30
M W O N G O Z O W A U S I M A M I Z I N A U H I F A D H I W A M A Z A O B A A D A Y A K U V U N A November, 2019 KITINI NAMBA 8:

KITINI NAMBA 8...SEHEMU YA 1 ... - Kushawishi panya na wadudu wengine waharibifu Udhibiti - Umakini wakati wa kukausha – Kukausha hadi kufikia kiwango kinachopendekezwa cha unyevu

  • Upload
    others

  • View
    9

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: KITINI NAMBA 8...SEHEMU YA 1 ... - Kushawishi panya na wadudu wengine waharibifu Udhibiti - Umakini wakati wa kukausha – Kukausha hadi kufikia kiwango kinachopendekezwa cha unyevu

MWONGOZO WA USIMAMIZI NA UHIFADHI WA MAZAO BAADA YA KUVUNA

November, 2019

KITINI NAMBA 8:

Page 2: KITINI NAMBA 8...SEHEMU YA 1 ... - Kushawishi panya na wadudu wengine waharibifu Udhibiti - Umakini wakati wa kukausha – Kukausha hadi kufikia kiwango kinachopendekezwa cha unyevu
Page 3: KITINI NAMBA 8...SEHEMU YA 1 ... - Kushawishi panya na wadudu wengine waharibifu Udhibiti - Umakini wakati wa kukausha – Kukausha hadi kufikia kiwango kinachopendekezwa cha unyevu

2

YALIYOMO 1. UTANGULIZI ................................................................................................................................................................. 3

SEHEMU YA 1. .................................................................................................................................................................. 3

2. UHIFADHI NA USIMAMIZI WA MAZAO YA NAFAKA BAADA YA KUVUNA ...................................... 3

3. HATUA MBALIMBALI AMBAMO UHARIBIFU WA MAZAO HUTOKEA ................................................ 3

4. VYANZO VYA UHARIBIFU KATIKA MAZAO YA NAFAKA NA KUNDE ................................................. 3

5. HIFADHI YA MBEGU NA NAFAKA – KANUNI MUHIMU ZA KUZINGATIA ILI KUZUIAUHARIBIFU ...................................................................................................................................................................... 10

6. MCHANGANYIKO WA MIMEA MBALIMBALI ...............................................................................................15

SEHEMU YA 2:................................................................................................................................................................ 16

7. UHIFADHI NA USIMAMIZI WA MAZAO AINA YA MATUNDA NA MBOGAMBOGA BAADA YAKUVUNA ........................................................................................................................................................................... 16

7.1 BILINGANYA ........................................................................................................................................................ 16

7.2 BAMIA ..................................................................................................................................................................... 17

7.3 MATIKITI ............................................................................................................................................................... 18

7.4. KABICHI ............................................................................................................................................................... 19

7.5 CHAINIZI KABICHI/MCHIHILI. .....................................................................................................................21

7.6. VITUNGUU. ......................................................................................................................................................... 22

7.7 PILIPILI HOHO .................................................................................................................................................... 23

7.8 NYANYA ................................................................................................................................................................ 24

MBINU /STADI ZILIZOFUNDISHWA ..................................................................................................................... 27

Page 4: KITINI NAMBA 8...SEHEMU YA 1 ... - Kushawishi panya na wadudu wengine waharibifu Udhibiti - Umakini wakati wa kukausha – Kukausha hadi kufikia kiwango kinachopendekezwa cha unyevu

3

1. UTANGULIZI Uhifadhi wa mazao ya kilimo ni hatua ya mwanzo kabisa mara baada tu ya kuvuna. Hatua zifuatazo huzingatiwa katika uhifadhi bora wa mazao ya kilimo; kuweka mazao

katika hali ya usafi, ubaridi, kuchambua, kutenga katika makundi kulingana na ubora nakufungasha.

Uhifadhi na usimamizi mzuri wa mavuno kwa kiasi kikubwa huamua ubora wa mwisho,kujua soko zuri la mazao kulingana na madaraja ya ubora.

Mazao yatokanayo na kilimo yanawezwa kuwekwa katika makundi makuu mawili;a) Mazao ya nafaka

- Yanajumuisha nafaka pamoja na mazao ambayo mbegu zake hukamuliwa na kutoamafuta mfano alizeti, ufuta na karanga.

b) Mazao ya mbogamboga, matunda na mazao yote ambayo yanatokana na mizizi mfanoviazi vitamu, viazi mviringo na mihogo.

SEHEMU YA 1. 2. UHIFADHI NA USIMAMIZI WA MAZAO YA NAFAKA BAADA YA KUVUNA

• Mazao ya nafaka, mbegu za mimea jamii ya kunde na mizizi ni mojawapo ya mazao

yanayolimwa hapa nchini Tanzania kwenye maeneo mengi. Mazao haya si tu kwamba ni

chakula muhimu kwa binadamu bali pia kwa viumbe wengine wengi, na pia yanatumika

kama mazao ya biashara.

• Upotevu wa mazao baada ya mavuno imethibitika kuwa ni changamoto kubwa kwa

wakulima kwani takwimu zinaonesha kwamba kwa nchi zetu (nchi zilizo kusini mwa

jangwa la sahara ikiwemo Tanzania) upotevu wa mazao baada ya mavuno unafikia

takribani asilimia 30% ya mazao yanayozalishwa.

3. HATUA MBALIMBALI AMBAMO UHARIBIFU WA MAZAO HUTOKEA

Upotevu na uharibifu mwingi wa mazao hutokea katika maeneo haya; • Wakati wa kuvuna• Wakati wa kusafirisha• Wakati kukausha• Wakati wa kupukuchua• Wakati wa usindikaji• Wakati kuhifadhi

4. VYANZO VYA UHARIBIFU KATIKA MAZAO YA NAFAKA NA KUNDE4.1. Matumizi mabaya ya vitendea kazi Visababishi - Utaratibu na njia isiyo sahihi ya Kuvuna- Utaratibu mbovu wa Kuvuna, kupukuchua, kupanga madaraja na kukausha- Miundo mbinu mibovu na upakiaji

Page 5: KITINI NAMBA 8...SEHEMU YA 1 ... - Kushawishi panya na wadudu wengine waharibifu Udhibiti - Umakini wakati wa kukausha – Kukausha hadi kufikia kiwango kinachopendekezwa cha unyevu

4

Madhara - Kushuka kwa uzito- Kupoteza ubora- Kushawishi panya na wadudu wengine waharibifu

Udhibiti - Umakini wakati wa kukausha – Kukausha hadi kufikia kiwango kinachopendekezwa cha

unyevu- Umakini wakati wakubeba magunia/Mifuko- Kurekebisha mbao za kukalishia magunia

4.2. Joto Visababishi - Miundo mbinu mibovu ya stoo- Kuzaliana kwa wadudu wa haribifu katika stoo- Mzunguko duni wa hewa katika stoo- Unyevu mwingi katika nafaka

Madhara - Kushuka kwa uzito- Kupoteza ubora- Kuweka mazingira mazuri ya kuzaliana wadudu waharibifu- Uwepo wa mazingira yakuzalisha fangasi katika mazao

Udhibiti - Kuboresha stoo- Kuweka kivuli katika silo au bini- Kushusha joto la ndani ya stoo- Kuangamiza wadudu waharibifu- Kupangilia vizuri mbao za kukalishia magunia (Paleti) kuruhusu hewa- Kuzingatia nafasi ya meta 1 kati ya kila fungu la magunia

4.3 Unyevu Visababishi - Kiwango cha juu cha unyevu- Nyufa na mashimo kwenye stoo- Magunia kugusa ukuta wa stoo- Kuongezeka wadudu waharibifu kwa kasi

Madhara - Kupoteza ubora- Kushuka uzito- Kuzalisha fangasi kwa kiasi kikubwa na kusababisha sumu kuvu (Afflatoxin)- Kuongezeka kasi ya kuzaliana wadudu waharibifu- Kuota kwa Mazao yakiwa stoo- Kuharibika miundo mbinu ya stoo

Page 6: KITINI NAMBA 8...SEHEMU YA 1 ... - Kushawishi panya na wadudu wengine waharibifu Udhibiti - Umakini wakati wa kukausha – Kukausha hadi kufikia kiwango kinachopendekezwa cha unyevu

5

Udhibiti - Kausha Mazao vizuri kabla yakuhifadhi- Rekebisha stoo na funga vizuri magunia- Punguza unyevu kadiri iwezekavyo katika stoo- Weka magunia juu ya mbao (palleti)- Zingatia nafasi ya meta 1 kati ya magunia- Dhibiti wadudu waharibifu kadiri uwezavyo- Zuia au dhibiti mabadiliko ya joto kupanda au kushuka ndani ya stoo.

