Pongezi Kwa HakiElimu HakiElimu Imehamasisha Elimu Na ...hakielimu.org/files/publications/SautiElimu 27.pdf · batiki, ubanguaji wa korosho, ufugaji wa kuku wa kienyeji na kadhalika

  • Upload
    lammien

  • View
    287

  • Download
    13

Embed Size (px)

Citation preview

  • SautiElimuToleo la 27, 2011 | ISSN 1821 5076

    HakiElimu Mtaa wa Mathuradas Na. 739 SLP 79401, Dar es Salaam, Tanzania Simu: (+255) 22 2152449. Barua pepe: [email protected] Tovuti: www.hakielimu.org

    Pongezi Kwa HakiElimuNa Agnes Amlima, Lindi

    HakiElimu ni shirika lisilo la kiserikali ambalo linashughulikia masuala ya kutetea elimu

    HakiElimu ni shirika lisilo la kiserikali ambalo linashughulikia masuala ya kutetea elimu nchini Tanzania na kuhakikisha usawa katika nchi yetu unapatikana kwa hali na mali na kutoa matokeo chanya ya utendaji wa kazi.

    Jamii inatoa shukrani kwa shirika la HakiElimu kwa kutoa matangazo mbalimbali kwenye redio, runinga, magazeti na vijarida mbalimbali kwa ajili ya kuboresha elimu katika ngazi ya jamii ikiwemo na utunzaji wa mazingira katika sehemu mbalimbali kama vile shuleni na nyumbani. Jamii pia inapenda kila wilaya ingekuwa na tawi maalum la HakiElimu ili huduma zipatikane kwa urahisi zaidi.

    Shirika la HakiElimu mnahitaji kuwa mstari wa mbele katika kutoa changamoto za kuboresha na kuinua elimu katika nchi yetu. Aidha shirika la HakiElimu lingekuwa linafanya vikao na serikali angalau mara tatu kwa mwaka ili kufanya mikakati ya kuboresha na kutanua wigo katika sekta ya elimu.

    Vile vile shirika hili lingeunda kamati maalumu ya Marafiki wa Elimu kila mkoa. Pia HakiElimu waishauri serikali kutoa mafunzo kwa walimu ili kuwapa msukumo wa kupata ufahamu wa kutosha katika kufundisha mitaala mbalimbali pamoja na kuboresha makazi yao.

    HakiElimu hushiriki katika maonesho mbalimbali na kugawa machapisho kwa wananchi. Pichani ni moja ya maonesho ya mwaka ya Serikali za mitaa yaliyofanyika mjini Kigoma mwezi Juni mwaka 2010.

    HakiElimu imesaidia kuleta mabadilikoNa Amina Saidi Jumla, Lindi Manispaa

    HakiElimu ni shirika la hiari linalolenga kufikia usawa, ubora na demokrasia katika elimu na jamii.

    HakiElimu ina kazi kubwa katika jamii zetu hususani katika kuchochea ubunifu wa mijadala ya umma, kuwezesha jamii kupata habari, kubadili shule na mfumo wa uundaji wa sera na jinsi ya kufuatilia fedha zipatikanazo na matumizi yake katika jamii husika.

    Kutokana na shughuli zinazofanywa na HakiElimu, wanajamii wanapenda kuona kwamba mnakuja kuwatembelea; vilevile muendelee katika suala zima la kuonya, kuhamasisha jamii katika mambo mbalimbali.

    Mabadiliko katika eneo langu yatokanayo na shughuli zinazofanywa na HakiElimu yapo kwani jamii inaelewa wajibu wake kama vile mzazi kumsomesha mtoto, kutoa kero walizokuwa nazo katika vyombo husika kama vile serikali za mitaa na kuweza kujieleza.

    Napendekeza, HakiElimu iendelee kuelimisha jamii, kuonya na kuhamasisha jamii katika suala zima la elimu hususani kupitia kipindi cha Tafakari Time. Kipindi hiki kiendelezwe kwani kinaleta mabadiliko na kinaweza kuboresha elimu na kufikia malengo

    Meneja wa Idara ya Upatikanaji wa Taarifa Robert Mihayo akimkabidhi mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya Sekondari ya Mpwapwa Kompyuta maalum kwa ajili ya wanafunzi walemavu wa macho.

    HakiElimu Imehamasisha Elimu LindiNa Asha Bilali, Lindi Mjini

    unaopinga unyanyapaa kwa wanafunzi walemavu kwa kutokaa nao dawati moja, sasa hivi hakuna kabisa unyanyapaa; wanafunzi wanashirikiana.

    Jamii ya Lindi tunaomba ujumbe tunaopata kuhusu elimu uendelee kwa kupitia TV, redio na vipeperushi ili elimu hii iwafikie pia jamii iliyoko vijijini.

    Changamoto tunazozipata ni pamoja na baadhi ya wazazi kuwaacha watoto wao kuwa machokoraa na kukosa elimu. Tunaomba Marafiki wa Elimu tushirikiane katika kukomesha hii tabia kwa kupanga mbinu itakayosaidia kukomesha tatizo hilo la kutokwenda shule.

    Natoa shukurani kwa HakiElimu kwa ujumbe kupitia vijarida mnavyotuletea, nasema asante. Jamii ya Lindi imehamasika kusoma vijarida na kuona kila mmoja wetu ana wajibu wa kuhamasisha jamii inayomzunguka kuhusu elimu bora.

    Naomba Marafiki wa Elimu wawaangalie zaidi walimu walevi wakati wa shule hasa kule vijijini; ndipo tutafanikiwa kufikia lengo la tamko la elimu bora kwa kila mtoto wa kitanzania.

