27
Joining Instructions Kiss 2017 Email: [email protected] Page 1 ن الرحيم لرحم بسمKIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL Maelekezo ya Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2017. Soma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya shule kisha uthibitishe kukubali nafasi hii kwa kulipa mkupuo wa kwanza wa ada kabla ya tarehe 22/12/2016. Ada isipolipwa katika muda uliotajwa, nafasi itatolewa kwa mwanafunzi mwingine. Shule itafunguliwa tarehe 31/12/2016. Utangulizi KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL ni Shule ya Kiislamu inayotazama elimu kuwa ni jambo la kwanza na muhimu kwa mwanadamu. Tunajifunza katika Qur’an kuwa Nabii Adam (a.s) kabla hajaletwa hapa ulimwenguni kwa kazi yake ya ukhalifa (uongozi), alielimishwa kwanza kuhusu mazingira yake (Rejea Qur’an, (2:31). Vile vile tunajifunza kuwa Mtume wa mwisho Muhammad (s.a.w) kabla hajaanza kazi yake kubwa ya kuhuisha uislamu alipewa kwanza amri ya kusoma (rejea Qur’an 96:1-5). Mtume (s.a.w) akasisitiza kuwa ni faradhi (lazima) kwa kila muislamu mwanamume na kila muislamu mwanamke kutafuta elimu. Pia Mtume (s.a.w) amesisitiza kuwa elimu itafutwe hata ikibidi ifungiwe safari ya mbali (Uchina). Tunalojifunza kutoka katika Qur’an na hadithi sahihi za Mtume (s.a.w) ni Kuwa, kwanza elimu ni zana ya kwanza ya msingi ambayo muislamu hana budi kuwa nayo ili aweze kuishi maisha ya kiislamu na awe Khalifa (kiongozi) wa Allah (s.w) hapa duniani. Pili, tunajifunza kuwa katika uislamu hapana ubaguzi wa elimu ya dunia na elimu ya akhera.Kila fani ya elimu inayomwezesha mwanadamu kufikia lengo la kuwa Khalifa wa Allah (s.w) hapa duniani ni faradhi (wajibu/lazima) kwa waislamu wote.

KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL - ipc.or.tzipc.or.tz/assets/uploads/news/join-kiss-F1-2018.pdfSoma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya ... Tunalojifunza kutoka katika Qur’an

  • Upload
    dangdat

  • View
    653

  • Download
    17

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL - ipc.or.tzipc.or.tz/assets/uploads/news/join-kiss-F1-2018.pdfSoma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya ... Tunalojifunza kutoka katika Qur’an

Joining Instructions Kiss 2017 Email: [email protected] Page 1

بسم هللا لرحمن الرحيم

KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL

Maelekezo ya Kujiunga na Kidato cha Kwanza

Mwaka 2017.

Soma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya shule kisha uthibitishe

kukubali nafasi hii kwa kulipa mkupuo wa kwanza wa ada kabla ya

tarehe 22/12/2016. Ada isipolipwa katika muda uliotajwa, nafasi

itatolewa kwa mwanafunzi mwingine. Shule itafunguliwa tarehe

31/12/2016.

Utangulizi

KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL ni Shule ya Kiislamu

inayotazama elimu kuwa ni jambo la kwanza na muhimu kwa

mwanadamu. Tunajifunza katika Qur’an kuwa Nabii Adam (a.s) kabla

hajaletwa hapa ulimwenguni kwa kazi yake ya ukhalifa (uongozi),

alielimishwa kwanza kuhusu mazingira yake (Rejea Qur’an, (2:31). Vile

vile tunajifunza kuwa Mtume wa mwisho Muhammad (s.a.w) kabla

hajaanza kazi yake kubwa ya kuhuisha uislamu alipewa kwanza amri

ya kusoma (rejea Qur’an 96:1-5).

Mtume (s.a.w) akasisitiza kuwa ni faradhi (lazima) kwa kila muislamu

mwanamume na kila muislamu mwanamke kutafuta elimu. Pia Mtume

(s.a.w) amesisitiza kuwa elimu itafutwe hata ikibidi ifungiwe safari ya

mbali (Uchina).

Tunalojifunza kutoka katika Qur’an na hadithi sahihi za Mtume (s.a.w)

ni Kuwa, kwanza elimu ni zana ya kwanza ya msingi ambayo muislamu

hana budi kuwa nayo ili aweze kuishi maisha ya kiislamu na awe

Khalifa (kiongozi) wa Allah (s.w) hapa duniani.

Pili, tunajifunza kuwa katika uislamu hapana ubaguzi wa elimu ya

dunia na elimu ya akhera.Kila fani ya elimu inayomwezesha

mwanadamu kufikia lengo la kuwa Khalifa wa Allah (s.w) hapa duniani

ni faradhi (wajibu/lazima) kwa waislamu wote.

Page 2: KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL - ipc.or.tzipc.or.tz/assets/uploads/news/join-kiss-F1-2018.pdfSoma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya ... Tunalojifunza kutoka katika Qur’an

Joining Instructions Kiss 2017 Email: [email protected] Page 2

1. LENGO LA SHULE:

KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL ina malengo ya jumla

yafuatayo:

(i) Kuwaelimisha na kuwalea vijana wa kiislamu kuanzia kidato

cha kwanza hadi kidato cha sita.

(ii) Kuwaandaa vijana kuwa viongozi (Makhalifa) wa kutegemewa

na jamii ya Kiislamu na Taifa kwa ujumla. Ili kufikia malengo

haya shule hii inatoa mafunzo katika kiwango cha kawaida

(O’Level) na kiwango cha juu (A’ Level).

Masomo yanayofundishwa kwa (O’level) ni:

(1)

(2) Qur’an

(3) Lugha ya kiarabu.

(4) English Language

(5) Kiswahili

(6) History

(7) Geography

(8) Basic Mathematics

(9) Pysics

(10)Chemistry

(11)Biology

(12)Commerce

(13)Book Keeping

(14)Civics

(15) Computer Applications

2. MAHALI SHULE ILIPO:

KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL ipo wilaya ya SAME, Mkoani

Kilimanjaro. Ukitokea Dar es Salaam au Tanga shule ipo kati ya

Makanya na SAME mjini umbali wa kilometa kumi (10 km) kabla ya

kufika Same Mjini. Ukitokea Moshi shule ipo kilometa kumi baada ya

kupita SAME mjini. Kutokea Kilipo kibao cha shule hadi shuleni ni

umbali wa kilometa 1.4.

Kwa maelezo zaidi fika Juhudi Studio SAME Mjini mkabala na benki

ya NMB.

Elimu ya Dini ya kiislamu.

Page 3: KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL - ipc.or.tzipc.or.tz/assets/uploads/news/join-kiss-F1-2018.pdfSoma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya ... Tunalojifunza kutoka katika Qur’an

Joining Instructions Kiss 2018 Email: [email protected]

4. USAFIRI:

Wanafunzi watajitegemea kwa usafiri wa kuja shuleni na kurudi

nyumbani wakati wa likizo. Uongozi wa shule utahusika kuwafanyia

mpango wa usafiri wa pamoja ili kutafuta nafuu ya gharama na usalama

wa watoto na hasa wakati wa kufunga shule kwenda likizo

5. ADA YA SHULE :

Ada ya shule kwa mwaka 2017 ni Tshs 1,850,000/=(milioni moja na

laki nane na elfu hamsini tu.)

Ada italipwa kwa mikupuo miwili;

a) Mkupuo wa kwanza Tshs 1,000,000 kabla ya tarehe

24/12/2016.

b) Mkupuo wa pili Tshs 850,000/= kabla ya tarehe za mwanzo

za muhula wa pili 2017.

Ada ya shule, na pesa za matumizi (Pocket money) zitalipwa kupitia

benki.

Majina ya benki, namba za A/c na jina la A/c ni kama ifuatavyo:

(i) Benki ya AMANA A/C No: 005120109690001 kwa jina la

Kirinjiko Islamic Secondary School.

(ii) Benki ya NMB A/C No: 40503500042. kwa jina la Kirinjiko

Islamic Secondary School.

Mambo muhimu ya kuzingatia juu ya malipo:

(a) Wazazi/Walezi wanaoishi au wanaosafiri katika miji yenye

matawi ya Amana Bank, yaani Dar Es salaam, Arusha, Mwanza

n.k wanatakiwa kufanya malipo kupitia Benki ya Amana.

(b) Stakabadhi(receipt) za malipo yote zitaandikiwa shuleni

Kirinjiko Islamic tu.

(c) Nakala kivuli (Photocopy) ya Pay-in-slip haitapokelewa kwa

sababu zozote zile.

Page 4: KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL - ipc.or.tzipc.or.tz/assets/uploads/news/join-kiss-F1-2018.pdfSoma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya ... Tunalojifunza kutoka katika Qur’an

Joining Instructions Kiss 2018 Email: [email protected]

(d) Malipo yakishafanyika hayatarudishwa kwa sababu yoyote ile.

