15
Big result now ufaulu mkubwa sasa Big result now ufaulu mkubwa sasa Big result now ufaulu mkubwa sasa MBINU ZA KUFAULU MITIHANI Mimi najiandaa kufaulu mtihani wewe je? GEOPHREY E. SANGA @2015 GEOPHREY E. SANGA 2015 GEOPHREY E. SANGA 2015 GEOPHREY E. SANGA Kitabu hiki kinalenga kumsaidia mwanafunzi kumwelekeza njia mbadala za usomaji na jinsi ya kujiandaa na mtihani. Kitabu hiki kinamsaidia mwanafunzi kujua namna ya kusoma namna na kukabiliana na mtihani na namna ya kujibu maswali ya mtihani. Kupitia kitabu hiki mwanafunzi atajiamini wakati wa mtihani na hivyo kupelekea ufaulu mkubwa. GEOPHREY E. SANGA ni mwalimu wa masomo ya sanaa na TEHAMA (ICT), amehitimu shahada ya kwanza ya elimu katika chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) (Bed ICT) Amehitimu kidato cha sita katika shule ya secondary TUKUYU, kidato cha nne katika shule ya sekondari IPANDE na alihitimu shule ya msingi NKOKWA Kimepigwa chapa na kabuje stationary @2015 Kyela-Mbeya- Tanzania

Mbinu za usomaji na kufaulu mitihani

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Mbinu za usomaji na kufaulu mitihani

Big result now ufaulu mkubwa sasa Big result now ufaulu mkubwa sasa Big result now ufaulu mkubwa sasa

MBINU ZA

KUFAULU

MITIHANI

Mimi najiandaa

kufaulu mtihani

wewe je?

GEOPHREY E. SANGA @2015 GEOPHREY E. SANGA 2015 GEOPHREY E. SANGA 2015 GEOPHREY E. SANGA

Kitabu hiki kinalenga kumsaidia mwanafunzi

kumwelekeza njia mbadala za usomaji na jinsi ya

kujiandaa na mtihani. Kitabu hiki kinamsaidia

mwanafunzi kujua namna ya kusoma namna na

kukabiliana na mtihani na namna ya kujibu maswali

ya mtihani.

Kupitia kitabu hiki mwanafunzi atajiamini wakati wa

mtihani na hivyo kupelekea ufaulu mkubwa.

GEOPHREY E. SANGA ni mwalimu wa

masomo ya sanaa na TEHAMA (ICT),

amehitimu shahada ya kwanza ya

elimu katika chuo kikuu cha Dodoma

(UDOM) (Bed –ICT)

Amehitimu kidato cha sita katika shule ya secondary

TUKUYU, kidato cha nne katika shule ya sekondari

IPANDE na alihitimu shule ya msingi NKOKWA

Kimepigwa chapa na

kabuje stationary @2015

Kyela-Mbeya- Tanzania

Page 2: Mbinu za usomaji na kufaulu mitihani

Kitabu hiki kimeandaliwa na

SANGA GEOPHREY

0655-425-315

0753 425 315

[email protected]

Na kupigwa chapa na

Kabuje stationary printer

[email protected]

© 2015

Kyela-Mbeya-Tanzania

Haki zote zimehifadhiwa huruhusiwi kunakili kitabu hiki au sehemu ya kitabu hiki bila idhini ya mchapishaji

au mwandishi wa kitabu hiki.

Page 3: Mbinu za usomaji na kufaulu mitihani

SHUKRANI

Shukrani zangu za pekee ziende kwa wenyezi mungu mwingi wa

rehema anayenijaalia afya njema na kunifanya niwe mzima ili

niendelee kuifanya kazi hii, na kunikarimu uwezo wa kiakiri na

maarifa katika kuandika kitabu hiki.

