278
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Arobaini na Moja – Tarehe 3 Juni, 2019 (Bunge Lilianza Saa 3:00 Asubuhi) Spika (Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa tukae. Waheshimiwa Wabunge tunaendelea na Mkutano wetu wa Kumi na Tano leo ni Kikao cha Arobaini na Moja. Katibu. NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka wa fedha 2019/ 2020. SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango tunashukuru. Sasa naomba nimuite Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti kwa niaba yake Mheshimiwa Martha Umbulla tafadhali. MHE. MARTHA J. UMBULLA (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI): Taarifa ya Kamati ya Bajeti kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka wa

MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

  • Upload
    others

  • View
    2

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

1

BUNGE LA TANZANIA_________

MAJADILIANO YA BUNGE_________

MKUTANO WA KUMI NA TANO

Kikao cha Arobaini na Moja – Tarehe 3 Juni, 2019

(Bunge Lilianza Saa 3:00 Asubuhi)

Spika (Job Y. Ndugai) Alisoma Dua

SPIKA: Waheshimiwa tukae. Waheshimiwa Wabungetunaendelea na Mkutano wetu wa Kumi na Tano leo ni Kikaocha Arobaini na Moja. Katibu.

NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE:

HATI ZA KUWASILISHA MEZANI

Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:-

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO:

Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi yaWizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Naibu Waziri waFedha na Mipango tunashukuru. Sasa naomba nimuiteMwenyekiti wa Kamati ya Bajeti kwa niaba yake MheshimiwaMartha Umbulla tafadhali.

MHE. MARTHA J. UMBULLA (K.n.y. MWENYEKITI WAKAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI):

Taarifa ya Kamati ya Bajeti kuhusu utekelezaji wamajukumu ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka wa

Page 2: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

2

fedha 2018/2019 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusuMakadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwakawa fedha 2019/2020.

SPIKA: Ahsante Mheshimiwa Martha Umbulla.Naomba nimuite Msemeji Mkuu wa Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni kuhusu Wizara ya Fedha na Mipango, MheshimiwaMwambe tafadhali.

MHE. CECIL D. MWAMBE (K.n.y. MSEMAJI MKUU WAKAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KUHUSU WIZARA YA FEDHANA MIPANGO):

Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizaraya Fedha na Mipango kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

SPIKA: Ahsante sana. Katibu

NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE:

MASWALI NA MAJIBU

Na. 338

Kupeleka Walimu wa Hisabati na Sayansi Wilayani Mbinga

MHE. JOSEPH K. MHAGAMA (K.n.y. MHE. MARTIN A.MSUHA) aliuliza:-

Uhaba wa walimu wa Hisabati na Sayansi umeathirisana matokeo ya darasa la saba mwaka 2017 WilayaniMbinga.

Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka walimu wamasomo hayo Wilayani Mbinga?

SPIKA: Majibu ya Serikali, Naibu Waziri, TAMISEMI,Mheshimiwa Mwita Mwikwabe Waitara tafadhali.

Page 3: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

3

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA W. WAITARA) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa niaba ya Waziriwa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI naomba kujibu swali laMheshimiwa Martin Alexander Msuha, Mbunge wa MbingaVijijini kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, zipo sababu mbalimbalizilizopelekea kushuka kwa ufaulu wa wanafuzi wa darasa lasaba wa mwaka 2017 Wilaya ya Mbinga ikiwemo. Upungufuwa walimu, ushiriki hafifu wa wazazi husasani kufatiliamaendeleo ya watoto wao, utoro na nyingine nyingi. Walimuwa shule za msingi wanaoajiriwa wanaweza kufundishamasomo yote yaani Sanaa na Sayansi pamoja na Hisabati.

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wafedha 2017/2018 na 2018/2019 Serikali imeajiriwa walimu14,422 ambapo 10,695 ni walimu wa shule za msingi za 3,727ni walimu wa shule za sekondari. Halmashauri ya Wilaya yaMbinga imepatiwa jumla ya walimu 143 kati hayo walimu112 ni wa shule za msingi na walimu 31 ni wa shule zasekondari. Kati yao 28 ni wa Sayansi na Hisabati, mmojamasomo ya biashara na wawili ni walimu wa fasihi kiingereza(English Literature). Serikali itaendelea kuajiri walimu nakuwapanga kwenye Halmashauri hasa zenye upunugufu wawalimu kwa kadri ya upatikanaji wa fedha. Ahsante.

SPIKA: Mheshimiwa Mhagama swali la nyongezatafadhali.

MHE. JOSEPH K. MHAGAMA: Mheshimiwa Spika,ahsante kwa kupata nafasi ya kuuliza maswali mawili yanyongeza.

Kwa vile uhaba huu wa walimu kwa sehemu nyingineunachangiwa na kutokuwa na msawazisho sawa wa shulezetu mbalimbali hasa baina ya shule za mijini na vijiji na hivikusababisha shule za vijiji ziwe na walimu wachache zaidiukilinganisha na sehemu za miji. Ni lini sasa Serikali itakamilisha

Page 4: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

4

mchakato wake wa kuhakikisha kwamba kuna kuwa namsawazisho wa walimu ili uhaba au toshelevu wa walimuulingane mijini na vijijini?

Mheshimiwa Spika, pili, kwa vile tumeona vijana wengiwaliohitimu taaluma ya ualimu bado wapo mtaani kwamuda mrefu sasa na wengine zaidi ya miaka minne/mitanona bado Serikali inawekeza fedha nyingi kwenye kusomeshavijana hawa katika vyuo vyetu vikuu kwa nini sasa Serikaliisiangalie utaratibu mpya wa kusomesha vijana wetu kwakulingana kwa mahitaji ya soko la ajira na mahitaji ya Taifakatika ujumla wake na kuwawezesha vijana wetu wawezekuwekeza zaidi katika ujasiliamali? (Makofi)

SPIKA: Majibu Mheshimiwa Naibu Waziri, TAMISEMI.Kwa nini tusisomeshe idadi tunayoihitaji ya walimu?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA W. WAITARA): MheshimiwaSpika, namshukuru Mheshimiwa Mbunge kwa maoni namtazamo wake, lakini wiki iliyopita nilitoa taarifa kwenyeBunge lako tukufu kwamba tumepeleka fedha katikaHalmashauri zote ambazo kazi, moja, nikumalizia mabomaya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi,Walimu na Makatibu Tawala wa Mikoa kwambawahahakishe kwamba fedha hii inatumika kuwahamishawalimu ili moja, kuangalia kusambaza walimu katikaupungufu uliopo katika maeneo ya mjini ili waende maeneoya pembezoni; lakini la pili kuangalia zile hoja kwamba kunashule ina mwalimu kike haina mwalimu wa kiume au wakiumehaina wakike pia izingatiwe hilo. Kwa hiyo kazi inafanyikatunatarajia kwamba Wakurugenzi na viongozi wa mikoawatasimamia hili na Waheshimiwa Wabunge ni kwa sababuni sehemu ya mikoa yenu hili ni taarifa rasmi naombamtusaidie kusimamia.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili anasematufundishe wanafunzi wetu kulingana na mahitaji, juziMheshimiwa Waziri wa Nchi alitangaza matokeo ya form four

Page 5: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

5

na mojawapo ya kazi iliyofanyika ni kugawanya wanafunzikatika maeneo mbalimbali, sasa hili la kusema tuwekekulingana na idadi, ni kweli kwamba walimu wapo mitaanilakini ukweli kwamba tunahitaji walimu wengi katika sektazote shule ya msingi na sekondari.

Mheshimiwa Spika, sasa kwa sababu kila mwanafunziamelekwa mahali ambapo anahitaji, na tunatarajia kunashule za Serikali na watu binafsi lakini pia na shughuli binafsina tunaendelea kuangalia mchakato wa kuhakikishawanafunzi hawa badala ya kutegemea kuajiriwa na Serikaliambalo ni jambo la kitaifa kwa kweli ni lazima tuanzisheutaratibu wa watu kufanya kazi hata kwa shughuli binafsiyaani isiwe ile knowledge based, iwe ni competent. Kwa hiyotunalichukua tunafanyia kwa siku za usoni tutawezakulizingatia, ahsante.

SPIKA: Ahsante sana, Mbunge Mlimba MheshimiwaLimbweni uliza lako la nyongeza.

MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Spika, ahsantesana, matatizo ya walimu wa sayansi yameikumba sanaWilaya Kilombelo hususani jimbo la Mlimba karibuni ina shule26 za sekondari. Lakini hivi karibu tumepata walimu wa sayansiwanne tu na kupelekea shule nyingi za sekondari kukosawalimu wa sayansi.

Je, Serikali ina mpango gani kutupelekea walimu wasayansi Wilaya ya Kilombero husani jimbo la Mlimbaukizingatia tunakula samaki, kwa hiyo, watoto wana akili sanaya mahesabu na sayansi kwa mfano bora angalia tumemtoaMheshimiwa Likwelile alikuwa kule Wizarani tumemtoa BennoNdulu kwa hiyo sasa hivi tunakosa wasomi kwa sababuhatuna walimu wa sayansi. Ahsante.

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa, kumbe wanatokaMlimba hawa. (Kicheko)

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA W. WAITARA): Mheshimiwa

Page 6: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

6

Spika, ni kweli Mheshimiwa Mbunge ameuliza mara kadhaaswali hili tunamshukuru, lakini tumepeleka walimu wachachekulingana na mahitaji yaliyopo, lakini tumeomba kibali chakuajiri walimu wa kutosha mwezi huu wa sita au mwaka wafedha mpya ukianza. Kwa hiyo, pindi tutakapopata hichokibali Mheshimiwa Mbunge ndio maana nakuhakikishakwamba suala Mlimba na maeneo mengine yenye upungufumkubwa kama kwako kule tunazingatia maombi yakomuhimu. Ahsante.

SPIKA: Ahsante Mheshimiwa Bura bado tunaendeleana swali hilo hilo la upungufu wa walimu.

Na. 339

Upungufu wa Walimu Shule za Msingi Mkoa wa Dodoma

MHE. FELISTER A. BURA aliuliza:-

Mkoa wa Dodoma una mahitaji ya walimu 11,676 kwauwiano wa 1:40 kwa shule za msingi. Kwa sasa walimu walioponi 7,382 na hivyo kuwa na upungufu wa walimu 4,410 sawana asilimia 38.

Je, ni lini Serikali itaajiri mwalimu wa kutosha MkoaniDodoma?

SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Waziri,TAMISEMI Mwita Mwikabe Waitara kuhusu upunguvu wawalimu katika Mkoa wa Dodoma.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA W. WAITARA) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisiya Rais, TAMISEMI,naomba kujibu swali la Mheshimiwa FelisterBura, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, kamaifuatavyo:-

Page 7: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

7

Mheshimiwa Spika, Serikali imekuwa ikiajiri nakuwapanga walimu kwenye Halmashauri kwa awamu. Kwakipindi cha mwaka wa fedha 2017/2018 na 2018/2019 Serikaliimeajiri walimu 14,422 ambapo 10,695 ni walimu wa shule zamsingi na 3,727 ni walimu wa shule za sekondari. Mkoa waDodoma umepatiwa walimu 699 wa shule za msingi kati yawalimu 10,695 walioajiriwa wa shule za msingi. Serikaliitaendelea kuajiri walimu kwa awamu kwa kadri yaupatikanaji wa fedha.

SPIKA: Swali la nyongeza Mheshimiwa Buranimekuona.

MHE. FELISTER A. BURA: Mheshimiwa Spika, elimu yamsingi ni kumjengea mtoto uwezo wa kujua, wa kuelewa nawa kuendelea na maisha ya elimu na ujuzi katika siku zambele; na unapoacha kumpa mwanafunzi wa shule yamsingi mwalimu wa kumsaidia hata huko sekondari hawezikufanya vizuri.

Mheshimiwa Spika, tuliomba walimu 4,410 lakinitumepewa walimu 699 hata nusu ya kiwango tulichoombahatujapata; na hapo kuna walimu waliostaafu, waliotolewakwa vyeti fake, kuna wanaougua ambao wamesafishwa kwaajili ya kuugua. Walimu 699 hawakidhi mahitaji ya walimu washule za msingi na kutokana na ujio wa makao makuu kunauhitaji mkubwa sana wa walimu wa shule za msingi.

Serikali ina mkakati gani sasa wakuongeza walimu wakutosha katika mkoa wetu wa Dodoma?

Mheshimwa Spika, swali la pili, tuna walimu 203ambao wamestaafu ambao mahitaji yao ya fedhawanazotakiwa kulipwa ni shilingi milioni 260. Walimu hawatangu mwaka 2014 hajalipwa stahil i zao nawamekwishastaafu wapo nyumbani.

Ni lini sasa Serikali itawalipa walimu hawa 203 ambaowamestaafu wameshindwa kurudi kwao kutokana nakutolipwa stahiki zao?

Page 8: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

8

SPIKA: Hili la pili sijui la TAMISEMI au la Waziri wa Fedha.Majibu Mheshimiwa Naibu Waziri.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA W. WAITARA): MheshimwaSpika, ni kweli kwamba tulipata kibali cha kuajiri walimu 4500lakini uhitaji wa walimu wa shule za msingi ni zaidi 66,000; uhitajiwa walimu wa sekondari ni zaidi ya 14,000; walimu 3,088tuliwapeleka shule za msingi na walimu waliobaki ndiotulipeleka sekondari. Kwa hiyo katika hesabu hiyo katika haliya kawaida lazima kutaendelea kuwa na upungufu na kunaHalmashauri na shule nyingine hazikupata walimu kabisa, huondio ukweli.

Mheshimwa Spika, lakini kama nilivyosema kwenyeswali lililotangulia tuliomba kibali cha kuajiri walimu tukipatakibali hicho tunaongeza walimu lakini tutapeleka maeneoambayo wana uhitaji makubwa ikiwepo na Mkoa waDodoma.

Mheshimwa Spika, swali la pili anauliza walimuwastaafu; malipo ya stahiki za walimu ziko za aina mbili, kunamalipo yanayolipwa na Halmashauri zetu lakini pia kunamalipo ambayo yanatoka katika Serikali Kuu. Katika Mkoawa Dodoma amezunguzumza walimu 203 lakini sisi tunajuakwamba tuna walimu hapa 599 katika Mkoa huu ambaowamestaafu na wadai fedha zaidi ya shilingi milioni 652. Lakinimadi yalipokuja TAMISEMI yamerudishwa kule kwa mambomanne.

Moja, ni kwamba madai hayo pia yanabidiyahakikiwe kamati za ukaguzi za mikoa na halmashaurihazikufanya hivyo; lakini jambo la pili kwa mfano nauli zawalimu inabidi Wakurugenzi walipe. Wakurugenzi hawakuwawameonesha wana mkakati gani wa kulipa walimu wastaafufedha kutoka kwenye mipango ambayo ni maelekezo yaSerikali; lakini jambo la tatu ni lazima fedha hizo baadhi yawatumishi waliomba wameletwa kwamba wadai wenginewanastaafu mwaka 2019 yaani mwaka Juni kimsingi walikuwahawajastaafu. Sasa tulipoangalia namna ya ukokotoaji wa

Page 9: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

9

zile nauli kwamba nani analipwa nini kutoka wapi kwendailikuwa imekosewa.

Mheshimwa Spika, kwa hiyo tukarudisha madai hayokatika viongozi wetu wa Mikoa na Halmashauri wayafanyiekazi tutawasiliana na Wizara ya Fedha, ukweli ni kwambawataafu wa Serikali wakiwemo na walimu baada ya kufanyakazi kubwa kutumikia taifa hili kwa unyenyekevu mkubwa nauaddilifu mkubwa ni lazima walipwe stahiki zao.

Kwa hiyo, naomba kwa Wakurugezi wahakikishekabla ya kuleta madai ni lazima wahayahakiki ili kondoausumbufu ambao walimu wetu na wastaafu wenginewanaupata, ahsante.

SPIKA: Ahsante upungufu huo mkubwa mno katika hii4000 Halmashauri tisa sijui za Dodoma hapa 1000 plus niKongwa peke yake. Kwa hiyo mnapogawa ni vizuri kuangaliauwiano ili..., vinginevyo baadhi ya Wilaya zinaumia sanamaana ugawaji unafanyika juu moja kwa moja.

Tunaenda Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia swalila Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa nil ikuonaMheshimiwa Kisangi kwa niaba yake.

Na. 340

Chuo cha Ikwiriri Kuwa VETA

MHE. MARIAM N. KISANGI (K.n.y. MHE. MOHAMED O.MCHENGERWA) aliuliza:-

Serikali imerejesha vyuo vilivyokuwa vya maendeleokuwa chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Je, Serikali haioni umuhimu wa kukibadili Chuo chaMaendeleo Ikwiriri FDC kuwa VETA ili kubadili fikra zawananchi wa Rufiji, Kibiti na Ikwiriri na hatimaye kuletamwamko wa elimu?

Page 10: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

10

SPIKA: Majibu ya swali hilo Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia, Mheshimiwa William OleNasha.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIAalijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa ElimuSayansi na Teknolojia napenda kujibu swali la MheshimiwaMohamed Omary Mchengerwa, Mbunge wa Rufiji kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, elimu ya ufundi na mafunzo ufundistadi hutolewa katika shule na vyuo katika viwango namadaraja mbalimbali kulingana na malengo yake. Katikangazi ya shule za sekondari, elimu ya ufundi hutolewa ilikumuandaa mwanafunzi kujiunga na vyuo vya ufundi stadina ufundi wa kati. Vyuo vya elimu ya ufundi na mafunzo yaufundi stadi huandaa mafundi mchundo na vyuo vya ufundiwa kati huandaa mafundi sanifu. Aidha, vyuo vikuu hundaawahandisi katika fani mbalimbali zinzohusiana na ufundi.

Mheshimiwa Spika, Vyuo vya Maendeleo yaWananchi vilianzishwa kwa lengo la kumsaidia wananchikubaliana na changamoto za kimaendeleo katika mazingirayake kwa kumapatia maarifa na stadi anuwai. Vyuo hivihutoa elimu ya ufundi stadi katika hatua ya kwanza hadi tatatu. Pia mafunzo ya ujasiliamali, kilimo, uvuvi, mifugo n.khutolewa kulingana na mahitaji ya eneo husika.

Mheshimiwa Spika, kwa sasa Serikali haina mapangowa kuvibadili Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi kuwa VETA.Badala yake, Serikali imejikitia katika viboresha vyuo hivyokwa kuvikarabati na kuviongezea vifaa vya kuviongezeavifaa vya kujifunzia na kufundishia ili viweze kutoa mafunzobora zaidi. Awamu ya kwanza ukarabati wa Vyuo vyaMaendeleo ya Wananchi 20 ipo katika hutua za mwisho zaukamishaji awamu ya pili inataraji kuanza mapema mweziJuni, 2019. Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Ikwiriri kilikuwakatika awamu ya kwanza na ukarabati umekamilika. Aidha,katika mwaka wa fedha 2019/2020 Rufiji n miongoni mwa

Page 11: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

11

Wilaya zilizotengewa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Chuo chaUfundi stadi cha Wilaya cha VETA.

SPIKA: Mheshimiwa Mariam Kisangi uliza swali lanyongeza.

MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Spika, ahsantesana kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuuliza maswali yanyongeza.

Kwa kuwa wananchi wa Rufiji wamekuwa na shidakubwa kupata Chuo cha VETA rufiji, pamoja na juhudu zaMbunge wao kupambana kutafuta jinsi gani ya kupata Chuocha VETA ndio sababu akaona hata kuna haja kubadilishavyuo vya FDC labda wanafunzi wa Rufiji waweze kupataelimu hiyo ya VETA, na Kwa kuwa Serikali sasa imeshatengafedha kwa ajili ya ujenzi wa VETA - Rufiji ni jambo la shukranina pongezi sana kwa Serikali, je, Serikali sasa ni lini ujenzi huoutaanza rasmi.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, Kwa kuwa katika Mkoawa Dar es Salaam kuna Chuo kikubwa sana cha VETAKipawa, chuo hiki ni kikubwa mno, lakini hatujawahi kuonamatangazo mbalimbali juu ya elimu inayotelewa hapo au nimwaka gani wa mafunzo ambao unaanza lini na liniwanafunzi waweze kuhamasika kujiunga na Chuo cha VETAKipawa?

Je, Serikali ina mpango gani sasa wa kukitangaza hikiChuo cha VETA Kipawa ambacho Serikali imewekeza fedhanyingi sana na chuo ni kizuri mno, ili wanafunzi kutoka maeneombalimbali waweze kujiunga na chuo hiko?

SPIKA: Majibu ya maswali hayo, Mheshimiwa NaibuWaziri Elimu.

NAIBU WAZIRI ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Spika, kuhusiana na lini ujenzi wa Chuo cha VETAcha Rufiji kitaanza, naomba nimhakikishie MheshimiwaMbunge kwamba fedha zimetengwa katika mwaka wa

Page 12: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

12

fedha unaokuja na fedha hizo zipo, kwa hiyo, siyo za kutafuta.Kwa hiyo, ujenzi utaanza mara moja, Rai yetu kwaHalmashauri ya Wilaya ya Rufiji ni kwamba watupatie eneolenye hati ili ujenzi uanze bila kuchelewa.

Mheshimiwa Spika, lakini pia swali lake la pili kuhusianana Chuo cha VETA Kipawa, naomba nimhakikishieMheshimiwa Mbunge kwamba VETA nchi nzima kawaidainakuwa na utaratibu wa kutangaza nafasi za masomo katikavyuo vyake vyote lakini kama Mheshimiwa Mbunge anaonahaitoshi katika Chuo cha Kipawa naomba nitumie fursa hiikumuagiza Mkurugenzi Mkuu wa VETA ahakikishe kwambamatangazo yale yanatolewa na aongeze kasi na wigo wakutangaza nafasi mbalimbali za VETA zote nchini.

SPIKA: Nimekuona Mheshimiwa Mbunge uliza swalilako tafadhali.

MHE. DEOGRATIAS F. NGALAWA: Mheshimiwa Spika,ahsante kwa kunipa fursa ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, Chuo cha VETA Ludewa kilipaswakiwe kimeshakamilika toka mwaka jana mwezi wa nane, lakinimpaka leo hivi ninavyozungumza Chuo cha VETA kile Ludewahakina dalili na mkandarasi hayupo. Je, ni lini Chuo cha VETALudewa kitakamilika? (Makofi)

SPIKA: Majibu ya swali hilo la Mheshimiwa DeogratiasNgalawa, Mbunge wa Ludewa tafadhali.

NAIBU WAZIRI ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Spika, naomba kwanza nitumie nafasi hii kukirina kuweka wazi kwamba Mheshimiwa Deogratias Ngalawaamekuwa akifuatilia sana ujenzi wa Chuo cha Ludewa auChuo cha VETA Mkoa wa Njombe.

Mheshimiwa Spika, uchelewaji wa ujenzi wa chuohusika umetokea kwa sababu mkandarasi ambaye alipewakazi ya kujenga chuo kile alifanya madudu na Serikali ilibidikusitisha mkataba. Kwa sasa tayari mfadhili wa mradi ambaye

Page 13: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

13

ni Benki ya Maendeleo ya Afrika tayari ameshatupa ruhusaya kutangaza kandarasi upya. Kwa hiyo, kwa sasa tupo katikahatua za kumpata mkandarasi mpya ili ujenzi uwezekuendelea.

Kwa hiyo, naomba nimhakikishie MheshimiwaMbunge kwamba ujenzi utaanza mara tu Mkandarasi mpyaatakapopatikana na hatutegemei ichukue tena muda mrefu.

SPIKA: Ahsante. Waheshimiwa Wabungetunaendelea na Wizara ya Maji, swali la Mheshimiwa EsterAmos Bulaya Mbunge wa Bunda Mjini, naona MheshimiwaEster hayupo. Nani nimemuona sijui Mheshimiwa Getere aunani yule, Mheshimiwa Sware uliza swali. (Makofi/Kicheko)

Na. 341

Upatikanaji wa Maji Safi na Salama

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI (K.n.y. MHE. ESTER A.BULAYA) aliuliza:-

Jimbo la Bunda Mjini ni miongoni mwa majimboyanayokabiliwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wamaji safi na salama?

(a) Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikishamaeneo yote yanayopitiwa na mradi mkubwa wa maji -Nyahebu hasa vijiji vya Nyatare yananufaika na mradi huo?

(b) Kwa kuzingatia kwamba siyo kila mwananchiatakuwa na uwezo wa kuvuta maji nyumbani kwakekutokana na ukubwa wa gharama katika utekelezaji wamradi tajwa hapo juu; je, Serikali inatarajia kujenga vituovingapi vya maji?

(c) Je, ni nini Serikali itatekeleza ahadi yake yausambazaji wa mabomba awamu ya pili katika Kata zaManyamanyama, Nyasura, Kabalimu, Bundastoo,Nyamakokoto, Balili na Bunda Mjini?

Page 14: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

14

SPIKA: Majibu ya swali hilo Naibu Waziri Maji,Mheshimiwa Aweso tafadhali.

NAIBU WAZIRI MAJI NA UMWAGILIAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji naUmwagiliaji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ester AmosBulaya, Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini lenye sehemu (a),(b) na (c) kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali imeshaunganisha vijiji vyaNyabeho, Guta na Tairo na mradi mkubwa ambapowananchi wa vijiji hivyo wanapata huduma ya maji kupitiamradi huo.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa kij i j i chaKinyambwiga Serikali inaendelea na ujenzi wa kuunganishakijiji hicho na Mradi mkubwa kwa gharama ya shilingi milioni923.3 na hadi kufikia mwezi Machi, 2019 ujenzi huoumekamilika kwa asilimia 70. Aidha, kijiji cha Nyantarekitaunganishwa na mradi huo katika mwaka wa fedha 2019/2020.

Mheshimiwa Spika, Serikali ilipanga kujenga vituo 42vya kuchotea maji katika maeneo mbalimbali ya Mji waBunda ambapo kwa sasa imeshakamilisha ujenzi wa vituo22, aidha, Serikali inaendelea na ujenzi wa vituo zaidi vyakuchotea maji kwa lengo la kusogeza huduma ya maji kwawananchi.

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na mradi wausambazaji wa maji ambapo hadi kufikia mwezi Machi, 2019jumla la km 32 zimelazwa katika maeneo mbalimbali ya kataalizozitaja Mheshimiwa Mbunge. Aidha, Serikali itaendeleana kazi ya upanuzi wa mtandao wa usambazaji ili kuhakikishawananchi wote wa Jimbo la Bunda wanapata huduma yamaji safi. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Dkt. Sware uliza swali la nyongeza.

Page 15: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

15

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Spika,nashukuru kwa nafasi, Mheshimiwa Bulaya ana swali lanyongeza, Mheshimiwa Bulaya anasema kwambamkandarasi anayehusika na mradi huu kwa miaka kumi namoja sasa hajatimiza/hajakamilisha Mradi huu na 2017Mheshimiwa Waziri Mkuu na 2018 Mheshimiwa Rais walitoatamko juu ya mkandarasi huyu apate kuwekewa nguvu iliaweze kumaliza mradi huu.

Sasa nini hatma ya Mkandarasi huyu ambaye badoyuko site ili mradi huo uweze kukamilika? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nirudi sasa Mkoa waDodoma hata Mkoa wa Dodoma kuna maeneo mengi tunashida ya maji, hususani katika Jimbo la Kibakwe, watu waJimbo la Kibakwe wana shida sana na maji safi na salama.Sasa ni lini Serikali itawaangalia wananchi hao ili kuwezakuimarisha afya zao? (Makofi)

SPIKA: Majibu ya maswali hayo Mheshimiwa NaibuWaziri hata Kongwa kule maji mtihani.

NAIBU WAZIRI MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaSpika, kwanza napenda nimpongeze Mheshimiwa Mbungekwa swali zuri, lakini kikubwa tukiri kwamba huu mradiulitekelezwa umechukua muda mrefu na hii yote inatokanakwa baadhi ya miradi kupewa wakandarasi wababaishaji,lakini sisi kama viongozi wa Wizara tumefatilia mradi ule natumeongeza nguvu yetu kubwa sana katika kuhakikishamradi ule unakamilika.

Mheshimiwa Spika, mpaka sasa umeshafikia asilimia92 na tunaendelea kuongeza nguvu katika kuhakikisha mradiule unakamilika ili wananchi wa Bunda waweze kupatahuduma ya maji safi, salama na yenye kuwatosheleza.

Mheshimiwa Spika, lakini kuhusu eneo hili la Dodomala Kibakwe, nataka nimuhakikishie Mheshimiwa Mbunge sisikama Wizara ya Maji na Umwagiliaji tumeliona hilo, natakatumuagize Mhandisi wa Maji aone namna sasa ya kufanya

Page 16: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

16

mradi haraka il i kuhakikisha wananchi wa Kibakwewanaweza kupata maji safi na salama.

Mheshimiwa Spika, lakini kikubwa katika kuhakikishaMji huu wa Dodoma unaondokana na tatizo la maji, tunaujenzi huu wa Bwawa la Farkwa, na tupo katika hatua yautafutaji wa fedha tunaamini upatikanaji utakapokuwaumepatikana Mradi ule utatatua kabisa tatizo la maji katikaMji huu wa Dodoma, ahsante sana.

SPIKA: Nil ikuona Mheshimiwa Justin Monko.Mheshimiwa Monko.

MHE. JUSTIN J. MONKO: Mheshimiwa Spika, ahsantesana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiaw Spika, Jimbo la Singida Kaskazini linauhaba wa maji kutokana na tatizo la kutumia visima vifupina visima virefu peke yake, lakini tunavyo vyanzo vyamabwawa, ambayo yangeweza kwa ajili ya mradi mkubwawa maji.

Je, Mheshimiwa Waziri yuko tayari kutembelea Bwawala Ntambuko na kuangalia chanzo hiki na tuanzishe Mradimkubwa utakaoweza kutoa maji yenye uhakika katika Jimbola Singida la Kaskazini? Ahsante sana.

SPIKA: Majibu ya swal hilo Mheshimiwa Naibu WaziriMaji tafadhali.

NAIBU WAZIRI MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaSpika, awali ya yote kwa niaba ya Waziri wa Maji naUmwagiliaji, nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa kazi nzurianayoifanya katika Jimbo lake na nataka nimuhakikishie, sisikama viongozi wa Wizara nipo tayari sasa kuongozana nayekatika kuhakikisha tunaangalia namna ya kuweza kusaidiatatizo lake.

SPIKA: Tunaendelea Waheshimiwa Wabunge naWizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasil iano swali la

Page 17: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

17

Mheshimiwa Ezekiel Magolyo Maige kwa niaba yakeMheshimiwa Mwanne Mchemba nimekuona.

Na. 342

Ahadi ya Ujenzi wa Reli ya Kati

MHE. MWANNE I. MCHEMBA (K.n.y. MHE. EZEKIEL M.MAIGE) aliuliza:-

Ilani ya CCM 2015 – 2020 imeielekeza Serikali ya CCMkujenga upya reli ya kati kwa kiwango cha standard gaugena Mheshimiwa Rais tayari ameshapata fedha za mkopokutoka Serikali ya China kwa ajili ya kutekeleza mradi huo.

(a) Je, utekelezaji wa ahadi hiyo ya CCM naMheshimiwa Rais Magufuli kwa mradi huu umefikia hatuagani?

(b) Kwa kuwa Isaka ni eneo la makutano ya reli yaTabora – Mwanza na reli mpya (itakayojengwa) kati ya Isakahadi Keza (Ngara) na hatimaye Kigali – Rwanda; je, Serikaliiko tayari kuifanya Isaka kuwa ndiyo karakana kuu ya ujenzina baadaye ukarabati wa reli hiyo?

(c) Je, Serikali imejipangaje kuwasaidia wananchiwaishio jirani na mradi huo ili wanufaike kiuchumi wakati waujenzi huo?

SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu WaziriUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Engineer Atashasta Nditiyetafadhali.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasil iano, napenda kujibu swali laMheshimiwa Ezekiel Magolyo Maige, Mbunge wa Msalalakama ifuatavyo:-

Page 18: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

18

(a) Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza Ilani yaChama cha Mapinduzi ya mwaka 2015 – 2020 kwa upandewa uendelezaji wa miundombinu ya uchukuzi, Serikali kupitiaShirika la Reli Tanzania (TRC) inaendelea na ujenzi wa reli yakisasa yaani standard gauge railway kwa awamu, ambapoawamu ya kwanza ni kutoka Dar es Salaam hadi Mwanzakilometa 1219; ujenzi wa reli kutoka Tabora hadi Kigomakilometa 411; Kaliua - Mpanda hadi Karema kilometa 320;Isaka hadi Lusumo - Kabanga kilometa 393 na Uvinza -Kalelema kuelekea Msongati kilometa 150.

Mheshimiwa Spika, hivi sasa ujenzi wa reli awamu yakwanza umeanza kutoka Dar es Salaam hadi Morogorokilometa 300 na utekelezaji wake umefikia asilimia 47.87 kwamujibu wa taarifa ya mwezi Machi, 2019. Aidha, ujenzi wakipande cha pili kutoka Morogoro hadi Makutuporaambacho kina urefu wa kilometa 422 ambao umefikia asilimia7.96 kwa mujibu wa taarifa ya mwezi Machi, 2019.

(b) Mheshimiwa Spika, mpango wa Serikali nikuendelea kuifanya Isaka kuwa bandari kavu yaani dry portkwa ajili ya kuhudumia shehena itakayobebwa na reli ya sasameter gauge na pia ile ya kisasa ya SGR. Aidha, kwenye mradiwa ukarabati wa reli iliyopo yaani meter gauge kupitia mkopowa Benki ya Dunia Tanzania Intermodal Railway Projectitahusisha ujenzi wa Kituo kikubwa cha kuhudumia shehena.

Mheshimiwa Spika, uamuzi wa kujenga au kutojengakarakana kuu Isaka utafanywa wakati wa kufanya usanifuwa msingi, yaani baseline design kutoka Makutupora hadiMwanza, kwa sasa reli mpya inayojengwa kutoka Dar esSalaam hadi Makutupora itakuwa na karakana kuu katikaeneo la Kwala lililopo Mkoa wa Pwani eneo la Ruvu.

(c) Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimuwa kuwasaidia wananchi waishio jirani na mradi huu kwakupata manufaa wakati wa ujenzi unaoendelea kwakuhakikisha kuwa kukamilika kwa mradi huo kutachocheashughuli za ukuaji wa uchumi kwa wananchi waishio jirani namradi huu na Watanzania wote kwa ujumla.

Page 19: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

19

Mheshimiwa Spika, mradi huu unatarajiwa kutoa ajirakwa wazawa, kutumia malighali za ndani kwa zilezinazopatikana nchini na pia kutoa fursa na kuwajengeauwezo wazawa.

SPIKA: Mheshimiwa Mchemba nilikuona uliza swali lanyongeza.

MHE. MWANNE I. MCHEMBA: Mheshimiwa Spika,ahsante kwa kunipa nafasi na mimi niulize swali dogo lanyongeza.

Kwa kuwa Tabora kuna karakana kubwa ambayo ipotangu wakati wa mkoloni na kwa kuwa sasa kuna ujenzi wastandard gauge. Je, Serikali iko tayari sasa kuboreshakarakana hiyo kupeleka mitambo ya kisasa ili iendane natreni hiyo ambayo ni ya kisasa? (Makofi)

SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu Waziri,Ujenzi, Uchukuzi Mawasiliano, Engineer Atashasta Nditiyetafadhali.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE): Mheshimiwa Spika, ni kwelikwamba tunayo karakana kubwa kabisa ya matengenezoya vichwa vya treni maeneo ya Tabora na nimhakikishie tuMheshimiwa Mbunge kwamba Serikali kupitia TRC bado inampango wa kuendelea kuirekebisha karakana ile natunamhakikishia kwamba tutaongeza vifaa na iko kwenyempango ambao tunakwenda kuutekeleza kuanzia mwakanimwezi wa pili.

SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Ndassa nilikuonaswali la nyongeza tafadhali.

MHE. RICHARD M. NDASSA: Mheshimiwa Spika,ahsante sana, mbali na Isaka kuwa dry port, stesheni yaBukwimba ambayo iko Wilaya ya Kwimba tulishaomba kupitiaTPA/kupitia TRL. Tunataka kujua sasa Mpango ni lini sasa

Page 20: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

20

mpango huo wa kuweka dry port katika Stesheni yaBukwimba utafanyika? (Makofi)

SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu WaziriUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mheshimiwa Nditiyetafadhali.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE): Mheshimiwa Spika,ahsante, Kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi naMawasiliano, naomba kujibu swali la Mheshimiwa RichardNdassa, Seneta, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa, Kwa niaba yaWaziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Wizara nzimakwa ujumla, naomba kumpongeza sana Mheshimiwa Ndassakwa jinsi anavyofuatilia masuala ya miundombinu katikaJimbo lake na nchi nzima kwa ujumla. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nipende tu kumjibu MheshimiwaNdassa kwamba eneo la Bukwimba lipo kwenye mipangoya Shirika la Reli pamoja na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandarikwa ajili ya kujenga bandari kavu, sasa hivi tunachosubiri niile layout plan ya watu wa Wilaya ya Bukwimba ambayotukishaipata tutaweka layout plan yetu tena ndani ya eneohilo kwa ajili ya kujenga hiyo dry port.

SPIKA: Tunaendelea bado tuko Wizara hii hii ya Ujenzi.Mheshimiwa Zaynabu Vulu tafadhali uliza swali lako. (Makofi)

Na. 343

Makakati wa Kuboresha Vituo Vidogo vya Reli

MHE. ZAYNABU M. VULU aliuliza:-

Serikali inajenga reli ya standard gauge na itapitiabaadhi ya maeneo ya Mkoa wa Pwani?

Page 21: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

21

Je, Serikali imeweka mkakati gani wa kuboresha vituovya zamani na hasa vituo vidogo vidogo ili kuimarisha njia yausafiri na vituo hivyo vidogo ni vipi?

SPIKA: Majibu ya swali hilo bado tuko Wizara Ujenzi,Mheshimiwa Nditiye tafadhali.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ahsante sana, kwa niaba ya Waziriwa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano napenda kujibu swali laMheshimiwa Zaynabu Matitu Vulu, Mbunge wa Viti Maalum- Pwani kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, mpango wa Serikali ni kuhakikishakuwa reli iliyopo meter gauge inaendelea kukarabatiwa ilikuhakikisha inatoa huduma za uchukuzi hasa kwa mizigo yandani ya nchi, hivi sasa Serikali inaendelea na ukarabati wareli hii kutoka Dar es Salaam hadi Isaka kupitia mkopo waBenki ya Dunia wa dola za Kimarekani milioni 300.

Mheshimiwa Spika, kwa ukarabati huo, wakatiukarabati huo unaendelea katika mwaka wa fedha 2019/2020 Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupitia Shirikala Reli Tanzania (TRC) imetenga fedha kupitia kifungu namba4216 kwa ajili ya kuendelea na ukarabati ikiwemo stesheniya Soga, Ruvu na Kwala zilizopo katika Mkoa wa Pwani.

Mheshimiwa Spika, pamoja na ukarabati huu,mpango wa Serikali ni kuunganisha stesheni za zamani nampya zinazoendelea kujengwa kupitia mradi wa ujenzi wareli ya kisasa yaani SGR. Yapo maeneo yatakayounganishwakwa barabara na pia kwa madaraja ya juu kwa baadhi yamaeneo yanayokaribiana na vituo hivyo, kwa mfano,Stesheni ya Soga ya zamani ya Mkoa wa Pwaniitaunganishwa na daraja la juu la Stesheni mpya ya SGR.

SPIKA: Mheshimiwa Zaynabu Matitu Vulu nimekuona.

Page 22: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

22

MHE. ZAYNABU M. VULU: Mheshimiwa Spika, ahsantesana kwa majibu yaliyokuwa na uhakika kutoka kwaMheshimiwa Naibu Waziri, lakini nina maswali madogo mawili.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, hapo zamanistesheni ndogo ndogo za reli zilikuwa zina stawi sana miji yakekutokana na kwamba reli zilikuwa zinasimama kwa mfanoStesheni ya Mpiji na Stesheni ya Kikongo na nyinginezo hadiMwanza, Kigoma na Tabora na kwa kuwa ujenzi huu wa relisasa hivi hakuonyeshi dalili ya kwamba kutakuwa na treniitasimama.

Je, kuna mpango gani na mkakati gani angalau kwaStesheni ya Kikongo ambayo stesheni hiyo inaunganishabarabara inayotoka Makofia hadi Mlandizi, Mlandizi hadiMzenga, Mzenga hadi Mwanarumango, Serikali haionikwamba barabara hii na stesheni hii ikiboreshwa na trenizikasimama itasaidia kusafirisha abiria na mizigo ambayowananchi wanataka kuipeleka kokote kule? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa Serikali naninaishukuru na kuipongeza, imepanga Stesheni ya Soga naKwala kuwa stesheni kubwa; je, Serikali haioni sasa kuna hajana umuhimu wa Halmashauri hizo kupewa ardhi, ardhi hiyoikapimwa, ikagaiwa kwa wananchi, wananchi haowakajenga na wakawa na miradi ambayo itaendeleza ulemji na wao kuwapatia kipato? (Makofi)

SPIKA: Majibu ya maswali hayo Mheshimiwa NaibuWaziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mheshimiwa EngineerNditiye tafadhali.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE): Mheshimiwa Spika, swalila kwanza ametaka kujua status ya vituo vya zamani kupitiameter gauge. Nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwambakati ya Dar es Salaam hadi Morogoro ambako tunapitia Mkoawa Pwani kuna vituo vya zamani 14. Nimhakikishie tu kwambavile vituo vitaendelea kuboreshwa kupitia mradi wa TIRPambao unafadhiliwa na Benki ya Dunia kwa dola milioni 300

Page 23: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

23

na mpaka sasa hivi vimekwishaanza kurekebishwa nakuwekwa katika hali nzuri. Reli itakapokuwa inapita ile metergauge itahudumia vituo vyote vile 14 kati ya Dar es Salaammpaka Morogoro.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa SGR kuna vituosita, Dar es Salaam mpaka Morogoro kuna vituo sita, vinneviko katikati na kimoja ni cha Dar es Salaam na kingine nicha Morogoro. Vinne kuna Kwala, Soga, Kingolwira naNgerengere. Nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwambautaratibu wa kuunganisha vituo hivyo na vile vituo vya zamaniunaendelea vizuri na reli ya kisasa inayojengwa kwa asilimia70 itakwenda na ile reli ya zamani ya meter gauge.

Mheshimiwa Spika, kwenye swali lake la pil i,Mheshimiwa alitaka kujua suala la upimaji wa ardhi kwa ajiliya maeneo yale. Naomba tu nimhakikishie MheshimiwaMbunge kwamba Mamlaka ya Mji wa Kibaha kwakushirikiana na Wizara ya Ardhi wamekwishaendeleakupanga mji ule wa maeneo ya Kwala, Soga na Kingolwirakwa ajili ya kuwa-accommodate watu watakapata viwanjapale. Kwa sababu vituo vile vitakuwa ni vya kisasa ambavyovitakuwa na huduma zote za kijamii na tunategemea hatawananchi nao waende wakae pale maeneo yao kwa ajiliya kufanya shughuli za kijamii.

SPIKA: Nilikuona Mheshimiwa Goodluck Mlinga.

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa Spika,ahsante sana. Ujenzi wa reli uendane sambamba na ujenziwa barabara hasa kwa maeneo yenye misongamanomkubwa wa abiria na mizigo. Kwa mfano barabara ya Dares Salaam – Chalinze – Morogoro, ile barabara ina hali mbayasana, ina msongamano mkubwa wa magari na inatumiamasaa matano hadi sita kwa basi la abiria. Serikali ilikuwa nampango wa kujenga barabara (highway) barabara sita,kutoka Dar es Salaam mpaka Chalinze – Morogoro na sasahivi imesitisha.

Page 24: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

24

Sasa nataka kusikia kauli ya Serikali, je, lini itafufua tenampango huu wa ujenzi wa hii barabara ili kuondoa kadhiahii?

SPIKA: Mheshimiwa Elias Kwandikwa, Naibu Waziri,Ujenzi majibu tafadhali.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Mheshimiwa Spika, Serikalihaijasitisha ujenzi wa barabara njia sita ya kutoka Dar esSalaam kuja Chalinze, isipokuwa ujenzi unaendelea kwahatua na hata juzi tu nimefanya ukaguzi wa barabara. Ilebarabara ya kutoka Kimara kuja Kibaha sasa tuko 28% namkandarasi anaendelea kulipwa vizuri.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo nikuombe MheshimiwaMlinga uvute tu subira kwamba tumejipanga vizuri kadritunavyopata fedha, tunaendelea na harakati za ujenzi wabarabara hiyo. Hata hivyo, tunaendelea kufanya maboreshombalimbali maeneo ambayo yanakuwa na uharibifu kwasababu ni kawaida maeneo ambayo yanaharibika Serikalitunaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kufanya maboreshombalimbali ili barabara ipitike wakati tunaendelea na hatuaupanuzi wa barabara.

SPIKA: Ahsante, Wizara ya Kilimo, swali la MheshimiwaEdwin Amandus Ngonyani uliza swali lako tafadhali.

Na. 344

Changamoto za Ununuzi wa Tumbaku Ruvuma

MHE. ENG. EDWIN A. NGONYANI aliuliza:-

Mkoa wa Ruvuma umepata mnunuzi wa tumbakuambaye amekubali kuwawezesha SONAMCU kufufuakiwanda cha kuchambua tumbaku na kugeuza green leafkuwa dry leaf. Aidha, kutokana na changamoto za kodi nasoko mnunuzi huyo hajaweza kutekeleza azma yake.

Page 25: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

25

Je, Serikali inasaidiaje kutatua changamotozinazomkabili mnunuzi huyo?

SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa InnocentLugha Bashungwa, Naibu Waziri Kilimo tafadhali.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. INNOCENT L.BASHUNGWA) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziriwa Kilimo naomba kujibu swali la Mheshimiwa MhandisiEdward Amandus Ngonyani, Mbunge wa Namtumbo kamaifutavyo:-

Mheshimiwa Spika, kufuatia kuondoka kwa kampunimbili za ununuzi wa tumbaku Mkoani Ruvuma msimu wa 2014/2015, wakulima walikosa soko la uhakika. Kutokana na halihiyo Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali pamojana Mheshimiwa Mbunge Ngonyani walifanya juhudi zakutatua changamoto hiyo.

Mheshimiwa Spika, jitihada hizo zilisaidia kupatikanakwa mnunuzi wa tumbaku ambaye ni Kampuni ya PremiumActive Tanzania Limited ambayo ilianza kununua kilo 250,000na sasa imeongeza hadi kilo 1,000,000. Serikali pia inapongezania ya kampuni hiyo ya kutaka kukiwezesha Chama Kikuucha Ushirika cha Mkoa huo cha SONAMCU kufufua kiwandacha kuchakata tumbaku.

Mheshimiwa Spika, kwa msingi huo Wizara ya Kilimoipo tayari kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango namwekezaji huyo kutafuta ufumbuzi wa changamoto zamnunuzi huyo ili kuhakikisha kuwa kampuni hiyo inatimizaazma hiyo njema kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma nataifa kwa ujumla, ahsante.

SPIKA: Mheshimiwa Ngonyani nimekuona, swali lanyongeza tafadhali.

MHE. ENG. EDWIN A. NGONYANI: Mheshimiwa Spika,namshukuru sana Mheshimiwa Waziri wa Kilimo na Serikali yetukwa ujumla kwa jibu hilo zuri.

Page 26: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

26

Hata hivyo ili tuwe na uelewa wa pamoja kati yaSerikali na wakulima wa tumbuku wa Namtumbo; je,Mheshimiwa Waziri yuko tayari kuzifafanua changamoto hizoza mnunuzi wa tumbaku zinavyotakiwa kutatuliwa na Serikalikwa ujumla wake? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali dogo la pili, wakulima waNamtumbo wanalishukuru sana Bunge lako tukufu na Serikaliya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa kwaumahiri mkubwa na Mheshimiwa John Pombe JosephMagufuli, Rais wetu kwa kuwawezesha wakulima waNamtumbo hadi sasa katika minada mitatu tu wamepatashilingi bilioni 5.5 la zao la ufuta kupitia mfumo wa stakabadhighalani. (Makofi)

Je, Serikali iko tayari kuendelea kutatua changamotoza wakulima wa Namtumbo hususan katika mazao yakorosho, soya, mbaazi na mengineyo na hasa katika koroshowale wakulima wachache ambao mpaka sasa hawajalipwa,wameuza korosho zao mwezi wa kumi hususan wa Tarafawa Sasawala, lini watalipwa? (Makofi)

SPIKA: Majibu ya maswali hayo muhimu kwa Wana-Namtumbo na watanzania kwa ujumla Mheshimiwa NaibuWaziri tafadhali.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. INNOCENT L.BASHUNGWA): Mheshimiwa Spika, swali la kwanzaMheshimiwa Ngonyani angependa kupata commitment yaSerikali kama tunaweza tukakaa pamoja na MheshimiwaMbunge, pamoja na wakulima wake ili kuweza kutatuachangamoto ambazo anakabiliana nazo huyu mwekezajiPATL. Kwa sababu ya muda na kwa vile MheshimiwaNgonyani ni mfuatiliaji mzuri, hili ni swali la pili katika kikao hikibasi nimuahidi kwamba nitakaa naye na tutafute mudakuweza kukaa pamoja na kuainisha hizi changamotoambazo tayari Wizara tunazifahamu na kuzijadili na kuangalianamna bora ya kuzitatua haraka iwezekanavyo ili mwekezajihuyo aweze kuendelea na uwekezaji, wakulima wetuwaweze kupata mahali pa kuchakata tumbaku yao. (Makofi)

Page 27: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

27

Mheshimiwa Spika, swali la pili, Mheshimiwa Ngonyanianauliza kama Serikali iko tayari kufanya maboresho nakuongeza jitihada za kuhakikisha mazao ya korosho, soya,mbaazi na mazao mengineyo yanamsadia mkulimaMtanzania na jibu ni ndiyo. Azma ya Serikali ni kuhakikishamazao yote haya na mengine tunaongeza uzalishaji natunawasaidia wakulima wetu kuwa na kilimo cha tija nasambamba na hilo tunawasaidia wakulima wetukuwaunganisha na masoko. Suala la malipo ya koroshonimhakikishie Mbunge kuwa Serikali inaendelea kufanya kilaiwezekanavyo kuhakikisha waliobaki ambao hawajalipwa naambao ni wachache waweze kulipwa malipo yao, ahsante.

SPIKA: Ahsante sana, Mheshimiwa Waziri wa Kilimomajibu ya nyongeza tafadhali.

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, kwanzanaomba nichukue nafasi hii kumpongeza Naibu Waziri kwamajibu mazuri aliyoyatoa.

Mheshimiwa Spika, ni kweli kabisa huyu mwekezajiamefanya jitihada kabisa kuhakikisha kwamba anawekezakatika kile kiwanda na amewekeza anadai zaidi ya dola zaMarekani milioni tatu na hivi sasa alikuwa amesimamakutokana na changamoto mbalimbali ambazo zimekuwazikimkabili. Lakini Serikali tumepanga kabisa kwamba ndaniya wiki mbili hizi tutakaa naye ili tuweze kuzungumza pamojaikiwa ni pamoja na kuangalia suala lile la madai ya VATambayo yalikuwa yamekaa muda mrefu ambayo anasemakwamba yamemuathiri katika kuendeleza hiki kiwanda. Kwahiyo, tutakaa naye pamoja na makampuni mengine yaleambayo nayo yana changamoto hiyo hiyo ili tuwezekuhakikisha kwamba hili suala linafikia mwisho na kusudiwaendelee kununua zao letu la tumbaku. Nakushukuru.(Makofi)

SPIKA: Ahsante, nilikuona Mheshimiwa Aida Khenani.

MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Spika,nakushukuru. Changamoto ya ununuzi wa tumbaku

Page 28: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

28

inafanana sana na changamoto wanayokabiliana nayowakulima wa zao la mahindi. Hivi sasa ni msimu wa mavuno,ningependa kujua kwa Serikali imejipangaje kwa mwaka huujuu ya ununuzi wa zao hili la mahindi?

SPIKA: Zao la mahindi Mheshimiwa Waziri wa Kilimotafadhali majibu.

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ni kweli kabisakatika msimu uliopita tulikuwa na changamoto ya masokoya zao la kilimo, lakini kama sote tunavyojua, Serikali imekuwaikihakikisha kwamba inatafuta masoko na muda huutunapoongea tumepata masoko makubwa sana ya mahindikatika nchi za Kusini. Hivi sasa Rwanda wanahitaji zaidi yatani 100,000; Burundi wanahitaji zaidi ya tani 100,000; lakininchi ya Zimbabwe wanahitaji tani 800,000 za mahindi na nchinyingine nyingi zinahitaji mahindi kwa wingi.

Kwa hiyo, ninachotaka kusema ni kwamba sasa hivisoko la mahindi ni kubwa sana, wakulima wote wenyemahindi tunaomba wajitokeze watuambie wana kiasi gani,washirikiane na Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuanzia wiki taasisi zetu ikiwemoNFRA pamoja na CPB wanaanza kununua mahindi nakukusanya mahindi kutoka kwa wakulima mbalimbali pamojana wafanyabiashara, lakini pia taasisi nyingine ambayotumeipa jukumu la kupeleka mahindi Zimbabwe nayoinaanza kununua mahindi wiki hii.

Kwa hiyo wakulima wakae mkao kila mahali wenyemahindi sasa hivi ni wakati wa kula mkate mzuri, nakushukuru.(Makofi)

SPIKA: Ahsante sana, ahsante sana. Mheshimiwa CecilMwambe.

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, ahsantesana kwa kunipa nafasi na mimi ya kuuliza swali la nyongeza,lakini tu nimuombe Waziri kwamba maneno mazuri

Page 29: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

29

anayoongea hapa alianza kuongea haya haya kwenye zaola korosho na sasa hivi hali iliyopo kule tunaifahamu.

Sasa swali langu, atakuwa tayari kuwajibika endapohaya anayoyasema hayatafanywa kadri anavyoongeahapa? (Makofi/kicheko)

SPIKA: Hilo siyo swali. Nimekuona Mheshmiwa Mbungetafadhali uliza swali lako. (Makofi/Kicheko)

MHE. JEROME D. BWANAUSI: Mheshimiwa Spika,nashukuru kupata nafasi ya kuuliza swali.

Mheshimiwa Spika, sasa tunaelekea kwenye msimuujao wa zao letu la korosho na nilitaka nipate maelezo kutokaSerikalini, mpaka hivi sasa wakulima hawajapata taarifazozote juu ya uwepo na lini na bei elekezi ya pembejeo. Kwahiyo, ningeomba Serikali itoe maelezo ili kuhakikisha wakulimawanapata ufahamu juu ya uwepo wa pembejeo lakini beielekezi itatolewa lini, lakini pia ni lini itasambazwa?(Makofi)

SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Waziri waKilimo tafadhali.

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ni kweli sasahivi ni msimu wa kilimo cha zao la korosho hasa katika kupuliziamadawa ikiwemo sulfur na maeneo mengine. Sasa hivi Serikalitumejipanga tumehakikisha kwamba sulfur ipo ya kutoshakatika maeneo yote tumeshapaleka na bado tunajaribukufanya tathmini kuangalia kama kuna sehemu tunaupungufu il i tuhakikishe kwamba hayo madawayanakuwepo. Sambamba na hilo tumeanza kujiandaa kabisakatika msimu unaokuja ikiwa ni pamoja na uteuzi wa Bodi yaKorosho ambayo tayari tumeshaiteua kwa ajili ya kuanza kazina kuweza kupanga mikakati mbalimbali ya kuendeleza hilizao la korosho.

Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge avute tu muda nikwamba kila tumejipanga na kitakwenda vizuri na ninauhakika wakulima wa korosho watafurahi sana, ahsante.

Page 30: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

30

SPIKA: Ahsante sana. Waheshimiwa Wabungetunaendelea, leo ni Wizara ya siku moja, kwa hiyo, inabidimambo yaende chap chap hapa mbele. Naomba sasaniwatumbulishie wageni walioko Bungeni kwetu siku ya leo.Nitaanza na wageni wangu mwenyewe ambao ni walimusita na wanafunzi 44 kutoka Shule ya Sekondari kuleSongambele, Kilimani Kongwa ambao wanaongozwa naMheshimiwa Diwani Patrick Messo. Wanafunzi waSongambele Sekondari naomba msimame. Ahsanteni sana,karibuni sana wanangu, karibuni sana. Mheshimiwa DiwaniPatrick Messo, ahsante sana na karibu sana, karibu sanaBungeni. (Makofi)

Nina wageni pia watano kutoka Kinondoni Jijini Dares Salaam, ni Bi. Radhia Solomon. Radhia naomba usimamemwenye mtoto pale na wale waliofuatana naye piawasimame, ahsanteni sana. Bi. Radhia ni binti aliyejifunguamapacha wanne kwa uzazi mmoja. Kwa bahati mbaya sanayule mwanaume ambaye ni responsible akakimbia,akamtaliki, akakimbia kuwajibika. Kwa hiyo,…. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Yupo humu?

SPIKA: Eeh, naam?

MBUNGE FULANI: Yupo humu?

SPIKA: Hapana, mwenye mtoto hayuko humu ndanihapana.

Lakini ni kwamba baada ya kupata watoto hawawanne ambapo amelazimika sasa yeye mwenyewe apatena wasaidizi kama mnavyoona muda wote wa kumsaidiana yule bwana amekimbia na maisha ya Dar es Salaam,Kinondoni ni maisha magumu kidogo. Mmoja wawanaomsaidia ni mama yake mzazi, Ester Mlinda naDorothea Benjamin ni mama mkubwa na Joyce Mtesigwa niAfisa Ustawi wa Jamii. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Mama ni yupi?

Page 31: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

31

SPIKA: Mama anyooshe mkono, Radhia anyooshemkono. (Makofi)

(Hapa Bi. Radhia Solomon alinyoosha mkono)

MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM: Sadaka, sadaka.

SPIKA: Kwa hiyo, ndugu zangu kwanza amekuja hapaili sisi kama Bunge kwa kweli tukemee jambo la wanaumeambao hawawajibiki, lakini kipekee nafikiri safari hii iwe zamuya Wabunge Wanawake. (Makofi)

WABUNGE FULANI: Wanaume.

SPIKA: Peke yao. (Kicheko/Makofi)

SPIKA: Au wanaume ambao ndiyo wamekimbia ndiyowawajibike? Au kama ilivyo kawaida wote tuwajibikepamoja, naona la wote linaenda vizuri. (Makofi)

WABUNGE FULANI: Ndiyo.

SPIKA: Haya nipeni.

MBUNGE FULANI: Shiilingi 100,000.

MBUNGE FULANI: Shilingi 20,000.

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Spika, poshoya siku moja, hiki ni kiwanda hiki.

MHE. ALLY SALEH ALLY: Shilingi 20,000.

MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM: Shilingi 100,000.

MHE. NEEMA W. MGAYA: Shilingi 100,000.

MHE. ALLY SALEH ALLY: Shilingi 20,000 nyingi sana kwajumla.

Page 32: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

32

SPIKA: Tumsikilize mwenzetu hapa.

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru.

MBUNGE FULANI: Utatuharibia.

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Hapana siku nzimabwana.

MBUNGE FULANI: Ataripuka yule.

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Ninyi hamjazaa ninyi.

MHE. RUKIA AHMED KASSIM: Mheshimiwa Spika, kwasababu wanaume wamezoea kutelekeza wanawake nawatoto, mimi nashauri Bunge wanawake tuchangie shilingi50,000 na wanaume shilingi 100,000.

MHE. ZAYNABU M. VULU: Naunga mkono hoja.

MHE. ALLY K. MOHAMED: Wewe usilete utani wewe,toa mwenyewe.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuatautaratibu)

MHE. ALLY K. MOHAMED: Wewe ulikimbiwa na mumewako.

SPIKA: Mpeni Mheshimiwa Musukuma.

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana.

SPIKA: Jamani jambo hili siyo la utani, tulifanyie seriousfulani.

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana.

Page 33: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

33

Mheshimiwa Spika, suala hili kiukweli siyo la utani nasiyo lawama tu kwa mwanaume aliyekimbia, lakini pia hatawanawake tumeona sehemu nyingi wanapopata tukio kamahili wanatelekeza watoto na wao wanawakimbia. Nilikuwanakuomba tukate posho ya siku nzima tumsaidie huyu mamakabisa. (Makofi)

SPIKA: Haya TWPG - Makamu wa Mwenyekiti. UmojaAkinamama wa Bunge tuwasikilize kupitia viongozi wao,Mheshimiwa Susan.

MHE. SUSAN A. J. LYIMO: Mheshimiwa Spika,nashukuru, nilikuwa naunga mkono alilosema MheshimiwaRukia na hii ni kwa sababu pia wanaume ni wengi kulikowanawake, kwa hiyo tusaidie hili jambo ni kubwa sana.Nadhani hiyo ni sawasawa tutoe shilingi 50,000 wanawakena wanaume shilingi 100,000. (Makofi/ Vigelegele)

MHE. ALLY K. MOHAMED: Msilete utani, hatutoi.

SPIKA: Ahsante sana. Makubaliano wanawake woteshilingi 50,000 na wanaume wote shilingi 100,000. (Makofi/Vigelegele)

MHE. ALLY K. MOHAMED: Tukatwe fedha za vyoo,apewe fedha za vyoo.

SPIKA: Tunaendelea na utambulisho, ahsante sanaRadhia, tunawashukuru. Mnaweza mkaenda na watotowakaenda kunyonya sasa. Kupitia Mbunge wenu,tutawasiliana namna gani ya kuweza kukupata na kukupatiamsaada huo. Ahsante sana. (Makofi)

Mgeni mwingine wa Mheshimiwa Spika, NduguGodfrey Mosha kutoka Mafinga, Mosha karibu sana. Ahsantesana. Karibu.(Makofi)

Mheshimiwa Waziri wa Fedha, Dkt. Phillip Mpango anawageni wake kama wafuatavyo..., naomba tusikilizaneWaheshimiwa Wabunge, hilo limepita. Yupo Katibu Mkuu -

Page 34: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

34

Ndugu Doto James, naomba usimame na karibu sana; NaibuKatibu Mkuu - Dkt. Khatibu Kazungu, ahsante sana; Gavanawa Benki Kuu - Profesa Florens Luoga, karibu Gavana;Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania - NduguCharles Kichere, ahsante sana; Kamishna wa Bajeti - NduguMary Maganga, ahsante sana, Kamishna wa Sera - NduguBenedicto Mgonya; Kamishna wa Fedha za Nje - Ndugu JohnRubuga; Mhasibu Mkuu wa Serikali - Ndugu FrancisMwakapalila; Msajili wa Hazina - Ndugu Athumani Mbutuka,Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu - Dkt. AlbinaChuwa; Kamishna wa Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramu- Ndugu Onesmo Makombe; Katibu wa Tume ya Pamoja yaFedha - Ndugu Ernest Mchanga; Kamishna wa Idara yaUsimamizi wa Sera ya Ubia wa Sekta ya Umma na Sekta Binafsi- Dkt. John Mboya na Kaimu Kamishna wa Idara ya Sera yaUnunuzi wa Umma - Ndugu Alex Haraba. Pia viongozi hawawameambatana na Wakurugenzi na Wakuu wa Idara naTaasisi zilizopo chini ya Wizara ya Fedha. (Makofi)

Mheshimiwa Jenista Mhagama - Waziri wa Nchi, Ofisiya Waziri Mkuu ana wageni wake ambao ni Wajumbe waBaraza la Taifa la Ushauri kwa Watu Wenye Ulemavuwakiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza hilo Dkt. Lucas KijaLuhende. Naomba msimame, ahsanteni sana, karibuni sana.(Makofi)

Wageni wa Waheshimiwa Wabunge, wageni 28 waMheshimiwa Constantine Kanyasu - Naibu Waziri wa Maliasilina Utalii ambao ni wanafunzi wa kidato cha tano na walimuwao kutoka Shule ya Sekondari ya Golden Ridge iliyoko Mkoawa Geita, Golden Ridge, karibuni sana. (Makofi)

Wageni watatu wa Mheshimiwa Mwita Waitara -Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, ni ndugu zake kutokaDar es Salaam wakiongozwa na Ndugu Joshua Joel, KaribuJoshua, wale pale. (Makofi)

Wageni sita wa Mheshimiwa Anna Lupembe ambaoni watumishi wa Mungu kutoka Jijini Dodoma, karibuni, walekule juu. (Makofi)

Page 35: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

35

Wageni 70 wa Mheshimiwa Emmanuel Papian ambaoni wanafunzi na walimu kutoka Shule ya Sekondari ya Kiteto,Mkoa wa Manyara. Wale wa Kiteto, karibuni sana. Majiranihawa wanatoka Kibaya, Kiteto hawa. (Makofi)

Wageni 21 wa Mheshimiwa Dkt. Steven Kiruswaambao ni wanafunzi kutoa Jimbo la Longido Mkoa wa Arushawanaosoma katika vyuo mbalimbali hapa Dodoma, haya.Karibuni sana, kabisa. (Makofi)

Wageni watano wa Mheshimiwa Maulid Mtuliaambao ni wapiga kura wake kutoka Kinondoni Dar es Salaamna ndiyo nimeshawatambulisha tayari wakiongozwa na Bi.Radhia.

Wageni 113, lakini sasa twende hivi; WaheshimiwaWabunge ningependa kuwatambulisha wanafunziwaliohitimu kidato cha nne mwaka 2018 Shule ya Sekondariya St. Anne Marie ya Dar es Salaam na kufaulu division onena two. Wako 86, wale wa Anne Marie, wako wapi? SimameniAnne Marie, wale kule wengi sana. Hongereni sana kupatadivision one na two Anne Marie. Wanaongozwa na MwalimuGladias Ndyetabura. (Makofi)

Pia tuna wanafunzi waliohitimu kidato cha nnemwaka 2018 Shule ya Sekondari ya Brilliant na kufaulu divisionone na two jumla wako 26 wakiongozwa na Kaimu Mkuu waShule - Ndugu Jafari Athumani, wale wa Brilliant na wenginewako kule tunawapongeza sana. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, shule zote hizi mbili AnneMarie ya Dar es Salaam na Brilliant pia ya huko huyo, shulehizi zinamilikiwa na Mbunge mwenzetu Ndugu JassonRweikiza. (Makofi)

Tunakushukuru sana Mheshimiwa Rweikiza kwa malezimazuri kwa watoto na kwa kweli kwa watoto hao kuwezakufaulu vizuri kiasi hiki. Mheshimiwa Rweikiza ahsante sanana wengine tuige mifano mizuri kama hiyo. (Makofi)

Page 36: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

36

Wageni 11 wa Mheshimiwa Edwin Ngonyani ambaoni wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya kutoka Namtumbo,Mkoa wa Ruvuma wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM waWilaya Ndugu Aggrey Mwansasu, karibuni sana na mmesikialeo swali lenu likiulizwa na Mbunge wenu na majibu ya Waziriwa Kilimo natumaini yamewapa moyo sana. (Makofi)

Mgeni wa Mheshimiwa Ritta Kabatti ambaye nimdogo wake kutoka Iringa Mjini, Ndugu Debora Christian,karibu sana. (Makofi)

Wageni watatu wa Mheshimiwa Japhary Michaelambao ni wapiga kura wake kutoka Moshi, Mkoa waKilimanjaro wakiongozwa na Diwani wa Manispaa ya MoshiMheshimiwa Dkt. Collins Mayuta, wale wa Moshi karibunisana. (Makofi)

Wageni waliokuja kwa ajili ya mafunzo ni wanafunzi60 na walimu sita kutoka shule ya awali ya Marangu HillsAcademy. Marangu Hills Academy msimame, karibuni sanaMarangu Hills. (Makofi)

Viongozi 17 na Mshauri wa Wanachuo kutoka Chuocha Madini kilichopo Dodom, Chuo cha Madini naombamsimame kwa sababu gallery zimejaa inawezekana wakobasement somewhere. (Makofi)

Wananchi wawili kutoka Dodoma ambao ni NduguDavison Mnyili na Ndugu Grace Mnyili waliotembelea Bungekwa ajili ya mafunzi. Davison na Grace, ahsante sana karibuni.Hawa ni wapiga kura wa Kongwa hawa. Ahsanteni sana.(Makofi)

Naendelea na matangazo mengine, weekend hiipalikuwa na mechi mbalimbali kama nilivyowatangazia;kwenye upande wa football Ndugai Boys ilipata goli mojana JKT Makutupora goli moja, kwa hiyo, walitoka sare na golihili lilifungwa na Mheshimiwa Alex Gashaza kwa upande huo,nyota wa mchezo alikuwa Mheshimiwa Venance Mwamoto,kocha mchezaji. (Makofi)

Page 37: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

37

Kwa upande wa mpira wa pete, Bungewaliwaduwaza wanajeshi wa JKT Makutupora kwakuwafunga magoli 26 kwa 18 kwenye netball, wafungaji waBunge walikuwa Mheshimiwa Grace Kiwelu na MheshimiwaAnna Gidarya na kwa maajabu makubwa kabisa, nyota wamchezo huo wa juzi alikuwa Mheshimiwa Hawa Mwaifunga.(Makofi/Kicheko)

Kuvuta kamba wanaume na wanawake, BungeSports Club waliwagaragaza JKT Makutupora kwa mbalikabisa. Inaelekea JKT lishe ndogo, wamezidiwa na Wabunge.(Makofi/Kicheko)

Siku ya Jumapili Bunge Sports Club walipata bao mbili,Muungano wakawa zero (mbili bila). Mfungaji wa BungeSports Club alikuwa Mheshimiwa Paschal Haonga na nyotawa mchezo wa football alikuwa ni Mheshimiwa WilliamMganga Ngeleja. (Makofi)

Kwenye netball, Bunge Queens waliendeleza doseyao kwa kuwafunga Muungano Veterans jumla ya magoli26 kwa 10. Karamu hiyo ya magoli ilikuwa imeandaliwa nawachezaji hatari wa Bunge Queens ambao ni MheshimiwaGrace Kiwelu na Mheshimiwa Esther Matiko na nyota wamchezo alikuwa Mheshimiwa Anna Lupembe. (Makofi)

Tunawashukuru sana viongozi wote na WaheshimiwaWabunge ambao mlienda kushambulia mechi hizo. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, naomba tusikilizane kidogokuhusiana na majumuisho kati ya Serikali na Kamati ya Bajeti.Kama mnavyojua baada ya leo tutasimama kidogo nahuenda keshokutwa Jumatano au Alhamisi ikawa sikukuu yaEid na baada ya hapo Kamati ya Bajeti inatakiwa iendeleekukutana na Serikali. Sasa nataka tutoe mwongozo mfupi tu.

Kwa mujibu wa masharti ya Kanuni ya 105(1) ya Kanuniya Bunge Toleo la Januari, 2016 kwenye ratiba ya Mkutanohuu unaoendelea tumetenga siku sita za majumuisho kati yaSerikali na Kamati ya Bajeti kwa ajili ya kuzingatia hoja

Page 38: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

38

zilizojitokeza wakati wa kujadili utekelezaji wa Bajeti za Wizarakwa mwaka wa fedha unaoisha na makadirio ya matumiziya Wizara hizo kwa mwaka wa fedha unaofuata.

Waheshimiwa Wabunge kwa kuzingatia mashartihayo ya Kikanuni, kazi hii itafanyika kuanzia siku ya Ijumaa hiiya mashauriano kati ya Kamati ya Bajeti na Serikali yaanitarehe 7 Juni hadi siku ya Jumatano tarehe 12 Juni, 2019.Aidha, kwa mujibu wa masharti ya Kanuni ya 105(3) katikakipindi hicho cha majumuisho Wajumbe wa Kamati yaUongozi kwa nafasi zao wanakuwa moja kwa moja niWajumbe wa Kamati ya Bajeti. Kwa hiyo, Kamati ya Bajeti naKamati ya Uongozi wanachanganyika pamoja kwa siku zotehizi za majadiliano ya kuanzia tarehe 7 hadi tarehe 12 Juni.

Hivyo basi, pamoja na kwamba Wabunge wengimtaondoka hapa Dodoma wakati wa kipindi hiki cha sikukuuza Eid, nawaomba Wajumbe wa Kamati hizo mbili yaaniKamati ya Bajeti na Kamati ya Uongozi wajipange kurejeamapema ili wafanye kazi hiyo muhimu ya majumuisho kuanziatarehe 7 Juni, 2019 kwa kuzingatia ratiba itakayoafikiwa katiya Kamati hizo na Serikali. Watakaa na kutengeneza ratibaya ndani ya namna ya kufanya kazi zao kwa pamoja nasmoothly.

Basi baada ya hayo kwa sababu muda ni mdogosana, naomba tusonge mbele.

Katibu!

NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE:

HOJA ZA SERIKALI

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Fedha naMipango kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020

SPIKA: Ahsante sana, ufafanuzi zaidi kuhusu hiiweekend tutatoa baadae kadri muda unavyoenda,tutafafanua zaidi. Nilichokuwa nakielezea hapa ni kwamba

Page 39: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

39

watu wa Kamati ya Bajeti na Kamati ya Uongozi kuanziaIjumaa kazi kama kawaida. Ndiyo ilikuwa umuhimu wa…

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Spika,Mwongozo.

SPIKA: Hatuna muda kabisa. Mheshimiwa Waziri waFedha nakuomba sasa uje mbele utusomee hotuba yakotafadhali. Karibu sana Waziri wa Fedha Mheshimiwa Dkt.Phillip Mpango, karibu.

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika,kutokana na Taarifa iliyowasilishwa ndani ya Bunge lakotukufu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge yaBajeti, naomba kutoa hoja kwamba sasa Bunge lako lipokeena kujadili mapitio ya utekelezaji wa mpango na bajeti yaWizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka 2018/2019 pamojana makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2019/2020.Aidha, naomba Bunge lako tukufu likubali kupitisha makadirioya mapato na matumizi ya Wizara ya Fedha na Mipango naTaasisi zilizo chini yake, pamoja na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzikwa mwaka 2019/2020.

Mheshimiwa Spika, awali ya yote napendakumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia uhai na afyanjema na kutuwezesha kukutana tena kushiriki Mkutano huuwa Bunge unaojadili bajeti ya mwaka 2019/2020 ambayo niya nne tangu Serikali ya Awamu ya Tano il ipoingiamadarakani.

Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee napendanitumie fursa hii kuwapongeza kwa dhati kabisa viongoziwakuu wa Serikali nikianza na Mheshimiwa Dkt. John PombeJoseph Magufuli - Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania; Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan - Makamu waRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na MheshimiwaKassim Majaliwa, Mbunge na Waziri Mkuu wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania kwa miongozo yao iliyojaa hekimana uzalendo. Ni dhahiri kwamba katika kipindi cha takribanimiaka mitatu na nusu ya uongozi wao tumepata mafanikio

Page 40: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

40

mengi ambayo kia mmoja wetu anapaswa kujivunia.Naomba Mwenyezi Mungu aendelee kuwajaalia afya njemaili dhamira zao za dhati za kuwaletea Watanzania maendeleoziendelee kuleta manufaa kwetu na kwa vizazi vijavyo.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, napenda pia nitumie fursa hiikuwapongeza sana Mheshimiwa Balozi Dkt. Augustine PhillipMahiga (Mbunge) kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Katiba naSheria pamoja na Mheshimiwa Profesa Palamagamba JohnAidan Kabudi (Mbunge) kwa kuteuliwa kuwa Waziri waMambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Nawaahidiushirikiano wa hali ya juu katika kutekeleza majukumu yetuya kumsaidia Mheshimiwa Rais ili shughuli za Serikali ziendeleekufanyika kwa ufanisi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, napenda kukupongeza wewebinafsi, Naibu Spika na Wenyeviti wote wa Bunge kwakuendesha vizuri majadiliano ya bajeti za Wizara mbalimbali.(Makofi)

Aidha, napenda kumpongeza Mwenyekiti wa Kamatiya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mheshimiwa George BonifaceSimbachawene (Mbunge) na Makamu MwenyekitiMheshimiwa Mashimba Mashauri Ndaki (Mbunge) kwakuongoza vizuri majadiliano ya Kamati. Lakini vilevilenawashukuru Wajumbe wote wa Kamati ya Bajeti kwamichango yao mizuri ambayo inasaidia sana katikakutekeleza majukumu ya Wizara kwa ufanisi. Aidha, Wizarainaahidi kuendelea kuzingatia maoni na ushauri kutoka kwaWaheshimiwa Wabunge wote wakati wa kujadili Taarifa hiiya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara yangu kwa mwaka 2018/2019 na Mpango na Bajeti ya mwaka 2019/2020. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, napenda kutoa shukrani zangu zadhati kwa Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji,Mbunge na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango kwa msaadamkubwa na ushirikiano anaonipatia katika kusimamiautekelezaji wa majukumu ya Wizara. (Makofi)

Page 41: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

41

Aidha, nawashukuru Bwana Doto James, Katibu MkuuHazina na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Naibu Makatibu Wakuu,Amina Shabaan, Khatibu Kazungu na Bwana Adolf Ndugurukwa kusimamia shughuli za kiutendaji za Wizara kwa ufanisi.Vilevile nawashukuru Makamishna, Wakurugenzi, Wakuu waTaasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango, Wakuuwa Vitengo, wafanyakazi wote wa Wizara kwa kutimizawajibu wao wa kuwatumikia Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya maneno haya yashukrani naomba sasa nijielekeze katika hoja yangu yenyemaeneo makuu mawili ambayo ni mapitio ya utekelezaji wampango na bajeti ya Wizara kwa mwaka 2018/2019 nampango na bajeti kwa mwaka 2019/2020.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2018/2019Bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango inatekelezwa katikamafungu nane ya kibajeti ambayo ni Fungu 50 – Wizara yaFedha ya Mipango, Fungu 21 – Hazina, Fungu 22 – Deni laTaifa, Fungu 23 – Mhasibu Mkuu wa Serikali, Fungu 7 – Ofisi yaMsajili wa Hazina, Fungu 10 – Tume ya Pamoja ya Fedha,Fungu 13 – Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramu na Fungu45 – Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa mpango na bajetiya Wizara kwa mwaka 2018/2019; katika kuhakikisha azmaya Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga uchumi waViwanda na kuwaletea Watanzania maendeleo inafikiwa,Wizara iliandaa mpango na bajeti ya mwaka 2018/2019 kwakuzingatia Miongozo mbalimbali ya kitaifa, kikanda nakimataifa ambayo ni pamoja na Dira ya Maendeleo ya Taifaya mwaka 2025, Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa MiakaMitano, Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti wamwaka 2018/2019, Sheria ya Bajeti Na. 11 ya mwaka 2015,Ilani ya Uchagu ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015,Ajenda ya Kamisheni ya Umoja wa Afrika 2063 na Malengoya Maendeleo Endelevu ya mwaka 2030. (Makofi)

Aidha mpango na bajeti ilizingatia hadi na maelekezoyaliyotolewa na Mheshimiwa Rais katika hotuba yake ya

Page 42: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

42

uzinduzi wa Bunge la Kumi na Moja la Jamhuri ya Muunganowa Tanzania, ushauri na maoni ya Kamati ya Kudumu yaBunge ya Bajeti pamoja na Sera Mbalimbali za Serikali.

