24
2 FURSA YA MAISHA YAKE. PAMBANO LA MAISHA YAKE. MWONGOZO WA UWEZESHAJI WA FILAMU KUTOKA KWA WATOAJI WA INSIDE STORY

MWONGOZO WA UWEZESHAJI WA FILAMU - The Lucky …luckyspecials.com/wp-content/uploads/2017/09/LuckySpecialsSwahili_2.10.17.pdfMuhtasari wa Mtiririko The Lucky Specials ni bendi ndogo

  • Upload
    others

  • View
    6

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: MWONGOZO WA UWEZESHAJI WA FILAMU - The Lucky …luckyspecials.com/wp-content/uploads/2017/09/LuckySpecialsSwahili_2.10.17.pdfMuhtasari wa Mtiririko The Lucky Specials ni bendi ndogo

2

FURSA YA MAISHA YAKE. PAMBANO LA MAISHA YAKE.

MWONGOZO WA UWEZESHAJI WA FILAMU

K U T O K A K W A W A T O A J I W A I N S I D E S T O R Y

Page 2: MWONGOZO WA UWEZESHAJI WA FILAMU - The Lucky …luckyspecials.com/wp-content/uploads/2017/09/LuckySpecialsSwahili_2.10.17.pdfMuhtasari wa Mtiririko The Lucky Specials ni bendi ndogo

3

Page 3: MWONGOZO WA UWEZESHAJI WA FILAMU - The Lucky …luckyspecials.com/wp-content/uploads/2017/09/LuckySpecialsSwahili_2.10.17.pdfMuhtasari wa Mtiririko The Lucky Specials ni bendi ndogo

1

Utangulizi wa The Lucky Specials 2

Madhumuni na Jumbe Muhimu 3 kwenye Filamu

Malengo ya Mafunzo 3

Muhtasari wa Mtiririko 4

Wahusika Wakuu 6

Vidokezo kwa Wawezeshaji 8

Mawazo ya Kusisimua Mjadala 12

TB: Kweli za Msingi Ambazo Kila 16 Mtu Anahitaji Kujua

TB: Baadhi ya Maneno Muhimu 20

Marejeo kwa Maelezo Zaidi 21

Yaliyomo

Page 4: MWONGOZO WA UWEZESHAJI WA FILAMU - The Lucky …luckyspecials.com/wp-content/uploads/2017/09/LuckySpecialsSwahili_2.10.17.pdfMuhtasari wa Mtiririko The Lucky Specials ni bendi ndogo

2

THE LUCKY SPECIALS NI NINI?

The Lucky Specials ni filamu nzima inayoelimisha watazamaji kuhusu kifua kikuu (TB) huku ikiteka mawazo ya watu kupitia hadithi yenye mtiririko unaovutia. Katika filamu hii “inayoelimisha huku ikiburudisha,” visa vya hadithi na katuni za kisayansi zilizohaishwa zinawaeleza watu wanachohitaji kujua kuhusu ugonjwa, matibabu, na uzuiaji wa kifua kikuu (TB).

Utangulizi wa The Lucky Specials

Ili kuimarisha jumbe za filamu hii na kuhimiza tabia nzuri zinazohusiana na uzuiaji na matibabu ya TB, tunapendekeza kwamba maonyesho kwa jamii yaambatanishwe na mijadala iliyosimamiwa. Tumia mwongozo huu kuwezesha mijadala hiyo.

Mtu yeyote anaweza kupakua filamu hii na mwongozo huu wa uwezeshaji katika lugha ya Kiingereza, Kifaransa, Kireno, na Kiswahili—zote bila malipo—kutoka www.luckyspecials.com.

NI NANI WALIOTENGENEZA THE LUCKY SPECIALS?The Lucky Specials ilitolewa na Discovery Learning Alliance na Quizzical Pictures ikishirikiana na HHMI Tangled Bank Studios—na usaidizi wa Howard Hughes Medical Institute (HHMI), the Wellcome Trust, na USAID na PEPFAR kupitia Mradi wa Uongozi, Usimamizi & Utawala, unaoongozwa na Management Sciences for Health (MSH).

Mwongozo huu uliandikwa na Carla Visser, Nathene Morley, na Carole Douglis.

SHUKRANI NA KANUSHOChapisho hili limefanikishwa na usaidizi wa dhati wa Wakala ya Marekani ya Maendeleo ya Kimataifa (USAID) chini ya Mkataba wa Ushirikiano wa Mradi wa Uongozi, Usimamizi na Utawala, AID-OAA-A-11-00015. Maoni yaliyopo katika chapisho hili si maoni wazi ya USAID au ya Serikali ya Marekani. © The Lucky Specials Productions.

(PTY) LTD MMXVII. Haki zote zimehifadhiwa.

Page 5: MWONGOZO WA UWEZESHAJI WA FILAMU - The Lucky …luckyspecials.com/wp-content/uploads/2017/09/LuckySpecialsSwahili_2.10.17.pdfMuhtasari wa Mtiririko The Lucky Specials ni bendi ndogo

3

The Lucky Specials ina uwezo wa kubadlisha ujuzi, mitazamo, na tabia za umma kuhusiana na TB. Huku ikiwa imeandaliwa Kusini mwa Afrika, filamu hii ni muhimu kwa maeneo mengi yanayokumbwa na changamoto mbalimbali na imeundwa:

• Kuwajulisha watazamaji wote—wanaotazama kila aina ya skrini—kuhusu kweli halisi za sasa za kijamii na kisayansi za TB;

• Kuwapa wafanyakazi wa afya katika viwango vyote, mbinu fanisi ya kuelimishia jamii kuhusu matibabu na uzuiaji wa TB;

• Kuhamasisha ubadilishaji wa tabia za mtu binafsi ili kuhimiza uzuiaji, uchunguzi, upimaji na umezaji wa dawa za TB kikamilifu.

JUMBE MUHIMU• TB ni ugonjwa wa kuambukiza

unaosambazwa kupitia hewa. Si laana. Si upotovu wa nidhamu. Inasababishwa na vimelea (viini). Mtu yeyote anaweza kupata TB.

• TB inatibika ukianza matibabu mapema na ukikamilisha msururu wote wa dawa.

• Hakikisha kwamba wewe na wapendwa wako mmepimwa haraka iwezekanavyo iwapo mmekutana kwa ukaribu na mgonjwa wa TB.

• Hakikisha kwamba umepimwa haraka iwezekanavyo ikiwa unakohoa kwa zaidi ya wiki mbili au ikiwa una dalili zingine za kawaida za TB kama vile kutokwa na jasho usiku, kupunguza uzito, na uchovu.