Pia shukrani zangu ziende kwa familia yangu (Mariamu Kabuje na

Jamaly Sanga) kwani wamenisaidia mchango wao wa hali na mali

na kunitia moyo katika uaandaaji wa kitabu hiki

Pia niwashukuru wale waliotoa mchango wao wa mawazo juu ya

kuandaa kitabu hiki. Wapo wengi sana ntawataja wachache tu,

nimshukuru Happiness George Tarimo mwalimu wa saikolojia,

Kiswahili na Geograph kwa mchango wake mkubwa

Mwisho niwashukuru walimu wangu wote wa walio nipa maarifa ya

kufika hapa nilipo. Shukrani kwa walimu wa shule ya msingi

nkokwa (1991-2005), walimu wa shule ya sekondari Ipande[o-level]

(2006-2009), walimu wa shule ya sekondari Tukuyu[A-level] (2010-

2012) pamoja na wahadhiri wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM)

kitibo cha elimu (2012-2015)

Page 4: Mbinu za usomaji na kufaulu mitihani

UTANGULIZI

Kitabu hiki kimeandaliwa kwa lengo la kumsaidia mwanafunzi kufaulu mitihadi

yake vizuri. Kitabu hiki kitamwongoza mwanafunzi namna ya kusoma wakati wa

kujiandaa na mitihani. Kitamwongoza na kumpatia mwanafuzi njia au mbinu bora za

kujiaandaa na mitihani

Pia kitabu hiki kinampa mwanafunzi mbinu bora za kukabiliana na mtihani siku ya

mtihani na siku zote awapo kwenye mchakato wa ufanyaji mtihani.

Kitabu hiki hakikusahau pia kumweleza mwanafunzi uhusiano wake na jamii yake

yaani wazazi na walimu wake kwani nao wana mchango mkubwa katika ufaulu wa

mwanafunzi.

Page 5: Mbinu za usomaji na kufaulu mitihani

TABARUKU

Kitabu hiki nakitabaruku kwa Familia yangu ya Mariamu Kabuje kwani wao ni

tegemeo langu la pekee.

Mungu awape maisha marefu na mzidi kumtegemea yeye.

Kupitia kuandika kitabu hiki nimejifunza vitu vingi sana na sitaacha kuandika kama

mwenyezi mungu ataendelea kunipa afya na akili

“si rahisi kupaza sauti kutoka nyikani na ukapata msaada kwa haraka”

Page 6: Mbinu za usomaji na kufaulu mitihani

SURA YA KWANZA

UTANGULIZI.

Wanafunzi wengi wamekuwa wakijiuliza maswali mengi juu ya namna ambayo wanaweza kufauru

mitihani yao.

Wingi wamekua wakijua swala la kufauru mitihani ni swala la watu wachache (wenye akili), lakini

ukweli ni kwamba hakuna mtu mwenye akili na asiye na akili wala mwenye akili bali

tunatofautiana IQ (uwezo binafsi) . uwezo huu ndio unamfanya mtu kuelewa haraka ama

kuchelewa kuelewa ila mwisho wa siku wote tunaelewa kwa pamoja haijalishi unaelewa haraka au

umechelewa kuelewa lengo ni kuelewa.

Licha ya IQ kutofautiana wengine huwa na IQ kubwa lakini bado wanachelewa kuelewa kutokana

na mbinu wanazotumia kusoma. Kitabu hiki kitakupa mbinu mbalimbali zitakazo kuwezesha

wewe kama mwanafunzi kuweza kufauru mtihani wako haijalishi unasoma shule ya kata (wengine

huziita shule za kayumba) au unasoma shule za private kitabu hiki kitasaidia sana kufikia malengo

yako ya ufauru mkubwa sasa (big result now)

MASWALI 10 YA KUJIULIZA.

1. Mtihani ni nini?

2. Kwa nini kuna mitihani?

3. Anayetunga mtihani ni nani?

4. Kwa nini anatunga mitihani?

5. Maswali ya mtihani yanatoka wapi?

6. Kwanini tunafeli mitihani?

7. Mtihani unajibiwa ukiwa na hali ganii (mud)?

8. Ntafanyeje ili kuweza kufaulu mitihani yangu?

9. Nifanye vitu gani kabla ya kuingia kwenye chumba cha mtihani?

10. Ni kina nani wanaopaswa kufaulu mitihani?

Maswali haya na mengine mengi yatajibiwa ndani ya kitabu hiki ili kuweza kumtoa mwanafunzi

katika hali ya kujiuliza maswali mengi kuhusiana na mtihani ili kumsaidia kuukabili mtihani bila

kuwa na maswali mengi ya kujiuliza mwisho wa siku matokeo makubwa.