4.4 Wadudu waharibifu Visababishi - Maambukizo kutoka kwa mazao ya zamani kuingia kwenye mazao mapya stoo.- Kuhama kwa wadudu waharibifu kutoka katika uchafu- Maeneo ya maficho katika stoo mfano mipasuko- Kutumia magunia machafu

Madhara - Kushuka uzito- Kupungua kwa ubora- Kuongezeka kwa joto na unyevu

Udhibiti - Kuvuna kwa muda muafaka- Kuchagua aina ya mbegu zinazostahimili uharibifu wa wadudu.- Tumia njia safi na sahihi za kusafirisha- Ondoa magunzi, punje na mabua kwenye nafaka- Hakikisha Mazao yamekauka vizuri kabla yakuhifadhi- Safisha stoo kila mara- Dhibiti kiwango cha joto na unyevu kwenye stoo kufikia 12% na halijoto lisilozidi 14.5oC- Tenga Mazao ya zamani na mapya katika stoo- Safisha magunia matupu na yakinge dhidi ya wadudu- Dhibiti wadudu waharibifu wa mazao kwa kutumia mimea dawa au vitu dawa (vya kilimo

hai)- Tumia vifaa vya kuhifadhia visivyoruhusu mwanga kupenya- Matumizi ya mbinu husishi za udhibiti wa wadudu

4.4.1 Mifano ya wadudu waharibifu maarufu 4.4.1.1 Fukusi wa Kunde Ni visumbufu wakuu wa mimea jamii ya kunde (Kunde, Mbaazi, soya n.k) Wanaathiri podi shambani hadi ghalani /stoo Upotevu unaweza kufikia 90% Matundu ya duara na mayai meupe kwenye mbegu ni kiashiria cha mashambulizi ya

fukusi

Page 7: KITINI NAMBA 8...SEHEMU YA 1 ... - Kushawishi panya na wadudu wengine waharibifu Udhibiti - Umakini wakati wa kukausha – Kukausha hadi kufikia kiwango kinachopendekezwa cha unyevu

6

Picha: Fukusi wa kunde

Kumdhibiti fukusi wa kunde o Vuna mara tu baada ya kukomaao Kausha juanio Hifadhi kwenye chombo kisichopenyeza fukusio Kupaka kunde mafuta ya kula kunaweza kuzuia ukuzi zaidi wa fukusi (mililita 5 za mafuta

ya kula kwa kilo 1 ya mbegu za mikunde)o Vitu dawa kama majivu ya kuni, pilipili kali au moshi unaotokana na motoo Kuhifadhi podi zisizopurwa (kunde kwenye maganda yake) kunaweza kupunguza athari

4.4.1.2 Fukusi wa maharage o Ana mabawa mafupi ambayo hayafuniki kiwiliwili choteo Ndie kisumbufu mkuu wa maharageo Anaanzia mashambulizi shambanio Anakamilisha mzunguko wake ndani ya mbegu

Picha: Fukusi wa maharage Jinsi ya kumdhibiti fukusi wa maharage o Kuchanganya mahindi na kunde, kuvuna kwa wakati kunapunguza mashambulizi ya

fukusi wa maharage na fukusi wa kunde.

4.4.1.3 Dumuzi (Scania) Ni kisumbufu sugu cha mahindi yaliyohifadhiwa ghalani /stoo na mihogo iliyokaushwa Anashambulia mahindi yaliyokaushwa iwe kabla au baada ya mavuno

Page 8: KITINI NAMBA 8...SEHEMU YA 1 ... - Kushawishi panya na wadudu wengine waharibifu Udhibiti - Umakini wakati wa kukausha – Kukausha hadi kufikia kiwango kinachopendekezwa cha unyevu

7

Picha: Dumuzi mkubwa (katika muonekano tofauti)

Picha: Dumuzi mdogo

Jinsi ya kumdhibiti Dumuzi o Kuhifadhi nafaka au mihogo kwa kuchanganya na majani ya kutosha ya Mvepe (Lantana

camara) yaliyokaushwa au majani ya milingotio Mwarobaini pia imeonekana kufanya vizuri katika kudhibiti dumuzi

4.4.1.4 Fukusi wa nafaka (tembo wa vihenge) Wana mkonga uliochongoka Wanashambulia nafaka nzima au iliyopata jeraha Wanashambulia shambani au ghalani/stoo Fukusi wa mpunga ndie kisumbufu kikuu wa mpunga, mahindi na nafaka maghalani

Picha: Fukusi wa nafaka (Tembo wa vihenge) picha ndogo (kushoto) Picha iliyokuzwa Zaidi (kulia)

Page 9: KITINI NAMBA 8...SEHEMU YA 1 ... - Kushawishi panya na wadudu wengine waharibifu Udhibiti - Umakini wakati wa kukausha – Kukausha hadi kufikia kiwango kinachopendekezwa cha unyevu

8

4.4.1.5 Vipepeo wa nafaka Anashambulia mpunga, mtama, mahindi na ngano Athari yake inalingana na ile inayosababishwa na fukusi Anaweza kuathiri mazao shambani kabla ya kuvunwa na uharibifu unaweza kuwa

mkubwa sana, hata kabla nafaka hazijahifadhiwa

Picha: Kipepeo wa nafaka

4.4.1.6 Vipepeo wa ghalani Kipepeo huyu anashambulia mazao kama Nafaka nzima, karanga, matunda

yaliyokaushwa, cocoa na vyakula vingine. Wanasababisha uharibifu mkubwa kwenye maua ya nafaka na bidhaa zingine zilizosagwa,

lakini pia kwenye nafaka nzima, zaidi wakila kiini. Wanashambulia pia karanga, matunda yaliyokauka, cocoa na vyakula vingine Mabuu ya vipepeo hawa mara nyingi hujishikiza kwenye mifuko Unaweza pia kuona mbegu zikiwa na uchafu na uchafu huu kimsingi unachafua chakula

na kupunguza ubora

Picha: Kipepeo wa ghalani/stoo

4.5 Vimelea (bakteria na Ukungu/kuvu) Visababishi - Kiwango kikubwa cha unyevu katika Mazao yaliyo hifadhiwa- Kiwango kikubwa cha unyevu katika store- Mvuke kutoka angani- Unyevu unaozalishwa na wadudu

Madhara - Kushuka ubora

Page 10: KITINI NAMBA 8...SEHEMU YA 1 ... - Kushawishi panya na wadudu wengine waharibifu Udhibiti - Umakini wakati wa kukausha – Kukausha hadi kufikia kiwango kinachopendekezwa cha unyevu

9

- kupungua uzito- Ongezeko joto na unyevu- Ongezeko la mvuke na gesi

Udhibiti - Kausha Mazao vizuri kabla ya kuyahifadhi- Kupunguza kiwango cha unyevu kadiri iwezekanavvyo katika stoo- Zingatia nafasi ya meta 1 kila baada ya magunia- Kumbuka kudhibiti wadudu waharibifu

Mfano wa vimelea

4.5.1 Ukungu (Fangasi) Wanahitaji hali ya unyevu hewani inayofikia 65 % (sawa na kiwango cha unyevu cha 13 %

kwenye nafaka) Wanakua kwenye halijoto ya nyuzi 10 hadi 40 Maambukizi ya baadhi ya aina za kuvu yanaweza kuanzia shambani,

Madhara Kupotea kwa virutubisho Nafaka kupoteza rangi yake Kupunguza uwezo wa mbegu kuota Kupandisha joto la bidhaa zilizohifadhiwa kufikia hatua ya kuungua Harufu na ladha ya ukungu Kuzalisha sumu mbalimbali ambazo zinabakia kwenye bidhaa zako m.f sumu kuvu

4.5.1.1 Sumu kuvu Haiwezi kuharibiwa kwa kuchemsha, kukamua na uchakataji Mazao yaliyoathiriwa lazima yaharibiwe Inaweza kupatikana kwenye mazao haraka sana baada ya athari za fangasi (saa 24) Kuzuia uchafuzi wa fangasi lazima mazao yakaushwe vizuri kabla ya kuhifadhiwa

4.6 Panya Visababishi - Kupenya kupitia mlangoni au dirishani kama hapajafungwa vizuri au kwa uwazi mwingine- Kutokuwa na vizuizi vya panya- Usafi kutozingatiwa stoo pamoja na mazingira yanozunguka

Madhara - Kupungua uzito

Page 11: KITINI NAMBA 8...SEHEMU YA 1 ... - Kushawishi panya na wadudu wengine waharibifu Udhibiti - Umakini wakati wa kukausha – Kukausha hadi kufikia kiwango kinachopendekezwa cha unyevu

10

- Mazao kumwagika kutokana na mifuko kutobolewa- Kupungua ubora kutokana na nafaka chafu, vinyesi na mikojo ya panya, nywele n.k- Kuharibu vitendea kazi magunia, madirisha, nyaya za umeme na miundombinu mingine.- Kueneza magonjwa kwa binadamu; mfano, Tauni.