• Usipomaliza dawa zako za TB, utakuwa katika hatari ya kuambukizwa tena na kuwa mgonjwa hata zaidi, kwa kuwa na TB iliyo sugu kwa dawa. Kufuatia hii, utahitaji matibabu ya muda mrefu yanayohusisha kuingiza vifaa ndani ya mwili.

• TB na VVU ni magonjwa tofauti. Lakini kuwa na VVU kunakuweka katika hatari kubwa zaidi ya kupata TB. Na hali huwa mbaya zaidi ikiwa “umeambukizwa na yote mawili kwa wakati mmoja,” au una magonjwa haya mawili.

Madhumuni na Jumbe Muhimu za Filamu

iKUHUSU FILAMU

Page 6: MWONGOZO WA UWEZESHAJI WA FILAMU - The Lucky …luckyspecials.com/wp-content/uploads/2017/09/LuckySpecialsSwahili_2.10.17.pdfMuhtasari wa Mtiririko The Lucky Specials ni bendi ndogo

4

Muhtasari wa Mtiririko

The Lucky Specials ni bendi ndogo ya muziki wa pop katika mji wa uchimbaji migodi nchini Afrika Kusini. Kiongozi wa bendi Mandla anafanya kazi migodini lakini anapenda sana gita na ana ndoto ya kuwa nyota. Bra Easy—mmiliki wa Kilabu cha Easy na pia mpiga ngoma wa bendi—anamhimiza Mandla na kumfundisha maskandi-gita ya (kisasa ya Kizulu). Mandla anampenda na anavutiwa na mwangalizi na mpwake Bra Easy, Nkanyiso.

Kinachojiri ni kwamba, Bra Easy amekuwa akipuuza dalili za TB kwa muda mrefu. Anazimia akiwa jukwaani na kupelekwa hospitalini. Wakati huo huo, Mandla pia anaonyesha dalili za TB. Wafanyakazi wa hospitalini wanaomba kwamba, marafiki wengine wa karibu wa Mandla na Bra Easy wapimwe. Kwa vile alisikia kwamba TB na VVU huambatana, Mandla anachelewa hadi Nkanyiso anapomhimiza kuenda kupata matokeo yake.

Mandla anatambuliwa kuwa ana TB, lakini hana VVU. Wiki mbili za kwanza za matibabu zinamtatiza—Mandla anatengwa, anahisi kuwa yeye ni mgonjwa, na anatatizika kula na kulala. Nkanyiso anamliwaza na kumsaidia Mandla katika wakati huu, na uhusiano wao unaanza kunawiri. Baada ya kutengwa, anahitajika kuendelea kumeza tembe kwa miezi sita, wakati ambapo hapaswi kuvuta sigara na kunywa pombe. Mandla ana wasiwasi kuhusu kile ambacho watu katika jamii yake wanawaza kuhusu ugonjwa wake, hadi rafikiye, Jose, anapomwambia kwamba, ijapokuwa unyanyapaa ulisababisha atoroke nyumbani nchini Msumbiji, amejifunza kusimamia ugonjwa wake (VVU) na kuishi maisha yenye afya. Hata aliwahi kuwa na TB, ikatibiwa akapona.

Baada ya muda mfupi, Mandla anaanza kuhisi ako sawa. Kwa vile ana nguvu nyingi, anakosa kuvumilia mfumo wa matibabu na anaacha kumeza dawa. Kile ambacho Mandla hajui ni kwamba, viini vya TB vinasalia mwilini mwake, kama ilivyoonyeshwa kwa katuni za kisayansi zilizohaishwa katika filamu.

Page 7: MWONGOZO WA UWEZESHAJI WA FILAMU - The Lucky …luckyspecials.com/wp-content/uploads/2017/09/LuckySpecialsSwahili_2.10.17.pdfMuhtasari wa Mtiririko The Lucky Specials ni bendi ndogo

The Lucky Specials wanapata mpiga ngoma mpya ambaye ni mwimbaji wao wa kike, Zwanga, na wanaanza kusahau kutokuwepo kwa Bra Easy.

Mdhamini wa muziki kutoka Msumbiji anataka kuwekea bendi yao nafasi katika tamasha jijini Maputo. Hata hivyo, Mandla anazimia wakati wa majaribio ya vipawa.

Sasa, Mandla anatambuliwa kuwa ana (MDR) TB ambayo ni TB iliyo sugu kwa dawa nyingi. Wakati huu matibabu ni makali zaidi: analazwa katika hospitali ya MDR TB kwa miezi kadhaa, anapewa dawa zenye nguvu nyingi zaidi zenye athari nyingi za kando, na anadungwa sindano mara kwa mara.

Lazima ameze tembe nyingi kila siku kwa zaidi ya mwaka mmoja. Lakini anapona. Bra Easy, ambaye mapafu yake yameharibiwa kabisa kutokana na ugonjwa huu, anaaga dunia.

Baada ya Mandla kurudi kutoka hospitalini, bendi hii inasafiri kuenda Msumbiji kwa tamasha ile ya muziki. Lakini wanakosa pahali pa kuishi na fursa ya kucheza muziki wao jukwaani. Jose anaipeleka bendi hii kwa nyumba ya wazaziwe, anapoungana upya na familia yake. Mtazamo chanya wa Jose unamkumbusha Mandla kufuata mfumo wa matibabu ya TB, na anamtafuta mfanyakazi wa afya amdunge sindano yake.

Wakati wa mwisho, mwimbaji wa bendi ya headliner katika tamasha ya muziki anakuwa mgonjwa, na The Lucky Specials wanaalikwa wachukue nafasi yao mbele ya umati mkubwa. Umati huu unawapenda, na The Lucky Specials wanapata kandarasi ya kurekodi muziki. Wanatumia malipo yao kuokolea Kilabu cha Easy (walipoanzia), inayokumbwa na shida za kifedha.

iKUHUSU FILAMU

5

Page 8: MWONGOZO WA UWEZESHAJI WA FILAMU - The Lucky …luckyspecials.com/wp-content/uploads/2017/09/LuckySpecialsSwahili_2.10.17.pdfMuhtasari wa Mtiririko The Lucky Specials ni bendi ndogo

6

Mandla

OROS MAMPOFU

Nkanyiso

SIVENATHI MABUYA

Msimuliaji na mhusika mkuu. Mchimbaji mgodi mchana na mwanamuziki usiku, Mandla anapata TB, anaacha matibabu mapema, anapata TB iliyo sugu kwa dawa nyingi, na mwishowe anafuata mfumo mgumu wa matibabu.

Bra Easy

BLONDIE MAKHENE

Mmiliki wa Kilabu cha Easy, mpiga ngoma wa bendi, na mshauri.

Bra Easy ana TB lakini anachagua kutumia dawa za kienyeji. Anapolazwa hospitalini, anasisitiza kwamba Mandla na wanabendi wengine wapimwe.