MAJIBU YA MASWALI

Page 7: Mbinu za usomaji na kufaulu mitihani

Maswali haya yatajibiwa kwa ufupi na kwaeleweka katika sehemu hii, yataendelea kujibiwa kwa

undani na kwa maelezo ya kina katika sehemu nyingine kadri utakavo edelea kusoma itabu hiki

utapata majibu ya ziada. Tuanze swali moja baada ya linguine.

1. Mtihani ni nini?

Mtihani ni jumla ya maswali yaliyoandaliwa kutoka kwenye mada alizosoma mwanafunzi darasani

kwa lengo la kumpima kama ameelewa ama hakuelewa kwenye mchakato wa ujifunzaji. Mtihani

uweza kufanyika mwanzoni mwa mchakato, katikati ama mwishoni mwa mchakato wa ujifunzaji

ili kumwamisha mwanafunzi kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine.

2. Kwa nini kuna mitihani?

Mitihani huwekwa ili kumpima mwanafunzi kama alielewa wakati wa mchakato wa ujifunzaji ili

kujua kitu gani alielewa ama hakuelewa sehemu gani au kumwamisha kutoka hatua moja ya

kielimu kwenda kwenye hatua nyingine ya juu zaidi. Wanafunzi wengi wanamini kuwa mitihani

hutungwa ili kupunguza idadi ya wasomi hivyo kuwafanya wakate tama ya kusoma.

3. Anayetunga mtihani ni nani?

Anayetunga mtihani ni mwalimu. Wanafunzi wengi huamini kuwa wanaotungamitihani ni watu

wenye malengo mabaya na wanafunzi ili kuwafelisha. wanasahau

kuwa anayetunga mtihani ni mwalimu mwenye uelewa wa soma

na maada husika.

4. Kwa nini anatunga mitihani?

Anatunga mitihani ili kuwapima wanafunzi wanaozingatia masomo na wasiozingatia masomo,

wanalio elewa na wasio elewa. Wanafunzi wengi huamini kuwa mwalimu hutunga mitihani ili

kumfelisha mwanafunzi, jambo lisilo kweli.

5. Maswali ya mtihani yanatoka wapi?

Maswali ya mtihani hutoka kwenye mada zilizofundishwa na mwalimu au mada zilizoainishwa

kwenye mtaala wa elimu na kupangiliwa kwenye muhtasari wa somo na si nje ya hapo. Hivyo

maswali hutoka kwenye vitabu

6. Kwanini tunafeli mitihani?

Page 8: Mbinu za usomaji na kufaulu mitihani

Wanafunzi wengi hufeli mitihani kutokana na kukosa mbinu bora za kusoma/kujiandaa na mtihani

na namna ya kujibu mtihani. Sio kila anayefeli hana akili bali alikosa mbinu za kujisomea na

kujibu mitihani.

7. Mtihani unajibiwa ukiwa na hali ganii (mud)?

Mtihani hujibiwa ukiwa katika hali ya kawaida ya kutokuwa na wasiwasi wala pressure yoyote.

Wanafunzi wengi huingia kwenye chumba cha mtihani wakiwa na wasiwasi mkubwa au pressure

kubwa ya kukabiliana na mtihani hivyo kuwapelekea kufeli mitihani.

8. Ntafanyeje ili kuweza kufaulu mitihani yangu?

Wanafunzi wengi wamekuwa wakijiuliza maswali mengi ya namna gani wanaweza kufahuru

mitihani yao. Wengi wamekuwa wakienda hadi kwa waganga wa kienyeji. Lakini mbinu pekee ni

kusoma na kuchagua mbunu sahihi za usomaji na ujibuji wa mitihani.

9. Nifanye vitu gani kabla ya kuingia kwenye chumba cha mtihani?

Kitu cha kwanza ni kujiandaa vya kutosha kabla ya siku ya mtihani kuhakikisha kila kitu

umekipitia na kukielewa kwa kutumia mbinu bora za usomaji na wakati wa mtihani hakikisha

unatoa wasiwasi wote kwa kujiamini kama unaweza, na mwisho kutumia mbinu bora za kuchagua

maswali na kujibu maswali.

10. Ni kina nani wanaopaswa kufaulu mitihani?

Wanafunzi wengi huona wanaopaswa kufaulu mitihani ni watu Fulani, kumbe kila mwanafunzi

ana uwezo wa kufaulu mtihani haijalishi anaelewa halaka au anaelewa taratibu.