Mheshimiwa Spika, mapato na matumizi ya Wizarakwa mwaka 2018/2019; muhtasari wa mapato na matumiziya Wizara kwa mwaka wa fedha 2018/2019 tumeyaoneshakwenye kitabu cha hotuba yangu kuanzia ukurasa wa sitampaka wa tisa.

Mheshimiwa Spika, napenda sasa nitumie fursa hiikulieleza Bunge lako tukufu kuhusu majukumu yaliyotekelezwana Wizara pamoja na taasisi zilizo chini yake kwa kipindi chakuanzia Julai, 2018 hadi kufikia April i, 2019 ambayoyameainishwa katika hotuba yangu kuanzia ukurasa wa tisahadi ukurasa wa 124.

Mheshimiwa Spika, kwanza ni kubuni na kusimamiautekelezaji wa sera za uchumi jumla; malengo ya uchumijumla kwa mwaka 2018/2019 yalikuwa kuhakikisha Pato laTaifa linakua kwa asilimia 7.2 mwaka 2018; mfumuko wa beiunabaki katika wigo wa tarakimu moja; mapato ya ndaniyanafikia asilimia 15.8 ya pato la Taifa na mapato ya kodiyanafikia asilimia 13.6 ya Pato la Taifa na nakisi ya bajetiinafikia asilimia 3.2.

Mheshimiwa Spika, uchumi wa nchi yetu umeendeleakuimarika ambapo mwaka 2018, Pato la Taifa kwa kutumiabei ya kizio ya mwaka 2015 li l ikua kwa asil imia 7.0ikilinganishwa na asilimia 6.8 mwaka 2017. Sekta zilizokua kwakasi kubwa ni pamoja na sanaa na burudani (asilimia 13.7);ujenzi (asilimia 12.9); usafirishaji na uhifadhi mizigo (asilimia11.8) na habari na mawasiliano (asilimia 9.1).

Mheshimiwa Spika, ukuaji huu wa uchumi umeendasambamba na utolewaji wa huduma bora kwa wananchizikiwemo maji, afya, umeme, elimu na ujenzi wa miundombinuya reli, bandari, viwanja vya ndege, madaraja na barabarapamoja na kuimarisha usafiri wa anga. (Makofi)

Page 43: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

43

Mheshimiwa Spika, mfumuko wa bei umeendeleakushuka na kubakia katika kiwango cha tarakimu moja. Kwamwezi Aprili, 2019 mfumuko wa bei ulikuwa asilimia 3.2ikilinganishwa na asilimia 3.8 katika kipindi kama hicho mwaka2018. Hali hii imetokana na kuimarika kwa upatikanaji wachakula katika masoko ya ndani na nchi jirani, kutengamaakwa bei za mafuta katika soko la dunia, usimamizi madhubutiwa sera za bajeti na fedha na utulivu wa thamani ya shilingiya Tanzania dhidi ya sarafu nyingine. Utulivu huu wa beiumesaidia wazalishaji, wanunuzi na walaji kuweka mipangona mikakati ya muda mrefu bila kuhofia mabadiliko ya marakwa mara ya bei ya malighafi na bidhaa.

Mheshimiwa Spika, upande wa uandaaji na ufuatiliajiwa Mpango wa Maendeleo wa Taifa; Wizara imefanikiwakufuatilia utekelezaji wa miradi 102 ya maendeleo kati ya 179.Miradi iliyofuatiliwa iko katika sekta za viwanda, maji, kilimo,nishati, uvuvi, afya, elimu, madini, sheria, ujenzi na uchukuzi.Ufuatiliaji huo umesaidia kurekebisha upungufu uliojitokezakatika utekelezaji na kuainisha hatua za kuzingatiwa katikakutayarisha Mpango wa mwaka 2019/2020.

Mheshimiwa Spika, kusimamia ukusanyaji wa mapatoya Serikali na nitaanza mapato ya kodi na yasiyo ya kodi;katika mwaka 2018/2019 Wizara il ipanga kusimamiaukusanyaji wa mapato ya ndani ikijumuisha mapato yaHalmashauri ya jumla ya shilingi trilioni 20.89. Kati ya hizomapato ya kodi yalikuwa shilingi trilioni 18.0, Halmashaurishilingi bilioni 735.6 na mapato yasiyo ya kodi shilingi trilioni2.16. Hadi kufikia Aprili, 2019 mapato ya ndani yakijumuishamapato ya Halmashauri yalifikia shilingi trilioni 15.46. Kati yakiasi hicho mapato ya kodi yalikuwa shilingi trilioni 12.9 sawana asilimia 87.4, mapato yasiyo ya kodi shilingi trilioni 2.04 sawana asilimia 122 na mapato ya Halmashauri shilingi bilioni 529.25sawa na asilimia 72 ya lengo la kipindi hicho.

Mheshimiwa Spika, kati ya mapato yasiyo ya kodi yakiasi cha shilingi trilioni 2.04 yaliyopatikana hadi kufikia Aprili,2019 jumla ya shilingi bilioni 600.45 zimekusanywa na Wizaraya Fedha na Mipango sawa na asilimia 100.44 ya lengo la

Page 44: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

44

kukusanya shilingi bilioni 597.81. Mafanikio haya yametokanana kuimarishwa kwa ufuatiliaji na usimamizi wa mashirika,makampuni na taasisi za umma ambazo Serikali imewekeza.

Mheshimiwa Spika,ili kuendelea kuleta uwazi na ufanisikatika ukusanyaji wa mapato, Wizara ilipanga kuunganishaWizara, Idara na Taasisi za Serikali 300 kwenye Mfumo waSerikali wa Kielektroniki wa Ukusanyaji na Usimamizi waMaduhuli (Government e-Payment Gateway). Hadi kufikiaAprili, 2019 jumla ya Taasisi 210 zimeunganishwa kwenyemfumo wa GePG ikiwa ni asilimia 70 ya lengo. Aidha, hadisasa jumla ya taasisi 410 kati ya taasisi 667 zimeunganishwana zinakusanya mapato kupitia mfumo huu. Mfumo huuunaiwezesha Serikali kuona moja kwa moja miamala yaukusanyaji wa mapato na kujua kiwango cha mapatokinachokusanywa kwa siku.

Mheshimiwa Spika, misaada na mikopo kutoka kwawashirika wa maendeleo; katika mwaka 2018/2019 Wizarailipanga kuratibu upatikanaji wa misaada na mikopo nafuuya kiasi cha shilingi trilioni 2.67 kutoka kwa washirika waMaendeleo ili kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo.Hadi kufikia mwezi Aprili, 2019 misaada na mikopo ilifikiashilingi trilioni 1.70 sawa na asilimia 86 ya lengo la kipindi hicho.

Mheshimiwa Spika, mikopo ya ndani na nje yenyemasharti ya kibiashara; katika mwaka 2018/2019 Wizarailitarajia kuratibu upatikanaji wa mikopo ya ndani na njeyenye masharti ya kibiashara ya jumla ya shilingi trilioni 8.90.Kati ya hizo shilingi trilioni 3.11 ni mikopo ya nje, shilingi trilioni1.19 ni mikopo ya ndani na shilingi trilioni 4.60 ni mikopo yandani ya kulipia hatifungani zilizoiva. Hadi kufikia Aprili, 2019kiasi cha shilingi bilioni 692.30 kilikopwa kutoka nje na shilingitrilioni 3.3 zilikopwa kutoka soko la ndani zikijumuisha malipoya dhamana za Serikali zilizoiva.

Mheshimiwa Spika, usimamizi wa deni la Serikali; hadikufikia Aprili, 2019 deni la Serikali liliongezeka na kufikia shilingitrilioni 51.03 kutoka shilingi trilioni 49.86 Aprili, 2018. Ongezekohili ni sawa na asilimia 2.35. Kati ya kiasi hicho, deni la ndani

Page 45: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

45

lilikuwa shilingi trilioni 13.25 na deni la nje lilikuwa shilingi trilioni37.78. Ongezeko la deni la Serikali linatokana na kupokelewakwa mikopo mipya kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbaliya maendeleo ikiwemo ujenzi wa Jengo la Tatu la Kiwanjacha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, ujenzi wa reliya kati kwa kiwango cha kimataifa, ujenzi wa miradi yaumeme na ujenzi wa barabara na madaraja makubwa.

Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kufanyatathmini ya Deni la Taifa kila mwaka ili kupima uhimilivu wake.Matokeo ya tathmini iliyofanyika Desemba, 2018 inaoneshakuwa Deni la Taifa ni himilivu katika kipindi cha muda mfupi,wa kati na mrefu. Tathmini hiyo ilionesha kuwa uwiano wathamani ya sasa ya Deni la Taifa (present value of total publicdebt) kwa Pato la Taifa ni asilimia 27.2 ikilinganishwa naukomo wa asilimia 70; thamani ya sasa ya Deni la nje pekee(present value of external debt) kwa Pato la Taifa ni asilimia22.2 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 55; thamani ya sasaya deni la nje kwa mauzo ya nje ni asilimia 157.3 ikilinganishwana ukomo wa asilimia 240 na ulipaji wa deni la nje kwakutumia mauzo ya bidhaa nje ni asilimia 15.2 ikilinganishwana ukomo wa asilimia 23.

Mheshimiwa Spika, Serikali ilitenga kiasi cha shilingitrilioni 1.41 kwa ajili ya kulipa riba ya deni la ndani. Hadi kufikiaAprili, 2019 kiasi cha shilingi trilioni 1.06 kimelipwa sawa naasilimia 75.18 ya lengo. Aidha, Serikali ilitenga shilingi bilioni689.67 kwa ajili ya kulipa riba ya deni la nje. Hadi kufikia Aprili,2019 shilingi bilioni 588.30 zimelipwa sawa na asilimia 85.30 yalengo. Vilevile Serikali ilitenga shilingi trilioni 1.66 kwa ajili yakulipia mtaji wa deni la nje ambapo hadi kufikia Aprili, 2019shilingi trilioni 1.23 zimelipwa sawa na asilimia 74.10 ya lengo.Wizara itaendelea kusimamia deni la Serikali kwa kuzingatiaSheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada, Sura 134 pamojana mkakati wa muda wa kati wa kusimamia madeni.

Mheshimiwa Spika, malipo ya pensheni na michangoya mwajiri kwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii; Serikali ilitengakiasi cha shilingi trilioni 1.19 kwa ajili ya kulipia mchango wamwajiri kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Hadi kufikia Aprili,

Page 46: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

46

2019 kiasi cha shilingi bilioni 797.29 sawa na asilimia 67.0 yalengo kililipwa ikiwa ni uwasilishaji wa michango ya mwajirikwa watumishi wote wa Umma walio kwenye payroll yaSerikali na kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019 Serikaliilitenga kiasi cha shilingi bilioni 424.74 kwa ajili ya kulipa mafaoya kustaafu na mirathi kwa wastaafu wanaolipwa na Hazina.Hadi kufikia Aprili, 2019 kiasi cha shilingi bilioni 314.92 sawa naasilimia 64.14 kilitumika kulipa wastaafu 4,016, mirathi ililipwakwa warithi 854 na pensheni kwa kila mwezi kwa wastaafu57,055. Katika kurahisisha ulipaji wa mafao ya wastaafu,Serikali imetengeneza mfumo wa ukokotoaji wa mafao,uhifadhi wa kumbukumbu pamoja na utoaji wa vitambulishovya kielektroniki kwa kutumia mfumo wa Treasury PensionersPayment System (TPPS).

Mheshimiwa Spika, kubuni na kusimamia mifumo yataarifa za fedha; Wizara imefanikiwa kubuni mfumo waufuatiliaji wa mali za Serikali ujulikanao kama GovernmentAsset Management Information System (GAMIS) kwa ajili yakurahisisha usimamizi na udhibiti wa mali za Serikali. Aidha,Wizara imebuni na kuanza kutengeneza mfumo wa usimamiziwa fedha za miradi ya Maendeleo kutoka kwa washirika wamaendeleo zinazopelekwa moja kwa moja kwa watekelezaji(Direct to Projects Funds) ambao unatarajiwa kuanzakutumika Julai, 2019. Lengo ni kutambua miradi yote nakuweka uwazi kuhusu fedha zinazotolewa na washirika wamaendeleo bila kupitia Mfuko Mkuu wa Serikali.

Mheshimiwa Spika, majukumu mengineyaliyotekelezwa chini ya usimamizi wa mifumo ya taarifa zafedha ni kama ilivyooneshwa kwenye kitabu cha hotubayangu kuanzia ukurasa wa 24 hadi ukurasa wa 28.

Mheshimiwa Spika, kuandaa na kufuatilia utekelezajiwa bajeti ya Serikali; katika kuhakikisha Mamlaka za Serikaliza Mitaa zinatoa huduma bora kwa wananchi, Wizaraimeendelea kuzijengea uwezo kwa kuzipatia fedha zakutekeleza miradi ya kimkakati ili ziweze kujitegemea

Page 47: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

47

kimapato na kupunguza utegemezi wa ruzuku ya Serikali Kuu.Kwa mwaka 2018/2019 Wizara imefanya uchambuzi wamiradi ya kimkakati 111 yenye thamani ya shilingi bilioni 749.63kutoka kwenye Halmashauri 67 kwa ajili ya kuzingatiwa katikabajeti ya 2019/2020.

Mheshimiwa Spika, matokeo ya uchambuzi huo nikuwa jumla ya miradi 15 yenye thamani ya shilingi bilioni137.38 kutoka Halmashauri 12 ilikidhi vigezo na mikatabakusainiwa. Orodha ya Halmashauri na idadi ya miradi ni kamaifuatavyo; Halmashauri ya Jiji la Tanga mradi mmoja;Halmashauri ya Mwanza miradi miwili; Halmashauri zaManispaa ya Kinondoni miradi miwili, Kigamboni mradimmoja, Iringa mradi mmoja, Ilemela miradi miwili; Halmashauriya Mji wa Tarime mradi mmoja; Halmashauri ya Wilaya yaBagamoyo mradi mmoja, Biharamuro mradi mmoja, Kibahamradi mmoja na Hanang mradi mmoja.

Mheshimiwa Spika, maelezo ya kina kuhusu kuandaana kufuatilia utekelezaji wa Bajeti ya Serikali ni kamainavyooneshwa kwenye kitabu cha hotuba yangu kuanziaukurasa wa 28 hadi ukurasa wa 32.

Mheshimiwa Spika, usimamizi na udhibiti wa matumiziya fedha za umma; Wizara kupitia Mkaguzi wa Ndani Mkuuwa Serikali imefanya uhakiki wa madeni ya malimbikizo yamishahara katika Wizara, Idara zinazojitegemea na Wakalawa Serikali 142; Sekretarieti za Mikoa 24 na Mamlaka ya Serikaliza Mitaa 185. Aidha, Wizara imeendelea kuhakikishausimamizi na udhibiti wa matumizi ya fedha za ummazinazotolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbaliya maendeleo kwa kufanya ukaguzi maalum katika Wakalawa Nishati Vijijini (REA) na katika Hospitali ya Taaluma na Tibaya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili,Kampasi ya Mloganzila, ambapo mapendekezo ya ukaguziyaliwasilishwa kwa taasisi husika kwa ajili ya kuyafanyia kaziili kuleta ufanisi katika utekelezaji wa miradi.

Mheshimiwa Spika, majukumu mengineyaliyotekelezwa katika kusimamia na kudhibiti matumizi ya

Page 48: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

48

fedha za umma tumeyaonesha kwenye kitabu cha hotubayangu kuanzia ukurasa wa 33 hadi ukurasa wa 35.

Mheshimiwa Spika, usimamizi wa mali za Serikali;Wizara ilifanya uhakiki wa mali na madeni katika taasisizilizounganishwa ambazo ni Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (PSPF,GEPF, PPF na LAPF) na Mamlaka za Maji Dar es Salaam(DAWASA na DAWASCO). Baada ya utambuzi wa mali namadeni ya taasisi hizo, Serikali itahakikisha kuwa inachukuahatua stahiki kulingana na matokeo ya uhakiki. Wizara piaimefanya uhakiki wa majengo yaliyobaki wazi Jijini Dar esSalaam baada ya Serikali kuhamishia shughuli zake JijiniDodoma kwa lengo la kuandaa utaratibu wa kugawamajengo hayo kwa baadhi ya taasisi za Serikali ambazo zinauhitaji wa majengo hayo.

Mheshimiwa Spika, majukumu mengineyaliyotekelezwa katika usimamizi wa mali za Serikali nitumeyaonesha kwenye kitabu cha hotuba yangu kuanziaukurasa wa 35 mpaka ukurasa wa 37.

Mheshimiwa Spika, udhibiti wa utakasishaji wa fedhaharamu na ufadhili wa ugaidi, Wizara kupitia Kitengo chaUdhibiti wa Fedha Haramu (FIU) imeendelea kusimamiautekelezaji wa Sheria za Udhibiti wa Fedha Haramu kwakutekeleza majukumu mbalimbali ikiwa ni pamoja nakupokea na kuchambua taarifa 1,305 za miamala shukukutoka kwa watoa taarifa na kuwasilisha taarifa fiche 32kwenye vyombo vinavyosimamia utekelezaji wa sheria kwaajili ya uchunguzi; kupokea taarifa 5,536 zinazohusu usafirishajifedha taslimu na hati za malipo mipakani; kuratibu nakusimamia zoezi linaloendeshwa na ESAAMLG la tathmini yamifumo ya udhibiti wa fedha haramu (AML/CFT MutualEvaluation); kuimarisha ushirikiano na FIU za nchi za Djibouti,Sudan, Ethiopia, Somalia, China, Mauritius na pia kufanyamajadiliano ya kuingia katika makubaliano ya ushirikiano naFIU za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jamaica, Japan,Trinidad and Tobago, Botswana, Canada, Jamhuri ya Kongona Kazakhstan. Aidha, Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu

Page 49: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

49

imekagua benki nne ili kujiridhisha na utekelezaji wa Sheriaza Udhibiti wa Fedha Haramu.

Mheshimiwa Spika, majukumu mengineyaliyotekelezwa katika udhibiti wa utakasishaji wa fedhaharamu na ufadhili wa ugaidi ni kama inavyooneshwakwenye kitabu cha hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 37 hadiukurasa wa 39.

Mheshimiwa Spika, Tume ya Pamoja ya Fedha;utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Pamoja ya Fedhaumeoneshwa kuanzia ukurasa wa 39 hadi ukurasa wa 40.

Mheshimiwa Spika, usimamizi wa mashirika na taasisiza umma; katika mwaka 2018/2019 Ofisi ya Msajili wa Hazinakwa kushirikiana na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu zaSerikali imefanya Ukaguzi Maalum katika Kampuni 34 ambazoSerikali ina umiliki wa hisa chache. Aidha, Ofisi ya Msajili waHazina imeandaa mpango kazi wa kutekeleza mapendekezoyaliyotolewa katika ripoti ya ukaguzi na utekelezajiunaendelea. Utekelezaji wa mpango kazi unajumuisha kupitiamikataba ya ubia, uendeshaji na utaalam kwa kampunihusika. Lengo kuu la zoezi hili ni kubaini sababu za Serikalikupata kiwango kidogo cha gawio au kutopata kabisa nakuchukua hatua stahiki ili kuongeza mapato ya Serikali. Aidha,ufuatil iaji wa madeni kwa wawekezaji waliobainikakutomaliza kulipa bei ya ununuzi wa kampuni hizounaendelea.

Mheshimiwa Spika, majukumu mengineyaliyotekelezwa katika usimamizi wa mashirika na taasisi zaumma tumeyaonesha kwenye kitabu cha hotuba yangukuanzia ukurasa wa 40 hadi ukurasa wa 47.

Mheshimiwa Spika, uratibuwa mikakati ya kupunguzaumaskini; katika mwaka 2018/2019 Wizara imefanyauchambuzi wa awali wa utafiti wa mapato na matumizi yakaya binafsi wa mwaka 2017/2018 ambao unaonesha kuwaumaskini wa mahitaji ya msingi umepungua kutoka asilimia28.2 mwaka 2011/2012 hadi asilimia 26.4 mwaka 2017/2018.

Page 50: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

50

Kiwango cha umaskini wa chakula kimepungua kutokaasilimia 9.7 mwaka 2011/2012 na kufikia asilimia 8.0 mwaka2017/2018.

Mheshimiwa Spika, tathmini ya viashiria vya umaskiniusio wa kipato unaonesha tumefanya vizuri katika kuboreshahali ya makazi, umeme, huduma za maji safi na salama, vyoo,umiliki wa vyombo vya usafiri na mawasiliano. Viashiriavinaonesha kuwa makazi yaliyojengwa kwa kutumia zege,mawe, saruji na vyuma yameongezeka. Vilevile kayazinazoishi katika nyumba zenye paa za kisasa zimeongezekakutoka asilimia 68 mwaka 2011/2012 hadi asilimia 84.1 mwaka2017/2018. Aidha, asilimia 78.8 ya kaya zinaishi kwenyenyumba zilizojengwa kwa kuta imara mwaka 2017/18ikilinganishwa na asilimia 46.0 mwaka 2011/2012. Vilevileasilimia 50.1 ya Kaya zinaishi kwenye nyumba zilizojengwakwa sakafu imara mwaka 2017/2018 ikilinganishwa na asilimia40 mwaka 2011/2012.

Mheshimiwa Spika, majukumu mengineyaliyotekelezwa katika kuratibu mikakati ya kupunguzaumaskini ni kama tumeionesha kwenye kitabu cha hotubayangu kuanzia ukurasa wa 48 mpaka ukurasa wa 52.

Mheshimiwa Spika, ununuzi wa umma; Wizaraimefanikiwa kufanya marekebisho ya Kanuni ya 164 ya Sheriaya Ununuzi wa Umma ili kumpa mzabuni haki ya kupatataarifa ya ukamilishwaji wa mchakato wa ununuzi. Aidha,Kanuni ya 226 imerekebishwa kumpa mamlaka Mlipaji Mkuuwa Serikali kutoa idhini kwa Maafisa Masuuli kuongeza idadiya wajumbe wa timu ya majadiliano kwenye miradi mikubwayenye maslahi kwa Taifa. Marekebisho hayo yamezingatiamaoni ya wadau juu ya changamoto za utekelezaji wa Sheriaya Ununuzi wa Umma, Sura 410.

Mheshimiwa Spika, majukumu mengineyaliyotekelezwa katika kusimamia ununuzi wa ummayameoneshwa kwenye kitabu changu yangu kuanzia ukurasawa 52 mpaka ukurasa wa 60.

Page 51: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

51

Mheshimiwa Spika, ubia kati ya sekta ya umma nasekta binafsi yaani (PPP); Wizara imepokea mapendekezoya miradi ya ubia ipatayo 33, kati ya hiyo miradi sita imekidhivigezo na kufanyiwa kazi. Miradi hiyo ni Mradi wa Uboreshajiwa Huduma za Usafiri Dar es Salaam Awamu ya Kwanza;Mradi wa Viwanda Vitatu vya Uzalishaji Dawa muhimu naVifaa Tiba; Mradi wa Usambazaji wa Gesi asilia katika Jiji laDar es Salaam, Lindi na Mtwara; Mradi ya Ujenzi ya Hoteli yaNyota Nne; Kituo cha Biashara katika Kiwanja cha Ndegecha Kimataifa cha Julius Nyerere na Mradi wa ujenzi wahosteli ya wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE).Aidha, Wizara imekamilisha uchambuzi wa mawasilisho yaawali ya miradi 22 ya Mamlaka za Serikali za Mitaa nawahusika watajulishwa kuhusu maeneo ya kufanyia kazi kwamujibu wa sheria, mwongozo na taratibu za PPP.

Mheshimiwa Spika, majukumu mengineyaliyotekelezwa kuhusu eneo hili Ubia tumeyaonesha kwenyekitabu cha hotuba kuanzia ukurasa wa 60 mpaka ukurasawa 65.

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa majukumu yamashirika na taasisi za umma; utekelezaji wa majukumu yataasisi na mashirika yaliyo chini ya Wizara kwa mwaka 2018/2019 ni kama inavyooneshwa kwenye kitabu cha hotubayangu ukurasa wa 65 mpaka ukurasa wa 114.

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi; katikamwaka 2018/2019 Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu zaSerikali imefanya ukaguzi wa hesabu za Wizara na Idara zaSerikali 65; Vyama vya Siasa 14; Sekretariati za Mikoa 26;Wakala za Serikali 33; Mifuko Maalum 16; Taasisi nyingine zaSerikali 42 na Balozi za Tanzania 41. Aidha, ukaguzi ulifanyikakwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa 185 na Mashirika yaUmma 176. Vilevile ofisi imefanya ukaguzi maalum kwenyeTaasisi zifuatazo; Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA); Mfukowa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF); Wakala wa VipimoTanzania (WMA); Taasisi ya Elimu Tanzania; Tume ya Taifa yaUchaguzi; Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA); Jeshila Polisi; na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege.

Page 52: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

52

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi pia ilifanyaukaguzi wa miradi ya maendeleo 469 na ripoti za ukaguzizimetolewa. Aidha, katika ukaguzi wa ufanisi, jumla ya taarifa10 zimetolewa katika kipindi kilichoishia Machi, 2019. Vilevile,mpaka kufikia Aprili, 2019 ofisi imetoa ripoti kuu tano. Taarifahizo ni muhtasari wa jumla ya taarifa 1,042 za ukaguzizilizotolewa kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2017/2018.

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa miradi yamaendeleo; maelezo ya utekelezaji wa miradi ya maendeleoiliyo chini ya Wizara kwa mwaka 2018/2019 tumeioneshakwenye kitabu cha hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 117mpaka ukurasa wa 121.

Mheshimiwa Spika, changamoto na mikakati yakukabiliana nazo; pamoja na mafanikio yaliyopatikana katikautekelezaji wa bajeti ya Wizara, changamoto zifuatazozilijitokeza katika mwaka huu wa fedha ambazo ni zifuatazo:-

(i) Masharti yasiyo rafiki ya mikopo kwenye masoko ya fedhaduniani;

(ii) Kupungua na kutokupatikana kwa wakati kwa fedhakutoka kwa washirika wa maendeleo katika kugharamiamiradi mbalimbali ya maendeleo; na

(iii) Ni Mwamko mdogo wa kulipa kodi kwa hiari, kudai aukutoa risiti za kielektroniki.

Mheshimiwa Spika, mkakati ya kukabiliana nachangamoto; katika kukabiliana na changamoto zautekelezaji wa bajeti Wizara inaendelea kuchukua hatuambalimbali zikiwemo zifuatazo:-

(i) Kuhakikisha kuwa Wizara na Taasisi zote za umma zinatumiaMfumo wa Serikali wa Kielektroniki wa ukusanyaji na usimamiziwa maduhuli yaani GePG;

(ii) Kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa lengo lakupunguza utegemezi;

Page 53: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

53

(ii i) Kuboresha mfumo wa usimamizi wa mashine zakielektroniki za kutolea risiti ili ziweze kutumika kwa kilamuamala unaofanywa. Uboreshaji huu utaondoa uwezekanowa kughushi risiti na kupunguza mianya ya ukwepaji wa kodi;

(iv) Kudhibiti biashara ya magendo kupitia bahari, maziwa,mipaka, na njia zisizo rasmi kwa kushirikiana na taasisi nyingineza Serikali kama TANROADS, Mamlaka ya Bandari, Jeshi laPolisi, Jeshi la Wanamaji na Usalama wa Taifa;

(v) Kuongeza jitihada za ukusanyaji wa kodi ya majengo kwakushirikisha wadau muhimu wakiwemo Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI,Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka ya Serikali za Mitaa na Ofisiya Taifa ya Takwimu;

(vi) Kuendelea kusimamia utekelezaji wa bajeti kwakuzingatia Sheria ya Bajeti Na. 11 ya mwaka 2015;

(vii) Kuendelea kuimarisha ushirikiano na washirika wamaendeleo kwa kutekeleza mwongozo wa ushirikiano ilikuhakikisha fedha zilizoahidiwa zinatolewa na kwa wakati;na

(viii) Kuendelea na majadiliano na taasisi za fedha zakimataifa ili kuhakikisha kuwa fedha zinazotokana na mikopoya kibiashara zinapatikana kwa kipindi kilichobaki.

Mheshimiwa Spika, malengo ya mpango na bajetikwa mwaka 2019/2020; naomba sasa nieleze kuhusumalengo ya mpango na bajeti ya Wizara ya Fedha naMipango na Taasisi zake kwa mwaka 2019/2020;

Mheshimiwa Spika, mwaka 2019/2020 Wizaraitaendelea kusimamia majukumu mbalimbali ikiwa ni pamojana yafuatayo:-

(i) Kubuni na kusimamia utekelezaji wa sera za uchumi jumlazinazolenga kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi;

Page 54: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

54

(ii) Kuratibu uandaaji na ufuatiliaji wa mipango ya maendeleoya Taifa;

(iii) Kusimamia hatua mbalimbali za ukusanyaji wa mapatoya ndani ili kuwezesha utekelezaji wa bajeti ya Serikali kwaufanisi;

(iv) Kuratibu upatikanaji wa misaada na mikopo kutoka kwawashirika wa maendeleo na kuhakikisha kuwa inaendeleakutolewa kama ilivyoahidiwa na kwa wakati ili kugharamiautekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo;

(v) Kusimamia Deni la Serikali kwa kuhakikisha inakopakwenye vyanzo vyenye riba nafuu;

(vi) Kufanya ufuatiliaji na tathmini ya mikopo iliyodhaminiwana Serikali ili kuhakikisha wadaiwa wanalipa madeni husikakwa wakati kuepusha uwezekano wa kuongeza mzigo kwaSerikali wa kulipa mikopo hiyo;

(vii) Kusimamia mifumo ya udhibiti wa matumizi ya fedha zaumma ikiwa ni pamoja na kufanya maboresho ya mfumowa Akaunti Jumuifu ya Hazina (Treasury Single Account) kwalengo la kuboresha mfumo wa matumizi ya umma ilikuiongezea Serikali uwezo wa kugharamia shughuli zake kwawakati;

(viii) Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa bajeti ya Serikali;

(ix) Kusimamia na kudhibiti matumizi ya fedha za umma ilikupata thamani halisi ya fedha katika utekelezaji wa miradiya maendeleo;

(x) Kuratibu zoezi la uthamini wa mali katika taasisi za Serikaliili kuwa na taarifa sahihi za mali pamoja na kuendeleakuondoa mali chakavu, na zile sinzia yaani dormant nazilizokwisha muda wake;

(xi) Kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Udhibiti wa FedhaHaramu kwa kupokea na kuchambua taarifa za miamala

Page 55: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

55

shuku zinazohusu utakasishaji wa fedha haramu na ufadhiliwa ugaidi;

(xii) Kusimamia zoezi linaloendelea la tathmini ya kitaifa yamifumo ya kudhibiti utakasishaji fedha haramu na ufadhili waugaidi yaani (mutual evaluation). Tathmini hiyo itaijengeanchi sifa na uwezo wa kushirikiana na nchi nyingine dunianikwa kubadilishana taarifa zinazohusu udhibiti na utakasishajiwa fedha haramu na ufadhili wa vitendo vya kigaidi;

(xiii) Kusimamia mashirika na taasisi za umma kwa kuimarishaukusanyaji wa maduhuli kutoka katika taasisi na mashirika yaumma na kampuni ambazo Serikali ina hisa, kuhakikishaviwanda vilivyobinafsishwa vinafanya kazi kwa ufanisi,kurejesha viwanda vilivyoshindwa kutekeleza majukumu yakekwa mujibu wa makubalianona kuwapatia wawekezajiwengine wenye uwezo na nia ya kuviendeleza;

(xiv) Kuratibu mikakati ya kupunguza umaskini;

(xv) Kusimamia ununuzi wa umma;

(xvi) Kuratibu shughuli za PPP nchini; na

(xvii) Kulipa mafao ya kustaafu na mirathi kwa wastaafuwanaolipwa na Hazina.

Mheshimiwa Spika, maelezo ya kina kuhusu mpangowa utekelezaji wa majukumu ya Wizara yangu ni kamailivyooneshwa kwenye kitabu cha hotuba kuanzia ukurasawa 125 hadi ukurasa wa 145.

Mheshimiwa Spika, usimamizi na uratibu wa taasisi namashirika ya umma chini ya Wizara; mipango katika mwaka2019/2020 kwa upande wa mashirika na taasisi za umma zilizochini ya Wizara ni kama ilivyooneshwa kwenye kitabu chahotuba kuanzia ukurasa wa 147 mpaka ukurasa wa 167.

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi; katikamwaka 2019/2020, Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi imepanga

Page 56: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

56

kutekeleza vipaumbele nane ikiwa ni pamoja na kufanyaukaguzi wa mafungu ya bajeti ya Wizara, Idara za Serikalizinazojitegemea, Wakala na Taasisi za Serikali, Sekretariati zaMikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa katika Mikoa yote nchini,Mashirika ya Umma; kufanya ukaguzi wa miradi yamaendeleo inayofadhiliwa na wahisani; kufanya kaguzi zakiufundi katika maeneo yenye uwekezaji mkubwa warasilimaliza umma kama vile ujenzi wa barabara na viwanjavya ndege, reli ya kisasa, miradi ya umeme; kufanyamaboresho ya mfumo wa ukaguzi kwa kutumia TEHAMA nakukagua ukusanyaji wa mapato ya kodi na yasiyo ya kodi;ukaguzi wa ufanisi, kaguzi maalum na kaguzi za kiuchunguziyaani (forensic audits) katika maeneo yatakayoainishwa; nakuwajengea wakaguzi uwezo wa kufanya ukaguzi katikamaeneo mapya ya ukaguzi pamoja na ukaguzi katika uhalifuwa kifedha kwa kutumia mtandao yaani financial crimesauditing.

Mheshimiwa Spika, makadirio ya mapato na matumizikwa mwaka 2019/2020 kwanza makadirio ya mapato; katikamwaka 2019/2020 Wizara inakadiria kukusanya maduhuli kiasicha shilingi bilioni 967,042,379,000kutoka katika vyanzombalimbali ikiwa ni pamoja na gawio, kodi za pango,marejesho ya mikopo, michango kutoka katika taasisi namashirika ya umma, mauzo ya leseni za udalali na mauzo yanyaraka za zabuni. Mchanganuo wa maduhuliyanayokadiriwa kukusanywa kwa mafungu ni kamainavyoonekana katika Jedwali Namba. 6 ukurasa wa 181 wakitabu cha hotuba yangu.

Mheshimiwa Spika, makadirio ya matumizi kwamwaka 2019/2020 kwa mwaka 2019/2020 Wizara ya Fedhana Mipango, Taasisi zake pamoja na Ofisi ya Taifa ya Ukaguziinakadiria kutumia kiasi cha shilingi 11,942,986,578,719; katiya fedha hizo, shilingi 11,212,404,636,988ni kwa ajili ya matumiziya kawaida na shilingi 730,581,941,731 ni matumizi yamaendeleo. Matumizi ya kawaida yanajumuisha shilingi608,371,517,988 kwa aji l i ya mishahara na shil ingi10,604,033,119,000 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo. Aidha,

Page 57: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

57

matumizi ya maendeleo yanajumuisha shilingi 677,000,000,000fedha za ndani na shilingi 53,581,941,731 fedha za nje.

Mheshimiwa Spika, maombi ya fedha kwa mafungu;Fungu 50 – Wizara ya Fedha na Mipango; katika Fungu hilikwa mwaka ujao wa fedha 2019/2020, Wizara inaombakuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:-

Matumizi ya Kawaida - shilingi 65,713,430,000; kati yahizo mishahara ni shilingi 37,920,916,000 na matumizimengineyo ni shilingi 27,792,514,000.

Miradi ya Maendeleo – shilingi 34,763,757,000; kati yahizo fedha za ndani ni shilingi 13,000,000,000; fedha za njeshilingi 21,763,757,000.

Mheshimiwa Spika, Fungu 21-Hazina; katika Fungu hilikwa mwaka ujao wa fedha 2019/2020, Wizara inaombakuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:-

Matumizi ya Kawaida shilingi 1,272,801,249,988ambapo mishahara ni shilingi 536,520,631,988; MatumiziMengineyo shilingi 736,280,618,000 ambazo ni kwa ajili yamatumizi ya Idara, Taasisi zilizo chini ya Fungu hili, pamoja namatumizi maalum. Miradi ya Maendeleo shil ingi683,713,888,733; kati ya hizo fedha za ndani ni shilingi656,000,000,000 na fedha za nje shilingi 27,717,888,733.

Mheshimiwa Spika, Fungu 22- Deni la Taifa; katikaFungu hili kwa mwaka ujao wa fedha, Wizara inaombakuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:-

Matumizi ya Kawaida – shilingi 9,730,012,708,000; katiya hizo mishahara ni- 8,885,708,000 na Matumizi Mengineyoshilingi 9,721,127,000,000.

Mheshimiwa Spika, Idara ya Mhasibu Mkuu wa SerikaliFungu 23; katika Fungu hili kwa mwaka 2019/2020, Wizarainaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:-

Page 58: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

58

Matumizi ya Kawaida shilingi 44,066,048,000 ambapomishahara ni shilingi 7,029,314,000 na Matumizi Mengineyoshilingi 37,036,734,000. Kwa upande wa Miradi ya Maendeleoshilingi 3,300,000,000 ambapo fedha za ndani ni shilingi2,000,000,000 na fedha za nje ni shilingi 1,300,000,000.

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Msajili wa Hazina - FunguNamba 7; katika Fungu hili kwa mwaka 2019/2020, Wizarainaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha Matumizi ya Kawaidashilingi 40,510,802,000na kati ya hizo mishahara ni 3,281,016,000na Matumizi Mengineyo shilingi 37,229,786,000. Miradi yaMaendeleo shilingi 2,300,000,000 Kati ya fedha hizo fedha zandani ni 1,000,000,000 na fedha za nje ni shilingi 1,300,000,000.

Mheshimiwa Spika, Fungu Namba10 – Tume yaPamoja ya Fedha; katika Fungu hili kwa mwaka 2019/2020Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha, Matumizi yaKawaida shilingi 2,207,935,000 kati ya hizo mishahara ni649,793,000 na Matumizi Mengineyo ni shilingi 1,558,142,000.

Mheshimiwa Spika, Fungu 13 – Kitengo cha Udhibiti waFedha Haramu; katika Fungu hili kwa mwaka ujao wa fedha,Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kamaifuatavyo; Matumizi Mengineyo shilingi 2,000,015,586,000 naMatumizi ya Maendeleo shilingi 200,295,998 ambazo ni fedhaza nje.

Mheshimiwa Spika, Fungu 45 - Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi;katika Fungu hili kwa mwaka ujao wa 2019/2020 Wizarainaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:-

(i) Matumizi ya Kawaida shilingi 55,076,878,000; kati ya fedhahizo mishahara ni shilingi 14,084,139,000 na MatumiziMengineyo ni shilingi 40,992,739,000.

(ii) Miradi ya Maendeleo ni shilingi 6,300,000,000. Kati ya hizo,fedha za ndani ni shilingi 5,000,000,000 na fedha za nje nishilingi 1,300,000,000.

Page 59: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

59

Mheshimiwa Spika, shukurani; napenda nirudie tenakumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kuwasilishahotuba hii mbele ya Bunge lako tukufu. Aidha, kwa namnaya pekee kabisa naomba nitumie fursa hii kuwashukuruwashirika wa maendeleo wote wakiwemo nchi na mashirikaya kimataifa ambao wamekuwa wakisaidia kwa namnambalimbali katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara.

Lakini vilevile napenda kuwashukuru Watanzaniawote wenye mapenzi mema na uzalendo kwa nchi yaoambao wamekuwa wakilipa kodi stahiki na kwa hiari.Naomba nitumie fursa hii kuwaambia kuwa mchango waokatika ujenzi wa Taifa letu unathaminiwa sana na Serikali nautaendelea kukumbukwa hata na vizazi vijavyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa napendanikushukuru tena wewe binafsi kwa kunipa nafasi yakuwasilisha hoja hii pamoja na Waheshimiwa Wabunge wotekwa kunisikiliza na hotuba hii inapatikana katika tovuti yaWizara kwa anuani ya www.mof.go.tz. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja. (Makofi)

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHESHIMIWADKT. PHILIP I. MPANGO (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI

MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA FEDHANA MIPANGO KWA MWAKA 2019/20 - KAMA

ILIVYOWASILISHWA MEZANI

1.0 Utangulizi

1. Mheshimiwa Spika, kutokana na taarifa iliyowasilishwandani ya Bunge lako Tukufu na Mwenyekiti wa Kamati yaKudumu ya Bunge ya Bajeti, naomba kutoa hoja kwamba,sasa Bunge lako lipokee na kujadili mapitio ya utekelezaji waMpango na Bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango kwamwaka 2018/19 pamoja na Makadirio ya Mapato naMatumizi kwa mwaka 2019/20. Aidha, naomba Bunge lakoTukufu likubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi

Page 60: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

60

ya Wizara ya Fedha na Mipango na Taasisi zilizo chini yakepamoja na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kwa mwaka 2019/20.

2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote, napenda kumshukuruMwenyezi Mungu, kwa kutujalia uhai na afya njema nakutuwezesha kukutana tena kushiriki mkutano huu wa Bungeunaojadili Bajeti ya mwaka 2019/20, ambayo ni ya Nne tanguSerikali ya Awamu ya Tano ilipoingia madarakani.

3. Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee kabisa, napendanitumie fursa hii kuwapongeza kwa dhati kabisa Viongoziwangu Wakuu wa Serikali, nikianza na Mhe. Dkt. John PombeJoseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa(Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kwa miongozo yao iliyojaa hekima, busara na uzalendo. Nidhahiri kwamba, katika kipindi cha takriban miaka mitatuna nusu ya uongozi wao, tumepata mafanikio mengi ambayokila mmoja wetu anapaswa kujivunia. Naomba MwenyeziMungu aendelee kuwajalia hekima, busara na afya njema ilidhamira zao za dhati za kuwaletea watanzania maendeleoziendelee kuleta manufaa kwetu na kwa vizazi vijavyo.

4. Mheshimiwa Spika, napenda pia nitumie fursa hii,kuwapongeza sana Mhe. Balozi Dkt. Augustine Philip Mahiga(Mb.), kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria,pamoja na Mhe. Prof. Palamagamba John Aidan Kabudi(Mb.), kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje naUshirikiano wa Afrika Mashariki. Nawaahidi ushirikiano wa haliya juu katika kutekeleza majukumu yetu ya kumsaidia Mhe.Rais ili shughuli za Serikali ziendelee kufanyika kwa ufanisi zaidi.

5. Mheshimiwa Spika, napenda kukupongeza wewe binafsi,Naibu Spika na Wenyeviti wote wa Bunge kwa kuendeshavizuri majadiliano ya Bajeti za Wizara mbalimbali. Aidha,napenda kumpongeza Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumuya Bunge ya Bajeti Mhe. George Boniface Simbachawene(Mb) na Makamu Mwenyekiti Mhe. Mashimba Mashauri Ndaki(Mb) kwa kuongoza vizuri majadiliano ya Kamati. Vilevile,

Page 61: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

61

nawashukuru wajumbe wote wa Kamati ya Bajeti kwamichango yao mizuri inayosaidia katika kutekeleza majukumuya Wizara kwa ufanisi. Wizara inaahidi kuendelea kuzingatiamaoni na ushauri watakaoutoa wakati wa kujadili taarifa hiiya utekelezaji wa Bajeti ya Wizara yangu kwa mwaka 2018/19 na Mpango na Bajeti ya mwaka 2019/20.

6. Mheshimiwa Spika, napenda kutoa shukrani zangu za dhatikwa Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji (Mb), NaibuWaziri wa Fedha na Mipango, kwa ushirikiano anaonipatiakatika kusimamia utekelezaji wa majukumu ya Wizara. Aidha,nawashukuru Bw. Doto M. James, Katibu Mkuu HAZINA naMlipaji Mkuu wa Serikali, Naibu Makatibu Wakuu Bi. AminaKh. Shaaban, Dkt. Khatibu M. Kazungu na Bw. Adolf H.Ndunguru kwa kusimamia shughuli za kiutendaji za Wizara kwaufanisi. Vilevile, nawashukuru Makamishna, Wakurugenzi,Wakuu wa Taasisi zilizoko chini ya Wizara ya Fedha naMipango, Wakuu wa Vitengo na wafanyakazi wote waWizara, kwa kutimiza wajibu wao wa kuwatumikiaWatanzania.

7. Mheshimiwa Spika, baada ya maneno haya ya shukrani,naomba nijielekeze katika hoja yangu yenye maeneo makuumawili ambayo ni: mapitio ya utekelezaji wa Mpango naBajeti ya Wizara kwa mwaka 2018/19 na Mpango na Bajetikwa mwaka 2019/20.

8. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2018/19, bajetiya Wizara ya Fedha na Mipango inatekelezwa katikamafungu nane ya kibajeti ambayo ni: - Fungu 50 - Wizara yaFedha na Mipango; Fungu 21 - HAZINA; Fungu 22 - Deni laTaifa; Fungu 23 - Mhasibu Mkuu wa Serikali; Fungu 7 - Ofisi yaMsajili wa HAZINA; Fungu 10 - Tume ya Pamoja ya Fedha;Fungu 13 - Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramu; na Fungu45 – Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.

2.0 Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara kwaMwaka 2018/19

9. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha azma ya Serikali yaAwamu ya Tano ya kujenga uchumi wa viwanda na

Page 62: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

62

kuwaletea Watanzania maendeleo inafikiwa, Wizara iliandaaMpango na Bajeti ya mwaka 2018/19 kwa kuzingatiamiongozo mbalimbali ya kitaifa, kikanda na kimataifaambayo ni pamoja na: Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025,Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17- 2020/21, Mwongozo wa kuandaa Mpango na Bajeti 2018/19, Sheria ya Bajeti Na.11 ya Mwaka 2015, Ilani ya Uchaguziya Chama Cha Mapinduzi 2015, Agenda ya Kamisheni yaUmoja wa Afrika 2063 na Malengo ya Maendeleo Endelevuya mwaka 2030. Aidha, Mpango na Bajeti ulizingatia ahadina maelekezo yaliyotolewa na Mheshimiwa Rais katikahotuba yake ya uzinduzi wa Bunge la 11 la Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, Ushauri na maoni ya Kamati yaKudumu ya Bunge ya Bajeti pamoja na Sera mbalimbali zaSerikali.

2.1 Mapato na Matumizi ya Wizara kwa Mwaka 2018/19

10. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Wizara yaFedha na Mipango iliidhinishiwa kiasi cha shilingi trilioni 12.05kwa ajili ya Matumizi ya Mafungu yake nane ya kibajeti. Katiya fedha hizo, shilingi trilioni 10.76 ni kwa ajili ya Matumizi yaKawaida na shilingi trilioni 1.29 ni kwa ajili ya matumizi yamaendeleo.

11. Mheshimiwa Spika, matumizi ya kawaida yalijumuishashilingi bilioni 313.67 kwa ajili ya mishahara ya Wizara naTaasisi zake, shilingi bilioni 445.34 kwa ajili ya matumizimengineyo na shilingi trilioni 10.00 ni malipo ya Deni la Serikalina michango ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Aidha, kati yafedha za matumizi ya maendeleo, shilingi trilioni 1.26 ni fedhaza ndani na shilingi bilioni 29.17 ni fedha za nje.

12. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili 2019, Wizaraimepokea jumla ya shilingi trilioni 8.25 kwa ajili ya Matumiziya Mafungu yake nane ya kibajeti, sawa na asilimia 68.46 yabajeti iliyoidhinishwa. Kati ya fedha hizo, shilingi trilioni 8.23 nikwa ajili ya Matumizi ya Kawaida, sawa na asilimia 76.49 yabajeti iliyoidhinishwa na shilingi bilioni 20.68 ni kwa ajili yamatumizi ya maendeleo. Aidha, kati ya fedha za maendeleo

Page 63: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

63

zilizopokelewa shilingi bilioni 15.37 ni fedha za ndani, na shilingibilioni 5.31 ni fedha za nje.

13. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili 2019, Wizaraimetumia jumla ya shilingi bilioni 191.97 kwa ajili ya mishahara,sawa na asilimia 61.20 ya fedha zilizoidhinishwa. Kati ya fedhahizo, shilingi bilioni 28.30 zimetumika kulipa mishahara yawatumishi katika mafungu ya Wizara, shilingi bilioni 7.01zimetumika kulipa mishahara ya Waheshimiwa Majaji,Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu, Tume yaKurekebisha Sheria Tanzania na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuuwa Hesabu za Serikali na shilingi bilioni 156.66 zimetumikakulipa ruzuku ya mishahara kwa Taasisi zilizo chini ya Wizara.Mchanganuo wa Matumizi ya Mishahara kwa kila Fungu nikama unavyoonekana katika Jedwali Na. 01.

14. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili 2019, Wizara ilitumiajumla ya shilingi trilioni 7.03 kwa ajili ya matumizi mengineyopamoja na deni la Serikali, sawa na asilimia 67.30 ya fedhazilizoidhinishwa. Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 301.61zimetumika kwa ajili ya matumizi ya mengineyo, sawa naasilimia 67.72 ya fedha zilizoidhinishwa na shilingi trilioni 6.73zimetumika kulipa Deni la Serikali na Huduma Nyingine, sawana asilimia 67.28 ya fedha zilizoidhinishwa. Mchanganuo waMatumizi kwa kila Fungu ni kama unavyoonekana katikaJedwali Na. 02.

15. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa fedha za maendeleo,hadi kufikia Aprili 2019, jumla ya shilingi bilioni 19.19 zilitumika.Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 15.37 ni fedha za Ndani nashilingi bilioni 3.82 ni fedha za Nje. Mchanganuo wa matumizikwa kila Fungu unavyoonekana katika Jedwali Na. 03.

2.2 Utekelezaji wa Majukumu

16. Mheshimiwa Spika, napenda sasa nitumie fursa hii kulielezaBunge lako Tukufu kuhusu majukumu yaliyotekelezwa naWizara kwa kipindi cha kuanzia Julai 2018 hadi kufikia Aprili2019.

Page 64: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

64

2.2.1 Kubuni na Kusimamia Utekelezaji wa Sera za UchumiJumla

17. Mheshimiwa Spika, malengo ya uchumi jumla kwamwaka 2018/19 yalikuwa kama ifuatavyo: kuhakikisha Patola Taifa linakua kwa asilimia 7.2 mwaka 2018, mfumuko wabei unabaki katika wigo wa tarakimu moja, mapato ya ndaniyanafikia asilimia 15.8 ya pato la Taifa, mapato ya kodiyanafikia asilimia 13.6 ya Pato la Taifa na nakisi ya bajetiinafikia asilimia 3.2.

18. Mheshimiwa Spika, uchumi wa nchi yetu umeendeleakuimarika ambapo mwaka 2018, Pato la Taifa kwa kutumiabei ya kizio ya mwaka 2015 li l ikua kwa asil imia 7.0ikilinganishwa na asilimia 6.8 mwaka 2017. Sekta zilizokua kwakasi kubwa ni pamoja na Sanaa na Burudani (asilimia 13.7),ujenzi (asilimia 12.9), uchukuzi na uhifadhi mizigo (asilimia 11.8)na habari na mawasiliano (asilimia 9.1). Ukuaji huu wa uchumiumeenda sambamba na utolewaji wa huduma bora kwawananchi zikiwemo maji, afya, umeme, elimu na ujenzi wamiundombinu ya reli, bandari, viwanja vya ndege, madarajana barabara pamoja na kuimarisha usafiri wa anga.

19. Mheshimiwa Spika, mfumuko wa bei umeendeleakushuka na kubakia katika kiwango cha tarakimu moja. Kwamwezi Aprili 2019, mfumuko wa bei ulikuwa asilimia 3.2ikilinganishwa na asilimia 3.8 kwa kipindi kama hicho mwaka2018. Hali hii imetokana na kuimarika kwa hali ya upatikanajiwa chakula katika masoko ya ndani na nchi j irani,kutengamaa kwa bei za mafuta katika soko la dunia,usimamizi madhubuti wa Sera za bajeti na fedha na utulivuwa thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya sarafu nyingine.Utulivu huu wa bei umesaidia wazalishaji, wanunuzi na walajikuweka mipango na mikakati ya muda mrefu bila kuhofiamabadiliko ya mara kwa mara ya bei ya malighafi na bidhaa.

2.2.2 Uandaaji na Ufuatiliaji wa Mpango wa Maendeleo waTaifa

20. Mheshimiwa Spika, ili kuhakikisha kuwa Tanzania inafikiamalengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, Wizara

Page 65: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

65

inaendelea kusimamia Utekelezaji wa Mpango wa Taifa waMaendeleo wa Miaka Mitano 2016/17 - 2020/21.

21. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Wizarailipanga kuandaa na kufuatilia utekelezaji wa Mpango waMaendeleo wa Taifa. Pamoja na mambo mengine, Wizaraimeandaa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka2019/20 na kufanya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleoiliyoidhinishwa katika mwaka 2018/19. Mpango wa mwaka2019/20 ni wa nne katika kutekeleza Mpango wa Pili waMaendeleo ya Taifa wa Miaka Mitano 2016/17-2020/21 wenyedhima ya “kujenga Uchumi wa Viwanda ili kuchocheaMageuzi ya kiuchumi na Maendeleo ya Watu” na kuiwezeshaTanzania kufikia uchumi wa kipato cha kati ifikapo 2025.Katika kutimiza azma hiyo, Serikali inaendelea kuboreshamazingira ya kufanya biashara na uwekezaji, kwa lengo lakuimarisha utekelezaji wa Mpango.

22. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Wizara kwakushirikiana na Wizara za kisekta ilipanga kufuatilia utekelezajiwa miradi 179. Hadi kufikia Aprili 2019, Wizara imefanikiwakufanya ufuatil iaji wa utekelezaji wa miradi 102 yamaendeleo, sawa na asilimia 57 ya lengo. Miradi iliyofuatiliwailijumuisha sekta za Viwanda, Maji, Kilimo, Nishati, Uvuvi, Afya,Elimu, Madini, Sheria, Ujenzi na Uchukuzi. Ufuatiliaji huoumesaidia kurekebisha upungufu uliojitokeza katikautekelezaji na kuainisha hatua za kuzingatiwa katikakutayarisha mpango wa mwaka 2019/20. Hadi kufikia Juni30, 2019 miradi yote itakuwa imefuatiliwa kama ilivyotarajiwa.

2.2.3 Kusimamia Ukusanyaji wa Mapato ya Serikali

Mapato ya Kodi na Yasiyo ya Kodi

23. Mheshimiwa Spika, katika kuboresha ukusanyaji wamapato ya ndani kwa mwaka 2018/19, Wizara ilipangakusimamia sera za fedha na kibajeti zinazolenga kuimarishauwekezaji na biashara; kusimamia dhana ya kulipa kodi kwahiari, kusimamia zoezi la uunganishaji wa Wizara, Idara,Wakala, Taasisi na Mashirika ya umma kwenye Mfumo wa

Page 66: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

66

Serikali wa Kielektroniki wa ukusanyaji wa mapato (GePG) ilikuboresha ukusanyaji na kudhibiti upotevu wa mapato yaSerikali.

24. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Wizarailipanga kusimamia ukusanyaji wa mapato ya ndaniyakijumuisha mapato ya Halmashauri ya jumla ya shilingitrilioni 20.89. Kati ya hizo, mapato ya kodi yalikuwa shilingitrilioni 18.0, Halmashauri shilingi bilioni 735.6 na mapato yasiyoya kodi shilingi trilioni 2.16. Hadi kufikia Aprili 2019, mapato yandani yakijumuisha mapato ya Halmashauri yalifikia shilingitrilioni 15.46. Kati ya kiasi hicho, mapato ya kodi yalikuwashilingi trilioni 12.9, sawa na asilimia 87.4, mapato yasiyo yakodi shilingi trilioni 2.04, sawa na asilimia 122 na mapato yaHalmashauri shilingi bilioni 529.25, sawa na asilimia 72 ya lengola kipindi hicho.

25. Mheshimiwa Spika, kati ya mapato yasiyo ya kodi yakiasi cha shilingi trilioni 2.04 yaliyopatikana hadi kufikia Aprili2019, jumla ya shilingi bilioni 600.45 imekusanywa na Wizaraya fedha na Mipango, sawa na asilimia 100.44 ya lengo lakukusanya shilingi bilioni 597.81. Mafanikio haya yametokanana kuimarishwa kwa ufuatiliaji na usimamizi wa mashirika nataasisi za umma, katika mashirika na kampuni ambazo Serikaliimewekeza.

26. Mheshimiwa Spika, ili kuendelea kuleta uwazi na ufanisikatika ukusanyaji wa mapato, Wizara ilipanga kuunganishaWizara, Idara na Taasisi za Serikali 300 kwenye mfumo waGePG. Hadi kufikia April i 2019, jumla ya Taasisi 210zimeunganishwa kwenye mfumo wa GePG ikiwa ni asilimia70 ya lengo. Aidha, hadi sasa jumla ya taasisi 410 kati yataasisi 667 zimeunganishwa na zinakusanya mapato kupitiamfumo huu. Mafanikio ya kuunganishwa kwa taasisi hizokwenye mfumo wa GePG ni kuongezeka kwa mapato yasiyoya kodi kutoka shilingi trilioni 1.78 katika kipindi cha Julai 2017hadi Aprili 2018 na kufikia shilingi trilioni 2.04 katika kipindi chaJulai 2018 hadi Aprili 2019. Pamoja na kuongezeka kwamapato yasiyo ya kodi, Mfumo huu pia unaiwezesha Serikalikuona moja kwa moja miamala ya ukusanyaji wa mapato

Page 67: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

67

na kujua kiwango cha mapato kinachokusanywa kwa siku.Hadi ifikapo Juni 30, 2019 Taasisi zote 300 zilizotarajiwakuunganishwa katika mfumo huu, zitakuwa zimeunganishwa.

Misaada na Mikopo kutoka kwa Washirika wa Maendeleo

27. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Wizarailipanga kuratibu upatikanaji wa misaada na mikopo nafuuya kiasi cha shilingi trilioni 2.67 kutoka kwa washirika waMaendeleo ili kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo.Hadi kufikia mwezi Aprili 2019, misaada na mikopo ilifikia shilingitrilioni 1.70, sawa na asilimia 86 ya lengo la kipindi hicho.

28. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha kuwa misaadana mikopo nafuu kutoka kwa Washirika wa Maendeleoinatolewa kama ilivyoahidiwa na kwa wakati, Wizaraimeendelea kufanya mazungumzo ya kimkakati na Washirikawa Maendeleo na kuhakikisha kuwa Mazungumzo ya Kisektayanafanyika ili kuhakikisha changamoto zinazojitokezazinatatuliwa kwa wakati. Aidha, Wizara kwa kushirikiana naWadau wa Maendeleo iliandaa Mpango Kazi wa kutekelezaMwongozo mpya wa Ushirikiano (Action Plan forImplementation of the Development CooperationFramework- DCF) ambao uliidhinishwa tarehe 07 Februari,2019. Mpango kazi huu utaisaidia Serikali kuongeza ukusanyajiwa misaada na mikopo nafuu kutoka kwa Washirika wamaendeleo. Aidha, nitoe rai kwa Washirika wa Maendeleokuendelea kutoa fedha walizoahidi kwa wakati na kwamujibu wa misingi ya ushirikiano.

Mikopo ya Ndani na Nje yenye Masharti ya Kibiashara

29. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Wizarailitarajia kuratibu upatikanaji wa mikopo ya ndani na njeyenye masharti ya kibiashara ya jumla ya shilingi trilioni 8.90.Kati ya hizo, shilingi trilioni 3.11 ni mikopo ya nje, shilingi trilioni

Page 68: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

68

1.19 ni mikopo ya ndani na shilingi trilioni 4.60 ni mikopo yandani ya kulipia hatifungani zilizoiva (rollover). Hadi kufikiaAprili, 2019 kiasi cha shilingi bilioni 692.30 kilikopwa kutoka nje,shilingi trilioni 3.3 zilikopwa kutoka soko la ndani zikijumuishamalipo ya dhamana za Serikali zilizoiva (rollover). Napendakulihakikishia Bunge lako Tukufu kuwa, Serikali inaendeleakufanya mazungumzo na wadau wa mikopo ya masharti yakibiashara ili kuhakikisha kwamba kiwango cha mikopokilichotarajiwa kinafikiwa ifikapo Juni 30, 2019.

2.2.4 Usimamizi wa Deni la Serikali

30. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Wizarailiendelea kusimamia Deni la Serikali na kuhakikisha kuwalinaendelea kuwa himilivu. Aidha, Wizara ilipanga kuendeleakuratibu ukopaji kwa kutoa kipaumbele kwenye mikopoyenye masharti nafuu na kuhakikisha kwamba mikopo yenyemasharti ya kibiashara inaelekezwa kwenye miradi yamaendeleo inayochochea ukuaji wa uchumi ikiwemo; ujenziwa miundombinu ya barabara, reli, viwanja vya ndege,bandari na mitambo ya kufua umeme. Hadi kufikia Aprili, 2019Deni la Serikali liliongezeka na kufikia shilingi trilioni 51.03 kutokashilingi trilioni 49.86 Aprili 2018. Ongezeko hilo ni sawa naasilimia 2.35. Kati ya kiasi hicho, deni la ndani lilikuwa shilingitrilioni 13.25 na deni la nje lilikuwa shilingi trilioni 37.78.Ongezeko la Deni la Serikali linatokana na kupokelewa kwamikopo mipya kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali yamaendeleo ikiwemo ujenzi wa Jengo la tatu la Kiwanja chandege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Ujenzi wa reli yakati kwa kiwango cha kimataifa, Ujenzi wa miradi ya umeme,Ujenzi wa barabara na madaraja makubwa.

31. Mheshimiwa Spika, sambamba na ukopaji, Wizaraimeendelea kufanya tathmini ya Deni la Taifa kila mwaka ilikupima uhimilivu wake. Matokeo ya tathmini iliyofanyikaDesemba, 2018 inaonesha kuwa, Deni la Taifa ni himilivu katikakipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu. Viashiria katikatathmini hiyo vinaonesha kuwa: thamani ya sasa ya Deni laTaifa (Present Value of Total Public Debt) kwa Pato la Taifa niasilimia 27.2 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 70; thamani

Page 69: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

69

ya sasa ya Deni la nje pekee (Present Value of External Debt)kwa Pato la Taifa ni asilimia 22.2 ikilinganishwa na ukomo waasilimia 55; thamani ya sasa ya deni la nje kwa mauzo ya njeni asilimia 157.3 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 240; naulipaji wa deni la nje kwa kutumia mauzo ya bidhaa nje niasilimia 15.2 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 23.

32. Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuhakikishainalipa deni kwa wakati kwa kadri linavyoiva. Katika mwaka2018/19, Serikali ilitenga kiasi cha shilingi trilioni 1.41 kwa ajiliya kulipa riba ya deni la ndani. Hadi kufikia Aprili, 2019 kiasicha shilingi trilioni 1.06 kimelipwa sawa na asilimia 75.18 yalengo. Aidha, Serikali ilitenga shilingi bilioni 689.67 kwa ajili yakulipa riba ya deni la nje. Hadi kufikia Aprili, 2019 shilingi bilioni588.30 zimelipwa sawa na asilimia 85.30 ya lengo. Vilevile,Serikali ilitenga shilingi trilioni 1.66 kwa ajili ya kulipia mtaji wadeni la nje, ambapo hadi kufikia Aprili, 2019 shilingi trilioni 1.23zimelipwa sawa na asilimia 74.10 ya lengo. Wizara itaendeleakusimamia Deni la Serikali kwa kuzingatia Sheria ya Mikopo,Dhamana na Misaada SURA 134 pamoja na Mkakati waMuda wa kati wa Kusimamia Madeni.

2.2.5 Malipo ya Pensheni na Michango ya Mwajiri kwaMifuko ya Hifadhi ya Jamii

33. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wizara ya Fedha naMipango inawajibika kulipa michango mbalimbali kwenyeMifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa ajili ya watumishi wake kwamujibu wa Sheria. Lengo la michango hiyo ni kuhakikishawatumishi wanaendelea kuishi maisha bora baada yakustaafu. Aidha, Wizara inawajibika kulipa mafao ya kustaafukwa watumishi wa Umma ambao hawachangii katika Mifukoya Hifadhi ya Jamii. Ili kutekeleza jukumu hili, Wizaraimeendelea kuhakikisha inalipa mafao ya kustaafu pamojana kupeleka michango ya mwajiri kwenye Mifuko ya Hifadhiya Jamii kwa wakati.

34. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuwasilisha kwawakati michango ya kisheria ya Mwajiri (Serikali) ya kila mwezikwa watumishi wa Serikali na taasisi zake kwenye Mifuko ya

Page 70: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

70

Hifadhi ya Jamii. Katika mwaka 2018/19, Serikali ilitenga kiasicha shilingi trilioni 1.19 kwa ajili ya kulipia mchango wa mwajirikwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Hadi kufikia Aprili 2019,kiasi cha shilingi bilioni 797.29 sawa na asilimia 67.0 ya lengokililipwa ikiwa ni uwasilishaji wa michango ya mwajiri kwawatumishi wote wa Umma walio kwenye “Payroll” ya Serikali.Hivyo, Serikali inalipa mchango wa mwajiri kwenye mifukoya hifadhi ya Jamii kwa wakati kila mwezi.

35. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Serikaliilitenga kiasi cha shilingi bilioni 424.74 kwa ajili ya kulipa mafaoya Kustaafu na mirathi kwa wastaafu wanaolipwa na HAZINA.Hadi kufikia Aprili 2019, kiasi cha shilingi bilioni 314.92 sawa naasilimia 74.14 kilitumika kulipa Wastaafu 4,016, Mirathi ililipwakwa Warithi 854 na Pensheni kwa kila mwezi kwa Wastaafu57,055. Katika kurahisisha ulipaji wa mafao ya wastaafu,Serikali imetengeneza mfumo wa ukokotoaji wa Mafao,uhifadhi wa kumbukumbu pamoja na utoaji wa Vitambulishovya kielektroniki kwa kutumia mfumo wa TPPS (TreasuryPensioners Payment System). Aidha, Serikali imeendeleakulipa Mafao ya kustaafu na Mirathi kwa Wakati kwa kutumiaMfumo wa TISS (Tanzania Inter-Bank Settlement System)ambao kwa sehemu kubwa umesaidia kuwaondoleawastaafu usumbufu wa kufuatilia mafao yao kila mwezi.

2.2.6 Kubuni na Kusimamia Mifumo ya Taarifa za Kifedha

36. Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2018/19, Wizarailipanga kubuni mifumo mbalimbali ya kuimarisha usimamiziwa mapato, matumizi na mali za Serikali. Hadi kufikia Aprili2019, Wizara imefanikiwa kubuni mfumo wa ufuatiliaji wa Maliza Serikali ujulikanao kama Government Asset ManagementInformation System-GAMIS kwa ajili ya kurahisisha usimamizina udhibiti wa Mali za Serikali. Aidha, Wizara imebuni nakuanza kutengeneza mfumo wa usimamizi wa fedha za miradiya Maendeleo kutoka kwa washirika wa maendeleozinazopelekwa moja kwa moja kwa watekelezaji (Direct toProjects Funds) ambao unatarajiwa kuanza kutumika Julai,2019. Lengo ni kutambua miradi yote na kuweka uwazi wa

Page 71: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

71

fedha zinazotolewa na Washirika wa Maendeleo bila kupitiaMfuko Mkuu wa Serikali.

37. Mheshimiwa Spika, katika kubuni mifumo mipya yakisasa, Wizara imezingatia umuhimu wa kuwa na mifumoinayobadilishana taarifa kwa lengo la kurahisisha upatikanajiwa taarifa za fedha na zile zinazohitajika kwenye mifumomingine. Mifumo hii itapunguza gharama na usumbufu wakutumia mfumo wa zamani (manual) wakati wakubadilishana taarifa, kupunguza makosa ya uingizaji wataarifa hizo na kuhakikisha taarifa inaingizwa mara mojakwenye mfumo na inapatikana kwenye mifumo mingine.

38. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili 2019, Wizara piaimefanikiwa kuunganisha mfumo wa kutolea Taarifa zaMishahara ya watumishi wa Umma (Government SalaryPayment Platform -GSPP) na taasisi tatu za awali ambazo niMfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF),Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) naBenki ya CRDB. Uunganishaji huu umerahisisha uoanishaji wataarifa za makato zilizoko kwenye mfumo wa Mishahara yawatumishi wa Umma na taarifa zilizoko kwenye mifumo yaMifuko ya Hifadhi ya Jamii ili kupunguza adha wanayopatawastaafu wanapobaini tofauti ya taarifa zao katika mifumohiyo. Aidha, uunganishaji huu umerahisisha upatikanaji wataarifa za makato ya watumishi wa Umma kwa njia yakielektroniki hivyo kuondoa usumbufu na gharama kwa taasisihizo kufuata taarifa HAZINA.

39. Mheshimiwa Spika, Wizara pia imefanikiwa kuunganishaMfumo wa Akaunti Jumuifu ya Hazina (Treasury SingleAccount-TSA) kwenye mifumo ya kihasibu (IFMS/Epicor) kwaTaasisi tano za Serikali ambazo ni Jeshi la Wananchi waTanzania, Jeshi la Kujenga Taifa, Mfuko wa Mahakama, Ofisiya Taifa ya Ukaguzi na Mfuko wa Bunge ili kuziwezesha taasisihizo kulipa moja kwa moja kwa utaratibu wa TSA. Aidha,mfumo wa TSA umeunganishwa na mifumo ya mapato namatumizi iliyoko Ofisi ya Rais – TAMISEMI ili kurahishaubadilishanaji wa taarifa za kifedha za Mamlaka za Serikaliza Mitaa na Serikali Kuu.

Page 72: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

72

40. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kutoa mafunzoya utumiaji wa mifumo mbalimbali ya Usimamizi wa fedha.Mafunzo yametolewa katika mfumo wa kutolea taarifa zamishahara ya watumishi wa umma (Government SalariesPayment Platform - GSPP) kwa Maafisa Utumishi 430 naWahasibu 430 wanaotumia mfumo huo kutoka Wizara, Idaraza Serikali, Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaana Taasisi. Mafunzo hayo yatawezesha maafisa hao kuhakikina kuidhinisha malipo ya mishahara kwa wakati, ambapokwa sasa mishahara ya watumishi wa Umma imekuwa ikilipwakwa urahisi. Aidha, Maafisa 370 kutoka katika Mamlaka zaSerikali za Mitaa 185 pamoja na Maafisa 351 kutoka Wizara,Mikoa na Hazina Ndogo wamefundishwa kutumia mfumo waAkaunti Jumuifu ya Hazina (Treasury Single Account) hususannamna ya kupata taarifa mbalimbali za malipoyanayofanyika kupitia Benki Kuu ya Tanzania pamoja nausuluhishi wa Kibenki (Bank Reconciliation).

2.2.7 Kuandaa na kufuatilia utekelezaji wa Bajeti ya Serikali

41. Mheshimiwa Spika, Bajeti ya Serikali ni nyenzo muhimuya kiutawala na kiuwajibikaji ya kuhakikisha utekelezaji waMipango na Sera, matumizi bora ya rasilimali, pamoja nausimamizi wa majukumu ya Serikali vinazingatiwa ipasavyo.Bajeti ya Serikali hutoa mwongozo wa makusudio namtazamo wa Serikali katika azma ya kutekeleza majukumuyake katika muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu,ugawaji wa rasilimali, maeneo ya vipaumbele, mapato namatumizi pamoja na usimamizi wa mikakati na mipango yaSerikali kwa ujumla katika kuleta maendeleo ya kiuchumi nakijamii.

42. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Wizarailipanga kuendelea kuboresha Mfumo mpya wa Uandaaji naUsimamizi wa Bajeti ya Serikali (CBMS), kuendelea kuchambuana kufanya tathmini ya miradi ya kimkakati kwa misingi yavigezo vilivyopo ili Halmashauri nyingi zaidi ziweze kunufaikana mkakati huu, pamoja na kufanya ufuatiliaji na tathmini yautekelezaji wa Bajeti ya Serikali.

Page 73: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

73

43. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili 2019, Wizaraimefanikiwa kuboresha Mfumo wa Uandaaji na Usimamizi waBajeti ya Serikali kwa kuweka moduli za uhamisho wa fedha,mpango wa mahitaji ya fedha na taarifa za utekelezaji wabajeti. Aidha, Wizara imefanikiwa kutoa mafunzo ya matumiziya mfumo wa CBMS kwa maofisa 186 kutoka kwenye Wizara,Idara Zinazojitegemea na Wakala, na Sekretarieti za Mikoa.

44. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha Mamlaka zaSerikali za Mitaa zinatoa huduma bora kwa Wananchi, Wizaraimeendelea kuzijengea uwezo kwa kuzipatia fedha zakutekeleza miradi ya kimkakati ili ziweze kujitegemeakimapato na kupunguza utegemezi wa ruzuku ya Serikali Kuu.Katika mwaka 2018/19, Wizara imefanya uchambuzi waMiradi ya Kimkakati 111 yenye thamani ya shilingi bilioni 749.63kutoka kwenye Halmashauri 67 kwa ajili ya kuzingatiwa katikabajeti ya 2019/20. Matokeo ya uchambuzi huo ni kuwa jumlaya miradi 15 yenye thamani ya shilingi bilioni 137.38 kutokakwenye Halmashauri 12 ilikidhi vigezo na mikataba kusainiwa.Orodha ya Halmashauri na idadi ya Miradi ni kama ifuatavyo:Halmashauri ya Jiji la Tanga mradi mmoja na Halmashauri yaJiji la Mwanza miradi miwili; Halmashauri za Manispaa yaKinondoni miradi miwili, Kigamboni mradi mmoja, Iringa mradimmoja, Ilemela miradi miwili; Halmashauri ya Mji wa Tarimemradi mmoja; Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo mradimmoja, Biharamuro mradi mmoja, Kibaha mradi mmoja naHanang mradi mmoja.

45. Mheshimiwa Spika, katika kudhibiti matumizi ya fedhaza Serikali na kuhakikisha thamani ya fedha inapatikana,Wizara ilifanya ufuatiliaji na uhakiki wa matumizi mbalimbalikatika utekelezaji wa bajeti ya Serikali. Baadhi ya maeneoyaliyofanyiwa uhakiki ni: Utekelezaji wa Programu yaKuimarisha Halmashauri za Miji na Manispaa (Urban LocalGovernment Strengthening Programme – ULGSP); mapato namatumizi ya taasisi zinazokusanya mapato ya ndani nakupata ruzuku ya Serikali; utekelezaji wa miradi ya kimkakatiya kuongeza mapato ya Mamlaka za Serikali za Mitaa nauhakiki wa madai ya fedha za fidia za miradi mbalimbali yamaendeleo.