Bra Easy anaaga dunia kutokana na TB.

Nkanyiso anasimamia Kilabu cha Easy mjombake Bra Easy anapolazwa hospitalini. Anairithi na kuendelea kuisimamia anapoaga dunia.

Page 9: MWONGOZO WA UWEZESHAJI WA FILAMU - The Lucky …luckyspecials.com/wp-content/uploads/2017/09/LuckySpecialsSwahili_2.10.17.pdfMuhtasari wa Mtiririko The Lucky Specials ni bendi ndogo

7

Jose

RICHARD LUKUNKU

Zwanga

FULU MUGOVHANI

Wahusika Wakuu

Mcheza besi wa The Lucky Specials.

Jose anaishi na VVU na amewahi kuwa na TB; anamhimiza Mandla akapimwe.

Zwanga anaanza kama mcheza ngoma na mwimbaji wa The Lucky Specials. Lakini anacheza pia ngoma za kidesturi za Kusini mwa Afrika—na anasaidia kuokoa bendi kwa kuwa mpiga ngoma baada ya Bra Easy kuzirai.

Page 10: MWONGOZO WA UWEZESHAJI WA FILAMU - The Lucky …luckyspecials.com/wp-content/uploads/2017/09/LuckySpecialsSwahili_2.10.17.pdfMuhtasari wa Mtiririko The Lucky Specials ni bendi ndogo

Vidokezo kwa Wawezeshaji

Kama mwezeshaji, kazi yako ni kuimarisha jumbe za afya ya umma kupitia mijadala na kuhusisha walengwa. Huenda ukahitaji kutunga maswali yako kulingana na kila kundi la washiriki, kwa sababu mashaka na viwango vya ujuzi ni tofauti. Kwa mfano, huenda watoa huduma ya afya wanufaike na taarifa tofauti kuliko wanaumma wa kawaida.

NINAPASWA KUJITAYARISHA VIPI? Ndiyo haya mapendekezo yatakayokusaidia kujitayarisha kwa uwezeshaji wa mjadala kuhusu filamu.

• Tazama filamu na upitie mwongozo huu kabla ya hafla husika. Unaweza kuyapakua bila kutozwa malipo kutoka www.luckyspecials.com.

• Pitia jumbe muhimu kwenye ukurasa wa 3. Ikiwa kuna jumbe mahususi zinazohusiana na walengwa wako, zingatia hizo.

• Hakikisha kwamba unaelewa TB—watu wanavyoambukizwa, dalili, upimaji na kutambuliwa kwake, vipengele vya hatari, na matibabu—ya TB ya kawaida na ile iliyo sugu kwa dawa nyingi. Kwa maelezo, angalia ukurasa wa 16 wa mwongozo huu. Hakikisha unaelewa kwa nini wanaoishi na VVU wako katika hatari kubwa ya kupata TB na wanahitaji kupimwa TB mara kwa mara.

• Tafuta huduma za karibu za TB na uwe na uhusiano mzuri na watoa huduma, ili ujue utakapowatuma washiriki walio na dalili. Isitoshe: waalike watoa huduma ili wachunguze na wapime TB papo hapo katika eneo la hafla.

• Fanya utafiti kuhusu takwimu za ndani za TB—idadi gani ya watu, wa umri gani, wana uwezekano wa kuwa na TB katika eneo lako? (Takwimu za kimataifa zinatueleza kwamba takriban thuluthi moja ya watu wameambukizwa TB, ingawa wengi hawatafika katika TB-tendaji yenye dalili.)

8

Page 11: MWONGOZO WA UWEZESHAJI WA FILAMU - The Lucky …luckyspecials.com/wp-content/uploads/2017/09/LuckySpecialsSwahili_2.10.17.pdfMuhtasari wa Mtiririko The Lucky Specials ni bendi ndogo

• Nchi tofauti zina mikakati yao ya TB. Ukipata nafasi, pitia sera za kitaifa za nchi yako kuhusu upimaji na matibabu ya TB.

UNAVYOPASWA KUZINGATIA UNAPOPANGA HAFLA HUSIKAZingatia yafuatayo kabla ya kutangaza hafla yako na kutuma mialiko.

• Je, unaenda kuwa na hafla ya kutazama na kujadiliana itakayotendeka mara moja tu? Au unapanga kuwa na hafla ya kuhudhuriwa mara nyingi? Kulingana na chaguo lako, na wakati mzuri kwa walengwa wako—utaonyesha filamu nzima, au sehemu chache tu za filamu?

• Je, hii itahusisha walioalikwa pekee, au utatangaza—mtandaoni/machapishoni/kwenye mitandao ya kijamii?

• Unda karatasi ya kutiwa saini ya washiriki, yenye jina, taarifa za mawasiliano, na majibu.

• Unda kanuni zitakazofuatwa kabla ya kikao hicho. Kwa mfano, zingatia yafuatayo: Je, simu za mkononi zinapaswa kuzimwa? Lugha ifaayo/chafu ni gani? Je, mshiriki anaweza kuzungumza kwa muda gani? Je, mjadala huu utawekwa siri?

• Zingatia kuanza hafla yako ya kuonyesha filamu na kinachosisimua mazungumzo (angalia mifano ya shughuli kwenye ukurasa wa 12).

TUMIA LUGHA YA HURUMA

Kila neno ni muhimu, hasa unapowezesha/kuhutubia hadhara. Kwenye ukurasa unaofuata kuna baadhi ya maneno ya kawaida ambayo yana mibadala muhimu, pamoja na mibadala inayozingatia watu inayopendelewa na jamii ya walio na TB.

VIDOKEZO

9

Page 12: MWONGOZO WA UWEZESHAJI WA FILAMU - The Lucky …luckyspecials.com/wp-content/uploads/2017/09/LuckySpecialsSwahili_2.10.17.pdfMuhtasari wa Mtiririko The Lucky Specials ni bendi ndogo

LUGHA ISIYOKUBALIKA

BADALA YAKE TUMIA

KWA NINI?

Mshukiwa wa TB

Anayeshukiwa kwamba ana TB

Anayepaswa kuchunguzwa TB

Aliye na dalili za TB

Neno mshukiwa linadokeza kushukiwa na kwamba mtu ana hatia. Neno hili linaweza kuchangia unyanyapaa na lawama kwa kuwa mgonjwa.

Anayeugua TB

Mwathiriwa wa TB

Aliye na TB

Mgonjwa wa TB

Anayeugua na mwathiriwa yanadokeza kutokuwa na nguvu, kana kwamba mhusika hawezi kudhibiti maisha yake.

Aliyeshindwa kumaliza dawa za TB

Mtu ambaye hajamaliza dawa zake za TB

Mtu ambaye hajamaliza matibabu.

