Upload
duonglien
View
294
Download
0
Embed Size (px)
Citation preview
Sheria ya Wakala wa Usimamizi wa Maafa
1
SHERIA YA WAKALA WA USIMAMIZI WA MAAFA, 2014
MPANGILIO WA VIFUNGU
Kifungu Kichwa cha habari
1. Jina na tarehe ya kuanza kutumika.
2. Matumizi.
3. Tafsiri.
SEHEMU YA PILI
WAKALA WA USIMAMIZI WA MAAFA
4. Uanzishwaji wa Wakala.
5. Kazi za Wakala.
6. Mamlaka ya Wakala.
7. Baraza la usimamizi wa maafa.
8. Kazi za Baraza.
SEHEMU YA TATU
USIMAMIZI WA WAKALA
9. Mkurugenzi Mkuu.
10. Mamlaka ya Mkurugenzi Mkuu.
11. Kurugenzi na watumishi wa Wakala.
12. Kitabu cha orodha ya vitu.
13. Kamati ya usimamizi ya Mkoa.
14. Kazi za Kamati ya Mkoa.
15. Kamati za Wilaya.
16. Kazi za Kamati za Wilaya.
17. Uwezo wa kamati za Mikoa na Wilaya.
18. Kamati za kata.
19. Kazi za Kamati za Kata.
20. Kamati za vijiji.
21. Kazi za Kamati za vijiji.
22. Miongozo ya Kamati za usimamizi.
23. Kanuni za shughuli za kamati ya maafa.
Sheria ya Wakala wa Usimamizi wa Maafa
2
SEHEMU YA NNE
HATUA ZA KULINDA RAIA
24. Hatua za kulinda raia.
25. Wajibu wa jumla.
SEHEMU YA TANO
SHUGHULI WAKATI WA MAAFA NA HALI YA HATARI
26. Kutangaza maafa.
27. Hali ya hatari inayojikusanya kwenye maeneo.
SEHEMU YA SITA
MPANGO WA TAIFA WA USIMAMIZI WA MAAFA
28. Mpango wa Taifa wa Usimamizi.
SEHEMU YA SABA
MFUKO WA USIMAMIZI WA MAAFA
29. Mfuko wa Taifa wa usimamizi wa maafa.
30. Usimamizi wa makusanyo na misaada.
SEHEMU YA NANE
MASHARTI YA FEDHA
31. Vyanzo vya fedha
32. Taarifa ya mwaka ya mahesabu.
33. Uwasilishaji wa taarifa ya mwaka.
34. Usimamizi na udhibitisho wa fedha.
35. Bajeti ya mwaka na ya nyongeza.
SEHEMU YA TISA
MAKOSA NA ADHABU
36. Kanuni za uendeshaji.
37. Uwezo wa kuwekeza.
38. Makosa na adhabu.
39. Makosa na bodi shirikishi.
Sheria ya Wakala wa Usimamizi wa Maafa
3
SEHEMU YA KUMI
MASHARTI YA MCHANGANYIKO
40. Jukwaa la Usimamizi wa maafa.
41. Kinga dhidi ya mashtaka.
42. Kanuni.
43. Kufuta na kubakiza Sura 242.
____
JEDWALI
______
Sheria ya Wakala wa Usimamizi wa Maafa
4
TAARIFA
________
Muswada huu utakaowasilishwa Bungeni umechapishwa pamoja na
Madhumuni na Sababu zake wa ajili ya kutoa taarifa kwa umma.
Dar es Salaam, OMBENI Y. SEFUE
15 Oktoba, 2014 Katibu wa Baraza la Mawaziri
MUSWADA
wa
Sheria kwa ajili ya kuanzishwa kwa Sheria ya Wakala wa Usimamizi
wa Maafa; usimamizi wa athari zitokanazo na maafa; uratibu
wa hatua za kuzuia, kukabiliana, kupunguza maafa, kujiandaa
na kurejesha hali ya awali na kuanzisha na kusimamia Mfuko
wa Usimamzi wa Maafa na kuhusiana na mambo
yanayohusiana nayo.
IMETUNGWA na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Sheria ya Wakala wa Usimamizi wa Maafa
5
SEHEMU YA KWANZA
MASHARTI YA AWALI
Jina na tarehe
ya kuanza
kutumia
1. Sheria hii itaitwa Sheria ya Uasimamizi wa Maafa
ya mwaka, 2014 na itaanza kutumika katika tarehe ambayo
itateuliwa na Waziri kupitia Tanganzo la Serikali
litakalochapishwa kwenye Gazeti.
