4
1 KWANINI MUNGU ANATUPA UTAJIRI MALI NA FEDHA ? 1. ILI KUIMARISHA AGANO LAKE (UFALME WAKE)* Kumb 8:18 (12-18) Agano la Mungu kwa siku za leo, ni Agano JIPYA. Kuimarisha Agano lake maana yake; ni kuimarisha kazi ya injili ya Yesu Kristo, ili wokovu uwafikie watu wote. Tunapotoa muda wetu na vipawa vyetu na mali zetu kwa ajili ya kazi ya Mungu, ili kuimarisha Ufalme wa Mungu, tunakuwa tumetimiza makusudi ya Mungu ya kutupa hizi mali; “kuimaisha agano lake” (Kumb 8:17-18) Soma pia, Gal 3:11,23-26,29; Rum 10:13 – 15; Fillip 4:15 –19) Mali zetu si pesa tu. Mali ni kitu chochote chenye thamani na kikitumiwa vizuri, kinaweza kuongeza ubora wa kitu. Kwa mfano; a) Muda wako ni mali ya thamani sana, ukiutumia vizuri, utakuletea kipato. b) Vipawa vyako pia ni mali, ukikitumia vizuri, kitakuletea kipato. c) Fedha yako pia ni mali, ukiipangilia a kuitumia vizuri, itakuboreshea maisha yako. Tunapotoa muda wetu na vipawa vyetu na mali zetu kwa ajili ya kazi ya Mungu, ili kuimarisha Ufalme wa Mungu, tunakuwa tumepanda mbegu katika ufalme wa Mungu na kwa wakati wa Mungu, zitarudi kwetu moja ikiwa imezaa 30, na nyingine itarudi imezaa 60, na nyingine 100. Hii ni kwasababu, mali zako na vipawa vyako na muda wako, ni sadaka mbele za Mungu.Hayo ndio makusudi ya Mungu ya kutupa hizi mali; “kuimaisha agano lake” (Kumb 8:17-18). Unapotoa sadaka kama hizi kwa Mungu, toa kwa imani, yaani toa kwa kutarajia kupokea tena kutoka kwa Mungu. Usione muda wako kama unapoteza au unajitolea tu. Bali vione hivi vitu kuwa ni sadaka, kwasababu kwa uhalisi, vitu hivi ni mali. Muda ni pesa; vipawa ni pesa pia, na mali zetu ni pesa. Unapotoa muda, vipawa na mali zako kwa Mungu, ona kwamba unatoa sadaka. Na sadaka ni mbegu. Na mbegu ikitolewa kwa usahihi, huzaa sana (Math 13:8).

Kwanini mungu anatupa utajiri

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Kwanini mungu anatupa utajiri

1

KWANINI MUNGU ANATUPA UTAJIRI

MALI NA FEDHA ?

1. ILI KUIMARISHA AGANO LAKE (UFALME WAKE)* Kumb 8:18 (12-18)

Agano la Mungu kwa siku za leo, ni Agano JIPYA. Kuimarisha Agano lake maana yake; ni

kuimarisha kazi ya injili ya Yesu Kristo, ili wokovu uwafikie watu wote. Tunapotoa muda

wetu na vipawa vyetu na mali zetu kwa ajili ya kazi ya Mungu, ili kuimarisha Ufalme wa

Mungu, tunakuwa tumetimiza makusudi ya Mungu ya kutupa hizi mali; “kuimaisha agano

lake” (Kumb 8:17-18)

Soma pia, Gal 3:11,23-26,29; Rum 10:13 – 15; Fillip 4:15 –19)

Mali zetu si pesa tu. Mali ni kitu chochote chenye thamani na kikitumiwa vizuri, kinaweza

kuongeza ubora wa kitu. Kwa mfano;

a) Muda wako ni mali ya thamani sana, ukiutumia vizuri, utakuletea kipato.

b) Vipawa vyako pia ni mali, ukikitumia vizuri, kitakuletea kipato.

c) Fedha yako pia ni mali, ukiipangilia a kuitumia vizuri, itakuboreshea maisha yako.

Tunapotoa muda wetu na vipawa vyetu na mali zetu kwa ajili ya kazi ya Mungu, ili

kuimarisha Ufalme wa Mungu, tunakuwa tumepanda mbegu katika ufalme wa Mungu na

kwa wakati wa Mungu, zitarudi kwetu moja ikiwa imezaa 30, na nyingine itarudi imezaa 60,

na nyingine 100. Hii ni kwasababu, mali zako na vipawa vyako na muda wako, ni sadaka

mbele za Mungu.Hayo ndio makusudi ya Mungu ya kutupa hizi mali; “kuimaisha agano

lake” (Kumb 8:17-18).

