15
GATEPASS REVISION KIT 111 102/1 KISWAHILI Karatasi ya 1 INSHA Okt./Nov. 2011 Muda: Saa 1 3 / 4 Maagizo 1. Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima. 2. Kisha chagua insha moja nyingine kittoka kwa hizo tatu zilizobakia. 3. Kila insha isipungue maneno 400. 4. Kila insha ina alama 20. 5. Karatasi hit ina kurasa 2 zilizopigwa chap a. 6. Watahiniwa ni lazima wahakikishe kwamba kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo. 1 Insha ya lazima. Wewe kama mwanafunzi umepata nafasi ya kumhoji Mkurugenzi wa Habari nchini kuhusu umuhimu wa magazeti kwa wanafimzi wa shule za sekondari. Andika mahoji.ano hayo. 2 "Magari ya matatu yameleta faida nyingi hapa nchini kuliko hasara." Jadili. 3 Pele hupewa msi kucha. 4 Andika insha itakayomalizika kwa: "Niliipapia ile bilauri ya maji kwa pupa. Sikuwa na uhakika kuwa kiu yangu ingekatika. Nikapiga mafunda mawili, matatu. Baada ya kugumia bilauri yote, ndipo nilipotambua kuwa kweli maji ni uhai." For More Free KCSE past papers visit www.freekcsepastpapers.com

Okt./Nov. 2011 - freekcsepastpapers.com · Mosi, unasaidia kujenga makini ya utendaji. Pili, hupevusha uwezo wa usomaji kwa kuufanya usomaji huo uwe na malengo wazi. Fauka ya hayo,

  • Upload
    others

  • View
    3

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

GATEPASS REVISION KIT

111

102/1KISWAHILI Karatasi ya 1 INSHA

Okt./Nov. 2011Muda: Saa 13/4

Maagizo

1. Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima.2. Kisha chagua insha moja nyingine kittoka kwa hizo tatu zilizobakia.3. Kila insha isipungue maneno 400.4. Kila insha ina alama 20.5. Karatasi hit ina kurasa 2 zilizopigwa chap a.6. Watahiniwa ni lazima wahakikishe kwamba kurasa zote za karatasi hii

zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.

1 Insha ya lazima.

Wewe kama mwanafunzi umepata nafasi ya kumhoji Mkurugenzi wa Habarinchini kuhusu umuhimu wa magazeti kwa wanafimzi wa shule za sekondari.Andika mahoji.ano hayo.

2 "Magari ya matatu yameleta faida nyingi hapa nchini kuliko hasara." Jadili.

3 Pele hupewa msi kucha.

4 Andika insha itakayomalizika kwa:

"Niliipapia ile bilauri ya maji kwa pupa. Sikuwa na uhakika kuwa kiu yanguingekatika. Nikapiga mafunda mawili, matatu. Baada ya kugumia bilauri yote,ndipo nilipotambua kuwa kweli maji ni uhai."

For More Free KCSE past papers visit www.freekcsepastpapers.com

GATEPASS REVISION KIT

112

102/2KISAWHILI

KARATASI ya 2LUGHA2011

UFAHAMU (Alama15)

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali.

Changamoto kubwa inayowakabili watu wengi katika mataifa yanayoendelea nisuala la chakula. Suala hili linaweza kuangaliwa katika sawia mbili tofauti.Kuna tatizo linalofungamana na uhaba wa chakula chenyewe, Uhaba huuunaweza kutokana na utegemezi mkubwa kwa zaraa kama nyenzo kuu yauzalishaji wa chakula.

Zaraa katika mataifa mengi hususan yanayoendelea, hutegemea mvua.Kupatikana kwa mvua huathiriwa na mabadiliko ya tabianchi ulimwenguni. Matendo naamali za watu kama ukataji wa miti na uchafuzi wa mazingira huwa na athari hasikwenye tabianchi hiyo. Mabadiliko ya tabianchi huweza kuvyaza ukame kutokana nangambi ya mvua.

