80
COUNSENUTH Information Series No.16 December, 2008 MODULE GFR4.indd 1 8/25/09 2:49:50 PM

MAFUNZO KWA WATOA HUDUMA MWONGOZO WA MKUFUNZI

Embed Size (px)

Citation preview

COUNSENUTHInformation Series No.16December, 2008

MODULE GFR4.indd 1 8/25/09 2:49:50 PM

MODULE GFR4.indd 2 8/25/09 2:49:50 PM

Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

LISHE KWA WATU

WALIOAMBUKIZWA VIRUSI VYA UKIMWI

MAFUNZO KWA WATOA HUDUMA

MWONGOZO WA MKUFUNZI

December, 2008

MODULE GFR4.indd 3 8/25/09 2:49:50 PM

Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)ii

LISHE KWA WATU WALIOAMBUKIZWA VIRUSI VYA UKIMWI

MAFUNZO KWA WATOA HUDUMA

MWONGOZO WA MKUFUNZI

© COUNSENUTH, 2008

ISBN 978 - 9987 - 9017 - 9 - 1

Mwongozo huu umetayarishwa na:

Kituo cha Ushauri Nasaha, Lishe na Afya (COUNSENUTH)United Nations Rd./ Kilombero Str.Plot No. 432, Flat No. 3S. L. P. 8218Dar es Salaam, TanzaniaSimu/Nukushi: +255 22 2152705 au +255 755 165 112Barua pepe: [email protected]

Kwa ufadhili wa:Global Fund Round Four Program

Sehemu yoyote ya kitabu hiki inaweza kunakiliwa kwa ajili ya matumizi yasiyo ya kibiashara ili mradi ionyeshe kwamba maelezo hayo yametolewa kutoka kwenye kitabu hiki.

MODULE GFR4.indd 4 8/25/09 2:49:50 PM

Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi) iii

YALIYOMO

VIFUPISHO ..................................................................................................................................................... iv

SHUKRANI ..................................................................................................................................................... v

UTANGULIZI ..................................................................................................................................................... vi

MAELEZO KUHUSU MWONGOZO ....................................................................................................................... 1

MAELEZO KUHUSU MAFUNZO ........................................................................................................................... 3

MADA YA 1: ELIMU YA MSINGI YA CHAKULA NA LISHE ............................................................................... 6

MADA YA 2: UKWELI KUHUSU VIRUSI VYA UKIMWI NA UKIMWI ................................................................ 13

MADA YA 3: UHUSIANO WA LISHE NA VIRUSI VYA UKIMWI ........................................................................ 16

MADA YA 4: MBINU ZA KUBORESHA CHAKULA ........................................................................................... 18

MADA YA 5: USAFI NA USALAMA WA CHAKULA NA MAJI ............................................................................ 20

MADA YA 6: LISHE NA ULAJI WAKATI WA MATATIZO YA KIAFYA

YANAYOAMBATANA NA KUAMBUKIZWA VIRUSI VYA UKIMWI ................................................ 22

MADA YA 7: UHAKIKA WA CHAKULA KATIKA KAYA ...................................................................................... 28

MADA YA 8: KUTATHMINI HALI YA LISHE YA MTU ALIYEAMBUKIZWA VIRUSI VYA UKIMWI .................... 31

MADA YA 9: MATUMIZI YA DAWA NA CHAKULA ............................................................................................ 36

MADA YA 10: LISHE KWA WANAWAKE WAJAWAZITO NA WANAONYONYESHA ......................................... 40

MADA YA 11: ULISHAJI WA MTOTO KATIKA HALI YA KAWAIDA. ................................................................... 43

MADA YA 12 : ULISHAJI WA MTOTO KATIKA HALI YA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI. ....................... 47

MADA YA 13: KUMLISHA MTOTO WA UMRI MIEZI 6 MPAKA 24 ..................................................................... 52

MADA YA 14: HUDUMA ENDELEVU ................................................................................................................. 56

MADA YA 15: MBINU ZA KUWASILIANA NA MLENGWA .................................................................................. 59

MADA YA 16: MTINDO BORA WA MAISHA KWA AFYA ..................................................................................... 63

MADA YA 17: WAJIBU WA MHUDUMU KATIKA KUTOA HUDUMA NA MATUNZO YA LISHE

KWA WATU WALIOAMBUKIZWA VIRUSI VYA UKIMWI ............................................................... 66

BIBLIOGRAFIA ..................................................................................................................................................... 68

MODULE GFR4.indd 5 8/25/09 2:49:51 PM

Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)iv

VIFUPISHO

AMREF African Medical Research Foundation

ART Antiretroviral Therapy

ARV Antiretroviral

AFASS Acceptable, Feasible, Affordable, Sustainable, Safe

BP Blood Pressure

BMI Body Mass Index

COUNSENUTH Centre for Counselling, Nutrition and Health Care

CHAC Council HIV and AIDS Coordinator

CTC Care and Treatment Clinic

Hb Haemoglobin

FANTA Food and Nutrtition Technical Assistance

IGA Income Generating Activities

PMTCT Prevention of Mother to Child Transmission

RFE Rapid Funding Envelop

TB Tuberculosis

TDHS Tanzania Demographic and Health Survey

TACAIDS Tanzania Commission for AIDS

VCT Voluntary Counselling and Testing

ORS Oral Rehydration Solution

UKIMWI Upungufu wa Kinga Mwilini

USAID United States Agency for International Development

UNICEF United Nations Children’s Fund

VVU Virusi vya UKIMWI

VCT Voluntary Counselling and Testing

WHO World Health Organization

MODULE GFR4.indd 6 8/25/09 2:49:51 PM

Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi) v

SHUKRANI

Kituo cha Ushauri Nasaha, Lishe na Afya (COUNSENUTH) kinatoa shukrani za dhati kwa Global Fund Round Four

Program kupitia Serikali ya Tanzania kwa kufadhli utayarishaji na uchapishaji wa mwongozo wa mkufunzi wa lishe kwa

watu walioambukizwa virusi vya UKIMWI.

COUNSENUTH inatoa shukrani za pekee kwa mradi wa TUMAINI chini ya ufadhili wa Shirika la Kimataifa la

Maendeleo la Marekani (USAID) kwa kufadhili utayarishaji wa mwanzo wa mwongozo huu. Shukrani kwa wakufunzi

wote walioshiriki kufundisha katika mafunzo ya lishe kwa watu waliombukizwa VVU katika mradi wa Tumaini, Tunajali

na mradi wa Rapid Funding Envelope for HIV/AIDS (RFE) kwa kutoa maoni ya kuboresha mwongozo huu.

Aidha COUNSENUTH inatoa shukrani za dhati kwa mashirika, wataalamu mbalimbali na watu binafsi ambao

wamechangia kwa njia mbalimbali katika kutayarisha na kukamilisha mwongozo huu.

COUNSENUTH inapenda pia kutambua mchango wa wataalamu wafuatao ambao walishiriki katika hatua mbalimbali

za utayarishaji wa mwongozo huu: Restituta Shirima; Dr. Lunna Kyungu; Tuzie Edwin; Belinda Liana na Mary G.

Materu. COUNSENUTH inathamini na kutambua sana michango yao yote na maoni ambayo yamechangia katika

kufanikisha na kukamilisha mwongozo huu.

Shukrani kwa Donald Navetta kwa kuhariri mwongozo huu.

MODULE GFR4.indd 7 8/25/09 2:49:51 PM

Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)vi

UTANGULIZI

Watu waliombukizwa virusi vya UKIMWI wapo katika hatari kubwa ya kupata utapiamlo kwani matatizo mengi

yanayowapata huathiri ulaji na uyeyushwaji wa chakula, pia usharabu wa virutubishi na matumizi yake mwilini. Vilevile,

virusi vya UKIMWI vinapokuwa mwilini mwa mtu huongeza mahitaji ya baadhi ya virutubishi.

Hali nzuri ya lishe ni muhimu katika kuboresha lishe na afya ya mtu. Hali nzuri ya lishe kwa mtu aliyeambukizwa virusi

vya UKIMWI, husaidia kurefusha kipindi cha tangu kuambukizwa virusi vya UKIMWI hadi kuugua UKIMWI. Vilevile,

husaidia kupunguza makali ya maradhi na kufanya dawa zinazotumiwa zifanye kazi kwa ufanisi na kuchangia katika

kuboresha hali ya maisha ya mtu kwa ujumla.

Mwongozo huu umetayarishwa ili kumwongoza mkufunzi katika kuwajengea uwezo watoa huduma katika ngazi

mbalimbali ili waweze kutoa matunzo na huduma bora za lishe kwa watu waliombukizwa virusi vya UKIMWI.

Mada mbalimbali zimeelezea kuhusu lishe na virusi vya UKIMWI ikiwa ni pamoja na, elimu ya msingi ya chakula na

lishe, ukweli kuhusu VVU, uhusiano wa lishe na VVU, mbinu za kuboresha chakula na usafi na usalama wa chakula

na maji. Mada nyingine ni lishe wakati wa matatizo mbalimbali ya kiafya yanayoambatana na kuambukizwa virusi

vya UKIMWI, uhakika wa chakula katika kaya, kutathmini hali ya lishe ya mtu aliyeambukizwa virusi vya UKIMWI,

matumizi ya dawa na chakula, lishe kwa wanawake wajawazito na wanaonyonyesha, ulishaji wa mtoto; ulishaji wa

mtoto aliyezaliwa na mama mwenye virusi vya UKIMWI na ulishaji wa mtoto wa umri miezi 6 mpaka 24. Mwongozo huu

pia umegusia mada kuhusu huduma endelevu, mbinu za kuwasiliana na mlengwa na wajibu wa mtoa huduma katika

kutoa huduma na matunzo ya lishe kwa watu walioambukizwa virusi vya UKIMWI na mtindo bora wa maisha kwa afya.

Aidha rejea kwa mkufunzi pia zimeoneshwa.

COUNSENUTH inaamini kuwa kwa kutumia mwomgozo huu, wakufunzi wataweza kutoa elimu na stadi muhimu kwa

watoa huduma kuhusu lishe hivyo kuchangia katika kuboresha matunzo na huduma za lishe kwa watu walioambukizwa

virusi vya UKIMWI.

MODULE GFR4.indd 8 8/25/09 2:49:52 PM

1Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

MAELEZO KUHUSU MWONGOZOUTANGULIZIWatu wote wanaowahudumia watu walioambukizwa virusi vya UKIMWI (VVU) inabidi wawe na taarifa na stadi za kutosha kuwawezesha kuwasiliana na walengwa wao na kuwasaidia ili waweze kufuata ulaji unaofaa.Katika harakati za kujenga uwezo katika ngazi mbalimbali ili kuboresha hali ya lishe ya watu walioambukizwa VVU, mafunzo huendeshwa kwa watoa huduma wa ngazi mbalimbali kutoka vituo vya afya na asasi zinazotoa huduma kwa watu walioambukizwa VVU.

LENGO KUU LA MWONGOZO: Kutoa stadi na elimu kuhusu lishe kwa watu walioambukizwa virusi vya UKIMWI kwa watoa huduma ili kuwawezesha kutoa ushauri kuhusu afya na lishe bora.

MALENGO MAHUSUSI: Kuinua kiwango cha uelewa cha washiriki kuhusu: Umuhimu wa vyakula mbalimbali kwa binadamu na ulaji unaofaa. Mambo muhimu kuhusu maambukizi ya Virusi vya UKIMWI. Uhusiano kati ya virusi vya UKIMWI na lishe. Mbinu mbalimbali za kuboresha chakula hususan cha mtu aliyeambukizwa virusi vya UKIMWI. Umuhimu wa usafi na usalama wa chakula na maji hususan kwa mtu aliyeambukizwa virusi vya UKIMWI. Jinsi ya kukabiliana kilishe na matatizo mbalimbali ya kiafya yanayoambatana na kuambukizwa virusi vya

UKIMWI. Mbinu mbalimbali za kuboresha uhakika wa chakula katika kaya. Stadi za kutathmini hali ya lishe ya mtu aliyeambukizwa virusi vya UKIMWI. Uhusiano kati ya chakula na baadhi ya dawa zinazotumiwa na watu walioambukizwa virusi vya UKIMWI au

UKIMWI. Umuhimu wa lishe bora kwa wanawake wajawazito na wanaonyonyesha. Namna ya kumlisha mtoto katika hali ya kawaida na katika hali ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Umuhimu wa kumwanzishia mtoto chakula cha nyongeza katika umri unaotakiwa na kufahamu jinsi ya

kumlisha mtoto mwenye umri wa miezi 6 – 24. Huduma mbalimbali za kuboresha afya na maisha ya mtu aliyeambukizwa virusi vya UKIMWI.

Umuhimu wa kufuata mtindo bora wa maisha. Wajibu wa watoa huduma katika kutoa huduma na mafunzo ya lishe kwa watu walioambukizwa virusi vya

UKIMWI katika jamii. Stadi na mbinu mbalimbali muhimu za kuwasiliana na mlengwa.

MODULE GFR4.indd 9 8/25/09 2:49:52 PM

2 Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

MADA ZA MWONGOZO DAKIKA

Elimu ya msingi ya chakula na lishe ................................................................................................... 180

Ukweli kuhusu vvu na UKIMWI ............................................................................................................ 60

Uhusiano wa lishe na virusi vya UKIMWI ............................................................................................. 60

Mbinu za kuboresha chakula ............................................................................................................... 30

Usafi na usalama wa chakula na maji .................................................................................................. 60

Lishe na ulaji wakati wa matatizo ya kiafya yanayoambatana na kuambukizwa

virusi vya UKIMWI ................................................................................................................................ 180

Uhakika wa chakula katika kaya .......................................................................................................... 60

Kutathmini hali ya lishe ya mtu aliyeambukizwa virusi vya UKIMWI .................................................... 180

Matumizi ya dawa na chakula .............................................................................................................. 60

Lishe kwa wanawake wajawazito na wanaonyonyesha ....................................................................... 60

Ulishaji wa mtoto katika hali ya kawaida .............................................................................................. 60

Ulishaji wa mtoto katika hali ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI .................................................... 60

Kumlisha mtoto wa umri miezi 6 mpaka 24 .......................................................................................... 60

Huduma endelevu ................................................................................................................................ 60

Mbinu za kuwasiliana na mlengwa ....................................................................................................... 60

Mtindo bora wa maisha kwa afya ......................................................................................................... 120

Wajibu wa mhudumu katika kutoa huduma na matunzo ya lishe kwa watu walioambukizwa

virusi vya UKIMWI ................................................................................................................................ 60

MODULE GFR4.indd 10 8/25/09 2:49:52 PM

3Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

MAELEZO KUHUSU MAFUNZOKUENDESHA MAFUNZO Sehemu hii inaelezea njia zitumikazo kuendeshea mafunzo haya. Unapaswa kusoma sehemu hii kabla hujaanza kufundisha somo lolote.Yawezekana baadhi ya washiriki wameambukizwa virusi vya UKIMWI, au wana ndugu na jamaa wa karibu au rafiki ambao wanaishi na virusi vya UKIMWI. Epuka kutoa maoni au maelezo ambayo yanalenga kukosoa watu walioambukizwa virusi vya UKIMWI wakati wa mafunzo kuepuka kukwaza washiriki.

KUUNDA VIKUNDIKufanya kazi katika vikundi huwezesha kufanya ufundishaji kuwa wa kuingiliana na shirikishi, na hutoa nafasi kwa kila mmoja kuuliza maswali. Washiriki ambao sio wazungumzaji sana pia wanapata nafasi ya kuchangia. Kila kikundi ni vema kiwe na uwiano wa washiriki wenye fani tofauti na watoke sehemu mbalimbali. Washauri washiriki wachanganyike na wabadilishane mawazo. Hii itasaidia washiriki kuondoa aibu, na hivyo kuwawezesha kuwasiliana na kusaidiana katika kipindi chote cha mafunzo.Jitahidi kufahamu majina ya washiriki wote mwanzoni mwa mafunzo, na tumia majina yao kila inapobidi. Tumia majina yao unapotaka wazungumze, kujibu maswali, unapozungumzia mchango wao au unapo washukuru.

KUjITAYARISHA KUTOA MADA

Soma maelezo Kabla ya kutoa mada, soma maelezo yote kwa uangalifu na angalia kwa makini vielelezo utakavyotumia katika

somo husika ili uvielewe.Ni muhimu uwe unaielewa mada kwa usahihi, ili uwe na mpangilio wa mawazo wakati wa kuitoa. Hii ni muhimu hata kama wewe ni mkufunzi mwenye uzoefu na uliyebobea katika masuala ya lishe. Soma maandiko, weka alama sehemu muhimu unazotaka kuzizungumzia au ongeza maelezo yako ya kukukumbusha kuhusu vipengele muhimu vya kusisitiza.

Husisha washiriki Wakati unatoa mada ni vema kuwauliza maswali washiriki, ili kuweza kupima uelewa wao na kuwafanya wafikiri.

Njia hii inafanya washiriki kuwa na hamasa ya kuendelea kusikiliza na kwa kawaida ni njia nzuri ya kujifunza. Uliza maswali yasiyo na majibu ya “ndiyo” au “hapana” ili washiriki waweze kujieleza zaidi ya kusema “ndiyo” au

“hapana.

Yapokee majibu ya washiriki na kuwatia moyo kujaribu tena. Zungumzia kidogo kuhusu majibu yao, pia sema “Asante” au “Ndiyo” pale inapobidi. Kama mshiriki akitoa jibu ambalo sio sahihi usiseme “Hapana au umekosea” hii itawafanya wengine waliotaka kuchangia waogope. Pokea majibu yote, na usiseme kitu ambacho kitawakatisha tamaa. Mshiriki anapotoa jibu sahihi, lijadili na kulipanua na hakikisha kuwa kila mshiriki amelielewa.

Usiruhusu washiriki wengi kuzungumza kwa wakati mmoja. Kama hii itatokea katisha mazungumzo na uwape nafasi ya kuzungumza mmoja mmoja. Kwa mfano sema tutamsikiliza Mariamu kwanza, halafu Florida na hatimaye Mwajuma. Kwa kawaida watu hawataingilia mazungumzo wakijua kuwa nao watapata nafasi ya kuzungumza.

Usiruhusu washiriki wachache (mmoja au wawili) kujibu maswali yote. Kama mshiriki mmoja akitaka kujibu maswali yote mwambie asubiri. Jaribu kuhusisha washiriki ambao kwa kawaida sio wazungumzaji sana. Mwite mshiriki ambaye hajajibu swali kwa jina na kumuomba achangie au nenda ukasimame karibu naye ili kuwa msikivu na kumfanya ajihisi kuwa unataka azungumze.

Washukuru washiriki ambao majibu yao yalikuwa ni sahihi.

KUjIANDAA KUFANYA MAONESHO KWA VITENDO

Soma kwa makini maelekezo na kusanya vifaa vya kufundishia Kabla ya kufanya maonesho kwa vitendo, chukua muda kusoma maelekezo kwa uangalifu, ili uelewe na usisahau hatua za muhimu. Hii ni muhimu hata kama umeshawahi kumwona mtu mwingine akifanya onesho hilo. Hakikisha kwamba una vifaa vinavyohitajika.Unaweza kuhitaji mtu wa kukusaidia, omba msaada siku moja au mbili kabla ya onesho kwa vitendo ili wasaidizi

MODULE GFR4.indd 11 8/25/09 2:49:53 PM

4 Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

wapate muda wa kujiandaa. Jadiliana nao kuhusu nini unataka wafanye na wasaidie kufanya maandalizi na mazoezi kabla ya siku.

Acha muda wa kuuliza maswali. Wape nafasi ya kujibu maswali hayo kutokana na mafunzo waliyopata, na uzoefu wao. Mkufunzi amalizie kwa kufafanua vipengele ambavyo havikueleweka na kutoa muhtasari wa ‘vipengele’ muhimu.Waelekeze pia kuhusu vitendea kazi wanavyoweza kurejea.

NjIA ZA KUFUNDISHIAMafunzo haya yatatumia njia mbalimbali za ufundishaji ikiwa ni pamoja na: Mihadhara na majadiliano Kazi za vikundi Bungua bongo Maswali na majibu Mazoezi kwa vitendo

VIFAA VYA KUFUNDISHIA Bango kitita/ubao Kalamu za kuchorea/chaki Gundi za karatasi Madaftari Kalamu Picha za rejea Vyakula vya aina mbalimbali Maziwa ya aina mbalimbali Mizani, Kikokoteo (calculator), Kipima urefu (height rod)

MAMBO YA KUZINGATIA Masomo yamepangwa kwa kufuatana yakiendeleza masomo yaliyotangulia. Mahudhurio ya kila siku na

kushiriki kwenye kila somo ni muhimu sana. Ili kutoa taarifa inayofanana mara nyingi wawezeshaji watakuwa wakisoma kwenye mwongozo wao ili

udumisha usahihi wa mafunzo. Kutakuwa na tathimini ya kila siku na ya kila somo ili kutoa mrejesho kwa wawezeshaji na washiriki. Pia

kutakuwa na tathmini ya mwisho ya mafunzo yote pamoja na ya vitendea kazi.

Jaribio la AwaliWashiriki watapewa maswali kuhusu mafunzo na huduma za lishe kwa watu walioambukizwa VVU. Washiriki wataombwa kujibu maswali yote. Madhumuni ya jaribio hili la awali ni kufahamu kiwango cha uelewa wa washiriki kabla ya mafunzo. Pia jaribio hili litatumika mwisho wa mafunzo kupima kiwango cha elimu alichoongeza mshiriki wakati wa mafunzo.

REjEA KWA MKUFUNZIInashauriwa mkufunzi kusoma vitabu vifuatavyo kabla ya kuendesha mafunzo:

Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI”: COUNSENUTH Information Series No. 2, January 1. 2004.

Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI: “Majibu ya Maswali Yanayoulizwa Mara kwa 2. Mara” COUNSENUTH Information Series No. 3, January, 2004.

Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI: “Vyakula Vinavyoboresha Uyeyushwaji wa 3. Chakula na Ufyonzwaji wa Virutubisho Mwilini” COUNSENUTH information Series No. 4, March 2003.

Unyonyeshaji Bora wa Maziwa ya Mama: Vidokezo Muhimu kwa Jamii COUNSENUTH Information Series 4. No. 5, June, 2003.

Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI: “Matumizi ya Viungo vya Vyakula katika 5. Kuboresha Lishe na Afya” COUNSENUTH Information Series No. 6, March, 2004.

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi Vya UKIMWI: Kitabu cha Mafunzo na Rejea.6.

MODULE GFR4.indd 12 8/25/09 2:49:53 PM

5Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

Ulishaji Bora wa Mtoto Kuanzia Umri wa Miezi Sita: Vidokezo Muhimu. COUNSENUTH, Information Series 7. No. 8, December 2004

Lishe kwa Mtoto Mwenye Virusi vya UKIMWI: Umri wa Miaka 2 – 9 COUNSENUTH Information Series No. 8. 11, Agosti, 2006.

Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI: Kitendea Kazi kwa Mtoa Huduma Nyumbani. 9. COUNSENUTH, 2005

Unasihi wa Lishe kwa Watu Wanaotumia Dawa za Kupunguza Makali ya UKIMWI: COUNSENUTH Information 10. Series No. 10, Agosti, 2006.

Maambukizo ya Virusi vya UKIMWI na ULishaji wa Watoto Wachanga. Maswali na Majibu Mwongozo kwa 11. Wanasihi): Majibu ya Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara na Wanawake, Familia na Jamii. URC/QAP, March 2005

Jedwali la Rejea kwa BMI: COUNSENUTH, Desemba, 2003.12.

Jinsi ya Kunyonyesha Mtoto Wako URC/QAP, July 200713.

Jinsi ya Kumlisha Mtoto Baada ya Miezi 6. URC/QAOP, July 200714.

Lishe Wakati wa Ujauzito na Kunyonyesha; Vidokezo Muhimu. URC/QAP, September 200515.

Ulishaji wa Watoto Wachanga katika Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI-Mwongozo kwa Mkufunzi: Draft 516.

Mkufunzi ahakikishe kuwa kila mshiriki anapewa Kitendea Kazi kwa Mtoa Huduma Nyumbani kwa ajili ya rejea na kumsaidia kufanya kazi kwa ufanisi.

MODULE GFR4.indd 13 8/25/09 2:49:53 PM

6 Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

MADA YA 1

ELIMU YA MSINGI YA CHAKULA NA LISHEI. LENGO:Kuwawezesha washiriki kuelewa umuhimu wa vyakula mbalimbali kwa binadamu na ulaji unaofaa.

II. MALENGO MAHUSUSI: Mwisho wa mada hii washiriki waweze:

Kueleza umuhimu wa chakula kwa binadamu; Kutambua virutubishi mbalimbali, umuhimu wake na vyanzo vyake; na Kujadili makundi ya vyakula na mlo kamili.

III. MAMBO YA KUjIFUNZA Maana ya chakula, lishe, virutubishi, mlo kamili na ulaji bora; Faida za chakula kwa binadamu; Aina za virutubishi;

- Kabohaidreti - Protini - Mafuta - Vitamini - Madini

Kazi za virutubishi, umuhimu na vyanzo vyake; Makundi ya vyakula; na Mlo kamili.

IV. MUDA: Dakika 180

V. MUHTASARI WA MADA

UTANGULIZIChakula ni muhimu kwa binadamu wote. Chakula uupatia mwili virutubishi mbalimbali kwa ajili ya lishe bora. Ili kuwa na hali nzuri ya lishe ni vyema kuzingatia ulaji bora ikiwa ni pamoja na mlo kamili. Ulaji bora ni muhimu zaidi kwa watu walioambukizwa virusi vya UKIMWI kwa sababu ya ongezeko la mahitaji ya baadhi ya virutubishi mwilini, ulaji duni, uyeyushwaji na usharabu duni wa virutubishi.

Maana ya chakula, lishe, virutubishi, mlo kamili na ulaji bora

Chakula ni nini?Chakula ni kitu chochote kinacholiwa na kuupatia mwili virutubishi mbalimbali. Chakula huupatia mwili nguvu, huulinda na huukinga dhidi ya maradhi mbalimbali. Mfano wa chakula ni pamoja na ugali, wali, maharagwe, ndizi, viazi vya aina zote, mchicha, machungwa, mkate, muhogo, nyama na samaki

Lishe ni nini?Lishe ni mchakato unaohusisha hatua mbalimbali za jinsi mwili unavyokitumia chakula kilicholiwa. Hatua hizi ni tangu chakula kinapoliwa, jinsi mwili unavyokisaga na kukiyeyusha na hatimaye virutubishi kufyonzwa na kutumika mwilini.

Virutubishi ni nini?Virutubishi ni viini vilivyoko kwenye chakula ambavyo vinauwezesha mwili kufanya kazi zake. Hakuna chakula kimoja ambacho kina virutubishi vyote vinavyohitajika mwilini isipokuwa maziwa ya mama kwa miezi sita ya mwanzo ya maisha ya mtoto. Karibu vyakula vyote huwa na virutubishi zaidi ya kimoja, ila hutofautiana kwa kiasi na ubora. Kila kirutubishi kina kazi yake mwilini na mara nyingi hutegemeana ili viweze kufanya kazi kwa ufanisi. Hivyo ni muhimu kula vyakula vya aina mbalimbali ili kuuwezesha mwili kupata virutubishi mchanganyiko vinavyohitajika.

MODULE GFR4.indd 14 8/25/09 2:49:53 PM

7Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

• Mlokamiliniupi?Ni mlo ambao una virutubishi vyote muhimu kwa ajili ya lishe na afya bora. Ni mlo unaotokana na mchanganyiko wa angalau chakula kimoja kutoka kila kundi la chakula. Mlo huu unapoliwa kwa kiasi cha kutosha kulingana na mahitaji ya mwili angalau mara tatu kwa siku huupatia mwili virutubishi vyote muhimu.

• Ulajiboraninini? Ulaji bora hutokana na kula chakula mchanganyiko na cha kutosha (mlo kamili) ili kukidhi mahitaji ya mwili ikiwa ni pamoja na kutumia mafuta, chumvi na sukari kwa kiasi kidogo. Ulaji bora huchangia katika kudumisha uzito wa mwili unaotakiwa na kupunguza magonjwa yasiyoambukiza. Ulaji bora unatakiwa kuzingatia mahitaji ya mwili kutokana na jinsi, umri, hatua mbalimbali za maisha, kazi/shughuli na hali ya afya.

Faida za chakula kwa binadamu- Kutengeneza seli za mwili na kurudishia seli zilizokufa au kuharibika;- Ukuaji wa akili na mwili;- Kuupa mwili nguvu, joto na uwezo wa kufanya kazi; na- Kuupa mwili kinga dhidi ya maradhi mbalimbali.