    Kumekuwa na mafanikio kadha katika shughuli za HakiElimu baadhi yake ni pamoja na; baada ya HakiElimu kutoa ujumbe

    Kila mwaka HakiElimu inatayarisha mashindano ya insha na michoro. Lengo ni kukusanya maoni ya wananchi kuhusiana na mada ya shindano husika. Pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu Bi. Elizabeth Missokia akikabidhi zawadi ya redio zitumiazo mionzi ya jua baadhi ya washindi wa shindano lililofanyika mwaka 2010.

    Karibuni MkurangaNa Fatuma Mpanga, Mkuranga-PwaniKujiunga na HakiElimu kumenisaidia kupata maoni mbalimbali katika machapisho na katuni na mimi nazidi kuboreka na ninapata mwanga wa maisha na kuwa na mwanaharakati.

    Idadi ya Marafiki wa Elimu Mkuranga bado ni ndogo. Nashauri HakiElimu mje kufanya mdahalo katika wilaya ya Mkuranga ili kuhamasisha wananchi wajiunge na mtandao wa Marafiki wa Elimu ili kuongeza hiyo idadi. Tukiwa wanachama wengi, itarahisisha kupata maoni mbalimbali kwa wanajamii. Karibuni Mkuranga.

  • HakiElimu Imeleta Mchango Mkubwa Katika Miaka 10 IliyopitaNa Mussa Kamtande, Kikundi cha WEMA, Mtwara

    Awali ya yote naomba niseme wazi kwamba HakiElimu katika kipindi cha miaka 10 imeweza kupata mafanikio makubwa ambayo leo hii tunayashuhudia katika nyanja za elimu na demokrasia hapa nchini.

    Kuanzishwa kwa vuguvugu la Marafiki wa Elimu kumewezesha kuiamsha jamii kwa kuipatia elimu sahihi juu ya mambo ambayo huko nyuma yalikuwa hayafamamiki. Aidha, hapo awali, wananchi hawakushirikishwa kikamilifu katika maamuzi mbalimbali. Elimu iliyotolewa na Marafiki wa Elimu katika maeneo mbalimbali hapa nchini imewapa wananchi utambuzi wa kujua haki zao, na namna ya kuzidai pale wanapohisi kuwa hawatendewi haki. Kwa upande wa pili wamepata utambuzi wa namna fedha nyingi zilizokuwa zikiletwa katika vijiji vyao, zilivyoweza kuwanufaisha watu wachache wakiwemo viongozi badala ya walengwa, ambao ni wananchi.

    Aidha, kupitia vikundi vya Marafiki wa Elimu, wananchi katika maeneo mbalimbali wameweza kuwa na chombo ambacho kimeweza kuwasemea mapungufu na matatizo yanayojitokeza katika maeneo yao. Mfano mzuri wa yale yanayofanywa na vikundi vya wanaharakati wa elimu, ni kutoka katika kikundi cha WEMA.

    Kikundi cha Wanaharakati wa Elimu, Mazingira na Afya WEMA kiliasisiwa mwezi Disemba 2007 na kuanza rasmi shughuli zake Januari 2008. Wanachama waanzilishi walikuwa 15. Kwa sasa idadi inakadiriwa kufikia 50. Kikundi kimesajiliwa. Mambo yanayofanywa na kikundi cha WEMA toka kianzishwe ni pamoja na:

    Januari 2008 WEMA ilianzisha Maktaba ya Jamii ambayo ina uwezo wa kukidhi viwango vyote vya elimu, kuanzia elimu ya awali, hadi chuo kikuu. Maktaba hiyo ilizinduliwa rasmi tarehe 11 Julai 2009 na viongozi kutoka taasisi ya kiraia ya HakiElimu.

    Kwa ufadhili wa HakiElimu, WEMA wamejenga ubao wa matangazo. Ubao huo umejengwa karibu na ofisi ya kijiji na umekabidhiwa rasmi kwa serikali ya kijiji kwa matumizi.

    Mwaka 2010 WEMA waliandaa mjadala wa wazi baada ya kufadhiliwa na HakiElimu. Mada iliyojadiliwa ilihusu; Athari za disco toto na kumbi za starehe kwa wanafunzi. Washiriki walikuwa Marafiki wa Elimu, wadau wa elimu, viongozi wa serikali, wazazi pamoja na wawakilishi wa wanafunzi.

    Mwaka 2009 na 2010 Marafiki wa Elimu kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara walishiriki katika mijadala iliyokuwa inaandaliwa na Marafiki wenyewe na kurushwa hewani kupitia kituo cha redio cha Pride fm 87.8 chini ya ufadhili wa HakiElimu. Vipindi hivyo vimeleta mwamko mkubwa kwa wananchi wa mikoa hii na imepanua uelewa wa mambo mbali mbali yakiwamo ya demokrasia.

    Tarehe 01 Julai 2010 kikundi cha WEMA kilishiriki maonesho ya Serikali za Mitaa ambayo yalifanyika kiwilaya mji mdogo wa Ndanda. WEMA waliweza kuonesha shughuli mbalimbali wanazozifanya zikiwemo ufinyanzi wa vyungu vya kupandia maua na miche pamoja na shughuli za maktaba.

    Kikundi cha WEMA kinawapatia huduma wanafunzi watatu, kutoka katika shule za msingi Liputu, Mkalapa na Mtunungu.

    Wanapewa huduma kama sare za shule, vifaa vya kuandikia na michango muhimu ya shule.

