23
Utamaduni, Sanaa na Michezo TOLEO NA.5 TOLEO LA JUNI 2017 NCHI YETU Jarida la Mtandaoni Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO www.maelezo.go.tz TANZANIA YA VIWANDA HII HAPA JPM Azindua Viwanda Vitano, Vyaajiri Zaidi ya Watu 900 Kiwanda cha Sharubati Chatoa Soko kwa Wakulima 30,000

NCHI YETU...Uzinduzi wa viwanda hivyo ni muendelezo wa kutekeleza ahadi yake aliyoitoa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 wa kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa nchi ya

  • Upload
    others

  • View
    8

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

  • Utamaduni, Sanaa na Michezo

    TOLEO NA.5 TOLEO LA JUNI 2017

    NCHI YETUJarida la Mtandaoni

    Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO

    www.maelezo.go.tz

    TANZANIA YA VIWANDA HII HAPAJPM Azindua Viwanda Vitano, Vyaajiri Zaidi ya Watu 900

    Kiwanda cha Sharubati Chatoa Soko kwa Wakulima 30,000

  • i

    Bodi ya Uhariri

    Idara ya Habari-MAELEZOS.L.P 8031

    Dar es Salaam-TanzaniaSimu : (+255) 22 -2122771

    Baruapepe:[email protected]: blog.maelezo.go.tz

    Rodney ThadeusJohn LukuwiElias MalimaJovina BujuluLilian Lundo

    MwenyekitiDkt. Hassan Abbasi

    Msanifu JaridaHassan Silayo

    Wajumbe

    Jarida hili hutolewa na:

    Mkurugenzi-Idara ya Habari-MAELEZO

    1.Kuuza picha za Viongozi wa Taifa na matukio muhimu ya Serikali.

    2.Kusajili Magazeti pamoja na Majarida3.Kukodisha ukumbi kwa ajili ya mikutano na Waandishi

    wa Habari.4.Rejea ya Magazeti na Picha za Zamani5.Kupokea kero mbalimbali za wananchi.

    Huduma zitolewazo MAELEZO

    Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO

  • ii

    TANZANIA YA VIWANDA, MKOA WA PWANI UMEONESHA NJIA

    TAHARIRI

    Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO

    Mwezi Juni mwaka huu, karata nyingine ya Mhe. John Pombe Magufuli ilichangwa na kwa wale weledi wa mchezo wa karata wanaweza kusema alilamba dume. Hii imedhihirika pale alipofanya ziara ya siku tatu katika mkoa wa Pwani na kuzindua viwanda vikubwa vitano ambapo alisema mkoa huo una zaidi ya viwanda 127 jambo ambalo kama angevitembelea vyote hata mwaka mmoja usingetosha kuvikagua.

    Kipindi cha kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Mhe. Magufuli aliwaomba wananchi wamchague na wamuamini kwani anadhamiria ya dhati kuitoa nchi katika lindi la umasikini na kuipeleka katika uchumi wa kati unaojengwa na ukuaji wa viwanda. Jambo hili limeanza kudhihirika.

    Mbali na ahadi hiyo, ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi CCM sura ya pili ibara za 32 na 33 zimeweka bayana mikakati ya kuanzisha viwanda vipya na kushirikiana na wawekezaji kuimarisha viwanda vilivyopo ikiwa ni pamoja na kuweka mazingira wezeshi kwa uwekezaji mkubwa wa viwanda ili kuzalisha ajira za kutosha.

    Mpango wa maendeleo wa taifa wa Miaka mitano 2016/17-2020/21 pia umeweka bayana mikakati itakayosaidia kukuza uchumi wa viwanda ikiwemo kushirikiana na Jumuiya za Kikanda katika masoko na uchumi kama Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ili kukuza uchumi wa viwanda.

    Juhudi zote hizo zinadhihirisha kuwa Tanzania ya viwanda inawezekana chini ya uongozi wa Jemedari Rais John Pombe Magufuli zimeanza kuzaa matunda. Mkoa wa Pwani ni kioo cha uwekezaji mkubwa wa viwanda hivyo ni vema kuwakaribisha viongozi wa mikoa mingine ili waweze kujifunza mbinu walizotumia kufikia mafanikio hayo ambayo yameonekana katika kipindi kifupi kwa ujenzi wa viwanda vingi ambavyo vitazalisha ajira kwa wingi na hatimaye kuwapunguzia vijana tatizo la ajira kwa vijana.

    Sisi NCHI YETU tuna unga mkono jitihada za Mhe. Rais za kuhakikisha kunakuwa na ongezeko la viwanda, pia tunaunga mkono onyo alilolitoa kwa watumishi wa umma wanaokwamisha wawekezaji kwa makusudi kwa kuwawekea mlolongo wa taratibu zisizokuwa na tija ambazo mara nyingi zimewakatisha tamaa na kusababisha wengine kuhamishia uwekezaji katika nchi jirani. Tanzania ni nchi yenye utajiri mkubwa wa rasilimali ikiwemo madini, misitu, mbuga za wanyama, hali nzuri ya hewa na tunu za taifa letu za amani na utulivu, ni vyema tukatumia baraka hizo tulizojaaliwa na Mungu katika kuhakikisha uchumi unakua kwa sababu mazingira yetu yanaruhusu. Pamoja na mambo yote mazuri ni vema kila mmoja wetu akatimiza wajibu wake ili tunufaike na ukuaji wa uchumi sambamba na utetezi wa maslahi ya wanyonge jambo ambalo kila mara Mhe. Rais amekuwa akilitilia mkazo.

    Tukiwa watanzania wenye uchungu na uzalendo wa nchi hii, tuendelee kumuunga mkono na kumuombea Rais wetu katika kuhakikisha azma yake ya kukuza uchumi kwa kuijenga Tanzania ya viwanda inawezekana. Tuna toa rai kwa viongozi wa mikoa ambayo haina viwanda wakajitathmini na kujitafakari ni kwa namna gani watamsaidia Mhe. Rais kwa kuanzisha kuweka mazingira wezeshi uanzishwaji wa viwanda. Aidha ni budi kuhakikisha kwamba wanaiga mfano wa mkoa wa Pwani kwa kuvutia wawekezaji wengi katika sekta ya viwanda ili kuweza kuongeza ajira na kuondoa umaskini miongoni mwa Watanzania. Tanzania ya viwanda imeanza kuonekana, kila mmoja atimize wajibu wake, Mungu ibariki nchi yetu, Mungu ibariki Tanzania ya viwanda.

  • Jarida la Nchi Yetu 2016Inaendelea Uk. 3

    Inatoka Uk. 1

    1 Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO

    Hivi karibuni Rais John Pombe Magufuli alifanya ziara ya kikazi ya siku tatu katika Mkoa wa Pwani na kuzindua viwanda vitano. Hatua hii inaelekea kutimiza ahadi yake wakati wa Uchaguzi Mkuu ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.