Kibinimethali hutokea wakati mafuriko yanapotokea na labda kuyasomba mazaomashambani na kusababisha baa la njaa. Hali hizi mbili husababisha matatizomakubwa ya chakula na kuathiri pakubwa suala zima la usalama wa chakula. Hikuzuia uwezekano wa kuwepo kwa shida hii, pana haja ya kuwepo kwa mikakati na seraza kuhakikisha kuna usalama wa chakula. Kwa mfano, pana haja ya kukuza kilimo chaumwagiliaji ili kuepuka adha inayosababishwa na ukosefu wa mvua. Kwa upandemwingine, sharti zichukuliwe hatua mufidi za kuzuia na kupambana na athari zagharika.

Changamoto nyingine inahusiana na usalama wa chakula chenyewe. Chakulakilichosibikwa na vijasumu au kwa njia nyingine ile huweza kumdhuru anayehusika.Msibiko wa chakula unatokana na vyanzo tofauti. Mathalan, uandalizi wa chakulakilichochafuliwa na choo, kutozingatia mbeko za usafi, uandaaji wa chakula nakukiweka katika hali ya uvuguvugu kabla ya kukipakua - hali inayochochea ukuaji waviini na ulaji wa chakula kisichoandaliwa vyema.

Ili kuepuka uwezekano wa kuadhirika, pana haja ya kuzingatia usafi wa chakulana uandalizi unaofaa. Fauka ya hayo, vyombo vya uandalizi viwe safi, kanuni za usafizifuatwe, upikaji na uandaaji uwe kamilifu. Hali hii isipozingatiwa, siha za raiawenyewezitaathirika pakubwa.

Maswali

For More Free KCSE past papers visit www.freekcsepastpapers.com

GATEPASS REVISION KIT

113

(a) Taja aina mbili za kuangalia suala la chakula katika mataifa yanayoendelea.(alama 2)

(b) Taja hatua mbili zmazoweza kuchukuliwa kupambana na tatizo lachakula.

(alama 2)

c) Eleza jinsi nne tofauti namna chakula kinavyoweza kuwa si salama?(alama 4)

(d) Kwa nini inahalisi kukipakua chakula baada ya kukiandaa tu?(alama 1)

(e) Ni mapendekezo gani anayoyatoa mwandishi kuhakikisha kuwa chakulakinafaa?

(alama 4)(f) Eleza maana ya maneno haya jinsi yalivyotumiwa: (alama 2)

(i) Ngambi yamvua ....................................................................................................

(ii)

Adha......................................................................................................................

MUHTASARI

Uwazaji tunduizi ni tendo ambalo huhusisha matumizi ya akili. Uwazaji huuumekitwa kwenye matumizi ya michakato kama makini, upangi l iaj i ,uteuzi na tathmini. Hata hivyo, uwazaji huu si mchakato mwepesi bali nimchakato changamano.

Mchakato wa uwazaji tunduizi unahusisha stadi na mikabala tofauti. Mathalan,kuweza kutambua na kubainisha misimamo ya watu wengine, hoja wanazozuana uamuzi waliofikia, kutathmini au kupima ushahidi uliopo ili kubainishamitazamo tofauti. Vilevile. uwazaji tunduizi hushirikisha kupima hoja zaupinzani na ushahidi uliopo kwa njia ya haki pamoja na kutambuayaliyofichwa au ukweli uliofunikwa na taswira ya juu juu. Hali kadhalika,uwazaji tunduizi hujumuisha kutambua mbinu zinazotumiwa kufikia misimamo

For More Free KCSE past papers visit www.freekcsepastpapers.com

GATEPASS REVISION KIT

114

fulani kwa mvuto zaidi na kwa matumizi ya mbinu za kishawishi. Aidha,uwazaji huu huhitaji kutathmini masuala kwa mtindo ulio wazi, kufikiauamuzi kama hoja zinazotumiwa zina mashiko au zinakubalika kuwa nzuri.Zaidi ya hayo, uwazaji tunduizi unahusisha kuwasilisha mtazarao kwa njia yenyeuwazaji mzuri na inayoshawishi.

