65
FORMATION MISSIONNAIRE THEOLOJIA Muhtasari: Elekeza kwa mada ilioko hapa chini nayo itakuelekeza kwa mada hiyo. I. Tafsiri ya Theolojia II. Lengo III. Mitandao Inayoweza Kukusaidia IV. Kanuni za Maandiko V. Upuzio wa Maandiko VI. Imani VII. Mungu Aliye na Nafsi Tatu A. Baba B. Mwana C. Roho Mtakatifu VIII. Malaika A. Malaika Watakatifu B. Malaika Walioanguka IX. Mwanadamu A. Uumbaji B. Kuanguka kwa Mwanadamu C. Dhambi D. Wokovu 1. Kuokolewa kwa Neema 2. Toba

MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

  • Upload
    others

  • View
    14

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

FORMATION MISSIONNAIRE

THEOLOJIA

Muhtasari: Elekeza kwa mada ilioko hapa chini nayo itakuelekeza kwa mada hiyo.I. Tafsiri ya Theolojia II. LengoIII. Mitandao Inayoweza KukusaidiaIV. Kanuni za MaandikoV. Upuzio wa MaandikoVI. ImaniVII. Mungu Aliye na Nafsi Tatu

A. BabaB. Mwana C. Roho Mtakatifu

VIII. Malaika A. Malaika WatakatifuB. Malaika Walioanguka

IX. MwanadamuA. UumbajiB. Kuanguka kwa MwanadamuC. DhambiD. Wokovu

1. Kuokolewa kwa Neema2. Toba3. Upatanisho wa Mungu na Mwanadamu

a. Tulizab. Ukuhani wa Waumini

Page 2: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

4. Sheria ya Neema5. Thibitisho6. Wongofu, Kutakaswa na Kukutukuza

X. Dhamana ya WokovuXI. Uchaguzi na Mada Zinazoambatana

A. UchaguziB. HiariC. Yaliyoamuliwa D. Kujua Jambo kabla HalijatokeaE. Msimamo wa Kipekee wa Kitheolojia

XII. Mambo ya MwishoA. Utatu usio MtakatifuB. MajonziC. Siku ya KiamaD. Kiti cha Hukumu cha KristoE. Vita vya Har-MagedoniF. Kuja kwa Kristo kwa Mara ya PiliG. Milenia

1. Mtazamio Kabla ya Milenia2. Mtazamio Baada ya Milenia3. Mtazamio wa Milenia

H. Uasi wa MwishoI. Kiti cha Enzi Kikubwa Cheupe cha HukumuJ. Mbingu Mpya na Nchi Mpya

XIII. Ufalme wa Mungu

XIV. Kanisa

XV. Agano

XVI. Maovu

XVII. Maombi

XVIII. Bibliografia

Haki ya Kunakili © 2008 Shirika la Mafunzo ya Umisheni. Haki Imehifadhiwa.

Page 3: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

THEOLOJIA

I. Tafsiri ya Theolojia

 Theolojia ni “mtalaa juu ya Mungu na uhusiano kati ya Mungu na vitu vyote.” 1 Theolojia ya Kikristo ni mtalaa huo katika taswira ya Kikristo. Theolojia ya Kikristo huchunguza kanuni zilizokuzwa na kanisa la Kikristo.

1 Webster’s New World Dictionary, College Edition, s.v. “theology.”

RUDI KWA MUHTASARI

Page 4: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

THEOLOJIA

II. Lengo

Baada ya kusoma kiunzi hiki cha mafundisho, unafaa kuelewa mambo yafuatayo:

Jinsi na wakati orodha rasmi ya Maandiko iliziduliwa. Jinsi tawi tatu za kanisa la Kristo zinavyotazama vitabu visivyothibitishwa

“Apocrypha.” Wakati Agano la Kale na vitabu visivyothibitishwa (Septuagint) zilimalizika na

umuhimu wake kuhusiana na unabii wa Agano la Kale. Tahini za kuweka kitabu katika orodha rasmi ya Agano Jipya. Kiini cha Biblia Utaratibu na mkazo wa Imani ya Mitume na imani ya Nicene. Imani kwamba kuna Mungu mmoja na jinsi ya kufafanua Utatu Mtakatifu. Tabia za Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Mahali unapoweza kupata orodha ya karama za Roho Mtakatifu katika

Maandiko. Tabia na umuhimu wa malaika. Maumbile na kazi ya Shetani na pepo zake. Maelezo ya Kibiblia kuhusu kuumbwa kwa mwanadamu. Dhambi ya Adamu na matokeo ya laana. Mpango wa Mungu wa ukombozi wa ulimwengu. Hali ya dhambi na matokeo yake. Kanuni ya soteriolojia na mada zilizo ndani yake. Uchaguzi na mada zinazohusiana. Mada zilizojumuishwa katika kanuni ya mambo ya mwisho. Ufalme wa Mungu. Kanisa na mwanzilishi wa kanisa. Mitazamo mitatu tofauti ya kanisa kuhusu elementi zinazotumika katika ushirika.

Kuwa na uwezo wa kueleza “ishara ya ukumbusho.” Mapatano nane ya Kibiblia Shida ya maovu. Jinsi ya kuomba.

RUDI KWA MUHTASARI

Page 5: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

THEOLOJIA

III. Mitandao Inayoweza Kukusaidia

Kwa kamusi ya Theolojia ya mtandao, tazama:

http://www.carm.org/dictionary.htm

Kutazama vifungu vya Biblia kwa haraka:

http://www.biblegateway.com/passage/

RUDI KWA MUHTASARI

Page 6: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

THEOLOJIA

IV. Kanuni za Maandiko

Neno Kanuni linatokana na neno la Kilatini lililo na maana ya “mstari wa kupima au amri.”2 Kanuni za Maandiko zinataja Vitabu ambavyo vimetambuliwa na kanisa kuwa na ufunuo wa Mungu. Kitabu ambacho ni sehemu ya sheria husemekana kuwa kinahusu kanuni za kanisa (canonical).  Kanisa la Orthodox la Mashariki, Kanisa la Katoliki la Kirumi, na Makanisa ya Kiprotestanti yote pamoja huzingatia vitabu vya Biblia vilivyopokelewa katika kanuni za Kiyahudi kuwa na ufunuo wa Mungu. Kufuatia uharibifu wa Yerusalemu na Warumi mwaka wa A.D. 70, kundi la Wayahudi wasomi lilikusanyika huko Jabneh au Jamnia, kijiji kilichoko maili thelathini magharibi mwa Yerusalemu , na kutoka mwaka wa A.D. 90 hadi A.D. 100, wakahitimisha sheria za kanisa la Kiyahudi.3 Makanisa ya Kikristo hugawa vitabu ishirini na nne vya Kanuni za Kiyahudu na kuwa vitabu thelathini na tisa. 

Kuongezea vitabu hivi thelathini na tisa ambavyo vilipokelewa na matawi matatu ya makanisa ya Kikristo, Kanisa la Orthodox la Mashariki na Kanisa la Katoliki la Kirumi hufikiria vitabu zaidi kuwa na ufunuo wa Mungu. Vitabu hivi zaidi vinajulikana kama vitabu visivyothibitishwa (kutokana na neno la Kigiriki linalo maana ya kufichwa au kisiri). Vitabu visivyothibitishwa havipokelewi katika Kanuni za Maandiko ya Kiyahudi. Kanisa la Orthodox la Mashariki huzingatia vitabu vyote kumi na vinne visivyothibitishwa vinavyopatikana katika Septuagint kuwa na ufunuo wa Mungu . Septuagint ni tafsiri ya Agano la Kale ambayo ilitafsiriwa kwa Kigiriki kutoka kwa Kiebrania karne ya tatu Kabla ya Kristo (BC).4 Kanisa la Katoliki la Kirumi hukubali vitabu kumi na moja visivyothibitishwa, lakini huvizingatia kuwa “kumbukumbu la kanuni,” au kuwa vinafuata vitabu thelathini na tisa katika umuhimu.5 Makanisa ya Kiprotestanti huzingatia vitabu visivyothibitishwa kuwa muhimu kwa kusudi la kihistoria, lakini Waprotestanti hawaamini kuwa Mungu alitoa ufunuo kwa vitabu hivyo visivyothibitishwa. 

Mwaka wa A.D. 367 Athanasius (ca. A.D. 296–373), Askofu wa Alexandria, Misri, alituma barua wakati wa pasaka akitoa orodha ya vitabu ishirini na saba vya Agano Jipya ambavyo hutumika kwa wingi makanisani. Kanuni hiyo ya Kanisa ilithibitishwa magharibi na azimio la baba mtakatifu mwaka wa A.D. 405. Katika Kaskazini mwa Africa, kanuni hii iliidhinishwa katika Sinodi za Hippo (A.D. 393) na Carthage (A.D. 397). Lakini baraza la kanisa nzima halikuthibitisha kanuni hiyo. Huku makanisa ya Orthodox ya mashariki, Kanisa la Katoliki la Kirumi na makanisa ya Kiprotestanti yakikubaliana juu ya kanunu ya Agano Jipya, kanisa la Kihabeshi (Ethiopian) lina kanuni tofauti.6  

Ni muhimu kujua wakati Maandiko yalikamilika. Hata kama Kanuni la Kiyahudi (Agano la Kale) halikumalizika mpaka mwisho wa karne la kwanza A.D., Agano la Kale lilimalizika kabla ya kutafsiriwa kwake katika karne la tatu B.C. katoka Kiebrania mpaka Septuagint ya Kigiriki. Kwa hivyo unabii wa Agano la Kale wa Kristo uliandikwa karne nyingi kabla ya Yesu kuja kwa njia ya kimwili. Unabii wa Masiha haukuandikwa baada ya Yesu kuishi duniani. 

Page 7: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

Vitabu vya Kanuni la Agano Jipya vilimalizika katika karne la kwanza A.D. Kama viliandikwa mamia ya miaka baadaye, watu wengine wangedai kuwa vilikuwa na hekaya au makosa. Lakini viliandikwa wakati watu wengi waliomuona Yesu walikuwa hai – Mtu mkubwa zaidi aliyewahi kuishi. Bila shaka mashahidi hawa walikuwa na kumbukumbu dhahiri za Masiha ambaye aliongea kwa hekima kubwa, aliyeponya magonjwa tofauti na pia kuwafufua wafu. Mashahidi hawa wangeweza kupinga vitabu vya Agano Jipya, kama vitabu hivyo vilikuwa vya uongo. Kwa kweli, kanisa limekataa vitabu vingi vya uongo ambavyo hudai kuwa andiko takatifu. Vitabu kama hivyo vya uongo viliandikwa kati ya 200 B.C. na 600 A.D. na huitwa Maandiko ya Pseudepigrafia (ambayo ina maana ya “Maandiko ya uongo”). 

Katika karne la kwanza, baadhi ya watu kanisani walikuwa wakitumia vitabu vya Agano Jipya. Lakini si mpaka karne la nne wakati vitabu hivyo viliidhinishwa na makanisa mengi ya Kikristo.

Fikiria juu ya tahini iliyotumiwa na kanisa kuamua ikiwa Kitabu kitajumuishwa katika kanuni la Agano Jipya.  

i. Mtume aliiandika au iliandikwa na mtu aliyekuwa na uhusiano na mtume?

ii. Ina imani halisi? Inakubaliana na mafundisho ya kale ya Maandiko?

iii. Yaweza kutumiwa na watu wote? Inatumika kwa kanisa nzima au ni kwa baadhi ya makundi madogo?

iv. Ina nguvu za kufanya upya na kuendeleza Wakristo.

Kwa mazungumzo zaidi kuhusu suala hili, tazama sehemu ya “Tulipataje Biblia” katika wavuti ufuatao:

http://www.letusreason.org/Apolo22.htm

Tawi kuu la makanisa ya kikristo hukubali kuwa baada ya kumalizika kwa Agano la Kale na Agano Jipya, hakuna Maandiko mengine yametolewa kutoka kwa Mungu.Ukizidisha mamilioni ya Wakristo, wakiongozwa na Roho Mtakatifu, hukubali jambo hili. Kutoka wakati huo, hata hivyo, baadhi ya makundi ya dini yamejiunga, yakidai kuwa Wakristo, lakini yakitoa Injili isiyo na imani halisi. Makundi haya ya kidini hudai kuwa na Maandiko mapya ambayo yana umuhimu wa kwanza kabla ya mafunzo ya Agano la Kale na Agano Jipya. Zingatia yale Biblia inayosema kuhusu mafundisho mapya.  

18) Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki. (19) Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki. (Ufunuo 22:18,19)

Tazama pia 2 Yohana 7-10.

Page 8: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

2Webster’s New World Dictionary, College Edition, s.v. “Kanuni.”

3 Kwa mengi kuhusu suala hili, tazama ukurasa huu wa wavuti. http://airspirit3.freehomepage.com/chap31.html

4Webster’s New World Dictionary, College Edition, s.v. “Vitabu visivyothibitishwa.”

5Ibid.

6 Kwa habari zaidi kuhusu habari za Kanuni za Agano Jipya, tazama wavuti ufuatao: http://www.ntgateway.com/canon.htm

RUDI KWA MUHTASARI

Page 9: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

THEOLOJIA

V. Upuzio wa Maandiko

Tunakubali vitabu thelathini na tisa vya Agano la Kale na Ishirini na saba vya Agano Jipya kuwa Neno la Mungu la pekee lenye uhakika na mamlaka. Hizi ndizo vitabu vya “maana” vilivyokubalika na Orthodox ya Mshariki, Kanisa la Katoliki la Kirumi na makanisa ya Kiprotestanti. Maandiko hayo ndicho kipimo cha mwisho cha kuamua imani na matendo na desturi za kidini.

Zingatia yale Biblia inayosema kujihusu:  

“Majani yakauka, ua lanyauka; Bali neno la Mungu wetu litasimama milele” (Isaya 40:8).

Zaidi ya watu arubaini waliongozwa na Roho Mtakatifu kuandika Biblia. Watu hawa hawakuwa wanaandika kama mitambo, kuandika bila ubinafsi. Badala yake, waliandika kwa mitindo yao ya kipekee. Mungu aliongoza watu kurekodi neno lake kwa karne nyingi.

 “20 Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. 21 Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu” (2 Petro 1:20, 21).

Tazama pia 2 Timotheo 3:16,17.

Hata kama Biblia iliandikwa kwa muda mrefu na watu tofauti, vitabu vya Biblia huafikiana katika kiini moja: Kuna Mungu mmoja ambaye anatawala ulimwengu, na njia ya pekee ya wokovu ni kupitia kwa Yesu Kristo. Tazama Kumbukumbu la Torati 6:4 na Yohana 14:6.

Maandiko yanaonyeshwa kuwa halali kwa sababu unabii wa Biblia unatimizwa. Tazama Kumbukumbu la Torati 18:18-22; Yohana 6:14. Pia tazama kiuzi cha mafundisho katika wavuti huu, ukurasa wa “Unabii wa Masiha” Mungu alisema kuwa alitoa unabii ili watu wasidai kuwa sanamu fulani ana nguvu za kiungu. Tazama Isaya 48:3,5. Maandiko pia yanaonyeshwa kuwa halali kwa sababu yanatimiza kusudi lake. Tazama Isaya 55:10, 11. Madai hayo ya uhalali wa Maandiko yalitolewa kupitia kwa baadhi ya manabii wakuu katika Agano la Kale: Musa na Isaya.