    Kuwepo kwa ongezeko la viwanda kunatimiza nia ya Serikali ya kuwezesha sekta binafsi kuongoza mendeleo ya viwanda kwa kuweka mifumo dhabiti ya usimamizi na muindombinu wezeshi ili kuchochea kasi ya maendeleo ya teknolojia katika viwanda hivyo. Hii ni pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa ardhi iliyopimwa na kuweka dira na mwongozo wa utekelezaji wake.

    Viwanda vitano vilivyozinduliwa na Rais ni pamoja na kiwanda cha vifungashio cha Global Packaging Tanzania chenye uwezo wa kutengeneza mifuko aina ya sandarusi 53, 000 kwa siku.

    Kiwanda hicho ambacho ujenzi wake umegharimu shilingi bilioni nane, kimeajiri wafanyakazi 110.

    Kiwanda kingine ni cha kutengeneza matrekta 2,400 aona ya Ursus kiwanda hiki kinamilikiwa na Serikali ya Tanzania kwa asilinia 100.

    Kiwanda kingine kilichozinduliwa ni cha chuma cha Kiluwa Steel Group kilichopo Mlandizi ambacho katika awamu ya kwanza kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 500,000 za nondo kwa mwaka na awamu ya pili kitaongeza uzalishaji hadi kufikia

    tani 1,200,000 kwa mwaka.

    Kiwanda hiki kinamilikiwa na Mtanzania Bwana Mohamed Said Kiluwa kwa asilimia 51 na mwekezaji kutoka China kwa asilimia 49.

    Katika kiwanda cha vinywaji baridi cha Sayona Drinks Ltd kinachomilikiwa na Mtanzania Subhash Patel ambapo Rais Magufuli aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa kiwanda hicho utakao gharimu shilingi bilioni 120 mpaka kukamilika.

    Aidha kiwanda hicho cha sharubati kitatoa ajira 800 na pia kufungua fursa ya soko la matunda kwa wakulima 30,000 ambao watakuwa wanakiuzi kiwanda hicho matunda.

    Serikali katika kuhakikisha inawasaidia wawekezaji wa viwanda kwa kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRL) tayari limejenga njia ya reli ya kilometa 3.5 inayounganisha kiwanda cha Chuma cha Kiluwa na reli ya kati ikiwa ni juhudi za kurahisisha usafirishaji wa malighafi na vyuma vinavyozalishwa kiwandani hapo kwenda ndani na nje ya nchi. Katika ziara hiyo, Rais Magufuli pia alizindua Barabara ya Bagamoyo – Makofia - Msata yenye urefu wa kilometa 64 ambayo imejengwa na wakandarasi wazawa kwa fedha za ndani.

    Barabara hiyo itasaidia kupunguza foleni iliyokuwa kero katika barabara ya

    Na Eliphace Marwa-MAELEZO

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua kiwanda cha kutengeneza matrekta URSUS

    kilichopo Kibaha mkoani Pwani.

    Inaendelea Uk. 2

    TANZANIA YA VIWANDA HII HAPA

  • “Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu” 2Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO

    Morogoro toka Dar es Salaam mpaka Chalinze.

    Aidha Rais Magufuli pia amezindua mradi wa upanuzi wa mtambo wa maji wa Ruvu Juu na ulazaji wa mabomba makubwa ya maji ya kutoka Mlandizi hadi Dar es Salaam uliojengwa na Serikali ya Tanzania kwa gharama ya shilingi bilioni 200 ikiwa ni mkopo nafuu kutoka Serikali ya India.

    Rais Magufuli pia ameitaka Wizara ya Maji na Umwagiliaji kuhakikisha inajipanga vizuri kusimamia utekelezaji wa miradi ya maji inayosuasua, kudhibiti upotevu na wizi wa maji na kuwakatia maji wadaiwa sugu wote.

    Akizungumza katika miradi hiyo, Rais Magufuli amepongeza uwekezaji huo na ameagiza vyombo vinavyohusika kutoa vibali kwa ajili ya ujenzi wa viwanda hapa nchini viondoe urasimu ambao umekuwa ukiwakatisha tamaa wawekezaji

    kujenga viwanda na kuwataka wamiliki wa viwanda hivyo kujali maslahi na usalama wa wafanyakazi waliowaajiri.

    Uzinduzi wa viwanda hivyo ni muendelezo wa kutekeleza ahadi yake aliyoitoa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa

    mwaka 2015 wa kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa nchi ya viwanda na kupelekea kuondoa tatizo la ajira nchini na pia kupunguza bei za bidhaa kwenye soko la biashara.

    Mkoa wa una zaidi ya viwanda vikubwa na vidogo 85 na ni kielelezo tosha cha kwamba azma ya Tanzania ya Viwanda inawezekana, hivyo watanzania hawanabudi kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais za kuanzisha na kufufua viwanda pamoja na kuhamasisha uwekezaji.

    Makamu wa Rais wa Kampuni ya Podravka ya Nchini Croatia Olivia Jakupec akimtembeza Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage

    katika maeneo mbalimbali ya kiwanda cha utengenezaji wa viungo vya chakula kilichopo Bagamoyo,Mkoani Pwani.

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua kiwanda cha Sharubati(Juisi) cha Sayona Fruits

    kilichopo Mboga Chalinze mkoani Pwani.

    TANZANIA YA VIWANDA HII HAPA

    “nawapongeza wawekezaji na pia naviagiza vyombo vinavyohusika kutoa

    vibali kwa ajili ya ujenzi wa viwanda hapa nchini viondoe urasimu ambao umekuwa ukiwakatisha

    tamaa wawekezaji”- Rais Magufuli

  • “Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu”3 Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO

    Inaendelea Uk. 4

    Pamoja na Tanzania kutajwa kuwa ni miongoni mwa nchi tano zenye uchumi unaofanya vizuri barani Afrika, lakini tangu kuingia utawala wa Awamu ya Tano kumekuwepo na dhana miongoni mwa baadhi ya watu na taasisi kuwa hali si hivyo ilivyo.

    Katika Makala hii Mwandishi Said Ameir anachambua kwa kifupi maeneo yanayopelekea kuwepo kwa dhana hiyo na kwa nini.

    Kwa mwaka mwingine tena mwenendo wa hali ya uchumi nchini umeendelea kuwa mzuri huku Tanzania ikitajwa kuwa ni moja kati ya nchi tano barani Afrika zenye uchumi unaofanya vizuri.

    Kwa mujibu wa taarifa za Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) uchumi wa Tanzania umeendelea kufanya vizuri ukiwa katika orodha ya nchi tano barani Afrika na nafasi ya kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki.

    Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF World Economic Outlook Database), uchumi wa Tanzania unakuwa kwa

    asilimia 7.1 ikiwa nyuma ya nchi ya Ivory Coast ilioongoza kwa uchumi wake kukua kwa asilimia 7.9.