(e) Malipo ya ada lazima yapitie Benki.Fedha taslim

hazitapokelewa shuleni kwa sababu yoyote ile.

(f) Mwisho wa kulipa mkupuo wa kwanza wa ada ni tarehe

24/12/2016. Kulipa mkupuo wa kwanza wa ada ndio

kuthibitisha kukubali nafasi. Kwa hiyo baada ya tarehe tajwa,

kwa mzazi ambaye atakuwa hajafanya malipo haya nafasi ya

mtoto wake itatolewa kwa mhitaji mwingine.

(g) Pay-in-slip ya ada na pocket money ziwe tofauti. Pay-in-slip

iandikwe/ziandikwe jina la mwanafunzi anayelipiwa na

kidato anachosoma ili kuondoa usumbufu unaoweza kujitokeza

(Mfano: 1.Ada ya Ahmed Ally- Form ID. 2.Pocket money ya

Amina Juma -Form IA).

(h) Baada ya kulipa, Tafadhali wasilisha nakala halisi (original)

Pay-in-slips kwa Mhasibu wa shule ili kupatiwa stakabadhi ya

malipo (receipt).

(i) Wanafunzi watakaokuja na pesa za matumizi wanatakiwa

kuziwasilisha kwa Mhasibu na kupatiwa stakabadhi. Upo

utaratibu maalum uliowekwa na shule wa kuwapatia fedha

hizi pale watakapozihitaji kwa matumizi.

(j) Mwanafunzi haruhusiwi kukaa na zaidi ya shs 5,000/-

bwenini.

(k) Shule haitahusika na upotevu wa aina yoyote wa fedha za

mwanafunzi.

6. SARE ZA SHULE

(A) Sare ya Darasani

i) Wavulana

1) Suruali 2 rangi ya “light blue”

Page 5: KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL - ipc.or.tzipc.or.tz/assets/uploads/news/join-kiss-F1-2018.pdfSoma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya ... Tunalojifunza kutoka katika Qur’an

Joining Instructions Kiss 2018 Email: [email protected]

2) Nusu kanzu nyeupe; urefu wa kufika magotini, mikono mirefu,

Isiyopasuliwa na isiyo na kola.

3) Kofia mbili nyeupe zisizokuwa na urembo wa aina yoyote na ziwe za

kitambaa sio za kufuma kwa nyuzi.

4) Viatu vyeusi vya ngozi vya kufunga kamba, unene wa soli

ya viatu usizidi nchi mmoja (1 inch), soksi nyeusi au dark blue.

ii) Wasichana

1) Nusu kanzu mbili (light blue), ndefu zenye mikono mirefu isiyo

na mifuko.

2) Suruali (pajama) 2 za rangi ya light blue.

3) Shungi (juba) 2 nyeupe kubwa ya duara yenye urefu wa

Kufika magotini.

4) Baibui 2 (pana na ndefu) zenye rangi ya zambarau. Aina ya

zambarau inayokusudiwa ni ile tu inayotambulika na kushonwa

shuleni. Ili kuepusha kuharibu vigezo vya sare yetu wanafunzi wote

watashonea sare zao shuleni.

5) Viatu vyeusi vya ngozi vya kufungwa kwa kamba, unene wa soli

ya viatu usizidi nchi moja (1 inch) vifunike miguu,na soksi za dark

blue au nyeusi.

Angalizo:

Mwanafunzi hataruhusiwa kuingia darasani na ikibidi anaweza

kurudishwa nyumbani iwapo atakiuka utaratibu wa sare ya shule hata

kwa kipengele kimoja.

(B) Sare za Nje ya Darasa

(a) Wavulana

i). Suruali 2 nyeusi (siyo Jeans, Lee, wala Corduroy) zilizoshonwa kwa

mshono wa suruali za kawaida na isiyobana.

ii). Fulana 2 za rangi ya dark blue, zenye nembo ya shule

Page 6: KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL - ipc.or.tzipc.or.tz/assets/uploads/news/join-kiss-F1-2018.pdfSoma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya ... Tunalojifunza kutoka katika Qur’an

Joining Instructions Kiss 2018 Email: [email protected]

iii) Kanzu nyeupe

iv) Track-suit nyeusi au Dark bluu na raba kwa ajili ya

michezo/mazoezi.

v) Jacket/sweta lenye rangi ya dark blue au nyeusi lisilo na picha wala

maandishi yoyote kwa ajili ya matumjzi ya kipindi cha baridi.

vi) Gun boot za kawaida.

(b)Wasichana

i). Gauni refu la mikono mirefu la rangi ya damu ya mzee lisilopasuliwa,

lisiloungwa na lisilokuwa na mikunjo kiunoni.

ii). Pajama ya rangi ya damu ya mzee.

iii). Ushungi mkubwa wa mviringo (juba), urefu wa kufika magotini wa

rangi ya damu ya mzee.

iv). Kitenge jozi moja. Kanga hairuhusiwi shuleni.

v). Nguo za michezo: Track suit dark blue au nyeusi na pana kiasi na

fulana isiyobana (dark blue au nyeusi) ya mikono mirefu.

vi). Nguo za kulalia (night dress) – shumizi ndefu 2.

vii) Gun boot za kawaida.

Zingatia:

i) Zaidi ya sare, mwanafunzi hataruhusiwa kuwa na nguo nyingine

yoyote.

ii) Nguo yoyote inayobana au inayoonesha ndani (transparent) au

iliyoshonwa kinyume na maagizo haitakubaliwa kama sare ya shule.

iii) Hairuhusiwi kwa wanafunzi kuvaa mapambo ya aina yoyote wakiwa

shuleni au nje ya shule (likizo) wakati bado ni mwanafunzi wa shule

hii.

iv) Mwanafunzi atakayekiuka utaratibu huu na kuthibitishwa na

uongozi wa Shule, atachukuliwa hatua kali za kinidhamu ikiwa ni

pamoja na Kunyang’anywa mapambo hayo na hatarudishiwa.

Page 7: KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL - ipc.or.tzipc.or.tz/assets/uploads/news/join-kiss-F1-2018.pdfSoma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya ... Tunalojifunza kutoka katika Qur’an

Joining Instructions Kiss 2018 Email: [email protected]

Muhimu:

Ili kuondoa tatizo la kutofautiana kwa rangi za vitambaa na muundo

wa Sare za shule; sare zote za shule zitashonwa hapa shuleni kwa

gharama zilizotajwa kwenye kifungu namba saba (7) (Gharama za

mashono).

7. GHARAMA ZA MASHONO YA SARE ZA SHULE

(A)Sare za Darasani

(i) Wavulana

1. Suruali 1

2. Nusu kanzu 1 Jumla = 30,000.

3. Kofia 1

(ii)Wasichana

1. Baibui 1

2. Pajama 1 Jumla = 30,000/=

3. Nusu kanzu 1

4. Ushungi (Juba) 1

Sare za Nje

(i)Wavulana

1. Suruali nyeusi @ 13,000/= Jumla = 25,000/=

2. Fulana @ 12,000/=

(ii)Wasichana

1. Gauni damu ya mzee 1

2. Pajama 1 Jumla = 27,000/=

3. Ushungi 1

Muhimu:

Page 8: KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL - ipc.or.tzipc.or.tz/assets/uploads/news/join-kiss-F1-2018.pdfSoma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya ... Tunalojifunza kutoka katika Qur’an

Joining Instructions Kiss 2018 Email: [email protected]

(i) Vipimo vya sare vitafanyika hapa shuleni.

(ii)Malipo ya sare za shule yatafanyika hapa shuleni kwa Mhasibu wa

shule.

8. VIFAA VYA MASOMO

Mwanafunzi atalazimika kununua vifaa vyote vya masomo

vinavyohitajika kama vile :

(a) Madaftari makubwa (counter books) ya kila somo. Madaftari ya saizi

ya kati (3Quires) yenye nembo ya shule yanapatikana kwa Tshs 2,5000.

(b) Kalamu na mkebe wa vifaa vya hisabati (Mathematical set).

(c)Licha ya uwepo wa maktaba ya shule, kila mwanafunzi anashauriwa

kujinunulia vitabu vinavyohusiana na masomo yake ili aweze

kujisomea kikamilifu akiwa ndani na nje ya shule.

(d)Kila mwanafunzi aripoti shuleni akiwa na Jalada(Box file) la

kutunzia mitihani na majaribio.

( e) Graph paper pad.

9. VIFAA VYA BWENI:

(i) Godoro la upana wa futi mbili na nusu ( ft x3 lnch). Ili kuondoa

tatizo la kusafiri na magodoro,magodoro yanapatikána hapa shuleni

kwa Tshs 30,000/=.

(ii) Shuka mbili za rangi ya pink pia zinapatikana shuleni kwa Tsh

12,000/= @ Ths 6,000/=.

(iii) Mto na foronya mbili.

(iv) Taulo na blanketi.

(v) Chandarua chá pembe nne. Vyandarua vinapátikana shuleni kwa

Tsh 9,000/=.