Kama tunataka kuelewa ukweli wa Maandiko, tunapokea Roho Mtakatifu. Tazama 1 Wakorintho 2:9-13. Huwa tunampokea Roho Mtakatifu mara tu tunapomwamini Kristo. Tazama Yohana 7:37-39. Roho Mtakatifu huishi ndani yetu na kutuongoza katika kweli.

RUDI KWA MUHTASARI

Page 10: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

THEOLOJIA

VI. Imani

Hata kama Maandiko ndicho kiwango cha kuamua imani na matendo ya dini, Imani hutumika kuwaongoza watu katika imani. Kwa jumla imani zimekuzwa ili kukabiliana na changamoto za theolojia iliyoshikiliwa na kanisa. Fikiria juu ya imani mbili za kale ambazo zimekubalika katika makanisa mengi.

Imani ya Mitume, inayotumika katika makanisa ya Katoliki na Kiprotestanti (Lakini si kwa kanisa la Orthodox la Mashariki), ilitokana na kukiri kwa makanisa fulani mwisho wa karne la pili. Tambua mkazo wa Utatu Mtakatifu.  

"Naamini Mungu Baba Mwenye enzi, muumba mbingi na dunia, na Yesu Kristo Mwana wake wa pekee, Bwana wetu; aliyezaliwa na bikira Maria, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akateswa wakati wa Pontio Pilato, akasulubishwa, akafa na akazikwa, akaenda kuzimu; siku ya tatu akafufuka, akapaa mbinguni, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu; atakuja kuwahukumu walio hai na waliokufa. Naamini Roho Mtakatifu; Kanisa takatifu la Katoliki; umoja wa watakatifu, msamaha wa dhambi; ufufuo wa mwili na maisha ya milele na milele. Amini."7

Imani ya mitume hutangaza ubinadamu wa Kristo, ikikanusha madai ya uongo ya makundi ya uasi (Gnostics, Marcionites, na baadaye Manicheans). Tazama 1 Yohana 4:1-3. Imani hiyo inashikilia kuwa Yesu alienda kuzimu, mahali ambapo watakatifu na wasio watakatifu huenda mara tu wanapokufa. Neno “Kanisa Katoliki” lina maana ya “Kanisa la Ulimwengu.” Linakanusha Gnostics, ambao hudai kuwa na maarifa ambayo wengi hawakuwa nayo kanisani, Imani hii inaeleza kuwa Injili ni ya kanisa ya ulimwengu. Kwa habari zaidi tazama wavuti uliko hapa chini. Elekeza kwa mada “Kale,” arafu uelekeza kwa “Maelezo ya Imani ya Mitume”

http://www.creeds.net/

Kama vile Imani ya Mitume, Imani ya Nicene husisitiza Utatu Mtakatifu. Tarehe yake ni wakati wa kamati ya Ekumeni, uliofanyika Constantinople, A.D. 381. Imani ya Nicene ni sahihisho na upanuzi wa Imani ya hapo awali – Imani ya Nicaea, ambayo ilikuzwa na kamati ya kanisa iliyokutanika Nice huko Bithynia, mwaka wa A.D. 325. Kanisa lote la Kristo, hukubali Imani ya Nicene, isipokuwa kanisa la Orthodox la Mashariki ambalo hukataa sura ya filioque (tazama hapo chini).  

"Ni naamini Mungu mmoja, muumba mbingu na dunia, na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana; na katika Mungu mmoja Yesu Kristo, Mwana wa pekee wa Mungu, aliyekuwepo na Mungu kabla ya ulimwengu wote, Mungu wa miungu, mwangaza wa miangaza, Mungu yule yule wa Mungu yule yule, wa pekee, asiyeumbwa, aliye na nguvu sawa na Baba; kupitia kwake vyote viliumbwa, kwa ajili, yetu wanadamu na kwa ajili ya wokovu wetu, alitoka mbinguni, na akawa na mwili wa mwanadamu kupitia kwa Roho Mtakatifu wa Bikira Maria, na akafanyika mwanadamu, na

Page 11: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

akasulubishwa chini ya Pontio Pilato. Akateswa na akazikwa; na siku ya tatu akafufuka kulingana na Maandiko, na akapaa mbinguni, amaketi katika mkono wa kuume wa Baba yake. Atakuja tena kwa utukufu kuhukumu waliohai na waliokufa; ambaye ufalme wake hautakuwa na mwisho. Naamini katika Roho, Mungu nayetoa uhai, ambaye anaendelea kutoka kwa Baba (na Mwana) (filioque), ambaye akiwa na Baba na Mwana wote pamoja huabudiwa na kutukuzwa; ambaye alinena kupitia kwa manabii. Naamini katika Kanisa moja la Katoliki na Mitume; natambua ubatizo mmoja kwa msamaha wa dhambi; na natazamia ufufuo wa wafu na maisha ya ulimwengu ujao."8

Imani ya Nicere iliandikwa na Kanisa ili kupambana na msimamo wa uasi wa Arius, mkubwa katika Alexandria, Misri. Arius alifunza kuwa Baba aliumba Mwana. Ili kupinga mafunzo ya Arius ( Arianism), Kanisa lilifunza kuwa Mwana alikuwepo milele pamoja na Baba. Katika Imani ya Mitume, Kanisa lilisisitiza kuwa Mwana alikuwa mwanadamu, na katika Imani ya Nicene, Kanisa lilisisitiza kuwa Mwana alikuwa Mungu. Hata leo, kuna waasi ambao hukana uungu au ubinadamu wa Yesu Kristo. Unapochunguza msimamo wa madhehebu yanayopenda mtu au vitu (cults) (ambao hudai kuwa Wakristo, lakini hukanusha kanuni muhimu za Kikristo), ni vyema kuamua mafunzo yao kulingana na uungu na ubinadamu wa Yesu Kristo. Unapozungumza nao, kwa uangalifu eleza jinsi unavyoelewa utu wa Yesu Kristo, na wao pia waeleze.

Imani ya Nicene inashikilia kuwa Kristo “alipatwa na Baba kabla ya ulimwengu.” Kwa maneno mengine, alikuweko kabla ya uumbaji. Kwa hivyo yuko nje ya uwanja wa nyakati, kama vile tunavyoeleza nyakati. Kristo “alipatwa hakuumbwa.” Neno la Kigriki “monogenes” (linalotamkwa “mo-nog-en-ace”), linalotafsiriwa kama “kupatwa” katika Kiingereza, lina maana ya kupatwa kama vile mtoto kutoka kwa wazazi, au laweza kuwa na maana ya kutoka kwa namna au jamaa fulani. Mungu aliumba wanadamu, lakini alipata mwana wake wa pekee. Kwa imani, mtu anaweza kuwa mwana wa kupanga wa Mungu, lakini hatawahi kuwa mwana wa Mungu wa Pekee. Mwanadamu ni kiumbe, lakini Kristo ni Muumba. Kristo ni “mmoja wa aina yake” au Mwana wa Mungu wa “kipekee”. Hoja hii inapatana na mafunzo ya Maandiko kwamba Yesu ni Mungu. Tazama Yohana 1:1-3,14; 14:8-10.  

Imani ya Nicene inasema kuwa Yesu atarudi “kuhukumu wote walio hai na waliokufa.”

“Maneno yaliyo kwa mabano, "na Mwana," ni ongezo la Magharibu kwa Imani kama ilivyokubaliwa mwanzoni na Kamati iliyowakilisha Kanisa lote, Mashariki na Magharibi. Maneno haya yanaambatana na neno la Kilatino FILIOQUE (FILI = Mwana, -O = Kutoka, -QUE = na; inatamkwa kwa lafudhi ya O), na mabishano yanayowahusu yanajulikana kama Mabishano ya Filioque.”9 Kanisa la Magharibi liliongeza Sharti la “filioque” mwaka wa A.D. 569. Sharti la filioque linasema kuwa Roho Mtakatifu anaendelea kutoka kwa Baba na Mwana, na sio tu kutoka kwa Baba. Kanisa la Orthodox la Mashariki lilikataa maneno “na Mwana” na yaliyofuata ni mgawanyiko kutoka kwa Kanisa la Magharibi mwaka wa A.D. 1054.

Kwa maelezo zaidi kuhusu Imani ya Nicene, tazama:

  http://www.creeds.net Elekeza mada kwa “Kale,” baadaye uelekeze kwa “Maelezo zaidi kuhusu Imani ya Nicene”

Page 12: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

Pia tazama wavuti zifuatazo:

http://www.bible-researcher.com/confessions.html

7 Tazama wavuti: http://www.bible-researcher.com/confessions.html

8 Tazama wavuti: http://www.bible-researcher.com/confessions.html

9James E. Kiefer. Source: CHRISTIA File Archives. See http://www.creeds.net Elekeza kwa “Kale,” baadaye uelekeze kwa “Maelezo zaidi kuhusu Imani ya Nicene”

RUDI KWA MUHTASARI

Page 13: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

THEOLOJIA

VII. Mungu Aliye na Nafsi Tatu

Kabla ya kujifunza kuhusu Utatu Mtakatifu, hebu tuangalie dhana tofauti za Mungu. Theism ni imani kwa mungu mmoja au miungu.Sanaa ya theism ni imani katika Mungu mmoja asiye kuwa na mwisho, ambayo imetengwa na ulimwengu; na hii Mungu aliumba, anadumisha na kuongoza ulimwengu. Sanaa ya theism, Mungu ni mvuka mipaka (ametolewa ulimwenguni ) na yupo kila mahali daima (yupo ulimwenguni). Sanaa ya theism inahusisha Ukristo, Ujuda na Uislamu. Imani ya Uungu hushikilia kuwa Mungu ni muumba wa ulimwengu, lakini haendelei kuuongoza. Katika Imani ya Uungu, Mungu ni mvuka mipaka, lakini hayupo mahali pote. Kuabudu miungu ni wazo kuwa Mungu ni ulimwengu. Imani kwa miungu, Mungu yupo kila mahali, lakini havuki mipaka. Imani ya kuabudu miungu wengi ni imani katika miungu wengi. Imani kwamba kuna Mungu mmoja tu ni imani katika Mungu mmoja. Sanaa ya theism huabudu Mungu mmoja.

Utatu Mtakatifu ni imani ya Kikristo katika Mungu mmoja, aliyejulikana katika watu watatu – Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu. Watu wote watatu katika Utatu Mtakatifu walikuwepo kabla ya uumbaji wa ulimwengu. Kifungu cha kwanza cha Biblia kinasema kuwa Mungu aliumba mbingu na nchi. Neno la Kihebrania “Elohim” ni jina la Mungu katika kifungu hiki, na ni wingi wa neno lenye maana “tatu au zaidi,” linalopendekeza watu watatu wa Utatu Mtakatifu. Tazama Mwanzo 1:1.

Mwanzo 1:26 tena huonyesha Mungu katika wingi (Elohim), lakini Mwanzo 1:27 huonyesha Mungu katika umoja na katika wingi (Elohim) na katika umoja wa kiwakilishi nomino (mme au mke).  

26 Mungu akasema, "Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu aliumba, mwanamume na mwanamke aliumba” (Mwanzo 1:26, 27).

Biblia inafunza kwamba kuna Mungu mmoja tu.

Sikiza, Ee Israeli: BWANA, Mungu wetu, BWANA ndiye mmoja. (Kumbukumbu la Torati 6:4).

Wakati neno BWANA limeandikwa kwa herufi kubwa katika Biblia zilizoandikwa kwa Kiingereza, linahusu jina la Mungu (lililonukuuliwa kutoka kwa neno la Kiebrania kama YHWH--“Yahweh” au JHVH--“Yehova”). Katika Kumbukumbu la Torati 6:4, neno “Mungu” linatokana na neno la Kiebrania “Elohim” (wingi wa Mungu), lakini Elohim linatumika katika kifungu kumaanisha Mungu mmoja mwenye mamlaka. Tambua kwamba kifungu halisi kinachotangulia “BWANA” kikionyesha Mungu mmoja. Kumbukumbu la Torati 6:4 inatangaza kwamba Yehova ni Mungu mmoja.

Page 14: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

Biblia inafunza kuwa Baba wa Mbinguni ni Mungu. Tazama Mathayo 6:9. Biblia inaonyesha kuwa Yesu ni Mungu. Tazama Wakolosai 2:9. Biblia inaonyesha kwamba Roho Mtakatifu ni Mungu. Tazama Matendo 5:3,4. Baba ni Mungu, Mwana ni Mungu na Roho Mtakatifu ni Mungu, lakini kuna Mungu mmoja. Kwa hivyo Mungu mmoja anajulikana katika watu watatu.

Ili kusaidia kuelewe Utatu Mtakatifu, fikiri kuhusu mifano kadhaa. Mwanzo 1:27 inasema, “Mungu akaumba mtu kwa mfano wake.” Kwa hivyo mfano mmoja ni kuwa mwanadamu ana mwili, akili na roho – mwanadamu mmoja anajulikana katika njia tatu. Kama vile Mungu mmoja anavyojulikana katika watu watatu, mwanadamu mmoja anajulikana katika njia tatu. Mfano mwingine ni ule wa maji, barafu, na mvuke vyote vimeundwa na kitu kimoja (vipande viwili ni haidrojen na sehemu moja ni hewa safi (oksijeni), lakini yanajulikana katika njia tatu - maji, imara and mvuke.

Agano la Kale linapendekeza Utatu Mtakatifu. Tazama Isaya 48:12,13,16. Vifungu vya 12 na 13 vinamuonyesha Muumba (Yesu) kama mnenaji; na kifungu cha 16 kinataja Bwana Mwenyezi (Baba) na Roho (Roho Mtakatifu).

Utatu Mtakatifu umeonyeshwa vyema katika Agano Jipya. Tazama Luka 1:35 (kuzaliwa kwake Yesu ); tazama Mathayo 3:16-17 (ubatizo wa Yesu); na tazama Mathayo 28:18-20 (Tume Kuu). Agano Jipya linapoonyesha watu watatu wakiwa na nguvu za Mungu, inasema kwamba kuna Mungu mmoja. Tazama Marko 12:29.

Neno “Utatu Mtakatifu” halipatikani katika Biblia. Lakini Maandiko yanaonyesha Utatu Mtakatifu na vifungu vya Imani ya Kikristo kutoka kwa karne la pili na kundelea vinaonyesha Utatu Mtakatifu.    

A. Baba.

 Mungu Baba ndiye Mungu aliyepo milele. Musa alipomwuliza Mungu alitambue jina lake, Mungu alisema kwamba yeye, “MIMI NIKO” (kutoka kwa neno la Kiebrania lililo na maana ya “kuwepo”). Kutoka 3:14.

Yesu alimtambulisha Mungu kama “Baba.” Tazama sala ya Bwana: Mathayo 6:9kf.

Mungu huvuka mipaka na yuko kila mahali daima. Mungu huvuka mipaka —ni mkuu zaidi kuliko ulimwengu. Aliumba ulimwengu. Yeye, ni Mwenye nguvu. Tazama Zaburi 33:6-11. Anajua vyote. Tazama Ayubu 37:14-16. Bwana habadiliki (tazama Malaki 3:6). Mungu ni nuru. Tazama Yohana 1:5. Mungu ni Roho. Tazama Yohana 4:24.