Matumizi 2. Sheria hii itatumika Tanzania Bara Tafsiri 3. Katika sheria hii, isipokuwa kama muktadha
utahitaji vinginevyo: “Wakala” maana yake ni Wakala wa Usimamizi wa Majanga
Tanzania inayoanzishwa chini ya kifungu cha 4; “afisa muidhiniwa” maana yake ni mtu yeyote aliyeidhinishwa
kutekeleza shughuli yeyote kama atakavyoelekezwa na
Wakala; “Baraza” maana yake ni Baraza la Usimamizi wa Majanga
Tanzania linaloanzishwa chini ya kifungu cha 7; “Mkurugenzi Mkuu” maana yake ni Mkurugenzi Mkuu wa
Wakala anayeteuliwa chini ya kifungu cha 9 cha
Sheria hii; “maafa” maana yake ni tukio au mfululizo wa matukio, ama
ya asili au yanayosababishwa na binadamu,
yanayosababisha au kutishia kutokea vurugu au tishio
kwenye shughuli za jamii, yanayosababisha kuenea
kwa majanga yanayosababishwa na binadamu au ya
asili katika uchumi au mazingira yanayozidi uwezo
wa jamii hiyo kupambana nayo kwa kutumia
rasilimali zake; “eneo la maafa” maana yake ni eneo lililotangazwa kuwa
eneo la maafa chini ya Sheria hii; “usimamizi wa maafa” maana yake ni juhudi endelevu za
mipango ya utekelezaji unaolenga- (a) kuzuia hatari au tishio la maafa; (b) kupunguza ukali au matokeo ya maafa; (c) kujizatiti dhidi ya na maafa; (d) kuanzisha au kuimarisha juhudi za kujiandaa dhidi
ya maafa;
Sheria ya Wakala wa Usimamizi wa Maafa
6
(e) kuanzisha njia za haraka za kukabiliana na maafa; (f) kuanzisha au kuimarisha njia za kurudisha hali ya
kawaida baada ya maafa na kurekebisha athari
zitokanazo na maafa. “kujiandaa na maafa” maana yake ni hali ya kuwa tayari
kukabiliana na tishio la hali ya maafa, maafa na athari
zake; “uzuiaji wa maafa” maana yake ni hatua zinazochukuliwa
kuondoa au kuzuia matukio ya kibinadamu au ya asili
yasisababishe kutokea kwa maafa; “urekebishaji wa athari za maafa” maana yake ni hatua
zinazosaidia kurejesha hali ya maisha, mali na
kiwango cha uzalishaji cha jamii zilizoathirika
kurejesha miundombinu muhimu, uwezo wa
uzalishaji, taasisi na huduma zilizoharibiwa au
kuonekana kutokufanya kazi kutokana na maafa na
kusaidia kuleta maendeleo endelevu kwa kufanya
marekebisho muhimu kwa mabadiliko
yaliyosababishwa na maafa au kuboresha na kurudisha
katika hali ya kawaida; “kukabiliana na maafa” maana yake ni hatua yoyote
inayochukuliwa kabla na mara baada ya athari za
maafa inayochukuliwa kuokoa maisha, kulinda mali na
mazingira au kushughulikia uharibifu uliotokea na
madhara mengine yaliyosababishwa na maafa; “upunguzaji wa hatari za maafa” maana yake ni hatua
zinazochukuliwa kupunguza uwezekano wa matokeo
yenye athari ya maafa kama vile vifo, majeruhi,
matarajio ya upotevu wa mali, maisha, kuathirika kwa
shughuli za uchumi au uharibifu wa mazingira
unaotokana na mwingiliano wa athari za asili
zinazotokana na mazingira magumu na shughuli za
binadamu; “Waziri” maana yake ni Waziri mwenye dhamana ya
usimamzi wa maafa; “kupunguza” maana yake ni hatua zinazoelekezwa
kupunguza athari, matokeo au athari za maafa;
Sheria ya Wakala wa Usimamizi wa Maafa
7
“Mpango wa Taifa wa Usimamizi wa Maafa” maana yake ni
mpango ambao unelezea hatua zitakazochukuliwa
katika kushughulikia, kupunguza hatari za usimamizi
wa maafa; “maafa ya asilia” maana yake ni maafa yanayotokana na
mwingiliano wa matukio ya asili bila kusababishwa na
binadamu na inajumuisha matukio kama vile,
tetemeko, kimbunga, mafuriko, ukame, moto au
magonjwa ya mlipuko; “Jukwaa” maana yake ni Jukwaa la Taifa la Usimamizi wa
Maafa lililoanzishwa chini ya Sheria hii; “Kamati ya Kata” maana yake ni Kamati ya Usimamizi wa
Maafa ya Kata iliyoanzishwa chini ya Sheria hii; “Kamati ya Kijiji” maana yake Kamati ya Kijiji ya Usimamzi
wa Maafa iliyoanzishwa chini ya Sheria hii; “Kamati ya Mkoa” maana yake ni Kamati ya Mkoa ya
Usimamizi wa Maafa iliyoanzishwa chini ya Sheria
hii; “udhaifu” maana yake ni kiwango cha uwezekano wa watu
kupatwa au kuathirika na maafa.
SEHEMU YA PILI
WAKALA WA USIMAMIZI WA MAAFA
Uanzishwaji
wa Wakala 4.-(1) Inaanzishwa wakala ambayo itajulikana kama
Wakala wa Usimamizi wa Maafa Tanzania. (2) Wakala itakuwa ni Bodi hodhi na kwa jina lake
hodhi litakuwa na uwezo wa- (a) kushtaki na kushtakiwa; (b) kuingia katika mikataba, makubaliano, waraka wa
maelewano, hati na kutekeleza mipangilio
mingine; (c) kumiliki mali inayohamishika na isiyohamishika;
na (d) kuwa na muhuri wake.
Sheria ya Wakala wa Usimamizi wa Maafa
8
(3) Mwanasheria Mkuu atakuwa na haki ya
kuunganishwa katika shauri lolote au jambo lolote
lililofunguliwa na au dhidi ya Wakala. (4) Endapo, Mwanasheria Mkuu ataunganishwa katika
shauri lolote, masharti ya Sheria ya Mwenendo wa Mashauri
ya Serikali yatatumika, katika shauri au jambo hilo kama
kwamba yamefunguliwa na au dhidi ya Serikali. (5) Kwa madhumuni ya vifungu (3) na (4), Wakala
itakuwa na wajibu wa kumfahamisha Mwanasheria Mkuu
kuhusu shauri lolote ambalo liko mahakamani au kusudio la
kufungua shauri au kupeleka suala au suala kwa au dhidi ya
Wakala.
Kazi za
Wakala 5.-(1) Wakala itakuwa ni kitovu cha taifa cha kuratibu
upunguzaji wa hatari ya maafa na usimamizi wake. (2) Katika utekelezaji wa kazi zake kufuatana na
masharti ya kifungu kidogo cha (1), Wakala- (a) itatayarisha sera na mipango kwenye shughuli zote
zinazohusiana na usimamizi wa maafa Tanzania
Bara; (b) itakuwa kituo cha mipango, asasi ya uratibu na
usimamizi wa uzuiaji, upunguzaji, utayarishaji,
kukabiliana, utekelezaji na uokoaji baada ya maafa
kwa kuzingatia uwezekano wa kuwepo kwa hatari
ya maafa; (c) itaratibu na kusimamia taasisi za wizara, sekta
mbalimbali na kamati za kitaalam zenye dhamana
ya usimamzi wa maafa katika ngazi zote; (d) itaunda Kituo cha Dharura cha Kusimamia Maafa; (e) itaunda mfumo wa tahadhari ya awali
utakaohusisha sekta zote na kuwa kiungo kati ya
asasi mbalimbali zinatoa huduma ya tahadhari; (f) itaendeleza elimu, uelewa na utumiaji wa taarifa,
teknolojia ya mawasiliano ya usimamizi wa maafa
kwa ajili ya kutoa elimu kwa umma; (g) kutafuta rasilimali kwa ajili ya usimamizi wa
shughuli za maafa; na
Sheria ya Wakala wa Usimamizi wa Maafa
9
(h) kuhitaji kutoka taasisi yoyote, idara, mamlaka, mtu
au watu, kupeleka taarifa inayotakiwa kwa ajili ya
shughuli za usimamzi wa maafa kama Mkurugenzi
atakavyoelekeza.