(vi) Sabuni za kutosha za kufulia (za unga) na za kuogea.

(vii) Vyombo vya chakula; sahani, bakuli, kikombe, na kijiko. Sahani

na bakuli visiwe vya udongo (nunua stainless steel au pembe).

(viii) Begi kwa ajili ya kuhifadhia vitabu na vitu vingine.

212

Page 9: KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL - ipc.or.tzipc.or.tz/assets/uploads/news/join-kiss-F1-2018.pdfSoma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya ... Tunalojifunza kutoka katika Qur’an

Joining Instructions Kiss 2018 Email: [email protected]

(ix) Ndoo ya kuhifadhia maji.

Zingatia:

Sanduku la chuma (tranker) HALIRUHUSIWI shuleni.

Muhimu:

Mwanafunzi atakapoacha, kufukuzwa au kuhama shule vifaa vyake

kama vile godoro, begi n.k ataondoka navyo. Pindi atakapoviacha, shule

haitakuwa na dhamana ya vifaa hivyo.

10. UANDIKISHWAJI

Siku ya kuripoti shuleni, mwanafunzi awe na vifaa vifuatavyo:

(i) Fomu za Utambulisho wa mwanafunzi na wazazi/walezi wa

mwanafunzi zikiwa zimejazwa na kubandikwa picha.

(ii) Fomu ya daktari (Medical Examination form). Kama mwanafunzi

ana matatizo maalum ya kiafya maelezo ya daktari

yaeleze tahadhari anazotakiwa kuchukua akiwa shuleni.(kiambatis

ho B).

(iii) Fomu ya wajibu wa mzazi/mlezi (kiambatisho C)

(iv) Fedha za kitambulisho TSh. 5,000/=

(v) Pay-in-slip ya malipo ya ada.

(viii) Kitabu-Mwongozo wa mafanikio katika Elimu(Supu ya Elimu)

Shilingi 12,000.

(ix) Msahafu wa tafsiri ya Kiswahili wenye tangulizi za sura wa

(Abdullah Saleh Al

Farsy).Kwa shuleni unapatikana kwa Tshs. 15,000/=.

(x) Kitabu cha kwanza Elimu ya Dini ya Kiislam.Tshs.9,000/=

(xi) Kitabu cha Riyadh Swalihina (Tafsiri ya Kiswahili) Tsh 20,000/=

(xii) Kitabu cha dua na adhkar (HisnulMuslim) cha kiarabu-

Kiswahili.Tsh.2,000.

(xiii) Kitabu cha Lugha ya Kiarabu kidato cha 1 sh.5,000/=

MUHIMU;

• Mwanafunzi atakayeshindwa kukamilisha mahitaji

hatapokelewa.

11. MAENDELEO YA DARASANI.

Page 10: KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL - ipc.or.tzipc.or.tz/assets/uploads/news/join-kiss-F1-2018.pdfSoma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya ... Tunalojifunza kutoka katika Qur’an

Joining Instructions Kiss 2018 Email: [email protected]

Kila mwanafunzi anatakiwa kufanya bidii katika masomo yake kwa

kuhudhuria vipindi vyote, kufanya kazi za darasani katika kila

kipindi, kufanya majaribio na mitihani yote inayotolewa shuleni,

kutumia maktaba ya shule kujisomea vitabu na majarida mbalimbali

ya kielimu ili kujiongezea maarifa zaidi.

Ili kufaulu kuingia kidato kingine, mwanafunzi anatakiwa afikishe

wastani wa angalau alama 50 (daraja C) au zaidi na crediti 7 au zaidi

katika masomo yake yote anayosoma. Crediti ni madaraja C, B na A.

12. KAZI ZA NJE YA DARASA.

Kujibidiisha katika kazi ni katika nidhamu ya kiislamu. Hivyo, kila

mwanafunzi atawajibika kushiriki kikamilifu katika kutenda kazi za

usafi wa mazingira, ujenzi na kazi nyinginezo kama atakavyoelekezwa

na walimu au viongozi wa wanafunzi. Kutegea kazi, iwe ya darasani au

nje ya darasa ni kukiuka maadili anayotarajiwa awe nayo mwanafunzi

wa shule hii na haitavumilika.

13. NIDHAMU

Shule hii ni ya Kiislamu. Hivyo mwenendo wa wanafunzi na

wafanyakazi wake unatarajiwa uwe wa kiislamu. Kukiuka maadili ya

kiislamu kwa mujibu wa Qur’ani tukufu na Sunnah sahihi za Mtume

(S.A.W) ni sawa na kukiuka maadili ya shule. Mwanafunzi yeyote

atakayekiuka kwa makusudi kanuni na mwenendo bora wa shule,

atachukuliwa hatua kali za kinidhamu.

14. KANUNI NA MWENENDO BORA WA SHULE

(i) Kila mwanafunzi wa shule hii anapaswa kutambua kuwa yupo hapa

kwa ajili ya Uislamu. Kwa sababu hiyo chochote kilichopo nje ya

Uislamu hakina nafasi katika shule hii, kiwe kwa maneno au kwa

vitendo.

(ii) Kila mwanafunzi atakuza pendo lake kwa Allah (s.w) na mtume

wake(s.a.w), dini yake na waumini wenzake.

Page 11: KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL - ipc.or.tzipc.or.tz/assets/uploads/news/join-kiss-F1-2018.pdfSoma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya ... Tunalojifunza kutoka katika Qur’an

Joining Instructions Kiss 2018 Email: [email protected]

Pamoja na haki za muumba zilizo juu ya kila Muislam, yamwajibikia

kila mwanafunzi achunge haki na nafasi yake na atumie vipaji vyake

katika uchamungu ndani na nje ya shule.

(iii) Kila mwanafunzi atatumia muda wake vizuri katika

kujielimisha kwa ajili ya Allah (s.w) ikizingatiwa kuwa

kujielimisha kwa ajili ya Alla(s.w) ni amri ya kwanza kwa

kila muislamu.

(iv) Kila mwanafunzi atalazimika kuhudhuria kila kipindi cha

somo, kufanya mazoezi, majaribio ya kila somo na mitihani

yote itakayotolewa shuleni. Mwanafunzi atakayeshindwa

kuhudhuria darasani mfululizo kwa siku tatu au zaidi bila

sababu yoyote ya msingi, atakuwa amejifukuzisha shule.

(v) Kila mwanafunzi anapaswa kuzingatia na kufuata ratiba na

utaratibu wa shule kikamilifu. Ni kosa kubwa kutoonekana

katika eneo husika kwa mujibu wa ratiba kama vile;

kuonekana bwenini wakati wa masomo. Wanafunzi wagonjwa

wanapaswa kuripoti kwa mwalimu wa zamu na darasa ili

wapewe kibali cha kwenda zahanati.

(vi) Wakati wote wa kuja shule au wakati wa kurudi nyumbani,

vazi rasmi ni sare ya shule ya darasani. Kutokuwa na sare

katika wakati huo ni kosa lisilovumilika.

(vii) Wanafunzi wote wanatakiwa wavae nguo za Kiislamu wakiwa

ndani na nje ya shule. Wasichana wavae nguo za kuenea mwili

mzima isipokuwa uso na vitanga vya mikono rejea Qur-an

{24:31}.

(viii) Ni marufuku kwa mwanafunzi wa jinsia yoyote kuvaa

mapambo wakati akiwa shuleni na nje ya shule.

a. Wavulana wavae nguo za heshima na zisizo na maandishi au

picha ya aina yoyote. Hairuhusiwi kuvaa kaptura, jeans, msuli

au carwash katika maeneo ya shule.

b. Hairuhusiwi kwa wasichana kuvaa nguo za kubana, fupi au

zinazoonesha ndani (Transparent) akiwa shuleni au nje ya

shule.

(ix) Ni marufuku kwa mwanafunzi yeyote kufuga kucha, kujipaka

rangi za kucha, rangi za midomo, kupaka hina, kunyoa nyusi,

Page 12: KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL - ipc.or.tzipc.or.tz/assets/uploads/news/join-kiss-F1-2018.pdfSoma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya ... Tunalojifunza kutoka katika Qur’an

Joining Instructions Kiss 2018 Email: [email protected]

kupaka wanja, kutumia manukato kwa wasichana, kuvaa viatu

vya kuchuchumia au vinavyotoa sauti, kukali nywele, kutia

rangi, kusuka rasta au kubadilisha nywele, kucha,kope au

ngozi kwa namna yoyote ile na kufuga nywele kwa wavulana.

Angalizo:

Kwa wasichana itakapobidi kutumia manukato watatumia Nivea ya kupaka kwapani tu (Rolling)ambayo harufu yake ataihisi mpakaji mwenyewe.Ama body spray na manukato ya aina zote ni makosa kukutwa nayo.

(x) Ni marufuku mwanafunzi kuchochea, kushawishi,

kuhamasisha,au kushiriki mgomo kwa namna moja au nyingine

hata kama kuna sababu za msingi. Ni kosa kubwa kugomea amri

au maelekezo ya viongozi wa serikali ya wanafunzi, walimu na

uongozi wa shule kwa ujumla.