Aliyeshindwa kumaliza dawa ni neno lingine linalodokeza lawama kwa mhusika. Kukatizika kwa matibabu mara nyingi husababishwa na huduma duni za afya kuliko makosa ya mhusika.

Utiifu/kutotii Ufuataji utaratibu

Mgonjwa ambaye amemaliza matibabu

Kutotii pia kunadokeza lawama kwa mgonjwa.

Kokteli ya dawa Dawa Wakati wagonjwa kwa kawaida humeza dawa zaidi ya moja, kokteli inaonekana kudunisha athari kali za kando zinazohusika hasa na matibabu ya MDR TB.

Kudhibiti TB Uzuiaji TB na huduma husika

Udhibiti wa TB linadokeza kwamba wataalamu wana nguvu juu ya vipengele vyote vya uzuiaji, matibabu, na huduma. Inapuuza jitihada kubwa za jamii na watu binafsi walio na TB.

10

Page 13: MWONGOZO WA UWEZESHAJI WA FILAMU - The Lucky …luckyspecials.com/wp-content/uploads/2017/09/LuckySpecialsSwahili_2.10.17.pdfMuhtasari wa Mtiririko The Lucky Specials ni bendi ndogo

VIDOKEZO KWA WAWEZESHAJI WAPYA• Kumbuka kwamba unaongoza mjadala—

huku ukiwahimiza watu washiriki ili wafikirie kwa kina kuhusu filamu na jumbe zake.

• Usihadhiri au kutoa maoni yako. Uliza watazamaji maoni yao, na uhakikishe kwamba unasikiliza zaidi kuliko unavyoongea.

• Mtu asipotaja ujumbe mkuu, endelea kuuliza. Ikiwa baada ya ufafanuzi, ujumbe mkuu bado haujazungumzwa, unaweza kuupeana wewe mwenyewe.

• Saidia watazamaji walinganishe filamu na maisha yao wenyewe: “Je, unafikiri kwamba ungefanya nini?” “Je, unajua yeyote katika maisha yako ambaye anaweza kufanya hivyo?”

• Jaribu kumhimiza kila mtu azungumze ikiwa kundi si kubwa sana. Ikiwa mmoja au wawili wanazungumza sana, waambie kwamba wana hoja nzuri, na ungependa kuwapa wengine nafasi wazungumze. Kwa wale walionyamaza, sema kitu kama, “Kwa wale ambao hatujapata maoni yao, tungependa kujua mnachofikiria.”

• Himiza kila mtu. Inapofaa, hakikisha umesema kwamba, “Hiyo ni hoja nzuri.” “Hilo ni swali nzuri.”

• Himiza washiriki wako wajibu maswali yako na wajadiliane wenyewe kwa wenyewe pia.

• Uliza ikiwa yeyote kati ya watazamaji amewahi kuwa na, au anajua mtu ambaye amewahi kuwa na, TB. Je, hali yao ilikuwa sawa au tofauti na ya Mandla kivipi? Ni nini ambacho wewe au rafikiyo angefanya vitofauti?

LUGHA ISIYOKUBALIKA

BADALA YAKE TUMIA

KWA NINI?

Mshukiwa wa TB

Anayeshukiwa kwamba ana TB

Anayepaswa kuchunguzwa TB

Aliye na dalili za TB

Neno mshukiwa linadokeza kushukiwa na kwamba mtu ana hatia. Neno hili linaweza kuchangia unyanyapaa na lawama kwa kuwa mgonjwa.

Anayeugua TB

Mwathiriwa wa TB

Aliye na TB

Mgonjwa wa TB

Anayeugua na mwathiriwa yanadokeza kutokuwa na nguvu, kana kwamba mhusika hawezi kudhibiti maisha yake.

Aliyeshindwa kumaliza dawa za TB

Mtu ambaye hajamaliza dawa zake za TB

Mtu ambaye hajamaliza matibabu.

Aliyeshindwa kumaliza dawa ni neno lingine linalodokeza lawama kwa mhusika. Kukatizika kwa matibabu mara nyingi husababishwa na huduma duni za afya kuliko makosa ya mhusika.

Utiifu/kutotii Ufuataji utaratibu

Mgonjwa ambaye amemaliza matibabu

Kutotii pia kunadokeza lawama kwa mgonjwa.

Kokteli ya dawa Dawa Wakati wagonjwa kwa kawaida humeza dawa zaidi ya moja, kokteli inaonekana kudunisha athari kali za kando zinazohusika hasa na matibabu ya MDR TB.

Kudhibiti TB Uzuiaji TB na huduma husika

Udhibiti wa TB linadokeza kwamba wataalamu wana nguvu juu ya vipengele vyote vya uzuiaji, matibabu, na huduma. Inapuuza jitihada kubwa za jamii na watu binafsi walio na TB.

VIDOKEZO

11

Page 14: MWONGOZO WA UWEZESHAJI WA FILAMU - The Lucky …luckyspecials.com/wp-content/uploads/2017/09/LuckySpecialsSwahili_2.10.17.pdfMuhtasari wa Mtiririko The Lucky Specials ni bendi ndogo

Mawazo ya Kusisimua Mjadala

Kuna njia nyingi za kusisimua na kuendeleza mjadala. Kuwa na uhuru wa kutumia yafuatayo na/au mawazo yako mwenyewe.

MFANO WA SHUGHULI: HADITHI AU UKWELI?

Soma ukweli au hadithi kuhusu TB na uliruhusu kundi liseme iwapo ni UKWELI au HADITHI TU. Uliza watazamaji waeleze kwa nini kila kauli ni ukweli au hadithi tu—huku ukirekebisha ipasavyo na kusema kweli husika ipasavyo. Ndiyo hii mifano michache inayoweza kutumiwa katika zoezi hilo

12

Page 15: MWONGOZO WA UWEZESHAJI WA FILAMU - The Lucky …luckyspecials.com/wp-content/uploads/2017/09/LuckySpecialsSwahili_2.10.17.pdfMuhtasari wa Mtiririko The Lucky Specials ni bendi ndogo

MJADALA

13

HADITHI TU KWELI

TB ni laana au adhabu kutoka kwa Mungu au wahenga.

TB ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea (viini) vinavyosafiri hewani watu wanapokohoa. Mtu yeyote anaweza kuupata, bila kujali hao ni nani.

TB haiwezi kutibiwa.Watu walio na TB wanaweza kutibiwa wakapona! Lakini lazima waanze matibabu mapema iwezekanavyo, na kumaliza matibabu yote yaliyoagizwa na daktari wao.

Ikiwa una TB, una VVU pia.