Aina za virutubishiKuna aina kuu tano za virutubishi ambavyo ni kabohaidreti, protini, mafuta, vitamini na madini. Kila kirutubishi kina kazi yake katika mwili wa binadamu na kiasi kinachohitajika hutofautiana.

Kabohaidreti

Hiki ni kirutubishi muhimu katika kuupa mwili nishati – lishe kwa ajili ya kazi mbalimbali pamoja na kuupa joto. Kabohaidreti ndio inayochukua sehemu kubwa ya mlo. Kabohaidreti inajumuisha wanga, sukari na makapi-mlo. Makapi - mlo ni muhimu katika uyeyushwaji wa chakula. Vyakula vyenye kabohaidreti kwa wingi ni pamoja na mahindi, mchele, uwele, ngano, viazi vya aina zote, mihogo, ndizi, sukari na baadhi ya matunda.

Protini

Protini ni muhimu kwa ukuaji wa mwili na akili. Protini husaidia mwili kutengeneza seli mpya, mfumo wa kinga, kutengeneza vimeng’enyo na vichocheo mbalimbali na wakati mwingine protini huupa mwili nishati kwa ajili ya matumizi mbalimbali. Ingawaje protini pia hupatikana kwenye vyakula vingine, baadhi ya vyanzo vizuri vya protini ni pamoja na aina zote za nyama, samaki, vyakula vya jamii ya kunde kama choroko, kunde, maharagwe, soya, karanga, korosho, maziwa, mayai, dagaa na wadudu wa aina mbalimbali wanaoliwa kama kumbikumbi na senene.

Mafuta

Mafuta huhitajika mwilini kwa ajili ya kuupa mwili nguvu na joto, pamoja na kusaidia usharabu wa baadhi ya vitamini. Mafuta pia hulainisha chakula na kukifanya kiwe na ladha nzuri, na hivyo kumfanya mlaji ale chakula cha kutosha. Mafuta hupatikana kwa wingi kwenye samli, siagi, baadhi ya nyama, baadhi ya samaki, soya, mbegu zitoazo mafuta kama ufuta, korosho, mbegu za maboga, karanga, alizeti, kweme, mawese pamoja na nazi.

VitaminiVitamini zinahitajika mwilini kwa ajili ya kulinda mwili dhidi ya maradhi pamoja na kuufanya mwili ufanye kazi zake vizuri. Vitamini ziko za aina nyingi na zinapatikana kwa wingi kwenye mboga-mboga, matunda, dagaa na samaki na kwenye vyakula vinavyotokana na wanyama kama maziwa, aina zote za nyama, na mayai.

Madini

Madini kama zilivyo vitamini hulinda mwili dhidi ya maradhi na kuusaidia ufanye kazi zake vizuri. Kuna aina nyingi za madini. Baadhi ya vyakula vyenye madini kwa wingi ni pamoja na vyakula vinavyotokana na wanyama, dagaa, samaki, mboga-mboga na matunda.

MODULE GFR4.indd 15 8/25/09 2:49:54 PM

8 Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

Virutubishi, Umuhimu, Vyanzo Vyake

jedwali Na. 1, linaonyesha baadhi ya virutubishi, umuhimu wake na vyanzo vyake na dalili zinazojitokeza upungufu unapotokea.

JedwaliNa.1:Baadhiyavirutubishi,umuhimu,vyanzovyakenadalilizaupungufu

Aina Umuhimu Vyanzo Dalilizaupungufu

1. Huupa mwili nishati-lishe (nguvu) kwa ajili ya kufanya kazi mbalimbali

Mahindi, mchele, ngano, uwele, mtama, ulezi, aina zote za viazi, mihogo, magimbi, ndizi, asali, sukari

Mwili kukosa nguvu na kupungua uzito

2. Protini Ukuaji wa mwili, kutengeneza seli mpya za mwili, kukarabati zilizochakaa au kuharibika, kutengeneza vimeng’enyo, vichocheo, damu na mfumo wa kinga, huupa mwili nishati lishe pale ambapo wanga hautoshelezi

Aina zote za nyama, vyakula vya jamii ya kunde (maharage, kunde, njegere, mbaazi, choroko, dengu, njugu, n.k), samaki, dagaa, wadudu (kama senene na kumbikumbi), maziwa, jibini, mayai

Utapiamlo, ukuaji na maendeleo hafifu kwa watoto, kuharibika kwa chembechembe na tishu

3. Mafuta Huupa mwili nishati-lishe (nguvu), joto na husaidia ufyonzwaji na usafirishwaji wa baadhi ya virutubishi kama vitamini A, D, E na K,

Siagi, samli, karanga, samaki wenye mafuta, jibini, nyama yenye mafuta, mbegu zitoazo mafuta kama alizeti, ufuta, maboga, korosho, karanga, mahindi na pamba, nazi na mawese

Mwili kukosa nguvu na kuwa dhaifu, ngozi kuwa ngumu na yenye magambadalili zitokanazo na upungufu wa vitamini A, D, E na K

4. Vitamini A (Retinol)

Ukuaji wa akili na mwili, huimarisha seli za ngozi, huimarisha kinga ya mwili dhidi ya maradhi, husaidia macho kuona vizuri, hulinda utando laini katika sehemu mbalimbali za mwili

Maini, mboga za majani za kijani, figo, mayai, samaki, jibini, siagi, viazi vitamu (hasa vya manjano), maboga, karoti, mawese na matunda hasa yenye rangi ya manjano au nyekundu kama papai, embe, n.k.

Kutoona kwenye mwanga hafifu (gizani), mtoto wa jicho (cataract), kuongezeka kwa maradhi ya kuambukiza ya mara kwa mara hasa katika mfumo wa hewa, ngozi kutokuwa nyororo

5. Vitamini B1 (Thiamin)

Husaidia umetaboli wa nishati-lishe, huongeza hamu ya kula na huboresha mfumo wa fahamu, moyo na misuli

Nafaka zisikobolewa, vyakula vya jamii ya kunde, nyama, samaki, kuku, mayai, maziwa, maini, matikiti, mbegu za alizeti na maboga, karanga na korosho

Kunyongea na kusikia uchovu, hamu ya kula hupungua au kupotea,kupungua uzito, maumivu ya hapa na pale ambayo hayana sababu, moyo na mfumo wa chakula kushindwa kufanya kazi vizuri

6. Vitamini B2 (Riboflavin)

Husaidia utumikaji wa nishati na protini, husaidia macho kuona vizuri na huboresha ngozi, kucha na nywele, husaidia katika utengenezaji wa chembe chembe za kinga na za damu

Maziwa, nyama, samaki, mboga za kijani, nafaka zisizokobolewa, vyakula vya jamii ya kunde, uyoga

Kuwashwa macho, vidonda kwenye kona za midomo,kuzorota, vipele kwenye ngozi

7. Vitamini B3 (Niacin)

Husaidia utumikaji wa nishati na protini, huboresha ngozi, mfumo wa chakula na fahamu

Maziwa, mayai, nyama, kuku, samaki, karanga, uyoga, nafaka zisizokobolewa

Kuharisha, magonjwa ya ngozi, kuchanganyikiwa,kukosa usingizi, misuli kukosa nguvu na kuumwa kichwa

MODULE GFR4.indd 16 8/25/09 2:49:54 PM

9Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

Aina Umuhimu Vyanzo Dalilizaupungufu

8. Vitamin B5 (Biotin)

Huimarisha mfumo wa kinga, husaidia katika matumizi ya vitamini nyingine, husaidia katika matumizi ya nishati-lishe na protini, husadia katika kutengeneza seli za mfumo wa kati wa fahamu

Nyama na mazao yake, mayai, nafaka zisizokobolewa, maziwa na mazao yake, viazi, kabichi, vyakula vya jamii ya kunde, mbogamboga na matunda,

Maumivu miguuni kama ya kuungua, ukuaji duni,kizunguzungu, kutapika

9. Vitamini B6 (Pyridoxine)

Husaidia ufyonzwaji na utumikaji wa mafuta, kabohaidreti na protini, kusaidia kutengeneza seli za kinga, husaidia kuweka sawa kiwango cha madini ya sodiyamu na fosforasi mwilini, husaidia kupunguza kushituka kwa misuli, kichefuchefu, huimarisha mfumo wa kati wa fahamu, husaidia kutengeneza seli nyekundu za damu

Viazi aina zote, maharagwe, nafaka zisizokobolewa, parachichi, kabichi, nyama, samaki, matikiti, mboga za majani, ndizi mbivu.

Kukosa usingizi, ngozi kuchanika, misuli kunyongea, magonjwa ya ngozi, mwili kuhifadhi maji mengi

10. Vitamini B9(Foleti)

Husaidia katika utengenezaji wa seli mpya, na ukuaji, pia husaidia seli nyekundu za damu kukua vizuri, husaidia matumizi ya protini , husaidia mfumo wa chakula

Jamii ya kunde, mboga za majani, machungwa maini, samaki, parachichi, mbegu zitoazo mafuta

Matatizo katika mfumo wa chakula, upungufu wa damuUkosefu wa vitamini B12, nywele kuwa na mvi kabla ya wakati wake, kuharibika kwa uti wa mgongo na msononeko

11. Vitamini B12 (Cyanoco- balamin)

Husaidia kutengeneza seli mpya na kukarabati seli za neva na seli nyekundu za damu, husaidia matumizi ya kabohaidreti, protini na mafuta mwilini, husaidia ukuaji kwa watoto, huongeza nguvu mwilini. Ni muhimu kwa ufyonzwaji wa madini ya chokaa

Nyama nyekundu, samaki, kuku, jibini, mayai, maziwa, vyakula vilivyochachushwa kama mtindi. (hupatikana kwenye vyakula vya asili ya wanyama tu)

Upungufu wa wekundu wa damu, kukosa hamu ya kula, kuzorota kwa ukuaji kwa watoto, uchovu, kuharibika kwa ubongo, kuharibika kwa uti wa mgongo msononeko

12. Vitamini C (Ascorbic acid)

Husaidia umetaboli wa protini, husaidia matumizi ya madini ya chokaa, husaidia ufyonzwaji wa madini ya chuma, huboresha kinga ya mwili na huondoa chembe haribifu mwilini. Hufanya mishipa ya damu kuwa imara, huzuia uvujaji wa damu ovyo, hutumiwa katika utengenzaji wa kuta muhimu za mishipa na tishu (collagen), husaidia kuzuia saratani

Mapera, machungwa, nyanya, ukwaju, malimau, ndimu, machenza, madalansi, ubuyu, pesheni, mabungo, na aina nyingine za matunda ya porini, mboga za majani

Kutokwa na damu katika fizi,kuvimba kwa viungio, vidonda kuchukua muda mrefu kupona, kuoza meno,kuvuja damu kwenye ngozi,mishipa ya damu kupasuka kwa urahisi, upungufu wa wekundu wa damu

13. Vitamini D (Calciferal)

Husaidia ufyonzwaji wa madini ya chokaa na fosforasi, hutumika katika kutengeneza mifupa na meno, huimarisha mfumo wa fahamu na huwezesha moyo kufanya kazi vizuri

Kiini cha yai, samaki wenye mafuta, maziwa, siagi na mionzi ya jua

Matege kwa watoto, mifupa kulainika na kushindwa kupona kwa urahisi kama imevunjika au kupata mpasuko, kuoza meno na misuli kukosa nguvu

MODULE GFR4.indd 17 8/25/09 2:49:54 PM

10 Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

Aina Umuhimu Vyanzo Dalilizaupungufu

14. Vitamini E Huondoa chembe haribifu mwilini, husaidia umetaboli wa seli nyeupe na nyekundu za damu, huimarisha kinga ya mwili, hupunguza kasi ya seli kuzeeka kiurahisi, hukinga seli nyekundu za damu kuharibiwa na chembe haribifu mwilini

Mboga za majani zenye rangi ya kijani, mbegu zitoazo mafuta, maini, mayai, siagi, nafaka zisizokobolewa, karanga na korosho

Upungufu hutokea kwa nadra pale ambapo kuna tatizo la ufyonzwaji wa mafuta mwilini. Misuli ya moyo na neva kuharibika

Vitamini K Husaidia kutengeza protini ambayo hufanya damu igande kwa urahisi, baada ya kuumia, hushiriki katika kutengeneza protini ya mifupa

Mboga za majani zenye rangi ya kijani, mbegu zitoazo mafuta, yai, siagi, nafaka zisokobolewa, maziwa ya ng’ombe na kabichi

Upungufu hutokea kwa nadra., ngozi kukauka, misuli ya moyo na mingine kuharibika. Utengenezaji hafifu wa mifupa

Madini chuma

Hutengeneza seli nyekundu za damu, husafirisha hewa ya oksijeni kwenye damu, husaidia utumikaji wa nishati-lishe, hudhibiti chembe haribifu mwilini

Maini, mboga za majani zenye rangi ya kijani, figo, bandama, nyama nyekundu, samaki, dagaa, mayai, kuku, vyakula jamii ya kunde, baadhi ya matunda yaliyokaushwa, rozela/choya na baadhi ya nafaka

Upungufu wa wekundu wa damu, ngozi na sehemu nyeupe ya macho kuwa nyeupe kuliko kawaidaMwili kukosa nguvu, kupumua kwa shida, moyo kwenda mbio

Madini ya Chokaa

Hujenga na kuimarisha mifupa na meno, husaidia damu kuganda baada ya kuumia, husaidia misuli na moyo kufanya kazi vizuri, huboresha kinga ya mwili, huboresha mfumo wa fahamu, husaidia figo kufanya kazi vizuri

Maziwa na bidhaa zake, mboga za majani zenye rangi ya kijani, samaki wakavu, maharagwe, ulezi, mtama, dagaa, bamia, mbegu zitoazo mafuta, karanga na korosho

Mifupa na meno kuwa laini na kuvunjika kwa urahisi, matege kwa watoto, ukuaji hafifu kwa watoto

Zinki Huboresha kinga ya mwili, husaidia uyeyushwaji wa chakula na usafirishwaji wa Vitamini A mwilini, huzuia chembe haribifu, husaidia kutengeneza protini mwilini na kupona kwa vidonda, husaidia katika ukuaji na maendeleo ya mfumo wa uzazi

Nyama, kuku, samaki, jibini, maziwa, nafaka zisizokobolewa, vyakula vya jamii ya kunde na mboga-mboga, uyoga, vitunguu maji, mayai, maini, mbegu za maboga, pilipili manga, karanga, korosho

Kuchelewa kwa wavulana kubalehe na wasichana kupata hedhi, vidonda kuchelewa kupona, mapele kwenye ngozi, kuharisha, ukuaji hafifu wa watoto, ugumba, kutokuwa makini, vidonda vya ngozi, kupungua hamu ya kula

Seleniamu Huzuia kudhoofu kwa misuli ya moyo, huondoa chembe haribifu

Nyama aina zote, mayai, vyakula vya baharini, jamii ya kunde, vitunguu, vyakula vya nafaka, karanga na korosho

Magonjwa ya moyo, kuzeeka mapema, ngozi kulegea, uwezo wa kuona kupungua, misuli kulegea, mtoto wa jicho

Madini joto Muhimu kwa ukuaji, husaidia ubongo na mfumo wa fahamu kufanya kazi vizuri, hutengeneza kichocheo katika tezi la shingo ambacho ni muhimu kwa ufanisi wa shughuli mwilini

Vyakula vya baharini, chumvi iliyowekwa madini joto, vyakula vyote vilivyozalishwa kwenye udongo wenye madini joto

Kuvimba tezi la shingo, uwezo mdogo wa ubongo kufanya kazi na pia wa darasani, kuzorota na mwili kukosa msukumo wa kufanya shughuli yeyote

Magnesia Huimarisha misuli hasa ya moyo, muhimu katika mfumo wa fahamu, ukuaji na huimarisha mifupa na meno, matumizi ya madini ya chokaa na Vitamini C

Nafaka, mboga za majani zenye rangi ya kijani, vyakula vya baharini, jamii ya kunde, karanga, nafaka zisisokobolewa

Misuli kupata msituko (spasms), kukanganyikiwa, mawe kwenye figo, kukosa choo, misuli kukaza (cramps)

Chanzo: Imeboreshwa na kutafsiriwa kutoka Network of African People Living with HIV/AIDS (1997

15.

16.

17.

18.

19.

20.

21.

MODULE GFR4.indd 18 8/25/09 2:49:55 PM

11Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

Makundi ya vyakulaPamoja na kuzungumzia virutubishi mbalimbali, umuhimu na vyanzo vyake; ni muhimu kuzungumzia makundi ya vyakula. Hii husaidia kupanga mlo kamili kwa urahisi na kuwezesha vyakula vyote muhimu kuwepo. Ili kuweza kupata virutubishi vyote muhimu vinavyohitajika na mwili ni vizuri kula vyakula kutoka katika makundi mbalimbali. Hii ni kwa sababu hakuna chakula cha aina moja ambacho kinaweza kuupatia mwili virutubishi vyote vinavyohitajika. Hivyo ni muhimu, kutumia makundi ya vyakula badala ya aina za virutubishi katika kujifunza ulaji bora. Makundi hayo ni:

Vyakula vya nafaka, mizizi na ndizi:Vyakula hivi ndivyo vinavyochukua sehemu kubwa ya mlo na kwa kawaida ndiyo vyakula vikuu. Vyakula katika kundi hili ni pamoja na mahindi, mchele, mtama, ulezi, ngano, uwele, viazi vikuu, viazi vitamu, mihogo, magimbi, viazi mviringo na ndizi.

Vyakula vya jamii ya kunde na vyenye asili ya wanyama:

Vyakula vilivyoko katika kundi hili ni pamoja na maharagwe, njegere, kunde, karanga, soya, njugu mawe, dengu, choroko na fiwi. Vile vyenye asili ya wanyama ni pamoja na nyama, samaki, dagaa, maziwa, mayai, jibini, maini, figo, senene, nzige, kumbikumbi na wadudu wengine wanaoliwa.

Mboga-mboga:Kundi hili linajumuisha aina zote za mboga-mboga zinazolimwa na zinazoota zenyewe. Mboga-mboga ni pamoja na mchicha, majani ya maboga, kisamvu, majani ya kunde, matembele, spinachi, mnafu, mchunga, pia aina nyingine za mboga-mboga kama karoti, pilipili hoho, biringanya, matango, maboga, nyanya chungu (ngogwe), bamia, bitiruti, kabichi na figiri.

Matunda:Kundi hili linajumuisha matunda ya aina zote kama mapapai, maembe, mapera, mapesheni, mananasi, mapeasi, machungwa, machenza, zambarau, maparachichi, ndizi mbivu, mafenesi, mastafeli, mabungo, madalansi, mapichesi na matopetope. Aidha ikumbukwe kuwa matunda pori au yale ya asili yana ubora sawa na matunda mengine. Matunda hayo ni kama ubuyu, ukwaju, embe ng’ong’o, mavilu na mikoche.

Mafuta na sukari:Mafuta na sukari ni muhimu ingawa vinahitajika kwa kiasi kidogo mwilini. Mafuta yanaweza kupatikana kutoka kwenye mimea kama mbegu za alizeti, ufuta, korosho, karanga, mawese na mbegu za pamba. Pia kutoka kwa wanyama kama siagi, samli na nyama yenye mafuta. Sukari hupatikana kwenye sukari ya mezani, miwa na asali.

MajiMaji kwa kawaida hayahesabiwi kama kundi la chakula, lakini yana umuhimu mkubwa katika afya na lishe ya binadamu. Inapaswa kunywa maji ya kutosha safi na salama, angalau lita moja na nusu au glasi nane kwa siku. Inashauriwa kunywa maji zaidi wakati wa joto kali ili kuzuia upungufu wa maji mwilini. Vile vile unaweza kuongeza maji mwilini kwa kunywa vinywaji kama supu, madafu na juisi halisi za matunda mbalimbali.

MODULE GFR4.indd 19 8/25/09 2:49:59 PM

12 Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

Mlo kamili na umuhimu wakeIli mtu awe na afya na lishe bora anapaswa kula mlo kamili na kuzingatia ulaji bora. Mlo mkamili unapoliwa kwa kiasi cha kutosha kulingana na mahitaji ya mwili huupatia mwili virutubishi vyote muhimu.

Kupangamlokamili Mlo kamili hupangwa kwa kuchanganya angalau chakula kimoja kutoka katika kila kundi la vyakula kama

inavyooneshwa katika picha inayofuata. Ni muhimu kula milo kamili angalau mitatu kila siku.

Umuhimu wa kula vyakula mchanganyiko Ni muhimu kula vyakula mchanganyiko kwa sababu baadhi ya virutubishi hutegemeana ili kuweza kufanikisha

kazi zake mwilini. Mfano wa virutubishi vinavyotegemeana ni: - Madini chuma yanayopatikana kwenye vyakula vya mimea kama mboga-mboga za kijani, hufyonzwa kwa

ufanisi mwilini iwapo katika mlo huo kuna Vitamini C ambayo hupatikana kwa wingi kwenye matunda, mfano chungwa, pera, nanasi, pesheni, ubuyu.

- Utumikaji wa vitamini A, D, E na K mwilini hutegemea kuwepo kwa mafuta. Hivyo basi ni muhimu kutumia mafuta kidogo wakati wa kupika hususan mbogamboga.

HITIMISHO:Ulaji bora ni muhimu kwa watu wote hususan wale walioambukizwa virusi vya UKIMWI. Kula aina mbalimbali za vyakula husaidia mwili kupata virutubishi vyote vinavyohitajika na mwili. Ujumbemuhimunikulamlokamili. Pale inapowezekana kila mlo uwe na chakula kutoka kila kundi. Tumia vyakula vinavyopatikana katika mazingira unayoishi na vile ambavyo vipo kwenye msimu, kwani huwa na bei nafuu na freshi.

VI. NjIA ZA KUFUNDISHIA: Mhadhara, majadiliano, maswali na majibu

VII. VIFAA VYA KUFUNDISHIA: Bango kitita/ubao, kalamu za kuchorea/chaki, gundi za karatasi, vitini, madaftari, kalamu, picha za vyakula mbalimbali na vyakula halisi.

VIII. KAZI KWA WASHIRIKI: Kuorodhesha aina za vyakula vinavyopatikana kwa urahisi katika maeneo yao na kuviweka katika makundi ya a. vyakula. Kuorodhesha vyakula vya asili pamoja na vile vilivyosahaulika vinavyopatikana katika maeneo yao. b. Kubuni mlo kamili wa siku nzima kwa familia ya kawaida katika sehemu wanazotoka. Zingatia upatikanaji wa c. vyakula pamoja na vyakula vya asili.

Vyakula vya nafaka, mizizi

na ndizi

Mboga-mboga

Mafuta na sukariMatunda

Kielelezo Na.1: Makundi ya Vyakula na Mlo Kamili

Vyakula vya mikunde na vyenye asili ya wanyama

MODULE GFR4.indd 20 8/25/09 2:50:03 PM

13Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

I. LENGO: Kuwawezesha washiriki kuelewa mambo muhimu kuhusu maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.

II. MALENGO MAHUSUSI: Baada ya mada hii washiriki waweze: Kueleza maana ya maneno UKIMWI na VVU; Kueleza njia kuu za maambukizi ya VVU; Kujadili mambo yanayochangia kasi ya maambukizi ya VVU; Kueleza athari za VVU; na Kueleza njia za kuzuia maambukizi ya VVU.

III. MAMBO YA KUjIFUNZA Maana ya maneno UKIMWI na Virusi vya UKIMWI; Jinsi VVU vinavyoambukiza; Njia za maambukizi ya VVU; Sababu zinazoongeza uwezekano wa maambukizi ya VVU; na Njia za kuzuia maambukizi ya VVU.

IV. MUDA: Dakika 60

V. MUHTASARI WA MADA

UTANGULIZIMaambukizi ya VVU yamekuwa ni tatizo kubwa katika nchi nyingi na hasa zinazondelea, Tanzania ikiwa mojawapo. Takwimu zinaonesha kuwa bado kuna idadi kubwa ya watu walioambukizwa VVU nchini.

Virusi vya UKIMWI vinapoingia mwilini vinaishi ndani ya chembe hai zinazokinga mwili dhidi ya maradhi na kuziharibu taratibu. Zinapoharibika, mwili unapoteza uwezo wake wa kupambana na magonjwa na hivyo mtu hudhoofu na kupata magonjwa nyemelezi na kufikia hatua ya UKIMWI na hatimaye kupoteza maisha.

Maana ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI Virusi vya UKIMWI - Ni vimelea vidogo vidogo ambavyo vinaharibu chembechembe zinazokinga mwili dhidi ya maradhi na hivyo kuvyodhoofisha na kufanya mwili kupoteza uwezo wa kupambana na maradhi.

UKIMWI - Ni kifupisho cha maneno Upungufu wa Kinga Mwilini. UKIMWI ni mkusanyiko wa maradhi yanayotokana na kudhoofika kwa uwezo wa mwili kujikinga na maradhi kunakosababishwa na VVU.

Mtu anapoambukizwa VVU haanzi kuugua mara moja, huweza kuishi na VVU kwa muda mrefu bila kuonyesha dalili zozote. Mtu mwenye UKIMWI ni yule ambaye amekwishaanza kuonyesha dalili za magonjwa nyemelezi yanayotokana na kinga yake ya mwili kuharibiwa na VVU. Magonjwa hayo ni kama kuharisha, kukohoa, kuvimba matezi, kifua kikuu, mkanda wa jeshi, harara kwenye ngozi, utando mweupe kinywani n.k. Ni muhimu kukumbuka kwamba siyo kila mtu anayeugua magonjwa hayo ana VVU. Kwa hiyo njia kuu ya kuthibitisha uambukizo ni kupima.

jinsi Virusi vya UKIMWI vinavyoambukizwa

Virusi vya UKIMWI huhitaji aina fulani ya majimaji ili kuweza kuishi. Majimaji yanayoweza kueneza VVU ni kama damu, uteute wa ukeni, maziwa ya mama, shahawa, majimaji mengine ya mwili kama ya vidonda, usaha n.k. Majimaji haya huhitaji mlango wa kupitia ili uambukizo utokee. Mlango unaweza kuwa:

MADA YA 2

UKWELI KUHUSU VIrUSI VYA UKIMWI NA UKIMWI

MODULE GFR4.indd 21 8/25/09 2:50:03 PM

14 Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

- Sehemu iliyokatwa au kuchubuka kama kidonda- Tishu laini inayoitwa utando telezi (mucus membrane) iliyoko kwenye uke, kichwa cha uume, sehemu ya haja

kubwa, macho au pua.

Njia za maambukizi ya VVUZipo njia kuu nne zinazoweza kufanya mtu aambukizwe VVU, nazo ni:- Kufanya ngono na mtu aliyeambukizwa VVU bila kutumia kinga. Ngono hiyo inaweza kuwa ya ukeni, sehemu

ya haja kubwa au mdomoni.- Mama kumwambukiza mtoto wakati wa mimba, uchungu na kujifungua au kunyonyesha.- Kupewa damu au vitu vitokanavyo na damu yenye VVU au majimaji mengine ya mwili.- Kuchangia sindano, mabomba ya sindano, nyembe na vifaa vyenye ncha kali ambavyo vimetumika kwa mtu

aliyeambukizwa VVU.

Njia zifuatazo haziambukizi VVU Kushikana mikono na mtu aliyeambukizwa VVU. Kubadilishana nguo na mtu aliyeambukizwa VVU ili mradi hazina majimaji au damu kutoka kwa mtu

aliyeambukizwa VVU. Kuishi pamoja na mtu aliyeambukizwa VVU. Kula pamoja na mtu aliyeambukizwa VVU. Kuchangia vifaa vya kulia na mtu aliyeambukizwa a VVU. Kugusana, kukumbatiana na kupeana busu kavu na mtu aliyeambukizwa VVU. Kushirikiana bafu, choo au bwawa la kuogelea na mtu aliyeambukizwa VVU. Kuumwa na mbu, viroboto, kunguni na wadudu wengine. Kukohoa au kupiga chafya kunakofanywa na mtu aliyeambukizwa VVU.

Sababu zinazoongeza uwezekano wa maambukizi ya VVUKuna sababu nyingi ambazo zinachangia maambukizi; nazo ni: Sababu za kimaumbile: Wanawake wako katika hatari zaidi ya kuambukizwa VVU mara 2 – 4. Kupata magonjwa ya zinaa: Kupata magonjwa haya mara nyingi na kwa mfululizo kunaongeza hatari ya

kupata maambukizi ya VVU mara 5 – 10.