(xii) Mwanafunzi asionekane katika vilabu vya pombe, nyumba za

Kupangisha wageni (Guest house), kumbi za dansi na sinema.

(xiii) Kila mwanafunzi ni mlinzi wa mali ya shule, mali yake binafsi

na ya wenzake. Mwanafunzi atakayeharibu,

kusababisha mali ya shule kuharibika, kuibiwa au kupotea

atachukuliwa hatua kali za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kulipa.

Hivyo mwanafunzi atakapogundua wizi au uharibifu wowote dhidi

ya mali ya shule au ya mwanafunzi mwingine atoe taarifa kwa walimu

au viongozi wanaohusika mara moja.

(xiv) Kuiba ni kosa kubwa, mwanafunzi atakayethibitika kuiba mali

ya shule au mwanafunzi mwenzake au nje ya shule atachukuliwa

hatua kali za

kinidhamu ikiwa ni pamoja na kufukuzwa shule.

(xv) Mwanafunzi anapokuwa na shida yoyote hapa shuleni, kwanza

aanze kwa viongozi wanafunzi na ndipo aende kumuona mwalimu wa

zamu au wa Darasa lake, au walimu wengine wanaohusika. Kama

mwanafunzi baada ya kufuata ngazi hizo shida yake haijatatuliwa,

aende kwa Makamu Mkuu wa shule, kisha kwa Mkuu wa shule

itakapobidi kufanya hivyo Mwanafunzi asishitakie shida zake nje ya

shule kabla hajamuona Mkuu wa shule.

Page 13: KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL - ipc.or.tzipc.or.tz/assets/uploads/news/join-kiss-F1-2018.pdfSoma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya ... Tunalojifunza kutoka katika Qur’an

Joining Instructions Kiss 2018 Email: [email protected]

(xvi) Kila mwanafunzi anatakiwa awe msafi wakati wote, ashiriki

vyema katika usafi wa mwili wake binafsi; kitanda, nguo, nywele,

kucha, na usafi wa madarasa, bweni,bwalo la chakula na mazingira ya

shule kwa jumla.

(xvii) Kelele za aina yoyote hazitaruhusiwa, ziwe darasani, kwenye

baraza za madarasa, ndani ya bweni, au popote iwe kwa mwanafunzi

mmoja au wengi (kundi). Tunalazimika kuonesha maadili ya Kiislalmu

katika mazungumzo yetu yote.(Rejea Qur’ani 31:19)

(xviii) Shule haimruhusu mwanafunzi kutoka ndani ya shule na

kulala nje ya eneo la shule bila ya kibali maalum cha maandishi

kilichoidhinishwa na Mkuu wa shule.

Wakati wa mapumziko mafupi (mid-term break) wanafunzi

watabakia katika eneo la shule.Hawataruhusiwa kwenda

nyumbani.

(xix) Mwanafunzi hatakiwi kulala au kwenda katika nyumba za

watumishi isipokuwa kwa dharura maalum itakayoidhinishwa na

Mkuu wa shule.

(xx) Wanafunzi wa jinsia tofauti hawaruhusiwi kuchanganyika katika

jambo lolote bila ya uangalizi wa mwalimu iwe faragha au bayana,

kufanya hivyo ni kosa la kukaribia zinaa ambalo adhabu yake ni

kufukuzwa shule.

(xxi) Kupigana ni kosa kubwa. Mwanafunzi atakayepigana au kumpiga

mwenzake atachukuliwa hatua kali za kinidhamu.

(xxii) Mwanafunzi anapaswa kuripoti shuleni katika tarehe na muda

uliopangwa baada ya likizo, atakapochelewa kwa dharura, taarifa

itolewe kwa Mkuu wa Shule kabla ya kufunguliwa shule, na baada ya

hapo aje na mzazi/mlezi wake anaetambulika kiofisi ndani ya siku

saba (7) baada ya shule kufunguliwa, atakayechelewa zaidi ya hapo

bila taarifa shule haitakuwa na dhamana naye.

(xxiii) Wazazi wa wanafunzi wanaruhusiwa kuwatembelea wanafunzi

(watoto wao)

shuleni siku za Jumapili tu ya kila mwisho wa mwezi. Hata hivyo

Page 14: KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL - ipc.or.tzipc.or.tz/assets/uploads/news/join-kiss-F1-2018.pdfSoma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya ... Tunalojifunza kutoka katika Qur’an

Joining Instructions Kiss 2018 Email: [email protected]

kutokana na uhaba wa makazi shuleni, shule haitahusika

kumpatia mzazi/mlezi malazi atakapomtembelea mwanae.

(xxiv) Wakati wa kuwatembelea wanafunzi, mzazi/mlezi haruhusiwi

kuleta vyakula au vinywaji vya aina yoyote kwa mwanafunzi. Vifaa

vitakavyoletwa kwa wanafunzi vikabidhiwe kwanza kwa mwalimu wa

zamu/darasa ili vikaguliwe.

(xxv) Zaidi ya mashine ya kufanyia hesabu (calculator), vifaa vyote

vya electronics kama vile simu, camera, radio, radio cassette n.k

haviruhusiwi mwanafunzi kuwa navyo katika mazingira ya shule.

Mwanafunzi atakayekutwa navyo vitu hivyo hapa shuleni, atapewa

adhabu kali ikiwa ni pamoja na kufukuzwa shule na havitarudishwa.

(xxvi Ni kosa kwa mwanafunzi kukaa na pesa taslimu bwenini

zinazozidi Tsh 5,000/=. Pesa zote zihifadhiwe kwa Mhasibu wa

shule. Kutakuwa na utaratibu wa kuchukua pesa kiasi kidogo kwa

ajili ya matumizi.

(xxvii) Shule imetenga maeneo maalum kwa ajili ya michezo.Hivyo ni

marufuku mwanafunzi kukutwa anacheza mpira na michezo mingine

ya kutimua vumbi na kushawishi kelele za kishabiki na mfano wake

katika maeneo yanayozunguka bweni,darasa na maeneo mengine mfano

wa hayo nje ya maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya michezo.

(xxviii) Swala ni nguzo kuu ya kumtambulisha mtu kuwa ni muislamu

na ufunguo wa milango ya mafanikio. Hivyo shule haitamvumilia

mwanafunzi yeyote atakayeonekana kupuuza swala kwa makusudi hata

kama ni kwa tabia ya kuchelewachelewa na kukosa jamaa msikitini.

(xxix) Mbali na mzazi kuruhusiwa kumtembelea mtoto wake na kujua

maendeleo yake kitaaluma na kitabia kila Jumamosi na Jumapili

ya mwisho wa mwezi, pia anakaribishwa shuleni au kuwasiliana

na uongozi wa shule wakati wowote kwa lengo la kuleta ufanisi kwa

mwanae na jamii ya waislamu kwa

ujumla.

15. MAKOSA YANAYOWEZA KUSABABISHA KUFUKUZWA SHULE.

Page 15: KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL - ipc.or.tzipc.or.tz/assets/uploads/news/join-kiss-F1-2018.pdfSoma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya ... Tunalojifunza kutoka katika Qur’an

Joining Instructions Kiss 2018 Email: [email protected]

Pamoja na maelezo yote hayo, mwanafunzi atakayechupa kwa makusudi

mipaka ya Uislamu na kuvunja maadili na kanuni za shule kwa

kutenda makosa makubwa kama yalivyoainishwa atafukuzwa shule;

(1) Kunywa pombe.

(2) Kwenda nyumba za starehe kama vile kwenye kumbi za

madansi, disko n.k

(3) Uzinzi au kukaribia zinaa kwa kuwa na rafiki wa jinsia

tofauti (boy Friend/girl friend).

(4) Kuvuta bangi, sigara, madawa ya kulevya, n.k

(5) Kutosimamisha swala

(6) Kumiliki vitu vya electronics kama simu au line, redio,

kamera n.k

(7) Kukaa nje ya shule kwa muda wa siku 3 bila kibali maalum

kilichoidhinishwa na Mkuu wa shule.

(8) Kuanzisha, kuchochea, kushiriki au kuongoza mgomo.

(9) Kuhatarisha amani ya shule kwa kupigana au kuchochea

watu wapigane.

(10) Wizi, uporaji na uharibifu wa mali ya shule na ya

wanafunzi au wakazi wa kituo.

(11) Kukosa mitihani/jaribio bila ya sababu za msingi.

(12) Kutohudhuria masomo/darasani bila sababu maalumu za

msingi.

(13) Kujirudiarudia katika makosa ya uvunjifu wa kanuni na

mwenendo bora wa shule.

16. HITIMISHO

Ni matumaini yetu kuwa Mzazi/ Mlezi na mwanafunzi mtarajiwa

mmeyasoma maelekezo haya vizuri na kwa makini na kuyaelewa

vilivyo.