    Mwaka 2010 shirika lisilo la kiserikali la CYODO (Children Youth Development Organization) liliandaa kongamano ambalo lilishirikisha wanafunzi wa shule za sekondari za mikoa ya Lindi na Mtwara, WEMA waliweza kumtafuta mwanafunzi mmoja na kumpeleka kuhudhuria kongamano hilo kwa gharama zao. Kongamano hilo lilifanyika Mtwara mjini.

    Kikundi cha WEMA kimeunda kitengo kinachojulikana kama WEMA Women Empowerment Generation (WEMA Women-EG). Kitengo hiki ni mahsusi kwa ajili ya akina mama na kimelenga kujishughulisha na utengenezaji wa mitungi ya kupandia maua, batiki, ubanguaji wa korosho, ufugaji wa kuku wa kienyeji na kadhalika. Sambamba na shughuli hizo wamejipanga kukutana na wanafunzi wa kike na kuwakumbusha juu ya umuhimu wa elimu na kuwataka waepuke kuendekeza mapenzi wangali bado wanafunzi.

    Oktoba mwaka 2010 WEMA walishiriki maonesho ya kanda yaliyoandaliwa na SIDO ambayo yalifanyika kikanda mjini Masasi. Katika maonesho hayo walionyesha vyungu vya kupandia maua pamoja na shughuli za maktaba. Wametunukiwa cheti cha ushiriki katika maonesho hayo.

    Kwa ujumla HakiElimu imeleta changamoto kubwa katika kipindi chote cha miaka 10.

    Katika harakati za kuboresha elimu Tanzania, Marafiki wa Elimu, huendesha maktaba ya jamii. Pichani ni moja wa maktaba hizo, inayoendeshwa na kikundi cha WEMA

    Shirika la LISAWE linapenda kutoa shukrani kwa kupewa nafasi ya kutoa maoni kupitia Jarida la SautiElimu. LISAWE ingependa kutoa shukrani kwa mambo yote ikiambatana na shughuli zote zinazohusiana na gurudumu la kuboresha elimu Tanzania, hususani katika kuonesha kupaumbele, haki na sera za elimu kwa ujumla.

    Yapo manufaa kemkem tuliyoyapata kutoka HakiElimu. Miongoni mwa manufaa hayo ni pamoja na kupata elimu mbalimbali hususani kuhusu umuhimu wa elimu kwa ujumla. Aidha, kwa msaada wa HakiElimu, kumekuwepo na uboreshaji wa vikundi vyetu katika shirika la LISAWE.

    Mathalani tumekuwa tukipata elimu kwa kutumia majarida na machapisho tunayoletewa, tumekuwa tukisoma na kupata ujumbe dhahiri.

    Tumepata redio jamii ambazo zinatusaidia kupata taarifa mbalimbali za maendeleo ya jamii na nchi kwa ujumla.

    Aidha, HakiElimu imetuwezesha kufanya ziara mbalimbali za mafunzo, zilizotuwezesha kuona wanachofanya katika vikundi na NGOs kwenye maeneo mbalimbali ya nchi.

    Pia tunashukuru kwa kuwezeshwa kutoa maoni yahusuyo uendeshaji wa vikundi vya jamii, kupitia kituo cha redio cha PRIDE kilichopo Mtwara.

    Vile vile kumekuwa na faida ya kutuunganisha na Marafiki wa Elimu nchini kiasi kwamba tuna mahusiano ya kina na marafiki wenzetu.

    Vilevile sasa bado tunaendelea kuangalia vipindi mbalimbali vinavyohusu mambo ya elimu katika runinga.

    Kiujumla, HakiElimu, kupitia Idara ya Upatikanaji wa Habari na Taarifa, imeweza kuleta mabadiliko katika jamii zetu. Ni matumaini yetu mtaendelea na mikakati na shughuli kama hizo zilizopelekea jamii iweze kufikia hatua iliyofikia.

    Shirika la LISAWE lingependa kuweka wazi mambo ambayo mnapaswa kuyaongezea na kuyatilia mkazo ili kuweza kuboresha shughuli zenu na kuweza kukubalika na wadau hususani jamii.

    Tungependa msaidie asasi kwa kuzifadhili (kifedha) zifanye kazi kwa jamii kuhusu masuala ya elimu kwa vile asasi hizo zipo karibu na jamii katika majukumu yake.

    Majarida yanayoandikwa na kuchapwa na HakiElimu yahusishe zaidi maoni ya jamii. Hii ni kwa vile majarida haya ni kama fasihi na fasihi ni ya jamii ambayo hubeba na huakisi yale yote yaliyopo katika jamii hiyo. Mmekuwa mkihusisha jamii isipokuwa ni msisitizo zaidi kuwa jamii ndio iwe na mchango mkubwa zaidi. Kwa namna hiyo hata yanayoandikwa lazima yawe ndani ya jamii hii.

    Pia tungependa HakiElimu ijikite zaidi katika kuandika taarifa kutokana na takwimu halisia ili kuweza kuwaonesha wasomaji na jamii kwa ujumla kuwa HakiElimu ipo makini, wanalenga kuinua maendeleo kwa kuipa kipaumbele elimu nchini.

    Shirika la LISAWE pia lingependa kuwasisitizia suala la Uwazi kwa uwajibikaji unaopaswa kufanywa katika taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali katika kuinua elimu. Na hii ikiambatana na kutoa kipaumbele kielimu katika jamii.

    Pia tungependa kusisitiza kuwa muongeze na muendeleze ushirikiano zaidi na asasi zisizo za kiserikali kama ilivyo hapa LISAWE. Kwa vile asasi hizi zipo na shughuli zake hufanywa na jamii na taarifa kuhusu jamii zaweza kupatikana kiurahisi kupitia katika asasi hizi zisizo za kiserikali. Tunasema asante sana!

