4
Wakazi wa kundi katika majadiliano mnamo. Februari 2018 Matokeo ya utafiti unaohusu usimamizi wa misitu na vyanzo vya maji katika msitu mdogo wa Saboti-Sosio katika Msitu wa Mlima Elgon Mradi wa Minara ya Maji Lengo Kuthibitisha ikiwa na jinsi mashirika ya jamii yanayohifadhi misitu na mashirika ya wanaotumia maji yanavyoshirikiana kusimamia msitu na maji. Kuhusu msitu mdogo wa Saboti-Sosio Misitu midogo ya Saboti na Sosio ina ukubwa wa ekari 11,158 jumla (Sosio una ekari 10035 huku Saboti ikiwa na ekari 1122.8) Misitu yote miwili ni mali ya serikali na ni sehemu ya msitu mkubwa wa Mlima Elgon. Chama cha Msitu wa Saboti-Sosio (CFA) kina jumla ya wanachama 2600 (wanaume 1800 na wanawake 800). Makundi ya wanachama yanayotumia rasilimali za misitu ni ya wafugaji nyuki, walishaji mifugo, wanaoteka maji na kukata kuni, wanaopanda miche katika nasari na (Mradi wa Mashamba Makubwa na Unaoboresha maisha ya wakazi (Plantation Establishment and Livelihood Improvement Scheme- PELIS). Shirika la Wanaotumia Maji (Water Resource User Association -WRUA) katika eneo la Sosio lina wanachama 70 (wanawake 38 na wanaume 32).

Mradi wa Minara ya Maji - CIFOR · • Kutambua mashujaa wa jamii kueneza elimu kuhusu majukumu ya wanawake na wanaume. • Kuhakikisha wanawake na wanaume wanajulishwa mapema kuhusu

  • Upload
    others

  • View
    5

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Mradi wa Minara ya Maji - CIFOR · • Kutambua mashujaa wa jamii kueneza elimu kuhusu majukumu ya wanawake na wanaume. • Kuhakikisha wanawake na wanaume wanajulishwa mapema kuhusu

Wakazi wa kundi katika majadiliano mnamo. Februari 2018

Matokeo ya utafiti unaohusu usimamizi wa misitu na vyanzo vya maji katika msitu mdogo wa Saboti-Sosio katika Msitu wa Mlima Elgon

Mradi wa Minara ya Maji

LengoKuthibitisha ikiwa na jinsi mashirika ya jamii yanayohifadhi misitu na mashirika ya wanaotumia maji yanavyoshirikiana kusimamia msitu na maji.

Kuhusu msitu mdogo wa Saboti-SosioMisitu midogo ya Saboti na Sosio ina ukubwa wa ekari 11,158 jumla (Sosio una ekari 10035 huku Saboti ikiwa na ekari 1122.8) Misitu yote miwili ni mali ya serikali na ni sehemu ya msitu mkubwa wa Mlima Elgon. Chama cha Msitu wa Saboti-Sosio (CFA) kina jumla ya wanachama 2600 (wanaume 1800 na wanawake 800). Makundi ya wanachama

yanayotumia rasilimali za misitu ni ya wafugaji nyuki, walishaji mifugo, wanaoteka maji na kukata kuni, wanaopanda miche katika nasari na (Mradi wa Mashamba Makubwa na Unaoboresha maisha ya wakazi (Plantation Establishment and Livelihood Improvement Scheme- PELIS). Shirika la Wanaotumia Maji (Water Resource User Association -WRUA) katika eneo la Sosio lina wanachama 70 (wanawake 38 na wanaume 32).

Page 2: Mradi wa Minara ya Maji - CIFOR · • Kutambua mashujaa wa jamii kueneza elimu kuhusu majukumu ya wanawake na wanaume. • Kuhakikisha wanawake na wanaume wanajulishwa mapema kuhusu

Maoni ya wakazi kuhusu hali ya msitu na majiWakazi walikubali kwamba msitu umepungua katika miaka 5-10, wanaposhuhudia miti ikipungua na kuona sehemu bila miti. Idadi kubwa ya watu, imesababisha watu kunyemelea misitu wakitafuta makazi na malisho ya mifugo. Kadhalika, miti asili imepungua na nafasi yake kuchukuliwa na Mradi wa PELIS. Msitu pia umeharibiwa na wakataji miti wanaotaka mbao na wachomaji makaa. Miti asili kama vile armotit, mwiri, tapaswet, tunguron, sesut na lamaiywet ilipotea na idadi ya miti mingine ya kiasili kama vile Elgon Teak na Cedar (mwerezi) kupunguka. Wakazi walisema kwamba eneo la msitu linalokaliwa na jamii ya Ogiek halijaharibiwa kwani jamii hiyo inazingatia mbinu bora za kuhifadhi miti.