Ikumbukwe kuwa tohara kwa wanaume hupunguza uwezekano wa kuambukizwa VVU kwa asilimia 60, lakini kwa wanawake huleta athari za kiafya.

Sababu za kijamii- Ngono isiyo salama/ngono zembe;- Kuwa na wapenzi/wenza wengi;- Watu kutokupenda kutumia kondomu;- Unyanyapaa kuhusu matumizi ya kondomu;- Kutaka kuwa na watoto wengi hata nje ya ndoa;- Mila na desturí:

- Kurithi wajane na kutakasa wajane;- Sherehe za kiutamaduni;- Ukeketaji wa wanawake;- Kutakasa kimila; na- Kutokuwepo mawasiliano kati ya wazazi na watoto kuhusu masuala ya ngono.

- Kusafiri kutokana na ajira: kama wachimba madini, wafanyabiashara, jeshi/polisi, madereva wa magari makubwa ya mizigo yaendayo safari za mbali: na- Unywaji wa pombe kwa wingi ambao huweza kuathiri maamuzi ya mtu.

Sababu nyingine ambazo huongeza uwezekano wa maambukizi ya VVU- Umaskini au utajiri Baadhi ya tafiti zimeonyesha kuwa: - Nchi tajiri zaidi Afrika zina viwango vikubwa zaidi vya maambukizi ya VVU.

MODULE GFR4.indd 22 8/25/09 2:50:03 PM

15Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

- Watu ambao ni tajiri zaidi Tanzania huambukizwa VVU (matajiri 10.5%; maskini 3.4%).- Katika ngazi ya jamii wananchi maskini ambao hawana nafasi nzuri ya kupata mahitaji yao ya msingi hujihusisha na mahusiano ya ngono ili kupata mahitaji yao ya kila kila siku.

Athari za VVU/UKIMWI Watu wengi huugua na kuhitaji matunzo ya hali na mali. Kuongezeka kwa gharama za huduma ya afya. Kupoteza wataalamu kwa sababu ya vifo kutokana na UKIMWI. Kushuka kwa uchumi kwa sababu ya watu wengi ambao ndio nguvu kazi wanakufa kutokana na UKIMWI. Ongezeko la watoto yatima, wa mtaani na wajane. Vifo huongezeka na jamii hupoteza muda mwingi kwenye maombolezo.

VI. NjIA ZA KUFUNDISHIA: Mhadhara na majadiliano, bungua bongo, maswali na majibu

VII. VIFAA VYA KUFUNDISHIA: Bango kitita/ubao, kalamu za kuchorea/chaki, vitini, madaftari, gundi za karatasi, kalamu, sampuli za vyakula vya madukani.

VIII. KAZI YA KIKUNDI KWA WASHIRIKI: Eleza njia ambazo huongeza uwezekano wa maambukizi ya VVU katika eneo lako la kazi/makazi. Nini kifanyike ili kupiga vita hali hii? Ni ujumbe gani mahususi HUWEZA kutumika ili kufikia jamii kuhusu kujikinga na maambukizi ya VVU na

hatimaye UKIMWI?

MODULE GFR4.indd 23 8/25/09 2:50:04 PM

16 Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

I. LENGO: Kuwawezesha washiriki kuelewa uhusiano kati ya VVU na lishe.

II. MALENGO MAHUSUSI: Mwisho wa mada hii washiriki waweze kueleza:

Uhusiano wa lishe na virusi vya UKIMWI; Athari za VVU kwenye lishe; na Umuhimu wa ulaji bora kwa mtu aliyeambukizwa VVU.

III. MAMBO YA KUjIFUNZA Uhusiano wa lishe na virusi vya UKIMWI. Athari za virusi vya UKIMWI kwenye lishe

- Ulaji duni;- Uyeyushwaji duni;- Usharabu duni; na

- Mabadiliko katika ujenzi na uvunjaji wa kemikali mwilini (umetaboli). Umuhimu wa ulaji bora kwa mtu aliyeambukizwa virusi vya UKIMWI.

IV. MUDA: Dakika 60

V. MUHTASARI WA MADA

UTANGULIZILishe na virusi vya UKIMWI vina uhusiano mkubwa. Kuna athari mbalimbali ambazo virusi vya UKIMWI husababisha kwenye hali ya lishe. Kwa upande mwingine lishe bora hupunguza makali ya matatizo ya kiafya yanayoambatana na kuambukizwa virusi vya UKIMWI hivyo huboresha afya.

MADA YA 3

UHUSIANO WA LISHE NA VIrUSI VYA UKIMWI

Uhusiano wa lishe na virusi vya UKIMWIKuna uhusiano mkubwa kati ya lishe na virusi vya UKIMWI. Ni dhahiri kwamba virusi vya UKIMWI husababisha kupungua kwa kinga ya mwili. Virusi vya UKIMWI pia husababisha ongezeko la mahitaji ya baadhi ya virutubishi mwilini. Ongezeko hilo linaposhindwa kukidhiwa huweza kusababisha utapiamlo. Utapiamlo husababisha kupungua kwa kinga ya mwili na wakati huo huo virusi vya UKIMWI navyo hupunguza kinga ya mwili. Hali hii husababisha kuongezeka kwa hatari ya kupata maambukizo mbalimbali. Haya yote husababisha kuongezeka kwa mahitaji ya virutubishi mwilini na hivyo kufupisha kipindi cha tangu mtu kuambukizwa virusi vya UKIMWI mpaka kufikia hatua ya UKIMWI. Kielelezo Na. 2: Uhusiano kati ya Lishe na Virusi vya UKIMWI

MODULE GFR4.indd 24 8/25/09 2:50:04 PM

17Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

Athari za virusi vya UKIMWI kwenye lisheKuna athari mbalimbali za virusi vya UKIMWI kwenye lishe. Athari hizi huweza kuleta utapiamlo. Athari hizo ni:

- Ulaji duni:Kukosa hamu ya kula, kichefuchefu, utando mweupe kinywani, vidonda kinywani na kooni, mawazo na sononeko humfanya mtu ashindwe kula chakula cha kutosha hata kama chakula kinapatikana.

- Uyeyushwaji na usharabu duni wa virutubishiKutapika na kuharisha huufanya mwili upoteze virutubishi kwani chakula anachokula hakikai tumboni kwa muda wa kutosha kuweza kuyeyushwa na kusharabiwa, hivyo mtu anakuwa kwenye hatari ya kupata utapiamlo. Pamoja na kuharisha na kutapika, mabadiliko au uharibifu wa seli za tumbo pia husababisha uyeyushwaji wa chakula na usharabu wa virutubishi kuwa duni.

- Mabadiliko katika ujenzi na uvunjwaji wa kemikali mwilini (umetaboli)Hali ya kuwa na virusi vya UKIMWI huweza kusababisha mabadiliko katika umetaboli. Pamoja na uyeyushwaji wa chakula tumboni na usharabu wa virutubishi mwilini kuwa duni, mwili pia hushindwa kutumia kikamilifu baadhi ya virutubishi hasa mafuta, protini na kabohaidreti.

Umuhimu wa ulaji bora kwa mtu aliyeambukizwa VVUNi muhimu sana kwa mtu aliyeambukizwa virusi vya UKIMWI kuzingatia ulaji ulio bora kwa ajili ya: Kuboresha kinga dhidi ya magonjwa nyemelezi; Kutengeneza seli mpya na kurudishia seli zilizochakaa; Kurudisha vitamini, madini na virutubishi vingine vinavyopotea kutokana na maradhi kama kuharisha na

kutapika; Kusaidia dawa zinazotumika kufanya kazi vizuri mwilini; Kumpa mtu nguvu ya kufanya shughuli mbalimbali; na Kuboresha afya, hivyo kuweza kurefusha muda wa kuishi tangu kupata uambukizo wa virusi vya UKIMWI

hadi kufikia hatua ya UKIMWI.

Ni muhimu kuhakikisha kwamba mtu aliyeambukizwa virusi vya UKIMWI anakula mlo kamili. Mlo huo utayarishwe katika hali ambayo unakuwa ni rahisi kula na kutumika mwilini kutegemea hali ya mtu wakati huo. Kutokana na ongezeko la mahitaji ya nishati mwilini, ni muhimu kuongeza idadi ya milo na ikiwezekana kula milo midogo midogo mara kwa mara hasa wakati ambapo mtu hawezi kula chakula cha kutosha kwa mara moja

HITIMISHOKuna uhusiano wa karibu kati ya VVU na lishe.

Mtu aliyeambukizwa virusi vya UKIMWI yuko

katika hatari ya kupata utapiamlo kutokana

na athari zinazosababishwa na VVU. Hivyo ni Chanzo : Imetafsiriwa kutoka Piwoz na Prebel 2003

KielelezoNa.3:UmuhimuwaUlajiBorakwaWatuWalioambukizwaVVU

muhimu sana kuzingatia ulaji wa mlo kamili

VI. NjIA ZA KUFUNDISHIA: Mhadhara na majadiliano, bungua bongo, maswali na majibu

VII. VIFAA VYA KUFUNDISHIA: Bango kitita/ubao, kalamu za kuchorea/chaki, vitini, madaftari, gundi za karatasi, kalamu, sampuli za vyakula vya madukani.

.

MODULE GFR4.indd 25 8/25/09 2:50:05 PM

18 Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

I. LENGO: Kuwawezesha washiriki kuelewa mbinu mbalimbali za kuboresha chakula hususan cha mtu aliyeambukizwa

virusi vya UKIMWI

II. MALENGO MAHUSUSI: Mwisho wa mada hii washiriki waweze kueleza:

Umuhimu wa kuboresha chakula; na

Mbinu za kuboresha chakula.

III. MAMBO YA KUjIFUNZAMbinu za kuboresha chakula Kuponda au kusaga chakula, Kuongeza vyakula vyenye virutubishi vingi, Kuchachusha chakula, Kuotesha chakula, Kuongeza viungo vya vyakula, na Kupika kwa mvuke.

IV. MUDA: Dakika 30

V. MUHTASARI WA MADA

UTANGULIZIZipo njia mbalimbali zinazoweza kutumika katika jamii kuboresha chakula bila kuhitaji gharama kubwa. Mbinu hizo zimetumika tangu zamani katika sehemu nyingi nchini. Ni vyema kuziboresha pale inapohitajika na kuziendeleza.

Mbinu za kuboresha chakula Baadhi ya mbinu zinazoweza kutumika ili kukifanya chakula kiwe bora zaidi, rahisi kula na kutumika mwilini ni pamoja na: Kuponda au kusaga chakula: Kuponda au kusaga chakula hufanya chakula kuwa rahisi kula na pia husaidia uyeyushwaji wake tumboni.

Kuongeza vyakula vyenye virutubishi vingi:Kuongeza vyakula vyenye virutubishi vingi kwenye vyakula hasa vya nafaka, mizizi na ndizi, huongeza ubora wa vyakula hivyo. Vyakula vinavyoweza kuongezwa ni pamoja na karanga, maziwa, mbegu mbalimbali zitoazo mafuta zilizopondwa, mafuta au tui la nazi.

Kuchachusha vyakula (fermented foods): Watu walioambukizwa virusi vya UKIMWI mara kwa mara huwa na matatizo ya uyeyushwaji wa chakula na usharabu wa virutubishi. Vyakula vilivyochachushwa huyeyushwa kwa urahisi na hatimaye virutubishi husharabiwa kwa wingi. Vilevile vimeonekana kusaidia uyeyushwaji wa vyakula vingine na usharabu wa virutubishi. Baadhi ya vyakula hivyo ni kama maziwa ya mgando (mtindi), togwa na vinywaji vingine vilivyochachushwa ambavyo havina kilevi kama maji ya uchachu ya nafaka na kabichi.

MADA YA 4

MBINU ZA KUBOrESHA CHAKULA

MODULE GFR4.indd 26 8/25/09 2:50:05 PM

19Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

Kuotesha mbegu mbalimbali/kimea (germinated/sprouted): Kama ilivyo kwa vyakula vilivyochachushwa, vyakula vilivyooteshwa huyeyushwa kwa urahisi na husaidia uyeyushwaji wa vyakula vingine. Mbegu mbalimbali za nafaka na jamii ya kunde huweza kuoteshwa na kutumika kama vyakula. Mbegu hizo ni kama; mahindi, mtama, ulezi, uwele, choroko, kunde na maharagwe. Mbegu zilizooteshwa sio lazima zikaushwe na kutengenezwa unga. Kwa mfano, mbegu za maharagwe, njegere, choroko na kunde zinaweza kupikwa mara tu baada ya kuota na kutumiwa kama mboga.

Kuchachusha vyakula na kuotesha mbegu mbalimbali kunaongeza kiasi cha protini, vitamini na madini kwenye vyakula hivyo na vile vile vyakula hivyo huwa na vimeng’enyo (enzymes) ambavyo husaidia uyeyushwaji wa vyakula mbalimbali.

Kutumia viungo vya vyakula:Matumizi ya baadhi viungo kama mdalasini, kitunguu saumu, iliki na tangawizi yameonekana kusaidia katika kuboresha ladha ya chakula na hivyo kuongeza hamu ya kula, kusaidia uyeyushwaji wa chakula na usharabu wa virutubishi mwilini.

Kuboresha njia za upishi (kupika kwa mvuke):Kupika chakula kwa mvuke ni njia mojawapo ya kuboresha chakula. Njia hii hufanya chakula kuwa rahisi kuyeyushwa na kusharabiwa mwilini. Vilevile, kupika kwa mvuke husaidia kuhifadhi virutubishi vilivyoko kwenye chakula. Hii ni njia nzuri ya kupika mboga-mboga za aina mbalimbali kama mboga za majani, karoti na vyakula vingine.

HITIMISHONi muhimu kutumia mbinu mbalimbali zinazowezekana katika mazingira yetu. Ikumbukwe kwamba mbinu nyingi zinaweza kutumika bila kuongeza gharama au kutumia vyombo maalum.

VI. NjIA ZA KUFUNDISHIA: Mhadhara na majadiliano, bungua bongo, majadiliano ya vikundi, maswali na majibu

VII. VIFAA VYA KUFUNDISHIA: Bango kitita/ubao, vitini, kalamu za kuchorea/chaki, madaftari, kalamu, gundi za karatasi, jedwali la uoteshaji wa mbegu mbalimbali.

VIII. KAZI KWA WASHIRIKI: Kujibu swali lifuatalo:

Katika eneo lako la kazi utamshauri mgonjwa aliyeambukizwa virusi vya UKIMWI atumie mbinu gani za kuboresha chakula?

Toa mfano wa vyakula unavyoweza kuviboresha kwa kutumia mbinu ulizotaja.

MODULE GFR4.indd 27 8/25/09 2:50:05 PM

20 Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

I. LENGO:

Kuwawezesha washiriki kutambua umuhimu wa usafi na usalama wa chakula na maji hususan kwa mtu aliyeambukizwa virusi vya UKIMWI.

II. MALENGO MAHUSUSI: Mwisho wa mada hii washiriki waweze kueleza:

Usafi wa mtu binafsi kwenye utayarishaji wa chakula; Usafi wa vyombo; Usafi na usalama wa vyakula; Usafi wa sehemu ya kutayarishia chakula; na Usafi na usalama wa maji ya kunywa.

III. MAMBO YA KUjIFUNZA: Usafi wa mtayarishaji wa chakula; Usafi wa vyombo; Usafi wa sehemu ya kutayarishia chakula; Usafi na usalama wa chakula; na Usafi na usalama wa maji ya kunywa.

IV. MUDA: Dakika 60

V. MUHTASARI WA MADA

UTANGULIZIWatu walioambukizwa virusi vya UKIMWI wapo katika hatari ya kupata maambukizi ya maradhi mbalimbali kwa urahisi kutokana na kupungua kwa kinga ya mwili. Chakula na maji vinaweza kuwa ni miongoni mwa vyanzo vya maambukizi mbalimbali ikiwa usafi na usalama wake hautazingatiwa. Ili chakula na maji viwe safi na salama ni muhimu kuzingatia usafi wa mtayarishaji wa chakula, usafi wa vyombo, usafi wa sehemu ya kutayarishia chakula, usafi na usalama wa chakula chenyewe na maji ya kunywa.

Usafi wa mtayarishaji wa chakulaMtayarishaji wa chakula ni muhimu:- Kuosha mikono kwa sabuni na maji yanayotiririka na ya kutosha kabla na baada ya kutayarisha chakula.

Majivu yanaweza kutumika pale ambapo hakuna sabuni.- Kunawa mikono mara baada ya kutoka chooni kujisaidia, kumsaidia mgonjwa au mtoto.- Kuzingatia usafi wa mwili na nguo ikiwa ni pamoja na kuoga, kuvaa nguo safi, kukata kucha/kuwa na kucha

fupi.- Kufunga vidonda vya mkononi ili kuzuia sibiko (contamination) wakati wa kutayarisha chakula.- Kuepuka matumizi ya kitambaa cha kufutia mikono kisicho kisafi kwani huweza kuwa chanzo cha maambukizo

ya vimelea vya maradhi.

Usafi wa vyombo:- Kutumia vyombo safi kwa kutayarishia chakula na kupakulia.- Kuosha kwa maji ya kutosha na sabuni vyombo na vifaa vinavyotumika kutayarishia vyakula na hasa nyama

mbichi, samaki wabichi, au mayai mabichi, kabla ya kuvitumia kwa matayarisho ya vyakula vingine. Majivu yanaweza kutumika pale ambapo hakuna sabuni.

- Kuwa na kichanja cha kuanikia vyombo. Vyombo viondolewe punde vinapokauka na kuhifadhiwa katika

MADA YA 5

USAFI NA USALAMA WA CHAKULA NA MAJI

MODULE GFR4.indd 28 8/25/09 2:50:05 PM

21Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

sehemu kavu na safi.- Iwapo kitambaa cha kukaushia vyombo kitatumika; ni muhimu kifuliwe mara baada ya kutumika, kianikwe

na kipigwe pasi pale inapowezekana.

Usafi wa sehemu ya kutayarishia chakula:- Kusafisha sehemu zote za kutayarishia chakula, ikiwa ni pamoja na kufagia jiko au kudeki mara kwa mara ili

kuzuia wadudu watambaao na panya.- Kukusanya uchafu na mabaki ya vyakula katika ndoo au chombo chenye mfuniko na baadaye kutupwa

ipasavyo kwenye shimo la takataka.

Usafi na usalama wa chakula:- Kuhakikisha vyakula vya aina ya nyama, samaki na mayai vimepikwa na kuiva vyema ili kuepuka maambukizi

mbalimbali kwenye mfumo wa chakula kama yanayosababishwa na vimelea vya “salmonella”. Vyakula hivi visiliwe vikiwa vibichi, kwani vina hatari kubwa ya kuleta madhara mwilini (food poisoning).

- Kupika chakula mpaka kiive vizuri na kuhakikisha vitu vya maji maji vimechemka sawasawa. - Chakula kilichopikwa kiliwe kingali cha moto.- Kuosha matunda na mboga-mboga kwa maji ya kutosha (ikiwezekana yaliyochemshwa), hasa zile zinazoliwa

bila kupikwa. Matunda pia yanaweza kumenywa.- Kufunika chakula daima ili kuzuia wadudu, hasa inzi na mende na vumbi.- Kuepuka kutumia vyakula vilivyosindikwa, kwani mara nyingi vyakula husindikwa kwa kemikali ambazo

wakati mwingine zinaweza kumdhuru mtumiaji hasa kama ni mgonjwa.- Kuepuka vyakula vilivyoota ukungu k.m. nafaka, unga wa nafaka, karanga, mikate na matunda.- Kupasha moto kiporo au chakula kilichokaa zaidi ya saa mbili baada ya kupikwa mpaka kichemke kabla ya

kula hata kama bado kina uvuguvugu.- Kuepuka kununua mbogamboga zilizoanza kuoza mfano nyanya ambazo hazina ubora.- Kuhakikisha hakuna mwingiliano wa vyakula vilivyopikwa na vyakula vibichi vinavyoweza kuleta maambukizo

kama nyama mbichi, samaki wabichi na mayai mabichi.- Kuhakikisha muda wa kutumia vyakula haujapita (expiry date) hasa kwa vyakula vya madukani.

Usafi na usalama wa maji ya kunywa:- Kuhakikisha maji ni safi na yachemshwe na kuachwa yaendelee kuchemka kwa muda wa dakika 5 – 10 ili

kuua vimelea vya magonjwa.- Kuepuka kutumia kikombe kinachotumika kuchotea maji kwa matumizi mengine kwa mfano kunywea.- Kuchemsha maji ya kutengenezea barafu, aiskrimu, lambalamba au juisi.- Kutunza maji katika chombo safi chenye mfuniko na kuweka mahali penye baridi.

HITIMISHONi muhimu kuhakikisha kwamba maji na vyakula vinavyotumiwa na watu walioambukizwa virusi vya UKIMWI ni safi na salama ili kuzuia maambukizi mbalimbali yanayoweza kusababishwa na maji na vyakula visivyo safi na salama. Hii ni kwa sababu kinga yao ya mwili imepungua hivyo kuwafanya kupata maambukizi kwa urahisi zaidi. Ili chakula na maji viwe safi na salama ni muhimu kuzingatia usafi wa mtayarishaji wa chakula, usafi wa vyombo, usafi wa sehemu ya kutayarishia chakula, usafi na usalama wa chakula chenyewe na maji ya kunywa.

VI. NjIA ZA KUFUNDISHIA: Mhadhara na majadiliano, bungua bongo, maswali na majibu.

VII. VIFAA VYA KUFUNDISHIA: Bango kitita/ubao, kalamu za kuchorea/chaki, vitini, madaftari, gundi za karatasi, kalamu, sampuli za vyakula vya madukani.

VII. KAZI KWA WASHIRIKI Jadili mbinu mbalimbali zinazotumika katika mazingira unayotoka kuhakikisha usafi na usalama wa chakula

na maji. Je kuna haja ya kuzirekebisha? Kitu gani kifanyike ili kuhakikisha mbinu hizo zimeboreshwa?

MODULE GFR4.indd 29 8/25/09 2:50:06 PM

22 Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

MADA YA 6

LISHE NA ULAJI WAKATI WA MATATIZO YA KIAFYA YANAYOAMBATANA NA KUAMBUKIZWA VIrUSI VYA UKIMWI

I. LENGO: Kuwawezesha washiriki kufahamu jinsi ya kukabiliana kilishe na matatizo mbalimbali ya kiafya yanayoambatana

na kuambukizwa virusi vya UKIMWI

II. MALENGO MAHUSUSI: Mwisho wa mada hii washiriki waweze: Kutambua matatizo mbalimbali ya kiafya yanayoambatana na kuambukizwa virusi vya UKIMWI; Kutambua sababu zinazochangia kuwepo kwa matatizo hayo; Kutambua vyakula mbalimbali na ulaji unaoweza kupambana na matatizo mbalimbali ya kiafya

yanayoambatana na kuambukizwa virusi vya UKIMWI; na Kutambua mbinu mbalimbali za kumwezesha mtu aliyeambukizwa virusi vya UKIMWI kula chakula cha

kutosha wakati wa matatizo ya kiafya.

III. MAMBO YA KUjIFUNZAMatatizo, sababu, vyakula na mbinu za kukabiliana na:

- Kukosa hamu ya kula;- Vidonda na utandu mweupe kinywani na kooni;- Kichefuchefu na kutapika; - Kuharisha;- Kupungua uzito;- Uzito uliozidi au unene uliokithiri;- Kukosa choo au kupata choo kigumu;- Mafua na kikohozi;- Homa;- Upungufu wa wekundu wa damu;- Kifua kikuu; na- Matatizo ya ngozi.

IV. MUDA: Dakika 180

V. MUHTASARI WA MADA

UTANGULIZIKuna matatizo mbalimbali ya kiafya yanayoambatana na kuambukizwa virusi vya UKIMWI ambayo yanaweza kukabiliwa kilishe. Zipo sababu mbalimbali kwa kila tatizo. Vyakula na mbinu mbalimbali vinaweza kutumika kupunguza ukali wa baadhi ya matatizo hayo. Ikumbukwe kwamba pamoja na chakula, ni muhimu mgonjwa amwone daktari kwa ajili ya matibabu na uchunguzi mapema. Mkufunzi awakumbushe washiriki kuhusu athari za VVU kwenye lishe na awashirikishe kutambua matatizo mbalimbali ya kiafya yanayoambatana na kuambukizwa VVU.

Kukosa hamu ya kula

Kukosa hamu ya kula ni tatizo linaloweza kujitokeza mara kwa mara kwa mtu aliyeambukizwa VVU. Tatizo hili huweza kusababishwa na maambukizi mbalimbali, msongo-mawazo, uchovu, maumivu ya kinywa au koo, athari inayotokana na dawa au kutokula kwa muda mrefu. Mgonjwa ajaribu yafuatayo:

MODULE GFR4.indd 30 8/25/09 2:50:06 PM

23Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

- Kuongeza viungo kama tangawizi, limau, mdalasini, kotimiri au iliki kwenye vinywaji au vyakula mbalimbali kwani viungo hivi na vingine vimeonekana kuongeza hamu ya kula.

- Kula milo midogo mara nyingi kwa siku.- Ikiwezekana, mgonjwa asitayarishe vyakula mwenyewe au kukaa jikoni ama karibu na jiko kwani harufu ya

vyakula vinavyopikwa huweza kupunguza hamu ya kula.- Kunywa vinywaji na kula vyakula anavyovipenda zaidi.- Ikiwezekana mgonjwa asile akiwa peke yake, ale pamoja na familia au marafiki.- Aepuke kunywa vinywaji wakati wa kula kwani hii itasababisha tumbo kujaa haraka. Mgonjwa anywe kinywaji

kati ya mlo mmoja na mwingine.- Kuongeza vyakula vyenye virutubishi vingi kama karanga, maziwa, mafuta kwenye vyakula mbalimbali ili

kuviongezea ubora na kuvifanya viwe rahisi kula na kumeza.- Kubadili ladha na aina ya vyakula anavyokula mgonjwa kwani hii huongeza hamu ya kula.- Kufanya mazoezi mbalimbali kama kutembea haraka haraka na mengine ili kusaidia kuongeza hamu ya

kula. Aina ya mazoezi hutegemea hali ya mgonjwa.- Endapo mgonjwa ana tatizo la kubadilika kwa ladha kinywani huweza kutumia viongeza ladha kama vile

chumvi kiasi, sukari, viungo, “vinegar”, ndimu au limau ambavyo huweza kusaidia kuongeza ladha ya chakula na kuficha ladha mbaya inayoletwa na dawa.

- Endapo njia zilizoshauriwa hazitasaidia mgonjwa ale chakula kwa kujilazimisha kwani chakula ni muhimu sana.

- Tatizo linapokwisha mgonjwa arudie ulaji wa kawaida.

Vidonda na utandu mweupe kinywani au kooni

Vidonda na utandu mweupe kinywani au kooni (fangasi) huweza kufanya ulaji wa vyakula kuwa mgumu na hivyo kupunguza kiasi cha chakula anachoweza kula mgonjwa. Yafuatayo huweza kusaidia:

- Kula vyakula laini kama mtindi na uji au vile vilivyopondwa kama mtori au matunda kama parachichi, papai au ndizi mbivu.

- Kuepuka vyakula vyenye viungo au ladha kali.- Kuepuka vyakula vya moto sana au vyenye pilipili kali.- Kuepuka vyakula vyenye sukari nyingi kwani sukari huchochea kuongezeka kwa utandu mweupe kinywani

(fangasi).- Kusukutua kinywa kwa kutumia maji yaliyochemshwa pamoja na kitunguu saumu au mdalasini. Rudia kila

baada ya saa 3 hadi 4.- Kutumia mrija wakati wa kunywa au kula pale inapowezekana.- Kujaribu kumung’unya barafu iliyotengenezwa kwa maji yaliyochemshwa kama inapatikana kwani huweza

kupunguza maumivu kinywani.- Kutumia maziwa ya mgando (mtindi) mara kwa mara kwani mtindi hutuliza maumivu na huzuia utandu

mweupe kinywani na kooni kuongezeka.

Kichefuchefu au kutapika

Kichefuchefu na kutapika huweza kusababishwa na njaa, maradhi mbalimbali, ukosefu wa maji ya kutosha mwilini na baadhi ya dawa au vyakula mbalimbali. Kichefuchefu hupunguza hamu ya kula. Mgonjwa ajaribu yafuatayo:

- Kuepuka vyakula vyenye viungo vingi, mafuta mengi au sukari nyingi kwani vyakula hivi huweza kuongeza kichefuchefu.

- Kujaribu kula vyakula vichachu kidogo au vikavu na vyenye chumvi kidogo kama muhogo, kiazi na mkate; kwani hivi hupunguza kichefuchefu.