    HakiElimu Imesaidia Kuleta Mabadiliko Katika JamiiNa Marafiki wa Elimu, Shirika la LISAWE, Lindi

    Rafiki wa Elimu akitoa risala kwenye mkutano wa Marafiki wa Elimu uliofanyika mkoani Lindi kati ya tarehe 6 hadi 10 Julai 2009 katika ukumbi wa TCCIA

    Wazazi Wawe Karibu na Watoto WaoNa Malundila Manzi Selemani, Lindi

    Kwanza ningependa kuwapongeza watendaji wote wa HakiElimu kupitia Idara ya Upatikanaji wa Taarifa kwa kutoa machapisho mbalimbali ili kuelimisha jamii. Wanajamii wana maoni mengi sana juu ya shirika la HakiElimu. Mojawapo ni kuhusu udogo wa machapisho kwa maana kuwa kurasa kidogo. Kwa maana hiyo kurasa ambazo zinachapishwa ziwe nyingi maana wasomaji wanapotaka kupata utamu wa kusoma ndipo mwisho umefika.

    Mabadiliko katika eneo langu yapo na ni makubwa sana kwa sababu, kutokana na machapisho ambayo tunayapata kutoka

    Wananchi wa kijiji cha Kitembe wilayani Rorya wakichukua machapisho kutoka kwa timu ya HakiElimu ilipotembelea kijijini hapo mwezi Julai mwaka 2010

    HakiElimu watu walio wengi wanapenda kusoma majarida ya HakiElimu.

    Nina mapendekezo machache ambayo yanaweza kuboresha shughuli za HakiElimu. Kwanza walimu wanatakiwa watambue kuwa wao ndio watu muhimu katika taifa lolote lile duniani kwani bila wao tusingekuwa na waganga, mawaziri, wakemia na kadhalika. Pia wazazi nao wawe karibu na watoto wao kufuatilia maendeleo darasani wakishirikiana na walimu. Kwa hiyo kitu ambacho kinaweza kuboresha na kufikia malengo ya HakiElimu ni ushirikiano kati ya wazazi na walimu ili kila mtoto wa kitanzania apate elimu bora na si bora elimu.

  • Saut iEl imu

    Tahariri

    Matokeo ya Kidato cha Nne ni Hali Halisi ya Mazingira na Muelekeo wa Elimu NchiniNa Haji S. Mswaki, TangaMwishoni mwa mwezi Januari mwaka 2011, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilitangaza matokeo ya mitihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka 2010.

    Kutokana na matokeo haya, kumekuwa na maoni na mawazo mengi kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa Serikali.

    Kwa ujumla matokeo hayakuwa mazuri, kwani kila mtu anajua hali halisi iliyotokea katika eneo analoishi. Viongozi mbalimbali pia wamekubali kwamba hali ni mbaya na wamekuwa wakitoa sababu mbalimbali.

    Hali ya elimu na mazingira yake ni vitu ambavyo haviwezi kuachana kamwe. Kutokana na mazingira ya shule zetu, tunastahili kupata matokeo haya.

    Serikali inajivunia kwa kufanikisha ujenzi wa shule za kata kwa wingi. Shule hizi zimeenea na zina wanafunzi wengi ambao miongoni mwao ndio wamehitimu kidato cha nne mwaka 2010. Hivyo wengi wao ndio wamesababisha matokeo haya ya leo.

    Miundombinu ya shule hizi ni mibovu ukilinganisha na elimu inayotakiwa kutolewa. Vyumba vya madarasa vimekuwa haba ukilinganisha na idadi ya wanafunzi. Hali hii inachangia wanafunzi kukosa uhuru wa kukaa darasani kwa amani na kupata kile walichokifuata.

    Pamoja na wingi wao bado wanaenda shuleni kuhesabu madawati na kupiga soga kutokana na kutokuwa na walimu wa kuwafundisha. Lakini pia vitabu vingekuwa vya kutosha, wangeweza kujisomea na kueleweshana japo kwa shida. Hali hii inachangia wanafunzi

    kuwa watoro na ukizingatia wengine wamepangishwa makazi mtaani na wazazi wao kwa pesa ya kulenga kwa manati. Kwa ujumla hali ni ngumu na juhudi za makusudi zinahitajika.

    Tatizo lingine ni mtaala wetu ambao unayumbayumba. Leo unasikia hivi kesho vile. Mitihani wa kidato cha pili ulikuwa kipimo kizuri cha kumpeleka mtu kidato cha nne, lakini kipimo hiki sasa hakipo, milango iko wazi na wanafunzi wenye sifa na wasio na sifa wanaingia kidato cha tatu. Je tunategemea nini mbeleni?

    Lakini pia kuna shule ambazo zimeuzwa kwa walimu wakuu, kwani unakuta shule haitembelewi na viongozi na taarifa zake hazijulikani, sasa zinashughulikiwa vipi? Kwani si ajabu kukuta shule ina kidato cha kwanza hadi cha nne huku ina mwalimu mmoja tu. Kweli viongozi wanaitambua hali hii?

    Nashauri serikali iangalie upya mfumo wa elimu na kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwa kuboresha majengo ya shule, maabara, maktaba, kuongeza walimu wenye sifa na vifaa vya kujifunzia.

    Naamini wanafunzi waliofanya vizuri kutoka shule zisizo za serikali walikuwa wanajifunza katika mazingira mazuri ambayo yametosheleza kila kitu.

    Kwa hiyo, serikali iboreshe mazingira ya kufundishia na kujifunzia ili tujivunie watanzania kwa kupata elimu bora na siyo bora elimu.