Mamlaka ya
wakala 6.-(1) Kwa madhumuni ya kutekeleza kazi zake,
Wakala itakuwa na mamlaka ya- (a) kuamuru watu kuondoka katika meneo ya maafa
au maeneo yanayopatwa na maafa mara kwa mara; (b) kusimamisha au kuzuia mauzo kutoa au
kushirikisha vileo, vinywaji, silaha, milipuko, au
mazao mengine ambayo hayapaswi kuwa kwenye
maeneo ya maafa; na (c) kuchukua na kutumia rasilimali za Serikali
itajumuisha maghala, vifaa na nyenzo nyingine
kama itakavyonekana ni lazima kwa shughuli za
dharura.
(2) Wakala itatumia mamlaka iliyopewa katika
utekekezaji wa maelekezo yoyote yaliyotolewa chini ya
mamlaka yake na kuchukua na kusababisha kuchukuliwa kwa
hatua hizo ikijumuisha kupeleka shauri mahakamani au
kwenye baraza.
(3) Wakala anaweza, baada ya kutoa taarifa ya
kuridhisha ya kusudio lake la kuchukua hatua hizo, kuelekeza
taasisi, idara, mamlaka, mtu au chombo cha watu, kutekeleza,
ndani ya muda utakaopangwa na kwanamna kama
itakavyoelekeza, kazi yoyote au nyingine iliyowekwa na au
chini ya Sheria hii au Sheria nyingine yoyote kuhusiana na
usimamizi na utekelezaji wa Sheria.
(4) Endapo itatokea kushindwa kutekelea maelekezo
hayo, Wakala inaweza kufanya au kusababisha kufanyika kazi
zinazotakiwa na gharama zitakazotumika zitarudishwa na
Wakala kutoka kwenye taasisi, idara, mamlaka, mtu au
chombo cha watu shirikishi kwa njia ya madai.
Sheria ya Wakala wa Usimamizi wa Maafa
10
Baraza la
usimamizi
wa maafa
7.-(1) Kutakuwa na Baraza la Usimamizi wa Maafa
Tanzania.
(2) Baraza litaundwa na wajumbe wafuatao- (a) Katibu Mkuu Wizara yenye dhamana ya
Usimamizi wa maafa ambaye atakuwa
Mwenyekiti; (b) Katibu Mkuu Wizara yenye dhamana ya ulinzi na
Jeshi la Kujenga Taifa ambaye atakuwa Makamu
wa Mwenyekiti; (c) Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali; (d) Katibu Mkuu Wizara yenye dhamana ya mamlaka
na tawala za mikoa na serikali za mitaa; (e) Katibu Mkuu Wizara yenye dhamana na fedha; (f) Katibu Mkuu Wizara yenye dhamana na afya na
ustawi wa jamii; (g) Katibu Mkuu Wizara yenye dhamana na
mawasiliano; (h) Katibu Mkuu Wizara yenye dhamana na
mazingira;
(i) Katibu Mkuu Wizara yenye dhamana na Kilimo; na
(j) Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Hali ya Hewa Tanzania.
(3) Mkurugenzi Mkuu wa Wakala atakuwa Katibu wa
Baraza.
(4) Baraza linaweza kumualika mtu yeyote wakati wa
Mkutano wake kama Baraza litakavyoona lazima.
(5) Masharti ya Jedwali la Sheria hii yatahusu
shughuli za Baraza na mambo mengine yanayohusiana nayo.
Kazi za
Baraza 8.-(1) Baraza litasimamia shughuli za Wakala.
(2) Katika kutekeleza kazi zake, Baraza litakuwa na
Sheria ya Wakala wa Usimamizi wa Maafa
11
jukumu la- (a) kuhakikisha kwamba juhudi za kupunguza athari
za maafa zinajumuisha taasisi muhimu za Serikali,
sera za maendeleo, mikakati na program za kitaifa,
kimkoa na kimtaa; (b) kutoa msaada katika utafutaji wa rasilimali kwa
azma ya kupata njia bora ya kupunguza na
kusimamia athari za maafa; (c) kuhamasisha maendeleo ya taarifa za Taifa na
uelewa wa mikakati ya usimamizi na uanzishaji wa
mtandao wa wadau wa athari za usimamizi wa
maafa; (d) kupitia na kuboresha sera za usimamizi wa athari
za maafa; na (e) kumshauri Waziri kuhusiana na usimamizi wa
maafa na mambo yote yanayohusiana nayo.
SEHEMU YA TATU
USIMAMIZI WA WAKALA
Mkurugnezi
Mkuu 9.-(1) Kutakuwa na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala
ambaye atateuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watumishi
wa umma wenye sifa husika.
(2) Mkurugenzi Mkuu atakaa madarakani kwa kipindi
cha miaka mitano na anaweza kuchaguliwa kwa mara
nyingine.
(3) Mkurugenzi Mkuu atakuwa Mtendaji Mkuu na
Afisa Masuhuli wa Wakala na atawajibika kwenye Baraza. Mamlaka ya
Mkurugenzi
Mkuu
10.-(1) Mkurugenzi Mkuu anaweza wakati wa hali ya
hatari na baada ya kushauriana na Mwenyekiti wa Baraza
kutoa maelekezo au amri ambayo ni muhimu katika
kushughulikia jambo husika.
(2) Mkurugenzi Mkuu baada ya kushauriana na
Mwenyekiti-
Sheria ya Wakala wa Usimamizi wa Maafa
12
(a) atamfahamisha Waziri kuhusu hatua za dharura
zilizochukuliwa ili kukabili hali iliyotokea; (b) kuelekeza kuwepo kwa mkutano wa dharura wa
Baraza ili kutoa maamuzi kuhusu hali iliyotokea. Kurugenzi
nawatumishi
wa Wakala
11.-(1) Wakala kwa idhini ya Mamlaka husika,
anaweza kuanzisha kurugenzi, vitengo kama itakavyoonekana
lazima kwa ajili ya utekelezaji wa kazi za Wakala.
(2) Wakala, kwa idhini ya Baraza itateua au kuajiri
idadi ya maofisa wa umma kama itakavyoonekana ni lazima
kwa ajili ya utekelezaji mzuri wa kazi chini ya sheria hii.