- Kunywa kiasi kidogo kidogo cha maji, supu na vinywaji vya viungo na kuendelea na vyakula laini. - Kula vyakula ambavyo si vya moto sana.- Kunywa juisi ya limau au ndimu iliyochanganywa na maji ya moto.- Kula milo midogo mara kwa mara (si chini ya mara 5 kwa siku).- Kula wakati amekaa wima au kujiegemeza kidogo kwenye mto. Asijilaze mara tu baada ya kula (asubiri

dakika 30 hadi saa 1 baada ya kula).- Kujaribu kula taratibu ili kupunguza kichefuchefu au kutapika.

MODULE GFR4.indd 31 8/25/09 2:50:06 PM

24 Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

- Kuepuka kukaa muda mrefu bila kula au kunywa chochote kwani kufanya hivyo huweza kusababisha kichefuchefu.

- Kuepuka aina zote za pombe au vyakula vyenye kafeini kama chai, soda na kahawa.

Kuharisha

Kuharisha mara nyingi husababishwa na kula vyakula au vinywaji vilivyosibikwa au vyenye vimelea vya maradhi, maambukizi mbalimbali katika mfumo wa chakula, minyoo na baadhi ya dawa kama kiua vijasumu (antibayotiki).

Kuharisha huweza kusababisha upotevu wa maji na virutubishi mwilini kwani uyeyushwaji wa chakula na ufyonzwaji wa virutubishi huwa duni. Wakati mwingine kuharisha husababisha kutokuwa na hamu ya kula. Mgonjwa ajaribu kufanya yafuatayo:

- Kunywa maji safi na salama kwa wingi ili kuzuia upungufu wa maji mwilini (zaidi ya lita moja na nusu au glasi 8 kwa siku).

- Kunywa vinywaji vingine kwa wingi zaidi isipokuwa vile vyenye kilevi au kafeini. Vinywaji kama supu ya mchele, madafu, togwa, supu, juisi ya matunda na maji yenye mchanganyiko maalumu wa sukari na chumvi (ORS) vinaweza kutumika.

- Kula matunda kama ndizi mbivu na mboga-mboga kama karoti, zilizopikwa ili kurudisha madini na vitamini zinazopotea kutokana na kuharisha.

- Kutafuna kwa muda mrefu au kula vyakula laini hurahisisha kumeza na virutubishi vyake kuyeyushwa na kusharabiwa mwilini.

- Kula vyakula ambavyo sio vya moto sana au baridi sana ili kupunguza kuharisha.- Kuepuka vyakula vyenye mafuta mengi, viungo vingi au pilipili nyingi kwani vyakula hivi huweza kuzidisha

kuharisha.- Kuepuka kutumia matunda yasiyoiva vizuri au yenye uchachu mkali kama nyanya, machungwa, machenza

na limau kwani huweza kuongeza tatizo.- Kuepuka vyakula na vinywaji vinavyosababisha gesi kwa wingi tumboni kama maharagwe, kabichi au

soda.- Kuepuka vinywaji vyenye kafeini kwa wingi kama chai na kahawa, kwani hivi husababisha upotevu zaidi wa

maji.- Kuepuka matumizi ya pombe za aina zote kwani huzuia baadhi ya virutubishi kusharabiwa na huongeza

upotevu wa maji mwilini.- Kuepuka maziwa freshi kwani yanawezesha kuongeza kuharisha, hata hivyo ajaribu kutumia mtindi.- Kuepuka vyakula vyenye makapi - mlo kwa wingi kama nafaka zisizokobolewa au vyakula vya jamii ya

kunde na baadhi ya mboga za majani kwani haviyeyushwi kwa urahisi na hivyo huongeza kuharisha.- Kuponda vitunguu saumu na kuchanganya kwenye vinywaji kama supu ya maji ya viungo.- Kula milo midogo mara kwa mara ili kurudisha virutubishi vinavyopotea.- Mgonjwa atumie nafaka zilizokobolewa au vyakula vya jamii ya kunde vilivyotolewa maganda.

Kupungua uzitoKupungua uzito kwa watu walioambukizwa virusi vya UKIMWI huweza kusababishwa na ongezeko la mahitaji ya baadhi ya virutubishi, ulaji, uyeyushwaji duni wa chakula, ufyonzwaji duni wa virutubishi mwilini na mabadiliko katika uvunjaji na ujengaji wa kemikali mwilini (umetaboli). Kupungua uzito huweza kukabiliwa kwa:

- Kuongeza aina, kiasi cha chakula na idadi ya milo kwa siku.- Kuongeza vyakula vyenye virutubishi na nishati-lishe kwa wingi kama karanga, mafuta, siagi, maziwa, sukari

na asali kwenye vyakula mbalimbali.- Kula vyakula vya nafaka, mizizi na ndizi kama mahindi, mchele, ngano, mtama, ulezi, uwele, viazi na pia aina

za nyama, samaki na vyakula vya jamii ya kunde kwa wingi.- Kutumia asusa kati ya mlo na mlo kama karanga, matunda au mtindi mara kwa mara kwani hii itasaidia

kukidhi mahitaji ya mwili ya siku.- Kuweka viungo katika chakula ili kuongeza hamu ya kula na kusaidia uyeyushwaji wake.

MODULE GFR4.indd 32 8/25/09 2:50:07 PM

25Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

- Kutumia vyakula vilivyochachushwa kama mtindi, togwa au mbegu zilizooteshwa ili kusaidia uyeyushwaji na ufyonzwaji wa virutubishi.

- Kufanya mazoezi kwani huongeza hamu ya kula na hujenga misuli.

Uzito uliozidi au unene uliokithiri

Kuzidi uzito huweza kusababishwa na matumizi ya baadhi ya dawa, kula chakula kingi kuliko mahitaji ya mwili, ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi, sukari nyingi au kutokufanya mazoezi ya mwili. Uzito uliozidi au uliokithiri unaweza kukabiliwa kwa:

- Kupunguza kiasi cha chakula katika kila mlo.- Kuepuka ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi.- Kuchagua asusa zenye virutubishi muhimu kama matunda, maziwa, juisi halisi za matunda, vyakula

vilivyochemshwa au kuchomwa kama ndizi, mihogo, mahindi au viazi.- Kubadili njia za mapishi. Badala ya kukaanga vyakula vichemshe au vichome.- Kuongeza ulaji wa mbogamboga na matunda hasa wakati wa mlo.- Kuepuka ulaji wa vyakula vilivyopikwa kwa mafuta mengi (kutumbukizwa kwenye mafuta) kama vile chipsi,

nyama zenye mafuta mengi, maandázi, keki nk.- Kufanya mazoezi kwani husaidia kupunguza kiasi cha mafuta mwilini.

Kukosa choo au kupata choo kigumu

Kukosa choo au kupata choo kigumu pia ni tatizo linalojitokeza kwa watu walioambukizwa virusi vya UKIMWI. Hii huweza kusababishwa na homa ambazo hupunguza maji mwilini au kutokula chakula cha kutosheleza mahitaji ya mwili na hasa chenye makapi-mlo. Mgonjwa anashauriwa kufanya yafuatayo:

- Kunywa maji mengi safi na salama angalau lita moja na nusu au glasi 8 na zaidi kwa siku.- Kutumia vyakula vinavyotokana na nafaka ambazo hazijakobolewa kama dona, unga wa ngano usiokobolewa,

mahindi ya kuchoma, kuchemsha n.k.- Kula matunda na mboga-mboga kwa wingi, na pia vyakula vya jamii ya kunde kama kunde, choroko na

maharagwe; kwani huwa na makapi mlo kwa wingi.- Kutumia matunda kama papai, parachichi, embe au matunda yaliyokaushwa kwani yameonekana kusaidia

kulainisha choo.- Kujaribu kufanya mazoezi kwani husaidia chakula kuyeyushwa.- Kujipa muda wa kutosha chooni wakati wa kujisaidia, hivyo ni vyema vyoo vyetu viwe katika hali ya usafi

Mafua na kikohozi

Mafua na kikohozi ni maambukizo yanayowapata mara kwa mara watu walioambukizwa VVU. Mafua na kikohozi huweza kusababishwa na aina fulani ya virusi au bakteria. Wakati mwingine mafua na kikohozi husababisha homa. Mgonjwa ajaribu yafuatayo:

- Kunywa maji ya kutosha au vinywaji vingine kama vile limau, tangawizi, kitunguu maji, nanaa, n. k. katika kipindi chote cha kuwa na mafua na/au kikohozi.

- Kujifukiza kwa kutumia mvuke wa maji.- Kuchanganya maji ya limau na asali na kutumia mara kwa mara katika kipindi chote cha ugonjwa.- Kupata muda wa kutosha wa kupumzika.

Homa

Homa husababishwa na maambukizi mbalimbali. Tatizo hili huwapata watu walioambukizwa virusi vya UKIMWI mara kwa mara. Mgonjwa ajaribu yafuatayo:

- Kunywa maji na vinywaji vingine kwa wingi mara kwa mara ili kupunguza joto la mwili na kuepuka upotevu wa maji mwilini.

- Kula milo midogo mara nyingi ili kukidhi ongezeko la mahitaji ya mwili wakati wa homa.- Kupunguza nguo nzito mwilini.- Kuoga kwa maji ya uvuguvugu ili kupunguza joto la mwili.

MODULE GFR4.indd 33 8/25/09 2:50:07 PM

26 Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

Upungufu wa wekundu wa damuUpungufu wa wekundu wa damu huweza kusababishwa na ulaji duni hasa wa vyakula vyenye madini chuma kwa wingi, malaria na minyoo. Mtu aliyeambukizwa virusi vya UKIMWI huathirika kiafya haraka zaidi iwapo ana tatizo la upungufu wa wekundu wa damu. Dalili za upungufu wa wekundu wa damu ni pamoja na uchovu, ulegevu, mapigo ya moyo kuongezeka, kizunguzungu, kupumua kwa shida, vidole kufa ganzi, kuvimba uso na miguu, masikio kuvuma, na weupe usio wa kawaida kwenye macho, midomo, kucha, viganja, ufizi, ulimi na hata ngozi. Upungufu wa wekundu wa damu huweza kukabiliwa kwa: - Kula vyakula vyenye madini chuma kwa wingi, kama vile maini, samaki, dagaa, figo, nyama, kisamvu,

matembele, majani ya kunde, mchicha, choya, maharagwe, choroko, njegere, kunde, dengu, njugu mawe, na korosho.

- Kula matunda kwa wingi pamoja na mlo, hasa yale yenye Vitamini C kwa wingi kama vile mapera, machungwa, machenza, mapesheni, mananasi, mabungo, ubuyu na ukwaju. Vitamini C husaidia ufyonzwaji na utumikaji wa madini chuma yaliyoko kwenye vyakula vyenye asili ya mimea.

- Kuepuka vinywaji kama chai, kahawa au soda wakati wa mlo, kwani vina kemikali iitwayo kafeini ambayo huzuia upatikanaji wa madini chuma yaliyoko kwenye vyakula vyenye asili ya mimea. Iwapo italazimu kutumia vinywaji hivyo ni vema kuvitumia saa moja kabla au saa moja baada ya kula chakula na si wakati wa kula.

- Kutibu maradhi kama vile malaria na minyoo mapema kwani huchangia kuleta upungufu wa wekundu wa damu.

- Kumuona daktari kwa ushauri zaidi ikiwa ni pamoja na kupewa vidonge vya madini chuma na foliki asidi ili kukabiliana na tatizo la upungufu wa wekundu wa damu.

Kifua kikuu

Kifua kikuu ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na vimelea vya bakteria ajulikanae kama Mycobacterium tuberculosis. Kifua kikuu kwa kawaida kinaathiri mapafu, lakini huweza kuathiri pia sehemu nyingine za mwili kama uti wa mgongo, mifupa, moyo, ubongo, figo na mfumo mzima wa njia ya chakula. Kifua kikuu ni mojawapo ya maradhi nyemelezi kwa watu walioambukizwa virusi vya UKIMWI. Dalili za kifua kikuu ni pamoja na kikohozi, kichefuchefu, kutapika, kuharisha, kukosa hamu ya kula, homa za usiku na kupungua uzito. Mtu mwenye kifua kikuu anashauriwa yafuatayo:

Kula mlo kamili angalau mara tatu kwa siku. Mlo kamili hutayarishwa kutokana na mchanganyiko wa angalau chakula kimoja kutoka katika makundi ya vyakula.

Kula vyakula vinavyoupatia mwili nguvu (nishati-lishe) kwa wingi ili kuzuia kupungua uzito, kuongeza nguvu na kusaidia kupona haraka. Vyakula vyenye nishati-lishe kwa wingi ni pamoja na mahindi, mtama, uwele, mchele, ngano, viazi aina zote, mihogo, magimbi na ndizi za kupikwa. Vyakula vingine ni mafuta ya alizeti, mawese, mbegu zitoazo mafuta, siagi, majarini, maziwa, jibini, asali na sukari.

Kula vyakula vyenye protini kwa wingi ili kusaidia kujenga misuli, kukarabati mwili na kuimarisha mfumo wa kinga. Vyakula vyenye protini kwa wingi ni kama maharagwe, choroko, njegere, kunde, dengu, njugu mawe, karanga, korosho, aina zote za nyama, samaki, mayai na maziwa.

Kula matunda na mboga-mboga kwa wingi ili kupata vitamini na madini kwa ajili ya kuwezesha kupona haraka na kuboresha kinga ya mwili.

Kula vyakula vyenye Vitamini B6 kwa wingi kama vile viazi vitamu, maharagwe, mahindi yasiyokobolewa,

parachichi, nyama na samaki kwani baadhi ya dawa za kutibu kifua kikuu huingilia matumizi ya vitamini hiyo mwilini.

Kula vyakula vyenye madini chuma kwa wingi ili kuzuia upungufu wa wekundu wa damu. Vyakula vyenye madini chuma kwa wingi ni kama maini, dagaa, figo, nyama, samaki, mbaazi, maharagwe, korosho, choya (rozela), kisamvu, majani ya kunde, matembele na mchicha.

Kula vyakula vyenye Vitamini A kwa wingi ili kuboresha mfumo wa kinga na kuzuia matatizo ya ngozi. Vyakula vyenye Vitamini A kwa wingi ni kama vile maini, mawese, samaki wenye mafuta, kisamvu, matembele, majani ya kunde, maboga, karoti, papai, embe na viazi vitamu vyenye rango ya manjano.

Kula vyakula vyenye Vitamini D kwa wingi kama vile nyama, samaki, mafuta ya samaki na maziwa. Vilevile, Vitamini D hupatikana kwenye jua. Upungufu wa vitamini hii huweza kufanya hali ya mgonjwa kuwa mbaya zaidi.

Kukabili dalili za kifua kikuu zinazofanana na matatizo yanayoambatana na kuambukizwa na virusi vya UKIMWI kwa kufuata ushauri uliotolewa hapo awali.

MODULE GFR4.indd 34 8/25/09 2:50:07 PM

27Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

Kupata muda wa kupumzika. Kuepuka matumizi ya pombe za aina zote, tumbaku na bidhaa zake na madawa ya kulevya. Kuendelea na matibabu ya kifua kikuu kama ilivyoshauriwa na wataalam wa afya.

Matatizo ya ngoziMatatizo ya ngozi huweza kumpata mtu yeyote, ingawa yameonekana zaidi kwa watu walioambukizwa virusi vya UKIMWI. Baadhi ya matatizo ya ngozi husababishwa na upungufu wa baadhi ya vitamini kwa mfano Vitamini A na B

6.

Magonjwa ya ngozi yanaweza kuhitaji matibabu, hata hivyo mgonjwa anashauriwa:- Kula vyakula vyenye Vitamini A kwa wingi kama mawese, maini, mayai, maziwa, jibini, matunda na mboga

zenye rangi ya njano kama embe, papai, karoti na maboga na vilevile mboga zenye rangi ya kijani.- Kula vyakula vyenye Vitamini B

6 kwa wingi kama vile maharagwe, mboga za kijani, karanga, mahindi, nyama

na parachichi.

HITIMISHOPamoja na mbinu na vyakula mbalimbali vilivyoshauriwa kukabili matatizo ya kiafya yanayoambatana na kuambukizwa virusi vya UKIMWI, ni muhimu kumuona daktari mapema tatizo linapojitokeza. Endapo mgonjwa ana tatizo zaidi ya moja ni vizuri asaidiwe kuchagua vyakula na mbinu ambazo zinamsaidia zaidi wakati huo. Ikumbukwe kuwa ni muhimu kurudia kula vyakula vya kawaida mara tu tatizo linapokwisha.

VI. NjIA ZA KUFUNDISHIA:

Mhadhara na majadiliano, maswali na majibu.

VII. VIFAA VYA KUFUNDISHIA:

Bango kitita/ubao, kalamu za kuchorea/chaki, vitini, madaftari, kalamu, gundi za karatasi.

VII. KAZI KWA WASHIRIKIEleza kwa kifupi utamsaidiaje mgonjwa huyu:Annet ameambukizwa virusi vya UKIMWI kwa miaka 3. Muda wote hali yake kwa ujumla ilikuwa inaendelea vizuri. Sasa ameambiwa na daktari kuwa ana ugonjwa wa kifua kikuu (TB) na wakati huo huo anaharisha.

Utamshauri afanye nini kuhusu: a) Chakula ili hali yake ya lishe isiwe mbaya?

b) Afya yake kwa ujumla?

MODULE GFR4.indd 35 8/25/09 2:50:07 PM

28 Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

MADA YA 7UHAKIKA WA CHAKULA KATIKA KAYA

I. LENGO: Kuwawezesha washiriki kufahamu mbinu mbalimbali za kuboresha uhakika wa chakula katika kaya.

II. MALENGO MAHUSUSI: Mwisho wa mada hii washiriki waweze kueleza:

Maana ya uhakika wa chakula katika kaya; Uhusiano kati ya uhakika wa chakula katika kaya na kuwepo kwa virusi vya UKIMWI; Jinsi ya kutambua kaya zisizokuwa na uhakika wa chakula; na Jinsi ya kuboresha uhakika wa chakula katika kaya.

III. MAMBO YA KUjIFUNZA Maana ya uhakika wa chakula katika kaya; Uhusiano kati ya uhakika wa chakula katika kaya na kuambukizwa virusi vya UKIMWI; Vigezo vya kutambua kaya zisizokuwa na uhakika wa chakula; na Jinsi ya kuboresha uhakika wa chakula katika kaya: - Majukumu ya kaya, Serikali ya kijiji, mtoa huduma majumbani, serikali kuu na taasisi zisizo za kiserikali.

IV. MUDA: Dakika 60

V. MUHTASARI WA MADA

UTANGULIZIUhakika wa chakula katika kaya ni muhimu katika kuhakikisha upatikanaji wa virutubishi muhimu na vya kutosha kwa ajili ya lishe na afya bora ya wanakaya. Ukosefu wa uhakika wa chakula katika kaya hufanya watu kuwa na hali mbaya ya lishe. Pamoja na sababu nyingine nyingi, maradhi na hasa ya muda mrefu kama UKIMWI huweza kusababisha ukosefu wa chakula cha kutosha katika kaya, kwa kupunguza nguvu kazi ya watu katika kaya.

Maana ya uhakika wa chakula katika kaya Ni upatikanaji wa chakula cha kutosha na chenye virutubishi muhimu kwa watu wote waliopo katika kaya kwa wakati wote kwa ajili ya afya bora.

Uhusiano kati ya uhakika wa chakula katika kaya na kuwepo kwa virusi vya UKIMWI Kuwepo kwa virusi vya UKIMWI katika jamii kumeathiri uhakika wa chakula katika kaya. Sababu zinazoweza kuchangia ni pamoja na:

- Watu wengi walioambukizwa virusi vya UKIMWI wako katika umri wa kuzalisha mali na chakula. Watu hawa uwezo wao wa kufanya kazi na kuzalisha mali hupungua, hivyo uhakika wa chakula katika kaya huathiriwa kwa kiasi kikubwa.

- Miili yao huwa dhaifu na hivyo kutoweza kufanya kazi ngumu na kwa muda mrefu. Hali hiyo inapunguza mapato na uzalishaji wa chakula.

- Huugua mara kwa mara na hivyo huhitaji kutunzwa na wanafamilia pamoja na ndugu. Hali hii hupunguza muda wa kuzalisha chakula au kufanya kazi zinazoleta kipato.

- Mali mbalimbali, akiba na mapato ya kaya huweza kutumika kwa ajili ya matibabu badala ya kutumika kwa kuzalishia mali au kununua chakula.

- Kutokana na vifo vya mapema, urithishaji wa maarifa ya kilimo, ufugaji na shughuli nyingine za mikono hukosekana.

- Kadri upatikanaji wa chakula unavyopungua, ndivyo hatari ya kupata utapiamlo na maradhi mengine kwa wanakaya inavyoongezeka.

- Kwa mantiki hiyo uhakika wa chakula katika kaya huweza kuathiriwa kwa kiasi kikubwa.

MODULE GFR4.indd 36 8/25/09 2:50:08 PM

29Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

Vigezo vya kutambua kaya zisizokuwa na uhakika wa chakula

Vigezo mbalimbali huweza kutumika katika kutambua kaya zisizokuwa na uhakika wa chakula. Vigezo hivyo ni:- Hali ya lishe ya watu na hasa watoto katika kaya. Lishe ya watoto chini ya umri wa miaka mitano huathirika

zaidi.- Maradhi ya mara kwa mara kwa wanakaya. Watu wasiopata chakula cha kutosha na chenye virutubishi

muhimu huugua mara kwa mara.- Kuuza vitu kama wanyama wanaofugwa, samani na vitu vingine vya thamani ili kupata fedha za kununua

chakula. Uuzaji wa namna hiyo unapofanyika kuliko ilivyo kawaida inaashiria kupungua kwa uhakika wa chakula katika kaya.

- Kupungua kwa kiasi na aina ya vyakula vinavyoliwa katika kaya. Mara nyingi wanakaya hupunguza kiasi na aina ya vyakula kama hatua ya kukabiliana na upungufu wa uhakika wa chakula katika kaya.

- Kubadili kazi toka kwenye kilimo kwenda kwenye kazi zenye ujira wa haraka hata kama kipato ni kidogo. Mara nyingi wanakaya wengi huacha mashamba na kaya zao na kwenda sehemu nyingine kutafuta kazi kwa ajili ya kipato.

- Kupungua kwa aina za mazao yanayolimwa. Watu hujaribu kubadili na kulima mazao ya muda mfupi na ambayo huhitaji pembejeo kidogo. Mara nyingi mazao hayo hutoa mavuno kidogo.

- Kupungua kwa chakula kilichohifadhiwa. Mara nyingi kabla ya kuuza mali za kaya, watu hujaribu kutumia kwanza chakula kilichohifadhiwa.

- Kupungua kwa shughuli za kuongeza kipato. Muda mwingi hutumika kutafuta chakula na kuhudumia wagonjwa kuliko shughuli za uzalishaji.

- Kuuza ardhi na hivyo kupungua kwa ardhi kwa ajili ya kilimo. Baada ya kuuza mali zote, kaya huishia kuuza mashamba na pengine hata nyumba.

jinsi ya kuboresha uhakika wa chakula katika kaya

Majukumuyakaya•- Kujikinga na maambukizi ya virusi vya UKIMWI.- Kuanzisha miradi midogo midogo ili kuongeza kipato kwa ajili ya matumizi ya kaya ikiwa ni pamoja na

chakula.- Kuboresha njia za kuhifadhi vyakula ikiwemo kusindika kwa njia za asili.- Kutumia njia bora za utayarishaji wa chakula hasa zile zinazohifadhi na kuboresha upatikanaji wa virutubishi

kama kupika kwa mvuke.- Kulima bustani za matunda, mboga-mboga na vyakula vingine.- Kufuga wanyama wadogo kama kuku na sungura na kuwatumia kwa chakula.- Kutumia vyakula vya asili, hasa vinavyopatikana kwa urahisi kwenye mazingira husika.- Kupata elimu kuhusu umuhimu wa uhakika wa chakula.- Kuzingatia usafi na usalama wa chakula.

MajukumuyaSerikaliyaKijiji/HalmashaurizaWilaya•- Kuhamasisha jamii kuhusu kujikinga na maambukizi ya virusi vya UKIMWI.- Kuhakikisha hakuna mnyanyapao na ubaguzi kwa watu walioambukizwa virusi vya UKIMWI. - Kufuatilia uhakika wa chakula katika kaya za watu walioambukizwa virusi vya UKIMWI.- Kuhamasisha wanajamii kusaidia watu walioambukizwa na virusi vya UKIMWI ili kuhakikisha uhakika wa

chakula katika kaya zao.

Majukumuyamtoahudumamajumbani•Kuzitambua familia zenye matatizo.- Kutoa taarifa kwa serikali ya kijiji.- Kuunganisha familia zenye matatizo na huduma nyingine zinazopatikana katika eneo husika.- Kuzisaidia familia zenye matatizo ili zitumie fedha au chakula kwa uangalifu ili kupata virutubishi muhimu.- Kuhamasisha matumizi ya matunda pori, vyakula na mboga za asili iwapo zinapatikana.- Kuhusisha wataalamu wa kilimo katika kusaidia kaya kuwa na uhakika wa chakula.-

MODULE GFR4.indd 37 8/25/09 2:50:08 PM

30 Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

MajukumuyaSerikaliKuu•- Kusimamia sera mbalimbali zinazolenga kuongeza kipato na chakula kwa wananchi.- Kusimamia programu za jamii zinazohusu chakula.- Kusimamia sera zinazohusu virusi vya UKIMWI na UKIMWI

Majukumuyataasisizisizozakiserikali•- Kuhamasisha jamii kuhusu kujikinga na maambukizi ya virusi vya UKIMWI na kuwahudumia watu

walioambukizwa virusi vya UKIMWI.- Kuhamasisha na kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa uhakika wa chakula katika kaya.- Kusaidia kaya zilizoathirika ili ziweze kupata kipato cha kutosha na hivyo kuwa na uhakika wa chakula.- Kuweka msukumo kwenye upangaji wa sera za serikali zinazoboresha uhakika wa chakula katika kaya.

HITIMISHO

Uhakika wa chakula katika kaya huweza kuathiriwa kwa kiasi kikubwa kwa kuwepo kwa virusi vya UKIMWI. Ni muhimu kwa kaya, serikali ya kijiji, watoa huduma serikali kuu na taasisi zisizo za serikali kutekeleza majukumu yake ili kuboresha uhakika wa chakula katika kaya. Wanajamii wanaweza kubuni mbinu mbalimbali za kuhakikisha kaya zina uhakika wa chakula. Ni muhimu kwa jamii kusaidia kaya ambazo zina upungufu wa chakula. Jamii zinaweza kuwa na utaratibu wa kuchangia chakula kwa ajili ya kaya zisizo na chakula cha kutosha hasa zenye watu walioambukizwa virusi vya UKIMWI.

VI. NjIA ZA KUFUNDISHIA: Mhadhara na majadiliano, maswali na majibu.

VII. VIFAA VYA KUFUNDISHIA:

Bango kitita/ubao, kalamu za kuchorea/chaki, vitini, gundi za karatasi, madaftari, kalamu.

VIII. KAZI KWA WASHIRIKI Kujadili katika vikundi vigezo vya kuitambua kaya yenye kuhitaji msaada ili kuboresha uhakika wa

chakula. Kujadili njia zinazoweza kutumika kusaidia kaya hizi kuwa na uhakika wa chakula katika mazingira

unayotoka.

MODULE GFR4.indd 38 8/25/09 2:50:08 PM

31Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

MADA YA 8

KUTATHMINI HALI YA LISHE YA MTU ALIYEAMBUKIZWA VIrUSI VYA UKIMWI

I. LENGO: Kuwapa washiriki stadi za kutathmini hali ya lishe ya mtu aliyeambukizwa virusi vya UKIMWI.

II. MALENGO MAHUSUSI: Mwisho wa mada hii washiriki waweze:

Kutaja njia mbalimbali zinazoweza kutumika kutathimini hali ya lishe ya mtu; Kutambua mambo ya kuzingatia wakati wa kuchukua historia ya ulaji; Kupima na kutafsiri baadhi ya vipimo vya umbile la mwili; na Kutambua mambo ya kuzingatia wakati wa kuchukua historia ya maradhi.

III. MAMBO YA KUjIFUNZA Mambo ya kuzingatia wakati wa kuchukua historia ya ulaji; Baadhi ya vipimo vya umbile la mwili; Vipimo vya kibailojia na kikemia; Kutambua dalili za upungufu wa wekundu wa damu; na Mambo ya kuzingatia wakati wa kuchukua historia ya magonjwa.