Page 74: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

74

46. Mheshimiwa Spika, katika uhakiki huo yafuatayoyalibainika: baadhi ya Halmashauri kutozingatia Mwongozona utaratibu unaotakiwa katika utekelezaji wa Programu yaUboreshaji wa Mazingira ya Miji na Manispaa; baadhi yataasisi zinazopata ruzuku kutoka Serikalini zina uwezo wakukusanya mapato ya ndani yanayokidhi kugharamiaMatumizi Mengineyo na baadhi ya Halmashauri kukiukamikataba na mwongozo wa utekelezaji wa miradi yakimkakati. Aidha, shilingi bilioni 10 ziliokolewa kutokana nauhakiki wa madai ya fedha za fidia za miradi mbalimbali yaSerikali ikiwemo Mradi wa Maendeleo ya Miundombinu katikaJiji la Dar es Salaam (DMDP), Ujenzi wa Reli ya Kati kwaKiwango cha Kimataifa (SGR) na Ujenzi wa Kituo cha Jeshicha Majini (Naval Military Base).

47. Mheshimiwa Spika, i l i kukabiliana na upungufuuliobainika wakati wa ufuatiliaji wa utekelezaji wa bajeti yaSerikali, Wizara inazitaka Wizara, Idara Zinazojitegemea naWakala, Taasisi, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikaliza Mitaa kuzingatia Sheria ya Bajeti Na. 11 ya mwaka 2015pamoja na miongozo mbalimbali ya utekelezaji wa bajeti.Pili, Wizara inaendelea kufanya tathmini ya kina ili kubainiuwezo wa Taasisi za Umma zinazoweza kugharamia matumizimengineyo kwa kutumia mapato yao ya ndani. Aidha, Wizaraimeweka kigezo cha kuangalia ufanisi wa utekelezaji wamiradi ya kimkakati ya awali iliyotekelezwa na Halmashauri,wakati wa mawasilisho na uchambuzi wa miradi mipya. Pili,fedha za miradi ya kimkakati zitatolewa baada yaHalmashauri kuwasil isha Hati ya Madai kutoka kwaMkandarasi.

2.2.8 Usimamizi na Udhibiti wa Matumizi ya Fedha za Umma

48. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Wizarailipanga kufanya uhakiki wa madeni ya Wizara, IdaraZinazojitegemea, Wakala wa Serikali, Sekretarieti za Mikoa,Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi za Serikali sambambana kuendelea kuwajengea uwezo Wakaguzi wa Ndanikuhusu miongozo ya ukaguzi wa miradi na ununuzi.

Page 75: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

75

49. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza majukumu haya,Wizara kupitia Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali imefanyauhakiki wa madeni ya malimbikizo ya mishahara katikaWizara, Idara zinazojitegemea na Wakala wa Serikali 142;Sekretarieti za Mikoa 24 na Mamlaka ya Serikali za Mitaa 185.Aidha, Wizara imeendelea kuhakikisha usimamizi na udhibitiwa matumizi ya fedha za Umma zinazotolewa kwa ajili yautekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kufanyaukaguzi maalum kwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) naHospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya naSayansi Shirikishi Muhimbili Kampasi ya Mloganzila, ambapomapendekezo ya ukaguzi yaliwasilishwa kwa taasisi husikakwa ajili ya kuyafanyia kazi ili kuleta ufanisi katika utekelezajiwa miradi.

50. Mheshimiwa Spika, kati ya Julai 2018 na Aprili 2019,Wizara iliwajengea uwezo Wakaguzi wa Ndani ambapoWakaguzi 65 walipewa mafunzo ya kutumia miongozo yaukaguzi wa miradi na ununuzi. Aidha, mafunzo ya Usimamiziwa Viashiria Hatarishi na Viashiria Hatarishi vya Udanganyifuna Udhibiti wa Ndani yametolewa kwa Wakuu wa Idara naVitengo pamoja na waratibu 191 wa usimamizi wa vihatarishikutoka kwenye Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala waSerikali na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Vilevile, wakaguzi268 kutoka Wizara 14, Sekretarieti za Mikoa 21, Halmashauri178 na Taasisi za Serikali 5 wamepatiwa mafunzo ya kutumiamfumo wa kielektroniki wa kufuatilia utekelezaji wa Hoja zaMdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) nahoja za Wakaguzi wa Ndani (Government AuditRecommendation Implementation Tracking System-GARI-ITS)na kutoa mafunzo mengine mbalimbali kwa Wakaguzi waNdani 1,359 na Wajumbe wa Kamati za Ukaguzi.

51. Mheshimiwa Spika, Mafunzo haya yanalengakuwajengea uwezo Watumishi katika kusimamia na kudhibitimatumizi ya fedha za Umma zinazoelekezwa katikautekelezaji wa miradi ya maendeleo na hatimaye kuletathamani halisi ya fedha za miradi hiyo (Value for Money).Hivyo, kuimarika kwa udhibiti wa fedha za Umma kutaongeza

Page 76: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

76

ufanisi na kuleta matokeo yaliyokusudiwa ya kukuza uchumina kuwaletea maendeleo wananchi.

2.2.9 Usimamizi wa Mali za Serikali

52. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Wizarailipanga kufanya uhakiki wa mali za Serikali katika Wizara,Idara na Wakala za Serikali sambamba na kutoa miongozoya namna bora ya uthamini wa mali za Serikali. Katika kufikialengo hili, Wizara imeendelea kufanya uhakiki wa mali zaSerikali katika Wizara, Idara na Wakala za Serikali kwa lengola kuimarisha usimamizi wa mali za Serikali.

53. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili 2019, Wizarail ifanya uhakiki wa mali na madeni katika taasisizilizounganishwa ambazo ni Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (PSPF,GEPF, PPF na LAPF) na mamlaka za maji Dar es Salaam(DAWASA na DAWASCO). Baada ya utambuzi wa mali namadeni ya taasisi hizo, Serikali itahakikisha kuwa inachukuahatua stahiki kulingana na matokeo ya uhakiki. Wizara piaimefanya uhakiki wa majengo yaliyobaki wazi Jijini Dar esSalaam baada ya Serikali kuhamishia shughuli zake JijiniDodoma kwa lengo la kuandaa utaratibu wa kugawamajengo hayo kwa baadhi ya Taasisi za Serikali ambazo zinauhitaji wa majengo hayo.

54. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kutoa miongozoya namna bora ya uthamini wa mali za Serikali katika taasisimbalimbali ili kuiwezesha Serikali kutambua mali zake kwaidadi, hali, mahali zilipo na thamani. Aidha, Wizara imeanzakutumia kwa majaribio Mfumo wa Usimamizi wa Mali zaSerikali (GAMIS) katika mikoa mitano ambayo ni Mwanza,Tabora, Mara, Shinyanga na Kagera na Mafungu matatu yaWizara (Fungu 50, Fungu 21 na Fungu 23). Mfumo huuutaongeza ufanisi katika usimamizi wa mali za Serikali ikiwa nipamoja na kuwezesha utunzaji na uhuishaji wa daftari la maliza Serikali kwa wakati, kupata taarifa sahihi za ajali, potevuna fidia za mali, kudhibiti mapato yatokanayo na ada zaleseni za udalali, malipo ya tozo za potevu na malipo ya uuzajiwa mali chakavu.

Page 77: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

77

2.2.10 Udhibiti wa Utakasishaji wa Fedha Haramu na Ufadhiliwa Ugaidi

55. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Wizarakupitia Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramu (FIU)imeendelea kusimamia utekelezaji wa Sheria za Udhibiti waFedha Haramu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniakwa kutekeleza majukumu mbalimbali ikiwa ni pamoja na:kupokea taarifa 1,305 za miamala shuku kutoka kwa watoataarifa na kuwasilisha taarifa fiche 32 kwenye vyombovinavyosimamia utekelezaji wa sheria kwa ajili ya uchunguzi;kupokea taarifa 5,536 zinazohusu usafirishaji fedha taslimu nahati za malipo mipakani; kuratibu na kusimamia zoezilinaloendeshwa na ESAAMLG la tathmini ya mifumo yaudhibiti wa fedha haramu (AML/CFT Mutual Evaluation);kuimarisha ushirikiano na FIU za nchi za Djibouti, Sudan,Ethiopia, Somalia, China (Taiwan) na Mauritius na pia kufanyamajadiliano ya kuingia katika makubaliano ya ushirikiano naFIU za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jamaica, Japan,Trinidad and Tobago, Botswana, Canada, Jamhuri ya Kongona Kazakhstan. Aidha, Wizara kupitia Kitengo cha KudhibitiFedha Haramu imekagua benki nne ili kujiridhisha nautekelezaji wa Sheria za Udhibiti wa Fedha Haramu.

56. Mheshimiwa Spika, kazi nyingine zilizofanyika nikuendelea kutoa elimu kwa wadau 102 ya jinsi ya kutumiamfumo maalum wa kompyuta (goAML – Anti MoneyLaundering System) katika kupokea na kuchambua taarifambalimbali ili kurahisisha uwasilishaji wa taarifa za miamalashuku kwa njia ya kielektroniki; kuendesha mafunzo ya udhibitiwa utakasishaji wa fedha haramu na ufadhili wa ugaidi kwawaheshimiwa Mahakimu, Makadhi na Majaji wa Zanzibar;kukamilisha rasimu ya Kanuni za utoaji wa taarifa za miamalaya fedha taslimu na utumaji na upokeaji wa fedha kwa njiaza kielekroniki.

2.2.11 Tume ya Pamoja ya Fedha

57. Mheshimiwa Spika, Tume ya Pamoja ya Fedhaimeendelea kutekeleza majukumu yake ya kutoa ushauri wa

Page 78: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

78

uhusiano wa kifedha kwa Serikali ya Jamhuri ya Muunganowa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Katikamwaka 2018/19, Tume imefanya uchambuzi katika Usimamiziwa Deni la Taifa baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muunganowa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar nauchambuzi wa takwimu za Mapato na Matumizi yaMuungano kuanzia Mwaka 2013/14 hadi 2016/17. Uchambuzihuo umebaini kuwa, ushiriki wa pande mbili za Muunganokatika usimamizi wa Deni la Taifa umeimarika. Aidha,miongoni mwa kero za Muungano za masuala ya fedhazilizofanyiwa kazi hadi kufikia Aprili 2019, ni kurekebishwa kwaSheria ya kodi ya ongezeko la thamani kwenye huduma yaumeme unaopelekwa Zanzibar.

2.2.12 Usimamizi wa Mashirika na Taasisi za Umma

58. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Ofisi ya Msajili waHazina ina jukumu la kusimamia rasil imali za Serikalizilizowekezwa katika taasisi, Mashirika ya umma na kampunibinafsi. Ili kutekeleza jukumu hili, Ofisi ya Msajili wa Hazinaimeendelea kutoa ushauri kwa Serikali juu ya uwekezaji nanamna ya kuimarisha uendeshaji wa taasisi, Mashirika yaumma na kampuni zilizo chini ya usimamizi wake. Aidha, Ofisiimeendelea na uangalizi wa mali za Serikali zilizobinafsishwazikijumuisha viwanda, majengo na mashamba kwa lengo lakuangalia tija iliyopo na utekelezaji wa mikataba ya mauzo.

59. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Ofisi ya Msajiliwa Hazina ilipanga kufanya ukaguzi maalum katika kampuniambazo Serikali ina umiliki wa hisa chache, kufanyauchambuzi wa uwekezaji unaofanywa na Mashirika ya Ummakatika Kampuni Tanzu na kampuni nyinginezo, kufanyauchambuzi wa Miundo na Mgawanyo wa majukumu yaTaasisi na Mashirika ya Umma pamoja na kufanya tathminina ufuatiliaji kwenye Mashirika ya umma yaliyobinafsishwakwa lengo la kukagua ufanisi na kuhakiki utekelezaji wamasharti ya mikataba ya mauzo.

60. Mheshimiwa Spika, ili kutekeleza majukumu haya,Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kushirikiana na Mdhibiti na

Page 79: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

79

Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali imefanya UkaguziMaalum katika Kampuni 34 ambazo Serikali ina umiliki wa hisachache. Aidha, Ofisi ya Msajili wa Hazina imeandaa MpangoKazi wa kutekeleza mapendekezo yaliyotolewa katika ripotiya ukaguzi na utekelezaji unaendelea. Utekelezaji waMpango Kazi unajumuisha kupitia mikataba ya ubia,uendeshaji na utaalam kwa kampuni husika. Pamoja namambo mengine, lengo la zoezi hili ni kufuatilia na kubainisababu za Serikali kupata kiwango kidogo cha gawio aukutopata kabisa na kuchukua hatua stahiki ili kuongezamapato ya Serikali. Aidha, ufuatiliaji wa madeni kwawawekezaji waliobainika kutomaliza kulipa bei ya ununuzi wakampuni hizo unaendelea.

61. Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Msaji l i wa Hazinaimekamilisha zoezi la kutambua Kampuni Tanzu zilizoanzishwana kuendeshwa na Mashirika inayoyasimamia kwa lengo lakupata taarifa za umiliki wa kampuni hizo na uwekezaji wahisa kwenye kampuni mbalimbali. Hadi kufikia Aprili 2019,Mashirika 106 yalikuwa yamewasilisha taarifa, ambapo kwamujibu wa taarifa hizo Mashirika nane yameanzisha kampunitanzu; Mashirika tisa yamewekeza kwenye hisa katikakampuni zipatazo 79; na Mashirika 89 yakiwa hayana umilikiwa hisa wala hayajaanzisha kampuni tanzu.

62. Mheshimiwa Spika, hatua inayofuata ni kufanyauchambuzi wa mikataba na nyaraka husika za uanzishwajiwa Kampuni hizo, ili kujiridhisha kama uanzishwaji na uwekezajiulifuata sheria na taratibu na una tija kwa Taasisi na Taifakwa ujumla. Aidha, Ofisi ya Msajili wa Hazina inafuatilia kwaukaribu kampuni hizo ili kuhakikisha kuna usimamizi na uongozithabiti.

63. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Ofisi ya Msajili waHazina, imeendelea kufanya uchambuzi wa Miundo naMgawanyo wa majukumu ya Taasisi na Mashirika ya Umma.Hadi kufikia Aprili, 2019, jumla ya Taasisi na Mashirika 60yalichambuliwa. Kati ya hayo, Taasisi na Mashirika ya Umma54 miundo yao imeidhinishwa na Mhe. Rais na imewasilishwakwenye taasisi na mashirika husika kwa utekelezaji. Aidha,

Page 80: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

80

miundo ya taasisi na mashirika sita iko katika hatua ya kupataidhini. Utekelezaji wa zoezi hili umeenda sambamba nauunganishaji wa Mashirika ya umma 15 na kubaki Mashirikasita. Lengo kuu la uunganishaji wa Taasisi na Mashirika yaUmma ni kuongeza ufanisi wa kiutendaji, kuondoamwingiliano wa majukumu, kupunguza gharama zauendeshaji na kuongeza tija. Mashirika yaliyounganishwa nipamoja na; Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ambapo mifuko yaGEPF, LAPF, PPF na PSPF iliunganishwa na kuunda Mfuko waHifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF); UTT-MFIna SELF-Microfinance kuunda SELF Microfinance; UTT-AMIS naUTT-PID kuunda UTT- AMIS; Mamlaka za Maji za DAWASA naDAWASCO kuunda DAWASA; Wakala wa Mbegu za Miti naWakala wa Misitu na kuunda Wakala wa Misitu Tanzania. Kwaupande wa taasisi za fedha, Benki ya Wanawake Tanzania,Benki ya Twiga na Benki ya Posta zimeunganishwa kuundaBenki ya TPB.

64. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili 2019, Ofisi ya Msajiliwa Hazina imekamilisha tathmini na uchambuzi wa mikatabaya utendaji kwa Taasisi na Mashirika yote 53 iliyoingiwa bainaya Msajili wa Hazina na Wenyeviti wa Bodi za Taasisi naMashirika ya Umma. Lengo la zoezi hili ni kupima utekelezajiwa mikataba hiyo kwa mujibu wa viashiria vya mafanikio,ambapo mambo ya msingi yaliyozingatiwa katika tathminini pamoja na utawala bora, usimamizi wa fedha, usimamiziwa rasilimali watu na huduma kwa mteja. Aidha, jumla yamikataba ya utendaji kwa Mashirika 126 kati ya Mashirika 169yenye Bodi imesainiwa. Mashirika 43 yaliyobaki yataingiamkataba na Ofisi ya Msajili wa Hazina mwaka wa fedha 2019/20.

65. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Ofisi ya Msajili waHazina ilifanya tathmini na ufuatiliaji kwenye Mashirika yaumma 32 yaliyobinafsishwa kwa lengo la kukagua ufanisi nakuhakiki utekelezaji wa masharti ya mikataba ya mauzo.Kupitia taarifa ya tathmini na ufuatiliaji, Wizara imechukuahatua mbalimbali zikiwemo kuwataka wawekezaji kuongezauzalishaji kwa viwanda vinavyosuasua. Aidha, kwa walewalioshindwa au kukiuka mikataba ya mauzo, Serikali

Page 81: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

81

imechukua hatua na inakusudia kuvunja mikataba na baadhiya wawekezaji na kuwapatia wawekezaji wengine wenyeuwezo wa kuwekeza ili kuchochea shughuli za kiuchumi nahatimaye kuchangia kwenye Pato la Taifa.

66. Mheshimiwa Spika, hadi Aprili 2019, Wizara kupitia Ofisiya Msajili wa Hazina imerejesha shirika moja na viwanda 12vilivyobinafsishwa ambavyo vimeshindwa kutekelezamasharti ya mikataba ya mauzo. Viwanda hivyo ni MoshiPesticide, Tembo Chipboard, Kilimanjaro Paddy, MkataSawmill, NAFCO Dakawa, Mang’ula Mechanical & MachineTools Ltd, Lindi Cashewnut, Newala Cashewnut, Utegi DairyFarm, Mafuta ya Ilulu Ltd, Kiwanda cha Korosho Mtama,Kiwanda cha Korosho Nachingwea na Shirika la New NationalSteel Corporation. Aidha, jumla ya viwanda 26 vimepewanotisi/taarifa ya kusudio la kuvirejesha Serikalini baada yakubainika kusuasua kutekeleza masharti ya mkataba.

67. Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Msajili wa Hazina kwakushirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara imeendeleana jitihada za kutafuta wawekezaji ili Viwanda vilivyorejeshwaSerikalini viweze kuendelezwa. Matokeo ya jitihada hizo nikupatikana kwa mwekezaji wa kiwanda cha Chai Mpondeambaye ni Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi waUmma (PSSSF) na SUMA JKT katika kiwanda cha Korosho Lindi,Shamba la Mifugo na Kiwanda cha Maziwa Utegi.

68. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Ofisi ya Msajili waHazina imeendelea kuweka mikakati thabiti ya kusimamiana kukusanya madeni yatokanayo na Ubinafsishaji pamojana madeni ya iliyokuwa Benki ya NBC. Kwa mwaka 2018/19,Ofisi imelenga kukusanya kiasi cha shilingi milioni 700, ambapohadi kufikia April i 2019, kiasi cha shil ingi milioni 590kimekusanywa, sawa na asilimia 84.29 ya lengo. Aidha, Ofisiinaendelea kufuatilia madai mbalimbali ili kukusanya kiasikilichosalia ifikapo tarehe 30 Juni, 2019.

2.2.13 Uratibu wa Mikakati ya Kupunguza Umaskini69. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2018/19, Wizarailiendelea kuratibu jitihada za kupambana na umaskini nchini

Page 82: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

82

kwa kufanya ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa jitihadaza kupunguza umaskini zilizoainishwa katika Mipango yaKitaifa na Kisekta na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs)2030.

70. Mheshimiwa Spika, Wizara imefanya uchambuzi waawali wa Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi 2017/18 ambao, unaonesha kuwa umaskini wa mahitaji ya msingiumepungua kutoka asilimia 28.2 mwaka 2011/12 hadi asilimia26.4 mwaka 2017/18. Kiwango cha umaskini wa chakulakimepungua kutoka asilimia 9.7 mwaka 2011/12 na kufikiaasilimia 8.0 mwaka 2017/18.

71. Mheshimiwa Spika, tathmini ya viashiria vya umaskiniusio wa kipato inaonesha tumefanya vizuri zaidi, katikakuboresha hali ya makazi, umeme, huduma ya maji safi nasalama, vyoo, umiliki wa vyombo vya usafiri na mawasiliano.Viashiria vinaonesha kuwa makazi yaliyojengwa kwa kutumiazege, mawe, saruji na vyuma yameongezeka. Vilevile, kayazinazoishi katika nyumba zenye paa la kisasa zimeongezekakutoka asilimia 68.0 mwaka 2011/12 hadi asilimia 84.1 mwaka2017/18. Aidha, asilimia 78.8 ya kaya zinaishi kwenye nyumbazilizojengwa kwa kuta imara mwaka 2017/18 ikilinganishwana asilimia 46.0 mwaka 2011/12. Vilevile, asilimia 50.1 ya kayazinaishi kwenye nyumba zilizojengwa kwa sakafu imaramwaka 2017/18 ikilinganishwa na asilimia 40.0 mwaka 2011/12. Kaya zinazomiliki simu za mkononi ni asilimia 78 kwa 2017/18 ikilinganishwa na asilimia 57 ya mwaka 2011/12.

72. Mheshimiwa Spika, Wizara ilifanya ufuatiliaji wa miradiya kuondoa umaskini na jitihada za vikundi visivyo rasmi katikawilaya za Kakonko, Kasulu, Uyui, Ikungi, Hai, Siha, Arumeru,Mkuranga, Morogoro vijijini, Kilosa, Kilombero, na Kondoa.Wizara ilibaini kuwa, miongoni mwa wilaya hizo nyingizimepiga hatua katika kupambana na Umaskini kwakuimarisha sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na kilimo chaumwagiliaji, mifugo, uvuvi, ufugaji wa samaki na ufugaji nyuki.Aidha, matumizi ya nishati mbadala, uanzishwaji wa viwandavidogo vya kusindika mazao ya kilimo, mifugo na uvuviyamepewa kipaumbele na yameleta tija katika kuongeza

Page 83: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

83

mapato ya halmashauri ya wilaya hizo na kuleta mabadilikochanya ya hali ya maisha ya watu. Vilevile, katika maeneoyaliyotembelewa, jitihada za vikundi kujiwekea akiba nakutumia akiba hizo kama mitaji ya kuanzisha na kuboreshabiashara pamoja na miradi ya maendeleo zinaendeleakuimarika.

73. Mheshimiwa Spika, Wizara ilifanya mapitio ya Sera yaTaifa ya Huduma Ndogo ya Fedha ya mwaka 2000 kwakutunga Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo ya Fedha yamwaka 2017. Sera hiyo imewatambua watoa huduma ndogoza fedha ikiwemo vikundi visivyo rasmi. Katika kufanikishautekelezaji wa sera hii, Bunge la Jamhuri ya Muungano waTanzania lilitunga Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha yamwaka 2018 ambayo inaipa mamlaka Benki Kuu ya Tanzaniaya kusimamia sekta ndogo ya fedha. Sheria hiyo imewekautaratibu wa kusimamia na kuratibu vikundi hivyo.

74. Mheshimiwa Spika, Wizara ilifanya uchambuzi waTaarifa ya Gharama na Faida (Cost Benefit Analysis Study)iliyohusu miradi ya umaskini na mazingira inayotekelezwakatika wilaya sita za mfano ambazo ni Bunda, Sengerema,Bukoba, Ikungi, Ileje na Nyasa. Matokeo ya uchambuzi huoyalionesha kuwa kuna upungufu katika eneo la ufanisiunaotokana na muundo na uwezo wa utendaji wa Maafisawa halmashauri wanaosimamia miradi ya umaskini namazingira. Aidha, Wizara ilitoa maelekezo kwa Mikoa naHalmashauri kujumuisha masuala ya umaskini na mazingirakatika mipango na bajeti zao.

75. Mheshimiwa Spika, Wizara ilitoa mafunzo kwa MaafisaMipango wa Halmashauri na Mikoa juu ya mbinu na umuhimuwa kujumuisha malengo na shabaha za kuhuisha juhudi zakuondoa Umaskini na Mazingira katika mipango na bajeti zao.Mafunzo hayo yalilenga kujenga uwezo na uelewa wawatendaji wa Halmashauri ili kupanua wigo kwa kuanzishamiradi (Poverty Environment Initiatives-PEI) katika maeneombalimbali.

Page 84: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

84

2.2.14 Ununuzi wa Umma

76. Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2018/19, Wizarailipanga kufanya marekebisho ya Sheria na kanuni za ununuziwa umma sura 410, Mwongozo wa Maadili ya Maafisaununuzi, Ugavi na Wazabuni, kusimamia utekelezaji waMfumo wa Ununuzi kwa Njia ya Mtandao (TANePS),kuyajengea uwezo makundi mbalimbali kuhusu Sheria yaUnunuzi wa Umma, kununua magari na vifaa mbalimbali kwapamoja, kusimamia Wataalam wa ununuzi na Ugavi pamojana kuendelea kupokea na kusikiliza rufaa za zabuni za umma.

77. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili 2019, Wizaraimefanikiwa kufanya marekebisho ya Kanuni ya 164 ya Sheriaya Ununuzi wa Umma ili kumpa mzabuni haki ya kupatataarifa ya ukamilishwaji wa mchakato wa ununuzi. Aidha,Kanuni ya 226 ilirekebishwa kumpa mamlaka Mlipaji Mkuuwa Serikali kutoa idhini kwa Maafisa Masuuli kuongeza idadiya wajumbe wa timu za majadiliano kwenye miradi mikubwayenye maslahi kwa Taifa. Marekebisho hayo yamezingatiamaoni ya wadau juu ya changamoto za utekelezaji wa Sheriaya Ununuzi wa Umma Sura 410.

78. Mheshimiwa Spika, Wizara imekamilisha rasimu yaMwongozo wa Maadili ya Maafisa ununuzi, Ugavi naWazabuni. Mwongozo huo umeweka misingi ya kimaadili yakuzingatia katika utekelezaji wa ununuzi wa umma kwamujibu wa Sheria ya Ununuzi wa Umma Sura 410. Aidha,Wizara imekamilisha rasimu ya Mwongozo wa Utekelezaji waShughuli za Ununuzi wa Umma ambao umeweka bayanataratibu za utekelezaji wa ununuzi wa umma kwa kuzingatiaSheria ya Ununuzi wa Umma. Vilevile, mafunzo ya uandaajiwa mikataba midogo (LPOs) kwa kutumia mfumo wa IFMIS/EPICOR yametolewa kwa Maafisa 100 wa ununuzi na Ugavi.

79. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Mamlaka yaUsimamizi wa Ununuzi wa Umma (PPRA) imeendeleakusimamia utekelezaji wa Mfumo wa Ununuzi kwa Njia yaMtandao (TANePS). Madhumuni ya kuanzishwa kwa mfumohuu ni kuboresha mchakato wa ununuzi ili ufanyike kwa

Page 85: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

85

urahisi, uwazi, haki na tija, ili kuongeza ushindani naupatikanaji wa thamani halisi ya fedha zinazotumika katikaununuzi. Hadi kufikia Aprili 2019, Taasisi Nunuzi 71 kati ya 540na Wazabuni 1,681 wamesajiliwa na kuanza kutumia mfumohuu kwa majaribio katika ununuzi wa vifaa na hudumamtambuka. Aidha, mfumo huu wa TANePS unatarajiwakupunguza vitendo vya rushwa, gharama katika michakatoya zabuni na muda wa mchakato na hivyo kuongeza ufanisikatika ununuzi wa umma. Matarajio ya Serikali ni kuona kuwaTaasisi zote Nunuzi za Serikali zinasajiliwa na kuunganishwakwenye mfumo wa TANePS.

80. Mheshimiwa Spika, PPRA imeendelea kujenga uwezona kuimarisha uelewa wa Sheria ya ununuzi kwa makundimbalimbali. Mafunzo maalum ya Sheria ya Ununuzi yalitolewakwa watumishi 763 kutoka Taasisi za Umma 26 kati ya Taasisi40 zilizopangwa kupatiwa mafunzo. Aidha, Mamlaka ilifanyawarsha mbili na kuhudhuriwa na washiriki 64 kutoka taasisinunuzi za Umma. Vilevile, ukaguzi wa ununuzi wa umma wamwaka 2017/18 ulifanyika katika taasisi 60 zilizopangwakukaguliwa. Kaguzi hizo zilifanyika katika maeneo yauzingatiaji wa sheria, kupima thamani ya fedha kwenyemiradi na ukaguzi kuhusu viashiria vya udanganyifu na rushwakwenye ununuzi wa umma. Matokeo ya ukaguzi huoyalionesha kuwa, kiwango cha uzingatiaji wa Sheria yaUnunuzi wa Umma katika 2017/18 ni sawa na kiwango chamwaka 2016/17 ambacho ni asilimia 74.

81. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili 2019, Wakala waHuduma ya Ununuzi Serikalini - GPSA amefanikiwa kufanyaununuzi wa pamoja kwa niaba ya taasisi 128 za Serikali wamagari 429 wenye thamani ya shilingi bilioni 64.14. Ununuzihuo wa pamoja umeisaidia Serikali kuokoa shilingi bilioni 2.6.Aidha, Wakala ameanzisha kituo cha pamoja One StopCentre’ kwa ajili ya kuhifadhi kumbukumbu na taarifa zaununuzi wa magari ya Serikali kwa pamoja. Pia, Wakalaamefanikiwa kukamilisha ujenzi wa kisima cha mafuta katikaMkoa wa Mwanza uliogharimu kiasi cha shilingi 73,457,200na hivyo kuongeza uwezo wa kuhifadhi ziada ya lita 57,000

Page 86: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

86

na kuanza mchakato wa ujenzi wa matanki ya mafuta katikaMikoa ya Morogoro, Tabora na Mtwara.

82. Mheshimiwa Spika, Ujenzi wa visima vya mafuta katikaMikoa ya Tanga na Lindi upo katika hatua za mwisho. Visimahivyo vitakuwa na uwezo wa kuhifadhi lita 30,000 kwa kilakimoja na kuongeza uwezo wa uhifadhi kutoka lita 21,700hadi 51,700 kwa Tanga na lita 25,000 hadi lita 55,000 kwamkoa wa Lindi. Vilevile, Wakala umepata Mkandarasi waujenzi wa Kituo cha mafuta, Ofisi na Ghala katika Mkoa waGeita. Mradi huu ukikamilika utaongeza uwezo wa Serikalikatika kutoa huduma za mafuta na vifaa katika Mkoa waGeita.

83. Mheshimiwa Spika, Wakala umefanikiwa kugomboamizigo yenye thamani ya shilingi bilioni 56.76 kwa niaba yataasisi za umma 67. Katika utaratibu huo, Taasisi hizo zimeokoajumla ya shilingi milioni 883.30. Kati ya kiasi hicho, shilingi milioni433.83 zinatokana na mchakato wa zabuni endapo kila taasisiingefanya mchakato yenyewe na shilingi milioni 449.47kimetokana na tozo ya ugomboaji ambapo Wakala unatozakati ya asilimia 0.4 hadi 0.8 ya thamani ya mzigo ikilinganishwana Wakala binafsi ambao hutoza asilimia 1.2 au zaidi yathamani ya mzigo. Vilevile, Wakala umetoa mikatabamaalum 7,223 kwa wazabuni na taasisi binafsi za kutoahuduma kwa Taasisi za Umma. Utaratibu huu umesaidiakuokoa gharama za michakato ya zabuni kwa Taasisi zaUmma kila zinapohitaji huduma na vifaa mtambuka.

84. Mheshimiwa Spika, Bodi ya Wataalam wa Ununuzi naUgavi – PSPTB iliendelea kusimamia Wataalam wa Ununuzina Ugavi kwa njia ya usajili, kukuza na kuratibu mafunzo yaelimu ya fani ya Ununuzi na Ugavi nchini na kuishauri Serikalikatika masuala yanayohusu Taaluma ya Ununuzi na Ugavi.Katika mwaka 2018/19, Bodi iliandaa na kusimamia mitihaniya kitaaluma katika fani ya ununuzi na ugavi kwa watahiniwa1,367 kwa ngazi za Awali, Msingi na Shahada. Kati yaoWatahiniwa 690 sawa na asilimia 50.48 walifaulu kuendeleana ngazi nyingine za mitihani. Aidha, Bodi ilifanya mahafalina kutunuku vyeti vinavyotambuliwa na taasisi ya kimataifa

Page 87: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

87

ya ununuzi na ugavi (International Federation of Purchasingand Supply Management – IFPSM) kwa wahitimu 263waliofaulu mitihani mwaka 2017/18. Vilevile, Bodi imesajiliwataalam wapya 1,870 katika ngazi mbalimbali za kitaalumana kufikia idadi ya wataalam 11,620.

85. Mheshimiwa Spika, Bodi imeendelea kutoa mafunzo naushauri wa kitaaluma kwa taasisi mbalimbali zikiwemo Mfukowa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bodi ya Taifa ya Wahasibuna Wakaguzi (NBAA) na Benki ya TPB, Mamlaka ya Maji Safina Maji Taka Morogoro (MORUWASA), Shirika la Wakala waMeli Tanzania (TASAC), Shirika la Maendeleo ya PetroliTanzania (TPDC) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).Aidha, mafunzo hayo yamesaidia kuongeza ufanisi katikautendaji kazi na ufanisi huo unatarajiwa kupunguza hoja zaukaguzi. Vilevile, Bodi imeendesha kongamano la mwakakwa wataalam wa Ununuzi na Ugavi lililohudhuriwa nawataalam 689 ambapo mada mbalimbali na maazimioyalitolewa kuhusu mchango wa taaluma ya ununuzi na ugavikatika kuhakikisha uwepo wa thamani ya fedha kwenyeununuzi wa umma.

86. Mheshimiwa Spika, Mamlaka ya Rufaa za Zabuni zaUnunuzi wa Umma (PPAA) imeendelea kupokea na kusikilizarufaa ili kuhakikisha wazabuni wanaopewa zabuni wanakidhivigezo vinavyohitajika kama vile kutokuwa na tuhuma zakugushi nyaraka na wana uwezo wa kutoa huduma kwakuzingatia thamani halisi ya fedha. Kwa mwaka wa fedha2018/19, PPAA ilikadiria kupokea na kusikiliza jumla yamashauri 30. Hadi kufikia Aprili 2019, PPAA imepokea jumlaya mashauri 47 sawa na asilimia 156.67 ya mashauri 30yaliyotegemewa kupokelewa kwa mwaka. Kati ya mashaurihayo, mashauri 30 yamesikilizwa na kutolewa maamuzi,mashauri 16 yako katika hatua mbalimbali za kusikilizwa nashauri moja limeondolewa na mlalamikaji kwa ridhaa yake.Serikali itahakikisha kuwa, Taasisi zote Nunuzi za Serikalizinaimarishwa kwa kupatiwa watumishi wenye weledi,vitendea kazi na rasilimali fedha ili kuhakikisha ununuzi waumma unaleta tija kwa Taifa.

Page 88: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

88

2.2.15 Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi - PPP

87. Mheshimiwa Spika, Serikali iliamua kuanzisha utaratibuwa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) kwalengo kuihusisha sekta binafsi kushiriki katika utekelezaji wamiradi ya maendeleo. Pia, utaratibu wa PPP umeanzishwa ilikuipunguzia Serikali mzigo mkubwa wa mahitaji ya fedha zabajeti na hivyo kuwa na wigo mpana wa kutoa huduma zakiuchumi na kijamii. Wizara imeendelea kutekeleza mikakatiya kuharakisha utekelezaji wa PPP, ikiwa ni pamoja nakuratibu marekebisho ya Sheria ya PPP ili kuimarisha mazingirawezeshi ya uwekezaji na ushiriki wa Mamlaka za Serikalikwenye miradi ya PPP, hususan wakati wa maandalizi yaBajeti. Kwa mujibu wa Marekebisho ya Sheria ya PPP yamwaka 2018, Wizara ina jukumu la kuchambua miradi ya ubiailiyowasilishwa na Taasisi za Serikali. Lengo ni kuhakikisha kuwa,miradi husika inakidhi vigezo vya uwekezaji chini ya utaratibuwa PPP. Mambo ya kuzingatia katika uchambuzi wa miradini pamoja na thamani halisi ya fedha, vihatarishi vya mradi,faida na tija kwa Taifa.

88. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Wizaraimepokea mapendekezo ya miradi ya ubia ipatayo 33. Katiya miradi 33 iliyopokelewa, miradi sita imekidhi vigezo nakufanyiwa kazi. Miradi hiyo ni pamoja na: Mradi wa Uboreshajiwa Huduma ya Usafiri jijini Dar es Salaam Awamu ya kwanza(Dar- Rapid Transit Project- Phase1); Mradi wa Viwanda Vitatuvya Uzalishaji wa Dawa muhimu na Vifaa Tiba; mradi waUsambazaji wa Gesi asilia katika Jiji la Dar es Salaam, Lindina Mtwara; Mradi ya Ujenzi ya Hoteli ya Nyota Nne; Kituocha Biashara katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa chaJulius Nyerere; na Mradi wa ujenzi wa hosteli ya wanafunziwa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE). Aidha, Wizaraimekamilisha uchambuzi wa mawasilisho ya awali ya miradi22 ya Mamlaka za Serikali za Mitaa na wahusika watajulishwakuhusu maeneo ya kufanyia kazi kwa mujibu wa Sheria,mwongozo na taratibu za PPP. Vilevile, miradi mitano ipokatika hatua mbalimbali za uchambuzi na uangalifu stahiki(Due Diligence).

Page 89: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

89

89. Mheshimiwa Spika, Mradi wa Wakala wa MabasiYaendayo Haraka Awamu ya Kwanza, umeidhinishwa naKamati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP SteeringCommittee) tarehe 2 Aprili, 2019 kwa hatua inayofuata yakutafuta mzabuni wa kutoa huduma. Aidha, Mradi waViwanda Vitatu vya Uzalishaji wa Dawa muhimu na Vifaa Tibauliidhinishwa na Kamati ya Kusimamia Ubia mwezi Novemba2018, na Bohari ya Dawa (MSD) imepewa idhini ya kuendeleana utaratibu wa kutafuta Wawekezaji. Taarifa ya awali yaUpembuzi Yakinifu ya Mradi wa Usambazaji wa Gesi asiliakatika Jiji la Dar es Salaam, Lindi na Mtwara uliidhinishwa naWizara ya Fedha na Mipango mwezi Machi, 2018 na TPDCwapo katika hatua ya maandalizi ya upembuzi yakinifukulingana na hitaji la Sheria ya Ubia Sura 103. UpembuziYakinifu wa awali wa Mradi ya Ujenzi ya Hoteli ya Nyota Nnena Kituo cha Biashara iliidhinishwa tarehe 22 Aprili, 2019 naMamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) imepewa muda wamwezi mmoja kukamilisha maandiko ya upembuzi yakinifukuwezesha kuendelea na hatua ya kuwapata wabia wakutekeleza miradi hiyo. Vilevile, upembuzi yakinifu wa awaliwa Mradi wa ujenzi wa hosteli ya wanafunzi wa Chuo chaElimu ya Biashara (CBE) uliidhinishwa tarehe 22 Septemba,2018 na Chuo kinaendelea na maandalizi ya upembuziyakinifu.

90. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kushirikiana naMamlaka za Serikali ili kuhakikisha kuwa miradi ya PPPinaibuliwa na kuendeshwa kwa kufuata Sheria, Kanuni nataratibu za PPP. Kutokana na umuhimu wa utaratibu huukatika kuleta maendeleo nchini, Wizara imeandaa nakusambaza Waraka wa Hazina Na. 2 wa mwaka 2018/19kuhusu uzingatiaji wa sheria katika utekelezaji wa miradi yaubia baina ya sekta ya umma na sekta binafsi. Waraka huuunasisitiza umuhimu wa kuzingatia kikamilifu Sheria, Kanunina taratibu za PPP na umepiga marufuku Mamlaka za Serikalikuingia mikataba ya PPP bila kufuata taratibu zilizowekwachini ya Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta BinafsiSura 103 na Kanuni zake. Nitoe wito kwa Mamlaka na Taasisizote za Serikali kubuni miradi yenye sifa ya miradi ya PPP katikasekta za kiuchumi na kijamii ili kufanikisha azma ya Serikali ya

Page 90: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

90

kutoa huduma bora kwa wananchi na kupunguza utegemezikwenye bajeti ya Serikali.

2.3 Utekelezaji wa Majukumu ya Mashirika na Taasisi zaUmma

91. Mheshimiwa Spika, baada ya mapitio ya taarifa yautekelezaji ya mafungu ya kibajeti, napenda sasa nielezekuhusu utekelezaji wa mashirika na Taasisi zilizo chini ya wizarakwa mwaka 2018/19.

2.3.1 Huduma za Kibenki

Benki Kuu ya Tanzania – BOT

92. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Benki Kuuya Tanzania imeendelea kutekeleza sera ya fedhainayolenga kudumisha kiwango cha kutosha cha ukwasikwenye uchumi kulingana na mahitaji ya malengo mapanaya kusimamia utulivu wa bei na ukuaji wa uchumi jumuishi.Katika kipindi hicho, Benki Kuu imeendelea kuchukua hatuambalimbali za kuongeza ukwasi kwenye uchumi i l ikuziwezesha benki na taasisi za fedha kuongeza utoaji wamikopo kwa sekta binafsi pamoja na kuendeleza shughulimbalimbali za uchumi. Njia zilizotumika katika kuongezaukwasi kwenye uchumi ili kuendana na mahitaji ni pamojana kununua fedha za kigeni kutoka katika benki za biashara,taasisi za fedha na taasisi za Serikali, kutoa mikopo ya mudamfupi kwa mabenki, na kushusha riba ya mikopo kwamabenki (discount rate) kutoka asilimia 9.0 hadi asilimia 7.0mwezi Agosti 2018.

93. Mheshimiwa Spika, hatua hizi zilisaidia kuongeza ukwasikwenye benki za biashara na kushusha riba katika masokoya fedha. Riba ya siku moja katika soko la fedha baina yamabenki (overnight interbank cash market rate) ilipunguakutoka wastani wa asilimia 3.15 kwa kipindi cha Julai 2017,hadi Februari 2018 na kufikia wastani wa asilimia 2.96 kwakipindi cha mwezi Julai, 2018 hadi Machi, 2019. Aidha, katikakipindi hicho, riba za dhamana za Serikali zilipungua hadi

Page 91: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

91

wastani wa asilimia 8.05 kutoka asilimia 8.17. Vilevile, riba zamikopo inayotolewa na benki za biashara zilishuka kutokawastani wa asilimia 17.97 katika kipindi cha Julai 2017 hadiJanuari 2018 mpaka wastani wa asilimia 17.15 kwa kipindicha Julai 2018 hadi Machi 2019. Aidha, Benki Kuu imeendeleakuhimiza mabenki kutumia kanzi data ya taarifa za wakopaji(credit reference system) ambayo imechangia kupunguakwa mikopo chechefu kutoka asilimia 10.18 Machi 2018 hadikufikia asilimia 9.61 Machi 2019.

94. Mheshimiwa Spika, Benki Kuu imeendelea kusimamiamasoko ya fedha ili kuhakikisha kuwa yanafanya kazi kwaufanisi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa viwango vya ribakatika masoko haya vinapatikana kwa kuzingatia nguvu halisiya soko ikiwemo kiwango cha ukwasi kilichopo kwa kipindihusika. Vilevile, kwa kushirikiana na wadau wengine, Benkiimeendelea kuimarisha mawasiliano kati ya Mfumo wa Sokola Dhamana za Serikali na Hati Fungani na Mfumo waDhamana wa Soko la Mitaji. Benki kuu pia imeendeleakuhakikisha kuwa mfumo wa mauzo ya Dhamana za Serikalipamoja na mifumo ya malipo inafanya kazi kwa ufanisi wakatiwote. Kadhalika, mfumo wa kielektroniki wa soko la fedhabaina ya mabenki ulianza kufanya kazi rasmi Novemba 2018hatua ambayo itaboresha upatikanaji wa viashiria halisi vyaukwasi nchini na kusaidia usimamizi wa utekelezaji wa seraya fedha. Hatua hizi kwa pamoja zilichangia ongezeko laukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi kutoka wastani wa asilimia3.4 mwaka 2018 hadi kufikia asilimia 9.6 Machi 2019.

95. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2018 hadiAprili 2019, Wizara kupitia Benki Kuu ya Tanzania ilifanyaukaguzi wa maduka ya kubadilisha fedha katika mkoa waArusha na Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya jukumu lake lamsingi la kusimamia sekta ya fedha. Katika ukaguzi huoilibainika kuwa, maduka mengi ya kubadilisha fedhayanaendesha shughuli zao bila kuzingatia Sheria na Kanuniza Kubadilisha Fedha za mwaka 1992 pamoja namarekebisho yake ya mwaka 2017. Miongoni mwa upungufuuliobainika ni pamoja na uondoshwaji wa fedha katikamfumo rasmi wa fedha na kuelekezwa kwenye mifumo ya

Page 92: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

92

utakatishaji wa fedha haramu, kupokea Amana kutoka kwawafanyabiashara kinyume cha matakwa ya leseni zabiashara husika, kudhoofisha thamani ya shilingi, pamoja namambo mengine ambayo yalianza kuathiri usalama wa nchikwa ujumla. Hata hivyo, Benki Kuu ya Tanzania ilichukuatahadhari ya kutosha kuhakikisha huduma ya ubadilishajifedha za kigeni inaendelea nchini kwa kutolewa na benkizote pamoja na Shirika la Posta.

96. Mheshimiwa Spika, hivi sasa Serikali inaandaa Kanunimpya kwa ajili ya biashara ya maduka ya kubadilisha fedhaza kigeni ambazo zitaelekeza jinsi ya kuomba leseni zauendeshaji wa maduka hayo kwa mtu binafsi au taasisiyeyote na masharti ya kuzingatiwa wakati wa shughuli hizo.Kanuni hizo zinalenga kuweka mazingira mazuri ya biasharaambayo hayatatoa athari kwa sekta ya fedha na uchumijumla, na inakuwa yenye manufaa kwa nchi. Ni matarajio yaSerikali kuwa udhibiti huu utaziwezesha Benki za biashara nataasisi nyingine kuuza fedha za kigeni kwenye soko la fedhana hatimaye kuongeza akiba ya fedha za kigeni. Aidha,Serikali inatoa tahadhari kwa wananchi kutoshiriki kwenyebiashara ya kubadilisha fedha za kigeni kwa njia zisizo halali.

Benki ya Maendeleo ya Kilimo - TADB

97. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Benki yaMaendeleo ya Kilimo ilipanga Kutoa mikopo kwa ajili yamiradi ya umwagiliaji na kilimo cha kisasa, kuendeleakutekeleza mpango wa kuwajengea uwezo wakulimawadogo wadogo kupitia mafunzo ya usimamizi wa fedha,uendeshaji wa vikundi na vyama, utunzaji wa kumbukumbuna utengenezaji wa miradi inayokidhi masharti ya mikopokutoka katika benki na taasisi za fedha na kukamilisha zoezila ufunguzi wa ofisi ya Benki Dodoma na Ofisi ya TADB Kandaya Ziwa Jijini Mwanza.

98. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili 2019, Benkiimefanikiwa kutoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni10.4 kwa ajili ya utekelezajiwa miradi ya umwagiliaji. Aidha,benki imefanikiwa kuidhinisha mikopo yenye thamani ya

Page 93: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

93

shilingi bilioni 3.4 kwa ajili ya ufadhili wa miradi 51 ya kilimocha kisasa cha zao la pamba na mpunga. Vilevile, Benkiimetoa mafunzo kwa wakulima wadogo wadogo, wafugajina wavuvi wapatao 7,469 katika mikoa mbalimbali. Mafunzohayo yalilenga kuwajengea wakulima uwezo katika masualaya usimamizi wa fedha, uendeshaji wa vikundi na vyama,utunzaji wa kumbukumbu na uandaaji wa miradi.

99. Mheshimiwa Spika, napenda kutumia fursa hii kulitaarifuBunge lako Tukufu kwamba, Benki ya Maendeleo ya Kilimoimefungua ofisi mpya mbili za kanda ili kusogeza hudumakaribu na wateja. Ofisi zilizofunguliwa ni pamoja na ofisi yaKanda ya Ziwa, Mwanza na Kanda ya Kati, Dodoma. Aidha,TADB ipo katika hatua za mwisho za ufunguzi wa Ofisi yakanda ya Nyanda za Juu Kusini, Mbeya. Vilevile, Benki ipokatika hatua za mwisho za ufunguzi wa Ofisi Ndogo ya Kigomaitakayohudumia wakulima wa mkoa huo pamoja na viungavyake. Ufunguzi wa matawi hayo mapya ni utekelezaji waazma ya Serikali ya kusogeza huduma za mikopo karibu nawakulima, wafugaji na wavuvi.

Benki ya Maendeleo Tanzania ya TIB - DFI

100. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Benki ya TIB– DFI ilipanga kutoa mikopo ya thamani ya shilingi bilioni 688.29na Waraka Mizania wa benki ulitarajiwa kukua kutoka shilingibilioni 757.06 mwaka 2017 hadi kufikia shilingi bilioni 864.94mwaka 2018. Benki pia ilipanga kuendeleza maeneo yaviwanda kwa wajasiriamali wadogo na wa kati kwakushirikiana na SIDO na Shirika la Ushirikiano wa KimataifalaJapan (JICA).

101. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi Machi 2019, benkiimefanikiwa kutoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni634.58 sawa na mafanikio ya asilimia 92.20 ya lengo. Katikakipindi hicho, mapato ya benki yalifikia shilingi bilioni 46.41na faida ya benki baada ya kodi ilikuwa shilingi milioni 499.88.Aidha, hadi mwezi Machi, 2019 Benki imeweza kukusanyamarejesho ya mikopo yenye jumla ya shilingi bilioni 62.72.Majadiliano yanaendelea baina ya benki, SIDO, JICA na

Page 94: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

94

Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa ajili ya kuendeleza maeneoya viwanda kwa wajasiriamali wadogo. Majadilianoyanaendelea vizuri na mradi unatarajiwa kuanza kutekelezwakatika nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha 2019/2020.

TIB Corporate Bank – TIB CBL

102. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019, Benki yaTIB – CBL ilipanga kutoa mikopo yenye thamani ya Shilingibilioni 40 kwa ajili ya ununuzi wa mazao ya biashara, Shilingibilioni 20 kwa ajili ya sekta mbalimbali za kiuchumi, kutoabarua na dhamana za mikopo ya thamani ya Shilingi bilioni15 na kukuza amana kutoka kwa wateja.

103. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili 2019, Benkiimefanikiwa kutoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni6.1 kwa ajili ya ununuzi wa Pamba na shilingi bilioni 6.9 kwaajili ya ununuzi wa Kahawa. Vilevile, benki imefanikiwakuidhinisha mikopo ya jumla shilingi bilioni 68.7 kwa ajili yasekta mbalimbali za kiuchumi, pamoja na barua na dhamanaza mikopo ya thamani ya shilingi bilioni 140 kwa Kampuni naTaasisi mbalimbali za umma na binafsi. Benki ilifanikiwa piakukuza amana kutoka kwa wateja hadi kufikia shilingi bilioni276.08 ikilinganishwa na shilingi bilioni 258.64 mwaka 2017/18, sawa na ongezeko la asilimia 6.7.

Benki ya TPB PLC

104. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018, Benki ya TPBiliweka lengo la kukuza amana za wateja hadi kufikia shilingibilioni 469.00 na kutoa mikopo ya shilingi bilioni 389. Aidha,benki inatarajia kuongeza mapato kutoka shilingi bilioni 107.96mwaka 2017 hadi kufikia shilingi bilioni 121.47 mwaka 2018.

105. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018, Benki ya TPBimeendelea kutoa huduma za kibenki kupitia matawi yake36. Mtandao huu wa matawi uliongezewa wigo na matawimadogo 40 yanayofanya kazi katika maeneo mbalimbalinchini. Katika kipindi hicho, amana za wateja ziliongezekakwa shilingi bilioni 25.45 na kufikia shilingi bilioni 446.11. Aidha,

Page 95: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

95

idadi ya wateja imeongezeka na kufikia wateja 576,264 sawana ongezeko la wateja 65,240.

106. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Desemba 2018, thamaniya mikopo katika Benki ya TPB ilikuwa shilingi bilioni 408.46sawa na ongezeko la shilingi bilioni 71.66. Thamani ya mikopoiliongezeka kutokana na Benki hii kuunganishwa na Benki yaTwiga na Benki ya Wanawake. Aidha, katika kipindi hicho,pato ghafi la Benki lilikuwa shilingi bilioni 117.40 likiwa niongezeko la kiasi cha shilingi bilioni 9.44.

107. Mheshimiwa Spika, Benki ya TPB imefanya juhudi zakuboresha mikopo iliyopokelewa kutoka katika Benki ya Twigana Benki ya Wanawake, kwa kufuatilia na kukusanya madenikutoka kwa wadaiwa wa muda mrefu pamoja na kuwekalengo la kukabili hasara katika madeni mengine. Jumla yataasisi 193 zenye wakopaji 2,130 zilitembelewa na wakopajikutambuliwa na kubaini mikopo iliyofutwa yenye thamani yashilingi bilioni 12.0. Fedha ambazo zimekusanywa kutokakwenye mikopo iliyofutwa kwa kipindi cha Januari, 2018 hadiMachi, 2019 ilifikia shilingi bilioni 2.5. Aidha, Benki inaendeleana juhudi ya kukusanya madeni ya mikopo iliyofutwa.

108. Mheshimiwa Spika, katika kipindi kilichoishia Desemba2018 Benki imeendelea na juhudi za kuimarisha ubora wamikopo yake, uimarishwaji huu wa mikopo uliwezesha benkikuwa na kiwango kidogo cha mikopo chechefu cha asilimia6.9, kiwango hicho cha ubora wa mikopo pamoja na wigompana wa bidhaa za TPB viliweka benki katika hali nzuri nahivyo kupata mapato ya shilingi bilioni 19 na faida kabla yakodi ya shilingi bilioni 17.2. Ukuaji huo ulionekana katikathamani za mtaji wa benki, rasilimali na amana za wateja.Juhudi zinaendelea katika kuboresha mikopo na kuongezauwezo wake katika kuleta faida. Matumaini ni kuwa namikopo ambayo kiwango cha mikopo chechefu ni chini yaasilimia 5. Aidha, matarajio ya benki ni kuendelea kufanyavizuri hasa baada ya kuongezewa wanahisa ambaowataendelea kuwekeza fedha katika benki yao na hivyokuipa uwezo wa kufanya biashara na hatimaye kuongezamapato yake yanayotokana na riba za mikopo.

Page 96: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

96

2.3.2 Taasisi za Kitaalam na Huduma Nyinginezo

Ofisi ya Taifa ya Takwimu -NBS

109. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai, 2018 hadiAprili, 2019 Ofisi ya Taifa ya Takwimu imefanya kazi zakukusanya, kuchambua, kutunza na kuwasilisha takwimurasmi zinazohitajika katika sekta mbalimbali za kiuchumi nakijamii kwa wakati kama ifuatavyo: Mfumuko wa Bei kwa kilamwezi; Pato la Taifa kwa robo mwaka hadi robo ya tatu yamwaka 2018/19; Takwimu za Pato la Taifa zilizorekebishwakwa mwaka wa kizio 2015; Fahirisi za Uzalishaji Viwandanihadi robo ya tatu ya mwaka 2018; Fahirisi za bei za uzalishajiviwandani hadi robo ya tatu ya mwaka 2018; Fahirisi za Uuzajina Uagizaji wa bidhaa nje ya Nchi kwa robo tatu ya mwaka2018/19; Takwimu za uchumi za Pato la Taifa kwa mwaka 2007– 2017; Makadirio ya idadi ya watu kwa umri kwa mwaka2013 hadi 2035; Tafiti za Sekta ya Utalii Tanzania, 2018; naTaarifa ya Hali ya Uhalifu Tanzania, 2018.

110. Mheshimiwa Spika, maandalizi kwa ajili ya sensa yaMwaka 2022 yameanza kwa kuandaa “Strategic Handbook”ambayo inabainisha namna sensa itakavyofanyika.Maandalizi mengine yaliyofanyika hadi sasa ni kufanya “Pilot”ya kutenga maeneo ya kuhesabia watu katika Wilaya yaChamwino ambayo imekamilika na kazi inaendelea kwaWilaya ya Bahi. Aidha, zoezi la kukusanya takwimu za utafitiwa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi (HBS) 2017/18lililoanza Desemba 2017 limekamilika Novemba 2018. Uhaririwa takwimu hizo ulikamilika Januari 2019 na uchambuzi waviashiria vya umaskini wa kipato na usio wa kipato ulikamilikaMachi 2019.

111. Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia umuhimu wamatumizi bora ya takwimu katika Sera na Mipango yaMaendeleo ya Nchi, jitihada zinaendelea kuwekwa katikakuimarisha na kuboresha takwimu za uchumi, kijamii namazingira hususan katika kipindi hiki ambacho Nchi zoteduniani zinaendelea na utekelezaji wa Mpango Endelevu waMaendeleo wa Dunia wa mwaka 2030 ambapo takwimu ni

Page 97: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

97

nyenzo ya kupima malengo yaliyofikiwa katika maeneoyanayohusu uwazi, utawala bora, matokeo na mabadilikoya sera. Vilevile, juhudi zinaelekezwa katika kuhamasishamatumizi bora ya takwimu katika ngazi zote za utawala kwalengo la kuhakikisha malengo yaliyowekwa katika kutekelezamipango ya maendeleo ya Nchi yanafikiwa kwa ukamilifu.

Mamlaka ya Mapato Tanzania – TRA

112. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Mamlaka yaMapato Tanzania (TRA) ilipanga kukusanya shilingi trilioni18.03, ikiwa ni ongezeko la asilimia 18.7 ikilinganishwa namakusanyo halisi ya mwaka wa fedha 2017/18. Kwa upandewa Zanzibar, TRA ilipanga kukusanya shilingi bilioni 301.47,ikiwa ni ongezeko la asilimia 17.8 ikilinganishwa na makusanyohalisi ya mwaka wa fedha 2017/18.

113. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2018 hadiAprili 2019, Mamlaka ya Mapato Tanzania ilifanikiwakukusanya shilingi trilioni 12.88 Tanzania Bara ikilinganishwana lengo la kukusanya shilingi trilioni 14.74 katika kipindi hicho.Makusanyo hayo ni ongezeko la asilimia 2.22 ikilinganishwana shilingi trilioni 12.60 zilizokusanywa katika kipindi kama hichomwaka 2017/18 (Jedwali Na. 4).

114. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Zanzibar,makusanyo yalifikia shilingi bilioni 241.12 ikilinganishwa nalengo la kukusanya shilingi bilioni 248.39 (Jedwali Na.5).Makusanyo hayo ni sawa na ufanisi wa asilimia 97.07 ya lengona ni ongezeko la asilimia 14.7 ikilinganishwa na makusanyoyaliyofikiwa katika kipindi kama hiki mwaka 2017/18.

115. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Bunge lako Tukufukatika mwaka wa fedha 2018/19, ilianzisha Mfumo Mpya waStempu za Kodi za kielektroniki (Electronic Tax Stamp – ETS)ambao ulianza kutumika tarehe 01 Septemba, 2018 kwalengo la kuiwezesha Serikali kutumia teknolojia ya kisasa yakupata taarifa sahihi za uzalishaji viwandani na kwa wakati.Mfumo huu mpya pia ulilenga kuiwezesha Serikali kudhibitiuvujaji wa mapato na kutambua mapema kiasi cha Kodi ya

Page 98: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

98

Ushuru wa Bidhaa, Kodi ya Mapato na ile ya Ongezeko laThamani. Aidha, mfumo wa Stempu za Kodi za kielektronikiutadhibiti tatizo la kugushi linalotokana na uwepo wa stempuza karatasi ambao umechangia uwepo wa bidhaa zisizokidhiviwango vya ubora na zinazoweza kuathiri afya za binadamu.

116. Mheshimiwa Spika, Mfumo wa ETS tayari umeanzakufanya kazi kwa viwanda vya awamu ya kwanza yaanisigara, pombe kali na bia. Hadi Aprili, 2019 wazalishaji wandani 33 na waagizaji 17 wa bidhaa kutoka njewameunganishwa katika mfumo ikiwemo Viwanda vyote vyasigara (4), viwanda vyote vya bia (7), na viwanda 22 vyapombe kali. Viwanda vinginge vya pombe kali viko katikahatua mbalimbali za usimikaji wa mfumo. Ufungwaji wamitambo ya ETS kwa viwanda vya awamu ya pili unaendeleaambapo unahusisha viwanda vya soda, maji na juisi.Utekelezaji wa mfumo wa ETS umechangia kuongezeka kwamakusanyo ya Ushuru wa Bidhaa kwenye bidhaa za sigara,Bia na Pombe kali kwa asilimia 6.5 toka shilingi bilioni 445.47mwaka 2017/18 mpaka shilingi bilioni 474.57 mwaka 2018/19.

117. Mheshimiwa Spika, Mamlaka ya Mapato Tanzaniaimeendelea kuhamasisha ulipaji kodi kwa hiari kwa kutumianjia mbalimbali ikiwa ni pamoja na utoaji wa elimu ya kodikwa walipa kodi kuhusu sheria na kanuni mbalimbali za kodi,namna ya ukokotoaji wa kodi na uwasilishaji wa pingamiziikiwa mfanyabiashara hakuridhishwa na makadirio ya kodi.Utoaji wa elimu ya kodi unafanyika kupitia makongamano,semina, televisheni na radio pamoja na mitandao ya kijamii.Aidha, Mamlaka imeanzisha kituo cha ushauri kwa mlipa kodikilichopo Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kurahisisha hudumakwa walipa kodi kwa kuwapatia ushauri kuhusu masuala yakodi. Vituo vingine vinaanzishwa katika mikoa ya Mwanza,Mbeya, Dodoma na Arusha. Vilevile, Mamlaka inaendeleakuboresha mifumo yake ya TEHAMA ili kurahisisha ulipaji wakodi kwa njia ya mitandao ya simu pamoja na mabenki.

118. Mheshimiwa Spika, Mamlaka ya Mapato Tanzaniaimeendelea kusimamia uboreshaji wa vitalu vya kodi kwakuongeza wafanyakazi wenye weledi kwenye maeneo

Page 99: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

99

yenye mchango mkubwa wa makusanyo ya kodi. Mamlakainashirikiana na Serikali za Mitaa ili kubadilishana taarifazitakazo imarisha usimamizi wa mapato kwenye vitalu vyakodi. Aidha, Mamlaka ya Mapato Tanzania inaendeleakuwajengea uwezo maafisa wa kodi kuhusu namna bora yakusimamia vitalu na kuimarisha mifumo ya kielektroniki kamavile Mfumo Jumuishi wa Usimamizi wa Mapato (e-TAX) naMfumo wa Usajili wa Walipa Kodi ili kuwa na taarifa sahihi zawalipa kodi.

Mfuko wa Huduma Ndogo za Fedha – Self Microfinance Fund

119. Mheshimiwa Spika, jukumu la msingi la Mfuko wa SELFni kukuza na kuongeza upatikanaji wa huduma za fedha kwaWananchi wenye kipato cha chini, hususan waishio vijijini napembezoni mwa miji. Lengo ni kuwawezesha kushiriki katikashughuli za uzalishaji mali, kujiongezea kipato na hatimayekuondokana na umaskini. Katika kutekeleza lengo lauwezeshaji, Mfuko umeendelea kukopesha wajasiriamalikatika sekta ya Kilimo na Biashara. Mikopo ya Kilimo imejikitakatika uzalishaji, pembejeo, zana za kilimo na mnyororo waongezeko la thamani. Aidha, mikopo ya biashara imejielekezakatika biashara za uchuuzi na huduma.

120. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19 Mfukoulipanga kutoa mikopo ya kiasi cha shilingi bilioni 25.0 nakukusanya jumla ya shilingi bilioni 21.28 kutoka kwa wakopaji.Hadi kufikia Aprili, 2019 Mfuko umefanikiwa kutoa mikopoyenye thamani ya shilingi bilioni 20.4 ikiwa ni ufanisi wa asilimia82.0. Mikopo hiyo iliwafikia wajasiriamali wadogo wapatao8,339 ambapo kati ya hao 4,443 ni wanawake na 3,896 niwanaume. Aidha, Mfuko ulifanikiwa kurejesha jumla ya shilingibilioni 19.25 kutoka kwa wakopaji sawa na asilimia 90.46 yalengo. Mfuko wa SELF utaendelea kutekeleza jukumu lake lamsingi la kuwawezesha wananchi kiuchumi na kuchangiakwenye huduma za kifedha. Napenda kuliarifu Bunge lakoTukufu kuwa, Mfuko wa SELF kwa sasa unachangia asilimia 3katika ukuaji wa huduma za kifedha hapa inchini. Nimatumaini ya Serikali kuwa kiwango cha mchango wa Mfuko

Page 100: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

100

wa SELF kwenye ukuaji wa huduma za kifedha utaongezekahususan baada ya kuunganishwa na UTT MFI.

Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi – NBAA

121. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2018/19, Bodi ya Taifaya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) il ipanga kusaji l iwatahiniwa, wanachama na kampuni za uhasibu na ukaguzi,kufanya ukaguzi na kusimamia ubora wa kazi za ukaguzi,kutoa miongozo ya viwango vya uhasibu na ukaguzi, kutoamafunzo endelevu kwa wanataaluma na wadau wengine,kutoa huduma ya ushauri elekezi na ufundi, kukamilishamuundo wa mifumo ya uwekaji kumbukumbu namawasiliano, na kuendelea kushirikiana na Taasisi nyinginekama TRA, BRELA na BoT katika kuwaelimisha wadau kuwezakuelewa na kutumia viwango vya uhasibu na ukaguzivinavyokubalika.

122. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili 2019, Bodi ya Taifaya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) imefanikiwa kufanyaukaguzi wa ubora wa uandaaji wa taarifa za fedha katikataasisi 66, kufanya ukaguzi wa kampuni 50 za uandaaji naukaguzi wa hesabu ili kujiridhisha kama zina mifumo thabitiya udhibiti ubora katika ukaguzi wa hesabu kwa kuzingatiaviwango vya kimataifa, kuendelea kuzihamasisha taasisi zaSerikali, mashirika yasiyo ya kiserikali na taasisi binafsi kutumiaviwango vya kimataifa vya utayarishaji na ukaguzi wa taarifaza hesabu nchini na kutoa ushauri elekezi na huduma zakiufundi kwa taasisi za umma na binafsi tano Tanzania Bara.

123. Mheshimiwa Spika, katika jitihada za kuendeleza kadaya uhasibu hapa nchini, Bodi ilitunga, kusimamia nakusahihisha mitihani muhula wa Agosti na Novemba 2018 naFebruari 2019, ambapo jumla ya watahiniwa 6,204 walifanyamitihani. Kati yao, 63 walifaulu mitihani ya Cheti cha Utunzajiwa Hesabu, 377 walifaulu Shahada ya Juu ya Uhasibu na 22walifaulu mitihani ya ulinganifu kwa wahasibu wenye sifa zanje wanaokuja kufanya kazi hapa nchini. Aidha, Bodi ilitoamafunzo ya diploma ya viwango vya uandaaji wa taarifa zafedha Serikalini kwa wahasibu 93. Vilevile, Bodi ilisajili kampuni

Page 101: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

101

za ukaguzi wa hesabu 15, wakaguzi wa hesabu katika ngaziya CPA-PP 68, wahasibu ngazi ya CPA 145, wahasibu wahitimuwanaopatiwa uzoefu wa kazi 373, watunza vitabu watanona kampuni moja ya uhasibu. Bodi itaendelea kusimamiataaluma ya uhasibu na ukaguzi wa hesabu ili kuhakikishakuwa hesabu zinazoandaliwa zinakidhi viwango vyakimataifa, taratibu, kanuni na miongozo stahiki.

Bodi ya Michezo ya Kubahatisha - Gaming Board

124. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Bodi yaMichezo ya Kubahatisha ilipanga kusimamia na kutoa leseni2,500 ya michezo ya kubahatisha na kuhakikishazinaendeshwa kwa mujibu wa sheria na taratibu. Aidha, Bodiilipanga kuanzisha mfumo wa kielektroniki wa Kusimamiamichezo ya kubahatisha ujulikanao kama Regulator CentralMonitoring System (RCEMS).

125. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili 2019, Bodiimefanikiwa kutoa jumla ya leseni 2,062 sawa na asilimia 82.48ya lengo. Idadi hii inajumuisha leseni mpya 779 na lesenizilizohuishwa 1,283. Vilevile, Bodi ilifanikiwa kukusanya jumlaya shilingi bilioni 3.7 ikiwa ni ada ya leseni sawa na asilimia 64ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 5.8. Bodi pia, ilifanyaukaguzi kwa waendeshaji wa michezo ya kubahatisha 53nchini kwa lengo la kuhakikisha kuwa michezo hiyoinaendeshwa kwa kuzingatia matakwa ya sheria ya michezohiyo pamoja na sheria nyingine za nchi. Katika ukaguzi huo,Bodi haikubaini ukiukwaji mkubwa wa sheria kwawaendeshaji wenye leseni. Hata hivyo, Bodi ilibaini baadhiya wafanyabiasha kuendesha biashara ya michezo yakubahatisha bila leseni. Bodi iliwachukulia hatua wale wotewaliobainika kuendesha biashara hiyo kinyume na sheria,kanuni na taratibu za nchi.

126. Mheshimiwa Spika, Bodi inaendelea na kazi ya kuundamfumo wa kielektroniki wa Kusimamia michezo yakubahatisha, kwa kushirikiana na wataalamu wa mifumo waWizara pamoja na Wakala wa Mifumo wa Serikali, na kazihiyo inatarajiwa kukamilika katika mwaka wa fedha 2019/

Page 102: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

102

2020. Kukamilika kwa mfumo huo kutaiwezesha Bodikusimamia kwa ufanisi sekta hiyo na hivyo kufikia malengoya kulinda maslahi mapana ya jamii, walaji pamoja nawawekezaji.

127. Mheshimiwa Spika, ili kulinda maadili ya jamii Bodiilichukua hatua ya kusitisha matangazo ya michezo yakubahatisha kupitia redio na runinga ili kutoa fursa kwa Serikalikuandaa utaratibu mpya wa kurusha matangazo bila kuletaathari kwa jamii. Aidha, Serikali iliunda timu ya wataalam kwaajili ya kufanya utafiti wa namna bora ya kuendesha BahatiNasibu ya Taifa na kuishauri Serikali ipasavyo. Taarifa namapendekezo ya utafiti huo yatasaidia kuweka utaratibumzuri wa kuendesha Bahati Nasibu ya Taifa, kwa faida yaserikali na jamii kwa ujumla.

2.3.3 Rufani za Kodi128. Mheshimiwa Spika, Bodi ya Rufani za Kodi (TRAB), katikamwaka 2018/19, imesajili mashauri 521 yenye kiasi cha kodikinachobishaniwa cha shilingi trilioni 1.3 na Dola za Marekanimilioni 5.3. Hadi kufikia Aprili, 2019 Bodi imesikiliza na kutoleauamuzi mashauri 431 yenye kiasi cha shilingi bilioni 880.7 chakodi kinachobishaniwa na Dola za Marekani billioni 6.2, kiasihiki kinajumuisha mashauri yaliyosajiliwa miaka ya nyuma.Aidha, Bodi katika kuongeza kasi ya usikilizaji wa mashauri yakodi imeanzisha vikao maalum “special sessions” kwa kusikilizana kutolea uamuzi mashauri ya muda mrefu.

129. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2018 hadiAprili 2019, Baraza la Rufani za Kodi (TRAT) lilikuwa na jumlaya mashauri 81 yaliyokuwa na kiasi cha kodikinachobishaniwa shilingi trilioni 22.83 na Dola za KimarekaniMilioni 1.45. Hadi kufikia Aprili 2019, mashauri 30 yaliyokuwana kiasi cha fedha kinachobishaniwa shilingi trilioni 21.43yalisikilizwa na kutolewa uamuzi.

2.3.4 Huduma za BimaMamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima – TIRA

130. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Mamlaka yaUsimamizi wa Shughuli za Bima imeandaa Rasimu ya Sera ya

Page 103: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

103

Taifa ya Bima. Sera hii itasaidia kuongeza wigo wa hudumaza bima; kuweka mifumo mahsusi ya kukabiliana na athariza majanga yatokanayo na mabadiliko ya mazingira na tabianchi; kuwapatia wananchi kinga ya bima ya uhakika na kwawakati; kuongeza mchango wa sekta ndogo ya bima katikaPato la Taifa; na kuongezeka kwa akiba, uwekezaji, ajira,umiliki wa watanzania, mitaji ya kampuni za bima na uelewawa shughuli za bima. Aidha, Mamlaka imeandaa kanuni zaBancassurance zitakazosaidia ukuaji wa soko la Bima nchini.Bancassurance ni utaratibu ambao benki au taasisi za fedhaushirikiana na kampuni za bima kusambaza na kuuza hudumaza bima. Kanuni za Bancassurance zimeanza kutumika Mei,2019.

131. Mheshimiwa Spika, Mamlaka imetengeneza mifumo yakielektroniki ili kurahisisha na kudhibiti uhalifu katika biasharaya bima nchini. Mifumo hiyo ni pamoja na Tanzania InsuranceRegulatory Authority Management Information System,Reinsurance Portal, Online Registration pamoja na TanzaniaImport Insurance Portal. Mifumo hii imerahisisha ukusanyajiwa taarifa za bima kutoka kwa kampuni za bima, upatikanajiwa taarifa za bima kwa wananchi, uhakiki wa taarifa za bimakwa umma na watumiaji wa huduma za bima pamoja naukusanyaji na udhibiti wa mapato, tozo na kodi zitokanazona biashara ya bima nchini. Mifumo hii pia inaongeza kodiitakanayo na biashara ya bima pamoja na kuongezamapato yatokanayo na bima mtawanyo. Vilevile, mifumohii yote inaweza kufikiwa na wanachi kwa kutumia simu yakiganjani pamoja na kompyuta.

132. Mheshimiwa Spika, katika kuendeleza mchango wasekta ya bima, Mamlaka imeendelea kuimarisha usimamizina ukaguzi wa Kampuni za Bima. Katika kipindi cha kuanziaJulai 2018 hadi Aprili 2019, Mamlaka imefanya kaguzi katikakampuni 15, kati ya hizo kampuni tatu ni za bima za mudamrefu na kampuni 12 ni za bima za muda mfupi. Aidha, hadikufikia Aprili, 2019, jumla ya kampuni 28 zilikuwa zimekidhimatakwa ya kisheria kuendelea kutoa huduma ya Bima.Vilevile, Mamlaka imeendelea kuchukua hatua stahiki zausimamizi kwa kampuni ambazo hazitekelezi matakwa ya

Page 104: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

104

kisheria na usimamizi wa biashara ya bima ikiwemo hitaji laukwasi (Solvency margin deficit), kutokutumia vizuri mfumowa kielektroniki wa kununulia bima za mizigo toka nje ya nchina mfumo wa kukagua bima za magari.

Shirika la Bima la Taifa – NIC

133. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Shirika laBima la Taifa lilipanga kuanzisha Bima ya Kilimo, kuanzishamfumo mpya wa kidij itali wa bima za COMESAutakaokomesha bima za bandia na kukusanya mapato yashilingi bilioni 99.79. Hadi kufikia Aprili 2019, Shirika kwakushirikiana na Wizara ya Kilimo limeanzisha bidhaa mpya yaBima ya Kilimo ambayo itakuwa inamkinga mkulima namajanga kipindi cha uzalishaji. Bima hiyo inatarajiwakuzinduliwa mwezi Agosti, 2019 na kuanza kufanya kazi kwamara ya kwanza kwa wakulima wa mkoa wa Simiyu. Aidha,Shirika limefanikiwa kuanzisha Mfumo wa kidigitali wakukusanya na kutoa miamala ya Bima za COMESA YellowCard. Mfumo huo umeongeza mapato ya Shirika kutokashilingi bilioni 1.63 katika kipindi cha Julai 2017 hadi Machi,2018 na kufikia shilingi bilioni 2.86 katika kipindi cha Julai 2018hadi Machi, 2019. Vilevile, Shirika lilikusanya Shilingi bilioni 43.04sawa na asilimia 43 ya makaridio. Shirika litaendelea kutoaelemu kwa umma ili kuhakikisha kuwa, bidhaa na hudumaza bima zinafahamika na kuwafikia watanzania waliowengi,hususan wakulima, wafugaji na wavuvi.