Mwanafunzi unatakiwa kuzingatia na kutekeleza maelekezo yote ili

kuepusha usumbufu.

Mzazi/Mlezi anashauriwa kujitahidi kushirikiana na shule kwa

kutekeleza wajibu wake kikamilifu ikiwa ni pamoja na kulipa ada kwa

Page 16: KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL - ipc.or.tzipc.or.tz/assets/uploads/news/join-kiss-F1-2018.pdfSoma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya ... Tunalojifunza kutoka katika Qur’an

Joining Instructions Kiss 2018 Email: [email protected]

wakati na kumsimamia mwanae katika maadili ya Kiislamu hasa

wakati wa likizo.

Kirinjiko Islamic Secondary School ni shule yenye mazingira mazuri

sana ya kusoma na malezi ya maadili mema ya kiislamu.

TUNAKUTAKIA MAANDALIZI MEMA NA KARIBU

KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL, KAMA

MWANAFAMILIA MPYA WA KIRINJIKO.

Kauli mbiu: “Soma kwa jina la Mola wako Aliyeumba”(96:1).

MKUU WA SHULE.

2017.

Wabillah Tawfiiq.

Page 17: KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL - ipc.or.tzipc.or.tz/assets/uploads/news/join-kiss-F1-2018.pdfSoma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya ... Tunalojifunza kutoka katika Qur’an

Joining Instructions Kiss 2018 Email: [email protected]

الرحيمبسم هللا لرحمن

KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL

Maelekezo ya Kujiunga na Kidato cha Kwanza

Mwaka 2017.

Soma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya shule kisha uthibitishe kukubali nafasi hii kwa kulipa mkupuo wa kwanza wa ada kabla ya tarehe 22/12/2017. Ada isipolipwa katika muda uliotajwa, nafasi itatolewa kwa mwanafunzi mwingine. Shule itafunguliwa tarehe 30/12/2018.

1.Utangulizi.

KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL ni Shule ya Kiislamu inayotazama elimu kuwa ni jambo la kwanza na muhimu kwa mwanadamu. Tunajifunza katika Qur’an kuwa Nabii Adam (a.s) kabla

hajaletwa hapa ulimwenguni kwa kazi yake ya ukhalifa (uongozi), alielimishwa kwanza kuhusu mazingira yake (Rejea Qur’an, (2:31). Vile vile tunajifunza kuwa Mtume wa mwisho Muhammad

(s.a.w) kabla hajaanza kazi yake kubwa ya kuhuisha uislamu alipewa kwanza amri ya kusoma (rejea Qur’an 96:1-5).

Mtume (s.a.w) akasisitiza kuwa ni faradhi (lazima) kwa kila muislamu mwanamume na kila muislamu mwanamke kutafuta elimu. Pia Mtume (s.a.w) amesisitiza kuwa elimu itafutwe hata ikibidi ifungiwe safari ya mbali (Uchina).

Tunalojifunza kutoka katika Qur’an na hadithi sahihi za Mtume (s.a.w) ni Kuwa, kwanza elimu ni zana ya kwanza ya msingi ambayo muislamu hana budi kuwa nayo ili aweze kuishi maisha ya kiislamu na

awe Khalifa (kiongozi) wa Allah (s.w) hapa duniani. Pili, tunajifunza kuwa katika uislamu hapana ubaguzi wa elimu ya dunia na elimu ya akhera. Kila fani

ya elimu inayomwezesha mwanadamu kufikia lengo la kuwa Khalifa wa Allah (s.w) hapa duniani ni faradhi (wajibu/lazima) kwa waislamu wote.

2. LENGO LA SHULE: KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL ina malengo ya jumla yafuatayo:

(i) Kuwaelimisha na kuwalea vijana wa kiislamu kuanzia kidato cha kwanza hadi kidato cha sita. (ii) Kuwaandaa vijana kuwa viongozi (Makhalifa) wa kutegemewa na jamii ya Kiislamu na Taifa

kwa ujumla. Ili kufikia malengo haya shule hii inatoa mafunzo ya elimu ya sekondari ngazi ya

awali (O’Level) na elimu ya sekondari ngazi ya juu (A’ Level).

Page 18: KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL - ipc.or.tzipc.or.tz/assets/uploads/news/join-kiss-F1-2018.pdfSoma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya ... Tunalojifunza kutoka katika Qur’an

Joining Instructions Kiss 2018 Email: [email protected]

Masomo yanayofundishwa kwa (O’level) ni: 1. Elimu ya diniya kiislam 2. Qur’an 3. Lugha ya kiarabu. 4. English Language 5. Kiswahili 6. History

7. Geography 8. Basic Mathematics

9. Pysics 10. Chemistry 11. Biology 12. Commerce 13. Book Keeping 14. Civics 15. Computer Applications

S/N TITLE PUBLISHER/AUTHOR FORM I

1 History for Secondary Schools Longhorn 8500

2 Kiswahili Shule za Sekondari Oxford 9000

3 Secondary English Oxford 10000

4 Geography For Secondary Schools Azika Juma 9000 5 Civics for Secondary Schools Longhorn 6500

6 Basic Mathematics TIE 10000

7 Fundamental Biology Form One longhorn/mwaniki Gofrey 9,000

8 Physics Oxford 10,500

9 Chemistry Oxford 10,500

10 Oxford Student Dictionary Oxford 21,000

11 Mabala The Farmer Ben and Company Ltd 4000

12 Hawa The Bus Driver Ben and Company Ltd 4000

13 Kalulu the Hare 4500

14 Magic Garden 4000

15 Commerce for sec schools forms 1&2 Nyambani Nyangwine publishers 9000

16 Book for sec schools forms 1&2 Nyambani Nyangwine publishers 9000

TOTAL 138500

ORODHA YA VITABU NA BEI ZAKE KIDATO CHA KWANZA 2017/218

Page 19: KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL - ipc.or.tzipc.or.tz/assets/uploads/news/join-kiss-F1-2018.pdfSoma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya ... Tunalojifunza kutoka katika Qur’an

Joining Instructions Kiss 2018 Email: [email protected]

3. MAHALI SHULE ILIPO:

KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL ipo wilaya ya SAME, Mkoani Kilimanjaro. Ukitokea Dar es Salaam au Tanga shule ipo kati ya Makanya na SAME mjini umbali wa kilometa kumi (10 km) kabla

ya kufika Same Mjini. Ukitokea Moshi shule ipo kilometa kumi baada ya kupita SAME mjini. Kutokea Kilipo kibao cha shule hadi shuleni ni umbali wa kilometa 1.4.

Kwa maelezo zaidi fika Juhudi Studio SAME Mjini mkabala na benki ya NMB.

4. USAFIRI: Wanafunzi watajitegemea kwa usafiri wa kuja shuleni na kurudi nyumbani wakati wa likizo. Uongozi wa shule utahusika kuwafanyia mpango wa usafiri wa pamoja ili kutafuta usalama wa watoto na hasa wakati wa kufunga shule kwenda likizo.

5. ADA YA SHULE : Ada ya shule kwa mwaka 2018 ni Tshs 2,000,000/= (milioni mbili tu.)

Ada italipwa kwa mikupuo miwili; a. Mkupuo wa kwanza Tshs 1,100,000 kabla ya tarehe 22/12/2017.

b. Mkupuo wa pili Tshs 900,000/= kabla ya tarehe 30/06/ 2018. Ada ya shule, na pesa za matumizi (Pocket money) zitalipwa kupitia benki. Majina ya benki, namba za A/c na jina la A/c ni kama ifuatavyo:

i. Benki ya AMANA A/C No: 005120109690001 kwa j ina la Kirinjiko Islamic Secondary School.

ii. Benki ya NMB A/C No: 40503500042. kwa jina la Kirinjiko Islamic Secondary School. Mambo muhimu ya kuzingatia juu ya malipo:

(l) Stakabadhi(receipt) za malipo yote zitaandikiwa shuleni Kirinjiko Islamic tu.

(m) Nakala kivuli (Photocopy) ya Pay-in-slip haitapokelewa kwa sababu zozote zile.

(n) Malipo yakishafanyika hayatarudishwa kwa sababu yoyote ile.

(o) Malipo ya ada lazima yapitie Benki. Fedha taslim hazitapokelewa shuleni kwa sababu yoyote ile.

(p) Mwisho wa kulipa mkupuo wa kwanza wa ada ni tarehe 20/12/2017. Kulipa mkupuo wa kwanza wa ada ndio kuthibitisha kukubali nafasi. Kwa hiyo baada ya tarehe tajwa, kwa mzazi ambaye atakuwa hajafanya malipo haya nafasi ya mtoto wake itatolewa kwa

mhitaji mwingine.

(q) Pay-in-slip ya ada na pocket money ziwe tofauti. Pay-in-slip iandikwe/ziandikwe jina la

mwanafunzi anayelipiwa na kidato anachosoma ili kuondoa usumbufu unaoweza

kujitokeza (Mfano: 1.Ada ya Ahmed Ally- Form ID. 2.Pocket money ya Amina Juma -Form IA). 3. Gharama za Vifaa na vitabu vya Najat Hudhaifa Form 1, n.k.