    Miaka 10 Ya HakiElimu Katika Kuboresha Elimu TanzaniaNa Mussa Msengi Gunda, Rafiki wa Elimu, Kigoma

    vya redio na matangazo mbalimbali katika televisheni yaliyochochea ufuatiliaji na ubainifu wa mambo mbalimbali ikiwamo haki za binadamu, demokrasia na utawala bora kwa wananchi na uwajibikaji wa kweli kwa viongozi katika ngazi mbalimbali.

    Pamoja na hayo HakiElimu bado wapo mstari wa mbele katika kuhakikisha kila mtoto ndani ya nchi hii anapata elimu iliyo bora itakayomfanya aweze kujitambua.

    Napenda kuchukua fursa hii kuwaomba HakiElimu kuongeza kasi ili kuwafikia wananchi wengi zaidi hususani wa vijijini na mimi kwa nguvu zangu nawaunga mkono katika shughili zenu zote.

    Elimu imekuwa nguzo muhimu sana duniani kote katika kurahisisha maendeleo ya jamii. Ushiriki wa wananchi unaongezeka kadri mtu anavyopata elimu sahihi inayomuwezesha kuchambua na kupambanua taarifa mbalimbali zinazomfikia na kisha kuzitolea maamuzi sahihi.

    HakiElimu leo hii wanatimiza miaka 10 tangu waingie kwenye mchakato wa kuwahabarisha wananchi katika kufahamu sera mbalimbali za nchi ili kuongeza ushiriki wao katika kuleta demokrasia na utawala bora wenye tija ya wananchi kuhoji na kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo.

    Napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza kwa kuweza kuwafikia wananchi wengi sana katika nchi hii hususani walio maeneo ya vijijini kupitia Marafiki wa Elimu. Mambo mengi wameweza kuyafanikisha katika maeneo mbalimbali ni pamoja na:

    Kuwawezesha wananchi kutambua sera mbalimbali ikiwamo sera ya elimu na kuwafanya wananchi katika maeneo mbalimbali kuona umuhimu wa kushiriki katika kuboresha elimu na demokrasia katika maeneo yao.

    Kuwajengea uwezo baadhi ya wananchi kuweza kujitolea na kuwaelimisha wananchi wenzao juu ya masuala mbalimbali ya elimu na demokrasia nchini kupitia Harakati za Marafiki wa Elimu.

    Kuongeza upatikanaji wa vitabu katika maeneo mbalimbali kwa kuchangia vitabu katika maktaba za shule na za kijamii hususani vijijini.

    Kuibua mijadala mbalimbali kupitia vipindi

    Na Noah Nzawila, Dar es salaam

    Tangu nilipojiunga na harakati za Marafiki wa Elimu nchini, mwaka 2003, binafsi kama mwananchi na raia wa Tanzania ninayependa kuwepo upatikanaji wa elimu bora unaozingatia haki, usawa na ubora kwa watoto wote wa kitanzania, nimenufaika sana na ninaendelea kunufaika kutokana na shughuli zinazofanywa na HakiElimu kupitia harakati za Marafiki wa Elimu nchini. Tokea wakati huo mpaka hivi sasa nimeweza kujitambua, pamoja na kutambua haki na wajibu wangu katika jamii. Ndiyo maana pia mpaka leo hii nimeweza kuwa tayari kutumia muda wangu wa ziada ili kuwezesha na watu wengine waweze kujitambua, kutambua haki na wajibu wao katika jamii zinazowazunguka na kisha kushiriki katika harakati za kuleta mabadiliko ya elimu na demokrasia. Hili ni suala ambalo limewezekana kutokana na matokeo yanayoendelea kuonekana.

    Mwaka huu HakiElimu inaadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwake, nikiwa kama Rafiki wa Elimu nimeshuhudia HakiElimu ikibisha hodi hadi vijijini kwenye vitongoji vilivyo mbali na miji kupitia harakati za Marafiki wa Elimu nchini. Maeneo hayo si ya vijijini tu bali hata mijini watu wengi walikuwa bado wanauchapa usingizi licha ya kuwa kumekucha. Lakini hiyo yote ni kutokana na giza la uelewa mdogo wa uboreshaji elimu na demokrasia lililokuwa limewazunguka katika maeneo yao.

    Ujio wa HakiElimu ni mwanga wa jamii katika kuboresha elimu na demokrasia nchini Tanzania, kwani mpaka sasa jamii nyingi hapa

    Tanzania zimefunguka kifikira na kimtazamo katika kuwezeshwa kupata taarifa mbalimbali zilizofanyiwa utafiti wa kina na kuwafikia huko waliko.

    Hali inayoonekana sasa ni kitu ambacho jamii imeamka na inatafakari matatizo yanayotokea ambayo yanasababishwa na kile kitu kinachoitwa bora elimu na kisha kuchukua hatua katika kuyatafutia ufumbuzi.

    Elimu ya sasa imepoteza muelekeo kabisa

    unaotolewa na shirika la HakiElimu.

    Watu 22 kati ya 28 kwa kuzingatia usawa wa kijinsia na katika maeneo tofauti walitoa maoni kwamba shirika ka HakiElimu limeleta manufaa makubwa katika jamii ya kitanzania kwa kuwezesha na kupigania haki za wananchi wanyonge walioachwa pembezoni zaidi kiuchumi na kijamii kwa kuwapatia taarifa zinazohusu elimu ili nao waweze kushiriki kikamilifu.