Ni ukweli kwamba anayeishi na VVU ako katika hatari kubwa ya TB kukolea kwake kwa sababu mfumo wao wa kinga umeharibiwa. Lakini TB na VVU ni magonjwa mawili tofauti, na unaweza kuwa na mmoja bila huo mwingine kuwepo.

Walio na VVU/maskini/wenye lishe duni/wanaofanya kazi migodini pekee ndio wanaoweza kupata TB.

Mtu yeyote anaweza kupata TB. Kwa kweli, mtu mmoja kati ya watatu ulimwenguni ana viini vya TB mwilini mwao—ijapokuwa wengi huwa hawana dalili, kama vile kukohoa.

TB inaweza kusambazwa kwa kushiriki chakula au kinywaji, au kupitia busu.

TB ni ugonjwa unaosambazwa hewani, kama mafua au homa ya kawaida. TB haisambazwi kupitia kugusana kimwili au kushiriki chakula.

Kila mtu aliye na TB anapaswa kutengwa.

Mtu anapotambuliwa kuwa ana ugonjwa wa TB tendaji, yeye anapaswa kubaki nyumbani kwa wiki mbili za kwanza za matibabu ili kupunguza kukutana na watu anapoweza kuwaambukiza. Baada ya hapo, huwa hawawezi kuwaambukiza watu—bora tu wamalize matibabu.

Unaweza kuacha kumeza dawa pindi tu unapohisi kwamba uko sawa.

Lazima ukamilishe msurusu kamili wa matibabu ili upone kabisa. Usipofanya hivyo, unaweza kupata TB iliyo sugu kwa dawa, ambayo ni ngumu sana kutibu.

Waponyaji wa kienyeji wanaweza kutibu TB bila viuavijasumu.

Baadhi ya dawa za kienyeji zinaweza kusaidia kutibu dalili za TB (kama vile kukohoa), lakini ni viuavijasumu pekee ndivyo vinavyoweza kutibu TB hadi mtu apone, na wagonjwa huwa wanahitaji kumeza aina mbili au zaidi pamoja.

Page 16: MWONGOZO WA UWEZESHAJI WA FILAMU - The Lucky …luckyspecials.com/wp-content/uploads/2017/09/LuckySpecialsSwahili_2.10.17.pdfMuhtasari wa Mtiririko The Lucky Specials ni bendi ndogo

Je, Mandla alipataje TB?• Bra Easy alikuwa na TB—tendaji na

alimsambazia Mandla ugonjwa huo, ingawa hakufanya hivyo kimaksudi.

• Bra Easy hakujua kwamba alikuwa na TB kwa muda mrefu kwa sababu alikataa kuzuru kliniki ili apimwe.

Je, Mandla alipataje MDR TB? • Baada ya muda, Mandla alihisi kwamba ako

sawa na akakosa kusubiri dawa zake zijazwe, kwa hivyo aliacha kumeza tembe zake.

• Viini vya TB vilibaki mwilini mwake, na vile vilivyokuwa vimebaki ndivyo vilivyokuwa vinavyoweza kuwa sugu kabisa kwa matibabu. Pindi Mandla alipoacha matibabu, viini hivi vilianza kuongezeka na kutawala.

Ni vipengele vipi vya hatari ambavyo vingeweza kuchangia maambukizi ya TB ya Mandla na Bra Easy? • Mandla alikuwa anafanya kazi mgodini,

ambapo alikuwa anafikiwa na vumbi ya silica inayoharibu mapafu (vumbi kutoka kwa miamba na madini). Pia, alikaa pahali ambapo hapakuwa na uingizaji hewa ya kutosha na Bra Easy, ambaye alikuwa na TB.

• Bra Easy alikuwa mkongwe ambaye alikuwa anavuta sigara na kunywa pombe sana. Badala ya kutafuta matibabu kutoka kwa madaktari, alitegemea suluhu za kienyeji kama vile muti, iliyosaidia kupunguza kikohozi chake lakini haingeweza kutibu maambukizi hayo.

Ni nini ambacho wagonjwa, muuguzi, marafiki wa Mandla, na wengine waliokuwa katika kliniki/nyumba/kilabu walifanya ili kujilinda?

• Barakoa na madirisha wazi: Wauguzi na madaktari klinikini walivalia barakoa zilizofunika midomo na mapua yao ili waepuke kupumua vimelea vya TB. Wagonjwa wa TB—Bra Easy na Mandla—pia walivalia barakoa walipokuwa wamelazwa hospitalini ili wasisambaze vimelea hivyo. Nkanyiso alipomtembelea Mandla nyumbani mwake, alivalia barakoa na akafungua madirisha ya chumba cha Mandla

MASWALI YA MOJA KWA MOJA, NA MAJIBU YALIYOPENDEKEZWA Tena, waruhusu washiriki wajibu na kujadiliana miongoni mwao wenyewe.

Unaweza kupeana majibu yaliyoko hapa chini ikiwa hakuna atakayeyasema, au uyasisitize utakavyo.

14

Page 17: MWONGOZO WA UWEZESHAJI WA FILAMU - The Lucky …luckyspecials.com/wp-content/uploads/2017/09/LuckySpecialsSwahili_2.10.17.pdfMuhtasari wa Mtiririko The Lucky Specials ni bendi ndogo

alipomtembelea. Mandla alipopokea wageni katika kituo cha MDR, alikutana nao nje kwenye bustani.

• Kutafuta walio karibu: Madaktari walipotambua ugonjwa wa Bra Easy, waliwashauri walio karibu naye (wanafamilia na marafiki) wapimwe TB.

• Utengaji uambukizaji unapowezekana: Mandla alipoanza matibabu ya TB kwa mara ya kwanza, alikaa katika chumba chake kwa wiki mbili ili wengine wasiambukizwe TB. Mandla alipoingia katika hospitali ya MDR TB, alikaa katika hospitali hiyo kwa miezi miwili wakati ugonjwa huo ulikuwa unaweza kuambukizika. Bra Easy alitoka hospitalini na kurudi nyumbani baada ya ugonjwa wake kuwa usioweza kuambukizika tu.

Ni nini kilichomfanya Mandla atatizike kufuata matibabu yake? • Ilibidi Mandla ajitenge kwa wiki mbili

mwanzoni mwa matibabu yake. Alipitia athari za kando—kichefuchefu, kukosa hamu ya kula, na udhaifu.

• Mandla anaishi pekee yake na hana wanafamilia au marafiki wengi wa karibu ambao wangeweza kumsaidia na matibabu yake. Hakutafuta msaada wa marafiki wengine kwa sababu aliogopa unyanyapaa.

• Baada ya kuhisi vizuri kidogo, alikuwa na pupa ya kuendelea na maisha yake, na hakutaka kusubiri kwenye foleni klinikini.