Unapotoa sadaka kama hizi kwa Mungu, toa kwa imani, yaani toa kwa kutarajia kupokea tena

kutoka kwa Mungu. Usione muda wako kama unapoteza au unajitolea tu. Bali vione hivi vitu

kuwa ni sadaka, kwasababu kwa uhalisi, vitu hivi ni mali. Muda ni pesa; vipawa ni pesa pia,

na mali zetu ni pesa. Unapotoa muda, vipawa na mali zako kwa Mungu, ona kwamba unatoa

sadaka. Na sadaka ni mbegu. Na mbegu ikitolewa kwa usahihi, huzaa sana (Math 13:8).

Page 2: Kwanini mungu anatupa utajiri

2

Hivyo, toa kwa imani, yaani toa kwa kutarajia kupokea tena kutoka kwa Mungu. Usione

muda wako kama unapoteza au unajitolea tu, bali ona kwamba umetoa sadaka. Tunapotoa

muda wetu na vipawa vyetu na mali zetu kwa ajili ya kazi ya Mungu, ili kuimarisha Ufalme

wa Mungu, tunakuwa tumepanda mbegu katika ufalme wa Mungu na kwa wakati wa Mungu,

zitarudi kwetu moja ikiwa imezaa 30, na nyingine 60, na nyingine 100; kama tulivyosoma

katika Mathayo 13:8.

2. ILI KUVITUMIA KWA MAHITAJI YETU BINAFSI *Yoh16:24

Soma tena 1Timotheo 6:17 na 2Wakorintho 9:8 – 11

Mungu kama Baba yetu na kama Mchungaji Mwema, anajali sana mahitaji yetu na haja zetu

au shauku za mioyo yetu. (vitu vitupavyo furaha na kuridhika). Ndio maana hutupa utajiri, ili

tufurahie maisha. Si mapenzi ya Mungu tuwe masikini. Ndio maana Yesu alifanyika maskini

(kimwili) ili kwa umasikini wake, (sisi) tupate kuwa matajiri (kimwili)” (2 Kor 8:9)

Ni mapenzi ya Mungu tupate vitu vyote vitakavyotufanya tufurahie maisha yetu duniani.

Nyumba nzuri, mavazi mazuri, chakula kizuri, kazi nzuri, magari mazuri, biashara nzuri,

mifugo mizuri, mashamba mazuri, mshahara mzuri, n.k.

(Zab23:1- 2; Fil 4:6-7,19; Zab37:4; Zab145:17- 19)

3. ILI KUWAGAWIA WAHITAJI *2KOR 9:8-13;

Pia soma 1Timotheo 6:17-19; Waefeso 4:28 na Luka 6:38.

Tunapowapa wahitaji fedha, nguo, viatu, chakula au vitu vya aina nyingine ili kuwasaidia

kimaisha, tunapata thawabu kubwa kwa Mungu. Kumsaidia mhitaji kitu, ni kumpa Mungu.

Hebu soma vizuri Mathayo 25:31-40; Mathayo 10:40 – 42 na Yohana 13:20.

Mungu ametupa mali, fedha na utajiri wa namna nyingi ili tuwasaidie wahitaji na masikini,

wajane na yatima, wagonjwa na walemavu. Thawabu yake ni kubwa mbele za Mungu, na

Mungu ataona sababu ya kukupa tena na kukuzidishia. Tena Mungu atakufanya uwe

njia/mkondo wa baraka zake kwa watu wengine.

Soma pia 2Kor 8:14-15, Mdo 20:35

Page 3: Kwanini mungu anatupa utajiri

3

TUMTUMIKIE MUNGU KWA MALI ZETU

Ushiriki wetu katika kazi ya Mungu, kwa njia ya kutoa muda, vipawa na mali, utamfanya

Mungu, kutufungulia madirisha na milango ya mbinguni, ili kutumwagia baraka nyingi,

tunazohitaji katika mashamba, mifugo, biashara, miradi mbalimbali tuliyonayo. Pia ushiriki

wetu katika kazi ya Mungu, kwa njia ya kutoa muda, vipawa na mali, utamfanya Mungu

azibariki familia zetu, watot wetu, ndoa zetu na afya zetu pia, ili tuzidi kumtumikia na kuwa

baraka kwa wengine pia. Baraka za Mungu zitatuzidishia mapato yetu, ili tuwe na vitu vya

kutosha kutumia na hata kuwa baraka kwa wahitaji wengi

Utoaji ni njia ya Mungu kutupa na kutujaza tunavyohitaji *1Fal 17:1-16

Mungu ndiye alieyewaka kanuni ya kupanda na kuvuna, kutoa na kupokea. Hivyo, mara

nyingi tunapomwomba Mungu atubariki/atujaze mahitaji yetu, anatuletea mafasi ya kutoa

kwanza, ili tupokee mahitaji yetu tumwombayo. Kwasababu, ndiyo kanuni ya kupokea. Ni

ajabu, sicho tunachotegemea (kutoa wakati wewe binafsi unahitaji). Badala ya Mungu

kukupa moja kwa moja kitu ulichomwomba, anakuletea nafsi ya kutoa hicho hicho kidogo

ulichonacho, kiwe kama mbegu, ili hatimaye upokee (uvune) kile ulichomwomba, na hata

zaidi ya ulivyoomba.