    Kuendelea kufanya vizuri huku kunaelezwa kuwa ni matokeo ya uboreshaji wa sera uliofanywa na unaoendelea kufanywa na uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli, kama alivyosema Naibu Mkurugenzi Mkuu wa IMF Bw. Tao Zhang, alipotembelea Tanzania Mei 2017, hususan katika uthabiti wa maeneo ya ukusanyaji wa mapato ya ndani na vita dhidi ya rushwa na ufisadi.

    Hata hivyo, pamoja na

    mafanikio hayo, wako wanaiona hali ya uchumi wa nchi kuwa si shwari kwa madai kuwa kutokana na baadhi ya hatua zilizochukuliwa na serikali bila kushirikisha wadau kumesababisha ukwasi katika uchumi, kufungwa kwa biashara, na madai kwamba sekta binafsi imepoteza matumaini na kujiamini.

    Katika hotuba yake ya Bajeti Bungeni, Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango alieleza kuwa hali ya ukwasi katika kipindi kilichoishia mwezi Machi 2017, kwa hali ya baadhi ya vigezo vya ukwasi inaonyesha kuwa ujazo wa fedha kwa tafsiri pana zaidi (M3) uliongezeka kwa asilimia 4.1 kutoka shilingi

    Na Said Ameir-MAELEZO

    Uchumi wa Tanzania Waongoza A. Mashariki

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Tao Zhang aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam Mei

    16,2017.

  • 4Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO

    Uchumi wa Tanzania Waongoza A. Mashariki

    trilioni 21.65 katika kipindi kama hicho mwaka 2016 hadi shilingi trilioni 22.53.

    Hotuba hiyo ya Waziri ilibainisha pia kuwa kwa sekta ya kibenki nayo iliendelea kuwa imara na himilivu huku uwiano kati ya mali inayoweza kubadilishwa kuwa fedha taslim na amana zinazoweza kuhitajika kwa muda mfupi ilikuwa asilimia 35.9 mwezi Machi 2017 ikilinganishwa na uwiano wa chini unaohitajika kisheria wa asilimia 20.

    Imekuwa ikidaiwa pia kuwa katika kipindi cha Awamu ya Tano kumekuwepo na kasi ya wafanyabishara kufunga biashara zao likitajwa jiji la Dar es Salaam kuwa moja miji iliyoathirika sana.

    Hata hivyo, takwimu rasmi toka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) zinaonesha

    kuwa katika kipindi cha kuanzia Julai 2016 hadi Machi, 2017 ni biashara 7,277 tu ndizo zilizofungwa katika mikoa mbalimbali nchini ikilinganishwa na biashara mpya zipatazo 224,738 zilizosajiliwa katika kipindi hicho hicho.

    Kufungwa huku kunaweza kusababishwa na mambo mengi lakini inawezekana sana kasi hiyo ya kufunga biashara inatokana na wito unaotolewa na Serikali kuwataka wale wote wanaofunga biashara watoe taarifa ili wasiendelee kutozwa kodi.

    Ni kweli tumekuwa tukisoma katika baadhi ya vyombo vya habari vikiwemo vya nje vikidai kuwa wawekezaji wanasita kuja Tanzania kwa madai kuwa wamepoteza imani kutokana na

    maamuzi yasiyotabirika yanayofanywa na Serikali.

    Wanaoeneza dhana hii potofu ambao baadhi ni mawakala wa washindani wa Tanzania katika kuvutia uwekezaji na biashara wanafanya hivyo huku takwimu zikionesha hali tofauti na kile wanachokieleza.

    Serikali imekuwa mara kwa mara, ikichukua hatua za kuimarisha mazingira ya uwekezaji na kufanya biashara na hata taarifa ya Benki ya Dunia ya mwaka 2017 inaonesha matokeo tofauti na hiyo dhana inayojengwa na baadhi ya watu.

    Taarifa hiyo ya Benki ya Dunia ya mwaka 2017 inaonesha kuwa, Tanzania imepiga hatua 12 kutoka kuwa nchi ya 144 hadi nchi ya 132 kwa urahisi wa kufanya biashara.

    Kwa upande wa uwekezaji, mwaka 2016 Tanzania ilikuwa nchi ya kwanza miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki kwa kuvutia uwekezaji na ya nane kwa Afrika, ikiwa imepiga hatua kutoka nafasi ya 19 mwaka 2015.

    Taarfa hii ni kwa mujibu wa “Fahirisi ya Uwekezaji Afrika ya mwaka 2016” (Africa Investment Index, 2016) iliyotolewa na taasisi ya “Quantum Global Research Lab” ya Uingereza.

    Katika kuendelea kuweka mazingira bora zaidi ya uwekezaji nchini, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)

    Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa tatu kulia) akielezea mpango wa Serikali wa kuboresha kilimo ili kukuza uchumi wa viwanda alipofanya Mkutano na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa

    (IMF), Tao Zhang (wa tatu kushoto), hivi karibuni jijini Dar es salaam

  • Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO5

    Inaendelea Uk. 6

    kimetangaza kuanzia Julai mwaka huu kitaanza kutoa kutoa vibali vya uwekeza ndani ya siku tatu tu.

    “Taasisi mbalimbali zinazotoa huduma kwa mwekezaji zinatakiwa zilete ofa na kukaa hapa kutoa vibali

    vyote ili kutokumfanya mwekezaji kuzunguka kwenye mamlaka kutafuta vibali, ningependa kuazia Julai mwaka huu tutoe vibali ndani ya siku tatu”, anaeleza Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Godfrey Mwambe.

    Kwa hivyo, wasiwasi

    wanaojaribu kuujenga wakosoaji wa hali uchumi nchini hauna msingi wowote. Kama alivyoeleza Waziri Fedha katika hotuba yake ya bajeti, Serikali imekuwa ikifanya jitihada za kujenga mazingira mazuri ya kuvutia uwekezaji kufanya biashara.

    Katika kufanya hivyo, Serikali imekuwa ikichukua hatua mbali mbali zikiwemo kuimarisha utulivu wa uchumi jumla, kupunguza urasimu, kuharakisha maamuzi, kuimarisha ulinzi na usalama na kuhakikisha upatikanaji wa miundombinu imara na huduma bora zikiwemo umeme wa uhakika na mikopo kwa sekta binafsi. Bwana Mwanri aliongeza kuwa ni vema Polisi wawe wanafanyakazi kwa kubadilishana ili kuepuka kujenga mazoea ya wachimbaji hao na hivyo kuathiri utendaji wao.

    Bunge Lapitisha Bajeti ya WananchiHivi Karibuni Bunge lilipitisha Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017-2018 ya trilioni 31.7 Katika Makala hii Mwandishi Said Ameir pamoja na kuchambua kwa ufupi baadhi ya maeneo anaeleza kuwa ni bajeti inayoleta unafuu kwa watu wa kila kipato.

    Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango

    akionesha mkoba wenye

    bajeti ya serikali mjini

    Dodoma

    Makao Makuu ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam

  • Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO6

    Inaendelea Uk. 7

    Ni bajeti iliyogusa hisia za watu wengi tangu wakati ilipotangazwa kwa mara ya kwanza tarehe 08 Juni, 2017, wakati wa kujadili wizara kwa wizara hadi kufikia tamati na kupitishwa tarehe 20 Juni, 2017.

    Hii ni bajeti ya pili katika kipindi cha kwanza cha miaka mitano ya Rais John Pombe Magufuli. Ni bajeti ambayo mchambuzi yeyote wa masuala ya siasa na uongozi anaweza kusema kuwa imezingatia sana mwelekeo na sura halisi ya uongozi wa Awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli.

    Unaliona hilo katika upangaji wa vipaumbele, mikakati ya utafutaji wa mapato na matumizi pamoja na ari na dhamira ya uongozi ya kutaka kuondoa kero zisizo za lazima zinazowakuta wananchi kutokana na baadhi ya maamuzi ya kisera au kisheria.

    Hii ni kusema kuwa bajeti ya mwaka huu imezidi kuweka mazingira wezeshi kwa uchumi na uwekezaji kushamiri huku wananchi wa kawaida wakipewa unafuu katika maeneo mbalimbali kwa kufutwa baadhi ya tozo na kodi ambazo zimeonekana kuwa kwaza.

    Fedha nyingi zimeendelea kutengwa kwa matumizi katika sekta muhimu za maendeleo kama vile ujenzi wa miundombinu ya uchumi, uimarishaji wa sekta ya nishati kwa ajili ya uwekezaji na wananchi mijini na vijijini pamoja na huduma za jamii kama elimu, afya na maji.

    Hapana shaka yeyote kuwa ushirikishaji wadau mbali mbali wakiwemo kutoka sekta binafsi umesaidia sana kuifanya bajeti hii kuwa bora zaidi kuliko ya mwaka uliopita na unathibitisha kwa vitendo utekelezaji wa

    dhana ya ushirikishwaji na pia ni kielelezo kuwa Serikali imezidi kuwa sikivu.

    Serikali haikuamka tu ikaamua kufuta kodi na tozo mbali mbali bali ni matokeo ya kusikiliza maoni ya wananchi wakiwemo walipa kodi na watumia huduma zinazotozwa kodi. Mwaka huu Serikali, kwa mfano, imefuta kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa magari ya kubebea wagonjwa, ada ya leseni ya magari, kodi kwa vifaa va walemavu, tozo na ada za zimamoto kwa shule binafsi.

    Aidha, serikali imeamua kutoza asilimia sufuri ya kodi kwenye usafirishaji wa bidhaa au mizigo nje ya nchi ili kuifanya Tanzania kuwa njia bora kwa usafirishaji/upitishaji wa mizigo kwenda nchi nyingine kama vile nchi jirani za Burundi, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Malawi.

    Hatua hii itasaidia kuongeza matumizi ya Bandari zetu za Dare es Salaam, Tanga na Mtwara na kwa kiasi kikubwa kuchangia ongezeko la ukusanyaji mapato ya serikali.

    Serikali imeondoa pia Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye bidhaa za mtaji ili kuhamasisha ukuaji wa viwanda, ada ya tathmini ya mazingira kwa wawekezaji wa viwanda, tozo ya VAT kwa vyakula vya mifugo vinavyotengenezwa

    Waziri wa Fedha na Mpango Mhe.Dr.Philip Mpango akiwasilisha Bungeni mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa

    mwaka 2017/18.

  • “Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu”

    “Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu”7 Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO

    Inaendelea Uk. 8

    hapa nchini chini ya alama ya HS CODE 2309, tozo ya VAT kwenye mayai ya kutotolea vifaranga na imepunguza ushuru wa mazao. Hatua hizi zote zinalenga kuongeza fursa zaidi sio tu kwa wawekezaji toka nje bali pia kwa wananchi kuwekeza katika viwanda kwa kuazisha vidogo vidogo na vya ngazi ya kati hatua ambayo itaongeza uwezo wao kiuchumi na hatimae kuinua kiwango cha maisha. Uchambuzi wa bajeti unaonesha kuwa mwaka huu wa fedha Serikali imepanga kutumia jumla ya shilingi trilioni 31.7 ambapo fedha kwa ajili ya maendeleo ni shilingi trioni 11.9 sawa asilimia 38 ya bajeti yote. Katika fedha hizo matumizi ya kawaida ni shilingi trilioni 19.7 ikijumuisha shilingi trilioni 7.2 za mishahara na shilingi trilioni 9.4 kwa ajili ya kulipia deni la Taifa na huduma nyinginezo.

    Bajeti hii imezidi kutoa matumaini kwa wananchi kwa sababu tofauti na bajeti ya mwaka uliopita, bajeti ya mwaka huu karibu asilimia 85 inatokana na vyanzo vya ndani hivyo utekelezaji wake unatarajiwa kuanza mara moja na kwa mafanikio zaidi.

    Tuna amini pia kuwa uzoefu wa upangaji na utekelezaji wa bajeti ya mwaka uliopita umesaidia sana kuimarisha utendaji na usimamizi wa bajeti ya mwaka huu.

    Miswada ya Kihistoria yawasilishwa BungeniKatika kutekeleza agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli lililotokana na mapendekezo ya kamati ya pili ya mchanga wa madini (makinikia) chini ya Mwenyekiti wake Prof. Nehemia Osoro, hatimaye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeanza kujadili miswada

    Na Mwandishi Wetu-MAELEZO

    Wabunge wakisikiliza hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/2018 leo Bungeni Mjini Dodoma Juni 8 2017.

    Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya Kamati

    ya pili ya Uchunguzi wa Madini yaliyo

    kwenye makontena yenye mchanga unaosafirishwa

    nje ya nchi kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa

    Nehemiah Osoro Ikulu jijini Dar es Salaam, kulia ni Waziri Mkuu

    Mhe. Kassim Majaliwa na Kushoto ni

    Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.

  • “Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu” 8Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO

    mitatu ya sheria iliyowasilishwa na Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba kwa ajili ya kufanyiwa marekebisha.

    Miswada iliyowasilishwa Bungeni ni pamoja na Muswada wa Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi wa Mwaka 2017, Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Maliasili wa Mwaka 2017 na Muswada wa kutungwa kwa Sheria mbalimbali ikiwemo sheria ya madini, petrol, kodi ya mapato, Kodi ya Ongezeko la Thamani na Sheria ya Bima.

    Sababu za kufanya marekebisho hayo ya sheria ni kuimarisha mifumo ya udhibiti na uwajibikaji, kupanua wigo wa makusanyo ya kodi yanayohusiana na sekta ya madini na petroli na kuweka masharti yatakayowezesha Watanzania kunufaika na maliasili ya madini, petroli na gesi asilia.