Je, ni mafunzo gani ambayo Mandla alijifunza kutokana na hali ya Jose? • Jose anaishi na VVU na anachagua

kuwajibikia afya yake. Yeye anakula vizuri, anafanya mazoezi, anachukua matibabu yake ya ARV, na anaepuka mihadarati na pombe. Kutoka kwake, Mandla anajifunza kwamba unaweza kusimamia ugonjwa bila aibu. Na kwamba kulinda afya yako mwenyewe ni zawadi kwa wapendwa wako pia.

• Jose pia alishiriki kwamba aliwahi kuwa na TB lakini alipambana nayo na akashinda—hata walio na VVU wanaweza kutibiwa hadi wakapona TB.

MASWALI MENGINE UNAYOWEZA KUULIZA:

• Je, bendi ingefaulu bila Zwanga?

• Je, kilabu ingefanikiwa bila mpwake Bra Easy Nkanyiso?

• Je, ni nini kilichokushangaza zaidi katika filamu hii?

• Je, ni taarifa gani katika filamu hii ilikuwa tofauti na ulichofikiri hapo awali kuhusu TB?

• Je, UTAFANYA nini ukianza kukohoa sana na kutokwa na jasho usiku?

• Je, unaweza kufanyia familia yako nini ukipata TB?

MJADALA

15

Page 18: MWONGOZO WA UWEZESHAJI WA FILAMU - The Lucky …luckyspecials.com/wp-content/uploads/2017/09/LuckySpecialsSwahili_2.10.17.pdfMuhtasari wa Mtiririko The Lucky Specials ni bendi ndogo

TB: Kweli za Msingi Ambazo Kila Mtu Anahitaji Kujua

Kifua Kikuu ni ugonjwa mbaya lakini unaoweza kutibiwa unaosambazwa kupitia hewa, unaosababishwa na vimelea—(Mycobacterium tuberculosis). Vimelea vya TB kwa kawaida huvamia mapafu (TB ya mapafu), lakini vinaweza kuharibu sehemu zingine za mwili, ikiwemo ubongo, figo, na uti wa mgongo. Watu wengi huishi na TB fiche, au bwete, miilini mwao. Kwa kweli, Shirika la Afya Duniani linakadiri kwamba thuluthi moja ya watu wote duniani wana TB fiche. Lakini ni baadhi ya watu tu ambao hufika katika hali ya TB tendaji—kile tunachofikiri tunaposema kwamba mtu “ana TB.”

MZUNGUKO WA MAISHA YA TB

Hatua ya Kwanza: TB inasambaa kupitia hewa kama tu mafua ya kawaida Mtu aliye na ugonjwa wa TB anapokohoa, au kupumua, matone yasiyoweza kuonekana yenye vimelea vya TB hupaa hewani na yanaweza kukawia hapo kwa saa kadhaa. Watu wengine wakipumua ndani matone haya, wanaweza kuambukizwa. Wanafamilia, marafiki, na wafanyakazi wenza—walio karibu nawe—wana uwezekano mkubwa wa kuambukizwa.

Hatua ya Pili: Maambukizi ya TB fiche Watu wengi walioambukizwa TB hawatahisi kwamba hao ni wagonjwa kwa sababu mfumo wa kinga wenye afya huwa unaweza kupambana na vimelea hivi. Katika TB fiche, vimelea hukawia mwilini lakini huwa vinakuwa bwete, au tuli. Watu walio na maambukizi ya TB fiche huwa hawana dalili—na hawawezi kuambukiza wengine. Kipimo cha ngozi au damu kinaweza kudhihirisha maambukizi ya TB fiche. Walio na TB fiche baada yake hufanyiwa vipimo zaidi ili kuona ikiwa wana TB tendaji. Hata ikiwa hawana, walio na TB fiche wanapaswa kuanza matibabu ya kuondoa vimelea hivyo kabisa.

Hatua ya Tatu: Ugonjwa wa TB tendaji TB tendaji, tunayoona Mandla na Bra Easy wakiwa nayo, hutokea wakati mfumo wa kinga hauwezi kudhibiti vimelea vya TB. Vimelea bwete “huamka” na kuanza kuongezeka, huku zikiharibu mapafu na viungo vingine. Watu wengine huwa na TB tendaji mara tu baada ya kuambukizwa. Watu wengine wanaweza kutoonyesha dalili kwa miaka au hata miongo. Ugonjwa mwingine, au uvutaji, au pengine mawazo mengi au uchovu unaweza kuchochea badiliko kutoka maambukizi fiche hadi ugonjwa wa TB tendaji.

KUMBUKA: TB INASAMBAZWA KUPITIA HEWA, BALI SIO KWA MGUSANO WA KIMWILI KAMA VILE:

• Kusalimiana kwa mikono• Kushiriki chakula na kinywaji

• Kushiriki mswaki• Kugusa matandiko au kushiriki bafu

• Kumbusu mtu • Kushiriki ngono

16

Page 19: MWONGOZO WA UWEZESHAJI WA FILAMU - The Lucky …luckyspecials.com/wp-content/uploads/2017/09/LuckySpecialsSwahili_2.10.17.pdfMuhtasari wa Mtiririko The Lucky Specials ni bendi ndogo

Mtu aliye na ugonjwa wa TB tendaji kwa kawaida huhisi kwamba ako mgonjwa na huonyesha dalili. Yeye anaweza kuwaambukiza wengi wengine kabla, na baada ya muda mfupi wa, kuanza matibabu. Bila matibabu kamili, aliye na TB tendaji atakuwa mgonjwa mahututi na huenda aage dunia.

VIPENGELE VYA HATARI

Mtu yeyote anaweza kupata TB, ingawa watu wengine wako katika hatari kubwa. Vipengele vya hatari vinajumuisha: • Kukaribiana na aliye na ugonjwa wa

TB tendaji • Uvutaji • Lishe duni• Maeneo yasiyo na uingizaji wa hewa ya

kutosha, yaliyojaa watu (jela, migodi, kambi la jeshi, na shule za bweni)

• Magonjwa ikiwemo VVU na kisukari

Isitoshe, baadhi ya makundi ya umri na kazi ziko katika hatari kubwa: • Wakongwe na watoto wenye umri wa

chini ya miaka mitano, wenye mifumo ya kinga iliyodhoofika au ambayo haijakomaa;

• Watoto waliozaliwa na wanawake wajawazito walio na ugonjwa wa TB tendaji (Watoto hawa huenda wazaliwe kabla ya wakati wao, huenda wawe na uzito mdogo wa kuzaliwa, na wako katika hatari ya kupata TB muda mfupi tu baada ya kuzaliwa.);

• Wachimba migodi, ambao hupumua ndani vumbi ya silica—vumbi itokayo kwenye miamba na madini—wanapofanya kazi. Baada ya muda, vumbi ya silica huharibu mapafu, na kuzidisha hatari ya TB;

• Wahudumu wa afya wanaokaribiana na wagonjwa wa TB;

• Wahamiaji, ambao huenda watatizike kupata matibabu;

• Wafungwa na wafanyakazi wa jela, wanaoishi na kufanya kazi pamoja katika maeneo yaliyofungwa, yasiyo na huduma ya afya ya kutosha na yenye watu wengi.