Udhibiti - Zuia panya kuingia ndani kwa kuziba vizuri stoo, kuweka wavu madirishani na sehemu za

kupitisha hewa- Stoo pamoja na mazingira yanayozunguka yawe safi- Tegesha mitego ya panya- Chukua tahadhari ya njia za kuzuia panya- Kufuga paka (wakulima wadogo)

4.7 Ndege

Visababishi - Madirisha au milango iliyo wazi, uwazi katika kuta za stoo

Madhara - Kushuka uzito- Uharibifu wa magunia- Uchafuzi wa Mazao yaliyohifdhiwa ikiwa ni pamoja na vinyesi na uchafu mwingine

Udhibiti - Kujenga au kurekebisha stoo ndege wasiweze kuingia- Ondoa nyumba zote za ndege zilizo stoo na kuzunguka stoo

5. HIFADHI YA MBEGU NA NAFAKA – KANUNI MUHIMU ZA KUZINGATIA ILI KUZUIAUHARIBIFU5.1 Aina na uchaguzi wa mbegu boraMbegu za asili zimekuwa katika mazingira husika kwa kipindi kirefu kwa hivyo mara nyingizimethibitika kuwa na uwezo mzuri wa kuhimili hali ya maeneo husika zinapokua. Mbegu zakisasa zinaweza kuwa na uzalishaji mkubwa lakini uwezo mdogo wa kuhimili visumbufu pamojana wale wa wale wa ghalani /stoo.

Hivyo ni muhimu kupima uzito baina ya ongezeko la mavuno dhidi ya uharibifu wa visumbufu. Jambo la msingi linalohitaji kuzingatiwa ni: Chagua mbegu zilizo bora kwa ajili ya kupanda misimu ijayo, epuka mbegu zilizoharibiwa au zisizo na afya.

5.2 Kupangilia vizuri muda wa kuvuna Kama uvunaji utafanywa wakati wa kiangazi, hakutakuwa na tatizo la ukaushaji. Mkulima anapozalisha zao jipya linalokomaa kwa muda mfupi kuna uwezekano uvunaji ukaangukia wakati wa kipindi cha mvua, na hii inaweza kuleta tatizo kwenye uhifadhi.

Baadhi ya visumbufu maghalani kama mbawakau wa maharage, fukusi wa kunde, dumuzi na baadhi ya vipepeo wanashambulia mazao shambani pale tu yanapokua yamekaribia kukauka

Page 12: KITINI NAMBA 8...SEHEMU YA 1 ... - Kushawishi panya na wadudu wengine waharibifu Udhibiti - Umakini wakati wa kukausha – Kukausha hadi kufikia kiwango kinachopendekezwa cha unyevu

11

kabisa. Kuvuna kwa wakati kunaweza kusaidia kuhakikisha kwamba visumbufu hawa hawahamishwa pamoja na nafaka au maharage kupelekwa ghalani.

Kanuni muhimu hapa ni: Usiache mazao shambani ikiwa yapo tayari kuvunwa, hii inaongeza nafasi ya maambukizi ya

visumbufu wa ghalani.

5.3 Ukaushaji Unazuia mbegu zisiote. Unazuia mashambulizi ya fangasi. Mbegu zote lazima zikaushwe hadi kufikia kiwango cha unyevu cha kati ya 12 – 13 % ili zihifadhiwe kwa usalama. Ili kuhakikisha mbegu imekauka ifaavyo weka mbegu moja mdomoni na kuing’ata kama haikuvunjika kwa urahisi itakuwa imekauka vizuri lakini ikisagika kati ya meno itakuwa haijakauka vizuri. Joto linalozalishwa wakati wa kukausha linaua wadudu kwenye hatua ya lava, na kufukuza wale visumbufu waliofikia hatua ya ukuzi kamili.

Uangalifu unahitajika ili kuepuka joto kuipita kiasi kwa kuwa linaweza kusababisha uharibifu wa mbegu au nafaka. Joto halipaswi kuzidi: nyuzi 35 kwa maharage, nyuzi 43 kwa mbegu, nyuzi 60 kwa Nafaka (Deg C)

5.3.1 Mbinu za kukausha zinahusisha: Kukausha juani kwa kusambaza kwenye sakafu safi au kichanja wakati wa jua na kukusanya pamoja muda wa jioni hadi zikauke vizuri.

Page 13: KITINI NAMBA 8...SEHEMU YA 1 ... - Kushawishi panya na wadudu wengine waharibifu Udhibiti - Umakini wakati wa kukausha – Kukausha hadi kufikia kiwango kinachopendekezwa cha unyevu

12

Kugeuza ni muhimu ili kuchochea ukaukaji mzuri na kwa haraka Makaushio rahisi: ipo miundo mbalimbali lkn kaushio la dohani (chimney) linaweza kuwa

rahisi zaidi na lenye ufanisi katika kukausha

5.4 Kupanga madaraja na usafi wa mazao Chukua sampuli na kutizama ikiwa mazao yemeanza kushambuliwa. Chunguza mipasuko, vishimo ambamo wadudu wanaweza kujificha. Kama mazao yameathirika yahifadhi kivyake na kuyatibu ili kuzuia maambukizi kwa mazao yaliyo safi. Kama yameathirika sana yatupilie mbali (yaondoe). Kama hayajaathirika sana yanaweza kutibiwa kwa joto lisilozidi nyuzi 50 0C ili kuua wadudu kama fukusi na vipepeo. Zaidi ya nyuzijoto 50 mbegu itapoteza uwezo wa kuota. Kuondoa nafaka au magunzi yaliyoathirika kunaweza kufanywa kwa mkono, kupepeta, kuchekecha au kutikisa. Unapotumia mbinu ambazo zinatenganisha visumbufu kutoka kwenye mazao yaliyohifadhiwa, hakikisha kwamba unaua visumbufu kuepuka kurudi tena kwenye mazao yako.

5.5 Eneo la ghala /stoo Weka ghala eneo la mbali na vyanzo vya maambukizi. Vipepeo wa viazi na nafaka ni mahodari wa kuruka na pamoja na kuathiri mazao ghalani wanaweza pia kuathiri mazao yakiwa shambani. Kuwa ghala sehemu ya mbali na shamba kunaweza kusaidia kupunguza mashambulizi.

5.6 Sifa za eneo la kuhifadhia mazao/ ghala/stoo Hewa ya kutosha, kivuli, ubaridi na ukavu. Isiwe na matundu au mipasuko wala sehemu zozote zinazoweza kuruhusu visumbufu kupenya. Madirisha, milango na sehemu za kupitisha hewa ziwekwe nyavu nyembamba. Kupiga plasta hata ya tope kuziba matundu na mipasuko.

Page 14: KITINI NAMBA 8...SEHEMU YA 1 ... - Kushawishi panya na wadudu wengine waharibifu Udhibiti - Umakini wakati wa kukausha – Kukausha hadi kufikia kiwango kinachopendekezwa cha unyevu

13

5.7 Usafi wa ghala /stoo la kuhifadhia Wakati wote mazingira ya kuzunguka ghala yawe safi. Kabla ya kuhifadhi mazao mapya, ghala /stoo lisafishwe mapema. Bidhaa za zamani ziondolewe na chumba kisafishwe kikamili. Sakafu, paa, mipasuko yote izibwe na chumba kitengezwe kwa namna ambayo hakiruhusu panya kupenya.