Mungu yuko kila mahali milele – Yuko ulimwenguni kote (Yuko kila mahali). Yupo hapa nasi (Tazama Matendo 17:24-27). Kwa vile Mungu ni Roho, hawezi kuonekana. Lakini Mungu amejionyesha kupitia kwa theophanies. Theophany ni kujitokeza wazi kwa Mungu. Mifano yake ni pamoja na Mungu kujitokeza kama

Page 15: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

nguzo la wingu na nguzo ya moto (Kutoka 13:21), na kama kijiti kilichowaka moto (Kutoka 3:4). Mungu ni mbinafsi —si nguvu. Nafsi ya Mungu inaonyeshwa na jinsi alivyopenda (1 Yohana 4:8) na kuchukia (Mithali 6:16-19).   

B. Mwana.

 Yesu Kristo ndiye Mwana wa pekee wa Mungu (Yohana 3:16). Jina “Yesu” ni umbo la neno la Kigriki la jina la Kiebrania ‘Yoshua,” kumaanisha “Yehovah—Aliyeokoka.” Kwa hivyo jina Jesu linafahamisha kuwa Yeye ni Mwokozi. “Kristo” linamaanisha “aliyepakwa mafuta,” kutoka kwa Waebrania “Masiha.” (Danieli 9:25,26).

Katika nyakati za Agano la Kale, manabii, makuhani, na wafalme walikuwa wanapakwa mafuta walipochaguliwa katika ofisi. Yesu ni Nabii aliyeahidiwa na Mungu atakuja (Kumbukumbu la Torati 18:18; tazama Luka 13:33; Yohana 6:14). Nabii hutangaza neno la Mungu. Yesu ni Kuhani wetu ( tazama Waebrania 7:21). Kama kuhani wetu, Yesu anatuombea kati ya Mungu Baba na Mwanadamu. Yeye ni mtetezi wa waumini. Makuhani katika Agano la Kale walitoa dhabihu ili kupatanisha wenye dhambi na Mungu. Yesu alikuja kama dhabihu kamili kutupatanisha na Bwana. Makuhani walibariki watu, na Yesu anatubariki – anatupa uzima wa milele. Yesu atarudi kuhukumu ulimwengu (tazama Mathayo 25:31-33), na atatawala kama Mfalme (tazama Ufunuo 11:15). Katika Kuja kwa Kristo kwa mara ya kwanza, Yesu alitambulisha Ufalme wa Mbinguni ( tazama Mathayo 4:17). Katika Kuja kwake kwa mara ya Pili, Yesu atatawala kama Mfalme katika Ufalme wa Mungu ( tazama Ufunuo 12:10; 19:16).

Kabla ya uumbaji wa ulimwengu, Yesu na Baba walikuwepo. Kwa hivyo haistaajabishi kwamba Yesu alikuwepo wakati wa Agano la Kale. Katika Agano la Kale Yesu anaitwa “Malaika wa Bwana” (tazama Mwanzo 22:8,11,12,15,16) au “malaika wa uwepo wake” (tazama Isaya 63:9). Kifungu chenye msimamo kinapojitokeza mbele ya “malaika” huenda Maandiko hayo yanataja Yesu.

Unabii wa Masiha ulitabili kujitokeza kwa Yesu kimwili duniani. Vifani vya Agano la Kale vilionyesha maisha ya Yesu kabla yake kuja duniani. Kiuzi cha mafunzo kuhusu Unabii wa Masiha kinaonyesha kuwa Unabii unaotimika na vifani ni vya kipekee katika imani ya Kikristo. Unabii na vifani huonyesha ukweli wa Maandiko na kuelekeza njia kwa Mwokozi.

Yesu alijitokeza kimwili duniani, ili uweze kujua jinsi Mungu alivyo (tazama Yohana 1:14,18; 14:9). Yesu alikuja kutafuta na kuokoa waliopotea (tazama Luka 19:10). Kristo aliokoa au komboa wenye dhambi kwa kujitoa kama dhabihu (tazama Waebrania 10:10). Ukombozi ni Kiini cha Mandiko (tazama Mambo ya Walawi 25:47-53). Katika kitabu cha Ruthu, Boazi alimkomboa Ruthu (tazama Ruthu 4:9-10). Boazi alikuwa mfano wa Kristo, Mkombozi wetu. Kristo alijitoa kama fidia ya kuokoa na kutoa watu kutoka ukombozi wa dhambi (tazama Wakolosai 1:13,14).

Page 16: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

Mwanadamu wa kwanza —Adamu—alitenda dhambi, na wanadamu wote wakarithi mwelekeo wa dhambi. Mungu alimwambia Adamu kwamba asipotii, atakufa. Adamu hakutii na akafa. Mungu hasemi uongo. Kila mwanadamu hutenda dhambi, na hufa. Hakuna aliye na cha kumpa Mungu ili kuzuia kifo. Lakini Mungu anapenda watu kwa hivyo alimtoa Mwanaye wa pekee kama fidia ya kulipia maisha kwa wale wanaomwamini Yesu. Wakati wote, Yesu alimtii Baba yake, kwa hivyo alikuwa na kitu cha kumpa Baba yake kama malipo kwa ajili ya dhambi za wanadamu. Yesu alitoa maisha yasiyo na dhambi (tazama 2 Wakorintho 5:21). Kwa sababu Yesu hakutenda dhambi, hakuwajibika kufa. Lakini Yesu – Adamu wa pili – kwa hiari alikufa badala ya mwanadamu mwenye dhambi. Kupitia kwa Adamu wa kwanza wote wanakufa, na kupitia kwa Yesu maisha yalikuja (tazama 1 Wakorintho 15:22).

Katika kuja kwa Yesu duniani kimwili, Yesu alikuwa Mungu na pia mwanadamu (tazama Wakolosai 2:9; Wafilipi 2:5-8). Yesu alikuwa Mungu katika mwili, na alifanya miujiza ambayo ilionyesha kuwa alikuwa na nguvu za Mungu ( tazama Yohana 20:30,31). Yesu alikuwa mwanadamu, kwa hivyo alipatwa na majaribu (tazama Mathayo 4:1), njaa ( tazama Mathayo 4:2), kiu ( tazama Yohana 19:28), na kifo ( tazama Yohana 19:33).

Yesu alikuwa Mwana wa Mungu (tazama Luka 1:32) na Mwana wa mwanamke. Alizaliwa na bikira Mariamu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu (tazama Luka 1:34, 35). Unabii wa Agano la Kale ulitabiri kuzaa kwa bikira (tazama Isaya 7:14).

Unabii wa Agano la Kale unatuelekeza kwa kifo cha Yesu kwa kusulubishwa na kufufuka kwake (tazama Zaburi 22:1-18; Isaya 53). Daudi alipoandika neno la unabii katika Zaburi 22 akieleza kusulubishwa kwa Yesu, Waebrania hawakuwa wanasulubisha watu. Kusulubisha kulianza baadaye kama desturi ya utawala wa ukatili wa Kirumi. Mungu aliweka maneno ya unabii katika akili za Daudi.

Juu ya msalaba, kwa hiari yake “akaitoa roho yake” kwa kifo (tazama Mathayo 27:50). Yesu aliwekwa kaburini, na siku ya tatu, akafufuka (tazama Mathayo 27:57—Mathayo 28:10). Yesu alifufuka katika mwili (tazama Mathayo 28:6). Ufufuo wa Yesu ni ukweli wa muhimu katika Injili (tazama 1 Wakorintho 15:14). Kama Kristo hakufufuka, hakuna haja ya kuhubiri. Lakini, kama Kristo alifufuka, ni muhimu tutangaze Habari Njema. Tunajua Kristo alifufuka, kwa hivyo tunashurutishwa kushiriki ujumbe huu na ulimwengu, ili wengine wainuke kutoka kaburini na kuishi pamoja na Kristo.

Baada ya kufufuka, Kristo aliwatokea mitume kwa muda wa siku arubaini (tazama Matendo 1:1-3). Baadaye alipaa mbinguni (tazama Matendo 1:9), ambako anatukuzwa pamoja na Baba (tazama Matendo 7:55). Ndiye mwombezi wetu na mpatanishi kati ya Baba na mwanadamu mwenye dhambi, kwa hivyo tunaomba kwa Mungu Baba katika jina la Yesu (Yohana 14:13,14).    

C. Roho Mtakatifu.

Page 17: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

 Roho Mtakatifu ni mtu wa tatu katika Utatu Mtakatifu. Roho Mtakatifu ana nafsi ya utu ili tuweze kutumia kiwakilishi nomino cha utu “mwanamume” tunapotaja Roho Mtakatifu. Yeye si nguvu tu, kwa hivyo tusimtaje kama “Kitu” Roho Mtakatifu hufikiria na kuongoza (tazama Matendo 15:28), na uhuzunika (tazama Waefeso 4:30). Roho Mtakatifu ni Mungu, ni mwenye kudura (tazama Mwanzo 1:2), na yuko kila mahali (tazama Zaburi 139:7-10). Roho Mtakatifu alihusika katika uumbaji wa uhai (tazama Mwanzo 1:26, 27; Zaburi 104:24,30).

Kutoka wakati wa siku ya Pentekoste ambayo imeelezwa katika Matendo 2, Roho Mtakatifu hukaa ndani ya waumini. Kabla ya wakati huo, alikuja juu ya watu na kuwaacha kwa hiari yake (tazama Hesabu 11:17,25,26; Mithali 1:23).

Yesu alipokufa kama dhabihu kamili, aliwapa maisha wale wote wanaoamini Mungu – wale walioishi zamani, wale wanaoishi sasa, na wale watakaoishi. Roho Mtakatifu huokoa na kuupa moyo wa mwanadamu maisha mapya. Bila Roho Mtakatifu, waumini wamekufa kiroho. Wale wasiokuwa na Roho Mtakatifu hawana uzima wa milele (tazama Yohana 3:5-6).

Roho Mtakatifu huwapa nguvu waumini ili waweze kumtumikia Kristo (Matendo 1:4,8). Baada ya kufufuka kwake, Yesu aliwaambia wanafunzi wangojee ahadi ya Baba (Roho Mtakatifu aliyeahidiwa). Kwa hivyo wanafunzi waliungana Yerusalemu, wakingojea. Siku ya Pentekoste, Roho Mtakatifu alikuja juu yao – wakabatizwa kwa Roho Mtakatifu (tazama Matendo 1:5; 2:4). Kama ishara ya muujiza huu, waumini walianza kusema kwa lugha nyingine. Wayahudi kutoka sehemu tofauti za ulimwengu walikuwa Yerusalemu kwa Sherehe ya Pentekoste. Waumini walipokuwa wakinena katika lugha zingine, Wayahudi waliweza kuwaelewa kwa lugha zao tofauti. Kwa hivyo ndimi za wakati wa Pentekoste zilieleweka na wale waliokuwa wakisikiza. Hii ni kinyume cha ndimi zilizonenwa baadaye katika kanisa la Korintho ambazo si kila mtu aliweza kuelewa, bali tu wale waliokuwa na kipawa cha kiroho cha kufafanua ndimi (tazama 1 Wakorintho 14:27,28).

Kanisa lilianza wanafunzi walipopokea Roho Mtakatifu (Matendo 2:1-4). Kuanzia wakati huo, waumini waliunda mwili wa Kristo – wakishirikiana na Roho (tazama Waefeso 1:22,23; 1 Wakorintho 12:13; 2 Wakorintho 13:14). Kutoka wakati huo na kuendelea, waumini wamekuwa na ushirika na kila mmoja kwa nguvu za Roho aliye ndani yao. Kwa nguvu za Roho Mtakatifu, waumini wana uwezo wa kuujenga Ufalme wa Mungu – kuwa mashahidi (Matendo 1:8).

Waumini wanazo nguvu za kuwa waaminifu kwa Mungu. Wakristo wanataka kufanya mema, naye Roho Mtakatifu huwapa Wakristo nguvu za kufanya mema. Fikiria mfano wa mabadiliko ambayo huletwa na Roho Mtakatifu. Kabla ya kumpokea Roho Mtakatifu, mara tatu Mtume Petro alimkana Yesu (tazama Mathayo 26:69-75). Baada ya kumpokea Roho Mtakatifu, Petro alihubiri kwa ujasiri na mara moja karibu watu 3,000 walimpokea Kristo (Matendo 2:14-41). Kabla ya kumpokea Roho Mtakatifu, Petro hakuwa na ufanisi kwa sababu ya uoga ya sulubishwa. Baada ya kumpokea Roho Mtakatifu, Petro alihatarisha maisha yake kueneza Injili (tazama Matendo 4:8,13,18-20). Kwa njia hiyo hiyo, kama tutakuwa na matokeo tunapomtumikia Kristo, ni lazima tufanye hivyo kwa

Page 18: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

nguvu za Roho Mtakatifu.

Roho Mtakatifu aliongoza manabii kuandika Maandiko (tazama 2 Petro 1:21). Siku hizi huongoza wahubiri kutangaza Injili.

Roho Mtakatifu husaidia Wakristo kwa njia tofauti. Hutufariji (tazama Yohana 14:16-18). Hutuongoza kufanya mambo yapasayo (tazama Wagalatia 5:16-18). Hutupa maneno ya kutetea imani yetu ndani ya Kristo (tazama Marko 13:11). Hutuhakikisha habari za dhambi, haki na hukumu ya Mungu (tazama Yohana 16:7-11). Kwa hivyo tunaongozwa na Roho Mtakatifu kumpokea Kristo, baadaye tunaendelea kuongozwa kuepukana na dhambi.

Roho Mtakatifu husaidia Wakristo kukua na kuzaa matunda ya Kiroho kama vile upendo na furaha (tazama Wagalatia 5:22, 23). Tunapoamini Kristo, tunapokea Roho Mtakatifu, naye Roho Mtakatifu hutupa kipawa kimoja au zaidi. Vipawa vya kiroho sio sawa na matunda ya kiroho. Vipawa vya kiroho vimeorodheshwa katika Warumi 12:3-9, 1 Wakorintho 12:4-11,27-31, na Waefeso 4:11-16.

Roho Mtakatifu anayeonyeshwa kwa ishara ya njiwa (tazama Luka 3:22), kwa mafuta iliyotumika kuweka wakfu makuhani ( tazama Kutoka 29:21; 1 Yohana 2:20), na kwa moto (tazama Matendo 2:3).

Tunapoamini Kristo na kupokea Roho Mtakatifu, tuna uhakika wa uzima wa milele.

  

13Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisika neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu. 14Ndiye aliye arabuni ya urithi wetu, ili kuleta ukombozi wa milki yake - kuwa sifa ya utukufu wake. (Waefeso 1:13,14)

RUDI KWA MUHTASARI

Page 19: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

THEOLOJIA

VIII. Malaika

Neno “malaika: lina maana ya “mtumwa”. Hapo mwanzo, malaika wote walikuwa mbinguni pamoja na Mungu, lakini baadaye malaika Shetani alimwasi Mungu, kwa hivyo yeye pamoja na malaika ambao walifuata Shetani wakatupwa kutoka mbinguni.

Malaika ni viumbe vilivyoumbwa (tazama Zaburi 148:1-5; Wakolosai 1:16,17). Zaburi 148:2 hutaja malaika na wenyeji wa mbinguni, na Zaburi 148:5 inaonyesha kuwa malaika hao na wenyeji wa mbinguni waliumbwa. Wakolosai 1:16 inasema kuwa Kristo aliumba vitu vyote vilivyo mbinguni.