2.3.5 Mitaji na DhamanaMamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana – CMSA

134. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Mamlaka yaMasoko ya Mitaji na Dhamana ilipanga kusimamia soko lamitaji ili kulinda maslahi ya wawekezaji, kuongeza idadi yawataalam wa masoko ya mitaji wenye weledi na ujuzi wangazi ya kimataifa, kutoa elimu kwa umma na kutoa mafunzoyenye lengo la kujenga uwezo wa Halmashauri za Serikali zaMitaa kutumia fursa ya kutoa Hatifungani za Serikali za Mitaakupata fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo ambayoinaweza kujiendesha kibiashara. Hadi kufikia Aprili 2019,

Page 105: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

105

Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana imeendeleakusimamia masoko ya hisa na dhamana ili kulinda maslahiya mwekezaji. Katika kipindi hicho, Idadi ya wawekezaji katikamasoko ya mitaji na dhamana imeongezeka na kufikiawawekezaji 685,625 kutoka wawekezaji 530,841 Aprili, 2018.

135. Mheshimiwa Spika, katika jitihada za kuongezawataalam wenye weledi na ujuzi kwa ngazi ya kimataifakwenye masoko ya mitaji na dhamana, Mamlaka iliendeshamafunzo yanayotambulika kimataifa kwa wataalam 131 kwakushirikiana na Taasisi ya Uwekezaji na Dhamana yaUingereza katika kipindi kilichoishia mwezi Aprili 2019,ikilinganishwa na wataalam 60 waliopatiwa mafunzo kamahayo katika kipindi kilichoishia mwezi Aprili 2018. Mafunzohaya yamewezesha kujenga uwezo na ufanisi kwa watendajiwa masoko ya mitaji hapa nchini. Aidha, Mamlakaimeendelea kutoa elimu ili kuongeza uelewa na ushiriki katikamasoko ya mitaji kwa kuendesha mafunzo kwa wataalam15,004 wa kada mbalimbali, ikilinganishwa na wataalam 7,872waliopatiwa mafunzo kama hayo katika kipindi kilichoishiamwezi Aprili 2018. Vilevile, katika kipindi hicho, Mamlakailiendesha semina kwa Waheshimiwa Wabunge 51 kuhusufursa na faida za uwekezaji katika masoko ya mitaji.

136. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa soko la hatifunganiza Serikali za Mitaa (Municipal Bonds), Serikali kupitia Mamlakaya Masoko ya Mitaji na Dhamana kwa kushirikiana na Mfukowa Maendeleo ya Mitaji wa Umoja wa Mataifa (UNCDF)imeendelea na jitihada za kujenga uwezo wa kutumia fursaya utoaji wa Hatifungani za Serikali za Mitaa katikakugharamia miradi ya Maendeleo. Jitihada hizi ni pamojana utoaji wa elimu kwa Halmashauri za Serikali za Mitaakuhusu faida na namna ya kutumia Hatifungani hizi katikakugharamia miradi ya maendeleo; na kutoa mwongozo kwaHalmashauri za Serikali za Mitaa wa jinsi ya kufanya upembuziyakinifu wa miradi ya maendeleo yenye uwezo wakujiendesha kwa njia ya kutoa Hatifungani za Serikali za Mitaa,ambapo mapato yatokanayo na miradi hiyo ndiyoyatatumika kulipa fedha zitokanazo na hatifungani hizo.

Page 106: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

106

137. Mheshimiwa Spika, kufuatia juhudi hizo, Halmashauri yaJiji la Mwanza, imepata idhini kutoka Ofisi ya Rais, Tawala zaMikoa na Serikali za Mitaa kuendelea na mchakato wa utoajiwa Hatifungani za Serikali za Mitaa kwa Umma. Hii imetokanana halmashauri hiyo kukidhi vigezo vya utoaji wa Hatifunganiza Serikali za Mitaa, ikiwa ni pamoja na Utawala Bora; kuwana hati safi ya ukaguzi wa taarifa za fedha; na kuwa na miradiiliyofanyiwa upembuzi yakinifu. Aidha, Mamlaka kwakushirikiana na Mfuko wa Maendeleo ya Mitaji wa Umoja waMataifa imeendelea na jitihada za utoaji wa elimu kwaHalmashauri za Serikali za Mitaa hapa nchini juu ya utoaji wahatifungani hizo.

Soko la Hisa la Dar es Salaam – DSE

138. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Soko la Hisala Dar es Salaam lilitarajia kuorodhesha kampuni nne mpyakwenye Soko la Hisa. Kampuni zilizotarajiwa kujiorodhesha nikampuni za simu na mawasiliano. Hata hivyo, matarajio hayohayakufikiwa hadi kufikia Aprili 2019, kutokana na kampunihizo kuchelewa kukamilisha taratibu. Aidha, hadi kufikia Aprili2019, jumla ya kampuni 28 zilikuwa zimeorodheshwa kwenyeSoko la Hisa Dar es Salaam. Kati ya hizo, 21 ni kampuni zandani na saba ni za nje. Aidha, katika kipindi hicho, Serikaliiliorodhesha hatifungani zenye thamani ya shilingi bilioni 9,402ikilinganishwa na hatifungani zenye thamani ya shilingi bilioni8,874 zilizoorodheshwa Aprili 2018. Vilevile, katika kipindi hichohatifungani za kampuni binafsi zenye thamani ya shilingi bilioni124.88 ziliorodheshwa katika soko. Jumla ya thamani ya hisazilizopo sokoni ni shilingi bilioni 19,380 ambapo shilingi bilioni9,161 ni za kampuni za ndani.

139. Mheshimiwa Spika, kwa kipindi cha Julai 2018 hadi Aprili2019, hisa zenye thamani ya shilingi bilioni 111 zilinunuliwaikilinganishwa na hisa zenye thamani ya shilingi bilioni 454mwaka 2017/18. Kupungua kwa shughuli za uuzaji na ununuziwa hisa katika mwaka 2018/19 kumechangiwa na mdororowa shughuli za uwekezaji katika masoko ya hisa ya nchizinazoendelea kulikosababishwa na mwenendo wawawekezaji duniani kupeleka uwekezaji wao katika masoko

Page 107: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

107

makubwa yaliyoendelea na hasa nchini Marekani. Aidha,katika kipindi hicho, DSE haikuweza kuorodhesha kampunikubwa kama ilivyotaratajiwa. Hata hivyo DSE ilipokeamaombi ya kampuni tatu za simu za mikononi (Tigo, Halotelna Airtel) ambazo bado ziko katika mchakato wa kukamilishataratibu za kisheria na kanuni zinazosimamia uendeshaji wamasoko ya hisa na dhamana nchini.

140. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili 2019, hatifunganizenye thamani ya shilingi bilioni 454 zilinunuliwa, sawa naasilimia 86 ya thamani ya mauzo yote ya hatifungani kwamwaka 2017/18, ambapo mauzo ya hatifungani yalikuwashilingi billioni 528.

Soko la Bidhaa Tanzania – Tanzania Mercantile Exchange(TMX)

141. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Soko laBidhaa lilipanga kukusanya mtaji wa Soko la Bidhaa kutokaSekta ya Umma na Binafsi, kushawishi vyama vya ushirika nawafanyabiashara wa mazao kuanzisha kampuni za kutoahuduma za uwakala kwenye soko la bidhaa na kukamilishaununuzi na kufunga mfumo wa kielektroniki wa mauzo,uhawilishaji bidhaa na malipo, na utoaji wa taarifa za masoko.Aidha, Soko lilipanga kutumia Balozi za Tanzania nje ya nchikutafuta masoko na kuongeza wanunuzi wa mazao kupitiaSoko la Bidhaa, kushirikiana na Idara ya Habari Maelezo, Bodiya Stakabadhi za Ghala na wadau wengine katika kutoaelimu kwa umma kuhusu Mfumo wa Stakabadhi Ghalani naSoko la Bidhaa, kutembelea wadau na kuhamasisha uzalishajimkubwa wa mazao ya chakula na biashara.

142. Mheshimiwa Spika, napenda kulitaarifu Bunge lakotukufu kuwa, Soko la Bidhaa limetekeleza baadhi ya shughulizilizopangwa kufanyika katika mwaka wa fedha 2018/19. Sokola Bidhaa lilitoa elimu kwa wakulima juu ya manufaa nanamna ya kuuza mazao yao katika Soko la Bidhaa, ikiwemokufanya mauzo ya majaribio katika mkoa wa Manyara. Aidha,Soko la Bidhaa lilifanikiwa kushawishi baadhi ya kampuni zaununuzi wa mazao kushiriki katika mauzo ya majaribio katika

Page 108: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

108

mkoa wa Manyara kama hatua ya kuelekea kwenyeuanachama wa Soko la Bidhaa. Soko la Bidhaa lilishiriki katikaziara ya kutafuta masoko ya mazao nchini Malawiiliyoratibiwa na Wizara ya Mambo ya nchi za Nje na Ushirikianowa Afrika Mashariki pamoja na TANTRADE ambakomazungumzo kuhusu ushirikiano wa kibiashara kati ya TMXna Soko la Bidhaa la nchi hiyo (AHL Commodity Exchange)ulijadiliwa na kuazimiwa.

143. Mheshimiwa Spika, Soko la Bidhaa halikuwezakukamilisha kufunga mfumo wa kielektroniki wa mauzo,uhawilishaji bidhaa na malipo, utoaji wa taarifa za masokokwa mujibu wa hadidu za rejea kutokana na kusitishwa kwamkataba na Mzabuni. Soko la Bidhaa lilianza taratibu zakumpata mzabuni mpya baada ya kupata kibali kutoka BenkiKuu ya Tanzania. Aidha, GPSA imekamilisha taratibu zakumpata mzabuni mpya anayetarajiwa kuanza kazi yakufunga mfumo wa kisasa Juni, 2019 na kukamilisha kazi hiyokatika kipindi cha miezi mitatu. Kuchelewa kuanza kwamfumo wa mauzo katika Soko la Bidhaa umeathiri juhudi zaukusanyaji mtaji toka Sekta Binafsi katika mwaka 2018/19.Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu na wananchi kwa ujumlakuwa, Soko la Bidhaa limeanza kufanya mauzo ya baadhiya mazao, hususan ufuta, dengu na mbaazi na hivyoinategewa kuwa Sekta Binafsi itavutiwa kuwekeza katika Sokola Bidhaa na hatimaye kuchochea uzalishaji wa mazao yabiashara.

2.3.6 Dhamana za Uwekezaji Tanzania

Taasisi ya Usimamizi wa Rasilimali za Uwekezaji - UTTAMIS

144. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Kampuni yaUsimamizi wa Rasilimali za Uwekezaji ilipanga kuongezarasilimali za mfuko kwa asilimia 15, kuongeza idadi yawawekezaji kwa asilimia 5, kuzihusisha zaidi Taasisi za Serikali,Mifuko ya Hifadhi za Jamii, Mashirika na vikundi mbalimbalivya kijamii kama vile SACCOS kujiunga na mifuko ya UTT AMIS.

Page 109: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

109

145. Mheshimiwa Spika, hadi Aprili 2019, UTT AMIS imeongezarasilimali za Mfuko kutoka shilingi bilioni 290.9 hadi shilingi bilioni294. Aidha, idadi ya wawekezaji iliongezeka kutoka 140,615hadi 144,749 sawa na ongezeko la asilimia 2.94. Vilevile, Taasisiiliuza vipande vya shilingi bilioni 39 na shilingi bilioni 36.7zilitolewa kwa ajili ya ununuzi wa vipande na kutoa gawiokwa wawekezaji. Kadhalika, Mfuko ulifanikiwa kuhamasishaTaasisi 25 kuwekeza kwenye Mifuko ya Pamoja ya Uwekezaji.

2.3.7 Taasisi za Mafunzo

Chuo cha Usimamizi wa Fedha – IFM

146. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Chuo chaUsimamizi wa Fedha kilitarajia kufanya udahili wa wanafunzi9,200 katika fani mbalimbali; kufanya tafiti na kutoa hudumaza ushauri elekezi; kuendeleza kituo cha Simiyu; na kukamilishaumiliki wa eneo la upanuzi wa Chuo katika Jiji la Dodoma(ekari 769).

147. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa masomo 2018/19, chuo kimefanikiwa kudahili jumla ya wanafunzi 10,421ikilinganishwa na wanafunzi 9,711 waliodahiliwa katikamwaka uliopita. Mafanikio haya ni sawa na asilimia 107.31,na kwa sehemu kubwa yamechangiwa na ongezeko lawataalam wa kada mbalimbali za fedha walioandaliwa nakujengewa uwezo na chuo. Aidha, chou kimefanya tafiti 23na kutoa shauri 4 katika kipindi cha kati ya Novemba 2018na Aprili 2019. Mafanikio mengine yaliyopatikana ni pamojaChuo kukamilisha malipo yote ya umiliki wa eneo lenyeukubwa wa ekari 783, kwa ajili ya ujenzi wa Kampasi yaDodoma. Vilevile, Chuo kimepewa eneo la zaidi ya ekari 29mkoani Simiyu katika kijiji cha Sapiwi, kilichopo katikaHalmashauri ya wilaya ya Bariadi kwa ajili ya kuanzisha kituokipya cha mafunzo. Kituo hicho kinalenga kunufaika na sokokubwa katika mikoa ya Mara, Simiyu na Shinyanga kutokanana kukosekana kwa huduma za vyuo vya elimu ya kati katikakanda hiyo.

Page 110: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

110

Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini – IRDP

148. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019, Chuo chaMipango na Maendeleo Vijijini kilipanga kuongeza udahili wawanafunzi kutoka wanafunzi 5,784 hadi kufikia wanafunzi7,000; kuboresha miundombinu ikiwa ni pamoja na kuanzakujenga jengo la tatu la mafunzo katika Kituo cha Kanda yaZiwa Mwanza; kuanza ujenzi wa Bweni la wasichana lenyeuwezo wa kuchukua wanafunzi 192 katika Kampasi yaDodoma; kuajiri watumishi wapya 90; na kuongeza uwezowa kiutendaji kwa watumishi 226. Hadi kufikia Aprili, 2019,Chuo kimedahili na kusajili jumla ya wanafunzi 8,098wakiwemo wanaume 3,622 na wanawake 4,476 katika fani27 ikiwa ni asilimia 115.7 ya lengo la Chuo la kudahili wanafunzi7,000. Aidha, katika mahafali ya 32 ya Chuo ya mwaka 2018/19, jumla ya wahitimu 3,799 wakiwemo wanaume 1,625 nawanawake 2,174 walihitimu mafunzo yao katika kozimbalimbali za mipango ya maendeleo. Kuhitimu kwawanafunzi hao kunaongeza idadi ya wataalam wenyeweledi wa kuandaa, kutekeleza, kufuatilia na kusimamiashughuli za maendeleo nchini.

149. Mheshimiwa Spika, miradi iliyotekelezwa ni pamoja naMradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi Kandaya Kati Tanzania unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya; Mradiwa Uboreshaji Miundombinu ya Masoko na Kuongezathamani katika zao la Vitunguu Saumu unaofadhiliwa naMfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo - IFAD na Benkiya Maendeleo ya Afrika – AfDB; na Mradi wa KuboreshaUstahimilivu wa Jamii ya wafugaji na wakulima wa Wilaya yaBunda kwa ajili ya kupunguza migogoro ya rasilimali zakiikolojia na rasilimali zinazofanana na hizo unaofadhiliwa naShirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa - UNDP. Aidha,Chuo kimeendelea kutoa huduma ya ushauri elekezi kwawadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo Halmashauriza Wilaya, Miji na Majiji; Sekta Binafsi na Mashirika yasiyo yaKiserikali. Huduma hizo zimesaidia kuboresha utoaji wahuduma na kuchochea shughuli za Maendeleo za kiuchumina kijamii.

Page 111: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

111

Chuo cha Uhasibu Arusha – IAA150. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Chuo chaUhasibu Arusha kimeendelea kutoa mafunzo ya msingi nambinu katika nyanja za uhasibu, ugavi, usimamizi wa kodi,benki, utawala wa biashara, teknolojia ya habari na sayansiya kompyuta katika ngazi ya Cheti, Stashahada, Shahadaya kwanza na Shahada ya Uzamili. Katika kutekeleza hilo,kwa mwaka 2018/19 chuo kil idahili wanafunzi 3,986ikilinganishwa na wanafunzi 3,849 waliodahiliwa mwaka 2017/18. Kati ya hao 791 ni ngazi ya cheti, 1,282 ni ngazi yastashahada 1,695 ni ngazi ya shahada ya kwanza na 218 nishahada ya uzamili. Aidha, chuo kwa kushirikiana na Wizara,PPRA, PSPTB, GPSA na wadau wengine kilishiriki kuandaa nakuendesha kongamano la kimataifa liitwalo “InternationalPublic Procurement Conference 2018” mwezi Agosti 2018ambapo washiriki zaidi ya 300 kutoka nchi zaidi ya 46walishiriki. Lengo la kongamano hilo lilikua kuwapa fursawatunga sera, wanataaluma na watu wengine kubadilishanauzoefu kuhusu sheria na taratibu za ununuzi wa ummazinazotumika katika nchi mbalimbali.

151. Mheshimiwa Spika, katika kipindi hicho, chuokimeanzisha programu mpya nne katika ngazi ya shahadaya uzamili ambazo ni Shahada ya Uzamili ya Usimamizi waBiashara katika TEHAMA (Master of Business Administration -Information Technology Management); Shahada ya Uzamiliya Usimamizi wa Biashara (Master of Business Administration);Shahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Biashara katika Ununuzina Ugavi (Master of Business Administration – Procurementand Supplies Management); na Shahada ya Uzamili yaSayansi ya Fedha na Uwekezaji (Master of Science- Financeand Investment). Aidha, ili kuboresha miundombinu yakufundishia na kujifunzia chuo kimechukua hatua mbalimbalizikiwemo, kujenga madarasa katika kampasi ya Babati,kukarabati madarasa na kuanza kutumia mfumo wakielektroniki kudahili na kuchakata matokeo ya wanafunzi.

Taasisi ya Uhasibu Tanzania – TIA152. Mheshimiwa Spika, ili kuendelea kutoa elimu bora,huduma za utafiti zenye tija na ushauri uliyo bora, Taasisi katika

Page 112: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

112

mwaka 2018/19 imeandaa sera inayosimamia masuala yautafiti, ushauri na machapisho. Sera hii inalengakuwawezesha wahadhiri kufanya tafiti na kuandikamachapisho mbalimbali yatakayoainisha jinsi ya kuendanana uchumi wa viwanda. Aidha, katika kuendelea kutoaushauri kwa jamii, Taasisi imetoa ushauri wa kitaalamu katikakutambua na kutathmini vyanzo vyote vya mapato katikaHalmashauri ya mji wa Tunduma. Vilevile, Taasisi imetoaushauri katika uandaaji wa daftari la mali kwa mujibu wamwongozo wa Serikali kwa Halmashauri ya Jiji la Mbeya.Kadhalika, Taasisi katika kuhakikisha inatoa elimu bora, kwamwaka 2018/19 imeandaa miongozo mitatu ya kufundishia.Miongozo hii inalenga kuwawezesha wanafunzi kuwa nauelewa mpana unaoendana na mazingira halisi katika fanizao.

153. Mheshimiwa Spika, Taasisi katika kuboresha suala lataaluma na kuhakikisha inakuwa na wahadhiri wa kutosha,kwa mwaka wa fedha 2018/19 imedhamini wahadhiri 18katika kozi ya Shahada ya Uzamivu (PhD) ndani ya nchi nawahadhiri watatu nje ya nchi. Aidha, Taasisi katika kutatuachangamoto ya uhaba wa madarasa imekamilisha ujenzi wajengo la taaluma kampasi ya Dar es Salaam. Kukamilika kwajengo hili kunapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto yamuda mrefu ya uhaba wa kumbi za kufundishia, madarasa,maktaba na maabara ya kompyuta. Vilevile, katikakuboresha majengo kwa ajili ya ofisi na malazi kwa wanafunzi,Taasisi imekarabati mabweni katika kampasi ya Singida naofisi katika kampasi ya Mbeya.

154. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai, 2018 hadiAprili, 2019 Taasisi ilidahili wanafunzi 16,720 katika kozimbalimbali. Kati ya hao wanawake ni 8,821 na wanaume ni7,899. Aidha, katika mwaka wa 2018 wanafunzi 6,416walihitimu mafunzo yao katika kozi mbalimbali. Kati ya hao,wanafunzi 1,678 walihitimu katika ngazi ya Cheti cha Awali,2,436 walihitimu katika ngazi ya Stashahada, 2,266 walihitimukatika ngazi ya Shahada na 36 walihitimu katika ngazi yaStashahada ya Uzamili.

Page 113: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

113

Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika – EASTC

155. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19 Chuo chaTakwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) kinaendelea kutoamafunzo ya Shahada ya Uzamili katika Takwimu Rasmi naTakwimu za Kilimo. Jumla ya wanafunzi 36 wanaendelea namasomo ya shahada za uzamili. Aidha, Mitaala ya Ngazi yaCheti, Diploma na Shahada imepitiwa upya na ukamilishajiwa maoni ya maboresho ya mwisho kutoka Baraza la Taifala Elimu ya Ufundi (NACTE) kwenye mitaala husika yapo hatuaza mwisho. Vilevile, chuo kimepitia mitaala ya shahada yaUzamili katika Takwimu rasmi na zimewasilishwa NACTE kwaajili ya kuomba ithibati. Kadhalika, Chuo kwa kushirikiana naBenki ya Dunia na Tume ya Umoja wa Mataifa ya uchumibarani Afrika kimetoa mafunzo mbalimbali kwa washiriki 80kutoka nchi za Zambia, Malawi, Zimbabwe, Gambia, Afrikaya Kusini, Lesotho, Swaziland, Botswana, Sudani, Sudani yaKusini, Kenya na Uganda kuhusu masuala ya takwimu.

2.3.8 Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi

156. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Ofisi ya Taifaya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali, imeendelea kutekelezamajukumu yake kwa mujibu wa Ibara ya 143 ya Katiba yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kufanya ukaguzi wamapato na matumizi ya Serikali kwa kipindi cha mwaka wafedha 2017/18. Kazi zilizofanyika ni pamoja na ukaguzi wahesabu za: Wizara na Idara za Serikali 65; Vyama vya Siasa14; Sekretariati za Mikoa 26; Wakala za Serikali 33; MifukoMaalum 16; Taasisi nyingine za Serikali 42; na Balozi za Tanzania41. Aidha, ukaguzi ulifanyika kwenye Mamlaka za Serikali zaMitaa 185 na Mashirika ya Umma 176. Vilevile, Ofisi imefanyaukaguzi maalum kwenye taasisi zifuatazo: Shirika la UsafiriDar-es-Salaam (UDA); Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii(NSSF); Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA); Taasisi ya ElimuTanzania; Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC); Mamlaka yaVitambulisho vya Taifa (NIDA); Jeshi la Polisi; na Mamlaka yaViwanja vya Ndege.

Page 114: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

114

157. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa miradi yamaendeleo, jumla ya miradi 469 imekaguliwa na ripoti zaukaguzi zimetolewa. Miradi iliyokaguliwa inajumuishainayotekelezwa kwa fedha za ndani za Serikali nainayofadhiliwa na Washirika wa Maendeleo. Aidha, katikaukaguzi wa ufanisi, jumla ya taarifa 10 zimetolewa katikakipindi kilichoishia Machi, 2019. Vilevile, hadi kufikia Aprili, 2019Ofisi imetoa ripoti kuu tano. Taarifa hizo ni muhtasari wa jumlaya taarifa 1,042 za ukaguzi zilizotolewa kwa kipindi cha mwakawa fedha 2017/18. Ofisi iliwasilisha ripoti hizo kwa MheshimiwaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tarehe 28 Machi,2019 na hatimaye kuwasilishwa kwenye Bunge lako tukufu,mnamo tarehe 10 Aprili, 2019 kwa mujibu wa Katiba yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania.

2.3.9 Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo

Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma -PFMRP

158. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Wizarakupitia Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha zaUmma ilipanga kuziwezesha Wizara, Idara Zinazojitegema,Wakala, Taasisi za Serikali, Sekretarieti za Mikoa na Mamlakaza Serikali za Mitaa ili kutekeleza maboresho ya usimamizi wafedha za umma. Maeneo yaliyolengwa ni pamoja na:marekebisho ya sheria za kodi (Sheria ya Kodi ya Mapato,Sheria ya Ongezeko la Thamani, Sheria ya Ushuru wa Bidhaana Sheria ya Ushuru wa Forodha); kuhuisha mikataba yamadini ambayo inapata misamaha ya kodi na kuhuishamfumo wa kufanya maoteo ya viashiria vya uchumi jumla;kuandaa na kukamilisha Sera ya Kitaifa ya Ufuatiliaji naTathmini; kuhuisha mikataba ya makubaliano na Mashirikaya Maendeleo; kufanya marekebisho ya sheria ya Udalali yamwaka 1928; kuimarisha ununuzi wa Umma kwa kuzingatiathamani ya fedha, kuweka udhibiti na usimamizi; kuingiaMikataba ya Utendaji na Bodi za Mashirika ya Umma; nakuimarisha mfumo wa ukusanyaji wa mapato katika ngaziya Mamlaka ya Serikali za Mitaa.

Page 115: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

115

159. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili 2018/19, Wizarakupitia Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha zaUmma Awamu ya Tano imefanikiwa kuwajengea uwezowataalam 130 kutoka kwenye Wizara, Idara Zinazojitegemeana Wakala na Sekretarieti za Mikoa kuhusu Mfumo waUandaaji na Usimamizi wa Bajeti ya Serikali (CentralisedBudget Management System-CBMS) na maafisa 15 kwenyemasuala ya majadiliano juu ya mikopo na madeni. Shughulinyingine zilizotekelezwa chini ya programu hii ni: Kufanyamarekebisho ya sheria za kodi (Sheria ya Kodi ya Mapato,Sheria ya Ongezeko la Thamani, Sheria ya Ushuru wa Bidhaana Sheria ya Ushuru wa Forodha) ili kuendana na Sheria yaUwekezaji; kuhuisha mfumo wa kufanya maoteo ya viashiriavya uchumi jumla (MACMOD); na kuandaa Mkakati wa Mudawa Kati wa Kutafuta Vyanzo vya Mapato kwa ajili ya bajetiya Serikali na Mpango kazi wa utekelezaji. Ni matarajio yetukwamba, shughuli zote zilizopangwa kufanyika katika mwakawa fedha 2018/19 chini ya Programu hii zitakuwa zimekamilikaifikapo Juni 30, 2019.

Utekelezaji wa Mpango Kabambe wa Kuimarisha naKuboresha Takwimu Tanzania -TSMP

160. Mheshimiwa Spika, baada ya utekelezaji wa awamuya kwanza ya Mpango Kabambe wa Kitaifa wa Kuboreshana Kuimarisha Takwimu Nchini (Tanzania Statistical MasterPlan-TSMP) kukamilika mwaka 2017/18, Ofisi ya Taifa yaTakwimu imeandaa mapendekezo ya awamu ya pili ya TSMP.Mapendekezo hayo yameainisha maeneo muhimu yampango yatakayozingatiwa katika kipindi cha miaka mitanoijayo. Maeneo hayo ni pamoja na: uendelezaji wa Rasilimaliwatu kwa kuwajengea uwezo ili kuwa na mfumo imara watakwimu wa Taifa; kuimarisha mifumo ya takwimu zakiutawala na kuendeleza tafiti na sensa mbalimbali kwamujibu wa ratiba ya tafiti; na kuendeleza miundombinu yatakwimu, Teknolojia ya Habari na Ofisi za Mikoa na vitendeakazi. Mpango huu utazingatia maelekezo yaliyotolewa nawadau wengine wa uboreshaji takwimu Afrika.

Page 116: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

116

Kusaidia Ufanisi wa Bajeti za Wizara na Idara za Serikali

161. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Wizarailipanga kulipa madeni yaliyohakikiwa katika Wizara, IdaraZinazojitegemea, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikaliza Mitaa na kugharamia ujenzi wa nyumba na Ofisi za SerikaliMjini Dodoma. Fedha zilizokasimiwa kwa ajili ya kutekelezaProgramu hii ni shilingi trilioni 1.13. Hadi kufikia Aprili 2019, jumlaya Shilingi bilioni 471.2 zimelipwa. Kati ya kiasi hicho, shilingibilioni 221.43 zimelipwa kwa Wakandarasi na wahandisiwashauri, shilingi bilioni 230.25 zimelipwa kwa Wazabuni nawatoa huduma, shilingi bilioni 19.51 zimelipwa kwa watumishi.Vilevile, shilingi bilioni 23 zimetolewa kwa ajili ya kugharamiaujenzi wa Ofisi za Wizara katika Mji wa Serikali, Jijini Dodoma.Aidha, Wizara inaendelea na zoezi la uhakiki wa madeni naulipaji utaendelea kufanyika kwa kadri taarifa za uhakikizitavyokuwa zikiwasilishwa.

2.4 Changamoto na Mikakati ya Kukabiliana nazo

2.4.1 Changamoto

162. Mheshimiwa Spika, pamoja na mafanikioyaliyopatikana katika utekelezaji wa bajeti ya Wizara,changamoto zifuatazo zilijitokeza katika mwaka huu wafedha ambazo ni:

(i) Masharti yasiyo rafiki ya mikopo kwenye masoko ya fedhaduniani kutokana na mabadiliko ya sera za nchi kubwakiuchumi;

(ii) Kupungua na kutopatikana kwa wakati kwa fedha kutokakwa Washirika wa Maendeleo katika kugharamia miradimbalimbali ya maendeleo;

(iii) Mwamko mdogo wa kulipa kodi kwa hiari, kudai au kutoarisiti za kielektroniki; na

(iv) Uelewa mdogo wa Halmashauri kuhusu mkakati waSerikali wa kuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa

Page 117: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

117

kuongeza mapato kwa kutekeleza miradi ya kimkakati, hivyokushindwa kuandaa na kuwasilisha nyaraka mbalimbali zamiradi ya kimkakati zinazokidhi vigezo.

2.4.2 Mikakati ya Kukabiliana na Changamoto

163. Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana na changamotoza utekelezaji wa bajeti kama zilivyobainishwa hapo juu,Wizara inaendelea kuchukua hatua mbalimbali zikiwemo:

(i) Kuhakikisha kuwa Wizara na Taasisi zote za umma zinatumiaMfumo wa Serikali wa Kielektroniki wa ukusanyaji na usimamiziwa maduhuli (Government e- Payment System Gateway -GePG);

(ii) Kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa lengo lakupunguza utegemezi;

(i i i) Kuboresha mfumo wa usimamizi wa mashine zakielektroniki za kutolea risiti ili ziweze kutumika kwa kilamuamala unaofanywa. Uboreshaji huu utaondoa uwezekanowa kughushi risiti na kupunguza mianya ya ukwepaji wa kodi;

(iv) Kuendelea kukusanya madeni ya kodi ya msingi (principaltax) inayotokana na mikataba iliyoingiwa na walipa kodikwenye zoezi la msamaha wa riba na adhabu (tax amnesty);

(v) Kudhibiti biashara ya magendo kupitia bahari, maziwa,mipaka, na njia zisizo rasmi kwa kushirikiana na Taasisi nyingineza Serikali kama TANROADS, Mamlaka ya Bandari, Jeshi laPolisi, Jeshi la Wanamaji na Usalama wa Taifa;

(vi) Kuongeza jitihada za ukusanyaji wa kodi za majengo kwakushirikisha wadau muhimu wakiwemo Wizara ya ArdhiNyumba na Maendeleo ya Makazi, OR-TAMISEMI, Sekretarietiza Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa, na Ofisi ya Taifa yaTakwimu;

(vii) Kuendelea kusimamia utekelezaji wa bajeti kwakuzingatia Sheria ya Bajeti Na. 11 ya Mwaka 2015;

Page 118: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

118

(viii) Kuendelea kuimarisha ushirikiano na Washirika waMaendeleo kwa kutekeleza Mwongozo wa Ushirikiano (DCF)ili kuhakikisha fedha zilizoahidiwa zinatolewa kwa wakati; na

(ix) Kuendelea na majadiliano na taasisi za fedha za kimataifaili kuhakikisha kuwa fedha zinazotokana na mikopo yakibiashara zinapatikana kwa kipindi kilichobaki.

(x) Kufanya mafunzo kwa wataalam wa Mikoa naHalmashauri kuhusu mkakati wa Serikali wa kuziwezeshaHalmashauri kuongeza mapato kwa kutekeleza miradi yakimkakati ili kuwezesha Halmashauri kuandaa na kuwasilishanyaraka mbalimbali za miradi ya kimkakati, mfano; andikola mradi na taarifa ya upembuzi yakinifu.

3.0 Malengo ya Mpango na Bajeti kwa mwaka 2019/20

164. Mheshimiwa Spika, naomba sasa nieleze kuhusumalengo ya mpango na bajeti ya Wizara na Taasisi zake kwamwaka 2019/20;

3.1 Mpango wa Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara

3.1.1 Kubuni na Kusimamia utekelezaji wa Sera zaUchumi Jumla

165. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2019/20, Wizaraitaendelea kusimamia sera za uchumi jumla zinazolengakuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi ikiwa ni pamoja na:kuendelea kudhibiti mfumuko wa bei na kuhakikisha kuwaunabaki kwenye wigo wa tarakimu moja; kuongeza mapatoya ndani ikiwa ni pamoja na mapato ya kodi na yasiyo yakodi; na kudhibiti nakisi ya Bajeti ya Serikali. Hivyo, shabahaza uchumi jumla katika kipindi cha mwaka 2019/20 ni Pato laTaifa kukua kwa asilimia 7.1 mwaka 2019, mfumuko wa beikuwa kati ya asilimia 3 hadi asilimia 4.5, kuongeza mapatoya ndani hadi kufikia asilimia 15.8 ya Pato la Taifa, kuongezamapato ya kodi hadi kufikia asilimia 13.1 ya Pato la Taifa nanakisi ya Bajeti ya Serikali kuwa asilimia 2.3 ya Pato la Taifa.

Page 119: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

119

3.1.2 Uandaaji na ufuatiliaji wa Mipango ya Maendeleo yaTaifa

166. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2019/20 Wizaraitaendelea kuratibu uandaaji na ufuatiliaji wa mipango yamaendeleo ya Taifa kwa kufanya yafuatayo: kufanyatathmini ya muda wa kati ya utekelezaji wa Mpango waMaendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17 - 2020/21;kuandaa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2020/21; kuanza maandalizi ya Mpango wa Maendeleo wa Taifawa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26; kufuatilia utekelezaji waMpango na Miradi ya Maendeleo; kuratibu kanzidata yakuhifadhi na kutoa taarifa za miradi ya maendeleo; kuandaamfumo wa kitaifa wa ufuatiliaji na tathmini ya Miradi yaMaendeleo (National M&E Framework); na kuandaa taarifaya kwanza ya utekelezaji wa Malengo ya MaendeleoEndelevu (SDGs).

3.1.3 Kusimamia ukusanyaji wa mapato ya ndani

167. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/20, Wizaraitaendelea kusimamia hatua mbalimbali za ukusanyaji wamapato ya ndani ili kuwezesha utekelezaji wa Bajeti ya Serikalikwa ufanisi. Hatua hizi ni pamoja na kuunganisha Wizara,Idara, Wakala, Taasisi na Mashirika ya Umma kwenye Mfumowa Serikali wa Kielektroniki wa ukusanyaji wa mapato (GePG)na kuboresha mfumo (Upgrade) ili kukidhi mahitaji naongezeko la watumiaji.

3.1.4 Kuratibu upatikanaji wa Misaada na Mikopo kutokakwa Washirika wa Maendeleo

168. Mheshimiwa Spika, Wizara itaendelea kushirikiana naWashirika wa Maendeleo katika kuhakikisha kuwa misaadana mikopo inaendelea kutolewa kama ilivyoahidiwa na kwawakati ili kugharamia utekelezaji wa miradi mbalimbali yamaendeleo nchini. Aidha, Wizara itaendelea kuratibuMpango Kazi wa Kutekeleza Mwongozo wa Ushirikiano wamaendeleo (Action Plan for the Implementation ofDevelopment Cooperation Framework) na kuendelea

Page 120: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

120

kuratibu mazungumzo ya Kimkakati (Strategic Dialogue)katika ngazi ya Taifa. Vilevile, Wizara itashiriki mazungumzokatika Ngazi ya Kisekta na yale yenye mwelekeo wa kisiasaambayo huongozwa na Wizara za Kisekta na Wizara yaMambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Wizaraitaendelea kushiriki kwenye Mikutano ya Kimataifa inayohusuupatikanaji wa Misaada na Mikopo na njia mbadala yakugharamia Miradi Mikubwa (Global Partnership forEconomic Development Cooperation), Jukwaa la Ushirikianowa Maendeleo (Development Cooperation Forum), mikutanoya Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) na mikutano ya Kipupwena ya Mwaka ya Benki ya Dunia/IMF.

3.1.5 Usimamizi wa Deni la Serikali

169. Mheshimiwa Spika, mwaka 2019/20, Wizara itaendeleakusimamia Deni la Serikali kwa kuhakikisha inakopa kwenyevyanzo vyenye riba nafuu kwa ajili ya utekelezaji wa miradiya maendeleo. Aidha, Wizara itafanya ufuatiliaji na tathminiya mikopo iliyodhaminiwa na Serikali ili kuhakikisha wadaiwawanalipa madeni husika kwa wakati kuepusha uwezekanowa kuongeza mzigo kwa Serikali wa kulipa mikopo hiyo.Wizara pia itahakikisha kuwa madeni yote yanayoivayanaendelea kulipwa kwa wakati ili kudhibiti ukuaji wa Denila Serikali.

3.1.6 Kubuni na Kusimamia Mifumo ya Taarifa za Fedha

170. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2019/20, Wizaraitaendelea kubuni, kusimamia na kuboresha uendeshaji nautumiaji wa mifumo ya taarifa za fedha ili kuwezesha utunzajiwa taarifa. Mifumo itakayoboreshwa ni Mfumo wa Usimamiziwa Fedha za Miradi ya Maendeleo kutoka kwa Washirika waMaendeleo zinazotolewa moja kwa moja kwa wahusika(Direct to Projects Funds) na Mfumo wa Aid ManagementPlatform (AMP). Aidha, Wizara itaendelea kutoa usaidizi kwawatumiaji wa mifumo ya taarifa za fedha ili kuhakikishakwamba mifumo hiyo inapatikana, inatunza taarifa kwausahihi na ni salama. Vilevile, katika kuboresha upatikanajiwa mawasiliano, Wizara itaendelea kulipia gharama za

Page 121: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

121

mtandao kwa taasisi zinazotumia Mfumo wa Usimamizi waFedha (IFMIS) ili kuwezesha taasisi hizo kufanya malipo kwaufanisi. Kadhalika, Wizara itaboresha mtandao wamawasiliano katika Ofisi tano za Hazina Ndogo ili kuongezaufanisi wa mtandao.

171. Mheshimiwa Spika, Mfumo wa Taarifa za Mishahara yaWatumishi wa Umma (GSPP) utaendelea kuboreshwa kwakuunganisha mfumo huo na taasisi za fedha kwa ajili yaurahisishaji wa huduma za mikopo na pensheni kwa wastaafu.Aidha, Wizara itakamilisha uunganishaji wa mfumo wamapato ya Serikali ili kuweza kufanikisha ukusanyaji wamaduhuli ya Serikali pamoja na kuendelea kutoa mafunzokwa taasisi zitakazounganishwa. Vilevile, katika kipindi hichoWizara itaendelea na zoezi la uunganishaji wa mifumo 10 yakielektroniki ya taarifa za fedha nchini ili iweze kubadilishanataarifa na kuanzisha ghala la taarifa za pamoja (DataWarehouse) ya mifumo ya taarifa za fedha na kiuchumi.

3.1.7 Usimamizi wa Malipo

172. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2019/20, Wizaraitaendelea kusimamia mfumo wa udhibiti wa matumizi yafedha za umma ikiwa ni pamoja na kufanya maboresho yamfumo wa Akaunti Jumuifu ya Hazina kwa lengo la kuboreshamfumo wa matumizi ya umma ili kuiongezea Serikali uwezowa kugharamia shughuli zake kwa wakati. Aidha, Wizaraitaendelea kutoa mafunzo kwa wahasibu wa Wizara, Idaraza Serikali, Sekretarieti za Mikoa na Serikali za Mitaa kuhusumfumo wa akaunti jumuifu ili kutoa uelewa wa dhumuni lauanzishwaji wa akaunti husika pamoja na kufahamu jinsi yakufanya usuluhisho wa Daftari la fedha la IFMS na akauntijumuifu ya hazina (TSA). Pia wizara itendelea kutoa mafunzokwa wahasibu wa wizara, Idara za Serikali, Mikoa na Serikaliza Mitaa yanayohusu uandaaji wa hesabu kwa kutumiaviwango vya kimataifa (IPSAS Accrual) vilivyohuishwa. Vilevile,kupitia ofisi za hazina ndogo zilizopo mikoa yote ya TanzaniaBara, Wizara ya Fedha na Mipango itaendelea kutoahuduma karibu na maeneo ya wananchi wakiwemo

Page 122: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

122

wastaafu, watoa huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na ofisiza serikali na taasisi zake.

3.1.8 Kuandaa na Kusimamia Utekelezaji wa Bajeti yaSerikali

173. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/20, Wizaraitaendelea na jukumu la kuandaa na kusimamia utekelezajiwa Bajeti ya Serikali ambapo pamoja na shughuli nyingineimepanga kutekeleza yafuatayo: kuendelea kuboreshaMfumo wa Uandaaji na Usimamizi wa Bajeti ya Serikali (CBMS)kwa kuunganisha na Mifumo ya Bajeti ya Mamlaka ya Serikaliza Mitaa (Plan Rep), ikiwa ni pamoja na kuendesha mafunzo;kuchapisha na kusambaza Kitabu cha Bajeti ya Serikali yamwaka 2019/20 Toleo la Wananchi; kuandaa na kusambazaMwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya mwaka2020/21; na kufanya uchambuzi wa bajeti za Wizara, IdaraZinazojitegemea na Wakala, Sekretarieti za Mikoa naMamlaka ya Serikali za Mitaa kwa Kipindi cha Muda wa Kati(MTEF) kwa mwaka 2020/21.

174. Mheshimiwa Spika, kazi nyingine zitakazotekelezwa nipamoja na: kuandaa na kuweka kwenye Tovuti taarifa zautekelezaji wa Bajeti ya Serikali za kila Robo Mwaka; kufanyaufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa Bajeti ya Serikalipamoja na matumizi ya fedha za umma ikiwemo Mishaharakwa Wizara, Idara Zinazojitegemea na Wakala, Sekretarietiza Mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa; kuendeleakuchambua na kufanya tathmini ya miradi ya Kimkakati kwakuzingatia vigezo vilivyowekwa; kuendelea kutenga bajetikwa ajili ya kulipa madeni yaliyohakikiwa kwa kuzingatiaMkakati wa Kulipa na Kuzuia Ulimbikizaji wa Madeni; nakuendelea kuimarisha uwazi na uwajibikaji kwa kushirikishawadau kwenye mapitio ya taarifa za utekelezaji wa Bajeti.

3.1.9 Usimamizi na Udhibiti wa Matumizi ya Fedha za Umma

175. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2019/20, Wizaraitaendelea kusimamia na kudhibiti matumizi ya fedha zaumma ili kupata thamani halisi ya fedha katika utekelezaji

Page 123: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

123

wa miradi ya maendeleo. Shughuli zitakazofanyika ni pamojana: kufanya uchambuzi na kuhakiki madai ya fidia mbalimbalikabla ya kufanya malipo; kufanya ufuatiliaji wa utekelezajiwa mapendekezo ya ukaguzi wa ndani kwenye Halmashauri40; kufanya kaguzi maalum kwenye miradi ya ujenzi; kufanyauchambuzi wa taarifa za ukaguzi wa ndani kutoka kwenyeHalmashauri 185; na kuandaa taarifa ya majumuisho ya hojakwa mwaka 2018/19.

3.1.10 Usimamizi wa Mali za Serikali

176. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2019/20, Wizaraimepanga kuendelea kuratibu uthamini wa mali katika taasisiza Serikali ili kuwa na taarifa sahihi za mali pamoja nakuendelea kuondosha mali chakavu, sinzia (dormant) nazilizokwisha muda wake kwa kufanya yafuatayo: kuhakiki malikatika Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala za Serikali,Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa naMashirika ya Umma kwa lengo la kuongeza ufanisi na tijakatika usimamizi wake; kutoa ushauri wa kupunguza hasarazinazotokana na matumizi yasiyo sahihi ya mali za Serikali;kuunganisha mfumo wa GAMIS kwenye taasisi 150 kwa lengola kuongeza ufanisi katika usimamizi wa mali za Serikali;kukamilisha marekebisho ya Sheria ya Uendeshaji wa Minadaya mwaka 1928 ili kuongeza ufanisi katika kusimamia shughuliza udalali; kufanya kaguzi za mali katika balozi tano zaTanzania; na kutoa elimu ya utunzaji bora wa mali katikataasisi mbalimbali za Serikali ili kuepusha hasara za mali.

3.1.11 Udhibiti wa Utakasishaji wa Fedha Haramu na Ufadhiliwa Ugaidi

177. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2019/20, Wizara kupitiaKitengo cha Udhibiti Fedha Haramu itaendelea kusimamiautekelezaji wa Sheria za Udhibiti wa Fedha Haramu kwakufanya yafuatayo: Kuendelea kupokea na kuchambuataarifa za miamala shuku zinazohusu utakasishaji wa fedhaharamu na ufadhili wa ugaidi na taarifa za usafirishaji wafedha taslimu na hati za malipo mipakani; kuendeleakuwasilisha taarifa fiche kwenye vyombo vinavyosimamia

Page 124: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

124

utekelezaji wa sheria kwa ajili ya uchunguzi na kufikishawahusika mahakamani; kuendelea kuratibu na kusimamiashughuli za Kamati ya udhibiti wa utakasishaji wa fedhaharamu na ufadhili wa ugaidi ikiwa ni pamoja na mikutanoya Kamati hiyo; kuendelea na utekelezaji wa mikakati yakitaifa na kimataifa ya udhibiti wa utakasishaji wa fedhaharamu na ufadhili wa ugaidi; kushiriki katika mikutano navikao kazi na wadau mbalimbali katika kusimamia kwa karibuzoezi linaloendelea la tathmini ya kitaifa ya mifumo yakudhibiti utakasishaji fedha haramu na ufadhili wa ugaidi(Mutual evaluation). Tathmini hiyo itaijengea nchi sifa nauwezo wa kushirikiana na nchi nyingine duniani kwakubadilishana taarifa zinazohusu udhibiti wa utakasishaji wafedha haramu na ufadhili wa vitendo vya kigaidi.

178. Mheshimiwa Spika, kazi nyingine zitakazo fanyika nikuendelea na ukaguzi wa watoa taarifa mbalimbali ikiwa nipamoja na taasisi za fedha ili kuhakikisha kuwa sheria namiongozo ya kudhibiti utakasishaji wa fedha haramu naufadhili wa ugaidi inafuatwa ipasavyo; kuandaa nakutekeleza mpango wa mafunzo kwa vyombovinavyosimamia utekelezaji wa sheria na watoa taarifa katikaJamhuri ya Muungano wa Tanzania; kuwapeleka mafunzowatumishi wa Kitengo kwa ajil i ya kujifunza mambombalimbali katika nyanja ya udhibiti wa utakasishaji wa fedhaharamu na ufadhili wa ugaidi na kuendelea kutekelezamapendekezo ya Taarifa ya Tathmini ya Kitaifa ya ViashiriaHatarishi vya Fedha Haramu.

3.1.12 Tume ya Pamoja ya Fedha

179. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2019/20, Tume yaPamoja ya Fedha itafanya Stadi kuhusu vikwazo vyakibiashara baina ya Tanzania Bara na Zanzibar na athari zakekatika mapato ya muungano. Aidha, Tume itaendeleakukusanya na kufanya uchambuzi wa takwimu za mapatona matumizi yanayohusu utekelezaji wa mambo yamuungano, pamoja na kutoa elimu kwa wadau kuhusuuhusiano wa masuala ya fedha katika Jamhuri ya Muunganowa Tanzania.

Page 125: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

125

3.1.13 Usimamizi wa Mashirika na Taasisi za Umma

180. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/20 Wizarakupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina, itaendelea Kuimarishaukusanyaji wa maduhuli kutoka katika Taasisi na Mashirikaya Umma na Kampuni ambazo Serikali ina hisa chache;Kuanzisha na kuboresha mifumo ya TEHAMA; Kuhakikishaviwanda vilivyobinafsishwa vinafanya kazi kwa ufanisi;Kuvirejesha viwanda vilivyoshindwa kutekeleza majukumuyake kwa mujibu wa makubaliano na kuwapatia wawekezajiwengine wenye uwezo na nia ya kuviendeleza.

3.1.14 Uratibu wa Mikakati ya Kupunguza Umaskini

181. Mheshimwa Spika, katika kuratibu mikakati yakupunguza umaskini kwa mwaka 2019/20, Wizara itafanyayafuatayo: kuwajengea uwezo Maafisa Mipango naMaendeleo ya Jamii wa Halmashauri zote nchini juu yaMuongozo wa Mfumo Shirikishi wa Kuleta Maendeleo yaUchumi katika Ngazi za Jamii ili kujumuisha katika mipangona bajeti zao; kukamilisha Mpango Kazi wa KupunguzaUmaskini pamoja na kukuza dhana ya biashara katikakupunguza umaskini; na itajielekeza katika uwezeshajiwananchi kiuchumi kwa kuanzisha na kuendesha programuza kukabiliana na changamoto ya umaskini kwa wananchihasa sekta ya fedha kwa kuhamasisha uanzishaji wa Ushirikawa Kuweka na Kukopa.

3.1.15 Ununuzi wa Umma

182. Mheshimwa Spika, kwa mwaka 2019/20 Wizaraimepanga kufanya yafuatayo: kuhuisha mifumo ya ununuziwa umma kati ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa; kuendeleakufanya vikao vya wadau na kupokea maoni yao juu yachangamoto za utekelezaji wa Sheria ya Ununuzi wa Umma,Sura 410 na kuzipatia ufumbuzi; kutoa mafunzo ya uandaajiwa mikataba midogo (LPOs) kwa maafisa ununuzi na ugavi100 wa Serikali kwa kutumia mfumo wa EPICOR; kupitia nakuhuisha mifumo inayohusiana na utunzaji wa kanzidata yamaafisa ununuzi na ugavi waliopo Serikalini; ukamilishaji wa

Page 126: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

126

Mwongozo wa utekelezaji wa shughuli za ununuzi wa umma;kukamilisha Mwongozo wa Maadili ya Maafisa ununuzi, ugavina Wazabuni; kupitia na kufuatil ia utekelezaji wamapendekezo ya taarifa za ukaguzi wa ununuzi wa ummaunaofanywa na CAG, PPRA na mamlaka nyinginezinazoruhusiwa kisheria.

183. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2019/20, Wizara kupitiaWakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini - GPSA imepangakutekeleza yafuatayo: Kuendelea na utaratibu wa ununuziwa magari ya Serikali kwa pamoja ili kupunguza gharamana kuongeza uwazi na uwajibikaji; kuendelea kuandaamikataba maalum ya ununuzi wa vifaa na hudumamtambuka kwa niaba ya Taasisi za Serikali ili kuokoa gharamaza michakato ya zabuni kwa taasisi za Umma kila zinapohitajihuduma na vifaa mtambuka; na kuongeza uwezo wa Wakalawa kuhifadhi mafuta katika mikoa ya Iringa, Kagera,Shinyanga, Mbeya, Dodoma, Arusha na Kilimajaro kufikiawastani wa lita 50,000 kila mkoa pamoja na ujenzi wa tenkila kuhifadhia mafuta yatakayonunuliwa moja kwa mojakutoka kwa wazalishaji. Lengo ni kununua mafuta kwa beirahisi na kuziuzia Taasisi za Umma kwa bei nafuu.

184. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Wakala wa Hudumaya Ununuzi Serikalini - GPSA imepanga kuimarisha uwezo wakusambaza mafuta kwa kuongeza gari la mafuta lenyeuwezo wa kubeba ujazo wa lita 40,000 kwa ajili ya kusambazamafuta mikoani na; kujenga kituo cha mafuta katika mji waSerikali, uliopo katika eneo la Mtumba - Dodoma kwa lengola kusogeza huduma hiyo kwa Taasisi za Umma zilizopo katikaeneo hilo. Ili kuboresha mazingira ya utoaji huduma Wakalaumepanga kujenga ofisi, ghala na kituo cha mafuta kwamikoa ya Simiyu, Njombe na Pwani. Vilevile, kufanya ukarabatiwa matanki ya kuhifadhia mafuta katika Mikoa ya Lindi,Kigoma, Kagera, Mara, Kilimanjaro, Ruvuma, Manyara naMorogoro.

185. Mheshimwa Spika, kwa mwaka 2019/20, Bodi yaWataalam wa Ununuzi na Ugavi inatarajia kutekelezamajukumu yafuatayo: kusajili wataalam 15,000 na taasisi 20;

Page 127: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

127

kuendesha mafunzo ya muda mfupi kwa washiriki 720; kusajiliwatahiniwa 5,000 katika mitihani ya Ununuzi na Ugavi;kuendesha huduma tano za ushauri; kuingia makubalianoya ushirikiano na taasisi za ndani na nje ya nchi; kufanya tafitimbili kwenye nyanja za ununuzi na ugavi ili kubainichangamoto na fursa zilizopo kwenye fani kwa lengo lakuishauri Serikali na wadau wengine jinsi ya kuboresha Sheriaza Ununuzi zilizopo; na kutengeneza kanuni na taratibu zaajira kwenye kada za Ununuzi na Ugavi.

186. Mheshimwa Spika, kwa mwaka 2019/20, Mamlaka yaUdhibiti wa Ununuzi wa Umma itafanya yafuatayo: ukaguziwa taasisi nunuzi 120; kufuatilia uzingatiaji wa mikataba yaununuzi; kufanya tathmini ya uwezo wa ununuzi; kuendeleana utekelezaji wa mfumo wa ununuzi kwa njia ya mtandao(TANePS) kwa kutoa mafunzo kwa watumishi 500 kwa TaasisiNunuzi na wazabuni 4,000 ambao wamejisajili kwenye mfumo;na kuendesha warsha, makongamano na mafunzokuhusiana na sheria ya ununuzi wa Umma kwa Taasisi Nunuzi40.

187. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2019/20, Mamlaka yaRufaa za Zabuni imepanga kupokea, kusikiliza na kutoleamaamuzi rufaa 50 na kuendelea kuimarisha Utawala Borakwa kuhakikisha kuwa michakato ya ununuzi wa Ummainazingatia matakwa ya sheria na hivyo zabunizitakazotolewa zinafuata taratibu na hatimaye kupatathamani halisi ya fedha katika ununuzi wa Umma.

3.1.16 Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi - PPP

188. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2019/20, Wizaraitaendelea kuratibu shughuli za PPP nchini kwa kuzingatiaSheria ya PPP Sura 103 kwa kufanya yafuatayo: kuanzishaKituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPCentre); kukamilisha mapitio ya Kanuni za kutekeleza Sheriaya PPP Sura 103; kusimamia uibuaji, uchambuzi na utekelezajiwa miradi ya PPP ili kuwa na miradi yenye tija na endelevuna hivyo kupunguza utegemezi wa Bajeti ya Serikali; kuandaana kuimarisha Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Miradi ya

Page 128: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

128

PPP nchini; na kujenga uwezo wa Mamlaka za Serikalizinazotekeleza miradi ya ubia.

3.1.17 Mafao ya Kustaafu na Mirathi

189. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/20, Wizaraitaendelea kutunza kumbukumbu na kuboresha huduma kwawastaafu ikiwa ni pamoja na: kulipa mafao ya kustaafu namirathi kwa wakati kwa wastaafu wanaolipwa na HAZINA;kufanya Uhakiki kwa wastaafu wanaolipwa na HAZINA ilikubaini wastaafu wanaostahili kulipwa pensheni; na kutoaelimu kwa wadau wanaohusika na uaandaji wa mafao yakustaafu na mirathi kwa watumishi wa Bunge, Wizara, Mikoa,Wilaya na baadhi ya taasisi za Serikali ili kuwawezeshawatendaji kuandaa mafao ya kustaafu kwa kufuata sheria,kanuni na taratibu na kuondoa ucheleweshaji wa malipo.

190. Mheshimiwa Spika, Kwa mara nyingine nasisitizaMaafisa Masuuli wote kuandaa nyaraka za watumishiwanaotarajia kustaafu kwa ukamilifu na kuziwasilisha HAZINAmapema ili kuwezesha malipo ya mafao ya kustaafu namirathi kufanyika kwa wakati ili kuondoa usumbufu kwawatumishi wanaostaafu. Aidha, nahimiza ofisi zote za ummakutunza taarifa za watumishi wao kielektroniki kwa kushirikianana Wakala wa Serikali Mtandao (eGA).

3.1.18 Michango ya mwajiri kwenye mifuko ya Hifadhi yaJamii

191. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/20, Wizaraitaendelea kuwasilisha kwa wakati michango ya kisheria yamwajiri ya kila mwezi kwa ajili ya watumishi wa umma kwenyeMfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF),Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mfuko wa Hifadhiya Jamii Zanzibar (ZSSF), Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF).

Page 129: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

129

3.2 Usimamizi na Uratibu wa Taasisi Na Mashirika YaUmma Chini Ya Wizara

3.2.1 Huduma za Kibenki

Benki Kuu ya Tanzania – BoT

192. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2019/20,Benki Kuu kwa kushirikiana na wadau wengine imepangakuanzisha Mfumo wa Usajili wa Huduma na Watoa Hudumaza Fedha (Financial Service Registry) unaolenga kukusanya,kuhifadhi, kuchakata na kutoa taarifa za sekta ya fedha kwauhakika na ufanisi zaidi, na utaunganisha mifumo mingineya wadau. Mfumo huu utasaidia kupunguza gharama zaukusanyaji takwimu kwa wadau wa huduma jumuishi zakifedha. Mfumo huu pia utasaidia kuimarishwa utambuzi wawatoa huduma kwa kuanzisha vitambulisho vya kipekeevitakavyoimarisha taratibu za kumjua mteja na kuimarishwaulinzi kwa watumiaji dhidi ya ulaghai.

193. Mheshimiwa Spika, Benki Kuu itaendelea na uundaji wamfumo wa Tanzania Instant Payment System (TIPS). Mfumohuu utasaidia kuongeza ufanisi kwa mifumo ya malipomadogo madogo, ushirikiano kati ya watoa huduma wafedha kwa njia ya kidigitali, uwazi na usahihi wa takwimu kwaajili ya kufanya maamuzi sahihi, na kupunguza gharama zahuduma za fedha, hivyo kuongeza ujumuishi katika sekta nahuduma za fedha.

194. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/20, Benki Kuuya Tanzania imepanga pia kutekeleza yafuatayo: kuendeleakutekeleza sera ya fedha yenye kuongeza ukwasi katikauchumi ili kuendeleza ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi nashughuli mbalimbali za uchumi bila kuchochea mfumuko wabei; kuendelea kuhakikisha kuwa kunakuwepo na ufanisikatika masoko ya fedha ikiwa ni pamoja na kuwepo kwautulivu wa viwango vya riba kama chachu ya kuongezaupatikanaji wa mikopo nafuu kwa sekta binafsi; na kuendeleakutumia mfumo mpya wa kutekeleza sera ya fedhaunaotumia riba ya Benki Kuu (Central Bank Policy Rate) katika

Page 130: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

130

kutoa mwelekeo wa sera ya fedha badala ya kutumia fedhataslimu.

Benki ya Maendeleo ya Kilimo - TADB

195. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2019/20, Benki yaMaendeleo ya Kilimo itatekeleza yafuatayo: kutoa mikopokwa ajili ya miradi ya uchakataji wa mazao, kilimo chaumwagiliaji na kilimo cha miradi ya mfumo wa nyukliasi; ujenziwa maghala ya kisasa; na kuanzisha vituo vya huduma zazana za kilimo. Aidha, TADB itaendelea kutekeleza mpangowa kuwajengea uwezo wakulima wadogo kupitia mafunzoya usimamizi wa fedha, oganaizesheni ya vikundi na vyama,utunzaji wa kumbukumbu na utengenezaji wa miradiinayokidhi masharti ya mikopo kutoka katika mabenki nataasisi za fedha. Vilevile, TADB itakamilisha ufunguzi wa Ofisiza kanda ya nyanda za juu kusini mkoani Mbeya na Kigomapamoja na kuendeleza uzalishaji na uchakataji wa maweseili kutengeneza mafuta ya kupikia na bidhaa nyingine.

Benki ya Maendeleo TIB – DFI

196. Mheshimiwa Spika, Benki ya Maendeleo TIB kwa mwaka2019/20 itafanya yafuatayo: kutoa mikopo yenye thamaniya shilingi bilioni 144.5 katika sekta ya viwanda, maji, nishati,utalii, kilimo na miundombinu ya Serikali za Mitaa kama vilevituo vya mabasi, masoko ya kisasa, machinjio ya kisasapamoja na upimaji wa viwanja; kukuza mizania ya benkikufikia kiasi cha shilingi bilioni 872.9; kupunguza kiwango chamikopo chechefu kutoka asilimia 32 ya mwaka 2018 mpakaasilimia 25 kwa mwaka 2019; na kuongeza faida kutoka shilingibilioni nane ya mwaka 2018 mpaka kufikia shilingi bilioni tisakwa mwaka 2019.

Benki ya Biashara TIB - CBL

197. Mheshimiwa Spika, lengo la benki hii kwa mwaka 2019/20 ni kufikia kiwango cha jumla ya mali kiasi cha shilingi bilioni500. Benki inaendelea kufanya mazungumzo na taasisi zaSerikali na Kampuni mbalimbali kwa ajili ya kutoa huduma

Page 131: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

131

na mikopo yenye thamani ya jumla ya shilingi bilioni 156kulingana na mahitaji ikiwemo mikopo ya muda mfupi, wakati na mrefu; mikopo ya uendeshaji (working capital) namikopo ya maendeleo. Baadhi ya taasisi hizo ni: SUMA JKT;Taasisi ya Mifupa Muhimbili – MOI; Taasisi ya Moyo ya JakayaKikwete; Hospitali ya Taifa Muhimbili; Wakala wa BarabaraMijini na Vijijini -TARURA; Mamlaka ya Maji Safi na TakaDodoma; na Kiwanda cha Madawa Simiyu. Aidha, Benkiitaendelea kutoa mikopo kwa ajili ya ununuzi wa mazao yakilimo na uchakataji wake kama vile pamba, kahawa,mahindi, korosho na kadhalika. Vilevile, Benki imejipangakutekeleza vipaumbele vya Serikali katika kukuza uchumi waviwanda kupitia uwezeshaji wa mitaji na uwekezaji ilikuongeza Pato la Taifa na kuwajibika kuchangia utoaji wahuduma kwa jamii katika maeneo mbalimbali ikiwemo afya,elimu na ujasiriamali kupitia faida itakayopatikana.

Benki ya TPB

198. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2019/20, Benki ya TPBitatekeleza yafuatayo: kupeleka huduma za kibenki kwawananchi wengi zaidi, na hasa vijijini, kupitia Programu yaFedha Jumuishi (Financial Inclusion Program). Mkakati huoutatekelezwa kupitia matumizi ya teknolojia ya simu zamkononi, mawakala wa huduma za fedha na kuimarishamatawi madogo wilayani; kukuza amana na kuelekezahuduma ya mikopo katika Sekta ya kilimo. Benki itafanyajuhudi kuwashirikisha wadau wa maendeleo ya sekta yakilimo ili kupata fedha za kuwakopesha wazalishaji na watoahuduma katika kilimo; na kuzalisha faida zaidi na kutoa gawiokwa wanahisa.

3.2.2 Rufani za Kodi

199. Mheshimiwa spika, kwa mwaka 2019/20, Bodi ya Rufaniza Kodi itaendelea kusikiliza na kutolea maamuzi migogoroya kodi kwa wakati. Aidha, Bodi itaendelea na mkakati wakufanya vikao maalum “special sessions” wa kusikiliza nakutolea maamuzi kesi za muda mrefu.

Page 132: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

132

200. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2019/20 Baraza laRufani za Kodi limepanga kusikiliza na kutolea maamuzi rufanizote za kodi kwa wakati. Aidha, Baraza litaendelea kutoaelimu kwa wadau juu ya taratibu za kukata rufaa na za utatuziwa migogoro ya kodi. Vilevile, Baraza limepanga kuchapishavitabu vya rejea (Tanzania Tax Law Reports) kwa kesizilizoamuliwa kuanzia mwaka 2013 hadi 2018. Lengo ni kuwana rejea za maamuzi yanayohusu mashauri ya kodi ambayoyatawasaidia walipa kodi, wadau wa kodi na wanazuonikatika kujifunza.

3.2.3 Huduma za Bima

Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima - TIRA

201. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2019/20, Mamlakaimepanga kutekeleza yafuatayo: kuanzisha Skimu ya Bimaya Kilimo na Mifugo; kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji wamapato na usimamizi wa kampuni za bima; kukamilishataratibu za fidia kwa wateja wa kampuni za bima ilikupunguza malalamiko ya kiwango cha fidia na kuanzishamkakati wa kumlinda mtumiaji wa huduma za bima nchini;kufanya marekebisho ya Sheria ya Bima Sura 394 ili kuletaufanisi katika ukuzaji na usimamizi wa biashara ya bima nchini;na kuendelea na utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wakuelimisha umma kuhusu masuala ya bima nchini. Aidha,Mamlaka kwa kushirikiana na Wizara itakamilisha Sera ya Taifaya Bima.

Shirika la Bima la Taifa - NIC

202. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2019/20, Shirikalimepanga kuanza kutoa huduma kupitia mitandao ya simuza mkononi ili kuwarahisishia wateja kulipia bima bilakulazimika kufika kwenye Ofisi za Shirika la Bima la Taifa. Aidha,Shirika linatarajia kufanya uhakiki wa wateja wake wa madaiya bima za maisha wa muda mrefu na muda mfupi kwakutumia mfumo wa K.Y.C (Know Your Customer). Vilevile,Shirika litahakikisha kuwa viwanda vinavyoanzishwa vinapataushauri wa kitaalam wa bima na kupatiwa kinga zinazofaa.

Page 133: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

133

3.2.4 Mitaji na DhamanaMamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana - CMSA

203. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2019/20, Mamlaka yaMasoko ya Mitaji na Dhamana imepanga kufanya yafuatayo:kuimarisha udhibiti na usimamizi wa masoko ya mitaji kwakutumia mfumo wa usimamizi unaozingatia vihatarishi (RiskBased Supervision); kutoa elimu kwa umma na kujenga uwezowa Mamlaka za Serikali za Mitaa kutumia masoko ya mitaji ilikupata fedha za kugharamia miradi ya maendeleo kwa njiaya utoaji wa Hatifungani za Serikali za Mitaa. Aidha, Mamlakaitaendelea kushirikiana na Taasisi ya Uwekezaji na Dhamanaya nchini Uingereza katika kutoa mafunzo yenye lengo lakuongeza wataalam wenye weledi na ujuzi wa ngazi yakimataifa kwenye masoko ya mitaji.

Soko la Bidhaa Tanzania -TMX

204. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2019/20, Soko la BidhaaTanzania litatekeleza yafuatayo: kutoa huduma ya kitaalamkuhusiana na uendeshaji na mahitaji ya taasisi ya Soko laBidhaa Tanzania na Bodi ya Stakabadhi za Ghala; kushirikikatika usimamizi wa minada ya bidhaa ikiwa ni sehemu yamaandalizi ya kuingiza mazao katika mfumo wa mauzo yaSoko la Bidhaa Tanzania; kusimamia utaratibu wa kuchaguaghala zitakazotumika katika mfumo wa Soko la Bidhaa;kutekeleza mpango wa elimu kwa umma kuhusu Soko laBidhaa na mfumo wa stakabadhi ghalani; kufanya ukaguziwa ghala zitakazosajiliwa kwa lengo la kupata taarifa ya kiasina ubora wa mazao yaliyopo ghalani kwa kushirikiana naBodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala; na kutoa nakusambaza taarifa za soko na bei kwa umma kwa kutumiavyombo vya habari na tovuti ya Soko la Bidhaa.

Soko la Hisa la Dar es Salaam - DSE

205. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2019/20, DSEitatekeleza yafuatayo: kuongeza ukwasi wa soko kutokaasilimia 2.2 hadi kufikia kiwango cha asilimia tano katikauwiano wa mauzo ya hisa kwa ukubwa wa soko na asilimia

Page 134: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

134

10 kwa mauzo ya hatifungani kwa thamani ya hatifunganizilizopo; kujenga uwezo wa kampuni za kati kuweza kuvutiauwekezaji wa mitaji pamoja na mikopo kutoka kwa mabenki,hisa na hatifungani; kuhuisha Kanuni za Uendeshaji wa Soko;na kuongeza ushiriki wa wawekezaji wa ndani na nje katikakuwekeza kupitia masoko ya hisa. Aidha, DSE itaendelezajuhudi za kupata uanachama wa kudumu katika Jumuiyaya Masoko ya Hisa Duniani (WFE) na Kupata hadhi yaClassification of Frontier Market Status.

3.2.5 Dhamana za Uwekezaji Tanzania

Taasisi ya Usimamizi wa Rasilimali za Uwekezaji - UTT AMIS

206. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2019/20, taasisiimeazimia kuongeza wigo katika masuala ya uwekezaji kwalengo la kuongeza mapato ya kampuni na kutoa gawio kwaSerikali. Ili kufikia lengo hilo, taasisi itafanya yafuatayo:kuongeza rasilimali za mifuko kwa asilimia 15 kwa mwaka;kuongeza idadi ya wawekezaji kwa asilimia tano ili wanufaikena fursa za uwekezaji zilizopo nchini kupitia mifuko ya UTT AMIS;kuendelea kutoa viwango shindani vya faida kwawawekezaji kwenye mifuko ya Uwekezaji wa pamoja nahuduma za usimamizi wa mitaji binafsi; kuendeleakuhamasisha Taasisi za Serikali, Mifuko ya Hifadhi za Jamii,Mashirika na vikundi mbalimbali vya kijamii kama vile SACCOSili zijiunge na mifuko ya UTT AMIS kwa lengo la kukuza mitajiyao; kuanzisha Mfuko wa Hatifungani ili kuongeza wigo wauwekezaji kwa wananchi; kuzindua na kutoa huduma zausimamizi wa mitaji binafsi; usimamizi wa majengo kwa niabaya wamiliki; na kuwawezesha wananchi kutumia njia za kisasakama simu za mikononi kununua vipande, kupata taarifa nahuduma mbalimbali za uwekezaji.

3.2.6 Taasisi za Mafunzo

Chuo cha Usimamizi wa Fedha – IFM

207. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2019/20, Chuo chaUsimamizi wa Fedha - IFM kitaendelea kutoa Mafunzo katika

Page 135: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

135

ngazi ya astashahada, shahada, na shahada ya uzamili.Aidha, Chuo kimepanga kutekeleza shughuli mbalimbaliambazo ni pamoja na kudahili wanafunzi 10,500 wa fanimbalimbali katika vituo vyote vya mafunzo vya Dar esSalaam, Mwanza, Dodoma na Simiyu; kuendeleza ujenzi wakampasi ya Dodoma ikianzia na Kituo cha BiasharaNjedengwa ambacho kitaongeza udahili wa kozi za shahadahususan kwa watumishi wa Umma wanaotaka kujiendelezakwa masomo ya jioni na wanafunzi wa Kanda ya Kati,kuendelea na ujenzi wa Kituo cha Mafunzo cha Simiyu,kuboresha shughuli za utafiti, machapisho/majarida nahuduma mbalimbali kwa jamii, kuendelea kujenga uwezowa wahadhiri kutoa huduma elekezi na kufanya tafitimbalimbali, ukarabati wa Majengo katika Kampasi ya Dares Salaam ili kuongeza ufanisi katika uendeshaji wa Chuo nautoaji huduma bora kwa wadau pamoja na kuendeleakuimarisha uwezo wa watumishi wake kupitia mafunzombalimbali ili kuboresha taaluma za wahitimu wawezekukubalika katika soko la ajira.

Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini - IRDP

208. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2019/20, Chuokimepanga kutekeleza yafuatayo: kuongeza udahili na usajiliwa wanafunzi kutoka 8,098 mpaka kufikia wanafunzi 9,500;kupitia mitaala ya mafunzo ya muda mrefu na kuandaamitaala ya kozi mpya 10; kukamilisha ujenzi wa bweni lawanafunzi wa kike lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 192Kampasi Kuu Dodoma; kukamilisha ujenzi wa jengo mojalenye madarasa ya kufundishia na ofisi za watumishi Kampasiya Mwanza; na kujenga jengo moja lenye madarasa yakufundishia na ofisi za watumishi Kampasi Kuu Dodoma.

Chuo cha Uhasibu Arusha -IAA

209. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2019/20, Chuokimepanga kufanya yafuatayo: kudahili wanafunzi 4,500katika kampasi za Arusha, Babati na Dar es Salaam; kujengakituo cha elimu mtandao (e-learning centre); kujengamabweni katika Kampasi za Arusha na Babati; na kukarabati

Page 136: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

136

miundombinu pamoja na kuanzisha kituo cha afya ndani yaKampasi Kuu ya Arusha.

Taasisi ya Uhasibu Tanzania – TIA

210. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/20 Taasisiimepanga kuboresha mafunzo ili kutoa wataalam borawatakaoendana na kasi ya kuleta mabadiliko chanya katikamapinduzi ya viwanda, kupanua Taasisi kwa kuimarisha nakuendeleza kampasi za Kigoma, Mtwara na Mwanza ilikuijengea uwezo Taasisi wa kudahili wanafunzi wengi,kudhamini wahadhiri wanaojiunga na kozi za Uzamili naUzamivu ili kuongeza idadi ya wahadhiri wenye shahada yaUzamili na Uzamivu; kuimarisha kitengo cha Utafiti na Ushauriwa Kibiashara ili kuweza kufanya tafiti na kutoa ushauri wakitaalam katika kuelekea Tanzania ya uchumi wa kati kupitiadhana ya Uchumi wa Viwanda, na kuboresha huduma zamaktaba na huduma ya mtandao kwenye kampasi zote ilikuongeza wigo wa udahili na ukusanyaji wa mapato yaTaasisi.

Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika - EASTC

211. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/20, Chuokimepanga kuongeza udahili wa wanafunzi katika ngazi zoteza programu zinazotolewa na chuo kwa kuendelea kutoana kuboresha huduma na mafunzo ya Takwimu rasmi naTakwimu za Kilimo. Katika ngazi ya shahada ya TakwimuRasmi, chuo kinatarajia kudahili wanafunzi 210 kutoka 168walipo sasa. Aidha, katika ngazi za Astashahada naStashahada, chuo kinatarajia kudahili wanafunzi 200 kutokaidadi ya sasa ya wanafunzi 145. Matumaini haya yanakujabaada ya chuo kuongeza juhudi za kujitangaza katika shuleza sekondari ambako ndiko wanafunzi hawa wanakotokea.Aidha, katika ngazi ya shahada ya uzamili, chuo kinalengakudahili wanafunzi 50 kutoka 36 waliopo hivi sasa. Chuokimetambua ugumu wanaoupata wanafunzi wanaojilipiaada katika ngazi hii, hasa wale wanaotoka makazini. Hivyobasi, chuo kimeunda mkakati wa kuwaruhusu kulipa ada zaokwa awamu nyingi zaidi ilimradi wasivuke muhula mmoja bila

Page 137: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

137

kukamilisha ada husika. Hali kadhalika Chuo kitaendeleakuwajengea uwezo wanataaluma kwa kuwapa mafunzo yavitendo katika maeneo ya mifumo ya uchakataji wa takwimu;kuendelea kutoa mafunzo ya muda mfupi ya cheti chaukusanyaji wa takwimu kama njia mbadala ya kuboreshamapato Chuoni; kuendelea kuboresha mazingira yakufundishia na kujifunzia; kupitia upya mitaala ya programuza Chuo; kuendelea na mchakato wa kuboresha namna yakutoa mafunzo kwa njia ya masafa (Distance Learning).

3.2.7 Taasisi za Kitaalam na Huduma nyinginezo

Mamlaka ya Mapato Tanzania - TRA

212. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2019/20, Mamlaka yaMapato Tanzania itaendelea kuimarisha ukusanyaji wamapato ya Serikali kwa: kuhamasisha ulipaji kodi kwa hiari,upanuzi wa wigo wa kodi na matumizi ya mifumo ya TEHAMAkatika usimamizi wa kodi; kuimarisha usimamizi wa sheria zakodi ili kutatua changamoto za ukwepaji kodi na kupunguzaupotevu wa mapato; na kuimarisha makusanyo yasiyo yakodi.