Viwango vya maji katika mito kama vile Mumwo, Nyanja, Karasa na Kulkul vimepungua katika miaka 5-10 iliyopita kutokana na ukataji miti na uharibifu wa miti asili. Hali hii imesababisha mmomonyoko wa udongo na matope kujazana katika mito, hasa mito ya Chepsagat, Tabason, Kipyawyon na Kumriony. Hali hii imebadili rangi ya maji kuwa ya kahawia (brown) ambayo si salama kutumia. Viwango vya maji maji vinapunguka katika mito Sikerker, Sosio na Nyanja. Mbali na misitu kuharibiwa, wakazi walisema misimu mirefu ya kiangazi imeathiriwa viwango vya maji katika visima kama vile Kirorei na Chemtei.

Washiriki wote wa katika makundi ya majadiliano walisema kwamba viwango vya maji vilipingua katika mito kwa sababu ya hali ya misitu inabadilika. Wanachama wa WRUA pia walitaja kuwa ukataji wa miti ulisababisha viwango vya maji kupungua, matope kujaa katika mito na maji kubadili rangi.

Mchoro 1. Jinsia na umri wa wahojiwa katika makundi yaliyolengwa.

Mchoro 2. Idadi ya majadiliano ya katika kila kundi la watumiaji.

Utaratibu wa utafitiTulifanya utafiti katika eneo la Sosio lililo na msitu asili. Makundi yafuatayo yanayotumia rasilmali za misitu yalichaguliwa; wafugaji nyuki, walishaji mifugo, wanaoteka maji na kuni, wanaopanda miche katika nasari na PELIS. Tuliandaa jumla ya mikutano 39 na wanachama wa makundi hayo, viongozi wa makundi hayo na wakazi wasio wanachama wa CFA na WRUA. Tena, tuliwahoji, mara sita (6), viongozi wa CFA na WRUA. Tulizungumza na washirika 451 (wanaume 87 na wanawake 62), wenye umri tofauti kama mchoro 1 unavyoonyesha.

0

2

4

6

8

Ufugaji

Nasari z

a miche

Ufugaji w

a nyuki

Kuni

Wasio

wanacham

a

Viongozi wa vikundi

la watu

miaji

Miti sh

amba

TELIS

WRUA

22%

16%

22%

31%

4% 5%

Wanawake wachanga (18-35)

Wanawake wazee (Zaidi ya 35)

Wanaume wachanga (18-35)

Wanawake wazee (Zaidi ya 35)

Wanawake wachanga na wazee

Wanaume wachanga na wazee

Page 3: Mradi wa Minara ya Maji - CIFOR · • Kutambua mashujaa wa jamii kueneza elimu kuhusu majukumu ya wanawake na wanaume. • Kuhakikisha wanawake na wanaume wanajulishwa mapema kuhusu

Uongozi Mwenyekiti wa CFA na katibu ni wanaume, na mwekahazina ni mwanamke. Chama cha WRUA kina aina mbili ya viongozi: wasimamizi na kamati nne ndogo zinazosimamia ununuzi wa bidhaa na huduma, fedha na kufuatilia miradi. Kila kamati ina wanachama watano (wanaume 3 na wanawake 2). Katika kiwango cha usimamizi, mwenyekiti msaidizi, mwekahazina na katibu msaidizi ni wanawake. Shirika la WRUA lilipanga kupunguza muda wa maafisa kuwa afisini kutoka miaka mitano hadi mitatu. Wanachama waliandaa uchaguzi wa mwisho mnamo Juni 2018. Wanachama wa CFA wameandaa uchaguzi mara mbili tangu waje pamoja. Maafisa huwa mamlakani kwa muda wa miaka mitano. Wanawake huchaguliwa kuwa waweka hazina kwani wanaaminika kuwa wakarimu, wenye uwazi na wepesi wa kueneza taarifa miongoni mwa wanachama wa makundi, tofauti na viongozi wanaume.

Wanawake wanadhaniwa kuwa waaminifu, wanaosimamia mali na fedha za makundi vyema, wanaofahamu kuhusu shughuli za makundi. Wanaume wanachaguliwa wenyeviti kwa kuwa wanadhaniwa kuwa wenye bidii, wenye ushawishi katika maamuzi, wavumilivu na wasiyoyumbayumba wakiendeleza shughuli.

Shughuli za CFA na WRUA Wanachama wa CFA na WRUA hawaendelezi shughuli pamoja.• Wanachama wa WRUA hawako katika CFA. Wanachama

wa WRUA walisema ilikuwa mara ya kwanza kuambiwa kuhusu CFA.

• Wanachama wa CFA hawana taarifa kuhusu WRUA katika eneo hilo kwa kuwa CFA wanapakana na maeneo ya maji upande wa juu ilhali wanachama wa wanapatikana katika maeneo ya kati na chini yenye maji.

• Wanachama wa CFA hawana habari kuhusu miradi ya WRUA ama umuhimu wa kushirikiana na WRUA.

• Wanachama wa CFA walishikilia kuwa viongozi wa makundi yanayotumia rasilmali ya misitu wanalenga miradi ya makundi yao na hawana nafasi ya kushiriki katika shughuli za pamoja.

Mapendekezo ya shughuli za pamoja• Kujifunza na kubadilishana taarifa kuhusu uhifadhi,

kwa mfano, wanachama wa CFA wanaweza kuwafunza wanachama wa WRUA aina ya miti inayofaa kupandwa huku WRUA wakiwafunza CFA mbinu bora za kuhifadhi maji kama vile kuhifadhi visima na ardhi kando ya mito.