Wakati wote, Biblia hutaja malaika kama jinsia ya kiume, lakini hakuna jinsia iliyopewa malaika. Malaika ni viumbe wanaoishi milele, hawaoi, na ni wazi hawazaani (tazama Luka 20:35-36). Ni wengi mno (Waebrania 12:22). Malaika ni roho, lakini wakati mwingine huonekana (tazama Yohana 20:12). Mikaeli, Malaika Mkuu (Yuda 1:9), alimtokea Danieli (tazama Danieli 10:18-20). Malaika Gabrieli alimtokea Zakaria (tazama Luka 1:11,19). 

A. Malaika Watakatifu.

Wale malaika wasiomfuata Shetani ni malaika watakatifu. Kwa sasa malaika watakatifu wana nguvu kushinda mwanadamu (tazama Zaburi 8:4-5). Lakini kwa Ufalme wa Mungu Ujao, mwanadamu atawahukumu malaika (tazama 1 Wakorintho 6:3). Yesu alipokuwa duniani katika mwili, aliwekwa chini ya malaika (tazama Waebrania 2:9). Alipofufuka, Kristo alirudishwa kwa utukufu, kwa hivyo ana nguvu kuliko malaika (tazama Waebrania 1:4-14). Hatupaswi kuabudu malaika, bali tumwabudu Mungu peke yake. Mojawapo ya kazi za malaika ni kumwabudu Mungu (Ufunuo 5:11-13).

Mungu huwatuma malaika kunena na watu (kwa mfano, tazama Luka 1:11-13). Malaika ni roho wanaotumika ambao huwajali watakatifu kutoka utotoni hadi kifo (tazama Waebrania 1:14; Mathayo 18:10; Zaburi 91:11). Malaika hutazama kinachofanyika duniani na wanafurahia mtu anapopokea uzima wa milele (tazama 1 Wakorintho 4:9; Luka 15:10). Malaika wataambatana na Kristo atakaporudi duniani (tazama Mathayo 25:31). 

B. Malaika Walioanguka.

Shetani, malaika mkuu aliyetenda dhambi na kutoka kwa neema ya Mungu, anajulikana kwa majina mengi. Anajulikana kama Shetani – “adui” (1 Mambo ya Nyakati 21:1), Ibilisi—“Kashfa,” njoka (Ufunuo 12:9), nyoka (Mwanzo 3:13), na muuaji na Baba ya uongo (Yohana 8:44). Mungu ni mkuu kuliko Shetani, lakini humruhusu Shetani kutawala ulimwengu huu hadi atakaporudi Kristo. Kwa hivyo Shetani anaitwa mungu wa ulimwengu huu (tazama 2 Wakorintho 4:4), na mwana mfalme wa ulimwengu huu (tazama Yohana 12:31). Shetani hudanganya watu, hata kujigeuza kuwa malaika wa nuru (tazama 2 Wakorintho 11:14).

Page 20: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

Biblia inaeleza Shetani kwa kumuonyesha kama mwenye nguvu za maovu yanayotendwa na watawala wa dunia. Nguvu za Shetani ndizo zilizoongoza Mfalme wa Tyre, kama vile ilivyoelezwa katika kitabu cha Ezekieli 28:11-19. Mfalme wa Tyre ameelezwa, na pia Shetani ameelezwa (tazama Ezekieli 28:12,15,17). Shetani alikuwa mwenye hekima na mrembo hadi alipokuwa mwovu. Nguvu za Shetani ndizo zilizoongoza wafalme wengine wa ulimwengu. Kiburi chake —cha kutaka kuwa mkuu kuliko Mungu –kilimfanya ashushwe (tazama Isaya 14:12-15). Wakati mmoja, Yesu alionyesha kuwa Shetani alikuwa anamtumia Mtume Petro (tazama Mathayo 16:23).

Shetani hutujaribu tufuate njia za ulimwengu bali na njia za Mungu. Kama vile Shetani, ambaye kupitia kwa kiburi alimwasi Mungu, pia sisi huongozwa na kiburi.

“Maanda kila kilichomo duniani, yaani, tama ya mwili, tama ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia” (1 Yohana 2:16).

  Pepo (Luka 10:17) ni wale malaika walioanguka wanaomfuata Shetani. Pepo wengine wako vifungoni wakingojea hukumu (2 Petro 2:4) na pepo wengine wanafanya kazi pamoja na Shetani kuendeleza maovu duniani. (tazama Waefeso 6:12).

Pepo wanaitwa kwa majina mengi kama vile “pepo wachafu” (Marko 1:23-27), “pepo wabaya” (Luka 7:21), “roho zidanganyazo” (1 Timotheo 4:1), au “pepo mchafu” (Marko 9:25 ). Wanaweza kupagaa miili ya watu (tazama Marko 5:1-9). Mtu Yule aliyepagawa huonekana kama ana kichaa, na aweza kuwa na nguvu za kimwili zaidi ya binadamu (Matendo 19:16). Kupagawa na pepo kwaweza kusababisha ububu wa kimwili ( tazama Mathayo 9:32). Pepo waweza kunena kupitia kwa mdomo wa yule aliyepagawa (tazama Marko 5:7, 8). Pepo huwaongoza watu kutenda dhambi (Yohana 8:44).

Pepo hutoa nguvu za kipekee kama vile nguvu za kutabili—roho ya utabiri (tazama Matendo 16:16). Wakristo wanafaa kuwa macho kwa wale wanaotenda vitendo vya kishetani kama vile uchawi (Wagalatia 5:20); uchawi (Matendo 8:9-11); na kuomba wafu (tazama Kumbukumbu la Torati 18:9-12).

Shetani na malaika wake walihukumiwa na dhabihu ya Kristo na ufufuo wake (tazama Yohana 12:31,32). Lakini bado Shetani anaeneza uovu duniani. Mwishowe, Shetani na malaika wake watatupwa katika ziwa la moto (tazama Ufufuo 20:10; 2 Petro 2:4; Yuda 6).

Wakristo wanaweza kumwepuka Shetani na malaika wake. Pepo wanamuogopa Mungu (tazama Yakobo 2:19). Wakristo wanaweza kuzitegemea nguvu za Roho Mtakatifu aishiye ndani yao kuwakinga kutokana na Shetani (tazama 1 Yohana 4:4). Wanapokubana na matendo ya kishetani wanaweza kuomba katika jina la Yesu (tazama Yohana 14:14).

RUDI KWA MUHTASARI

Page 21: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

THEOLOJIA

IX. Mwanadamu

Mwanadamu ni kiumbe kilichoumbwa. Biblia haifundishi kwamba mwandamu aligeuka kutoka kwa spishi. Badala yake, Mungu aliumba kila mnyama kulingana “na aina yake” (tazama Mwanzo 1:24). Nadharia ya kugeuka inashikiria kuwa spishi moja iligeuka na kuwa nyingine hadi wanyama walipogeuka wakawa wanadamu. Kama haya ni ya kweli, kunafaa kuwa na wingi wa visukuku “vya katikati” kati ya kila spishi inayoonyesha kuendelea kutoka kwa spishi moja hadi nyingine. Lakini hakuna wingi wa visukuku vya kati vinavyounganisha spishi. Mwanadamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu (tazama Mwanzo 1:26, 27). Mwanadamu anafanana na wanyama wengine, lakini pia ana tofauti na wanyama. Biblia haisemi ya kwamba wanyama waliumbwa kwa mfano wa Mungu, bali mwanadamu ana mfano wa Mungu.  

A. Uumbaji.

Uhasibu wa uumbaji wa mwanadamu umetolewa katika Mwanzo 1:26, 27. Mwanadamu aliumbwa mume na mke. Mwanadamu—kiumbe cha juu duniani – alipewa nguvu za kutawala viumbe vingine. Ujumbe zaidi wa uumbaji wa mwanadamu umetolewa katika Mwanzo 2:7, 21-23. Mwanzo 2:7 inaeleza kuwa mwanadamu aliumbwa kutoka kwa mavumbi. Neno la Kiebrania la “Mwanadamu” ni Adamu” na neno hilo limetumiwa kumwita mwanadamu wa kwanza. Pia, neno la Kiebrania “arthi” ni “Adamah,” ambalo lina mlio kama “adamu.” Mwanadamu wa kwanza aliumbwa kutoka kwa mavumbi ya ardhi, na Mungu alipumua kwa mapua yake pumzi za maisha. Baadaye, Mungu akamfanya mwanadamu kupata usingizi mzito na akamuumba mwanamke wa kwanza – Hawa – kutoka kwa ubavu wa mwanamume.

Stringfellow aliandika kuwa mwanadamu aliumbwa na asili tatu – mwili, nafsi na roho ( tazama 1 Wathesalonike 5:23; Waebrania 4:12). Kwa hivyo mwanadamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu – ambaye ni Utatu Mtakatifu. Mwili wa mwanadamu uliumbwa na hisia tano za kuona, kunusa, kusikia, kuoja na kushika ambazo humpa ufahamu wa dunia. Nafsi (akili) ya mwanadamu- uwezo wake wa kufikiria, mhemko, kukumbuka, upendo na dhamiri— ina maana sawa na ya “nafsi” kama ilivyotumika katika Maandiko. Nafsi yake ni ufahamu wake. Roho ya mwanadamu inamtofautisha na viumbe vingine. Roho yake ni ufahamu wa Mungu wake10. Mwanadamu anamjua Mungu. Anamuomba Mungu. Je, viumbe wengine huomba nini? Nani anaweza kusema wanyama wanamfahamu Mungu kwa njia yo yote?

Maana ya “nafsi” na “roho” yana uhusiano wa karibu. Maandiko yanaonyesha ufanano wa mawazo haya, yakisema kuwa neno la Mungu lina nguvu la kuzigawa nafsi na roho (tazama Waebrania 4:12).

Mungu aliumba bustani katika edeni, na akamweka Adamu pale ailime na kuitunza (Mwanzo 2:8,15). Kabla ya dhambi kuingia duniani, kazi haikuelezwa kama mzigo.

Page 22: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

Kazi ilimpa mwanadamu lengo—hisia ya kutimiza.  

B. Kuanguka kwa Mwanadamu

Mungu alimruhusu Adamu kula matunda ya kila mti katika Edeni isipokuwa matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Alimuonya kuwa akila matunda ya mti huyo kwa hakika atakufa. (Mwanzo 2:15-17). Shetani, kwa mfano wa nyoka, akamjaribu Hawa kula matunda waliyokatazwa, na akampa Adamu tunda hili, ambaye pia alilila (tazama Mwanzo3:1-6). Shetani alimjaribu Hawa kwa kupendeza tamaa ya mwili – tunda lilionekana nzuri “lilifaa kwa chakula” tamaa ya macho – tunda lilionekana “lilipendeza macho” na kiburi cha uzima - tunda lilionekana “lilitamanika kwa maarifa” (Mwanzo 3:6 ). Majaribu yote huwa sawa kwa vizazi vyote.

 “Maanda kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia” (1 Yohana 2:16).

Kwa sababu Adamu na Hawa walitenda dhambi, Mungu alisema kwamba kuna laana kwa mwanadamu na kwa ardhi. Uchungu wa mwanamke anapozaa umeongezwa, na atatawaliwa na mume wake (tazama Mwanzo 3:16). Ardhi imelaaniwa, ili izae miimba na mbaruti, na mwanadamu atafanya kazi katika hali ngumu (tazama Mwanzo 3:17-19). Kwa kutomtii Mungu, mwanadamu alipatwa na hatia — akajua tofauti ya mema na mabaya (tazama Mwanzo 3:22). Mwanadamu akaanza kujifahamu na akaanza kujihukumu (tazama Mwanzo 3:7,11, 21). Mungu akamzuia mwanadamu kuishi milele katika hali ya dhambi – alimzuia kukula kutoka kwa mti wa uzima (tazama Mwanzo 3:24). Kwa sababu ya dhambi, mwanadamu wa kwanza alikufa.

Matokeo ya dhambi kuingia duniani kupitia kwa Adamu na Hawa, watu wote walirithi mwelekeo wa kufanya dhambi. Kwa imani katika Kristo, watu wanaweza kusamehewa dhambi na kuupokea uzima wa milele (tazama 1 Wakorintho 15:21,22).

Mwanzo 3:15 unatabili ushindi wa Kristo juu ya Shetani. Kwa sababu Shetani alimjaribu Hawa, Mungu alimlaani Shetani na akamwambia kuwa uzao wa mwanamke utaponda kichwa cha nyoka. Bila kuhesabu ukoo huu, ukoo wa Kiebrania umenakiliwa kupitia kwa waume (wana wa wanaume). Lakini kuna kisa kimoja ambacho kulikuwa na mama na hakukuwa na baba wa kibinadamu wa mtoto—Yesu alizaliwa na bikira. Kwa hivyo Mwanzo 3:15 inaonyesha kwamba wakati wa kuanguka kwa mwanadamu kwa sababu ya dhambi, Mungu alikuwa na mpango wa kumuokoa mwanadamu. Kifo cha Yesu msalabani kilimpa ushindi dhidi ya Shetani. Atarudi kuponda kichwa cha Shetani. Katika Mwanzo 3:15, Mungu pia alitabili kuwa Shetani ataponda kisigino cha Kristo. Shetani alikiponda kisigino cha Kristo kwa kuufanya muhimu kifo cha Kristo ili watu waishi. Kifo cha Yesu msalabani kilikuwa kupondwa kwa muda, lakini kifo cha Shetani cha kiroho ni cha milele.   

C. Dhambi

Page 23: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

Neno la Kigriki lililo na tafsiri ya “dhambi” lina maana ya “kukosa alama” 11 Tunapotenda dhambi, tunakosa alama au tunapungukiwa na kiwango kilichowekwa na Mungu. Dhambi ilitokana na Shetani (Isaya 14:12-14), na kuingia duniani kupitia kwa Adamu na Hawa. Kila mtu ni mwenye dhambi (tazama Warumi 3:23).

Watu hawapendi kukubali kuwa wao ni wenye dhambi. Hii ni sababu ya kimsingi ya watu wengi kuukataa Ukristo. Wakimkubali Kristo, ni lazima waachane na dhambi. Hawataki kuacha kutenda dhambi. Kwa hivyo wanaleta kila aina ya sababu ili kuukataa ukweli wa Kikristo.

Dhambi hutokana na upovu wa kiroho (tazama Yohana 9:39), dhamiri yenye ugumu (tazama Waefeso 4:19), mawasiliano na Mungu yaliyokatika (tazama Mithali 15:29), maumivu ya roho na shida duniani, ufungwa na kifo (tazama Warumi 6:20-23), na kutengwa milele kutoka kwa Mungu (tazama Luka 12:15).

Kukiri kwa dhambi ni muhimu kwa wokovu (tazama Warumi 10:9,10) na ushirika wa kila siku—kutembea na Kristo kila siku (tazama Yohana 13:6-10).

Kwa ujumbe zaidi kuhusu dhambi, tazama “dhambi” katika kamusi ya Kitheolojia katika wavuti ufuatao:

http://www.carm.org/dictionary.htm

 

D. Wokovu

Mafundisho ya wokovu yanajulikana kama soteriolojia.

Kristo alikuja duniani kuokoa watu kutokana na adhabu ya dhambi. Watu ni kama kondoo waliopotea, na Kristo ni mchungaji mwema ambaye huwaita kwa usalama katika maisha ndani yake.