Baada ya kukabiliana na maswali mengi yanayo wasumbua wanafunzi wengi sasa najua

wanafunzi wengi watakuwa na uelewa juu ya mtihani. Hivyo mwanafunzi anapoenda kuzitumia

mbinu za kufauru mtihani atajitambua yeye ni nani na mtihani ni nini hivyo kumfanya awe tayari

kuzitumia mbinu tutakazozieleza hapo mbele.

Page 9: Mbinu za usomaji na kufaulu mitihani

SURA YA PILI

MBINU ZA KUJIANDAA NA MTIHANI KABLA YA MTIHANI

1: kuhuzuria vipindi vyote vya darasani.

2: Kuchukua/ kuandika mambo muhimu wakati wa kipindi.

3: kuandika nukuu (notes) zote unazopewa na mwalimu

4: kutafuta nukuu (notes) nyingine mbali na za mwalimu

5: kusoma material zote ulizonazo

6: kupitia mitihani ya nyuma kutafuta past paper

1: kuhuzuria vipindi vyote vya darasani.

Wanafunzi wengi wamekuwa wavivvu wa kuhuzuria vipindi vya

darasani na badalaa yake kutumia nguvu zao kusoma kile

kilichofundishwa na mwalimu darasani. Na hakikisha unashiriki

kujibu na kuliza maswali darasani ili uelewe zaidi

Kuna umuhimu gani mwanafunzi kuhuzuria darasani?

Kwanza itakusaidia kukumbuka maelezo ya point muhimu hivyo kukusaidia wakati wa

kusoma kutotumia nguvu nyingi kuelewa.

Humsaidia mwanafunzi kunukuu point muhimu wakati mwalimu anafundisha

Humsaidia kujua ni mambo gani anapaswa kuyafahamu kwenye mada husika hivyo

kumpunguzia mzigo wa kusoma mambo mengi yasiyo na umuhimu (yaliyo nje ya

muhtasali wa somo) kwani mwalimu atakupa mwongozo wa mambo unayotakiwa kusoma

Itakusaidia kuchambua mambo uliyokuwa uana uelewa nayo awali kama ulikuwa sahihi au

la na kama hukuwa sahihi kubadilisha na kuingiza jambo jipya unalopewa na mwalimu.

Namna ya kuandika nukuu (notes) darasani.

Wakati wa kuandika notes mwalimu akiwa anafundisha huitaji umakini mkubwa. Sio kila

mwalimu anachoandika ubaoni lazima uandike mengine huyandika ili kumsaidia kuelezea point ili

aeleweke. Hivyo unavyo kuwa unandika notes wakati mwalimu anafundisha zingatia yale mambo

Page 10: Mbinu za usomaji na kufaulu mitihani

mhimu hasa yale yanayotiliwa mkazo na mwalimu. Na kuwa makini kusikiliza maelezo kuliko

kukazania kuandika tu.

Andika pointi, maelezo kidogo, mfano. Maelezo mengine utasikiliza tu na kuyaweka kichwani.

2: Kuchukua/ kuandika mambo muhimu wakati wa kipindi.

Mwanafunzi unatakiwa kuwa na daftari ndogo ambayo itakusaidia

kuandikia pointi muhimu wakati wa kipindi. Kwenye hilo daftari

utandika summary na sio notes hivyo utandika point tu. Zitakusaidia

wakati wa usomaji ili ujikite zaidi kwenye mambo muhimu pia

itakusaidika kutosinzia wakati wa kipindi

3: kuandika nukuu (notes) zote unazopewa na mwalimu.

Mwanafunzi unatakiwa kuandika nukuu zote unazopewa na mwalimu kabla,

baada na wakati wa kipindi. Kuna baadhi ya walimu hupenda kutoa notes

kabla ya kipindi wenginee baada na wengine wakati wa kipindi hivyo uwe

makini kuzipata notes zote maana ndizo zitakuwa mwongozo wako wakati

wa usomaji. Usipendelee kuandika notes kutoka kwa mwanafunzi

mwenzako maana unaweza ukakopi makisa aliyo andika yeye ni vyema

kuandika nukuu mwenyewe kutoka kwa mwalimu.

