidia wao kujua pale pa kugeukia ukombozi.Andika neno sababu kwenye ubao chini ya maelezo ya omboleza. Waalike wanafunzi kadhaa kuchukua zamu kusoma kwa sauti Mosia 7:20–28. Uliza darasa kutafuta vitendo ambavyo Limhi alitambua kama sababu za majaribu na huzuni wa watu wake. (Inaweza kusaidia kuwaelezea wanafunzi kwamba nabii aliyetajwa katika Mosia 7:26 ni Abinadi, ambaye alichomwa hadi kifo wakati wa utawala wa Nuhu baba yake Limhi.) Baada ya vi-fungu kusomwa, waalike wanafunzi wachache kuorodhesha kwenye ubao chini ya sababu kile wamegundua.• Ni nini kinachoonekana kuwa sababu kubwa ya huzuni ya watu hawa? (Uovu, au dhambi.)Waulize wanafunzi kusoma Mosia 7:29–32 kimya. Waalike wao kuchagua kishazi amba-cho kinaonyesha uelewa wa Limhi juu ya uhusiano kati ya dhambi za watu na huzuni ya watu. (Unaweza kuhitaji kuelezea kwamba neno kapi linamaanisha mabaki ya mvunjiko baada ya nafaka kutawanywa kutoka kwa mabua ya ngano. Katika Mosia 7:30, “vuna kapi” humaanisha kupata kitu kilicho bure.) Waalike wanafunzi wachache kusoma na kuelezea vishazi ambavyo wameona.• Je! Kutambua matokeo ya dhambi zetu kunawezaje kutusaidia?Alika mwanafunzi asome Mosia 7:33 kwa sauti. Uliza darasa kutafuta kile Limhi aliwasihi watu wake kufanya.• Ni kanuni gani tunaweza kujifunza kutoka kwa Limhi na watu wake kuhusu athari ya

kutambua na kuhisi huzuni ya dhambi zetu? (Wanafunzi wanapotambua kweli kutoka kwa sura hii, wasaidie kuona kwamba kutambua na kuhisi huzuni wa dhambi zetu kunaweza kutuelekeza sisi kumgeukia Bwana kwa ukombozi. Unaweza kutaka kuandika kanuni hii kwenye ubao.)

Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa vyema kanuni hii, waulize kufikiria kwamba wana mpendwa ambaye anahisi kujuta kwa ajili ya dhambi zake na ambaye ana hamu ya kutubu na kumgeukia Bwana lakini hana uhakika wa kufanya hivyo. Shuhudia kwamba ushauri

Maelezo ya Jumla ya Safari katika Mosia 7–24

Nchi ya Zarahemla

Nchi ya Nefi (Lehi- Nefi)

Kundi la Wanefi lililo-ngozwa na

zenifu Kundi la utafutaji

lililoongzwa na amoni

Page 223: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

208

SoMo la 56

wa Limhi kwa watu wake katika Mosia 7:33 una funguo za kushinda huzuni na majuto ambayo yanaambatana na dhambi. Waalike wanafunzi kupekua Mosia 7:33 kimya, wakita-futa vishazi ambavyo vinaweza kusaidia mtu kujua jinsi ya “kumgeukia Bwana.” (Unaweza kutaka kupendekeza kwamba waweke alama vishazi hivi.)Baada ya muda wa kutosha, waalike wanafunzi wachache kuelezea vishazi ambavyo vinaonekana wazi. Acha kila mwanafunzi kuelezea maana ya kishazi alichochagua kwa (1) akiyaweka kwa maneno yake mwenyewe au (2) kutoa mfano wa vitendo au sifa za mtu ambaye anajitahidi kutumia kanuni zilizoelezewa katika kishazi hiki.Waalike wanafunzi kutafakari kama wana dhambi ambazo hawajatubu ambazo zinawale-tea huzuni na majuto wao na wale wanaowapenda. Waalike wanafunzi kuandika majibu ya maswali yafuatayo katika shajara zao za maandiko:• Unaweza kutumia Mosiah 7:33 katika maisha yako leo?Shiriki ushuhuda wako kwamba tunapomgeukia Bwana kwa moyo wetu wote na akili, Yeye atatukomboa kutokana na kuomboleza kunakotokana na dhambi zetu.

Mosia 8Amoni anajua kuhusu mabamba 24 ya dhahabu na kumwambia Limhi juu ya muonaji ambaye angeweza kutafsiri michoro iliyokuwepoUliza wanafunzi wawili kuja mbele ya darasa. Mfumbe macho mwanafunzi mmoja, na kisha uweke vitabu, vipande vya karatasi, au vitu vingine visivyokuwa na hatari kwenye

sakafu kote katika chumba. Muulize mwanafunzi wa pili kutoa maelekezo kwa sauti kumsaidia mwanafunzi wa kwanza kuvuka darasa bila kugusa kitu chochote kwenye sakafu. Kisha acha mwanafunzi wa pili kuweka kifumba macho. Vipange upya vile vitu kwenye sakafu, na acha mwanafunzi wa kwanza atoe maelekezo. Wakati huu, hata hivyo, mwanafunzi aliyefumbwa macho kwa makusudi ata-puuza maelekezo. (Ongea na mwanafunzi huu kisiri kabla ya darasa, na muulize yeye kupuuza maelekezo.)• Kuna thamani gani kumsikiliza mtu mwingine ambaye anaweza kuona vitu ambavyo sisi hatuwezi kuona?Fanya muhtasari Mosia 8:5–12 kwa kuelezea kwamba Li-mhi alituma kikundi maalum kutafuta usaidizi kutoka Za-rahemla wakati fulani kabla kuwasili kwa Amoni. Kikundi hiki kilitangatanga nyikani, na badala ya kupata Zarahemla, kilipata vifusi vya mabaki ya ustawi ulioangamizwa. Hapo waligundua mabamba 24 ya dhahabu yaliyo na mchoro. (Unaweza kutaka kuelezea kwamba magofu yaliyogundu-liwa na watu wa Limhi yalikuwa kile kilichobaki cha ustawi wa Wayaredi. Kumbukumbu ya Wayaredi, iliyotwaliwa kutoka kwa mabamba 24 ya dhahabu, imejumlishwa katika Kitabu cha Mormoni kama kitabu cha Etheri.) Ongeza

safari hii katika mchoro kwenye ubao, kama inavyoonyeshwa kwenye ukurasa huu. Acha wanafunzi waiongezee kwenye michoro yao pia. Elezea kwamba Mfalme Limhi alitaka kuelewa maandishi yaliyochorwa kwenye mabamba 24. Alimuuliza Amoni kama alijua mtu yeyote ambaye angeyatafsiri Alika mwanafunzi asome majibu ya Amoni katika Mosia 8:13–15. Uliza darasa kutafuta jina ambalo Amoni alitumia kuonyesha mtu ambaye alikuwa na uwezo wa kutafsiri ku-mbukumbu kama hizo. Uliza wanafunzi kupekua Mosia 8:16–19 kimya, wakitafuta uwezo wa ziada wa muonaji. Uliza wanafunzi kadhaa kuelezea kile walichopata.Andika taarifa ifuatayo kwenye ubao: Bwana hutoa manabii, waonaji, na wafunuzi kwa manufaa ya binadamu.• Kuna waonaji wangapi ulimwengu leo? (Washiriki—kumi na watano wa Urais wa Kwa-

nza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili.)

Maelezo ya Jumla ya Safari katika Mosia 7–24

Magofu ya Taifa la Wayaredi katika Nchi ya Kaskazini

Kundi la utafutaji

lililoongozwa na amoni

Kundi la Wanefi lilio-ngozwa na

zenifu

Mabamba 24 ya dhahabu (kitabu

cha etheri)

jaribio la kutafuta

zarahemla

Nchi ya Zarahemla

Nchi ya Nephi (Lehi- Nefi)

Page 224: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

209

MoSia 7– 8

• Ni baadhi vitu gani ambavyo manabii, waonaji, na wafunuzi hutujulisha sisi? (Kama wanafunzi wana shida ya kujibu, uliza kile waonaji wamejulisha kuhusu mada kama vile ndoa na familia, elimu, burudani, na vyombo vya habari, au usafi wa maadili.)

• Je! Maisha yako yamebarikiwa vipi na manabii wa siku za mwisho, waonaji, na wafunuzi?Unaweza kutaka kunena kuhusu vile manabii, waonaji, na wafunuzi wamebariki maisha yako. Waalike wanafunzi kusoma na kutafakari peke yao kuhusu hotuba ya mkutano mkuu wa majuzi ya mshiriki wa Urais wa Kwanza au Akidi ya Mitume Kumi na Wawili na kufu-ata ushauri wa hotuba hio

Page 225: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

210

UtanguliziWakati wa utawala wa Mfalme Benyamini, Zenifu alio-ngoza kundi la Wanefi kutoka Zarahemla kufanya ma-kazi miongoni mwa Walamani katika nchi ya Nefi. Mosia 9–22 ina simulizi juu ya uzoefu wa watu hawa. Mfalme wa Walamani aliwaruhusu watu wa Zenifu kufanya

makazi miongoni mwao na kwamba kwa siri alipanga njama ya kuwaweka katika utumwa. Desturi za uongo za Walamani na chuki kwa Wanefi hatimaye zilileta vita. Watu wa Zenifu walitegemea nguvu za Bwana, na wali-weza kuwafukuza Walamani nje ya nchi yao.

SOMO LA 57

Mosia 9–10

Mapendekezo ya Kufundisha

Mosia 9:1–13Zenifu anaongoza kundi la Wanefi kurudi katika nchi ya NefiUliza wanafunzi wafikirie wakati ambapo walitaka kitu sana. Alika wachache wao kuele-zea kuhusu uzoefu huu. Elezea kwamba leo watajifunza kuhusu mtu aliyetaka kitu sana kwamba alikosa kuona uwezekano wa matokeo ya tamaa yake.Waalike wanafunzi kutazama mchoro wa safari walianza kuchora wakati wa somo la awali. Wakumbushe kwamba mtu aliyeitwa Amoni aliongoza kundi ambalo lilisafiri kutoka Za-rahemla na kumpata Limhi na watu wake katika nchi ya Nefi. (Unaweza kutaka kuelezea kwamba Kitabu cha Mormoni husimulia juu ya watu wawili wanaoitwa Amoni. Mmoja alikuwa mtu ambaye wanafunzi wanajifunza kumhusu leo. Yule mwengine alikuwa mwana wa Mosia ambaye alikuwa mmisionari mkuu kwa Walamani. Wanafunzi wataanza kusoma juu yake katika Mosia 27.) Acha wanafunzi warudi kwenye Mosia 7–8 na watafute tarehe ambayo inatokea hapo chini ya kurasa au katika muhtasari wa sura (karibu na miaka 121 K.K.). Acha walinganishe tarehe hiyo na tarehe iliyopo katika Mosia 9 (karibu miaka 200 K.K., takribani miaka 80 mapema). Uliza ikiwa kuna mtu anayeweza kuelezea mabadiliko ya ghafula katika tarehe.Elezea kwamba kutoka Mosia 8 hadi Mosia 9, mfululizo wa hadithi unaenda nyuma sana mi-aka 80 kusimulia kuhusu Zenifu babu ya Mfalme Limhi. Alika mwanafunzi asome kwa sauti dibaji ya Mormoni kwa kumbukumbu ya Zenifu hapo mwanzoni wa Mosia 9. Kisha muulize

mwanafunzi mwingine asome Mosia 9:1–2 kwa sauti.Acha wanafunzi waongezee katika michoro mshale unao-ashiria safari iliyochukuliwa na kundi la kwanza ambalo li-liondoka Zarahemla hadi nchi ya Nefi. Taja kwamba Zenifu alikuwa sehemu kundi hili. Kama inavyoonyeshwa kwenye mchoro kwenye ukurasa huu, mshale unapaswa kuonyesha kwamba kundi ili lilirudi Zarahemla. Kibandiko kinapaswa kusomeka “Wanefi fulani walitafuta kumilki tena nchi ya Nefi.” (Kwa mchoro kamili, ona kiambatisho hapo mwisho wa kitabu cha kiada hiki.)Muulize mwanafunzi mwingine asome Mosia 9:3–4. Alika wengine wa darasa kufuatilia, wakitafuta (1) kile Zenifu alitaka kukipata sana na (2) kile alizembea kukumbuka.• Inamaanisha nini kuwa na raghba? (Kutamani sana kuzidi kiasi au kupendelea sana kuzidi kiasi katika kutafuta kitu.)• Unafikiria inamaanisha ni kuzembea kumkumbuka Bwana?Elezea kwamba kwa sababu Zenifu alikuwa na raghba na alizembea kumkumbuka Bwana, alifanya makosa. Acha wanafunzi wasome Mosia 9:5–7, 10, wakitafuta lile kosa.

Tarehe katika tanbihi na muhtasari ya suraWaonyeshe wanafunzi makisio ya tarehe zina-zotokea hapo chini ya kila ukurasa (au katika muhtasari wa sura) wa Kitabu cha Mormoni ili kusaidia kuthibitisha muktadha wa matukio kihistoria inavyoelezwa katika kurasa hizo. Wanafunzi wanapoji-fahamisha tarehe hizi, wataona jinsi mtukio ya-lioelezwa katika Kitabu cha Mormoni yanahusi-ana moja na lingine na yale matukio mengine katika historia.

Maelezo ya Jumla ya Safari katika Mosia 7–24

Nchi ya Zarahemla

Magofu ya Taifa la Wayaredi katika Nchi ya Kaskazini

Nchi ya Nephi (Lehi- Nefi)

Kundi la Wanefi lilio-ngozwa na

zenifu jaribio la kupata

zarahemla

Mabamba 24 ya dhahabu (kitabu

cha etheri)

Wanefi fulani walitafuta kumilki tena nchi ya nefi

Kundi la utafutaji

lililoongozwa na amoni

Page 226: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

211

MoSia 9 –10

• Zenifu akikosa kuona nini kwa sababu ya hamu yake ya raghba ili kuimilki nchi ya Nefi?• Kuna hatari gani kuwa na tamaa sana kuzidi kiasi unapofanya maamuzi?• Kuna hatari gani katika kufanya maamuzi bila kushauriana na Bwana? Fanya muhtasari wa Mosia 9:11–13 kwa kuwaambia wanafunzi baada ya miaka 12, watu wa Zenifu walikua sana kwa ufanisi kwamba mfalme Mlamani alikuwa na wayowayo kwa-mba angeweza kuwaweka katika utumwa, kwa hivyo ‘alianza kuwachochea watu wake kwamba wabishane na watu [Zenifu]” (Mosia 9:13).

Mosia 9:14–10:22Walamani walijaribu kuwaweka watu wa Zenifu katika utumwaAndika maneno na vishazi vifuatavyo kwenye ubao: kazi ya shule, kustahimili majaribu, shida na marafiki, uongozi, ajira, mzozo na wanafamilia, michezo.(Kutegemea na mahitaji na hamu za wanafunzi, unaweza kuongeza kitu kingine kwenye orodha.)Alika mwanafunzi kuja mbele ya darasa na ushikilie mkono wake. Weka vitu vidogo, kama vile vitabu au mawe, katika mikono ya mwanafunzi na umuulize kuinua juu. Elezea kwa-mba vitu hivi vinaashiria changamoto zilizoorodheshwa kwenye ubao. Uliza darasa:• Ni katika maeneo gani ungependa kuwa na nguvu zaidi na usaidizi?Ongeza kitu kimoja au viwili kwenye mikono ya mwanfunzi. Uliza darasa:• Umeshahisi kama unabeba zaidi sana na ukatamani ungekuwa na uwezo au nguvu zaidi

za kupambana na changamoto zako?Waalike wanafunzi wawili kuja mbele ya darasa na kuhimili mikono ya mwanafunzi anayeshikilia vitu. Elezea kwamba somo la leo lililosalia ni kuhusu kundi la watu ambao walijipata katika mahitaji ya nguvu za ziada. Pendekeza kwamba, kote katika somo hili, wanafunzi watafute njia ambazo wanaweza kupokea nguvu za ziada katika maisha yao. (Alika wanafunzi waliopo mbele ya darasa kurudi katika viti vyao.)Elezea kwamba Mosia 9 na 10 husimulia mara mbili wakati ambao Walamani walikuja kupigana vita dhidi ya Zenifu na watu wake. Nakili chati ifuatayo kwenye ubao, lakini usijumuishe majibu yaliyo kwenye mabano. Waambie wanafunzi kwamba watapekua vifungu vya maandiko vilivyo katika chati, wakitafuta majibu ya maswali hapo juu ya chati. Alika nusu ya darasa kutumia vifungu vilivyo katika safu ya kwanza ili kupata majibu kuhusu Zenifu na watu wake. Alika ile nusu ingine ya darasa kupekua vifungu katika safu ya pili kwa majibu kuhusu Walamani. Acha mwanafunzi kutoka kwa kila kikundi kuandika majibu yao waliyopata kwenye ubao.

Watu walifanya nini ili kujiatayarisha?

ni nini walichowekea imani yao katika bwana?

Matokeo yalikuwa nini?

zenifu na watu wake

Mosia 9:14–16; 10:1–2, 7, 9–10(Walijiami na kwenda vitani.)

Mosia 9:17; 10:19(Waliomba na kuku-mbuka kwamba bwana alikuwa amewakomboa babu zao.)

Mosia 9:18; 10:20(bwana aliwaimarisha wao, na walifanikiwa kuwafurusha Walamani kutoka kwa nchi yao.)

Walamani Mosia 10:6–8(Walijiami na kwenda vitani.)

Mosia 10:11(hamna chochote. Walitegemea nguvu zao wenyewe.)

Mosia 10:19–20(Walamani walifurushwa kutoka kwenye nchi kwa mauaji makali.)

Baada ya wanafunzi kukamilisha chati, uliza:• Kuna mfanano na tofauti gani unazoona kati ya watu wa Zenifu na Walamani za jinsi

walijiaanda kipigana vita?• Ni kweli gani tunaojifunza kutokana na ulinganishi huu?Andika kanuni ifuatayo kwenye ubao: Bwana atatuimarisha tunapofanya kile tunacho-weza na tukiweka imani yetu Kwake.Rejea nyuma kwenye changamoto zilizoorodheshwa kwenye ubao, na uwakumbushe wanafunzi somo la vitu.

Page 227: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

212

SoMo la 57

• Je! Unafikiria kanuni hii inaweza kutumiwa kwa baadhi ya changamoto hizi?Fikiria kutumia mifano ifuatayo ili kuwasaidia wanafunzi kufikiria kuhusu jinsi wanaweza kutenda sehemu yao na kuwa na imani katika Bwana wanapotafuta nguvu: 1. Una mtihani muhimu unaokuja shuleni, na ungependa kuwa na nguvu za kufanya vyema. 2. Umekuwa unajaribu kuachana na tabia mbaya, na hauhisi kama wewe una uwezo wa

kutosha kutenda hivyo peke yako. 3. Unapata kuwa na shida katika familia yako, na hauhisi kama unaweza kustahamili mhe-

mko mkali unaokuja bila usaidizi fulani.Uliza wanafunzi kurejelea mistari mitatu ya kwanza katika Mosia 9:18. (Unaweza kutaka kupendekeza kwamba waweke alama mistari hii katika maandiko yao.)• Ni wakati gani ulipata uzoefu wa ukweli ulioelezwa katika mistari hii?Unaweza kutaka kuelezea uzoefu wako mwenyewe ambao unaonyesha upendeleo wa Bwana wa kutuimarisha tunapofanya yote tuwezayo na kuweka imani yetu Kwake.Elezea kwamba kabla Zenifu na watu wake kuenda vitani mara ya pili, Zenifu aliwaelezea watu wake kwa nini Walamani walikuwa wamejawa na chuki dhidi ya Wanefi. Andika ma-neno ghadhabu na dhulumiwa kwenye ubao, na uliza wanafunzi ikiwa wanaweza kuelezea kile maneno haya yanamaanisha. (Kughadhabika ni kukasirika sana; kudhulumiwa ni kukosewa au kutendewa pasipo haki au kuonewa.)Ili kuwasaidia wanafunzi kuona kwamba kukasirika, kuwa ghadhabu, na kukataa kusamehe kunaweza kuathiri vizazi, wagawe wao katika majozi na kila uwenzi usome Mosia 10:12–18. Waulize wao kutafuta sababu za kwa nini uzao wa Lamani na Lemueli uliendelea kuchukia uzao wa Nefi.Baada ya wenzi kusoma mistari pamoja, acha wajadili majibu ya maswali yafuatayo. (Fikiria kuandika maswali yafuatayo kwenye ubao wakati wanafunzi wanasoma mistari waliopa-ngiwa, au patiana maswali kwa kila jozi ya wanafunzi kwenye kitini.)• Kwa nini Walamani waliwachukia Wanefi sana hivi?• Ni nani anayeumia wakati tunakasirika au tunakataa kusamehe?• Je! Ghadhabu ya mtu inaweza vipi kuathiri familia yake, sasa na katika siku za usoni?Soma kauli ifuatayo ya Mzee Donald L. Hallstrom wa Sabini. Waulize wanafunzi kusikiliza kile tunaweza kufanya wakati tunahisi kuwa tumekosewa au tumemkasirikia mtu.“Ikiwa unahisi kuwa umekosewa —na mtu yeyote (mwanafamilia, rafiki, muumini mwi-ngine wa Kanisa, kiongozi wa Kanisa, mwenzi wa kibiashara) au na chochote (kifo cha mpendwa, shida za kiafya, kupinduka kwa kifedha, dhuluma, uteja)—shughulikia hilo jambo moja kwa moja na kwa nguvu zote ulizonazo. Na bila kuchelewa, mgeukie Bwana. Fanya imani yote uliyonayo katika Yeye. Acha Yeye akusaidie mzigo wako. Ruhusu neema Yake ipunguze mzigo wako. Kamwe usiache hali za kilimwengu kukulemeza kiroho” (“Turn to the Lord,” Ensign au Liahona, May 2010, 80).Waulize wanafunzi kutafakari kila moja ya maswali yafuatayo. (Unaweza kutaka kuwahi-miza kuandika majibu yao katika shajara zao za kujifunza maandiko au daftari za darasani.)• Je! Una hisia zozote za kuwa umekosewa au hisia za kughadhabika dhidi ya mtu yeyote?• Ni nani unaweza kwenda kwake kwa usaidizi katika juhudi zako za kusamehe? Je! Una-

weza kuepuka vipi hisia za kukosewa na ghadhabu katika siku za usoni?Waulize wanafunzi kufikiria wakati walimsamehe mtu. Waulize wachache wao kushiriki kile walihisi kusamehe na kuachilia mbali hisia zao za kukosewa au ghadhabu. Fikiria kutoa ushuhuda wako mwenyewe kuhusu kutafuta usaidizi wa Bwana ili uweze kuwa-samehe wengine.

Page 228: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

213

UtanguliziKwa sababu ya kiburi cha Mfalme Nuhu na maisha ya anasa yalipeleka wengi wa watu wake katika uovu, Bwana alimtuma nabii Abinadi kumuonya Nuhu na watu wake. Abinadi aliwaonya wao kwamba

watawekwa chini ya utumwa kama hawatatubu. Watu walichagua kutotii maonyo haya, na Mfalme Nuhu aliamuru kwamba Abinadi atupwe gerezani.

SOMO LA 58

Mosia 11–12:17

Mapendekezo ya Kufundisha

Mosia 11:1–19Mfalme Nuhu aliwaongoza watu kwa uovuAndika maswali yafuatayo kwenye ubao kabla ya darasa:

Je! Unaweza kujibu vipi kama wazazi wako wangependekeza kwamba baadhi ya marafiki zako wana ushawishi mbaya juu yako?Je! Unaweza kujibu vipi ikiwa kiongozi wa Kanisa alisema kwamba moja ya shughuli uzipe-ndazo zilikuwa zinaingiliana na ukuaji wako wa kiroho?Je! Ungejibu vipi ikiwa nabii angenena dhidi ya burudani fulani ambayo unaipendelea?

Waalike wanafunzi kutafakari maswali haya kimya kimya. Kisha uliza:• Kwa nini hali hizi zina changamoto?• Je! Ungefanya nini ili kufuata ushauri wa wazazi wako au viongozi wako katika hali

kama hizi?• Kwa nini watu wema wako tayari kufuata ushauri hata kama inahitaji mabadiliko ma-

gumu katika maisha yao?Elezea kwamba katika somo hili, wanafunzi watajifunza kuhusu kundi la watu ambao hawakuwa tayari kufuata ushauri kutoka kwa nabii.Ili kupatiana muktadha wa somo hili, wakumbushe wanafunzi kwamba Zenifu alio-ngoza kundi la watu hadi nchi ya Nefi, pale waliwekwa chini ya utumwa na Walamani. Ingawa raghba ya Zenifu ilimwongoza yeye kudanganywa na Walamani, yeye alikuwa mtu mwema, na aliwafundisha watu wake kuweka imani yao katika Bwana. Kabla Zenifu kufariki, alimkabidhi ufalme kwa Nuhu Mwanawe. (Ona Mosia 9–10.)Elezea kwamba Nuhu alikuwa mtu mwovu. Ili kuonyesha jinsi uovu wake ulivyo shawi-shi watu wake, gawa darasa katika makundi mawili. Uliza kundi la kwanza lisome Mosia 11:1–2, 5–7, na uulize kundi la pili kusoma Mosia 11:14–19. Alika makundi yote kutafuta utondoti wa jinsi uovu wa Mfalme Nuhu ulishawishi watu. Wasaidie wanafunzi kuchanga-nua mistari hii kwa kuuliza maswali kama yafuatayo:• Kwa nini unafikiri watu walikuwa tayari kumhimili Nuhu katika uovu wake?• Kwa nini “maneno bure na kusifu mno” yanaweza kupelekea watu kudanganywa?

(Wanafunzi wanapojadili swali hili, unaweza kutaka kutaja kwamba kusifu mno ni sifa za uongo, kwa kawaida upatianwa ili kuadaa mtu anayesifiwa.)

• Kutoka kwa tukio la watu wa Nuhu, tunaweza kujifunza nini kuhusu jinsi tunafaa kujibu maneno bure na ya kisifu mno? (Tunapoamini maneno bure na ya kusifu mno ya we-ngine, tunajiweka wazi kulaghaiwa.)

• Tunaweza kufanya nini wakati watu wanatuzunguka wanaishi kwa uovu?

Tohoa masomo kwa mahitaji ya wanafunziMasomo mengi yana kweli nyingi za ki-maandiko kuliko vile unaweza kukamilisha katika muda uliopa-tiwa. Unapojifunza maandiko na mtaala, tafuta mwongozo wa Roho Mtakatifu kujua ni mafundisho na kanuni gani zilizo muhimu sana kwa wanafunzi wako kujifunza na kujadili katika somo hili. Roho Mtakatifu atakusaidia kutohoa kila somo kwa mahitaji ya wanafunzi.

Page 229: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

214

SoMo la 58

Mosia 11:20–12:17Abinadi alionya watu kwamba watawekwa chini ya utumwa kama hawatatubuAlika mwanafunzi asome Mosia 11:20 kwa sauti.• Bwana alifanya nini ili kuwasidia watu Nuhu? (Yeye alituma nabii kuwaita wao katika toba.)Andika kanuni ifuatayo kwenye ubao: Mungu hutuma manabii ili kutusaidia kutubu na kuepuka taabu. Elezea kwamba Bwana alimtuma Abinadi mara mbili kuwaonya watu.Nakili chati ifuatayo kwenye ubao. Acha nafasi ya kutosha ya kuandika muhtasari chini ya kila mtajo wa maandiko.

Ujumbe wa abinadi jibu la Watu

onyo la Kwanza Mosia 11:20–25 Mosia 11:26–29

onyo la pili Mosia 12:1–8 Mosia 12:9–17

Ili kusaidia wanafunzi kuelewa ujumbe wa Abinadi, uliza nusu yao kusoma Mosia 11:20–25, ambayo inalezea onyo la kwanza la Abinadi, na uliza ile nusu ingine kusoma Mosia 12:1–8, ambayo inaeleza kuhusu onyo la pili. Alika wanafunzi katika kila kikundi kufanya muhtasari ujumbe wa Abinadi wakati huo mwanafunzi anaandika muhtasari huo kwenye ubao chini ya mistari ifaayo.• Je! Unaona tofauti gani kati ya maonyo mawili ya Abinadi?Ili kuwasaidia wanafunzi kuona tofauti hizi, fikiria kuvuta usikivu wao kwenye Mosia 11:20–25 na warudie vishazi “wasipotubu” na “watu hawa wasipotubu.” Unaweza kutaka kuwatia wao moyo kuweka alama vishazi hivi. Kisha wahimize kugundua tofauti kati ya maneno katika vishazi hivi na maneno katika Mosia 12:1–8. Unaweza kupendekeza kwa-mba wanafunzi wafanye usikivu mahususi kwa maneno nita na wata katika vifungu hivi. (Wasaidie wanafunzi kuona kwamba watu wangeweza kuepuka matokeo haya kama wa-ngetubu baada ya onyo la kwanza. Kwa sababu watu walikataa kutubu, matokeo yakawa lazima na makali sana katika onyo la pili la Abinadi.)• Je! Hizi tofauti zinakufundisha nini kuhusu matokeo ya kutosikia onyo la nabii?• Je! Kuna hatari gani katika kuendelea katika dhambi na kutotubu?Ili kuwasaida wanafunzi kuelewa majibu ya watu kwa jumbe za Abinadi, uliza nusu ya wa-nafunzi kusoma Mosia 11:26–29, wakiangalia majibu ya watu na mfalme wao kwa ujumbe wa kwanza wa Abinadi. Uliza ile nusu ingine ya wanafunzi kusoma Mosia 12:9–17, waki-angalia majibu kwa ujumbe wa pili wa Abinadi. Uliza wanafunzi katika kila kundi kufanya muhtasari wa majibu mwanafunzi mmoja anapoandika muhtasari kwenye chati.• Je! Unafikiria ni kwa nini watu walimjibu Abinadi kwa ghadhabu, ambaye alikuwa ana-

jaribu kuwasaidia? Je! Unafikiria ni kwa nini walimtetea Mfalme Nuhu, ambaye alikuwa anawaelekeza kwenye taabu?

• Katika Mosia 11:29, tunasoma kwamba “macho ya watu yanapofushwa.” Je! Hawa watu walikuwa wamekuwa vipofu kwa ukweli vipi?

Wanafunzi wanapojadili maswali haya, wasaidie kutambua kanuni ifuatayo: Dhambi inaweza kutopofusha tusiweza kutambua ukweli wa maneno ya manabii. Elezea kwamba, katika upofu wao, watu walifikiria kwamba Nuhu alikuwa rafiki yao na kwamba Abinadi alikuwa adui yao, hali kinyume ndio ilikuwa kweli. Waulize wanafunzi kutafakari kimya kimya maswali yafuatayo:• Je! Umeshapata kukasirika au kutetea makosa yako wakati mtu alikukosoa, hata kama

ulijua walikuwa sahihi?

Alika wanafunzi kuandika kwenye ubaoWanafunzi wanapo-andika kwenye ubao, unaweza kutazama darasa na kuendelea ku-endesha mazungumzo. Hii inaelekeza usikivu wa wanafunzi kwenye ubao na wakati huo huo kushiriki. Wakumbushe wanafunzi kwamba hawahitaji kuandika majibu yote —maneno muhimu tu kutoka kwa majibu ya watu. Ili kuongezea ushiriki, unaweza kumwalika mwanafunzi mmoja kua-ndika kwa dakika chache na kumpatia mwanafu-nzi mwingine nafasi ya kuwa mwandishi.

Page 230: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

215

MoSia 11–12:17

• Je! Unaweza kufanya nini kukubali ushauri wa wanafamilia, viongozi wa Kanisa, na manabii wanapokushauri jinsi ya kufuata neno la Mungu?

Taja kwamba watu wengi hutuhimiza kuishi kulingana na neno la Mungu. Ili kuwasaidia wanafunzi kufikiria zaidi kuhusu jinsi ya kuwajibu ipasavyo wale ambao wanatushauri kubadilika au kutubu, rudi kwenye maswali matatu yaliyoandkiwa ubaoni kabla ya darasa. Waulize wanafunzi kujibu mojawapo wa maswali katika shajara zao za maandiko au daftari za darasa. Wanapokuwa na muda wa kutosha wa kuandika, alika wachache wao kuelezea kuhusu wakati walibarikiwa kwa sababu walifuata ushauri kutoka kwa wazazi au viongozi. Wahimize wao kutafuta na kufuata ushauri wa wazazi, viongozi wa Kanisa, na manabii.

Rejeo la Umahiri wa MaandikoUelewa wao wa vifungu vya maandiko utaongezeka wanapobuni maswali yao wenyewe kuhusu vifungu. Waalike wanafunzi kufanya kazi pamoja, kama darasa au vikundi vidogo, kuandika dokezo ambazo zinalenga vifungu mahususi vya umahiri wa maandiko. (Una-weza kutaka kuchagua kikundi cha vifungu ambavyo ungependa wanafunzi kujifunza au kurejea) Kisha acha wao wasome dokezo zao kwako. Alama itatolewa kwako kama utataja kifungu cha umahiri wa maandiko kwa usahihi. Alama zitatolewa kwa darasa kama hauta-weza kutaja kwa usahihi.Tazama: Ikiwa hauna muda wa kutumia kwa shughuli hii kama sehemu ya somo hili, unaweza kuitumia siku ingine. Kwa shughuli zingine za marejeo, ona kiambatisho hapo mwisho wa kitabu hiki cha kiada.

Page 231: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

216

UtanguliziWakati Mfalme Nuhu na makuhani wake wakimhoji Abinadi, nabii aliwakemea kwa kutofundisha au ku-shika amri. Mfalme Nuhu aliwaamuru makuhani wake kumuua Abinadi, lakini Mungu alimlinda Abinadi na

kumpatia nguvu za kuendelea na ujumbe wake. Akim-nukuu Isaya, Abinadi alishuhudia juu ya Yesu Kristo na Upatanisho Wake.

SOMO LA 59

Mosia 12:18–14:12

Mapendekezo ya Kufundisha

Mosia 12:18–13:26Abinadi alimkemea Mfalme Nuhu na makuhani wake kwa kukataa kushika na kufunza amriKuanza somo ili, andika taarifa zifuatazo kwenye ubao:

MIMI NAJUA inamaanisha nini kuishi injili ya Yesu Kristo.MIMI NAISHI injili ya Yesu Kristo.

Waulize wanafunzi kufikiria kimya kimya jinsi taarifa zinawaelezea wao vyema, ukitumia kipimo cha 1 hadi 10 (10 ikiashiria kwamba taarifa iliwaelezea wao vyema sana). • Kwa nini unafikiria ni muhimu kuweza kwa uaminifu kutengeneza taarifa hizi zote?Elezea kwamba wanafunzi wanapojadili maneno ya Abinadi, watajifunza zaidi kuhusu umuhimu wa kujua na kuishi injili. Wakumbushe kwamba katika somo la awali, walija-dili tukio la Mfalme Nuhu na makuhani wake wakimtupa Abinadi gerezani kwa sababu ya unabii wake dhidi yao (ona Mosia 12:1–17). Fanya muhtasari wa Mosia 12:18–24 kwa kuelezea kwamba baadaye Abinadi aliletwa mbele ya Mfalme Nuhu na makuhani wake. Makuhani walimhoji yeye, wakijaribu kumkanganya aseme kitu wangeweza kukitumia dhidi yake. Kisha mmoja wao alimuuliza kuelezea kifungu cha maandiko.Waalike wanafunzi kusoma Mosia 12:25–30 kimya, wakitafuta sababu za Abinadi za kum-kemea Nuhu na makuhani wake. Baada ya wanafunzi kusema kile wamepata, uliza:• Abinadi alisema kwamba Nuhu na makuhani wake walikuwa wamechafua njia za

Bwana (ona Mosia 12:26). Kwa maneno mengine, walikuwa wameharibu vitu vitakatifu na kugeukia njia sahihi ya kuishi. Ni kwa njia gani Nuhu na makuhani walikuwa na hatia ya kuchafua njia za Bwana?

Ili kuwasaidia wanafunzi kujibu swali hili, unaweza kutaka kutaja kwamba makuhani walidai kwamba wokovu ulikuja kwa sheria ya Musa (ona Mosia 12:32). Hata hivyo, hawa-kuweka Amri Kumi, ambazo zilikuwa sehemu ya sheria, na hawakuwafunza watu kuweka amri (ona Mosia 11:1–15; 12:27–29, 37; 13:25–26).Alama kwa taarifa kwenye ubao.• Katika kipimo cha 1 hadi 10, unafikiria kila taarifa inawaelezea vyema Nuhu na

makuhani?Alika mwanafunzi asome Mosia 12:31–33 kwa sauti. Uliza darasa kutambua kanuni Abinadi aliwafunza Nuhu na makuhani wake. (Yeye alifunza kwamba kama tutashika amri za Mungu, tutaokolewa.)Elezea mifano ifuatayo iliyotolewa na Mzee F . Melvin Hammond wa wale Sabini. Wahi-miza wanafunzi kusikiliza umuhimu wa yote kujua na kushika amri.“Miaka mingi iliyopita mmisionari aliyerejea alisimama kwa ujasiri katika mkutano wa sa-kramenti na kutangaza kwa sauti kwamba alijua kutokana kujifunza kwake kwa maandiko kwamba injili ni kweli na kwamba angejitolea maisha yake kwa Bwana na Kanisa Lake. Wiki mbili baadaye alisimama mbele ya askofu wa kata ya wanafunzi, akiwa amedhalilika na kushituka, alipokuwa anakiri kwamba katika wakati wa udhaifu alipoteza maadili yake.

Page 232: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

217

MoSia 12:18 –14:12

Kwa njia ingine uchaji kwa Mwokozi aliokuwa ametangaza ulikuwa umesahaulika katika vuguvugu la shauku yake. Ingawa mwanafunzi ana neno la Mungu, hakuwa ameungani-sha kujifunza kwake na matumizi halisi ya kila siku, kujihusisha na mambo halisi ya, kuishi kama Kristo.“Msichana mrembo alifanya bidii kufikia masharti yote ya kupata Utambuzi wa Usichana. Malengo binafsi yalikuwa yameandikwa kwa makini na ungalifu katika kitabu chake cha ukumbusho. Katakata, aliandika kwamba yeye atafanya miadi na wavulana wastahiki tu na kumpata yule mmoja maalum ambaye atampeleka hekaluni. Alipokuwa umri wa miaka kumi na nane, malengo yake yalisahauliwa; alitoroka na kijana ambaye hakuwa muumini wa Kanisa. Majonzi mengi yalimwagwa na wale waliompenda sana —wazazi wake, wa-limu, na marafiki. Alikuwa ameanguka katika utupu mbaya sana kati ya masharti ya sheria na uhalisi wa ufuasi wa ukweli” (“Eliminating the Void between Information and Applica-tion,” CES satellite training broadcast, Aug. 2003, 17, si. lds. org).• Kwa nini kujua amri haitoshi kutufikisha sisi kwenye wokovu?Onyesha picha ya Abinadi mbele ya Mfalme Nuhu (62042; Gospel Art Book [2009], no. 75). Waulize wanafunzi kuelezea kile kinachotokea katika picha hii. (Mfalme aliamuru kwamba Abinadi auawe. Bwana anamkinga Abinadi.) Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa tukio hili, fikiria kuwauliza wanafunzi watatu kusimama na kufanya drama ya kusoma. Mwanafunzi mmoja atakuwa kama msimulizi. Mwanafunzi wa pili atasoma maneno ya Mfalme Nuhu. Mwanafunzi wa tatu atasoma maneno ya Abinadi. Kwanza, muulize msimulizi na mwana-funzi anayecheza kama Nuhu asome sehemu yake Mosia 13:1–2. Kisha acha mwanafunzi anayecheza kama Abinadi kujibu na Mosia 13:3–4. Msimulizi kisha atasoma Mosia 13:5–6. Kisha mwanafunzi anayecheza Abinadi amalizie na Mosia 13:7–11.Elekeza usikivu wa wanafunzi katika Mosia 13:11.• Unafikiria inamaanisha nini kupata amri kuandikwa katika mioyo yao? (Wasaidie wa-

nafunzi kuelewa kwamba kupata amri kuandikwa katika mioyo yetu, ni sharti tujue na kuishi injili.)

Taja kwamba kabla ya Nuhu kutaka kumuua Abinadi, Abinadi alikuwa ameanza kukariri kifungu cha maandiko ambacho labda kilifanana na mfalme na makuhani wake na hiyo ilikuwa ushahidi wa uovu wao. Acha darasa lisome Mosia 12:34–36 kimya kimya ili kuona kama maandiko Abinadi alimsomea Nuhu na makuhani wake yanaonekana yakifanana. Wasaidie kuona kwamba Abinadi alikuwa ameanza kukariri Amri Kumi.Chora vibao viwili vikubwa, ambavyo havijaandikwa kwenye ubao. Alika mwanafunzi kua-ndika mojawapo ya Amri Kumi katika mojawapo ya vibao hivi. Acha mwanafunzi apitishe chokaa ili mwanafunzi mwingine aandike Amri Kumi. Rudia zoezi hili mpaka wanafunzi waorodheshe yote wanayoweza kukumbuka. Waalike kutafuta majibu yao katika Mosia 12:34–36 na 13:12–24. Unaweza kutaka kuwahimiza wao kuweka alama Amri Kumi katika mistari hii na katika Kutoka 20:3–17 (kifungu cha umahiri wa maandiko).

Shiriki taarifa ifuatayo ya Rais Gordon B. Hinckley:“Amri Kumi ziliandikwa kwa kidole cha Yehova kwenye vibao vya mawe kwa wokovu na usalama, kwa ulinzi na furaha ya watoto wa Isreali, na kwa vizazi vyote ambavyo vitakuja baada ya wao” (“Our Solemn Responsibilities,” Ensign, Nov. 1991, 51).Himiza wanafunzi kurejea Amri Kumi na kufikiria kimya kimya juhudi zao za kibinafsi na kuzishika.

Usomaji wa kidramaUsomaji wa kidrama wa maandiko unaweza kuwasaidia wanafu-nzi kupiga twasira ya watu na matukio katika maandiko. Wahimize wanafunzi kufanya uzo-efu huu kuwa wakupe-ndeza na kufurahia bila kuwaondoa kutoka kwa utakatifu wa matukio ya kimaandiko.

Page 233: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

218

SoMo la 59

Mosia 13:27–14:12Abinadi anafunza kuhusu wokovu kupitia Upatanisho wa Yesu KristoAndika yafuatayo kwenye ubao (unaweza kutaka kuandika kabla ya darasa kuanza). Wau-lize wanafunzi kufikiria kuhusu kile kinachoweza kuingia katika pengo.

“Baada ya utiifu wetu wote na kazi nzuri, hatuwezi kuokolewa kutokana na kifo au athari za dhambi binafsi bila . . .”

Soma kwa sauti taarifa ifuatayo ya Mzee Dallin H. Oaks:“Baada ya utiifu wetu wote na kazi nzuri, hatuwezi kuokolewa kutokana na kifo au athari za dhambi zetu binafsi bila neema zinazotolewa na upatanisho wa Yesu Kristo. Kitabu cha Mormoni huweka haya wazi. Hufunza kwamba ‘wokovu hauji kwa sheria pekee’ (Mosia 13:28). Kwa maneno mengine, wokovu hauji tu kwa kushika amri. . . . Hata wale ambao wanajaribu kutii na kumtumikia Mungu kwa moyo wao wote yote, uwezo, akili, na nguvu zote ni watumishi wasio na faida’ (Mosia 2:21). Mtu hawezi kupata wokovu wake mwe-nyewe” (“Another Testament of Jesus Christ,” Ensign, Mar. 1994, 67).Kamilisha taarifa iliopo kwenye ubao kwa kuandika neema hutolewa na upatanisho wa Yesu Kristo. Kisha uliza wanafunzi wachache kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka kwa Mosia 13:28, 32–35. Uliza darasa kutafuta maneno na vishazi ambavyo vinahusiana na taa-rifa ya Mzee Oaks. Waalike wanafunzi kadha kushiriki kile walichogundua. (Majibu yakini yanaweza kuwa “upatanisho,” “ukombozi wa Mungu,” “kuja kwa Masiya,” na ahadi ya kwamba “Mungu mwenyewe [atakuja] duniani miongoni mwa watoto wa watu.”Elezea kwamba taarifa ya Abinadi kuhusu “sheria’ katika Mosia 13:28 na 32 ni marejeo ya sheria ya Musa, ambayo inajumuisha seti kali za amri zinazohusisha dhabihu, sherehe, na matendo mengine. Sheria ilitolewa ili kuwasaidia Waisraeli kumkumbuka Mungu na kutarajia Upatanisho wa Yesu Kristo. Baada ya muda, Waisraeli wengi walishindwa kuelewa kazi ya Yesu Kristo kama Mwokozi, kufikiria wangeweza kuokolewa tu kwa kupitia utiifu wa sheria ya Musa.• Abinadi alishuhudia kwamba hakuna anayeweza kuokolewa isipokuwa tu kupitia

Upatanisho wa Yesu Kristo (ona Mosia 13:28, 32). Kwa nini ni muhimu kwetu kuelewa ukweli?

Elezea kwamba Abinadi alipokuwa akisema na Nuhu na makuhani, alinukuu unabii wa Isaya kuhusu Yesu Kristo. Waalike wanafunzi kusoma Mosia 14:3–12 kimya. Waulize wata-fute maneno au vishazi ambavyo vinaelezea kile Mwokozi alifanya ili kuleta wokovu wao.Baada ya wanafunzi kujifunza vifungu hivi kwa dakika chache, waulize wao kushiriki kile wamepata. Unaweza kufikiria kuandika majibu yako kwenye ubao. Ili kuwasaidia wanafu-nzi kuhusu huzuni na simanzi kwamba Mwokozi alibeba kwa ajili yao na kuwasaidia wao kufikiria kuhusu kuteseka Kwake kwa ajili ya dhambi zetu, kuwasomea taarifa zifuatazo. Waalike kukamilisha taarifa hizi katika akili zao:Yesu Kristo alibeba huzuni wetu, kama vile . . .Yesu Kristo aliumizwa na kuchubuliwa kwa sababu ya makosa yetu, kama vile . . .Waulize wanafunzi kile taarifa zifuatazo zinamaanisha kwao: “Kwa kuchapwa kwake sisi tuliponywa” (Mosia 14:5). Unaweza kuhitaji kuelezea kwamba neno vichapo inamaanisha vidonda vilivyoachwa kwenye mwili wa Mwokozi wakati alipopigwa kwa mjeledi, au ku-chapwa (ona Yohana 19:1). Kwa kawaida, neno hili humaanisha mateso Yake yote.Baada ya wanafunzi kuelezea hisia zao kuhusu taarifa hii, shuhudia kwamba kupitia ma-teso ya Mwokozi na juhudi zetu wenyewe za kushika amri, na tunaweza kupokea amani na msamaha katika maisha haya na wokovu katika maisha yanayokuja (ona M&M 59:23; Makala ya Imani 1:3). Waalike wanafunzi kuonyesha upendo wao na kumfurahia Mwokozi kwa kushika amri.

Page 234: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

219

UtanguliziAbinadi alipoendelea kumhubiria Mfalme Nuhu na makuhani wake, alishuhudia juu ya kazi ya Yesu Kristo kama Mkombozi. Mmoja wa makuhani wa Nuhu, Alma, alimwamini Abinadi. Mfalme Nuhu alimtupa Alma nje ya kasri lake na kuwaamuru watumishi wake kumuua, lakini Alma alitoroka na kuandika mafundisho

aliyosikia kutoka kwa Abinadi. Baada ya Abinadi kutoa ujumbe wake Bwana aliomtuma kuutoa, Mfalme Nuhu na makuhani wake walitishia kumuua kama hangeka-nusha yale aliyokuwa amesema. Kukata kukana ushu-huda wake, “akapata kifo kwa moto” na “akatia mhuri ukweli wa maneno yake kwa kifo chake” (Mosia 17:20).

SOMO LA 60

Mosia 15–17

Mapendekezo ya Kufundisha

Mosia 15–16Abinadi anafunza kuhusu kazi Yesu Kristo kama MkomboziWapatie wanafunzi dakika mbili za kupata maneno komboa, ukomboa, kombolewa, na ukombozi katika Mosiah 15–16. Unaweza kutaka kupendekeza kwamba waweke alama maneno haya. Elezea kwamba wakati maumbo tofauti ya neno sawa yanatumika katika umbo la maandiko, inaweza kuashiria kwamba neno hili ni muhimu kwa ujumbe wa mwandishi. Wahimize wa-nafunzi kuangalia mafundisho ya Abinadi kuhusu kukombolewa katika somo la leo.Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa kazi ya Yesu Kristo kama Mkombozi, chora mchoro ufuatao kwenye ubao:

Onyesha kwenye mchoro ulioandikwa “Mkosaji” na uwaulize wanafunzi kufikiria kwamba wamefanya jinai. Wamehukumiwa kulipa faini kubwa kama adhabu, na hakuna njia ya kisheria na uaminifu wanayoweza kuepuka kulipa faini wao wenyewe. Waulize wanafu-nzi jinsi wanahisi kukabiliwa na adhabu kama hiyo. Kisha waulize wao kufikiria kwamba mwanafamilia au rafiki anajitolea kulipa faini kwa niaba yao.• Je! Ungehisi vipi kuhusu mtu huyu?Elezea kwamba katika kulipa faini, mwanafamilia au rafiki ambaye amewakomboa kutoka kwa adhabu yao. Neno komboa humaanisha kuachilia kutoka kwa deni au kufanya kuwa huru kwa kulipa fidia. Unaweza kutaka kuwahimiza wanafunzi kuandika maelezo haya karibu na mojawapo wa vifungu katika Mosia 15 vilivyo na umbo la neno komboa.Andika Sisi chini ya Mkosaji. Andika Haki chini ya Adhabu. Elezea kwamba kwa sababu sisi tumetenda dhambi na kuvunja sheria za Mungu, ni sharti tuadhibiwe. Kwa maneno mengine, sisi sharti tulipe madai ya haki. Soma taarifa ifuatayo ya Mzee Richard G. Scott wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili. Waulize wanafunzi kusikiliza baadhi ya matokeo ya kuvunja sheria za Mungu:“Haki inahitaji kwamba kila sheria inayovunjwa iliridhishwe. Unapotii sheria za Mungu, unabarikiwa, lakini hamna muamana wa ziada unaopata ambao unaweza kudunduiza ku-ridhisha sheria ulizovunja. Ikiwa haitatatuliwa, sheria iliyovunjwa inaweza kufanya maisha yako kuwa mabaya na kukuzuia kurudi kwa Mungu” (“The Atonement Can Secure Your Peace and Happiness,” Ensign au Liahona, Nov. 2006, 42).• Kulingana na Mzee Scott, ni nini baadhi ya matokeo ya kuvunja sheria za Mungu?

Mkosaji

faini

adhabu

Page 235: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

220

SoMo la 60

Wanafunzi wanapotambua matokeo ya kuvunja sheria za Mungu, futa neno Faini kutoka ubaoni. Mahali pake, andika Taabu na Kufungiwa kutoka kwa uwepo wa Mungu. Acha wanafunzi wasome Mosia 15:1, 8–9 kimya. Unaweza kutaka kuuliza maswali yafuatayo ili kuwasaidia wao kuelewa baadhi ya mafundisho katika vifungu hivi:• Neno sala ya kuombea humaanisha mtu anakuja kati ya watu wawili au makundi ya watu

ili kuwasaidia wao kupatana—kwa maneno mengine, kuja katika uwiano kwa mmoja na mwingine. Unafikiria inamaanisha nini kwamba Yesu Kristo alikuja “kutuombea”sisi?

• Neno kati humaanisha baina. Unafikiria inamaanisha nini kwamba Mwokozi husimama “kati[yetu] na haki”? Unafikiria inamaanisha nini kuridhisha “madai ya haki”?

Wasaidie wanafunzi kuelewa kwamba haki hudai kwamba tuadhibiwe kwa dhambi zetu. Mwokozi hafuti madai ya haki; Yeye husimama kati yetu na haki ili kuridhisha madai ya haki kwa kuchukua adhabu kwa niaba yetu. Yeye alilipa bei ya kutukomboa sisi—ili kutu-toa kutoka kwa adhabu. Kwenye ubao, weka picha ya Mwokozi (picha kama ile iliyo na kichwa cha Bwana Yesu Kristo [64001]) kati ya mkosaji na adhabu.

Waulize wanafunzi kusoma Mosia 15:5–7 kimya kimya, wakifikiria kuhusu bei Yesu Kristo aliyolipa ili kuwakomboa—ili kusimama kati yetu na madai ya haki.Andika yafuatayo kwenye ubao:

Wale waliochagua kukombolewa Wale wanaokataa kukombolewa

Mosia 15:11–12 Mosia 16:2–5, 12

Gawa darasa nusu. Uliza nusu ya darasa kupekua Mosia 15:11–12, ikitafuta hukla ya watu waliochagua kukombolewa. Uliza ile nusu ingine ya darasa kupekua Mosia 16:2–5, 12, ikitafuta hulka ya watu ambao walikataa kukombolewa. Baada ya muda wa kutosha, uliza kundi la kwanza la wanafunzi kushiriki kile walichopata.• Kulingana na Mosia 15:11–12, ni kina nani watakaokombolewa kutoka kwa dhambi zao?

(Hakikisha wanafunzi wanaelewa kwamba Yesu Kristo anaridhisha madai ya haki kwa wale wanaosikia maneno ya manabii, kuamini katika uwezo Wake wa kuko-mboa, na kutubu dhambi zao.)

Elezea kwamba bei Mwokozi alilipa ni zawadi binafisi kwa yeyote ambaye atachagua kuhitimu kwa ukombozi kwa kutubu na kujitahidi kushika amri na maagano yao pamoja na Bwana.Ili kusisitiza uhalisi wa kibinafsi wa Upatanisho, muulize mwanafunzi kusoma Mosia 15:10 kwa sauti. Kisha elekeza usikivu wa wanafunzi kwa kishazi “ataona mbegu yake” katika kifungu hicho. Unaweza kutaka kupendekeza kwamba waweke alama kishazi hiki. Elezea kwamba katika kifungu hiki, neno mbegu humaanisha watoto.• Ni wakati gani tujifunza kuwa kama “watoto wa Kristo”? (Wakumbushe wanafunzi

kuhusu maneno ya Mfalme Benyamini juu ya somo hili linalopatikana katika Mosia 5. Ona pia somo la 55.)

Unaweza kutaka kupendekeza kwamba wanafunzi wabinafsishe Mosia 15:10 kwa kua-ndika majina yao katika kishazi “mbegu yake.” Waalike wao kutafakari kwa muda kile hii inamaanisha.• Je! Mafundisho haya yanaathiri vipi uelewa wako wa Upatanisho?Waulize wanafunzi ambao walisoma Mosia 16:2–5, 12 kushiriki kile walipata kuhusu wale ambao walikataa kukombolewa. Ili kusisitiza uzito wa kukataa kukombolewa, waulize wanafunzi kusoma Mosia 16:5 kimya.• Ni nini kitafanyika kwa mchoro kwenye ubao ikiwa mkosaji ataendelea katika dhambi

na kukataa kutubu? (Wanafunzi wanapojibu, ondoa picha ya Yesu Kristo kutoka kwa

MkosajiSisi

adhabuhaki

taabuKufungiwa kutoka kwa

uwepo wa Mungu.

Page 236: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

221

MoSia 15 –17

mchoro. Unaweza kusisitiza kwamba kwa mtu kama huyu, “ni kama vile hakukuwa na ukombozi uliofanywa.”)

Waalike wanafunzi kusoma Mafundisho na Maagano 19:16–17 ili kugundua kile kitaka-chotokea kwa wale wanaokataa kutubu na kukubali ukombozi wa Mwokozi. Unaweza kutaka kuwahimiza kuandika M&M 19:16–17 katika maandiko yao karibu na Mosia 16:5.Weka picha ya Mwokozi tena katika mahali pake kwenye ubao.• Ni kweli gani ambazo umejifunza leo kuhusu Mkombozi wako?Baada ya wanafunzi kujibu swali hili, elezea kwamba katika ziada ya kufundisha kwa-mba Mwokozi amejitolea kutukomboa sisi kutokana na adhabu ya dhambi zetu, Abinadi alifunza kwamba Mwokozi hutukomboa kutoka kwa kifo. Waulize wanafunzi kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka kwa Mosia 16:6–11. Shiriki ushuhuda wako kwamba kwa sababu Upatanisho wa Yesu Kristo, watu wote watafufuliwa. Unaweza kutaka kutaja kwamba watu wema watafufuliwa katika hali ya furaha.Waalike wanafunzi kuandika katika shajara zao za kujifunza maandiko au daftari za dara-sani kuhusu hisia zao kwa Mkombozi wao na kile watafanya ili waweze kupokea uko-mbozi Yeye hupatiana.

Mosia 17Alma alimwamini Abinadi na akatupwa nje; Abinadi alichomwa motoWaulize wanafunzi:• Je! Ushaona mtu akisimama imara kwa kile kilicho sahihi wakati ni vigumu kwao kufa-

nya hivyo? Ni nini kilitendeka?Onyesha picha ya Abinadi mbele za Mfalme Nuhu (62042; Gospel Art Book [2009], no. 75). Fanya muhtasari wa Mosia 17:1–6 kwa kuelezea kwamba wakati Abinadi alihitimisha uju-mbe wake, kuhani aliyeitwa Alma alijaribu kumshawishi mfalme kwamba Abinadi alikuwa ananena ukweli na anafaa kuachiliwa. Mfalme alimtupa Alma nje na kuwatuma watumishi kumuua. Alma alijificha na kuandika maneno ya Abinadi. Siku tatu baadaye, mfalme na makuhani wake walimhukumu Abinadi kifo.Gawa wanafunzi katika jozi. Waulize wao kujifunza vifungu vya maandiko vifuatavyo pamoja na wenzi wao: Mosia 17:7–10, ambavyo ni kuhusu chaguo za Abinadi, na Mosia 17:11–12, ambayo ni kuhusu chaguo za Mfalme Nuhu. Waulize wao kulinganisha chaguo za Abinadi na chaguo za Mfalme Nuhu. Pia waulize wao kujadili maswali yafuatayo. (Una-weza kutaka kuandika maswali haya kwenye ubao.)• Kwa nini unafikiria maneno ya Abinadi yalimwathiri Mfalme Nuhu katika njia hiyo?

(Ona Mosia 17:11.) Makuhani wa Mfalme Nuhu walimuathiri vipi? (Ona Mosia 17:12–13.)

• Ni mafunzo gani tunaweza kujifunza kutokana mfano wa Abinadi? (Jibu moja wanafu-nzi wanaweza kupatiana ni tunaweza kuwa wakweli kwa Mungu katika hali zote.)

Ikiwa inawezekana, wapatie wanafunzi nakala ya taarifa ifuatayo ya Rais Gordon B. Hinckley:“Kuwa thabiti—katika kusimama katika haki.Tunaishi katika nyakati za mahafikiano. Katika hali ambayo kwayo tunakabiliana nayo kila siku, tunajua kile kilicho haki. Sisi lazima tu-kuze nguvu za kufuata imani yetu” (“Building Your Tabernacle,” Ensign, Nov. 1992, 52).Unaweza kutaka kuwaalika wanafunzi kuandika mimi nitakuwa mkweli kwa Mungu katika hali zote katika maandiko yao karibu na Mosia 17:9–12. Elekeza usikivu wa wanafunzi kwa maneno ya mwisho ya Abinadi, yaliyopo katika Mosia 17:19—“Ee Mungu, pokea nafsi yangu.” Kisha muulize mwanafunzi asome Mosia 17:20 kwa sauti.• Ni nini kinacho kupendeza kuhusu maneno ya mwisho ya Abinadi?Waulize wanafunzi kujibu maswali yafuayo katika shajara zao za kujifunza maandiko:• Utafanya nini ili kuwa mkweli kwa Mungu katika hali zote?Baada ya muda wa kutosha, waalike wanafunzi kadhaa kushiriki kile wameandika. Pia waulize ikiwa kuna wanafunzi wanaotaka kushiriki kile injili inamaanisha kwao na kile wamefanya hapo awali kuwa wakweli kwa Bwana wakati wa nyakati ngumu. Hitimisha kwa ushuhuda wako.

Page 237: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

222

Vifaa vya Matayarisho kwa Mwalimu wa Mafunzo ya NyumbaniMuhtasari wa Masomo ya Kila Siku ya Mafu-nzo ya NyumbaniMuhtasari ufuatao wa mafundisho na kanuni wanafunzi walijifunza walipokuwa wakijifunza Mosia 7–17 (kitengo cha 12) haikupangiwa kufunzwa kama sehemu ya somo lako. Somo unalofunza linazingatia tu chache ya haya mafundisho na kanuni. Fuata msukumo wa Roho Mtakatifu unapofikiria mahitaji ya wanafunzi.

Siku ya 1 (Mosia 7–8)Walipokuwa wanajifunza Mosia 7–8, wanafunzi walizingatia juu ya uhusiano kati uovu na kifungo. Pia walijifunza kutoka kwa maneno ya Mfalme Limhi kwa kutambua uovu wetu na hisia za huzuni kwayo kunaweza kutupelekea kumgeukia Bwana kwa ukombozi. Amoni alimhakikishia Limhi kwamba Bwana amepatiana manabii, waonaji, na wafunuaji kwa faida ya binadamu.

Siku ya 2 (Mosia 9–10)Wanafunzi walijifunza zaidi kuhusu jinsi kundi la Wanefi, lilioitwa watu wa Zenifu, lilifanya makazi miongoni mwa Walamani. Ukweli ufuatao ulimulikwa wakati Zenifu na watu wake walikwenda kupingana dhidi ya Walamani wapenda vita: Bwana atatuimarisha kama tutafanya yote tuwezayo na kufanya imani katika Yeye.

Siku ya 3 (Mosia 11–14)Mfalme Nuhu alisababisha watu wake kufanya madhambi na uovu. Wanafunzi waligundua kwamba Mungu hutuma manabii ili kutusaidia kutubu, kuepuka taabu, na kupata wokovu. Kupitia mafundisho ya nabii Abinadi, wanafunzi walijifunza kwamba ikiwa tunaweka amri za Mungu tutao-kolewa. Pia walijifunza kwamba Upatanisho wa Yesu Kristo in chanzo cha wokovu.

Siku ya 4 (Mosia 15–17)Kabla kifo chake cha kishahidi, Abinadi alitamka kwa ujasiri kwamba Upatanisho wa Yesu Kristo huridhisha madai ya haki kwa wale wanaoamini katika nguvu za ukomboaji za Mwokozi, wakatubu dhambi zao na kushika amri. Abinadi pia alifunza kwamba kwa sababu ya Upatanisho wa Yesu Kristo, watu wote watafufuka. Kupitia kujifunza mafundisho haya, wanafunzi waliakisi juu ya umuhimu wa kutegemea Mwokozi na kuwa mkweli kwa Mungu katika hali zote.

UtanguliziMosia 7–17 inaelezea safari na uzoefu wa watu kadhaa na ma-kundi ya watu. Uchaguzi wa Zenifu ulisababisha kundi la Wanefi kufanya makazi miongoni mwa Walamani ambao ulikuwa na athari kwa mataifa yote. Kwa mfano, watu wa Zenifu na uzao wao walipata majaribu, uasi, utumwa, kuzaliwa upya kiroho, na ukombozi. Sehemu ya kwanza ya somo hili itawapatia wana-funzi nafasi ya kurejea majina, maeneo, na matukio ambayo walisoma wiki hii. Sehemu ya pili ya somo hili itawasaidia wa-nafunzi kutambua mada muhimu ya ujumbe wa nabii Abinadi kwa watu—Yesu Kristo na Upatanisho Wake. Ulikuwa ni ujumbe ambao Abinadi akiwa radhi kufa kwa ajili yake.

Mapendekezo ya Kufundisha

Mosia 7–17Marejeo ya mazingira ya kihistoria na mafundishoIli kukusaidia kuelezea matukio katika somo ili, rejelea chati katika “Maelezo ya Jumla Mosia 7–24” katika kitengo cha 12, siku ya 1 ya mwongozo wa kujifunza wa mwanafunzi. Waalike wanafunzi kusoma Mosia 7:1–2, na acha watambue nchi mbili ambazo zimetajwa. Waulize waeleze kwa nini baadhi ya maku-ndi ya Wanefi yalitaka kusafiri kutoka nchi moja hadi nyingine.

Andika majina ya nchi mbili katika pande mkabala kwenye ubao (au kipande cha karatasi):

Nchi ya Zarahemla Nchi ya Nefi (Lehi- Nefi)

Maswali yafuatayo yanaweza kusaidia wakati wewe na wa-nafunzi mnaporejea matukio. Andika kwenye ubao majina ya watu binafsi mnapojadili. Unaweze kutumia yote au baadhi ya maswali yafuatayo, kutegemea na maoni ya wanafunzi:

• Kwa nini Zenifu alitaka kuhama kutoka nchi ya Zarahemla? (Ona Mosia 9:1, 3.)

• Zenifu, Nuhu, na Limhi wanahusiana vipi? (Ona Mosia 7:9.)• Nuhu alikuwa mfalme wa aina gani? (Ona Mosia 11:1–5, 11.)• Mungu alifanya nini ili kumshawishi Nuhu na watu wake ku-

geuka kutoka kwa uovu wao mkubwa na madhambi? (Yeye alimtuma Abinadi Nabii Wake kuwaonya watubu.)

• Unaweza kutuambia nini kuhusu Alma? (Majibu yanaweza kujumuisha kwamba yeye alikuwa mmoja wa makuhani wa Mfalme Nuhu, kwamba aliamini na kuyaandika maneno ya Abinadi, na kwamba aliatoroka kuepuka kuuawa.)

• Kwa nini Musa na Isaya ni muhimu katika sura hizi, ingawa waliishi zamani sana kabla ya Abinadi na katika sehemu ingine ya ulimwengu?

• Kwa nini Limhi aliwatuma watu 43 kati ya watu wake huko nyikani? (Limhi na watu wake walikuwa utumwani chini ya Walamani na walitaka usaidizi kutoka kwa watu wa Zarahe-mla.) Walipata nini badala ya Zarahemla? (Walipata magofu ya ustawi na mabamba 24 ya dhahabu yenye maandishi juu yake.)

Somo la Mafunzo- NyumbaniMosia 7–17 (Kitengo cha 12)

Page 238: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

223

SoMo la MafUnzo- nyUMbani

• Amoni na watu wengine 15 walifanya nini? (Walitumwa na Mosia kujulia ni kitu gani kilichowatokea watu wa Zenifu. Walipata uzao wa watu hawa katika utumwa. Zenifu mjukuu wa Limhi alikuwa mfalme wao.)

• Ni nani alikuwa mfalme katika Zarahemla na kama nabii, muonaji, na mfunuaji? (Mosia.) Kwa nini kazi yake kama mu-onaji ilikuwa muhimu kwa Limhi? (Limhi alijua kwamba Mosia angeweza kutafsiri maandishi yaliyokuwa kwenye mabamba 24 ya dhahabu.)

Taja kwamba takribani miaka 80 ilikuwa imepita kati ya Zenifu na watu wake kuondoka Zarahemla na kuwasili kwa Amoni na wenzake katika nchi ya Nefi.

Baada ya kuwasaidia wanafunzi kuelewa vyema matukio ya ki-historia, wakumbushe kwamba kuna mtu mwengine walijifunza juu yake wiki hii ambaye jina lake bado halipo kwenye ubao.

Muulize kila mwanafunzi kusoma Mosia 16:6–8 na kutambua jina la huyu mtu. Waambie wanafunzi kwamba ingawa hii se-hemu ya Kitabu cha Mormoni inashughulikia wingi wa historia, pia inaangazia mafundisho ya wokovu kupitia Yesu Kristo.

Ili kusisitiza umuhimu wa wokovu kupitia Yesu Kristo, nakili chati ifuatayo kwenye ubao au ipatiane katika kitini. Waalike wanafu-nzi kufanya kazi katika majozi ili kujifunza marejeo ya maandiko yaliyoorodheshwa katika chati na wajadili kile wamepata. Kwa sababu baadhi ya matumizi maswali haya ni ya kibinafsi sana katika uasili, wanafunzi wanaweza kuamua kama watayajibu kwa sauti kwa kila moja, kuandika majibu katika shajara zao za kujifunza maandiko, au kimya wafikirie majibu yao.

Ili kuwasidia wanafunzi kuakisi juu ya kile wamejifunza katika shughuli hii ya maandiko na masomo haya ya wiki, uliza: Je! Kanuni na mafundisho uliyojifunza wiki hii yanasaidia vipi kuta-zamia ondoleo la dhambi zako?

Wapatie wanafunzi nafasi ya kushuhudia juu ya Yesu Kristo.

Njia moja unaweza kuhitimisha somo la leo ni kusoma Mosia 16:13–15 na kushiriki ushuhuda wako kwa haja yetu kwa Mwokozi. Njia ingine ambayo ya kusisitiza kwa wanafunzi wako mafundisho au kanuni mbili walizojifunza wiki hii: kwamba Upatanisho wa Yesu Kristo ni chanzo cha wokovu na kwa-mba Yesu Kristo huridhisha madai ya haki kwa wale wote watakaotubu.

Kitengo Kifuatacho (Mosia 18–25)Mosia 18–25 hufunua jinsi makundi mawili yalitoroka kutoka utumwani wa maadui zao na kurejea salama hadi Zarahemla. Utajifunza jinsi Mungu aliongoza kila kikundi kutoroka. Kundi moja lilifuata mpango wa Gidioni wa kuwalewesha walinzi, na lile kundi lingine lilitoroka kwa kumfuata Alma wakati Walamani walikuwa wamelala. Ni nini kiliwafanya Walamani kulala?

andiko Kile cha Kutafuta. Matumizi ya Maswali

Mosia 7:33 je! tunaokolewa vipi kutokana ya kifungo cha kiroho na kimwili.

Kati ya vitu vitatu limhi alisisitiza, ni kitu gani unahisi unahitaji kufanyia kazi katika kujiimarisha wakati huu?

Mosia 13:11 Kwa nini Mfalme nuhu na wengi wa watu wake walishi-ndwa kuelewa misheni ya yesu Kristo.

Kuna ushahidi gani katika maisha yako kwamba amri zimeandikwa katika moyo wako? ni kwa njia gani unaji-funza na kufunza wema?

Mosia 14:3–7 Maneno na vishazi muhimu kuhusu mateso na kukata-liwa kwa Mwokozi.

ni kwa njia gani ambazo watu humpuuza na kumkataa Mwokozi leo? je! Mtu anaweza kuficha uso kutoka Kwake vipi? je! Mtu anaweza kufanya kinyume vipi?

Mosia 15:6–9, 11 Kile yesu Kristo “alivunja” na kile yeye ‘alipata”; pia , kile tunapata kwa sababu ya dhabihu ya Mwokozi.

ni kwa njia gani bwana majuzi aliingilia kati kwa niaba yako? je! yeye ameshasimama kati yako na madai ya haki vipi?

Page 239: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

224

UtanguliziBaada ya kifo cha Abinadi, Alma kisiri alifunza maneno ya Abinadi miongoni mwa watu. Wale ambao wali-omwamini walikusanyika katika Maji ya Mormoni ili kujifunza zaidi. Alma alihubiri ujumbe juu ya “toba, na ukombozi, na imani katika Bwana” (Mosia 18:7). Wale

ambao walikubali mafundisho yake na kutubu dhambi zao waliingia katika agano la ubatizo. Watu walikuwa waaminifu kwa hili agano, na walisaidiana mmoja na mwingine kwa mali na kiroho.

SOMO LA 61

Mosia 18

Mapendekezo ya Kufundisha

Mosia 18:1–16Alma anafunza na kubatiza watuOnyesha picha ya Abinadi mbele za Mfalme Nuhu (62042; Gospel Art Book [2009], no. 75). Onyesha makuhani katika usuli wa picha. Elezea kwamba Mosia 18 husimulia uzoefu wa Alma, ambaye alikuwa mmoja wa makuhani wa Mfalme Nuhu.

Alika wanafunzi asome Mosia 18:1, 3–6 kimya. Uliza darasa litafute kile Alma alifanya baada ya kusikia ushuhuda wa Abinadi. Baada ya wanafunzi kusema kile wamejifunza, waalike wao kurejelea michoro yao inayoonyesha maelezo ya jumla katika Mosia 7–24. Waelekeze wao kuchora Maji ya Mormoni katika eneo lifaalo. (Kwa mchoro kamili, ona kiambatisho hapo mwisho wa kitabu cha kiada hiki.)Elezea kwamba Alma alidhamiria mafundisho yake kuwa-tayarisha watu kwa ubatizo. Waulize wanafunzi kufikiria kwa muda kuhusu ubatizo wao. Ili kuwasaidia wao kutafa-kari kile ubatizo wao unamaanisha kwao, unaweza kuuliza maswali kama yafuatayo:• Ni utondoti gani unaweza kukumbuka kuhusu uzoefu wako?• Je! Wazazi, walimu, na viongozi wako walikusaidia kuji-tayarisha vipi kwa ubatizo?• Ni kitu gani unachothamini zaidi kuhusu ubatizo sasa kuliko ilivyokuwa wakati ulibatizwa?Elezea kwamba hadithi ya Alma akifundisha na kubatiza watu katika Maji ya Mormoni inaweza kutusaidia kupata uelewa wa kina wa agano la ubatizo.

Waulize wanafunzi kusoma Mosia 18:2, 7 kimya, wakitafuta kile Alma alifunza watu alipo-kuwa akiwatayarisha wao kwa ubatizo.• Kulingana na vifungu hivi, ni mafundisho na kanuni gani ambazo Alma alisisitiza?• Je! Unafikiria uelewa wa kweli hizi unaweza kumsaidia mtu vipi kujitayarisha kwa

ubatizo?Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa kile wanapaswa kufanya ili kuweka agano la ubatizo, na kuwasaidia wao kutathimni baraka walizopokea kama matokeo, nakili chati ifuatayo kwenye ubao. Husijumuishe mtajo wa taarifa au marejeo ya maandiko katika sehemu ya chini ya chati.

Maelezo ya Jumla katika Mosia 7–24

Nchi ya Zarahemla

Magofu ya Taifa la Wayeradi katika Nchi ya Kaskazini

Maji ya Mormoni

Nchi ya Nefi (Lehi- Nefi)

Kundi la Wanefi lililo-ongzwa na

zenifu jaribio la kupata

zarahemla

mabamba 24 ya dhahabu (kitabu

cha etheri)

Wanefi fulani walitafuta kumilki tena nchi ya nefi

Kundi la utafutaji

lililoongozwa na amoni

Page 240: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

225

MoSia 18

Mimi niko tayari ku . . . Mungu alihadi . . .

Saidia kubeba mzigo wa wengine ili kwamba iwe rahisi (ona Mosia 18:8).omboleza na wale ambao wanaomboleza (ona Mosia 18:9).Wafariji wale ambao wanaohitaji faraja (ona Mosia 18:9).Simama kama shahidi wa Mungu nyakati zote, katika vitu vyote, na katika mahali popote (ona Mosia 18:9).Mtumikie Mungu na kuweka amri zake (ona Mosia 18:10).

Kwamba mimi nitakombolewa na Mungu (ona Mosia 18:9).Kwamba mimi ni sehemu ya ufufuo wa kwanza (ona Mosia 18:9).Kwamba nitapokea uzima wa milele (see Mosiah 18:9).yeye atamimina Roho yake juu yetu (ona Mosia 18:10).

Elezea kwamba kabla ya kuwaalika watu kubatizwa, Alma aliwaambia wao kuhusu mi-tazamo na vitendo ambavyo vinaonyesha wako tayari kufanya na kuweka agano hili na Bwana. (Unaweza kutaka kuwakumbusha wanafunzi kwamba agano ni makubaliano kati ya Mungu na mtu lakini kwamba Mungu na mtu “hawafanyi kama watu wanaotoshana katika makubaliano. Mungu hutoa masharti ya agano, na watu wanakubali kufanya kile yeye atawauliza kufanya. Mungu kisha ameahidi baraka fulani kwa utiifu wao” [Guide to the Scriptures, “Covenant,” scriptures.lds.org]. Kwa maelezo ya watakatifu wa siku za mwisho kuhusu masharti ya kubatizwa Mafundisho na Maagano 20:37.)Gawa darasa katika nusu. Alika nusu moja ya darasa kupekua Mosia 18:8–11 kutafuta kile Alma alifunza tunapaswa kuwa radhi kufanya tunapobatizwa. Alika ile nusu ingine ya darasa kupekua kifungu hicho hicho na kutambua jinsi Bwana aliahidi kutubariki kama tutaweka agano letu. Baada ya wanafunzi kuwa na muda wa kujifunza mistari, waulize baadhi yao kuja kwenye ubao na kuandika katika safu ifaayo kile wamegundua.Ili kuwasaidia wanafunzi kuthamini agano lao la ubatizo, uliza:• Je! Vitendo gani na mitazamo gani katika safu ya kwanza vinamaanisha nini kwako?• Kwa nini ahadi zilizoorodheshwa katika safu ya pili ni muhimu kwako?Waulize wanafunzi kupekua Mosia 18:12–16 kimya, wakitafuta njia ambazo kwazo Alma na watu wake walibarikiwa walipofanya agano la kumtumikia Bwana. Waalike wanafunzi kutoa ripoti ya kile wamepata. Unaweza kutaka kutaja kwamba Alma alijawa na Roho wa Bwana alipokuwa akijitayarisha kumbatiza Helamu na kwamba wote Alma na Helamu walijawa na Roho wakati ubatizo ulikamilika, kuonyesha kwamba Bwana alikuwa tayari ameanza kutimiza agano lake la kumimina Roho Yake kwa watu.Shiriki ushuhuda wako kwamba tunapokea Roho wa Bwana na ahadi ya uzima wa milele kwa kufanya na kuweka agano la ubatizo.

Mosia 18:17–30Alma anaanzisha Kanisa la Yesu Kristo miongoni mwa watuSoma taarifa ifuatayo ya Rais Henry B. Eyring wa Urais wa Kwanza:Kutoka siku ya ubatizo kupitia matukio muhimu ya kiroho katika maisha yetu, tunafanya ahadi na Mungu na Yeye anafanya ahadi nasi. Yeye daima huweka ahadi Zake zinazotolewa kupitia watumishi Wake wenye mamlaka, lakini ni jaribio la maisha yetu la kuona kama tutafanya na kuweka maagano yetu Kwake” (“Witnesses for God,” Ensign, Nov. 1996, 30).Warejeshe wanafunzi kwenye chati katika ubao. Elezea kwamba sasa watajifunza ku-husu jinsi watu wa Alma waliishi kulingana na agano la ubatizo na jinsi walibarikiwa kwa kufanya hivyo. Gawa wanafunzi katika makundi mawili. Uliza kundi moja lijifunze Mosia 18:17–23 na lile kundi lingine lijifunze Mosia 18:24–30. Wanaposoma, alika makundi yote kutafuta baadhi ya njia Alma alifunza watu ambazo walifaa kuishi ili kuweka agano lao la ubatizo. Uliza wanafunzi binafsi kutoka kwa kila kikundi kuripoti kile wamepata kwa we-nzi wao kutoka kwa kikundi kingine. Au pata mwakilishi kutoka kwa kila kikundi kuripoti kile yeye amejifunza kwa darasa lote. • Je! Agano lako la ubatizo linaathiri vipi jinsi unavyoishi kila siku? (Fikiria kuwaalika wanafunzi

kujibu swali hili kwa kuongea kuhusu jinsi agano lako la ubatizo linaathiri jinsi wanawatendea wanafamilia, ni aina gani ya burudani wanachagua, au jinsi wanaingiliana na wenzi wao.)

Page 241: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

226

SoMo la 61

Waalike wanafunzi kurejelea Mosia 18:17, 22, 29 ili kupata maneno na vishazi ambavyo vinaonyesha jinsi watu walibarikiwa kwa kuweka maagano yao. Orodhesha baraka kwenye ubao chini ya chati ya agano la ubatizo. (Unaweza kutaka kuwakumbusha kwamba kishazi “watoto wa Mungu” [Mosia 18:22] ina maana ya sisi kuwa warithi wa uzima wa milele kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo [ona Mosia 5:6–8, 15].)Ili kuwasidia wanafunzi kuona kwamba baraka kuu huja kwa wale ambao wanaweka agano la ubatizo, warejeshe wanafunzi kwenye chati kwenye ubao, na uulize:• Ni kwa njia gani umeona marafiki zako, wanafamilia wako, au washiriki wa kata yako

wakibarikiwa kwa kuweka maagano yao?• Je! Bwana amekubariki vipi kwa kuweka maagano yako ya ubatizo?Toa ushuhuda wako kuhusu jinsi kuweka maagano kumeleta baraka katika maisha yako.

Mosia 18:31–35Wale ambao walikuwa wa Kanisa walitoroka udhalimu wa Mfalme NuhuFanya muhtasari wa Mosia 18:31–33 kwa kuelezea kwamba siku moja, Alma na watu wake walipokuwa wamekusanyika kusikia neno la Bwana, waligunduliwa na watumishi wa Mfalme Nuhu. Mfalme kisha alituma jeshi lake kuwaangamiza.Alika mwanafunzi asome Mosia 18:34 kwa sauti. Taja kwamba tanbihi a inawarejesha wasomaji kwa Mosia 23:1. (Unaweza kutaka kuwaalika wanafunzi kuweka alama tanbihi hii.) Elezea kwamba tukio katika Mosia 18:34 linaendelea katika Mosia 23:1, baada ya sura ya 19–22 imeandikwa uzoefu wa watu wa Limhi. Uliza mwanafunzi asome Mosia 23:1–2 kwa sauti.• Ni kwa jinsi gani Alma “aliarifiwa” juu ya hatari iliyowakabili watu wake?Andika kanuni ifuatayo kwenye ubao: Bwana anaweza kuwaonya watu wema wana-pokuwa hatarini. (Unaweza kutaka kuwaalika wanafunzi kuandika kanuni hii ukingoni karibu na Mosia 18:34.) Ili kuonyesha ukweli huu, soma hadithi ifuatayo ya Mzee Neil L. Andersen wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili:“Akifanya kazi kama ajenti maalum wa FBI, rafiki yangu alichunguza makundi ya jinai yaliyokuwa yanasafirisha madawa haramu hadi Marekani.“Wakati mmoja, yeye na ajenti mwenzi walikwenda kwa nyumba ambayo ilidhaniwa kuwa na muuza madawa aliyekuwa anasambaza kokeini. Rafiki yangu anaeleza kile kilichotokea:“‘Tulipogonga mlango wa muuza madawa. Mshukiwa alifungua mlango, na alipotuona sisi, alijaribu kutuzuia tusione. Lakini alikuwa amechelewa; tungeweza kuona kokeini kwenye meza.“‘Mwanaume na mwanamke ambao walikuwa mezani mara moja wakaanza kuondoa kokeini. Tulihitaji kuwazuia wasiharibu ushahidi, kwa hivyo nilimsukuma kando yule mshukiwa wa madawa ambaye alikuwa anazuia mlango. Nilipokuwa nikimsukuma, macho yangu yalikutana na yake. Cha kustaajabisha, hakuonekana kukasirika au kuogopa. Alikuwa anatabasamu.“Macho yake na tabasamu la kuzima ilinipatia onyesho kwamba yeye alikuwa hana hatari, mara kwa upesi nikamuacha na kuanza kwenda kwenye meza. Mshukiwa sasa alikuwa nyuma yangu. Wakati huo, nikapata msukumo wa kipekee, na wa nguvu sana kuja akilini mwangu: “Jihadhari na muovu aliye nyuma mwenye macho ya tabasamu.”“‘Mara moja nikageuka nyuma kumwendea yule mshukiwa. Mkono wake ulikuwa kwenye mfuko wake wa mbele mkubwa. Bila kufikiria nikaushika ule mkono na kuutoa kutoka kwa mfuko wake. Hapo tu ndio niliona, alishika mkononi mwake, bastola otomatiki tayari kuipiga. Kitendo cha haraka sana kilifuata, na nikimdhibiti mtu huyu.’ . . .“. . . Roho Mtakatifu alimuonya rafiki yangu kuhusu hatari ya kimwili; Roho Mtakafitu pia atawaonya kuhusu hatari ya kiroho” (“Beware of the Evil behind the Smiling Eyes,” Ensign au Liahona, May 2005, 46–47).Tamka kwa dhati kwamba Bwana kila mara huonya watu wema hatari inayojiri, lakini tusifikirie kuwa sisi si wema kama hatuhisi onyo kutoka kwa Roho Mtakatifu kila mara tunapokabiliana na hali za hatari.• Je! Ni wakati ulihisi Bwana akikuonya wewe juu ya hatari ya kimwili au kiroho? (Wana-

funzi wanaposhiriki uzoefu wao, unaweza kutaka kushiriki mmoja wako mwenyewe.)

Page 242: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

227

UtanguliziBaada ya Alma na watu wake kukwepa jeshi la Mfalme Nuhu, Mfalme Nuhu na watu wake walianza kupata matokeo ya uovu wake, kama ilivyotabiriwa na Abinadi— walishambuliwa na kuwekwa chini ya utumwa na Walamani, Mfalme Nuhu alikufa kifo cha moto. Limhi mwana wa Nuhu akawa mfalme baada ya kifo cha Nuhu. Wakati makuhani wa zamani wa Nuhu

walipowateka kundi la mabinti wa Walamani, Wala-mani waliwalaumu watu wa Limhi na wakajiaanda ku-washambulia. Watu wa Limhi walipingana kwa ujasiri, na wakamjeruhi na kumkamata mfalme wa Walamani. Limhi alimtuliza mfalme wa Walamani, ambaye aliwa-shawishi watu wake kurudi kwenye nchi yao wenyewe kwa amani.

SOMO LA 62

Mosia 19–20

Mapendekezo ya Kufundisha

Mosia 19–20Wanefi katika nchi ya Lehi- Nefi waliona tukio la utimilifu wa unabii wa AbinadiWaalike wanafunzi kufikiria wakati mtu fulani aliwaonya kuhusu hatari ambayo hawaku-weza kutarajia. Waulize wao kusimulia kuhusu jinsi wamebarikiwa kwa sababu walifuata onyo. Wasidie wanafunzi kujadili madhumuni ya maonyo kwa kuuliza maswali yafuatayo:• Ni nini madhumuni ya onyo? Ni nani anayekuonya vitu unavyopaswa kuepuka au vitu

vinavyoweza kuwa na madhara kwako?• Ni kwa nani ambaye Mungu hufunua maonyo ya kiroho katika Kanisa Lake?Wakumbushe wanafunzi kwamba Bwana alimtuma Abinadi kuwaonya Wanefi matokeo ya dhambi zao. Wasaidie wanafunzi kurejelea unabii wa Abinadi kwa Wanefi katika nchi ya Lehi- Nefi, nakili chati ifuatayo kwenye ubao. Hakikisha kuacha nafasi ya kutosha kwa wanafunzi kuandika chini ya seti za marejeo ya maandiko.

Unabii kuhusu watu wa Mfalme nuhu (Mosiah 12:1–2; 17:17)

Utimilifu (Mosia 19:10, 14–15; 20:20; 21:2–4)

Unabii kuhusu Mfalme nuhu (Mosia 12:3; 17:18) Utimilifu (Mosiah 19:18–20)

Alika mwanafunzi asome Mosia 12:1–2 kwa sauti. Uliza darasa litambua kile Abinadi alitabiri kitatokea kwa watu wa Mfalme Nuhu kwa sababu hawakutubu. Alika mwanafunzi aorodheshe matokeo haya katika kijisaduku hapo kwenye upande wa kushoto wa chati iliyopo kwenye ubao. Acha mwanafunzi mwengine asome Mosia 12:3 kwa sauti. Uliza darasa litambue kile Abinadi alitabiri kitamtokea Mfalme Nuhu. Acha mwanafunzi aandike matokeo haya kwenye chati.Ili kuwasaidia wanafunzi kufikiria kuhusu umuhimu wa maonyo ya kiroho tunayopokea kupitia manabii, shiriki hadithi aliyosimuliwa na David R. Stone wa wale Sabini:“Jumapili moja asubuhi, zaidi ya mwaka mmoja uliopita, tuliamka katika siku nzuri sana katika Santo Domingo katika Jamhuri ya Dominika. Jua la Karibiani lilikuwa linaangaza, na mawingu ya meupe. Upepo ororo ulikuwa unavuma, karibu tu kuodondoa majani kwenye miti; ilikuwa joto na ya amani na tulivu. Lakini huko baharini, pasipofika hisi zetu za kimwili siku hiyo, mwangamizi hatari alikuwa anakuja upande wetu, haisiyetulizika na hasiyezuilika. Kituo cha Tufani, kilicho na wajibu wa kufutatilia na kutabiri mapito ya Tufani Georges, kilikuwa kila dakika kinatoa taarifa zilizoweza kupatikana katika Intaneti. Katika

Page 243: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

228

SoMo la 62

amani, utulivu mwanana wa asubuhi hiyo, kwa uwezo wa yale macho yanayoona angani, niliona mapito ya kimbunga, kilicholenga katikati mwa Santo Domingo. “Katika masaa 48 kimbunga kilipiga kisiwa hiki kwa ukali, ghadhabu, kikiacha mapito ya uangamizaji, ukiwa, na kifo. . . ."Jinsi ukubwa wa uharibifu na maangamizo na kifo kutokana jambo la kutisha la nguvu za asili unavyoweza kuwa, kuna hata pia ukiwa zaidi unaosababishwa katika maisha ya watu na tufani za kiroho. Hizo nguvu kali mara nyingi zina uharibifu mbaya sana kushinda vimbunga asili, kwa sababu zinaangamiza nafsi zetu na kutuibia sisi mtazamo na ahadi yetu ya milele. . . .Lakini pia tuna walinzi wetu wa kiroho, ambao wito wao ni kutunza na kuonya, kutusaidia sisi kuepuka uharibifu, maangamizo ya kiroho na hata kifo. Walinzi wetu kwenye mnara wanajulikana kwetu kama mitume na manabii. Wao ndiyo macho yetu ya kiroho angani, na wanajua, kupitia maongozi na umaizi na akili halisi, njia hivi vimbunga vitachukua. Wanaendelea kupazaa sauti zao katika kuonya ili kutuambia sisi matokeo mabaya ya ku-vunja amri za Bwana kwa utundu na kwa makusudi. Kupuuza kwa makusudi maonyo yao ni kuiita taabu, huzuni, na maangamizo. Kuwafuata wao ni kufuata watumishi wateule wa Bwana katika malisho ya kiroho ya amani na utele” (“Spiritual Hurricanes,” Ensign, Nov. 1999, 31–32).• Je! Hadithi hii inafanana vipi na kazi ya Abinadi miongoni mwa watu wa Mfalme Nuhu?Waambie wanafunzi kwamba shughuli ifuatayo itawasaidia wao kujifahamisha vyema na mfululizo wa hadithi ya Mosia 19–20 na kuona utimilifu wa unabii wa Abinadi katika sura hizi. Baada ya shughuli hii, wanafunzi wanaweza kujaza katika safu ya kulia ya chati kwenye ubao.Andika taarifa 11 zifuatazo kwenye ubao kabla ya darasa, au uzitayarishe kama kitini kwa kila mwanafunzi. Alika wanafunzi wapitie Mosia 19–20. Wanaposoma, acha wao wapatie nambari msururu wa matukio katika orodha. Unaweza kutaka kuwaambia wanafunzi kwamba muhtasari wa sura unapatiana dokezo zenye usaidizi.

Gidioni anatafuta kumuua Mfalme Nuhu. Wanawake na watoto wa Kinefi waliwasihi Walamani wasiwachinje. Mfalme Nuhu anakufa kifo cha moto. Jeshi la Walamani linakuja katika mipaka ya Shemloni. Makuhani wa Nuhu wanawateka mabinti 24 wa Kilamani. Mfalme Mlamani anasihi jeshi lake kuwasamehe watu wa Limhi. Nuhu na baadhi ya watu wake wanatoroka kutoka kwa Walamani, wakiwaacha

nyuma wake na watoto wao. Limhi anaamuru watu wake wasimuue mfalme Mlamani. Kunakuwa na amani kati ya Wanefi na Walamani kwa miaka miwili. Limhi anaahidi kwamba watu wake watalipa nusu ya mali yao kwa Walamani. Wanefi wanashinda shambulizi la Walamani na kumteka mfalme Mlamani.

Wapatie wanafunzi dakika 5 hadi 10 ili wakamilishe shughuli hii. Kisha tumia orodha kure-jelea mfululizo wa Mosia 19–20. (Msururu sahihi wa matukio, kuanzia hapo juu ya orodha, ni kama ifuatavyo: 1, 4, 5, 2, 8, 11, 3, 10, 7, 6, 9.)Warejeshe wanafunzi kwenye chati ubaoni. Gawa darasa katika makundi mawili. Uliza kundi kupekua Mosia 19:10, 14–15; 20:20; 21:2–4 ili kuona unabii wa Abinadi kuhusu watu wa Mfalme Nuhu ambao ulitimizwa. Uliza kundi la pili kupekua Mosia 19:18–20 ili kuona jinsi unabii wa Abinadi kuhusu Mfalme Nuhu ulitimizwa. Alika mwanafunzi kutoka kwa kila kikundi kufanya muhtasari wa jinsi unabii wa Abinadi ulitimizwa. Alika mwanafunzi mwingine kuandika muhtasari katika chati.Waalike wanafunzi kusoma Mosia 20:21 kimya.• Gidioni alisema nini ndio kilikuwa chanzo cha kuteseka kwa watu?Waulize wanafunzi kuelezea kwa maneno yao wenyewe kile Gidioni alikuwa anataka watu waelewe. Hali kuwa wanaweza kutumia maneno tofauti, wanafunzi wanapaswa kuonye-sha uelewa wa kwamba kukataa maneno ya watumishi wa Bwana huleta mateso na huzuni. (Unaweza kutaka kuandika kanuni hii kwenye ubao.)

Page 244: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

229

MoSia 19 –20

Waambie wanafunzi kwamba Bwana amepatiana onyo kama hili kwa wale katika siku za mwisho ambao hawatasikia sauti ya Yake. Uliza mwanafunzi asome Mafundisho na Ma-agano 133:70–72 kwa sauti. Unaweza kutaka kupendekeza kwamba wanafunzi kuandika mtajo huu katika pembeni mwa maandiko yao karibu na Mosia 20:21.• Ni nini baadhi ya vitu ambavyo manabii na mitume hufunza katika siku yetu ambavyo

vitatusaidia kuepuka mateso na huzuni? Ni nini wanachofunza ambacho kutasaidia kutuletea amani na furaha na kutusaidia kurudi katika uwepo wa Mungu? (Unaweza kuwaonyesha wanafunzi toleo la mkutano mkuu wa majuzi la Ensign na hutaje baadhi ya vichwa vya hotuba zilizotolewa na manabii.)

Waalike wanafunzi kusimulia kuhusu nyakati walipobarikiwa kwa sababu ya kufuata usha-uri wa viongozi wa Kanisa.Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa kwamba kutii maneno ya manabii kunaweza kutuletea amani na kutusaidia sisi kurudi katika uwepo wa Mungu, shiriki taarifa ifuatayo ya Mzee

Robert D. Hales wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili:“Usalama wetu wa kiroho unategemea kugeukia sauti ya nabii wetu aliye hai. Ikiwa tunasikiza sauti yake na kutii ushauri wake, tunaweza kuishi kama vile Kristo angependa sisi tuishi na kuvumilia hadi mwisho ili kwamba siku moja sisi, pamoja na familia zetu, turudi katika uwepo wa Baba yetu wa Mbinguni na Mwanawe Yesu Kristo” (“Hear the Prophet’s Voice and Obey,”

Ensign, May 1995, 17).Hitimisha somo hili kwa kushuhudia amani na usalama wa kiroho ambao huja kutoka kwa kufuata ushauri wa watumishi wa Bwana.

Rejeo la Umahiri wa MaandikoIkiwa muda unaruhusu, unaweza kutaka kurejelea vifungu vya umahiri wa maandiko uli-vyofunza kufikia hapo mwaka huu ili kuwasaidia wanafunzi kukumbuka maneno muhimu katika kila kifungu.Wapatie wanafunzi dakika chache za kurejelea vifungu vya umahiri wa maandiko walivyo-jifunza kufikia hapa katika mwaka huu wa shule. Alika mwanafunzi kuja mbele ya darasa pamoja na maandiko yake. Uliza mwanafunzi kuwenda kwenye mojawapo wa vifungu vya umahiri wa maandiko bila kumuonyesha mtu yeyote. (Ikiwa kadi za umahiri wa maandiko zinapatikana, unaweza kumuacha mwanafunzi kutumia moja.) Acha mwanafunzi aa-ndike neno moja kutoka kwa kifungu cha umahiri wa maandiko kwenye ubao. (Wahimize mwanafunzi kuchagua maneno muhimu kutoka kwa kifungu badala ya maneno ambayo hayana sifa kama vile na au - le.)Alika sehemu ya darasa iliyobaki kupekua maandiko yao wakitafuta kifungu cha umahiri wa maandiko wanachofikiria neno hili linatoka. Ikiwa hakuna yeyote anayeweza kupata kifungu sahihi akitumia neno moja, acha mwanafunzi aandike neno lingine kutoka kwa kifungu cha umahiri wa maandiko kwenye ubao. Rudia mfanyiko huu mpaka angalao mwanafunzi mmoja amepata kifungu sahihi. Alika wengine wa darasa kugeukia kifungu hiki, na acha wanafunzi wakikariri kwa pamoja. Kisha rejelea shughuli hii na mwanafunzi mwengine na kifungu kingine cha umahiri wa maandiko.

Page 245: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

230

UtanguliziBaada ya kushindwa mara tatu kujitoa kutoka katika utumwa wa Walamani, watu wa Limhi mwishowe walimgeukia Bwana ili awakomboe. Kisha, Amoni na ndugu zake waliwasili katika nchi ya Lehi- Nefi. Baada

ya kufanya agano za kumtumikia Bwana, watu wa Limhi walitoroka kutoka kwa utumwa wa Walamani, na Amoni aliwaongoza wao hadi Zarahemla

SOMO LA 63

Mosia 21–22

Mapendekezo ya Kufundisha

Mosia 21:1–22Baada ya uasi wa watu wa Limhi dhidi ya Walamani na kushindwa mara tatu, walijinyenyekeza wenyewe mbele za Bwana na kuanza kufanikiwaAndika maneno utumwa na ukombozi kwenye ubao.• Ni picha gani zinazokujia akilini unapofikiria maneno haya?• Ni mhemko gani unayoifikiria katika uhusiano na maneno haya?• Maneno haya yana uhusiano gani na mpango wa wokovu?Elezea kwamba Mosia 21–24 ina matukio ya makundi mawili ya watu ambao walikuwa utumwani chini ya majeshi ya Walamani na hatimaye wakakombolewa na Bwana. Katika Mosia 21–22, tunasoma kuhusu Limhi na watu wake, ambao walikuwa watumwa kama matokeo ya uovu wao. Utumwa wao wa kimwili uliakisi utumwa wa kiroho waliopata uzoefu kwa sababu ya dhambi zao. Tukio la kundi la pili, katika Mosia 23–24, litashughu-likiwa katika somo lijalo. Linasimulia kuhusu watu wa Alma, ambao walipata kuwa katika utumwa na kuteseka baada ya wao kubatizwa. Matukio yote yanafunza ukweli muhimu kuhusu nguvu za Bwana za kutukomboa sisi kutoka kwa dhambi na mateso. Wahimize wanafunzi kufikiria kuhusu nguvu za Bwana za kutukomboa kutoka kwa dhambi wanapo-jifunza kuhusu utumwa na ukombozi wa watu katika Mosia 21–22.Waalike wanafunzi kusoma Mosia 21:2–6 kimya. Waulize wao kutambua maneno na vishazi ambavyo vinaelezea kile Limhi na watu wake walipatwa nacho na jinsi walihisi kukihusu. Ili kusisita shida zilizowakabili watu wa Limhi, unaweza kutaka kuwahimiza wanafunzi kuweka alama kishazi “hapakuwa na njia yoyote ya kujikomboa” katika. Mosia 21:5.• Ni utondoti gani katika Mosia 21:6 unaopendekeza kwamba watu hawakuwa wameji-

nyenyeka wenyewe na kumgeukia Bwana?• Ni suluhu gani ambayo watu wa Limhi walipendekeza ili kupata nafuu kutokana na

mateso yao?Fanya muhtasari wa Mosia 21:7–12 kwa kuwaambia wanafunzi kwamba watu wa Limhi walienda kupingana vita mara tatu kujikomboa wenyewe kutoka kwa Walamani, lakini walishindwa na kupata hasara kubwa kila mara.• Ni baadhi ya njia gani watu wangejibu baada ya jaribio lao la tatu kushindwa kujiko-

mboa wenyewe?Waalike wanafunzi kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka kwa Mosia 21:13–16 ili kuji-funza jinsi watu walijibu. Fikiria kuwauliza baadhi yao au wote kujibu maswali yafuatayo:• Watu walibadika vipi baada ya kushindwa mara ya tatu?• Kulingana na Mosia 21:15, kwa nini Bwana alikawia kusikia maombi yao?• Katika Mosia 11:23–25, ni kitu gani Abinadi aliwaambia watu walipaswa kufanya kabla

ya Bwana kusikia maombi yao kwa ukombozi?• Ingawa watu hawakumbolewa mara moja kutoka utumwani, Bwana aliwabariki kwa

jinsi gani walipoanza kutubu? (Wanafunzi wanapojibu, fikiria kuwahimiza wao kuweka alama kishazi “wakafanikiwa kiasi kwa kiasi” katika Mosia 21:16.)

Page 246: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

231

MoSia 21–22

• Hii inafunza nini kuhusu kile Bwana atafanya watu wanapojinyenyekeza wenyewe, wakianza kutubu, na kumuomba Yeye usaidizi?

Fanya muhtasari wa Mosia 21:16–22 kwa kuelezea kwamba katika wakati uliobaki ambao watu wa Limhi wakiwa utumwani, Bwana aliwafanikisha wao hata kwamba hakuwa na njaa. Pia “hakukuwa na ghasia yoyote miongoni mwa Walamani na watu wa Limhi” (Mosia 21:22).Waalike wanafunzi kutaja kanuni walizojifunza kuhusu habari za watu wa Limhi. Ingawa wanafunzi wanaweza kushiriki kanuni tofauti, hakikisha wanaelewa kwamba tunapoji-nyenyekeza wenyewe, kumuomba Bwana, na kutubu dhambi zetu, Yeye atasikia maombi yetu na kuondoa mzigo wa dhambi zetu katika wakati Wake mwenyewe. (Unaweza kutaka kuandika kanuni hii kwenye ubao. Unaweza kutaka pia kuwauliza wa-nafunzi kuandika katika maandiko yao karibu na Mosia 21:15–16 au katika shajara zao za kujifunza maandiko au daftari za darasani.• Unafikiria tunaweza kufaidika kwa kuongojea Bwana atukomboe sisi kutokana na mzigo

wa dhambi zetu?Ili kuwasaidia wanafunzi kutumia kile walichojifunza, wapatie dakika chache za kutafakari maswali yafuatayo na kuandika majibu katika shajara zao za kujifunza maandiko. (Una-weza kutaka kuandika maswali kwenye ubao.)• Je! Unafanya nini kutafuta nguvu za Bwana za ukombozi kutoka kwa dhambi zetu?• Ni kwa njia gani “umefanikiwa kiasi kwa kiasi” ulipotafuta usaidizi wa Bwana?

Mosia 21:23–22:16Limhi, Amoni, na Gidioni walifanya kwa pamoja ili kuwasaidia watu kutoroka kutoka utumwani na kurudi ZarahemlaTazama: Unaweza kutaka kuwakumbusha wanafunzi kwamba Mosia 7 na 8 ikijumuisha habari za Amoni na ndugu zake kuwatafuta Mfalme Limhi na watu wake. Sura 14 zifu-atazo, Mosia 9–22, zinasimulia historia ya watu wa Limhi, kuanza karibu miaka 80 kabla Amoni kuwapata. Historia hii inamalizika kwa kusimulia tena baadhi ya matukio ambayo yanashughulikia sura zilizopita. Kwa sababu hii, wingi wa maudhui ya Mosia 21:23–30 yalishughulikiwa katika masomo ya Mosia 7–8 na Mosiah 18. Ili kuwasidia wanafunzi kukumbuka matukio yaliyoandikwa katika Mosiah 21:23–30, inaweza kusaidia kurejelea maelezo ya jumla ya safari kwa kifupi katika Mosia 7–24 katika kiambatisho hapo mwisho wa kitabu cha kiada hiki.Wakumbushe wanafunzi kwamba watu wa Limhi walitambua kwamba mateso yao yali-tokana na kukataa kwao mwaliko wa Bwana wa kutubu (ona Mosia 12:1–2; 20:21). Kwa kukiri dhambi zao, watu wa Limhi walianza mfanyiko wa toba na uongofu. Shiriki maelezo ya toba yafuatayo:“[Toba] ni muhimu kwa faraha yako katika maisha haya na milele yote. Toba ni zaidi ya kukiri makosa. Ni mabdiliko ya akili na moyo. Inajumuhisha kugeuka kabisa kutoka kwa dhambi na kumgeukia Mungu kwa msamaha. Yanaletwa na upendo wa Mungu na hamu ya uaminifu ya kutii amri Zake” (True to the Faith: A Gospel Reference [2004], 132).Waalike wanafunzi kusoma Mosia 21:32–35 kimya. Waache wao kutambua maneno na vishazi ambavyo vinaonyesha kwamba Limhi na watu wake walikuwa wametubu na kugeuza mioyo yao kwa Bwana. Unaweza kutaka kupendekeza kwamba waweke alama maneno na vishazi hivi. Waalike wanafunzi wachache kushiriki kile wamepata. (Majibu yao yanafaa kujumisha kwamba Limhi na wengi wa watu wake kwa kuingia katika agano la kumtumikia Mungu na kuweka amri Zake, kwamba walikuwa na hamu ya kubatizwa, na kwamba walikuwa tayari kumtumikia Mungu kwa mioyo yao yote.)Shughuli ifuatayo itawasaidia wanafunzi kuona kwamba Bwana aliwasaidia watu wa Limhi kutoroka kutoka utumwani walipoweka maagano yao ya kumtumikia Yeye na kuweka amri Zake. Andika maswali yafuatayo na marejeo ya maandiko kwenye ubao kabla ya darasa:

Je! Kuwasili kwa Amoni na ndugu zake kulikuwa jibu kwa maombi ya watu wa Limhi vipi? (Ona Mosia 7:14–15, 18–20; 21:14–15, 22–24.)Katika ziada ya kutafuta usaidizi wa Bwana kupitia maombi, watu wa Limhi walifanya nini, na uongozi wa Gidioni, katika kukombolewa? (Ona Mosia 21:36; 22:1–10.)

Page 247: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

232

SoMo la 63

Ni utondoti gani katika mistari hii unaoonyesha kwamba Bwana aliwasidia watu wa Limhi kutoroka salama? (Ona Mosia 22:11–16; 25:15–16.)

Gawa wanafunzi katika makundi matatu. Acha kila kundi litayarishe jibu la mojawapo wa maswali haya yaliyopo ubaoni kwa kujifunza yanayoambatana na vifungu vya maandiko. Baada ya dakika chache, alika mwanafunzi mmoja kutoka kwa kila kikundi kuripoti majibu

waliyotayarisha. Hii pia unaweza kuwa wakati mzuri wa kuwaacha wanafunzi kuongezea “kutoroka kwa watu wa Limhi” kwenye mchoro wa maelezo ya jumla ya safari katika Mosia 7–24. (Kwa mchoro kamili, ona kiambatisho hapo mwisho wa kitabu cha kiada hiki.) Unaweza pia ku-taka kuwaacha wanafunzi kuangalia alamisho la Kitabu cha Mormoni ili kutambua kile ambacho hatimaye kitawatokea watu wa Limhi (ona Mosia 22:13–14).Taja kwamba ingawa hatutaweza kuwa na haja ya kutafuta ukombozi kutoka kwa utumwa wa kimwili kama vile watu wa Limhi, tuna haja ya ukombozi kutoka kwa dhambi.• Ni nini ulichojifunza kutoka kwa Mosia 21–22 ambacho kinamtia moyo mtu yeyote ambaye alihitaji kupata uzo-efu wa nguvu za Bwana za kutukomboa sisi kutoka kwa dhambi?Hitimisha kwa kutoa ushuhuda wako wa nguvu za Bwana wa kutukomboa sisi kutoka kwa dhambi. Sisitiza kwamba tunapojinyenyekeza wenyewe, na kumuomba Bwana, na kutubu dhambi zetu, Yeye atasikia maombi yetu na kuondoa mzigo wa dhambi zetu katika wakati Wake mwenyewe.

Maelezo ya Jumla katika Mosiah 7–24

Nchi ya Zarahemla

Magofu ya Taifa la Wayeradi katika Nchi ya Kaskazini

Maji ya Mormoni

Nchi ya Nefi (Lehi- Nefi)

Kundi la Wanefi lilio-ngozwa na

zenifu

Kutoroka kwa watu wa limhi

jaribio la kupata

zarahemla

Mabamba 24 ya dhahabu (kitabu

cha etheri)

Wanefi fulani walitafuta kumilki tena nchi ya nefi

Kundi la watafutaji

liliongozwa na amoni

Page 248: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

233

MoSia 21–22

Tangazo na Habari za UsuliMosia 21:15, 29–30. Kuteseka kunakotokana na dhambi kunaweza kuwa na madhumuni

Tunapofanya dhambi na kukataa kutubu, kama vile watu wa Mfalme Limhi, sisi wenyewe tunajiletea ma-umivu ya ziada—wakati mwengine kimwili na daima kiroho. Mzee Kent F. Richards wa wale Sabini alielezea jinsi maumivu yanaweza kuwa sehemu ya uponyaji wa kiroho na ukuaji:

“Maumivu ni kipimo cha mfanyiko wa uponyaji. Mara nyingi hutufunza sisi subira. . . .

“Mzee Orson F. Whitney aliandika: ‘Hamna maumivu ambayo tunapata, hamna majaribu ambayo tunayo-pata ambayo ni bure. Yanatuhudumia elimu yetu, kwa ukuaji wa sifa kama vile subira, imani, ustahamilivu, na unyenyekevu. Ni kupitia huzuni na kuteseka, kazi ya su-lubu na masumbuko, ambapo tunapata elimu ambayo tunakuja hapa kuipata.”

“Vivyo hivyo, Mzee Robert D. Hales alisema:

“‘Maumivu hukuletea unyenyekevu ambao hukuruhusu kutafakari. Ni uzoefu ambao mimi ninashukurani kuwa nimevumilia. . . .

“Nimejifunza kwamba maumivu ya kimwili na uponyaji wa mwili . . . yanafanana kiajabu na maumivu ya kiroho na uponyaji wa nafsi katika mfanyiko wa toba’” (“The Atonement Covers All Pain,” Ensign au Liahona, May 2011, 15).

Mosia 21:15–16. Je! Mitazamo yako ni ipi wakati wa masumbuko?

Mzee Richard G. Scott wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alifunza kuhusu mitazamo tunayofaa kujita-hidi kuepuka na mitazamo ya kujitahidi kukuza katika masumbuko yetu:

“Bwana atakupatia nafuu kwa nguvu za utakatifu unapotafuta ukombozi katika unyenyekevu na imani katika Yesu Kristo.

“Usiseme, ‘Hakuna anayenielewa mimi; Siwezi kutatua, au siwezi kupata usaidizi ninaohitaji.’ Haya maoni ni ya kuvunja moyo. Hakuna anayeweza kukusaidia bila imani na juhudi katika sehemu yako. Ukuaji wako wa kibinafsi unahitaji kwamba. Usitafute maisha yaliyo huru kutokana na usumbufu, maumivu, shinikizo, changamoto, au huzuni, kwani hivyo ndivyo vyombo ambavyo Baba mwenye upendo hutumia kusisimua ukuaji wa kibinafsi na uelewa wetu. Kama maandiko yanavyodhihirisha kila mara, utasaidiwa unapofa-nya imani katika Yesu Kristo. . . . Imani katika Kristo humaanisha kumwamini Yeye; kuamini mafundisho Yake. Haya uelekeza kwenye matumaini, na matumiani huleta hisani, upendo kamili wa Kristo—ambao huleta hisia ambazo huja wakati tunahisi husu Yake, upendo Wake, na uwezo Wake wa kutuponya sisi au kuondoa mizigo yetu pamoja na nguvu za uponyaji Wake” (“To Be Healed,” Ensign, May 1994, 8).

Page 249: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

234

Nchi ya Zarahemla

Nchi ya Nefi (Lehi- Nefi

UtanguliziBaada ya Alma na watu wake kutoroka kutoka kwa jeshi la Mfalme Nuhu, walianzisha mji wa haki. Ingawa wali-kuwa wameongolewa katika injili, walipata usumbufu na changamoto. Walamani waliwaweka utumwani. Jinsi

Alma na watu wake walivyofanya imani na subira, Bwana aliondoa mizigo yao na hatimaye kuwakomboa kutoka utumwani. (Tazama kwamba Mosia 23–24 hushughulikia karibu kipindi hicho hicho kama vile Mosia 19–22.)

SOMO LA 64

Mosia 23–24

Mapendekezo ya Kufundisha

Mosia 23:1–20Bwana anamsaidia Alma na watu wake kutoroka kutoka kwa majeshi ya Mfalme Nuhu na kuanzisha mji wa hakiWaonyeshe wanafunzi picha ya Alma Akibatiza katika Maji ya Mormoni (62332; Gospel Art Book [2009], no. 76). Alika mwanafunzi kuliambia darasa kile yeye anajua kuhusu mtu ambaye anambaatiza wengine katika picha hii. (Ikiwa wanafunzi wana shida kujibu, una-weza kupendekeza kwamba wasome muhtasari wa sura ya Mosia 18 ili kuwakumbusha wao habari za Alma wa watu wake katika Maji ya Mormoni.)Gawa wanafunzi katika majozi. Alika kila jozi kuchukua zamu kusomaena mmoja na mwengine kutoka kwa Mosia 23:1–5, 19. Waulize wao kutafuta vishazi ambavyo vinaonye-sha jinsi Bwana alimbariki Alma na watu wake walipotubu na kuchagua kuishi kwa wema, (Unaweza kutaka kupendekeza kwamba waweke alama vishazi hivi.) Waulize wanafunzi kusema kile wamepata,

Waalike wanafunzi kutazama katika michoro yao inayoo-nyesha maelezo ya jumla ya safari katika Mosia 7–24. Wae-lekeze wao wachore nchi ya Helamu kwenye michoro yao katika sehemu ifaayo. Pia waache wachore mshale kutoka Maji ya Mormoni hadi nchi ya Helamu, na uwaache waite mshale huu “Alma na watu wake wanaondoka.” (Kwa mchoro kamili, ona kiambatisho hapo mwisho wa kitabu cha kiada hiki,)Elezea kwa kifupi kwamba katika Mosia 23:6–14, tuna-soma kwamba Alma alikataa mombi ya kwamba yeye awe mfalme wao. Alika mwanafunzi asome Mosia 23:9–10, 12 kwa sauti. Uliza darasa kuangalia maelezo ya Alma ya athari ya Mfalme Nuhu ambayo alikuwa nayo juu yake na watu wake. Waulize wanafunzi waseme kile wamepata.• Vishazi “kushikwa katika mtego” na “kufungwa kwa ka-mba za uovu” vinafunza nini kuhusu madhara ya dhambi?• Kwa nini ni msaada kwetu kutambua ushawishi ambao unaweza kutuelekeza kwenye dhambi za awali?• Baada ya kutubu, kwa nini inaweza kuwa muhimu kuku-mbuka jinsi toba inaweza kuwa “chungu?

Uliza mwanafunzi asome Mosia 23:13 kwa sauti. Taja kwamba ushauri wa Alma wa “msi-mame imara kwenye huo uhuru ambao kwa hii mmekombolewa.”• Je! Ushauri huu unatumika vipi katika mfanyiko wa toba? (Wasaidie wanafunzi kuelewa

kwamba mara Bwana ametukomboa sisi kutoka kwa dhambi na tunapata uzoefu wa uhuru wa msamaha, ni lazima tufanye chaguo njema ili kudumisha uhuru huu.)

Waalike wanafunzi wapekue Mosia 23:14–18 kimya kimya, wakitafuta baadhi ya vitu ambavyo Alma aliwafunza watu kufanya ili kudumisha uhuru wao. Waulize wanafunzi wachache kuripoti kile wamepata.

Maelezo ya Jumla katika Mosia 7–24

Magofu ya Taifa la Wayaredi katika Nchi ya Kaskazini

Nchi ya Helamu

Maji ya Mormoni

Kundi la Wanefi lililo-ongozwa na

zenifu

Kutoroka kwa watu wa limhi.

Mabamba 24 ya dhahabu (kitabu

cha etheri)

alma na watu wake

wanaondoka.

jaribio la kuipata

zarahemlaWanefi fulani

walitafuta kumilki tena nchi ya nefi

Kundi la watafutaji la

amoni

Page 250: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

235

MoSia 23–24

Alika mwanafunzi kusoma Mosia 23:19–20 kwa sauti. Uliza darasa kutambua kishazi ambacho kinaonyesha kwamba Bwana aliwabariki watu walipochagua kuishi kwa wema (“kufanikiwa zaidi”).• Je! Unaweza kufanya muhtasari vipi kile umejifunza kutokana na uzoefu wa Alma na

watu wake? (Miongoni mwa kweli zingine, wanafunzi wanaweza kusema kwamba tunapotubu na kuchagua kuishi kwa wema, Bwana atatubariki sisi na kutuweka huru kutoka kwa kamba za uovu.)

• Je! Uliona hii kanuni ikitimizwa katika maisha yako au katika maisha ya rafiki au mwa-nafamilia? (Wakumbushe wanafunzi kwamba hawahitaji kushiriki uzoefu ambao ni wa kibinafsi au siri.)

Mosia 23:21–29Jeshi la Walamani na makuhani waovu wa Nuhu walimuweka Alma na watu wake utumwaniIli kuwasaidia wanafunzi kuelewa kwamba wale ambao ni wema sharti bado wapate uzoefu wa majaribu, waulize wanafunzi kufikiria wakati katika maisha yao ambapo wangeweza kufananisha taarifa ifuatayo ya Mzee Richard G. Scott wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili:

“Majaribio yanahitajika hata wakati unaishi maisha ya ustahiki, na wema na umtiifu kwa amri za [Mungu]. Pale inapoonekana mambo yote yanaenda sawa, changamoto kila mara ujitokeza katika chembe nyingi kwa pamoja” (“Trust in the Lord,” Ensign, Nov. 1995, 16).Waulize wanafunzi kupekua Mosia 23:21–22 ili kugundua kwa nini Bwana angekubali wale ambao wamechagua kuishi kwa wema upatwa na majaribu

na dhiki. Wanafunzi wanaporipoti kile ambacho wamepata, wasaidie wao kuelewa kwa-mba Bwana atajaribu subira yetu na imani yetu ili kutusaidia kuongezea imani yetu katika Yeye.Waalike wanafunzi kuandika maswali yafuatayo katika sharaja zao za kujifunza maandiko au daftari za darasani. Waulize wao kutafakari maswali haya wanapojifunza salio la Mosia 23. Hawapaswi kuandika majibu yao mpaka uwasukume wao kufanya hivyo baadaye katika somo ili.• Je! Ni majaribu gani ambayo yanakupata kwa sasa?• Je! Unaweza vipi kutumia imani na matumaini katika Mungu katika nyakati zako za

majaribu?Waulize wanafunzi kusoma Mosia 23:23–29. Waalike wao kutafuta njia ambazo Alma na watu wake walijaribiwa na kile walifanya ili kuonyesha imani yao katika Mungu.• Je! Kuomba na kufuata ushauri wa nabii kunatusaidia vipi wakati wa majaribu? (Ina-

weza kutusaidia kuongezea subira na imani. Inaweza pia kutusaidia kupokea nguvu, ufunuo wa kibinafsi, amani, na imani ili tuweze kuvumilia hadi mwisho majaribu yetu au kupata ukombozi kutoka kwayo.)

Mosia 23:30–24:25Alma na watu wake walipatwa na mateso, lakini Bwana aliondoa mizigo yao na kimiujiza kuwakomboaIli kuwasaidia wanafunzi kuelewa uhusiano wa Amuloni na Walamani na mfalme wao, fanya muhtasari wa Mosia 23:30–39 na 24:1–7. Elezea kwamba Amuloni alikuwa kiongozi wa makuhani waovu wa Mfalme Nuhu, ambaye alikuwa amemfurusha Alma kwa kum-tetea Abinadi. Amuloni, pamoja na makuhani waovu wengine na wake wao Walamani, walikuwa wameungana na Walamani. Amuloni alipata upendeleo wa mfalme Mlamani, ambaye kisha alimteua yeye kutawala Wanefi wote katika nchi ya Helamu, ikijumuisha watu wa Alma.Alika mwanafunzi kuja mbele ya chumba, na muulize yeye kujitweka mkoba wa mgongoni mtupu. (Mwanafunzi atahitaji maandiko yake.) Uliza mwanafunzi jinsi itakuwa rahisi kubeba mkoba wa mgongoni siku nzima. Alika mwanafunzi huyu asome Mosia 24:8–11

Page 251: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

236

SoMo la 64

kwa sauti. Kila mara mwanafunzi anaposoma kuhusu kitu ambacho kimekuwa jaribu kwa Alma na watu wake, weka jiwe au kitu kingine kizito katika mkoba wa mgongoni. Wakati mwanafunzi ameshamaliza kusoma, muulize vile ilivyo kubeba mkoba uliojaa kwa wakati uliobakia wa siku. (Mwanafunzi anafaa kubakia mbele za darasa na kujitweka mkoba wa mgongoni mpaka pale utakapomwambia akae chini.) Uliza darasa:• Je! Mawe au vitu vizito kwenye mkoba wa mgongoni vinaashiria nini katika maisha yetu?• Je! Mizigo ya aina hii inatuathiri sisi vipi?Uliza mwanafunzi asome Mosia 24:10–12 kwa sauti. Alika darasa kutafuta kile watu wa Alma walifanya ili wapokee usaidizi kwa mizigo yao. Waalike wanafunzi kuelezea kile wamepata.• Je! Maombi yanaweza kutusaidia vipi wakati tuna mizigo mizito?• Tunapopatwa na majaribu, kwa nini inaweza kuwa faraja kujua kwamba Mungu anajua

“fikira za mioyo [yetu]”?Waalike wanafunzi kusoma Mosia 24:13–15 ili kujua kile kilichowatokea watu wa Alma walipoendelea kuomba usaidizi.• Je! Bwana aliahidi kufanya nini kwa watu wa Alma? (Wanafunzi wanapojibu, unaweza

kumuuliza mwanafunzi mwingine au wawili kuinua chini ya mkoba wa mgongoni ili kurahisisha mzigo wa mwanafunzi anayeubeba— ili kuonyesha mfano jinsi Bwana hu-rahisisha mizigo yetu.) Je! Ahadi hii unahusiana vipi na agano walilofanya kule Maji ya Mormoni? (Ona Mosia 18:8–10.)

• Je! Kwa nini inasaidia kujua kwamba Bwana kila mara haondoi mizigo yetu au kuondoa changamoto zetu?

• Je! Tunaweza kujifunza nini kutokana njia Alma na watu wake walijibu majaribu yao?• Je! Ni wakati gani ambapo ulihisi Bwana amekupatia nguvu za kuvumilia majaribu au

kubeba mzigo?Waalike wanafunzi kusoma Mosia 24:16–17, 21 kimya. Waulize watafute maneno na vishazi ambavyo vinaelezea zaidi jinsi watu wanavyofanya kwa majaribu yao na jinsi Bwana amewasaidia wao. Alika mwanafunzi mmoja au wawili kuelezea kwa maneno yao we-nyewe uhusiano wowote walioona kati ya matendo ya watu na matendo ya Bwana. Andika kanuni ifuatayo kwenye ubao: Tunapojiweka kwa subira chini ya mapenzi ya Bwana, Yeye atatuimarisha na kutukomboa kutokana na majaribu yetu katika wakati Wake. Alika mwanafunzi mbele ya darasa kuvua mkoba wa mgongoni. Muulize jinsi inavyohisika kuwa huru kutokana na mzigo. Muulize mwanafunzi huyo huyo asome Mosia 24:21–22. Unaweza kumuuliza mwanafunzi kushiriki jinsi yeye analingana na kile watu walifanya katika mistari hii.

Fanya muhtasari wa Mosia 24:18–25 kwa kuelezea kwamba Alma na watu wake waliweza kutoroka kwa sababu Bwana alifanya usingizi wa kina kuwajia Walamani. Bwana kisha alimwelekeza Alma na watu wake hadi Zarahemla, ambapo Mfalme Mosia aliwakaribisha wao kwa shangwe. Alma na watu wake “walitoa shukrani zao kwa Mungu,” wakijua kwamba “kuwa ni Bwana Mungu wao ambaye alikuwa amewakomboa. (Mosia 24:21; ona pia Mosia 25:16).Katika michoro yao inayoonyesha maelezo ya jumla ya safari katika Mosia 7–24, acha wanafunzi kuchoro mshale kutoka nchi ya Helamu hadi nchi ya Zarahemla. Waelekeze wao kuita safari hii “Kutoroka kwa watu wa Alma.”Ili kuhitimisha, waalike wanafunzi kuandika majibu ya maswali mawili walioandika katika shajara zao za kujifunza maandiko hapo mapema katika somo hili. Waulize wao kuakisi juu ya majaribu yao na jinsi walifanya imani na ma-tumaini katika Mungu ili kuwasaidia wao kuvumilia. Shiriki ushuhuda wako kwamba ikiwa sisi tutajiweka kwa subira chini ya mapenzi ya Bwana, Yeye atatuimarisha sisi na kutu-komboa sisi kutokana na majaribu yetu katika wakati Wake. Unaweza pia kutaka kuwaalika wanafunzi kushiriki mifano ya jinsi Bwana amewaimarisha katika majaribu yao.

Ushiriki wa mwanafunziKuwaalika wanafunzi kushiriki katika shughuli hapa mbele za darasa husaidia wanafunzi wote kujihisi kujumuika katika kujifunza, kwa sababu mmoja wa wenzi wao anasaidia katika kujifunza. Unapowaa-lika wanafunzi kushiriki hapo mbele za darasa kwa muda mrefu, wao-mbe walete maandiko yao pamoja nao ili waweze pia kushiriki katika kusoma maandiko na kujadili na wengine wa darasa.

Nchi ya Zarahemla

Maelezo ya Jumla katika Mosia 7–24

Magofu ya Taifa la Wayaredi katika Nchi ya Kaskazini

Nchi ya Helamu

Maji ya Mormoni

Kundi la Wanefi lililo-ongozwa na

zenifu

Watu wa limhi wanatoroka

Mabamba 24 ya dhahabu (kitabu

cha etheri)

alma na watu wake

wanaondoka

Watu wa alma wanatoroka

jaribio la kuipata

zarahemla

Wanefi fulani walitafuta kumilki tena nchi ya nefi

Kundi la utafutaji

lililoongozwa na amoni

Nchi ya Nefi (Lehi- Nefi)

Page 252: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

237

UtanguliziMosia 25 hupatiana hitimisho la tukio la watu wa Zenifu (ona Mosia 7–24). Watu wa Limhi na wafuasi wa Alma walirudi hadi Zarahemla na waliungana chini ya ulinzi wa utawala wa Mfalme Mosia. Baada ya makundi

haya kuwasili, Limhi na watu wake walibatizwa. Mfalme Mosia alimpatia Alma mamlaka ya kuanzisha makanisa kote katika nchi na kusimamia mambo ya Kanisa la Mungu miongoni mwa watu wa Nefi.

SOMO 65

Mosia 25

Mapendekezo ya Kufundisha

Mosia 25:1–13Wale waliokusanyika katika Zarahemka wanaungana na kujulikana kama Wanefi.Waalike wanafunzi kufikiria matukio waliyosoma au kusikia ambayo yanaonyesha jinsi Bwana amemsaidia mtu kutoa mwongozo, nguvu, ulinzi, au ukombozi. Unaweza kupe-ndekeza kwamba wafikirie matukio katika maandiko, historia ya Kanisa, au maisha ya wanafamilia au marafiki. Kama mfano, shiriki hadithi ifuatayo iliyosimuliwa na msichana ambaye alitanga mbele ya kundi lake na akateremka chini mlima wakati wa shughuli za nje za kata:“Sauti ya onyo, kimya bali ya dhati, akisema ‘Rudi nyuma.’ Karibu niipuuze, lakini ilikuja tena. Wakati huu nilisikiliza na kurudi kwenye kundi. Tulipoanza kwenda chini, tuliwaona madume wawili weusi wakubwa sana wakitembea kasi na kwa hasira wakipanda mlima. Yule mkubwa alianza kuparura mchangani na kututazama. Kiongozi wetu wa ukuhani alivuta mawazo yake, na tuliweza kupanda ua hadi kwenye usalama.“Tulipokuwa tunaingia kambini, niligundua kwamba kama singesikiliza onyo kutoka kwa Roho, ningeumizwa vibaya sana au hata kuawa. Nilijua kwamba Baba wa Mbinguni ananijali mimi na aliniweka salama. Mimi ninashukrani kwa Bwana kwa onyo hilo. Uzoefu huu uliimarisha ushuhuda wangu na kunipatia mimi upendo mkubwa kwa Bwana” (“Turn Back,” New Era, Nov. 2010, 47).Alika mwanafunzi mmoja au wawili kushiriki hadithi waliyofikiria kwamba inaonyesha wema na nguvu za Mungu katika maisha ya mtu mwingine. Uliza darasa:• Je! Inakusaidia vipi kusikiliza mifano ya wema na nguvu za Mungu katika maisha ya

wengine?Fanya muhtasari wa Mosia 25:1–6 kwa kuelezea kwamba baada ya watu wa Limhi na watu wa Alma (wote ambao walikuwa uzao wa watu wa Zenifu) kutoroka kutoka utumwani na kuungana na watu walioishi katika Zarahemla, Mfalme Mosia alisoma kumbukumbu zao kwa watu wote. Acha wanafunzi wasome Mosia 25:7 kimya, wakitafuta majibu ya kawaida ya watu ya matukio ya kushughulika kwa Mungu na watu wa Zenifu. Alika mwanafunzi kushiriki kile yeye amepata.Nakili chati ifuatayo kwenye ubao. Elezea kwamba katika Mosia 25:8–11, tunajifunza zaidi kuhusu jinsi watu wanajibu matukio ya watu wa Zenifu na Alma. Waulize wanafunzi ku-pekua marejeo ya maandiko kwa kile watu walisikia na jinsi walihisu kukihusu. Majibu ya mtajo wa kwanza ulio katika mabano kama mfano.

Page 253: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

238

SoMo 65

Watu walisikia nini. jinsi watu walihisi.

Mosia 25:8 (Walisikia jinsi watu wa limhi walikombolewa kutoka utumwani.)

(iliwajaza wao na shangwe kuu.)

Mosia 25:9

Mosia 25:10

Mosia 25:11

Wakati wanafunzi wamekuwa na muda wa kutosha wa kujifunza marejeo ya maandiko, waalike wanafunzi wachache kuandika ubaoni kile wamepata. Waulize wanafunzi kufanya muhtasari wa kile wamejifunza kutoka kwa Mosia 25:8–11 kwa kutaja kanuni kutoka kwa kishazi ambacho kinaweza kutumika kwao wenyewe. Wanafunzi wanapojibu, wasaidie wao kutambua kwamba kwa kujifunza kumbukumbu za kushughulika kwa Mungu na wengine, tunaweza kuhisi shangwe na shukrani kwa wema wa Mungu. (Wanafu-nzi wanaposoma mistari hii, wanaweza pia kuona huzuni na hasara ambayo inatokana na dhambi.)• Ni katika nyenzo gani tunaweza kujifunza uzoefu wa wengine kwa wema wa Mungu?

(Andika majibu ya wanafunzi kwenye ubao. Wanaweza kujumuisha maandiko, hotuba za mkutano mkuu, magazeti ya Kanisa, wasifu wa viongozi wa Kanisa na wengine, na historia ya familia.)

Waalike wanafunzi kufikiria nyakati ambapo wamepata kujua wema wa Mungu kwa we-ngine kutokana nyenzo zilizoorodheshwa kwenye ubao.• Je! Umefaidika vipi kutoka kwa kujifunza wema wa Mungu kwa wengine kutokana

mojawapo wa nyenzo hizi?• Je! Unafikiria nini inaweza kuwa athari ya muda mrefu juu ya mtu ambaye kila mara

hujifunza kuhusu wema wa Mungu katika kushughulika Kwake na wengine?Wahimize wanafunzi kuchukua muda wao wenyewe kuchagua mojawapo wa nyenzo zilizoorodheshwa kwenye ubao na kutafuta hadithi za wema wa Mungu.

Mosia 25:14–24Alma alianzisha Kanisa la Mungu kote katika nchi ya WanefiIli kuwatayarisha wanafunzi kujifunza utaratibu na mafundisho ya Kanisa miongoni mwa Wanefi, uliza:• Je! Ni lini ulihudhuria kata au tawi la Watakatifu wa Siku za Mwisho lingine isipokuwa

kata au tawi lako la nyumbani? Ni mfanano gani uliona baina ya kata au tawi lako la nyumbani na lile ulilotembelea?

• Inasaidia vipi kuona kwamba utaratibu na mafundisho ya Kanisa ni sawa katika kila kata au tawi la Kanisa?

Fanya muhtasari wa Mosia 25:14–17 kwa kuelezea kwamba baada ya Mosia kunena na kuwasomea, yeye alimwalika Alma kuwafundisha. Kisha Mfalme Limhi na watu wake waliomba wabatizwe. Alma aliwabatiza na akaanza kuanzika Kanisa kote katika nchi.Waalike wanafunzi wachache kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka kwa Mosia 25:18–22. Uliza darasa litafute jinsi Kanisa lilianzishwa na kusimamiwa miongoni mwa Wanefi katika siku za Alma. Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa kwamba utaratibu wa Kanisa huhakikisha kwamba washiriki wote wanapokea ukweli, uliza maswali kama yafuatayo:• Je! Kanisa miongoni mwa Wanefi linafanana vipi na Kanisa la siku hizi? (Tuna kata na

matawi ambayo ni kama “vikundi tofauti” vilivyotajwa katika Mosia 25:21. Marais wa matawi, maaskofu, na marais wa vigingi walikuwa kama makuhani na walimu ambao walisimamia Kanisa siku za Alma.)

Page 254: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

239

MoSia 25

• Kulingana na Mosia 25:15–16, 22, ni kweli gani makuhani na walimu wa Kanisa walisisi-tiza siku za Mosia? (Unaweza kutaka kutaja kwamba Bwana alitoa maelekezo sawa kwa wazazi, viongozi wa Kanisa, na wamisionari katika siku za mwisho. [Ona M&M 15:6; 19:31; 68:25.])

• Kwa nini ni muhimu kuendelea kufunza toba na imani katika Mungu?Waulize wanafunzi kusoma Mosia 25:23–24, wakitafuta vishazi ambavyo vinaelezea baraka zilizopokelewa na wale waliojiunga na Kanisa la Mungu.• Je! Watu wanabarikiwa vipi kama matokeo ya kubatizwa na kujiunga na Kanisa la Mungu?• Ni kwa njia gani Bwana amekubariki kupitia ushiriki wako katika Kanisa?Andika kanuni ifuatayo kwenye ubao: Tunapojichukulia juu yetu wenyewe jina la Yesu Kristo na kuishi kwa ulinganifu, Bwana atamwaga juu yetu Roho Yake.Shuhudia kwa wanafunzi kwamba baraka wanazopata kama washiriki wa Kanisa zinaweza kuongezeka wanapoweka maagano yao na kupokea Roho.

Shuhudia juu ya baraka zilizoahidiwaNdugu Russell T. Osgu-thorpe, rais mkuu wa Shule ya Jumapili, alishi-riki mpangilio rahisi wa ufunzaji bora: (1) funza mafundisho muhimu, (2) waalike wanafunzi kutenda, na (3) shuhudia baraka zilizoahidiwa (ona “Teaching Helps Save Lives,” Ensign or Liahona, Nov. 2009, 15). Unaposhuhudia juu ya ahadi zinazopatikana katika maandiko na maneno ya manabii wa siku za mwisho, mwana-funzi wanaweza kuhisi motisha kuu ya kutumia kile wamejifunza.

Tangazo na Habari za UsuliMosia 25:17–22. Mamlaka ya ukuhani miongoni mwa Wanefi

Kitabu cha Mormoni hakipatiani utondoti mahususi kuhusu ukuhani ulioshikiliwa na manabii na ndugu wengine miongoni mwa Wanefi na Walamani. Hata hivyo, marejeo kwa maagizo na njia ambayo kwayo Kanisa liliendeshwa hutoa ushahidi wa kutosha kwa-mba walikuwa wanashikilia Ukuhani wa Melkizedeki. Nabii Joseph Fielding Smith alifunza kwamba “ukuhani

ambao [Wanefi] walishikilia na ambao kwake walisima-mia ulikuwa Ukuhani kulingana na mpango mtakatifu, mpango wa Mwana wa Mungu [ona Alma 13:1–20]. Ukuhani mkuu huu unaweza kusimamia kila agizo la injili” (Doctrines of Salvation, ed. Bruce R. McConkie, 3 vols. [1954–56], 3:87).

Kwa maelezo ya ziada kuhusu mamlaka ya ukuhani katika Kitabu cha Mormoni, ona Tangazo na Habari za Usuli Mosia 18.

Page 255: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

240

Vifaa vya Matayarisho kwa Mwalimu wa Mafunzo ya NyumbaniMuhtasari wa Masomo ya Kila Siku ya Mafu-nzo ya NyumbaniMuhtasari ufuatao wa mafundisho na kanuni ambazo wanafunzi walijifunza walipokuwa wakijifunza Mosia 18–25 (kitengo cha 13 haikupangiwa kufunzwa kama sehemu ya somo lako. Somo unalofunza linazingatia tu chache ya haya mafundisho na kanuni. Fuata msukumo wa Roho Mtakatifu unapofikiria mahitaji ya wanafunzi.

Siku ya 1 (Mosia 18)Baada ya kifo cha Abinadi, Alma alitubu na kuwafundisha wengine injili ya Yesu Kristo katika Maji ya Mormoni. Kwa kujifunza uzoefu huu, wanafunzi walijifunza kwamba sisi tunaweza kupokea Roho wa Bwana na ahadi za uzima wa milele kwa kufanya na kuweka agano la ubatizo na kwamba baraka kuu uja kwa wale wanaoweka agano la ubatizo.

Siku ya 2 (Mosia 19–20)Baada ya Mfalme Nuhu na watu wake kukataa mafundisho ya Abinadi na walitaka kumwangamiza Abinadi na wafuasi, walishambuliwa na Walamani. Nuhu aliuawa na watu wake, na Limhi mwanawe akawa mfalme. Wanafunzi waliposoma jinsi watu wa Limhi waliwekwa utumwani na Walamani, walijifunza kwamba kukataa maneno ya watumishi wa Bwana huleta mateso na huzuni. Walihimizwa kufikiria juu ya wakati walipata uzoefu wa amani na usalama wa kiroho kwa kufuata ushauri wa watumishi wa Bwana.

SIku ya 3 (Mosiah 21–24)Wanafunzi walijifunza kwamba Alma na watu wake, ingawa walikuwa wema, pia waliwekwa utumwani na Walamani. Wanafunzi walitengeneza chati katika shajara zao za kujifu-nza maandiko ambazo zililingana na utumwani na ukombozi wa Limhi na watu wake, na ule wa Alma na watu wake. Tukio la pili la watu wa Limhi lilifunza kwamba tunapokuwa na hamu ya kufanya na kuweka maagano, Bwana atapati-ana njia ya ukombozi wetu. Kutoka kwa kundi la Alma, wa-nafunzi walijifunza kwamba tunapojiweka chini ya mapenzi ya Bwana kwa subira, Yeye atatuimarisha na kutukomboa kutokana na majaribu katika wakati Wake.

Siku ya 4 (Mosia 25)Baada ya watu wa Limhi na watu wa Alma kuungana tena salama chini ya Mfalme Mosia katika Zarahemla, matukio yao yalisomwa kwa watu wote. Wanafunzi walijifunza kwamba kwa kujifunza kumbukumbu za Mungu za utendaji Wake kwa wengine, tunaweza kuhisi shangwe na shukrani kwa wema wa Mungu. Wanafunzi walipotafakari jinsi ushi-riki wa Kanisa katika siku za Wanefi unafanana na ushiriki wa Kanisa siku hizi, walijifunza kwamba tunapojichukulia juu yetu wenyewe jina la Yesu Kristo na kuishi kwa ulinganifu, Bwana atatubariki kwa Roho Yake. Wanafunzi waliandika jinsi kuwa radhi kujichukulia juu yetu wenyewe jina la Yesu Kristo huleta tofauti katika maisha yao.

UtanguliziKulinganisha na kutofautisha uzoefu wa watu wa Alma na watu wa Limhi kunaweza kuwasidia wanafunzi kugundua kanuni ze-nye thamani kuhusu vyanzo vya majaribu yetu na jinsi tunaweza kukombolewa kutokana na taabu kupitia imani yetu katika Yesu Kristo. Wasaidie wanafunzi kujua kwamba wanapofanya na kuweka maagano matakatifu, kufanya imani katika Bwana, na kwa unyenyekevu kumuomba Yeye usaidizi, Yeye atawaimarisha na kuwakuomboa kutokana na taabu zao katika njia Yake mwe-nyewe na katika wakati Wake mwenyewe.

Mapendekezo ya Kufundisha

Mosia 18Alma alihubiri injili kwa watu wa Mfalme Nuhu, wengi wakatubu na kutamani kubatizwaWaulize wanafunzi wanafikiria nini kuhusu ubatizo wao we-nyewe. Waalike wao kushiriki baadhi utondoti wa kukumbukwa kuhusu uzoefu wao. Kisha onyesha, kama inapatikana, picha ya Alma Akibatiza katika Maji ya Mormoni (62332; Gospel Art Book [2009], no. 76), na kisha uwaulize wao kukumbuka matu-kio yaliyoelezewa katika Mosia 18:8–11. Waulize wanafunzi kile walielewa kuhusu madhumuni ya ubatizo na agano la ubatizo wakati walibatizwa.

Baada ya wanafunzi kujadili tukio katika Mosia 18, acha wa-rejee kwenye siku ya 1, kazi ya 1 katika shajara zao za kujifu-nza maandiko, ambapo walichora kile Alma alifunza kuhusu agano la ubatizo kama ilivyoelezwa katika Mosia 18:8–11.

Somo la Mafunzo ya NyumbaniMosia 18–25 (Kitengo cha 13)

Page 256: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

241

SoMo la MafUnzo ya nyUMbani

Alika mwanafunzi kuchora tena mchoro wake kwenye ubao au kuushiriki na darasa, na uwaulize wanafunzi wengine ikiwa wana chochote cha kuongezea kwenye safu za “Mimi naahidi” na “Mungu anaahidi." Kisha andika kanuni ifuatayo kwenye ubao au kipande cha karatasi: Tunapokea Roho wa Bwana na ahadi ya uzima wa milele kwa kufanya na kuweka agano la ubatizo. Unaweza kutaka kupendekeza kwamba wanafunzi waandike kanuni hii kwenye maandiko yao karibu na Mosia 18:8–11.

Uliza: Je! Uelewa wako wa agano la ubatizo unaathiri vipi hamu yako ya kuweka agano hili?

Mosia 19–24Watu wa Limhi na wafuasi wa Alma walikombolewa kutoka utumwani wa WalamaniUliza mwanafunzi asome taarifa ya kwanza ya Mzee Richard G. Scott wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili katika somo la siku ya 3 ya kitengo hiki katika mwongozo wa kujifunza wa mwana-funzi. Waulize wanafunzi kile Mzee Scott alisema ni majaribu aina mbili ya majaribu tunayokabiliana nayo katika maisha yetu. (Wanapaswa kuwa waliweka laini chini ya haya katika vitabu vya kiada vyao.) Andika Changamoto ambazo huja kutokana na kuvunja amri na Utakaso ambao huja kutokana na majaribu kwenye ubao.

Waulize wanafunzi kurejea majibu yao ya siku ya 3, kazi ya 1 katika shajara zao za kujifunza maandiko. Kisha andika watu wa Limhi chini ya “Changamoto ambazo huja kutokana na kuvunja amri” (ona Mosia 19:10, 25–28; 20:20–21) na watu wa Alma chini ya “Utakaso ambao huja kutokana na majaribu” (ona Mo-sia 23:18–21). Waalike wanafunzi kuorodhesha kwenye ubao baadhi ya mifano ya jinsi siku hizi wanaweza kupata uzoefu wa changamoto za aina hii.

Unaporejea kanuni zifuatazo pamoja na wanafunzi wako, zia-ndike kwenye ubao.

Waalike wanafunzi kusoma Mosia 21:13–16 katika majozi. Waulize wao kutambua maneno na vishazi ambavyo vinafunza kwamba tunapojinyenyekeza wenyewe, na kumuomba Bwana, na kutubu dhambi zetu, Mungu atasikia maombi yetu na kuondoa mizigo ya dhambi zetu katika wakati Wake mwenyewe. Waulize wanafunzi kushiriki jinsi wanafikiria mtu anaweza kutumia kanuni hii ikiwa wanapata uzoefu wa mojawapo wa changamoto zilizopo ubaoni.

Waalike wanafunzi kusoma Mosia 21:31–32, 35 na wafanye muhtasari wa kutoroka kwa watu wa Limhi katika Mosia 22 ili kuonyesha kwamba tunapofanya agano la kumtumikia Mu-ngu na kuweka amri Zake, Bwana atapatiana njia ya uko-mbozi wetu. Unaweza kutaka kuwahimiza wanafunzi kuandika kanuni hii katika maandiko yao karibu na Mosia 21:31–35.

Ili kurejelea kanuni wanafunzi walijifunza kutokana na kujifunza kuhusu watu wa Alma, muulize mwanafunzi afanye muhtasari wa tukio la jinsi watu wa Alma waliwekwa kwenye utumwa na

Walamani (ona Mosia 23:25–24:11). Alika wanafunzi wachache kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka kwa Mosia 24:12–17. Waulize wataje maneno au vishazi ambavyo vinafunza kwamba tunapojiweka kwa subira chini ya mapenzi ya Bwana, Yeye atatuimarisha na kutukomboa kutokana na majaribu yetu katika wakati Wake. Unaweza kutaka kuwahimiza wana-funzi kuweka alama maneno au vishazi katika mistari hii.

Nakili mifano ifuatayo kwenye ubao au itayarishe katika kitini. Waulize wanafunzi kuelezea jinsi wanaweza kutumia kweli hizi walizojifunza kutokana na kujifunza kuhusu watu wa Limhi na watu wa Alma ili kumsaidia mtu katika kila mfano.

1. Rafiki ametambua haja ya kutubu na amepata uzoefu mkali wa hisia za kutokuwa mastahiki na kuvunjika moyo, akisha-ngaa ikiwa kamwe itawezekana kushinda majaribu na hisia za hatia. Je! Unaweza kutumia tukio la watu wa Limhi vipi kumpatia rafiki yako moyo na matumaini ya kutubu. (Una-weza kutaka kuwatia moyo wanafunzi kutambua mistari mahususi katika Mosia 21 ambayo wanaweza kushiriki na rafiki huyu. Waalike wanafunzi kuelezea kwa nini wanafiki-ria mistari waliyochagua inaweza kumsaidia rafiki huyu.)

2. Rafiki ni mchangamfu kijamii na anataka kuishi kulingana na viwango vya injili. Baadhi ya watu hawataki kujihusisha na mtu huyu, wakisema kwamba yeye ni “bora sana” kwao. Je! Unaweza kutumia tukio la watu wa Alma vipi ku-msaidia rafiki yako kuwa na imani katika Bwana na kupata nguvu na faraja wakati wa majaribu haya? (Unaweza ku-taka kuwatia moyo wanafunzi kutambua mistari mahususi katika Mosia 24 ambayo wanaweza kushiriki na rafiki huyu. Waalike wanafunzi kuelezea kwa nini wanafikiria mistari waliyochagua inaweza kusaidia.)

Waalike wanafunzi kusimulia kuhusu nyakati wao au watu wanaojua walishuhudia nguvu za Bwana za ukombozi katika maisha yao. (Kuwa makini usiwahimize moyo au usiwaruhusu wanafunzi kushiriki utondoti usiofaa wa uvunjaji wa amri wa zamani darasani.) Watie moyo wanafunzi kuweka maagano yao, kumuomba Bwana usaidizi, na kuwa na imani na nguvu za ukombozi Wake kwa majaribu yoyote yale wanayokumbana nayo katika maisha yao. Hitimisha darasa kwa kushiriki ushu-huda wako wa nguvu za Bwana za kutukomboa kutokana na changamoto na dhiki zinazokuja kutokana na uvunjaji wetu wa dhambi au kutokana na majaribu ambayo yanatutakasa sisi.

Kitengo kifuatacho (Mosia 26–Alma 4)Katika wiki inayokuja, wanafunzi watajifunza kuhusu malaika ambaye alitumwa kumsitisha Alma Mdogo kuacha kuangamiza Kanisa. Watajifunza kile kilitendeka kwa Alma baada ya uzoefu huu na kusoma baadhi ya mafundisho muhimu sana juu ya kuzaliwa upya kiroho kunakopatikana katika maandiko. Wakati Mfalme Mosia alifariki, Alma alichaguliwa kuwa kiongozi wa Wanefi. Amlisi, mtu muovu, alijaribu kumpendua. Wahimize wanafunzi kutafuta kile Alma alifanya kualika nguvu za Bwana za ukombozi katika hali hii.

Page 257: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

242

UtanguliziWakati wa enzi za Mosia, wengi wa vizazi vinavyochi-puka—ambavyo vilikuwa watoto wadogo katika wakati wa hotuba ya mwisho ya Mfalme Benyamini—ambao hawakuamini katika mafundisho ya Kanisa na kukataa kumuomba Bwana. Vijana waliokuwa hawaamini wa-likuwa na ushawishi kwa washiriki wengine wa Kanisa wa kutenda dhambi mbaya. Wengi wa haya watenda dhambi waliletwa mbele za Alma, kiongozi wa Kanisa.

Alma hakujua la kufanya hapo mwanzoni, lakini mishowe yeye alimuomba Bwana mwongozo wa jinsi ya kuhukumu washiriki wasio watiifu. Bwana alifunua mfanyiko ambao Alma alipaswa kufuata katika kuwa-fanya washiriki wa Kanisa kuwajibika kwa dhambi zao. Alma pia alijifunza juu ya neema za Mungu na upe-ndeleo wa kuwasamehe wale waliotubu. Alma alifuata ushauri wa Bwana na kuleta utulivu katika Kanisa.

SOMO LA 66

Mosia 26

Mapendekezo ya Kufundisha

Mosia 26:1–6Wengi wa vizazi vinavyochipuka hawaamini injili na wanawaelekeza wengine kutenda dhambiKabla ya darasa, andika maswali yafuatayo kwenye ubao:

Je! Unaweza kuelezea ushuhuda wako kuwa vipi leo?Je! Ni kwa njia gani unaweza kutaka ushuhuda wako ukue?

Waulize wanafunzi kujibu maswali haya katika shajara zao za kujifunza maandiko au daf-tari ya darasani. Baada ya muda wa kutosha, elezea kwamba Mosia 26 ina tukio la kundi la watu ambao hawakufanya kile walihitajika kufanya kukuza shuhuda zao. Kama matokeo, imani yao katika Mungu kamwe haikukua, na waliwaelekeza waumini wengi wa Kanisa katika dhambi na makosa. Pendekeza kwamba wanafunzi wanapojifunza tukio hili, wafiki-rie kile linafunza kuhusu ukuaji na uimarishaji wa shuhuda zao.Alika mwanafunzi asome Mosiah 26:1–3 kwa sauti. Kisha uliza darasa:• Je! Ni chaguo gani wengi wa kizazi kinachochipuka wanafanya? (Wao hawachagui kua-

mini tamaduni za wazazi wao.)• Je! Kwa nini unafikiria kutokuamini kwa watu kunazuia uwezo wao wa “kuelewa neno

na Mungu”? (Mosia 26:3).Elezea kwamba kuamini (au hata kuwa na hamu ya kuamini) uelekeza kwenye matendo ambayo huimarisha shuhuda zetu. Kwa upande mwengine, watu wanapochagua kutoa-mini, pia wanachagua kutofanya vitu fulani ambavyo vingeweza kuwasaidia wao kukuza shuhuda thabiti. Waalike wanafunzi kusoma Mosia 26:3–4, 6 kimya. Uliza nusu ya darasa kutafuta kile kizazi kinachochipuka hakitaki kufanya kwa sababu ya kutokuamini kwao. Uliza ile nusu ingine ya darasa kutafuta matokeo ya kutokuamini huku.• Je! Kizazi kinachochipuka kilikataa kufanya nini kwa sababu ya kutokuamini kwao?• Je! Madhara ya kutokuamini kwao yalikuwa nini?Baada ya wanafunzi kujadili maswali haya, andika yafuatayo kwenye ubao: Kukuza na kudumisha ushuhuda, tunaohitaji . . .

Muulize mwanafunzi asome kwa sauti taarifa ifuatayo ya Rais Henry B. Eyring wa Urais wa Kwanza. Uliza darasa lisikilize njia za kukamilisha sente-nsi kwenye ubao.“Ushuhuda unahitaji kulewa kwa maombi ya imani, kutamani sana neno la Mungu katika maandiko, na kutii ukweli tuliyopokea. Kuna hatari katika ku-puuza kuomba. Kuna hatari kwa ushuhuda wetu katika kujifunza na kusoma

maandiko kijuujuu tu. Kuna rutuba muhimu kwa ushuhuda wetu. . . .

Kuwafunza vijanaRais J. Reuben Clark Mdogo. wa Urais wa Kwanza alifunza:“Vijana wa Kanisa wana njaa ya vitu vya Roho; wana hamu ya kujifu-nza injili, na wanaitaka moja kwa moja, bile kuzimuliwa. . . .“. . . Hauna haja ya kufunika kweli za kidini kwa pazia ya vitu vya kilimwengu; unaweza kuleta kweli hizi [kwao] wazi wazi” (The Charted Course of the Church in Education, rev. ed. [pa-mphlet, 1994], 3, 9).

Page 258: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

243

MoSia 26

“Kusherekea neno la Mungu, maombi ya moyo, na kutii amri za Bwana sharti kutumike sawa sawa na kuendelea kwa ushuhuda wako wa kukua na kufanikiwa” (“A Living Testi-mony,” Ensign or Liahona, May 2011, 127).• Ni mazoezi gani Rais Eyring alitambua ambayo yatatusaidia sisi kulisha shuhuda zetu?

(Wanafunzi wanapotambua mazoezi haya, yaweke katika sentensi kwenye ubao: Ili ku-kuza na kudumisha ushuhuda, tunahitaji kula neno la Mungu, kuomba kwa imani, na kutii amri za Bwana.)

• Je! Mazoezi haya yanaweza kushawishi vipi ushuhuda wako?Waalike wanafunzi kusoma Mosia 26:5–6 kimya, wakitafuta jinsi vijana wasio na imani walishawishi washiriki fulani wa Kanisa.• Fikiria taarifa ifuatayo: “Kwani iliwasababisha kutenda dhambi nyingi; kwa hivyo ilibidi

wale ambao walikuwa kanisani, na kutenda dhambi, waonywe na kanisa. (Mosia 26:6). Je! Unafikiria haya yanamaanisha nini? (Ilikuwa muhimu kwa waumini wa Kanisa ambao walitenda dhambi kuhukumiwa na kuwajibika.)

Mosia 26:7–14Alma alimuomba Bwana mwongozo wa jinsi ya kuhukumu wale waliotenda dhambiAcha wanafunzi wafikirie vile ingekuwa kuwa askofu wa kata akiwa na waumini wake ambao wametenda dhambi mbaya sana na hawataki kutubu. Waulize wanafunzi kimya kutafakari kile wangefanya katika hali hii. Je! Wanawezaje kutimiza majukumu yao ya ku-wawajibisha waumini kwa dhambi zao na kuwasaidia wao kutubu? Elezea kwamba Alma, kiongozi wa Kanisa, alikabiliana na changamoto kama hizo.Fanya muhtasari wa Mosia 26:7–12 kwa kuelezea kwamba wale ambao walitenda dhambi waliletwa mbele za Alma. Kulikuwa hakujatokea jambo kama hili hapo mapema katika Kanisa, na Alma hakujua cha kufanya. Aliamua kuwepeleka watenda dhambi kwa Mfalme Mosia kuhukumiwa. Mfalme Mosia aliwarudisha kwa Alma, ambaye alikuwa na mamlaka kutoka kwa Mungu ya kuhukumu waumini wa Kanisa waliotenda dhambi.Alika mwanafunzi asome Mosia 26:13–14 kwa sauti. Uliza darasa kutafuta jinsi Alma alihisi kuhusu majukumu yake ya kuhukumu wale ambao walikuwa wametenda dhambi.• Wakati Alma alihisi kusumbuka kuhusu wajibu wake wa kuwahukumu watenda dhambi,

alifanya nini?• Kwa nini ni muhimu kujua kwamba maaskofu na marais wa matawi hutafuta na kupo-

kea mwongozo wa Bwana wanapowasidia wale ambao wametenda dhambi?

Mosia 26:15–32Bwana anamfunulia Alma jinsi ya kuwawajibisha waumini wa Kanisa kwa dha-mbi zao na kuweka masharti ya tobaIli kuwasaidia wanafunzi kuelewa maudhui ya Mosia 26:15–32, taja kwamba hii mistari ina jibu la Bwana kwa swali la Alma kuhusu kile alipaswa kufanya kuhusu watenda dhambi. Wanafunzi wanapojifunza jibu la Bwana, wahimize wao kutafuta kanuni na mafundisho ambayo yanawasaidia kuelewa vyema kazi ya waamuzi wa kikuhani, kama vile maaskofu na marais wa matawi (na kwa wenye Ukuhani wa Melkizedeki, marais wa vigingi, wilaya, na misheni). Pia waulize wao kutafuta kanuni na mafundisho kuhusu kutatuta msahama.Waalike wanafunzi kusoma Mosia 26:17–28 kimya kimya, wakiona kila mara Bwana ana-potumia neno yangu au Mimi. Unaweza kutaka kupendekeza kwamba wanafunzi waweke alama maneno haya kila mara yanapotokeza. Kisha uliza darasa:• Katika Mosia 26:17–28, maneno haya Mimi na yangu yanapendekeza vipi kuhusu nafasi

ya Bwana katika mfanyiko wa toba? (Unaweza kutaka kuwaalika wanafunzi kushiriki vishazi au mistari mahususi ambayo inahimili majibu yao.)

• Ni kweli gani tunazojifunza kutoka kwa Mosia 26:20–21 kuhusu kazi ya watumishi wa Bwana katika mfanyiko wa toba? (Wasaidie wanafunzi kuelewa kwamba viongozi wa ukuhani humwakilisha Bwana na kwamba katika hali ya dhambi mbaya sana, ma-askofu na marais wa matawi wanaweza kutusaidia kutubu na kupokea msamaha.)

Page 259: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

244

SoMo la 66

• Ni kwa njia gani askofu au rais wa tawi anaweza kuwasaidia wale ambao wanataabi-shwa na dhambi na majaribu?

Elezea kwamba Bwana alimfunza Alma kuhusu kile wale wanaotafuta msamaha wa-napaswa kufanya ili watubu. Waalike wanafunzi kupekua Mosia 26:29–32 katika majozi na kutambua kanuni ambazo zinawasaidia kuelewa kile Bwana anahitaji kutoka kwetu tunapotubu.Baada ya wanafunzi kuwa na muda wa kujifunza mistari hii, waalike wanafunzi kadhaa kuandika kwenye ubao, wakitumia maneno yao wenyewe, kanuni walizogundua. Majibu yao yanaweza kujumuisha yafuatayo:Kukiri dhambi kunaelekeza kwa msamaha.Bwana atawasamehe wale ambao wanatubu kwa uaminifu wa mioyo yao.Sisi sharti tuwasamehe wengine ili wapokee msamaha wa Bwana.Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa vyema kanuni hizi, uliza baadhi yao au wote maswali yafuatayo:• Katika Mosia 26:29, ni nini maana ya kishazi “ataungama dhambi zake mbele yako na

mimi”? (Unaweza kuhitaji kutaja kwamba katika mistari hii, neno zake inamaanisha Alma.)• Wakati mtu ametenda dhambi mbaya sana, kwa nini unafikiria mtu huyu anahitaji kuu-

ngama kwa Bwana na kiongozi wa Kanisa anayefaa? (Kutenda dhambi mbaya, uvunjaji wa sheria ya usafi wa kimwili kama huu, unaweza kuhatarisha ushiriki wa mtu katika Kanisa. Kwa hivyo, katika hali kama hizo mtu anahitaji kuungama dhambi kote kwa Mungu na mwakilishi Wake katika Kanisa. Maaskofu na marais wa tawi wanashikilia fu-nguo za ukuhani za kuwasaidia wale waliotenda dhambi wanaotafuta msamaha. Ingawa ni Bwana tu anayeweza kusamehe dhambi, viongozi wa ukuhani wana nafasi ya usaidizi katika kuwasaidia watu kupokea msamaha huo. Wanaweza kuweka kuungama kote kwa siri na huwasaidia wale ambao wamekiri kote katika mfanyiko wa toba.)

• Je! Unafikiria inamaanisha nini mtu kutubu “kwa moyo wake wa kweli”? (Mosia 26:29).• Je! Kwa nini unafikiria Bwana anahitaji sisi tusamehane? Je! Kutubu na kusamehana

kunahusiana vipi? (Ona 3 Nefi 13:14–15; M&M 64:8–11.)• Ni vishazi gani katika mistari hii vinavyoweza kumtia moyo au kumfaraji mtu ambaye

ana hamu ya kutubu lakini hahisi anaweza kusamehewa?

Mosia 26:33–39Alma anatii ushauri wa Bwana, kuwahukumu wale ambao walikuwa wametenda dhambi na kuleta utulivu katika KanisaElezea kwamba Mosia 26:33–37 husimulia jinsi Alma alivyofuata maelekezo ya Bwana, kuwahukumu washiriki wa Kanisa ambao walikuwa wametenda dhambi, na kuleta utulivu katika Kanisa. Waalike wanafunzi kusoma Mosia 26:34–37 kimya, wakitafuta matokeo ya juhudi za Alma za kufuata ushauri wa Bwana. Shiriki ushuhuda wako kwamba tunapotubu na kuishi kwa wema, tunawezza kuwa na amani katika mioyo yetu na kufanikiwa kiroho.

Page 260: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

245

UtanguliziAlma Mdogo na wana wa Mfalme Mosia waliasi dhidi ya baba zao na Bwana na walijaribu kuangamiza Kanisa la Mungu. Juhudi zao ziliisha wakati malaika, alitumwa katika jibu la maombi ya wema, waliombwa

kutubu. Kama matokeo ya uzoefu huu wa kimiujiza, walizaliwa tena kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo, na walisafiri kote katika nchi ya Zarahemla kuhubiri injili na kuponya madhara walioleta.

SOMO LA 67

Mosia 27

Mapendekezo ya Kufundisha

Mosia 27:1–22Malaika anamwita Alma Mdogo na wana wa Mosia kutubuIli kupatiana maudhui ya somo hili, fanya muhtasari wa Mosia 27:1–7 kwa kuelezea kwamba wengi wa wasioamini katika Zarahemla walianza kuwatesa wale waliokuwa wa Kanisa. Baada ya Mfalme Mosia kutangaza tamko kupiga marufuku vitendo kama hivyo, wengi wa watu walitii na amani ilirejeshwa. Hata hivyo, watu fulani waliendelea kujaribu kuangamiza Kanisa. Watano wa watu hawa walikuwa Alma mwana wa Alma na wana wa Mfalme Mosia, Amoni, Haruni, Omneri, na Himni. Alma mwana wa Alma sana sana anaitwa Alma Mdogo.Alika mwanafunzi asome Mosia 27:8–10 kwa sauti. Uliza darasa kutambua maneno au vishazi ambavyo vinawaeleza Alma Mdogo na wana wa Mosia.• Ni sehemu gani inayowaelezea Alma na wana wa Mosia iliyo wazi sana kwako? Kwa

nini?” (Orodhesha maneno na vishazi kwenye ubao wanafunzi wanapovitambua. Acha nafasi kwenye ubao ya kutengeza orodha ya pili baadaye katika somo.)

Waulize wanafunzi watafakari kimya maswali yafuatayo:• Kama ungekuwa unaishi Zarahemla wakati huo, unadhania ungejibu vipi vitendo vya

Alma na wana wa Mosia.Onyesha picha ya Kuongoka kwa Alma Mdogo (Kitabu cha Sanaa za Injili [2009], no. 77). Waulize wanafunzi kusoma Mosia 27:11–13, ambalo ni tukio linaloonyeshwa katika mchoro. Kisha alika mwanafunzi asome Mosia 27:14 kwa sauti. Uliza darasa kutafuta sababu ambazo malaika alipatiana za kujawajia Alma na wana wa Mosia.• Mstari huu unafunza nini kuhusu jinsi tunaweza kuwasaidia wengine ambao wanasu-

mbuka? (Hakikisha kwamba wanafunzi wanaelewa kwamba Bwana hujibu maombi yetu ya uaminifu kwa wengine. Unaweza kutaka kuandika kanuni hii kwenye ubao na kupendekeza kwamba wanafunzi waandike katika maandiko yao karibu na Mosia 27:14. Unaweza pia kutaka kupendekeza kwamba waongeze marejeleo Yakobo 5:16. Taja kwamba Bwana hujibu maombi yetu si tu ya wale wanaotaabika kiroho bali pia wale ambao wana aina ingine ya changamoto na mahitaji.)

• Ni wakati gani maombi ya mtu mwigine yalileta tofauti katika maisha yako?• Ni wakati gani umehisi kwamba maombi yako yameleta tofauti kwa maisha ya mtu

mwingine?Wahimize wanafunzi waendelee kuwaombea wengine. Shuhudia kwamba tukio la Alma Mdogo na wana wa Mosia ni ushahidi wa kwamba Bwana husikia maombi yetu kwa niaba ya wengine. Yeye hataruka wakala wa wale ambao tunawaombea, lakini Yeye atasikia mao-mbi yetu, na Yeye atajibu katika njia Yake na wakati Wake.Alika mwanafunzi asimame mbele ya darasa na kusoma Mosia 27:15–16 kwa sauti. Elezea kwamba maneno haya ni ya malaika kwa Alma na wana wa Mosia. Sisitiza kwa malaika alisema “kwa sauti kama radi, iliyosababisha ardhi kutetemeka” (Mosia 27:11).• Ni nini kinachokupendeza kuhusu kile malaika alifanya na kusema? Kwa nini

kilikupendeza ?

Kufindisha kwa Roho MtakatifuBwana amesema kwa-mba tunafaa “kuhubiri injili [Yake] kwa Roho, hata Mfariji ambaye alitumwa kufunza ukweli” (M&M 50:14). Unapofundisha, tafuta mwongozo wa Roho kukusaidia kutohoa somo kwa mahitaji ya wanafunzi wako.

Page 261: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

246

SoMo la 67

Fanya muhtasari wa Mosia 27:19–22 kwa kuelezea kwamba baada ya malaika kushiriki ujumbe wake, Alma hangeweza kusema, alikuwa mdhaifu, na alibebwa akiwa hoi hadi kwa baba yake (ona Mosia 27:19). Wakati baba ya Alma alisikia kile kilichokuwa kimete-ndeka, yeye “alifurahi, kwani alijua kwamba ulikuwa ni uwezo wa Mungu” (Mosia 27:20). Yeye aliwakusanya watu “ili washuhudie yale ambayo Bwana alikuwa amemtendea mwana wake” (Mosia 27:21). Yeye pia aliwakusanya makuhani, na walifunga na kuomba kwamba mwanawe aweze kupokea nguvu zake na aweze kuongea (ona Mosia 27:22).

Mosia 27:23–31Alma Mdogo alitubu na kuzaliwa tenaRudi kwenye orodha inayoelezea Alma na wana Mosia ambayo uliandika kwenye ubao mapema. Ipatie nembo orodha hiyo Mapema. Andika Baadaye kwenye upande mwengine wa ubao. Waalike wanafunzi kusoma Mosia 27:23–24, 28–29, wakitafuta maneno na vishazi ambavyo vinaonyesha vile Alma alibadilika. Wapatie wanafunzi wachache nafasi ya kuandika maneno na vishazi hivi kwenye ubao.• Kulingana na Mosia 27:24 na 28, Alma alifanya nini ambacho kilimpelekea kubadilika?

Bwana alifanya nini? Tunapotafuta kubadilika na kumfuata Mwokozi, kwa nini ni mu-himu kuelewa kile ambacho ni sharti tufanye? Kwa nini ni muhimu kuelewa kile Bwana atatufanyia sisi?

• Je! Kujifunza kuhusu uzoefu wa Alma kunaweza kumsaidia vipi mtu anayefikiria kwa-mba yeye hawezi kusamehewa?

Alika mwanafunzi asome Mosia 27:25–26 kwa sauti. Uliza darasa kutambua fundisho ambalo Bwana alimfunza Alma. (Ingawa wanafunzi wanaweza kutumia maneno tofauti, hakikisha wanaelewa kwamba kila mmoja wetu lazima azaliwe tena kupitia Upatani-sho wa Yesu Kristo. Unaweza kutaka kuandika ukweli huu kwenye ubao.Elezea kwamba kuzaliwa tena humaanisha kupata Roho wa Bwana kusababisha maba-diliko makubwa katika moyo wa mtu hata kwamba mtu yule hana hamu tena ya kutenda maovu bali ana hamu ya kutafuta vitu vya Mungu (ona Mosia 5:2).Unaweza kutaka pia kuelezea kwamba ingawa mabadiliko makubwa ya moyo yalitokea upesi kwa Alma na wana wa Mosia, wengi wetu ubadilika kupitia Upatanisho kidogo ki-dogo. Ni mfanyiko badala ya tukio. Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa vyema fundisho hili, alika mmoja wao kusoma taarifa ifuatayo ya Rais Ezra Taft Benson:“Ni sharti tuwe makini, tunapotafuta kuwa zaidi na zaidi kama mungu, kwamba tusivu-njike moyo na kukata tamaa. Kuwa kama Kristo ni jambo la maishani yote na kila mara hujumuisha ukuaji na mabadiliko ambayo uwa pole pole, karibu sana yasitambulika. Maandiko yameandikwa matukio ya ajabu ya watu ambao maisha yao yabadilika kwa kiajabu, ghafula kama ilivyokuwa: Alma Mdogo, Paulo kwenye barabara kwenda Dameski, Enoshi akiomba usiku wa manane, Mfalme Lamoni. Mifano ya ajabu kama hiyo ya nguvu za mabadiliko hata wale waliokuwa katikati ya dhambi yanapatiana matumaini kwamba Upatanisho unaweza kuwafikia hata wale walioko ndani ya kina cha kukata tamaa.“Lakini sharti tuwe na tahadhari tunapojadili mifano hii ya ajabu. Ingawa ilikuwa halisi na ya nguvu, ilikuwa ya kipekee zaidi ya kuwa kawaida. Kwa kila Paulo, kwa kila Enoshi, na kwa kila Mfalme Lamoni, kuna mamia na maefu ya watu ambao wanapata mfanyiko wa toba kuwa mgumu sana kueleweka, usiotambulika sana. Siku baada ya siku wanasonga karibu na Bwana, kutambulika kidogo sana wanajenga maisha ya kiungu. Wanaishi maisha ya wema sana, ya huduma, na azimio” (“A Mighty Change of Heart,” Ensign, Oct. 1989, 5).Baada ya wanafunzi kushiriki kile walichojifunza kutoka kwa taarifa, waalike wachukue dakika chache kujibu mojawapo wa maswali yafuatayo katika shajara zao za kujifunza maandiko. (Unaweza kutaka kuandika maswali haya kwenye ubao kabla ya darasa, ku-tayarisha kitini kikiwa na maswali, au kusoma maswali pole pole ili wanafunzi waweze kuyaandika katika shajara zao za kujifunza maandiko.)• Je! Umeshabadilishwa kupitia Upatanisho ulipotubu na kufanya yote uwezayo kumfuata

Mwokozi?• Je! Ni kitu kimoja gani unaweza kufanya kiukamilifu zaidi ili kuja kwa Bwana ili kwamba

uweze kubadilika kupitia Upatanisho?

Kushiriki taarifa za kinabiiKama dondoo ni ndefu, inaweza kuwa usaidizi mkubwa kuiwasilisha kwa wanafunzi kama kitini au kuiandika kwe-nye ubao. Bila usaidizi kama huo, wanafunzi waweza kukangayika au kutatizika katika kuielewa.

Page 262: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

247

MoSia 27

Waalike wanafunzi wachache kushiriki kile wameandika na kusimulia kuhusu mabadiliko ambayo yanaweza kututokea tunapotubu na kufanya imani katika Yesu Kristo na Upata-nisho Wake. (Wakumbushe wanafunzi kwamba hawahitaji kushiriki chochote ambacho ni cha kibinafsi au siri. Hakikisha kwamba wanaelewa kwamba hawafai kuongea kuhusu dhambi zao za zamani.)

Mosia 27:32–37Alma Mdogo na wana wa Mosia walisafiri kote katika nchi, wakijitahidi kurekebi-sha madhara waliyokuwa wamefanya na kuimarisha KanisaElezea kwa toba ya kweli ni mabadiliko ya moyo, si tu azimio la kusitisha kufanya makosa. Alika wa mwanafunzi asome Mosia 27:32–37 kwa sauti. Uliza darasa kutambua kile Alma na wana wa Mosia walifanya zaidi ya tu kusitisha kile walikuwa wanafanya ambacho kili-kuwa makosa.• Je! Kuna ushahidi gani unaouona kwamba Alma na wana wa Mosia walikuwa wameba-

dilika kweli?• Je! Tunaweza kujifunza nini kutokana na mfano wao?Majibu ya wanafunzi yanaweza kujumuisha yafuatayo:Hata wale ambao wanaasi dhidi ya Bwana na mafundisho Yake wanaweza kusamehewa.Kutubu kikweli, mtu sharti afanye kila kitu kinachowezekana kurekebisha uha-ribifu ambao ametenda. Unaweza kuelezea kwamba sisi wakati mwengine tunatumia neno kulipia kumaanisha kitendo cha kurekebisha uharibifu ambao umefanywa na kureke-bisha chaguo zetu zisizo za hekima.)Kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo, tunaweza kubadilishwa hadi kwa hali ya wema.Hitimisha kwa kushuhudia kwamba tukio la Alma na wana wa Mosia ni mfano wa nguvu za Upatanisho wa Yesu Kristo za kutubadilisha sisi. Shuhudia juu ya hamu ya Mwokozi ya kutusamehe sote ambao, kama vijana hawa, walifanya imani katika Yeye na kutafuta kumfuata Yeye.

Page 263: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

248

SoMo la 67

Tangazo na Habari za UsuliMosia 27:25. Kuzaliwa tena

Mzee David A. Bednar wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alielezea mfanyiko huu wa kuzaliwa tena:

“Tunaanza mfanyiko wa kuzaliwa tena kupitia kufanya imani katika Kristo, kutubu dhambi zetu, na kubatizwa kwa kuzamishwa kwa ondoleo la dhambi na mtu aliye na mamlaka ya ukuhani.

“. . . Baada ya kutoka nje ya maji ya ubatizo, nafsi zetu zinahitaji kuendelea kuzamishwa ndani na kuloweshwa na ukweli na nuru ya injili ya Mwokozi. Kujichovya kijuujuu mara kwa mara katika mafundisho ya Kristo na ushiriki nusu nusu katika Kanisa Lake la urejesho hakuwezi kuzaa mabadiliko ya kiroho ambayo yana-tuwezesha kutembea katika upya wa maisha. Badala, uaminifu kwa maagano, na sharti la daima, na kujito-lea nafsi zetu zote kwa Mungu ndicho kinachohitajika ikiwa sisi tutapokea baraka za milele. . . .

“Uzamisho kamili ndani na ulowesho kwa injili ya Mwokozi ni hatua muhimu katika mfanyiko wa kuzaliwa tena” (“Ye Must Be Born Again,” Ensign or Liahona, May 2007, 21).

Mzee Bruce R. McConkie, pia wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, alielezea:

“Tunazaliwa tena tunapokufa kulingana na uovu na tunapoishi kulingana na vitu vya Roho. Lakini haya hayatokei mara moja, ghafula. Huu ni mfanyiko. Ku-zaliwa tena ni kitu cha polepole, isipokuwa kwa hali chache za kipekee ambazo ni za kimiujiza sana ambazo zimeandikwa katika maandiko. Almradi idadi kubwa ya washiriki wa Kanisa inavyohusika, tunazaliwa tena kwa viwango, na tunazaliwa tena kwenye nuru iliyoonge-zeka na elimu iliyoongezeka na hamu iliyoongezeka kwa wema tunapoweka amri. . . .

“Kama waumini wa Kanisa, ikiwa tutapanga uelekeo unaongoza hadi uzima wa milele; ikiwa tutaanza kufanyiza kuzaliwa tena kiroho, na kuelekea katika uelekeo sahihi; ikiwa tutapanga uelekeo wa kutakasa nafsi zetu, na kiwango kwa kiwango tukielekea katika uelekeo huo; ikiwa tutapanga uelekeo wa kuwa waka-milifu, na, hatua kwa hatua, na awamu kwa awamu, tunakamilisha nafasi zetu kwa kushinda malimwengu, kisha ni hakikisho kamili hamna—swali lolote kui-husu—tuatapata uzima wa milele. Hata ingawa tuna kuzaliwa tena kiroho mbele yetu, ukamilisho mbele yetu, kiwango kamili cha utakaso mbele yetu, ikiwa tutapanga uelekeo na kuufuata kwa uwezo wetu wote katika maisha haya, basi tunapoondoka kutoka kwa maisha haya tutaendelea kisahihi katika uelekeo huu huu” Brigham Young University 1976 Speeches, Sept. 5, 1976, 5–6, speeches. byu. edu).

Page 264: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

249

UtanguliziBaada ya kuogolewa, wana wa Mfalme Mosia wali-hisi hamu kuu ya kuhibiri injili kwa Walamani. Baada ya kumuuliza Bwana na kupokea hakikisho kwamba watabarikiwa na ufanisi na ulinzi, Mosia aliwaruhusu waondoke. Wakati huo huo, Mosia alikuwa anajishu-ghulisha na kutunza kumbukumbu takatifu ambazo

alikuwa amekabidhiwa. Yeye alitafsiri kumbukumbu za Wayaredi na kisha kumpatia kumbukumbu zote Alma Mdogo. Kwa sababu wanawe walikataa nafasi ya kuwa mfalme, yeye alianzisha mfumo wa waamuzi kama mpango mpya wa serikali katika nchi.

SOMO LA 68

Mosia 28–29

Mapendekezo ya Kufundisha

Mosia 28:1–9Wana wa Mosia walikuwa na hamu ya kuwahubiria WalamaniKabla ya darasa, andika taarifa zifuatazo kwenye ubao: 1. Nina hamu ya kweli ya furaha ya milele kwa wengine. 2. Niko tayari kujitolea kuwasadia wengine. 3. Nina hamu ya kushiriki injili na wengine.Ili kuanza darasa, waulize wanafunzi kutumia taarifa zilizopo kwenye ubao kimya kujita-thimini wenyewe. Acha watumia kipimo cha 1 kwa 10, kipimo cha 1 kikionyesha kwamba taarifa hii haiwaelezei wao kisahihi na kipimo cha 10 kikionyesha kwamba taarifa hii inawaelezea wao kisahihi kabisa.Waalike wanafunzi kusoma Mosia 27:8–10 kimya.• Je! Alma na wana wa Mosia wangeonyeshwa vipi katika kipimo hicho hicho katika wa-

kati huu katika maisha yao?Uliza mwanafunzi asome Mosia 28:1–4 kwa sauti.• Je! Wana wa Mosia wangeonyeshwa vipi katika kipimo hicho hicho baada ya kuongo-

lewa kwao? Ni vishazi gani katika Mosia 28:1–4 vinavyoonyesha kiasi ambacho wali-kuwa wamebadilika?

• Je! Kwa nini hamu za wana wa Mosia zilibadilika? (Walifanya imani katika Yesu Kristo, wakatubu dhambi zao zote, na wakaongoka; ona Mosiah 27:34–36. Unaweza pia kutaka kurejelea Mosia 28:4 ili kuonyesha jinsi Roho ya Bwana aliwashawishi wao.)

• Kutokana na kile umejifunza kuhusu Walamani kwa wakati katika historia yao, ni ugumu gani wamisionari wangekumbana nao miongoni mwao?

• Kulingana na Mosia 28:2, ni tofauti gani wana wa Mosia waliamini kuhubiri kwao ku-ngeleta katika maisha ya Walamani?

• Je! Mazungumzo ya wana wa Mosia yalishawishi hamu yao vipi ya kushiriki injili? Ni kanuni gani tunaweza kujifunza kutokana uzoefu wake? Fanya muhtasari majibu ya wanafunzi kwa kuandika kanuni ifuatayo kwenye ubao: Mazungumzo yetu yanapoe-ndelea kupata kina, hamu yetu ya kushiriki injili itaongezeka.)

Uliza mwanafunzi asome taarifa ya Mzee Dallin H. Oaks wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili. Unaweza kutaka kuwahimiza wanafunzi kuandika taarifa hii katika ulingo wa maandiko yao karibu na Mosia 28:1–4.“Uzito wa hamu yetu ya kushiriki injili ni kielelezo kikubwa cha kiwango cha uongofu wetu binafsi” (“Sharing the Gospel,” Ensign, Nov. 2001, 7).Waalike wanafunzi kutafakari jinsi hamu yao ya kushiriki injili pamoja na

wengine inaongezeka wanapokuwa kuwa karibu na Bwana.• Je! Ni uzoefu gani katika maisha yetu uliokupelekea kushiriki injili na wengine?

Page 265: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

250

SoMo la 68

Waulize wanafunzi kufikiria kwamba wanajua kijana ambaye ni muumini wa Kanisa lakini ana hamu ndogo ya kuhudumu misheni ya muda.• Je! Kijana huyu anaweza kufanya nini ili kuongezea hamu ya kushiriki injili? (Wanafunzi

wanaposhiriki umaizi wao, wahimize wao kukumbuka kile kilichofanya uongofu wao kupata kina kwa injili ya Yesu Kristo na jinsi wanaweza kupendekeza shughuli kama hizo au uzoefu kwa kijana huyu. Wasaidie wao kuona kwamba uongofu mkuu unaele-keza kwenye hamu ya kushiriki injili na wengine.)

Unaweza kutaka kuelezea jinsi ulipokea hamu ya kufunza injili ya wengine. Unapofanya hivyo, fikiria kushiriki ushuhuda wako kwamba tunapokaribia karibu na Bwana na kuhisi Roho Yake, hamu yetu ya kushiriki injili na wengine itaongezeka.Acha wanafunzi wasome Mosia 28:5–8 na watambue kwa nini Mosia aliacha wanawe kuenda kwenye kazi hatari.• Katika jibu la mombi ya Mosia, ni baraka gani Bwana aliwaahidi wana wa Mosia?

Mosiah 28:10–20Mosia alitafsiri mabamba ya Wayaredi na kumkabidhi Alma kumbukumbu takatifuChoro yafuatayo kwenye ubao:

Onyesha picha ya taji, na acha wanafunzi asome Mosia 28:10. Uliza darasa kuangalia shida mfalme aliyokuwa nayo wakati wanawe waliondoka kwenda misheni. (Yeye alihitaji kum-pata mtu wa kuchukua nafasi yake kama mfalme.)Fanya muhtasari wa Mosia 28:11–19 kwa kuelezea kwamba Mosia alikuwa anazeeka, na aligeuza usikivu wake kwa kumbukumbu takatifu ambazo alizokuwa amekabidhiwa: kumbukumbu ambazo baba yake alikuwa amempatia yeye na kumwambia azichunge na kumbukumbu ambazo Limhi alikuwa amempatia. Katika nafasi yake kama muonaji, ali-tafsiri kumbukumbu ya mabamba ya—Wayaredi ambayo yalikuwa yamepatikana na kundi ambalo Mfalme Limhi alikuwa ametuma kutafuta nchi ya Zarahemla (ona Mosia 8:7–9). Waelekeze wanafunzi usikivu wa picha mabamba ya dhahabu kwenye ubao.Elezea kwamba zaidi ya kumteua kiongozi wa ufalme, Mosia pia alihitaji kuteua mtunzaji wa mabamba. Waulize wanafunzi kusoma Mosia 28:20 kimya.• Je! Ni nani alipokea kumbukumbu takatifu?• Kwa nini Alma alikuwa chaguo zuri la kutunza kumbukumbu hizi?

Mosia 29Watu walifuata ushauri wa Mosia wa kuanzisha mfumo wa waamuzi kama mpa-ngo wao wa serikaliAcha wanafunzi kuinua mikono yao kama wangependa kuwa mfalme au malikia. Chagua mmoja wa wanafunzi hawa kuja mbele ya darasa na kusimama karibu na taji lililochorwa kwenye ubao (au weka taji la karatasi kwenye kichwa chake). Acha mwanafunzi aelezee ni manufaa gani yeye atapata kutoka kwa kuwa mfalme au malikia.Uliza mwanafunzi asome Mosia 29:1–3 kwa sauti.• Je! Ni nani watu hawa walikuwa wanataka awe mfalme wao?• Je! Ni nini wana wa Mosia waliachana navyo ili waweze kuhubiri kwa Walamani?• Ni zipi baadhi ya nafasi wavulana na wasichana wanazowacha au kuhairisha leo ili wao

waweze kuhudumu misheni?

Hali halisi ya maishaKulinganisha kanuni ya injili na hali halisi ya ma-isha inaweza kuwasaidia wanafunzi kuchanganua kanuni hii na kutambua uhusiano wake katika maisha yao. Unaweza kutaka kuwashauri wanafunzi kwamba wa-navyojibu kwa uaminifu kwa mfano kama huo, vile itakavyofaa zaidi katika mfanyiko wao wa kujifunza.