    Hata hivyo watu wanne walisema upo umuhimu mkubwa wa HakiElimu kushirikiana na serikali kwa ukaribu sana kufanya kazi ili kuhakikisha jamii inanufaika zaidi na rasilimali na fursa zilizopo katika sekta ya elimu nchini. Baadhi yao walitoa mfano kuwa kama mpango wa MMEM utatumika vizuri, unaweza kuleta mabadiliko makubwa ya elimu hapa nchini.

    Kwa upande mwingine watu wawili walikuwa na mtazamo tofauti. Maoni yao ni kuwa, shirika la HakiElimu limekuwa likifanya shughuli zake kwa kukosoa sana sera za serikali kitu ambacho wanadai kuwa ni kuichonganisha serikali na wananchi.

    Katika kipindi chote hicho kuna mabadiliko yaliyotokana na shughuli zinazofanywa na HakiElimu. Viongozi na watendaji wa mitaa sasa wanatambua umuhimu wa taarifa kwa wananchi na hivyo taarifa hizo hubandikwa hata kwenye kuta za ofisi. Mijadala midogo

    Inaendelea ukurasa wa 4

    kwani walimu wengi wa shule za msingi sasa imekuwa ni bora walimu. Ukijaribu kutafakari kwa kina hali hii, sidhani kama serikali haitambui kuwa watu wanaoingia kusomea fani nyeti ya ualimu hasa wa shule za msingi, wengi wao wanakuwa wamefaulu kwa kiwango cha chini zaidi. Aidha wengine wamefikia hata kughushi vyeti ili mradi tu

    Mmoja wa Marafiki wa Elimu, Noah Nzawila, akiwa ndani ya maktaba ya jamii iliyopo Maeneo ya Kitunda, Gongolamboto, jijini Dar es Salaam.

    kutimiza malengo yao. Hali hii inatokana na wengi kushindwa masomo yao. Je kutokana na hali hiyo tunatarajia kuwa na elimu bora?

    Leo hii Hakielimu kupitia nyaraka zake za msimamo imeweza kuelimisha jamii na watu walioko serikalini wanaohusika na elimu kutambua umuhimu wa mafunzo bora ya walimu kwa maendeleo ya elimu. Lengo ni kuondoa mapungufu yaliyopo na vilevile kuwaandaa walimu katika ulimwengu unaobadilika mara kwa mara ili waweze kuwaandaa wanafunzi kusoma kwa makini na kuwapa mazoezi ya kutosha kwa vitendo.

    Mwanzoni mwa miaka ya tisini, wanafunzi walikuwa na uwezo na ujasiri wa kutatua kero za walimu kuishi mbali na shule. Waliweza kushirikiana na walimu wao kukata miti, fito, kamba, nyasi kisha kujenga nyumba za walimu karibu na shule. Nyumba hizi zinatumika mpaka sasa ambapo zimefanyiwa maboresho ya kuondoa nyasi zilizotumika kuezeka kipindi kile na badala yake kupiga bati. Je mwanafunzi anayemaliza elimu ya msingi miaka hii ya sasa anaweza kufanya hivyo?

    Yapo baadhi ya maoni ya wanajamii kuhusu shughuli zinazofanywa na Shirika la HakiElimu. Kwa mujibu wa utafiti mdogo nilioufanya siku chache zilizopita kupitia wananchi waliotembelea katika maktaba ya jamii na katika eneo ninaloishi ni kwamba watu wengi wanatambua na kuthamini mchango

    Baadhi ya maeneo mbalimbali ya Gunda Foundation iliyopo wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma

    HakiElimu Ni Mwanga wa Jamii Katika Kuboresha Elimu na Demokrasia Nchini

  • midogo ya wanajamii inafanyika na pia uanzishaji wa maktaba za jamii imesaidia watu wengi kuhabarika na kupata taarifa nyingi zilizofanyiwa utafiti wa kina.

    Ufahamu wa wanajamii juu ya sera za serikali na haki katika jamii umeongezeka. Watoto wametambua haki na wajibu wao kwa wazazi, walezi na jamii zao. Pia watoto ambao ni taifa la kesho wamejenga utamaduni wa kuazima vijitabu, machapisho, majarida mbalimbali ili kujisomea na kuongeza maarifa badala ya kuwa na mtazamo hasi wa kufikiria kwamba maarifa yanapatikana darasani tu. Hii imesaidia watoto wengi kupunguza kwa kiasi kikubwa muda mwingi kucheza na kuzurura mitaani.

    Aidha, wanawake wanajiunga na vikundi mbalimbali vya maendeleo kupitia taarifa mbalimbali wanazozipata za kiuchumi na kijamii; na kupitia chapisho la Rafiki Sema Usikike, wananchi wameandika kero zao katika magazeti.

    Watu wengi sasa wanamiliki simu za mkononi na wengine huamua kuwa hata na namba ya simu tu na kila baada ya siku chache huomba kwa jamaa na marafiki zao simu ili kusoma ujumbe. Kwa kuwa suala la elimu linamgusa kila mmoja wetu hapa nchini, napendekeza kuwa itakuwa ni vizuri kama HakiElimu itaweza kusambaza taarifa za elimu kupitia ujumbe mfupi wa simu za mikonononi. Hii itawawezesha watu kupata taarifa nyingi popote pale walipo na kwa wakati muafaka zaidi. Hongereni sana kwa kutimiza miaka 10.

    Kutoka ukurasa wa 3

    Na Prisca Unga, Lindi

    HakiElimu ni shirika lisilo la kiserikali ambalo limejikita zaidi katika kuboresha elimu kwa Nyanja mbalimbali kuanzia upatikanaji wa elimu toka elimu ya awali hadi elimu ya juu. Pia inajihusisha katika suala zima la uboreshaji wa mitaala iliyopo, walimu, majengo husika, vitendea kazi pamoja na kuwaunganisha wadau wote wa maendeleo wanaojishughulisha na masuala ya elimu. Suala kubwa katika yote yaliyotajwa ni ushawishi na utetezi kwa jamii na makundi yote.