Ofisi ya Taifa ya Takwimu - NBS

213. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2019/20, Wizara kupitiaOfisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) itaendelea kutayarisha nakutoa takwimu rasmi kwa wakati na kumalizia ujenzi wa jengola Ofisi ya Takwimu Mkoa wa Kigoma. Aidha, NBS itaendeleana maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022ambayo itatoa taarifa zitakazowezesha utengenezaji,utekelezaji, ufuatiliaji na kufanya tathmini ya programu nasera za idadi ya watu na itatumika kupima mafanikio yaSerikali katika mipango mbalimbali.

Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi - NBAA

214. Mheshimwa Spika, katika mwaka 2019/20, Bodi ya Taifaya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) itaendeleakutekeleza majukumu yake kama yalivyoainishwa katika

Page 138: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

138

Sheria ya Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Sura286; kusimamia utumiaji wa viwango vya kimataifa vyautayarishaji na ukaguzi wa taarifa za fedha nchini; kutoamafunzo ya diploma ya viwango vya kimataifa vya uandaajiwa taarifa za fedha Serikalini; kutoa ushauri elekezi nahuduma za kiufundi; kusimamia ubora wa wakaguzi wahesabu; na kufanya usajili wa wahasibu na kutunza takwimuzinazohusiana na taaluma ya uhasibu na ukaguzi wa hesabu.

Bodi ya Michezo ya Kubahatisha

215. Mheshimwa Spika, kwa mwaka 2019/20, Bodiitaendelea kuratibu na kudhibiti matangazo ya michezo yakubahatisha ili kuepuka ushawishi wa kupitiliza. Aidha, Bodiitaendelea kutoa elimu kwa umma juu ya dhana ya“responsible gaming” ili ushiriki katika michezo hii uwe ni kwaajili ya burudani na siyo kama chanzo kikuu cha mapato.Vilevile, Bodi inatarajia kukamilisha utengenezaji wa mifumoya TEHAMA. Mifumo hii imekusudiwa kuunganisha mifumo yauendeshaji wa michezo ya kubahatisha kwenye Mfumo Mkuuwa Bodi kwa lengo la kurahisisha ukusanyaji wa taarifambalimbali za fedha zitokanazo na uendeshaji wa michezohiyo.

Mfuko wa Huduma Ndogo za Fedha - SELF Microfinance Fund

216. Mheshimwa Spika, kwa mwaka 2019/20, Mfuko wa SELFumepanga kutoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni36. Mikopo hiyo inatarajiwa kuwafikia wajasiriamalitakriban 15,000 wakiwemo wajasiriamali wadogo na wakati, hususan wale wanaoongeza thamani katika mazao yakilimo. Aidha, katika kutekeleza jukumu la kuwafikia wananchiwalio vijijini na pembezoni mwa miji, Mfuko utatoa mafunzokwa viongozi na watendaji wa Asasi ndogo za fedha zipatazo200 na mafunzo ya moja kwa moja kwa wajasiriamaliwapatao 2,000.

3.2.8 Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi217. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/20, Ofisi ya Taifaya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali itaendelea kuimarisha

Page 139: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

139

ukaguzi wa mapato na matumizi ya Serikali kwa lengo lakuimarisha uwajibikaji na uwazi kwenye matumizi ya rasilimaliza Umma. Katika kufikia malengo hayo, Ofisi imepangakutekeleza vipaumbele nane ikiwa ni pamoja na: kufanyaukaguzi wa mafungu ya Bajeti ya Wizara, Idara za Serikalizinazojitegemea, Wakala na Taasisi za Serikali, Sekretariati zaMikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa katika Mikoa yote nchini,Mashirika ya Umma; kufanya ukaguzi wa miradi yamaendeleo inayofadhiliwa na Wahisani; kufanya kaguzi zakiufundi katika maeneo yenye uwekezaji mkubwa warasilimali za Umma kama vile ujenzi wa barabara na viwanjavya ndege, reli za kisasa, na Miradi ya nishati (umeme);Kufanya maboresho ya mfumo wa ukaguzi kwa kutumiaTEHAMA; na Kukagua ukusanyaji wa mapato ya kodi nayasiyo ya kodi; ukaguzi wa ufanisi, kaguzi maalum, na kaguziza kiuchunguzi (forensic audits) katika maeneoyatakayoainishwa; na kuwajengea Wakaguzi uwezo wakufanya ukaguzi katika maeneo mapya ya ukaguzi pamojana ukaguzi katika uhalifu wa kifedha kwa kutumia mtandao(financial crimes auditing).

4.0 Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2019/20

4.1 Makadirio ya Mapato

218. Mheshimwa Spika, katika mwaka 2019/20, Wizarainakadiria kukusanya maduhuli kiasi cha shilingi967,042,379,000 (bilioni 967.04) kutoka katika vyanzombalimbali ikiwa ni pamoja na gawio, kodi za pango,marejesho ya mikopo, michango kutoka katika taasisi namashirika ya umma, mauzo ya leseni za udalali na mauzo yanyaraka za zabuni. Mchanganuo wa maduhuliyanayokadiriwa kukusanywa kwa mafungu ni kamainavyoonekana kwenye Jedwali Na. 6:

4.2 Makadirio ya Matumizi kwa Mwaka 2019/20

219. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2019/20 Wizara yaFedha na Mipango, Taasisi zake pamoja na Ofisi ya Taifa yaUkaguzi inakadiria kutumia kiasi cha shilingi 11,942,986,578,719

Page 140: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

140

(trilioni 11.94). Kati ya fedha hizo, shilingi 11,212,404,636,988(trilioni 11.21) ni kwa ajili matumizi ya kawaida na shilingi730,581,941,731 (bilioni 730.58) ni matumizi ya maendeleo.Matumizi ya kawaida yanajumuisha shilingi 608,371,517,988(bilioni 608.37) kwa aji l i ya mishahara na shil ingi10,604,033,119,000 (trilioni 10.60) kwa ajili ya matumizimengineyo. Aidha, matumizi ya maendeleo yanajumuishashilingi 677,000,000,000 (bilioni 677.00) fedha za ndani nashilingi 53,581,941,731 (bilioni 53.58) ni fedha za nje.

4.3 Maombi ya Fedha kwa Mafungu

4.3.1 Fungu 50 – Wizara ya Fedha na Mipango

220. Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwa mwaka 2019/20, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kamaifuatavyo:

(a) Matumizi ya kawaida - shilingi 65,713,430,000 (bilioni 65.71).Kati ya hizo:

(i) Mishahara - shilingi 37,920,916,000 (bilioni 37.92)

(ii) Matumizi mengineyo – shilingi 27,792,514,000 (bilioni 27.79)

(b) Miradi ya Maendeleo – shilingi 34,763,757,000 (bilioni34.76). Kati ya hizo:

(i) Fedha za Ndani – shilingi 13,000,000,000 (bilioni 13.00)(ii) Fedha za Nje - shilingi 21,763,757,000 (bilioni 21.76)

4.3.2 Fungu 21 – HAZINA

221. Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwa mwaka 2019/20, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kamaifuatavyo:

(c) Matumizi ya Kawaida – shilingi 1,272,801,249,988(trilioni 1.27). Kati ya hizo:(i) Mishahara - shilingi 536,520,631,988 (bilioni 536.52).

Page 141: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

141

(ii) Matumizi mengineyo – shilingi 736,280,618,000 (bilioni736.28) ambazo ni kwa ajili ya matumizi ya idara, taasisi zilizochini ya Fungu hili, pamoja na matumizi maalum.

(b) Miradi ya maendeleo – shilingi 683,717,888,733 (bilioni683.71). Kati ya hizo:

(i) Fedha za Ndani - shilingi 656,000,000,000 (bilioni 656.00)(ii) Fedha za Nje - shilingi 27,717,888,733 (bilioni 27.71)

4.3.3 Fungu 22- Deni la Taifa

222. Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwa mwaka 2019/20, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kamaifuatavyo:

(a) Matumizi ya kawaida – shilingi 9,730,012,708,000 (trilioni9.73). Kati ya hizo:(i) Mishahara - shilingi 8,885,708,000 (bilioni 8.88)(ii) Matumizi mengineyo - shilingi 9,721,127,000,000 (trilioni 9.72)

4.3.4 Fungu 23 – Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali

223. Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwa mwaka 2019/20, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kamaifuatavyo:-

(a) Matumizi ya kawaida - shilingi 44,066,048,000 (bilioni 44.07).Kati ya hizo(i) Mishahara – shilingi 7,029,314,000 (bilioni 7.03)(ii) Matumizi mengineyo - shilingi 37,036,734,000 (bilioni 37.04)

(b) Miradi ya Maendeleo – shilingi 3,300,000,000 (bilioni 3.30).Kati ya hizo:(i) Fedha za ndani – shilingi 2,000,000,000 (bilioni 2.00)(ii) Fedha za Nje - shilingi 1,300,000,000 (bilioni 1.30)

4.3.5 Fungu 7 – Ofisi ya Msajili wa HAZINA

Page 142: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

142

224. Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwa mwaka 2019/20, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kamaifuatavyo:

(a) Matumizi ya kawaida – shilingi 40,510,802,000 (bilioni40.51). Kati ya hizo:-(i) Mishahara – shilingi 3,281,016,000 (bilioni 3.28)(ii) Matumizi mengineyo – shilingi 37,229,786,000 (bilioni 37.23)

(b) Miradi ya Maendeleo – shilingi 2,300,000,000 (bilioni 2.30).Kati ya hizo:(i) Fedha za ndani – shilingi 1,000,000,000 (bilioni 1.00)(ii) Fedha za Nje - shilingi 1,300,000,000 (bilioni 1.30)

4.3.6 Fungu 10 – Tume ya Pamoja ya Fedha

225. Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwa mwaka 2019/20, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kamaifuatavyo:-

Matumizi ya Kawaida - shilingi 2,207,935,000 (bilioni 2.20)Kati ya hizo:-(i) Mishahara - shilingi 649,793,000 (milioni 649.79)(ii) Matumizi mengineyo - shilingi 1,558,142,000 (bilioni 1.55)

4.3.7 Fungu 13 – Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramu

226. Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwa mwaka 2019/20, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kamaifuatavyo:

(a) Matumizi ya mengineyo - shilingi 2,015,586,000 (bilioni 2.01)(b) Matumizi ya Maendeleo – shilingi 200,295,998 (milioni200.29) ambazo ni fedha za nje.

4.3.8 Fungu 45 – Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi

227. Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwa mwaka 2019/20, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kamaifuatavyo:

Page 143: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

143

(a) Matumizi ya kawaida – shilingi 55,076,878,000 (bilioni55.07). Kati ya hizo:-(iii) Mishahara – shilingi 14,084,139,000 (bilioni 14.08)(iv) Matumizi mengineyo – shilingi 40,992,739,000 (bilioni 40.99)

(b) Miradi ya Maendeleo – shilingi 6,300,000,000 (bilioni 6.30).Kati ya hizo:(iii) Fedha za ndani – shilingi 5,000,000,000 (bilioni 5.00)(iv) Fedha za Nje - shilingi 1,300,000,000 (bilioni 1.30)

5.0 Shukrani

228. Mheshimiwa Spika, napenda nirudie tena kumshukuruMwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kuwasilisha hotuba hiimbele ya Bunge lako Tukufu. Aidha, kwa namna ya pekeekabisa naomba nitumie fursa hii kuwashukuru Washirika waMaendeleo wote wakiwemo nchi na mashirika ya kimataifaambao wamekuwa wakisaidia kwa namna mbalimbali katikautekelezaji wa majukumu ya Wizara. Vilevile, napendakuwashukuru Watanzania wote wenye mapenzi mema nauzalendo kwa nchi yao ambao wamekuwa wakilipa kodistahiki na kwa hiari. Naomba nitumie fursa hii kuwaambiakuwa, mchango wao katika ujenzi wa Taifa letuunathaminiwa sana na utaendelea kukumbukwa hata kwavizazi vijavyo.

229. Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa, napendanikushukuru tena wewe binafsi, kwa kunipa nafasi yakuwasilisha hoja hii pamoja na Waheshimiwa Wabunge wotekwa kunisikiliza. Hotuba hii inapatikana katika tovuti ya Wizarakwa anuani ya www.mof.go.tz

230. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika,naafiki.

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha naMipango. Hoja imetolewa na imeungwa mkono,tunakushukuru sana kwa hotuba yako nzuri ambayo

Page 144: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

144

imetusaidia kufafanua mambo mengi ya kuhusu Wizara yako,tunakushukuru sana. Sasa moja kwa moja nimuite Mwenyekitiwa Kamati ya Bajeti, anakuja Makamu Mwenyekiti,Mheshimiwa Ndaki tafadhali karibu sana una si zaidi ya nususaa.

MHE. MASHIMBA M. NDAKI - MAKAMU MWENYEKITIKAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana.

Mheshimiwa Spika, ninaomba Taarifa hii ya Kamatiya Bejeti yote iingie kwenye Kumbukumbu Rasmi za Bungeyaani Hansard kwa sababu sitaweza kusoma yote hapa kwasababu ni kubwa na naomba Waheshimiwa Wabungewafuatilie kwenye kitabu cha taarifa yetu ili kuhakikishakwamba wanapata kila kilichoelezwa na Kamati ya Bajetikwenye taarifa yetu.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 99(9)ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016 nakwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bejeti, naombakuwasilisha Taarifa ya Kamati ya Bunge ya Bajeti kuhusuutekelezaji wa bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango kwamwaka wa fedha 2018/2019 pamoja na Makadirio yaMapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha2019/2020 ambayo inajumuisha mafungu saba ambayo niFungu 07 - Ofisi ya Msajili wa Hazina; Fungu 10 - Tume yaPamoja ya Fedha; Fungu 13 - Kitengo cha Kudhibiti FedhaHaramu; Fungu 21- Hazina; Fungu 22 - Deni la Taifa; Fungu 23- Mhasibu Mkuu wa Serikali; Fungu 50 - Wizara ya Fedha naMipango. Taarifa hii itajumuisha pia Fungu 45 – Ofisi ya Taifaya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali.

Mheshimiwa Spika, moja ya jukumu la Kamati yaBunge ya Bajeti kama yalivyoainishwa kwenye Nyongeza yaNane kifungu cha 9 cha Kanuni za Kudumu za Bunge Toleola Januari, 2016 ni pamoja na kusimamia shughuli za Wizaraya Fedha na Mipango na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo.Aidha, kifungu cha 9(1)(c) cha Sheria ya Bajeti Namba 11 yamwaka 2015 pia kinaipa Kamati jukumu la kupitia na

Page 145: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

145

kuidhinisha makadirio ya mapato na matumizi ya Fungu – 45- Mfuko wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali.

Kwa muktadha huo, katika nyakati tofauti Kamatiilikutana na kufanya mashauriano na Serikali na hatimayekupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara yaFedha na Mipango na mafungu yote pamoja na Fungu 45ambalo ni Mfuko wa Ofisi ya Taifa ya Mdhibiti na MkaguziMkuu wa Hesabu za Serikali.

Mheshimiwa Spika, majukumu ya Wizara ya Fedha naMipango yameorodheshwa kwenye Tangazo la SerikaliNamba 144 la terehe 22 Aprili, 2016. Pamoja na mambomengine Wizara ina jukumu la kusimamia utekelezaji wa seraza mapato na matumizi ya umma pamoja na kusimamia seraza fedha na uchumi kwa jumla. Majukumu hayoyanatekelezwa kupitia mafungu hayo niliyoyataja mafunguhayo ambayo yametajwa kwenye taarifa yetu na naombakama nilivyoomba Wabunge waendelee kupitia.

Mheshimiwa Spika, sasa nijielekeze kwenye mapitioya utekelezaji wa Bajeti na majukumu ya Wizara ya Fedhana Mipango kwa mwaka wa fedha 2018/2019; katika mwakawa fedha 2018/2019 Wizara ya Fedha na Mipangoili idhinishiwa na Bunge kutumia jumla ya shil ingi12,058,714,013,500 kwa mafungu yote saba. Kati ya fedhahizo shilingi 10,763,501,474,000 zilikuwa kwa ajili ya matumiziya kawaida ambayo yanajumuisha malipo ya deni la Serikalipamoja na riba na shilingi 1,295,212,539,500 zilikuwa kwa ajiliya matumizi ya maendeleo. Aidha, Kamati ilipitia Bajeti yaOfisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali ambapo kiasicha shilingi 69,106,308,000 kiliidhinishwa kwa matumizi ya Ofisihii katika mwaka 2018/2019. Kati ya fedha hizo, shilingi55,394,216,000 zilikuwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida nashilingi 13,712,092,000 zilikuwa kwa ajili ya matumizi yamaendeleo.

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi Aprili, 2019 jumlaya shilingi 8,253,791,005,658 zilikuwa zimetolewa kwa Wizaraya Fedha na Mipango pamoja na mafungu yake yote hii ikiwa

Page 146: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

146

ni sawa na asilimia 68.4 ya bajeti yote ya Wizara kwa kipindihusika. Kati ya fedha hizo shilingi 8,233,112,879,443 sawa naasilimia 76.5 ya lengo zilikuwa ni kwa ajili ya matumizi yakawaida na shilingi 20,678,126,214 zilikuwa ni kwa ajili ya miradiya maendeleo sawa na asilimia 1.6 tu ya bajeti. Aidha, kwaupande wa Fungu 45 - Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabuza Serikali lilitengewa jumla ya shilingi 57,735,146,884 kwa ajiliya matumizi ya kawaida na maendeleo.

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi Aprili, 2019lilikuwa limepokea kiasi cha shilingi 41,736,336,731 sawa naasilimia 75.3. Kati ya fedha hizo shilingi 41,536,336,731 zilikuwakwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi 1,602,930,884zilikuwa kwa ajili ya matumizi ya maendeleo ambayo ni sawana asilimia 11.7 ya bajeti iliyoidhinishwa. Lipo jedwali naombatu Waheshimiwa Wabunge waweze kuangalia.

Mheshimiwa Spika, uchambuzi wa Kamati kuhusuutekelezaji wa bajeti kwa mafungu ya Wizara ya Fedha naMipango kwa mwaka wa fedha 2018/2019; uchambuzi waKamati katika mafungu haya ulibaini kuwa:-

(i) Mafungu matano 5; Fungu 13, Fungu 22, Fungu 23, Fungu45 na Fungu 50 yalipokea zaidi ya asilimia 60 ya fedha zamatumizi ya kawaida zilizoidhinishwa na Bunge; na

(ii) Mafungu mawili 2; Fungu 10 - Tume ya Pamoja ya Fedhana Fungu 21- Hazina yalipokea zaidi ya asilimia 50 na Fungumoja, Fungu 07-Msajili wa Hazina lilipokea asilimia 20 tu yabajeti nzima ya fedha za matumizi ya kawaida.

Mheshimiwa Spika, kati ya shilingi 1,295,212,539,500zilizoidhishwa na Bunge kwa Wizara kwa mwaka wa fedha2018/2019 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo nishilingi 20,678,126,214 sawa na asilimia 1.6 ndiyo zimetolewa.Aidha, ni fungu moja tu, Fungu 23 - Idara ya Mhasibu Mkuuwa Serikali ndilo lilopata zaidi ya asilimia 50 ya bajeti yamaendeleo kama ilivyoidhinishwa na Bunge. Aidha, kati yafedha zote, fedha za ndani ndizo zilizotolewa kwa kiasikikubwa ikilinganishwa na fedha za nje. Hivyo, utekelezaji huu

Page 147: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

147

hafifu wa bajeti za mafungu ulichangiwa kwa kiasi kikubwana kutopatikana kwa fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleokutoka nje. Mwenendo huu wa utolewaji wa fedhausioridhisha unaathiri utekelezaji wa majukumu ya msingi yaWizara.

Mheshimiwa Spika, mafungu mengine kadri ambayoyametajwa Waheshimiwa Wabunge wanaweza kuangalialakini mimi nijielekeze kwenye mafungu machache tu; Fungumojawapo ni Fungu 10 - Tume ya Pamoja ya fedha; hadikufikia mwezi Machi, 2019 Tume ilikuwa imepokea kiasi chashil ingi 1,440,202,822 kati ya shil ingi 2,155,075,000zilizoidhinishwa ikiwa ni sawa na asilimia 66.8 ya bajeti yote.Kamati inasisitiza ukamilishaji wa haraka wa mchakato wamapitio ya mapendekezo ya mwongozo wa uendeshaji nausimamizi wa Akaunti ya Fedha ya Pamoja na hatimayekufunguliwa kwa akaunti hiyo. Suala hili ni la muda mrefutangia kuanza kwa chombo hiki mwaka 2003 lakini badoutekelezaji haujafanyika ipasavyo.

Mheshimiwa Spika, Fungu 13 – Kitengo cha KudhibitiFedha Haramu; hadi mwezi Aprili, 2019 Kitengo kilikuwakimepokea kiasi cha shilingi 1,575,970,211 fedha kwa ajili yamatumizi ya kawaida ikiwa ni sawa na asilimia 69.6. Aidha,kwa upande wa fedha za maendeleo, Kitengo kilitengewakutumia kiasi cha shilingi 248,363,000; lakini hadi Aprili, 2019hamna fedha zozote zilizotolewa na hivyo kufanya bajeti yamaendeleo kutotolewa kabisa.

Mheshimiwa Spika, pamoja na utolewaji wa fedhaunaoridhisha kwa upande wa fedha za matumizi ya kawaida,bado Kitengo hiki hakijaweza kufanya kazi iliyokusudiwa kwaufanisi kutokana na changamoto zifuatazo:-

(i) Kitengo kufanya kazi kwa kutegemea watumishi wakuazima kutoka Idara nyingine za Serikali.

(ii) Kitengo kutegemea taarifa kutoka vyombo vinginepamoja na uwezo wa kimfumo wa Kitengo kugundua nakudhibiti miamala shuku.

Page 148: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

148

Hivyo Kamati inaishauri Serikali kushughulikia harakachangamoto hizo ili kitengo kiweze kufanya kazi kwa ufanisiikiwemo kutoa fedha za miradi ya maendeleo.

Mheshimiwa Spika, Fungu 21- Hazina; hadi kufikiamwezi Aprili, 2019 Fungu hili lilikuwa limepokea shilingi1,599,643,826,107 kwa ajili ya matumizi ya kawaida sawa naasilimia 20.4 ya bajeti nzima ya fedha za matumizi ya kawaida.Aidha, kwa fedha za maendeleo fungu lilikuwa limepokeashilingi 11,659,660,085 fedha za maendeleo sawa na asilimia0.93. Aidha, bajeti nzima ya Fungu 21 katika kipindi hichoilikuwa imetolewa kwa asilimia 20.4 tu.

Mheshimiwa Spika, Fungu hili pamoja na majukumumengine ndilo hasa linasimamia sera ya fedha na sera zakibajeti. Aidha, kwa kiasi kikubwa fungu hili linahusika mojakwa moja na mikakati ya kupunguza umasikini na kukuzauchumi hivyo, utolewaji wa fedha za maendeleo kwa asilimia0.93 tu ni kuathiri juhudi za Serikali ambazo kimsingi zina niaya kutokomeza umasikini na kukuza uchumi.

Mheshimiwa Spika, Fungu 22 – Deni la Taifa naHuduma Nyingine; malipo ya deni la Serikali ambayo ni mtajipamoja na riba yameongezeka kutoka shil ingi7,817,118,000,000 mwaka 2017/2018 hadi shil ingi8,372,951,000,000 mwaka 2018/2019 sawa na ongezeko laasilimia 7.11.

Mheshimiwa Spika, tathimini ya uhimilivu wa Deni laTaifa iliyofanyika mwezi Desemba, 2018 na matokeo ya awaliyanaonesha kuwa deni ni himilivu kwa muda mfupi, wa katina mrefu. Takwimu zinaonesha kwa wastani katika kipindi chamiaka mitatu Serikali hutenga shilingi 8,017,549,000,000 kwamwaka kwa ajili ya kugharamia Deni la Taifa hivyo, Kamatiinaendelea kuishauri Serikali kuendelea kutafuta vyanzovingine vya mikopo ya masharti nafuu ili kugharamia miradiya maendeleo. Kuna jedwali namba tatu WaheshimiwaWabunge mnaweza mkapitia.

Page 149: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

149

Mheshimiwa Spika, lakini niendelee sasa kwenyemakadirio ya mapato ma matumizi ya Wizara ya Fedha naMipango pamoja na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu zaSerikali kwa mwaka wa fedha 2019/2020; katika mwaka wafedha 2019/2020 imekadiriwa kutumia jumla ya shilingi11,286,170,133,820 kwa mafungu yote saba. Kati ya fedhahizo, shilingi 10,604,033,118,820 ni kwa ajili ya matumizimengineyo na kwa ajili ya kulipia Deni la Serikali na HudumaNyingine. Shilingi 608,371,517,988 ni kwa ajili ya mishahara nashilingi 730,581,941,731 ni kwa ajili ya kutekeleza miradi yamaendeleo inayotarajiwa kutekelezwa na Wizara katikakipindi husika.

Mheshimiwa Spika, Kamati ya Bajeti ilikutana na Waziriwa Fedha na Mipango pamoja na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuuwa Hesabu za Serikali ili kujadiliana na kufanya mashaurianokuhusu nyongeza ya shilingi 3,000,000,000 iliyokuwa ikiombwabaada ya kupewa ukomo wa bajeti. Fedha hizo zinazohitajikakwa ajili ya kaguzi maalum nje ya zile zinazopangwa na Ofisiya Taifa ya Ukaguzi ambapo maombi hupokelewa kutokataasisi mbalimbali za Serikali, kaguzi maalum kwa Halmashaurizilizopata hati chafu pamoja na kaguzi za Mamlaka 13 zaMaji ambazo hazina uwezo wa kugharamia kaguzi zake.Kukosekana kwa nyongeza hiyo ya fedha kutaathiri utendajikazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi katika mwaka wa fedha2019/2020. Baada ya majadiliano Serikali iliridhia kuongezafedha hizo kwa Ofisi ya NAOT pindi mahitaji hayoyatakapojitokeza.

Mheshimiwa Spika, Ofisi kwa mwaka wa fedha 2019/2020 imelenga kuimarisha ukaguzi wa mapato na matumiziya Serikali, kuimarisha uwajibikaji na uwazi kwenye matumiziya rasilimali za umma ambapo ilipanga kutumia shilingi64,917,248,417 kulingana na vipaumbele na kazi za ofisizilizolengwa kutekelezwa. Aidha, kwa mujibu wa ukomouliotolewa na Wizara ya Fedha na Mipango, Fungu 45limetengewa jumla ya shilingi 61,376,878,000; kati ya fedhahizo, shilingi 14,084,139,000 ni kwa ajili ya mishahara yawatumishi, shilingi 34,305,459,417 ni fedha kutoka Mfuko Mkuuwa Serikali, shilingi 6,227,650,000 ni fedha kutoka ukaguzi wa

Page 150: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

150

Wakala, Taasisi na Mashirika ya Umma na shilingi 6,300,000,000ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo ambazo shilingi5,000,000,000 ni fedha za ndani na shilingi 1,300,000,000 nifedha za nje.

Mheshimiwa Spika, Kamati bado inasisitiza umuhimuwa kuhakikisha Fungu 45 linapatiwa rasilimali fedha za kutoshazinazoendana na vipaumbele, kazi na mahitaji halisi ya ofisiili iweze kutekeleza majukumu yake ya msingi.

Mheshimiwa Spika, sasa niende kwenye maoni namapendekezo ya Kamati ya Bunge; baada ya Kamati kupitiautekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango pamojana Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwakawa fedha 2018/2019 pamoja na mapato na matumizi yamafungu husika kwa mwaka wa fedha 2019/2020; Kamatiinaendelea kutoa maoni na mapendekezo yake.

Mheshimiwa Spika, la kwanza mamlaka yaMheshimiwa Waziri wa Fedha katika masuala yote ya fedha;Kamati inatambua majukumu ya Wizara ya Fedha naMipango na Taasisi zake katika kusimamia sera za fedha nasera za kiuhasibu (monetary and fiscal policies) na kuwa ndiyemsimamizi mkuu wa masuala yanayohusu fedha. Hata hivyo,hivi karibuni kumeibuka utaratibu kwa baadhi ya Wizara naMamlaka ya Mikoa na Wilaya kutoheshimu mamlaka hayaya Wizara ya Fedha na Mipango na hivyo kutoishirikishaWizara katika uanzishwaji wa tozo, ushuru na ada katika sektazao. Jambo hili limepelekea baadhi ya tozo, ada na ushuruunaoanzishwa kuwa kero kwa wananchi nawafanyabiashara. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Wizara ya Fedha naMipango ndiyo yenye instrument ya kusimamia masuala yoteya fedha na taratibu zake ni vema kukafanyika harmonizationya sheria zote ili kuzitaka Wizara na mamlaka nyingine zotekulazimika kukubaliana na Wizara ya Fedha na Mipangokabla ya kuanzisha tozo, ada au ushuru wa aina yoyote ile.(Makofi)

Page 151: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

151

Mheshimiwa Spika, namba mbili utaratibu wakubakiza kiasi cha mapato yaani (retention); wakati wamapitio wa bajeti ya Fungu 50 - Wizara ya Fedha na Mipango,Kamati ilibaini kuwa kuna baadhi ya taasisi zilizo chini yaWizara ya Fedha na Mipango ambazo zinapokea mishaharakutoka Serikali Kuu bado zinatumia utaratibu wa retention.Taasisi hizo ni pamoja na taasisi za mafunzo IFM, IAA, TIA; Bodiya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi, Wakala wa Ununuzi waSerikali (GPSA) na PSPTB.

Mheshimiwa Spika, taasisi hizo zinatumia mapato yaoya ndani kama matumizi mengineyo ndio maana hakunafedha zozote za OC ambazo taasisi hizi zinapokea kutokaSerikali Kuu. Ni ushauri wa Kamati kuwa kwa kuwa mapatoya chuo yatokanayo na ada, ni muhimu Serikali ikawekautaratibu wa kuyatambua mapato haya ili kudhibiti matumiziyasiyo ya lazima kwenye taasisi hizo.

Mheshimiwa Spika, usimamizi na utekelezaji wa sheriaya bajeti; moja ya lengo la kuanzisha Sheria ya Bajeti ilikuwani kuwa na Sheria ya mahsusi ya kuongoza mchakato mzimawa bajeti ya Serikali pamoja na kubainisha vema mipaka yakiutendaji na kimajukumu kati ya Serikali na Bunge kwakuweka bayana kazi na majukumu ya Serikali na Bungepamoja na Kamati zake katika mchakato wa Bajeti ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, pamoja na uwepo wa sheria hiina sheria nyingine za fedha, bado kuna viashiria vidogovinavyoonesha Wizara ya Fedha na Mipango kutozingatiaSheria ya Bajeti katika upangaji na utekelezaji wa Bajeti zamafungu mbalimbali. Mathalani, wakati wa mjadala huu waBunge la Bajeti, Serikali kupitia Wizara na Fedha na Mipangoilihamisha kiasi cha takribani shilingi bilioni 152 kutoka katikaFungu 21 - Hazina kwenda Fungu 56 - TAMISEMI shilingi bilioni33; Fungu 98 -Ujenzi shilingi bilioni 90 na Fungu 46 -Elimu shilingibilioni 29 pasipo kushauriana na Kamati ya Bajeti, licha yakuwa hapo awali Kamati ya Bajeti ilikwishapitisha Bajeti yamafungu yote ya Wizara ya Fedha na Mipango kwakuzingatia ukomo wa bajeti ambao umekuwa ukisisitizwa naWizara ya Fedha na Mipango kwa mafungu yote. Kamati

Page 152: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

152

inashauri Wizara ya Fedha na Mipango kuhakikishainasimamia na Sheria ya Bajeti katika kupanga na kutekelezabajeti ya Serikali kwa mafungu yote.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, uhakiki na ulipaji wa madeni yawatumishi, wakandarasi na wazabuni; Kamati inaipongezaSerikali kwa jitihada za kendelea kuhakiki na kulipa madeniya wafanyakazi, wazabuni na watoa huduma. Hata hivyo,suala hili limekuwa la muda mrefu na madeni mapyayanaendelea kuzalishwa. Kati ya mwaka 2016/2017 hadiMachi, 2019 jumla ya shilingi 2,299,836,402,880.07 zilikuwazimetolewa kwa ajili ya kulipa madeni mbalimbali yawatumishi, wazabuni, wakandarasi/wahandisi washauri,watoa huduma na madeni mengineyo. Kuhusu madeniyaliyokataliwa kwa hesabu zilizoishia tarehe 30 Juni 2018 nijumla ya shilingi 407,009,218,378.55; dola za Marekani29,650,115.78; euro 162,009; paundi za Uingereza 7,477; randza Afrika Kusini 1,122,852 na korona za Uswis 95,986. Madenihayo yalikataliwa kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamojana kukosekana kwa nyaraka zinazostahili.

Mheshimiwa Spika, ni rai ya Kamati kuwa Serikaliihakikishe inaendelea na ulipaji wa madeni yoteyaliyohakikiwa ili kupunguza gharama kwa Serikali hasa kwamadeni yenye ongezeko la riba, lakini pia gharama kwawatoa huduma waliokopa kwenye mabenki kupata mtaji iliwaweze kutoa huduma kwa Serikali. Aidha, kwa madaiyaliyokataliwa Serikali ihakikishe inawapa taarifa wadaikuhusu mapungufu katika madai yao na hivyo kuwatakawayawasilishe tena yakiwa yamekamilika ikiwa endapoyatastahili kulipwa malipo yaweze kufanyika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwisho, muda unaotumikakuhakiki madeni umekuwa mrefu hivyo Serikali ihakikishe kuwamchakato wa uhakiki unafanyika ndani ya muda il ikuwezesha ulipaji wa mdeni hayo kwa wakati. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Kitengo cha Kudhibiti FedhaHaramu; Kitengo hiki kina jukumu muhimu la kupokea nakuchambua taarifa za miamala shuku toka kwa watoa taarifa

Page 153: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

153

na kupeleka intelejensia kwenye vyombo vya utekelezaji waSheria kwa uchunguzi. Pamoja na kwamba kitengo hichokimeongezewa majukumu lakini Bajeti ya kitengo hicho nisawa na ile ya mwaka wa fedha wa 2018/2019. Katikamwaka wa fedha 2019/2020 kitengo kimeidhinishiwa kutumiajumla ya kiasi cha shilingi 2,015,586,000 kwa ajili ya matumiziya kawaida ikiwa sawa na bajeti ya mwaka 2018/2019.Kutokana na umuhimu wa chombo hiki, Serikali ikiangaliechombo hiki kwa jicho la kipekee, ihakikishe kuwa kitengohiki kinatengewa rasilimali fedha za kutosha ili kitekelezemajukumu yake kikamilifu.

Mheshimiwa Spika, Sheria ya Udhibiti wa FedhaHaramu Sura ya 423; Kamati inaishauri Serikali iangalie upyaSheria Udhibiti wa Fedha Haramu (The Anti-Money LaunderingAct Cap 423) na majukumu yake yaangaliwe upya ili iendanena hali halisi ya sasa ili kiweze kufanya zaidi ya kaziiliyokusudiwa. Maboresho hayo yajikite katika maeneoyanayohusu dhamana na kiwango cha fedha ambacho mtuanaruhusiwa kubeba hasa kwa wafanyabiashara wa madinibaada ya kuanzisha masoko ya madini nchini.

Mheshimiwa Spika, Sheria ya Anti-Money Launderingya mwaka 2006 imetaja kiwango cha juu cha fedhaambacho mtu anaweza kukibeba kama fedha taslimu kuwani shilingi 10,000,000 tu. Kiwango hiki kwa biashara ya dhahabuni kidogo sana, hivyo sheria iweke utaratibu ambaoutawezesha biashara hii kufanyika bila ya kuwa na vikwazovyovyote.

Mheshimiwa Spika, uanzishwaji wa Akaunti ya Pamojaya Fedha; Ibara ya 133 ya Katiba ya Jamhuri ya Muunganoya Tanzania inatamka kuwa kutaanzishwa Akaunti ya Fedhaya Pamoja kwa madhumuni ya shughuli za Jamhuri yaMuungano kwa mambo ya Muungano ambamo kutawekwafedha yote itakayochangwa na Serikali mbili kwa kiasikitakachoamuliwa na Tume ya Fedha ya Pamoja kwa mujibuwa sheria iliyotungwa na Bunge. Aidha, pamoja na Tume hiikuanzishwa mwaka 2003 hadi hivi sasa akaunti hii badohaijafunguliwa.

Page 154: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

154

Mheshimiwa Spika, wakati wa kupitia bajeti ya Funguhili Kamati ilijulishwa kuwa suala hili linafanyiwa kazi na Serikaliambapo taarifa ya mapendekezo ya mwongozo wauendeshaji na usimamizi wa Akaunti ya Fedha ya Pamojaimewasilishwa Serikalini kwa ajili ya kufanyiwa maamuzi. Hivyobasi, Kamati inashauri Serikali kuharakisha mchakato wakuandaa Mwongozo kwani suala hili ni la muda mrefu. Uwepowa akaunti hiyo sio tu utapelekea Tume kufanya kaziil iyokusudiwa lakini pia itasaidia kupunguza kero nachangamoto za Muungano.

Mheshimiwa Spika, uunganishwaji wa taasisi zamafunzo zilizo chini ya Wizara mbalimbali; taasisi za mafunzohasa zile zilizochini ya Wizara mbalimbali mathalani IAA, IFM,Chuo cha Madini, Chuo za Hombolo na kadhalika zimekuwazikiongezeka kwa kasi nchini. Pamoja na nia nzuri zauanzishwaji wa taasisi hizi ambazo zililenga kutoa mafunzoya kinadharia katika taaluma za Wizara husika taasisi hizi sasazinatoa hadi shahada. Hivyo basi, imefika wakati sasa waSerikali ifanye mapitio ya sheria zilizoanzisha taasisi ilikuendana na dhima ya uanzishwaji wa taasisi hizo.

Mheshmiwa Spika, utitiri wa mifumo ya malipo;kumekuwa na mifumo mingi sana ambayo inasimamiwa naWizara mfano TANePS, IFMs, GePG, GSSP, GAMIS, GARI-ITS,IDEA, PMS-Poverty Management System na CBMS. Mifumoyote hii inasimamiwa na Wizara moja na uendeshaji wake niwa gharama kubwa. Mathalani kwa mwaka wa fedha 2019/2020 mifumo hii inakadiriwa kutumia takribani jumla ya shilingi3,000,000,000 kwa mwaka. Ni maoni ya Kamati kuwa Serikaliije na namna bora ya kuunganisha mifumo hii hasa ileambayo inafanya kazi moja.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, Kamati pia ilibaini kuwa asilimiakubwa ya mifumo hiyo ni ya nje yaani ya kununua kutoka njena hivyo kuongeza gharama za kiuendeshaji ikiwa ni pamojana ada za leseni yaani hosting na subscription fees.

Mheshimiwa Spika, pamoja na changamotozilizotajwa hapo juu, Kamati inaipongeza Serikali kwa jitihada

Page 155: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

155

zake ilizoanza katika kuhakikisha kuwa inakuja na mifumoyake yenyewe ambapo hadi sasa imeweza kutengezamifumo yake kadhaa ikiwa ni pamoja na mfumo wa PMIS,TANePS, GePG, EFD na GAMIS. Hivyo basi, Serikali iharakishemchakato wa kujenga mifumo yake na kuondokana namifumo mengine kutoka kwa Makampuni au watu binafsikutoka nje.

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa Akaunti Jumuifu yaFedha (TSA); pamoja na dhamira nzuri ya Serikali ya kuhuishaakaunti zote za Serikali na kuanzisha Akaunti Jumuifu ilikudhibiti matumizi, mfumo huu umekumbwa na changamotombalimbali za kiutendaji. Mfumo huu kwa kiasi kikubwaunategemea ubora wa mifumo ya mawasiliano na kwa haliilivyosasa hasa katika ngazi za Halmashauri kumekuwa nachangamoto kubwa sana. Tatizo hil i la kimtandaolimepelekea ucheleweshawaji wa malipo kutokana na kuwataarifa za malipo hazifiki Benki Kuu kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, changamoto nyingineinayopelekea ufanisi wa mfumo huu kupungua ni mlundikanowa server katika kituo kimoja. Server zote za malipozimehifadhia katika ofisi za TAMISEMI Makao Makuu Dodomana hivyo kupelekea kituo hiki kuelemewa au kushindwakufanya kazi iwapo...

SPIKA: Ahsante sana, Mheshimiwa Makamu Mwenyekitinakushukuru.

MHE. MASHIMBA M. NDAKI – MAKAMU MWENYEKITIKAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJAETI: Mheshimiwa Spika,ahsante, nakushukuru na naomba nihitimishe dakika mbilinihitimishe dakika moja.

Mheshimiwa Spika, naomba nihitimishe kwakukushukuru wewe Mheshimiwa Spika na Dkt. Tulia Ackson -Naibu Spika na Wenyeviti wa Bunge na niwashukuruWajumbe wa Kamati ambao naomba nawatambuliwe naKumbukumbu zako za Bunge kama ambavyo wameandikwakwenye taarifa hii.

Page 156: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

156

Lakini pia mwisho nitoe shukurani zangu za dhati kwaKatibu wa Bunge ndugu Stephen Kagaigai pamoja nawatendaji wote wa Ofisi ya Bunge kwa kuiwezesha Kamatikuitekeleza majukumu yake ipasavyo. Aidha, kwa namna yapekee napenda kuishukuru Sekretarieti ya Kamati ya Bajetikwa kuratibu shughuli za Kamati pamoja na kutoa ushauriwa kitaalam na hatimaye kukamilisha kwa taarifa hii kwawakati.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha na naombakuunga mkono hoja (Makofi)

MAONI YA KAMATI KUHUSU UTEKELEZAJI WA BAJETI YAWIZARA YA FEDHA NA MIPANGO KWA MWAKA WA FEDHA

2018/19 PAMOJA NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZIKWA MWAKA WA FEDHA 2019/20 - KAMA

ILIVYOWASILISHWA MEZANI

1.0 UTANGULIZI.Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 99 (9) ya Kanuniza Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016, naombakuwasilisha Taarifa ya Kamati ya Bunge ya Bajeti kuhusuUtekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango kwamwaka wa fedha 2018/19, pamoja na Makadirio ya Mapatona Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/20ambayo inajumuisha Mafungu Saba (7)ambayo ni Fungu 07- Ofisi ya Msajili wa Hazina, Fungu 10 - Tume ya Pamoja yaFedha, Fungu 13 - Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu, Fungu21- Hazina, Fungu 22 - Deni la Taifa, Fungu 23 - Mhasibu Mkuuwa Serikali,Fungu 50 - Wizara ya Fedha na Mipango. Taarifahii itajumuisha piaFungu 45 – Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi waHesabu za Serikali.

Mheshimiwa Spika, moja ya jukumu la Kamati ya Bunge yaBajeti kama yalivyoainishwa kwenye Nyongeza ya Nanekifungu cha 9 chaKanuni za kudumu za Bunge Toleo laJanuari, 2016 ni pamoja na kusimamia shughuli za Wizara yaFedha na Mipango na taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo. Aidha,kifungu cha 9 (1) (c) cha Sheria ya Bajeti Na. 11 ya mwaka2015 pia kinaipa Kamati jukumu la kupitia na kuidhinisha

Page 157: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

157

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fungu – 45, Mfuko waOfisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali. Kwa muktadhahuo, katika nyakati tofauti,Kamati ilikutana na kufanyamashauriano na Serikali na hatimaye kupitisha Makadirio yaMapato na Matumizi ya Wizara ya Fedha na Mipango naMafungu yake pamoja Fungu 45 - Mfuko wa Ofisi ya Taifa yaMdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Mheshimiwa Spika, majukumu ya Wizara ya Fedha naMipango yameorodheshwa kwenye Tangazo la Serikali Na.144 la terehe 22 Aprili, 2016. Pamoja na mambo mengineWizara ina jukumu la kusimamia utekelezaji wa sera zamapato na matumizi ya umma pamoja na kusimamia seraza fedha na uchumi kwa ujumla. Majukumu hayoyanatekelezwa kupitia mafungu yaliyo chini yake kamaifuatavyo: -

i. Fungu 07 - Ofisi ya Msajili wa Hazina imepewa jukumu lakusimamia na kulinda rasilimali zilizowekezwa na Serikali katikaMashirika na Taasisi za Umma na majukumu mengine kamayalivyoainishwa kwenye Sheria ya Msajili wa Hazina Sura Na.370.

ii. Fungu 10 – Tume ya Pamoja ya Fedha ni Asasi ya Muunganowa Tanzania iliyoundwa kwa mujibu wa Ibara 134 ya Katibaya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 nakuanzishwa kwa Sheria ya Tume ya Pamoja ya Fedha yamwaka 1996, Sura 140. Jukumu kuu la Tume ni kuwa chombocha ushauri kuhusiana na mambo yote ya Muunganoyanayohusu fedha baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muunganowa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja namajukumu mengine kama yalivyoainishwa kwenye Ibara ya134(2) ya Katiba.

iii. Fungu 13 – Kitengo cha kudhibiti Fedha Haramu; Kitengohichi ni chombo cha kiinteligensia kilichoanzishwa chini yaSheria ya Udhibiti wa Fedha Haramu ya Mwaka 2006, SuraNa. 463 mahsusi kwa ajili ya kupambana na utakatishaji wafedha haramu pamoja na ufadhili wa vitendo vya ugaidinchini.

Page 158: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

158

iv. Fungu 21- Hazina;Ofisi hii ina majukumu makuu matatu.Jukumu la kwanza ni kusimamia ukusanyaji wa mapato namatumizi ya fedha za Serikali, Pili nikusimamia utekelezaji wabajeti ya Serikali na Tatuni kuhakikisha kunakuwa na kudhibitiDeni la Taifa ili liendelee kuwa himilivu.

v. Fungu 22 – Deni la Taifa; Idara hii inajukumu kubwa la kulipamadeni ya ndani na nje ya nchi (Principal debt) pamoja nariba (Interest). Aidha Idara hii pia inajishughulisha na mafaoya pensheni kwa wastaafu pamoja na michango ya mwajiri.vi. Fungu 23- Mhasibu Mkuu wa Serikali; Idarahii inajukumu lakusimamia matumizi ya fedha za Serikali na kutoa miogozoya mifumo ya kifedha inayopaswa kutumiwa na taasisi zoteza umma.

vii. Fungu 50 -Wizara ya Fedha na Mipango inajukumu lamsingi la kusimamia uchumi jumla kupitia sera za fedha (FiscalPolicy) na matumizi na mifumo ya kifedha kwa ajili yakuimarisha ukuaji wa uchumi (Monetary Policy).

2.0 MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA BAJETI NA MAJUKUMUYA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO KWA MWAKA WAFEDHA 2018/19

2.1. Mapato na Matumizi ya Wizara ya Fedha na Mipango

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa Fedha 2018/19, Wizaraya Fedha na Mipango iliidhinishiwa na Bunge kutumia jumlaya shilingi 12,058,714,013,500 kwa mafungu yote saba (7) .Kati ya fedha hizo Shilingi 10,763,501,474,000 zilikuwa kwaajili ya matumizi ya kawaida ambayo yanajumuisha malipoya deni la Serikali (pamoja na riba) na Shilingi1,295,212,539,500 zilikuwa kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.Aidha, Kamati ilipitia Bajeti ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi waHesabu za Serikali ambapo kiasi cha shilingi 69,106,308,000kiliidhinishwa kwa matumizi ya Ofisi hii katika mwaka 2018/19. Kati ya fedha hizo, Shilingi 55,394,216,000 zilikuwa kwa ajiliya matumizi ya kawaida na shilingi 13,712,092,000 zilikuwakwa ajili ya matumizi ya maaendeleo.

Page 159: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

159

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi Aprili, 2019 jumla yashilingi 8,253,791,005,658 zilikuwa zimetolewa kwa Wizaraya Fedha na Mipango pamoja na mafungu yake yote hii ikiwani sawa na asilimia 68.4 ya Bajeti yote ya Wizara kwa kipindihusika. Kati ya fedha hizo Shilingi 8,233,112,879,443 sawa naasilimia 76.5 ya lengo zilikuwa ni kwa ajili ya matumizi yakawaida na Shilingi 20,678,126,214 zilikuwa ni kwa ajili yamiradi ya maendeleo sawa na asilimia 1.6 tu ya Bajeti.

Aidha, kwa upande wa Fungu 45 - Ofisi ya Taifa ya Ukaguziwa Hesabu za Serikali , l i l itengewa jumla ya shilingi57,735,146,884 kwa ajil i ya matumizi ya kawaida namaendeleo. hadi kufikia mwezi April, 2019 lilikuwa limepokeakiasi cha shilingi 41,736,336,731 sawa na asilimia 75.3 Kati yafedha hizo shilingi 41,536,336,731 zilikuwa kwa ajili ya matumiziya kawaida na Shilingi 1,602,930,884 zilikuwa kwa ajili yamatumizi ya maendeleo ambayo ni sawa na asilimia 11.7 yaBajeti iliyoidhinishwa na Bunge.

Aidha,Jedwali Na. 1 hapo chini linaonyesha mgawanyo wabajeti kwa kila fungu pamoja na utekelezaji wa bajeti kwakipindi cha robo tatu ya mwaka wa fedha 2018/19.

Mheshimiwa Spika, Kama ambavyo jedwali linaonyesha,Utekelezaji wa bajeti ya Mafungu ya Wizara ya Fedha naMipango umekuwa si wakuridhisha hasa kwa upande waBajeti ya maendeleo. Katika mafungu yote matanoyanayopokea fedha za maendeleo ni fungu moja tu (Fungu-50) ambalo limepokea fedha za maendeleo zaidi ya asilimia50

Page 160: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

160

Jedwali Namba 1. Utekelezaji wa Bajeti Kwa Mafungu yaWizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka 2018/19

Jedwali Namba 2. Utekelezaji wa Bajeti ya Maendeleo KwaMafungu ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka 2018/19

FUNGU JINA LA FUNGU BAJETI ILIYOIDHINISHWA 2018/19

FEDHA ILIYOTOLEWA HADI APRILI, 2019

ASILMIA YA FEDHA ZILIZOTOLEWA HADI

APRILI, 2019

ASILIMIA KIASI

CHOTE KILICHO-TOLEWA

Matumizi ya kawaida

Maendeleo Matumizi ya Kawaida

Maendeleo Matumizi ya Kawaida

Maendeleo (%)

07 Msajili wa Hazina 54,592,065,000 1,650,000,000 15,771,612,109 649,895,000 28.9 39.4 29.2

10 Tume ya Pamoja ya Fedha

2,155,075,000 - 1,440,202,822 - 66.8 0 66.8

13 Kitengo cha Udhibiti Fedha Haramu

2,015,586,000 248,363,000 1,575,970,211 0 78.2 0.00 69.6

21 Hazina 531,890,056,000 1,247,611,267,500 352,032,558,607 11,659,660,085 66.2 0.93 20.4

22 Deni la Taifa 10,013,706,140,000 - 7,734,740,415,117 - 77.2 0 77.2

23 Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali

46,725,409,000 3,200,000,000 40,155,147,427 2,726,434,843 85.9 85.2 85.9

50 Wizara ya Fedha na Mipango

57,022,927,000 28,790,817,000 27,851,947,727 3,301,205,402 48.8 11.5 36.3

JUMLA 45 Ofisi ya Taifa ya

Ukaguzi wa Hesabu ya Serikali

55,394,216,000 13,712,092,000 41,736,336,731 2,340,930,884 75.3 17.0 63.8

 

FUNGU JINA LA FUNGU BAJETI YA MAENDELEO ILIYOIDHINISHWA 2018/19

FEDHA ILIYOTOLEWA HADI APRILI, 2019

ASILMIA YA FEDHA ZILIZOTOLEWA

Ndani Nje Ndani Nje Ndani Nje

07 Msajili wa Hazina 1,000,000,000 650,000,000 0 649,895,000 0 99.9

10 Tume ya Pamoja ya Fedha

- - - - -

13 Kitengo cha Udhibiti Fedha Haramu

- 248,363,000 - 0 0

21 Hazina 1,236,190,593,500 11,420,674,000 10,950,000,000 709,660,085 0.89 6.2

22 Deni la Taifa - -

23 Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali

2,000,000,000 1,200,000,000 1,620,641,093 1,105,793,750 81.0

92.1

50 Wizara ya Fedha na Mipango

19,642,535,000 9,148,282,000 1,276,831,402 2,024,374,000 6.5

22.1

JUMLA

45 Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu ya Serikali

7,200,000,000 6,512,092,000 1,520,535,884 820,395,000 21.1

12.6

 

Page 161: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

161

2.2. Uchambuzi wa Kamati kuhusu Utekelezaji wa Bajetikwa mafungu ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa Mwakawa Fedha 2018/19.

Mheshimiwa Spika, uchambuzi wa Kamati katika mafunguhaya ulibaini kuwa :-

i. Mafungu matano 5 (Fungu 13- Kitengo cha Udhibiti waFedha Haramu, Fungu 22- Deni la Taifa, Fungu 23- Idara yaMhasibu Mkuu wa Serikali, Fungu 45- Ofisi ya Taifa ya Ukaguziwa Hesabu za Serikali na Fungu 50- Wizara ya Fedha naMipango) yalipokea zaidi ya asilimia 60 ya fedha za matumiziya kawaida zilizoidhinishwa na Bunge; na

ii. Mafungu mawili 2 (Fungu 10- Tume ya Pamoja ya Fedhana Fungu 21- Hazina) yalipokea zaidi ya asilimia 50 na Fungumoja, (Fungu 07 Msajili wa Hazina) lilipokea asilimia 20 tu yabajeti nzima ya fedha za matumizi ya kawaida.

Mheshimiwa Spika, kati ya Shilingi 1,295,212,539,500zilizoidhishwa na Bunge kwa Wizara kwa mwaka wa fedha2019/20 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ni20,678,126,214 sawa na asilimia 1.6 ndiyo zimetolewa. Aidha,ni fungu moja tu, Fungu 23- Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikalindilo lilopata zaidi ya asilimia 50 ya bajeti ya maendeleokama iliyoidhinishwa na Bunge. Aidha, kati ya fedha zote,fedha za ndani ndizo zil izotolewa kwa kiasi kikubwaikilinganishwa na fedha za nje. Hivyo, utekelezaji huu hafifuwa bajeti za mafungu ulichangiwa kwa kiasi kikubwa nakutopatikana kwa fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleokutoka nje.

Mheshimiwa Spika, mwenendo huu wa utolewaji wa fedhausioridhisha unaathiri utekelezaji wa majukumu ya Msingi yaWizara.

2.1.1. Fungu 07 - Ofisi ya Msajili wa HazinaMheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2018/19, Funguhili liliidhinishiwa jumla ya shilingi 56,242,065,000 hata hivyohadi kufika mwezi Aprili, 2019 kiasi cha shilingi 16,421,507,109

Page 162: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

162

ndicho kilikuwa kimetolewa na Hazina ikiwa ni sawa naasilimia 29.1 ya lengo.

Mheshimiwa Spika, utolewaji wa fedha kwa fungu hiliumekuwa ni chini ya asilimia 50 katika kipindi husika kwamiaka mitatu mfululizo. Katika kipindi kama hiki kwa mwakawa fedha 2017/18 na 2016/17 Ofisi ilipokea bajeti kati yaasilimia asilimia 7.7 hadi 17.25 ya fedha yote iliyoidhinishwana Bunge. Mwenendo huu si wa kuridhisha hata kidogoukizingatia umuhimu wa majukumu ya Ofisi ya Msajili waHazina. Aidha, katika mafungu yote 7, ya Wizara ya fedhana Mipango Fungu 07 ndio fungu pekee ambalo limekuwalinapokea fedha kwa ajili ya matumizi ya kawaida chini yaasilimia 30.

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa mwaka wafedha 2018/19 ilitenga shilingi 45,000,000,000 fedha kwa ajiliya matumizi maalum yanayojumuisha kulipa madeni yamashirika ya umma na kurekebisha mashirika yenye matatizoya kimtaji. Hadi kufikia mwezi Machi, 2019 zilikuwa zimetolewashilingi 6,300,000,000 tu sawa na asilimia 14 sawa. Hii ikiashiriakwamba Serikali bado haijatekeleza kwa vitendo nia yakeya kuwekeza kwenye mashirika ya umma ili yaweze kutoamchango mkubwa zaidi katika Maendeleo ya Taifa.

2.1.2. Fungu 10 – Tume ya Pamoja ya Fedha

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi Machi, 2019, Tumeilikuwa imepokea kiasi cha shilingi 1,440,202,822 kati ya shilingi2,155,075,000 zilizoidhinishwa ikiwa ni sawa na asilimia 66.8ya bajeti yote. Kamati inasisitiza ukamilishaji wa haraka wamchakato wa mapitio ya mapendekezo ya mwongozo wauendeshaji na usimamizi wa Akaunti ya Fedha ya Pamoja(AFP) na hatimaye kufunguliwa kwa akaunti hiyo. Suala hili nila muda mrefu tangia kuanza kwa chombo hiki mwaka 2003lakini bado utekelezaji haujafanyika ipasavyo.

2.1.3. Fungu 13 – Kitengo cha kudhibiti Fedha HaramuMheshimiwa Spika, hadi mwezi Aprili, 2019 Kitengo kilikuwakimepokea kiasi cha shilingi 1,575,970,211 fedha kwa ajili ya

Page 163: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

163

matumizi ya kawaida ikiwa ni sawa na asilimia 69.6 Aidha,kwa upande wa fedha za maendeleo, Kitengo kilitengewakutumia kiasi cha shilingi 248,363,000 lakini hadi Aprili, 2019hamna fedha zozote zilizotolewa na hivyo kufanya bajeti yamaendeleo kutotekelezwa.

Mheshimiwa Spika, pamoja na utolewaji wa fedhaunaoridhisha kwa upande wa fedha za matumizi ya kawaida,bado kitengo hiki hakijaweza kufanya kazi iliyokusudiwa kwaufanisi kutokana na changamoto zifuatazo;

i. Kitengo kufanya kazi kwa kutegemea watumishi wa kuazimakutoka Idara nyingine za Serikali na

ii. Kitengo kutegemea taarifa kutoka vyombo vingine pamojana uwezo wa kimfumo wa kitengo kugundua na kudhibitimiamala shuku.

Hivyo kamati inaishauri Serikali kushughulikia harakachangamoto hizo ili kitengo kiweze kufanya kazi kwa ufanisiikiwemo kutoa fedha za miradi ya maendeleo.

2.1.4. Fungu 21- Hazina

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi Aprili, 2019 fungu hilililikuwa limepokea shilingi 1,599,643,826,107 kwa ajili yamatumizi ya kawaida sawa na asilimia 20.4 ya bajeti nzimaya fedha za matumizi ya kawaida. Aidha, kwa fedha zamaendeleo fungu lilikuwa limepokea shilingi 11,659,660,085fedha za maendeleo sawa na asilimia 0.93 Aidha, bajetinzima ya Fungu 21 katika kipindi hicho ilikuwa imetolewa kwaasilimia 20.4 tu.

Mheshimiwa Spika, Fungu hili pamoja na majukumu menginendilo hasa linasimamia sera ya fedha na sera za kibajeti.Aidha, kwa kiasi kikubwa fungu hili linahusika moja kwa mojana mikakati ya kupunguza umasikini na kukuza uchumi. Hivyo,utolewaji wa fedha za maendeleo kwa asilimia 0.93 tu nikuathiri juhudi za Serikali ambazo kimsingi zina nia yakutokomeza umasikini na kukuza uchumi.

Page 164: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

164

2.1.5. Fungu 22 – Deni la Taifa na Huduma Nyingine

Mheshimiwa Spika, Malipo ya deni la Serikali ambayo ni mtajipamoja na riba yameongezeka kutoka Shilingi trilioni7,817,118,000,000 mwaka 2017/18 hadi Shilingi trilioni8,372,951,000,000 mwaka 2018/19 sawa na ongezeko laasilimia 7.11.

Mheshimiwa Spika, Tathimini ya uhimilivu wa deni la taifailiyofanyika mwezi Desemba 2018 na matokeo ya awaliyanaonesha kuwa deni ni himilivu kwa muda mfupi, wa katina mrefu. Takwimu zinaonyesha kwa wastani katika kipindicha miaka 3 Serikali hutenga shilingi 8,017,549,000,000 kwamwakakwa ajili ya kugharamia deni la taifa. Hivyo, Kamatiinaendelea kuishauri Serikali kuendelea kutafuta vyanzovingine vya mikopo ya masharti nafuu ili kugharamia miradiya maendeleo.

Jedwali Namba 3: Malipo ya Deni la Serikali

2.1.6. Fungu 23- Mhasibu Mkuu wa Serikali

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi Aprili, 2019 Idara hiiilikuwa imepokea jumla ya shilingi 42,881,582,270 sawa naasilimia 82.9 ya bajeti yote iliyoidhinishwa na Bunge. Funguhili, ni fungu pekee la Wizara ya Fedha na Mipango ambalolimepokea fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwaasilimia 85.2 ya fedha zote za maendeleo.

Mheshimiwa Spika, Kamati inaipongeza Idara hii kwa kuwezakusimamia mfumo wa udhibiti wa matumizi ya fedha zaumma ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa Akaunti Jumuifuya Hazina (TSA). Aidha, pamoja na mafanikio yaliyopatikana,utekelezaji wake bado unaathiriwa na upatikanaji wa

Na. 2017/18 2018/19 2019/20

1. Ndani 5,973,775,000,000 6,013,631,000,000 4,899,168,000,000 2. Nje 1,903,343,000,000 2,359,320,000,000 2,963,410,000,000 3. Jumla 7,817,118,000,000 8,372,951,000,000 7,862,578,000,000

 

Page 165: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

165

mtandao wa uhakika hivyo unaathiri pia mifumo mingine yamalipo hasa katika ngazi za chini za Halmashauri. Hivyo,Serikali itafute namna ya kuondokana na changamoto hii ilimfumo uweze kufanya kazi kwa ufanisi Zaidi.

2.1.7. Fungu 50 -Wizara ya Fedha na Mipango

Mheshimiwa Spika, Fungu 50 – Wizara ya Fedha na Mipangokatika mwaka wa fedha 2018/19 liliidhinishiwa jumla ya shilingi85,813,744,000 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na miradi yamaendeleo. Hadi kufikia mwezi Aprilii, 2019 Wizara ilikuaimepokea jumla ya shilingi 31,153,153,129 sawa na asilimia36.3 ya bajeti iliyoidhinishwa. Kati ya fedha hizo shilingi20,393,917,182 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo, shilingi5,479,287, 356 kwa ajili ya mishahara na shilingi 3,301,205,402kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa Idara na Taasisi zilizochini ya fungu hili.

Mheshimiwa Spika, ili Wizara iweze kutekeleza majukumu yakekwa ufanisi kuna umuhimu wa Serikali kuhakikisha kuwa Wizarahii inapelekewa fedha zake kama zilivyoidhinishwa na Bunge.Kushindwa kufikiwa kwa malengo ya Wizara kutapelekeakushindwa kufikiwa kwa malengo ya nchi hasa kwa upandewa ukuaji wa uchumi.

2.1.8. Fungu 45 - Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu zaSerikali

Mheshimiwa Spika, Kamati ya Bajeti ilikutana na Waziri waFedha na Mipango pamoja na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuuwa Hesabu za Serikali ili kufanya mashauriano kuhusuMakadirio ya Mapato na Matumizi ya Fungu hili.

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu zaSerikali ni taasisi yenye jukumu la kufanya ukaguzi wa mapatona matumizi ya Serikali, kama yalivyoidhinishwa na Bunge.Kwa mujibu wa Hati ya Majukumu ya mwaka 2018, Ofisiimepewa majukumu yafuatayo:

Page 166: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

166

i. Kukagua hesabu za Wizara, Mikoa, Halmshauri za Wilaya,Miji, Manispaa na Majiji, Ofisi za Balozi za Tanzania zilizoko njeya nchi, Wakala za Serikali, Mashirika ya Umma, pamoja naMiradi ya Maendeleo inayogharamiwa na wafadhili na kutoataarifa ya ukaguzi huo Bungeni juu ya mapato na matumiziya fedha za Umma;

ii. Kujenga, kukuza na kuimarisha utamaduni wa uwajibikajikatika Wizara na Taasisi za Serikali, Mikoa na Halmshauri;

iii. Kuhakikisha kwamba, inajiridhisha kuwa upo uwajibikaji wakutosha katika kusimamia na kudhibiti ipasayo ukusanyaji wamapato na matumizi ya Serikali; na

iv. Kuhakikisha kuwa jamii ya Tanzania inapata faida au tijakutokana na matumizi bora ya fedha za Umma, na mali zaUmma zinahifadhiwa, kutunzwa na kulindwa ipasavyo.

Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2018/19 Ofisi yaTaifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali iliidhinishiwa jumla yakiasi cha Shilingi 62,878,658,000 kutoka Mfuko Mkuukwa ajiliya matumizi ya kawaida na maendeleo.Kati ya fedha hizomishahara ni Shilingi 16,647,699,000 matumizi mengineyo (OC)Shilingi 32,518,867,000 na Shilingi 13,712,092,000 zilitengwakwaajili ya miradi ya maendeleo ambapo fedha za ndani zilikuwashilingi 7,200,000,000 na shilingi 6,512,092,000 ni fedha za nje.Kwa upande wa maduhuli, Ofisi ilikadiriwa kukusanya kiasicha shilingi 6,227,650,000. Maduhuli ya Ofisi hii yanatokananamarejesho ya gharama za ukaguzi (reimbursable costs) waMashirika ya Umma, ukaguzi wa Miradi ya Maendeleoinayosimamiwa na Wizara chini ya Divisheni ya Serikali Kuupamoja na ile ya miradi chini ya Divisheni ya Hesabu za Taifa.

Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza Bajeti hiyohadi kufikiamwezi Aprilii, 2019 Ofisi ilikuwa imepokea jumla ya kiasi chashilingi 44,077,267,615 kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali. Kiasihicho ni sawa na asilimia 54.05. Kati ya kiasi hicho, shilingi16,647,699,000 ni kwa ajili ya mishahara, Shilingi 30,789,493,681ni kwa Matumizi ya kawaida na shilingi shilingi 2,340,930,884ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Page 167: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

167

Mheshimiwa Spika, kiasi hicho cha bajeti kilichotolewakimeiwezesha Ofisi kutekeleza shughuli mbalimbali zilizokuwazimepangwa kulingana na fedha zilizopokelewa kutokaMfuko Mkuu wa Serikali na makusanyo ya ndani. Aidha,mwenendo wa utolewaji wa fedha kutoka Mfuko Mkuu kwaOfisi kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo umebakikuwa wa changamoto ambapo hadi kufikia mwezi Machi,2019 kiasi kilichokuwa kimepokelewa ni asilimia 54 tu ya lengola mwaka.

Mheshimiwa Spika, Kamati ilifanya tathmini ya mwenendowa sura ya bajeti ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi za Hesabu zaSerikali iliyokuwa inatengewa na Serikali kwa kipindi chamiaka 3 kuanzia 2017/18 hadi 2019/20 na ilibaini kuwa bajetiya Ofisi imekuwa ikishuka mwaka hadi mwaka na hivyokuifanya Ofisi kutofikia malengo yake ya kiukaguzi inayokuwaimejiwekea na hatimaye kushindwa kuendana na viwangovya kimataifa vilivyowekwa kwa uhuru wa Ofisi ya Mdhibitina Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Kutolewa kwakiwango cha chini cha bajeti kwa Ofisi hii kumepelekea Ofisihii kushindwa kufanya ukaguzi katika maeneo mengi zaidiyaliyokuwa na umuhimu wa kufanyiwa ukaguzi.

Mheshimiwa Spika, ufinyu huo wa bajeti umeisababisha Ofisikushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo. Baadhi yashughuli zilizoshindwa kutekelezwa ni zifuatazo: -

i. Ofisi imeshindwa kupanua mawanda ya ukaguzi kufikiamaeneo ambayo Ofisi inaona yana viashiria vya mwenendowenye shaka katika mapato na matumizi ya fedha za Serikali;

ii. Ofisi imeshindwa kufanya uhakiki wa kina hasa utekelezajiwa mapendekezo yanayotolewa kwa Halmsahuri kupitiataarifa za Mdhibiti na Mkaguzi yanayotolewa kwaHalmashauri kupitia taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu waHesabu za Serikali. Fedha nyingi za Umma zinaelekezwa katikaHalmshauri, ni muhimu Ofisi ya CAG ikawezeshwa ili kufanyaufuatiliaji wa karibu wa utekelezaji wa mapemdekezoyanayotolewa kwa Halmshauri husika;

Page 168: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

168

iii. Ofisi imeshindwa kukamilisha ujenzi wa majengo ya Ofisikatika mikoa iliyolengwa kutokana na kutopata fedha zamaendelo kama zinavyoidhinishwa;

iv. Ofisi imeshindwa kuendana na viwango vya kimataifavilivyowekwa kwa uhuru wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuuwa Hesabu za Serikalu (ISSAI 10); na

v. Ofisi imeshindwa kuwajengea uwezo wakaguzi kwa mujibuwa viwango vya kimataifa vya ukaguzi na katika maeneomapya ya kipaumbele ya kikaguzi.

3.0 MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YAFEDHA NA MIPANGO PAMOJA NA OFISI YA TAIFA YAUKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI KWA MWAKA WA FEDHA2019/20.

3.1 Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mafungu 7 yaWizara ya Fedha na Mipango kwa Mwaka wa Fedha2019/20.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2019/20imekadiriwa kutumia jumla ya Shilingi 11,286,170,133,820 kwamafungu yote Saba (7). Kati ya fedha hizo, Shilingi10,604,033,118,820 ni kwa ajili ya Matumizi mengineyo (OC)na kwa ajili ya kulipia Deni la Serikali na huduma nyingine,shilingi 608,371,517,988 ajili ya mishahara na Shilingi730,581,941,731 ni kwa ajil i ya kutekeleza Miradi yaMaendeleo inayotarajiwa kutekelezwa na Wizara katikakipindi husika.

3.2 Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Taifaya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali (NAOT)kwa Mwakawa Fedha 2019/20.

Mheshimiwa Spika, Kamati ya Bajeti ilikutana na Waziri waFedha na Mipango pamoja na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuuwa Hesabu za Serikali ili kujadiliana na kufanya mashaurianokuhusu nyongeza ya Shilingi bilioni 3, 5000,000,000 iliyokuwaikiombwa baada ya kupewa ukomo wa Bajeti. Fedha hizo

Page 169: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

169

zinazohitajika kwa ajili ya kaguzi maalum nje ya zilezinazopangwa na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi ambapo maombihupokelewa kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali, kaguzimaalum kwa Halmshauri zilizopata hati chafu pamoja nakaguzi za mamlaka 13 za maji ambazo hazina uwezo wakugharamia kaguzi zake. Kukosekana kwa nyongeza hiyo yafedha kutaathiri utendaji kazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzikatika mwaka wa fedha 2019/20. Baada ya majadilianoSerikali iliridhia kuongeza fedha hizo kwa ofisi ya NAOT pindimahitaji hayo yatakapojitokeza.

Mheshimiwa Spika, Ofisi kwa mwaka wa fedha 2019/20imelenga kuimarisha ukaguzi wa mapato na matumizi yaSerikali kuimarisha uwajibikaji na uwazi kwenye matumizi yarasilimali za umma ambapo ilipanga kutumia shilingi64,917,248,417 kulingana na vipaumbele na kazi za Ofisizilizolengwa kutekelezwa. Aidha, kwa mujibu wa ukomouliotolewa na Wizara ya Fedha na Mipango, Fungu 45limetengewa jumla ya shilingi 61,376,878,000. Kati ya fedhahizo, shilingi 14,084,139,000 ni kwa ajili ya mishahara yawatumishi, shilingi 34,305,459,417 ni fedha kutoka Mfuko Mkuuwa Serikali, shilingi 6,227,650,000 ni fedha kutoka ukaguzi waWakala/Taasisi na Mashirika ya Umma na shilingi 6,300,000,000ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo ambazo shilingi5,000,000,000 ni fedha za ndani na shilingi 1,300,000,000nifedha za nje.

Mheshimiwa Spika, Kamati bado inasisitiza umuhimu wakuhakikisha Fungu 45 linapatiwa rasilimali fedha za kutoshazinazoendana na vipaumbele, kazi na mahitaji halisi ya Ofisiili iweze kutekeleza majukumu yake ya kikatiba. Aidha, nimaoni ya Kamati kuwa maombi yote ya kaguzi kutoka taasisina wizara za Serikali zipitie kwanza Hazina ili kuwezeshaupatikanaji wa fedha kwa ajili ya kufanya kaguzi hizo na siomaombi hayo kupelekwa moja kwa moja kwa Mkaguzi Mkuu.

Page 170: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

170

Jedwali Namba 4. Maombi ya Fedha Kwa Wizara ya Fedhana Mipango na Mafungu yaliyo Chini Wizara Pamoja na Ofisiya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka 2019/20.

4.0 MAONI NA MAPENDEKEZO YA KAMATI YA BUNGE YABAJETI

Mheshimiwa Spika, baada ya Kamati kupitia utekelezaji waBajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Ofisi yaTaifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha2018/19 pamoja na mapato na matumizi ya mafungu husikakwa mwaka wa fedha 2019/20; Kamati inapenda kutoamaoni na mapendekezo yake kama ifuatavyo: -

4.1 Mamlaka ya Waziri wa Fedha katika masuala yoteya Fedha

Mheshimiwa Spika, Kamati inatambua majukumu ya Wizaraya Fedha na Mipango na Taasisi zake katika kusimamia Seraza Fedha na Sera za Kiuhasibu (Monetary and Fiscal Policies)na kuwa ndiye msimamizi mkuu wa masuala yanayohusufedha. Hata hivyo, hivi karibuni kumeibuka utaratibu kwabaadhi ya Wizara na mamlaka ya Mikoa na Wilayakutoheshimu mamlaka haya ya Wizara ya fedha na Mipangona hivyo kutoishirikisha Wizara (Consultation) katika

FUNGU MATUMIZI MENGINEYO (OC)

MISHAHARA MIRADI YA MAENDELEO

JUMLA

07 37,229,786,000 3,281,016,000 2,300,000,000 42,810,802,000 10 1,558,142,000 649,793,000 - 2,207,935,000 13 2,015,586,000 - 200,295,998 2,215,881,998 21 736,280,618,000 536,520,631,988 683,717,888,733 1,956,519,138,721 22 9,721,127,000,000 8,885,708,000 - 9,730,012,708,000 23 37,036,734,000 7,029,314,000 3,300,000,000 47,366,048,000 50 27,792,514,000 37,920,916,000 34,763,757,000 100,477,187,000

JUMLA 10,563,040,380,000 594,287,378,988 724,281,941,731 11,881,609,700,717

45 40,992,739,000 14,084,139,000 6,300,000,000 61,376,878,000 JUMLA KUU 10,604,033,119,000 608,371,517,988 730,581,941,731 11,942,986,578,719

Page 171: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

171

uanzishwaji/uwekaji wa tozo, ushuru na ada katika sekta zao.Jambo hili limepelekea baadhi ya tozo, ada na ushuruunaoanzishwa kuwa kero kwa wananchi nawafanyabiashara.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Wizara ya Fedha na Mipangondiyo yenye Instrument ya kusimamia masuala yote ya fedhana taratibu zake ni vema kukafanyika harmonization yaSheriazote ili kuzitaka Wizara na mamlaka nyingine zotekulazimika kukubaliana na Wizara ya Fedha na Mipangokabla ya kuanzisha tozo, ada au ushuruwa aina yoyote.

4.2 Utaratibu wa Kubakiza kiasi cha mapato (Retention)

Mheshimiwa Spika, wakati wa mapitio wa bajeti ya Fungu 50- Wizara ya Fedha na Mipango, Kamati ilibaini kuwa kunabaadhi ya taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha na mipangoambazo zinapokea mishahara kutoka Serikali kuu badozinatumia utaratibu wa retention. Taasisi hizo ni pamoja naTaasisi za Mafunzo IFM, IAA, TIA; Bodi ya Taifa ya Wahasibuna Wakaguzi (NBAA), Wakala wa Ununuzi wa Serikali (GPSA)na PSPTB.

Mheshimiwa Spika, Taasisi hizo zinatumia mapato yao yandani kama matumizi mengineyo (OC) ndio maana hakunafedha zozote za OC ambazo Taasisi hizi zinapokea kutokaSerikali Kuu. Ni ushauri wa Kamati kuwa kwa kuwa mapatoya Chuo yatokanayo na ada, ni muhimu Serikali ikawekautaratibu wa kuyatambua mapato hayaili kudhibiti matumiziyasiyo ya lazima.