• Kupanda nasari za miche, kugawa miche na kupanda miti katika maeneo ya misitu, maeneo ya chemichemi na kando ya mito.

• Wanachama wa CFA na WRUA kufunzwa pamoja matumizi bora ya maji na misitu.

Mikutano kati ya CFA na WRUA Wakazi walitoa maoni tofauti kuhusu kushiriki katika mikutano. Jamii ya Ogiek walisema hawashiriki katika mikutano wakidai wanabaguliwa na viongozi wa CFA, wanaotoka jamii zingine. Wanawake walisema wanatatizika kuhudhuria mikutano kwa sababu ya kulemewa na kazi za nyumbani. Tena, mikutano hufanyika mbali na makwao.

Viongozi wanawake wa CFA wanapata shida kuhudhuria mikutano kwa sababu hawafahamishwi mapema kuhusu mikutano, mikutano hufanyika mbali na kwao, kubaguliwa na viongozi wanaume. Wanaume walisema wanakosa kuhudhuria mikutano kwa sababu viongozi wa CFA wanapuuza maoni yao, kwa mfano yanayohusiana na utengaji wa ardhi. Baadhi ya wanachama wa WRUA wanaokosa kuhudhuria mikutano walisema wanajishughulisha na shughuli za kujitafutia mahitaji muhimu kama vile chakula.

Ili kuhimiza wanachama zaidi kuhudhuria mikutano, wanachama wa CFA na WRUA walipendekeza viongozi kutangaza tarehe ya mikutano mapema, kutumia mbinu thabiti za mawasiliano kama vile ujumbe kupitia simu (sms), mabango, mabaraza, na kuwatoza faini, wanaokosa kuhudhuria, kulingana na sheria za chama.

Page 4: Mradi wa Minara ya Maji - CIFOR · • Kutambua mashujaa wa jamii kueneza elimu kuhusu majukumu ya wanawake na wanaume. • Kuhakikisha wanawake na wanaume wanajulishwa mapema kuhusu

cifor.org/water-towers forestsnews.cifor.org

Center for International Forestry Research (CIFOR)CIFOR advances human well-being, equity and environmental integrity by conducting innovative research, developing partners’ capacity, and actively engaging in dialogue with all stakeholders to inform policies and practices that affect forests and people. CIFOR is a CGIAR Research Center, and leads the CGIAR Research Program on Forests, Trees and Agroforestry(FTA). Our headquarters are in Bogor, Indonesia, with offices in Nairobi, Kenya; Yaounde, Cameroon and Lima, Peru.

The CGIAR Research Program on Forests, Trees and Agroforestry (FTA) is the world’s largest research for development program to enhance the role of forests, trees and agroforestry in sustainable development and food security and to address climate change. CIFOR leads FTA in partnership with Bioversity International, CATIE, CIRAD, ICRAF, INBAR and TBI.

FTA’s work is supported by the CGIAR Trust Fund.

Mwisho Wanachama wa CFA na WRUA wanafahamu uhusiano kati ya misitu bora na athari kwa thamani na viwango vya maji. Wanatambua kuwa miti asili imepungua, hali ambayo imesababisha matope kujaa mitoni, viwango vya maji kuanguka na maji kubadili rangi. Wanajamii ya Ogiek wanaona utamaduni wao unachangia pakubwa katika uhifadhi wa maji na mazingira. Hakuwa na shughuli za pamoja kati ya wanachama CFA na WRUA kwani kila upande haukujua shughuli wala kuweko kwa upande mwingine. Mchango wa wanawake katika CFA na WRUA bado ni changamoto. Baadhi ya wanachama wa jamii ya Ogiek wanahisi viongozi wa CFA wanawabagua. Viongozi kutowasiliana kwa wakati na wanachama, haswa wanawake ni shida. Ni muhimu kuongeza mafunzo ya uongozi ili kujumuisha wanawake na jamii asili katika kufanya uamuzi, miradi ya kuhifadhi misitu na maji na mikutano kwa jumla.

Mapendekezo • Kutoa mafunzo kuhusu majukumu ya wanawake

na wanaume na vikwazo vinavyozuia wanawake kushiriki.

• Kutambua mashujaa wa jamii kueneza elimu kuhusu majukumu ya wanawake na wanaume.

• Kuhakikisha wanawake na wanaume wanajulishwa mapema kuhusu mahali pa mikutano, tarehe na ajenda ili wapange kuhudhuria.

• Kuwahamasisha zaidi wanachama wa CFA na WRUA kuhusu kusimamia pamoja misitu na maji ili wanachama wa mashirika yote washiriki katika miradi ya kuhifadhi misitu na maji.

• Kuandaa vikao vya mafunzo kati ya wanachama wa CFA na WRUA kuimarisha ushirikiano kati ya mashirika hayo.

• Kuendeleza mikutano kati ya viongozi wa CFA na WRUA kama hatua ya kwanza ya kufikia ushirikiano thabiti.