    Katika muswada wa kutungwa kwa Sheria mbalimbali ikiwemo sheria ya madini, petrol, kodi ya mapato, Kodi ya Ongezeko la Thamani na Sheria ya Bima, marekebisho ni yale ya kutambua na kuweka umiliki wa madini, petroli na gesi chini ya usimamizi wa Rais kwa niaba ya wananchi, tofauti na ilivyokuwa awali ambapo bidhaa hizo zilikuwa chini ya wizara yenye dhamana ya nishati madini.

    Marekebisho hayo pia

    yataipa Serikali haki na mamlaka ya umiliki wa mazao yote yanayopatikana katika uchimbaji, uchakataji na uchenjuaji wa madini na kuweka utaratibu wa kuyahifadhi migodini ikiwa ni pamoja na kuweka ulinzi mahsusi wa maeneo yote ya uchimbaji wa madini.

    Muswada huo pia utaanzisha Kamisheni ya Madini na kuanisha kazi zake ambapo ikiwa ni pamoja na kufanyia mapitio madaraka ya Waziri na Kamishna wa madini kwa lengo la kupunguza baadhi ya majukumu yao na kuyahamishia katika kamisheni hiyo.

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mwenyekiti wa Barrick Gold Corporation ya Canada

    Profesa John L. Thornton mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es salaam Juni 14, 2017. Kulia ni balozi wa Canada nchini Mhe. Ian Myles

    Malori yakisomba mawe na mchanga wa dhahabu katika mgodi wa Buzwagi.

  • “Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu”9 Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO

    Pia serikali itakuwa na uwezo kisheria wa kufanya majadiliano na kupitia upya baadhi ya masharti kwenye mikataba iliyokwisha fanyika.

    Aidha muswada huu pia utaipa serikali uwezo wa kutambua viwango vya madini yote yanayotolewa kwenye migodi na kuanzishwa kwa hifadhi ya dhahabu na vito chini ya Benki Kuu pamoja na kuanzisha maghala ya serikali ya kuhifadhi madini nchini.

    Pia Serikali itaanzisha mfumo mahsusi wa kukusanya na kuhifadhi taarifa zote za shughuli za madini.

    Kupitia muswada huu baadhi ya sheria zimependekezwa kurekebishwa. Sheria hizi ni pamoja na sheria ya madini sura ya 123 na sheria ya petroli ya sura 392, ambazo zitatambua na kuweka umiliki wa sekta ya madini mikononi mwa Watanzania na kuweka utaratibu bora wa kulinda mazingira

    kwenye shughuli za madini.

    Akizungumza hivi karibuni, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai amesema kuwa Bunge lake linaloendelea kujadili miswada hii, litahakikisha linafanya mabadiliko ya sheria hizo kwa maslahi mapana ya Taifa.

    Marekebisho ya sheria hizi yamekuja kufuatia kubainika kuwa nchi imekuwa ikipoteza mapato mengi katika sekta

    ya madini na rasilimali za taifa kutokana na udanganyifu na udhaifu wa baadhi ya sheria na mikataba.

    Upoteaji wa mapato na udhaifu wa sheria katika sekta ya madini ulibainika wakati Mwenyekiti wa Kamati ya Pili ya kuchunguza mchanga wa madini uliozuiliwa kusafirishwa nje nchi, Prof.

    Nehemia Osoro alipo bainisha kuwa makontena 61,320 yalisafirishwa nje ya nchi katika kipindi cha mwaka 1998-2017 na yalikuwa na thamani ya shilingi za kitanzania trilioni 183.597 kwa kiwango cha chini na trilioni 380.499 kwa kiwango cha juu.

    Aidha alisema kuwa serikali imepoteza mapato kiasi cha shilingi trilioni 108.46 ambazo ni sawa na bajeti ya serikali inayokaribia miaka mitatu kwa kigezo cha makadirio ya matumizi ya mwaka 2017/2018 pamoja na gharama ya kujenga reli ya Standard Gauge kutoka Dar es salaam hadi Mwanza.

    Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akioneshwa maeneo katika mgodi wa chuma cha liganga uliopo ludewa alipotembelea mgodi huo mapema mwaka

    huu

  • 6

    10Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO

    KATUNI NA MSAMIATI WA LEO

  • “Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu”11 Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO

    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi la Kituo cha Kutoa Huduma kwa Waathirika

    wa Dawa za Kulevya mjini Dodoma Juni 29, 2017. Kulia ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya

    Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu

    Rais Dk. John Pombe Magufuli akisoma ripoti ya Kamati ya Pili ya kuchunguzi wa mchanga wa Madini

    yaliyo kwenye makontena yaliyozuiwa kusafirishwa nje ya nchi.Wanaoshuhudia kushoto ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na kulia ni Waziri Mkuu

    Mhe. Kassim Majaliwa.

    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia

    namna samaki anaweza kufugwa vizuri bila kuharibu mazingira na kuleta manufaa kabla ya kuhutubia kwenye kilele cha siku ya mazingira

    duniani ambapo kilele chake kimefanyika kwenye viwanja vya Mwenge,Butiama

    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipozindua Kamusi Kuu ya Kiswahili

    kwenye ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma Juni 19, 2017.

    TANZANIA JUNI HII

  • 12Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO

    Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akipata maelekezo kutoka kwa mtaalam katika moja ya kiwanda alipokitembelea enzi za

    uongozi wake.

    Rais wa Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi akiweka mchanga kwenye tofali wakati akizindua

    moja ya jengo enzi za uongozi wake

    Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwa anasaidia katika kuponda udongo

    kwa ajili ya nyumba katika kijiji cha ujamaa Mkoani Dodoma.

    Rais wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na mwakilishi wa Shirika la Misaada la

    Ujerumani KFW Bi. Katrin Brandes na aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Lindi Bibi Mwantum Mahiza

    wakifunua kitambaa kuzindua ujenzi wa mradi wa maji wa mji wa Lindi eneo la Ng’apa mjini Lindi

    NCHI YETU KATIKA HISTORIA

  • 13 Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO

    Upanuzi Kina cha Bandari Kugharimu Bilioni 926Na Benjamin Sawe-MAELEZO

    Hivi karibuni Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), imesaini mkataba wa upanuzi na uongezaji wa kina cha bandari utakaowezesha bandari ya Dar es Salaam kupokea meli kubwa za mizigo na kushindana na bandari nyingine katika Pwani ya Bahari ya Hindi.

    Upanuzi huo utakaofanywa na kampuni ya China Harbor Construction ya China utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 926 na utadumu kwa miezi 36, ambapo utahusisha uongezaji wa kina cha lango la bandari na uongezaji wa kina cha maji kati ya gati namba moja hadi saba.

    Akizungumza katika hafla ya utiaji saini mkataba huo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema hatua hiyo inalenga kuifufua upya bandari ya Dar es Salaam ili ifanye kazi kwa ushindani na kuhudumia wateja wengi kuliko ilivyo sasa.