 “Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea" (Luka 19:10 ).  

1. Kuokolewa kwa Neema Kupitia kwa Imani

Tunaokoka tunapozaliwa katika Roho (tazama Yohana 3:5-7). Mbali na imani katika Kristo, tumekufa kiroho. Tunapomwamini Yesu, tunapokea Roho Mtakatifu, ambaye anaongoa roho zetu. Kwa hivyo kupitia kwa imani, tunazaliwa tena kiroho. Yohana 3:5 inasema kwamba ili kuingia ufalme wa mbinguni, lazima mtu azaliwe kwa Roho na maji.

Ryrie alifanya muhtasari wa ufafanuzi tofauti wa maana ya “maji” katika Yohana 3:5. Kama hii inamaanisha Ubatizo wa maji, inaonekana kukanusha andiko lingine (Yohana 3:16; Waefeso 2:8,9). Haya yamezungumziwa kwa kina katika kiuzi “Huduma ya Uchungaji” katika mada ya Ubatizo. Maana ya maji inayowezekana katika Yohana 3:5 inahusisha:

 

Page 24: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

1. Kuzaliwa kwa kimwili (linganisha na Yohana 3:6—“kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.”

2. Neno la Mungu (tazama Waefeso 5:26; Yohana 15:3).

3. Wokovu kama ulivyoonyeshwa na Yohana Mbatizaji.

4. Maji ni kisawe na Roho Mtakatifu, kwa hivyo Yohana 3:5 yaweza kutafsiriwa “kwa maji, hata Roho Mtakatifu.”12 Tazama Tito 3:4,5.

Kwa muhtasari, hatuamini kuwa kubatizwa ndani ya maji inahitajika kwa wokovu. Hata kama maana ya neno “maji” katika Yohana 3:5 haina uhakika, kutoka kwa maandiko mengine, ni wazi kuwa imani ndani ya Kristo ndiyo tu inayohitajika kwa wokovu (kwa mfano, tazama Yohana 3:16).

Maandiko yanafunza tuwabatize waumini ndani ya maji. Ubatizo katika Biblia ulikuwa kwa kuzamisha. Kwa hivyo huwa tunabatiza kwa kuzamisha.

Kama anayebatizwa ni mtoto, mtoto huyo awe na umri wa kuelewa kujitolea kwake kumfuata Kristo. Muda tu baada ya muumini kukiri imani yake ndani ya Kristo, muumini abatizwe.

Wokovu ni kwa neema ya Mungu (tazama Tito 3:4, 5). Neema ina maana ya “upendo usiostahili.” Kwa hivyo, wokovu ni kipawa cha bure. Hatuwezi kupata wokovu kwa nafsi yetu, sisi ni wenye dhambi. Bidii zetu hupungukiwa na maisha kamili ambayo Mungu anatutakia. Ni kwa imani tu katika Kristo, mpatanishi kati ya Mungu na mwanadamu, tunapata wokovu. Tumeokolewa ili tufanye matendo mema. Kwa hivyo tumeokolewa kwa neema kupitia kwa imani, ili tufanye matendo mema.

 8 Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani – ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu - 9wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. 10Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo. (Waefeso 2:8-10).

Wokovu ni kwa njia ya imani. Imani inayookoa inahusisha kubadilisha roho – kujitolea kumwamini na kumfuata Kristo. Tazama “hakikisho la Maisha ya Milele” katika kiuzi cha “Mwito wa Umisheni.” Kama tumeokoka, tunataka kutenda matendo mema na tutatenda matendo mema (tazama Yakobo 2:14-24).

Imani ni kuweka tumaini letu kwa Mungu na ahadi zake. Imani yetu ni ishara ya mabadiliko ambayo Roho Mtakatifu huleta katika maisha yetu (tazama Waebrania 11:1). Kwa muhtasari wa mashujaa wa imani, tazama Waebrania 11. Hata kabla ya Yesu kuja duniani katika mwili, watu walikuja kwa Mungu kwa imani. Waliamini Mungu asiyeonekana. Mungu alituma manabii kuwafunza watu jinsi ya kusamehewa dhambi.

Page 25: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

Imani ni kipawa kutoka kwa Mungu, kwa hivyo tuombe Mungu aweze kuongeza imani yetu (tazama Warumi 12:3). Utajiri wa mali hupunguza imani yetu. Matajiri huweka imani yao katika mali badala ya kumwamini Mungu. Mungu amewachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani (tazama Yakobo 2:5). Mara nyingi, maskini kabisa ndio huitikia Injili kwa haraka. Kwa hivyo wale kati yetu ambao ni maskini tunaweza kujihesabu kuwa tumebarikiwa kama umaskini wetu utatuongoza kuwa matajiri wa imani.

Tunapoamini Kristo tunampokea kama Bwana wetu, tunapangwa kama wana wa Mungu au watoto wa Mungu (tazama Yohana 1:11,12).  Stringfellow aliandika kuwa kupangwa kama huku ni zaidi ya kupangwa kisheria. Wazazi wanapopanga mtoto kisheria, huchukua wajibu wa kumtunza mtoto huyo, lakini hawawezi kumpa mtoto huyo tabia za jenasi zao. Lakini Mungu akitupanga, tunafanywa upya kwa nguvu za Roho Mtakatifu. 13 Kwa hivyo baada ya wokovu, tunakuwa na tofauti. Weka maanani kuwa tunakuwa wana wa kupanga wa Mungu, lakini hatuko sawa na Mwana wa Mungu wa kipekee. Wakati wote Kristo yuko juu yetu.  

2. Toba

Mafunzo wa Toba inakaribiana na imani (tazama Matendo 20:21). Kutubu kuna maana ya kubadilisha mawazo yako —baada ya kufikiria sana. Ina maana ya kubadilika kutoka kwa dhambi na kumfuata Kristo (tazama Matendo 3:19). Tunapopata imani ya kweli ya kiroho katika Kristo, tunabadilika, tunaacha njia za Shetani na kufuata njia za Kristo. 

3. Upatanisho wa Mungu na Mwanadamu

Soteriolojioa inajumuisha mafunzo ya upatanisho wa Mungu na mwanadamu. Katika Theolojia ya Kikristo, upatanisho wa Mungu na mwanadamu unataja upatanisho wa uhusiano uliovunjika kati ya Mungu na mwanadamu. Upatanisho huu unatimizwa kupitia kwa maisha na kifo cha Yesu. 14 Tunaweza kukumbuka wazo hili la upatanisho kwa kugawa neno katika sehemu: “at one ment.” Tumefanyika “moja” na Mungu tunapoamini dhabihu ya Kristo.

Chini ya Sheria za Agano la Kale (Agano la Kale), Waebrania walitoa wanyama kama sadaka “kulipia kosa” la dhambi zao au “kufunika” dhambi zao (tazama Mambo ya Walawi 16). Sadaka kama hizo hazikuchukua dhambi, bali zilieleza kuhusu sadaka moja kamili itakayokuja—Yesu Kristo—Mwana- Kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu (tazama Yohana 1:29). Chini ya Sheria za Agano la Kale, mara moja kwa mwaka, Siku ya Upatanisho, Kuhani Mkuu alitoa wanyama kama sadaka, kufunika dhambi za wana wa Israeli. Kristo, Kuhani Mkuu, alifanya upatanishi wa kudumu kwa ajili ya dhambi (tazama Waebrania 10:12). Kristo hakufunika tu dhambi zetu, aliziondoa. Kwa hivyo Kristo ni mpatanishi wa Neema ya Agano Jipya (Agano Jipya). Tazama Waebrania 8:6-13. 

 

Page 26: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

a. Tuliza   

Tuliza kuna maana ya kuridhisha Mungu kwa kutoa sadaka inayofaa. Kwa hivyo upatanishi una maana ya “kusuluhisha” na kutuliza kuna maana ya “kuridhika.” Ili kuridhisha Mungu bila kulegeza masharti juu ya haki yake, kuhani mkuu wa wana wa Israeli alinyunyiza damu ya wanyama juu ya kiti cha huruma (juu ya kisanduku cha ahadi) Siku ya Upatanishi. Kiti cha Huruma ni mahali ambapo kuhani mkuu walikutana na Mungu. Kristo, sadaka ya mwisho, ndiye tulizo la dhambi zetu (tazama 1 Yohana 4:10). 

 

b. Ukuhani wa Waumini  

Chini ya Sheria za Agano la Kale, ni Kuhani Mkuu peke yake aliyeingia mbele za Mungu, mahali palipo patakatifu zaidi ndani ya Hekalu. Naye Kuhani Mkuu angefanya hivyo mara moja kwa mwaka – Siku ya Upatanishi. Kristo alipokufa msalabani, pazia la Hekalu, lililogawanya mahali patakatifu kutoka kwa patakatifu pa patakatifu lilipasuka vipande viwili toka juu hata chini (tazama Mathayo 27:50,51). Kupasuka kwa pazia ni ishara kuwa waumini wako kama kuhani mkuu, wanaweza kumwendea Mungu mara moja. Kwa hivyo tunashikilia mafundisho ya ukuhani wa waumini. Yesu ndiye Kuhani wetu Mkuu huko mbinguni, kwa hivyo hatuhitaji kuhani hapa duniani wa kutuombea. Kwa ujasiri tunaweza kuja mbele ya kiti cha enzi cha Mungu cha neema (tazama Waebrania 10:19-22).  

4. Sheria na Neema

Agano Jipya ya neema huleta msamaha, lakini Sheria za Agano la Kale zilileta shutuma. Kwa nini Mungu alitoa Agano la Kale? Sheria zilitolewa kutuonyesha kuwa hatuwezi kutii Mungu kikamilifu kwa hivyo tunahitaji Mwokozi ( tazama Wagalatia 3:24).

Kwa sababu Agano Jipya limechukua mahali pa Agano la Kale, inamaanisha tusiangalie sheria zote? Kwa kweli hapana, Agano la Kale lilikuwa na sheria za utaratibu, sheria za serikali, na sheria za maadili . Sheria za Utaratibu na mfumo wake wa kutoa sadaka za wanyama mahali pake pamechukuliwa na sadaka moja ya Kristo. Sheria za Serikali – sheria za Kiebrania za kuongoza jamii – hazitumiki katika jamii zetu siku hizi. Tunaweza pata kanuni muhimu kutokana na sheria za serikali, lakini sheria hizo hazitumiki siku hizi. Mfano wa sheria za serikali umetolewa katika Mambo ya Walawi 19:27. Sheria za Maadili zinatakiwa kufuatwa. Mungu alitoa sheria za maadili kama vile “usiue,” “Usizini,” “Usiibe.” Kwa nema ya Mungu, tunaweza kusamehewa tukivunja sheria kama hizi, lakini tunatakiwa kujitahidi kusitii.

 

5. Thibitisha

Page 27: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

Soteriolojia inajumuisha mafunzo ya thibitisho. Thibitisho ina maana kuwa kwa njia ya imani katika Kristo, wenye dhambi wanafikiriwa kuwa wenye haki. Wakati tu mtu anapomwamini Kristo, anathibitishwa. Wenye dhambi huthibitishwa kwa njia ya imani katika Kristo, si kwa matendo. Tunaweza kukumbuka wazo hili “kuthibitishwa” kwa kulinganisha na kifungu “kama sikuwa nimefanya” “Kwa njia ya imani katika Kristo, ni kama sijawahi fanya dhambi. Au kupitia kwa njia ya imani katika Kristo, ni kama sijawahi tenda dhambi.” Hata kama tunatenda dhambi, tumethibitishwa na damu ya dhabihu ya Kristo. Kwa hivyo Mungu hukubali dhabihu hiyo na kuhesabiwa kuwa haki (tazama Warumi 3:23, 24.  

6. Wongofu, Kutakaswa, na Kutukuzwa

Wokovu ina awamu tatu: wongofu, kutakaswa, na kutukuzwa. Wongofu ina maana ya kuzaliwa tena kiroho (tazama Yohana 1:12,13; 3:3). Mtu anapoweka imani yake katika Kristo, mtu huyo huwa mtoto aliyezaliwa wa kiroho. Mara moja, mtu huyo hupokea Roho Mtakatifu na ana hakikisho la uzima wa milele (tazama Luka 23:42,43; Warumi 10:9,10; Waefeso 4:30).

Mtoto wa kimwili hukaa kwa muda wa miezi tisa katika tumbo la mamake kabla ya kuzaliwa. Watu wengi huchukua muda kujitayarisha kuzaliwa kiroho. Mtu anaweza kusikia Injili na kutafakari habari hii njema katika roho yake. Wakati mmoja, anaweka imani yake katika Kristo, na mara moja anazaliwa tena. Hageuki tu, bali yeye ni kiumbe kipya (tazama 2 Wakorintho 5:17).15

Mtu anapoongoka au anapozaliwa tena, mtu huyo hufanywa mtakatifu. Kutakaswa kuna maana ya “kufanywa mtakatifu”.16 Mafunzo haya yanahusiana kwa karibu na mafunzo ya kuthibitisha. Mungu huthibitisha au hutangaza mtu kuwa mtakatifu. Kuthibitishwa ni jambo ambalo Mungu ameshamfanyia muumini. Kutakaswa ni yale Mungu anaendelea kufanya katika maisha ya muumini yote. Mungu humfanya mtu kuwa mtakatifu – huwatakasa kwa ajili ya kazi takatifu ya huduma. Kwa hivyo mtu aliyefanywa mtakatifu ameteuliwa ili amtumikie Mungu.

Mtu anapoendelea kujifunza neno la Mungu na kumtumikia Mungu, hukua katika imani. Kwa hivyo, kutakaswa ni jambo linalofanyika maishani yako yote. Mkristo anatakiwa kuwa mwaminifu na mwenye upendo katika maisha yake (tazama I Wathesalonike 3:12, 13). Hata kama waumini hawatapata ukamilifu katika maisha haya, ukamilifu unatakiwa kuwa lengo (tazama Mathayo 5:48). Mungu ndiye hutufanya watakatifu, lakini ni lazima muumini atii Mungu ili aweze kukua katika imani (tazama Yohana 17:17-19; Wafilipi 2:12,13).

Baada ya kuokoka, tumeitwa kuwa kama Kristo. Tunafaa kukua katika maarifa ya Maandiko (Waebrania 5:12-14). Tunatakiwa kufuata sheria za maadili zilizotolewa katika Agano la Kale na katika Agano Jipya. Maisha ya Mkristo ni maisha ya mapambano ya kuepuka dhambi (tazama Warumi 7:15-25). Lakini sisi Wakristo twaweza kufurahia kwa kujua kwamba tuko huru kutokana na hukumu (tazama Warumi 8:1-3).

Mfuatano wa kufanyika mtakatifu humalizika wakati muumini ametukuzwa – ameenda kuwa pamoja na Mungu na baadaye kupokea mwili mpya. Kwa hivyo

Page 28: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

kutukuzwa kunafanyika baada ya maisha ya hapa duniani (tazama 1 Wakorintho 15:52). Katika maisha haya, hatukai bila dhambi yo yote. Kwa hivyo Mungu hututakasa – kutufanya watakatifu na kutusamehe dhambi zetu. Katika maisha yajayo, tutakuwa bila dhambi.