Kitabu cha
orodha ya
vitu
12.-(1) Mkurugenzi Mkuu ataanzisha na kutunza
Ktabu cha orodha ya vitu kwa ajili ya misaada ya kimaisha na
uhakiki wa muundo mbinu kwa ajili ya shughuli za usimamizi
wa majanga.
(2) Kitabu au orodha iliyoandaliwa na Wakala
itakuwa ni mali ya kiofisi kwa matumizi ya Wakala, na
Wakala anaweza akawashirikisha taarifa zilizomo katika
kitabu au orodha na mtu mwingine yeyote, idara au taasisi
kama atakavyoona inafaa.
(3) Uhakiki wa miundombinu kama, ilivyotumika
katika kifungu kidogo cha (1), ina maana yake, mchakato wa
mfumo, nyenzo, teknolojia, mtandao, mali na huduma
maalum za afya, usalama, au uchumi mzuri na utekelezaji wa
kazi za Serikali na jamii. Kamati ya
usimamizi ya
Mkoa
13.-(1) Sekretarieti ya Mkoa ilianishwa chini ya
Sheria ya Tawala za Mikoa, itakuwa Kamati ya usimamizi ya
Maafa ya Mkoa katika mamlaka ya mipaka yake.
(2) Bila kuathiri masharti ya kifungu kidogo cha (1)
na kifungu cha (2) cha sheria ya Tawala za Mikoa, Kamati ya
Mkoa pamoja na Wajumbe wa Sekretarieti ya Mkoa
ikiwajumuisha wajumbe wafuatao waliochaguliwa na Katibu
Tawala wa Mkoa-
Sheria ya Wakala wa Usimamizi wa Maafa
13
(a) mratibu wa usimamizi wa maafa wa mkoa, (b) mwakilishi kutoka jumuiya asasi zisizo za serikali
za mkoa; (c) wawakilishi wawili kutoka sekta binafsi ndani ya
mkoa; (d) mwakilishi wa Mkoa wa Chama cha Msalaba
Mwekundu na asasi nyingine za kibinadamu na za
kujitolela; (e) wawakilishi watatu kutoka taasisi za dini; na (f) watu wawili mashuhuri.
(3) Bila kujali masharti ya kifungu kidogo cha (2),
kamati ya Mkoa inaweza, kumwita mtu yeyote ambaye si
mjumbe wa kamati kuhudhuri na kutoa maamuzi ya kamati.
(4) Mratibu wa kamati ya usimamizi wa maafa ya
mkoa kwa madhumuni ya kifungu hiki atakuwa Katibu wa
Kamati ya Mkoa.
Kazi za
Kamati ya
Mkoa
14. Kazi za Kamati za Mkoa zitakuwa-
(a) kumshauri Mkuu wa Mkoa kwenye masuala ya
usimamizi wa maafa na shughuli zinazofanywa
mkoani na mambo mengine yoyote yatakayoletwa
na Kamati ya Mkoa; (b) kuangalia na kuratibu upungazaji wa athar za
usimamzi wa maafa na shughli za dhamila
miongoni mwa taasisi za kisekta za Serikali,
Serikali za mitaa, jamii na wahenga wengine
wanaojihusisha katika upunguzaji wa athari za
usimamiziw a maafa; (c) kuhamasisha rasilimali kwa ajili ya usimamizi wa
maafa na kushughulika na maafa yanayotokea
katika mikoa yao;
(d) kulinganisha mfumo wa awali wa tahadhari wa
Mkoa na kuwezesha uanzishaji wa kuwa na data za
taarifa ya athari za maafa kimkoa kwa kushirikiana
Sheria ya Wakala wa Usimamizi wa Maafa
14
na Wakala; na (e) kuratibu mipango ya Wilaya katika kuzuia maafa
na namna ya kuyapunguza iliyowasilishwa na
Kamati ya Wilaya.
Kamati za
Wilaya 15.-(1) Kamati ya Baraza la Usimamizi lililoanzishwa
chiniya Sheria ya Serikali ya Mtaa (Mamlaka ya Mji) na
Sheria ya Serikali ya Mtaa (Mamlaka ya Wiaya) kwa ajili ya
Sheria hii, zitakuwa Kamati za usimamizi za maafa za Wilaya
katika maeneo ya mamlaka ya Wilaya husika.
(2) Bila kuathiri kifungu akidogo cha (1) na masharti
ya sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka ya Wilaya) kuhusu
uundwaji wa Baraza la usimamizi, Kamati za Wilaya
zitajumuisha pamoja na wajumbe wa Kamati ya Usimamizi
wa Baraza ikiwajumuisha wajumbe walioteuliwa na
Mkurugenzi Mtendaji wafuatao- (a) mratibu wa Wilaya wa usimamzi wa maafa; (b) wawakilishi wawili wa sekta binafsi ndani ya
Wilaya; (c) wawakilishi katoka jumuiya ya Mkoa ya Asasi
zisizo za Serikali; (d) watu wawili mashuhuri; (e) mwakilishi wa Wilaya wa chama cha Msalaba
Mwekundu na taasisi za hiari na za kujitolea; (f) wawakilishi watatu wa taasisi za dini;
(3) Bila kujali masharti ya kifungu kidogo cha (2),
Mkurugenzi wa Halmashauri ikiwa ataonekana lazima,
kumwita mtu yeyote ambaye si mjumbe wa kamati
kuhudhuria maazimio ya kamati.
(4) Mratibu na msimamizi wa maafa wa Wilaya kwa
madhumuni ya kifungu hiki atakuwa katibu wa kamati wa
Wilaya;
Kazi za
Kamati za
Wilaya
16. Kazi za Kamati ya Wilaya zitakuwa-
Sheria ya Wakala wa Usimamizi wa Maafa
15
(a) kumshauri Kamishna kuhusu masuala ya
usimamizi wa maafa na kufanya shughuli za
wilaya na mambo mengine yaliyoletwa na Mkuu
wa Wilaya; (b) kuangalia na kuratbu athari za usimamizi wa maafa
na shughuli za dharura katika ngazi ya wilaya; (c) kuhamasisha rasilimali zinazohusiana na
usimamizi wa maafa.