Page 266: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

251

MoSia 28 –29

Fanya muhtasari wa Mosia 29:4–10 kwa kuelezea kwamba Mfalme Mosia alikuwa na hofu kwamba kuteuliwa kwa mfalme mpya angewaelekeza kwenye mabishano na hata vita. Yeye pia alitaja shida zingine ambazo zinaweza kuzuka kama mfalme mwovu angekuja mamlakani. Acha wanafunzi wasome Mosia 29:16–18 na kutambua shida hizi.Elezea kwamba Mfalme Mosia alipendekeza kwamba serikali ya Wanefi haikufaa tena kusimamiwa na mfalme. Badala yake, alipendekeza mfumo wa waamuzi, na waamuzi wakichaguliwa na sauti ya watu.Acha wanafunzi wasome Mosia 29:11, 25 kimya, wakitafuta jinsi waamuzi wangehukumu watu. (Kulingana na amri za Mungu” na “kulingana na sheria ambazo zimetolewa kwenu na baba zetu.”)Andika Mosia 29:26–27, 30, 33–34, 37–38 kwenye ubao. Gawa darasa katika majozi. Acha wanafunzi wapekue mistari hii na kutambua majukumu ya watu katika serikali iliyope-ndekezwa na Mfalme Mosia. Acha kila jozi lijadili maswali yafuatayo. (Unaweza pia kutaka kuandika maswali haya kwenye ubao au kupatiana katika kitini.)• Kulingana na Mfalme Mosia, ni manufaa gani yatakayokuja kutokana na maamuzi

ya sauti ya watu? (Yeye alisema kwamba sauti ya watu kawaida haina hamu ya vitu ambavyo ni “kinyume na kile kilicho sahihi.” Yeye pia aliongea kuhusu haja ya raia wote kushiriki katika mzigo wa serikali yao na kuwa na “nafasi sawa.”)

• Ni matokeo gani ambayo yangekuja ikiwa sauti ya watu itachagua uovu? (Hukumu ya Mungu itakuja juu yao, na wataangamizwa.)

• Katika Mosia 29:34, unafikiria maana ya kishazi hiki ni nini “kwamba kila mtu aweza kubeba sehemu yake”? Kishazi hiki kinaweza kutumika kwa majukumu ya raia katika kushiriki katika serikali zao za mitaa na kitaifa?

Soma taarifa ifuatayo ya Mzee Neal A. Maxwell wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili:“Kwa kile kinachotendeka katika tamaduni zinapodorora kote kwa viongozi na wafuasi wanawajibika. . . . Ni rahisi kulaumu viongozi, lakini hatupaswi kuwapatia wafuasi ruhusa ya bure” (“Repent of [Our] Selfishness,” Ensign, May 1999, 24).• Kwa nini ni muhimu kwa wote viongozi na wafuasi kuwajibika kwa vitendo vyao?• Unaweza kufanya nini kuhimili sheria na viongozi wa haki? (Unaweza kutaka kurejesha

wanafunzi kwa Makala ya Imani 1:12.)Onyesha uhakikisho wako kwamba hali si kila taifa katika dunia ambalo lina nafasi ya ku-chagua viongozi wao wenyewe, Bwana daima atawasaidia ambao wanaamini katika Yeye, bila kujali wanapoishi.Alika mwanafunzi asome Mosia 29:41–43 kwa sauti.• Ni nani watu walimchagua kuwa mwamuzi mkuu wa kwanza? Je! Aliishi kulingana

na jukumu lake kuwa kiongozi mwenye haki na mwema? Matokeo ya uongozi wake yalikuwa nini?

Waulize wanafunzi kuelezea kwa maneno yao wenyewe kile wamejifunza kutoka kwa Mosia 29. Wanaweza kutambua baadhi ya kweli zifuatazo:Uongozi wa uovu unaweza kuleta ubishani na dhambi.Si kawaida kwa sauti ya watu kuchagua kitu fulani ambacho si sahihi.Ikiwa watu wanachagua uovu, hukumu ya Mungu itakuja juu yao.Kila mtu ana wajibu wa kuhimili sheria na viongozi wa haki.Hitimisha kwa kutoa ushuhuda wa kanuni zilizopo katika somo la leo.

Rejeo la MosiaChukua wakati wa kuwasidia wanafunzi kurejea kitabu cha Mosia. Waulize wao kufikiria kile wao wamejifunza kutoka kwa kitabu hiki, kote katika seminari na katika shajara zao za kujifunza maandiko. Kama inahitajika, waalike wapitie kitabu hiki ili kuwasidia wao kukumbuka. Baada ya muda wa kutosha, waalike wanafunzi kadha kushiriki mawazo yao na hisia zao kuhusu kitu fulani ambacho kiliwapendeza katika kitabu hiki.

Page 267: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

252

UtangUlizi Wa

Kitabu cha almaKwa nini kujifunza kitabu hiki?Katika kujifunza kitabu cha Alma, wana-funzi watajifunza kuhusu Yesu Kristo na umuhimu wa Upatanisho na Ufufuo Wake katika mpango wa wokovu. Pia watajifu-nza kuhusu nguvu ya neno la Mungu ili kushinda ukuhani wa uongo, mafundisho ya uongo, dhambi, chuki, ukengeufu na kuwaongoza watu binafsi ili wapate uzoefu wa mabadiliko makuu ya moyo. Wanafunzi wanaweza kuandilishwa na kupata mao-ngozi wanaposoma kuhusu jitihada za ki-misionari za Alma, Amuleki, na watoto wa Mosia, pamoja na uongofu na uaminifu wa Anti- Nefi- Lehi (watu wa Amoni) Wanapo-soma kwa kina sura zinazoeleza mapigano kati ya Wanefi na Walamani, watajifunza kanuni zitakazowaongoza katika nyakati za shida wanazoziishi na kuwasaidia kushinda vita binafsi dhidi ya adui.

Nani alikiandika kitabu hiki?Mormoni alikusanya na kufupisha kumbu-kumbu kutoka katika mabamba makubwa ya Nefi ili kutengeneza kitabu cha Alma. Kitabu kimeitwa jina la Alma, ambaye, kama mwana wa Alma, mara nyingi hui-twa Alma Mdogo. Wakati Mfalme Mosiah alianzisha utawala wa waamuzi miongoni mwa Wanefi, Alma Mdogo akawa mua-muzi mkuu wa kwanza na kurithi nafasi ya baba yake kama kuhani mkuu katika Kanisa. (ona Mosia 29:42) Hatimaye aliji-uzulu nafasi yake kama mwamuzi mkuu ili ajitolee mwenyewe kabisa kwa ule ukuhani mkuu na kuwatolea watu neno la Mungu kote katika nchi ya Wanefi (Alma 4:20; 5:1). Mormoni ilitumia kumbuku-mbu za huduma ya Alma (ona Alma 1–44) na maandiko ya wana wa Alma Helamani (ona Alma 45–62) na Shibloni (ona Alma 63) kutunga kitabu cha Alma.

Kitabu hiki kiliandikwa kina nani na kwa nini?Mormoni hakukielekeza kitabu cha Alma kwa watu fulani wala hakusema ni kwa nini alikiandika. Hata hivyo, mafundisho mbalimbali kuhusu huduma ya ukombozi ya Yesu Kristo yamechangia kwenye lengo kuu la Kitabu cha Mormoni, ambayo ni kushuhudia kwamba Yesu ni Kristo, Mungu wa milele (ukurasa wa jina wa Kitabu cha Mormoni, ona pia Alma 5; 7; 13; 32–34; 36; 39–42).

Kiliandikwa lini na wapi?Kumbukumbu za asili zilizotumika kama vyanzo vya kitabu cha Alma vinadhaniwa kuwa viliandikwa kati ya mwaka wa 91 K.K mwaka wa 52 K.K Mormoni alifupisha kumbukumbu hizo kati ya mwaka wa 345 B.K na mwaka wa 385 B.K. Mormoni ha-kuandika pale alikuwa alipokuwa akiandika kitabu hiki.

Nini baadhi za sifa bainifu za kitabu hiki?Ingawa kitabu cha Alma ni kirefu zaidi katika Kitabu cha Mormoni, kinajumui-sha kipindi cha miaka 39 tu — takriban miaka 91 K.K hadi miaka 52 K.K. Kitabu hiki kinaeleza tukio la kwanza la mafani-kio ya kazi za umisionari miongoni mwa Walamani. Pia kinaangazia uaminifu wa

waongofu wa Walamani katika kuweka maagano yao (ona Alma 23:6–7; 24). Zaidi ya hayo, kitabu cha Alma kinajumuisha mafunzo kuhusu mafundisho ya kutawa-zwa kabla na huduma ya Melkizedeki (ona Alma 13), nguvu ya neno la Mungu (ona Alma 31); jinsi ya kukuza imani katika Yesu Kristo (ona Alma 32–34); uzito wa kuvunja sheria ya usafi wa mwili (ona Alma 39); hali ya roho zetu kufuatia kifo (ona Alma 40); mafundisho ya ufufuo na urejesho (ona {Alma 40–41); na majukumu ya haki na neema katika mpango wa ukombozi wa Baba wa Mbinguni (ona Alma 42). Kitabu hiki pia kina maelekezo ya Bwana kuhusu ulinzi binafsi na uhalalisho wa vita (ona Alma 43:45 –47).

MuhtasariAlma 1–3 Nehori anaanzisha ukuhani wa uongo miongoni mwa Wanefi. Alma anaongoza Wanefi wenye haki katika kujitetea wenyewe dhidi ya Amlisi na wafuasi wake, ambao wamejiunga pamoja na jeshi la Walamani. Baada ya kuzuia jaribio la Amlisi la kuwa mfalme na kuanga-miza Kanisa, Wanefi wanalishinda jeshi lingine la Walamani.

Alma 4–16 Alma ajiuzulu kama mwa-muzi mkuu. Alisafiri katika nchi yote ya Wanefi kupambana na kiburi na uovu kwa kuhubiri neno la Mungu. Amuleki aungana na Alma, na wanafundisha juu ya Upatanisho wa Yesu Kristo, ufufuo, na haja ya imani katika Bwana na toba. Zeezromu aongoka na kubatizwa.

Alma 17–28 Wana wa Mosia na we-ngine wanahubiri neno la Mungu miongoni mwa Walamani katika nchi ya Nefi. Maelfu waongoka kwa Bwana. Waongofu waziacha silaha zao za vita na kwenda kukaa mi-ongoni mwa Wanefi. Watu wengi wanakufa katika pambano kuu kati ya Wanefi na Walamani.

Alma 29–42 Alma ana hamu ya kuleta nafsi nyingi kwenye toba. Anamchanganya Korihori, mpinga Kristo. Wakati akiwafundisha Wa-zoramu, kundi la wapinzani Wanefi,

Alma analinganisha neno la Mungu na mbegu ambayo ni lazima irutu-bishwe kwa imani. Amuleki anashu-hudia Upatanisho, na kuwafundisha Wazoramu kufanya imani hadi toba. Alma anatoa ushauri wake binafsi na ushuhuda kwa wanawe Hela-mani, Shibloni, na Koriantoni. Alma anakabidhi kumbukumbu takatifu kwa Helamani. Anafundisha kuhusu dunia ya kiroho baada ya kifo, ufu-fuo, na majukumu ya haki na neema katika mpango wa Mungu.

Alma 43–45 Anachochea hasira na wapinzani Wanefi, Walamani wana-kuja vitani dhidi ya Wanefi. Moroni anawaongoza Wanefi katika ushindi dhidi ya jeshi la Zerahemna. Alma anamhoji na kumbariki Helamani, anatabiri juu ya maangamizi ya Wa-nefi, na kuondoka katika nchi ile.

Alma 46–63 Moroni, Lehi, Teankum, Helamani, na Pahorani wawao-ngoza Wanefi katika ushindi dhidi ya majeshi ya Walamani, wakisima-miwa na Amalikia na Amoroni. Mo-roni na Pahorani pia wanazima uasi wa Wanefi walioasi waliojulikana kama watu wa mfalme. Shibloni apokea kumbukumbu za Wanefi na baadaye anazipatiana kwa mwana wa Helamani, Helamani. Jeshi la Moroniha lashinda Walamani katika mapigano mengine.

252

Page 268: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

253

SOMO LA 69

alma 1–2UtanguliziMuda mfupi baada ya Alma kuwa mwamuzi mkuu, mtu aitwaye Nehori akajiimarisha mwenyewe kama mhubiri kati ya watu. Alizungumza dhidi ya Kanisa na mafundi-sho yake, na akawashawishi wengi kumwamini yeye na kumpa fedha. Wakati Nehori alipomwuua Gideoni, ambaye alikuwa mshiriki mwaminifu wa Kanisa, yeye aliletwa mbele ya Alma. Akimpata Nehori na hatia ya ukuhani wa uongo na kujaribu kutekeleza ukuhani wa uongo kwa upanga, Alma alimhukumu Nehori kifo.

Kanisa lilifanikiwa, wakiongozwa na makuhani we-nye bidii na wanyenyekevu, lakini ukuhani wa uongo uliendelea. Amlisi, mtu mjanja wa utaratibu wa Nehori, alipata msaada kati ya watu wengi na alijaribu bila ma-fanikio kuwa mfalme wa Wanefi. Yeye na wafuasi wake wakaasi, wakaja dhidi Wanefi kwa vita, na hatimaye wakaunganisha nguvu zao pamoja na jeshi la Walamani. Wakiimarishwa na Bwana, Wanefi walipata hasara nyi-ngi, lakini walishinda mashambulizi ya majeshi hayo.

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 1Licha ya kuenea kwa haraka ukuhani wa uongo na mateso, wengi wanasimama imara katika imaniAndika maarufu ubaoni.• Ni zipi baadhi ya hatari ya kutafuta umaarufu? Ni zipi baadhi ya hatari ya kufuata watu

kwa sababu tu wao ni maarufu?Eleza kwamba mtu mmoja aitwaye Nehori alikuwa maarufu na baadhi ya watu katika Zarahemla. Alika wanafunzi wasome Alma 1:2–6 kimya wakitafuta kile Nehori alifundisha na jinsi watu walivyojibu. Baada ya wanafunzi kutoa taarifa ya walichopata, fikiria kuuliza maswali kama yafuatayo:• Kwa nini mafundisho ya Nehori katika Alma 1:4 ni hatari? (Kama wanafunzi wana-

hangaika kujibu swali hili, waelezee kwamba Nehori alifundisha kwamba watu wote [watapata] uzima wa milele, bila kujali nini watafanya. Mafundisho haya yanapuuza haja ya toba, maagizo, na kushika amri za Mungu. Ona pia Alma 15:15.)

• Ni matokeo gani yanayoweza kumtokea mtu ambaye anaamini fundisho hili?• Mafanikio ya Nehori yalimwathiri vipi? (Ona Alma 1:6.)Fanya muhtasari wa Alma 1:7–15 kwa kueleza kwamba siku moja Nehori alikuwa anakwe-nda kuhubiri kwa kundi la wafuasi wake alipokutana Gideoni, ambaye alikuwa amesaidia kuwaokoa watu wa Limhi kutoka katika utumwa na ambaye alikuwa sasa anahudumu kama mwalimu katika Kanisa. Nehori “akaanza kubishana na [Gideon] kwa ukali, ili awapotoshe watu wa kanisa; lakini [Gideon] alimpinga, na kumwonya kwa maneno ya Mungu” (Alma 1:7). Nehori, katika hali ya hasira kali, akauchomoa upanga wake na kumwua Gideoni. Watu wa Kanisa walimpeleka Nehori kwa Alma, aleyekuwa mwamuzi mkuu, ahukumiwe kwa uhalifu wake. Alma alimhukumu Nehori kifo, na Nehori “akapata kifo cha aibu.” (Alma 1:15). Unaweza kuhitajika kueleza kuwa cha aibu humaanisha cha kufedhehesha ama chenye soni au kisicho na heshima. Waalike wanafunzi kutafuta mistari michache ya kwanza ya Alma 1:12 kwa neno ambalo Alma alitumia kueleza nini Nehori alileta kwa watu wake mara ya kwanza. Waalike wana-funzi kutazama tanbihi ya chini ya12a. wafanye kugeukia rejeo la kwanza lililoorodheshwa: 2 Nefi 26:29. Waambie wasome mstari huu kimya. • Kwa maneno yako mwenyewe, ukuhani wa uongo ni nini? Unafikiri inamaanisha nini

kwa watu “kujiinua wawe nuru ya ulimwengu”? Kwa nini hii ni hatari?• Kuhubiri kwa Nehori kulikuwaje mfano wa ukuhani wa uongo?• Kulingana na Alma, nini kingetokea kwa watu kama ukuhani wa uongo ungetekelezwa

miongoni mwao?

Kutumia vitabu vya kiada vya Kanisa na kutohoa masomoVitabu vya kiada vya Kanisa vimetayarishwa kwa makini ili kuhaki-kisha kuwa mafundisho ya Kanisa yamewekwa safi. Zingatia kwa makini mapendekezo ya kufu-ndisha katika kitabu cha kiada hiki, ambayo yata-kusaidia kuwa ni mkweli kwa dhamira ya manabii walioandika maandiko. Hata hivyo, unaweza ku-tumia masomo kulingana na mahitaji na mazingira ya wanafunzi wako.

Page 269: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

254

SoMo la 69

• Kwa nini unafikiri inatamanisha kwa watu kufundisha ili wengine wawasifu?Mualike mwanafunzi asome Alma 1:16 kwa sauti. Uliza darasa litambue jinsi na kwa nini ukuhani wa uongo uliendelea kuenea, hata baada ya kifo cha Nehori? Baada ya Wanafunzi kutoa taarifa za walichopata, uliza: • Kulingana na Alma 1:16, ni nini makusudi ya watu wanaotekeleza ukuhani wa uongo?

(Wanautekeleza “ili wapate utajiri na heshima”—kwa maneno mengine, ili wapate fedha na umaarufu.)

Eleza kuwa ukuhani wa uongo na athari zake ziliwakumba Wanefi kwa miaka mingi (ona Alma 2; 15:15; 24:28). Eleza kwamba, katika siku zetu, tunapaswa kuwa na tahadhari dhidi ya ukuhani wa uongo, ndani ya Kanisa na hata nje ya Kanisa. Tusikubali kudanganywa na watu wanaoshiriki ukuhani wa uongo. Tunapaswa pia kujilinda dhidi ya tabia na vitendo vya ukuhani wa uongo katika juhudi zetu za kufundisha injili.• Ni nafasi zipi ulizo nazo za kufundisha injili? (Wasaidie wanafunzi kuona kuwa wana nafasi

nyingi za kufundisha injili. Wanafundishana wanaposhiriki katika seminari na katika Akidi zao na madarasa yao. Wanaweza kufundisha familia zao katika jioni za familia nyumbani. Vijana wanahudumu kama walimu wa nyumbani. Wavulana na wasichana wanaweza kuo-mbwa kunena katika mikutano ya Sakramenti. Wanaweza kushiriki injili na wengine sasa, na wanaweza kuwa wanajitayarisha kuhudumu kama wamisionari wa muda.)

Mwalike mwanafunzi asome taarifa ifuatayo ya Mzee David A. Bednar wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili:

"Chochote ambacho ninyi au mimi tunafanya kama walimu ambacho kwa makusudi tunavuta nathari kwa nafsi zetu —katika ujumbe tunatoa, katika mbinu tunazotumia, au katika tabia zetu kibinafsi —ni aina ya ukuhani wa uongo unaozuia ufundishaji muafaka wa Roho Mtakatifu ” (“Seek Learning by Faith,” Ensign, Sept. 2007, 66–67).Sisitiza kuwa tukijivutia nathari kimakusudi katika majukumu yetu ya kufu-

ndisha injili, tutazuia ufundishaji muafaka wa Roho MtakatifuSoma orodha ifuatayo ya vihamasisho ambavyo watu wanaweza kuwa navyo wanapo-fundisha. Waalike wanafunzi kujadili vihamasisho vipi vinavyoweza kuwa mifano ya ukuhani wa uongo.Kuwaongoza wengine kwa Mwokozi.Kuonyesha jinsi walivyo wacheshi.Kuwasaidia wengine kuhisi Roho.Kuonyesha akili zao.Kuwasaidia wengine kutumia kweli za injili katika maisha yao.Mualike mwanafunzi asome Alma 1:26–27 kwa sauti. Uliza darasa kutambua njia ambazo makuhani wa Mungu walifanya tofauti na Nehori.• Mfano wa makuhani wa Wanefi unawezaje kutusaidia kuepukana na ukuhani wa

uongo?• Makuhani hawa walionyesha vipi kujitolea kwao kwa Mungu?Eleza kuwa ukuhani wa uongo ulisababisha ubishi na mateso kati ya Wanefi. Ili kuwasaidia wanafunzi, kujitayarisha kujifunza Alma 1:19–33, uliza maswali yafuatayo:• Ni lini umewaona watu wakidhihaki, kukashifu au kuwatesa wale wanaozishika amri za

Mungu?• Umewahi kuhisi kudhihakiwa, kukashifiwa au kuteswa kwa kuweka amri? Ikiwa hivyo,

ulijibu vipi?Waalike wanafunzi wasome Alma 1:19–20 kimya, wakitafuta mifano ya waumini wa Kanisa wakiteswa. Baada ya wanafunzi kutoa taarifa ya walichopata, andika maswali yafuatayo uba-oni na kuwaalika wanafunzi kuyanakili katika daftari zao au katika shajara zao za kujifunza maandiko. Wape muda kusoma aya za maandiko kimya na kujibu maswali wao wenyewe.

Kulingana na Alma 1:21–24, waumini walijibu vipi mateso? Ni yapi yalikuwa matokeo ya matendo yao?Kulingana na Alma 1:25–31, waumini wa Kanisa waliishi vipi licha ya mateso? Je! Ni baraka gani walizopokea?

Page 270: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

255

alMa 1–2

Wanafunzi wakishakuwa na muda wa kutosha kusoma aya hizi waulike kile tunachoweza kujifunza kutoka kwa aya hizi? Wanafunzi wanaweza kutambua baadhi au kanuni zote zifuatazo: Hata wakati watu walio karibu nasi wakikosa utiifu, tunaweza kuwa imara na kutotikisika katika kuziweka amri. Tunapoishi injili, tunaweza kuwa na amani maishani mwetu hata kama tunateswa.• Ni lini umeona kanuni hizi kuwa ni za kweli?

Alma 2Amlisi na waasi wengine hatimaye waliungana na Walamani kupigana na WanefiEleza kuwa takribani miaka minne baada ya kifo cha Nehori, Wanefi walikumbana na mtu mwingine mwovu ambaye aliweza kupata kuungwa mkono na wengi. Gawa wanafunzi katika majozi. Katika kila jozi, acha mmoja mwanafunzi mmoja asome Alma 2:1–7 wakati yule mwingine anasoma Alma 2:8–18. Waagize wanafunzi kuandaa makala ya muhtasari wa habari kutokana na aya walizopewa wakieleza kile watu walio na haki walifanya ili ku-uzuia uovu. Baada ya dakika nne au tano hivi, waalike wanafunzi washiriki muhtasari wao pamoja na wenzao. Unaweza kutaka kuwauliza wanafunzi wachache washiriki muhtasari wao na darasa. Uliza maswali yafuatayo ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaelewa aya ambazo wamejifunza;• Amlisi alitaka kufanya nini?• Kulingana na Alma 2:18, kwa nini Wanefi waliweza kuzuia jaribio la Amlisi la kuwa

mfalme? (Bwana aliutia nguvu mkono wa Wanefi. Unaweza kutaka kuwahimiza wanafu-nzi kualamisha kauli hii katika maandiko yao.)

Uliza darasa kuorodhesha mifano ya uovu ambayo vijana wanakumbana nayo hivi leo. Wana-weza kutaja majaribu, na wanaweza pia kutaja majaribio wanayokumbana nayo kwa sababu ya uovu wa wengine. Wapoendelea kujifunza Alma 2, waalike watafakari njia wanazoweza kupokea msaada wa Bwana ili kushinda majaribu na changamoto wanazokabiliana nazo.Eleza kwamba wapiganaji Wanefi waliwashinda wengi wa Waamlisi, lakini walishangazwa kuona kwamba Waamlisi waliosalia walijiunga na jeshi la Walamani. (ona Alma 2:19–25). Kabla ya majeshi ya Wanefi halijarejea jijini Zarahemla, jeshi lililoungana liliwashambulia. Waulize wanafunzi wapekue Alma 2:27 katika kishazi kinachoonyesha ukubwa wa jeshi lililoungana ya Walamani na Waamlisi. Waalike wanafunzi watue kwa muda na kuwaza kile wangefikiria na jinsi wangehisi kama wangekuwa sehemu ya jeshi la Wanefi. Waulize mwanafunzi wasome Alma 2:28–31, 36 kwa sauti, na ulize darasa kutafuta njia ambayo mapigano yaliisha. Baada ya wanafunzi kutoa taarifa kile walichopata, unaweza kutaka kupendekeza kuwa waalamishe maneno akawapa nguvu na akapewa nguvu katika aya hizi.• Kulingana na Alma 2:28, kwa nini Bwana aliwatia nguvu Wanefi? (Wanafunzi wanaweza

kushiriki majibu tofauti kwa swali hili. Wasaidie kutambua kanuni ifuatayo: Tunapo-mwita Mungu kutusaidia kusimama dhidi ya uovu, Yeye atatupatia nguvu. )

• Kwa nini unafikiri ni muhimu kupokea nguvu kutoka kwa Mungu ili kusimama dhidi ya uovu badala ya kuwa na ushawishi wa uovu kuondolewa kabisa kutoka maishani mwetu?

• Unawezaje kufuata mfano wa Alma unaposimama dhidi ya uovu?Waalike wanafunzi kuandika majibu ya mojawapo ya maswali haya:• Bwana amekupatia nguvu vipi wakati umekumbana na uovu?• Ni njia moja gani unayoweza kusimama dhidi ya uovu sasa?Wanafunzi wakishakuwa na wakati wa kuandika, waalike wachache wao kushiriki ma-jibu yao. Unaweza kutaka kushiriki majibu yako pia. Wahimize wanafunzi kufuata mfano wa Wanefi — kuomba usaidizi wa Bwana na kustahili kupatiwa nguvu na Mungu katika juhudi zao. Hitimisha kwa kushuhudia kuwa Mungu atatupatia nguvu tunaposimama dhidi ya uovu.

Page 271: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

256

UtanguliziBaada ya kujiunga na jeshi la Walamani, Waamlisi walijitofautisha kutoka kwa Wanefi kwa kujipaka rangi nyekundu utosini mwao. Waamlisi na Walamani walipigana dhidi ya Wanefi na “maelfu na makumi ya maelfu” walikufa kwenye mapigano (ona Alma 3:26). Kufuatia mapigano haya, Wanefi wengi walijinyenye-keza na “walikumbushwa jukumu yao” (Alma 4:3). Takribani 3,500 walibatizwa na kujiunga na Kanisa.

Hata hivyo, mwaka uliofuata, washiriki wengi wa Kanisa walikuwa wenye kiburi na wakaanza kuwatesa wengine. Akihofia juu ya uovu huu, Alma alijiuzulu kutoka kwanye majukumu yake kama mwamuzi mkuu na kuendelea kuhudumu kama kuhani mkuu juu ya Kanisa. Katika cheo chake, alipanga kusafiri kote katika jimbo, akitoa ushuhuda msafi na kuwaita watu kwa toba.

SOMO LA 70

alma 3–4

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 3:1–19Wanefi wapambana na Waamlisi na WalamaniGawa darasa katika vikundi vidogo vidogo. Kipe kila kikundi kipande cha karatasi kikiwa kimeandikwa maneno yafuatayo: nguo, mitindo ya nywele, vipuli na virembesho, michoro ya mwili. Viulize vikundi kujadili jumbe ambazo watu wanaweza kutuma ama kwa makusudi au bila kukusudia, na vitu hivi. Wakumbushe wanafunzi kuwa Waamlisi walijitenga na Wanefi na kuungana na jeshi la Walamani (ona Alma 2). Waalike wanafunzi wasome Alma 3:4 na kutambua jinsi Waamlisi walipobadilisha sura zao. • Waamlisi walitaka “kutofautishwa na nani?”• Jinsi gani baadhi ya watu leo wanajitofautisha kutoka kwa wenye haki kupitia muone-

kano wao wa nje? (Wanafunzi wanapojibu, hakikisha kueleza wazi kuwa watu wengine kwa makusudi hubadilisha muonekano wao ili kujitenga na walio haki au kuasi dhidi ya viwango vya Kanisa. Wengine hufuata mitindo ya ulimwengu bila kutambua kuwa wanatuma jumbe kuhusu wao wenyewe.)

Eleza kwamba wakati Waamlisi walipoweka alama katika tosi zao ili kujitofautisha na Wa-nefi, walionyesha kuwa walikuwa wajiletea laana ya Walamani juu yao. Waalike wanafunzi wachache kuchukua zamu katika kusoma kwa sauti kutoka kwa Alma 3:14–19. Lisaidie darasa kutathmini aya hizi kwa kuuliza baadhi au yote ya maswali yafuatayo:• Ni kishazi kipi katika Alma 3:18 kinaeleza matendo na msimamo wa Waamlisi kwake

Mungu? (Uasi wa wazi dhidi ya Mungu.”)• Waamilsi walijiletea vipi laana “juu yao”? (Alma 3:19).• Tunajifunza kweli zipi kutoka kwa mistari hii? (Majibu yanaweza kujumuisha kuwa

wale wanaokuja katika uasi wa wazi dhidi ya Mungu huleta matokeo hasi juu yao. na kuwa kama tumetwengwa kutoka kwa Mungu ni kwa sababu tumejitenga wenyewe kutoka kwake.)

Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa umuhimu wa kujitambulisha wenyewe katika njia zilizo za haki, uliza swali lifuatalo:• Ni baadhi ya njia zipi tunazoweza kuonyesha kupitia kwa nguo zetu na muonekano

wetu kuwa sisi ni wafuasi wa Yesi Kristo? (Ikiwa wanafunzi watahangaika katika kujibu swali hili, unaweza ukawacha wasome ingizo “Mavazi na Siha” katika Kwa Nguvu za Vijana [2011], uk 6–8. Sisitiza kuwa ushuhuda wetu kindani wa injili unapaswa kuathiri nguo na siha yetu. )

Wahimize wanafunzi kuonyesha kuwa wanamfuata Bwana wanapofanya chaguo za kila siku, ikijumuisha chaguo kuhusu nguo na siha zao. Sisitiza kwamba kupitia kwa mavazi na siha yetu, tunaweza kujitofautisha kama wafuasi wa Yesu Kristo.

Page 272: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

257

alMa 3– 4

Alma 3:20–27Maelfu wauawa katika mapigano kati ya Wanefi, na Walamani na WaamlisiFanya muhtasari Alma 3:20–25 kwa kueleza kuwa Wanefi waliwasukuma nyuma Walamani lakini pande zote mbili zilipata na maelfu ya majeruhi. Mualike mwanafunzi asome Alma 3:26–27 kwa sauti. Uliza darasa kusikiliza somo ambalo Mormoni alitaka sisi tulielewe.• Kulingana na aya hizi, ni zawadi ipi inawajia wale wanaomtii Bwana?• Ni matokeo yapi yanayowapata wale wasiomfuata Bwana?Kama muhtasari, unaweza kutaka kuandika kanuni ifuatayo ubaoni: Tunapokea furaha au simanzi kulingana na yule tunayechagua kumtii. Waalike wanafunzi kufikiria kuhusu baraka zinazowajia kutokana na kuchagua kumfuata Bwana. • Ni baraka gani umepokea kutoka kwa Bwana ulipochagua kumfuata?

Alma 4:1–14Baada ya muda wa ukuaji katika Kanisa, waumini wa Kanisa walikuwa wenye kiburi na wakibishana wao kwa waoAndika nyenyekevu na kiburi ubaoni.• Inamaanisha nini kuwa mnyenyekevu? (Kuwa mnyenyekevu inamaanisha kuwa mwe-

nye kufundishika na kutambua kwa shukrani tegemeo letu kwa Bwana— na kuelewa kuwa tuna haja daima ya usaidizi Wake.

Waalike wanafunzi wachache kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka kwa Alma 4:1–5. Uliza darasa kutafuta ushahidi kuwa Wanefi walikuwa wanyenyekevu. Na wanafunzi wa-napoeleza kile walichopata, inaweza kusaidia kueleza kuwa hatuhitaji kuvumilia janga ili kuwa wanyenyekevu — tunaweza kuchagua kuwa wanyenyekevu.Eleza kuwa maelezo ya Wanefi katika Alma 4:6 ni tofauti sana na maelezo yaliyo katika Alma 4:3–5. Ashiria neno kiburi ubaoni.• Inamaanisha nini kuwa na kiburi? Kiburi ni kinyume cha unyenyekevu. Watu walio na

kiburi hujiweka katika upinzani mmoja na mwengine na kwa Mungu. Watajiweka juu ya wale walio karibu nao na kufuata tamaa zao binafsi badala ya mapenzi ya Mungu.)

Alika nusu ya darasa isome Alma 4:6–8 kimya na ile nusu nyingine ya darasa isome Alma 4:9–12 kimya. Viulize vikundi vyote viwili kutambulisha matendo yenye kiburi ya baadhi ya Wanefi na jinsi matendo haya yalivyowaathiri wengine. Baada ya muda wa kutosha, acha vikundi vyote viwili visimulie kile walichopata. • Aya hizi zinatufundisha nini kuhusu jinsi kiburi kinavyoathiri jinsi tunavyowatendea

wengine?• Ni onyo gani unaloliona katika Alma 4:10? (Hakikisha kuwa wanafunzi wanaelewa kwa-

mba kama tukiweka mfano usio wa haki, matendo yetu yanaweza kuzuia wengine kukubali injili.)

Mualike mwanafunzi asome Alma 4:13–14 kwa sauti. Uliza darasa kutafuta mifano ya jinsi baadhi ya Wanefi walikuwa wanyenyekevu wakati wengine walikuwa na kiburi.• Aya hizi zinafundisha nini kuhusu jinsi unyenyekevu unavyoathiri jinsi tunavyowate-

ndea wengine. Sisitiza kuwa maamuzi yetu kuwa wanyenyekevu au wenye kiburi hutuathiri binafsi na wengine. Muda ukiruhusu, waalike wanafunzi waandike katika daftari zao au shajara za kuji-funza maandiko kuhusu uzoefu waliokuwa nayo ambao umedhihirisha ukweli wa kauli hii.

Alma 4:15–20Alma anajiuzulu kama mwamuzi mkuu, ili aweze kutumia wakati wake kuwaita watu kwenye tobaWaalike wanafunzi wafikirie kwamba wapo kwenye nafasi ya Alma. Wao ni mwamuzi mkuu, na wengi wa watu wamekuwa na kiburi na wanawatesa wale wanaobakia kuwa wanyenyekevu.

Page 273: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

258

SoMo la 70

• Ungefanya nini ili kuwasaidia watu kubadilika?Mualike mwanafunzi asome Alma 4:15–19 kwa sauti. Uliza darasa litafute nini Alma ali-chagua kufanya.• Alma aliamua kufanya nini? (Aliamua kujiuzulu cheo chake kama mwamuzi mkuu ili

kutenga wakati wake kufundisha watu.)• Ni nini kishazi "kuwashawishi ushuhuda halisi" (Alma 4:19) kinapendekeza kuhusu

jinsi Alma angefundisha? • Ni lini ulisikia watu wakitoa “ushuhuda halisi? Jinsi gani uzoefu huu umekuathiri?• Ni kweli gani unazoweza kujifunza kutoka kwa mfano wa Alma katika Alma 4:19?Majibu ya wanafunzi kwa swali hili yanaweza kujumuisha yafuatayo:Kutimiza majukumu yetu ya kiroho kunaweza kuhitaji kujitolea. Kutoa ushuhuda halisi husaidia wengine kumkaribia Mungu.Wahimize wanafunzi kutafuta ushuhuda halisi wa Alma wanaposoma Alma 5–16 katika masomo yao ya kibinafsi na walipojadili milango hii katika masomo yajayo. Pia wahimize wawe makini kwa matokeo ya ushuhuda wa Alma ulivyokuwa kwa watu.

Rejeo la Umahiri wa MaandikoWatambulishe wanafunzi kwa aya chache mpya za umahiri wa maandiko, au rejea vifungu vichache ambavyo tayari wanavifahamu. Tayarisha maswali ambayo yatawasaidia kugu-ndua kanuni katika vifungu hivyo. Waalike kuandika lengo katika daftari au shajara za kujifunza maandiko kuhusu kile watakachofanya ili kuishi vizuri kulingana na mojawapo ya kanuni hizi. Wape muda maalum wa kukamilisha malengo yao na uwaulize wajitayari-she kutoa taarifa kwa mshiriki wa darasa au darasa zima watakapokamilisha.Tazama: Kama hauna muda wa kutumia shughuli hii kama sehemu ya somo hili, itumie siku nyingine. Kwa shughuli zingine za rejeo, ona kiambatisho mwishoni mwa kitabu cha kiada hiki.

Tangazo na Habari za UsuliAlma 3:6–17. Alama na Laana

Wanafunzi wanapojifunza Alma 3, wanaweza kuwa na maswali kuhusu alama na laana iliyowekwa kwa Walamani. Unaweza ukataka kueleza kuwa kuna tofauti kati ya alama na laana. Alama iliyowekwa kwa Walamani ilikuwa ni ngozi nyeusi (ona Alma 3:6). Madhumuni ya alama hii ilikuwa ni kutofautisha na kuwatenga Walamani kutokana na Wanefi (ona Alma 3:8). Laana, iliyokuwa mbaya zaidi, ilikuwa hali ya “kuondolewa kutoka uwepo wa Bwana” (2 Nefi 5:20). Walamani na Waamlisi walijiletea laana hii kwa sababu ya uasi wao dhidi ya Mungu (ona 2 Nefi 5:20; Alma 3:18–19). Ingawa ngozi nyeusi ilitumika katika wakati huu kama alama ya laana iliyowekwa kwa Walamani, Kitabu cha Mormoni kinafundisha kuwa Bwana “ham-katazi yeyote anayemjia, weusi kwa weupe, wafungwa

na walio huru, wake kwa waume; . . . na wote ni sawa kwa Mungu” (2 Nefi 26:33). Injili ya Yesu Kristo ni ya kila mtu. Kanisa dhahiri inalaani ubaguzi wa rangi, ikijumuisha wowote ule na ubaguzi wote wa rangi wa zamani kwa watu binafsi ndani na nje ya Kanisa. Rais Gordon B. Hinckley alitangaza:

Hakuna mtu anayefanya mazungumzo ya dharau kuhusu wale wa rangi ingine na kujifikira kuwa mfuasi wa kweli wa Kristo. Wala hawezi kujifikiria kuwa katika uwiano na mafundisho ya Kanisa. 

Acha tutambue kuwa kila mmoja wetu ni mwana au binti wa Baba yetu wa Mbinguni, anayewapenda watoto Wake wote.” (“The Need for Greater Kindness,” Ensign or Liahona, Mei 2006, 58). Kwa usaidizi wa ziada kuhusu mada hii ona somo la 27

Waalike wanafunzi kwa ugunduzi zaidiMara kwa mara, hitimi-sha somo kwa kuwapa wanafunzi kitu cha ku-tafuta katika maandiko. Mapendekezo kama hayo yanawasaidia kuzingatia masomo ya kibinafsi na yanaweza kuwasaidia kupata ufahamu kuhusu jinsi mlango mmoja una-vyohusiana na mlango mwingine au kundi la milango.

Page 274: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

259

Somo la Mafunzo- NyumbaniMosia 26–Alma 4 (Kitengo cha 14)

Vifaa vya Matayarisho kwa Mwalimu wa Mafunzo ya NyumbaniMuhtasari wa Masomo ya Mafunzo ya Nyumbani Kila SikuMuhtasari ufuatao wa mafundisho na kanuni ambazo wa-nafunzi walijifunza waliposoma Mosia 26–Alma 4 (kitengo cha 14) hayakusudiwi kufundishwa kama sehemu ya somo lako. Somo unalofundisha linazingatia machache tu ya mafu-ndisho haya na kanuni. Fuata maongozi ya Roho Mtakatifu unapofikiria mahitaji ya wanafunzi wako.

Siku ya 1 (Mosia 26)Kwa kujifunnza kuhusu uzao wa Wanefi ambao hawakukuza shuhuda za injili, wanafunzi waligundua kuwa ili kukuza na kudumisha ushuhuda, tunahitaji kusherehekea neno la Mu-ngu, kuomba kwa imani na kutii amri za Bwana. Kutokana na juhudi za Alma za kuwasaidia wengine kutubu, wanafu-nzi walijifunza kuwa Bwana atawasamehe wale wanaotubu kwa dhati ya mioyo yao.

Siku ya 2 (Mosia 27)Wanafunzi walipojifunza kuhusu kuongoka kwa Alma Mdogo na wana wa Mosia, walijifunza kweli hizi tatu za injili zifuatazo: Bwana hujibu maombi yetu ya imani kwa ajili ya wengine, na hali anawaruhusu wakala wao; kila mmoja wetu ni sharti azaliwe tena kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo; na atubu kikweli, mtu ni sharti afanye kila kitu kina-chowezekana ili kurekebisha madhara ambayo yeye ameya-fanya. Wanafunzi waliandika katika shajara zao za kujifunza maandiko jinsi walivyobadilishwa kupitia kwa Upatanisho.

Siku ya 3 (Mosia 28–29)Wanafunzi walipojifunza kuhusu hamu ya wana wa Mosia kuhubiri injili kwa Walamani, walijifunza kuwa jinsi kuongo-lewa kwetu kunavyopata kina, hamu yetu ya kushiriki injili huongezeka. Waliandika pia kuhusu uzoefu waliopata ambao umewasaidia kutaka kushiriki injili. Wanafunzi walisoma ku-husu mabadiliko ya kiserikali ya Wanefi, na kujifunza kwamba raia wana jukumu la kuimarisha sheria za haki na viongozi.

Siku ya 4 (Alma 1–4)Kwa kujifunza mifano ya Wanefi wanyenyekevu, Wanafunzi walijifunza kuwa tunapoishi injili tunaweza kupata amani mai-shani mwetu, hata kama tunateswa. Waliposoma kuhusu uasi wa Waamlisi, waligundua kuwa tunapokea furaha au dhiki kutegemea na ni nani tunayechagua kumtii. Alma alikuwa mfano wa yule aliyechagua kumtii Bwana. Kujitolea kwake kusikoyumba katika kuwaita Wanefi wenye kiburi kwenye toba kuliwasaidia wanafunzi kuona kwamba watumishi wa Bwana wanatoa ushuhuda na kuwaita wenye dhambi kutubu.

UtanguliziSomo hili linaruhusu wanafunzi kutathmini kanuni za toba na kutafakari haja yetu ya kubadilika kupitia kwa Upatanisho wa Yesu Kristo— kama walivyokuwa Alma Mdogo na wana wa Mo-sia. Omba kwa maongozi wa kujua jinsi unavyoweza kuwasaidia vizuri wanafunzi kutafuta mabadiliko haya maishani mwao.

Mapendekezo ya Kufundisha

Mosia 26Alma anapokea mwongozo kuhusu jinsi ya kuwahukumu wale wanaofanya dhambi mbaya zaidiKwa kuanza somo hili, mwalike mwanafunzi asome muhtasari wa mlango katika mwanzo wa Mosia 26. Soma hali zifuatazo kwa darasa. Waulize wanafunzi wafikirie kuhusu kile wange-weza kufanya kumsaidia mtu katika kila hali.

1. Msichana amefanya dhambi mbaya sana, lakini anaogopa kuzungumza na askofu wake.

2. Mvulana ana hamu ya kutubu, lakini hajui jinsi ya kufanya hivyo. 3. Msichana anarudia dhambi ambayo awali alikuwa amefanya

na anahofia kuwa Bwana hatamsamehe tena. 4. Mvulana anaamua kutubu, lakini anakataa kumsamehe mtu

ambaye alimkosea.

Andika rejeleo lifuatalo la maandiko ubaoni Mosia 26:21–23, 29–31. Waeleze wanafunzi kwamba aya hizi zimeandikwa ufunuo wa Bwana kwa Alma juu ya watu ambao walikuwa wa-metenda dhambi nzito. Waalike wanafunzi wasome mistari hii na watambue angalau kanuni moja ambayo inaweza kumsaidia mmoja wa watu waloelezwa katika orodha iliyotangulia. Waulize wanafunzi kadhaa kushiriki majibu yao na darasa. Unaweza pia kutaka kushiriki jibu na ushuhuda wako wa kanuni juu ya toba inayopatikana katika Mosia 26.

Wakumbushe wanafunzi kwamba walipanga kutumia moja ya kanuni waliojifunza kutoka Mosia 26 katika juhudi zao wenyewe za kutubu. Wahimize kufuatilia hiyo mipango yao.

Mosia 27–28Alma Mdogo na wana wa Mosia wanatubu na kuzaliwa upya Ili kuwapa wanafunzi mfano wa mtu ambaye alipata mabadi-liko makuu ya moyo, waalike wachache wao kuchukua zamu kusoma kwa sauti uzoefu ufatao wa Mzee Keith K. Hilbig wa wale Sabini:

"[Mzee kijana akihudumu katika Ulaya ya Mashariki] na mwe-nzake alimpata na kumfundisha mtu wa makamo aitwaye Ivan. Mchunguzi wao alitoka kwenye historia ngumu, kama ilivyoo-nyeshwa katika mavazi yake yaliyochakaa sana, ndevu chakavu, na mwenendo wa kusita. Maisha yalikuwa magumu na yasiyo na upole kwake.

Page 275: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

260

SoMo la MafUnzo- nyUMbani

"Bila ya mafunzo yoyote ya kidini mapema, Ivan alikuwa na me-ngi ya kushinda. Mazoea yasiyo na uwiano na injili ya urejesho ilibidi yawekwe kando. Kanuni mpya zilihitajika ili kukubaliwa na kisha kujumuishwa. Ivan alitaka kujifunza, na yeye alijitayarisha mwenyewe kwa bidii kwa ajili ya ubatizo wake na uthibitisho. Mavazi yake yalibaki yasiyo nadhifu na ndevu zake chakavu, lakini yeye alikuwa amechukua hatua ya kwanza. Muda mfupi baada ya ubatizo wa Ivan, mmisionari alihamishwa. Alitumai kwamba angepata tena kukutana na Ivan.

"Miezi sita baadaye rais wa misheni alimtuma mmisionari huyo katika tawi lake la zamani. Akishangaa lakini akiwa na hamu ya kurudi, mzee huyu na mwenzi mpya, wakaja mapema Jumapili katika mkutano wake wa kwanza wa sakramenti aliporejea katika tawi. 

"Mzee huyo alitambua karibu kila mtu katika mkusanyiko huu mdogo. Hata hivyo, yeye alitafuta bila mafanikio kati ya nyuso mtu ambaye yeye na mwenzi wake walikuwa wamefundisha na kumbatizwa miezi sita mapema. Kulitokea ndani ya yule mzee hisia ya kukata tamaa na huzuni. 

"Hofu ya mzee yule na tafakari iliingiwa na mkabala wa mtu asio wa kawaida ambaye alikuwa akija kwa haraka kumkumbatia mi-sionari huyu. Mtu aliyenyolewa kinadhifu alikuwa na tabasamu la ujasiri na wema dhahiri uliomeremeta kutoka usoni mwake. Akivaa shati jeupe na tai iliyofungwa kwa makini, alikuwa njiani kuandaa sakramenti kwa ajili ya mkutano mdogo wa Sabato asubuhi hio. Ni wakati tu mtu huyu alipoanza kusema ndipo mzee akamtambua. Ilikuwa ni Ivan mpya, si Ivan wa zamani waliokuwa wamemfundi-shwa na kumbatiza! Mzee huyo aliona katika rafiki yake muujiza wa imani, toba na msamaha; aliona hali halisi ya Upatanisho.

 " ... [Ivan] alipata uzoefu wa mabadiliko ya moyo (Alma 5:26) kutosha kubatizwa na kusogea mbele katika mchakato wa kuendelea wa uongofu (Experiencing a Change of Heart, Ensign, June 2008, 29–31).

Uliza: Ni ushahidi gani katika hadithi unaonyesha jinsi Ivan ali-kuwa amebadilika? (Hakikisha kwamba ni wazi kwamba maba-diliko ya nje ambayo Ivan alifanya yalikuwa dalili za mabadiliko ya kina zaidi ndani yake.)

Wakumbushe wanafunzi kwamba Mosia 27 inaeleza uzoefu mwingine wa mabadiliko kupitia Upatanisho. Mwalike mwa-nafunzi asimame mbele ya darasa na kufanya muhtasari wa Mosia 27. Kama inapatikana, mwanafunzi anaweza pia kuo-nyesha picha ya kuongoka kwa Alma Mdogo (Gospel Art Book [2009], no. 77). Muulize mwanafunzi mwingine asome Mosia 27:24–26. Kisha uliza darasa kubainisha nani ambaye lazima kubadilishwa kupitia kwa Upatanisho, au kuzaliwa na Mungu. Wanafunzi wanapojibu, wanapaswa kueleza kuelewa ukweli ufuatao: Kila mmoja wetu lazima kuzaliwa upya kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo.

Uliza: Je! Ni kwa jinsi gani umeweza kuona, mtu akibadilika kuwa bora kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo?

Waalike wanafunzi kutafakari maswali ambayo mmisionari katika hadithi alijiuliza mwenyewe baada ya kukutana tena na Ivan: ni kiasi gani cha mabadiliko ya moyo ambayo Mimi

nimepata katika miezi sita iliyopita? Je, mimi nimezaliwa upya? (imenukuliwa katika Keith K. Hilbig, “Experiencing a Change of Heart,” 31).

Alika wanafunzi wasome Mosia 27:24, 28, wakitafuta kile Alma alifanya na nini Bwana alifanya ambacho kilicholeta mabadiliko kwa Alma. Waulize waeleze kwa nini wao wanaamini kwamba mtu binafsi na Bwana lazima wote wawili washiriki katika maba-diliko makuu ya moyo.

Wakumbushe wanafunzi kwamba wao walijaza kwenye chati vishazi ambavyo vilionyesha tofauti katika Alma kabla na baada ya mabadiliko yake ya moyo (katika somo kwa siku 2). Katika mgawo wa kazi ya 2 kwa siku ya 2, wanafunzi waliandika katika shajara zao za kujifunza maandiko kishazi kimoja kutoka safu ya "Baada" ambacho wao walitumaini kingewalezea wao katika maisha yao na kueleza kwa nini. Waalike wanafunzi kadhaa washiriki kile walichoandika. Shuhudia kwamba mabadiliko makuu ya moyo yanawezekana kwetu sisi kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo.

Waulize wanafunzi kutafakari jinsi walivyobadilishwa kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo. Waalike kushiriki mawazo yao, kama wanataka. Unaweza pia ukitaka kushiriki jinsi wewe ulivyobadili-shwa kupitia Upatanisho.

Wahamsishe wanafunzi kufanya bidii kuelekea kupata uzoefu wa mabadiliko ya moyo ili waweze kukua karibu na Bwana na kuruhusu Upatanisho kufanya tofauti katika maisha yao.

Nakili chati ifuatayo kwenye ubao kabla ya darasa, au tengeneza nakala yake kwa kila mwanafunzi:

Mosia 27:32–37 Mosiah 28:1–4

ni kwa jinsi gani alma na wana wa Mosia walibadilika?ni kanuni gani ulizojifunza kutoka mistari hii?Kwa nini unafikiri kuhuisha ni sehemu muhimu ya kutubu?

ni kwa jinsi gani wana wa Mosia walibadilika?ni kanuni gani ulijifunza kutoka mistari hii?ni uzoefu gani katika maisha yako ambao umekuongoza wewe kutaka kushiriki injili na wengine?

Uliza nusu ya darasa ijibu maswali katika safu ya kwanza na nusu nyingine ijibu maswali katika safu ya pili. Acha kila mwa-nafunzi afanye kazi peke yake. Waalike wanafunzi wachache kutoka katika kila kundi kutoa taarifa ya majibu yao.

Waalike wanafunzi kutafakari jinsi wanavyoweza kufanya mare-jesho kwa ajili ya dhambi zao na kuongeza hamu yao ya kushiriki injili na wengine.

Mosiah 29–Alma 4Mungu aliwabariki Wanefi ambao walibaki kuwa wenye haki katika nyakati za matesoWakumbushe wanafunzi kwamba sura za kwanza za Alma zinaeleza nyakati za matatizo na mateso kwa wanefi wenye haki. Waalike wanafunzi wasome Alma 1:25, 27 kimya. Waambie wabainishe nini hawa Wanefi walifanya wakati wa mateso.

Page 276: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

261

SoMo la MafUnzo- nyUMbani

Eleza wazi kwamba Bwana aliwabariki Wanefi wenye haki ili wa-weze kufanikiwa zaidi kuliko wale ambao walikuwa waovu (ona Alma 1:29–32). Waambie wanafunzi wajitahidi kufuata mfano wa Wanefi hawa waaminifu wanapokabiliana na matatizo katika maisha yao.

Kitengo kinachofuata (Alma 5–10)Utajuaje kama wewe umezaliwa upya? Inamaanisha nini ku-zaliwa upya? Wanafunzi wanapojifunza Alma 5–10, watapata baadhi ya maswali wanayoweza kujiuliza wenyewe ili kutathmini kama wao wamezaliwa upya na wamepata wa uzoefu wa ma-badiliko makubwa ya moyo. Kwa nyongeza, watapata ufahamu mkubwa wa kuelewa kwa kina na nguvu ya Upatanisho.

Page 277: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

262

UtanguliziWakati Kanisa lilipotishiwa na ubishi wa ndani na uovu (ona Alma 4:9–11), Alma aliachia kiti cha hukumu ili aweze kuimarisha juhudi zake katika kuimarisha Ka-nisa. Alikwenda kwenye misheni kuwakomboa Wanefi kwa kutoa ushuhuda halisi dhidi yao (Alma 4:19). Alma alianza misheni yake kwa kuwakumbusha watu wa

Zarahemla kuwa Bwana alikuwa amewaokoa mababu zao kutoka katika utumwa wa kimwili na kiroho. Ali-wahimiza kujitayarisha kwa siku ya mwisho ya hukumu kwa kuamini katika neno la Mungu na kutathmini hali ya kiroho ya mioyo yao.

SOMO LA 71

alma 5:1–36

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 5:1–14Alma anasimulia wongofu wa babaye na wale waliomfuataAndika neno mabadiliko ubaoni. Waulize wanafunzi kushiri mifano ya njia ambazo watu wanaweza kubadili muonekano au tabia zao. Waalike waeleze nini kinaweza kuwaongoza kwa au kuleta baadhi ya mabadiliko haya katika watu.Wakumbushe wanafunzi kwamba Alma alikuwa na wasiwasi juu ya uovu ambao uli-kuwa umeanza kukua kati ya Wanefi. Aliweza kuona kwamba kama hawangebadilika, wangeweza kupoteza baraka zilizo ahidiwa za maagano waliyoyafanya. Alikiacha kiti cha hukumu na kujitoa mwenyewe kwa kuwatumikia watu na kuwaita kwa toba. Alianza kwa kuwafundisha watu wa Zarahemla.Waalike wanafunzi kadhaa wachukue zamu kusoma kwa sauti kutoka Alma 5:3–6. Uliza darasa lifuatilie pamoja, wakitafuta matukio ambayo Alma alisisitiza wakati alipoanza kuwafundisha watu.• Jinsi gani ingewezekana kuwasaidia watu wa Alma kusikia simulizi za utumwa, uko-

mbozi, na uongofu wa baba yake Alma na wote waliomfuata ?• Tazama Alma 5:7. Kwa mujibu wa aya hii, ni aina gani ya mabadiliko yalikuwa yametokea

katika maisha ya baba yake Alma na watu wake?Ubaoni, ongeza maneno ya moyo baada ya mabadiliko, ili isome mabadiliko ya moyo.• Unafikiri inamaanisha nini kupata mabadiliko ya moyo? (Ili kuwasaidia wanafunzi

kujibu swali hili, unaweza kuwaambia kwamba Mzee Gerald N. Lund wa Wale Sabini alifundisha kwamba katika maandiko, neno moyo mara nyingi inahusu mtu wa kweli, kindani [Understanding Scriptural Symbols, Ensign, October 1986, 25].)

• Nini tofauti kati ya mabadiliko ya moyo na kila aina ya mabadiliko ambayo tulijadili katika mwanzoni mwa somo?

Eleza kwamba katika Alma 5:7–9, 14, Alma alitumia aina tofauti ya misemo ambayo inae-leza jinsi mabadiliko ya moyo yalivyo. Ongeza kishazi kwenye ubao ili isome, mabadiliko ya moyo ni kama . . .Waulize wanafunzi wasome Alma 5:7–9, 14 kimya, wakitafuta maelezo ya Alma ya jinsi mabadiliko ya moyo yalivyo. Waalike watoe taarifa kile walichopata. Wanafunzi wanapotoa taarifa, ongeza vishazi ubaoni. (Orodha yako inaweza kuonekana kama ifuatavyo: maba-diliko ya moyo kama . . . kuamka kutoka usingizi mzito; kujazwa na nuru; kuwa huru kutoka minyororo; kuwa na roho iliyopanuka; kuimba kuhusu upendo unaokomboa; kuwa uliyezaliwa na Mungu ;. kupokea mfano ya Bwana katika muonekano wako. )• Mabadiliko ya moyo yanafanana vipi na maelezo ya yaliotajwa ubaoni?• Mabadiliko ya moyo yanaweza kuonekana vipi katika vitendo ya mtu? Ni vipi mabadi-

liko ya moyo wakati mwingine huonekana katika muonekano wa mtu? Unaweza kutaka kuuliza wanafunzi kuelezea muonekano au mwenendo wa mtu fulani wanaemjua ambaye wanahisi ameupokea mfano [ wa Bwana] katika muonekano [wake].)

Page 278: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

263

alMa 5:1– 36

Alika mwanafunzi asome Alma 5:10 kwa sauti, na uulize darasa kubainisha maswali matatu Alma aliwauliza watu. (Unaweza kutaka kupendekeza kwamba wanafunzi waweke alama katika maswali haya.) Kusoma maswali haya kutawasaidia wanafunzi kutambua katika mistari inayofuata sababu zilizosababisha Alma na watu wake kupata mabadiliko makuu ya moyo.Mwalike mwanafunzi asome Alma 5:11–13 sauti, na uliza darasa kubainisha kile kilicho-leta mabadiliko makuu ya moyo kwa baba yake Alma na wafuasi wake. (Kuamini kwao katika neno la Mungu na, kwa ugani, imani yao na matumaini katika Mungu. Unaweza pia kutaka kuonyesha ushawishi wa neno la Mungu uliotajwa katika Alma 5:5, 7.)• Ni uhusiano gani unaouona kati ya kuamini katika neno la Mungu na kupata mabadi-

liko ya moyo? (Wasaidie wanafunzi kutambua kanuni zifuatazo: Wakati tunapoamini katika neno la Mungu na kutumia imani katika Yesu Kristo, tunaweza kupata mabadiliko makuu ya moyo. Sisitiza kwamba neno la Mungu kama lilivyo hubiriwa na Abinadi na Alma kwa kulenga ukombozi ambao huja kupitia kwa njia ya Yesu Kristo [ona Mosia 16:4–9; 18:1–2].)

Eleza kwamba njia nyingine ya kueleza kwamba mtu fulani ameweza kuwa amepata ma-badiliko makuu ya moyo ni kusema kwamba wamezaliwa upya. Wasaidie wanafunzi kue-lewa kwamba kuwa umezaliwa na Mungu au kuzaliwa upya inahusu mabadiliko ambayo mtu hupata wakati unapomkubali Yesu Kristo na kuanza maisha mapya kama mfuasi wake. Ili Kuwasaidia wanafunzi kuelewa kwamba kupata mabadiliko makuu ya moyo, au kuwa umezaliwa upya, mara nyingi ni mchakato wa taratibu, soma kauli ifuatayo ya Mzee D. Todd Christofferson wa Akidi ya Mitume kumi na Wawili:"Unaweza kuuliza, Kwa nini mabadiliko haya makuu hayatokei haraka zaidi kwangu mimi? Kwa wengi wetu, mabadiliko hasa ni ya taratibu na hutokea baada ya muda. Kuza-liwa mara ya pili . . . ni zaidi mchakato kuliko tukio. Na kushiriki katika mchakato huo ni lengo kuu la maisha ya muda” (“Born Again,” Ensign au Liahona, May 2008, 78).• Ni lini wewe ulihisi mabadiliko katika moyo wako wewe ulipojitahidi daima kuishi kuli-

ngana na neno la Mungu?• Ni jinsi gani unaweza kuelezea hisia na vitendo vinavyoandamana na mabadiliko ya moyo?• Ni jinsi gani moyo wako umebadilika ulipokisoma Kitabu cha Mormoni katika seminari

mwaka huu?Waruhusu wanafunzi dakika chache kuandika katika daftari au shajara zao za kujifunza maandiko kuhusu jambo moja au mawili watakayotenda kwa uaminifu zaidi ili kuishi kulingana na neno la Mungu.

Alma 5:15–36Alma anafundisha kwamba mabadiliko makuu ya moyo yanahitajika ili kuingia katika Ufalme wa mbinguniMpe kila mwanafunzi kitini chenye chati ifuatayo , au onyesha chati kwenye ubao ili wana-funzi wainakili.

Kadiogramu ya Kiroho

alma 13:15 alma 5:16 alma 5:19 alma 5:26 alma 5:27 alma 5:28

Kila Mara

Karibu kila mara

Kwa kawaida

Wakati mwingine

Mara chache, kama vile

Page 279: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

264

SoMo la 71

Eleza kwamba kadiogramu ni chati ambayo madaktari wakati mwingine hutumia kuta-thmini au kufuatilia utendaji kazi wa mioyo yetu ya kimwili. Inawasaidia kutambua mata-tizo au hali zinazohitaji matibabu.Waeleze wanafunzi kwamba baada ya Alma kufundisha kwamba neno la Mungu lilikuwa limemwongoza baba yake na watu wengine kupata mabadiliko makuu ya moyo, aliwauliza watu maswali ambayo yangewasaidia kutathmini hali ya mioyo yao wenyewe. Waalike wa-nafunzi wasome Alma 5:14 kimya, wakitafuta maswali matatu ambayo Alma aliwauliza watu. (Unaweza kutaka kupendekeza kwamba wanafunzi waweke alama katika maswali haya.)Eleza kwamba Alma aliuliza maswali kadhaa zaidi ya kusaidia watu wake kufikiria hali ya mioyo yao. Waalike wanafunzi kutumia dakika chache wajifunze na kutafakari mafungu ya maandiko yaliyoorodheshwa juu ya kadiogramu ya kiroho. Wahimize waweke alama katika masanduku katika chati ambavyo ineleza vizuri zaidi jinsi wanavyohisi wanafanya kuhusiana na maswali katika kila fungu. (Kumbuka kwamba baadhi ya mistari ina zaidi ya swali moja.) Kwa sababu ya asili ya binafsi ya shughuli hii, wanafunzi hawapaswi kutakiwa kushiriki majibu yao kwa darasa.Wakati wanafunzi wamemaliza kadiogramu, waalike wasome Alma 5:29–31 kimya, waki-tafuta maswali machache zaidi ambayo Alma aliuliza ili kuwasaidia watu wake kutathmini nyoyo zao. (Unaweza kutaka kupendekeza kwamba wanafunzi wabadilishe kidogo ma-neno ya maswali ili kuyatumia wenyewe: Je, mimi nimevuliwa wivu? Je! Mimi huwafanyia mzaha wengine?” Je! mimi huwatesa wengine?Waalike wanafunzi wachache kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka Alma 5:17–18, 20–25. Uliza darasa litafute kwa nini mioyo yetu ni lazima kubadilishwa katika maanda-lizi kwa ajili ya siku ya hukumu. Uliza maswali yafuatayo kusaidia wanafunzi kuelewa kwamba kwa kupata mabadiliko ya moyo, sisi tunajiandaa kupokea nafasi katika ufalme wa mbinguni: • Ni Maneno gani na vishazi vipi ambavyo Alma alitumia kuelezea hali ambayo ungepe-

nda kuwa wakati wewe utakapo simama mbele ya Mungu kuhukumiwa? (Wanafunzi wanapojibu swali hili, unaweza kuelekeza mawazo yao kwa Alma 5:16, 19.)

• Ni vipi unapopata mabadiliko ya moyo sasa kunakusaidia kujiandaa kupokea mahali katika Ufalme wa mbinguni?

Andika maswali yafuatayo kwenye ubao: (Unaweza ukataka kuyaandika ubaoni kabla darasa kuanza.)

Bwana anatualika tufanye nini?Nini matokeo ya kukataa au kukubali mwaliko huu?Mistari hii inafundisha nini kuhusu Mwokozi?

Muulize mwanafunzi asome Alma 5:33–36 kwa sauti wakati wanafunzi wengine wakita-futa majibu kwa maswali yaliyo ubaoni. Waalike wanafunzi kushiriki majibu waliyopata.Hitimisha kwa kuwapa wanafunzi dakika chache kuandika. Waulize wao kuchagua mstari au kishazi kutoka Alma 5:1–36. Waalike waandika kuhusu kile aya au kishazi kinamaanisha kwao na jinsi gani wanaweza kufanya kile kinachopendekezwa wanapotafuta kuwa na nyoyo zilizobadilishwa kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo. Shuhudia kwamba kama tuki-endelea kupata uzoefu wa mabadiliko ya moyo na kuzaa matendo yenye haki, tutakuwa tumejitayarisha kuingia ufalme wa Mungu.

Wape wanafunzi muda wa kutafakariKutoa muda wa kuta-fakari kwa wanafunzi wakati wa darasa ni njia mojawapo ya kuwasai-dia kujifunza kwa Roho. Wakati huu, epuka kuongezea maswali ya ziada, maelekezo, au mazungumzo ambayo yanaweza kuwavuruga.

Page 280: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

265

UtanguliziAlma pia alimliganisha Yesu Kristo na mchungaji mwema ambaye aliwaita na akatamani kuwarejesha katika zizi lake. Aliwahimiza watu watubu na kuepuka

mambo machafu ya ulimwengu ili waweze kurithi ufalme wa mbinguni.

SOMO LA 72

alma 5:37–62

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 5:37–42, 53–62Alma anaonya waovu na kuwaalika wote kwa kuisikiliza sauti ya Mchungaji MwemaOnyesha picha ya Yesu akibeba Mwanakondoo Aliyepotea (Gospel Art Book [2009], no. 64).• Ni katika njia zipi Mwokozi ni Mchungaji Mwema?Baada ya wanafunzi wachache kujibu, soma kauli ifuatayo ya Rais Ezra Taft Benson:"Katika wakati wa Yesu, mchungaji Mpalastina alibainishwa kwa ulinzi wake wa ko-ndoo. Tofauti na wachungaji wa kisasa, mchungaji daima alitembea mbele ya kundi lake. Aliwaongoza. Mchungaji alijua kila moja ya kondoo na kwa kawaida alikuwa na jina kwa kila mmoja. Kondoo walijua sauti yake na kumwamini na hawangemfuata mgeni. Hivyo, wakati wangeitwa, kondoo wangekuja kwake. (Ona Yohana 10:14, 16.) . . ."Yesu alitumia mfano huu wa kawaida siku zake ili kutangaza kwamba alikuwa Mchungaji Mwema, Mchungaji wa Kweli. Kwa sababu ya upendo wake kwa ndugu na dada Zake, kwa hiari yake na bila kushurutishwa angetoa maisha yake kwa ajili yao. (A Call to the Priesthood: ‘Feed My Sheep, Ensign, May 1983, 43; ona pia John R. Lasater, “Shepherds of Israel, Ensign, May 1988, 74–75).Wasaidie wanafunzi kukumbuka muktadha wa Alma 5 kwa kueleza kwamba Alma alienda kuhubiri kwa watu wa Zarahemla, ambao walikuwa kama kondoo wasio na mchungaji (Alma 5:37). Waulize wanafunzi kukumbuka changamoto watu wa Zarahemla walikabi-liana nazo na nini Alma aliwahimiza kufanya. Unaweza kwa ufupi kupitia mistari kadhaa muhimu kutokana na somo lililopita, kama vile Alma 5:14–20, ili kuwasaidia wanafunzi kukumbuka baadhi ya usuli huu. Hakikisha kwamba wanafunzi wanaelewa kwamba watu wa Zarahemla walikuwa katika hali ya kutisha kwa sababu ya uovu wao (ona Alma 7:3).Waalike wanafunzi wawili au watatu kwa kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka Alma 5:37–42. Uliza darasa liangalia njia ambazo mtu anaweza kujua kama yeye ni mmoja wa kondoo ya Mwokozi. Baada ya wanafunzi kushiriki walichopata, uliza maswali yafuatayo:• Ni kwa jinsi gani watu ni kama kondoo wanaohitaji mchungaji?• Kulingana na Alma 5:37–38, jinsi gani Mchungaji Mwema huonyesha upendo wake na

wasiwasi kwa ajili ya kondoo? (Yeye anaendelea kuwaita kwa jina Lake mwenyewe.)• Kulingana na Alma 5:41, tunawezaje kujua ikiwa tunasikiliza sauti ya Mchungaji Mwema?• Ni nini baadhi ya matendo yanayoweza kuonyesha kwamba mtu anamfuata Mchungaji

Mwema?Baada ya wanafunzi kujibu, waulize mwanafunzi wasome kauli ifuatayo ya Rais Ezra Taft Benson, ambaye alieleza wanaume na wanawake ambao wamejizatiti kumfuata Yesu Kristo. (Unaweza kutaka kuandaa nakala ya taarifa hii kwa kila mwanafunzi.)"Wakati unachagua kumfuata Kristo, unachagua kubadilishwa. . . ."Wanaume [na wanawake] waliobadilishwa kwa ajili ya Kristo, wataongozwa na Kristo. "Mapenzi yao yamemezwa kwa mapenzi Yake. (Ona Yohana 5:30.)"Wao hufanya daima mambo ambayo humpendeza Bwana. (Ona Yohana 8:29.)

Page 281: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

266

SoMo la 72

"Siyo tu wangekufa kwa ajili ya Bwana, lakini muhimu zaidi wanataka kuishi kwa ajili yake."Ingieni majumbani mwao, na picha kwenye kuta zao, vitabu kwenye rafu zao, muziki hewani, maneno yao na matendo yao yanawaonyesha kuwa wao ni Wakristo."Wanasimama kama mashahidi wa Mungu wakati wote, na katika mambo yote, na katika mahali popote. (Ona Mosia 18:9.)"Wana Kristo katika akili zao, wanapomtazamia yeye katika kila wazo. Ona M&M 6:36.)"Wana Kristo katika mioyo yao mapenzi yao yakiwekwa Kwake milele. (Ona Alma 37:36.)"Karibu kila wiki wanapokea sakramenti na kushuhudia upya kwa Baba yao wa milele kwamba wao wako tayari kuchukua juu yao jina la Mwana wake, daima kumkumbuka Yeye, na kutunza amri zake. (Ona Moroni 4:3)." ("Born of God,” Ensign, Nov. 1985, 5, 6–7).Waalike wanafunzi wasome Alma 5:53 – 56 kimya, wakitafuta mitazamo na vitendo amba-vyo hufanya vigumu kwa mtu yeyote kuisikiliza sauti ya Mwokozi. Baada ya dakika chache, waalike wanafunzi wachache waandike matokeo yao ubaoni. Waache waandike majibu yao ili waweze kujaza kiasi cha ubao kama iwezekanavyo. Waulize waongeze mitazamo yoyote au vitendo ambavyo wameona karibu nao ambavyo hufanya vigumu kuisikia sauti ya Mwokozi. (Majibu ya wanafunzi yanaweza kujumuisha kuweka kando [kupuuza] mafu-ndisho ya Mungu, kiburi, ubatili, kuweka mioyo yetu juu ya utajiri na mambo ya kidunia, kufikiri sisi ni bora kuliko wengine, kutesa watu wema, au kugeuza migongo yetu kwa maskini na wenye shida. Unaweza kutaka kuvuta nathari ya wanafunzi kwa matumizi ya Alma ya neno linalorudiwa ya dumu ukisisitiza kwamba watu wa Zarahemla walidumu katika tabia na mitazamo hii ya dhambi.)Tengeneza nafasi fulani ya kuandika katikati ya ubao kwa kufuta sehemu ya majibu ya wanafunzi. Katika nafasi hiyo, andika fuata sauti ya Mchungaji Mwema.Mualike mwanafunzi asome Alma 5:57 kwa sauti. Uliza darasa libainishe vishazi vinavyo-fundisha jinsi tutakavyojibu kwa athari ovu. (Njooni ninyi kutoka kwa waovu, Mkatengwe, na msiguse vitu vyao vichafu.) Unaweza kutaka kupendekeza kwamba wanafunzi watie alama vishazi hivi katika maandiko yao. Taja kwamba vishazi hivi vinasisitiza haja ya kue-puka kitu chochote kinachoweza kutuharibu au kutuchafua kiroho. Ili kuwasaidia wana-funzi kujadili jinsi gani wanaweza kuondoa vishawishi, kuepuka athari mbaya na kufuata sauti ya Mchungaji Mwema, uliza maswali kama yafuatayo:• Kijana Mtakatifu wa Siku za Mwisho anaweza kufanya nini ili kujitenga kutoka kwa

waovu? (Ili kuimarisha majibu ya wanafunzi, fikiria kushiriki mfano chanya ambao ume-ona katika mmoja wa wanafunzi katika darasa lako. Unaweza pia kuwaalika wanafunzi kushiriki mifano miema waliyoiona kati yao.)

• Kulingana na Alma 5:56 –57, ni nini matokeo ya kuendelea katika uovu? (Kama tuki-endelea katika uovu, hatutaweza kusikia sauti ya Mchungaji Mwema na hatuta-weza kuhesabiwa miongoni mwa watu wema. )

Kama kuna muda, wape wanafunzi muda wa dakika chache na kutafakari swali lifuatalo. Unaweza kuwataka wao wajibu swali katika daftari au shajara za kujifunza maandiko.• Ni nini Bwana angetaka wewe ufanye kwa ubora ili ukubali mwaliko Wake wa kuja

Kwake? (Unaweza kupendekeza kwamba jibu linaweza kuwa kitu ambacho wao wamehisi haja ya kufanya vizuri zaidi, au inaweza kuwa ni kitu ambacho wanahitaji kuacha kufanya.)

Waalike wanafunzi wasome Alma 5:58–62 kimya wakitafuta baraka zilizoahidiwa kwa wale ambao wanakusanyika na Bwana na watu Wake. Unaweza kutaka kupendekeza kwamba wanafunzi watie alama baraka hizi katika maandiko yao.• Ni vipi unaweza kufanya muhtasari wa ahadi ya Bwana kwa wale ambao huisikia sauti

Yake? (Ingawa wanafunzi wanaweza kupendekeza kanuni mbalimbali, hakikisha kuwa wao wanaelewa kwamba kama sisi tutafuata sauti ya Bwana [Mchungaji Mwema], tutakusanywa katika ufalme wake. Unaweza ukataka kuandika kanuni hii ubaoni.)

• Umekuza tabia gani ambazo hukusaidia kuisikia sauti ya Mchungaji Mwema?• Ni vipi tabia hizi zimekusaidia kupuuza baadhi ya vivutio viovu vilivyo orodheshwa ubaoni? Shuhudia kwamba kama tunaposikiliza maneno ya Mwokozi, tutakuwa miongoni mwa watu wema waliokusanyika katika ufalme wa Bwana.

Page 282: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

267

alMa 5:37– 62

Alma 5:43–52Alma anatimiza wajibu wake kuhubiri tobaWaulize wanafunzi waorodhesha hisia tano za kimwili (kuona, sauti, kugusa, harufu, na ladha). Fikiria kuleta baadhi ya vitu ambayo vitaruhusu wanafunzi kutumia hisia hizi.• Ni nini ulichojifunza kutoka kila moja ya hisia zako tano?• Je! Kuna njia ya kujua au kujifunza kitu bila kutumia hisia zako tano?Waalike wanafunzi wachache kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka Alma 5:44–48. Uliza darasa litafue nini Alma alisema alijua na jinsi alivyosema alikijua.• Kulingana na Alma 5:48, Alma alijua nini?• Alma alisema ni nini kilikuwa chanzo cha ushuhuda wake?• Alma alikuwa amefanya nini ili kupokea huu ushuhuda kutoka Roho Mtakatifu?• Ni vipi sala na kufunga kunatusaidia kupata au kuimarisha ushuhuda wa injili?• Ni lini wewe umehisi kwamba ushuhuda wako umeimarishwa kwa njia ya maombi

au kufunga?Shuhudia kwamba tunaweza kujua wenyewe, kwa njia ya Roho Mtakatifu, kwamba Yesu Kristo ni Mkombozi wa wanadamu. Ili kusisitiza umuhimu wa kutafuta na kupata ushuhuda wa kibinafsi kwamba Yesu Kristo ni Mkombozi wa watu, soma kauli ifuatayo ya Mzee M. Russell Ballard wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili:

"Ushuhuda wa kibinafsi wa ukweli wa injili, hasa ya maisha ya kiungu na huduma ya Bwana Yesu Kristo, ni muhimu kwa uzima wetu wa milele. Kwa maneno mengine, uzima wa milele unathibitishwa kuwa ni wa kweli juu yetu sisi wenyewe, ufahamu binafsi wa Baba yetu wa Mbinguni na Mwanae Mtakatifu. Kujua tu kuwahusu wao hakutoshi. Lazima tuwe na uzoefu wa kibinafsi, uzoefu wa kiroho kututia nanga. Haya huja kwa kutafuta sana, njia

pekee ya mawazo ambayo mtu mwenye njaa hutafuta chakula." (“Feasting at the Lord’s Table,” Ensign, May 1996, 80).Wape wanafunzi muda wa kuandika majibu yao kwa maswali yafuatayo. Pia wahamasishe kuandika watafanya nini ili kupata au kuimarisha ushuhuda wao wa Yesu Kristo. Wahama-sishe kukamilisha malengo yao, hata kama inachukua siku nyingi (Alma 5:46).• Ni lini umemhisi Roho Mtakatifu akikushuhudia kwamba Yesu Kristo ni Mkombozi wa

dunia?Waalike wanafunzi wasome Alma 5:49–52 kimya wakitafuta ni nini Alma aliwaambia watu kuwa walihitaji kufanya ili kujiandaa kuurithi ufalme wa mbinguni.• Kwa nini toba ni muhimu katika kuingia katika Ufalme wa Mungu?Ili Kuwasaidia wanafunzi kutumia mafundisho ya Alma kuhusu kujiandaa kuingia ufalme wa Mungu, mwalike mwanafunzi asome kauli ifuatayo ya Mzee Dallin H. Oaks wa Jamii ya Mitume kumi na Wawili:"Vipi kama siku ya kuja Kwake ingekuwa kesho? Kama tungejua kwamba tungekutana na Bwana kesho— kupitia kifo chetu katika umri mdogo au kwa njia zisizotarajiwa za kuja Kwake — tutafanya nini leo? Maungamo gani tungefanya? Ni mazoea gani ambayo sisi tu-ngeyacha? Tungekamilisha madeni yapi? Tungetoa Misamaha gani? Tungetoa shuhuda gani?"Kama tungetaka kufanya mambo hayo basi, kwa nini si sasa? Kwa nini tusitafute amani wakati amani inaweza kupatikana?" (Matayarisho ya Ujio wa pili, Ensign au Liahona, May 2004, 9).Hitimisha kwa kuwapa wanafunzi muda wa kutafakari kile wangehitaji kubadilisha katika maisha yao kujitayarisha kukutana na Mwokozi na kuingia katika ufalme wake. Waalike wao waandike mawazo yao na hisia zao ili waweze kusoma tena mawazo yao baadaye na wakumbushwe kufuata njia ya uvuvio wanaoupokea.

Himiza matumiziRais Thomas S. Monson alisema, Lengo [la mafundisho ya injili] ni kuhamasisha mtu kufikiri, kuhisi kuhusu, na kisha kufanya kitu kuhusu kuishi kanuni za injili (Katika Conference Report, Oct. 1970, 107). Unapofundisha kanuni za injili kwa wanafunzi, waalike watafute uvuvio wa Roho Mtakatifu katika kuchagua njia zinazoweza kuboresha tabia zao na kuimarisha imani yao katika Yesu Kristo.

Page 283: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

268

UtanguliziBaada ya kuweka Kanisa katika hali ya utulivu katika Zarahemla, Alma akaenda mji wa Gideoni. Aliwakuta watu huko wakiwa waaminifu zaidi kuliko wale wa Zarahemla walivyokuwa. Kwa hivyo, ujumbe wake katika Gideoni ulikuwa tofauti na ujumbe wake katika Zarahemla. Aliwahimiza watu kuendelea kumtegemea

Bwana na kutafuta kutumia Upatanisho Wake katika maisha yao. Alishuhudia kwamba Mwokozi angechu-kua juu yake mwenyewe mauti na dhambi zetu, na kwamba anaweza pia kuchukua juu Yake Mwenyewe maumivu yetu, mateso, magonjwa, na udhaifu, ili aweze kujua jinsi ya kutusaidia.

SOMO LA 73

alma 6–7

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 6Alma anaweka utaratibu Kanisani katika Zarahemla na kwenda na kuhubiri katika GideoniKabla ya somo, mwalike mwanafunzi kujiandaa kushiriki kwa ufupi na darasa baadhi ya njia yeye alihisi kubarikiwa kwa ajili ya juhudi zake za kuhudhuria kanisa. Kwa kuanza somo, muulize mwanafunzi huyu kuja mbele ya darasa na kushiriki mawazo ambayo yeye ameyandaa. Unaweza pia kushiriki jinsi ulivyobarikiwa kupitia mahudhurio ya Kanisa.Tanguliza Alma 6 kwa kueleza kwamba mlango huu unafundisha jinsi Alma na viongozi wengine wenye ukuhani waliimarisha Kanisa katika Zarahemla.Mwalike mwanafunzi asome Alma 6:4–6 kwa sauti. Uliza darasa lifuate pamoja, likitafuta ni nini washiriki wa Kanisa katika Zarahemla walifanya kwa wale ambao hawakumjua Mungu. Waalike wanafunzi kutoa taarifa ya kile wanachojifunza. Andika ukweli ufuatao kwenye ubao: Kanisa huwekwa imara kwa ajili ya ustawi wa watu wote. Ili Kuwasaidia wanafunzi kufikiri kuhusu jinsi ukweli huu unaweza kuathiri maisha yao, uliza:• Je! Unafikiri Kanisa leo linaweza kubariki wale ambao hawamjui Mungu?Waalike wanafunzi wafikirie juu ya mtu ambaye anahitaji kumjua Mungu vizuri zaidi. Mtu huyu anaweza kuwa muumini wa Kanisa au wa imani nyingine. Shuhudia baraka ambazo sisi hupokea kwa sababu sisi ni waumini wa Kanisa, na wahamasishe wanafunzi kuwaalika wengine washiriki katika baraka hizo.

Alma 7:1–13Alma anatoa unabii wa ujio wa Yesu KristoGawa darasa katika majozi. Uliza kila jozi kujadili majibu yao kwa maswali yafuatayo:• Ni nini baadhi ya matukio ya siku za usoni ambayo wewe una msisimko nayo?Baada ya majozi kuwa na muda wa kujadili majibu yao kwa swali hili, uliza wanafunzi wachache kuchangia majibu yao kwa darasa zima. Kisha eleza kuwa baada ya Alma kuweka utaratibu katika Kanisa katika Zarahemla, alikwenda katika jiji la Gideoni. Aliwaambia watu pale kwamba kwa mambo yote yatakayotokea katika siku za usoni, jambo moja ilikuwa la umuhimu zaidi kuliko hayo yote (Alma 7:7). Alifundisha kanuni ambazo zingesaidia watu kujiandaa kwa ajili ya baraka ambazo zingekuja kwa sababu ya tukio hili la siku zijazo.Mualike mwanafunzi asome Alma 7:3–6 kwa sauti. Uliza darasa litafute matumaini ambayo Alma alikuwa nayo kuhusu watu katika Gideoni. Kisha mwalike mwanafunzi mwingine asome Alma 7:18–19 kwa sauti. Waulize wanafunzi waeleze ni nini Alma alijifu-nza kwa mwongozo juu ya watu wa Gideoni.Waalike wanafunzi wasome Alma 7:7, 9–10 kimya, wakitafuta tukio ambalo Alma alihisi lilikuwa la muhimu zaidi kwa watu kulifahamu.

Fundisha kutoka kwenye maandikoKatika juhudi zao za kuwa tayari, baadhi ya walimu wa injili hutumia viyanzo nje ya maa-ndiko. Hali baadhi ya nyenzo za ziada, kama vile kitabu cha kiada hiki, zinaweza kuwa na manufaa kwako, zinga-tia kufundisha moja kwa moja kutoka kwenye maandishi ya Kitabu cha Mormoni yenyewe. Hii itaruhusu Roho Mta-katifu kutoa ushuhuda kwa wanafunzi wako kuhusu ukweli wa maandiko na thamani ya kuyasoma.

Page 284: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

269

alMa 6 –7

• Kulingana na Alma, ni nini lilikuwa jambo moja ambalo [lilikuwa] la umuhimu zaidi ku-liko kitu kingine chochote kitakachokuja? Kwa nini unafikiri kuja kwa Mwokozi ni tukio muhimu zaidi la wakati wote?

• Kwa nini unafikiri Alma angewaambia watu ambao tayari waliamini na kuwa na imani imara kwamba walihitaji kutubu?

Eleza kwamba Alma kisha akafundisha kwa nini kuja kwa Yesu Kristo kulikuwa tukio muhimu katika historia yote ya binadamu. Waulize wanafunzi wachache kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka Alma 7:11–13. Waalike waliobaki darasani kufuatilia pamoja na kutambua nini Mwokozi alichukua juu yake mwenyewe kwa ajili yetu. (Unaweza kutaka kueleza kwamba kusaidia ina maana ya kutoa ahueni au kutoa msaada kwa mtu.)Eleza kuwa Alma 7:11–13 ni aya ya umahiri wa maandiko. Unaweza kutaka kupendekeza kwamba wanafunzi waalamishe kifungu hiki katika njia tofauti ili waweze kukipata kirahisi.Orodhesha majibu ya wanafunzi kama vichwa kote juu ya ubao. Majibu yanaweza kujumui-sha maumivu, mateso, majaribu, magonjwa, kifo, magonjwa (udhaifu au kutojiweza), na dhambi.Unaweza kupendekeza kwamba wanafunzi waweke alama kishazi "kila aina" katika Alma 7:11. Waulize wataje mifano ya kila hali iliyoandikwa kwenye ubao. Wanafunzi wanapotoa mifano, andika chini ya vichwa vinavyofanana. (Kwa mfano, saratani inaweza kutajwa chini ya magonjwa, na ulemavu wa kimwili unaweza kutajwa chini ya udhaifu. )Alika mwanafunzi asome kauli ifuatayo ya Mzee Bruce C. Hafen wa Wale Sabini:"Upatanisho si tu kwa ajili ya wenye dhambi" (Beauty for Ashes: The Atonement of Jesus Christ, Ensign, Apr. 1990, 7). Unaweza kutaka kuandika kauli hii ubao na kupendekeza kwamba wanafunzi waiandike katika maandiko yao karibu na Alma 7:11–13.• Kulingana na kile tulichosoma katika Alma 7:11–13, nini unafikiri Mzee Hafen alimaani-

sha aliposema kwamba Upatanisho si tu kwa ajili ya wenye dhambi?Andika ukweli ufuatao kwenye ubao: Yesu Kristo aliteseka kutuokoa kutoka katika dhambi na kifo na kutusaidia kupitia changamoto za maisha ya muda.Ili Kuwasaidia wanafunzi kuelewa zaidi jinsi gani wanaweza kutegemea Upatanisho ya Mwo-kozi, soma kauli ifuatayo ya Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Mitume kumi na Wawili:

"Je! Wewe unapigana na pepo ya uteja — tumbaku au madawa ya kulevya au kamari, au maradhi yanayothuru ya kuchukiza ya picha za ngono? Unachanganyikiwa na utambulisho wa kijinsia au kutafuta kujiheshimu? Je! Wewe—au mtu upendaye—unakumbwa na ugonjwa au mfadhaiko au kifo? Hatua nyingine zozote zile unazoweza kuchukua ili kutatua matatizo haya, njoo kwanza kwenye Injili ya Yesu Kristo. Amini ahadi za mbinguni 

"Huku kutegemea asili ya huruma ya Mungu kuko katika kitovu cha injili ambayo Kristo alifundisha. Nashuhudia kwamba Upatanisho wa Mwokozi hauinui kutoka kwetu tu mzigo wa dhambi zetu lakini pia mzigo wa kuvunjika moyo kwetu na huzuni, uchungu wa mioyo yetu na kukata tamaa kwetu. (Ona Alma 7:11–12.] Kutoka mwanzo, imani katika msaada kama huu ilikuwa itupatie sote sababu na njia ya kuboreka, motisha ya kuitua mizigo yetu na kuchukua wokovu wetu” (“Broken Things to Mend,” Ensign au Liahona, May 2006, 70–71• Ni kwa jinsi gani uelewa wa Alma 7:11–13 unaweza kutusaidia wakati tunakabiliwa na

changamoto?Ili kuonyesha baadhi ya njia tunazoweza kupokea msaada na nguvu kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo, soma hali zifuatazo. Baada ya kusoma kila moja, waulize wanafunzi kueleza jinsi Yesu Kristo, kwa njia ya Upatanisho Wake, anaweza kumsaidia mtu anayekabiliwa na changamoto hizo. 1. Msichana alipata ajali ya gari ambayo ilisababisha miguu yake kupooza. 2. Mvulana anaona aibu juu ya chaguo mbaya alizofanya. Anahisi kufadhaika na kukosa

thamani. 3. Baba wa mvulana hivi karibuni alifariki, na mvulana huyu amehamia mji mpya na mama

yake. Anahisi huzuni na upweke, na yeye hawezi kuona jinsi kitu chochote kinavyoweza kuwa sawa sawa tena.

Shiriki ushuhuda wako wa nguvu ya Upatanisho na kiwango unachofikia. Kisha wape wa-nafunzi dakika chache za kujibu katika madaftari au shajara za kujifunza maandiko moja

Alma 7:11–13 ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Rejea wazo la kufundisha mwishoni mwa somo ili kuwasaidia wanafunzi na umahiri wao wa kifungu hiki.

Page 285: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

270

SoMo la 73

ya maswali yafuatayo. (Unaweza ukataka kuandika maswali haya ubaoni kabla ya darasa, andaa kitini chenye maswali au soma maswali taratibu ili wanafunzi waweze kuyaandika.) • Ni wakati gani Upatanisho ulikusaidia wewe au mtu yeyote unayemjua katika moja ya

njia zilizotajwa katika Alma 7:11–13?• Utafanya nini ili utegemee Upatanisho wakati unakabiliwa na changamoto?Waalike wanafunzi wachache kushiriki na darasa kile wao wameandika. (Wakumbushe kwa-mba hawana haja ya kushiriki kitu chochote ambacho ni cha binafsi sana au siri.)

Alma 7:14–27Alma awahimiza watu kuendelea katika njia ya ufalme wa MunguIli Kuwakumbusha wanafunzi jinsi Alma alielezea kuhusu hali ya kiroho ya watu katika Gideoni, alika mmoja wao asome Alma 7:19 kwa sauti. Sisitiza kwamba watu walikuwa katika njia ambayo inaelekeza kwenye Ufalme wa Mungu. Eleza kwamba Alma alitaka kuwasaidia kukaa kwenye njia ile.Ili Kuwasaidia wanafunzi kuona kwamba kwa kuishi kanuni za injili, sisi tunafuata njia ya kwenye ufalme wa Mungu, chora njia ubaoni kote. Katika mwanzo wa njia, andika Maisha ya muda. Mwishoni mwa njia, andika Ufalme wa Mungu. Gawa darasa ka-tika makundi mawili. Alika kundi moja kujifunza Alma 7:14 – 16 na kundi lingine kijifunza Alma 7:22–24. Uliza vikundi kutafuta kile tunachotaka kufanya na kile tunahitaji kuwa ili kufuata njia inayoelekeza kwenye kwa ufalme wa Mungu.Baada ya wanafunzi kuwa na muda wa kutosha wa kusoma, waalike wachache wao kuja ubaoni. Waulize wao waandike kufuata njia ile vitendo na sifa ambazo wamegundua ambazo huongoza kwenye ufalme wa Mungu. Unaweza kufikiria kuuliza wanafunzi ni baadhi ya vitendo au sifa gani njiani zinamaanisha nini kwao. Unaweza pia kuwauliza kufikiri juu ya jinsi wanavyoweza kufuata njia hii katika maisha yao. Shuhudia kwamba wakati sisi tunapoishi kwa uaminifu, tuko katika njia ambayo inayoelekeza kwenye ufalme wa Mungu ( Alma 7:19 ).

Umahiri wa Maandiko—Alma 7:11–13Kwa sababu Alma 7:11–13 ni kifungu kirefu cha umahiri wa maandiko, inaweza kuwa vi-gumu kwa wanafunzi kukikariri. Hata hivyo lugha ya Alma ina maneno maalum ambayo yanaweza kuwasaidia wanafunzi kukumbuka katika maisha yao yote nguvu na kufikia kwa kina kwa Upatanisho. Ili kuwasaidia wao kukariri maneno haya muhimu, andika maandishi ya Alma 7:11–13 ubaoni kabla ya darasa, ukiacha nafasi kwa ajili ya maneno muhimu yafuatayo popote yatakapotokea: maumivu, mateso, majaribu, magonjwa, kifo, ulemavu, dhambi uovu. (Kwa mfano, maandishi yako ya Alma 7:11 yataanza hivi: Naye atatoka, akiteseka ... na ... na ya kila aina. )Mnaposoma Alma 7:11–13 kwa sauti kama darasa, waulize wanafunzi wajaze maneno yasiyokuwepo. Baada ya kufanya hivi mara chache, waulize wanafunzi kama wanaweza kuandika kwenye karatasi tofauti maneno haya kuonyesha nini Mwokozi alijichukulia juu yake mwenyewe kwa ajili yao. Waalike wanafunzi daima kumbuka kile Yesu Kristo ame-fanya kwa ajili yao, ili wakati wanapopata changamoto wanaweza kuwa na imani kubwa katika nguvu ya ukombozi wake.Tazama: Unaweza kuchukua dakika chache katika mwanzo wa darasa lako lijalo ili kuona kama wanafunzi wanaweza bado kukumbuka maneno haya muhimu kuhusu Upatanisho wa Mwokozi usio na mwisho.

Page 286: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

271

UtanguliziBaada ya watu wengi kukubali ujumbe we Alma huko Zarahemla, Gideoni na Meleki, watu wa Amoniha walimkataa Alma na kumfukuza kutoka kwenye jiji lao. Wakati Alma akihuzunikia kwa uovu wa watu hawa, malaika yuleyule ambaye alimtokea yeye na wana wa Mosia alimjia tena. Malaika alimsifu Alma kwa uaminifu

wake na kumwamuru kurudi Amoniha. Alma kwa uami-nifu alitii Amri ya Bwana, na Bwana akamwita Amuleki amsaidie katika huduma yake. Alma na Amuleki kwa uaminifu wakatoka kwenda kuwafundisha watu wa Amoniha, wakijazwa Roho Mtakatifu na nguvu ya kufa-nya kazi ya Bwana.

SOMO LA 74

alma 8

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 8:1–6Watu wengi wa Meleki wakubali ujumbe wa Alma na kubatizwaWaulize wanafunzi wanyooshe mikono yao kama wana ndugu au rafiki aliyehudumu mi-sheni katika Kanisa. Alika wanafunzi wawili au watatu washiriki uzoefu ambao ndugu au rafiki zao wamewasimulia kuhusu jinsi wamisionari wanavyohisi wakati ujumbe wao una-pokubalika (Unaweza pia kufikiria kuwaalika wanafunzi waseme kuhusu nyakati ambapo mtu alikuwa mpokevu kwa juhudi zao za kushiriki injili. Unaweza pia ukataka kushiriki uzoefu wako mwenyewe.)Waalike wanafunzi wasome Alma 8:1–5 kimya. Acha wao watambue miji mitatu ambapo Alma alikuwa amehubiri injili. Andika majina ya miji hii mitatu ubaoni (Zarahemla, Gide-oni, na Meleki.)• Ni nini yalikua matokeo ya Alma kuhubiri katika miji hii mitatu? (Unaweza kupende-

keza kwamba wanafunzi warejee katika ufupisho wa sura za Alma 6–8 ili kuwasaidia kujibu swali hili.

Eleza kuwa ingawa watu wa miji hii walikubali ujumbe wa Alma, huduma yake ya umisionari haikukosa changamoto.

Alma 8:7–32Baada ya Alma kukataliwa huko Amoniha, Bwana anamwamuru kurudi tenaWaulize wanafunzi kama ndugu zao au marafiki zao ambao wamehudumu misheni ya muda wote wamewahi kuona watu wakikataa ujumbe wa injili. Fikiria kualika wanafunzi wachache waeleze jinsi ndugu zao au marafiki zao walivyofanya katika hali hiyo. Alika wanafunzi wachache wachukuwe zamu kusoma kwa sauti kutoka Alma 8:7–14. Lihi-mize darasa kufikiria jinsi Alma alijihisi alipojaribu kufundisha injili kwa watu wa Amo-niha. Wakati wanafunzi wanaposoma vifungu hivi, acha watue kidogo wakati mwingine ili wajibu maswali kama yafuatayo:• Ni nini vifungu hivi vinatuambia kuhusu tabia za Alma? (Ona Alma 8:8–10.)• Ungejibu vipi endapo ungefanyiwa kama Alma? (Ona Alma 8:11–13.)• Ni jinsi gani matendo ya Alma yanafanana na au yanatofautiana na yale yangekuwa ya

kwako katika hali sawa? (Ona Alma 8:14. Unaweza kutaka kupendekeza kuwa uamuzi wa Alma wa kuendelea na kazi ya Mungu katika mji wa Haruni unaonyesha kuwa ali-kuwa na imani na Bwana na hakukata tamaa.)

Taja kwamba ingawa sala za Alma kwa ajili ya watu wa Amoniha zilikuwa za uaminifu ona Alma 8:10), maombi yake hayakujibiwa mara moja. (Baadhi ya watu wa Amoniha walitubu hapo baadaye. ona Alma 14:1.)Soma taarifa ifuatayo ya Mzee Russell M. Nelson wa Akidi ya wale Mitume Kumi na Wawili:

Page 287: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

272

SoMo la 74

“Natambua kuwa wakati mwingine, baadhi ya maombi yetu ya dhati yanaweza kuonekana kutojibiwa. Tunashangaa, “Kwa nini?” Naijua hisia hiyo! Ninajua hofu na manjozi ya nyakati kama hizo. Lakini pia ninaelewa kuwa sala zetu kamwe huwa hazipuuzwi. Imani yetu kamwe haidharauliwi. Najua kuwa mtazamo wa Baba yetu wa Mbinguni ajuaye yote ni mpana sana kuliko wetu. Wakati tukijua matatizo ya maisha ya muda na maumivu, Yeye

anajua maendeleo yetu na uwezo wa kiroho wa milele” (“Jesus Christ—the Master Healer,” Ensign au Liahona, Nov. 2005, 86).• Ni nini alichofundisha Mzee Nelson kinachoweza kutusaidia kuwa na imani hata wakati

sala zetu zenye haki zisipojibiwa mara moja au kwa njia tunazotegemea?Alika mwanafunzi asome Alma 8:14–17 kwa sauti. Uliza darasa lifuatilie likitafuta jumbe za faraja katika maneno ya malaika na kwa amri ambayo huenda ilikuwa ngumu kwa Alma kutii.• Ni kwa namna gani maneno ya malaika katika Alma 8:15 yalimpa faraja Alma? Ni kwa

jinsi gani maneno ya malaika yanaweza kuwa ya faraja kwako?• Kwa nini ilikuwa vigumu kwa Alma kuwa mtiifu katika hali hii?Waache wanafunzi wasome Alma 8:18, wakitafuta maneno yanayoelezea jinsi Alma alivyo-itikia amri ya Mungu ya kurudi katika mji wa Amoniha (Unaweza kupendekeza wanafunzi waweke alama kwenye maneno haya kwa haraka.)• Ni kitu gani tunachoweza kujifunza kuhusu Alma kutokana na kuwa alirudi kwa haraka

Amoniha?Soma kauli ifuatayo ya Rais Henry B. Eyring wa Rais Urais wa Kwanza Waulize wanafunzi wasikilize ni jinsi gani tunaweza kufaidika kwa kumtii Bwana kwa haraka.

“Hata hivyo imani kubwa tuliyonayo ya kumtii Mungu, tunahitaji kuendelea kuiimarisha na kuiboresha kila mara. Tunaweza kufanya hivi kwa kuamua sasa kuwa na haraka zaidi katika kumtii na kuamua kuwa wavumilivu. Kujifunza kuanza mapema na kuwa thabiti ni ufunguo wa maandalizi ya kiroho. . . .". . . Baba yetu wa Mbinguni mwenye upendo na Mwanawe Mpendwa wametupa msaada wote wanaoweza ili kushinda majaribu yote katika ma-

isha yaliyo mbele yetu. Lakini tunatakiwa kuamua kutii na kisha kufanya hivyo. Tunaje-nga imani ya kushinda majaribu ya utiifu kwa muda na kupitia chaguo zetu za kila siku. Tunaweza kuamua sasa kufanya kwa haraka chochote Mungu anachotaka tufanye. Na tunaweza kuamua kuwa thabiti katika majaribu madogo ya utiifu ambayo yanajenga imani ya kutuvusha katika majaribu makubwa ambayo kwa hakika yatakuja” (“Spiritual Prepare-dness: Start Early and Be Steady,” Ensign, Nov. 2005, 38, 40). • Kulingana na Rais Eyring, ni kitu gani kinachotokea kwenye imani yetu tunapoamua

kumtii Bwana haraka?• Ni lini umewahi kuhisi imani yako kwa Bwana imeimarishwa kwa sababu ya utiifu wako

wa haraka na uthabiti?Katika kila hali zifuatazo, waulize wanafunzi ni jinsi gani utiifu wa haraka unaweza kuwabariki: 1. Msichana mdogo anapoondoka kwenda shule mama yake anamwambia avae shati la

uadilifu. 2. Katika wa mahojiano na askofu wake, kuhani mpya anapewa changamoto ya kupata

Tuzo la Wajibu kwa Mungu. 3. Wamisionari wawili katika mipango yao ya kila siku wanaongozwa kuitembelea familia

isiyoshiriki kikamilifu kanisani ambayo mama sio muumini wa Kanisa.Eleza kuwa Mungu alimbariki Alma kwa utiifu wake wa haraka. Alika wanafunzi watatu mbele ya darasa wafanye igizo la kukutana kwa Alma na Amuleki katika Alma 8:19–26. Acha mwanafunzi mmoja asome maneno ya Alma na wa pili maneno ya Amuleki na wa tatu maneno yanayoeleza hadithi hiyo. Wahimize wanafunzi wasome sehemu zao kwa hisia wanazohisi Alma na Amuleki walizipata.Baada ya igizo uliza:• Bwana alimbariki vipi Alma kwa kuwa mtiifu?

Masomo ya maigizoWanafunzi wanaweza kupata ufahamu mku-bwa zaidi wa kanuni za injili kwa kuigiza masi-mulizi kutoka kwenye maandiko. Wahimize wanafunzi wafanye uzoefu kuwa wa kuvutia na kufurahisha bila kupotoka kutoka kwa utakatifu wa matukio yaliyoonyeshwa katika maandiko.

Page 288: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

273

alMa 8

• Ni vipi uzoefu wa Alma na Amuleki ni ishara kuwa Mungu alisikia na kujibu sala za Alma? (Ona Alma 8:10 .)

• Ni kanuni gani tunajifunza kutokana na uzoefu wa Alma? (Wanafunzi wanaweza ku-pendekeza kanuni kadhaa. Jibu moja linaweza kuwa tunapoitikia haraka maneno ya Bwana, anatusaidia kutii amri zake.)

Alika wanafunzi wasome Alma 8:27–32 kimya, wakitafuta ushahidi zaidi kwamba kama tu-kiwa waaminifu na kufanya kazi kwa bidii na uvumilivu Bwana atatusaidia kutii amri zake.• Ni changamoto gani Alma na Amuleki walikutana nazo walipokwenda kufundisha

watu? (Ona Alma 8:28–29. Watu walikuwa wamezidi kuwa waovu, na Mungu akawaa-muru Alma na Amuleki kuwaita watu kwenye toba.)

• Bwana aliwasaidia vipi Alma na Amuleki? (Ona Alma 8:30–31.) Walijazwa Roho Mta-katifu na walipokea nguvu za kiungu za kuwalinda. Unaweza kupendekeza kwamba wanafunzi waweke alama maelezo ya hizi baraka katika maandiko yao.

• Ni wakati gani umehisi Bwana amekusaidia wakati umekuwa mwaminifu na mwenye bidii?Alika wanafunzi waandike maneno yafuatayo ya Rais Howard W. Hunter katika daftari zao au shajara za kujifunza maandiko:"Kwa hakika Bwana anapenda, zaidi kuliko kitu chochote, uamuzi usioyumba katika kutii ushauri wake” ((“Commitment to God ,” Ensign, Nov. 1982, 58).Kisha wape wao dakika chache kuandika na kujibu maswali yafuatayo:• Ni kitu gani utafanya leo ili kumwonyesha Baba yetu wa Mbinguni kuwa utatii ushauri

wake mara moja na kumtumikia kwa uaminifu na bidii?Shuhudia kuhusu baraka tunazopata kwa kutii ushauri wa Mungu kwa uaminifu. Unaweza pia kuwapa wanafunzi nafasi ya kushiriki shuhuda zao kuhusu ukweli huu.

Tangazo na Habari za UsuliAlma 8:10. Maombi ya nguvu

Kishazi “maombi ya nguvu” kinaonyesha mawasiliano yaliyojaa nguvu, na imani kwa Mungu. Mzee Joseph B. Wirthlin wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alipende-keza njia tunazoweza kutathmini na kutafuta kuimari-sha nguvu za maombi yetu:

“Naweza kukuuliza leo kufikiria ufanisi wa maombi yako? Ni kwa kiasi gani unahisi kuwa karibu na Baba yako wa Mbinguni? Unahisi kuwa maombi yako yanajibiwa? Je! Unahisi muda unaotumia katika sala unakuza na kuimarisha nafsi yako? Je! Kuna nafasi ya kuboresha?

Kuna sababu nyingi zinazofanya maombi yetu yakose nguvu. Saa ingine yanakuwa ya kawaida. Maombi yetu yanakuwa tupu pale tunaporudia maneno yale

yale kwa njia ile ile kila mara mpaka maneno yana-kuwa kama ya kunakili badala ya kuwa mawasiliano. Hii ndiyo Mwokozi alieleza kama “kupayukapayuka” (Mathayo 6:7). Maombi kama haya, Alisema, hayatasi-kilizwa . . . .

Je! Sala zako wakati mwingine zina sikika na kuhisiwa kuwa ni zilezile? Umeshawahi kusema sala bila kufiki-ria, maneno yanamiminika kama yanatoka kwenye ma-shine? Je! Wakati mwingine hujichosha unapoomba?

“Maombi ambayo hayahitaji fikira zako ni nadra ya-tastahili nathari kutoka kwa Baba yetu wa Mbinguni. Unapojikuta ukiingia katika mtindo wa kawaida katika maombi yako, tua na ufikirie. Tafakari kwa muda mambo ambayo kwayo kwa hakika una shukrani ” [(“Improving Our Prayers,” [Brigham Young University devotional address, Jan. 21, 2003], 2, speeches. byu. edu).

Page 289: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

274

UtanguliziAlma na Amuleki walikuwa na mafanikio kidogo katika kuwahubiria watu wa Amoniha kwa sababu Shetani ali-kuwa na nguvu kubwa katika mioyo ya watu ” (ona Alma 8:9). Wengi wao walikuwa wamefanya mioyo yao kuwa migumu dhidi ya injili na walikinza mwaliko wa Alma na Amuleki wa kutubu. Hata hivyo Alma na Amuleki kwa imani waliwaita ili watubu wakishuhudia kwamba kwa

sababu walikuwa wamefundishwa ukweli na walikuwa na uzoefu na nguvu za Mungu, Bwana aliwatarajia wao kuwa wenye haki kuliko Walamani ambao hawakuwa wamefundishwa ukweli. Alma na Amuleki walifundisha kwamba kama watu wa Amoniha hawangetubu wange-kumbana na maangamizo. Pia walifundisha watu kuwa ukombozi ungewezekana kupitia kwa Yesu Kristo.

SOMO LA 75

alma 9–10

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 9Alma awaonya watu wa Amoniha kutubu na kujiandaa kwa ujio wa Yesu KristoWasilisha mpangilio ufuatao: Wanafunzi wawili wanafika shuleni na mwalimu wao anatangaza kuwa ni lazima wafanye mtihani wa ghafla. Mwanafunzi wa kwanza alikuwa darasani kila siku lakini yule mwanafunzi wa pili hakuhudhuria wiki mbili kwa sababu alikuwa anaumwa.• Ni mwanafunzi yupi unategema atafanya vizuri mtihani huu?Waalike wanafunzi wapitie Alma 9:1–7, wakitafuta maneno na vishazi ambavyo vinaeleza vipi watu wa Amoniha walielewa injili na nguvu ya Mungu. Waulize watoe taarifa ya kile walichogundua.Waalike wanafunzi wachache wachukue zamu kusoma kwa sauti kutoka Alma 9:8–13. Uliza darasa litafute maneno na vishazi ambavyo vinaonyesha kama hawa watu walifundi-shwa injili au walikuwa na ufahamu wa nguvu ya Mungu. (Majibu yanapaswa kujumuisha “mmesahau” na “hamkumbuki.”)• Je! Watu wa Amoniha walikuwa wamewahi kujifunza injili au kufundishwa kuhusu

nguvu ya Mungu?• Ni baadhi sababu gani kwa nini watu waliofundishwa injili wanaweza kusahau nini

walichojifunza au wasiweze kuelewa nini walicho fundishwa?Waalike wanafunzi wapatie Alma 8:9, 11; 9:5, 30; na 12:10–11, wakitafuta maneno na vishazi vinavyopendekeza kwa nini watu wa Amoniha walikuwa wamesahau au hawaku-elewa vitu walivyofundishwa. (“Shetani alikuwa ameshikilia mioyo yao kwa kiasi kikubwa wameifanya mioyo yao “iwe migumu," “walikuwa na mioyo migumu na watu wenye shingo ngumu," “ mioyo [yao] ilikuwa imekuwa migumu sana dhidi ya neno la Mungu.")Nakili chati ifuatayo ubaoni na waulize wanafunzi wanakili kwenye daftari zao au shajara za kujifunza maandiko. (Hakikisha unaacha nafasi kubwa ya kuandika.)

historia fupi ya kiroho ya wale watu.

Mungu anatarajia nini kwa wale watu na nini bwana aliwaahidi watu wale.

Walamani(alma 9:14–17)

Watu wa amoniha (alma 9:18–24)

Gawa wanafunzi katika majozi. Alika kila jozi likamilishe chati kwa kutumia maandiko kama marejeo. Baada ya kukamilisha chati waambie wanafunzi waandike sentensi chini ya chati yao wakifanya muhtasari wa kile walichojifunza. Waalike wachache wao kushiriki

Page 290: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

275

alMa 9 –10

walichokiandika. Wanafunzi wanaweza wakatumia maneno tofauti, lakini majibu yao yanapaswa kuonyesha ukweli ufuatao: Bwana anatarajia utiifu mkubwa kutoka kwa wale waliopokea elimu na baraka za injili. Ili Kuwasaidia wanafunzi kuona jinsi hizi kanuni zinavyotumika katika maisha yao, waulize maswali yafuatayo:• Unafikiri kwa nini Mungu alikuwa na matarajio makubwa kwa watu wa Amoniha?• Kwa nini ni haki kwa Mungu kuwa na matarajio makubwa kwa wale ambao wamepokea

elimu na baraka za injili?Onyesha kishazi "waliopendelewa sana na Bwana" katika Alma 9:20. (Unaweza kutaka kupendekeza kwamba wanafunzi waalamishe kishazi hiki.)• Ni kwa njia gani waumini wa Kanisa leo ni “watu waliopendelewa sana wa Bwana”?• Kulingana na Alma 9:19–23, ni vipawa na baraka gani Wanefi walipata (ikijumuisha watu

wa Amoniha) kwa sababu walikuwa watu wa agano wa Bwana?• Ni vipawa na baraka gani ushapata kwa sababu wewe ni muumini wa Kanisa la Bwana?• Ni baadhi ya vitu gani Bwana anatarajia kutoka kwetu kwa sababu ya vipawa na baraka

tulizopokea kutoka Kwake?Pangia nusu ya darasa kujifunza Alma 9:24–27 kibinafsi na ile nusu ingine ijifunze Alma 9:28–30 kibinafsi. Waulize wanafunzi watayarishe muhtasari wa vifungu vyao walivyopa-ngiwa katika maneno yao wenyewe. Andika maswali yafuatayo kwenye ubao ili kuwao-ngoza wanapotayarisha miuhtasari yao.

Ni ushahidi gani unauona katika mistari hii kwamba Bwana anatajarajia utiifu mkuu kutoka kwa wale ambao wana elimu kubwa ya injili?Ni baraka Alma aliwakumbusha watu kuwa wangepokea?Ni nini Alma alisema watu walihitaji kufanya hili kupokea baraka hizi?

Baada wanafunzi kuwa na muda wa kutosha wa kusoma, mwite mwanafunzi mmoja kutoka kwa kila nusu ya darasa kufanya muhtasari vifungu walivyopangiwa. Kisha uliza darasa:• Ni zipi baadhi ya njia tunazoweza kuwa wakweli kwa nuru na elimu tuliyopokea?

(Wanafunzi wanaweza kupendekeza kujifunza maandiko, wakionyesha shukrani kwa Mungu kwa baraka zao, wakitoa shuhuda zao kila mara, wakihudhuria mikutano ya Kanisa kila wiki, wakiandika shajara, na alkadhalika.)

Alma 10:1–12Amuleki anaitikia mwito wa Bwana na kuthibitisha utakatifu wa wito wa AlmaElezea kwamba baada ya Alma kuwahutubia watu, walikasirika na wakataka kumtupa ge-rezani. Amuleki kwa ujasiri alihutubia watu na kuongezea ushahidi wake kwa ule wa Alma (Ona Alma 9:31–34.) Fanya muhtasari wa Alma 10:1–4 kwa kueleza kuwa Amuleki alikuwa ni wa ukoo wa Nefi. Alikuwa mfanyakazi mwenye bidii aliye jijengea utajiri mkubwa. Pia alijulikana sana na alikuwa “sio mtu aliye na heshima ndogo” miongoni mwa wanafamilia wengi na marafiki (ona Alma 10:4). Hata hivyo hakuwa anaishi kulingana na kweli za injili aliyokuwa amefundishwa.• Unafikiri kwa nini ingekuwa jambo la msaada kwa Amuleki, ambaye alifahamika katika

jumuia, kuandamana na Alma?Waulize wanafunzi walivyoamka asubuhi ya leo. (Kwa mfano, waliamshwa na kengele ya saa au mwanafamilia mwingine aliwaamsha wao? Kama una saa yenye kengele au picha ya saa yenye kengele, fikiria kuionyesha.) Waulize wanafunzi ni wangapi kati yao wame-kuwa “wakiitwa” zaidi ya mara moja kutoka kitandani.Mualike mwanafunzi asome Alma 10:5–6 kwa sauti. Uliza darasa litafute majibu ya Amu-leki kwa “miito ya muamko” ya kiroho ambayo alikuwa amepokea kutoka kwa Mungu. • Unafikiri Amuleki alimaanisha nini aliposema nisingesikia na nisingeweza kujua? • Ni kwa njia zipi Mungu anatuita sisi? (Majibu yamkini yanajumuisha minong’ono kutoka

kwa Roho Mtakatifu, maelekezo kutoka kwa wazazi na viongozi wa Kanisa , na miito ya Kanisa.)

Waalike wanafunzi wasome Alma 10:7–10 kimya wakitafuta vipengele muhimu vya ushu-huda wa mwanzo wa Amuleki kwa watu wake.

Waalike wanafunzi wafanye muhtasariUnapowauliza wanafu-nzi wafanye muhtasari makundi ya mistari, una-waalika wachanganue maandiko kwa makini zaidi. Ukihisi kwamba mwanafunzi amekosea utondoti muhimu katika muhtasari wake, una-weza kuwaita wanafunzi wengine kama wana utondoti wa maana wa kuongezea.

Page 291: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

276

SoMo la 75

• Uzoefu wa Amuleki ulimuandaa vipi kuwa shahidi wa pili wa ujumbe wa Alma kwa watu wa Amoniha?

• Unafikiri vipi uamuzi wa Amuleki wa kukubali kutii ulifanya mabadiliko katika maisha yake?

Alika mwanafunzi asome Alma 10:11–12 kwa sauti na uulize darasa kuangalia njia ambazo wengine waliathiriwa na uamuzi wa Amuleki kusikia mwito wa Mungu. Waalike wanafu-nzi washiriki kile walichopata.Andika kanuni ifuatayo ubaoni pale tunaposikia na kutii sauti ya Mungu baraka zina-kuja kwetu na kwa wengine. Unaweza kutaka kupendekeza kwamba wanafunzi waandike kanuni hii kwenye maandiko yao karibu na Alma 10:11–12.) Ili kuwasaidia wanafunzi kuhisi ukweli na umuhimu wa kanuni hii, uliza: • Ni lini umehisi kuwa umebarikiwa kwa sababu ulitii mwito kutoka kwa Bwana?• Jinsi gani umeshawahi kuona baraka zikiwajia wengine sababu wewe au mtu mwingine

ameitikia mwito wa Bwana?• Jinsi gani uzoefu huu unaathiri hamu yako ya kusikiliza na kutii miito kutoka kwa Bwana?

Alma 10:13–32Amuleki anajibu wale wanaompinga na kuwasihi watu watubuAndika vishazi vifuatavyo ubaoni:

1. Kukasirika na kujitetea. 2. Kutilia shaka umuhimu wa ushauri. 3. Kumkosoa mtu aliyetoa ushauri. 4. Kushuku au jadili ushauri. 5. Kwa unyenyekevu sikiliza na utii.

Waulize wanafunzi wasikilize kwa ukimya ni kishazi kipi ubaoni kinafanana kwa karibu jinsi gani wanaweza kujibu kama mzazi au kiongozi wa Kanisa angewasahihisha au kuwa-taka wabadilishe kitu fulani wanachofanya. • Ni zipi baadhi ya sababu za watu wanaweza kujibu marekebisho kwa njia hizi?Andika marejeo ya maandiko yafuatayo ubaoni: Alma 9:2–3; Alma 9:4–5; Alma 10:13, 16–17; Alma 10:24, 28–30Waalike wanafunzi kuchagua kifungu kimoja kwenye ubao ili wajisomee wenyewe. Waulize watafute jinsi gani vifungu vya maandiko vinaelezea watu wa Amoniha wakijibu ujumbe wa Alma na Amuleki. Pia acha wachague kishazi kwenye ubao ambacho kinaakisi kabisa mjibizo wa watu. Baada ya muda wa kutosha, waulize wanafunzi waaelezee ni upi kati ya mijibizo mitano kwenye ubao ambao unawiana na kifungu walichojifunza.• Kwa nini mijibizo ya kwanza minne kwenye ubao ni hatari kiroho?Waalike wanafunzi wachache wachukue zamu kusoma kwa sauti kutoka Alma 10:19–23. Wahimize wao watafute kile Amuleki alifunza kuhusu matokeo ya dhambi na kuwatupa nje wenye haki.Ili kuwasaidia wanafunzi kufikiria matokeo angamizi ya kutotubu dhambi zetu, soma kauli ifuatayo ya Rais Gordon B. Hinckley:

"Kuna uovu mwingi sana kila mahali. Majaribu, na vishwawishi vyote vya kuvutia, vinatuzunguka kila mahali. Tunashindwa na hizi nguvu angamizi, kwa bahati mbaya. Tunahuzinika kwa ajili ya mmoja ambaye amepotea. Tunawafikia ili kuwasaidia, kuwaokoa, lakini katika hali nyingi kusihi kwetu kunakataliwa. Janga ni njia wanayofuata. Ni njia ambayo inaelekeza hata kwenye maangamizo" (My Testimony, Ensign, May 2000, 69).

• Ni nini baadhi ya matokeo ambayo uja kwa watu au makundi ya watu wanapokaidi amri za Mungu?

Kama kuna wakati, waalike wanafunzi waandike majibu yao kwa swali lifuatalo:• Je! Kweli mmejifunza kutoka kwa somo la leo zitawabariki vipi?

Page 292: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

277

Somo la Mafunzo ya- NyumbaniAlma 5–10 (Kitengo cha 15)

Vifaa vya Matayarisho kwa Mwalimu wa Mafunzo ya - NyumbaniMuhtasari wa Masomo ya Mafunzo ya - Nyumbani Kila SikuMuhtasari ufuatao wa mafundisho na kanuni ambazo wana-funzi walijifunza walipokuwa wanasoma Alma 5–10 (kitengo cha 15) hakikusudiwa kufundishwa kama sehemu ya somo lako. Somo unalofundisha linasisitiza mafundisho na kanuni chache tu. Fuata minong’ono ya Roho Mtakatifu unavyofiki-ria mahitaji ya wanafunzi wako.

Siku ya 1 (Alma 5:1–36)Wanafunzi wanaposoma mahubiri ya Alma kwa watu wa Zarahemla waligundua kuwa wakati tunaamini neno la Mungu na kufanya imani katika Yesu Kristo tunaweza tu-kapata mabadiliko makuu ya moyo. Wanafunzi walipojibu maswali ya Alma walijifunza pia kuwa kwa kupata badiliko la moyo tunajiandaa binafsi kupokea sehemu katika ufalme wa mbinguni

Siku ya 2 (Alma 5:37–62)Wanafunzi walipojifunza nusu ya pili Alma 5, walijifunza kanuni hizi: Tukifuata sauti ya Bwana (Mchungaji Mwema), tutajumuishwa kwenye ufalme Wake. Tunaweza kujijulia wenyewe kupitia kwa Roho Mtakatifu kuwa Yesu Kristo ni Mkombozi wa wanadamu.

Siku ya 3 (Alma 6–7)Kwa kujifunza Alma 6, wanafunzi walijifunza kuwa siku za Wanefi na katika siku zetu Kanisa litaanzishwa kwa ajili ya watu wote. Kutokana na mahubiri ya Alma kwa watu wa Gideoni wanafunzi walijifunza kuwa Yesu Kristo aliteseka ili kutuokoa kutoka kwenye dhambi na kifo na kutusaidia katika changamoto ya maisha ya muda. Pia walijifunza kwa-mba kwa kuziishi kanuni za injili, tunafuata njia ya ufalme wa Mungu.

Siku ya 4 (Alma 8–10)Kwa kujifunza kuhusu hiari ya Alma kurudi kwa watu wa Amoniha baada ya wao kumkataa yeye, wanafunzi walijifu-nza kuwa wanapoitikia kwa haraka neno la Bwana, Yeye ana-tusaidia sisi kufuata amri Zake. Alma aliwaita watu kutubu na kuwafundisha kuhusu haja ya wao kujiandaa kwa ujio wa Mwokozi. Kutoka kwa uzoefu wa Amuleki na malaika, wana-funzi walijifunza kuwa wakati tunaposikia na kufuata mwito wa Bwana, baraka zinakuja kwetu na kwa wengine.

UtanguliziKatika somo hili tafuta kuwasaidia wanafunzi kulenga kwenye kanuni ambazo zitapelekea mabadiliko ya moyo. Tafuta njia ambazo zitawasaidia wao kutegemea neno la Mungu na kuo-ngeza shuhuda zao juu ya Mkombozi.

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 5:1–36Alma afundisha kuwa mabadiliko makuu ya moyo yanahitajika ili kuingia katika ufalme wa mbinguniAndika neno mabadiliko kwenye ubao au kipande cha karatasi. Waulize wanafunzi kushiriki mifano ya njia ambazo watu wa-naweza wakabadilika kama vile kwenye muonekeno, tabia au mtazamo. Waalike kuelezea kile kinasababisha watu kufanya mabadiliko.

Waulize wanafunzi wasome Alma 5:14 na kutambua maswali matatu ambayo Alma aliwauliza watu huko Zarahemla kuzinga-tia. Fikiria kualika wanafunzi wachache waelezee inamaanisha nini mabadiliko haya makuu ndani ya mioyo yenu.

Waalike wanafunzi wasome Alma 5:3–7 na kutambua kile Alma aliwaambia watu wa Zarahemla ambacho kilichowasaidia kua-ndaa mioyo yao kubadilika.

Alma aliwaambia watu wa Zarahemla kuhusu kuongoka kwa baba yake na wengine, pamoja na kufunguliwa kutoka kwenye vifungo. Uliza: Unafikiri kujifunza kuhusu uzoefu huu kunasai-dia vipi watu kujiandaa kupata mabadiliko ya moyo? Unaweza kutaka kuwakumbusha wanafunzi kwamba waliandika jibu la swali hili katika somo kwa siku ya 1 katika miongozo yao kwa masomo ya wanafunzi.

Uliza kama mwanafunzi angekuwa na hiari kushiriki uzoefu ambao ulisababisha mabadiliko katika moyo wake. Unaweza kutaka kushiriki uzoefu wako mwenyewe. Unaweza pia kutaka kuwakumbusha wanafunzi kauli ya Mzee D. Todd Christofferson (kwenye somo la siku ya 1 katika ya mwongozo kwa mafunzo ya mwanafunzi). Eleza kuwa kwa watu walio wengi, mabadiliko makuu katika ya mioyo yetu yanatokea kidogo kidogo tunapoji-funza na kukua kwenye injili.

Waulize wanafunzi waangalie kwenye Alma 5 "Chati ya Kadio-gramu ya Kiroho" katika somo kwa siku ya 1 katika mwongozo wa mafunzo kwa mwanafunzi. Waalike kutathmini baadhi ya maandiko kwenye Alma 5 ambayo yako kwenye chati. Halafu uliza maswali yafuatayo:

• Yapi kati ya maswali ya Alma yana maana maalumu kwako?• maswali haya yanawezaje kumsaidia mtu kuhisi mabadiliko

ya moyo?

Waeleze wanafunzi kuwa matarajio makubwa ya Mkombozi kuwa watu wote wanakuja kwake na kuhisi mabadiliko makuu

Page 293: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

278

SoMo la MafUnzo ya- nyUMbani

ya moyo ili waweze kupokea uzima wa milele. Muulize mwana-funzi asome Alma 5:33–36 kwa sauti. Uliza:

• Ni nini Mungu anatualika sisi tufanye?• Ni zawadi gani tutapata kwa kukubali mwaliko Wake?

Alma 5:43–52Alma anaeleza jinsi alivyopata ushuhuda na anafundisha kuhusu tobaElezea kuwa ili kuwahamasisha watu wa Zarahemla kutafuta mabadiliko ya moyo, Alma alitoa ushuhuda wake na kuelezea jinsi alivyoupokea. Kutoka kwa ushauri wake tunaweza kujifunza jinsi ya kupata au kuimarisha shuhuda zetu. Waalike wanafunzi wasome Alma 5:45–48 kimya. Waambie watambue kitu gani Alma alisema anakijua. Pia waambie watambue majibu ya Alma kwa swali hili “Na mnadhaniaje kwamba ninajua ukweli wao?

Waulize wanafunzi washiriki kile walichojifunza, na waandike majibu yao ubaoni. Pia andika kanuni hii: Sisi tunaweza tukajua kupitia Roho Mtakatifu kwamba Yesu Kristo ni Mkombozi wa wanadamu.

Wasaidie wanafunzi kuelewa kwamba kuna siku shuhuda zao zitapata changamoto kutoka kwa mtu au kitu fulani. Hii inaweza ikawa imeishatokea. Ushauri wa Alma unatupa njia ya kusimama imara na thabiti licha ya changamoto katika shuhuda zetu. Fikiria kuwaambia kuhusu kipindi ulichopitia changamoto ya ushuhuda wako na ukashinda au kipindi mtu unayemjua alipopitia changamoto kama hiyo. Unaweza pia ukashiriki nao uzoefu kutoka katika hotuba za mkutano mkuu au makala katika jarida la Kanisa. Unaweza pia ukamwalika mwanafunzi kushiriki uzoefu kama huo.

Elezea kuwa Alma alienda kufundisha watu kuhusu toba. Unaweza ukataka mwanafunzi asome Alma 5:50 na maelezo ya Mzee Dallin H. Oaks yanapatikana katika sura ya 15, siku ya pili katika mwongozo wa mafunzo wa wanafunzi. Waulize wanafu-nzi washiriki mawazo yao kuhusu kwa nini inatubidi kuishi kila siku kama tulikuwa tunajiandaa kukutana na Bwana.

Alma 7–10Alma anafundisha huko Gidioni na AmonihaWasilisha hali zifuatazo na uwaambie wanafunzi waweke akilini wanapofanya marejeo mafundisho ya Alma kwa watu wa Gidioni.

1. Msichana anajua kuwa Upatanisho unaweza kumsaidia kuka-biliana na dhambi zake, lakini amegunduliwa ameathirika na ugonjwa mkali na hadhani kama Upatanisho unaweza kusaidia.

2. Mvulana anahangaika wakati wazazi wake wanataka kutalaki-ana, lakini hatafuti msaada wa Mwokozi.

3. Msichana anajitahidi kudhibiti hasira yake ya haraka. Hajafiki-ria jinsi gani Upatanisho unaweza kumsaidia.

Waalike wanafunzi wasome Alma 7:11–13 na warejee hali ambazo Mkombozi alikuwa tayari “kuzichukua juu” Yake mwenyewe kwa faida yetu. Alika wanafunzi wachache wafanye muhtasari wa kile vifungu hivi vinafundisha kuhusu Upatanisho wa Yesu Kristo. Pia wahamasishe wanafunzi waangalie chati inaoonyesha baadhi ya hali zinazotupa shida katika maisha ya muda (katika somo la siku la 3 katika mwongozo wa mafunzo ya mwanafunzi.)

Waeleze wanafunzi kuwa kupitia nguvu za Upatanisho, ma-umivu na uchungu wa mateso unaweza kuondolewa kutoka kwetu. Hakikisha wanafunzi wanaielewa kanuni hii: Yesu Kristo aliteseka kutuokoa kutoka dhambini na kifo na kutusaidia katika changamoto za maisha ya muda.

Alika wanafunzi washiriki kitu gani watawaambia wavulana na wasichana katika hali hizo tatu ulizoelezea hapo juu. Uliza; ni vipi mafundisho ya Alma kuhusu Upatanisho yanaweza kutumika katika hali hizi?

Wakumbushe wanafunzi kuhusu picha tatu na marejeo ya maandiko kuhusu Alma katika Amoniha (katika somo la siku ya 4 kwenye mwongozo wa mafunzo ya mwanafunzi) ambayo walijifunza na kuandikia maandishi mafupi kwa. Unaweza ukawaambia wanafunzi wachache washiriki maandishi mafupi waliyoyaandika kuhusu uzoefu wa Alma na malaika. Waombe wanafunzi washiriki hisia zao kuhusu jinsi tukio hili linaahusiana na kanuni zifuatazo: Tunapoitikia haraka neno la Bwana anatusaidia kutii amri Zake.

Kitengo kinachofuata (Alma 11–16)Waulize wanafunzi wafikirie kuhusu maswali yafuatayo wakati wanajiandaa kujifunza kazi walizopangiwa: Ungejisikiaje kama ungelazimishwa kuangalia watu wasio na hatia wakiuwawa kwa sababu ya imani yao katika Yesu Kristo na injili Yake? Unafikiri Alma na Amuleki walijisikia vipi kuangalia haya yakitokea? Wali-ambiana nini walipoona haya yakitokea? Walifanya nini?

Page 294: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

279

UtanguliziWakati Alma na Amuleki wakiendelea kufundisha watu wa Amoniha, mwanasheria aitwaye Zeezromu alimpa Amuleki hela ili akatae uwepo wa Mungu. Zeezromu pia alijaribu kubadilisha maneno ya Amuleki na kuya-shusha thamani mafundisho yake kuhusu Yesu Kristo. Wakati Amuleki alijitetea dhidi ya juhudi za Zeezromu

za kumtega, alishuhudia kuwa uokozi kutoka kwenye dhambi unatoka kwa Yesu Kristo peke yake. Amuleki pia alishuhudia kuwa binaadamu wote watafufuliwa na wataletwa na kusimamishwa mbele ya Kristo Mwana na Mungu Baba na Roho Mtakatifu” katika Siku ya Hukumu (Alma 11:44).

SOMO LA 76

alma 11

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 11:1–25Amuleki akataa majaribu ya Zeezromu ya kukana uwepo wa MunguWaulize wanafunzi kufikiri kitu walichonacho ambacho kina thamani kubwa kwao na kwamba wasingeweza kamwe kukiuza. Waalike wanafunzi wachache kusema kile wamefi-kiri na kwa nini hivyo vitu ni vya thamani kwao.Eleza kwamba Alma 11 inendelea na maelezo ya Alma na Amuleki wakifundisha watu wa Amoniha. Wakati Amuleki anafundisha alikabiliwa na mwanasheria aliyeitwa Zeezromu ambaye alitoa hela kwa kubadilishana na kitu ambacho ni cha thamani kubwa kwa Amuleki.Waalike wanafunzi watafute Alma 11:21–22 kugundua ni kiasi gani cha hela Zeezrom ali-yompa Amuleki na kwa sababu gani. Waalike wanafunzi kutoa taarifa ya wanachojifunza Taja kuwa maelezo ya Mormoni kuhusu mfumo wa Wanefi wa fedha katika Alma 11:4–19 unatusaidia kuelewa ukubwa wa hongo la Zeezromu. Wasaidie wanafunzi kuelewa kuwa onti ilikuwa kipande cha fedha chenye gharama kubwa (ona Alma 11:6, 11–13). Onti moja ni sawa kwa kukadiria na mshahara wa wiki moja wa mwamuzi (ona Alma 11:3, 11–13), ikimaanisha kuwa onti sita ni sawa na mishahara ya wiki sita wa mwamuzi.• Kwa nini toleo la Zeezromu lilikuwa linawashawishi watu fulani?Mwalike mwanafunzi asome Alma 11:23–25 kwa sauti.• Kujibu kwa Amuleki kunaonyesha nini kumhusu?• Kulingana na Alma 11:25, ni nini Zeezromu alipanga kufanya kama Amuleki angekubali

toleo lake? Hii inafanana vipi na kile Shetani anafanya wakati watu wakisalimu amri kwa majaribu yake?

Kuwasaidia wanafunzi kuelezea ni vipi Amuleki aliweza kukataa toleo ya Zeezromu andika yafuatayo ubaoni: Nita . . . hakuna kitu ambacho ni tofauti kwa roho ya Bwana. Alika mwanafunzi asome Alma 11:22. Uliza darasa litafute neno ambalo Amuleki alilitumia ili kukamilisha kauli hii.• Ni maneno gani mengine tunayoweza kuweka katika pengo lililoachwa wazi ambayo

yanaweza kutusaidia kumtegemea Roho Mtakatifu kuyakabili majaribu? (Fanya, fikiri au angalia)

Acha wanafunzi wataje kanuni iliyojikita kwenye Alma 11:22 ambayo inaweza kuwasaidia kukumbuka jinsi wanavyoweza kushinda majaribu. Wakati majibu ya wanafunzi yanaweza kutofautiana, yanatakiwa kuonyesha kanuni ifuatayo: Tunapomtegemea Roho Mtaka-tifu, tunaweza kuyashinda majaribu. Unaweza kutaka kupendekeza kuwa wanafunzi waandike kanuni hii katika maandiko yao karibu na Alma 11:22.)• Unafikiri kuwa msikivu kwa hisia za Roho Mtakatifu kunaweza vipi kutusaidia kushinda

majaribu?

Mwalike Roho MtakatifuWahiimize wanafu-nzi kualika nguvu za Roho Mtakatifu wakati wanajifunza maandiko pamoja. Baadhi ya ma-tendo yanayomwalika Roho ni maombi ya ua-minifu, mafundisho ku-toka kwenye maandiko, na kuonyesha upendo kwa Mungu na wengine ,na kushiriki uzoefu wa kiroho. Kwa wakati mwingine unaweza kuhisi kushawishiwa kuwasaidia wanafunzi kutambua ushawishi wa Roho Mtakatifu wakati wa masomo.

Page 295: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

280

SoMo la 76

Soma ushauri ufuatao wa Rais Boyd K. Packer wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili:"Kama unateleza kwenye vitu ambavyo hutakiwi kuteleza kwavyo au kama unajiunga na watu wanaokuvuta mbali upande usio sahihi, huo ndio wakati wa kutangaza uhuru wako, wakala wako. Sikiliza sauti ya Roho na hutapotoshwa.  "Kama Mtumishi wa Mungu ninaahidi kuwa utalindwa na kukingwa ku-tokana na mashambulizi ya adui kama utafuata hisia zinazokuja kutoka kwa

Roho Mtakatifu" (Counsel to Youth,” Ensign or Liahona, Nov. 2011, 18).Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa na kuhisi umuhimu wa kufuata msukumo wa Roho Mtakatifu, uliza maswali yafuatayo: • Ni hali zipi ambazo vijana wanaweza kushawishiwa kufanya kinyume na shuhuda zao?• Unafanya nini ili kumtegemea Roho Mtakatifu? Hii inakusaidia vipi?• Ni lini Roho Mtakatifu alikusaidia kushinda majaribu?Wahamasishe wanafunzi kutumia kile walichokisoma kwa kukumbuka mfano wa Amuleki wakati mwengine ambapo watajaribiwa kutoa suluhu isiyofaa kwa imani yao. Shuhudia kwamba wanapoishi kwa ustahiki wa uenzi wa Roho Mtakatifu watahisi ujasiri mkubwa na kusimama kwenye ukweli na kuyashinda majaribu.

Alma 11:26–40Amuleki anashuhudia kuhusu Mwana wa Mungu na kushinda majaribu ya Zeezromu kutia fedheha neno lakeWaulize wanafunzi kama kuna mtu yeyote aliyejaribu kushuku au kupinga imani yao kwa njia ya mabishano au udanganyifu. Alika mwanafunzi mmoja au wawili kushiriki uzoefu wao.Eleza kwamba baada ya Zeezromu kushindwa kumfanya Amuleki akatae uwepo wa Mungu, alibadilisha mipango yake na ilianza kushambulia imani ya Amuleki katika Yesu Kristo. Waalike wanafunzi wachache wachukue zamu kusoma kwa sauti kutoka Alma 11:26–35. Uliza darasa litafute njia ambayo Zeezromu alijaribu kuyageuza maneno ya Amuleki. Wau-lize wanafunzi kutoa taarifa ya kile walichokipata. Alafu mwalike mwanafunzi asome Alma 11:36–37 kwa sauti. Uliza darasa kunakili jinsi Amuleki anavyosahihisha uongo ambao Ze-ezromu aliufundisha. Waalike wanafunzi kuangalia tanbihi 34a. (Unaweza kutaka kushauri kuwa wanafunzi waweke alama tanbihi 34a katika maandiko yao.) Mwalike mwanafunzi asome Helamani 5:10–11 kwa sauti.• Kwa nini ihaiwezekani kuokolewa kwenye dhambi zetu ? Kuna tofauti gani kati ya kuo-

kolewa kwenye dhambi zetu na kuokolewa kutoka kwenye dhambi zetu?Mwalike mwanafunzi asome Alma 11:40 kwa sauti. Eleza kuwa kifungu hiki kina kanuni ambayo tunatakiwa tuifuate ili tuweze kuokolewa kutoka kwenye dhambi zetu. Andika kanuni ifuatayo ubaoni: Tunapomwamini Yesu Kristo tunaweza kuokolewa kutoka kwenye dhambi zetu.• Inamaanisha nini kwako kumwamini Yesu Kristo?• Kwa nini tunahitaji kumwamini Yesu Kristo ili tuokolewe kutoka kwenye dhambi zetu?Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa jinsi imani katika Yesu Kristo inavyoelekeza kwenye uko-mbozi kupitia toba , soma kauli ifuatayo ya Rais Dieter F. Uchtdorf wa Urais wa Kwanza:

"Tunahitaji imani ya nguvu katika Kristo ili kuweza kutubu. Imani yetu haina budi kujumuisha “mawazo sahihi ya sifa za [Mungu] tabia, ukamilifu, na uadilifu ‘ (Lectures on Faith [1985], 38). Kama tukiamini kuwa Mungu anajua mambo yote, mwenye upendo na, ni mwenye huruma, tutaweza kuweka matumaini yetu Kwake kwa wokovu wetu bila wasiwasi. Imani katika Kristo itabadilisha mawazo yetu, imani na tabia ambazo hazina uwiano na mapenzi

ya Mungu” (“Point of Safe Return,” Ensign or Liahona, May 2007, 100).Wapange wanafunzi kwenye majozi. Uliza kila jozi lichukue zamu kuelezana jinsi wa-takavyojibu kama kijana angeuliza maswali yafuatayo: (Unaweza kutaka kuandika haya maswali kwenye ubao.)• Kwa nini ninahitaji kumwamini Yesu Kristo ili nitubu na kuokolewa kutoka kwenye

dhambi zangu?

Himiza matumizi kwa wanafunziKama uelewa wa kanuni ya injili umefunzwa lakini haukutumika, mafunzo hayajatimia. Matumizi yanafanyika wakati mtu anapokubali ukweli katika ya moyo na akili yake, na kisha anatenda kulingana na ukweli ule. Wahimize wanafunzi kutenda ku-lingana na minong’ono ya kiroho wayopokea na kutumia ukweli wa injili waliojifunza.

Page 296: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

281

alMa 11

• Ni jinsi gani kuwa na imani katika Yesu Kristo kumekusaidia kutubu?Shuhudia kwamba kwa kuwa na imani katika Kristo tunaweza kutubu, kuokolewa kutoka dhambi zetu na kupokea uzima wa milele.

Alma 11:41–46Amuleki anafundisha kuhusu ufufuo na hukumu ya wanadamu woteIli kuwasaidia wanafunzi kufikiria kwa nini ni muhimu kujua kuwa hatimaye tutafufuliwa na tutahukumiwa, uliza:• Mtu anaweza kuishi maisha kitofauti kama wangejua hakuna maisha baada ya kifo. Andika maneno ufufuo na Hukumu ubaoni. Alika wanafunzi watafute Alma 11:41–45 ki-mya, wakitafuta taarifa nyingi kadri wawezavyo kuhusu ufufuo na hukumu. Wakati wana-funzi wanapotoa taarifa ya kile walichokipata, andika majibu yao ubaoni. Hakikisha kuwa mojawapo ya maelezo ubaoni yanaeleza ukweli kuwa watu wanaoishi duniani mwishowe watafufuliwa. Sema maelezo rahisi ya ufufuo katika Alma 11:45: “Kwamba hawatakufa tena; roho zao zikiungana na miili yao, wala hazitatenganishwa tena." (Unaweza kutaka kuwahimiza wanafunzi waweke alama katika kauli hii.) Baada ya wanafunzi kutoa taarifa ya kile walichojifunza, unaweza kupendekeza kwamba waandike ukweli ufuatao juu ya ukurasa katika maandiko yao: Kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo, wote watafufuliwa, na kuhukumiwa kufuatana na kazi zao. • Ni kweli zipi zilizopo ubaoni zinakuchochea kujitayarisha kukutana na Mungu?• Kwa nini kweli kuhusu ufufuo zinaleta amani na matumaini kwa wenye haki?Alika wanafunzi wasome Alma 11:46 kimya, wakitafuta matokeo ya mafundisho ya Amuleki kwa Zeezromu.• Kwa nini unafikiri mtu anaweza akafanya hivi baada ya kusikiliza mafundisho ya Amuleki?• Ni mafundisho yapi katika Alma 11:41–45 unafikiri yaliweza kumsumbua Zeezromu?

Kwa nini?Shuhudia kuwa kwa sababu ya Upatanisho wa Yesu Kristo, watu wote watafufuliwa na watasimama mbele ya Mungu ili kuhukumiwa kulingana na kazi zao” (Alma 11:44). Wape wanafunzi muda wa kutafakari kile walichojifunza leo na jinsi kinavyohusiana nao. Kisha acha waandike majibu kwa maswali yafuatayo kwenye daftari au shajara za kujifunza maa-ndiko: (Unaweza kutaka kuandika maswali haya ubaoni.)• Unajihisi vipi unapofikiria kuhusu kufufuliwa na kuhukumiwa?• Unahitaji kufanya nini ili kujiandaa kusisimama mbele ya Mungu?• Imani yako ya kwamba utafufuliwa na kuhukumiwa inaathiri vipi jinsi unavyochagua

kuishi kila siku?

Tangazo na Habari za UsuliAlma 11:38–39. Yesu Kristo ni Baba wa Milele vipi?

Kama wanafunzi wanahitaji kuelewa ni vipi Yesu Kristo anaweza kuwa Mwana wa Mungu na Baba wa

Milele, unaweza ukafundisha au kurejea wazo la ziada la kufundishia la Mosia 15:1–9 katika somo la 60.

Page 297: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

282

UtanguliziBaada ya maneno ya Amuleki kusababisha Zeezromu “kutetemeka katika dhamira yake ya hatia, (Alma 12:1), Alma alifungua kinywa chake na akaanza kuelezea, na kuimarisha maneno ya Amuleki, Alma akalenga kwenye ukweli ambao ungesaidia watu wa Amoniha kutubu

ugumu wa mioyo yao na dhambi nyingine. Alisisitiza mitego iliyojificha ya Shetani, hukumu inayowaangu-kia waovu na mpango wa ukombozi, ambao utafanya uwezekano kwa wale ambao wanaotubu kusamehewe dhambi zao.

SOMO LA 77

alma 12

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 12:1–7Alma anaufichua mpango wa — Zeezromu na mpango wa adui—kwa watu wa Amoniha Fuata ufafanuzi ulioambatana ili kufunga kifundo au mtego, kwa kipande cha kamba au waya. Onyesha jinsi mtego unavyofanya kazi kwa kushika kamba iliyozungushwa mbele ya kipande cha peremende au chakula kwenye meza au dawati. Waulize wanafunzi wafikie chakula kupitia kwenye mtego. Wakati ambapo anafanya hivyo kaza mtego. (Kuwa makini usiwaumize wanafunzi.)

Mwalike mwanafunzi arudie kwenye darasa ni vipi Zeezromu alijaribu kumshika Amuleki kwenye mtego (ona Alma 11:21–25). Fafanua kuwa baada ya Amuleki kuelewa dhamira ya Zeezromu alimjibu, Alma pia alisimama kumwelezea Zeezromu na watu waliokuwa wakisikiliza (ona Alma 12:1–2). Waalike wanafunzi wasome Alma 12:3–6kimya, wakitafuta maneno na vishazi ambavyo Alma alivitumia kuelezea njama za Zeezromu. (Unaweza ukataka kuwatia moyo wanafunzi kuweka alama maneno au vishazi hivi.) Acha watoe taarifa ya kile wanachokipata. • Zeezromu alikuwa akifuata mpango ya nani?• Alma alisema ni nini ilikuwa dhamira za Ibilisi?• Nini kilimuwezesha Alma kuona kupitia mpango huu?Waalike wanafunzi kusema kanuni ambazo zinafanya muhtasari wa kile walichojifunza kutoka Alma 12:3 na kuhusu jinsi wanavyoweza kugundua uongo wa adui. Ingawa wana-funzi wanaweza wakatumia maneno tofauti wanapaswa kutambua kanuni ifuatayo: Roho Mtakatifu anaweza kutusaidia kutambua uongo wa adui. Unaweza kutaka kuwaku-mbusha wanafunzi kuwa somo lililopita walijifunza kuwa tunapomtegemea Roho Mta-katifu, tunaweza kuyashinda majaribu. Fafanua kuwa ili kuyashinda majaribu au uongo, kwanza ni lazima tuutambue na madhara yanayoweza kutuletea. Kisha ni sharti tufanye yote tuwezavyo kuepukana nao.• Ni wakati gani Roho Mtakatifu amekusaidia kugundua na kuepuka majaribu? (Wanafi-

nzi wakishajibu, unaweza pia kutaka kushiriki uzoefu wako mwenyewe.) Wape wanafunzi dakika chache kuandika kwenye daftari au shajara za kujifunza maandiko kuhusu jinsi wanavyoweza kuongeza usikivu wao kwa Roho Mtakatifu ili waweze kugu-ndua na kuepuka mitego ya adui.

Page 298: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

283

alMa 12

Alma 12:8–18Alma afundisha kuhusu hukumu ya mwisho ya watu woteWaulize wanafunzi kufikiri kuhusu fani zao wanazopenda kuchukua. Waalike wachache wao kuongea kuhusu fani ambayo wanayoipenda. Waulize kukisia kiwango wanachoweza kulipia mafunzo katika chuo au chuo kuu, au shule ya ufundi ili kupata ujuzi na utaalamu wanaou-hitaji ili kuweza kufanikisha fani zao? Mwalike mwanafunzi asome taarifa ifuatayo ya Mzee David A. Bednar wa wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili: Uliza darasa lisikilize “mafundi-sho binafsi” ambayo Mzee Bednar alisema ni lazima tulipie ili kupata elimu ya kiroho.

"Uelewa wa kiroho hauwezi tu kutolewa kirahisi kwetu [sisi]. Mafundisho binafsi ya bidii na ya kujifunza kwa kusoma na pia kwa imani lazima ilipwe ili, kupata na kibinafsi kuwa na elimu kama hii. Kwa njia hii pekee ndipo kile kinachojulikana kwenye mawazo ndicho kinachosikika moyoni” (“Watching with All Perseverance,” Ensign or Liahona, May 2010, 43).Mwalike mwanafunzi asome Alma 12:7–8 kwa sauti. Uliza darasa lifuatilie,

likitafuta ushahidi kuwa Zeezromu alikuwa anaanza kulipa mafundisho binafsi ya kiroho yanayotakiwa ili kupata elimu ya kiroho. Waalike wanafunzi waelezee wanachokiona ka-tika vifungu hivi kinachoonyesha moyo wa Zeezromu ulikuwa unaanza kubadilika.Eleza kuwa Zeezromu alimuuliza Alma swali kuhusu ufufuo. Badala ya kumjibu swali hilo mara moja, Alma alimfundisha kuhusu kupata elimu ya kiroho. Mwalike mwanafunzi asome Alma 12:9–11 kwa sauti. Waambie wanafunzi watafute kile Alma alichomfundisha Zeezromu kuhusu kupata elimu ya kiroho. Eleza kuwa “Siri za Mungu ni kweli za ki-roho zinazojulikana tu kwa ufunuo . . . kwa wale walio watiifu katika injili” (Guide to the Scriptures, “Mysteries of God,” scriptures.lds.org). (Unaweza ukataka kuandika hii taarifa ubaoni. Unaweza pia kupendekeza kuwa wanafunzi waiandike katika maandiko yao ka-ribu na Alma 12:9.)Waulize wanafunzi waelezee kwa maneno yao kile Alma 12:9 inafundisha kuhusu tu-nachotakiwa kufanya ili kupokea ukweli wa kiroho. (Wanafunzi wanaweza wakatumia maneno tofauti lakini majibu yao yanapaswa yaelezee kuwa Bwana hufunua kweli za ki-roho kwetu kulingana na usikivu na bidii yetu katika maneno yake. Unaweza kutaka kuwahimiza wanafunzi waandike kanuni hii katika maandiko yao karibu na Alma 12:9.)• Kuna uhusiano gani kati ya hali ya roho zetu na uwezo wetu wa kupokea ukweli wa kiroho?Kwenye Alma 12:10–11, sema wazi matokeo yanayo tofautiana kwa wale ambao hawai-weki migumu mioyo yao, dhidi ya ukweli, na wale wanaofanya hivyo. • Ni kwa jinsi gani kujua madhara haya kunachochea shauku yako ya kutaka kupata

elimu ya kiroho kuu?Eleza kuwa baada ya Alma kufundisha jinsi tunavyojua ukweli wa kiroho, alijibu swali ambalo Zeezromu alimuuliza mapema. Waambie wanafunzi waseme tena swali la Ze-ezromu kwenye Alma 12:8 kwa kutumia maneno yao wenyewe. Waalike wasome Alma 12:12–15 kimya, wakitafuta kile Alma alichomfundisha Zeezromu kuhusu ufufuo na hu-kumu. Wakati wanafunzi wanaposoma andika yafuatayo ubaoni: Tutawajibishwa mbele ya Mungu kwa ajili ya . . . , . . . , na . . .Wakati wanafunzi wamemaliza kusoma, waulize wamalizie sentensi kwenye ubao: Tuta-wajibishwa mbele ya Mungu kwa mawazo yetu, maneno, na matendo.• Unafikiri ni kwa jinsi gani ukweli huu ungeweza kumwathiri Zeezromu? (Acha wanafu-

nzi wafungue Alma 14:6 na 15:3 ili wapate jibu.) Kwa nini unafikiri ukweli huu ulikuwa na mguso wa nguvu kwa Zeezromu? (Unaweza kutaka kutaja kuwa Zeezromu hakujali tu kuhusu nafsi yake peke yake. Alijali kuhusu watu aliokuwa amewapotosha.)

• Ni mawazo aina gani, maneno na vitendo ambavyo watu wanapigana navyo ambavyo vitawalaani kama wasipotubu? (Ili Kuwasaidia wanafunzi kutafakari na kujadili ni jinsi gani uchaguzi wao ya burudani na vyombo vya habari unaweza kuathiri mawazo, ma-neno na vitendo vyao, unaweza ukafananisha na ushauri kuhusu burudani na vyombo vya habari katika Kwa Nguvu ya Vijana.)

• Ni tofauti gani inaweza kutokea katika chaguo zako za kila siku kama utakumbuka ukweli ulioandikwa ubaoni?

Page 299: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

284

SoMo la 77

Elezea marejeo ya Mosia 4:30 katika Alma 12:14, tanbihi 14a, na umwalike mwanafunzi asome Mosia 4:30 kwa sauti (Unaweza ukataka kushauri wanafunzi waweke alama katika marejeo haya.) Kama kuna muda wa kutosha waambie wanafunzi warejee nyuma kwe-nye kile walichoandika kuhusu kuongeza hisia zao katika ushawishi wa Roho Mtakatifu. Waalike waongeze mawazo machache kuhusu jinsi kuelewa uwajibikaji wao binafsi mbele ya Mungu kunavyochochea shauku yao ya kutambua na kuepuka majaribu.

Alma 12:19–37Alma anaelezea jinsi mpango wa ukombozi unatusaidia kushinda matokeo ya KuangukaWaonyeshe wanafunzi picha ya Adam na Hawa wakipiga magoti kwenye madhabahu (Gospel Art Book [2009], no. 4) Elezea kuwa mtu aliyeitwa Antiona, ambaye alikuwa mmoja kati ya viongozi wakuu huko Amoniha, aliuliza swali kuhusu mafundisho ya Alma na Amuleki kuhusu ufufuo. Alikuja kumuuliza Alma ni vipi binadamu anaweza akawa anayei-shi milele. (Ona Alma 12:20–21.)Waulize wanafunzi ni kiasi gani watapata ujasiri kuelezea kwa mtu ambaye sio muumini wa Kanisa jinsi gani tutaokolewa kutoka Kuanguka. Ili kuwasaidia wajiandae kufundisha ukweli huu kwa mtu mwingine, waambie watafute mistari hii katika chati ifuatayo na waandike watakachojifunza katika nguzo sahihi. (Unaweza ukanakili chati ifuatayo ubaoni kabla da-rasa halijaanza. Waalike wanafunzi wanakili katika daftari yao au shajara za maandiko.)

Matokeo ya Kuanguka (alma 12:22, 24)

Mungu amefanya nini kuleta ukombozi wetu (alma 12:24–25, 28–33)

tunapaswa kufanya nini ili tukombolewe? (alma 12:24, 30, 34, 37)

Wakati wanafunzi wanamalizia chati, wengine wanaweza wakahitaji usaidizi wako. Njia moja ya kuwasaidia wanafunzi waelewe maandiko hayo ni kuwaelekeza kwenye tanbihi. Kwa mfano, marejeo ya maandiko yaliyotolewa kwenye tanbihi 22 c yaweza kusaidia wanafunzi kuelewa inamaanisha nini kwa binadamu wote kupotea na kuanguka.) Wakati wanafunzi wamemaliza chati, waulize maswali yafuatayo: (Unaweza ukataka kuandika maswali haya ubaoni kabla ya darasa ili wanafunzi waweze kufikiria majibu yao wakiwa wanajaza chati.)• Ni vipi Upatanisho wa Yesu Kristo unaturuhusu kushinda matokeo ya Kuanguka? (Kwa

sababu ya Upatanisho wa Yesu Kristo, sisi sote tutashinda mauti kupitia ufufuo.) Na kwa kupitia Upatanisho wa Mwokozi na toba yetu, tunaweza kurudi kwa Mungu kutoka kwenye hali yetu ya kupotea na kuanguka.)

• Kulingana na Alma 12:24, ni nini Alma alifundisha kuhusu lengo la maisha? (Alisema kuwa maisha haya ni muda wetu wa kujiandaa kukutana na Mungu. Unaweza kutaka kupendekeza kuwa wanafunzi waweke alama katika vishazi katika Alma 12:24 vinavyofundisha ukweli huu.)

Ili kuwasaidia wanafunzi kutumia kile walichojifunza waulize maswali yafuatayo:• Ni kwa njia gani kujua lengo la maisha kulisaidia kukuongoza? • Ni kwa jinsi gani imani yako katika Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo imekusaidia kujia-

ndaa kukutana nao?Hitimisha kwa ushuhuda wako kuwa sasa ni muda wa kujiandaa kukutana na Mungu.

Wasaidie wanafunzi kibinafsiWakati wa kazi iliyopa-ngwa ya darasa ikiende-lea zunguka taratibu darasani ili kuwasaidia na kazi waliyopangiwa au kuwasaidia waendelee na kazi. Kwa kufanya hivyo itakupa nafasi ya kuima-risha uhusiano wako na wanafunzi na uelewa bora wa mahitaji yao.

Page 300: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

285

alMa 12

Tangazo na Habari za UsuliAlma 12:24. Hali ya Majaribio

Katika maandiko yote, neno “hali ya majaribio” au “ki-pindi cha majaribio” hutokea katika kitabu cha Alma pekee (ona Alma 12:24; 42:4, 10, 13). Mzee L. Tom Perry wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alielezea kuhusu kipindi hiki cha majaribio.

Lengo kuu la maisha ya duniani ni kuruhusu roho zetu, zilizokuwepo kabla ya dunia, ziungane na miili yetu kwa muda wa nafasi tuliyonayo ya maisha ya muda.

Uhusiano wa hivi vitu viwili umetupa nafasi ya kukua, kuendelea na kukomaa jinsi tunavyoweza kwa roho na mwili vikiungana. Tukiwa na miili yetu, tunapitia kiasi fulani cha majaribio kinachoitwa hali ya majaribio ya uwepo wetu. Huu ndio wakati wa kujifunza na kuji-pima ili kujihakiki tu wastahiki wa nafasi za milele. Ni sehemu ya mpango wa kiungu ambao Baba yetu anao kwa watoto Wake” (Hubirini Injili Yangu kutoka Nchi hadi Nchi,”) Ensign, Mei 1989, 14).

Page 301: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

286

UtanguliziWakati Alma alipowafundisha kwa mara ya kwanza waasi wa Amoniha,walimpinga na kumuuliza “Wewe ni nani?” na kuhoji mamlaka yake (ona Alma 9:1–6). Walikuwa kwenye hali ya ukengeufu wakiwa wame-kumbatia tamko la Nehori —ukuhani wa uongo, na lengo lake la manufaa ya kibinafsi (ona Alma 1:2–15; 15:15; 16:11). Tofauti ya mafundisho ya Nehori, Alma aliwafundisha kuhusu ukuhani mkuu wa agizo takatifu

la Mungu na lengo lake la kuwasaidia wengine kutubu na kuingia katika pumziko la Bwana (ona Alma 13:6). Alitoa mfano wa Melkizedeki, ambaye alihubiri imani na toba na kusaidia watu wake waishi kwa amani. Alma pia alifundisha kuhusu maisha kabla ya duniani na kutawazwa awali. Alihitimisha mahubiri yake kwa kuwaalika watu kusikia maneno yake ili wajiandae kuingia katika mapumziko ya Bwana.

SOMO LA 78

alma 13

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 13:1–12Alma anawafundisha watu wa Amoniha kuhusu mwito wa makuhani wakuuEleza kwamba Alma 13 ina mafundisho ya Alma kuhusu kundi la watu ambao ni faida kubwa kwa Kanisa. Kwa hakika, washiriki wote wa Kanisa wamebarikiwa kupitia huduma za watu hawa. Waambie wanafunzi kuwa wanawajua watu ambao ni sehemu ya kundi hili. Kisha waulize wanafunzi wasome Alma 13:1 kimya ili kuamua watu hawa ni kina nani. Wakishapata muda wa kutosha kusoma kifungu hiki washauri wasome pia Alma 13:10, 14 na Mafundi-sho na Maagano 107:1–3. Unaweza ukataka kupendekeza kuwa waandike marejeo haya kwenye pambizo karibu na Alma 13:1.Eleza kuwa Alma alizungumza kuwahusu makuhani wa utaratibu wa Mwana wa Mungu, ambao ni Ukuhani wa Melkizedeki. Kwa maneno mengine aliongea kuhusu watu ambao wa-lishikilia ofisi ya kuhani mkuu katika ukuhani wa Melkizedeki. Mwalike mwanafunzi asome taarifa ifuatayo ya Mzee Bruce R. McConkie wa Akidi ya wale Mitume Kumi na Wawili:“Hawa Wanefi ambao walikuwa waaminifu na wa kweli katika kufuata sheria ya Musa wa-likuwa na Ukuhani wa Melkizedeki, hii inamaanisha pia walikuwa na ukamilifu wa injili. . . . Baadhi ya taarifa zetu nzuri kuhusu Ukuhani wa Melkizedeki zinapatikana katika Alma 13” ( The Promised Messiah [1978], 421).• Ni baraka zipi zimekuja kwenye maisha yako kupitia Ukuhani wa Melkizedeki? (Wa-

nafunzi wanaweza wakataja karama ya Roho Mtakatifu baraka za baba mkuu, baraka zingine za kikuhani, uongozi wa Viongozi Wakuu Wenye Mamlaka, uongozi wa kawa-ida kama maaskofu na marais wa matawi na baraka wanazozipokea kupitia maagano ambayo wazazi wao wameweka Hekaluni. Wanaweza pia kutaja ubatizo na sakramenti, ambayo hutekelezwa kwa mamlaka ya Ukuhani wa Haruni lakini chini ya uongozi wa viongozi wa Ukuhani wa Melkizedeki.)

Onyesha maswali yafuatayo ubaoni au yajumuishe kwenye kitini. Wape wanafunzi muda wa kusoma Alma 13:2–10 na kutafuta majibu ya maswali.

Ni lini wenye Ukuhani wa Melkizedeki waliitwa mara ya kwanza na kutayarishwa? (Ona Alma 13:3–5.)Ni wajibu gani ambao wenye Ukuhani wa Melkizedeki wote wanao? (Ona Alma 13:6.)Ni vishazi gani kwenye Alma 13:7 vinaelezea kuhusu Ukuhani wa Melkizedeki?Ni zipi baadhi ya sifa zitakiwazo ili kutawazwa kwenye Ukuhani Melkizedeki? (Ona Alma 22:18.)

Wakati wanafunzi wameshakuwa na muda wa kutafuta majibu ya maswali waulize watoe taarifa ya majibu yao. Unaweza kutaka kuandika majibu yao kwenye ubao.Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa zaidi na kujadili walichojifunza, fikiria kuuliza maswali yafuatayo

Wafundishe wanafunzi na wala si kifaa cha somoKipaumbele chako ni kusaidia wanafunzi kuelewa ukweli wa injili na kutumia kweli hizo katika maisha yao. Epuka majaribu yeyote ya ku-harakisha kupitia somo ili tu ukamilishe kifaa chote. Kumbuka kuwa unafundisha wanafunzi na sio kifaa cha somo.

Page 302: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

287

alMa 13

• Ni kwa njia zipi huduma za wenye ukuhani zinatusaidia sisi kujua jinsi ya kumtegemea Yesu Kristo kwa ajili ya ukombozi? (Ona Alma 13:2, 8, 16. Kupitia kwa mifano na mafu-ndisho yao na kupitia maagizo wanayoyafanya, wanatuelekeza kwa Mwokozi.)

• Alma alimaanisha nini wakati aliposema kuwa makuhani mkuu “wakiitwa na kutaya-rishwa kabla ya msingi wa ulimwengu”? (Alma 13:3) Alimaanisha kuwa watu wengine walitawazwa kimbele kabla ya kupokea ofisi fulani za ukuhani.

Ili Kuwasaidia wanafunzi kuelewa kutawazwa kimbele na jinsi gani inatumika kwenye maisha yako, unaweza ukataka kumwambia wanafunzi wasome kauli zifuatazo:Nabii Joseph Smith alifundisha: “Kila mtu aliye na mwito wa huduma waishio duniani alitawazwa kwa lengo hilo katika Baraza Kuu la mbinguni kabla ulimwengu haujaumbwa. Nadhani kuwa nilitawazwa kwenye ofisi hii katika lile Baraza kuu” (Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith [2007], 511).Rais Spencer W. Kimball alisema: “Kwenye ulimwengu kabla hatujaja wanawake waami-nifu walipangiwa kazi fulani maalumu wakati wanaume waaminifu walitawazwa kimbele kwa kazi fulani za ukuhani. Ingawa sasa hatukumbuki vipengee hasa, hii haibadilishi ukweli wa utukufu wa kile sisi mara moja tulikubaliana nacho (Teachings of Presidents of the Church: Spencer W. Kimball [2006], 215–16).• Je! Alma 13:3 inafundisha nini kuhusu kile tunahitaji kufanya ili kutimiza huduma za

uteuzi wetu wa kimbele?• Wakati mtu anatawazwa katika ofisi ya ukuhani, kutawazwa huko kunamaanisha nini

kwake? (Ona Alma 13:8.) Tazama kwamba swali hili linaweza kujibiwa na wasichana na wavulana vile vile. Vijana wanaweza wakapata faida kusikia majibu ya wasichana.)

Waulize wanafunzi wasome Alma 13:11–12 kimya, wakitafuta njia ambazo wenye ukuhani wa Melkizedeki waliotajwa na Alma walibadilika kupitia kwa Upatanisho wa Yesu Kristo.• Unafikiri inamaanisha nini “mavazi ya mtu kuoshwa kuwa meupe kwa damu ya

Mwanakondoo”?• Kwa nini unafikiri wenye Ukuhani wa Melkizedeki wanahitaji kubadilishwa kupitia

Upatanisho wa Yesu Kristo? Ni kwa njia gani tunaweza kufuata mifano yao?Wakumbushe wanafunzi kuwa Alma alifundisha kweli hizi kwa watu wa Amoniha. Watu wengi kati ya hawa walikuwa wa fani ya Nehori” (Alma 14:18; 15:15), ikimaanisha kuwa walikuwa wameyakubali mafundisho ya Nehori. Nehori alikua mwanaume aliyeanzisha agizo la uongo ambalo Alma aliliita “ukuhani wa uongo” (ona Alma 1:12–15).• Ni kwa namna gani wenye Ukuhani wa Melkizedek waaminifu ni tofauti na wale waliofu-

ata mafundisho ya Nehori? Unaweza ukataka kuwaalika wanafunzi kurejelea Alma 1:2–6, wakitafuta tofauti kati ya ukuhani wa uongo wa Nehori na ukuhani wa Melkizedeki.)

• Watu wa Amoniha walikuwa walishafundishwa kuhusu Ukuhani wa Melkizedeki na kupokea baraka kupitia Ukuhani wa Melkizedeki (ona Alma 9:21; 13:1). Kwa nini una-dhani ilikua ni muhimu kwa watu wa Amoniha kukumbushwa walichofundishwa hupo mapema kuhusu Ukuhani wa Melkizedeki?

• Umejifunza nini kuhusu ukuhani katika somo hili? (Hali wanafunzi wanaweza kupe-ndekeza kweli mbalimbali, majibu yao yanapaswa yaelezee kuwa maagizo ya ukuhani na huduma za wenye ukuhani inatusaidia kujua jinsi ya kumtafuta Yesu Kristo kwa ajili ya ukombozi.)

Unaweza kutaka kupendekeza kwamba wanafunzi waandike kwenye daftari au shajara za kujifunza maandiko, kanuni hii na kanuni zingine walizozitambua. Kama muda unaru-husu, waambie waandike ni vipi kanuni hizi zinaweza kuchochea mtazamo wao kuhusu nguvu na baraka za ukuhani.

Alma 13:13–20Alma anafundisha kuhusu Melkizedeki, kuhani mkuu sana aliyeijenga amani miongoni mwa watu wakeAndika maneno yafuatayo na vishazi ubaoni: kuhani mkuu, mfalme, alifanya imani kuu, kuhubiri toba, kujenga amani, mfalme wa amani, alitawala chini ya baba yake. Tua baada ya kuandika kila neno au kishazi ili kuacha wanafunzi wakisie, bila kuangalia kwenye maa-ndiko yao, nani Alma alimwelezea kwa maneno na vishazi hivi. (Alimuelezea Melkizedeki)

Page 303: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

288

SoMo la 78

Kama wanafunzi hawajakisia sahihi wakati umeandika maneno na vishazi hivyo vyote ubaoni waambie wasome Alma 13:14.Kama baadhi ya wanafunzi walikisia kuwa Alma alikuwa anazungumza kuhusu Yesu Kristo, waulize kwa nini maelezo ya kuhani mkuu wenye haki yatawakumbusha kuhusu Mkombozi. Wasaidie kuelewa kuwa wenye Ukuhani wa Melkizedeki ”ni baada ya agizo la Mwana, Mwana pekee wa Baba (Alma 13:9; ona pia M&M 107:2–4). Sema kuwa wenye Ukuhani wa Melkizedeki wanatakiwa kujitahidi kufuata mfano wa Yesu Kristo katika hu-duma na mafundisho yao. Pia wakumbushe wanafunzi kuwa maagizo yanayotolewa kwa mamlaka ya Ukuhani wa Melkizedeki yanasaidia kutuvuta karibu zaidi na Mwokozi.Muulize mwanafunzi asome Alma 13:14–19 kwa sauti. Litie moyo darasa lifikirie kuhusu jinsi watu waovu wa Amoniha wangeweza kufaidika kutokana na kujifunza kuhusu Melkizedeki. • Katika Alma 13:17, ni maneno gani yanaeleza kuhusu watu wa Melkizedeki? Ni vipi

watu hawa walifanana na watu wa Amoniha? (Ona Alma 8:9; 9:8.)• Ni nini Melkizedeki alifanya kama kiongozi wa watu wake? Jinsi gani uongozi wake uliwa-

shawishi watu? Ni kwa vipi ushawishi huu unatofautiana na ushawishi wa wale waliokuwa katika Amoniha ambao walifuata mafundisho ya Nehori? (Ona Alma 8:17; 10:27, 32.)

Waalike wanafunzi wafanye muhtasari wa Alma 13:16–18, kuelezea kweli vifungu hivi hufundisha kuhusu majukumu ya viongozi wa ukuhani. Wanapopendekeza majumuisho, hakikisha wanaeleza kuwa viongozi wa ukuhani wanatusaidia kumtegemea Yesu Kristo, kutubu, na kuishi kwa amani. (Unaweza kutaka kuwatia moyo wanafunzi kuandika muhtasari wao kwenye maandiko yao karibu na Alma 13:16–18.) Eleza kuwa viongozi wengine wa Kanisa kama vile Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama na viongozi wa Wasichana ni washiriki muhimu katika juhudi hii. Kuhudumu pamoja na viongozi wa ukuhani, wanasaidia kuogoza watu binafsi na familia kuja kwa Kristo.• Umebarikiwa vipi kupitia huduma ya viongozi wa Kanisa?

Alma 13:21–31Alma anawaalika watu kusikiliza sauti ya Mungu na kuingia katika mapumziko yakeWaalike wanafunzi kutafuta wazo linalorudiwa katika Alma 13:12, 13, 16, 29. Wanapaswa kutafuta neno pumziko na kishazi “pumziko la Bwana” Unaweza kutaka kuwatia moyo wao waweke alama wazo hili kwenye kila aya. Ili Kuwasaidia wanafunzi kuelewa inama-anisha nini kuingia katika pumziko la Bwana katika maisha haya na baada ya kufa, soma maelezo yanayofuata: Manabii wa kale wanazungumzia kuingia kwenye pumziko la Mungu [ona Alma 12:34 ; M&M 84:23–24 ]; inamaanisha nini? Kwa mawazo yangu inamaanisha kuingia kwenye elimu na upendo wa Mungu na kuwa na imani katika lengo lake na mpango wake, kwa kiwango cha kujua kwamba tuko sahihi, na kwamba hatuwindi kitu kingine” (Joseph F. Smith, Teachings of Presidents of the Church: Joseph F. Smith [1998], 56).Watakatifu wa kweli huingia kwenye pumziko la Bwana wakati wa maisha haya na kwa kushi-kilia ukweli, wanaendelea kwenye hali hii ya baraka hadi wanapopumzika pamoja na Bwana mbiguni. Pumziko la Mungu katika hali ya milele ni kurithi uzima wa milele, kupata utukufu wote mkamilifu wa Mungu” (Bruce R. McConkie, Mormon Doctrine, 2nd ed. [1966], 633).Elezea kuwa Alma aliwahimiza watu wa Amoniha kutubu na kujiandaa kwa kuja kwa Kristo (ona Alma 13:21–26). Pia alishiriki kanuni wanazotakiwa kuzifuata ili kuingia kwenye pumziko la Bwana.Waulize wanafunzi wasome Alma 13:27 kimya. • Ni maneno gani kwenye Alma 13:27 yanayoonyesha jinsi Alma alijisikia kuhusu watu na

kuhusu ujumbe wake?Waalike wanafunzi wachache wachuke zamu kusoma kwa sauti kutoka Alma 13:27–29. Uliza darasa litafute zile kanuni Alma alizotarajia watu watazifuata. Kisha waulize wa-nafunzi waorodhesha kanuni walizozipata. Kwa mfano wanaweza wakasema kuwa na tunapojibu kwa unyenyekevu mwaliko wa kutubu Roho itatupelekea sisi kwenye pumziko la Bwana. Waalike wanafunzi kuandika malengo kuhusu jinsi watakavyofuata ushauri huu katika Alma 13:27–29. Shuhudia kuwa tutaingia kwenye pumziko la Mungu katika maisha haya na yajayo tunapofuata kanuni Alma alizofundisha.

Page 304: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

289

UtanguliziBaada ya kuwasikia Alma na Amuleki wakifundisha, ba-adhi ya watu wa Amoniha waliamini na kutubu. Watu wengi walikuwa na hasira na kutamani kuwaangamiza Alma, Amuleki na wale walioamini maneno yao. Alma na Amuleki walikamatwa, wahukumiwa, na hatimaye wafungwa gerezani. Watu waovu katika Amoniha

waliwafurusha watu ambao waliamini na waliwachoma wake, watoto, na maandiko yao hali Alma naAmuleki walilazimishwa katazama. Baada ya siku nyingi, Bwana aliwakomboa Alma na Amuleki kutoka gerezani na kuwaangamiza viongozi waovu wa Amoniha.

SOMO LA 79

alma 14

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 14:1–13Alma na Amuleki kufungwa gerezani, na waumini wa Amoniha wakafukuzwa au kuchomwa motoWaalike wanafunzi wafikirie juu ya changamoto walizokumbana nazo au walizokuwa wanakumbana nazo. Kisha waalike wanafunzi wasome kauli ifuatayo kwa sauti:“Dhiki huja kutoka vyazo tofauti. Unaweza wakati mwengine kukabiliwa na majaribio kama matokeo ya kiburi chako mwenyewe na utovu. Majaribio haya yanaweza kuepukika kupitia kuishi kwa haki. Majaribio mengine kwa urahisi ni sehemu halisi ya maisha na yanaweza kuja nyakati wewe unaishi kwa haki. Kwa mfano, unaweza kupatwa na majaribio katika nyakati za ugonjwa au msukosuko au vifo vya wapendwa wako. Dhiki inaweza kuja wakati fulani kwa sababu ya chaguo mbaya, maneno na matendo ya kuumiza ya wengine.“Ufanisi na furaha yako, yote sasa na katika milele, hutegemea sana na majibu yako katika magumu ya maisha” (True to the Faith: A Gospel Reference [2004], 8–9).Elezea kwamba katika somo la leo, wanafunzi watajadili juu ya tukio la watu ambao walipatwa na majaribio makali. Mengi ya haya majaribio yaliletwa na wengine. Wahimize wanafunzi wafikirie jinsi kweli watakazojadili katika somo hili zinahusiana na wao, bila kujali ni majaribio gani wanakabiliana nayo.Andika maswali yafuatayo kwenye ubao:

Waalike wanafunzi kadhaa kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka Alma 14:1–10. Uliza darasa lifuatie, likitafuta mifano ya mateso yaliwapata watu walioorodheshwa kwenye ubao.• Watu hawa walipatwa na mateso gani? (Orodhesha majibu ya wanafunzi kwenye ubao.)Sema kwamba wakati Amuleki aliona kuteseka kwa wanawake na watoto, yeye alitaka kutumia nguvu za ukuhani kuwaokoa wao. Mwalike mwanafunzi asome Alma 14:11 kwa sauti, na kisha uulize darasa litafute majibu ya Alma kwa maombi ya Amuleki.• Kwa nini Bwana aliruhusu wanawake na watoto hawa kuchomwa? (Unaweza kuwa na

haja ya kuelezea kwamba katika mstari huu, kishazi “yeye huteseka“ inamaanisha “yeye huruhusu.” Bwana aliruhusu watu wateseke ili vifo vyao viweze kusimama kama usha-hidi dhidi ya watu ambao waliwaua wao. Ona pia Alma 60:13.)

• Kulingana na Alma, ni kwa jinsi gani wanawake na watoto watabarikiwa kwa imani katika Bwana?

Unaweza kuwa na haja ya kusisitiza kwamba kwa wakati huu mahususi, ilikuwa ni ma-penzi ya Bwana kuruhusu watu wateseke. Hata hivyo, hii si hali ya kawaida. Wahakikishie wanafunzi kwamba Bwana anawapenda na anataka wao wawe na furaha na kuwa na amani katika maisha yao. Kama wanaumizwa au kudhulumiwa kwa njia yeyote, wanapa-swa kutafuta msaada kutoka kwa mzazi au kiongozi wa Kanisa ili watatue shida hiyo.

Alma na Amuleki Zeezromu Waongofu wanaume Waongofu wanawake na watoto

Page 305: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

290

SoMo la 79

• Ni sababu zipi zingine Bwana anaweza kuruhusu sisi kuteseka? (Majibu yanaweza ku-jumuisha kuwa anataka sisi kuelewa matokeo ua uamuzi usio wa busara, kwamba Yeye anataka sisi tukuze uvumilivu, kwamba Yeye anataka sisi tukuze huruma kwa wengine wanaoteseka na kwamba Yeye anatutaka tuelewe kwamba tunahitaji kumtegemea Yeye.)

Andika ukweli ufuatao ubaoni tunapomwamini Mungu atatuimarisha wakati wa ma-jaribio yetu. Kisha muulize mwanafunzi asome Alma 14:12–13 kwa sauti• Ni kwa insi gani maneno ya Alma yalionyesha imani yake kwa Bwana?Unaweza kutaka kuwauliza wanafunzi wasome kauli zifuatazo za Mzee Richard G. Scott wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili:

"Mfano wa Alma na Amuleki unaelimisha. Wakati walipokuwa wakijitahidi kufanya mema kwa watu wa Amoniha, walitekwa. Amuleki alimwamini mwenzi wake mzoefu sana, Alma, ambaye alimwongoza kwenye kujiamini sana katika Bwana. Wakilazimishwa kuwatazama wanawake na watoto wakiteketezwa na moto, Amuleki alisema “pengine watatuteketeza nasi pia” Alma alijibu ‘Na iwe hivyo kulingana na mapenzi ya Bwana” —kanuni ya

muhimu. “Lakini . . .kazi yetu haijaisha; kwa hiyo hawawezi kututeketeza’ [Alma 14:12–13; mkazo imeongezwa (“To Be Healed,” Ensign, May 1994, 8)."Maisha haya ni uzoefu katika imani kuu—imani kwa Yesu Kristo. Kuamini maana yeke ni kutii kwa hiari bila kujua mwisho kutoka mwanzo (ona Mithali. 3:5–7). Ili kuzaa matunda, imani yako kwa Bwana ni lazima kuwa na nguvu na yenye kuvumilia kuliko ujasiri wako kwenye hisia zako binafsi na uzoefu.” (“Trust in the Lord,” Ensign, Nov. 1995, 17).Elezea kuwa kwenye Alma 14:14–29 wanafunzi wataona mifano mingi ya Alma na Amuleki wakimwamini Bwana. Wataona pia jinsi Bwana alivyowaimarisha ili waweze kufanya kazi Zake.

Alma 14:14–29Mungu awaokoa Alma na Amuleki kutoka gerezani na kuwaangamiza viongozi wengi waovu wa Amoniha Gawa darasa mara mbili. Acha nusu moja ya darasa kupekua Alma 14:14–19 wakati nusu ingine ikipekua Alma 14:20–25. Uliza makundi yote mawili yatafute nini Alma na Amuleki waliteseka mikononi mwa viongozi waovu wa Amoniha? Wakati wanafunzi wamepata muda wa kutosha wa kusoma, waulize washiriki kile walichokipata. Orodhesha majibu yao ubaoni chini ya “Alma na Amuleki”• Yapi kati ya majaribio haya yangekuwa magumu sana kwako? Kwa nini?”• Ni lini umeona watu wakiteseka na majaribio hata ingawa wanajitahidi kuwa wenye haki?Waalike wanafunzi wachukue zamu na kusoma kwa sauti kutoka Alma 14:25–29. Uliza da-rasa lifuatilie, likitafuta kile Bwana alifanya ili kuwaokoa Alma na Amuleki kutoka gerezani. Ili kusaidia wanafunzi kugundua na kuelewa kanuni katika mistari hii, uliza baadhi au yote ya maswali yafuatayo:• Kwa nini Alma na Amuleki waliweza kupokea nguvu na uwezo kutoka kwa Bwana?

(Ona Alma 14:26, 28.)• Ni kanuni zipi tunazoweza kujifunza kutoka kwa uzoefu wa Alma na Amuleki wakiwa

gerezani? (Majibu ya wanafunzi yanaweza kutofautiana, lakini yanapaswa yadhihirishe ukweli kwamba kama tutamuita Mungu kwa imani atatuimarisha kwenye mateso yetu na kutuokoa katika njia Yake na kwa wakati Wake. Unaweza kutaka kusha-uri kuwa wanafunzi waweke alama vishazi katika Alma 14:26, 28 ambavyo vinasisitiza kanuni hii.)

• Ni baadhi ya njia zipi watu wanaweza kutumia imani kwa Yesu Kristo nyakati ngumu?Waalike wanafunzi kushiriki uzoefu waliokuwa nao wakati wameshuhudia nguvu ina-yoweza kuja katika maisha yetu tunapotumia imani katika Yesu Kristo na kumsubiri Yeye kwa unyenyekevu. Wanaweza kushiriki uzoefu wao au uzoefu kutoka kwa maisha ya watu wanaowajua. Unaweza pia kushiriki uzoefu kutoka kwenye maisha yako au maisha ya mtu unaemjua.

Uzoefu wa kibinafsiWanafunzi watafai-dika kusikia uzoefu wa kibinafsi wa wengine. Wahimize kushiriki uzo-efu katika njia ambayo itaalika ushawishi wa Roho Mtakatifu na ambao utawaongoza kumfuata Mwokozi. Wa-tahadharishe kutoshiriki uzoefu ambao ni wa kibinafsi au wa kisiri au ule unaoweza kuwaletea fedheha au aibu.

Page 306: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

291

alMa 14

Hitimisha kwa kutoa ushuhuda kuhusu nguvu za Bwana za kutuimarisha na kutuokoa kutoka kwenye majaribio kwenye njia Yake kwa wakati Wake. Wahakikishie wanafunzi kuwa tunapoamini mpango wa Bwana, ataongeza nguvu zetu na uwezo wa kuvumilia mambo magumu.

Tangazo na Habari za UsuliAlma 14:7–11. “Bwana anawapokea mwenyewe.”

Ingawa tunahuzunika kwa vifo vya wenye haki, tufu-rahie katika kujua zawadi zao katika dunia ya roho na (ona Alma 40:12 na hali yao ya mwisho katika Ufalme wa Selestia (ona M&M 76:50–70). Bwana alisema, “Wale wanaokufa ndani yangu hawataonja mauti, kwani itakuwa vyema kwao” (M&M 42:46). Rais Jo-seph F. Smith alielezea:

Ni kweli mimi ni mdhaifu vya kutosha kulia kwa kifo cha marafiki na ndugu zangu. Ninaweza nikatiririsha machozi ninapoona huzuni ya wengine. Nina huruma katika nafsi yangu kwa watoto wa watu. Ninaweza ku-lia pamoja nao wanapolia; ninaweza kufurahi pamoja nao wanapofurahi; lakini sina haja ya kuomboleza wala kuwa na huzuni kwa sababu kifo huja duniani. Woga wote wa kifo hiki umeondolewa kutoka kwa Wataka-tifu wa Siku za Mwisho. Hawana uoga kwa kifo cha

muda, kwa sababu wanajua kwamba kama vile kifo kilipokuja juu yao kwa kuvunja sheria kwa Adamu, hivyo kwa haki ya Yesu Kristo uzima utakuja kwao, na hata kama watakufa wataishi tena. Kuwa na elimu huu, wana furaha hata katika kifo, kwani wanajua watainuliwa tena na wataonana tena baada ya kaburi. (in Conference Report, Oct. 1899, 70).

Mzee Bruce R. McConkie wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alifundisha:

“Wakati mwingine watu wa Bwana wanawindwa na kuteswa. Wakati mwingine Yeye kwa makusudi huruhusu watakatifu Wake waaminifu wazurure na ku-teseka, yote kimwili na kiroho ili kuwathibitisha katika mambo yote, na kuona kama watashika agano Lake, hata katika kifo, ili waweze kupatikana wastahiki wa uzima wa milele. Kama haya yatakuwa ni maamuzi kwa yeyote kati yetu, basi na iwe hivyo” (“The Dead Who Die in the Lord,” Ensign, Nov. 1976, 108).

Page 307: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

292

UtanguliziBaada ya Bwana kuwaokoa Alma na Amuleki kutoka gerezani, walienda kuhubiri kwa watu katika jiji la Sidomu. Kule waliwakuta waumini waliowafukuza kutoka Amoniha akiwemo Zeezromu ambaye alikuwa anateseka kimwili na kiroho kwa sababu ya dhambi zake. Zeezromu alipotangaza imani yake katika Yesu Kristo, Alma alimponya na kumbatiza. Alma alilianzisha Kanisa huko Sidomu, na ndipo aliporudi na Amuleki

hadi Zarahemla. Kwa kutimiza unabii wa Alma, Wala-mani waliangamiza mji wa Amoniha katika siku moja. Zaidi ya hayo, Walamani waliwateka baadhi ya Wanefi kutoka nchi jirani. Kuchagua kufuata uongozi wa kina-bii wa Alma, majeshi ya Wanefi lilikomboa wafungwa na kuwafurusha Walamani kutoka kwenye nchi ile. Wa-kati wa kipindi cha amani, Alma, Amuleki na wengine wengi waliimarisha Kanisa kote katika nchi ya Wanefi.