Uwazaji tunduizi una manufaa anuwai. Mosi, unasaidia kujenga makini yautendaji. Pili, hupevusha uwezo wa usomaji kwa kuufanya usomaji huo uwe namalengo wazi. Fauka ya hayo, unamsaidia mtumiaji kutambua hoja kuu katikamatini au ujumbe fulani bila ya kuzongwazongwa na hoja duni za pembeni.Uwazaji huu unasaidia kuuchonga uwezo wa kuikabili au kuiitikia hali fulani nakukuza stadi za uchanganuzi. Mwanadamu huwa mtu tofauti na boraanapoujenga na kuuimarisha uwazaji tunduizi wake.

Maswali

(a) Bila kubadilisha maana aliyokusudia mwandishi, fupisha ay a mbili zamwanzo.

(Maneno 70 - 80) (alama 10; alama 2 za utiririko)Matayarisho:

For More Free KCSE past papers visit www.freekcsepastpapers.com

GATEPASS REVISION KIT

115

Nakala safi:

(b) Andika kwa muhtasari mambo muhimu katika aya ya tatu.(Maneno 35 - 40) (alama 5; alama I ya utiririko)Matayarisho:

For More Free KCSE past papers visit www.freekcsepastpapers.com

GATEPASS REVISION KIT

116

Nakala safi:

3 MATUMIZI YA LUGHA.

(a) Tumiamzizi '-enye'katika

sentensi kama:

(i)

Kivumishi...................................

.....

(ii) Kiwakilishi ......................................

(alama 2)

(b) Andika sentensi ifuatayo katika ukubwa:-

Paka mweupe araenaswa mguuni .(alama 2)

(c) Taja mfano mmoja mmoja wa sauti zifuatazo:-

(i) Kiyeyusho

..............................................................................................................

(ii)

Kimadende......................................................................................................

........

For More Free KCSE past papers visit www.freekcsepastpapers.com

GATEPASS REVISION KIT

117

(alama 1)

(d) Onyesha shamirisho kitondo, kipozi na ala katika sentensi ifuatayo:-

Kipkemboi alimbebea mwalimu mzigo kwa gari. (alama 3)

For More Free KCSE past papers visit www.freekcsepastpapers.com

(e) Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia jedwali.

Maria alipika taratibu huku mama akimwelekeza vizuri. (alama 4)

(f) Nomino 'furaha' iko katika ngeli gani?

......................................................................................................................... (alama

1)

(g) Andika kinyume cha sentensi:

Watoto wameombwa waanike nguo. (alama 2)

(h) Andika sentensi ifuatayo upya kwa kufuata maagizo uliyopewa. Mama alishangilia

arusi ya mwana. Anza: Mwana

.................................................................................................. (alama 2)

(i) Tumia kirejeshi 'O' katika sentensi ifuatayo:-

Mtu ambaye hutupa tope hujichafua mwenyewe. (alama 2)

(j) Kanusha sentensi ifuatayo:

Mgonjwa huyo alipona na kurejea nyurabani. (alama 2)

For More Free KCSE past papers visit www.freekcsepastpapers.com

(k) Ainisha vihusishi katika sentensi:

Ame aliwasili mapema kuliko wengine halafu akaondoka. (alama 2)

(1) Tunga sentensi mbili kuonyesha maana tofauti za neno "chuma". (alama 4)

(i) .................................

(ii) .................................

(m) Unda noniino kutokana na kitenzi 'tafakari' .................................................

(alama 1)

(n) Eleza maana mbili za sentensi:

Tuliitwa na Juma ...........................................................................................