Biblia pia inasema hivi katika kitabu cha Waefeso 3:20 na Wafilipi 4:15-19; kwamba, “Basi

atakuzwe Mungu awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tumwombaye au kuliko

yote tuyawazayo, kwa kadri ya nguvu, itendayo kazi ndani yetu” (Efe 3:20; Fil 4:15-19).

1Wafalme 17:13-16; Eliya akamwambia (yule mama mjane); usiogope (kutoa hicho kidogo

kilichobaki) … enenda ukafanye kwa ajili yangu (kwa maana ukinipa mimi, utakuwa

umempa Mungu) na Mungu wa Isarael anasema, unga wako wala mafuta yako

hayatapunguka kamwe, mpaka njaa itakapoondoka juu ya nchi. Yaani Mungu atavizidisha. Si

ajabu anliongezea Kama ukikubali na kutii, utakula mema ya nchi. Lakini ukikataa,

utaangamia (kama wengine wanavyoangamia). (Isa 1:19)

Si jambo rahisi kutoa wakati wewe mwenyewe umepumgukiwa au una uhitaji. Inahitajika

imani kubwa kutoa kidogo kilichobaki, ili uhitai wako ujazwe. Hivyo, usishangae siku

utakapomwomba Mungu pesa au vitu, halafu badala ya kukupa, anakuletea mhitaji ili umpe

pesa au vitu, au analeta nafasi ya wewe kutoa sadaka. Kumbuka kanuni yake, huwezi kuvuna

bila kupanda!

Page 4: Kwanini mungu anatupa utajiri

4

Hivyo, ukikubali na kutii, utavuna na kupata mema, tena zaidi ya ulivyotarajia. Hii ni kanuni

ya Mungu; ukipanda haba utavuna haba, ukipanda nyingi, utavuna nyingi. Huwezi kuvuna

bila kupanda

Utoaji wa sadaka, hufungulia na kutuletea mahitaji yetu (2Wafalme 4:8-41)

Huyu mama Mshunami pamoja na mume wake, japo walikuwa ni watu wenye fedha nyingi

na cheo kikubwa, lakini walikuwa hawajapata mtoto, pengine kwa miaka mingi sana.

Inaawezekana walishaombewa na watumishi wengi wa Mungu, lakini bado maombi yao

hayakuleta muujiza waliokuwa wanausubiri kwa hamu kubwa. Kumbe ufunguo wa muujiza

wao, haukuwa katika maombi pekee, bali katika utoaji wao pia. Yamkini Mungu alishawapa

mtot wao katika ulimwengu wa kiroho, ila sadaka ndio ilikuwa inahitajika, ili kutelemsha

Baraka yao ya mtoto.

Neno la Mungu linasema, Mungu akaweka mzigo ndani ya mama huyu, kumjengea Nabii

Elisha nyumba, ili asipate shida katika utumishi wake. Na huyu mama akamshirikisha

mumewe. Nao wakaiweka azma yao katika matendo. Walipotii na kufanya kile kitu ambacho

Mungu aliweka mioyoni mwao, kwa ajili ya Elisha mtumishi wa Mungu, ndipo muujiza wao

wa kupata mtoto, ukatimia.

Biblia inasema, Elisha akapewa Neno la Mungu kwa ajili ya familia hii, juu ya kupewa mtoto

wao (ambaye tayari alishatolewa kwao, kwa njia ya maombi, lakini ni katika ulimwengu wa

kiroho). Sadaka yao, iliushuhsa ule muujiza wao, kutoka rohoni, ukawa halisi katika mwili,

kwasababu ya Utii wao. Sadaka ina nguvu ya kutupa mahitaji yetu.

Kwahiyo Ushiriki wetu katika kazi ya Mungu, kwa njia ya kutoa muda, vipawa na mali,

utamfanya Mungu, kutufungulia madirisha na milango ya mbinguni, ili kutumwagia baraka

nyingi, tunazohitaji katika mashamba, mifugo, biashara, miradi mbalimbali tuliyonayo.

Pia ushiriki wetu katika kazi ya Mungu, kwa njia ya kutoa muda, vipawa na mali, utamfanya

Mungu azibariki familia zetu, watot wetu, ndoa zetu na afya zetu pia, ili tuzidi kumtumikia na

kuwa baraka kwa wengine pia. Baraka za Mungu zitatuzidishia mapato yetu, ili tuwe na vitu

vya kutosha kutumia na hata kuwa baraka kwa wahitaji wengi (Malaki 3:10–12, Luk 6:38)