SOMO LA 80

alma 15–16

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 15Alma anamponya Zeezromu, anaanzisha Kanisa katika Sidomu na anarudi pamoja na Amuleki hadi ZarahemlaIli kuwasaidia wanafunzi kukumbuka watu muhimu na matukio yaliyoelezwa katika Alma 11–14, andika maneno yafuatayo ubaoni:

ZeezromuWaontiMotoAlmaAmulekiAmoniha

Wape wanafunzi dakika moja ya kujaribu kutumia majina yote na maneno yote ubaoni ku-fanya muhtasari matukio yaliyosimuliwa katika Alma 11–14. (Unaweza kupendekeza kuwa warejelee muhtasari wa sura hiyo kwa msaada.) Baada ya wanafunzi wachache kujibu, futa maneno yote kasoro Zeezromu.Elezea kuwa baada ya kuondoka Amoniha, Alma na Amuleki wakaja Sidomu ambapo walikuta waumini ambao walikuwa wamefukuzwa kutoka Amoniha, pamoja na Zeezromu. Alika wanafunzi wasome Alma 15:3–5 kimya,wakitafuta maneno na vishazi vinavyoelezea hali ya Zeezromu. Wakati wanafunzi wanapotoa taarifa ya wanachokipata, andika majibu yao ubaoni chini ya jina la Zeezromu.• Kwa nini unadhani hatia ya Zeezromu ilimfanya ateseke yote kiroho na kimwili? Watu

walio katika hali hii wanatakiwa kufanya nini ili hali yao ibadilike?• Zeezromu aliutafuta msaada wa nani? (Ona Alma 15:4.) Kwa nini unadhani alitumana

Alma na Amuleki? (Majibu yanaweza kujumuisha kwamba aliwaamini na kwamba alijua walikuwa ni watu wa Mungu na walikuwa na mamlaka ya ukuhani.)

Alika wanafunzi wachache wachukue zamu kusoma kwa sauti kutoka Alma 15:6–10. Uliza darasa litafute maneno aliyoyasema Alma ili kumsaidia Zeezromu kufanya imani katika Yesu Kristo na Upatanisho Wake.• Kwa nini unadhani Zeezromu alihitajika kuwa na imani katika Yesu Kristo na Upatani-

sho Wake kabla ya kuponywa?Waulize wanafunzi wasome Alma 15:11–12 kimya kutafuta kile kilimtokea Zeezromu. Wa-kati watakapokuwa na muda wa kutosha wa kusoma, futa maneno na vishazi vyote ubaoni chini ya jina la Zeezromu.

Page 308: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

293

alMa 15 –16

• Ni ushahidi gani unaouona kwamba Zeezromu alitubu na kupokea huruma ya Bwana? (Aliponywa kupitia kwa imani katika Yesu Kristo, akabatizwa na akaanza kuihubiri injili.)

Andika kanuni ifuatayo ubaoni: Kupitia imani yetu katika Yesu Kristo tunaweza kupo-nywa na kuimarishwa.Sema kwamba Alma, kama kiongozi wa ukuhani hakujiletea sifa mwenyewe. Lengo lake katika maongezi haya na Zeezromu yalikuwa ni kumsaidia Zeezromu kuwa na imani katika Yesu Kristo na kupokea neema kupitia Upatanisho. Ili kuonyesha njia moja ambayo viongozi wetu wa ukuhani wanatusaidia kupokea baraka za upatanisho, soma uzoefu ufuatao ulioshirikiwa na Mzee Jay E. Jensen wa wale Sabini:“Wakati nikihudumu kama askofu, nilishuhudia baraka za Upatanisho katika maisha ya waumini wa Kanisa ambao walikuwa wamefanya dhambi nzito. . . .“Kijana mzima mmoja katika kata yetu alikuwa na miadi na msichana. Wakaruhusu huba yao kuvuka mipaka. Alinijia kwa ajili ya ushauri na msaada. Kulingana na alichoungama na uvuvio wa Roho Mtakatifu kwangu miongoni mwa vitu vingine, hakuruhusiwa kushiriki sakramenti kwa muda. Tulikutana mara kwa mara ili kuhakikisha toba imefanyika na baada ya muda wa kutosha, nilimruhusu kupokea tena sakramenti. “Nikiwa nimekaa kwenye jukwaa katika mkutano wa sakramenti, macho yangu yavutiwa kwake alipokuwa akipokea sakramenti kwa ustahiki. Nilishuhudia mikono ya huruma, upendo na usalama ikimzunguka yeye kama uponyaji wa Upatanisho ukikumbatia nafsi yake na ukainua mzigo wake, ikiwa ni matokeo aliyoahidiwa ya msamaha, amani, na furaha" (Arms of Safety, Ensign or Liahona, Nov. 2008, 49).Shuhudia kuwa maaskofu na viongozi wengine wa ukuhani wanaweza kutusaidia kupokea huruma na nguvu tunayohitaji kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo.Ili Kuwasaidia wanafunzi kuona viongozi wa Kanisa wanahudumia makundi ya watu na watu binafsi, acha wasome Alma 15:13–18. Wapange wanafunzi kufanya kazi kwa majozi. Muulize mwanafunzi mmoja katika kila jozi apekue Alma 15:13–15, 17, akitafuta njia ambazo watu wa Sidomu walibarikiwa kupitia huduma ya Alma. Muulize mwanafunzi mwingine katika kila jozi apekue Alma 15:16, 18, akitafuta njia ambazo Amuleki alibarikiwa kupitia huduma ya Alma. Baada ya kuwa na muda wa kutosha, waalike waelezane walichokipata.Alika majozi yafikirie njia tatu hadi tano ambazo viongozi wa Kanisa leo wanaweza ku-saidia makundi na watu binafsi. Wahimize wanafunzi wafikirie majukumu yao wenyewe kama viongozi katika akidi zao za ukuhani na madarasa ya Wasichana. Uliza kila jozi, ishiriki moja ya mawazo yao na darasa.

Alma 16:1–12Walamani waliharibu Amoniha lakini hawakuweza kuwashinda Wanefi wanaofuata ushauri wa AlmaWaulize wanafunzi wafikiri wakati ambao walijisikia kushangazwa au kutishika ghafula. Una-weza kutaka kumuuliza mwanafunzi mmoja au wawili kushiriki uzoefu wao. Waalike wana-funzi wasome Alma 16:1–3 kimya, wakitafuta jinsi Wanefi huko Amoniha walivyoshangazwa na kwa nini baadhi yao yaelekea walitishika. Waulize wanafunzi watoe taarifa ya kile walicho-kipata. (Kama ni muhimu, wasaidie kuona kuwa Walamani walivamia ghafla mji wa Amoniha na kuwaangamiza wakazi wake kabla Wanefi kukusanya jeshi la kupigana dhidi yao. Alika mwanafunzi asome Alma 16:4–6 kwa sauti, na liambie darasa litambue wapi Wanefi wenye haki walitafuta mwongozo. Alika mwanafunzi mwingine asome Alma 16:7–8 kwa sauti wakati wengine walio baki wanatafuta matokeo ya msaada walioupata.• Ni kwa jinsi gani mwongozo wa kinabii wa Alma uliwasaidia Wanefi?• Ni kanuni gani tunaweza kujifunza katika maelezo haya? (Wanafunzi wanaweza kuta-

mbua kanuni mbalimbali. Hakikisha wanaelewa kuwa tunapotafuta na kufuata mwo-ngozo kutoka kwa manabii wa Bwana, Bwana hutuimarisha na kutulinda. Andika kanuni hii ubaoni.)

• Vijana wanabarikiwa vipi wanapofuata mwongozo wa kinabii? Ili Kuwasaidia wanafunzi wajibu swali hili, fikiria kuwaacha waangalie sehemu mbili au tatu katika kijitabu cha Kwa Nguvu ya Vijana. Waalike wajibu swali hili kulingana na kila sehemu uliyochagua)

Page 309: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

294

SoMo la 80

Waulize wanafunzi wafikirie uzoefu wakati mwongozo wa kinabii uliwasaidia kufanya chaguo sahihi katika hali ngumu. Alika wanafunzi wachache washiriki uzoefu wao na darasa. (Hakikisha kuwa wanaelewa hawahitaji kujisikia wamelazimishwa kushiriki uzoefu wao ambao ni wa kibinafsi sana au wa siri) Unaweza pia ukashiriki nao uzoefu wako mwenyewe. Ili kuthibitisha ukweli kuwa maneno ya manabii siku zote yanatimia, unaweza kusisitiza kwamba Alma 16:9–11 inaonyesha kutimizwa kwa unabii wa Alma kuhusu watu wa Amoniha (ona Alma 9:12).

Alma 16:13–21Alma, Amuleki na wengine wajenga Kanisa miongoni mwa WanefiWakati wanafunzi wanamaliza kujifunza Alma 16, wahamasishe watafute mifano ya ka-nuni hizo mbili ulizoandika ubaoni. Fanya muhtasari wa Alma 16:13–15 kwa kueleza kuwa Alma na Amuleki waliendelea kuhubiri neno la Mungu katika nchi yote kwa msaada wa wengine ambao walikua wamechaguliwa kwa ajili ya kazi hiyo.” (Alma 16:15). Alika wa-nafunzi wasome Alma 16:16–21 kimya,wakitafuta matokeo ya juhudi hizo. Baada ya muda wa kutosha, waulize wanafunzi waseme kuhusu kile walichokipata. Waulize ni kwa jinsi gani mifano hii inaelezea kanuni moja au zote mbili zilizoandikwa ubaoni.Hitimisha somo kwa kuwahimiza wanafunzi wanakili moja kati ya kanuni hizi kwenye daf-tari au shajara za maandiko. Waalike waandike muhtasari wa kile walichojifunza leo kuhusu kanuni hiyo. Pia waulize waandike kuhusu jinsi wanavyopanga kutumia kile walichojifunza.

Tathmini ya Umahiri wa maandikoSomo hili linaonyesha alama katikati ya kozi hii. Ili kusaidia wanafunzi kuimarisha elimu yao ya umahiri wa vifungu vya maandiko, fikiria kuwapa zoezi au jaribio kuwapima ni kwa kiasi gani wana uzoefu wa umahiri wa vifungu vya maandiko mlivyovipitia darasani. Unaweza ukaandaa zoezi la usimulizi au la kuandika, kama vile kuwapa dokezo kutoka kwenye alamisho ya kitabu ya seminari na kuruhusu wanafunzi kuandika marejeo sahihi, au unaweza ukafikiria kufanya marejeo ya baadhi ya vifungu ambavyo wanafunzi wameka-riri. Unaweza ukataka kuwaambia wanafunzi kuhusu zoezi au jaribio mapema ili wajiandae.Tazama: Kama hauna muda wa kutumia kwa shughuli hii kama sehemu ya somo, unaweza kutumia siku nyingine. Kwa kazi nyingine za tathmini, angalia kiambatanisho mwishoni mwa kitabu cha kiada hiki.

Tangazo na Habari za UsuliAlma 15:3–5. Mateso ya kimwili yanayosababishwa na matatizo ya kiroho

Wakati Zeezromu alikuwa anatubu dhambi zake, “aka-yachimba sana mawazo yake mpaka yakawa kidonda chenye maumivu makali” (Alma 15:3). Rais Boyd K. Packer wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alizungu-mzia uhalisi wa mateso ya kimwili ambayo yanawezwa kusababishwa na matatizo ya kiroho.

“Mimi [wakati mmoja] nilimuuliza daktari wa familia ni muda gani wake anaoutumia hasa kwa ajili ya kureke-bisha matatizo ya kimwili? Ana kliniki kubwa, baada ya kuwaza kwa muda akajibu, Sio zaidi ya asilimia 20. Muda uliobaki wote huwa naonekana hujishughulisha na matatizo ambayo kwa kiasi kikubwa yanaathiri uzima wa miili ya wagonjwa wangu lakini ambayo hayatoki mwilini.

"'Haya matatizo ya kimwili,' daktari alimalizia, hizi ni dalili tu za aina nyingine ya matatizo.'

"Katika vizazi vya hivi karibuni, moja baada ya mwi-ngine wa magonjwa makubwa yamekubali kutibika au kudhibitika. Baadhi yake makubwa sana bado yame-baki, lakini sasa tunaonekana tunaweza kufanya kitu kuhusu mengi kati yao.

"Kuna sehemu nyingine yetu isiyoonekana lakini halisi kabisa kama miili yetu. Hii sehemu yetu isiyoonekana imeelezwa kama ni mawazo, hisia, akili na mambo mengine mengi. Kwa nadra sana imeelezwa kama ni kiroho.

“Lakini kuna roho katika mtu; kuipuuzia ni kuupuuzia uhalisi. Kuna matatizo ya kiroho pia, na magonjwa ya kiroho ambayo yanaweza kusababishia mateso makali.

“Mwili na roho ya binadamu vimeunganishwa pa-moja”( The Balm of Gilead,” Ensign, Nov. 1977, 59).

Page 310: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

295

Somo la Mafunzo- NyumbaniAlma 11–16 (Kitengo cha 16)

Vifaa vya Matayarisho kwa Mwalimu wa Mafunzo - NyumbaniMuhtasari wa Masomo ya Mafunzo- Nyumbani Kila SikuMuhtasari ufuatao wa mafundisho na kanuni walizojifunza wanafunzi walipowanasoma Alma 11–16 (kitengo cha 16) haijakusudiwa kufundishwa kama sehemu ya somo lako. Somo ulilofundisha linazingatia machache tu ya mafundisho na kanuni hizi. Fuata mwongozo wa Roho Mtakatifu upofiki-ria mahitaji ya wanafunzi.

Siku ya 1 (Alma 11)Kupitia mfano wa Amuleki akibishana na Zeezromu, wana-funzi walijifunza kuwa tunapomtegemea Roho Mtakatifu, tunaweza kushinda majaribu. Katika kumfundisha Zeez-romu na watu wa Amoniha, Amuleki alisisitiza mafundisho yafuatayo kuhusu nafasi ya Mwokozi: Imani ya kweli katika Yesu Kristo ni mwanzo wa hatua za ukombozi kutoka katika dhambi zetu. Kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo, wote wata-fufuliwa na kuhukumiwa kulingana na kazi zao.

Siku ya 2 (Alma 12)Kama Amuleki, Alma alifundisha Zeezromu na watu wa Amoniha. Alielezea malengo ya Ibilisi na kutangaza kuwa Zeezromu alikua chini ya nguvu za Ibilisi. Alma na Amuleki walithibitisha kuwa Roho Mtakatifu anaweza kutusaidia ku-tambua vishawishi vya adui. Alma aliwasaidia watu kuelewa kuwa Bwana anaonyesha ukweli wa kiroho kwetu kulingana na usikivu wetu wa makini na bidii tunayo toa kwa maneno Yake. Na pia alifundisha kuhusu Hukumu ya Mwisho, akie-lezea kuwa tutawajibishwa mbele ya Mungu kwa maneno yetu, kazi na mawazo yetu. Akasisitiza kuwa ubinadamu ndio kipindi cha kujiandaa kukutana na Mungu.

Siku ya 3 (Alma 13)Alma alimkumbusha Zeezromu na watu kuwa Mungu aliwata-waza wenye ukuhani toka mwanzo wa dunia. Watu wanaofa-nya imani kubwa na kuchagua haki, wanapokea Ukuhani wa Melkizedeki ili kuwapeleka wengine kwa Mungu. Wanafunzi walijifunza kuhusu Melkizedeki na watu wake na kuakisi ukweli huu: tukiitikia kwa unyenyekevu mwaliko wa toba, Roho Mtakatifu atatuongoza kwenye pumziko la Bwana.

Siku ya 4 (Alma 14–16)Wanafunzi walisoma kuhusu wanawake na watoto wasio na hatia wakifa mikononi mwa watu waovu. Walitafakari juu ya kauli za kinabii zinazofundisha kuwa Mungu huruhusu wenye haki kuteseka kwenye mikono ya waovu ili hukumu yake iwe ya haki. Wanafunzi waliona katika maisha ya Alma na Amuleki kwamba tunapomwamini Bwana, Yeye hutu-imarisha wakati wa majaribio. Kama tutamuita kwa imani atatuimarisha kwenye majonzi yetu na kutuokoa kwenye njia Yake kwa wakati Wake.

UtanguliziAlma na Amuleki walipoanza kuwafundisha watu wa Amoniha walikumbana na upinzani. Baada ya kueleza baadhi ya kweli za milele watu wengi “walianza kutubu na kupekua maandiko” (Alma 14:1). Masimulizi katika Alma 11–16 yanafafanua toleo ambalo watu wako radhi kufanya kwa ajili ya ushuhuda wao wa ukweli. Sura hizi pia zinaonyesha ushahidi kuwa wakati waovu “wanapowafukuza wenye haki” Bwana atawapiga kwa njaa, na kwa maradhi, na kwa upanga” (Alma 10:23). Alma na Amuleki waliwatahadharisha watu wa Amoniha kwamba kama wata-shindwa kutubu, hukumu ya Mungu itakuja juu yao. Kupuuza mwito wa kutubu, watu wa Amoniha baadaye waliangamizwa na jeshi la Walamani.

Somo hili litalenga kwenye Alma 14–15. Kwa nyongeza, una-weza ukataka kufundisha au kutathimini ukweli kutoka kwenye sura zingine zilizopangiwa juma hili.

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 14–15Mungu huwabariki wale ambao wanaomwamini Yeye katika majonzi yaoFikiria kuanza somo la leo kwa kutaja matukio ya hivi sasa ambapo watu wasio na hatia wameteseka kwa sababu ya chaguo za wengine. Au unaweza kuwauliza wanafunzi kushiriki mifano kutoka kwenye maandiko juu ya watu walioteswa kwa sababu ya shuhuda zao za injili. Baada ya kujadili mifano micha-che waalike wanafunzi wachache kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka Alma 14:7–11na Alma 60:13.

Uliza: Ni sababu zipi zinatolewa kwenye aya hizi na kwa nini wenye haki wakati mwingine wanaruhusiwa kuteseka kwenye mikono ya waovu? (Ukweli mmoja wanafunzi walijifunza wakati wanasoma sehemu hii ya Alma 14 ni kwamba Bwana anaru-husu wenye haki wapate shida kwenye mikono ya waovu ili hukumu yake iwe ya haki. )

Eleza kuwa haki na neema ya Mungu inapita kifo ili kuwawajibi-sha wale waliotenda dhambi na kuotoa neema kwa wenye haki. Kisha shiriki maelezo yafuatayo ya Rais James E. Faust wa Urais wa kwanza:

“Mateso haya yote yanaweza kwa hakika kuwa si ya haki kama kila kitu kingeishia kwenye kifo, lakini sivyo. Maisha si kama igizo lenye sehemu moja. Yana sehemu tatu. Tulikuwa na tendo lililopita, tulikuwepo kabla ya duniani, na sasa tuna wakati uliopo, ambao ni maisha ya muda na tutakuwa na sehemu ijayo tutakaporudi kwa Mungu. . . .Tuliletwa katika maisha ya muda ili kutahiniwa na kujaribiwa (ona Ibrahimu 3:25]. . . .

“Mateso yetu ya awali na ya sasa hayawezi, kama Paulo alivyo-sema, ‘kufananishwa na utukufu ambao utafunuliwa kwetu’ [Warumi 8:18] katika milele. “Kwani baada ya taabu kubwa huja baraka. Kwa hiyo siku yaja ambayo ninyi mtavikwa utukufu

Page 311: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

296

SoMo la MafUnzo- nyUMbani

mkubwa’ [M&M 58:4]. Kwa hiyo mateso yana faida kwa maana ya kuwa yanasaidia kuingia katika ufalme wa selestia. . . .

“Si vile kuhusu kinachotutokea lakini ni jinsi tunavyokabiliana na yanayotutokea (“Where Do I Make My Stand?” Ensign au Liahona, Nov. 2004, 19–20).

Eleza kuwa mateso na majonzi yanatusaidia kupata kuinuliwa kwa kukomaza imani yetu. Kubaki mwaminifu wakati wa majaribio na matatizo unaonyesha imani dhabiti kwa Mungu na mipango Yake, hivyo kuimarisha imani yetu na uwezo wetu kuvumilia mpaka mwisho.

Uliza maswali yafuatayo:

• Ni vipi kuwa na ushuhuda wa mpango wa wokovu, ukiju-muisha maisha kabla na baada ya kuja duniani yanapunguza mateso tunayokumbana nayo katika maisha ya muda?

• Ukifikiria kile ulijifunza juma hili katika Alma 14–15, ni kwa njia zipi wenye haki wanabarikiwa kwenye majonzi yao?

• Wakati wa majonzi tunawezaje kuonyesha kuwa tunamwa-mini Mungu?

Acha wanafunzi walinganishe maswali ya Alma yaliyouliza katika Alma 14:26 na maswali Joseph Smith aliuliza katika Mafundisho na Maagano 121:3. Kisha uliza: kulingana na Alma 14:26, ni kwa jinsi gani Alma na Amuleki waliweza kuyashinda majonzi yao?

Elezea kuwa wakati Nabii Joseph Smith alipofungwa bila haki huko Missouri, aliuliza swali lililoandikwa katika Mafundisho na Maagano 121:3. Tofauti na Alma na Amuleki hakuoko-lewa muda huo huo kutoka gerezani. Tunaweza kujifunza nini kutokana na jibu la Mungu kwa ombi lake? (Ona D&C 121:7–9; 122:4–9.) Ukweli ufuatao umesisitizwa wiki hii kwa wanafunzi kwenye masomo yako kibinafsi: Kama tutamwita Bwana kwa imani, atatuimarisha na kwenye majonzi yetu na kutuo-koa kwa njia Yake na kwa wakati Wake.

Uliza maswali yafuatayo:

• Mungu amekusaidia vipi wakati umekumbana na majaribu?

• Ni nini hukusaidia kujiweka chini ya mapenzi Yake na kukubali wakati Wake?

Wasaidie wanafunzi kuelewa kwamba Zeezromu na Amuleki walimwamini Mungu wakati wa mateso na walizawadiwa kuli-ngana na mapenzi Yake na wakati Wake.

Agiza nusu ya darasa isome Alma 15:5–12 na kutambua taarifa kuhusu Zeezromu zinazoonyesha kukua kwa imani yake katika Bwana. Agiza ile nusu nyingine ijifunze Alma 15:16, 18 na ku-tambua taarifa kuhusu kile Amuleki alichojitolea ili kumtumikia Bwana.

Wahimize wanafunzi kumwamini Bwana na kukubali mapenzi Yake na wakati Wake pindi matatizo na majonzi yanapowajia. Wahakikishie kuwa Mungu atanyoosha nguvu na uwezo Wake kwa njia tofauti za kimiujiza na njia za kibinafsi.

Tathmini ya Umahiri wa Maandiko.Somo hili linaalamisha sehemu ya kati ya mtaala wa seminari wa Kitabu cha Mormoni. Ili kuimarisha juhudi za wanafunzi za kujifunza na kuelewa vifungu vya umahiri wa maandiko fikiria kuwapa jaribio la kupima jinsi walivyo na uzoefu wa vifungu 13 ambavyo wamejifunza mpaka sasa. Huu unaweza kuwa mfano rahisi wa jaribio la kusema au kimaandishi, ukiwapa wanafunzi wazo kutoka kwenye alamisho la kitabu na waache waandike marejeo, au inaweza kuwa marudio ya baadhi ya vifungu wali-yokariri. Urefu wa somo hili unaweza kuruhusu muda wa jaribio la kutolewa wiki hii, au unaweza kutangaza kuwa kutakuwa na jaribio linalokuja ili wanafunzi waweze kujiandaa.

Kitengo Kinachofuata (Alma 17–24)Wana wa Mosia wanaenda kuwahubiria watu waovu na wakali. Mwanzoni walipata majonzi mengi, lakini walipohubiri injili kwa Walamani miujiza inatokea. Tazama uaminifu wa Amoni kwa Mungu na mfalme unaleta wema mwingi.

Page 312: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

297

UtanguliziKatika maandalizi ya kufundisha injili kwa Walamani, wana wa Mosia waliutafuata mwongozo wa Bwana kwa kufunga na kusali. Mungu aliwafariji na kuwaa-hidi kuwa wangekuwa vyombo kwenye mikono Yake kwa ukombozi wa roho nyingi (Alma 17:11). Awali aliwaahidi wao, kupitia ufunuo kwa baba yao kuwa

atawaokoa kutoka kwenye mikono ya Walamani (Mosiah 28:7). Wakiimarishwa kwa ahadi za Bwana na kuamini kuwa kuna siku wataonana tena walitengena kwenda kushiriki injili katika maeneo tofauti. Amoni alikwenda nchi ya Ismaeli, ambapo alijiandaa kuwafu-ndisha watu kwa kumhudumia mfalme wao.

SOMO LA 81

alma 17

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 17:1–16Wana wa Mosia walipekua maandiko, kusali, na kufunga ili walijue neno la Mungu na kufundisha kwa nguvuKabla ya darasa, andika maelezo yasiyo kamilika ubaoni: Kitu kimoja muhimu zaidi unacho-weza kufanya ili kujiandaa kwa ajili ya wito wa kuhudumu [misheni] ni (Unaweza kurejelea hii muda kidogo baadaye katika somo hili.)Waulize wanafunzi kama wamekuwapo wakati ndugu au marafiki wamekuja nyumbani kutoka misheni baada ya kuhudumu kwa uaminifu. Waalike wanafunzi wachache kufafa-nua tabia za wamisionari zinazofanana na Yesu waliporejea. • Ni mabadiliko gani uliyaona kwao baada ya misheni? Unafikiri nini kilisababisha

mabadiliko haya?Eleza kwamba baada ya kufundisha injili kwa miaka 14 katika nchi ya Wanefi wana wa Mosia walikuwa wanarudi Zarahemla wakati walikutana na Alma. Ikiwa wanafunzi wana-hitaji tathmini fupi ya hadithi ya Alma na wana wa Mosia, uliza: • Kulikuwa na mahusianao gani kati ya Alma na wana wa Mosia? Kama wanafunzi wanahi-

taji msaada kujibu swali hili, fikiria kuwaambia wasome muhtasari wa sura wa Mosia 27.)Eleza kuwa wakati Alma alikuwa akihubiri toba na kuanzisha Kanisa miongoni mwa Wanefi katika nchi ya Zarahemla na nchi zingine, wana wa Mosia walikuwa wakihubiri injili kwa Walamani katika nchi ya Nefi. (Unaweza kutaka kurejelea alamisho la Kitabu cha Mormoni kama sehemu ya maelezo.) Majina ya wana wa Mosia yalikwa Amoni, na Haruni, na Om-neri, na Himni (ona Mosia 27:34). Alma 17–26 inasimulia baadhi ya matukio ya misheni.Mualike mwanafunzi asome Alma 17:1–2 kwa sauti.• Alma alijihisi vipi alipowaona rafiki zake tena? Kwa nini unafikiri alijihisi hivi?Elekeza nathari ya wanafunzi kwa maelezo yasiyokamilika uliyoandika ubaoni kabla ya darasa. Waalike wanafunzi kupendekeza njia za kamilisha kauli. Kisha shiriki pamoja nao jinsi Mzee David A. Bednar wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alivyokamilisha maelezo hayo. “Jambo moja muhimu unaloweza kufanya ili kujiandaa kwa ajili ya wito wa kuhu-dumu [misheni] ni kuwa mmisionari muda mrefu kabla ya kwenda misheni” (“Becoming a Missionary,” Ensign or Liahona, Nov. 2005, 45). Kamilisha kauli iliyopo kwenye ubao.Eleza kuwa njia moja tunayoweza kujua jinsi ya kuwa mmisionari ni kujifunza kuhusu huduma ya wamisionari waaminifu katika maandiko. Waalike wanafunzi wasome kimya Alma 17:2–4, wakitafuta sababu za wana wa Mosia kufanikiwa kuwaleta watu kwenye elimu ya ukweli. • Wana wa Mosia walifanya nini ambcho kiliwasaidia kuwa wamisionari wafanisi? (Majibu

yanaweza kujumuisha “ kuwa ” waliyapekua maandiko kwa bidii,” walisali na kufunga.)• Ni baraka gani walizipokea kwa sababu ya kujifunza, kufunga na kusali kwao? Wa-

nafunzi wanapojibu swali hili, wasaidie kutambua kanuni zifuatazo: Tunapopekua

Tathmini ya muktadhaTathimi ya taarifa ya kimuktadha inaweza kuongeza kina cha uelewa wa wanafunzi wa tukio au fundi-sho katika maandiko. Wakati unapowasaidia wanafunzi kutathmini kifaa kama hiki, wape marejeo mahususi ya ku-wasaidia kupata habari wanazohitaji.

Page 313: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

298

SoMo la 81

maandiko, kuomba, na kufunga, tunaweza kupokea Roho Mtakatifu na kufundi-sha kwa nguvu.)

Waambie wanafunzi wasome kauli ifuatayo ya Mzee Bednar, akisisitiza nini tunachoweza kufanya ili kuwa wamisionari:

"Unaweza kuongeza hamu yako ya kumtumikia Mungu (ona M&M 4:3), na unaweza kuanza kufikiri kama wamisionari wanavyofikiri, kusoma kile wamisionari wanachosoma, kuomba kama wamisionari wanavyoomba, na kuhisi kile wamisionari wanachohisi. Unaweza kuepuka shinikizo za kidunia ambalo husababisha Roho Mtakatifu kujiondoa, na unaweza kukua katika kujiamini katika kutambua na kuitikia na misukumo ya kiroho. Mstari juu ya

mstari na agizo juu ya agizo, hapa kidogo na pale kidogo, unaweza polepole kuwa mmisionari unayetumaini kuwa na mmisionari ambaye Mwokozi anamtarajia. "Maandalizi ninayoelezea si tu yanayoelekeza katika huduma yako ya umisionari kama mtu wa umri wa miaka 19 au 20 au 21. Unajiandaa kwa kazi za umisionari ya maisha yako yote. Sisi daima ni wamisionari” (“Becoming a Missionary, 46).Ili kuwasaidia wanafunzi kutumia kanuni zilizofundishwa na Mzee Bednar na katika Alma 17:2–4, waulize waandike katika daftari au shajara za kujifunza maandiko kuhusu kile watafanya ili kuwa wamisionari kabla ya kuitwa kuhudumu. Waalike wanafunzi wasome Alma 17:9 kimya, wakitambua kile wana wa Mosia na wenzao waliomba. Baada ya wanafunzi kutoa taarifa ya kile walichokipata, waombe wasome Alma 17:10–12, wakitafuta majibu ya Bwana kwa maombi yao. • Kwa nini unafikiri mioyo yao “ilikuwa na ujasiri” walipopokea jibu la Bwana kwa

maombi yao?• Alma 17:11 inajumuisha ahadi ya Bwana kuwa atawafanya wamisionari hawa kuwa vyo-

mbo mikononi Mwake. Hii inamaanisha nini kwako? Ni kwa njia gani tunaweza kuwa vyombo mikononi mwa Mungu?

• Bwana aliwaelekeza wamisionari hawa kuonyesha mifano mingi mizuri (Alma 17:11). Kwa nini unafikiri kuweka mfano mzuri ilikuwa sehemu muhimu ya kazi yao ya umisio-nari? Wanafunzi wanaposhiriki majibu yao, wasaidie kutambua kanuni ifuatayo: Wakati tunaweka mfano mzuri, Bwana anaweza kutufanya vyombo katika mikono Yake. Unaweza ukataka kuandika ukweli ufuatao ubaoni.)

• Ni nini baadhi ya vitu watu wanaweza kujifunza kuhusu injili wanapoona mifano yetu mizuri?

• Ni lini mifano mizuri ya wengine ilikusaidia?Shuhudia umuhimu wa kuweka mifano mizuri na kuwahimiza wanafunzi kuwa mifano mizuri kwa wale walio karibu nao. Kama unaweza kufikiria nyakati mahususi ambapo umewaona wanafunzi wakiweka mifano mizuri, unaweza kutaka kuwasifu wanafunzi kwa kile walichokifanya. Hata hivyo, usitumie sifa za jumla au zisizo dhahiri, ambazo zinaweza kuonekana kutokuwa za uaminifu.Waulize wanafunzi wasome Alma 17:13–16 kimya, wakifikiria kuhusu ugumu wa kufundi-sha Walamani wakati ule.• Kwa nini wana wa Mosia walikuwa radhi kupatwa na majonzi na kwenda miongoni

mwa Walamani? (Ona Alma 17:16 pia ona Mosia 28:1–3.)

Alma 17:17–39Amoni anakuwa mtumishi kwa Mfalme Lamoni na analinda zizi la wanyama la mfalmeFanya muhtasari wa Alma 17:18–20 kwa kuelezea kuwa kabla ya wamisionari hawa kute-ngana ili kuhubiri injili katika sehemu tofauti, Amoni aliwafundisha na kuwabariki. Kisha akaenda nchi inayoitwa Ismaeli. Alipoingia nchi hiyo, alitekwa na kupelekwa mbele ya mfalme. Waombe wanafunzi wawili wasome kwa zamu kwa sauti kutoka Alma 17:21–25.• Unafikiri ni nini muhimu kwa Amoni kumwambia mfalme “Mimi nitakuwa mtumishi

wako? (Alma 17:25).• Ni lini umeona huduma ikisababisha nafasi za kushiriki injili?

Page 314: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

299

alMa 17

Kwa ufupi fanya muhtasari wa Alma 17:26–27 kwa kueleza kwamba wakati Amoni alikuwa akichunga zizi la kondoo wa mfalme, kundi la Walamani lilitawanya lile zizi. Gawa darasa kwenye makundi ya wanafunzi watatu watatu. Andika marejeo ya maandiko yafuatayo ubaoni: Alma 17:28–32; Alma 17:33–35; Alma 17:36–39. Waulize wanafunzi kwenye kila kundi kugawanya vifungu hivi baina yao. Waulize wanafunzi wasome vifungu walivyopewa kimya wakitafuta majibu ya maswali yafuatayo. (Unaweza ukitaka kuandika maswali haya ubao.)• Nini kilitokea kwenye sehemu yako ya hadithi?• Hii iliwezaje kusaidia kuwatayarisha watu kupokea injili?• Amoni alionyesha sifa zipi?Vipe vikundi muda wa kujadili majibu yao. Kisha uliza:• Tunaweza kujifunza nini kutoka kwenye simulizi hii? (Wanafunzi wanaweza kushiriki

majibu tofauti. Kwa mafano wanaweza kusema kwamba kutokana na huduma, tuna-weza kawasaidia wengine kujiandaa kukubali injili au kwamba wakati tupo ka-tika huduma ya Bwana, tunaweza kuwa na ujasiri na kuwa na shangwe. Unaweza ukitaka kuwahamasisha wanafunzi kuandika kanuni hizi kwenye maandiko yao.)

Waalike wanafunzi kuandika kwenye shajara zao za kujifunza maandiko kuhusu kile wa-naweza kufanya kuweka mifano mizuri ya kuishi injili. Kwa wasichana, lengo hili linaweza kuwasaidia kukamilisha uzoefu wa ziada kwenye Maendeleo ya Kibinafsi chini ya Kazi Nzuri. Kwa makuhani, lengo hili linaweza kuwasaidia kujifunza na kutimiza majukumu yao kama ilivyoorodheshwa katika kijitabu cha Wajibu kwa Mungu chini ya Wajibu wa Ukuhani na Waalike Wote Kuja kwa Kristo.

Tangazo na Habari za UsuliAlma 17. Huduma ya umisionari kwa wote wavulana na wasichana.

Rais Thomas S. Monson aliwapa ushauri ufuatao wavulana na wasichana kuhusu wajibu wa kuhudumu misheni:

"Kwa wavulana wa Ukuhani wa Haruni na ninyi wavulana ambao mnakuwa wazee, mimi narudia kile manabii kwa muda mrefu wamefundisha — kwamba kila anayestahili, mvulana aliye na uwezo anapaswa kujiandaa kuhudumu misheni. Huduma ya umisionari ni wajibu wa ukuhani— sharti ambalo Bwana ana-tarajia kutoka kwetu ambao tumepewa mengi sana.

Wavulana, nawasihi mjitayarishe kwa huduma kama wamisionari. Jiwekeni wasafi na halisi na wastahiki kumwakilisha Bwana. Dumisheni afya na nguvu zenu. Jifunzeni maandiko. Pale ambapo inapatikana, shiriki katika seminari au chuo. Jizoeshe kitabu cha maelekezo ya umisionari Hubiri Injili Yangu.

Neno kwa nyinyi kina dada wadogo: ingawa hamna wajibu wa ukuhani kama walionao wavulana wa kuhudumia kama wamisionari wa muda kamili, ninyi pia mnafanya mchango wa thamani kama wamisionari na tunakaribisha huduma yenu. (As We Meet Together Again, Ensign au Liahona, Nov. 2010, 5–6).

Page 315: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

300

UtanguliziMfalme Lamoni alishangazwa na nguvu Amoni ali-zoonyesha katika kulinda mifugo ya mfalme. Mpaka akaamini kuwa Amoni ni yule Roho Mkuu. Amoni akayasoma mawazo ya mfalme kwa nguvu za Roho

Mtakatifu na Amoni akaanza kumfundisha injili. Mfalme Lamoni aliamini alichofundisha Amoni, aka-gundua kuhitajika kwa Mwokozi, akalilia neema ya Bwana na akajawa na Roho.

SOMO LA 82

alma 18

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 18:1–11Mfalme Lamoni anavutiwa na uaminifu wa AmoniTathimini ya haraka mwishoni mwa Alma 17 itawasaidia wanafunzi kuona muktadha kwenye Alma 18. Pia itawasaidia kuelewa jumbe katika Alma 18. Ili kutathimini Alma 17, waulize wa-nafunzi kama hoja zifuatazo ni kweli au uongo. Unaweza ukawaambia waandike majibu yao. 1. Kwa sababu mfalme Lamoni alifurahishwa na Amoni,alimpa mmoja wa binti zake awe

mkewe. (Kweli. Ona Alma 17:24.) 2. Amoni akasema anataka kuwa mtumishi wa mfalme. (Kweli Ona Alma 17:25.) 3. Amoni alihofia maisha yake pale kundi la Walamani lilipotawanya kundi la mifugo ya

mfalme. (Uongo. Ona Alma 17:28–30.) 4. Kwa nguvu kubwa, Amoni alipigana na Walamani na kuwakata mikono wale walioinua

rungu zao dhidi yake. (Kweli. Ona Alma 17:37–38.)Baada ya kuendesha zoezi hili, hakikisha kwamba wanafunzi wanajua majibu sahihi.Waulize wanafunzi kama wamewahi kupata woga au kujisikia kuwa na mapungufu au kama wamewahi kujisikia kazi waliopangiwa au jukumu lilikuwa ni gumu mno kwao kute-keleza. Waambie kwamba kwenye somo la leo, watajifunza kanuni zitakazowasaidia katika hali kama hizo.Gawa darasa nusu mbili. Ipangie nusu moja isome Alma 18:1–4 na nusu ingine isome Alma 18:8–11. Wakati wanasoma, acha wafikirie jinsi uaminifu wa Amoni ulimwandalia njia ya kumfundisha Lamoni na watu wake. Wakishapata muda wa kutosha wa kusoma, waulize maswali yafuatayo:• Ni mawazo gani mfalme na watumishi wake walikuwa nayo kuhusu utambulisho wa

Amoni?• Kulingana na Alma 18:2, 4, ni nini Lamoni alifikiri lilikuwa lengo la kuja kwa Amoni?

(Kuwaadhibu watu kwa makosa yao ya mauaji na kumzuia Lamoni asiue tena kikatili watumishi wake.)

• Kulingana na Alma 18:10, ni nini kilimvutia Lamoni licha ya nguvu za Amoni kutetea kundi la mifugo ya mfalme? (Unaweza ukawahimiza wanafunzi waweke alama maneno uaminifu and aminifu.)

Andika kauli ifuatayo isiyokamili ubaoni: Tunapowatumikia wengine kwa uaminifu, Waulize wanafunzi wafikirie jinsi watakavyoikamilisha sentensi hiyo wakati wanaendelea na mafunzo yao ya Alma 18.

Alma 18:12–43Wakati Amoni anafundisha mpango wa ukombozi,Lamoni anagundua anavyomhitaji MwokoziIl kuwasaidia wanafunzi kuelewa nguvu za mafundisho ya Amoni na mabadiliko makuu ambayo Mfalme Lamoni alianza kuhisi, onyesha Alma 18:12–35 kama igizo la wasomaji. Chagua wanafunzi wanne na wapangie kila mmija sehemu yake. Mmoja awe msomaji, na

Page 316: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

301

alMa 18

wengine watatu wasome maneno ya Amoni, Mfalme Lamoni na mwingine awe mtumishi wa mfalme. Fikiria kuwasaidia wanafunzi kuandaa kwa kuwapangia nafasi zao kabla, labda siku moja kabla ya darasa au kabla darasa halijaanza. Acha wanafunzi wanne wasome sehemu zao katika Alma 18:12–15. Waulize wanafunzi wafuatilie kwenye maandiko yao, wakitafuta huduma ya Amoni ilikuwa na athari gani kwa Lamoni. Baada ya aya ya 15 imesomwa, simamisha igizo la wasomaji na uwaulize wanafu-nzi watoe taarifa ya kile walichokipata. • Kwa nini unadhani Lamoni alikuwa kimya mbele za Amoni? (Kama ikibidi, wasaidie

wanafunzi kukumbuka kuwa Lamoni alipatwa na uoga kwa sababu ya mauaji aliyoyafanya na alikuwa na wasiwasi kuwa Amoni alikuwa ni Roho Kuu na amekuja kumwadhibu.)

Endelea na igizo la wasomaji kwa kuwaalika wahusika wasome sehemu zao kwenye Alma 18:16–21. Lihamasishe darasa kutafuta ushahidi kwamba nguvu za Mungu zilikuwa na Amoni. • Ni kwa vipi Roho wa Mungu alimsaidia Amoni kwenye hali hii?• Ni nini Lamoni alitaka kukijua kutoka kwa Amoni?• Katika sehemu hii kwenye maelezo, ni nini Lamoni alijua kuhusu Amoni? (Alijua kwa-

mba Amoni alifanya kazi kwa nguvu zisizo za kawaida na anaweza kusoma mawazo ya watu wengine.)

Warudishe wanafunzi kwenye maelezo yasiyokamilika uliyoyaandika ubaoni: Tunapowatu-mikia wengine kwa uaminifu, . . .• Kutokana na tulichojifunza leo kutoka Alma 17–18, utawezaje kukamilisha sentensi hii?

(Wanafunzi wanaweza wakajibu kwa njia tofauti. Ili kufanya muhtasari wa majibu yao, kamilisha maelezo ubaoni kama ifuatavyo: Tunapowatumikia wengine kwa uaminifu, tunaweza kuwasaidia kujiandaa kupokea ukweli wa injili )

Waalike washiriki wasome sehemu zao kwenyeAlma 18:22–32. Uliza darasa lifuatilie, litafuta ukweli mahususi ambao Amoni alimfundisha Lamoni. Unaweza ukataka kusha-uri kwamba wanafunzi watie alama kweli hizi katika maandiko yao. Kisha waulize watoe taarifa za kweli walizotambua. Andika majibu yao ubaoni.Alika wahusika wasome sehemu zao katika Alma 18:33–35. Uliza darasa litafute ni kwa jinsi gani Amoni alielezea uwezo wake wa kujua mawazo ya mfalme na uwezo wake wa kulinda mifugo ya mfalme. Baada ya wahusika katika igizo kumaliza kusoma, washukuru kwa msa-ada wao. Waalike wanafunzi watoe taarifa ya walichokipata. Ili kuwasaidia wanafunzi kuona jinsi Mungu alivyombariki Amoni aweze kumtumikia Lamoni na watu wake, uliza:• Ni baadhi ya vitu gani ambavyo Amoni aliweza kuvifanya ambavyo vilikuwa zaidi ya

uwezo wake wa kawaida?Sema kwamba wakati Amoni alipokuwa anamtumikia Mfalme Lamoni, alikuwa pia anam-tumikia Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Andika yafuatayo ubaoni: Tunapomtumikia Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo kwa uaminifu, . . .• Kulingana na ulichojifunza kutoka kwa mfano wa Amoni, ni kwa jinsi gani utaikamilisha

kauli hii? (Wanafunzi wanaweza wakajibu kwa nja tofauti. Ili kufanya muhtasari wa ma-jibu yao, kamilisha maelezo ubaoni kama ifuatavyo: Tunapomtumikia Baba wa Mbi-nguni na Yesu Kristo kwa uaminifu, uwezo wetu wa kufanya kazi Zao unaongezeka.)

• Ni kwa jinsi gani kanuni hii inatumika katika maisha ya mtu anayejisikia kuogopa au kuwa na mapungufu au anayejisikia kuwa alichopangiwa au jukumu alilopewa ni gumu sana?

• Wakati gani umejisikia kuwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wamekusaidia kufanya kazi Zao? (Unaweza ukataka kusema jinsi Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wameo-ngeza uwezo wako katika utumishi wako Kwao. Au unaweza ukashiriki mfano kutoka kwa maisha ya mtu mwingine.)

Ili kuwasaidia wanafunzi waitumie kanuni hii, andika maswali yafuatayo ubaoni: Waulize wanafunzi waandike majibu yao kwa moja ya maswali haya.

Ni kwa jinsi gani kanuni hii inaweza kukusaidia katika majukumu yako ya sasa na baadaye?Ni kwa jinsi unaweza kuwa mwaminifu zaidi ili uweze kuhisi Bwana anaongeza uwezo wako wa kufanya kazi Yake?

Eleza kwamba mwongozo wa Amoni wa kumfundisha Lamoni kwenye Alma 18:36–39 ni mpangilio unaotumiwa na wamisionari leo. Alifundisha kuhusu mpango wa ukombozi, akijumuisha uumbaji, kuanguka kwa Adamu na Hawa, na Upatanisho wa Yesu Kristo. Waulize wanafunzi watafakari maswali yafuatayo:

Waandae wanafunzi mapema kwa igizo la wasomajiKatika igizo, wahu-sika hawaigizi zaidi ya sehemu zao. Hata hivyo, wanatakiwa wajiandae kusoma sehemu zao kwa uhakika na kwa njia ya maana. Hakikisha wanaelewa sehemu zao na wana muda wa ku-tosha kujifunza sehemu zao. Unaweza ukataka kuwapangia sehemu zao mapema ili waweze kuzoea kwa maelezo na wafanye mazoezi ya kusoma sehemu zao.

Page 317: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

302

SoMo la 82

• Kwa nini unadhani kwamba ni muhimu kufundisha kuhusu Uumbaji na Kuanguka wakati tunafundisha kuhusu Upatanisho wa Yesu Kristo?

Mwalike mwanafunzi asome taarifa ifuatayo ya Mzee Russell M. Nelson wa Akidi ya wale Mitume Kumi na Wawili:“Kabla hatujaelewa Upatanisho wa Kristo, . . . tunatakiwa kwanza kuelewa Kuanguka kwa Adamu. Na kabla ya kuelewa Kuanguka kwa Adamu, tunatakiwa kwanza kuelewa Uumbaji. Hivi vitu vitatu vya muhimu vya mpango wa wokovu vinahusiana. . . .“. . . Uzima wa milele, uliwezeshwa na Upatanisho, ni lengo kuu la Uumbaji” (“The Atonement,”Ensign, Nov. 1996, 33, 35).Kama mafundisho haya matatu tayari hayapo ubaoni, yaongeze kwenye orodha uliyoia-ndika wakati wa igizo. Mwalike mwanafunzi asome Alma 18:36–39 kwa sauti. Uliza darasa lifuatilie, likitafuta vipengele vya Uumbaji, Kuanguka, na Upatanisho katika mafundisho ya Amoni kwa Lamoni. Acha watoe taarifa ya kile walichokipata.• Ni kwa jinsi gani kujifunza mafundisho ya Uumbaji, Kuanguka, na Upatanisho kumem-

saidia Lamoni kugundua kumhitaji kwake kwa Mwokozi?Waambie wanafunzi wasome Alma 18:40–43 kimya kimya na watambue kile Lamoni ali-kiomba kama jibu kwa mafundisho ya Amoni. Unaweza ukawahimiza wanafunzi waweke alama ombi la Lamoni.• Ni nini sala ya Lamoni ilionyesha kwamba alielewa kuhusu nafsi yake na watu wake?

(Alielewa kuwa walitenda dhambi na walihitaji msamaha.)• Ni nini tunaweza kujifunza kutoka kwa Lamoni kuhusu nini kinatokea tunapoelewa

kwamba tunamhitaji Mwokozi? (Wakati wanafunzi wanajibu swali hili, wasaidie wao kutambua kanuni zifuatazo: Tunapoelewa umuhimu wa Mwokozi kwetu, tutata-mani kutubu. Unaweza ukawaalika wanafunzi waandike kanuni hii katika maandiko yao karibu na Alma 18:40–41. Sema kwamba wakati uzoefu wetu wa kibinafsi wa toba unaweza kutofautiana, tunaweza sote kufuata mfano wa Mfalme Lamoni tukiomba kwa uaminifu neema za Mungu.)

Alika wanafunzi waandike majibu yao kwa maswali yafuatayo:• Ni nini unaweza kufanya kile kitakacho kukumbusha haja yako wa Mwokozi?

Tangazo na Habari za UsuliAlma 18:36–39. Kufundisha mpango wa wokovu

Wakati Amoni alipomfundisha Lamoni, “alianzia kwenye uumbaji wa dunia, halafu akafundisha kuhusu kuanguka kwa binadamu” (Alma 18:36). Hatimaye “alifafanua kwao [ mfalme na watumishi wake] mpa-ngo wa ukombozi” hasa kuhusu kuja kwa Kristo (Alma 18:39). Alikadhalika Haruni alifundisha mafundisho haya kwa baba ya Lamoni (ona Alma 22:12–14).

Mzee Bruce R. McConkie wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili aliita misingi hii ya mafundisho— Uumbaji, Kuanguko, na Upatanisho— nguzo tatu za milele na matukio makuu ambayo yameweza kutokea katika kweli za milele yote. Yeye alielezea:

"Kama tunaweza kupata uelewa wake, ndipo mpango wote wa milele wa vitu utaangukia katika sehemu yake, na tutakuwa katika nafasi ya kufanyia kazi wokovu wetu. 

"Haya matatu ndio misingi ambao juu yake mambo yote yapo. Bila moja wapo ya hivi, vitu vyote vitapo-teza maana yake na mipango na usanifu wa Uungu utakuwa bure (The Three Pillars of Eternity [Brigham

Young University devotional address, Feb. 17, 1981], 1, speeches. byu. edu).

Mzee Russel M.Nelson wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alielezea jinsi kila sehemu mojawapo ni muhimu katika mpango:

"Mpango ulihitaji Uumbaji, na hiyo pia ulihitaji Ku-anguka , na Upatanisho. Hizo ndizo sehemu tatu za msingi za mpango huu. Uumbaji wa sayari ya paradiso ulitoka kwa Mungu. Maisha ya muda na kifo vilikuja duniani kutokana na Kuanguka kwa Adamu. Kutokufa na uwezekano wa kuishi milele kuliletwa na Upatani-sho wa Yesu Kristo. Uumbaji, Kuanguka na Upatanisho vilipangwa kabla ya kazi yenyewe ya Uumbaji haijaa-nza” (“The Creation,” Ensign, May 2000, 84).

Kwa nyongeza kufundisha mafundisho yaleyale, Amoni na Haruni walitumia njia sawa katika mafundisho yao. Walifundisha kwa urahisi kwa njia ambayo wasikilizaji wao waliweza kuelewa (ona Alma 18:24–30; 22:7–11). Walifundisha kutoka kwenye maandiko (ona Alma 18:36–39; 22:12–14). Mafundisho yao yaliwapelekea wengine kusali (ona Alma 18:40–41; 22:15–18).

Page 318: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

303

UtanguliziMfalme Lamoni alipata mabadiliko ya moyo, yaliyo-sababisha uongofu wa mke wake na wengi wa watu wake. Amoni na Mfalme Lamoni ndipo walisafiri kwenda Midoni kuwafungua ndugu za Amoni waliofu-ngwa. Njiani walikutana na baba yake Lamoni, mfalme juu ya nchi yote. Mfalme alishangazwa kwa maneno

ya Lamoni na Amoni, kwa nguvu ya Amoni na upendo Amoni kwa Lamoni. Moyo wake ulilainishwa, na ali-wahakikishiwa kwamba ndugu za Amoni wataachiwa kutoka gerezani. Alionyesha hamu ya kujifunza kuhusu maneno aliyoyasikia kutoka kwa mwanae na Amoni.

SOMO LA 83

alma 19–20

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 19Mfalme Lamoni na wengi wa watu wake walitubu na kubatizwaUliza wanafunzi • Unapoangusha jiwe kwenye bwawa la maji nini kinatokea kwenye maji?Wakati wanafunzi wanaeleza matokeo ya kuangusha jiwe kwenye maji chora mchoro ufuatao kwenye ubao, ukiacha maneno.

Andika yafuatayo kwenye ubao:Kwa kushiriki shuhuda zetu na kuweka mifano ya haki, tunaweza . . .

Waalike wanafunzi wakumbuke maelezo haya muda wote wa somo na wafikirie jinsi wata-vyoweza kuyakamilisha. • Ni kwa jinsi gani matendo ya mtu yanaweza kuwa kama jiwe lililoangushwa kwenye

maji? (Wasaidie wanafunzi waone kwamba, kama mawimbi yanavyotanuka kutoka kwe-nye jiwe, watu wengine wanaweza kuvutiwa na matendo yetu.)

Andika Amoni kwenye duara ya kwanza ya mchoro.• Ni nani Amoni alimfundisha kwanza? (Kama wanafunzi watahitaji msaada kujibu swali

hili, unaweza kupendekeza kuwa wapitie muhtasari ya sura katika Alma 18. Andika Mfalme Lamoni kwenye duara ya pili ya mchoro.)

Fanya muhtasari wa Alma 18:40–43 na 19:1–5 kwa kueleza kwamba wakati mfalme Lamoni alipomsikiliza Amoni, aligundua dhambi zake na haja yake ya Mwokozi. Alimlilia Bwana na kuomba msamaha na kisha alianguka arithini. Akiamini kuwa alikuwa amekufa, watumishi wake walimbeba mpaka kwa mke wake na kumlaza katika kitanda. Siku mbili mchana na usiku baadaye wafanyakazi walikuwa karibu kuchukua mwili wake kuweka kwenye jengo la wafu ndipo malkia akasema kuwa alitaka kuongea na Amoni. Hakufikiria kuwa Lamoni alikuwa amekufa, na alitaka Amoni aende kwake.)Waulize wanafunzi wasome Alma 19:6 kimya, na wakitafuta kishazi ambacho wanahisi kinaelezea uzoefu wa Lamoni hasa vizuri zaidi. Waombe wanafunzi wachache wasome vishazi walivyovichagua. Waulize kwa nini wamechagua vishazi hivyo?Kwenye mchoro, andika malkia kwenye duara inayofuata. Acha wanafunzi wapekue Alma 19:7{en }11 ili kuona jinsi uzoefu huu ulivyomvutia Malkia.

amoni Mfalme lamoni

Malkia Watumishi wa lamoni

abishi Walamani

wengine wengi

Page 319: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

304

SoMo la 83

• Nini tunaweza kujifunza kuhusu malkia kutoka kwenye mistari hii? (Majibu yanaweza yakajumuisha kuwa alimpenda mume wake, kwamba alimwamini Amoni, na kwamba alikuwa na imani kubwa.)

Waulize wanafunzi wasome Alma 19:12–14 kwa sauti. Waalike wanafunzi wengine kufuati-lia, wakiwa usikivu maalum kwa onyesho la Lamoni la imani. • Ni kweli gani alizojifunza Lamoni siku mbili zilikuwa zimepita? • Lamoni, malkia, na Amoni walikuwa wamejazwa na nguvu za Roho na wamejazwa na

shangwe Ni lini umehisi hamasa za Roho kwa njia ya nguvu kuu? Ni lini umehisi sha-ngwe kuu?

Andika watumishi wa Lamoni kwenye duara inayofuata katika mchoro. Mwalike mwana-funzi asome Alma19:15–16 kwa sauti. Uliza darasa litafute ushahidi kwamba watumishi hawa walikuwa wanamgeukia Mungu. • Ni maneno na vishazi gani vinavyoonyesha kwamba watumishi walikuwa wanamge-

ukia Mungu?Andika Abishi kwenye duara inayofuata. Mwalike mwanafunzi asome Alma 19:17 kwa sauti. Alika darasa litafute ni kwa jinsi gani Abishi alishawishiwa na matukio haya.• Abishi alifanya nini? Alitumaini nini kingetokea kwa sababu ya matendo yake?Fikiria kuwapa wanafunzi nafasi ya kufanya muhtasari Alma 19:18–28. Wape muda ku-soma mistari hii kimya. Kisha mwombe mmoja ajitolee kusimulia hadithi hii kwa maneno yake. Waruhusu wanafunzi wengine wasaidie. Inapohitajika wasaidie kujumuisha taarifa ifuatayo: baada ya kusikia habari kutoka kwa Abishi watu walikusanyika kwenye nyumba ya mfalme. Walipomwona Amoni, mfalme, malkia, na watumishi wamepoteza fahamu, mabishano makubwa yalizuka miongoni mwao. Mtu mmoja alijaribu kumwua Amoni lakini alikufa kwenye jaribio hilo. Wengine walisema kuwa Amoni alikuwa ni yule Roho Mkuu na wengine walisema alikuwa ni jinamizi. Abishi alipoona mabishano yote ambayo yamesababishwa kwa yeye kukusanya watu pamoja alihuzunika sana. Wafanye wanafunzi wafikirie nini wangeweza kufanya wangekuwa kwenye hali ya Abishi. Kisha muulize mwanafunzi asome Alma 19:29 kwa sauti.• Ni kwa jinsi gani matendo ya Abishi yalionyesha nguvu ya ushuhuda wake? Ni kwa jinsi

gani malkia alidhihirisha kuwa alikuwa amepokea ushuhuda?Soma Alma 19:30–36 kwa sauti. Waulize wanafunzi kufuata na kufikiria athari ya ushu-huda wa Amoni na mfano wa Amoni kwa wengine.Andika Walamani wengine wengi kwenye duara ya mwisho katika mchoro.Waulize wanafunzi kukamilisha kauli ambayo uliandika ubaoni mwanzoni mwa darasa. Kanuni moja ambayo wanaweza kueleza ni kwamba kwa kushiriki shuhuda zetu na kuweka mifano ya haki, tunaweza kuwasaidia wengine kumgeukia Bwana.• Ni lini mfano wa mtu fulani au ushuhuda ulikuvutia kwa wema ? Waalike wanafunzi kutafakari ni vipi shuhuda zao na mifano yao inaweza kuwaathiri wa-nafamilia, marafiki, na jamii yao. Waulize waandike jibu kwa swali lifuatalo kwenye daftari au shajara ya kujifunza maandiko: • Unaweza kufanya nini leo kinachoweza kuwa na ushawishi mzuri kwa watu walio ka-

ribu nawe?Wahimize wanafunzi waruhusu shuhuda zao na mifano ya haki kushawishi wengine, kama jiwe lifanyavyo viwimbi katika bwawa. Waambie wanafunzi kuwa kwenye somo linalokuja (Somo la 85) unaweza ukawataka watoe taarifa za jitihada zao.

Alma 20Baba wa mfalme Lamoni atamani kujifunza kuhusu injili na anaanza kuona mabadiliko ya moyoWaalike wanafunzi kufikiri kuhusu wakati ambao walihisi kuwa wamefanyiwa visivyo au kuonewa. Eleza kuwa Amoni na Lamoni walikumbana na hali ambayo walitendewa visivyo. Sema kwamba tunaweza kujifunza masomo muhimu kutoka kwenye majibu yao kwa njia ambayo walitendewa.

Page 320: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

305

alMa 19 –20

Kuwasaidia wanafunzi wawe na mazoea na simulizi katika Alma 20, fupisha Alma 20:1–7 kama ifuatavyo: Lamoni alitaka kumchukua Amoni akutane na Baba yake ambaye alikuwa Mfalme wa nchi yote. Bwana alifunua kwa Amoni kwamba Amoni asiende kwa sababu baba yake Lamoni atajaribu kumuua. Bwana alifunua pia kwamba kaka yake Amoni, Haruni na wafuasi wawili walikuwa gerezani kwenye nchi ya Midoni. Amoni alitaka kuwaweka huru ndugu zake. Kusikia kwamba Amoni alijifunza mambo haya kwa ufunuo , Lamoni alienda kumsaidia Amoni kuwaweka huru kaka zake Mbele ya darasa, nakili chati ifuatao kwenye ubao au kwenye kitini kwa kila mwanafunzi.

1. alma 20:8–13 ni hisia zipi ungeweza kuwa nazo kama ungekuwa katika hali ya amoni na mtu fulani anakutuhumu kuwa wewe ni mwongo na jambazi?

2. alma 20:14–16 ni masomo gani tunaweza kujifunza kutoka majibu ya lamoni kwa baba yake?

3. alma 20:17–25 Wakati baba yake lamoni alipoona kuwa amoni angemuua, alimpa nini amoni? amoni aliomba nini badala yake?

4. alma 20:26–27 ni kwa jinsi gani upendo wa amoni kwa lamoni ulimshawishi baba yake lamoni? Kwa njia zipi maneno ya amoni na lamoni yalimshawishi baba yake lamoni?

Wapange wanafunzi wafanye kazi katika majozi. Katika majozi haya, acha wasome aya zi-lizoorodheshwa katika safu 1–2 na kujadili majibu yanayoambatana na maswali. Wahimize wao kujiandaa ili kushiriki majibu yao na darasa zima. Baada ya wanafunzi kujadili safu 1–2 katika jozi, waulize wachache wao watoe taarifa ya kile walichojifunza. Kisha uliza:• Tunaweza kujifunza kanuni gani kutoka kwa mistari hii? Wanafunzi wanaweza kushiriki

majibu kadha, lakini wasaidie kutambue kanuni zifuatazo: Tunaweza kutoa shuhuda zetu kwa maneno na mfano hata kama wengine wanajaribu kutushawishi tufanye makosa. Unaweza kutaka kupendekeza kuwa waandike kanuni hii karibu na Alma 20:15.)

Waalike wenzi wajifunze aya zilizoorodheshwa katika mistari 3–4 na kujadili maswali yanayoambatana nayo. Waulize watoe taarifa ya kile walichogundua. Kisha uliza:• Tunaweza kujifunza kanuni zipi kutoka kwenye aya hizi? (Ingawa wanafunzi wanaweza

kushiriki aina tofauti za kanuni, hakikisha yafuatayo ni wazi: Tunapoonyesha upendo na kufundisha ukweli, tunaweza kuwasaidia wengine kupunguza ugumu wa mioyo yao na kuwa wapokeaji wa injili. Unaweza kutaka kuwahimiza wanafunzi kuandika kanuni hizi karibu na Alma 20:26–27.)

Waalike wanafunzi kushiriki uzoefu waliowahi kuwa nao ambao unaonyesha ukweli wa mojawapo wa kanuni walizogundua katika Alma 20. Unaweza pia ukataka kushiriki uzoefu wako mwenyewe.Hitimisha kwa kuhimiza wanafunzi watafute uongozi wa Roho kuhusu ni kwa jinsi gani wanaweza kutumia hizi kanuni mbili katika maisha yao.

Page 321: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

306

UtanguliziKaka yake Amoni, Haruni alifundisha Waamaleki lakini walikataa ujumbe wake kuhusu Upatanisho wa Yesu Kristo. Kisha alihubiri huko Midoni ambako yeye na baadhi ya wenziwe hatimaye walifungwa. Walibaki waaminifu wakati wa kipindi chao cha mateso, na waliendelea katika misheni yao kushiriki injili baada ya

Amoni na mfalme Lamoni kuwawezesha kuachiliwa. Baada ya baba yake Lamoni kuandaliwa kupitia mfano wa Amoni, alijifunza kutoka kwa Haruni jinsi ya “kuza-liwa na Mungu” (Alma 22:15). Babake Lamoni alijifunza kwamba kwa kutubu dhambi zake angekuja kumjua Mungu na hatimaye kupokea uzima wa milele.

SOMO LA 84

alma 21–22

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 21Haruni na ndugu zake walihubiri injili licha ya majaribio na kifungoWaulize wanafunzi kama walishawahi kuhisi kwamba walikuwa wanajitahidi kwa uwezo wao kufuata amri na hata hivyo wakakabiliwa na changamoto au kuhisi kukatishwa tamaa. Waalike wanafunzi kutaja baadhi ya hali ambazo watu wanaweza kuhisi hivyo.Eleza kuwa wakati Amoni alikuwa amefanikiwa kumfundisha mfalme Lamoni na watu wake, Haruni na wenzake walipambana na matatizo makali kwenye sehemu mbalimbali za nchi. Wakati wanafunzi wanajifunza mfano wa haruni na wenzake, wahimize kutafuta masomo ambayo yanayoweza kuwasaidia wakati wanapopatwa na changamoto au kuhisi kukatishwa tamaa.Andika marejeo yafuatayo ubaoni: Alma 21:1–4; Alma 21:5–8; Alma 21:9–11; Alma 21:12–15; na Alma 20:29–30. Gawa darasa katika makundi matano. Pangia kila kundi kifungu kimoja kati ya vilivyoandikwa kwenye ubao. Waulize wanafunzi kuandaa kutoa muhtasari wa vi-fungu walivyopangiwa na kuelezea shida zozote Haruni na wenzake walivumilia. Baada ya dakika chache, waalike wanafunzi kutoka kwenye kila kundi kushiriki kile walichokipata.• Haruni na wenziwe waliwezaje kuvumilia mateso yao? (Ona Alma 20:29; 21:9, 12, 15.)• Moja ya majaribio ambayo Haruni alipata yalikuwa upinzani kutoka kwa Waamaleki ali-

pokuwa akiwafundisha. (ona Alma 21:5–10). Tunaweza kufanya nini kama mtu anataka kubishana na sisi kuhusu dini au kushindana na imani zetu?

Wakumbushe wanafunzi swali hilo mwanzoni mwa somo hili. Haruni na nduguze wa-lifanya kazi kwa bidii jinsi Mungu alivyowaongoza, lakini bado walikutana na matatizo. Waulize wanafunzi kufikiria kwa ukimya jinsi wangehisi kama wangekumbana na kile Ha-runi na wenzake walikumbana nacho. Wanaweza kutaka kufanya nini baada ya kuteseka na kufungwa kwa ajili ya injili mbali na nyumbani? Unaweza kuwauliza kama watataka kurudi nyumbani.Andika ubaoni kanuni ifuatayo: kama kwa imani tutajizatiti kupitia mateso, Bwana atatusaidia kufanya kazi Yake. Alika mwanafunzi asome Alma 21:16–17 kwa sauti. Uliza wengine wa darasa kufuatilia wakitambua, jinsi Bwana alivyowasaidia Haruni na nduguze kufanya kazi Yake. Waalike wanafunzi kutoa taarifa ya kile walichotambua. Ili kuwasaidia wanafunzi kutumia kanuni zilizoandikwa kwenye ubao, wauulize ni aina gani ya kazi ambazo Mungu anazo kwa ajili yao wazifanye sasa na changamoto gani wa-nazoweza kuzipata wanapojaribu kutimiza kazi hizo. (Unaweza kutaka kuonyesha kuwa pamoja na kujumuisha na kazi za umisionari, wanafunzi wanaweza kushiriki kazi za Mu-ngu kwa kuhudhuria mikutano ya Kanisa, kutimiza miito na kupangiwa kazi, kuhudumia wengine na kuimarisha shuhuda zao, na kuwa zaidi kama Yesu.)Waalike wanafunzi kushiriki jinsi wameweza kujua kwamba kanuni uliyoandika ubaoni ni kweli. Unaweza kutaka kushiriki ushuhuda wako jinsi ambavyo Bwana anatusaidia kutimiza kazi Yake wakati kwa uaminifu tunajizatiti kapitia majaribio. Waulize wanafunzi

Wasaidie wanafunzi kutumia mafundisho na kanuniKwa maombi amua jinsi ya kuwasaidia wanafunzi kutambua na kutumia mafundisho na kanuni katika somo kulingana na mazingira yao binafsi.

Page 322: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

307

alMa 21–22

mifano ya nyakati za siku za usoni ambapo wanafikiri wanaweza kuhitaji kujizatiti kupitia majaribio wanapofanya kazi za Bwana. Fanya muhtasari Alma 21:18–23 kwa kuelezea kwamba baada ya kusaida kumtoa Haruni na nduguze kutoka gerezani, Amoni na Lamoni walirudi kwenye nchi ya Ismaeli ambako waliendelea kuhubiri Injili. Lamoni aliruhusu uhuru wa kidini kwa watu wake.

Alma 22Haruni afundisha injili kwa baba yake Lamoni ambaye aliamini na alizaliwa upya kwa Mungu Andika maswali yafuatayo kwenye ubao:

Kwa nini unataka kupokea uzima wa milele?Ungekuwa radhi kuacha nini ili kupokea uzima wa milele?

Eleza kuwa “Uzima wa milele au kuinuliwa, ni kurithi sehemu kwenye daraja ya juu zaidi ya ufalme wa selestia ambapo tutaishi kwenye uwepo wa Mungu na kuendelea kama familia (ona D&C 131:1–4). Karama hii inawezeshwa kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo (True to the Faith: A Gospel Reference [2004], 52). Waambie wanafunzi kwa kifupi kwa nini unataka kupokea uzima wa milele. Unapofanya hivyo, unaweza kuonyesha picha ya fami-lia yako na picha ya Mwokozi. Kisha waulize wanafunzi kutafakari maswali yaliyo ubaoni wanapojifunza Alma 22 pamoja.Mualike mwanafunzi asome Alma 22:1 kwa sauti.• Unakumbuka nini kuhusu baba yake Lamoni kutoka kwenye somo lililopita? (Unaweza

kutaka kumwaalika mwanafunzi afanye muhtasari Alma 20.)• Kulingana na Alma 20:27, baba yake Lamoni alimwuliza Amoni kufanya nini?

(Kumfundisha)Fanya muhtasari Alma 22:2–3 kwa kuelezea kuwa hata ingawa baba yake Lamoni alitaka kumuona Amoni na kufundishwa naye, alikuwa anatamani sana kujifunza wakati Haruni alipokuja kwake badala yake. Mualike mwanafunzi kusoma Alma 22:5–6 kwa sauti. Uliza darasa lifuatilie, likitafuta kile baba yake Mfalme Lamoni alitaka kujua. Watake wao watoe taarifa ya kile wanachokipata. Gawa darasa katika makundi madogo. Yaalike makundi yasome Alma 22:7–14 pamoja na yatayarishe orodha ya mafundisho ambayo Haruni alifundisha kwa baba yake Lamoni. (Kwa mfano, wanaweza wakataja kuwa alifundisha kuhusu Uumbaji, Kuanguka na Upata-nisho.) Baada ya makundi kutayarisha orodha zao, waulize wanafunzi kushiriki na darasa orodha ya mafundisho ambayo kundi lao limeunda. Unaweza ukataka kuwauliza wanafu-nzi kuandika orodha hiyo ubaoni. Kisha alika wanafunzi wengine waandike mafundisho mengine ya ziada ambayo makundi yao yaliorodhesha.• Mafundisho haya yanajibu vipi swali la mfalme katika Alma 22:6?Waalike wanafunzi kupekua Alma 22:15 kimya, wakitafuta kile baba ya mfalme Lamoni alikuwa yuko radhi kuacha ili apate kupokea furaha na uzima wa milele.• Ni mawazo gani uliyonayo unapofikiria kile mfalme alikuwa radhi kukiacha?Sisitiza kwamba ingawa Mfalme alikuwa yu radhi kuacha vyote alivyokuwanavyo, Haruni alimfundisha kuhusu toleo kubwa ambalo alitakiwa kulifanya. Mwalike mwanafunzi asome Alma 22:16 kwa sauti. Uliza darasa lisikilize kile Haruni alisema mfalme alitakiwa kukifanya. • Ni nini Aaron alisema mfalme alitakiwa kukifanya? (Kutubu dhambi zake na kuomba

kwa Mungu kwa imani.) Mwalike mwanafunzi asome Alma 22:17–18 kwa sauti. Uliza darasa lifuatilie, likitafuta jibu la Mfalme kwa maagizo ya Haruni.• Mfalme alidhihirisha vipi hamu yake ya kupata uzima wa milele?• Unafikiri inamaanisha nini “kuacha” dhambi zetu? Kwa nini unadhani ni muhimu ku-

tubu dhambi zetu zote, wala si baadhi ya dhambi? (Wasaidie wanafunzi kuelewa kwamba inachukua muda kwa mtu kutubu dhambi zake zote.)

• Tunaweza kujifunza nini kutoka kwa baba yake mfalme Lamoni kuhusu kujiandaa kwa ajili ya Uzima wa milele? (Ingawa wanafunzi watatumia maneno tofauti, hakikisha

Page 323: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

308

SoMo la 84

wanaelewa ukweli ufuatao: Ni sharti tuwe radhi kuacha dhambi zetu zote ili kujia-ndaa kwa Uzima wa milele. Unaweza kutaka kupendekeza kuwa wanafunzi waweke alama kishazi “nitaacha dhambi zangu zote ili nikujue wewe,” katika Alma 22:18.)

Waulize wanafunzi wasome kwa sauti maneno yafuatayo ya Mzee Dallin H. Oaks wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili.

“Injili ya Yesu Kristo inatupa changamoto ya kubadilika” ‘Tubu’ ni ujumbe wa mara kwa mara zaidi, na kutubu kunamaanisha kuacha tabia zetu zote—za kibinafsi, za kifamilia, kikabila na kitaifa—ambazo ni kinyume na amri za Mungu. Lengo la injili ni kubadilisha viumbe wa kawaida kuwa raia wa kiselestia, na hiyo inahitaji mabadiliko” (“Repentance and Change,” Ensign au Liahona, Nov. 2003, 37).

Sisitiza kuwa baadhi ya watu hushangaa kama wanaweza kweli kutubu na kubadilika. We-ngine wanajiuliza kama Bwana atawasamehe. Kuwasaidia wanafunzi ambao wana shaka juu ya haya, soma maelezo yafuatayo ya Dada Elaine S. Dalton, Rais Mkuu wa Wasichana:“Je! Una kitu fulani katika maisha yako ambacho unahitaji kubadili? Unaweza kufanya hi-vyo. Unaweza kutubu kwa sababu ya dhabihu ya upatanisho ya Mwokozi isiyo na mwisho. Alifanya uwezekano kwangu mimi na wewe kubadilika, na kuwa wa asili na wasafi tena na kuwa kama Yeye. Na ameahidi kuwa tukifanya hivyo, hatakumbuka dhambi zetu na ma-kosa yetu tena,” (“Now Is the Time to Arise and Shine!” Ensign au Liahona, Mei 2012, 124).Eleza kwamba tukiwa na imani na kutubu dhambi zetu, tunakuwa tunastahili kupokea ma-agizo na maagano ya ukuhani ambayo hutusaidia kujiandaa kwa ajili ya uzima wa milele. Waalike wanafunzi waandike kwenye daftari au shajara za kujifunza maandiko majibu yao ya swali lifuatalo. (Ukitaka unaweza kuliandika swali ubaoni au kulisoma taratibu ili wanafunzi waweze kuliandika.) • Kutoka kwa kile ulichojifunza kuhusu kinachohitajika ili kupokea uzima wa milele, una-

hisi ni nini Bwana atakuambia ufanye leo ili uweze kuwa karibu Naye?Wakati wanafunzi wameshapata muda wa kutosha kutafakari na kuandika, uliza:• Ni ushahidi gani unaouona kuwa mfalme alikuwa ameongolewa kwa Bwana? (Wakumbu-

she wanafunzi kuwa mfalme alibadilika kutoka kutaka kumuua mwanawe mwenyewe na kuwa tayari kuacha ufalme wake wote na dhambi zake zote ili kuzaliwa tena na Mungu.)

Fanya muhtasari Alma 22:19–21 kwa kuelezea kuwa baada ya mfalme kushindwa na nguvu za Roho, watumishi wake walikimbia na kwenda kumwambia malkia yaliyotokea. Alikasirika na kuwaamuru watumishi wawauwe Haruni na ndugu zake. Kwa kuogopa nguvu za wamisionari Wanefi, watumishi walikataa. Malkia pia aliogopa lakini alikuwa na lengo la kuhakikisha kwamba Wanefi wanauawa. Akawaamuru watumishi waende na kuwaleta watu wa kuwaua Haruni na wenzi wake.Waulize wanafunzi wasome Alma 22:22–26 kimya,wakitafuta matendo ambayo Haruni na mfalme walifanya ili malkia na wengine waweze pia kuongoka na wapate furaha. Hitimi-sha kwa kushiriki ushuhuda wako wa toba na baraka za kubadilishwa kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo.

Tathmini ya Umahiri wa MaandikoVijana wanaweza kujifunza kutumia maandiko ili kufundisha kweli za injili. Gawa wanafu-nzi katika majozi, na ualike kila jozi kutayarisha wasilisho la dakika moja au mbili ambalo watafundisha mafundisho ya msingi ambayo utawapangia. Uliza watumie angalau kifungu kimoja cha umahiri wa maandiko katika kufundisha mafunzo haya. Waulize pia wafikirie kutumia maelezo, mifano, uzoefu na ushuhuda katika mafundisho yao. Wanafunzi wote katika kila jozi wanapaswa kushiriki katika wasilisho hili. Baada ya muda wa kutosha wa kujiandaa, waulize mawili au matatu ya majozi kufundisha darasa. Fikiria kuwauliza majozi mengine yajiandae kutoa mawasilisho yao katika ibada zijazo au baada ya somo fupi. Tazama: Kama hauna muda kwa ajili ya shughuli hii kama sehemu ya somo hili, unaweza ukaitumia siku nyingine. Kwa shughuli zingine za tathmini, angalia maelezo ya ziada katika mwisho wa kitabu cha kiada hiki.

Page 324: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

309

UtanguliziKufuatia uongofu wake, mfalme wa Walamani akata-ngaza uhuru wa dini miongoni mwa watu wake. Ta-ngazo hili liliwaruhusu Haruni na ndugu zake kuhubiri injili na kuanzisha makanisa katika miji ya Walamani. Maelfu ya Walamani waliongoka na hawakuanguka kamwe. Walamani hawa walioongoka waliweka agano kuweka chini silaha zao za vita, na walijitofautisha na wale ambao hawakuongoka kwa kujiita Anti- Nefi- Lehi. Walipovamiwa na Walamani wasio waongofu, baadhi

ya Anti- Nefi- Lehi walitoa dhabihu maisha yao ili kutu-nza agano lao.

Tazama: Katika somo la 83, unaweza kuwa uliwahi-miza wanafunzi waruhusu shuhuda na mifano yao ya haki kuwahamasisha wengine, kama jiwe linavyofanya mawimbi kwenye bwawa. Kama ulifanya hivyo, fikiria kuanza somo hili kwa kuwataka wanafunzi watoe taarifa juu ya juhudi zao.

SOMO LA 85

alma 23–24

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 23Maelfu ya Walamani waongolewa kwa BwanaJuu ya ubao, chora picha ya watu wawili (sanamu rahisi za vifimbo zitatosha). Soma mae-lezo yafuatayo ya Mzee Richard G. Scott wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili: Uliza darasa lisikilize maelezo ya Mzee Scott ya aina mbili za watu.

“Kila mmoja wetu ameona jinsi baadhi ya watu wanavyopitia kwenye maisha wakitenda mambo mema kila mara. Wanaonekana kuwa wenye furaha, hata wachangamfu kuhusu maisha. Wakati chaguo ngumu zinata-kiwa zifanywe, wanaonekana bila kubadilika kufanya zilizo sahihi, hata kama kulikuwa na vivutio mbadala mbele yao. Tunajua kwamba wako chini ya majaribu, na lakini hawaonekani kuwa wazi kwa hilo. Hivyo hivyo, tumeona

jinsi wengine hawana ujasiri katika maamuzi wanayoyafanya. Katika mazingira ya kiroho yenye nguvu, wanaamua kufanya mema, kubadilisha mfumo wao wa maisha, kuacha tabia mbaya za kudhoofisha. Wako waaminifu sana katika azimio lao la kubadilika, hali punde wanarudia kufanya yale yale ambayo waliamua kuyaacha. Ni nini ambacho kinafanya tofauti katika maisha ya makundi haya mawili? Unawezaje daima kufanya chaguo sahihi? (Full Conversion Brings Happiness, Ensign, May 2002, 24).Waulize wanafunzi jinsi watakavyoweza kuziita picha mbili ubaoni katika msingi wa maoni ya Mzee Scott. Weka kibandiko kimoja kwenye picha ubaoni Waaminifu na ile nyingine Vige-ugeu. Waulize wanafunzi ni vipi wangeweza kujibu maswali ambayo Mzee Scott aliuliza:• Nini ni ambacho kinaleta tofauti katika maisha ya makundi haya mawili?• Unawezaje bila kubabaika kufanya chaguo sahihi?Darasa linapojifunza Alma 23 24 , hamasisha wanafunzi kufikiri kuhusu nini kilichowasu-kuma washiriki wengi wa Kanisa kubaki wa kweli na waaminifu katika maisha yao yote.Fanya muhtasari Alma 23:01 5 kwa kueleza kwamba baada ya mfalme wa Walamani kuo-ngolewa, alituma tangazo kati ya watu likisema kwamba wamruhusu Haruni na nduguze kuhubiri neno la mungu katika nchi yote bila ya kuzuiliwa na bila kudhuriwa. Tangazo hili liliwezesha wamisionari kuanzisha makanisa miongoni mwa Walamani. Na matokeo yake, maelfu ya Walamani wakaongolewa.Mualike mwanafunzi asome Alma 23:6 30 kwa sauti. Uliza darasa lifuatilie, likitafuta mambo mawili ambayo yalisaidia kuleta uongofu wa Walamani. Waalike wanafunzi watoe taarifa ya kile walichopata.• Kwa nini unafikiri ilikuwa ni muhimu kwamba Amoni na ndugu zake waliwafundisha

Walamani kufuatana na roho wa ufunuo na wa unabii?

Fuatilia mialikoWakati walimu wanafu-atilia mwaliko na kazi zilizowapangwa kwenye masomo yaliyopita, wanafunzi watakuja kuelewa na kuhisi umu-himu w akutenda juu ya kanuni za kiungu na kuzitumia katika maisha yao nje ya madarasa.

Page 325: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

310

SoMo la 85

• Unafikiri inamaanisha nini kwamba nguvu ya Mungu zilitenda miujiza miongoni mwa Walamani?

• Ni lini umepata uzoefu wa nguvu ya Mungu ikikusaidia kuwa mwongofu? Ni lini ume-ona nguvu ya Mungu ikifanya kazi kusaidia mtu mwingine kuwa mwongofu?

Waalike wanafunzi wasome Alma 23:6 tena, wakitambua vishazi vinavyoelezea Walamani ambao waliamini mahubiri ya Amoni na ndugu zake. Hakikisha wanafunzi wanaelewa kwamba Walamani hawa walikuwa wameongolewa kwa Bwana, si kwa Kanisa au kwa wamisionari ambao waliwafundisha. Pia hakikisha kwamba wanafunzi wanaona kwamba watu hawa kamwe hawakuanguka. Andika Waliongolewa kwa Bwana na hawakuanguka kamwe juu ya ubao ya chini ya picha inayoitwa Waaminifu .)• Tunapokabiliwa na hali ngumu na dhiki, kwa nini ni muhimu kwamba tuongolewa kwa

Bwana kuliko watu wengine au mawazo?Waalike wanafunzi wasome Alma 23:7, 16 18 kimya, wakitafuta maneno na vishazi vina-vyotoa ushahidi wa uongofu wa Walamani. Waulize wanafunzi watoe taarifa ya kile wana-chokipata. Unaweza kuorodhesha maneno na vishazi hivi ubaoni chini ya picha inayoitwa Waaminifu. Ili kuwasaidia wanafunzi kuchambua zaidi aya hizi, unaweza ukitaka kuuliza maswali yafuatayo:• Ilikuwaje hamu ya watu kupata jina jipya ni ushahidi kwamba walikuwa wamebadilika?• Ni kwa jinsi gani wale walioongolewa hivi leo wanaweza “kutofautishwa” na wengine?• Kwa mujibu wa Alma 23:18, Walamani waongofu walianza kuwa na bidii na kuwa na

urafiki na Wanefi. Wakati mtu anajaribu kutubu au kubadilisha maisha yake, ni kwa jinsi gani inaweza kuwa na manufaa kwake kushirikiana na watu wengine ambao wameongolewa?

Andika maneno yafuatayo ubaoni: Kuongoka humaanisha Waalike wanafunzi kufanya muhtasari wa yale waliyojifunza kutoka Alma 23 kwa kukami-lisha kauli ubaoni. Wanafunzi wanaweza kutumia maneno tofauti katika majibu yao, lakini wanapaswa kueleza ukweli ufuatao: kuongolewa humaanisha kubadilika na kuwa mtu mpya kupitia nguvu ya Mungu. Kamilisha kauli iliyo ubaoniRejesha ya wanafunzi kwa maneno Waaminifu na Vigeugeu ubaoni. Wahimize wao kufiki-ria yapi kati maneno haya yanaeleza vizuri zaidi kiwango cha uongofu wao.

Alma 24Watu wa Anti- Lehi- Nefi walifanya maagano ya kutoshika tena silahaWaalike wanafunzi kufikiria kimya kama wamewahi kuamua kuepuka kurudia makosa fulani au dhambi lakini baadaye wakafanya lile kosa au dhambi tena. Eleza kwamba kama wamepata uzoefu huu, wanapaswa kuendelea kujaribu kujiboresha. Wanapojifunza Alma 24, watajifunza kweli ambazo zitawasaidia.Fanya muhtasari wa Alma 24:1–5 kwa kuelezea kwamba Waamaleki na Waamuloni, ambao walikuwa zamani Wanefi, walichochea hasira za Walamani wengi dhidi ya mfalme wao na wale Anti- Nefi- Lehi wengine. Katika hasira yao, hawa Walamani walijitayarisha kusha-mbulia watu wa Anti- Nefi- Lehi. Wakati huu wa ugomvi, mfalme wa Anti- Nefi- Lehi ali-kufa. Ufalme ulipewa kwa mmoja wa wanawe. Amoni walijikusanyika pamoja na mfalme mpya pamoja na Lamoni na wengine ili kushauriana pamoja na kuamua jinsi ya kujilinda dhidi ya Walamani.Waalike wanafunzi wasome Alma 24:6 kimya, wakitafuta kile watu wa Anti- Nefi- Lehi waliamua wasingeweza kufanya. Baada ya wanafunzi kutoa taarifa ya kile walichokipata, waulize baadhi ya wanafunzi wachukue zamu kusoma kwa sauti kutoka Alma 24:7–10, 12–14. Acha darasa lifuate, lisikiliza njia zote ambazo mfalme wa Anti- Nefi- Lehi alikiri kwamba Mungu alikuwa amewabariki.• Kulingana na Alma 24:9, nini ilikuwa mojawapo ya dhambi ambazo watu wa Anti- Nefi-

Lehi walikuwa wametenda hapo awali?• Kulingana na Alma 24:13, kwa nini walikataa kupigana katika vita?Gawa darasa katika vikundi viwili. Alika kundi la kwanza lisome Alma 24:11, 15, likitafuta vishazi ambavyo vinvyoonyesha jitihada za watu wa Anti- Nefi- Lehi za kutubu. Uliza kundi la pili lisome Alma 24:16–19, wakitafuta nini Anti- Nephi- Lehies walifanya ili kuhakikisha

Page 326: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

311

alMa 23–24

kwamba wangeweza kubaki wasafi. Baada ya wanafunzi kuwa na muda wa kutosha wa kusoma, waalike kuelezea kile walichopata. Unaweza kutumia maswali yafuatayo ya kuleta mawazo ya ziada:• Unafikiri Mfalme alimaanisha nini wakati aliposema, imekuwa yote ambayo tungeweza

kufanya kutubu? (Alma 24:11). (Kishazi hiki kinaelezea juhudi kubwa na azimio la watu wa Anti- Nefi- Lehi la kutubu dhambi zao.)

• Neno ushuhuda linaonekana mara tatu katika Alma 24:15–16, 18. Ni kwa jinsi gani kuzika silaha zao kina kirefu katika ardhi kunathihirisha kama ni ushuhuda? (Ilionyesha kwa watu wengine na Mungu kwamba walikuwa kweli wameacha, au kuziacha dhambi zao.)

Alika mwanafunzi asome kauli ifuatayo ya Rais Spencer W. Kimball:"Katika kuacha dhambi mtu hawezi tu kutamani hali bora zaidi. ... Ni lazima awe na uhakika si tu kwamba yeye ameachilia mbali dhambi bali kwamba yeye amebadilisha hali zinazozunguka dhambi hiyo. Anapaswa kuepuka maeneo na hali na mazingira ambapo dhambi ilitokea, kwani hizi zinaweza kwa urahisi zaidi kuzalisha ile dhambi tena. Yeye lazima kuachana na watu ambao walitenda dhambi hii pamoja. Anaweza asiwachukie watu wanaohu-

sika lakini ni lazima kuepukana nao na kila kitu kinachohusishwa na dhambi ile" (The Miracle of Forgiveness [1969], 171 72).• Watu wa Anti- Nefi- Lehi walifanya nini ili kuepuka hali na watu ambayo wangeweza

kuwavuta waendelea na dhambi zao za zamani?Unaweza kutaka kuwapa wanafunzi muda wa kutafakari kama kuna hali yoyote katika maisha yao ambapo wanahitaji kubadilisha ili kutubu na kuacha dhambi ambayo wame-kuwa wakikabiliana nayo.Andika yafuatayo ubaoni: Ikiwa sisi . . . , mapenzi ya Mungu . . . Waulize wanafunzi watathmini Alma 24:10–18, wakitafuta njia ambayo itawawezesha kukamilisha kauli iliyopo ubaoni. (Unaweza kupendekeza kwamba wanafunzi waandike maelezo kama yafuatayo katika maandiko yao: Tukifanya yote tuwezayo kutubu, Mu-ngu ataondoa hatia yetu na kutusaidia kubaki wasafi. )Rejesha wanafunzi tena kwa Alma 24:17.• Je! Ni ipi baadhi ya mifano ya silaha za uasi (ona Alma 23:7) ambayo watu wanaweza

kuweka chini au kuzika wapokuwa waongofu kwa Bwana? (Wasaidie wanafunzi kuona kwamba silaha za uasi zinaweza kuwa ni pamoja na mitazamo ya dhambi au vitendo ambayo watu lazima waviache ili waweze kuongoka Bwana.)

Mwalike mwanafunzi asome taarifa ifuatayo ya Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya wale Mitume Kumi na Wawili:

"Inachukua muda sawa kabisa kutubu kama inavyo chukua kusema 'Nitaba-dilika' — na kumaanisha hivyo. Bila shaka kutakuwa na matatizo ya kutatua na malipizo ya kufanya. Unaweza kwa kweli kutumia—hakika ungeweza kutumia—muda wa maisha yako yote kuthibitisha toba yako kwa ilivyo-dumu" (For Times of Trouble, New Era, Oct. 1980, 11 12).Waulize wanafunzi waeleza hatua ambazo mvulana au msichana anaweza

kuchukua ili kuepuka kurudia kila dhambi zifuatazo: kuvunja Neno la Hekima, kutazama picha za ngono, na kuwa mkatili kwa ndugu.Alika wanafunzi kufikiria jinsi watu wa Anti- Nefi- Lehi walivyojisikia baada ya kuzika si-laha zao na kisha wakagundua kwamba jeshi la Walamani lilikuwa linakuja kuwashambu-lia. Waulize wanafunzi wafikiri hali hii wakati wanaposoma Alma 24:20 22 kimya.Andika ukweli ufuatao kwenye ubao: Tunapoweka maagano yetu, tunaweza kuwasai-dia wengine kuwa waongofu. Alika wanafunzi wachache wachukue zamu kusoma kwa sauti kutoka Alma 24:23 27. Uliza darasa lifuatilie pamoja, likitafuta maneno au vishazi ambavyo vinavyofundisha kanuni iliyoandikwa ubaoni.• Ni kwa jinsi gani maelezo haya yanahamasisha hamu yako ya kuweka maagano?• Tunaweza kufanya nini ili kuimarisha hamu na uwezo wetu wa kuweka maagano tuliyo-

yafanya na Bwana?Alika wanafunzi kushiriki uzoefu wowote ambao wamekuwa nao na kanuni iliyopo uba-oni. Hitimisha kwa kushiriki ushuhuda wako wa kanuni zilizofundishwa katika somo hili.

Page 327: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

312

Somo la Mafunzo- NyumbaniAlma 17–24 (Kitengo cha 17)

Vifaa vya Matayarisho kwa Mwalimu wa Mafunzo - NyumbaniMuhtasari wa Masomo ya Mafunzo- Nyumbani Kila SikuMuhtasari ufuatao wa mafundisho na kanuni ambazo wana-funzi walijifunza waliposoma Alma 17–24 (kitengo cha 17) haijanuiwa kufundishwa kama sehemu ya somo lako. Somo unalofundisha huzingatia tu machache ya mafundisho na kanuni hizi. Fuata uvuvio wa Roho Mtakatifu unapofikiria mahitaji ya wanafunzi.

Siku ya 1 (Alma 17–18)Kutoka kwa mfano wa Amoni, na ndugu zake wakifundisha Walamani, wanafunzi walijifunza kwamba kwa kupekua ma-andiko, na kuomba, na kufunga, tunaweza kupokea Roho Mtakatifu na kuwafundisha wengine kwa nguvu. Huduma ya Amoni kwa Mfalme Lamoni pia ilifundisha kipengele muhimu cha huduma ya umisionari —kwamba tunapoweka mifano mizuri, Bwana anaweza kutufanya vyombo katika mikono Yake. Wanafunzi waliweza kuona kwamba huduma ya Amoni kwa Lamoni ilitayarisha mtawala Mlamani na wengine kukubali injili. Uongofu wa mfalme Lamoni unafu-ndisha kwamba wakati tunapoelewa haja yetu ya Mwokozi, tutakuwa na hamu ya kutubu.

Siku ya 2 (Alma 19–20)Wanafunzi walijifunza kwamba ushuhuda na mfano wa haki wa Amoni ulisaidia kumgeuza baba yake Lamoni kwa Bwana. Walijifunza pia kwamba vitendo vyetu vya upendo vinaweza kusababisha wengine kupunguza makali ya nyoyo zao na kutafuta kujua ukweli.

Siku ya 3 (Alma 21–22)Masimulizi ya kazi ya Haruni ya umisionari yaliwasaidia wana-funzi kuona kwamba kama kwa uaminifu tutaendelea kupitia kwa majaribio yetu, Bwana atatusaidia kufanya kazi Yake. Haruni alimsaidia baba ya Mfalme Lamoni kuelewa kwamba angeweza kupokea wokovu tu kwa njia ya kustahili ya Yesu Kristo. Kama mfalme, ni lazima tuwe radhi kuacha dhambi zetu zote ili kubadilishwa kiroho kuzaliwa na Mungu.

Siku ya 4 (Alma 23–24)Maelfu ya Walamani waliokubali injili walionyesha kwamba uongofu ni mabadiliko ya kiroho, —kuwa mtu mpya kwa njia ya nguvu ya Mungu. Kupitia kwa mfano wa Walamani ambao walikuwa Anti- nefi- Lehi, wanafunzi walijifunza kwamba kama tukifanya yote tunayoweza kutubu, Mungu ataondoa hatia yetu na kutusaidia kubaki wasafi. Uongofu wa Walamani unaonyesha kwamba tunaweza kusaidia we-ngine kuwa waongofu wakati tukiwa waaminifu.

UtanguliziWana wanne wa Mfalme Mosia walichagua kukataa fursa na anasa nyumbani ili waweze kuhubiri injili miongoni mwa Wala-mani. Masimulizi ya wamisionari hawa wanne yanaonyesha jinsi wanafunzi wanaweza kujiandaa kwa ufanisi katika kufundisha injili ya Yesu Kristo kwa wengine.

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 17–22Amoni na nduguze wawili wanawafundisha wafalme wawili wa WalamaniMbele ya darasa, andika kauli ifuatayo isiyokamilika ubaoni au kwenye kipande cha karatasi: Jambo moja muhimu unaloweza kufanya ili kujiandaa kwa ajili ya wito kuhudumu [misheni] ni ku ... 

Alika wanafunzi wachache waeleze jinsi ilivyokuwa walipo-mwona mwanafamilia au rafiki akirudi kutoka kuhudumu kwa uaminifu misheni ya muda kamili. Kisha waulize wanafunzi: Jinsi gani mtu huyo alikuwa tofauti baada ya misheni wake? Unafikiri nini kilisababisha mabadiliko haya?

Waulize wanafunzi ni kwa jinsi gani wanaweza kukamilisha taarifa iliyopo ubaoni. Baada ya wanafunzi kujibu, shiriki nao jinsi Mzee David A. Bednar wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alivyokamilisha taarifa: "Jambo moja muhimu unaloweza kufa-nya ili kujiandaa kwa ajili ya wito kutumikia [misheni] ni kuwa mmisionari muda mrefu kabla ya kwenda misheni" (Becoming a Missionary, Ensign or Liahona, Nov. 2005, 45).

Uliza: Ni katika njia gani wavulana na waischana wanafuata ushauri wa Mzee Bednar na kuwa wamisionari kabla ya wao kutumikia misheni za muda kamili?

Shiriki kauli ifuatayo ya Rais Thomas S. Monson:

"Huduma ya umisionari ni jukumu la ukuhani—, sharti ambalo Bwana anatarajia kutoka kwetu sisi ambao tumepewa mengi sana. Wavulana, nawasihi mjitayarishe kwa huduma kama mmisionari. Jiwekeni wasafi na halisi na wastahiki kumwakilisha Bwana. Dumisha afya na nguvu zako" Soma maandiko. Pale ambapo inapatikana, shiriki katika seminari na chuo. Jizoeshe na kitabu cha maelekezo cha misionari Hubiri Injili Yangu.

Neno kwenu kina dada vijana: "Ingawa hamna majukumu ya ukuhani sawa na waliyonayo wavulana kuhudumu kama wa-misionari wa muda kamili pia mnatoa mchango muhimu kama wamisionari, na tunakaribisha huduma yenu." (As We Meet Together Again, Ensign or Liahona, Nov. 2010, 6).

Andika yafuatayo ubaoni: Bwana atatubariki kwa Roho Mtaka-tifu na nguvu ya kufundisha neno lake tunapo 

Gawa darasa katika vikundi vinne. Pangia kila kundi moja ya vifungu vifuatavyo vya maandiko: Alma 17:1–4; Alma 17:9–13;

Page 328: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

313

SoMo la MafUnzo- nyUMbani

Alma 17:19–25; 18:26–30; Alma 17:26–30. (Rekebisha shughuli hii kama una darasa ndogo.)

Waalike wanafunzi wasome vifungu walivyopangiwa kimya, wakitafuta kile wana wa Mosia walichofanya ambacho kiliwa-bariki kwa Roho na kwa nguvu walipokuwa wakifundisha injili. Eleza kwamba wakati wanafunzi wakishakamilisha, waulize washiriki kile walichogundua na jinsi watakavyoweza kukamili-sha sentensi ubaoni.

Baada ya muda wa kutosha, alika mtu kutoka kila kundi kueleza kile wana wa Mosia walichofanya na jinsi washiriki wa kundi wangekamilisha kanuni iliyopo ubaoni. Majibu ya wanafunzi ya-naweza kujumuisha yafuatayo: kupekua maandiko, kufunga na kuomba, kuwa na subira, kuweka mfano mzuri, uaminifu kwa Bwana, kutumikia wengine kwa dhati, na kuwapenda wengine kama ndugu na dada zetu. Wanafunzi wanaposhiriki majibu yao, yaorodheshe ubaoni. Waulize wanafunzi waeleze jinsi kila kitendo au tabia inavyoweza kusaidia mtu binafsi kushiriki injili kwa ufanisi zaidi.

Kama wowote wa mwanafunzi wako wangeongolewa katika injili baada ya kufundishwa na wamisionari wa muda wote, unaweza ukawataka washiriki jinsi walivyojisikia walipokuwa wakijifunza injili.

Wakumbushe wanafunzi kwamba baada ya Amoni kulilinda kundi la mifugo ya mfalme, Mfalme Lamoni alishangazwa na nguvu za Amoni na vilevile utii na uaminifu wake katika kutimiza amri za mfalme (ona Alma 18:8–10). Lamoni alikuwa tayari kusi-kiliza ujumbe wa Amoni ambao alikuwa amekuja kushiriki naye. Waalike wanafunzi kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka Alma 18:24–29. Uliza darasa litafute jinsi Amoni alivyojengea kwa ufahamu wa Lamoni juu ya Mungu ili aweze kumwandaa Lamoni kuelewa mafundisho ya kweli.

Waulize wanafunzi maswali yafuatayo:

• Kama ungekuwa na mazungumzo kuhusu Mungu na rafiki wa imani ingine, ungewezaje kutumia imani mnazoshiriki nyote, kama Amoni alivyofanya? Juhudi hii inawezaje kumsai-dia rafiki yako?

• Mada gani nyingine za injili mgezugumza na marafiki zako kufungua fursa ya kushiriki injili pamoja nao?

Wakumbushe wanafunzi kwamba Mfalme Lamoni alikuwa msikivu kwa injili ya Yesu Kristo, kama alivyofanya baba yake. Muulize mwanafunzi mmoja asome kwa sauti Alma 18:39–41— majibu ya Lamon kwa kujifunza kuhusu Yesu Kristo. Muulize mwanafunzi mwingine asome Alma 22:14–18— majibu ya babake Lamoni. Alika darasani lifuatilie katika maandiko yao na litafuta majibu yanayofanana katika watu hawa.

Uliza: Je! Watu wote wawili walitaka kufanya nini wakati wali-pojifunza kuhusu Yesu Kristo?

Eleza kwamba Lamoni na baba yake waliguswa na Roho kwa njia ya mafundisho ya wamisionari. Kwa hivyo, walitaka baraka za injili na walikuwa radhi kuacha dhambi zao na kutubu. Wa-kumbushe wanafunzi ukweli waliojifunza juma hili: Ni lazima tuwe radhi kuziacha dhambi zetu zote ili tubadilishwe kiroho na kuzaliwa kwa Mungu.

Mualike mwanafunzi asome kwa sauti taarifa ya Mzee Dallin H. Oaks inayopatikana katika mwongozo wao wa kujifunza: "Injili ya Yesu Kristo inatupa changamoto kubadilika. Tubuni ni ujumbe wa kila mara, na kutubu ina maana ya kuacha matendo yetu yote ya — kibinafsi, familia, kabila, na kitaifa — ambayo ni kinyume na amri za Mungu. Madhumuni ya injili ni kugeuza viumbe vya kawaida na kuwa raia wa selestia, na hiyo inahitaji mabadiliko" (Repentance and Change, Ensign au Liahona, Nov. 2003, 37).

Waalike wanafunzi kufikiria kuhusu maisha yao na kufikiria kama wanahitaji kuacha dhambi yoyote ili kubadilishwa kiroho kama vile Lamoni na baba yake walivyobadilishwa. Hitimisha kwa kushirikiana himizo lako na ushuhuda kwamba tukiwa radhi kuacha dhambi zetu, Bwana atatusaidia kubadilika na kukua.

Kitengo Kinachofuata (Alma 25–32)Waulize wanafunzi kufikiria swali hili: Ungeweza kusema nini kwa mtu ambaye ni mpinga Kristo? Katika kitengo cha pili, wanafunzi watajifunza jinsi Alma alishughulikia maswali na kejeli ya Korihori, ambaye alikuwa mpinga Kristo. Kwa nyongeza, watajifunza zaidi kuhusu imani kama wanavyosoma kuhusu jinsi Alma na wengine walivyofanya kazi ya kufundisha Wazoramu waliokengeuka, ambao walikuwa kuzipotosha njia za Bwana.

Page 329: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

314

UtanguliziBaada ya kuharibu mji wa Amoniha, Walamani wali-kuwa na vita vingi vingine na Wanefi na walisukumwa nyuma. Wakiwa wamepata hasara kubwa, Walamani wengi waliweka silaha zao za kivita chini, na kutubu, na walijiunga na Anti- Nefi- Lehi. Wakati wana wa Mosia

na wenzi wao walipohitimisha misheni yao ya miaka 14 miongoni mwa Walamani, Amoni alimsifu Bwana na kuonyesha shukrani kwa baraka ya kuwa vyombo katika mikono ya Mungu kuleta injili kwa Walamani.

SOMO LA 86

alma 25–26

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 25:1–12Unabii wa Abinadi na Alma watimiaKabla ya darasa, nakili chati ifuatayo ubaoni:

Unabii Kutimizwa kwa Unabii

alma 9:27. alma alitabiri nini kwa watu wa amoniha?

alma 25:1–2 (ona pia alma 16:2–3, 9–11)

Mosia 17:14–19. ni nini abinadi alitabiri kingetokea kwa uzao wa Mfalme nuhu na makuhani wake?

alma 25:4–9

Andika neno amini ubaoni. Watake wanafunzi kutaja baadhi ya watu ambao mara nyingi sisi huweka matumaini yetu kwao. Majibu yanayowezekana ni pamoja na Bwana, manabii, wazazi, walimu, na makocha. Waulize wanafunzi:• Kwa nini ni rahisi kuamini katika baadhi ya watu fulani kuliko wengine?• Kati ya watu wote duniani leo, ni nani aliye rahisi zaidi kwako kuweka matumaini yako?Waambie wanafunzi kwamba Alma 25 ina ushahidi kwamba neno la Bwana kwa manabii wake daima hutimia. Eleza kwamba wanafunzi watatumia chati kwenye ubao ili kujifunza unabii muwili wa manabii wa Kitabu cha Mormoni na kutimizwa kwa unabii huo. Waulize wanafunzi wanakili chati katika daftari au shajara za kujifunza maandiko. Katika safu ya kwanza, waandike majibu ya maswali, kwa kutumia marejeo ya maandiko yaliyotolewa. Katika safu ya pili, wafanye waandike kuhusu utimilifu wa utabiri. Waalike wanafunzi wa-chache watoe taarifa ya nini walichokipata.Mualike mwanafunzi asome Alma 25:11–12 kwa sauti. Waulize wengine darasani kufuata pamoja, wakitafuta nini ambacho Mormoni alisema kilitokea na maneno ya Abinadi. Una-weza kutaka kupendekeza kwamba wanafunzi waweke alama katika kishazi maneno hayo yalithibitishwa katika mstari wa 12 .• Kishazi hiki "maneno hayo yalithibitishwa" kina maana gani?Unaweza kupendekeza kuwa wanafunzi waandike M&M 1:38 katika maandiko yao karibu na Alma 25:12. Mwalike mwanafunzi asome Mafundisho na Maagano 1:38 kwa sauti. Uliza darasa lifuatilie, likitafuta kishazi kilicho sawa na "maneno haya yalithibitishwa." Yote yatatimia.• Tunajifunza nini kutoka Alma 25:1–12 kuhusu utabiri na ahadi zilizofanywa na ma-

nabii? (Andika ukweli ufuatao ubao. Maneno ya manabii yaliyo ya maongozi yote yatatimizwa )

Page 330: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

315

alMa 25 –26

Sisitiza kwamba mifano katika chati inaonyesha kwamba maonyo ya manabii kwa wasio na haki daima yatatimia. Manabii pia wanashiriki ahadi kwa wale ambao wanarejea kwa Bwana. Ahadi hizi pia zitatimia. Ili kusaidia wanafunzi kuona matumizi ya kanuni hii katika maisha yao, soma kauli ifuatayo ya Urais Kwanza kutoka Kwa Nguvu ya Vijana. Wa-ulize wanafunzi kusikiliza ahadi kwa wale ambao wanaweka viwango katika kijitabu hiki.Viwango katika kijitabu hiki vitakusaidia kwa chaguo muhimu ambazo wewe unafanya sasa na bado utafanya katika siku zijazo. Tunaahidi kwamba unapoweka maagano uliyoyaweka na viwango hivi, utabarikiwa kwa kuwa na Roho Mtakatifu, imani yako na ushuhuda wako utakuwa imara, na utafurahia ongezeko la furaha Kwa Nguvu ya Vijana [kijitabu,2011] , ii). • Urais wa Kwanza uliahidi nini?• Ni lini umeona ahadi hizi zikitimizwa?

Alma 25:13–17Walamani wengi wanatubu na kujiunga na watu wa Anti- Nefi- LehiMwambie mwanafunzi asome Alma 25:13–14 kwa sauti. Uliza darasa lifuatilie, likitafuta kile wengi wa Walamani walikifanya baada ya kugundua wasingeweza kuwashinda Wanefi.• Nini kinachokuvutia kuhusu vitendo vya Walamani?Fanya wanafunzi wasome Alma 25:17 kimya, wakitafuta hisia za wana wa Mosia kuhusu mafanikio waliyokuwa nayo miongoni mwa Walamani.• Ilikuwaje mafanikio ya wana wa Mosia ni mfano kuwa maneno ya Bwana yanathibi-

tishwa? (Kama wanafunzi wanahitaji msaada kujibu swali hili, warejeshe kwa Mosia 28:5–7na Alma 17:11.)

Alma 26Amoni anafurahi katika huruma za Bwana kwake na ndugu zake na kwa WalamaniOnyesha baadhi ya vifaa (kama vile nyundo, bisibisi, spana, kalamu au penseli, brashi ya rangi, mkasi, tarakilishi, na chombo cha muziki). Eleza kwamba neno lingine kwa kifaa ni chombo. • Je! Ni baadhi ya vitu gani ambavyo fundi mwenye ujuzi au msanii anaweza kufanya na

chombo sahihi?• Unafikiri inamaanisha nini kwa mtu fulani kuwa chombo katika mikono ya Bwana?Waalike wanafunzi wachache kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka Alma 26:1–5, 12. Uliza darasa libainishe njia ambazo Amoni na wamisionari wenzake walikuwa vyombo katika mikono ya Mungu.• Ni nini Bwana alitimiza kupitia Amoni na wamisionari wenzake?• Ungewezaje kuelezea tena Alma 26:12? Ni jinsi gani kauli ya Amoni katika aya hii ina-

husiana na kuwa chombo katika mikono ya Bwana?Waalike wanafunzi wasome Alma 26:11, 13, 16 kimya kimya, wakitafuta nyakati ambazo maneno shangwe na furahia yanaonekana. Unaweza kutaka kupendekeza kwamba wa-nafunzi watie alama maneno haya katika maandiko yao. Alika mwanafunzi asome Alma 26:13–16 kwa sauti, kisha uliza darasa litafute sababu ambazo Amoni alitoa kwa ajili ya kufurahia kwake.• Kwa nini Amoni alifurahia?• Tunaweza kujifunza kanuni gani kutoka kwa mistari hii? Wanafunzi wanaweza kutaja

kanuni nyingi tofauti. Kanuni ifuatayo inaweza kutumika kama muhtasari wa maoni yao: Sisi tunapata furaha tunapomtumikia kwa uaminifu Bwana na watoto Wake. Unaweza kutaka kuandika kanuni hii ubaoni.)

• Kwa nini unafikiri tunapata furaha tukiwa katika huduma ya Bwana?Andika marejeo ya maandiko na maswali yafuatayo kwenye ubao. Fikiria kuyaandika kabla ya darasa. Gawa wanafunzi katika majozi. Uliza kila jozi lichague na kusoma moja ya vifu-ngu na kujadili majibu ya maswali yanayoambatana nacho.

Alma 26:17–20. Amoni na ndugu zake walikuwa watu wa namna gani kabla hawajaongolewa?

Page 331: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

316

SoMo la 86

Alma 26:23–25. Kulingana na kile Wanefi walimwambia Amoni na ndugu zake, Walamani walikuwaje kabla ya kuongolewa?

Toa muda kwa wanafunzi wachache kuelezea majibu yao ya maswali haya. Waalike wana-funzi wasome Alma 26:23–29 kimya, wakitambua vikwazo ambavyo Amoni na ndugu zake walikabiliwa navyo katika huduma yao kwa Bwana na Walamani.• Ni vikwazo vipi unafikiri wamisionari wanaweza kukumbana navyo hivi leo?• Kulingana na Alma 26:27, 30, nini kiliwapatia motisha Amoni na wamisionari wenzake

kuendelea kuhudumu? Faraja na ahadi kutoka kwa Bwana na hamu ya "kuwa njia ya kuokoa baadhi ya roho.")

Waulize wanafunzi wasome Alma 26:31–34 kimya, wakitafuta baadhi ya matokeo ya kazi za wana wa Mosia. Wakati wao wamekuwa na muda wa kutosha wa kusoma, waulize washiriki kile walichopata.Alika mwanafunzi asome Alma 26:35–37 kwa sauti. Uliza darasa lifuatilie, litafakari sababu walizonazo za kufurahia wema wa Mungu.• Nini jumbe gani unaziona katika aya hizi?Sisitiza kwamba moja ya jumbe nyingi katika aya hizi ni kwamba Bwana ni mwenye huruma kwa wale wote wanaotubu na kuamini katika jina lake. Ili kuwasaidia wana-funzi kuhisi ukweli na umuhimu wa kanuni hii, soma kauli ifuatayo ya Rais Boyd K. Packer wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili:

"Barua huja kutoka kwa wale ambao wamefanya makosa ya tanzia. 'Wana kuuliza, Je, mimi kamwe naweza kusamehewa?'"Jibu ni ndio!"Injili inafundisha kwamba afueni kutoka kwenye mateso na hatia zina-weza kupatikana kupitia toba. Ila kwa wale wachache ambao wamehamia kwenye laana ya milele baada ya kujua ukamilifu, hakuna tabia, hakuna

uteja, hakuna uasi, hakuna kuvunja sheria, hakuna kosa, lililondolewa kutoka kwa ahadi ya msamaha kamili" (The Brilliant Morning of Forgiveness, Ensign, Nov. 1995, 19).Shuhudia nguvu ya Upatanisho inayoruhusu msamaha wa dhambi, kubwa au ndogo, kwa wale ambao wana imani katika Yesu Kristo na kutubu. Pia shuhudia kuhusu furaha inayo-kuja katika maisha yetu wakati tunapohudumu kama vyombo katika mikono ya Bwana.

Page 332: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

317

UtanguliziWakati Walamani walikuwa hawafanikiwi katika ma-shambulizi yao juu Wanefi, wakageuza hasira yao ku-elekea watu wa Anti- Nefi- Lehi. Kwa Sababu ya agano ambalo watu wa Anti- Nefi- Lehi walifanya kwamba kamwe tena hawangemwaga damu ya wengine, wali-kataa kuchukua silaha ili kujilinda. Amoni aliwaongoza watu wa Anti- Nefi- Lehi kwenda Zarahemla, ambapo walipata ulinzi kutoka kwa Wanefi na kujulikana

kama watu wa Amoni. Wanefi walipowalinda watu wa Amoni dhidi Walamani, maelfu ya Wanefi na Walamani walikufa katika vita. Licha ya huzuni ambayo Wanefi walihisi kwa ajili ya vifo vya wapendwa wao, wengi wao walipata matumaini na furaha katika ahadi ya Bwana kwamba wenye haki "watainuliwa na kuishi upande wa kulia wa Mungu, katika hali ya furaha isiyo-isha kamwe" (Alma 28:12).

SOMO LA 87

alma 27–29

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 27Amoni awaongoza watu wa Anti Nefi- Lehi kwenye usalama miongoni mwa WanefiWaulize wanafunzi wanyooshe mikono yao juu kama wamewahi kuwa na mtu aliye waahidi na kisha akaivunja ahadi hiyo. Kisha waulize wanafunzi kuinua mikono juu kama wamewahi kuwa na mtu aliye waahidi na akaweka ahadi hiyo. • Mnahisi vipi kuhusu watu wanaoweka ahadi zao? Kwa nini?• Je! Unafikiri Bwana anahisi vipi kuhusu wale ambao wanatimiza ahadi zao kwake?Tambulisha Alma 27 kwa kueleza kuwa baada ya Walamani kujaribu bila mafanikio ku-waangamiza Wanefi, waliwashambulia watu wa Anti- Nefi- Lehi, wale Walamani ambao walikuwa waongofu kwa njia ya huduma ya Amoni na ndugu zake. Waulize wanafunzi kukumbuka kile watu wa Anti- Nefi- Lehi walifanya ili kumwonyesha Bwana kuwa wata-weka ahadi yao kwamba kamwe tena hawata zitumia silaha kwa ajili ya kumwaga damu ya mtu (Alma 24:18). (Walizika silaha zao za vita.) Ili kujua jinsi walivyojizatiti watu wa Anti- Nefi- Lehi walikuwa waweke ahadi zao, alika mwanafunzi asome Alma 27:2–3 kwa sauti. (Unaweza pia kupendekeza kwamba wanafunzi wasome Alma 24:18–19 na andika rejeleo pembeni karibu na Alma 27:3.)• Kama ungekuwa mmoja wa watu wa Anti- Nefi- Lehi ingekuwa vigumu jinsi gani kwako

kuweka agano lako na usiende vitani kujilinda mwenyewe na wapendwa wako?Waalike wanafunzi wasome Alma 27:4–10 kimya, wakitafuta kile Amoni alipendekeza ku-fanya ili kuwalinda watu wa Anti- Nefi- Lehi na kuwasaidia kushika maagano yao. Waulize mwanafunzi wafanye muhtasari wa kifungu hiki.Alika mwanafunzi asome Alma 27:11-12 kwa sauti, na uliza darasa litafute maelekezo ambayo Amoni alipokea kutoka kwa Bwana. Eleza kwamba watu wa Anti- Nefi- Lehi walim-fuata Amoni kwenda Zarahemla (ona Alma 27:13–15). Unaweza pia kutaka kufanya muh-tasari wa Alma 27:16–19, ukitoa angalizo kuwa ilikuwa katika hali hii na kwamba Amoni na wana wengine wa Mosia waliungana tena na Alma, kama ilivyoelezwa katika Alma 17:1–4.)Eleza kuwa mwamuzi mkuu wa Wanefi aliuliza watu kama wangeweza kuruhusu watu wa Anti- Nefi- lehi kuishi miongoni mwao. Alika wanafunzi wasome Alma 27:22–24kimya, wakitafuta majibu ya Wanefi kwa tangazo la mwamuzi mkuu.• Wanefi walisema wangewasaidia vipi watu wa Anti- Nefi- Lehi?• Kwa nini unafikiri Wanefi walikuwa tayari kulinda adui zao wa zamani?Watake wanafunzi wasome Alma 27:26 kimya ili kugundua kile Wanefi walianza kuwaita watu wa Anti- Nefi Lehi.

Page 333: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

318

SoMo la 87

Waulize wanafunzi wachache kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka Alma 27:27–30. Acha darasa lifuatilie pamoja, likitafuta kile watu wa Amoni walijulikana nacho. Waalike wanafunzi watoe taarifa ya kile wanachokipata. • Ni nini kinachokuvutia kuhusu watu wa Amoni? Kwa nini?• Ni nini ambacho Alma 27:27–30 inafundisha kuhusu uhusiano kati ya kuongolewa kwa

Bwana na kuweka ahadi? Wanafunzi wanaweza kutumia maneno tofauti, lakini wana-paswa kuonyesha kwamba wanaelewa ukweli ufuatao: Wakati tumeongolewa kika-milifu kwa Bwana, tunaweka maagano ambayo tumefanya naye. Unaweza kutaka kuandika kanuni hii ubaoni.)

• Ni nani katika maisha yako amekuwa mfano wa kanuni hii?

Alma 28Wanefi wanawashinda Walamani katika vita vikubwaSisitiza kwamba hata ingawa wengi wa Wanefi walikuwa waaminifu, bado walikabiliwa na majaribio magumu.Eleza kwamba Rais Thomas S. Monson alishiriki simulizi ifuatayo ya tukio lililotokea katika ujana wake. Baada ya kusikia kwamba rafiki yake Arthur Patton alikuwa amekufa katika Vita Kuu ya II, kijana Thomas Monson alikwenda kumtembelea mama yake Arthur, ambaye alikuwa si muumini wa Kanisa. Baadaye alikumbuka:"Mwanga uliondoka katika maisha ya Bi. Patton. Yeye alikuwa akitafuta katika giza keke, na kukata tamaa kabisa. "Pamoja na maombi katika moyo wangu, nilifikia njia ya miguu nilioifahamu ilioelekea nyu-mbani kwa Patton, nikistajabu ni maneno gani ya faraja yangeweza kutoka kwa kijana tu."Mlango ulifunguliwa, na Bi. Patton akanikumbatia kama ambavyo angemkumkumbatia mwanawe mwenyewe. Nyumbani ikawa kanisa wakati mama mwenye majonzi mengi na mvulana asiyehisi kutosha walipopiga magoti katika maombi."Tukiinuka kutoka kwenye magoti yetu, Bi. Patton alitazama macho yangu na kusema: 'Tommy, mimi si wa kanisa lolote, lakini wewe ni wa Kanisa. Niambie, Arthur ataishi tena?" (Mrs.) Patton—the Story Continues, Ensign au Liahona, Nov. 2007, 22).• Ungejibu vipi swali la Bi. Patton?Soma majibu ya Rais Monson:"Kwa kadri ya uwezo wangu, nilimshuhudia kuwa Arthur bila shaka ataishi tena" (Mrs. Patton—the Story Continues, 22).• Ufahamu wa mpango wa wokovu unabadili vipi mtazamo wa wale ambao wapendwa

wao wamekufa?Waulize wanafunzi wachache wachukue zamu kusoma kwa sauti kutoka Alma 28:1–3. Uliza darasa litafute gharama ambayo Wanefi walilipa ili kuwasaidia watu wa Amoni kuweka ahadi zao. Alika wanafunzi wasome Alma 28:4–6 kimya, wakitafuta kiasi amba-cho vifo vingi viliwaathiri Wanefi. Waulize wanafunzi wapekue Alma 28:11–12 wakitafuta sababu ya baadhi ya watu kupata uzoefu wa hofu wakati wapendwa wetu wakifa, wakati wengine wanaweza kuhisi matumaini.• Kwa nini baadhi ya watu hupata hofu wakati wapendwa wao wanapokufa?• Kwa nini baadhi ya watu wanaweza kuhisi matumaini wakati wapendwa wao wana-

pokufa? Wanafunzi wanaweza kutumia maneno tofauti, lakini wanapaswa kueleza kwamba wakati tuna imani katika Yesu Kristo na ahadi za Bwana, tunaweza kuwa na matumaini na furaha wakati wa kifo. )

Andika sentensi ifuatayo isiyokamili ubaoni: Na hivyo tunaona Waulize wanafunzi jinsi watakavyokamilisha sentensi hii kwa mujibu wa kile walichosoma katika Alma 28.Baada ya wanafunzi kuwa na muda wa kujibu, alika mwanafunzi asome Alma 28:13–14. Wafanye wanafunzi kulinganisha majibu yao na kanuni zinazofundishwa katika aya hizi.

Page 334: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

319

alMa 27–29

Unaweza kutaka kupendekeza kwamba wanafunzi waweke alama kwenye kishazi "na hi-vyo tunaona" kila wakati inapotokea katika aya hizi. Eleza kwamba Mormoni mara nyingi alitumika kishazi hiki kutanguliza masomo muhimu tunayoweza kujifunza kutoka kwa masimulizi katika Kitabu cha Mormoni.)• Umesoma nini katika Alma 27–28 ambayo inasaidia kauli ya Mormoni "na hivyo

tunaona?"• Lini umeona mtu akikumbana na kifo au kifo cha mpendwa wake kwa matumaini kwa

sababu ya imani katika Yesu Kristo?• Ungeelezaje ufufuo ili kumsaidia mtu kuwa na matumaini katika kukabiliana na kifo

chake mwenyewe au kifo cha mpendwa?

Alma 29Alma anatukuza katika kuleta roho kwa MunguWaambie wanafunzi kwamba Alma 29 ina maelezo ya Alma ya hamu yake ya kuwa cho-mbo katika mikono ya bwana. Mualike mwanafunzi asome Alma 29:1–3 kwa sauti. Acha darasa litafute kile Alma angefanya kama angeweza kuwa na matakwa ya moyo [yake]. Yeye angekuwa [amelilia] toba kwa watu wote.)• Kulingana na Alma 29:2, kwa nini Alma alitamani hii? Acha wanafunzi wasome Alma 29:4–5 kimya, wakitafuta kile Bwana huwapa wale ambao wana hamu ya haki. Kama wanafunzi wanahitaji msaada kujibu swali hili, unaweza kutaja kishazi "Najua ya kwamba yeye anawapa watu kulingana na matakwa yao." Eleza kwamba kama tunatamani mambo mema, Bwana atatubariki kulingana na haja hizo. Sisitiza kwamba kama hamu zetu zote za haki hazitimizwi katika maisha haya, zitatimizwa katika maisha ya milele.)Waulize wanafunzi wapekue Alma 29:10, 14, 16 kibinafsi, wakitafuta baraka ambazo Alma alipokea alipowasaidia wengine kuja kwa Kristo. Waulize wanafunzi washiriki kile wanachopata.• Ni neno gani Alma alitumia kueleza jinsi alivyohisi kuhusu kuwasaidia wengine kuja

kwa Kristo? (Unaweza kutaka kupendekeza kwamba wanafunzi waweke alama kila matumizi ya neno shangwe katika aya hizi)

• Ni kanuni gani tunayoweza kujifunza kutokana na uzoefu wa Alma wa kuwasaidia we-ngine kutubu na kuja kwa Yesu Kristo? Wanafunzi wanaweza kutumia maneno tofauti, lakini wanapaswa kuonyesha kwamba wanaelewa kanuni ifuatayo: Tutapata furaha tunapowasaidia wengine kutubu na kuja kwa Yesu Kristo. )

• Ni Wakati gani umehisi furaha inayokuja kutokana na kuwasaidia wengine kuja kwa Kristo?Wahimize wanafunzi kutafuta fursa za kusaidia watu wengine kuja kwa Yesu Kristo. Fikiria kushiriki uzoefu wa furaha yako ya umisionari.

Wasaidie wanafunzi kutambua kanuni zinazofundishwa katika maandikoKatika baadhi ya ma-tukio, kanuni za injili zinazofundishwa katika maandiko hutanguliwa na kishazi "na kwa hivyo tunaona." Kwa mfano, katika Alma 28:13–14, Mormoni anatumia "na kwa hivyo tunaona" ku-teka mawazo yetu kwa kanuni ambazo tuna-weza kujifunza kutokana na uzoefu wa Amoni na watu wa Anti Nefi- Lehi. Wafundishe wanafunzi kwamba wanapojifunza na kutafakari maandiko, wanaweza kupata kanuni wao wenyewe, "Aya hizi zinanifundisha nini mimi?"

Page 335: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

320

SoMo la 87

Tangazo na Habari za UsuliAlma 28:11 12. Kupata amani wakati kifo kinapotokea

Mzee Russell M. Nelson wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alizungumzia jinsi matendo yetu katika maisha haya yanaweza kutuletea amani wakati kifo kinapotokea:

"Akina kaka na akina dada, tunaishi ili tufe na tuna-kufa ili tuishi—katika ufalme mwingine. Kama tu-mejitayarisha vizuri, kifo hakileti hofu. Kutokana na mtazamo wa milele, kifo ni cha mapema tu kwa wale ambao hawako tayari kukutana na Mungu.

"Sasa ni wakati wa kujitayarisha. Basi, wakati kifo kinapokuja, tunaweza kuelekea kwenye utukufu wa selestia ambapo Baba wa Mbinguni ameandaa kwa ajili ya watoto Wake waaminifu. Wakati huo huo, kwa wa-pendwa walioachwa nyuma wakihuzunika uchungu wa kifo hutulizwa kwa imani thabiti katika Kristo, mwa-ngaza kamili wa matumaini, upendo kwa Mungu na wa watu wote na hamu kubwa ya kuwatumikia" (Now Is the Time to Prepare, Ensign or Liahona, May 2005, 18).

Mzee Wilford W. Andersen wa wale Sabini alisimulia jinsi baadhi ya marafiki walivyoshugulikia kifo cha baba yao:

"Hivi karibuni rafiki yangu mpendwa alifariki dunia kutokana na saratani. Yeye na familia yake ni watu wa imani kubwa. Ilikuwa ni msukumo wa kuona jinsi imani yao iliwalibeba kupitia wakati huu mgumu sana. Walijawa na amani ya ndani ambayo iliwaendeleza na kuwaimarisha. Kwa ruhusa yao napenda kusoma ku-toka barua iliyoandikwa na mwanafamilia siku chache tu kabla ya baba yake kuaga dunia:

"'Siku chache zilizopita zimekuwa hasa ngumu. Jana usiku tulipokusanyika kandoni mwa kitanda cha Baba, Roho wa Bwana alikuwa wa kushikika na kwa kweli ali-tenda kama mfariji kwetu. Tuko na amani. ... Iimekuwa jambo gumu sana yoyote kati yetu aliyewahi kuwa na uzoefu nalo, lakini tunajisikia amani kwa kujua kwamba Baba yetu wa Mbinguni ameahidi kwamba tutaishi pamoja kama familia tena. Baada ya daktari kumwambia Baba katika hospitali ya kwamba hapa-kuwa na kitu kilichosalia cha kufanya, alitutazama sote kwa imani kamilifu na kwa ujasiri aliuliza, Je kuna mtu yeyote katika chumba hiki aliye na tatizo na mpango wa wokovu? Sisi tunashukuru kwa baba na mama ambao wametufundisha kuwa na imani kamili katika mpango huu" (The Rock of Our Redeemer, Ensign au Liahona, May 2010, 17 18).

Page 336: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

321

UtanguliziKufuatia vita vikubwa kati ya Wanefi na Walamani, amani ilitulia nchini. Karibu miaka miwili baadaye, mtu aitwaye Korihori alianza kuhubiri kwamba Mungu hayupo, kwamba hakutakuwa na Kristo, na kwamba kulikuwa hakuna dhambi. Yeye aliwatukana viongozi wa Kanisa, akidai wao walikuwa wakifundisha mila za ujinga. Mafundisho yake ya uongo yalisababisha watu wengi kutenda dhambi kubwa. Korihori alile-twa mbele ya Alma, ambaye alimshuhudia Yesu Kristo

na alifundisha kwamba mambo yote yanashuhudia Muumba Mkuu. Hatimaye Korihoir alikuwa bubu kwa nguvu ya Mungu na akashawishika juu ya ukweli. Hata hivyo, wakati alipoomba sauti yake kurejeshwa, Alma alikataa ombi lake, akisema kwamba angefundisha mafundisho ya uongo tena kama angerudishiwa sauti yake. Korihori alitumia maisha yake yote akiomba chakula mpaka alipokanyagwa kanyagwa hadi kifo na kundi la wapinzani Wanefi walioitwa Wazoramu.

SOMO LA 88

alma 30

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 30:1–18Korihori, mpinga Kristo, akashifu mafundisho ya KristoKabla ya darasa kuanza, dunga tundu ndogo chini ya kopo la soda na ruhusu kilichomo kitiririke nje. Onyesha darasa kopo bila kufafanua kuwa ni tupu. Uliza nani anaitaka na kiasi gani watakuwa radhi kuilipia. Mwite mwanafunzi aje mbele, kuchunguza kopo, na kuliambia darasa ni nini kilichopo ndani (Badala ya kopo la soda, unaweza pia kutumia sanduku lolote tupu, mfuko, au kifungashio ambacho kwa kawaida kina kitu ambacho wanafunzi wangependa.)• Mafundisho ya uongo yanafanana vipi na mkebe huu wa soda? (Mara nyingi huvutia

kwa nje lakini ni tupu kwa ndani.)Eleza kwamba katika somo la leo, wanafunzi watajifunza kuhusu mtu mmoja aliyeitwa Korihori. Wanapojifunza Alma 30, wahimize kufikiria jinsi mafundisho ya Korihori yali-mwacha na wengine wakiwa tupu kiroho.Waambie wanafunzi kwamba baada ya wakati wa vita dhidi ya Walamani, watu wa Amoni (Anti- Nefi- Lehi) na Wanefi waliingia katika kipindi cha amani. Kisha Korihori akavuruga amani yao. Waulzie wanafunzi wasome Alma 30:6, 12, wakitafuta neno linalomwelezea mtu huyu. Neno ni Mpinga- Kristo Eleza kwamba ufafanuzi mmoja wa neno hili ni mtu yeyote au kitu chochote ambacho kina karama za bandia za injili ya kweli ya mpango wa wokovu na ambacho kwa uwazi au kwa siri kinampinga Kristo [Guide to the Scriptures, Antichrist, scriptures.lds.org].)Andaa zoezi lifuatalo kwenye kitini au kwenye ubao kabla ya darasa. Kama utaliweka ubaoni, waulizie wanafunzi kulinakili katika daftari au shajara zankujifunza maandiko. Itawasaidia kuona jinsi Shetani na wale wanaomtumikia hutumia mafundisho ya uongo kutushawishi kutenda dhambi.

Mafundisho ya Uongo ya Korihori Mpinga- Kristo

Mafundisho ya Uongo Ujumbe

1. alma 30:13–14 a. hamwezi kujua vitu ambavyo hamuoni. Kwa hivyo, huwezi kujua kwamba kutakuwa na Kristo.

2. alma 30:15 b. hakuna kitu chochote kama dhambi. hakuna kiwango cha dunia nzima kilicho sahihi au makosa.

Page 337: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

322

SoMo la 88

Mafundisho ya Uongo Ujumbe

3. alma 30:16 c. Watu hufanikiwa kwa juhudi zao pekee. hakuna chochote kama Upatanisho.

4. alma 30:17 (ikianza na kila mtu alifanikiwa )

d. haiwezekani kujua kuhusu mambo yatakayotokea katika siku zijazo, hivyo hupaswi kuamini katika Kristo au kufuata maneno ya watu ambao wanasema wao ni manabii.

5. alma 30:17 (ikianza na chochote ambacho mtu alifanya )

e. Msamaha wa dhambi ni wazo la wenda wazimu ambalo linatokana na desturi za uongo.

6. alma 30:18 f. hakuna maisha baada ya kifo, hivyo hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu hukumu baada ya maisha haya.

Gawa wanafunzi katika majozi. Waulize wasome Alma 30:12 18 pamoja. Waelekeze kuli-nganisha mafundisho ya uongo ya Korihori, ambayo yapo upande wa kushoto wa zoezi, na jumbe za mafundisho hayo, ambazo zipo upande wa kulia. (Majibu: 1 d, 2 a, 3 e, 4 c, 5 b, 6 f.)Ili kuwasaidia wanafunzi kuchambua mafundisho Korihori na kutumia walichojifunza, uliza maswali yafuatayo:• Ni mafunzo gani umeweza kukutana nayo ambayo ni sawa na mafundisho ya Korihori?• Kulingana na Alma 30:18, mafundisho ya Korihori yaliwaongoza watu kufanya nini?• Kwa nini unafikiri mafundisho haya huwaongoza watu kushindwa katika majaribu?• Tunaweza kujifunza nini kutoka mistari hii kuhusu hatari ya mafundisho ya uongo?

(Wasaidie wanafunzi kutambua kanuni ifuatayo: Shetani hutumia mafundisho ya uongo kutushawishi kutenda dhambi.)

Waulize wanafunzi kujifikiria wenyewe katika hali zifuatazo:Rafiki anakualika kucheza mchezo wa video. Unapowasili katika nyumba ya rafiki yako, unagundua kwamba mchezo ni wa vurugu na kwamba unajumuisha na wahusika ambao wamevaa nguo zisizo na heshima. Wakati unaposita kucheza mchezo, rafiki yako anaku-taka umweleze kwa nini hutaki kucheza.• Utasema nini? (Wanafunzi wanaweza kueleza kwamba mchezo unakiuka viwango vya

imani yao.)• Kama rafiki yako ataanza kukukosoa wewe au imani yako, na kusema kwamba inaweka

mipaka katika uhuru wako, unaweza kujibu vipi?

Alma 30:19–60Korihori anadai ishara kutoka kwa Alma na anapigwa kuwa bubu kwa nguvu ya MunguFanya muhtasari wa Alma 30:19–30 kwa kueleza kwamba Korihori alifundisha mafundi-sho ya uongo katika miji mitatu tofauti ya Wanefi. Hatimaye, aliletwa mbele ya mwamuzi mkuu wa nchi na mbele ya Alma, ambaye alikuwa kiongozi wa Kanisa. Unaweza kusema kwamba moja ya hoja kubwa za Korihori ni kwamba viongozi wa Kanisa waliwaweka watu katika utumwa — kwamba dini yao ilichukua uhuru kutoka kwa watu. Pia aliwashutumu viongozi wa Kanisa kuwa walitafuta faida ya kibinafsi kutokana na kazi za watu.Waulize wanafunzi wasome Alma 30:31 kimya, wakitafuta mashitaka ya Korihori dhidi ya Alma na viongozi wengine wa Kanisa.Waalike wanafunzi wasome Alma 30:32–35 ili kugundua jinsi Alma alivyomjibu Korihori.• Jinsi gani umeona ukweli wa majibu ya Alma katika maisha ya viongozi wa Kanisa?Waalike wanafunzi wawili waje mbele ya darasa. Uliza wasome Alma 30:37–45kwa sauti, na moja asome maneno ya Alma na mwingine akisoma maneno ya Korihori. Waalike wali-obaki darasani kutafuta kile Alma aliwasilisha kama ushahidi wa kuwepo kwa Mungu.

Page 338: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

323

alMa 30

• Alma alitoa ushahidi gani wa kuwepo kwa Mungu? (Wanafunzi wanapojibu, unaweza kuandika majibu yao ubaoni. Unaweza pia kutaka kuwahimiza wanafunzi kuyaweka alama katika maandiko yao. Kama sehemu ya mjadala huu, sisitiza kwamba vitu vyote vinamshuhudia Mungu.

• Kati ya ushahidi ambao Alma aliorodheshwa, ni upi maalumu wenye nguvu kwako? Kwa nini?

Wape wanafunzi muda wa dakika chache kuandika. Waulize wao kuorodhesha ushahidi ambao wameuona unaoashiria kuwa kuna Mungu (Alma 30:44). Waalike wanafunzi ka-dhaa kushiriki orodha zao pamoja na darasa.• Uhahidi huu unakushawishi vipi wewe? Ni katika njia gani unazoweza kuimarisha

imani na ushuhuda wako?Fanya muhtasari Alma 30:46–50 kwa kueleza kwamba Korihori, akiwa bado hakubali ishara alizokuwa amepewa, alidai kuwa Alma amwonyeshe ishara ya kuwepo kwa Mungu. Katika kujibu, Korihori alipigwa kuwa bubu kwa nguvu ya Mungu. Akiamini nguvu ya Mu-ngu, Korihori aliandika kuhusu kwa nini alikuwa akihubiri dhidi ya Mungu Baba na Yesu Kristo. Alika mwanafunzi asome kwa sauti maelezo Korihori katika Alma 30:51–53.• Unafikiri Korihori alimaanisha nini wakati aliposema kwamba yeye alifundisha ma-

mbo ambayo yalikuwa yanapendeza katika akili za kimwili? Unaweza kuhitaji kueleza kwamba mafundisho ya Korihori yalifurahisha hamu za kimwili za watu wasio waadilifu badala ya hamu zao za haki za kiroho.

Fanya muhtasari wa Alma 30:54–59kwa kueleza kwamba Korihori alimwomba Alma aombe ili laana iweze kuondolewa kutoka kwake. Alma alikataa, na kusema kwamba kama Korihori akipokea uwezo wa kusema, angekufundisha tena mafundisho ya uongo kwa watu. Korihori akatupwa nje na alikwenda nyumba hadi nyumba, akiomba chakula. Hati-maye alikwenda kwa Wazoramu, ambao walikuwa wametengana na Wanefi, na akakanya-gwa kanyagwa hadi kifo.Waulize wanafunzi wasome Alma 30:60 kimya, wakitafuta kanuni ambazo Mormoni alifundisha.• Ni kanuni gani Mormoni anafundisha katika mstari huu?Hakikisha wanafunzi wanaelewa kwamba shetani hawezi kuwatetea watoto wake [wa-fuasi wake] siku ya mwisho.• Je! Hii ina tofauti gani na njia Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanavyotujali? (Wakati

wanafunzi wanapojadili swali hili, unaweza kuwataka wasome Alma 36:3 .)Shuhudia kweli ambazo wewe na wanafunzi mmejadili katika somo hili.

Page 339: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

324

SoMo la 88

Tangazo na Habari za UsuliAlma 30:52. Nilijua siku zote kwamba kulikuwa na Mungu

Mzee Robert D. Hales wa Akidi ya Mitume Kumi na Wa-wili alifundisha kuhusu umuhimu wa kutambua ishara ambazo tumepata kuhusu ukweli wa Injili:

"Kama hatutajisalimisha kwa ya ushawishi mpole wa Roho Mtakatifu, tunasimama katika hatari ya kuwa kama Korihori, mpinga- Kristo katika Kitabu cha Mor-moni. Si tu kwamba Korihori hakuamini kwa Mungu, lakini pia alimdharau Mwokozi, Upatanisho, na roho ya unabii, akifundisha uongo kwamba hakuna Mungu na hakuna Kristo.

"Korihori hakuridhika tu kumkataa Mungu na kimya kimya kwenda njia yake mwenyewe. Aliwadhihaki waumini na alidai kwamba nabii Alma amshawishi kwa ishara ya uwepo na nguvu za Mungu. Majibu ya Alma ni ya maana leo kama yalivyokuwa wakati ule: 'Wewe umepata ishara za kutosha; utamjaribu Mungu wako? Je! Utasema, nioneshe ishara, wakati una ushuhuda wa ndugu zako hawa, na pia Manabii wote watakatifu?

Maandiko yamewekwa mbele yako, wewe na vitu vyote vinaonyesha kuna Mungu; naam hata Dunia, na vitu vyote ambavyo vipo juu yake, naam na mwendo wake, naam na pia sayari zote ambazo huenda katika taratibu zake zina shuhudia kwamba kuna Muumba Mkuu.' [Alma 30:44.]

"Hatimaye Korihori alipewa ishara. Yeye alipigwa kuwa bubu. 'Na Korihori alinyoosha mkono wake na kua-ndika, akisema: ... Najua kwamba hakuna kingine isipo-kuwa nguvu ya Mungu pekee ndiyo iliyoweza kuniletea mimi haya; ndio, na nilikuwa kila siku najua kwamba kuna Mungu." [Alma 30:52.]

"Akina Kaka na Akina Dada, mnaweza mkawa tayari mnajua, ndani ya roho zenu, kwamba Mungu yu hai. Unaweza kuwa hujui yote kuhusu Yeye na huelewi njia Zake zote, lakini nuru ya kuamini ipo pamoja nawe, ukisubiri kuamshwa na kuimarishwa na Roho wa Mungu, na nuru ya Kristo, ambayo umezaliwa nayo." (Seeking to Know God, Our Heavenly Father, and His Son, Jesus Christ, Ensign or Liahona, Nov. 2009, 31 32).

Page 340: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

325

UtanguliziAlma alijifunza kwamba kundi la wapinzani wa Wanefi walioitwa Wazoramu walikuwa wamepotea kutoka katika ukweli wa injili na kuanguka katika mazoea ya uongo. Akisikitishwa na taarifa hizi za uovu, Alma ali-chukua kundi la wamisionari kufundisha neno la Mungu kwa Wazoramu. Alma na wenzake waliona ibada za uasi

za Wazoramu, uyakinifu, na kiburi. Alma aliomba kwa dhati kwamba Bwana angewafariji na wenzake wali-pokuwa wanakabiliwa na changamoto hii na kwamba wangeweza kupata mafanikio katika kuwarejesha Wazoramu kwa Bwana.

SOMO LA 89

alma 31

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 31:1 7Alma na wenzake waondoka Zarahemla kuhubiri neno la Mungu kwa Wazoramu wakengeufuWaulize wanafunzi kufikiri kuhusu nini watafanya kama rafiki au mwanafamilia angeanza kupotea kutoka kuiishi injili.• Ungeweza kufanya nini ili kumwasaidia mtu huyu kurudi kwenye Kanisa? Unawezaje

kuamsha katika mtu hamu ya kushika amri? Kwa nani ungeweza kumgeukia kwa msa-ada katika kufanya kazi na wanafamilia au rafiki yako?

Waeleze wanafunzi kwamba somo la leo linaonyesha jinsi Alma na wengine kadhaa waja-ribu kusaidia kundi la watu ambao walikuwa wamepotoka kutoka kwenye injili. Mualike mwanafunzi asome Alma 31:1 4 kwa sauti. Uliza darasa litafute wasiwasi ambao Alma na wengine walikuwa nao kuhusu Wazoramu.• Ni zipi zilikuwa hisia za Alma aliposikia kuhusu uovu wa Wazoramu?• Kwa nini Wanefi walianza kuwa na hofu kwa sababu ya Wazoramu?Waulize wanafunzi wafikirie kuwa wana nafasi ya kumshauri Alma jinsi ya kutatua ma-tatizo yake kuhusu Wazoramu. Waulize wanafunzi kile wangeweza kupendekeza yeye afanye. Mualike mwanafunzi asome Alma 31:5 kwa sauti. Uliza darasa litafute kile Alma alijua kingekuwa njia ya ufanisi zaidi ya kuwasaidia Wazoramu.• Alma aliamua kufanya nini ili kuwasaidia Wazoramu?• Katika jitihada za kuwasaidia watu kubadilika, kwa nini unafikiri neno la Mungu lina

nguvu zaidi kuliko nguvu au mbinu nyingine?Kulingana na Alma 31:5, tunaweza kujifunza nini kuhusu nguvu ya neno la Mungu katika maisha yetu? (Wanafunzi wanaweza kutumia maneno tofauti, lakini hakikisha kuwa wao wanatambua ukweli ufuatao: Tunapojifunza neno la Mungu, litatuelekeza tufanye kilicho cha haki. Unaweza kuandika ukweli huu ubaoni.)Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa vyema nguvu ya neno la Mungu katika kutusaidia kufa-nya kilichocha haki, shiriki kauli ifuatayo ya Rais Boyd K. Packer wa Akidi wa Mitume Kumi na Wawili. Unaweza ukataka kuandika kauli hii kwenye ubao au kuiandaa kama kitini.)

"Mafundisho ya kweli, yakieleweka, hubadilisha mtazamo na tabia. "Mafunzo ya mafundisho ya injili yataboresha tabia kwa upesi kuliko ma-funzo ya tabia yanavyoweza kuboresha tabia. Ndio maana tunasisitiza kwa nguvu sana kujifunza ya mafundisho ya injili" (Little Children, Ensign, Nov. 1986. 17).Waalike wanafunzi waeleze kuhusu wakati ambapo wao au mtu fulani

wanayemjua alipata hamu kubwa ya kufanya kilicho haki kwa sababu ya maandiko au mafundisho ya viongozi wa Kanisa.

Page 341: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

326

SoMo la 89

Fanya muhtasari wa Alma 31:6–7 kwa kuwaambia wanafunzi kwamba kama matokeo ya imani ya Alma katika nguvu ya neno la Mungu, yeye na watu wengine saba walikwenda kuhubiri kwa Wazoramu.

Alma 31:8–23Wazoramu waomba na kuabudu kwa namna ya uongoWaeleze wanafunzi kwamba wakati Alma na wenzake walipoenda miongoni mwa Wazo-ramu, waliona watu wakimwabudu Mungu kwa namna ya kushangaza.Alika wanafunzi wasome Alma 31:8–11 kimya, wakitambua maneno na vishazi vinavyo-eleza kuabudu kwa Wazoramu. Sisitiza kwamba tanbihi 10 a inapendekeza kuwa kishazi maonyesho ya kanisa ni kuhusiana na ibada na vile vile sala na dua kwa Mungu kila siku.• Kwa mujibu wa aya ya 10, Wazoramu walikuwa wanafanya nini kilicho wafanya wawe

katika mazingira hatari kwa majaribu? • Tunaweza kujifunza nini kutokana na kushindwa kwa Wazoramu kuendelea katika ma-

ombi na dua kwa Mungu kila siku? Majibu ya wanafunzi yanaweza kutofautiana, lakini wanapaswa kueleza kwamba juhudi zetu za kuomba kila siku na kushika amri hutuimarisha dhidi ya majaribu. Unaweza kuandika kanuni hii ubaoni. Unaweza pia kupendekeza kwamba wanafunzi waandike hili katika maandiko yao matakatifu karibu na Alma 31:9–11.)

• Ni wakati gani umeona kwamba maombi ya kila siku yanaweza kutusaidia kukinza majaribu?

Kama sehemu ya mjadala wa wanafunzi kwa swali hili, soma kauli ifuatayo ya Mzee Ru-lon G. Craven wa Wale Sabini:"Wakati wa kipindi cha miaka iliyopita nimekuwa nikiombwa wakati mwingine na Ndugu kukutana na washiriki wa kanisa waliotubu na kuwasahili kwa ajili ya marejesho ya baraka zao za Hekaluni. Hii imekuwa siku zote ni mwendelezo wa uzoefu wa kiroho kurejesha baraka za wale watu wa ajabu ambao wametubu. Mimi nimewauliza baadhi yao swali, 'Ni nini kilichotokea katika maisha yako kilichokusababishia wewe kupoteza ushiriki wako katika Kanisa kwa muda?' Kwa macho yaliyojawa na machozi wao walijibu: 'Mimi si kutii kanuni za msingi za injili: sala, kuhudhuria kanisa kila mara, kuhudumu katika kanisa na kujifunza Injili. Mimi kisha nilijisalimisha kwa majaribu na kupoteza uongozi wa Roho Mtakatifu'" (Temptation, Ensign, May 1996, 76).Mualike mwanafunzi asome Alma 31:12–14 kwa sauti. Kisha alika mwanafunzi mwingine asome Alma 31:15–18 kwa sauti. Kabla ya mwanafunzi wa pili kusoma, liambie darasa lifikirie juu ya jinsi wangeweza kujibu kama wangesikia mtu akiomba kwa njia hii.• Ungekuwa na hofu gani kama ungesikia mtu akiomba kwa namna hii?• Ni yapi baadhi ya mafundisho ya uongo ambayo Wazoramu walikariri katika maombi yao?• Ni upi msimamo wa Wazoramu kwa watu wengine? Unaweza kutaka kuelekeza nathari ya

wanafunzi kwa kasi ambayo maneno sisi na sisi huotokea katika maombi ya Wazoramu.)Mualike mwanafunzi asome Alma 31:19–23 kwa sauti. Uliza darasa lifuatilie na litafute matatizo ya ziada ya muundo wa kuabudu kwa Wazoramu. Waulize wanafunzi watoe taarifa ya kile wanapata.• Unafikiri Wazoramu wangehitaji kufanya mabadiliko yapi ili kuabudu kwao kuwe na

staha kuu na kumpendeza Bwana?Eleza kwamba sisi humwabudu Mungu kwa kutoa kwake upendo wetu, staha, na ibada. (Unaweza ukataka kuorodhesha vipengele vya kuabudu kwenye ubao.) Tunapaswa kuwa wenye kuabudu si tu katika mtazamo wetu na vitendo wakati tunaomba, kufunga, na kuhudhuria Kanisani lakini katika mtazamo wetu na matendo katika kila siku. Wahimize wanafunzi kutathmini mwelekeo na uamini wa kuabudu kwao wenyewe.Waulize wanafunzi watambue njia mbalimbali ambazo tunaweza kumwabudu Mungu vizuri. Ruhusu muda wa kutosha kwao ili kushiriki mawazo. Unaweza ukataka kuwa na mwanafunzi aandike haya ubaoni.

Page 342: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

327

alMa 31

• Tunapaswa kuwa na mtazamo gani tunapoabudu? Tunawezaje kuendelea kuweka msi-mamo huo kila siku?

Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa jinsi tabia zetu huathiri kuabudu kwetu, alika mwanafu-nzi asome kauli ifuatayo ya Mzee Dallin H. Oaks wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili:

"Kuabudu mara nyingi hujumuisha vitendo, lakini kuabudu kwa kweli daima huhusisha tabia fulani ya akili."Msimamo wa kuabudu huleta hisia za ndani kabisa za utii, kuabudu, na heshima. Kuabudu unachanganya upendo na staha katika hali ya ibada ambayo huleta roho zetu karibu na Mungu" (Pure in Heart [1988], 125).Alika wanafunzi waandike katika daftari au shajara za kujifunza maandiko

tathmini fupi ya muundo wa kibinafsi wa sasa na tabia zao za kuabudu katika makundi yafuatayo: sala ya binafsi ya kila siku, mafunzo ya maandiko ya kibinafsi, utiifu wa amri, na kuhudhuria kanisani na kushiriki sakramenti kila juma. Waulize wanafunzi kuweka lengo la kuboresha kuabudu kwao kwa kibinafsi kwa kila siku.

Alma 31:24 38Alma anaomba nguvu na mafanikio katika kuwarudisha Wazoramu kwa BwanaWaalike wanafunzi wasome Alma 31:24–25 kimya, wakitafuta mitazamo na tabia ambazo zili-ambatana na ukengeufu wa Wazoramu. Waulize wanafunzi watoe taarifa ya kile walichopata.Eleza kuwa Alma alipoona uovu wa Wazoramu, aliomba. Waulize wanafunzi kujigawa ka-tika majozi. Acha majozi yajifunze Alma 31:26–35 na kujadili maswali yafuatayo. Unaweza kutaka kutoa maswali haya kama kitini au yaandike ubaoni kabla ya darasa kuanza.)• Ni nini kilikuwa lengo la maombi wa Wazoramu? (Walijizingatia wenyewe.)• Ni nini kilikuwa lengo la maombi ya Alma? (Alilenga kuwasidia wengine) Hata alipoo-

mba kwa ajili yake mwenyewe na wenzake, aliomba nguvu za kuwahudumia Wazoramu.)• Ni vipengele vipi vya sala ya Alma ungependa kuingiza katika maombi yako ya kibinafsi?Andika yafuatayo kwenye ubao:

Kama tukiomba na kutenda kwa imani, ... Eleza kuwa baada ya Alma kuomba msaada katika kufikia Wazoramu, yeye na wenzake walianza kuhudumu, bila kujifikiria wenyewe. (Alma 31:37 ). Waulize wanafunzi wasome Alma 31:36–38 kimya, wakitafuta baraka ambazo ziliwajia Alma na wenzake walipopokea baraka za ukuhani na kuhubiri injili. (Unaweza kutaka kueleza kwamba katika Alma 31:36, kishazi alipiga mikono yake juu hao inamaanisha kuwekewa mikono. Ona tanbihi 36b.)• Baraka gani ziliwajia Alma na wenzake kwa sababu ya maombi na vitendo yao?Kulingana na kile ulichojifunza kutoka kwa mfano wa Alma na wenzake, ni kwa jinsi gani unaweza kukamilisha taarifa iliyo ubaoni? Wanafunzi wanaweza kutoa majibu kadhaa tofauti ambayo ni ya kweli. Fanya muhtasari wa majibu yao kwa kukamilisha taarifa iliyo ubaoni: kama tukiomba na kutenda katika imani, Bwana ataitumarisha katika majaribio yetu).Eleza kuwa kufuatia maombi yake, Alma na wenzake walionyesha imani yao kwa kwenda kufanya kazi na kuamini kuwa Bwana angewakimu walipokuwa wakimhudumu. Alika wanafunzi wafuate mfano Alma wa kuomba katika imani.

Wahimize wanafunzi kuweka malengo na kutumia waliyojifunzaRais Thomas S.Monson alifundisha umuhimu wa kuwaalika wanafunzi kuchukua hatua ya kile walichojifunza darasani. Lengo la mafundisho ya injili si kwa kumwaga habari ndani ya mawazo ya washiriki wa darasa. Lengo ni kushawishi mtu kufikiria juu ya, kuhisi juu ya, na kisha kufa-nya kitu kuhusu kuishi kanuni za Injili. ... "Ninasikia na ninasahau"Ninaona na ninakumbuka "Ninafanya na ninaji-funza" (katika Confe-rence Report, Oct. 1970, 107 8).

Page 343: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

328

UtanguliziBaada ya kushuhudia kuabudu kwa Wazoramu kwa ukengeufu, Alma na wenzake walianza kuhubiri neno la Mungu kwa Wazoramu. Wakaanza kupata mafani-kio miongoni mwa watu ambao walikuwa maskini na

ambao walikuwa wametupwa nje ya masinagogi yao. Kwa kulinganisha neno la Mungu na mbegu, Alma aliwafundisha watu jinsi ya kupokea neno la Mungu na kuongeza imani yao.

SOMO LA 90

alma 32

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 32:1–16Wazoramu wanyenyekevu waonyesha kwamba wako tayari kusikia neno la MunguWaalike wanafunzi wafikirie kwamba wewe ni rafiki ambaye umewauliza jinsi una-vyoweza kujua kama injili ya Yesu Kristo ni kweli. Waulize kile wangesema kukusaidia kupokea ushuhuda.Baada ya wanafunzi kushiriki mawazo yao, andika kwenye ubao Jinsi ya kupokea na kuima-risha ushuhuda. Waambie wanafunzi kwamba katika somo lote, utaorodhesha kanuni na umaizi ambao watagundua kuhusu jinsi ya kupokea na kuimarisha ushuhuda.Wakumbushe wanafunzi kwamba Alma na ndugu zake walikuwa wameona kuabudu kwa uo-ngo kwa Wazoramu, kundi kengeufu la Wanefi. Kwa Sababu ya huzuni yake ya uovu wa watu, alikuwa ameomba faraja na nguvu ya kuwa na uwezo wa kuwafundisha. (Ona Alma 31.)Mualike mwanafunzi asome Alma 32:1–3 kwa sauti. Uliza darasa litafute kundi gani la Wazoramu ambalo lilionyesha kuvutiwa na ujumbe wa wamisionari. Waulize watoe taarifa ya kile walichopata.• Kulingana na Alma 32:3, ni kwa njia gani watu hawa walikuwa maskini? (Walikuwa

maskini kwa vitu vya ulimwengu; na pia walikuwa maskini katika mioyo yao.) • Unafikiri inamaanisha nini kuwa maskini katika moyo?Ili Kuwasaidia wanafunzi kujibu swali hili, alika baadhi yao kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka Alma 32:4–12. (Wanafunzi wanaweza kupendekeza kwamba kuwa maskini katika moyo ni pamoja na kuwa mnyenyekevu, mwenye toba, na tayari kusikia neno la Mungu.)• Ni kwa jinsi gani swali katika Alma 32:5 linaonyesha kwamba Wazoramu walikuwa mas-

kini katika mioyo? • Umaskini ulipelekea vipi baraka kwa kikundi hiki cha Wazoramu?• Aya hizi zinafundisha nini kuhusu kupokea na kuimarisha ushuhuda? (Wanafunzi wa-

naposhiriki kanuni tofauti, ziandike chini ya mada iliyopo ubaoni. Hakikisha kuwa wa-natambua kanuni ifuatayo: Unyenyekevu hututayarisha kupokea neno la Mungu.)

• Kwa nini unyenyevu ni muhimu katika mchakato wa kupokea na kuimarisha ushuhuda?Alika wanafunzi wachache wachukue zamu kusoma kwa sauti kutoka Alma 32:13–16. Uliza darasa litafute njia mbili tofauti ambazo watu wanaweza kuwa wanyenyekevu. (Watu wanaweza kuchagua kuwa wanyenyekevu au wanaweza kushurutishwa kuwa wanyenyekevu.)• Tunaweza kujifunza nini kuhusu unyenyekevu kutoka kwenye aya hizi? (Wasaidie wa-

nafunzi kutambua kanuni ifuatayo: sisi hubarikiwa zaidi wakati tukichagua kuwa wanyenyekevu kuliko wakati tunapolazimishwa kuwa wanyenyekevu.) Kwa nini unafikiri ni bora kuchagua kuwa wanyenyekevu?

• Unafikiri inamaanisha nini kujinyenyekeza kwa sababu ya neno? (Alma 32:14) Hii ina-wezaje kutumika kwa mitazamo yetu katika kanisa, seminari, au mafunzo ya familia ya maandiko?

Page 344: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

329

alMa 32

Alma 32:17–43Alma anawafundisha Wazoramu jinsi ya kuongeza imani yao.Eleza kwamba Alma alitambua dhana potovu ambayo watu wengi wanayo kuhusu kupata ushuhuda. Waulize mwanafunzi wasome Alma 32:17–18 kwa sauti wakati darasa likibaini-sha wazo hili la uongo.• Ni dhana ipi ya uongo ambayo watu wengi walikuwa nayo kuhusu kupata ushuhuda?• Kuna ubaya gani katika kudai ishara kabla ya kuamini? (Unaweza kutaka kuwakumbu-

sha wanafunzi juu ya mfano wa Sheremu katika Yakobo 7:13–16 na mfano wa Korihori katika Alma 30:43–52. Unaweza pia kuwaacha wasome Mafundisho na Maagano 63:9 na kusisitiza kwamba ishara ni zao la imani, na sio kitu ambacho tunadai kabla ya kuwa na imani.

Elezea kwamba Alma aliwafunza watu imani ni nini. Waalike wanafunzi wasome Alma 32:21 kimya kimya, wakitafuta maelezo ya imani ya Alma. Elezea kwamba mstari huu ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Unaweza kutaka kuwahimiza wanafunzi kuualamisha kwa njia ya kipekee ili waweze kukipata kwa urahisi.Waombe wanafunzi wasome Alma 32:22 kimya kimya, wakitafuta ushauri wa jinsi ya ku-pokea na kuimarisha ushuhuda. Waalike watoe taarifa za kile wamegundua.Ongeza Kukumbuka rehema za Mungu na Kuamini neno la Bwana katika orodha kwenye ubao.• Kwa nini vitendo hivi ni muhimu katika ukuzaji wa imani yenu?Elezea kwamba ili kuwasaidia Wazoramu kuelewa jinsi kuamini katika neno la Mungu, Alma alipendekeza kwamba wanaweza kufanya majaribio.• Kwa nini watu wanafanya majaribio ya kisayansi? (Ili kugundua kama nadharia au

wazo ni kweli.)Waulize wanafunzi waelezee majaribio wanayofanya katika madarasa yao ya sayansi au katika mazingira mengine. Wasaidie wao kuona kwamba majaribio yanahitaji kitendo, siyo tu makisio, katika sehemu ya mtafiti. Mfanyiko wa kupokea au kuimarisha ushuhuda pia huhitaji kitendo.Acha mwanafunzi asome Alma 32:27 kwa sauti. Uliza darasa litafute jaribio Alma aliwaa-lika Wazoramu kufanya. Ongeza Kujaribu juu ya neno katika orodha kwenye ubao.• Unafikiria Alma alimaanisha nini aliposema "kujaribu juu ya maneno [yangu]?"• Unafikiria Alma alimaanisha nini aliposema "mtaamka na kuziwasha akili zenu" (Una-

weza kuhitaji kuelezea kwamba neno akili inarejea uwezo wa kufikiria na kutenda na kukamilisha mambo. Alma alikuwa anawaalika watu kutenda juu ya maneno yake. Una-weza kutaka kuongeza Mtaamka na Kuziwasha akili zenu katika orodha kwenye ubao.)

• Unafikiria inamaanisha nini “kufanya chembe ya imani”?Ili kuwasaidia wanafunzi kugundua jinsi wanaweza kuanza kufanya majaribio haya katika maisha yao, waalike wao wasome Alma 32:28 kimya kimya.• Alma alilinganisha nini na neno la Mungu? (Mbegu.)• Ni baadhi ya vyanzo vya neno la Mungu? (Majibu yanapaswa kujumuisha maandiko, mafu-

ndisho ya manabii wa siku za mwisho na ufunuo wa kibinafsi kutoka kwa Roho Mtakatifu.)• Alma alisema sharti tufanye nini na “mbegu” hii?Orodhesha majibu ya wanafunzi kwenye ubao. Unaweza kutaka kuyaandika chini ya Kujaribu juu ya neno, ambayo ulikuwa umeandika mapema. Orodha inaweza kujumuisha kauli zifuatazo:

1. Toa nafasi kwa neno (au mbegu) kupandwa katika moyo wako. 2. Usitupilie mbali neno kwa kutoamini kwako. 3. Tambua ukuaji wa neno ndani yako.

Ili Kuwasaidia wanafunzi kuelewa nini walichosoma kuhusu majaribio, uliza maswali yafuatayo:• Ni kwa jinsi gani neno la Mungu ni kama mbegu inayoweza kupandwa katika mioyo

yetu? (Majibu yanaweza kujumuisha kwamba inaweza kukua, kwamba inaweza kutupa nguvu, na kwamba tunatakiwa kuilirutubisha.)

Alma 32:21 ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Rejelea wazo la kufundisha hapo mwisho wa somo ili kuwasaidia wanafunzi kwa umahiri wao wa kifungu hiki.

Page 345: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

330

SoMo la 90

Wanafunzi wanapojadiliana kufananishwa kwa neno la Mungu na mbegu, waalike wa-some Alma 33:22–23 kimya. Kabla hawajasoma, waulize watafute maelezo ya Alma ya “neno hili.” Wasaidie kuona kwamba linamaanisha Yesu Kristo na Upatanisho Wake.• Je! Unafikiri inamaanisha nini “kutoa nafasi” kwa neno kupandwa katika mioyo yetu? (Ona

Alma 34:32–34. Majibu yanaweza kujumuisha kwamba tunahitaji kufungua mioyo yetu na kwamba tunahitaji kutoa nafasi katika maisha yetu kwa ajili ya kujifunza maandiko.

• Je! Unafikiria inamaanisha nini kuhisi kwamba neno la Mungu “linavimba” ndani yako? Kama neno la Mungu linavimba ndani yako, basi ni nini kinatokea katika ushuhuda na imani yako?

• Ni lini Neno la Mungu lilijaza nafsi yako na kuelimisha uelewa wako?Waulize wanafunzi wachukue zamu kusoma kutoka Alma 32:29–34. Alika darasa lifuatilie, likitafuta neno ama vishazi ambavyo vinaelezea kile tulichojifunza kuhusu neno la Mungu. Kisha waulize wanafunzi wasome maneno na vishazi walivyovipata na welezea kwa nini wamevichagua. Rejea katika picha ubaoni na uliza:• Kwa nini imani yetu bado haijakamilika baada ya kufanya jaribio hili? Je! Ni kitu gani

zaidi unafikiri tunakiitaji kukifanya ili kupokea ushuhuda wa kudumu wa injili?• Je! Mchakato wa kusaidia mti kuota unafanana vipi na mchakato wa kuimarisha ushuhuda?Waalike wanafunzi wachukue zamu kusoma kwa sauti kutoka Alma 32:35 40. Uliza darasa litafute ushauri wa Alma kuhusu jinsi ya kukamilisha jaribio.• Kulingana na Alma 32:37–40, ni nini ambacho ni sharti tukifanye ili imani yetu ka-

tika neno la Mungu iweze kuendelea kukua? (Ongeza Rutubisha neno kwenye orodha ubaoni.)

• Tunaweza kukifanya nini ili kurutubisha neno? (Majibu yanaweza kujumuisha kwamba tunaweza kusoma maandiko kila siku, kuomba kwa ajili ya mwongozo tunapojifunza, kutafuta njia ambazo maandiko na mafundisho ya manabii wa siku za mwisho yanavyo-fanya kazi katika maisha yetu, na kushiriki kile tunachojifunza.)

• Nini kitatokea tunapotelekeza mti ama kushindwa kuurutubisha? Je! Ni nini hutokea wakati tusipopuuza neno la Mungu ambalo limepandwa katika mioyo yetu?

Waulize wanafunzi waandike katika daftari au shajara za kujifunza maandiko kile wali-chojifunza kutoka Alma 32 kuhusu jinsi ya kupokea na kuimarisha ushuhuda. Unaweza kia kushauri kwamba waandike mafupisho haya katika maandiko yao karibu na Alma 32:37–43.Waalike wanafunzi kushiriki kile walichokiandika. Wanaposhiriki, hakikisha wanaelezea kwamba kama tutarutubisha kwa bidii neno la Mungu katika mioyo yetu, imani yetu na ushuhuda wetu wa Yesu Kristo na injili Yake utakua.Waulize wanafunzi wasome Alma 32:41–43, wakitafuta maelezo ya Alma kuhusu mti na matunda. • Ni wapi tena Kitabu cha Mormon kinajumuisha maelezo ya mti wenye matunda ambayo

ni “matamu kupita utamu wote”? (Unaweza kuhitaji kuwakumbusha wanafunzi mae-lezo ya mti wa uzima katika 1 Nefi 8:11–12 na 1 Nefi 11:9–24.)

• Katika ono la Lehi na Nefi la mti wa uzima, je, ni nini mti na tunda vinawakilisha? (Mti unawakilisha upendo wa Mungu kama unavyoonyeshwa kupitia Mwokozi na Upatani-sho Wake, na tunda linawakilisha baraka tunazoweza kupokea kupitia Upatanisho Ona soma la 12 katika kitabu hiki.)

• Katika ono la Lehi na Nefi, watu wanaweza kufika vipi katika mti ule? (Kwa kufuata fi-mbo ya chuma, ambayo inawakilisha neno la Mungu.) Hii inafanana vipi na mfananisho wa Alma wa neno la Mungu na mbegu?

Waalike wanafunzi wachache washiriki jinsi wamefuata desturi iliyoelezewa katika Alma 32. Waulize wao jinsi desturi hii imeathiri maisha yao. Fikiria kushiriki uzoefu wenu we-nyewe wakati mmehisi nguvu za neno la Mungu.

Page 346: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

331

alMa 32

Umahiri wa Maandiko —Alma 32:21Waombe wanafunzi watumie Alma 32:21 kutathimini jinsi watu katika hali zifuatazo wa-nafanya imani au hawafanyi imani. 1. Msichana ana ushahidi asili kwamba Kitabu cha Mormoni ni kweli kabla ya kukiamini. 2. Mvulana anasikia kwamba wavulana wote wastahiki wanahudumu misheni ya muda.

Ingawa familia yake ni maskini, yeye ana azimio la kuhudumu na anajitayarisha kuhudumu. 3. Msichana anataka kuwa msafi kutoka kwa dhambi zake kupitia Upatanisho wa Yesu

Kristo. Anajua anahitaji kukiri baadhi ya uvunjaji amri kwa askofu wake ili kutubu kika-milifu. Anapanga miadi ya kumwona askofu wake.

Angalia: Unaweza kutumia wazo hili wakati wa somo unapotanguliza kifungu cha umahiri wa maandiko, au unaweza kulitumia hapo mwisho wa somo.

Page 347: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

332

Somo la Mafunzo - NyumbaniAlma 25–32 (Kitengo cha 18)

Vifaa vya Matayarisho kwa Mwalimu wa Mafunzo - NyumbaniMuhtasari wa Masomo ya kila siku ya Mafunzo - Nyumbani. Muhtasari ufuatao wa mafundisho na kanuni ambazo wa-nafunzi walijifunza waliposoma Alma 25 32 (kitengo cha 18) haitarajiwi kufundishwa kama sehemu ya somo lako. Somo unalofundisha linazingatia machache tu ya mafundisho na kanuni hizi. Fuata uvuvio wa Roho Mtakatifu unapofikiria mahitaji ya wanafunzi.

Siku ya 1 (Alma 25–29)Wanafunzi walijifunza kanuni zifuatazo walipojifunza kuhusu furaha ya Amoni katika mafanikio ambayo yeye na ndugu zake waliyopata wakihubiri injili: Tunapojinyenyekeza, Bwana alituimarisha na anatutumia kama chombo katika mikono yake; tunapata furaha tunapomtumikia kwa uaminifu Bwana na watoto Wake. Kama walamani walioongolewa katika Injili na kukataa kutumia silaha, wanafunzi walijifunza kwa-mba tunapoongolewa kikamilifu katika Bwana, tunaweka maagano tuliyofanya Naye. Kutoka kwa mfano wa Alma, wanafunzi wametambua tunapata furaha tunapowasaidia wengine kutubu na kuja kwa Yesu Kristo.

Siku ya 2 (Alma 30)Kwa kusoma kuhusu mafundisho ya Korihori, mpinga- Kristo, wanafunzi walijifunza kwamba Shetani anatumia mafundisho ya uongo kutushawishi kutenda dhambi. Alma alijibu mafundi-sho ya Korihori kwa kusema kwamba vitu vyote vinamshuhudia Mungu kama Muumbaji Mkuu. Baada ya kusoma kwamba Ko-rihori alikanyagwa mpaka kufa, wanafunzi walielewa kanuni za Mormoni zilizoandikwa: “Shetani hatawaunga mkono watoto wake [wafuasi wake] katika siku za mwisho” (Alma 30:60).

Siku ya 3 (Alma 31)Wanafunzi waliposoma kuhusu nia ya Alma ya kuwaokoa Wazoramu kutoka katika ukengeufu, walijifunza kanuni zifu-atazo: Tunapojifunza neno la Mungu, litatuongoza kutenda kile kilicho sahihi. Juhudi za kila siku za kuomba na kuweka amri zinatuimarisha na zinatulinda dhidi ya majaribu. Kama tunaomba na kutenda kwa imani, ndipo tutapokea msaada wa kiungu katika majaribio yetu.

Siku ya 4 (Alma 32)Wanafunzi waliposoma kuhusu mafanikio ya Alma katika kuwahubiria maskini miongoni mwa Wazoramu, wanafunzi walijifunza kwamba unyenyekevu unatuandaa kupokea neno la Mungu. Alma alilinganisha kufanya imani na kupa-nda mbegu na kuirutubisha. Wanafunzi walijifunza kwamba kama watarutubisha kwa bidii imani katika neno la Mungu mioyoni mwetu, imani yetu na ushuhuda wetu katika Yesu Kristo na Injili Yake utakua.

UtanguliziAnza somo hili na shughuli ya kuwasaidia wanafunzi kutafuta kuwa vifaa katika mikono ya Mungu. Sehemu kubwa ya somo, hata hivyo, italenga katika matokeo ya kuamini na kutenda katika mawazo potofu kinyume na kuamini na kutenda katika Neno la Mungu, kama ilivyodhihirishwa katika Alma 30–32.

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 25–29Amoni na watoto wa Mosia wafurahia katika Bwana kwa jinsi Walamani wengi walivyoongolewa katika injiliKama ilivyonakiliwa katika Alma 26, Amoni na ndugu zake walifurahia mafanikio yao katika kazi ya Bwana. Acha wanafunzi wasome Alma 26:1–4, 11–13 na kutafuta kile ambacho Amoni na ndugu zake walikimilisha na jinsi walivyoweza kukamilisha. Wakumbushe wanafunzi kwamba mistari hii hufundisha kanuni ifuatayo: Tunapojinyenyekeza, Bwana hutuimarisha na kutumia kama vyombo katika mikono yake.

Alma 30Korihori adhihaki mafundisho ya KristoOnyesha darasa mbegu. Uliza waorodhesha mifano ya vitu wanavyovipenda vinavyotokana na mbegu. Kinyume na baadhi ya mimea, matunda, na mboga ambazo wanafunzi wameweza kuzitaja, onyesha kwamba kuna uwezekano kwamba mbegu inaweza kuota kuwa mmea ambao unazalisha matunda machu-ngu au hata matunda yenye sumu au kwamba inaweza kuimeza mimea mingine mizuri.

Andika maneno wazo na imani katika ubao na uliza: Jinsi gani wazo au imani vinaweza kuwa kama mbegu?

Elezea kwamba wanafunzi wanapojifunza na kujadili Alma 30–32 darasani hivi leo, watatofautisha matokeo ya kufuata mawazo potovu na matokeo ya kufuata neno la Mungu.

Waulize wanafunzi kuelezea Korihori alikuwa nani. Waalike wao wasome Alma 30:12–18, 23 na kutambua mawazo potovu aliyoyafundisha Korihori. Baada ya kuwa na muda wa kusoma, waalike waorodhesha ubaoni au katika kipande cha karatasi mawazo potovu mawili ama matatu ya Korihori ambayo wana-fikiria yanaweza kuwa ya hatari kwa imani ya dini ya mtu. Kisha waulize maswali yafuatayo:

• Ni baadhi ya matendo gani ambayo mawazo haya yanaweza kusababisha? (Wanafunzi wanapojibu, sisitiza kwamba wazo linaloelekea katika kitendo ni kama mbegu inayokua iwe mti.)

• Kulingana na Alma 30:18, mafundisho ya Korihori yaliwae-lekeza watu kufanya nini? (Wanafunzi wanapojibu, sisitiza kwamba Shetani hutumia mafundisho ya uongo kutu-shawishi ili kutenda dhambi.)

Page 348: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

333

SoMo la MafUnzo - nyUMbani

Mwalike wanafunzi wafanye muhtasari wa kile kilichomtokea Korihori. (Kama wanafunzi watahitaji msaada, waalike kutumia kichwa cha sura cha Alma 30 au kusoma Alma 30:52–53, 59 60.)

Alma 31Alma aongoza misheni kuwaokoa Wazoramu wakengeufuWakumbushe wanafunzi kwamba Wazoramu waliamini mawazo potovu na walianguka kwenye uongo au ukengeufu na matendo potovu. Katika Alma 31:5 tunajifunza kwamba tunaposoma neno la Mungu, litatuongoza kufanya kile kilicho sahihi.

Alma 32Alma anafundisha maskini wa Wazoramu jinsi ya kufanya imaniWakumbushe wanafunzi kwamba ingawa wengi wa Wazoramu walikataa kupokea neno la Mungu, Alma alianza kuwa na ma-fanikio miongoni mwa maskini. Aliwafundisha jinsi ya kufanya imani. Waulize wanafunzi kutathmini Alma 32:21, kifungu cha umahiri wa maandiko. Waulize wao waelezee kile mstari huu unawafundisha kuhusu imani.

Wakumbushe wanafunzi kwamba Alma alitumia mbegu kufundisha kuhusu mchakato wa ukuaji wa imani. Kisha uliza maswali yafuatayo:

• Ni vishazi vipi katika Alma 32:28 vinavyoonyesha kuwa mbegu hiyo, au kwa hali hii ni neno la Mungu, ni zuri?

• Je! Ni athari gani neno la Mungu linayo kwetu wakati tunapo-liruhusu lipandwe kwenye mioyo yetu?

Waulize wanafunzi kwamba Alma aliwahimiza Wazoramu kulijaribu neno la Mungu, au kupanda katika mioyo yao kwa kuliamini na kutenda kulingana na neno. Waalike wao wasome Alma 33:22–23, wakitafuta ni neno gani ambalo Alma alitamani hasa kwamba watu wapande katika mioyo yao. Unaweza ku-taka kuwahimiza wanafunzi kuandika mistari hii kama kielelezo cha marejeo karibu na Alma 32:28.

Acha wanafunzi wasome Alma 32:28–29, 31, 37, 41–42, wa-kitafuta zawadi tunazopokea kutokana na kuamini na kutenda katika neno la Mungu. Wanafunzi wanapojibu, hakikisha kanuni ifuatayo ni dhahiri: kama tukirutubisha kwa bidii imani yetu katika neno la Mungu mioyoni mwetu, imani yetu na ushuhuda wetu katika Yesu Kristo na Injili Yake utakua.

Kwa kuhitimisha somo hili, waalike wanafunzi kushiriki majibu yao kwenye somo la 4, kazi ya 4 katika shajara zao za kujifunza maandiko— kuhusu matokeo waliyoyaona katika maisha yao walipofuata jaribio ambao Alma alilielezea katika Alma 32.

Kitengo kinachofuata (Alma 33–38)Kuna hatari gani katika kuchelewesha toba? Amuleki anajibu swali hili na kutoa onyo. Pia, Alma anawashauri wawili wa wanawe anapokaribia mwisho wa maisha yake. Anasimulia utondoti kuhusu uongofu wake— akibadilika kutoka kwa mtu aliyepigana dhidi ya Mungu hadi kwa mtu aliyepigana kwa ajili ya Mungu— na jinsi alivyohisi wakati alipoachiwa huru kutoka katika hatia na maumivu ya dhambi zake.

Page 349: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

334

UtanguliziKikundi cha Wazoramu kilikuwa na hamu ya kujua jinsi ya kufuata ushauri wa Alma wa kupanda neno la Bwana katika mioyo yao na kufanya imani. Kwa kutumia maandiko, Alma alifundisha watu kuhusu kuabudu, sala, na neema tunayoweza kupokea kutoka kwa Mungu kwa sababu ya Mwokozi. Aliwahimiza watu kumtazamia Yesu Kristo na kuamini katika nguvu ya Upatanisho Wake.

Tazama: Somo la 94 hutoa nafasi kwa wanafunzi wa-tatu kufundisha. Unaweza kutaka kuchagua wanafunzi watatu sasa na kuwapa nakala ya sehemu iliyotengwa ya somo la 94 ili waweze kujiandaa. Wahimize wao kusoma nyenzo za somo kwa maombi na kwa kutafuta mwongozo wa Roho Mtakatifu ili waweze kujua jinsi ya kutohoa mahitaji ya somo kwa wanafunzi wenzao.

SOMO LA 91

alma 33

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 33Alma anawafundisha Wazoramu kuanza kuamini katika Yesu KristoAndika zoezi ubaoni• Inamaanisha nini kufanya zoezi kitu fulani? (Wanafunzi wanapokuwa wanajibu swali

hili, unaweza kumwambia mwanafunzi aonyeshe jinsi ya kutumia mikono yake, labda kwa kufanya mazoezi, au miguu yake, labda kwa kukimbia kwenye sehemu.)

Acha wanafunzi wasome Alma 33:1 kimya, wakitafuta zoezi ambalo Wazoramu walitaka kulielewa. Baada ya wanafunzi kutoa taarifa ya kile walichokipata, andika swali lifuatayo ubaoni: Je! Tunafanya vipi imani? Waalike wanafunzi watafute angalau majibu matatu kwa swali hili wanaposoma na kujadili Alma 33.Elezea kwamba Alma alipoanza kujibu maswali ya Wazoramu kuhusu jinsi ya kufanya imani, alisahihisha wazo potovu walilokuwa nalo kuhusu kuabudu. Mualike mwanafu-nzi asome Alma 33:2 kwa sauti. Uliza darasa litambue wazo potovu la Wazoramu kuhusu kumwabudu Mungu.• Kwa nini Wazoramu hawa walifikiria wasingeweza kumwabudu Mungu? (Kwa sababu

hawakuruhusiwa katika masinagogi yao)Waulize wanafunzi wafanye muhtasari wa kile walichojifunza katika Alma 31 kuhusu mfumo wa kuabudu wa Wazoramu. (Ona Alma 31:22.) Wazoramu walitoa sala hiyo hiyo mara moja kwa wiki katika masinagogi, na hawakuwahi kuzungumzia kuhusu Mungu tena wiki mzima)• Kwa nini mahudhurio ya Kanisa ni sehemu muhimu ya kuabudu kwetu? Ni njia gani

zingine tunaweza kumwabudu Mungu zaidi ya kuhudhuria katika mikutano ya Kanisa kila wiki?

Elezea kwamba Alma alinukuu mafundisho ya nabii aliyeitwa Zenosi kurekebisha mawazo potovu ya Wazoramu kuhusu kumwabudu Mungu. Waulize wanafunzi wasome Alma 33:3 kimya, wakitafuta neno ambalo Alma alilitumia bila kubadilisha mara zote na abudu (Neno ni sala.)Waalike wanafunzi wasome Alma 33:4–10 kimya, wakitambua kila hali ambayo Zenosi alisema alisalia.• Ni lini na wapi Zenosi aliposali?• Alma alifundisha nini kuhusu kuabudu aliponukuu maneno ya Zenosi? (Wasaidie

wanafunzi kugundua ukweli ufuatao: Tunaweza kumwabudu Mungu wakati wote kupitia sala.)

Rejea kwenye swali lililo ubaoni: Je! tunafanya imani? Chini ya swali hilo, andika Sali daima. • Ni kwa njia gani sala ni zoezi la imani kwa Baba yetu wa Mbinguni na Yesu Kristo?

Page 350: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

335

alMa 33

• Ni lini umesali katika hali kama hizo alizozitaja Zenosi? Sala yako ilijibiwa vipi? (Wa-kumbushe wanafunzi kwamba hawahitaji kushiriki uzoefu wao ambao ni wa kibinafsi sana au siri. )

Waalike wanafunzi kutathmini Alma 33:4–5, 8–9 kimya. Waulize watafute vishazi vinavyotaja neema za Mungu (kama vile wewe u mwenye rehema na wewe ulikuwa mwenye rehema).Ili kuwasaidia wanafunzi kuona kiunganishi kati ya Upatanisho wa Yesu Kristo na rehema ya Baba Yetu wa Mbinguni, mwalike wanafunzi asome Alma 33:11–16 kwa sauti Uliza darasa lifuatilie, likitafuta kishazi ambacho kinachoonekana mara nne katika mistari hii. (Maneno ni “kwa sababu ya Mwanao." Unaweza kutaka kuwahimiza wanafunzi kuweka alama katika kishazi hii.)• Unafikiria Zenosi alimaanisha nini aliposema, “Umegeuza hukumu yako dhidi yangu,

kwa sababu ya mwanao”? Wasaidie wanafunzi kutambua ukweli ufuatao: Tunapokea rehema ya Baba yetu wa Mbinguni, ikijumuishwa na msamaha wa dhambi zetu, kwa sababu ya Upatanisho wa Yesu Kristo. Unaweza kutaka kuwaalika wanafunzi kuandika ukweli huu katika maandiko yao karibu na Alma 33:11–16.)

Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa vyema rehema tunayoweza kuipokea kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo, fikiria kushikiri hadithi ifuatayo iliyonukuliwa na Rais Gordon B Hinckley:

"Mwalimu alisema, ‘Habari za Asubuhi, wavulana, tumekuja kuendesha shule.’ Walipiga kelele na wakafurahia kwa sauti zao za juu. Sasa, Nataka shule nzuri, lakini nakiri kwamba sijui vipi isipokuwa unisaidie. Fikiria kama tuna sheria chache. Hebu niambie, na nitaziandika ubaoni.’"Jamaa mmoja akasema kwa sauti, Hakuna kuiba! Na mwingine akasema kwa sauti, Katika saa Mwishowe, sheria kumi zilitokea ubaoni.