(alama 2)

(o) Ainisha viambishi katika kitenzi:-

Tutaonana................................................................................................ (alama 2)

(p) Tunga sentensi moja ukitumia kiunganishi cha kinyume. (alama 2)

(q) Huku ukitoa mifano eleza miundo miwili ya silabi za Kiswahili. (alama 2)

(r) Akifisha kifungu kifuatacho:

For More Free KCSE past papers visit www.freekcsepastpapers.com

Mzee alimwambia mwanawe njoo nikupeleke kwa babu yako angalau umjuemtoto aliuliza nani babu? (alama 4)

ISIMUJAMII

(a) Bainisha changamoto tano zinazoikabili lugha ya Kiswahili kama somo katikashule za upili nchini Kenya. (alama 5)

(b) Eleza namna tano za kukabiliana na changamoto ulizobainisha hapo juu.(alama 5)

For More Free KCSE past papers visit www.freekcsepastpapers.com

KISAWHILIKARATASI ya 3

FASIHI2011

SEHEMU A: TAMTHILIA

KITHAKA WA MBERIA: Kifo KisimaniSwali la lazima

1 "Alijiona pwagu. Lakini Butangi ina pwaguzi pia."Eleza tofauti baina ya wahusika wanaorejelewa. (alama 20)

SEHEMU B: RIWAYA

S.A.MOHAMED: UtenganoJibu swali la 2 au la 3

2 Eleza namna mbinu zifuatazo zilivyotumiwa na mwandishi wa riwaya ya Utengano:

(i) Kwelikinzani(ii) Sadfa. (alama 20)

3 "Uhuru alioutaka na ulimwengu alioufahamu Maimuna umemdhuru hatimaye."Thibitisha kauli hii kwa kutoa mifano kumi. (alama 20)

SEHEMU C: USHAIRIJibu swali la 4 au la 5

KUJITEGEMEA

1. Nchi ni ile ambayo, imekita ardhiniSiyo ile iombayo, ghaibu na majiraniTaratibu siyo hiyo, wanachi twambizaneniDaima hukaa chini, maganja ya mpewaji

2. Chumo lote na mitaji, leo limo maganjaniBepari na wanyonyaji, wasalie maguguniShime utekelezaji, vingine havifananiDaima hukaa chini, maganja ya mpewaji

For More Free KCSE past papers visit www.freekcsepastpapers.com

3. Twaishije tujihoji, wanachi humu nchiniKila tunachohitaji, kupatakwe ugeniniHiyo ni tete haviji, tongo tupangusaneniDaima hukaa chini, maganja ya mpewaji

4. Kuomba wataalamu, ni mwendo haulinganiTupate wa humu humu, wajuzi wa kila faniMbele washike hatamu, kwa mapimo na makiniDaima hukaa chini, maganja ya mpewaji

5. Tuufuate wongozi, pamwe na nyingi imaniTushiriki kila kazi, na mambo yalomkiniMikopo ina kinyezi, si kitu cha tumainiDaima hukaa chini, maganja ya mpewaji

6. Yote hatuyatimizi, alotimiza ni naniLakini tuwe maizi, tusizurure mijiniTukamshabilii kozi, kipanga au kunguniDaima hukaa chini, maganja ya mpewaji

7. Shujaa itakiwavyo, aonekane vitaniNa sisi vita tunavyo, roho kwa roho ugani'Kutegemea' vilivyo, kondo tujiamueniDaima hukaa chini, maganja ya mpewaji

Boukhet Amana: Malenga waMrimaMwinyihatibu Mohammed

Oxford University Press1977

(a) Mtunzi wa shairi hili ana dhamira gani? (alama 2)

(b) Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu moja. (alama 2)

(c) Eleza mambo matatu ambayo mshairi anashauri nchi ifanye ilikujitegemea. (alama 3)

(d) Taja aina moja ya idhini ya kishairi iliyojitokeza kwa wingi zaidi katika shairi na utoe

mifano mitano ya matumizi yake. (alama 7)

(e) Andika ubeti wa pili kwa lugha ya nathari. (alama 4)

(f) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika

shairi:

For More Free KCSE past papers visit www.freekcsepastpapers.com

(i) Ghaibu

(ii) Tukamshabihi.(alama 2)

HAKI1. Haki watutisha, tusikuandame, kwa matendo yetu,

Watukorofisha, tusikuandame, kila penye kitu, Mbona watugwisha, miba ituchonie, kwenye huu mwitu,

Tutokwe nautu!