    HakiElimu Iimarishe Mitandao

    Tokea nimeanza kuwatambua na kushirikana na HakiElimu mabadiliko ninayoyaona ni pamoja na Lindi imeweka mkazo katika elimu; watoto wanaoandikishwa ni wengi. Idadi ya watu wanaojiendeleza kielimu hadi chuo kikuu huria inaongezeka. Wanaosoma majarida yanayoandaliwa na HakiElimu ni wengi hasa wanaoyafuata hapa LISAWE. Midahalo ihusuyo uboreshaji wa elimu inafanyika mara kwa mara na mashirika yasiyo ya kiserikali hapa wilayani. Suala la

    Mikutano ya Wazi Itasaidia VijijiNa Rehema Ngelekele, MkurangaPongezi kubwa sana tunatoa kwa shirika la HakiElimu kwa harakari zenu za kuboresha elimu hapa nchini. Ndani ya miaka 10, wananchi mbalimbali tumepata ufahamu mkubwa kuhusu nini tufanye juu ya mabadiliko katika elimu katika sehemu zetu. Pia mmefanya kazi kubwa kuunganisha wanaharakati wa elimu kiwilaya, kikanda na kimataifa. Tunakutana na kujengeana uwezo kwa kubadilishana uzoefu na kujifunza kutoka kwa wengine. Mlikumbana na changamoto mbalimbali kutoka serikalini lakini mlisimama imara. Nasi Marafiki wa Elimu tulikuwa nanyi kwani ni watetezi wa elimu,

    waelimishaji wa jamii kwa njia mbalimbali kama vile vijarida, redio, mikutano ya wazi ya Marafiki. Mnastahili sifa na jamii nzima inafaa kuiga mfano wenu na kujifunza kutoka kwenu.

    Maoni yangu ni kuwa mikutano ya hadhara ishuke vijijini na vitongojini kuwalenga wanaoathirika zaidi. Harakati za ana kwa ana ni nzuri zaidi kwa huku vijijini. Kutuma majarida ni vizuri, lakini wengi wa wakazi wa vijijini hawafahamu kusoma. Hivyo mikutano ya wazi itasaidia zaidi vijijini, kwenye jamii kubwa zaidi.

    Baadhi ya wanakijiji wilayani Rorya, wakiwa katika mijadala wa pamoja na timu ya HakiElimu ilipotembelea wilayani hapo mwezi Julai 2010

    jinsia katika kuwabagua watoto wa kike wasipate elimu mkoani Lindi limepungua pia.

    Ili tufikie malengo ya kumwelimisha kila mtanzania yafuatayo inabidi yafanywe na HakiElimu. Kubwa ni kujikita katika kuunganisha na kuimarisha mitandao ya elimu Tanzania. Kuvitafutia vikundi vya jamii NGOs na CBOs wafadhili ambao wataweza kusaidia makundi tete kama wanafunzi walemavu n.k.

    Mafanikio Niliyoyapata Katika Miaka Kumi ya Ushirikiano na HakiElimuchangamoto hizo. Aidha, nilipata maarifa ambayo ninayatumia kuboresha elimu katika eneo langu.

    Vile vile, nilijifunza mbinu ya kuandika habari, kuchambua hotuba, maarifa ya ufuatiliaji wa bajeti ya serikali, uchambuzi sera, jinsi ya kujieleza na uhuru wa kutoa mawazo binafsi. Niliweza kutambua majukumu yangu kama mwanaharakati wa mtandao wa Marafiki wa Elimu. Nilipata maarifa ya kutambua kero na jinsi ya kutatua kero hizi katika jamii yangu.

    Pia nilijifunza jinsi ya kuanzisha huduma ya maktaba, ujuzi ambao uliyoniwezesha kuanzisha huduma hiyo katika eneo niliopo sasa la Kilwa.

    Ipo kila sababu ya marafiki walio hai na wasio hai kiwilaya/kikanda kufahamiana ili kuhamasishana na kuwezeshana ili kueneza dhana nzima ya Marafiki wa Elimu.

    Ili kuleta mabadiliko/mageuzi ya haraka katika elimu, upo umuhimu wa kufanya mikutano ya Marafiki wa Elimu katika vijiji, kata hadi tarafa au kiwilaya angalau mara moja kwa mwaka.

    Nashauri Marafiki wa Elimu wawe wabunifu ili kuiwezesha jamii kubadilika na kuondoa kero kama vile kushuka kwa uwezo wa kufikiri kwa wanafunzi waliopo shule za msingi na

    sekondari na vile vile kukosekana kwa maadili mema ndani ya jamii na mashuleni.

    Aidha, wazazi wanakwepa kutambua umuhimu wa kuwaanda watoto wao kifra/kimawazo ili kusaidia kumweka mwanafunzi katika mazingira ya kujifunza/kujisomea ili mwanafunzi apende masomo kuanzia nyumbani na kisha shuleni. Wajitahidi kuwajali watoto wao hususani wa kike.

    Uzazi usiofuata mpango, mimba zisizotarajiwa katika familia au urafiki wa mapenzi, kutengana kwa wazazi, kutelekeza familia ni baadhi ya sababu zinazochangia wanafunzi kukosa huduma ya elimu, hivyo ipo haja ya marafiki kuandaa michezo ya kuigiza na filamu kwa ajili ya kuelimisha jamii.