5.8 Kuchunguza/ Kukagua ghala /stoo Ukaguzi wa mara kwa mara na kuondoa mazao yaliyo athiriwa na mashambulizi ni muhimu. Kagua vinyesi na alama zozote za ndege na panya. Chunguza vipepeo wowote wanaoruka mida ya jioni. Inua mifuko ili kuchunguza mabuu ya vipepeo kwenye sehemu za mifuko zilizounganishwa.

5.8.1 Kutafuta Mbawakau: Chunguza mipasuko, masikio ya mifuko wanamojificha mara nyingi Chunguza mifuko tupu kama utaona dalili zozote za mbawakau na lava(funza) wao Haya yanapaswa kufanywa kivulini ili wadudu wasikimbie haraka Unaweza kutumia chekeche ya milimita 1 au 2 kuwatenganisha na kuwatambua ili kuchukua

hatua stahiki

Hatua zinazochukuliwa zinapaswa kuzuia pia mazalia ya wadudu kutoka kwenye mazao ya awali. Mazingira yawekwe katika hali ya usafi ili kuepuka kuchochea maambukizi mengine ya wadudu na panya.

5.8.2 Mashambulizi ya fangasi: Yanaweza yanaweza kutambuliwa kwa harufu ya ukungu, ambayo unaweza kuibaini hata

kabla mabadiliko yoyote kwenye mazao yanayoweza kuonekana hayajaanza kuonekana. Chunguza pia alama za umajimaji kwenye mifuko zinazoweza kugundulika hata kama mfuko

umekauka.

5.9. Kuvukisha moshi ghalani Kuwasha moto ambamo pilipili zinachomwa chini ya ghala mara moja kwa mwezi kunasaidia kufukuza visumbufu wa ghalani. Changamoto inaweza kuwa ukali wa moshi unaweza kuumiza macho ya mtu na kukohoa.

Page 15: KITINI NAMBA 8...SEHEMU YA 1 ... - Kushawishi panya na wadudu wengine waharibifu Udhibiti - Umakini wakati wa kukausha – Kukausha hadi kufikia kiwango kinachopendekezwa cha unyevu

14

5.10 Kudhibiti vimelea na wadudu ghalani (Disinfection) Baada ya kufanya usafi kwenye stoo na kuondoa uchafu wote wa nyuma ni vizuri kunyunyiza chokaa, au majivu kama njia ya kuongeza udhibiti dhidi ya matatizo ya visumbufu.

5.11 Vitu dawa Majivu ya kuni, Mchanganyiko wa majivu ya kuni na pilipili zilizosagwa, Mchanganyiko wa majivu na mbangi pori ni kinga nzuri pia dhidi ya wadudu.

Zingatia Kwamba: Majivu hayadhibiti Dumuzi (Scania).

5.11.1 Chokaa Kuchanganya gram 300 za chokaa kwenye kilo 100 za mbegu kumetoa matokeo mazuri katika udhibiti wa fukusi.

5.11.2 Mchanga laini Unachanganywa na mbegu kubwa, Lengo ni kuziba nafasi zote kati ya mbegu kubwa kubwa, Mbegu hizi zinachanganywa na mchanga ambao baadae utaondolewa tena kwa kuchekecha, Angalau kiasi cha mchanga kinapaswa kilingane na kiwango cha mbegu.

5.11.3 Mafuta ya mimea Mafuta ya nazi, mnyonyo, pamba, karanga, mahindi, alizeti, mwarobaini na soya yanaathiri uwezo wa kutaga mayai, mayai na ukuzi wa lava wa visumbufu wa ghalani. Kutumia mafuta mimea kunasaidia hasa kulinda mimea jamii ya kunde dhidi ya mbawakau wa mikunde (bruchid). Upotevu unaweza kuzuiwa kwa kutumia 5 mililita kwa kilo 1 ya mbegu za mikunde.

Ili kuwa na matokeo mazuri mbegu inapaswa kupakwa yote vizuri. Mafuta ya alizeti hayana ufanisi mkubwa sana. Athari ya mafuta inapungua kadri muda unavo kwenda kwa hiyo mara tu mbegu zinapoanza kuonesha dalili ya kushambuliwa zinapaswa zipakwe tena. Mbegu chache zinaweza kupoteza uwezo wa kuota baada ya kutibiwa na mafuta.

Ukitumia mafuta ya mwarobaini au mafuta yoyote ambayo si ya kula uchungu unaweza kuondolewa kwa kuloweka mbegu kwenye maji moto kwa dakika chache kabla ya kuziandaa kwa chakula.

Page 16: KITINI NAMBA 8...SEHEMU YA 1 ... - Kushawishi panya na wadudu wengine waharibifu Udhibiti - Umakini wakati wa kukausha – Kukausha hadi kufikia kiwango kinachopendekezwa cha unyevu

15

6. MCHANGANYIKO WA MIMEA MBALIMBALIJina la mmea

Sehemu za mmea Tiba

Alovera Mmea mzima Kausha, saga ili kupata unga na changanya na nafaka

Pili pili za kuwasha

Pilipili zilizoiva, zinaweza kukaushwa na kuchanganywa na majivu, samadi ya ng’ombe au udongo laini

Pilipili zinaweza kuchanganywa na nafaka au unga wa pilipili unaweza kunyunyizwa kwenye maharage

Pareto Maua Chuma kipindi cha joto kali Kausha kivulini Saga ili kupata unga na uchanganye na nafaka/ mbegu

Marejea Mbegu Changanya mbegu kwenye uwazi ulio katikati ya nafaka kubwakubwa

Ndulele Shina na majani (uangalifu unahitajika kwa kuwa mbegu zake zina sumu)

Kausha na kuchanganya na mazao

Mikaratusi Majani Majani yapangwe kwenye matabaka au yachanganywe na mazao yaliyohifadhiwa

Lantana Majani Unasagwa na kuchanganywa na mbegu Mmelia (Mwarobaini nusu)

Majani, mbegu zilizoiva Kausha, saga, unga wake changanya na nafaka kwa kiwango cha 2kg/ 100kg (ukitumia unga wa mbegu), kama unatumia unga wa majani tumia 4kg /100kg

Mbangi pori Mmea wote Panga mmea uliokaushwa kwenye matabaka au changanya changanya mmea uliosagwa au weka matabaka ya Sm 3 – 5 ya mmea uliosagwa kwenye kitako cha chombo cha kuhifadhia nafaka

Mint Mmea wote Mwarobaini Majani, mbegu zilizosagwa

na mabaki yake pamoja na mafuta ya mbegu

Kilo 4 za unga wa mwarobaini zitahifadhi kilo 100 kwa zaidi ya miezi minne (4)

Page 17: KITINI NAMBA 8...SEHEMU YA 1 ... - Kushawishi panya na wadudu wengine waharibifu Udhibiti - Umakini wakati wa kukausha – Kukausha hadi kufikia kiwango kinachopendekezwa cha unyevu

16

SEHEMU YA 2:

7. UHIFADHI NA USIMAMIZI WA MAZAO AINA YA MATUNDA NA MBOGAMBOGA BAADA YAKUVUNA

7.1 BILINGANYA 7.1.1 Uvunaji 7.1.1.1 Sifa za uvunaji Bilinganya zote ziwe sawa na zenye umbo la yai au kuelekea umbo la duara; ziwe na kushikio cha tunda cha kijani chenye ubichi; matunda yaliyojaza vizuri yenye Ngozi ya rangi ya zambarau iliyokolea.

7.1.1.2 Mambo ya kuzingatia wakati wa kuvuna • Vuna wakati hali ya hewa ni kavu• Zinaweza kupakiwa shambani• Vuna kwa kutumia kisu au mkasi maalumu• Kikonyo cha tunda kiwe kifupi• Usikwaruze matunda

7.1.2 Ukusanyaji na upakiaji

7.1.2.1 Madraja Ziwe na sifa na sifa za aina moja kulingana na aina halisi, rangi nzuri zimejaa safi umbo zuri na zisiwe na uozo na vitobo vya funza/viwawavi, Pia zisiwe na majeraha yanayotokana na mabaka, baridi kali, magonjwa, wadudu au mikandamizo au sababu nyingine yeyote.

7.1.2.2 Upoozaji • Upoozaji wa haraka kufikia nyuzijoto 10 mara tu baada ya kuvuna ni lazima• Upooza kwa kutumia maji• Upoozaji kwa hewa ya kusukumwa• Upoozaji wa ndani ya chumba baada ya kuosha (hii haina uwezo sana)• Upoozaji wa ndani ya jokofu asiliaBilinganya na nyanya chungu zinaweza kuoshwa kwa makundi au kuzamishwa /kuchovyakwenye maji kwa ajili ya kuondoa vumbi la shambani.