(r) Baada ya kulipa, Tafadhali wasilisha nakala halisi (original) Pay-in-slips kwa Mhasibu wa shule ili kupatiwa stakabadhi ya malipo (receipt). Hakikisha unatunza stkabadhi ya shule

kipindi chote mpaka mtoto kuhitimu masomo katika ngazi husika.

Page 20: KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL - ipc.or.tzipc.or.tz/assets/uploads/news/join-kiss-F1-2018.pdfSoma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya ... Tunalojifunza kutoka katika Qur’an

Joining Instructions Kiss 2018 Email: [email protected]

(s) Wanafunzi watakaokuja na pesa za matumizi wanatakiwa kuziwasilisha kwa Mhasibu na kupatiwa stakabadhi. Upo utaratibu maalum uliowekwa na shule wa kuwapatia

fedha hizi pale watakapozihitaji kwa matumizi. (t) Mwanafunzi haruhusiwi kukaa na zaidi ya shs 5,000/- bwenini.

(u) Shule haitahusika na upotevu wa aina yoyote wa fedha za mwanafunzi. (v) MWANAFUNZI ASIYEKAMILISHA ADA YA MUHULA HUSIKA HATAPOKELEWA KWA

SABABU YOYOTE NA HATARUHUSIWA KUFANYA MITIHANI YA SHULE.

6. SARE ZA SHULE (A) Sare ya Darasani i ) Wavulana 1. Suruali 2 rangi ya “l ight blue” 2. Nusu kanzu nyeupe; urefu wa kufika magotini, mikono mirefu, Isiyopasuliwa na isiyo na kola. 3. Kofia mbili nyeupe zisizokuwa na urembo wa aina yoyote na ziwe za kitambaa sio za kufuma

kwa nyuzi. 4. Viatu vyeusi vya ngozi vya kufunga kamba, unene wa soli ya viatu usizidi nchi moja (1 inch),

soksi nyeusi au dark blue. i i ) Wasichana

1. Nusu kanzu mbili (l ight blue), ndefu zenye mikono mirefu isiyo na mifuko. 2. Suruali (pajama) 2 za rangi ya light blue.

3. Shungi (juba) 2 nyeupe kubwa ya duara yenye urefu wa Kufika magotini. 4. Baibui 2 (pana na ndefu) zenye rangi ya zambarau. Aina ya zambarau inayokusudiwa ni ile tu

inayotambulika na kushonwa shuleni. Ili kuepusha kuharibu vigezo vya sare yetu wanafunzi wote watashonea sare zao shuleni.

5. Viatu vyeusi vya ngozi vya kufungwa kwa kamba, unene wa soli ya viatu usizidi nchi moja (1 inch) vifunike miguu, na soksi za dark blue au nyeusi.

Angalizo: Mwanafunzi hataruhusiwa kuingia darasani na ikibidi anaweza kurudishwa nyumbani iwapo atakiuka

utaratibu wa sare ya shule hata kwa kipengele kimoja.

(B) Sare za Nje ya Darasa

(a) Wavulana

1. Suruali 2 nyeusi (siyo Jeans, Lee, wala Corduroy) zilizoshonwa kwa mshono wa suruali za kawaida na isiyobana.

2. Fulana 2 za rangi ya dark blue, zenye nembo ya shule

3. Kanzu nyeupe 4. Track-suit nyeusi au Dark bluu na raba kwa ajili ya michezo/mazoezi.

5. Jacket/sweta lenye rangi ya dark blue au nyeusi lisilo na picha wala maandishi yoyote kwa ajili ya matumjzi ya kipindi cha baridi.

6. Gun boot za kawaida.

Page 21: KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL - ipc.or.tzipc.or.tz/assets/uploads/news/join-kiss-F1-2018.pdfSoma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya ... Tunalojifunza kutoka katika Qur’an

Joining Instructions Kiss 2018 Email: [email protected]

(b)Wasichana

1. Gauni refu la mikono mirefu la rangi ya damu ya mzee lisilopasuliwa, lisiloungwa na lisilokuwa

na mikunjo kiunoni. 2. Pajama ya rangi ya damu ya mzee.

3. Ushungi mkubwa wa mviringo (juba), urefu wa kufika magotini wa rangi ya damu ya mzee. 4. Kitenge jozi moja. Kanga hairuhusiwi shuleni.

5. Nguo za michezo: Track suit dark blue au nyeusi na pana kiasi na fulana isiyobana (dark blue

au nyeusi) ya mikono mirefu. 6. Nguo za kulalia (night dress) – shumizi ndefu 2.

7. Gun boot za kawaida.

Zingatia:

i. Zaidi ya sare, mwanafunzi hataruhusiwa kuwa na nguo nyingine yoyote.

ii. Nguo yoyote inayobana au inayoonesha ndani (transparent) au iliyoshonwa kinyume na maagizo haitakubaliwa kama sare ya shule.

iii. Hairuhusiwi kwa wanafunzi kuvaa mapambo ya aina yoyote wakiwa shuleni au nje ya shule

(likizo) wakati bado ni mwanafunzi wa shule hii. iv. Mwanafunzi atakayekiuka utaratibu huu na kuthibitishwa na uongozi wa Shule,

atachukuliwa hatua kali za kinidhamu ikiwa ni pamoja na Kunyang’anywa mapambo hayo na hatarudishiwa.

MUHIMU:

Ili kuondoa tatizo la kutofautiana kwa rangi za vitambaa na muundo wa Sare za shule; sare zote za shule zitashonwa hapa shuleni kwa gharama zilizotajwa kwenye kifungu namba saba (7) (Gharama za mashono).

7. GHARAMA ZA MASHONO YA SARE ZA SHULE (A)Sare za Darasani

( i ) Wavulana 1. Suruali 1 2. Nusu kanzu 1 Jumla = 30,000.

3. Kofia 1

( i i)Wasichana

1. Baibui 1 2. Pajama 1 Jumla = 30,000/= 3. Nusu kanzu 1 4. Ushungi (Juba) 1

Page 22: KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL - ipc.or.tzipc.or.tz/assets/uploads/news/join-kiss-F1-2018.pdfSoma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya ... Tunalojifunza kutoka katika Qur’an

Joining Instructions Kiss 2018 Email: [email protected]

Sare za Nje (i )Wavulana

1. Suruali nyeusi @ 13,000/= Jumla = 25,000/= 2. Fulana (dark blue) @ 12,000/=

( i i)Wasichana

1. Gauni damu ya mzee 1

2. Pajama 1 Jumla = 27,000/= 3. Ushungi 1 Muhimu: (i) Vipimo vya sare vitafanyika hapa shuleni. (ii)Malipo ya sare za shule yatafanyika hapa shuleni kwa Mhasibu wa shule.

8. VIFAA VYA MASOMO Mwanafunzi atalazimika kununua vifaa vyote vya masomo vinavyohitajika kama vile :

(a) Madaftari makubwa (counter books) ya kila somo. Madaftari ya saizi ya kati (3Quires) yenye nembo ya shule yanapatikana kwa Tshs 2,5000.

(b) Kalamu na mkebe wa vifaa vya hisabati (Mathematical set). (c) Licha ya uwepo wa maktaba ya shule, kila mwanafunzi anashauriwa kujinunulia vitabu

vinavyohusiana na masomo yake ili aweze kujisomea kikamilifu akiwa ndani na nje ya shule. (d) Kila mwanafunzi aripoti shuleni akiwa na Jalada(Box file) la kutunzia mitihani na majaribio. (e) Graph paper pad.

9. VIFAA VYA BWENI:

i. Godoro la upana wa futi mbili na nusu ( ft x3 lnch). Ili kuondoa tatizo la kusafiri na

magodoro, magodoro yanapatikána hapa shuleni kwa Tshs 38,000/= ii. Shuka mbili za rangi ya pink pia zinapatikana shuleni kwa Tsh 13,000/= @ Ths 6,500/=.

iii. Mto na foronya mbili. Tsh. 12,000. iv. Blanketi Tsh. 15,000.

v. Chandarua chá pembe nne. Vyandarua vinapátikana shuleni kwa Tsh 9,000/=. vi. Sabuni za kutosha za kufulia (za unga) na za kuogea.

vii. Vyombo vya chakula; sahani, bakuli, kikombe, na kijiko. Sahani na bakuli visiwe vya udongo (nunua stainless steel au pembe).

viii. Begi kwa ajili ya kuhifadhia vitabu na vitu vingine. ix. Ndoo ya LITA 10 kwa ajili ya kuhifadhia maji.

Zingatia: Sanduku la chuma (tranker) HALIRUHUSIWI shuleni.

Muhimu: Mwanafunzi atakapoacha, kufukuzwa au kuhama shule vifaa vyake kama vile godoro, begi n.k

ataondoka navyo. Pindi atakapoviacha, shule haitakuwa na dhamana ya vifaa hivyo.