    Ingekuwa vema mngewapatia Marafiki wa Elimu wawezeshaji vifaa na misaada ya vitendea kazi kama vile kamera, kompyuta au hata pikipiki angalau kwa awamu hasa kwa marafiki waliopo kanda ya kusini ili waweze kufika maeneo mbalimbali na kisha kusaidia kutatua kero zilizopo katika maeneo yao.

    Nawatakia kila la kheri kiutendaji kazi kwa mwaka 2011.

    Mazungumzo hayo haliwafanya wanafunzi walioshiriki kujitambua na kubadilika kitabia na kuwa na tabia njema.

    Shughuli ambazo ninazifanya zimekuwa zinatangazwa katika machapisho, vitabu n.k., hali inayonifanya nijiamini na nitambulike kiasi cha kunitia moyo kuendelea na harakati.

    Nikiwa Liwale, nilipokea machapisho na kufanya vikao vya mara kwa mara, hali iliyonifanya nibaini kuwa kuna baadhi ya watoto/vijana hawana elimu kiasi tuliwashawishi kujiunga na madarasa ya MEMKWA, hadi hivi sasa baadhi yao wapo sekondari.

    Tabia ya kusoma machapisho, kufanya vikao na wanafunzi, wazazi na walimu kulinisaidia kwa kiasi kukubwa kuleta mahusiano mazuri ndani ya jamii.

    Shughuli ninazofanya Liwale na Kilwa zimetambulika sana ndani ya wilaya na nje ya wilaya kwa ujumla.

    Kwa kuhudhuria mikutano, midahalo na majadiliano na Marafiki wa Elimu na HakiElimu, niliweza kuwatambua na kuunganishwa na marafiki wengine. Nilijifunza changamoto zinazowakumba na kujifunza mbinu za kupambana na

    Mwezi Julai mwaka 2010, HakiElimu ilitembelea shule za msingi na kukabidhi mipira kwa lengo la kuhamasisha michezo mashuleni. Pichani ni mmoja wa wafanyakazi wa HakiElimu akikabidhi mipira kwa kaka mkuu wa shule ya msingi Changuge iliyopo wilaya ya Tarime, mkoani mara.

    Na Sylvester T. R. Karigita, Kilwa, Lindi

    Nilijiunga na harakati za Marafiki wa Elimu mwaka 2000. Nilianza harakati hizi nikiwa wilaya ya Liwale lakini kwa sasa nipo wilaya ya Kilwa mkoani Lindi . Yafuatayo ni baadhi ya mafanikio ambayo nimepata.

    Nilipata fursa ya kuunganishwa na marafiki waliopo wilaya zingine. Hii ilinisaidia kutambua shughuli wanazofanya wanaharakati wenzangu katika maeneo yao kiasi niliweza kupata ubunifu na uweza kutekeleza shughuli zifuatazo:

    Kati ya mwaka 2000-2005, nilishirikana na vijana waliopo katika kikundi cha Upendo, kwa pamoja tuliweza kuboresha mazingira ya shule katika shule ya msingi Nanjegeja wilaya ya Liwale kwa kupanda miti ya vivuli.

    Mwaka 2003-2006 tulikutana na walimu, wanafunzi pamoja na wazazi wao katika shule za msingi Kawawa, Liwale, Kambarage, Naluleo na Liwale B na kufanikiwa kupunguza tatizo la utoro katika shule hizo.

    Tulitumia machapisho na majarida kuanzisha utaratibu wa kila mwisho wa juma kufanya vikao na vijana/wanafunzi waliopo katika kikundi cha Upendo na kujadili kuhusu maeneo ambayo yanawagusa kimasomo.

    HakiElimu ni shirika la hiari linalolenga kufikia usawa, haki na demokrasia katika elimu na jamii kwa ujumla. Tunafanya hivyo kwa kuwezesha jamii

    kupata habari, kubadili shule na mfumo wa uundaji wa sera; kuchochea ubunifu wa mijadala ya umma; kufanya utafiti yakinifu, uchambuzi wa sera na

    utetezi na kushirikiana na wadau ili kuendeleza manufaa ya pamoja na kuzingatia haki za jamii.

    Je una kero, kisa au mafanikio kuhusu elimu, demokrasia na haki za binadamu katika eneo lako na ungependa maoni yako yachapishwe kwenye

    Toleo lijalo la Jarida hili la SautiElimu? Tuandikie makala nasi tutachapisha kwenye toleo lifuatalo. Toleo la 28 la Jarida la SautiElimu litabeba mada

    kuhusu nidhamu ya wanafunzi. Tutafurahi kupata maoni/mawazo kuhusiana na hiyo mada. Tuandikie kupitia anuani ifuatayo

    HakiElimu SautiElimu

    S. L. P 79401

    Dar es Salaam

    Tanzania

    Simu: (022) 2151852 au 3

    Faksi: (022) 2152449

    Barua Pepe: [email protected]

    Tovuti: www.hakielimu.org

    Shukurani kwa wachangiaji, wapiga picha, wachoraji na kwa wote walioandaa habari zilizochapishwa katika jarida hili. Unaruhusiwa kunakili sehemu yoyote ya jarida hili kwa minajili isiyo ya kibiashara. Unachotakiwa kufanya no kunukuu chanzo cha sehemu iliyonakiliwa na kutuma

    nakala mbili kwa HakiElimu.

    WahaririElizabeth Missokia

    Robert Mihayo

    MtayarishajiWambura Wasira

    WachangiajiAgnes Mangweha

    Benedicta Mrema

    Edwin Mashasi

    Honoratus Swai

    PichaHakiElimu

    HakiElimu 2011

    Pata Machapisho Mapya!