10 Alan B. Stringfellow, Through The Bible in One Year, Vol. 3 Great Truths of the Bible, 95.

11 Strong’s, G. 264.

12 Charles Caldwell Ryrie, The Ryrie Study Bible (Chicago: Moody Press, 1978), note to John 3:5.

13Alan Stringfellow, Through the Bible In One Year . Vol. 3. Great Truths of the Bible. 191.

14 Van A. Harvey,. A Handbook of Theological Terms, (New York: Macmillan Publishing Co., Inc., 1964), “atonement,” 33.

15 Alan Stringfellow, Through the Bible In One Year . Vol. 3. Great Truths of the Bible. , 124-126

16 Strong’s Concordance, s.v. Greek “sanctify.”

RUDI KWA MUHTASARI

Page 29: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

THEOLOJIA

X. Dhamana ya Wokovu

Dhamana ya wokovu ni muhimu kwa waumini ili kuishi maisha ya usalama na ya furaha. Wakati mwingine dhamana hiyo huelezwa kama usalama wa muumini. Tunaamini kuwa Wakristo hawapotezi wokovu wao. Tunapomwamini Kristo, huwa tunapokea Roho Mtakatifu, ambayo ni hakikisho la uzima wa milele (tazama Waefeso 4:30). Nguvu za Mungu hutulinda tuzianguke (tazama 1 Petro 1:3-5). Yesu aliahidi kuwa hakuna atakayewapokonya katika mkono wake (tazama Yohana 10:28). Biblia hufundisha kuwa, tunaweza kujua kwamba tumeokolewa (tazama 1 Yohana 5:13).

Wakristo wengine hushikilia kuwa tunaweza kuchagua kuacha Kristo na kupoteza wokovu wetu. Wanatoa hoja kwamba hakuna anayeweza kutupokonya kutoka mkononi mwake lakini tunaweza kuchagua kutoka kwa mkono wake. Hutaja maandiko kama vile Waebrania 6:4-6 yakionyesha kwamba tunaweza kupoteza wokovu wetu. Ryrie ameandika kwamba Waebrania 6:4-6 imeeleweka kwa njia zifuatazo:  

1. Watu wanaweza kupoteza wokovu wao. Kama jambo hili ni la kweli, hawawezi kuokolewa tena.

2. Kifungu hiki cha Waebrania 6:4-6 kinazungumzia watu wale ambao hukiri imani yao, lakini hawajaokolewa. Kwa hivyo wanatoka tu kwa ufahamu wa ukweli, si kwamba wamejitolea kumfuata Kristo. Tambua kwamba Waebrania 6:9 inaonekana kuonyesha kuwa Paulo hatarajii Wakristo wa kweli watoke katika imani.

3. Maandiko yanaonya Wakristo kukomaa. Ni vigumu kutoka kwa imani. Vifungu hivi ni kama vinazungumzia kundi la wanafunzi kwa njia hii: Haiwezekani mwanafunzi, anapojiandikisha kwa mafunzo haya, kurudisha wakati nyuma (ambalo haliwezekani), kuanza mafunzo tena. Kwa hivyo, ni vyema wanafunzi wote waendelee kupata elimu ya kina.”17

Huwa tunadumisha ushirika na waumini ambao wanaamini kuwa mtu anaweza kutoka kwa wokovu. Hao ni ndugu na dada zetu katika Kristo. Pengine wako sahihi nasi tunakosea.

Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu na yasio muhimu katika wokovu. Warumi 10:9,10 hufunza kuwa tukimkiri Yesu kwa kinywa chetu ya kuwa ni Bwana na tuamini moyoni mwetu ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu tutaokoka. Kwa hivyo watu wakishikilia mambo muhimu kama vile vifungu hivi, hao ni ndugu na dada zetu katika Kristo. Mungu anajua kwamba tutatofautiana kwa mambo mengine ya kitheolojia, na kama tunakubaliana katika mambo muhimu, tunatakiwa tuwe na ushirika. Kwa njia hii, tunaweza kuwa mashahidi duniani (tazama Yohana 17:20, 21).

Tunadhania kwamba Biblia hutupa hakikisho la kutosha kwa waumini kuwa na tumanini

Page 30: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

katika wokovu wao. Kama kwa kweli kunatafuta kumfuata Mungu, tunaweza kuwa na amani na hakikisho la uzima wa milele. 

Na kazi ya haki itakuwa amani; na mazao ya haki yatakuwa ni utulivu na matumaini daima (Isaya 32:17).

Kama tunataka kumfuata Mungu, tunalo onyo – twaweza kuwa hatuna imani ya kweli, kwa hivyo twaweza kuwa hatujaokoka. Kwa muhtasari, tuna hakikisho na onyo.

Kwa habari zaidi kuhusu hakikisho la wokovu, tazama “Hakikisho la Uzima wa Milele” katika kiuzi cha mafunzo, “Mwito wa Umisheni.”

17 Ryrie, Ryrie Study Bible, Note to Hebrews 6:4-6.

RUDI KWA MUHTASARI

Page 31: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

THEOLOJIA

XI. Uchaguzi na Mada Zinazoambatana

Mawazo nne zimejadiliwa kwa karne nyingi: uchaguzi, kwa hiari, Kujua jambo kabla halijatokea, Yaliyoamuliwa. Nitatoa kila wazo baadaye nitoe msimamo wa kitheolojia ambao umetolewa kutoka kwa mawazo yote manne. 

A. Uchaguzi

Uchaguzi ni imani kuwa Mungu huwachagua watu fulani ili waokoke. Kulingana na Agano la Kale, Mungu alichagua uzao wa Ibrahimu – kupitia kwa mwana wake Isaka na mjukuu wake Yakobo (Israeli) – kuwa watu wake (tazama Mwanzo 12:2, 3). Mungu alichagua watu binafsi na alichagua taifa kama watu wake. Mungu alichagua watu binafsi kama vile Ibrahimu kuwa watu wake (tazama Mwanzo 12:1). Alichagua taifa la Israeli kuwa taifa la makuhani ambalo litawashuhudia watu wa mataifa (Kutoka 19:6).

Mungu alichagua watu wake lini? Kulingana na Agano Jipya, kabla ya kuumba ulimwengu, Mungu aliwachagua watu ili waokolewe (tazama Waefeso 1:4-12).

Biblia hufunza kuwa Mungu aliwachagua wengine wapate kuokolewa. Wale anaochagua ni wateule. Lakini watheolojia hujadiliana kama mwanadamu ana uchaguo wo wote wa kuitikia au kukataa mwito wa wokovu. Watheolojia wengine wamechukua msimamo kuwa Mungu alichagua wateule, na mwanadamu ana hiari yake katika mambo hayo. Mmoja wa watheolojia ambao wanajulikana kwa msimamo huu ni John Calvin (1509-64), Mprotestanti wa Kifaranza. Alama tano za mafundisho ya Calvin yalielezwa kwa usahihi kama jibu kwa Kitheolojia la Waminia. Waminia walisisitiza mwanadamu apokee au akatae wokovu kwa hiari yake. Alama tano za mafunzo ya Calvin ni kama zifuatavyo:

Upotovu kamili

Uchaguzi usio na masharti

Upatanisho ulio na mipaka

Neema isiyozuilika

Uvumilivu wa watakatifu

Kwa maelezo kuhusu alama hizi tano, tazama mafundisho ya Calvin (Calvinism) kwenye kamusi la Theolojia katika wavuti ufuatao:

 

http://www.carm.org/dictionary.htm

Page 32: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

  Mafunzo ya Calvin yanatia mkazo mamlaka ya Mungu. Mfuasi wa Calvin anaweza kuuliza, “Kama Mungu hafanyi kazi ya kuokoa watu, anawezaje kuitwa `mwenye nguvu?’”    

B. Hiari

Hiari ni imani kuwa mwanadamu anaweza kuchagua kuitikia au kukataa toleo la Mungu la wokovu.  Mtheolojia anayetambulika siku hizi kwa sababu ya msimamo huu ni Jacobus Arminius (c.1559-1609), mleta mabadiliko wa Kiholanzi. Biblia inafundisha kwamba kila atakayeliita jina la Mungu ataokoka (tazama Warumi 10:13). Na Biblia inafundisha kuwa mtu ye yote atakayemfuata Kristo ataokolewa (Tazama Marko 8:34, 35). Mungu hapendi mtu ye yote apotee, bali wote watapokea uzima (tazama 2 Petro 3:9).

Kwa muhtasari wa msimamo wa Arminianism, tazama “Arminianism” kwenye kamusi la theolojia katika wavuti ufuatao:

 http://www.carm.org/dictionary.htm

 Mafunzo ya Arminianism hutilia mkazo upendo wa Mungu. Mfuasi wa Arminian anaweza kuuliza, “Mungu asipompa kila mtu nafasi ya kuokolewa kutoka kwa mateso ya milele, anawezaje kuitwa Mungu mwenye upendo?”  

 

C. Yaliyoamuliwa

Yaliyoamuliwa ni imani kuwa Mungu huwa ameamua majaliwa ya mwanadamu – mbinguni au jehannamu.

  

“Maana wale waliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi” (Warumi 8:29). 

D. Kujua Kitu Kabla Hakijatokea

Imani ya Mungu kujua mambo kabla hayajatokea hufunza kuwa Mungu hujua kile kitakachotendeka, lakini hasababishi kila kitu kutendeka. Kwa hivyo anajua, nani atakayeokoka, lakini hawalazimishi kuokoka. Biblia hufunza kwamba Mungu anajua kesho (tazama Matendo 15:18).  

E. Msimamo wa Kipekee wa Kitheolojia  

Biblia yaweza kudondolewa kuunga mkono mawazo yote manne yanayohusu uchaguzi, na kuna mvutano kati ya mawazo hayo. Tunawezaje kuyapatanisha? Wakristo wengi huwa hawajaribu kupatanisha mawazo hayo. Wanachukua msimamo wa mafunzo ya Calvin ya yaliyoamuliwa au wa Arminia wa kujua

Page 33: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

mambo kabla hayajatokea. Bila kujali msimamo wo wote, zote tuko chini ya amri za Maandiko. Wafuasi wa Calvin na wa Arminia wameamriwa kutii Tume Kuu katika kueneza Injili. Wafuasi wa calvin na wa Arminia wamefunzwa kutii Amri Kuu – Kupenda Mungu na kumpenda jirani yako. Tukitii Maandiko, haitakuwa muhimu kama tunafuata au hatufuati Calvin au Arminia. Hata hivyo, mtazamo wa Mungu unaweza kutofautiana kama mtu anashikilia mafunzo ya Calvin au Armania kabisa. Wafuasi wa Calvin waweza kuona Mungu kuwa na mamlaka na sio mwenye upendo. Na wafuasi wa Arminia weweza kuona Mungu kuwa mwenye upendo, lakini sio mwenye mamlaka.

Stringfellow anatupa msimamo ambao umetoka kwa mawazo yote manne. Ameandika kuwa Mungu alihusika katika kuwachagua na kuwaita watu kama vile Ibrahimu (Mwanzo 12:1), lakini Ibrahimu anatii Mungu kwa hiari (Waebrania 11:8). Mungu alichagua kumwita Ibrahimu, na Ibrahimu angechagua kukataa mwito huo. Mungu alijua ni nani ataitikia mwito wake, kwa hivyo, akaamua wale ambao watafananishwa na mfano wa Mwana wake (tazama Warumi 8:25 ilioko hapo juu).18 Mungu alijua ni nani atakayeitikia mwito wake, kwa hivyo akaamua watu watakaoitikia kuokoka. 19

18 Stringfellow, Through the Bible In One Year . Vol. 3. Great Truths of the Bible, 198.

19 Stringfellow, Through the Bible In One Year . Vol. 3. Great Truths of the Bible, 206,207.

RUDI KWA MUHTASARI

Page 34: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

THEOLOJIA

XII. Mambo ya Mwisho

Kuja kwa Kristo kwa mara ya kwanza ndiko kulikuwa mwanzo wa siku za mwisho za dunia. Mafunzo ya mambo ya mwisho au Eschatolojia inaelezea yale yatakayofanyika mwisho wa dunia ukikaribia, na Mungu akikaribisha mbingu mpya na nchi mpya.    

A. Utatu Usio Mtakatifu  

Katika siku za mwisho, utatu usio mtakatifu, ukiwa na Shetani, mpinga Kristo na nabii wa uongo watatawala ulimwengu. Kinyume cha Utatu Mtakatifu, utatu usio mtakatifu ni uigaji mbaya, ukitaka kuwa kama Mungu. Shetani anaweza kuingia ndani ya wapinga Kristo na manabii wa uongo, lakini utatu usio mtakatifu sio watatu ndani ya mmoja. Utatu Mtakatifu ni watu watatu katika uungu. Utatu usio mtakatifu ni watu watatu tofauti. Shetani ameelezwa katika kitabu cha Ufunuo kama joka mkubwa na nyoka wa zamani – Ibilisi na Shetani (ufunuo 12:9).

Wapinga Kristo wengi wamekuwapo duniani (tazama 1 Yohana 2:18), lakini mtawala wa mabavu muovu atatawala ulimwengu. Mpinga Kristo atatawala shirikisho la mataifa zaidi ya kumi (ufalme wa Kirumi uliotengenezwa), na shirikisho la mataifa kumi litakuwa lenye nguvu juu ya nguvu za ulimwengu. Mpinga Kristo anajulikana kama mwenye kuharibu (tazama Danieli 9:27), chukizo la uharibifu (tazama Mathayo 24:15), na mnyama akitoka katika bahari (tazama Ufunuo 13:1).

Kama vile Shetani amekuwa akiwatumia viongozi waovu wa ulimwengu, Shetani atawapa nguvu mpinga Kristo (tazama Ufunuo 13:4). Shetani atashawishi nabii wa uongo kuongoza wasio Wakristo kuabudu mpinga Kristo (tazama Ufunuo 13:8; 16:13). Nabii wa uongo atahitaji watu wote wapate alama ya mnyama (au jina la mnyama yule au namba ya jina lake - 666) katika mkono wao wa kuume au katika vipaji vya nyuso zao (tazama Ufunuo 13:16-18). Wale ambao hawatapokea alama hiyo hawataweza kununua au kuuza. Na wale wasioisujudu sanamu ya mpinga Kristo watauawa (tazama Ufunuo 13:14,15). Lakini Mungu atahukumu wale watakaomsujudu mnyama kwa kuteswa kwa moto na kiberiti milele na milele (tazama Ufunuo 14:9-11).   

B. Majonzi

 Miaka saba ya uharibifu na machafuko unakaribia – mbaya zaidi kuliko dhiki iliyo kuu duniani (tazama Ufunuo 7:14). Wakati mwingine sehemu ya pili ya majonzi inaitwa majonzi makuu, kwa sababu uharibifu utakuwa mbaya zaidi katika miaka mitatu na nusu ya mwisho. Mpinga Kristo atafanya agano na Israeli, lakini katikati ya kipindi cha majonzi, atavunja agano na kunajisi Hekalu la Wayahudi (tazama Danieli 9:27).

Page 35: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

C. Siku ya Kiama  

Siku ya Kiama ni tukio ambalo Kristo atawanyakua Wakristo ulimwenguni na kumlaki hewani (tazama 1 Wathesalonike 4:16,17; 1 Wakorintho 15:51-58). Wakati huo, mwanadamu anayekufa atabadilishwa na kuwa kiumbe kinachoishi milele.