    “Kukamilika kwa upanuzi na uongezaji wa kina cha maji katika gati namba moja (1) hadi saba (7) kutoka mita 8 hadi 15 kutawezesha meli kubwa na za kisasa zenye uwezo wa kubeba hadi makontena elfu kumi na tisa kutia nanga katika bandari ya Dar es Salaam na kuongeza ufanisi na

    kukuza uchumi wa Tanzania”, amesema Prof. Mbarawa.

    Prof. Mbarawa anasisitiza kuwa pamoja na upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam Serikali inaendelea na ujenzi wa miundombinu wezeshi ya reli na barabara ili kuhakikisha mizigo haikai muda mrefu bandarini.

    “Ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge toka Dar es Salaam hadi Kanda ya Ziwa na Kigoma na ufufuaji wa reli ya Tazara kutawezesha bandari ya Dar e s Salaam kufanya kazi kwa ufanisi na kuvutia wafanyabiashara wengi hivyo nawataka wafanyakazi wote wa bandari kufanyakazi kwa bidii na uadilifu”, amesisitiza Prof. Mbarawa.

    Naye Mkurugenzi Mkuu wa TPA Mhandisi Deusdedit Kakoko anasema kiasi cha dola za Marekani milioni 421, kitapatikana kwa ajili ya ujenzi huo ambapo kati ya fedha hizo Benki ya Dunia itatoa mkopo wa masharti nafuu wa dola milioni 345.

    Kukamilika kwa ujenzi huo kutaondoa adha ya baadhi ya meli kusubiri kwa muda mrefu kupata nafasi ya kutia nanga na kutaongeza hadhi ya bandari ya Dar es salaam na kuvutia wasafirishaji wengi kutoka ndani na nje ya nchi.

    Rais Tayari amezindua ujenzi huo na kutoa maagizo kuwa ukamilike haraka ikiwezekana ndani ya miezi 28 badala ya 36

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird mara baada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa Uboreshaji wa

    Bandari ya Dar es Salaam.

  • 14Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO

    Serikali ya Awamu ya Tano imeonesha jitihada za makusudi katika ukusanyaji wa kodi ambapo mapato yameongezeka kwa kipindi kifupi kutoka bilioni 8 hadi wastani wa trilioni 1.3 kwa mwezi.

    Katika kutekeleza suala la ukusanyaji wa mapato kielektroniki, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imezindua Mfumo wa kukusanya kodi ya pango la ardhi kwa njia ya kielektroniki. Mfumo huu umeonyesha kuwa ni bora katika kuongeza ukusanyaji wa mapato.

    Katika mahojiano maalumu na mwandishi wa makala hii, Mkuu

    Ukusanyaji Kodi ya Ardhi Kielektroniki Waongeza Mapato

    Na Jovina Bujulu-MAELEZOwa Kitengo cha Kodi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Denis Masami amesema kuwa tangu kuanza kutumika rasmi kwa mfumo huu mwanzoni mwa mwezi Juni mwaka huu, makusanyo yameongezeka kutoka bilioni mbili hadi bilioni 2.9 kwa kipindi cha wiki tatu.

    “Kwa mfumo wa kawaida watu walikuwa wanalipa kodi ya pango la ardhi kwa siku tano tu ambazo ni siku za kazi, lakini baada ya kuanza kutumia mfumo wa elektroniki watu wanaweza kulipa wakati wowote, muda wowote na mahali popote, hivyo ni dhahiri kuwa taratibu za malipo kwa mfumo huu zimekuwa ni rafiki” anasema Masami.

    Aliongeza kuwa kwa mfumo huo, mlipaji kodi hahitaji kwenda

    Wizarani au kituo cha malipo kulipa kodi bali anaweza kufanya hivyo akiwa mahali popote kwa kutumia simu yake ya mkononi kwa kupitia menyu kuu ya Taifa ambayo ni *152*00#. Njia hii itamwondolea usumbufu mlipaji ikiwemo kupoteza muda mwingi kutoka anapokaa hadi kufika Wizarani kwa ajili ya kulipia kodi.

    Masami aliongeza kusema kuwa hadi sasa Wizara imekusanya shilingi bilioni 90, ukilinganisha na shilingi bilioni 74 ambazo zilikusanywa kwa kipindi cha mwaka 2015/16, na kwamba bado wana imani kuwa makusanyo yataongezeka kwani zoezi linaendelea hadi kufikia Juni 30, mwaka huu.

    Pamoja na kuongezeka kwa makusanyo, Masami alisema bado wanakabiliwa na changamoto za kimtandao na uelewa mdogo wa wananchi katika matumizi ya mtandao.

    “Ili kutatua changamoto hii elimu inaendelea kutolewa kwa maofisa wa Wizara, taasisi na wananchi wa kawaida ili waweze kutumia njia ya kielektoniki kwa wingi na kuongeza makusanyo”, alisisitiza Masami.

    Naye Mkurugenzi wa Mifumo ya Kifedha wa Wizara ya Fedha na Mipango John Sausi amesema kuwa kwa kutumia mfumo huo mtu atatumiwa ujumbe wa majibu kuonyesha kiasi cha fedha alicholipia ambao utahesabika kama risiti.

    Mkuu wa kitengo cha kodi, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi, Denis Masami(kushoto),akizungumza na waandishi wa habari,katikati ni Mkurugenzi wa mifumo ya kifedha kutoka Wizara

    ya fedha, John Sausi.

  • 15

    Jumatatu tarehe 19-06-2017, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) ilionyesha kuwa sasa haitaki mchezo na suala la wahujumu uchumi na wanaochezea rasilimali za taifa kwa kuwafikisha Mahakamani watuhumiwa wawili wakuu waliohusika katika kashfa ya Akaunti ya Tegeta ESCROW.

    Ni dhahiri kuwa taasisi hiyo inayoongozwa na Mkurugenzi wake Mkuu, Kamishna Valentino Mlowola kuwa sasa imelivalia njuga suala la wabadhirifu na wala rushwa bila kujali hadhi, vyeo wala ushawishi wao katika jamii, kama inavyosisitizwa mara kwa mara na kinara wa mapambano hayo ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

    Katika hali iliyowashangaza mamilioni ya watanzania Taasisi hiyo ilifanikiwa kuwafikisha Mahakamani wafanyabiashara maarufu waliowahi kulitikisa Bunge katika serikali iliyopita aliyekuwa mmiliki wa Kampuni ya VIP Engineering and Marketing Limited, James Rugemarila na mmiliki wa Kampuni ya PAP, Habinder Seth Sigh.

    Ni wazi kuwa juhudi za kupambana na ufisadi

    TAKUKURU Inastahili Kongole

    pamoja na ubadhirifu wa mali za umma na rasilimali za Watanzania zimeanza kuungwa mkono na taasisi zenye dhamana ya kumsaidia Mhe. Rais katika mapambano hayo.