212

Page 23: KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL - ipc.or.tzipc.or.tz/assets/uploads/news/join-kiss-F1-2018.pdfSoma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya ... Tunalojifunza kutoka katika Qur’an

Joining Instructions Kiss 2018 Email: [email protected]

10. UANDIKISHWAJI Siku ya kuripoti shuleni, mwanafunzi awe na vifaa vifuatavyo:

i) Fomu za Utambulisho wa mwanafunzi na wazazi/walezi wa mwanafunzi zikiwa zimejazwa na kubandikwa picha.

ii) Fomu ya daktari (Medical Examination form). Kama mwanafunzi ana matatizo maalum ya kiafya maelezo ya daktari

yaeleze tahadhari anazotakiwa kuchukua akiwa shuleni.(kiambatisho B). iii) Fomu ya wajibu wa mzazi/mlezi (kiambatisho C)

iv) Fedha za kitambulisho TSh. 5,000/= v) Pay-in-slip ya malipo ya ada. vi) Kitabu-Mwongozo wa mafanikio katika Elimu (Supu ya Elimu) Shilingi 12,000. vii) Msahafu wa tafsiri ya Kiswahili wenye tangulizi za sura wa (Abdullah Saleh Al Farsy).Kwa

shuleni unapatikana kwa Tshs. 15,000/=. viii) Kitabu cha kwanza Elimu ya Dini ya Kiislam.Tshs.9,000/= ix) Kitabu cha Riyadh Swalihina (Tafsiri ya Kiswahili) Tsh 20,000/=

x) Kitabu cha Lugha ya Kiarabu kidato cha 1 sh.5,000/= xi) Qur-an na sunna Juzuu ya tatu DWW. Tsh.9000/=

xii) Jalada la kuhifadhia nyaraka za taaluma. 5000/= MUHIMU

• Mwanafunzi atakayeshindwa kukamilisha mahitaji haya hatapokelewa. 11. MAENDELEO YA DARASANI. Kila mwanafunzi anatakiwa kufanya bidii katika masomo yake kwa kuhudhuria vipindi vyote,

kufanya kazi za darasani katika kila kipindi, kufanya majaribio na mitihani yote inayotolewa shuleni, kutumia maktaba ya shule kujisomea vitabu na majarida mbalimbali ya kielimu ili kujiongezea maarifa zaidi. Ili kufaulu kuingia kidato kingine, mwanafunzi anatakiwa afikishe wastani wa angalau alama 50 (daraja C) au zaidi na crediti 7 au zaidi katika masomo yake yote anayosoma. Crediti ni madaraja C, B na A. 12. KAZI ZA NJE YA DARASA.

Kujibidiisha katika kazi ni katika nidhamu ya kiislamu. Hivyo, kila mwanafunzi atawajibika kushiriki kikamilifu katika kutenda kazi za usafi wa mazingira, ujenzi na kazi nyinginezo kama

atakavyoelekezwa na walimu au viongozi wa wanafunzi. Kutegea kazi, iwe ya darasani au nje ya

darasa ni kukiuka maadili anayotarajiwa awe nayo mwanafunzi wa shule hii na haitavumilika. 13. NIDHAMU

Shule hii ni ya Kiislamu. Hivyo mwenendo wa wanafunzi na wafanyakazi wake unatarajiwa uwe wa kiislamu. Kukiuka maadili ya kiislamu kwa mujibu wa Qur’ani tukufu na Sunnah sahihi za Mtume (S.A.W) ni sawa na kukiuka maadili ya shule. Mwanafunzi yeyote atakayekiuka kwa makusudi kanuni na mwenendo bora wa shule, atachukuliwa hatua kali za kinidhamu.

Page 24: KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL - ipc.or.tzipc.or.tz/assets/uploads/news/join-kiss-F1-2018.pdfSoma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya ... Tunalojifunza kutoka katika Qur’an

Joining Instructions Kiss 2018 Email: [email protected]

14. KANUNI NA MWENENDO BORA WA SHULE

(i) Kila mwanafunzi wa shule hii anapaswa kutambua kuwa yupo hapa kwa ajili ya Uislamu. Kwa sababu hiyo chochote kilichopo nje ya Uislamu hakina nafasi katika shule hii, kiwe kwa maneno au kwa vitendo.

(ii) Kila mwanafunzi atakuza pendo lake kwa Allah (s.w) na mtume wake (s.a.w), dini yake na

waumini wenzake. Pamoja na haki za muumba zilizo juu ya kila Muislam, yamwajibikia kila mwanafunzi

achunge haki na nafasi yake na atumie vipaji vyake katika uchamungu ndani na nje ya shule.

(iii) Kila mwanafunzi atatumia muda wake vizuri katika kujielimisha kwa ajili ya Allah (s.w) ikizingatiwa kuwa kujielimisha kwa ajili ya Alla(s.w) ni amri ya kwanza kwa kila muislamu.

(iv) Kila mwanafunzi atalazimika kuhudhuria kila kipindi cha somo, kufanya mazoezi, majaribio ya kila somo na mitihani yote itakayotolewa shuleni. Mwanafunzi atakayeshindwa

kuhudhuria darasani mfululizo kwa siku tatu au zaidi bila sababu yoyote ya msingi, atakuwa amejifukuzisha shule.

(v) Kila mwanafunzi anapaswa kuzingatia na kufuata ratiba na utaratibu wa shule kikamilifu.

Ni kosa kubwa kutoonekana katika eneo husika kwa mujibu wa ratiba kama vile; kuonekana bwenini wakati wa masomo. Wanafunzi wagonjwa wanapaswa kuripoti kwa mwalimu wa

zamu na darasa ili wapewe kibali cha kwenda zahanati. (vi) Wakati wote wa kuja shule au wakati wa kurudi nyumbani, vazi rasmi ni sare ya shule ya

darasani. Kutokuwa na sare katika wakati huo ni kosa lisilovumilika. (vii) Wanafunzi wote wanatakiwa wavae nguo za Kiislamu wakiwa ndani na nje ya shule.

Wasichana wavae nguo za kuenea mwili mzima isipokuwa uso na vitanga vya mikono rejea Qur-an {24:31}.

(viii) Ni marufuku kwa mwanafunzi wa jinsia yoyote kuvaa mapambo wakati akiwa shuleni na nje ya shule.

a. Wavulana wavae nguo za heshima na zisizo na maandishi au picha ya aina yoyote. Hairuhusiwi kuvaa kaptura, jeans, msuli au carwash katika maeneo ya shule.

b. Hairuhusiwi kwa wasichana kuvaa nguo za kubana, fupi au zinazoonesha ndani (Transparent) akiwa shuleni au nje ya shule.

(ix) Ni marufuku kwa mwanafunzi yeyote kufuga kucha, kujipaka rangi za kucha , rangi za

midomo, kupaka hina, kunyoa nyusi, kupaka wanja, kutumia manukato kwa wasichana, kuvaa viatu vya kuchuchumia au vinavyotoa sauti, kukali nywele, kutia rangi, kusuka rasta

au kubadilisha nywele, kucha,kope au ngozi kwa namna yoyote ile na kufuga nywele kwa wavulana.

Angalizo: Kwa wasichana itakapobidi kutumia manukato watatumia Nivea ya kupaka kwapani tu

(Rolling)ambayo harufu yake ataihisi mpakaji mwenyewe. Ama body spray na manukato

ya aina zote ni makosa kukutwa nayo. (x) Ni marufuku mwanafunzi kuchochea, kushawishi, kuhamasisha, au kushiriki mgomo kwa

namna moja au nyingine hata kama kuna sababu za msingi. Ni kosa kubwa kugomea amri au maelekezo ya viongozi wa serikali ya wanafunzi, walimu na uongozi wa shule kwa

ujumla.

Page 25: KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL - ipc.or.tzipc.or.tz/assets/uploads/news/join-kiss-F1-2018.pdfSoma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya ... Tunalojifunza kutoka katika Qur’an

Joining Instructions Kiss 2018 Email: [email protected]

(xi) Mwanafunzi asionekane katika vilabu vya pombe, nyumba za Kupangisha wageni (Guest house), kumbi za dansi na sinema.

(xii) Kila mwanafunzi ni mlinzi wa mali ya shule, mali yake binafsi na ya wenzake. Mwanafunzi atakayeharibu, kusababisha mali ya shule kuharibika, kuibiwa au kupotea atachukuliwa

hatua kali za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kulipa. Hivyo mwanafunzi atakapogundua wizi au uharibifu wowote dhidi ya mali ya shule au ya mwanafunzi mwingine atoe taarifa kwa

walimu au viongozi wanaohusika mara moja. (xiii) Kuiba ni kosa kubwa, mwanafunzi atakayethibitika kuiba mali ya shule au ya mwanafunzi

mwenzake au nje ya shule atachukuliwa hatua kali za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kufukuzwa shule.