7.1.3 Vifungashio Uzito: 11 Kg

Ukubwa /Wingi

Daraja Urefu (Sm) Idadi ya matunda(namba)

Ndogo 12-14 32

Saizi ya kati (Wastani) 19-20 24

Saizi kubwa 21-24 18

Saizi kubwa zaidi 24.5-26 16

Page 18: KITINI NAMBA 8...SEHEMU YA 1 ... - Kushawishi panya na wadudu wengine waharibifu Udhibiti - Umakini wakati wa kukausha – Kukausha hadi kufikia kiwango kinachopendekezwa cha unyevu

17

Mahitaji/Vifaa; Maboksi/vifungashio kwa ujumla huwa ni maboksi ya jamii ya mbao nyembamba yaliyo pakwa nta au makreti ya plastiki. Kila tunda linaweza kuzingirwa na karatasi laini kuzuia uharibifu.

7.1.4 Uhifadhi • Nyuzi Joto 10-12• Kiwango cha unyevu; 90-95%.• Upumuaji wa hewa; 32-41ml/kg kwa saa kwenye kiwango cha joto la sentigredi 12.5o C.• Mchanganyiko wa hewa; Haina faida/madhara.• Utoaji wa hewa ya ethylene: 0.1 – 0.7µL/Kg kwa saa. Zinaathirika sana zikiwekwa kwenye

hewa ya ethylene.• Madhara tarajiwa; Madhara ya baridi kali.• Muda wa ubora; siku 14 au pungufu.

7.1.5 Wadudu na magonjwa • Uozo wa ukungu mweusi, uozo wa ukungu wa kijivu, uozo wa vinywelea na uozo laini.• Epuka madhara ya baridi kali• Epuka kuhifadhi kwa muda mrefu sana

7.2 BAMIA

7.2.1 Uvunaji 7.2.1.1 Sifa za ubora • Matunda ya viwango vya juu yana urefu wa sentimita 5 hadi 15, yamenenepa, yana mng’aro

wa kijani na yamejaza vizuri.• Mbegu hazitakiwi kuvimba na kujionesha kwenye Ngozi na migongo isiwe meusi na

kuchubuka.• Bamia zivunwe zikiwa teke na unato mwingi kabla hazijawa na nyuzinyuzi nyingi. Kawaida

ni wiki mbili hadi sita baada ya kutoa maua.

7.2.2 Ukusanyaji /Upakiaji

7.2.2.1 Madaraja Bamia za aina moja zenye sifa ya aina halisi ambazo ni teke, laini na zenye umbo zuri, hazina uozo na uharibifu unaosababishwa na uchafu au kitu chochote, isiwe na magonjwa, wadudu, au mikandamizo au miburuzo yoyote ile.

7.2.2.2 Upoozaji Bamia ziuzwe ndani ya masaa thelathini na sita (36) baada ya kuvunwa na zisafirishwe kwenye hali ya hewa ya jokofu (refrigeration). Hifadhi kwenye stoo yenye maboksi/vifungashio visivyopitisha hewa. Bila ya kuwa na hali ya hewa ya jokofu inaweza kuathiri rangi ya bamia. Baadhi ya wakulima wanatumia upoozaji kwa njia ya maji au upoozaji kwa usukumaji wa hewa. Bamia zisilowe.

Page 19: KITINI NAMBA 8...SEHEMU YA 1 ... - Kushawishi panya na wadudu wengine waharibifu Udhibiti - Umakini wakati wa kukausha – Kukausha hadi kufikia kiwango kinachopendekezwa cha unyevu

18

7.2.3 Vifungashio - Uzito wa kawaida 0.45kg- Uzito mkubwa 11kg

7.2.4 Uhifadhi Joto 7-10 sentigredi Kiwango cha nyuzi joto>90% Mchanganyiko wa hewa: 4-10 % hewa ya ukaa Utoaji wa hewa ya Ethylene; kiwango cha chini. zinaathiriwa kiasi zikiwekwa kwenye hewa

ya ethylene (hewa inayochochea mazao kuiva) Madhara tarajiwa; zinaathirika sana na baridi kali. Muda wa ubora; siku 7-14

7.2.5 Wadudu na magojwa Ukungu wa Kijivu /Gray mold (Botrytis cinereal) Ubwiru (Mildew) Kuvu (Yeast)

7.3 MATIKITI

7.3.1 Kuvuna 7.3.1.1 Sifa za ubora Limejaa vizuri la uzungusho mzuri na usawa katika maumbile, liwe na muonekano wenye

gundi na kung`ara. Ganda/ Ngozi isiwe na mabakabaka, kuungua na jua, na isiwe na miburuzo au mikwaruzo

yoyote, isiwe na magojwa au kuoza au hali ya kuiva kwa kupitiliza.

7.3.1.2 Mambo ya kuzingatia Vigezo vya kukomaa; Kunyauka kwa vikonyo vya matunda, vidoti vya njano hini ya tunda

tunda, tofauti kubwa ya rangi ya Ngozi na sauti ya mvumo tunda linapogongwa kwa kidole Aina zenye ngozi nyembamba inabidi kuzihudumia kama yai. Endesha polepole. Ondoa udongo kwenye matunda shambani kwa kutumia glovu. Matikiti hayaendele kuiva kufika mwisho baada ya kuvunwa. Joto lisibadilike baada ya kuvuna; usiyaondoe sehemu ya ubaridi yalipoifadhiwa na

kuyapeleka kwenye joto. Matunda yaliyopasuka huwavutia nyuki, hii inaweza kuwa ni hatari kwa wafanya kazi.

Matunda yaliyokatwa yafunikwe au kuilaza hii ni sehemu iliyokatwa ili kuepuka kuwavutiang`ombe na nyuki.

7.3.2 Ukusanyaji/upakiaji Madaraja

Yamekomaa, aina moja, yamekuwa vizuri kwa wastani, na hakuna yaliyoiva kupitiliza. Hayana ugonjwa wa Anthracnose, hayajaoza na hayana mabaka ya kuungua na jua na hayana weupe wa joto. Hayaja haribiwa na kitu chochote.

Page 20: KITINI NAMBA 8...SEHEMU YA 1 ... - Kushawishi panya na wadudu wengine waharibifu Udhibiti - Umakini wakati wa kukausha – Kukausha hadi kufikia kiwango kinachopendekezwa cha unyevu

19

7.3.2.2 Upoozaji wa joto na Uoshaji Kwa ujumla hayafanyiwi upoozaji wa awali. Upoozaji wa ndani ya nyumba Kuooza kwa hewa ya kusukuma

Uoshaji; Futa kwa kitambaa kisafi shambani; Pia yanaweza kuoshwa kwa kutumia maji kama ni

lazima

Ukubwa wa maboksi/vifungashio (Sifa za vifaa vya kufungashia/kubebea)

Maboksi au vifungashio viwe na uwezo maalumm wa kuhimili uzito wa matunda Maboksi au vifungashio vipya tu ndiyo vitumike 7.3.3 Uhifadhi Kiwango cha joto; nyuzijoto 10-15 Kiwango cha unyevu; 90% Upumuaji wa hewa: 3-5ml/kg kwa saa kwenye kiwango cha joto cha nyuzijoto 10 Mchanganyiko wa hewa; Hayanufaiki Utoaji wa hewa ya Ethylene; Kiwango cha chini. Yanaathirika sana yakiwekwa kwenye hewa

ya ethylene (hewa inayochochea uivaji). Madhara tarajiwa; Athari ya baridi kali. Muda wa ubora; Wiki 3 hadi 3.

7.3.4 Wadudu na Magonjwa Vijidudu/Vimelea mbalimbali. Ondoa matunda yenye magonjwa. Dhibiti magonjwa vizuri shambani.

7.4. KABICHI

7.4.1 Kuvuna 7.4.1.1 Sifa za Ubora Isiwe imepooza, imejaza na imefunga vizuri. Iwe rahisi kuvunika na isiwe na majani yaliyojiachia au sehemu ya kichwa iliyopasuka.