Kulingana na ufafanuzi wa Maandiko, Wakristo huwa na mtazamo unaotofautiana kuhusu mpangilio wa siku ya kiama. Wengine huamini kuwa siku ya kiama itakuwa kabla ya majonzi, wengine husema itafanyika wakati wa majonzi (katikati ya majonzi), na wengine hufikiria itafanyika baada ya majonzi.

D. Kiti cha Hukumu cha Kristo  

Kiti cha Hukumu cha Kristo ni hukumu ile Kristo atatoa kwa Wakristo kwa ajili mambo waliyotenda kwa mwili ( tazama 2 Wakorintho 5:10; Warumi 14:10). Wakristo wameshaokolewa klwa neema kwa njia ya imani. Hawapotezi wokovu wao, lakini wengine watapokea thawabu kwa matendo yao mema (tazama I Wakorintho 3:11-15).  

 

E. Vita vya Har-Magedoni  

Vita vya Har-Magedoni vitafanyika katika bondo na mlima wa Magedoni, katika uwanda wa Jezreel, katika Uyahudi. Shetani mpinga Kristo na nabii wa uongo ataongoza majeshi ya ulimwengu kupigana na Uyahudi, lakini Kristo na malaika wake watatokea kwa ghafla na kuangamiza maadui (tazama Ufunuo 16:16; 19:11-21). Vita hivi vitafanyika mwisho wa wakati wa majonzi utakapokaribia.  

F. Kuja kwa Kristo kwa Mara ya Pili

Yesu atakuja duniani kwa mara ya pili kutakuwa wakati wa vita vya Har-Magedoni. Kwa hivyo kuja kwa Yesu kwa mara ya pili duniani kunaweza kuwa wakati tofauti na siku ya kiama. Au kuja kwa Yesu duniani kwa mara ya pili kwaweza kufanyika siku ya kiama. Yesu atakaporudi, atakuja na mawingu na kila jicho litamwona (tazama Ufunuo 1:7). Yesu alieleza ishara zitakazotangulia kuja kwake (tazama Mathayo 24:3-51). Ahadi ya mwisho ya Maandiko ni ile ya Yesu anaposema, “Naam; naja upesi” (Ufunuo 22:20).

G. Milenia

Muda tu baada ya vita vya Har-Magedoni, Kristo atatawala duniani kama mfalme pamoja na watakatifu wakati wa Milenia (Milania ina maana ya “miaka elfu moja”). Huu utakuwa wakati wa amani na ustawi. Shetani atakuwa amefungwa gerezani wakati huo. Umilenia unataja mitazamo mbalimbali ya kumbukumbu

Page 36: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

za Kibiblia za muda huu wa miaka elfu moja. Zifuatazo ni shule za mawazo za kimsingi. Kwa kuongezea, wanatheolojia wanatoa maoni yao tofauti.  

 

1. Mtazamio kabla ya Milenia umeonyeshwa hapa. Unaeleza kuwa kufuatia majonzi, Kristo atarudi kukaribisha Milania. Mwisho wa Milania, Shetani atawachiliwa, kutakuwa na vita vya mwisho na baadaye kiti cha enzi cheupe cha hukumu kitawasili (tazama hapo chini)

2. Mtazamio baada ya Milenia ni kuwa Milania itarejea kabla ya kuja kwa Yesu duniani kwa mara ya pili. Kristo, kukaa mbinguni wakati wa Milenia, atafanya kazi kupitia kwa kanisa kuleta nyakati za amani na ustawi. Kufuatia Milenia kutakuwa na vita kati ya mema na maovu, na baadaye Kristo atarudi duniani. Kwa sababu ya vitisho vya vita vya dunia vya kwanza na vya pili, na kuongezeka kwa vifaa hatari vya vita, mtazamo huu umepoteza umaarufu. Ulimwengu umekuwa na hatari nyingi sio amani.

3. Mtazamio wa Milenia huchukulia milania kama ishara. Hakuna miaka elfu moja hasa – bali sisi tuko katika Milenia. Kristo atarudi kwa hukumu la mwisho. Kufuatia hukumu mbingu na dunia zitaharibiwa na mbingu mpya na dunia mpya zitaundwa. 

H. Uasi wa Mwisho

Kufuatia Milenia, Shetani atafunguliwa, atoke kifungoni chake. Tena atawadanganya mataifa na kuwaongoza dhidi ya watu wa Mungu. Lakini moto utashuka kutoka mbinguni utawaangamiza waasi naye Shetani atatupwa katika ziwa la moto na kuteswa milele (tazama Ufunuo 20:7-10).  

 

I. Kiti cha Enzi Kikubwa Cheupe cha Hukumu

Baada ya Shetani kutupwa katika ziwa la moto, kiti cha enzi kikubwa cheupe cha hukumu kitarejea. Mungu ataketi katika kiti cha enzi kuwahukumu watu waovu (wafu) kulingana na matendo yao, na kuwatupa katika ziwa la moto (tazama Ufunuo 20:11-15). Kwa hivyo wasioamini wataishi milele mbali na Mungu.    

J. Mbingu Mpya na Nchi Mpya

Mbingu, mahali anapokaa Mungu, patafanywa upya. Dunia itahukumiwa kwa moto, kama vile wakati mmoja ilihukumiwa kwa maji (tazama 2 Petro 3:6,7). Kwa hivyo kutakuna na nchi mpya, nao watakatifu wataishi milele kwa furaha pamoja na Mungu duniani (tazama Ufunuo 21:1-5; 22:1-5).

  RUDI KWA MUHTASARI

Page 37: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu
Page 38: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

THEOLOJIA

XIII. Ufalme wa Mungu

Ladd anashikilia mwelekeo wa kabla ya Milenia kuhusu Ufalme wa Mungu. Ameandika kuwa kuna maana tatu za ufalme wa Mungu katika Agano Jipya. 

1. Maana ya msingi ni utawala wa Mungu au mamlaka (tazama 1 Wakorintho 15:24, 25).

2. Ufalme au mahali anapotawala Mungu.

a. Ufalme wa Mungu wa siku hizi ( tazama Marko 1:15).

b. Ufalme ujao utakaozinduliwa Kristo atakaporudi na kufikia kilele na ufalme wa milele wa nyakati zijazo (tazama Marko 25:34).

3. Watu ambao Mungu anatawala (tazama Ufunuo 1:6). 20

Ufalme wa Mungu ulianza Yesu alipokuja duniani kwa mara ya kwanza. Mungu alianzisha utawala wake au mamlaka kupitia kwa kafara ya Kristo. Ufalme wa Mungu unajumuisha mataifa yote ya Kikristo – mahali ambapo Injili imeenezwa.

Katika jambo la tatu hapo juu, Ladd anapendekeza kuwa ni Wakristo pekee walio katika Ufalme wa Mungu. Stringfellow ameandika kuwa wale wote walio kanisani – waumini wa kweli na wale wanaokiri kumwaminiri Kristo - wako katika Ufalme wa Mbinguni. Stringfellow anatofautisha kati ya Ufalme wa Mungu na ufalme wa Mbinguni. Ufalme wa Mbinguni umetajwa katika Injili ya Mathayo peke yake, lakini waandishi wengine wote wa Agano Jipya hutaja Ufalme wa Mungu. Yesu alieeleza Ufalme wa Mbinguni katika mifano kumi na miwili iliyoko katika Injili ya Mathayo. Kristo alifafanua mifano ya kwanza miwili (tazama Mathayo 13:3-23, 24-29, 36-43 ), na ufafanuzi wake unatumika kama mwongozo wa kufafanua mifano hiyo mingine kumi. Katika mfano wa ngano na magugu, ngano (waumini wa kweli) na magugu (wale ambao wanakiri kuwa waumini waliruhusiwa kuishi pamoja (katika Ufalme wa Mbinguni) mpaka wakati wa mavuno (wakati Kristo atakaporudi). Ufalme wa Mbinguni unadumu kuanzia kuja kwa Yesu duniani wa mara ya kwanza mpaka mwisho wa Milenia, na mwisho wa dahari, Kristo atakabidhi Ufalme wa Mbinguni kwa Mungu Baba, ili uwe Ufalme wa Mungu (tazama 1 Wakorintho 15:24 ).21

Si wanathelojia wote hutofautisha kati ya Ufalme wa Mbinguni na Ufalme wa Mungu. Wacha tutumie Ufalme wa Mungu. Kulingana na mambo yaliyo hapo juu, ufafanuzi ufuatao umetolewa: Ufalme wa Mungu ni utawala juu ya kanisa kati ya mataifa ya Kikristo. Kanisa la siku hizi linajumuisha baadhi ya wasio amini, lakini katika siku zijazo, waumini pekee ndio watakaokuwa katika Ufalme. Mwisho wa dahari, ufahamu wa Mungu utakuwa umeenea kote katika nchi mpya, kwa hivyo kila mmoja katika Ufalme wa Mungu atakuwa Mkristo.

Page 39: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

20 George E. Ladd, “Kingdom of God,” Pictorial Bible Dictionary, (Nashville, Tennessee: Southwestern Company, 1968), p. 466.

21 Stringfellow, Through the Bible In One Year . Vol. 3. Great Truths of the Bible, 277-279.

RUDI KWA MUHTASARI

Page 40: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

THEOLOJIA

XVI. Kanisa

Katika Agano Jipya, neno “kanisa” kwa kawaida hutaja kusanyiko la waumini wa mahali.Pia hutaja Mwili wa Kristo, ambao unajumuisha waumini wote wa nyakati zote. Kanisa lenye mpangilio sio sawa na kanisa la kweli. Kanisa lenye mpangilio lina waumini wa kweli na wale ambao hukiri tu kuwa waumini. Kanisa la kweli ni mwili wa Kristo. Kristo, ndani ya Roho Mtakatifu, huishi ndani ya waumini, akiwapa nguvu za kutenda kazi ya kanisa. Kila muumini ana kusudi katika Mwili wa Kristo. Waumini wote wanapaswa kufanya kazi pamoja ili kuhimiza kazi ya kanisa (tazama 1 Wakorintho 12:13-27). Kristo ndiye kichwa cha Mwili (tazama Wakolosai 1:18).

Kristo, kichwa cha kanisa, amefananishwa na mume, ambaye ni kichwa cha uhusiano wa ndoa (tazama Waefeso 5:25, 32). Kwa hivyo, huwa tunafikiria kanisa kama bibi arusi wa Kristo.

Kristo aliamuru kanisa kuadhimisha agizo mbili – ubatizo na ushirika. Wale watakaoamini Kristo wabatizwe kwa kuzamishwa. Waumini wanatakiwa kubatizwa muda mfupi baada ya kutangaza imani yao katika Kristo. Kwa habari zaidi kuhusu Ubatizo, tazama “kuabudu kwa Ubatizo” katika kiuzi cha mafunzo cha “Huduma ya Uchungaji.”

Ushirika au “Ushirika Mtakatifu” umefafanuliwa kwa njia tatu: Mafunzo ya Wakatoliki wa Kirumi kwamba mkate na mvinyo hubadilika kuwa mwili na damu ya Yesu, Mfunzo ya Kilutheri kuwa damu na mwili wa Yesu Kristo upo pamoja na divai na mkate na mafunzo ya Protestanti kuwa ni ishara ya ukumbusho. Kanisa la Katoliki la Kirumi hushikilia kuwa elementi (mkate na kikombe) hubadilika hasa na kuwa mwili na damu ya Kristo, na kama sakaramenti, ina thamani ya kumpokea Kristo. Kanuni ya Kilutheri ya damu na mwili wa Kristo kuwepo pamoja na divai na mkate husema kuwa elementi hazibadiliki na kuwa mwili na damu ya Kristo, bali, kuna kuwepo kwa Kristo katika, chini na pamoja na elementi. Huwa tunashika ishara ya ukumbusho – tukiamini kuwa elementi ni ishara ya mwili na damu ya Kristo, na ushirika unasherehekewa kama ukumbusho wa kifo cha Yesu. Wakati Yesu alitaja elementi kuwa mwili na damu, alikuwa anavitumia kama sitiari ya Roho na maneno yake (tazama Yohana 6:51-56, 61-63). Tunapotwaa mkate na kikombe, huwa hatuli au kunyua mwili na damu hasa wa Kristo, kwa kuwa “mwili haufai kitu ” (Yohana 6:63). Badala yake, huwa tunaamini maneno ya Kristo, na tunaokolewa kwa sababu ya Roho wake Mtakatifu aliye ndani yetu. Kwa habari zaidi kuhusu ushirika, tazama “Kuabudu kupitia kwa Ushirika” katika kiuzi cha mafunzo cha “Huduma ya Uchungaji.”

Kanisa liliundwa wakati Roho Mtakatifu aliwajaza waumini siku ya Pentekoste (tazama Matendo 2:1-4). Matendo ya Mitume hutoa historia ya kanisa wakati wa karne la kwanza. Msingi wa kanuni za kanisa umetokana na Nyaraka za Mtume Paulo. Msingi wa kanisa ni Kristo (tazama 1 Wakorintho 3:11). Petro alikuwa kiongozi wa kanisa la kwanza, lakini msingi wa kanisa ni Kristo, sio Petro. Na tuchunguze maneno ya kifungu kinachohusika na uongozi wa kanisa. 

Page 41: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

Nami nakuambia, wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda (Mathayo 16:18).

Kristo alimuita Simoni “Petro,” au “Petros” kwa Kigriki, iliyo na maana ya “mwamba” au “jiwe dogo.” Neno “mwamba” katika Mathayo 16:18 ni “Petra” kwa lugha ya Kigriki, linalo maanisha “Jiwe kubwa.” Kwa hivyo maana ya kifungu hiki ni: “Wewe ndiwe Petro — jiwe dogo, na juu ya jiwe hili kubwa (Kristo), nitalijenga kanisa langu.” Ni jambo la kushangaza kuwa Petro baadaye alidondoa Isaya akisema kuwa Kristo ndiye jiwe kuu la pembeni na watu wanatakiwa kumwamini Kristo (tazama 1 Petro 2:6).

Kristo alituma kanisa lienende na kuwafanya watu kuwa wanafunzi (tazama Mathayo 28:18-20). Muhtasari wa kusudi la Kanisa umetolewa katika kiuzi cha mafundisho, “Uongozi na Utawala wa kanisa.” Maofisa wa kanisa ni pamoja na Wachungaji, wazee wa kanisa, na mashemasi. Ofisi ya Mchungaji imeelezwa katika kiuzi cha mafundisho, Huduma ya Uchungaji,” na maofisi ya wazee na mashemasi yameelezwa katika kiuzi cha mafundisho, “Uongozi na Utawala wa Kanisa.”

Kila muumini awe mshiriki hai wa kanisa la mtaa. Biblia hufundisha Wakristo kukutanika pamoja kwa ajili ya kuhimizana.  

24 Tukaangaliane sisi kwa sisi na kuhimizana katika upendo na kazi nzuri. 25Wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia (Waebrania 10:24,25).

RUDI KWA MUHTASARI

Page 42: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

THEOLOJIA

XV. Agano

Agano la Kibiblia ni mapatano kati ya Mungu na mwanadamu, ambapo Mungu ndiye huweka masharti. Agano kama hilo ni ahadi kutoka kwa Mungu. Kati ya agano nane zilizoko katika Biblia, sita hazina masharti – Mungu atatenda jambo bila kujali matendo ya mwanadamu. Mbili kati yake zina masharti (Agano la Edeni na Agano la Musa) – Mungu atatenda jambo kulingana na jinsi mwanadamu anavyojibu.