4: kutafuta nukuu (notes) nyingine mbali na za mwalimu

Mwanafunzi unatakiwa kufanya jitihada kubwa ya kutafuta notes

nyingine mbali na zile ulizopewa na mwalimu ili kuongeza ujuzi

zaidi. Nukuu hizo unaweza kuzipata kwenye mtandao, vitabu vya

kiada na ziada, vitini nk.

5: kupitia mitihani ya nyuma kutafuta past paper

Mwanafunzi inakubidi uwe na jitihada ya kutafuta mitihani ya nyuma, mitihani hii tafuta ya

shuleni kwenu, shule nyingine na mitihani ya mocko na mitihani ya taifa hii itakusaidia wakati wa

usomaji. Tutangalia kwenye point ya sita namna ya kusoma kwa kutumia mitihani ya nyuma.

5: kusoma material zote ulizonazo

Njiia za usomaji.

Kuna njia nyingi zitumikazo katika usomaji lakini tutangalia njia tatu muhimu.

Page 11: Mbinu za usomaji na kufaulu mitihani

Kusoma pekeyako (individual studies)

Kusoma kwenye vikundi (group discussion)

Kusoma kwa kuliza maswali

Kusoma pekeyako (individual studies)

Katika jia ya kusoma pekeyako, mwanafunzi unakaa pekeyako

kwenye meza na kusoma. Katika usomaji huu mwanafunzi unaweza

ukawa unatumia notes kusoma, au maswali yaliyomo kwenya past

paper au sehemu yoyote.

Namna ya kusoma notes. Wanafunzi wengi wamekuwa wakisoma notes kama wasomavyo vitabu

vya hadithi au gazeti na kuwapelekea kusinzia haraka au kuto kuelewa.

Unaposoma notes epuka kukalili soma na uelewe points hii itakua rahisi kwa wewe kukumbuka

kwa ulahisi points na maelezo yake. Na unapo soma note kumbuka kuwa na karatasi au daftari la

lafu kila unapo maliza kusoma sehemu unarudia kwa kuandika point zote ulizozisoma kama

unazikumbuka usihame kama bado hukuzishika vizuri rudia tena kusoma.

Pia unaweza kutumia maswali ya mada husika kusoma notes ili yakuongoze katika kusoma au

kujua maeneo unayotakiwa kutilia mkazo katika usomaji wako ( unaweza kutumia maswali ya past

paper au yaliyomo kwenye vitabu vya kiada au vya zaiada.)

Kusoma maswali. unapo soma maswali kumbuka kuwa na nukuu zote ili kupitia pale ambapo

unakuwa umeshindwa kujibu swali. Hapa pia unatakiwa kuwa na karatasi utakalo tumia kuandika

point au kusolvia swali lako. Na kama umesahau point au kanuni ya kufanya swali lako unarejea

kwenye nukuu zako. Au uatajibu maswali yote na baadaye kurejea kwenye notes zako kama

ulikuwa sahihi au hukuwa sahihi na kama hukuwa sahihi unajifanyia usahihi.

Kusoma kwenye vikundi (group discussion)

Hapa unavyotengeneza vikundi vya kujisomea hakikisha unalia

watu mnaoendana mwenendo na itikadi na mwenendo yenu na

usawa wa masomo yenu sciences au arts.

Mnapo fanya discussion mnaweza kutumia maswali au kupitia

notes na kuelekezana maeneo ambayo hayakueleweka darasani

Kuwa huru kuuliza swali lolote pasipo kuogopa maana unakuwa upon a wanafunzi wenzako hivyo

ni lahisi kuwauliza maswali.

Page 12: Mbinu za usomaji na kufaulu mitihani

Hakikisha unachangia mawazo ili kutoa kile ulicho nacho na unapo waelekeza wenzako inakuwa

rahisi wewe kuhifadhi zaidi kichwani

Usisahau kuandika opoint mnazofikia mwafaka kuwa ni sahihi.

Epuka kuingiza maada zilizo nje na somo, kwani wanafunzi wengi hujikuta wakiongelea mambo

yaliyonje na somo na kutumia mda mwingi kulijadili na kutumia mda mchache kujadili vitu vya

msingi.

Hakikisha unakuwa naratiba ya discussion ili upitie

kwanza yale mtakayoenda kujadili na wenzio ili usije

ukaenda ukiwa mtupu na ukashindwa kuchangia.