Uwezo wa
kamati za
Mikoa na
Wilaya
17. Kamati za Usimamizi maafa na mkoa na wilaya
zitashirikiana na Wakala, zitakuwa na uwezo wa-
(a) kuelekeza taasisi zote katika Mkoa na Wiaya
kutayarisha, kuzuia au kupunguza maafa; (b) kuamuru watu kuondoka katika maeneo ambayo
yameathirika au kufikiwa na maafa na kuwapangia
maeneo mengine; (c) kumuomba mtu yeyote au asasi ndani ya mkoa au
wilaya kutoa usafiri, jingo oote, vifaa, bidhaa muhimu
na usambazaji mwingine kwa ajili ya kusaidia juhudi
za usimamizi katika wilaya; (d) kuanzisha kamatiai ndogo kwa ajili ya kuhakikisha
utekelezaji mzuri wa kazi zake; (e) kufanya jambo lolote ambalo ni la lazima kufanywa au
kulingana na utekelezaji wa kazi zake chini ya sheria
hii kutegemeana na sera iliyoanzishwa, mipango na
taratibu; Kamati za
kata 18.-(1) Vikundi vya usimamizi vya Kata
vinavyoundwa chini ya sheria ya Serikali za mitaa (Mamlaka
ya Wilaya) kwa madhumuni ya sheria hii, zitakuwa kamati za
usimamizi wa maafa za Kata kutoka maeneo ya mamlaka zao.
(2) Bila kuathiri kifungu kidogo cha (1), na masharti
ya Sheria ya Seriakli za Mitaa (Mamlaka ya Wilaya)
kuhusiana na uundaji wa vikundi vya usimamizi vya kata,
kamati za Kata kwa kujumuisha wajumbe wa vikundi vya
usimamizi za kata, ikijumuisha wajumbe wafuatao ambao
wameteuliwa na Mkurugenzi wa Baraza kwa kushauriana na
Sheria ya Wakala wa Usimamizi wa Maafa
16
Afisa Kaa Mtendaji. (a) wawakilishi wawili kutoka sekta binafsi ndani ya
Kata; (b) wawakilishi wa taasisi za kijamii ndani ya Kata; (c) watu wawili mashuhuri; (d) mwakilishi kutoka chama cha msalaba mwekundu
na taasisi nyingine za kibinadamu na hiari; na
(2) wawakilishi watatu kutoka taasisi za dini.
(3) Afisa mtendaji wa kata aweza, iwapo ataona kuna
ulazima, kumjumuisha mtu yeyote ndani ya kata husika
ambaye si mjumbe wa Kamati kuhudhuria kikao cha kamati.
(4) Mkurugenzi wa Halmashauri wa Kata, atamfanya
afisa yeyote wa kata kuwa Katibu wa kamati ya Kata kwa
madhumuni ya kifungu hiki.
Kazi za
Kamati za
Kata
19. Kazi za Kmati ya Kata zitakuwa ni:
(a) kuangalia na kuratibu athari za usimamizi wa
maafa na shughli za dhamira katika ngazi ya Kata; (b) kuhamasisha rasilimali klingana na usimamizi wa
maafa; (c) kusaidia utekelezaji wa mipango ya usimamizi wa
mafaa ya kata; (d) kutoka katika utaratibu ulioratibiwa,hali yoyote ya
dharura katika ngazi ya kata.
Kamati za
Kata 20.-(1) Kikundi cha usimamizi wa kijiji
kinachoanzishwa chini ya sheria ya serikali (mamlaka ya
wilaya) kwa madhumuni ya sheria hii, Kamati ya usimamizi
ya maafa ya vijiji katika maeeo ya mamlaka yake.
(2) Bila kuathiri kifungu kidogo cha (1) na masharti
ya sheria ya Serikari (Mamlaka za Wilaya) kuhusu aina na
uundaji wa kikundi cha wilya kwa kujumuisha wajumbe wa
kikundi cha utawala wa kijiji. Ikijumuisha wajumbe wafuatao
walioteuliwa na Mkurugezi wa Halmashauri kwa kushauriana
Sheria ya Wakala wa Usimamizi wa Maafa
17
na Afisa Mtendaji wa Kijiji: (a) wawakilishi wa sekta binafsi zilizopo katika kijiji; (b) mwakilishi wa jumuiya za asasi zisizo za Serikali
zilizopo katika kijiji; (c) watu wawili mashuhuri; (e) mwakilishi kutoka chama cha msalaba mwekundu
na taasisi dini.
(3) Bila kujali masharti ya kufungu kidogo (2), Afisa
Mtendaji wa kijiji aweza, pale anapoona ni lazima kumwita
mtu yeyote kutoka ndani ya kijiji husika ambaye si mjumbe
wa kamati kuhudhuria kikao cha maamuzi cha Kamati.
(4) Mkurugenzi wa Baraza kwa kushuriana na Afisa
Mtendaji wa Kijiji atamfanya afisa yeyote wa kijiji kuwa
Katibu wa Kamati ya Kijiji kwa madhumuni ya kifungu hiki.
Kazi za
Kamati za
vijiji
21.-(1) Kazi za Kamati za Kijiji zitakuwa-
(a) kuangalia na kuratibu athari za usimamizi wa
maafa na shughuli za dharura katika ngazi ya
kijiji; (b) kuwa kama chombo cha taarifa kuhusiana na
utoaji taarifa za athari mapema; (c) kuhamasisha rasilimali kuhusu usimamizi wa
maafa; (d) kutekeleza mipango ya utoaji taarifa na
uwelewa katika vijiji; na (e) kuitikia katika utaratibu ulioratibiwa hali
yoyote ya dharura katika ngazi ya kijiji.
(2) Katika utekelezaji wa kazi zake, Kamati ya kijiji
kama itakavyowekana itatumia sheria za kimira, taratibu za
kimila na mbinu za wazawa ya tahadhari na mawasiliano.
Miongozo ya
Kamati za
usimamizi
22.-(1) Waziri anaweza kutengeneza mwongozo kwa
ajili ya usimamizi mzuri kamati za wilaya, Kata na vijiji.
Sheria ya Wakala wa Usimamizi wa Maafa
18
(2) Miongozo iliyotengenezwa chini ya kifungu hiki
zitaelezea- (a) utayarishaji wa mipango kwa ngazi mbalimbali ya
Kamati; (b) njia za mawasiliano na usambazaji wa taarifa
kuhusiana na kupunguza athari za maafa na
usimamizi; (c) usambazaji wa taarifa mapema kuhusiana na
tahadhari; (d) uendeshaji wa shughuli za Kamati.