IV. MUDA: Dakika 180

V. MUHTASARI WA MADA

UTANGULIZIUfuatiliaji na tathmini ya hali ya lishe ya mtu aliyeambukizwa virusi vya UKIMWI ni muhimu katika kugundua mapema dalili zozote za matatizo ya kiafya na utapiamlo. Lishe duni ni moja ya matatizo makuu kwa mtu aliyeambukizwa virusi vya UKIMWI. Lishe duni huweza kusababisha matatizo mengi ya kiafya na hata kifo cha mapema. Hivyo ni muhimu kufuatilia na kutathmini hali ya lishe mara kwa mara ili kuboresha hali ya lishe na afya ya mtu aliyeambukizwa virusi vya UKIMWI. Lengo hasa la kutathmini hali ya lishe ya mtu aliyeambukizwa virusi vya UKIMWI ni kuangalia au kufuatilia maendeleo ya kilishe ya mtu huyo ili kuweza kumshauri ipasavyo. Zifuatazo ni baadhi ya mbinu zinazotumika kutathmini hali ya lishe:

- Kuchukua historia ya ulaji;- Kutumia vipimo vya umbile la mwili;- Kutumia vipimo vya kibaologia na kikemia; na- Kuchukua historia ya maradhi.

Kuchukua historia ya ulajiMamboyakuzingatianipamojana:

- Kiasi na aina ya chakula mgonjwa anachokula; - Idadi ya milo; - Vyakula anavyopendelea na asivyopendelea; - Miiko katika vyakula; - Matatizo katika ulaji wa vyakula kama kukosa hamu ya kula; - Usafi katika uandaaji wa vyakula; - Jinsi mlengwa anavyohifadhi vyakula, wapi anakula chakula;

MODULE GFR4.indd 39 8/25/09 2:50:08 PM

32 Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

- Nani anapika; - Anatumia nishati gani kupikia; - Anapataje chakula chake; - Muda gani anakula na anakula baada ya muda gani; - Ubora wa chakula anachokula (quality of the meal/food); pamoja na - Matumizi ya virutubishi vya nyongeza na dawa.

Huu ni msingi mzuri kwa ajili ya kutoa ushauri wa lishe.

Vipimo vya umbile la mwili

Tathminiyahaliyalishehuwezapiakufanyikakwakuangaliavipimovyaumbilelamwili.Vifuatavyo ni baadhi ya viashirio vinavyotumika:

U• wiano wa uzito na urefu (Body Mass Index (BMI)): Kiashirio hiki hutumia uwiano wa uzito na urefu ili kutathmini hali ya lishe ya mtu. BMI inapotumika kwa watoto na vijana walio katika umri kati ya miaka 5 na 19, chati maalumu ambayo inahusisha umri na jinsi hutumika kuonyesha hali ya lishe ya wahusika. Uwiano huo wa uzito katika kilogramu (kg) na urefu katika mita (m) hupatikana kwa kutumia kanuni ifuatayo:

BMI = Uzito (kg) Urefu (m) ²

Njia hii hutumika kutathmini hali ya lishe ya mtu kwa haraka. Pia hutumika kupima watu wengi, ni rahisi kutumia mahali popote na haina gharama kubwa. Mahitaji yake ni mizani ya kupimia uzito na kifaa cha kupimia urefu. BMI huwa na viwango mbalimbali vinavyoashiria hali ya lishe ya mtu. Ifuatayo ni tafsiri ya viwango hivyo kama ilivyowekwa na Shirika la Afya Duniani (WHO). Tafsiri hii ni kwa watu wazima.

BMI chini ya 18.5 = Hali duni ya lishe

BMIkatiya18.5mpaka24.9 = Uzitounaofaa

BMI kati ya 25.0 na 29.9 = Unene uliozidi

BMI ya 30.0 au zaidi = Unene uliokithiri au kiribatumbo

Tafsiri ya viwango hivi haitumiki kwa wanawake wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano.

Kielelezo Na. 4: Chati ya BMI

MODULE GFR4.indd 40 8/25/09 2:50:09 PM

33Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

Uwiano wa uzito na umri:• Kiashirio hiki mara nyingi hutumika sana kutathmini hali ya lishe kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano. Kipimo hiki kinahitaji kumpima mtoto mara kwa mara angalau mara moja kwa mwezi ili kuweza kupata picha kamili ya kasi ya ukuaji wa mtoto na hali yake ya lishe. Kipimo hiki hutumika kwenye kliniki za ufuatiliaji wa ukuaji na maendeleo ya mtoto.

jINSI YA KUPIMA UZITO, UREFU NA KUTUMIA KADI YA BMI

MODULE GFR4.indd 41 8/25/09 2:50:10 PM

34 Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

KutafsirivipimovyaukuajiwamtotokwausahihiMchirizi wa mtoto anayekua vizuri huambaa sambamba na mchirizi wa ulinganisho ambao huwa kati ya asilimia

80 - 100 na uko kwenye rangi ya kijani katika kadi ya ukuaji wa mtoto.- Mabadiliko ya ghafla ya mchirizi aidha kwa kubaki pale pale kwa kipindi cha miezi mitatu mfululizo au kushuka

kunaashiria tatizo na uchunguzi wa kina unatakiwa ufanyike ili kujua sababu na jinsi ya kulitatua.- Mstari uliolala pale pale mfululizo kwa miezi mitatu au zaidi hata kama uko katika viwango gani (asilimia 60 - 80

au 80 -100) unaonyesha kuwa mtoto huyu hakui vizuri na anahitaji kuchunguzwa.- Mtoto ambaye mchirizi wake wa ukuaji upo kati ya asilima 60 na 80 ( rangi ya kijivu katika kadi) ni mtoto ambaye

ana uzito pungufu kwa umri wake. Lakini kama uzito wa mtoto huyu unaongezeka kila wakati na hana tatizo lolote la kiafya huenda mtoto huyu ana umbo dogo, labda alizaliwa njiti au ana uzito pungufu. Mfuatilie mtoto huyu na mjengee mama kujiamini na uendelee kumuelimisha mama kuhusu ulishaji unaofaa kwa mtoto huyu.

- Mtoto ambaye yuko chini ya asilimia 60 (katika rangi nyekundu) inaonyesha kuwa hali yake ya afya na lishe si nzuri, kwa hiyo inabidi afuatiliwe kwa karibu zaidi na kuhakikisha kuwa mchirizi wake wa ukuaji haushuki wala kubaki umelala pale pale bali uwe unaelekea juu wakati wote. Mtoto huyu huweza kuwa amezaliwa njiti; amezaliwa na uzito pungufu au amepata utapiamlo mkali. Hatua za haraka zinatakiwa zichukuliwe kwa mtoto huyu hata rufaa kama itabainika ana matatizo yoyote na mara nyingi tatizo dogo tu la kiafya humweka mtoto katika hatari hata ya kupoteza maisha yake.

- Kama mchirizi wa ukuaji uko juu kabisa ya mstari wa asilimia 100 (sehemu nyeupe baada ya kijani) mtoto huyu pia hana hali nzuri ya afya na lishe. Mhudumu wa afya anapaswa kujadiliana na mama au mlezi ili kujua tatizo na jinsi ya kumsaidia.

- Kitu muhimu katika ufuatiliaji wa ukuaji na maendeleo ya mtoto ni kuchunguza mwelekeo wa mchirizi wa ukuaji wa mtoto na kuchukua hatua za haraka na zinazofaa bila kujali mchirizi wa ukuaji uko wapi.

KielelezoNa.5:ChatiyaKufuatiliaUkuajinaMaendeleoyaMtotoMwenyeUmriChiniyaMiaka5

MODULE GFR4.indd 42 8/25/09 2:50:12 PM

35Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

Uzito wa mwili: •Kiashirio hiki hutumika kuangalia mabadiliko ya umbile la mwili. Uzito wa mwili hupimwa kwa kutumia mizani. Kipimo hiki cha uzito kinashauriwa kufanywa mara kwa mara, angalau mara moja kwa wiki ili kuweza kutambua kasi ya kuongezeka au kupungua kwa uzito wa mwili. Kama kuna upotevu wa uzito wa kilo 6 – 7 kwa mwezi bila kukusudia basi huashiria hali mbaya ya lishe na afya.

Kutumia vipimo vya kibaiolojia na kikemiaHii inajumuisha tathmini ya vitamini na madini mbalimbali mwilini. Hata hivyo kiashirio cha kibailojia na kikemia kinachotumika zaidi ni kipimo cha wekundu wa damu (Haemoglobin (Hb)).

Kupima wekundu wa damu: Upungufu wa wekundu wa damu unaweza kuonekana kwa macho au kupimwa maabara. Unaweza kutambua upungufu wa wekundu wa damu kwa kuona kuna weupe usio wa kawaida katika viganja vya mikono, nyayo, macho, ulimi na kucha. Tathmini ya maabara inahusisha kupima kiasi cha wekundu wa damu (haemoglobin) na kuona kama wekundu unafikia kiwango rasmi kilichowekwa na shirika la Afya Duniani (WHO) kama inavyoonyeshwa katika jedwali na. 2:

jedwali Na. 2: Kiwango cha HaemoglobinKinachoashiriaUpungufuwaWekunduwaDamu

Kundi la watu Kiwango cha haemoglobin chini ya:

Watoto kati ya miezi sita na miaka 5Watoto kati ya miaka 5 na miaka 11Watoto kati ya miaka 12 na 14Wanawake wajawazitoWanawake wasio wajawazito zaidi ya miaka 15Wanaume watu wazima zaidi ya miaka 15

11.0 g/dl11.5 g/dl12.0 g/dl11.0 g/dl12.0 g/dl13.0 g/dl

Imetafsiriwa kutoka: WHO/UNICEF/UNU (2001); values used in Demographic and Health Surveys

Kuchukua historia ya maradhiTathmini ya lishe ya mtu aliyeambukizwa virusi vya UKIMWI inaweza pia kufanyika kwa kuchukua historia ya magonjwa yanayompata mara kwa mara. Dadisi juu ya:

- Maradhi katika mfumo mzima wa chakula, mfano kuharisha, kichefuchefu, kutapika, n.k.- Upataji choo;- Magonjwa nyemelezi;- Magonjwa kama kisukari, malaria, n.k.

HITIMISHO:

Ni muhimu kutatmini hali ya lishe ya mtu aliyeambukizwa virusi vya UKIMWI ili kuweza kufuatilia maendeleo yake ya afya na lishe na kumshauri ipasavyo. Inashauriwa kutumia vipimo au vigezo zaidi ya kimoja kutathmini hali ya lishe ya mtu. Ikumbukwe kuwa vigezo na vipimo vilivyoongelewa hutumika kwa watu wote na si maalumu kwa watu walioambukizwa virusi vya UKIMWI.

VI. NjIA ZA KUFUNDISHIA: Mhadhara na majadiliano, majadiliano ya vikundi, maswali na majibu

VII. VIFAA VYA KUFUNDISHIA: Bango kitita/ubao, vitini, kalamu za kuchorea/chaki, madaftari, kalamu, gundi za karatasi, mizani, kipimo cha urefu,

kikokoteo, chati ya BMI, kadi ya kliniki ya watoto.

VIII. KAZI KWA WASHIRIKI: Washiriki wakae katika vikundi ili wafanye mazoezi ya kupima uzito na urefu wa kila mwanakikundi na

kukokotoa na kutafsiri BMI yake na kumpa ushauri kutegemeana na hali yake.

NB: Usahihi wa kupima urefu na uzito uzingatiwe.

MODULE GFR4.indd 43 8/25/09 2:50:13 PM

36 Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

MADA YA 9

MATUMIZI YA DAWA NA CHAKULA

I. LENGO: Kuwawezesha washiriki kuelewa uhusiano kati ya chakula na baadhi ya dawa zinazotumiwa na watu

walioambukizwa virusi vya UKIMWI au UKIMWI.

II. MALENGO MAHUSUSI: Mwisho wa mada hii washiriki waweze:

Kueleza uhusiano kati ya chakula na baadhi ya dawa; Kutoa ushauri wa matumizi sahihi ya chakula na dawa; na Kutambua athari za baadhi ya dawa.

III. MAMBO YA KUjIFUNZA Jinsi chakula kinavyoingiliana na dawa; Ushauri wa matumizi sahihi ya chakula na dawa.

IV. MUDA: Dakika 60

V. MUHTASARI WA MADA

UTANGULIZIWatu walioambukizwa virusi vya UKIMWI mara nyingi huwa wanatumia dawa za aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na dawa za kupunguza makali ya UKIMWI (ARVs) na dawa za kutibu au kupunguza kasi ya magonjwa nyemelezi na matatizo mengine ya kiafya yanayotokana na maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Pamoja na umuhimu wa chakula kwa mgonjwa yeyote, chakula na dawa huweza kuwa na mwingiliano ambao huwa na faida au hasara. Hivyo ni muhimu kwa mtoa huduma kwa watu walioambukizwa virusi vya UKIMWI, kuwasaidia wagonjwa kutambua athari zinazojitokeza wakati wanapotumia dawa fulani na kuwasaidia kukabiliana nazo.

jinsi chakula kinavyoweza kuiingiliana na dawa Chakula huweza kuingilia usharabu wa dawa tumboni, usambazwaji wake mwilini na pia utoaji wa mabaki ya

dawa mwilini. Baadhi ya vyakula huweza kuboresha ufyonzwaji na namna dawa inavyofanya kazi, na vingine huweza kupunguza. Hali kadhalika baadhi ya dawa huweza kuingilia ufyonzwaji wa virutubishi, matumizi ya virutubishi mwilini na utoaji mabaki mwilini. Tatizo hili linaweza kukabiliwa kwa kuepuka au kupunguza aina ya chakula kinachoingiliana na dawa hiyo mwilini, kuongeza kiasi cha chakula au kutumia virutubishi vya nyongeza ili kuongeza kiwango cha aina ya virutubishi vinavyoathiriwa na dawa hiyo.

Baadhi ya athari zitokanazo na dawa huweza kumfanya mgonjwa ashindwe kula chakula cha kutosha, pia kudhoofisha ufyonzwaji wa virutubishi mwilini. Kwa mfano, baadhi ya dawa husababisha kichefuchefu, mabadiliko ya ladha, kukosa hamu ya kula, kutapika, n.k. Baadhi ya athari hizi ni kama zile za matatizo ya kiafya yanayoambatana na kuambukizwa virusi vya UKIMWI au UKIMWI, hivyo zinaweza kukabiliwa kama ilivyoelekezwa hapo awali katika mada husika (Mada ya 6).

MODULE GFR4.indd 44 8/25/09 2:50:13 PM

37Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

Ushauri wa matumizi sahihi ya chakula na dawaJedwali na. 3 linaonyesha dawa mbalimbali, ushauri wa chakula na athari zinazoweza kujitokeza:

jedwali Na. 3 : Baadhi ya dawa, ushauri wa chakula na athari zinazoweza kujitokezajina la dawa Ushauri wa chakula Atharizinazowezakujitokeza

Rifampin - Itumiwe wakati tumboni hamna kitu yaani muda wa saa moja kabla ya kula au masaa mbili baada ya kula

- Usinywe pombe

Kichefuchefu, kutapika, kuharisha na kukosa hamu ya kula. Mabadiliko hayo yanaweza kuingiliana na kiasi cha foleti na Vitamini B

12

Isoniazid - Saa moja kabla au mbili baada ya kula.

- Usinywe pombe

Kukosa hamu ya kula, kuharisha.Inaweza kusababisha matatizo kama ikitumika na vyakula kama ndizi, pombe, parachichi, maini, samaki wakavu, yeast na mtindi, inaweza kuathiri umetaboli wa Vitamin B

6, kwa hiyo Vitamini B

6 ya nyongeza inahitajika

Fluconazole - Itumike na chakula Kichefuchefu, kutapika, kuharisha

Nystatin - Itumike na chakula Kuharisha kunakotokea ghafla, kutapika, kichefuchefu

Efavirenz(EFZ)

- Isitumiwe na chakula chenye mafuta mengi. Mafuta mengi huzorotesha usharabu wa dawa hii.

- Epuka pombe

Kiasi cha lehemu kwenye damu huongezeka, vipele, kizunguzungu, kukosa hamu ya kula, kichefuchefu, kutapika, kuharisha, kiungulia, tumbo kuuma na kuvimbiwa

Nevirapine (NVP)

- Kula kama kawaida (hakuna mwingiliano na chakula)

- Epuka pombe

Kichefuchefu, kutapika, vipele, kichwa kuuma, kuchoka, inflamesheni ya midomo, kusinzia, msisimko usio wa kawaida katika ngozi, sumu nyingi kwenye ini

Abacavir(ABC)

- Kula kama kawaida (hakuna mwingiliano na chakula)

- Epuka pombe

Kukosa hamu ya kula, kichefuchefu, kutapika, homa, mzio, tumbo kuuma, kuharisha, upungufu wa wekundu wa damu, vipele, kupungua kwa msukumo wa damu, matatizo katika kongosho, Kupumua kwa shida, ulegevu, kukosa usingizi, kikohozi, kichwa kuuma

Didanosine(ddl)

- Meza wakati tumboni hakuna chakula, yaani saa moja kabla ya kula au saa 2 baada ya kula, kwani chakula hupunguza ufyonzwaji wa dawa hii

- Epuka pombe- Isimezwe na juisi- Isimezwe na dawa zenye

“Aluminium” au “Magnesium”

Kichefuchefu, kuharisha, kukosa hamu ya kula, kutapika, kichwa kuuma, vipele, kinywa kukauka, kubadilika ladha, ulegevu, kukosa usingizi, kukosa choo, imflamesheni ya midomo, upungufu wa wekundu wa damu, homa, kizunguzungu, matatizo katika kongosho

Lamivudine(3TC)

- Kula kama kawaida (hakuna mwingiliano na chakula

- Epuka pombe

Kichefuchefu, kutapika, kichwa kuuma, kizunguzungu, kuharisha, tumbo kuuma, kikohozi, kuchoka, matatizo katika kongosho, kukosa usingizi, upungufu wa wekundu wa damu, misuli kuuma, vipele

MODULE GFR4.indd 45 8/25/09 2:50:13 PM

38 Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

Stavudine(d4T)

- Kula kama kawaida kwani hazina mwingiliano na chakula

- Epuka pombe

Kichefuchefu, kutapika, kuharisha, matatizo katika wa mfumo wa neva, homa, kukosa hamu ya kula, imflamesheni ya midomo, upungufu wa wekundu wa damu, kichwa kuuma, vipele, matatizo ya uboho wa mifupa, matatizo katika kongosho, huweza kusababisha matatizo ya umetaboli wa mafuta (lipodistrophy)

Zidovudine(ZDV/AZT)

- Ni vizuri zaidi ikimezwa bila chakula.

- Kama inasababisha kichefuchefu au matatizo ya tumbo inaweza kumezwa na chakula chenye mafuta kidogo

- Epuka pombe

Kukosa hamu ya chakula, kichefuchefu, upungufu wa wekundu wa damu, kutapika, matatizo katika uboho wa mifupa, kichwa kuuma, kuchoka, kukosa choo, kiungulia, homa, kizunguzungu, kupumua kwa shida, kukosa usingizi, misuli kuuma, vipele

Lopinavir(LPV)

- Kula kama kawaida.(hakuna mwingiliano na chakula)

- Epuka pombe

Tumbo kuuma, kuharisha, kichwa kuuma, udhaifu, kichefuchefu. Huweza kusababisha matatizo ya umetaboli wa mafuta (lipodistrophy) huweza kusababisha kisukari.

Nelfinavir(NFV)

- Itumike pamoja na chakula au asusa.

- Ikimezwa pamoja na vyakula au vinywaji vyenye uchachu husababisha dawa kuwa chungu.

- Epuka pombe

Kuharisha, kuvimbiwa, kichefuchefu, tumbo kuuma, vipele. Huweza kusababisha matatizo ya umetaboli wa mafuta (lipodistrophy)

Ritonavir(RTV)

- Inapowezekana itumike pamoja na chakula

- Epuka pombe

Kichefuchefu, kutapika, kuharisha, uambukizo wa ini, homa ya manjano, udhaifu, kukosa hamu ya kula, tumbo kuuma, homa, ugonjwa wa kisukari, kichwa kuuma, kizunguzungu. Huweza kusababisha matatizo ya umetaboli wa mafuta (lipodistrophy)

Saquinavir(SQV)

- Imezwe pamoja na chakula au asusa. Imezwe baada ya kula chakula chenye mafuta au madini ya chokaa kwani husaidia ufyonzwaji wa dawa hii

- Epuka kutumia vitunguu saumu kwa wingi

- Epuka pombe.

Vidonda vya kinywani, kubadilika ladha, kichefuchefu, kutapika, tumbo kuuma, kuharisha, kukosa choo, kuvimbiwa, udhaifu, vipele, kichwa kuuma, kukosa usingizi. Huweza kusababisha matatizo ya umetaboli wa mafuta (lipodistrophy)

Imetafsiriwa kutoka: FANTA, Food and Nutrition Implications of Antiretroviral Therapy in Resource Limited Settings. Academy for Educational Development, Washington DC, June 2003

Mambo muhimu ya kuzingatia

jina la dawa Ushauri wa chakula Atharizinazowezakujitokeza

MODULE GFR4.indd 46 8/25/09 2:50:14 PM

39Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

Kujua aina mbalimbali za dawa anazotumia mgonjwa. Kumsaidia mgonjwa kupanga utaratibu wa kumeza dawa na kula chakula kwa kuzingatia masharti ya dawa. Kumuhimiza kutumia maji kumeza dawa na si vinywaji kama juisi, soda, chai au kahawa. Kunywa maji safi na salama kwa wingi ili kuondoa mabaki ya dawa mwilini. Kumshauri aepuke kunywa pombe. Kumuhimiza mgonjwa kuzingatia muda wa kumeza dawa na kuendelea kuzitumia kama inavyoshauriwa hata

kama amepata nafuu ili kuepuka kuathiri matibabu au hali yake ya lishe.- Dawa ikielekezwa imezwe kabla ya kula au wakati tumboni hakuna chakula (tumbo tupu) ina maana imezwe

saa 1 kabla ya kula au saa 2 baada ya kula. - Dawa ikielekezwa imezwe wakati wa kula au wakati tumboni kuna chakula ina maana imezwe wakati wa kula

au katika muda wa saa 1 baada ya kula.- Dawa iliyoelekezwa kumezwa mara 3 kwa siku imezwe kila baada ya saa 8.- Mara 2 kwa siku imezwe kila baada ya saa 12.

Vilevile kumueleza mgonjwa kwamba si rahisi kuwa na ushauri wa matumizi ya dawa na chakula unaofanana kwa kila dawa.

Mgonjwa asaidiwe kukabiliana na athari mbalimbali za dawa k.m kichefuchefu, kutapika, kuharisha n.k. Mtumiaji wa dawa ahimizwe kuripoti tatizo lolote linalojitokeza kutokana na matumizi ya dawa fulani.

Mkufunzi aeleze washiriki kwamba mada hii ni kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kuwasaidia walengwa kutumia dawa kama inavyoshauriwa na kuwasaidia kukabiliana na baadhi ya athari za dawa kilishe na si kushauri walengwa kutumia dawa fulani. Iwapo kuna tatizo ni vyema watumie mbinu za kuwasiliana na mgonjwa kwa kutoa rufaa ili mlengwa aweze kumuona mtaalamu kwa ushauri zaidi.

HITIMISHONi muhimu kupata na kufuata maelekezo yanayotolewa na mtengenezaji wa dawa au daktari kuhusu matumizi ya dawa na chakula ili kuepuka kuathiri matibabu na lishe ya mgonjwa. Ikumbukwe kwamba si rahisi kuwa na ushauri wa chakula wa kufanana kwa dawa aina zote kwani mwingiliano kati ya dawa fulani na chakula huweza kutofautiana. Mtumiaji wa dawa ashauriwe kuchunguza na kuripoti hali mbalimbali au tatizo linapojitokeza ili kupata ushauri zaidi.

VI. NjIA ZA KUFUNDISHIA: Mhadhara na majadiliano, maswali na majibu.

VII. VIFAA VYA KUFUNDISHIA: Bango kitita/ubao, vitini, kalamu za kuchorea/chaki, gundi za karatasi, madaftari, kalamu, jedwali la dawa.

MODULE GFR4.indd 47 8/25/09 2:50:14 PM

40 Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

MADA YA 10

LISHE KWA WANAWAKE WAJAWAZITO NA WANAONYONYESHA

I. LENGO: Kuwawezesha washiriki kuelewa umuhimu wa lishe bora kwa wanawake wajawazito na wanaonyonyesha

II. MALENGO MAHUSUSI: Baada ya somo hili washiriki waweze:

Kueleza umuhimu wa lishe bora kwa wanawake wajawazito na wanaonyonyesha;•Kueleza matatizo ya kilishe yanayowapata wanawake wajawazito na wanaonyonyesha; na•Kujadili mikakati ya kuboresha hali ya lishe ya wanawake wajawazito na wanaonyonyesha.•

III. MAMBO YA KUjIFUNZA Umuhimu wa lishe bora kwa wajawazito na wanaonyonyesha;•Matatizo ya lishe yanayoweza kuwapata wajawazito na wanaonyonyesha; •Sababu za lishe duni kwa wajawazito na wanaonyonyesha;•Athari za lishe duni wakati wa ujauzito na kunyonyesha;•Mambo ya kuzingatia wakati wa ujauzito na kunyonyesha; na•Mahitaji maalumu kwa wanawake wajawazito walioambukizwa VVU•Mikakati ya kuboresha lishe ya wajawazito na wanaonyonyesha.•

IV. MUDA: Dakika 60

V. MUHTASARI WA MADA

UTANGULIZI Mwanamke anatakiwa awe na hali nzuri ya lishe kabla hajapata ujauzito, hii ina maana tangu akiwa mtoto mdogo. •Lishe bora itamsaidia kujengeka kwa maumbile yake hasa urefu na nyonga ambavyo vitamsaidia kuwa na uzazi salama na hatimaye kuweza kunyonyesha vizuri. Miezi miwili kabla ya kupata ujauzito ni vyema mama akajiandaa vizuri kilishe na kupata ushauri wa mtaalamu wa afya na lishe ili kutumia vidonge vya madini chuma kwa ajili ya kuongeza wekundu wa damu. Lishe na afya bora wakati wa ujauzito ni muhimu kwa mama mwenyewe na mtoto aliye tumboni na ni muhimu pia •wakati wa kunyonyesha.Wakati wa ujauzito na kunyonyesha mahitaji ya virutubishi mwilini huongezeka.•Lishe duni wakati wa ujauzito huweza kusababisha athari mbalimbali kwa mama na mtoto aliye tumboni.• Ongezeko la uzito wa kutosha wakati wa ujauzito ni muhimu sana kwani ni kiashiria cha lishe nzuri. Mama •anatakiwa aongezeke wastani wa kilo 12 kwa kipindi chote cha ujauzito. Sehemu ya akiba ya mafuta yatatumika kwa ajili ya ya kutengeneza maziwa katika miezi sita ya kwanza.

Umuhimu wa lishe bora kwa wanawake wajawazito na wanaonyonyeshaLishe bora husaidia:

Kuongeza uzito angalau kilo 12 wakati wa ujauzito. Uzito huongezeka wastani wa kilo moja kwa mwezi. •Kuzuia upungufu wa wekundu wa damu.•Kuboresha ukuaji na maendeleo ya mtoto wake.• Kuutayarisha mwili kwa ajili ya kunyonyesha. Mahitaji ya nishati na virutubishi wakati wa kunyonyesha ni makubwa •kuliko wakati wa ujauzito. Kupunguza uwezekano wa kujifungua kabla ya wakati, mtoto mwenye uzito pungufu, mtoto mwenye ulemavu au •mfu.

MODULE GFR4.indd 48 8/25/09 2:50:14 PM

41Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

Matatizo ya lishe duni yanayowapata wanawake wajawazito na wanaonyonyeshaMatatizo makubwa yanayowapata wanawake hao ni pamoja na upungufu wa wekundu wa damu, ukosefu wa madini joto na upungufu wa nishati na protini.

Upungufu wa wekundu wa damu wakati wa ujauzito ni moja ya sababu kubwa za vifo vya wanawake.•Ukosefu wa madini joto huweza kusababisha mimba kuharibika, kuzaa mtoto mfu, vifo vya watoto wachanga, •udumavu na utaahira kwa watoto.Utapiamlo wa nishati na protini husababisha mama kuongezeka uzito kidogo wakati wa ujauzito na watoto kuzaliwa •na uzito pungufu.