Baada ya discussion tenga mda wa kuyapitia yote mlio

jadili. Na sehemu ambazo hamkufikia mwafaka ni vema

mkamwona mwalimu wa somo au kikundi kingine cha

wanafunzi wenzenu au mwanafunzi mmoja mwenye

uelewa na sehemu hiyo.

Na ni vyema mkajiwekea utaratibu wa kutungiana mitihani angalau mara moja kwa wiki.

Mtapeana zamu ya kutunga mtihani ili kujipima kama mnayo jadiliana mnaelewa na kama hiyo

haitoshi mnaweza kumwomba mwalimu akawatungia maswali na mtafanya kwa uaminifu kwa

kujisimamia wenyewe na kumrudishia mwalimu awasahihishe.

Kusoma kwa kuliza maswali

Hapa unaweza kuwa unandaa maswali angalau matano kila

siku unayoona yamekushinda na ukampelekea mwalimu wa

somo husika au mwanafunzi mwenzako. Unapokuwa

unaelekezwa ndivyo utajifunza zaidi.

Nb: jitahidi kutumia njia zote wakati wa kusoma, usije ukatumia njia moja tu ya kusoma mfano

kusoma peke yako muda wote au mda wote kwenye group kufanya discussion bila kuwa na mda

wako binafsi wa kupitia mliyo discussi na uliyosoma darasani au kuliza maswali tu. Tenga mda

wako kusoma pekeyako mda mwingine kwenye discussion na kuliza maswali hivyohivyo kuwa

na ratiba inayoeleweka na hakikisha unaifuata vyema ratiba yako.

Page 13: Mbinu za usomaji na kufaulu mitihani

SURA YA TATU

NAMNA YA KUJIBU MASWALI WAKATI WA MTIHANI

Baada ya kujiandaa kwa muda mrefu sasa unatakiwa kuyawasilisha yaleyote uliyosoma kwa muda

mfupi sana masaa mawili au matatu. Hapa ndipo wanafunzi weengi huingiwa na wasiwasi

mkubwa sana.

Kabla ya kuingia kwenye chumba cha mtihani

Kabla hujaenda kwenye chumba cha mtihani hakikisha unajikagua na kuhakikisha

una vifaa vyote vinavyorhusiwa kwenye chumba cha mtihani. Hii itakusaidia

kuwa huru kwenye mtihani pasipo kumsubiria mwenzako amalize kufanya swali

ndipo uazime, hiyo itakuharibia mudi ya kufanya mtihani na kwangukia katika

kufeli

Hakikisha huungii na kitu kisichoruhusiwa kuingia nacho kwenye chumba cha

mtihani maana ukiingia nacho kitakufanya uwe na wasiwasi mkubwa kukamatwa

na unajikuta unashindwa kufanya mtihani wako kwa uhuru.

Ni vyema kuingia na saa kwenye chumba cha mtihani hii itakusaidia kutenga

mda wako ili ujue swali moja utatumia dakika ngapi ili ukamilishe maswali

yako kwa wakati na ukijiona uko nje ya mda uongeze speed ya kuandika,

kuliko kusubiria msimamizi aseme wengine huwa wanajisahau kusema

utasikia bado dk 10 wakati wewe bado hujafanya maswali mengi hiyo nayo

siyo njeme.

Baada ya kuingia kwenye chumba cha mtihani

Unapofika na kukaa kwenyekiti jitahidi kusali kwa imani yako (imani huponya)

Baada ya kukabidhiwa karatasi relax kuwa huru usiwe na pressure chukulia ni sawa na test au

maswali uliyowahi kufanya darasani au sehemu yoyote ile.

Usifunue karatasi hadi pale utambiwa funua karatasi na msimamizi. Unaweza ukachungulia

mtihani afu ukakutana na swali gumu likakutia pressure na ukauona mtihani wote ni mgumu.

Andika taarifa zako za msingi (no ya mtihani au jina kama linahitajika) kabla hujaingia kuagalia

mtihani

Page 14: Mbinu za usomaji na kufaulu mitihani

Baada ya kuambiwa fungua mtihani soma kwanza maelekezo ya juu kabla ya kusoma maswali.

Baada ya kumaliza kusoma maelekezo ya mtihani kagua karatasi yako kama ina idadi sawa za

kurasa kama ulivo kwisha kuelezwa kwenye maelekezo, kagua idadi ya sehemu kama mtuhani

umegawanyika katika sehemu, pia kagua idadi ya maswali kama yako sawa na maelezo ya juu.