Mambo ya kuzingatia

Vuna wakati wowote wa siku ila tu epuka joto kali. Kupakia shambani ni jambo zuri lakini kabichi lazima ziwe safi. Bakiza jani moja hadi mawili ya chini wakati wa kuvuna. Si vibaya kama majani ya chini yameshambuliwa na wadudu lakini kabichi yenyewe iwe

nzima. Usisafirishe kabichi zenye vinyesi vya wadudu vya wadudu. Pasua baadhi ya kabichi kuona kama kuna shida kwa ndani. Vuna kabichi ambazo zimefunga na kukomaa vizuri lakini kabla ya kuasuka. Baadhi ya aina ya kabichi zote hukomaa kwa pamoja lakini aina nyingine zinatofautiana.

Page 21: KITINI NAMBA 8...SEHEMU YA 1 ... - Kushawishi panya na wadudu wengine waharibifu Udhibiti - Umakini wakati wa kukausha – Kukausha hadi kufikia kiwango kinachopendekezwa cha unyevu

20

Kwa hiyo kuna aian za kabichi ambazo zote zinaweza kuvunwa mara moja kwa wakatimmoja, lakini aina nyingine zinaweza kuvunwa mara mbili, tatu na hata Zaidi kwa wakatitofautitofauti.

Kabichi zikivunwa wakati wa joto kali zipelekwe haraka stoo kwa ajili ya kuondoa joto lashamabani.

Kuwa mwangalifu usijeruhi kabichi wakati unabeba. Uondoaji maganda/majani ya nje hupelekea kuwa na kabichi nyeupe. Hata hivyo zingatia

kwamba wateja wengi hawapendi kabichi nyeupe.

7.4.2 Kukusanya /Kupakia

7.4.2.1 Madaraja Aina moja au aina zenye sifa zinazofanana, ngumu na hazija sinyaa, zimejifunga vizuri, hazijapasuka, na hazina uozo au vitawi vya kutolea mbegu, hazijapoteza rangi ya asili, hazijaathirika na baridi, magonjwa, wadudud au uharibifu mwingine wowote. Shina lisizidi nusu inchi (1/2) kutoka majani ya chini. Ondoa zilizo na maumbo yasiyo ya kawaida, majani yasiyo jishika vizuri (yanayoning`inia).

Upoozaji wa awali;

- Hewa ya kusukumwa wakati wa kuhifadhi.

Kuosha; Haishauriwi kuosha.

7.4.2.2 Vifungashio na Ukubwa wa kabichi. Ukubwa; (kuweka kwa makundi ni hiyari) kabichi zilizo chongoka nchani.

7.4.3 Uhifadhi - Nyuzijoto 0.- Kiwango cha unyevu;98-100%.- Mchanganyiko wa hewa;4-5%hewa ya ukaa,2-3%hewa ya oksijeni.- Utoaji wa hewa ya Ethylene; kiwango cha chini. Yanaaathirika sana yakiwekwa kwenye

hewa ya Ethylene.- Madhara tarajiwa; Kiwango cha chini.- Muda wa ubora; Mwezi mmoja hadi sita (1-6).

7.4.4 Wadudu na magonjwa Ukungu wa kijivu

- Ni kisaababisho kikubwa cha uozo baada ya mazao kuvunwa.- Tumia aina za kabichi zenye kuhimili ugonjwa huu.- Tumia dawa za kilimo hai za kudhibiti wadudu kabala ya kuvuna.- Kuwa makini kwenye usafi na fanya usafi wa hali ya juu.- Epuka michubuko au madhara ya baridi iliyokithiri.- Fanya upoozaji wa haraka kwenye kiwango cha joto la sentigredi 0.- Dhibiti hali ya hewa kwenye sehemu ya hifadhi.

Page 22: KITINI NAMBA 8...SEHEMU YA 1 ... - Kushawishi panya na wadudu wengine waharibifu Udhibiti - Umakini wakati wa kukausha – Kukausha hadi kufikia kiwango kinachopendekezwa cha unyevu

21

Uozo Mweusi au madoa ya kijivu kwenye jani(altenaria)

- Inashambulia mazao mengi ya jamii ya kabichi.- Tumia dawa ya kudhibiti ukungu kabla ya kuvuna.- Fanya upoozaji wa haraka.

7.5 CHAINIZI KABICHI/MCHIHILI.

7.5.1. Uvunaji 7.5.1.1 Dalili za kukomaa/utayari wa kuvuna Kutambua utayari wa kuvuna (kukomaa) si rahisi na hakuna kiashiria kimoja cha

kukitegemea. Chainizi kabichi huvunwa kwa kukatwa majani au kukata kichwa chote karibu na udongo

wa wakati majani yakiwa ya kijani iliyokolea. Kwa baadhi ya aina, majani ya nje/pembeni hufungwa pamoja wiki chache kabla ya

kuvunwa ili kuweza kuwa na chanizi kabichi iliyojifunga vizuri na iliyonyooka vizuri.

7.5.1.2 Sifa za ubora Kuwa sawa/kufanana/kulingana, vichwa vikiwa vimejifunga vizuri na kuwa na rangi ya kijani kahawia na majani yakiwa yamejikunja kwenye ukingo. Kusiwe na dalili zozote za ukaukaji au upoteaji wa rangi kwenye majani.

Angalizo wakati wa uvunaji;

Ondoa majani yaliyohaharibika kabla ya kupeleka kwenye stoo. Kuongeza muda ubora hufanywa kwa kulima chainizi kabichi msimu wa baridi na

kuviinamisha vichwa wakati wa kuhifadhi kwenye stoo. Zinahifadhika vizuri Zaidi wakati chainizi kabichiji zikiwa zimejaa vizuri zaidi wakati wa

kuvunwa.

7.5.2.1 Madaraja; Kwa kawaida hazina madaraja.

7.5.2.2 Upoozaji Weka kwenye vyombo vya kusafirisha na pooza haraka. Upoozaji kwa kutumia upepo na maji. Kupooza kwa msukuma wa upepo/hewa.

Kuosha haishauriwi.

Mahitaji/vifaa; Zinasafirishwa kwenye maboksi ya ukubwa mablimbali. Upotevu wa maji unaweza kupunguzwa kwa kuweka kwenye vifungashio vinavyoweza kupitisha hewa ili kuongeza Maisha rafuni.

7.5.3 Uhifadhi Joto; Ikaribie kwenye nyuzijoto 0 lakini pasiwe na kugandana. Kiwango cha unyevu; 98-100%.

Page 23: KITINI NAMBA 8...SEHEMU YA 1 ... - Kushawishi panya na wadudu wengine waharibifu Udhibiti - Umakini wakati wa kukausha – Kukausha hadi kufikia kiwango kinachopendekezwa cha unyevu

22

Mchanganyiko wa hewa 1-2%Okisijeni, na hewa ya ukaa 0-5% kulingana na aina ya chainizikabichi, joto lililokuwepo na muda wa kuhifadhi. Kama mazingira yakidhibitiwa, rangi yamajani na uwingi wa sukari hautaathirika na hali ya uozo haitaendelea.

Utoaji wa hewa ya Ethylene; Kiwango cha chini inaaathirika sana kwenye hewa ya ethylene. Hifadhi kwenye joto na unyevunyuevu wa hewa ulioshauriwa.

7.6. VITUNGUU.

7.6.1 Uvunaji 7.6.1.1 Sifa za ubora Vitunguu viwe vimekomaa, vimejaza vizuri na vigumu; vyenye maganda mapya. Ukubwa, umbo na rangi ya ganda lililokauka viwe sawa na aina halisi. Visiwe vimeharibiwa na vyombo vya kuvunia au wadudu, kuoza, jua, ukijani kwenye ganda,

kuchipua, michubuko, mapacha, shingo ya chupa, vitunguu vyenye ukubwa au udogo kulikokawaida na madhara mengine yeyote yale.

7.6.1.2 Viashiria vya vya ukomaaji. - Vinavyunwa wakati majani yakiwa yameanza kunyauka.

7.6.2 Kukusanya na kupakia. 7.6.2.1 Madaraja. Aina moja, ukomavu ulifanana, ugumu mzuri, na umbo la kufanana. Zisiwe na dalili za kuoza, kuungua na jua, kuchipua na mapacha. Kusiwe na majeraha, kupasuka, uchafu, magonjwa na athari za wadududu.

7.6.2.2 Ukomazaji; Vinakomazwa shambani kwa siku 3-5 ili mradi hakuna mvua, halafu viwekwe kwenye sehemu yenye mzunguko wa hewa na joto dogo kukamilisha ukomazaji.