Ni muhimu kujua agano ili tuweze kuelewa mpango kamili wa Mungu kama ulivyoonyeshwa kupitia kwa Maandiko. Agano ni sehemu ya Mpango wa Mungu wa Ukombozi wa ulimwengu, kwa hivyo hutimizwa kupitia kwa Yesu Kristo. Zifuatazo ni agano, pamoja na maelezo ya jinsi Yesu alivyotekeleza ahadi hizo. 

1. Agano la Edeni (tazama Mwanzo 2:16,17). Mungu alimpa Adamu uhuru wa kula kutoka mti wo wote katika bustani ya Edeni isipokuwa matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Kwa matokeo yake Mungu akasema, ukinitii utaishi, lakini usipotii, utakufa.”

Kristo, Adamu wa pili, alitimiza agano hili kwa kumtii Mungu (Warumi 14-19).

2. Agano la Adamu (tazama Mwanzo 3:14-19). Mungu aliweka laana kama tokeo la dhambi, lakini alitoa mpango wa ukombozi kupitia kwa uzao wa mwanamke – Yesu Kristo.

3. Agano la Nuhu (tazama Mwanzo 9:1-17). Mungu aliahidi kamwe hataharibu ulimwengu kwa mafuriko tena, aliongeza nyama kuwa chakula cha mwanadamu, na kuanzisha utakatifu wa maisha ya mwanadamu – kwa sababu mwandamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu. Alithibitisha agano hilo kwa ishara ya upinde wa mvua.

Mungu alimbariki Shemu, mmoja wa wana watatu wa Nuhu, na Yesu akazaliwa kutoka kwa ukoo wa Shemu (Mwanzo 9:26).

4. Agano la Ibrahimu (tazama Mwanzo 12:1-3). Mungu aliahidi kuufanya ukoo wa Ibrahimu kuwa taifa kubwa, alibariki marafiki wa Ibrahimu, na kubariki jamaa zote za dunia kupitia kwa Ibrahimu.

Kupitia kwa Yesu, ambaye ni wa ukoo wa Ibrahimu, jamaa zote za dunia walibarikiwa kwa kupata nafasi ya kupokea uzima wa milele.

5. Agano la Musa (tazama Mwanzo 19:5, 6). Mungu aliahidi kwamba, wana wa Israeli wakitii sheria za Mungu (zilizotolewa kupitia kwa Musa), watakuwa watu wateule – ufalme wa makuhani.

Page 43: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

Yesu alitimiza mahitaji ya sheria, kwa kuishi maisha yasiyokuwa na dhambi (tazama Mathayo 5:17).

6. Agano la Palestino (tazama Kumbukumbu la Torati 30:1-10). Mungu aliahidi kwamba wana wa Israeli watakapomrudia, atawapa nchi ya Palestino. Agano hili halikuwa na masharti – watu wa Mungu watamrudia Mungu.

Yesu atatimiza Agano hili kwa kuwaongoza watu wake katika nchi la ahadi katika dunia mpya.

7. Agano la Daudi (tazama 2 Samweli 7:8-17). Mungu aliahidi kuthibitisha nyumba na ufalme wa Daudi milele (2 Samweli 7:16).

Yesu, uzao wa Daudi kupitia kwa Mariamu, ndiye Mfalme wa milele.

8. Agano Jipya (tazama Waebrania 8:7-13). Tofauti na Agano la Kale, Agano Jipya limeandika katika roho za watu wa Mungu.

Kupitia kwa dhabihu ya Kristo, Agano Jipya la neema hutolewa (Mathayo 26:28).

RUDI KWA MUHTASARI

Page 44: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

THEOLOGIA

XVI. Maovu

Harvey aliandika kuwa siku za nyuma hadi wakati wa Pilato (c. 427-347 B.C.), watu wamekuwa wakijaribu kueleza shida ya maovu. Imani yo yote ya (Ukristo, Uyuda, Uislamu n.k.) ambayo husema kuwa mema na nguvu hutokana na uungu yamekabiliwa na shida hii. Mfumo wa utawala ni njia moja ya kueleza wema wa Mungu ukilinganishwa na maovu yalioko duniani. Wakristo hueleza shida ya maovu kwa njia ifuatayo: Mungu aliye mwenye nguvu na mwenye upendo anawezaje kuruhusu kuwepo kwa maovu? Kama yeye ni mwenye nguvu na mwenye upendo, anatakiwa awe na uwezo wa kuzuia maovu, na angeonekana kutaka kuzuia maovu. Wakristo wengi ambao hujaribu kutatua mtanziko huu huwa katika aina mbili zifuatazo: 

1. Huwezi kuzuia maovu katika utaratibu wo wote mahali palipo na viumbe huru.

a. Shetani hutumia uhuru wake kwa kuasi dhidi ya Mungu, na kuleta maovu ulimwenguni kupitia kwa Adamu na Hawa. Adamu na Hawa walitumia uhuru wao na kutenda dhambi.

2. Hakuna jibu linalopatikana kwa mwanadamu. Tunahitaji kuwa na imani kama ya mtoto katika Maandiko ambayo inatwambia kuhusu ukuu na upendo wa Mungu.22

Hata kama hatuwezi kuamua kuhusu shida ya dhambi, tunaweza kuelewa kweli kadhaa kuhusiana na shida hii.  

1. Mungu aliumba vitu vyema na kuhuluku ubaya:

  “ Mimi naiumba nuru, na kulihuluku giza       mimi nafanya suluhu, na kuhuluku ubaya;        Mimi ni BWANA, niyatendaye hayo yote” (Isaya 45:7).

 

2. Tunaweza kujaribu kuelewa sababu za kuwepo kwa maovu, lakini hatuwezi uliza swali kuhusu ukweli wa Neno la Mungu au uaminifu wake:

 9 "Ole wake ashindanaye na Muumba wake!        Kigae kimoja katika vigae vya dunia!        Je! Udongo umwambie yeye aufinyangaye; Unafanya nini? Au kazi yako, Hana mikono?  10 Ole wake amwambiaye baba yake,        `Wazaa nini?'

Page 45: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

       Au mwanamke,        'Una utungu wa nini?'  11  "BWANA, Mtakatifu wa Israeli - na Muumba wake asema hivi:        Niulize habari za Mambo yatakayokuja;        mambo ya wana wangu,        na habari ya kazi ya mikono yangu; haya! Niagizeni. (Isaya 45:9-11)

 

3. Mungu huleta uzuri kutokana na uovu.

  “Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, [a] yaani [b] wale walioitwa kwa kusudi lake” (Warumi 8:28).  

a. Warumi 8:28 Muswada mwingine, nasi twajua ya kuwa mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema

 

b. Warumi 8:28 au kufanya kazi pamoja na wale wampendao kuleta mema – pamoja na wale

 Ufafanuzi wa uovu, si wema. Lakini Mungu anaweza kutumia uovu kuleta wema. Na Mungu anaweza kufanya kazi kati ya uovu kuleta wema. Ingawa uovu upo, mema yatajitokeza kwa wale wameitwa kutimiza kusudi la Mungu.

 

4. Ingawa hatuwezi kueleza fumbo la dhambi, tunajua kwamba Mungu anatupenda. Mungu, katika utu wa Kristo, aliteswa masalabani. Hangeweza kuepuka mateso kama (tazama Luka 22:42). Mungu ana nguvu za kutosha kumshinda Shetani na uovu, bali ni lazima uovu uwepo kwa muda. Mungu anatupenda sana hadi akateswa pamoja nasi na akatufia.

22 Van A. Harvey,. A Handbook of Theological Terms, (New York: Macmillan Publishing Co., Inc., 1964), “theodicy,” 236,237.

RUDI KWA MUHTASARI

Page 46: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

THEOLOJIA

XVII. Maombi

Maombi ni mawasiliano ya njia mbili kati ya Mungu na wanadamu. Ni mojawapo ya karama kuu ambayo imetolewa na Mungu. Maombi hubadilisha ulimwengu. Maombi hubadilisha kanisa. Maombi hubadilisha mtu.

Yesu aliwafundisha wanafunzi wake jinsi ya kuomba (tazama “Maombi” katika kiuzi cha mafundisho “Mwito wa Umisheni”) kupitia kwa Sala ya Bwana (Mathayo 6:9-15). Maombi na Kufunga huambatana (tazama Mathayo 6:9-18). Tunapofunga, njaa yetu hutukumbusha kuomba kila siku.

Mtu alindokeza kutumia aina ya chemshabongo ya kiingereza ACTS kutukumbusha jinsi ya kuomba:  

A   Adoration of God - Kumsujudu Mungu

C   Cofession of Sin -  Kukiri dhambi

T   Thanksgiving to God - Kutoa shukrani kwa Mungu

S   Supplication—asking God to supply needs – Kumsihi Mungu atimize mahitaji

Zingatia kila sehemu ya sala. Tunamsujudu Mungu kwa kumsifu na kumheshimu, kwa kuzungumzia sifa zake – utakatifu wake, ukuu wake, upendo, fadhili, neema na uaminifu (tazama Ufunuo 4:10, 11). Tunakiri dhambi zetu ili tusamehewe na tuwe na ushirika na Mungu (tazama 1 Yohana 1:9). Tunamshukuru Mungu kwa baraka zake katika hali zote (tazama 1 Wathesalonike 5:16-18). Shukrani kama hizo zinatufurahisha na hufurahisha Mungu (tazama Luka 17:12-18). Maombi ni kitendo cha kumsihi Mungu kutimiza mahitaji (tazama Mathayo 7:7-8; Wafilipi 4:6). Tunaweza kumsihi Mungu atutimizie mahitaji ama tunaweza kuyaombea mahitaji ya wengine.

Ni lazima tumuombe Mungu Baba (tazama Mathayo 6:9) katika jina la Yesu (tazama Yohana 16:4) kwa nguvu za Roho Mtakatifu (tazama Warumi 8:26,27). Kuomba jina la Yesu sio kutaja jina lake tu, bali ni kuomba kulingana na asili yake. Kuomba kwa jina la Yesu ni kusihi mamlaka ya Yesu, ambaye ameshinda dhambi na mauti kupitia kwa dhabihu yake msalabani (tazama Ufunuo 3:20). Ni asili ya Yesu kutamani kufanya mapenzi ya Baba (tazama Luka 22:42).

Tusiongee na Mungu kwa maombi tu, bali tunafaa kumsikiza na kungojea majibu yake (tazama Yohana 10:27; Zaburi 5:2). Ni vyema kuomba katika mahali patulivu pasiri, tunapomsikiza Mungu ajibu maombi yetu. Kama inawezekama tuombee katika mahali pasipo na shughuli nyingi. Mungu naweza kujibu kwa sauti tulivu, akivutia mioyo yetu na akili kwa neno lake. Inasaidia kuwa na Biblia na kutafakari Maandiko tunapoomba. Kwa njia hii, Mungu anaweza kunena kupitia kwa Maandiko kutusisitizia jambo. Tunapoyatafakari Maandiko tuliyoyasoma au tuliyoyakariri, tunaweza kumuuliza Mungu, “Ninawezaje kuyatumia mafunzo haya katika maisha yangu?” Au tunaweza kuomba

Page 47: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

Maandiko kwa Mungu, kwa kusema, “Naamini ahadi zako zilizoko katika Maandiko.” Kama tumejitolea kwa Yesu na kudumu katika mafunzo yake, maombi yetu yatajibiwa (tazama Yohana 15:7).

Ni wakati gani tunafaa kuomba? Wakati wo wote. Maombi yaweza kuwa neno moja au mawili. Inaweza kuchukua masaa kadhaa. Inasaidia kutenga wakati fulani kwa ajili ya maombi. Tunaweza kuomba tunapoamka (tazama Zaburi 5:3), kabla ya kulala, ama mara tatu kila siku kama nabii Danieli (tazama Danieli 6:10). Maombi si maneno tu – ni mtazamo. Tuwe na mtazamo wa shukrani.

Maombi hufanyika mahali pa siri (tazama Mathayo 6:6), pamoja na jamii (tazama Mathayo 18:19, 20), na katika kanisa (tazama Luka 19:46). Maombi yanaweza kuwa pamoja na kundi lo lote la Wakristo. Je, elementi za maombi yakufana ni zipi? Elementi zingine zimetolewa hapo juu.

Pia, zingatia yafuatayo:  

1. Jambo la muhimu, anayeomba lazima awe Mkristo – mtu aliyetangazwa kuwa mtakatifu kwa damu ya Yesu (tazama Yakobo 5:16). Kristo ameukaribisha ufalme wa mbinguni, na Wakristo katika ufalme wana uhusiano wa kipekee na Mungu (tazama Mathayo 11:11). Maombi ya Wakristo yana nguvu.

2. Mungu hawasikilizi watenda dhambi, kwa hivyo ni lazima tutafute msamaha na kushirikiana na Mungu (tazama 66:18). Dhambi moja ni kutesa mume au mke katika ndoa, na dhambi kama hiyo huzuia nguvu za maombi (tazama 1 Petro 3:7).

3. Ni lazima tuwasamehe wengine ili dhambi zetu zisamehewe, na kwa hiyo maombi yetu yatajibiwa (tazama Marko 11:25-26).

4. Maombi lazima yafanywe kawa imani (tazama Mathayo 17:20).

5. Lazima tuvumilie katika maombi (tazama Luka 11:1-8).

6. Lazima maombi yatoke kwa moyo mnyenyekevu (tazama 2 Kumbukumbu la Torati 7:14).

Je, tunaweza kumtarajia Mungu ayajibu maombi yote? Kama tunaishi katika dhambi, hatajibu (Zaburi 66:18). Kama tumejitolea kwa Yesu na kudumu katika mafundisho yake, maombi yetu yatajibiwa (tazama Yohana 15:7). Tukikaa ndani ya Kristo, tunaomba kulingana na mapenzi ya Mungu. Maombi kama hayo hujibiwa.

Mungu anaweza kuyajibu mambo katika mojawapo ya njia zifuatazo: 

Ndio

La

Ngoja

Page 48: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

Niko na mpango mwema

Akisema, “La,” au “Niko na mpango mwema,” tuwe na shukrani kwamba yeye hufanya uamuzi mwema kutuliko. Akisema, “Ngoja,” tuombe atupe subira. Maombi yetu yanapojibiwa, tumshukuru Mungu.

RUDI KWA MUHTASARI

Page 49: MWITO WA UMISHENI - Missions Trainingmissionstraining.org/Kiswahili/Courses/KiswahiliTheology.doc · Web viewPengine wako sahihi nasi tunakosea. Ni jambo la maana kutambua mambo muhimu

THEOLOJIA

XVIII. Bibliografia

     Harvey, Van A. A Handbook of Theological Terms. New York: Macmillan Publishing Co., Inc., 1964.

Hunt, T. W., and Walker, Catherine. Disciple’s Prayer Life. Nashville, Tennessee: Lifeway Press, 1997.

Stringfellow, Alan B. Through the Bible In One Year. Vol. 3. Great Truths of the Bible. Tulsa, Oklahoma: Virgil W. Hensley, Inc., 1981. Inawezekana usiweze kupata nakala ya kitabu hiki, lakini waweza kukipata kupitia kwa wavuti wa E-Bay.

RUDI KWA MUHTASARI