Usisahau kukagua aina ya mtihani kama ni civics hakikisha umepewa mtihani wa civics na kama

ni form II hivyo hivyo.

Baada ya kufanya hivyo tulia kwa muda wa sekunde kadhaa vuta pumzi hadi mwili ukae katika

usawa.

Sasa anza kusoma swali moja baada ya jingine soma kwa umakini swali zima sio kusoma maswali

nusu nusu. Soma maswali yote rudia mara mbili a tatu na uyaelewe maswali vizuri.

Baada ya kusoma maswali yako angalia swali lililo lahisi zaidi dilo uanze nalo. na unavyo anza

tena kujibu angalia swali hilo uliloanza nalo lipo sehemu gani na soma kwa umakini maelezo ya

sehemu hiyo. Faida ya kuanza na swali jepesi linakupa mwanga wa kujibu maswali mengine na

linakupunguzia pressure ya mtihani ili unapo fuata maswali magumu unakuwa huna pressure tena

ya mtihani.

Na unapochagua swali hakikisha umeandika point pembeni (mwishoni mwa kitabu cha kujibia

mtihani) ukiona unakumbuka point chache chagua linguine na kama ni hesabu hakikisha unandika

kanuni na unaikumbuka vizuri ndipo uanze kujibu na kama hukumbuki vizuri kanuni anza na

linguine ili pressure ikipungua utakumbuka vizuri kanuni.

Na unapo jibu swali hakikisha unangalia idadi ya alama katika swali unalo fanya usije ukatumia

muda mwingi kwenye swali la alama chache. Swali la alama chache maanake ulijibu kwa ufupi na

kwa kueleweka.

Epuka kumsumbua mau kusumbuliwa na mtu kwenye chumba cha mtihani. Mfano mwenzako

anakuomba umsaidie swali la kumi wakati wewe umelifanya mda, unaanza kurudi nyuma

kumwonyesha, kwanza unapoteza mda wako, pili mtiririko wako wa kujibu swali ulilokua unajibu

kwa wakati huo hupotea tatu unaingiza pressure tena kwa kuogopwa kukutwa na msimamizi hivyo

kupoteza umakini wa kujibu maswali.

Epuka kuangalia kwa mwenzako, maana mwenzako anaweza akawa amekosa na ukajiona wewe

ndo umekosa na kukata jibu lako sahihi na ukandika la mwenzako la uongo au lisilo sahihi.

Page 15: Mbinu za usomaji na kufaulu mitihani

Epuka kutoka toka nje wakata wa mtihani na kujikuta unatumia mda mwingi nje badala ya kujibu

maswala labda kama hali yako ya kiafya sio nzuri na kama upo fizuri mambo yote maliza kabla ya

kuingia kwenye mtihani.

Hakikisha unandika namba ya swali katika kila ukurasa wa karatisi yako

Baada ya kumaliza kufanya maswali yako hakikisha umejibu maswali yote ulio ambiwa ujibu.

Kuwa makini sana na maswali ya lazima.

Kama umejiona umekamilisha maswali yote, sasa kagua namba za maswali katika kila ukurasa na

kisha kagua taarifa zako kama uliandika katika kila ukurasa wa kitabu cha kujibia mtihani.

Unapotoka kwenye chumba cha mtihani epuka kusimuliana ya kwenye mtihani. Maana unaweza

ukambiwa umekosa swali ikakuharibia hata katika mtihani mwingine. Mambo ya mtihani yaishie

kwenye chumba cha mtihani.

NB: hakikisha kipindi chote cha mitihani unakuwa na ratiba ya mtihani inayokuongoza ni somo

gani linaanza na lipi linafuata, ili usije changanya ratiba.

Na kwa kipindi chote cha mtihani epuka kukaa peke yako, usije ukasinzia na ukapitiliza mda wa

mtihani, pia ukikaa peke yako hata ukikosea kunakili ratiba hakuna atakaye kurekebisha. Hivyo si

vyema kukaa peke yako kipindi chote cha mti

Kwa kusoma kitabu hiki najua utajifunza kitu na ukiyazingatia yote kufeli mtihani

kwako itakuwa si rahisi.

MWISHO