(3) Waziri anaweza kutunga miongozo ambavyo
itatumwa na Kamati zilizoainishwa. Kanun za
shughuli za
kamati ya
maafa
23. Kamati za Mkoa, Wilaya, Kata na vijiji zitaweka
kanuni za kujiongoza katika mamlaka zao husika.
SEHEMU YA NNE
HATUA ZA KULINDA RAIA
Hatua za
kulinda raia 24.-(1) Wakala itaweka hatua za kulinda raia kwa asasi
za Serikali za mitaa na asasi za Sekta mbalimbali
zinazojihusisha na usimamizi wa maafa.
(2) Kwa madhumuni ya kifungu kidogo cha (1) wakala
atachukua watu kama itakavyoweza kuona ni lazima
kuendeleza mipango kwa kupanga uwezao kwa Kamati za
Mikoa na Wilaya, taasisi za serikali na taasisi mbalimbali za
kisekta mufuata na masharti ya huduma za lazima na taratibu
zitakazofuatwa katika kutekeleza shughuli za uokoaji wa
maafa. (3) “Kulinda raia mali” ilivyotumika katika kifungu
hiki, ina maana ya juhudi za pamoja za vitengo tofauti za
dharura katika kuandaa jamii kujilinda na hatari ya
kuongezeka ka maafa.
Wajibu wa
jumla 25. Kila mtu ana wajibu wa -
(a) kuweka mpangilio wa ustawi wa jamii na kutunza
Sheria ya Wakala wa Usimamizi wa Maafa
19
amani na mapatano; (b) kutunza tatbia ambazo zinapunguza athari za
maafa; na (c) kuwa tayari kuonyesha na kuridhia kushiriki katika
shguhuli za usimamizi wa maafa.
SEHEMU YA TANO
SHUGHULI WAKATI WA MAAFA NA HALI YA HATARI
Kutangaza
maafa 26.-(1) Pale wakala atakaporidhika kwamba hali ya
Hatari inajikusanya kwenye eneo la maafa, itahuisha mpango
wa dhamira wa kujiandaa na kutekelezaji wa Taifa kwa
kutumika katika eneo hilo kwa kipindi cha miezi mitatu.
(2) Pale ambapo mpango wa dharura wa Taifa wa
kujiandaa na utekelezaji una huishwa katika eneo, Waziri
atatoa amri kwenye Gazeti, kuweka utaratibu wa shughuli
ambazo zitatumika katika eneo hilo.
(c) Hali ya Hatari
Hali ya hatari
inayojikusan
ya kwenye
maeneo
27.-(1) Pale hali ya hatari inapojikusanya kwenye
maafa ni ya aina ambayo kwamba inahitaji hatua za kipekee,
Baraza litapendekeza kwa Waziri kwamba hali ya hatari
itatangazwa katika eneo lolote au kwa Tanzania Bara pale,
baada ya waziri kuridhika kwamba hali ya hatari ya maafa
inaruhusu kutangazwa kwa hali ya hatari, Waziri atamuomba
Rais kutumia uwezo wake alipopewa na Katibu kutangaza hai
ya htari kwa eneo husika au Tanzania Bara yote.-
(2) Tangazo la hali ya Hatari litajumuisha na kueleza
hatua za haraka ambazo zitakazochukuliwa ikijumuisha- (a) kuwahamisha au kuwaondoa watu na mali zao; (b) kutumia msaada wa Jeshi; (c) kupata msaada wa kimataifa; (d) hatua nyingine kama itakavyokuwa lazima
kulingana na hali halisi ya mazingira.
Sheria ya Wakala wa Usimamizi wa Maafa
20
SEHEMU YA SITA
MPANGO WA TAIFA WA USIMAMIZI WA MAAFA
Mpango wa
Taifa wa
Usimamizi
28-(1) Wakala kwa kibali cha Waziri, atatayarisha na
kutunza mpango wa Taifa wa usimamizi wa maafa.
(2) Mpango wa Taifa wa usimamizi wa maafa
utaunganishwa katika mpango wa maendeleo wa Taifa wa
mwaka na utakuwa unahuishwa na kutengenezwa kama ni
lazima. (3) Mpango wa Taifa na usimamizi wa maafa
itawezesha mwelekeo wa upunguzaji wa athari za maafa na
usimamizi katika maendeleo na kisekta na itatumiwa na
Wakala, Kamati za Mkoa na Wilaya na Serikali na asasi
mbalimbali.
(4) Kwa madhumuni ya kifungu kidogo cha (3) Kila
Wakala, Kamati za Mikoa na Wolaya, Serikali na asasi
mbalimbali za kisekta zitakayarisha na kuwasilisha taarifa ya
mwaka kwenye Jukwaa la Taifa la Usimamizi wa Maafa kwa
majadiliano na kupeana uzoefu.
(5) Waziri, kwa kanuni atatoa tamko kwa mambo
ambayo atayajumuisha katika mpango wa Taifa wa usimamizi
wa maafa.
SEHEMU YA SABA
MFUKO WA USIMAMIZI WA MAAFA
Mfuko wa
Taifa wa
usimamizi
wa maafa
29.-(1) Kutakuwa na Mfuko wa Taifa wa Usimamizi
wa maafa.
(2) Vyanzo vya fedha vya Mfuko vitakuwa- (a) kiasi cha fedha ambacho kitakachoainihswa na
Bunge kwa madhumuni ya usimamizi wa maafa; (b) mchango wa hiari kwa Mfuko kutoka kwa mtu
yeyote au taasisi; (c) fedha yoyote ambayo imetolewa kwa njia kya
msaada au mkopo kutoka ndani na nje ya Jamhuri
Sheria ya Wakala wa Usimamizi wa Maafa
21
ya Muungano. (d) fedha yoyote iliyopatikana kwa njaa mauzo ya vitu
vilivyotolewa kama msaada; na (e) kutokana na harambee;
(3) Mfuko utasimamiwa na kuongozwa na wakala na
Mkurugenzi Mkuu atakuwa ndiye afisa masuhuli.
(4) Mfuko utatumika kwa- (a) masharti ya bidhaa muhimu na misaada mingine
kwa waathirika wa maafa yoyote, hatari au
dharura; na (b) kuzuia, kupunguza, kutayarisha katika maafa na
shughuli nyingine zinazohusu usimamizi wa
maafa.