Sababu za lishe duniUlaji duni ambao hauzingatii ulaji wa chakula mchanganyiko na cha kutosha•Maradhi kama vile malaria na minyoo;•Kazi nyingi na nzito/kandamizi ambazo humkosesha mama muda wa kupumzika ikiambatana na ulaji duni, •hupunguza pia nguvu ya mwili wa mama, mama kutokuongezeka uzito na anaweza kushindwa kunyonyesha ipasavyo; Uzazi wa karibu karibu;•Ujauzito katika umri mdogo chini ya miaka 18;•Ufahamu mdogo kuhusu umuhimu wa lishe bora;•Mila na desturi potofu; na•Kipato duni.•

Athari za lishe duni wakati wa ujauzitoKuzaa mtoto mwenye uzito pungufu yaani chini ya kilo 2.5;•Udhaifu wa mwili;•Kuzaa mtoto kabla ya wakati;•Mimba kuharibika;•Matatizo wakati wa kujifungua kama vile kushindwa kuzaa;•Kuzaa mtoto mwenye akili taahira au mwenye ulemavu; na•Utengenezwaji duni wa maziwa ya mama baada ya kujifungua ambao husababisha lishe duni kwa mtoto.•

Mambo ya kuzingatia wakati wa ujauzito na kunyonyeshaKula chakula mchanganyiko na cha kutosha kinachopatikana kwenye mazingira husika (kula mlo kamili).•Kuongeza kiasi cha chakula katika mlo au kula milo midogo mara nyingi.•Kula asusa kati ya mlo na mlo.•Kula matunda na mboga-mboga kwa wingi katika kila mlo.•Kuzingatia usafi na usalama wa chakula na maji.•Kuepuka kunywa vinywaji vyenye kafeini kama chai, kahawa na baadhi ya soda pamoja na mlo, kwani huzuia •usharabu wa madini chuma na huweza kuchangia katika kuleta upungufu wa wekundu wa damu. Pale inapobidi ni vyema vinywaji hivi vitumike saa moja kabla ya kula au saa moja baada ya kula chakula.Kunywa maji ya kutosha kila siku angalau glasi 8 au lita 1.5.•Kuwa na muda wa kutosha kupumzika angalau saa moja wakati wa mchana.•Kuepuka unywaji wa pombe za aina zote, uvutaji wa sigara na matumizi ya madawa ya kulevya.•

Mahitaji maalumu kwa wanawake wajawazito walioambukizwa VVUWanawake wajawazito na wanaonyonyesha ambao wamepima na kuthibitika kuwa wameambukizwa virusi vya UKIMWI wanahitaji kushauriwa kuonana na wataalamu wanaohusika na kuzuia maambukizo ya virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Ni vyema wanawake hawa wahimizwe kuendelea kuhudhuria kliniki ili kupata ushauri wa kitaalamu.

Mikakati ya kuboresha hali ya lishe kwa wanawake wajawazito na wanaonyonyeshaKutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa lishe bora kwa wanawake wajawazito na wanaonyonyesha. •Kuzuia upungufu wa wekundu wa damu wakati wa ujauzito kwa kula vyakula vyenye madini chuma na Vitamini •C kwa wingi.Kuwahimiza wanawake kutumia dawa za kuongeza damu na kutumia chumvi iliyowekwa madini joto.•Kuwapunguzia wanawake kazi nzito na kandamizi. •

MODULE GFR4.indd 49 8/25/09 2:50:15 PM

42 Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

Kufuata uzazi wa mpango.•Familia na jamii iwajibike na ijue umuhimu wa kuwasaidia wanawake wajawazito na wanaonyonyesha kuwa na •hali nzuri ya lishe ili waweze kujifungua salama na kufanikisha unyonyeshaji.

HitimishoNi muhimu mwanamke kuwa na hali nzuri ya lishe kabla ya ujauzito, wakati wa ujauzito na wakati wa kunyonyesha. Mama mjamzito na anayenyonyesha ale chakula cha kutosha na cha mchanganyiko kutoka katika makundi yote ya vyakula. Matatizo yatokanayo na lishe duni yatatuliwe haraka ili kunusuru afya ya mama na mtoto.

VI. NjIA ZA KUFUNDISHIA: Mhadhara na majadiliano, maswali na majibu.

VII. VIFAA VYA KUFUNDISHIA: Bango kitita/ubao, vitini, kalamu za kuchorea/chaki, gundi za karatasi, madaftari, kalamu, kipeperushi cha Lishe Wakati wa Ujauzito na Kunyonyesha.

MODULE GFR4.indd 50 8/25/09 2:50:15 PM

43Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

MADA YA 11ULISHAJI WA MTOTO KATIKA HALI YA KAWAIDA

I. LENGO: Kuwawezesha washiriki kufahamu namna ya kumlisha mtoto katika hali ya kawaida

II. MALENGO MAHUSUSIMwisho wa mada hii washiriki waweze: Kueleza umuhimu wa maziwa ya mama kwa mtoto; na Kufahamu mbinu za kufanikisha unyonyeshaji.

III. MAMBO YA KUjIFUNZA Mapendekezo ya unyonyeshaji unaofaa Hali ya unyonyeshaji Tanzania Faida za kunyonyesha maziwa ya mama kwa mtoto na mama; Mbinu za kufanikisha unyonyeshaji wa maziwa ya mama.

IV. MUDA: Dakika 60

V. MUHTASARI WA MADA

UTANGULIZIKunyonyesha maziwa ya mama ni tendo la kumpa mtoto maziwa kutoka katika titi la mama moja kwa moja au kumnywesha mtoto maziwa ya mama yaliyokamuliwa kwa kutumia kikombe. Maziwa ya mama ni chakula na kinywaji pekee kinachotosheleza mahitaji ya mtoto tangu anapozaliwa mpaka anapotimiza umri wa miezi 6. Mtoto anapotimiza umri wa miezi 6 apewe vyakula vya nyongeza ili kukidhi mahitaji yake ya kilishe yanayoongezeka kadri anavyokua na aendelee kunyonyeshwa maziwa ya mama hadi atimize umri wa miaka miwili au zaidi.

Mapendekezo ya unyonyeshaji unaofaaIli mama na mtoto waweze kunufaika kikamilifu na faida za kunyonyesha ni lazima mama anyonyeshe ipasavyo. Inashauriwa mtoto:

Aanze kunyonya maziwa ya mama mara tu baada ya kuzaliwa katika saa moja ya kwanza;• Anyonyeshwe kila anapohitaji, usiku na mchana;• Anyonyeshwe maziwa ya mama pekee bila hata maji mpaka atakapotimiza umri wa miezi 6; • Aanzishiwe chakula cha nyongeza anapotimiza miezi 6; na • Aendelee kunyonyeshwa pamoja na kupewa chakula cha nyongeza mpaka atimize umri wa miaka 2 au zaidi.•

Hali ya Unyonyeshaji TanzaniaTakwimu za TDHS za mwaka 2004/2005 zinaonyesha:

Asilimia 98 ya wanawake hunyonyesha watoto wao;• Asilimia 59 huanza kunyonyesha (katika saa 1) ya kujifungua; • Asilimia 41 hunyonyesha maziwa ya mama pekee katika miezi 6 ya mwanzo;• Umri wa kuanzisha chakula cha nyongeza: •

- Chini ya miezi 2 asilimia – 7.5- Miezi 2-3 asilimia – 32.1- Miezi 4-5 asilimia – 58

Asilimia 91 ya watoto wanaonyonya wenye umri wa miezi 6-9 wanapewa chakula cha nyongeza. Takwimu hizi zinaonyesha kuwa pamoja na wanawake wengi kunyonyesha watoto wao hawanyonyeshi ipasavyo hivyo wanahitaji taarifa sahihi na msaada ili waweze kufanya hivyo.

MODULE GFR4.indd 51 8/25/09 2:50:15 PM

44 Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

Faida za kunyonyesha maziwa ya mama kwa mtoto na mamaKwa mtoto

Humpatia virutubishi kwa uwiano sahihi kwa ukuaji na maendeleo yake;• Humpatia kinga dhidi ya maradhi mbalimbali kama kuharisha na magonjwa ya njia ya hewa;• Huyeyushwa kwa urahisi na kufyonzwa na mwili kwa ufanisi; na• Huleta uhusiano mzuri na wa karibu kati ya mama na mtoto. •

Kwa mamaHusaidia tumbo la uzazi kurudi katika hali yake ya kawaida mapema;• Huchangia kuzuia upungufu wa wekundu damu kwa kuzuia utokaji wa damu kwa wingi baada ya kujifungua na • husitisha hedhi kwa muda;Huzuia uwezekano wa kupata ujauzito katika miezi 6 ya mwanzo;• Hupunguza uwezekano wa kupata saratani ya ovari na matiti; na• Humsaidia mama kurudia umbile lake la kawaida mapema.•

Faida nyingineNi safi na salama, hupatikana muda wote katika joto sahihi na hayahitaji matayarisho;• Hayaharibiki yakiwa ndani ya matiti. Yakikamuliwa hukaa saa 8 bila kuharibika katika joto la kawaida na saa 72 • kwenye jokofu;Gharama yake ni ndogo ukilinganisha na ile ya maziwa mbadala;• Huokoa muda wa mama na fedha za familia;• Huokoa fedha za kigeni (kununulia dawa na maziwa mbadala);• Hayaleti matatizo ya mzio; na• Hutunza mazingira kwani hayaachi mabaki kama makopo au chupa.•

Faida zote hizo zinatokana na virutubishi vilivyoko kwenye maziwa ya mama ambavyo ni maalumu kwa ukuaji bora na maendeleo ya mtoto.

Kielelezo Na. 6: Faida za Maziwa ya Mama

Maziwa ya Mama

• Yana virutubishi vinavyo-tosheleza mahitaji ya mtoto

• Huyeyushwa kwa urahisi na kutumika kwa ucanisi;

• Hukinga mwili dhidi ya maradhi

Kunyonyesha

• Huboresha mahusiano

• Huchelewesha kupata mimba nyingine

• Hulinda afya ya mama (LAM,PPH)

• Hupunguza uwezekano wa kupata upungufu wa wekundu wa damu

• Yana gharama ndogo kuliko maziwa mbadala

MODULE GFR4.indd 52 8/25/09 2:50:15 PM

45Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

Mbinu za kufanikisha unyonyeshaji wa maziwa ya mama

Ili mtoto aweze kunyonya kwa ufanisi ni muhimu apakatwe na kuwekwa kwenye titi kwa njia inayofaa.

Mkao wa mama Mama anaponyonyesha akiwa amekaa aegemeze mgongo wake kwenye kitu, kwa mfano kiti, ukuta au

tendegu la kitanda; na Kama atakuwa amelala anyonyeshe titi la upande alilolalia.

Mtotoanaponyonya Tumbo la mtoto lielekee tumbo la mama. Midomo ya mtoto igusishwe na chuchu. Mtoto akiachama

asogezwe haraka kwenye titi akilenga mdomo wa chini. Sehemu kubwa ya eneo jeusi linalozunguka chuchu liingie kinywani mwa mtoto kwani ndipo maziwa

yanapohifadhiwa.

Hakikisha unaona yafuatayo:1. Kichwa cha mtoto na mwili wake viko katika mstari ulionyooka;2. Uso wake uangalie titi la mama na pua yake iwe mkabala na chuchu;3. Mwili wa mtoto usogezwe karibu na mwili wa mama; na4. Iwapo ni mtoto mchanga sana, mama ashikilie makalio ya mtoto na sio mabega tu.

Anyonye taratibu na kugugumia na kupumzika katikati na unaweza pia kumsikia akimeza maziwa; Anyonye titi moja mpaka liishe maziwa au aachie mwenyewe ndipo apewe titi la pili. Kuachia titi ni dalili

kwamba mtoto amepata maziwa yote kutoka kwenye titi hilo na pia virutubishi vyote vya kukidhi mahitaji yote;

Mtoto anyonye mara kwa mara usiku na mchana kadiri anavyotaka, angalau mara 10 katika saa 24. Iwapo mtoto atahitaji kunyonya mara kwa mara ni kawaida na inaashiria kuwa mtoto anakua; na Kunyonyesha mara kwa mara husaidia mwili kutengeneza maziwa ya kutosha na pia huzuia matiti kujaa sana, • kuvimba na kuuma. Usiku mtoto alale karibu na mama ili iwe rahisi kumnyonyesha.

KielelezoNa.7:JinsiyaKumpakatanaKumwekaMtotokwenyeTitiAngalia michoro ifuatayo: Mtoto akiwa ananyonya anaweza kuwa amewekwa vizuri au hakuwekwa vizuri kwenye titi.

Dalili unazoweza kuziona vizuri ni: Mtoto yuko karibu na titi na uso wake umeelekezwa kwenye titi; Kinywa chake kimeachama kiasi cha kutosha; Mdomo wa chini umebinuka kwa nje; Kidevu chake kinagusa titi la mama; Mashavu yake ni ya mviringo; Sehemu nyeusi ya titi inayozunguka chuchu inaonekana zaidi juu ya kinywa cha

mtoto kuliko chini.

Kutambua dalili zinazoashiria mtoto hakuwekwa vizuri kwenye titi

Dalili unazoweza kuziona waziwazi ni: Kidevu cha mtoto hakigusi titi la mama; Midomo yake imeelekezwa mbele; Mashavu yake yamebonyea kwa ndani; Mtoto yuko mbali na mwili wa mama yake; Kinywa chake hakikufunguka kiasi cha kutosha, midomo yake imeelekea mbele; na Sehemu nyeusi ya titi inayozunguka chuchu iko sawa chini na juu ya kinywa cha

mtoto.

Mama anayenyonyesha mtoto kwa njia ya kawaida na akiwa

amempakatwa ipasavyo

Mtoto amewekwa vizuri kwenye titi

MODULE GFR4.indd 53 8/25/09 2:50:16 PM

46 Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

Uwekaji mbaya wa mtoto kwenye titi huleta madhara kwenye chuchu na huweza kumfanya mtoto asipate maziwa ya kutosha hivyo kuathiri ukuaji na maendeleo yake. Ni muhimu sana mtoto kupakatwa na kuwekwa vizuri kwenye titi.

HITIMISHO

Maziwa ya mama ndiyo chakula pekee kwa mtoto kwa miezi sita ya mwanzo kwani humpatia virutubishi vyote anavyahitaji kwa ukuaji na maendeleo yake pamoja na kumkinga dhidi ya maradhi mbalimbali. Kunyonyesha humpatia mama faida mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuzuia upungufu wa wekundu wa damu, kuzuia asipate mimba mapena na kupunguza uwezekano wa kupata saratani ya ovari na matiti. Mbinu sahihi zinahitajika ili mama aweze kunyonyesha ipasavyo.

VI. NjIA ZA KUFUNDISHIA:Mhadhara, majadiliano, maswali na majibu.

VII. VIFAA VYA KUFUNDISHIA: Bango kitita/ubao, vitini, kalamu za kuchorea/chaki, gundi za karatasi, vitini, michoro ya namna ya kumpakata na kumuweka mtoto kwenye titi.

VIII. Kazi ya kikundi Taja dalili tatu za kuonyesha mtoto amepakatwa vizuri. • Taja dalili tatu za kuonyesha mtoto hajapakatwa vizuri. • Taja faida nne za maziwa ya mama kwa mtoto.• Taja faida mbili za kunyonyesha kwa mama. •

Mtoto hajawekwa vizuri kwenye titi

MODULE GFR4.indd 54 8/25/09 2:50:16 PM

47Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

MADA YA 12ULISHAJI WA MTOTO KATIKA HALI YA MAAMBUKIZI YA

VIrUSI VYA UKIMWI

I. LENGO: Kuwawezesha washiriki kufahamu namna ya kumlisha mtoto katika hali ya kawaida na yule aliyezaliwa na mama

aliyeambukizwa Virusi vya UKIMWI.

II. MALENGO MAHUSUSI: Mwisho wa mada hii washiriki waweze: Kueleza njia za kuambukiza virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto; Kueleza ulishaji wa mtoto aliyezaliwa na mama aliyeambukizwa virusi vya UKIMWI; na Kueleza mambo ya kuzingatia kutegemea njia ya ulishaji aliyochagua mama.

III. Mambo ya kujifunza Njia za kuambukiza virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto:

- Wakati wa ujauzito;- Wakati wa uchungu na kujifungua;- Wakati wa kunyonyesha.

Mambo yanayochangia kuongezeka kwa hatari ya maambukizi ya VVU; Namna ya kumlisha mtoto aliyezaliwa na mama aliyeambukizwa virusi vya UKIMWI;

(a) Kunyonyesha maziwa ya mama:- Kunyonyesha maziwa ya mama pekee tangu mtoto anapozaliwa hadi miezi sita;- Kunyonyesha maziwa ya mama pekee kwa muda mfupi (chini ya miezi sita);- Maziwa ya mama yaliyokamuliwa na kupashwa moto;- Mambo ya kuzingatia wakati wa kutumia maziwa ya mama;

(b) Kutumia ulishaji mbadala- Maziwa yaliyotengenezwa maalumu kwa watoto wachanga;- Maziwa freshi ya wanyama kama ng’ombe au mbuzi yaliyorekebishwa;- Maziwa yenye mafuta maziwa yaliyokaushwa (dried full cream milk) au maziwa yaliyochevushwa yenye

mafuta (full cream evaporated); na- Mambo ya kuzingatia wakati wa kutumia maziwa mbadala.

Vyakula na maziwa yasiyofaa kumlisha mtoto mwenye umri chini ya miezi sita.

IV. MUDA: Dakika 60

V. UTANGULIZIVVU huweza kuambukizwa kupitia: Kubadilishana maji maji ya mwili ya mtu anayeishi na VVU, kama shahawa, maji maji au damu itokayo ukeni

wakati wa kufanya ngono isiyo salama; Kuongezewa damu ya mtu anayeishi na VVU; kutumia sindano zilizosibikwa; kuchangia vifaa vyenye ncha kali

kuchanja mwili au kutahiri; na Kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, wakati wa ujauzito, wakati wa uchungu na kujifungua au wakati wa

kunyonya maziwa ya mama.

Njia bora ya kuzuia maambukizi kwa watoto ni kuwasaidia wazazi wao kuepuka kuambukizwa VVU. Wajibu wa wanaume wa kulinda familia zao lazima usisitizwe.

MODULE GFR4.indd 55 8/25/09 2:50:16 PM

48 Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

Njia za maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto Takwimu za utafiti uliofanywa na Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI mwaka 2004/5 zimeonyesha kwamba • asilimia 8.7 ya wanawake wajawazito waliohudhuria kliniki ya uzazi walikuwa wameambukizwa VVU. Kwa kawaida sio wanawake wote walioambukizwa virusi vya UKIMWI huambukiza watoto wao. Inakadiriwa kuwa • kiasi cha asilimia 60 ya watoto wanaozaliwa na wanawake walioambukizwa virusi vya UKIMWI hawaambukizwi kabisa virusi vya UKIMWI hata kama hakuna hatua zozote zilizochukuliwa. Asilimia 30 hadi 40 ya watoto huambukizwa virusi vya UKIMWI ambapo:- Asilimia 5 – 10 ya watoto wanaambukizwa wakati wa ujauzito;- Asilimia 10 – 20 wanaambukizwa wakati wa uchungu na kujifungua; na- Asilimia 5 – 20 wanaambukizwa wakati wa kunyonyeshwa.

Kielelezo Na. 8: Uwezekano wa Maambukizi ya VVU Kutoka kwa Mama Kwenda kwa Mtoto kama HatuazaKuzuiaauKupunguzaMaambukizi(PMTCT)Hazikuchukuliwa

Wanawake 100 na Watoto wao

Ufafanuzi:Rangi ya zambarao wanaweza kupata maambukizi wakati wa ujauzito, uchungu na kujifungua (25%).Rangi ya manjano wanaweza kuambukizwa VVU wakati wa kunyonya maziwa ya mama (15%).Rangi ya kijani wanaweza wasipate maambikizi ya VVU hata kama hatua yoyote ya kuzuia haijachukuliwa (60%).

Kielelezo Na. 9: Uwezekano wa Maambukizi ya VVU Kutoka kwa Mama Kwenda kwa Mtoto kama Hatua za PMTCT Zimechukuliwa

Wanawake 100 na Watoto wao

Rangi ya zambarao wanaweza kupata maambukizi wakati wa ujauzito, uchungu na kujifungua (10%).Rangi ya manjano wanaweza kuambukizwa VVU wakati wa kunyonya maziwa ya mama (5%).Rangi ya kijani wanaweza wasipate maambikizi ya VVU (85%).

MODULE GFR4.indd 56 8/25/09 2:50:17 PM

49Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

Mambo yanayochangia kuongezeka kwa hatari ya maambukizi

Maambukizi mapya ya VVU Kama mwanamke akiambukizwa VVU wakati wa ujauzito au anaponyonyesha, atakuwa na kiasi kikubwa cha

virusi kwenye damu yake, hivyo mtoto wake anakuwa kwenye hatari kubwa ya kuambukizwa. Ni muhimu sana kumkinga mama asipate maambukizi ya VVU wakati huu kwa sababu mtoto atakuwa katika hatari kubwa ya kuambukizwa. Wanaume na wanawake wote wanapaswa kujua kwamba ngono isiyo salama inawaweka katika hatari ya kuambukizwa VVU. Wakati wa ujauzito au kipindi cha kunyonyesha ni muhimu wakazingatia ngono salama.

Makali ya maambukizi ya VVU Kama mama anaumwa kutokana na magonjwa yanayohusiana na maambukizi ya virusi vya UKIMWI au ana

UKIMWI, ana virusi vingi mwilini mwake hivyo ana uwezekano mkubwa wa kumwambukiza mtoto wake.

Maambukizi ya magonjwa ya kujamiana Mwanamke mwenye ugonjwa wowote wa ngono wakati wa ujauzito ana uwezekano mkubwa wa kuambukizwa

VVU na hivyo huweza kumwambukiza VVU mtoto wake wakati wa ujauzito, wakati wa kujifungua na kunyonyesha. Kugundulika na kutibiwa mapema kwa magonjwa haya kunaweza kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Uambukizo utokanao na ngono isiyo salama husababisha kulainika na kuchubuka kwa ngozi ya ukeni na hivyo kuongeza maji maji ya mwili katika njia ya uzazi.

Huduma na taratibu zinazofanyika wakati wa ujauzito na kujifungua Imeonekana kuwa kutumia taratibu ambazo zinaingilia mwili wa mama wakati wa kujifungua kama kuchana utando

na kuongeza njia ya uzazi inaongeza uwezekano wa mama kumwambukiza mtoto wake VVU. Inawezekana ni kwa sababu mtoto anagusana na damu na maji maji ya mama. Taratibu hizo zitumike pale tu inapolazimu ili kupunguza maambukizi ya VVU.

Urefu wa kipindi cha kunyonyesha Mtoto anaweza kupata maaambukizi ya VVU wakati wowote wa kipindi cha kunyonya. Watoto waliozaliwa na

wanawake walioambukizwa VVU na kunyonyeshwa kwa miaka miwili au zaidi wana uwezekano mkubwa zaidi wa kuambukizwa VVU kuliko wale wanaoachishwa kunyonya baada ya miezi michache.

Ulishaji unaochanganya maziwa ya mama pamoja na na vyakula au vinywaji vingine Kumlisha mtoto maziwa ya mama pamoja na vyakula au vinywaji vingine hata maji, hupunguza kinga dhidi ya

maradhi inayopatikana katika maziwa ya mama pekee. Vilevile, vyakula au vinywaji hivi huweza kudhuru mfumo wa chakula wa mtoto. Hali hii huweza kuruhusu VVU kuingia kwenye mwili wa mtoto kwa urahisi.

Hali ya matiti ya mama Vidonda kwenye chuchu, hasa kama chuchu inatoa damu, uvimbe wa titi au jipu la titi vinaweza kuongeza

hatari ya maambukizi ya VVU kupitia kunyonyesha. Uwekaji mzuri wa mtoto kwenye titi wakati wa kunyonyesha husaidia kuzuia matatizo hayo kutokea na pia huweza kupunguza uwezekano wa maambukizi ya VVU.

Hali ya kinywa cha mtoto Kinywa cha mtoto kikiwa na vidonda au vipele inakuwa rahisi kwa VVU kupenya kwa mtoto kupitia sehemu hizo.

Namna ya kumlisha mtoto aliyezaliwa na mama aliyeambukizwa VVU tangu anapozaliwa hadi miezi sitaInashauriwa kuwa katika miezi sita ya mwanzo ya maisha ya mtoto yeyote, maziwa ndiyo chakula pekee na ni muhimu sana. Kuna njia kuu mbili zinazoweza kutumika kumlisha mtoto aliyezaliwa na mama aliyeambukizwa virusi vya UKIMWI. Njia hizi ni kutumia maziwayamamaaukutumiaulishajimbadala. Ikumbukwe kuwa kila njia ina hasara na faida zake. Mama anahitaji msaada wa kitaalam kuweza kuchagua njia iliyo bora kwake.

MODULE GFR4.indd 57 8/25/09 2:50:17 PM

50 Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

1. Kunyonyesha maziwa ya mama Mama anaweza kunyonyesha mtoto wake maziwa yake pekee tangu mtoto anapozaliwa hadi miezi sita au

kunyonyesha maziwa yake pekee kwa muda mfupi (chini ya miezi sita) au kutumia maziwa yake yaliyokamuliwa na kupashwa moto. Ikumbukwe kupasha moto maziwa ya mama huua VVU vilivyomo kwenye maziwa bila kuharibu virutubishi vingi kwenye maziwa hayo.

• Mamboyakuzingatiawakatiwakutumiamaziwayamama- Kumnyonyesha mtoto kila anapohitaji, usiku na mchana;- Kumpakata na kumweka mtoto vizuri kwenye titi; - Kuhakikisha matatizo kinywani mwa mtoto yanatibiwa mapema;- Kuepuka kumpa mtoto vinywaji au vyakula vingine;- Kuomba msaada zahanati/kituo cha afya/hospitali iwapo kuna tatizo lolote;- Kumwachisha mtoto kunyonya endapo mama atakuwa na dalili za UKIMWI; na- Kufanya ngono salama.

2. Kutumiaulishajimbadala Maziwa mbadala yanayoweza kutumika ni pamoja na:

- Maziwa yaliyotengenezwa maalumu kwa watoto wachanga;- Maziwa freshi ya wanyama kama ng’ombe au mbuzi yaliyorekebishwa; na- Maziwa yenye mafuta maziwa yaliyokaushwa (dried full cream milk) au maziwa yaliyochevushwa yenye

mafuta (full cream evaporated milk). Inabidi mama kufanyiwa unasihi na kupewa taarifa za kutosha ili kuamua aina ya maziwa ambayo inafaa kwake

katika mazingira yake binafsi. Endapo mama atachagua ulishaji mbadala aelezwe kuhusu kuyamudu maziwa hayo; “kukubalika, kuwezekana, kumudu gharama, kuwa endelevu na salama” (AFASS – Acceptable, Feasible, Affordable, Sustainable, Safety).

• Mamboyakuzingatiawakatiwakutumiamaziwambadala- Mama atayarishwe kabla ya kujifungua kwa kuangalia jinsi ya kutengeneza maziwa aliyochagua kwa

vitendo na kisha kutengeneza maziwa mwenyewe mbele ya mnasihi. Apewe msaada au maelekezo iwapo yatahitajika.

- Katika wiki moja baada ya kujifungua, mama atembelewe na aombwe kutengeneza maziwa mbele ya mnasihi. Mama aelezwe kuwa anaweza kuomba ushauri au msaada wakati wowote.

- Mtoto apewe maziwa mbadala kwa kutumia kikombe.- Mtoto aonwe na daktari au mtaalamu wa afya kwa ajili ya ushauri kuhusu mikronutrienti za nyongeza.- Ulishaji mbadala lazima ukubalike, uwe unawezekana, familia imudu gharama, uwe enedelevu na salama. - Mama ashauriwe kuhusu uzazi wa mpango.

Vyakula na maziwa yasiyofaa kumlisha mtoto mwenye umri chini ya miezi sitaMaziwa yaliyotolewa mafuta • (skimmed milk) na yale yaliyopunguzwa maji na kuongezwa sukari (sweetened, condensed milk);Maji ya matunda au maji ya sukari;•Maziwa yaliyoganda (mtindi); na•Chai au uji. •

Taarifa ambazo zimewekwa kwenye mada hii ni za kumwezesha mtoa huduma kupata mwanga au kuelewa kwa kiasi hali hiyo ya ulishaji wa mtoto aliyezaliwa na mama aliyeambukizwa virusi vya UKIMWI. Ili kuweza kutoa huduma kamilifu kwa mama aliyeambukizwa virusi vya UKIMWI kuhusu kumlisha mtoto, mtoa huduma anahitaji mafunzo zaidi kama itakavyokuwa imeelekezwa na sekta ya Afya. Mtoa huduma ambaye hajapata mafunzo ya kutosha atahitaji kuwafahamu watoa huduma ambao wamepata mafunzo hayo ili waweze kushirikiana nao kutoa rufaa kwa mama ili apate huduma kamilifu.