"'Sasa,' mwalimu akasema, sheria sio mzuri isupokuwa iambatanishwe na adhabu. Tutam-fanya nini yule anayevunja sheria?’"'Tumpige mgongoni mara kumi bila koti lake,’ likaja jibu kutoka kwa mmoja wa wanafunzi."'Hiyo ni kali sana, vijana. Mna uhakika kwamba mko tayari kuitetea?’ Mwingine aka-sema kwa sauti, ‘Nakubaliana na hoja,’ na mwalimu akasema, ‘Haya, basi tutayazingatia! Darasa, tulieni!’"Katika siku moja au kadhaa, ‘Tom Mkubwa’ alikuta chakula chake cha mchana kimei-biwa. Mwizi alipatikana —ni kijana mdogo mwenye njaa, wa umri wa karibu miaka kumi hivi. Tumempata mwizi na lazima aadhibiwe kulingana na sheria yenu —viboko kumi mgongoni mwake. Jim, njoo hapa!’ mwalimu alisema"Kijana mdogo, huku akitetemeka, alikuja taratibu akiwa na koti kubwa lililofungwa mpaka kwenye shingo na kuomba, ‘Mwalimu, Unaweza kunichapa kadri uwezavyo, lakini tafadhali, usiondoe koti langu!’ [Tazama: Unaweza kutaka kuelezea kwamba katika hadithi hii, neno lamba linamaanisha kumchapa mtu.]"'Vua koti lako,’ mwalimu alisema. 'Ulisaidia kuzitunga sheria hizi!’"'O, Mwalimu, usinifanye nifanye hivyo!’ Akaanza kutoa vifungo, na mwalimu aliona nini? Mvulana hakuwa ameva shati, na ulionekana mwili mdogo wenye mifupa ulio na kilema. "'Ninawezaje kumpiga mtoto huyu?’ alifikiri. Lakini lazima, lazima nifanye kitu kama ninataka kuhifadhi shule hii.’ Kila kitu kilikuwa kimya kama mauti."'Kwa nini haujavaa shati, Jim?’"Alijibu, ‘Baba yangu alikufa na mama yangu ni maskini sana. Nina shati moja tu na anali-fua leo, na nimevaa koti kubwa la kaka yangu ili linipe joto.’"Mwalimu, akiwa na fimbo mkononi, alisita. Hapo ndipo Tom Mkubwa aliruka kwa miguu yake na kusema, 'Mwalimu, kama hupingi, nitachukua kipigo cha Jim kwa ajili yake.""' Vyema sana, kuna sheria fulani ambayo mtu anaweza kuwa mbadala wa mwenzake. Je! Mnakubaliana na hili?’“Tom akalivua Koti lake na baada ya fimbo tano fimbo ikavunjika! Mwalimu aliinamisha kichwa chake katika mikono yake na kufikiria, ‘Je nawezaje kumaliza kazi hii mbaya?’ Halafu akaona darasa likilia, na aliona nini? Jim Mdogo alimfikia na kumshika Tom kwa mikono yake miwili katika shingo yake. ‘Tom, naomba unisamehe kwa kuiba chakula

Kutambua maneno na vishazi vilivyorudiwaManabii mara nyingi wanasisitiza kweli kupitia marudio. Wanafunzi wanapogu-ndua marudio katika maneno,vishazi,na ma-wazo, waulize kufikiria ukweli gani mwandishi anafundisha na kwa nini ni muhimu kuelewa ukweli huo.

Page 351: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

336

SoMo la 91

chako cha mchana, lakini nilikuwa na njaa ya kutisha. Tom, Nitakupenda mpaka nife kwa kupigwa kwa ajili yangu! Ndio, nitakupenda milele!’” [Mtunzi hajulikani.]Baada ya kunukuu hadithi hii, Rais Hinckley alisema, “Kutwaa kishazi kutoka katika ha-dithi hii ya kawaida, Yesu, Mkombozi wangu, alipata ‘kipigo kwa ajili yangu’ na yako pia” (“The Wondrous and True Story of Christmas,” Ensign, Dec. 2000, 4).• Je ni kwa jinsi gani maelezo haya yanahusiana na mafundisho ya Alma kuhusu Upata-

nisho wa Mwokozi? (Kama ikihitajika, elezea kwamba kukubali kwa Tom “kupigwa kwa ajili ya Jim” inawakilisha Upatanisho. Mwokozi amechukua adhabu kwa ajili ya dhambi zetu juu yake ili tusiweze kuvumilia adhabu hiyo kama tukitubu.)

Elezea kwamba baada ya kunukuu maneno ya Zenosi, Alma alinukuu maneno ya Zenoki, nabii mwingine. Soma Alma 33:15–16 kwa sauti kwa wanafunzi. Sisitiza kutoridhishwa kwa Baba yetu wa Mbinguni wakati watu wanapokataa kuelewa kile ambacho Mwanawe amekifanya kwa ajili yao. Waulize wanafunzi wasome Alma 33:12–14 kimya, wakitafuta chanzo ambacho Alma alitu-mia wakati aliposhiriki mafundisho haya. • Kwa nini Alma alikuwa anaelewa vizuri maneno ya Zenosi na Zenoki? (Kwa sababu

maneno yalikuwa katika maandiko. Ungependa kutoa sisitizo kwamba maneno ya Alma katika mistari ya 12 na 14 yanapendekeza kwamba Wazoramu pia walikuwa na uwezo wa kupata maandiko haya. Sisitiza kwamba maandiko yanashuhudia juu ya Yesu Kristo.)

Chini ya swali katika ubao, andika Jifunze na kuamini maandiko. Onyesha kwamba Alma alirejea kwenye maandiko mengine kuwasaidia Wazoramu kukuza imani yao katika Yesu Kristo. Onyesha picha ya Musa na Nyoka wa Shaba(62202; Gospel Art Book [2009], no. 16). Fanya muhtasari wa usimulizi huu kwa kuelezea kwamba wakati Musa alipokuwa akiwaongoza Waisraeli nyikani, watu wengi walianza kuasi dhidi yake na Bwana. Kutokana na kutotii kwao, Bwana alituma nyoka wenye sumu ambao waliwa-uma watu. Watu walienda kwa Musa kwa ajili ya msaada. Musa aliomba na alielekezwa kutengeneza nyoka juu ya mti kwa watu kuangalia. Alitii, akatengeneza nyoka wa shaba. (Ona Hesabu 21:4–9.) Acha wanafunzi wasome{ Alma 33:19 –20 kwa sauti. Alika darasa litambue kile kilitokea kwa wale ambao waliangalia nyoka wa shaba na nini kilitokea kwa wale ambao walichagua kutoangalia. • Kulingana na Alma 33:20, kwa nini watu wengi walichagua kutoangalia? Waulize wanafunzi watafakari kama wangechagua kutazama kama wangekuwa katika hali hiyo.Onesha picha ya Kusulubiwa (62505; Gospel Art Book, no. 57). Elezea kwamba nyoka wa shaba katika mti alikuwa ni wa “aina” (Alma 33:19). Katika maneno mengine, ilikuwa ni ishara ya kitu ambacho kingetokea siku sijazo. Iliwakilisha Yesu Kristo msalabani (ona Yohana 3:14).Waulize wanafunzi wasome Alma 33:21– 23 kimya, wakitafuta jinsi gani Alma alifananisha maelezo haya kwa Wazoramu. Baada ya wanafunzi kutoa taarifa ya kile waligundua, rejea tena kwenye swali ubaoni: Ni kwa jinsi gani tunaweza kufanya imani? • Ni nini maelezo ya Waisraeli na nyoka wa shaba yanafundisha kuhusu nini tunatakiwa

tufanye ili tuponywe kiroho? • Je! Alma 33:22– inajibu vipi swali hili? (Wanafunzi inabidi wagundue ukweli ufuatao:

Tunafanya imani kwa kuchagua kuamini katika Yesu Kristo na Upatanisho Wake.)Chini swali ubaoni, andika Amini katia Yesu Kristo na Upatanisho Wake. • Ni matendo gani ama mtazamo gani unauona katika watu wanaoamini katika Upatani-

sho wa Mwokozi?Kusisitiza imani hiyo kwa Yesu Kristo ni chaguo tunalofanya, elekeza usikivu wa wanafu-nzi kwenye kishazi kifuatacho katika Alma 33:23: “Na haya yote mnaweza kufanya kama mtaweza. Unaweza ukitaka kutia moyo wanafunzi kuwekea alama kishazi hiki. Andika maelezo yafuatayo ubaoni, na fikiria kuwapa moyo wanafunzi kuandika katika maandiko yao. (Kauli inapatikana katika “Inquire of the Lord” [address to CES religious educators,, Feb. 2, 2001] 1, si. lds. org.)

“Kila mtoto katika kila kizazi anachagua imani au kutoamini. Imani siyo urithi; ni chaguo” (Rais Henry B. Eyring).

Page 352: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

337

alMa 33

Waulize wanafunzi wajibu mojawapo ya maswali yafuatayo kwenye daftari au shajara ya kujifunza maandiko. (Unaweza ukitaka kuandika maswali haya ubaoni mbele ya darasa, andaa kitini na maswali, au soma maswali taratibu ili wanafunzi waweze kuyaandika.)• Je! Ni kwa jinsi gani chaguo yako ya kuamini katika Mwokozi imeshawishi maisha yako

ya kila siku? • Je! Ni kwai jinsi gani kujifunza kibinafsi maandiko kumeimarisha imani yako katika

Baba yako wa Mbinguni na Yesu Kristo?• Je! Sala zako za kibinafsi za kila siku na kuabudu kumeimarishaje imani yako katika

Baba yako wa Mbinguni na Yesu Kristo? • Unahisi ni nini Baba wa Mbinguni angependa ukifanye ili kufanya imani kuu?Waalike wanafunzi wachache kushiriki majibu yao. Shuhudia umuhimu wa kuchagua kuamini katika Mwokozi.

Page 353: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

338

UtanguliziBaada ya Alma kuwafundisha Wazoramu kuamini katika Mwana wa Mungu, Amuleki alitangaza ushu-huda wake mwenyewe wa Yesu Kristo, akitoa ushahidi wa pili. Amuleki, mwenza wa Alma, alisisitiza kwamba Upatanisho wa Yesu Kristo ni muhimu kwa ajili ya wo-kovu wa binadamu wote na kwamba kila mtu anaweza kupokea baraka zote za Upatanisho wanapoifanya imani hata toba. Wazoramu wengi walikubali mwaliko

wa Amuleki wa kutubu. Wakati Wazoramu waliotubu walipotupwa nje ya nchi yao na viongozi wao waovu na makuhani, Wanefi na watu wa Amoni waliwapa chakula, nguo, na ardhi kwa urithi wao. Matokeo yake, ni kwamba Walamani na Wazoramu ambao walikuwa hawajatubu walianza kujitayarisha kwa ajili ya vita dhidi ya Wanefi na watu wa Amoni.

SOMO LA 92

alma 34–35

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 34:1–14Amuleki anawafundisha Wazoramu kuhusu Upatanisho wa Yesu KristoAndika kauli zifuatazo ubaoni kabla ya darasa. Waulize wanafunzi waandike katika daftari au kipande cha karatasi kama wanafikiri kila kauli ni ya kweli ama uongo.

1. Wakati Yesu Kristo alipofanya upatanisho kwa ajili ya dhambi za binadamu, Yeye alipata mateso tu kwa watu wenye wema.

2. Watu wote wanahitaji upatanisho ili waweze kuokolewa. 3. Mtu yeyote anaweza kufanya upatanisho au kulipa kwa ajili ya dhambi za mwingine.

Baada ya wanafunzi kupata muda wa kunakili majibu yao, wakumbushe kwamba Alma alifundisha kundi la wa Wazoramu jinsi ya kupokea neno la Mungu na kufanya imani katika Yesu Kristo (Ona Alma 32–33). Fanya muhtasari Alma 34:1–7 kwa kuelezea kwamba Amuleki alimfuata Alma kwa kushiriki naye ushuhuda wake kuhusu Mwokozi. Waulize wanafunzi wapekue mafundisho ya Amuleki katika Alma 34:8 –9, 11 kimya, wakigundua vishazi ambayo vinaonyesha kama kila kauli ubaoni ni ya kweli ama uongo. Kisha tathimi kauli kama darasa. Majibu sahihi ni: 1. Uongo— “Atalipia dhambi za ulimwengu” (Alma 34:8 ). 2. Kweli— “Lazima upatanisho ufanywe, la sivyo wanadamu wote ni lazima bila kuepuka

wapotee” (Alma 34:9). 3. Uongo— “Sasa hakuna mtu yeyote ambaye anaweza kutoa dhabihu ya damu yake

ambayo italipia dhambi ya mwingine” (Alma 34:11).Baada ya wanafunzi kujadiliana majibu katika kauli ya 3, uliza: • Kwa nini unafikiria Yesu Kristo ni mtu wa pekee ambaye anaweza kufanya upatanisho

kwa ajili ya dhambi za ulimwengu? Kwa kuwasaidia wanafunzi kujibu swali hili, waalike wasome Alma 34: 10 14 kimya. Halafu soma kauli zifuatazo na Mzee Russell M, Nelson wa Akidi ya Kumi na Wawili:

“Upatanisho wake usio na kikomo— bila mwisho. Pia ilikuwa hauna kikomo ili wanadamu wote waweze kuokolewa kutoka katika kifo kisichokuwa na mwisho. Ulikuwa hauna kikomo katika masharti ya mateso Yake mazito. . . . Ulikuwa hauna mwisho katika mawanda— ulikuwa ufanyike mara moja kwa ajili ya wote. Na rehema ya Upatanisho imepanuliwa siyo tu kwa idadi ya watu isiyo na kikomo, bali pia kwa idadi kubwa isiyo na kikomo ya dunia

zilizoumba Naye. Ulikuwa hauna kikomo kupita kipimo cha mwanadamu au uelewa wa mwili unaokufa.

Fundisha kwa Roho na shuhudia kuhusu Yesu KristoFanya yote uwezayo ku-jenga mazingira ambayo wanafunzi wanaweza kufundishwa kwa Roho Mtakatifu. Moja kati ya njia za maana sana za kujenga mazingira kama hayo ni kulenga mifano yako na majadiliano yako kwa Mwokozi, mshuhu-die yeye kila mara, na kutoa nafasi kwa wana-funzi kutoa shuhuda zao kumhusu yeye.

Page 354: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

339

alMa 34 – 35

“Yesu alikuwa ni wa pekee ambaye aliweza kutoa, upatanisho wa usiyo na kipomo. Kwa vile alikuwa amezaliwa katika mwili wa kufa na mama yake na Baba yake aliyekuwa na mwili usiokufa. Kwa sababu ya upekee wa uzao wa kwanza, Yesu alikuwa Kiumbe wa milele”(“Atonement,” Ensign, Nov. 1996, 35).“Kulingana na sheria ya milele, upatanisho ulihitaji dhabihu ya kipekee kwa kiumbe kisichokufa ambacho hakiko chini na kifo. Hivyo lazima afe na kuchukua tena Mwili wake. Mwokozi alikuwa ni mtu pekee ambaye angeweza kutimiza hili. Kutoka kwa mama yake alirithi uwezo ya kufa. Kutoka kwa Baba yake alipata uwezo juu ya kifo” (“Constancy amid Change,” Ensign, Nov. 1993, 34).• Je! Mafundisho ya Amuleki na kauli za Mzee Nelson zinatusaidia kuelewa kwa nini Yesu

Kristo alikuwa mtu pekee ambaye angeweza kuleta upatanisho kwa ajili ya dhambi za ulimwengu?

• Je! Mnawezaje kufanya muhtasari wa kile mlichojifunza mpaka sasa kutoka Alma 34 kuhusu Upatanisho wa Yesu Kristo? (Wanafunzi wanaweza kupendekeza kweli nyingine, lakini hakikisha wanaelewa kwamba Upatanisho wa Yesu Kristo wa milele na usio na mwisho unafanya wokovu kuwezekana kwa wanadamu wote. )

Ili kuwasaidia wanafunzi kuthamini zaidi umuhimu wa Upatanisho katika mpango wa wo-kovu wa Baba wa Mbinguni, fikiria kutumia shughuli ifuatayo. Unaweza ukipenda kufanya shughuli hii kuyafikia mahitaji na hamu za wanafunzi unaowafundisha.Andika kishazi kifuatayo ubaoni: Fikiria maisha bila . . . Inua kitu juu ambacho vijana wengi hukithamini (kama vile simu tamba) na uulize: • Je! Unafikiria maisha yatakuwaje bila kitu hiki? Kisha, nyanyua chupa au glasi ya maji (au kitu kingine ambacho ni muhimu katika kubo-resha maisha).• Je! Maisha yangekuwaje bila maji?Baada ya wanafunzi kuwa na majadiliano ya umuhimu wa maji, malizia kauli ubaoni ili isomeke kama ifuatavyo: Fikiria maisha bila Upatanisho wa Yesu Kristo. • Je! Maisha yangekuwaje tofauti bila Upatanisho wa Yesu Kristo? (Wape wanafunzi muda

kiasi wa kutafakari swali hili kabla ya kutaka majibu. Kama muda utaruhusu, unaweza ukipenda kuwaalika kuandika majibu ya swali hili. )

Alma 34:15–41Amuleki awafundisha Wazoramu jinsi ya kufanya imani hata tobaSisitiza kwamba ingawa Yesu Kristo alifanya upatanisho kwa watu wote, hatupokei mara moja baraka zake zote. Amuleki alifundisha kile tunachokihitaji kukifanya kupokea baraka zote zilizotolewa kupitia Upatanisho. Waalike wanafunzi wasome Alma 34:15–17 kimya na kutambua kishazi Amuleki alikisema mara nne. (“Imani mpaka toba.”)• Tunaweza kujifunza nini kutoka Alma 34:15– 17 kuhusu kile sharti tufanye ili kupokea

baraka kamili za Upatanisho? (Hakikisha wanafunzi wanaelewa kwamba ili kupokea baraka kamili za Upatanisho, lazima tufanye imani mpaka toba. )

• Je! Unafikiri inamaanisha nini kufanya imani mpaka toba? Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa inamaanisha nini kufanya imani mpaka toba, soma kauli ifuatayo ya Rais Dieter F. Uchtdorf wa Urais wa Kwanza:“Tunahitaji imani thabiti katika Kristo ili tuweze kutubu. . . .Imani katika Kristo itabadilisha fikra zetu, imani, na tabia ambazo haziendani na mapenzi ya Mungu. . . .Toba inamaanisha mabadiliko ya akili na moyo—tunaacha kufanya mambo yasiyo sahihi, na tunaanza kufa-nya vitu vilivyo sahihi” (“Point of Safe Return,” Ensign au Liahona, May 2007, 100).• Kwa nini ni muhimu kuelewa kwamba toba inahitaji kwamba siyo tu tuache yale yaliyo

mabaya, lakini tunaanza kufanya yale yaliyo sahihi?• Kulingana naAlma 34:16, ni nini matokeo tunapofanya imani mpaka toba?

Page 355: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

340

SoMo la 92

• Nini kinatokea kama hatufanyi imani mpaka toba? (Unaweza ukitaka kuelezea kwamba kuwa “ikiwa imewekwa wazi katika sheria yote ya dai la haki” inamaanisha kuteseka matokeo kamili kwa ajili ya dhambi zetu na kukosa baraka za uzima wa milele.)

• Kulingana na Alma 34:17, ni kitu gani kimoja tunaweza kukifanya ili kufanya imani yetu mpaka toba?

Waalike wanafunzi wasome Alma 34:17 –28 kimya. Waulize wao watafute kile ambacho Amuleki aliwafundisha Wazoramu kuhusu sala, ikijumuisha wakati wa kusali na nini cha kuomba. • Ni nini Amuleki alifundisha kuhusu sala ambacho kinahusika katika maisha yenu? Kwa

nini unafikiri sala ni sehemu muhimu kwa kufanya imani mpaka toba?• Amuleki alisema kwamba sala zetu hazitatusaidia chochote, au hazitakuwa na maana,

kama hatutawasaidia wale walio miongoni mwetu (ona Alma 34:28). Kwa nini unafiki-ria hii ni kweli?

Ili kuuwasaidia wanafunzi wafikirie njia za ziada ambazo tunaweza kufanya imani mpaka toba, waambie wajibu mifano ifuatayo: 1. Mvulana ameanza tabia ya kutumia lugha isiyofaa. Ni njia gani anaweza kuonyesha

imani mpaka toba ili awe huru na tabia hiyo? (Majibu yanaweza kujumuisha kuomba kwa ajili ya msaada, kuomba wanafamilia na marafiki msaada, na kushiriki katika shu-ghuli ambazo humwalika Roho.)

2. Msichana na mvulana wamejihusisha katika mahusiano yasiyofaa. Wamemhisi Roho Mtakatifu akiwaonya kuacha uhusiano wao mara moja. Je! Kufuata hisia hizi kunaweza ashiria imani mpaka toba vipi? Ni hatua gani zingine watakazohitaji za kuhakikisha wako katika njia toba kamili? (Majibu yanaweza kujumuisha kutafuta mwongozo kutoka kwa askofu au rais wa tawi na kuomba kwa ajili ya nguvu na msamaha.)

• Kuahirisha kunamaanisha nini? Ni sababu gani chache ambazo hufanya watu kuahirisha? Waalike wanafunzi wasome Alma 34:33 kimya, wakitatufa kitu ambacho Amuleki aliwao-nya Wazoramu wasiahirishe? Waalike wanafunzi wachache kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka Alma 34:32. Wanaposoma, acha darasa litafute matokeo ya kuahirisha toba yetu. Wanafunzi wanapotoa taarifa ya kile walichojifunza, andika ukweli ufuatao ubaoni: Maisha haya ni muda wetu wa kujitayarisha kukutana na Mungu.• Je! unawezaje kuelezea ukweli huu kwa mtu fulani? • Fikiria una rafiki ambaye kwa makusudi hatii baadhi ya amri lakini anapanga kutubu

baadaye. Je! Utamfundisha nini rafiki huyu kulingana na kile ulichojifunza kutoka Alma 34:32–35?

Elezea kwamba Amuleki hakuonya tu juu ya matokeo ya kuahirisha toba; bali pia alifu-ndisha kuhusu baraka za kuchagua kutubu sasa. Waalike wanafunzi wasome Alma 34:30 kimya na kutambua baraka hii. • Katika Alma 34:31, ni hakikisho gani limetolewa kwa wale wanaotubu sasa? (“Na kwa

haraka mpango mkubwa wa ukombozi utaletwa kwenu.”)Soma taarifa ifuatayo ya Rais Boyd K Packer wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili:“Hauhitaji kujua kila kitu kabla ya nguvu ya upatanisho ifanye kazi kwako. Kuwa na imani katika Kristo; inaanza kufanya kazi siku unapoomba!” (“Washed Clean,” Ensign, May 1997, 10).• Ni kwa vipi kuelewa hakikisho hili kunatusaidi sisi? Kwa njia gani umehisi Upatanisho

umeanza kufanya kazi kwa ajili yako wakati ulipoanza kuutegemea? Soma kauli ifuatayo ya Rais Harold B. Lee. Waambie wanafunzi wasikilize kile ambacho Rais Lee aliita “amri ya muhimu sana.”“Sasa, kama umefanya makosa, fanya leo ni mwanzo wa kubadilisha maisha yako. Geuka kutoka kwa yale mambo ambayo umekuwa ukiyatenda ambayo ni makosa. Amri ya mu-himu sana kati ya zote za Mungu ni ile ambayo inakuwa ngumu kwako kuitii leo. Kama ni ile ya kutokuwa mwaminifu, kama ni ile ya uasherati, kama ni ile ya kudanganya, kuto-sema ukweli, leo ni siku yako ya kuifanyia kazi mpaka utakapoweza kuushinda udhaifu

Page 356: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

341

alMa 34 – 35

huo. . . .Weka hiyo sawa sawa na hapo ndio unaanza kwa nyingine inayofuata ambayo ni ngumu sana kwako kuitekeleza”Mafundisho ya marais wa Kanisa: Harold B.Lee [2000],30)• Kulingana na Rais Lee, ni amri gani iliyo muhimu sana? Kwa nini?”Andika kauli zifuatazo zisizokamili ubaoni. Waulize wanafunzi kuzimalizia katika daftari au shajara za kujifunza maandiko.

Leo, amri ya muhimu sana kwangu mimi ni . . .Nitaanza leo kufanya imani mpaka toba na . . ..

Alma 35Wazoramu waliotubu wanakwenda kuishi miongoni mwa wenye hakiFanya muhtasari Alma 35 kwa kuelezea kwamba wengi wa Wazoramu walitubu dhambi zao. Walitupwa nje ya nchi na viongozi wao waovu na makuhani, na walienda kuisha katika nchi ya Jershomu na watu wa Amoni. Watu wa Amoni waliwapa ardhi, na Wanefi waliwatumia wanajeshi yao kuwalinda. Shuhudia kwamba tunaweza kupokea baraka za Upatanisho wa Mwokozi mara tu tuna-pofanya imani mpaka toba. Watie moyo wanafunzi kufuata mfano wa watu wa Amoni na Wanefi kwa kuonyesha upole na kuwaunga mkono wale wanaotafuta toba.

Page 357: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

342

UtanguliziBaada ya misheni yake kwa Wazoramu, Alma aliwa-shauri kila mmoja wa watoto wake. Ushauri wake kwa mwanawe Helamani unapatikana katika Alma 36 na 37. Alma anashuhudia kwa Helamani kwamba Mungu angewakomboa wale walio na imani katika Yeye. Kutoa kielezo cha ukweli huu, Alma anaelezea uzoefu wake wa miaka iliyopita alipokombolewa kutoka katika machungu ya dhambi zake kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo. Pia alielezea juhudi zake za kuwaleta wengine kwa Kristo na kupata furaha ya toba kwao wenyewe.

Tazama: Somo la 94 linatoa nafasi kwa wanafunzi wa-tatu kufundisha. Kama hujafanya hivyo bado, unaweza ukipenda kuchagua wanafunzi watatu sasa na kuwapa nakala za sehemu zilizochagulia katika somo la 94 ili waweze kujiandaa. Wape moyo kujifunza nyenzo za somo kwa kuomba na kutafuta mwongozo wa Roho Mtakatifu ili waweze kujua jinsi ya kutohoa somo kwa mahitaji ya wanafunzi wenzao.

SOMO LA 93

alma 36:3

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 36:1–5Alma anafundisha Helamani kuhusu nguvu ya Mungu ya kukomboaWaulize wanafunzi wafikirie kuhusu njia chanya ambazo ushuhuda au mafundisho fulani ya wazazi wao yamewashawishi wao. Alika mwanafunzi mmoja au wawili kushiriki ma-wazo yao na darasa.Eleza kwamba milango ya 36–42 katika kitabu cha Alma ina ushauri kutoka kwa Alma hata kwa watoto wake. Milango 36–37 imeelekezwa kwa Helamani, mlango 38 umeeleke-zwa kwa Shibloni, na milango 39–42 imeelekezwa kwa Koriantoni.Wahimize wanafunzi kujifikiria wenyewe katika sehemu ya Helamani aliposikiliza ushu-huda wa baba yake katika Alma 36:1–5. Acha wanafunzi wasome mistari hii kimya, wakita-futa kile kilichowafurahisha kuhusu ushuhuda wa Alma. • Katika mistari hii, ni kitu gani kinachokufurahisha zaidi? Kwa nini?

Alma 36:6–22Alma alielezea uasi wake na kueleza jinsi alivyopokea msamahaEleza kwamba kama ushuhuda zaidi wa nguvu ya Mungu ya kukomboa wale walioweka imani yao Kwake, Alma alishiriki uzoefu wake wa kukombolewa kutoka katika machungu ya dhambi zake. Waulize wanafunzi kuangalia Alma 36:6–9 na kufanya muhtasari kile kili-chotokea kwa Alma wakati yeye na wana wa Mosia walipoenda huku na huko wakitafuta kuliangamiza Kanisa. Mualike mwanafunzi asome Alma 36:10 kwa sauti. Waulize wanafunzi kutambua ni kwa muda gani Alma aliteseka kwa ajili ya dhambi zake. Eleza kwamba katika Alma 36:11–17 tunapokea maelezo ya kina ya kile Alma alikipata wakati wa siku tatu mchana na usiku za mateso yake zaidi ya yale tunayoyapata katika maelezo mengine ya uongofu wake. (ona Mosia 27 na Alma 38). Wapangie wanafunzi wafanye kazi katika majozi. Alika kila jozi lijifunze Alma 36:11–17, likitafuta maonyesho ya Alma ya woga au uchungu. Unaweza ukipenda kupendekeza kwamba wanafunzi waweke alama kile wanachogundua. Acha wa-nafunzi watoe taarifa ya maneno na vishazi wanavyovipata. (Unaweza ukitaka kuyaandika ubaoni.) Unaweza ukitaka kuuliza maswali yafuatayo kuzidisha ufahamu wa wanafunzi wa maneno na vishazi wanavyotolea taarifa. • Je! Unafikiri kile kishazi (au neno) linamaanisha nini? Nini kilimfanya Alma kuhisi vile? Ili Kuwasaidia wanafunzi kuelewa vyema maneno kitanda cha kutesea, sehemu ya kutia uchungu, na mateso makali, soma maelezo yafuatayo ya Raisi Boyd K. Packer wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili:

Wape moyo wanafunzi kusali kwa ajili ya mwongozo wanapokamilisha masomo waliyopangiwaWakati unapowapa-ngia wanafunzi somo, kama vile kufundisha sehemu ya somo, wape moyo wasali kwa ajili ya mwongozo wanapoma-liza somo lao walilopa-ngiwa. Kuhimiza kwako kutawaongeza ujasiri ili waweze kupokea ue-lewa zaidi kupitia Roho (ona M&M 6:14–15).

Page 358: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

343

alMa 36:3

“Kitanda cha mateso humaanisha ‘kuteswa.’ Zamani kitanda cha mateso ilikuwa ni fremu ambayo kwayo mwathiriwa alilazwa huku kila kisigino na kifundo cha mkono vilifu-ngwa katika pembezo ambayo inaweza kuzungushwa na kusababisha maumivu makali yasiyovumilika. “Haro ni Fremu yenye miiba iliyopitiliza. Inapovutwa aridhini, hurarua na kuchana chana udongo. Mara kwa mara maandiko yanazungumza kuhusu roho na akili vikiwa ‘vimete-seka’ kwa hatia. Mateso makali yanamaanisha ‘kukunja ,’ njia ya kutesa inayoumiza sana kwamba hata mtu ambaye hana hatia atakiri” ” (“The Touch of the Master’s Hand,” Ensign, Mei 2001, 23).• Je! uzoefu wa Alma unatufundisha nini kuhusu madhara ya dhambi? (Wasaidie wa-

nafunzi kutambua ukweli ufuatao: Dhambi hutuongoza kwenye maumivu makali, mateso na kujuta.)

• Je! inaonekana kama Alma alipata maumivu na majuto kwa ajili ya dhambi zake mara moja baada ya kuzitenda? Kwa nini unafikiri ni muhimu kuelewa kwamba tunaweza kukosa kuhisi madhara ya dhambi zetu mara moja?

Waulize wanafunzi watafakari matukio ambayo wamehisi maumivu au majuto kwa ajili ya dhambi zao. Kisha soma kauli ifuatayo ya Rais Packer:“Kila mmoja wetu angalau ameonja maumivu ya dhamira ambayo yanakuja baada ya makosa yetu. . . .“Kama umelemewa na huzuni mzito wa hatia ama kukatisha tamaa, ya kushindwa au aibu, kuna tiba” (“The Touch of the Master’s Hand,” 22).Sisitiza kwamba wakati Alma alikuwa akihisi maumivu makali na majuto kwa ajili ya dhambi zake, alikumbuka tiba ya maumivu yake. • Kulingana na Alma 36:17, Alikumbuka nini? Acha mwanafunzi asome Alma 36:18 kwa sauti. Alika darasa litafute kile ambacho Alma alikifanya ili kutenda kulingana na mafundisho ya baba yake. Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa vyema aya hizi, muulize mwanafunzi asome kauli ifuatayo ya Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili:

“Alma alikuwa ameguswa na mafundisho ya baba yake, lakini ni muhimu sana kwamba unabii alioukumbuka ulikuwa ule unaohusu ‘ujio wa Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, kuleta upatanisho kwa ajili ya dhambi za ulimwengu.’ (Alma 36:17.) Hili ndilo jina na huo ndio ujumbe ambao kila mtu sharti ausikie. . . .Sala zozote tunazoomba, mahitaji mengine yoyote tuliyonayo, yote kwa njia moja hutegemea katika ombi lile: ‘Ee Yesu, Mwana

wa Mungu, unirehemu.’ Amejiandaa kutoa rehema hiyo. Alilipia kwa maisha yake mwenyewe ili kuitoa” ( However Long and Hard the Road [1985], 85).• Kwa nini unafikiri ni muhimu kwetu sio tu kujifunza kuhusu Yesu Kristo lakini pia kuo-

mba baraka za Upatanisho Wake? Wahimiza wanafunzi kufikiria kimya kama wameomba kupokea baraka za Upatanisho wa Yesu Kristo, ikijumuisha baraka ya msamaha. Waalike wanafunzi kupekua Alma 36:19– 22 kimya, wakitafuta maneno ama vishazi amba-vyo vinaeleza jinsi hisia za Alma zilivyobadilika baada ya kuomba rehema. • Ni maneno au vishazi gani ulivyovipata ambavyo vinaeleza jinsi hisia za Alma

zilivyobadilika?Uliza swali lifuatalo kuhusu kila moja ya maneno na vishazi ambavyo wanafunzi wamevipata:• Kishazi hiki (au neno) linatufundisha nini kuhusu nguvu ya Upatanisho ya Mwokozi?

(Wanafunzi wanapojibu, wasaidie waone kwamba siyo tu maumivu ya Alma yaliondo-lewa, lakini vile vile alijawa na shangwe.)

Andika kauli ifuatayo ambayo haijakamilika ubaoni: Kama tutafanya imani katika Yesu Kristo na Upatanisho Wake, basi Yeye atatu . . .• Kutoka uzoefu wa Alma, tunaweza kujifunza nini kuhusu kile ambacho Bwana anatufa-

nyia tunapotubu kwa dhati? (Wanafunzi wanaweza kushiriki kanuni tofauti, lakini haki-kisha wanaeleza kwamba kama tutafanya imani katika Yesu Kristo na Upatanisho Wake, basi tutakombolewa kutoka katika maumivu ya dhambi zetu na atatujaza na shangwe. Unaweza kutaka kukamilisha kauli ubaoni.)

Page 359: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

344

SoMo la 93

• Tunaweza kufanya nini ili kufanya imani katika Yesu Kristo ili tuweza kukombolewa kutoka katika hisia za maumivu au majuto yanayosababishwa na dhambi zetu?

Soma kwa sauti hali ifuatayo, na waulize wanafunzi kufikiria jinsi watakavyojibu: Rafiki ambaye amekuwa akisoma Kitabu cha Mormon alionyesha dukuduku lake ku-husu maneno ya Alma katika Alma 36:19. Rafiki yako anakuuliza, “Kama naweza ku-kumbuka dhambi zangu na bado najuta kuhusu dhambi hizo, je! inamaanisha kwamba sijasamehewa?”Waulize wanafunzi waeleza jinsi uzoefu wa Alma unavyohusika katika hali hii. Baada ya wanafunzi kujibu, soma kauli ifuatayo ya Rais Dieter F. Uchtdorf wa Urais wa Kwanza:

“Shetani atajaribu kutufanya tuamini kwamba dhambi zetu hazijasamehewa kwa sababu sisi tunaweza kuzikumbuka. Shetani ni muongo; anajaribu kutuziba kuona kwetu na kutupotosha kutoka kwa njia ya toba na msamaha. Mungu hakuahidi kwamba sisi hatutakumbuka dhambi zetu. Kukumbuka kutatusaidia kuepuka kutenda makosa hayo hayo tena. Lakini kama tutakuwa wakweli na waaminifu, kumkukumbu ya dhambi zetu italainishwa

muda baada ya muda. Hii itakuwa ni sehemu ya uponyaji na mchakato wa utakaso. Alma alishuhudia kwamba baada ya kulia kwa Yesu kwa ajili ya rehema, alikuwa bado anaweza kuzikumbuka dhambi zake, lakini kumbukumbu ya dhambi zake haikumkandamiza na kumtesa, kwa sababu alijua alikuwa amesamehewa (ona Alma 36:17–19).“Ni jukumu letu kuepuka chochote ambacho kinaweza kurudisha kumbukumbu za zamani za dhambi. Tunapoendelea kuwa na ‘mioyo iliyovunjika na roho zilizopondeka’ (3 Nefi 12:19), tunaweza kuamini kwamba Mungu ‘hatozikumbuka [dhambi zetu] tena (“Point of Safe Return,” Ensign or Liahona, Mei 2007, 101).• Kulingana na kauli ya Rais Uchtdorf, je unawezaje kueleza inamaanisha nini “kutoteswa

na kumbukumbu ya dhambi zetu tena”? Alma 36:3Shuhudia kwamba tukifanya imani katika Yesu Kristo na Upatanisho Wake, atatukomboa kutoka katika maumivu ya dhambi zetu na kutujaza na shangwe. Wahimize wanafunzi kufikiria jinsi wanavyoweza kuyatumia yale waliyoyasoma kutoka kwenye uzoefu wa Alma. Muda ukiruhusu, acha wanafunzi waimbe “Where Can I Turn for Peace?” Hymns, no. 129).

Alma 36:23–30Alma anaeleza kwa nini anaendelea kufanya kazi daima kuwaleta wengi katika tobaKuwasaidia wanafunzi kufahamu kwa nini Alma alifanya kazi kuwaleta wengi katika toba, fikiria kutumia shughuli ifuatayo. (Kama haiwezekani kutoa vitafunwa kwa ajili ya darasa lako, unaweza badala yake kueleza shughuli yenyewe.)Onesha kitafunwa (kama vile biskuti au kipande cha peremende) na waulize kama yeyote darasani hupenda kitafunwa kama hicho. Kula kipande, na onesha jinsi gani kilivyo kitamu. Waambie wanafunzi kwamba kitafunwa ni kizuri sana na kwamba ungependa kushiriki darasa zima. Onyesha vitafunwa vingi vya aina hiyo na uliza kama yeyote mwi-ngine angependa kukionja. Gawa vitafunwa kwa yeyote ambaye angependa kidogo. Mualike mwanafunzi asome Alma 36:23–24 kwa sauti. Waulize wanafunzi wafuatilie, waki-tafuta jinsi shughuli ya kuonja inahusisha uzoefu wa Alma baada ya kuongolewa kwake. • Je! Ni kwa jinsi gani matendo ya Alma yalikuwa sawa na shughuli ya kuonja? Ni kitu

gani Alma alitaka watu wengine waonje? Mualike mwanafunzi asome Alma 36:25–26 kwa sauti. Waulize wanafunzi wagundue jinsi juhudi za Alma za kufundisha injili zilivyomshawishi yeye na wengine. • Je! Ni kwa jinsi gani mafundisho ya Alma yalimshawishi yeye na wengine?• Je! Ni kanuni gani tunayoweza kujifunza kutoka kwenye mistari hii? (Wanafunzi wana-

weza kutumia maneno tofauti, lakini hakikisha kwamba wanaeleza kwamba tunaweza kupokea furaha kubwa tunavyojitahidi kuwaleta wengine kwa Kristo.)

Fanya muhtasari Alma 36:27–30 kwa kueleza kwamba Alma tena alishuhudia kwa Hela-mani kwamba Bwana angewakomboa wale wanaoweka imani yao katika Yeye. Shuhudia juu shangwe tunayoweza kupata tunapofanya imani katika Yesu Kristo na tunapowapa moyo wengine kufanya vivyo hivyo. Ili kuwasaidia wanafunzi kutumia kile walichojifunza

Page 360: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

345

alMa 36:3

kutoka Alma 36, waalike wao wamalizie moja ya shughuli hapa chini. (Unaweza kuandika haya kwenye ubao.) 1. Fikiria kama umeshahisi Mwokozi amekukomboa kutoka katika dhambi na amekujaza

na shangwe. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, eleza nini utakachofanya ili uweze kupokea baraka hizi.

2. Fikiria mtu (kama vile rafiki, ndugu, au mshiriki wa kata) ambaye anaweza kunufaika kutoka kwa ushuhuda wako juu ya Mwokozi. Andika barua kwa mtu huyu na ujumuii-sha ushuhuda wako wa jinsi Yesu Kristo anaweza kutukomboa kutoka katika maumivu ya dhambi na kutujaza na furaha.

Page 361: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

346

UtanguliziAlma aliendelea na ushauri wake kwa mwanawe Hela-mani na akampa mamlaka ya kumbukumbu takatifu. Alimkubushwa Helamani kwamba maandiko mataka-tifu yalikuwa tayari ni njia ya kuwaleta maelfu ya Wala-mani kwa Bwana, na akatabiri kwamba Bwana alikuwa na madhumuni makubwa kwa ajili ya kumbukumbu katika siku za usoni. Alma alimwelekeza mwanawe ku-husu kile cha kufundisha watu. Akilinganisha maneno

ya Kristo katika Liahona, alisisitiza kwa Helamani umu-himu wa kuyategemea kwa ajili ya Muongozo.

Tazama: Somo hili linatoa nafasi kwa wanafunzi watatu kufundisha darasa. Ili kusaidia kuwaandaa wa-nafunzi hawa kufundisha, mpatie kila mwanafunzi na nakala ya kifungu ambacho atakifundisha siku moja ama mbili kabla. Au unaweza kuchagua kufundisha sehemu hizi mwenyewe.

SOMO LA 94

alma 37

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 37:35.Alma amkabidhi Helamani rekodi, amshauri kushika amri na kumkumbusha kuwa Liahona ilifanya kazi kwa njia ya ImaniNakili mchoro ufuatao kwanye ubao

Waulize wanafunzi kuorodhesha ubaoni baadhi ya vitu vidogo na rahisi. Unaweza kutaka kuwauliza kueleza majibu yaoEleza kuwa Alma 37 ina ushauri wa Alma wa kumsaidia mwanawe Helamani kujitayarisha kuwa mtunzaji wa rekodi takatifu. Alma alimfundisha kuhusu jukumu la vitu vidogo rahisi katika kazi ya Bwana. Mualike mwanafunzi kusoma Helamani 3:29–30 kwa sauti.Tunajifunza nini kuhusu aya hizi kuhusu thamani ya “vitu vidogo na rahisi”? (Wanafunzi wanaweza kutumia maneno tofauti lakini wanapaswa kueleza kuwa Bwana hufanya kazi kwa njia ndogo na rahisi ili kutimiza madhumuni yake ya milele.)Waalike wanafunzi kusoma Alma 37:1–5 kimoyomoyo, wakitafuta mfano wa kitu kidogo na rahisi ambacho chaweza kuwa na athari kubwa katika maisha ya watu (rekodi takatifu au maandiko). Baada ya wanafunzi kuripoti walichopata andika neno Maandiko ubaoni chini ya vitu vidogo na rahisi.Wafanye wanafunzi kutafuta Alma 37:8–10 kwa njia ambazo maandiko yaliathiri watu wa Kitabu cha Mormoni. Wanafunzi wanaporipoti walichopata, unaweza kutaka kuandika majibu yao chini ya ATHARI KUU.• Ni kwa njia gani maandiko yamekuwa na athari maishani mwako?Fupisha Alma 37:11–32 kwa kueleza kuwa Alma alimfundisha Helamani kwamba Bwana angeonyesha nguvu zake katika kuja kwa Kitabu Mormoni. Alimwagiza Helamani kufuata amri za Bwana na kuweka rekodi zile kwa uangalifu. Alimwagiza pia Helamani kutumia rekodi zile kuwafundisha watu kuepukana na kufunua maelezo yote ya uovu wa Wayaredi uliopelekea uangamizi.Waalike wanafunzi kupekua Alma 37:13–16 kimyakimya, wakitafuta kanuni ambazo Alma alimfunza Helamani alipomkabidhi kumbukumbu. (Wanafunzi wanaweza kushiriki baadhi ya Kanuni, lakini hakikisha kuwa majibu yao yanaonyesha kwamba tukitii amri za Bwana, atatusaidia kutimiza majukumu yetu. Unaweza kuuliza jinsi kanuni hii inahu-siana na dhana kwamba vitu vidogo na rahisi vinaweza kuwa na athari kubwa)Sehemu iliyosalia ya somo hili inapaswa kufundishwa na wanafunzi watatu. Ikiwa darasa ni kubwa waulize wanafunzi kusonga kwenye sehemu tatu tofauti. Gawa darasa katika vikundi vitatu. Alika kila kikundi kuchukua maandiko yao, daftari zao, shajara za kujifunza maandiko, kalamu au penseli na kukusanyika na mmoja wa walimu wanafunzi.

vitu vidogo na Rahisi athaRi KUbWa

Page 362: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

347

alMa 37

Baada ya walimu wanafunzi kukamilisha masomo yao makundi yatabadilishana nafasi. Ikiwa darasa ni dogo, walimu wanafunzi wanaweza kuchukua zamu katika kufundisha darasa zima. Kwa vyovyote walimu wanafunzi wanapaswa kuchukua karibu dakika saba kutoa masomo yao na kuongoza mjadala.

Mwalimu mwanafunzi 1—Alma 37:33–34Waulize wanafunzi wenzako kufikiria kiongozi wa kanisa katika sehemu yao au Mkuu Mwenye Mamlaka ambaye amewafundisha kitu kilicholeta tofauti katika maisha yao. Wa-alike wanafunzi wachache kushiriki kile kiongozi huyu alifunza na jinsi kilivyowashawishi. Unaweza kutaka kushiriki mfano kutoka kwa maisha yako.Waulize wanafunzi wawili kuchukua zamu wakisoma kwa sauti kutoka kw a Alma 37:33–34. Waulize wanafunzi wengine kufuatilia wakitafuta kile Alma alimshauri Helamani kufundisha watu. Unaweza kupendekeza kuwa waweke alama kwenye vishazi “wafundishe” na “wa-hubirie” wanaposoma. Kwenye ubao ama kipande cha karatasi andika Mafunzo ya Viongozi wa Kanisa. Wakati wanafunzi wamekamilisha kusoma aya hizi, waulize kuripoti walichopata. Andika majibu yao chini ya Mafunzo ya viongozi wa kanisa. Uliza maswali yafuatayo:• Mafundisho haya yanawezaje hasa kuwa ya manufaa kwetu hivi leo? Kwa nini?”Waulize wanafunzi wenzako kuuliza kishazi cha Alma 37:34 ili kuona ni baraka gani huja kutokana na kufuata mafunzo ya viongozi wa Kanisa. Andika kanuni ifuatayo ubaoni: Kwa kufuata mafunzo ya viongozi wa Kanisa, tunaweza kupata pumziko la roho zetu. Waulize kinachomaanisha “kupata pumziko kwa roho zao.” (Majibu yanaweza kujumu-isha kuwa huru kutokama na matokeo ya dhambi, kupokea amani kutoka kwa Roho, na kubarikiwa na nguvu ya kuhimili na kushinda changamoto.)Shiriki ushuhuda wako wa jinsi kanuni hii imekuwa halisi katika maisha yako. Ukiwa na wakati wa ziada waalike wengine kushiriki shuhuda zao za kanuni hii.

Mwalimu mwanafunzi 2—Alma 37:35–37Waeleze wanafunzi wenzako kuwa ni kawaida kwa wale ambo hupanda miti kufunga kamba kwa kigingi kisha kutoa huo usaidizi baada ya mti kukomaa. Wauliza kwa nini hili hufanyika. Kisha soma hadithi ifuatayo kuhusu mti ambao Rais Gordon B. Hinckley alipa-nda katika ua lake.

Rais Gordon B. Hinckley alipanda mche mdogo karibu na nyumba yake mara tuu baada ya kuoa. Hakuujali sana miaka ilipopita siku moja akaona kuwa mti ulikuwa na kasoro la umbo na ulikuwa ukiegemea magharibi. Alijaribu kuusukuma usimame lakini shina lilikuwa zito sana. Alijaribu kutumia kamba na kapi kuunyoshoa lakini kamwe hangeinama. Hatimaye alichukua msumeno na kulikata tawi zito katika sehemu ya magharibi,

ikiacha kovu baya. Baadaye alisema hivi kuhusu ule mti:“Zaidi ya nusu karne imepita tangu nilipoupanda mti ule. . . .juzi niliutazama tena mti ule Ni mkuu. Umbo lake ni bora. Ilikuwa mali ya thamani kwa nyumba ile. Lakini ilikuwa kali vipi mshtuko wa ujana wake na katili hali niliyotumia kuunyosha.“Wakati ulipopandwa, kamba ndogo ingeushikilia dhidi ya nguvu za upepo. Ningeweza, na nilipaswa kuupa kamba kwa urahisi sana. Lakini sikufanya hivyo, na ukajikunja kufuatia nguvu zilizokuwa dhidi yake” (“Bring Up a Child in the Way He Should Go,” Ensign, Nov. 1993, 59).Wafanye wanafunzi kusoma ushauri wa Alma kwa Helamani katika Alma 37:35. Waulize kufikiria jinsi aya hii inavyohusiana na uzoefu wa Rais Hinckley na ule mti.Waalike wanafunzi kufupisha Alma 37:35 kwa maneno yao wenyewe (Majibu yao yanapa-swa kueleza kuwa tunapaswa kujifunza ujanani mwetu kuweka amri za Mungu. ) Pia waalike kuandika majibu yao kwa maswali yafuatayo. Unaweza kutaka kuandika maswali ubaoni au kuyasoma polepole ili wanafunzi waweze kuyaandika)• Unafikiri tofauti gani hutokea katika maisha ya mtu kujifunza kutii amri za Mungu

akiwa angali bado kijana?• Unaweza kufikiria watu waliobarikiwa katika maisha yao yote kwa sababu walijifunza

kutii Amri katika ujana wao? Andika kuhusu jinsi walivyobarikiwa.Waalike wanafunzi wachache kutoa taarifa ya kile walichokiandika. Kisha alika mwanafu-nzi asome Alma 37:36–37 kwa sauti. Waulize wanafunzi wote waliobakia kufuatilia, waki-tafuta ushauri dhahiri ambao unaweza kuwasaidia kutii amri wakati wangali vijana.

Alma 37:35 ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Unaweza kutaka kuwasaidia wanafunzi katika umahiri wa kifungu hiki kwa kuwaalika kukamilisha kazi ya ziada mwishoni mwa somo la leo.

Page 363: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

348

SoMo la 94

• Je kwa kufuata ushauri huu kunawezaje kukusaidia kila siku kutii Amri? • Ni kwa njia zipi unajaribu kumweka Bwana mbele katika mawazo, maneno, matendo,

na upendo wako? (Wahimize wanafunzi kufikiria jinsi wanavyoweza kuwa bora zaidi.)Shiriki hisia zako kuhusu jinsi kushauriana na Bwana kumekusaidia kutii amri. Wahimize wanafunzi wenzako kushauriana na Bwana katika yote wayoyafanya.

Mwalimu Mwanafunzi 3 —Alma 37:38–45 Onesha ya picha ya Liahona (62041; Gospel Art Book [2009], no. 68). Wakumbushe wanafu-nzi wenzako juu ya dira ambayo Bwana aliitumia kusaidia familia ya Lehi kusafiri kwenda nchi ya ahadi. Katika Alma 37:38, tunajifunza kwamba dira iliitwa Liahona. Eleza kwamba Alma alizugumzia Liahona ili kumfundisha Helamani kanuni ya muhimu kuhusu jinsi Bwana huongoza watoto Wake. Waeleze wanafunzi wenzako kwamba utawauliza maswali na kisha waulize wachukue zamu kusoma mistari michache kwa sauti wakati kila mmoja akitafuta majibu. Acha wao wajibu kila swali baada ya kifungu kilichohusiana na maandiko ambacho kimekwisha somwa. • Je! Liahona ilifanya kazi vipi? (Ona Alma 37:38–40.)• Kwa nini Liahona iliacha kufanya kazi wakati mwingine? (Ona Alma 37:41–42.)• Je! tunaweza kulinganisha vipi Liahona na maneno ya Kristo? (Ona Alma 37:43–45.)Unaweza kutaka kueleza kwamba katika mistari hii maneno kivuli na aina ilielekeza kwa “mtu, tukio, au tamaduni zinazofananishwa na mtu mwingine, tukio, au tamaduni zenye umuhimu mkubwa ambao unafuata. . . . Aina halisi zitakuwa na vipengele vinavyoone-kana vinavyofanana, onyesha ushahidi wa uteuzi wa kiungu, na kuwa utabiri wa matukio yajayo” (Joseph Fielding McConkie, Gospel Symbolism [1985], 274). Chaguo la kufuata au kutofuata mwelekeo wa Liahona ni kama chaguo letu kuhusu jinsi tunavyojibu katika mwelekeo ambao unakuja kutokana na maneno ya Kristo. • Ni wapi tunaweza kupata maneno ya Kristo? (Majibu yanaweza kujumuisha maandiko,

maneno ya manabii wa siku za mwisho, baraka za Baba Mkuu, na minong’ono ya Roho.)Waalike wanafunzi wenzako kufanya muhtasari maneno ya Alma katika Alma 37:38–45, hasa mistari ya 44–45. Mjadala huu unapaswa ujumuishe ukweli ufuatao: Kama tutafuata maneno ya Yesu Kristo, yatatuongoza kupokea uzima wa milele. Shiriki jinsi maneno ya Kristo yamekuathiri kiroho na jinsi yanavyokusaidia kuendelea kuelekea kwenye uzima ya milele. Unaweza kupendekeza kwamba wanafunzi wafikirie kupata baraka za Baba Mkuu, au kama tayari wameshapokea, waisome mara kwa mara na kwa maombi.

Muhtasari kwa mwalimu: Baada ya wanafunzi kumaliza kufundisha sehemu zao za somo, washukuru na, muda ukiruhusu, waalike wanafunzi wachache kushuhudia moja ya kanuni walizojifunza leo. Unaweza pia kutaka kushiriki ushuhuda wako wa kanuni hizi. Hitimisha kwa kuwaalika wanafunzi kufuatilia unaposoma Alma 37:46–47 kwa sauti.

Umahiri wa Maandiko —Alma 37:35Tazama: Shughuli ifuatayo ya kuchukua nyumbani itawaandaa wanafunzi kwa mwanzo wa somo linalofuata (Alma 38). Andaa muda darasani ili kuelezea zoezi kwa wanafunzi na kuwataarifu kuhusu mpango wako wa kufuatilia juu ya uzoefu wao wakati mwingine mtakapokutana. Sisitiza kwamba Alma 37:35 ni kifungu cha Umahiri wa Maandiko. Unaweza kuwahimiza wanafunzi kuweka alama katika njia ya wazi ili waweze kukipata kwa urahisi. Waalike wanafunzi wakariri kifungu hiki cha maneno nyumbani usiku na kuyatogoa kutoka katika kumbukumbu kwa mzazi au mtu mzima mwingine anaeaminika. (Au wanaweza kusoma mistari pamoja na mtu mzima.) Wahimize kumwuliza yule mtu mzima maswali yafuatayo: (Unaweza kutaka kuwaambia wanafunzi kuandika maswali katika kipande cha karatasi na kuchukua nyumbani.)Je! Utii kwa amri za Mungu umekusaidiaje?Ni ushauri gani ulionao kwangu ambao unaweza kunisaidia kuwa na hekima zaidi katika ujana wangu?Wajulishe wanafunzi kwamba utawataka wao kutoa taarifa za uzoefu wao wakati wa kipi-ndi cha darasa kifuatacho.

Page 364: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

349

UtanguliziShibloni alitumika pamoja na baba yake, Alma, kama mmisionari miongoni mwa Wazoramu (ona Alma 31:7). Baada ya misheni hii, Alma alionyesha furaha katika uthabiti na uaminifu ambao Shibloni aliuonyesha

wakati akivumilia mateso. Alma pia alishuhudia kwa Shibloni kuhusu Nguvu ya Mwokozi ya ukombozi na kutoa ushauri kuhusu juhudi endelevu za Shibloni za kufundisha injili.

SOMO LA 95

alma 38

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 38:1–3Alma alionyesha furaha katika uaminifu wa ShibloniKama uliwaambia wanafunzi kuifanya matumizi ya shughuli nyumbani, mwishoni mwa somo liliopita, wakumbushe kuhusu maswali mawili uliyowaalika wao waulize wazazi wao au mtu mzima anayeaminika. • Je! Ni kwa jinsi gani utiifu katika amri za Mungu umekusaidia?• Je! Una ushauri gani kwangu ambao unaweza kunisadia kuwa na hekima zaidi katika

ujana wangu? Waulize wanafunzi kutoa taarifa ya uzoefu wao wa shughuli hiyo. Baada ya wanafunzi kushiri, uliza: • Je! Uzoefu huu ulishawishi vipi hamu yako ya kutii amri za Bwana?Eleza kwamba Alma 38 imeandikwa ushauri ambao Alma aliutoa kwa mwanawe Shibloni. Mwambie mwanafunzi asome Alma 38:1–3 kwa sauti. Uliza darasa lifuatilie, likitafuta vi-shazi vinavyoelezea jinsi Alma alivyojisikia kuhusu Shibloni na kwa nini. Waalike wanafu-nzi watoe taarifa ya kile wanachopata. • Tunaweza kujifunza nini kutoka Alma 38:2–3 kuhusu athari ambayo watoto wenye

haki wanaweza kuwa nayo kwa wazazi wao? (Wanafunzi wanaweza kutofautiana katika majibu yao. Hakikisha kwamba wanatambua ukweli kwamba kama vijana wana msimamo na ni waaminifu katika kutii amri, wanaweza kuwaletea furaha kubwa wazazi wao.)

• Lini wazazi wako wamekuwa na furaha kwa sababu ya uamuzi wako mzuri uliyoufanya au kwa sababu ya juhudi zako za kuishi ukifuata injili?

• Je! Ni kwa jinsi gani juhudi zako za kutii amri zinashawishi uhusiano wako na wazazi wako? Unaweza ukipenda kushiriki mfano wa jinsi familia yako imeshawishika kwa chaguo za haki ya watoto katika familia.

Alma 38:4–9Alma anashuhudia kuhusu nguvu ya Mwokozi katika kukomboaElezea kwamba Alma alimkumbusha Shibloni kwamba wote walipitia nguvu za Mwokozi za ukombozi. Andaa chati ifuatayo kama kitini, au uonyesha ubaoni na uwaulize wanafu-nzi wainakili katika daftari au shajara za kujifunza maandiko.

Fuatilia baada ya kutoa kaziWakati unapofuatilia kwa wanafunzi katika mialiko iliyopita kutumia kanuni za injili, wape nafasi kushuhudia juu ya baraka ambazo huja kutokana na kuishi injli. Wakati wanafunzi wa-nashiriki kile walichoji-funza walipotumia kweli za injili, waliimarisha shuhuda zao na kusaidia kuimarisha shuhuda za wengine.

Page 365: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

350

SoMo la 95

Shibloni (alma 38:4–5) alma (alma 38:6–8)

alikombolewa kutoka katika nini?

Kwa nini alipokea baraka ya ukombozi?

tunaweza kujifunza nini kutoka kwa uzoefu wake.

Malizia chati kama darasa, au wapangie wanafunzi kuimalizia wakiwa katika majozi. Acha wanafunzi warejee vifungu vya maandiko vilivyoorodheshwa kwenye chati wanapojibu maswali. Wape moyo wanafunzi kujumuisha kile wanachokijua tayari kuhusu Bwana kum-komboa Shibloni (ona Alma 38:2–3) na Alma (ona Mosia 27; Alma 36). Baada ya wanafu-nzi kuimaliza chati, waulize maswali yafuatayo kuwasaidia kujadili kanuni walizojifunza. • Tunaweza kujifunza nini kutoka uzoefu wa Shibloni? (Wanafunzi wanaweza kutambua

kanuni tofauti. Hakikisha wanatambua ukweli ufuatao: Kama tunabeba vitu vyote kwa uvumulivu na imani katika Mungu, Yeye atatukomboa kutoka kwenye maja-ribio, shida, na majonzi, na kutuinua siku ya mwisho.)

• Tunaweza kujifunza nini kutoka kwa uzoefu wa Alma? (Ingawa wanafunzi wanaweza kujibu kwa utofauti, hakikisha wanaelezea kwamba kupokea ondoleo la dhambi zetu na kupata amani katika mioyo yetu, lazima tufanye imani katika Yesu Kristo na kutafuta rehema Yake.)

Mwalike mwanafunzi asome Alma 38:9 kwa sauti. Waulize wanafunzi wafuatilie, wakita-futa kile ambacho Alma alitaka mwanawe ajifunze kuhusu Mwokozi.• Kwa nini ni muhimu kwetu sisi kujua kwamba Yesu Kristo ndio pekee “njia au namna

ambayo [sisi] tunaweza kuokolewa”?• Ni katika njia gani umeona ukombozi kupitia nguvu ya Mwokozi? (Unaweza ukipenda

kuwapa wanafunzi muda wa kutafakari swali hili kabla ya kutaka majibu yao.) Ulifanya nini kutafuta ukombozi huo?

Toa muda kiasi kwa wanafunzi kutafakari jinsi wanavyoweza kutafuta msaada wa Bwana kwa changamoto binafsi.

Alma 38:10–15Alma anamshauri Shibloni kuendelea kufundisha injili na kukuza sifa za haki za kiasiliElezea kwamba Alma alimpa moyo Shibloni kukuza ubora ambao ungemsaidia alivyoe-ndelea kufundisha injili na kuwatumikia wengine. Ushauri wa Alma kwa Shibloni una-weza kutumika kwa mtu yeyote ambaye anataka kutumika, kufundisha, au kuwashawishi wengine kwa wema. Waalike wanafunzi wasome Alma 38:10–15 kimya, wakitafuta ushauri ambao unaweza kuwa wa msaada mzuri hasa kwao. Unaweza ukipenda kushauri kwamba wanafunzi waweke alama kile wanachokipata.Wape wanafunzi nakala ya mwongozo wa kujifunza mwishoni mwa somo. Elezea kwamba wanapotumia mwongozo huu, wataona jinsi juhudi zetu za kukuza sifa za haki za ki-asili zinatuandaa kufundisha na kuwatumikia wengine. Waalike wao wachague moja ya sehemu ya ushauri wa Alma katika safu ya wima ya kushoto ya mwongozo na kumalizia shughuli ya mafunzo yanayofanana katika safu ya wima ya kulia. (Kama hauwezi kutenge-neza nakala za mwongozo wa kujifunza, badili shughuli kwa kuongoza mjadala wa darasa na kwa kutumia maelezo katika mwongozo wa kujifunza kama nyenzo.)Wakati wanafunzi watakapokuwa wamepata muda wa kutosha kumalizia moja ya shughuli za mwongozo wa kujifunza, fikiria kuwaambia baadhi yao kushiriki kile walichojifunza kutoka shughuli hii na jinsi wanavyopanga kukitumia. Kama umewapa wanafunzi nakala ya mwongozo wa kujifunza, wape moyo kuchukua nyumbani na kujifunza zaidi kuhusu ushauri wa Alma kwa Shibloni.

Badili shughuli ya kujifunzaUtaratibu wa kufundisha uliowekwa katika kitabu cha kiada hiki ni mape-ndekezo. Tumia busara kuyatohoa kulingana na mazingira yako na kulingana na mahitaji mwanafunzi binafsi na darasa zima kwa ujumla. Kwa maombi tafuta mwongozo wa Roho Mtakatifu.

Page 366: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

351

alMa 38

Mwongozo wa Kujifunza wa Alma 38:10–12Chunguza sehemu tofauti za ushauri wa Alma zilizoorodheshwa hapa chini, na chagua moja ambayo ungependa kuiboresha. Malizia shughuli ya mafundisho yanayofanana ili kukusaidia kutumia ushauri huu katika maisha yako.

Ushauri wa alma Shughuli za Kujifunza

“Kuwa mwenye bidii na mwenye kiasi ka-tika kila kitu” (alma 38:10).

bidii haibadiliki, yenye umakini, na juhudi yenye umakini sana. Kuwa na umakini ni “kutumia wastani katika kila kitu au kuwa na uwezo wa kuji-zuia” (Kent d. Watson, “being temperate in all things,” Ensign or Liahona, nov. 2009, 38). Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika kuhusu kwa nini tabia hizi mbili zinahitajika wakati mtu anapofundisha injili na kuwatumikia wengine. pia andika kuhusu maeneo mengine yoyote katika maisha yako ambayo ungeweza kuwa na bidii zaidi au mwenye kiasi na kuhusu jinsi ya kuendelea katika maeneo hayo kutakusaidi kuwafundisha na kuwatumikia wengine kwa ufasihi zaidi.

“hakikisha kwamba hujiinui kwa kiburi, hujisifu” (alma 38:11).

Moja katika vipengele vya kiburi ni kujiaminii kuliko kumwamini Mungu. Kiburi pia ni dhahiri wakati mtu anapofikiria kwamba yuko juu au ni mu-himu sana kuliko wengine. andika katika shajara ya kujifunza maandiko kuhusu kile kinachoweza kutokea kama mshiriki wa Kanisa ni mwenye kiburi katika mwito wake. Mzee Robert d. hales wa akidi ya Mitume Kumi na Wawili alifundisha, “Wafuasi wa kweli huongea kwa ujasiri wa upole, sio kwa majivuno ya kiburi” (“christian courage: the price of disciple-ship,” Ensign or Liahona, nov. 2008, 73). fikiria mtu unayemjua anaye-fundisha injili “kwa ujasiri wa upole.” Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika kuhusu mtu huyu na athari ambayo mafundisho yake yameleta kwako. pia andika njia mbili au tatu unazoweza kuepuka kuwa mwenye kiburi.

“tumia ujasiri, lakini usiwe ujeuri” (alma 38:12).

Soma maneno ya Mtume paulo katika Wafilipi 1:14 (katika agano jipya) kuona jinsi mtumishi wa Mungu anaweza kuonyesha ujasiri. Rais james e. faust wa Urais wa Kwanza alifundisha jinsi tunavyoweza kuepuka kuwa mtu mwenye ujeuri: “Siamini kwamba tunatakiwa kuwa wenye sauti, wa kusukuma, au tusiojali hisia katika mwenendo wetu [wa kazi ya umisheni] (katika james p. bell, In the Strength of the Lord: The Life and Teachings of James E. Faust [1999], 373). Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika kuhusu mtu anavyoweza kuwa jasiri bila kuwa jeuri. andika njia mahususi ambayo utatumia ushauri wa kuwa jasiri lakini sio mjeuri. pia andika jinsi ushauri huu unaweza kukusaidia kuwa mwenye mafanikio katika kuwafundisha na kuwatumikia wengine.

“zuia tamaa zako zote,” (alma 38:12).

Kuzuia humaanisha kudhibiti, kuongoza, au kuamrisha. tamaa ni hisia kali. tafakari maswali yafuatayo, na uandike majibu yako katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Kwa nini unafikiri ni muhimu kwetu kuzuia tamaa zetu? ni kwa jinsi gani unafikiri kuzuia tamaa zako kunaweza kukusaidia kujazwa na upendo? Utafanya nini kufuata ushauri wa alma kuzuia tamaa zako zote?

“epuka kuwa mvivu” (alma 38:12).

tathmini vifungu vya maandiko vilivyoorodheshwa katika kielelezo katika muungano wa vitabu vitatu chini ya maneno “Uvivu, vivu, mvivu” tafuta ushauri kuhusu kile humaanisha kuwa mvivu na kuhusu kinyume cha kuwa mvivu. chagua mistari miwili ilivyoorodheshwa chini ya kiingizo na hujifunze juu yake. andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kuhusu kile unachojifunza kutoka katika mistari hii uliyoichagua. andika kuhusu jinsi ushauri kuepukana na uvivu utakusaidia kuwafundisha na kuwahudumia wengine kwa umakini zaidi. Mwishowe, andika njia mahu-susi unayoweza kujizuia kuwa mvivu.

Page 367: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

352

Somo la Mafunzo- NyumbaniAlma 33–38 (Kitengo cha 19)

Vifaa vya Matayarisho kwa Mwalimu wa Mafunzo- NyumbaniMuhtasari wa Masomo ya Mafunzo- Nyumbani Kila SikuMuhtasari ufuatao wa mafundisho na kanuni wanafunzi walijifunza waliposoma. Alma 33–38 (kitengo cha 19) haitarajiwi kufundishwa kama sehemu ya somo lako. Somo unalofundisha huzingatia katika sehemu chache tu za mafundisho na kanuni. Fuata ushawishi wa Roho Mtakatifu unapofikiria mahitaji ya wanafunzi.

Siku ya 1 (Alma 33–35)Alma aliwafundisha Wazoramu kwamba tunaweza ku-mwabudu Mungu wakati wote kupitia sala. Alma baadaye anafundisha kwamba tunapokea rehema ya Baba yetu wa Mbinguni, ikijumuisha msamaha wa dhambi zetu, kwa sa-babu ya Upatanisho wa Yesu Kristo. Amuleki aliwafundisha Wazoramu kwamba Upatanisho wa Yesu Kristo usiokuwa na mwisho na wa Milele unaleta wokovu kwa binadamu wote. Wanafunzi pia walijifunza kwamba ili kupokea baraka kamili ya Upatanishao, lazima tufanye imani mpaka toba.

Siku ya 2 (Alma 36) Kutoka katika uzimulizi wa Alma kuhusu kuongoka kwake, wanafunzi walijifunza kwamba dhambi inaweza kutuletea uchungu mkali na majuto. Kwa kuongezea, walijifunza kwamba kama tutafanya imani katika Upatanisho wa Yesu Kristo, atatukomboa kutoka katika maumivu ya dhambi zetu na kutujaza na shangwe. Kama Alma, tunaweza kupokea shangwe kuu tunapotafuta kuweleta wengine kwa Kristo.

Siku ya 3 (Alma 37)Alma alimpa mwanawe Helamani mamlaka ya kuziweka na kuzitunza kumbukumbu takatifu. Kwa kujifunza maneno ya Alma, wanafunzi walijifunza kwamba kuleta madhumuni Yake ya milele, Bwana anafanya kazi kwa njia ndogo na rahisi. Pia walijifunza kwamba kama tutatii Amri za Bwana, tutafanikiwa. Alma aliwafundisha wanawe kwamba tukiji-funza katika ujana wetu kuzitii Amri za Mungu na kwamba kama tutayashika maneno ya Yesu Kristo, yatatuongoza katika kupokea uzima wa milele.

Siku ya 4 (Alma 38)Wanafunzi walipojifunza ushauri wa Alma kwa Shibloni, walijifunza kwamba wanapoanza katika ujana wao kuwa na msimamo na waaminifu katika kutii Amri, wanaweza kuleta shangwe kuu kwa wazazi wao. Alma alishuhudia kwa wa-nawe kwamba Mungu hukomboa watu kutoka katika ma-jaribio, shida na majonzi wakati wanapofanya mambo yote kwa uvumilivu na imani katika Yeye. Alma pia alishuhudia kwamba kupokea ondoleo la dhambi zetu na amani nafsi zetu, lazima tumlilie Bwana kwa ajili ya rehema. Mwishowe, wanafunzi walijifunza kwamba kukuza sifa ya kiasili ya haki kunatuandaa kuwafundisha na kuwatumikia wengine.

UtanguliziAmuleki aliwafundisha Wazoramu kwamba Upatanisho “hauna mwisho na ni wa milele” (Alma 34:10). Wanafunzi walijifunza ukweli huu katika mafunzo yao ya wiki, na somo hili litawaletea nafasi zaidi ya kuelewa na kuthamini Upatanisho wa Yesu Kristo.

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 33–35Alma na Amuleki wanafundisha Wazoramu kuhusu Upatanisho wa Yesu KristoUliza: Kwa nini ni Yesu Kristo pekee ambaye aliweza kuleta upatanisho kwa ajili ya dhambi za ulimwengu?

Wakumbushe wanafunzi kwamba, kama sehemu ya mazoezi walipangiwa kila wiki, walisoma Alma 34:10– 14 na waliweka alama vishazi ambavyo vinajumuisha maneno isiyo na mwisho na ya milele. Muombe mwanafunzi asome mistari hii kwa sauti, na kisha waulize wanafunzi kushiriki vishazi walivyotambua.

Mwalike mwanafunzi asome kauli ifuatayo ya Mzee Russel M. Nelson wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili ili kuwasaidia kuelewa jinsi Upatanisho wa Yesu Kristo hauna kikomo na ni wa milele:

Page 368: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

353

SoMo la MafUnzo- nyUMbani

“Upatanisho Wake hauna kikomo— hauna mwisho. Na pia uli-kuwa hauna kikomo kwa vile wanadamu wataokolewa kutoka kwenye kifo kisicho kuwa na mwisho. Ulikuwa hauna mwisho hali ya mateso Yake makali. Ulikuwa hauna mwisho katika na-fasi— ulikuwa ufanyike mara moja tu. Na rehema ya Upatanisho imetolewa siyo tu kwa idadi ya watu isiyo na mwisho, bali pia kwa idadi ya dunia zisizo na mwisho zilizoumba Naye. Ulikuwa hauna mwisho kuzidi kipimo chochote cha mwanadamu cha kupima au uwezo wa kibinadamu wa kuelewa.

“Yesu alikuwa ndio mtu pekee aliyeweza kutoa upatanisho huu usio na mwisho, kwa vile alizaliwa na mama mwenye mwili unao kufa na baba mwenye mwili usiokufa. Kwa sababu ya upe-kee wa uzao wake, Yesu alikuwa ni Kiumbe asiye na mwisho” (“The Atonement,” Ensign, Nov. 1996, 35).

Uliza: Je! Ni kwa jinsi gani mafundisho ya Amuleki na maelezo haya kutoka kwa Mzee Nelson yanatusaidia kuelewa kwa nini Yesu Kristo alikuwa mtu pekee ambaye aliyeweza kuleta upata-nisho kwa ajili ya dhambi za ulimwengu?

Waombe mwanafunzi wafanye muhtasari kile walichojifunza mpaka sasa kutoka Alma 34 kuhusu Upatanisho wa Yesu Kristo. Elezea kwamba kanuni ya msingi tunayoweza kujifunza kutoka katika kifungu hiki ni kwamba Upatanisho wa Yesu Kristo usio na mwisho na wa milele unaufanya wokovu kuweze-kana kwa binadamu wote.

Andika kishazi kifuatacho ubaoni au katika kipande cha karatasi: Fikiria maisha bila 

Nyanyua kitu ambacho vijana wengi wanakidhamini (kama vile simu tamba). Uliza: Je! Maisha yatakuwaje bila kitu hiki?

Halafu, nyanyua chupa au glasi ya maji (au kitu ambacho ni muhimu katika kutupa uhai). Uliza: Je! Maisha yatakuwaje bila kuwa na maji?

Baada ya wanafunzi kujibu maswali haya, malizia kauli ubaoni; Fikiria maisha bila Upatanisho wa Yesu Kristo.

Uliza maswali yafuatayo:

• Je! Unafikiri watu wanachukulia vipi maisha kama hawajui ku-husu Yesu Kristo au kama hawaamini kwamba kuna Mungu?

• Je! Unafikiria maisha yangekuwa tofauti vipi kwako bila Upa-tanisho wa Yesu Kristo? (Wape wanafunzi muda wa kutafa-kari swali hili kabla ya kuuliza majibu yao.)

Elezea kwamba Amuleki alifundisha Wazoramu kwamba wa-lihitaji kutubu ili waweze kupata baraka za Upatanisho katika maisha yao (ona Alma 34:15–17). Waombe wanafunzi kama walishawahi kuchelewesha kutubu kwa sababu walikuwa

wanaogopa kuungama dhambi zao au walikuwa wanaogopa kwamba hawakuwa imara vya kutosha kubadilika. Kisha uliza: Kwa nini ni hatari kuchelewesha toba?

Waalike wanafunzi wachukue zamu kusoma kwa sauti kutoka Alma 34:30–35, wakitafuta kile ambacho Amuleki alifundisha kuhusu kwa nini hatupaswi kuchelewesha toba. Jadili mistari hii kwa kuuliza maswali yafuatayo:

• Tazama katika Alma 34:32. Kwa nini tunapaswa kutubu leo? (Wanafunzi wanapojibu, wasaidie kuelewa kanuni hii: Maisha haya ni wakati wetu wa kujiandaa kukutana na Mungu.)

• Tazama katika Alma 34:33. Je! Ni nini Madhumuni ya maisha haya? Kutatokea nini kwa wale ambao wanaahirisha toba?

• Tazama katika Alma 34:31. Je! Ni ahadi gani imetolewa kwa wale ambao wanaotubu sasa?

Soma kauli ifuatayo ya Rais Boyd K. Packer wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili.

“Hautakiwi kujua mambo yote kabla nguvu ya Upatanisho kufanya kazi ndani yako. Kuwa na imani katika Kristo; inaanza kufanya kazi siku unayoiomba!” (”Washed Clean Safi,” Ensign, May 1997, 10.)

Uliza: Je! Kauli hii ya Rais Packer inakufundisha nini? Kwa nini ni ya msaada kwako?

Alma 36Alma anamshauri mwanawe HelamaniWanafunzi wako walijifunza ushauri wa Alma kwa mwanawe Helamani, ulionakiliwa katika Alma 36, na kujifunza kuhusu furaha ambayo Alma aliipata alipotubu dhambi zake kwa dhati. Wanafunzi waliulizwa wasome Alma 36:19–22 na kisha waandike katika shajara zao za kujifunza maandiko kile mistari hii iliwafundisha kuhusu nguvu ya Upatanisho (siku ya 2, kazi ya 3). Waalike wanafunzi wachache kushiriki kile walichokiandika. Hitimisha na ushuhuda wako wa Upatanisho wa Yesu Kristo na shangwe inayokuja kutokana na toba.

Kitengo kinachofuata (Alma 39– 44)Waombe wanafunzi kufikiria kuhusu jinsi mzazi anayejali na mwenye upendo anavyoweza kumrekebisha mwanawe ambaye ametenda dhambi mbaya ya uasherati. Alma alikumbana na hali hii na akafundisha ukweli muhimu kwa mwanawe Koriantoni, aliyetenda dhambi wakati akitumikia katika misheni.

Page 369: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

354

UtanguliziAlma alimrudi mwanawe mpotevu Koriantoni, ambaye alikuwa ameacha kazi yake na kutenda dhambi ya uasherati. Alma alimfundisha umuhimu wa vitendo vyake na akaonyesha kusikitishwa kwamba Koriantoni

alikuwa na hatia ya dhambi mbaya. Alma alimwamuru mwanawe kuacha kukimbilia shauku za macho yake na kutubu. (Ushauri wa Alma kwa Koriantoni kwenye ma-somo mengine unaendelea katika milango ya 40– 42.)

SOMO LA 96

alma 39

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 39:1–8Alma anamweleza mtoto wake Koriantoni ubaya wa dhambi ya uasheratiAndika swali lifuatalo ubaoni: kwa nini baadhi ya dhambi ni mbaya sana kuliko zingine? Waalike wanafunzi kufikira kimya majibu ya swali hili. Pendekeza kwamba ushauri wa Alma ulionakiliwa katika Alma 39 unaweza kutusaidia kuelewa ubaya na uhalisi wa baadhi ya dhambi. Waalike wanafunzi waangalie muhtasari juu ya kichwa cha ukurasa wa 39. Waulize wam-tambue nani anaongea katika sura hii na anaongea na nani (Alma anaongea na mwanawe Koriantoni). Elezea kwamba Koriantoni alikuwa amefuatana na kaka yake Shibloni na Alma kuhubiri injili miongoni mwa Wazoramu, lakini alianguka katika dhambi. Sisitiza kwamba kuelewa nini ambacho Koriantoni alifanya makosa itawasaidia wanafunzi kue-lewa vyema ushauri wa Alma kwake katika sura hii na sura tatu zinazofuata. Mualike mwanafunzi asome Alma 39:1–5 kwa sauti. Omba darasa litafute ni kile Kori-antoni alifanya ambacho kilikuwa makosa. (Unaweza kuhitaji kuelezea kwamba neno kahaba katika mstari wa 3 linahusu mwanamke asiye msafi au malaya.)• Ni kitu gani Koriantoni alikifanya kilichokuwa makosa? Ni ipi kati ya dhambi zake

ilikuwa mbaya sana? (Kuzini.)• Miongoni mwa Wazoramu, Koriantoni alikuwa amejisifia kuhusu nguvu zake na hekima

(ona Alma 39:2). Ni kwa njia gani tabia ya kiburi inaweza kutupelekea kwenye kutenda dhambi kama vile kuzini? Nini baadhi ya mifano ya kisasa ya siku hizi yenye tabia za kiburi zinazosababisha watu kufanya dhambi ya uasherati? (Wanafunzi wanapojadili maswali haya, sisitiza kwamba wakati watu wana majivuno, mara nyingi hujiona wenye nguvu sana, ikijumuishwa na uwezo wao wa kukinza majaribu. Baadhi ya mifano ya kisasa ya siku hizi ni mahusiano ya mapema na uhusiano wa mtu mmoja pekee.)

Waambie wanafunzi wasome Alma 39:5 kimya, wakitafuta jinsi Alma alivyoelezea madhara ya dhambi ya uasherati. (Inaweza kusaidia kuelezea kwamba neno machukizo linahusu kitu fulani ambacho ni chenye dhambi, kiovu, au cha kuchukiza.) • Je! Bwana anahisi vipi kuhusu dhambi uasherati? (Wakati wanafunzi wanapojibu, wasai-

die kutambua ukweli kwamba kuzini ni chukizo machoni pa Bwana.) • Kwa nini unafikiria kuzini na uasherati yamewekwa karibu na kuua katika uzito wake? Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa kiwango cha Bwana na ahadi inayojumuishwa ka-tika usafi wa kimwili, waalike wanafunzi kusoma kimya aya mbili za mwanzoni kwenye kifungu chenye jina “Usafi wa Kijinsia” katika Kwa nguvu ya Vijana.Waombe wao wata-fute majibu ya maswali yafuatayao wanaposoma. (Unaweza ukipenda kuandika swali hili ubaoni. Unaweza ukipenda pia kupendekeza kwamba wanafunzi waweke alama katika vijitabu vyao majibu wanayoyapata.)• Ni nini faida ya kuendelea kuwa msafi ?Baada ya wanafunzi kupata muda wa kusoma na kutoa taarifa ya majibu waliyoyapata, waombe wasome sehemu iliyobaki ya Usafi wa Kijinsia kimya, wakitafuta majibu kwa maswali yafuatayo.

Page 370: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

355

alMa 39

• Je! Ni viwango gani Bwana anatuwekea kuendelea kuwa wasafi kijinsia?Waalike wanafunzi watafakari ni ujumbe gani wanahisi Bwana angewapatia wajifunze kutoka katika kile walichosoma. Shuhudia uzito wa dhambi ya uasherati na baraka zinazo-tokana kwa kuwa msafi kimwili.Sisitiza kwamba kwa kumshauri mwanawe kuhusu umuhimu wa jambo hili, Alma alikuwa akitimiza wajibu wake kama mzazi. Waulize wanafunzi wafikirie jinsi wanavyoweza kujibu ushauri kutoka kwa wazazi wao au viongozi wa Kanisa kuhusu usafi wa kimwili. Waalike wasome Alma 39:7–8 kimya, wakitafuta sababu ya Alma katika kumfundisha Koriantoni uzito wa dhambi ya uasherati. • Nini ilikuwa Sababu ya Alma kumfundisha Koriantoni kuhusu uzito wa dhambi yake?

(Kumsaidia Koriantoni kutubu ili asiweze kusimama na hatia mbele ya Mungu.)• Je! Tunaweza kujibu vipi pale mtu anapotualika sisi kutubu?Kuwasaidia wanafunzi kuelewa kwa nini wazazi, kama Alma, wangewaalika watoto wao kutubu, soma kauli ifuatayo ya Mzee D. Todd Christofferson wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili:

“Mwaliko wa kutubu ni mwonyesho wa upendo. Kama hatutawaalika wengine kubadilika au kama hatutaki toba sisi wenyewe, tunashindwa katika kazi muhimu tunayodaiwa na wengine na kwetu sisi wenyewe. Mzazi anayeruhusu, rafiki anayependa raha, kiongozi wa kanisa mwenye hofu kwa ukweli wanahuzunika kuhusu wao wenyewe zaidi ya hali za furaha za wale wanaoweza kuwasaidia. Naam, mwito wa toba mara nyingine unatambuliwa

kama usiyovumilika au wa kuudhi na unaweza kubishiwa, lakini kwa kuongozwa na Roho, kwa kweli ni tendo la kuonyesha kujali” (“The Divine Gift of Repentance,” Ensign or Liahona, Nov. 2011, 39).

Alma 39:9–19Alma anampa moyo Koriantoni kutubuKuwasilisha ushauri Alma alioutoa kwa mwanawe kuhusu jinsi ya kutubu na kumgeukia Bwana, andika yafuatayo ubaoni: Toba inajumuisha . . .Waalike wanafunzi wachache wachukue zamu kusoma kwa sauti kutoka Alma 39:9–13 Tua katikati ya kila mstari kuwauliza wanafunzi maswali yafuatayo:

Alma 39:9• Inaamanisha nini “kuzikana dhambi zako”? (Kuacha kuzitenda.)• Ni nini vishazi “usiviendee tena vishawishi vya macho yako” na “jifunge katika vitu

hivi” vina uhusiano gani na kuzikana dhambi? (Inaweza kusaidia kuelezea kwamba ka-tika siku zetu kishazi “vishawishi vya macho” vinaweza kuhusu taswira na viburudisho ambavyo ni vya picha za ngono katika njia yoyote. Kusisitiza hatari ya picha za ngono, firikiria kuwaomba wanafunzi kusoma ushauri kwenye somo hili katika ukurasa wa 12 wa Kwa Nguvu ya Vijana. Unaweza pia kueleza kwamba kishazi “jifunge” kinamaanisha kufanyia kazi kujizuia au kujihimili; ona tanbihi 9b.)

• Ni njia gani zingine vijana Watakatifu wa Siku za Mwisho wanaweza kujishughulisha kwa kujizuia katika mambo ya usafi wa kimwili na kuepuka kufuata vishawishi vya ma-cho yao. (Kuwasaidia wanafunzi kujadili swali hili kwa kina zaidi, unaweza ukataka ku-elezea baadhi ya hali ambazo ni za muhimu kwa tamaduni na hali za wanafunzi wako. Kwa mfano, unaweza kusema kitu kama kifuatacho: Msichana Mtakatifu wa Siku za Mwisho ameamua “kujifunga” lakini baada ya hapo mvulana anayempenda anamwalika katika sherere isiyo na maadili. Je anapaswa kujibu vipi?)

Sisitiza kwamba Alma 39:9 ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Unaweza ukitaka kupe-ndekeza kwamba wanafunzi waweke alama katika kifungu hiki katika maandiko yao ili waweze kukipata kirahisi.

Alma 39:10• Ni kwa njia gani kutafuta kurutubishwa kiroho— ikiwezekana kutoka kwa wazazi, vio-

ngozi wa Kanisa, ndugu, au marafiki wanaoaminika— hutusaidia kutubu?

Alma 39:9 ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Rejea katika mawazo ya mafundisho mwishoni mwa somo ili kuwasaidia wanafunzi kwa umahiri wao wa kifungu hiki.

Page 371: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

356

SoMo la 96

Alma 39:11• Inamaanisha nini “usiamini kudanganywa”? (Unaweza ukitaka kueleza kwamba neno

kubali linamaanisha kuruhusu.)• Ni nini baadhi ya vitu “visivyofaa au vya kijinga” ambavyo unawaona watu wakipoto-

shwa navyo leo hii?

Alma 39:12• Je! inamanisha nini kujiepusha kutoka katika uovu? (Keupuka dhambi.)

Alma 39:13Eleza kwamba toba inamaanisha “kugeuza moyo na matakwa kwa Mungu” (ona Kamusi ya Biblia, “Toba”). Katika maandiko matakatifu, kishazi “geukia kwa Bwana” mara nyingi kinamaanisha toba. • Je! Unafikiri inamaanisha nini “kumgeukia kwa Bwana kwa akili zako zote, uwezo, na

nguvu”?Wakubushe wanafunzi kwamba wakati wa misheni kwa Wazoramu, tabia ya Koriantoni iliwaelekeza watu wasiamini maneno ya Alma (ona Alma 39:11).• Wakati dhambi zetu zinapowaathiri wengine, je, tufanye nini kama sehemu ya toba

yetu? (Kukiri au kuungama makosa yetu kwa wale tuliowaumiza na kutafuta jinsi ya kurekebisha walioumia. )

Andika ukweli ufuatao ubaoni: Toba inajumuisha kukiri na kuachana na dhambi zetu na kumgeukia Bwana kwa akili zetu zote, uwezo, na nguvu. Unaweza kutaka kupende-keza kwamba wanafunzi waandike kauli hii katika maandiko yao karibu na Alma 39:13. Waombe wanafunzi waandike katika daftari au shajara za kujifunza maandiko kuhusu nini wanachohisi Bwana angewataka kufanya ili kumgeuzia mioyo na matakwa yao Kwake kwa ukamilifu zaidi. Ili kusisitiza kazi ya Mwokozi katika mchakato wa toba, waombe wanafunzi wasome Alma 39:15–16, 19 kwa sauti. Uliza darasa litafute kishazi ambacho kimerudiwa mara tatu katika mistari hii. (Kishazi ni “habari njema,” ambayo ungependa kuielezea inama-anisha “habari nzuri.”)• Ni “habari njema” gani ambazo Alma alimfundisha mwanae? (Kati ya majibu wanafu-

nzi watakayotoa yanapaswa kuwa na ukweli kwamba Yesu Kristo alikuja kuondoa dhambi za ulimwengu. Unaweza kutaka kuandika hili ubaoni.)

• Kwa nini ujio wa Yesu Kristo ulikuwa ni habari njema kwa Koriantoni? (Wanafunzi wanapojibu swali hili, unaweza kutaka kuwaambia kwamba Koriantoni baadaye alitubu dhambi zake na kurudi kuwa mmisionari [ona Alma 49:30].)

Fikiria kushiriki na darasa jinsi ujumbe wa Upatanisho waYesu Kristo umekuwa “habari njema” kwako au kwa wale unaowajua. Ongezea ushuhuda wako kuhusu kanuni ambazo wanafunzi wamezijadili kutoka katika Alma 39. Wahimize wanafunzi kufuata ushawishi ambao wameweza kuupata wakati wa somo la kulinda usafi wao na kumgeukia Bwana kupitia toba.

Umahiri wa Maandiko—Alma 39:9Gawa darasa katika makundi ya wanne wanne au watano watano. Kipe kila kikundi dadu ya pande sita na penseli. (Kama chapa haipo, fikiria kutohoa shughuli kwa kuweka vipande vya karatasi, kila kimoja kikiwa kimeandikwa namba kutoka 1 mpaka 6, katika bahasha au kifungashio chochote.) Kila mwanafunzi atahitaji pia kipande cha karatasi kisichoandikwa. Acha kila kundi la wanafunzi kukaa kwa kukaribiana kuzunguka meza au ndani ya duara. Waalike wafungue maandiko yao kwenye Alma 39:9.Eleza kwamba nia ya shughuli hii ni kuwa mtu wa kwanza katika kundi kuandika wazi Alma 39:9 kwa ukamilifu wake. Hata hivyo, kwa sababu kuna penseli moja kwa kila kundi, mtu mmoja tu katika kundi anaweza kuandika katika wakati mmoja. Mtu atahitimu kutu-mia penseli kwa kipata 1 kwenye dadu. Waambie washiriki wa kila kundi kuchukua zamu kuzungusha dadu (au kuchukua kipa-nde cha karatasi na kuirudisha). Wakati mtu anaporusha dadu ( au kuchagua) 1, huchukua penseli nakuanza kuandika, akisema kwa sauti kila moja ya maneno wakati akiyaandika.

Page 372: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

357

alMa 39

Kwa sasa, wengine katika kundi wanachukua nafasi wakirusha dadu ili kustahili kutumia penseli. Wakati mwanafunzi mwingine katika kundi akirusha 1, mtu huyo anachukua penseli kutoka kwa mwandishi aliyepita na anaaza kuandika mstari katika karatasi yake wakati akisema maneno. Mwandishi aliyetangulia anaungana na kundi lililobaki katika kurusha dadu. Wakati wanafunzi wanapostahili kupata penseli na tayari wameshaandika sehemu ya mstari katika karatasi zao, ni lazima wasome kwa sauti kipande walichokia-ndika kabla ya kuandika zaidi kwenye mistari. (Hii inaleta kurudiarudia ambako kutawa-saidia wanafunzi kukariri mstari.) Shughuli inamalizika wakati mwanafunzi kutoka katika kila kundi anapoandika Alma 39:9 kwa ukamilifu wake. Uliza darasa lirudia mstari kwa umoja baada ya shughuli hiyo. Tazama : Kwa sababu ya asili na urefu wa somo hili, unaweza ukipenda kutumia shughuli hii siku ingine, unapokuwa na muda wa ziada.

Page 373: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

358

UtanguliziKama Alma alivyomuonya mwanawe Koriantoni ku-husu madhara ya dhambi, alifundisha pia kuhusu mai-sha baada ya kifo. Alieleza kwamba kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo, watu wote watafufuliwa. Alifundisha kuhusu ulimwengu wa kiroho, ambako wafu, kulingana na chaguo zao katika maisha ya duniani, wanasubiri ama paradiso au gerezani mpaka ufufuko.

Tazama: Katika somo hili, wanafunzi watakuwa na nafasi ya kufundishana mbele ya darasa, andaa vitini vilivyo na maelekezo kwa ajili ya wenza. Kuwa mwe-lewa wa kila seti ya maelekezo ili uweze kuwasaidia wanafunzi wanapojiandaa kufundisha.

SOMO LA 97

alma 40

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 40Alma anafundisha Koriantoni kuhusu dunia ya kiroho na ufufuoAndika maswali yafuatayo ubaoni mbele ya darasa:

1. Nini kinachotuwezesha kuishi baada ya kufa? Ni nani atafufuliwa? 2. Tutaenda wapi tutakapokufa? Kukoje huko? 3. Ufufuko ni nini? Je! Miili yetu iliyofufuka itakuwaje tofauti na miili yetu ya kufa? Tutafanya

nini baada ya kufufuliwa?Waalike wanafunzi wafikirie kwamba wao ni wamisionari na kwamba wana mpango kukutana na mtu ambaye anatafuta majibu kwa maswali yaliyoandikwa ubaoni. Eleza kwamba Alma 40 ni mwendelezo wa mafundisho ya Alma kwa mwanawe Koriantoni na ina majibu ya maswali hayo.Waalike wanafunzi wasome Alma 40:1 kimya. Waulize wanafunzi kutambua kwa nini Alma alijadili ufufuo na mwanawe.• Kwa nini Alma alimfundisha Koriantoni kuhusu ufufuo?• Unapokumbuka uamuzi wa Koriantoni, kwa nini angekuwa na shaka kuhusu ufufuo?Gawa darasa katika majozi. Wapangie kila jozi nambari: 1, 2, au 3. Alika kila jozi lifanye kazi kama vile wamisionari wenza, wakijitayarisha kufundisha somo fupi kujibu maswali yaliyo ubaoni yanayoshabihiana na nambari walizopangiwa. Ili kuwasaidia kujiandaa, wape nakala ya maelekezo yanayoshabihiana na nambari zao (ona hapa chini) Wanafunzi wanapofanya kazi unaweza kutaka, kutembea tembea kwenye chumba ili uweze kusikiliza na kusaidia inapohitajika.

Uwenza 1—Alma 40:1–5Maswali: Nini kinatuwezesha kuishi baada ya kufa? Ni nani atakayefufuliwa?Jiandae kutumia Alma 40:1–5 kujibu maswali haya. Unapojiandaa, amua sehemu gani ya somo kila wenza watafundisha. Kuwa tayari kufanya yafuatayoToa maelezo machache ya usuli kwa kifungu ulichopangiwa. (Unapofundisha kutoka katika maandiko, eleza nani anazungumza, nani anazungumziwa, na hali zingine zozote ambazo zinaweza kuwasaidia wanafunzi kuelewa kifungu cha maneno.) Soma mistari ambayo inajibu maswali. Eleza jinsi ukweli katika mistari hii unavyosaidia kujibu maswali. Unapofanya hivyo, hakikisha kila mtu anaelewa kwamba kwa sababu ya Yesu Kristo, wanadamu wote watafufuliwa. Unaweza pia kupendekeza kwamba wale unaowafundisha waandike ukweli huu katika maandiko yao karibu na Alma 40:1–5.Shiriki kwa nini ahadi ya ufufuo ni muhimu kwako. Unaweza pia kuwauliza wale unaowa-fundisha kwa nini wanafurahia ahadi ya ufufuko. Shuhudia juu ya kweli ulizofundisha.

Wasaidie wanafunzi katika jozi au makundiWanafunzi wanapofa-nya kazi wakiwa katika jozi ama makundi, fikiria kutembea tembea ndani ya chumba na kusikiliza mijadala yao. Hii inaweza kukusaidia kujua ni muda gani wanaohitaji ili waweze kumaliza kazi zao. Hii inaweza kukuwezesha kuwasikiliza wanafu-nzi wakishiriki umaizi ambao ungependa kuurejea baadaye katika somo. Tazama kwa-mba wanafunzi mara kwa mara watajisikia vizuri zaidi kuwa nawe ukisikiliza majadiliano yao utakapowasifia kwa juhudi na umaizi wao.

Page 374: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

359

alMa 40

Uwenza 2—Alma 40:6–14Maswali: Tutaenda wapi tutakapokufa? Je! Kukoje huko? Jiandae kutumia Alma 40:6–7, 11–14 kujibu maswali haya. Unapojiandaa, amua ni sehemu gani ya somo kila mwenza utafundisha. Kuwa tayari kufanya yafuatayo: Toa maelezo machache ya usuli kwa fungu la maneno ulilopangiwa. (Unapofundisha kutoka kwenye maandiko matakatifu, eleza nani anazungumza, nani anazungumziwa, na mazingira mengine yeyote ambayo yanaweza kusaidia wanafunzi kufahamu fungu la maneno.)Soma mistari inayojibu maswali. Eleza jinsi ukweli katika mistari hii unavyosaidia kujibu maswali. (Inaweza kusaidia kutoa msisitizo kwamba wakati Alma alipotumia kishazi giza nene la nje hakumaanisha hali ya mwisho ya Shetani na wale waliolaaniwa. Alionyesha hali ya waovu kati ya wakati wa vifo vyao na muda wa ufufuo wao. Hivi leo huwa tuna-onyesha hali hii kama gereza la kiroho.) Unaposoma mistari hii, hakikisha kila mmoja anaelewa kwamba kati ya kifo na ufufuo, roho za walio na haki zinaishi paradiso na roho za waovu zinaishi gerezani. Unaweza kupendekeza kwamba wale unaowafundisha waandike ukweli huu katika maandiko yao karibu na Alma 40:11–14.Shiriki jinsi uelewa wako wa ukweli huu unavyoshawishi maamuzi unayoyafanya katika maisha. Unaweza kuwauliza pia wale unaowafundisha jinsi uelewa wao wa maisha baada ya kifo umewasaidia.Shuhudia kuhusu kweli ulizofundisha.

Uwenza 3—Alma 40:21–26Maswali: Ufufuo ni nini? Miili yetu iliyofufuliwa itakuwaje tofauti na miili yetu ya sasa? Tutafanya nini baada ya kufufuliwa?Jiandae kutumia Alma 40:21–26 kujibu maswali haya. Unavyojiandaa, amua sehemu gani ya somo kila mwenza atafundisha. Kuwa tayari kufanya yafuatayo:Toa habari fupi za usuli kwa taarifa uliyopangiwa. (Unapofundisha kutoka katika maa-ndiko, eleza nani anazungumza, anazungumziwa na nani, na hali ingine yoyote ambayo inaweza kuwasaidia wanafunzi kuelewa kifungu cha maneno.)Soma mistari ambayo inajibu maswali. Elezea jinsi ukweli katika mistari hii umesaidia kujibu maswali. (Unapojiandaa kufundisha, inaweza kusaidia kufahamu kwamba neno roho katika mistari hii linamaanisha roho ya mtu.) Hakikisha kila mtu anaelewa kwamba ufufuo ni muungano wa roho na mwili, na vitu vyote vikiwa vimerejeshwa katika sehemu zake sahihi na kimilifu. Unaweza kutaka kupendekeza kwamba wale unaowa-fundisha waandike ukweli huu katika maandiko yao karibu ya Alma 40:21–23.Shiriki kwa nini unashukuru kujua kwamba mwili wako na roho siku moja vitarejeshwa katika sehemu zake sahihi na kikamilifu. Unaweza pia kueleza jinsi maamuzi yako yame-adhiriwa na ufahamu wako kwamba siku moja utasimama mbele ya Mungu na kuhuku-miwa. Waombe wale unaowafundisha kushirikisha hisia zao kuhusu mafundisho ya ufufuo na hukumu ya mwisho. Shuhudia juu ya kweli ulizofundisha.Baada ya wanafunzi kujiandaa kujibu maswali waliyopangiwa, wapange katika vikundi vidogo ili waweze kufundishana katika igizo la wamisionari. Kila kundi liwe na wenza watatu, na kila wenza wakiwa wameandaa majibu katika mpangilio ya maswali tofauti. (Kama darasa ni dogo, waambie kila kundi kufundisha darasa zima.) Wape moyo wanafu-nzi kujiamini wanapofundisha na wanapojifunza kutoka kwa wengine wakati wa kuigiza. Wahakikishie kwamba Roho Mtakatifu anaweza kuwatia hamasa na wale wanaowafundi-sha kama ni wakweli katika maelekezo yao na majibu yao. Wasikilize wanapofundishana, na toa mitazamo kama unahisi kufanya hivyo. Baada ya wanafunzi kuwa na muda wa kufundishana katika makundi, fikiria kuuliza wa-nafunzi baadhi ya maswali yafuatayo: • Umejifunza nini ulipojiandaa kujibu maswali uliyopangiwa? Ulijifunza nini ulipokuwa

ukifundishwa na wenza wengine?• Kujua kwamba Koriantoni alijitahidi kutii sheria ya usafi wa kimwili, unafikirije kufahamu

asili ya maisha baada ya kifo kungeweza kumsaidia kujizuia na majaribu ya baadaye?• Kwa nini ukweli tuliojadiliana leo una maana kwako?

Page 375: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

360

SoMo la 97

Waalike wanafunzi wasome Alma 40:25–26 kimya, wakitafuta tofauti kati ya hatima ya hali za wenye haki na hatima za hali za waovu. Baada ya kuelezea walichokipata, waulize ku-shiriki jinsi kifungu hiki cha maneno kinashawishi uamuzi wao wa kuishi injili. Unaweza kutaka kushiriki majibu yako kwa swali hilo hilo. Shuhudia kuhusu nafasi yaYesu Kristo katika kutoa baraka za ufufuo.

Rejeo la Umahiri wa MaandikoUfahamu wa wanafunzi wa vifungu vya maandiko utaongezeka wakati watakapotunga maswali yao wenyewe katika vifungu hivyo. Waalike wanafunzi wafanye kazi pamoja, kama darasa au vikundi vidogo, waandike dondoo ambazo zinaonyesha vifungu vya umahiri vya maandiko mahususi. (Unaweza ukipenda kuchagua vikundi vya vifungu vilivyotengwa ambavyo ungependa wanafunzi wajifunze au kurejelea.) Halafu waambie wakusomee dokezo zake. Alama zinatolewa kwako kama utakisia kifungu cha umahiri wa maandiko kwa usahihi. Alama zinatolewa kwa darasa kama huataweza kukisia kwa usahihi. Angalizo: Urefu wa somo hili unaweza kuruhusu muda kwa shughuli ya umahiri wa maandiko. Hata hivyo, kuhakikisha kwamba wanafunzi wana muda wa kutosha kujiandaa kwa ajili ya kushiriki katika somo, unaweza ukitaka kutumia shughuli hili mwishoni mwa darasa, kama muda utaruhusu. Kama huna muda wa kutumia shughuli hii kama sehemu ya somo, unaweza kuitumia siku nyingine. Kwa shughuli zingine za tathmini, ona kiamba-tanisho mwishoni mwa kitabu cha kiada hiki.

Tangazo na Habari za UsuliAlma 40:11. “Kuchukuliwa nyumbani kwa Mungu yule aliyewapa maisha”

Rais Joseph Fielding Smith alieleza kwamba maneno katika Alma 40:11 hayafundishi kwamba tutaletwa katika uwepo wa Mungu mara moja baada ya kufa:

“Maneno haya ya Alma [Alma 40:11–14] kama ninavyo-yaelewa, hayakusudiwi kupelekea wazo kwamba roho zote zitarudi katika uwepo wa Mungu kwa ajili ya kupa-ngiwa mahali pa amani au mahali pa adhabu na mbele yake kupokea hukumu binafsi. ‘Kuchukuliwa nyumbani kwa Mungu,’ [linganisha Mhubiri 12:7] inamaanisha kwamba maisha yao ya hapa duniani yamefika mwisho, na wamerudi kwenye ulimwengu ya kiroho, ambako wamepangiwa kwenye sehemu kulingana na kazi zao pamoja na wenye haki au pamoja na wasio na haki, pale wakisubiri ufufuo. ‘Kumrudia Mungu’ ni kishazi kinacho-pata uwiano katika hali zingine nyingi zinazojulikana vizuri. Kwa mfano: mtu anatumia muda uliopangwa katika misheni ya kigeni. Wakati anapumzishwa na aka-rudi Marekani, anaweza kusema, ‘Ni furaha sana kurudi nyumbani’; bado nyumbani kwake inaweza kuwa Utah au Idaho au sehemu nyingine za magharibi.” (Answers to Gospel Questions, comp. Joseph Fielding Smith Jr., 5 vols. [1957–66], 2:85).

Alma 40:11–15. Ulimwengu wa Kiroho uko wapi?

Rais Brigham Young alifundisha:

Ulimwengu wa Kiroho uko wapi? Uko hapa hapa. Je [roho za wale waliokufa] zinaenda kupita mipaka ya dunia iliyopangwa? Hapana, hawafanyi hivyo. Wana-letwa kutoka dunia hii” (Discourses of Brigham Young, sel. John A. Widtsoe [1954], 376).

Alma 40:11–15. Nini kinatokea kwa roho zilizo katika ulimwengu wa kiroho?

Wakati mwili unapokufa, roho inaendelea kuishi. Katika ulimwengu ya kiroho, roho za wenye haki zinapokelewa kwa hali ya furaha, ambayo inaitwa paradiso, hali ya kupumzika, hali ya amani, ambapo zitapumzikia kutoka kwenye taabu zao zote na kutoka kwa mashaka yote na masikitiko (Alma 40:11–12). Sehemu inayoitwa gereza la kiroho imewekwa kwa wale ‘ambao wamekufa ka-tika dhambi zao, bila ufahamu wa ukweli, au dhambi, wakiwa wamewakataa manabii’ (M&M 138:32). Roho katika gereza la kiroho ‘zinafundishwa imani katika Mungu, toba kutoka kwenye dhambi, kazi za ubatizo mbadala kwa ondoleo la dhambi, zawadi ya Roho Mta-katifu kwa kuwekewa mikono, na kanuni zingine zote za injili ambazo ni za muhimu kwa wao kuzijua (M&M 138:33–34). Kama watakubali kanuni za injili, wakatubu dhambi zao, na wakakubali maagano yanayofanywa kwa niaba yao hekaluni, watakaribishwa paradiso” (True to the Faith: A Gospel Reference [2004], 46–47).

Page 376: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

361

UtanguliziAkiendelea kumshauri mwanawe Koriantoni, Alma alifundisha kwamba mpango wa urejesho unajumuisha siyo tu kufufuka kwa mwili lakini pia urejesho wa roho

ambamo hali yetu ya milele inaonyesha matendo na hamu zetu za duniani. Alma alisisitiza kwamba uovu hauwezi kamwe kuelekeza kwenye furaha.

SOMO LA 98

alma 41

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 41Alma anamfundisha Koriantoni kuhusu mpango wa urejeshoUliza darasa lifikirie vipi matendo ya mtu yanaweza kushawishiwa kama wataamiini kauli zifuatazo (tua kidogo baada ya kila kipengele kuruhusu wanafunzi kujibu):Hakuna maisha baada ya kifo.Baada ya kufa, tutafanywa wakamilifu bila kujali kazi zetu hapa duniani. Katika hukumu ya Mwisho, tutazawadiwa kwa matendo yetu mema na kuadhibiwa kwa matendo yetu mabaya. • Kwa nini ni muhimu kuwa na ufahamu sahihi wa kile kitakachotutokea baada ya kufa?Wakumbushe wanafunzi kwamba katika Alma 40 walijifunza kuhusu mafundisho ya Alma kwa Koriantoni kuhusu ulimwengu wa kiroho, ufufuo, na hukumu. Eleza kwamba katika Alma 41 tunajifunza kwamba Koriantoni alichanganyikiwa kwa kile ambacho baadhi ya watu walikuwa wanakifundisha kuhusu ufufuo. Sisitiza kishazi “wamepotelea mbali” katika Alma 41:1, na waalike wanafunzi wasome mstari huu wakitafuta kile kilichokuwa kikiwasababishia baadhi ya watu kupotoka.• Kwa nini baadhi ya watu walikuwa wanapotoka? (Unaweza ukitaka kueleza kwamba

kupotosha maandiko ni kuyabadilisha, kuharibu, au kubadilisha maana yake.)• Je! Alma alisema atamweleza nini Koriantoni?Mara wanafunzi wanapotambua neno urejesho, unaweza ukipenda kuliandika ubaoni. Eleza kwamba urejesho humaanisha kurudisha au kuweka tena katika hali yake ya mwanzoni.Eleza kwamba Alma alitaka Koriantoni aelewe kwamba kuna dhana ya kimwili na dhana ya kiroho kwa kile alichokiita “mpango wa urejesho” (Alma 41:2). Waalike wanafunzi kupekua Alma 41:2–5 kimya, wakitafuta vitu ambavyo vitarejeshwa kimwili kwetu baada ya kufa na vitu ambavyo vitarejeshwa kiroho. Unaweza ukipenda kupendekeza kwamba wanafunzi waweke alama ya kile walichokipata. Kabla wanafunzi hawajasoma, inaweza kusaidia kwako kueleza kwamba mahitaji inamaanisha inahitajika au lazima.• Je, Ni kipengee gani cha kimwili cha mpango wa urejesho kilichotajwa katika Alma

41:2? (Katika urejesho, roho itarejeshwa kwenye mwili, na viungo vyote vya mwili vitarejeshwa.)

• Je! Ni kipengee gani cha kiroho cha mpango wa urejesho kilichoelezewa katika Alma 41:3–5? (Wanafunzi wanapojibu, andika ukweli ufuatao ubaoni: Tutarejeshwa kwenye furaha au kwenye taabu kulingana na kazi na hamu zetu katika maisha duniani.)

Waalike wanafunzi wafikirie wanafundisha mistari hii kwa darasa la Msingi.• Je! Unaweza kuelezea vipi mafundisho ya urejesho wa kiroho ili kwamba watoto wa-

weze kuulewa? Wakumbushe wanafunzi kwamba Koriantoni alikuwa amevunja amri ya usafi wa kimwili na akaacha jukumu lake la umisionari (ona Alma 39:2–4).

Page 377: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

362

SoMo la 98

• Je! Ufahamu sahihi wa mafundisho ya urejesho wa kiroho ungeweza kumsaidia vipi Koriantoni kufanya maamuzi bora? Je! Kufahamu mafundisho haya kunaweza kuathiri vipi matendo na hamu yetu?

Shuhudia ukweli wa mafundisho haya, na ushiriki mawazo yako kuhusu haki ya Mungu katika kuturejeshea mazuri au mabaya kulingana na hamu zetu na matendo yetu. Andika swali lifuatalo ubaoni: Itakuwaje kama nimetenda dhambi?• Kulingana na mpango wa urejesho, tunapokea nini kama tumetenda dhambi?• Je! Kuna njia yeyote ya kurejeshewa uzuri na furaha wakati tumetenda makosa? Mwalike mwanafunzi asome Alma 41;6–9 kwa sauti. Waombe wanafunzi watafute kile tunachoweza kukifanya kurejeshewa uzuri na furaha hata kama tumetenda dhambi. (Sisi lazima tutubu na tuwe na hamu ya haki katika maisha yetu yote .)• Ni maneno au vishazi gani katika Alma 41:6–7 vinavyopendekeza kwamba tunawa-

jibika kwa kile tunachopokea katika ufufuo? Ni katika hali gani sisi tu waamuzi wetu wenyewe? (Chaguo zetu katika maisha haya uamua aina ya hukumu tutakayoipokea tutakaposimama mbele za Mungu.)

Sisitiza kwamba baadhi ya watu wanafikiri wanaweza kurudi na kuishi na Mungu bila kuchukua jukumu la kibinafsi kwa matendo yao. Mara nyingi wanasema kwamba chaguo zao za dhambi zilikuwa ni mchezo. Mara nyingine wale wanajiingiza kwenye dhambi wanaweza kuonekana kuwa wana furaha.Waalike wanafunzi wasimame na kusoma Alma 41:10 kwa sauti kwa pamoja. Sisitiza kwamba Alma 41:10 ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Unaweza ukipenda kupende-keza kwamba wanafunzi waweke alama katika kifungu hiki kwa njia ya pekee ili waweze kukipata kwa urahisi. (Kwa sababu hiki ni kifungu cha umahiri wa maandiko, unaweza kuwaacha warudie pamoja zaidi ya mara moja. Unaweza kuwauliza kama yeyote darasani anaweza kurudia kutoka kichwani.) Wanapokuwa wamemaliza, liombe darasa kukaa. Uba-oni, andika “Uovu kamwe haujawa furaha.”• Kwa nini ni kweli kwamba ”Uovu kamwe haujawa furaha”?• Ni mfano gani wa jinsi Shetani angetufanya tuzivunje amri na kuamini kwamba tuna-

weza bado kuwa na furaha?Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa utofauti kati starehe fupi za ulimwenguni na furaha ambazo Bwana anazitoa, soma kauli ifuatayo ya Mzee Glenn L. Pace wa Sabini:“Shughuli zilizokatazwa na Bwana mara yote na kwa miaka mingi zilizochukiwa na jamii kwa sasa zinakubalika na kuinuliwa na jamii hiyo hiyo. Vyombo vya habari vinatumia shu-ghuli kama hizi kwa njia inayozifanya zionekane kuwa zinakubalika. . . .“. . . Usikosee raha ya telestia na furaha ya selestia na shangwe. Usikosee kukosa kujinyima na uhuru. Uhuru uliokamilika bila kizuizi sahihi unatufanya watumwa kwenye hamu zetu wenyewe. Usitamanie maisha ya kawaida na ya chini. . . .“. . . Amri unazozitii hazikutolewa na Mungu asiye na upendo kukuzuia kupata furaha, lakini na Baba wa Mbinguni mwenye upendo anayekutaka uwe na furaha wakati unaishi katika dunia hii na vilevile dunia ijayo” (“They’re Not Really Happy,” Ensign, Nov. 1987, 39–40).Andika maelezo yafuatayo kwenye ubao: Unaweza ukitaka kupendekeza kwamba wanafu-nzi wayaandike katika maandiko yao karibu na Alma 41:10. (Kauli inapatikana katika “To ‘the Rising Generation,’” New Era, June 1986, 5.)

“Huwezi kufanya mabaya na kuhisi vyema. Haiwezekani!” (Rais Ezra Taft Benson)Waambie wanafunzi kwamba Alma 41:11 inaelezea kwa nini haiwezekani kuwa na furaha ya kweli wakati unafanya maamuzi mabaya. Nakili chati ifuatayo ubaoni (unaweza uki-penda kufanya hivyo kabla ya darasa kuanza), au utayarishe kama kitini kwa kila mwana-funzi. Wapange wanafunzi katika majozi, na waagize kuoanisha kila kishazi kutoka Alma 41:11 na maana yake. Pia waalike kujadiliana maswali yayoambatana.

Soma kwa pamojaKusoma kwa pamoja kunaongeza msisitizo katika kifungu cha maa-ndiko na vile vile kucha-ngia umoja darasani. Pia ni njia moja kuongeza utofauti katika somo. Tumia wazo hili wakati uona kwamba wanafu-nzi wanaweza kuhitaji kubadilisha mwendo. Wape moyo wao kwa kusema maneno kwa ku-kusudia na kwa pamoja wanapoyasoma.

Alma 41:10 ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Rejea wazo la kufundishia mwishoni mwa somo ili kuwasaidia wanafunzi na umahiri wao wa kifungu hiki.

Page 378: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

363

alMa 41

vishazi katika alma 41:11 ambavyo vinaeleza kuwa katika “hali ya asili”

Maana

1. “Katika hali ya kimwili” a. tukizuiwa na kulemewa na dhambi zetu

2. “Katika nyongo ya uchungu na katika minyororo ya dhambi”

b. Kupungukiwa na baraka na mwelekeo wa Mungu; kupotea kwa uenza wa Roho Mtakatifu.

3. “bila Mungu ulimwenguni” c. Kutawaliwa na mapenzi ya kimwili.

Katika mstari huu, tunaona kwamba “asili ya Mungu” ni “asili ya furaha.” hii inakuambia nini kuhusu kwa nini kuwepo na dhambi ni kinyume cha asili ya furaha?ni baadhi ya mifano gani mahususi ya kwa nini watu wanaweza kujikuta katika hali ya kutokuwa na furaha?

(Majibu: 1- c, 2- a, 3- b)Ili kuwasaidia wanafunzi kuona kung’angania katika “hali ya uhalisi” inahusisha mafu-ndisho ya urejesho, waalike wanafunzi wasome Alma 41:12. Baada ya mistari kusomwa, Waombe wanafunzi wajibu swali la Alma. Halafu waambie wanafunzi wasome majibu ya Alma katika swali lake yeye mwenyewe katika Alma 41:13. Unaweza ukitaka kupendekeza kwamba waweke alama kile ambacho Alma alisema kitarejeshwa kwetu kama sehemu ya mpango wa urejesho.)Waombe wanafunzi kufikiria kuwa wana rafiki anayechagua kutenda katika njia ambazo ni kinyume na amri za Bwana lakini anataka kurejeshwa kwenye haki. Waambie wanafunzi kuelezea mafundisho ya urejesho kwa mwenzake, kama kwamba wao ni yule rafiki, waki-tumia Alma 41:12–13. (Wanafunzi wanaweza kutumia maneno yao wenyewe au maneno ya kauli iliyoandikwa ubaoni: “Tutarejeshwa aidha kwenye furaha au huzuni kulingana na kazi na hamu zetu katika maisha haya.”)Waonyeshe wanafunzi bumarengi au uichore picha yake ubaoni. Waulize wanafunzi kile bumarengi hufanya inaporushwa kisahihi. (Inarudi katika sehemu ilipokuwa imerushiwa.) Waulize wasome Alma 41:14–15 kimya, wakitafuta njia ambazo bumarengi inaweza kuashiria kweli zilizofundishwa katika mistari hii. (Unaweza ukitaka kupendekeza kwamba wanafunzi waweke alama mistari hii.) Waalike wanafunzi kueleza kile walichokipata.• Je! Ni baadhi ya mambo gani unayotumainia kuyapokea kutoka kwa wengine na kutoka

kwa Bwana katika maisha haya na katika maisha yajayo? (Majibu yanaweza kujumuisha upole, rehema, na upendo. Fikiria kuorodhesha majibu ya wanafunzi katika ubao.)

• Ni lini umetoa wema, rehema, au upendo kwa wengine na baadaye ukaupokea tena?Wahimize wanafunzi kuweka lengo, kutenda katika njia na kukuza mitazamo ambayo inayoakisi kile wanachotumaini kurejeshewa kwao katika maisha haya na yajayo. Shuhudia juu ya furaha inayokuja tunapotenda katika haki.

Umahiri wa Maandiko—Alma 41:10Tazama: Kwa sababu ya asili na urefu wa somo hili, shughuli ifuatayo ingekuwa nzuri zaidi ikitumiwa siku nyingine mkiwa na muda wa ziada.Andika yafuatayo ubaoni: . . . ni furaha.Waalike wanafunzi wabuni kauli kinyume ya mafundisho yanayofundishwa katika Alma 41:10. (Jibu moja linaweza kuwa “Haki ni Furaha” Kisha waalike wanafunzi kuorodhesha matendo halisi ya haki ambayo wanafikiri yangeweza kutosha katika sehemu iliyowazi. (Kwa mfano, “Kuwatumikia wengine ni furaha.”) Waulize wanafunzi kama wanaweza kushuhudia kwamba kitendo chochote kati ya hivi kinaongoza kwenye furaha. Baada ya wanafunzi wachache ku-changia ujuzi wao na shuhuda, waalike wanafunzi kuandika katika kadi ndogo au kipande cha karatasi au mawili wanayoweza kuyafanya katika wiki kuongeza furaha yao. Wape moyo ku-beba karatasi zao kama kumbukumbu na kutoa taarifa ya juu ya juhudi zao katika siku zijazo.

Waalike wanafunzi waeleze mafundisho na kanuniWape wanafunzi nafasi ya kuwaeleza wengine mafundisho na kanuni walizojifunza darasani. Wanapojiandaa kueleza ukweli wa injili, wataji-funza kutafakari vifungu vya maandiko kwa kina zaidi na kuyapanga mawazo yao. Wanapoe-leza ukweli huu kwa we-ngine, Roho Mtakatifu atazidisha ufahamu wao na ushuhuda wa ukweli wanaoufundisha.

Page 379: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

364

UtanguliziAlma alihitimisha ushauri wake kwa mwanawe Koria-ntoni kwa kuelezea kwamba Baba yetu wa Mbinguni ametoa njia kwa wale wanaotenda dhambi kupata neema. Alifundisha kwamba haki ya Mungu inadai kwamba watenda dhambi waondolewe kwenye uwepo

wa Mungu. Na ndipo alishuhudia kwamba Yesu Kristo “angetuliza madai ya haki” (Alma 42:15) kwa kuteseka kwa ajili ya wote ambao wametenda dhambi na kwa kutoa neema kwa wanao tubu.

SOMO LA 99

alma 42

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 42:1–14Alma anafundisha Koriantoni kuhusu Haki ya MunguMbele ya wanafunzi, chora michoro miwili rahisi ya mizani ubaoni, kama ilivyooneshwa katika ukurasa ufuatao. (Usiongeze maneno katika mchoro mpaka utakovyoelekezwa ku-fanya hivyo katika somo. Unaweza ukitaka kuhamasisha wanafunzi kunakili mchoro huu katika daftari au shajara za kujifunza maandiko. )Juu ya mizani, andika kauli ifuatayo Ninataka Hukumu ya Mwisho kuwa ya haki.Waalike wanafunzi wainue mikono yao kama wanakubaliana na kauli iliyo ubaoni.• Kwa nini unataka Hukumu ya Mwisho kuwa ya haki?• Neno ya haki linamaanisha nini?Pendekeza kuwa ya haki inaweza kumaanisha kupata unachostahili. Wazo la haki linahusi-ana na neno la kimaandiko haki. Andika neno haki ubaoni chini ya mizani.Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa dhana ya haki, mwambie mwanafunzi asome maelezo yafuatayo ya Mzee Dallin H. Oaks wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili: "Haki ina maana nyingi. Moja ni usawa. Alama ya kawaida ya haki ni mizani iliyo sawa. Hivyo, wakati sheria za mtu zinapokuwa zimekiukwa, sheria kwa kawaida inahitaji kwamba adhabu itolewa, adhabu ambayo itarejesha uwiano [kwenye mizani]. "Sheria za Mungu ni vivyo hivyo zinahusiana na haki. Wazo la haki kama kile mtu anasta-hili ni nguzo ya kimsingi ya maandiko yote yanayozungumzia watu kuhukumiwa kuli-ngana na kazi zao." (“Sins, Crimes, and Atonement” [address to CES religious educators, Feb. 7, 1992], 1, si. lds. org).Eleza kwamba Koriantoni mwana wa Alma alikuwa na wasiwasi kuhusu haki ya Hukumu ya Mwisho. Alika mwanafunzi asome Alma 42:1 kwa sauti wakati darasa likitafuta kile Koriantoni alifikiria kingekuwa sio sawa au cha haki, kuhusu Hukumu ya Mwisho?• Koriantoni alihisi nini kilikuwa sio haki? (Kwamba wenye dhambi watapelekwa au

kukabidhiwa kwenye hali ya majonzi). • Kwa nini Koriantoni angetaka kuamini kwamba ingekuwa si haki kwa wale waliofanya

dhambi kuadhibiwa? (Kama wanafunzi wanahitaji kukumbushwa kwamba Koriantoni alikuwa akihangaika na dhambi mbalimbali, warejeshe kwa Alma 39:2–3.)

• Kama haki ina maana ya kupokea kile tunastahili na kuadhibiwa kwa ajili ya dhambi zetu, jinsi gani hii pia ingeweza kututia mashaka? (Sisi sote tunafanya dhambi na tuko chini ya madai ya sheria.)

Fanya muhtasari Alma 42:2–11 kwa kueleza kuwa Alma alishughulikia hofu ya Koriantoni. Alifundisha kwamba Kuanguka kwa Adamu kuliwaleta wanadamu wote katika hali ya ku-anguka ambako ni lazima wapitie kifo cha kimwili na kifo cha kiroho (ona Alma 42:9 ). Pia alielezea kuwa bila ya njia ya kuokolewa kutoka hali hii ya kuanguka, roho za watu wote zitakuwa na huzuni na kuondolewa kutoka uwepo wa Mungu milele. (ona Alma 42:11).

Page 380: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

365

alMa 42

Mwalike mwanafunzi asome Alma 42:12 kwa sauti. Elezea kwamba aya hii inasisitiza kuwa kuanguka na madhara yake, ikiwa ni pamoja na kuondolewa mbali kutoka uwepo wa Mungu, ililetwa na kutotii kwa Adamu kwa sheria za Mungu. Wasaidie wanafunzi waelewa kwamba wakati tunapovunja amri za Mungu — wakati tunapofanya dhambi — sisi wenyewe tunajiweka mbali zaidi tunajiweka wenyewe katika matakwa ya sheria. (Unaweza ukitaka kumwalika mwanafunzi asome Makala ya Imani 1:2 kwa sauti.) Waambie wanafunzi wa-some Alma 42:14 kimya, wakitafuta matokeo ambayo sheria inahitajika kwa ajili ya kutotii.• Inamaanisha nini “kuondolewa” katoka uwepo wa Mungu? (Kutengwa kutoka kwa

Mungu na kutoweza kurudi kuishi katika uwepo Wake. Unaweza kutaka pia kutaja kuwa tunapofanya dhambi, tunajiondoa wenyewe kutoka kwa uenzi wa Roho Mtakatifu, ambaye ni mshiriki wa Uungu.

Ubaoni, ongeza vishazi Kutotii au dhambi na kuondolewa mbali kutoka uwepo wa Mungu kwa mchoro, kama inavyooneshwa hapo chini.

Kutokana na kile ulichojifunza katika Alma 42:1–14, unaweza kufanya muhtasari vipi katika sentensi moja kile sheria ya haki inahitaji wakati mtu si mtiifu? (Andika ukweli ufuatao kwe-nye ubao chini ya mizani: Kwa sababu ya kutotii kwetu, sheria ya haki inahitaji kuwa sisi tuondolewe kutoka uwepo wa Mungu. Unaweza ukitaka kupendekeza kuwa wanafu-nzi waandike ukweli huu katika maandiko yao matakatifu karibu na Alma 42:1–14.)Waalike wanafunzi wasome Alma 42:18 kimya, wakitafuta matokeo mengine ya dhambi.• Inamaanisha nini kuwa na majuto ya dhamira? Waalike wanafunzi watafakari wakati walipopata uzoefu wa majuto na huzuni au kutoku-wepo kwa Roho Mtakatifu kwa sababu wamefanya dhambi. Waombe wao wafikirie kwa-mba hisia zikizidishwa na kila kitu walichowahi kufanya kimakosa. Halafu watake kufikiria kwamba hisia hiyo inabaki pamoja nao milele.Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa na kuhisi haja ya huruma, unaweza kuuliza swali lifuatalo:• Kulingana na kile ulichojifunza katika Alma 42:1–14, unataka Hukumu ya Mwisho isi-

mame kwenye misingi ya haki tuu?

Alma 42:15–31Alma anamfundisha Koriantoni kuhusu mpango wa rehemaIli kuwasaidia wanafunzi kuelewa kwamba madai ya haki lazima kuridhishwa, onyesha sehemu ya adhabu kwenye mizani ubaoni. Unaweza kufikiria kushikilia kifutio kama una-kwenda kufuta madai ya haki. Uliza:• Kuna njia yoyote ambayo madai ya haki yanaweza kufutwa au kuondolewa? (La, Wakati

amri za Mungu zimevunjwa, sheria huhitaji adhabu. Madai ya haki ni lazima yaridhishwe.Wasaidie wanafunzi kuelewa kwamba itakuwa sio haki kufuta matokeo ambayo haki ina-dai. Mualike mwanafunzi asome Alma 42:25 kwa sauti.• Kulingana na Alma, nini kingetokea kama matokeo ya dhambi yangeondolewa na haki

ikaachwa bila kuridhishwa?Waambie wanafunzi kutafakari swali lifuatalo kabla ya kuwapa marejeo ya maandiko ili kupata jibu:• Kama madai ya haki hayawezi kufutwa, basi vipi wale ambao wamefanya dhambi (kila

mmoja wetu) kweli watapata amani ya dhamiri na kurejeshwa kwenye uwepo wa Mungu? (Baada ya kuwapa wanafunzi muda kutafakari swali, alika mwanafunzi asome

Kutotii au dhambi

Kuondolewa mbali kutoka

uwepo wa Munguhaki

Waalike wanafunzi kutafakari swaliKuuliza swali ambalo linahitaji wanafunzi kufikiria kabla ya kujibu huchochea tamaa yao ya kujua jibu na husababi-sha wao kuangalia kwa kina katika maandiko au katika uzoefu wao binafsi kwa ajili ya kue-lewa. Waruhusu wanafu-nzi muda kufikiri kuhusu swali kabla ya kuwaele-keza kwenye maandiko kwa ajili ya jibu.

Page 381: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

366

SoMo la 99

Alma 42:15. Inaweza kuwa na msaada kueleza kwamba kishazi "kuridhisha madai ya haki" humaanisha ya kulipa deni, au kupata adhabu, ambayo haki inadai.)

• Kulingana na Alma 42:15, inawezeka vipi kuwa huruma utaendelezwa kwetu?Kwa kutumia majibu ya wanafunzi futa kishazi "Kuondolewa kutoka uwepo wa Mungu" kutoka ubaoni na kuandika Upatanisho wa Yesu Kristo na Rehema. Chini ya mizani, andika ukweli ufuatao: Upatanisho wa Yesu Kristo ulitosheleza madai ya haki ili huruma iweze kutolewa kwetu.

• Inamaanisha nini kwako kujua kwamba Mwokozi kwa hiari yake atateseka katika nafasi yako ili huruma iweze kutolewa kwako?.

Waambie wanafunzi wasome Alma 42:22–24 na watafuta kile kinachohitajika ili huruma itolewe kwetu.• Kinatakiwa nini kutoka kwetu ili tupate huruma na kuepuka madai kamili ya sheria?

(Wakati wanafunzi wametambua toba kama njia ambayo sisi hupata huruma, andika ka-nuni ifuatayo kwenye ubao chini ya mizani: kama tukitubu, tutapata huruma kupitia Upatanisho ya Mwokozi. Unaweza pia kutaka kupendekeza kwamba waandike hili katika maandiko yao karibu na Alma 42:22–24.)

• Unafikiri kishazi “waliotubu kwa ukweli” humaanisha nini? (Kutubu kwa dhati)• Kwa nini ni muhimu kwetu kuelewa kwamba Mwokozi aliteseka adhabu kwa dhambi

zetu katika nafasi yetu?Elezea kwamba Yesu Kristo ni Mpatanishi wetu. Mpatanishi ni yule anayesimama kati ya watu wawili kuwasaidia kutatua kutoelewana. Mwambie wanafunzi asome kwa sauti kauli ifuatayo na Rais Boyd K. Packer wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili. Omba darasa lisikilize sababu za kwa nini mtu wa tatu anahitajika kwa ajili ya rehema iweze kutolewa kwa mwenye dhambi:"Kwa sheria ya milele, rehema haiwezi kutolewa isipokuwa kuwe na mmoja ambaye ana hiari na anaweza kuchukua deni letu na kulipa thamani na kuweka masharti kwa ajili ya ukombozi wetu."Kusipokuwa na mpatanishi, tusipokuwa na rafiki, uzito mzima wa sheria isiyobadilishwa, isiyo na huruma, lazima, kwa hali chanya iangukie kwetu. Malipo kamili ya kila kosa ijapo dogo namna gani au zito namna gani, yatatakiwa kutoka kwetu kwa njia yoyote hata kwa kiwango kidogo sana, "Lakini jua kwamba: Ukweli, ukweli mtukufu, unaonyesha kuwa kuna Mpatanishi. . . ."Kupitia Kwake, rehema inaweza kutolewa kwa kila mmoja wetu bila kuvunja sheria ya milele ya haki. "Kutolewa kwa rehema hakutakuwa moja kwa moja. Itakuwa ni kupitia kwa agano na Yeye. Itakua kwenye masharti Yake, masharti Yake ya ukarimu" (The Mediator, Ensign, May 1977, 55–56).Waombe wanafunzi wasome Alma 42:29–31 kimya, wakitafuta kile ambacho Alma alita-mani kwa ajili ya Koriantoni. (Unaweza ukitaka kupendekeza kwamba wanafunzi waweke alama kile walichokipata.)• Unafikiri inamaanisha nini kuacha haki na rehema na mateso ya Bwana viwe na uthibiti

kamili kwenye moyo wako? Waalike wanafunzi waandike mpango mfupi wa somo ambao unaonyesha jinsi wanaweza kufundisha mawazo ya haki na rehema kwa wengine. Wahimize kufundisha familia zao kile walichojifunza leo.

Kutotii au dhambi

Upatanisho wa yesu Kristohuruma

haki

Page 382: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

367

alMa 42

Wakumbushe wanafunzi kuhusu shaka ya Koriantoni kuhusu usawa wa haki ya Mungu. Unaweza ukitaka kushuhudia kuwa Hukumu ya Mwisho itakua ya haki na kuwa sote tutapata tunachostahili, kutokana na haki na rehema ya Mungu. Unaweza pia kusisitiza kwamba Koriantoni alitubu dhambi zake na alikuwa na athari chanya kwenye ukuaji wa Kanisa (ona Alma 49:30). Waombe wanafunzi kutafakari jinsi watakavyohitaji kuendelea katika mchakato wao wa kutubu.Waalike wanafunzi wachache kushiriki shukrani na shuhuda zao kwa hiari ya Mwokozi kuleta upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu na kutosheleza madai ya haki kwa niaba yetu. Shiriki ushuhuda wako wa rehema na ukombozi uliyopo kupitia kwa dhabihu ya upatani-sho ya Mwokozi.

Page 383: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

368

UtanguliziWakati Alma na wanawe wakiendelea kuhubiri injili, Wazoramu walijiunga na jeshi la Walamani kuwasha-mbulia Wanefi. Kapteni Moroni alidhihirisha imani na busara katika kuwaongoza Wanefi kujilinda dhidi jeshi la Walamani. Ijapokua walizidiwa kwa idadi,

maandalizi ya wanajeshi Wanefi na imani yao katika Yesu Kristo iliwasaidia vitani. Walamani walipoona wa-likuwa dhahiri wanashindwa, walifanya agano la amani na kuondoka kutoka kwa nchi hiyo kwa kipindi fulani.

SOMO LA 100

alma 43–44

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 43Maandalizi na mikakati ya Kapteni Moroni ilisaidia kushinda mbinu za jeshi la WalamaniWaalike wanafunzi waandike kwenye daftari au shajara za kujifunza maandiko orodha ya mipango, malengo na hamu zao za siku za usoni. Wanapoandika, wakumbushe wafikirie kuhusu malengo na hamu zao za kiroho kama vile kuhudumu misheni, kufungishwa he-kaluni na kulea familia. Kabla ya darasa, unaweza kuandika orodha kama hiyo ya malengo na hamu yako mwenyewe ya siku za usoni. Unaweza kushirikisha baadhi ya mipango na hamu zako kama mifano ili kuwasaidia wanafunzi kuanza kuandika.Baada ya wanafunzi kuandika orodha yao, waalike kutambua hamu na malengo wanahisi Shetani hatataka wao wayatimize. Alika wanafunzi wachache kushiriki malengo waliyo-yatambua. Waombe waelezee kwa nini Shetani hatotaka wao wayatimize malengo hayo. Unaweza pia kuwauliza kwa nini wanahisi kwa nguvu kuhusu kutimiza hayo malengo. Pendekeza kuwa somo la Alma 43–44 linaweza kusaidia kuonyesha jinsi tunavyoweza kutimiza malengo yetu maadilifu licha ya juhudi za uharibifu za adui.Fanya muhtasari wa Alma 43:1–4 kwa kuelezea kuwa licha ya juhudi za Alma kuwarudi-sha tena Wazoramu katika Kanisa, wengi wao walijiunga na Walamani na kujitayarisha kuwavamia Wanefi. Waliungana pia na Waamaleki, ambao, kama Wazoramu walikuwa kwa wakati mmoja Wanefi lakini walikuwa wamepotoka kutoka kwenye kweli. Mualike mwanafunzi asome Alma 43:5–8 kwa sauti. Omba darasa lifuatilie likitafuta mipa-ngo au “ mbinu” za kiongozi Mlamani, Zerahemna.Eleze kuwa tunapojifunza masimulizi ya vita vya kimwili katika Kitabu cha Mormoni, tunaweza kufananisha na mapigano ya kiroho tunayokabiliana nayo.• Mbinu za Zerahemna dhidi ya Wanefi zinaweza vipi kuwa kama mbinu alizonazo Shetani?Mualike mwanafunzi asome Alma 43:9–12 kwa sauti. Uliza darasa litambue mbinu za Wanefi.• Mbinu za Wanefi zilikuwa ni nini?Waalike wanafunzi wasome Alma 43:16–19 kimya. Waalike wakitafute kile Moroni, kapteni mkuu wa Wanefi, alikifanya kuwaandaa watu kulinda nchi yao na familia zao.• Ni vitu gani halisi ambavyo Wanefi walifanya ili kujiandaa kwa shambulizi la Walamani? Mualike mwanafunzi asome Alma 43:20–22 kwa sauti, na omba darasa litafute majibu ya Walamani kwa maandalizi ya Wanefi.• Kwa nini Walamani waliondoa shambulizi lao ijapokuwa walikuwa wengi kushinda Wanefi?• Tunaweza kujifunza nini kutoka tukio hili kuhusu kujilinda sisi wenyewe dhidi ya mbinu

za Shetani? Waalike wanafunzi wasomeAlma 43:23–24 kimya wakitafuta kile Moroni alifanya alipo-kuwa hana uhakika jinsi adui yake alivyopanga kufanya shambulio lingine.

Page 384: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

369

alMa 43– 44

• Kwa nini Moroni aliwatuma wajumbe kuzungumza na Alma?• Mfano wa Moroni unaweza kutufundisha nini kuhusu jinsi tunavyoweza kujitayarisha

kiroho dhidi ya adui? (Wasaidie wanafunzi kutambua kanuni ifuatayo: Kama tukitafuta na kufuata ushauri wa kinabii, tutaweza vizuri zaidi kujilinda dhidi ya adui.)

Kwa ufupi fanya muhtasari wa Alma 43:25–43 kwa kuelezea kwamba Moroni alitumia ufahamu ambao alipata kutoka kwa Nabii. Aliligawa jeshi lake katika sehemu mbili. Baadhi ya wanajeshi walikaa katika mji wa Jershoni na kuwalinda watu wa Amoni. Jeshi lililobakia lilikwenda katika nchi ya Manti. Moroni alituma wapelelezi kutafuta wapi walikuwepo Walamani, na alikuwa na wanajeshi wengine waliojificha katika njia ambayo Walamani wangepitia. Walamani walipokaribia, wanajeshi Wanefi waliwazingira. Walamani walipo-ona kuwa wamezungukwa, walipigana vikali. Wengi wa Wanefi walikufa, lakini Walamani hata walipata waadhiriwa zaidi. Waalike baadhi ya wanafunzi wachukue zamu kusoma kwa sauti kutoka Alma 43:43–54. Uliza darasa litafute tofauti kati ya motisha na chanzo cha nguvu za Walamani na motisha na chanzo cha nguvu za Wanefi. • Umegundua nini kuhusu sababu za Walamani za kwenda vitani? Umegundua nini

kuhusu sababu za Wanefi za kwenda vitani? Chanzo cha nguvu za Wanefi kilitofautiana vipi na kile chanzo cha nguvu za Walamani? Kama inahitajika, sisitiza kwamba wakati Walamani walipigana kwa sababu ya chuki na hasira, Wanefi walivutiwa na sababu bora zaidi [ona Alma 43:45–47]. Walimlilia Bwana kwa msaada, na Yeye aliwaimarisha [ona Alma 43:49–50].)

• Tunaweza kujifunza nini kutokana na mfano wa Moroni na jeshi lake cha kutusaidia kupigana dhidi ya adui?

Waalike wanafunzi waandike majibu yao kwa swali hili. Kisha waombe wao washiriki kile walichoandika. Wanaweza kutaja baadhi ya kanuni zifuatazo:Na tunapoomba msaada katika kutimiza mipango yetu ya haki na haja adilifu, Mu-ngu atatusaidia kuyatimiza.Tunaongozwa na nia bora kuliko hao wanaoukataa ukweli. Bwana atatusaidia kutimiza wajibu wetu kulinda familia zetu, uhuru wetu, na dini yetu.Waalike wanafunzi waelezee kuhusu wakati ambapo walipata msaada wa Bwana katika kutimiza malengo mema. Fikiria kushirikisha uzoefu wako mwenyewe. Shuhudia uwezo wa Bwana wa kutusaidia kutimiza mbinu njema. Waalike wanafunzi waweka malengo mema kama sehemu endelevu ya maombi yao.

Alma 44Kapteni Moroni anawaamuru Walamani kufanya agano la amaniMualike mvulana ambaye yupo radhi kusoma kwa sauti aje mbele ya chumba na maa-ndiko yake. Kumbusha darasa kwamba wakati kapteni Moroni alipoona hofu kubwa ya Walamani, aliamrisha watu wake kuacha kupigana (ona Alma 43:54). Acha yule mvulana asome maneno ya Moroni katika Alma 44:1–6. Omba darasa lisikilize maelezo ya Moroni kuhusu ushindi wa Wanefi.• Moroni alitaka Zerahemna kuelewa nini kuhusu chanzo cha nguvu za Wanefi kwenye

vita? Alitoa nini kwa Walamani? (Alisema kwamba Wanefi wasingewadhuru tena kama wangeweka silaha zao chini na kuingia kwenye agano la amani.)

• Tunaweza kujifunza ukweli gani kutoka katika Alma 44:4–6 ambacho kinaweza kutu-saida kwenye vita vyetu vya kiroho. (Wanafunzi wanaweza kushiriki kanuni kadhaa, baadhi yake tayari zimekwishapitiwa kwenye somo hili. Hakikisha watajumuisha ukweli unaofuata: Bwana atatuimarisha na kutuhifadhi kulingana na imani yetu Kwake. Unaweza ukitaka kupendekeza kwamba wanafunzi waweke alama kwenye maneno katika aya hizi yanayofundisha ukweli huu.)

Mualike mwanafunzi asome kwa sauti ushauri ufuatao kwa vijana wa Kanisa, kutoka kwa Rais Boyd K. Packer wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili. Unaweza ukitaka kutoa nakala kwa kila mwanafunzi.

Page 385: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

370

SoMo la 100

"Vijana wa leo wanalelewa kwenye himaya ya adui lililo na viwango vya maadili vinavyodorora. Lakini kama mtumishi wa Bwana, ni naahidi kwamba mtalindwa na kukingwa kutokana na mashambulizi ya adui kama mtatii uvuvio ambao unaletwa na Roho Mtakatifu. "Valieni kwa staha; ongeeni kwa adabu; sikiliza muziki uinuao. Epukeni uasherati na vitendo vinavyoshusha hadhi. Chukua hatua ya maisha yako na

jiamrishe kuwa shujaa. Kwa sababu tunakutegemea sana wewe, utabarikiwa sana. Haupo mbali machoni pa Baba yako wa Mbinguni mwenye upendo” (“Ushauri kwa Vijana),” Ensign au Liahona, Nov. 2011, 18).• Katika maneno ya Rais Packer, nini kinachokuvutia zaidi? Kwa nini?”Fanya muhtasri Alma 44:7–10 kwa kuelezea kuwa Zerahemna alitangaza kwamba yeye na watu wake hawakuamini kwamba Wanefi waliimarishwa na Mungu. Alijitolea kuhakiki-sha Walamani wanasalimisha silaha zao, lakini alikataa kuweka agano la amani Mualike mwanafunzi aliyesoma Alma 44:1–6 asome kwa sauti jibu alilotoa Moroni kwa Zerahemna, ambalo linapatikana katika Alma 44:11. Uliza darasa:• Unadhani kulikua na umuhimu gani kwa Moroni kuhakikisha wanaweka agano la

amani na Walamani?Fanya muhtasari Alma 44:12–20 kwa kuelezea kwamba wakati wengi wa Walamani wali-fanya agano la amani, Zerahemna aliwakusanya watu wake waliosalia kushindana na jeshi la Moroni. Na Wanefi walipoanza kuwaua, Zerahemna aliona maangamizo yao yaliyokuwa karibu sana na akaahidi kuingia kwenye agano la amani.Shuhudia juu ya mkono wa ulinzi wa Bwana katika maisha ya wale wenye imani Kwake. Wahimize wanafunzi kupigana kishujaa kwa malengo yao ya haki na haja na kuamini katika ahadi za Mungu za kutusaidia, na kutunza, na kutulinda, almradi tuna imani na Yeye (Alma 44:4).

Tangazo na Habari za UsuliAlma 36:3. Vita tunayopigana ilianza katika maisha kabla ya hapa duniani

Rais Gordon B. Hinckley alizungumzia uhalisia wa vita tuliyoingia kabla ya dunia kuanza.

“Kuna vita ambayo imeendelea kabla ya dunia kuu-mbwa na ambayo inaonekana itaendelea kwa muda mrefu ujao. . . .

“Vita hiyo . . ..ni vita kati ya ukweli na makosa, kati ya uhuru na shuruti, kati ya wafuasi wa Kristo na wale wa-liomkataa Yeye. Maadui Zake wametumia kila mbinu kwenye huo mgongano. . . .

 "Ni kama ilivyokuwa mwanzoni. Waathiriwa wanao-anguka ni tunu kama wale ambao walioanguka hapo awali. Ni mapigano yanayoendelea. . . .

"Vita inaendelea Inapiganwa katika maisha yetu we-nyewe, usiku na mchana, katika nyumba zetu, katika

kazi zetu, katika vyama vyetu vya shule; inapiganwa kwenye masuala ya mapenzi na heshima, ya utiifu na uaminifu, ya utiifu na uadilifu. Sote tunahusika navyo. Tunashinda, na siku za usoni hazijapata kuwa na mwa-nga zaidi ya sasa (The War We Are Winning, Ensign, Nov. 1986, 42, 44–45).

Alma 43:9, 45. Linda na imarisha familia

Dada Virginia U. Jensen wa Urais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama alirejelea onyo katika tangazo kuhusu familia "Kuwa kuvunjika kwa fami-lia kutawaletea watu binafsi, jamii na mataifa maafa yaliyotabiriwa na manabii wa kale na wale wa kisasa (Familia: Tangazo kwa Ulimwengu, Ensign au Liahona, Nov. 2010, 129). Dada Jensen alisema hivi: Ndugu na kina dada, tumo katikati ya uhalisi huo wakati huu. Ni wajibu wetu wote kulinda na kuimarisha familia" (Come, Listen to a Prophet’s Voice, Ensign, Nov. 1998, 13–14).

Page 386: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

371

Somo la Mafunzo - NyumbaniAlma 39–44 (Kitengo cha 20)

Vifaa vya Matayarisho kwa Mwalimu wa Mafumzo- NyumbaniMuhtasari wa Masomo ya Mafunzo - Nyumbani ya Kila SikuMuhtasari ufuatao ni wa mafundisho na kanuni ambazo wanafunzi walijifunza waliposoma Alma 39–44 (kitengo cha 20) haikusudiwi kufundishwa kama sehemu ya somo lako. Somo unalofundisha huzingatia machache ya mafundi-sho na kanuni hizi. Fuata uvuvio wa Roho Mtakatifu unapofi-kiria mahitaji ya wanafunzi.

Siku ya 1 (Alma 39)Wakati wakisoma maneno ya Alma kwa mwanawe mpotevu Koriantoni, wanafunzi walijifunza kwamba dhambi ya uzinzi ni chukizo machoni pa Bwana. Alma pia alimfundisha mwa-nawe kwamba toba inajumuisha kukubali na kuacha dhambi zetu na kumgeukia Bwana kwa akili, nguvu na uwezo wetu. Wanafunzi walisoma ushuhuda wa Alma kwamba Yesu Kristo alikuja kuchukua dhambi za ulimwengu.

Siku ya 2 (Alma 40–41)Koriantoni alihofia kuhusu ufufuo na Hukumu ya Mwisho. Kutokana na majibu ya Alma kwa hofu hizi, wanafunzi wa-lijifunza mafundisho mbalimbali yanayohusiana na ufufuo, ikijumuisha ukweli kwamba tutarejeshwa kwa furaha au mateso kulingana na kazi na hamu katika maisha ya muda. Alma pia alisisitiza kuwa “uovu haujapata kuwa furaha” (Alma 41:10).

Siku ya 3 (Alma 42)Alma alimsaidia Koriantoni kuona kwamba kutotii kunasa-babisha watu binafsi kuondolewa kutoka kwa uwepo wa Mungu. Hivyo basi wanafunzi walijifunza jinsi mpango wa ukombozi ambao unaruhusu watu binafsi kushinda hali yao ya kuanguka. Mafundisho ya Alma yanathibitisha kwamba mateso ya Yesu Kristo yalitosheleza mahitaji ya haki ili re-hema iwafikie wale wote wanaotubu.

Siku ya 4 (Alma 43–44)Wanafunzi walijifunza kuhusu vita kati ya Walamani na Wanefi. Moja ya somo walilojifunza kutoka kwa Alma 43–44 ni kwa-mba kama tukitafuta na kufuata ushauri wa kinabii, tutaweza vizuri zaidi kujilinda wenyewe dhidi ya adui. Zaidi ya hayo, wa-nafunzi waligundua kwamba tunapoomba kwa Bwana kuhusu mipango ya haki na haja adilifu, atatusaidia kuitimiza.

UtanguliziKama ilivyoandikwa katika Alma 39–42, Alma alimsaidia mwanawe Koriantoni kuelewa umakini wa dhambi ya kuzini, mafundisho yanayohusiana na ufufuo na Hukumu ya Mwi-sho, na matokeo ya milele ya sheria za haki na rehema. Somo hili litawapa wanafunzi fursa ya kufundishana na kuelezeana mafundisho haya.

Mapendekezo ya KufundishaKabla ya darasa, andaa vitini vyenye maelekezo katika somo hili. Jifahamishe wewe mwenyewe maelekezo haya ili uweze kuwa-saidia wanafunzi kufanikiwa katika juhudi zao za kufundishana.

Alma 39–41Alma anafundisha kwamba toba huleta furahaAnza darasa kwa kualika wanafunzi pamoja kwa sauti wakariri Alma 39:9, kifungu cha umahiri wa maandiko waliyohimizwa ku-kariri kama sehemu ya somo lao la juma hili. Uliza kama kuna mtu anayeweza kukumbusha darasa kwa nini Alma alimshahuri mwa-nawe Koriantoni kutubu na kuacha dhambi zake katika aya hii.

Wakumbushe wanafunzi kwamba katika Alma 40–41, Alma pia alizungumzia hofu ya Koriantoni kuhusu ufufuo wa wafu na Hukumu ya Mwisho. Ili kuwasidia wanafunzi kuelezea kile walichojifunza na washiriki hisia na shuhuda zao kuhusu ukweli unaopatikana katika Alma 39–41, andika maswali yafuatayo na marejeo ya maandiko ubaoni kabla ya darasa halijaanza.

1. Kwa nini ni muhimu kutii sheria ya usafi wa kimwili? (Ona Alma 39:1–9).

2. Ufufuo ni nini? Ni nini tofauti kati ya miili inayowezakufa na miili iliyofufuka? Nini kinatokea baada ya kufufuliwa? (Ona Alma 40:21–26.)

3. Nitahukumiwa vipi katika Hukumu ya Mwisho? (Ona Alma 41:1–7.)

4. Inaonekana kama wengine wanovunja amri wana furaha. Je! Hii ni kweli? (OnaAlma 41:10–15.)

Waulize wanafunzi wafikirie kuwa wao ni wamisionari na kwa-mba wana miadi ya kukutana na mtu anayetafuta majibu kwa maswali haya. Wajulishe kwamba watapewa muda kidogo wa kujiandaa, na kisha watapata fursa ya kujibu baadhi ya maswali haya wakitumia kile walichojifunza kutoka Alma 39–41.

Kama ukubwa wa darasa lako unaruhusu, gawa darasa kwenye majozi yanayowakilisha uenza wa wamisionari. Wapangie kila wenza mojawapo wa maswali kutoka ubaoni. (Kama darasa lako ni dogo, unaweza kupanga maswali kwa kila mwanafunzi.) Wape kila wenza nakala ya maelekezo hapa chini, na waambie

Page 387: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

372

SoMo la MafUnzo - nyUMbani

kutumia mistari iliyorejelewa mwishoni mwa swali walilo-pangiwa kujibu maswali ya mchunguzi wao. Toa muda kwa wanafunzi kutathimini mistari hii na kuandaa somo fupi kwa ajili ya mchunguzi. Wahimize wenza waamue sehemu ya maelekezo ambayo kila mtu atawajibika kufundisha.

Na wanafunzi wanapoandaa, unaweza kupenda kutembe-lea miongoni mwa wanafunzi ili uweze kusikiliza na kuwapa msaada wanapohitaji. Kama kunahitajika, wasaidie wanafunzi kutambua mafundisho kutoka Alma 39–41 ambayo yatasaidia kujibu maswali waliyopangiwa. Tumia mafundisho yafuatayo kama mwongozo:

Dambi ya uasherati ni chukizo machoni pa Bwana (ona Alma 39:1–9).

Ufufuo ni muunganisho wa mwili na roho, pamoja na vitu vyote kurejeshwa kwenye hali yake ya halisi na ukamilifu (ona Alma 40:21–26).

Tutarejeshwa kwenye furaha ama mateso kulingana na kazi zetu na hamu yetu katika maisha ya muda (ona Alma 41:1–7).

Uovu haujapata kamwe kuwa furaha (ona Alma 41:10–15).

MaelekezoKuwa tayari kufanya yafuatayo unapofundisha: 1. Toa habari ya usuli kuhusu mistari hii (kama vile kuelezea

nani anazungumza, na nani walikuwa wanazugumzia nani, na kwa nini.)

2. Soma sehemu za kifungu cha maandiko yaliyotolewa ili kuku-saidia kujibu maswali mliyopangiwa.

3. Andika mafundisho au kanuni iliyofundishwa kwenye mistari mliyojifunza ambayo inatumika kwenye swali ulilopewa.

4. Elezea jinsi mafundisho au kanuni ulioandika inasaidia kujibu swali ulilopewa. Unaweza ukitaka kupendekeza kwamba wale unaowafundisha waandike mafundisho au kanuni hii katika maandiko yao.

5. Shiriki kwa nini mafundisho au kanuni hii ni muhimu kwako, na shuhudia ukweli uliofundisha.

Baada ya wanafunzi kujiandaa kujibu maswali waliyopangiwa, waweke kwenye vikundi vidogo ili waweze kufundishana. Kama darasa lako ni dogo, acha kila mwanafunzi au kila wenza kufu-ndisha darasa zima. Baada ya wanafunzi kumaliza kufundishana, uliza darasa maswali yafuatayo:

• Unapofikiria dhambi za Koriantoni, kwa nini unadhani ufa-hamu wa mafundisho haya ungemsaidia yeye?

• Kwa nini ingekuwa ni muhimu kuweza kueleza kweli hizi kwa wale utakaoshirikiana nao katika maisha yako?

• Kwa nini ni muhimu kwamba uelewe na kuishi kweli hizi?

Alma 42Alma anamfundisha Koriantoni kuhusu haki na rehemaChora seti rahisi ya mizani ubaoni. Mwalike mwanafunzi afundi-she darasa dhana za haki na rehema kwa kutumia kielezo na kitu ambacho alijifunza kutoka kwa maelekezo ya Alma kwa Koria-ntoni katika Alma 42. Waalike wanafunzi kwenda kwa Alma 42 katika maandiko yao na kutafuta vishazi na kauli kuhusu haki na rehema ambazo waliweka alama au kupiga mstari.

Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa hali ambazo rehema hupati-kana, waulize maswali yafuatayo:

• Yesu Kristo alifanya nini ili rehema ipatikane kwetu?• Tunapaswa kufanya nini ili kupokea rehema?

Waalike wanafunzi wachache kushiriki kwa nini wana shukrani kwa ajili ya Uptanisho wa Yesu Kristo.

Alma 43–44Kutii ushauri wa manabii kunaotulinda sisi kutoka kwa aduiKama muda utabaki, fikiria kuwauliza wanafunzi kutathimini walichojifunza kutoka Alma 43–44 kwa kushiriki walichokia-ndika kwenye shajara zao za kujifundisha maandiko kuhusu kupigana na mashambulizi yao ya kiroho (siku ya 4, kazi ya 3 na 4) Shuhudia juu ya Yesu Kristo na nguvu Zake za kuendeleza rehema tunapotubu na kutulinda tunapokwenda Kwake.

Kitengo kinachofuata (Alma 45–63)Kwa nini Wanefi walifanikiwa sana dhidi ya maadui zao? Wa-liweza vipi kupigana kwa nguvu za Bwana? Majibu yanaweza kupatikana kwa kusoma mifano ya Kapteni Moroni na Helamani na askari wake vijana.

Page 388: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

373

UtanguliziBaada ya Alma kutoa maelekezo ya mwisho kwa mwanawe Helamani, aliondoka kutoka kwa watu wa Nefi na hakusikika tena. Helamani alikuwa kio-ngozi muhimu wa kiroho na Kapteni Moroni alikuwa kiongozi muhimu wa kijeshi wakati wa kipindi kigumu

cha Wanefi. Amalikia, kiongozi wa kikundi cha waasi Wanefi, aliweka mpango wa ujanja wa kupata nguvu juu ya Wanefi. Kapteni Moroni aliwasaidia wa Wanefi kujiimarisha dhidi ya mashambulizi ya maadui zao ili waweze kudumisha uhuru wao na uhuru wa kuabudu.

SOMO LA 101

alma 45–48

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 45Helamani anamini maneno ya Alma na kuanzisha huduma yakeWaalike wanafunzi wafikirie kuhusu mahojiano ambayo wamewahi kuwa nayo na mzazi au kiongozi wa ukuhani.• Ni maswali ya aina gani ambayo wazazi au viongozi wa ukuhani huwa wanauliza

katika mahojiano?Baada ya mazungumzo mafupi, eleza kwamba kabla ya Alma hajamkabidhi Helamani kumbukumbu takatifu na kuondoka kwenye hiyo nchi (ona Alma 45:18–19), alimuuliza Helamani maswali mfululizo. Waalike wanafunzi wasome Alma 45:2–8 kimya, wakitafuta maswali ambayo Alma alimuuliza na majibu aliyotoa Helamani.• Wanefi na Walamani walikuwa vitani wakati Alma na Helamani walipokuwa katika ma-

zungumzo haya. Unafikiri ni kwa vipi imani ya Helamani iliweza kumsaidia wakati wa vita na wakati wote wa huduma yake?

• Ni lini umepata nguvu kutokana na imani yako kwa Yesu kristo na maneno ya manabii na kutokana na kuwajibika kwako kutii amri?

Fanya muhtasari Alma 45:9–19 kwa kuwaambia wanafunzi kwamba baada ya Alma kutoa unabii kuhusu maangamizo ya taifa la Wanefi ambayo yangefuatia, aliondoka kwenye nchi na hakusikika tena. Kabla ya kuondoka, alitoa unabii wa mwisho. Mwambie mwanafunzi asome Alma 45:16 kwa sauti.• Kweli gani tunaweza kujifunza kutoka unabii huu? Wanafunzi wanaweza kusema

kanuni mbalimbali, lakini hakikisha wanadhihirisha ufahamu wa kuwa Bwana hawezi kutazama dhambi na kuivumilia hata kidogo.)

Eleza kwamba Helamani alianzisha huduma yake kwa kuwateua makuhani na walimu wa Kanisa katika nchi yote. Waalike wanafunzi wapekue Alma 45:23–24, wakitafuta jinsi watu walivyowajibu viongozi hawa wa Kanisa.• Watu waliwajibu vipi viongozi wao wa Kanisa? Kwa nini watu wengine walikataa kuwa-

sikiliza viongozi wa Kanisa?

Alma 46Kapteni Moroni anajiunga na waadilifu katika kulinda haki zao na dini yaoFanya muhtasari wa Alma 46:1–3 kwa kueleza kwamba wale ambao hawangewasikia viongozi wa Kanisa waliongozwa na mtu aliyeitwa Amalikia. Waulize wanafunzi wasome Alma 46:4–5 kimya, wakitafuta nini Amalikia na wafuasi wake walitamani. Waalike wana-funzi kuelezea walichokigundua.Waalike wanafunzi wasome Alma 46:6–7 kimya, wakitafuta matokeo ya athari ya Amalikia kwa wale waliomfuata. • Ni nini kilitokea kama matokeo ya athari za Amalikia?

Page 389: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

374

SoMo la 101

Waalike wanafunzi wasome Alma 46:8–10 kimya, wakitafuta masomo ambayo Mormoni alitaka tujifunze kutokana na vitendo vya Amalikia. Unaweza kusisitiza kwamba baadhi ya masomo haya yanatanguliwa na maneno kwa hiyo tunaona au tunaona. Unaweza ukitaka kupendekeza kwamba wanafunzi watie alama maneno haya katika maandiko yao. Wana-funzi wanaweza kugundua masomo yafuatayo:Watu wengi ni wepesi kumsahau Bwana na kufanya uovu.Mtu mmoja mwovu anaweza kuleta maovu zaidi.Kupambanua kati ya Amalikia na Kapteni Moroni, waulize wanafunzi wasome Alma 46:11–18 na Alma 48:11–13, 17 kimya. Alika nusu ya darasa itafute kile Moroni alitamani. Alika ile nusu ingine ya darasa itafute maneno na vishazi vinavyoeleza jinsi Moroni alivyo-kuwa. (Wasaidie wanafunzi kuona tofauti kati ya maazimio maadilifu ya Moroni na maa-zimio maovu ya Amalikia. Moroni aliunga mkono jambo la uhuru na haki, hali Amalikia alikuwa na ulafi wa madaraka na kutafuta kuwaleta Wanefi utumwani.) • Kutokana na unachokisoma, ni kwa vipi utamuelezea Kapteni Moroni? Ni kanuni zipi

tunaweza kujifunza kwenye aya hizi? Wanafunzi wanaweza kupendekeza kanuni ka-dhaa tofauti ikiwemo ukweli kuwa mtu mwadilifu anaweza kuleta uadilifu zaidi.)

• Kulingana na Alma 46:11–18, Moroni aliombea nini? Kwa baraka za kuwa uhuru na haki zibaki na Wanefi na kwa chanzo cha Wakristo kupendelewa na Mungu.

Moroni aliomba kuhusu chanzo cha Wakristo. Kulingana na, Alma 46:12, ni mawazo gani matatu ambayo Moroni anahisi kwamba Wakristo wanapaswa wayalinde na kuyadumi-sha? (Wasaidie wanafunzi kuona kwamba ni wajibu wetu kulinda familia, dini yetu na uhuru wetu. Ona pia Alma 43:45–48.)• Ni changamoto gani zilizopo dhidi ya familia, Wakristo, na uhuru kwa leo? Ni zipi baa-

dhi ya njia mwafaka tunazoweza kulinda familia zetu, dini yetu, na uhuru wetu?Waulize wanafunzi wasome Alma 46:18–22 kimya, wakitafuta kile Moroni aliwaambia watu wake wafanye. (Unaweza kupendekeza kwamba wanafunzi waweke alama neno agano kwenye aya hizi.)• Watu walifanya maagano kufanya nini? (Kudumisha haki zao na dini yao; kutomuacha

Bwana; kutovunja amri za Mungu; kutoona haya kujichukulia jina la Kristo juu yao.)• Kulingana na Alma 46:22, watu walifanya nini kama ishara ya agano walilofanya. (Wali-

rarua au kuchana nguo zao na kutupa vipande kwenye miguu ya Moroni.)Chukua kipande cha nguo, na kichane nusu kwa nusu. Unaweza ukitaka kueleza kwamba kwa kurarua au kuchana, nguo zao, watu walikuwa wanadhihirisha maamuzi yao kwa agano walilokuwa wamefanya.• Kulingana na Alma 46:21–22, watu walisema nini kingetokea kama wangevunja agano lao? • Hii inakusaidia vipi kuelewa umakini wa asili ya maagano tunayofanya na Mungu?Wakumbushe wanafunzi kuwa Moroni na watu wake walikuwa wanakabiliwa na maadui waliotaka kuwaangamiza.• Kulingana na Alma 46:18, Moroni alisema nini ingewaletea watu wake maangamizo?Andika yafuatayo ubaoni: kama tutaweka maagano yetu, Mungu ata ... Waalike wanafunzi kushiriki jinsi wangeweza kukamilisha kauli kutokana na kile wali-chokisoma kutoka Alma 46:18–22. Waulize pia wao watoe mfano wa jinsi wanavyojua kuwa kauli hii ni kweli. Majibu yanaweza kutofautiana. Fanya muhtasari wa majibu kwa kukamilisha kishazi kwenye ubao kama ifuatavyo: Kama tutayashika maagano yetu, Mungu atatubariki. Wahimize wanafunzi watafute ushahidi ambao unadhibitisha kanuni hii wanapojifunza milango iliyobakia katika Alma. Unaweza ukitaka kuwaambia kuhusu wakati Bwana alikubariki kwa ajili ya kuheshimu maagano yako.Fanya muhtasari Alma 46:29–41. Eleza kwamba Amalikia na wafuasi wake waligundua walikuwa wamezidiwa kwa idadi, kwa hivyo walikwenda katika nchi ya Nefi, wakitaka ku-jiunga na Walamani. Jeshi la Moroni lilizuia wengi wa kikundi cha Amalikia kufika kwenye nchi ya Nefi. Wengi wa wafuasi wa Amalikia waliingia katika maagano ya kutetea uhuru. Wachache ambao hawangeingia katika agano waliuawa. Amalikia na idadi ndogo ya watu wake walitoroka na kujiunga na Walamani.

Page 390: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

375

alMa 45 – 48

Alma 47Kwa udanganyifu, Amalikia akawa mfalme wa WalamaniWaulize wanafunzi wangehisi vipi kama wangekuwa kwenye mchezo wa mashindano au shindano lingine na walikuwa na kitabu kilicho na orodha ya vitu ambavyo mahasimu wao walitaka kufanya ili washinde mashindano. Waambie wanafunzi kwamba kwa kulingani-sha Alma 47 na sisi, tunaweza kujifunza zaidi mafunzo muhimu kuhusu mbinu za Shetani za kujaribu kutushinda.Fanya muhtasari Alma 47:1–6 kwa kuwambia wanafunzi kwamba Amalikia hakukata tamaa kwa malengo yake ya kupata madaraka juu ya Wanefi. Alibuni mpango wa ujanja wa kumuondoa madarakani mfalme wa Walamani na kuwa mfalme wao ili aweze kuwa-ongoza Walamani kipigana dhidi ya Wanefi. Wakati Amalikia alipoungana na Walamani, alipata upendeleo kutoka kwa mfalme wao, aliyempa amri juu ya sehemu ya jeshi la Wa-lamani. Mfalme alimwamuru Amalikia na jeshi lake kufuata sehemu ya jeshi la Walamani lililoasi, lililoongozwa na mtu aliyeitwa Lehonti. Amalikia aliamrishwa kushurutisha jeshi la Lehonti kuchukua silaha dhidi ya Wanefi lakini Amalikia alikuwa na mipango mingine.Waalike wanafunzi wajifunze Alma 47:7–19 kama wao walikuwa Lehonti na kama Ama-lickia alikuwa ni Shetani. Waulize wao wasome Alma 47:7–10 kimya, wakitafuta ni wapi Lehonti alikwenda kulinda jeshi lake na kile Amalikia alijaribu kumfanya Lehonti afanye.• Lehonti alikusanya jeshi lake wapi kwa maandalizi ya mapigano? Jeshi lina uwezo gani

zaidi kama lipo kwenye sehemu ya juu kuliko maadui wao?• Ni nini Amalikia alimtaka Lehonti afanye? Ni zipi baadhi ya mbinu ambazo Shetani

hutumia kutufanya sisi tushuke chini kutoka nyanda za juu? (Majibu yanaweza kujumu-isha kutujaribu kushusha viwango vyetu na kutushawishi kwenda sehemu ambazo sio salama kiroho.)

Waalike wanafunzi kadha wachukue zamu kusoma kwa sauti kutoka Alma 47:11–19. Uliza darasa lifuatilie, likizingatia jinsi mbinu za Amalikia zinaweza kufananishwa na mbinu Shetani anazotumia kutuangamiza.• Ni kwa njia gani mbinu za Amalikia zinafanana na mbinu Shetani anazotumia kutu-

angamiza? (Majibu yanaweza kujumuisha kwamba Shetani ni mganganizi, mlaghai, mjanja na katili.)

• Ni baadhi ya mifano gani ya njia ambazo Shetani anajaribu kutumia kutupa sumu hatua kwa hatua?

Fanya muhtasari Alma 47:20–36 kwa kueleza kwamba Amalikia aliendelea kudanganya na kuua hadi alipokuwa mfalme wa Walamani. Sisitiza kwamba maazimio na mbinu za Amalikia zilikuwa karibu sawa na maazimio na mbinu za Shetani kwetu sisi. Andika ka-nuni ifuatayo kwenye ubao: Shetani anajaribu kutuangamiza na anatushawishi kwa kushusha taratibu viwango vyetu.

Alma 48Kapteni Moroni anawahamasisha Wanefi kujiandaa na kuwa waaminifuWaalike wanafunzi wasome Alma 48:7–10 kimya wakitafuta ni nini Moroni alikuwa anafa-nya wakati Amalikia alipokuwa anatafuta madaraka miongoni mwa Walamani.• Moroni alikuwa anafanya nini wakati Amalikia alipokuwa anatafuta madaraka miongoni

mwa Walamani?• Moroni alifanya nini kuimarisha watu wake na miji yao dhidi ya mashambulizi ya siku za

usoni? Ni sehemu gani maalumu ambazo Moroni alizitilia mkazo maalum?Wape wanafunzi muda wa kutafakari sehemu zenye mapungufu katika maisha yao na kile wangefanya kuimarisha sehemu hizo. Waulize waandike fikra zao• Kulingana na Alma 48:10, kwa nini Moroni alifanya kazi kwa nguvu nyingi kuimarisha

watu wake dhidi ya mashambulizi ya maadui wao? (Sisitiza kuwa Moroni alitaka kuwa-saidia Wanefi kuhifadhi uhuru wa kuabudu katika dini yao.)

• Ni baadhi ya mifano gani ya vitu ambavyo viongozi wa sasa wa Kanisa wanatufundisha kutusaidia kuimarisha sehemu zetu zenye mapungufu ya kiroho.

Page 391: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

376

SoMo la 101

• Kwa nini viongozi wa Kanisa wafanya kazi kwa nguvu kutuimarisha kiroho?Wahakikishie wanafunzi kwamba tunapofuata ushauri wa watumishi wa Bwana, tutaweza kuimarishwa dhidi ya majaribu.Wahimize wanafunzi kuangalia kwa makini milango iliyosalia ya Alma kwa kanuni zinazohusu thamani ya kuweka maagano na umuhimu wa kujiimarisha sisi wenyewe kumkinza Shetani.

Page 392: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

377

UtanguliziMaandalizi ya kujilinda ya Moroni yalikuwa ni mu-himu katika kuwalinda Wanefi dhidi ya maadui zao. Wanefi walifanikiwa katika kujilinda dhidi ya Wala-mani mpaka uasi na uovu kati ya watu wao ulipoanza

kuwadhoofisha. Moriantoni na watu wa mfalme walitafuta mgawanyiko na kuchochea mabishano kati ya watu. Moroni alijaribu kuondoa mgawanyiko na mabishano na kuleta amani.

SOMO LA 102

alma 49–51

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 49; 50:1–24Wanefi walijenga ngome, kustawi, na kuudumisha uhuru waoSoma tukio la kufikiria lifuatalo kwa darasa lako na uliza maswali yanayoambatana nalo (au unda la kwako tukio la kufikiria na seti ya maswali): Mvulana alikuwa anahisi amechoka lakini hakutaka kwenda kulala, kwa hiyo akaanza kupekua kwenye mtandao. Akajikuta anajaribiwa kutembelea tovuti zenye picha za ngono.• Ni maandalizi gani ambayo mvulana huyu angefanya ili kuepuka majaribu hayo?• Angeweza kufanya nini ili kuepuka majaribu wakati ujao?Waeleze wanafunzi kwamba wanaposoma Alma 49–51, wanaweza kutafuta jinsi maanda-lizi aliyofanya Kapteni Moroni dhidi ya Walamani yanaweza kufananishwa na maandalizi tutayofanya dhidi ya majaribu ya Shetani leo. Eleza kwamba wakati Amalikia alipokuwa anachochea jeshi la Walamani kwenda kwenye mapigano, Kapteni Moroni alikuwa anaimarisha miji ya Wanefi. Waalike wanafunzi wa-some Alma 49:1, 6–7 kimya. Waulize wao kufikiria jinsi maandalizi ya Kapteni Moroni ya kukinza Walamani yanaweza kufananishwa na haja yetu ya kujiandaa kwa mashumbulizi ya Shetani kwetu. Waulize wanafunzi wasome Alma 49:2–4; 50:1–6 kimya, wakitafuta jinsi Wanefi walivyojiandaa kwa mashambulizi ya Walamani ya siku za usoni.• Kama ungekuwa mwanajeshi wa Mlamani, ungejihisi vipi ulipoona ngome hizi kwa

mara ya kwanza?Waombe wanafunzi wachache wachukue zamu kusoma kwa sauti kutoka Alma 49:8–12. Uliza darasa lifuatilie likitafuta jinsi Walamani walijibu kwa maandalizi ya Wanefi.• Walamani walifanya nini walipoona kwamba Amoniha ilikuwa imejengewa ngome?

(Walirudi nyuma.)Waombe wanafunzi wasome kwa sauti kauli ifuatayo ya Rais James E. Faust wa Urais Wa Kwanza.“Shetani ni adui yetu mkubwa na anafanya kazi usiku na mchana kutuangamiza. Lakini hatuhitaji kupooza kwa kuogopa nguvu za Shetani. Hawezi kuwa na mamlaka juu yetu isipokuwa tukimruhusu. Yeye kwa hakika ni mwoga, na kama tukisimama imara atarejea nyuma ” (“Be Not Afraid,” Ensign, Oct. 2002, 4).Waalike wanafunzi wachache wachukue zamu kusoma na kwa sauti kutoka Alma 49:18–20, 23. Uliza darasa lifuatilie na kifikirie jinsi tunavyoweza kutumia matayarisho ya Wanefi kwa vita kama mfano wa kutusaidia kujiandaa vita vyetu vya kiroho dhidi ya Shetani. • Kapteni Moroni alifanya kazi kubwa kuwalinda Wanefi kutoka kwa Walamani. Jinsi gani

viongozi wetu wanafanya kazi kwa bidii na kutulinda dhidi ya adui? • Tutafanya nini kujenga kuta ndefu za kiroho dhidi ya majaribu ya shetani? (Majibu yana-

weza kujumuisha sala ya dhati ya kila siku, mafunzo ya maandiko kila siku, kuhudhuria kanisani kila mara, kuwahudumia wengine, na kufunga.)

Fikiria kuwaalika wanafunzi kujibu maswali yafuatayo kwenye daftari au shajara za kujifu-nza maandiko. (Unaweza ukitaka kuandika maswali haya ubaoni kabla ya darasa.)

Kutohoa matukio ya kufikiriaWewe uko katika nafasi nzuri ya kuelewa utamaduni na haiba za wanafunzi waliopo da-rasani mwako, pamoja na majaribu yanayowa-kabili. Chagua matukio ya kufikiria ambayo yataruhusu wanafunzi kutafakari juu ya hali zi-nazofanana na zao. Hii itawapa fursa ya kiroho kuwaweka tayari wana-funzi kulingana na ma-hitaji yao. Unapotafuta muongozo wa Baba wa Mbinguni, Yeye atakusa-idia kutohoa matukio ya kufikiria katika katibu cha kiada kwa karibu zaidi ifae katika maisha ya wanafunzi wako.

Page 393: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

378

SoMo la 102

• Ungeeleza vipi bidii zako za kila siku kuimarisha ulinzi wa kuta zako za kiroho? • Chagua kitu kimoja unachofanya kujiimarisha kiroho au kitu kimoja usichokichafanya.

Ungefanya nini ili kuongeza umahiri wa shughuli ile katika kujiimarisha wewe mwe-nyewe dhidi ya uovu?

Mwalike mwanafunzi asome Alma 49:28–30 kwa sauti. Uliza darasa kumtambua ni nani, licha ya Moroni, alikuwa akifanya kazi kwa bidii ili kuwalinda Wanefi dhidi ya Walamani. Sisitiza kwamba kwa kuwasidia Wanefi kubaki waadilifu, Helamani na ndugu zake wali-kuwa wakiwasaidia kupokea baraka na ulinzi kutoka kwa Bwana.Wape wanafunzi muda wa kujifunza Alma 50:10–12. Kisha waache wajadiliane hali za kufi-kiria zifuatazo na mwanafunzi mwenzake. (Kama inawezekana, tayarisha kitini chenye hali ya kufikiria mbele ya darasa. Kama hii haitowezekana, soma hali moja baada ya nyingine, ukiruhusu muda wa kutosha kwa ajili ya kujadili kila moja wapo.) 1. Moroni “alizingira ngome zote za Walamani” Ni kwa jinsi gani msichana “ataacha” hali

ya kusengenya anapokutana na rafiki zake wakati wa chakula cha mchana. 2. Moroni alijenga na kuimarisha mstari, au mpaka, kati ya Wanefi na Walamani. Ni kwa

jinsi gani mvulana na msichana wanaweza kuimarisha mstari kati ya kuweka amri ya usafi wa kimwili na kuvuka na kwenda kwenye kuto kufa?.

3. Jeshi la Moroni lilijenga ngome ili kulinda watu wake dhidi ya maadui zao. Mvulana anakuja kubaini kwamba amekuwa akitumia muda mwingi kwenye vyombo vya habari vya kijamii (mtandaoni au kwa kutuma ujumbe fupi). Tabia hii inaonyesha kupunguza kuhusika kwake na familia yake ya karibu, na yeye hupuuza majukumu yake ya nyu-mbani. Tunaweza kufanya nini ili kuimarisha na kulinda uhusiano wake na familia yake?

Waalike wanafunzi wachache kufanya muhtasari kile walichojifunza kutoka kwenye matendo ya Kapteni Moroni kuhusu jinsi tunavyoweza kujilinda dhidi ya mashambulizi ya adui. Haki-kisha kuwa wanafunzi wanaelewa kwamba kama tutajiandaa, tunaweza kukinza masha-mbulizi (majaribu) kutoka kwa adui. Unaweza ukapenda kuandika kanuni hii ubaoni.Mwalike mwanafunzi asome Alma 50:1 kwa sauti. Uliza darasa:• Kutokana na mafanikio ya maandalizi ya Kapteni Moroni, ni kitu gani cha ziada tuna-

weza kujifunza kwenye aya hii? (Moroni “hakusitisha” kufanya maandalizi; aliendelea na kuimarisha ulinzi wake, hata wakati ilikuwa inaonekana kama hamna tishio lililo wazi.)

Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa haja ya kuimarisha kiroho kunakoendelea, soma kauli ifuatayo ya Rais Henry B. Eyring wa Urais wa Kwanza:

“Nguvu zinazotuzunguka zinapoendelea katika ukali, nguvu zozote za kiroho ambazo zilikuwa zinatosha wakati fulani sasa hazitoshi. Na ukuaji wowote katika nguvu za kiroho wakati mmoja tulifikiria zinatosha, ukuaji mkuu utaweza kupatikana kwetu. Yote haja ya nguvu za kiroho na nafasi za kuipata zitaongezeka katika kasi ambayo sisi tunapuuza kwa kujihatarisha wenyewe” (“Always,” Ensign, Oct. 1999, 9).

Andika maswali yafuatayo kwenye ubao:Nitajitayarisha kukinza majaribu kwa . . .Nitasimama imara ninapo . . .

Waalike wanafunzi wakamilishe kauli hizi katika daftari au shajara za kujifundisha maandiko. Baada ya wanafunzi kumaliza kuandika, soma kuali ifuatayo ya Rais Ezra Taft Benson. (unaweza kutaka kupendekeza kwamba wanafunzi waandike kauli hii katika maandiko yao karibu na Alma 50:10–12.)“Ni vyema kujitayarisha na kukinga kuliko kurekebisha na kutubu” (The Teachings of Ezra Taft Benson [1988], 285).• Kwa unafikiria kauli hii ni kweli? Ni lini umewahi kuona mfano wa kanuni inayofunzwa

na kauli hii?Elezea kwamba maandalizi ya Wanefi yalisababisha miaka michache ya ufanisi mkuu na imani. Sisitiza kwamba wakati Amalikia alimtukana Mungu kwa sababu yeye alishindwa, Wanefi “walimshukuru Bwana Mungu wao” (Alma 49:28).Waalike wanafunzi wafikirie wana rafiki ambaye huishi katika eneo ambalo vita vimeki-thiri. Yeye huhisi kwamba haiwezekani kupata amani na furaha kwa sababu ya vurugu inayomzunguka. Andika marejeo ya maandiko yafuatayo ubaoni: Alma 50:18–23. Waalike

Page 394: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

379

alMa 49 – 51

wanafuzi wasome kifungu hiki na kutengeneza majibu wanayoweza kumfanyia rafiki yao. Waulize wanafunzi wachache kushiriki kile wangesema. Ukweli mmoja wanaoweza kujumuisha katika majibu yao ni kwamba uaminifu kwa Mungu huleta furaha, hata katikati ya vurugu. (Unaweza kutaka kuandika kanuni hii ubaoni.) Wasaidie wanafu-nzi kuelewa kwamba ukweli huu unatumika si tu kwa vita bali pia kwa changamoto za kibinafsi kama vile mdororo wa kifedha, kupoteza ajira, kifo cha mpendwa, mahusiano ya wanafamilia yaliyozongwa, na mikasa ya asili.• Kulingana na Alma 50:18–23, ni kwa nini Wanefi wapata kipindi cha furaha?• Ni wakati gani wewe umehisi Bwana ametoa uwezo na baraka Zake kwako kwa kuwa

mtiifu na kwa kujiimarisha mwenyewe dhidi ya majaribu?• Ni lini Bwana amekubariki wewe au mtu unayemjua kwa ufanisi, amani, na furaha

katika nyakati ngumu? (Baada ya wanafunzi kujibu, fikiria kushiriki mfano kutoka kwa maisha yako.)

Alma 50:25–40; 51Ulinzi wa Wanefi ulidhoofika na Moroni alikabiliana na uasi miongoni mwa watu wake(Tazama: Kwa kuwa urefu wa somo hili kufikia hapa, unaweza kuhitaji kufanya muhtasari mfupi wa nyenzo iliyobakia. Kama ukifanya hivyo, elezea kwamba Alma 50:25–40 ina taa-rifa za uasi wa Moriantoni na kifo na kuteuliwa kwa Parihani kama mwamuzi mkuu. Alma 51 Inasimulia kuhusu kikundi kilichoitwa watu wa- mfalme ambao walibadilisha sheria ili kumruhusu mfalme atawale juu ya Wanefi. Majaribio yao yaliangukia patupu. Katika ghadhabu yao juu ya kushindwa, watu wa- mfalme walikataa kujiami wakati Amalikia na Walamani walikuja kupigana dhidi ya Wanefi. Kilingana na sheria, Moroni aliwahitaji wa-jiami au waadhibiwe. Jeshi la Amalikia liliteka miji mingi ya Wanefi na kuwachinja Wanefi wengi. Amalikia alipokuwa anajaribu kuteka nchi ya Utele, yeye alikutana na Teankumu na jeshi lake. Teankumu alimchinja Amalikia na kuzuia kusonga kwa jeshi la Walamani.)Andika kauli ifuatayo ubaoni: Pamoja twasimama; tukigawanyika twaanguka.Waalike wanafunzi wasome Alma 50:25–26 kimya, wakitafuta neno katika kila kifungu ambalo linaelezea sababu za mgawanyiko miongoni mwa Wanefi.• Ni nini kilichosababisha mgawanyiko miongoni mwa watu?Fanya muhtasari wa salio la Alma 50 kwa kuelezea kwamba Moriantoni na watu wake wa-lijaribu kuwaacha Wanefi na kutorokea katika nchi ya kaskazini. Moroni alihofia kwamba mgawanyiko huu ungeleta kupotea kwa haki za Wanefi. Yeye alituma jeshi, lililoongozwa na mtu aliyejulikana kama Teankumu, ili kuwazuia watu Moriantoni wasiondoke. Jeshi la Teankumu liliwazuia watu wa Moriantoni wasifikie mwisho wa safari yao, na Moriantoni aliuawa. Masalio ya watu wake “walifanya agano kudumisha amani” (Alma 50:36). Punde baada ya uasi wa Moriantoni, mgawanyiko hatari wa kisiasa ulianza miongoni mwa watu wa Nefi. Baadhi ya Wanefi walitaka kumuondoa Pahorani kutoka kwenye kiti cha hukumu na kumbadilisha yeye na mfalme. Watu wengine walikuwa wanataka kubakia na mfumo wa serikali ya waamuzi.Alika wanafunzi kupekua Alma 51:5–6 kwa majina ya makundi haya mawili yanayopi-ngana ( watu wa - mfalme na watu huru.) Wape wanafunzi muda wa kutambua katika Alma 51:8 azimio la watu wa- mfalmeAndika ukweli ufuatao ubaoni: mgawanyiko na mabishano yanaharibu amani yetu. • Ni kwa jinsi gani kanuni hii imeoonyeshwa katika masimulizi ya mgawanyiko na mabi-

shano yaliyonakiliwa katika Alma 50 na 51?• Ungefanya nini katika familia yako, miongoni mwa rafiki zako, au katika jumuiya yako

kusuluhisha mabishano? • Ni lini uliona baraka zitokanazo na familia iliyoimarishwa na umoja wa familia au jamii

au darasa?Shuhudia kweli hizo ambazo unahisi zimekuvutia kuzisisitiza. Wakumbushe wanafunzi kwamba masomo machache yafuatayo yatawapa fursa zaidi ya kutambua kanuni na kuji-funza masomo kutokana na vita kati ya Wanefi na Walamani.

Page 395: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

380

UtanguliziKufikia hapa katika vita na Walamani, Wanefi wali-kuwa wamepoteza miji mingi kwa sababu ya mabi-shano miongoni mwao. Moroni, Teankumu, na Lehi waliteka mji wa Muleki na kulishinda mojawapo ya je-shi kubwa la Walamani. Moroni alikataa ombi la Amo-roni, kiongozi wa Walamani, kubadilishana wafungwa na kutekeleza mpango wa kuwaachilia wafungwa wa Wanefi bila ya kumwaga damu. Moroni alisimama

imara na hakutaka mafikiano na uovu wa Amoroni na wafuasi wake.