DALILI

Dalili za ugonjwa wa TB zinaweza kuwa zifuatazo: • Kukosa hamu ya kula

• Maumivu kifuani

• Uchovu na udhaifu

• Jasho na joto usiku

• Kikohozi kilichokithiri (kwa wiki mbili au zaidi, au kwa muda wowote ikiwa mhusika ana VVU). Kukohoa damu ni dalili ya ugonjwa wa TB uliokomaa.

• Kupunguza uzito

Dalili zinaweza kuwa tofauti katika watoto. Kwa mfano, watoto wadogo huenda wasiwe na kikohozi kilichokithiri, lakini wawe na mgongo wenye kasoro na wakose kustawi. Katika watoto na hata watu wazima, dalili za TB zinaweza kubakia kuwa kidogo kwa miezi mingi—lakini upimaji unapaswa kufanywa haraka iwezekanavyo.

KWELI KUHUSU TB

17

Page 20: MWONGOZO WA UWEZESHAJI WA FILAMU - The Lucky …luckyspecials.com/wp-content/uploads/2017/09/LuckySpecialsSwahili_2.10.17.pdfMuhtasari wa Mtiririko The Lucky Specials ni bendi ndogo

UTAMBUZI NA MATIBABU• Ikiwa una dalili za TB au umekaribiana

sana na mtu aliye nazo, kimbia SASA HIVI hadi klinikini ili upimwe TB. Utambuzi na matibabu ya mapema yanaweza kukuzuia kuwa mgonjwa kabisa. Muhimu pia ni kwamba, itakuzuia kusambazia wanafamilia na marafiki ugonjwa huu.

• Klinikini, muuguzi atauliza maswali kuhusu dalili zako, kisha atachukua sampuli ya kohozi ya kupelekwa maabarani. Kohozi ni balaghamu (kamasi) iliyokoholewa kutoka ndani kabisa mwa mapafu.

• Kuna uwezekano mkubwa kwamba muuguzi atakuomba upimwe VVU. VVU hudhoofisha mfumo wa kinga, inayokufanya uwe katika hatari kubwa ya kupata TB na magonjwa mengine. Kuwa na TB HAKUMAANISHI kwamba una VVU. Lakini unahitaji kujua hali yako ili upate matibabu bora zaidi.

• Wataalamu wa maabarani wakipata vimelea vya TB kwenye kohozi lako, utaagiziwa tembe za ugonjwa huo, na labda tembe zingine za athari za kando. Unahitaji kumeza dawa zako zote kila siku, na kwa muda wote ambao wahudumu wa afya wamependekeza, ili kuhakikisha kwamba vimelea vimekwisha kabisa. Usipofanya hivyo, unaweza kupata TB iliyo sugu kwa dawa kama alivyopata Mandla.

MDR AND XDR TBMgonjwa akipata TB ILIYO SUGU KWA DAWA NYINGI (MDR TB), kama alivyopata Mandla katika filamu, vimelea vilivyoko mwilini mwake haviwezi kuuliwa kamwe na viuavijasumu viwili ambavyo kwa kawaida hutumiwa kutibu TB—isoniazid (INH) na rifampicin (RIF). Aina hii ya ugonjwa ni ngumu na ghali kutibu ikilinganishwa na TB ya kawaida (inayoaangamizwa kwa urahisi na dawa) na inahitaji matibabu ya hadi miaka miwili ukitumia dawa nyingi. Pamoja na tembe, wagonjwa hudungwa sindano nyingi na hutengwa katika kituo

WAGONJWA WA TB LAZIMA WAMALIZE DAWA ZOTE!

Wagonjwa wakimeza dawa zote kama ilivyoagizwa, kwa kawaida huwa wanapona. Wasipomaliza dawa—wakikosa dozi fulani au wakiacha matibabu mapema—wanaweza kuwa wagonjwa tena na kuwasambazia wengine TB. Pia, wanaweza kupata TB iliyo sugu kwa dawa nyingi, ambayo ni ngumu sana kutibu.

18

Page 21: MWONGOZO WA UWEZESHAJI WA FILAMU - The Lucky …luckyspecials.com/wp-content/uploads/2017/09/LuckySpecialsSwahili_2.10.17.pdfMuhtasari wa Mtiririko The Lucky Specials ni bendi ndogo

UHUSIANO KATI YA TB NA VVU NI GANI?

TB na VVU ni magonjwa mawili tofauti. Hata hivyo, VVU huathiri mfumo wa kinga, na kumfanya aliye na VVU kuwa katika hatari kubwa ya kupata TB tendaji, au kuwa na “virusi zaidi ya moja.” TB haikuzidishii hatari ya kuambukizwa VVU. Hata hivyo, kwa vile mfumo wa kinga wenye afya kwa kawaida huweza kupambana na TB, kuwa na TB kunaweza kuwa ishara kwamba mtu anaishi na VVU pia. Leo, watu wengi zaidi kote duniani wanakufa kutokana na TB kuliko VVU, na mara nyingi ni TB ndiyo hatimaye husababisha kifo cha watu wengi wanaoishi na VVU.

Ni muhimu kukumbuka kwamba sio kila mtu anayeishi na VVU ana TB tendaji, na kinyume chake.

cha matibabu ya MDR kwa miezi mingi. Wagonjwa wa MDR TB pia wanaweza kuwasambazia wengine walio karibu nao MDR TB, kama vile tu TB ya kawaida isiyo sugu kwa dawa.

KIFUA KIKUU KILICHO SUGU KABISA KWA DAWA (XDR TB) ni aina ya TB ambayo ni sugu kwa angalau dawa nne kuu za TB. Walio na XDR TB huhitaji matibabu makali ya miaka miwili yatumiayo dawa na ndiyo aina ya TB ipeanayo changamoto kubwa sana unapoitibu.

UNAWEZA KUZUIA KUSAMBAA KWA TB Njia muhimu zaidi ya kukomesha kusambaa kwa TB ni wagonjwa wa TB kufunika mdomo na pua lao wanapokohoa na kumeza dawa zote za TB ilivyoagizwa kikamilifu. Njia zingine za kuzuia TB:

• Kuwa na afya njema iwezekanavyo. Kula vyakula vyenye rutubishi, ikiwemo protini na mboga nyingi. Fanya mazoezi na udumishe usafi. Epuka kuvuta sigara, mihadarati, na kunywa pombe sana.