    Wafanyabiashara hao, ambao wanatuhumiwa kufanya udanganyifu na kuisababishia serikali hasara ya Shilingi bilioni 309, ni miongoni mwa watuhumiwa ambao walipewa jina la ‘mapapa’ ikimaanishwa kuwa ni ‘wasiogusika’.

    Tunaipongeza Serikali ya Rais John Pombe Magufuli kwanza kwa kuisuka upya TAKUKURU chini ya Kamishna Valentino

    Mlowola, lakini pia kwa taasisi hiyo jinsi ilivyojipanga kushughulika na watuhumiwa mbali mbali wa uhujumu uchumi, jambo ambalo linairudishia heshima Tanzania iliyojengeka tangu enzi za Baba wa Taifa hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

    TAKUKURU ilikuwa ni miongoni mwa taasisi za umma ambazo zilionekana kushindwa kuwachukulia hatua watuhumiwa mbali mbali wa kesi za rushwa pamoja na ufisadi ambazo ziliibuliwa na kamati mbali mbali za Bunge katika awamu iliyopita na mwanzoni mwa Awamu ya Tano.

    Na Mwandishi Wetu-MAELEZO

    Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO

    Inaendelea Uk. 16

    Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) Juni 19, 2017 iliwafikisha mahakamani wafanyabiashara wawili James Rugemalira na Harbinde Seth watuhumiwa wawili wa kesi za

    ESCROW na IPTL.

  • 16

    Kitendo cha kuwafikisha watuhumiwa wa ESCROW Mahakamani sio tu kimewafurahisha watu wengi bali hata wakosoaji wa juhudi za Mh. Rais Magufuli za kupambana na ufisadi wameanza kumkubali na kumuunga mkono. Kwa mfano, aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ambaye pia ni kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zito Kabwe hakuficha hisia zake na kumpongeza Mh.Rais na TAKUKURU alipoandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter.

    Kwa kuwa mwarobaini wa rushwa sio TAKUKURU pekee,

    ni vyema wananchi na wao kwa upande wao kukataa kutoa au kupokea rushwa lakini pia kusaidia katika juhudi za kuwafichua wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo. Kwa kufanya hivyo itasaidia kujenga taifa lenye wazalendo wa kweli watakaosaidia ndoto ya Tanzania ya viwanda na yenye uchumi wa kati kufikiwa.

    Pongezi hizi zisiwafanye Kamishna Mlowola na timu yake kulewa sifa na kuona wameshafanikiwa, wanatakiwa kuhakikiksha kuwa wale wote walioshiriki kwa namna moja ama nyingine katika kashfa ya Akaunti ya Tegeta ESCROW wanachukuliwa hatua

    za kisheria pamoja na wale wote wanaoliingiza taifa kwenye umaskini mkubwa kwa kuhujumu rasilimali za watanzania.Katika muktadha huu ni vyema sasa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Kamishna Valentino Mlowola na timu yake waendelee na moyo huo wa kuchapa kazi bila woga na kuhakikisha kuwa hata wale waliotajwa katika ripoti ya pili ya mchanga wa madini maarufu kama Makinikia, wanachunguzwa na wakibainika wafikishwe mbele ya vyombo vya Sheria ili imani ya Watanzania kwa aliyeianzisha vita hivi Rais Magufuli iendelee kuimarika. Mapambano haya yakisimamiwa kwa dhati na yakiungwa mkono na Watanzania wote, bila kujali itikadi za vyama, itawezesha serikali kutekeleza majukumu yake ipasavyo kwa kujenga mazingira mazuri ya kuiwezesha kufikia lengo la Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.

    Viva Magufuli, viva TAKUKURU kila kitu k i n a w e z e k a n a tukiwa na nia ya dhati.

    Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amepokea toka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU

    Kamishna Valentino Mlowola Taarifa ya Utendaji kazi wa TAKUKURU ya mwaka 2015/2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

  • Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO

    PPF Yajipanga Kufanikisha Uchumi wa Viwanda

    Mfuko wa Pensheni PPF umejipanga kuwekeza kwenye viwanda ili kufanikisha azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kujikita kwenye uchumi wa viwanda utakaowezesha Taifa kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

    Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Bw. William Erio wakati akizungumza kwenye kipindi maalum cha TUNATEKELEZA kinachoratibiwa na Idara ya Habari-MAELEZO na kutangazwa na Televisheni ya Taifa (TBC 1) Jijini Dar es Salaam.

    Akifafanua kuhusu uwekezaji huo, Erio amesema kuwa PPF kwa kushirikiana na Shirika la Hifadhi ya Jamii NSSF wanajenga viwanda viwili vya sukari mkoani Morogoro kwenye maeneo ya Mkulazi na Mbigiri na vinatarajiwa kukamilika ifikapo mwaka 2019.

    “Mchakato wa ujenzi wa viwanda hivyo umeshaanza na vitakapokamilika vitaweza kuzalisha tani laki 2.5 kwa mwaka na vitasaidia kupunguza tatizo la uhaba wa sukari hapa nchini.” Anasema Erio.

    “Uwekezaji kwenye viwanda hivyo utasaidia kukuza pato la taifa na kutoa ajira kwa

    Na Fatma Salum-MAELEZO

    zaidi ya Watanzania laki moja hasa vijana.” Anasema Erio.

    Akieleza kuhusu maeneo mengine ya uwekezaji, Mkurugenzi Mkuu wa PPF amesema kuwa Mfuko huo pia umewekeza kwenye ujenzi wa hoteli, ofisi na nyumba za kuishi na kwamba kuanzia mwaka 2015 hadi 2017 mfuko huo umelipa kodi ya Serikali shilingi bilioni 73.9 kutokana na uwekezaji.

    Aidha amebainisha kuwa

    thamani ya mfuko huo inaendelea kukua kila mwaka ambapo hadi mwaka wa fedha 2016/2017 imefikia shilingi trilioni 2.5 na una wanachama zaidi ya laki 3 na elfu 30 kutoka sekta rasmi na isiyo rasmi.

    PPF ni Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ulioanzishwa mwaka 1978 na jukumu lake kubwa ni kutoa pensheni pamoja na mafao mengine kwa mujibu wa sheria.

    “Mchakato wa ujenzi wa viwanda hivyo umeshaanza na vitakapokamilika

    vitaweza kuzalisha tani laki 2.5 kwa mwaka na vitasaidia kupunguza tatizo la uhaba

    wa sukari hapa nchini.” William Erio.

    Kamishna Jenerali wa Magereza nchini (CGP) Dkt. Juma Malewa akisainiana mkataba wa makubaliano na Mkurugenzi wa Muda wa Kampuni ya Mkulazi

    Holdings Co. Ltd, Nicander Kileo huku wakishuhudiwa na Wakurugenzi wa NSSF (Prof. Godius Kahyarara) na PPF (William Erio),

    17

  • Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO

    Urasimishaji Makazi Holela Dar Wanufaisha Wananchi

    Ukuaji wa makazi yasiyopangwa ni mojawapo ya changamoto kubwa ya miji yetu hususan katika majiji na Manispaa nchini.