7.6.2.3 Upoozaji Vitunguu vya kuhifadhiwa kwa muda mrefu vinahitaji upoozaji wa awali kwenye joto la nyuzijoto 0 mara tu baada ya kukomazwa.

7.6.3 Uhifadhi NyuziJoto; 20-30 kwa kukomaza, nyuzijoto 0 kwa hifadhi ya muda mrefu. Hali ya unyevu hewani 65-75%. Mchanganyiko wa hewa:5% hewa ya ukaa,3% hewa ya oksijeni inaweza kutumika. Utoaji wa hewa ya Ethylene, Kiwango cha chini sana. Hivi uathiriki kabisa vikiwekwa

kwenye hewa ya Ethylene, ingawa kiwango cha juu sana kinaweza kuhamasisha kuchipua. Muda wa ubora: Miezi 6-9.

7.6.4 Wadudu na Magonjwa. Uozo wa shingo: Ukungu wa kijivu kwanza kwenye shingo na baadae kwenye kitunguu chote. Kausha vitnguu vizuri. Uozo wa ukungu mweusi.

Page 24: KITINI NAMBA 8...SEHEMU YA 1 ... - Kushawishi panya na wadudu wengine waharibifu Udhibiti - Umakini wakati wa kukausha – Kukausha hadi kufikia kiwango kinachopendekezwa cha unyevu

23

- Hifadhi kwenye nyuzi joto nyuzijoto 0.- Hifadhi kwenye unyevu wa hewa ya wastani.

Uozo wa ukungu wa bluu

- Vuna vitunguu vilivyo komaa tu.- Kausha vitunguu vizuri.- Hifadhi kwenye nyuzi joto 0 sentgradi.- Hifadhi kwenye unyevu wa hewani ya wastani.

Uozo laini unaosababishwa na bacteria

- Vuna vitunguu vilivyo komaa tu.- Kausha vitunguu vizuri.- Punguza michubuko.- Dhibiti kiwango hali ya uhifadhi kwenye stoo.

7.7 PILIPILI HOHO

7.7.1 Uvunaji 7.7.1.1 Sifa za Ubora Pilipili zenye ubora wa hali ya juu zina fanana kwa maumbo, ukubwa na rangi ya aina halisia. Ngozi ya tunda iwe mbichimbichi, imejaza vizuri na imara na iwe na rangi ya mng`ao na

harufu nzuri isiwe na uharibifu wowote kama mipasuko, kuoza na madhara ya jua. Epuka matunda yaliyosinyaa au yaliyofifia au yaliyotobolewa.

7.7.1.2 Vigezo vya uvunaji Vuna kukiwa kukavu. Usifungashie shambani. Pilipili zenye rangi zinaitajika ziwe na angalau 95% ya rangi.

7.7.2 Ukusanyaji, Upakiaji na Ufungishaji 7.7.2.1 Madaraja Hoho zilizo komaa za kijani zenye sifa sawa na aina halisi (isipokua kama kuna aina zaidi ya moja), ziwe zimejaa vizuri, umbo haliko vibaya sana, na hazina madhara ya jua, madhara ya baridi kali, uozo uliokithiri kikonyo au tunda na zisiwe na majeraha yeyote kama vile magonjwa, wadudu au mikandamizo yoyote ile.

7.7.2.2 Upoozaji Upoozaji wa haraka si chini ya nyuzi joto 7. Hewa ya kusukumwa husaidia upoaji. Upoozaji wa maji huweza kutumika.

7.7.3 Uhifadhi. Joto: Nyuzi joto 7. Unyevu hewani: 90-95%. Mchanganyiko wa hewa: iSiyo zidi 5% ya hewa ya ukaa na 2-5% hewa ya oksijeni. Madhara tarajiwa: Madhara ya baridi kali chini ya nyuzi joto (7.2). Muda wa ubora: wiki 2-3.

Page 25: KITINI NAMBA 8...SEHEMU YA 1 ... - Kushawishi panya na wadudu wengine waharibifu Udhibiti - Umakini wakati wa kukausha – Kukausha hadi kufikia kiwango kinachopendekezwa cha unyevu

24

7.7.4 Wadudu na Magonjwa Ukungu wa kijivu: Ni kawaida sana kwenye pilipili.

- Fanya usafi wa shambani.- Zuia vidonda.- Chovya katika maji ya moto yenye joto la nyuzi 53-55 kwa dakika 4.

Uozo mweusi (Altenaria blackrot)- Epuka madhara ya baridi kali.

Uozo laini unaosababishwa na bakteria (bacterial soft rot)- Tumia maji ya kutosha unaposafisha au unapopooza kwa maji.

7.8 NYANYA

7.8.1 Uvunaji 7.8.1.1 Sifa za Ubora Mtunda ya kiwango cha juu huwa magumu, yanafanana, yamejaza na yanang`ara, hayana dalili za michubuko, mikwaruzo au kugandamizwa, hazijasinyaa/pooza au kuoza.

7.8.1.2 Mambo ya Kuzingatia Kwa ujumla matunda yaliyofikia hatua ya kuanza kubadilika rangi ndiyo yanayopendelewa

zaidi na wanunuzi wa jumla; Wasiliana na wateja juu ya hatua ya uivaji wanayoipenda Zungusha tunda ukivuta kuelekea chini ili ulitoe tunda bila mshikio/kikonyo cha tunda.

Kwa baadhi ya aina kikonyo kinaweza kutolewa kama bado kimejishikilia. Vikonyo huwavinabaki kwa nyanya aina ya tunguja (ndogondogo za kienyeji) na uvunaji wake huwa nikwa kutumia mkasi.

Usikandamize matunda wala usiyachubue. Panga matunda sehemu ya kikonyo ielekee pembeni kwa chini. Epuka kuvuna kukiwa na hali ya umande/majimaiji kwenye mimea na matunda. Vaa glovu za pamba shambani na zitumie kufuta uchafu wa kwenye matunda. Nyanya zilizoharibika na mabaki ya nyanya yatumike kuandaa mboji. Kwa kawaida nyanya zinawekwa kwenye maboksi/vifungashio shambani. Matunda ya nyanya yanaitaji yaonekane na sio kusikika, Yahudumie kwa uangalifu sana. Vuna angalau kila baada ya siku moja.

7.8.1.3 Hatua a uivaji/Ukomaaji. Hatua 1: Zimekomaa za kijani: Hatua hii ni nzuri kwa kusafirisha kwenda masoko ya mbali. Hatua ya kijani kuelekea pinki inaweza kuhifadhiwa kwa wiki 1-2 kwenye jokofu, Kama nyanya zina mbegu zilizoanza kubadilika rangi na ute mwingi kuzizunguka huweza kuvunwa na kuiva kwa ubora wa wastani. Kama mbegu zikitolewa na kuonesha kuna rangi nyekundu kiasi, nyanya uiva kwa ubora wa juu

Hatua 2: Hatua ya pink. Hii ni hatua ya uvunaji kwa ajili ya soko la jumla. Nyanya inakua na rangi ya pinki kwenye kitako. Kwa hatua hii, nyanya uiva baada ya siku 3 kwenye joto la kawaida.

Page 26: KITINI NAMBA 8...SEHEMU YA 1 ... - Kushawishi panya na wadudu wengine waharibifu Udhibiti - Umakini wakati wa kukausha – Kukausha hadi kufikia kiwango kinachopendekezwa cha unyevu

25

Hatua 3: Zilizoiva: Nyekundu lakini ngumu. Zitumike mara moja. Hizi hazifai kwa soko la jumla na la mbalimbali kwa soko la moja kwa moja. Hatua hii ndio maarufu sana kwenye masoko ya wakulima.

7.8.2 Ukusanyaji, Upakiaji na Ufungashaji. 7.8.2.1 Madaraja. Aina moja na matunda yenye sifa zinazofanana zimekomaa, hazijaiva kwa kupitiliza au kwa kua laini, safi, zimekua vizuri, kwa wastani zina maumbo mazuri na wastani. Hazina uozo, madhara ya baridi na madhara ya jua. Hazijaathiriwa na kitu chochote kile.

Ustahimilivu:

Madhara kwenye kituo cha usafirishaji: 10% kwa matakwa ya daraja (5%) kwa madhara yanayosababisha uharibifu mkubwa ni 1% kwa kua laini au kuwa na uozo).