2. Hatutakufanya, mwana kwa mvyele, aliyemzaa, Haki watunyima, machumi ya mbele, na nyingi hadaa,

Tuchumayo nyanya, uchungu umbele, hatuna wasaa,Haki twashangaa!

3. Na kambi nzima, kunaiyenea, hasa hapa petu,Tunakutazama, kwa kuulizia, kuweza thubutu,Na kwenye milima, ilotueka, kupandia watu,

Usifanyekatu!

4. Sio hao mabwana, waloteuliwa, kupata mwangaza,Haki wakubana, lilotarajiwa, kwenye hichi kiza,Ndevu kuchomana, wengine kuliwa, tukijiingiza,

Kambi yatuviza!

5. Haki huna njia, kizuizi mali, ndio njia panda,Tukiifatia, hatufiki mbali, wengi tunaganda,Sio yetu nia, lakini akili, mali ishapenda,

Haki yatuponza!

6. Wala hutasemwa, sababu ni nyoyo, kwisha haribika,Ya mali kuchumwa, vyovyote iwavyo, itavyopatika,Wakati mtumwa, ushatumwa ndivyo, na ushatufika, Kwetu ni mashaka!

7. Haki hufanyiki, papitapo mambo, na vikubwa visa,Watu hawataki, kutenda kijambo, tunu yao pesa,Sisi kwetu dhiki, yatunisha tumbo, wao hata hisa,

Nandio yasasa!

8. Haki husimami, kwa viumbe sisi, tuvyojaaliwa,Na huna ulimi, kuweza tukisi, tukageukiwa,Zama za uchumi, zishashika kasi, nguvu zishapewa,

For More Free KCSE past papers visit www.freekcsepastpapers.com

Haki wauliwa!

9. Iwe hivi haki, hakuna mmoja, akukumbukae,Hatuna ashiki, kuvuta la haja, haki ituvae,Mbona hatutaki, twalia na tija, haki iambae,

Hakitamati!

Suleiman A. Ali: Malenga Wapya

(a) Eleza dhamira ya shairi hili. (alama 2)

(b) Huku ukitoa mfano, eleza aina ya shairi hili. (alama 3)

(c) Taja na ufafanue tamathali ya usemi inayotawala katika shairi hili. (alama 3)

(d) Kwa kutoa mfano mmoja mmoja, onyesha aina tatu za idhini ya kishairi

katika shairi hili. (alama 6)

(e) Andika ubeti wa saba kwa lugha ya nathari. (alama 4)

(f) Mshairi ana maana gani kwa kusema;

(i) Kambi yatuviza

(ii) Kuwezatukisi.(alama 2)

SEHEMU D: HADITHI FUPI

K.W. WAMITILA: Mayai Waziri Wa Maradhi na Hadithi Nyinginezo

Jibu swali la 6 au la 7

6 "Cheche ndogo hufanya moto mkubwa,"

(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)

(b) Fafanua maudhui manne yanayohusiana na chanzo cha tukio linalorejelewakatika dondoo hilo. (alama 8)

For More Free KCSE past papers visit www.freekcsepastpapers.com

(c) Eleza matokeo manne ya tukio linalorejelewa katika dondoo. (alama 8)

7 "Mganga na wateja wake wote walikosa busara." Fafanua ukweli wa kaulihii kwa mifano kumi kutoka hadithi ya 'Siku ya Mganga.'

(alama 20)

SEHEMU E: FASIHI SIMULIZI

(a) Eleza maana ya malumbano ya utani. (alama 2)

(b) Bainisha sifa nne za malumbano ya utani. (alama 8)

(c) Fafanua majukumu matano ya malumbano ya utani katika jamii. (alama

10)For More Free KCSE past papers visit www.freekcsepastpapers.com