Tazama: Somo hili linalenga kwenye matukio katika maisha ya Moroni, Teankumu, na Lehi. Katika somo lifuatalo, wanafunzi watajifunza zaidi kuhusu askari vijana 2,000 wa Helamani waliotajwa katika Alma 53:16–23.

SOMO LA 103

alma 52–55

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 52–53Moroni, Teankumu, na Lehi walifanya kazi kwa pamoja kuwashinda WalamaniKabla ya darasa, andika kauli ifuatayo kwenye ubao:

“Vijana wa leo wanalelewa kwenye himaya ya adui” (Rais Boyd K. Packer)Mwanzoni mwa darasa, mwalike mwanafunzi asome kauli hii. Kisha uulize:• Nani ndiyo adui? (Shetani.)• Ni ushahidi gani wa vitendo vya Shetani unavyoviona kwenye dunia inayokuzunguka?

(Wanafunzi wanaweza kutaja lugha isiyofaa na mavazi, kukosa uaminifu , utovu wa maadili na majaribu ambavyo kila mara hukuzwa kwa kutumia teknolojia na vyombo vya habari.)

Wahimize wanafunzi kufikiri njia ambazo wanaweza kufananisha changamoto wazokabi-liana nazo kwa matukio na hali zinazoelezwa katika Alma 52–55. Kisha soma endelezo la Kauli ya Rais Packer: “Vijana wa leo wanalelewa kwenye himaya ya adui kwa viwango vya maadili vilivyoshuka. Lakini kama mtumishi wa Bwana, ninaahidi kwamba mtalindwa na kukingwa kutoka ma-shambulizi ya adui kama mtafuata uvuvio unaokuja kutoka kwa Roho Mtakatifu. (“Counsel to Youth,” Ensign or Liahona, Nov. 2011, 18).Wahimize wanafunzi kutafuta mwongozo wa Roho Mtakatifu ili kwamba waweze kuzuia uovu. Wakumbushe wanafunzi kwamba wakati Moroni alipokuwa anauzima uasi wa watu wa mfalme, Walamani waliteka miji mingi iliyojengewa ngome ya Wanefi (ona Alma 51:26). Waalike wanafunzi wasome Alma 52:14 kimya, wakitafuta maelezo ya Mormon kuhusu hali ya Wanefi wakati huu. Kisha muulize mwanafunzi asome Alma 53:9 kwa sauti. Uliza darasa litambue kwa nini hali ya Wanefi ilikuwa ni ya hatari.• Ni zipi baadhi ya njia watu hujiweka wenyewe katika hali ambazo ni hatari kiroho?Andika rejeo la maandiko lifuatalo kwenye ubao: Alma 52:5–10, 16–19. Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa muktadha na umbo la hadithi unaohusisha aya hizi, waambie wanafu-nzi wawili wasome muhtasari wa milango katika Alma 52 na 53 kwa sauti. Kisha waalike wanafunzi wajifunze aya ulizoziandika kwenye ubao, wakitafuta kanuni zinazoweza kuwa-saidia kuepuka au kuzuia uovu. Baada ya muda wa kutosha, uliza:• Ni kanuni gani tunazoweza kujifunza kutoka kwenye hizi aya? (Kati ya baadhi ya ka-

nuni, wanafunzi wataweza kugundua ukweli ufuatao: kama tutaepuka ngome za adui, tunaweza zaidi kuepuka na kuzuia majaribu.)

Waalike wanafunzi wafikirie mahali halisi, mazingira ya kijamii, au hali zinazohusisha matumizi ya teknolojia (kama mtandao) ambayo wanahisi kuwa inaweza kuleta athari kwenye maisha yao.

Wasaidie wanafunzi kutambua kanuni zilizodokezwaKanuni nyingi huwa hazitamkwi moja kwa moja na wale walioa-ndika maandiko. Badala yake, kanuni inaweza kufichwa kwenye umbo la hadithi au kwenye tu-kio maalumu au methali. Inaweza ikadhihirishwa na kitabu kizima cha maandiko, mlango au aya moja. Kanuni zilizo-ashiriwa zinaweza mara nyingi kugundulika kwa kuchanganua matendo na misimamo ya watu au makundi kwenye maandiko na kisha kutambua matokeo ya matendo hayo na misi-mamo hiyo.

Page 396: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

381

alMa 52– 55

Elezea kwamba Mormoni alieleza kuhusu msimamo wa Teankumu dhidi ya Walamani kwa kutumia maneno kama kulinda, kuimarisha, kuthibiti, kusababisha mateso, na kuimarisha. Waulize wanafunzi watafakari nini kinahitajika kusuguliwa au kuondolewa, kutoka kwenye maisha yao kuwasaidia wawe salama zaidi kiroho. Mwalike mwanafunzi asome Alma 52:19–30 kwa sauti. Uliza darasa:• Viongozi wa Wanefi walifanya nini kabla ya kwenda kwenye mapigano? (Walikutana

katika baraza la vita.)• Ni kwa njia zipi baraza la familia au baraza la kanisa linaweza kufanana na “baraza la

vita”? Mabaraza kama haya yanatuimairisha vipi kwenye mapigano dhidi ya adui?Fanya muhtasari Alma 52:20–40 na Alma 53 kwa kuelezea kuwa baada ya baraza la vita, Kapteni Moroni na jeshi lake waliuteka tena mji wa Muleki kwa kuwatoa Walamani kutoka kwenye ngome zao. Wanefi walichukua mateka wengi wa Walamani na kuwapeleka kufa-nya kazi ya kuimarisha mji wa Utele. Hata hivyo, Walamani waliendelea kupata mafanikio kwenye mikoa mingine kwa sababu ya mabishano ya hasira kati ya Wanefi.

Alma 54–55Moroni akataa masharti ya Amoroni ya kubadilishana wafungwa na akatumia busara kuwatoa wafungwa wa WanefiElezea kwamba Alma 54 ni kumbukumbu ya barua zilizotumwa kati ya Amoroni (mfalme wa Walamani) na Kapteni Moroni. Kabla ya hili, Walamani na Wanefi walikuwa wamechu-kua wafungwa wa vita wengi. Sura hii imeandikwa kumbukumbu ya majibu ya Moroni kwenye ombi la Amoroni kwamba Walamani na Wanefi wabadilishane wafungwa.Elezea kwamba Alma 54:9–12 ina maneno ya Kapteni Moroni kwa Amoroni. Mwalike mwanafunzi asome hizi aya kwa sauti. Kisha mwambie mwanafunzi mwingine asome majibu ya Amoroni kwa Kapteni Moroni katika Alma 54:18–20.• Maazimio ya Kapteni Moroni ya kubadilishana wafungwa yalitofautiana vipi na yale ya

Amoroni? (Unaweza ukitaka kusisitiza kwamba Moroni alionea huruma familia, huku Amoroni aliwajali watu wake wa vita tu kwa sababu alitaka kuwaangamiza Wanefi.)

• Ni kwa jinsi gani kauli za Amoroni kwenye Alma 54:18–20 zinaonyesha maazimio ya shetani katika vita vyake dhidi yetu?

Mwalike mwanafunzi asome Alma 55:1–2 kwa sauti. Alika darasa litafute majibu ya Moroni kwa matakwa ya Amoroni.• Kwa nini Moroni hakuwa tayari kufanya kile Amoroni alisema? (Alijua Amoroni alikuwa

anadangaya, na hakutaka kumpa Amoroni nguvu zaidi ya alizokuwa nazo tayari.)• Tunajifunza nini kutoka kwa majibu ya Moroni kwa Amoroni? (Japokuwa wanafunzi

wanaweza kusema idadi fulani ya kweli, uwe na uhakika wanaelewa kwamba Tunapo-simama imara kwa kile kilicho cha haki, tunaweza kuzuia athari za uovu kupata nguvu juu yetu.)

Kauli zifuatavyo za Joseph Smith zinaweza kusaidia kwenye majadiliano ya aya hizi.“Shetani hawezi kututongoza kwa vishawishi vyake isipokuwa mioyo yetu imekubali na kujitoa” (Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith [2007], 213).“Shetani hana nguvu juu yetu ni pale tu tunapomruhusu” (Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith, 214)Andika marejeo ya maandiko yafuatao kwenye ubao: Alma 55:15–24, 28–31.Elezea kwamba katika Alma 55 tunajifunza kuwa Kapteni Moroni waliwaachia huru wafu-ngwa katika mji wa Gidi kwa tabasuri (ni njia inayotumika vitani kumadanganya au kumshi-nda adui.) Katika Alma 55:3–14, tunajifunza kwamba Moroni aliweza kumtumia mwanajeshi Mnefi aliyeitwa Lamani kusababisha wanajeshi Walamani waliokuwa wanawalinda wafu-ngwa Wanefi kulewa. Waalike wanafunzi wasome kimya aya ulizoziandika kwenye ubao, wakitafuta kile Kapteni Moroni alifanya mara moja alipolisababisha Walamani kuzungukwa katika mji wa Gidi. Wakumbushe wanafunzi kuangalia kanuni wanapojifunza. Baada ya muda wa kutosha, waulize watoe taarifa ya kile walichogundua. Unaweza pia kuuliza:• Aya hizi zinakufundisha nini kuhusu Moroni?Andika kauli ifuatayo kwenye ubao na waalike wanafunzi kujaza mapengo:

Page 397: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

382

SoMo la 103

Hatupaswi kufurahi katika . . . ; bali,tunapaswa kufurahi katika . . .• Jinsi gani tunaweza kutumia mfano wa Moroni wa kutofurahia umwagaji damu? Kwa

mfano, tunaweza kutumia vipi mfano wa Moroni kwenye vitu tunavyosoma na kuona au kwa michezo tunayocheza?

Waalike wanafunzi kufikiria maswali yafuatayo:• Unahisi Mormoni alitaka ujifunze nini kwenye somo la leo litakalokusaidia kuwa

mwaminifu unapopigana dhidi ya adui?Fikiria kuwapa wanafunzi muda wa kuandika kwenye daftari au shajara za kujifunza maandiko kuhusu nini watafanya kuzuia kuingia kwenye himaya ya Shetani na kusimama imara dhidi ya mashambulizi yake. Hitimisha kwa kushuhudia ukweli uliyoujadili leo darasani.

Wazo la Kufundusha la ZiadaAlma 53:20–21. Kutembea wima mbele ya Mungu

Mwalike mwanafunzi asome Alma 53:20–21 kwa sauti.

• Ina maana gani kutembea wima mbele ya Mungu?

Waulize wanafunzi kutafakari jinsi wao, kama wale askari vijana, wanaweza kuwa wakweli wakati wote katika kitu chochote ambacho wamekabidhiwa. Soma kauli ifuatayo, ambayo Rais George Albert Smith alishiriki ushauri wa busara aliopewa na babu yake George A. Smith:

"Babu yangu alikuwa akisema kwa familia yake, ‘Kuna mstari wa mpaka ulio ainishwa vizuri kati ya himaya ya Bwana na himaya ya Ibilisi. Kama utakaa kwenye upa-nde wa mstari wa Bwana utakuwa chini ya himaya yake na hautokuwa na haja ya kufanya maovu; lakini ukiruka kwenye upande wa mstari wa Ibilisi inchi moja utakuwa chini ya nguvu za mshawishi na kama akifanikiwa, hau-takuwa na uwezo wa kufikiri au hautawaza sawasawa kwa sababu utakuwa umepomteza Roho wa Bwana.

“Wakati mwingine ninapokuwa nimejaribiwa kufa-nya kitu fulani, nilijiuliza, ‘ni upande gani wa mstari

nimeegemea?’ Kama niliamua kuwa kwenye upande salama, Upande wa Bwana, nitafanya kitu kizuri kila wakati. Hivyo wakati majaribu yanapokuja fikiria kwa maombi kuhusu matatizo yako na ushawishi wa Bwana utakusaidia kuamua kwa busara. Kuna usalama kwetu tu kwenye upande wa mstari wa Bwana” (“A Faith Fou-nded upon Truth,” Deseret News, June 17, 1944, Church Kipengele, 9).

Fikiria kuchora mstari wa wima chini katikati ya ubao. Andika upande mmoja wa ubao Himaya ya Bwana na upande mwingine wa ubao Himaya ya Ibilisi. Waulize wanafunzi

• Kuhusiana na mstari unaogawanya himaya hizi mbili, ni wapi ni salama zaidi kuwepo? (Kwenye upande wa Bwana mbali na mstari huo kama inavyowezeka.)

• Ni hatari gani itakuwepo utapojaribu kuishi kwe-nye upande wa Bwana lakini karibu na mstari inavyowezekana?

• Nini kinakusaidia kukaa mbali sana na mstari?

Page 398: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

383

UtanguliziHelamani na Kapteni Moroni walipigana na Walamani katika sehemu mbalimbali za nchi. Helamani alituma barua kwa Moroni akieleza a mapigano ya jeshi lake na Walamani na kueleza kujiamini kwake katika imani

ya askari vijana 2060 waliojiunga na jeshi lake. Hela-mani pia alielezea jinsi jeshi lake lilifanya ili kushinda mapigano na kupata matumaini na nguvu wakati wa majonzi.

SOMO LA 104

alma 56–58

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 56Majeshi ya Antipa na Helamani ndiyo washindi dhidi ya jeshi lenye nguvu la Walamani Waulize wanafunzi kama walishawahi kupata barua au ujumbe ambao uliwaimarisha kuvumilia tatizo fulani. Elezea kwamba Alma 56–58 ina waraka wenye ujumbe au barua, ambayo Helamani aliandika kwa Kapteni Moroni wakati wa kipindi kigumu cha vita. Waulize wanafunzi wasome Alma 59:1–2 kimya ili kugundua jinsi Kapteni Moroni alivyo-jibu barua hiyo. Wahimize wanafunzi wanaposoma barua kutambua sababu ya kwa nini Kapteni Moroni alifurahia licha ya wakati mgumu aliokuwa nao. Fanya muhtasari Alma 56:2–17 kwa kuelezea kwamba Helamani aliamrisha jeshi dogo lililojumuisha wana 2000 wa Anti- Nefi- Lehi, au watu wa Amoni. Hawa wanajeshi mara kwa mara wanajulikana kama askari 2000 vijana wapiganaji. (Unaweza kuhitaji kuelezea kuwa neno mvulana linamaanisha kijana.) Wazazi wa hawa mvulana walikuwa wameweka agano kamwe wasijiami tena. Wavulana, ambao hawakufungwa na agano hilo, walijitolea kuwali-nda wazazi wao na Wanefi wengine walipokuwa wanatishwa na jeshi la Walamani.Elezea kuwa Helamani aliwaongoza vijana wapiganaji 2000 kwenda kwenye mji wa Yudea kuwasidia jeshi la Wanefi likiongozwa na Antipo. Walamani walikuwa wameteka miji ka-dha ya Wanefi na kupunguza kwa kiasi kikubwa jeshi la Antipo. Antipo alishangilia wakati Helamani na wanajeshi wake walipofika kumsaidia.Waalike wanafunzi wasome Alma 53:17–21 kimya wakitafuta maneno na vishazi ambavyo vinaeleza uwezo wa kiroho ambao hawa wavulana waliouleta kwenye jeshi. Wanaposoma, nakili mchoro ufuatao kwenye ubao. Waalike wanafunzi wachache waje ubaoni na waa-ndike maneno na vishazi walivyovipata chini ya kichwa cha habari “Kabla ya mapigano”

• Unafikiri Helamani alitaka kumaanisha nini wakati alipoelezea vijana wapiganaji 2000 kama wanaume wa ukweli na makini? (Unaweza kutaka kuelezea kuwa neno umakini ni sawa na ukweli, utulivu na kujidhibiti.)

• Ni kwa jinsi gani tabia zilizoorodheshwa kwenye ubao zitatusaidia kukabiliana na mapi-gano ya kiroho na changamoto zingine?

Kwa ufupi fanya muhtasari wa mwanzo wa mapigano ya kwanza ya vijana wapiganaji katika Alma 56:29–43. Antipo aliwatumia Helamani na wapiganaji wake 2000 kama mtego wa kuliondoa jeshi lenye nguvu nyingi la Walamani katika mji wa Antipara. Wengi wa jeshi la Walamani waliondoka Antipara kufuata jeshi la Helamani, na kulipa jeshi la Antipo fursa ya kuwafuta kwa nyuma na kuwashambulia. Wakati jeshi la Antipo lilipofikia jeshi la Walamani, waliwashambulia kulingana na mpango wao. Wakati jeshi la Walamani liliposi-mamisha harakati zao kulifuata jeshi la Helamani,Helamani hakuweza kujua kama jeshi la Walamani lilikuwa linajaribu kuwadanganya askari wake waingie kwenye mtego au kama

Kabla ya mapigano Wakati wa mapigano

askari vijana/ vijana Watakatifu wa Siku za Mwisho

Page 399: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

384

SoMo la 104

jeshi la Antipo limeanza mapigano na Walamani kutoka nyuma. Helamani na askari wake vijana ilibidi waamue kuendelea kukimbia au kushambulia Walamani.Waalike wanafunzi wasome Alma 56:44–48 kimya. Waulize watafute maneno na vishazi ambavyo vinaonyesha ushahidi wa jinsi hawa wavulana walipigana kwa imani. Waalike wana-funzi wachache kuandika kile walichokipata ubaoni chini ya kichwa cha habari “Kabla ya vita”• Kitu gani hawa wavulana hawakuwa na shaka nacho? (Kuwa Mungu atawaokoa.)• Kwa nini hawakuwa na shaka kwamba Mungu atawaokoa?• Ni kwa jinsi gani sifa walizokuwa nazo kabla ya mapigano ziliwasaidia wakati wa mapigano?Andika ukweli ufuatao kwenye ubao: Tunapotenda kwa imani, tunaweza kupata uwezo kutoka kwa Mungu. Waaulize wanafunzi watafute ushahidi wa ukweli huu wanapojifunza Alma 56.Fanya muhtsasari wa Alma 56:49–53 kwa kuelezea kwamba jeshi la Helamani lilikuta jeshi la Antipo katika hali ngumu. Antipo na viongozi wengi wa jeshi walikuwa wamekufa na Wanefi waliochoka na kuchanganyikiwa walikuwa wanakaribia kushindwa.Mualike mwanafunzi asome Alma 56:54–56 kwa sauti. Uliza darasa lifuatilie, likitafuta jinsi Mungu alivyowabariki wapiganaji wa Helamani kwa sababu ya imani yao. • Unafikiri sifa za kiroho zilizoorodheshwa kwenye ubao zilichangia vipi matukio yaliyoa-

ndikwa katika Alma 56:56?• Ni lini wewe au mtu unayemjua alifanya kitu kwa imani na kupokea nguvu za Mungu

katika hali ngumu?

Alma 57Helamani na askari wake vijana wapiganaji wauteka tena mji wa Kumeni na wanalindwa katika mapiganoElezea kwamba Alma 57 ni muendelezo wa barua ya Helamani kwa Kapteni Moroni. Ina-anza na simulizi ya Wanefi wakichukua tena miji yao miwili kutoka kwa Walamani. Wakati wa kipindi hiki, Helamani alipokea watu 6000 kuimarisha jeshi lake, pamoja na wana 60 zaidi wa watu wa Amoni. Walamani pia walipata askari wa kuongeza nguvu na kuendelea kuimarisha miji waliyoiteka.Sisitiza kwamba katika pigano moja, Walamani walikuwa karibu wawazidi nguvu Wanefi (ona Alma 57:18). Waaulize wanafunzi wasome Alma 57:18) kimya, wakitafuta sababu za Wanefi kuweza kushinda.• Kwa nini Wanefi waliweza kushinda dhidi ya Walamani?• Helamani alisema askari wake walitii na kuwa waangalifu kufanya kila neno la amri kwa

uhakika (Alma 57:21). Unafikiri hii inamaanisha nini? Ni kwa jinsi gani utiifu huu ni dhihirisho la imani yao?

Ili kuwaongezea wanafunzi majibu kwa maswali haya, soma maelezo yafuatayo ya Mzee Russell M.Nelson wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili:

"[Wewe] utakutana na watu ambao wanachagua amri zipi watazitii na kupuuza zingine ambazo wanachagua kuzivunja. Nauita huu ni mfumo wa utiifu wa mkahawa. Haya mazoea ya kuchukua na kuchagua hayawezi kufanya kazi. Itasababisha huzuni. Ili Kujiandaa kukutana na Mungu, mtu anaweka amri Zake zote. Inahitaji imani ili kuzitii, na kuweka amri Zake kutaimarisha imani ile” (“Face the Future with Faith,” Ensign or Liahona, Mei 2011, 34).

Maulize mwanafunzi wasome Alma 57:23–27 kwa sauti. Uliza darasa litafute ni kwa muda gani Bwana aliwahifadhi askari vijana na kwa nini aliwahifadhi. Ili Kuwasaidia kujadiliana nini wanapata, uliza maswali haya yafuatayo:• Kuhusu askari wake Helamani alisema “Wana akili imara” Ufikiri hii ina maana gani ?

Kwa nini tunahitaji kuweka akili zetu imara tunapokutana na changamoto?• Askari wa Helamani walionyesha vipi kuwa “daima waliweka imani yao kwa Mungu”?Inaweza kusaidia kueleza kwamba katika baadhi ya mifano, wenye haki watateseka au kufa, kama ilivyokuwa kwa askari vijana waliteseka na kama baadhi katika jeshi la wanefi waliuawa. Hata hivyo, Mungu siku zote atawaheshimu wale wanaomheshimu, na wenye haki wanaokufa watabarikiwa.

Page 400: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

385

alMa 56 – 58

• Ni mifanano gani unayoiona kati ya mapigano ya vijana wapiganaji na maadui zao na mapigano yetu na adui?

Mwalike mwanafunzi asome taarifa ifuatayo ya Mzee M. Russell Ballard wa Akidi ya Mi-tume Kumi na Wawili:“Hivi leo tunapigana mapigano ambayo kwa njia nyingi ni ya hatari zaidi. . . kuliko mapigano kati ya Wanefi na Walamani. Adui yetu ni mjanja na mwenye nyenzo. Tunapigana dhidi ya Lusiferi, baba wa uwongo wote, adui wa yale yote ambayo ni mema na, ya haki na takatifu. . . .“. . . Tunapigana kwa ajili ya roho za watu. Adui hana msamaha wala hasiti. Anawachukuwa wafungwa wa milele kwa kiwango cha kutisha. Na haonyeshi ishara yoyote ya kuachilia."Wakati tukiwa tunashukuru kwa dhati washiriki wengi wa kanisa ambao wanafanya mambo makubwa kwenye mapigano ya ukweli na haki, lazima niwaambieni kwa kweli kuwa bado haitoshi. Tunahitaji msaada zaidi. Tunakuhitaji wewe. Kama vijana wapiganaji 2000 wa Helamani, wewe pia unaweza kupewa nguvu za kujenga na kutetea ufalme wake. Tunakuhitaji uweke maagano matakatifu, kama walivyofanya. Tunakuhitaji uwe mwanga-lifu mtiifu na mwaminifu, kama walivyokuwa" (The Greatest Generation of Missionaries, Ensign or Liahona, Nov. 2002, 46–47).Andika yafuatayo kwenye ubao kama tukimwamini Bwana na kumtii Yeye kwa ukamilifu, ... • Kwa misingi ya ulichosoma kuhusu wapiganaji wa Helamani, utakamilisha vipi sentensi

hii? (Kamilisha sentensi kwenye ubao kulingana na mapendekezo ya wanafunzi. Kwa mfano unaweza kuandika ukweli ufuatao: kama tunamwamini Bwana na kumtii kwa ukamilifu, atatusaidia kwenye mapigano yetu.)

Waulize wanafunzi wajikumbushe wakati wao au mtu wanayemfahamu alitii kwa ukami-lifu katika hali ngumu shuleni, nyumbani au katika mazingira ya kijamii. Waalike wanafu-nzi wachache kushiriki uzoefu wao. Waulize jinsi Bwana alivyowasidia kwenye hiyo hali.Wape muda wanafunzi kuandika kwenye daftari au shajara ya kujifundisha maandiko kuhusu kile watakachofanya ili kutii amri za Mungu “kwa ukamilifu” (Alma 57:21) “na kuweka imani yao kwa Mungu daima” (Alma 57:27).

Alma 58Wanajeshi Wanefi waliamini kuwa Mungu angewalinda katika matatizo yaoElezea kwamba Alma 58 inajumuisha mwisho wa waraka wa Helamani kwa Moroni. Hela-mani alielezea jinsi jeshi la Wanefi lilivyopata wakati mgumu uliozidisha kufanya hali wali-zokabiliana nazo kuwa mbaya zaidi. Waalike wanafunzi wachache wachukue zamu kusoma kwa sauti kutoka Alma 58:2, 6–9, na uliza darasa kutambua hizo hali za ugumu (ukosefu wa chakula, ukosefu wa nguvu za ziada, woga kwamba wataangamizwa na adui zao).Waulize wanafuzi wasome Alma 58:10–12 kimya, wakitafuta majibu kwa maswali yafu-atayo. (Andika maswali kwenye ubao kabla ya darasa. Soma maswali kwa darasa kabla ya wao kusoma kifungu cha maandiko, na kisha yatathmini baada ya wao kuyasoma. Hii itawasaidia wanafunzi kuzingatia jinsi jeshi la Helamani lilivyojibu katika hali hii ngumu.)

Wanefi walifanya nini walipokabiliana na hali hii ngumu?Bwana alijibu vipi kusihi na maombi yao ya dhati?Jinsi gani mahakikisho ambayo Bwana aliwapa yaliwasaidia Helamani na jeshi lake?

Waalike wanafunzi kuandika kwa ufupi ukweli waliojifunzi kutoka Alma 58:10–12. (Wa-nafunzi wanaweza kutumia maneno tofauti, lakini hakikisha kuwa wanatambua kanuni ifuatayo: Ikiwa tutamgeukia Mungu katika wakati mgumu, tutaweza kupata hakiki-sho la kiungu ambalo linaweza kuimarisha imani yetu na kutupa matumaini.)• Ni lini Bwana amekubariki na amani na hakikisho wakati wa hali ngumu?Elezea kwamba sehemu ya mwisho ya Alma 58 inaelezea kufanikiwa kwa jeshi la Wanefi kuchukua tena miji ambayo ilikuwa imetekwa na Walamani (Ona Alma 58:31). Mwalike mwanafunzi wasome Alma 58:39–40 kwa sauti.• Wapiganaji vijana wa Helamani walionyesha vipi imani yao kwa Mungu, licha ya

“majeraha mengi ” waliyopata?• Unapokabiliana na changamoto maishani, unaweza kupata faida gani kutoka kwa

mfano ufuatao wa wana wa Helamani?Hitimisha kwa kushiriki ushuhuda wako wa kanuni zilizofundishwa katika somo hili.

Page 401: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

386

UtanguliziKapteni Moroni alifurahia mafanikio ya Helamani katika kufanikiwa kurudisha baadhi ya miji ya Wanefi ambayo ilikuwa imepotezwa kwa Walamani. Hata hivyo, wakati alipotaarifiwa kwamba mji wa Nefiha uli-kuwa umetekwa na Walamani alikasirikia kwa serikali kwa kuzembea kutuma nguvu za ziada. Kwenye barua kwa Pahorani, mwamuzi mkuu, alilalamika mateso ya waadilifu na kumkemea Pahorani kwa kutojali mcha-kato wa uhuru. Bila kujulikana na Moroni, Pahorani

alitoroka kwenye nchi ya Gidioni kwa sababu ya uasi wa Wanefi waliotaka kuchukua ufalme. Pahorani hakuchukizwa kwa kurudiwa na Moroni; bali alifurahia mapenzi ya Moroni katika uhuru. Bwana aliwaimarisha Wanefi, na kwa pamoja, Moroni, Pahorani na watu wao waliwashinda watu wa - mfalme na Walamani. Baada ya miaka kadhaa ya vita, Wanefi tena walipata amani na Helamani alianzisha upya Kanisa.

SOMO LA 105

alma 59–63

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 59Wanefi wanapoteza ngome, na Kapteni Moroni anahuzunika kwa sababu ya uovu wa watuKabla ya darasa, andika ubaoni kauli ifuatayo ya Rais Ezra Taft Benson kutoka kwenye The Teachings of Ezra Taft Benson [1988], 285): “Ni vyema kujitayarisha na kukinga kuliko kurekebisha na kutubu” (President Ezra Taft Benson).Unaweza kuwa umeshanukuu maelezo haya kama sehemu ya somo kwenye Alma 49–51. Kama ulifanya hivyo, fikiria kuacha mapengo kwenye sehemu ya maneno fulani wakati unaandika ubaoni. Uliza wanafunzi wajaze mapengo.Waalike wanafunzi kusimulia kuhusu nyakati katika maisha yao au kwenye maisha ya mtu wanayemjua wakati maandalizi yaliwasaidia kuzuia masikitiko au huzuni. Wakumbushe wanafunzi kwamba katika masomo ya hivi karibuni wamejifunza milango ya kuhusu mapigano kati ya Wanefi na Walamani. Waalike wanafunzi wasome Alma 59:5–11 ki-mya, wakifikiri kuhusu jinsi kauli iliyopo ubaoni inahusika na hali inayoelezwa katika aya hizi.• Ni nini kinachoonekana kuwa kiliwawezesha Walamani kushinda mji wa Nefiha? (Ma-

ovu ya watu wa Nefiha.)• Mlipata nini kwenye aya hizi zinazohusiana na kauli iliyoandikwa ubaoni?Kama wanafunzi hawatotaja kauli ifuatayo kwenye Alma 59:9, sisitiza kwao: “Ilikuwa rahisi sana kuweka mji kutoanguka katika mikono ya Walamani kuliko kuuchukua tena kutoka kwao” Unaweza ukitaka kupendekeza kwamba wanafunzi watie alama maelezo haya ka-tika maandiko yao. Ili kuwasaidia wanafunzi kufikiri kuhusu jinsi ukweli huu unavyotumika kwenye maisha yao, waulize wafananishe miji katika simulizi hili na wao wenyewe na vita vya kiroho wanavyokumbana navyo. Kisha uliza moja au zaidi ya maswali yafuatayo:• Ukweli huu unatuhusu vipi sisi? (Wasaidie wanafunzi kuona kwamba ni rahisi na bora

kubaki mwaminifu kuliko kurudi kwenye imani baada ya kupotea.)• Kwa nini kubaki mwaminifu katika Kanisa ni rahisi zaidi kuliko kurudi Kanisani baada

ya kipindi fulani cha kutoshiriki kikamilifu? • Kwa nini ni rahisi kudumisha ushuhuda kuliko kujipatia upya ushuhuda baada ya

kuanguka?Waalike wanafunzi kutafakari njia ambazo adui na wafuasi wake wanaweza kuwa wana-washambulia. Wahimize wao waandike kwenye daftari au shajara ya kujifundisha maa-ndiko kuhusu kile watafanya kujiandaa kwa mapigano ya kiroho.

Masomo yanayojumuisha milango kadhaaSomo linapojumuisha milango kadhaa katika maandiko, huhitaji kutoa msisitizo katika kila kitu kilicho katika milango hiyo. Unaweza kufanya muhtasari se-hemu za umbo la maa-ndiko na kisha kutenga muda zaidi kwa sehemu za umbo ambazo zinahusiana hasa na wanafunzi wako.

Page 402: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

387

alMa 59 – 63

Alma 60–62Moroni anamshitaki kiuongo Pahorani, ambaye anajibu kwa upendo na heshimaSoma Alma 59:13 kwa sauti. Hakikisha kuwa wanafunzi wanaelewa kwamba Moroni ali-kuwa amekasirika kwa sababu alifikiri serikali ilikuwa haijali au kujihusisha, kuhusu uhuru wa watu. Katika hasira yake, aliandika barua kwa Pahorani, mwamuzi mkuu wa Zarahemla Waalike wanafunzi wachache wasoma kwa zamu na kwa sauti kutoka Alma 60:6–11.• Kapteni Moroni alimshitaki Pahorani kwa nini?• Unahisi mhemuko upi katika mashitaka ya Moroni?Andika marejeo yafuatayo ya maandiko kwenye ubao Alma 60:17–20, 23–24. Waalike wanafunzi wasome aya hizi kimya. Wahimize jinsi wangelihisi kama wangekuwa kwenye hali ya Pahorani.• Ni kwa njia gani mashitaka ya Kapteni Moroni yameweza kumuumiza Pahorani?Waalike wanafunzi wachache wachukue zamu kusoma kwa sauti kutoka Alma 60:33–36. Uliza darasa lifuatilie, likitafuta kile Kapteni Moroni alijitayarisha kufanya kama Pahorani hakujibu vyema maombi yake. Baada ya kuruhusu wanafunzi kutoa taarifa ya kile wali-chokipata, waulize watambue maneno au vishazi katika aya hizi ambavyo vinavyoonesha sababu za Moroni au nia yake ya kutoa maombi. Waalike wanafunzi wasome Alma 61:1–5 kimya ili wagundue kwa nini Moroni hakuwa amepokea nguvu ya ziada ya wapiganaji.• Ni taarifa gani ambayo Pahorani alishirikiana na Moroni?• Ni zipi baadhi ya njia ambazo watu wanajibu wanaposhitakiwa juu ya kitu fulani kwa

uongo?• Umewahi kushitakiwa kwa jambo lolote kimakosa? Ulihisi vipi kuhusu mashitaka na

aliye kushitaki?Waalike wanafunzi wasome Alma 61:9–10, 15–18 kimya, wakitafuta chochote kinachoonye-sha ukuu wa sifa ya Pahorani. Baada ya muda wa kutosha, waalike wanafunzi wachache washiriki kile walichopata. • Tunaweza kujifunza masomo gani kutokana na jinsi Pahorani alivyojibu mashitaka ya

Moroni? (Wasaidie wanafunzi kutambua kanuni ifuatayo: Tunaweza kuchagua kuto-chukizwa kwa maneno na vitendo vya wengine. Kweli zingine ambazo wanafunzi wanaweza kutambua zinajumuisha kwamba tunapaswa kuepuka kutoa hukumu zisizo na huruma kuhusu wengine na kwamba tunapoungana katika haki na we-ngine, tunakuwa wenye nguvu katika vita vyetu dhidi ya uovu. (Unaweza ukitaka kuandika kweli hizi kwenye ubao.)

• Ni kwa jinsi gani tunaweza kuchagua kutochukizwa?Fikiria kuwauliza wanafunzi kama wapo tayari kushiriki uzoefu wowote waliokuwa nao katika kuchagua kutochukizwa wakati watu wamesema mabaya au vitu vya uongo kuwahusu. Unaweza pia kufikiria kuwaeleza kuhusu uzoefu wako mwenyewe. Shuhudia umuhimu wa kusamehe wengine kwa maneno yao au vitendo vyao dhidi yetu. Wahimize wanafunzi wafuate mfano wa Pahorani.Mwalike mwanafunzi asome Alma 62:1 kwa sauti. Uliza darasa lionyeshe jinsi Moroni alivyohisi alipopokea majibu ya Pahorani.Eleza kwamba hata kama Kapteni Moroni alikosea katika mashitaka yake ya Pahorani, Alifundisha kanuni za kweli ambazo tunaweza kuzitumia katika maisha yetu. Mwalike mwanafunzi asome Alma 60:23 kwa sauti. Sisitiza kwamba maneno ya Moroni kuhusu kusafisha chombo kwa ndani inaweza kumhusu yeyote anayehitaji kutubu. Eleza kwa-mba chombo ni kifaa, kama kikombe au bakuli. Weka uchafu au matope ndani na nje ya kikombe (kama kipo, kikombe kinachoonyesha ni vizuri zaidi.) Waulize wanafunzi kama watapenda kukinywea kikombe hicho. Safisha nje ya kikombe halafu waulize wanafunzi kama watahisi sawa kukinywea sasa.• Kama tukijifikiria sisi wenyewe kama vyombo, itamaanisha nini kusafisha sehemu ya

ndani, au ndani ya chombo?Soma maelezo yafuatayo ya Rais Ezra Taft Benson:

Page 403: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

388

SoMo la 105

"Ni lazima tuoshe ndani ya chombo (ona Alma 60:23 kuanzia kwanza na sisi wenyewe, halafu kwa familia zetu, na mwishowe kwa Kanisa” (“Cleansing the Inner Vessel,” Ensign, May 1986, 4).• Kwa nini ni muhimu kwamba tuwe wasafi kwa ndani (ambako watu hawawezi kuona)

vilevile kwa nje (ambako watu wanaweza kuona)?• Kwa nini ni muhimu kusafisha ndani ya chombo cha maisha yetu kabla hatujaweza

kutumika kikamilifu katika ufalme wa Bwana?Fanya muhtasari Alma 62:1–38 kwa kueleza kwamba Kapteni Moroni alileta sehemu ya jeshi lake kumsaidia Pahorani kupindua watu wa mfalme katika Zarahemla. Ndipo, wa-kiwa na jeshi lao lililoungana na msaada wa vikosi vingine vya Wanefi, Moroni na Pahorani waliiteka tena miji iliyobaki ambayo walikuwa wameipoteza kwa Walamani. Waliwafurusha Walamani kutoka katika nchi na wakajenga amani miongoni mwa watu.• Nini baadhi ya changamoto gani ambazo watu binafsi na familia wanaweza kukabiliana

nazo baada ya muda wa vita? Waalike wanafunzi wasome Alma 62:39–41 kimya ili waone jinsi Wanefi walivyoadhirika na majaribio ya vita.• Ni kanuni gani unazoweza kuzitambua katika Alma 62:40–41?Wakati wanafunzi wakijadiliana swali hili, wanaweza kuwa na majibu kama haya:Sala zetu za haki zinaweza kuwa na matokeo mazuri katika jumuia zetu.Katika wakati wa matatizo, baadhi ya watu hunyenyekea mbele za Mungu wakati wengine wanakuwa sugu.• Kwa nini unafikiri baadhi ya watu huwa karibu sana na Bwana wanapokabiliwa na

majaribio? Kwa nini baadhi ya watu ugeuka kutoka kwa Bwana wanapokabiliwa na ma-jaribio? (Wasaidie wanafunzi kuelewa kwamba katika wakati wa matatizo, chaguo zetu zinaamua kama tutakuwa karibu zaidi kwa Bwana.

• Kama ulivyosoma milango ya Kitabu cha Mormoni juu ya vita, imekufundisha nini wewe kuhusu kuwa mfuasi wa Yesu Kristo wakati wa vita au mabishano?

Alma 63Wanefi wengi walisafiri kwenda nchi iliyo kaskaziniFanya muhtasari maneno ya Mormoni katika sura hii kwa kueleza kwamba wanefi wengi walianza kuhamia upande wa kaskazini, kwa njia ya nchi kavu na kwa bahari. Shibloni alimkabidhi Helamani zile kumbukumbu takatifu. Kapteni Moroni alikufa, na mwanawe wa kiume Moroniha akaongoza jeshi lililosukuma nyuma shambulio lingine la Walamani.Unaweza kutaka kuhitimisha somo hili kwa kuwaeleza kuhusu mtu fulani ambaye alipa-twa na shida na matatizo na amechagua kuwa na moyo wa upole na akaongeza imani kwa Mungu. Fikiria kushirikisha uzoefu wa kibinafsi.

Tathmini ya AlmaChukua muda kiasi kuwasaidia wanafunzi kutathmini kitabu cha Alma. Waalike wafi-kiri kuhusu nini wamejifunza kutoka kitabu hiki, katika seminari na katika mafunzo yao kibinafsi ya maandiko. Kama itahitajika, waalike warudie baadhi ya muhtasari ya milango katika Alma ili iwasaidie kuikumbuka. Baada ya muda wa kutosha, waalike wanafunzi kadhaa waje washiriki mawazo na hisia zao kuhusu kitu fulani katika kitabu ambacho kimewavutia.

Page 404: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

389

Somo la Mafunzo - NyumbaniAlma 45–63 (Kitengo cha 21)

Vifaa vya Matayarisho kwa Mwalimu wa Mafunzo ya NyumbaniMuhtasari wa Masomo ya Kujifunza Nyumbani Kila SikuMuhutasari ufuatao wa mafundisho na kanuni wanafunzi walijifunza walipokuwa wakisoma Alma 45–63 (kitengo 21) haikusudiwa kuwa sehemu ya somo lako. Somo unalofu-ndisha limekazia sehemu chache za mafundisho na kanuni. Fuata maelekezo ya Roho Mtakatifu unapo waza mahitaji ya wanafunzi.

Siku 1 (Alma 45–49)Alma alimweleza mwanawe wa kiume kwamba Bwana hawezi kuiangalia dhambi kwa nia ndogo sana ya kuiruhusu. Kwa kulinganisha vita za Wanefi na vita vyao, wanafunzi walijifunza kweli zifuatazo: Tunapo kuwa mashujaa kwa kufuata amri kama Kapteni Moroni alivyofanya, Mungu atatuimarisha na kutubariki. Shetani anatafuta kutuharibu, na anatushawishi kwa kila njia kushusha viwango vyetu.

Siku 2 (Alma 50–52; 54–55)Ingawa wanefi walifanikiwa kwa muda baada ya kuondoka kwa Amalikia Moroni aliendelea kuwatayarisha watu kwa mashambulizi yajayo. Mfano wa wanefi wakati wa hali ngumu uliwasaidia wanafunzi kuelewa kwamba uaminifu kwa Mungu unaleta furaha, hata katika machafuko—hata hivyo mgawanyiko na mabishano yanaweza kuharibu amani yetu. Wanafunzi pia walijifunza kwamba tunaposimama imara kwa yale yaliyo ya haki tunaweza kuzuia ushawishi mwovu usiwe na nguvu juu yetu.

Siku 3 (Alma 53; 56–58)Wakati wa baadhi ya mapigano magumu sana, Helamani ali-ongoza jeshi la vijana ambao walikuwa wa watu wa Amoni. Hawa wapiganaji vijana wadogo walionesha kwamba tunapowajibika kiimani, twaweza kupata nguvu kutoka kwa Mungu. Wanafunzi walijifunza kutoka kwa mfano wa hawa wapiganaji shujaa kwamba kama tutamwamini Bwana na kumtii kwa uhakika, atatusaidia katika mapigano yetu. Licha ya vidonda vingi walivyovipata na shida nyingi walizovumilia, jeshi la Wanefi na vijana wadogo wapiganaji walionesha kwamba tukimgeukia Mungu nyakati za matatizo, tunaweza kupokea uhakika wa kiungu ambao unaweza kuimarisha imani zetu na kutupa matumaini.

Siku ya 4 (Alma 59–63)Kwa sababu ya uasi wa ndani, Wanefi walipoteza baadhi ya miji; hii iliwaonyesha wanafunzi kwamba ni rahisi na vizuri kubaki mwaminifu kuliko kurudi kwenye imani baada ya kupotea. Moroni kabla mashitaka yasiyokamili alimshi-taki mwamuzi mkuu Pahorani kwa kutojali kazi zake, na wanafunzi walijifunza kutoka majibu ya Pahorani kwamba twaweza kuchagua kutoudhiwa kwa maneno na vitendo vya wengine. Kwa nyongeza, wanafunzi walijifunza kwamba tunapoungana katika haki na wengine, tunakuwa wenye nguvu zaidi katika vita vyetu na uovu, kama ilivyooneshwa na Moroni na Pahorani.

UtanguliziKwa sababu somo hili linajumuisha milango 19 ya kitabu cha Alma, hautaweza kuwa na uwezo wa kufundisha au kusisitiza mahusiano yote ya kihistoria na mafundisho yote na kanuni ambazo wanafunzi walijifunza juma zima. Mapendekezo ya kufundisha yafuatayo yanawapa wanafunzi fursa ya kutumia kweli walizojifunza kutoka mafundisho ya vita vya Wanefi na vita katika maisha yao. Kwa maombi jifunze maandiko kwa ajili ya somo hili ili upate mwongozo wa kusisitiza kweli ambazo wana-funzi wanahitaji ili wawe makini wakati wakiwa darasani.

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 45–63Kwa kumwamini Mungu na kuwafuata viongozi waliopewa mwongozo, Wanefi waliweza kuwashinda WalamaniAndika kauli ifuatayo ya Rais Ezra Taft Benson ubaoni kabla ya darasa: "Kutoka Kitabu cha Mormon tunajifunza jinsi wafuasi wa Kristo wanavyoishi wakati wa vita" (The Book of Mormon—Keystone of Our Religion, Ensign, Nov. 1986, 7).

Waulize wanafunzi wataje baadhi ya vita ambazo vimepiganwa katika nchi wanaoishi. Kisha waulize wataje baadhi ya changa-moto ambazo watu wanaweza kukabiliwa nazo wakati wa vita.

Uliza: Kwa nini inaweza kuwa vigumu kuwa mfuasi wa Yesu Kristo wakati wa vita?

Waulize wanafunzi wafikirie kuhusu vita walivyojifunza karibu juma zima lililopita, kama ilivyonakiliwa katika Alma 45–63. Unaweza ukitaka kuwahamasisha kwa haraka wafanye marejeo ya baadhi ya muhtasari wa milango kwa Alma 45–63. Waalike wataje baadhi ya changamoto Wanefi walikumbana nazo wakati wa vita vyao.

Page 405: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

390

SoMo la MafUnzo - nyUMbani

Wakumbushe wanafunzi kwamba hata kama kamwe hatupi-gana vita halisi, sisi sote twapigana vita vya kiroho. Mwalike mwanafunzi asome maelezo yafuatayo ya Rais Henry B. Eyring wa Urais wa Kwanza, ambaye alieeleza vita ya kiroho ambayo tunapambana navyo. Unaweza kutaka kuwapa nakala kila mwanafunzi.

“Umesajiliwa katika jeshi la Bwana katika muda huu wa mwi-sho. Huu sio wakati wa amani. Na imekuwa hivyo tangu Shetani alipovipanga vikosi vyake dhidi ya mpango wa Baba yetu wa Mbinguni katika uwepo wetu mbinguni Hatujui kwa utondoti pambano lile. Lakini twajua tukio moja. Shetani na wafuasi wake walitupwa chini duniani. Na tangu kuumbwa kwa Adamu na Hawa, mgogoro umeendelea. Tumeuona ukiongezeka. Na maandiko yameashiria kwamba vita vitakuwa vikali sana na waathirika wa kiroho upande wa Bwana wataongezeka. (Man Down) Ensign or Liahona, May 2009, 63).

Warejeshe wanafunzi kwenye maelezo ya Rais Benson ubaoni Waambie kwamba iwe tunazugumzia kuhusu vita vya kimwili au vita vya kiroho, maelezo ni ya kweli. Eleza kwamba kujifunza maisha ya wafuasi walioishi wakati wa vita katika wakati wa Kitabu cha Mormoni inaweza kutusaidia sisi kujenga sifa ambazo zitakuwa muhimu katika vita vyetu vya kiroho.

Andika majina yafuatayo na marejeo ya maandiko ubaoni au yatayarishe kama vitini. Waulize wanafunzi wamchague mmoja wa watu hawa au makundi kujifunzia. Jaribu kuwa na mwafunzi angalau mmoja ajifunze kila mtu au kundi.

1. Moroni—Alma 46:11–21; 48:7–17 2. Helamani—Alma 48:19–20; 56:2–9; 58:4–12, 32–37 3. Wale vijana wapiganaji 2060—Alma 53:16–22; 56:47–56;

57:19–27 4. Pahorani—Alma 50:39–40; 51:1–7; 61:1–21

Wape wanafunzi dakika kadhaa kusoma maandiko mengi kadri iwezekanavyo kuhusu mtu binafsi au kikundi walichochagua. Waulize wawe tayari kufundisha mawazo yafuatayo kwa darasa (unaweza ukitaka kuandika haya ubaoni au kuweka kwenye kitini pia):

• Tukio kutoka maisha ya mtu huyu au kikundi linaloonyesha watu walikuwa wafuasi wa kweli wa Mwokozi.

• Sifa moja au zaidi ya mtu huyu au kikundi ambazo ziliwasaidia kubaki mashujaa wakati wa vita na Walamani.

• Kanuni moja ya injili tunayoweza kujifunza kutokana na mtu huyu au kikundi ambazo zinaweza kututia nguvu katika vita vyetu vya kiroho hivi leo.

Alika wanafunzi wengi kadri iwezekanavyo kushiriki kile walicho-jifunza pamoja na darasa. Unaweza ukitaka uwaulize wanafunzi waandike kanuni za injili ambazo wamejifunza ubaoni.

Fikiria kuuliza maswali yafuatayo kusaidia wanafunzi kutumia kile walichojifunza kutoka kwenye mafunzo yao ya Alma 45–63:

• Fikiria sifa za mfuasi wa Yesu Kristo ambazo uliziona katika watu ambao waliishi wakati wa vita na Walamani. Sifa gani kati ya hizi ambazo wewe ungependa zaidi kukuza katika maisha yako? Kwa nini?”

• Ni baadhi ya vita vya kiroho gani ambavyo sisi hukumbana navyo hivi leo? Ni kwa jinsi gani mifano ya wafuasi hawa wa Mwokozi inaweza kukusaidia kuwa na imani na ujasiri unapo-kumbana na vita hivi?

Unaweza ukitaka kushiriki mojawapo ya vifungu unavyopenda za-idi kutoka Alma 45–63. Shuhudia kuwa kanuni tunazojifunza ku-toka kwa milango hii zinaweza kutusaidia kuwa wafuasi wa kweli wa Yesu Kristo wakati wa vita vya kiroho vya siku za mwisho.

Kitengo kinachofuata (Helamani 1–9)Waambie wanafunzi kuwa mlango wa kwanza wa Helamani umeandikwa vifo vya waamuzi wakuu watatu. Waambie wata-pata majibu kwa maswali yafuatayo: Waamuzi hawa walikufa vipi? Mwujiza gani ulitokea kwa Nefi na Lehi walipokuwa gerezani? Walisikia sauti ya nani? Waambie wanafunzi kwamba Nabii Nefi aliweza kutatua suala la mauaji kupitia kwa uwezo wa unabii.

Page 406: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

391

UtangUlizi Wa

Kitabu cha helamaniKwa nini ujifunze kitabu hiki?Katika masomo yao ya kitabu cha Hela-mani, wanafunzi watajifunza kutoka kwa mifano na mafundisho ya watu wakuu kama vile Helamani, wanawe Nefi na Lehi, na Samueli Mlamani, ambao kwa ushujaa walimtii Bwana na kushuhudia kumhusu. Utume wa wanaume hawa unaonyesha kuwa Mungu hupeana uwezo kuwasaidia watumishi Wake kutekeleza matakwa Yake na kuwa jitihada za watu wenye haki zinaweza kubariki maelfu ya watu. Wana-funzi pia watajifunza kuhusu madhara ma-baya ya kiburi, uovu, na makundi ya siri.

Nani aliandika kitabu hiki?Mormoni alikusanya na kufupisha kumbu-kumbu kutoka kwa mabamba makubwa ya Nefi ili kutunga kitabu cha Helamani. Kitabu kimeitwa kwa ajili ya Helamani, ambaye alikuwa mwana wa Helamani na mjukuuu wa Alma Mdogo. Helamani ali-pokea kumbukumbu kutoka kwa Shibloni, mjomba wake, na alihudumu kama mwa-muzi mkuu mwenye haki juu ya Wanefi. Aliwafundisha wanawe Nefi na Lehi kutii amri na kumkumbuka Mkombozi wao na kumweka awe msingi wa maisha yao (ona Helamani 5:9–14). Wakiwa wamesha-wishiwa na mafundisho haya na wakisi-kitishwa na uovu wa watu, Nefi na Lehi walihubiri toba kwa Wanefi na Walamani. Nefi aliwacha wadhifa wake kama mwa-muzi mkuu ili kufanya hivyo. Baada ya ma-elfu ya Walamani kuogoka, nabii Mlamani aliyeitwa Samueli alishawishiwa kuhubiri toba na kutoa unabii miongoni mwa Wa-nefi. Kitabu cha Helamani kinazidua kutoka kwa kumbukumbu zilizowekwa wakati wa utawala na uchungaji wa Helamani (Helamani 1–3) na Nefi (Helamani 4–16). Kumbukumbu za Nefi zilijumuisha unabii na mafundisho ya Samueli Mlamani.

Kitabu hiki kiliandikiwa nani na kwa nini?Mormoni aliandika kitabu cha Helamani kwa watu wa siku za mwisho ambao wa-ngepokea rekodi yake. Kama fupisho zake zingine kutoka kwa mabamba makubwa ya, kitabu cha Helamani kinashuhudia misheni tukufu na ya kukomboa ya Yesu Kristo (ona Helamani 3:27–30; 5:9–12; 8:13–23; 14:1–29; 16:4–5).

Kiliandikwa lini na wapi?Kumbukumbu asili zilizotumiwa kama nyenzo za kitabu cha Helamani huenda zi-liandikwa kati ya miaka 52 K.K. na mwaka 1 K.K. Mormoni alizifupisha kumbukumbu hizo wakati fulani kati ya miaka 345 B.K. na 385 B.K. Mormoni hakuelezea mahali alikuwa wakati alitunga kitabu hiki.

Ni zipi baadhi ya sifa bainifu za kitabu hiki?Kitabu cha Helamani kinawaonyesha Wa-nefi wakibadilikabadilika kati ya wema na uovu kwa marudio wa juu zaidi kushinda wakati wowote mwingine katika historia yao. Kitabu kinaeleza matokeo mengi ya ugomvi, vita, mauaji na makundi ya siri. Pia kinatambulisha na kueleza shughuli za wezi wa Gadiantoni, ambao vitendo vyao vya giza hatimaye vilileta uangamiaji wa Wanefi (ona Helamani 2:13–14). Kitabu cha

Helamani pia ni cha kipekee kwa sababu ki-naelezea wakati ambapo “sehemu kubwa” ya Walamani waliongoka na “uzuri wao ulizidi ule wa Wanefi” (Helamani 6:1). Zaidi ya hayo, kinaonyesha uwezo ambao Mu-ngu huwapa manabii Wake, kama vile Nefi alipofunua mauaji ya mwamuzi mkuu na kutoa unabii wa kukiri kwa ndugu ya mwa-muzi (ona Helamani 8–9 na wakati Nefi alipokea uwezo wa kufunganisha kutoka kwa Bwana na kisha akautumia kuwezesha na kusitisha njaa (ona Helamani 10–11). Aidha, katika kuhifadhi maneno ya Samueli, kitabu hiki kina kumbukumbu ya pekee ya mahubiri ya nabii Mlamani yaliyohubiriwa Wanefi (ona Helamani 13–15). Katika ma-hubiri haya, Samueli alitoa unabii wa ishara za kuzaliwa na kufa kwa Yesu Kristo.

Muktasari Helamani 1–3 Waamuzi wakuu wawili, Pahorani na Pacumeni, wauawa. Moroniha azuia uvamizi wa Walamani ulioongozwa na Ko-riantumuri. Kishkumeni auliwa aki-jaribu kumua Helamani, mwamuzi mkuu aliyeteuliwa hivi karibuni. Ingawa Gadiantoni na wezi wake wanaeneza makundi ya siri, miongo ya maelfu ya watu wanabatizwa katika Kanisa. Nefi akawa mwamuzi mkuu baada ya kifo cha Helamani.

Helamani 4–6 Jeshi la wapinzani Wa-nefi na Walamani wateka nchi zote za kusini za Wanefi, ikijumuisha pia Zarahemla. Wanefi wanakuwa wa-nyonge kwa sababu ya uovu wao. Nefi ampatia Kezorami kiti cha hu-kumu. Nefi na Lehi wanakumbuka maneno ya baba yao, Helamani, na kujitolea kuhubiri injili. Wapinzani wengi wanatubu na kurudi kwa Wanefi. Baada ya Bwana kuwalinda Nefi na Lehi kimiujiza gerezani, we-ngi wa Walamani waongoka na ku-rudisha nchi walizokuwa wameteka kwa Wanefi. Wakati wa mafanikio, wezi wa Gadiantoni waongezeka. Wengi wa Wanefi waungana katika

uovu wao, kusababisha ufisadi wa serikali ya Wanefi.

Helamani 7–12 Nefi anaomba juu ya mnara wa bustani yake na kuwa-onya watu kutubu. Anaangazia shuhuda za wengi ambao walita-biri kuhusu Kristo. Anafunua pia kuwa Siizoramu, mwamuzi mkuu, ameuliwa na nduguye Seantumi. Nefi apokea uwezo wa kufunga-nisha na aendelea kuhubiri toba. Amwomba Bwana abadili vita na njaa, na maombi yake yafanya mvua kuja kusitisha njaa baada ya watu kutubu. Baada ya kipindi kifupi cha mafanikio na amani, ubishi na uovu unaenea miongoni mwa watu. Mor-moni aomboleza kuhusu njia zisizo thabiti na za upumbavu za watu.

Helamani 13–16 Samueli Mlamani aonya Wanefi kutubu, atabiri ku-husu maangamizo yao ya baadaye, na kubashiri ishara zilizoashiria kuzaliwa na kufa kwa Yesu Kristo. Wale ambao wanaamini maneno yake wanabatizwa. Hata hivyo, wengi wa watu wamkataa Samueli na kupuuza ishara na matukio ya maajabu yanayopeanwa.

391

Page 407: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

392

SOMO LA 106

helamani 1–2UtanguliziBaada ya Pahorani kuaga, kulitokea ubishi miongoni mwa Wanefi kuhusu nani alistahili kuwa mwamuzi mkuu mrithi. Mwanawe Pahorani aliteuliwa na sauti ya watu. Hata hivyo, mwamuzi mkuu mpya aliuliwa na Kishkumeni, ambaye alikuwa sehemu ya kundi la

siri. Wakichukua fursa ya ubishi na mgawanyiko huu, Walamani waliteka mji mkuu wa Zarahemla. Wanefi walimiliki tena Zarahemla, na Kishkumeni aliuliwa akijaribu kumua Helamani ( mwana wa Helamani), mwamuzi mkuu mpya.

Mapendekezo ya Kufundisha

Helamani 1Ubishi unawatenganisha Wanefi na kuwawezesha Walamani kuteka ZarahemlaKabla ya darasa, andika yafuatayo ubaoni:

Helamani 1:1–4. Ni nini kilichosababisha ubishi na migawanyiko miongoni mwa watu Wanefi?Helamani 1:5–8. Ni nani aliyeteuliwa mwamuzi mkuu, na nduguze wawili waliichukulia vipi?

Ili kuanzisha somo, uliza wanafunzi waeleze tofauti kati ya kujadiliana swala fulani na kubishana kuhusu swala fulani. Ikiwa wanafunzi wanahitaji usaidizi kuelewa tofauti hizi, waulize wazingatie hali zifuatazo na watambue zipi ni mifano ya ubishi. (Wanapaswa watambue hali ya pili na ya tatu) 1. Kueleza msimamo wako kupitia ushawaishi wa kirafiki na ukweli. 2. Kuonyesha kutomuheshimu mtu ambaye mitazamo yake ni tofauti na yako. 3. Kuhisi kuwa kushinda ubishi ni muhimu zaidi kuliko hali nzuri ya mtu mwingine.Alika wanafunzi watafute hatari za ubishi wanaposoma Helamani 1. Wahimize wazingatie faraghani jinsi ubishi unaweza kuwa dhahiri maishani mwao.Waulize wanafunzi wasome kimya vifungu vya maandiko ambavyo umeandika ubaoni, wakitafuta majibu ya maswali sambamba. Waalika waelezee walichopata.Chora njia ubaoni, na ipatie jina ubishi .

Eleza kuwa ubishi unaweza kuwa kama njia inayoelekeza kwa dhambi zingine na matokeo mabaya. Alika mwanafunzi asome Helamani 1:9 kwa sauti.Uliza darasa libainishe kile ubishi kati ya Wanefi hatimaye ulisababisha. (Mauaji) Andika mauaji ubaoni, mahali fulani kwenye njia uliochora.Alika wanafunzi wasome Helamani 1:10–12 kimya, wakibainisha kile Kishkumeni na wale waliomtuma walifanya ili kuficha mauaji aliyokuwa ametekeleza. • Kwa nini Kishkumeni na wafuasi wake wangetaka kuweka vitendo vyao siri?• Ni gani baadhi ya mifano ya kisasa ya watu kujaribu kuweka vitendo vyao visivyo vya

haki kuwa siri? (Majibu yanaweza kujumuisha kuwadangany’a wazazi au katika mahoji-ano na askofu au rais wa tawi)

• Kwa nini ingekuwa si busara kusaidia mtu mwingine kuficha dhambi zake?Alika mwanafunzi asome Helamani 1:18–21 kwa sauti. Uliza darasa lifuatilia na libaini-she matokeo mengine ya ubishi kati ya Wanefi. Wanafunzi wanapoelezea walichokipata,

ubishi

Page 408: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

393

helaMani 1–2

wawezeshe waandike majibu yao mahali fulani kwenye njia ubaoni. Unaweza pia kuwaa-lika wapendekeze na waandike matokeo mengine ya ubishi ambayo wameona.Fupisha Helamani 1:22–30 kwa kueleza kuwa baada ya Walamani kuteka Zarahemla, ma-jeshi ya Wanefi yaliwashinda katika vita ambako wengi waliuliwa.Alika wanafunzi wafanye muhtasari wa kanuni kuhusu ubishi ambao wamejifunza kwa kusoma Helamani 1. Kanuni moja ambao wanafunzi wanaweza kubainisha ni kuwa ubishi hutufanya tuwe katika hatari ya uvutio wa adui. Unaweza amua kuandika haya ubaoni.Ili kuwasaidia wanfunzi waelewe kanuni hii zaidi na kuitumia katika maisha yao, zingatia kuuliza baadhi ya maswali yafuatayo: • Ikiwa msichana amekuwa akibishana na wazazi wake kwa sababu ya marafiki wake,

inawezaje kuathiri mtazamo wake kwa ushauri wa wazazi wake katika sehemu zingine za maisha yake?

• Ikiwa watoto wa familia wamekuwa wabishi, ni jinsi gani tabia yao inaweza kuathiri uhusiano wao wa muda mrefu? Inawezaje kuathiri familia mzima?

• Ubishi katika kata au tawi unawezaje kuwafanya washiriki wa Kanisa kuwa katika hatari zaidi ya mashambulizi ya Shetani?

• Ikiwa mvulana ana hisia za hasira kwa mtu katika jamii yake ya ukuhani, ni jinsi gani hisia zake zinaweza kuathiri vitendo vyake kanisani? Zinawezaje kuathiri ushiriki wake kanisani?

• Hisia za ubishi zinawezaje kutudhoofisha wakati tunakumbana na majaribio?Alika wanafunzi wapendekeze hali zingine ambako ubishi unaweza kutufanya tuwe dhaifu na katika hatari na mipango ya adui.Wape wanafunzi muda wa kutafakari sehemu katika maisha yao ambako wanaweza kuwa wanachangia hisia za ubishi. Waalike wabainishe hatua moja maalum ambayo wanaweza kuchukua ili kuepuka tabia ya ubishi.

Helamani 2Helamani akuwa mwamuzi mkuu, na mfanyikazi wake amzuia Kishkumeni kumuua • Kwa nini ni vyema zaidi kusafisha machafuko kuliko kuyaficha?• Kwa nini mtu anaweza taka kuficha kitu alichofanya?Alika wanafunzi wasome Helamani 2:3–4 na M&M 58:43 kimya.• Kulingana na mistari hii, ni nini tofauti kati ya jinsi Bwana anataka tukabiliane na dha-

mbi na jinsi wezi wa Gadiantoni walikabiliana na dhambi?Eleza kuwa katika Helamani 2, tunasoma kuhusu jaribio ya Kishkumeni kumuua Hela-mani, mwamuzi mkuu mrithi. Uliza wanafunzi kufikiria kwamba wao ni waandishi walio-patiwa jukumu la kuripoti jaribio la kumuua mwamuzi mkuu. Waalike wasome Helamani 2:2–9 na mwenzi na waandike kichwa cha habari ili kufupisha kile kilichotendeka. Uliza wanafunzi kadhaa wasome vichwa vyao vya habari kwa darasa.Alika wanafunzi wasome Helamani 2:10–11 kimya, wakitafuta hatua ambayo Helamani alichukua dhidi ya wezi wa Gadiantoni. Uliza mwanafunzi afupishe mistari hii.Elezea kuwa kundi la Gadiantoni ni mfano wa kundi la siri. Alika mwanafunzi asome He-lamani 2:12–14 kwa sauti. Uliza darasa libainishe athari ambayo makundi ya siri yalikuwa nayo kwa Wanefi• Tunaweza kujifunza nini kutoka kwa mistari hii kuhusu hatari ya makundi ya siri?

(Wanafunzi wanapojibu, hakikisha kuwa ukweli ufuatao ni wazi: Makundi ya siri yanaweza kusababisha kuangamizwa kwa jamii. Unaweza amua kueleza kuwa pamoja na kuleta kuangamizwa kwa Wanefi, makundi ya siri yalisababisha kuangami-zwa kwa Wayaredi, ambao kuwahusu wanafunzi watasoma katika kitabu cha Etheri; ona Etheri 8:20–21.)

Soma kauli ifuatayo ya Mzee M Russell Ballard wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili. Uliza wanafunzi wasikilize mifano ya makundi ya siri leo:

Kutambua mafundisho na kanuniWakati mwingine, wanafunzi hueleza mafundisho na kanuni wanapojibu maswali ama kufupisha kile wamejifundisha katika umbo la maandiko. Kwa vile saa zingine wao huwa hawajui kuwa wanaelezea ukweli wa kimsingi, inaweza kusai-dia kuuandika ubaoni au kuwahimiza wanafunzi waandike katika vitabu vyao ama shajara ya kujifunza maandiko.

Page 409: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

394

SoMo la 106

“Kitabu cha Mormoni kinafundisha kuwa makundi ya siri yanayoshiriki katika uhalifu yanatoa changamoto kuu, si tu kwa watu binafsi na familia lakini kwa ustaarabu mzima. Miongoni mwa makundi ya siri ya leo ni magenge, muungano wa wakiritimba wa madawa ya kulevya, na familia za uhalifu uliopangwa. . . .“Tusipokuwa waangalifu, makundi ya siri ya leo yanaweza kupata nguvu na uvutio haraka tu na kwa ukamilifu kama vile yalifanya katika Kitabu

cha Mormoni. . . . "[Shetani] hutumia makundi ya siri, ikiwa ni pamoja na magenge, ‘kutoka kizazi hadi kingine kulingana na vile anavyoweza kupata mioyo ya watoto wa watu.’ [Helamani 6:30.] Lengo lake ni kuangamiza watu binafsi, familia, jamii na mataifa. [Ona 2 Nefi 9:9.] Kwa kiwango fulani, alifaulu wakati wa Kitabu cha Mormoni. Na anapata ushindi mwingi sana leo. Ndiposa ni muhimu sana kwetu kuchukua msimamo dhabiti kwa ajili ya ukweli na haki kwa kufanya kile tunaweza ili kusaidia kulinda jamii zetu” (“Standing for Truth and Right,” Ensign, Nov. 1997, 38).Alika wanafunzi watafakari jinsi wanaweza kutumia mafunzo ya Mzee Ballard. Waalike waandike katika madaftari ama majarida ya kujifunza maandiko kuhusu kile watakacho-fanya kuepuka aina yoyote ya makundi ya siri na kile watafanya “kuchukua msimamo dhabiti kwa ajili ya ukweli na haki” katika jamii zao.

Tangazo na Habari za UsuliHelamani 1:1–21. Ubishi unaangamiza Kitabu cha Helamani kinaelezea wakati wa uovu mkuu miongoni mwa Wanefi. Wezi wa Gadiantoni walisitawi, na watu walipitia vipindi vya uovu, uangamizo, na toba, ili tu kurejea kwenye uovu. Nyingi ya shida hizi zilianza na ubishi, kama ilivyoelezwa katika mlango wa kwanza wa Helamani. Watu wengine hudhania ubishi kuwa dhambi ndogo. Lakini, kauli mbili zifuatazo za manabii wa siku za mwisho zinahimiza uzito wa dhambi hii:

Rais James E. Faust wa Urais wa Kwanza alionya, “Wa-kati kuna ubishi, Roho wa Bwana ataondoka, bila kujali ni nani amekosea” (“What I Want My Son to Know before He Leaves on His Mission,” Ensign, Mei 1996, 41).

Mzee Joseph B. Wirthlin wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili alionya; “Dhambi za ufisadi, uongo, mabi-shano, ubishi na maovu mengine katika ulimwengu huu hayapo hapa kwa bahati. Ni ushahidi wa kam-peni ya dhati ya Shetani na wale wanaomfuata. Yeye

hutumia vifaa na mbinu zote ambazo anazo kuda-ng’anya, kuchanganya na kupotosha” (“Deep Roots,” Ensign, Nov. 1994, 76).

Tofauti na matokeo ya uharibifu ya ubishi, Rais Henry B. Eyring wa Urais wa Kwanza alisisitiza umoja na amani ambayo Roho wa Bwana huleta.

“Ambapo watu wana Roho hio pamoja nao, tunaweza kutarajia umoja. Roho huweka ushuhuda wa kweli katika mioyo yetu, ambayo huunganisha wale ambao wanashiriki huo ushuhuda. Roho wa Mungu kamwe huwa haleti ubishi (ona 3 Ne. 11:29). Kamwe huwa haleti hisia za tofauti baina ya watu ambazo huelekeza kwa mabishano (ona Joseph F. Smith, Gospel Doctrine, 13th ed. [1963], 131). Huelekeza kwa amani ya kibinafsi na hisia ya umoja na wengine. Huunganisha nafsi. Familia iliyoungana, Kanisa lilioungana, na dunia katika amani inategemea nafsi zilizounganishwa. (“That We May Be One,” Ensign, Mei 1998, 67).

Page 410: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

395

UtanguliziWakati huu katika historia ya Kitabu cha Mormoni, Wanefi walifurahia muda wa amani lakini pia walipitia nyakati za ubishi. Miongo ya maelfu ya Wanefi waliji-unga na Kanisa wakati wa amani. Kufuatia hali hii ya muda wa mafanikio makubwa, kiburi kikaanza kuingia

mioyoni mwa watu. Hata hivyo, washiriki wanyenye-kevu zaidi wa Kanisa walikuwa katika imani yao, licha ya wao kudhulumiwa na wale waliokuwa na kiburi. Kwa sababu ya uovu miongoni mwa wengi wa Wanefi, walipoteza nchi zao zote za kusini kwa Walamani.

SOMO LA 107

helamani 3–4

Mapendekezo ya Kufundisha

Helamani 3Wanefi wengi wahamia kaskazini, wakati Kanisa linastawi miongoni mwa uovu na matesoAndika maneno yafuatayo ubaoni (unaweza amua kufanya hivi kabla ya darasa):

Watu katika (jina la nchi yako)Watu Katika (jina la jiji lako)Watu katika kata au tawi langu Watu katika familia yanguMimi Mwenyewe

Uliza wanafunzi ni nani kati ya watu wote walioorodheshwa ubaoni, wanahisi wanaweza kudhibiti. Kisha waulize wainue mikono yao kama wamewahi kuvunjika moyo kwa sababu ya vitendo vya wengine. Wawezeshe kuwacha mikono yao juu kama wameshavunjika moyo hivi karibuni kwa sababu ya vitendo vibaya vya wengine. Elezea kwamba wanapo-soma Helamani 3, watapata ufahamu kuhusu kile wanaweza kufanya wakati wale karibu nao hawaishi kulingana na injili.Alika mwanafunzi asome Helamani 3:1–2 kwa sauti. Uliza darasa lifuatilie, likitafuta mato-keo ya kishazi “hakuna ubishi” Alika wanafunzi wasome Helamani 3:3, 19 kimya, wakita-futa maneno na vishazi vinavyoashiria jinsi mambo yalibadilika miongoni mwa Wanefi.• Kwa nini unafikiri Wanefi walipita haraka kutoka kwa muda wa kutokuwa na ubishi hadi

kwa moja wenye ubishi mwingi.Fupisha Helamani 3:3–16 kwa kueleza kuwa wakati huu wa ubishi, Wanefi wengi waliha-mia kaskazini. Alika mwanafunzi asome Helamani 3:20 kwa sauti. Uliza darasa litambue jinsi Helamani alivyoelezewa katika wakati huu wa ubishi.• Ni nini kinakuvutia kuhusu mfano wa Helamani wakati huu wa ubishi? (Wanafunzi

wanapojibu, unaweza amua kupendekeza kuwa waweke alama kwenye neno siku zote katika Helamani 3:20.)

Alika wanafunzi wasome Helamani 3:22–26 kimya na watambue jinsi hali miongoni mwa Wanefi ilibadilika.• Nini kiliwafanya viongozi wa Kanisa washtuke ?• Tunaweza kjifunza nini kutoka kwa mistari hii kuhusu uwezo wa kuvutia ambao Kanisa

linaweza kuwa nao kwa watu?Kumbusha wanafunzi kuwa Mormoni alipotayarisha kumbukumbu ya Kitabu cha Mor-moni, wakati mwingine aliashiria mafunzo ambayo alitaka wasomaji wajifunze kutoka kwa maelezo fulani. Kwa upande wa Helamani 3, alitumia vishazi “hivyo tunaweza kuona,” “hivyo tunaona” na “tunaona” kuanzisha mafunzo yake. Alika wanafunzi wa-some Helamani 3:27–30 kimya na watambue ni mafunzo gani Mormoni alitaka tujifunze. Baada ya wanafunzi kuripoti kile wamepata, uliza:

Kubainisha kauli na jinsi tuonavyoKatika kutayarisha Kitabu cha Mormoni, nabii Mormoni wakati mwingine alitumia vishazi kama vile “ na hivyo tunaona” ili kusisitiza kweli alizotaka kufundisha. Kwa kusi-sitiza vishazi hivi katika Helamani 3, unaweza kuwatayarisha wanafu-nzi kugundua mafu-nzo ambayo Mormoni alinuia katika sehemu zingine za Kitabu cha Mormoni.

Page 411: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

396

SoMo la 107

• Ni nini Mormoni alitaka tujue kuhusu neno la Mungu? Wape wanafunzi muda wa kutafakari jinsi masomo yao ya maandiko yamewawezesha kupokea baraka kama zile zilizoaidiwa katika Helamani 3:29. Zingatia kuwaita wanafunzi wachache washiriki yale waliyopitia wenyewe.Eleza kuwa yote iliyobaki ya Helamani 3 inasimulia jinsi, baada ya muda wa mafanikio makubwa, kiburi kilienea miongoni mwa Wanefi. Washiriki wengi wanyenyekevu wa Kanisa walipitia mateso kutoka kwa washiriki wengine wa Kanisa ambao walikuwa na kiburi mioyoni mwao. Soma hali zifuatazo kwa sauti. Uliza wanafunzi watafakari siku waliona au wamepitia hali hizo hizo. 1. Msichana amdhiaki msichana mwingine katika kata yake. 2. Mvulana amkejeli mshiriki wa jamii yake kwa kuwa na hamu ya kujibu maswali darasani

au kujitolea kwa ajili ya majukumu ya ukuhani. 3. Kundi la wavulana katika kata wamtenga mvulana mwingine kutoka kwa mazungumzo

yao na shughuli nje ya kanisa. 4. Kundi la wasichana watoa matamshi ya kuumiza kuhusu nguo ambazo wasichana

wengine huvaa. Alika mwanafunzi asome Helamani 3:33–34 kwa sauti. Uliza darasa litambue uhusiano kati ya hali ya Wanefi na hali zilizoelezwa hapo juu. Baada ya wanafunzi kupata muda ya kujibu, uliza maswali yafuatayo: • Kwa nini unafikiri mateso ya washiriki wa Kanisa na washiriki wengine wa Kanisa

ilidhaniwa “uovu mkuu” miongoni mwa Wanefi? • Ni kanuni zipi za injili tunakiuka tunapowatendea vibaya au kutokuwa wema kwa wa-

shiriki wengine wa Kanisa? Tunawezaje kuhimili upendo wetu kwa Watakatifu wenzetu?Alika wanafunzi wasome Helamani 3:35 kimya na watambue jinsi wale wanyenyekevu miongoni mwa Wanefi walikabiliana na kudhulumiwa. • Je, imani ya waliodhulumiwa iliongezeka, ilipunguka, ama ilibaki vivyo hivyo? • Waliodhulumiwa walichukua hatua gani ambayo ilichangia kuongezeka katika imani

yao? (Walifunga na kuomba kila mara, wajitahidi kuwa wanyenyekevu, na kuelekeza mioyo yao kwa Mungu.)

• Licha ya ongezeko katika imani, ni mengine yapi yalisababishwa na vitendo vya Wanefi wanyenyekevu? (Furaha, ukombozi, na usafishaji na utakaso wa mioyo yao.)

Andika yafuatayo ubaoni: Tunapo . . . , imani yetu katika Yesu Kristo itaongezeka, licha ya mateso na majaribu. Uliza wanafunzi wakamilishe kauli hii kulingana na kile walichojifunza kutoka kwa Helamani 3:33–35. Unaweza amua kuwaalika wanafunzi kadhaa washiriki ji-nsi walivyokamilisha kauli. Ingawa majibu ya wanafunzi yanaweza kutofautiana, hakikisha wameeleza ukweli ufuatao: Tunapojitahidi kuishi kwa haki, imani yetu katika Yesu Kristo itaongezeka, licha ya mateso na majaribu. Ili kuwasaidia wanafunzi kuimarisha ufahamu wao wa mafundisho katika aya hizi, unaweza amua kuuliza maswali yafuatayo:• Maombi na kufunga kumekusaidiaje katika wakati wa mateso au majaribu?• Unafikiri inamaanisha nini kutoa moyo wako kwa Mungu?• Kwa nini kutoa moyo wako kwa Mungu ni muhimu katika kuongeza imani yako katika

wakati wa mateso au majaribu?Waulize wanafunzi kama wamewahi kuhisi imani yao kuongezeka walipopitia mateso kwa haki. Alika wanafunzi wachache washiriki yale waliyoyapitia wenyewe. Unaweza pia kutaka kushiriki uzoefu wa kibinafsi.Ili kuwatayarisha wanafunzi kusoma Helamani 4, waalike wasome Helamani 3:36 kimya. Waulize wabainishe hali ya jumla ya Wanefi. (Wanefi walikuwa wanaongezeka katika kiburi, licha ya mfano wa wafuasi wanyenyekevu wa Kristo.)

Helamani 4Kwa sababu ya uovu, Roho wa Bwana ajiondoa kutoka kwa Wanefi, na Walamani wateka nchi zote kusini za WanefiEleza kuwa Helamani 4:4–8 inaelezea kuhusu vita ambavyo Wanefi walipigana dhidi ya wapinzani wa Walamani na Wanefi. Alika mwanafunzi asome mistari hii kwa sauti.

Page 412: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

397

helaMani 3– 4

Uliza darasa lifuatilie pamoja, likitambua ni nchi zipi za Wanefi zilitekwa wakati wa vita hivi.Andika maelekezo yafuatayo ubaoni: (Unaweza amua kufanya hivi kabla ya darasa kuanza.) Alika wanafunzi wayanakili katika madaftari au majarida ya kujifunza maandiko.

Andika vishazi vitatu ambavyo vinaonyesha tabia na vitendo vya Wanefi.Andika vishazi vitatu ambavyo vinaonyesha kile kilichotokea kwa sababu ya matendo haya.

Wagawe wanafunzi katika majozi. Uliza kila jozi lisome Helamani 4:11–13, 23–26 pamoja, likitafuta na kuandika vishazi muhimu kulingana na maelekezo kwenye ubao.Alika makundi machache yaripoti majibu yao. Wanafunzi wanaposhiriki yale waliyoandika, unaweza amua kupendekeza kuwa watie alama kwenye vishazi vifuatavyo katika maa-ndiko yao: "waliwachiliwa wategemee nguvu zao" (Helamani 4:13), "walikuwa wamekuwa walegevu" (Helamani 4:24), na "hivyo walikuwa wamekuwa wanyonge" (Helamani 4:26).Uliza wanafunzi ni kanuni zipi wanaweza kubainisha kutoka mafunzo yao ya Helamani 4. Wasaidie watambue kanuni ifuatao: Kiburi na uovu hututenganisha na Roho wa Bwana na kutuacha kwa nguvu zetu wenyewe. Unaweza amua kuandika kanuni hii ubaoni. Unaweza pia kupendekeza kwamba wanafunzi waiandike katika maandiko yao karibu na Helamani 4:23–24.Ili kuwasaidia wanafunzi waelewe kanuni hii, alika mmoja wao aje mbele ya darasa. Uliza mwanafunzi afikirie kwamba ameitwa kupigana pekee yake katika vita dhidi ya Walamani. Uliza mwanafunzi ni nafasi gani angeweza kuwa nayo dhidi ya jeshi la ukubwa zaidi. Uliza mwanafunzi mwingine aje mbele ya darasa na asimame karibu na mwanafunzi wa kwanza. Uliza mwanafunzi wa kwanza ikiwa kuwa na msaada wa mwanafunzi wa pili ingeweza kuongeza nafasi yake kwa ajili ya ushindi dhidi ya nguvu za adui. (Dhidi ya jeshi la ukubwa zaidi, kuongeza mwanafunzi wa pili hakutaongeza vikubwa nafasi ya ushindi.) Kisha andika Bwana ubaoni. Uliza mwanafunzi wa kwanza:• Unafikiri nafasi yako ya kushinda vita itakuwa vipi Bwana akiwa upande wako?Waulize wanafunzi ni jinsi gani shughuli hii inahusiana na kanuni zilizobainishwa kutoka Helamani 4. Zingatia kuuliza swali lifuatalo:• Katika tukio la Wanefi, kuwachwa kwa nguvu zao wenyewe kulimaanisha kupoteza vita

na nchi. Ni “vita” gani tunaweza kupoteza kama hatuna Roho Mtakatifu kuwa nasi?Waulize wanafunzi watafakari jambo moja wanaweza kufanya ili kudumisha uhusiano wa Roho Mtakatifu katika maisha yao, na wakaribishe walifanye. Shiriki ushuhuda wako juu ya umuhimu wa Roho katika maisha yako.

Tangazo na Habari za UsuliHelamani 3:33–34, 36; 4:12. Athari ya kiburi kwa KanisaMormoni alisema kuwa kiburi hakikuwa sehemu ya Ka-nisa la Bwana lakini kwamba sababu ya utajiri mkubwa, kilianza kuingia katika mioyo za baadhi ya waumini wa Kanisa (ona Helamani 3:33, 36).

Rais Ezra Taft Benson alifundisha:

“Fikiria kuhusu kile kiburi kimetugharimu katika siku zilizopita na kile kinatugharimu sasa katika maisha yetu wenyewe, familia zetu, na Kanisa.

“Fikiria kuhusu toba ambayo ingeweza kutendeka na maisha ikibadilishwa, ndoa kuhifadhiwa, na nyumba kuimarishwa, ikiwa kiburi hakingetuzuia kutubu dha-mbi zetu na kuziacha. (Ona M&M 58:43.)

“Fikiria kuhusu wengi ambao ni waumini wa Kanisa wasioshiriki kikamilifu kwa sababu walikasirishwa na kiburi chao hakiwaruhusu kusamehe au kula kikamilifu katika meza ya Bwana.

“Fikiria kuhusu miongo ya maelfu ya wavulana na wanandoa ambao wangekuwa misheni isipokuwa kwa kiburi kinachowazuia kutoka kujitoa mioyo yao kwa Mungu. (Ona Alma 10:6; Helamani 3:34–35.)

“Fikiria jinsi kazi ya hekalu ingeongezeka kama muda uliotumika katika huduma hii ya kumcha Mungu unga-likuwa muhimu zaidi kuliko shughuli nyingi za kiburi ambazo zinashindana kwa wakati wetu” (“Beware of Pride,” Ensign, Mei 1989, 6).

Page 413: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

398

UtanguliziWanefi waliendelea kuwa waovu hadi wengi wao wakachagua uovu badala ya wema. Nefi na Lehi wa-lijitolea kuhubiri neno la Mungu Baba yao, Helamani, alikuwa amewafundisha kumkumbuka Mwokozi wao na kumfanya awe msingi wa maisha yao. Baada ya

kufundisha Wanefi, Nefi na Lehi waliwahubiria Wala-mani, ambao waliwatupa gerezani. Bwana aliwaokoa kimiujiza, na wengi wa Walamani walitubu na kuo-ngoka kwa ajili ya injili.

SOMO LA 108

helamani 5

Mapendekezo ya Kufundisha

Helamani 5:1–13Helamani awashauri wanawe kushika amri za Mungu, kuhubiri Injili, na kuku-mbuka nguvu za ukombozi wa Yesu KristoKabla ya darasa, tayarisha vishoroba sita vya karatasi ya kuonyesha. Cha kwanza kina-paswa kuwa na jina lako limeandikwa juu yake. Vile tano vingine vinapaswa kuwa na maneno na vifungu vifuatavyo: Wazazi, Upatanisho wa Yesu Kristo, Manabii, Toba huelekeza kwa wokovu, na Tii amri.Mpe kila mwanafunzi kipande cha karatasi. Eleza kwamba utawaonyesha kwa kifupi vishoroba sita vya karatasi vikiwa na maneno yaliyoandikwa juu yao. Kisha wataandika, kutoka kwa kumbukumbu, maneno hayo. Onyesha wanafunzi kishoroba kimoja cha kara-tasi kwa wakati.Waulize wanafunzi waandike maneno wanayokumbuka. Kisha onyeshe vishoroba hivyo sita vya karatasi tena. Uliza:• Je, ilikuwa ni rahisi au vigumu kukumbuka maneno haya na vishazi?• Ni tofauti gani unadhani ilileta kwa kuambiwa mapema kwamba ungehitajika kuku-

mbuka kile kilichokuwa kwenye vishoroba vya karatasi?Uliza mwanafunzi wasome maelezo yafuatayo ya Rais Spencer W. Kimball. Alika darasa lisiki-lizie yale aliyosema juu ya umuhimu wa kukumbuka mafundisho ya injili ambayo tumepokea:

“Unapoangalia katika kamusi ukitafuta neno muhimu zaidi, unajua ni nini? Inaweza kuwa kumbuka. Kwa sababu kila mmoja wenu mmefanya maagano — mnajua kile cha kufanya na jinsi ya kukifanya— haja yetu kubwa ni kukumbuka” (“Circles of Exaltation” [address to CES religious educators, Juni 28, 1968], 5, si. lds. org).Elezea darasa kwamba leo watajifunza kuhusu watu wawili ambao walileta

tofauti katika maisha ya maelfu ya wengine kwa sababu walikumbuka na kutenda kwa ajili ya kweli fulani. Wahimize wanafunzi watafakari wakati wa somo la leo kile wanachofikiri Bwana anawataka wakumbuke.Fupisha Helamani 5:1–4 Elezea kwamba kwa sababu ya uovu wa watu, Nefi alijiuzulu kama mwamuzi mkuu ili yeye na ndugu yake Lehi waweze kujishughulisha kwa kuhubiri neno la Mungu.Andika rejeleo ya maandiko yafuatayo kwenye ubao. (Usijumuishe maneno katika mabano.)

Helamani 5:5–7 (Tii amri;. Kumbuka mifano ya haki ya wahenga)Helamani 5:9–11 (Kumbuka Upatanisho wa Kristo; Kukumbuka kwamba hatuwezi kuokolewa katika dhambi zetu lakini kwamba tunaweza kuokolewa kutokana na dhambi zetu kwa njia ya toba na nguvu ya Upatanisho)Helamani 5:12 (Kumbuka kwamba Yesu Kristo ni lazima awe msingi wetu.)

Alika wanafunzi wapitie kwa juu mistari iliyoorodheshwa kwenye ubao, wakitafuta neno kukumbuka. Unaweza amua upendekeze kwamba watie alama kwa kila tokeo la neno hili.

Fundisha kwa njia ya Roho MtakatifuUnapojiandaa kufu-ndisha, omba kwamba Roho Mtakatifu atakuwa nawe na wanafunzi.

Page 414: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

399

helaMani 5

Kisha wape wanafunzi muda wa dakika chache wasome vifungu hivi kimya, wakitafuta kile Helamani aliwataka wanawe wakumbuke. Alika wanafunzi waripoti walichopata. Unaweza amua kuandika majibu yao kwenye ubao karibu mkabala na andiko rejeo.Ili kuwasaidia wanafunzi kuchambua na kuelewa mistari hii, uliza maswali yafuatayo:• Kukumbuka mifano ya haki ya watu wengine kunawezaje kukusaidia kuchagua “kufa-

nya kile ambacho ni chema”?• Huwa unafanya nini ili kukumbuka Upatanisho wa Yesu Kristo?Andika maelezo yafuatayo ubaoni. Tuki . . . , Shetani hatakuwa na nguvu juu yetu.Alika mwanafunzi asome Helamani 5:12 kwa sauti. Uliza darasa kufuata pamoja, wakita-futa njia wanaweza kukamilisha kauli iliyo ubaoni. Ingawa wanafunzi wanaweza kutumia maneno tofauti, hakikisha kuwa wameeleza kwamba tukijenga msingi wetu juu ya Yesu Kristo, Shetani hatakuwa na nguvu juu yetu. Unaweza amua kuwaalika wanafunzi wa-tie alama kwenye vishazi katika Helamani 5:12 vinavyoelezea kanuni hii. Eleza kuwa He-lamani 5:12 ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Unaweza amua kupendekeza kwamba wanafunzi watie alama ya kipekee kwenye kifungu hiki ili waweze kukipata kwa urahisi.Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa kanuni iliyofundishwa katika mstari huu, jenga mnara mdogo au nyumba ukitumia vifaa (kama vile vitalu au vitabu), na uulize maswali kama haya yafuatayo:• Kwa nini ni muhimu kwamba jengo liwe na msingi imara?• Unafikiri ina maana gani kujenga msingi wetu juu ya Yesu Kristo?• Ni ahadi gani zinazopewa wale ambao hujenga msingi yao juu ya “mwamba wa Mko-

mbozi wetu?”• Tunaweza kufanya nini ili kujenga msingi wetu juu ya mwamba wa Yesu Kristo? (Una-

weza amua uwauliza wanafunzi jinsi kweli zinazofundishwa katika Helamani 5:6–11 ni mifano ya njia tunaweza kujenga msingi wetu juu ya Yesu Kristo.)

Unaweza amua kuhimiza kwamba kujenga juu ya msingi wa Mwokozi si kuzuia masha-mbulizi ya Shetani, lakini kunatupatia nguvu kuyashinda.• Ni lini umeweza kustahimili majaribu au kuvumilia majaribu kwa sababu msingi wako

ulijengwa juu ya Yesu Kristo?Shuhudia juu ya nguvu uliyopokea kwa sababu umejenga msingi wako juu ya mwamba wa Yesu Kristo. Wape wanafunzi muda wa kuandika katika madaftari au majarida ya kujifu-nza maandiko kuhusu njia moja watajitahidi zaidi kujenga msingi yao juu ya mwamba wa Mkombozi wao.

Helamani 5:14–52Bwana awalinda Nefi na Lehi gerezani, na Walamani wengi waongokaFupisha Helamani 5:14–19 kwa kueleza kwamba Nefi na Lehi walihubiri injili kwa nguvu nyingi miongoni mwa Wanefi na Walamani. Kwa sababu ya hayo, wapinzani wengi wa Wa-nefi walirudi katika imani. Kule Zarahemla na maeneo jirani, Walamani 8000 walibatizwa.Nakili chati ifuatayo ubaoni. Gawa darasa katika majozi, na uulize kila jozi linakili chati kwenye kipande cha karatasi. Uliza majozi hayo yashirikiane pamoja ili kusoma vifungu vi-livyoorodheshwa katika chati na kisha wachore picha rahisi au waandike muhtasari mfupi wa kile kila kifungu kinaelezea. (Wanafunzi wanaponakili chati, wahimize waache nafasi ya kutosha chini ya kila rejeo la andiko kwa ajili ya picha zao au muhtasari.)

helamani 5:20–21 helamani 5:22–25 helamani 5:26–28

helamani 5:29–34 helamani 5:35–41 helamani 5:42–44

Baada ya muda wa kutosha, alika wanafunzi waonyeshe kwa ufupi na kuelezea picha zao au muhtasari kwa jozi lingine la wanafunzi. Ili kuwasaidia wanafunzi waimarishe ufasihi wao wa aya hizi, uliza maswali yafuatayo:

Helamani 5:12 ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Rejea wazo la kufundisha mwishoni mwa somo ili kuwasaidia wanafunzi na umahiri wao wa kifungu hiki.

Page 415: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

400

SoMo la 108

• Wakati Walamani walikuwa wamefunikwa na giza, sauti iliwahimiza wafanye nini? (Ona Helamani 5:29, 32.)

• Jinsi gani Helamani 5:30 inaelezea sauti hiyo?• Ni wakati gani umehisi au kusikia mnong’ono wa Sauti ya upole mkamilifu ?• Aminadabu alifundisha ndugu zake kufanya nini ili waepushe giza? (Ona Helamani 5:41.)• Ni nini kilitendeka wakati Walamani walitii ushauri wa Aminadabu na kuweka imani

katika Kristo? (Ona Helamani 5:43–44.)Alika wanafunzi wasome Helamani 5:44–47 kimya, wakitafuta maneno yanayoeleza baadhi ya matokeo ya toba.• Kutoka mistari hii, je, unaweza kujifunza nini kuhusu kutubu? (Wasaidie wanafunzi ku-

bainisha ukweli ufuatao: Tunapoweka imani katika Yesu Kristo na kutubu dhambi zetu, Roho Mtakatifu atajaza mioyo yetu na amani na shangwe.)

Fupisha Helamani 5:48–52 kwa kueleza kwamba wapinzani wa Walamani na Wanefi ambao walipata muujiza huu walienda na kuwahutubia watu, na “sehemu zaidi ya Wala-mani” waliongoka katika Injili.Wahimize wanafunzi wazingatie kama wanahisi amani na furaha katika maisha yao kwa sasa. Kama hawahisi, waalike watafakari kile wanaweza kufanya ili kujenga msingi wao juu ya Yesu Kristo na kufukuza mawingu ya giza kutoka karibu nao.

Umahiri wa Maandiko—Helamani 5:12Alika wanafunzi wasome Helamani 5:12. Ili kuwasaidia wakariri mstari huu,wape karatasi ambayo haijaandikiwa. Wawezeshe kuandika mstari huu kwenye karatasi wakitumia picha na herufi moja. Kwa maneno yanayopendekeza picha (kama vile mwamba, msingi, upepo, mvua ya mawe, na dhoruba), wawezeshe wachore picha rahisi. Kwa maneno yasiyopende-keza picha (kama vile sasa na wangu), wawezeshe waandike herufi ya kwanza ya neno. Alika wanafunzi wafanye mazoezi ya kukariri mstari wakitumia picha peke yake na herufi ambazo wamechora na kuandika. Unaweza pia kuwaalika wabadilishane makaratasi na kukariri kifungu wakitumia vikumbusho ambavyo wanafunzi wenzao wamechora na kua-ndikwa. Wahimize wanafunzi wabebe karatasi zao nyumbani na kuziweka mahali ambapo wataziona mara kwa mara ili waweze kutia bidii katika kukariri kifungu hiki.Kumbuka: Kwa sababu ya urefu wa somo la leo, unaweza amua utumie shughuli hii siku nyingine, ambapo una muda zaidi.

Tangazo na Habari za UsuliHelamani 5:12 Tunawezaje kuustahimili upepo wenye nguvu wa adui?Rais Spencer W. Kimball alifundisha kwamba ni lazima tushike injili ya Yesu Kristo wakati adui anatuma maje-shi yake dhidi yetu:

"Sisi, pia, tunakabiliwa na nguvu kali za uharibifu zinazotumwa na adui. Mawimbi ya dhambi, uovu, ufisadi, uharibifu, ukorofi, hila, njama, na udanganyifu yanatutishia sote. Huja kwa nguvu nyingi na kasi na yatatuangamiza ikiwa sisi si waangalifu.

“Lakini onyo linaenezwa kwa ajili yetu. Inatupasa tuwe waangalifu na tusikize na kutoroka kutokana na maovu kwa ajili ya maisha yetu ya milele. Bila usaidizi hatuwezi kusimama dhidi yake. Lazima tukimbilie

mahali pa usalama au tushikilie kwa dhati kwa kile ambacho kinaweza kutukinga kutokana na kutupiliwa mbali. Kile ambacho ni lazima tushikilie kwa dhati ni injili ya Yesu Kristo. Ndio nguzo yetu kutokana na nguvu yoyote ambao mwovu anaweza kutumia. Nabii aliyeongozwa wa Kitabu cha Mormoni aliwashauri watu wake: 'Kumbukeni kwamba ni juu ya mwamba wa Mkombozi wetu, ambaye ni Kristo, Mwana wa Mu-ngu, kwamba lazima mjenga msingi wenu, kwamba ibilisi atakapotuma mbele pepo zake kali, naam , mi-shale yake kimbungani, wakati mvua yake wa mawe na dhoruba kali itapiga juu yenu, haitakuwa na uwezo juu yenu kuwavuta chini kwenye shimo la taabu na msiba usioisha’ (Hel. 5:12)” (“Hold Fast to the Iron Rod,” Ensign, Nov. 1978, 6).

Page 416: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

401

Mapendekezo ya Kufundisha

Helamani 6Walamani wakawa wenye haki na wapigana dhidi ya wezi wa Gadiantoni, wakati Wanefi waongezeka katika uovu na kusaidia wezi wa GadiantoniChora mchoro ufuatao katikati mwa ubao:

Ushawishi wa Roho Mtakatifu katika maisha yako

Alika wanafunzi wabainishe na kufikiri juu ya mitazamo na vitendo ambavyo huelekeza katika kuongezeka kwa ushawishi wa Roho Mtakatifu katika maisha yao na yale ambavyo huelekeza katika upungufu wa ushawishi wa Roho Mtakatifu.Eleza kwamba Mormoni aliandika kwamba Bwana aliondoa Roho wake kutoka kwa Wanefi na akaanza kumimina Roho wake juu ya Walamani (ona Helamani 6:35–36). Wa-kumbushe wanafunzi kwamba Wanefi walikuwa “wadhaifu, kwa sababu ya makosa yao” (Helamani 4:26). “Roho wa Bwana hakuwahifadhi” (Helamani 4:24), na walikuwa “wanaji-tayarisha kwa maangamizo” (Helamani 5:2).Alika mwanafunzi asome Helamani 6:2 kwa sauti. Uliza darasa lifuate pamoja, likitafuta vitendo na mitazamo ambayo ingeweza kusababisha Wanefi kuendelea “[kuiva] kwa maangamizi ya milele” (Helamani 6:40). Wanafunzi wanaporipoti kile walichopata, weze-sha mwanafunzi kuandika majibu yao kwenye nusu ya chini ya ubao, chini au karibu na mshale unaoangalia chini. (Unaweza amua kueleza kwamba neno wasiotubu inamaanani-sha wasiotubu na wasio na majuto.)Wakumbushe wanafunzi kwamba kwa sababu ya juhudi za umisionari za Nefi na Lehi katika mwaka uliopita, maelfu ya Walamani kule Zarahemla walibatizwa, na wengi wa Walamani katika nchi ya Nephi waliongoka katika injili (ona Helamani 5:19–20, 50–51). Uliza mwanafunzi asome Helamani 6:1, 3–5 kwa sauti. Alika darasa lifuate pamoja, waki-tafuta vitendo na tabia ambazo zilisababisha Walamani kufurahia ushawishi zaidi wa Roho. Wanafunzi wanaporipoti kile wanachopata, uliza mwanafunzi aandike majibu yao kwenye nusu ya juu ya ubao, juu au karibu na mshale unaoangalia juu.• Inamaanisha nini kwako kuwa imara na thabiti katika imani? (Ona Helamani 6:1.)• Watu wa Kanisa walipokea uongofu wa Walamani kwa njia gani ? (Unaweza amua kuhi-

miza kwamba kushiriki injili na kushiriki na Watakatifu kunaweza kuleta furaha kubwa, hata wakati tumezungukwa na uovu.)

Fupisha Helamani 6:7–14 kwa kueleza kwamba kwa takriban miaka mitatu, Wanefi na Walamani walifurahia amani. Viwanda na biashara ilivyoongezeka baina yao, wote wawili walistawi. Kisha, katika mwaka wa 66 wa utawala wa waamuzi, waamuzi wawili wakuu waliuwawa. Alika mwanafunzi asome Helamani 6:16–17 kwa sauti. Uliza darasa lifuate pamoja, likitafuta mitazamo na vitendo ambavyo vilisababisha Roho kuondoka kutoka

UtanguliziKufuatia jitihada za umisionari za Nefi na Lehi, Wala-mani waliongezeka katika wema. Hata hivyo, Wanefi wakawa waovu na kuanza kusaidia wezi wa Gadia-ntoni, na Roho wa Bwana akaondoka kutoka kwao.

Nefi alitoa unabii kwamba ikiwa Wanefi wataendelea kuishi katika uovu, wangeangamia. Alitoa unabii pia kwamba kwa sababu ya wema wa Walamani, Bwana angewahurumia na kuwalinda.

SOMO LA 109

helamani 6–7

Page 417: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

402

SoMo la 109

Wanefi. Wanafunzi wanaporipoti kile walichopata, uliza mwanafunzi aandike majibu yao kwenye nusu ya chini ya ubao, chini au karibu na mshale unaoangalia chini.Shiriki kweli zifuatazo na wanafunzi wako:Moyo ni muhimu kwa maisha yetu ya kimwili. Hupiga damu kupitia miili yetu ili oksijeni na virutubisho vingine viweze kufikia seli zetu zote. Karibu ukubwa wa ngumi, moyo was-tani wa watu wazima hupiga galoni 2,000 (lita 7,570) ya damu kila siku. Hupiga takriban mara 70 kwa dakika, au pigo 100,000 kwa siku.• Kujua asili muhimu ya moyo wako wa kimwili, ungekuwa tayari kufanya nini ili kutunza

afya yake?Andika marejeo ya maandiko yafuatayo ubaoni: Helamani 6:17, 21, 26, 28–31. Himiza kwamba kila mstari katika rejeleo hili inatumia neno moyo au mioyo, ikirejea mioyo yetu ya kiroho. Wape wanafunzi muda wa kusoma mistari hii na kutafakari majibu ya maswali ya-fuatayo. (Ili kuokoa muda, andika maswali haya ubaoni kabla ya darasa au yaandae kama kitini cha wanafunzi kuirejea wanaposoma mistari iliyoorodheshwa ubaoni.)

Kwa nini unafikiri Shetani anatamani mioyo ya watoto wa Mungu?Wanefi walifanya nini ili kumwezesha Shetani ashike mioyo yao? (Ona Helamani 6:17.)Ni nini kinachotokea kwa mtu ambaye moyo wake unashawishiwa au kudhibitiwa na Shetani? (Ona Helamani 6:21, 28, 30–31.)

Alika wanafunzi wachache wajibu maswali. Kisha alika mwanafunzi asome kwa sauti ma-elezo yafuatayo na Rais Boyd K. Packer wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili. Uliza darasa lisikilize kwa makini ili kubaini njia Shetani hujaribu kupanda majaribu katika mioyo yetu.

“Kunaweza kuwa na ufunuo bandia, ushawishi kutoka kwa shetani, majaribu! Ila tu unapoishi, kwa njia moja an nyingine adui atajaribu kukupotosha. . . ."Ukiwahi pokea ushawishi kufanya kitu ambacho kinakufanya kujisikia kutotulia, kitu unajua katika akili yako kuwa ni makosa na ni kinyume na kanuni za haki, wala usiutii!" (“Personal Revelation: The Gift, the Test, and the Promise,” Ensign, Nov. 1994, 61).

Ongeza kusikiliza na kukubali majaribu katika orodha kwenye nusu ya chini ya ubao. Alika wanafunzi wachache wachukue zamu kusoma kwa sauti kutoka Helamani 6:20–21, 37–38. Uliza darasa lifuate pamoja, likitafuta njia tofauti Walamani na Wanefi walichukulia usha-wishi wa wezi wa Gadiantoni.Waeleze wanafunzi kwamba baada ya Mormoni kuandika kilichowafanyikia Wanefi na Wa-lamani, alihimiza mafunzo tunayoweza kujifunza kutokana na yale waliyopitia wenyewe. Andika kauli ifuatayo isiyokamilifu ubaoni:

Wanefi walipoteza Roho kwa sababu . . .Bwana alimwaga Roho Wake kwa Walamani kwa sababu . . .

Alika wanafunzi wasome Helamani 6:34–36, wakitafuta taarifa ambayo itawasaidia kuka-milisha kauli iliyo ubaoni.• Kutokana na yale umesome katika mistari hii, unaweza kamilisha vipi kauli iliyo ubaoni?

(Unaweza amua kukamilisha kauli ubaoni ukitumia majibu ya wanafunzi.)• Mistari hii inafundisha nini juu ya kile tunaweza kufanya ili Roho kuwa pamoja nasi?

(Ingawa wanafunzi wanaweza kutoa majibu kadhaa, hakikisha kuwa wanaeleza kwa-mba tunapoamini na kutii maneno ya Bwana, atamimina Roho Wake juu yetu. Wanafunzi wanapaswa pia waeleze kwamba tunapomruhusu Shetani ateke mioyo yetu, Roho wa Bwana atatuwacha.)

Elekeza nadhari ya wanafunzi kwa orodha walioandika juu na chini ya mishale ubaoni. Eleza kuwa vitendo na mitazamo iliyo juu ya nusu ya ubao inawakilisha nia ya kuamini na kutii maneno ya Bwana, wakati vitendo na mitazamo iliyo nusu ya chini ya ubao inawakili-sha uovu na ungumu wa moyo.• Unafanya nini ili kukaribisha kwa bidii ushawishi wa Roho Mtakatifu katika maisha yako

na kuweka ushawishi wa Shetani nje ya moyo wako?• Ni jinsi gani kufanya moja ya vitendo vilivyo kwenye nusu ya juu ya ubao kumekusai-

diwa kukaribisha Roho Mtakatifu maishani mwako? (Unaweza pia kuwauliza wanafunzi watafakari iwapo wamefanya vitendo vyovyote au kuwa na mitazamo iliyotajwa kwenye

Page 418: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

403

helaMani 6 –7

nusu ya chini ya ubao na kuzingatia jinsi vilisababisha upungufu wa ushawishi wa Roho maishani mwao.)

Uliza wanafunzi waandike kwenye madaftari au majarida ya kujifunza maandiko jambo moja watafanya ili kukaribisha Roho wa Bwana katika maisha yao. Wahimize wao wateke-leze malengo yao.

Helamani 7Nefi awahubiria Wanefi waovu na awaamuru watubuKwa kila moja ya maswali yafuatayo,waalike wanafunzi watumie maandiko yao ili kupata majibu haraka wawezavyo. Waeleze wasimame wapatapojibu. Alika mtu wa kwanza asima-maye ajibu kila swali. Kisha alika wanafunzi wakae chini kabla ya kusoma swali lifuatalo.• Kulingana na Helamani 7:1, jina la nabii ambaye alirejea kutoka nchi kaskazini lilikuwa?• Ni kishazi gani katika Helamani 7:2 kinachoeleza kile Nefi alifundisha umati wa watu

katika nchi upande wa kaskazini?• Kulingana na Helamani 7:3, kwa nini Nefi aliondoka nchi ya kaskazini?• Kulingana na Helamani 7:4, nani alikuwa katika kiti cha hukumu wakati Nefi alirudi

Zarahemla?Alika mwanafunzi asome Helamani 7:5 kwa sauti, na kisha uliza darasa libainishe jinsi wezi wa Gadianton waliwatawala watu.Fupisha Helamani 7:6–12 kwa kueleza kwamba Nefi alipoona hali ya watu wake, moyo wake ulifura kwa huzuni (Helamani 7:6). Akapanda juu ya mnara katika bustani yake ili kuomba na kuomboleza uovu wa watu. Watu waliposikia akisali na kuomboleza, umati wa watu ulikusanyika ili kujua ni kwa nini alikuwa na huzuni hivyo. Alitumia fursa hio kuwafundisha.Alika wanafunzi wasome Helamani 7:15–16 kimya.• Kwa nini Nefi alisema watu “wanapaswa kustaajabu”?• Shetani anatafuta nini?Alika wanafunzi watue na kutafakari juu ya taswira Nefi alitumia. Baada ya Shetani kuteka mioyo ya watu, kisha hutaka kuvuta nafsi zao chini hadi katika mateso ya milele.• Kwa nini unafikiri Nefi aliwaonya watu kuhusu nia ya Shetani? Ni nini Nefi alitaka

waepuke?Alika wanafunzi wachache wachukue zamu kusoma kwa sauti Helamani 7:17–22, 26–28. Alika nusu ya darasa libainishe dhambi za Wanefi, na uliza ile nusu ingine ya darasa libai-nishe madhara Nefi alionya yatakuja ikiwa watu hawatatubu.Nusu ya kwanza ya darasa inaporipoti walichopata, eleza mifanano na yale yaliyoandikwa juu ya nusu ya chini ya ubao. Nusu ya pili ya darasa inaporipoti, uliza maswali yafuatayo:• Ni maneno gani katika Helamani 7:22 yanaonyesha kitu ambacho Bwana huzia kutoka

kwa wale wanaokataa kutubu? (Unaweza amua kupendekeza kwamba wanafunzi watie alama kishazi hiki katika maandiko yao.)

• Kulingana na Helamani 7:28, ni nini hufanyika watu wanapokataa kutubu? (Wataanga-mia. Unaweza kueleza kwamba katika hali ya Wanefi, kukataa kutubu kwao kulimaani-sha wangeangamia kimwili na kiroho.)

Andika ukweli ufuatao ubaoni: tukikataa kutubu dhambi zetu, tutapoteza ulinzi wa Mungu na baraka ya uzima wa milele .Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa kanuni hii,waalike waeleze madhara ambayo yanaweza kuja kwa watu katika hali zifuatazo: (1) kijana anakataa kutubu kutawaliwa kwake na ponografia; (2) msichana ambaye kipaumbele chake cha juu zaidi ni kujulikana na kuwa na umaarufu, licha ya kufundishwa tofauti na wazazi wake; (3) Ingawa amesikiliza mafundisho ya manabii kusoma maandiko na kuomba, mvulana , anakataa kufanya yoyote kati ya hayo.Alika wanafunzi watafakari njia wanaweza kuhitaji kutubu. Wahimize watubu ili waweze daima kuwa na nguvu za Bwana na ulinzi katika maisha yao.

Page 419: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

404

UtanguliziBaada Nefi kutangaza kwamba watu lazima watubu au waangamizwe, waamuzi waovu walichochea watu wengi dhidi yake. Baadhi ya watu walimtetea kwa ujasiri. Nefi alifundisha kwamba watu waliokanusha ushahidi wake pia walikanusha shuhuda za manabii

wote waliokuja kabla yake, wote ambao walikuwa wameshuhudia juu ya Yesu Kristo. Kama ushuhuda kwamba alikuwa nabii, Nefi alifunua kuwa mwamuzi mkuu alikuwa ameuawa. Maneno ya Nefi yalipohakiki-shwa, baadhi ya watu walimkubali kuwa nabii.

SOMO LA 110

helamani 8–9

Mapendekezo ya Kufundisha

Helamani 8:1–10Waamuzi wafisadi wajaribu kuwachochea watu dhidi ya Nefi• Ni baadhi gani ya shawishi zinazojaribu kukushawishi usiamini maneno ya manabii?Wanafunzi wanapojadili swali hili, uliza mwanafunzi aandike majibu yao ubaoni. Alika wa-nafunzi watafute umaizi kuhusu kile wanachopaswa kufanya wanapokabiliana na shawishi kama zile watakazosoma kuhusu katika Helamani 8 leo.Wakumbushe wanafunzi kwamba Nefi alitoa ujumbe wa toba kwa ujasiri kwa watu wake (ona Helaman 7). Alika wanafunzi kadhaa wachukue zamu kusoma kwa sauti kutoka He-lamani 8:1–6. Uliza darasa lifuate pamoja, likitambua jinsi waamuzi walichukulia mafundi-sho ya Nefi. Unaweza amua kueleza kuwa baadhi ya waamuzi walikuwa sehemu ya genge la siri la Gadiantoni.• Ujumbe wa waamuzi kwa watu ulikuwa nini? (Walijaribu kuwashawishi watu wam-

kasirikie Nefi.)• Kulingana na Helamani 8:4, kwa nini waamuzi hawangemwaadhibu Nefi?Uliza wanafunzi wafikirie kuhusu kile wangefanya ikiwa mtu angejaribu kuwashawishi wapuuze maneno ya manabii.Wajulishe wanafunzi kuwa baadhi ya watu walipinga mawazo ya waamuzi. Alika mwa-nafunzi asome Helamani 8:7–9 kwa sauti. Himiza kwamba, kama baadhi ya watu katika umati, tunaweza kupaza sauti zetu kumtetea nabii, hata wakati si kitu kinachope-ndelewa kufanywa.• Je, kumekuwepo wakati katika maisha yako umeongea kutetea nabii aliye hai, ingawa

mafundisho yake yamekuwa si ya kupendelewa? Ni jinsi gani jambo hili lilileta tofauti katika maisha yako? Liliwavutia watu wengine jinsi gani?

Uliza wanafunzi wasome Helamani 8:10 kimya ili kujua jinsi maneno ya watu hawa yalileta tofauti.• Ilileta tofauti gani wakati baadhi ya watu walimuunga mkono nabii? Kwa nini unafikiri

ni muhimu kwetu kufanya hivi siku ya leo?Alika mwanafunzi asome kauli ifuatayo ya Mzee M. Russell Ballard wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili:

“Tunahitaji kukumbuka kauli ya Edmund Burke: ‘Kitu muhimu tu kinachohi-tajika ili uovu ushinde ni kwa watu wema kutofanya chochote.’ [Husishwa katika John Bartlett, comp., Familiar Quotations, 15th ed. (1980), ix.] Tunahi-taji kupaza sauti zetu na raia wengine wahusika duniani kote katika upinzani wa mitindo ya sasa. Tunahitaji kuwaambia wadhamini wa vyombo vya habari vya kukera kwamba tumechoshwa. Tunahitaji kusaidia mipango na bidhaa

ambazo ni nzuri na za kuinua. Kujiunga pamoja na majirani na marafiki ambao wanashi-riki matatizo yetu, tunaweza kutuma ujumbe wa wazi kwa wale wanaohusika" (“Let Our Voices Be Heard,” Ensign ama Liahona, Nov. 2003, 18).

Page 420: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

405

helaMani 8 – 9

• Tunawezaje kupinga mvuto ambao unajaribu kutushawishi dhidi ya maneno ya manabii?• Je, ni baadhi ya njia gani sahihi kuongea dhidi ya mvuto wa maovu na katika kuunga

mkono maneno ya manabii?Alika wanafunzi waongee kuhusu wakati wao au mtu wanayemjua alipinga mvuto kama huo.

Helamani 8:11–24Helamani anafundisha kwamba manabii wote hushuhudia juu ya Yesu KristoAlika mwanafunzi asome Helamani 8:13 kwa sauti. Uliza darasa lifuate pamoja na lita-mbua kile Nefi alisema watu walikikana. Waonyeshe wanafunzi picha ya Musa an Nyoka wa Shaba (62202; Gospel Art Book [2009], no. 16). Waulize wasome Helamani 8:14–15 na watambue kile Musa alifundisha kuhusu Mwokozi• Ni baadhi ya njia zipi mtu anaweza “kumtegemea Mwana wa Mungu kwa imani”? • Kuwa na “Roho iliovunjika” kama ilivyoelezwa katika Helamani 8:15, ni kuwa mnyenye-

kevu, mwenye toba, na mpokevu wa matakwa ya Bwana. Kwa nini tabia hii ni muhimu tunapomtegemea Mwokozi?

• Kujua utume wa Mwokozi kunawezaje tusaidia kushinda uovu?Alika wanafunzi waseme upya fundisho kutoka Helamani 8:15, wakitumia maneno yao wenyewe. Kwa mfano,wanaweza kusema tukizingatia juu ya Yesu Kristo na kuweka imani Kwake, tutapokea uzima wa milele. Alika mwanafunzi asome Helamani 8:16 kwa sauti. Uliza darasa lifuate pamoja, likibaini-sha wengine ambao wamefundisha ujumbe ulioelezwa katika Helamani 8:15. Kisha uliza wanafunzi wapekue kwa upesi Helamani 8:17–22 wakitafuta majina ya manabii wengine ambao walishuhudia kuhusu Kristo. Alika wanafunzi watafakari shuhuda nyingi juu ya Yesu Kristo ambazo wamesoma au kusikia kutoka kwa manadbii wa kale na manabii wa siku za mwisho.Eleza kuwa watu wengi walimkataa Nefi na ujumbe wake. Alika wanafunzi wasome Helamani 8:24–26 na wabainishe matokeo yaliyowakumba Wanefi kwa sababu walikataa shuhuda za manabii.• Kwa nini unadhani kuwa wale ambao mara kwa mara hukana ukweli na kuaasi dhidi ya

Mungu hukumbana na madhara makali vile?• Ni wakati gani ujumbe wa nabii umekusaidia kumgeukia Bwana?Alika wanafunzi wazingatie jinsi wanaweza kuimarika katika juhudi zao za kumgeukia Mwokozi. Wahimize waweke lengo katika njia moja wataweza kuwa bora wiki ijayo.

Helamani 8:25–9:41Nefi anafunua kuwa mwamuzi mkuu ameuawaFupisha Helamani 8:25–28 kwa kueleza kuwa kama thibitisho kwamba watu walikuwa katika hali ya dhambi na kuwa Nefi alinena neno la Mungu, Nefi alifunua kuwa mwamuzi mkuu alikuwa ameuliwa. Gawa darasa katika majozi. Alika kila jozi lifikirie kuwa wao ni wapelelezi katika kesi kudhibitisha ni nani aliyemuuwa mwamuzi mkuu. Andika maswali yafuatayo ubaoni au yaweke katika kitini kwa ajili ya kila jozi.

Siku ya Kwanza ya Upelelezi: 1. Wakati watu watano walipochunguza madai ya Nefi, walipata nini? Ni kwa nini walia-

nguka ardhini? (Ona Helamani 9:1–5). 2. Watu walidhani ni akina nani waliokuwa wauaji? (Ona Helamani 9:7–9.)

Siku ya Pili ya Upelelezi: 3. Ni nani aliyeachwa huru? (Ona Helamani 9:10–13, 18.) 4. Ni nani aliyestakiwa? (Ona Helamani 9:16–17, 19.) 5. Nefi alishiriki habari gani ya ziada? (Ona Helamani 9:25–36.) 6. Nani alikuwa muuaji? (Ona Helamani 9:37–38.)

Alika majozi yapate majibu ya swali la 1 na la 2 Wakati wamekuwa na muda wa kutosha, uliza:

Wape wanafunzi muda wa kutafakariUliza maswali yaliyo-undwa kwa makini ili kusisimua wazo. Baadhi ya maswali yanaweza kuhitaji wanafunzi wa-chukue muda wa kutafa-kari kabla wajibu. Katika hali kama hizo, unaweza kusema, “Tafadhali chu-kua muda kufikiria juu ya majibu yako, kisha nitauliza nipate majibu.”

Page 421: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

406

SoMo la 110

• Wakati wanaume watano walipogundua mwamuzi mkuu aliyeuliwa, waliamini nini? Walihofia nini? (Ona Helamani 9:5.)

Alika majozi yajibu maswali yote mengine ili kukamilisha upelelezi wao. Kisha uliza:• Kulingana na Nefi, Siantumi angesema nini baada ya kukiri hatia yake? (Ona Helamani 9:36.)• Kulingana na Helamani 9:39–41, kwa nini baadhi ya watu walimwamini Nefi?Alika wanafunzi wafupishe kile walichojifunza kutoka Helamani 9 kuhusu maneno ya manabii. Wanafunzi wanaweza kueleza fikra nyingi tofauti, lakini hakikisha wamebainisha kanuni zifuatazo: Maneno ya manabii yatatimizwa. Ili kutilia mkazo ukweli huu, una-weza amua kuwawezesha wanafunzi wasome Mafundisho na Maagano 1:37–38.• Ni matukio gani ambayo yameimarisha ushuhuda wako kuwa tunao manabii wa kweli

duniani leo?Tamatisha na ushuhuda wako kuwa maneno ya manabii yatatimizwa.

Tangazo na Habari za UsuliHelamani 8:14–15. “ Nyoka wa shaba”Nefi alipozungumuzia juu ya Musa akiinua "nyoka wa shaba,” alirejea wakati watoto wa Israeli walikuwa wakikabiliwa na “nyoka za moto”(ona Hesabu 21:6–9; zingatia kuwa neno shaba linamaanisha shaba). Mwa-nzo wa shida ya Waisraeli ulikuwa kwamba walikuwa wamezungumza maovu juu ya Mungu na manabii Wake (ona Hesabu21:5). Wale waliotazama nyoka wa shaba waliponywa, na wale waliochagua kutotazama waliangamia (ona Hesabu 21:9; 1 Nefi 17:41).

Kama hao Waisraeli, watu wengi katika siku za Nefi walizungumza kwa kupinga Mungu na nabii Wake. Nefi aliporejelea tukio la nyoka wa shaba, alihimiza kuwa watu wake “wataangalia juu kwa Mwana wa Mungu na imani” na kuishi (Helamani 8:15; ona pia Yohana 3:14–15, ambako Yesu Kristo Mwenyewe alirejea nyoka wa shaba kama ishara ya Usulubisho Wake). Nefi kisha aliwakumbusha watu kuwa manabii wote walikuwa wameshuhudia Kristo (Ona Helamani 8:16–23).

Mapendekezo ya Ziada ya KufundishaHelamani 7–9. Onyesho la VideoBadala ya kutumia shughuli ya upelelezi katika somo hili, unaweza amua kuonyesha onyesho la video

linaloitwa “The Pride Cycle” ambalo ni onyesho la tukio katika Helamani 7–9 na aya chache za kwanza katika Helamani 10. Onyesho linapatikana katika Book of Mormon DVD Presentations 1–19 (54011) na LDS. org.

Page 422: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

407

Somo la Mafunzo ya NyumbaniHelamani 1–9 (Kitengo cha 22)

Vifaa vya Matayarisho kwa Mwalimu wa Mafunzo ya NyumbaniMuhtasari wa Masomo ya Mafunzo ya Kila Siku ya Nyumbani Muhtasari ufuatao wa mafundisho na kanuni wanafunzi wamejifunza waliposoma Helamani 1–9 (kitengo cha 22) haudhamiriwi kufunzwa kama sehemu ya somo lako. Somo unalofundisha linazingatia tu mafundisho na kanuni chache ya hizi. Fuata ushawishi wa Roho Mtakatifu unapozingatia mahitaji ya wanafunzi.

Siku ya 1 (Helamani 1–2)Wanafunzi walipojifunza ubishi wa kisiasa na mauaji miongoni mwa Wanefi na kutekwa kwa jiji la Zarahemla na Walamani, walijifunza kuwa ubishi hutenganisha na hutuweka katika hatari ya kushindwa na uvutio wa adui. Walijifunza pia kuwa makundi ya siri yanaweza kuelekeza katika maangamizo ya jamii.

Siku ya 2 (Helamani 3–4)Kwa kujifunza jinsi wafuasi Wanefi wanyenyekevu wa Mwokozi walivumilia mateso mengi, wanafunzi walijifunza kwamba licha ya mateso na majaribu, imani yetu katika Yesu Kristo inaweza kuongezeka tunapomwita Mungu kwa unyenyekevu na kutoa mioyo yetu Kwake. Wanafunzi walipojifunza jinsi kiburi cha Wanefi kilichoongezeka kiliwa-ruhusu Walamani kupata nusu ya nchi ya Wanefi, walijifunza kwamba kiburi na uovu hututenga na Roho wa Bwana na kutuacha kwa nguvu zetu wenyewe.

Siku ya 3 (Helamani 5)Kwa kujifunza ushauri aliotoa Helamani kwa wanawe Nefi na Lehi, wanafunzi walijifunza kwamba tukijenga msingi wetu juu ya Yesu Kristo, Shetani hatakuwa na nguvu juu yetu. Kupitia nguvu za Mungu na imani na juhudi za umisi-onari za Nefi na Lehi, Walamani wengi walitubu. Wanafunzi walijifunza kwamba tunapoweka imani katika Yesu Kristo na kutubu dhambi zetu, Roho Mtakatifu huijaza mioyo yetu na amani na shangwe.

Siku ya 4 (Helamani 6–9)Wanafunzi walijifunza kwamba tunapoamini na kutii maneno ya Bwana, atamimina Roho Wake juu yetu. Nefi aliwaonya Wanefi waovu juu ya matokeo ya uovu wao na akasisitiza kuwa tukikataa kutubu dhambi zetu, tutapo-teza ulinzi wa Mungu na baraka za uzima ya milele. Baada ya kusikiliza maneno ya Nefi, baadhi ya watu walimuu-nga mkono Wanafunzi walijifunza kuwa tukikana uovu, tunaweza kuuzuia kuenea. Nefi aliwakumbusha watu kuwa manabii wengi walitabiri kuhusu Mwokozi na kufundisha kwamba tunapolengea Yesu Kristo na kuweka imani Kwake, tutapokea uzima wa milele. Kutoka kwa mafundisho ya Nefi katika Helamani 7–9, wanafunzi walijifunza kuwa maneno ya manabii yatatekelezwa.

UtanguliziMiongoni mwa uvumi na uovu uliokuwa ukiongezeka, Nefi ali-wafundisha wanawe kuwa msingi wa imani yao inapaswa kuwa Yesu Kristo. Mafunzo ya Nefi kuhusu toba na kusikiliza maneno ya manabii wa Bwana yalikuwa muhimu kwa ajili ya furaha ya watu.

Mapendekezo ya Kufundisha

Helamani 1–5Wanefi washindwa kwa sababu ya ubishi na uovu; Walamani wengi waongoka wakati Nefi na Lehi wanapohubiri injiliUliza wanafunzi wazingatie ni kwa nini baadhi ya majengo husi-mama kwa muda mrefu inhali mengine hubomoka. Kisha uliza: Kwa nini ni muhimu kwa jengo kuwa na msingi dhabiti?

Alika mwanafunzi asome Helamani 5:12–30 kwa sauti. Kwa vile hii ni mstari wa umahiri wa maandiko, alika mwanafunzi ajaribu kuukariri. Wahimize wajaribu hata ikiwa huenda hawajaukariri kikamilifu. Kisha uliza maswali yafuatayo:

• Ni nini kinachoahidiwa katika mistari hii tukijenga maisha yetu katika msingi wa Yesu Kristo? (Majibu ya wanafunzi yanapa-swa kuelezea kuwa tukijenga msingi wetu juu ya Yesu Kristo, Shetani hatakuwa na nguvu juu yetu.)

• Umefanya nini ili kujenga maisha yako kwenye msingi wa Yesu Kristo?

Page 423: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

408

SoMo la MafUnzo ya nyUMbani

Alika wanafunzi wasimulie kuhusu nyakati ambapo shuhuda zao juu ya Mwokozi ziliwasaidia kustahimili majaribu au kuvumi-lia majaribio. Shiriki ushuhuda wako juu ya uwezo wa kiroho uliopokea kwa sababu umejenga maisha yako kwenye msingi wa Yesu Kristo. Himiza wanafunzi wafikirie juu ya njia moja au zaidi ambazo watafanya wawezalo ili kujenga maisha yao vyema zaidi kwenye mwamba wa Kristo

Helamani 6–7Walamani wanakuwa wema zaidi wakati Wanefi wakuwa waovu zaidi; Nefi awahubiria Wanefi waovu na kuwaamuru watubuWakumbushe wanafunzi kuwa wakati Walamani wengi walitubu na kuwa imara katika injili, Wanefi waliishi katika uovu na Roho Mtakatifu aliondoka kutoka kwao. Waulize wanafunzi wafikire kuhusu wakati maishani mwao ambapo walihisi Roho akiondoka kutoka kwao kwa sababu ya chaguo zao.

Elezea kuwa wakati Nefi alipoona hali ya watu wake, “moyo wake ulifura kwa huzuni” (Helamani 7:6). Alipanda juu ya mnara katika bustani yake ili kuomba na kuomboleza uovu wa watu. Umati wa watu ulimzingira, na Nefi alitumia fursa hiyo kuwafundisha.

Alika mwanafunzi aje mbele ya darasa kumwakilisha Nefi katika mnara. Uliza mwanafunzi asome Helamani 7:15–22, 26–28 kwa sauti, darasa linapofuatilia. Kabla asome, gawa darasa kwa nusu mbili. Uliza nusu moja itafute kile Nefi alifundisha kuwa dhambi za Wanefi, na uliza nusu ingine itambue matokeo ambayo Nefi alishuhudia kuwa yangekuja ikiwa Wanefi hawangetubu. Kisha uliza wanafunzi waripoti kile walichopata.

Baada ya wanafunzi kujibu, waalike waeleze kanuni ambazo tunaweza kujifunza kutoka kwa tukio hili. Wanafunzi wana-weza kushiriki kanuni tofauti, lakini wanapaswa kueleza kuwa ikiwa tutakataa kutubu dhambi zetu, tutapoteza ulinzi wa Bwana na baraka za uzima wa milele.

Ili kuwasaidia wanafunzi waelewe kanuni hii, waalike wae-leze matokeo yanayoweza kuwajia watu katika hali zifuatazo: (1) Mvulana anakataa kutubu kutawaliwa kwake na ponogra-fia. 2) Msichana ambaye kipaumbele chake cha juu zaidi ni kujulikana na kuwa na umaarufu, licha ya kufundishwa tofauti na wazazi wake. (3) Mvulana amesikiliza mafundisho ya manabii kusoma maandiko na kuomba, lakini anakataa kufanya yoyote kati ya hayo.

Alika wanafunzi watafakari kama kuna chochote ambacho wa-nahitaji kutubu ili waweza kuwa na nguvu za Bwana kikamilifu maishani mwao.

Helamani 8Nefi afundisha kuwa kila nabii hushuhudia kuhusu Yesu KristoAndika maneno kubali na kana ubaoni. Uliza wanafunzi waeleze tofauti kati ya haya maneno mawili. Alika mwanafunzi asome Helamani 8:13 darasa linapobainisha kile Nefi alisema kuwa watu walikana. Unaweza amua kuwahimiza wanafunzi watie alama kile walichogundua.

Onyesha wanafunzi picha ya Musa na Nyoka ya Shaba (62202; Gospel Art Book [2009], no. 16). Waalike wasome Helamani 8:14–15 na wabainishe kile Musa alifundisha kuhusu Mwokozi. Waalike waripoti kile walichojifunza. Kisha uliza:

• Ni baadhi njia gani mtu anaweza kumtegemea Mwokozi kwa imani?

• Inamaanisha nini kuwa na “roho iliyopondeka?” (Kuwa mnye-nyekevu, mwenye toba, na mpokevu wa matakwa ya Bwana) Kwa nini sifa hii ni muhimu tunapomtegemea Mwokozi?

• Kujua kuhusu Upatanisho wa Mwokozi kunawezaje kutusai-dia kushinda uovu na kutubu tunapotenda dhambi?

Alika wanafunzi waeleze kanuni tunayojifunza kutoka kwa mistari hii. Wanafunzi wanaweza kutumia maneno tofauti, lakini wanapaswa waeleze kuwa tukimzingatia Yesu Kristo na kuweka imani Kwake, tutapokea uzima wa milele.

Alika mwanafunzi asome Helamani 8:16 kwa sauti, na uliza da-rasa libainishe ni nani mwingine aliyefundisha kuhusu utume wa Mwokozi. Wawezeshe wanafunzi wapekue kwa upesi Helamani 8:17–22 majina ya manabii wengine walioshuhudia kuhusu Yesu Kristo. Alika wanafunzi wafikirie kuhusu jinsi manabii katika nyakati za kale, na pia katika siku zetu, wametoa ushuhuda wa huduma na dhabihu ya upatanisho ya Mwokozi.

Alika wanafunzi washiriki shuhuda zao kuhusu kile ambacho Upatanisho wa Mwokozi unamaanisha maishani mwao. Una-weza pia kushiriki ushuhuda wako.

Kitengo kifuatacho (Helamani 10–16)Uliza wanafaunzi wafikirie kuwa Bwana amewaahidi atafanya chochote watakachomwomba Yeye afanye. Nefi alikuwa mwa-minifu sana hadi Bwana akampa ahadi hii na kumpa nguvu ya kufunganisha. Himiza wanafunzi wasome Helamani 10–11 wiki hii, wakitafuta njia Nefi alitumia nguvu alizopewa na Bwana ili kusaidia watu wake. Pia waalike watafute ni ishara ngapi za ku-zaliwa na kufa kwa Yesu Kristo wanaweza kutambua wanapoji-funza unabii wa Samueli Mlamani katika Helamani 13–16.

Page 424: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

409

UtanguliziJaribio la kubainisha ni nani aliyemuua mwamuzi mkuu liliisha wakati ufunuo wa Nefi kuhusu mauaji ulipodhi-bitishwa. Akiwa ameepuka mateso kutoka kwa madai ya uongo ambayo yalikuwa yameelekezwa kwake, Nefi alianza kutembea kwenda nyumbani. Alitafakari yale ambayo Bwana alikuwa amemuonyesha, akiwa anahisi

huzuni kwa sababu ya uovu wa watu. Katika muda huo wa kutafakari na huzuni, aliisikia sauti ya Bwana. Bwana alimbariki na nguvu ya kufunganisha na aka-muamuru aendele kuhubiri toba kwa watu. Nefi mara moja akatii amri ya Bwana

SOMO LA 111

helamani 10

Mapendekezo ya Kufundisha

Helamani 10:1–11Nefi apokea nguvu ya kufunganishaKumbusha wanafunzi kuhusu ufunuo wa Nefi juu ya mauaji ya mwamuzi mkuu, yaliyore-kodiwa katika Helamani 8–9. Alika wanafunzi wajifikirie kuwa katika nafasi ya Nefi, punde tu baada ya kufunua ni nani aliyemuua mwamuzi mkuu.• Ungejisikia vipi? Ungetazamia wengine wafanye nini?• Ungetaka kuwaambia watu nini?• Ungehisi vipi ikiwa watu wangekupuuza na kukuwacha peke yako?Eleza kuwa baada ya kuwachiliwa kwa ajili ya mauaji ya mwamuzi mkuu, Nefi alianza mwendo kurudi nyumbani. Alika mwanafunzi asome Helamani 10:1–3 kwa sauti, na uliza darasa litafute kile Nefi alifanya alipokuwa akitembea kwenda nyumbani. Unaweza amua kupendekeza kuwa wanafunzi watie alama neno kutafakari mahali ambapo linajitokeza katika mistari hii. • Ni kwa nini Nefi alikuwa “amehuzunika”?• Ni nini kilichotokea Nefi alipokuwa akitafakari? (Sauti ya Bwana ilimjia) Kuna uhusiano

gani kati ya kutafakari na kupokea ufunuo?Wanafunzi wanapojibu, wasaidie kutambua kanuni ifuatayo: Kutafakari mambo ya Bwana kunatutayarisha kupokea ufunuo. Unaweza amua kuandika kanuni hii ubaoni.Uliza wanafunzi kama wanaweza kufikiria juu ya matukio katika maandiko ama historia ya Kanisa ambapo watu walipokea ufunuo kama matokeo ya kutafakari mambo ya Bwana. Mifano inajumuisha Nefi mwanawe Lehi, ambaye alipokea ono baada ya kutamani kuona vitu ambavyo babake aliviona na “akiwa anawaza moyoni mwake” [ona 1 Nefi 10:17; 11:1]; Joseph Smith ambaye Ono lake la Kwanza lilikuja baada yake “kuwazia tena na tena” kwenye Yakobo 1:5 [ona Joseph Smith—Historia 1:11–17]; na Joseph F. Smith, ambaye alipokea ono la uokovu wa wafu baada ya kutafakari na kuwazia maneno ya Bwana [ona M&M 138:1–6, 11].)• Ni wakati gani kutafakari kumekusaidia kupokea ufunuo wa kibinafsi? (Unaweza

amua kutaja kuwa kupokea ufunuo wa kibinafsi huwa si tukio kubwa la ajabu kama vile baadhi ya mifano katika maandiko. Matukio ya ufunuo huwa mara nyingi ni muda wa ufahamu wa ghafla, kama vile tunapoelewa kwa ghafla jambo ambalo tumesumbu-liwa nalo hapo awali)

• Ni zipi baadhi ya nyakati na hali ambapo kutafakari mambo ya Bwana kungestahili ka-bisa. (Mifano ya nyakati hizo inajumuisha wakati wa mkutano wa sakramenti na baada ya mkutano huo, kabla na baada ya maombi ya kibinafsi na kujifunza maandiko, baada ya kutazama au kusikiliza mkutano mkuu, tunapofunga, tunaposhiriki hekaluni, na tunapomtukuza Bwana siku ya Sabato.)

Himiza wanafunzi watenge muda wa kutafakari mara kwa mara. Pendekeza kuwa waa-ndike hisia wanazopata wanapotafakari.

Mazingira ya darasaniMazingira yanayofaa ya kujifunza injili hukuza hisia za upendo, he-shima, staha na amani. Ni mahali pa utaratibu, pa kuchangia hisia ya azma. Mzee Boyd K. Packer alifunza kwamba “ushawishi huja kwa urahisi katika mazingira ya amani,” na kwamba “staha hualika ufunuo” (“Reverence Invites Revelation,” Ensign, Nov. 1991, 21–22).

Page 425: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

410

SoMo la 111

Ili kuwatayarisha wanafunzi waendele kujifunza tukio hili katika maisha ya Nefi, waalike wafikirie kuwa majirani wao wataenda kwa muda na wanahitaji mtu wa kuchunga nyumba yao na mali yao.• Ni mtu wa aina gani mnafikiri majirani wenu wangetaka wachunge nyumba yao?• Mnawezaje kuoonyesha majirani wenu kuwa mko tayari kukabithiwa jukumu kama hilo?Uliza wanafunzi wasome Helamani 10:4–5 kimya, wakitafuta ni kwa nini Bwana alimkabi-thi Nefi baraka kuu na majukumu. (Unaweza kuhitajika kuelezea kuwa kutosita inamaani-sha bila kuchoka ama bidii) Alika wanafunzi waripoti kile walichopata.• Ni jinsi gani huduma ya kutosita kunaonyesha kuwa Bwana anaweza kutukabithi baraka

na majukumu?• Ni vipi kufauta mfano wa Nefi wa kutowaogopa watu kunaweza kututayarisha kwa ajili

ya majukumu katika ufalme wa Bwana?• Kishazi “hujatazamia maisha yako” kinamaanisha nini kwako?Andika ifuatavyo ubaoni: Bwana hutukabithi baraka na majukumu tunapo .... Uliza wana-funzi jinsi wangekamilisha kauli hii, kulingana na kile walichojifunza kuhusu Nefi katika Helamani 10:4–5. Njia moja wanafunzi wanaweza kukamilisha kauli hii ni kama ifuatavyo: Bwana hutukabithi baraka na majukumu tunapoweka matakwa Yake mbele ya yetu wenyewe. Unaweza amua kupendekeza kwamba wanafunzi waandike ukweli huu katika maandiko yao ama kwenye madaftari ama majarida ya kujifunza maandiko.Alika wanafunzi watafakari maswali yafuatayo na waandike majibu yao ya mmoja yao:• Umefanya nini maishani mwako hivi karibuni ili kuonyesha Bwana kuwa matakwa Yake

ni muhimu zaidi kuliko yako mwenyewe?• Ni sehemu gani moja maishani mwako unaweza kutafuta matakwa ya Bwana vyema zaidi?Shuhudia upendeleo wa Bwana kutukabithi baraka kuu na kuu sana tunapotafuta mata-kwa Yake na kutii amri Zake.Alika wanafunzi wasome Helamani 10:5–7 kimya, wakitafuta baraka na majukumu Bwana alimpa Nefi Wanafunzi wanaposoma, andika yafuatayo ubaoni:

Aya ya 5Aya ya 6Aya ya 7

Alika wanafunzi wachache waandike ubaoni, kando ya nambari ya aya inayolingana, ba-raka Bwana alimpa Nefi.Himiza kuwa moja ya baraka Bwana alimpa Nefi ilikuwa nguvu ya kufunganisha. Kisha andika ukweli ufuatayo ubaoni: nguvu ya kuunganisha inafunga na kufungua duniani na mbinguni. Unaweza amua kupendekeza kuwa wanafunzi waandike ukweli huu katika maandiko yao kando ya Helamani 10:7.Uliza wanafunzi kama wanajua kuhusu wengine ila Nefi ambao wamepewa nguvu ya ku-funganisha. Baada ya wanafunzi kujibu, unaweza kuwaalika warejee mtambuko Helamani 10:7 na maandiko yafuatayo: 1 Wafalme 17:1 (Eliya); Mathayo 16:15–19 (Petro); Mafundi-sho na Maagano 132:46 (Joseph Smith).Eleza kuwa funguo za nguvu hiyo hiyo zimeshikiliwa leo na Rais wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Kama Nefi, Marais wa Kanisa wamehudumu bila kusita na kuonyesha kuwa Bwana anaweza kuwakabithi baraka na majukumu makuu. Sisi mara nyingi hurejea nguvu ya kufunganisha kwa uhusiano na kufunganishwa kwa familia kupi-tia ibada za hekalu.Ili kuwasaidia wanafunzi waelewe zaidi nguvu ya kufunganisha, alika mwanafunzi asome kauli ifuatayo ya Mzee Russell M. Nelson wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawaili:

“Hekalu, ibada, maagano, endaumenti, na kufunganishwa zimerejeshwa, kama vile ilivyotabiriwa. Ibada za hekalu zinatoa fursa ya upatanisho na Bwana na huunganisha familia pamoja milele. Utiifu kwa maagano mataka-tifu yanayofanywa katika hekalu kunatuhitimisha kwa ajili ya uzima wa milele— karama kuu ya Mungu kwa binadamu” (“Prepare for the Blessings of the Temple,” Ensign, Oct. 2010, 42).

Page 426: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

411

helaMani 10

• Umebarikiwa kwa njia gani na maarifa kuwa familia zinaweza kuwa pamoja milele?• Unaweza kutafuta baraka za nguvu ya kufunganisha kwa njia gani katika siku zijazo?

(Majibu yanaweza kujumuisha kuwa wanafunzi wanaweza kujitayarisha kwa ajili ya ndoa hekaluni na kuwa wanaweza kufanya kazi ya hekalu na historia ya familia sasa ambayo itawawezesha kuunganishwa na mababu zao walioaga.

Shiriki hisia zako kuhusu baraka za nguvu ya kuunganisha na umuhimu wa kupokea ibada za kuunganisha hekaluni.

Helamani 10:12–19Nefi atii amri ya Bwana kuwahubiria watu tobaUliza wanafunzi kama wamewahi chelewa kufanya jambo walioulizwa wafanye (Mifano inaweza kujumuisha kuchelewa kutekeleza kazi za nyumbani ama kazi shuleni ama kazini.)• Ni ujumbe upi tunaweza kutuma kwa wengine tunapochelewa kufanya kile wanacho-

tuuliza tufanye?Alika mwanafunzi asome Helamani 10:11–12 kwa sauti. Uliza darasa lifuate, likitafuta jinsi Nefi alishughulika; Bwana alipomwamuru kuwahubiria watu toba.• Tunamuonyesha nini Bwana tunapoitikia kwa haraka kwa ajili ya ushauri na amri Zake?Alika mwanafunzi asome Helamani 10:13–14 kwa sauti. Kisha uliza mwanafunzi mwi-ngine asome Helamani 10:15–17 kwa sauti.• Mfano wa Nefi katika aya hizi unatufunza nini?• Bwana alimsaidia Nefi vipi?Wasaidie wanafunzi kuona kwamba kwa sababu ya uaminifu wa Nefi, Bwana alimlinda na kumbariki na nguvu ya ajabu. Nefi alikuwa amejitahidi kutekeleza huduma ambayo Bwana alikuwa amempa.• Unawezaje kuonyesha jitihada yako kumtumikia Bwana?Himiza wanafunzi watafute njia za kuweka matakwa ya Bwana mbele ya yao wenyewe na kutii kwa haraka. Shuhudia juu ya baraka zinazokuja tunapomtii Bwana.

Marejeo ya Umahiri wa MaandikoUrefu wa somo hili unaweza kuruhusu muda wa shughuli ifuatayo ya kurejea umahiri wa maandiko.Patia kila mwanafunzi jukumu asome mojawapo wa aya za umahiri wa maandiko ifuatayo kimya: 1 Nefi 3:7; 2 Nefi 2:27; 2 Nefi 31:19–20; Mosia 2:17. Uliza wanafunzi wasome kifu-ngu walichopewa na wazingatie jinsi kinahusiana na Nefi na huduma yake kama ilivyoa-ndikwa katika Helamani 10. Baada ya muda wa kutosha, alika wanafunzi wachache wajibu.

Page 427: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

412

Mapendekezo ya Kufundisha

Helamani 11Wanefi wapitia mzunguko wa nyakati za haki na uovu.Nakili mchoro ufuatao kwenye ubao. Eleza kuwa mchoro huu unasimamia kile ambacho mara mingi huitwa mfuatano wa kiburi

Uliza wanafunzi wazingatie kile wangeandika kwa ajili ya jambo la msingi la nne la mfu-atano. Waruhusu wanafunzi wajadiliane majibu yamkini. Baada ya mjadala kiasi, andika Unyenyekevu na Toba kando ya nambari 4 kwenye mchoro. Eleza kuwa shughuli ifuatayo ya maandiko itaonyesha jinsi watu katika Kitabu cha Mormoni walipitia mfuatano huu. Eleza kuwa mfuatano huu huonekana mara nyingi katika jamii kubwa, lakini inaweza kuakisia kielelezo katika maisha ya familia na watu binafsi.Kumbusha wanafunzi kuwa hata baada ya Nefi kuwaambia watu kuhusu kifo cha mwa-muzi wao mkuu, “walishupaza mioyo yao na hawakutii maneno ya Bwana” (Helamani 10:13). Mwishoni mwa mwaka wa 71 wa utawala wa waamuzi, watu walikuwa “wamega-wanyika dhidi yao wenyewe na wakaanza kuuana na upanga (Helamani 10:18).• Wakati huu, mnafikiri Wanefi hawa walikuwa katika sehemu gani ya mfuatano huu wa

kiburi?Kabla ya darasa, nakili chati ifuatayo ubaoni. Usijumuishe majibu ya italiki katika safu ya tatu na nne. Kama inawezekana, tengeneza nakala ya chati kama kitini ya kila mwana-funzi. Kama hii haiwezekani, waulize wanakili chati kwenye madaftari ama majarida ya kujifunza maandiko.Panga jinsi ya kukamilisha chati kwa kufanya laini ya kwanza pamoja kama darasa. Alika mwanafunzi asome Helamani 11:1–2 kwa sauti. Uliza darasa litoe muhtasari mfupi wa hali ya watu kama ilivyoelezwa katika mistari hii. Andika majibu yao ubaoni. Kisha uliza wa-nafunzi wabainishe; watu walikuwa katika kipindi ama vipindi vipi vya mfuatano. Andika majibu yao kwenye chatiWanafunzi wanapoelewa jinsi ya kukamilisha chati, wape muda wa kufanya hivyo. Una-weza kuwauliza wafanye kazi kibinafsi, katika majozi ama vikundi vidogo, ama pamoja kama darasa.

1. Wema na Ustawi

2. Kiburi na Uovu

3. Mateso na Maangamizo

4.

Kupanga mtindo wa shughuli za maandikoUnapotayarisha kuwa-wezesha wanafunzi wakamilishe shughuli ya maandiko, amua kiwango cha ugumu cha shughuli na uwezo wa wanafunzi wako. Katika hali chache, unaweza amua kupanga sehemu ya shughuli wewe mwenyewe ili wana-funzi waweze kuona kile watahitaji kufanya watakapokamilisha kazi peke yao.

UtanguliziMilango ya 11 na 12 katika kitabu cha Helamani inajumuisha miaka 14 ya historia ya Wanefi ambapo watu walipitia mzunguko wa nyakati za haki na uovu.

Historia hii inaonyesha jinsi watu humsahau Bwana kwa haraka na jinsi Yeye huwarudi ili kuwasaidia kutubu na kurudi Kwake.

SOMO LA 112

helamani 11–12

Page 428: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

413

helaMani 11–12

Miaka ya utawala ya waamuzi

Mistari katika helamani 11

Maelezo ya hali ya watu vipindi katika mfuatano

miaka 72–73 1–2 Ubishi na vita vyaongezeka, na genge la siri la wezi laendeleza kazi ya maangamizo

2, 3

miaka 73–75 3–6 Kwa sababu ya ombi la Nefi kwake Bwana, baa la njaa lina kuja balada ya vita, na maelfu waanza kuangamizwa na njaa.

2, 3

Miaka 75 7–11 Watu waanza kumkumbuka Bwana na kuji-nyenyekeza wenyewe, na kufukuza genge la Gadiantoni miongoni mwao.

3, 4

miaka 76 17–20 Watu wafurahia na kumtukuza Mungu. Wa-nakuwa wema, na kuanza kufanikiwa tena.

4, 1

miaka 77–79 21–23 Ustawi na amani yarejeshwa. Ubishi uko kwa kiwango cha chini, na zinatatuliwa na ufunuo na mafundisho ya injili.

1

miaka 80 24–26 Watu wakuwa wenye kiburi, kukasirika na waovu tena. Genge ovu la wezi laanzishwa tena miongoni mwa watu, na mauwaji yao na mipango ya siri.

2, 3

miaka 80–81 27–35 Wezi wasababisha vurumai na maanga-mizo, na majeshi ya Wanefi na Walamani yashindwa kulimaliza genge ovu. Wezi waua watu wengi na kuwateka nyara baadhi ya watu, ikiwa ni pamoja na akina mama na watoto, nyikani. Majaribio yawaelekeza watu kumkumbuka Bwana.

3, 4

Baada ya wanafunzi kuwa na wakati wa kukamilisha chati, waulize waripoti kile walichoji-funza kutokana na shughuli hii. Kisha uliza maswali yafuatayo:• Kulingana na, Helamani 11:4, kwa nini Nefi aliomba kuwe na baa la njaa? (Alitarajia

kuwa baa la njaa lingewaelekeza watu wamkumbuke Bwana na kutubu.)• Watu wangefanya nini ili kuepuka awamu ya “mateso na maangamizo” ya mfuatano?Wanafunzi wanaweza kutoa majibu mengi mazuri ya swali hili. Hakikisha wametambua kanuni ifuatayo: Kupitia unyenyekevu na toba, tunaweza kuepuka kiburi na maa-ngamizo. Eleza kuwa Wanefi wangeruka kipindi cha pili na tatu cha mfuatano. Wangeishi kwa wema na unyenyekevu daima, wakitubu bila kuchelewa wanapotenda dhambi. Ikiwa wangeishi hivi, bado wangepitia majaribio kadhaa, lakini hawangehitaji kuvumilia mateso makali na maagamizo yaliyokuja kwa sababu ya uovu wao.Alika mwanafunzi asome Helamani 11:36–37 kwa sauti. Uliza darasa lifuate pamoja, waki-sikiza mabadiliko yaliyotokea katika muda mfupi.• Iliwachukuwa Wanefi muda gani baada ya kumkumbuka Bwana “kuiva tena kwa maa-

ngamizo”? (Miaka Minne)• Ni kipindi gani ya mfuatano kinaelezwa mwishoni mwa Helamani 11?Uliza wanafunzi wabainishe na kufikiria kuhusu wakati maalum ambapo wameona mfuatano huu kwa kiwango fulani maishani mwao wenyewe ama maishani mwa watu ambao wao wanawajua. Waalike watafakari kile wanaweza kufanya ili kuepuka kipindi cha pili na tatu cha mfuataano. Wahimize wanadike mawazo ya kipekee wanayopokea wanapotafakari.

Page 429: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

414

SoMo la 112

Helamani 12Mormoni aeleza ni kwa nini Bwana huwarudi watuAndika yafuatayo ubaoni: “Na hivyo tunaweza kuona . . .” Eleza kuwa Mormoni alitumia kishazi hiki kuashiria masomo ya kujifunza kutoka kwa matokeo aliyoandika.• Kulingana na Helamani 11, unaweza kukamilisha kauli hii vipi?Alika mwanafunzi asome Helamani 12:1 kwa sauti, na uliza darasa litafute jinsi Mormoni aliikamilisha kauli.• Kishazi “kutoaminika kwa mioyo ya watoto wa binadamu” kinamaanisha nini kwako?• Ni nini kinachosaidia moyo wako kubaki imara katika kujitolea kwa Bwana?Uliza wanafunzi wasome Helamani 12:2–3 kimya, wakitafuta masomo ambayo Moroni alitaka tujifunze kutoka kwa historia ya Wanefi. Kumbusha wanafunzi kuwa Mormoni kwa mara nyingi alitumia vishazi kama vile “tunaweza kuona” (mstari wa 2) na “hivyo tunaona” (mstari wa 3) aliposhiriki kweli ambazo tunaweza kujifunza kutoka kwa matokeo katika maandiko.• Kwa maneno yako mwenyewe, ni masomo yapi Mormoni alitaka tujifunze? (Wana-

funzi wanaweza kutoa majibu kama yafuatayo: Ikiwa hatuko makini, ustawi wetu unaweza kutuelekeza kumsahau Bwana; Bwana hurudi watu Wake ili kuwaa-musha katika kumkumbuka Yeye.)

• Kwa nini unafikiri kuwa watu waliofanikiwa saa zingine humsahau Bwana?• Kwa nini unafikiria watu saa zingine wanahitaji kurudiwa kabla wamkumbuke Bwana?

(Unaweza kuhitajika kueleza kuwa neno rudi linamaanisha kurekebisha mtu kupitia adhabu ama mateso ya aina fulani.

Uliza wanafunzi watafakari maswali yafuatayo:• Bwana anaweza kuturudi kwa njia gani siku hizi?Ili kuwasaidia wanafunzi wajibu maswali haya, soma kauli ifuatayo na Mzee D. Todd Christofferson wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili:“Kurudi kiungu kuna madhumuni angalau matatu: (1) kutushawishi kutubu, (2) kutusafi-sha na kututakasa, na (3) wakati mwingine kurekebisha mwelekeo wetu maishani kwa ile Mungu anajua ni njia bora zaidi” (“As Many as I Love, I Rebuke and Chasten,” Ensign au Liahona, Mei 2011, 98).• Rudi ya Bwana ni ushahidi wa upendo Wake kwa njia gani?Alika mwanafunzi asome Helamani 12:4–6 kwa sauti. Uliza darasa lifuate, likitafuta mitazamo ambayo hufanya iwe vigumu kwa watu kumkumbuke Mungu. Alika wanafunzi washiriki kile wamepata.Eleza kuwa Mormoni aliwaelezea watu wanaokataa kumwacha Bwana awe kiongozi wao kama “hafifu kuliko mavumbi ya dunia” (Helamani 12:7). Alika mwanafunzi asome Hela-mani 12:7–8 kwa sauti.• Ni kwa nini watu kama hao wanafikiriwa kuwa “hafifu kuliko mavumbi ya dunia”? (Wa-

sadie wanafunzi waelewe kuwa Moroni hakuwa anafundisha kuwa watu wana thamani ndogo kwa Baba wa Mbinguni kuliko mavumbi ya dunia. Ila, alikuwa anavutia mawazo kwa ukweli kuwa vumbi daima hutii amri ya Mungu, lakini watu mara nyingi huwa hawatii.)

Fupisha Helamani 12:9–22 kwa kutaja kuwa katika mistari hii Mormoni anatukumbusha kuhusu nguvu kuu ya Bwana — kuwa Bwana anaweza kuamuru vipengele vya kimwili vi-songe ama vibadilike na kuwa anaweza kumfanya mtenda dhambi atupiliwe mbali kutoka kwa uwepo Wake. Alika wanafunzi wasome Helamani 12:23–26, wakitafuta ushahidi una-oonyesha kuwa tuna thamani ya juu kuliko vumbi ya dunia. Unaweza amua upendekeze kuwa wanafunzi watie alama kwa maneno na vishazi ambavyo ni muhimu kwao.• Ni kipawa gani kinachopatikana kwa ajili yetu tunapotubu na kutii sauti ya Bwana?• Huu ni ushahidi kwa njia gani wa thamani yetu kwa Mungu?Andika kauli zifuatazo zisizokamilika ubaoni. Alika wanafunzi waandike hitimisho kwa somo la leo kwa kukamilisha kauli zifuatazo katika madaftari ama majarida ya kujifunza maandiko.

Na hivyo ninaona katika Helamani 11–12 kuwa . . .Hivyo basi nita . . .

Shuhudia kuwa tunapomkumbuka Bwana, na kutii sauti Yake, na kutubu, tunaonyesha unyenyekevu wetu na imani katika Yeye. Hatimaye, Yeye huweka ahadi Yake kutubariki na kutustawisha, mwishowe akitupa uzima wa milele

Page 430: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

415

SOMO LA 113

helamani 13UtanguliziMiaka michache kabla ya kuzaliwa kwa Mwokozi, Bwana alituma nabii Mlamani aliyeitwa Samweli kuhubiri toba kwa Wanefi. Aliwahubiria Wanefi kule Zarahemla habari njema ya wokovu kupitia Upatanisho

wa Yesu Kristo. Pia aliwakabili kuhusu kukataa kwao manabii na tabia yao ya kutaka furaha katika uovu. Aliwaonya kuhusu maangamizo ambayo yangewajia ikiwa hawangetubu.

Mapendekezo ya Kufundisha

Helamani 13Samweli awaonya Wanefi juu ya maangamizo yao ikiwa hawatatubuKabla ya darasa, tayarisha kitini kinachopatikana mwishoni mwa somo hili. Unaweza amua kukata kitini katika theluthi, ukiwa na kazi moja ya kikundi kwenye kila kipande cha karatasi. Pia kabla ya darasa, nakili muhtasari ufuatao wa Helamani 13 ubaoni

Helamani 13:1–4. Bwana amwita Samweli Mlamani awahubirie Wanefi.Helamani 13:5–23. Samweli awaonya Wanefi juu ya maangamizo ambayo yatawajia ikiwa

hawatatubu.Helamani 13:24–39. Samweli awaonya watu juu ya matokeo ya kuwakataa manabii na

kukataa kutubu.Anzisha somo kwa kuonyesha picha ya Samweli Mlamani Ukutani (62370; Gospel Art Book [2009], no. 81). Uliza wanafunzi ikiwa wanajua ni kwa nini Wanefi walitaka kumuua Samweli. Baada ya wanafunzi kujibu, eleza kuwa Helamani 13–16 ina maelezo ya nabii Sa-mweli, Mlamani. Maelezo haya ni ya kipekee kwa sababu kwa mara ya pekee katika Kitabu cha Mormoni tunajifunza kuhusu nabii Mlamani akiwaita Wanefi watubu. Wakati huu, Walamani walikuwa wema zaidi ya Wanefi. Rejea muhtasari ubaoni ili kuwapa wanafunzi maelezo mafupi ya juu ya Helamani 13.Gawa darasa katika vikundi vitatu. (Ikiwa inawezekana, kila kikundi kinapaswa kiwe na idadi sawa ya wanafunzi.) Patia kila mwanafunzi nakala ya kazi ya kikundi chake (inayo-patikana mwishoni mwa somo). Waambie wanafunzi watajifunza sehemu ya Helamani 13 kibinafsi na kisha wafundishane kile walichojifunza. Uliza kila mwanafunzi ajitayarishe kufundisha kanuni kutoka kwa kifungu cha maandiko alichopewa na kutayarisha majibu kwa ajili ya maswali yanayoambatana. Wape wanafunzi chaguo la kuandika majibu yao. (Shughuli hii itaruhusu kila mwanafunzi ashiriki na itatoa mazingira ya salama ambapo wanafunzi wanaweza kushiriki hisia, mawazo na shuhuda zao pamoja na wengine.)Baada ya wanafunzi kuwa na muda wa kutosha kujifunza binafsi, wapange wafanye kazi katika vikundi vya wanafunzi watatu. Ikiwa inawezekana, kila kikundi kinapaswa kiwe na mwanafunzi mmoja aliyesoma Helamani 13:1–7, 11, mwengine aliyesoma Helamani 13:17–23, na aliyesoma Helamani 13:24–33. Ruhusu muda wa kutosha kwa kila mwanafu-nzi kushiriki majibu yake na washiriki wengine wa kikundi . Wakati wa majadiliano mafupi ya kikundi, tembea darasani na uchunguze majibu ya wanafunzi. Kama ifaavyo, changia mawazo yako kwenye majadaliano unayosikiliza.Wanafunzi wakishakuwa na muda wa kufundishana, alika wachache wao kushiriki na darasa zima ukweli ama umaizi ambao wamejifunza kutoka kwa mwanafunzi mwingine wakati wa shughuli hii.Fupisha Helamani 13:9–14 kwa kueleza kuwa Wanefi wangeangamizwa kwa miaka 400 (ona Helamani 13:9–10), na sababu ya pekee ya kuwa hawakuwa wameangamizwa tayari ilikuwa kwamba watu wema waliishi miongoni mwao bado (ona Helamani 13:13–14 ) Shuhudia kuwa Samweli alitumwa kwa Wanefi na Bwana, na alizungumza kile ambacho Bwana aliweka moyoni mwake alipowaalika Wanefi watubu na wamrudie Bwana (ona Helamani 13:11).

Ruhusu wanafunzi waeleze walichojifunza kutoka kwa kila mmojaKupitia nguvu ya Roho Mtakatifu, maneno na maelezo ya wanafunzi yanaweza kuwa na matokeo ya maana kwe-nye mioyo na akili za wenzao. Unapowauliza waeleze kweli walizoji-funza kutoka kila moja, unawasaidia kukuza mazingira ya upendo, heshima na umoja.

Page 431: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

416

SoMo la 113

Alika mwanafunzi asome Helamani 13:27–28 kwa sauti. Uliza darasa lifuate, likitafuta jinsi Wanefi walikuwa wamewachukulia manabii waongo.• Kulingana na Samweli, Wanefi waliwachukulia vipi wale waliofundisha uongo? Unafikiri

ni kwa nini wengine walikubali ushauri wake na wengine waliukataa?• Kauli na mitazamo tunayosoma kuhusu katika Helamani 13:27 iko dhahiri kwa njia gani

katika siku zetu?Uliza mwanafunzi asome kwa sauti kauli ifuatayo ya Rais Ezra Taft Benson.“Jinsi tunavyochukulia maneno ya nabii aliye hai anapotuambia kile tunapaswa kujua, lakini hatungependa kusikia, ni jaribio la uaminifu wetu” (“Fourteen Fundamentals in Following the Prophet” [BYU devotional address, Feb. 26, 1980], 3–4, speeches. byu. edu).• Ni ushauri gani kutoka kwa manabii ambao unaweze kuwa mgumu kwa baadhi ya

watu kufuata leo?• Ni mfano gani wa ushauri wa kinabii umechagua kufuata? Umebarikiwa jinsi gani kwa

sababu umefuata ushauri huu?Alika wanafunzi waandike katika madaftari ama majarida ya kujifunza maandiko kuhusu njia moja wanaweza kufanya bora zaidi katika kufuata ushauri wa manabii walio hai.Wanafunzi wakishapata muda wa kutosha wa kuandika, uliza mwanafunzi asome Hela-mani 13:33–37 kwa sauti. Uliza darasa lifuate, likitafuta ni nini Wanefi wasiotubu hati-maye wangepitia na kile wangesema kujihusu. Kisha alika mwanafunzi mwengine asome Helamani 13:38 kwa sauti. Uliza darasa litafute ukweli wa kuhuzunisha ambao Samweli alitangaza kuhusu vizazi vijavyo vya Wanefi.• Samweli alitangaza ukweli gani wa kuhuzunisha kuhusu vizazi vijavyo vya Wanefi?• Unafikiri Samweli alimaanisha nini aliposema kuwa “siku (zao) za majaribio zimepita”?

(Vizazi vijavyo vya Wanefi vingeahirisha kutubu kwao hadi ingekuwa imechelewa kwao kutubu. Na kwa sababu hawangetubu, dhambi zao zingepelekea maangamizo yao.)

• Ni nini mbaya na kutaka “furaha kwa kufanya uovu”? (Saidia wanafunzi waone kuwa furaha ya kweli huja tu tunapotii amri za Mungu.)

• Ni baadhi gani ya njia ambazo watu hutafuta kupata furaha kwa kufanya uovu?Kumbusha wanafunzi juu ya matokeo mengine katika Kitabu cha Mormoni ambapo watu binafsi waliendelea katika uasi na maovu hadi mioyo yao ikawa migumu hata kwa ushawi-shi wa Roho Mtakatifu. (Mifano inajumuisha Lamani na Lamueli, waliokuwa “wamekufa ganzi” [1 Nefi 17:45] na kukataa kumsikiliza Mungu, na Mfalme Nuhu na watu wake, wa-liokataa kutubu licha ya maonyo ya nabii Abinadi.) Samweli alisisitiza kuwa kukataa kwa Wanefi kutubu kungepelekea kwa maangamizo ya watu wao katika vizazi vijavyo.Saidia wanafunzi wafahamu kuwa, kwa kiwango cha binafsi, kuna tumanini kwa wote ambao watachagua kutubu. Kupitia toba, tunaweza kupokea msamaha wa Bwana na kuzuia mioyo yetu kuwa migumu. Ili kuwasaidia wanafunzi waelewe kuwa tunaweza kurekebisha mkondo wetu kupitia toba, soma kauli ifuatayo ya Rais Dieter F. Uchtdorf wa Urais wa Kwanza:“Nilipokuwa nikijifunza kuwa rubani wa ndege, ilinibidi nijifunze jinsi ya kuendesha ndege kwa masafa marefu. Safari kwa ndege juu ya bahari kuu, kupitia majangwa maku-bwa, na kupitia mabara kunahitaji kujipanga kwa makini ili kuhakikisha kufika salama mwishoni mwa safari. Baadhi ya hizi safari kwa ndege bila kusimama zinaweza kuchukua masaa 14 na kuwa na umbali wa takriban maili 9,000.“Huwa kuna hatua fulani ya maamuzi muhimu wakati wa safari kama hizo ndefu za ndege inayojulikana kwa kawaida kama hatua ya kurudi kwa salama. Hadi mahali hapa ndege ina mafuta ya kutosha kupinduka na kurudi salama kwa uwanja wa ndege ilipotoka. Akiwa amepita hatua hii ya kurudi salama, rubani amepoteza chaguo hili na ni lazima aendelee mbele. Ndiposa hatua hii inajulikana kwa kawaida kama hatua ya kutorudi“. . . Shetani anataka tufikirie kuwa tunapotenda dhambi tumepita “hatua ya kutorudi” — kuwa tumechelewa kubadilisha mkondo wetu. . . .“. . . Ili kutufanya tupoteze tumanini, tujihisi kuhuzunika kama yeye, na kuamini kuwa tumepita kusamehewa, Shetani anaweza hata kutumia vibaya maneno kutoka kwa maa-ndiko yanayohimiza haki ya Mungu, ili kudokeza kuwa hakuna huruma. . . .“Kristo alikuja kutuokoa. Ikiwa tumechukua njia isiyo sahihi, Upatanisho wa Yesu Kristo unaweza kutupatia hakikisho kuwa dhambi si hatua ya kutorudi. Kurudi salama

Page 432: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

417

helaMani 13

kunawezekana ikiwa tutafuata mpango wa Mungu kwa ajili ya wokovu wetu (“Point of Safe Return,” Ensign ama Liahona, Mei 2007, 99).• Maneno ya Rais Uchtdorf yanawezaje kumpa matumaini mtu aliyetenda dhambi?Himiza wanafunzi watafakari kweli walizojadili. Wahimize wafuatilie ushawishi wowote ambao wamepokea kutoka kwa Roho Mtakatifu. Shuhudia kuwa furaha itawajia wale ambao wanazingatia mwaliko wa Bwana na kutubu.Tazama: Tayarisha kitini kifuatacho cha vikundi vitatu vilivyoelezewa hapo awali katika somo.

Kikundi cha 1—Helamani 13:1–7, 11Manabii huongea ujumbe Mungu ameweka mioyoni mwao. 1. Mistari gani unahisi inafundisha ukweli huu? 2. Ni ujumbe gani Mungu aliweka katika moyo wa Samweli? 3. Kwa nini unafikiria ingekuwa vigumu kwa Samweli kutoa ujumbe huu? 4. Samweli alitumaini ujumbe huu ungekuwa na athari gani kwa Wanefi? 5. Lini umehisi kuwa mzazi ama kiongozi wa Kanisa ameshawishiwa kutoa ujumbe kwa

ajili yako? Ulikuathiri vipi? 6. Ni kweli gani za ziada unaweza kupata katika mistari hii?

Kikundi cha 2—Helamani 13:17–23Wakati hatumkumbuki Bwana, tunaadhiriwa kwa urahisi na kiburi na uovu. 1. Ni mistari gani unahisi inafundisha ukweli huu? 2. Ni laana gani Samweli alisema ingewajia Wanefi ikiwa wangeendelea katika uovu? 3. Ni dhambi gani zingine ambazo zililetwa na tamaa ya Wanefi ya mali? 4. Ni baadhi ya vitu gani vijana wanaweza kutamani ambavyo vinaelekeza kwa kiburi

na dhambi? 5. Kwa nini unafikiria ni muhimu “kumkumbuka Bwana Mungu wenu kwa vitu ambavyo

amewabariki navyo?” (Helamani 13:22). 6. Ni kweli gani za ziada unaweza kupata katika mistari hii?

Kikundi cha 3—Helamani 13:24–33Tukikataa maneno ya manabii wa Bwana, tutapatwa na majuto na huzuni. 1. Ni mistari gani unahisi inafundisha ukweli huu? 2. Kulingana na Samweli, kwa nini Wanefi waliwakataa manabii wa kweli? 3. Kwa nini unafikiria baadhi ya watu hukubali manabii waongo, kama vile Samweli alieleza? 4. Ni baadhi ya mafundisho gani maalum ya mitume na manabii walio hai? 5. Ni baadhi ya “wapumbavu na vipofu" gani (Helamani 13:29) mitume na manabii walio

hai wametuonya tuepuke? 6. Ni kweli gani za ziada unaweza kupata katika mistari hii?

Page 433: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

418

SOMO LA 114

helamani 14UtanguliziAkiendelea kuhubiri kwa Wanefi kule Zarahemla, Samweli Mlamani alitangaza ishara ambazo zingea-shiria kuzaliwa na kifo cha Yesu Kristo. Alieleza kuwa alitoa unabii wa ishara hizi ili kuwasaidia watu waamini katika Yesu Kristo na kuwasihi watubu dhambi zao. Alifundisha kuwa kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo,

kila binadamu atarudishwa katika uwepo wa Mungu. Akiwaita watu watubu, aliahidi kuwa walio na moyo wa toba wangesamehewa dhambi zao lakini kuwa wale waliokataa kutubu wangetupwa nje kutoka kwa uwepo wa Mungu.

Mapendekezo ya Kufundisha

Helamani 14:1–13Samweli atabiri kuhusu ishara zinazohusiana na kuzaliwa kwa MwokoziKabla ya darasa, chora mishale mitatu ubaoni kama ifuatavyo. Utaandika maneno na vishazi kando ya mishale somo linapoendelea.

Alika wanafunzi wakumbuke kile walichojifunza katika somo lililopita, ambalo lilikuwa linahusu Helamani 13. Ikiwa wanahitaji usaidizi kukumbuka, wakumbushe kuwa waliji-funza kuhusu nabii aliyeitwa Samweli. Waulize washiriki yale wanayokumbuka kumhusu, kama vile yeye alikuwa nani, alienda wapi, kile alichofundisha, na hali ya kiroho ya wale aliyewafundisha. Uliza wanafunzi wakumbuke jinsi watu walipokea ujumbe wa Samweli. Eleza kuwa Helamani 14 ina mwendelezo wa mafundisho ya Samweli.Eleza kuwa Samweli alitoa unabii kuhusu matukio ambayo yangetendeka katika siku za usoni, mengine maelfu ya maili kutoka Zarahemla. Uliza wanafunzi wapitie Helamani 14:1–2 na watambue tukio moja ambalo Samweli alitoa unabii kulihusu (kuzaliwa kwa Yesu Kristo).Uliza wanafunzi wasome Helamani 14:3–6 kimya, wakitafuta ishara ambazo Wanefi wa-ngeona wakati wa kuzaliwa kwa Mwokozi. Unaweza amua upendekeze kuwa wanafunzi watie alama maneno haya katika maandiko yao. Unaweza amua pia kuwaelekeza wanafu-nzi kwenye tanbihi za mistari hii, zinazolenga utimizaji wa unabii wa Samweli. • Kuzaliwa kwa Mwokozi kunamaanisha nini kwako?Soma Helamani 14:8–9 kwa sauti. Himiza umuhimu wa kuamini katika Mwokozi ili kupokea uzima wa milele. Andika Maisha ya Milele baada ya alama ya mshale ya mwisho ubaoni. Eleza kuwa “maisha ya milele” humaanisha jambo sawa na “uzima wa milele” Inamaanisha kuishi maisha sawa na yale Mungu anayoishi na kuishi milele katika uwepo Wake pamoja na familia zetu. Samweli aliwafundisha Wanefi kule Zarahemla kile walicho-hitaji kufanya ili kupokea maisha ya milele.Alika wanafunzi wasome Helamani 14:11–13 kimya, wakitafuta kile Samweli alitaka watu wajue na kufanya. Unaweza amua upendekeze kuwa wanafunzi watie alama kwenye vitu ambavyo Samweli alitaka watu wajue na kufanya.Kwa upande wa kushoto wa alama ya mshale ya kwanza, andika Maarifa. Kisha uliza wana-funzi kile walichopata ambacho Samweli aliwataka watu wajue Alika wanafunzi wachache waorodheshe vitu hivi ubaoni chini ya neno Maarifa (Majibu yanapaswa yajumuishe kuwa Samweli aliwataka watu wajue kuhusu hukumu ya Mungu kwa wale ambao wanatenda dhambi, masharti ya toba, kuja kwa Yesu Kristo, na ishara zinazohusiana na kuja Kwake,)• Samweli alitumaini kuwa maarifa haya yangewaelekeza watu wafanye nini? (Waamini

katika Yesu Kristo na kutubu dhambi zao.)

Kutoa UshuhudaUshuhuda ni tangazo rahisi na wazi la ukweli. Toa ushuhuda wako juu ya Yesu Kristo na injili Yake ya urejesho kila mara. Hii itaalika ushawishi wa Roho Mtakatifu, ambao utaimarisha wanafunzi katika jitihada zao za kujifunza, kuelewa na kuishi injili.

Tafuta nia ya mwandishi ama mnenajiKatika kutayarisha maa-ndiko, manabii wa kale walishawishiwa kuju-muisha jumbe ambazo zingehusiana na mahitaji yetu leo. Unapotafuta kujua nia ya mwandishi ama mnenaji katika Ki-tabu cha Mormoni, kuwa mwangalifu usije ukapita mpaka na yale yaliyo-wazi katika maandishi. Kumbuka kuwa nia ya msingi ya manabii daima imekuwa kushuhudia juu ya Yesu Kristo.

Page 434: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

419

helaMani 14

Uliza wanafunzi waandike kanuni iliyo na msingi katika Helamani 14:13. Kisha uliza wanafunzi wachache wasome kwa sauti kile walichoandika. (Jibu moja yamkini linaweza kuwa imani katika Yesu Kristo inaelekeza kutubu na kusamehewa dhambi. )Ili kuwasaidia wanafunzi waelewe maana ya kishazi “kupitia uzuri wake,” eleza kuwa uzuri ni sifa ama vitendo ambavyo humfanya mtu kustahili kupata tuzo. Ili kustahili kupo-kea msamaha wa dhambi zetu, lazima tufanye vitu fulani, kama vile kutubu kwa dhati, ku-batizwa na kudhibitishwa, na kutii amri. Lakini, sisi hupokea karama ya kusamehewa kwa sababu ya uzuri wa Mwokozi, si uzuri wetu. Unaweza amua uwakumbushe wanafunzi juu ya 2 Nefi 25:23, kifungu cha umahiri wa maandiko: “ Ni kwa neema kwamba tunaokolewa, baada ya kutenda yote tunayoweza.” Unaweza pia kupendekeza kuwa wanafunzi wasome Alma 22:14 na Alma 24:10–11. Kamilisha picha ubaoni kama ifuatavyo:

Maarifa imani katika Kristo toba Uzima wa Milele

• Kuongeza maarifa yako juu ya Mwokozi kumeimarisha vipi imani yako juu Yake?• Kuamini Mwokozi kwako kumekuelekeza vipi kutubu na kujitahidi kuwa zaidi kama Yeye?Shuhudia kuwa ni kupitia uzuri wa Yesu Kristo peke yake ndipo tunaweza kupokea msa-maha wa dhambi zetu na kupokea uzima wa milele.

Helamani 14:14–31Samweli anatoa unabii wa ishara zinazohusiana na kifo cha MwokoziAlika mwanafunzi asome Helamani 14:14 kwa sauti. Kisha uliza wanafunzi wasome Hela-mani 14:20–27 kimya, wakitafuta ishara ambazo Wanefi wangeona wakati wa kifo cha Yesu Kristo. Unaweza amua upendekeze kuwa watie alama kwenye ishara hizi. Wakiwa wame-pata muda wa kutosha kusoma, waalike waripoti kile walichopata. Waeleze kuwa utekelezi wa ishara hizi umerekodiwa katika 3 Nefi (ona Helamani 14:20, tanbihi a).Alika mwanafunzi asome Helamani 14:28–29 kwa sauti. Uliza darasa lifuate, likitafuta sababu Bwana hutoa ishara na matukio ya maajabu. Uliza wanafunzi wachache waeleze sababu hizi kwa maneno yao wenyewe. (Wanafunzi wanaweza kutumia maneno tofauti, lakini hakikisha wametambua ukweli ufuatao: Bwana hutoa ishara na matukio ya maa-jabu ili kuwasaidia watu wamuamini.)• Ukweli huu unaweza kutufunza nini kuhusu ishara ambazo zitatangulia Ujio wa Pili

wa Mwokozi?Uliza wanafunzi wafikirie kuhusu ishara ama ushahidi ambao Bwana amewapa ili kuwa-saidia kumuamini Yeye. Unaweza kuwahimiza wanafunzi washiriki yale waliyopitia (lakini wakumbushe kuwa hawapasi kuhisi kulazimishwa kushiriki chochote ambacho ni cha kibinafsi sana ama cha siri). Shuhudia kuwa Bwana hutoa ishara na hutuma manabii, kama Samweli, katika siku zetu ili kutusihi tumuamini Yeye.Tazama: Kwa sababu vifungu vingi vya maandiko vinatuonya tusitafute kupata ishara, wanafunzi wanaweza kuhusi kukanganywa na mjadala huu wa ishara. Wasaidie waelewe kuwa kuna tofauti kati ya kutambua ishara za upendo wa Mungu na kutafuta kupata ishara kwa sababu za ubinafsi (ona Yakobo 7:9–14; Alma 30:43–50; M&M 46:9; 63:7–11). Manabii wanapoonya kuhusu kutafuta ishara, huwa wanalenga watu ambao hukataa kuamini ila wanapoonyeshwa ishara, si watu ambao wanatumia imani katika kutafuta miujiza kuli-ngana na matakwa ya Bwana.Eleza kuwa ingawa ni vyema kujua kuhusu ishara ambazo Wanefi wangeona zinazohusi-ana na kifo cha Mwokozi, ni muhimu zaidi kuelewa mafundisho ya Samweli kuhusu umu-himu wa kifo na ufufuo wa Yesu Kristo. Chora picha ifuatayo ubaoni, ukiondoa maaelezo yaliyohesabiwa. Ongeza maelezo haya kwa wakati unaofaa wakati wa mjadala juu ya Hela-mani 14:15–19. (Unaweza zingatia kualika wanafunzi wanakili picha hii katika madaftari ama majarida ya kujifunza maandiko.)

Page 435: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

420

SoMo la 114

Eleza kuwa kishazi “kifo cha kiroho” kinarejea kutengwa kutoka kwa uwepo wa Mungu. Alika mwanafunzi asome Helamani 14:15–16 kwa sauti.• Kifo cha kiroho cha kwanza, kinachozungumuziwa katika Helamani 14:16 ni nini? (Una-

weza hitajika kueleza kuwa kwa sababu ya Kuanguka kwa Adamu na Hawa, tumete-ngwa kutoka kwa uwepo wa Mungu.)

Alika mwanafunzi asome Helamani 14:17 kwa sauti. Uliza darasa lifuate na litafakari jinsi wanaweza kushinda kifo cha kiroho cha kwanza. Andika ukweli ufuatayo ubaoni: Yesu Kristo akomboa kila mwanadamu kutokana na Kuanguka ili tuweze kurudi kwa uwepo wa Mungu. Eleza kuwa kila mwanadamu atarejea kwenye uwepo wa Mungu ku-hukumiwa (ona 2 Nefi 2:10).Alika mwanafunzi asome Helamani 14:18–19 kwa sauti.• Kifo cha kiroho cha pili, kinachozungumziwa katika Helamani 14:18–19 ni nini?

(Unaweza hitajika kueleza kuwa wale ambao hawatatubu watatengwa tena kutoka kwa uwepo wa Baba.)

• Tunaweza kufanya nini ili kuepuka kifo cha pili kilichozungumuziwa na Samweli? (Zingatia kualika wanafunzi wasome Helamani 14:13 na Mormoni 7:7–8. Eleza kuwa kupitia Upata-nisho wa Yesu Kristo, wale wanaotubu wataishi katika uwepo wa Mungu milele.)

Ili kuhimiza umuhimu wa wakala tunapotafuta kupata baraka za Upatanisho wa Mwo-kozi, alika wanafunzi wasome Helamani 14:30–31 kimya. Waulize watafute maneno na vishazi kuhusu wakala wao. Waalike washiriki maneno na vishazi ambavyo wamepata. Waulize waeleze jinsi maneno na vishazi hivi vinawasaidia kuelewa umuhimu wa chaguo wanazofanya kila siku.

Tangazo na Habari za UsuliHelamani 14:18–19. Karama tukufu ya tobaMzee D. Todd Christofferson wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alishuhudia juu ya furaha ambayo huja kupitia toba:

“Nakiri kwa shukrani na kushuhudia kuwa mateso yasiyoeleweka, kifo na Ufufuo wa Bwana wetu

“inasababisha kutimiza hali ya toba” (Helamani 14:18). "Karama tukufu ya toba ni ufunguo wa furaha hapa na baadaye. Katika maneno ya Mwokozi na katika unyenyekevu wa kina na upendo, nawaalika nyote ‘mtubu: kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia” (Mathayo 4:17). Najua kuwa katika kukubali mwaliko huu, utapata furaha sasa na milele” (“The Divine Gift of Repentance,” Ensign ama Liahona, Nov. 2011, 41)

Uwepo wa Mungu

dunia

Kifo na Ulimwengu

wa Roho

1. Kuanguka kwa adamu na hawa kulileta kifo cha kiroho cha kwanza (ona helamani 14:16).

2. Ufufuo unarejesha binadamu wote katika uwepo wa Mungu kuhukumiwa (ona 2 nefi 2:10; helamani 14:17).

3. Wale wanaotubu na kupokea msamaha wa dhambi zao wa-naishi katika uwepo wa Mungu milele (ona helamani 14:13; Mormoni 7:7–8).

4. Wale ambao hawatubu watatengwa kutoka kwa uwepo wa Mungu, wakipi-tia kifo cha kiroho cha pili (ona helamani 14:18).

Page 436: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

421

UtanguliziSamweli Mlamani aliwaonya Wanefi kuwa wasipotubu, wangeangamizwa. Alitangaza kuwa Bwana angere-fusha siku za Walamani, ambao walikuwa wamekuwa wenye haki zaidi ya Wanefi. Baadhi ya Wanefi waliamini

mafunzo ya Samweli na wakabatizwa na Nefi. Wale ambao hawakumuamini Samweli walijaribu kumuua. Lakini Samweli alilindwa na nguvu ya Mungu, na aka-rudi katika nchi yake mwenyewe.

SOMO LA 115

helamani 15–16

Mapendekezo ya Kufundisha

Helamani 15Samweli awaonya Wanefi na anaeleza jinsi Walamani wamekuwa watu wa ahadiSoma maelezo yafuatayo kwa sauti:Mvulana mmoja alilelewa na wazazi ambao hawakuwa waumini wa Kanisa na hawaku-himiza mafunzo ya Yesu Kristo. Walimruhusu kunywa pombe, tabia ambayo aliendelea hata chuoni. Kisha akakutana na Wamisionari wa kanisa la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Baada ya kukutana na wamisionari mara kadhaa, aliahidi kuacha pombe. Siku chache baadaye, alikuwa na kikundi cha marafiki walimpa kinywaji chenye mvinyo.Mvulana mwingine alilelewa katika familia ya Watakatifu wa Siku za Mwisho. Wazazi wake walikuwa na mkutano wa jioni wa familia nyumbani na vikao vya kujifunza maadiko kwa familia. Alikuza tabia ya kusoma maandiko kila siku na kutoa maombi ya kibinafsi. Alihudhuria darasa la Msingi kanisani, akahudumu katika akidi ya Ukuhani wa Haruni, na kuhitimu kutoka seminari, akipata maarifa juu ya amri na njia za Bwana. Akihudhuria chuo, alikuza urafiki mpya. Usiku mmoja rafiki alimpa kinywaji chenye mvinyo.• Je, kukubali kinywaji chenye mvinyo kungekuwa kosa kubwa zaidi kwa mvulana wa

kwanza ama wa pili? Ndio ama la, kwa nini?Andika maswali yafuatayo ubaoni:

Hali ya kiroho ya Wanefi —Helamani 15:1–3, 17Hali ya kiroho ya Walamani—Helamani 15:4–6

Alika wanafunzi wasome kimya vifungu vya maandiko vilivyoorodheshwa ubaoni. (Kabla wasome, unaweza amua kuelekeza nadhari yao kwa neno uangalifu katika Helamani 15:5. Kufanya kitu kwa uangalifu kunamaanisha kutenda kwa makini sana.) Uliza wanafunzi waandike sentensi mbili— moja ikifupisha hali ya kiroho ya Wanefi na ingine ikifupisha hali ya kiroho ya Walamani. Baada ya muda wa kutosha, uliza:• Ni yupi wa wavulana hawa walili tuliowajadili mwanzoni mwa somo anafanana na Wa-

nefi walioelezwa katika mistari hii? Yupi anafanana na Walamani?• Ingawa Walamani walikuwa na historia ndefu ya uovu, kwa nini waliweza kupokea

baraka nyingi?• Kwa nini Wanefi walikuwa katika hatari ya kuangamizwa?• Kurudi kwa Bwana ni ishara ya upendo Wake kwa njia gani? (Unaweza hitajika kueleza

kuwa neno rudi linamaanisha kurekebisha mtu kupitia adhabu ama mateso ya aina fulani.)

Andika maswali yafuatayo ubaoni:Watu wanapojua ukweli na kuamini maandiko, wao huelekezwa kwa ... na ... , ambayo huleta ...