    Katika utafiti uliofanyika mwaka 2013 ukihusisha majiji na Manispaa nane, asilimia 66 ya maeneo yaliyoendelezwa yalikuwa ni maeneo yasiyopangwa.

    Maeneo yaliyojengwa kiholela hayana huduma muhimu za kiuchumi na kijamii kama vile maji safi na maji taka, mitaro ya maji ya mvua, barabara, umeme huduma za elimu na afya. Ili kukabiliana na hali hiyo, juhudi mbalimbali zimekuwa zikifanyika zikiwemo uboreshaji wa miundombinu kwenye maeneo husika (Community Infrastructure Upgrading) urasimishaji (regularization), utoaji wa leseni za makazi na ujenzi upya wa maeneo hayo hususan yale yaliyoko kwenye maeneo yaliyoiva kiuendelezaji upya (redevelopment).

    Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imepima viwanja 4,333 hadi mwishoni mwa Mei, 2017 na hatua za umilikishaji zimeanza katika utekeleza wa kurasimisha maeneo yaliyojengwa kiholela jijini Dar es Salaam.

    Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Mipango Miji na Vijiji wa Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bertha Mlonda anafafanua katika makala hii.

    Kwa mujibu wa Mlonda, jumla ya viwanja 6,000 vinatarajiwa kupimwa na kumilikishwa katika jiji la Dare es Salaam katika zoezi zima la urasimishaji wa makazi holela.

    “Pamoja na urasimishaji katika Jiji la Dar es Salaam halmashauri nyingine sita (6) zimepangwa kutekeleza mradi huo. Halmashauri hizo ni; Manispaa za Musoma, Kigoma-Ujiji, Tabora, Singida, Sumbawanga na Lindi”, amesema Mlonda.

    Aidha, Mlonda amesema kuwa mradi unatekelezwa katika Kata za Kimara na Saranga Manispaa ya Ubungo ambazo zina ukubwa wa hekta 3,960. Kata ya Kimara, inajumuisha mitaa sita (6) ambayo ni Kilungule “A”, Kilungule “B”, Mavurunza, Baruti, Kimara Baruti na Golani. Kata ya Saranga ina jumla ya mitaa saba (7)

    ambayo ni Kimara B, King’ong’o, Matangini, Michungwani, Saranga, Stopover na Upendo.

    Ameongeza kuwa kwa pamoja kata hizo zina wastani wa viwanja 34,000. Mradi umeanzia kutekelezwa katika Kata ya Kimara kwenye Mitaa ya Kilungule ‘A’, Kilungule ‘B’ na sasa Mavurunza. Lengo la Mradi ni kutambua, kupanga, kupima na kumilikisha viwanja 6,000.

    Mkurugenzi Msaidizi huyo amesema kuwa baada ya kukamilisha michoro ya Mipango miji na Ramani za Upimaji na kupata upana wa barabara, kazi iliyofuata ni kufungua barabara.

    Barabara zenye urefu wa kilomita 9.128 zimechongwa katika Mitaa ya Kilungule ‘A’, Kilungule ‘B’ na Mavurunza, amesema Mlonda.

    Na Jonas Kamaleki-MAELEZO

    Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akionyeshwa moja ya vifaa vinavyotumika katika upimaji wa Ardhi katika Mkutano mkuu na

    Kongamano la Wapimaji Ardhi uliofanyika Jijini Dar es Salaam

    18

  • Katika urasimishaji huo, Mlonda anaainisha mafanikio ya mradi ni pamoja na kuboresha mazingira katika makazi, kuongeza huduma za jamii na miundombinu katika maeneo ambayo awali yalikuwa hayafikiki kwa gari sasa yanafikika na kuongeza usalama wa miliki ya ardhi kwa wananchi na kuongeza fursa ya kutumia ardhi kama mtaji na kupunguza umasikini.

    Ameyataja mafanikio mengine kuwa kanzi data inajenga uwezo wa halmashauri kusimamia na kutoa huduma za ardhi kwa ufanisi, kuwa na maeneo yaliyopangwa, kupimwa na kumilikishwa,kupunguza au kupunguza kwa kiasi kikubwa migogoro ya ardhi na kuongeza wigo wa mapato ya serikali kwa kupitia tozo mbalimbali za ya kodi ya ardhi.

    Urasimishaji huu unatekelezwa kwa mkopo wa Benki ya Dunia ambapo viwanja 3,000 vinatarajiwa kupimwa katika

    kila Halmashauri. Utekelezaji utatumia uzoefu uliopatikana wakati wa utekelezaji wa mradi Jijini Dar es Salaam na Mwanza.

    Mmoja wa wataalamu wa upimaji ardhi akiweka alama katika eneo lililorasimishwa.

    Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO19

    Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amezindua Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) ikiwa ni mkakati wa kuharakisha utatuzi wa changamoto za usafiri katika maeneo hayo.

    Akifanya uzinduzi mapema mwezi huu mjini Dodoma, Waziri Mkuu amesema kuwa wakala huo utasaidia kuimarisha mtandao wa barabara za vijijini na kuwawezesha wananchi wengi kusafiri na kusafirisha bidhaa zao kwa urahisi.

    “Wakala huu tunaouzindua leo utakuwa na manufaa makubwa kwa ustawi wa nchi yetu kwa kuongeza chachu ya uzalishaji mali mashambani kutokana na urahisi wa kufika sokoni na pia utasaidia kushusha bei ya vyakula mijini na vijijini pamoja na bidhaa za viwandani kutokana na gharama za usafirishaji kupungua,” ameeleza Mhe. Majaliwa.

    Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na

    Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. George Simbachawene amesema TARURA ni muhimu kwani ujenzi wa barabara za vijijini zitawagusa wananchi moja kwa moja na ni kichocheo kikubwa cha uchumi

    kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

    Kwa sasa Tanzania ina zaidi ya kilomita 108,942 za mtandao wa barabara za Mamlaka ya Serikali za Mitaa ambao ni zaidi ya nusu ya mtandao wa barabara kuu za Kitaifa.

    Na Mwandishi Wetu-MAELEZO

    Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi kitabu cha Muongozo wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini , Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala Barabara Vijini na Mijini Mhandisi Victor Seif, katikati ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI George Simbachawene . Uzinduzi huo umefanyika July 2, 2017 katika ukumbi wa

    mikutano wa Chuo cha Mipango Mkoani Dodoma

    Waziri Mkuu azindua Wakala wa Barabara Vijijini

  • LIMEANDALIWA NA

    @TZ_MsemajiMkuu Msemaji Mkuu wa Serikali

    Idara ya Habari-MAELEZOS.L.P 8031

    Dar es Salaam-TanzaniaSimu : (+255) 22 -2122771

    Baruapepe:[email protected]: www.maelezo.go.tz

    Blogu: blog.maelezo.go.tz

    MaelezoTv

    Waziri Mkuu azindua Wakala wa Barabara Vijijini