4.3 Usimamizi na utekelezaji wa Sheria ya Bajeti .

Mheshimiwa Spika, moja ya lengo la kuanzisha sheria ya Bajetiilikuwa ni kuwa na Sheria ya mahsusi ya kuongoza mchakatomzima wa bajeti ya Serikali pamoja na kubainisha vemamipaka ya kiutendaji na kimajukumu kati ya Serikali na Bungekwa kuweka bayana kazi na majukumu ya Serikali na Bunge(pamoja na Kamati zake) katika mchakato wa Bajeti yaSerikali

Page 172: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

172

Mheshimiwa Spika, Pamoja na uwepo wa Sheria hii na Sherianyingine za fedha, bado kuna viashiria vidogovinavyoonyesha Wizara ya Fedha na Mipango kutozingatiaSheria ya Bajeti katika upangaji na utekelezaji wa Bajeti zamafungu mbalimbali. Mathalani, wakati wa mjadala huu waBunge la Bajeti, Serikali kupitia Wizara na Fedha na Mipangoilihamisha kiasi cha takribani shilingi Bilioni 152 kutoka katikafungu 21 (HAZINA) kwenda TAMISEMI-56 (Bilioni 33), Ujenzi-98(Bilioni 90) na Elimu – 46 (Bilioni 29) pasipo kushauriana naKamati ya Bajeti, licha ya kuwa hapo awali Kamati ya Bajetiilikwishapitisha Bajeti ya mafungu yote ya Wizara ya Fedhana Mipango kwa kuzingatia ukomo wa bajeti ambaoumekuwa ukisisitizwa na Wizara ya Fedha na Mipango kwamafungu yote. Kamati inashauri Wizara ya Fedha na Mipangokuhakikisha inasimamia na Sheria ya Bajeti katika kupangana kutekeleza Bajeti ya Serikali kwa mafungu yote.

4.4 Uhakiki na Ulipaji wa Madeni ya Watumishi,Wakandarasi na Wazabuni.

Mheshimiwa Spika,Kamati inaipongeza Serikali kwa jitihadaza kendelea kuhakiki na kulipa madeni ya wafanyakazi,wazabuni na watoa huduma.Hata hivyo, suala hili limekuwala muda mrefu na madeni mapya yanaendelea kuzalishwa.Kati ya mwaka 2016/17 hadi Machi 2019 jumla ya shilingi2,299,836,402,880.07 zilikuwa zimetolewa kwa ajili ya kulipamadeni mbalimbali ya watumishi, wazabuni, wakandarasi/wahandisi washauri, watoa huduma na madeni mengineyo.Kuhusu madeni yaliyokataliwa kwa hesabu zilizoishia tarehe30 Juni 2018 ni jumla ya shilingi 407,009,218,378.55, Dola zaMarekani 29,650,115.78, Euro 162,009, Paundi za Uingereza7,477, Randi za Afrika Kusini 1,122,852 na Korona za Uswis95,986. Madeni hayo yalikataliwa kwa sababu mbalimbaliikiwa ni pamoja na kukosekana kwa nyaraka zinazostahili.

Mheshimiwa Spika, ni rai ya Kamati kuwa Serikali inahakikishainaendelea na ulipaji wa madeni yote yaliyohakikiwa ilikupunguza gharama kwa Serikali hasa kwa madeni yenyeongezeko la riba lakini pia gharama kwa watoa hudumawaliokopa kwenye mabenki kupata mtaji ili waweze kutoa

Page 173: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

173

huduma kwa Serikali. Aidha, kwa madai yaliyokataliwa Serikaliihakikishe inawapa taarifa wadai kuhusu mapungufu katikamadai yao na hivyo kuwataka wayawasilishe tena yakiwayamekamilika ili endapo yatastahili kulipwa malipo yawezekufanyika. Mwisho, muda unaotumika kuhakiki madeniumekuwa mrefu hivyo Serikali ihakikishe kuwa mchakato wauhakiki unafanyika ndani ya muda ili kuwezesha ulipaji wamdeni hayo kwa wakati.

4.5 Fungu 13 – Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu

Mheshimiwa Spika, Kitengo hiki kina jukumu muhimu lakupokea na kuchambua taarifa za miamala shuku toka kwawatoa taarifa na kupeleka intelligensia kwenye vyombo vyautekelezaji wa Sheria kwa uchunguzi. Pamoja na kwambakitengo hicho kimeongezewa majukumu lakini Bajeti yakitengo hicho ni sawa na ile ya mwaka wa fedha wa 2018/19. Katika mwaka wa fedha 2019/20 kitengo kimeidhinishiwakutumia jumla ya kiasi cha shilingi 2,015,586,000 kwa ajili yamatumizi ya kawaida ikiwa sawa na bajeti ya mwaka 2018/19. Kutokana na umuhimu wa chombo hiki, Serikali ikiangaliechombo hiki kwa jicho la kipekee, ihakikishe kuwa kitengohiki kinatengewa rasilimali fedha za kutosha ili kitekelezemajukumu yake kikamilifu.

4.6 Sheria ya Udhibiti wa Fedha Haramu Sura ya 423 “TheAnti Money Laundring Act Cap 423)

Mheshimiwa Spika, Kamati inaishauri Serikali iangalie upyasheria Udhibiti wa Fedha Haramu (The Anti Money LaunderingAct cap 423) na majukumu yake yaangaliwe upya ili iendanena hali halisi ya sasa ili kiweze kufanya zaidi ya kaziiliyokusudiwa. Maboresho hayo yajikite katika maeneoyanayohusu dhamana na kiwango cha fedha ambacho myanaruhusiwa kubeba (cash) hasa kwa wafanyabiashara wamadini baada ya kuanzisha masoko ya madini nchini. Sheriaya Anti-Money Laundering ya mwaka 2006 imetaja kiwangocha juu cha fedha ambacho mtu anaweza kukibeba kamafedha taslimu “cash” kuwa ni shilingi 10,000,000tu. Kiwangohiki kwa biashara ya dhahabu ni kidogo sana, hivyo Sheria

Page 174: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

174

iweke utaratibu ambao utawezesha biashara hii kufanyikabila ya kuwa na vikwazo vyovyote.

4.7 Uanzishwaji wa Akaunti ya Pamoja ya FedhaMheshimiwa Spika, Ibara ya 133 ya Katiba ya Jamhuri yaMuungano ya Tanzania inatamka kuwa kutaanzishwa Akauntiya Fedha ya Pamoja kwa madhumuni ya shughuli za Jamhuriya Muungano kwa Mambo ya Muungano ambamokutawekwa fedha yote itakayochangwa na Serikali mbili kwakiasi kitakachoamuliwa na Tume ya Fedha ya Pamoja kwamujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge. Aidha, pamoja naTume hii kuanzishwa mwaka 2003 hadi hivi sasa akaunti hiibado haijafunguliwa.

Mheshimiwa Spika, wakati wa kupitia bajeti ya Fungu hiliKamati ilijulishwa kuwa suala hili linafanyiwa kazi na Serikaliambapo taarifa ya mapendekezo ya mwongozo wauendeshaji na usimamizi wa Akaunti ya Fedha ya Pamoja(AFP) imewasilishwa Serikalini kwa ajili ya kufanyiwa maamuzi.Hivyo basi, Kamati inashauri Serikali kuharakisha mchakatowa kuandaa Mwongozo kwani suala hili ni la muda mrefu.Uwepo wa akaunti hiyo sio tu utapelekea Tume kufanya kaziil iyokusudiwa lakini pia itasaidia kupunguza kero nachangamoto za Muungano.

4.8 Uunganishwaji wa Taasisi za Mafunzo zilizo chini yaWizara mbalimbali

Mheshimiwa Spika, Taasisi za mafunzo hasa zile zilizochini yaWizara mbalimbali mathalani IAA, IFM, Chuo cha Madini,Chuo za Hombolo n.k. zimekuwa zikiongezeka kwa kasi nchini.Pamoja na nia nzuri za uanzishwaji wa Taasisi hizi ambazozililenga kutoa mafunzo ya kinadharia katika taaluma zaWizara husika taaisi hizi sasa zinatoa hadi shahada. Hivyobasi, imefika wakati sasa wa Serikali ifanye mapitio ya Sheriazilizoanzisha Taasisi ili kuendana na dhima ya uanzishwaji wataasisi hizo.

Mheshimiwa Spika, kwa hali i l ivyo sasa gharama yauendeshaji wa vyuo hivi imekuwa kubwa na vimekuwa

Page 175: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

175

vikipata ruzuku kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali kwa ajili yakugharamia mishahara ya Taasisi hizo. Kamati inashauri Serikalikuangalia uwezekano wa kuziunganisha taasisi hizi zamafunzo ili baadhi ziwe makao makuu (Kampasi Kuu) nanyingine kuwa kampasi ndogo. Ama kuziacha Taasisi hizizijiendeshe kama vyuo vikuu ili kupunguza mzigo wa kibajetikwa Serikali.

4.9 Utitiri wa Mifumo ya Malipo

Mheshmiwa Spika, kumekuwa na mifumo mingi sana ambayoinasimamiwa na Wizara mfano TANePS, IFMS, GePG, GSSP,GAMIS, GARI-ITS, IDEA, PMS-Poverty Management System naCBMS. Mifumo yote hii inasimamiwa na Wizara moja nauendeshaji wake ni wa gharama kubwa. Mathalani kwamwaka wa fedha 2019/20 mifumo hii inakadiriwa kutumiatakribani jumla ya shilingi 3,000,000,000 kila mwaka. Ni maoniya Kamati kuwa Serikali ije na namna bora ya kuunganishamifumo hii hasa ile ambayo Inafanya kazi moja.

Mheshimiwa Spika, Kamati pia ilibaini kuwa asilimia kubwaya mifumo hiyo ni ya nje (kununua) na hivyo kuongezagharama za kiuendeshaji ikiwa ni pamoja na ada za leseni,hosting na subscription fees.

Mheshimiwa Spika, Pamoja na changamoto zilizotajwa hapojuu, Kamati inaipongeza Serikali kwa jitihada zake ilizoanzakatika kuhakikisha kuwa inakuja na mifumo yake yenyeweambapo hadi sasa imeweza kutengeza mifumo yake kadhaaikiwa ni pamoja na mfumo wa PMIS, TANePS,GePG, EFD naGAMIS. Hivyo basi, Serikali iharakishe mchakato wa kujengamifumo yake na kuondokana na mifumo mengine kutokakwa Makampuni au watu binafsi.

4.10 Utekelezaji wa Akaunti Jumuifu ya Fedha (TSA)

Mheshimiwa Spika, pamoja na dhamira nzuri ya Serikali yakuhuisha akaunti zote za Serikali na kuanzisha Akaunti Jumuifuil i kudhibiti matumizi, mfumo huu umekumbwa nachangamoto mbalimbali za kiutendaji. Mfumo huu kwa kiasi

Page 176: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

176

kikubwa unategemea ubora wa mifumo ya mawasiliano nakwa hali ilivyosasa hasa katika ngazi za Halmashaurikumekuwa na changamoto kubwa sana. Tatizo hili lakimtandao limepelekea ucheleweshawaji wa malipokutokana na kuwa taarifa za malipo hazifiki Benki Kuu kwawakati.

Mheshimiwa Spika, changamoto nyingineinayopelekeaufanisi wa mfumo huu kupungua ni mlundikano wa “server”katika kituo kimoja. Server zote za malipo zimehifadhia katikaofisi za TAMISEMI makao makuu Dodoma na hivyo kupelekeakituo hiki kuelemewa au kushindwa kufanya kazi iwapokutatokea hitilafu ya umeme au kimtandao. Ili kuondokanana adha hii na mfumo uweze kufanya kazi kwa ufanisi nakwa matarajio yaliyokusudiwa ni vema Serikali ikatatua tatizohili la kimtandao na kulipatia ufumbuzi wa kudumu ikiwa nipamoja na kuzitaka taasisi, idara na wizara zotekuonganishwa katika mkongo wa Taifa. Aidha, Serikali ioneumuhimu wa wa kuanzisha kituo cha server kwenye kilakanda ambapo kuna ofisi za Benki Kuu kwa lengo lakupunguza mzigo uliopo Ofisi ya Rais – TAMISEMI kuongezaufanisi.

4.11 Fedha kwa ajili ya Ujenzi wa Maboma

Mheshimiwa Spika, katika kuunga mkono juhudi za wananchiza ujenzi wa miundombinu ya mandeleo, Kamati ilikubalianana Serikali kuhusu suala la kumalizia maboma na ikatengakiasi cha shilingi bilioni 271.33. Aidha Serikali ilikubali kupelekafedha hizo katika Halmashauri kwa awamu, ambapo hadimwezi Januari ilipeleka kiasi cha shilingi bilioni 29.9 kwa ajiliya miradi ya elimu na shilingi bilioni 38.9 kwa miradi ya afya.Shilingi 54.75 zilitolewa kupitia mradi wa Lipa Kulingana naMatokeo kwa ajili ya kumalizia miradi ya elimu. Aidha, miradiya afya imeendelea kutengewa fedha kwa kuzingatiatathmini ya mahitaji ambapo jumla ya shilingi bilioni 100.5zilmetolewa kwa mwaka 2018/19. Kamati inaendeleakusisitiza upelekaji wa fedha zilizobaki katika mwaka wa fedha2019/20 kwa ajili ya kuendelea na ukamilishaji wa maboma144 ya miradi ya afya na elimu.

Page 177: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

177

4.12 Taasisi zinazosimamia manunuzi ya Umma

Mheshimiwa Spika,Kamati ilipata fursa ya kupitia bajetipamoja na utendaji wa mashirka yaliyo chini ya Wizara hii.Kati ya mashirika ilikutana nayo ni pamoja na taasisizinazohusiana na masuala ya ununuzi wa umma zikiwemoGPSA – Wakala wa Hudma ya Ununuzi Serikalini, PPRA –Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma, PSPTB – Bodi yaWataalam wa Ununuzi na Ugavi Tanzania na PPAA – Mamlakaya Rufaa ya Zabuni za Umma.

Mheshimiwa Spika, uchambuzi wa Kamati ulibaini kuwepona mwingiliano wa majukumu baina ya hizi taasisi kwanibaadhi ya taasisi hizi zinafanya kazi zinazofanana. HivyoKamati inashauri kuwa kuwepo nakutafsiri majukumu kwauwazi baina ya taasisi hizi. Taasisi zihakikishe kuwa zinatekelezamajukumu yake kama yalivyoanishwa kwenye Sheriailizozianzisha. Aidha, Kamati ilibaini kuwepo na changamotoya wataalam wa ununuzi waliosajiliwa na bodi ya PSPTBkwenye taasisi na mashirika ya Serikali na hivyo kwendakinyume na Sheria suala ambalo ni lazima Serikali ilifanyie kazikwa haraka.

4.13 Usiamamizi wa Maduka ya Ubadilishaji Fedha (bureaude change)

Mheshimiwa Spika, Kamati inaipongeza Serikali kwa jitihadazake katika kusimamia biashara ya ubadilishaji wa fedhanchini. Hatua hii itaendelea kuimarisha ulinzi na usalama nakukabiliana na mianya yote ya ubadilishaji wa fedha haramu.Hata hivyo, endapo Serikali haitaimarisha mifumo yake itatoamianya ya kuwepo kwa maduka ya ubadilishaji fedha yasiyorasmi “black market”.

Mheshimiwa Spika, Ni vema Serikali ikaangalia viwango vyaubadilishaji fedha vinavyotolewa na mabenki kwani ni vyajuu ukilinganisha na vile vinavyotumika na maduka yaubadilishaji fedha. Hivyo basi, Serikali iangalie ni kwa namnagani itaweza kudhibiti viwango vya fedha vinavyotolewa namabenki, viwango ambavyo vilitegemea kuwa vya chini

Page 178: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

178

vikilinganishwa na vya bureau de change ikizingatiwa kuwamabenki yanafanya shughuli nyingine Zaidi ya kubadilishafedha za kigeni.

4.14 Sheria ya Sekta Ndogo ya Fedha ya 2018 (TheMicrofinance Act 2018).

Mheshimiwa Spika, Novemba 2018, Serikali ilileta Muswadawa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha (The MicrofinanceAct 2018) uliokuwa na madhumuni ya kuwezesha usimamizina udhibiti wa huduma ndogo za kifedha na Bunge lakotukufu lilipitisha Muswada huo na kuwa Sheria. Pamoja nania njema ya Serikali ya kusimamia na kudhibiti Sekta ndogoya fedha nchini ikiwa ni pamoja na kuwatambua wananchina wafanya biashara nchini walioko katika sekta hiyokumekuwa na malalamiko kutoka kwa wadauwanaoitekeleza Sheria hii.

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa Sheria hii umekuwa mgumukutokana na masharti yaliyowekwa katika Sheriayanayolenga kundi la Tier 4. Masharti hayo ni pamoja namatumizi ya benki katika ukusanyaji na uhifadhi wa fedha zawanakikundi; matumizi ya credit bureau reference pamojana ulazima wa kikundi kuwa na mtaalam wa fedha yaanimhasibu. Masharti hayo yamekuwa vikwanzo kwa Tier 4 nahivyo kushindwa kutekeleza sheria.

4.15 Ugharamiaji wa Miradi ya Maendeleo

Mheshimiwa Spika, Sheria ya Misaada, Mikopo na Dhamanainaipa mamlaka Wizara ya Fedha na Mipango kuchambuana kuishauri Serikali kuhusu fedha za ugharamiaji wa miradimbalimbali ya maendeleo. Kwa msingi huo, Kamati inashauriSerikali badala ya kutumia fedha za ndani katika ujenzi wamiradi ya maendeleo ambayo ina muelekeo wa kibiasharaione umuhimu wa kutafuta fedha nje kupitia mikopo yenyemasharti nafuu au kutekeleza miradi hiyo kwa kwa njia yaubia. Hatua hii itasaidia fedha za ndani kuelekezwa kwenyemiradi ya kijamii.

Page 179: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

179

4.16 Mwenendo wa Utolewaji wa Fedha za Bajeti kwaMafungu ya Wizara

Mheshimiwa Spika, Kamati inaisistizia Wizara kuhakikisha kuwafedha za bajeti kwa ajili ya mafungu yake zinatolewa kamazilivyoidhinishwa na Bunge. Kamati inashauri kuwa wakati wauandaaji wa bajeti hasa bajeti ya maendeleo Wizara isitengekiasi kikubwa cha fedha kwa kutegemea fedha za wafadhilikutoka nje,kwani mwenendo wa upokeaji fedha zamaendeleo za nje sio wa kuridhisha na hivyo kukwamishautekelezaji wa bajeti na shughuli za Wizara.

4.17 Ukusanyaji wa Mapato ya Kodi na yasio ya Kodi

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha miaka mitatu,Mamlakaya mapato Tanzania imekuwa ikikusanya kwa wastani katiya shilingi 1,2000,000,000,000 hadi 1,300,000,000,000kwamwezi. Hatua hii ni ya kupongeza kwasababu kabla ya hapoMamlaka ilikuwa ikikusanya wastani wa bilioni 800,000,000,000hadi shilingi 900,000,000,000 kwa mwezi.

Mheshimiwa Spika, pamoja na pongezi hizo, Kamati inaishauriSerikali na Mamlaka ya Mapato Tanzania mambo yafuatayo;kwanza kupanua wigo wa kodi na pili ni kuhakikisha kwambaMaofisa wa TRA pindi wanapokuwa wanatekelezejamajukumu yao kuzingatia sheria, taratibu na kanuni.

4.18 Mapungufu ya usimamizi wa Sera za Kibajeti naKifedha (Fiscal and Monetary Policies

Mheshimiwa Spika, Kamati inatambua jukumu laWizara ya Fedha na Mipango pamoja na taasisi zakekatika kusimamia Sera za Kibajeti na Fedha (Fiscal andMonetary Policies) ili kuleta uchumi tulivu na hivyo kusaidiaukuaji wa uchumi (economic growth) unaoendana namaendeleo ya uchumi (economic development). A i d h a ,pamoja na makujukumu haya, Wizara ya Fedha na taasisizake zimekuwa zikichukua baadhi ya hatua za kisheria,kikanuni pamoja na za kiutawala (administrative measures)katika kusimamia shughuli za kiuchumi. Hata hivyo,

Page 180: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

180

mapungufu katika utekelezaji wa baadhi ya hatua hizoumekuwa ukiathiri uendeshaji wa shughuli za kibiashara nahivyo kudhoofisha kasi ya uwekezaji katika sekta mbalimbali,mathalani utozaji wa 15% ya amana kwa waagizaji wa sukariya viwandani, usitishwaji wa kutoa huduma ya kubadilishiafedha kwa baadhi ya maduka, na kuchelewa kurudishwakwa rejesho la Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT refunds).Kamati inaishauri Wizara ya Fedha na Mipango pamoja nataasisi zake kuhakikisha inazingatia sheria, kanuni na taratibuilizojiwekea katika kusimamia sera za kibajeti na fedha katikakuhakikisha zinasaidia kuweka mazingira wezeshi ya ufanyajibiashara nchini pamoja na uwekezaji na hivyo kusaidia ukuajiwa uchumi.

5.0 HITIMISHO

Mheshimiwa Spika, naomba nihitimishe kwa kukushukuruwewe Mhe. Spika, Dkt. Tulia Akson, Mb - Naibu Spika naWenyeviti wa Bunge kwa miongozo yenu ambayo mmekuwamkitupatia. Shukrani pia ziwaendee Mhe. Dkt Philip Mpango(Mb) Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt Ashatu K. Kijaji(Mb), Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Katibu Mkuu naNaibu Makatibu Wakuu pamoja na wataalamu wote waWizara ya Fedha na Mipango kwa ushirikiano wao mkubwawaliotupa wakati wote wa kujadili utekelezaji wa majukumuya Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Makadirio yamapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2019/2020. Aidha,Kamati inatoa shukrani kwa Wakuu wa Taasisi na Idara zotezilizo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa ushirikianona ufafanuzi walioutoa kwa Kamati katika kipindi chote chautekelezaji wa majukumu yake.

Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee kabisanapendakumshukuru Mheshimiwa Mashimba Mashauri Ndaki, Mbungewa Maswa MagharibiMakamu Mwenyekiti wa Kamatipamoja na Wajumbe wote wa Kamati kwa umahiri, umakinina ushirikiano wao walionipatia wakati wote wa kuchambuabajeti ya Wizara hii na hatimaye kukamilika kwa taarifa hii.Aidha, naomba niwatambue Wajumbe wa Kamati kwamajina yao kama ifuatavyo: -

Page 181: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

181

1. Mhe.George Boniface Simbachawene, Mb – Mwenyekiti2. Mhe.Mashimba Mashauri Ndaki, Mb - Makamu Mwenyekiti3. Mhe. Balozi Adadi Mohamed Rajabu, Mb4. Mhe. Ali Hassan Omar, Mb5. Mhe. Abdallah Majura Bulembo, Mb6. Mhe. Prof. Anna Kajumulo Tibaijuka, Mb7. Mhe. Albert Obama Ntabaliba, Mb8. Mhe. Dkt. Dalaly Peter Kafumu, Mb9. Mhe. David Ernest Silinde, Mb10. Mhe. Freeman Aikael Mbowe, Mb11. Mhe. Hasna Sudi Katunda Mwilima, Mb12. Mhe. Dkt. Immaculate Sware Semesi, Mb13. Mhe.Dkt. Balozi Diodorus Buberwa Kamala, Mb14. Mhe. Makame Kassim Makame, Mb15. Mhe. Maria Ndilla Kangoye, Mb16. Mhe. Martha Jachi Umbulla, Mb17. Mhe. Mendrad Lutengano Kigola, Mb18. Mhe. Marwa Ryoba Chacha, Mb19. Mhe. Mbaraka Kitwana Dau, Mb20. Mhe. Oran Manase Njeza, Mb21. Mhe. Riziki Said Lulida, Mb22. Mhe. Stephen Julius Masele, Mb23. Mhe. Andrew John Chenge, Mb24. Mhe. Hussein M. Bashe, Mb25. Mhe. Shally Josepha Raymond, Mb26. Mhe. Suleiman A. Sadiq, Mb27. Mhe. Jumanne Kishimba, Mb.

Mheshimiwa Spika,mwisho naomba nitoe shukrani zangu zadhati kwa Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigaipamoja na watendaji wote wa Ofisi ya Bunge kwakuiwezesha Kamati kutekeleza majukumu yake ipasavyo.Aidha, kwa namna ya pekee napenda kuishukuru Sekretarietiya Kamati ya Bajeti kwa kuratibu shughuli za Kamati pamojana kutoa ushauri wa kitaalamu na hatimaye kukamilika kwataarifa hii kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo naliomba Bungelako tukufu sasa lijadili na kuidhinisha Makadirio ya Mapatona Matumizi ya Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na

Page 182: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

182

mafungu manane (8) yaliyo chini yake kwa Mwaka wa Fedha2019/2020 kama yalivyowasilishwa na Mheshimiwa Waziri waFedha na Mipango.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha na naunga mkonohoja.

George B. Simbachawene (Mb)MWENYEKITI

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI

03 Juni, 2019

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Mashimba Ndaki -Makamu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti kule ambakohukufika Waheshimiwa wote wana nakala. Niwashauri tuWaheshimiwa mnakuja kusoma taarifa kitu muhimu sanahuwa ni maoni na mapendekezo ya Kamati, hata kama kulembele ukiruka lakini kitu muhimu sana ni maoni namapendekezo ya Kamati ambayo yanalisaidia sana Bungekatika kuona tunaendaje.

Saa saba kamili mchana tukimaliza naombaWajumbe wa Tume tukutane hapa nyuma hapo Speaker’sLounge Wajumbe wa Tume ya Huduma za Bunge kunamambo mawili/matatu ya kufanya kwa pamoja.

Kwa kawaida anayepaswa kufuata ni Msemaji Mkuuwa Kambi Rasmi ya Upinzani lakini kwa bahati mbaya sanaleo haitakuwa hivyo kwa sababu ya makosa ya obvisousambayo wameyafanya wao wenyewe, nafikiri sijui kama ninahaja hata ya kueleza. Nafikiri mkishika kitabu hiki mtaona tujinsi ambavyo hakiwezi kuingia na sijui kwa nini mnawafanyahivyo mnavyofanya, ukiacha habari ya huko ndani mambomnayoyaandika, lugha mnazozitumia ni masikitiko makubwa.Vitabu hivi vinakaa muda mrefu sana, hata miaka 100 nakadhalika mbele, watakuja wajukuu zetu na vitukuu kufanyareferences ni vizuri sana vikaandikwa katika namna ambayoinaandikwa kibinadamu vizuri, huo ni ushauri wa jumla tu

Page 183: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

183

niliousema. Lakini sababu yake ya kwa nini haiwezi kuingiamnaiona kuanzia ukurasa wa kwanza wala huna haja yakwenda hata ukurasa wa pili wala wangapi.

Haiwezekani wewe Bunge limekuweka pembenihalafu wewe huyo unaingiza kazi zako kupitia mlango wanyuma, kupitia Bunge hilo kwa wakati huo. Kwa hiyo, ni jamboambalo haliwezekani.

Basi tutaendelea na uchangiaji baada ya rullingyangu hiyo tunaanza na Mheshimiwa Albert ObamaNtabaliba wachangiaji wa leo si wengi kwa hiyo ambayeatakuwe kwenye chai au wapi nikimuita kama amekosekanainakuwa bahati mbaya. Mheshimiwa Ntabaliba dakika 10,atafuatiwa na Mheshimiwa Dkt. Diodorus Kamala.Mheshimiwa Ntabaliba tafadhali.

MHE. ALBERT O. NTABALIBA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kunipa nafasi hii niweze kuchangia hii Wizara,kwanza kabisa nimpongeze Waziri, Naibu Waziri na MakatibuWakuu na Wakuu wa Vitengo vyote vya ndani ya Wizara hii,kwa kweli wameendelea kutupa ushirikiano ndani ya Kamatiya Bajeti, naomba niwapongeze sana. Lakini niendeleekumpongeza Mheshimiwa Rais kwa kuendelea kuwapamwongozo mzuri katika usimamizi wa fedha ambayo ni jambozuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba kabisa nipongezeKamishna Mkuu wa TRA, kwa taarifa zake za ukusanyaji wamapato hasa ukiangalia kule kwenye jedwali la makusanyoukurasa wa 180 utaona kwamba average yake imekuwa niasilimia 87 ambayo ni nzuri, kwa hiyo nampongeza sana.Lakini niendelee kumpongeza Magavana wote wa Benki Kuukwa kazi nzuri wanayoendelea kutoa miongozi ya fedhakatika nchi hii.

Mheshimiwa Spika, nilitaka tu kumuuliza MheshimiwaWaziri ukiangalia page yake 178 Ofisi ya Msajili wa Hazinaimepewa asilimia 17 ya fedha za OC, sasa nilitaka kujua nikitu gani kinawafanya wakati Wizara zako na Taasisi zako

Page 184: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

184

zilizoko kwako zina asilimia 70, 60 hao wana asilimia 17 nawanasimamia mashirika ya umma. Ni kitu gani wamefanyamakosa au ni shughuli gani hawaifanyi mpaka sasa wasiwezekupata fedha? Hilo nilitaka Mheshimiwa Waziri uweze kutupaufafanuzi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini lingine ni uhakiki, Wizara yaFedha imechukua majukumu ya kuhakiki fedha, sasa witowito kwamba speed ya kuhakiki imekuwa ni ndogo na kamakuna timu za uhakiki basi muweze ku-recruit watu wenginekutoka kwenye Wizara nyingine kwa sababu kwa kweli malipoya wazabuni, wakandarasi yamechelewa sana na halafuhatuna deadline ya kuona ni lini tutaweza kuhakiki. Lakinifeedback kwa wale ambao hawakufanikiwa hakunautaratibu ambao mmeuleza kwenye Kamati ambaounawapa feedback wale ambao madai yao hayakupitaqualification zenu, kwa hiyo kule wanaendelea kubakiwanakijua wanadai kumbe ninyi mmeshayatupa pembeni.

Mheshimiwa Spika, lakini la pili kuna sheria hii ya asilimia15 kama wanazo-deposit hawa wenye viwanda vya sukari,hebu tunaomba maana yake wanakuja kwenye Kamati zetu,wanaonesha mitaji yao imeyumba. Sasa Serikali inahimizaviwanda lakini inachukua fedha zao, lakini haiwarudishii sasaunachohimiza ni nini na unachotaka kufanya ni nini.

Mheshimiwa Spika, ukiangalia Mheshimiwa Wazirikwenye hotuba yako yote ni control, hakuna mahali kwenyeWizara hapa unachosema kwamba nitahamasishawafanyabiashara wafanye hivi, nitahamasisha wakulimawafanye hivi. Sasa ni mambo umejaza mambo ya kodi tuambayo kwa kweli ni vizuri huko mbele style hii nawanaposikia hotuba yako wapate faraja wafanyabiashara,wachimbaji waone faraja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lingine nipongeze BOT kwa hatuayao kwa kupitia Sheria hii ya Bureau De Change sisi tuwapenguvu tuwaombe waendelee walete kanuni na walewanafanya biashara ya Bureau De Change ambao hawanamakosa basi waweze kufunguliwa waweze kwenda vizuri.

Page 185: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

185

Mheshimiwa Spika, lingine ni kuchelewa kwa madaiya wastaafu. Wastaafu wanadai, wastaafu inachukuamwaka mzima bado hajalipwa fedha zake, hebutunakuomba hicho kitengo kinachoshughulikia wastaafu kwasababu ile database ya watu wanaostaafu MheshimiwaWaziri mnayo kila Idara na kila sekta. Kwa hiyo, ni vizuri nayohii iweze kuangaliwa vizuri iweze kwenda haraka.

Mheshimiwa Spika, lakini la mwisho ni mambo yabusiness license. Sasa hivi Watanzania wote hatuwezikuajiriwa, watu wanatafuta namna ya kujiajiri, lakinibureaucracy iliyopo unapotaka leseni mpaka unaambiwauende kwenye TRA ukapate tax clearance; tax clearanceunaipataje na hujaanza biashara?

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ni vizuri huu mfumouliopo hebu tuurahisishe mtu akienda kutafuta leseni sikuhiyohiyo au siku ya pili aweze kuipata, lakini kuliko kuzungukaaende TRA kumbe hajaanza biashara na akifika kule anaanzakukadiriwa biashara, unataka kufanya biashara gani?Unaanza kukadiriwa kodi na huku biashara haujaanza, kwahiyo, ni vizuri sana muweze kuiangalia hiyo, ili tuweze kwendavizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nisiseme mengi. Mengitumeyasema kwenye Kamati yetu ya Bajeti na nisipendekuyarudia kwa sababu tumeyaandika na Wabunge wotewameyaona. Nakushukuru sana. (Makofi)

SPIKA: Nakushukuru sana, asante sana MheshimiwaObama Ntabaliba. Nilishakutaja Mheshimiwa DiodorousKamala na atafuatiwa na Mheshimiwa Zitto Kabwe naMheshimiwa George Simbachawene ajiandae. MheshimiwaDkt. Kamala, dakika 10.

MHE. BALOZI DKT. DIODORUS B. KAMALA: MheshimiwaSpika, ahsante sana. Nashukuru kwa kunipa fursa yakuchangia bajeti hii muhimu iliyo mbele yetu, ni bajeti muhimusana kwa sababu ndio roho ya uchumi wa nchi, inasimamiaroho ya uchumi wa nchi.

Page 186: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

186

Kwanza nianze kwa kusema kwamba naunga mkonohoja, lakini ninayo mambo machache ambayo ningependanishauri, ili Wizara iweze kuyazingatia na Serikali iwezekuyazingatia.

Mheshimiwa Spika, ukiangalia ukurasa wa 10Mheshimiwa Waziri ameeleza vizuri kwamba uchumi wa Taifaau pato la Taifa limekua kwa asilimia saba, ni jambo jema naninampongeza kwa kazi hiyo, lakini alipoanza kubainishasekta ambazo zimekua kwa kasi; sekta ya kwanza ambayoameonesha kwenye kitabu, nitatumia yaliyoandikwa tukwenye kitabu, ya kwanza amesema ni sanaa na burudaniimechangia kwa asilimia 13.7. Nikasema hilo ni jambo jema,sanaa na burudani. Sekta iliyofuata ni ujenzi asilimia 12.9, sektailiyofuata ni uchukuzi na uhifadhi wa mizigo asilimia 11.8 nasekta nyingine aliyoitaja ni habari na mawasiliano asilimia 9.1.

Mheshimiwa Spika, sasa nilipofika hapo nikastukakidogo nikasema sasa kilimo vipi, mbona wala hakitajwihapa? Maana ukiona uchumi sasa sanaa na burudani ndioinachangia kwa kasi, ndio imekua kwa kasi, ni jambo jema,lakini lazima ujiulize kilimo vipi?

Mheshimiwa Spika, sasa kilimo baada ya kuangaliakwenye nyaraka nyingine ni kwamba chenyewe kimekuakwa asilimia 5.3. Sasa kwa nchi yetu hii ambayo wananchiwengi ni wakulima na sehemu kubwa kwa kweli yaWatanzania ni wakulima, ukiona kilimo hakikui vizuri basi ujuehata ukienda kwa wananchi kuwaelezea kwamba uchumiunakua wao watashangaa kwa sababu sio sehemu ya kukuahuko. Ndio maana namuomba Mheshimiwa Waziri akijawakati wa kufafanua atualeze kidogo walao na wakulimawasikie na wao wamekua kwa kiasi gani, walau wawe namatumaini kwamba sasa Serikali kuna mambo inayafanyayatakayosaidia na kilimo na chenyewe kukua. Wasanii naburudani barabara, lakini huenda ni kwa sababu tu sikwamba wasanii wamefanya mambo mengi ila kwa sababusekta zilizo muhimu hazijakua kwa hiyo na zilizokua palepalezinaweza kuonekana kwamba sasa zenyewe ndio zinakuakwa kasi, hilo jambo la kwanza.

Page 187: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

187

Mheshimiwa Spika, jambo la pili ambalo ningependakuchangia ni mfumuko wa bei. Ukisoma kitabu chaMheshimiwa Waziri kinatueleza vizuri kwamba mfumuko wabei ni asilimia 3.2. Ni jambo jema, nampongeza kwa hatuahiyo, lakini mimi nikajiuliza, nikaangalia huu mfumuko wa beiunachangiwa na nini hasa kutokua, kwa nini tunafanya vizuri?

Mheshimiwa Spika, nikagundua tunafanya vizuri sasatuwapongeze wakulima kwa sababu mfumuko wa wakulimawa chakula wenyewe umekua tu kwa asilimia 3.2 na ni kwasababu wakulima wetu hawa wanaweza kuzalisha chakulakwa wingi na cha uhakika na ndio maana wanalindamfumuko wetu wa bei. Kwa hiyo, lazima tuwapongezewakulima wetu hawa, lakini nikajaribu kujiuliza sasa ni wapiambapo sasa huyu Mheshimiwa Waziri ambaye mfumukowake wa bei unaendelea kuwa mdogo kwa sababu tuwakulima wana mazao, bei hazipandi za mazao ya wakulimakwa sababu tuna sera ambazo zinahakikisha wakulima hawawanalipwa kidogo.

Sasa kama tuna sera zinazohakikisha wakulima hawawanalipwa kidogo ili mfumuko wa bei usipande ukaharibuvitu vingine, je, wakulima hawa tunawapelekea ruzukumaalum kiasi gani ya kuwawezesha kunufaika na mfumukowa wa bei unaoendelea kwa kidogo? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, maana mtu akikutendea jamojema basi na yeye lazima umpe fadhila na fadhila ya kwanzakabisa ka mkulima ni ruzuku ya mbolea, lakini sioni. Nimejaribukupitia sana labda kwenye sekta, labda tutaona badae,sijaona ruzuku ya mbolea tunayopeleka kwenye kilimo,sijaona mkakati maalum. Nchi nyingine duniani zinakuwa namfumuko kidogo wa mazao ya kilimo, lakini kwa mfano kuleUbelgij i wakulima wanaambiwa kwamba bwanatunakuomba wewe usizalishe eneo lako na kwa kuwahautazalisha sisi tunajua ungezalisha ungeweza kuzalishamaziwa mengi, kwa hiyo, kwa mwaka huu tunakulipa pesahii ya maziwa ambayo ungezalisha, lakini wewe pumzikausizalishe, ili kulinda bei ya mazao, lakini sasa sioni mikakatiya makusudi ya namna hiyo, ndio maana nashauri Waziri wa

Page 188: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

188

Fedha aanze kuangalia ni kwa namna gani huu mfumukowa bei ambao unakuwa wa chini na anayechangia sana nimkulima na kwa sababu anazalisha kwa wingi, kwa ninitusimfikirie huyu mkulima kumwezesha, kumsaidia?

Mheshimiwa Spika, hoja nyingine ni uhimilivu wa Denila Taifa; ukisoma kitabu cha Mheshimiwa Waziri ametuambiadeni la Taifa limepanda kutoka trilioni 49.86 mpaka trilioni 51.03na akatueleza vizuri tu akasema hiyo ni sawasawa nakupanda kwa asilimia 2.35. Sasa na mimi nikasema ngoja namimi nijifanye nisiyejua hesabu, nijifanye sijui hesabu na sijuihesabu ngumu ngumu; nikasema kama kwa mwaka mmojaDeni la Taifa limeongezeka kwa asilimia 3.5 je, kwa miakamitano deni hili litaongezeka kwa asilimia ngapi? Hesabuzikaniambia litaongezeka kwa asilimia 17.2. Nikapata mstukokidogo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini namuomba sasaMheshimiwa Waziri akija baadae anihakikishie kwambaMheshimiwa Kamala usiwe na wasiwasi, deni hili halitakuwahivyo kama unavyofikiri, bali litakuwa kidogo. Akishaniambiahivyo, ajiandae kwa sababu nitamuuliza litakuwaje kidogokwa sababu bado tunaendelea, Stiegler’s Gorge ndiotumeanza na fedha nyingi lazima ziende huko, lakininitamueleza pia SGR ndio tumeanza na fedha nyingi lazimaziende huko na ametueleza yeye kwamba, fedha katikamasoko ya nje, misaada ya wahisani imekua migumu migumusana kwa hiyo, lazima tuendelee kutafuta fedha ndani nanje, nitamuuliza maswali hayo kwa hiyo, kukopa lazimakuendelee na kukopa si dhambi, cha msingi mnajipanga vipikulipa na mkopo huo unautumia namna gani?

Mheshimiwa Spika, lakini mambo haya lazimatuyazungumze kwa sababu ndio kazi ya Mbunge. Kazi yaMbunge ni kuzungumza, ni kutumia microphone na kushauri.Na lazima tushauri kwa msisitizo.

Kwa hiyo, lakini uhimilivu wa deni mwinginewanasema mauzo ya nje sasa tumeweza kufikia asilimia 157.3hii tuko chini ya ukomo ambayo ni asilimia 240, lakini kwa

Page 189: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

189

hesabu ya haraka haraka ni kwamba asilimia 82 tu ndiozimebaki, hiyo maana yake hiyo. Nikaangalia na kutumiamapato ya ndani kulipa deni nikaona sasa ni asilimia 15 naukomo ni asilimia 22 nikajua sasa kumbe tumebakiza asilimiasita. Kwa hiyo, hivi viashiria vya ukomo wa deni pamojakwamba ni vizuri hapa, lazima tukubaliane kuna taa ya njanoimeanza kuwaka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, na ukiwa unaendesha gariukakutana na taa ya njano lazima kwanza ushike brakekidogo na kama gari lako ulikuwa hujakagua brakeusiendeshe tu, uanze kukagua brake ziko namna gani, nakama mafuta yameanza kwisha ile taa ya mafuta ikiwakabasi simama kwenye kituo cha karibu ujaze mafuta iliuendelee na safari. Ukiyadharau haya ukasema garihalijasimama ukaendesha tu, utapata tatizo na uendeshajiwa gari wa style hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la mwisho naomba niseme nikokwenye Kamati ya Bajeti na ninakushukuru Mheshimiwa Spikaulinipeleka kwenye hiyo Kamati, nakushukuru sana,nimejifunza mambo mengi. Moja nililojifunza ni kwambatunakusanya saa nyingine fedha ambazo tunajua hizi fedhahatukutakiwa kuzikusanya, tunasema tuta-refund, lakini hatu-refund.

Mheshimiwa Spika, kwa mfano kwenye madini pekeyake wanadai bilioni 600, ukienda kula TBL wanadai-refundbilioni nyingi tu, ukienda viwanda vya soda wanadai fedha.Sasa shida ya fedha ambazo humrudishii mtu na ulitakiwaumrudishie fedha yake unapokaanazo ni kwamba unakuwaumeshikilia mtaji. Unaposhikilia mtaji ni kwamba unakuwaumeshikilia ajira; unaposhikilia mtaji, unaposhikilia fedha zakampuni maana yake umeshikilia ajira za Watanzania. Huyubadala angeweza kuwa na mipango ya kuajiri zaidi inabidiasitishe ajira ili aweze kuendelea kiwanda chake kwenye …,kwa hiyo, nasema eneo hili ambako ni mabilioni ya fedhanyingi tu yapo. (Makofi)

Page 190: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

190

Mheshimiwa Spika, lakini hakuna kinachoshindikanakatika Bunge. Kama Serikali inaona zile fedha lazimaaendelee kuzitumia basi ituletee hapa turekebishe sheriakwamba wasisubiri chochote fedha hizi sasa zinakuwa rasmiza Serikali na wajipange vizuri kwa siku zijazo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Diodorus Kamala.Unajua kitabu hiki cha Waziri ni kizito, tulikuwa tunakipitiapitiahapa, kumbe sekta ya Mheshimiwa Mwakyembe ndioinayokua kwa haraka, hatari kubwa hii, lakini ni habari njema.(Kicheko)

Mheshimiwa Zitto nil ishakutaja, MheshimiwaSimbachawene anafuata, halafu Mheshimiwa Mattar Salumna Mheshimiwa Justin Monko watafuata. (Makofi)

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Spika, nashukurukwa kunipa nafasi nami ya kuchangia bajeti, makadirio yabajeti ya Wizara ya Fedha, mafungu yote saba ya Wizara hii.Na nitakuwa na maeneo matatu ya kuchangia, kamanitapata muda nitaongeza eneo la nne na ningependakuanza na upande wa makusanyo ya kodi.

Mheshimiwa Spika, kwa muda wa miaka minne sasatumekuwa tukielezwa kwamba tumeongeza sana uwezowetu wa makusanyo ya kodi, lakini ukitazama takwimu zaSerikali yenyewe kuhusiana na uwezo wetu wa kukusanyakodi ukilinganisha na huku ambako tunatoka story hii sio storyya kweli. Ni story ambayo inapaswa tuelezwe upya, ili tuwezekuona changamoto ni nini na tuweze kutatua namna gani.

Mheshimiwa Spika, kwa mfano wakati Serikali yaAwamu ya Tano inaingia madarakani mwaka 2015, kipimocha makusayo ya kodi kwa kutumia Pato la Taifa, yaani taxGDP ratio ilikuwa tumefikia asilimia 15 na lengo letu na WaziriMpango atakumbuka kwamba katika Mpango waMaendeleo wa Kwanza ilikuwa na lengo la asilimia 16 ambalondio sasa lengo la bajeti ambayo inakwisha sasa hivi na

Page 191: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

191

Mpango wa Maendeleo wa Pili tufike asilimia 19 ya pato laTaifa.

Mheshimiwa Spika, lakini kwa mujibu wa Taarifa yaMdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali tax GDP ratioya mwaka wa fedha 2017/2018 ni asilimia 12 tu. Na hiiinatuweka sisi kuwa hata chini ya nchi kama Burundi ambayotax GDP ratio ni asilimia 13, Kenya asilimia 18.1, Ugandaasilimia 16, Rwanda asilimia 16. Katika nchi za Afrika Masharikisisi ni wa mwisho ukitumia kiashiria cha kupima makusanyoya ndani kulingana na Pato la Taifa yaani shughuli za uchumikatika nchi. Hii inathibitisha ya kwamba hatuendi mbelekatika makusanyo ya kodi, bali tunarudi nyuma, lakini kwasababu tunaangalia tarakimu tumetoka bilioni 800 mpakatrilioni 1.2 au trilioni 1.3 tunajiona kana kwamba tunakusanyasana, lakini ukiangalia bilioni 800 ya Pato la Taifa kwa mwakahusika na trilioni 1.3 ya Pato la Taifa la mwaka huo maanayake ni kwamba tunashuka sana.

Mheshimiwa Spika, nimepita l ibrary asubuhi,nimejaribu kuangalia miaka mitatu ya mwisho ya Serikali yaAwamu ya Nne ongezeko la makusanyo ya kodi lilikuwa niasilimia ngapi kulingana na miaka mitatu ya mwanzo mpakahuu mwaka wa fedha tunaoumaliza sasa ya Serikali yaAwamu ya Tano.

Mheshimiwa Spika, miaka mitatu ya mwisho ya Serikaliya Awamu ya Nne wastani wa ongezeko la makusanyo yakodi lilikuwa ni asilimia 16. Wastani wa makusanyo ya Serikaliya Awamu ya Tano toka wameanza mpaka bajeti hii ambayotunaimalizia ni asilimia 11.3; kwa hiyo, hakuna sababu yoyoteya kujidanganya kwamba tuna makusanyo makubwa ilhalimakusanyo si mazuri.

Mheshimiwa Spika, na makusanyo si mazuri kwasababu biashara zinafungwa; sekta binafsi ndioinayotengeneza kodi, sekta ya umma haitengenezi kodi. Zaidiya asilimia 95 ya watu wanaoajiriwa, ajira rasmi katika nchiyetu, wanatoka sekta binafsi, kwa miaka mitatu iliyopitatumeinyonga sekta binafsi.

Page 192: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

192

Mheshimiwa Spika, leo tunavyozungumza, nitakupamifano tu ya siku za karibuni; Kampuni ya Mwananchiimepunguza wafanyakazi zaidi ya 100 ndani ya wiki mbilizilizopita. Kampuni ya New Habari Corporation ya akinaMheshimiwa Bashe imepunguza kutoka wafanyakazi 300wamebakiwa na wafanyakazi 43. Tunavyozungumza sasaKampuni inayonunua tumbaku asilimia 40 ya tumbaku ya nchihii, Kampuni ya TLTC, Kiwanda cha Morogoro wamefungana wame-retrench wakati wa season watu 3,000 walipotezakazi. Katika mazingira kama haya mtapata wapi kodi? Kwasababu sehemu kubwa ya kodi ni kodi za wafanyakazi.

Mheshimiwa Spika, wala tusijidanganye tukadhanikwamba wenye mitaji wanalipa kodi kubwa, angalienitakwimu za Serikali 2/3 ya makusanyo ya kodi za mapato nikodi za wafanyakazi. Kwa hiyo, ni lazima mjenge mazingiraya kazi watu wapate kazi ili Serikali ipate pesa, lakini Serikaliinanyonga, biashara zinafungwa, wapi Serikali itapata pesa?Ndio maana takwimu hizi zinaonekana hivi kwamba tax GDPratio imeshuka na hata ongezeko la hizo kitarakimu ambazotunaambiwa bado ukilinganisha na Serikali i l iyopita,zimeshuka sana ni lazima tufanye marekebisho ya uhakikaya kuhakikisha ya kwamba, tunakusanya kodi ya kutosha.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili ambalo natakanilizungumzie nalo kwa kina kidogo ni usimamizi wa Deni laTaifa. Siendi kwenye mjadala kama deni ni himilivu au sihimilivu, usimamizi wa Deni la Taifa ni tatizo. Tazama recordza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa miakamiwili iliyopita, wanatoa maelezo yanayoonesha ya kwambamoja, kuna upotoshaji mkubwa katika taarifa za Deni la Taifakwa sababu mfumo wa malipo ya Deni la Taifa na mfumowa utunzaji wa kumbukumbu za Deni la Taifa havisomani.Matokeo yake ni kwamba tuna madeni ambayo hayakorecorded.

Mheshimiwa Spika, kwa mfano kwenye Taarifa yaCAG ya mwaka jana kuna zaidi ya shilingi trilioni mbili ambazorecord yake haionekani, lakini Mdhibiti amekwenda kwawaliotukopesha, kuna fedha ambazo waliotukopesha

Page 193: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

193

wanasema tumezitoa, ukienda Hazina wanasema hizombona hatujazipata kwa sababu ya mfumo mbovu wausimamizi wa deni. Kwa hiyo, hata deni ambalo tunaambiwahapa na Mheshimiwa Waziri Mpango ndugu yangu kwamba,ni kiasi hiki, ni asilimia hii ya Pato la Taifa sijui ya mauzo nje, nakadhalika, ni deni ambalo record yake sio sahihi.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba kwa ruhusayako, for the first time in the history of this country, ruhusuUkaguzi Maalum wa Deni la Taifa tuweze kupata takwimusahihi kwa sababu takwimu za sasa hivi sio sahihi na mimihapo nimesoma ripoti mbili tu ya mwaka jana na ya mwakahuu ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikaliambayo inaonesha kuna tatizo kubwa sana katika utunzajiwa kumbukumbu; wanatunza kumbukumbu za deni kwenyemadaftari ya shule, ma-counter book, unawezaje kutunzakumbukumbu za deni kwenye ma-counter book? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, aah, ndio ukweli huo MheshimiwaMwakyembe na Mheshimiwa Spika, mwambie MheshimiwaMwakyembe tumeingia wote Bungeni humu, tuko sawa kwahiyo, aniheshimu wakati naongea kwa hiyo, atulie kidogo.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba hili jambouruhusu Ukaguzi Maalum wa Deni la Taifa kwa maslahi yanchi tuweze kujua kwamba tunadaiwa kiasi gani natunadaiwa na nani? Kwa sababu inawezekana tukawatunalipa madeni ambayo ni hewa, hayapo. Kuna kitukinaitwa odious debts, debts ambazo zimekuwa created,hazipo na hii inawezekana kabisa ipo katika mfumo wetukwa sababu haufanyi kazi sawasawa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la mwisho ni jambo ambalonaishukuru sana Kamati ya Bajeti na naipongeza sanaimefanya kazi nzuri sana ya Bunge. Kuna fedha ambazozinakusanywa kinyume na Katiba na sheria. Kwa mujibu waIbara ya 138 ya Katiba, Bunge lako hili unaloliongoza ndilolenye mamlaka ya kutamka kodi. Ibara ya 138 ya Katiba;hakuna kodi ya aina yoyote itakayotozwa isipokuwa kwa

Page 194: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

194

mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge au kwa mujibu wautaratibu uliowekwa kisheria na uliotiliwa nguvu kisheria nasheria iliyotungwa na Bunge.

Mheshimiwa Spika, l ini hapa Bungeni tulikaatukapanga ushuru wa vitambulisho vya wamachinga? Wapikwenye revenue book unaona hayo mapato? Tutawa-account namba gani hawa? Haipo kwenye sheria…

SPIKA: Ahsante sana, muda hauko upande wako.

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Spika, naombadakika moja tu ya kiti, dakika moja ya kiti. Ahsante sana.

Mheshimiwa Spika, haipo kwenye sheria ya utaratibuwala kwenye revenue book, hakuna mahali ambapo fedhazinazokusanywa kwa wananchi wetu zimo, sasatunatuvunjaje sheria na Katiba namna hii? Kwamba Bungehalijakaa kutunga, Serikali inatekeleza, watu wetuwanaumizwa, nimesikia Tunduma huko leo wafanyabiasharawameshindwa kufanya biashara kwa sababu wameambiwahawana vitambulisho, haimo kwenye revenue book, kwenyesheria, tunavunja Katiba kwa nini? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba maoni yaliyotolewa naKamati ya… (Makofi)

SPIKA: Nakushukuru sana. Mheshimiwa GeorgeSimbachawene atafuatiwa na Mheshimiwa Mattar naMheshimiwa Monko.

MHE. GEORGE B. SIMBACHAWENE: Mheshimiwa Spika,kwanza kabisa nichukue nafasi hii kuipongeza Serikali nanimpongeze sana Waziri wa Fedha na Mipango na Naibuwake, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu na watendaji wotewa taasisi zote zilizopo chini ya Wizara ya Fedha na Mipangokwa kazi nzuri wanayoifanyia taifa hili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, unapojenga uchumi wa nchikama ya kwetu, ambayo zipo falsafa tofauti, wengine

Page 195: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

195

wanaona tunakimbia, wengine wanaona tunachelewa,wengine wanaona tunakosea na wengine wanaonatunapatia, ni lazima uwe na msimamo ili kuweza kufanyaunayofikiria kufanya na hasa kama umepewa dhamana yahaki na halali ya kuongoza nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Chama cha Mapinduzi kimepewadhamana hii kwa kushinda uchaguzi na Chama chaMapinduzi ndicho kinachoshika historia ya nchi hii kwasababu ndicho kilichoongoza nchi hii toka tulivyopata uhuru.Tunafahamu wapi tulipotembea tukaona mabonde,tunafahamu wapi tulioona kuna miteremko mikali na tunajuanamna ya kushika brake au kuongeza mwendo. Niwasihi naniwaombe wenzetu waliopo humu na Watanzania kwaujumla waunge mkono jitihada hizi nzuri zinazofanywa naSerikali ya Awamu ya Tano. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunajaribu kutekeleza miradiambayo ilikuwa haijaweza kutekelezwa tangu katikamipango ya kwanza kabisa tulipopata uhuru, leo inafanyika.Tunafanya miradi mikubwa ambayo inajenga msingi wauchumi wa nchi kwa ajili ya vizazi vyetu vijavyo, siyo kwa ajiliya sisi. Ukijenga reli, haujengi kwa ajili ya sisi leo na kwa hiyo,hata ukikopa hatukopi kwa ajili yetu sisi, tunakopa kwa ajiliya watoto na wajukuu zetu na kukopa si dhambi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, leo tunajenga mradi mkubwa wakuzalisha umeme wa Stiegler’s Gorge ambao hata tukikopasi kwa ajili ya sisi tu tunaoishi leo, ni kwa ajili ya vizazi vijavyo.Ni muhimu katika kuangalia hii mikubwa ikiwemo ya ufufuajiwa Shirika la Ndege kwa sababu ipo miundombinu muhimuikiwemo barabara, ujenzi na huduma za afya, haya yoteyanafanyika kwa gharama kubwa lakini pia uwekezaji kwawatoto wetu katika kutoa elimu bure ni mambo makubwaambayo yakifanyika leo yana maana sana kwa kizazi kijachokuliko sisi tunaoishi leo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, limezungumzwa hapa suala lakukopa na pengine nianze na hili ambalo Mheshimiwa Zittoamelisema juu ya masuala ya mamlaka ya fedha.

Page 196: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

196

Mheshimiwa Zitto ukiisoma Katiba Ibara ya 99 unayaonamamlaka ya Rais katika masuala ya fedha pia. Sasa lazimausome zote mbili na kwa sisi wanasheria huwa tunazisoma ilituweze kujua kama sheria hizi zinasomeka kwa pamoja auzinaenda mutatis mutandis au zinaenda kwa kupingana.Ninachokiona hapa ni kwamba hiyo uliyoisoma lazima uisomepia na Ibara ya 99. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Ibara ya 99 inasema hivi; “Bungelitashughulikia jambo lolote kati ya mambo yanayohusika naibara hii isipokuwa kama Rais amependekeza kwambajambo hilo lishughulikiwe na Bunge na pendekezo hilo la Raisliwe limewasilishwa kwenye Bunge na Waziri. Na mamboyanayohusika na Ibara hii ni haya yafuatayo; Muswada waSheria kwa ajili ya lolote kati ya mambo yafuatayo; kutozakodi au kubadilisha kodi kwa namna nyingine yoyoteisipokuwa kupunguza.”

Sasa katika madaraka haya na ukisoma na hizinyingine ni lazima uisome na hiyo. kwa hiyo, kuamuakuwatambua Watanzania wakajulikana kwa shughuliwanazozifanya ili waweze kupata msaada wa Serikali labdalingehojiwa msaada wa Serikali uko wapi dhidi ya hawa.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, mimi nasema…

MHE. KABWE Z. R. ZITTO:Mheshimiwa Spika, taarifa.

SPIKA: Mheshimiwa Simbachawene pokea taarifa.

T A A R I F A

MHE. KABWE Z. R. ZITTO:Mheshimiwa Spika, naombaMheshimiwa George Simbachawene, Mwenyekiti wa Kamatiya Bajeti aangalie taarifa ya Kamati ambayo yeyemwenyewe ameiongoza ambayo imesomwa hapa Bungeniukurasa wa 27 aya ya 4.1 kuhusu namna ambavyo mamlakazinajiamulia kukusanyakusanya mapato bila consultation yaWizara ya Fedha na Bunge hili kuleta sheria, arejee katika

Page 197: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

197

hilo kabla hajanijibu mimi ndiyo atajua kwamba nilichokuwanakiongea mimi ni kile ambacho kamati imeleta hapa.

SPIKA: Mheshimiwa Simbachawene unapokea hiyotaarifa?

MHE. GEORGE B. SIMBACHAWENE: Mheshimiwa Spika,anavyoitafsiri ni tofauti, tumezitaja kabisa; tumesema Wizara,taasisi/mamlaka ya mikoa na wilaya. Ni kwa sababu ya vilevikodi/vitozo vidogo vidogo ambavyo vinahitajika kwa mujibuwa sheria Serikali i-coordinate siyo kila mamlaka itoke na kodi/tozo yake, zinaleta shida na kero kwa wananchi na huu ndiyoulikuwa ushauri kwa Serikali na bahati nzuri Serikaliilishaupokea ushauri huu kutoka kwenye Kamati. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa nini tunakopa leo? Lakini pialazima nieleze ipo tofauti kati ya Deni la Taifa na Deni laSerikali; hapa tunachanganya mambo. Deni la Serikali ni lileambalo Serikali imekopa kwa mujibu wa Sheria ya Mikopo,Misaada na Dhamana na lina utaratibu wake. Haiwezekaniikasemekana eti halieleweki, sheria ipo inakuwaje deni liwehalieleweki? Deni la Serikali linaeleweka vizuri kabisa ingawaSerikali pia ina udhibiti wa Deni la Taifa lakini Deni la Taifalinahusisha pia mikopo ya sekta binafsi. Kwa hiyo, lazimakuelewa namna ya ku-balance, isijeikachukuliwa yote kwaujumla wake halafu ikawachanganya Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, inadaiwa hapa kwamba eti sisitunakopa sana na pengine deni hili limeongezeka. Madenitunayolipa leo kama nchi yalikopwa toka awamu ya kwanzaya uongozi wa nchi hii, kwenye ule mkeka yapo madeni naKamati yako iko well informed. Vipo vitu tunavipata kule namimi namshukuru Mungu kuwepo kwenye Kamati hiinimejifunza mambo makubwa ambayo nilikuwa siyajui.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, madeni tunayolipa leo ni ya miakaya 1980, 1990 yaani ya siku za nyuma ndiyo tunalipa leo nahaya tunayokopa sisi yatalipwa huko mbele, lakini lazimatuhakikishe tunakopa kwa ajili ya kitu gani. Sasa tunapokopa

Page 198: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

198

kwa ajili ya reli ambayo watoto wetu wataikuta kwa miaka100 ijayo, tunapokopa kwa ajili ya kuzalisha umeme ambaowajukuu zetu wataukuta, kuna ubaya gani! (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukopaji una uwiano wake nauwiano muhimu ni kipimo cha debt to GDP ratio. Deniukilinganisha na GDP (Pato la Taifa), kwa mfano Tanzanianilishanishe tu kidogo, Marekani debt to GDP ni asilimia 106.1;Kenya debt to GDP ni asilimia 52; Zambia debt to GDP niasilimia 54; Ugiriki debt to GDP ni asilimia 179 yaani GDP yaoinaingia kama mara mbili na zaidi, lakini Tanzania debt toGDP yetu ni asilimia 32, tupo chini ya wengine wote. Kwahiyo deni letu ni himilivu, tena bado tuna nafasi ya kukopa ilituweze kuwekeza, cha msingi ni kuwekeza kwa ajili ya watotowetu na wajukuu zetu na vizazi vijavyo, hicho ndicho chamsingi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, yamesemwa mambo hapa…

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: Mheshimiwa Spika,taarifa.

MHE. DAVID E. SILINDE: Achana nae unapoteza muda.

SPIKA: Mwakajoka nini tena? Maana yake hiyo shule…

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: Mheshimiwa Spika,unajua amejisahau…

SPIKA: Ngoja kidogo, subiri, hujaruhusiwa bado.

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: Unasikia mzeeamejisahau anasema kwamba…

SPIKA: Hujaruhusiwa kwanza, nitakupa nafasi.

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: Aah sorry.

SPIKA: Usiwe unaongea kabla hujapewa nafasi.Nilikuwa nasema kwamba shule hii inayotolewa na lawyer

Page 199: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

199

kwa Zitto economist i l itakiwa...; Mheshimiwa Zitto niMwakajoka amesimama kwa hiyo…, Mwakajoka nakupadakika moja. (Makofi/Kicheko)

T A A R I F A

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: Mheshimiwa Spika,miminampa taarifa Mheshimiwa Mbunge anayezungumzakwamba anazungumza kama Waziri, ajue kabisa kwambasasa hivi ni Mbunge wa kawaida, kwa hiyo, anatakiwa kutoamichango yake. (Makofi)

SPIKA: Aah! Yaani kwa kweli umechezea wakatiwangu, hapa wanaongea professionals na Mwakajokahujawahi kuniandikia professional yako ni nini hasa?Mheshimiwa Simbachawene endelea. (Kicheko)

MBUNGE FULANI: Darasa la nne huyo.

MHE. GEORGE B. SIMBACHAWENE: Mheshimiwa Spika,nataka Mwakajoka afahamu kwamba kila Mbunge wa CCMni Waziri mtarajiwa. (Makofi/Vigelegele)

Mheshimiwa Spika, ni vizuri wakati mwinginetukafahamu historia ya uchumi wa nchi yetu na namnatunavyoujenga. Tulipopata uhuru tulijenga uchumi wakijamaa na mpaka leo misingi ya kijamaa hatujaiondoakwenye Katiba hii. Ukisoma Ibara ya 9 inaeleza vizuri namnaya kujenga uchumi wetu, kwa sababu ya muda sitainukuu,lakini nataka wafahamu kwamba ni tofauti na baadatulipofika mwaka 1967 tukajenga uchumi mwingine, lakini piatumejenga uchumi wa aina tofauti katika kipindi cha kilaawamu ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, leo hii tunajikuta tunasahihishamakosa ya uchumi wa soko huria ambao ulikuwa ni fashionna sera ya mashirika ya fedha duniani including World Bank.Tumefika tulipofikana inadaiwa kwamba hatujapiga hatuakubwa ukilinganisha na wenzetu kwa sababu ya aina yauchumi tulioujenga. Mataifa ya Asia ambayo yali-harmonize

Page 200: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

200

ujamaa na ubepari na ndiyo maana Wachina wanasemawanajenga scientific socialism leo, ndiye aliyefanikiwa kupigahatua.

Mheshimiwa Spika, kwa ninavyoona mimi, ninaonakama Serikali ya Awamu ya Tano inaenda kwenye aina yaujenzi wa uchumi wa scientific socialism. Mwelekeo huu nisahihi, ndiyo uliofanya nchi za Asia, Malaysia, Singapore,Bangladesh na zingine kupiga hatua kubwa kiuchumiincluding China yenyewe na nchi zingine. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tupewe nafasi kama Chama chaMapinduzi, tuipeleke hii nje, tufike mahali tuje tupimwe kwakura za wananchi na nataka niwaambie Watanzaniakwamba leo hii ukitaka kujenga nyumba, lazima ujinyimekabisa, ni lazima tujinyime kidogo ili tuweze kujenga nchi yetu,haiwezekani tukawa tunafanya sherehe huku tunafanyamaendeleo, haiwezekani. Ni lazima tukubali, tusikilizane,tulete utulivu tuone nchi inavyojengwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Watanzania ni mashahidi, kilamahali nchi hii inajengwa, katika kila sekta nchi inajengwa,sasa ni lazima tujenge nchi, haya mambo mengine yatakujatu. The highest good in life is happiness, Plato alisema, we willbe happy kama tumejenga misingi ya uchumi imara.Tumefika tulipofika leo kwa sababu hatukuweka misingi imarasana ingawa awamu zilizopita zilifanya kazi nzuri, lakini kilaregime ina fashion yake, let’s follow this fashion. Twendetumuunge mkono Rais, tujenge misingi ya uchumi na miminaamini ndani ya miaka 10 na kama tutaendeleakumchagua Magufuli kuwa Rais wa nchi hii, tutayaonamakubwa ambayo hatukuwahi kuyafikiria. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipanafasi na ninaunga mkono hoja. (Makofi/Vigelegele)

SPIKA: Ahsante sana Mwenyekiti wa Bajeti,Mheshimiwa Zitto alikuwa anakusikiliza kwa umakini mkubwasana na amepata nondo nyingi.

Page 201: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

201

Waheshimiwa Wabunge kwanza nimtambueMheshimiwa Mwakyembe kwamba ndiyo Kiongozi waShughuli za Serikali humu Bungeni kwa sasa na nashukurusana. Wakati na acknowledge kazi ya Wizara yake, haikunijiakwamba yupo, niliangalia kwenye kiti chake kule basinikasema kidogo kwa sababu nili-assume hayupo, lakini kwakweli tukupongeze sana kwa takwimu hizi za Waziri wa Fedhasekta yako inakwenda vizuri sana. (Makofi)

Inanikumbusha enzi zile sisi wazee wakati huotunasoma kwenye chuo kile kikongwe kuliko vyote, ilikuwamtu akisoma mambo hayo ya theatre arts na nini na ninitulikuwa tuna neno, ukiulizwa aah anasoma unamwambiaaah anasoma mahoka, ndiyo ilikuwa neno la hao watu wasampuli hiyo. Ilikuwa inaendana na dharau na kejeli na sikuwakiingia Nkurumah pale kufanya demo zao na nini basitunaenda kucheka hasa tuliokuwa tukifanya sayansi,tunaona yaani hawa, lakini sasa unaona mamboyanavyokwenda, Mheshimiwa Mwakyembe hongera sana,kabisa, ni badiliko kubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Simbachawene tunakushukuru sanakama Mwenyekiti wa Bajeti kwa mchango mzuri, ni kwelibwana hatuwezi kujenga nchi gizani, hivi inawezekana kwelikujenga nchi gizani? Stiegler’s Gorge lazima ijengwe, nchiiwake yaani umeme, viwanda nini. (Makofi)

Kwa hiyo, tunaendelea Waheshimiwa, nilitakakumtambua Mheshimiwa Mwakyembe na kuwajulishakwamba Serikali ipo. Mheshimiwa Mattar nilikutaja dakikatano, yupo? Kama hayupo, Mheshimiwa Justin Monko dakikatano pia, atafuata Mheshimiwa David Silinde.

MHE. JUSTIN J. MONKO:Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana kwa kunipa na mimi nafasi ya kuchangiakatika bajeti hii ya Wizara ya Fedha. Nianze kwa kuipongezasana Wizara kwa bajeti nzuri ambayo wametuletea hapa nanina imani kubwa akiitekeleza hivi wanavyosema, watawezakututoa hapa tulipo.

Page 202: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

202

Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabungewaliotangulia wameanza kuzungumza mengi na mojawapolimekuwa ni Deni la Taifa na mimi niiombe tu Wizara kwa sasaDeni la Taifa kweli pamoja na kwamba limeongezeka, naMheshimiwa Simbachawene amelielezea vizuri sana kwasasa lakini tunaona kwamba deni hili linaendelea kuongezekapamoja na kwamba inafanya miradi mikubwa ambayo kwakweli tunaihitaji na ni miradi ya kimkakati ya nchi hii.

Mheshimiwa Spika, sasa wito wangu kwa Wizara nikujaribu kuangalia kwamba deni hili liwe stahimilivu kamawanavyoendelea kusema kwa sababu ukiangalia sasa zaidiya trilioni 50 wakati sisi uwezo wetu tunakusanya mapato yandani kwa trilioni 20, kidogo linakuwa na mashaka na hasakwa sisi ambao siyo wachumi. Kwa hiyo, niiombe sana Wizaraitupie macho kuhusiana na suala hili la Deni la Taifa nakuangalia tusijetukateleza.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ni ukusanyaji wamapato. Tunaipongeza sana Wizara wamefanya kazi nzuriya kukusanya mapato na mimi nilitaka baadaye MheshiwaWaziri atakapokuja, mwaka jana tulipitisha hapa, tulitoamsamaha wa kodi kwa mfano kwenye kulipia magari na nini.Nilitarajia sana kuweza kuona kwamba tuone msamaha huouliotoka, mapato ambayo yalikuwa yamekusanywayametusaidia kuongeza mapato kwa kiwango gani, lakinisijaliona hilo. Kwa hiyo, tunataka tuone namna ambavyoWizara hii inaweza ikasimamia mapato hayo ambayoyanatusaidia katika utekelezaji wa miradi mbalimbali na hataulipaji wa pensheni, nyongeza hata za mishahara pamojana mambo mengine ambayo yanatokana na kuongezekakwa mapato.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ninataka nimuombeWaziri atakapokuja tuweze kujua, kitu ambachoWaheshimiwa Wabunge walipitisha mwaka jana hapakimeleta manufaa gani.

Mheshimiwa Spika, na labda kazi kubwa ambayoWizara inatakiwa kufanya sasa ni kujaribu kuendelea

Page 203: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

203

kuboresha mazingira ya ukusanyaji wa kodi, hasa kwenyemaeneo mengi ili wananchi wengi waweze kulipa kodi. Badowako wananchi ambao wanaendelea kukwepa kodi kwasababu wakati mwingine mazingira ya ulipaji au kodizenyewe siyo rafiki. Kwa hiyo, niombe sana Wizara iwezekuboresha kwenye maeneo haya ili wananchi waweze kulipakodi inavyostahili.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na suala la miradi nahasa miradi ya PPP; hotuba ya Mheshimiwa Waziri imeelezavizuri sana, na kwamba sasa hivi wana mikakati ya kuwezakuzisaidia Halmashauri ili ziweze kuongeza uwezo wake waukusanyaji wa mapato. Kwa hiyo, niombe Wizara iwezekuwasaidia.

Mheshimiwa Spika, kwa sababu tukiangalia, kwamfano katika Halmashauri yangu ya Singida DC tuna miradiambayo tumekwishakuiandika lakini imekwenda kwa mudamrefu na hatujapata fedha. Tumeomba kwa ajili ya ujenziwa mradi wa soko pale Njiapanda ya Meriya na andiko hililimekuja muda mrefu, limepita katika hatua mbalimbali katikangazi za mkoa na limekwishakwenda huko Wizarani, lakinikatika bajeti hii sijaona kama limepata kibali cha kupatafedha.

Mheshimiwa Spika, Halmashauri ile bado ni duni sana,mwaka uliopita tulikusanya chini ya shilingi bilioni moja. Kwahiyo, tunahitaji sana fedha hizi kwa ajili ya miradi hii mkakatiili tuweze kuongeza uwezo wetu na kuweza kuwasaidiawananchi. Kwa sababu mapato ya ndani ya halmashauriyanategemewa sana na vijiji vyetu, yanategemewa sana naakina mama, vijana na walemavu na yanategemewa sanana Waheshimiwa Madiwani katika kutekeleza miradimbalimbali kule kwenye Halmashauri zetu.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo niombe sana Wizaraijaribu kuliangalia suala hili, ipitie na kama liko tatizo lamaandiko ambayo tunaandika kutoka kwenye Halmashauribasi Wizara itusaidie ili maandiko haya na yenyewe yawezekukidhi vigezo.

Page 204: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

204

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Justin Monko.

MHE. JUSTIN J. MONKO: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana kwa kunipa nafasi, ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana, Mheshimiwa David Silindeatafuatiwa na Mheshimiwa Hussein Bashe.

Mheshimiwa Silinde ni dakika kumi.

MHE. DAVID E. SILINDE: Mheshimiwa Spika, ahsantesana na mimi kunipa fursa hii kuchangia bajeti ya Wizara yaFedha na Mipango kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

Mheshimiwa Spika, naomba nianze kwa kum-quoteMakamu wa Rais wa Ghana, Dkt. Mahamudu Bawumia,anasema; “Huwezi kuendesha uchumi kwa propaganda.”Never, haijawahi kutokea, haitakuja kutokea, kwa sababuhali halisi ya maisha ya wananchi itakuumbua. Maswalimadogo tu sisi mioyoni mwetu tunaridhika na namna Wizaraya Fedha inavyoendesha uchumi wa nchi hii? Mioyoni mwetu.. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Wabunge tukiwa tumekaa kantini,tukiwa Wajumbe wa Kamati ya Bajeti kila taasisi inayokujatumewapelekea bango kitita, taasisi zote, hakunainayoridhika, watu wanalalamika. Tuna uwezo wa kusemapropaganda kadri tunavyoweza, lakini uchumi hauendeshwikwa propaganda, uchumi ni fact. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Wizara ya Fedha iliyo chini yaMheshimiwa Dkt. Mpango. Dkt. Mpango yule wa Tume yaMipango leo wakikutana na Mheshimiwa Dkt. Mpango waWizara ya Fedha leo, ni watu wawili tofauti. Hakuna mahaliwana-merge, yaani huwezi kuwakutanisha, yaani yule waTume ya Mipango wana-differ kwenye kila kitu, ndiyo ukweli,whether mnakubali ama mnakataa, ndiyo ukweli. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, leo Wizara ya Fedha na Mipango,mwaka jana mimi nilizungumza hapa Bungeni, inafanya

Page 205: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

205

mambo ya reallocation ya fedha bila mamlaka ya Bunge.Kosa hilo hilo wamelirudia tena mwaka huu, wametengenezarevised budget zaidi ya bilioni 355, Bunge halijapitisha walahakuna reallocation warrant kwenye vitabu vyetu. Hukowamekiuka Sheria ya Bajeti… (Makofi)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Spika,taarifa.

SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Nchi.

T A A R I F A

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Spika,naomba tu nimpe taarifa mchangiaji, pamoja na hizopersonal attacks kwa Mheshimiwa Dkt. Mpango, MheshimiwaDkt. Mpango hapa yuko kama Waziri na kanuni zinamtakaamu-address kama Waziri na siyo Dkt. Mpango.

Mheshimiwa Spika, lakini nataka nimpe taarifakwamba kifungu cha 28(2) cha Sheria ya Bajeti, Sura ya 439kimempa Waziri wa Fedha mamlaka ya kufanya uhamishobaina ya mafungu kwa kiasi kisichopungua asilimia tisa. Hiyobilioni 355 anayoisema ni asilimia moja tu ya hizo asilimia tisaambazo Mheshimiwa Waziri wa Fedha amepewa kwa mujibuwa sheria. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo ninataka nimpe taarifaMheshimiwa Silinde, asi-take advantage ya haya yanayojirikupotosha fulani hivi, hiki kiasi cha fedha cha hizo bilioni 355kiko ndani ya sheria na kanuni hiyo niliyoisema ambayoinampa mamlaka Waziri wa Fedha kufanya hayoaliyoyafanya. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Waziri wa Nchi,Mheshimiwa Silinde ni taarifa kwako hiyo, iko ndani ya uwezowake.