Uliza wanafunzi wasome Helamani 15:7 kimya, wakitafuta jinsi wanaweza kukamilisha kauli iliyo ubaoni. Baada ya muda wa kutosha, uliza baadhi ya wanafunzi jinsi wangekami-lisha kauli. (Kwa mfano, wanafunzi wanaweza kueleza kanuni ifuatayo: Watu wanapojua

Page 437: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

422

SoMo la 115

ukweli na kuamini maandiko, wao huelekezwa kwa imani na toba, ambayo huleta mabadiliko ya moyo.)Alika mwanafunzi asome Helamani 15:8 kwa sauti. Uliza darasa lifuate, likitafuta maelezo ya Samweli ya Walamani ambao walikuwa wamepata mabadiliko ya moyo. (Walikuwa “imara na dhabiti katika imani.”)Wape wanafunzi muda watafakari ikiwa kusoma maandiko kumewaelekeza kuwa na imani zaidi katika Bwana. Pia waulize watafakari ikiwa hii imewaelekeza kuwa imara na dhabiti katika imani. Zingatia kualika mwanafunzi moja ama wawili waeleze jinsi kusoma maa-ndiko kumeongeza imani yao katika Yesu Kristo.Elekeza nadhari ya wanafunzi kwa Helamani 15:9–17. Eleza kuwa katika mistari hii, neno wewe linarejelea Wanefi na maneno wao na yao yanarejelea Walamani. Soma mistari hii kwa sauti kwa darasa, ukitua kama inavyohitajika ili kutoa maelezo ama kujibu maswali. Kisha wape wanafunzi muda wa kuangalia mistari tena na kuandika sentensi ambayo inaeleza ukweli uliofundishwa katika mistari hii.Alika wanafunzi wachache wasome kile walichoandika. Miongoni mwa kweli zingine, wanfunzi wanaweza kuandika jambo kama: watu wakiwa wakutoamini baada ya kupo-kea ukamilifu wa injili, watapokea laana kuu zaidi. Unaweza amua upendekeze kuwa wanafunzi waandike ukweli huu katika maandiko yao kando ya Helamani 15:9–17.Wanafunzi wanapojadili ukweli huu, sisitiza baraka kuu ambazo huja kwa kuelewa na kui-shi injili sasa. Mafunzo ya Samweli hayakubalishi muumini mpya wa Kanisa kutenda dha-mbi. Wala hayadokezi kuwa tunaweza kuepuka kuwajibika na laana kwa kukataa kujifunza kuhusu injili. Ingawa ni kweli kwamba kuwa na maarifa ya injili kunaelekeza kwa kuwaji-bika zaidi tukifanya kitu kibaya, pia kunaelekeza kwa nguvu zaidi katika juhudi zetu za ku-tenda haki. Na tunapofuata matakwa ya Mungu na kusaidia wengine kufanya vivyo hivyo, Yeye hutubariki na amani na furaha ambayo hatuwezi kupokea kwa njia ingine yoyote.

Helamani 16Wale wanaomuamini Samweli wanatubu na kubatizwa, wakati wengine wanafa-nya mioyo yao kuwa migumuOnyesha picha ya Rais wa sasa wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Uliza wanafunzi waeleze njia tofauti ambayo wameona watu (kanisani na nje ya Kanisa) wakichukulia ujumbe wa nabii.Uliza nusu ya darasa isome Helamani 16:1–5 kimya, ikitafuta vitendo vya watu ambao waliamini ujumbe wa Samweli. Uliza nusu hio ingine ya darasa isome Helamani 16:2–3, 6–7 kimya, ikitafuta vitendo vya watu ambao hawakuamini ujumbe wa Samweli. (Unaweza amua uandike marejeo haya ya maandiko kwenye ubao.) Uliza mwanafunzi aripoti juu ya kile walichojifunza.• Kwa nini unadhani watu huchukulia manabii na jumbe zao kwa njia tofauti hivi?• Kwa nini unadhani baadhi ya watu hukasirika manabii wanapotoa ushauri kama vile

maneno katika kijitabu cha Kwa Nguvu ya Vijana ?Alika mwanfunzi asome kwa sauti kauli ifuatayo ya Rais Ezra Taft Benson.

“Nabii anapoonyesha dhambi za dunia, walimwengu, badala ya kutubu dhambi zao, hutaka kufunga mdomo wa nabii ama kutenda kana kwamba nabii hayuko. Upendeleo na wengi kamwe si upimaji wa ukweli. Manabii wengi wameuliwa ama kufurushwa. Tunapowadia ujio wa pili wa Bwana, unaweza kutarajia kwamba watu wa dunia wanapokuwa waovu zaidi, nabii hatapendwa nao” (The Teachings of Ezra Taft Benson [1988], 133).

• Ni ipi baadhi ya mifano ya watu wanaofuata ushauri wa manabii hata kama wengine walikataa ushauri huo?

Uliza wanafunzi wafunge maandiko yao. Alika mwanafunzi mmoja afungue maandiko yake na asome Helamani 16:13–14 wakati wanafunzi wengine wanasikiliza. Uliza darasa jinsi linafikiria wasioamini wangechukulia ishara na matukio haya.Uliza wanafunzi wafungue maandiko yao na wafuate unapowasomea Helamani 16:15–16 . Kisha waulize wafikirie kuwa wameruhusiwa kuzungumza na watu ambao walikuwa kule

Page 438: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

423

helaMani 15 –16

Zarahemla wakati ishara zilitolewa. Waalike wafikirie juu ya maswali ambayo wangependa kuuliza muumini au asiyeamini. Baada ya wanafunzi kuwa na muda wa kufikiria juu ya maswali, uliza baadhi yao washiriki maswali yao na darasa.Uliza wanafunzi watafakari swali lifuatalo bila kujibu kwa sauti:• Ikiwa ungekuwa hapo na kushuhudia ishara na matukio hayo ya maajabu, unafikiri

ungeyachukulia vipi?Wanafunzi wakiwa wamepata muda wa kutafakari, uliza:• Kulingana na Helamani 16:16, kwa nini baadhi ya watu walikana kutimizwa kwa unabii,

ikiwa ni pamoja na ishara kutoka mbinguni?Wape wanafunzi dakika chache wasome Helamani 16:17–21 kimya, wakitafuta sababu za ziada ambazo wasiowema walitoa kwa kutoamini unabii wa Samweli. Alika wanafunzi wachache waseme sababu ambazo wametambua katika mistari hii.• Ni gani miongoni mwa sababu ama majadiliano dhidi ya manabii unadhani ni ya kawa-

ida zaidi kwa siku zetu?Alika wanafunzi wasome Helamani 16:22–23 kwa sauti, na uulize darasa litafute kile kilichotendeka watu wengi walipoendelea kupuuza maonyo ya Samweli. Alika wanafunzi washiriki kile walichopata.• Nini kitatutendekea tukikataa manabii wa Bwana wa siku za mwisho?Wanafunzi wanapojibu, sisitiza kanuni ifuatayo: Tunapokataa mashahidi wa Bwana, tunamkubalia Shetani ateke mioyo yetu. (Unaweza amua uandike kauli hii ubaoni kabla ya darasa.)Ili kuhitimisha somo la leo, alika mwanafunzi asome kauli ifuatayo ya Rais Henry B. Eyring wa Urais wa Kwanza. Uliza darasa lisikize kile hakika tunachagua tunapokataa ushauri kutoka kwa Mungu, ambao wingi wake huja kupitia manabii wa siku za mwisho:“Tunapokataa ushauri unaokuja kutoka kwa Mungu, hatuchagui kujitenga na ushawishi wa nje. Tunachagua ushawishi mwingine. Tunakataa ulinzi wa Baba wa Mbinguni anaye-penda kwa kikamilifu, mwenye nguvu zote, mwenye maarifa yote, ambaye lengo lake lote, kama lile la Mwana Wake Mpendwa, ni kutupa uzima wa milele, kutupatia yote ambayo anayo, na kuturejesha nyumbani tena katika familia kwa mikono Yake ya upendo. Kwa kukataa ushauri Wake, tunachagua ushawishi wa nguvu zingine, ambazo lengo lake ni kutufanya tuwe na huzuni na ambazo kusudi kwake ni chuki. Tunao wakala wa kimaadili kama karama ya Mungu. Badala ya haki ya kuchagua kuwa huru kutokana na ushawishi, ni haki isiyobanduka ya kujiweka chini ya nguvu zozote za zile tunazochagua” (“Finding Safety in Counsel,” Ensign, May 1997, 25).• Kulingana na Rais Eyring, ni nini hasa tunachochagua tukikataa ushauri kutoka kwa

Mungu na manabii Wake?Alika wanafunzi wafikirie kimya ikiwa wamefanya mioyo yao kuwa migumu kwa njia yoyote dhidi ya ushauri ambao Mungu ametoa kupitia manabii na mitume. Wahimize wawe imara na dhabiti katika kuishi injili na kwa kusikiliza ushauri wa Bwana kutoka kwa manabii Wake. Shuhudia kweli ambazo mmejadili katika somo hili.

Rejeleo la HelemaniChukua muda ili kuwasaidia wanafunzi warejelee kitabu cha Helamani. Waulize wafikirie kuhusu kile walichojifunza kutoka kwa kitabu hiki, katika seminari na kujifunza maandiko kibinafsi. Waalike warejelee kwa kifupi baadhi ya muhtasari ya milango katika Helamani ili kuwasaidia kukumbuka. Uliza wanafunzi wachache washiriki kitu kutoka kwa Helamani kilichowavutia ama kilichowasaidia kuwa na imani kuu zaidi katika Yesu Kristo. Baada ya muda wa kutosha, uliza baadhi ya wanafunzi washiriki mawazo na hisia zao.

Page 439: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

424

Somo la Mafunzo ya NyumbaniHelamani 10–16 (Kitengo cha 23)

Vifaa vya Matayarisho kwa Mwalimu wa Mafunzo ya NyumbaniMuhtasari wa Masomo ya Mafunzo ya Kila Siku ya NyumbaniMuhtasari ufuatao wa mafundisho na kanuni ambazo wanafunzi walijifunza waliposoma Helamani 10–16 (kitengo cha 23 hakitarajiwi kufunzwa kama sehemu ya somo lako. Somo unalofundisha linamakinisha tu baadhi ya mafundisho na kanuni hizi. Fuata ushawishi wa Roho Mtakatifu unapozi-ngatia mahitaji ya wanafunzi.

Siku ya 1 (Helamani 10)Helamani 10 Iliwapatia wanfunzi fursa ya kujifunza zaidi kuhusu nguvu ya kiroho ya Nefi. Kupitia mfano wake, wanafunzi walijifunza kuwa kutafakari mambo ya Bwana ku-natutayarisha kupokea ufunuo. Walijifunza pia kuwa Bwana hutukabithi baraka na majukumu tunapoweka matakwa Yake mbele ya yetu wenyewe. Nefi alipoweka matakwa ya Bwana mbele ya yake mwenyewe, Bwana alimpatia nguvu ya kuunganisha.

Siku ya 2 (Helamani 11–12)Kwa kujifunza miaka 14 ya historia ya Wanefi, wanafunzi walijifunza kuwa kupitia unyenyekevu na toba tunaweza ku-epuka kiburi na maangamizo. Ikiwa sisi si waangalifu, ustawi wetu unaweza kutuelekeza kumsahau Bwana. Nefi alifu-ndisha kuwa ili kuwasaidia watu waepuke kosa hili, Bwana hurudi watu Wake ili kuwaamusha katika kumkumbuka Yeye.

Siku ya 3 (Helamani 13–14)Samweli, nabii Mlamani, alionyesha kuwa manabii hunena jumbe ambazo Mungu huweka mioyoni mwao. Katika kusoma maonyo yake ya kinabii, wanafunzi walijifunza kuwa tukikataa maneno ya manabii wa Bwana, tutapata majuto na huzuni. Samweli aliwahimiza watu waamini katika Yesu Kristo na alishuhudia kuwa Bwana hutoa ishara na matukio ya maajabu ili kusaidia watu wamuamini Yeye.

Siku ya 4 (Helamani 15–16)Kwa sababu Bwana alikuwa amewabariki Wanefi sana, Samweli alikuwa anajaribu kuwasaidia waelewe hukumu za Mungu ambazo wangekabiliana nazo ikiwa hawange-tubu. Kutokana na haya, wanafunzi walijifunza kuwa watu wakiwa wa kutoamini baada ya kupokea utimilivu wa injili, watapata laana kuu zaidi. Kutoka kwa jinsi Wanefi walivyo-mchukulia Samweli, wanafunzi walijifunza kuwa tunapocha-gua kukataa mashahidi wa Bwana, tunamruhusu Shetani ateke mioyo yetu.

UtanguliziKatika Helamani 10–16 jukumu la manabii katika kutangaza toba limesisitizwa. Wiki hii mzima, wanafunzi walikuwa na fursa ya kujifunza uaminifu wa manabii Nefi, na Samweli Mlamani. Wanaume wote wawili walipata maonyesho ya kiroho na walikuwa na mamlaka ya kuhudumu miongoni mwa Wanefi wa-liopotoka. Licha ya ugumu wa mioyo ya watu, wanaume wote wawili walitangaza toba. Walifundisha kuwa furaha inapatikana katika kuishi kanuni zilizotolewa na Yesu Kristo na si katika kutenda maovu.

Mapendekezo ya Kufundisha

Helamani 10–16Helamani na Samweli wanatumikia watu kwa uaminifuUliza wanafunzi kama wamewahi kuwa katika hali ambayo kusimamia viwango vilivyofundishwa katika kijitabu Kwa Nguvu ya Vijana kungekuwa hakupendezi kwa marafiki zao. Unaweza alika wanafunzi wachache washiriki kile walichopitia na wazu-ngumzie kile walichohisi na kujifunza.

Ambia wanafunzi kuwa Helamani 10–16 inatupatia mifano ya wanaume wawili waliosimama kwa ajili ya viwango vya Bwana hata kama ilikuwa haipendezi kwa watu. Alika wanafunzi wazi-ngatie kile wanachoweza kujifunza kutoka kwa mifano ya Nefi na Samweli Mlamani kinachoweza kuwasaidia katika hali kama hizo.

Chora chati ifuatayo ubaoni ama kwenye kipande cha karatasi.

Mifanano kati ya nefi na Samweli Mlamani

nefi (helamani 10:1–5, 12, 15–16)

Samweli (helamani 13:1–6; 16:1–2)

Uliza wanafunzi wasome mistari iliyoorodheshwa katika chati, wakitafuta mifanano kati ya Nefi na Samweli. Alika wanafunzi wachache waorodheshe mifanano hii katika nafasi tupu kwenye chati. Orodha inaweza kujumuisha yafuatayo: walikataliwa na watu, walisikia sauti ya Bwana, walifuata maelekezo ya Bwana kwa haraka, walizungumza kile Bwana alichoweka mioyoni mwao, waliwaonya Wanefi kuwa wasipotubu, watanagamizwa, walilindwa na nguvu ya Mungu ili waweze kutoa ujumbe Wake.

Baada ya wanfunzi kuorodhesha mifanano waliogundua, uliza mwanafunzi asome Helamani kwa sauti. Kisha uliza maswali yafuatayo:

• Ni zipi baadhi ya sababu yamkini za kutochoka kwa Nefi?• Samweli alionyesha kutochoka pia kwa njia gani? Tunawezaje

kukuza kutochoka kama huku?

Uliza mwanafunzi asome kwa darasa kauli ifuatayo ya Mzee Neal A. Maxwell wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, ambapo anatufunza jinsi ya kukuza sifa hii:

Page 440: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

425

SoMo la MafUnzo ya nyUMbani

“Tukimtazamia Yesu na kazi Yake, furaha pamoja na uwezo wetu wa kubaki huongezwa. Nefi hakuwa amefuata kwa kibinafsi “maisha yake” lakini alikuwa amefuata kufanya mata-kwa ya Mungu. Hii ilimpatia nguvu ya ziada na isiogawanywa ambayo ilifanya kujitahidi kwake kwa jitihada isiyoisha kuweze-kana. Nefi alijua upande aliokuwa anaangalia: kwake Mungu” (If Thou Endure It Well [1996], 116).

Uliza:

• Kulingana na Mzee Maxwell , tunaweza kufanya nini ili kuhu-dumu na jitihada isiyoisha.

• Vishazi vipi katika Helamani 10:4 vinaonyesha kuwa Nefi “alimwangalia Mungu” ama vingine, alilenga kufanya ma-takwa ya Mungu?

• Vishazi vipi katika Helamani 13:3–5 vinaonyesha kuwa Sa-mweli aliweka matakwa ya Mungu juu ya yake mwenyewe?

• Tunaweza kujifunza ukweli upi kutoka kwa yale ambayo Nefi na Samweli walipitia? Jibu moja yamkini linaweza kuakisi ukweli ambao wanafunzi walijifunza katika masomo yao ya kibinafsi wiki hii: Bwana hutukabithi baraka na majukumu tunapoweka matakwa Yake mbele ya yetu wenyewe.)

Soma hadithi ifuatayo, iliyotolewa na Mzee Dallin H. Oaks wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, juu ya msichana mwenye umri wa miaka 12 ambaye alikubali matakwa ya Mungu mbele ya yake mwenyewe:

“Hatuwezi kuwa na imani ya kweli katika Bwana bila kuwa na tumaini kamili pia katika matakwa ya Bwana na wakati wa Bwana. Tunapokuwa na aina hiyo ya imani na tumaini katika Bwana, tuna ulinzi wa kweli maishani mwetu. . . .

“Nilisoma juu ya msichana aliyeonyesha aina hiyo ya imani na tumanini. Kwa miezi mingi mamake alikuwa amegonjeka vibaya. Mwishowe, baba mwaminifu aliwaita watoto kando ya kitanda chake na kuwaambia wampigie kwaheri mama yao kwa sababu alikuwa anakufa. Binti mwenye umri wa miaka kumi na miwili alilalamika:

Papa, sitaki mamangu afe. Nimekuwa naye hospitalini kwa miezi sita; na mara kwa mara umemuombea, na ametuliziwa uchungu wake na kwa kimya akalala. Nataka uweke mikono yako juu ya mamangu na umponye.’

“Baba, ambaye alikuwa ni Mzee Heber J. Grant, aliwaambia watoto kuwa alihisi moyoni mwake kwamba wakati wa mama yao ulikuwa umewadia. Watoto waliondoka, na akapiga magoti kando ya kitanda cha mkewe. Baadaye alikumbuka ombi lake: ‘Nilimwambia Bwana nilikiri mkono wake katika maisha na katika kifo. Lakini nilimweleza Bwana kwamba nilikosa nguvu za kumwacha mke wangu afe na kufanya iathiri imani ya watoto wangu wadogo.’ Alimsihi Bwana ampe binti yake “fahamu kuwa ilikuwa ni mawazo yake na matakwa yake kwamba ma-make angeaga.’

Katika saa moja mama aliaga. Mzee Grant alipowaita watoto warejee kwenye chumba chake na kuwaambia, mvulana wake mdogo mwenye umri wa miaka sita (aliyeitwa Heber) alianza ku-omboleza kwa huzuni. Dadake mwenye umri wa miaka kumi na miwili akamchukua mikononi mwake na kusema: “Usiomboleze,

Heber; tangu tulipotoka nje ya chumba hiki, sauti ya Bwana kutoka mbinguni imeniambia, Katika kifo cha mamako matakwa ya Bwana yatatekelezwa” (Bryant S. Hinckley, Heber J. Grant: Highlights in the Life of a Great Leader, Salt Lake City: Deseret Book Co., 1951, pp. 243–44).

Tunapokuwa na aina ya imani na matumaini yaliyoonyeshwa na msichana huyo, tunayo nguvu ya kutuhimili katika tukio lolote muhimu maishani mwetu” (“Faith in the Lord Jesus Christ,” Ensign, Mei 1994, 100).

Uliza:

• Nini kilimsaidia Rais Heber J. Grant na familia yake kuweka matakwa ya Bwana mbele ya yao wenyewe?

• Je, umewahi kuwa na tukio ambapo ulihitaji kuweka matuma-nini yako katika Mungu na kuweka matakwa Yake mbele ya yako mwenyewe? (Zingatia kuwaalika wanafunzi wachache washiriki na darasa yale ambayo wamepitia. Wakumbushe kuwa hawapaswi kushiriki lolote la kibinafsi sana ama la siri.)

Hakikishia wanafunzi kuwa tunapoweka matumaini yetu kwa Mungu na kuweka matakwa Yake mbele ya yetu wenyewe, atatuhimili wakati wa shida.

Eleza kuwa sehemu muhimu wa huduma ya Nefi ilikuwa ni kuwasaidia watu wamkumbuke Mungu na watubu dhambi zao. Lakini, waliendelea kufanya mioyo yao kuwa migumu na hawa-kutaka kurekebishwa.

Gawa darasa kwa vikundi viwili. Uliza kikundi kimoja kisome Helamani 10:15–18; 11:3–10 na kile kingine kisome Helamani 11:30–37; 12:1–3. (Unaweza amua uandike marejeo haya uba-oni.) Uliza kila kikundi kiwe tayari kujadili sababu za Bwana ku-warudi watu Wake. Wanafunzi wanaweza kutaja sababu chache tofauti, lakini hakikisha kuwa wameeleza kuwa Bwana hurudi watu Wake ili kuwaamsha katika kumkumbuka Yeye.

• Bwana alitumia aina gani ya kurudi ili kupata usikilivu wa watu?• Kulingana na Helamani 12:3, watu wengi huwa hawamkumbuki

Bwana ila tu awarudi. Kwa nini unadhani hivi ndivyo ilivyo?

Alika mwanafunzi asome Helamani 15:3 kwa sauti.

• Kurudi kwa Bwana ni onyesho la upendo kwa njia gani?

Uliza wanafunzi washiriki majibu yao ya zoezi la 5 siku ya 2 ya wiki hii. Unaweza amua kutia mkazo kuwa kupitia unyenye-kevu na toba, tunaweza kuepuka kiburi na maangamizo na kuwa ikiwa hatuko waangalifu, ustawi wetu unaweza kutuelekeza kumsahau Bwana.

Kitengo Kifuatacho (3 Nefi 1–11)Katika zoezi linaofuata la wanafunzi, watasoma kuhusu nchi yote ya Wanefi ikikusanyika kupigana na wezi wa Gadiantoni katika vita kuu. Wanefi waliwezaje kuwashinda wezi waovu? Wanafunzi pia watasoma kuhusu maangamizo mkubwa yali-yotendeka katika Amerika wakati wa kifo cha Yesu Kristo kule Yerusalemu. Gizani, watu walisikia sauti ya Yesu Kristo. Kisha Mwokozi aliyefufuka akaja kuwahudumia kibinafsi. Uliza wana-funzi wazingatie jinsi wangehisi ikiwa wangekuwa hapo.

Page 441: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

426

UtangUlizi Wa

Kitabu cha tatu cha nefi: Kitabu cha nefiKwa nini kujifunza hiki kitabu?Katika masomo yao ya 3 Nefi wanafunzi watajifunza kuhusu maneno na matendo ya Mwokozi wakati wa huduma yake ya siku tatu kati ya Wanefi. Rais Ezra Taft Benson alifundisha “3 Nefi inayo baadhi ya taarifa zenye nguvu na za kugusa ka-tika maandiko yote. Inashuhudia kuhusu Yesu Kristo,manabii Wake, na mafundisho ya wokovu”(The Saviors Visit to Ame-rica,” Ensign, May 1987, 6). Wanafunzi wanapoona jinsi Yesu Kristo alivyoonye-sha huruma kwa watu “mmoja mmoja,” wanaweza kutambua vyema zaidi huruma zake kwao kibinafsi (ona 3 Nefi 11:15; 17:21) Wanaweza kujifunza masomo mu-himu kutoka kwa mifano ya utakatifu wa wale waliojitayarisha kukutana na mwo-kozi. Wanaweza pia kujifunza kutokana na utovu wa utakatifu wa wale ambao hawakujitayarisha kukutana na mwokozi

Nani aliyeandika kitabu hiki?Mormoni alifupisha kumbukumbu kutoka kwenye bamba za Nefi ili kutengeneza kitabu cha 3 Nefi. Kitabu hiki kimeitwa kwa Nefi (Mwana wa Nefi) ambaye kazi zake zilijumuisha misimu kabla, wakati wa, na baada ya ujio wa mwokozi kwa watu. Mnamo wakati wa uovu mkubwa uliotangulia kuja kwa Yesu Kristo, Nefi alihudumu“kwa uwezo na mamlaka maku-bwa” (3 Nefi 7:17). Juhudi zake zilikuwa utangulizi kwa huduma ya Yesu Kristo ambaye maneno yake na matendo yake yalianzisha kiini cha 3 Nefi. Akifupisha rekodi ya Nefi, Mormoni aliongeza maoni yake na ushuhuda (ona 3 Nefi 5:8–26; 26:6–12; 29–30)

Kitabu hiki kiliandikiwa nani, na kwa nini?Mormoni alikusudia maandishi katika 3 Nefi kwa vikundi viwili Kwanza alieleza kuwa alikuwa ameyaandika kwa uzao wa Lehi (ona 3 Nefi 26:8). Pili, Mormoni aliwazungumzia Wayunani katika siku za mwisho na kurekodi onyo la Bwana kwamba waje kwake na kuwa sehemu ya watu wake wa agano (ona 3 Nefi 30) Kitabu cha 3 Nefi kinahimiza mwaliko huu kwa ushuhuda wake wenye nguvu wa Yesu Kristo na kutilia mkazo juu ya umuhimu wa maagano

Kuliandikwa lini na wapi?Rekodi asili zilizotumiwa kama chanzo cha kitabu cha 3 Nefi zinawezekana kuwa ziliandikwa kati ya 1 K.K. na 35 B.K.. Mormoni alifupisha kumbukumbu hizo wakati fulani kati ya 345 B.K. na 385 B.K. Mormoni hakurekodi mahali alipokuwa akitunga kitabu hiki.

Ni zipi baadhi ya sifa bainifu za kitabu hiki?3 Nefi anaandika kutimia kwa unabii kuhusu kuzaliwa, kufa na kukufuka kwa Yesu Kristo (ona 3 Nefi 1; 8; 11).)

Kumbukumbu yake ya ujio wa Mwokozi kwa Wanefi kunawakilisha kile ambacho Mzee Jeffrey R. Holland amekita “kitovu, wakati muhimu, katika Historia mzima ya Kitabu cha Mormoni” (Christ and the New Covenant: The Messianic Message of the Book of Mormon [1997], 250). Milango ishirini kati ya thelethini katika 3 Nefi ina mafundisho ya mwokozi yali-yotolewa moja kwa moja kwa watu (ona 3 Nefi 9–28)

Mpangilio3 Nefi 1–5 Nefi anapokea kumbuku-mbu kutoka kwa baba yake. Ishara za kuzaliwa kwa Kristo zinatolewa, mpango wa kuwaangamiza waa-minio unashindwa na watu wengi wanaokolewa Wanefi na Wala-mani waungana kupigana dhidi ya wanyanganyi wa Gadiantoni. Wanatubu dhambi zao na hatimaye kuwashinda wanyang’anyi chini ya uongozi wa Lakonea na Gidgiddoni. Mormoni azungumzia majukumu yake kama mfuasi wa Kristo na mweka kumbukumbu.

3 Nefi 6–7 Ufanisi miongoni mwa wa Wanefi unaongoza kwenye kiburi, uovu, na makundi ya siri. Serikali inapinduliwa na watu wanagawa-nyika katika makabila. Nefi anahu-dumia kwa uwezo mkubwa.

3 Nefi 8–10 Tufani, uharibifu na giza yanaashiria kusulubiwa na kifo cha Mwokozi Watu waaomboleza vifo vya wale waliouwawa katika uhari-bifu Sauti ya Yesu Kristo inawalika manusura kutubu na kuja kwake.

3 Nefi 11–18 Yesu Kristo awajia umati hekaluni na kumwalika kila mtu aguse alama za misumari katika mikononi yake na miguu. Anawa-teua wafuasi kumi na wawili na kuwapa mamlaka ya kufanya ibada na kusimamia kanisa. Mwokozi anafundisha mafundisho yake, atoa sheria za utakatifu na kueleza kuwa

ametimiza sheria ya Musa. Anapo-nya magonjwa ya watu, awombea na kuwabariki watoto wao. Baada ya ya kuanzisha Sakramenti, na ku-toa mafunzo ya ziada, aondoka.

3 Nefi 19–26 Wafuasi kumi na wawili wanahudumia watu na Roho Mtaka-tifu anashushwa juu yao. Yesu Kristu aja mara ya pili na kuwaombea wote watakaomwamini yeye. Anasima-mia Sakramenti na kufundisha jinsi baba atakavyotimiza agano lake na Israeli. Mwokozi aamuru watu ku-tafuta maneno ya Isaya na manabii wote na anamwagiza Nefi aweke kwenye kumbukumbu kutimia kwa unabii uliotangazwa na Samueli Mlamani. Anatoa maneno ambayo baba alimpa Malaki na kueleza vitu vyote kutoka mwanzo mpaka wakati ambao angekuja katika utukufu Wake (3 Nefi 26:3). Kisha anaondoka.

3 Nefi 27–28 Yesu Kristo anatokea na kuwaagiza wafuasi kumi na wawili kuliita kanisa kwa jina lake. Anatoa injili yake na kuwaagiza wafuasi wake kuwa kama alivyo. Yesu Kristo awapa wafuasi kumi na wawili kulingana na matakwa yao.

3 Nefi 29–30 Mormoni aeleza kwa-mba ujio wa Kitabu cha Mormoni ni ishara kuwa Mungu ameanza kuwa-kusanya Israeli katika siku za mwi-sho. Bwana anawasihi mataifa yasio jua injili kutubu na kuwa sehemu ya watu wake wa Agano.

Page 442: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

427

UtanguliziWakati ulipofika wa kutimia kwa unabii wa Samweli Mlamani kuhusu kuzaliwa kwa Mwokozi, waumini walingoja ishara ambazo Samweli alikuwa alisema zitakuja. Wasioamini walitisha kuwaua waumini kama unabii usingetimia kufikia siku fulani Nefi, mwana wa Nefi na, mjukuu wa Helamani alimsihi Bwana kwa niaba ya waumini. Katika kujibu ombi la Nefi, sauti ya

Bwana ilimjia, ikitangaza kwamba ishara ingetolewa utatolewa usiku ule. Jua lilipotua, hapakuwa na giza, na nyota mpya ikatokea. Licha ya majaribio ya Shetani ya kuangamiza imani ya watu, wengi wa watu wali-ongolewa kwa Bwana. Lakini miaka miwili baadaye, wezi wa Gadiantoni walianza kuwaongoza Wanefi na Walamani wengi katika uovu.

SOMO LA 116

3 nefi 1

Mapendekezo ya Kufundisha

3 Nefi 1:1–26Unabii kuhusu kuzaliwa kwa Yesu Kristo Yatimia na Wanefi wengi waongolewaWaalikewanafunzi wafikirie kuhusu watu ambao wametoa kafara maisha yao kwa ajili ya injili. (Baadhi ya mifano ni Yesu Kristo, Abinadi, baadhi ya Anti-Nefi-Lehi, Joseph and Hyrum Smith. Waulize wanafunzi waeleze ni kwa nini wanafikiri watu wanahitaji kutoa kafara kama hiyo. Wape wanafunzi muda kutafakari wanavyofikiria wangejibu iwapo wangekuwa katika hali ambayo ingewahitaji kutoa maisha yao kwa ajili ya injili. Eleza kwamba miaka mitano baada ya Samweli, Mlamani kuhubiri huko Zarahema, kikundi cha Wanefi waaminifu kilikumbana na uwezekano huu.Fupisha 3 Nefi 1:1–3 kwa kuwaambia wanafunzi kwamba mwana wa Helamani, Nefi, alimkabidhi kumbukumbu takatifu kwa mwanawe Nefi kisha akaondoka nchini. Hakuna aliyejua alikokwenda.Waalike baadhi ya wanafunzi tofauti kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka kwa 3 Nefi 1:4–9. Litake darasa kufuatilia wakitafuta changamoto ambazo Wanefi wauminifu walikumbana nazo.• Ni changamoto gani ambayo waumini walikumbana nayo?• Kwa nini watu wengine wanaweza kuona shida kusalia waaminifu katika hali hii?• Ni nani unayemjua unayeamini kuwa angesalia mwaminifu katika hali hii? Kwa nini

unafikiri watu wale wangebaki waaminifu? Waulize wanafunzi wasome 3 Nefi 1:10–12 kimoyomoyo, wakitafuta kile Nefi alifanya katika wakati huu muhimu.• Ni nini kinachokufurahisha kuhusu majaribu ya Nefi kwa hali hii. Kwa nini?”Alika mwanafunzi asome 3 Nefi 1:13–14 kwa sauti na kuuliza darasa kulipa nathari maa-lum jibu la Bwana kwa maombi ya Nefi. • Bwana alisema nini “angeonyesha kwa ulimwengu? Majibu ya wanafunzi yanapaswa

kuonyesha kwamba Bwana atatimiza maneno yote ambayo alikuwa amesababisha kunenwa na manabii wake.

• Wakati Bwana alipozungumza kuja katika ulimwengu, “kufanya mapenzi ya Baba na Mwana”, Alirejelea upatanisho wake. Ujumbe huu unatusaidia vipi “kujipa moyo."

Waambie wanafunzi wasome 3 Nefi 1:4, 14, –15, 19–21 kimoyomoyo wakitafuta vishazi vinavyosisitiza kwamba Bwana hutimiza maneno ya manabii.• Unafikiri ungejihisi vipi kama ungekuwa miongoni mwa waumini wakati ishara ilipokuja.• Kujua kuwa Bwana hutimiza maneno ya manabii kunakusaidiaje wakati mtu akikashifu

viwango vyako au kukutesa kwa ajili ya imani yako?Waalike wanafunzi wawili au watatu kuchukua zamu wakisoma kwa sauti kutoka 3 Nefi 1:16–18. Uliza darasa kufuatilia wakitafuta jinsi waovu wallivyojibu walipoona ishara iliyo-kuwa imetabiriwa.

Page 443: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

428

SoMo la 116

• Waovu walifahamu nini baada ya ishara kutolewa?• Kwa nini dhambi na kutoamini huelekeza kwenye hofu?Alika mwanafunzi asome 3 Nefi 1:22–23 kwa sauti. Uliza darasa kufuatilia wakitafuta kile shetani alifanya ili kushawishi watu kutoamini kalika ishara za kuzaliwa kwa Bwana.• Shetani alifanya nini? (Aliutuma uongo miongomi mwa watu) Ni nini baadhi ya uongo

ambao shetani hutumia hivi leo?• Ni ukweli upi tunaoweza kujifunza kutoka kwa majibu ya watu kwa uongo wa shetani?

Wasaidie wanafunzi kutambua kanuni ifuatayo: tunapokumbana na uongo wa she-tani, tunaweza kuchagua kumwamini Yesu Kristo na kuongoka. Unaweza kutaka kuandika kanuni hii ubaoni

Ili kuwasaidia wanafunzi kuhisi ukweli na umuhimu wa kanuni hii, shiriki kauli hii na As-kofu Richard C. Edgeley wa Uaskofu Msimamizi. Fikiria kuwapa wanafunzi nakala ya kauli hii inayoweza ambayo inaweza kuwekwa katika maandiko yao.“Kwa sababu ya ukinzani na changamoto tunazo kumbana nazo katika ulimwengu wa leo, ningependa kupendekeza chaguo— moja, chaguo la amani na ulinzi na chaguo ambalo-linafaa kwa wote. Chaguo hilo ni amani.. . . Chagua imani dhidi ya shuku, chagua imani dhidi ya hofu, chagua imani dhidi ya kisichojulikana na kusichoonekana,na chagua imani dhidi ya usorajua. . . .“Wakati mantiki, fikira au akili ya kibinafsi inapokinzana na mafunzo na mafundisho matakatifu au jumbe zenye ukinzani zinapovamia imani yako . . . , chagua kutotupa mbegu nje ya moyo wako kwa kutoamini [ona Alma 32:28]. Kumbuka hatupokei ushuhuda hadi baada ya jaribu la imani yetu(ona Etheri 12:6)” (“Faith—the Choice Is Yours,” Ensign au Liahona, Nov. 2010, 31, 32–33).• Tunaweza kufanya nini ili kuchagua imani dhidi ya kushuku au usorajua? (majibu yana-

weza kujumuisha kuwa tunaweza kuchagua kuomba na kutafuta usaidizi wa Bwana, ku-soma maandiko, kuweka amri, kuhudhuria mikutano ya kanisa na kuwahudumia wengine.

Waaalike wanafunzi kusoma 3 Nefi 1:24–25 kimoyomoyo na kutambua changamoto za ziada ambazo baadhi ya waumini walikumbana nazo.• Baadhi ya watu walijaribu kuhakikisha nini kuhusu sheria ya Musa?• Ni nini kinacho kufurahisha kuhusu majibu ya watu hawa walipojua kuwa walikuwa

wamekosea?Andika swali lifuatalo ubaoni: Wakati adui anapojaribu kuniletea shaka nitadumisha vipi imani katika yesu Kristo na injili yake iliyorejeshwa? Waulize wanafunzi kunakili swala hili katika madaftari yao au katika majarida ya mafunzo ya maandiko. Wape dakika chache kuandika majibu yao.

3 Nefi 1:27–30Waasi wa Kinefi na baadhi ya vijana wa Kilamani waungana na wanyang’nanyi wa GadiantoniWaalike wanafunzi wawili kuja mbele ya chumba. Uliza mwanafunzi moja kufunga macho na kusimama kwa mguu moja. Eleza kuwa mwanafunzi huyu anamwakilisha mtu anaye-fahamu ukweli lakini hatumii imani katika baba wa mbinguni na Yesu Kristo na hana bidii katika kuishi injili. Eleza kuwa katika onyesho hili, mwanafunzi wa pili anawakilisha ushawishi unaoweza kumwongoza mtu kukengeuka. Uliza mwanafunzi wa pili kusukuma kwa utaratibu mkono wa mwanafunzi wa kwanza hadi atakapopoteza kapani yake na kuyumbayumba. Eleza kuwa wakati mtu haweki bidii kuishi injili, yeye ni rahisi kudanganywa na uongo na majaribu ya shetani. • Mwanafunzi wa kwanza anahitaji kufanya nini ili kuwa imara? (Mwanafunzi anapaswa

kufungua macho yake na kusimama kwa miguu yote miwili.)Agiza mwanafunzi wa kwanza kufungua macho yake na kusimama kwa miguu yote miwili kwa umbali ulio sawa na mabega*. Eleza kuwa mwanafunzi huyu sasa anawakilisha mtu ambaye ni “imara na asiyetikisika katika imani”(Helamani 15:8). Kisha mwambie Mwa-nafunzi wa pili kusukuma kwa utaratibu mkono wa mwanafunzi wa kwanza tena. Toa

Page 444: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

429

3 nefi 1

angalizo kwamba wakati mtu akiwa anabidii ya kujifunza injili na kuweka amri za Mungu yeye huwa imara hata pingamizi zikija.Waambie wanafunzi hawa wawili kurudi vitini mwao. Eleza kuwa miaka michache baada ya ishara za kuzaliwa kwa Yesu Kristo, Shetani aliendelea kujaribu kuwafanya watu kuwa na shaka kuhusu ukweli wa injili.Alika wanafunzi wachache wachukue zamu kusoma kwa sauti kutoka kwa 3 Nefi 1:27–29. Uliza darasa lifuatilia wakitafuta ushawishi ambao watu waisokuwa wa haki walikuwa nao kwa baadhi ya vijana wa kilamani.• Ni nini kilitendeka kwa baadhi vijana wa Kilamani? (“Walipotoshwa na baadhi ambao

walikuwa Wazoramu,”na walijiunga na wanya’ganyi wa Gadiantoni)• Kulingana na 3 Nefi 1:29, kwa nini baadhi ya vijana Walamani waliamaini “uongo” na

“sifa bandia za Wazoramu? (Kama mwanafunzi wasipotaja kauli ya Mormoni kuwa vijana “walijitegemea wenyewe” toa angalizo kwao,)

• Unafikiria kishazi “walijitegemea wenyewe” kinamaanisha nini?Wanafunzi wanapojadili swali hili,soma kile dada Kathleen H. Hughes,mshiriki wa Urais Mkuu wa muungano wa Usaidizi wa kina mama,alisema kuhusu kishazi hiki:“Inaonyesha kwangu kuwa waliangalia wenyewe kwanza na kujiingiza kwenye shauku ambazo manabii walikuwa wamewaonya waziepuke. Walijisalimisha kwenye ushawishi wa shetani na mavutio ” (“Grow Up unto the Lord,” Ensign, Feb. 2010, 18).Mualike mwanafunzi kusoma 3 Nefi 1:30 kwa sauti. Uliza darasa kufuatilia wakitafuta ushawishi wa “Kizazi kinachoinukia” (vijana) kwa wengine.• Ni athari gani ambayo kizazi kinachoinukia kilikuwanacho kwa imani ya wale waliokuwa

karibu nao.Ili kuwasaidia wanafunzi kulinganisha masimulizi haya na hali za siku hizi, uliza maswali yafuatayo:• Ni nini baadhi ya “uongo” na maneno ya “sifa za uongo”ambazo zinazoweza kushawi-

shi vijana hivi leo kujihusisha na vikundi visivyo vya haki?• Ni wakati gani umeona vijana wakiwa na athari mbaya kwa imani ya wengine?Waulize wanafunzi kutaja kanuni inayofupisha kile tunachoweza kujifunza kutokana kwa 3 Nefi 1:29–30. Wanaweza kutumia maneno tofauti kueleza majibu yao lakini hakikisha wanatambua ukweli ufuatawo Tukijisalimisha katika majaribu mifano yetu inaweza kuwa na mgongano hasi katika imani na haki za wengine. Unaweza kutaka kuwahi-miza wanafunzi kuandika ukweli huu katika maandiko yao.Toa angalizo kwamba ingawa vijana waliotajwa katika 3 Nefi 1:30 walikuwa na athari hasi kwa imani za wengine, vijana pia wanaweza kuwa na athari ya haki kwa wale waliokaribu nao. Alika mwanafunzi aje ubaoni na kuwa kama mwandishi wa darasa. Mwambie mwa-ndishi aandike majibu ya wanafunzi kwa swali lifuatalo:• Ni zipi baadhi ya njia unazoweza kuwa nazo zenye athari nzuri kwenye imani ya familia

yako, kata au tawi na jamii yako?Himiza mwanafunzi kuchagua wazo moja au mawili ubaoni ambayo watafanya mara moja. Wahakikishie kwamba wanaweza kuimarisha imani za wengine kupitia kwa nguvu ya mifano yao ya haki.

Tangazo na Habari za Usuli3 Nefi 1:29–30. Uovu wa kizazi kinachoinukia”

Rais Henry B. Eyring wa Urais wa kwanza anaeleza athari ya mtu mmoja anayepotoka inavyoweza kuwa kwa familia:

"Vijana wa Kanisa wana siku za usoni mikononi mwao. Kanisa daima limekuwa kizazi kimoja kutoka kwenye

maangamizi. Ikiwa kizazi kizima kingepotea,ambacho hakiwezi kutendeka, tungepoteza kanisa. Lakini hata mtu mmoja akipotea kwa injili ya Yesu Kristo kunafu-nga milango kwa vizazi vya uzao, ila Bwana anyoshe mkono wake kurejesha baadhi yao” (“We Must Raise Our Sights” [address to CES religious educators, Aug. 14, 2001], 1, si. Lds. Org).

Page 445: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

430

UtanguliziBaada ya watu kuona ishara za kuzaliwa kwa Yesu Kristo, walianza kutoshangazwa na ishara, na wakafa-nya mioyo yao kuwa migumu. Wengi wa watu waalipu-uza ishara zaidi na maajabu na wakaongezeka katika uovu. Kwa hivyo, wanyag’anyi wa Gadiantoni wakawa imara zaidi hata Wanefi na walamani wakalazimika kuchukua silaha dhidi yao. Walamani walioongolewa

waliungana na Wanefi na wakajulikana kama Wanefi. Lakoneo, mwamuzi mkuu wa Wanefi, akawataka watu watubu na akawatayarisha kwa vita. Kwa sababu ya toba yao, imani yao katika Bwana na matayarisho yao ya bidii, Wanefi waliwashinda wanyag’anyi wa Ga-diantoni. Kufuatia ukombozi wao, watu walitambua uwezo wa Mungu katika kuhifadhi kwao

SOMO LA 117

3 nefi 2–5

Mapendekezo ya Kufundisha

3 Nefi 2Walamani walioongolewa waliungana na Wanefi ili kujilinda dhidi ya wanyag’anyi wa GadiantoniWaalike wanafunzi wachukue dakika chache kuorodhesha katika madaftari au majarida ya mafunzo na maandiko baadhi ya matukio ya kiroho waliyo yapata. Wakumbushe kwamba matukio ya kiroho hayahitaji kuwa ya maigizo au yasiyo ya kawaida ili kuwa na maana. Pendekeza kuwa watafakari nyakati ambapo wamehisi upendo wa baba yao wa mbinguni au ushawishi wa Roho Mtakatifu. Kwa mfano, wanaweza kuandika kuhusu matukio wali-yokuwanayo wakati walipopokea majibu ya sala, wakati walipopokea baraka za ukuhani, au wakati walipo wahudumia wengine. Watakapomaliza kuandika, waulize kwa nini wana-fikiri ingekuwa muhimu kukumbuka matukio ya kiroho ya sasa na katika miaka 10 au 20 katika siku za usoni.Mwalike mwanafunzi asome 3 Nefi 2:1–3 kwa sauti. Uliza darasa kufuatilia wakitafuta nini ki-lichotokea wakati watu walipoanza kusahau ishara zilizohusiana na kuzaliwa kwa Mwokozi.• Ni kweli zipi zinazofundishwa na simulizi hili kuhusu hatari ya kusahau matukio ya kiroho. Wanafunzi wanaposhiriki kweli walizotambua sisitiza kanuni ifuatayo: Kama Tukisahau matukio ya kiroho ya awali, tunakuwa katika hatari zaidi ya majaribu ya Shetani na udanganyifu. Unaweza ukitaka kuandika kanuni hii ubaoni. Unaweza pia kutaka kuwahimiza wanafunzi kuiandika chini ya orodha zao za matukio ya kiroho.• Unafikiri ni kwa nini kusahau matukio ya kiroho hutufanya tuwe katika hatari ya Shetani.• Tunaweza kufanya nini ili kuhakikisha kuwa hatusahau matukio ya kiroho tuliyokuwa

nayo? (Majibu yanaweza kujumuisha kushirikiana matukio na wengine panapofaa, kua-ndika katika jarida la binafsi, au kunakili uzoefu kutoka kwa shughuli za Duty to God au Personal Progress.)

Mwalike mwanafunzi asome kauli ifuatayo ambapo Rais Henry B. Erying wa Urais wa kwanza anaeleza jinsi kunakili matukio ya kiroho katika jarida kulimsaidia. Uliza darasa lisikilize baraka ambazo zinaweza kuja kutokana na kuweka kumbukumbu kama hiyo:

“Niliandika mistari michache kila siku kwa miaka. Sikukosa kamwe hata siku moja bila ya kujali nilivyochoka, au jinsi gani ilibidi niamke mapema kuanza siku iliyofuata. Kabla sijaandika, nilitafakari swali hili: ”Nimeona mkono wa Mungu ukinyooka kutugusa, au watoto wetu au familia yetu hivi leo?” "Nilivyoendelea kitu fulani kilianza kutokea. Nilivyotupa mawazo yangu siku mzima, niliweza kuona ushahidi wa kile Mungu amefanya kwa

mmoja wa [wanafamilia wetu]ambacho sikuweza kutambua katika, nyakati za shughuli nyingi za siku. Na yale yalipotokea,na yalitokea mara kwa mara, nilielewa kwamba kujaribu kukumbuka kulimruhusu Mungu kunionesha nini alichokifanya.“Zaidi ya shukrani ilianza kuwa ndani ya moyo mwangu. Ushuhuda ukakuwa. Nikawa daima mwenye hakika kwamba Baba yetu wa mbinguni husikia na kujibu maombi. Nilihisi

Page 446: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

431

3 nefi 2– 5

shukrani zaidi kwa kulainika na kusafishwa kunakokuja kwa sababu ya upatanisho wa Mwokozi Yesu Kristo. Na nilikuwa na uhakika zaidi kwamba Roho Mtakaifu anaweza kuleta mambo yote katika kumbukumbu zetu —hata vitu ambavyo hatukuviona au kuvipa nathari ni lini vilitokea” (“O Remember, Remember,”) Ensign or Liahona, Nov. 2007, 67).Waalike wanafunzi washiriki jinsi kukumbuka matukio ya Kiroho— kupitia kuandika katika shajara au kwa njia nyingine —kumewasaidia kubaki waaminifu licha ya juhudi za Shetani kuwajaribu au kuwadanganya.Fupisha 3 Nefi 2:4–19 kwa kueleza kwamba watu walipoendelea katika uovu, wanya’ganyi wa Gadiantoni waliongezeka katika idadi na nguvu. Wanya’ganyi wa Gadiantoni walikuwa na fujo na hasira, na Walamani walioongolewa waliungana na Wanefi na kupigana dhidi yao. Ingawa walikuwa na mafanikio kiasi katika kuwafukuza wanya’ganyi wa Gadiantoni kutoka kwenye arthi yao, Wanefi (pamoja na Walamani walioongolewa, ambao sasa waliitwa Wa-nefi) walikuwa bado katika hali ya hatari miaka 15 baada ya ishara ya kuzaliwa kwa Kristo.

3 Nefi 3:1–10Kiongozi wa wanyag’anyi wa Gadiantoni anaamuru kuwa Wanefi wasalimu amriEleza kwamba katika 3 Nefi 3:1–10, tunaona mfano wa jinsi adui anaweza wakati mwi-ngine kuwatumia wengine kujaribu kudhoofisha imani yetu na kutupotosha. Giddianhi, kiongozi wa wanyag’anyi wa Gadiantoni aliandika barua kwa Lakoneyo, hakimu mkuu wa Wanefi kumshawishi ajisalimishe kwa Wanyang’anyi wa GidiantoniAndika Giddianhi anamjaribu Lakoneyo ubaoni. Waambie nusu ya darasa wasome 3 Nefi 3:2–5 kimoyomoyo na nusu nyingine wasome 3 Nefi 3:6 –10 kimoyomoyo. Wanafunzi wa-naposoma, wafanye watafute maneno au vishazi vinavyoonyesha mbinu ambazo Giddia-nhi alitumia kujaribu kudhoofisha imani ya Lakoneyo na kumpotosha. Baada ya wanafunzi kumaliza kusoma, waambie watoe taarifa ya nini walichokipata. Mwalike mwanafunzi aandike majibu yao ubaaoni.Ili kufupisha mbinu ambazo wanafunzi wametambua katika 3 Nefi 3:2–10, andika ukweli ufuatao ubaoni chini ya orodha ya wanafunzi: shetani na wafuasi wake mara nyingi hutumia sifa za uongo, ahadi za uongo, vitisho ili kupotosha watu. Waalike wanafunzi kuchukua moja ya mbinu za Giddianhi zilizoandikwa ubaoni na kueleza jinsi shetani na wafuasi wake wanavyoweza kutumia mbinu kama hiyo kwa vijana siku hizi. Ili kuwasaidia wanafunzi kutafuta baadhi ya vifananisho hivi, unaweza kutaka kuuliza maswali kama yafuatayo:• Ni ipi baadhi ya mfano ambayo adui anaweza kutumia sifa za uongo (sifa zisizo za kweli au

sifa kupita kiasi) kwa vijana siku hizi? Ni zipi baadhi ya ahadi za uongo au vitisho vya uo-ngo ambavyo adui anaweza kutumia? Unafikiri vijana wanaweza kukinza vipi mbinu hizi?

3 Nefi 3:11–5:7Watu wa Lakoneyo wajitayarisha kujilinda, na wanalishinda wanyag’anyi wa Gadiantoni?Mualike mwanafunzi kusoma 3 Nefi 3:11–30 kwa sauti. Uliza darsa kufuatilia wakitafuta jinsi Lakoneyo alivyo jibu barua ya vitisho ya Giddianhi.• NI kweli zipi tunazoweza kujifunza kutokana na jinsi Lakoneyo alivyo mjibu Giddianhi.

(Ukweli moja wanafunzi huenda wakatambua ni kwamba wanaume na wanawake wenye haki hawahitaji kuogopa waovu na hawapaswi wakubali vitisho vyao)

Gawa darasa katika vikundi vinne. Kipatie kila kikundi kipande kikubwa cha karatasi. Fanya vikundi kugawanya karatasi zao katika masafu mawili, moja iliyo andika Matayarisho ya Lakoneyo na nyingine iloyoandikwa vifananisho vya Kisasa. Andika mafungu yafuatazo ya maandiko ubaoni na mpangie mmoja afundishe kikundi: 3 Nefi 3:12–15; 3 Nefi 3:16–21; 3 Nefi 3:22–26; 3 Nefi 4:1–4. Waambie wanafunzi wasome mistari waliyopangiwa wakitafuta njia ambazo Lakoneyo aliwatayarisha watu wake kiroho na kimwili ili kuzuiya mashambullizi ya wanyag’anyi wa Gadiantoni. Chini ya Matayisho ya Lakoneyo. Wezesha mwanafunzi kutoka kila kikiundi kuandika kile watu walifanya ili kujitayarisha. Angalizo: Wanafunzi wanaposoma mistari hii, hakikisha kuwa wana tofautisha kati ya Giddianhi, kiongozi wa wanyag’anyi wa Gadiantoni, na Gidgiddoni, nabii mkuu na kapteni mkuu wa Wanefi.

Page 447: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

432

SoMo la 117

Baada ya wanafunzi kuwa na wakati wa kutosha kukamilisha orodha zao chini ya Mata-yarisho ya Lokoneyo waabie waorodheshe chini ya Vilinganisho vya kisasa. Matayarisho ya kiroho na kimwili ambayo tumeshauriwa kufanya katika siku za mwisho. Wakati Wana-funzi wakisha kuwa na muda wa kutosha kukamilisha kazi hii waliyo pangiwa Mwalike mwanafunzi mmoja kutoka kwa kila kikundi kishiriki pamoja na darasa kile kikundi chake kimejifunza. Ili kuwasaidia wanafunzi kuamua jinsi wanavyoweza kutumia walichojifunza, uliza maswali kama yafuatayo wakati wa au baada ya maonyesho. • Tunawezaje kuimarisha nyumba zetu dhidi ya mashambulizi ya adui?• Kwa nini matayarisho ya muda— kama vile kupata elimu na uhifadhi wa nyumbani —

yana umuhimu katika siku za mwisho.• Kujikusanya katika familia na kata au matawi yanatoaje ulinzi kwetu?• Ni wakati gani maombi yamekusaidia kupata nguvu za kiroho? • Toba inawezaje kututayarisha kwa siku za usoni?• Ni baraka zipi huja tunapofuata manabii walio hai na mitume?• Tunawezaje kualika roho ya ufunuo katika maisha yetu?Waalike wanafunzi wachache kuchukua zamu ya kusoma kwa sauti kutoka 3 Nefi 4:7–12. Litake darasa kufuatilia wakitafuta njia ambazo watu walibarikiwa kwa sasbabu ya mataya-risho yao ya kiroho na muda.• Ni kweli zipi ulizojifunza kutoka kwa simulizi hili? Wanafunzi wanaposhiriki majibu yao,

sisitiza kanuni ifuatayo Tunapojitayarisha kiroho na kwa muda Bwana atatuimari-sha kushinda changamoto.)

Fupisha 3 Nefi 4:13–29 kwa kueleza kwamba Lakoneyo na watu wake waliwashinda wanyag’nyi wa Gadiantoni na kuwauwa viongozi wao. Soma 3 Nefi 4:30–33 kwa sauti. Wa-alike wanafunzi kufuatilia wakitafuta jinsi watu walivyojibu ushindi huu.• Watu walijibu vipi baada ya Bwana kuwaokoa kutoka kwa maadui zao.• Watu walitambua nini kama chanzo cha kuokolewa kwao kutoka kwa wanyang’anyi wa

Gadiantoni. (Toba yao na unyenyekevu wao na wema wa Mungu. Unaweza kutoa anga-lizo kwamba tunapotubu na kunyenyekea, Mungu atatuidhinisha na kutuokoa kutoka kwa majaribu yetu.)

Unaweza kutaka kushiriki tukio ambapo ulimtegemea Mungu na akakusaidia kuvumilia au kushinda jaribio. Unaweza pia kualika mwanafunzi mmoja au wawili kushiriki tukio kama hilo.Alika mwanafunzi asome 3 Nefi 5:1–4 kwa sauti. Uliza darsa kufuatilia wakitafuta kile Wanefi walifanya kutokana na usaidizi wa baraka walizopokea katika vita vyao dhidi ya wanyang’anyi wa Gadiantoni. Wanafunzi wanaposhiriki walichopata sisitiza, kwamba mo-jawapo ya njia ambayo watu walijibu ilikuwa ni kuhubiri injili kwa wengine.

3 Nefi 5:8–26Amani inarejeshwa miongoni mwa watu: Mormoni ueleza kuhusu ufupishaji wake wa kumbukumbuWaalike wanafunzi kuwa salio la 3 Nephi 4:13–29 lina maelezo ya Mormoni ya kwa nini alifupisha kumbukumbu hii. Waambie wanafunzi wasome 3 Nefi 5:12–15 kimoyomoyo wakitafuta kile Mormoni alisema kuhusu jukumu lake la kuandika ufupisho wa kumbu-kumbu za Wanefi.• Ni kweli ipi uliyojifunza kutoka kwenye mistari hii inayoeleza jukumu letu kama wafuasi

wa Yesu Kristo? (Ingawa wanafunzi wanaweza kutumia maneno tofauti, wanapaswa kutambua kweli ifuatayo: kama wafuasi wa Yesu Kristo, tuna jukumu la kufundi-sha wengine njia ya kwenda kwenye uzima wa milele. Unaweza ukitaka kuandika ukweli huu ubaoni.

Toa angalizo kwamba moja wapo ya njia muhimu tunayoweza kuonyesha shukrani zetu kwa Bwana kwa baraka anazotupa ni kwa kuwasidia wengine kuja kwake na kupokea ba-raka hizo hizo. Waambie wanafunzi wapendekeze njia chache ambazo wao kama wafuasi wa Yesu Kristo wanaweza kufundisha wengine njia ya uzima wa milele. Wahimize wana-funzi kuchagua moja au mawili ya mapendekezo haya kwa kushiriki injili na kwa maombi kutuafuta msaada wa Bwana katika kutekeleza kile wanachochagua kufanya.

Page 448: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

433

UtanguliziKufuatia kuokolewa kwao kimiujiza kutoka kwa wa-nyang’anyi i wa Gadiantoni, Wanefi walifurahia amani kwa takribani miaka mitatu. Lakini kiburi, migawanyiko ya matabaka, na mateso yalianza miongoni mwa watu. Wakati baadhi walibakia waaminifu kwa Bwana, wengi

waalingia katika makundi ya kisiri. Kwa sababu ya ma-kundi ya siri, mwamuzi mkuu aliuawa na serikali ya Wa-nefi kupinduliwa. Watu waligawanyika katika makabila na kuchagua viongoni wao wenyewe. Nefi alihudumia watu kwa uwezo na mamlaka makubwa.

SOMO LA 118

3 nefi 6–7

Mapendekezo ya Kufundisha

3 Nefi 6:1–18Kufuatia msimu wa ufanisi, Wanefi wakawa na kiburi na kanisa likavunjikaAndika maswali yafuatayo ubaoni mbele ya darasa. Waambie wanafunzi wajibu na kuelezea majibu yao.

Je! Inawezekana kwa mtu kuwa . . .Tajiri na mnyenyekevu?Maskini na jeuri?? Mwenye Elimu na mnyenyekevu? Asiye na elimu na mwenye kiburi?

Wahimize wanafunzi waendelee kufikiri kuhusu maswali haya wanapojifunza 3 Nefi 6. Fu-pisha 3 Nefi 6:1–9 kwa kuelezea kwamba baada ya Wanefi na Walamani kushinda Wanya-nganyi wa Gidiatoni walidumisha amani katika nchi na walianza kufanikiwa. Lakini baada ya muda mfupi, amani yao na ufanisi ukawa katika tishio.Alika mwanafunzi kusoma 3 Nefi 6:5, 10–12 kwa sauti na litake darasa kutafuta kile kili-choanza kutishia amani na ufanisi wa watu.• Ni nini kilianza kutokea ambacho kilitishia amani na ufanisi wa watu?• Umewahi kuona malimbikizo ya mali au kujifunza kunasababisha matatizo kama haya

katika shule. Ikiwa hivyo, ni kwa njia gani?Chora mstari wima chini katikati mwa ubao ili kutengeneza safu mbili Andika - enye kiburi juu ya safu moja na Mnyenyekevu juu ya safu nyingine Waambie wanafunzi wapekue 3 Nefi 6:13–14, wakitafuta maneno na vishazi ambavyo vinaeleza jinsi watu walivyofanya wakati mali na elimu vilipoanza kuwagawanya. (Unaweza ukitaka kueleza kwamba ku-tukana au kutusi kunamaanisha kukosoa kwa hasira na kuzungumza kwa madharau kwa mtu.) Wanafunzi watakapomaliza kusoma, waambie waandike katika safu inayositahili ubaoni maneno na vishazi walivyopata• Ni ushahidi gani unaoona katika 3 Nefi 6:13 kwamba baadhi ya waliokuwa wakiteswa

kwa kiburi walikuwa wanajibu mateso haya na kiburi?• Kwa nini unafikiri kurudisha “matusi kwa matusi ” (au ukosoaji kwa ukosoaji) ni ishara

ya kiburi?• Ni nini kinacho kufurahisha kuhusu jinsi Walamani walioongolewa walijibu wakati huu?• Ni kanuni zipi tunazoweza kujifunza kutoka 3 Nefi 6:13–14? (majibu ya wanafunzi yana-

weza kutofautiana lakini wanapaswa kutambua kanuni ifuatayo: Tunaweza kuchagua kuwa wanyenyekevu na waaminifu licha ya hali zetu.)

Warejeshe wanafunzi kwenye safu ubaoni ambayo inaoorodhesha majibu ya unyenyekevu Uliza maswali yafuatayo.

Page 449: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

434

SoMo la 118

• Ni matendo yapi tunayoweza kufanya kutusaidia kubaki wanyenyekevu na waaminifu katika hali yoyote? (Orodhesha majibu ya wanafunzi ubaoni katika safu iliyoalamishwa Wenye unyenyekevu.)

• Fikiria mtu ambaye unahisi ni mfano mzuri wa kuchagua kuwa mnyenyekevu na mwe-nye imani licha ya hali yake. Je ni jinsi gani mtu huyu ni mfano wa unyenyekevu?

Eleza kuwa kwa sababu wengi wa Wanefi hawakutubu juu ya kiburi chao, hali yao ilizidi kuwa mbaya. Waambie wanafunzi wachache kuchukuwa zamu kusoma kwa sauti kutoka 3 Nefi 6:15–18. Uliza darasa lifuatilie likitafuta jinsi kiburi cha watu kilivyomruhusu Shetani kuwaathiri. • Aya hizi zinafundisha nini kuhusu uhusiana kati ya kiburi na uwezo wa Shetani wa kutu-

jaribu? (Wanafunzi wanapojibu,wasaidie kutambua ukweli ufuatao: Wakati Tunapokuwa na kiburi, tunamruhusu Shetani uwezo mkubwa zaidi kutujaribu na kutuelekeza kutenda dhambi zaidi. Unaweza ukitaka kuwahimiza kuandika kanuni hii katika maa-ndiko yao matakatifu au katika majarida au vitabu vya mafunzo ya maandiko.)

• Kulingana na 3 Nefi 6:15–18, ni maneno yapi na vishazi vipi vinavyoeleza kuhusu mba-diliko wa moyo wa uovu ambao watu hawa walipata kwa sababu ya kiburi. (Walihanga-ishwa na majaribio mahali pote [Shetani] alipotaka kuwapeleka, na kufanya aina yote ya maovu aliyotaka wafanye. Walikuwa katika hali ya "uasi kwa makusudi” na walikuwa “kwa makusudi wakiasi dhidi ya Mungu”)

• Kwa nini unafikiria kiburi hutuadhiri hadi kiwango ambapo Shetani anaweza kutushawishi. Zaidi ya majibu ambayo wanafunzi walitoa, fikira kumwalika mwanafunzi kusoma kauli ifuatayo kutoka kwa Rais Henry B. Eyring. Waambie wanafunzi kusikiliza kile Rais Eyring alionya kuwa ni mojawapo ya hatari za kiburi.“Kiburi hujenga kelele ndani yetu inayofanya sauti tulivu ya roho kuwa vigumu kuisikia. Na punde, katika anasa zetu, hatuhitaji hata kuisikiliza. Tunaweza kuja haraka kufikiria kuwa “hatuihitaji” (“Prayer,” Ensign, Nov. 2001, 16).

• Kwa nini ni hatari kutosikiliza tena sauti ya roho. Wasaidie wanafunzi kuelewa kwamba wakati tunapopuuza minong’ono ya roho mtakatifu, tunakuwa wapesi kwa majaribu ya Shetani.

Rejesha wanafunzi tena kwenye orodha ya majibu ya unyenyekevu ubaoni. Waambie wa-chague jibu moja la unyenyekevu ambalo wanahisi litakuwa lenye msaada mkubwa kwao binafsi. Wape dakika chache kuandika kuhusu jinsi watakavyoanza mara moja kutupia pendekezo hilo shuleni au nyumbani.

3 Nefi 6:19–7:14Makundi ya kisiri yaangamiza serikali ya Wanefi na watu kugawanyika katika makabilaNakili mstari ufuatao wa wakati ubaoni

Gawanya darasa katika makundi manne na pangia kila kundi mojawapo ya mafungu ya maandiko ubaoni. Waambie wanafunzi wasome mafungu waliyopangiwa kimoyomoyo, wa-kitafuta matukio maalumu yaliyotokea miongoni mwa Wanefi. Baada ya wanafunzi kuwa na muda wa kutosha wa kusoma. Mwalike mwanfunzi kutoka kwa kila kundi kuandika matukio maalum kutoka kwa aya waliyopangiwa kusoma chini ya sehemu inayolingana katika mistari wa wakati (wanafinzi wengine katika kila kundi wanaweza kusaidia) Watakapomaliza, eleza kwamba orodha ya matukio yanaonesha jinsi vikundi vya kisiri vilisababisha kuanguka kwa serikali ya Kinefi na kugawanyika kwa watu katika makabila. Waaite wanafunzi wachache kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka 3 Nefi 6:27–30. Uliza darasa kufuatilia na kutambua mwanzilishi na kusudi la makundi ya kisiri. Wanafunzi wakishamtambua mwanzilishi wa makundi ya kisiri (Ibilisi), uliza:• Ni maneno yapi na vishazi vinavyoeleza makusudi ya makundi ya kisiri? (Majibu yana-

weza kujumuisha “Ungana dhidi ya haki yote,” “Angamiza ” watu wa Bwana, “walidha-rau sheria na haki za nchi yao,” na “nchi isiwe na uhuru”.)

3 nefi 6:19–24 3 nefi 6:25–30 3 nefi 7:1–8 3 nefi 7:9–14

Page 450: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

435

3 nefi 6 –7

• Wale waliowaua manabii waliwezaje kukwepa adhabu? (Marafiki na familia zao, ambao pia walikuwa washiriki wa makundi ya kisiri, waliungana ili kuwasaidia kuweka mate-ndo yao siri kuepuka na matokeo ya matendo yao.

• Fikiria kama una baadhi ya marafiki wanaotaka kuepuka na matokeo ya matendo yao. Unaweza vipi kuwasaidia kuishi injili na viwango vyake badala yake.

Waalike wanafunzi wachache wachukue zamu kusoma kwa sauti kutoka kwa 3 Nefi 7:1–8. Uliza darasa kufuatilia wakitafuta matokeo ya makundi ya kisiri miongoni mwa Wanefi. Eleza kuwa ibilisi huwashawishi watu kuingia makundi ya kisiri katika juhudi ya kuangamiza haki na kuongeza uovu. Wasaidie wanafunzi kuelewa kwamba mbinu na nia za makundi ya kisiri mara nyingi huwa za kificho, na siku zote sio rahisi kugundua. Wahimize kuepukana na kuungana na vikundi vyovyote au watu binafsi wanaofanana na makundi ya kisiri kwa njia yoyote ile.

3 Nefi 7:15–26Wakati wa muda ambapo wachache ni waaminifu, Nefi aendelea kuhudumu na baadhi waongelewa• Unafikiria angehisi vipi kama ungeishi miongoni mwa Wanefi baada ya serikali yao

kupinduliwa? Kwa nini?”• Unafikiri ni wapi ungegeukia kwa ajili ya uongozi na mwongozo?Waambie wanafunzi wachache wachukue zamu kusoma kwa sauti kutoka kwa 3 Nefi 7:15–20. Uliza darasa kufuatilia wakitafuta sababu kwa nini wangetaka kumfuata Nefi katika hali hii. Fikiria kuwafanya wanafunzi kutua baada ya kila aya au mbili ili uweze kuwauliza wanafunzi kueleza kwa nini wangeweza kuhamasishwa kumfuata Nefi.• Nini ulikuwa ujumbe wa Nefi kwa watu wakati huu? (Ona 3 Nefi 7:16.)• Ni vipi viongozi wa kanisa hivi leo ni kama Nefi. • Ni lini umemwona kiongozi wa kanisa “akihudumu kwa uwezo na mamlaka makuu”?

(3 Nefi 7:17).Waambie wanafunzi wasome 3 Nefi 7:21–26 kimoyomoyo na watambue jinsi wale wali-oongolewa walibarikiwa kwa kumfuata Nefi na kutubu dhambi zao. Waalike wanafunzi kadha waeleze kile walichokipata• Ni kanuni zipi tunazoweza kujifunza kutoka kwa mfano wa wale waliotubu na kum-

fuata Nefi?Wanafunzi wanaweza kushiriki kweli tofauti lakini wanapaswa kutambua kanuni ifua-tayo: kama Tukitubu na kuwafuata watumishi wa Bwana, tutapokea ushawishi wa roho mtakatifu:• Kwa nini toba ni muhimu kwetu ili tuweze kuwa na roho mtakatifu?• Unafikiri ni kwa nini kufuata watumishi wa Bwana kunatusaidia kuwa wapokezi zaidi

kwa mwongozo wa roho Mtakatifu?. Soma kauli ifuatayo ya Rais James E. Faust wa Urais wa Kwanza.

"Nimeamua kuwa uongozi wa kiroho kwa kiwango kikubwa hutegemea kuwa katika hali ya uwiano na Rais wa Kanisa, Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili —wote ambao tunawaidhinisha. . . kama manabii, waonaji na wafunuzi. Sijui ni vipi tunavyoweza kutegemea kuwa katika uwiano mtimilifu na Roho wa Bwana kama hutupo katika uwiano na Rais wa Kanisa, na manabii wengine, waonaji na wafunuzi. ” (Called

and Chosen,” Ensign au Liahona, Nov. 2005, 53).• Ni lini umehisi ushawishi wa Roho Mtakatifu kwa sababu umechagua kuwa mtiifu kwa

watumishi wa Bwana?Wahimize wanafunzi kuandika hisia walizopokea kuhusu nini wanachoweza kufanya ili kutumia kweli walizojifunza leo. Sisitiza kwamba hata wakati wengine wanapochagua kuishi kinyume na amri za Mungu, kama ilivyokuwa kwa baadhi ya Wanefi, tunaweza kuchagua kwa unyenyekevu kumfuata Mungu na watumishi wake wateule.

Page 451: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

436

UtanguliziMiaka thelathini na mitatu baada ya kuona ishara ya kuzaliwa kwa Mwokozi, Wanefi walianza kutafuta ishara ambayo Samueli Mlamani alitabiri kuhusu kifo cha Mwokozi. Ingawa ishara nyingi zilitolewa, wasiwasi na mabishano yalianza miongoni mwa watu. Katika mwaka uliofuata, utabiri wa Samueli ulitimia. Baada ya dhoruba kubwa, mitetemeko ya ardhi, na majanga

mengine, yalisababisha uharibifu, giza likatanda juu ya nchi kwa muda wa siku tatu. Katika giza, watu walio-nusurika uharibifu walisikia sauti ya Yesu Kristo. Aliwa-alika kutubu na kurejea Kwake. Wakati giza lilipoinuka, maombolezo ya watu yaligeuka kuwa furaha na sifa kwa Yesu kristo.

SOMO LA 119

3 nefi 8–10

Mapendekezo ya Kufundisha

3 Nefi 8:1–18Uharibifu mkubwa unaashiria kifo cha Yesu Kristo, ukitimiza utabiri wa Samueli Mlamani Anza darasa kwa kuuliza swali lifuatalo.: • Unafahamu ishara zozote ambazo zimetimia, zikionyesha kuwa ujio wa pili wa

Mwokozi uko karibu? (Unaweza kutaka kutoa angalizo kwamba utabiri mwingi kama ule wa Urejesho wa injili, ujio wa nabii Eliya, na injili kuhubiriwa kote ulimwenguni, umetimia. Au unatimia)

• Unahisi vipi unapotambua kitu kama ishara ya wazi kwamba Ujio wa Pili wa Mwokozi unakaribia?

Eleza kuwa tunaishi katika wakati uliofanana na wakati kabla ya Yesu Kristo kuwatembelea Wanefi. Kama vile Wanefi walipotazama ishara ambazo Samueli Mlamani alikuwa ameta-biri kuwa zingeashiria kifo na Ufufuo wa Yesu kristo, nasi tunapaswa, kutazamia ishara za Ujio wa Pili wa MwokoziWaambie wanafunzi wasome 3 Nefi 8:3–4 kimoyomoyo, wakitambua tofauti katika jinsi baadhi ya Wanefi walihisi kuhusu ishara hizi waambie wanafunzi watoe taarifa ya walicho-pata. (Ingawa watu walingojea ishara kwa hamu kubwa, wasiwasi mkubwa na mabishano yalikuwepo kati yao.)• Ni kwa njia gani hali inayoelezwa katika 3 Nefi 8:3–4 ni sawa na hali ya ulimwengu

hivi leo?• Tunawezaje kuimarisha imani yetu katika Yesu Kristo hata wakati wengi waliotuzunguka

wanaonyesha shaka?Uliza wanafunzi kama wamewahi kupatwa na dhoruba kali, tetemeko la ardhi au janga lo-lote. Wanafunzi wanapojibu, waalike washiriki jinsi walivyohisi wakati na baada ya tukio hilo.Alika mwanafunzi asome 3 Nefi 8:5–7 kwa sauti. Litake darasa kufuatilia, wakitafuta nini kilitokea katika mwaka wa 34 baada ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Kisha walike wanafunzi wasome 3 Nefi 8:8–18 kimoyomoyo, wakitafuta nini kilitokea kwa wakaazi wa miji hiyo. Fanya wanafunzi watoe taarifa nini wamepata. Wakumbushe wanafunzi kuwa Samueli Mlamani ali-kuwa ametabiri mambo haya (ona Helamani 14:20–27). Sisitiza kwamba maneno ya manabii yatatimizwa yote na kwamba Mungu atawataka waovu kuwajibika kwa matendo yao.

3 Nefi 8:19–25Giza linatanda juu ya nchi kwa muda wa siku tatuEleza kuwa baada ya dhoruba na mitetemeko ya ardhi kusimama, giza lilitanda juu ya ilin-chi kwa siku tatu. Zima taa katika chumba kwa muda. Kisha uliza wanafunzi kama wame-wahi kuwa katika mahali pa giza kabisa, kama vile pango au chumba kisicho na madirisha.

Page 452: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

437

3 nefi 8 –10

• Ulijisikia vipi wakati ulipokuwa mahali pale?Toa angalizo kwamba giza ambalo lilifunika nchi kwa siku tatu lilikuwa tofauti na giza ambalo linalokuja wakati sisi tunapozima taa au kwenda mahali pasipo na madirisha. Waa-mbie wanafunzi wasome 3 Nefi 8:19–23 kimoyomoyo wakiafuta vishazi ambavyo vinaeleza giza ambalo Wanefi walipata (Majibu yanaweza kuwa pamoja na giza nenemvuke wa giza mawingu ya giza, na hakuna mwanga.)Waambie wanafunzi wasome 3 Nefi 8:23–25 kimoyomyo, wakitafuta athari giza lilileta kwa Wanefi ambao walikuwa wamenusurika uharibifu. Fanya wanafunzi watoe taarifa nini wanapata.

3 Nefi 9:1–14Katika giza, Yesu Kristo anawakaribisha wale ambao wamenusurika uharibifu ili kutubu na kuja kwakeAndika maswali yafuatayo kwenye ubao: Watake wanafunzi wasome 3 Nefi 9:1–12 kimo-yomoyo, wakitafuta majibu kwa maswali haya.

Kwa nini uharibifu huu ulitokea?Jinsi gani Shetani alijibu uharibifu huu?Je, hii inafundisha nini kuhusu Shetani na jinsi yeye huwafanyia wale wanao mfuata?.

Soma 3 Nefi 9:13–14 kwa sauti kwa darasa. Waalike wanafunzi kufuatilia pamoja, wakita-futa mwaliko wa Mwokozi kwa wale waliokuwa wameachwa kutoka katika uharibifu. Waa-mbie wanafunzi kufikiria wale Wanefi, wakisikiliza sauti ya Mwokozi katika giza totoro. Waliachwa kwa sababu walikuwa wenye haki zaidi ya hao ambao walikuwa wamehari-biwa, lakini bado walihitajika kutubu na kubadilika (ona 3 Nefi 9:13; 10:12).• Je unafikiri Wanefi walihisi vipi waliposikia mwaliko huu kutoka kwa Mwokozi? Kwa nini?”Mwalike mwanafunzi asome maelezo yafuatayo na Mzee C. Scott Grow wa Wale Sabini:"Yesu Kristo ni Mponyaji Mkuu wa roho zetu"Tunapofanya dhambi, Shetani hutuambia tumepotea. Katika kutofautisha, mkombozi wetu anatoa ukombozi kwa wote — bila kujali tumefanya makosa gani —hata wewe na mimi (The Miracle of the Atonement, Ensign au Liahona, Mei 2011, 109).Thibitisha kwamba mwaliko wa Mwokozi katika 3 Nefi 9:13— kuja kwake na kuponywa —unaelekezwa kwa kila mmoja wetu. Ili Mwokozi aweze kutuponya, ni lazima tukubali mwaliko wake wa kuja kwake, kutubu dhambi zetu, na kuongolewa. Watake wanafunzi kufikiria kuhusu masuala ya maisha yao ambapo wanayo haja ya uponyaji ya Mwokozi. Kisha wakaribishe wajibu swali lifuatalo katika madaftari au majarida ya mafundisho ya maandiko:• Je, unahitaji kufanya nini ili uweze kupokea uponyaji wa Mwokozi katika maisha yako?

3 Nefi 9:15–22Mwokozi anatangaza kwamba kupitia dhabihu yake, sheria ya Musa imetimiaSoma 3 Nefi 9:19 kwa sauti. Uliza darasa kufuatilia pamoja, wakitafuta ni nini Yesu Kristo alisema hangeweza tena kukubali kutoka Wanefi. Inaweza kuwa muhimu kuwakumbu-sha wanafunzi kwamba Wanefi walikuwa wakiishi sheria ya Musa kwa wakati huu. Kama sehemu ya sheria ya Musa, Bwana aliamuru watu wake kutoa toleo la wanyama kama aina na kivuli cha toleo ambalo Mwokozi angetoa kupitia Upatanisho wakeKaribisha wanafunzi wasome 3 Nefi 9:20 kimoyomoyo wakitafuta kile Mwokozi alisema Wanefi walikuwa sasa watoe kama toleo. Wafanye wanafunzi watoe taarifa ya nini wanapata. • Unafikiri inamaanisha nini kutoa toleo la moyo uliovunjika na roho iliyopondeka? • Mwokozi anaahidi baraka gani kwa wale wanaomjia na moyo uliovunjika na roho

iliyopondeka?Eleza kwamba Mzee D. Todd Christofferson wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alifu-ndisha njia moja ya kufikiria kuhusu vishazi “moyo uliovunjika” na “roho iliyopondeka” Soma kauli ifuatayo, ukiwataka wanafunzi kusikiliza maneno ambayo Mzee Christofferson alitumia kutusaidia kuelewa vishazi hivi:

Maswali ya KibinafsiMaswali ya binafsi yana-weza kusaidia wanafunzi kutumia kweli za injili. Hata hivyo, kwa sababu ya asili ya maswali haya, wanafunzi wanaweza kusita kujibu kwa sauti. Kuwakaribisha wana-funzi kujibu maswali binafsi kwa maandishi kunawaruhusu kujibu binafsi, pamoja na uwazi zaidi na majibu ya dhati. Hata hivyo, unapaswa kuwatahadharisha wasi-andike kuhusu mambo ya siri, kama vile dhambi za zamani au makosa.

Page 453: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

438

SoMo la 119

"Unaweza kumtolea Bwana zawadi ya moyo wako uliyovunjika, au kutubu, na majuto yako, au roho ya utiifu. Kihalisi, ni zawadi ya wewe mwenyewe — vile ulivyo na vile unavyokuwa."Je, kuna kitu kwako au katika maisha yako ambacho ni kichafu au kisi-chostahili? Wakati wewe unapokiondoa, hiyo ni zawadi kwa Mwokozi. Je, kuna tabia nzuri au ubora ambao unakosekana katika maisha yako? Wakati

unapokirithi na kukifanya sehemu ya tabia yako, unatoa zawadi kwa Bwana (When Thou Art Converted, Ensign au Liahona, Mei 2004, 12).• Ni neno gani Mzee Christofferson alitumia kutusaidia kuelewa kishazi moyo uliovunjika?

(mwenye kutubu) Unafikiri nini maana ya kuwa na moyo wa toba?• Ni neno gani Mzee Christofferson alitumia ili kutusaidia kuelewa kipengele roho iliyo-

pondeka? (Mtiifu) Utaelezaje mtu mwenye roho ya utiifu?Waambie wanafunzi wasome 3 Nefi 9:21–22 kimoyomoyo, wakitafuta maelezo ya Mwo-kozi ya jinsi tunapaswa kuja kwake. Watake watoe taarifa ya nini wanachokipata. Onyesha picha ya mtoto mdogo, labda mtu kutoka kwa familia yako.• Unaweza kufikiria mtoto mdogo akimjia Mwokozi? Hii inakukusaidia vipi kuelewa jinsi

sisi tunapaswa kumjia Mwokozi?Andika yafuatayo kwenye ubao:

Kama tukimjia Kristo na moyo uliovunjika na roho iliyopondeka, Yeye ata . . .Waambie wanafunzi warejee 3 Nefi 9:13–15, 19–22 ili kutambua njia za kukamilisha kauli ubaoni. Waambie watoe taarifa ya nini walichopata. Majibu yanaweza kujumuisha kwamba atatuponya (ona 3 Nefi 9:13), atatupa uzima wa milele (ona 3 Nefi 9:14), na atatupokea (ona 3 Nefi 9:22). Baada ya wanafunzi kujibu, kamilisha taarifa ubaoni: Kama sisi tuta-kuja kwa Kristo na moyo uliovunjika na roho iliyopondeka, Atatupokea, kutuponya, na kutupatia uzima wa milele.

3 Nefi 10Bwana anataka kuwakusanya watu wake kama kuku anavyokusanya vifaranga vyakeFupisha 3 Nefi 10:1–3 kwa kueleza kwamba baada ya kusikia sauti ya Mwokozi, watu walisha-ngaa mno kwamba walikaa kimya kwa masaa mengi. Kisha Yeye alizungumza tena na watu.Watake wanafunzi wachache kuchuka zamu kusoma kwa sauti kutika 3 Nefi 10:4–6. Toa angalizo kwamba katika mistari hii, Mwokozi anazungumza juu ya nyumba ya Israeli, watu wake wa agano. • Ni katika njia zipi Mwokozi ni kama kuku anaelinda vifaranga vyake kutoka kwenye

hatari? Kwa nini Mwokozi hakuwa amekusanyika na kulinda nyumba yote ya Israeli? (Wao hawangekuja kwake.)

• Mwokozi aliwaahidi nini wale ambao wangetubu na kurudi kwake? (Yeye angekuwaku-sanya kama kuku anavyokusanya vifaranga vyake.)

Waambie wanafunzi wajibu swali lifuatayo katika madaftari au majarida ya mafunzo ya maandiko. (Unaweza ukitaka kuandika swali hili ubaoni au kusoma polepole ili wanafunzi wanaweza kuandika.)• Lini umeweza kuhisi mwaliko wa mwokozi wa kupokea urutubisho na ulinzi?Alika mwanafunzi asome 3 Nefi 10:9–11 kwa sauti. Uliza darasa kufuatilia pamoja, kua-ngalia nini kilitokea baada ya Mwokozi kusema na watu. Unaweza ukitaka kuhitimisha kwa kushuhudia kwamba Mwokozi ni mwenye huruma kwa wale wote wanaokuja kwake na moyo ulivunjika na roho iliyopondeka. Unaweza pia ukitaka kueleza kwamba katika somo lijalo, wanafunzi watajadili ziara ya Mwokozi kwa watu na jinsi Yeye binafsi alivyo-wahudumia kila mmoja wao.

Page 454: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

439

UtanguliziKufuatia maangamizi na siku tatu za giza zilizoashiria kifo cha Mwokozi, takriban wanaume, wanawake na watoto 2,500 wa Wakinefi walikusanyika kuzunguka hekalu katika nchi ya Bountiful (ona 3 Nefi 17:25). Wa-lipokuwa wakizungumuza walisikia sauti ya Baba wa Mbinguni akimtambulisha Mwana Wake, Yesu Kristo,

ambaye kisha akajitokeza. Yesu Kristo aliwaalika watu washuhudie kibinafsi kwamba alikuwa amaeuliwa kwa ajili ya dhambi za dunia. Mmoja baada ya mwingine, walimwendea na kugusakovu katika upande Wake na alama za misumari katika mikono na miguu Yake.

SOMO LA 120

3 nefi 11:1–17

Mapendekezo ya Kufundisha

3 Nefi 11:1–7Wanefi wanasikia sauti ya Baba akitangaza kutokea kwa Mwana WakeWanafunzi wanapoingia darasani, kuwa na kanda la muziki tukufu ama mkutano mkuu ukicheza kimya katika usuli —kwa sauti kiasi ya kutosha kusikika. Zima kanda wakati wa maombi ya kufungua na ibada. Kufuatia maombi, uliza wanafunzi kama walisikia kanda. (Ikiwa hauna vifaa vya kutekeleza shughuli hii, fikiria kuwezesha mwanafunzi asome kwa sauti ya chini kutoka kwa 3 Nefi 11wanafunzi wanapoingia chumbani. Ukichagua chaguo hili, lifanyika kwa ubora zaidi kama utapanga siku moja kabla ya wakati, pengine kwa mwanafunzi ambaye kwa kawaida hufika mapema.)• Ni nini lazima mtu afanye ili kusikia na kuelewa sauti ya chini?• Ujumbe wa wimbo ulikuwa nini (ama hotuba ya mkutano mkuu ama fungu la maandiko

matakatifu) ambao ulikuwa ukicheza mlipokuwa mkiingia darasani leo?• Je, ilikuwa rahisi ama vigumu kusikia na kuelewa maneno kila mmoja alipokuwa anai-

ngia darasani? Kwa nini?”Alika mwanafunzi asome 3 Nefi 11:1–3 kwa sauti. Uliza darasa lifuate, likitafuta kile Wanefi walikuwa na ugumu kuelewa.• Sauti imeelezewa vipi katika 3 Nefi 11:3? (Unaweza ukitaka kupendekeza kwamba wa-

nafunzi waalamishe maelezo ya sauti katika maandiko yao matakatifu.)• Ni adhari gani sauti ilikuwa nayo kwa wale walioisikia?Waambie wanafunzi wasome 3 Nefi 11:4–7 kimoyomoyo, wakitafuta kile Wanefi walifanya tofauti ili waweze kuelewa sauti mara ya tatu walipoisikia.• Wanefi walifanya nini tofauti mara ya tatu waliposikia sauti?• Kulingana na kile unachosoma katika 3 Nefi 11:7, watu walisikia sauti ya nani? (Walisikia

sauti ya Baba wa Mbinguni, akimtambulisha Mwana Wake, Yesu Kristo.)Fikiria kuwataka wanafunzi wasome Helamani 5:30, wakitafuta maelezo mengine ya sauti ya Bwana.• Ni vipi ambavyo sauti Wanefi walisikia ilikuwa sawa na maongozi tunayopokea kutoka

kwa Roho Mtakatifu? Wanafunzi wanaweza kutumia maneno tofauti, lakini wanapa-swa watambue ukweli ufuatao: Roho Mtakatifu mara nyingi huzungumza kwetu kupitia hisia zetu.

• Kwa nini ni muhimu kuzingatia ushawishi tunaopokea kutoka kwa Bwana kupitia Roho Mtakatifu?

Waalike wanafunzi washiriki matukio ambayo wamekuwa nayo wakati wamehisi ushawi-shi wa Roho Mtakatifu ukija akilini na mioyoni mwao. Watake waeleze jinsi walivyohisi. Unaweza pia ukipenda kushiriki tukio lako mwenyewe.

Kupima urefu wa somoPima urefu wa kila somo ili uweze kutumia muda wa kutosha kwenye ma-mbo ya muhimu zaidi. Kwa mfano, mwishoni mwa somo hili, wanafu-nzi watakuwa na fursa ya kutoa ushuhuda wa Yesu Kristo. Ingawa sehemu zingine za somo ni muhimu, hakikisha kwamba muda wa kuto-sha umebaki kwa ajili ya kutoa ushuhuda.

Page 455: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

440

SoMo la 120

Alika mwanafunzi asome kauli ifuatayo ya Rais Boyd K. Packer wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili kuhusu nini tunachohitaji kufanya ili tusikilize na kuelewa sauti ya Bwana kupi-tia Roho Mtakatifu:

“Roho huwa hapati nadhari yako kwa kupiga kelele. Huwa hatutikisi kwa mkono wa mzito. Roho hunong’ona. Hupapasa pole pole sana, kwa kweli, kwamba kama tunashughulika, hatuwezi kuhisi kamwe.“Mara nyingine, Roho atatusukuma kwa nguvu tu ya kutosha ama mara nyingi ya kutosha kwetu kuzingatia; lakini kutokana na uzoefu wangu, mara nyingi, kama tusiposikiza hisia hiyo tulivu, kama tusiposikia pamoja na hisia

hizo, Roho ataondoka na kungoja hadi tuje tukitafuta na kusikiliza, katika njia yetu na maelezo” (“How Does the Spirit Speak to Us?” New Era, Feb. 2010, 3).• Ni kanuni gani tunaweza kujifunza kutoka kwa 3 Nefi 11:1–7 na kutoka kwa Rais Pa-

cker? (Wanafunzi wanaweza kutoa aina mbali mbali za majibu, lakini hakikisha wana-tambua ukweli ufuatao: Tunapojifunza jinsi ya kusikiliza sauti ya Bwana kupitia Roho Mtakatifu, tutaweza kuelewa mawasiliano anayotupa.)

• Nini kinachokusaidia kutayarisha akili na roho yako kusikiliza na kuelewa minog’ono ya Roho Mtakatifu?

3 Nefi 11:8–17Yesu Kristo anawatokea Wanefi, na kuwaalika mmoja mmoja kuhisi alama za vidonda katika mikono yake, miguu na upande wakeAlika mwanafunzi asome 3 Nefi 11:8–10 kwa sauti. Litake darasa kufuatilia na kufikiria ingekuwa vipi kuwa miongoni mwa Wanefi wakati huu. Onyesha picha ya Yesu akifundisha katika Nchi za Magharibi (62380; Gospel Art Book [2009], no. 82), na uliza: • Ni fikira na hisia zipi unazofikiri ungekuwa nazo kama ungekuwa miongoni mwa Wa-

nefi wakati mwokozi alipowatembelea. Wakumbushe wanafunzi kuhusu giza na maangamizi ambayo Wanefi walipitia kabla tu ya Mwokozi kutokea. Kisha mwalike mwanafnzi asome kwa sauti kauli ifuatayo ya Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili kuhusu umuhimu wa kuonekana kwa Mwokozi kwa Wanefi.

“Kuonekana huko na tangazo hilo linajumuisha kiini, wakati muhimu, katika historia yote ya Kitabu cha Mormoni. Ilikuwa ni onekano la wazi na tangazo ambalo lilimfahamisha na kuwaongoza kila nabii wa Kinefi kwa miaka mia sita iliyopita, bila kusema lolote kuhusu babu zao wa kiisraeli na Wayaredi kwa maelfu ya miaka kabla ya hapo. "Kila mtu alimzungumzia, alimwimba, alimuota, na kuomba kwa ajili ya ku-

onekana kwake— lakini sasa hapa alikuwapo. Siku ya Siku! Mungu anayegeuza kila usiku wa giza kuwa mwanga wa asubuhi amewasili" (Christ and the New Covenant: The Messia-nic Message of the Book of Mormon [1997], 250–51).Elezea darasa kwamba sehemu ijayo ya somo imetengwa ili kuwaruhusu kutafakari ma-tembezi ya Mwokozi wao wenyewe. Kabla ya darasa, tayarisha maelekezo yafuatayo na maswali katika kipeperushi kwa kila mwanafunzi (au andika ubaoni au kwenye bango). Waruhusu wanafunzi muda wa kutosha kusoma 3 Nefi 11:11–17 na kufuata maagizo ka-tika kipeperushi. Wahimize kutafakari kwa makini maana ya aya hizi wanapojifunza. 1. Soma 3 Nefi 11:11–12 kimoyomoyo. Tafuta kile Yesu Kristo alitaka watu kujua kumhusu

na kuhusu alichokuwa amefanya wakati wa huduma yake katika maisha ya kufa. Tafakari maswali yafuatayo: • Ni kauli zipi za mwokozi katika 3 Nefi 11:11 zina maana zaidi kwako? Kwa nini?”• Mwokozi alimaanisha nini aliposema “nimekunywa kutoka kwenye kikombe kile ki-

chungu ambacho Baba amenipa” Kwa nini ni muhimu kujua kwamba Yesu Kristo kila mara amekuwa akijitoa kwa ajili ya Matakwa ya Baba Yake?

2. Soma 3 Nefi 11:13–15, na tafakari maswali yafuatayo: • Mwokozi aliwaalika Wanefi kufanya nini? Aliwataka wajue nini kama matokeo ya

uzoefu huu?

Page 456: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

441

3 nefi 11:1–17

• Watu walienda kwa Mokozi “mmoja mmoja mpaka walipoenda wote” (3 Nefi 11:15). Fikiria kulikuwa na takriban watu 2,500 katika umati (ona 3 Nefi 17:25), hii inakufu-ndisha nini kuhusu jinsi Mwokozi anahisi kuhusu kila moja wetu?

3. Jibu maswali yafuatayo katika daftari au jarida la mafundisho ya maandiko;• Unafikiri kwa nini Bwana alitaka watu kumwona na kumshika “mmoja mmoja”?• Unafikiri vipi ingekugusa kuweza kugusa vidonda Mwokozi alivyovipata alipokuwa

akipatanisha kwa ajili ya dhambi zako? 4. Fikiria kuandika ukweli ufuatao katika ukingo wa maandiko yako karibu na 3 Nefi

11:11–15. Yesu Kristo ananialika kupokea ushuhuda wa kibinafsi kwamba Yeye ni Mwokozi wangu. Jibu maswali yafuatayo katika daftari au katika jarida la mafundisho ya maandiko.• Ni uzoefu upi umekuongoza kupata ushuhuda wako mwenyewe kwamba Yesu Kristo

ni Mwokozi wako?• Unafikiri nini Mwokozi angependa ufanye ili kuimarisha ushuhuda wako Kwake?• Ni lini umehisi kuwa Mwokozi anakufahamu na amekubariki wewe kibinafsi?

Baada ya wanafunzi kuwa na muda wa kutosha kukamilisha shughuli hii, Mwalike mwa-nafunzi asome 3 Nefi 11:16–17 kwa sauti. Litake darasa kufuatilia wakitafuta ni nini watu walifanya baada ya kuwa na uzoefu huu wa kibinafsi pamoja na Mwokozi. Unaweza ku-taka kueleza kuwa hosanna ni neno la Kiebrania linalomaanisha “okoa sasa” au “tafadhali tuokoe” na hutumika kote katika maandiko matakatifu kama ishara ya sifa na ibada. (ona Bible Dictionary, “Hosanna”; Guide to the Scriptures, “Hosanna,” scriptures. Lds. Org).• Kwa nini unafikiri watu waliimba “Hosanna” baada ya uzoefu wao pamoja na Mwokozi?Waambie wanafunzi waangalie kwa makini 3 Nefi 11:15. Waambie watambue nini watu walifanya baada ya kumwona na kuhisi makovu ya Mwokozi? (Watu walitoa kumbuku-mbu, au kushuhudia, kwamba alikuwa ni Yesu Kristo.)• Je, tunahitaji kuwa na uwezo wa kumwona na kumgusa Mwokozi ili kujua kuwa yu hai?

(Ona Moroni 10:5.) Tunawezaje “kutoa kumbukumbu ya” Yesu Kristo?• Tunawezaje kufananisha 3 Nefi 11:15 na sisi wenyewe? Kila mmoja wetu anapaswa ku-

fanya nini baada ya kupokea ushuhuda wa Yesu Kristo? (Tunapopokea ushuhuda wa kibinafsi wa Yesu Kristo, ni jukumu letu kuweka kumbukumbu yake.)

Hitimisha darasa kwa kuwaalika wanafunzi kusimulia kuhusu nyakati ambapo wameshiriki shuhuda zao za Yesu Kristo na wengine. Muda unaporuhusu, waalike wale wote wanaota-mani kufanya hivyo kushiriki ushuhuda mfupi wa Mwokozi. Na pengine, waseme nini wa-lichofanya ili kupata shuhuda zao. Kama Muda ukiruhusu unaweza pia kuwaalika kushiriki baadhi ya kile walichoandika au kuhisi wakati wa mafunzo yao ya 3 Nefi 11 hivi leo.

Tangazo na Habari za Usuli3 Nefi 11:3. “Sauti Ndogo”

Rais Boyd K. Packer wa Akidi ya Mitume Kumi na Wa-wili alieleza jinsi sauti ya Roho Mtakatifu inavyofanya kazi katika akili na miyoyo yetu.

“Sauti ya Roho Mtakatifu huja kama hisia badala ya sa-uti. Mtajifunza, kama nilivyojifunza, ‘kusikiliza’ ile sauti ambayo inahisiwa badala ya kusikika. . . .

“Kipawa cha Roho Mtakatifu, kama ukikubali, itakuo-ngoza na kukulinda na hata kusahihisha matendo yako. Ni sauti ya Kiroho inayokuja kwenye akili kama fikira au hisia iliyowekwa moyoni mwako. . . .

“Haitarajiwi kuwa utaishi maishani bila kufanya makosa, lakini hautafanya kosa kubwa bila kwanza kuonywa kwa uvuvio wa Roho.” (“Counsel to Youth,” Ensign or Liahona, Nov. 2011, 17–18).

Page 457: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

442

UtanguliziZoezi kwa 3 Nefi 1–7 katika somo hili linahimiza baadhi ya ma-fundisho na kanuni zinazoweza kuwasaidia wanafunzi kuelewa vyema zaidi nini maana ya kuongolewa kwa injili ya Yesu Kristo. Shughuli za kufundishia kwa 3 Nefi 8–10 zitawatayarisha wana-funzi kutafakari shuhuda zao za Mwokozi wanapojifunza kuhusu kuonekana kwake kwa uzao wa Lehi katika 3 Nefi 11.

Mapendekezo ya Kufundishiia

3 Nefi 1–7Ishara na miujiza yatangaza kuzaliwa kwa Yesu Kristo; watu wazunguka kati ya haki na uovu hadi serikali ikaangukachora mstari kama ifuatavyo ubaoni

Uliza: Kutokana na masomo yako ya wiki iliyopita, jinsi gani mstari huu unaweza kuwakilisha Wanefi katika 3 Nefi 1–7? (Unaweza ukitaka kuwaalika wanafunzi kutathmini vichwa vya sura kwa 3 Nefi 1–7 ili kiwakumbusha jinsi Wanefi walivyobadi-lika badilika kati ya haki na uovu kutoka 1 B.K. hadi 33 B.K.)

Ili kuwasaidia wanafunzi kufikiria nini 3 Nefi 1–7 inaweza kutu-fundisha kuhusu kuongolewa kikweli kwa Yesu Kristo na Injili Yake, mwalike mwanafunzi asome kwa sauti kauli ifuatayo ya Rais Marion G. Romney wa Urais wa kwanza. (Kama inawe-zekana toa nakala kwa kila mwanafunzi, na waambie wapige

Somo la Mafunzo ya Nyumbani3 Nefi 1–11:17 (Kitengo cha 24)

Vifaa vya Matayarisho kwa Mwalimu wa mafunzo ya nyumbani. Muhtasari wa Masomo ya kila siku ya mafunzo ya nyumbani. Muhutasari ufuatao wa kanuni na mafundisho wanafunzi waliojifunza waliposoma 3 Nefi 1 –11:17 (kitengo cha 24) haikusudiwi kufundishwa kama sehemu yako ya somo. Somo unalofundisha huzingatia machache tu ya mafundisho na kanuni hizi. Fuata uvuvio wa Roho Mtakatifu unapofikiria mahitaji ya wanafunzi wako.

Siku 1 (3 Nefi 1)Wanafunzi walipojifunza kuhusu kutimia kwa unabii wa Sa-mweli Mlamani kuhusu kuzaliwa kwa Yesu Kristo, walijifunza kuwa Bwana atatimiza maneno yote ambayo amesababisha kusemwa na manabii wake. Kutoka kwa mfano wa wale waliokuwa waaminifu hata wakati wasiokuwa waaminifu walipopanga kuwaangamiza, wanafunzi walijifunza kwamba tunapokumbana na uongo wa Shetani, tunaweza kuchagua kumwamini Yesu Kristo na kubakia waaminifu. Uasi wa baa-dhi ya vijana wa Walamani uliwaonyesha wanafunzi kwamba kama tukikubali majaribu, mifano yetu inaweza kuwa na athari hasi kwa imani na haki za wengine.

Siku 2 (3 Nefi 2–5)Walipokuwa wakijifunza kuhusu watu kupungukiwa kwa haki, wanafunzi waliona kuwa kama tukisahau matukio ya kiroho ya wakati uliopita, tutakuwa katika hatari zaidi kwa majaribu ya Shetani na udanganyifu. Walipotathmini barua ya uongo ya Giddiani kwa Lakoneyo, wanafunzi waligundua jinsi Shetani na wafuasi wake mara nyingi wanatumia sifa za uongo, ahadi za uongo na vitisho ili kuwapotosha watu. Wanafunzi waliji-funza kutoka kwa Wanefi na walamani waliofaulu kujitetea dhidi ya wanyag’anyi wa Gadiantoni kwamba tunapojita-yarisha kiroho na kimwili, Bwana atatuimarisha ili kushinda changamoto. Wanafunzi waliposoma kuwahusu Wanefi, wakimsifu Mungu kwa kuokolewa kwao, walijifunza kwamba kutambua wema na huruma za Mungu katika kuokolewa kwetu kutoka shida hutusaidia kubakia wanyenyekevu. Juhudi za Wanefi kuhubiri injili na tangazo la Mormoni la kazi yake inaonesha kwamba kama wafuasi wa Yesu Kristo, tuna jukumu kuwafundisha wengine njia ya maisha ya milele.

Siku ya 3 (3 Nefi 6–10)Wanafunzi waliposoma kuhusu jinsi Wanefi na Walamani wali-vyoanguka tena kwenye uovu, waligundua kuwa tunapokuwa wenye kiburi, tunamruhusu Shetani nguvu nyingi za kutuja-ribu na kutuongoza kufanya dhambi zaidi. Lakini mfano wa uaminifu wa baadhi ya watu ulidhihirisha kwamba tunaweza kuchagua kuwa wanyenyekevu na waaminifu licha ya hali

zetu. Wakati serikali ya Kinefi ilipodhihirika, wale waliomfuata Nefi walionyesha kwamba kama tukitubu na kuwafuata wa-tumishi wa Bwana, tutafurahia ushawishi wa Roho Mtakatifu katika maisha yetu. Kufuatia maangamizi ya kutisha, watu wote kote nchini walisikia sauti ya Yesu Kristo ikitangaza katika giza kwamba kama tukija kwake na mioyo iliyovunjika na roho iliyopondeka, atatuponya na kutupa uzima wa milele.

Siku ya 4 (3 Nefi 11:1–17)Wanafunzi walipojifunza tangazo la Baba la Yesu Kristo, wa-ligundua kwamba Roho Mtakatifu mara nyingi hunena nasi kupitia hisia zetu. Walijifunza pia kwamba tunapojifunza jinsi ya kusikiliza sauti ya Bwana kupitia Roho Mtakatifu, tutaweza kuelewa mawasiliano anayotupa. Kutoka kwa masimulizi ya Mwokozi kuanza huduma yake miongoni mwa Wanefi, wanafunzi walijifunza kwamba Yesu Kristo anatualika sote kupokea ushuhuda wa kibinafsi kwamba Yeye ni Mwokozi wetu, na kwamba mwanzo tulipokea ushuhuda ule, tuna jukumu la kutoa kumbukumbu yake.

Page 458: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

443

SoMo la MafUnzo ya nyUMbani

mstari vishazi au maneno ambayo wanahisi yanaeleza vyema zaidi mtu mwongofu

"Uongofu ni mabadiliko ya kiroho na ya kimaadili. Kuongoka kunamaanisha si tu kumkubali akilini Yesu na mafundisho yake lakini imani ya kuhamasisha katika Yeye na injili Yake. katika mmoja ambaye kwa kweli ameongoka, haja ya vitu vilivyo ki-nyume na injili ya Yesu Kristo imekufa kwa kweli. Na kilichowe-kwa mbadala basi, ni upendo wa Mungu, pamoja na uthibiti wa mwongozo kuweka amri zake" (in Conference Report, Guatemala Area Conference 1977, 8).

Uliza: Ni vishazi au maneno yapi unayohisi yanaeleza bora zaidi mtu aliyeongolewa?

Chora mchoro ufuatayo ubaoni, au tayarisha kama kipeperushi kwa wanafunzi

imani na Matendo yanayoelekeza katika Uongofu

imani na Matendo ambayo yanayo-dhoofisha Uongofu

3 nefi 1:15–23, 27–30

3 nefi 2:1–3; 3:1–10

3 nefi 4:7–12, 30–33

3 nefi 6:13–18; 7:1–5

3 nefi 7:15–22

Mpangie kila mwanafunzi moja ya vifungu vya maandiko kutoka kwenye mchoro. Wape washiriki wa darasa muda wa kutafuta vifungu walivyopangiwa kwa imani na matendo ambayo yanaele-keza kwenye au kudhoofisha uongofu. Nyingi za kanuni ambazo wanafunzi wanaweza kupata zimewekwa kwenye Ufupisho wa Masomo ya mafunzo ya nyumbani ya kila siku 1–3 katika mwanzo wa somo hili. Wanafunzi wanapotoa taarifa ya kile wanachopata, andika majibu yao ubaoni au wahimize kuandika katika vipeperu-shi vyao. Wasaidie wanafunzi watumie kanuni walizozipata kwa kuwauliza maswali kama yafuatayo kuhusiana na moja au mawili ya kweli ambazo wanafunzi wamezitambua

• Jinsi gani wewe au mtu unayemjua ameishi kulingana na kweli hiyo au kupata uzoefu wa kanuni hiyo?

• Kutokana na ukweli uliogundua, ni ushauri gani unaoweza kutoa kumsaidia mtu kuwa mwongofu zaidi na kuwa imara kiroho

3 Nefi 8–11:17Maangamizi mkubwa na giza iliashiria kifo cha Yesu Kristo; baada ya Ufufuo Wake, Anawatembelea Uzao wa LehiMwalike mwanafunzi kufupisha matukio katika 3 Nefi 8 na kushiriki na darasa hisia zozote au mawazo ambayo amepata

wakati akijifunza sura hii katika wiki iliyopita. Mwambie mwa-nafunzi asome 3 Nefi 8:20–23. Litake darasa kueleza kwa nini ishara ambayo hizi aya zinaeleza ni ishara ifaayo kuonyeasha kifo cha Yesu Kristo. Ili Kusisitiza kuwa giza ambalo Wanefi walipata, unaweza ukitaka utumie shughuli ifuatayo:

Mpe kila mwanafunzi kurunzi, na kuzima taa chumbani (ikiwa huna kurunzi zakutosha, wanafunzi wanaweza kuhitaji kutumia pamoja) Fanya wanafunzi kuwasha tochi zao, na waalike wacha-che kati yao kupokezana kusoma kwa sauti kutoka kwa 3 Nefi 9:13–20. Uliza darasa kufuatilia wakitafuta kweli ambazo watu walijifunza kumhusu Yesu Kristo walipokumbana na giza baada ya kifo chake. Pamoja na taa kuwashwa tena, fupisha ubaoni kweli ambazo wanafunzi wametambua. Sisitiza kanuni zifuatazo: Yesu Kristo ni mwanga na uhai wa ulimwengu. Tukimjia Yesu Kristo na moyo uliovunjika na roho iliyopondeka, atatupokea na kutupa uzima wa milele.

Fupisha 3 Nefi 11:1–7 kwa kueleza kwamba watu walionusurika maangamizi walikusanyika hekaluni katika Bountiful.

Onyesha picha ya Yesu akifundisha bara la magharibi (62380; Gospel Art Book [2009], no. 82) au Yesu akiponya Wanefi (Gospel Art Book, no. 83). Waalike wanafunzi kutaswiri 3 Nefi 11:8–17 unapowasomea. Tua mara kwa mara katika usomaji wako, na waalike wanafunzi kushiriki jinsi wanavyohisi wanapotaswiri tukio hili, hasa tukio la “moja kwa moja” ambalo Wanefi walipata pamoja na Mwokozi kama lilivyoelezwa katika 3 Nefi 11:15.

Baada ya kusoma 3 Nefi 11:8–17, waulize wanafunzi maswali yafuatayo. Watake wachukue muda mfupi kutafakari kwa ukimya maswali kabla hawajajibu. (Hakikisha umeacha muda wa kutosha kwa wanafunzi kujibu maswali haya ili wasihisi kama wamehara-kishwa wanapotafakari na kushiriki hisia na shuhuda zako.)

• Kama ungelikuwa miongoni mwa Wanefi na kuwa nafasi ya kuhisi vidonda vya Mwokozi, je ungemwambia nini?

• Wakati Yesu Kristo alipojitambulisha kwa Wanefi, kwa nini unafikiri ni muhimu kuwa alivuta nathari kwa “kikombe kichungu” (3 Nefi 11:11).

• Je ni nini “kikombe kichungu” ambacho Yesu Kristo alizungu-mzia? (Ona M&M 19:16–19.)

Shiriki ushuhuda wako wa Mwokozi na Mwanga uliokuja katika maisha yako wakati umemfuata Yeye. (Unaweza pia ukitaka kuwahimiza wanafunzi kukumbuka hisia walizopata wakati wa somo hili na kuziwekea kumbukumbu katika shajara zao za kibinafsi za nyumbani.

Kitengo Kinachofuata (3 Nefi 11:18–16:20)Waambie wanafunzi wafikirie maswali yafuatayo wanapojifunza kitengo kinachofuata: Ninamfikiria yeyote kuwa adui yangu? Kama ni hivyo, ninawatendea vipi watu kama hao? Ni maadili yapi ambayo Mungu huhisi ni muhimu maishani mwangu? Je inakubalika kuwahukumu watu wengine? Wanafunzi wanaweza kupata majibu kwa maswali haya wanapojifunza maneno ya Mwokozi katika kitengo cha 25.

Page 459: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

444

UtanguliziBaada ya Wanefi kuja na kugusa makovu ya majeraha katika mikono, miguu na ubavu wa Mwokozi, Bwana alimpa Nefi na wengine uwezo wa kubatiza na kuteke-leza kazi zingine za ukuhani. Mwokozi pia aliwaonya

watu kuepukana na ubishi na aliahidi kwamba wale wanaoishi kulingana na mafundisho yake wangerithi ufalme wa Mungu.

SOMO LA 121

3 nefi 11:18–41

Mapendekezo ya Kufundisha

3 Nefi 11:18–27Yesu Kristo anampa Nefi na wengine uwezo wa KubatizaMbele ya darasa, andika maswali yafuatayo ubaoni: Nani anayeweza kunibatiza? Ubatizo unafanywa vipi?Kama ukifundisha mwanafunzi mmoja au zaidi ambao hivi majuzi wamejiunga na Kanisa, unaweza kuanza somo hili kwa kuwataka kushiriki baadhi ya uzoefu waliokuwa nayo wali-pokuwa wakijifunza kuhusu Kanisa. Waulize kama walishangaa kuhusu majibu ya maswali mawili ubaoni walipoamua kubatizwa.Unaweza pia kuanza somo hili kwa kuwaalika wanafunzi kufikiria kwamba mmoja wa marafiki zao wameamua hivi karibuni kujiunga na Kanisa na wamewauliza hayo maswali mawili ubaoni. Waambie wanafunzi waeleze jinsi wavyoweza kujibu maswali haya. Au unaweza ukitaka kuwaita wanafunzi wawili kuigiza majadiliano kati ya muumini wa Ka-nisa na rafiki yake kwa kutumia maswali haya.Wakumbushe wanafunzi kwamba katika somo lililopita walijifunza kuhusu kutokea kwa Yesu Kristo kwa kikundi cha Wanefi. Yesu kristo aliwaalika kushuhudia wenyewe Ufufuo Wake na uungu kwa kuhisi alama za vidonda mikononi, miguuni na katika upande wake. Eleza kwamba mara tu kufuatia tukio hili, Mwokozi alifundisha watu mafundisho yake ambayo yalikuwa ni kumwamini yeye, kubatizwa na kupokea Roho Mtakatifu.Mwalike mwanafunzi asome 3 Nefi 11:18–26 kwa sauti. Litake darasa kufuatilia, wakitafuta majibu ya swali nani anaweza kunibatiza? Mpate mwanafunzi aandike majibu ubaoni chini ya swali hili. Ingawa wanafunzi wanaweza kutumia maneno tofauti, wanapaswa kutambua ukweli ufuatao Ubatizo ni sharti ufanywe na mtu aliye na mamlaka sahihi. (Ikiwa wazo hili halijaandikwa tayari ubaoni, unaweza ikitaka kuuongeza katika orodha ya majibu.)Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa zaidi ukweli huu, unaweza kueleza kwa ufupi kwamba ubatizo unaweza kufanywa tu na mtu mwenye mamlaka katika ofisi ya kuhani katika uku-hani wa Haruni (ona M&M 20:46) au na mtu aliyekuwa amepasishwa ukuhani wa Melki-zediki (Ona M&M 20:38–39; 107:10–11). Zaidi ya hayo, mtu huyu ni sharti atende chini ya uongozi wa kiongozi wa ukuhani mwenye funguo zinazotakiwa kuidhinisha ibada (kama vile askofu, rais wa kata, au rais wa misheni)• Kwa nini unafikiri Bwana anahitaji ibada ya ubatizo kutekelezwa na mwenye ukuhani

aliyeidhinishwa?Alika mwanafunzi asome 3 Nefi 11:23–27 kwa sauti. Uliza darasa kufuatilia, wakitafuta majibu ya swali Ubatizo hufanywa vipi? Mpate mwanafunzi aandike majibu yao ubaoni chini ya swali. • Ni nini kinafanyika wakati wa ubatizo kama maneno ya ibada hayasemwi kwa usahihi au

kama mtu anayebatizwa hakuzamishwa kikamilifu chini ya maji? (Ibada inarudiwa) Ni ukweli gani tunaoweza kujifunza kutoka kwa haya? (Ingawa wanafunzi wanaweza kutu-mia maneno tofauti. Wanapaswa kutambua ukweli ufuatao: Ubatizo ni sharti ufanywe kwa njia iliyowekwa na Bwana. (Unaweza kutaka kuandika taarifa hii kwenye ubao.)

• Kwa nini unafikiri ni muhimu kwamba ubatizo ufanywe sawasawa kwa njia iliyowekwa na Bwana?

Tohoa somoMasomo mengi ka-tika mwongozo huu huanza kwa kupende-keza shughuli au swali ambalo linakusudiwa kuwatayarisha wanafu-nzi kujifunza maandiko matakatifu. Mapende-kezo haya yanaweza kutoholewa kulingana na mahitaji na hali za wanafunzi.

Page 460: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

445

3 nefi 11:18 – 41

Ili kuwasaidia wanafunzi kuhisi umuhimu wa kweli mliojadili katika 3 Nefi 11:18–27, una-weza kutaka kuuliza baadhi ya maswali yafuatayo:• Ulikuwa na hisia gani ulipobatizwa? Ina maana gani kwako kujua kwamba ulibatizwa na

mtu aliye na mamlaka sahihi na kwa jinsi Bwana alivyoweka?• Umeshuhudia ubatizo hivi karibuni? Ulipata hisia zipi?Kama yeyote kati ya wanafunzi wako anashikilia ofisi ya kuhani katika Ukuhani wa Haruni, uliza:• Kujua kuwa una mamlaka ya kubatiza kunakushawishi vipi? (Unaweza kutaka kujua

kama wanafunzi yeyote darasani mwako amewahi kuwa na nafasi ya kubatiza mtu. Kama wamewahi, waalike washiriki kile walichohisi na kujifunza wakati wa uzoefu wao.)

Unaweza ukitaka kushiriki uzoefu wako na hisia kuhusu ibada takatifu ya ubatizo.

3 Nefi 11:28–30Yesu Kristo aonya kuwa ubishi ni wa shetaniAndika neno ubishi ubaoni.• Ubishi ni nini? (mabishano, ukinzano, ugomvi)Waambie wanafunzi kuorodhesha kwa ufupi katika shajara zao au majarida yao ya kuji-funzia maandiko matakatifu baadhi ya hali au shughuli ambapo ubishi huweza kutokea. Baada ya wanafunzi kuwa na muda wa kutosha kuandika, mwambie mwanafunzi asome 3 Nefi 11:28–30 kwa sauti. Alika darasa kufuatilia na kutambua ni nini baadhi ya Wanefi walibishana kuhusu.• Yamkini vilihusu nini baadhi vitu vya wazi ambavyo Wanefi waligombania? (Ibada ya

ubatizo [ona pia 3 Nefi 11:22] na mafundisho ya Kristo.)• Kulingana na 3 Nefi 11:29, ni wapi ambapo roho wa ubishi hutoka? (Andika ukweli

ufuatao ubaoni: Roho wa ubishi si wa Mungu, lakini ni wa Shetani. unaweza kutaka kupendekeza kwamba wanafunzi waalamishe ukweli huu katika 3 Nefi 11:29.)

• Kwa nini unafikiri ni muhimu kuepuka ubishi wakati una jadili injili na wengine. Kwa nini kubishana ni njia isiyofaa kufundisha injili? (Wanafunzi wanaweza kutoa majibu mbalimbali, lakini kuwa na uhakika wanaelewa kwamba wakati sisi tukishindana au kubishana na wengine kuhusu injili, Roho Mtakatifu hatakuwepo kutusaidia kufundisha au kushuhudia ukweli katika mioyo ya wale tunaowafundisha.)

Ili Kusisitiza matokeo muhimu ya ubishi, andika juu ya ubao ya maelezo ya yafuatayo na Rais James E. Faust wa Urais wa kwanza. Unaweza kutaka kuhamasisha wanafunzi kua-ndika katika maandiko yao matakatifu karibu na 3 Nefi 11:29. (Kauli hii inapatikana katika “What I Want My Son to Know before He Leaves on His Mission,” Ensign, Mei 1996, 41).

“Wakati kuna ugomvi, Roho wa Bwana ataondoka, bila kujali nani ana makosa.” Rais James E. Faust).

• Ni Wakati gani wewe umehisi Roho ya Bwana ikiondoka kwa sababu ya ubishi? Ulijuaje Roho ameshaondoka?

Toa angalizo kauli ya Mwokozi kuhusu ubishi katika 3 Nefi 11:30: “hili ndilo fundisho langu, kwamba vitu kama hivi viondolewe mbali.”• Tunawezaje “kuondolea mbali” ubishi na ugomvi? (Majibu yanaweza kujumuisha yafua-

tayo: Tunaweza kutafuta kuwa wapatinishi [ona 3 Nefi 12:9]. Tunaweza kuomba kwa ajili ya hekima na uvumilivu kushinda ubishi. Tunaweza kujaribu kuepuka hali ambayo sisi tungeshawishika kushindana na wengine.)

• Ni lini wewe umehisi kubarikiwa kwa juhudi zako za kuepuka au kushinda ugomvi?• Ni vipi kukumbuka mafundisho ya Mwokozi katika Nefi 11:29–30 kukusaidia wakati

wewe mwenyewe unajikuta katika hali iliyo au inayoweza kuwa ya mabishano? Unaweza kutaka kushiriki uzoefu ambao umekuwa nao wakati ulipohisi kubarikiwa kwa juhudi zako ili kuepuka au kushinda ubishi. Kuhamasisha wanafunzi kutumia kile amba-cho wamejifunza kutoka 3 Nefi 11:28–30, wawakaribishe kurejea nyuma kwenye orodha yao ya hali au shughuli ambazo wanaweza kukabiliwa na ubishi. Waalike kuweka na kua-ndika lengo kwa jinsi wao watajaribu kuepuka au kushinda ubishi katika hali au shughuli ambazo wao waliorodhesha.

Page 461: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

446

SoMo la 121

3 Nefi 11:31–41Yesu atangaza fundisho LakeIli kuwatayarisha wanafunzi kujifunza 3 Nefi 11:31–41, andika yafuatayo ubaoni:

tendo Matokeo

Waite wanafunzi waeleze kwa ufupi kwa mwanafunzi mwenzao kitu walichofanya hivi karibuni ambacho kili sababisha matokeo chanya na kueleza matokeo haya yalikuwa ni nini. Unaweza pia kuwataka waseme kuhusu kitu fulani walichofanya au kuona amba-cho kilisababisha matokeo hasi (Tahadharisha wanafunzi dhidi ya kushiriki kitu chochote ambacho kinaweza kuwa kisicho cha muafaka au kibinafsi zaidi.)Soma 3 Nefi 11:31 kwa sauti kwa darasa. Eleza kuwa salio la 3 Nefi 11 linahusu tangazo la Yesu Kristo la fundisho lake kwa watu wa Nefi. Sura hii pia inatoa matokeo ya kukubali au kukataa mafundisho yake.Andika marejeo ya maandiko yafuatayo ubaoni: 3 Nefi 11:32–34; 3 Nefi 11:35–36; 3 Nefi 11:37–38; 3 Nefi 11:39–40. Wagawanye wanafunzi wawiliwawili na pangia kila kikundi kujifunza mojawapo ya vifungu vya maandiko. Waambie wabainishe vitendo na matokeo ambayo Yesu Kristo alifundisha kuhusu. (Unaweza kupendekeza kwamba wanafunzi wali-nganishe mafundisho haya na makala ya nne ya imaniBaada ya wanafunzi kuwa na muda wa kutosha wa kujifunza, waambie wachache kati yao watoe taarifa ya vitendo na matokeo waliyoyapata katika mistari waliyopangiwa. Waambie waandike majibu yao ubano chini ya Kitendo au Matokeo. Wanafunzi wanapotoa taarifa juu ya kila fungu, uliza maswali haya sambamba chiniKwa kikundi kilichopangiwa 3 Nefi 11:32–34, uliza:• Roho Mtakatifu anatusaidia vipi kuamini katika Yesu Kristo na Baba wa Mbinguni?

Roho Mtakatifu hushuhudia, juu ya Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Ni lini Roho Mtakatifu ametoa ushahidi kwenu wa ukweli na upendo wa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo?

Kwa makundi yaliyopangiwa 3 Nefi 11:35–36, uliza:• Kulingana na mistari hii, kuchagua kuamini katika Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo

kunakaribisha vipi ushawishi wa Roho Mtakatifu katika maisha yetu?Kwa makundi yaliyopangiwa 3 Nefi 11:37–38, uliza:• Ni nini ulichopata ambacho kilikuwa sawa kati ya 3 Nefi 11:37 na 3 Nefi 11:38?• Je, ni nini sifa mzuri za mtoto mdogo? Kwa nini unafikiri ni muhimu kuwa kama

mtoto mdogo?Kwa kikundi kilichopangiwa 3 Nefi 11:39–40, uliza:• Ni jinsi gani mafundisho ya Mwokozi katika mistari hii yanasisitiza umuhimu wa ucha-

guzi wetu kutii au kutotii mafundisho yake?Waambie wanafunzi kufupisha hatua muhimu ambazo Yesu Kristo alifundisha kwamba ni lazima tuchukue kuingia katika Ufalme wa Mbinguni. Wanafunzi wanaweza kutumia maneno tofauti, lakini wanapaswa kueleza ukweli ufuatao: Ili kuingia katika Ufalme wa mbinguni, ni lazima tutubu, tuamini katika Yesu Kristo, tubatizwe, na kupokea Roho Mtakatifu. Unaweza kuhitimisha kwa kushirikisha ushuhuda wako wa ukweli huu. Wahimize wanafunzi kuishi kulingana na mafundisho ya Yesu Kristo ili waweze kuwa na uwezo wa kurithi ufalme wa Mungu. Unaweza pia kutaka kuwakumbusha kufanya kazi katika malengo yao ili kuepuka na kushinda ubishi.

Page 462: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

447

UtanguliziYesu Kristo aliwafundisha Wanefi jinsi ya kupokea baraka za injili Yake na akawaelekeza kushawishi wengine kwa wema. Alitangaza kwamba alikuwa

ametimiza sheria ya Musa, na akawapa watu sheria ya juu ili kuwatayarisha kuwa kama Yeye na Baba yetu wa Mbinguni.

SOMO LA 122

3 nefi 12

Mapendekezo ya Kufundisha

3 Nefi 12:1–12Yesu Kristo anafundisha mkusanyiko kuhusu baraka tunazopokea tunapoishi injili YakeMbele ya darasa, andika maswali yafuatayo ubaoni:

Je, Baba wa Mbinguni anatutarajia kuwa wakamilifu?Je, tunahitaji kuwa kamilifu katika maisha haya ili kuingia ufalme wa selestia?Je, tunaweza kweli kuwa kamilifu?

Mwanzoni mwa somo,waambie wanafunzi watafakari maswali haya. Waambie wafikirie maswali haya wakati wote wa somo.Mwalike mwanafunzi asome 3 Nefi 12:48 kwa sauti. Toa angalizo kwamba hiki ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Unaweza ukitaka kupendekeza kwamba wanafunzi waalamishe kifungu hiki kwa njia ya kipekee ili waweze kukipata kwa uraisi.Mwalike mwanafunzi asome kauli ifuatayo ya Mzee Russell M. Nelson wa Akidi ya Mi-tume Kumi na Wawili kuhusu amri ya kuwa kamili:

“Hatupaswi tufe moyo ikiwa jitihada zetu za dhati kuelekea ukamilifu sasa zinaonekana kuwa ngumu na zisizo na mwisho. Ukamilifu unangoja. Unaweza kuja kwa ukamilifu mara tu baada ya Ufufuo na tu kupitia Bwana. Inawangojea wale wote wanaompenda na kutii amri zake” (“Perfection Pending,” Ensign, Nov. 1995, 88).• Kwa nini unafikiria ukamilifu unaweza kuja “tu kupitia Bwana”?

Rejea maswali matatu mwanzoni mwa somo. Waulize wanafunzi kama wangebadilisha majibu yao kwa maswali hayo baada ya kusoma 3 Nefi 12:48 na kusikiliza maelezo ya Mzee Nelson. Wasaidie wanafunzi kuelewa kwamba Baba wa Mbinguni hatutarajii tuwe wakamilifu wakati wa maisha yetu duniani lakini kwamba tukijitahidi kwa bidii kutii amri na tunapotegemea Upatanisho, hatimaye tunaweza kuwa wakamilifu.Andika neno barikiwa ubaoni. Waambie wanafunzi wasome 3 Nefi 12:1–12 kimoyomoyo, wakitafuta sifa ambazo Mwokozi anatusihi tutukuze na baraka anazoahidi kama matokeo.• Ni baraka zipi zimekuja maishani mwako kama matokeo ya kuishi mafundisho ya Yesu

Kristo katika 3 Nefi 12:1–12?Toa angalizo ni mara ngapi neno barikiwa linatokea katika mistari hii. Shiriki ushuhuda wako wa jinsi ulivyobarikiwa ulipoishi kulingana na mafunzo ya Mwokozi.Waambie wanafunzi waandike katika madaftari ama majarida ya kujifunzia maandiko kuhusu baraka wanayotamani ambayo imeelezewa katika 3 Nefi 12:1–12. Watake waa-ndike sifa ambayo ni lazima waikuze ili kupokea baraka hio. Kisha waambie waandike nini wangependa kufanya ili kukuza sifa hiyo. Waambie wanafunzi wachache washiriki kile walichoandika na kwa nini.

3 Nefi 12:48 ni kifungu cha umahiri wa maandiko Rejea pendekezo la kufundi-shia mwishoni mwa somo hili ili kuwasaidia wanafunzi na umahiri wao wa kifungu hiki.

Page 463: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

448

SoMo la 122

3 Nefi 12:13–16Mwokozi ahimiza umati kuwa mfano mwema kwa duniaOnyesha chombo chenye chumvi. Uliza darasa litambue manufaa ya chumvi. Wanafunzi wanapojibu, hakikisha kwamba ni wazi kwamba chumvi hukipa ladha chakula na kwamba ni dawa inayotumika kuzuia nyama isiharibike. Unaweza pia ukitaka kuelezea kwamba chini ya sheria ya Musa, makuhani waliamuriwa kutoa chumvi pamoja na toleo lao la sadaka (ona Mambo ya Walawi 2:13). Basi, chumvi ilikuwa ni ishara ya agano kati ya Bwana na watu Wake.Waambie wanafunzi wasome 3 Nefi 12:13 kimoyomoyo na watambue ni nani Mwokozi alimlinganisha na chumvi. Wanafunzi wanapojibu, eleza kuwa Mwokozi alikuwa akiwazu-ngumzia si tu umati kwenye hekalu siku ile bali kwa wale wote waliobatizwa katika kanisa lake na kuishi injili Yake.• Ni kwa njia zipi tunaweza kama wafuasi wa Yesu Kristo kuwa kama chumvi? (Tunata-

kiwa kusaidia kuwahifadhi au kuwaokoa watu na kuboresha ulimwengu kwa kuwasha-wishi n wengine kwa wema.

• Unafikiri inamaanisha nini chumvi ikipoteza ladha yake?Wanafunzi wanapojadili swali hili, unaweza kutaka kusoma kauli ifuatayo ya Mzee Ca-rlos E. Asay wa Wale Sabini. “Chumvi haitapoteza ladha yake kwa uzee. Ladha hupotezwa kupitia kwa mchanganyiko na uchafuzi. Ladha na ubora humtoka mtu anapochafua akili zake kwa mawazo yasiyo masafi, anachafua mdomo wake kwa kusema mambo yasiyo ya kweli, akitumia nguvu zake visivyo kwa kutenda mambo maovu.” (“Salt of the Earth: Savor of Men and Saviors of Men,” Ensign, May 1980, 42).• Kwa nini ni lazima tuwe wasafi ili kuwashawishi wengine kwa mazuri?Eleza kuwa Mwokozi alitumia alama nyingine kufundisha jinsi washiriki wa agano wa Kanisa lake wanavyopaswa washawishi wengine kwa wema. Alika mwanafunzi asome 3 Nefi 12:14–16 kwa sauti. Litake darasa kufuatilia wakutafuta jinsi mwokozi alivyotumia mwanga kufundisha kuhusu jukumu la watu wake wa agano duniani. Kabla ya mwanafu-nzi hajasoma, unaweza kutaka kueleza kuwa pishi ni kikapu.• Washiriki wa kanisa wanawezaje kuwa mwanga kwa wengine? Unafikiri inamaanisha

nini kufanya mwanga wetu uangaze? (Wanafunzi wanapojibu swali hili, wasaidie kuona jinsi mifano yao ya kuishi kwa haki inaweza kuwasaidia watu wengine.

• Ni kwa njia zipi baadhi ya washiriki wa Kanisa wanaweza kufunika mwanga wao?• Kulingana na 3 Nefi 12:16, kwa nini mwokozi anataka tuache mwanga wetu uangaze?

(Tunapoweka mfano wa haki, tunaweza kuwasaidia wengine kumtukuza Baba wa Mbinguni. Unaweza kutaka kupendekeza kwamba wanafunzi waandike kanuni hii kwa maneno yao wenyewe katika maandiko yao.)

• Ni mfano wa nani wa haki imekusaidia kujongea karibu zaidi kwa Baba wa Mbinguni na kuiarisha hamu yako ya kuishi injili?

Waambie wanafunzi kutafakari mfano walioweka kwa ajili ya wale walio wazunguka. Wahimize kufikiri jinsi wanavyoweza kuwasaidia zaidi wengine kuweka kina upendo wao kwa baba wa Mbinguni na hamu yao ya kumfuata.

3 Nefi 12: 17–48Yesu Kristo anafundisha umati sheria kuu ambayo itakayowasaidia kuwa kama yeye na Baba wa MbinguniEleza kuwa Mwokozi aliendelea kuwafundisha Wanefi jinsi ya kumjia Yeye na kuingia ka-tika ufalme wa mbinguni. Alika mwanafunzi asome 3 Nefi 12:19–20 kwa sauti. Uliza darasa kufuatilia wakitafuta neno linalotokea mara kadha katika aya hizi.• Ni neno ipi muhimu ambalo mwokozi anatumia mara tatu kama sehemu ya mwaliko wa

kumjia Yeye? Amri

Page 464: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

449

3 nefi 12

Eleza kwamba 3 Nefi 12:21–47 ina amri kadha maalumu ambazo Mwokozi alitoa ambazo zitatusaidia kumjia Yeye na kuwa zaidi kama Yeye. Alipofundisha amri hizi kwa Wanefi, alirejea mwongozo ambao ulikuwa sehemu ya sheria ya Musa na kisha akafundisha amri kuu. Alielekeza kwa utamaduni wa kuelewa sheria ya Musa wakati alipotumia vishazi kama "ilisemekana wale wa wakati wa kale”, na “imeandikwa.” Aliposema “Lakini nina-waambia,” alitanguliza njia ambayo alitaka tuweke amri hiyo hivi leo.Ili kuwasaidia wanafunzi kujifunza aya hizi, nakili mchoro ufuatao ubaoni. Gawa darasa katika vikundi vinne. Pangia kila kikundi safu moja katika mchoro, na kuwaalike wasome aya zinazoambatana na kujibu maswali.

je uelewa wa kitamaduni wa sheria ya Musa ulikuwa upi?

Mwokozi alitushauri kuishi vipi?

Kijana au msichana anaweza kufanya nini ili kutumia mafundisho ya Mwokozi?

3 nefi 12: 21 3 nefi 12: 22–26

3 nefi 12: 27 3 nefi 12:48

3 nefi 12:38 3 nefi 12:39–42

3 nefi 12:43 3 nefi 12:44–46

kwa manufaa ya wanafunzi kusoma 3 Nefi 12:22, unaweza kutaka kueleza kuwa Raka ni neno la dharau au kejeli linalodhihirisha bezo au dharau (ona Mathayo 5:22, tanbihi d). Unaweza pia kutaka kueleza kwamba Mzee David E. Sorensen wa wale sabini alifundisha kwamba kishazi “kubaliana na adui yako haraka” (3 Nefi 12:25) inamaanisha “kutatua tofauti zetu mapema ama mhemko wa wakati huo unaongezeka na kuwa ukatili wa kihisia au kimwili na tunaanguka na kuwa mateka wa hasira” (“Forgiveness Will Change Bitter-ness to Love,” Ensign au Liahona, Mei 2003, 11).Wakati wanafunzi wanekamilisha kusoma aya walizopangiwa, alika kila kikundi kutoa taarifa ya majibu yao. Unaweza kuwataka kuandika majibu yao katika mchoro ubaoni• Ni nini kilichoonekana kubadilika kati ya sheria za Musa na amri kuu iliyofundishwa na

Yesu Kristo?Unaweza ukitaka kutoa angalizo kwamba sheria kuu inalenga zaidi juu ya tamaa, mawazo, na hamasa zetu kuliko juu ya matendo yetu ya nje.• Tunapojibidiisha kuwa wakamilifu, kwa nini ni muhimu sana kulenga hamu zetu, ma-

wazo na hamasa? Waalike wanafunzi wachagua mojawapo ya mafundisho ya Mwokozi katika 3 Nefi 12 na waandike kifungu kuhusu jinsi watakavyofanya maendeleo katika eneo hilo. Alika mwanafunzi asome 3 Nefi 12:19–20 kwa sauti. Wasaidie wanafunzi kuelewa kwamba kwa kutubu na kuweka amri ambazo Bwana alifundisha kwa bidii tunaweza kuwa waka-milifu kupitia kwa Upatanisho na “kuingia katika ufalme wa mbinguni” (3 Nefi 12:20).Baada ya wanafunzi kukamilisha shughuli hizi, waalike kushiriki kile kilichokuwa na maana zaidi kwao. Fupisha mlango huu kwa kuandika kanuni ifuatayo ubaoni: Tunapomjia Kristo na kuweka amri zake, tunaweza kuwa zaidi kama Yeye, na Baba wetu wa Mbingu ambao ni wakamilifu. Wakumbushe wanafunzi kwamba ili kupata kiwango chochote cha ukamilifu ni lazima tutegemee Upatanisho wa Yesu Kristo. Waalike wanafunzi waandike kuhusu njia moja au mbili ambazo wangependa kutumia mafundisho ya mwokozi waliyoji-funza hivi leo. Hitimisha kwa kushiriki ushuhuda wako wa kanuni uliyoandika ubaoni.

Umahiri wa Maandiko—3 Nefi 12:48Waalike wanafunzi kufungua maandiko yao matakatifu katika 3 Nefi 12:48. Waambie wasome kwa sauti aya hiyo kwa pamoja. Wape wanafunzi muda wa kusoma aya kisha wa-ambie wafunge maandiko yao na wakariri aya hiyo tena kwa ukamilifu wawezavyo. Wape kurudia mchakato wa kuangalia aya hiyo, wakifunga maandiko yao na kisha kukariri aya kutoka kichwani.

Page 465: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

450

SoMo la 122

• Ulikuwaje bora zaidi pamoja na juhudi? • Shughuli hii inakusaidia vipi kuelewa safari yako kuelekea ukamilifu?Toa angalizo kwamba juhudi zetu maishani ni muhimu. Wakumbushe wanafunzi kwamba hata hivyo, Bwana hatutarajii kuwa wakamilifu katika mambo yote katika maisha yetu ya kufa. Kupitia kwa Upatanisho na juhudi zetu za bidii za kumfuata Mwokozi, tunaweza hatimaye kukamilishwa. Waalike wanafunzi wafikirie njia moja wanayoweza kujitahidi kumfuata Mwokozi.

Page 466: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

451

UtanguliziMwokozi aliendeleza mahubiri Yake katika hekalu katika nchi ya Bountiful. Aliwaonya watu dhidi ya unafiki na kuwafundisha kufanya matendo ya haki ili kumpendeza Baba wa mbinguni. Pia aliwaagiza umati

kujiwekea hazina mbinguni na kuwaelekeza wanafunzi wake kutafuta ufalme wa Mungu kabla ya mahitaji yao ya muda.

SOMO LA 123

3 nefi 13

Mapendekezo ya Kufundisha

3 Nefi 13:1–18Mwokozi awaonya Wanefi dhidi ya unafiki na kuwafundisha kufanya matendo ya haki ili kumpendeza Baba wa MbinguniMbele ya darasa, tayarisha kipeperushi cha tathmini ya kibinafsi ifuatayo, na fanya nakala kwa kila mwanafunzi. Kama hiyo haiwezekani, unaweza kutoa tathmini kwa maneno au kuyaandika ubaoni. 1. Ninafanya wema (matendo ya kujitolea kidini au huduma) kwa sababu:

A. Ninapaswa ku B. Ninampenda Bwana na ninafurahia kuwasaidia watu wengine C. Ninataka wengine wanifikirie vyema.

2. Ninaomba kwa sababu A. Ninataka kuweza kuwaambia wazazi wangu au askofu wangu “ndiyo” wakati

wanaponiuliza kama ninasali B. Ni sehemu tu ya mazoea yangu ya kila siku C. Ninataka kuwasiliana na Baba yangu wa mbinguni

3. Ninafunga kwa sababu A. Kufunga kunasaidia kunileta karibu na Bwana B. Watu wengine watafikiri mimi ni mnyonge nisipofunga. C. Wazazi wangu huniambia ninapaswa kufunga

Ili kuanza somo, waulize wanafunzi kukamilisha tathmini ya kibinafsi (ama kwenye kipeperushi au katika madaftari au majarida ya mafundisho ya maandiko) kwa kuonyesha ni vishazi vipi vinaeleza vizuri zaidi njia bora au sababu zao za kufanya wema, kuomba na kufunga. Wahakikishie wanafunzi kuwa hutawataka k washirikishe majibu yao na wengine. Baada ya wanafunzi kukamilisha tathmini zao kibinafsi, toa angalizo kwamba majibu yanayowezekana yaliyoorodheshwa chini ya kufanya wema, kuomba na kufu-nga yanaonyesha sababu au nia tofauti tunazoweza kuwa nazo kwa kufanya vitu hivi au shughuli zingine zinazolingana na injili. (tunaweza kuzifanya, kwa mfano, kwa sababu ya wajibu, au sharti, ili kuwafurahisha watu wengine, au kumfurahisha Baba wa Mbinguni)• Je ina maana kwa nini tunafanya kazi za haki? Kwa nini au kwa nini isiwe?Andika mada zifuatazo na marejeo ya maandiko yanayoambatana ubaoni (unaweza kutaka kufanya hivi kabla ya darasa):

Matendo ya wema: 3 Nefi 13:1–4Sala: 3 Nefi 13:5–6Kufunga: 3 Nefi 13:16–18

Eleza kwamba 3 Nefi 13 inasimulia tena jinsi Yesu Kristo alivyoendelea kuwaagiza umati wa Wanefi katika hekalu na kuwafundisha kuhusu umuhimu wa nia ya mtu ya kufanya matendo ya wema, kusali na kufunga.

Page 467: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

452

SoMo la 123

Waambie wanafunzi wachague mojawapo ya mada zilizoorodheshwa ubaoni. Waambie wasome kifungu cha maandiko kinachohusiana kimoyomoyo, wakitafuta majibu ya ma-swali yafuatayo (unaweza kutaka kuandika maswali haya ubaoni):• dhidi ya nia gani Bwana alionya tunapofanya shughuli hii? • Ni kwa jinsi gani Bwana alisema tunapaswa kufanya shughuli hii? Kabla ya wanafunzi hawajaanza, inaweza kuwa na manufaa kueleza mnafiki kama mtu ambaye anavaa muonekano wa uongo wa haki au ambaye anasema jambo moja lakini anafanya lingine.Karibisha wanafunzi wachache kushiriki majibu waliopata kwa maswali haya mawili. (Ku-tokana na kutafuta kwao, wanafunzi wanapaswa kugundua kwamba Bwana alionya dhidi ya kufanya matendo ya haki ya kuonekana na watu na kufundisha kwamba tunapaswa kufanya matendo ya haki ili kumpendeza Baba yetu wa Mbinguni.) Ili kuwasaidia wanafu-nzi kufikiria zaidi kuhusu na kutumia mafundisho ya Mwokozi, uliza maswali yafuatayo:• Ni vipi nia zetu za kufanya matendo ya haki zinaathiri jinsi tunavyofanya?• Ni zipi baadhi ya nia za haki ambazo zinaweza kuhamasisha mtu kufanya wema, kusali,

au kufunga kwa siri? Andika yafuatayo ubaoni: Tukifanya matendo ya haki ili kumpendeza Baba wa Mbinguni . . .• Kulingana na 3 Nefi 13:4, 6, 18, ni baraka gani huja kwa wale ambao hufanya matendo

ya haki kumpendeza Baba wa Mbinguni? (wanafunzi wanapojibu, kamilisha taarifa juu ya ubao: Kama Tukifanya matendo ya haki kumpendeza Baba wa Mbinguni, Yeye atatuzawadia hadharani.

Karibisha wanafunzi kwa ufupi kupitia tathmini yao ya binafsi na kutathmini nia zao kwa ajili ya kufanya sadaka, kusali, au kufunga. Wahimize kufikiria jinsi gani wanaweza kutumia mafundisho ya Mwokozi kuboresha nia zao kwa kufanya shughuli hizi au nyingine, kama vile masomo ya maandiko matakatifu, kulipa zaka, kuhudhuria kanisani, na kushiriki sakramenti.

3 Nefi 13:19–24Yesu Kristo awafundisha umati wa watu kujiwekea hazina mbinguniAndika vishazi vifuatavyo kwenye ubao: Hazina Duniani na Hazina Mbinguni. Waalike wanafunzi kujadili maswali yafuatayo pamoja na mwenza:• Je, nini baadhi ya mifano ya hazina hapa duniani na hazina mbinguni?Baada ya wanafunzi kuwa na muda wa kujadili swali hili wawiliwawili, unaweza kuuliza wachache kuchangia majibu pamoja na darasa. Fikiria kutaja mfano kutoka kwenye ma-isha yako ya hazina duniani (unaweza kuonyesha milki ya thamani yako mwenyewe) na mfano wa hazina mbinguni (unaweza kuonyesha picha ya familia yako au kutaja umuhimu wa ushuhuda wako). Alika mwanafunzi asome 3 Nefi 13:19–23 kwa sauti. Uliza darasa ku-fuatilia pamoja na kutambua ushauri ambao Mwokozi alitoa kuhusu kutafuta hazina hapa duniani na hazina mbinguni.• Kulingana na 3 Nefi 13:19–20, ni vipi hazina hapa duniani ni tofauti na hazina mbinguni?• Kutafuta hazina hapa duniani kunawezaje kutuvuruga kutoka kwenye kutafuta hazina

mbinguni? (Unaweza ukitaka kufafanua kwamba Mwokozi hakufundisha kwamba fedha au mali ya kidunia ni mbaya, bali, yeye alisisitiza umuhimu wa kuweka mioyo yetu juu ya hazina ya mbinguni ambayo ni ya kudumu.)

• Unafikiri kishazi "kama. . . jicho lako likiwa moja" ‘kinamaanisha nini katika 3 Nefi 13:22? (Ili kusaidia wanafunzi kuelewa maana ya kishazi hiki, waelekeze kwenye ku-mbukumbu ya Topical Guide katika tanbihi 22c.) tunawezaje kuonyesha kujitolea katika kuweka hazina mbinguni?

Mwambie mwanafunzi aandike neno Mungu kwenye kipande cha karatasi na kukiweka kwenye upande mmoja wa darasa. Mwalike mwanafunzi mwingine aandike neno Kuipe-nda dunia kwenye kipande cha karatasi na kukiweka juu ya upande mwingine wa darasa. Mwalike mwanafunzi wa tatu asimame mbele ya darasa na kutazama karatasi iliyoandikwa Mungu. Kisha, mfanye mwanafunzi ageuke na kutazama karatasi iliyoandikwa Kuipenda dunia. Mwambie mwanafunzi ajaribu kutazama karatasi zote mbili kwa wakati mmoja. Uliza darasa kusoma 3 Nefi 13:24 kimoyomoyo na kufikiria jinsi aya hii inahusiana na jaribio la mwanafunzi kutazama karatasi zote kwa mara moja. Eleza kwamba neno mali inawakilisha kuipenda dunia au utajiri.

Kuelezea maneno magumu au vipengele vigumuLugha ya Kimaandiko wakati mwingine inaweza kuwa changa-moto kwa wanafunzi kuelewa. Kufafanua maneno magumu au vipengele inaweza kuwasaidia wanafunzi kuelewa vizuri si tu maudhui ya aya maalum lakini pia ujumbe wa jumla wa mwandishi wa kinabii. Makamusi, tanbihi, na usaidizi wa mafunzo ya maandiko inaweza kuwa zana za manufaa kuwasaidia wanafunzi kugundua maana ya neno fulani au kishazi.

Page 468: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

453

3 nefi 13

• Ni kwa njia gani kutafuta kumtumikia Mungu na mali ni kama kujaribu kutazama kuta zote mbili kwa wakati mmoja?

• Nini kinaweza kuwa baadhi ya Mifano ya kujaribu kumtumikia Mungu na Mamoni kwa wakati mmoja?

Alika darasa kusimama na kuangalia karatasi iliyoandikwa Mungu.• Kwa nini ni muhimu kwako kuwa na Mungu kama Bwana wako?• Kutokana na maneno ya Mwokozi katika 3 Nefi 13:24, unawezaje kujua kuwa Mungu

ni Bwana wako? (Ingawa wanafunzi wanaweza kutoa majibu mengi sahihi, hakikisha wao wanatambua kanuni ifuatayo: Ili kuwa na Mungu kama Bwana wetu, ni lazima tumpende na kumtumikia zaidi ya mambo ya dunia)

Wakati wanafunzi wamebaki wakisimama, soma mifano hapo chini na waambie wata-zame upande wa darasa ambayo inawakilisha Bwana ambaye wanafikiri mtu anamtumikia —Mungu au Kupenda dunia (mali). Waalike wanafunzi waeleze kwa nini walichagua kuge-uka kwa njia walivyofanya. (Unaweza kutaka kurekebisha mifano hii ili kukidhi mazingira na maslahi ya wanafunzi unaowafundisha.) 1. Kijana anakataa kazi ambayo itamtaka kukosa mikutano yake ya Jumapili na badala yake

anachagua kazi ya malipo ya chini ambayo hamhitaji kukosa mikutano yake. 2. Msichana mara nyingi analalamika kwa wazazi wake kuhusu haja yake ya nguo mpya.

Nguo ambayo anataka kununua zina gharama ya zaidi zile familia yake inaweza kumudu. 3. Kijana analipa zaka yake mara kwa mara na fedha anayopata kutokana na kazi yake.

Hata hivyo, anatumia mapato yake yaliyobaki kununua vitu vya burudani, ikiwa ni pa-moja na baadhi ya sinema sizizofaa na nyimbo, na hajaweka akiba fedha yoyote kwa ajili ya misheni au elimu.

4. Msichana mara nyingi anatumia baadhi ya mapato yake kununua zawadi ndogo ya kuo-nyesha upendo kwa wengine.

Kufuatia shughuli hii, waambie wanafunzi wakae, na kisha waulize maswali yafuatayo :• Kulingana na uzoefu wako, nini inaweza kuwa vigumu daima kumpenda na kumtumikia

Mungu juu ya mambo ya dunia? Kwa nini kumweka Mungu kwanza kunastahili juhudi?

3 Nefi 13:25–34Mwokozi anawaagiza wafuasi kumi na wawili kutafuta ufalme wa Mungu kabla ya matatizo yao ya kiduniaFupisha 3 Nefi 13:25–31 kwa kuwaambia wanafunzi kwamba Yesu Kristo aliwaagiza wafu-asi wake kumi wawili wasiwe wasiwasi juu ya mahitaji yao ya kidunia ya chakula na nguo. Toa angalizo kwamba ingawa mafundisho haya yalipewa hasa kwa wanafuasi kumi na wawili, kanuni za msingi zinaweza kutumika kwa ujumla. Alika mwanafunzi asome 3 Nefi 13:32–33 kwa sauti. Uliza darasa kufuata pamoja na kutambua jinsi Mwokozi alivyowafariji wanafuasi wake kuhusu mahitaji yao ya kidunia.• Ni vipi kutambua kwamba Mungu anajua mahitaji yetu kunatusaidia?• Kulingana na 3 Nefi 13:33, nini Yesu Kristo aliwahidi wale ambao humweka Mungu na

ufalme wake kwanza katika maisha yao? (Ingawa wanafunzi wanaweza kujibu kwa njia tofauti, hakikisha kuwa wao wanatambua kanuni zifuatazo: kama Tukitafuta ufalme wa Mungu kwanza, atatusaidia kukimu mahitaji yetu. Unaweza ukitaka kuandika kanuni hii juu ya ubao.)

• Unahisi vipi wakati rafiki wa karibu au mwana familia akiweka maslahi na mahitaji yako juu ya yake? Je, sisi huwasiliana nini na Baba wa Mbinguni na Mwokozi wakati tunapo-waweka juu ya mahitaji yetu ya kidunia na maslahi?

Waambie wanafunzi waandike katika madaftari au majarida ya kujifunzia maandiko lengo kuhusu jambo moja wanaloweza kufanya kikamilifu zaidi ili kumweka Mungu kwanza katika maisha yao. Unaweza ukipenda kuhitimisha somo kwa kutoa ushuhuda wa baraka ambazo umepata ulipotafuta kumweka Mungu na ufalme wake wa kwanza katika maisha yako.

Page 469: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

454

Utangulizi Yesu Kristo alipoendelea na mahubiri yake kwenye he-kalu katika Bountiful, Aliwatahadharisha watu kuhusu kuwahukumu wengine na kuwaagiza kutafuta baraka kutoka kwa Baba wa Mbinguni kwa kusali na kufanya

mapenzi Yake. Mwokozi pia aliwaonya kuhusu ma-nabii wa uongo na alisisitiza umuhimu wa kufanya mapenzi ya Mungu.

SOMO LA 124

3 nefi 14

Mapendekezo ya Kufundisha

3 Nefi 14:1–6Mwokozi anafundisha kuhusu kufanya hukumu za hakiIli kuandaa wanafunzi kujifunza mafundisho ya Mwokozi juu ya kufanya maamuzi ya haki, soma hadithi ifuatazo iliyosimuliwa na Rais Thomas S. Monson:

"Wanandoa vijana, Lisa na John, walihamia katika kitongoji kipya. Asubuhi moja wakati walikuwa wakila kifungua kinywa, Lisa alitazama nje ya dirisha na kummwangalia jirani wa mlango unaofuata akianika nguo zake."Nguo sio safi! Lisa alisema. Jirani yetu hajui jinsi ya kufanya nguo kuwa safi!"John aliangalia lakini alibaki kimya.

"Kila wakati jirani yake ataanika nguo zake zikauke, Lisa atatamka maoni yaleyale."Wiki chache baadaye Lisa alishangaa kutazama nje ya dirisha yake na kuona nguo safi zimeanikwa katika ua la jirani yake. Alisema kwa mume wake, `Angalia, John — hatimaye amejifunza jinsi ya kufua vizuri! Nashangaa jinsi alivyofanya. "John akajibu, Naam, mpendwa, Nina jibu kwa ajili yako. Utapenda kujua kwamba mimi niliamka mapema asubuhi na kuosha madirisha yetu! (Charity Never Faileth, Ensign au Liahona, Nov. 2010, 122).• Tunaweza kujifunza masomo yapi kutoka hadithi hii?Eleza kwamba 3 Nefi 14 ina muendelezo wa mafundisho ya Mwokozi kwa Wanefi heka-luni. Alika mwanafunzi asome 3 Nefi 14:1–2. Uliza darasa kufuata pamoja na kutambua onyo ambalo Yesu Kristo alitoa kuhusu kuwahukumu wengine. Unaweza kutaka kueleza kwamba neno pima linalopatikana katika 3 Nephi 14:2, lina maana ya kupima au kuhu-kumu. Kishazi na kile kipimo ninyi mnachopima kinahusu kiwango ambacho mtu anatu-mia kupima au kuwahukumu watu wengine.• Unaweza kueleza vipi ukweli katika 3 Nefi 14:2 kwa maneno yako mwenyewe? (majibu

ya Wanafunzi lazima yaonyeshe ukweli ufuatao: Sisi tutahukumiwa kulingana na jinsi tunavyohukumu wengine.)

Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa amri ya Mwokozi ya Msihukumu katika 3 Nefi 14:1, alika mwanafunzi asome kauli ifuatayo ya Mzee Dallin H. Oaks wa Akidi ya Mitume kumi na wawili. Liambe darasa kusikiliza aina hukumu tunayopaswa kuepuka kuwafanyia wengine.

"Hukumu ya mwisho ni lile tukio la baadaye ambalo sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo kuhukumiwa kulingana na matendo yetu. Naamini kwamba amri ya maandiko ya Msihukumu inahusu kwa uwazi zaidi hukumu hii ya mwisho. "Kwa nini Mwokozi aliamuru kwamba tusihukumu kwa hukumu ya mwi-sho? Naamini amri hii ilitolewa kwa sababu sisi tunakisia kufanya hukumu

ya mwisho wakati tunapotangaza kwamba mtu fulani anakwenda jehanamu (au mbi-nguni) kwa ajili ya tendo fulani au kwa wakati fulani. Tunapofanya hivi —na kuna jaribio kubwa kufanya hivyo —tunajiumiza wenyewe na mtu ambaye tunajifanya kumhukumu . . .

Page 470: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

455

3 nefi 14

"... Injili hii ni Injili ya matumaini, na hakuna hata mmoja wetu aliyepewa mamlaka ya kukana nguvu za Upatanisho ili kuleta utakaso wa dhambi ya mtu binafsi, msamaha, na kuyarejesha maisha katika hali sahihi" (Judge Not’ and Judging, Ensign, Aug. 1999, 7, 9).• Kauli ya Mzee Oaks inakusaidia vipi kuelewa amri ya Mwokozi ya msihukumu?Onyesha kipande kidogo cha kifaa, kama vile kibanzi kidogo cha mbao. Eleza kwamba neno lingine la kipande ni kibanzi. Kisha onyesha (au chora ubaoni) boriti ya mbao au kipande kirefu cha kuni. Wajulishe wanafunzi kuwa Mwokozi alielekeza kibanzi na boriti ili kutusaidia kuelewa matatizo yanayotokea wakati tunapowahukumu wengine kwa njia isiyo ya haki. Alika mwanafunzi asome 3 Nephi 14:3–5 kwa sauti, na Uliza darasa kufikiri kuhusu nini kibanzi na boriti vinawakilisha.• Kibanzi kinawakilisha nini? (Kosa tunaloliona kwa mtu mwingine) Boriti inawakilisha

nini? (makosa yetu wenyewe)Toa angalizo kwamba mlinganisho wa Mwokozi unalenga vitu vilivyoingia katika jicho. Vitu kama hivi huathiri maono ya mtu.• Makosa yetu yanawezaje kuathiri jinsi tunavyowaona wengine?Waambie wanafunzi wafikirie kama kamwe sahihi kufanya hukumu kwa watu wengine. Wape muda kutafakari swali hili. Kisha eleza kwamba katika tafsiri ilyoongozwa ya Mat-thew 7:1, Nabii Joseph Smith alifafanua mafundisho ya Mwokozi kuhusu kuwahukumu wengine. Kulingana na Joseph Smith, Mwokozi akasema, Msihukumu pasipo na haki, ili nanyi msihukumiwe: lakini toeni hukumu ya haki, (Joseph Smith Translation, Mathayo 7:1 [katika Mathayo 7:1, tanbihi a]). Alika mwanafunzi ya asome maelezo yafuatayo katika True to the Faith:"Wakati mwingine watu huhisi kwamba ni makosa kuhukumu wengine kwa njia yoyote. Ingawa ni kweli kwamba hatupaswi kuwalaumu wengine au kuwahukumu pasipo haki, utahitaji kufanya hukumu za mawazo, hali, na watu katika maisha yako. Bwana ametoa amri nyingi ambazo huwezi kuweka bila kufanya hukumu" (True to the Faith: A Gospel Reference [2004], 90).Ili Kuwasaidia wanafunzi kuona kwamba Mwokozi alifundisha umuhimu wa kufanya hukumu za haki, waalike wasome 3 Nephi 14:6 kimoyomoyo. Waambie wabainishe baadhi ya hukumu ambazo alituagiza kufanya. Waambie watoe taarifa nini wanakipata. • Inamanisha nini kutoa kile ambacho ni kitakatifu kwa mbwa au kutupa lulu mbele ya

nguruwe? (Kushiriki kitu ambacho ni kitakatifu na wale ambao hawezi kuweka thanani ya juu au kuheshima utakatifu wake.)

• Ni kwa jinsi gani ushauri wa Mwokozi katika 3 Nefi 14:6 unatuhitaji kufanya hukumu kwa wengine?

Baada ya wanafunzi kujibu, soma maelezo yafuatayo na Mzee Dallin H. Oaks kuhusu hali nyingine ambazo tunahitaji kufanya hukumu za haki :"Sote tunafanya maamuzi katika kuchagua marafiki zetu, katika kuchagua jinsi tunavyotu-mia muda wetu na fedha zetu, na, bila shaka, katika kuchagua mwenza wa milele . . . " ... ya haki itaongozwa na Roho wa Bwana, na si kwa hasira, kisasi, wivu, au maslahi ya ubinafsi" (Judge Not and Judging, 9).• Kwa nini ni muhimu kufanya hukumu ya haki katika hali kama vile kuchagua marafiki,

kuamua jinsi ya kutumia muda wetu na fedha, na kuchagua mwenza wa milele?• Je, ni nini baadhi ya hali nyingine ambazo tunahitaji kufanya hukumu ya wengine? (Wa-

nafunzi wanaweza kutaja kuchagua kati ya wanaoweza kuwa waajiri au kuamua ama kukubali mwaliko kwenda miadi.)

3 Nefi 14:7–11Mwokozi anafundisha kuhusu kutafuta baraka kutoka kwa Baba wa MbinguniWaalike wanafunzi wasome 3 Nefi 14:7–11 kimoyomoyo, wakitafuta mafundisho ya Mwo-kozi kuhusu utayari wa Baba wa Mbinguni kujibu maombi yetu. Eleza kwamba kama baba wa kidunia, ambao ni wapole na wenye upendo lakini si wakamilifu, watawapa watoto wao mkate na samaki badala ya mawe na nyoka, Baba yetu wa Mbinguni, ambaye ni mka-milifu mpole na mwenye upendo, hakika atajibu sala za watoto wake kwa ajili ya msaada.

Page 471: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

456

SoMo la 124

• Tunaweza kujifunza kanuni gani kutoka 3 Nefi 14:7–11? (Wanafunzi wanaweza kuta-mbua aina mbalimbali za kanuni. Kanuni moja unayoweza kutaka kusisitiza ni kwamba Baba wa Mbinguni hutubariki tunapoomba msaada wake.)

• Kwa nini ni muhimu kwako kujua kwamba Baba wa Mbinguni atajibu maombi yako?• Ni lini umehisi upendo wa Baba wa Mbinguni kwako kupitia njia ambayo Yeye amejibu

maombi yako? (Unaweza kuwapa wanafunzi muda wa kutafakari swali hili kabla ya kulijibu. Pia fikiria kushiriki uzoefu wako mwenyewe.)

3 Nefi 14:12–27Mwokozi afundisha umuhimu wa kufanya mapenzi ya Baba wa MbinguniWaalike wanafunzi wasome 3 Nefi 14:12 kimoyomoyo na watake kufikiria jinsi ya ma-fundisho ya Mwokozi katika aya hii yanaweza kuwasaidia kuwa zaidi kama Baba wa Mbinguni.• Kutii ushauri katika 3 Nefi 14:12 kunaweza kutusaidia vipi kuwa zaidi kama Baba yetu

wa Mbinguni?Wajulishe wanafunzi kwamba na Mwokozi alipoendelea kufundisha, alitumia milinganisho ya nguvu kutusaidia kuelewa umuhimu wa kufanya mapenzi ya Baba wa Mbinguni.Ili Kuwandaa wanafunzi kujifunza milinganisho ya Mwokozi katika 3 Nefi 14, fanya shu-ghuli zifuatazo:Gawanya wanafunzi katika vikundi viwili vya 2–4. Mpe kila mwanafunzi kipande cha kara-tasi. Andika marejeo ya maandiko yafuatayo ubaoni, na mpangie mmoja wao kwenye kila kundi: 3 Nefi 14:13–14; 3 Nefi 14:15–20; 3 Nefi 14:24–27. Kama una darasa kubwa, pangia vitalu vya maandiko kwa zaidi ya kundi moja. Waambie wanafunzi wasome maandiko wa-liyopangiwa na kuchora vielelezo ya milinganisho ambayo Mwokozi alitumia. Pia watake waandike nini walichojifunza kutoka kwa milinganisho hiyo.Baada ya muda wa kutosha, watake wanafunzi kuonyesha picha zao darasani na kueleza nini walichojifunza. Wanafunzi wanapowasilisha nini walilojifunza, uliza maswali kama haya yafuatayo:• Ni kwa njia gani kutii mafundisho ya Yesu Kristo kama kutembea kwenye njia nyemba-

mba? Ni kwa njia gani kukataa mafundisho ya Yesu Kristo ni kama kutembea kwenye njia pana? (Ona 3 Nefi 14:13–14.) Ni zipi baadhi ya njia ambazo mafundisho ya Mwo-kozi ni tofauti na mafundisho ya ulimwengu?

• Kwa nini mbweha avae mavazi ya kondoo? (Ona 3 Nefi 14:15.) Je mlinganisho huu unatuambia nini kuhusu tamaa na matendo ya manabii wa uongo?

• Kama miti katika 3 Nefi 14:16–20 inawakilisha watu, matunda yanaweza kuwakilisha nini? (Majibu yanaweza kujumuisha mawazo ya watu, maneno, matendo, na ushawishi juu ya wengine.)

• Tunaposikia maneno ya Mwokozi na kuyafuata, ni kwa jinsi gani tunakuwa kama mtu aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba? (Ona 3 Nefi 14:24–25.) Kama tukichagua kutokufuata maneno ya Mwokozi, tunakuwaje kama mtu anaejenga nyumba yake juu ya mchanga? (Ona 3 Nefi 14:26–27.)

Baada ya mawasilisho ya wanafunzi na majadiliano, mwambie mwanafunzi asome 3 Nefi 14:21–23 kwa sauti.• Tunaweza kujifunza nini kutoka 3 Nefi 14:21? (Wanafunzi wanaweza kutumia maneno

tofauti, lakini wanapaswa kutambua ukweli ufuatao [andika ukweli huu juu ya ubao]: Ni lazima tufanye mapenzi ya Baba wa Mbinguni ili kuingia katika Ufalme wa mbinguni.)

• Je ukweli huu huhusiana vipi na vielelezo ya njia nyembamba na pana, miti mizuri na mibaya, na mtu mwenye busara na mtu mpumbavu?

Wape wanafunzi muda wa kutafakari na kutumia yale waliyojifunza kutoka 3 Nefi 14. Waalike kuandika katika madaftari au majarida ya mafundisho ya maandiko kuhusu jinsi watakavyoboresha jitihada zao za kufuata mafundisho ya Mwokozi katika 3 Nefi 14. Muda ukiruhusu, karibisha wanafunzi wachache kufupisha kile walichojifunza na kushiriki kile watakachofanya kwa sababu ya kile walichojifunza. Unaweza kuhitimisha kwa kutoa ushu-huda wa baraka ambazo umepokea wakati umefuata mapenzi ya Baba wa Mbinguni.

Page 472: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

457

UtanguliziYesu Kristo alipoendelea kuwafundisha watu katika hekalu katika nchi Bountiful, alitangaza kwamba sheria ya Musa ilitimizwa na kwamba alikuwa mwanga na sheria ambayo watu wanapaswa kutazamia. Yeye kisha alielezea kwa wanafunzi wale kumi na wawili kwamba

watu katika Amerika walikuwa kondoo wengine ambao Yeye alikuwa amesema katika Yerusalemu (Ona Yohana 10:14–16). Pia aliahidi kwamba wale wanao-tubu na kurudi kwake watahesabiwa miongoni mwa watu wake wa agano.

SOMO LA 125

3 nefi 15–16

Mapendekezo ya Kufundisha

3 Nefi 15:1–10Mwokozi anatangaza kwamba ametimiza sheria ya MusaKabla ya darasa kuanza, andika maswali yafuatayo ubaoni:

Kwa nini kulipa zaka? Kwa nini kuweka siku ya Sabato takatifu? Kwa nini kuwatii wazazi?Ili kuanza somo, onyesha maswali juu ya ubao na kuuliza:• Watu wengine hushangaa kwa nini Bwana hutoa amri. Unaweza kueleza vipi madhu-

muni ya amri?Waalike wanafunzi kwamba Yesu Kristo alipowaelekeza Wanefi, aliwafundisha kwamba lengo moja la amri zake lilikuwa kuwaelekeza watu Kwake. Waalike wanafunzi kutafuta kusudi hili wanapojifunza 3 Nefi 15.Eleza kwamba Mwokozi alipozungumza na umati wa watu, Yeye alijua kwamba baadhi miongoni mwao walikuwa na swali. Waambie wanafunzi wasome kwa haraka 3 Nefi 15:1–2 ili kupata ni nini watu hawa walitaka kujua. (Wao walishangaa nini Mwokozi aliwataka kufanya kuhusu sheria ya Musa. Ibada za Wanefi,vitendo na muundo wa Kanisa lilikuwa limejengwa juu ya sheria ya Musa ili kuandaa watu kwa ajili ya ujio wa Yesu Kristo na kuwasaidia kutazamia dhabihu Yake ya kupatanisha. Inavyoonekana, baadhi walikuwa wamechanganyikiwa juu ya nini cha kufanya badala ya kushika sheria ya Musa.)Mwambie mwanafunzi asome 2 Nefi 15:3–5, 9 kwa sauti. Alika darasani ili kufuata pamoja, wakitafuta vishazi katika maelezo ya Mwokozi ambavyo vinaweza kuwa viliwahakikishia Wanefi kwamba imani yao haikuwa na haja ya kubadilika. Wapate wanafunzi wachache kushiriki vipengele walivyotambua. Waambie waeleze kwa nini wanafikiri vishazi hivi vina-weza kuwa na manufaa kwa Wanefi.• Kwa nini unafikiri Yesu alikuwa akifundisha wakati Yeye alitangaza kwamba Yeye ni she-

ria? (3 Nefi 15:9).Wanafunzi wanaweza kutoa aina tofauti ya majibu. Wanapojibu, wasaidie kutambua kweli zifuatazo (andika kweli hizi kwenye ubao): Yesu Kristo ni chanzo cha sheria. Sheria zote za injili hutuelekeza kwa Yesu Kristo na Upatanisho wake. Kama Tukifuata sheria Zake tutapokea uzima wa milele.• Kwa nini kweli hizi zilikuwa muhimu kwa Wanefi kuelewa wakati huu? (Unaweza kutaka

kutoa angalizo kwamba kama sheria ya Musa, sheria mpya ilielekaza kwa Mwokozi na Upatanisho Wake. Wakati baadhi ya mbinu za ibada ya watu ingebadilika, wangeweza kuendelea kuwa na imani katika Yesu Kristo na kumwabudu Baba katika jina lake.)

Fupisha 3 Nefi 15:6–8 kwa kueleza kwamba Mwokozi aliwahakikishia watu kwamba kama maneno ya manabii kuhusu Mkombozi yalikuwa yametimia kwake, unabii wao kuhusu matukio ya baadaye pia utatimia. Pia alielezea kuwa agano alilolifanya na watu wake bado lilikuwa na nguvu na lingetimia.Mwalike mwanafunzi asome 3 Nefi 15:9–10 kwa sauti. Uliza darasa kufuata pamoja, wakitafuta ni nini Mwokozi anataka watu wake kufanya na maarifa yao ya ukweli ambayo yameandikwa kwenye ubao.

Page 473: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

458

SoMo la 125

• Ina maanisha nini kwako “kumtazama” Kristo?Waalike wanafunzi kupitia 3 Nefi 15:9–10 na kufanya muhtasari wa jinsi Bwana anatutaka kutazama njia tunayoishi injili na baraka zinazokuja kama matokeo. (Wanafunzi wanaweza kufanya muhtasari wa kifungu hiki kwa njia tofauti, lakini majibu yao lazima yadhihirishe kanuni ifuatayo: Kama Tukimtazamia Yesu Kristo kwa kushika amri zake na kuvumi-lia mpaka mwisho, atatupa uzima wa milele.)• Je, inawezekana kwa kumfuata Yesu Kristo bila kushika amri zake? Kwa nini?Waalike wanafunzi wazingatie maswali uliyoyaandika ubaoni kabla ya darasa.• Je, inawezekana kwa mtu kushika amri kwa nje bila kumtizamia Yesu Kristo?• Je, ni zipi baadhi ya sababu ambazo mtu anaweza kutii amri kwa nje bila kumtazamia

Yesu Kristo? (Majibu yanaweza kujumuisha wajibu, hofu ya adhabu, hamu ya kufaa au ili kuonekana, au upendo wa sheria.)

• Nini inapaswa kuwa sababu yetu ya kutii amri? (Tunapaswa kushika amri kwa sababu tunampenda Bwana, tunataka kumpendeza, na tunataka kuja kwake.)

• Umebarikiwa vipi wakati wewe umetii amri kwa dhamira ya kweli? Watake wanafunzi kufikiria amri au kiwango cha injili ambacho kimekuwa kigumu kwao kuelewa na kufuata. Waalike kufikiria jinsi hisia zao kuhusu amri hii au kiwango kinaweza kubadilika kama upendo wao kwa Bwana inakuwa sababu yao ya kutii. Watie moyo kutii amri kwa upendo kwa ajili ya Bwana. Shiriki njia ambazo amri zimekusaidia kusongea karibu kwa Baba wa Mbinguni na Mwokozi.

3 Nefi 15:11–16:5Yesu Kristo ananena na wanafuasi wake juu ya kondoo wake wengineWaalike wanafunzi wainue mikono yao kama wamewahi kujihisi kuwa na umuhimu wa chini kuliko mtu mwingine. Watake kufikiria kama wamewahi kuhisi wamesahaulika au wakiwa peke yao au kama wamewahi kushangazwa kama Baba wa Mbinguni anawajua wao ni nani.Andika kauli ifuatayo ubaoni Mungu anawajali watoto wake wote, na Yeye alijionye-sha kwao. Wahakikishie wanafunzi ukweli wa kauli hii, na kuwakaribisha kutafuta usha-hidi wa ukweli wake wanapojifunza salio la of 3 Nefi 15 and mwanzo wa 3 Nefi 16.Alika mwanafunzi asome 3 Nefi 15:11–17, na uliza wanafunzi kutambua kile Bwana ali-sema kwa watu katika Yerusalemu kuhusu ya watu wake katika Amerika. Unaweza pia ku-wataka wanafunzi kusoma Yohana 10:14–16. (Wasaidie wanafunzi kuelewa kuwa kondoo wengine ni rejeo kwa wafuasi wengine wa Mchungaji, Yesu Kristo. Neno kundi linaweza kurejea kwa zizi la kondoo, lakini pia inaashiria kundi la watu wenye imani moja.)• Kwa mujibu wa 3 Nefi 15:17, Bwana aliahidi kujidhihirisha Mwenyewe kwa njia gani

kwa kondoo wake wengine, au wafuasi? (Wangesikia sauti Yake)Mwambie mwanafunzi asome 2 Nefi 15:18–19 kwa sauti. Uliza darasa kufuata pamoja, wakitafuta sababu kwa nini Baba wa Mbinguni alimuamuru Yesu Kristo kuzuia ufahamu kondoo wake wengine kutoka kwa watu katika Yerusalemu. Baada ya wanafunzi kutoa taarifa nini walichopata,uliza:• Tunaweja kujifunza kanuni gani kutoka kwa hili? (Majibu ya wanafunzi lazima kudhi-

hirisha kanuni ifuatayo: Mungu anatupa maarifa na ukweli kulingana na imani yetu na utiifu.)

Fanya muhtasari wa 3 Nefi 15:21–23 kwa kueleza kwamba Bwana aliwaambia Wanefi kwamba walikuwa kondoo wengine ambao Yeye alikuwa amesema, hata hivyo, Wayahudi wa Yerusalemu walifikiri Alikuwa akizungumzia watu wa Wayunani, au wasio Waisraeli. Hawakuwa wameelewa kuwa watu wa mataifa wasingeweza binafsi kusikia sauti yake. Alika mwanafunzi asome 3 Nefi 15:24 kwa sauti, na uulize darasa kusikiliza jinsi Bwana aliwahakikishia Wanefi utunzaji wake kwao. Unaweza kuuliza wanafunzi vipi wanaweza kuhisi kama wangemsikia Bwana akisema maneno haya kwao.Waambie wanafunzi wasome 3 Nefi 16:1–3 kimoyomoyo na kutambua ni nani mwingine angesikia sauti ya Mwokozi. Eleza kwamba hatuna kumbukumbu ya maeneo mengine na

Page 474: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

459

3 nefi 15 –16

watu Mwokozi alitembelea, lakini ni wazi kwamba Yeye alitembelea makundi mengine au wanachama wa kanisa.Ili kutanguliza wazo kwamba Mwokozi pia alijionyesha kwa wale ambao hawasikii sauti yake, uliza maswali yafuatayo kabla ya kuwaalika wanafunzi tafuta maandiko matakatifu kwa majibu:• Nini vipi kuhusu wale ambao hawapati kusikia sauti ya Mwokozi? Yeye huwaonyesha

vipi kwamba Yeye anawajali? Waalike wanafunzi kupekua 3 Nefi 15:22–23 na 3 Nefi 16:4, wakitafuta jinsi Bwana alivyo-tangaza atajionyesha mwenyewe kwa Watu wa mataifa (kwa njia ya mahubiri ya wengine, kwa njia ya ushuhuda wa Roho Mtakatifu, na kwa njia ya maandiko ya manabii).• Maonyesho haya yanadhihirisha vipi kwanba Mungu anawajali watoto wake wote? • Ni kwa njia gani Bwana amejidhihirisha mwenyewe kwako na kwa familia yako? • Unawezaje kusaidia katika juhudi za Bwana kujidhihirisha kwa watu wake wote?

3 Nefi 16:6–20Yesu Kristo anatangaza baraka na maonyo kwa Watu wa mataifa ambao wata-pata injili katika siku za mwishoWaulize wanafunzi kama wamewahi kutaka kuwa sehemu ya kundi, klabu, au timu. Uliza ni sifa gani zilitakiwa ili kuwa mwanachama wa kundi walilotaka kuwa sehemu yake. Pende-keza kwamba kundi kubwa tunaloweza kuwa wanachama ni lile la watu wa agano la Bwana.Alika mwanafunzi asome 3 Nefi 16:6–7 kwa sauti. Uliza darasa kufuata pamoja, wakitafuta nini Bwana alisema kingetokea katika siku ya mwisho kwa sababu watu wa mataifa wange-mwamini na nyumba ya Israeli haingeamini katika Yeye. (Unaweza kueleza kwamba manabii wa Kitabu cha Mormoni walitumia neno Watu wa mataifa kumaanisha watu ambao hawa-kutoka kwa Nchi Takatifu. Kwa hiyo, neno hilo linaweza kumaanisha washiriki wa Kanisa vi-levile wasioamini na washiriki wa dini zingine.) Baada ya wanafunzi kujibu, fanya muhtasari wa 3 Nefi 16:8–9 kwa kueleza kwamba Kristo Yesu alitabiri kwamba kuna pia wasioamini wa mataifa mengine katika siku za mwisho ambao watawatawanya na kuwanyanyasa washiriki wa nyumba ya Israeli. Alika mwanafunzi asome 3 Nefi 16:10 kwa sauti. Uliza darasa kufuata pamoja, wakitafuta ni nini kitatokea kwa hawa watu wa mataifa wasioamini.• Bwana alitangaza kwamba watu wa mataifa wasioamini wangepoteza nini?• Hii inaweza kutumika vipi kwa wale wanaojua ukweli lakini wakainuliwa kwa kiburi?Eleza kwamba Bwana aliahidi kuweka agano lake na nyumba ya Israeli kwa kuleta injili kwao (ona3 Nefi 16:11–12). Alika mwanafunzi asome 3 Nefi 16:13 kwa sauti. Uliza darasa kufuatilia wakitafuta kile kinachohitajika kwa mtu kuwa mshiriki wa watu wa agano la Bwana. Andika yafuatayo ubaoni: “kama sisi.. . . . , kisha sisi .. . . . ” Waambie wanafunzi watumie 3 Nefi 16:13 kukamilisha kauli hii. Wanafunzi wanapaswa kuwa na uwezo wa ku-tambua ukweli ufuatao: Kama tukitubu na kurudi kwa Yesu Kristo, ndipo tutahesabiwa miongoni mwa watu Wake. • Kwa nini ni baraka kuhesabuliwa miongoni mwa watu wa Bwana?Hitimisha kwa kushiriki ushuhuda wako wa kweli zilizofundishwa katika somo hivi leo.

Tangazo na Habari za Usuli3 Nefi 15:5–8. Agano lote halijatimia

Yesu alimaanisha nini aliposema, agano ambalo mimi nimefanya na watu wangu lote halijatimia? (3 Nefi 15:8). Yehova alifanya agano na Ibrahimu nyakati za

kale. Ibrahimu aliahidiwa (1) ukoo wa milele, (2) nchi ya urithi na (3) Nguvu za ukuhani wa Mungu. Ahadi hizi pia zilifanywa kwa uzao wa Ibrahimu (ona M&M 132:30–31) na itatimizwa katika siku zijazo.

Maswali ya upekuzimaswali ya upekuzi huwasaidia wanafunzi kujenga uwelewa wao wa msingi wa mafungu ya maandiko na kuwaka-ribisha kutafuta maelezo muhimu wanaposoma. Inasaidia kuuliza ma-swali kama hayo kabla ya wanafunzi kusoma mistari ambako jibu li-napatikana. Hii inalenga nathari ya wanafunzi na kuwasaidia kugu-ndua majibu ndani ya maandishi ya maandiko wanaposoma.

Page 475: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

460

Utangulizi Katika somo hili wanafunzi watazingatia jinsi ubishi huathiri uwezo wao wa kuhisi Roho. Pia wataweza kufikiri kuhusu wale ambao wamekuwa mifano chanya kwao na kufikiria ni jinsi gani wanaweza kutumikia kwa ubora kama mifano kwa wengine.

Mapendekezo ya Kufundisha

3 Nefi 11:18–41Yesu Kristo anapanga namna ya ubatizo, analaani ubishi, na kutangaza mafundisho yakeAndika neno ubishi juu ya ubao, na uliza wanafunzi kufafanua neno hili (hoja, migogoro, au kujadiliana).

Waambie wanafunzi waorodheshe kwa ufupi juu ya ubao baadhi ya hali au shughuli ambazo wanaweza kukabiliwa na uzoefu wa ubishi. (Unaweza kuwa na mwanafunzi mmoja kama mwandishi wakati darasa linatoa majibu.) Wakati Unapofanya shughuli hii epuka kile Mzee Dallin H. Oaks wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili aliita mbinu za adui ambazo zinazoweza kuhi-miza “mjadala na utata" (Kwa njia ya Bwana [1991], 139).

Wakumbushe wanafunzi kwamba katika 3 Nefi 11 walisoma kwamba Yesu Kristo alionekana kwa Wanefi ambao walikuwa wamekusanyika katika hekalu. Alika mwanafunzi asome 3 Nefi 11:28 kwa sauti, na kuuliza darasa kubainisha baadhi ya mada ambayo Wanefi walikuwa wamebishana juu yake. (Ili kusaidia wanafunzi kuelewa vizuri mstari huu, unaweza ukataka kueleza kwamba neno mabishano humaanisha ubishi au kutoelewana.)

Uliza: Kwa nini unafikiri ni muhimu kuepuka mabishano au ubishi wakati wa kujadili injili na wengine?

Andika yafuatayo ubaoni: roho ya ugomvi sio ya Mungu, la-kini. . . Mualike mwanafunzi asome 3 Nefi 11:29–30 kwa sauti, na waulize wanafunzi kutambua wapi roho ya ubishi inakotoka. Ukweli wanaoupata unaweza kuonyeshwa kama ifuatavyo: roho wa ugomvi sio wa Mungu, bali ni wa shetani. Una-weza ukipenda kupendekeza kwamba wanafunzi watie alama maneno haya katika maandiko yao.

Uliza: Kukumbuka mafundisho ya Mwokozi katika 3 Nefi 11:29–30 kunaweza kukusaidia vipi ukiwa katika hali inayoweza

Somo la Kujifunza Nyumbani3 Nefi 11:18–16:20 (Kitengo cha 25)

Vifaa vya Matayarisho kwa Mwalimu wa mafunzo ya nyumbaniMuhtasari wa Mafunzo ya Nyumbani ya Kila SikuMuhtasari ufuatao wa mafundisho na kanuni ambayo wana-funzi walijifunza walipokuwa wakisoma 3 Nefi 11:18–16:20 (kitengo 25) Haikusudiwi kufundishwa kama sehemu ya somo lako. Somo unalofundisha huzingatia machache tu ya mafundisho haya na kanuni. Fuata uvuvio wa Roho Mtaka-tifu unapozingatia mahitaji ya wanafunzi wako.

Siku ya 1 (3 Nefi 11:18–12:48)Wanafunzi walijifunza kwamba ubatizo ni lazima kufanywa na mtu ambaye ana mamlaka sahihi na lazima kufanyika katika namna ambayo imeelezwa na Bwana. Pia walijifunza mafundi-sho ya Kristo na kujifunza kwamba Roho Mtakatifu anamshu-hudia Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Katika mafunzo yao ya Heri na maelezo ya Mwokozi ya sheria ya juu, walijifunza kwamba kama tukiishi kulingana na mafundisho ya Yesu Kristo, tutabarikiwa na kutayarishwa kuingia katika Ufalme wa mbinguni. Walijifunza pia kwamba tunapokuja kwa Kristo na kushika amri zake, tunaweza kuwa zaidi kama yeye na Baba yetu wa Mbinguni walivyo, ambao ni wakamilifu.

Siku 2 (3 Nephi 13)Kutoka katika mafundisho ya Mwokozi kuhusu motisha kwa kutoa sadaka, kusali, na kufunga, wanafunzi walijifunza kwamba tukifanya matendo ya haki ili kumpendeza Baba wa Mbinguni, Yeye atatulipa waziwazi. Walipojifunza mafu-ndisho ya Mwokozi kuhusu kutowezekana kuwahudumia mabwana wawili, walijifunza kanuni zifuatazo: Ili kuwa na Mungu kama mkuu wetu, ni lazima kumpenda na kumtumi-kia yeye juu ya mambo ya dunia. Kama tukitafuta ufalme wa Mungu kwanza, atatusaidia kwa kutupa mahitaji yetu.

Siku 3 (3 Nefi 14)Mafundisho ya Mwokozi kuhusu hukumu kwa haki yaliwa-saidia wanafunzi kuelewa kwamba tutahukumiwa kulingana na njia ya sisi tunavyowahukumu wengine. Pia walijifunza kwamba Baba wa Mbinguni hutubariki tunapoomba msaada kutoka kwake. Wanafunzi walichora picha inayoonyesha mafundisho ya Mwokozi na kujifunza kwamba ni lazima kufanya mapenzi ya Baba wa Mbinguni ili kuingia katika Ufalme wa mbinguni.