MODULE GFR4.indd 58 8/25/09 2:50:17 PM

51Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

Mama aliye na dalili za UKIMWI hashauriwi kunyonyesha. Kwa wanawake ambao hawana virusi vya UKIMWI, wale ambao hawajui hali yao ya maambukizi na wale waliopima lakini hawakuchukua majibu; wote wanakuwa katika kundi moja la kushauriwa kumlisha mtoto kama kawaida na kufuata taratibu za kawaida za kunyonyesha.

Njia yoyote ambayo mama atachagua kutumia kumlisha mtoto, apewe msaada ili aweze kufanikisha njia hiyo kwa usahihi na usalama iwezekanavyo.

HITIMISHO

Kuna njia kuu mbili zinazoweza kutumika kumlisha mtoto aliyezaliwa na mama aliyeambukizwa virusi vya UKIMWI. Njia hizi ni kutumia maziwayamamaaukutumiaulishajimbadala. Ikumbukwe kuwa kila njia ina hasara na faida zake. Mama anahitaji unasihi na msaada wa kitaalam kuweza kuchagua njia iliyo bora kwake. Mama akichagua kunyonyesha asaidiwe kunyonyesha kwa usalama. Endapo mama atachagua ulishaji mbadala aelezwe kuhusu kuyamudu maziwa hayo; “kukubalika, kuwezekana, kumudu gharama, kuwa endelevu na salama”.

VI. NjIA ZA KUFUNDISHIA: Mhadhara na majadiliano, maswali na majibu, mazoezi kwa vitendo.

VII. VIFAA VYA KUFUNDISHIA: Bango kitita/ubao, vitini, kalamu za kuchorea/chaki, gundi za karatasi, madaftari, kalamu.

VIII. KAZI KWA WASHIRIKI: Taja njia mbili kuu za kumlisha mtoto aliyezaliwa na mama aliyeambukizwa VVU. Mambo gani ya kuzingatia ili kufanikisha ulishaji wa mtoto wake?

MODULE GFR4.indd 59 8/25/09 2:50:18 PM

52 Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

MADA YA 13

KUMLISHA MTOTO WA UMrI MIEZI 6 MPAKA 24I. LENGO: Kuwawezesha washiriki kutambua umuhimu wa kumwanzishia mtoto chakula cha nyongeza katika umri

unaotakiwa na kufahamu jinsi ya kumlisha mtoto mwenye umri wa miezi 6 – 24.

II. MALENGO MAHUSUSI: Mwisho wa mada hii washiriki waweze:

Kueleza ulishaji wa vyakula vya nyongeza; Kueleza umuhimu wa kumwanzishia mtoto chakula cha nyongeza katika umri unaofaa; Madhara ya kuwahi au kuchelewa kumwanzishia mtoto chakula cha nyongeza; Kujadili aina ya vyakula vinavyofaa kumpa mtoto; na Kueleza jinsi ya kumlisha mtoto.

III. MAMBO YA KUjIFUNZA Ulishaji wa vyakula vya nyongeza; Madhara ya kumwanzisha mtoto chakula cha nyongeza kabla ya kutimiza umri wa miezi 6; Vyakula vya nyongeza vinavyoweza kutumika; Jinsi ya kumwanzishia mtoto chakula cha nyongeza; Njia za kuboresha chakula cha mtoto; Jinsi ya kumlisha mtoto katika umri wa miezi 6 – 24; na Ulishaji shirikishi.

IV. MUDA: Dakika 60

V. MUHTASARI WA MADA

UTANGULIZIKatika miezi sita ya kwanza chakula cha mtoto ni maziwa tu. Mtoto anapotimiza umri wa miezi 6 anatakiwa kupewa vyakula vya nyongeza kwa vile maziwa pekee hayatoshelezi mahitaji ya mwili wake.

Ulishaji wa vyakula vya nyongeza Ulishaji wa vyakula au vinywaji vingine zaidi ya maziwa hujulikana kama ulishajiwavyakulavyanyongeza kwa

sababu vyakula hivyo ni nyongeza kwa maziwa ya mama au mengine. Vyakula vya nyongeza viwe vya kutosha na vyenye virutubishi vingi ili kumwezesha mtoto kukua kimwili na kiakili.

Kwa mtoto anayenyonya, maziwa ya mama humpatia mtoto nusu au zaidi ya mahitaji yake ya lishe katika miezi 6 - 12 na theluthi ya mahitaji hayo katika umri wa miezi 12 - 24. Hivyo, kama mtoto hanyonyi maziwa ya mama ni muhimu kumpatia maziwa ya aina nyingine mpaka atimize umri wa miaka miwili au zaidi.

Ni vigumu sana kutosheleza mahitaji ya lishe ya mtoto chini ya umri wa miaka miwili kwa kutumia vyakula vya nyongeza tu bila maziwa au aina nyingine ya chakula cha asili ya wanyama.

Madhara ya kumwanzisha mtoto chakula cha nyongeza kabla ya kutimiza umri wa miezi sitaIwapo mtoto ataanzishiwa chakula cha nyongeza kabla ya miezi sita madhara yafuatayo yanaweza kutokea:

Chakula hicho huchukua nafasi ya maziwa ya mama hivyo kusababisha mtoto akose virutubishi muhimu kutoka kwenye maziwa ya mama;

Mtoto huweza kupata utapiamlo endapo vyakula anavyopewa havina ubora kilishe kwa mfano uji mwepesi, maji ya mbogamboga, chai, michuzi ya nyama, maji yaliyowekwa rangi, sukari au ladha za matunda;

Uwezekano wa mtoto kupata maradhi ya kuhara huongezeka kwani vyakula hivi vinaweza visiwe safi na salama au kushindwa kuyeyushwa na mfumo mchanga wa tumbo la mtoto;

MODULE GFR4.indd 60 8/25/09 2:50:18 PM

53Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

Uwezekano wa mtoto kupata mzio huongezeka; na Uwezekano wa mama kupata mimba nyingine mapema huongezeka kama unyonyeshaji haukufanywa

ipasavyo.Athari za kuchelewa kumwanzishia mtoto (zaidi ya umri wa miezi 6) vyakula vya nyongeza

- Mtoto hatapata virutubishi vya kutosheleza mahitaji ya ukuaji; - Inapunguza kasi ya ukuaji na maendeleo ya mtoto; na- Mtoto atakuwa kwenye hatari ya kupata upungufu wa virutubishi na hatimaye utapiamlo.

Ni muhimu jamii kupewa taarifa sahihi kuhusu umri wa kumwanzishia mtoto chakula cha nyongeza ili watoto wakue wakiwa na afya njema.

Vyakula vya nyongeza vinavyoweza kutumikaNi muhimu kuvijua vyakula vinavyopatikana kwa urahisi katika sehemu husika ili kumsaidia mama kupanga mlo •wenye kutosheleza mahitaji ya kilishe ya mtoto wake.Mara nyingi vyakula vya nafaka mizizi na ndizi hutumika kutengeneza chakula cha nyongeza cha mtoto. Kwa •kawaida bei yake ni nafuu, hupatikana kwa urahisi, ni rahisi kutayarisha na watoto wengi wanavipenda. Hata hivyo, vyakula hivi pekee haviwezi kutosheleza mahitaji ya mwili kwa hivyo ni lazima viliwe kwa kuchanganya •na vyakula vingine ili kumpatia mtoto virutubishi vya kutosha. Vyakula vya nyongeza vitokane na mchanganyiko wa angalau chakula kimoja kutoka katika makundi yafuatayo: •

- Vyakula vya nafaka, mizizi na ndizi (km mahindi, mtama, uwele, ngano, ulezi, mihogo, viazi na ndizi za kupika);

- Vyakulavya jamiiyakundenavilevyenyeasiliyawanyama (kmmaharage,choroko,mbaazi,nyama, samaki, mayai, maziwa, dagaa, senene, kumbikumbi);

- Mboga-mboga (mchicha, matembele, kisamvu, figili, karoti);- Matunda (ubuyu, chungwa, papai, nanasi, parachichi);- Mafuta na sukari ( nazi, mbegu za mafuta kama za maboga, matango karanga, korosho, alizeti, asali na

sukari ya mezani).

jinsi ya kumwanzishia mtoto chakula cha nyongeza Chakula cha mtoto kiwa laini ila kisiwe chepesi sana Mtoto aanze kwa kupewa chakula cha aina moja katika kila mlo. Vyakula vya aina nyingi visichanganye kwa mara

moja. Hii itamsaidia mtoto kuzoea kwa urahisi chakula na kujua vyakula vinavyoweza kumletea mtoto uzito

Kielelezo Na. 10: Uzito na Ulaini wa Vyakula

Chepesiaumajimajisana Uzito unaofaa Chakula ambacho kina uzito wa kutomiminika kwa urahisi kutoka kwenye kijiko humpatia mtoto nishati zaidi.

Njia za kuboresha chakula cha mtotoKuna njia mbalimbali za kuweza kuongeza nishati na virutubishi vingine kwenye chakula cha mtoto ambazo ni:a) Nishati

- Tumia maji kidogo kutengeneza uji mzito;- Kaanga nafaka kabla ya kusaga;- Ongeza mafuta, mbegu za mafuta zilizopondwa, tui la nazi, sukari au asali;- Tumia vyakula vilivyochachushwa kama togwa na maziwa ya mgando; na- Tumia vyakula vilivyooteshwa kama uji wa kimea.

MODULE GFR4.indd 61 8/25/09 2:50:18 PM

54 Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

b) Madini chuma

- Nyama nyekundu ni chanzo kizuri cha madini chuma, hivyo ni muhimu chakula cha mtoto kiongezewe nyama;

- Pale ambapo nyama haipatikani, chakula cha mtoto kiongezwe mboga za majani zenye rangi ya kijani pamoja na matunda yale yenye Vitamini C kwa wingi; na

- Iwapo itahitajika mtoto apatiwe madini chuma ya nyongeza kwa ushauri wa daktari.

c) Vitamini A- Chakula cha mtoto kiongezwe mayai, dagaa, mboga za majani na matunda yenye rangi ya kijani na manjano

(maboga na viazi vya rangi ya manjano) na maziwa; na- Watoto wapelekwe kwenye vituo vinavyotoa huduma ya afya kupata matone ya Vitamini A kulingana na

utaratibu uliopo.

jinsi ya kumlisha mtoto wa miezi 6 – 24i) Kumlisha mtoto wa miezi 6 – 12

- Mtoto anapoanza kupewa chakula cha nyongeza anahitaji muda wa kuzoea ladha na mchanganyiko wa chakula;

- Anahitaji muda wa kujifunza kula. Kwa kuanzia, mtoto apewe vijiko 2 – 3 vya mezani mara mbili kwa siku;- Kila mara mtoto anyonyeshwe kwanza kabla ya kupewa chakula;- Mtoto anavyoendelea kukua aongezewe kiasi na mchanganyiko wa chakula taratibu mpaka atimize umri wa

miezi 12 ili aweze kumaliza kikombe au kibakuli cha ujazo wa mililita 250 kwa mlo mmoja; na- Kadri mtoto anavyokua na kujifunza kula anaendelea kuacha vyakula laini sana kwenda vyakula vilivyopondwa

hadi kufikia vyakula vyenye vipande vya kutafuna na hatimaye kula chakula cha familia.

ii) Kumlisha mtoto wa miezi 12 – 24

- Mtoto mwenye umri huu apewe vyakula vinavyoliwa na familia, vikatwekatwe au kupondwa kama ikibidi;- Apewe milo mitatu kwa siku pamoja na asusa mbili; na- Apewe kikombe au kibakuli cha ujazo wa mililita 250 kwa mlo mmoja.

Mtoto anayetumia ulishaji mbadala utaratibu wa kupewa chakula cha nyongeza ni huo uliojadiliwa awali. Ni muhimu apatiwe maziwa angalau mililita 500 kwa siku.

Ulishaji shirikishi- Matunzo na malezi ya mtoto yanajumuisha ulishaji, huduma ya afya, msaada wa kiakili na kisaikolojia ambayo ni

muhimukwaafya,ukuajinamaendeleoyamtoto. Haya yanategemea tabia na mwenendo wa mlezi na familia inayomlea. Wakati mzuri wa kuonyesha malezi mazuri ni wakati wa kumlisha mtoto. Ulishaji mzuri ni ulishaji shirikishi;

- Ulishaji shirikishi ni ule ambao mtoto anasaidiwa na kuhimizwa kula na mazingira ya kula ni ya furaha na upendo;

- Mwangalizi anapaswa kuwa makini wakati wa kumlisha mtoto;- Mtoto asilazimishwe kula iwapo ameshiba; na- Ni muhimu kuwaelimisha wanawake jinsi ya kuwalisha watoto wao kama ilivyo muhimu kuwaeleza nini cha

kuwalisha.

Mbinu za ulishaji shirikishi- Mlishe mtoto akiwa mwenye furaha na huku ukimhimiza kwa upendo;- Mlishe mtoto taratibu na kwa uvumilivu;- Jaribu kumlisha vyakula vyenye mchanganyiko, ladha nzuri na uzito tofauti;- Mpe chakula ambacho mtoto anaweza kushika na kula mwenyewe;- Punguza vivutio ambavyo vitamfanya mtoto asiendelee kula; na- Kuwa karibu na mtoto wakati wote wa kula na uwe makini.

MODULE GFR4.indd 62 8/25/09 2:50:18 PM

55Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

HITIMISHO

Kuanzia umri wa miezi sita, watoto wote wanahitaji kupewa vyakula vya nyongeza vinavyotokana na vyakula vya familia ambavyo vina nishati ya kutosha, vitamini na madini hasa madini chuma kwa ajili ya ukuaji na maendeleo yao. Maziwa pekee hayatoshelezi tena mahitaji ya lishe ya mtoto.Chakula cha nyongeza kiwe cha mchanganyiko uliotokana na makundi yote ya vyakula na kiwe cha kutosha kwa kuzingatia ubora, kiasi na idadi ya milo; kiasi na uzito wa chakula huongezeka kadiri mtoto anavyokua; na ulishaji shirikishi unahitajika ili kumpa mtoto moyo wa kula chakula cha kutosha. Ulishaji shirikishi unaweza kujenga uhusiano mzuri kati ya mzazi/au mlezi na mtoto.

VI NjIA ZA KUFUNDISHIA: Mhadhara na majadiliano, bungua bongo, maswali na majibu.

VII. VIFAA VYA KUFUNDISHIA:

Bango kitita/ubao, kalamu za kuchorea/chaki, vitini, madaftari, gundi za karatasi, kalamu, sampuli za vyakula vya madukani.

VII. KAZI KWA WASHIRIKI Jadili ulishaji wa watoto katika jamii husika na mbinu za kuboresha hali hiyo? Jadili mbinu mbalimbali zinazotumika kuboresha chakula cha mtoto katika jamii? Buni mlo wa siku nzima kwa mtoto mwenye umri wa:

- miezi 8 -11;- miezi 12 – 15; na- miezi 24.

MODULE GFR4.indd 63 8/25/09 2:50:19 PM

56 Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

MADA YA 14 HUDUMA ENDELEVU

I. LENGO: Washiriki waweze kuelewa huduma mbalimbali za kuboresha afya na maisha ya mtu aliyeambukizwa virusi vya

UKIMWI

II. MALENGO MAHUSUSI: Mwisho wa mada hii washiriki waweze kueleza:

Mahitaji mbalimbali ya watu walioambukizwa virusi vya UKIMWI; Mambo yanayojumuishwa katika huduma endelevu; Kanuni za msingi za huduma endelevu.

III. MAMBO YA KUjIFUNZA Umuhimu wa huduma endelevu; Baadhi ya mahitaji ya watu walioambukizwa na VVU; na Mambo yanayojumuishwa katika huduma endelevu.

IV. MUDA: Dakika 60

V. MUHTASARI WA MADA

UTANGULIZIKukiwa na muunganisho wa huduma zinazotolewa kati ya kituo cha huduma za afya na jamii, hali hii huongeza ubora, umuhimu, umiliki na ufanisi na kuweza kuwa na HUDUMA ENDELEVU. Unapotoa huduma ni muhimu kumwangalia mlengwa katika mahitaji yake yote kwa ujumla ili kuweza kumpa nafasi ya kusaidiwa na watu mbalimbali wanaotoa huduma. Hali hii huimarisha huduma na kuzuia matatizo yanayoweza kujitokeza. Kaya zilizoathirika na UKIMWI na watu walioambukizwa VVU wanahitaji mambo yafuatayo: - kisaikolojia, - kisosholojia, - kisheria, - matibabu,- matunzo, na- huduma na taarifa mbalimbali.

Ikumbukwe kuwa mahitaji haya hubadilika kutegemeana na hali ya mgonjwa. Huduma endelevu haiwezi kutolewa na mtu au taasisi moja hivyo ushirikiano na kufanya kazi kwa pamoja ni muhimu kuweza kutoa huduma kwa wakati na ubora unaotakiwa. Huduma endelevu hufanya kazi kwa ufanisi pale ambapo mfumo wa kutoa rufaa wadau wote wanafahamiana, wanafahamu aina ya huduma zinazotolewa, mahali ambapo huduma zinatolewa na anayezitoa, wakati gani zinatolewa na utaratibu mzima wa kufuata ili kupata huduma.

Umuhimu wa huduma endelevu Watu walioambukizwa VVU wana mahitaji tofauti ambayo ni muhimu. Mahitaji hayo hubadilika kadiri hali ya

ugonjwa inavyoendelea. Mahitaji muhimu ni pamoja na yale ya kisaikolojia, kijamii, kisheria, kitabibu na ya uuguzi.

Huduma zitolewazo zinalenga hasa katika kukidhi mahitaji ya mlengwa. Mahitaji hayo yanaweza kutokana na sababu za kimazingira au kijamii ambazo ni pamoja na unyanyapaa, ubaguzi, hofu/ woga, kukosa matunzo, umaskini, kutokuwa na uhakika wa chakula katika kaya. Mambo haya yanaweza kutokea katika jamii, sehemu za kazi au katika huduma za matibabu.

MODULE GFR4.indd 64 8/25/09 2:50:19 PM

57Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

Baadhi ya mahitaji ya watu walioambukizwa VVUHuduma za afya za msingi

- Mahitaji ya kifedha; - Ajira;- Mahitaji ya binafsi - chakula, sabuni, malazi, mavazi, matandiko, hifadhi; - Taarifa sahihi kuhusu masuala mbalimbali (ngono salama, uzazi wa mpango, lishe nk.);- Rufaa na usafiri;- Mahitaji ya kiroho na upendo (emotional);- Mwenzi (companionship);- Huduma za matibabu;- Usafi; na- Huduma za kisheria.

Mambo yanayojumuisha huduma endelevuHuduma za uuguzi na matibabu:•- Huduma za kupima hali ya uambukizo wa VVU (VCT); na ile ya kupunguza maambukizi ya VVU kutoka

kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT);- Huduma za tiba na kinga; - Tiba ya magonjwa nyemelezi na magonjwa ya ngono;- Tiba ya kupunguza makali ya UKIMWI (ART);- Huduma ya tiba za kupunguza maumivu yatokanayo na ugonjwa (palliative care);Huduma za kisaikolojia na kijamii; •Huduma za haki za binaadamu na kisheria; na•Huduma za kiuchumi na kijamii.•

Kanuni za msingi za huduma endelevuSikiliza• : Sikiliza mahitaji ya mlengwa na familia yake na wasaidie kupanga mikakati/ mipango yao ya baadaye. Heshima• : Heshima inayohusiana na haki za binadamu, maadili (ethics), usiri, ruhusa/ ridhaa , faragha na hadhi ya mtu. Usawa• : Huduma/matunzo yanayotolewa ni lazima yawe wanayoweza kumudu na yanayokubalika kiubora kwa watu wote bila kujali jinsi, jamii/ asili ya mtu (race), kabila au kipato. Ubora• : Huduma/matunzo lazima ziwe zenye ubora. Vigezo vya kuhakiki ubora wa huduma viwe muda wa kusubiri huduma, mtazamo (attitude) wa watoa huduma na aina ya vituo vya kutoa huduma vilivyopo. Upatikanaji• : Huduma za afya za aina zote ni lazima ziwe zinawafikia na kupatikana kwa watu wengi kadri inavyowezekana. Endelevu• : Uwezo wa kuanzisha huduma na matunzo utakuwa wa maana zaidi iwapo kanuni zake zitakuwa za kujitosheleza/kujitegemea na zikiwa zimewekwa katika mpango wa huduma ulio endelevu. Mpango huu unahitaji kutilia maanani masuala yote ya mahitaji ya kibinadamu, kiutaratibu na kifedha.

MODULE GFR4.indd 65 8/25/09 2:50:19 PM

58 Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

Ainayahudumazinazopatikanakatikajamii

KielelezoNa.12:AinayaHudumaZinazopatikanakatikaJamiiambazoWatuWalioambukizwaVVUWanawezaKuhitajiKupewaRufaa

Ni muhimu kwa watoa huduma kutambua asasi na mashirika katika jamii yanayotoa huduma kwa watuwalioambukizwa VVU ili kuweza kuwaunganisha walengwa na huduma hizo katika jamii husika. Mfano; msaada wa chakula, shughuli za kuinua kipato, msaada wa kisheria au wa kiroho n.k.

HITIMISHO

Watu walioambukizwa virusi vya UKIMWI wana mahitaji mengi ambayo yanatofautiana kulingana na hatua ya ugonjwa na hali ya familia. Huduma endelevu ni muhimu katika kukidhi mahitaji hayo ambayo yanaweza kuwa ni ya kimazingira au ya kijamii. Mtoa huduma anapaswa kufahamu mahitaji yote ya mlengwa na huduma zinazopatikana katika maeneo husika. Huduma hizo zinapotolewa kwa pamoja au katika muunganiko kati ya huduma moja na nyingine huongeza ufanisi katika kuboresha afya na maisha kwa walioambukizwa virusi vya UKIMWI.

VI. NjIA ZA KUFUNDISHIA:

Mhadhara na majadiliano, bungua bongo, maswali na majibu.

VII. VIFAA VYA KUFUNDISHIA:

Bango kitita/ubao, kalamu za kuchorea/chaki, vitini, madaftari, gundi za karatasi na kalamu.

MODULE GFR4.indd 66 8/25/09 2:50:19 PM

59Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

MADA YA 15MBINU ZA KUWASILIANA NA MLENGWA

I. LENGO: Washiriki waweze kuelewa stadi na mbinu mbalimbali muhimu za kuwasiliana na mlengwa

II. MALENGO MAHUSUSI: Mwisho wa mada hii washiriki waweze kueleza:

- Stadi za kuwasiliana na mlengwa;- Hatua za kuwasiliana na mlengwa

III. MAMBO YA KUjIFUNZA Stadi za mawasiliano; - Stadi za kusikiliza na kujifunza - Stadi za kujenga kujiamini na kutoa msaada

Hatua za kuwasiliana na mlengwa - Kujenga uhusiano kati ya mtoa huduma na mlengwa wake; - Kuchunguza tatizo linalomkabili mlengwa wake; na - Kutengeneza mkakati wa pamoja wa kutatua tatizo.

IV. MUDA: Dakika 60

V. MUHTASARI WA MADA

UTANGULIZIMtoa huduma anahitaji stadi za mawasiliano ili aweze kuhojiana na mlengwa na kujua jinsi anavyojisikia au kutambua matatizo yake na kumsaidia ili aweze kufikia uamuzi wa jambo la kufanya.

Mtoa huduma anatakiwa kujenga mahusiano mazuri na mlengwa wake ambayo ni msingi muhimu wa kuweza kumsaidia yeye na mlengwa wake kutambua na kutatua matatizo yanayomkabili. Mtoa huduma anatakiwa kupitia na kutumia hatua na mbinu mbalimbali za kujenga mawasiliano mazuri kati ya mtoa huduma na mlengwa wake.

Stadi za mawasiliano zinajumuisha stadi za kusikiliza na kujifunza na stadi za kujenga kujiamini na kutoa msaada.

(i) Stadi za kusikiliza na kujifunza Stadi ya 1: Tumia mawasiliano ya vitendo au ishara inayofaa Mawasiliano ya vitendo au ishara maana yake ni kuonyesha mtazamo kupitia vitendo, mwonekano au kutumia viungo vya mwili bila kuongea. Mtoa huduma anapoongea na mlengwa inabidi azingatie yafuatayo:- Kuketi usawa na mlengwa;- Kusikiliza kwa makini;- Kuondoa vizuizi;- Kutumia muda wa kutosha na mlengwa; na- Kumgusa mlengwa inavyokubalika.

Stadi ya 2: Uliza maswali yanayotoa mwanya wa kujieleza Ni muhimu kuuliza maswali kwa namna ambayo itamfanya mlengwa atoe maelezo. Hii inakusaidia usiulize maswali mengi na inakufanya ujifunze zaidi kutoka kwake kwa muda ulio nao. Maswali yanayohitaji majibu ya kujieleza kwa kawaida yanaanza na ”Ni jinsi gani?, Nini? Wakati gani? Wapi? na Kwa nini?”

Stadi ya 3: Tumia viitikio na ishara zinazoonyesha kuvutiwa na mazungumzo Kama unataka mlengwa aendelee kuongea, unapaswa kuonyesha kwamba unamsikiliza na unavutiwa na anachosema. Njia nzuri ya kuonyesha kwamba unasikiliza na unavutiwa na mazungumzo ni kwa vitendo, kwa mfano, kumwangalia,

MODULE GFR4.indd 67 8/25/09 2:50:20 PM

60 Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

kutingisha kichwa na kutabasamu au kwa kuitikia, kwa mfano unasema “Aha”, “Mmm”, “Oh, “Enhe”.Stadi ya 4: Kurudia maelezo ya mlengwaInasaidia sana kurudia maelezo aliyosema mlengwa. Inaonyesha kuwa unaelewa na itamfanya mlengwa aongee zaidi kile anachoona ni muhimu kwake. Ni vyema zaidi kurudia kwa maneno tofauti ili isionekane kwamba unamuigiza anachosema. Kama utaendelea kurudia mara kwa mara anachosema, inaweza kuleta hisia mbaya. Ni vyema kuchanganya yaani kurudia maelezo na viitikio vingine. Kwa mfano, “Ahaa?” au ”Ohoo”; au uliza maswali yanayotoa mwanya wa kujieleza.

Stadi ya 5: Onyesha kuwa unatambua hisia ya mlengwaMlengwa anaposema jambo fulani linaloonyesha anavyojisikia, ni vizuri kuitikia kwa namna ambayo inaonyesha kwamba umesikia alichosema na kwamba unatambua anavyojisikia. Kutambua jinsi mtu anavyojisikia ni tofauti na kuonyesha huruma. Unapoonyesha huruma, unasikitika na unaliangalia suala hilo kwa mtazamo wako. Inafaa pia kuonyesha unatambua hisia nzuri na sio hisia mbaya tu

Stadi ya 6: Epuka kutumia maneno yanayohukumuManeno ya kuhukumu ni kama ‘sawa’, ‘si sawa’, ‘nzuri’, ‘mbaya’, ‘vizuri’, ‘inatosha’, ‘sawasawa’. Kama ukitumia maneno yenye kuhukumu wakati unapozungumza na mlengwa, hasa wakati unauliza maswali, unaweza kumfanya ajisikie amekosa au ana tatizo. Kwa mfano: Usiseme: “unakula vizuri?” Badala yake sema: “kwa kawaida unakula nini?”

Wakati mwingine unaweza kuhitaji kutumia maneno ya kuhukumu, wakati unapomjengea mlengwa kujiamini. Hata hivyo jizoeze kutoyatumia maneno hayo kwa kiasi kikubwa, labda kukiwa na sababu muhimu ya kuyatumia. Unaweza kuona maswali ya kuhukumu mara nyingi ni yale yanayotoa majibu ya “ndiyo” au “hapana”. Kutumia maswali yanayotoa mwanya wa kujieleza mara nyingi husaidia kuepuka maneno ya kuhukumu.