Page 206: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

206

MHE. DAVID E. SILINDE: Mheshimiwa Spika, nashukuru.Bahati mbaya Waziri hakuelewa na Mheshimiwa Dkt.Mpango, Mheshimiwa Waziri wa Fedha unajua.

Mheshimiwa Spika, hawa watu hii ni sheria, Sheria yaBajeti iko wazi, Sheria ya Fedha iko wazi. Sisi baada ya mudawako kuisha tutakutana mahakamani kule kwa hii kazi.Wasikudanganye, utafungwa kwa mambo haya. Sheria haifi,criminal huwa haifi. Mheshimiwa Waziri hajaelewa ni bahatimbaya sana. Watu wanaokushangilia sana usiwafurahiekuliko wanaokuambia ukweli. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba mimi niendelee na hojaza msingi ambazo nilikuwa nazungumza, kwamba makosahaya ya revised budget bila kuleta kwenye Bunge mamlakaaliyonayo ya kwenye mafungu ile asilimia moja hayoyanaeleweka. Lakini tutakwenda mwisho wa siku haya, sisitunarekodi tu, tunaweka kwenye rekodi, utawalautakavyobadilika watakuja kusema akina Mheshimiwa Silindemlituambia na mlitushauri vizuri na utawala siyo lazima ajeCHADEMA nawaambia huko huko ndani, umenielewa. Kwahiyo, hicho ndicho tunachokisema. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la pili, Wizara ya Fedhaimeshindwa kusimamia sera zake nyingi za fedha natunapojadili hapa, tatizo la nchi hii, sera za nchi tulizonazolazima ziendane na malengo (objectives) ambayotumejiwekea. Sasa leo ukiangalia Sera ya Fedha, Sera yaBiashara, Sera ya Kilimo zinatofautiana kabisa when it comesto industrialization. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunajadili uchumi wa viwandalakini nenda kaangalie Sera ya Fedha, angalia Sera yaBiashara na Kilimo yaani hivi vitu vitatu tu vinatofautiana. Sasaunajiuliza unafikiaje malengo ya uchumi wa viwanda ambaotunauhubiri humu ndani wakati sera zenyewe zinatofautiana.

Mheshimiwa Spika, Serikali ikaja na blueprint, mkaletaopinion hapa kwamba twende na blueprint; leo kila

Page 207: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

207

unayemuita sasa twendeni tukatekeleze hakuna hata mmojaambaye yuko tayari. Kuna mikanganyiko kibao mule ndani.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, UWEKEZAJI:Mheshimiwa Spika, taarifa.

SPIKA: Mheshimiwa Silinde, taarifa, MheshimiwaAngellah Kairuki nimekuona.

T A A R I F A

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, UWEKEZAJI:Mheshimiwa Spika, nimuombe tu Mheshimiwa Silinde aachekupotosha. Tayari tumeshatoa taarifa, mpango kazi wablueprint uko tayari na kuanzia Julai mwaka huu utekelezajiunaanza na hakuna anayepinga hilo na hata sekta binafsiyenyewe, bahati nzuri tarehe 28 Mei, nilikuwa nao, wanasubirikwa hamu utekelezaji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini si hilo tu, yako maeneoambayo tayari utekelezaji umeanza. Ukiangalia katika kufutatozo mbalimbali za OSHA, zaidi ya tozo tano; ukiangalia katikaWizara ya Madini katika uzalishaji wa chumvi zaidi ya tozotisa zimefutwa. Lakini pia Wizara ya Afya kupitia TFDA, TBS,kwenye Bodi ya Nyama na Maziwa na bodi nyinginezo.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo nimuombe sana kwakweli Mheshimiwa Silinde asitumie hadhara hii kuwezakufanya upotoshaji huo na niwahakikishie wananchi nawafanyabiashara wawe macho, Serikali inatambua kwambawao ndiyo engine ya ukuaji wa uchumi, tuko pamoja nao,tunawathamini, tutawalea na kuhakikisha kwambawanafanikiwa na hata Mheshimiwa Rais muda si mrefuanakutana nao kuhakikisha kwamba mambo yaoyanakwenda vizuri. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Silinde taarifa hiyoipokee.

Page 208: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

208

MHE. DAVID E. SILINDE: Mheshimiwa Spika, uzuri hawawatu ukipiga kwenye fact huwa lazima wajitokeze. Miminapokea taarifa yake, naipokea kwa sababu ndichoninachokizungumza. Hii taarifa ya blueprint tangu mwaka2016, leo nasema hata Bunge halijui ndiyo taarifa inatolewahumu ndani kwa kushtukiza. Hii biashara ya kushtukiza kilakitu itaendelea mpaka lini? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ndiyo maana mimi nasemanaipokea, lakini bado ukiona vitu anavyovitaja ni vitu petty,yaani vitu vidogo vidogo. Kuna haja na ndiyo maana mojaya proposal yangu kwenye mchango wangu kabla huyu hajainterfere nil itaka nikuombe uunde Kamati Maalumitakayopitia ile blueprint kuishinikiza Serikali ianze utekelezajiwake kwa sababu mambo mengi yanakwama, ndilo jamboambalo nilikuwa nauliza.

Mheshimiwa Spika, na ndiyo maana kuna vitu hapatunaweza tukaulizana maswali, nchi hii kwenye masuala yasera kuna swali tumewahi kujiuliza siku moja, hivi leo kwamfano Wizara ya Kilimo isingekuepo watu wasingekuwawanalima humu ndani, hii nchi watu wasingekuwawanalima? Au Wizara ya Viwanda na Biashara isingekuepowatu wasingefanya biashara? Wangefanya. Sijui kamaumenielewa.

Mheshimiwa Spika, lakini sasa angalia hawawataalam walikokaa kule, ndiyo wanatumika kama kuvurugautaratibu. Sasa ukipitia, hii nilikuwa najaribu kuiunganisha kwasababu sera yetu ya sasa ni sera ya uchumi wa viwanda.Sasa hivi vitu vitatu vikubwa nilikuwa naona ni vitu ambavyolazima ilikuwa tuvi-merge ili kuhakikisha tunaisaidia.

Mheshimiwa Spika, kwenye Kamati ya Bajeti amekujaWaziri wa Viwanda na Biashara wanalalamikia kuhusu mtiririkowa makodi, amekuja Waziri wa Fedha na wenyewewanawalalamikia watu wa upande mwingine. Kwa hiyo,imekuwa ni lawama juu ya lawama ya kila moja wao. Kwahiyo, hilo nikasema ni bora kulisema.

Page 209: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

209

Mheshimiwa Spika, lakini cash economy is veryexpensive na Mheshimiwa Dkt. Mpango anajua. Wakati Dkt.Mpango anaanza kuwa Waziri alisema bajeti yetu nikasungura, sasa hivi amebadilisha kutamka yeye mwenyewesasa hivi anatamka kwamba unajua uchumi wetu sasa nikasimbilisi, kwamba makusanyo ya fedha ni madogo. Sasatunapoiambia Wizara ya Fedha irekebishe, iongeze uzalishajimaana yake tunataka kodi, wigo wa kodi uongezeke.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, na ndiyo maana lengo letu lilikuwani nini, Wizara ya Fedha ni lazima i-promote, iweke incentiveskwenye private sector ili kuongeza uzalishaji na wigo wa kodi.Lakini Wizara ya Fedha inajikita kwenye kodi peke yake, yaaniyenyewe inafikiri kwamba kodi baada ya kodi ndiyo suluhisho.

Mheshimiwa Spika, kuna maswali ya kujiuliza hapa,swali namba moja, kwa mfano hivi kupunguza kodi ndiyosuluhu ya kupata kodi nyingi? Jibu linaweza kuwa ndiyo auhapana. Kwa sababu gani, moja, unaweza kuangaliaefficiency, kama kukiwa na efficiency nzuri mtakusanya kodi,lakini efficiency ikiwa mbovu kodi itakuwa hakuna.

Mheshimiwa Spika, suala la pili, uchumi unakwendaje?Kama uchumi ni mbovu hiyo kodi haiwezi kupatikana,mtahangaika haitakusanywa mahali popote. Ni masualaambayo tunapaswa tuangalie. Jambo la tatu, compliance,mazingira ya kibiashara. Wakati mwingine wafanyabiasharahawataki wapunguziwe hata kodi, ni bureaucracyiliyokuwepo mle ndani, kuna kanuni zinakwenda contrary nasheria ambazo tumepitisha ndani ya Bunge.

Mheshimiwa Spika, sasa haya yote ndiyo kazi yetu sisikuishauri Wizara ya Fedha iyafanyie kazi ili ku-rescue uchumiwa nchi. Lakini hapa watu wanataka kusikia zile lugha zakupendeza tu, jamani reli imepata, Stiegler’s imekwenda hivi,sijui nini; hizo lugha hazisaidii, tunaangalia mapungufu iliyarekebishwe, nchi iende mbele na hiyo ndiyo kazi yetukubwa ambayo tunaifanya humu ndani. Sasa bahati mbayabinadamu huwa hapendi kusikia maneno mabaya. (Makofi)

Page 210: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

210

Mheshimiwa Spika, Mwalimu Nyerere wakatianaondoka madarakani…

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Silinde.

MHE. DAVID E. SILINDE: Mheshimiwa Spika, ahsantesana. (Makofi)

SPIKA: Nakushukuru sana. Nilishakutaja MheshimiwaHussein Bashe atafuatiwa na Mheshimiwa Peter Serukamba.

MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Spika, nashukurukwa kunipa fursa. Kwanza nimshukuru Mwenyezi Mungu kwakutujalia sote afya na nguvu ya kuja kutimiza wajibu wetu.

Mheshimiwa Spika, mimi nianze kwa manenoyafuatayo; litmus paper ya sera za fedha na fiscal measuresya kwanza ni Revenue Authority, kwamba je, malengotuliyojiwekea na mimi niingie on record, siyo sahihi na Waziriwa Fedha anajua hili, siyo sahihi kusema Watanzania hawalipikodi. Labda tuseme ni sahihi kusema kuna Watanzaniawachache hawalipi direct tax, kila Mtanzania wa nchi hiianalipa kodi whether ni direct or indirect. Kwa hiyo, hii dhananaiona siyo dhana sahihi kwa sababu hakuna Mtanzaniahanunui bidhaa, anaponunua bidhaa amelipa kodi. Kwahiyo, hii ni dhana ambayo ni vizuri sana ikawa inaelezwa vizuri.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi mkononi hapa na hii ni Wizaraya Fedha yenye jukumu la kusimamia fiscal measures.Mkononi hapa nina takwimu za miaka kumi zinazooneshatrend ya makusanyo ya kodi ya nchi yetu. Kati ya matarajiona hali halisi, the focus error kwa kipindi cha miaka kumikwenye Revenue Authority ni asilimia 17 yaani kwa miakakumi asilimia 17 haijawahi kufikiwa, kila ukitenga shilingi mojakwamba ndiyo tutakusanya maana yake kuna asilimia 17 yahiyo shilingi moja hatutafikia. Ukichukua focus error ya miakakumi ya bajeti nzima ni asilimia 27, hizi hapa ni takwimu zaSerikali za miaka kumi.

Page 211: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

211

Mheshimiwa Spika, sasa kwa nini nimesema litmuspaper ni TRA? Kwa sababu kule ndiko tunakoenda kukusanyamapato. Sasa unakusanya mapato kutoka wapi? Hapa ndiyolinakuja jukumu la Wizara ya Fedha kusimamia fiscal measureszake. Nataka nitoe mifano, kuna makosa ya kiutawalayanayofanyika katika nchi yetu yana-destroy economy.

Mheshimiwa Spika, ripoti ya IMF ambayo ni leakedambayo hatupendi kuisikia imezungumzia jambo moja,business environment. Tunapozungumzia businessenvironment ni hatua tunazochukua ambazo nyingizinakwenda kuathiri TRA function. Mfano, kuna watuwanaingiza sukari za viwandani wanapitisha kwa njia zapanya kuziingiza sokoni. Tumeamua kuazisha kodi ambayoni unconstitutional ya withholding ya 15%. Hili ni suala laadministrative, ni suala la usimamizi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa nini kinachotokea, hivi kweliWaziri, Mheshimiwa Dkt. Mpango, Coca Cola ataingizaindustrial sugar aipeleke Kariakoo akauze? Kwa nini weziwatatu tu wanaojulikana, wanaoingiza sukari za viwandanisokoni tunakwenda ku-destroy the entire sector, why?(Makofi)

Mheshimiwa Spika, yaani mimi hili swali nimeliulizandani ya Kamati ya Bajeti kwa miaka miwili halipati majibu.Yaani tunawajua ambao huwa wanaingiza sukari zaviwandani ambazo wanaziingiza sokoni, hawazidi watatukatika nchi, tunawajua. Lakini hatua gani tunachukua?Tunaanzisha kodi ambayo inakwenda kuua cash flow zaviwanda. It is unfair. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri Dkt. Mpango,tunakubebesha dhambi nyingi katika nchi hii, malawamamengi, because you are the one, be bold kaka. Walazimishepolisi, walazimishe Wizara ya Mambo ya Ndani, walazimishewengine wachukue hatua, don’t kill the sector, sector nzimaina-suffer.

Page 212: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

212

Mheshimiwa Spika, kinachotokea ni hivi, anatakiwaalipe withholding tax ambayo refund yake haipo na tulipitishakuanzisha Escrow Account na nikwambie mimi nampongezasana Rais, Dkt. Magufuli, najua anakwenda kukutana nawafanyabiashara kila Wilaya wanakwenda watano. I swearzitakuja sheria hapa za kubadilishwa, kama ilivyokuwakwenye madini, akienda kuwasikiliza.

Mheshimiwa Spika, mimi nasikitika, it is very painful.The business sector is suffering. Nataka nikupe mfanomwingine, these are administrative issues ambayeanakwenda kuathirika ni Wizara ya Fedha, TRA, kuna kiwandakinakwenda kupigwa mnada kinaitwa Salahi CompanyLimited kiko Iringa. Angalia hii movie ya kihindi, kile kiwandakiko kwenye eneo la EPZA, anazalisha pipi na biscuit, kapatacertificate zote na kila kitu input yake mojawapo ni sukarikwa ajili ya pipi na biscuit. Document zote zimeendaamezipeleka Bodi ya Sukari unajua Bodi ya Sukariwamewajibu nini? Sisi hatutambui EPZA hizo incentivewanazokupa, kwa hiyo hatukupi kibali.

Sasa nini kimetokea? Kiwanda hiki kilifunguliwa for trialmwaka 2016 for trial for two months kwa ajili ya watu EPZAkujiridhisha quality na TBS na kila kitu baada ya hapowakazima wame-importraw material ngano yao sasa hivi ikounder bounded warehouse ya TRA imeoza. Sukari waliyoimport kwasababu hawajapata kibali cha Bodi ya Sukariangalia bureaucracy hii sukari wamezuiliwa mpaka ime-expire bandarini angalia hili, wananchi 120 wa Iringa mjiniwaliokuwa wameajiriwa wamerudishwa nyumbani. Benki yaAmana leo ina-recall mkopo, asset zao zinapigwa mnada,he is a Tanzanian ame-invest two billion shillings atapata wapikodi TRA atapata wapi? (Makofi)

Sasa ushauri wangu, Dkt. Mpango leta kasheria humumimi sijui procedure. Economic Intelligence Unit iliyoko chiniya TRA ipewe mamlaka makubwa ya kisheria kufanya analysisna kukuletea ripoti na kukupa mamlaka ya kum-summonWaziri yeyote anaye-hinder your productivity ili tuondokekwenye haya matatizo. (Makofi)

Page 213: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

213

Mheshimiwa Spika, nikupe mfano mwingine, miminimeamua kuongelea hii tu hebu tuulizane maswali kwa ninitumeenda na ambush na mapolisi na mabunduki kwendakufunga Bureau de Change, why? hatuna sheria, hamnasheria inayosimamia biashara ya fedha ya nje kwa sababuya luxity ya watu walioajiriwa kusimamia kazi yao tunatafutashortcut we are going to destroy the sector matokeo yaketutaandikwa kwenye international news kwamba hawa watuare not friend in business inatu-take ages ku-clean that mess,it’s not because we don’t have laws, we have good laws inthis country. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la tatu tumbaku hapa WaziriMpango ametaja sekta zinazochangia zilizokua kwa haraka,mwaka huu sekta ya kilimo imekuwa kwa asilimia tano na hiiimekuwa kwa kudra ya Mwenyezi Mungu, ninarudia kwakudra ya Mwenyezi Mungu. Mvua mwaka jana zimekuwanyingi growth yetu imetoka 3.7 to 5% ingawa marginal growthna hili ni jambo muhimu sana wachumi wawe wanafanyaanalysis tunasema tu sekta imekuwa, imekuwa kwa kiwangogani compared na mwaka jana marginal growth yetu is lessthan ourpopulation growth, ndiyou kweli sasa nini inatokeatumbaku, Zitto kataja Kampuni ya TLTC.

Mheshimiwa Spika, nataka nikwambie hivi it is a badnews again Alliance One ambaye ananunua tumbaku Mkoawa Tabora, TLTC ndiyo wanunuzi wakubwa wa kwetukinachotokea umeona hii karatasi ina page 14 haya yote nimautitiri ya kodi na nini, crisis VAT returns hawarudishiwi hawawatu wa TLTC leo wanafunga Waziri amejitahidi wa-investment mwezi Aprili amekutana nao, lakini mimi najuahawajafikia muafaka wala kutatua tatizo kwahiyo mwakahuu tumbaku tuliyozalisha mwaka juzi ilikuwa kilo milioni 1.2imeshuka mpaka 370,000 uzalishaji wa tumbaku unashuka….

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Bashe.

MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Spika, mojatunimalize nataka niombe kwa heshima kabisa WaziriMpango unaweza ukawa unaweza ukawa unafanya kazi

Page 214: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

214

kubwa tutajenga Stigler’s, tutajenga TRC, tutajengaeverything if hatu-encourage productivity na kufanyabiashara katika nchi hii miradi mikubwa yote inayoifanyahaiwezi kusaidia kukua kwa uchumi, ni lazima Serikali watu,wabadilike TRA rudisheni VAT mna-suffocate economy yawatu na cash flow za wafanyabiashara. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nashukuru na naunga mkono hoja.(Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Hussein Bashe,Mheshimiwa Peter Selukamba, dakika kumi.

MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Spika,na miminianze kwa kumpongeza Waziri wa Fedha kwa speech yakenzuri sana.

Mheshimiwa Spika, mimi nitaongelea kwa kweli jambomoja biashara na financial institutions. Asilimia 97 ya kaziTanzania zinakuwa-offered na private sector, kwa hiyo,nataka tuelewane hapa vizuri kama kuna mwajiri wa kwanzamkubwa Tanzania ni private sector, so lazima huyu mwajirihuyu tumlinde, lazima tuje na instrument za kufanya huyuafanye vizuri zaidi.

Mheshimiwa Spika, tuna benki za biashara tuna benkiya maendeleo ama investment benki kazi yake ni nini. Kaziya benki hizi ni kuchochea uchumi na biashara hata kamawatapata faida lakini cha kwanza ni biashara wachochee.Sasa kinachotokea tungalie investment bank tunaifanyia niniili iweze kufanya hiyo kazi vizuri. Lazima tuandae mazingira ilihii development bank ifanye vizuri zaidi watu wakope,wawekeze ili biashara ichangamke. Kwenye commercialbank biashara haiwezi kwenda kama commercial bankhaziendi.

Mheshimiwa Spika, leo Ndugai umeanzisha biasharautanisamehe, umeweka mkopo benki/umeenda kukopamkopo benki umeweka mortgage ukishaweka mortgageunapewa pesa. unakwenda kufanyabiashara unashindwa

Page 215: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

215

kulipa deni, ukishindwa kulipa deni benki inasema tunauzanyumba TRA wanakuja wanaweka kitu kinaitwa ganesh orderkwamba sasa kabla hujachukua hela zako benki huyutunamdai kodi, tupe kodi yetu, kinachotokea benkiinafanyaje NPL zinapanda so leo TRA kwa... kwenye mortgagewao ni super power kuliko aliyetoa fedha maana yake ni nini,maana yake ni moja tu. Watu wengi hawatokopeshwakwenye mabenki kwa sababu itabidi utajikutawanaokopeshwa ni hao hao breweries, wakina Azam walewale wakubwa, wadogo inaanza kuwa shida tukija hapambele tunasema kuna mikopo chechefu. Lakini wakati huohuo mabenki yanatoa fedha ikitoka hapo watu wanaendamahakamani wanaweka order hawezi ku-escute ile order somahakama inashughulika na banks, TRA inashughulika nabanks, NPL zinapanda mabenki yanafanya nini yataanzakufunga branches, yataanza kufanya nini yataanzakupunguza wafanyakazi, yataanza kufanya nini fedhaambazo walikuwa wanalipa za cooperate tax zitaanzakupungua.

Sasa naomba Serikali au contract firming mtuanataka kujenga barabara anakuja anachukua mkopoanapewa anajenga barabara TRA wanakwenda TANROADShuyo mtu huyo tunamdai kabla hujamlipa kule benki tupehela zetu kabisa, so the priority now is TRA kwa maana yarevenue ni jambo jema, lakini tusisahau kama hizi financialinstitutions zisipochangamka biashara haitochangamka.

Mheshimiwa Spika, mimi nasema kwa sababu ndiyomaana leo BOT wameshusha treasury bills rate, lakini badokama unajua interest rate hazijashuka za mikopo kwa sababugani? Risk bado ni kubwa na ni kwa sababu ya serahizitunajichanganya. Kwa hiyo, mimi naomba jamanibiashara ndiyo itakayofanya nchi hii twende kwa kasi .

Mheshimiwa Spika, kwa mfano mwaka 2015/2016fedha iliyokuwa inakopwa kwa ajili ya agriculture ilikuwaasilimia 11.2, mwaka 2018 ikashuka to negative four, 2019kumetokea jambo zuri na ningependa baadaye Waziri

Page 216: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

216

atuambie tumepanda kwa asilimia 45. Je, tumepanda 45%kwenye sekta moja hiyo ya korosho tu au na mazao mengine?

Mheshimiwa Spika, personal lending mwaka 2015/2016 ilikuwa asilimia 37.2; leo hii personal lending imeshukakwa asilimia 17.5 maana yake ni nini? Kuna retrenchmentwatu hawaaminiki, kwa hiyo hawakopesheki. Waziri waUwekezaji anisikie mwaka 2015 investment kwa GDP ratioilikuwa asilimia tano, leo investment imeshuka kwa 2.3 to ratio.

Mheshimiwa Spika, kwa nini nayasema haya maanaenvironment ya biashara ndiyo itafanya kodi iongezeke,ndiyo itafanya tuweze kupata ajira. So lazima tunapotengapolicy zetu tulinde biashara na Waziri amesema vizuri sananimemsikia leo anasema katika sekta ambazo zimekua sanaya Mwakyembe na nyingine, lakini kilimo hakijakua sana,lakini kilimo ni 80% yaani population yetu wanaolima ni asilimia80 hawa asilimia 80 growth yake asilimia tano sababu ni nini?

Mheshimiwa Spika, sababu ya kwanza tumeendeleakuwa na traditional agriculture bila ku-embrace commercialfarming hatuwezi, mifano ipo Zimbabwe ni mfano madhubutikwa kiburi cha Mugabe aliua commercial farming, leowanakufa njaa na mashamba/ardhi si wanayo tuna ardhikubwa sana nilisema juzi, lakini lazima tuje na mkakati wagrowth, tujiulize maswali kwenye tumbaku tumekuwa?Kwenye kahawa tumekua? Kwenye pamba tumekua?Kwenye korosho tumekua? Twende huko lazima Waziri waFedha mwambie Waziri wa Kilimo tuanze kupambana kwagrowth kwamba mwaka kesho seme tumetoka tani tanotumeenda tani kumi haya ndiyo maendeleo, lakini kamahakuna growth leo pamoja Tanzania tuna ardhi kubwatunazalisha tani 50,000 za kahawa. Uganda tani 288,000maana yake ni nini kuna kitu hatujafanya na ndiyo narudikule tukifanya mabenki yafanye vizuri watakopeshawakulima, watakopesha wafanyabiashara, tutapata growthkwenye biasharara na tutapata growth kwenye kilimo.

Mheshimiwa Spika, kil imo ndiyo jambo pekeelitakalofanya industrialization iwezekane, maana kilimo ndiyo

Page 217: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

217

raw material. Sasa lazima tuulizane hapa, hivi kweli tuna ardhikubwa tunazalisha tani 19,000 za mkonge wakati tunacapacity installed ya tani milioni moja shida ni nini tunachukuamashamba tunakwenda kuwagawia watu wadogowadogo, na mimi nasema mimi jamani naomba leo ni-declare kama kuna jambo siliamini ni ujamaa, siamini.(Makofi)

SPIKA: Ahsante sana.

MHE. PETER J. SERUKAMBA: Baada ya kusema hayolakini nimalizie kwa neno moja tu, jambo moja, Waziri waFedha mwaka jana alitoa amnesty ya watu walipe kodiambao hawajalipa kodi za nyuma, kuna watu wamelipaasilimia 50, asilimia 70 mpaka kwenda juu, ningemuombaWaziri wa Fedha wale ambao wameonesha interest ya kulipaover 50% a-extend time kwa sababu hawa wana niahawajamaliza kwasababu hali ya biashara ngumu.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo naombakuunga mkono hoja. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana na nashukuru sana.

Waheshimiwa Wabunge, naomba mnivumiliehatutaenda sana ninawachangiaji kama wachache sana,nipate upande wa CUF na tumalizie na MheshimiwaNsanzugwako. Upande wa CUF mnagawana dakika tano/tano Mheshimiwa Katani, halafu Mheshimiwa Mbarouk halafuMheshimiwa Nsanzugwako utatufungia pazia. Dakika tanoMheshimiwa Katani.

MHE. KATANI A. KATANI: MheshimiwaSpika,nikushukuru sana na nadhani unajua kwamba miminikizungumza bajeti ya Wizara ya Fedha mimi naangalia sanakwenye kilimo kwa sababu asilimia 95 ya watu wangu waTandahimba ni wakulima.

Mheshimiwa Spika, ukisoma Fungu 43 la Wizara yaKilimo fedha iliyokuwa imetengwa ilikuwa kama shilingi bilioni

Page 218: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

218

98.11 ya kugharamia miradi ya maendeleo, lakini hadi kufikiaMachi, 2019 fedha iliyokwenda ni asilimia 42 tu. Sasa kwa sisiwakulima maana sisi wengine ni wakulima typical kamaimekwenda asilimia 42 Waziri wa Fedha nadhani hapa sisawa, pana namna ambayo unapaswa uangalie uone sektahii ya kilimo ambayo kwa Taifa la Tanzania asilimia 85 niwakulima, fedha inayotengwa ya maendeleo inakwendaangalau asilimia 70 ili kilimo hicho tunachokisema tukionekimekuwa.

Mheshimiwa Spika, lakini mmezungumza suala laukuwaji wa asilimia tano kwenye sekta ya kilimo ambayo miminapata mashaka kidogo, kwa sisi wakulima wa koroshoambao tulizalisha tani zaidi ya 300,000 mwaka 2017/2018 namsimu uliopita tumezalisha tani laki mbili na kitu tukaonakwamba kuna ukuaji unaongezeka kidogo ninyi wataalamuwa hesabu mnaweza mkatupa tathmini hiyo mnaitoa kwavigezo gani.

Mheshimiwa Spika, lakini limezungumzwa hapakwenye suala la kilimo tulikuwa na mfumo ule wa fedha ileexport levy ambayo iliondolewa na mzee wangu paleKamala alikuwa ameomba kwamba Serikali sasa ione namnabora ya kuleta pembejeo za ruzuku kwa ajili ya kusaidiawakulima. Hili nadhani Mheshimiwa Waziri uangalie kwanamna ya pekee sana, itakuwa jambo muhimu na busarasana kwa wakulima suala la ruzuku. Kwetu sisi kwenye koroshomfano msimu huu tusipopata ruzuku kutoka tani 200,000 hizozinazozungumzwa kuna uwezekano mkubwa msimu huutunaokwenda tunakwenda kuzalisha tani 80,000.

Kwa hiyo, ni ombi langu kwa Wizara ya Fedhaambayo mwaka jana fedha zetu zimechukuliwa,tumesamehe, zimekwenda, tuone basi namna ya ku-recoverhili jambo at least wakulima wapate ruzuku ya pembejeo yakorosho ili tuende kuanza msimu vizuri.

Mheshimiwa Spika, lakini nizungumze suala la miradiya mikakati, Mheshimiwa Waziri na Mheshimiwa Naibu Wazirikuna siku nilikuandikia memo pale nikiwa nakwambia

Page 219: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

219

Tandahimba ambayo ndiyo wazalishaji wakubwa wa koroshomradi wa mkakati ambao walishaleta na mradi ule godownmmeshindwa kupeleka Tandahimba ambako wanazalishatani zaidi ya 70,000 unakwenda kujenga ghala sehemuinayozalisha tani 10,000 hizo fedha mnazopeleka kwenye tani10,000 return yake itakuwa kwa muda gani? Kwa sababu hizofedha mngepeleka Tandahimba wanakozalisha tani 70,000maana yake baada ya miaka miwili, mitatu kulikuwa napossibility kubwa ya fedha zenu kurudi, lakini unapopelekafedha, mmepeleka fedha Mkuranga ambako wanazalishatani 4,000 ukaacha kupeleka fedha Tandahimbawanakozalisha tani 74,000 ninyi wenyewe wataalamu wauchumi sijajua, sijajua kitaalamu mnafanya utaalamu wanamna gani? Mnataka fedha zirudi ziweze kuwasaidiawatanzania wengine au mnapeleka sehemu ambako fedhazitakaa miaka 15, 20 tukawa tunaendelea kulalamikamatatizo ya fedha.

Ombi langu kwa Serikali, miradi hii ya mikakatipelekeni kwenye Halmashauri ambazo zinaweza kurudishafedha, mfano Tandahimba ambayo inazalisha koroshozinauwezo wa kuzalisha tani 70,000 ina uwezo wa kuzalishatani 80,000 ungepeleka mradi wa mkakati kama wa godownambao Halmashauri ishawaletea mradi huo na bahati nzuriulikuwa vizuri sana, return yake ilikuwa ya muda mfupi, leoinawezekana tungekuwa tumeshaanza kurejesha.Niwaombe sana muangalie mambo haya kwa namna yakibiashara na kuona namna mnavyoweza kuzichukua fedhakupeleka sehemu nyingine.

Mheshimiwa Spika, niwaombe sana watu wa Wizaraya Fedha tumeona Benki ya Kilimo, Mwanza wakatitumeenda wakati wa Kamati ya Kilimo tumeona wenzetummewapelekea tawi kule, lakini nimesoma kitabu chakoMheshimiwa Waziri nimeona Dodoma pana tawi, lakininimeona mna maandalizi ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusinikule Mbeya, nione sasa kuna umuhimu wa makusudi kabisakwa sehemu yenye uzalishaji mkubwa mfano wa koroshoMtwara nako kuwe kwenye mpango wa kupeleka Benki yaKilimo ili at least watu wale wapate mikopo…

Page 220: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

220

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Katani, MheshimiwaMbarouk halafu Mheshimiwa Nsanzugwako.

MHE. MUSSA B. MBAROUK: Mheshimiwa Spika, ahsantelabda na mimi nianze kwa kumshukuru Mwenyezi mungu kwakutujaalia kuwa katika Bunge letu hili tukiwa na afya njema.

Mimi niseme tu kwamba pamoja na kumpongezaMheshimiwa Waziri, lakini bado hali yetu ya maishaWatanzania ni ngumu hususan ukiangalia hali ya kiuchumikila siku inaendelea kuwa ngumu na maisha katika Tanzaniakila ni afadhali ya jana na hii inatokana na nini kwanzamazingira kibiashara na kodi sio rafiki na hili nalisema kwasababu ukiangalia tuna tofauti kubwa na wenzetu.

Sisi watanzania unaanza kulipa kodi kabla hujafanyabiashara, ukitaka kufungua biashara kwanza upate TINNumber, uende TRA wakufanyie assessment, kabla ya hilihalijafanyika unaanza kulipa sasa inakuwa ni taabu nahususan niende kwa akina mama, akina mama wengi niwafanyabiashara wadogo wadogo, wajasiriliamali, wenyemaduka ya nguo, wenye maduka ya vyakula, lakiniwanapata tabu hali ya kuwa kwanza hata mikopowanapochukua msharti ni magumu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa hili naliona ni tatizo kubwakibiashara ukinagalia baadhi ya nchi jirani kama Kenya,labda Rwanda au Uganda wenzetu wafanyabiashawanapaanza wanapewa tax holiday ya karibu miezi sitaangalau wajiimarishe waweze kujua faida wanapata vipi naaangalie mtiririko wa biashara unaendaje, lakini kwetu nitofauti. Sasa nashauri Mheshimiwa Waziri jambo jema huigwa,hebu tuige wenzetutuwasidie wafanyabiasha wetu wadogo.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, yamesemwa maneno mengihapa na wenzangu, lakini kiukweli hata ukija kwenyemfumuko wa bei tunasema tu kwamba mfumuko wa beiumepungua kwa 3.9%. Lakini h ivi tuulizane Wabunge ni kwelimfumuko wa bei umepungua? Twende kwenye petrol na

Page 221: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

221

diesel tunayoitumia mwaka jana ilikuwa takribani shilingi 1800leo shilingi 2290. Hapa mfumuko wa bei umepungua auumepanda? Wale tunoafunga tunajua mwaka jana bei yakilo moja ya tambi ilikuwa shilingi 1800 leo shilinig 2500.Maharage yalikuwa kilo moja shilingi 1700 leo shilingi 2400,sukari ilikuwa shilingi 1900 au shilingi 2000 leo shilingi 2500.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa mwananchi wa kawaidaunapomwambia kwamba mfumuko wa bei umepunguahakuelewi hata tukienda kwenye shilingi yetu ta Tanzania kilakukicha thamani ya shilingi ina shuka. Tujilinganishe na Kenya,tujilinganishe na dola ya Marekani hela yetu inazidi kupunguathamani kila uchao, lakini tunasema uchumi unakuwa patona Taifa linaongeza, lakini mwananchi wa kawaida mtaaniukimtanzama amechoka hohe hahe, hajielewi kabisa yaanihaelewi somo.

Mheshimiwa Spika, sasa mimi nisemetunaponzungumza mambo mengine tuwafikirieni hawawatanzania wenzetu ambao asilimia kubwa wapo vijiji namijini na ambapo wengine hawana hata ajir iunapomwambia mtu uchumi umekuwa hata hakuelewi. Kwahiyo, niseme hebu tuwaeleze ukweli lakini vilevile piatuwaweke mazingira rafiki ya biashara kwa sababuwafanyabiashara wengi sasa hivi wanalalamika.

Mheshimiwa Spika, juzi hapa nilikuta Katibu waChama cha Biashara Mkoa wa Tanga ananiambiaMheshimiwa kutokana na ukali wa kodi nina barua 60 zawafanyabiashara ambao wanataka kufunga biasharawanaandika barua TRA ili wasidaiwe tena kodi. Sio Tanga tu,Dar es Salaam leo ukitaka frame katikati ya Jiji Kariakoo leounapata. Kwa sababu gani watu wanashindwa kufunguabiashara, mzunguko wa fedha umekuwa ni mdogo biasharazinafungwa na mwaka jana nilishauri hili Mheshimiwa Wazirialisema katika moja ya mafanikio Wizara ni kwambawamefunga biashara takribani 300 kwa Dar es Salaam. Nanilisema kufunga biashara sio mafanikio kwa sababu kilabiashara moja uliyoifunga pana wafanyakazi labda hao

Page 222: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

222

kwenye duka ua kampuni hao wanategemewa na watu 11mgongoni, sasa unaposema umefunga biashara kwanzatunakosa mapato, lakini pili tunateketeza familia zaWatanzania.

Kwa hiyo mimi niseme kufunga biashara kodi kubwasio mafanikio ni matatizo watu hawana ajira Tanzaniawanakimbilia kwenye biashara. Kwenye biashara napo kodikubwa wakienda kwenye kilimo ndio hivyo, kwenye koroshokuna matatizo, sasa tunaelekea mpaka kwenye mahindi.

Mheshimiwa Spika, amezungumza hapa Waziri waKilimo kwamba wenye mahindi mengi wampe taarifa. Lakiniwatakapokuwa wemeleta hiyo taarifa kodi itapungua?Hawawezi kutoa taarifa kwa Waziri wa Kilimo kwa sababuwanajua nikisema nina tani 50 za mahindi tayari TRAwatanikalia benet, hawawezi kukupa, lazima tupunguze kodinafikiri wajua katika commerce kuna the law of demand.

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Mbarouk.

MHE. MUSSA B. MBAROUK: Mheshimiwa Spika,kwamba the low price, high demand and the high price,low demand. Tuweke mazingira hayo angalu tuwasaidiewafanyabishara. Wafanyabiasha hasa sisi wa mikoa ya karibuna mipakani wananchi wetu wanakwenda Kenya, Ugandana Congo kuchukua bidhaa ili waweze kuuza wajipate kipatocha kila siku, ahsante. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Nsanzugwankodakika kumi utufungie uchagiaji kwa siku ya leo.

MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Spika,ahsante nashukuru kwa kunipa nafasi hii nitakuwa namachache.

Mheshimiwa Spika, la kwanza kabla sijasahauningependa Mheshimiwa Waziri wa Fedha atakapokujaatueleze zile kodi zinazodaiwa (tax refund) kwa mwakammoja kwa sababu kuna mashirika mengi na baadhi ya

Page 223: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

223

mashirika ni yale hata Serikali yenyewe ina hisa, lakini wanadaitax refund. Ningependa Waziri aje na figure atueleze angalaukodi ambayo TRA wanapaswa kui-refund kwawafanyabiashara na makampuni ni kiasi kadhaa. Kwa hiyo,nilikuwa naomba hilo kabla sijasahau.

Mheshimiwa Spika, nina mawili madogo tu, la kwanzaningependa sana sana hayo yaliyozungumzwa jambo nimoja ni menejimenti ya uchumi wa nchi yetu. Bahati nzuriWaziri wa Fedha na Naibu wake ni wataalam wa masualahaya, ukisikiliza michango ya Wabunge yote hata Wapinzaniwetu walivyosema ni kwamba lipo tatizo la msingi laeconomic management ya uchumi wa nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, hili jambo ushauri wangu mamboni mengi na nchi ni kubwa. Nchi hii lazima tu-source talent zawenye uwezo mkubwa. Kuna watu wana uwezo mkubwakatika nchi yetu. Watu kama akina Profesa Ndulu kwa mfano,natoa mfano watu kama wakina Mafuru yule aliyekuwa TRkwa mfano na wengine wengi wapo wengi ndani ya CCMna nje ya CCM. Watu ambao tunaweza tukawafanya kamathink tank ya nchi yetu wakamsaidia Waziri wa Fedha katikaku-manage uchumi wa nchi hii yako mambo mengi, mengiambayo nina hakika yangetuletea fedha nyingi sana katikanchi yetu.

Mheshimiwa Spika, maana hapa shida ni kwambauchumi ni mdogo, sungura ni mdogo lakini bado vipo vyanzovingi sana fedha ambavyo havijaguswa, kwa mfano, chukuaitem moja uvuvi wa bahari kuu, alikuja mtaalam mmojakutoka Zanzibar, alikuwa Mzanzibar mwenye maarifa mengisana wakati nipo Kamati ya Kilimo na Mifugo. Alitupitishakwenye uchumi wa bahari kuu, alitushawishi kabisa kwambakile ni chanzo ambacho hakijaguswa kabisa. Kwa sababukuna nchi zinaendeshwa kwa kodi ya uvuvi wa bahariniSeychelles, Maldives ni nchi ambazo zitegemea uchumi wabahari kuu, lakini sisi hatuzungumzi na hata kwenye kitabuhusikii kama Waziri wa Fedha anazungumza kama kunasource revenue nyingine muhimu sana ambayo imejifichakwenye bahari yetu.

Page 224: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

224

Mheshimiwa Spika, ningeshauri sincerely bado kabisakwamba Waziri wa Fedha una mamlaka kwa mujibu wainstrument yako unda timu ya wataalam, wazee kama kinaMzee Ndulu wakushauri mambo ya msingi yakufanya.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili ambalo ningependanizungumze ni haya mashirika na makapuni ambayo Serikalizina hisa. Tuchukue mfano hivi Kampuni kama KilomberoSugar Company, kama TPC, Kampuni kama Puma Energyhivi Serikali ina maximize hisa zake zilizopo kule? Ni mamboya kujiuliza tu. Sisi tulitembelea wakati nipo Kamati ya Kilimotulitembea Kilombero Sugar Company, tukakuta pale kunahisa kubwa za Serikali; 25% ya hisa za Kilombero SugarCompany ni za Serikali. Ukienda TPC 30% ni za Serikali naukienda Puma Energy 50% ni za Serikali, lakini kweli Serikaliina maximize?

Mheshimiwa Spika, nafikiri wakati umefika Msajili waHazina ifanye kazi yake kwa umakini mkubwa ili mashirikahaya ambayo Serikali iliwekeza hisa zake yaweze kuwa faida.Mheshimiwa Waziri Mpango naamini ile dividend ya bilioniya tano/bilioni saba/bilioni mbili/milioni 500 ni kidogo mno.Naamini kabisa haya mashirika na yapo mengi kweli kweliyapo mengi tunapata kidogo sana ukilingaisha na investmentya hisa Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukianga dividend ambayoinalipwa njoo kwenye kodi malipo ya kodi, njoo kwenye ajirana Mheshimiwa Jenista wewe ni Waziri wa Ajira, jambo linginekubwa katika nchi yetu ni suala la ajira jamani. Suala laemployment ni jambo kubwa sana, ni jambo kubwa, vijanawanatoka vyuo vikuu na wote tunaona kwamba ni mamboya kawaida.

Kwa hiyo, mashirika hayo mwenyekiti yapo mengiyapo zaidi ya 200 na mimi na hakika bado mchango wakekwa uchumi wa Taifa letu, mchango wake kwa pato letu,mchango wake kwenye Mfuko wa Hazina bado ni kidogo nikidogo ni kidogo sana.

Page 225: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

225

Mheshimiwa Spika, jambo la pili ambalo ningependanilizungumze ni jambo la TRA. Nashukuru nah ii tunamshukuruMheshimiwa Rais mwenye ndio ameingilia kati kwamba TRAwawe marafiki wa wafanyabiashara, otherwise ilikuwaimefika mahali sasa TRA kazi yao ni kuwindawafanyabiashara. Na rafiki yangu ana kiwanda kule Arushaalifuatwa na bunduki na polisi wakachukua computer zakena maskini ya Mungu akaamua kuacha biashara ame-reallocate amekwenda Jinja nchini Uganda.

Mheshimiwa Spika, sasa angalau tunaona TRAwameanza angalau kuwa marafiki wa wafanyabiashara,hiyo inatutia moyo na TRA sasa waende na trend hiyo,kwamba kazi ya TRA iwe ni ya kukusanya kodi na kamwewasiwe maadui wa wafanyabiashara na wewe responsiblekwa wafanyabiashara, wawasikilize wafanyabiashara, bilawafanyabiashara hawa kusaidia uchumi wa nchi hii tutapatamatatizo na hatuwezi kujidai kwamba nchi itakwendayenyewe bila kuwa na private sector na bila kuwa na hawawafanyabiashara. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambaloningependa nitoe angalizo kwa Wizara ni matumizi makubwaya Serikali. Ninaamini bado Serikali ina matumizi ya hovyo namakubwa sana. Kwa mfano, hivi nchi maskini kama hii nchiinayoendelea kama hii inawezaje ku-afford misaada yaSerikali inanunua magari ya kifahari ndio wanayotumiawatendaji wetu ambapo maskini wanapaswa watumiemagari ya kawaida kabisa. Unakuta gari shangingi, Vx 8, DFPiko Kasulu kule, mambo ya ajabu kabisa haya.

Mheshimiwa Spika, huko nyuma ilikuwa mkazo natrend ni matumizi ya Serikali hovyo ya Serikali ili fedha nyingikama anavyosema Mheshimiwa Rais Magufuli tuzipeleke kwawatu tukajenge vituo vya afya tukajenge shule zetu nakadhalika na kadhalika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini Mheshimiwa Waziri badoyapo matumizi ya hovyo ya magari ya anasa kabisa ambayohajapaswi kuwepo katika nchi yetu. Ukienda Uganda na

Page 226: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

226

nilibahatika kwenda Uganda mwaka jana tulikweda kwenyeziara ya wakimbizi. Ukienda Uganda hawana trend hiyo, hiyoluxury hiyo wameshaiacha. Hatusemi watembee na baiskeliMheshimiwa Jenista no, no hoja sio hiyo, hiyo ni kupotoshahivi kwa mfano una mpaje Regional Manager wa TANROADSshanging Vx 8 why?

Mheshimiwa Spika, Regional Manager wa TANROADSkwa nini usimpe a good pickup car akikuta bango labarabara limeanguka, akatoka kwenye gari yake,akachukua bango lake, akaweka kwenye gari yake nimetoamfano mgodo tu. Kwanini umpe Vx 8 nani ana service gariile? (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, hoja ya msingi ni kwambaMheshimiwa Waziri nenda kaangalie kwenye archives yakobado matumizi ya hovyo ya Serikali ni makubwa sana naSerikali ina kazi nyingi sana za kufanya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la mwisho nikukumbusheMheshimiwa Waziri, sisi Halmshauri ya Mji wa Kasulutumeshatoa kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya TRA, kwamaana ya Buhigwe na Kasulu tumetoa kiwanja bure kwa TRAkujenga ofisi zake na mwaka wa jana uliniahidi kwamba TRAwataanza kujenga ofisi pale na kile kiwanja tumewapa bure,sasa mambo mawili au mnajenga au hamjengi turudishienikiwanja chetu tukitumie kwa mtumizi mengine. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimshauri Waziri wa fedha afanyeziara katika Wilaya ya Buhigwe na Kasulu ajionee hali halisiyamambo yalivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada kusema hayo nakushukurunaunga mkono hoja hii, ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa DanielNsanzigwako, nakushukuru sana. Umenikumbusha piaKongwa kule yaani Ofisi ya TRA ukiitembelea ni chumba nasebule. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri na Bwana Kichere huko

Page 227: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

227

muangalie angalie baadhi ya mambo hatutaki ghorofanyumba nzuri inayofanana na TRA.

Waheshimiwa Wabunge, nawatangazieni kwambataasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kwa kushirikiana nawadau mbalimbali kama alivyosema Waziri wa Nishati naMadini siku ile ya kuwasilisha hotuba yake ya bajeti wameletahapa mfano wa magari ambayo yanayotumia nature gasambayo unaweza ukabaili gari lako la mfumo wa petrolilikatumia gesi.

Waheshimiwa Wabunge, kwa kuzingatia umuhimu wateknolojia hii, wameleta pale nyuma ya Ukumbi wa Msekwaunaweza ukapita kwa wakati wako ukaangalia hilo gariambalo lipo pale linatumia mfumo wa gesi asilia.

Kwa hiyo, tunaomba mkipata muda mchana huummpite pale muweze kujionea wenyewe utaalamuunapoelekea kwa matumizi ya nishati ya gesi asilia.

Basi tutarudi saa kumi jioni ataanza Mheshimiwa NaibuWaziri kadri watakavyogawana labda dakika kumi na tanoau zaidi kidogo, lakini mna saa moja kwa pamoja. Kwa hiyotukianza saa kumi ataanza Naibu halafu atakuja Wazirimwenyewe na tutamaliza kwa wakati leo. Leo hatutazidishahata dakika moja.

Kwa hiyo, nasitisha shughuli za Bunge hadi saa 10:00jioni ya leo.

(Saa 7:16 Mchana Bunge lilisitishwa hadi Saa 10:00 Jioni)

(Saa 10.00 Jioni Bunge lilirudia)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu.

Page 228: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

228

NDG. MOSSY LUKUVI - KATIBU MEZANI:

HOJA ZA SERIKALI

Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Wizara ya Fedha naMipango kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020

(Majadiliano Yanaendelea)

SPIKA: Sasa naomba nimuite Mheshimiwa Naibu Waziriunaweza ukaja mbele hapa tafadhali, karibu sana, karibusana Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji una dakika ishirini, karibu,pitia hoja za Waheshimiwa Wabunge. (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaSpika, ahsante sana, kwa kunipa fursa hii ya kuchangia hojahii ya hotuba ya makadirio ya bajeti ya Wizara ya Fedha naMipango kwa mwaka 2019/2020 kama ilivyowasilishwa naMheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango.

Mheshimiwa Spika, naomba nianze kwa kumshukuruMwenyezi Mungu kwa kutupatia fursa tena ya kukutanakatika Bunge lako tukufu kwa ajili ya jambo hili kubwa kwaajili ya Taifa letu na Watanzania kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, naomba nimpongeze sanaMheshimiwa Rais wetu Mheshimiwa Makamu wa Rais naMheshimiwa Waziri Mkuu kwa kazi kubwa wanayoifanya kwaniaba ya Watanzania, kwani waliwaamini na sisi tunaona naWatanzania wanaona utekelezaji wa Ilani ya Chama chaMapinduzi unavyotekelezwa kwa kasi kubwa kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nikushukuru na wewebinafsi pamoja na Mheshimiwa Naibu Spika, Wenyeviti wotewa Bunge kwa miongozo yenu mnayotupa tunapokuwakwenye Bunge hili Tukufu ili tuweze kuwatumikia Watanzaniakwa ujumla wake tunawashukuruni sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nimshukuru sana,Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango Kaka yangu Dkt.

Page 229: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

229

Philip Mpango kwa kazi kubwa anayoifanya kwa ajili yaWatanzania kwenye Wizara hii ngumu kama ambavyoimeelezwa na Waheshimiwa Wabunge huu ndiyo moyo waSerikali yetu, ndiyo roho ya Taifa letu hakika nakupongezasana Dkt. Philip Mpango kwa kazi kubwa unayoendeleakuifanya na mimi nakutia moyo uendelee kulitumikia Taifaletu wala usirudi nyuma kwamba lazima apatikaneMtanzania wa kulibeba hili kwa kipindi hiki na Mtanzaniaaliyechaguliwa, Mtanzania aliyeaminiwa, Mtanzaniaaliyeteuliwa na Mwenyezi Mungu ni wewe kwa ajili ya Taifaletu, usikate tamaa endelea kusimama imara naaminimishale yote inapiga lakini naamini bado uko imara, endeleakusimama imara Mheshimiwa Waziri wangu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema maneno hayo,naomba pia niwapongeze sana, watendaji wetu ndani yaWizara ya Fedha na Mipango na wao pia naomba niwatiemoyo, waendelee kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu wahali ya juu, wameipata nafasi ya kuwatumikia Watanzania,wawatumikie Watanzania kwa moyo wote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya maneno hayo yautangulizi naomba sasa niseme maneno machache kwenyehoja ambazo zimechangiwa na Waheshimiwa Wabunge nanianze na hoja ya kwanza ambayo ilisema makusanyo yakodi yameshuka sana kipindi hiki cha Serikali ya Awamu yaTano.

Mheshimiwa Spika, naomba niseme jambo hili siyo lakweli hata kidogo, siyo la kweli kwa sababu Watanzaniawanaona, Watanzania wanaona yanayotendeka ndani yaTaifa lao, ni kupitia makusanyo ya kodi haya ambayo leotunaambiwa yameshuka.

Mheshimiwa Spika, kama makusanyo ya Kodiyameshuka, tungeweza wapi kuanza utekelezaji wa mradiwa reli ya kisasa, isingewezakana hata kidogo,isingewezekana leo hii Stiegler’s Gorge kule Rufiji, mradi uleumeanza kutekelezwa kama makusanyo yangekuwa ni yachini kama inavyodaiwa kwenye Bunge hili tukufu. (Makofi)

Page 230: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

230

Mheshimiwa Spika, niwaombe Waheshimiwawabunge, tuwape moyo watumishi wetu wanaoshughulikana kazi hii ngumu ya ukusanyaji wa mapato ya Taifa letu,wanaifanya kazi katika mazingira magumu, wanaifanya kazihii kwa kujitolea maisha yao, ni kazi ngumu, ni kazi yenyeviahatarishi vingi lakini wanaifanya kwa nguvu zao zote.

Mheshimiwa Spika, nimeanza kusema kwamba siyokweli makusanyo yamepungua kwa sababu ukiangalia kwamiaka mitano mfululizo, tukianza mwaka 2014/2015 makadirioya ukusanyaji wa Kodi yalikuwa ni shilingi trilioni 11.9, kipikilikusanywa mwaka 2014/2015.

Mheshimiwa Spika, kilichokusanywa ilikuwa ni trilioni10.66 hicho ndicho kilichokusanywa 2014/2015 kabla Serikaliya Dkt. John Pombe Magufuli ya Awamu ya Tano haijaingiamadarakani, leo tunapoongea mwaka 2017/2019 kipikimekusanywa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi yaAwamu ya Tano.

Mheshimiwa Spika, makadirio yalikuwa shilingi trilioni17.3 haya ni ya kodi, na nini kilikusanywa, kilichokusanywailikuwani trilioni 15.25 ukilinganisha haya mambo mawiliunaweza ukaelewa, ni kweli mapato yamepungua,makusanyo yamepungua, taarifa hizi bahati nzuri, takwimuza kikodi huwa hazijawahi kudanyanya na hili naombaWaheshimiwa Wabunge tuwatendee haki Watanzania.

Mheshimiwa Spika, Kwa sababu wao ni mashahidiwanaona, wao ni mashahidi wanadhihirisha kile ambachokinatendwa na Serikali yao waliyoiamini.

Mheshimiwa spika, limeunganishwa jambo hili najambo la pili kwamba tunaangalia sasa kati ya uwiano, katiya mapato ya Kodi na Pato la Taifa. Wanasema kwambalimepungua ni kweli uwiano wa Kodi dhidi ya Pato la Taifakutoka asilimia 13.2 mwaka 2016/2017 hadi imefika Pato laTaifa asilimia 12.8 kwa mwaka 2017/2018.

Page 231: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

231

Mheshimiwa Spika, nini kimetokea? Kilichotokea hiindiyo naomba Watanzania waelewe, calculations hizizimefanyika kwa kufuata rebasing ambayo ni marekebishoyaliyofanywa kwenye takwimu za Pato la Taifa, kwambayamefanywa mabadiliko, na kama tusingetumia rebasingmabadiliko ya takwimu za Pato la Taifa, mchango, uwianowa kodi dhidi ya Pato la Taifa ilikuwa ni asilimia 3.6. Kwa hiyokama tungetumia mwaka wa kizio wa 2017, uwiano huuusingekuwa umepungua.

Kwa hiyo, hili linadhihirisha kwamba mapato hayahayajapungua, mapato yako vizuri tukiangalia makadirioyameongezeka na makusanyo halisi yameongezeka, kwahiyo, tuwatendee haki Watanzania, tuwaeleze ukweli kileambacho Serikali yao waliyoiamini kipi Serikali inafanya.

Mheshimiwa Spika, naomba niseme kuhusu jambo lapili nayo ni kuhusu Ofisi ya Msajili wa Hazina kwamba ofisi hiibado haijaonyesha uimara wake kwenye kusimamiakampuni na mashirika ya umma. Naomba kulihakikishiaBunge lako tukufu kwamba Ofisi ya Msajili wa Hazina kwasasa, ni imara sana, na sisi sote ni mashahidi tunaona utendajimzuri wa watumishi wetu kwenye ofisi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nasema hili kwa sababu tunaionaOfisi ya Msajili wa Hazina ikiendelea kufanya tathmini naufuatiliaji ili kuimarisha usimamizi na ufanisi wa mashirika yaumma pamoja na kampuni ambazo Serikali yetu imekezahuko, tunafatilia kwenye hisa chache, lakini pia kule ambakoSerikali yetu ina hisa nyingi.

Mheshimiw Spika, matokeo ya hili tumeona kabisakwamba hata mapato yaliyokusanywa kutoka kwenyegawio, kutoka kwenye kampuni hizi na mashirika ambapoSerikali yetu ina hisa yameongezeka kwa kiwango kikubwasana.

Mheshimiwa Spika, kwa mfano, kwa mwaka huu wa2018/2019 ambapo hadi tarehe 30 Aprili, 2019 Ofisi ya Msajiliwa Hazina il ikuwa imekusanya shil ingi bil ioni 602.64

Page 232: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

232

ikilinganishwa na ilichokuwa kimetarajiwa kukusanywaambayo ilikuwa ni shilingi bilioni 597.77 hii tunaiona ni zaidi yaasilimia 101 na hii ni tarehe 30 Aprili; je, tukienda mpaka tarehe30 Juni, 2019 tunaiona Ofisi ya Msajili wa Hazina ikiwa inafanyakazi yake vizuri katika kipindi hiki.

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Msaji l i wa Hazinainaendelea pia kushughulikia ukaguzi maalum katika taasisiambazo Serikali yetu ina hisa chache ambapo tayari mpakatarehe 30 tulishakagua taasisi 33 na tayari tumeonamapungufu yaliyokuwa yamebainika na mapungufu hayoyanaendelea kufanyiwa kazi ili sasa tuweze kuona taasisi hizina mashirika haya yakifanya kazi kwa tija kwa ajili yaWatanzania.

Mheshimiwa Spika, Serikali yetu pia imechukua hatuambalimbali, haya yote yasingewezekana kama Serikaliisingeimarisha Ofisi hii ya Msajili wa Hazina na Serikaliinaendelea na mambo mbalimbali kuhakikisha Ofisi hiiinaendelea kuwa imara ili tuweze kupata faida kwenye taasisina mashirika haya ambayo tumewekeza, kwa mfano, Serikalitayari imeandaa Waraka wa Baraza la Mawaziri wenye lengola kurekebisha Sheria ya Ofisi ya Msajili wa Hazina ili kuendeleakuiimarisha zaidi, ili iweze kufanya kazi kwa tija zaidi kwa ajiliya Watanzania wote, lakini pia tumeona Serikali yetuimeongeza Bajeti ya kutosha kwenye Bajeti ya maendeleokwenye Ofisi hii ya Msajili wa Hazina hadi kufikia shilingi bilioni2.3 kwa mwaka wa fedha 2019/2020 kutoka bilioni 1.6 tuzilizokuwa za mwaka 2018/2019.

Mheshimiwa Spika, hii yote inalenga kuimarishamifumo ya usimamizi ya kielektoniki ili tuweze kuyafatiliamashirika na taasisi ambazo tumewekeza kama Serikali yetu.

Mheshimiwa Spika, kuhusu utendaji wa Ofisi ya Msajiliwa Hazina, liko jambo ambalo limehojiwa nalo ni malipo yamafao ya wastaafu 1071 wa TAZARA yamefikia wapi.

Mheshimiwa Spika, napenda kuliambia Bunge lakotukufu kwamba kundi la kwanza ni la wastaafu 1172walioacha kazi baada ya muda wao wa kustaafu kutimia

Page 233: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

233

kama ambavyo ilivyoainishwa katika makubaliano yapamoja kati ya TAZARA na watumishi hao.

Mheshimiwa Spika, hivyo basi, kwa kuwa wastaafuhawa hawakustahili kulipwa kiinua mgongo kwa sababuwalikuwa wametimiza vigezo vya kupata malipo ya pensheniambayo yanaendelea kulipwa kila mwezi. Pia kulikuwa nakundi la pili ambalo kundi la pili la wastaafu hawa wanastahilikulipwa ambapo Serikali imeridhia kuwalipa kama ifuatavyona hatua za malipo zimefikia katika hatua mbalimbali, kundila kwanza ilikuwa ni Shauri la S. Dagaa na wenzake 271 kesinamba 88 ya mwaka 2009 hawa Serikali imeridhia baada yakesi kuisha waweze kulipwa shilingi trilioni 1.422.

Mheshimiwa Spika, kundi la pili lilikuwa ni Shauri laKiobya na wenzake ambapo Serikali inatakiwa kulipa jumlaya shilingi bilioni 41.549; Shauri la tatu ambalo ni kundi la tatuwanaostahili kulipwa ilikuwa ni Shauri la Kassim Mshana nawenzake 79 ambapo jumla ya shilingi 814,695,000 zinatakiwakulipwa kwa ajili ya Kassim Mshana na wenzake 79.

Mheshimiwa Spika, kundi la nne, ilikuwa ni Shuari laKaduma na wenzake 130 ambapo wanatakiwa kulipwajumla ya shilingi bilioni 8.042, Ofisi ya Msajili wa Hazinainaendelea kushughulikia malipo yao kwa makundi hayaniliyoyataja na muda siyo mrefu basi watalipwa mafao yaokama ambavyo imeelekezwa na mahakama.

Mheshimiwa spika, jambo lingine ambalo limeelezwakwa urefu na ambalo limekuwa likirudia mara kwa mara nayoilikuwa ni malipo ya wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya AfrikaMashariki.

Mheshimiwa Spika, malipo kwa ajili ya wastaafu hawaSerikali i l ishayamaliza, hii ni kwa mujibu wa hati yamakubaliano yaani deed of settlement ya tarehe 20Septemba, 2005 na kuthibitishwa na mahakama kamahukumu tarehe 21 Septemba, 2005 Serikali tayari ilishawalipastahiki zao wastaafu hawa waliokuwa 31,788 wa iliyokuwaJumuiya ya Afrika Mashariki iliyovunjika tarehe 30 Juni, 1977.

Page 234: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

234

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema haya, naombanirejee kusema naunga mkono hoja hii ya Wizara ya Fedhana Mipango na nakushukuru sana kwa kunipa nafasi. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Naibu Waziri kwa wasilisho hilozuri Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kijaji, tunakushukuru sana,ahsante sana.

Sasa moja kwa moja nimuite mtoa hoja Waziri waFedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango, sasahapa Mheshimiwa Silinde ajiandae kujua Mpango anayekujani yupi. Mheshimiwa Waziri karibu sana. (Makofi/Kicheko)

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika,napenda kwanza nitumie fursa hii kukushukuru sana wewemwenyewe umeongoza kikao hiki toka asubuhi na umerudimchana tunakushukuru sana, sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini, naomba pia nitambuemichango ambayo imetolewa na Kamati ya Bajeti chini yaMwenyekiti wake - Mheshimiwa George BonifaceSimbachawene, Makamu Mwenyekiti - MheshimiwaMashimba Ndaki, Waheshimiwa Wabunge wotewaliochangia kwa kuzungumza na kwa maandishi na badotunaendelea kupokea hata maoni mengine nikiwa hapamezani nimepokea maoni ya maandishi kutoka kwaWaheshimiwa Wabunge wawili.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo jumla ya Wabunge 22niliyo nao mpaka sasa wamechangia hii hoja na kati yao,waliochangia kwa maandishi sasa ni 11 na waliochangia piakwa kuzungumza ni 11. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa kweli nafurahi kwambamichango ni mizuri ambayo imetolewa na WaheshimiwaWabunge wote na nitaeleza kwa muhtasari majibu ya hojambalimbali ambazo zimetolewa, ingawa sijui kama nitawezakujibu hoja zote zilizosemwa kwa sababu ya muda, lakininaomba niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge kwamba

Page 235: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

235

majibu ya hoja zote zilizochangiwa tutaziwasilisha kwamaandishi kabla ya kuahirishwa kwa Mkutano huu wa Bunge.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nianze na baadhi ya hojaambazo zimechangiwa na Kamati ya Bajeti, moja lilikuwa nilile la ukiukwaji wa taratibu katika kuanzisha tozo, ada naushuru kwa baadhi ya Wizara na Mamlaka ya Serikali za Mitaana ambazo zimeendelea kuleta kero kwa baadhi yawananchi, lakini pia wafanyabiashara.

Mheshimiwa Spika, pana ukweli kiasi fulani na Wizaraya Fedha na ikijumuisha hivi karibuni tumeziandikia Wizarazote na mamlaka nyingine wahakikishe kwambawanazingatia utaratibu uliobainishwa katika Sheria ya Bajeti.Pia kwa kawaida mwezi Desemba tunawaandikia wadaundani na nje ya Serikali kuwasilisha mapendekezo ya tozo,ada na ushuru kabla hazijaanzishwa ili ziweze kuchambuliwana tuweze pia kuziwianisha ili kuondoa migongano. Wizarainaitisha pia maoni ya wadau mbalimbali kuhusu hizo kodiambazo zinapendekezwa kuanzishwa au kuzifuta ili kuondoakero kwa wananchi. Kubwa hapa ni kwamba ndugu zanguwote Serikalini wazingatie huu utaratibu ambao ni wa kisheria.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati pia ilibaini baadhiya taasisi ambazo zinapokea mishahara kutoka Serikali Kuu,lakini bado zinatumia utaratibu wa retention. Ushauri waKamati umepokelewa na kwa mujibu wa sheria zilizoanzishahizi taasisi, Bodi za taasisi hizo zimepewa mamlaka yakuidhinisha bajeti husika katika ngazi ya awali. Vilevile Sheriaya Bajeti Na. 11 ya mwaka 2015 na hususan kifungu kile cha17 na kifungu cha 22 vimetoa mamlaka kwa Msajili wa Hazinana Katibu Mkuu Hazina kupitia na kuidhinisha bajeti za taasisina mashirika hayo ambayo tumeyaona. Tutalitazamatunavyokwenda mbele tuone namna ya kuondoa upungufuhuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati i l itupongezatunawashukuru sana kwa jitihada ambazo tunaendelea

Page 236: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

236

kuhakiki na kulipa madeni ya wafanyakazi, wazabuni, watoahuduma na wakandarasi na ni kweli suala hili limekuwa ni lamuda mrefu. Pamoja na kupokea ushauri wa Kamati, nisemetu kwamba Serikali inaendelea kutenga fedha kwa ajili yakulipa madeni ambayo yamehakikiwa kila mwaka. Baadaya uhakiki kukamilika taarifa ya matokeo ya uhakiki huwainawasilishwa kwa Maafisa Masuuli ambayo inaonesha wadaiambao madeni yao yamekubaliwa na wale madai yaoyamekataliwa na sababu za kukataliwa kwake.

Kwa hiyo, nitumie nafasi hii kuwataka Maafisa Masuulikuwajulisha wahusika ambao walikuwa na madai lakinimadai yao yalikataliwa, maana wao ndiyowanaowafahamu. Uhakiki wa madeni ya mwaka 2017/2018na 2018/2019 umeanza na tunatarajia kwamba itakapofikamwezi wa nane, Serikali itakuwa imemaliza na tutaanzautaratibu wa kuyahakiki kwa kila robo mwaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati ilishauri Serikalikutenga fedha za kutosha kwa ajili ya Kitengo cha Udhibitiwa Fedha Haramu ili kiweze kufanya majukumu yakekikamilifu. Ni kweli kabisa tunatambua umuhimu wa kitengohiki na kwenye mwaka ujao wa fedha Fungu 13 ambayondiyo kitengo cha udhibiti wa fedha haramu, kimetengewajumla ya shilingi bilioni 2.01 kwa ajili ya OC na shilingi milioni200.29 kwa ajili ya maendeleo. Tunatenga fedha hizi kwakuzingatia kiwango cha makadirio ya mapato kwa mwakaujao wa fedha, lakini pia vipaumbele vya kimkatabaambavyo tunavyo ikiwa ni pamoja na Deni la Taifa lakini piamishahara ya watumishi wa umma. Kwa hiyo, kwa kuzingatiaumuhimu wa kitengo hiki, tutaendelea kukitengea fedha,lakini tunafungwa tu na mapato ambayo yanawezayakapatikana katika mwaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati pia ilihoji juu ya Sheriaile ya Udhibiti wa Fedha Haramu ya mwaka 2006 ambayoinataja kiwango cha juu cha fedha ambazo mtu anawezakukibeba kama fedha taslimu kuwa ni shilingi milioni 10 tu nakwamba kwa biashara na hususan biashara ya dhahabukwamba hiki kiasi ni kidogo sana.

Page 237: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

237

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni zaKusimamia Usafirishaji wa Fedha Taslimu ambazo zinavukamipaka ya nchi (The Anti-Money Laundering (Cross BorderDeclaration of Currency and Bearer Negotiable InstrumentsRegulations) ya mwaka 2016 wasafiri wakiwa na fedhataslimu, sawa na dola za Marekani 10,000 au zaidiwanatakiwa kutoa taarifa kwa Maafisa Forodha.

Naomba ifahamike kuwa kanuni hizi hazimzuii mtukubeba fedha taslimu zaidi ya kiwango kilichotajwa, lakinitunachosema ni kwamba ni lazima a-declare, lazima atoetamko kwa Maafisa Forodha ili tuweze kudhibiti usafirishajiwa fedha haramu kupitia mipakani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati pia il ioneshakwamba pamoja na kuwa Tume ya Pamoja ya Fedhaimeanzishwa tangu mwaka 2003 mpaka sasa Akaunti yaPamoja bado haijafunguliwa, japokuwa jambo hili linafanyakazi ni muhimu tuliharakishe. Naomba tu niseme kwambatarehe 9 Februari, 2019 Mheshimiwa Makamu wa Raisaliongoza kikao hapa Mjini Dodoma na moja ya ajendailiyojadiliwa katika kushughulikia changamoto za Muunganolilikuwa ni hili. Maelekezo ambayo sisi tulipatiwa ni kwambatuandae Waraka mpya wa Baraza la Mawaziri kuhusumapendekezo ya kufungua akaunti ya pamoja. Naombakulijulisha Bunge lako tukufu kwamba utekelezaji wa maagizohayo unafanyiwa kazi hivi sasa, kwa hiyo muda si mrefu Serikaliitaweza kutoa maamuzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati pia ilibaini kwambakumekuwa na mifumo mingi sana ambayo inasimamiwa naWizara yangu ikiwemo IFMS, GPG, GSSP, GAMIS na kadhalika;mifumo yote inasimamiwa na Wizara yangu, uendeshaji wakeuna gharama kubwa na kwamba ni muhimu sana sasa tuonenamna ya kuiwianisha na kuiunganisha na hasa ile ambayoinafanya kazi moja. Pia Kamati ilitusisitiza tuharakishemchakato wa kujenga mifumo yake na kuondokana namifumo mingine kutoka makampuni au watu binafsi.

Page 238: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

238

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara imekuwaikitengeneza mifumo kulingana na mahitaji mbalimbaliambayo hayaingiliani katika business process. Hata hivyokupitia mradi wa PFMRP tayari Wizara imeanza kuunganishamifumo mbalimbali ya ndani na taasisi nyingine za kifedha ilikubadilishana taarifa na kupunguza gharama za uendeshajiwa mifumo. Pia Serikali imeanza kutengeneza mifumo yakena nashukuru Kamati ya Bajeti imeliona hili, ili tuwezekupunguza gharama kubwa mno ambazo tumekuwa tukilipawakandarasi mbalimbali. Kwa hiyo, tumetumia wataalamwetu ndani ya Serikali kutengeneza mifumo ya GPG, GSPPna GAMIS, lakini pia mfumo wa kiuhasibu. Pia kwa kutumiawataalam wetu wa ndani tunaendelea kutengeneza mifumomingine ya nje iliyobaki ili kuondokana na utegemezi wamalipo ya leseni (subscription fee) pamoja na utegemezi wautalaam kutoka makampuni binafsi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati pia iliona kwambapamekuwepo na mwingiliano wa majukumu baina ya baadhiya taasisi za Serikali na hususan GPSA ambao ni Wakala waHuduma za Ununuzi Serikalini, lakini PPRA - Mamlaka yaUdhibiti wa Manunuzi Umma, lakini pia Bodi ya Wataalamwa Ununuzi na Ugavi Tanzania na Mamlaka ya Rufaa zaZabuni za Umma. Walitushauri kwamba ni vizuri majukumuya taasisi hizi kuwa wazi na tuhakikishe zinatekeleza majukumuyake kama ambavyo zimebainishwa kwenye sheriazilizozianzisha. Kamati pia iliona zipo changamoto zawataalam wa ununuzi waliosajiliwa na Bodi ya PSPTB kwenyetaasisi na mashirika ya Serikali na hivyo inakwenda kinyumena sheria na suala hilo lazima Serikali ilifanyie kazi haraka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme tu kwambatunapokea ushauri wa Kamati na Wizara yangu kwakushirikiana na hizo taasisi tutapitia na kuchambua majukumuya kila mmoja ili kubaini maeneo yenye muingiliano kwa lengola kurekebisha ili taasisi hizo ziweze kutekeleza majukumu yakekwa mujibu wa sheria iliyozianzisha. Bodi kuendelea kutoaelimu kwa waajiri na waajiriwa juu ya matakwa ya Sheria yaPSPTB inayowataka kuwaajiri au kuajiriwa wataalam waununuzi na ugavi waliosajiliwa na hii Bodi. Lakini bodi

Page 239: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

239

itawachukulia hatua waajiri wanaoajiri Maafisa Ununuzi naUgavi ambao hawajasajiliwa kwa mujibu wa Sheria Na. 23ya PSPTB.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pia nianze kutoleaufafanuzi baadhi ya hoja ambazo zilitolewa; kwanzaMheshimiwa Obama Ntabaliba tunazipokea pongezi zakekwa Serikali na hususan Mheshimiwa Rais, viongozi wa Wizaralakini pia Mamlaka ya Mapato na Benki Kuu ya Tanzania.(Makofi)

Suala la Ofisi ya Msajili a Hazina, Mheshimiwa NaibuWaziri ameshalitolea maamuzi. Naomba niseme kuhusuhotuba yangu niliyoitoa asubuhi imejaa hatua za udhibiti(controls) na hakuna hatua ambazo zinaleta faraja kwawafanya biashara, naomba Mheshimiwa Obama na Bungelako wasubiri kidogo, wavute subira hotuba ya Bajeti Kuu yaSerikali itasomwa alasiri ya tarehe 13 Juni, 2019 na baadhi yahaya mambo atapata majibu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa na suala la walewalikuwa wanaendesha maduka ya kubadilisha fedha zakigeni na wapo wachache ambao walikuta wanaendeshahiyo biashara kwa mujibu wa sheria na taratibu za lesini zao,hoja ilikuwa kwamba hawa waruhusiwe kuendelea nabiashara yao. (Makofi)

Naomba nilifahamishe Bunge lako tukufu kwambabaada ya Benki Kuu kukamilisha lile zoezi kwa baadhi yamaeneo, wote waliokutwa wanafanya biashara hiyo kwamujibu wa leseni, masharti ya leseni zao waliruhusiwakuendelea na biashara zao. Ni wale tu ambao walikutwawanafanya kinyume cha taratibu hizo ndiyo walifungiwakuendelea na biashara zao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Obama piaalituambia kwamba malipo ya wastaafu yanachelewa sanana pengine tuangalie kwa macho makali kile kitengokinahusika. Naomba kulitaarifu Bunge lako tukufu kwambahivi sasa tunaweka mfumo wa kielektroniki ambao

Page 240: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

240

utapunguza sana ucheleweshaji, lakini hususan shida kubwaiko kwenye kumbukumbu (records). Kwa hiyo, sisi tunaaminikwamba njia hiyo itaturahisishia na muda si mrefu suala lakuchelewesha malipo ya wastaafu litakuwa ni historia, lakinipia tunapokea ushauri, tutakitazama pia kitengo hiki kwakaribu, kwa maana ya mahitaji ya watumishi lakini piavitendea kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Balozi Dkt.Kamala alisema vizuri sana kuhusu ukuaji wa uchumi na zilesekta ambazo zinakuwa kwa kasi. Ni kweli kabisa sektaambayo inaongozwa na Mheshimiwa Mwakyembe ndiyoinayokuwa kwa kasi zaidi kuliko nyingine kwa hivi sasa. Kwaupande wa kilimo naomba kwa kweli niwapongeze sanawakulima wa nchi hii, siyo tu wanatupatia chakula, lakiniwanatupatia fedha nyingi za kigeni kupitia mazao ambayotunauza nje. Kwa mwaka 2016 kilimo kimeendelea kutoatakribani asilimia 27.4 ya pato la Taifa, mwaka 2017 kilichangiaasilimia 28.8 na mwaka 2018 kimechangia asilimia 28.2. Hataukiangalia kwenye mauzo yetu nje kwa wastani kwa hiyomiaka mitatu kwa kila mwaka mazao ya kahawa, pamba,katani, chai, tumbaku, korosho na cloves, kwa ujumla kilamwaka zinaliletea taifa letu mapato ya takribani dola milioni4197. Hii unaondoa fedha ambazo tunapata kutoka kwenyemauzo ya samaki na yanayotokana na samaki, lakini piamazao ya mboga mboga na hata mazao ambayoyameongezewa thamani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa ukuaji wasekta ya kilimo kwa kutumia takwimu mpya za pato la Taifakwa kweli tumeona, hapo zamani kilimo kilikuwa kinakuwakwa karibu asilimia 3/3.2. Kwa takwimu mpya kilimo kimekuwakwa asilimia 4.8 mwaka 2016, asilimia 9.2 mwaka 2017 naasilimia 5.3 mwaka 2018. Kwa hiyo kwa kweli wamefanya vizurisana wakulima wetu wanastahili pongezi. Ukienda kwenyemchanganuo kilimo cha mazao ndiyo kinaongoza kwa kasikubwa ambacho kimekuwa kwa wastani wa asilimia 5.0mwaka 2018 na kinafuatiwa na mifugo ambayo nayo sektandogo ya mifugo nayo ilikuwa kwa asilimia 4.9, uvuvi imekuwakwa kasi zaidi ya asilimia 9.2 mwaka 2018. Tunawapongeza

Page 241: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

241

sana wavuvi wetu ambao wameleta mafanikio hayo.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kabisa mfumuko wabei katika nchi hii unachangiwa kwa kiasi kikubwa namfumuko mdogo wa bei za chakula. Kwa hiyo MheshimiwaBalozi Kamala alikuwa anasema ni vema nieleze mikakati yaSerikali kusaidia wakulima ambao ndiyo wanachangiakushusha mfumuko wa bei katika nchi yetu. (Makofi)

Naomba niseme tu kwa kifupi kwamba, maelezoyalitolewa wakati wa hatuba ya bajeti ya Wizara ya Kilimolakini siyo vibaya nikarudia kwamba sisi kama Serikalitunajielekeza kuhakikisha kwamba pembejeo muhimuzinawekewa fedha kwenye bajeti ya Serikali kupitia bajetiya Wizara husika, hizi zote zinazohusika na mazao, mifugo nauvuvi, lakini pia kwa upande wa misitu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme pia, mkakatimwingine ni kuondoa kodi na tozo za kero. Kodi na tozo zakero kwa wakulima wetu tumekuwa tunazifuta kwa miakayote mitatu na mimi kabisa ninaamini kwamba tutaendeleana jitihada hizi katika mwaka ujao wa fedha. Lingine nikuwatafutia mikopo nafuu, na hii tumekuwa tunafanya kwakuzungumza na taasisi mbalimbali ikiwemo AfricanDevelopment Bank lakini pia Kuwait Fund ambao tumekuwana majadiliano nao ili watupatie fedha kwa ajili ya miradi yaumwagiliaji, lakini pia ADB kwa ajili mradi ambao utawekakongani za kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, lakini piajitihada za kuongeza na kutafuta masoko. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa naomba kidogo nijielekezekwenye Deni la Taifa ambalo limesemwa na watu wengi nanaomba nimshukuru sana Mheshimiwa George BonifaceSimbachawene kwa darasa zuri sana ambalo amelitoakuhusu Deni la Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Sika, labda nianze na hili ambaloalilisema Mheshimiwa Kamala maana yeye hakuwa na shidasana na sisi kukopa, lakini suala alikuwa na wasiwasi kwamba

Page 242: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

242

viashiria vya uhimilivu wa deni vimeanza kuwaka na hivyoSerikali ipunguze kasi ya kukopa. Pia alihoji kwamba tunamkakati gani wa kuhakikisha kwamba Deni la Serikalihaliendelei kukua sana kwa kuwa tunajua tutaendeleakukopa kugharamia miradi yetu mikubwa ya maendeleo,SGR, umeme Mto Rufiji na kadhalika.