Siku 4 (3 Nefi 15–16)Wanafunzi walijifunza kwamba Yesu Kristo ni chanzo cha sheria zote na amri za injili. Kama tukitazama kwake kwa kushika amri zake na kuvumilia mpaka mwisho, atatupa-tia uzima wa milele. Wanafunzi waliposoma maneno ya Mwokozi kuhusu kondoo wengine (3 Nefi 15:21), walijifunza kwamba Mungu anawajali watoto wake wote na alijionyesha kwao. Pia walijifunza kwamba Mungu anatupa maarifa na ukweli kulingana na imani yetu na utii.

Page 476: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

461

SoMo la KUj ifUnza nyUMbani

kuwa ya ubishi? (Unaweza kuonyesha hali maalum iliyoandikwa kwenye ubao au wafanye wanafunzi kufikiria hali ambayo mtu anataka kuleta ubishi juu ya vipengele vya injili.)

Ili Kuwasaidia wanafunzi kuelewa tokeo moja muhimu la ubishi, soma au onyesha kauli ifuatayo ya Rais James E. Faust wa Urais wa Kwanza: "Wakati kuna ugomvi, Roho wa Bwana ataondoka, bila kujali nani aliye katika kosa (What I Want My Son to Know before He Leaves on His Mission, Ensign, May 1996, 41).

Unaweza ukitaka kupendekeza kwamba wanafunzi waa-ndike kauli hii katika maandiko yao au katika majarida yao ya maandiko.

Uliza: Je, umewahi kuhisi Roho wa Bwana akiondoka kwa sa-babu ya ubishi? Ilihisi vipi?

Toa angalizo maneno ya Mwokozi kuhusu ubishi katika 3 Nefi 11:30: "Hili ndilo fundisho langu, kwamba vitu kama hivi vio-ndolewe mbali." Kisha uliza maswali yafuatayo:

• Tunawezaje kuondoa ubishi na migogoro?• Tunawezaje kutokubaliana na wengine na kuepuka ubishi?• Ni kwa njia zipi umehisi kubarikiwa kwa juhudi zako za kue-

puka au kushinda ugomvi?

Unaweza kutaka kushiriki uzoefu ambao umekuwa nao wakati umehisi kubarikiwa kwa juhudi zako za kuepuka au kushinda ubishi. Waalike wanafunzi warejee kwenye orodha ubaoni na wachague hali ambayo wanaweza mara nyingi kuhisi kuwa na ubishi. Wape muda wa kuandika shabaha ya jinsi watakavyota-futa kuepuka au kushinda ugomvi katika hali hiyo.

3 Nefi 12–16Yesu kristo afundisha kanuni ambazo husaidia watoto wake kukaribia ukamilifuAlika wanafunzi wasimame na kukariri 3 Nefi 12:48. Unaweza kutaka wafanye zoezi mara kadhaa ili waweze kukariri kifu-ngu hiki cha umahiri wa maandiko matakatifu kwa ukamilifu. Waambie wanafunzi watumie maandiko yao kuonyesha baadhi ya sifa za ukamilifu zilizotajwa katika 3 Nefi 12:1–12 ambazo wanatumaini ya kuendeleza katika kipimo cha juu zaidi.

Weka kiasi kidogo cha chumvi kwenye kijiko, na uliza wanafunzi kukisia kitu kile ni nini?. Kisha alika mwanafunzi kuja mbele na kubainisha kile kitu kwa kuionja. Baada ya mwanafunzi kubainisha kitu kile kuwa ni chumvi, uliza darasa, kuorodhesha faida ya chumvi. Wanapojibu, hakikisha ni dhahiri kwamba zaidi ya kitia ladha chakula, chumvi hutumika kama kihifadhi nyama isiharibike.

Waambie wanafunzi wasome 3 Nefi 12:13 ili kugundua yule ambaye Mwokozi alimlinganisha na chumvi. Wanafunzi wa-napojibu, eleza kwamba Alikuwa akimaanisha si tu kwa umati katika hekalu siku ile lakini pia wale wote ambao wamebatizwa katika agano lake.

Uliza: Kwa njia gani tunaweza, kama wafuasi wa Yesu Kristo, kuwa kama chumvi? (Tunapaswa kuhifadhi au kuokoa watu na kuboresha ulimwengu kwa kushawishi wengine kwa mema.)

Eleza kwamba katika 3 Nefi 12:13 neno ladha inahusu si tu ladha ya chumvi, bali pia na kazi yake ya kuhifadhi.

Mwambie mwanafunzi asome maelezo ya yafuatayo na Mzee Carlos E. Asay wa Wale Sabini kuhusu jinsi chumvi inavyoweza kupoteza ladha yake:

"Chumvi haiwezi kupoteza ladha yake kwa umri. Ladha hupotea kwa njia ya mchanganyiko na uchafuzi. Vile vile ladha na ubora humkimbia mtu anapochafua akili yake kwa mawazo machafu, akiharibu kinywa chake kwa kusema yasiyo kweli, na anapo-tumia vibaya nguvu zake katika kutekeleza matendo ya uovu" (Salt of the Earth: Savor of Men and Saviors of Men, Ensign, Mei 1980, 42).

Uliza: Kwa nini ni lazima tujitahidi kuwawasafi ili kushawishi wengine kwa mema?

Onyesha wanafunzi kurunzi. Washa, na wakaribishe wanafunzi wasome 3 Nefi 12:14–16 na tafuta jinsi Mwokozi alivyotumiwa mwanga kufundisha zaidi kuhusu jukumu la watu wake wa agano ulimwenguni. Kabla hawajasoma inaweza ikasaidia kue-leza kwamba pishi ni kikapu.

Uliza: Jinsi gani waumini wa Kanisa ambao hushika maagano yao wanaweza kuwa nuru kwa watu wengine?

Funika mwanga na kikapu au kitambaa, na uliza maswali yafuatayo:

• Ni zipi baadhi ya njia tunaweza kujaribiwa kufunika mwanga wetu?

• Kwa mujibu wa 3 Nefi 12:16, kwa nini Mwokozi anatutaka tuweke mfano wa haki kwa wengine? Tunapoweka mfano wa haki, tunaweza kuwasaidia wengine kumtukuza Baba wa Mbinguni. Unaweza ukitaka kupendekeza kwamba wanafunzi waandike kanuni hii katika ukingo wa maandiko yao.

• Ni nani ambaye mfano wake wa haki umekusaidia wewe ku-songea karibu zaidi kwa Baba wa Mbinguni au umeimarisha hamu yako ya kuishi injili kikamilifu zaidi?

Wahimize wanafunzi kuwa kama chumvi na kama mwanga kwa ulimwengu kwa kuchagua kuwa mifano ya haki.

Eleza kwamba Mwokozi aliendelea kufundisha Wanefi kwamba malipo halisi kwa ajili ya kuweka kwa haki amri zitakuja waki-mwabudu bila unafiki na bila kuweka mioyo yao juu ya hazina za kidunia au thawabu. Andika marejeo ya maandiko yafuatayo kwenye ubao: 3 Nefi 13:22; 13:31–33; 14:7–8; 15:9; 16:13. Waambie wanafunzi watafute vifungu hivi na kutambua baadhi ya tuzo ambazo Baba wa Mbinguni alituahidi ikiwa mioyo yetu italenga kuishi maisha ya haki. Baada ya muda wa kutosha, waalike kutoa taarifa ya kile wamekipata.

Shiriki na wanafunzi ushuhuda wako kwamba Baba wa Mbi-nguni na Yesu Kristo watasaidia na kuwabariki katika jitihada zao za kuondoa ubishi na kuwa mfano mwema kwa ulimwengu.

Kitengo kifuatacho (3 Nefi 17–22)Waeleze wanafunzi kwamba wanaposoma 3 Nefi 17–22 wata-soma kwamba Yesu Kristo alilia alipokuwa na watoto wa Wa-nefi. Wahimize kutafuta majibu ya maswali yafuatayo: Alifanya nini kwa ajili yao? Ni miujiza gani mingine Yesu alifanya wakati akihudumu miongoni mwa Wanefi?

Page 477: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

462

UtanguliziWakati siku ya kwanza ya Mwokozi na Wanefi ilipo-karibia kumalizika, Yeye alijua kwamba wengi ha-wakuelewa kikamilifu maneno yake. Aliwafundisha jinsi ya kupokea uelewa wa ziada, na alisisitiza umu-himu wa maombi na kutafakari. Watu walilia wakati

alipotangaza kwamba alikuwa anaondoka. Akiwa amejazwa na huruma, Mwokozi alibakia tena kidogo ili kuponya wagonjwa, ili kuwaombea watu, na kubariki watoto wao. Wanefi walijawa na furaha.

SOMO LA 126

3 nefi 17

Mapendekezo ya Kufundisha

3 Nefi 17:1–3Yesu awaagiza Wanefi kutafakari maneno yake na kuomba waelewe Waambie wanafunzi wajifikirie wenyewe katika hali zifuatazo: Wewe na rafiki mmepata viti vya mstari wa mbele katika mkutano Mkuu au katika mkutano wa kanda ambapo nabii ni mnenaji. Wakati mkiwa pale, nyote mnapata kukutana naye. Wakati wa mwisho wa mku-tano, wewe na rafiki yako mnaenda nyumbani.• Unafikiri wewe na rafiki yako mgezungumzia nini baada ya mkutano?Wakumbushe wanafunzi kwamba Yesu Kristo alikuwa akifundisha Wanefi kwa kile kinachoonekana kama siku nzima. Alipokuwa akijitayarisha kuondoka, alijua kwamba watu hawakuelewa kikamilifu alichokuwa akifundisha. Waalike wanafunzi wasome 3 Nefi 17:1–3 kimoyomoyo, wakitafuta ni kile Mwokozi aliwaambia Wanefi wanapaswa kufanya ili kupata uelewa zaidi. (Unaweza kupendekeza kwamba wanafunzi waweke alama wana-chopata.) Baada ya wanafunzi kutoa taarifa ya nini walichopata, uliza:• Kutafakari kunamaanisha nini?Mwalike mwanafunzi asome kwa sauti maelezo ya yafuatayo na Rais Henry B. Eyring wa Urais wa Kwanza. Uliza darasa kusikiliza kwa kile alichofundisha kuhusu nini maana ya kutafakari.

"Kusoma, kujifunza, na kutafakari si sawa. Tunasoma maneno na tunaweza kupata mawazo. Tunajifunza na tunaweza kugundua mifumo na mahusiano katika maandiko. Lakini tunapotafakari, tunakaribisha ufunuo wa Roho. Kutafakari, kwangu, ni kufikiri na kuomba mimi ninayofanya baada ya kusoma na kujifunza katika maandiko kwa makini (Serve with the Spirit, Ensign or Liahona, Nov. 2010, 60).

• Je unafikiri kutafakari na sala vinaweza kufanya kazi pamoja ili kutusaidia kuelewa kile tunachojifunza kanisani au seminari?

Toa angalizo kwamba mafundisho ya Mwokozi katika 3 Nefi 17:3 kwamba Wanefi wanapa-swa kuandaa akili [zao ] kwa ajili ya kesho wakati atakaporudi kuwafundisha tena.• Je, mtu anaweza kufanya nini ili kuandaa akili yake kabla ya kuhudhuria kanisa au seminari?• Kuna tofauti gani wakati tunapoandaa akili zetu kwa fursa kama zile za kujifunza?Ili kuwasaidia wanafunzi kutambua kanuni iliyofundishwa katika 3 Nefi 17:1–3, andika kauli isiyokamilika ifuatayo ubaoni, na watake wanafunzi kukamilisha kwa mujibu wa kile walichojifunza.

Kwa kutafakari na kuomba kwa Baba, tunaweza . . .Ingawa wanafunzi wanaweza kutumia maneno tofauti, wanapaswa kutambua kanuni ifua-tayo: Kwa kutafakari na kuomba kwa Baba, tunaweza kupokea uelewa mkubwa.Andika yafuatayo kwenye ubao:

Andaa akili yangu kabla ya kuhudhuria kanisa au seminariTafakari kile ninachosikia katika kanisa au seminariOmba kuhusu kile ninachosikia katika kanisa au seminari

Page 478: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

463

3 nefi 17

Waambie wanafunzi wachague moja ya vitendo vilivyoandikwa juu ya ubao. Wape muda wa kufikiri juu ya (1) jinsi walivyofanya na (2) jinsi ilivyowasaidia kujifunza zaidi kutoka kwenye uzoefu wao Kanisani au seminari. Alika wanafunzi wachache kushiriki mawazo yao na darasa. Himiza wanafunzi kufikiria jinsi wanavyoweza kuwa bora katika moja ya maeneo matatu na kufanya mipango ya namna ya kufanya hivyo. Unaweza kupendekeza kuwa waandike mipango yao katika madaftari au majarida ya mafundisho ya maandiko. Waalike wanafunzi kwamba sehemu ya pili ya somo itatoa nafasi kwao kufanya mazoezi ya kutafakari.

3 Nefi 17:4–25Mwokozi aponya mgonjwa miongoni mwa Wanefi, anaomba kwa Baba kwa ajili ya watu, na kubariki watoto waoOnyesha picha ya Yesu akifundishia katika nchi za Magharibi (62380; Gospel Art Book [2009], no. 82). Alika mwanafunzi asome 3 Nefi 17:4. Toa angalizo kishazi "sasa naenda kwa Baba."Waulize wanafunzi kufikiria wameshinda siku moja na Mwokozi na Yeye ametangaza kwamba ni wakati wake wa kuondoka. Waalike wanafunzi wachache kushiriki jinsi wange-weza kuhisi katika hali hii. Alika mwanafunzi asome 3 Nefi 17:5 kwa sauti, na litake darasa kubainisha jinsi Wanefi walivyoitikia wakati Mwokozi alipoeleza nia yake ya kuondoka.Eleza kwamba kama haingekuwa kwa hamu ya haki ya Wanefi, matukio yaliyowekwa kwenye kumbukumbu katika 3 Nefi 17 na 18 kamwe hayangetokea. Shughuli zifuatazo zimepangwa kusaidia wanafunzi zaidi kuelewa upendo Yesu Kristo alionao kwa watu wake na kuwasaidia kupata ukweli wenyewe katika maandiko kuhusu tabia za Yesu Kristo. Andika marejeo ya maandiko yafuatayo juu ya ubao, na waambie wanafunzi kuyanakili katika madaftari yao au majarida ya mafundisho ya maandiko.

3 Nefi 17:6–103 Nefi 17:11–183 Nefi 17:19–25

Soma kauli ifuatayo ya Rais Ezra Taft Benson :"Kwamba mtu ni mkubwa sana na aliyebarikiwa mno na mwenye furaha ambaye maisha yake yanakaribia zaidi mfumo wa mfano wa Kristo. Hii haihusiani na mali ya dunia, nguvu, au heshima. Mtihani wa kweli pekee wa ukuu, baraka,furaha, shangwe ni jinsi maisha yalivyo karibu na kuwa kama Bwana, Yesu Kristo. Yeye ni njia ya haki, ukweli kamili, na uzima tele" (“Jesus Christ—Gifts and Expectations,” Ensign, Des. 1988, 2).

Wape wanafunzi muda wa dakika 5 hadi 10 kwa ukimya kila mmoja ajifunze vifungu vya maandiko ulivyoandika ubaoni. Waalike kutambua ukweli kuhusu sifa za Mwokozi. Wana-pojifunza, wanapaswa kupata angalau ukweli mmoja kwa kila fungu la maandiko. Watake kuandika ukweli wanaoupata.Wakati wanafunzi watakapomaliza kujifunza, karibisha baadhi yao waandike ubaoni, chini ya marejeo ya maandiko yanayo fanana na andiko, ukweli mmoja ambao wamejifunza ku-husu Mwokozi. Wakati wanafunzi watakapomaliza shughuli hii, uliza maswali yafuatayo:• Kwa nini ni muhimu kwetu kujua kweli hizi kuhusu Mwokozi? • Ulipata ushahidi gani kwamba Mwokozi anajali mahitaji yetu na hamu zetu?• Sehemu gani ya simulizi hii ilikuvutia sana? Kwa nini?• Kwa nini unafikiri watu walijawa na furaha? (Ona 3 Nefi 17:18.)• Kwa nini unafikiri furaha ya Mwokozi ilikuwa kamili siku hiyo? (Ona 3 Nefi 17:20.)Waambie wanafunzi wafupishe kile walichojifunza kutoka 3 Nefi 17:6–25. Wanafunzi wa-naweza kutoa aina tofauti ya majibu. Ukweli mmoja wanaoweza kutambua ni Mwokozi anahisi huruma mwingi kwetu. Andika ukweli huu ubaoni. Unaweza kutaka kupende-keza kwamba wanafunzi waandike ukweli huu, au ukweli mwingine ambao wao wameta-mbua, katika kingo za maandiko yao karibu na 3 Nefi 17:6.Ili kuwasaidia wanafunzi kuthamini jinsi kuelewa sifa za Yesu Kristo kunatusaidia kuo-ngeza imani yetu, soma kauli ifuatayo:

Page 479: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

464

SoMo la 126

Unaweza kutumia imani katika Kristo wakati una uhakika kwamba yeye yuko, wazo sahihi la sifa zake, na ufahamu kwamba wewe unajitahidi kuishi kulingana na mapenzi yake (True to the Faith: A Gospel Reference [2004], 54).• Kuelewa asili ya huruma ya Mwokozi kunaweza kukusaidia kwa jinsi gani kuwa na

imani kwake?Toa angalizo "kuteswa kwa namna yoyote" katika 3 Nefi 17:9.• Ni aina gani ya maradhi inayoweza kujumuishwa kwa mateso ya "namna yoyote?"

(Aina zote za maradhi ya kimwili, kihisia, kiakili, na kiroho.)Waambie wanafunzi kutafakari njia ambazo wanaweza kuteswa na kile wangeweza kumu-uliza Mwokozi kuwaponya kama angewabariki kibinafsi. Wakumbushe kwamba ingawa Mwokozi hayuko hapa kutuhudumia mwenyewe uwezo wake wa kubariki na kuponya unapatikana kupitia ukuhani.• Wewe humwendea nani kwa baraka za ukuhani? • Ni lini ilikuwa mara ya mwisho ulihisi ushawishi wa uponyaji wa Mwokozi katika

maisha yako?Wakumbushe wanafunzi kanuni kuhusu kutafakari ambayo walijadili katika mwanzo wa darasa. Pendekeza kwamba njia moja wanaweza kutafakari ni kwa kutaswiri wenyewe katika hali iliyoelezwa katika masimulizi ya maandiko waliyosoma. Waambie wanafunzi ku-jitaswiri wenyewe miongoni mwa wa Wanefi wakati wa matukio yaliyoelezwa katika 3 Nefi 17. Wape wanafunzi muda wa kuandika katika madaftari au majarida ya mafundisho ya maandiko kuhusu nini walichoweza kusikia, kuona, kuhisi, na kujifunza kama wangekuwa miongoni mwa Wanefi na kuzungumza na Mwokozi kwenye muda ule muafaka. Unaweza kupendekeza kwamba waandike kuhusu mateso ambayo wangeweza kuomba Mwokozi kuponya. Watakapomaliza kuandika, fikiria kuwakaribisha wanafunzi wachache wasome kile walichoandika kwa darasa. Hakikisha wanaelewa kwamba hawapaswi kuhisi shuruti-sho kushiriki kitu chochote ambacho ni cha binafsi sana au siri.Baada ya wanafunzi wachache kushiriki walichoandika, unaweza kutaka kumkaribisha mmoja au wawili wao kushiriki jinsi walivyokuja kujua kwamba Yesu Kristo anawapenda na anawaonea huruma. Himiza wanafunzi kutafakari somo hili na kuamini katika huruma ya Mwokozi wakimtegemea kwa ajili ya usaidizi kwa hamu zao, udhaifu, matatizo, na majaribu.

KutafakariKutafakari ni ujuzi wa kujifunza maa-ndiko ambao unaweza kusaidia wanafunzi kuchambua, kuelewa, na kutumia kile wa-nachosoma. Wasaidie wanafunzi kujifunza kutafakari matukio ya maandiko kwa kuwahi-miza kujaribu kujenga picha katika akili zao za watu, mahali, na matu-kio waliosoma. Njia moja ya wanafunzi kuweza kukamilisha hili ni kwa kufikiria kwamba wao ni washiriki katika hadithi wanayosoma

Page 480: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

465

UtanguliziYesu Kristo alipokuwa akihitimisha siku ya kwanza ya huduma yake miongoni mwa Wanefi, Yeye alia-nzisha sakramenti. Aliwaamuru kushiriki sakramenti, Sali kwa Baba daima, na kupanua ushirika kwa watu wote. Mwokozi aliahidi baraka kubwa kwa wale

ambao walitii. Baadaye aliwapa wanafunzi wake kumi na wawili wa Kinefi maelekezo yanayohusu huduma yao katika Kanisa. Kabla ya kupaa mbinguni, aliwapa uwezo wa kutoa kipawa cha Roho Mtakatifu.

SOMO LA 127

3 nefi 18

Mapendekezo ya Kufundisha

3 Nefi 18:1–14Yesu Kristo alianzisha sakramenti kwa WanefiMwalike mwanafunzi asome kauli ifuatayo ya Mzee Gerald N. Lund wa wale Sabini. (Mwambie mwanafunzi kwamba jina czenkusch hutamkwa kama ZEN - kush.) Himiza darasa kufikiria nini kingeweza kuwa kama mpanda mlima aliyetajwa na Mzee Lund."Wakati fulani uliyopita kulikuwa na makala ya kuvutia kuhusu kupanda mlima katika jarida la kimatibabu. . . ."Makala yalihusu mtu mmoja aliyeitwa Czenkusch ambaye anaendesha shule ya upandaji. Czenkusch alikuwa akieleza kwa msahili mfumo wa belay katika kupanda mlima. Huu ni mfumo ambao wakweaji hujilinda kutokana na maporomoko. Mpandaji mmoja anakuwa katika sehemu ya salama na kuweka imara kamba kwa mpandaji mwingine, kwa kawaida kuzunguka mwili wake mwenyewe. 'Upo kwenye belay,' maana yake, 'Mimi nimekupata. Kama kutatokea kituchochote, nitakukinga usianguke.' Ni sehemu muhimu ya kupanda mlima. Sasa angalizo la nini kilifuata karibu katika makala: 'kufanya belay kumemletea Czenkusch hali bora na mbaya zaidi katika kupanda.' Czenkusch aliwahi kuanguka kutoka kilele cha juu, aking’oa visaidizi vitatu na kuvuta belayer wake kutoka kwenye korongo. Alisimamishwa, kichwa chini, futi 10 kutoka ardhini wakati belayer wake [Don] aliyekuwa amenyosha mkono yake yenye nguvu sana. 'Don aliokoa maisha yangu," anasema Czenku-sch. "Utamjibu vipi mtu kama huyo? Mpe kamba iliyotumika ya kupandia kama zawadi ya Krismasi? Hapana, unamkumbuka. Unamkumbuka daima." [Eric G. Anderson, “The Vertical Wilderness, Private Practice, November 1979, 21; shadda imeongezwa] (The Grace and Mercy of Jesus Christ, in Jesus Christ: Son of God, Savior, ed. Paul H. Peterson, Gary L. Hatch, and Laura D. Card [2002], 48).• Kwa nini unafikiri mpanda mlima alihisi kumpa zawadi ya vitu mwokoaji ingekuwa njia

isiyotosha kuonyesha shukrani? Waambie wanafunzi wasome 3 Nefi 18:1–7 kimoyomoyo, wakitafuta kile Mwokozi aliwa-ambia Wanefi kufanya ili kumkumbuka yeye. (Unaweza kupendekeza kwamba wanafunzi waweke alama maneno ukumbusho na kumbuka katika 3 Nefi 18:7.) Baada ya wanafunzi kutoa taarifa nini walichopata, uliza maswali yafuatayo:• Ni kwa njia gani kushiriki sakramenti hutusaidia kukumbuka dhabihu ya Mwokozi kwa

niaba yetu?• Kwa mujibu wa 3 Nefi 18:7, Wanefi walikuwa wakumbuke nini waliposhiriki mkate?Wape wanafunzi muda wa kuangalia nyuma katika 3 Nefi 11:14–15. Kisha uliza maswali yafuatayo:• Kwa nini kukumbuka mwili wa Mwokozi kuwe muhimu hasa kwa Wanefi? • Ingawa hujaona majeraha katika mwili wa Mwokozi kama Wanefi walivyofanya, kwa

nini bado ni muhimu kwako kushiriki mkate wa sakramenti katika kuukumbuka mwili wa Mwokozi? M&M 20:77

Page 481: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

466

SoMo la 127

• Nini unaweza kufanya ili daima kumkumbuka Mwokozi?Andika kishazi kifuatacho ubaoni: Tunaposhiriki sakramenti, tunashuhudia kwa Baba kwamba . . .Waalike wanafunzi wasome 3 Nefi 18:8–11 kimoyomoyo, wakitafuta maneno au vishazi ambavyo vinakamilisha taarifa ubaoni. Waambie wanafunzi wachache washirikishe kile wa-lichopata. (Wanafunzi wanaweza kukamilisha maelezo kwa njia hii: Tunaposhiriki sakra-menti, tunashuhudia kwa Baba kwamba daima tutamkumbuka Yesu Kristo. Jawabu jingine liwezekanalo linaweza kuwa lifuatalo Tunaposhiriki sakramenti, sisi hushuhudia kwa Baba kwamba tuko tayari kufanya yote ambayo Mwokozi aliagiza.)Tumia baadhi au yote ya maswali yafuatayo kuwasaidia wanafunzi kuimarisha uelewa wao na shukrani kwa ajili ya jukumu sakramenti katika kutusaidia tumkumbuke Mwokozi :• Je, nini baadhi ya vipengele vya maisha ya Mwokozi na huduma ambavyo tunavyoweza

kukumbuka wakati wa ibada ya sakramenti? (Majibu huenda yakajumuisha kifo chake na kafara ya upatanisho, kuzaliwa kwake kwa unyenyekevu, miujiza Yake na mafundisho, huduma yake ya upendo kwa wengine, na kujitoa kwake kwa Baba wa Mbinguni.)

• Ingawa kushiriki sakramenti kunachukua kiasi kidogo cha muda, matokeo ya kujita-yarisha kwa na kushiriki katika ibada hii ya milele. Tufanye nini ili daima tumkumbuke Mwokozi baada kushiriki sakramenti na wakati uliobaki wa wiki?

• Ni vipi tunaweza kwa uaminifu na umakini tunayotoa kwa kushiriki sakramenti kunatu-saidia kumkumbuka mwokozi wakati wa juma zima.?

• Sakramenti ina maana gani kama tukikosa kumkumbuka?• Kwa mujibu wa 3 Nefi 18:7, 11, Mwokozi aliahidi nini kwa hao wanaoshiriki sakramenti

na kumkumbuka? (Tunaposhiriki sakramenti na daima kumkumbuka Mwokozi, tutakuwa na Roho wake awe nasi.)

Mwambie mwanafunzi asome 3 Nefi 8:12–14 kwa sauti, na kisha mwalike mwingine asome 3 Helamani 5:12 kwa sauti. Waambie wanafunzi waliobaki wafuate pamoja, kutafa-kari uhusiano kati ya vifungu hivi viwili katika maandiko.• Kushiriki mara kwa mara sakramenti kunakusaidia vipi kumfanya Yesu Kristo msingi

ambao juu yake unajenga maisha yako?Ili kuwasaidia wanafunzi kumkumbuka Yesu Kristo zaidi, waalike kuandika kila siku kwa wiki ijayo katika madaftari, majarida ya mafundisho ya maandiko, au majarida yao binafsi kuhusu nini wanachofanya kumkumbuka Mwokozi. Wahimize kufikiria kuandika kuhusu mawazo waliyokuwa nayo wakati wa sakramenti au jinsi kumkumbuka Mwokozi kulivyo-shawishi mawazo, maneno, na matendo yao.Fuatilia pamoja na wanafunzi kwa vipindi vichache vya darasa vijavyo kwa kuwahimiza waendelee kuandika kila siku. Wakati wa wiki, unaweza kutaka kuwapa dakika chache ka-tika mwanzo wa darasa ili kuweka taarifa ya kile wanachokifanya kumkumbuka mwokozi.

3 Nefi 18:15, –25Yesu anawafundisha Wanefi kusali kwa Baba daima na kukutana pamoja mara kwa maraGawanya wanafunzi wawili wawili. Waambie kila wenza wasome 3 Nefi 18:15–21 pamoja, wakitafuta nini Mwokozi alitufundisha kufanya ili kupinga majaribu. Wakati watakapo maliza kusoma, watake kila wenza kuandika sentensi moja ambayo wanahisi kuwa ni muhtasari wa mafundisho haya kuhusu kushinda majaribu. Uliza baadhi ya wenza washi-riki kile walichoandika. (Ingawa wanafunzi wanaweza kutumia maneno tofauti ya kueleza muhtasari wao, wanapaswa kutambua ukweli ufuatao: Kama tukiwa macho na kuomba daima kwa Baba, tunaweza kuzuia majaribu ya Shetani.)• Unafikiri neno kuwa macho linamaanisha nini katika 3 Nefi 18:18? kuwa macho kiroho,

kujitayarisha kwa lolote, au kujilinda.)• Kwa nini unafikiri kuwa macho na kuomba ni muhimu kwa kuzuia majaribu?Toa angalizo kwamba 3 Nefi 18:15, 20–21 ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Unaweza kupendekeza kwamba wanafunzi waweke alama kifungu hiki katika njia tofauti ili waweze kukipata kwa urahisi.

3 Nefi 18:15, 20–21 ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Rejea wazo la kufundi-shia mwishoni mwa somo ili kuwasaidia wanafunzi pamoja na umahiri wao wa kifungu hiki.

Page 482: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

467

3 nefi 18

• Sala hutusaidia kwa jinsi gani kukaa macho na kutahadhari kuhusu jitihada za Shetani kutujaribu?

Waalike wanafunzi kujibu mojawapo wa maswali yafuatayo katika daftari au majarida ya kujifunzia s maandiko: Unaweza ukataka kuandika maswali ubaoni au kusoma pole pole ili wanafunzi waweze kuandika:• Maombi yamekusaidia vipi kuzuia majaribu ya Shetani?• Unaweza kufanya nini ili kuboresha maombi yako ya kibinafsi?• Umeona baraka zipi kutokana na kuomba na familia yako?• Unaweza kufanya nini ili kuisaidia familia yako kuwa na maombi ya familia thabiti na

ya maana?Kama muda unaruhusu, fikiria kuwaambia wanafunzi wachache kushiriki na darasa nini walichoandika.Waambie wanafunzi wamfikirie mtu ambaye wangependa kumsaidia kusongea karibu na Mwokozi. Andika kanuni ifuatayo kwenye ubao na kuhamasisha wanafunzi kuiandika: Tu-napowahudumia wengine, tunaweza kuwasaidia kuja kwa Kristo. Waalike wanafunzi kusoma 3 Nefi 18:22–24 kimoyomoyo.• Je Mwokozi anatuuliza kufanya nini ili kuwasaidia wengine kuja kwake? (Hatupaswi ku-

wafukuza wengine kutoka kwenye mikutano yetu ya Kanisa, na tunapaswa kuwaombea.)• Mwokozi alisema kwamba Yeye ni mwanga ambao tunapaswa kuushikilia juu kwa uli-

mwengu. Je tunawezaje kila mmoja wetu kuishi maisha yetu tukiushikilia juu mwanga wa Mwokozi?

Soma kwa sauti maelezo ya yafuatayo na Mzee Robert D. Hales wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili. Waalike wanafunzi wasikilize kwa nini Mzee Hales alisema kitatokea wakati tukiishi maisha ya haki.

"Je, si ingempendeza Yesu kama tungeweza kuacha mwanga wetu kuangaza ili wale ambao walitufuata sisi wangemfuata Mwokozi? Kuna wale ambao wanatafuta mwanga ambao wangefurahia kupitia lango la ubatizo hadi kwa njia nyofu na nyembamba iendayo kwenye uzima wa milele (ona 2 Nefi 31). Je, utakuwa mwanga huo ambao utawaongoza kwenye bandari ya usalama? (That Ye May Be the Children of Light [Brigham Young University fireside

address, Nov. 3, 1996], 8, speeches. Byu. Edu).• Unapata mawazo gani wakati unapofikiria swali, Je, si ingempendeza Yesu kama tu-

ngeweza kuacha mwanga wetu uangaze ili wale ambao walitufuata sisi wangekuwa wanamfuata Mwokozi?

Eleza kuwa kuwaombea wengine, kuwaalika kuhudhuria mikutano ya kanisa, na kuweka mfano ulio kama wa Kristo ni njia ambazo tunaweza kuwahudumia wengine. Waalike wa-nafunzi wachache kushiriki tukio ambalo walishikilia juu mwanga wa Mwokozi kumsaida mtu kumjia Yeye.

3 Nefi 18:26–39Mwokozi anafundisha wanafunzi wake kupanua ushirika kwa watu woteFanya muhtasari wa 3 Nefi 18:26–39 kwa kueleza kuwa baada ya Mwokozi kuzungumza na umati wa watu, aligeukia wanafunzi Kumi na Wawili Aliokuwa amechagua na kuwaa-giza juu ya jinsi ya kuongoza na kuelekeza mambo ya Kanisa. Waalike wanafunzi wasome 3 Nefi 18:32 kimoyomoyo, wakitafuta jinsi tunavyopaswa kuitikia kwa watu ambao wame-potea kutoka katika imani.• Kwa nini ni muhimu kwamba tuendelee kuwahudumia watu ambao wamepotea kutoka

kwenye imani?Fikiria kushiriki uzoefu ambao umesaidia kumhudumia mmoja wa watoto wa Mungu na kumsaidia mtu kuja kwa Kristo.

Page 483: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

468

SoMo la 127

Umahiri wa maandiko—3 Nefi 18:15, 20–21Angalizo: Kwa sababu ya urefu wa somo hili, unaweza kuanza somo lifuatalo pamoja na shughuli zifuatazo za umahiri wa maandiko. Au shughuli hii inaweza kutumika katika somo la siku zijazo wakati una muda zaidi kwa kupitia vifungu vya umahiri wa maandiko.Tumia dakika kadhaa kuwasaidia wanafunzi kukariri 3 Nefi 18:15, 20-21. Andika aya zote tatu ubaoni, na watake wanafunzi wafanye mazoezi ya kuzisema kwa sauti. Baada ya wanafunzi kusoma mistari yote mara chache, anza kufuta sehemu mbalimbali za mistari wakati wanafunzi wanapoendelea kusoma kifungu kizima. Rudia mchakato huu hadi maneno yote yamefutwa kutoka ubaoni.

Page 484: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

469

UtanguliziBaada ya Mwokozi kukamilisha ziara yake ya kwanza kwa Wanefi, habari za ziara yake zilienea kati ya watu usiku ule wote. (Matukio yaliyoandikwa katika 3 Nefi 11–18 yote yalifanyika katika siku moja.) Usiku wote, watu "walijishughulisha sana ili wapate kuwa kesho yake katika sehemu ile" ambapo Mwokozi alikuwa anaenda kuonekana tena (3 Nefi 19:3). Asubuhi, wale

Wanafunzi Kumi Na Wawili waliwafundisha watu na kuomba pamoja nao. Yesu Kristo alitokea na kuwa-amuru watu kuomba, naye Akiomba kwa Baba kwa niaba yao. Kwa sababu ya imani yao, Wanafunzi Kumi na Wawili walitakaswa. Yesu aliomba kwamba wafuasi na wale wote walioamini maneno yao waweze kuwa wamoja pamoja Naye na Baba yake.

SOMO LA 128

3 nefi 19

Mapendekezo ya Kufundisha

3 Nefi 19:1–14Wanafunzi kumi na wawili wawahudumia watu kama Mwokozi alivyoamuruWaambie wanafunzi kufikiria wanachoweza kufanya au jinsi gani wanaweza kuhisi kama wa-ngejua kwamba kesho Yesu Kristo atakuwa anakuja hekaluni (au makao ya kigingi, au katikati ya jiji, au mahali pengine ambapo patahitaji juhudi fulani kwa upande wa wanafunzi kusafiri).• Ungewezaje kufika huko?• Ungemtaka nani kwenda nawe?• Ungefanya nini ili kujitayarisha kwa tukio hili?Wakumbushe wanafunzi kwamba karibu na hitimisho la ziara ya Mwokozi kwa Wanefi siku ya kwanza, Yeye aliwatia moyo watu kwenda kwenye majumbani mwao na kutafakari na kuomba kuhusu mafundisho yake ili kujiandaa kwa ajili ya ziara yake siku ya pili (ona 3 Nefi 17:3). Waambie wanafunzi wasome 3 Nefi 19:1–3 kimoyomoyo, wakitafuta mwitikio wa Wanefi kwa ahadi ya Mwokozi kwamba yeye angerudi siku ya pili. Baada ya wanafunzi kutoa taarifa nini walichopata, fanya muhtasari 3 Nefi 19:4–8 kwa kueleza kuwa baada ya umati wa watu kukusanyika siku ya pili, Wanafunzi Kumi na Wawili waligawanywa watu katika makundi kumi na mawili na, wakaanza kuwafundisha. Baada ya kuuelekeza umati kupiga magoti katika sala, wale Wanafunzi Kumi na Wawili pia waliomba na kisha kuwafu-ndisha watu kweli zilezile ambazo Mwokozi alikuwa amewafundisha siku iliyopita. Kisha wanafunzi wakapiga magoti katika maombi tena.Alika mwanafunzi asome 3 Nefi 19:8–9 kwa sauti. Uliza darasa kufuata pamoja, wakitafuta kile nini wanafunzi waliombea.• Je wafuasi walitamani nini zaidi? • Wanafunzi kumi na wawili walikuwa waendeshe moja kwa moja shughuli za Kanisa mi-

ongoni mwa Wanefi baada ya Mwokozi kuondoka. Kwa nini unafikiri walimhitaji Roho Mtakatifu katika huduma zao?

• Katika sala unayotoa, ni yapi mambo machache ambayo wewe unatamani zaidi?• Je, wewe huomba kwa ajili ya Roho Mtakatifu? Kwa nini? Au kwa nini isiwe hivyo?Alika mwanafunzi asome 3 Nefi 19:10–12 kwa sauti. Baada ya yeye kumaliza kusoma, eleza kuwa ubatizo huu wa pili ulikuwa wa hali maalum. Ingawa Wanefi walikuwa wamebatizwa hapo awali kwa ajili ya ondoleo la dhambi na walikuwa wanastahili kuwa katika uwepo wa Yesu Kristo, Mwokozi aliwaamuru wabatizwe tena kwa sababu alikuwa amepanga Kanisa upya.Alika mwanafunzi asome 3 Nefi 19:13–14 kwa sauti. Uliza darasa kufuata pamoja, wa-kitafuta baraka ambazo wafuasi walipokea kama jibu kwa hamu zao za haki. Ili kusaidia kuongeza hamu ya wanafunzi kwa ushawishi wa Roho Mtakatifu katika maisha yao, fanya shughuli zifuatazo:

Page 485: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

470

SoMo la 128

Gawa wanafunzi katika majozi. Waambie kila wenza kutengeneza orodha katika madaftari au majarida ya mafundisho ya maandiko kile Roho Mtakatifu anafanya kwa wale ambao wanaishi maisha yanayostahili. Kisha, waalike wanafunzi kulinganisha orodha yao na ma-elezo ya yafuatayo na Mzee Robert D. Hales wa Akidi ya Mitume Kumi Na Wawili. (Mbele ya darasa, fanya nakala ya taarifa au iandike ubaoni.) Wafanye wanafunzi waongeze kwenye orodha yao mawazo yoyote mapya walioyapata wakisoma taarifa.

"Roho Mtakatifu ... ni chanzo cha ushuhuda wetu wa Baba na Mwana. . . ."Tunahitaji Roho Mtakatifu kama mwenza wetu mara kwa mara kutusaidia kufanya chaguzi bora katika maamuzi yanayotukabili kila siku. Uenza wa Roho utawapa [vijana wetu] nguvu ya kuzuia uovu, na kunapohitajika, tubu na rudi kwenye njia nyofu na nyembamba. Sote tunahitaji urutubishaji unaopatikana kupitia njia ya Roho Mtakatifu. Kuwa na karama ya Roho Mtakatifu husaidia

familia kufanya chaguzi yenye hekima— chaguzi ambazo zitawasaidia kurudi pamoja na familia zao kwa Baba yao wa Mbinguni na Mwana wake, Yesu Kristo, kuishi nao milele (The Covenant of Baptism: To Be in the Kingdom and of the Kingdom,” Ensign, Nov. 2000, 8).• Ni kwa njia gani Baraka kwenye orodha yako zingekuwa zenye msaada kwa vijana katika

Kanisa? Waite wanafunzi wapitie orodha ya baraka ambazo wameandika na kufikiria nini tunahitaji kufanya ili kustahili baraka hizi. Waambie wasome 3 Nefi 19:9, 13 kimoyomoyo, wakitafuta kanuni kuhusu kupokea ushawishi wa Roho Mtakatifu. Wafanye wanafunzi waandike kanuni wanayotambua. Watake wachache wao kushirikiana kile walichoandika. (Wanafu-nzi wanaweza kushirikiana kitu kama kifuatacho: hamu zetu za haki na sala zinaweza kutufanya tusitahili kujazwa Roho Mtakatifu.)• Ni lini hamu yako ya haki na sala zimekusaidia kuhisi ushawishi wa Roho?Andika kauli ifuatayo isiyokamilika ubaoni. Waalike wanafunzi kuandika sehemu hii ya kauli na kisha kukamilisha kwa maneno yao wenyewe.

Mimi nitamwonyeshea Baba wa Mbinguni shauku yangu ya uenza wa Roho Mtakatifu, kwa . . .

3 Nefi 19:15–36Mwokozi anatokea na kuomba kwa ajili ya watu watakaswe kupitia njia ya imani yaoMwambie mwanafunzi asome 2 Nefi 19:15–16 kwa sauti. Toa angalizo kwamba wakati watu walipokuwa wamepiga magoti, walishuhudia Yesu Kristo akitoa sala tatu tofauti kwa ajili ya wanafunzi wake na umati. (Eleza hiyo baadaye katika somo ambalo darasa litajifu-nza sala ya tatu ya Mwokozi.)Andika marejeo ya maandiko na maswali yafuatayo kwenye ubao mbele ya darasa (au kuyaandaa kwenye kipeperushi kwa kila mwanafunzi):

3 Nefi 19:17–18, 24–26, 303 Nefi 19:19–233 Nefi 19:27–29Unaweza kujifunza nini kuhusu maombi kutoka kifungu hiki?Ungewezaje kutumia kile ulichojifunza katika aya hizi kwa maombi yako ya kibinafsi?

Gawanya darasa katika makundi ya wanafunzi watatu kila moja. (Kama darasa lako ni dogo, unaweza kuhitaji kugawa darasa katika vikundi vidogo vidogo.) Mpangie mwana-funzi katika kila kikundi kusoma moja ya vifungu vya maandiko vilivyoandikwa ubaoni. Wajulishe wanafunzi kwamba lazima wote wawe tayari kujibu katika makundi yao maswali yaliyopo ubao.Baada ya muda wa kutosha, watake wanafunzi kuchangia majibu yao kwa maswali na washiriki wengine wa makundi yao. Kuwa tayari kujibu kama wanafunzi watauliza kwa nini wanafunzi waliomba kwa Mwokozi (ona 3 Nefi 19:18). Toa angalizo kwamba katika mfano huu wa kipekee, wanafunzi waliomba kwa Yesu Kristo kwa sababu alikuwa pamoja nao kimwili kama mwakilishi wa Baba (ona 3 Nefi 19:22).Alika mwanafunzi asome 3 Nefi 19:31–34 kwa sauti. Uliza darasa kufuata pamoja na kufikiria kwa nini maombi ya Mwokozi yaliwaathiri watu kwa undani. Alika wanafunzi wachache watoe taarifa ya kile wanachokipata. Wakati wanafunzi wataweza kujifunza kweli nyingi kutoka kwa wengine wanaposhiriki shughuli ifuatayo itasisitiza kanuni mbili wanazoweza kugundua katika masomo yao.

Page 486: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

471

3 nefi 19

Andika ubaoniyafuatayo: Tunapotumia imani katika Yesu Kristo, . . .Waambie wanafunzi kupitia 3 Nefi 19:28 kimoyomoyo, Wakitafuta njia ya kukamilisha kauli iliyoandikwa kwenye ubao. (waalike wanafunzi kuandika majibu yao. Ifuatayo ni njia moja wapo ya wanafunzi kukamilisha kauli: Tunapotumia imani katika Yesu Kristo, tunaweza kutakaswa.)• Inamaanisha nini kutakaswa? Kutumia imani katika Yesu Kristo kunatusaidiaje kuwa wasafi?• Ni katika njia zipi wafuasi walitumia imani wakati wa matukio yaliyowekwa kumbuku-

mbu katika 3 Nefi 19?Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa kwamba sisi tunatakaswa kwa Roho Mtakatifu, wa-kumbushe kwamba wanafunzi walipokea Roho Mtakatifu na "walijazwa ... kwa moto" (3 Nefi 19:13). Eleza kwamba kishazi "kujazwa ... kwa moto" ni ishara ikimaanisha baraka ya kutakaswa kwa njia ya ushawishi wa Roho Mtakatifu.Waambie wanafunzi wasome tena 3 Nefi 19:23, 29 kimoyomoyo, wakitafuta baraka nyi-ngine inayokuja kwa wale ambao wana Roho wa Bwana pamoja nao. (Baada ya wanafunzi kusoma, unaweza kutaka kupendekeza kwamba waweke alama katika aya zote mbili kishazi "Ili tuwe pamoja.")• Yesu Kristo na Baba ni wamoja kwa jinsi gani? (Wao ni viumbe tofauti, wanaoonekana,

lakini ni wamoja katika kusudi na mafundisho. Wakiwa katika umoja mkamilifu, wana-leta mpango wa kiungu wa Baba wa Mbinguni wa wokovu.)

• Ina maana gani kwetu kuwa wamoja na Mungu Baba na Mwana?• Tunajifunza nini kutoka 3 Nefi 19:23, 29 kuhusu jinsi tunavyoweza kuwa wamoja pamoja

nao? (Kwa njia ya imani, tunaweza kutakaswa na kuwa wamoja na Yesu Kristo, kama Yeye alivyo mmoja na Baba.)

Mwalike mwanafunzi asome taarifa ifuatayo ya Mzee D. Todd Christofferson wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili: Litake darasa kusikiliza jinsi tunavyoweza kuwa wamoja na Baba na Mwana.

"Yesu alitimiza mafanikio ya umoja kamili na Baba kwa kujitoa mwenyewe, mwili na roho, kwa mapenzi ya Baba. Huduma yake ilikuwa daima ya umakini kwa sababu hapakuwa na kudhoofisha au bughudha ya mawazo mawili katika Yeye. Akizungumzia Baba yake, Yesu alisema, 'nafanya daima yale yanayompendeza' (Yohana 8:29)..."Hakika sisi hatuwezi kuwa wamoja na Mungu na Kristo hadi tutakapofanya

mapenzi yao na maslahi yao kuwa hamu yetu kubwa. Kujisalimisha huko hakuwezi kufikiwa kwa siku, lakini kupitia Roho Mtakatifu, Bwana atatufundisha kama tukiwa radhi mpaka, katika mchakato wa muda, inaweza kusemwa kwa usahihi kuwa Yeye yu ndani yetu kama Baba alivyo katika Yeye" (That They May Be One in Us, Ensign, Nov. 2002, 72, 73).Waalike wanafunzi wasome 3 Nefi 19:35–36 kimoyomoyo na kutafakari nguvu ya maombi yao wenyewe. Waahidi wanafunzi kwamba sisi pia tunaweza kuwa na uzoefu mkubwa wa kiroho na kukua kuelekea kuwa wamoja na Baba na Mwana kama tukiongeza imani yetu na kuomba kwa bidii kwa ajili ya uenza wa Roho.

Tangazo na Habari za Usuli3 Nefi 19:18, 22. waliomba kwa Yesu

Kutokana na maandiko na mafundisho ya manabii wa siku za mwisho, tunajua kwamba tunapaswa kumwa-budu Mungu Baba, na kuomba kwake tu. Hatupa-swi kuomba kwa Yesu Kristo kwa mfano, Mwokozi aliwafundishwa Wanefi, Ninyi lazima msali daima kwa Baba kwa jina langu (3 Nefi 18:19). Hata hivyo, muda mfupi baada ya Mwokozi kufundisha hili, wanafunzi wake Wanefi waliomba moja kwa moja kwake (ona 3 Nefi 19:18). Walifanya hivyo, alisema, kwa sababu alikuwa pamoja nao (ona 3 Nefi 19:22). Mzee Bruce R.

McConkie wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alieleza kuwa hii ilikuwa hali tofauti — ya kipekee:

Kulikuwa na sababu maalum kwa nini hili lilifanyika ka-tika hali na kwa msingi wa wakati mmoja tu. Yesu ali-kuwa tayari amewafundisha kuomba kwa jina lake kwa Baba, ambayo wao kwanza walifanya. Yesu alikuwepo mbele yao kama ishara ya Baba. Kwa kumwona Yesu, ilikuwa ni kana kwamba walimwona Baba; kuomba kwake, ilikuwa ni kama waliomba kwa Baba. Ilikuwa ni hali maalumu na ya kipekee (The Promised Messiah [1978], 560, 561).

Page 487: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

472

UtanguliziSiku ya pili ya huduma yake miongoni mwa Wanefi, Yesu Kristo tena alisimamia sakramenti kwa watu. Alishuhudia kwamba maagano na ahadi za Baba

zitatimizwa katika siku za mwisho. Israeli itakusanywa, na mataifa yote ya dunia yatabarikiwa.

SOMO LA 129

3 nefi 20

Mapendekezo ya Kufundisha

3 Nefi 20:1–9Mwokozi asimamia sakramenti kwa watu tenaIli kuanza somo, eleza kwamba ungependa vijana na wasichana katika darasa kujibu maswali tofauti. Waite vijana wachache ambao wana Ukuhani wa Haruni kuambia darasa kuhusu majukumu yao ya kuandaa, kubariki, au kupitisha sakramenti. Wasaidie kushiriki hisia zao kuhusu kutekeleza majukumu haya kwa kuwauliza maswali yafuatayo:• Ina maana gani kwako kusaidia kusimamia sakramenti? • Unawezaje kuonyesha kwa Bwana kwamba unaelewa asili takatifu ya ibada hii?Wasaidie wasichana wachache kushiriki hisia zao kuhusu utakatifu wa sakramenti kwa kuwauliza maswali yafuatayo:• Unajihisi vipi wakati unapoona vijana wanaostahili wakisimamia sakramenti? • Wewe hufanya nini wakati wa usimamizi wa sakramenti ambacho kinachoonyesha kwa-

mba unaelewa asili yake takatifu?Eleza kwamba wakati wa siku ya pili ya huduma Yake miogoni mwa Wanefi, Mwokozi na wanafunzi wake walisimamia sakramenti kwa watu mara ya pili. Waalike wanafunzi wasome 3 Nefi 20:1 kimoyomoyo. Toa angalizo sentensi ifuatayo: Na aliwaamuru kwamba hawapaswi kusitisha kuomba katika miyoyo yao.• Ina maanisha nini kwako kutokuacha kuomba katika moyo wako?Mwambie mwanafunzi asome 3 Nefi 20:3 kwa sauti.• Jinsi gani unafikiri kuomba moyoni mwako kunaweza kushawishi uzoefu wako wa kila

wiki wa kushiriki sakramenti? • Kwa nini unafikiri ni muhimu kudumu katika kumzingatia Mwokozi tunaposhiriki

sakramenti? Mwalike mwanafunzi asome 3 Nefi 20:8 kwa sauti. Uliza darasa kufuata pamoja, wakita-futa ni nini mkate na mvinyo huwakilisha. (Ni inaweza kuwa na manufaa kueleza kwamba utaratibu wa sasa wa Kanisa ni kutumia maji badala ya mvinyo. [Ona M&M 27:2.])• Mkate wa sakramenti na maji huwakilisha nini? (Mwili na damu ya Mwokozi.)Unaweza kutaka kusoma maelezo ya yafuatayo na Mzee James E. Talmage wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa maana ya kiishara ya mwaliko wa Mwokozi kula mwili wake na kunywa damu yake."Kula nyama na kunywa damu ya Kristo kulikuwa na bado ni kuamini katika na kumkubali kama Mwana halisi wa Mungu na Mwokozi wa dunia, na kutii amri Zake. Kwa njia hizi tu ndipo Roho wa Mungu anaweza kuwa sehemu ya kudumu ya nafsi ya mtu binafsi, hata kama kiini cha chakula anachokula kinatumiwa na misuli ya mwili wake" (Jesus the Christ, 3rd ed. [1916], 342; italics added).• Ni ishara gani iliyopo katika kushiriki mkate na maji?• Kwa mujibu wa 3 Nefi 20:8, Yesu Kristo aliahidi nini kwa wale wanaoshiriki sakramenti?

(Nafsi zao zitashibishwa.)

Page 488: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

473

3 nefi 20

Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa nini maana ya kushibishwa kwa nafsi zao, watake kufi-kiri juu ya kiasi cha mkate na maji wao kwa kawaida hula na kunywa wakati wanaposhiriki sakramenti. Kisha uliza:• Kama ungekuwa na njaa na kiu, ungeweza kushibishwa navyo?Mwambie mwanafunzi asome 3 Nefi 20:9 kwa sauti, na uliza darasa:• Ni kanuni gani tunayoweza kujifunza kutoka katika mafundisho ya Mwokozi katika

3 Nefi 20:8–9? (Wanafunzi wanaweza kutumia maneno tofauti, lakini wanapaswa kutambua kanuni ifuatayo: Kama tunashiriki sakramenti kwa kustahili, tunaweza kujazwa na Roho Mtakatifu.)

Mwalike mwanafunzi asome taarifa ifuatayo ya Mzee Dallin H. Oaks wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili: Litake darasa kusikiliza njia tunazoweza kubarikiwa tunapo jazwa na Roho:

"Hebu tujihitimishe wenyewe kwa ajili ya ahadi ya Mwokozi wetu kwamba kwa kushiriki sakramenti sisi tutajazwa (3 Ne. 20:8; ona pia 3 Ne. 18:9), ambayo ina maana kuwa tutajazwa na Roho (3 Ne. 20:9). Roho hiyo— Roho Mtakatifu —ni mfariji wetu, mtafutaji wa mwelekeo wetu, mwasili-shaji wetu, mkalimani wetu, shahidi wetu, na mtakasaji wetu —mwongozo wetu asiyeanguka na msafishaji kwa ajili ya safari yetu ya maisha ya kufa

tukielekea uzima wa milele. "... Katika ya kitendo kinachoonekana kidogo cha uangalifu na kwa heshima tukifanya upya maagano ya ubatizo huja kufanywa tena baraka za ubatizo kwa maji na kwa Roho, ili tuweze daima kuwa na Roho wake awe nasi. Kwa njia hii sisi sote tutaongozwa, na kwa njia hii sisi sote tunaweza kutakaswa" (Always Have His Spirit, Ensign, Nov. 1996, 61).• Ni njia zipi tunazoweza kubarikiwa tunapojazwa na Roho? • Ni lini kushiriki sakramenti kumekusaidia kujazwa na Roho Mtakatifu?Shuhudia baraka ulizopokea kwa kushiriki sakramenti na kujazwa na Roho. Thibitisha kwamba kuomba kwa mioyo yetu ni njia moja tunayoweza kujitayarisha kushiriki sakra-menti na kujazwa na Roho Mtakatifu. Himize wanafunzi kutumia muda katika maombi kabla ya kushiriki sakramenti.

3 Nefi 20:10–46Mwokozi anawafundisha Wanefi juu ya maagano yatakayotimizwa katika siku za mwishoWaalike wanafunzi kuandika katika daftari au majarida ya mafundisho ya maandiko maelezo mafupi ya sifa zao muhimu zaidi. Wakiisha kumaliza, waalike kuangalia aina za sifa walizozingatia. Je zilikuwa sifa za kimwili? Sifa za umaarufu? Sifa za kiroho? (Kama kuna muda unaweza kuwaalika wanafunzi wachache kusoma walichoandika) Soma kauli ifuatayo ya Mzee David A. Bednar wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, na Uliza darasa kusikiliza kile anachosema kinachopaswa kuelezea utambulisho wa mtu:

“Unaweza kuwa unafurahia muziki, riadha au kuegemea umakanika, na siku moja unaweza kufanya kazi katika biashara au taaluma au katika usanii. Na shughuli kama hizi zilivyo muhimu, na ajira zinaweza kuwa,hazielezei sisi ni nani. Kwanza kabisa sisi ni viumbe vya kiroho Sisi ni [watoto] wa Mungu na Uzao wa Ibrahimu.” (“Becoming a Missionary,” Ensign or Liahona, Nov. 2005, 47).

• Mzee Bednar alielezaje kuwa sisi ni nani? Kwa nini unafikiri ni muhimu kwetu kujiona “Kwanza kabisa” kama viumbe vya Kiroho ambao ni watoto wa Mungu?

Toa angalizo kwamba kwa nyongeza kusema kwamba sisi ni watoto wa Mungu, Mzee Bednar alisema kwamba sisi ni uzao wa Ibrahimu. Eleza kwamba kishazi “uzao wa Ibra-himu” kinaweza kuelekeza watu ambao ni uzao wa moja kwa moja wa Ibrahimu. Inaweza pia kuelekeza watu ambao, kwa kukubali na kutii sheria na ibada za injili ya Yesu Kristo, wanapokea ukamilifu wa injili, baraka za ukuhani na ahadi zile zile na maagano ambayo Mungu aliweka na Ibrahimu.Waalike wanafunzi kuwa katika salio la 3 Nefi 20, watajifunza mafundisho ya Mwakozi kwa Wanefi kuhusu maagano na ahadi zilizofanywa kwa Ibrahimu na uzao wake (nyumba ya Israeli) Alisema kuwa wangejifunza kuhusu maagano haya kwa kusoma maneno ya

Page 489: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

474

SoMo la 129

Isaya. Alika mwanafunzi asome 3 Nefi 20:11–12 kwa sauti. Litake darasa kufuatilia, wakita-futa nini Mwokozi alisema kingefanyika wakati maneno ya Isaya yangetimizwa. Baada ya Wanafunzi kutoa taarifa nini walichopata, unaweza kuhitaji kueleza kwamba maneno ya Isaya yatatimizwa katika siku za mwisho.Alika mwanafunzi asome 3 Nefi 20:13 kwa sauti na waulize wanafunzi watambue jinsi Baba wa Mbinguni atakavyotimiza maagano yake na Nyumba ya Israeli katika siku za mwisho. Waambie wanafunzi wafupishe kweli wakizojifunza kutoka 3 Nefi 20:11–13. (Majibu ya wanafunzi yanaweza kuwa tofauti, lakini wanapaswa kutambua ukweli ufuatao: Bwana atatimiza agano lake la kukusanya nyumba ya Israeli katika siku za mwisho. Fikiria kuandika ukweli huu ubaoni.)• Kulingana na 3 Nefi 20:13, ni ufahamu gani watu wa nyumba ya Israeli watapata kama

sehemu muhimu ya mkusanyiko huu? (Watapata “ufahamu wa Bwana Mungu wao, aliyewakomboa.”)

Ili kuwasaidia wanafunzi kuona jinsi ya kupata ufahamu wa Yesu Kristo kuwa sehemu mu-himu ya kukusanyika kwa Israeli, mwambie mwanafunzi asome kwa sauti kauli ifuatayo ya Mzee Bruce R. McConkie wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili. Waambie wanafunzi kusikiliza kile kukusanyika kwa Israeli kinahusisha. “Kukusanyika kwa Israeli kunajumuisha kuamini na kukubali kuishi kwa uwiano na yale yote ambayo Bwana mwanzo aliwapa watu wake wateule. Inajumuisha kuwa na imani ka-tika Bwana Yesu Kristo, ya kutubu, ya kubatizwa na kupokea karama ya Roho Mtakatifu, na ya kuweka amri za Mungu. Inajumuisha kuamini injili, kujiunga na Kanisa, na kuja katika ufalme. Inajumuisha kupokea ukuhani mtakatifu, kupewa nguvu katika sehemu takatifu pamoja na uwezo kutoka juu, na kupokea baraka zote za Ibrahimu, Isaka na Yakobo kupitia kwa ibada ya ndoa ya selstia Na inaweza pia kujumuisha kukusanyika kwenye sehemu au nchi iliyochaguliwa ya kuabudu” (A New Witness for the Articles of Faith [1985], 515).• Je ni kwa njia gani kumwamini na kumfuata Yesu Kristo ni sehemu muhimu ya kuku-

sanyika kwa Israeli?Fupisha 3 Nefi 20:14–22. Eleza kuwa Mwokozi aliwafundisha Wanefi kwamba kama sehemu ya kukusanyika kwa Israeli na katika kutimiza agano la Bwana na Ibrahimu, Baba wa Mbinguni aliwapa uzao wa Lehi nchi ambamo waliishi kama urithi. Alieleza pia njia nyingine Wanefi walibarikiwa kama wana wa agano. Waalike wanafunzi wasome 3 Nefi 20:23–24 kimoyomoyo wakitafuta ni nani Musa alitabiri kuwa angebariki nyumba ya Israeli. Baada ya wanafunzi kutoa taarifa ya nini walichokipata, waalike wasome 3 Nefi 20:25–26 kimoyomoyo. Waambie watambue jinsi uazo wa Lehi walibarikiwa kwa sababu ya agano ambalo Mungu aliweka na Ibrahimu. Wanafunzi wanapotoa taarifa ya kile wali-chopata, sisitiza kwamba Baba wa Mbinguni alimtuma Yesu Kristo kuwatembelea uzao wa Lehi na kuwaokoa kutoka kwenye dhambi “kwa kuwa [walikuwa] wana wa agano.”• Jinsi gani tumebarikiwa kwa maagano tunayofanya na baba wa mbinguni? Sisi tumeba-

rikiwa vipi kwa maagano tuliyoweka na Baba wa Mbinguni?Mwambie mwanafunzi asome 3 Nefi 20:27 kwa sauti, na uliza darasa kutambua jukumu ambalo linalokuja pamoja na maagano tunayofanya na Mungu.• Mara tufanyapo maagano na Bwana, ni nini wajibu wetu kwa watu wengine kote duniani?

(wanafunzi wanapaswa kutambua ukweli ufuatao: kama uzao wa Ibrahimu, tuna ju-kumu la agano kuwabariki watu wote wa dunia. Fikiria kuandika ukweli huu ubaoni.)

• Unafikiri vipi tunaweza kuwa baraka kwa watu wote wa dunia? (Kama umeandika kauli hii ya mafundisho ubaoni, ongeza maneno “kwa kushirikiana injili pamoja nao.”)

Fupisha 3 Nefi 20:29–46 kwa kueleza kwa ufupi kwamba ukijumuisha kufundisha Wanefi kuhusu baraka zao na majukumu kama watoto wa agano, Mwokozi alihakikisha kwamba nchi ya urithi ya wayahudi itakuwa Yerusalemu. Alinukuu tabiri za Isaya ambazo zili tabiri muda ambapo wayahudi watarejeshwa kwenye nchi yao ya urithi baada ya wao kumwa-mini Yesu Kristo na kuomba kwa baba katika jina lake. Ili kuhitimisha, mwalike mwanafunzi asome 3 Nefi 20:46 kwa sauti. Waambie wanafunzi kufuatilia na kutambua njia moja wanayoweza kubariki maisha ya mtu mwingine kwa injili katika wiki inayokuja. Panga kufuatilia na wanafunzi katika darasa lijalo ili kuwapa fursa ya kutoa taarifa ya uzoefu wao. Shuhudia umuhimu wa kutimiza wajibu wetu wa kusaidia kukusanya Israeli.

Page 490: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

475

UtanguliziYesu Kristo alipoendelea kuwafundisha Wanefi, alieleza kuwa kuja kwa Kitabu cha Mormoni katika siku za mwi-sho kungekuwa ishara kwamba ameanza kuwakusanya Israeli na kutimiza agano lake na watu wake. Akisisitiza

upendo wake mkuu kwa watu wake wa agano, Mwo-kozi alinukuu utabiri wa Isaya kuhusu urejesho wa watu wa agano.

SOMO LA 130

3 nefi 21–22

Mapendekezo ya Kufundisha

3 Nefi 21:1–11Yesu kristo anafundisha kwamba kuja kwa Kitabu cha Mormoni kutakuwa ni ishara ya kukusanyika kwa Israeli katika siku za mwishoMbele ya darasa, chora ishara zifuatazo kwenye ubao (au tumia ishara ambazo ni za kawa-ida unakoishi).

Waulize wanafunzi kutambua maana ya kila ishara. Kisha uliza maswali yafuatayo:• Ishara hutumiwa kwa nini (Kutayarisha, kuonya na kutuelekeza.)• Kwa nini ni muhimu kwamba ishara iwekwe kisahihi na kwamba ujumbe kwenye ishara

uwe rahisi kueleweka? Wakumbushe wanafunzi kwamba maandiko mara nyingi huzumgumzia ishara zinazota-yarisha, kuonya na kutuagiza kuhusu utimizo wa Mpango wa Baba wa Mbinguni. Waalike wanafunzi kupitia 3 Nefi 21:1–2, 7, wakiutafuta neno ishara. Unaweza kutaka kupendekeza kwamba wawekee alama neno popote linapoonekana katika aya hizi. Kisha waambie kusoma kwa makini aya 1 kimoyomoyo.• Kwa nini Bwana alisema angetupa ishara hii maalumu? (Ili watu waweze kujua kuwa

anawakusanya nyumba ya IsrealiWaambie wanafunzi wasome 3 Nefi 21:1–7 kimoyomoyo na waambie watoe angalizo la vishazi “vitu hivi” na “kazi hizi” na kuzingatia kile vishazi hivi vinamaanisha.• Akizungumza na Wanefi, Mwokozi alinena juu ya mambo haya ambayo mimi natangaza

kwenu (3 Nefi 21:2). Ni wapi ambapo maneno yake kwa Wanefi yagewekwa kumbuku-mbu? (Katika Kitabu cha Mormoni.)

• Kulingana na mistari hii, ni nini moja ishara kwamba Mungu anatimiza maagano yake katika siku za mwisho? (Wasaidie wanafunzi kutambua ukweli ufuatao [andika kwenye ubao]: Kuja kwa Kitabu cha Mormoni ni ishara kwamba Mungu anatimiza ahadi yake ya kukusanya Israeli katika siku za mwisho.)

Mwalike mwanafunzi asome kwa sauti taarifa ifuatayo ya Mzee Russell M. Nelson wa Akidi ya wale Mitume Kumi na Wawili: Uliza darasa kusikiliza njia ambazo Kitabu cha Mormoni husaidia watu kukusanyika kwa kazi ya Bwana.

Kitabu cha Mormoni ni muhimu kwa kazi hii. Inatangaza mafundisho ya Mkusanyiko. Na kinasababisha watu kujifunza kuhusu Yesu Kristo, kuamini injili yake, na kujiunga na kanisa lake. Kwa kweli, kama kusingekuwa na Kitabu cha Mormoni, mkusanyiko ulioahidiwa wa Israeli haungetokea (The Gathering of Scattered Israel,” Ensign or Liahona, Nov. 2006, 80).

Fundisha kwa Roho MtakatifuOmba uongozi wa Roho Mtakatifu unapojitayari-sha na unapofundisha.

Page 491: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

476

SoMo la 130

• Ni lini Kitabu cha Mormoni kimekusaidia katika njia hizi? Ni lini umeona Kitabu cha Mormoni kikiwasaidia watu wengine katika njia hizi?

Mwalike mwanafunzi asome 3 Nefi 21:9 kwa sauti, na omba darasa liangalie maneno "kazi kubwa na ya ajabu." Toa angalizo kwamba kishazi hiki kinahusu Urejesho wa injili ya Yesu Kristo, ambao ni pamoja na kuja kwa Kitabu cha Mormoni• Je, ni nini kilicho kikubwa na cha kushangaza kuhusu Urejesho wa injili ya Yesu Kristo?Toa angalizo kwamba 3 Nefi 21:9 inahusu “mtu. Watake wanafunzi kufikiria mtu huyu anaweza kuwa ni nani. Kisha onyesha picha ya Joseph Smith (pengine picha ya Kaka Jo-seph au picha The First Vision [Gospel Art Book (2009), no. 87 or no. 90]). Waeleze wanafu-nzi kwamba Mzee Jeffrey R. Holland wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili alimtambua mtu huyo kuwa ni Joseph Smith (angalia Christ and the New Covenant: The Messianic Message of the Book of Mormon [1997], 287–88). Waambie wanafunzi wasome 3 Nefi 21:10–11 kimoyo-moyo, wakitafakari jinsi Nabii Joseph Smith anafaa katika maelezo ya aya hizi.• Ni jinsi gani Mungu ameonyesha kupitia Joseph Smith kwamba hekima yake ni kubwa

kuliko hila za shetani? • Kwa mujibu wa 3 Nefi 21:11, nini kitatokea kwa wale ambao hawaamini katika maneno

ya Kristo yaliyoletwa kupitia Joseph Smith? ("Watakatiliwa mbali” kutoka kwa baraka zinazokuja kupitia kwa maagano).

3 Nefi 21:12–22:17Mwokozi anasema juu ya uharibifu wa wasiotubu na urejesho wa watu wake ambao watatubu na kurudi kwakeFanya muhtasari 3 Nefi 21:12–21 kwa kueleza kwamba Mwokozi alitoa onyo kwa wale walio katika siku za mwisho ambao hawataamini katika yeye na kutubu. Alisema kwamba vifaa na mali zao, miji, ngome, na mazoea maovu yangeangamizwa. Pia alisema kwamba wangekatiliwa mbali kutoka kwa watu wake wa agano.Waalike wanafunzi wasome 3 Nefi 21:22, 25–28 kimoyomoyo, wakitafuta baraka na wajibu ambao utakuja kwa wale walio katika siku za mwisho watakaotubu na kuyasikiliza ma-neno ya Mwokozi.Uliza wanafunzi jinsi wanavyoweza kufupisha mafundisho katika 3 Nefi 21:12–22, 25–28. Mwalike mwanafunzi aandike majibu yao ubaoni. Kisha andika ufupisho wa majibu yote ubaoni kwa kutoa angalizo kwamba tunapotubu na kusikiliza maneno ya Mwokozi tunakusanywa kama sehemu ya watu Wake wa agano. (Unaweza kutaka kuandika ukweli huu ubaoni.)Chora hema ubaoni au katika bango (unaweza kufanya hili kabla ya darasa) Eleza kuwa Yesu Kristo alinukuu utabiri ambao alikuwa amemvuvia nabii Isaya kuandika karne nyingi awali. Katika utabiri huu, Isaya alifananisha Kanisa pamoja na maagano yake na baraka, na hema.

• Ni nini baadhi ya manufaa ya kuwa chini ya kivuli cha hema? (Majibu yanaweza kuju-muisha hema hutoa ulinzi kutokana na tufani na kivuli kutokana na jua.)

• Ni kwa njia gani Kanisa ni kama Hema?Mwambie mwanafunzi asome 3 Nefi 22:2 kwa sauti.• Hili “hema” linaweza kuhitaji nini ili kupanuliwa na kuimarishwa katika siku za mwi-

sho? Kwa sababu watu wengi watajiunga na Kanisa au kurudia maagano yao na Bwana) Unaweza kufanya nini ili kusaidia kupanua hema na kuimarisha vigingi? (Wahimize wanafunzi kutumia majibu yao kwa swali hili)

Eleza kuwa katika utabiri huu huu, Isaya alitumia istiari nyingine. Alihusisha nyumba ya Isreali kama mke ambaye mumewe ni Bwana. Mwambie mwanafunzi asome 3 Nefi 22:4–5 kwa sauti, na ulize darasa kutafuta maneno ya faraja kwa mke.

pazia (ukuta)

Kigingi

Kamba

Page 492: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

477

3 nefi 21–22

• Ni maneno gani ya faraja unaweza kuona katika 3 Nefi 22:4? (Majibu yanaweza kuju-muisha "wewe hutafedheheshwa na ... hutakumbuka aibu [ soni ] ya ujana wako.) Kwa nini inafariji kujuwa kuwa mume ndiye Mkombozi, Mtakatifu wa Isreali? (3 Nefi 22:5).

• Aya hizi zinafanana vipi kwa jibu la Mwokozi kwetu tunapofanya dhambi?Waambie wanfunzi wasome 3 Nefi 22:7–10 kimoyomoyo wakitafuta ahadi ambazo Mwo-kozi huzifanya kwa watu wake wa Agano wanaomrudia• Mwokozi anawaahidi nini wale wanaomrudia. • Ni zipi baadhi ya kweli tunazojifunza kuhusu Bwana katika aya hizi? (wanafunzi wana-

weza kushiriki majibu machache tofauti kwa swali hili. Hakikisha wanatambua ukweli ufuatao: Bwana huonyesha huruma na wema wa milele kwa watu wanaomrudia. Unaweza kutaka kuandika ukweli huu ubaoni. Unaweza pia kufikiria kupendekeza kwa-mba wanafunzi waandike katika maandiko yao matakatifu karibu na 3 Nefi 22:7–10.)

Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa zaidi 3 Nefi 22:4–10, fikiria kusoma kauli ifuatayo ya Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili:

"Hata ingawa kumekuwa na ukame na wakati mwingine kutokuwa waami-nifu, lakini mume (Kristo) humrudisha na kumkomboa mke wake (Israeli). Taswira ya Yehova kama bwana harusi na Israeli kama bibi harusi ni miongoni mwa mifano ya kawaida inayotumika katika maandiko ikitumiwa na Bwana na manabii wake kuelezea uhusiano kati ya Uungu na wana wa agano. "... Kristo amekuwa, wakati fulani, na hasira ya haki kwa uasi wa Israeli, bali

hiyo imekuwa kwa muda mfupi —kitambo kidogo. Huruma na wema wakati wote hurejea na kuwepo katika njia ya uhakika. Milima na vilima vinaweza kutoweka. Maji ya bahari kubwa yanaweza kukauka. Mambo yenye uwezekano mdogo katika ulimwengu yanaweza kutokea, lakini wema wa Bwana na amani havitaweza kuchukuliwa kutoka kwa watu wake wa agano. Yeye ameapa kwa kiapo cha mbinguni kwamba yeye hatawakasirikia milele (Christ and the New Covenant, 290).• Umeona ushahidi gani wa wema na huruma za Mwokozi maishani mwako? (Hakikisha

kuwa wanafunzi wanaelewa kwamba hawahitaji kushiriki chochote kilicho cha kibinafsi sana au cha siri.)

• Jinsi gani Kuwa na ufahamu wa huruma na wema wa Mwokozi kunashawishi kuathiri uaminifu wetu kwa maagano?

Eleza kwamba Mwokozi aliendelea kuwafundisha Wanefi juu ya baraka zinazowangoja wenye haki. Waambie wanafunzi wapekue 3 Nefi 22:13–17 kimoyomoyo, wakitafuta ba-raka moja iliyoahidiwa ambayo ina maana sana kwao. Toa angalizo kwamba tunaposoma kuhusu baraka hizi zilizoahidiwa, tunaona kwamba watu wa Bwana watakuwa imara katika haki na watashinda uovu.Hitimisha kwa kutoa ushuhuda wako wa kweli ambazo zimejadiliwa katika somo hili. Waambie wanafunzi waandike sentensi tatu au nne katika madaftari au majarida yao ya mafundisho ya maandiko kuhusu jambo moja wanaloweza kufanya leo ili kustahili baraka ambazo Bwana anataka kuwapa.

Tangazo na Habari za Usuli3 Nefi 21:22–25. Yerusalemu Mpya

Daniel H. Ludlow alifafanua ni nani atajenga mji wa Yerusalemu Mpya:

"Yerusalemu Mpya ya siku za mwisho itajengwa katika bara la Marekani na (1) salio la Yakobo, (2) mataifa

ambayo yataingia katika agano na kuhesabiwa mio-ngoni mwa salio la Yakobo, na (3) wengi wa nyumba ya Israeli kama watakuja. (3 Nefi 21:22–25. Soma pia 3 Nefi 20:22; Etheri 13:1–12.) (A Companion to Your Study of the Book of Mormon [1976], 281).

Page 493: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

478

UtanguliziSomo hili linaweza kusaidia wanafunzi kuelewa upole na hu-ruma ambao Mwokozi anahisi kwa watu Wake. Zaidi ya hayo, wanafunzi wanapotathmini ushauri wa Bwana wa kuomba, wa-naweza kufikiria njia ya kufanya maombi yao binafsi na familia kuwa ya maana zaidi.

Mapendekezo ya Kufundisha

3 Nefi 17Mwokozi aponya wagonjwa, anaomba, kwa Baba kwa ajili ya watu, na kuwabariki watoto waoWaambie wanafunzi kufikiri juu ya mtu anayejali zaidi ambaye wanamjua. Kisha uliza: ulimfikiria nani? Ni kwa jinsi gani mtu huyu huonyesha upendo kwa wengine na kwako?.

Onyesha picha ya Yesu akiwapoya Wanefi (Gospel Art Book [2009], no. 83) na Yesu anawabariki watoto Wanefi (Gospel Art Book, no. 84). Kisha uliza: Mmejifunza nini kuhusu upendo wa Mwokozi kwa watu wakati wa mafunzo yenu ya Kitabu cha Mormoni wiki hii iliyopita?

Andika ukweli ufuatao kwenye ubao: Mwokozi anahisi hu-ruma mwingi kwa ajili yetu. Chini ya kauli hii, andika marejeo yafuatayo ya maandiko matakatifu: 3 Nefi 17:7, 9, 11, 15–17, 21, 24. Waambie wanafunzi kupitia aya hizi na kuchagua moja ambayo hasa inaeleza ukweli ulioandikwa ubaoni. Baada ya muda wa kutosha, unaweza kuuliza maswali yafuatayo:

• Ni kwa njia gani mstari uliochagua huonyesha kwamba Mwo-kozi anahisi huruma mwingi kwa ajili yetu?

• Unajifunza nini kuhusu Mwokozi kutokana na ukweli kwamba Yeye aliwahudumiwa watu moja moja? 3 Nefi 17:21).

• Kwa jinsi gani kujua kuhusu huruma ya Mwokozi kunakusai-dia kutumia imani kuu kwake na kuhisi upendo mkubwa kwa ajili yake?

Somo la Mafunzo ya Nyumbani 3 Nefi 17–22 (Kitengo cha 26)

Vifaa vya Matayarisho kwa Mwalimu wa Mafunzo ya nyumbaniMuhtasari wa Masomo ya kila siku ya Mafunzo ya nyumbani. Muhtasari ufuatao wa mafundisho na kanuni ambazo wanafunzi walijifunza waliposoma 3 Nefi 17–22 (kitengo 26) haikusidiwi kufundishwa kama sehemu ya somo lako. Somo unalofundisha huzingatia machache tu ya mafundisho haya na kanuni. Fuata uvuvio wa Roho Mtakatifu unapofikiria mahitaji ya wanafunzi wako.

Siku ya 1 (3 Nefi 17)Wanafunzi waliposoma maneno ya Yesu Kristo kwa umati wa wanefi, walijifunza kwamba kwa kutafakari na kuomba kwa Baba, tunaweza kupokea uelewa mkubwa wa mafundisho ya Mwokozi. Mwokozi aliitikia hamu ya Wanefi kwamba Yeye akae nao kwa muda mrefu kidogo kwa kuponya wagonjwa wao na kubariki watoto wao. Wanafunzi wanaposoma juu ya matukio hayo, walijifunza kwamba Yesu Kristo anahisi huruma mwingi kwa ajili yetu.

Siku 2 (3 Nefi 18)Mwokozi alisimamia sakramenti kwenye umati. Wanafunzi walijifunza kwamba kama tunaposhiriki sakramenti, tunashu-hudia kwa Baba kwamba sisi tu tayari kufanya yoteambayo Yeye ameamrisha na kwamba daima tutamkumbuka Yesu Kristo. Wao pia walijifunza kwamba tunaposhiriki sakramenti na daima kumkumbuka Mwokozi, tutakuwa na Roho wake awe pamoja nasi. Mafundisho ya Mwokozi kuhusu maombi yaliwasaidia wanafunzi kuelewa kwamba kama tukiwa ma-cho na kuomba daima kwa Baba, tunaweza kuzuia majaribu ya Shetani. Wao pia walijifunza kwamba tunapo tunapowa-hudumia wengine, tunaweza kuwasaidia kuja kwa Kristo.

Siku 3 (3 Nefi 19)Baada ya Mwokozi kuondoka mwishoni mwa siku yake ya kwanza na Wanefi, wanafunzi waliwafundisha watu. Wao waliomba kwa ajili na kupokea Roho Mtakatifu. Wanafunzi walijifunza kwamba hamu yetu ya haki na sala zinaweza ku-tuwezesha kustahili kujazwa Roho Mtakatifu. Mwokozi alito-kea tena, na Yeye alimshukuru Baba kwa ajili ya kuwatakasa wanafunzi wake. Wanafunzi walijifunza kwamba tunapotu-mia imani katika Yesu Kristo, tunaweza kutakaswa na kuwa wamoja na Yesu Kristo, kama Yeye alivyo mmoja na Baba.

Siku ya 4 (3 Nefi 20–22)Yesu kristo tena alisimamia sakramenti. Wanafunzi waliji-funza kwamba kama tukishiriki sakramenti kwa kustahili, tunaweza kujazwa na Roho Mtakatifu. Mwokozi kisha akawafundisha Wanefi kwamba Baba atatimiza ahadi yake ya kukusanya nyumba ya Israeli katika siku za mwisho. Wa-nafunzi pia walijifunza kwamba kama mbegu ya Ibrahimu, tuna wajibu wa agano kubariki watu wote wa dunia kwa kushiriki injili nao.

Page 494: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

479

SoMo la MafUnzo ya nyUMbani

3 Nefi 18–19Yesu alifundisha watu kuomba kwa Baba daima na kukutana pamoja mara kwa mara Wagawanye wanafunzi katika majozi, na litake kila kundi kute-ngeneza orodha ya majaribu matano yenye changamoto kubwa ambayo wanaamini yanawakumba vijana leo. Watakapomaliza, karibisha kila jozi kusoma 3 Nefi 18:15–20 na kutafuta ushauri ambao Mwokozi alitoa kwa ajili ya kushinda majaribu. Waulize wanafunzi wachache kushiriki kanuni wanayopata katika mistari hii. Kanuni moja wanayoweza kutambua ni kwamba kama tu-takuwa waangalifu na kusali daima kwa Baba, tunaweza kuzuia majaribu ya Shetani.

Waulize wanafunzi maswali yafuatayo:

• Unafikiri kijana anapaswa kuwa mwangalifu kwa kitu kipi ili kuhimili moja ya majaribu katika orodha yako?

• Je, kujana anaweza kuomba nini ambacho kinaweza kum-saidia kuhimili moja ya majaribu katika orodha yako? Ni vipi kuomba kwa Baba wa Mbinguni hukusaidia kubaki imara?

Ili kuwasaidia wanafunzi kuimarisha ushuhuda wao wa maombi ya familia, mkaribishe mwanafunzi asome 3 Nefi 18:21 kwa sauti. Kisha uliza: Je, ni baraka zipi wewe umepokea kutokana na kuomba na familia yako?

Mwambie mwanafunzi asome taarifa ifuatayo kutoka kwa Rais James E. Faust wa Urais wa Kwanza ambaye alizungumza juu ya nguvu ya maombi ya familia :

"Maombi ya familia ni ushawishi wenye nguvu wa unaohimili. Wakati wa siku za giza za Vita Vikuu ya Dunia II bomu la pauni 500 lilianguka nje ya nyumba ndogo ya Kaka Patey, baba kijana katika Liverpool, Uingereza, lakini bomu halikulipuka. Mke wake alikuwa amefariki, hivyo alikuwa akiwalea watoto wake watano peke yake. Aliwakusanya wote wakati huu wa wasiwasi sana kwa ajili ya sala ya familia. Wao wote waliomba kwa bidii na walipokwisha kuomba, watoto alisema: Baba, tutakuwa salama. Tutakuwa salama katika nyumba yetu usiku huu.

"Na kwa hiyo walikwenda kulala, fikiria, na bomu la kutisha likiwa nje ya mlango limezama nusu ardhini. . . .

"Asubuhi iliyofuata kitongoji kizima kiliondolewa kwa masaa arobaini na nane na bomu hatimaye liliondolewa.. . . .

"Wakiwa njiani kurudi Kaka Patey alimuliza msimamizi wa Kikosi cha ARP: Naam, ni nini mligundua?

"Bw. Patey, tulipata bomu nje ya mlango wako na kukuta ikiwa tayari kulipuka wakati wowote. Hapakuwa na kasoro yoyote katika bomu hilo. Sisi tumeshangazwa kwa nini halikulipuka Mambo ya miujiza kutokea wakati familia ikiomba pamoja" (The Lifeline of Prayer, Ensign, May 2002, 61).

Waulize wanafunzi maswali yafuatayo, kuwa makini kwa wana-funzi ambao familia zao huenda hawaombi pamoja :

• Unaweza kufanya nini ili kusaidia familia yako kuwa na utha-biti zaidi na maombi ya maana ya sala ya familia?

• Jinsi gani unaweza kupanga ili kufanya maombi ya familia yawe ya mihimu katika familia yako ya siku za usoni?

Eleza kwamba wakati Yesu aliporudi kwa siku ya pili kuwafundi-sha Wanefi, kama ilivyoandikwa katika 3 Nefi 19, Yeye tena ali-wasihi wanafunzi Wanefi kuomba. Mwalike mwanafunzi asome 3 Nefi 19:9, 13 kwa sauti, na wafanye wanafunzi kutambua kile wanafunzi waliomba. Uliza: Ni kanuni gani tunayoweza kujifu-nza kutokana na uzoefu wa wafuasi wa Kinefi? (Ifuatayo ni njia moja ya wanafunzi wanaweza kueleza kanuni hii: Hamu zetu za haki na sala zinaweza kutuwezesha kustahili kujazwa Roho Mtakatifu.)

Kisha uliza wanafunzi: Ni lini wewe umetaka kwa dhati na kuo-mba kwa ajili ya uenza wa Roho Mtakatifu? Ulibarikiwa vipi kwa kufanya hivyo?

3 Nefi 20–22Katika siku za mwisho, Mungu ataanza kukusanya nyumba ya IsraeliEleza kuwa baada ya kuwafundisha Wanefi kuhusu maombi, Mwokozi alianza kuwafundisha kuhusu mkusanyiko wa nyumba ya Israeli katika siku za mwisho. Alika mwanafunzi asome 3 Nefi 21:9. Uliza darasa kufuata pamoja, wakitafuta maneno ambayo yanayoelezea kazi ya Bwana. Kisha uulize:

• Unafikiri "kazi kubwa na ya ajabu" inahusu nini? (Urejesho wa injili ya Yesu Kristo, ambao unajumuisha kuja kwa Kitabu cha Mormoni.)

• Kwa maoni yako, ni nini kilicho kikubwa na ya kushangaza kuhusu urejesho wa injili ya Yesu Kristo?

Waulize wanafunzi wapitie 3 Nefi 21:10–11 na fikiria kuhusu ni nani Bwana alikuwa anamzungumzia kama mtumishi wangu. Uliza: Ni maneno gani au vishazi vinavyokusaidia kujua kwamba Bwana anamwelezea Nabii Joseph Smith? Kisha onyesha picha ya Joseph Smith katika Jela ya Liberty (Gospel Art Book, no. 97).

Uliza: Ni vipi Mungu ameonyesha kupitia kwa Joseph Smith kwamba hekima yake ni kuu kuliko hila za shetani?

Kwa kuhitimisha, waambie wanafunzi kushirikiana ushuhuda wao wa Nabii Joseph Smith na urejesho wa injili. Shirikisha ushu-huda wako wa mambo haya pamoja na wanafunzi wako.

Kitengo kifuatacho (3 Nefi 23–30)Waalike wanafunzi kufikiria kwamba Mwokozi aliwaambia angewakubalia chochote walichotamani. Eleza kwamba wana-pojifunza 3 Nefi 23–30 katika juma lijayo, watajifunza kuhusu watu kumi na wawili ambao walikuwa na uzoefu huu na nini walichoomba.

Page 495: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

480

UtanguliziBaada ya kunukuu maneno ya Isaya (angalia 3 Nefi 22), Yesu Kristo aliwaamuru Wanefi kupekua maneno ya nabii huyu. Alisema kwamba maneno ya Isaya ni baraka kwa sababu Isaya alinena na kugusa mambo yote ya-nayohusu watu wangu ambao ni wa nyumba ya Israeli

(3 Nefi 23:2). Pia alisema kwamba maneno yote ya Isaya yametimizwa au yatatimizwa. Mwokozi kisha akawa-amuru Wanefi kupekua maneno ya manabii wote na kuwaelekeza kuongeza nyenzo kwa kumbukumbu zao.

SOMO LA 131

3 nefi 23

Mapendekezo ya Kufundisha

3 Nefi 23:1–5Yesu Kristo anawaamuru watu kupekua maneno ya manabiiAndika kishazi kifuatacho kwenye ubao: Baraka kutoka kwa mafunzo ya maandiko yangu. Waulize wanafunzi kutafakari uzoefu wao katika kujifunza Kitabu cha Mormoni nyumbani na katika seminari mwaka huu. Waalike waje ubaoni na kuandika neno au vishazi vifupi ambavyo vinavyoeleza baraka iliyokuja katika maisha yao kama matokeo ya kujifunza maandiko. Unaweza kutaka kuuliza wanafunzi wachache kuelezea kwa undani zaidi nini walichoandika. Kisha onesha baraka zilizoandikwa ubaoni.• Kwa nini unafikiri tunabarikiwa kwa njia hizi tunaposoma maandiko matakatifu? Waulize wanafunzi wakumbuke kutoka somo lililopita ni maneno ya nani Yesu Kristo alinukuu alipowafundisha Wanefi. (Maneno ya Isaya Mwalike mwanafunzi asome 3 Nefi 23:1–3 kwa sauti. Uliza darasa kufuata pamoja, wakitafuta kile Mwokozi alisema tuna-paswa kufanya na maneno ya Isaya. Unaweza kutaka kupendekeza kwamba wanafunzi waweke alama maneno na vishazi ambavyo vina umuhimu zaidi kwao katika mistari hii. Waalike kushiriki kile wanachogundua.• Kwa nini Bwana anataka watu kupekua maneno ya Isaya? (Ona 3 Nefi 23:2–3.)• Kwa nini ni baraka kujua kwamba maneno yote ya Isaya yatatimizwa? Mwalike mwanafunzi asome 3 Nefi 23:4–5 kwa sauti. Toa angalizo kwamba baada ya Mwokozi kusema tupekue maneno ya Isaya, Alisema na tupekue manabii. Andika ukweli ufuatao kwenye ubao: Mwokozi anatuamrisha kukagua kwa bidii maneno ya Isaya na manabii wengine.• Kwa mujibu wa 3 Nefi 23:5, ni sharti tufanye nini ili tupate kuokoka? Ni kwa jinsi gani

maneno ya manabii hutusaidia kufuata amri hizi? • Ni katika njia zipi kupekua maneno ya manabii kwa bidii ni tofauti na kusoma tu ma-

neno ya manabii? Kwa nini unafikiri ni muhimu kupekua maneno ya Isaya na manabii wengine kwa bidii?

• Nini mbinu mzuri zaidi za kujifunza maandiko zinazokusaidia kufanya upekuzi wa ma-neno ya Isaya na manabii wengine sehemu ya maana ya maisha yako?

Mwalike mwanafunzi asome maelezo ya yafuatayo na Mzee Merrill J. Bateman wa Wale Sabini:Kuna baadhi ya baraka zinazopatikana wakati mtu anapopekua maandiko. Mtu anapo-soma maneno ya Bwana na kuyatii, yeye husongea karibu na Mwokozi na anapata hamu kubwa ya kuishi maisha ya haki. Nguvu ya kupinga majaribu huongezeka, na udhaifu wa kiroho unashindwa. Majeraha ya kiroho yanaponywa (Coming unto Christ by Searching the Scriptures, Ensign, Nov. 1992, 28).• Pamoja na maandiko, ni wapi ambapo tunaweza kupata maneno ya manabii? Waambie wanafunzi wajibu katika madaftari au majarida yao ya mafundisho ya maandiko swali lifuatalo:• Ni mabadiliko gani unayoweza kufanya ili kujifunza maneno ya manabii kwa bidii zaidi?

Page 496: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

481

3 nefi 23

Waalike wanafunzi wachache kushuhudia baraka ambazo huja kutokana na kupekua maneno ya manabii.

3 Nefi 23:6–14Mwokozi anawaelekeza wanafunzi wake kuongeza tukio muhimu kwenye ku-mbukumbu zao za kimaandikoWaite wanafunzi wachache wataje simulizi wanazopenda zaidi katika Kitabu cha Mormoni. Orodhesha majibu yao ubaoni. Kisha futa mojawapo ya majibu. Waulize wanafunzi kufiki-ria kwamba Mormoni au Nefi au mweka kumbukumbu mwingine angepuuza kujumuisha simulizi ile. • Ni masomo gani muhimu yangekosekana kutoka Kitabu cha Mormoni kama simulizi hii

isingekuwa imejumuishwa?Eleza kwamba wakati Yesu alipofundisha Wanefi, Alitoa angalizo kwamba watunza kumbu-kumbu wao walikuwa wamepuuza kujumuisha tukio muhimu ambalo lilikuja katika kutimiza utabiri. Waambie wanafunzi kadhaa kwa zamu kusoma kwa sauti kutoka 3 Nefi 23:6–13. Uliza darasa kufuata pamoja, wakitafuta nini Wanefi walishindwa kuweka kumbukumbu. • Wanefi tayari walikuwa na kumbukumbu ya unabii wa Samweli (Ona Helamani 14:25).

Kwa nini unafikiri ingekuwa ni muhimu kwao kuwa na kumbukumbu ya utimilifu wake? Toa angalizo kwamba ingawa hatukuamriwa kuweka kumbukumbu ya maandiko kwa ajili ya kanisa tumeshauriwa kuweka majarida ya binafsi..• Jinsi gani Ushauri wa mwokozi katika 3 Nefi 23:6–13 unatumika kwenye juhudi zetu za

kuweka majarida ya kibinafsi?Ili kusaidia wanafunzi kuona njia moja wanayoweza kuweka jarida, alika mwanafunzi asome kwa sauti uzoefu ufatao wa Rais Henry B. Eyring wa Urais wa Kwanza

"Nilikuja nyumbani nikiwa nimechelewa kutoka kwenye kazi niliyopangiwa na Kanisa. Ilikuwa baada ya giza Baba mkwe wangu aliyeishi karibu nasi alinishangaza nilipokuwa natembea kuelekea mlango wa mbele wa nyumba yangu. Yeye alikuwa amebeba mzigo wa mabomba ya juu ya bega lake, akitembea haraka sana na akiwa amevaa nguo za zake za kufanyia kazi. Nilijua kwamba alikuwa akijenga mfumo wa kusukuma maji kutoka kwenye

kijito chini yetu hadi juu kwenye shamba letu."Yeye alitabasamu, alizungumza kwa upole, na kisha akapita kwa haraka nyuma ya-ngu kwenye giza kuendelea na kazi yake. Mimi nilipiga hatua chache kuelekea kwenye nyumba, nikifikiri ni nini alikuwa akifanya kwa ajili yetu, na mara nilipofika tu mlangoni, nilisikia katika akili yangu— si kwa sauti yangu mwenyewe, —maneno haya: Mimi sikupi uzoefu huu kwa ajili yako mwenyewe. Uandike'"Niliingia ndani. Sikwenda kitandani. Ingawa nilikuwa nimechoka, nilitoa karatasi kadha na nilianza kuandika. Na nilipofanya hivyo, nilielewa ujumbe niliyokuwa nimeusikia katika akili yangu. Mimi nilipaswa kuweka kumbukumbu kwa ajili ya watoto wangu kusoma, siku moja katika siku zijazo, jinsi gani nilivyoona mkono wa Mungu ukibariki familia yetu. Haikumbidi babu kufanya kile alichokuwa akifanya kwa ajili yetu. Angeacha mtu mwi-ngine afanye au hangefanya kamwe. Lakini alikuwa akituhudumia, familia yake kama vile wafuasi wa agano la Yesu Kristo wanafanya siku zote. Nilijua kwamba hiyo ilikuwa kweli. Na hivyo mimi niliandika, ili kwamba watoto wangu wangeweza kuwa na kumbukumbu siku moja wakati wangekuwa na haja nayo. Niliandika mistari michache kila siku kwa miaka mingi. Mimi kamwe sikukosa siku bila kujali jinsi nilivyokuwa nimechoka au mapema jinsi gani ningeanza siku iliyofuata. Kabla ya kuandika, ningetafakari swali hili: Je, mimi nimeuona mkono wa Mungu ukitufikia ili ku-tugusa au watoto wetu au familia yetu leo?'" (O Remember, Remember, Ensign or Liahona, Nov. 2007, 66–67).• Kwa nini unafikiri ni muhimu kwetu kuandika kuhusu uzoefu ambao ulituimarisha kiroho?• Tunawezaje kufaidika kwa kufuata mfano wa Rais Eyring? Ni vipi kumbukumbu yetu

inaweza kuwasaidia wengine?Eleza kwamba Rais Eyring alizungumza juu ya baraka alizopokea kwa sababu aliweka kumbukumbu ya kila siku ya baraka ya Mungu, kwa familia yake. Mwambie mwanafunzi

Page 497: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

482

SoMo la 131

asome taarifa hii kwa sauti. (Unaweza kuwa umeshiriki sehemu ya kauli hii katika somo la 117. Wanafunzi wanaweza kunufaika kwa kusikia tena.)"Nilipoendelea kuwa hivyo, kitu kilianza kutokea. Na nilivyotupa mawazo yangu juu ya siku, ningeona ushahidi wa kile Mungu alichokifanya kwa mmoja wetu ambacho sikukitambua katika wakati wa kazi nyingi za siku. Hayo yalifanyika, na yalifanyika mara nyingi, niligundua kwamba kujaribu kukumbuka kulikuwa kumemruhusu Mungu anio-nyeshe kile alichokifanya."Shukrani zaidi zikaanza kukua katika moyo. Ushuhuda ulikua. Nikawa na uhakika zaidi kuwa Baba yetu wa Mbinguni husikia na kujibu maombi. Nilihisi zaidi shukrani kwa ku-lainishwa na kusafishwa ambako kunaokuja kwa sababu ya Upatanisho wa Mwokozi Yesu Kristo. Na mimi nilikuwa katika kujiamini zaidi kwamba Roho Mtakatifu anaweza kuleta mambo yote kwenye kumbukumbu zetu —hata mambo ambayo hatukuona au kuwa na makini na wakati yalipotokea" (O Remember, Remember, 67).• Ni kanuni gani tunayoweza kujifunza kutokana na simulizi katika 3 Nefi 23 na kutokana

na uzoefu wa Rais Eyring? (Wanafunzi wanaweza kujibu swali hili katika njia kadhaa tofauti. Majibu yao lazima kuonyesha ukweli ufuatao: Wakati sisi tunaweka kumbu-kumbu za uzoefu wa kiroho, tutabarikiwa kibinafsi na katika familia zetu.)

Ili kuwasaidia, unaweza kutaka kumkaribisha mwanafunzi asome kwa sauti kauli ifuatayo ya Mzee John H. Groberg wa Wale Sabini:"Baadhi ya watu wanasema, sina kitu cha kuweka kumbukumbu. Hakuna kitu cha kiroho kinachotokea kwangu. Nasema, anza kuweka kumbukumbu, na mambo ya kiroho yata-tokea. Yapo wakati wote, lakini sisi huhisi zaidi tunapoindika (“Writing Your Personal and Family History,” Ensign, May 1980, 48).Waambie wanafunzi wajiulize wenyewe kama wamepuuza kuandika kuhusu uzoefu ambao umewaimarisha kiroho. Wahimize waandike kuhusu uzoefu huu na kuendelea ku-weka kumbukumbu uzoefu mwingine katika maisha yao. Unaweza kupendekeza kwamba wafuate mfano wa Rais Eyring, kuandika kitu fulani kila siku.

Rejeo la Umahiri wa MaandikoKujifunza jinsi ya kutatua matatizo kwa kutumia maandiko kunaweza kusaidia wanafunzi katika maisha yao. Mpe kila mwanafunzi kipande kidogo cha karatasi. waalike kuandika kuhusu swali walilo nalo au changamoto zinazowakabili. Eleza kwamba utakusanya maka-ratasi na kusoma baadhi kwa darasa. Waelekeze wanafunzi wasiweke majina yao kwenye karatasi, na wakumbushe wasijumuishe maelezo ya kina ambayo ni ya binafsi au yasiyofaa kujadiliwa darasani. (Baada ya kukusanya makaratasi, unaweza kutaka kupitia kwa ufupi maoni ili kuhakikisha kuwa ni sahihi na sio ya kibinafsi sana.) Soma swali au changamoto darasani na ona kama wanafunzi wanaweza kutumia vifungu vya umahiri wa maandiko kusaidia kushughulikia swali au changamoto hii.Eeleza kwamba Mwokozi alituamuru kuwafundisha wengine kile alichotufundisha. (ona 3 Nefi 23:14). Ili kusaidia kuandaa wanafunzi kushika amri hii, wahimize kutumia stadi za kufundishia, kama vile kueleza mafundisho au kanuni, kubadilishana uzoefu, na kushuhu-dia wanapotumia vifungu vya umahiri wa maandiko kutatua matatizo. Unaweza kuataka kuhifadhi maswali mengine au changamoto ambazo wanafunzi walitoa na uzijadili kwa njia kama hiyo kwa siku ambazo una muda wa ziada.Angalizo: Urefu wa somo hili unaweza kuruhusu muda kwa ajili ya marejeo ya umahiri wa maandiko. Unaweza kufanya shughuli hii mwanzo wa darasa, kama mapumziko kati ya sehemu za somo, au mwisho wa darasa. Fanya hii shughuli kuwa fupi ili uruhusu muda kwa ajili ya somo. Kwa shughuli nyingine za marejeo, angalia kiambatanisho mwi-shoni mwa kitabu hiki.

Fuatilia malengo na changamotoBaada ya kuwapa changamoto wanafunzi kufanya kitu fulani, kama vile kuandika katika jarida, fikiria njia za kufuatilia, kuwaku-mbusha juu ya ahadi walizotoa. Wape fursa ya kubadilishana uzoefu wao wanapotumia ukweli wanaojifunza katika darasa. Kupitia kwa kushirikiana uzoefu wao, wanaweza kuji-hamasisha kuishi injili. Unaweza kufikiria kutoa fursa kama hizi mwa-nzoni mwa somo. Si kila mwanafunzi anayehitaji kushiriki.

Page 498: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

483

UtanguliziYesu Kristo alitimiza amri kutoka kwa Baba wa Mbi-nguni kushiriki na Wanefi baadhi ya utabiri kutoka kwa nabii Malaki (ona 3 Nefi 26:2). Huu utabiri ulifundisha kwamba washiriki wa nyumba ya Israeli walihitajika kutubu na kurudi kwa Bwana kama maandalizi kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Mwokozi. Yesu Kristo pia alifafanua

kwa Wanefi mambo yote, hata kutoka mwanzo hadi wakati atakapokuja katika utukufu wake (3 Nefi 26:3). Mormoni alifundisha kwamba wale ambao wanaamini Kitabu cha Mormoni hata watakuwa na mambo zaidi yatayofanywa wazi kwao (ona 3 Nefi 26:9).

SOMO LA 132

3 nefi 24–26

Mapendekezo ya Kufundisha

3 Nefi 24:1–6Yesu Kristo ananukuu Utabiri wa Malaki kuhusu Ujio wa PiliAnza darasa kwa kushikilia kijiti cha kiberiti na mche wa sabuni (au chora ubaoni picha ya moto na mche wa sabuni). Waulize wanafunzi nini moto na sabuni vina wiana. (Sabuni na moto zinaweza kutumika kama nguvu za kusafisha au kutakasa.)Eleza kuwa Yesu Kristo alitimiza amri kutoka kwa Baba (ona 3 Nefi 26:2) kuwapa Wanefi baadhi ya tabiri za Malaki, nabii wa Agano la Kale ambaye aliishi katika Nchi Takatifu ka-ribu miaka 170 baada ya Lehi na familia yake kuondoka Yerusalemu. Waambie wanafunzi wasome 3 Nefi 24:1–3 kimoyomoyo, wakitafuta mtu ambaye Malaki amemfananisha na moto wa mtu usafishaye na sabuni ya dobi.• Ni nani ambaye amefananishwa na moto wa mtu asafishaye na sabuni ya dobi?

(Yesu Kristo.)• Tukio gani linaelezwa katika aya hizi? (Siku ya kuja kwake. Kwa maneno mengine, Ujio

wa Pili wa Yesu Kristo. Ili kuwasaidia wanafunzi kujibu swali hili, unaweza kupendekeza kwamba wasome upesi mada ya sura au tanbihi.)

• Je mfananisho wa Yesu Kristo wa moto na sabuni unapendekeza kuwa utafanyika katika Ujio Wake wa pili? (Wanafunzi wanaweza kutumia maneno tofauti, lakini wanapaswa kutambua ukweli ufuatao: Wakati wa Ujio wake wa Pili, Yesu Kristo atatakasa du-nia. Unaweza kutaka kuwaambia wanafunzi kuandika ukweli huu katika maandiko yao matakatifu karibu na Nephi 24:2–3

Eleza kwamba msafishaji hutumia moto kupasha joto chuma kama fedha au dhahabu mpaka ifikie hali ya uoevu. Mchakato wa kupasha moto huruhusu takataka, au uchafu, ku-panda juu ya uso wa chuma iliyo maji maji, ambapo asafishaye anaweza kuuondoa, hivyo kusafisha chuma kutokana na uchafu wake. Dobi ni mtu anayesafisha au kufanya vitambaa kuwa vyeupe vitambaa kwa kutumia sabuni. Unaweza pia kuwa na haja ya kueleza kuwa "wana wa Lawi" walikuwa wamiliki wa ukuhani katika Israeli ya kale. Hivi leo kishazi kinaweza kuhusu wamiliki wa ukuhani wa siku za kisasa (ona M&M 84:33–34).Alika mwanafunzi asome 3 Nefi 24:5–6 kwa sauti. Uliza darasa kufuata pamoja na kuta-mbua nani wataangamizwa, au kuharibiwa, wakati wa Ujio wa Pili wa Mwokozi na ambao hawataangamizwa. (Unaweza kueleza kwamba kishazi wana wa Yakobo linahusu watu wa agano wa Mungu katika nyumba ya Israeli. • Kulingana na 3 Nefi 24:5, Yesu Kristo atafanya nini katika Ujio Wake wa Pili? (Ingawa

wanafunzi wanaweza kutumia maneno tofauti, wanapaswa kutambua ukweli huu: Yesu Kristo atawaangamiza waovu katika Ujio wake wa Pili.)

Amua Kitu cha Kufundisha Somo hili lina nyenzo zaidi kuliko utaka-vyokuwa na muda wa kufundisha. Kwa mao-mbi fikiria mafundisho, kanuni, na mawazo ya kufundishia yatakayo kuwa na manufaa zaidi kwa ajili ya wanafunzi katika darasa lako.

Page 499: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

484

SoMo la 132

3 Nefi 24:7–18Yesu Kristo ananukuu mafundisho ya Malaki kuhusu jinsi nyumba ya Isreali ina-vyoweza kurudi kwa BwanaWaambie wanafunzi kufikiria kuwa wana rafiki wa karibu au mwanafamilia ambaye ana-pambana na kuhisi upendo na ushawishi wa Bwana na kuweka ushuhuda wa injili. • Ungefanya nini ili kujaribu na kumsaidia mtu huyu?Waambie wanafunzi wasome 3 Nefi 24:7 kimoyomoyo, na waambie watambue ushauri wa Bwana kwa wale walioanza kusonga mbali kutoka kwake na kuto kuweka maagano yao naye. • Unafikiri inamaanisha nini kuwa watu ‘wamekwenda zao ‘) kutoka kwenye ibada za

Bwana? (Hawakuwa wanaweka maagano na ibada za injili.)• Ni ahadi gani Bwana alitoa kwa wale ambao hawakuwa wanaweka maagano yao? (“Ni-

rudieni nami nitawarudia) • Unafikiri inamaanisha nini “kurudi” kwa Bwana? Unafikiri inamaanisha nini kwamba

Bwana “atawarudia” wale wanaomrudia?Andika kanuni ifuatayo ubaoni: kama tukimrudia bwana, Naye ataturudia.• Kanuni hii inakufundisha nini wewe kuhusu Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Kwanye ubao andika Rudini kwa Bwana. Waambie wanafunzi wasome 3 Nefi 24:8–12 kimoyomoyo wakitafuta, njia moja ambayo Bwana alionyesha kuwa watu wanaweza kum-rudia. Wanafunzi wanapojibu, andika lipa zaka na matoleo chini ya Rudini kwa Bwana.• Ni kwa vipi hiari ya kulipa zaka ni ishara kuwa mtu fulani ameweka upendo wake na

mapenzi kwa Bwana?Alika mwanafunzi asome taarifa ifuatayo ya Rais Gordon B. Hinckley:“Sisi tunaweza kulipa zaka zetu. Hili hasa si jambo la fedha kama lilivyo jambo la imani. ” (“Let Us Move This Work Forward,” Ensign, Nov. 1985, 85).• Ni jinsi gani hiari yetu ya kulipa zaka na matoleo ni ishara ya imani yetu kwa Bwana?Wape wanafunzi muda wa kurejea 3 Nefi 24:10–12 kimoyomoyo. Waambie watambue ahadi za Bwana kwa wale wanaolipa zaka kamili na kwa uaminfu• Ni kwa njia gani umebarikiwa kutokana na kulipa kwako zaka? Ni kwa vipi mifano hii

ya “madirisha ya mbingu” yanafunguliwa kwako?Fupisha 3 Nefi 24:13–18 kwa kueleza kuwa katika aya hizi Bwana alitoa angalizo kwa-mba wengine katika Israeli ya kale walikuwa wameshuku haja ya kuweka ibada za injili. Walilalamika kwamba wenye kiburi na waovu walionekana kufanikiwa licha ya uovu wao. Katika 3 Nefi 24:16, Bwana alijibu kwamba “kitabu cha kumbukumbu” kitawe-kwa ambamo majina ya walio waaminifu yatawekwa kumbukumbu (ona M&M 85:7–9; 128:6–7; Musa 6:5–8). Kisha Bwana Akaonyesha kwamba atakaporudi tena atawahifadhi walio waaminifu na kuwaweka kwake kama hazina au “ urembo[vito vyake] ”• Ni jinsi gani ni baraka kujua kwamba Bwana atawahifadhi walio waaminifu na kuwafa-

nya kuwa hazina yake.• Katika 3 Nefi 24:16, ni vishazi vipi vinavyoeleza wale ambao Bwana atawaweka kama

hazina Yake? (“Wale ambao walimcha Mungu” na wale “waliofikiria jina lake” Andika kumcha Bwana na na kulifikiria jina la Bwana chini ya Kumrudia Bwana. (Unaweza kutaka kueleza kwamba katika muktadha huu neno kumcha linamaanisha heshima au ibada.) Waambie wanafunzi wajibu swali lifuatalo katika daftari au majarida ya mafundisho ya maandiko matakatifu: • Fikiria jinsi unavyofanya katika maeneo ya kulipa zaka na matoleo na kimfikiria Kristo kila

mara. Ni kwa njia gani unaweza “kurudi” Kwake au kujiboresha katika maeneo haya?

3 Nefi 25Yesu ananukuu utabiri wa Malaki kwamba Eliya atarudi kabla ya Ujio wa piliAlika mwanafunzi asome 3 Nefi 25:1–3 kwa sauti. Litake darasa kufuatilia wakitafuta sababu kwa nini Ujio wa Pili utakuwa baraka kwa wake walio waaminifu kwa Yesu Kristo. Waambie wanafunzi watoe taarifa ya kile wamepata. Unaweza kuhitaji kueleza kuwa

Page 500: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

485

3 nefi 24 –26

3 Nefi 25:1, neno mzizi inaweza kuwa linahusu mababu na neno tawi kwa uzao. Hivyo, katika maisha yajayo, waovu hawatafurahia baraka za kufungishwa kwa mababu zao na uzao. Katika 3 Nefi 25:2, kishazi “ndama zizini ” linahusu ndama walio salama, walioli-shwa vyema, na kutunzwa. Bwana anaahidi kwamba vivyo hivyo atawalinda na kutunza wale ambao “wanaomcha jina lake.”Eleza kuwa Malaki alitabiri kuhusu tukio ambalo lingefanyika kabla ya Ujio wa Pili na kwamba lingejumuisha Nabii Eliya wa Agano la Kale. Mwalike mwanafunzi asome 3 Nefi 25:5–6 kwa sauti, na uulize darasa litafute Eliya angelifanya nini ili kusaidia kutayarisha Ulimwengu kwa ujio wa Bwana. Waulize wanafunzi nini wanajua kuhusu kurejea kwa Eliya duniani kama sehemu ya ure-jesho wa injili. Unaweza kuongeza majibu yao kwa kueleza kuwa mnamo Aprili 3, 1836, Eliya alimtokea Joseph Smith na Oliver Cowdery katika hekalu jipya lililowekwa wakfu hivi karibuni la Kirtland (ona M&M 110:13–16). Kwa wakati ule, Eliya alirejesha funguo za ukuhani zinazohitajika kufunganisha familia milele katika mahekalu matakatifu ya Mungu. Kupitia utafiti wa historia ya familia, tunatambua wanafamilia ambao ibada za hekaluni zinaweza kufanywa.• Unafikiri inamaanisha nini kuwa Eliya “angeigeuza miyoyo ya baba iwaelekee watoto,

na ya watoto iwaelekee mababa zao”? • Ni baraka kwako vipi kujua kwamba unaweza kufunganishwa kwa familia yako kwa milele?Shuhudia kuwa mioyo yetu inapogeukia baba zetu kupitia kwa historia ya familia na kazi ya hekalu, tunasaidia kutayarisha dunia kwa Ujio wa Pili wa Yesu Kristo.

3 Nefi 26:1–12Yesu Kristo afafanua maandiko maandiko, na Mormoni anafundisha kile kina-chpaswa kufanywa ili kupokea vitu vikuu ambavyo Bwana amefunuaFupisha 3 Nefi 26:1–5 kwa kueleza kuwa baada ya Mwokozi kushiriki utabiri wa Malaki, aliwafundisha watu “vitu vyote ambavyo vingekuja juu ya uso wa dunia” kutoka kuumbwa mpaka Hukumu ya Mwisho (3 Nefi 26:3–4).Mwalike mwanafuzi asome 3 Nefi 26:6–8 kwa sauti na litake darasa kutafuta ni kiasi gani cha yale Yesu Kristo alifundisha yaliwekwa katika Kitabu cha Mormoni. Kisha waalike wa-nafunzi wasome 3 Nefi 26:9–11 kimoyomoyo wakitafuta, sababu ya Mormoni kutojumu-isha katika ufupisho wake kila kitu ambacho Bwana aliwafundisha Wanefi. Sisitiza kuwa neno amini katika aya hizi linamaanisha tunahitaji kutumia mafundisho na kanuni ambazo Mungu amefunua na si tu kutumaini kuwa ni za kweli. • Kulingana na 3 Nefi 26:9, Bwana anawaahidi nini wale wanaoamini na kutumia kile

ambacho amefunua? (Wanafunzi wanapojibu, sistiza kwamba na tunapoamini na kufa-nya kile Mungu ametufunulia, sisi tunajiandaa kupokea ufunuo mkubwa zaidi.)

• Kwa nini unafikiri ni muhimu kwamba tuamini katika kweli ambazo tayari tumepokea kabla ya kupokea kweli za ziada?

• Tunawezaje kuonyesha kwamba tunaamini kile Bwana amefunua?Waahidi wanafunzi kwamba wanapojifunza kwa uaminifu na kutumia kanuni katika Kitabu cha Mormoni, watapokea ufahamu uloongezeka wa injili. Wasaidie wanafunzi ku-afakari jinsi wanavyopokea vizuri kweli katika Kitabu cha Mormoni kwa kuwataka wajibu maswali yafuatayo katika daftari zao au majarida ya kujifunzia maandiko) (unaweza kutaka kuandika maswali haya ubaoni) • Unafanya nini katika maisha yako kinachodhihirisha imani yako katika Kitabu cha

Mormoni?• Ni lini kusoma Kitabu cha Mormoni kwa nia hasa kumekuongoza kupokea ufunuo

wa kibinafsi.

Page 501: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

486

SoMo la 132

3 Nefi 26:13–21Mwokozi akamilisha huduma yake duniani miongoni mwa Wanefi, na Wafuasi wake wafuata mfano wake katika huduma yaoEleza kwamba katika 3 Nefi 26, Mormoni alifanya muhtasari salio la huduma ya Mwokozi miongoni mwa Wanefi Waalike wanafunzi wasome 3 Nepfi 26:13–16 kimoyomoyo. Una-weza kutaka kupendekeza kuwa waweke alama baadhi ya vitu ambavyo Mwokozi alifanya ambavyo Mormoni alichagua kuhimiza. Kama Wakati ukirihusu, waalike wanafunzi kutathmini na kutafakari hoja zao na maa-ndiko waliyoweka alama kutoka kwenye mafunzo ya 3 Nefi 11–25. Wahimize kutafuta mafindisho na matukio kutoka kwa huduma ya Mwokozi miongoni mwa Wanefi ambayo ni ya maana au ni ya kumbukumbu kwao. Waalike wanafunzi wachache kushiriki fikira na hisia zao kuhusu huduma ya mwokozi miongoni mwa Wanefi.

Page 502: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

487

UtanguliziMara baada ya huduma ya Mwokozi miongoni mwa Wanefi, wale kumi na wawili wapya walioitwa wafuasi wa Kinefi walikutana pamoja katika maombi makuu na

kufunga. Yesu Kristo aliwatokea na kujibu maswali yao kuhusu jina wanalopaswa kulipa Kanisa. Aliwafundisha kuhusu injili yake na kuwaamuru kuwa kama Yeye alivyo.

SOMO LA 133

3 nefi 27

Mapendekezo ya Kufundisha

3 Nefi 27:1–12Yesu Kristo anawafundisha wafuasi kumi na wawili kuwa Kanisa lake linapaswa kuwa na jina LakeGawa darasa katika vikundi vya watatu ua wanne. Ikiwa darasa lako ni dogo, acha kila mwanafunzi kufanya kazi kibinafsi. Kiambie kila kikundi (au mtu binafsi) kufikirie kwamba kinakwenda kuanzisha klabu kipya au timu ya michezo. Kiambie kila kikundi kiamue aina ya timu ya michezo au klabu watakayounda, kama vile klabu ya kisayansi, au timu ya kandanda na, kisha waambie wachague jina kwa shirika lao. Fanya kila kikundi kiandike jina lao katika kipande cha karatasi. Kisha kusanya karatasi za kila kikundi (Shughuli hii inapaswa kuwa fupi. Haifai kuchukua muda mrefu au nathari kutoka kwa mafundisho na kanuni katika 3 Nefi 27.)Soma kwa sauti jina kutoka kila karatasi. Baada ya kusoma kila jina, litake darasa kukisia kutokana na jina aina ya klabu au timu hiyo.• Jina linaweza kuwasilisha nini kuhusu shirika na watu waliomo ndani yake?Eleza kwamba punde baada ya ujio wa Yesu Kristo kwa Wanefi, wafuasi wake kumi na wawili wa Kinefi walijiunga katika kufunga na sala. (ona 3 Nefi 27:1). Waite wanafunzi wachache wachukue zamu kusoma kwa sauti kutoka 3 Nefi 27:2–7. Uliza darasa kufuatilia, wakitafuta swali la wafuasi na jibu la Mwokozi.• Mwokozi alisema Kanisa lake linapaswa kuitwa vipi?• Ni sababu zipi alizotoa za kulipa Kanisa jina lake?Waaike wanafunzi kupekua 3 Nefi 27:8–12 kimoyomoyo wakitafuta maelezo ya Mwokozi kwa Kanisa lake la kweli. Wakati Wanapojifunza, andika kauli ifuatayo isiyokamilika ubaoni:

Kanisa la kweli la Yesu Kristo sharti liwe....Baada ya wanafunzi kuwa na muda wa kutosha kupekua aya hizi, waulize jinsi wange-kamilisha sentesi iliyo ubaoni kwa mujibu wa kile walichosoma. (Wanafunzi wanapaswa kuwe na uwezo wa kutambua ukweli ufuatao: Kanisa la kweli la Yesu Kristo ni sharti kuitwa kwa jina lake na kujengwa juu ya injili yake.)• Kwa nini unafikiri ni muhimu kwa Kanisa la Mwokozi kuwa na jina lake?• Unafikiri inamaanisha nini kwa “kanisa kujengwa juu ya injili yake? (3 Nefi 27:10). Unafikiri

kwa nini ni mihumu kwa Kanisa kujengwa juu ya injili yake badala ya juu ya kazi za watu?Waambie wanafunzi kukamilisha sentensi ifuatayo katika daftari au majarida yao ya ma-fundisho ya maandiko “Kuwa muumini wa Kanisa la Yesu Kristo ni muhimu kwangu kwa sababu.

3 Nefi 27:13–22Yesu Kristo anaelezea injili Yake na kufundisha kile tunachopaswa kufanya ili kusimama bila hatia mbele yake na Baba yakeWaulize wanafunzi kufikiria jinsi walivyohisi wakati walipokamatwa wakifanya makosa. (Usiwatake kushirikisha uzoefu huu) Kisha watake kufikiria itakavyokuwa kusimama mbele ya Bwana kuhukumiwa. Wahimize kutafakari swali lifuatalo:

Page 503: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

488

SoMo la 133

• Utahisi vipi mbele za Bwana ikiwa una hatia ya dhambi?Eleza kuwa neno injili inamaanisha habari njema. Watake wanafunzi wachache kuchukua zamu kusoma kutoka kwa 3 Nefi 27:13–16, na omba darasa kutafuta habari njema katika aya hizi. Pia waambie wafikirie jinsi habari hii njema inahusiana na siku ambapo watasi-mama mbele ya Mungu kuhukumiwa.• Mwokozi alishuhudia kwamba alikuja duniani kufanya mapenzi ya Baba Yake. Kulingana

na 3 Nefi 27:14, Baba wa Mbinguni alimtuma Yesu Kristo kufanya nini duniani?• Kwa mujibu wa 3 Nefi 27:13–14, ni nini msingi wa injili? (Ingawa wanafunzi wanaweza

kutumia maneno tofauti, wanapaswa kutambua ukweli ufuatao: Msingi wa injili ni kwamba Yesu Kristo alifanya mapenzi ya Baba yake katika kutimiza upatanisho. Unaweza kutaka kuwaalika wanafunzi kuandika ukweli huu katika maandiko yao karibu na 3 Nefi 27:13–14.)

• Kwa sababu mwokozi alitimiza matakwa ya baba yake, ni nini kitatokea kwa wanadamu wote? (Tutainuliwa juu mbele Yake ili kuhukumiwa kwa ajili ya kazi zetu.)

Waalike wanafunzi kupekua 3 Nefi 27:16 kimoyomoyo, wakitafuta kazi ambazo sharti tufa-nye ili kupokea baraka zote za Upatanisho na kujitayarisha kwa ajili ya hukumu. Uliza wa-nafunzi watoe taarifa ya nini wanachopata. Alika mwanafunzi kuandika majibu yao ubaoni.• Kulingana na aya hii, ni baraka zipi zitakazowajia wanaotubu, kubatizwa na kuvumilia

hadi mwisho? (Majibu ya wanafunzi yanapaswa kuonyesha ukweli ufuatao: kama tuki-tubu, kubatizwa; na kuvumilia hadi mwisho, tutakuwa bila hatia tutakaposimama mbele ya Mungu ili kuhukumiwa.)

Alika mwanafunzi asome 3 Nefi 27:17–19 kwa sauti. Liambie darasa kufuatilia wakitafuta kile kitakachofanyika kwa wale wasiotubu au kuvumilia hadi mwisho.• Kutoka kwa ulichosoma, kwa nini wote wa watoto wa Baba wa Mbinguni wanahitaji

Upatanisho wa Yesu Kristo?• Ni habari gani njema iliyoko kwa ajili yetu tunapofikiria kuhusu kusimama mbele ya

Bwana ili kuhukumiwa?Mwalike mwanafunzi asome taarifa ifuatayo ya Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Mi-tume Kumi na Wawili:

"Habari njema [ni] kuwa kifo na jehanamu [vinaweza] kuepukika, kwamba makosa na dhambi zinaweza kushindwa, kwamba kuna tumaini, kwamba kuna msaada, kwamba isiyotatuliwa inaweza kutatuliwa, kwamba adui ameshindwa. Habari njema [ni] kwamba kaburi la kila mtu siku moja litakuwa tupu, kwamba nafsi ya kila mmoja inaweza tena kuwa safi, kwamba kila mtoto wa Mungu anaweza tena kurejea kwa Baba aliyewapa uzima"

(Missionary Work and the Atonement, Ensign, Machi. 2001, 8, 10).Alika mwanafunzi asome 3 Nefi 27:20–21 kwa sauti na omba darasa kutafuta mwaliko wa Mwokozi kwetu. • Ni nini mwaliko wa Mwokozi katika aya hizi?Ili kuwasaidia wanafunzi kufikiria kuhusu juhudi zao kukubali mwaliko huu, waalike ku-jibu maswali yafuatayo katika daftari zao au majarida ya mafunzo ya maandiko. (Unaweza kutaka kuandika maswali haya ubaoni mbele ya darasa au kuyasoma pole pole ili wanafu-nzi waweze kuandika.)• Kwa nini Mwokozi anakutaka kutubu na kumjia Yeye?• Ni kwa njia gani unakubali mwaliko wa Mwokozi katika 3 Nefi 27:20–21?• Unaweza kufanya nini leo ili kujitayarisha kusimama bila mawaa mbele ya Bwana?Alika wanafunzi asome Mafundisho na Maagano 76:40–42 kwa sauti. Uliza darasa kufuatilia wakitafuta uelewa mwingine kuhusu kwa nini injili ni habari njema. (Unaweza kupendekeza kuwa wanafunzi waandike M&M 76:40– 42 katika maandiko yao karibu na 3 Nefi 27:13.)Awali katika somo, uliwataka wanafunzi kutafakari jinsi wangehisi mbele ya Bwana kama wangekuwa na hatia ya dhambi. Katika wakati huu kwenye somo, waalike kutafakari jinsi wangeweza kuhisi mbele ya Mwokozi kama wangejua kuwa wamesafishwa kupitia kwa Upatanisho wake na kwa utiifu kwa kanuni, amri, na ibada za injili.• Kama ungezungumza na Mwokozi wakati huo, ungesema nini?

Page 504: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

489

3 nefi 27

• Kulingana na kile ulichojifunza hivi leo, ungeelezea vipi habari njema ya injili ya Yesu Kristo kwa Rafiki?

3 Nefi 27:23–33Yesu Kristo awaagiza wafuasi Wake kuwa kama AlivyoFupisha 3 Nefi 27:23–26 kwa kueleza kuwa Mwokozi aliwapa maagizo wafuasi wake kumi na wawili wa Kinefi na kuwafundisha kuhusu majukumu yao. Waambie wanafunzi wasome 3 Nefi 27:27 kimoymoyo, wakitafuta sheria aliyowapa wanafunzi ili kuwasaidia kutimiza majukumu yao kama waamuzi wa watu.• Kwa nini ingekuwa muhimu kwa waamuzi wa watu kuwa kama Mwokozi?Waambie wanafunzi kutathmini 3 Nefi 27:21.• Mwokozi aliwaamuru wafuasi kufanya nini?• Ni uhusiano gani uliopo kati ya kufanya kazi za Bwana na kuwa kama alivyo?Wanafunzi wanapojadili swali hili, andika kanuni ifuatayo ubaoni: Bwana anategemea wafuasi Wake kufanya kazi zake na kuwa kama Alivyo. • Ni zipi baadhi ya njia ambazo kwazo tunaweza kuwa kama Mwokozi? Ni zipi baadhi ya

kazi tunazoweza kufanya tunapofuata mfano wake?• Ni kwa njia gani umebarikiwa wakati ulipojaribu kufuata mfano wa Mwokozi?Hitimisha darasa kwa kushuhudia baraka zinazotujia tunapojibidiisha kuwa kama Yesu Kristo alivyo.

Tangazo na Habari za Usuli3 Nefi 27:13–21. Injili ya Yesu Kristo

Nabii Joseph Smith alieleza ujumbe wa kimsingi wa injili ya Yesu Kristo:

"Kanuni za msingi za dini yetu ni ushuhuda wa Mitume na Manabii, kuhusu Yesu Kristo, kwamba alikufa, akazikwa, na akafufuka tena siku ya tatu, na kupaa mbinguni; na mambo yote mengine ambayo yanahu-siana na dini yetu ni viambatisho vyake" Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith [2007], 49).

Mzee Russell M. Nelson wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili alifundisha:

"Neno injili linamaanisha Habari njema. Habari njema ni Bwana Yesu Kristo na ujumbe wake wa wokovu. [Ona Kamusi ya Biblia. Bible Dictionary, Gospels, 682–683. Yesu alifananisha injili pamoja na ujumbe wake na huduma yake katika maisha ya kufa. Katika kauli ya ujumbe wake Yesu alisema:

"Hii ndiyo injili ambayo nimewapatia—kwamba nilikuja ulimwengu kufanya mapenzi ya Baba yangu, kwa sababu Baba yangu alinituma.

'"Na Baba yangu alinituma ili nipate kuinuliwa juu kwenye msalaba.' [3 Nefi 27:13–14.]

"Misheni ya Mwokozi duniani tunaifahamu kama Upatanisho.

"Huduma ya Mwokozi inajumuisha kila kitu kingine—mafundisho yake, madhihirisho yake ya upendo, nathari kwa ibada, mipango ya sala, uvumilivu, na zaidi. Aliishi ili kuwa Mfano wetu, ambayo pia alifa-nanisha na injili katika kauli yake ya huduma. Hii ni injili yangu, Alisema, kwa kazi mlizoniona nikifanya, kwamba nanyi pia mzifanye. 3 Nefi 27:21. Hivyo, imani, toba ubatizo kwa maji mengi, moto na wa Roho Mtakatifu;mkusanyiko wa wateule; na kuvumilia hadi mwisho, yote ni sehemu ya injili," (Senior Missionaries and the Gospel, Ensign or Liahona, Nov. 2004, 81).

(3 Nefi 27:27). Kuwa Kama Yesu Kristo

Rais Ezra Taft Benson alifundisha:

"Kwamba mtu ni mkuu zaidi na aliyebarikiwa zaidi na mwenye furaha ambaye maisha yake kwa mara nyingi hufikia mfano wa Kristo. Hili haihusiani na mali ya kilimwengu, nguvu au sifa. Jaribio la kweli la ukuu, kubarikiwa na kujawa na furaha ni jinsi maisha yana-vyoweza kuwa karibu kama Bwana,Yesu Kristo. Yeye ndiye njia ya kweli, ukweli wote, na uzima tele" (Jesus Christ—Gifts and Expectations [BYU devotional address, Dec. 10, 1974], 1, speeches. Byu. Edu).

Shuhudia juu ya Yesu KristoUpatanisho wa Yesu Kristo ni ukweli wa kimsingi ambao kwake mafundisho yote ya injili na kanuni zimejengwa. Inapaswa kuwa katika kitovu cha mafundisho yote na kujifunza injili. Tafuta nafasi za ku-shudia mara kwa mara kumhusu Yesu Kristo na kuwasaidia wanafu-nzi kuongezeka katika upendo wao kwake na hamu yao ya kuwa wa-fuasi wake wa kweli.

Page 505: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

490

UtanguliziWakati Yesu Kristo alipouliza kila mmoja wa wafuasi wake wa Kinefi kile walichohitaji kutoka kwake, tisa waliomba upesi kurejea kwake wakati huduma yao ulimwenguni ulipokamilika. Watatu waliomba kubaki duniani ili kuleta mioyo kwake hadi ujio wake wa pili.

Bwana alitimiza haja za haki za vikundi vyote viwili. Mormoni atoa maelezo ya kina ya huduma za Wanefi watatu, na pia anashiriki kile Bwana alichokuwa ame-mfunulia kuhusu mabadiliko ya kimwili wale Wanefi waliopata ili waweze kubaki duniani.

SOMO LA 134

3 nefi 28

Mapendekezo ya Kufundisha

3 Nefi 28:1–11Yesu Kristo akubali mahitaji ya wafuasi wake wa KinefiWatake wanafunzi kutafakari jinsi wangejibu kama Yesu Kristo angewatokea na kuwauliza "Mnahitaji nini kutoka kwangu?" Waambie waandike majibu yao katika daftari zao au ma-jarida ya kujifunza maandiko. Wape nafasi ya kushiriki kile walichoandika ikiwa watahisi sawa kufanya hivyo.Waambie wanafunzi wasome 3 Nefi 28:1–3 kimoyomoyo, wakitafuta majibu ya wale wafuasi tisa wakati Bwana alipowauliza swali hili. Baada ya wanafunzi kutoa taarifa ya nini walichojifunza, uliza:• Mwokozi alihisi nini kuhusu hamu ya wafuasi hawa tisa?Waambie wanafunzi wasome 3 Nefi 28:4–9 kimoyomoyo wakitafuta kile wafuasi watatu waliosalia walitaka kutoka kwa Mwokozi. Acha wanafunzi watoe taarifa za kile walicho-pata. (Inaweza kuwa jambo la maana kuweka nathari ya wanafunzi kwa kauli ifuatayo katika 3 Nefi 28:9: Mmetamani kwamba muweze kuleta roho za watu kwangu.)• Mwokozi alihisi vipi kuhusu hamu za wafuasi hawa?• Kulingana na 3 Nefi 28:8–9, Mwokozi aliwaahidi nini Wanefi Watatu ili hamu yao ya

haki iweze kutimizwa?Waalike wanafunzi wasome 3 Nefi 28:10 kwa sauti, ana Uliza darasa kutafuta Baraka Bwana alizowaahidi wale Wanefi Watatu. • Bwana aliwaahidi nini wale Wanefi Watatu? Ni lini umeona kuwa hudua kwa wengine

huleya shangwe?• Tunaweza kujifunza nini kuhusu Bwana kutoka kwa 3 Nefi 28:1–10? (Majibu ya wa-

nafunzi kwa swali hili yanaweza kujumuisha kuwa Bwana hutubariki kulingana na haja zetu za haki na kwamba Bwana anafurahia wakati tunapotamani kuwasaidia wengine kumjia yeye.)

Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa umuhimu wa haja za haki, soma kauli zifuatazo:Mzee Neal A. Maxwell wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alisema:"Tunachokitamani bila kukoma, kwa muda mrefu, ni kile hatimaye kitakuwa na kwamba tutapokea katika umilele . . ."Hivyo, haja za haki zinapaswa kuwa thabiti, (“According to the Desire of [Our] Hearts, Ensign, Nov. 1996, 21–22).Rais Brigham Young alifundisha:"Wanaume na wake wanaotamani kupata makao katika ufalme wa Selestia, watagundua kwamba ni sharti wapigane na adui wa haki zote kila siku" (Remarks, Deseret News, Dec. 28, 1864, 98).• Kwa nini unafikiri tunapaswa kupigana kila siku ili haja zetu za haki ziweze kutimizwa?• Wakati unapohisi kuwa Bwana amekubariki kwa sababu ya haja zako za haki?

Epukana na makisio kuhusu wale Wanefi WatatuWengi wamesikia ha-dithi kuhusu kukisiwa kwa matembezi ya Wale Wanefi Watatu. Badala ya kushiriki hadithi hizi, fundisha kile kinachofu-ndishwa katika maa-ndiko. Kumbuka kauli ya Mormoni kwamba wale Wanefi watatu wangekuwa miongoni mwa Watu wa mataifa na Wayahudi ambao “hawangewafahamu” (3 Nefi 28:27–28). Jizuie kutokana na kujadili ha-dithi au habari zingine ambazo hazipatikani katika vyanzo vilivyoi-dhinishwa na Kanisa.

Page 506: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

491

3 nefi 28

Warejeshe wanafunzi kwenye haja walizoziandika mwanzoni wa darasa. Waambie waa-ndike santensi chache kuhusu kile watakachoanza kufanya leo ili kuhakikisha kwamba zile haja za kweli zinaweza kutimizwa.

3 Nefi 28:12–35Mormoni aeleza kuhusu huduma ya wale Wanefi WatatuAlika mwanafunzi asome 3 Nefi 28:12–16 kwa sauti. Uliza darasa kufuatilia wakitafuta kilichotokea kwa wafuasi wa Kinefi baada ya Bwana kuondoka kutoka kwao. Eleza kuwa wafuasi walipata mageuzi—mabadiliko ya muda katika miili yao.• Kulingana na 3 Nefi 28:15, ni sababu gani moja wafuasi walihitaji kugeuzwa? (Ili “wa-

weze kutazama mambo ya Mungu.”)Eleza kwamba kuanzia kwa 3 Nefi 28:17, tunasoma maelezo ya Mormoni ya huduma ya wale Wanefi Watatu. Waambie wanafunzi wasome 3 Nefi 28:17 kimoyomoyo, wakitafuta kile Mormoni hakufahamu kuhusu hali ya kimwili ya wale Wanefi Watatu alipoandika usimulizi huu. (Unaweza kutaka kuwaambia wanafunzi kwamba baadaye katika somo, watajifunza zaidi kuhusu mabadiliko ambayo wale Wanefi Watatu walipata.Waalike wanafunzi wachache kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka kwa 3 Nefi 28:18–23. Litake darasa kufuatilia wakitafuta jinsi Bwana alivyowabariki wale Wanefi Watatu ili waweze kutimiza haja zao za haki.• Wale Wanefi Watatu walifanya nini ili kutimiza haja yao kuwaleta wengine kwa Mwokozi?• Ni kwa njia gani Bwana aliwabariki ili waweze kutimiza haja zao?Waalike wanafunzi wasome 3 Nefi 28:25–32 kimoyomoyo, wakitambua watu waliofai-dika na bado watafaidika kutoka kwa huduma ya wale Wanefi Watatu. Unaweza kutaka kupendekeza kuwa wanafunzi waweke alama kile wanachopata. (Angalizo kwamba 3 Nefi 28:27–28 inaonyesha sababu moja kwa nini tunapaswa kuwa wangalifu kuhusu kuamini na kushiriki hadithi kutoka kwa watu wengine ambao wanadai kuwa wamekutana na wale Wanefi Watatu: Mormoni alisema kuwa watu ambapo miongoni mwao wale Wanefi Watatu watahudumu “hawatawajua.”)

3 Nefi 28:36–40Mormoni ajifunza kuhusu asili ya viumbe waliobadilishwa Waulize wanafunzi kama wamewahi kuwa na swali kuhusu injili au ikiwa wamewahi kusoma kitu katika maandiko ambacho hawakukielewa. Wakumbushe kwamba wakati Mormoni alipoandika kwanza kuhusu kubadilishwa kwa Wanefi Watatu, alisema kuwa hakuelewa kikamilifu badiliko katika hali yao ya kimwili wakati wa huduma yao duniani. (ona 3 Nefi 28:17).• Wewe humgeukia nani kwa kawaida unapokuwa na maswali kuhusu injili au kuhusu

vifungu vya maandiko? Kwa nini?Waalike wanafunzi wasome 3 Nefi 28:36–37 kimoyomoyo ili kugundua nini kile Mormoni alifanya kupata jibu kwa swali yake..• Ni kanuni gani tunaweza kujifunza kutoka kwa Mormoni kuhusu jinsi ya kupokea ufa-

hamu ziada? (Ingawa wanafunzi wanaweza kujibu swali hili kwa njia tofauti, hakikisha wanatambua kanuni ifuatayo: Wakati tunapokosa ufahamu, tunapaswa kumuuliza Baba wa Mbinguni na sisi tutapokea mwongozo.)

• Je, ni baadhi ya mifano gani ambayo inaonyesha kanuni hii?• Ni nini baadhi ya hali ambazo tunaweza kumuhitaji Baba wa Mbinguni kwa ufahamu

mkubwa?Soma maelezo yafuatayo, ambayo Rais Spencer W. Kimball anaonyesha hali chache ambazo tunapaswa kuomba kwa ajili ya msaada:"Kila mmoja wetu huwa na haja sana ya msaada wake tunapotafuta kujifunza kweli za injili na kisha kuziishi, tunapotafuta msaada wake katika maamuzi makubwa ya maisha yetu, maamuzi yanayohusiana na masomo, ndoa, ajira, nafasi ya makazi, kulea familia zetu, kuhudumiana kila mmoja

katika kazi ya Bwana, na kutafuta msamaha wake na uongozi wa daima na ulinzi katika yote tunayofanya. Orodha yetu ya mahitaji ni ndefu, na ya kweli na dhati. . . .

Page 507: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

492

SoMo la 134

"Baada ya maisha ya sala, najua kuhusu upendo na uwezo na nguvu inayotokana na sala na uaminifu wa dhati. Najua juu ya utayari wa Baba yetu kutusaidia katika uzoefu wetu wa maisha ya muda, kutufundisha, na kutuongoza. Hivyo, kwa upendo mkubwa, Mwo-kozi wetu amesema, Nisemacho kwa mmoja ninasema kwa wote; ombeni daima." (M&M 93:49). (“Pray Always,” Ensign, Oct. 1981, 3, 6).• Ni vipi unavyoweza kuongeza imani yako katika nguvu ya sala? Ni lini wewe na familia

yako mmepokea majibu ya maombi yenu?Wahimize wanafunzi kwenda kwa Baba wa Mbinguni katika maombi wanapotaka kuelewa injili na kukumbana na changamoto za maisha. Shuhudia baraka ambazo zimekuja katika maisha yako wakati wewe umepeleka changamoto zako na maswali kwa Baba wa Mbinguni.Eleza kwamba mabadiliko ambayo Wanefi Watatu walipata inaitwa kubadilishwa. Baa-dhi ya watumishi wa Bwana waaminifu wamebadilishwa ili waweze kuendeleza huduma zao duniani. Mormoni alipoendelea kuuliza kuhusu mabadiliko hayo, alijifunza kuhusu asili ya viumbe waliobadilishwa.Andika Viumbe Waliobadilishwa ubaoni. Alika mwanafunzi asome 3 Nefi 28:37–38 kwa sauti. Uliza darasa kufuata pamoja, wakitafuta nini Mormoni alijifunza kuhusu mabadiliko ambayo yalitokea katika miili ya Wanefi Watatu.• Mormoni alijifunza nini kuhusu viumbe waliobadilishwa? (Mwalike mwanafunzi

ahudumie kama mwandishi na aandike majibu ya wanafunzi wengine ubaoni. Majibu yanapaswa kujumuisha kwamba viumbe waliobadilishwa hawakuonja kifo, na kwamba hawasikii maumivu, na kwamba hawana uzoefu wa huzuni isipokuwa kwa huzuni wa-nahisi kwa sababu ya dhambi za ulimwengu.)

• Kwa nini mabadiliko haya kwenye miili yao ni muhimu? (Unaweza ukawataka wanafu-nzi kupitia 3 Nefi 28:6–7. Mabadiliko yalikuwa muhimu ili waweze kutimiza matakwa yao ya haki ya kubaki duniani na kuendelea kuleta roho kwa Kristo mpaka Ujio wa Pili wa Mwokozi.

Waambie wanafunzi wasome 3 Nefi 28:39–40 kimoyomoyo, wakitafuta maelezo ya ziada kuhusu viumbe waliobadilishwa. Wanafunz wanapotoa taarifa, kuwa na mwandishi mwingine aandike matokeo yao ubaoni. (Majibu yanapaswa kujumuisha kwamba viu-mbe waliobadilishwa hawawezi kujaribiwa na Shetani, kwamba wao wametakaswa na ni watakatifu, na kwamba “nguvu za dunia haziwezi kuwashikilia.”) Unaweza kutaka kueleza kwamba ingawa viumbe waliobadilishwa hawateseki maumivu ya kifo, wao hawajafufuka. Hawatapokea lile badiliko kuu mpaka siku ya Hukumu, watakapobadilishwa kutoka kwa kufa hadi kutokufa haraka katika —“kufumba na kufumbua (ona 3 Nefi 28:8, 40).Hitimisha kwa kutoa ushuhuda wa kanuni na mafundisho yaliyojadiliwa katika darasa. Waalike wanafunzi kutenda kufuatana na minong’ono waliyopokea kutoka kwa Roho.

Tangazo na Habari za Usuli3 Nefi 28. Kubadilishwa na kugeuzwa

Wale Wanefi Watatu walibadilishwa na kuhuishwa.

Kubadilishwa ambako kunatajwa katika 3 Nefi 28:13–17, ni hali ya watu ambao wanabadilishwa kwa uonekano wao — kwa muda na asili—, yaani wanainuliwa kwa ki-wango kikuu cha kiroho— ili waweze kustahimili uwepo na utukufu wa nafsi za mbingu. (Guide to the Scriptu-res, Transfiguration,” scriptures. Lds. Org; see also D&C 67:11; Moses 1:11). Maandiko yanasimulia kuhusu watu waliogeuzwa, pamoja na Musa, (ona Musa 1:9–11); Yesu

Kristo, Petro, Yakobo, na Yohana (ona Mathayo 17:1–8); na Joseph Smith (ona Joseph Smith—Historia1:14–20).

Nafsi zilizobadilishwa ni watu waliobadilishwa ili wasi-pate maumivu au kifo hadi ufufuo wa wafu (Guide to the Scriptures, Translated Beings, scriptures.lds.org; ona pia 3 Nefi 28:7–9, 20–22, 37–40). Madhumuni yao ni ku-waleta roho kwa Kristo (ona 3 Nefi 28:9). Maandiko yana masimulizi ya watu ambao wamebadilishwa, pamoja na Henoko (ona Mwanzo 5:24; Wahebrania 11:5), Musa (ona Alma 45:19), Eliya (ona 2 Wafalme 2:11), Na Yohana Mpendwa (ona Yohana 21:22–23; M&M 7).

Page 508: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

493

UtanguliziMormoni alipohitimisha masimulizi yake ya matembezi ya Mwokozi kwa Wanefi, alieleza kuwa kuja kwa Kitabu cha Mormoni kungekuwa ishara kuwa Bwana alikuwa anatimiza agano lake kwa nyumba ya Israeli. Pia alionya

kuwa wale wanaokataa kazi za Mungu wataletwa chini ya hukumu ya Mungu. Hatimaye aliweka kumbukumbu ya mwaliko wa Mwokozi kwa watu wote kutubu na kuhesabiwa kuwa miongoni mwa nyumba ya Israeli

SOMO LA 135

3 nefi 29–30

Mapendekezo ya Kufundisha

3 Nefi 29Mormoni ashuhudia kwamba Bwana atatimiza agano lake na nyumba ya Israeli katika siku za mwishoNakili mchoro ufuatao ubaoni kabla ya darasa kuanza (au utayarishe kama kipeperushi kwa kila mwanafunzi):

1. Wayunani a. Maana mbili: (1) Watu wa uzao wa nabii yakobo wa agano la Kale (israeli) ambaye pamoja na bwana alifanya maagano, na (2) waumini wa kweli katika yesu Kristo waliofanya maagano na Mungu.

2. nyumba ya israeli b. ahadi kwa walio waaminifu iliyojumuisha baraka za injili, mamlaka ya ukuhani, familia za milele, na nchi ya urithi.

3. Wabeuzi c. Maana mbili: (1) watu wasio wa uzao wa Kiisraeli au wasio wa ukoo wa kiisraeli na (2) watu wasio na injili

4. agano la bwana na israeli d. huzuni ya kina na kujuta

5. ole e. Kupuuza au kukataa kwa madharau au bezo

Anza darasa kwa kuwaalika wanafunzi kulinganisha maneno katika safu ya kwanza ya chati na maelezo katika safu ya pili (majibu: 1- c, 2- a, 3- e, 4- b, 5- d). Wanafunzi wanapotoa taarifa ya majibu, hakikisha kuwa wanaelewa kila moja ya maelezo haya. Unaweza kufanya hivi kwa kuwaalika wanafunzi kueleza maelezo katika maneno yao au kwa kutumia kila neno au kishazi katika sentensi. Wajulishe wanafunzi kuwa maelezo haya yatawasaidia kuelewa vyema zaidi 3 Nefi 29–30.Elezea kuwa baada ya Mormoni kuandika kuhusu matembezi ya Mwokozi kwa Wanefi, anatabiri kutimizwa kwa ahadi za Bwana katika siku za mwisho. Waulize wanafunzi kama wamepata timizo la ahadi ya kiungu, iwe iliyotolewa katika maandiko, na nabii, kupitia kwa Roho Mtakatifu au kupitia kwa baraka ya ukuhani. Waalike wanafunzi wachache ku-simulia uzoefu wao, lakini hakikisha kuwakumbusha kwamba hawapaswi kushiriki uzoefu ambo ni wa siri au wa kibinafsi.• Kwa nini unafikiri watu wengine wanaweza kuwa na shaka kwamba Mungu ataweka

ahadi zake?• Unajuaje kuwa Mungu anaweka ahadi zake?Andika maneno Wakati na kisha ubaoni. Waalike wanafunzi wasome 3 Nefi 29:1–3 ki-moyomoyo, wakitafuta maneno haya ubaoni. Eleza kwamba maneno haya yatawasaidia

Kufuatilia malengo na changamotoKama sehemu ya somo la 131, uliwahimiza wana-funzi kuandika kuhusu uzoefu wao ambao ume-waimarisha kiroho. Kabla ya kuanza somo la leo, fikiria kuwakumbusha kuhusu changamoto hii. Unaweza pia kuwapa na-fasi ya kuzungumzia jinsi walivyofaidika kutokana na kuweka kumbukumbu ya uzoefu wao.

Page 509: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

494

SoMo la 135

kutambua tukio ambalo linawaonyesha kwamba Bwana anaweka ahadi zake kwa nyumba ya Israeli katika siku za mwisho. (Inaweza kuwa ya msaada kuelezea kishazi "haya ma-neno" katika 3 Nefi 29:1 kinarejea maandiko ya Kitabu cha Mormoni.)• Unaweza kufupisha vipi unabii uliowekwa kumbukumbu katika aya hizi? (Wanafunzi

wanaweza kutumia maneno tofauti, lakini wanapaswa kutambua ukweli ufuatao: Kuja kwa Kitabu cha Mormoni ni ishara kuwa Bwana anatimiza agano lake la kuwaku-sanya Israeli katika siku za mwisho. Unaweza kutaka kuwahimiza wanafunzi kuweka alama ukweli huu katika muhtasari wa mlango wa 3 Nefi 29.)

Waambie wanafunzi kuinua juu nakala zao za Kitabu cha Mormoni. Eleza kuwa wanalo mikononi mwao timizo la unabii wa Mormoni na kuwa wanaweza kuhakikishiwa kwamba Bwana anawatayarisha watu wake kwa ujio wake. Mwalike mwanafunzi asome kwa sauti kauli ifuatayo ya Mzee Russell M. Nelson wa Akidi ya wale Mitume Kumi na Wawili:

"Kitabu cha Mormoni ni ishara dhahiri kwamba Bwana umeanza kuwakusa-nya watoto wake wa agano la Israeli. . . ."Hakika Bwana hajasahau! Ametubariki na wengine duniani kote na Kitabu cha Mormoni ... Kinatusaidia kufanya maagano na Mungu. Kinatualika kum-kumbuka na kumjua Mwana wake mpendwa. Ni ushuhuda mwingine wa Yesu Kristo" (Covenants,” Ensign au Liahona, Nov. 2011, 88).

• Jinsi gani ukweli kuwa tuna Kitabu cha Mormoni ni ushahidi kuwa Mungu ataweka ahadi zake?

Andika swali lifuatalo ubaoni: Kwa nini Watakatifu wa Siku za Mwisho wana haja na agano la Bwana kwa nyumba ya Israeli? Waambie wanafunzi wasikilize majibu kwa swali hili wanaposoma maelezo yafuatayo ya Mzee Russell M. Nelson, ambaye aliorodhesha ahadi ambazo ni sehemu ya agano la Bwana na watu Wake. (Unaweza kutaka kumpa kila mwa-nafunzi nakala ya kauli hii)"Agano ambalo Mungu alifanya na Ibrahimu, na baadaye kuhakikishwa na Isaka na Ya-kobo lilijumuisha ahadi kadha, pamoja na:“• Yesu Kristo angezaliwa kupitia kwa ukoo wa Ibrahimu.“• Uzao wa Ibrahimu itakuwa mwingi, ukiwa na haki ya ongezeko la milele, na pia na

haki ya kuwa na ukuhani.“• Ibrahimu atakuwa baba wa Mataifa mengi“• Nchi fulani zitarithiwa na uzao wake.“• Mataifa yote ya ulimwengu yatabarikiwa kwa uzao wake. “• Na agano lile litakuwa la milele —hata kupitia vizazi elfu."Baadhi ya hizi ahadi zimetimizwa, zingine bado zinasubiri. . . ."Wengine wetu ni mbegu hasa ya Ibrahimu, wengine wamekusanya katika familia yake kwa kuasiliwa. Bwana hatofautishi. Pamoja tunapokea baraka —hizi zilizoahidiwa kama tukimtafuta Bwana na kutii amri zake. . . . "... Brigham Young alisema: Watakatifu wote wa siku za mwisho huingia katika agano jipya la milele wanapoingia katika Kanisa hili.'" (Covenants, 87–88; quoting Teachings of Presi-dents of the Church: Brigham Young [1997], 62).• Kwa kutumia kile ulichojifunza kutoka kwa kauli ya Mzee Nelson, unaweza kujibu swali

lililo ubaoni? (Wanafunzi wanaweza kutoa majibu tofauti, lakini hakikisha kuwa wana-tambua ukweli ufatao: Watakatifu wa Siku za mwisho ni sehemu ya watu wa agano wa Mungu, na tuna jukumu la kuyabariki mataifa yote.)

• Watakatifu wa Siku za Mwisho wanatafuta vipi kubariki mataifa ya ulimwengu?• Kitabu cha Mormoni kinatekeleza jukumu gani katika jitihada hizo?Rejea maneno kana na ole kutoka kwa zoezi la kulinganisha. Eleza kwamba Mormoni alijua kwamba katika siku za mwisho kutakuwa na wale ambao watakataa Kitabu cha Mor-moni na ushahidi mwingine wa kutimiza agano la Bwana pamoja na watu wake. Watake wanafunzi wasome 3 Nefi 29:4–9 kimoyomoyo, wakitafuta kile kitakachotokea kwa wale wanaompuuza Mwokozi na kazi zake. Baada ya wanafunzi kuelezea nini walichopata, unaweza kutaka kupendekeza kwamba waandike ukweli ufuatao katika maandiko yao: Huzuni itawajia wale wanaomkana Yesu Kristo na kazi Zake.

Page 510: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

495

3 nefi 29 – 30

• Kwa nini huzuni ni matokeo ya kiasili ya kumpuuza Mwokozi na kazi Zake?• Ungejibu vipi kwa mtu anayesema kwamba Bwana haneni na wanadamu au kufanya

miujiza?• Tunawezaje kutambua vyema zaidi na kumfurahia Bwana na kazi zake maishani mwetu?

3 Nefi 30Bwana awausia Watu wa mataifa kutubu na kumjia YeyeRejea neno Watu wa mataifa kutoka kwa zoezi ya kulinganisha. Wajulishe wanafunzi kuwa katika 3 Nefi 30, Mormoni alitimiza amri kutoka kwa Bwana ya kuweka kumbukumbu ya mwaliko kutoka kwa Yesu kristo hasa kwa Watu wa mataifa, au watu wasio na injili. Waa-like wanafunzi wasome 3 Nefi 30:1–2 kimoyomoyo, wakitafuta mialiko mingi iwezekanvyo kwa Watu wa mataifa. Baada ya kutoa taarifa ya nini walichopata, uliza:• Ni upi kati ya mialiko hii unaweza kuwa muhtasari ya ile ingine yote? (Mwaliko wa

kumjia Kristo unajumuisha toba, ubatizo, kupokea Roho Mtakatifu, na kuhesabiwa mio-ngoni mwa watu wake)

• Ni baraka zipi ambazo Yesu Kristo anawaahidi watu wa mataifa ikiwa watamjia yeye? (Ondoleo la dhambi, kujazwa kwa Roho Mtakatifu, na kuhesabiwa miongoni mwa watu wake.)

• Kwa nini ni baraka kuhesabika miongoni mwa watu wa Bwana?Andika kanuni ifuatayo ubaoni: kama tukimjia Kristo, tutahesabika miongoni mwa watu wake. Eleza kuwa hata ingawa 3 Nefi 30:2 ilikusudiwa kwa wale wasio washiriki wa Kanisa, tunaweza kutumia mwaliko wa Yesu Kristo kupima juhudi zetu wenyewe katika kuweka maagano tuliyofanya na Mungu. Shuhudia baraka zinazotokana na kuweka maa-gano yetu na amri za Bwana.

Tathmini ya 3 Nefi Chukua muda fulani kuwasaidia wanafunzi kutathmini kitabu cha 3 Nefi. Waambie wafikirie kuhusu kile walichojifunza kutoka kwenye kitabu hiki, katika seminari na katika masomo yao ya kibinafsi ya maandiko. Ikihitajika, waalike kutathmini kwa ufupi baadhi ya muhtasari ya milango katika 3 Nefi ili kuwasaidia kukumbuka. Baada ya muda wa kuto-sha, waalike wanafunzi kadha kushiriki kitu kutoka kwa 3 Nefi ambacho kiliwasisimua au ambacho kiliwasaidia kuwa na imani kuu zaidi katika Yesu kristo.

Tathmini ya Umahiri wa MaandikoMpe kila mwanafunzi karatasi iliyo tupu. Waambie waandike barua kwa mtu (wa kufiki-riwa au mtu wanayemjua) asiye mshiriki wa Kanisa. Pendekeza kuwa wapekue vifungu vya umahiri wa maandiko kwa kweli wanazoweza kutumia kuwaalika wapokeaji wa barua ya kuja kwa Kristo na kuhesabiwa miongoni mwa watu Wake. Watake wanafunzi wachache kushirikiana kile walichoandika.Angalizo: Urefu wa somo hili unaweza kuruhusu muda kwa zoezi hili. Kwa mazoezi mengine ya tathmini ya umahiri wa maandiko tazama kiambatanisho mwisho wa mwongozo huu.

Tangazo na Habari za Usuli3 Nefi 30:1–2. Kukusanyika kwa Israeli

Rais Spencer W. Kimball alifundisha:

"Kukusanyika kwa Israeli kunajumuisha kujiunga na ka-nisa la kweli na kuja kwao katika ufahamu wa Mungu wa Kweli. Mtu yeyote, kwa hiyo, ambaye amekubali

injili ya urejesho, na ambaye sasa anatafuta kumwa-budu Bwana katika ulimi wake mwenyewe na pamoja na Watakatifu katika mataifa wanakoishi amefuata sheria ya kuwakusanya Israeli, na ni mrithi wa baraka zote walizoahidiwa Watakatifu katika siku hizi za mwisho. (The Teachings of Spencer W. Kimball, ed. Edward L. Kimball [1982], 439).

Page 511: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

496

UtanguliziHuku kukiwa na kanuni nyingi za thamani katika 3 Nefi 23–30, sehemu ya kwanza ya somo hili inazingatia kile wanafunzi wana-choweza kujifunza katika 3 Nefi 24–25 kuhusu kujitayarisha kwa Ujio wa Pili wa Yesu Kristo. Sehemu ya pili ya somo inazinga-tia kanuni katika 3 Nefi 27 zinazoweza kusaidia mwanafunzi kutafakari kinachomaanisha kuwa mfuasi wa Yesu Kristo na jinsi wanavyoweza zaidi kuwa kama alivyo.

Mapendekezo ya Kufundisha

3 Nefi 23–26Yesu Kristo aliyefufuka awafafanulia Wanefi MaandikoWaambie wanafunzi kutoa mifano ya matukio yanayohitaji matayarisho kwa uangalifu kwa muda fulani. (Mifano inaweza kujumuisha mbio za masafa marefu, onyesho la muziki au mchezo wa kuigiza.) Waulize wanafunzi kueleza nini kinacho-weza kutokea kwa mtu atakayejaribu kushiriki katika matukio haya bila matayarisho yanayohitajika.

Mwalike mwanafunzi asome 3 Nefi 24:2, kisha uliza darasa tukio ambalo wanafikiri Nabii Malaki alikuwa anatabiri. Mara wanafunzi wakishatambua “siku ya kuja kwake” kama Ujio wa Pili wa Yesu Kristo, waambie kuweka alama swali ambalo Malaki aliuliza: “nani atakayestahimili siku ya kuja kwake na nani ataka-esimama wakati atakapotokea?

Uliza: Kwa nini hili ni swali muhimu kwa wale wanaoishi katika siku za mwisho kufikiria?

Mwalike mwanafunzi asome kwa sauti maelezo yafuatayo ya Rais Henry B. Eyring wa Urais wa Kwanza kuhusu jinsi ulipaji zaka unavyoweza kutusaidia kuwa tayari kwa Ujio wa Pili wa Mwokozi:

Somo la Mafunzo Nyumbani 3 Nefi 23–30 (Kitengo cha 27)

Vifaa vya Matayarisho kwa Mwalimu wa Mafunzo nyumbani Muhtasari wa Masomo ya Kila siku ya mafunzo nyumbani. Ufuatao ni muhtasari wa mafundisho na kanuni ambazo wanafunzi walijifunza waliposoma 3 Nefi 23–30 (Kitengo 27) hakikukusudiwa kufundishwa kama sehemu ya somo lako. Somo unalofundisha linazingatia tu machache ya mafundisho haya na kanuni. Fuata ushawishi wa Roho Mtakatifu unapofi-kiria mahitaji ya wanafunzi wako.

Siku 1 (3 Nefi 23)Wanafunzi waliendelea kujifunza maneno ya Yesu Kristo kwa Wanefi. Walijifunza kuwa Mwokozi aliwaamuru watu kupekua kwa bidii maneno ya Isaya na manabii wengine. Mwokozi alipowakaripia watu kwa kutoweka kumbukumbu sahihi za historia yao ya Kiroho, wanafunzi walijifunza kwa-mba tunapoweka kumbukumbu za matukio yetu ya kiroho, tunamwalika Bwana kutupa ufunuo zaidi.

Siku 2 (3 Nefi 24–26)Wanafunzi walipotafakari maneno ya Malaki ambayo Yesu Kristo alishiriki na Wanefi, walikumbushwa kuwa katika Ujio wa Pili wa Mwokozi, Atatakasa watu wake na kuwahukumu waovu. Tafakari zaidi kuhusu kanuni ya kulipa zaka na utabiri wa kurejea katika siku za mwisho kwa Eliya kuliwasaidia wa-nafunzi kutambua kuwa tukimkrudia Bwana, atarudi kwetu na kwamba mioyo yetu imewageukia baba zetu, tunasaidia kutayarisha dunia kwa Ujio wa pili wa Yesu Kristo. Maelezo ya Mormoni kuhusu kwa nini hakujumuisha mafundisho yote ya Mwokozi miongoni mwa Wanefi yaliwasaidia wanafunzi kugundua kuwa tunapoamini kile ambacho Mungu amefu-nua, tunajitayarisha kupokea ufunuo mkuu zaidi.

Siku 3 (3 Nefi 27)Huku wafuasi kumi na wawili wa Kinefi wakiendelea katika maombi na kufunga, Mwokozi aliwatembelea na kuwaeleza kuwa Kanisa la kweli la Yesu Kristo linaitwa kwa jina lake na kujengwa katika injili Yake. Kutokana na kile Mwokozi alichofundisha wafuasi wake, wanafunzi pia walijifunza kuwa msingi wa injili ya Yesu Kristo ni kwamba alifanya mapenzi ya Baba yake katika kuukamilisha upatanisho. Pamoja na uelewa huu wa injili, wanafunzi walijifunza pia kuwa tukiishi kanuni za injili, basi tutaweza kusimama bila mawaa mbele za Mungu katika siku ya mwisho.

Siku 4 (3 Nefi 28–30)Kama vile Yesu Kristo aliyefufuka alivyotimiza matamanio ya wafuasi wake wa Kinefi, wanafunzi walijifunza kuwa Bwana hutubariki kulingana na hamu zetu za haki. Kutokana na mfano wa Mormoni kumwomba Bwana ujuzi zaidi kuhusu wale Wanefi Watatu, wanafunzi walijifunza kuwa kama tukimwomba Bwana uelewa, tutapokea ufunuo. Hitimisho la Mormoni la Huduma ya Mwokozi miongoni mwa Wanefi lili-wafundisha wanafunzi kwamba ujio wa Kitabu cha Mormoni ni ishara kwamba Bwana anatimiza agano lake na nyumba ya Israeli na kuwa tukimjia Kristo, tunaweza kuhesabiwa miongoni mwa watu Wake.

Page 512: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

497

SoMo la MafUnzo nyUMbani

“Kwa uamuzi wetu sasa kuwa walipaji kamili wa zaka na wenye uthabiti katika juhudi zetu za kutii, tutaimarishwa katika imani yetu, na kwa wakati, mioyo yetu italainishwa. Ni badiliko hilo mioyoni mwetu kupitia kwa Upatanisho wa Yesu Kristo, zaidi ya kutoa pesa au mali yetu, kunako wezesha kwa Bwana kuwa-ahidi wenye kulipa zaka kamili ulinzi katika siku za mwisho. Tunaweza kuwa na ujasiri kuwa tutastahili baraka hiyo ya ulinzi ikiwa tutajitolea sasa kulipa zaka kamili na kuwa wenye uthabiti katika kufanya hivyo” (“Spiritual Preparedness: Start Early and Be Steady,” Ensign or Liahona, Nov. 2005, 40).

Uliza: Kulingana na Rais Eyring, kulipa zaka kunawezaje kutusai-dia kujitayarisha kukutana na Mwokozi?

Mwalike mwanafunzi asome kwa sauti unabii wa Malaki kuhusu ujio wa Eliya katika 3 Nefi 25:5–6. Ili kuwasaidia kuelewa vyema zaidi jinsi kutimizwa kwa unabii huu kunavyoweza kuwaathiri, Mwalike mwanafunzi asome mwaliko ufuatao kutoka kwa Mzee David A. Bednar wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili:

“Mimi ninawaalika vijana wa Kanisa kujifunza kuhusu na kupata uzoefu wa Roho ya Eliya. . . .

“Mnapojibu katika imani mwaliko huu, mioyo yenu itageuka kwa mababu. Ahadi alizopewa Ibrahimu, Isaka na Yakobo zitapandwa katika nyoyo zenu. Upendo wenu na shukrani kwa ajili ya mababu zenu utaongeza. Ushuhuda wenu na kuongoka kwa Mwokozi kutakuwa kwa kina na kwa kudumu. Nami ninawaahidi mtalindwa dhidi ya ushawishi uliopamba moto wa adui. Unaposhiriki katika na kupenda kazi hii takatifu, utalindwa katika ujana wako na katika maisha yako yote" (“The Hearts of the Children Shall Turn,” Ensign or Liahona, Nov. 2011, 26–27).

Uliza: Ni uzoefu gani umekuwa nao ukifanya historia ya familia na kazi ya hekalu ambao umekuimarisha kiroho?

3 Nefi 27–30Yesu Kristo afununua jina na sifa muhimu za Kanisa lake na ku-heshimu hamu ya haki ya wanafunzi wake, Mormoni anahitimi-sha rekodi yake ya huduma ya Mwokozi miongoni mwa WanefiAndika kauli ifuatayo ya Nabii Joseph Smith kwenye ubao (una-weza kutaka kufanya hivyo kabla ya darasa na kuifunika mpaka hatua hii katika somo) Muulize mwanafunzi kusoma taarifa hii kwa sauti. (Kauli hii inapatikana katika Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith [2007], 49.)

"Kanuni za kimsingi ya dini yetu ni ushahidi wa Mitume na Manabii, juu ya Yesu Kristo, kwamba Yeye alikufa, akazikwa, akafufuka siku ya tatu, na kupaa mbinguni" (Joseph Smith)

Eleza kwamba kama vile Nabii Joseph Smith alivyotangaza, Mwokozi aliwafundisha Wanefi kwamba katikati ya injili yake ni dhabihu ya upatanisho wake. Andika ukweli ufatao ubaoni: msingi wa injili ya Yesu Kristo ni kuwa alifanya mapenzi ya Baba Yake katika kutimiza upatanisho.

Alika wanafunzi wasome kwa upesi 3 Nefi 27 na kutambulisha vishazi ambavyo kwavyo Mwokozi alifundisha fundisho hili. Uliza wanafunzi kushiriki aya walizopata.

Eleza kuwa 3 Nefi 27:16–20 ina mfundisho ya Mwokozi juu ya jinsi tunavyoweza kualika nguvu ya upatanisho wake maishani mwetu. Andika kauli ifuatayo ubaoni: tuki.. . . . , basi tuta. . .. Alika wanafunzi wasome 3 Nefi 27:20 kimoyomoyo wakitafuta maneno au vishazi wanavyoweza kutumia kujaza mapengo uba-oni. Uliza: kufuata kanuni kunawezaje kutusaidia kuwa wafuasi halisi wa yesu Kristo?

Eleza darasa kuwa changamoto na kilele cha ufuasi wetu ina-patikana katika 3 Nefi 27:21, 27. Alika wanafunzi kusoma aya hizi kimoyomoyo wanaposoma, andika kauli ifuatavyo ubaoni: Bwana Yesu Kristo anawatarajia wafuasi wake kufanya kazi zake na kuwa ... 

Waulize wanafunzi jinsi wangekamilisha kauli hii kwa mujibu wa kile walichosoma katika 3 Nefi 27:27. (wanafunzi wanapojibu, kamilisha kauli ubaoni ifuatavyo: Bwana Yesu Kristo anawa-tarajia wafuasi wake kufanya kazi zake na kuwa kama Alivyo) Soma kwa sauti kauli ifuatayo ya Rais James E. Faust wa Urais wa Kwanza;

"Na tufikirie baadhi ya vitu ambavyo Yesu alivifanya ambavyo sote tunaweza kuiga.

“1. Yesu “Alizunguka huko na huko, akitenda kazi njema” Matendo ya Mitume 10:38. Sote tunweza kufanya jambo zuri kila siku —kwa mwanafamilia, rafiki au hata mgeni —tukitafuta nafasi hizo.

“2. Yesu alikuwa Mchungaji Mwema aliyewachunga kondoo wake na kuwajali waliopotea. Tunaweza kutafuta walio pweke au wale wasioshiriki kikamiliku na kufanya urafiki nao.

“3. Yesu alikwa na huruma kwa wengi, hata maskini mwenye ukoma. Sisi pia tunaweza kuwa na huruma. Tunakumbushwa katika Kitabu cha Mormoni kuwa “kuomboleza na wale wanao-omboleza” [Mosia 18:9.]

“4. Yesu alishuhudia huduma yake ya kiungu na ya kazi kuu ya Baba Yake. Kwa sehemu yetu, sote tunaweza “kusimama kama mashahidi wa Mungu nyakati zote” Mosia 18:9 (Discipleship,” Ensign au Liahona, Nov. 2006, 21).

Gawanya wanafunzi katika majozi au vikundi vidogo alika kila jozi au kikundi kuandika njia mbili au tatu wanayoweza kuteke-leza mapendekezo manne ya Rais Faust katika maisha yao.

Baada ya wao kukamilisha, alika kila jozi au kikundi kushiriki wazo moja kwa zamu kutoka katika orodha zao. Ubaoni, andika mawazo yao ya jinsi tunavyoweza kufanya kazi za Mwokozi na kuwa zaidi kama Alivyo. Waalike wanafunzi kujitolea kimyaki-mya kufanya moja au mawili ya mawazo haya katika juma lijalo. Toa ushuhuda wako kuwa sote tunaweza kuwa kama Mwokozi tukiweka imani kwake.

Kitengo kifuatacho (4 Nefi 1–Mormoni 8)Wahimize wanafunzi kutafuta majibu ya maswali yafuatayo wa-naposoma kitengo kifuatacho: Watu wanawezaje kutoka kuwa wenye amani na ufanisi hadi kuwa waovu? Wanefi waliendaje kutoka kwa watu waliofanikiwa na wenye baraka kuliko wote waliowahi kuishi duniani hadi kuwa waovu kabisa? Ni yapi ma-neno ya mwisho ya Mormoni?

Page 513: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

498

UtangUlizi Wa

nefi nne: Kitabu cha nefiKwa nini kusoma kitabu hiki?Wanafunzi wanaposoma 4 Nefi, watajifu-nza kuhusu baraka zinazowajia watu walio-ungana katika kuishi injili ya Yesu Kristo. Kufuatia huduma ya Mwokozi miongoni mwa uzao wa Lehi, watu wote wa nchi waliongolewa. Walipotii amri, walifura-hia amani, ufanisi na baraka za ajabu za kiroho. Mormoni alitangaza, “kwa hakika hapawezi kuwa na watu wenye furaha zaidi miongoni mwa watu wote ambao wameumbwa kwa mkono wa Mungu”. (4 Nefi 1:16). Wanafunzi pia watajifunza masomo muhimu kutoka kwa kushuka ki-taratibu kwa watu hadi katika hali ya uovu.

Ni nani aliyeandika kitabu hiki?Mormoni alikusanya na kufupisha kumbu-kumbu za waandishi wanne ili kuunda kitabu cha 4 Nefi. Wa kwanza wa hawa alikuwa Nefi, ambaye kitabu kilipewa jina lake Nefi alikuwa mwana wa Nefi, aliyekuwa mmoja wa mitume kumi na wawili waliochaguliwa na Bwana wakati wa huduma Yake miongoni mwa uzao wa Lehi (angalia 3 Nefi 11:18–22; 12:1). Waandishi wengine watatu walikuwa wana wa Nefi, Amosi na wana wa Amosi, Amosi na Amaroni (angalia 4 Nefi 1:19, 21, 47).

Kitabu hiki kiliandikiwa nani na kwa nini?Mormoni hakuelekeza kitabu cha 4 Nefi kwa hadhara maalumu, na hakusema kwa nini alikiandika. Hata hivyo, kitabu hiki kinachangia katika madhumuni ya nia za uunganishi wa Kitabu cha

Mormoni— kushuhudia kuwa Yesu ndiye Kristo na kufanya maagano ya Bwana yajulikane. angalia ukurasa wa kwanza wa Kitabu cha Mormoni) Kinafanya hivyo kwa kudhihirisha baraka ambazo hutokea wa-kati watu wanapotubu. Kuja kwa Kristo na kufanya maagano naye. Kinaonyesha pia matokeo ya kuangamiza yanayotokea wakati watu wakimkana Mwokozi na injili Yake na kuacha maagano yao.

Kiliandikiwa wapi na lini?Kumbukumbu za asili zilitumika kama vya-nzo vya kitabu cha 4 Nefi zinaelekea kuwa ziliandikwa kati ya miaka 34 B.K na miaka 321 B.K. Mormoni alifupisha kumbuku-mbu hizo wakati fulani kati ya miaka 345 B.K na miaka 385 B.K Mormoni hakusema alipokuwa wakati alipotunga kitabu hiki.

Ni nini baadhi ya sifa bainifu za kutabu hiki?Katika aya 49 tu, kitabu cha 4 Nefi kina-simulia muda wa takribani miaka 300. karibu theluthi moja ya historia nzima ya Wanefi iliyojumlishwa katika Kitabu cha Mormoni. Ufupi wa 4 Nefi huchangia nguvu zake. Kinaangazia umuhimu dhahiri na tofauti kati ya utakatifu wa watu mara tu baada ya huduma ya Mwokozi kati yao na uovu wao vizazi vinne baadaye. Aya 18 za kwanza za kitabu hiki zinadhihirisha baraka zilizofurahiwa na jamii iliyojengwa kwenye injili ya Yesu Kristo. Aya za baa-daye zinatoa ushuhuda wa uangamizaji wa kiburi, zikionyesha jinsi jamii hii pole pole ilidhoofika hadi ilikawa karibu kume-zwa kabisa katika dhambi.

Muhtasari4 Nefi 1:1–18 Kufuatia huduma ya Yesu Kristo, watu wote katika nchi wanaongolewa na kuba-tizwa. Hawajigawi tena kati yao kama wanefi na Walamani “Vitu vyao vyote vilitumiwa kwa usawa miongoni mwao” (4 Nefi 1:3), walipata miujiza mingi, na kufanikiwa na kuishi kwa umoja na furaha kwa miaka 110.

4 Nefi 1:19–34 Nefi anafariki, na mwanawe Amosi anaweka kumbukumbu. Baadaye Amosi anamkabidhi kumbukumbu kwa mwanawe Amosi. Watu wengi wanamruhusu Shetani “kushikilia mioyo yao” (4 Nefi 1:28). Miga-wanyiko, kiburi, na makanisa ya uongo yanatokea kati ya watu. Waovu wanaanza kuwatesa washiriki wa Kanisa la Kweli na “wafuasi wa Yesu ambao wali-baki nao” (4 Nefi 1:30).

4 Nefi 1:35–49 Watu tena wanaji-gawa kama Wanefi na Walamani. Walamani kwa makusudi wanaasi dhidi ya injili na kuanzisha makundi ya siri ya Gadiantoni. Hatimaye, Wanefi pia wana-kuwa waovu. Amosi anafariki, na nduguye, Amaroni anaweka kumbukumbu kwa muda kabla ya kuhimizwa na Roho Mtakatifu kuzificha.

498

Page 514: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

499

Mapendekezo ya Kufundisha

4 Nefi 1:1–18Watu wote wanaongolewa na kupata amani na furahaKabla ya darasa, tayarisha vipande viwili vitupu vya karatasi kwa kila mwanafunzi ikiwe-zekana, kimoja cheupe na kingine cha rangi tofauti (nusu karatasi zitatosha) Weka karatasi nyeupe katika dawati za wanafunzi kabla ya wao kufika. Weka kando karatasi za rangi kwa matumizi ya baadaye katika somo hili. Andika swali hili ubaoni: Ni nini hukufanya kuwa na furaha ya kweli? Wanafunzi wanapowasili, waalike kuandika ubaoni majibu yao kwa swali hili.Anza darasa kwa kujadili majibu walioandika ubaoni. Waulize wanafunzi swali hili:• Ni tofauti gani iliyopo kati ya vitu vinavyotufanya kuwa na furaha kwa muda na vitu vina-

vyoelekeza kwenye furaha ya kudumu? (Wanafunzi wanapojibu, unaweza kutaka kusi-sitiza kuwa furaha ya kweli haiwezi kupatikana kwa vitu vya muda kama vile umaarufu, utajiri, au mali.)

Eleza kuwa 4 Nefi ni kumbukumbu za vizazi kadha vya uzao wa Lehi walioishi baada ya ujio wa Kristo. Waalike wanafunzi kusoma 4 Nefi 1:16 kimyakimya, wakitafuta jinsi Mormoni alivyoeleza kuhusu watu walioishi takribani miaka mia moja baada ya ujio wa Mwokozi. Unaweza kutaka kupendekeza kuwa wanafunzi waweke alama kishazi “kwa ha-kika hapengeweza kuwa na watu waliokuwa na furaha zaidi.” Waulize wanafunzi kuandika Hapangeweza kuwa na watu waliokuwa na furaha zaidi. Juu ya kipande cha karatasi nyeupe ulichowapatia. Kisha waulize wachore duara kubwa katikati ya karatasi zao.

Waambie wanafunzi wasome 4 Nefi 1:1–2, wakitafuta kile watu walichofanya ambacho kilifanya furaha hii kuwezekana. Waalike kuorodhesha walichopata ndani ya duara (Majibu yanapaswa kujumuisha kuwa watu walitubu, walibatizwa, walipokea Roho Mtakatifu na “wote wakaongolewa kwa Bwana” • Inamaanisha nini kuongolewa?Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa kuwa uongofu wa kina ni zaidi ya kuwa tu na ushuhuda au kuwa muumini wa Kanisa, alika mwanafunzi kusoma kwa sauti kauli ifuatayo ya Mzee Richard G. Scott wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili. Ikiwezekana, wapatie wanafunzi na-kala za kauli hii, na kuwahimiza kutambua maneno na vishazi ambavyo vinaeleza uongofu.

Husisha nadhari ya wanafunzi wanapowasiliTafuta njia za kuwasa-idia wanafunzi kuanza kufikiria kuhusu somo mara tu wanapoingia darasani. Unaweza ku-andika swali ubaoni, au unaweza kuonyesha kitu au picha. Hii inawasaidia wanafunzi kuzingatia nadhari yao na kutaya-risha akili na mioyo yao kujifunza.

hapangeweza kuwa na watu waliokuwa na furaha zaidi.

Watu walitubu, walibatizwa, walipokea

Roho Mtakatifu na “wote wakaongolewa

kwa bwana”

SOMO LA 136

4 nefi UtanguliziBaada ya huduma ya Kristo miongoni mwa uzao wa Lehi, watu walitumia mafunzo yake na kufura-hia zaidi ya miaka 100 ya umoja, ufanisi na furaha. Waliungana kama “wana wa Kristo” na hawakujiita tena Wanefi au Walamani (4 Nefi 1:17). Hata hivyo,

hatimaye walikuwa wenye kiburi na waovu zaidi, na walijigawanya kama Wanefi na Walamani. Karibu Mi-aka 300 baada ya ujio wa Mwokozi, karibu watu wote walikuwa wamekuwa waovu.

Page 515: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

500

SoMo la 136

“Furaha yako sasa na milele inategemea kiwango chako cha uongofu na yale mabadiliko yanayoletwa maishani mwako. Unawezaje basi kuongoka kikweli? Rais [Marion G.] Rom-ney alieleza hatua ambazo ni sharti ufuate :“Ushirika Kanisani na uongofu sio lazima viwe na maana sawa. Kuongolewa na kuwa na ushuhuda sio lazima viwe vitu sawa. Ushuhuda huja wakati Roho Mtakatifu anapompatia mtafutaji wa kweli ushahidi wa ukweli. Ushuhuda wa kusisimua huimarisha imani Yaani, inahimiza toba na utiifu kwa amri. Uongofu ni tunda au zawadi ya toba na utiifu” [Katika Taarifa ya Mkutano mkuu, Guatemala Area Conference 1977, 8–9.]“Ikielezwa kwa njia rahisi, uongofu wa kweli ni tunda la imani, toba, na utiifu wa kila mara. . . .“Uongofu wa kweli huzaa tunda la uvumilivu wa furaha ambao unaweza kufurahiwa hata wakati. Ulimwengu unakuwa katika misukosuko na wengi hawana chochote bali furaha.” (“Full Conversion Brings Happiness,” Ensign, May 2002, 25, 26).• Ni maneno gani na vishazi vipi ulivyosikia vinavyoelezea uongofu?• Unafikiri ingekuwaje kama kila mtu karibu nawe angekuwa mwongofu kwa Bwana?Andika marejeo yafuatayo ya maandiko ubaoni: 4 Nefi 1:2–3, 5, 7, 10–13, 15–18. Alika baadhi ya wanafunzi wasome kwa zamu kwa sauti kutoka aya hizi. Uliza darasa lifuatilie, likita-futa maneno na vishazi vinavyoelezea uzoefu watu walioupata kwa sababu wote walikuwa wameongoka kwa Bwana. Alika wanafunzi waandike maneno na vishazi kuzunguka duara katika karatasi zao. (Majibu yanaweza kujumuisha yafuatayo: hapakuwa na mabishano wala kutoelewana, walitendeana haki mmoja na mwingine, walitumia vitu vyote kwa umoja, miu-jiza mingi ilifanywa katika jina la Yesu Kristo, Bwana aliwafanikisha watu, walijenga upya miji ambayo ilikuwa imeangamizwa, walioa na kujenga familia, waliongezeka na kuwa imara, upendo wa Mungu ulikuwa mioyoni mwao, walikuwa wenye furaha na umoja.)Waalike wanafunzi watambue kanuni kuhusu furaha ambayo wamejifunza kutoka kwa nusu ya kwanza ya 4 Nephi 1. Ingawa wanafunzi wanaweza kutambua kanuni kadha, hakikisha kuwa wanaelezea kuwa watu wakifanya kazi pamoja ili kuongoka kwa Bwana, wanaunganishwa na kupata uzoefu wa ongezeko la furaha. Unaweza ku-taka kuandika kanuni hii ubaoni• Ni baraka zipi unazofikiria zingekuja kwa darasa letu kama sote tungeishi kama vile

watu hawa walivyoishi? Ni baraka gani unazofikiri zingekuja kwa familia yako? Ni ba-raka gani unazofikiri zingekuja kwa kata au tawi lako?

Alika wanafunzi kusimulia kuhusu wakati walipokuwa sehemu ya kikundi kilichoungani-shwa kwa haki, kama vile familia yao, jamii au darasa, au kikundi cha marafiki. Unaweza pia kushiriki uzoefu.• Bidii yako ya kuwa muadilifu inawezaje kuathiri furaha na wema wa waliokuzunguka.

(Hakikisha wanafunzi wanaelewa kuwa mazungumzo yetu na matendo matakatifu yanachangia, si tu kwa furaha yetu bali pia furaha na wema wa wengine. Wakati wana-familia, jamii, darasa au kikundi kingine wanaunganishwa katika haki wanaweza kupata uzoefu wa furaha kuu zaidi kuliko ambavyo wangepata wakiwa pekee yao.

• Dhambi za mtu mmoja zinawezaje kuathiri kikundi kizima kinachojaribu kuwa kitakatifu?Wahimize wanafunzi kuimarisha uongofu wao kwa Bwana na kuwasaidia wale walio karibu nao kufanya vivyo. Ili kuwasaidia wanafunzi na changamoto hii, waulize kutathmini maneno na vishazi walivyoorodhesha katika karatasi zao. Waalike kuchagua kishazi kimoja au viwili vinavyoeleza njia za kuishi ambazo wangependa kupata uzoefu. Wapatie dakika chache kuandika katika daftari zao au shajara zao za kujifunza maandiko kuhusu jinsi wanavyoweza kutafuta kuishi katika njia hizi. Shuhudia kuhusu upendo unaokuja kutoka kwa uongofu wa kweli na kuungana katika haki.

4 Nephi 1:19–49Wanefi wazidi kuwa waovu hadi wakabakia watu wachache tu wenye haki• Unafikiria ni kitu ngani kingeweza kuangamiza jamii kama ile inayoelezewa katika

4 Nefi 1:1–18?Acha wanafunzi wasome 4 Nefi 1:20, 23–24 kimya wakitafuta kile kilichohatarisha umoja na furaha ya watu. Unaweza kupendekeza kuwa waalamishe wanachokipata. Baada ya kutoa taarifa ya kile walichopata, andika ubaoni kauli ifuatayo ya Rais Henry B. Eyring

Page 516: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

501

4 nefi

wa Urais wa Kwanza. (Kauli hii inapatikana katika “Mioyo Yetu Kufumwa kuwa Mmoja,” Ensign or Liahona, Nov. 2008, 70.) Unaweza kutaka kupendekeza kuwa wanafunzi wanakili kauli hii katika maandiko yao karibu na 4 Nefi 1:24.