(xiv) Mwanafunzi anapokuwa na shida yoyote hapa shuleni, kwanza aanze kwa viongozi wanafunzi na ndipo aende kumuona mwalimu wa zamu au wa Darasa lake, au walimu wengine wanaohusika. Kama mwanafunzi baada ya kufuata ngazi hizo shida yake haijatatuliwa, aende kwa Makamu Mkuu wa shule, kisha kwa Mkuu wa shule itakapobidi kufanya hivyo Mwanafunzi asishitakie shida zake nje ya shule kabla hajamuona Mkuu wa

shule. (xv) Kila mwanafunzi anatakiwa awe msafi wakati wote, ashiriki vyema katika usafi wa mwili

wake binafsi; kitanda, nguo, nywele, kucha, na usafi wa madarasa, bweni,bwalo la chakula na mazingira ya shule kwa jumla.

(xvi) Kelele za aina yoyote hazitaruhusiwa, ziwe darasani, kwenye baraza za madarasa, ndani ya bweni, au popote iwe kwa mwanafunzi mmoja au wengi (kundi). Tunalazimika kuonesha maadili ya Kiislalmu katika mazungumzo yetu yote.(Rejea Qur’ani 31:19)

(xvii) Shule haimruhusu mwanafunzi kutoka ndani ya shule na kulala nje ya eneo la shule bila ya kibali maalum cha maandishi kilichoidhinishwa na Mkuu wa shule. Wakati wa mapumziko mafupi (mid-term break) wanafunzi watabakia katika eneo la shule. Hawataruhusiwa kwenda nyumbani.

(xviii) Mwanafunzi hatakiwi kulala au kwenda katika nyumba za watumishi isipokuwa kwa

dharura maalum itakayoidhinishwa na Mkuu wa shule. (xix) Wanafunzi wa jinsia tofauti hawaruhusiwi kuchanganyika katika jambo lolote bila ya

uangalizi wa mwalimu iwe faragha au bayana, kufanya hivyo ni kosa la kukaribia zinaa ambalo adhabu yake ni kufukuzwa shule.

(xx) Kupigana ni kosa kubwa. Mwanafunzi atakayepigana au kumpiga mwenzake atachukuliwa hatua kali za kinidhamu.

(xxi) Mwanafunzi anapaswa kuripoti shuleni katika tarehe na muda uliopangwa baada ya likizo, atakapochelewa kwa dharura, taarifa itolewe kwa Mkuu wa Shule kabla ya kufunguliwa shule, na baada ya hapo aje na mzazi/mlezi wake anaetambulika kiofisi ndani ya siku saba

(7) baada ya shule kufunguliwa, atakayechelewa zaidi ya hapo bila taarifa shule haitakuwa na dhamana naye.

(xxii) Wazazi wa wanafunzi wanaruhusiwa kuwatembelea wanafunzi (watoto wao) shuleni kulingana na ratiba iliyoainishwa na uongozi wa shule hapo chini na si vinginevyo. Hata

hivyo kutokana na uhaba wa makazi shuleni, shule haitahusika kumpatia mzazi/mlezi malazi atakapomtembelea mwanae.

Page 26: KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL - ipc.or.tzipc.or.tz/assets/uploads/news/join-kiss-F1-2018.pdfSoma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya ... Tunalojifunza kutoka katika Qur’an

Joining Instructions Kiss 2018 Email: [email protected]

RATIBA YA KUWATEMBELEA WANAFUNZI KWA MUHULA HUU NI KAMA INAVYOONEKANA HAPA

CHINI.

1. TAREHE: 28/01/2018.

2. TAREHE : 25/02/2018.

3. TEREHE : 01/04/2018. 4. TAREHE: 29/04/2018. ANGALIZO: Tunapenda kuwakumbusha wazazi kuwa mtu pekee anayeruhusiwa kumtembelea mwanafunzi ni mzazi au mlezi anayetambulika katika nyaraka muhimu za utambulisho wa wazazi/walezi za shule tu, na si vinginevyo. Haturuhusu vyakula wala vinywaji vya aina yoyote wakati wa kumtembelea mwanafunzi.

(xxiii) Wakati wa kuwatembelea wanafunzi, mzazi/mlezi haruhusiwi kuleta vyakula au vinywaji vya aina yoyote kwa mwanafunzi. Vifaa vitakavyoletwa kwa wanafunzi vikabidhiwe kwanza

kwa mwalimu wa zamu/darasa ili vikaguliwe. (xxiv) Zaidi ya mashine ya kufanyia hesabu (calculator), vifaa vyote vya electronics kama vile simu,

camera, radio, radio cassette n.k haviruhusiwi mwanafunzi kuwa navyo katika mazingira ya shule. Mwanafunzi atakayekutwa navyo vitu hivyo hapa shuleni, atapewa adhabu kali ikiwa ni pamoja na kufukuzwa shule na havitarudishwa.

(xxv) Ni kosa kwa mwanafunzi kukaa na pesa taslimu bwenini zinazozidi Tsh 5,000/=. Pesa zote zihifadhiwe kwa Mhasibu wa shule. Kutakuwa na utaratibu wa kuchukua pesa kiasi kidogo

kwa ajili ya matumizi. (xxvi) Shule imetenga maeneo maalum kwa ajili ya michezo.Hivyo ni marufuku mwanafunzi

kukutwa anacheza mpira na michezo mingine ya kutimua vumbi na kushawishi kelele za kishabiki na mfano wake katika maeneo yanayozunguka bweni,darasa na maeneo mengine

mfano wa hayo nje ya maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya michezo. (xxvii) Swala ni nguzo kuu ya kumtambulisha mtu kuwa ni muislamu na ufunguo wa milango ya

mafanikio. Hivyo shule haitamvumilia mwanafunzi yeyote atakayeonekana kupuuza swala kwa makusudi hata kama ni kwa tabia ya kuchelewachelewa na kukosa jamaa msikitini.

(xxviii) Mbali na mzazi kuruhusiwa kumtembelea mtoto wake na kujua maendeleo yake kitaaluma na kitabia kila Jumapili ya mwisho wa mwezi, pia anakaribishwa shuleni au kuwasiliana na uongozi wa shule wakati wowote kwa lengo la kuleta ufanisi kwa mwanae na jamii ya waislamu kwa ujumla.

Page 27: KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL - ipc.or.tzipc.or.tz/assets/uploads/news/join-kiss-F1-2018.pdfSoma kwa makini taarifa na maelekezo juu ya ... Tunalojifunza kutoka katika Qur’an

Joining Instructions Kiss 2018 Email: [email protected]

15. MAKOSA YANAYOWEZA KUSABABISHA KUFUKUZWA SHULE.

Pamoja na maelezo yote hayo, mwanafunzi atakayechupa kwa makusudi mipaka ya Uislamu na kuvunja maadili na kanuni za shule kwa kutenda makosa makubwa kama yalivyoainishwa

atafukuzwa shule; i. Kunywa pombe.

ii. Kwenda nyumba za starehe kama vile kwenye kumbi za madansi, disko n.k iii. Uzinzi au kukaribia zinaa kwa kuwa na rafiki wa jinsia tofauti (boy Friend/girl friend).

iv. Kuvuta bangi, sigara, madawa ya kulevya, n.k v. Kutosimamisha swala vi. Kumiliki vitu vya electronics kama simu au line, redio, kamera n.k

vii. Kukaa nje ya shule kwa muda wa siku 3 bila kibali maalum kilichoidhinishwa na Mkuu wa shule.

viii. Kuanzisha, kuchochea, kushiriki au kuongoza mgomo. ix. Kuhatarisha amani ya shule kwa kupigana au kuchochea watu wapigane.

x. Wizi, uporaji na uharibifu wa mali ya shule na ya wanafunzi au wakazi wa kituo. xi. Kukosa mitihani/jaribio bila ya sababu za msingi.

xii. Kutohudhuria masomo/darasani bila sababu maalumu za msingi . xiii. Kujirudiarudia katika makosa ya uvunjifu wa kanuni na mwenendo bora wa shule.

16. HITIMISHO Ni matumaini yetu kuwa Mzazi/ Mlezi na mwanafunzi mtarajiwa mmeyasoma maelekezo haya vizuri na kwa makini na kuyaelewa vilivyo. Mwanafunzi unatakiwa kuzingatia na kutekeleza maelekezo yote ili kuepusha usumbufu. Mzazi/Mlezi anashauriwa kujitahidi kushirikiana na shule kwa kutekeleza wajibu wake kikamilifu ikiwa ni pamoja na kulipa ada kwa wakati na kumsimamia mwanae katika maadili ya Kiislamu hasa wakati wa likizo.

Kirinjiko Islamic Secondary School ni shule yenye mazingira mazuri sana ya kusoma na malezi ya maadili mema ya kiislamu.

TUNAKUTAKIA MAANDALIZI MEMA NA KARIBU

KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL, KAMA MWANAFAMILIA MPYA WA

KIRINJIKO.

Kauli mbiu: “Soma kwa jina la Mola wako Aliyeumba”(96:1). MKUU WA SHULE.

2017. Wabillah Tawfiiq.