Mheshimiwa Spika, kwa maana ya mkakati, napendakusisitiza kwamba mikopo ambayo inapewa kipaumbelekatika kukopa ni ile yenye masharti nafuu. Ile ya kibiasharakwa kweli tunakuwa waangalifu sana, we are very verycautious na tunapokopa mikopo ya kibiashara tunaielekezakwenye maeneo mahsusi ya kuchochea uchumi. Kwa hiyo,hatukopi tu mikopo ya kibiashara tukaipeleka popote,hapana.

Mheshimiwa Spika, la pil i tumejielekeza sanakuboresha ukusanyaji wa mapato ya ndani na lengo letu nikuwa sehemu kubwa ya bajeti iwe inagharamiwa na fedhaza ndani na wakati huo huo tukifanya jitihada kupunguzamatumizi ambayo yanaepukika. Lakini mkakati wa tatu nikufanya marekebisho ya Sheria ya Mikopo, Dhamana naMisaada, Sura ile ya 134 ili dhamana ya Serikali ambayoinatolewa itolewe tu kwa taasisi za Serikali ambazozinajiendesha na ambazo tuna uhakika zinaweza zikarudishadeni.

Mheshimiwa Spika, mkakati mwingine ni kufuatilia kwakaribu mwenendo wa Deni la Taifa ndiyo sababu kila mwakani lazima tufanye uchambuzi wa uhimilivu wa deni (debtsustainability assessment) kila mwaka ndiyo maana nilitoataarifa kwamba Desemba, 2018 tumefanya assessment hiyona bado tunaona kwamba kwa vigezo vyote vya Kimataifabado tuko vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mkakati mwingine tunaendeleamajadiliano na majadiliano nan chi ambazo sio wanachamawa Paris Club na lengo letu hapa ni kuona kama tunawezatukafikia makubaliano ili nao waweze kutusamehe madeni

Page 243: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

243

yao kama ilivyokuwa wakati ule wa HIPC kwa nchi ambazoni za Club ya Paris.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa mikopo ya ndani,tunazingatia uwezo wa soko na pia tunazingatia liquiditykatika uchumi, lakini pia tunafanya hivyo, tunapokopatunahakikisha kwamba hatupunguzi uwezo wa taasisi mbalimbali kuikopesha sekta binafsi ya ndani. Kamamnavyofahamu, tumeruhusu pia nchi za Afrika Masharikikushiriki kwenye ununuzi wa dhamana kwenye soko letu hapanchini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema vigezo vyotevya uhimilivu tuko vizuri kabisa na niseme tu kwamba kumtoawasiwasi Mheshimiwa Dkt. Kamala na wengine ni kwambatunapofanya ule uchambuzi wa uhimilivu wa deni tunafanyakitu tunaita debt stress test na hizi maana yake ni kwambatunaweka zile namba zote ambazo tunakuwa tumezikusanyakwamba deni letu liko hapa hivi sasa. Je, kama ikitokea tatizokubwa labda tumepata tatizo kubwa moja ya mazao yetuyanayotuingizia fedha za kigeni imeporomoka, kwa hiyomwenendo wa upataji fedha za kigeni unakuwaje namwenendo wa deni letu la Taifa utakuwaje. Kwa hiyo,tunatumia vigezo mbalimbali kujiridhisha kwamba badotutabakia sawasawa na kwa hiyo, tunapotoa taarifakwamba deni letu ni himilivu tunakuwa pia tumezingatia debtstress test ambazo tumekuwa tumefanya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia nirudie kusisitiza kukopa siodhambi ilimradi mikopo hiyo ielekezwe kuongeza uwezo wakuzalisha mali nchini na pia izingatie uwezo wa nchi yetukulipa. Nadhani hicho ndicho kitu cha msingi na bahati nzurini kwamba Serikali imeendelea kulipa kulingana na mikatabaya madeni hayo kila yanapoiva. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, labda naomba nilisemee hili tenakwa Mheshimiwa mdogo wangu Zitto Kabwe ambayealituambia usimamizi wa Deni la Taifa ni tatizo na kwambakuna upotoshaji kwa mujibu wa Taarifa ya CAG ambayoalikuwa anainukuu. Naomba niseme, tena yupo, afadhali!

Page 244: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

244

Naomba niseme allegation aliyoitoa ni very serious.Mheshimiwa Zitto Kabwe allegation aliyoisema ni very serious,haiwezekani Taifa kama letu tukatunza takwimu za Deni laSerikali kwenye counter book. Hii si kweli na ni udhalilishaji waSerikali. Kwa kweli Mheshimiwa Zitto Kabwe ulitakiwa ufutekabisa yale maneno, hayafai, sio sahihi na ninajuaunafahamu kwamba hatuweki takwimu za Deni la Taifakwenye counter book. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika kutunza kumbukumbu zaDeni la Taifa, Wizara ya Fedha inatumia mfumo wakielektroniki wa kutunza kumbukumbu za Deni la Serikaliambao unajulikana kama Commonwealth Secretariat DebtRecording and Management System (CSDRMS) na mfumohuu unatumiwa na nchi za Jumuiya ya Madola naunahuishwa mara kwa mara kulingana na mahitaji. Aidha,mfumo huu kwa Tanzania ulianza kutumika toka mwaka 1996mpaka 1997. Kwa hiyo, Mheshimiwa Zitto Kabwe hilo sio sahihi,usipotoshe umma hata kidogo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, takwimu za deni letu ni sahihi, lakinipia niseme CAG hazuiliwi kufanya ukaguzi wa Deni la Taifana wala sio mara ya kwanza amefanya, kwa hiyo, kwa mujibuwa taratibu zake alizojipangia akitaka kuhakiki Deni la Taifaatafanya hivyo. Sasa labda niseme tu inawezekana penginepakawa na tofauti, alikuwa anasema inawezekana kabisakwamba wale waliotukopesha wana namba tofauti na sisihili ni jambo la kawaida, tofauti zinaweza kuja kwa sababuya matumizi ya exchange rate, lakini inawezekana pia hatajust human error katika uandishi wa zile takwimu, lakinikikubwa ni kuhakikisha kwamba ile marginal of error inakuwani kidogo na kwetu sisi marginal of error ndogo na inakubalika.Hata kukiwa na error baadae reconciliation inafanyika. Kwahiyo hili sio tatizo hata kidogo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba pia nitoe maelezo yanyongeza pale alipoishia Mheshimiwa Naibu Waziri kuhusuukusanyaji wa mapato ya kodi. Mheshimiwa Zitto Kabwe miminakumbuka wakati ule, nadhani siasa inakuchanganyakidogo siku hizi. Wakati ule ukiwa darasani kwangu nadhani

Page 245: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

245

ungeweza kuona kwa urahisi kabisa. Uwiano wa mapato yakodi kwa Pato la Taifa kwa nchi yetu ni kweli umepunguakama Mheshimiwa Naibu Waziri alivyosema, lakini ni rahisi tu,tax effort tunachukua makusanyo ya kodi unagawanya kwaPato la Taifa. Sasa kilichofanyika baada ya kufanya rebasingni kwamba GDP imeongezeka kwa kasi kuliko kasi yaongezeko la kodi na kwa hiyo ndiyo maana utaona kwambatax effort imepungua, lakini ni kwa sababu ya mabadilikoambayo tumefanya kwenye Pato la Taifa kwa sababu nimuhimu pia. Ni muhimu kwamba Pato la Taifa liwezekuendana na hali halisi ya uchumi. Wakati ule tulikuwatunatumia Pato la Taifa kwa kizio cha mwaka 2007 sasa tokamwaka 2007 mpaka mwaka 2019 pametokea tofauti kubwasana katika structure ya uchumi wetu na ndiyo maanaunaona kwamba sekta anayoongoza MheshimiwaMwakyembe sasa imekuwa ni sekta ambayo inakua kwa kasikuliko zote wakati hapo nyuma tu haikuwa hivbyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo ni rahisi tu kamadenominator inaongezeka kwa kasi zaidi kuliko numerator nihesabu za kawaida tu Mheshimiwa Zitto Kabwe unatakiwaukumbuke tu hiyo. Lakini pia ni muhimu kuzingatia kwambabaadhi ya nchi za Afrika Mashariki bado hazijakamilisharebasing na katika makubaliano tuliyonayo tumekubalianakwamba tutafanya rebasing ya nchi zote za Afrika Masharikikwa pamoja na hapo ndiyo unaweza ukafanya ulinganifumzuri wa hiyo tax effort kwa maana ya uwiano wa mapatoya kodi na GDP.

Mheshimiwa Spika, labda niseme pia kuhusu rai yaMheshimiwa Peter Serukamba, tunaisaidiaje Benki yaMaendeleo iweze kufanya vizuri zaidi, lakini pia benki zinginekwa ajili ya kuchochea maendeleo ya uchumi katika Taifaletu. Labda tu niseme kwamba pamekuwepo changamotoza mtaji na hususan kwa benki zetu mbili zile za TIB Corporatena ile ya Maendeleo. Lakini tumekuwa tunashirikiana na benkihizi kama Wizara ili kushughulikia suala la mtaji na ukwasi ilikuweza kuleta tofauti na mafanikio yameanza kuonekana.Mikopo ya mashirika ya umma iliyokuwa hailipwi kwaushrikiano wa karibu na Ofisi ya Msajili wa Hazina sasa mikopo

Page 246: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

246

hii imeanza kurejeshwa. Pia benki imefanikiwa kupata vibalistahiki kutoka kwa Mamlaka ya Masoko na Mitaji naDhamana (CMSA) na Soko la Hisa la Dar es Salaam kwa ailiya kutoa hati fungani ya kiasi cha shilingi bilioni 135 nampango huu unatazamiwa kukamilika ndani ya mwezi Juniambao tumeanza, 2019.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo nataka tu kusemakwamba zipo jitihada za makusudi kabisa ambazo Serikaliinafanya ili kuweza kuhuisha utendaji wa benki hizi.

Mheshimiwa Spika, naomba pia nisemee juu yamarejesho ya Kodi ya Ongezeko la Thamani. Kamautakumbuka palikuwepo na udanganyifu ambao umekuwaukijitokeza kwa baadhi ya wafanyabiashara wanapodaikurejeshewa kodi ambazo hawastahili na ndiyo sababutuliamua kwamba ni lazima tufanye uhakiki wa marejeshohayo kwa kiwango cha asilimia 100 na kwa hiyo, tunahakikinyaraka zote ambazo zinawasilishwa na mwombaji, lakininyaraka zote pia ya yule aliyemuuzia bidhaa au hudumamuombaji wa marejesho na uhakiki wa nyarakazilizowasilishwa kwa kiwnago cha asilimia umefanyika nahatua inayoendelea sasa ni uhakiki wa nyaraka za muuzajiwa bidhaa iliyonunuliwa yaani third part verification.Tunachukua hatua hii kwa waombaji wote wa marejesho yakodi ya ongezeko la thamani ili tujiridhishe kwamba hakunauwezekano wa kurejesha fedha zaidi ya kiwango sahihikinachostahil i. I l i kukabiliana na changamoto yaucheleweshaji, Serikali kupitia TRA imefanya maboresho yamifumo yake ya usimamizi wa kodi ikiwemo EFDMS ili kuwezakutoa risiti moja moja kwa kila muamala badala ya mfumowa zamani wa kutoa risiti kwa makundi mwisho wa siku.Mfumo huu utaweza kusomana na mifumo mingine kama i-tax ambao unatumika kuwasilisha return za VAT na hivyokufanya uhakiki kuwa rahisi.

Mheshimiwa Spika, kiasi cha madai yaliyopokelewani maombi 1,854 ambayo yana thamani ya shilingi bilioni 697.2na kati ya hayo, madai yaliyohakikiwa ni 451 ambayo yanathamani ya shil ingi bil ioni 22.6 na madai ambayo

Page 247: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

247

hayajahakikiwa ni 1292 ambayo thamani yake ni shilingi bilioni713.2. madai yaliyolipwa mpaka sasa ni 152 ambayo yanathamani ya shilingi bilioni 10.6 na madai haya ni takwimu hadikufikia mwezi wa Aprili, 2019.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa malipo ya ileasilimia 15 kwa waingizaji wa sukari, napenda niseme tukwamba Serikali imelifanyia kazi na hivi karibuni Serikaliitatangaza kwa umma juu ya hatua stahiki ambazozitachukuliwa kuhusiana na eneo hili.

Mheshimiwa Spika, naomba pia nitolee ufafanuzikidogo juu ya suala la vitambulisho vya wajasiriamali. Nisemetu kwa sababu kulikuwa na allegation hapa kwamba ile tozo/gharama ya kitambulisho kwamba haipo kisheria, sio sahihikabisa kabisa. Suala hili ni kwa mujibu wa sheria nalinaratibiwa na kutekelezwa kwa asilimia 100 na Wizarayangu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, labda niseme tukwamba Sheria ya Usimamizi wa Kodi Sura 438 pamoja namarekebisho yake ambayo yalifanywa na Bunge hili tukufumwaka 2017 katika kifungu cha 22(a) kilimpa mamlakaKamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)kuwatambua na kuwasajili wafanyabiashara wadogo nawatoa huduma ambao ni washereheshaji, machinga, mamalishe, baba lishe na wengineo ambao mauzo ghafi hayazidishilingi milioni nne.

Kwa hiyo, hil i jambo liko kisheria kabisa.Wafanyabiashara wadogo na watoa hudumawanaoangukia kwenye Sekta isiyo rasmi hivyo huwekamazingira ya ushirikiano na Ofisi ya Rais, TAMISEMI na TRAkatika mchakato wa ugawaji wa vitambulisho, ni utaratibuwa makusanyo ya malipo ya gharama ya vitambulisho naushirikiano huo umegawanyika katika sehemu mbili; kwanzani kutumia mtandao mpana wa kiutawala ambao uko kuleTAMISEMI katika kuwatambua wajasiriamali wadogo pamojana kugawa hivyo vitambulisho kwenye huo mtandao. Ndiyouliotumika kugawa hivyo vitambulisho.

Page 248: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

248

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa pili ni ule sasaambao unahusu ukusanyaji wa fedha na gharama zavitambulisho na Wizara ya Fedha kupitia TRA ndiyo inafanyakazi hiyo na fedha zinazokusanywa zote zinapelekwa mojakwa moja kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo nirudie tena kwambajambo hili liko kisheria na sheria ilipita hapa Bungeni, kwa hiyo,ni suala tu la mgawanyo wa majukumu na kama Serikali nilazima tutumie mtandao mpana wa Serikali kule kwa waleambao wanaweza kuwafikia wananchi kwa karibu zaidi.

Mhesimiwa Spika, Mheshimiwa Nsanzugwankonilishatolea maelezo juu ya suala la tax refunds.Hili la kutumiawataalam kunishauri tutalitafakari, lakini pia nikuhakikishiekabisa kwamba Serikali inafanya jitihada kuhakikishakwamba yale mashirika ambayo Serikali inahisa kama NaibuWaziri alivyozieleza tunajitahidi ku-maximize mapatoyanayotokana na taasisi hizo kwa kuzingatia uwekezaji waSerikali na pia kwa kuzingatia kama ulivyosema umuhimu wakulinda ajira lakini pia michango ya hayo mashirika.Tunafanya jitihada kubwa na wewe mwenyewe umeonamabadiliko makubwa katika kipindi kifupi kwamba hata sasahata taasisi ambazo kwa miaka mingi zilikuwa haziletichochote Serikali sasa zimeanza kuleta gawio.

Mheshimiwa Spika, rai ya kwamba TRA iwe rafiki kwawafanyabiashara, ahsante kwa kutupongeza kwamba walaumnaona tunaanza kusikiliza, lakini ni rai yangu kwambatutaendelea kulitilia mkazo ili TRA kweli iwe rafiki wawafanyabiashara.

Mheshimiwa Spika, kuhusu ujenzi wa Ofisi ya TRA Kasuluna kule Kongwa kwa Mheshimiwa Spika, niseme tu kwamba,nitalitazama kwa jicho la karibu tunavyokwenda mbele katikamwaka ujao wa fedha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja mbalimbalikutoka kwa Mheshimiwa Katani, labda tu niseme kwambatulipochagua ule mradi wa kimkakati kule Mkuranga nadhani

Page 249: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

249

ilikuwa timing problem, lakini tutaliangalia kuhusu mradi wakimkakati wa kujenga ghala kule Tandahimba kwa kuwatunatambua kweli Tandahimba ni moja ya Wilaya ambazozinazalisha korosho kwa wingi. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Waziri ahsante, sasa.

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika,baada ya maelezo hayo nakushukuru tena kwa nafasi,naomba kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO:Mheshimiwa Spika, naafiki.

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha naMipango. Hoja imetolewa na imeungwa mkono,tunakushukuru sana kwa kutupitisha katika ushauri mwingi waWaheshimiwa Wabunge na sasa tunaingia kwenya hatuainayofuata. Katibu!

NDG. MOSSY V. LUKUVI-KATIBU MEZANI:

KAMATI YA MATUMIZI

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge tukae. Katibu!

NDG. YONA KIRUMBI-KATIBU MEZANI:

MATUMIZI YA KAWAIDA

Fungu 50 - Wizara ya Fedha na Mipango

Kif. 1001– Administration and Human Resources Management...…………Sh. 8,007,734,000

MWENYEKITI: Haya tunaanza mchakato sasa,Mheshimiwa Ndassa.

MHE. RICHARD M. NDASSA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nikushukuru sana kwa nafasi hii.

Page 250: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

250

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa sera ya kukuzauchumi ni pamoja na kurasmisha shughuli za biashara ndogondogo, Mheshimiwa Rais wetu mpendwa alitoa vitambulishovya ujasiriamali kwa nchi nzima, lakini kila mkoa kumekuwana approach yake hali iliyopelekea sintofahamu kwavitambulisho hivi. Nini kauli ya Serikali? Nisipopata majibunitachukua shilingi na kuondoka nayo.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Ndassa, juzi si Serikali ilitoakauli humu ndani, ulikuwa umetoka kidogo? MheshimiwaNaibu Waziri TAMISEMI alitoa msimamo wa Serikali na maelezokabisa, labda kama kuna jambo specific ambaloungelipenda kuliuliza, lakini mambo yote ya vitambulishoalisema, ila kama una jambop specific, sikukatazi.

MHE. RICHARD M. NDASSA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ni kweli, baada ya maelezo ya Serikali, na ndiyo maananikasema kwamba, mikoani huko mpaka leo na janayamefanyika mambo ambayo huwezi kuamini kwamba hayayanafanywa na watendaji wa Serikali. Wamekwenda kwenyeeneo moja wakamkuta mjenzi na makoleo yake na sururuyake, wakabeba sururu, hao ni watendaji wa Serikali. Ndiyomaana ninasema, kwa sababu hapa, kila mkoa umekuwana approach yake. Nini kauli ya Serikali, mbali na siku ileMheshimiwa Waziri kusema, nini kauli ya Serikali, kwa sababuimekuwa ikichanganya, kila mkoa umekuwa na approachyake. (Makofi)

MWENYEKITI: Ufafanuzi, Mheshimiwa Naibu Waziri,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa!

NAIBU WAZIRI, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZAMITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru, naomba nijibu hoja ya Mheshimiwa Mbunge,Senator, ni juzi ulitoa nafasi kwenye Bunge lako tukufu nikatoamaelezo ya Serikali/ufafanuzi wa jambo hil i nakilichoelekezwa na Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niendelee kusisitiza kwambani kweli kuna changamoto ya jambo hili, lakini kama Serikali

Page 251: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

251

tumeliona na maneno yaliyozunguzwa kwenye Bunge hili nimaneno sahihi. Sisi tulikusudia kupeleka vitambulisho kwawafanyabiashara wadogo na watoa huduma wadogo,ambao kipato chake kuanzia sifuri mpaka, isiyozidi milioni nnekwa mwaka mzima. Sasa hayo mengine ambayoyanafanyika, tumeona kwamba kweli kwa sababu watuwalikuwa wanaendesha zoezi hili kila mtu anavyojisikia,pamoja na maelekezo yote tukasema, tumetengeneza sasamwongozi, ambao utasambazwa na WaheshimiwaWabunge mtapata nakala, ni nani anapaswa kupewakitambulishi cha mjasiriamali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili sasa kama kutakuwa namtu anachukua hatua tofauti na maelekezo ya Serikali,nadhani huyo atakuwa na jambo lingine la ziada. Kwa hiyo,naomba tuvumiliane hili jambo tumeshalichukua na ni kwelitumeendelea kupata taarifa mbalimbali tunazifanyia kazikwa haraka kubwa kweli kweli. Ahsante.(Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Ndassa.

MHE. RICHARD M. NDASSA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nikubaliane na maelezo ya Serikali, lakini niombe tu kwasababu suala hili halijaanza leo, kila siku limekuwa likijirudia,likijirudia, likijirudia.Naomba elimu ipelekwe kwa kila mkoa,kila wilaya, kila eneo ili wananchi waelewe, nini maana yavitambulisho vya ujasiriamali na ni kiasi gani na ni nanianastahili kulipa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana na kwa kweli hata miminingewashaurini mfanye hivyo, lakini kuwa kidogo makinikwamba kama tumeamua kuelekeza kulipa kodi, watuwalipe kodi jamani. Kama mamaa vitumbua analipa,anakuwa na hicho kitambulisho, huyu na masururu yake nanini anapiga plasta, sasa huyo asilipe kwa nini. Kwa hiyo,kama tunalipa kodi tuseme jamani, watu walipe kodi.(Kicheko)

Page 252: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

252

Kama tumeshamshika yule wa chini kabisa, hawawengine tunawaachaachaje hawa wanaoelealea hapakatikati hapa. Kwa hiyo, it’s only twenty thousand a year, isnot twenty million. Wanazo, kuna mtu utampa kazi ya kupigaplasta ayemlipa chini ya laki! Tunaendelea na MheshimiwaJoseph Mkundi.

MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru, pamoja na maelezo ya Mheshimiwa Waziri, mimihoja yangu iko kwenye Deni la Taifa. Ukiangalia Deni la Taifamwaka jana tulikuwa na deni la trilioni 49.86 na mwaka huuinasomeka trilioni 51.03 na ukiangalia hili ni ongezeko laasilimia 2.4 almost hivi na ukifanya hesabu hapa, ina maanatukienda kama miaka mitano, deni hili linaweza likaongezekakwa asilimia zaidi ya 10, ni ongezeko kubwa na tukiangaliamambo jinsi yanavyokwenda, sehemu kubwa ya deni hili nikwa sababu ya mikopo ambayo tumekuwa tukikopa kwaajili ya miradi, lakini bado miradi hii inaendelea. NiipongezeSerikali inaonyesha jitihada za kulipa deni hili, lakini ni mkakatigani hasa ambao tunaweza kuwa nao ili pamoja na kulipalakini vilevile deni hili lisiongezeke kwa kasi? Nashukuru.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Waziri ufafanuzitafadhali, mkakati.

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza nimshukuru Mheshimiwa Mkundi kwahoja yake, hii ni hoja muhimu ambayo ndiyo maana nilijaribukuieleza kwa kirefu ni hoja ambayo inagusa watu wengi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kilicho kikubwa, ni kwelikama nilivyokiri kwamba deni letu la Serikali linaongezeka,lakini katika kupima uhimilivu wa deni hili, kwa vigezo vyotevinavyotumika kimataifa, liko sawasawa! Ile kasi ya ongezekoni moja ya vitu ambavyo vinaangaliwa, kwa sababutunatazama pia uwezo wa Serikali, uwezo wa taifakurejeshayale madeni, siyo leo tu, tunafanya hata estimate kwambahuko mbele, miaka 10 ijayo, kwa assumptions ambazotunakuwa tumeweka. Je, tutaweza kulipa hilo deni.

Page 253: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

253

Mheshimiwa Mwenyekiti, na ikumbukwe kwamba hilideni tunalipa vitu vingi, tunalipa riba na principal ya madeniambayo tulikopa huko nyuma kuanzia hata miaka ya 1980siyo ya leo tu. Kwa hiyo, kinachoonekana ni accumulationpamoja yaani ni compounded mpaka leo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na kwa mana sasa yamikakati, nilijaribu kueleza kwamba kwanza tunawekakipaumbele katika namna ya kukopa ili kuweza kudhibiti ilekasi ya ongezeko. Hatuendi, tunapendelea zaidi kukopamikopo yenye masharti nafuu, yenye riba ndogo, yenyemuda wa malipo ambao ni mrefu zaidi. Ndiyo maana maranyingi tunakwenda kukopa World Bank ambapo unakuwana muda mrefu wa kurejesha na interest rates ambazo nindogo sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hiyo ni moja, napale ambapo tunalazimika kwenda kukopa sasa kibiasharaambako gharama ya kurejesha ile mikopo ni kubwa zaidi,tunakuwa waangalifu sana. Naomba tu nikiri tu hapakwamba hata sasa tumekuwa na mjadala, kwa sababuukienda kwenye Pato la Taifa, wastani wa Pato la Taifa kwakila mtanzania, tunakaribia sasa kuingia kipato cha kati nawatu wameanza kutuambia sasa ninyi muondoke hukokupata mikopo yenye masharti nafuu, muende huku kwenyewindow nyingine ambako ni masharti ya kibiasharaukichanganya na haya masharti nafuu mtapata fedha nyingizaidi, lakini we are very conscious, we are very very cautiousili tuhakikishe kwamba deni letu hili linakuwa ni endelevu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la pili nimesema,tunaweka nguvu kubwa kuongez amapato ya ndani, ndiyomaana tumejikita kutumia mifumo ya kisasa ya TEHAMA,tumejikita sasa kuanza kupanua wigo wa walipa kodi ilituondokane na hao kidogo milioni 2.3 kwa population yetukwa kweli ni asilimia ndogo ili tuhakikishe kwamba hiiitapunguza ile drive ya kwenda kukopa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nimesema pia hapa,tunafanya kila mwaka, kwa kushirikiana na wadau wetu

Page 254: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

254

International Monetary Fund na wengine, tunafanyaassessment ya hili deni ili tujiridhishe kwamba nchi haitaingiamahali ikashindwa kulipa haya madeni yake. Kwa hiyo,naomba tu ndugu yangu, Mheshimiwa Mkundi, aridhike tukwamba Serikali tunafanya jitihada kubwa kuhakikishakwamba hii kasi bado inabaki k atika wigo ambaounavumilika kimataifa.(Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mkundi ameridhika,tunaendelea na Mheshimiwa Mattar Salum.

MHE. MATTAR ALI SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti,nikushukuru kunipa nafasi, nataka ufafanuzi wa kina, kamasikupata ufafanuzi wa kina, naomba kushika shilingi ya Waziri.

Mheshimiwa mwenyekiti, Serikali/Wizara yake inakuwaikisuasua katika kutia saini baadhi ya mikataba ambayo yakujenga miradi ambayo itafaidisha watanzania kwa kiasikikubwa. Kuna miradi mikubwa ambayo inataka itekelezwekatika nchi yetu ambayo ina maslahi mapana kwaWatanzania na inaweza ikaisaidia Tanzania kufanyamaendeleo makubwa sana. Mfano kama Mradi wa MsimbaziCity, wa kwanza, lakini wa pili, Mradi wa Bandari yaMpigaduri, lakini mradi wa tatu ni Mradi wa Airport yaZanzibar. Wizara ya Fedha bado inasuasua katikakukubaliana na kutia saini ili miradi hii itekelezwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba ufafanuzi, hiiWizara ya Fedha ni lini miradi hii itaanza kutekelezwa iliWatanzania wapate maslahi mapana? Ahsante.

MWENYEKITI: Miradi hii ni ya Wizara ya Fedha au ni yaupande wa pili? Mheshimiwa Waziri ufafanuzi.

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaMwenyekiti, namshukuru Mheshimiwa Mbunge.

Kwanza naomba nimwambie kabisa kwamba Wizarayangu haiwezi kusuasua kutia saini mradi wenye maslahi kwa

Page 255: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

255

Taifa kama masharti yake hayana tatizo. Tunasuasua paleambapo masharti yake ni magumu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ngoja nitoe mfano, miradimingi sasa ambayo inafadhiliwa na China Exim Bank imekuwana sharti kwamba turidhie pale ambapo tutashindwa kulipawaweze kuja kukamata mali za Jeshi, Migodi, Bandari,hatuwezi kukubari masharti kama haya. Haiwezekani kabisa!Nitakuhukumiwa na mimi siko tayari kuhukumiwa kwa hilo!Sasa hilo ni moja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini baadhi ya miradiunakuta wamechomeka vitu ambavyo kwa kweli havikosawa, haviendi kutupatia the maximum benefit ambayotungetaka kama Taifa. Kwa hiyo, unaona kwamba Mradi waMsimbazi ni kweli, na mafuriko ambayo tunapata kila siku Dares Salaam, na mimi mwenyewe nakubwa na mafuriko,nimewahi kulala majini kwa sababu hakuna mifereji hakunanini.ningekuwa wa kwanza kuichangamkia, lakini unapoingiakule ndani sasa kwenye zile terms na nini watafanya,components zile, hapana! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niwaombe nanimuombe tu Mheshimiwa Mbunge, iki Bandari ya Mpigadurito be very specific, hii tuliwaomba wenzetu wa Serikali yaMapinduzi Zanzibar iweze kutupatia lile andiko ili tujiridhishena zile gharama. Tatizo ni kwamba hizi gharama zinafanywana watu tofautitofauti na nilipokuwa nimeelemewa tuliamuakutafuta utaalam kwa taasisi za kitafiti, ESRF, Chuo Kikuu chaDar es Salaam na REPOA ambao wanaendelea na kazi hiyokuchambua upya zile gharama.

Kwa hiyo, punde tutakapokuwa tumejiridhishakwamba zile gharama zinaendana na zile ambazo tunaonani muhimu kwa taifa, hatutasita kuidhinisha mradi huu.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana, Mheshimiwa Mattarameridhika.

Page 256: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

256

MHE. MATTAR ALI SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti,nikushukuru kwa mara ya pili, niombe kidogo nipe nafasi. Huumradi wa Mpigaduri, ambayo ni bandari kubwa ambayo inatakribani miaka 15 mpaka sasa inakwenda katika michakato,wanafika wakati wafadhili au watoaji wa fedha wanakuwawako tayari, na ukiangalia ile view ya Zanzibar, zaidi yakupata bandari sisi kubwa, hatuna uchumi mwingine wowoteambao tuliokuwa nao, hatuna mashamba, hatuna kilimo,hatuna madini, tunategemea biashara ndiyo kazi yetu kubwaZanzibar. Kile kibandari ambacho kilikuwepo pale chaMalindi, kazi yake ni abiria tu, ndicho kilichojengwa na mizigomidogo midogo, nia yetu kupata hii Bandari ya Mpigaduriiwe kubwa, tuweze kushusha mizingo mingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa ukileta meli moja,ikikaa Bandari ya Malindi zaidi ya wiki mbili huwezi kuwekameli nyingine, ni hasara kubwa, wafanyabiashara wotewamebobea.

Kwa hiyo, nimuonbesana Mheshimiwa Waziri, tuwezeku, atupe ufafanuzi wa kina, ni lini bandari hii itaanzakujengwa hata kama kwa mfadhili mwingine, ili wazanzibarwaweze kupata mafanikio makubwa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba hilo nipateufafanuzi wa kina tena. Ahsante sana.

MWENYEKITI: Ufafanuzi Mheshimiwa Waziri anauliza nilini? Kwa kifupi tu.

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaMwenyekiti, naomba niseme kwamba jambo hili, mradi huuni moja ya miradi ambayo tumekuwa tunaijadili kwenye ileKamati ambayo inaongozwa na Mheshimiwa Makamu waRais, kwa hiyo hili jambo liko katika ngazi ya juu kabisa yakujadiliana, lakini kama nilivyosema, kikubwa ni hizi timu zawataalam ambazo tumeziteua zikamilishe uchambuzi wagharama za mradi huu ili tuone kama zinawiana na fedhaambazo tunakwenda kukopa, tukishajiridhisha hakuna mtu

Page 257: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

257

ambae hajui umuhimu wa Bandari kama anavyoieleza.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana tunaendelea, MheshimiwaZitto Kabwe.

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza nashukuru sana kwa maelezo ya kina ambayo Waziriwa Fedha, Mheshimiwa Dkt. Mpango, mwalimu wanguameyatoa kuhusiana na suala la Deni la Taifa na napendanikumbushe kwamba hoja yangu mimi haikuwa ukubwa wadeni, hoja yangu mimi ilikuwa ni menejimenti ya deni, hojawala siyo yangu ni hoja ya ukaguzi ambako kulikuwa kunahoja tatu ya mifumo hiyo hiyo ambayo umeitaja kwanza huowa Commonwealth, pili, EPICOR na huo wa Commonwealthkutosomana na tatu ni madeni ambayo disbursement reportyake haipo kwenye taarifa yenu na ndiyo maana nikaombana bahati nzuri umekiri kwamba CAG anaweza ukaguziwakati wowote, lakini tunachoomba ni Special Audit onManagement ya Public Dedt kwa sababu pia MheshimiwaWaziri wewe mwenyewe hapa umeona michango yaWabunge, hata takwimu ambazo wewe unazitoa naWabunge wanazitoa zinatofautiana sana. Kwa mfano, sasanimeangalia MER, Monthly Economic Review ya Benki Kuukuhusu deni la Taifa. External Debt mpaka Machi, 2019 ni dolabilioni 21.5, Domestic Dedt trilioni 14, ukichukua ukabadilishakwa exchange rate ya chini kabisa utakuta external debttrilioni 62.8.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwezi Juni, 2018 deni lotekwa ujumla wake lilikuwa 50 trillion; kwa hiyo kati ya Juni, 2018na Machi, 2019 deni limeongezeka kwa 50 percent, hapotunaachana na mikopo ambayo tayari mmekubaliana naWorld Bank ya 1.9 billion dollars ambayo bado haijawadisbursed kwa sababu ya masharti ambayo mmepeana naWorld Bank.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo by June kamamkikubaliana na World Bank maana yake tunakwenda

Page 258: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

258

kwenye deni la mpaka 64 trillion kutoka 50 trillion nyongezaya 14 trillion.

Kwa hiyo mimi ninachokiomba, Waziri ukubali hapandani ya Bunge kwamba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu waHesabu za Serikali afanye special audit (ukaguzi maalum) wamenejimenti ya Deni la Taifa. (Makofi)

Naomba maelezo yako Mheshimiwa Waziri,nisiporidhika kaka yangu itabidi niende nayo shilingi Buhigwetu hamna namna. (Makofi)

MWENYEKITI: Ufafanuzi Mheshimiwa Waziri wa Fedhatafadhali.

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaMwenyekiti, nilitoa statement fupi kwenye maelezo yangunikitumaini kwamba mdogo wangu, Mheshimiwa Zitto Kabweamenipata.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kiutaratibu yeyeamekwenda anasema ni hoja ya ukaguzi ya CAG, kama nihoja ya CAG ina nafasi yake itapelekwa kwenye Kamati yaPAC na italetwa humu ndani, tutaizungumza kwa hiyo sijuikama nalazimika kwenda huko. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la pili, nirudie tenakwamba mimi sipangi ajenda ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuuwa Hesabu za Serikali, hiyo ni mandate yake akitaka kupangaatapanga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la tatu, hizi tofauti zakitakwimu, kwa uzoefu wangu watu wanaposoma hizitakwimu ni vizuri wakaziangalia. Kuna tofauti ya muda wareporting yaani hata kama pana tofauti ya miezi miwili, mwezimmoja unapata completely different figure, kwa hiyo watuwanasoma tu ni Deni la Taifa, ni Deni la Taifa kwahiyo nimuhimu sana kuwa careful na muda unaotolewa taarifa.

Page 259: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

259

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la pil i, kunakuchanganya pia Deni la Serikali na Deni la Taifa, kwa hiyo nimuhimu, sipendi kuamini kwamba Mheshimiwa Zitto Kabwehajui hizi tofauti, lakini hiyo michanganyiko ambayo unaisikiakutoka kwa Waheshimiwa Wabunge inatokana na tofautikama hizi, lakini hata hizo exchange tare zenyewe ambazounasema, exchange rate mwingine anatumia averageexchange rate, mwingine anatumia exchange rate yamwisho wa mwaka you get a different figure.

Kwa hiyo, namuomba tu mdogo wangu aniachieshilingi yangu asiende huko sasa wale wajukuu zangu kuleBuhigwe utawaweza? Ahsante.

MWENYEKITI: Ahsante sana. Tunaendelea kwa sababuhilo ni jambo liko kwenye Kamati ya PAC. Mheshimiwa Silinde.

MHE. DAVID E. SILINDE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana na mimi kunipa fursa hii angalau nimuulizeMheshimiwa Waziri wa Fedha juu ya jambo dogo la masualaya fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika majibu yaMheshimiwa Waziri amejaribu kuainisha kwamba aligusiakidogo kuhusu vitambulisho ya Wamachinga, lakini miminajikita zaidi kwenye sera ya fedha na usimamizi ambaoWizara ya Fedha inapaswa kuwa nao.

Mheshimiwa Spika, uki[itia Ibara ya 38(1) ya Katibaambayo yenyewe inazungumzia mamalaka ya Bungekwenye kutunga sheria zote zinahusu kodi na Ibara ya 99ambayo inazungumzia mamlaka ya Rais, lakini ikimuelekezamambo gani hapaswi kufanya yaani kuna mambo ambayoRais anatakiwa atekeleze ambayo anamtuma Waziri waFedha kuleta Bungeni. Miongoni mwa mambo hayo ni kamamasuala yanayohusu kutoza kodi au kubadilisha kodi kwanamna yoyote, malipo au matumizi ya fedha, kuagiza malipona matumizi ta fedha kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina namengine kwa maana ya Ibara yote kama ilivyo.

Page 260: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

260

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwenye issue yavitambulisho pamoja na uzuri wake wote uliotajwa pale kunakitu kinaitwa mapato yanayotokana na vitambulisho, lakinimapato yale ya shilingi 20,000 ambayo yanakusanywa hukochini nimejaribu kupitia kwenye kitabu cha mapato (VolumeI) hii yote.

Nimeangalia kwenye TRA hayaonekani humu ndani,nimeangalia kwenye Ofisi za Sekretarieti za Mikoa ikiwemoMkoa wangu wa Songwe, vyanzo vyao vya nadni haipo,nimeangalia TAMISEMI haionekani humu ndani, nimekwendaOfisi ya Waziri Mkuu sijaona hicho chanzo, kwa hiyo, mimiambacho nilikuwa nataka kutoka kwa Waziri wa Fedhaatueleze hapa mapato hayo yanayotokana na vitambulishokwa nini hayaonekani kwenye Kitabu Namba Moja na sisihapa tupo kupitisha bajeti ya Bunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na unajua kabisa hakunashilingi yoyote inayokusanywa nchi hii popote pale hatakama ni senti moja lazima ionekane kwenye kitabu chamapato kwa maana ya Volume I, kwa hiyo nilitaka kupatamajibu.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Slinde na lile la MheshimiwaNdassa?

MBUNGE FULANI: Tofauti kabisa.

MHE. DAVID E. SILINDE: Tofauti kabisa.

MWENYEKITI: Yana tofauti?

MHE. DAVID E. SILINDE: Tofauti kabisa.

MWENYEKITI: Wewe unachoulizia ni kuonekanakwenye kitabu?

MHE. DAVID E. SILINDE: Mapato yawe kwenye kitabu.

MWENYEKITI: Haya umeeleweka.

Page 261: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

261

MHE. DAVID E. SILINDE: Kwa hiyo isipojibiwa vizurinitatoa shilingi. Ahsante.

MWENYEKITI: Ufafanuzi wa Serikali, Mheshimiwa Waziritafadhali.

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza nimshukuru Mheshimiwa Silinde muulizaswali kwa sababu ni suala la msingi na yeye najua ni mfuatiliajimzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mapato haya siyo kilamapato ya Serikali yanakuwa yanaoneshwa item by itemkwenye Volume I; kwa hiyo viko vyanzo ambavyo tunaviingizakwenye mfuko mkuu as a block, nilitaka nimuoneshe kidogo.Kwa hiyo, naomba tu anikubalie kwamba fedha hizi zipotumezi-budget kama sehemu ya mapato ya Mfuko Mkuu.(Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Silinde zipo hizo hela.(Kicheko)

MHE. DAVID E. SILINDE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru sana…

MWENYEKITI: Sasa mnataka muonyeshwe ninye siWaheshimiwa Wabunge nyinyi kwani ninyi ni watoto waprimary mpaka muonyeshwe kama vile…

WABUNGE FULANI: Yeye mwenyewe hajui zilipo.

MHE. DAVID E. SILINDE: Mheshimiwa Mwenyekiti, katikakitu ambacho nina uhakikanacho ni kwamba Serikali haijuizile fedha zilizpo watakwambia tu Mfuko Mkuu wa Hazina.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kwa nini nimeombajambo hili? Jambo hili ni jipya kwenye Taifa. Mwaka janalililetwa yaani katikati ya bajeti kwa maana lilitokea kwaMheshimiwa Rais likashuka chini. Kwenye Kamati ya bajetisisi tuliwahoji Serikali hizi hela zinaonekana wapi? Wakatupa

Page 262: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

262

urataibu kwamba hela hizi zinakusanywa, zinapelekwa TRA,zikitoka TRA zinapelekwa Mfuko Mkuu wa Hazina.

Mheshimiwa Mwenyekiti, chanzo kipya, kinapokuwakipya na sisi Bunge ndiyo tulikuwa na jukumu la kutunga sheriajamani tumepata chanzo kipya hapa cha haya mapato nani lazima hizi fedha za umma zionekane huku ndani, lakinibahati mbaya huu ni mwaka mpya sizungumzii mwaka wafedha uliopita 2018/2019 nazungumzia mwaka wa fedhampya ni hiki kitabu. Ni kwa nini Serikali inashindwa tu kukubalihapa kuleta addendum ya kufanya mabadiliko ili chanzocha hizo fedha kiweze kuonekana humu ndani kwa sababuvyanzo vyote vinafahamika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo kwa kusemabaadhi ya maneno naomba nitoe hoja ili Wabunge wapatekuchangia.

MWENYEKITI: Hoja ya nini sasa Bwana Silinde?

MHE. DAVID E. SILINDE: Kujadili.

MWENYEKITI: Umeongea vizuri Mheshimiwa Silinde,point yako ni muhimu na Waziri naye ameongea vizuri sanamnachotofautiana ni mahali tu pa kufanya kiweconspequancy zaidi na kadhalika. Sisi tunalitupa kwenyeKamati ya Bajeti kwa ufuatiliaji na wewe ni Mjumbe hukokwenye Kamati ya Bajeti. Mfuatilie vizuri huko, likae sawa,kama tutalazimika sisi Bunge kufanya follow up ya karibu walahakuna tatizo, haliwezi kutukwamisha hilo. (Makofi)

Ahsante sana Mheshimiwa Silinde kwa ukumbushohuo, bajeti mtafanya kwa niaba yetu. Mheshimiwa Mlinga.

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi suala languMheshimiwa Waziri amejitahidi kulifafanua lakini badosijamuelewa.

Page 263: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

263

Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo la Serikali kubinafsishamashirika ya umma moja ilikuwa ni kuondoa mzigo wakuyahudumia matokeo yake yajiendeshe yenyewe kwa faidana Serikali ipate gawio. Tuna mashirika ya umma zaidi ya 230lakini mpaka leo hi yanayotoa mgao wa Serikali hayazidimashirika 10.

Kwa hiyo nataka majibu ya Serikali (ufafanuzi) wanamkakati gani kuhakikisha haya mashirika yanajiendeshakifaida na matokeo yake nayatoa gawiwo Serikalini nakuacha kuwa mzigo tena kwa Serikali kwa sababu yapompaka leo mishahara Serikali inatoa kwa ajili ya kuwalipawatumishi, la sivyo nitashika shilingi. (Makofi)

MWENYEKITI: Ufafanuzi wa jambo hilo, MheshimiwaNaibu Waziri wa Fedha, Dkt.Kijaji.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaMwenyekiti, naomba nimshukuru Mheshimiwa Mlinga kwahoja hii muhimu kuhusu mashirika yetu ambayoyalibonafsishwa na sasa taasisi na mashirika ambayo yanatoagawio kwa Serikali na mkakati uliopo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati naijibu hoja hiinilijaribu kueleza mambo mbalimbali ambayo Ofisi ya Msajiliwa Hazina imeanza kuyashughulikia ili kuhakikisha mashirikana taasisi hizi ambazo Serikali imewekeza au Taasisi za ummaziweze kutoa gawio kwenye Serikali. Nikasema kwanzatumeimarisha Ofisi ya Msajili wa Hazina yenyewe, lakini pilinikasema Ofisi ya Msajili imeanza kushughulika na Shirika mojabaada ya lingine kusainiana mikataba (performancecontract) ili kila shirika liweze kuonyesha nini wanatakiwakufanya ili Serikali iweze kupata gawio.

Kwa hiyo nimuombe Mheshimiwa Mlinga aipe nafasiOfisi ya Msajili wa Hazina, tumeiboresha kwa kiwango kikubwana wameanza kufanyakazi yao vizuri na tayari tumeonaSerikali imeanza kupata gawio tofauti na kipindi cha nyuma.Nina uhakika ndani ya kipindi kifupi kijacho mashirika mengi

Page 264: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

264

na taasisi nyingi zitaweza kufanya vizuri kwa sababutunasainiana hizi performance contract.

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Mlingaameridhika. Mheshimiwa Zainab Katimba.

MHE. ZAINAB A. KATIMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa kunipa fursa hii ili niweze kuuliza swali kwaWaziri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi sote tunafahamukwamba ajira kwenye Serikali lakini kwenye sekta binafsihazitoshi kuajiri vijana wote na tunawahamasisha vijanawaweze kujiajiri wao wenyewe kwa kufanya shughulimbalimbali ikiwemo ujasiriamali. Sasa pindi vijanawanapoanzisha biashara, wanapokwenda kukata leseni yabiashara, wanakutana na kigezo cha kuwa na Tax ClearanceCertificate na ili waweze kupata hiyo Tax ClearanceCertificate wakienda TRA wanapewa makisio ya kodi yamapato ambayo wanalazimika walipe first installment priorkabla hata hawajapata hiyo leseni ya biashara. Kwa hiyowanalipa hiyo kodi ya mapato, wanapata Tax ClearanceCertificate, wanarudi kwenye mamlaka ya leseni ya biasharandipo wanapata leseni ya biashara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa sisi tunafahamukwamba kwanza vijana wamepata changamoto kwanza yakukosa ajira lakini pili, wamehangaika kutafuta mitaji nanamna zote ili waweze kujiajiri wao wenyewe, lakiniwanapokwenda kujiajiri wao wenyewe wanakutana navikwazo kama hivi.

Je, Serikali haioni sasa iweze kutoa kama six monthgross period kwa startup yaani biashara zinazofunguliwa zilebiashara mpya kabla ya kuanza kulipa first installment yamakisio ya kodi. (Makofi)

Naomba majibu ya Serikali na kama nisipopatamajibu ya kina nitawaomba Wabunge wenzangu waniungemkono, nitashika shilingi ya Waziri. (Makofi)

Page 265: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

265

MWENYEKITI: Wala suala hili, tunakushukuru sana, walasiyo la vijana peke yake, yoyote anayeanza biashara hatauwe mzee vipi utaratibu ni huo huo kwa hiyo inamfanya mtuapate tabu kweli wakati wa kuanza. Ndiyo Mheshimiwa Waziriufafanuzi tafadhali. (Makofi)

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza nimpongeze sana mdogo wangu kwaobservation nzuri sana na ni jambo ambalo kwa kwelilimekuwa linasumbua sana na Kamati ya Bajeti imelijadili nawaliishauri Serikali ipasavyo.

Naomba tu nimuombe mdogo wangu MheshimiwaKatimba avute subira kidogo tu kwa sababu Serikaliimelifanyia kazi na itatangaza uamuzi hivi karibuni. (Makofi)

MWENYEKITI: Nafikiri Zainab umesoma maandikokwenye ukuta, una cha kusema? Mheshimiwa Zainab.

MHE. ZAINAB A. KATIMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwa sabau Mheshimiwa Waziri ametoa commitmentkwamba wataliangalia hili suala na wataweza kutoa kaulina maamuzi basi sitoshika tena shilingi ya Waziri. Nashukuru.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Usihofu bado tuko nayeWaziri, bado tuko naye, huko mbele bado tuko naye kwasababu kusema ukweli hili ni moja ya vikwazo vikubwa sabavya watu kuweza kuanza kwenda mbele, haraka ya nini siutampata tu huyo mtu katika miezi sita, atatakaja tu TRA,Mheshimiwa Masoud tafadhali.

MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni mara kadhaa mkakati waSerikali umekuwa ukituahidi hapa Bungeni kwambawataboresha maslahi ya wastaafu na hasa kwenye sualazima la pensheni, ni mara kadhaa pensheni ya kima cha chinikwa wastaafu wetu ambao wamefanyia kazi kwenye Serikali

Page 266: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

266

kwa muda mrefu kwenye mazingira magumu, lakini hadi leoSerikali hili jambo wamekuwa wakiliachia na hawatakikuweza kuboresha pensheni ya wastaafu wetu.

Mheshimiwa Spika, pensheni ya kima cha chini hivisasa ni shilingi 100,000 sawa na shilingi 3,300 kwa siku ni maraBunge lililopita Serikali iliweza kupandisha pensheni kutokashilingi 51,144 hadi shilingi 100,000, tangu awamu hii iingie sasahuu ni mwaka wa nne sasa imekuwa ikituahidi hapa Bungenikwamba itaandaa mazingira ya kuboresha pensheni kwawastaafu.

Mheshimiwa Spika, ninaomba Serikali itupe ahadi yakweli ahadi ya Mwezi wa Ramadhani, ahadi maridhawaambayo itaboresha maslahi ya wastaafu wetu hawa nakama nisipopata jibu sahihi basi naona kama shilingi ya kakaninaweza nikaondoka nayo, nakuomba sana jibumaridhawa, pensheni wastaafu ambayo kima chao cha chinini shilingi 3,300 kwa siku watafanya nini? Kama sitopata jibuzuri basi nahisi kama shilingi nitaweza kuondoka nayo.

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Waziriufafanuzi wa jambo hili muhimu sana, Mheshimiwa Waziri wawazee, Mheshimiwa Waziri wa Nchi.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, VIJANA, AJIRA NA WALEMAVU: Mheshimiwa Spika,naomba tu niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge kwambabaada ya kutungwa kwa Sheria mpya ya Mifuko ambayoimeunganisha mifuko mingi kuwa na mfuko mmoja kwa ajiliya public sector na kuwa na mfuko mmoja kwa ajili ya privatesector, sasa hivi Bodi zote za Mifuko zinafanya kazikushughulikia matatizo na kero zote ambazo zimekuwazikiwakumba wastaafu na ninaomba niwahakikishieWaheshimiwa Wabunge tutakapokuwa tume-settle kila kitukitakuwa kiko mahali pake. Kwa hiyo, kuunganishwa kwasheria mbili hizi kunasaidia sana kupunguza kero na matatizoyaliyokuwa yanaikuta sekta nzima ya hifadhi ya jamii, lakiniwastaafu wote katika nchi yetu ya Tanzania.

Page 267: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

267

Kwa hiyo namuomba tu Mheshimiwa Masoudarudishe shilingi kwa Mheshimiwa Waziri ajue kwamba baadaya kazi ile nzito iliyofanyika sasa Serikali inaanza kufanyamaboresho makubwa kwenye sekta nzima ya hifadhi ya jamiina masuala yote ya pensheni kwa ajili ya ustawi wa wastaafuwote katika nchi yetu ya Tanzania. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Masoud bado liko kwako.

MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM: MheshimiwaMwenyekiti, nashukuru kauli ya Mheshimiwa Waziri mzee nawewe ndio mzee mwenzako.

Kwa hiyo mimi kwangu suala la kuunganishwa kwamifuko ni jambo jema, maboresho yanafanyika sina pingamizina mzee mwenzangu, mchakato uwe unaendelea, lakiniyote ambayo yanafanyika haiwezekani huu ni mwaka wanne bado kauli ni zile zile maboresho, mifuko imeunganishwahivi karibuni sawa namkubalia, lakini watupe ahadi ya kweli,ahadi ya mwezi wa Ramadhani Mheshimiwa Ashatu naonaunafanya kichwa hivi kwa ahadi aya mwezi wa Ramadhanimtuambie ukweli shil ingi 3,300 zinakwendaje hapamaboresho ni lini mtafikia hicho kipindi angalau mtu mkatupabaada ya miezi miwili, mitatu, minne na kama haiwezekanikweli na nikwambie jambo moja kubwa wengine walikuwavyombo vya ulinzi leo unakuwa Sargent Jeshi la WananchiSargent aliyestaafu mwaka 1985 anapewa shilingi 98,000vyombo vya ulinzi na usalama yaani unafika mpaka unapatawakati hivi kweli ndio vyombo vya ulinzi tunafikisha hapa.

Kwa hiyo, hebu mtuambie kauli ya ziada wasikiewanataka kusikia ya ziada wanataka kusikia jambo la ziadamzee mwenzangu tafadhali anasikia mzee mwenzetu nayeMheshimiwa Ashatu, Ramadhani Karim, nashukuru.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Ashatu Kijaji.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaMwenyekiti, nawashukuru na nimshukuru sana MheshimiwaWaziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu kwa jibu halisi na rasmi la

Page 268: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

268

Serikali, lakini nimshukuru sana Mheshimiwa Masoud kwakuwajali wazee kama ambavyo Serikali yetu imekuwa ikiwajaliwazee miaka yote na ndio maana vipindi hadi vipindiimekuwa ikiongeza pensheni kwa ajili ya wastaafu wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo kama alivyosemaMheshimiwa Waziri wa Nchi kuunganishwa kwa mifuko kujana sheria hii moja ni mwanzo mzuri, nimekuwa nikilielezaBunge lako tukufu siku zote kwamba unapoongeza chochotelazima tuangalie mifuko yote ina nini na Mheshimiwa Waziriwa Nchi amesema tayari tathimini imefanyika, sasa tunawezakukaa chini na kufikiri ni kipi kiongezeke baada ya kujuamifuko ya mifuko yetu hii ina nini ndani yake.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo nimuombe tuMheshimiwa Masoud kwamba Serikali inalitambua jambo hilivizuri tu na kama ambavyo uchumi wetu unaendeleakuimarika na mifuko yetu inaendelea kufanya vizuritutaongeza, ni ahadi ya Serikali hatuwezi kuangushawastaafu wetu wamefanya kazi nzuri kwa Taifa letu, ahsantesana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Masoudtunashukuru, Serikali imesikia jamani Serikali wazee walehawasubiri yaani wanaondoka mmoja mmoja kila siku hukoyaani tunazika. Kwa hiyo mchakato wao ungeweza kuwamaalum kabisa wakati wa wengine unakwenda taratibu,lakini wao ukawa faster kidogo waambulie kidogowasomeshe wajukuu nao. Tunatumaini mwakani wakati huutatakapokutana Inshallah kutakuwa na kitu fulani kuhusuhawa wastaafu kwa kweli itatia moyo sana maana wazeewetu jamani mwezi mtukufu huu, guillotine.

Fungu 50 – Wizara ya Fedha na Mipango

Kif. 1001 – Administration and Human Resources Management.............…Sh.8,007,734,000

Kif. 1002 – Finance and Accounts Unit……………….…….......Sh.1,253,084,000

Kif. 1003 – Planning Division…………………..…Sh.36,560,508,000

Page 269: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

269

Kif. 1004 – Legal Services Unit…………………….Sh.1,120,403,000Kif. 1005 – Government Communication Unit…Sh.539,243,000Kif. 1006 – Internal Audit Unit……………………….Sh.509,204,000Kif. 1008 – Procurement Management Unit…….Sh.799,722,000Kif. 1010 – Information and

Communication Technology….......Sh.1,081,213,000Kif. 3001 – Internal Auditor General…………….Sh.3,282,560,000Kif. 5001 – Government Asset

Management Division........................Sh.5,336,593,000Kif. 6001 – Financial Management Information

Systems Division……...........………….Sh.7,223,166,000

(Vifungu Vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

Fungu 21 – Hazina

Kif. 1002 – Finance and Accounts Unit…….. …Sh.1,075,024,000Kif. 1009 – Public Procurement

Policy Unit (PPU)…...............................Sh.1,360,322,000Kif. 2001 – Government Budget division…. …Sh.864,742,056,000Kif. 2002 – Policy Analysis Division…….……….Sh.379,353,862,000Kif. 4001 – External Finance Division…….……...Sh.42,366,153,780Kif. 4002 – Public Private Partnership Unit…….…Sh.1,671,504,220Kif. 5001– Financial Sector

Development Division...............…......Sh.3,149,030,000Kif. 6001 – Debt Management Division……….Sh.3,218,280,000Kif. 7001 – Poverty

Eradication Department….............Sh.1,734,378,000Kif. 8001 – National Planning Division…….......Sh.3,532,380,000

(Vifungu Vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

Fungu 22 – Deni la Taifa

Kif. 1001 – Administration and Human Resources Management..……Sh.9,730,012,708,000

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

Page 270: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

270

Fungu 23 – Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali

Kif. 3001 – Public Debt Management…………….Sh.222,750,000Kif. 3002 – Expenditure Management………….Sh.4,756,237,500Kif. 3003 – Financial Management………..….Sh.31,489,820,544Kif. 3004 – Financial Operations

and Standards................................…Sh.4,554,180,000Kif. 3005 – Sub Treasury Arusha………….………….Sh.95,900,000Kif. 3006 – Sub Treasury Coast………........……..….Sh.91,230,000Kif. 3007 – sub Treasury Dodoma ………….......….………….Sh.0Kif. 3008 – Sub Treasury Iringa……………………….Sh.90,845,000Kif. 3009 – Sub Treasury Kagera…………………….Sh.90,965,000Kif. 3010 – Sub Treasury Kigoma…………………….Sh.88,380,000Kif. 3011 – Sub Treasury Kilimanjaro………………….Sh.91,320,000Kif. 3012– Sub Treasury Lindi…………………………..Sh.90,890,000Kif. 3013 – Sub Treasury Mara………………………...Sh.90,810,000Kif. 3014 – Sub Treasury Mbeya…………………….Sh.90,820,000Kif. 3015 – Sub Treasury Morogoro………………….Sh.98,000,000Kif. 3016 – Sub Treasury Mtwara…………………….Sh.91,300,000Kif. 3017 – Sub Treasury Mwanza………………...….Sh.90,650,000Kif. 3018 – Sub Treasury Rukwa………………………Sh.90,760,000Kif. 3019 – Sub Treasury Ruvuma……………..…….Sh.90,800,000Kif. 3020 – Sub Treasury Shinyanga………………..Sh.89,950,000Kif. 3021 – Sub Treasury Singida…………………….Sh.91,290,000Kif. 3022 – Sub Treasury Tabora………………....….Sh.86,450,000Kif. 3023 – Sub Treasury Tanga……………………….Sh.90,915,000Kif. 3024 – Sub Treasury Manyara………………….Sh.98,710,000Kif. 3025 – Sub Treasury Njombe………………….Sh.107,310,000Kif. 3026 – Sub Treasury Geita……………..……….Sh.90,790,000Kif. 3027 – Sub Treasury Katavi…………….……….Sh.90,730,000Kif. 3028– Sub Treasury Simiyu………………...…….Sh.90,810,000Kif. 3029 – Sub Treasury Songwe…………………….Sh.88,400,000Kif. 3030 – Sub Treasury Dar es Salaam………….Sh.141,420,000Kif.4001 – Local Government Finances………….Sh.143,902,000Kif. 7001 – Pension and Gratuity………………….Sh.549,712,956

(Vifungu Vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

Page 271: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

271

Fungu 07 – Ofisi ya Msajili wa Hazina

Kif. 1001 – Administration and Human Resources Management..…………Sh.3,785,444,185

Kif.1002 – Finance and Accounts Unit……….......Sh.451,630,070Kif. 1003 – Planning Unit…….............…………..…Sh.413,190,276Kif. 1004 – Legal Services Unit…..……………...….Sh.303,990,140Kif. 1005 – Procurement Management Unit..…Sh.305,420,140Kif. 1006 – Information and Communication

Technology Unit...............................….Sh.650,377,209Kif. 1007– Information, Education and

Communication Unit……................…..Sh.277,598,549Kif. 1008 – Internal Audit Unit…………………..…..Sh.427,420,140Kif. 2001 – Public Investment Management

Division ……..........................…..…..Sh.31,279,825,000Kif. 3001– Privatization and Monitoring………..Sh.1,514,424,349Kif. 4001– Management Service Division……..Sh.1,101,481,942

(Vifungu Vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

Fungu 10 – Tume ya Pamoja ya Fedha

Kif. 1001 – Administration General…..…………Sh.1,735,515,000Kif.1002 – Internal Audit Unit………..............….......Sh.90,040,000Kif. 2001– Technical Department…………….……Sh.270,940,000Kif. 2002 – Zanzibar Office…….............……….......Sh.111,440,000

(Vifungu Vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

Fungu 13 – Kitengo cha Udhibidi wa Fedha Haramu

Kif. 1001 – Administration and Human Resources Management...........……Sh.1,286,213,000

Kif.1002 – Finance and Accounts Unit………….......Sh.72,480,000Kif. 1003- Internal Audit…………………….……..…Sh.23,580,000Kif. 1004 – Monitoring Unit…..………….……...….Sh.165,080,000Kif. 1005 – Inspection Unit ……………............….…Sh.79,925,000Kif. 1006 – Procurement Management Unit……….Sh.18,130,000

Page 272: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

272

Kif. 1007– Legal Service Unit………………………..Sh.67,590,000Kif. 1008 – Management Information

Systems Unit….........................................Sh.302,570,000

(Vifungu Vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

Fungu 45 – Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi

Kif. 1001 – Administration and Human Resources Management Division……......……Sh.12,006,968,000

Kif.1002 – Finance and Accounts Unit………......Sh.1,097,667,000Kif. 1003- Internal Audit………………........……..…Sh.294,974,000Kif. 1004 – Ministerial Audit Division………...….Sh.7,101,411,500Kif. 1005 – Local Government

Authorities Division..............................Sh.11,783,769,000Kif. 1006 – Performance Audits Division……..….Sh.2,317,499,000Kif. 1007– National Account Division…….……..Sh.4,779,369,000Kif. 1008 – Technical Support Service Unit….…..Sh.4,166,997,000Kif. 1009 – Public Authorities Audit Division……..Sh.5,308,784,000Kif. 1010 – Planning Monitoring and

Evaluation Division………............……..Sh.909,510,000Kif. 1011 – Procurement

Management Unit…............……..…..Sh.477,952,000Kif. 1012 – Information and Communication

Technology Unit............................…..Sh.1,568,094,000Kif. 1013 – Forensic Audit Unit………..……..…..Sh.2,092,710,000Kif. 1008 – Technical Support Service Unit……..Sh.4,166,997,000Kif. 1014 – Quality Assurance Unit……………..…..Sh.707,708,000Kif. 1015 – Government Communication Unit…….Sh.97,360,000Kif. 1016 – Risk Management and

Compliance Unit……….............…..…..Sh.128,097,500Kif. 1017 – Legal Services Unit………………….…..Sh.143,518,000Kif. 1018 – Parliamentary

Coordination Unit…........................……..Sh.94,490,000

(Vifungu Vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

Page 273: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

273

MATUMIZI YA MAENDELEO

Fungu 50 – Wizara ya Fedha na Mipango

Kif. 1001 – Administration and Human Resources Management Division…Sh.1,118,270,000

Kif.1003 – Planning Division ………………….....Sh.18,937,221,000Kif.1004 – Legal Services Unit ………………………..……......Sh. 0Kif.1010 – Information and Communication

Technology Unit..................................Sh. 5,000,000,000Kif. 3001 – Internal Auditor General ……………Sh. 1,229,500,000Kif. 5001 – Government Asset

Management Division…..…............Sh. 2,950,000,000Kif. 6001 – Financial Management, Information

Systems Division......……………........Sh.5,289,050,000

(Vifungu Vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

Fungu 21 – Hazina

Kif. 2001 – Government Budget Division……....……………Sh.585,500,000,000

Kif. 2002 – Policy Analysis Division ……………….…Sh.324,280,000Kif. 4001 – External Finance Division ……………Sh.3,031,830,000Kif. 4002 – Public Private Partnership Unit…………...………Sh. 0Kif. 6001 – Debt Management Division…………..Sh. 397,160,000Kif. 7001 – Poverty Eradication Department……Sh. 288,868,000Kif. 8001 – National Planning Division……………Sh. 238,130,000

(Vifungu Vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

Fungu 23 – Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali

Kif. 3002 – Expenditure Management…………………………Sh.0Kif. 3003– Financial Management ……………Sh.2,973,560,000

Page 274: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

274

Kif. 3004 – Financial Operations and Standards...................................…Sh.269,640,000

Kif. 4001 – Local Government Finances …..…....Sh.56,800,000

(Vifungu Vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

Fungu 07 – Ofisi ya Msajili wa Hazina

Kif. 1001 – Administration and Human Resources Management…........................................…….…Sh. 0

Kif.1002 – Finance and Account Unit............…………….....Sh. 0Kif.1003 – Planning Unit …………………...............Sh.827,550,000Kif.1004 – Legal Services Unit ………………………..…….....Sh. 0Kif.1006 – Information and Communication

Technology Unit..…...............................Sh.685,450,000Kif. 2001 – Public Investment Management

Division........................…......................Sh.472,450,000Kif.3001 – Privatization and Monitoring..............Sh.341,550,000Kif.4001 – Management Service Division.............................Sh.0

(Vifungu Vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

Fungu 13 – Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramu

Kif. 1001 – Administration and Human Resources Management Unit..............Sh.200,295,998

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

Fungu 45 – Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi

Kif. 1001 – Administration and HumanResources Management Division….…Sh. 4,200,000,000

Kif.1010 – Planning Monitoring and Evaluation Division.............................………........Sh.2,100,000,000

(Vifungu Vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

Page 275: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

275

NDG. YONA KIRUMBI - KATIBU MEZANI: MheshimiwaMwenyekiti, naomba kutoa taarifa kwamba Kamati yaMatumizi imekamilisha kazi yake.

(Bunge lilirudia)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tukae.MheshimiwaWaziri wa Fedha na Mipango, Taarifa.

T A A R I F A

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika,naomba kutoa taarifa kuwa Bunge lako limekaa kamaKamati ya Matumizi limekamilisha kazi zake. Naomba taarifaya Kamati ya Matumizi ikubaliwe na Bunge.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO:Mheshimiwa Spika, naafiki.

SPIKA: Hoja imetolewa na imeungwa mkono,ahsanteni sana. sasa kama ilivyo ada napaswa niwahojikuhusiana na hoja iliyotolewa na Mheshimiwa Waziri kwambasasa mkubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwaWizara hii ya Fedha na Mipango kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

(Hoja ilitolewa Iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

(Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa 2019/2020

Wizara ya Fedha na Mipango yalipitishwa na Bunge)

SPIKA: Mtakufa njaa ninyi. (Makofi)

Kwa niaba yenu Waheshimiwa Wabunge tukushukurusana Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango, MheshimiwaNaibu Waziri, Katibu Mkuu, Naibu Makatibu Wakuu na

Page 276: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

276

wengine wote walio chini yetu kwa kazi kubwa sana ambayommekuwa mkiifanya all through kipindi chote hiki cha Bungemmekuwa na Kamati ya Bajeti kwa karibu sana, tunaaminimmejadili mambo mengi sana yenye manufaa kwa nchi yetu,lakini pia ninyi ndio tuseme waratibu wa mambo ya kifedhakwa ujumla wake kwa Wizara zote, kwa hiyo mko katikati yatimu kama ni timu ya mchezo basi ninyi ndio mko midfiledpale. Na kawaida midfield ikiwambo mbovu hiyo timuitafungwa tu, kwa hiyo tunawategemea sana tunawaaminiasana munajitahidi sana kufanya kazi zenu tunawapongezasana. Na tunajua bado kazi ya kuwa na sisi bado ni kubwambele baada ya hapa sisi tunaenda kwenye Eid na nini lakiniwewe tunajua hakuna cha Eid na Naibu wako na wataalamwote hawa sasa mkaandae hotuba ya bajeti ili tarehe 13Juni, siku ya alhamisi tukutane hapa isomwe hotuba ambayoitazingatia pamoja na mambo mengine ushauri ambaoWaheshimiwa Wabunge mmeutoa tangu tulipoanza shughulizetu hapa. (Makofi)

Kwa hiyo, kwa Wizara wao bado ni kwamba leowamepita hatua moja tu, lakini sasa kazi ndio inaanza kabisa.Kwa hiyo tunawatakia kila la kheri tunawaombeeni kila lakheri na fanaka katika kazi za mwaka unaokuja wa fedha,tunajua fedha tuliyowapa si nyingi kihivyo kama Wizara, lakinitujitahidi hivyo hivyo.

Waheshimiwa Wabunge, tutambue kazi ya kuwaMheshimiwa Waziri wa Fedha ni kazi ngumu sana na ni kazimojawapo ambayo huwezi kupendwa, ukishakuwa Waziri waFedha wewe ni wa kupewa pole tu maana kila mtuanakulaumu sasa wasikulaumu wewe walaumu nani sasa,kwa sababu fedha siku zote huwa haitoshi na katika nchikama za kwetu ambazo rasilimali fedha ni adimu zaidi basina lawama zinakuwa nyingi zaidi.

Lakini lazima tukulaumu kwa sababu mwakani kipimokinaanza kwa Wabunge wakati wote huo tena hutajwi wewesasa, inakuwa hii barabara si Mbunge fulani bwana yuko tuhata barabara haichongwi, sasa hapo tena Waziri wa Fedhahayupo tena, Wabunge wanakuwa wameshabeba, hatuna

Page 277: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

277

maji huyu Mbunge anakaa tu hapa, safari iliyopita asilimia70 hawakurudi hapa, sasa sijui safari hii itakuwaje. Kwa hiyotunawapongeza sana, safari nasikia kuna upande fulani waondio kwa kweli wanaugulia zaidi. (Makofi/ Kicheko)

Basi baada ya kuwatakia kila la kheri Wizara ya Fedhana Mipango sasa niwatambue vijana wetu walio kwenyegallery ambao ni wanafunzi 75 na walimu wao watano, jumlayao 80 kutoka Shule ya Msingi ya Southern Highland yaMafinga Mkoa wa Iringa wakiongozwa na Mwalimu Ally Mrutuni wageni wa Mheshimiwa Cosato Chumi, ahsanteni sanakaribuni sana Southern Highland karibuni Bungeni. (Makofi)

Eeh, wanapendeza wavulana na wasichana eeh ilebaridi vipi kule? Poleni sana kwa baridi wako vizuri sanamnapendeza sana. Mheshimiwa Cosato utatusalimia watotowetu, ahsante sana safi sana. Hapa Profesa MheshimiwaNdalichako kwa kweli shule zako siku hizi yaani wanaokujahapa wako vizuri inaonekana viwango vimepanda kabisa,viwango cha elimu vimepanda sana.(Makofi)

Wako wageni wawili wa Mheshimiwa Flatei Massayambao ni wapiga kura wake kutoka Mbulu Vijjini, Mkoa waManyara wale pale, karibuni sana wageni wetu kutokaMbulu. (Makofi)

Basi Waheshimiwa Wabunge kama tulivyokubalianaile majuzi kwamba tuiweke vizuri ratiba yetu nanawashukuruni sana kwa pamoja tumeweza kuiweka vizuri,kwa jinsi hiyo, tunataraji kwamba kesho wanaosafiri mnawezamkasafiri kwenda sehemu mbalimbali za nchi yetu, tunaaminitutapewa maelekezo Eid ni lini na wahusika ambao ni viongoziwetu wa dini, basi tutakuwa na wapiga kura wetu waleambao tutakuwepo Dodoma basi vema na Spika nayeatakuwepo Dodoma, kwa hiyo tunaweza tukatafutanatukapata pilau la Eid.

Lakini matarajio kwa Kamati ya Bajeti na Kamati yaUongozi watarudi siku ya Alhamisi ili Ijumaa kazi hiyo ianze auvinginevyo kadri ambavyo mtakuwa mmepanga na

Page 278: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku-balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

278

Mheshimiwa Waziri wa Fedha. Lakini mjitahidi basi by Ijumaaau Jumamosi muanze, lakini sisi kwa maana ya Bungetumewapa zile siku sita zenu tumewapa Ijumaa, Jumamosi,Jumapili na tumewapa Jumatatu, Jumanne, Jumatano yaanimpaka tarehe 12 Juni. Kwa hiyo nyinyi jipangeni vizuri peanenitaarifa ili kazi hiyo iweze kufanyika. (Makofi)

Lakini sisi hapa tutakutana Jumatatu kama leoWabunge wote kipindi cha maswali asubuhi, naaminitutakaporudi tutakuwa tupo fresh watu wote kabisa kwa ajiliya kuelekea kwenye Bajeti ya Taifa ambayo itasomwa tarehe13 Juni, 2019 siku ya alhamis. Nadhani itakuwa imekaa vizuri,baada ya kipindi hiki kirefu hiki ambacho tumeshuhgulikanacho iko haja kidogo ya ku- stretch muscles kidogo, halafututakaporudi kuanzia Jumatatu tutakuwa na vipindi vyamaswali asubuhi baada ya hapo Kamati ya Bajeti inaendeleana kama kuna mambo mengine vilevile tutayabeba wakatihuo.

Basi sasa kwa muda ulipofika naomba sasa niahirisheshughuli za Bunge had Jumatatu ya tarehe 10 Juni, 2019.(Makofi)

(Saa 11:58 Jioni Bunge liliahirishwa hadi Siku ya Jumatatu,Tarehe 10 Juni, 2019 Saa Tatu Asubuhi)