Madhara kwenye kituo cha mwisho: 15% kwa matakwa ya daraja (5% kwa laini au kwa kuwa na uozo, 10% kwa michubuko kwenye mabega ya matunda au kupoteza rangi au kua na kovu zilizozama, 10% kwa kuwa na madhara mengineyo na 5% kwa kuwa na madhara makubwa sana kwa sababu yeyote ila isipokua laini au kua na nyanya zilizooza).

7.8.2.2 Kupooza Upoozaji wa ndani ya chumba. Kupooza kwa hewa ya kusukuma kunaleta matokeo mazuri.

7.8.2.3 Ukubwa wa Vifungashio Sifa ya vifungashio

Vifungashio/maboksi yawe masafi, kina kifupi, na kwa chini yawe nyororo/yasiyo namikwaruzo.

Nyanya zinaweza kupangwa kwenye ngazi moja au mbili Uzito: 11 kg cartons (12” ×16” ×91/2”)4.5 kg kwa ngazi moja.

7.8.2.4 Rangi za Matunda: Kijani: Asilimia (100%) ni kijani kuanza kubadilika rangi ya kahawia, Njano, Pinki au nyekundu chini ya asilimia kumi (≤ 10% kwenye tunda).

Kubadilika: 10-30% chini na sio kijani Pinki: 30-60% siyo kijani.

7.8.3 Uhifadhi Joto: nyuzi joto 19-21 kwa kuivisha; ≤ chini ya nyuzi joto 1 kusitisha kuivisha (Hii itumike kwa

nyanya zilizoiva hadi kuwa nyekundu; Inaweza kusababisha madhara ya baridi kali kwanyanya ambazo hazijaiva kabisa); Chini ya nyuzi joto 13 (ladha inaathirika sana inakuambaya sana).

Hali ya unyevunyevu hewani: 90-95%. Upumua wa hewa ya Ethylene :15.5-22.8 Ml/kg kwa saa kwenye nyui joto 20. Mchanganyiko wa hewa: 2-3% hewa ya ukaa kwa zilizoiva lakini bado za kijani, 3-5% hewa

ya ukaa, kwa zilizoiva nyekundu; 3-5% hewa ya oksijeni kwa aina zote.

Page 27: KITINI NAMBA 8...SEHEMU YA 1 ... - Kushawishi panya na wadudu wengine waharibifu Udhibiti - Umakini wakati wa kukausha – Kukausha hadi kufikia kiwango kinachopendekezwa cha unyevu

26

Utoaji wa hewa ya Ethylene:1-10 µL/kg kwa saa. Nyanya zilizoiva za kijani zikiwekwa uivaharaka. Nyanya zilizoanza kutoa rangi hazihitaji ethylene kwani inaweza harakisha uivaji.

Madhara tarajiwa: Zinaathirika na baridi kali, michubuko. Muda wa ubora: Inategemea na hatua ya ukomaaji wakati wa uvunaji.

7.8.4 Wadudu na Magonjwa Aina mbalimbali za uozo: Uozo laini, na aina nyingine za uozo Epuka michubuko au

uharibifu kwenye matunda. Dumisha masharti bora ya usafi na afya. Ondoa na teketeza matunda yaliyoathirika. Uhifadhi wa mazao ya kilimo ni hatua ya mwanzo kabisa mara baada tu ya kuvuna. Hatua zifuatazo huzingatiwa katika uhifadhi bora wa mazao ya kilimo, kuweka mazao

katika hali ya usafi, ubaridi, kuchambua, kutenga katika makundi kulingana na ubora nakufungasha.

Uhifadhi na usimamizi mzuri wa mavuno kwa kiasi kikubwa huamua ubora wa mwisho,kujua soko zuri la mazao kulingana na madaraja ya ubora.

Upotevu na uharibifu hutokea katika Mazao baada ya Kuvuna wakati wa shughuli zifuatazo:Kuvuna, kukausha, kusindika, kusafirisha na katika Uhifadhi.

Mambo makuu yanayosababisha uharibifu huo ni pamoja na joto, unyevu waduduwaharibifu ghalani na uharibifu wakati wa kusafirisha.

Page 28: KITINI NAMBA 8...SEHEMU YA 1 ... - Kushawishi panya na wadudu wengine waharibifu Udhibiti - Umakini wakati wa kukausha – Kukausha hadi kufikia kiwango kinachopendekezwa cha unyevu

27

MBINU /STADI ZILIZOFUNDISHWA 1. Jinsi ya kutambua wadudu mbalimbali na mbinu za udhibiti

1.1 Fukusi wa kunde

1.2 Fukusi wa maharage

1.3 Dumuzi

1.4 Tembo wa Vihenge

1.5 Mbawakau wa unga

1.6 Vipepeo

1.6.1 Vipepeo wa nafaka

1.6.2 Vipepeo wa ghalani

2. Kukabiliana na Ukungu kwenye mazao yaliyokaushwa

2.1 Athari za ukungu na sumu kuvu2.2. Jinsi ya kuzuia uchafuzi unaosababishwa na fangasi / Kuvu

3. Hifadhi ya Mbegu za nafaka – Kanuni muhimu za kuzingatia ili kuzuia uharibifu

3.1 Aina na Uchaguzi wa mbegu 3.2 Kupangilia vizuri muda wa kuvuna 3.3 Ukaushaji 3.4 Kupanga Madaraja na usafi wa Mazao 3.5 Enelo la ghala 3.6 Sifa za Ghala 3.7 Usafi wa ghala la kuhifadhia 3.8 Kuchunguza au Kukagua Ghala 3.9 Kufukiza moshi Ghalani (pilipili) 3.10 Unyunyiziaji wa majivu Ghalani ili kudhibiti vimelea na wadudu 3.11 Matumizi ya Vitu Dawa

3.11.1 Chokaa 3.11.2 Mchanga laini 3.11.3 Mafuta ya Mimea

3.12 Matumizi ya Mchanganyiko wa Mimea mbalimbali katika udhibiti na uhifadhi wa Mazao yaliyokaushwa

3.13 Mbinu za Usimamizi na Uhifadhi wa mazao ya bustani 3.13.1 Uvunaji 3.13.2 Ukaushaji 3.13.3 Usafirishaji 3.13.4 Ufungashaji 3.13.5 Upangaji madaraja 3.13.6 Upoozaji 3.13.7 Uhifadhi

Page 29: KITINI NAMBA 8...SEHEMU YA 1 ... - Kushawishi panya na wadudu wengine waharibifu Udhibiti - Umakini wakati wa kukausha – Kukausha hadi kufikia kiwango kinachopendekezwa cha unyevu
Page 30: KITINI NAMBA 8...SEHEMU YA 1 ... - Kushawishi panya na wadudu wengine waharibifu Udhibiti - Umakini wakati wa kukausha – Kukausha hadi kufikia kiwango kinachopendekezwa cha unyevu

SHUK RANI

Kitini hiki cha “Uhifadhi na usimamizi wa Mazao baada ya kuvuna” kimeandaliwa na shirika la

Kilimo Endelevu Tanzania (SAT – Sustainable Agriculture Tanzania) kwa ushirikiano na

SWISSAID Tanzania. Kitini hiki kimepitiwa na kuidhinishwa na wawakilishi wa Ofisi ya Kilimo

ya Mkoa wa Mtwara, Ministry of Agriculture Training Institute (MATI) Naliendele, Sustainable

Agriculture Tanzania (SAT), Tanzania Organic Agriculture Movement (TOAM), Tanzania

Alliance for Biodiversity (TABIO), Tanzania Official Seed Certification Institute (TOSCI-Mtwara),

Shirika la Kuhifadhi Misitu Asilia Tanzania (TFCG), wawakilishi wa wakulima na SWISSAID

Tanzania katika warsha iliyofanyika tarehe 25 – 27 September 2019 katika Wilaya ya

Masasi, mkoani Mtwara. Pia, msaada wa kifedha kutoka Ubalozi wa Ufaransa nchini

Tanzania, Liechtenstein Development Service (LED) na Swiss Agency for Development

and Cooperation (SDC) umefanikisha kwa kiwango kikubwa katika kugharamia uandaaji,

kupitia na kukamilisha uchapishaji wa kitini hiki.

“Kitini hiki cha mafunzo kipo chini ya hati miliki ya kimataifa nambari 4.0 (CC BY-NC-DC 4.0), hairuhusiwi kuuzwa ama kunakiriwa pasipo idhini ya mmiliki.”

"This training manual is licensed under a Creative Commons Attribution-Non Commercial-NoDerivatives 4.0 International (CC BY-NC-ND 4.0) license"