“Kiburi ni adui mkubwa wa umoja” (Rais Henry B. Eyring).• Ni kwa njia gani unafikiri kiburi ni adui wa umoja?Alika mwanafunzi kusoma kwa sauti kauli hii ya Rais Dieter F. Uchtdorf wa Urais wa Kwa-nza. Uliza darasa lisikilize jinsi kiburi kinavyoweza kuangamiza umoja.

“Katika kitovu chake, kiburi ni dhambi ya kulinganisha, kwani ingawa kwa kawaida kinaanza na “Tazama jinsi nilivyo bora na vitu vikuu nilivyofanya, kila mara huonekana kuishia “kwa hivyo mimi ni bora kuliko wewe”.“Wakati mioyo yetu imejawa na kiburi, tunatenda dhambi mbaya kwani tunavunja amri kuu mbili za Mungu. [ona Mathayo 22:36–40]. Badala ya kumwabudu Mungu na kumpenda jirani yetu, tunafunua lengo la kweli la

ibada yetu na upendo —picha tunayoiona katika kioo.” (“Kiburi na Ukuhani,” Ensign au Liahona, Nov. 2010, 56).• Kulingana na kauli ya Rais Uchtdorf, kiburi kinawezaje kuangamiza umoja?Waalike wanafunzi wachache kuchukua zamu kusoma kutoka kwa 4 Nefi 1:24–35, 38–45. Waulize darasa wafuatilie wakitafuta athari za kiburi kati ya watu. Unaweza kutaka kupe-ndekeza kwamba wanafunzi waweke alama walichokipata. (Majibu yanaweza kujumuisha yafuatayo: kuvaa mavazi ghali, kugawanyika katika matabaka, au vikundi vya kipekee vya marafiki, kujenga makanisa ili kufaidika, kukataa kanisa la kweli, kuwatesa waumini, kuu-nda vikundi vya siri, na uovu.)Mmoja bada ya mwingine, muulize kila mwanafunzi atoe taarifa ya kitu kimoja mvulana au msichana alichopata. (Wanafunzi wanaweza kurudia majibu ya wengine) Kila mwana-funzi anapojibu, andika majibu yake kwenye karatasi iliyotiwa rangi ambayo uliweka ka-ndo kabla ya darasa. Mpe manafunzi karatasi iliyotiwa rangi kwa kubadilisha na ile nyeupe inayoeleza furaha na umoja wa watu. Rudia mchakato huu hadi wanafunzi wote darasani wabadilishane karatasi zao nyeupe kwa zilizotiwa rangi.Waulize wanafunzi kuangalia na kuhakikisha kuwa kila mmoja darasani ana karatasi yenye rangi inayoashiria kiburi. Waalike watafakari jinsi wafuasi watatu wa Yesu walivyohisi wali-poona kiburi na uovu ukienea kati ya watu ambao kwa wakati mmoja walikuwa na furaha sana na kuungana.• Ni kweli gani tunayoweza kujifunza kutoka kwa aya hizi? (Ingawa wanafunzi wana-

weza kutumia maneno tofauti, wanapaswa kutambua kanuni ifuatayo; Dhambi ya kiburi huleta mgawanyiko na huongoza hadi kwenye uovu. Unaweza kutaka kuandika ukweli huu ubaoni.)

• Kiburi cha watu wachache kinawezaje kuathiri furaha ya kikundi kizima?Waalike wanafunzi kufikiria jinsi kiburi cha mtu mmoja kinavyoweza kuwaathiri wengine katika mifano ifuatayo. 1. Licha ya kuhimizwa na familia yake, kaka mkubwa anaamua kufuata haja za uchoyo

kuliko kutumikia misheni. 2. Mshiriki wa darasa la Wasichana au jamii ya Ukuhani wa Haruni anakuwa msumbufu

kimakusudi, anakataa kushiriki darasani na anapinga kufuata maelekezo. 3. Kijana au msichana anaendelea kumchokoza au kumdharau mshiriki mwingine wa

kikundi chake cha marafiki.Waulize wanafunzi kufikiria nyakati ambapo wameona kiburi kikiharibu furaha na umoja.Waalike wanafunzi kufikiria majukumu yao katika vikundi vyao tofauti kama vile familia zao, jamii au darasa, kata au matawi na darasa la seminari. (Unaweza kutaka kutaja viku-ndi vingine ambavyo wanafunzi wako ni washiriki.) Waulize kufikiria ikiwa wamefanya au wanafanya kitu chochote kinachodhihirisha kiburi katika mahusiano yao na watu wengine katika vikundi hivi. Wahimize kutubu na kufikiria njia ambazo wanaweza kushinda kiburi na kujenga umoja na haki katika vikundi hivi. Pia wahimize kutafakari kile walichoandika kuhusu jinsi wanavyopanga kuishi zaidi ya vile uzao wa lehi ulioongolewa kwa Bwana.Shuhudia kuwa tunapotafuta kuongoka zaidi kwa Yesu Kristo na kuishi na wengine kwa umoja, tunaweza kupata furaha kama ile iliyoelezwa katika 4 Nefi 1:1–18.

Page 517: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

502

UtangUlizi Wa

Kitabu cha MormoniKwa nini kujifunza kitabu hiki?Wanafunzi wanapojifunza kitabu hiki, watajifunza masomo ya thamani kutoka kwa Mormoni, mfuasi wa Yesu Kristo aliyeishi kwa uaminifu licha ya kuzungu-kwa maisha yake yote na “mfululizo wa muonekano wa uovu na machukizo” (Mormoni 2:18). Wanafunzi pia watafa-idika kwa kusoma maneno ya Moroni, ambaye alishuhudia kwa wasomaji wa siku za mwisho kwamba “Yesu Kristo amewaonesha nyinyi kwangu, na ninajua yale mnayofanya” (Mormoni 8:35). Wa-nafunzi wanaposoma kuhusu angamizo ambalo lilikuja kama matokeo ya uovu wa Wanefi watajifunza umuhimu wa kuishi kufuatana na Amri na maagano ya injili ya Yesu Kristo.

Ni nani alikiandika kitabu hiki? Mormon aliandika milango saba ya kwa-nza kama maelezo mafupi ya uovu na vita kati ya Wanefi na Walamani katika siku yake. Alifanya maelezo kamili ya matukio kutoka kwa maisha yake katika mabamba makubwa ya Nefi (ona Mormoni 2:18; 5:9). Wakati Mormoni alipokuwa na umri wa miaka 10, Amaroni mweka kumbuku-mbu alimpatia jukumu la kutunza kumbu-kumbu takatifu umri ulipotimia. Alikuwa aandike kila kitu alichoona kuhusu watu (angalia Mormoni 1:4). Katika umri wa miaka 15, Mormoni “alitembelewa na Bwana, na kuonja na kujua uzuri wa Yesu.(Mormon 1:15). Katika mwaka huo huo Nefi alimteua Mormoni kuongoza majeshi yao (angalia Mormoni 2:1). Kwa utiifu wa ushauri wa Amaroni, baadaye alipata mabamba makubwa ya Nefi na kuanza kutengeneza kumbukumbu yake. Pia alifupisha mabamba makubwa ya Nefi; ambayo yalijumuisha maandishi kutoka kwa manabii na waweka kumbukumbu kutoka kwa Lehi hadi kwa Amaroni na akaingiza mabamba madogo ya Nefi katika ufupisho huo. Karibu na mwisho wa maisha yake, Mormoni aliweka rekodi zote katika mlima Kumorah, isipokuwa mabamba machache ambayo alimpatia mwanawe Moroni (ona Mormoni 6:6). Kisha aliwaongoza Wanefi katika vita vyao vya mwisho dhidi ya Walamani. Kabla Mormoni kufa, alimwagiza Moroni kukamilisha kumbukumbu yake. Moroni aliongeza maneno yanayounda milango. –9 ya kitabu hiki.

Kitabu hiki kiliandikwa nani na kwa niniMormoni aliwaandikia wayunani na washiriki wa nyumba ya Israeli katika siku za mwisho, akitamani “kushawishi kila mtu aishiye duniani atubu na ajitayarishe kusimama mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo.” (Mormoni 3:22). Moroni alipoma-liza kitabu cha babaye, yeye alilenga moja kwa moja kwa wale ambao wangesoma maneno yake. Aliwaonya juu ya matokeo ya dhambi zao na kuwaalika “mje kwa Bwana na mioyo yenu yote” (Mormoni 9:27).

Kiliandikwa wapi na lini?Mormoni inawezekana aliandika milango ya 1–7 ya kitabu hiki kati ya miaka 345 B.K na miaka 401 B.K (angalia Mormoni 2:15–17; 8:5–6). Alikamilisha maandishi yake baada ya vita vya mwisho kati ya Wanefi na Walamani katika Kumora miaka 385

B.K (angalia Mormoni 6:10–15; 7:1). Labda Moroni aliandika nyenzo iliyopo katika milango ya 8–9 kati ya miaka 401 B.K na miaka 421 B.K, alipokuwa kuwa anatanga “kwa usalama wa maisha [yake]” (angalia Mormoni 8:4–6; Moroni 1:1–3).

Ni zipi baadhi ya sifa bainifu za kitabu hiki?Kitabu hiki kinaeleza utimilifu wa unabii wa Nefi, Samweli Mlamani, na Yesu Kristo kuhusu kuangamizwa kwa Wanefi (angalia 1 Nefi 12:19; Alma 45:9–14; Helamani 13:8–10; 3 Nefi 27:32). Mor-moni anarejelea baadhi ya maandishi yake kama “maandishi yangu kuhusu kuanga-mizwa kwa watu wangu” (Mormon 6:1). Alionyesha kuwa kuanguka kwa Wanefi kulikuwa matokeo ya uovu wao (ona Mormoni 4:12; 6:15–18).

MuhtasariMormoni 1 Amaroni anamwamuru Mormoni kuweka kumbukumbu ya watu katika siku zake. Wanefi wawashinda Walamani vitani. Uovu wa watu waenea kote nchini, wafuasi watatu wanefi waacha kuhudumu miongoni mwa watu, na karama za Roho kwa jumla zina-ondoshwa. Hata hivyo, Mormoni “anatembelewa na Bwana”.

Mormoni 2–3 Wanefi wamteua Mor-moni kuongoza majeshi yao. Anawa-ongoza vitani dhidi ya Walamani kwa zaidi ya miaka 30. Licha ya maanga-mizo na mateso, Wanefi walikataa kutubu. Mormoni anarejesha maba-mba ya Nefi kutoka mlima uitwao Shimu na kuanza kumbukumbu yake. Baada ya ushindi mara kadha. Watu walianza kujigamba kwa nguvu zao na kuapa viapo vya kulipiza kizazi dhidi ya Walamani. Mormoni akataa kuwaongoza zaidi. Anaandika ili ku-washawishi watu wote katika siku za mwisho kutayarisha kusimama mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo.

Mormoni 4 Hawakuongozwa tena na Mormoni, majeshi ya Wanefi yaendelea kupigana dhidi ya Walamani. Maelfu katika pande

zote mbili wauawa. Uzao wa Lehi unakuwa muovu zaidi kuliko wakati mwingine wowote katika historia yako na Walamani waanza kuwaa-ngamiza kabisa Wanefi. Mormoni ahifadhi kumbukumbu zote za Wanefi na kuzihamisha kutoka kwa mlima uitwao Shimu hadi katika mlima uitwao Kumora.

Mormoni 5–7 Mormoni arejelea uamiri wa majeshi ya Wanefi ingawa anajua wangeangamizwa. Anatabiri kuhusu ujio wa Kitabu cha Mormoni. Anawakusanya Wanefi katika Ku-mora kwa vita vya mwisho dhidi ya Walamani. Baada ya vita, anaombo-leza kuangamizwa kwa watu wake. Mormoni anandika ili kuwashawishi uzao wa Walamani kuamini katika Yesu Kristo na kubatizwa.

Mormoni 8–9 Baada ya kifo cha Mor-moni, Moroni aendeleza kumbu-kumbu. Anatabiri kuhusu Kitabu cha Mormoni kikija kwa nguvu za Mungu katika siku ya kutoamini na uovu. Anashuhudia juu ya Yesu Kristo na kufundisha kuwa miujiza na ishara zinandamana na imani ka-tika Yeye. Anawausia wale wanao-soma maneno yake kuja kwa Bwana na kuokolewa.

Page 518: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

503

UtanguliziIngawa Mormoni alikua katika wakati wa uovu mkubwa alichagua kuwa mwaminifu. Kwa sababu ya uaminifu wake, aliambiwa kuwa angekabidhiwa ku-mbukumbu takatifu za watu baadaye maishani mwake. Katika umri wa miaka 15 “alitembelewa na Bwana. (Mormoni 1:15). Alitamani kuwasaidia Wanefi kutubu

lakini kwa sababu ya uasi wao wa makusudi, alika-nywa na Bwana kuwahubiria. Katika umri huu mdogo, aliteuliwa kuongoza jeshi la Wanefi. Kwa sababu wengi wa Wanefi walikuwa wamepoteza Roho Mtakatifu na karama zingine za Mungu, waliachwa kwa nguvu zao wakipigana na Walamani.

SOMO LA 4

Mormoni 1–2

Mapendekezo ya Kufundisha

Mormoni 1:1–5Mormoni anajua kuwa siku moja angekabidhiwa kumbukumbu takatifu za WanefiAndika swali lifuatalo ubaoni mbele ya darasa ili wanafunzi waweze kulifikiria wanapowa-sili: Je! Unahisi vipi watu wanapokuita wewe Mmormoni?Mwanzoni mwa darasa, waalike wanafunzi kujibu swali lililo ubaoni. Baada ya wao kujadili swali, mwambie mwanafunzi asome kauli ifuatayo ya Raisi Gordon B. Hinckley.

“Ingawa wakati mwingine mimi hujuta kuwa watu hawaliiti kanisa hili kwa jina lake sahihi, ninafurahi kuwa jina la utani wanalotumia ni mojawapo wa heshima kuu iliyofanywa na mtu wa sifa na kitabu kinachotoa ushuhuda usiolinganishwa kumhusu Mkombozi wa dunia.“Mtu yeyote ajaye kumjua mtu Mormoni, kupitia kwa kusoma na kuyatafa-kari maneno yake, mtu yeyote anayesoma dafina hii ya thamani ya historia

iliyokusanywa na kuhifadhiwa naye, atakuja kujua kuwa Mormoni si neno la dharau, bali linawakilisha wema mkuu— wema huo ulio wa Mungu.” (“Mormon Should Mean ‘More Good,’” Ensign, Nov. 1990, 52–53).Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa muktadha wa Mormoni 1–2, eleza kuwa miaka 320 baada ya Mwokozi kutokea kwa Wanefi, karibu kila mtu nchini alikuwa anaishi katika uovu. Kwa wakati huu, Amaroni, mtu mwenya haki ambae alikuwa amehudumu kama mtunza rekodi, “akilazimishwa na Roho Mtakatifu, alificha maandishi yote matakatifu” (angalia 4 Nefi 1:47–49). Karibu wakati huo, Amaroni alimtembelea mvulana wa umri wa miaka 10 aliye-itwa Mormoni na kumwelekeza kulingana na jukumu lake la siku za usoni la kumbukumbu.Waulize wanafunzi wasome Mormoni 1:2. kimya wakitafuta maneno na vishazi ambavyo Amaroni alitumia kumwelezea Mormoni. Waulize watoe taarifa waliyopata. Andika jina Mormoni ubaoni na kuorodhesha majibu yao chini yake. Unaweza kuhitaji kueleza kuwa neno enye busara humaanisha tulivu, makini na mwangalifu.• Unafikiri tunapaswa kuwa makini kuhusu nini? Majibu yanaweza kujumuisha kutu-

mia na kupokea sakramenti, mafunzo ya maandiko, usafi wa kimwili, kuzungumza na kushuhudia kuhusu Mwokozi.) Kwa nini tuwe makini kuhusu mambo haya?

Eleza kuwa mtu anaweza kuwa makini na huku akiwa na raha na kucheka. Hata hivyo, mtu aliye mtulivu anaelewa wakati wa kuwa na raha na wakati wa kuwa makini.• Unafikiri inamaanisha nini kuwa “mwepesi wa kuzingatia”?Kama sehemu ya mjadala huu mwalike mwanafunzi kusoma maelezo yafuatayo ya mzee David A. Bednar wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili.“Tunapokuwa wepesi wa kuzingatia, tunatazama mara au kuona na kutii. Vipengele hivi viwili —kuona na kutii—ni muhimu katika kuwa wepesi wa kuzingatia. Na nabii Mormoni ni mfano wa ajabu wa karama hii katika vitendo. . . .“. . . Karama ya kiroho ya kuwa wepesi wa kuzingatia ni muhimu sana kwetu katika dunia tunamoishi sasa na tutakamoishi. ” (“Quick to Observe,” Ensign, Dec. 2006, 34).

Page 519: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

504

SoMo la 4

• Je! Uwezo wa kuona upesi na kutii ushauri wa Bwana utatusaidia vipi?Waalike wanafunzi kuandika katika daftari zao au shajara zao za kujifunza maandiko kuhusu jambo ambalo wanapaswa kuchukulia kwa uzito zaidi, jambo ambalo wanapaswa kuwa makini na watulivu. Pia waulize kuorodhesha maelekezo kutoka kwa Bwana ili wa-weze kutii kwa wepesi zaidi. Wahimize kutafuta kuwa makini na wepesi wa kuzingatia.Alika mwanafunzi kusoma Mormoni 1:3–5 kwa sauti na omba darasa kutambua maele-kezo ya Amaroni kwa Mormoni.• Amaroni alimwuliza Mormoni kufanya nini?• Unafikiri ni kwa nini Mormoni alihitaji kuwa makini na mwepesi wa kuzingatia ili kuti-

miza majukumu haya?

Mormoni 1:6–19Kwa sababu ya uasi wa makusudi wa watu, Bwana anamkanya Mormoni asiwahubirieWaulize wanafunzi ikiwa wamewahi kupoteza kitu walichothamini au kitu cha thamani kimewahi kutwaliwa kutoka kwao. Waalike wanafunzi wachache kushiriki uzoefu huu.Fanya muhtasari Mormoni 1:6–12 kwa kueleza kuwa wakati Mormoni alipokuwa ujanani alishuhudia vita kadha kati ya Wanefi na Walamani. Pia alishuhudia kuenea kwa uovu miongoni mwa watu wote nchini.Eleza kuwa kwa sababu Wanefi walikuwa waovu sana, walipoteza karama za thamani kutoka kwa Bwana. Gawa darasa kwa nusu. Wape nusu moja kusoma Mormoni 1:13–14, 18. kimya wakitafuta karama ambazo Bwana alianza kuondoa kutoka kwa Wanefi. Wape ile nusu nyingine kusoma Mormoni 1:14, 16–17, 19, wakitafuta sababu ambazo Bwana aliondoa karama hizi kutoka kwa Wanefi. Waalike wanafunzi kutoka katika kila kikundi kushiriki walichopata pamoja na darasa.• Kulingana na Mormoni 1:13–14, ni nini kinachotokea wakati watu wakiasi na kuge-

uka kutoka kwa Bwana? (Wanafunzi wanaweza kutoa majibu tofauti. Fikiria kufupisha majibu yao kwa kuandika ukweli huu ubaoni: Wakati watu ni waovu na wasioamini, wanapoteza karama za kiroho walizopokea kutoka kwa Bwana na hawawezi ku-pokea ushawishi wa Roho Mtakatifu. )

Eleza kuwa Uasi wa Wanefi ulikuwa umekithiri. Hata hivyo, kanuni hii hutumika kwetu kibinafsi tunapokosa kutii amri za Mungu.• Ni zipi kati ya karama zilizoorodheshwa katika Mormoni 1:13–14, 18 ambazo zingekuwa

vigumu sana kwako kuzipoteza.Alika mwanafunzi asome Mormoni 1:15 kwa sauti. Uliza darasa kufuatilia wakitafuta kile Mormoni alikuwa anapata wakati wengi wa Wanefi walikuwa wakipoteza karama za Mu-ngu na ushawishi wa Roho Mtakatifu.• Kwa nini unafikiri Mormoni aliweza kuwa na uzoefu wa kiroho ingawa alikuwa mio-

ngoni mwa uovu mwingi?

Mormoni 2:1–15Mormoni aongoza majeshi ya Wanefi na kuhuzunika kwa sababu ya uovu waoUliza mwanafunzi mwenye umri wa miaka 15 (au karibu na umri wa miaka 15) kusoma Mormoni 2:1–2 kwa sauti. Litake darasa kutafuta majukumu ambayo Mormoni alipewa ali-pokuwa na umri wa miaka 15 (katika mwaka wake wa “kumi na sita”). Waulize wanafunzi kufikiria jinsi ingekuwa kwa mwenye umri wa miaka 15 kuongoza jeshi.• Ni kwa njia gani sifa zilizotajwa katika Mormoni 2:1 zimemsaidia Mormoni kama

kiongozi wa jeshi. Fanya muhtasari wa Mormoni 2:3–9 kwa kuwaambia wanafunzi kuwa Walamani walisha-mbulia majeshi ya Wanefi kwa nguvu hata Wanefi wakaogopa na kurudi nyuma. Walamani waliwafukuza kutoka sehemu moja hadi nyingine hadi Wanefi walipokusanyika mahali pamoja. Hatimaye, jeshi la Mormoni lilikinza Walamani na kuwafanya kutoroka.Waalike wanafunzi kusoma Mormoni 2:10–15 kimyakimya wakitafuta hali ya kiroho ya Wanefi baada ya vita hivi.

Page 520: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

505

MoRMoni 1–2

• Kwa nini Wanefi walikuwa wakihuzunika? (Ona Mormoni 2:10–13. Walihuzunika kwa sababu hawakuweza kutunza mali zao. Kwa maneno mengine, walihuzunika kwa sa-babu ya matokeo ya dhambi zao tu, si kwa sababu walijutia matendo yao.)

• Kulingana Mormoni 2:13–14, ni vipi Mormoni alijua kuwa huzuni ya watu haikuwa onyesho la toba ya kweli?

Ili kuwasaidia wanafunzi kuona tofauti kati ya “kuhuzunika hadi toba” na “kuhuzunika kwa walio laaniwa.” Andika yafuatayo ubaoni.

Wale wanaohuzunika hadi toba . . .Wale wanaohuzunika kwa ajili ya matokeo ya dhambi . . .

Waulize wanafunzi kurejea Mormoni 2:12–15, wakitafuta sifa za vikundi hivi viwili vya watu. Waalike kutoa taarifa ya walichogundua. Majibu yao yanapaswa kudhihirisha kweli hizi:Wale wanaohuzunika hadi toba wanatambua wema wa Mungu na huja kwa Kristo na mioyo minyenyekevu. Wale wanaohuzunika tu kwa sababu ya matokeo ya dhambi huendelea kumwasi Mungu.Eleza kuwa Mormoni alitumia kishazi “huzuni ya waliolaaniwa” (Mormoni 2:13) kueleza kuhuzunika kwa wale wanaoteseka kwa sababu ya matokeo ya matendo yao lakini hawako tayari kutubu. Mtazamo huu haungozi kwenye toba na amani. Unaongoza kwenye laana inayomaanisha kuwa mtu huyo aliacha kuendelea kukua kuelekea uzima wa milele.Waalike wanafunzi kutafakari jinsi wanavyofanya wanapogundua kuwa wamefanya dha-mbi. Wahimize kuja kwa Mwokozi na mioyo minyenyekevu ili wapate kusamehewa, wahisi amani na kupatanishwa na Mungu.

Mormoni 2:16–29Mormoni anapata mabamba na kuandika matukio ya uovu wa watu wakeFanya muhtasari wa Mormoni 2:16–18 kwa kueleza kuwa wakati mapigano na Wala-mani yalipoendelea, Mormoni alijikuta karibu na mlima uitwao Shimu, ambapo Amaroni alikuwa ameficha kumbukumbu za Wanefi. Aliyachukua mabamba ya Nefi na kuanza kuandika kile alichokiona miongoni mwa ya watu tangu wakati alipokuwa mtoto.Alika mwanafunzi asome Mormoni 2:18–38 kwa sauti. Litake darasa kufuatilia, wakitafuta maelezo ya Mormoni ya hali ya kiroho ya watu kati siku yake. Pia waulize kutafuta mao-nyesho yake ya kibinafsi ya matumaini• Mormoni alieleza vipi hali ya kiroho katika siku yake? (“Mandhari ya maendelezo ya

uovu na machukizo.”)• Kutokana na kile ulichojifunza kumhusu Mormoni, unafikiri angeweza kuwa na uhakika

kuwa “angeinuliwa siku ya mwisho?” (Unaweza kutaka kuwasaidia wanafunzi kuelewa kuwa wakati Mormoni alipozungunzia “kuinuliwa siku ya mwisho,” alimaanisha kufu-fuliwa na kuletwa katika uwepo wa Mungu ili kubaki naye milele.)

• Vipi mfano wa haki wa Mormoni ni wa msaada kwako. (Wanafunzi wanaweza kushiriki hisia tofauti) Majibu yao yanapaswa kuelezea kanuni ifuatayo: Tunaweza kuchagua kuishi kwa haki, hata katika jamii iliyo ovu. Unaweza kutaka kumwalika mwanafu-nzi kuandika kweli huu ubaoni)

• Ni lini uliwaona marafiki au wanafamilia wakisimama imara katika kutii mapenzi ya Mungu hata wakati wale walio wazunguka hawakufanya hivyo?

Wahimize wanafunzi kufikiria kuhusu sehemu maalumu ya maisha yao ambapo wanaweza kufanya zaidi kusimama kwa ajili ya kilicho haki. Waalike kuandika katika daftari zao au katika shajara za kujifunza maandiko jinsi wangependa kujibu wakati ujao wanapopata changamoto katika sehemu hiyo maalumu. Shuhudia kuwa, kama Mormoni, tunaweza kuchagua kuishi kwa haki na kwamba Bwana atatusaidia kusimama imara kwa ajili ya kile kilicho haki hata wakati wale walio tuzunguka hawafanyi hivyo.

Page 521: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

506

UtanguliziBaada ya kuchukua tena nchi zao kutoka kwa Wala-mani, Wanefi walijitayarisha tena kwa vita. Mormoni aliwasihi Wanefi watubu. Badala yake, walijidai katika nguvu zao na kuapa kulipiza kisasi kwa ndugu zao wa-liouawa. Kwa kuwa Bwana alikuwa amewakataza watu

wake kulipiza kisasi, Mormoni alikataa kuliongoza jeshi la Wanefi na wakashindwa. Wanefi walipozidi katika uovu, Mungu alimwaga hukumu zake juu yao na Wala-mani wakaanza kuwafagia kutoka duniani.

SOMO LA 138

Mormoni 3–4

Mapendekezo ya Kufundisha

Mormoni 3:1–8Bwana anawalinda Wanefi vitani na kuwapa nafasi ya kutubu, lakini walifanya mioyo yao kuwa migumuMbele ya darasa, andika swali lifuatalo ubaoni: Umewahi kuhisi kuwa Bwana alikuwa akija-ribu kupata nathari yako na kukuhimiza kubadilisha kitu fulani maishani mwako?Anza kwa kuwataka wanafunzi kushiriki majibu yao kwa swali lililo ubaoni. (Hakikisha kuwa hawahisi kushurutishwa kushiriki chochote kilicho cha kibinafsi au cha siri.) Una-weza pia kufikiria kushiriki uzoefu fulani.Eleza kwamba Bwana alitaka kushika nathari ya Wanefi ili waweze kubadilisha njia zao ovu. Hata hivyo Wanefi walifanya mioyo yao migumu na kushindwa kutambua kuwa Bwana alikuwa anawabariki katika vita vyao na Walamani. Baada ya Wanefi kufanya mka-taba na Walamani na wale wanyang'anyi wa Gadiantoni (angalia Mormoni 2:28), Bwana aliwalinda, akiwakubalia kuishi miaka 10 bila vurugu. Wakati wa miaka hiyo, Mormoni aliwasaidia Wanefi kujitayarisha kwa mapigano yaliyokuwa yakija (angalia Mormon 3:1).Alika mwanafunzi asome Mormoni 3:2–3 kwa sauti. Litake darasa kufuatilia, wakitafuta kile Bwana alichotaka Wanefi kufanya wakati wa amani ambayo Yeye alikuwa amewapa.• Ni ujumbe gani Bwana alimwamrisha Mormoni kuwapa Wanefi? Je! Wanefi walielewa

ujumbe huu? Wanefi walijibu vipi ujumbe huo?• Kulingana na Mormoni 3:3, kwa nini Bwana aliwahifadhi Wanefi katika vita vyao vya hivi

karibuni licha ya uovu wao?• Ni ukweli upi unaoweza kutambua kutoka kwa matendo ya Bwana na Wanefi yali-

yoandikwa katika Mormoni 3:2–3? (Wanafunzi waweza kutoa majibu tofauti. Fanya muhtasari wa majibu yao kwa kuandika ukweli ufuatao ubaoni: Bwana hutupa nafasi za kutosha kutubu dhambi zetu. Unaweza kutaka kupendekeza kuwa wanafunzi waa-ndike ukweli huu katika maandiko yao.)

Fanya muhtasari wa Mormoni 3:4–8 kwa kueleza kuwa Bwana aliwahifadhi Wanefi mara mbili vitani, licha ya uovu wao, na kutokuwa tayari kumgeukia. • Uhifadhi wa Bwana kwa Wanefi unakufundisha nini kuhusu sifa Zake? (Majibu yana-

weza kujumuisha kuwa Bwana ni mwenye huruma na subira)Eleza wazi kuwa Bwana hutupa sisi sote “nafasi ya kutubu” (Mormoni 3:3). Kisha waulize wanafunzi kwa kimya kutafakari maswali yafuatayo:• Je! Umekuwa tayari kutubu na kufanya mabadiliko ambayo Mungu anataka ufanye?

Kuna mabadiliko unayoweza kufanya sasa ili uwe yule mtu ambaye Mungu anataka uwe?Shuhudia wema na subira ya Bwana katika kutupa nafasi za kutubu. Waalike wanafunzi kutafuta nafasi na mialiko ya kufanya mabadiliko katika maisha yao na kuwahimiza kufa-nya mabadiliko haya upesi.

KutafakariNjia moja ya kuwasaidia wanafunzi kuzidisha ufahamu wao wa kile wanachojifunza ni kuwapa wakati darasani ya kutafakari. Ungeweza kuwaalika wanafunzi kwa kimya kufikiria jinsi kanuni fulani ilivyoathiri maisha yao na jinsi wana-vyoweza kuitumia. Wa-nafunzi wanapojifunza maandiko darasani na peke yao, Roho Mtakata-ifu kila mara atawafunu-lia ukweli kwao.

Page 522: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

507

MoRMoni 3– 4

Mormoni 3:9–22Wanefi wazidi katika uovu, na Mormoni anakataa kuyaongoza majeshi yaoEleza kuwa Wanefi hawakujibu mialiko ya Bwana ya kutubu lakini badala yake wa wakafa-nya mioyo yao kuwa migumu. Alika mwanafunzi asome Mormoni 3:9–10 kwa sauti. Omba darasa kufuatilia wakitafuta kile Wanefi walitenda katika kujibu ushindi wao mara nyingi kwa Walamani. (Unaweza kuhitaji kuwaambia wanafunzi neno lipiza kisasi katika aya ya. inamaanisha kutafuta kulipiza kisasi.)• Wanefi walijibu vipi kufuatia ushindi wao kwa Walamani?• Kwa nini ilikuwa makosa kwa Wanefi kujisifu kwa nguvu zao wenyewe? Huku kujisifu

kunaonyesha nini kuhusu uhusiano wao na Mungu?Alika mwanafunzi asome Mormoni 3:11–13 kwa sauti. Litake darasa kutafuta majibu ya Mormoni wakati Wanefi walipoapa kulipiza kisasi.• Mormoni alifanya nini wakati Wanefi walipoeleza ari ya kulipiza kisasi kwa Walamani?• Umewahi kutaka kutafuta kulipiza kisasi kwa mtu fulani? Kwa nini unafikiri kutafuta

kulipiza kisasi ni jawabu la asili kwa watu wengi?• Mormoni alikuwa akiongoza majeshi ya Wanefi kwa zaidi ya miaka 30 licha ya uovu

wao. Kukataa kwa Mormoni kuongoza majeshi kunafundisha nini kuhusu uzito wa maana ya kutafuta kulipiza kisasi?

Alike mwanafunzi asome Mormoni 3:14–16, na kuhimiza darasa kutafuta kile Bwana alifu-ndisha Mormoni kuhusu kutafuta kulipiza kisasi. • Bwana anahisi vipi kuhusu kulipiza kisasi? (Majibu ya wanafunzi yanaweza kuwa tofa-

uti. Fanya muhtasari wa majibu yao kwa kuandika ukweli huu ubaoni: Bwana ameka-taza kutafuta kulipiza kisasi.)

Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa vyema ushauri wa Bwana katika aya 14–16, waulize wanafunzi kusema tena sehemu ya kwanza ya Mormoni 3:15 (“Kulipiza kisasi ni kwangu, na nitalipa”) katika maneno yao wenyewe.• Kwa nini ni muhimu kutotafuta kulipiza kisasi? Tunawezaje kushinda haja zetu za kuta-

futa kulipiza kisasi?Ili kuwasaidia wanafunzi kujifunza jinsi ya kushinda hisia za kulipiza kisasi, alike mwa-nafunzi kusoma kwa sauti ushauri ufuatao kutoka kwa Rais James E. Faust wa Urais wa Kwanza. Ikiwezekana, toa nakala ya dondoo kwa kila mwanafunzi.

“Tunahitaji kutambua na kukubali hisia za kukasirika. Itachukua unyenye-kevu kufanya hivi lakini tukipiga magoti na kumwomba Baba wa Mbi-nguni hisia za msamaha, atatusaidia. Bwana anatuhitaji “kuwasamehe watu wote” [M. M 64:10] kwa ajili ya wema wetu kwa sababu chuki hudumaza ukuaji wa kiroho” [Orson F. Whitney, Gospel Themes (1914), 144.] Ni pale tu tunapojiondolea chuki na machungu ndipo Bwana

anapoweza kuweka faraja mioyoni mwetu. . . .“. . . Maafa yanapotokea, hatupaswi kujibu kwa kutafuta kulipizia kisasi,lakini badala yake tuache haki ichukue mkondo wake na kisha tuache. Si rahisi kuachia na kuondoa mioyoni mwetu maudhi yanayochoma. Mwokozi ametupa sote amani yenye thamani kupitia kwa Upatanisho Wake, lakini hii inaweza kuja tu tunapokuwa radhi kutupa nje hisia za hasira, dharau au kulipiza kisasi.” (“The Healing Power of Forgiveness,” Ensign or Liahona, Mei 2007, 69).Alike mwanafunzi asome Mormoni 3:17, 20–22 kwa sauti, na agiza darasa kutafuta kile Mormoni alitaka tujue. Unaweza kutaka kuwaalika wanafunzi kuweka alama ushauri wa Mormoni wa “kutubu na kujitayarisha kusimama mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo.” (Mormoni 3:22).

Mormoni 4Walamani waanza kuwafagia Wanefi kutoka dunianiWaulize wanafunzi kuinua mikono yao ikiwa wanamjua mtu ambaye amefanya kitu kibaya lakini bado hajashikwa au kukumbana na matokeo ya kufanya makosa. Waalike wanafunzi kutafakari swali lifuatalo:

Page 523: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

508

SoMo la 138

• Je! Unashangaa wakati matokeo ya uchaguzi mbaya yatapompata mtu fulani ambae kwa kujua anachagua ubaya.

Waalike wanafunzi kusoma Mormoni 4:1–2 kimya, wakitafuta nini kilitokea kwa jeshi la Wanefi walipotafuta kulipiza kisasi kwa Walamani. Kisha waulize wanafunzi wasome Mormoni 4:4 kimya, wakitafuta kwa nini jeshi la Wanefi halikufanikiwa. Waulize wanafunzi watoe taarifa walichopata.Mtake mwanafunzi asome Mormoni 4:5 kwa sauti. Alika darasa kufuatilia, wakitafuta kweli ambazo aya hii hufundisha kuhusu matokeo ya kudumu katika uovu. Wakati wanafunzi wakishirikiana walichopata, andika ubaoni ukweli ufuatao kutoka kwa Mormoni 4:5: “Hukumu za Mungu zitawashinda waovu." Unaweza kupendekeza kuwa wanafunzi waweke alama ukweli huu katika maandiko yao.Alika wanafunzi wasome Mormoni 4:10–12 kimya, wakitafuta maelezo ya uovu wa Wanefi. waulize wanafunzi kuto taarifa walichopata.Waalike wanafunzi wachache wasome kwa zamu kwa sauti kutoka kwa Mormoni 4:13–14, 18, 21–22. Litake darasa kufuatilia wakitafuta jinsi hukumu za Mungu zilivyomwagwa kwa Wanefi.• Kwako wewe, ni sehemu ipi iliyo ya huzuni zaidi katika hadithi hii?Rejesha mwanafunzi katika kanuni ulizoandika ubaoni. Waalike kutafakari jinsi wanavyo-weza kutumia kweli hizi katika maisha yao. Wahimize kutenda kulingana na ushawishi wa Roho Mtakatifu wanaoupokea wanapotafakari. Shuhudia wema na upendo wa Bwana katika kutupa nafasi za kutosha za kutubu. Pia shuhudia kuwa matokeo yatakuja kila mara kwa wale wanaodumu dhambini.

Tangazo na Habari za UsuliMormoni 3:9–10. Kuapa kiapo

Mormoni alisema Wanefi waliapa kwa mbingu, na pia kwa kiti cha enzi cha Mungu” kwamba wangelipiza kisasi kwa Walamani. (ona Mormoni 3:9–10). Kauli ifu-atayo ya Mzee Bruce R. McConkie wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili inaeleza umuhimu wa kuapa kiapo katika nyakati za Kitabu cha Mormoni, hivyo kutupa ufahamu wa hali ya kukufuru ya Wanefi ya kujaribu kumhusisha Mungu katika kulipiza kisasi kwao.

“Jambo hili la kuapa kiapo katika siku za zamani lilikuwa la muhimu sana kuliko jinsi wengi wetu wanavyotambua.

“Kwa mfano: Nefi na nduguze walikuwa wakitafuta mabamba ya shaba kutoka kwa Labani. Maisha yao yalikuwa hatarini. Hata hivyo Nefi aliapa kiapo hiki: “Kama Bwana aishivyo,. na tuishivyo sisi, hatutarudi kwa baba yetu nyikani mpaka tukamilishe kile kitu ambacho Bwana ametuamuru sisi.” (1 Ne. 3:15.)

“Hivyo Nefi alimfanya Mungu mwenzi wake. Kama angeshindwa kupata mabamba, ingemaanisha Mungu alikuwa ameshindwa. Na kwa sababu Mungu hashi-ndwi, Nefi alikua hana budi kuyapata mabamba au ku-poteza maisha yake katika jabirio hilo” (“The Doctrine of the Priesthood,” Ensign, May 1982, 33).

Page 524: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

509

UtanguliziMormoni alitabiri kuwa kumbukumbu yake ingekuja katika siku za mwisho ili kuwashawishi wale wanao-isoma kwamba Yesu ndiye Kristo. Aliwahimiza wale ambao wangesoma kumbukumbu kutubu na kujitaya-risha kwa ajili ya hukumu mbele za Mungu. Miongoni mwa watu wake, Mormoni alifikiria tena kujiu-zulu kwake kama amiri jeshi wa Wanefi, akikubali

kuwaongoza tena vitani. Hata hivyo watu walikataa kutubu, na walifukuzwa na Walamani hadi taifa lote la Wanefi likaangamizwa. Mormoni anapotazama mandhari haya ya kifo na maangamizo, aliomboleza kuanguka kwa watu wake na kutopendelea kwao kurudi kwa Yesu Kristo.

SOMO LA 139

Mormoni 5–6

Mapendekezo ya Kufundisha

Mormoni 5:1–9Mormoni anamua kuwaongoza Wanefi, lakini walamani wakashindaTaja tukio la kiasili ambalo linaweza kuwa tishio katika sehemu yako— kwa mfano, tetemeko la ardhi, tsunami, ufushi wa volkano au kimbunga. Waulize wanafunzi kufikiria kuwa wameonywa kuwa janga hili la kiasili litatokea katika jamii yao katika muda wa siku chache zijazo.• Utageukia wapi kwa ajili ya usaidizi?Wakumbushe wanafunzi kuwa Wanefi walikumbana na hali sawa ya hatari, lakini janga li-lilokuwa likija lilikuwa la kiroho. Pia wakumbushe wanafunzi kuwa Wanefi walikuwa vitani na kwa sababu ya uovu wao, Mormoni alikataa kuongoza jeshi lao (ona Mormoni 3:16).Alika mwanafunzi asome Mormoni 5:1–2 kwa sauti. Litake darasa kufuatilia na kutambua Wanefi waliamini nani angewakomboa kutokana na mateso yao.• Ingawa ni kweli kuwa Mormoni angeongoza majeshi ya Wanefi vitani, kwa nini Mor-

moni aliamini kuwa watu hawangekombolewa kutokana na mateso yao.• Tunaweza kujifunza nini kutoka kwa Mormoni 5:1–2 kuhusu tunakopaswa kwenda kwa-

nza kwa usaidizi katika mateso yetu. (Tunapaswa kumgeukia Mungu kwanza ambaye atawajibu wale wanaotubu na kumwita kwa usaidizi katika mateso yao.)

Fanya muhtasari wa Mormoni 5:3–7 kwa kuelezea kuwa chini ya uongozi wa Mormoni, Wanefi walikinza mawimbi machache ya mashambulizi ya Walamani. Lakini hatimaye Walamani “waliwakanyaga watu wa Wanefi chini ya miguu yao” (Mormoni 5:6). Wanefi walipokuwa wakirudi nyuma, wale ambao hawakukimbia haraka waliangamizwa.Alika mwanafunzi asome Mormoni 5:8–9. Litake darasa kutafuta sababu ya Mormoni ya kutoandika habari kamilifu ya vitu alivyoviona.• Kwa nini Mormoni alijizuia kutoa maelezo kamili ya yale aliyoyashuhudia?

Mormoni 5:10–24Mormoni anaeleza kuwa kusudi la kumbukumbu ya Kitabu cha Mormoni ni ku-washawishi watu kumwamini Yesu KristoAlika mwanafunzi asome Mormoni 5:10–38 kwa sauti. Litake darasa kufuatilia na ku-tambua neno ambalo Mormoni alilotumia mara tatu kueleza jinsi watu katika siku za mwisho wangehisi wanaposoma kuhusu kuanguka kwa taifa la Wanefi. (Alisema kwamba “tungehuzunika”)• Unapata nini cha kuhuzunisha zaidi katika hadithi hii?Vuta mawazo ya wanafunzi kwa kauli ya Mormoni katika Mormoni 5:11 kwamba kama watu wake wangelitubu “wangekumbatiwa katika mikono ya Yesu.”

Page 525: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

510

SoMo la 139

• Unafikiri inamaanisha nini “kukumbatiwa katika mikono ya Yesu”? (Unaweza kutaka kueleza kuwa neno kukumbatiwa linamaanisha kushikiliwa kwa karibu au kwa usalama au kuwekwa kifuani.)

• Kishazi hiki kinatufundisha sisi nini kuhusu matokeo ya toba yetu? (Wasaidie wanafunzi kutambua kanuni ifuatayo: kupitia toba tunaweza “kukumbatiwa katika mikono ya Yesu.” Andika kanuni hii ubaoni.)

Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa vyema kanuni hii, alika mmoja wao asome kauli ifuatayo ya Mzee Kent F. Richards wa wale Sabini“Wote wanaokuja wanaweza 'kukumbatiwa katika mikono ya Yesu.’ [Mormoni 5:11.] Roho zote zinaweza kuponywa na nguvu Zake. Uchungu wote unaweza kutulizwa. Katika Yeye, tunaweza “kupata pumziko kwenye mioyo [yetu].’ Mathayo 11:29.] Hali yetu ya maisha ya muda huenda isibadilike mara moja, lakini uchungu wetu, hofu, mateso na uoga unaweza kumezwa katika amani Yake na mafuta ya zeri.”("The Atonement Covers All Pain,” Ensign or Liahona, Mei 2011, 16).Waalike wanafunzi kuandika jibu kwa mojawapo ya maswali yafuatayo katika daftari au shajara za kujifunza maandiko. (Unaweza kutaka kuandika maswali haya ubaoni au uya-some pole pole ili wanafunzi waweze kuyaandika.)• Ni lini umehisi “kukumbatiwa katika mikono ya Yesu?”• Unaweza kufanya nini zaidi ili kupokea zaidi faraja, ulinzi na msamaha wa Bwana?Eleza kuwa Mormoni 5:12–13 ina utabiri wa Mormoni kuwa maandiko yake yangefichwa na kutolewa tena ili kusomwa na watu wote. Alika wanafunzi wasome Mormoni 5:14–15 kimya, wakitafuta kile Bwana alikusudia maandiko ya Mormoni kufanya kwa watu katika siku za mwisho. Unaweza kutaka kupendekeza kuwa wanafunzi waweke alama vishazi vilivyo muhimu kwao.• Kulingana na Mormoni 5:14–15, ni nini madhumuni ya Kitabu cha Mormoni? (Hakiki-

sha kuwa wanafunzi wanaeleza kuwa Kitabu cha Mormoni kiliandikwa ili kuwa-shawishi watu wote kuwa Yesu ndiye Kristo, kumsaidia Mungu kutimiza agano Lake na nyumba ya Israeli na kuwasaidia uzao wa Walamani kuamini injili kwa ukamilifu zaidi. )

Wanafunzi wanapojibu kuwa maandishi ya Mormoni yamekusudiwa kuwashawishi watu kuwa Yesu ndiye Kristo, toa ushuhuda wako kuhusiana na hili kama kusudi kuu la Kitabu cha Mormoni.• Ni kwa njia gani kusudi hili kuu la Kitabu cha Mormoni huwabariki wale wanaokisoma?• Kujifunza kwako Kitabu cha Mormoni kumekusaidia vipi kuamini kwa ukamilifu zaidi

na kumpenda Yesu Kristo?Eleza kuwa Kitabu cha Mormoni kwa sasa kinawasaidia wengi kutubu na “kukumba-tiwa katika mikono ya Yesu” lakini kwamba bado kuna watu wengi wanaokataa kuamini katika Kristo.Ubaoni, karibu na kanuni kuhusu toba uliyoandika hapo awali katika somo, andika yafua-tayo: Tukikataa kutubu . . . Alika mwanafunzi kusoma Mormoni 5:16–19 kwa sauti, na ku-uliza darasa kutafuta matokeo ya kukataa kutubu kwa Wanefi. Waulize wanafunzi kutumia kile walichogundua katika aya hizi ili kukamilisha sentensi ubaoni. Wanapojibu, unaweza kuuliza baadhi ya maswali haya ili kuwasaidia kuelewa maneno na vishazi katika aya hizi.• Unafikiri inamaanisha nini kuwa “bila Kristo na Mungu duniani”? (Mormoni 5:16).

(Majibu yanaweza kujumuisha kuwa inamaanisha kuishi bila imani katika Yesu Kristo wala Baba wa Mbinguni, na bila ushawishi na mwongozo wa kiungu.)

• Kapi ni ganda jepesi la juu ya nafaka. Wakati nafaka inapovunwa, kapi hutupwa. Unafikiri nini maana ya kishazi “kupeperushwa kama makapi yanavyopeperushwa na upepo? (Mor-moni 5:16).

• Ingekuwaje kuwa katika merikebu bila namna ya kusafiri au usukani na bila nanga? Angalia Mormoni 5:18.) Hali hii inafanana vipi na ile ya Wanefi?

• Maneno ya Mormoni yanatufundisha nini kuhusu wale wanaokataa kutubu? (Majibu ya wanafunzi yanapaswa kueleza kuwa kukataa kutubu kunasababisha kupotea kwa mwo-ngozo kutoka kwa Bwana. Kamilisha kauli iliyo ubaoni kwa kuandika ukweli ufuatao: Tukikataa kutubu, Roho ataondoka na tutapoteza mwongozo wa Bwana.)

Page 526: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

511

MoRMoni 5 – 6

Waulize wanafunzi kutafakari kimya kimya jinsi walivyoona kanuni hii maishani mwao au maishani mwa wengine.Waalike wanafunzi kurejea kwa haraka Mormoni 5:11, 16–18 na zile kanuni mbili ulizoa-ndika ubaoni.• Kwa maneno yako mwenyewe, ungeelezaje tofauti kati ya matokeo ya kutubu kwa dhati

na matokeo ya kukataa kutubu?Alika wanafunzi wasome Mormoni 5:22–24 kimya, wakitafuta kile Mormoni aliwausia watu wafanye katika siku za mwisho. Unaweza kutaka kupendekeza kuwa wanafunzi waweke alama kile wanachopata. Shuhudia ukweli wa hizi kanuni mbili zinazotofautiana ubaoni.

Mormon 6Mormoni anakumbuka vita vya mwisho vya Wanefi na kuomboleza kuangamizwa kwa watu wakeUliza maswali yafuatayo:• Unaweza kuhisi vipi katika kifo cha mpendwa wako aliyekuwa mwaminifu kwa Mungu

katika maisha yake yote?• Unaweza kuhisi vipi katika kifo cha mpendwa wako ambaye si mtiifu kwa amri za Mu-

ngu katika maisha yake yote? Eleza kuwa Mormoni alihisi huzuni mwingi kwa vifo vya watu wake wote kwa sababu alijua hawakuwa tayari kukutana na Mungu. Fanya muhtasari Mormoni 6:1–6 kwa kueleza kuwa Walamani waliwaruhusu Wanefi kukusanyika katika nchi ya Kumora kwa vita. Mormoni alikuwa anazeeka na alijua hii ingekuwa “juhudi ya mwisho ya watu [wake]” (Mormoni 6:6). Alikabidhi kumbukumbu chache kwa mwanawe Moroni, na alificha kumbukumbu zilizosalia katika Mlima Kumora. Aliandika kile alichoshuhudia kuhusu kuangamizwa kwa mwisho kwa watu wake. Waulize wanafunzi wasome Mormoni 6:7–15 kimya, wakitafakari kuhusu jinsi Mormoni alivyojiona wakati alipoandika maneno haya. • Kwa nini unafikiri Wanefi walingojea kifo kwa “uoga wa kutisha”? (Mormoni 6:7).Soma Mormoni 6:16–22 kwa sauti kwa wanafunzi wanapofuatilia katika maandiko yao. Ki-sha waulize waandike katika daftari au shajara za kujifunza maandiko kuhusu mawazo na hisia zilizowajia waliposoma na kusikiliza aya hizi. Baada ya muda wa kutosha, unaweza kuwapa nafasi ya kushiriki baadhi ya mawazo yao waliyoandika.Shuhudia kwa wanafunzi kuhusu upendo ambao Baba wa Mbinguni, Yesu Kristo, mana-bii, viongozi na wazazi wao wanao kwao. Wahimize kufanya imani katika Yesu Kristo na kutubu dhambi zao ili waweze “kukumbatiwa katika mikono ya Yesu” (Mormoni 5:11).

Tangazo na Habari za UsuliMormoni 5:11. “Kukumbatiwa katika mikono ya Yesu”

Mzee Russell M. Nelson wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alieleza kiunganishi kati ya neno Upatanisho na kishazi “kukumbatiwa katika mikono ya Yesu”

“Maana kuu inapatikana katika kujifunza kuhusu neno upatanisho katika lugha za Kisemiti za nyakati za Agano la Kale. Katika Kihebrania neno la kimsingi la upatanisho ni kaphar, kitenzi kinachomaanisha

‘kufunika’ au ‘kusamehe.’ Ikikaribiana na hili kwa karibu ni neno la Kiaramai na Kiarabu, kafat, ikimaani-sha ‘mkumbatio wa karibu’— bila shaka inakaribiiana na mkumbatio wa matambiko ya Kimisri. Marejeo kwa mkumbatio huo yanaonekana katika Kitabu cha Mor-moni. Moja inasema kuwa ‘Bwana ameikomboa nafsi yangu . . . ; nimeuona utukufu wake, na nimezingirwa milele katika mikono ya upendo wake.’ [2 Nefi 1:15 .] Lingine linatoa tumaini tukufu la sisi “kukumbatiwa katika mikono ya Yesu.’ [Mormoni 5:11.]” (“The Atone-ment,” Ensign, Nov. 1996, 34).

Page 527: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

512

UtanguliziBaada ya mapigano ya mwisho kati ya Wanefi na Wa-lamani, Mormoni aliandika kwa uzao wa siku za usoni wa watu wa Kitabu cha Mormoni kuhusu umuhimu wa kujua walikuwa ni nani na kile sharti wafanye ili kuokolewa. Kwa upendo mwingi kwa uzao wa maadui

zake, Mormoni alifundisha umuhimu wa kufuata injili ya Yesu Kristo ili iwe “vema [kwao] katika ile siku ya hukumu” (Mormoni 7:10). Kufuatia kifo cha Mormoni, mwanae Moroni aliachwa peke yake kuandika kuhusu maangamizo ya watu wake.

SOMO LA 140

Mormoni 7–8:11

Mapendekezo ya Kufundisha

Mormoni 7Katika ushuhuda wa mwisho wa Mormoni, anawausia uzao wa Walamani ku-mwamini Yesu Kristo na kufuata injili YakeAndika nambari 230,000 ubaoni. Waulize wanafunzi kama wanakumbuka nambari hii inahusiana na maangamizo ya Wanefi. (Ni nambari ya askari wa Wanefi waliokufa katika mapigano ya mwisho, yaliyoandikwa katika Mormoni 6. Unaweza kutaka kutilia mkazo kuwa nambari katika Mormoni 6:10–15 inaonekana ni kwa wale tu waliopigana vitani, si kwa wale wengi waliokufa kutokana na matokeo ya vita. Acha wanafunzi kufikiria kama wangenusurika na vita vikuu ambayo wanafamilia wao na marafiki wameuawa na taifa lao limetekwa. Wape muda watafakari nini wangeweza kusema kama wangeandika ujumbe kwa uzao wa watu waliowaua wapendwa wao na kuteka taifa lao. Waalike wanafunzi kusoma Mormoni 7:1–4 kimya kimya, wakitafuta baadhi ya maneno ya mwisho ya Mormoni kwa uzao wa Walamani. • Mormoni alitaka uzao wa Walamani kujua nini?• Ni sifa zipi za Mwokozi unazoziona katika maneno ya Mormoni kwa maadui zake? Wasaidie wanafunzi kuelewa kuwa Mormoni alifundisha uzao wa Lamani kile walihitaji kujua ili kuokolewa. Alikuwa na hisani kwa watu wote, hata maadui zake. Waulize wanafunzi kusoma Mormoni 7:5, 8, 10 kimya kimya wakitambua nini Mormoni aliwafundisha wasomaji wake kuwa ni sharti wafanye. Waulize wanafunzi kushiriki wali-chopata, na kuorodhesha majibu yao ubaoni. Unaweza kutaka kutaja kuwa mafundisho ya Mormoni ni sawa na kanuni za injili ambazo zingewaokoa Wanefi kutoka kwa Maanga-mizo (ona Mormoni 3:2).Alika mwanafunzi asome Mormoni 7:6–7 kwa sauti. Litake darasa kufuatilia wakitafuta kile Bwana anawapa wale wote wanaomwamini Yeye na kukubali injili Yake. Baada ya wanafunzi kutoa taarifa za kile walichopata, wahimize kuandika ukweli ufuatao karibu na Mormoni 7:6–7: Bwana anatoa wokovu kwa wote na atawakomboa wale wanaoku-bali kanuni na maagano ya injili Yake.Andika swali lifuatalo kwenye ubao: Waalike wanafunzi kuandika majibu yao kwa swali katika daftari au shajara za kujifunza maandiko.

Kulingana na Mormoni 7:7, ni baraka gani zitakazokuwa kwa wale ambao watapatikana “bila hatia” mbele za Mungu?

Waalike wanafunzi wachache kushiriki wanachoandika.

Mormoni 8:1–11Baada ya Mormoni kufa, mwanawe, Moroni anabaki peke yake kuandika kuhusu kuangamizwa kwa watu wakeWaulize wanafunzi kufikiri wakati ambapo walikuwa peke yao katika hali fulani iliyoleta changamoto katika imani zao— pengine hali ambapo wangefanya kitendo kiovu kwa

Page 528: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

513

MoRMoni 7– 8:11

urahisi bila yeyote kuwaona. Waalike wafikiri kama uamuzi wao kumfuata Mwokozi na kutii amri Zake wakati huo uliongezeka, ulibaki sawa au ulipungua• Kwa nini baadhi ya watu wanaweza kuchagua kubaki waaminifu wakiwa peke yao

katika hali ambayo inatia changamoto imani yao?• Kwa nini watu wengine wanaweza kuchagua kubaki waaminifu katika hali kama hiyo?Eleza kuwa Mormoni aliuawa baada ya mapigano ya mwisho kati ya Wanefi na Walamani na mwanawe Moroni aliachwa pekee yake bila wanafamilia wowote au watu wake. Alika mwanafunzi asome kwa sauti maneno ya Moroni katika Mormoni 8:1–9 na litake darasa kutafuta maelezo ya hali ya Moroni. Waulize watoe taarifa kuhusu kile walichopata.• Unafikiri unaweza kuhisi vipi kama ungekuwa katika hali ya Moroni?Ukitumia tarehe chini ya kurasa au katika muhtasari wa milango, wasaidie wanafunzi ku-ona kuwa karibu miaka 16 ilipita kati ya maneno ya mwisho yaliyoandikwa ya Moroni na wakati Moroni alipoanza kuandika katika mabamba. Kisha waalike wanafunzi kuangalia tena Mormoni 8:1–4 kuona kile Moroni alikuwa ameamua kufanya, hata ingawa alikuwa peke yake kwa muda mrefu sana. Waulize kuripoti walichopata (Wanapaswa kuona kuwa alikuwa ameamua kumtii baba yake na kuandika kwenye mabamba)• Ni kanuni gani tunayojifunza kutokana na utiifu wa Moroni licha ya hali yake? (Wanafu-

nzi wanaposhiriki mawazo yao, himiza ukweli huu: Hata wakati tukiwa peke yetu, tu-naweza kuchagua kuwa waaminifu. Unaweza kutaka kuwaalika wanafunzi kuandika ukweli huu katika maandiko yao karibu na Mormoni 8:1–4.)

Eleza kuwa Moroni alikuwa na misheni ya kipekee. Yeye “alibakia peke yake ili kuandika hadithi ya huzuni ya maangamizo ya watu wake.” (Mormoni 8:3). Ingawa wanafunzi hawatakumbana na hali hizo hasa, wanaweza kukumbana na hali ambazo watakuwa peke yao na watahitaji kubaki waaminifu. Pia wanaweza kukabiliwa na hali ambapo wanahisi wapo peke yao hata wakiwa na watu wengine kama vile nyakati wanapokuwa na watu wasioishi viwango vilivyowekwa na Bwana na manabii Wake. • Unamjua nani ambaye amekuwa mwaminifu hata wakati ambapo amekuwa peke yake

katika hali ya changamoto?Wanafunzi wanapojibu swali hili, uliza baadhi au yote ya haya maswali ya kufuatilia:• Mtu huyu alifanyaje katika hali hizo? • Mtu huyu hatimaye alibarikiwa vipi kwa kufanya kile Mungu alikuwa amemwamrisha

kufanya?• Mifano hii inakusaidia vipi?Waalike wanafunzi kusoma Mormoni 8:10–11 kimya. Waulize kutambua njia moja ambapo Bwana aliwahifadhi Moroni na Mormoni kwa wakati uliokuwa mgumu wali-okumbana nao. (Bwana aliwatuma Wanefi Watatu kuwahudumia Mormoni na Moroni; angalia pia 3 Nefi 28:25–26.) Sisitiza kuwa tukiwa waaminifu kwa Mungu katika hali ya upweke au ngumu, atatusaidia kubakia kuwa waaminifu. Tumia maswali yafuatayo kujadili ukweli huu:• Ni wakati gani umekuwa mtiifu kwa mojawapo ya amri za Baba wa Mbinguni hasa

katika hali iliyokuwa ngumu? Unahisi vipi kuwa ulibarikiwa kwa kufanya hivyo?• Kwa nini unafikiri ni muhimu kujitayarisha sasa kuwa waaminifu katika hali ngumu

katika siku za usoni?Ili kuwapa moyo wanafunzi kubakia waaminifu hata katika hali ambazo wanapaswa kusi-mama peke yao, shiriki kauli ifuatayo ya Rais Thomas S. Monson:

“Tunapoendelea na kuishi siku hadi siku, inakua haiepukiki kuwa imani yetu itajaribiwa. Tunaweza wakati mwingine kujikuta tumezungukwa na wengine ilhali tunasimama kati ya walio wachache au hata kusimama peke yetu kulingana na kile kinachokubalika na kisichokubalika. Je, tuna ujasiri wa kiadilifu kusimama imara kwa ajili ya imani yetu, hata kama kwa kufanya hivyo tunalazimika kusimama peke yetu? . . . Acha daima tuwe wajasiri na

tayari kusimama kwa ajili ya kile tunachoamini, na kama ni lazima tusimame peke yetu katika mchakato, na tufanye hivyo kwa ujasiri, tukiimarishwa na ufahamu kuwa kwa kweli kamwe hatuko peke yetu tunaposimama na Baba yetu wa mbinguni.” (“Dare to Stand Alone,” Ensign or Liahona, Nov. 2011, 60, 67).

Maswali ya kufuatiliaKuuliza maswali ya kufuatilia kwa majibu ya kwanza ya mwanafunzi kunaweza kuwasaidia kufikiria kwa undani kuhusu jibu walilotoa na kushiriki mawazo na hisia zenye maana. Una-weza kuuliza maswali ya kufuatilia kwa mwa-nafunzi aliyetoa jibu la awali, au unaweza kujenga mjadala kwa kupeleka maswali ya ku-fuatilia kwa wanafunzi wengine.

Page 529: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

514

SoMo la 140

Hitimisha kwa kuelezea uzoefu wa wakati Bwana alipokubariki kwa kuwa mwaminifu katika hali ya upweke au ngumu.

Rejeo la Umahiri wa MaandikoAndika sihi ubaoni. Eleza kuwa neno sihi linamaanisha kuwahimiza wengine kwa nguvu kutenda jambo kwa njia fulani. Eleza kwamba maneno ya mwisho ya Mormoni katika Mormoni. Ni mfano mzuri wa mahubiri. Wape vipande vya karatasi wanafunzi na ku-waambia wataandika mahubiri yenye msingi wa mojawapo wa vifungu vya umahiri wa maandiko wanavyopenda zaidi katika Kitabu cha Mormoni. Juu ya kipande cha karatasi acha wanafunzi waandike. “Nitanena kwa namna fulani na vijana wa siku za mwisho.” Alika kila mwanafunzi kuchagua vifungu vya umahiri wa maandiko anavyopenda sana kisha aandike mahubiri kwa vijana wa siku za mwisho kwa msingi ya vifungu walivyo-chagua. Mahubiri yao yanaweza kujumuisha muhtasari wa kweli muhimu zinazopatikana katika taarifa ya umahiri wa maandiko, elezo la kwa nini kweli hizi ni muhimu kwa vijana hivi leo, na mwaliko kutenda kulingana na kweli hizi. Mahubiri yanaweza kuhitimishwa na ahadi kama ile inayopatikana katika Mormoni 7:7 au Mormoni 7:10. Ungeweza kuwau-liza wanafunzi wachache kushiriki mahubiri yaliyo kamilika pamoja na darasa. Unaweza kutaka kukusanya mahubiri haya yatumike kama vidokezo kwa shughuli za umahiri wa maandiko za siku za usoni au kuyaonesha darasani.Chunga: Unaweza kutaka kutumia shughuli hii wakati wowote katika somo hilo. Kwa mfano, unaweza kuitumia katika mwisho wa somo au unaweza kutumia baada ya kuja-dili Mormoni 7.

Tangazo na Habari za UsuliMormoni 7. Ombi la mwisho la Mormoni la kuamini katika Kristo

Mzee Jeffrey R. Holland wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili alieleza kuhusu ombi la mwisho la Mormoni kuamini katika Kristo, ombi aliloandika kwa watu katika siku zetu baada ya kuona maangamizo ya taifa lake zima:

“Katika mazungumzo ya nafsi juu ya mauti, Mormoni alifikia wakati na upeo kwa wote, hasa kwa salio la nyumba ya Israeli” ambao siku moja wangesoma kumbukumbu yake tukufu. Wale walio wa wakati na upeo mwingine ni lazima wajifunze kile wale wanao-lala mbele zake walikuwa wamesahau— kuwa wote ni sharti “kuamini katika Yesu Kristo, kwamba yeye

ni mwana wa Mungu,” kwamba kufuatia kusulubiwa kwake Yerusalemu alikuwa na “uwezo wa Baba akafu-fuka tena, hivyo, kupata ushindi juu ya kaburi; na pia katika yeye uchungu wa mauti unamezwa.

“Na alitimiza ufufuo wa wafu [na] ukombozi wa ulimwengu.’ Wale waliokombolewa wanaweza basi, kwa sababu ya Kristo, kufurahia ‘hali ya furaha isiyo na mwisho.’ [Mormoni 7:2, 5–7.] . . .

“Kuamini katika Kristo,’ hasa kukipimwa dhidi ya mato-keo kama hayo yanayoweza kuepukika, lilikuwa ombi la mwisho la Mormoni na tumaini lake tu. Ni kusudi kuu la kitabu kizima ambacho kingekuja duniani katika siku za mwisho kikiwa na jina lake. (Kristo na agano jipya: Ujumbe wa kimasiya wa Kitabu cha mormoni [1997], 321–22).

Wazo la Ziada la KufundishiaMormoni 7:8–9. Biblia na Kitabu cha Mormoni

Onyesha nakala ya Kitabu cha Mormoni kilichobandi-kwa "hiki." Kisha onyesha nakala ya Biblia kilichoba-ndikwa “hicho” Waalike wanafunzi kusoma Mormoni 7:8–9 kimya kimya wakitafuta nini Mormoni alisema

kuhusu uhusiano kati ya “hiki”(Kitabu cha Mormoni) na “hicho” (Biblia).

• Kujifunza kwako Kitabu cha Mormoni kumeimarisha vipi ushuhuda wako wa kweli katika Biblia? Kujifu-nza kwako Biblia kumeimarisha vipi ushuhuda wako wa kweli katika Kitabu cha Mormoni ?

Page 530: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

515

Utangulizi wa SomoKatika somo hili, wanafunzi watarejea maangamizo ya Wanefi na kujifunza kuhusu hamu ya Mormoni kwa watu wake “kuku-mbatiwa katika mikono ya Yesu” (Mormoni 5:11). Wanafunzi watajifunza jinsi ya kualika kumbatio la Bwana maishani mwao. Kutokana na Wanefi kukataa kutubu, wanafunzi wataelewa matokeo ya huzuni watu wanapata wanapokataa kutubu.

Mapendekezo ya Kufundisha

4 Nefi 1–Mormoni 4Watu wa Wanefi wanaanguka kutoka katika haki na furaha hadi kwenye uovuWaulize wanafunzi kuhakikisha ni miaka mingapi ya historia ya Wanefi wamesoma wiki hii. Wasaidie kutumia tarehe katika muhtasari wa milango au chini ya kurasa katika 4 Nefi 1 na Mor-moni 8 ili kuelewa haya. (Milango hii inajumuisha karibu miaka 400 au zaidi ya thuluthi ya historia ya Wanefi.)

Litake nusu ya darasa kutumia maandiko yao na shajara zao za kujifunza maandiko kurejea kile walichojifunza kuhusu furaha ya Wanefi katika 4 Nefi 1. Acha ile nusu nyingine ya darasa kutumia Mormoni 1–2 na shajara zao za kujifunza maandiko ili kurejea Mormoni alikuwa nani na kwa nini alikuwa wa kupe-ndeza sana. Waulize kila kikundi kufupisha walichojifunza. Kisha alika vikundi kuonyesha muhtasari wao.

Waulize wanafunzi: Ni nini kweli moja umejifunza kutokana na kujifunza milango hii, na kwa nini ni muhimu kwako?

Eleza kuwa licha ya juhudi za Mormoni kuwasaidia Wanefi kiroho kujitayarisha kwa mapigano, walikataa kutubu na kum-geukia Bwana. Kutokana na uovu wao, waliachiwa nguvu zao wenyewe, na Walamani wakaanza kuwashinda nguvu (angalia Mormon 3–4).

Mormoni 5:8–24Mormoni anaeleza kuwa kumbukumbu ya Kitabu cha Mormoni iliandikwa ili kuwashawishi watu kuamini katika KristoWaulize wanafunzi kama wamewahi kuhisi huzuni kwa sababu ya mtu aliyepatwa na matokeo ya chaguo mbaya. Unaweza ku-shiriki mfano unaofaa (usio wa kuhukumu) wa huzuni ambayo umehisi kwa sababu ya mtu aliyepitia matokeo machungu kwa chaguo walilofanya. Eleza kwamba Mormoni aliandika kwa-mba watu katika siku za mwisho wangehuzunika wanaposoma kuhusu maangamizo ya Wanefi.

Waalike wanafunzi kusoma Mormoni 5:10–11 kimya wakitafuta kile Mormoni alisema kuwa Wanefi wangefurahia. Baada ya wanafunzi kujibu, uliza maswali yafuatayo:

• Unafikiri inamaanisha nini “kukumbatiwa katika mikono ya Yesu”? (Neno kumbatia linamaniisha kushikilia kwa nguvu,

Somo la Kujifunza Nyumbani4 Nefi 1–Mormoni 8:11 (Kitengo cha 28)

Vifaa vya Matayarisho kwa Mwalimu wa Mafunzo ya NyumbaniMuhtasari wa Masomo ya Kujifunza Nyumbani Kila SikuMuhtasari ufatao wa mafundisho na kanuni ambazo wanafu-nzi walijifunza waliposoma 4 Nefi 1–Mormoni 8:11 (kitengo cha 28) haikusudiwi kufundishwa kama sehemu ya somo lako. Somo unalofundisha linatilia mkazo baadhi tu ya mafu-ndisho haya na kanuni. Fuata ushawishi wa Roho Mtakatifu unapofikiria mahitaji ya wanafunzi wako.

Siku ya 1 (4 Nefi 1)Wanafunzi walipojifunza hali miongoni mwa Wanefi katika muda wa karibu miaka 200 baada ya ujio wa Mwokozi, wali-jifunza kuwa watu wanapofanya juhudi pamoja kuongolewa kwa Bwana, wanakuwa na umoja na kupata furaha iliyoo-ngezeka. Pia, walitambua kuwa kiburi hujenga utengano na hupelekea uovu mkubwa.

Siku ya 2 (Mormoni 1–2)Kutokana na mfano wa maisha ya haki ya Mormoni, wanafunzi walijifunza kuhusu sifa za kuwa makini na wepesi wa kuzinga-tia. Walijifunza kuwa tunaweza kuchagua kuishi kwa haki hata katika jamii iliyo na uovu. Kutokana na mfano wa uovu wa watu wa Wanefi, wanafunzi walikuja kuelewa kanuni ifuatayo: Uovu na kutoamini kunaondoa karama za Bwana na ushawishi wa Roho Mtakatifu. Ikiwa huzuni yetu kwa dhambi ni hadi toba, itatuongoza kuja kwa Kristo kwa moyo mnyenyekevu. Huzuni ambayo ni ya matokeo ya dhambi husababisha maangamizo (au kusitishwa katika maendeleo yetu kuelekea uzima wa milele).

Siku ya 3 (Mormoni 3–6)Waliposoma umilivu wa Bwana kwa Wanefi, wanafunzi walijifunza kuwa Bwana hutupa nafasi za kutosha za kutubu dhambi zetu. Hata hivyo, Wanefi walikataa kutubu na walitaka kutafuta kulipiza kisasi kwa Walamani. Kwa sababu Bwana hukataza kutafuta kulipiza kisasi, Mormoni alichagua kujiuzulu kutoka kuongoza majeshi ya Wanefi. Matokeo ya juhudi za Wanefi kutafuta kulipiza kisasi iliwawezesha wana-funzi kuelewa kuwa hukumu za Mungu zitawashinda waovu. Mormoni alishuhudia maangamizo yote ya watu wake na akaomboleza kuanguka kwao.

Siku ya 4 (Mormoni 7:1–8:11)Mormoni alikamilisha kumbukumbu yake akiwazungumzia uzao wa Walamani. Wanafunzi walijifunza kuwa Bwana hutoa ukombozi kwa wale wanaokubali kanuni na maagano ya injili Yake. Mormoni alikufa, na Moroni akaandika kuhusu hali ya maangamizo ya Wanefi. Kutokana na mfano wa Moroni, wanafunzi walijifunza kuwa hata wakiwa peke yao, wanaweza kuchagua kubakia waaminifu.

Page 531: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

516

SoMo la KUj ifUnza nyUMbani

au kwa usalama, au kukumbatia, ambalo ni ishara ya ulinzi na upendo.)

• Kulingana na Mormoni 5:11, tunaweza kufanya nini ili kupokea aina hii ya mkumbatio? (Kupitia toba tunaweza “kukumbatiwa katika mikono ya Yesu.” Andika kanuni hii ubaoni.)

Soma au ualike mwanafunzi kusoma kauli ifuatayo ua Mzee Kent F. Richards wa wale Sabini. Litake darasa kusikiliza kinacho-maanisha “kukumbatiwa katika mikono ya Yesu”

“Wote wanaokuja wanaweza 'kukumbatiwa katika mikono ya Yesu.' [Mormoni 5:11.] Roho zote zinaweza kuponywa na nguvu Zake. Uchungu wote unaweza kutulizwa. Katika Yeye, tunaweza “kupata pumziko la mioyo yetu.’ [Mathayo 11:29.] Hali yetu ya maisha ya muda huenda isibadilike mara moja, lakini uchungu wetu, hofu, matatizo na uoga yanaweza kumezwa katika amani Yake na mafuta ya zeri." ("The Atonement Covers All Pain,” Ensign au Liahona, May 2011, 16).

Waalike wanafunzi kufikiria kuhusu nyakati ambapo wamehisi “kukumbatiwa katika mikono ya Yesu” kama matokeo ya toba. Pia, waulize kutafakari watakachohitaji kufanya ili kukumbatiwa katika mikono Yake sasa. Shuhudia kuhusu matokeo ya toba katika kufariji na kulinda.

Ili kuelezea kanuni nyingine katika Mormoni 5, weka kizibo au kitu kingine cha kuelea katika beseni ya maji. Wafanye wanafu-nzi wawili au watatu kupuliza kuelekeza pande tofauti. Uliza ni ushawishi kiasi gani kizibo kilionao kuhusu pale kinaenda. Hi-miza wanafunzi, wanapoendelea kusoma, kuangalia kwa makini jinsi kizibo hiki kinavyoweza kuwa kama Wanefi.

Andika ubaoni: Tunapokataa kutubu . . . kisha alika mwanafunzi kusoma Mormoni 5:2, 16–19 kwa sauti huku darasa likitafuta matokeo ya kukataa kwa Wanefi kutubu. Waulize wanafunzi kutumia kile wanachopata katika aya hizi kukamilisha sentensi ubaoni. Wanapojibu, unaweza kuuliza baadhi ya maswali yafu-atayo ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa baadhi ya maneno na vishazi katika aya:

• Katika aya ya 16, unafikiri inamaanisha nini kuwa “bila Kristo na Mungu duniani”? (Kuishi bila imani katika Yesu Kristo wala Baba wa Mbinguni, na bila ushawishi na mwongozo wao.)

• Unafikiri inamaanisha nini “kupeperushwa kama pumba zitimuliwavyo mbele ya kibunga”? (Mormoni 5:16). (Unaweza

kutaka kueleza kuwa kapi ni unyasi na ganda la juu la nafaka linalopeperushwa na upepo wakati wa kupukuta.)

• Unafikiri ungehisi vipi kama ungelikuwa kwenye mashua isiyo na nanga baharini, bila tanga wala mwongozo? Hali hii inafa-nana vipi na hali ya Wanefi?

Eleza kuwa Mormoni 5 inafundisha kuwa tunapokataa ku-tubu, Roho hujionda na tunapoteza mwongozo kutoka kwa Bwana. Andika kanuni hii ubaoni ili kukamilisha kauli uliyokuwa umeanza kuandika hapo awali. Waulize wanafunzi kutafakari nyakati maishani mwao ambapo wanaweza kuwa wamepata juu kanuni hii.

Unaweza kutaka kufanya wanafunzi watofautishe kanuni mbili ulizoandika ubaoni kwa kuwauliza swali lifuatalo: kutokana na kweli mbili zilizoandikwa ubaoni, je, matokeo ya kutubu yanato-fautiana vipi na matokeo ya kukataa kutubu?

Waalike wanafunzi kusoma Mormoni 5:22–24 kimya, wakitafuta kile Mormoni ametualika sote kufanya ili tusiwe kama Wanefi wa wakati wake. Unaweza kutaka kuwahimiza wanafunzi ku-weka alama kile wanachopata.

Shuhudia ukweli wa kanuni mbili zilizoandikwa ubaoni.

Mormoni 6:1–8:11Baada ya kushuhudia maangamizo ya mwisho ya watu wake, Mormoni aliwaandikia uzao wa Walamani, kisha afa, akiacha mwanawe Moroni peke yakeWaalike wanafunzi kufanya muhtasari wa maangamizo ya mwisho ya Wanefi wakitumia mada ya milango ya Mormoni 6–8 kama inabidi .

Waalike wanafunzi kusoma kimya na kutafakari Mormoni 7:10, maneno ya mwisho ya Mormoni aliyoyaandika kablahajafa.

Kitengo Kifuatacho (Mormoni 8:12–Etheri 3)Moroni alizungumza na Yesu Kristo na akaonyeshwa siku yetu. Moroni alituonya dhidi ya nini? Ndugu ya Yaredi pia alikuwa na imani kuu. Alimwona Yesu na kunena naye ana kwa ana. Je! Kujua kwamba Moroni na Nduguye Yaredi walimwona na kuzu-ngumza na Kristo kunakusaidiaje kuamini maneno yao?

Page 532: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

517

UtanguliziBaada ya kuandika kuhusu maangamizo ya watu wake na kifo cha babake, Moroni alitabiri kuhusu ujio wa Ki-tabu cha Mormoni na akaonya kuhusu matokeo ya ku-kikataa. Moroni aliona kuwa kumbukumbu ya Wanefi ingekuja katika siku ya uovu mkubwa, wakati ambapo

wengi wangependa mali ya ulimwengu kuliko Mungu. Alishuhudia kuwa Kitabu cha Mormoni kingekuwa cha thamani kuu licha ya hali hatari za kiroho ambazo zingekuwepo siku za mwisho.

SOMO LA 141

Mormoni 8:12–41

Mapendekezo ya Kufundisha

Mormoni 8:12–32Moroni alitabiri kuhusu ujio wa Kitabu cha MormoniMbele ya darasa tayarisha onyesho la vitu au picha zinazoonyesha maendeleo ya kitekno-lojia. Mwanzoni mwa darasa, elekeza mawazo ya wanafunzi kwenye onyesho. Mwalike mwanfunzi asome kwa sauti kauli ifuatayo ya Rais Ezra Taft Benson.

“Ningependa kunena kuhusu mojawapo ya zawadi muhimu iliyotolewa kwa dunia katika nyakati za kisasa. Zawadi ninayofikiria ni ya muhimu zaidi kuliko uvumbuzi wowote uliotokea kutokana na mapinduzi ya kiviwanda na kitekno-lojia. Hii ni zawadi iliyo ya thamani kuu zaidi kwa binadamu hata kuliko maendeleo ya ajabu tuliyoona katika utabibu wa kisasa. Ni ya thamani kuu kwa wanadamu kuliko maendeleo ya kupaa au safari za angani Nazungumzia

Zawadi ya . . .” (“The Book of Mormon—Keystone of Our Religion,” Ensign, Nov. 1986, 4).• Ungependa kuwa na zawadi hii ambayo Rais Benson alizungumzia? Kwa nini?• Unafikiri zawadi hiyo itakuwa nini?Eleza kuwa Moroni alifundisha kuhusu hii karama. Waulize wanafunzi kusoma Mormoni 8:12 ili kutambua hii karama ni nini. Wasaidie wanafunzi kuelewa kuwa kishazi ”kumbu-kumbu hii” inamaanisha Kitabu cha Mormoni. Eleza kuwa Rais Benson alizungumzia karama ya Kitabu cha Mormoni.Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa thamani ya Kitabu cha Mormoni, waalike wasome Mor-moni 8:13–16 kimya kimya. Kabla ya wao kusoma, waagize kutafuta kile ambacho Moroni alifundisha kuhusu thamani ya Kitabu cha Mormoni. Kisha uliza baadhi au maswali yote yafuatao kuwasaidia kujadili na kuchanganua kile walichopata:• Watu wengine wanaweza kufikiri juu ya thamani ya kifedha ya mabamba ya dhahabu.

Kulingana na Mormoni 8:14, ni sifa ipi ya mabamba kwa kweli ilikuwa ya “thamani kuu”? (Wasaidie wanafunzi kuona kuwa kwa sababu Bwana hataruhusu yeyote “kupata faida” kutokana na mabamba ya dhahabu, mabamba yenyewe “hayana thamani yoyote” Hata hi-vyo, kumbukumbu ambayo iliyokuwa imeandikwa kwenye mabamba “ni ya thamani kuu”)

• Moroni alisema kuwa Kitabu cha Mormoni kingeweza tu kuletwa na mtu aliye na “jicho lenye utukufu wake [wa Mungu]” (Mormoni 8:15). Unafikiri hii inamaanisha nini? (Wa-nafunzi wanapojadili swali hili, unaweza kutaka kuwaalika kusoma Joseph Smith—His-toria 1:46, iliyo na maelekezo ya baadaye ya Moroni kwa Joseph Smith, kabla ya kuleta Kitabu cha Mormoni.)

• Katika Mormoni 8:16, maelezo ya Moroni ya ujio wa Kitabu cha Mormoni yanasaidiaje kueleza thamani kuu ya kitabu hiki?

Kama ilivyoandikwa katika Mormoni 8:17–21, Moroni alionya wale ambao wangeshu-tumu au kupinga Kitabu cha Mormoni. Waalike wanafunzi kusoma aya hizi na kutafuta maonyo ya Moroni.• Ni yapi maonyo ya Moroni kwa wale wanakataa au kushitumu Kitabu cha Mormoni?

Page 533: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

518

SoMo la 141

• Ni ukweli upi unaojifunza kutoka katika Mormoni 8:22? Ujio wa Kitabu cha Mormoni katika siku za mwisho unasaidiaje kutimiza makusudi ya milele ya Mungu?

Eleza kwamba Mormoni 8:23–25 ina maneno ya Moroni kuhusu maombi ya watakatifu waaminifu waliokuwa wameishi kabla ya wakati wake. Aliwazungumzia wakimlilia Bwana “kutoka mavumbini.” Waulize wanafunzi kusoma kifungu hiki kimya, wakitafuta kile Wa-takatifu wa Amerika ya kale waliombea kuhusiana na Kitabu cha Mormoni.• Watakatifu wa kale walimwombea nani? (Waliombea ndugu zao— kumaanisha Wala-

mani na uzao wao— na kwa yule mtu ambaye angeleta Kitabu cha Mormoni—, kumaa-nisha Joesph Smith.)

Eleza kuwa Moroni alieleza kuhusu hali ambayo ingekuwepo wakati Kitabu cha Mormoni kingekuja. Kisha waulize kujitwasiri wakiwa katika hali ya Moroni, wakiishi zaidi ya miaka 1,600 na kupokea ono la siku zetu.Waalike wanafunzi kuandika aya katika daftari au shajara za kujifunza maandiko wakie-leza kuhusu hali ya kiroho ya siku zetu. Wanafunzi wakishakuwa na wakati wa kutosha kuandika, alika baadhi yao kushiriki walichoandika. Kisha waulize wanafunzi kusoma Mormoni 8:26–32 kimya na kulinganisha aya zao na maelezo ya kinabii ya Moroni ya siku zetu. Gawanya darasa katika majozi. Uliza kila jozi kushiriki vifananisho na tofauti chache kati ya maelezo yao na maelezo ya Moroni.• Nini unachokigundua kuwa sahihi kuhusu maelezo ya Moroni ya siku zetu?Andika muhtasari ufuatao wa unabii wa Moroni ubaoni: Kitabu cha Mormoni kitakuja kwa nguvu ya Mungu katika siku ya uovu mkuu. Ikiwa umeonyesha vifaa au picha zina-zowakilisha mavumbuzi ya kiteknolojia au ya kimatibabu, fikiria kuweka nakala ya Kitabu cha Mormoni karibu nazo. Ili kuwasaidia wanafunzi kutafakari na kushuhudia thamani ya Kitabu cha Mormoni maishani mwao, uliza maswali kama yafuatayo:• Kitabu cha Mormoni kinaweza kutusaidia vipi kukinza uovu katika siku zetu?• Ni kwa njia gani Kitabu cha Mormoni ni cha thamani zaidi kuliko uvumbuzi wa ya kite-

knolojia au wa kimatibabu?• Kwa nini unafikiri Kitabu cha Mormoni ni “mojawapo wa karama muhimu zaidi iliyo-

pewa ulimwengu katika nyakati za kisasa,” kama alivyosema Rais Benson?• Kama rafiki akikuuliza kwa nini Kitabu cha Mormoni kina thamani kwako, ungesema nini?

Mormoni 8:33–41Moroni anaona siku za mwisho na kulaani uovu wa kiroho wa wakati wetuAlika mwanafunzi asome Mormoni 8:35 kwa sauti. Kabla hajasoma, eleza kuwa katika aya hii Moroni anatuzungumzia sisi moja kwa moja.• Aya hii inawezaje kuathiri jinsi tunavyosoma Kitabu cha Mormoni?Wakati wanafunzi wameshajadili swali hili, soma kauli ifuatayo ya Rais Ezra Taft Benson, ambapo alinena kuhusu manabii wa Kitabu cha Mormoni.“Kama waliona siku zetu, na wakachagua mambo yale ambayo yangekuwa ya thamani kuu kwetu, si hiyo ndiyo sababu tunapaswa kujifunza Kitabu cha Mormoni? Tunapaswa kujiuliza wenyewe kila mara, ‘Kwa nini Bwana alimpatia maongozi Mormoni (au Moroni au Alma) kujumuisha hayo katika kumbukumbu zake? Ni somo gani ninaloweza kujifunza kutokana na hayo linaloweza kunisaidia katika siku hizi?'" (“The Book of Mormon—Keys-tone of Our Religion,” 6).Wahimize wanafunzi kufuata ushauri huu wanapojifunza masalio ya maneno ya Moroni katika Mormoni 8.Uliza wanafunzi kufikiria wakati walipomwona mtu aliyekuwa na shida— ya muda, ya kuhisia, ya kijamii au ya kiroho. Waalike kufikiria walichofanya kumsaidia mtu yule— au kama hawakutoa usaidizi, ni nini wangelifanya. Waualike pia kutafakari kwa nini walicha-gua kusaidia au kutosaidia.Alika wanafunzi wachache kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka Mormoni 8:33–41. Litake darasa kufuatilia, wakitafuta sababu za watu wengine katika siku za mwisho hawa-tawasaidia wale walio na mahitaji.

Waulize wanafunzi kushiriki majibu yaliyoandikwaMara kwa mara wahimize wanafunzi kushiriki kile walicho-andika katika daftari zao au katika shajara za kujifunza maandiko. Hakikisha kuwashukuru wanafunzi kwa kushiriki na kuwasifu kwa dhati. Unapochukua muda darasani kufanya hivi, utawasaidia kujenga mazingira ya kujifunza ya upendo na heshima.

Page 534: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

519

MoRMoni 8 :12– 41

• Kwa nini baadhi watu katika siku za mwisho hawatawasaidia walio na shida? (Majibu yanaweza kujumuisha kiburi, dhambi, kupenda pesa na nguo za kifahari kuliko kuwape-nda wale walio na shida , na kutamani sifa za ulimwengu.)

• Katika Mormoni 8:38, Mormoni anatumia neno uchafuzi. Ni upi baadhi ya ushawishi katika dunia hivi leo unaoweza kuonekana kama ni uchafuzi? (Majibu yanaweza kuju-muisha kiburi, picha za ngono na kupenda pesa.)

Waulize wanafunzi waandike sentensi ambayo inatoa muhtasari wa kile walichojifunza kutoka kwa Mormoni 8:36–41 kuhusu wajibu wetu kuwajali maskini na walio na shida. Waalike wanafunzi wawili au watatu kusoma sentensi zao kwa darasa. Ingawa maneno ya wanafunzi yanaweza kutofautiana, wanapaswa kuweza kutambua ukweli huu: Mungu atataka uwajibikaji wetu kwa njia tunavyowatendea maskini na walio na shida.• Unafikiri ni nini baadhi ya mahitaji ya kawaida katika shule yako au jamii? Vijana wa

Kanisa wanaweza kufanya nini ili kuwajali watu walio na shida hizi. Wasaidie wanafunzi kuelewa kuwa hawatarajiwi kutoa pesa zao na wakati wao kwa kila mradi unaofaa au kwa kila mtu anaomba usaidizi. Katika familia zao na Kanisani, vijana hupokea nafasi nyingi za kuwasaidia walio na shida. Zaidi ya hao, wanaweza kufuata mwongozo wa Roho kutoa huduma kwa hiari yao.)

• Unafikiri vijana Kanisani wanaweza kufanya nini ili kuwajali maskini? (Ikiwa wanafunzi hawatataja matoleo ya mfungo, unaweza kutilia mkazo ulipaji wa matoleo ya mfungo kwa kusoma aya chini “Fast Sunday” katikaTrue to the Faith:. Gospel Reference [2004], pages 67–69.)

Kufuatia mjadala huu, waalike wanafunzi kuandika katika daftari zao au shajara za kujifu-nza maandiko kuhusu kitu kimoja au viwili wanavyoweza kufanya ili kuwajali maskini na walio na shida. Wanaweza kuandika mapendekezo waliyosikia darasani au mawazo yao wenyewe. Waalike kuandika lengo la kufanya mojawapo ya mambo haya katika wiki zijazo. Wahimize kutimiza malengo yao.

Tangazo na Habari za UsuliMormoni 8:14–18. Amebarikiwa yule ambae ataleta vitu hivi katika mwanga”

Moroni alitabiri kumhusu nabii Joseph Smith, aliye-teuliwa kuleta Kitabu cha Mormoni ulimwenguni. (angalia Mormoni 8:15–16). Manabii wengine wa kale walifahamu kuhusu Joseph Smith na waliomba kufaulu kwake katika kutafsiri na kuchapisha mabamba ya dha-habu, hivyo basi kutimiza madhumuni ya Mungu. (ona Mormoni 8:23–25; M&M 10:46). Rais Boyd K. Packer wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alizungumzia wajibu wa Joseph Smith katika kuleta Kitabu cha Mormoni:

“Ukweli ni, kwa njia rahisi, kwamba alikuwa nabii wa Mungu— bila kuongeza wala kupunguza hata chembe moja!

“Maandiko hayakuja hasa kutoka kwa Joseph Smith kama jinsi yalivyokuja kupitia kwake. Alikuwa mpito ambapo kupitia kwake funuo zilitolewa . . . .

“Nabii Joseph Smith alikuwa mvulana wa shamba asiye msomi. Ili kusoma baadhi ya barua zake za mwanzo

katika asili kunamwonyesha kuwa kwa njia fulani si mfasaha katika tahajia na sarufi na maelezo.

“Kwamba funuo zilikuja kupitia kwake katika hali ya maandishi fasihi si lolote ila muujiza.” (“We Believe All That God Has Revealed,” Ensign, May 1974, 94).

Mormoni 8:37–38. Je, kuwajali maskini na wenye shida kunahusiana vipi na furaha ya milele?

Askofu H. David Burton, Askofu Msimamizi, alishuhudia matokeo ya milele ya kuwajali maskini na wenye mahitaji.

“Madhumuni, ahadi na kanuni zinazoimarisha kazi yetu ya kuwajali maskini na wenye shida huenea mbali na mafungo ya maisha ya muda. Kazi hii takatifu si tu ya kunufaisha na kubariki wale wanaoumia au wenye shida. Kama wana na binti wa Mungu, hatuwezi kurithi kipimo kamili ya uzima wa milele bila kuwekeza kikami-lifu katika kujaliana mmoja na mwengine tukiwa hapa duniani. Ni katika tendo la ukarimu la toleo na kujitolea kwa wengine ndipo tunapojifunza kanuni za selestia za kujitolea na kuweka wakfu” (“The Sanctifying Work of Welfare,” Ensign or Liahona, Mei 2011, 81–82).

Page 535: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

520

Utangulizi Moroni alimaliza kumbukumbu ya baba yake kwa kuwaita wale wasiomwamini Yesu Kristo kumgeukia Bwana kupitia toba. Alifundisha kuwa Mungu ni Mu-ngu wa miujiza asiyebadilikia na kuwa miujiza hukoma

tu kwa sababu ya kukosa kuamini. Aliwahimiza watu kumwamini Yesu Kristo na kumwomba Baba na mioyo yao yote katika jina la Yesu Kristo ili kupokea vitu wanavyohitaji.

SOMO LA 142

Mormoni 9

Mapendekezo ya Kufundisha

Mormoni 9:1–6Moroni anawaita wale wasioamini katika Yesu Kristo watubuWaulize wanafunzi kufikiria hali ambapo walihisi kutokustarehe. Waalike wanafunzi wa-chache kueleza kuhusu uzoefu wao na kueleza kwa nini walihisi kutukustarehe.. Unaweza pia kutaka kuwauliza kile ambacho kingewafanya kustarehe katika hali hizo. Waalike wanafunzi wasome Mormoni 9:1–5 kimya, wakitafuta hali ya kutokustarehe ambayo Mormoni alielezea .. (Unaweza pia kutaka kuwaalika wanafunzi wasome Alma 12:12–15 na kuandika rejeleo hili karibu na Mormoni 9:1–5.)• Wakati wa Hukumu ya Mwisho, waovu watahisi vipi katika uwepo wa Mungu Baba na

Yesu Kristo? Kwa nini watahisi hivi?Alika mwanafunzi wasome kauli ifatayo ya Rais Joseph Fielding Smith:

“Hapawezi kuwa na wokovu bila toba. Mtu hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu katika dhambi zake. Ingekuwa kitu kisichosahihi kwa mtu kuja katika uwepo wa Baba na kuishi katika uwepo wa Mungu katika dhambi zake. . . .“Ninafikiri kuna watu wengi katika dunia, wengi wao pengine katika Kanisa. kwa kweli baadhi katika Kanisa —walio na dhana kuwa wanaweza kupitia maisha haya wakifanya watakavyo, wakivunja amri za Bwana na hali hati-

maye watakuja katika uwepo wake. Wanafikiri watatubu, labda katika dunia ya kiroho.“Wanapaswa kusoma maneno haya ya Moroni [kunukuu Mormoni 9:3–5].“Unafikiri kuwa mtu ambaye maisha yake yamejawa ufisadi, ambaye amekuwa mwasi kwa Mungu, asiyekuwa na roho wa toba, angeweza kuwa na furaha au kuhisi vyema akikuba-liwa kuja katika uwepo wa Mungu?” (Doctrines of Salvation, ed. Bruce R. McConkie, 3 vols. [1954–56], 2:195–96; italiki katika nakala asili zilitolewa).• Kwa nini tunahitaji kutubu leo na si kungoja hadi siku ya hukumu? (Ili kuwasaidia wa-

nafunzi kujibu swali hili, unaweza kutaka kuwaalika kusoma Alma 34:33–38.)Alika mwanafunzi asome Mormoni 9:6 kwa sauti. Uliza darasa kufuatilia, wakitafuta kile wale wasioamini wanapaswa kufanya ili wahisi vyema katika uwepo wa Mungu. Baada ya wanafunzi kuripoti walichopata, waulize kutambua maneno na vishazi katika Mormoni 9:6 vinavyoeleza kuhusu wale waliomgeukia Bwana na kuomba msamaha. Unaweza kutaka kupendekeza kuwa wanafunzi waweke alama maneno na vishazi wanavyopata.Waalike wanafunzi kuandika katika daftari au katika shajara za kujifunza maandiko kanuni inayotoa muhtasari wa Mormoni 9:6. Waite wanafunzi wawili au watatu kusoma wali-choandika. Ingawa wanafunzi wanaweza kutumia maneno tofauti, majibu yao yanapswa kueleza ukweli ufuatao. Ikiwa tutatubu, tutapatikana kuwa bila mawaa tutakapokuja katika uwepo wa Mungu.Shuhudia kuwa kupitia toba na kuishi kwa haki, tunaweza kujitayarisha kuwa wenye faraja katika uwepo wa Bwana. Waalike wanafunzi kutafakari kile wanachopaswa kufanya sasa ili kuwa tayari kukutana na Bwana.

Kuwaita wanafunzi binafsiKuwaita wanafunzi binafsi kunaweza kuhi-miza kushiriki kutoka kwa wale wasioshiriki kila mara. Wasaidie wanafunzi kujitayarisha kushiriki kwa kuwapa muda kufikiri kabla ya kuwaita. Kuwa mwa-ngalifu usiwaaibishe au kuwashinikiza kushiriki ikiwa hawapendi kufa-nya hivyo.

Page 536: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

521

MoRMoni 9

Mormoni 9:7–20Moroni atangaza kuwa Mungu hufanya miujiza na kujibu maombi ya waaminioAndika miujiza ubaoni. Waulize wanafunzi jinsi wangeeleza neno hili. Baada ya wanafunzi wachache kujibu, alika darasa kutazama miujiza katika Kamusi ya Biblia. Waulize kusoma ingizo, wakitafuta habari inayoweza kueleza au kuongeza maelezo waliyopendekeza.• Kwa nini unafikiri watu wengine hawaamini katika miujiza?Fanya muhtasari Mormoni 9:7–8 kwa kueleza kuwa Moroni aliwalenga watu katika siku za mwisho ambao wangedai kuwa ufunuo, unabii, vipawa vya kiroho na miujiza hayafanyiki tena. Wagawe wanafunzi wawili wawili. Mwalike mwenzi mmoja kusoma Mormoni 9:9–11 kimya, huku yule mwingine akisoma Mormoni 9:15–19 kimya. Waulize kila mwanafunzi kuandika mambo muhimu ambayo Moroni alisema ili kuwashawishi watu kuamini katika miujiza. Wanafunzi wakishakuwa na wakati wa kutosha kukamilisha, waalike kutoa taarifa kwa wenzi wao kile walichoandika.Upande wa kushoto wa ubao, andika, Miujiza hukoma tunapo . . .Upande wa kulia ya ubao, andika Miujiza huweza kufanyika tuki . . .Alika mwanafunzi asome Mormoni 9:20 kwa sauti, na uulize darasa kutafuta sababu tatu kwa nini Mungu anaweza kukoma kufanya miujiza miongoni mwa watoto wake. Mwalike mwanafunzi kuandika sababu hizi ubaoni kukamilisha kauli katika upande wa kushoto wa ubao kama ilivyoonyeshwa katika chati ifuatayo.Waulize wanafunzi kueleza upya kila kauli kwa nini miujiza hukoma kwa njia ya kueleza sharti linalofanya miujiza kuwezekana. Majibu yao yanapaswa kuwa sawa na mifano iliyo upande wa kulia wa chati.

Miujiza hukoma tunapo . . . Miujiza huweza kufanyika tunapo . . .

fifia katika kutoamini ongezeka katika imani

ondoka kutoka katika njia iliyo sahihi ishi kwa njia inayofaa; au kutii amri za Mungu

hatumjui Mungu tunayepaswa kumwamini Kuja kumjua Mungu na kumwamini

Waalike wanafunzi kurejea kwa upesi Mormoni 9:9, 19, wakitafuta mafundisho ya Mor-moni kuhusu asili ya Mungu. Baada ya wanafunzi kutoa taarifa ya walichopata, uliza:• Kwa kuwa tunajua Mungu habadiliki na kwamba alitenda miujiza kati ya watoto Wake

katika siku za awali, je tunaweza kujua nini kuhusu kupendelea kwake kufanya miujiza katika maisha yetu hivi leo? (Ingawa wanafunzi wanaweza kutumia maneno tofauti, wanapaswa kueleza kanuni ifuatayo: Mungu kila mara amefanya miujiza, na kwa sababu Yeye habadiliki, Yeye angali anatenda miujiza kulingana na imani yetu. Unaweza kutaka kuandika kanuni hii ubaoni na kupendekeza kuwa wanafunzi waa-ndike kanuni hii karibu na Mormoni 9:19–20 kwenye maandiko yao.)

Eleza kuwa tunaweza kupata uzoefu wa nguvu za kimiujiza za Mungu kwa njia nyingi. Ili ku-wasaidia wanafunzi, fikiria njia ambayo kwayo Mungu yungali Mungu wa miujiza, mwalike mwanafunzi asome kauli ifuatayo ya Dada Sydney S. Reynolds wa Urais Mkuu wa Msingi:“Nimejifunza kuwa Bwana atatusaidia katika kila hali ya maisha yetu tunapojaribu kum-hudumia na kufanya mapenzi yake. “Ninaamini kuwa sote tunaweza kushuhudia miujiza hii midogo. Tunawafahamu watoto wanaomba msaada ili kupata kitu kilichopotea na wanakipata. Tunawafahamu vijana wa-naopata ujasiri kusimama kama mashahidi wa Mungu na kuhisi Mkono wake wa usaidizi. Tunawafahamu marafiki wanaolipa zaka yao kutoka katika pesa zao zote kisha, kupitia mwujiza, hujikuta wanaweza kulipa karo zao au pesa za kukodi nyumba au kwa jinsi fulani kupata chakula kwa familia zao. Tunaweza kuelezea uzoefu wa maombi yaliyojibiwa na baraka za kikuhani zilizotupa ujasiri, kuleta faraja au kurejesha siha. Miujiza hii ya kila siku inatufanya tuujue mkono wa Bwana maishani mwetu” (“A God of Miracles,” Ensign, Mei 2001, 12).• Ni uzoefu gani uliokuwa nao unaohakikisha kuwa Mungu bado ni Mungu wa miujiza?

Page 537: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

522

SoMo la 142

Mormoni 9:21–37Moroni anawausia wasioamini kumwamini Yesu Kristo na kuomba katika jina LakeAlika mwanafunzi asome Mormoni 9:21 kwa sauti. Litake darasa kufuatilia, wakitafuta kile Moroni alifundisha kuhusu kuomba kwa Baba wa Mbinguni.• Mormoni alitoa ahadi gani? (Majibu ya wanafunzi yanapaswa kuonyesha kanuni ifuatayo:

Tukiomba kwa imani na katika jina la Yesu Kristo, Baba wa Mbinguni atatupatia chochote tunachoomba.)

Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa inamaanisha nini kuomba “katika jina la Kristo” alika mwanafunzi asome kauli ifuatayo“Tunaomba katika jina la Kristo wakati mawazo yetu yako katika mawazo ya Kristo na matakwa yetu ni matakwa ya Kristo —wakati maneno yake yanapokaa ndani yetu (Yohana 15:7). Ndipo tunapoomba vitu ambavyo vinawezekana kwa Mungu kutupatia. Maombi mengi hubaki bila kujibiwa kwa sababu hayako katika jina la Kristo hata kidogo, na haya-wakilishi kwa njia yoyote akili yake, lakini hutokana na uchoyo wa moyo wa binadamu” (Bible Dictionary, “Prayer”).Unaweza kutaka kuuliza maswali yafuatayo:• Tunawezaje kuhakikisha kuwa vitu tunavyoomba vinadhihirisha kile Bwana anachotaka

kwetu?• Ni lini umeona ahadi zilizotolewa katika Mormoni 9:21 zikitimizwa? (Unaweza kuhitaji

kuwapa muda wanafunzi kufikiria kuhusu swali hili kabla ya kulijibu.)Fanya muhtasari wa Mormoni 9:22–25 kwa kueleza kuwa Mwokozi aliwaahidi wafuasi wake baraka alipowatuma kwenda kufunza injili. Waulize wanafunzi kupitia Mormoni 9:22–25 na kutambua baadhi ya baraka hizo.• Ina maana gani kwako kuwa Mwokozi atathibitisha maneno [Yake] yote”? (Mormoni 9:25).Waalike wanafunzi kusoma Mormoni 9:27–29 kimya, wakitafuta mitazamo na matendo yata-kayowasaidia kustahili na kupokea usaidizi wa Mungu. Unaweza kutaka kuwauliza wanafunzi kuandika muhtasari wa aya hizi katika daftari zao au katika shajara za kujifunza maandiko.Ili kuhitimisha somo hili, fanya muhtasari wa Mormoni 9:30–34 kwa kuwaambia wanafu-nzi kuwa Moroni alikuwa ana shaka kuwa watu wengine katika siku za mwisho wangeka-taa ujumbe wa Kitabu cha Mormoni kwa sababu ya mapungufu ya wale waliokiandika na kwa lugha iliyotumiwa kukiandika. Alika mwanafunzi asome Mormoni 9:35–37 kwa sauti. Litake darasa kufuatilia, likitafuta sababu za kwa nini Moroni na wengine waliomba kuwa Kitabu cha Mormoni kingetokea katika siku za mwisho. (Kwa hivyo uzao wa ndugu zao, Walamani, wangerejeshwa katika “ufahamu wa Kristo” na kwa maagano ambayo Mungu alikuwa amefanya na nyumba ya Israeli.)Ili kuwasaidia wanafunzi kufanya muhtasari wa kile walichojifunza leo, uliza maswali yafuatayo:• Je, ni vipi Kitabu cha Mormoni ni ushahidi kuwa Mungu ni Mungu wa miujiza na kwa-

mba hujibu maombi?• Ni kweli gani ulizojifunza hivi leo zitakazoathiri maombi yako ya kibinfasi?

Rejeo la MormoniChukua muda kuwasaidia wanafunzi kurejea kitabu cha Mormoni. Waulize wao kufikiria kile walichojifunza katoka kitabu hiki, katika seminari na kujifunza kwao kwa kibinafsi. Waalike wao kurejea kwa kufupi baadhi ya muhtasari wa sura katika Mormoni ili kuwasa-idia kukumbuka. Waulize wanafunzi wachache kushiriki kitu kutoka kwa Mormoni kilicho-wahamasisha au kuwasaidia kuwa na imani kuu zaidi katika Yesu Kristo.

Page 538: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

523

UtangUlizi Wa

Kitabu cha etheriKwa nini ujifunze kitabu hiki?Wanafunzi wanapojifunza kitabu cha Etheri, watajifunza kuhusu Wayaredi—ku-ndi la watu ambao walisafiri hadi Nusu Tufe ya Magharibi na waliishi huko kwa karne nyingi kabla ya kuwasili kwa watu wa Lehi. Wanafunzi watajifunza kanuni muhimu kuhusu maombi, ufunuo, na uhusiano kati ya imani katika Yesu Kristo na kupokea elimu ya kiroho. Pia wata-jifunza kuhusu nafasi ya manabii katika kuwashawishi watu kutubu na kuhusu matokeo ambayo yatakuja kwa wale wa-naomkataa Yesu Kristo na manabii Wake.

Nani aliandika kitabu hiki?Moroni alifupisha kitabu hiki kutoka ka-tika mabamba 24 ya dhahabu yaliyoitwa mabamba ya Etheri. Kitabu hiki kinaitwa kwa jina la nabii Etheri, ambaye alikuwa nabii wa mwisho wa Wayaredi na ambaye alitengeneza kumbukumbu ya historia yao (ona Etheri 15:33–34). Karibu miaka 500 kabla ya Moroni kufanya ufupisho wake wa kumbukumbu takatifu, baadhi ya watu wa Limhi waligundua mabamba ya Etheri walipokuwa wakitafuta nchi ya Zarahemla (ona Mosia 8:7–11; Ether 1:2). Manabii Wanefi na watunza kumbu-kumbu walikabidhiana mabamba ya Etheri hadi yalipomfikia Moroni. Moroni alisema kwamba yeye hakujumuisha hata “sehemu moja ya mia” ya kumbukumbu katika ufupisho wake (Etheri 15:33).

Hiki kitabu kiliandikiwa kina nani na kwa nini?Kwa sababu Moroni alifupisha mabamba ya Etheri baada ya Wayaredi na watu wake mwenyewe walikuwa wameanga-mizwa, yeye alidhamiria kitabu hiki kwa ajili ya watu wa siku hizi. Moroni aliwausia Wayunani wa siku za mwisho watubu, wamtumikie Mungu, na waachane na makundi ya kisiri (ona Etheri 2:11–12; 8:23). Yeye pia aliandika maneno ya Yesu Kristo, akiwaalika “enyi miisho ya dunia” tubuni, njooni Kwake, batizweni, na mpo-kee ufahamu ambao ulikuwa umefichwa kutoka kwa ulimwengu kwa sababu ya kutoamini (ona Etheri 4:13–18).

Kiliandikwa lini na wapi?Etheri alikamilisha kumbukumbu ya watu wake wakati wa, na baada ya vita kuu ya mwisho ambayo iliwaua wote isipokuwa Wayaredi wawili—yeye mwenyewe na Koriantumuri (ona Etheri 13:13–14; 15:32–33). Kisha yeye alificha maandishi yake “kwa njia ambayo watu wa Limhi waliyapata”(Etheri 15:33; ona pia Mosia 8:7–9). Moroni alifupisha kumbukumbu za Etheri kati ya miaka 400 B.K na miaka 421 B.K (ona Mormoni 8:3–6; Moroni 10:1). Moroni aliandika kwamba Wa-yaredi waliangamizwa katika “nchi hii ya magharibi” (Etheri 1:1), ikionyesha inawezekana kuwa alikuwa katika nchi ambayo waliangamizwa wakati akifupisha kumbukumbu zao.

Ni zipi baadhi ya sifa bainifu za kitabu hiki?Tofauti na vitabu vingine katika Kitabu cha Mormoni, kitabu cha Etheri hakielezei historia ya uzao wa Lehi. Kitabu hiki kina-simulia jinsi Wayaredi walivyotoka kutoka kwenye Mnara wa Babeli na kusafiri hadi nchi ya ahadi, ambapo hatimaye walia-ngamizwa. Kitabu cha Etheri ni ushuhuda wa pili kwa kumbukumbu za Wanefi kikionyesha kwamba “taifa lolote litakalo-imiliki [nchi ya ahadi] litamtumikia Mungu, au wataangamizwa baada ya wao kuwa waovu” (Etheri 2:9).Kujitokeza kwa Yesu Kristo kwa ndugu ya Yaredi kabla ya maisha haya “kume-wekwa miongoni mwa matukio makuu katika historia iliyoandikwa.” Tukio hili “li-lidhiriisha ndugu ya Yaredi kuwa miongoni mwa manabii wakuu wa Mungu milele” (Jeffrey R. Holland, Christ and the New Covenant: The Messianic Message of the Book of Mormon [1997], 17). Maelezo ya Moroni ya ono hili yanatoa ushuhuda wa nguvu wa Yesu Kristo na huonyesha mafundisho mahususi kuhusu uhalisi wa miili ya kiroho (ona Etheri 3:4–17).

MuhtasariEtheri 1–3 Bwana anahifadhi lugha ya Wayaredi katika Mnara wa Babeli na kuahidi kuwao-ngoza hadi kwenye nchi teule na kuwafanya wawe taifa kubwa. Yeye anawaongoza hadi pwani na kuwaelekeza kutengeneza mashua kwa ajili ya safari yao ya kuvuka bahari. Bwana anaji-dhihirisha Mwenyewe na “vitu vyote” (Etheri 3:26) kwa ndugu ya Yaredi.

Etheri 4–5 Moroni anafunga maandishi ya ndugu ya Yaredi. Yeye anaandika maelezo ya Yesu Kristo kwamba maandishi haya yatafunuliwa kwa wale waonye-shao imani katika Yeye. Moroni anafundisha kwamba mashahidi watatu wa siku za mwisho wata-ungana na Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu katika kushuhu-dia juu ya Kitabu cha Mormoni.

Etheri 6–11 Wayaredi wanasafiri hadi nchi ya ahadi. Watu wali-zaana na kuanza kuenea katika nchi. Mfululizo wa wafalme wema na waovu wanatawala vizazi vingi. Wayaredi wanakari-bia kuangamizwa kwa sababu ya makundi ya siri. Manabii wengi wanawaonya watu watubu, lakini watu wanawakataa.

Etheri 12 Moroni anafundisha kwa-mba imani inahitajika kabla ya mtu kupokea ushahidi wa kiroho. Yeye anaonyesha kwa Bwana hofu yake kwamba Wayunani katika siku za usoni watakejeli udhaifu wake katika kuandika kumbu-kumbu takatifu, na anaandika majibu ya Bwana kwake. Moroni anawasihi wasomaji wa siku za mwisho kumtafuta Yesu Kristo.

Etheri 13–15 Moroni anajadili una-bii wa Etheri juu ya Yerusalemu mpya. Baada ya Wayaredi kumka-taa Etheri, yeye anashuhudia na kuandika maangamizo yao yote.

Page 539: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

524

Mapendekezo ya Kufundisha

Etheri 1:1–32Moroni anaandika nasaba ya Etheri hadi ya Yaredi wakiwa katika Mnara wa BabeliIli kuwasadia wanafunzi kukumbuka kilipotoka kitabu cha Etheri, tathmini pamoja nao msu-ruru wa safari zao katika Mosia 7–24 katika kiambatisho cha hiki kitabu cha kiada. Waambie wao kutazama safari ya 4: jaribio la kuitafuta Zarahemla. Kisha waalike watafute kile watu wa Limhi walikipata katika safari hii. Kisha waambie wafungue kwenye ukurasa wa kwanza wa kitabu cha Etheri. Muhtasari uliopo chini ya kichwa cha habari unaelezea kwamba kitabu cha Etheri kilitwaliwa kutoka kwenye mabamba 24 yaliyopatikana na watu wa Limhi.Elezea kwamba baada ya Moroni kukamilisha kumbukumbu ya baba yake, aliandika ufupisho, au toleo fupi, la kumbukumbu zilizopatikana kwenye mabamba 24 ya dhahabu. Kumbukumbu hizi zina historia ya Wayaredi, ambao waliishi kwenye bara la Amerika kabla

ya Wanefi na Walamani. Waambie wanafunzi wasome Etheri 1:1–5 kimya, wakitafuta kile Moroni alichagua kukijumuisha katika ufupisho wake wa kumbukumbu za Wayaredi. Waambie wanafunzi waripoti kile walichokipata.Kama una uwezo wa kupata picha ya Mnara wa Babeli, unaweza kufikiria kuuonyesha. Waambie wanafunzi kufa-nya muhtasari wa kile wanachojua kuhusu mnara uliotajwa katika Etheri 1:5 na kilitokea nini kwa wale waliojaribu kuujenga. (Uliitwa Mnara wa Babeli. Bwana alichanganya lugha ya watu ambao walijaribu kuujenga na kuwatawanya kwa sababu ya uovu wao; ona Mwanzo 11:1–9.)Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa uhusiano kati ya historia ya Wayaredi na historia ya Wanefi, unaweza kuwataka wao wa-angalie mwenendo kwenye alamisho la Kitabu cha Mormoni (chombo nambari 32336). Elezea kwamba Moroni alianza usi-mulizi wake wa historia ya Wayaredi kwa kuandika nasaba ya nabii Etheri, ambaye aliandika historia kwenye mabamba 24 ya dhahabu. Moroni aliandika nasaba toka Etheri hadi kwa mtu anayeitwa Yaredi, ambaye aliishi nyakati za Mnara wa Babeli.

Etheri 1:33–43Kupitia maombi ya ndugu ya Yaredi, familia na marafiki zake wanapokea rehema na mwongozoWaulize wanafunzi kama kuna yeyote yule ambaye amewahi kuwa mahali ambapo haku-elewa lugha ambayo watu walio karibu naye walikuwa wakiongea. Waalike waelezee jinsi walivyohisi katika mazingira yale. Kisha waambie wao wafikirie jinsi watu walivyohisi pale kwenye Mnara wa Babeli wakati walipogundua kwamba lugha ya kila mtu ilikuwa imecha-nganywa. Waambie watafakari kimya kimya maswali yafuatayo:

Maelezo ya jumla ya safari katika Mosia 7–24

Nchi ya Zarahemla

Nchi ya Nefi (Lehi- Nefi)

Kundi la Wanefi lililoongozwa na zenifu

Kundi la watafutaji lililoongozwa

na amoni

jaribio la kuitafuta zarahemla

Mahame ya Taifa la Wayaredi katika Nchi ya Kaskazini

Mabamba 24 ya dhahabu (kitabu cha etheri)

Wanefi kadhaa wanatafuta kuimiliki

tena nchi ya nefi

Maji ya Mormoni

Watu wa limhi wanatoroka

alma na watu wake wanaondoka

Nchi ya Helamu

Watu wa alma wanatoroka

UtanguliziMoroni anafupisha kitabu cha Etheri kutoka mabamba 24 ya dhahabu yaliyopatikana na kundi la watafutaji waliotumwa na Limhi (ona Mosia 8:7–11). Mabamba haya yana historia ya watu wa Yaredi. Taarifa za Wayaredi zinaanza na Yaredi na kaka yake wakitafuta fadhila za Bwana na mwongozo Wake kwa familia na marafiki zao wakati Bwana alipochanganya ndimi za watu katika

Mnara wa Babeli (ona Mwanzo 11). Kwa sababu ndugu ya Yaredi aliomba kwa Bwana kwa uaminifu, Bwana alihifadhi lugha ya Wayaredi, kaka yake, na familia na marafiki zao. Bwana alitangaza kwamba Yeye angewao-ngoza hadi kwenye nchi ya ahadi, ambako wangekuwa taifa kubwa.

SOMO LA 143

etheri 1

Page 540: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

525

etheRi 1

• Kama ungekuwa katika hali hiyo, ni mawasiliano ya nani ambayo ungeyakosa sana? Kwa nini?”

Waalike wanafunzi wasome Etheri 1:33–34 kimya kimya. Kabla hawajasoma, waulize wa-tafute (1) ni nani Yarefi alitaka kuwasiliana naye na (2) jinsi gani alipendekeza kusuluhisha shida hii. (Yeye alitaka kuwasiliana na familia yake, na alimuomba ndugu yake aombe ili lugha yao isikanganywe.) Baada ya wanafunzi kuripoti kile walichokigundua, waulize:• Kishazi “mlilie Bwana” kina maanisha nini kwako?• Kutoka Etheri 1:33–34, unajifunza nini kuhusu jinsi Yaredi alivyohisi kuhusu ndugu yake

na kuhusu maombi ya ndugu yake?Gawa darasa katika makundi. Katika kila kundi, waambie wanafunzi wachukue zamu kusoma kwa sauti kutoka Etheri 1:35–42. Waambie watafute maombi ya ndugu ya Yaredi na majibu ya Bwana kwa maombi yale. Baada ya wanafunzi kupata muda wa kutosha wa kusoma, waulize:• Nini kinachokupendeza kuhusu maombi ya ndugu ya Yaredi?• Bwana alijibu vipi maombi ya ndugu ya Yaredi?• Ni kanuni gani tunazoweza kujifunza kwa jinsi ndugu ya Yaredi alivyoomba na jinsi

Bwana alivyojibu maombi yake? Wakati wanafunzi wakitoa mawazo, wahimize wao ku-tafakari kuhusu huruma na upendo wa Baba wa Mbinguni kwa ajili yao. Andika kanuni ifuatayo kwenye ubao: Tunapomlilia Mungu kila mara katika imani, Yeye atakuwa na huruma juu yetu.)

Kabla ya darasa, andika maswali yafuatayo kwenye ubao. (Au unaweza kufikiria kuwapa karatasi za maswali au kuwasomea kwa sauti pole pole ili wanafunzi waweze kuyaandika.)

Ni kwa njia gani kumlilia Baba wa Mbinguni ni tofauti na “kutoa sala” tu?Ni wakati gani ulihisi huruma za Baba wa Mbinguni katika kujibu maombi? Ni wakati gani wa-nafamilia au marafiki walikuambia juu ya huruma za Baba wa Mbinguni katika kujibu maombi?Ni majibu gani ya Mungu yanayohusu maombi yetu hutufundisha hisia Zake kwetu?Unaweza kufanya nini kuyafanya maombi yako yawe na maana zaidi?

Waalike wanafunzi kujibu maswali haya katika daftari au shajara za kujifunza maandiko. Una-weza kutaka kuwapa nafasi ya kuchangia kile walichoandika. Shuhudia kwamba unajua Baba wa Mbinguni anatupenda sisi na ana hamu ya kutubariki tunapomuomba yeye kila mara.Elezea kwamba tukio katika Etheri 1 linaweza kutupa umaizi wa ziada katika upendo wa Mungu kwetu na baraka ambazo huja kwa njia ya maombi. Waambie wanafunzi kupitia Etheri 1:34, 36, 38 kimya kimya, wakitafuta kile Yaredi alikiomba kwamba ndugu yake aombe katika maombi yake. Mwalike mwanafunzi kutenda kama mwandishi na kuoro-dhesha majibu ya wanafunzi kwenye ubao. Unaweza kupendekeza kwamba mwandishi aandike majibu haya chini ya maneno “kumlilia Baba wa Mbinguni” katika kanuni ulizoa-ndika kwenye ubao.Unaweza kupendekeza kwamba wanafunzi waweka alama kishazi “acha tuwe waaminifu kwa Bwana” mwishoni mwa Etheri 1:38. Tilia mkazo kwamba matendo ya Yaredi na ndugu yake yanaonyesha imani yao na hiari yao ya kuwa watiifu kwa Bwana. Waliomba kwa imani kwa ajili ya baraka walizohitaji.Waalike wanafunzi wapitie Etheri 1:35, 37, 40–42 kimya, wakitafuta njia ambazo Mungu alimbariki Yaredi na ndugu yake na familia zao na marafiki zao. Acha mwanafunzi ana-yetenda kama mwandishi aandike uvumbuzi wa wanafunzi kwenye ubao chini ya neno huruma katika kanuni ambayo umeiandika. Hakikisha wanafunzi wanaona uhusiano kati ya maombi ya ndugu ya Yaredi na baraka ambazo Bwana alitoa.Mwambie mwanafunzi asome Etheri 1:43 kwa sauti. Liambie darasa lifuatilie, likitafuta baraka ambazo Mungu aliahidi ingawa Ndugu ya Yaredi hakuwa ameziomba kimahususi.• Ni baraka gani za ziada ambazo Bwana aliwaahidi watu? (Yaredi alikuwa ameomba

kwamba ndugu yake amuombe Bwana mahali pa wao kwenda. Yaredi alikuwa amefikiria kwamba Bwana atawaelekeza hadi nchi ambayo “iliyochaguliwa kuliko zote duniani kote” [Etheri 1:38]. Bwana aliwaahidi kuwaongoza hadi nchi ya ahadi. Kwa nyongeza, Yeye aliwapa maelekezo mahususi kuhusu jinsi ya kufanya matayarisho ya mwanzo kwa safari yao. Yeye pia aliahidi kwamba Yeye atakuza taifa kuu kutoka katika familia zao na kwamba hakutakuwa na taifa kuu hapa ulimwenguni.)

Page 541: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

526

SoMo la 143

Waalike wanafunzi kufungua 2 Nefi 4:35. (Unaweza kupendekeza kwamba waandike 2 Nefi 4:35 karibu na Etheri 1:43 katika maandiko yao.) Kisha waombe wasome 2 Nefi 4:35 na Etheri 1:43 kimya kimya, wakitafuta kile kinachofundishwa kwenye mistari hii kuhusu baraka ambazo Mungu anatupa kama majibu ya maombi yetu.• Katika 2 Nefi 4:35, Nefi anafundisha nini kuhusu majibu ya Mungu kwa maombi? (Mu-

ngu atawapa kwa ukarimu wale wanaomtafuta Yeye katika maombi. Unaweza kuhitaji kuelezea kwamba neno ukarimu linamanisha bila choyo.) Je! Tukio katika Etheri 1:43 huthibitisha kile Nefi alitamka katika 2 Nefi 4:35?

• Kulingana na Etheri 1:43, ni kwa nini Bwana alitoa kwa kuahidi baraka zaidi ya zile Wayaredi walikuwa wameomba? (Bwana aliahidi baraka zaidi kwa sababu wao wali-kuwa waaminifu katika maombi yao. Unaweza kutaka kupendekeza kwamba wanafunzi waweke alama kishazi kifuatacho katika Etheri 1:43: “kwa sababu ya muda huu mrefu ambao umeomba kwangu.”)

• Ni kanuni gani tunazoweza kujifunza kutoka katika Etheri 1:43? (Wanafunzi wanaweza kutumia maneno tofauti, lakini wanafaa kutambua kanuni ifutayo: Ikiwa tunaomba kwa Mungu kila mara kwa imani, tunaweza kupokea baraka zaidi ya zile tunazoomba. Unaweza kutaka kupendekeza kuwa wanafunzi waandike kanuni hii katika maandiko yao.)

• Ni lini umeiona kanuni hii katika maisha yako au maisha ya mtu mwingine unayemjua?Baada ya wanafunzi kushiriki majibu yao, unaweza kutoa mifano kutoka katika maisha yako au maisha ya wengine. Nabii Joseph Smith ni mfano mzuri wa kanuni hii. Yeye ali-pokea baraka zaidi ya zile alizoomba wakati aliposali ili kujua kanisa gani lilikuwa la kweli (ona Joseph Smith—Historia 1:10–20) na wakati yeye alipoomba ili kujua msimamo wake mbele ya Bwana (ona Joseph Smith—Historia 1:29–47).Ili kuhitimisha, wahimize wanafunzi ili wafanye juhudi za kuomba kwa uaminifu mkuu. Pia wahimize kukumbuka kwamba Baba wa Mbinguni amejawa na huruma na kwamba Yeye atajibu maombi yao kulingana na uaminifu wao na kulingana na kile Yeye anachoki-jua kitawaletea baraka kuu katika maisha yao.

Rejeo la Umahiri wa MaandikoGawa darasa katika jozi. Wape muda ili wasaidiane kurejea marejeo na vishazi muhimu vya vifungu vyote 25 vya umahiri wa maandiko vya Kitabu cha Mormoni. Unaweza kupendekeza kwamba watumie kadi za umahiri wa maandiko ili kuulizana maswali (ona wazo la rejeo la umahiri wa maandiko hapo mwisho wa somo la 45). Kisha wape maswali toka kwenye vile vifungu, labda kwa kutumia vidokezo kutoka kwenye kadi za umahiri wa maandiko. Sahihisheni maswali kwa pamoja kama darasa. Waambie wanafunzi wanukuu kutoka kwenye vifungu wanavyotakiwa kuvipitia, na wape moyo wa kujisomea. Mwaka wa shule unapofikia mwisho, fikiria kutoa mtihani wa mwisho juu ya vifungu vya umahiri wa maandiko vya Kitabu cha Mormoni.Tazama: Unaweza kuendesha shughuli hii mwanzoni au mwishoni mwa darasa. Kama uta-tumia shughuli hii mwanzoni mwa darasa, fanya iwe fupi ili kutoa muda kwa ajili ya somo. Kwa tathmini ya shughuli zingine, ona kiambatisho katika kitabu hiki cha kiada.

Tangazo na Habari za UsuliEtheri 1:34–35. Jina la ndugu ya Yaredi ni nani?

Mzee George Reynolds wa Sabini anasimulia tukio lifutaalo, ambalo linaonyesha kwamba jina la ndugu ya Yaredi lilifunuliwa kwa Nabii Joseph Smith:

“Nilipokuwa nikiishi katika Kirtland Mzee Reynolds Cahoon alipata mwana. Siku moja wakati Rais Joseph Simth alipokuwa anapita mlangoni kwake alimuita Nabii ndani na akamwomba ambariki mtoto na kumpatia jina.

Joseph alifanya hivyo na kumpa mvulana jina la Mahonri Moriancumer. Wakati yeye alikuwa amemaliza baraka hizo alimweka mtoto kitandani, na kumgeukia Mzee Cahoon yeye alisema, jina nililompatia mwanao ni jina la ndugu ya Yaredi; Bwana amenionyesha mimi. Mzee William F. Cahoon, ambaye alikuwa amesimama karibu alimsikia Nabii akitamka maneno hayo kwa baba yake; na hii ilikuwa ni mara ya kwanza jina la ndugu ya Yaredi lilijulikana katika Kanisa katika kipindi hiki” (“The Jare-dites,” Juvenile Instructor, May 1, 1892, 282).

Page 542: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

527

UtanguliziBaada ya kuondoka kutoka Mnara wa Babeli, Yaredi na kaka yake na familia zao na marafiki zao waliongo-zwa na Bwana kupita nyikani. Bwana alimwelekeza ndugu ya Yaredi kujenga mashua nane ili kuwabeba

watu wake kuvuka bahari hadi nchi ya ahadi. Ndugu ya Yaredi na watu wake walipomtii Bwana kwa imani, Bwana aliwapa mwongozo na maelekezo yaliyohitajika ili kufanikiwa katika safari yao.

SOMO LA 144

etheri 2

Mapendekezo ya Kufundisha

Etheri 2:1–12Wayaredi wanaanza safari yao kwenda nchi ya ahadi.Ili kuwasaidia wanafunzi kuona jinsi tunavyofuata maelekezo tunayopokea kutoka kwa Mungu yanaweza kututayarisha sisi kupokea mwongozo zaidi na maelekezo kutoka Kwake, endesha shughuli ifuatayo:Kabla darasa kuanza, ficha kitu kinachowakilisha hazina katika chumba mnachokutania. Tayarisha msururu wa vidokezo vitatu au vinne ambavyo vinawaongoza wanafunzi hadi kwenye hazina. Wewe utatoa kidokezo cha kwanza kwa wanafunzi. Hicho kidokezo kita-waalekeza kwenye kile kinachofuata, ambacho kitaelekeza kwa kile kingine, na vivyo hivyo hadi wanafunzi wafikie hazina. Baada ya wao kupata hazina, waulize:• Ni nini kingetokea kama ungepuuza kidokezo cha kwanza? (Hawangepata kidokezo

cha pili.)Waalike wanafunzi kurejelea Etheri 1:41–42 kimya, wakitafuta seti ya kwanza ya maelekezo ya kuwaongoza Wayaredi hadi nchi ya ahadi.Ili kuwasidia wanafunzi kuona jinsi Wayaredi walivyojibu maelekezo haya, mwalike mwa-nafunzi asome Etheri 2:1–3 kwa sauti.• Wayaredi walijibu vipi kwa ile seti ya kwanza ya maelekezo ya Bwana?Alika mwanafunzi asome Etheri 2:4–6 kwa sauti. Uliza darasa lifuatilie, likitafuta baraka ambazo Wayaredi walipokea baada ya kufuata seti ya kwanza ya maelekezo.• Ni nini kilitokea baada ya Wayaredi kufuata seti ya kwanza ya maelekezo ya Bwana?

(Bwana aliwapa maelekezo ya ziada kupitia kwa ndugu ya Yaredi.)• Tunaweza kujifunza nini kutoka kwenye tukio hili kuhusu jinsi ya kupokea mwongozo

kutoka kwa Bwana? (Wanafunzi wanaweza kutumia maneno tofauti, lakini majibu yao yanafaa kuonyesha kufuata kanuni: Tunapotenda kwa imani juu ya maelekezo aliyo-tupa Bwana, tunaweza kupokea mwongozo zaidi kutoka Kwake. Unaweza kutaka kupendekeza kwamba waandike ukweli huu katika maandiko yao karibu na Etheri 2:6.)

Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa vyema na kutumia kanuni hii, waalike wao kufikiria juu ya onyesho au msukumo waliopokea hivi majuzi kutoka kwa Bwana. Kisha soma taarifa ifuatayo ya Mzee Richard G. Scott wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili kuhusu jinsi tuna-vyopokea ufunuo kila mara:

“Utakuja sehemu kwa wakati, katika pakiti, ili kwamba ukue katika uwezo. Kila sehemu itafuatiwa na imani, utaongozwa hadi sehemu nyingine mpaka utakapopata jibu lote. Utaratibu ule unahitaji ufanye imani katika uwezo wa kujibu wa Baba yetu. Hali wakati mwingine ni vigumu sana, huleta ukuaji muhimu wa kibinafsi” (“Using the Supernal Gift of Prayer,” Ensign or Liahona, May 2007, 9).

Waalike wanafunzi kujibu maswali yafuatayo kwenye daftari au shajara za kujifunza ma-andiko. Unaweza kutaka kuyaandika kwenye ubao au kuyasoma pole pole ili wanafunzi waweze kuyaandika.

Kujenga hamu na lengo.Panga shughuli ambazo zitajenga hamu na kuwasaidia wanafunzi kulenga usikivu wao kwenye maandiko katika somo. Hizi shughuli zinakuwa zinafana zaidi wakati zinakuwa fupi na wakati wanafunzi wana-polenga kanuni muhimu za somo.

Page 543: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

528

SoMo la 144

• Ni wakati gani ulifuata msukumo wa kiroho na kisha kupokea maelekezo zaidi kutoka kwa Mungu?

• Kwa nini unafikiri wakati mwingine tunahitaji kujibu msukumo wa kiroho kabla ya sisi kupokea ufunuo zaidi?

Fanya muhtasari wa Etheri 2:8–12 kwa kuelezea kwamba Bwana alimwambia ndugu ya Yaredi kwamba wakati Wayaredi walipowasili katika nchi ya ahadi, wangehitaji “kumtumikia yeye, Mungu wa kweli na pekee” (Etheri 2:8) kama wangetaka kuwa taifa kubwa Yeye ali-kuwa amewaahidi na wangeweza kuwa. Ikiwa hawatamtumikia Yeye, “wangefagiliwa mbali” (Etheri 2:8–10). Moroni alisema kwamba hii ilikuwa “amri ya milele” (Etheri 2:10), ikimaani-sha kwamba ingekuwa hivyo kwa wale wote ambao wangeishi katika nchi hio.

Etheri 2:13–15Bwana anamrudi ndugu ya Yaredi kwa kutomwita Yeye katika maombiWaalike wanafunzi wasome Etheri 2:13–15 kimya kimya, wakitafuta kile Wayaredi walikifa-nya walipofika pwani.• Wayaredi walifanya nini? (Walijenga mahema yao na kukaa pwani kwa miaka minne.)• Kwa nini Bwana alimrudi ndugu ya Yaredi?• Tunaweza kujifunza nini kutoka kwa Etheri 2:14? (Wanafunzi wanaweza kutambua

kweli tofauti, ikijumuisha ifuatayo: Bwana anataka sisi tumwite Yeye kila mara katika maombi; Bwana hapendezwi wakati tunapokosa kumwita Yeye katika maombi; na Roho hawezi kukaa nasi ikiwa tunatenda dhambi.)

Waambie wanafunzi wafikirie kuhusu maombi yao kibinafsi unaposoma taarifa ifuatayo ya Mzee Donald L. Staheli wa Sabini.“Maombi ya dhati ya kila siku ya kutafuta msamaha na usaidizi maalum na maelekezo ni muhimu kwa maisha yetu na kustawisha shuhuda zetu. Wakati tunaharakisha, kurudia, kuzembea, au kusahau katika maombi yetu, tunakosa kuwa karibu na Roho, ambaye ni muhimu katika mfululizo wa maelekezo tunayohitaji ili kufanikiwa kudhibiti changamoto za maisha yetu ya kila siku” (“Securing Our Testimonies,” Ensign au Liahona, Nov. 2004, 39).Andika maswali yafuatayo kwenye ubao kabla ya darasa. (Au unaweza kutaka kuyata-yarisha kwenye kitini au kuyasoma polepole ili wanafunzi waweze kuyaandika.) Wape wanafunzi dakika mbili au tatu ili waandike majibu mafupi ya maswali haya katika daftari au shajara za kujifunza maandiko.

Unahisi vipi kuhusu marudio ya maombi yako ya kibinafsi?Unahisi vipi kuhusu uaminifu wa maombi yako ya kibinafsi?Katika maombi yako ya kibinafsi, unahisi kwamba wewe kweli unawasiliana na Baba wa Mbinguni? Ndio kwa nini au la kwa nini?Kama ungeweza kufanya badiliko moja ili kuboresha maombi yako ya kibinafsi, lingekuwa badiliko gani hilo?

Etheri 2:16–25 (pia Etheri 3:1–6; 6:4–9)Wayaredi walijenga mashua ili kuvuka bahari hadi kwenye nchi ya ahadiWaambie wanafunzi wafikirie juu ya changamoto wanazoweza kuwa nazo au maamuzi muhimu wanayoweza kuyafanya, sasa au katika siku za usoni. Kwa mfano, wanaweza kufikiria kuhusu hali ngumu ya familia, changamoto shuleni, kuamua ni nani wa kuoa, au kuchagua kazi ya ajira. Waalike wao watafakari jinsi Bwana anaweza kuwapa maelekezo au usaidizi. Wanapojifunza sehemu zingine za Etheri 2, wahimize wao kutafuta kanuni ambazo zitawasaidia wao kupokea usaidizi wa Bwana katika kufanya uamuzi mzuri.Alika mwanafunzi asome Etheri 2:16,–17 kwa sauti. Liambie darasa lifuatilie, likitafuta kile Bwana aliwaambia Wayaredi kufanya ili kufanikiwa kwenda nchi ya ahadi. Wakati mwana-funzi amemaliza kusoma, uliza kama mmoja wao angependa kuja ubaoni na kwa haraka akachora vile anafikiria mashua ya Wayaredi ilivyofanana.Nakili chati ifuatayo kwenye ubao bila kujumuisha majibu katika mistari mitatu ya chini. Wagawie chati kama kitini au waambie wanafunzi wainakili katika daftari au shajara za kujifunza maandiko.

Page 544: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

529

etheRi 2

etheri 2:18–19 etheri 2:20–25; 3:1–6; 6:4–9

Shida za mashua. Suluhisho alichokifanya bwana. alichokifanya ndugu ya yaredi.

hamna hewa. Weka matundu ambayo yanaweza kufunguliwa na kufu-ngwa kwa juu na chini ya mashua.

alimpa yaredi maelekezo.

Waliweka matundu.

hamna usukani. Upepo utasukuma mashua kwenda nchi ya ahadi.

alifanya upepo uvume.

amini katika bwana.

hamna mwanga. tayarisha mawe maalum na muombe bwana ayaguse ili yang’ae.

alimshauri ndugu ya yaredi kuhusu vitu ambavyo havitafanya kazi na kumwelekeza yeye kutafuta suluhisho ambalo litafanya kazi.aliyagusa mawe baada ya ndugu ya yaredi kuyatayarisha.

alitayarisha mawe na kumwomba bwana ayaguse ili yaweze kung’aa gizani.

Waalike wanafunzi wapekue Etheri 2:18–19 peke yao ili kutafuta shida tatu ambazo ndugu ya Yaredi aliziona katika mashua hizo.• Ni shida gani ambazo ndugu ya Yaredi aligundua? (Andika majibu ya wanafunzi katika

safu ya kwanza ya chati, kama inavyoonyesha. Wahimize kufanya vivyo hivyo kwenye nakala zao za chati.)

Baada ya wanafunzi kutambua shida, waalike wao kujifunza Etheri 2:20–25; 3:1–6; 6:4–9. (Tazama: Vishazi katika Etheri 3 na 6 vitazungumziwa kwa utondoti zaidi katika masomo ya 145 na 147.) Wape muda wa kukamilisha sehemu zilizobaki za chati.Wanafunzi watakapokuwa na muda wa kutosha wa kukamilisha chati, waulize maswali yafuatayo ili kuwasaidia kutambua kanuni kutoka katika uzoefu wa ndugu ya Yaredi:• Kulingana na suluhisho la shida ya hewa, Bwana wakati mwingine huwa anatusaidia

vipi kusuluhisha shida zetu au kujibu maswali yetu? (Wakati mwingine Bwana hutua-mbia jinsi ya kutatua tatizo na hutarajia sisi kufuata maelekezo Yake.)

• Kulingana na suluhisho la shida za usukani, ni kwa jinsi gani wakati mwingine Bwana hutusaidia kutatua matatizo yetu au kujibu maswali yetu? (Wakati mwingine Bwana ushughulikia suluhisho Yeye mwenyewe.)

• Kulingana na suluhisho la kuhusu mwanga, ni jinsi gani wakati mwingine Bwana hutu-saidia kutatua matatizo yetu au kujibu maswali yetu? (Wakati mwingine Bwana hututaka sisi tutafute suluhisho na kumuomba idhinisho Lake na usaidizi katika kulitekeleza.)

Andika kanuni ifuatayo kwenye ubao: Tunapomuomba Bwana na kutenda sehemu yetu ya kutatua shida zetu, tunaweza kupokea usaidizi wa Bwana. Ili kuwasaidia wanafunzi kutumia kanuni hii, waambie wafikirie maamuzi muhimu waliyoyawaza dakika chache zilizopita. Kisha waambie watafakari maswali yafuatayo:• Unafikiria Bwana anaweza kutarajia nini kutoka kwako katika kufanya maamuzi haya?• Bwana anaweza kufanya nini ili kukusaidia?• Unaweze kuuonyesha vipi imani katika Bwana unavyofikiria kuhusu maamuzi haya?Wape wanafunzi dakika chache kuandika kuhusu kile walichojifunza leo. Toa ushuhuda wako kwamba tunapomwita Bwana kwa uaminifu na kutenda tunayopaswa ili kutatua matatizo yetu, Yeye atatuelekeza na kutusaidia kulingana na hekima na uwezo Wake.

Page 545: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

530

UtanguliziKujibu swali la Bwana —“Ungetaka nifanye nini ili muwe na mwangaza kwenye mashua zenu? —ndugu ya Yaredi alitayarisha mawe kumi na sita na kwa unye-nyekevu alimuomba Bwana kuyagusa “ili yaangaze kwenye giza” (Etheri 2:23; 3:4). Kwa sababu ndugu ya Yaredi alikuwa na imani kuu, yeye aliona kidole cha

Mwokozi kikigusa mawe. Kisha Bwana alijionyesha Mwenyewe kwa ndugu ya Yaredi na kufunua mambo mengi. Bwana alimwamuru ndugu ya Yaredi kuandika kile yeye ameona na kusikia na kufunga maandishi hayo hadi Bwana atakapotaka yatokeze.

SOMO LA 145

etheri 3

Mapendekezo ya Kufundisha

Etheri 3:1–20Bwana anayagusa mawe ili kuyapa mwanga kwa ajili ya mashua za Wayaredi na anajionyesha Mwenyewe kwa ndugu ya YarediMwalike mwanafunzi awe kama mwandishi. Kisha waulize wanafunzi swali lifuatalo na mwambie mwandishi kuorodhesha majibu ya wanafunzi kwenye ubao.• Ni nini baadhi ya vitu ambavyo vijana wanaomba kwa uaminifu?Waambie wanafunzi kufikiria kwamba mmoja wa marafiki zao anaomba kwa mojawapo ya vitu vilivyoorodheshwa kwenye ubao. Rafiki huyu angependa kujua jinsi ya kuboresha maombi na matendo yake ili aweze kupokea usaidizi na mwongozo wa Bwana. Wahimize wanafunzi kufikiria kuhusu maombi haya wanapojifunza mfano wa ndugu ya Yaredi katika Etheri 3, wakitafuta umaizi ambao wanaweza kushiriki na rafiki yao.Wakumbushe wanafunzi kwamba katika somo lililopita, walijadili tukio la ndugu ya Yaredi akimuuliza Bwana kuhusu jinsi ya kupata mwanga katika mashua za Wayaredi.• Ndugu ya Yaredi alifanya nini ili kusaidia kuleta mwanga kwenye mashua? (Ona Etheri 3:1.)• Ndugu ya Yaredi alimuomba nini Bwana ili kuleta mwanga? (Ona Etheri 3:1, 4.)• Nini kinachokupendeza kuhusu juhudi za ndugu ya Yaredi?Taja kwamba ndugu ya Yaredi alifanya juhudi kubwa ili kutayarisha mawe. Kisha waalike wanafunzi kufikiria jinsi hayo mawe yanavyoweza kuwa na nguvu za kutoa mwanga kama Bwana asingeyagusa. Waalike wanafunzi wasome Etheri 3:2–5 kimya, wakitafuta vishazi ambavyo vinaonyesha kwamba ndugu ya Yaredi alitambua utegemezi wake kwa Bwana.Baada ya wanafunzi kuwa na muda wa kusoma, wagawe katika makundi. Waambie wao waelezeane walichopata mmoja kwa mwingine. Pia pendekeza kwamba waelezane kile kinachowapendeza kuhusu maombi ya ndugu ya Yaredi.Wakati wanafunzi wakisoma Etheri 3:2, wanaweza kuwa na maswali kuhusu vishazi “sisi hatufai mbele yako” na “maumbile yetu yamekuwa maovu siku zote.” Wasaidie wao kuona kwamba wakati ndugu ya Yaredi akitumia maneno haya, alimaanisha hali tuliyoirithi “kwa sababu ya anguko.” Sisi tunatenganishwa kimwili na kiroho kutoka kwa Mungu, na tuna-jitenga zaidi kutoka kwake tunapotenda dhambi. Tukilinganishwa na Yeye, sisi ni wadhaifu na hatufai. Bila ya usaidizi Wake, sisi hatungeweza kurudi kuishi katika uwepo Wake.Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa zaidi maana ya vifungu walivyosoma, waulize maswali yafuatayo:• Unafikiri kwa nini ni muhimu kwetu kutambua utegemezi wetu juu ya Bwana tunapoo-

mba usaidizi Wake?• Katika Etheri 3:1–5, ni ushahidi gani unaona ambao ndugu ya Yaredi alikuwa na imani

ambayo Bwana angeweza kumsaidia kusuluisha shida yake? (Kama inavyohitajika, washauri wanafunzi watafute vishazi ambavyo vinaelezea juhudi za ndugu ya Yaredi na vishazi ambavyo vinaonyesha imani yake katika Bwana.)

Page 546: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

531

etheRi 3

Ili kusisitiza nguvu za imani za ndugu ya Yaredi, waambie wanafunzi wasome taarifa ifua-tayo ya Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili:“Hakika Mungu, vile vile msomaji, huhisi kitu kinachosisimua katika umaasumu ya utoto na ari ya imani ya mtu huyu. ‘Tazama, Ee Bwana, hauwezi kufanya hivi.’ Labda hakuna tena nguvu, mstari mmoja wenye nguvu wa imani uliosemwa na mtu katika maandiko. . . . Hata hivyo vyovyote nabii anavyohofia kuhusu uwezo wake wenyewe, yeye hana hofu kuhusu nguvu za Mungu” (“Rending the Veil of Unbelief,” in Nurturing Faith through the Book of Mormon: The 24th Annual Sidney B. Sperry Symposium [1995], 12).Onyesha picha ya ndugu ya Yaredi Anakiona Kidole cha Bwana (62478; Gospel Art Book [2009], no. 85). Alika mwanafunzi kusoma Etheri 3:6. Liambie darasa lifuatilie pamoja na kufikiria kile uzoefu ulioandikwa katika kifungu hiki inaweza kuwa kama ilivyokuwa kwa ndugu ya Yaredi.• Unaweza kufikiria au kuhisi nini kama wewe ungepata uzoefu kama ule wa ndugu ya

Yaredi?Fanya muhtasari Ether 3:6–8 kwa kuelezea kwamba wakati ndugu ya Yaredi aliona kidole cha Bwana, yeye “alianguka chini mbele ya Bwana” (Ether 3:6). Yeye alishangaa kuona kwamba kidole cha Bwana “kilikuwa kama kidole cha mtu, sawa kama mwili na damu” (Etheri 3:6). (Ndugu ya Yaredi baadaye alijifunza kwamba yeye alikuwa ameona sehemu ya mwili wa kiroho wa Bwana [ona Etheri 3:16].)Alika wanafunzi wasome Etheri 3:9 kimya kimya, wakitafuta sababu za kwa nini ndugu ya Yaredi aliweza kuona kidole cha Bwana.Baada ya wanafunzi kujibu, andika taarifa isiyokamili kwenye ubao:

Tunapomwita Bwana kwa unyenyekevu, Yeye atatubariki kulingana na yetu na mapenzi Yake.Waambie wanafunzi wapendekeze maneno ambayo yanaweza kutumika ili kujaza taarifa hii. Wanafunzi wanafaa kupendekeza kwamba neno imani linakamilisha sentensi. Wana-weza pia kupendekeza maneno kama vile juhudi, unyenyekevu, haja, na ukweli.Wasaidie kuona kwamba maneno haya yote yanawakilisha muonekano wa imani zetu. Kisha kami-lisha taarifa hii kwenye ubao: Tunapomwita Bwana kwa unyenyekevu, Yeye atatubariki kulingana na imani yetu na mapenzi Yake.Rejelea nyuma kwenye orodha kwenye ubao kutoka mwanzoni wa somo. Chagua kitu kimoja au viwili kutoka kwenye orodha. Waalike wanafunzi kushiriki mawazo yao juu ya jinsi mtu anaweza kuonyesha imani katika Bwana katika hizo hali mahususi. Baada ya wanafunzi kushiriki mawazo, rejea kanuni ulizoziandika kwenye ubao.• Ni uzoefu gani umeshapata ambao umekusaidia kujua kwamba kanuni hii ni ya kweli?Ili kuwasaidia wanafunzi kutumia kanuni hii katika maisha yao, waalike wao kufikiria tukio ambalo wanahitaji usaidizi wa Bwana. Wapatie muda wa kuandika katika daftari au shajara za kujifunza maandiko kuhusu njia moja wanayoweza kuwa na imani zaidi wanapotafuta usaidizi wa Bwana kwa unyenyekevu. Wahimize wanafunzi kufuatilia kwa makini yale waliyoyaandika. Unaweza kutaka kuelezea uzoefu uliopata wakati ulipopokea baraka kwa sababu ulionyesha imani katika Bwana.Alika mwanafunzi asome taarifa ifuatayo, ambayo Mzee Jeffrey R. Holland anaelezea kwa-mba uzoefu wetu uliopita unaweza kuimarisha imani yetu.“Imani ya matayarisho hujengwa kwa uzoefu katika wakati uliopita—kwa yanayojulikana, ambayo yanatoa msingi wa imani” (Christ and the New Covenant: The Messianic Message of the Book of Mormon [1997], 18).• Kuanzia kwenye Mnara wa Babeli, ni matukio gani ndugu ya Yaredi aliyapata ambayo ya-

limwezesha kuimarisha imani yake katika Bwana? Unafikiri uzoefu huu ulimtayarishaje yeye kufanya imani yake iwe kubwa kiasi hicho wakati alipoyapeleka mawe kwa Bwana?

Alika wanafunzi kugawanyika katika majozi na kujadili maswali yafuatayo:• Ni uzoefu gani ambao uliimarisha imani yako katika Bwana? Uzoefu kama huu unaweza

vipi kukutayarisha kufanya imani kuu baadaye katika maisha yao?Waalike wanafunzi wachache kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka Etheri 3:9–12. Liambie darasa lifuatilie nyuma. Kisha uliza swali lifuatalo:• Wakati Bwana alipouliza “Utaamini maneno ambayo nitayasema?” Ndugu ya Yaredi ali-

sema, “Ndio, Bwana” (Etheri 3:11–12) Kwa nini unafikiria ni muhimu kwamba ndugu ya Yaredi angeweka sharti kuamini maneno ya Bwana kabla ya yeye kuyasikia?

Kuelezea uzoefu wa kibinafsiWakati unapoelezea uzoefu uliopata ulipo-tafuta kuishi kanuni za injili, unaweza kuwasai-dia wanafunzi kuelewa jinsi ya kutumia kanuni hizo wenyewe. Fanya hadithi zako kuwa fupi, na kila mara jumuisha taarifa za ushuhuda ambazo zinafafanua kile ulichojifunza au jinsi ulivyobarikiwa kupitia uzoefu wako. Hii itaalika Roho Mtakatifu kutoa ushahidi wa kweli unazoshiriki.

Page 547: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

532

SoMo la 145

Elezea kwamba baada ya Mzee Holland kufundisha kuhusu imani ambayo inahusu ma-tukio yaliyopita, yeye alifundisha kuhusu imani kamili zaidi ambayo tunahitaji kuikuza. Mwalike mwanafunzi kusoma kwa sauti taarifa ifuatayo ya Mzee Holland:

“Imani ya ukombozi lazima kila mara ifanywe kwa uzoefu katika siku za usoni—zisojulikana, ambazo zinatoa nafasi ya miujiza. Kufanyiza imani, imani ya kuondosha milima, imani kama ile ya ndugu ya Yaredi, inapita muujiza na maarifa. Imani ni kukubali bila masharti—na mapema—katika hali yoyote ambayo Mungu anaweza kuhitaji kwa wakati huu na siku za usoni.“Imani ya ndugu ya Yaredi ilikuwa kamili” (Christ and the New Covenant, 18–19).

Wahimize wanafuzni kufikiria kama wana imani ya kutosha katika Bwana hata kuweka sharti la kuamini na kufuata kile Yeye atafunua kwao hata kabla Yeye hajakifunua.Waalike wanafunzi wasome Etheri 3:13–20 kimya, wakitafuta baraka alizopokea ndugu ya Yaredi kwa sababu ya imani yake. Unaweza kutaka kuwapa wao muda wa kuandika ku-husu kweli alizojifunza na uzoefu aliokuwa ameupata. Wanafunzi wanapokuwa wamepata muda wa kuandika, fikiria kuwauliza wachache wao kushiriki kile walichokiandika.Mapema katika somo hili, wakati wanafunzi waliposoma kuhusu ndugu ya Yaredi akiona kidole cha Bwana, uliuliza jinsi wangehisi kama wao wangekuwa na uzoefu kama huu. Sasa, baada ya wao kusoma zaidi kuhusu uzoefu wa ndugu ya Yaredi, unaweza kufikiria kuuliza swali hilo tena.Shuhudia kwamba tunapofanya imani kama ile ya ndugu ya Yaredi, tutamkaribia zaidi Bwana.

Etheri 3:21–28Bwana anamwamuru ndugu ya Yaredi kuandika mambo aliyokuwa ameyaona na kufunga kumbukumbu yakeAlika mwanafunzi asome Etheri 3:25–26, na liambie darasa kutambua kile Bwana alimwo-nyesha ndugu ya Yaredi katika ono. Waalike wanafunzi kuripoti kile walichojifunza.Fanya muhtasari wa Etheri 3:21–24, 27–28 kwa kuelezea kwamba Bwana alimwamuru ndugu ya Yaredi kuandika mambo aliyokuwa ameyaona na kusikia na kufunga maandishi yake. Bwana pia alielezea kwamba Yeye atatayarisha njia kwa ajili ya maandishi ya ndugu ya Yaredi yaweze kutafsiriwa katika siku za usoni—kupitia mawe mawili. Haya mawe yalikuwa sehemu ya kile kilichoitwa Urimu na Thumimu (ona M&M 17:1; ona pia Bible Dictionary, “Urim and Thummim”).Hitimisha kwa kuwahimiza wanafunzi kutumia kile walichojifunza leo—ili kutafuta njia za kuonyesha imani yao na kuamini katika Bwana. Toa hakikisho lako kwamba tunapofanya imani katika Yesu Kristo, Mungu atatubariki kama alivyombariki ndugu ya Yaredi.

Tangazo na Habari za UsuliEther 3:15. “Kamwe sijajionyesha kwa binadamu”

Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alionyesha maelezo yanayowezekana kwa ta-arifa ya Yesu kwamba Yeye kamwe hajajionyesha kwa mtu kabla ya kujionyesha Yeye Mwenyewe kwa ndugu ya Yaredi:

“Kristo alikuwa anasema kwa ndugu ya Yaredi, ‘Kamwe sijajionyesha kwa binadamu katika njia hii, bila ya hiari yangu, iliyosababishwa kabisa na imani ya anayeona.’ Kama sheria, manabii hualikwa katika uwepo wa Bwana, na wanakaribishwa kuingia uwepo wake na yeye na tu kwa ruhusa yake. Ndugu ya Yaredi, kwa

upande mwingine, huonekana alijisukuma mwenyewe kupitia katika pazia, lakini si kama mgeni ambaye ha-kukaribishwa bali kama mtu ambaye hakualikwa. Kwa kweli Bwana mwenyewe alikuwa anaunganisha imani ambayo haijapata kuonekana na ono hili ambalo halija-pata kuonekana tena. Ikiwa ono lenyewe halikuwa la kipekee, basi ilikuwa sharti iwe ni imani na jinsi ono lilivyopatikana hiyo haijapata kuonekana tena. Njia pe-kee ambayo imani ingeweza kuwa ya ajabu ilikuwa ni uwezo wake wa kumpeleka nabii, ambaye hakualikwa, pale wengine wameweza kwenda tu kwa ruhusa ya Mungu” (Christ and the New Covenant: The Messianic Message of the Book of Mormon [1997], 23).

Page 548: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

533

Somo la Mafunzo - NyumbaniMormoni 8:12–Etheri 3 (Kitengo cha 29)

Vifaa vya Matayarisho kwa Mwalimu wa Mafunzo - NyumbaniMuhtasari wa Masomo ya Kila Siku ya Mafu-nzo - NyumbaniMuhtasari ufuatao wa mafundisho na kanuni wanafunzi walijifunza walipokuwa wakisoma Mormoni 8:12–Etheri 3 (kitengo cha 29) haidhamiriwi kufundishwa kama sehemu ya somo. Somo unalofundisha linazingatia machache tu ya haya mafundisho na kanuni. Fuata msukumo wa Roho Mtakatifu unapofikiria mahitaji ya wanafunzi wako.

Siku ya 1 (Mormoni 8:12–41)Wanafunzi waligundua kwamba Moroni aliona siku yetu na kwamba yeye aliandika maelezo ya kinabii ya hali ambayo sisi tunaishi. Walikuwa wameweza kuona kwa nini Kitabu cha Mormoni ni zawadi ya thamani kutoka kwa Bwana ambacho kinaweza kutuongoza hadi siku za mwisho. Kuli-ngana na maelezo ya Moroni ya siku za mwisho, wanafunzi pia walijifunza kwamba Mungu atatuwajibisha kwa jinsi tunavyowatendea maskini na wale walio na mahitaji.

Siku ya 2 (Mormoni 9)Moroni alikamilisha kumbukumbu ya baba yake kwa kuta-ngaza kwamba ikiwa sisi tutatubu na kumwita Mungu, tuta-kuwa bila mawaa wakati tutakapokuja katika uwepo Wake. Kutoka Moroni, wanafunzi wamejifunza kwamba kwa sababu Mungu habadiliki, Yeye atafanya miujiza kulingana na imani ya watoto Wake na kwamba kama sisi tutaomba kwa imani kwa Baba wa Mbinguni katika jina la Yesu Kristo, Yeye atatupa baraka ambazo zitatusaidia sisi kufanyia kazi wokovu wetu.

Siku ya 3 (Etheri 1–2)Wanafunzi walijifunza kwamba kitabu cha Etheri ni ufupisho wa Moroni wa mabamba 24 ya dhahabu yaliyopatikana na watu wa Limhi, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Mosia. Mabamba haya yalitoa maelezo ya Wayaredi, ambao walio-ngozwa na Bwana hadi kwenye nchi ya ahadi. Kwa kujifunza uzoefu wa Wayaredi, wanafunzi walijifunza kwamba kama tutatenda kwa imani juu ya maelekezo ambayo Bwana ame-tupatia, tunaweza kupokea mwongozo zaidi kutoka Kwake. Wakati mmoja katika safari yao hadi nchi ya ahadi, Bwana alimrudi ndugu ya Yaredi kwa kukataa kumwita Yeye. Kwa kujifunza uzoefu huu, wanafunzi wamejifunza umuhimu wa kumwita Baba wa Mbinguni kila mara katika maombi. Uzoefu wa ndugu ya Yaredi na Bwana alipokuwa akijenga mashua uliwasaidia wanafunzi kutambua kwamba tuna-pomwita Bwana na kutenda sehemu yetu ili kutatua shida zetu, tunaweza kupokea usaidizi wa Bwana.

Siku ya 4 (Etheri 3)Ndugu ya Yaredi alipojaribu kutatua shida ya kupata mwa-nga katika mashua, yeye alionyesha kwamba tunapomwita Bwana kwa unyenyekevu, Yeye atatubariki sisi kulingana na imani yetu na mapenzi Yake. Wanafunzi wamejifunza kwa-mba sisi tunapofanya imani katika Bwana, tutakuwa karibu na Yeye. Ndugu ya Yaredi aliishi kanuni hizi, na yeye aliona mwili wa kiroho wa Mwokozi na ono la ajabu la wakazi wote wa ulimwenguni.

UtanguliziKitabu cha Etheri ni ufupisho wa Moroni wa kumbukumbu ya Wayaredi. Nabii Etheri alitengeneza kumbukumbu kwenye ma-bamba 24 ya dhahabu, ambazo yalipatikana na kundi la Mfalme Limhi. Wazo la kufundisha lifuatalo litawasaidia wanafunzi kuelewa kanuni fulani kuhusu maombi ambayo yanafundishwa katika Etheri 1.

Mapendekezo ya Kufundisha

Etheri 1Kupitia maombi ya ndugu ya Yaredi, yeye na familia yake walipo-kea neema na mwongozoAnza darasa kwa kuwauliza wanafunzi kuhusu hali waliyokuwa nayo wakati walihisi hasa haja ya kuomba usaidizi. Waalike wa-nafunzi wachache kushiriki uzoefu wao, au kushiriki mojawapo wa uzoefu wao wenyewe.

Wakumbushe wanafunzi kwamba kitabu cha Etheri ni ufupisho wa Moroni wa kumbukumbu ya Wayaredi. Yaredi, ndugu yake, marafiki zao, na familia zao waliishi wakati wa Mnara wa Babeli (takribani miaka 2200 K.K), Alika mwanafunzi asome Etheri 1:33–35 kwa sauti, na uwaulize washiriki wa dararsa watafute kwa nini Yaredi na ndugu yake walihitaji maombi ya usaidizi. Kabla ya mwanafunzi kusoma, unaweza kutaka kuuliza kwamba kishazi “mlilie Bwana” ni njia nyingine ya kusema “kuomba.” Kisha uliza maswali yafuatayo:

• Ni usaidizi gani Yaredi na ndugu yake walihitaji kutoka kwa Bwana?

• Vifungu hivi vinakuambia nini kuhusu jinsi Yaredi alihisi ku-husu imani ya ndugu yake?

Gawa wanafunzi katika jozi. Alika kila jozi kuchukua zamu kusoma kwa sauti mmoja kwa mwingine kutoka Etheri 1:35–42. Kabla ya wao kusoma, waambie watafute (1) kila wakati ndugu ya Yaredi alimlilia Bwana na (2) kila wakati Bwana akionyesha huruma kwa ndugu ya Yaredi kama matokeo ya maombi yake. Baada ya muda wa kutosha, alika jozi chache kushiriki mfano wa

Page 549: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

534

SoMo la MafUnzo - nyUMbani

Bwana wa kuonyesha huruma kwa ndugu ya Yaredi na familia yake kwa sababu ya maombi yao ya kila mara.

Uliza: Ni kanuni gani tunaweza kujifunza kuhusu maombi katika vifungu hivi? (Wanafunzi wanaposhiriki kanuni walizotambua, sisitiza kanuni ifuatayo: Tunapomsihi Mungu kila mara kwa imani, Yeye atakuwa na huruma kwetu. Andika kanuni hii kwenye ubao.)

Elezea wanafunzi kwamba ni muhimu kukumbuka kwamba “maombi ni kitendo ambacho kwacho mapenzi ya Baba na mapenzi ya mtoto yanaletwa katika uwiano na kila mmoja na mwingine. Madhumuni ya maombi si kubadilisha mapenzi ya Mungu, bali ni kupata kwetu na wengine baraka ambazo Mungu alikuwa tayari anataka kutupa, lakini hutendeka chini ya masharti ya kuziuliza” (Bible Dictionary, “Prayer”)

Waulize wanafunzi kurejea Etheri 1:34, 36, 38 na kutafuta kile ndugu ya Yaredi aliomba katika maombi yake. Muombe mwanafunzi kuorodhesha mambo ambayo wanafunzi walita-mbua chini ya kishazi “kusihi Mungu” katika kanuni ulioandika kwenye ubao.

Sisitiza kwamba Yaredi na ndugu yake walikuwa na imani na walikuwa tayari kuwa watiifu kwa Bwana. Pendekeza kwamba wanafunzi waweke alama kishazi “acha tuwe waaminifu kwa Bwana” hapo mwisho wa Etheri 1:38.

Waalike wanafunzi kurejea Etheri 1:35, 37, 40–42 na kutafuta njia mahususi ambazo Mungu alimbariki ndugu ya Yaredi na familia yake na marafiki zake. Wanafunzi wanapotambua baraka hizi, acha mwanafunzi aziorodheshe chini ya neno huruma ka-tika kanuni iliyoandikwa kwenye ubao. Sisitiza kwamba Bwana alimpa ndugu ya Yaredi baraka ambazo yeye aliomba.

Andika maswali yafuatayo kwenye ubao, au yatayarishe kwenye kitini. Waambie wanafunzi warejee kanuni zilizoandikwa kwenye ubao na, katika makundi yao, wajadili maswali. Maswali haya yatawasaidia wao kuelewa na kuhisi umuhimu wa kanuni hii.

Unafikiria “kumlilia Mungu” kunatofautinaje na “kutoa maombi”?

Wakati gani wewe au mtu fulani unayemjua waliona huruma ya Baba wa Mbinguni katika majibu ya maombi?

Unaweza kujifunza nini kuhusu Bwana kutokana na majibu Yake ya maombi ya ndugu ya Yaredi?

Wanafunzi watakapopata muda wa kujadili maswali haya, unaweza kuwaomba waelezee uzoefu waliojadili katika makundi yao au waelezee umaizi kutokana na majadiliano.

Shiriki ushuhuda wako juu ya upendo wa Baba wa Mbinguni kwetu na hamu Yake ya kutubariki sisi tunapomwita Yeye kila mara. Waalike wanafunzi kufikiria jinsi wanaweza kutumia kanuni hii kwenye ubao. Kwa mfano, wanaweza kuweka lengo

la kuomba kila mara zaidi au kuchagua njia moja ya kufanya maombi yao kuwa ya uaminifu zaidi. Unaweza kupendelea kuwapatia wao muda wa kuandika kile wanachotamani kufanya katika shajara zao za kujifunza maandiko.

Elezea kwamba kujifunza juu ya maombi ya ndugu ya Yaredi kunaweza kutupa ufahamu wa ziada juu ya upendo wa Bwana kwetu na baraka ambazo zitakuja kupitia maombi. Mualike mwanafunzi asome1 Etheri1:43–15 kwa sauti. Liombe darasa kufuatilia, wakitafuta baraka za ziada ambazo Mungu alimuahidi Yaredi na ndugu yake. Baada ya wanafunzi kuripoti kile walicho-jifunza, sisitiza kwamba ndugu ya Yaredi hakuwa ameomba ma-hususi baraka za kuwa na uzao wake kuwa taifa kuu. Unaweza kupendekeza kwamba wanafunzi waweke alama katika maa-ndiko yao hapo mwisho wa Etheri 1:43 ambayo itaonyesha kwa nini Mungu alijibu maombi ya ndugu ya Yaredi katika njia hii: “kwa sababu ya muda huu mrefu ambao umeomba kwangu.”

Uliza: Ni kanuni gani tunaweza kujifunza kutokana na ukarimu wa Bwana kwa Yaredi na ndugu yake, kama inavyoonyeshwa katika Etheri 1:43?

Kuna kanuni kadhaa ambazo zinaweza kujifunzwa kutoka katika maandiko haya. Kanuni moja muhimu ni: Ikiwa tutaomba kila mara kwa Mungu kwa imani, tunaweza kupokea baraka zaidi ya zile tulizoomba.

Uliza: Ni lini ulipata uzoefu ambao unaonyesha kanuni hii ni ya kweli? Je! Unamjua mtu ambaye ameshapata kuwa na uzoefu kama huo, au unaweza kufikiria mtu katika maandiko ambaye ameshaupata? (Waambie wanafunzi utawapatia muda wa kufi-kiria mifano kabla ya wewe kuwataka wao kujibu. Pia unaweza kutaka kushiriki mfano kutoka katika maisha yako mwenyewe.)

Ili kuhitimisha somo hili, toa ushuhuda wako kwamba Mungu husikia na hujibu maombi yetu. Yeye amejawa na hekima na hu-ruma na hufurahia kuwabariki watoto Wake. Yeye upendezwa wakati sisi tunamuomba Yeye kwa uaminifu kila mara. Wahimize wanafunzi kufanya juhudi za kuomba kwa imani zaidi. Wahi-mize wao kukumbuka kwamba Baba wa Mbinguni amejawa na huruma na atajibu maombi yao kulingana na kile Yeye anakijua kitaleta baraka kuu katika maisha yao.

Kitengo Kifuatacho (Etheri 4–12)Katika kitengo kifuatacho, wanafunzi watajifunza zaidi kuhusu Wayaredi. Ingawa manabii wanawaonya Wayaredi wasiteue wafalme, watu wanafanya hivyo, na wafalme wanawaingiza watu kwenye utumwa. Watu ambao wanatamani uwezo wa kilimwengu kwa kawaida wanatumia makundi ya siri kuende-leza ubinafsi wao. Moroni ameandika mambo mengi ya ajabu ambayo yalifanywa kwa sababu watu fulani walikuwa na imani kuu. Anafundisha kwamba wale ambao hujinyenyekeza we-nyewe mbele za Mungu na kuwa na imani katika Yeye watapo-kea neema Yake ili kuwasidia kushinda udhaifu wao.

Page 550: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

535

UtanguliziBwana alimwamuru Moroni kufunga ono lililoandikwa la ndugu ya Yaredi na kuelezea kwamba maandishi haya yangefunuliwa wakati watu watakapokuwa na

imani kama ndugu ya Yaredi alivyokuwa. Moroni alitoa unabii kwamba mashahidi watatu watatoa ushuhuda wa ukweli wa Kitabu cha Mormoni katika siku za mwisho.

SOMO LA 146

etheri 4–5

Mapendekezo ya Kufundisha

Etheri 4:1–7Moroni aliandika na kufunga taarifa kamili ya ono la Ndugu ya YarediWaalike wanafunzi kufikiria juu ya kitu ambacho hasa ni cha thamani kwao au familia yao na kwamba wanaweza kutaka kuweka mbali na watoto wadogo. Kama mfano, unaweza kutaka kuonyesha au kuelezea kitu ambacho ni cha thamani kwako.• Kwa nini wewe haungetaka kumruhusu mtoto kushika kitu hicho?• Mtoto angehitaji kujifunza au kufanya nini kabla wewe hujamwamini yeye na kitu hicho?Elezea kwamba kweli za injili ni za thamani kwa Bwana. Yeye anataka kushiriki zote pa-moja nasi, lakini Yeye hungojea hadi tunapokuwa tayari kuzipokea. Wanafunzi wanapojifu-nza Etheri 4 wakati wa somo hili, wahimize watafute kanuni ambazo zinaweza kuwasaidia kujitayarisha kupokea kweli kutoka kwa Bwana.Alika mwanafunzi kusoma Etheri 4:1–5, na liombe darasa kutafuta kile Bwana alimwa-muru Moroni kuandika na kufunga.• Ni nini Moroni aliamuriwa “kufunga”?Elezea kwamba Moroni alijumuisha kumbukumbu ya ndugu ya Yaredi katika kile ambacho kwa kawaida kinaitwa sehemu iliyofungwa ya Kitabu cha Mormoni. (Unaweza kutaka kuonyesha chati inayoitwa Vyanzo vya Kitabu cha Mormoni, ambavyo viko katika kiamba-tisho hapo mwishoni mwa kitabu hiki cha kiada.)• Moroni alielezea vipi kile ambacho ndugu ya Yaredi alikiona? (Ona Etheri 4:4.)Ili kuwasaidia wanafunzi kujifunza zaidi kuhusu kile Bwana alimuonyesha ndugu ya Yaredi, waalike wao kusoma Etheri 3:25–26 na 2 Nefi 27:8–10 kimya kimya. Kisha uliza maswali yafuatayo:• Kulingana na Etheri 3:25–26, ni nini Bwana alimuonyesha ndugu ya Yaredi?• Kulingana na 2 Nefi 27:10, sehemu iliyofungwa ya Kitabu cha Mormoni inajumuisha nini?Alika mwanafunzi asome Etheri 4:6–7 kwa sauti. Liombe darasa kufuatilia pamoja na ku-tambua masharti ambayo lazima yawepo kabla ya funuo hazijatolewa kwa ndugu ya Yaredi. Unaweza kutaka kuwahimiza wanafunzi kuweka alama kile wao wametambua katika maandiko yao.• Ni masharti gani ambayo ulitambua?• Ni kanuni gani kuhusu kupokea ufunuo tunaweza kujifunza kutoka katika kishazi hiki?

(Wasaidie wanafunzi kuona kwamba tunapotubu na kufanya imani katika Yesu Kristo, tunaweza kupokea ufunuo wa ziada.)

• Kwa nini unafikiria tunahitaji kutubu na kuwa wasafi ili kupokea ufunuo wa ziada?Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa nini maana ya kuendeleza imani hata kama ndugu ya Yaredi (Etheri 4:7), waalike wao kuorodhesha katika daftari au shajara za kujifunza maandiko njia nyingi kama unavyoweza kukumbuka kwamba ndugu ya Yaredi alionye-sha imani katika Bwana. Unaweza kupendekeza kwamba wao warejee Etheri 1–3 kama ilivyoandikwa katika orodha zao. Wakati watakapokuwa na muda wa kutosha kutafakari na kuandika, alika wanafunzi wachache kusoma mifano fulani ambayo wameorodhesha na kuelezea kwa nini mifano hii inawapendeza wao.

Page 551: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

536

SoMo la 146

Wakumbushe wanafunzi juu ya kitu cha thamani walichofikiria hapo mwanzoni mwa da-rasa na masharti ambayo kwayo wangemthaminisha nayo mtoto. Shuhudia kwamba kwa njia hii, Bwana anahitaji watoto Wake kufikia masharti fulani kabla Yeye hajafunua kweli Zake zote. Yeye hutuhitaji sisi kuonyesha utayari wetu wa kiroho na imani.

Etheri 4:8–19Bwana hutufundisha kile ambacho lazima tufanye ili kupokea ufunuo zaidiShika kipande cha kitambaa. Elezea kwamba Bwana alifundisha kanuni ambazo zinaweza kutusaidia kupokea ufunuo. Wakati Yeye alipofundisha kanuni hizi, Yeye alirejea katika pa-zia. Shela ni pazia au kipande cha kitambaa ambacho kinatumika kufunika au kuficha kitu.Alika wanafunzi wasome Etheri 4:15 kimya na kutafuta kishazi ambacho kinajumuisha neno pazia.• Ni aina gani ya pazia ambayo Bwana aliifananisha? (“Pazia la kutoamini.”) Kutoamini

kunafanana vipi na pazia?• Neno pasua humaanisha rarua au gawa. Unafikiria inamaanisha nini “kupasua pazia la

kutoamini”?Alika mwanafunzi mmoja asome Etheri 4:8 kwa sauti, na mwingine asome Etheri 4:11 kwa sauti, na mwingine asome Etheri 4:15 kwa sauti. Liombe darasa kufuatilia pamoja na kutambua kile kinachoweza kutuzuia sisi kupokea ufunuo na kile kinaweza kutusaidia sisi “kupasua pazia ya kutoamini” na kupokea ufunuo zaidi.• Unafikiri inamaanisha nini “kubishana dhidi ya neno la Bwana”? (Etheri 4:8).• Kulingana na Etheri 4:8, ni matokeo gani ambayo yanatukabili tunapobishana dhidi ya

neno la Bwana?• Kulingana na Etheri 4:11, ni baraka gani tunayopokea wakati tunaamini neno la Bwana?Andika taarifa ifuatayo isiyo kamili kwenye ubao:

Tunapoamini neno la Bwana, . . .Waambie wanafunzi kukamilisha taarifa hii kulingana na kile wao wamejifunza katika vifungu hivi. Ingawa majibu ya wanafunzi yanaweza kuwa tofauti, hakikisha wao wana-tambua kanuni ifuatayo: Wakati sisi tunaamini neno la Bwana, Bwana atatubariki sisi na ufunuo zaidi. Andika kanuni hii kwenye ubao. Unaweza pia ukataka kuwahimiza wanafunzi kuiandika katika maandiko yao karibu na Etheri 4:11.Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa kanuni hii, uliza:• Kwa nini unafikiria sisi tunahitaji kuamini kweli ambazo tayari tumezipokea kabla ya

Bwana kutupatia sisi zaidi?Mwambie mwanafunzi aandike kwenye ubao mifano ifuatayo ya kuendeleza imani katika neno la Bwana: kujifunza maandiko kibinafsi; kufuata msukumo kutoka kwa Roho Mtakatifu; kuwafuata viongozi wa Kanisa wa sehemu zetu; kujifunza maandiko kanisani na seminari; kufuata maneno ya manabii wa siku za mwisho.Waalike wanafunzi kutafakari jinsi ya kuonyesha imani katika neno la Bwana katika mojawapo ya njia hizi kumewawezesha wao kupokea ufunuo zaidi. Wahimize wanafunzi wachache kushiriki kile walichopata uzoefu nacho.Rejea tena kwenye mifano iliyoandikwa ubaoni. Waambie wanafunzi wafikirie ile mifano wanapotafakari kimya ni kwa jinsi gani wanaonyesha imani yao katika neno la Mungu. Pendekeza kwamba kwa kila mfano, wanajipima wenyewe katika kiwango cha 1 hadi 10, kiwango cha 10 kikimaanisha kwamba mfano huo unalenga kitu wanachofanya vyema. Waalike wanafunzi kuandika katika daftari zao au shajara za kujifunza maandiko kuhusu njia moja wanayoweza kuonyesha imani zaidi katika maelekezo ambayo tayari wamepo-kea kutoka kwa Bwana. Toa ushuhuda wako juu ya kanuni uliyoandika kwenye ubao, na wahimize wanafunzi kufuatilia wakiwa na malengo waliyoyaandika.Futa kishazi “amini neno la Bwana” kutoka kwenye ubao. Taja kwamba Bwana alifundisha kanuni za ziada kuhusu kupokea ufunuo. Waambie wanafunzi wasome Etheri 4:13–15 kimya kimya, wakitafuta vitu vingine wanavyoweza kufanya ili kupokea ufunuo kutoka kwa Bwana.Wanafunzi watakapopata muda wa kusoma, waambie wao kupendekeza njia za kukami-lisha taarifa hii. Majibu yanaweza kujumuisha kanuni zifuatazo: Wakati tunapokuja kwa

Page 552: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

537

etheRi 4 – 5

Bwana, Bwana atatubariki sisi kwa ufunuo zaidi. Wakati tunaomba kwa unyenye-kevu, Bwana atatubariki sisi kwa ufunuo zaidi.Ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa kanuni hizi vyema, fikiria kuuliza maswali yafuatayo:• Inamaanisha nini kwako kuja kwa Bwana? (Majibu yanaweza kujumuisha kujifunza

maneno Yake, kugeuza mioyo yetu Kwake, kutubu, na kumfuata na kumtii Yeye.)• Inamaanisha nini kuwa na moyo uliovunjika na roho iliyopondeka? (Kuwa mnyenye-

kevu, mwenye toba, na mpokeaji wa mapenzi ya Bwana. Kwa nini hii misimamo ni muhimu tunapoomba mfululizo wa ufunuo kutoka kwa Bwana?

Waalike wanafunzi kufikiria jinsi wao wanaweza kuingiza hizi kanuni katika juhudi zao za kupokea ufunuo.Fanya muhtasari wa Etheri 4:17–19 kwa kuelezea kwamba Bwana alitangaza kwamba kuja kwa Kitabu cha Mormoni kungekuwa ishara kwamba kazi ya Mungu katika siku za mwi-sho imeanza. Yeye pia alihimiza watu wote kutubu na kuja Kwake.

Etheri 5Moroni alitangaza kwamba mashahidi watatu wataona na kutoa ushuhuda wa mabamba hayaInua juu picha ya Joseph Smith akitafsiri Kitabu cha Mormoni (Gospel Art Book [2009], no. 92). Alika mwanafunzi asome Etheri 5:1–3 kwa sauti. Liambie darasa kufuatilia pamoja na kufikiria vile ingekuwa kwa Joseph Smith kutafsiri Kitabu cha Mormoni na kutambua kwa-mba ushauri huu uliandikwa moja kwa moja kwake na Moroni zaidi ya miaka 1400 iliyopita.• Moroni alisema nini kuhusu mabamba ambayo alikuwa “ameyafunga”?• Kulingana na Etheri 5:2–3, Joseph angekuwa na fursa ya kufanya nini na mabamba haya?Waulize wanafunzi kama wao wanaweza kuwataja Mashahidi Watatu wa Kitabu cha Mor-moni na wakumbuke kile wao walichokipata. (Kama wanafunzi wanahitaji usaidizi, wa-alike kusoma “Ushuhuda wa Mashahidi Watatu” mwanzoni mwa Kitabu cha Mormoni.) Unaweza kuelezea kwamba kama ziada ya Mashahidi Watatu, wengine wameshuhudia uhalisi wa mabamba ya dhahabu, ikijumuisha washiriki wa Uungu (ona Etheri 5:4), Moroni (ona Etheri 5:6), Joseph Smith, na Washahidi Nane.• Ni kwa njia gani wewe unaweza kuwa shahidi wa Kitabu cha Mormoni, hata bila ku-

yaona mabamba? Je! Ushuhuda wako wa Kitabu cha Mormoni unawezaje kuwaathiri vipi wengine?

Ili kuhitimisha somo hili, waambie wanafunzi wachache kutoa ushuhuda wao wa Kitabu cha Mormoni.

Page 553: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia

538

UtanguliziBaada ya kufanya matayarisho kulingana na amri za Bwana, Wayaredi wapanda kwenye vyombo vyao, wa-kitumaini kwamba Bwana angewapeleka wao kupitia safari yao ngumu hadi nchi ya ahadi. Bwana alituma upepo ambao ulisukuma mashua juu ya mawimbi na

kuwafunika wao katika bahari mara nyingi, hali upepo huo ulisukuma vyombo kuelekea nchi ya ahadi. Baada ya kujiendeleza wenyewe katika nchi mpya, watu wakamchagua mfalme, licha ya maonyo kutoka kwa ndugu ya Yaredi.

SOMO LA 147

etheri 6

Mapendekezo ya Kufundisha

Etheri 6:1–12Bwana alifanya upepo kuendesha mashua za Wayaredi hadi nchi ya ahadiKabla ya darasa, andika yafuatayo kwenye ubao:

Kushiriki injili na rafiki.Kukaa msafi kimaadili.Kuchagua marafiki walio na viwango vya juu.Kuweka vipaumbele sahihi katika maisha.

Sisitiza kwamba hii ni mifano ya mambo ambayo Bwana anataka sisi tuyafanye. Hata hi-vyo, watu fulani wanafikiria vitu hivi ni vigumu sana. Waalike wanafunzi kufikiria mifano mingine ambayo inaweza kuongezewa kwenye orodha. Elezea kwamba habari za safari ya Wayaredi hadi nchi ya ahadi zina kanuni ambazo zinaweza kutuongoza sisi wakati tu-naona ugumu wa kufanya yale ambayo Bwana ameamuru. Wahimize wanafunzi wanapo-jifunza Etheri 6 watafute kanuni ambazo zitawasaidia wao katika changamoto kama zile zilizoorodheshwa kwenye ubao.Alika mwanafunzi asome Ether 2:24–25 kwa sauti. Liombe darasa lifuatilie pamoja, liki-tafuta maonyo ya Bwana kwa Wayaredi kuhusu ugumu wa safari yao ya kwenda kwenye nchi ya ahadi.• Bwana aliahidi atafanya nini ili kuwasaidia Wayaredi kwenda salama hadi nchi ya ahadi?Wakumbushe wanafunzi kwamba ili kustahimili mawimbi na upepo, Wayaredi walite-ngeneza mashua ambazo “zilikazwa kama sahani” (Etheri 2:17), zikiwa na mashimo juu na chini ambayo yangefunguliwa kuleta hewa. Alika mwanafunzi kusoma Etheri 6:1–4 kwa sauti. Liambie darasa kufuatilia pamoja na kutambua njia zingine Wayaredi walijita-yarisha kwa ugumu huu.• Je! Unafikiria inamaanisha nini kwamba Wayaredi walijiandaa kusafiri “ wao wenyewe

wakimsifu Bwana Mungu wao”? (Walimtegemea sana Mungu kwa ajili ya ulinzi na usalama.)

• Kwa nini unafikiria ni muhimu kwa Wayaredi wao wenyewe kumsifu Bwana baada ya kuwafanyia yote waliyoweza kufanya kwa matayarisho yao wenyewe?

• Kwa nini inaweza kuwa ilikuwa vigumu kumwamini Bwana katika hali hii? (Kama wanafunzi hawatataja yafuatayo, unaweza kutaka kutaja kwamba Wayaredi iliwabidi kujenga mashua zao wenyewe, hawakuweza kuelekeza vyombo vyao, na inawezekana kabisa hawakujua njia ya kwenda nchi ya ahadi au safari ingechukua muda gani.)

Ili kuwasaidia wanafunzi kuona matukio yaliyosimuliwa katika Etheri 6, waambie wachore umbo rahisi la mashua ya Wayaredi katika daftari au shajara za kujifunza maandiko. Kisha acha wao wachore au waorodheshe vitu vya mashua kulingana na Etheri 6:1–4.Waalike wanafunzi wachache kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka kwa Etheri 6:5–11. Liambie darasa kutazama michoro yao wanaposikiliza na kufikiria vile wangeweza kusafiri katika vyombo kama hivyo.

KuonaWakati wanafunzi wa-napiga twasira au picha katika akili zao, matukio ya habari za maandiko, hayo matukio yanakuwa halisi zaidi na kuwa wazi kwao. Hii inaweza kuwa-saidia wanafunzi kulinga-nisha watu na hali vyema katika maandiko na kuchambua na kuelewa matukio vyema zaidi.

Page 554: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 555: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 556: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 557: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 558: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 559: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 560: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 561: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 562: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 563: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 564: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 565: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 566: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 567: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 568: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 569: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 570: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 571: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 572: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 573: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 574: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 575: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 576: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 577: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 578: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 579: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 580: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 581: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 582: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 583: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 584: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 585: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 586: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 587: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 588: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 589: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 590: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 591: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 592: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 593: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 594: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 595: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 596: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 597: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 598: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 599: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 600: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 601: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 602: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 603: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 604: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 605: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 606: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 607: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 608: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 609: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 610: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 611: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 612: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 613: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 614: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 615: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 616: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 617: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 618: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 619: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 620: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 621: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 622: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 623: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 624: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 625: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia
Page 626: Kitabu cha Mormoni - Church of Jesus Christ...iii Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni Mwongozo wa Mwalimu wa Seminari..... vi Dhamira Yetu ..... vi Matayarisho ya Somo ..... vi Kutumia