• Saidia unaowajua wanaopokea matibabu ya TB. Wahimize wafuate utaratibu wa dawa zao hata kama wanapitia athari za kando na hata kama wanahisi vyema.

• Walio katika hatari kubwa ya kuambukizwa TB lazima wapimwe kila mwaka. Wanafamilia na marafiki wote wa wagonjwa walio na ugonjwa wa TB tendaji lazima wapimwe TB.

• Ikiwa unaanza matibabu, epuka kukaribiana na watoto wadogo, wakongwe, au watu wengine wanaoweza kuwa na mifumo dhaifu ya kinga. Watu hawa wako katika hatari kubwa ya maambukizi ya vimelea.

KWELI KUHUSU TB

19

Page 22: MWONGOZO WA UWEZESHAJI WA FILAMU - The Lucky …luckyspecials.com/wp-content/uploads/2017/09/LuckySpecialsSwahili_2.10.17.pdfMuhtasari wa Mtiririko The Lucky Specials ni bendi ndogo

Tiba ya kupunguza makali ya VVU (ART)

Matumizi ya dawa za aina fulani (dawa za kupunguza makali ya VVU) kutibu maambukizi ya VVU; Lazima umezee ART katika maisha yako yote.

Kifua kikuu kilicho sugu kabisa kwa dawa (XDR TB)

XDR TB ni aina nadra ya TB iliyo sugu kwa karibu dawa zote na kwa hivyo ni ngumu sana kutibu.

Mfumo wa kinga

Sehemu ya mwili wako inayokulinda kwa kupambana na viini; ikiwa mfumo wako wa kinga ni dhaifu kutokana na VVU au sababu zingine, una uwezekanao mkubwa wa kuambukizwa TB.

Maambukizi ya TB Fiche

Hali ambayo umeambukizwa vimelea vya TB na unavyo mwilini mwako, lakini havikuuguzi; walio na maambukizi ya TB fiche hawana dalili. Hawawezi kusambaza vimelea vya TB kwa wengine, lakini wanapaswa kutibiwa au wawe katika hatari ya kuwa na ugonjwa wa TB tendaji baadaye.

Kifua kikuu kilicho sugu kwa dawa nyingi (MDR TB)

Ni ugonjwa wa TB unaosababishwa na aina ya vimelea vya TB ulio sugu kwa angalau dawa mbili za TB zinazotumiwa sana: isoniazid (INH) na rifampicin (RIF).

Kohozi

Balaghamu (kamasi) iliyokoholewa kutoka ndani kabisa mwa mapafu. Wataalamu wa maabarani hutafuta vimelea vya TB kwenye kohozi, kwa darubini au zana zingine, ili kutambua TB.

Unyanyapaa

Unyanyapa ni chuki bila sababu kwa kikundi fulani cha watu. Walio na TB (na pia VVU) hubaguliwa mara nyingi kwa sababu wengine hawaelewi ugonjwa huo na wanaogopa.

Ugonjwa wa TB (Ugonjwa wa TB Tendaji)

Ugonjwa ambao vimelea vya TB huongezeka na kushambulia sehemu fulani ya mwili, kwa kawaida mapafu lakini sio daima. Dalili za TB tendaji zinajumuisha udhaifu, kupunguza uzito, joto, kupoteza hamu ya kula, na kutokwa na jasho usiku. Dalili zingine za ugonjwa wa TB hulingana na sehemu ya maambukizi: ikiwa ugonjwa wa TB upo kwenye mapafu (TB ya mapafu), dalili zinaweza kuwa kikohozi kibaya kinachodumu zaidi ya wiki mbili, maumivu kifuani, na kukohoa damu.

Baadhi ya Maneno Muhimu

20

Page 23: MWONGOZO WA UWEZESHAJI WA FILAMU - The Lucky …luckyspecials.com/wp-content/uploads/2017/09/LuckySpecialsSwahili_2.10.17.pdfMuhtasari wa Mtiririko The Lucky Specials ni bendi ndogo

Centers for Disease Control and Prevention (CDC): http://www.cdc.gov/tb/default.htm

• CDC MDR TB fact sheet: http://www.cdc.gov/tb/publications/factsheets/drtb/mdrtb.htm

The National Institute for Communicable Diseases (Division of the National Health Laboratory Service), South Africa

• TB information: http://www.nicd.ac.za/?page=tuberculosis&id=17• TB resources: http://www.nicd.ac.za/?page=tb_resources&id=220

The Stop TB Partnership

• United to End TB—Every Word Counts: http://www.stoptb.org/assets/documents/resources/publications/acsm/LanguageGuide_ForWeb20131110.pdf

World Health Organization (WHO): http://who.int/tb/en/

• Global Tuberculosis Report 2016: http://www.who.int/tb/publications/global_report/en/

• Tuberculosis in Mozambique: http://www.who.int/countries/moz/areas/tuberculosis/en/

• WHO End TB Strategy, http://www.who.int/tb/post2015_strategy/en/• WHO Tuberculosis Fact Sheet N°104, updated October 2016 http://

www.who.int/mediacentre/factsheets/fs104/en/

Marejeo mengine ya tovuti:

• TBfacts.org, TB in South Africa: http://www.tbfacts.org/tb-statistics-south-africa/

iMAREJEO

21

Marejeo kwa Maelezo Zaidi

Page 24: MWONGOZO WA UWEZESHAJI WA FILAMU - The Lucky …luckyspecials.com/wp-content/uploads/2017/09/LuckySpecialsSwahili_2.10.17.pdfMuhtasari wa Mtiririko The Lucky Specials ni bendi ndogo

1

K U T O K A K W A W A T O A J I W A I N S I D E S T O R Y

FURSA YA MAISHA YAKE. PAMBANO LA MAISHA YAKE.

© The Lucky Specials Productions (PTY) LTD MMXVII. Haki zote zimehifadhiwa.

The Lucky Specials ni bendi ndogo ya muziki katika

mji wa uchimbaji mgodi kusini mwa Afrika. Mandla

(Oros Mampofu) anafanya kazi kama mchimbaji

mgodi mchana, lakini anapenda sana kucheza gita

na ana ndoto za kufanikiwa pakubwa katika ulingo

wa muziki.

Janga linapowakumba, Mandla, rafikiye Nkanyiso

(Sivenathi Mabuya) na bendi nzima lazima wajizatiti

ili wafanikishe ndoto zao. Huku kifua kikuu kikitishia

kuvunja bendi yao, je, watapata njia ya kuzindua aina

yao mpya ya muziki wa Kiafrika?