Usimamizi
wa
makusanyo
na misaada
30.-(1) Wakala unaweza kuendesha mchango maalum
au wa jumla kwa jamii kuchangia vitu au fedha kwa
madhumuni ya kuokoa maisha, vitu, kupunguza uharibifu au
kuhifadhi maisha ya jamii iliyoathirika na maafa.
(2) Pale ambapo kuna mantiki kwa ombi la wakala,
mtu yeyote au taasisi inayokusanya vitu au fedha
zilizochangwa, itatakiwa kuwasilisha taarifa kwa wakala,
kuelezea vitu vilivyokusanywa na fedha ambayo vitu hivyo
au fehda ziligawiwa kwa jamii iliyoathirika na maafa.
(3) Kwa madhumuni ya kifungu kidogo cha (2),
misaada kwa jamii iliyoathirika na maafa itapelekwa moja
kwa moja kwa jamii husika au kupitia kamati za Mkoa au
Wilaya, Wakala au viongozi wa Kitaifa.
SEHEMU YA NANE
MASHARTI YA FEDHA
Vyanzo vya
fedha 31.-(1) Vyanzo vya fedha za Wakala vitajumuisha-
(a) fidia kama zitakavyoainishwa na Bunge ; (b) fedha zozote au rasilimali ambayo inaweza
kuwekwa au kupatikana kutoka kwenye vyanzo
Sheria ya Wakala wa Usimamizi wa Maafa
22
vingine; (c) ada zinazowekewa na gharama nyingine
zilizokusanywa kutoka katika huduma
zilizotolewa. (d) zawadi, mikopo na michango; (e) fedha inayopatikana kutokana na mauzo ya
rasilimali za wakala; na (f) fedha nyingine yoyote, iliyokopwa, kupokelewa
na, au iliyopatikana kwa ajili ya Wakala kwa
madhumuni ya kazi zake.
(2) Ada na malipo yanalipwa chini ya Sheria hii
yataelezewa na kanuni.
Taarifa ya
mwaka ya
mahesabu
32.-(1) Katika sheria “mwaka wa fedha” ina maana ya
mwaka wa fedha wa Serikali.
(2) Mkurugenzi Mkuu, katika kila “mwaka wa fedha”
atatayarisha taarifa ya utekelezaji wa mwaka wa shughuli
zinazochukuliwa na wakala na kuwasilishwa kwa Waziri
baada ya kuidhinishwa na Bodi.
(3) Mkurugenzi Mkuu, atahakikisha kwamba taarifa ya fedha
ya mwisho wa mwaka inaandaliwa na kukaguliwa ndani ya
miezi mitatu baada ya mwaka wa fedha.
(4) Taarifa ya fedha itajumuisha- (a) taarifa ya utendaji wa fedha; (b) taarifa ya hali ya fedha; (c) taarifa ya mtiririko wa fedha; (d) taarifa ya mabadiliko ya hisa; na (e) tangazo la taarifa ya fedha.
Uwasilishaji
wa tarifa ya
mwaka
33.-(1) Mkurugenzi Mkuu atawasilisha kwa Waziri
taarifa ya fedha iliyokaguliwa pamoja na taarifa ya Mkaguzi
wa Mahesabu hayo miezi mitatu baada ya mwisho wa mwaka
wa fedha wa kila mwaka.
(2) Mkurugenzi Mkuu atatayarisha na kuwasilisha
Sheria ya Wakala wa Usimamizi wa Maafa
23
kwenye bodi makadirio ya mapato na matumizi ya wakala
miezi mitatu kabla ya mwisho wa mwaka unaoisha.
(3) Hakuna matumizi yatakayofanywa ndani ya
makadirio ya mwaka wa fedha kutoka katika fedha za Wakala
isipokuwa kama itaidhinishwa na Mkurugenzi .
Usimamizi
na
uthibitisho
wa fedha
34.-(1) Wakala itatunza vitabu vya mahesabu na
kuweka kumbukumbu za shughuli zake kulingana na viwango
vya mahesabu ya Kitaifa.
(2) Wakala atasababisha kutayarisha na kutunza vizuri
vitabu vya mahesabu na kumbukumbu kufuata na- (a) rasilimali na madeni; (b) mapato na matumizi ya fedha na Ankara nyingine
za fedha; (c) taarifa ya hali ya fedha na taarifa inayoonyesha
maelezo ya utendaji wa fedha utakaotayarishwa
kila mwaka wa fedha;
(3) Feha na rasilimali za Wakala zitatumika kwa ajili
ya utekelezaji mzuri wa malengo ya sheria hii.
(4) Matumizi ya Wakala yatakuwa kwa mujibu wa
usimamizi wa kupitiwa. Bajeti ya
mwaka na ya
nyongeza
35.-(1) Bodi itaidhinisha bajeti ya mwaka ya kiasi
kinachotarajiwa kupokelewa na kulipwa kwa kipindi cha
mwaka huo wa fedha, si chini ya mwezi mmoja kabla ya
kuanza kwa mwaka wa fedha wowote.
(2) Pale ambapo katika mwaka wowote wa fedha,
Wakala inataka kufanya malipo yoyote ambayo
hayakutolewa au kiasi chochote kinachozidi kiasi ambacho
kiliwekwa katika bajeti ya mwaka huo, Bodi itaidhinisha
bajeti ya nyongeza inayoelezea malipo hayo.
(3) Bajeti ya Mwaka na kila bajeti ya nyongeza
itakuwa katika fomu na itajumuisha maelezo kama
Sheria ya Wakala wa Usimamizi wa Maafa
24
yatakavyotakiwa na sheria.
Kauni za
uendeshaji 36. Wakala-
(a) itafungua na kuendesha vitabu vyote vya
mahesabu, leja, jarada na vitabu vingine vya
mahesabu kufuatana na kitabu cha mwongozo wa
mahesabu; (b) itapitia na kubadili hati kwa ajili ya kurejesha
uwekaji mzuri wa vitabu vya mahesabu kama
itakavyoelekezwa na mamlaka husika.
Uwezo wa
kuwekeza 37. Wakala inaweza kwa idhini ya Waziri mwenye
dhamana ya mambo ya fedha, kuwekeza fedha yoyote katika
namna ambayo itaona inafaa.