(ii) Stadi za kujenga kujiamini na kutoa msaada

Stadi ya 1: Pokea mlengwa anachofikiri na kuhisiWakati mwingine mlengwa anafikiri jambo ambalo hukubaliani nalo, yaani ana wazo potofu au anafadhaishwa na jambo ambalo unajua sio tatizo kubwa. Kama hukubaliani naye, au ukamkosoa, au ukamwambia kuwa hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi unaweza kumfanya ajisikie kwamba anafanya makosa. Hii itapunguza kujiamini kwake na anaweza asitake kusema chochote tena kwako. Ni muhimu kuepuka kutokubaliana na mlengwa. Ni muhimu pia kutokukubaliana na wazo potofu la mlengwa. Ni vyema kutoa ushauri kuhusu kusahihisha wazo hilo potofu, lakini itakuwa vigumu kama umeishakubalina na wazo lake potofu. Badala yake unapokea tu kile mlengwaa anachofikiria au kuhisi. Kupokea kuna maana ya kusikiliza bila kukubali au kukataa.

Stadi ya 2: Tambua na sifu kile mlengwa anachofanya sahihi Kusifia matendo mazuri kuna faida zifuatazo:

- Kunamjengea mtu kujiamini;- Kunamtia moyo kuendelea na yale matendo mazuri; na- Kunamrahisishia kupokea ushauri baadaye.

Ni vyema kutambua mazuri anayofanya mlengwa badala ya kuangalia yale mabaya tu.

Stadi 3: Toa msaada kwa vitendoWakati mlengwa anapojisikia kuchoka, ana maumivu au kujisikia hana raha; akiwa na njaa au anasikia kiu; au anapokuwa na tatizo la wazi kabisa anahitaji msaada kwa vitendo. Msaada utolewe kumwezesha mlengwa kujisikia nafuu ili kufanya mazungumzo yawe katika mazingira yanayoridhisha.

Stadi ya 4: Toa maelezo machache na yanayofaa Toa maelezo machache, yanayofaa na kuhusiana na hali ya mlengwa ya wakati huo. Mweleze mambo ambayo anaweza kuyatumia kwa wakati huu na sio kwa wiki zijazo. Jaribu kutoa maelezo machache kwa wakati mmoja hasa kama mlengwa amechoka na amekwishapata ushauri kuhusu mambo mengi.

Stadi ya 5: Tumia lugha rahisi

MODULE GFR4.indd 68 8/25/09 2:50:20 PM

61Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

Wataalamu wanajifunza juu ya magonjwa na matibabu yake kwa kutumia maneno ya kitaalamu au kisayansi. Maneno hayo yanapozoeleka, ni rahisi kusahau kuwa watu wengine ambao siyo wa fani ya afya wanaweza wasielewe. Watoa huduma mara nyingi hutumia maneno haya ya kitaalamu wakati wanapoongea na wagonjwa ambao hawaelewi.

Stadi ya 6: Toa pendekezo moja au mawili na siyo amriUnaweza kuamua kuwa itamsaidia mlengwa iwapo atabadilisha jinsi ya kufanya jambo fulani, kwa mfano, kula milo midogo mara nyingi, au kuongeza kiasi cha mbogamboga anachokula. Unapaswa kuwa mwangalifu usimpe amri ya kufanya hayo mabadiliko. Hii haimsaidii yeye kujiamini. Inabidi upendekeze kitu ambacho anaweza kufanya. Yeye ataamua kujaribu au la. Hii inamwezesha kutawala hisia zake na kujiamini.

(iii) Hatua za kuwasiliana na mlengwa 1. Kujenga uhusiano Mtoa huduma anatakiwa kujenga mahusiano mazuri na mlengwa wake. Mtoa huduma anatakiwa kuwa

mchangamfu, kumtaja mlengwa wake kwa jina, kumjali na kumheshimu. Inashauriwa mahusiano baina ya mtoa huduma na mlengwa yawe na mipaka. Kila unapomtembelea mlengwa unatakiwa kumsalimia na kumjulia hali kwanza na sio kumuuliza una tatizo gani? Au unajisikiaje?

2. Kuchunguza tatizo Mtoa huduma anatakiwa kutumia mbinu mbalimbali za mawasiliano ili aweze kuelewa matatizo ya

mlengwa wake kwa kina au mambo mazuri anayofanya. Ni muhimu kwa mtoa huduma:

Kumtazama mlengwa wake usoni ili aweze kutambua mawasiliano ya vitendo na kusikiliza vizuri sauti • yake.Kumuuliza mlengwa maswali yaliyo wazi ambayo yanatoa mwanya wa kujieleza. Hii itamfanya mlengwa • aeleze zaidi na siyo kujibu ndio au hapana.Kutoa taarifa chache zinazoeleweka na kwa usahihi.• Kutumia lugha ambayo ni rahisi na inayoeleweka na mlengwa.• Kumjengea mlengwa kujiamini kwa kupokea kile mlengwa anachofikiri au kuhisi.• Kutambua na kusifu kile mlengwa anachofanya vizuri.• Kurudia ujumbe aliosema mlengwa kwa maneno mengine ili kufafanua na kuhakikisha ujumbe aliosema • mlengwa umeeleweka.Kutoa muhtasari wa taarifa aliyotoa mlengwa na pia taarifa alizompa mlengwa.• Kuonyesha kwa maneno au vitendo kuwa unalielewa tatizo la mlengwa bila ya kukumbwa na hisia. Kwa • mfano kama tatizo ni la huzuni mtoa huduma amueleze mlengwa kuwa anaona tatizo hilo ni la kuleta huzuni lakini asilie.Kumsaidia mlengwa maelezo yake yawe yanalenga tatizo na yanaendena na mada unayozungumzia.• Kuhakiki uelewa wa mlengwa kwa kumuuliza maswali kuhusiana na taarifa alizompa.• Kuepuka kutumia maneno yanayohukumu.• Kutoa mapendekezo badala ya amri. • Kutoa msaada kwa vitendo.• Kukubaliana na mlengwa siku ya kumtembelea tena.• Kumpa mlengwa nafasi ya kuuliza maswali.•

3. Kutengeneza mkakati wa pamoja Mtoa huduma amsaidie mlengwa kupanga namna atakavyotatua matatizo yake hasa yanayohusu kufuata ushauri

wa chakula. Kwa mfano, iwapo kuna ushauri umempa unaohusiana na ulaji wa chakula, jadiliana naye na msaidie namna atakavyotekeleza ushauri huo.

KUMBUKA Mgonjwa ni wa familia na jamii hivyo husisha wanafamilia katika majadiliano kuhusu ulaji na

matunzo ya mlengwa wako.

MODULE GFR4.indd 69 8/25/09 2:50:20 PM

62 Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

HITIMISHO Stadi za mawasiliano ni muhimu kwa ajili ya kujenga mahusiano kati ya mtoa huduma na mlengwa. Mawasiliano mazuri humwezesha mtoa huduma kutambua matatizo ya mlengwa wake na kumsaidia katika kuyapatia ufumbuzi. Wakati wa kuwasiliana na mlengwa mbinu mbalimbali hupaswa kutumika ikiwa ni pamoja na kumsikiliza na kujifunza kutoka kwake, kujiamini na kutoa msaada unaohitajika. Kwa hiyo, ni vyema mbinu hizo zikatumika katika kumsaidia mlengwa kupanga namna ya kutatua matatizo yake.

VI. NjIA ZA KUFUNDISHIA: Mhadhara na majadiliano, bungua bongo, maswali na majibu.

VII. VIFAA VYA KUFUNDISHIA: Bango kitita/ubao, kalamu za kuchorea/chaki, vitini, madaftari, gundi za karatasi na kalamu.

VIII. KAZI YA KIKUNDI

1. Mtoa huduma ajiandae kwa kukutana na mlengwa wake kwa mara ya kwanza. Mtoa huduma anajua kuwa mlengwa wake aliambukizwa VVU hivyo anatakiwa kumueleza umuhimu wa lishe bora na uhusiano wa lishe na VVU (athari za VVU kwenye lishe) kwa lugha rahisi atakayoelewa.

2. Mtoa huduma amueleze mlengwa faida za kuwa na lishe bora ili aweze kufanya mabadiliko/ marekebisho atakayomweleza iwapo yatahitajika.

Mtoa huduma ajiandae kukutana na mlengwa wake kwa mara ya pili. Ajadiliane naye kuhusu umuhimu wa kula mlo kamili.

Mtoa huduma ajadiliane naye pia kuhusu makundi ya vyakula. Amsaidie kutambua jinsi ya kupanga mlo kamili kwa kutumia vyakula vinavyopatikana kwa urahisi na vile vya asili au vilivyosahaulika. Ruhusu maswali na jibu mpaka mlengwa aridhike.

3. Mtoa huduma atumie stadi tulizojifunza kumshauri mgonjwa mwenye upungufu wa wekundu wa damu. Jadili kwa kina vyakula anavyoweza kutumia na afanye nini iwapo tatizo litazidi.

MODULE GFR4.indd 70 8/25/09 2:50:20 PM

63Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

MADA YA 16MTINDO BOrA WA MAISHA KWA AFYA

I. LENGO: Washiriki waweze kuelewa umuhimu wa kufuata mtindo bora wa maisha.

II. MALENGO MAHUSUSI: Mwisho wa mada hii washiriki waweze kueleza:

Umuhimu wa ulaji bora; Umuhimu wa mazoezi ya mwili katika kudumisha afya njema; Madhara yatokanayo na matumizi ya pombe, sigara na bidhaa nyingine za tumbaku na madawa ya kulevya.

III. MAMBO YA KUjIFUNZA Ulajibora

- Kula mlo kamili angalau mara tatu kwa siku; - Kuanza siku kwa kifungua kinywa;- Kula vyakula vya aina mbalimbali;- Kuchagua asusa zenye virutubishi muhimu;- Kuzingatia idadi na kiasi cha milo;- Kunywa maji ya kutosha; na- Kuzingatia taarifa na maelezo yaliyopo katika kifungashio (kasha, paketi) cha chakula. Kufanya mazoezi ya mwili Kuepukamatumiziyapombe Kuepukamatumiziyasigaranabidhaanyinginezatumbakunamadawayakulevya.

IV. MUDA: Dakika 120

V. MUHTASARI WA MADA

UTANGULIZIMtindo bora wa maisha ni ule unaozingatia kanuni bora za afya. Mtindo bora wa maisha ni muhimu ili kuendeleza afya ya mtu na kuzuia magonjwa yanayotokana na mtindo wa maisha usiofaa.

Mtindo bora wa maisha unahusisha ulaji bora, mazoezi ya mwili na kuepuka matumizi ya pombe, sigara na bidhaa nyingine za tumbaku na madawa ya kulevya.

Vifuatavyo ni baadhi ya vidokezo muhimu vya mtindo bora wa maisha:

Zingatia ulaji boraKula mlo kamili angalau mara tatu kwa siku•Ni muhimu kula mlo kamili ili kuwezesha mwili kupata virutubishi muhimu kwa ajili ya mahitaji ya mwili. Mlo wa asubuhi unakupatia nguvu ya kuanza siku na pia kuweza kukusaidia kufanya shughuli vizuri. Kumbuka kuanza siku kwa kifungua kinywa kilicho bora.

Kula vyakula vya aina mbalimbali•Ni muhimu kubadilisha aina ya vyakula hata vilivyoko katika kundi moja mara kwa mara kutegemeana na upatikanaji ili kupata virutubishi vyote muhimu kwa ajili ya lishe na afya bora. Kwa mfano; katika kundi la nafaka mizizi na ndizi, unaweza kubadilisha ugali, ndizi, viazi, mihogo, mkate na magimbi. Pia unaweza kubadilisha maharage, njegere, nyama, yai, maziwa, samaki, dagaa, njugu mawe, mbaazi na choroko. Mbogamboga na matunda pia huweza kubadilishwa. Kuwa mwangalifu, usile chakula chochote kwa wingi kupindukia. Jifunze kula kila chakula kwa wastani. Katika kila mlo chagua zaidi vyakula vya nafaka zisizokobolewa, vyakula vya jamii ya kunde, matunda na mbogamboga ambavyo huupatia mwili nguvu pamoja na vitamini, madini na makapi mlo. Zingatia vyakula vilivyoko katika msimu, kwani bei zake huwa nafuu na pia huwa ni freshi.

MODULE GFR4.indd 71 8/25/09 2:50:21 PM

64 Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

Chagua asusa zenye virutubishi muhimu•Asusa ni kiasi kidogo cha chakula ambacho sio mlo kamili, kinachoweza kuliwa bila ya matayarisho makubwa. Mara nyingi huliwa kati ya mlo mmoja na mwingine.

Kuwa mwerevu kwa kuchagua asusa zenye virutubishi muhimu kama tunda, maziwa, juisi halisi ya matunda, karanga, vyakula vilivyochemshwa au kuchomwa kama ndizi, mihogo, mahindi au viazi.

Epuka vyakula na asusa zifuatazo: - Zilizokaangwa au kupikwa kwa mafuta mengi kama sambusa, chipsi, vitumbua, mihogo, ndizi na kachori. - Zenye sukari kwa wingi kama biskuti, visheti, kashata, ubuyu wenye sukari nyingi, keki, chokoleti, juisi bandia,

barafu na soda. - Zenye chumvi nyingi kama krisps, bisi, soseji nk.

Zingatia idadi na kiasi cha milo•Inashauriwa kula angalau milo mitatu iliyo kamili na asusa zilizo bora kilishe kati ya mlo mmoja hadi mwingine. Kumbuka kuwa kiasi cha chakula katika kila mlo kiwe pia na wastani mzuri.

Kunywamajiyakutosha•Inashauriwa kunywa maji safi na salama ya kutosha baada ya mlo au kati ya mlo mmoja na mwingine. Wakati wa joto inashauriwa kunywa maji mengi zaidi. Inashauriwa pia kunywa vinywaji vingine kama madafu, togwa, juisi ya matunda halisi, matunda yenye maji mengi kama machungwa na matikiti maji.

Zingatiataarifanamaelezoyaliyopokatikakifungashio(kasha,paketi)chachakula•Mara nyingi vyakula vinavyotoka viwandani huwa vimewekwa katika vifungashio vya aina mbalimbali kama chupa, boksi, paketi na kopo. Ni vyema kusoma kwa makini maelezo yaliyopo kwenye kifungashio. Angalia kiwango cha virutubishi vilivyomo na mara nyingi kile kinachotajwa cha kwanza ndiyo kipo kwa kiasi kikubwa. Zingatia maelekezo kuhusu matumizi sahihi na muda wa mwisho kutumika.

Fanya mazoezi ya mwiliNi muhimu kufanya mazoezi ya mwili kila siku. Mazoezi husaidia kujenga misuli ya mwili na kuyeyusha chakula kwa urahisi ili kiweze kutumika mwilini kwa ufanisi. Inashauriwa kufanya mazoezi kila siku kwa angalau nusu saa. Hii inakufanya kuwa na afya njema, kukuwezesha kutumia kalori zilizozidi mwilini hivyo kuepuka unene uliokithiri. Mazoezi ya mwili pia husaidia mzunguko wa damu, hupunguza msongo na kupunguza uwezekano wa kupata shinikizo la damu na kisukari.

Yafuatayo yazingatiwe:Tenga muda wa kufanya mazoezi kama kucheza mpira, kukimbia au kutembea angalau kwa dakika 30 kila siku. •Pia shiriki kikamilifu na furahia somo la michezo.

Kielelezo Na. 12: Aina Mbalimbali za Mazoezi ya Viungo

MODULE GFR4.indd 72 8/25/09 2:50:25 PM

65Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

Kama unapanda ghorofa tumia ngazi badala ya lifti. Tembea badala ya kupanda gari kila wakati inapowezekana. Pia unaweza kufanya mazoezi mengine kama kuruka kamba, kuendesha baiskeli, kukimbia taratibu, kutembea na

shughuli mbalimbali kama kazi za bustani, kufyeka na kazi za nyumbani. Inashauriwa kupunguza muda wa kuangalia luninga na kutumia kompyuta, kukaa sana ofisini badala yake

kuongeza muda wa kufanya mazoezi.

Epuka matumizi ya pombeWatu wote wanashauriwa kuepuka unywaji wa pombe kwani haina virutubishi muhimu. Pombe huingilia uyeyushwaji wa chakula, ufyonzwaji na utumikaji wa virutubishi mbalimbali mwilini. Vilevile, pombe huweza kusababisha saratani hususan ya kinywa, koo na ini. Unywaji wa pombe unaweza pia kuchangia kuwa na ulaji usiofaa kwa kiasi kikubwa.

Epuka matumizi ya sigara na bidhaa nyingine za tumbaku na madawa ya kulevyaInashauriwa kutotumia sigara, tumbaku au ugoro kwa sababu matumizi ya vitu hivi huongeza hatari ya kupata magonjwa ya mfumo wa hewa na saratani hasa ya mapafu na koo.

Mambo mengine ya kuzingatia Ulajiboranamazoeziyaweyaburudani

- Furahia mazoezi ikiwezekana fanya na rafiki au familia yako.- Kula mlo kamili.- Kuwa na uthubutu wa kujaribu michezo mipya na shughuli mbalimbali ambazo ni salama.- Fanya mabadiliko taratibu ili kuboresha mtindo wa maisha.

Matumizi ya virutubishi vya nyongezaKinga ya mwili inapopungua, mahitaji ya virutubishi mwilini huongezeka. Hata hivyo, mahitaji hayo yanaweza kukidhiwa kwa kula chakula mchanganyiko. Mara chache mgonjwa huhitajika kutumia virutubishi vya nyongeza (nutrient supplements). Ni vizuri kupata ushauri wa daktari au mtaalam wa afya ili kufahamu ni aina gani inahitajika na kwa kiasi gani. Hata hivyo ikumbukwe kwamba:- Vipo virutubishi vya nyongeza ambavyo ni bora na vinavyoweza kupatikana kwa bei nafuu.- Virutubishi vya nyongeza visitumike badala ya chakula bali vitumike baada ya kupata mlo kamili.- Virutubishi vya nyongeza visichukuliwe kama dawa ya kutibu UKIMWI.

HITIMISHO Kutozingatia mtindo bora wa maisha ndiyo chanzo kikubwa cha maradhi mbalimbali yanayosumbua na kuathiri mfumo mzima wa maisha katika jamii. Hali duni ya lishe ambayo hutokana na ulaji usiozingatia ulaji bora, kutofanya mazoezi na matumizi ya pombe, tumbaku na bidhaa zake na madawa ya kulevya huchangia kwa kiasi kikubwa katika kudhofisha afya za wanajamii. Ili kuepukana na athari hizo, mtindo bora wa maisha ni muhimu na unapaswa kuzingatiwa katika hatua zote za maisha ya mwanadamu.

VI. NjIA ZA KUFUNDISHIA: Mhadhara na majadiliano, bungua bongo, maswali na majibu

VII. VIFAA VYA KUFUNDISHIA: Bango kitita/ubao, kalamu za kuchorea/chaki, vitini, madaftari, gundi za karatasi na kalamu

VII. KAZI YA KIKUNDI1. Jadili ni mambo gani katika ulaji bora ambayo mgonjwa wako anapaswa kuzingatia ili aweze kuwa na afya

bora?2. Je wagonjwa wote wanaweza kufanya mazoezi? Jadili mazoezi yanayowafaa wagonjwa walio katika hatua

mbalimbali.

MODULE GFR4.indd 73 8/25/09 2:50:30 PM

66 Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

MADA YA 17

WAJIBU WA MHUDUMU KATIKA KUTOA HUDUMA NA MATUNZO YA LISHE KWA WATU WALIOAMBUKIZWA

VIrUSI VYA UKIMWI

I LENGO: Kuwawezesha washiriki kutambua wajibu wao katika kutoa huduma na matunzo ya lishe kwa watu walioambukizwa

virusi vya UKIMWI katika jamii.

II. MALENGO MAHUSUSI: Mwisho wa mada hii washiriki waweze: Kueleza majukumu yao ya kuwahudumia watu walioambukizwa virusi vya UKIMWI katika masuala

yanayohusiana na lishe.

III. MAMBO YA KUjIFUNZA Majukumu ya watoa huduma katika masuala yanayohusiana na lishe.

IV. MUDA: Dakika 60

V. MUHTASARI WA MADA

UTANGULIZIWatoa huduma ni watu ambao wamekubalika katika jamii kutokana na sifa zao ili kutoa huduma mbalimbali kwa jamii husika. Watoa huduma kwa watu walioambukizwa virusi vya UKIMWI pia ni miongoni mwa wahudumu wa jamii. Ni muhimu kwa watoa huduma mbalimbali kutambua majukumu yao katika jamii husika na hivyo kuyatekeleza ipasavyo. Huduma hizi huweza kutolewa na watoa huduma wa afya au watoa huduma katika jamii.

Majukumu ya watoa hudumaBaadhi ya majukumu ya mhudumu katika kutoa huduma na matunzo ya lishekwa watu walioamukizwa VVU ni: Kutoa elimu kuhusu lishe na virusi vya UKIMWI kwa watu walioambukizwa VVU. Kutoa unasihi wa lishe kwa walengwa na familia zao kuhusu mlo kamili, athari za VVU kwenye lishe na umuhimu

wa ulaji bora kwa watu walioambukizwa VVU. Kuwezesha familia kuwa na ujuzi na mbinu za kuboresha chakula cha mtu aliyeambukizwa VVU. Kutoa elimu ya lishe kwa jamii. Kuwatambua walengwa wanaohitaji msaada na kuchukua hatua stahili. Kujenga mahusiano na walengwa ili kuweza kutambua matatizo yanayowakabili. Kutathmini hali za lishe za walengwa. Kusaidia jamii kupanga mlo kamili kwa kutumia vyakula vinavyopatikana kwa urahisi. Kuwa kiunganishi kati ya walengwa na serikali ya kijiji, uongozi wa mtaa n.k. Kutunza siri za walenga. kuwa mkweli na kufanya kazi kwa mipaka. Kutambua kaya zisizo na uhakika wa chakula na kutoa taarifa kwa serikali ya kijiji na wadau wengine. Kuwashauri wanawake wajawazito na wanaonyonyesha kuhusu umuhimu wa lishe bora. Kutambua huduma zinazopatikana katika jamii zinazolenga kuwasaidia watu walioambukizwa VVU. Kuhamasisha jamii kutumia mbogamboga na matunda kwa wingi. Kutoa mrejesho kwa shirika husika. Kuhamasisha kaya kuwa na uhakika wa chakula kwa kushirikiana na wataalamu wa kilimo: Kuzisaidia familia zenye matatizo zitumie fedha/chakula kwa uangalifu na kupata virutubishi muhimu.

MODULE GFR4.indd 74 8/25/09 2:50:30 PM

67Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

Mfano; matumizi ya chakula kwa kupika pombe, utumiaji wa vyakula visivyo na virutubishi kwa mahitaji ya mwili n.k.

Kuhamasisha matumizi ya matunda pori, vyakula na mboga za asili iwapo zinapatikana. Kuwasaidia walengwa kutumia dawa kama inavyoshauriwa na pia jinsi ya kukabiliana na athari za dawa kilishe. Kuhamasisha walengwa na jamii kutumia vyakula vinavyopatikana kwa urahisi katika mazingira yao. Kutoa rufaa kwa huduma husika kama vile matibabu, shughuli za kuinua kipato, n.k. Kuhamasisha jamii na familia katika kuhudumia watu walioambukizwa VVU kwa kushirikiana na serikali za kijiji na

kupiga vita unyanyapaa.

HITIMISHONi muhimu kwa watoa huduma kutambua wajibu wao katika kuwahudumia watu walioambukizwa VVU. Pia ni muhimu kutambua huduma zinazopatikana katika jamii zinazolenga kuwasaidia watu walioambukizwa VVU. Watoa huduma wanapaswa kuhudumia watu walioambukizwa VVU kwa moyo wa upendo na kwa ushirikiano na familia na jamii inayowazunguka. Jamii pia inapaswa itambue kuwa ina wajibu wa kuhudumia watu walioambukizwa VVU.

VI. NjIA ZA KUFUNDISHIA:Mhadhara na majadiliano, bungua bongo, maswali na majibu.

VII. VIFAA VYA KUFUNDISHIA: Bango kitita/ubao, vitini, kalamu za kuchorea/chaki, gundi za karatasi, madaftari na kalamu.

MODULE GFR4.indd 75 8/25/09 2:50:30 PM

68 Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

BIBLIOGRAFIA 1. Bijlsma, M., Living Positively: Nutrition Guide for People with HIV/AIDS, Muntare City Health Department,

Zimbabwe, Second Edition, 1997.

2. Bijlsma, M., Nutritional Care and Support for People with HIV: Review of Literature, Initiatives and Educational Materials in Sub-Sahara Africa, and Recommendations for Developing National Programmes. Report to FAO, July 2000.

3. Burgess, A. and others, Community Nutrition for Eastern Africa, African Medical and Research Foundation, Nairobi, Kenya; 1994.

4. COUNSENUTH, “Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI”: COUNSENUTH Information Series No. 2, Toleo la Pili, January 2000.

5. COUNSENUTH, Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI: “Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara”: COUNSENUTH Information Series No. 3, Toleo la Pili, March 200.

6. COUNSENUTH, Unyonyeshaji Bora wa Maziwa ya Mama: Vidokezo Muhimu kwa Jamii. June, COUNSENUTH Information Series No. 5, 2003.

7. FAO/WHO, Living Well with HIV/AIDS: A manual on Nutritional Care and Support for People Living with HIV/AIDS, Rome, 2002.

8. Food and Nutrition Technical Assistance (FANTA), Food and Nutrition Implications of Antiretroviral Therapy in Resource Limited Settings. Academy for Educational Development, Washington DC, June 2003.

9. Food and Nutrition Technical Assistance (FANTA), HIV/AIDS: A Guide for Nutrition, Care and Support. Academy for Educational Development, Washington DC, 2001.

10. Friis, H. “The Possible Effect of Micronutrients in HIV Infection. SCN News, United Nations Systems Forum on Nutrition, Number 17, December 1998.

11. IBFAN Africa, Infant Feeding Options in HIV/AIDS: Information for Health Workers. Mbabane, Swaziland, may 2002.

12. Ndungi, H.K., Food and Nutrition for Schools and Colleges, Nairobi, 1992.

13. NFTRC, (Botswana) Healthy Eating, is Shopping for Food and Food Safety Guidelines.

14. Sir Davidson S., Passmore R., Brock J.F., Truswell A. S. Human Nutrition and Dietetics; Seventh Edition. Wilture Enterprises, (International) Ltd. 1979.

15. The Network of African People Living in HIV/AIDS (NAP+). Food for People Living with HIV/AIDS, July 1996.

16. The United Republic of Tanzania, Ministry of Health. A National Guide on Nutrition Care and Support for People Living With HIV/AIDS, TFNC 2003.

17. Tull, A., Food and Nutrition, GCSE Edition, Oxford University Press, 1991.

18. UNICEF/UNAIDS/WHO/UNFPA, HIV and Infant Feeding: A Guide for Health Care Mangers and Supervisors, September 2003.

19. UNICEF/UNAIDS/WHO/UNFPA, HIV and Infant Feeding: Guidelines for Decision Makers, September 2003.

20. Anaemia Prevention and Control . What Works, Tools and Resources. The Population, Health and Nutrition Information. 2003

21. The Republic of Uganda, Nutritional Care and Support for PLHA: Guideline for Service Providers.

22. Nutrient Requirements for People Living with HIV/AIDS. Report of the Technical Consultation Geneva. 2003

23. Ulishaji wa Watoto Wachanga katika Maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI-Mwongozo kwa Mkufunzi: Draft 5

MODULE GFR4.indd 76 8/25/09 2:50:31 PM

MODULE GFR4.indd 77 8/25/09 2:50:31 PM

MODULE GFR4.indd 78 8/25/09 2:50:31 PM

MODULE GFR4.indd 79 8/25/09 2:50:31 PM

72 Mafunzo kwa Watoa Huduma (Mwongozo wa Mkufunzi)

Mwongozo huu umetayarishwa na:The Centre for Counselling, Nutrition and

Health Care (COUNSENUTH)United Nations Rd./Kilombero Str.

Plot No. 432, Flat No. 3P.O Box 8218, Dar es Salaam, Tanzania.

Tel/Fax: +255 22 2152705, Cell: +255 755 165112Email: [email protected]

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:Mkurugenzi Mtendaji

The Centre for Counselling, Nutrition and Health Care (COUNSENUTH)

ISBN 978 - 9987 - 9017 - 9 - 1

© COUNSENUTH, 2008

Kimefadhiliwa na:GLOBAL FUND ROUND 4 PROGRAM

Designed & Printed by:DeskTopProductionsLimited

P.O. Box 20936, Dar es Salaam, Tanzania.

MODULE GFR4.indd 80 8/25/09 2:50:34 PM