SEHEMU YA TISA
MAKOSA NA ADHABU
Makosa na
adhabu 38. Mtu ambaye-
(a) anachelewesha au kumzuia afisa yeyote
kutekeleza kazi zake chini ya Sheria hii. (b) anakataa kumpa afisa yeyote msaada unaofaa
kama atakavyoombwa na afisa kwa
madhumuni ya kutekeleza kazi zake chini ya
sheria hii. (c) anatoa taarifa za uongo na huku anajua
kwamba si za kweli, anatenda kosa na akitiwa
htiani atalipa adhabu ya fehda zisizopungua
shilingi milioni moja au kifungo kwa kipindi
kisichozidi miaka miwili au vyote viwili.
Makosa na
bodi
shirikishi
39. Pale kosa linapokuwa linatendeka na bodi
shirikishi au shirika, mtu yeyote ambaye wakati kosa hilo
linatendwa alihusika na usimamizi wa bodi shirikishi hiyo au
shirika atachukuliwa kuwa amefanya kosa hilo yeye.
Sheria ya Wakala wa Usimamizi wa Maafa
25
SEHEMU YA KUMI
MASHARTI YA MCHANGANYIKO
Jukwaa la
Usimamizi
wa maafa
40.-(1) Kutokana na Jukwaa la Taifa la usimamizi wa
maafa ambalo litatoa nafasi ya wadau kukutana na kujadili
mambo yanayohusu usimamizi wa maafa na kuishauri Serikali
kikamilifu.
(2) Jukwaa litaundwa na- (a) Mkurugenzi Mkuu ambaye atakuwa ni
mwenyekiti; (b) Wakuu wa Idara yenye dhamana na usimamizi wa
maafa kutoka: (i) Wizara yenye dhamana ya Kilimo na
Chakula; (ii) Wizara yenye dhamana ya Mambo ya
Ndani ; (iii) Wizara yenye dhamana ya Fedha; (iv) Wizara yenye dhamana ya Serikali za
Mitaa; (v) Wizara yenye dhamana ya Afya na Ustawi
wa Jamii; (vi) Wizara yenye dhamana ya Mazingira (vii) Wizara yenye dhamana ya Madini; (viii) Wizara yenye dhamana ya Mawasiliano; (ix) Wizara yenye dhamana ya Ardhi na
Nyumba; (x) Wizara yenye dhamana ya Usafiri; na (xi) `Wizara yenye dhamana ya nguvu za
atomu. (c) Wakuu wa taasisi zifuatazo: (i) Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano
Tanzania; (ii) Kikosi cha zimamoto; (iii) wakala wa taifa wa akiba ya chakula;
(iv) kituo cha chakula na Lishe Tanzania; (v) upimaji wa jeologia Tanzania; (vi) mamlaka ya chakula na dawa.
Sheria ya Wakala wa Usimamizi wa Maafa
26
(d) mwakilishi wa wakala wa Hali ya hewa; (e) watu wanne wanaowakilisha Vyuo vya Elimu ya
Juu; (f) mwakilishi wa Jeshi la Wananchi; (g) mwakilishi wa taasisi ya dhamana na mipango ya
Taifa; (h) wawakilishi watatu kutoka Jumuiya ya Taasisi ya
Vyama vya kiraia; (i) wawakilishi watatu kutoka taasisi za dini;
(2) Jukwaa linaweza kumualika mtu mwingine
yeyote kama itakuwa ni lazima.
(3) Jukwaa litakutana mara mbili kwa mwaka lakini
linaweza kukutana wakati mwingine wowote kama kutakuwa
na suala ambalo linahitaji kujadiliwa haraka.
(4) Jukwaa litaweka taratibu zake lenyewe.
(5) Jukwaa laweza kuunda kamati ambazo wajumbe
wake watateuliwa kutoka miongoni mwao.
Kinga dhidi
ya mashtaka 41.-(1) Mwajiriwa yeyote wa Wakala hatashtakiwa
binafsi kwa jambo lolote alilolitenda au kuacha kutenda kwa
nia njema akitekeleza au kuchukuliwa kutotekeleza kazi
yoyote akiwa kama mwajiriwa wa wakala.
(2) Wakala itamlipa na kumrudishia kwa kiwango
cha namna kama itakavyoelezwa mtu anayejitolea na mtu
mwingine aliyeshughulika na usimamizi wa maafa gharama
za msingi alizoingia ikiwa ni matokeo ya- (a) kutekeleza mwitikio wa kutoa huduma za maafa
kwa mujibu wa sheria hii; (b) kupatikana kwa ajali ya maafa, ardhi , yoyote au
vituo.
Kanuni 42. Waziri atatunga Kanuni kuhusu jambo lolote
ambalo ni la lazima kwa madhumuni ya utekelezaji au wa
kuipa nguvu ya utekelezaji wa sheria hii.
Sheria ya Wakala wa Usimamizi wa Maafa
27
Kufuta na
kubakiza
Sura 242
43.-(1) Sheria ya Uratibu wa Maafa inafutwa.
(2) Bila kujali kufutwa kwa sheria ya maafa, kanuni
zozote, amri, mashtaka au matangazo ya serikali yaliyofanywa
chini ya Sheria ya Maafa na ambayo bado yatakuwa na nguvu
kabla ya sheria hii kuanza kutumika yatabakia kuwa na nguvu
kama yametengenezwa chini ya sheria hii.
______
JEDWALI
______
(Imetengenezwa chini ya kifungu cha 7(4))
_________
UTARATIBU WA MIKUTANO YA BARAZA NA MAMBO
MENGINE
Mikutano 1.-(1) Baraza litakutana kwa kufanya shughuli zake
katika muda na sehemu itakayoamuliwa na Baraza.
(2) Mikutano ya kawaida ya Baraza itafanyika mara
moja kwa kila miezi mitatu.
(3) Mwenyekiti au ikiwa kama hauyupo Makamu
Mwenyekiti anaweza katika wakati wowote kuitisha kikao cha
dharura cha Baraza, baada ya kupokea ombi la kimaandishi
kutoka kwa wajumbe wengi wa Baraza.
(4) Mwenyekiti au kama hayupo, Makamu
mwenyekiti ataongoza mikutano ya Baraza.
(5) Mwenyekiti au kama hayupo, Makamu
Mwenyekiti anaweza kumwalika mtu mwingine ambaye si
mjumbe kuhudhuria mkutano wowote wa kamati isipokuwa
kupiga kura.
Akidi 2. Akidi ya mkutano wowote wa Baraza itakuwa ni
nusu ya wajumbe wa Baraza.
Sheria ya Wakala wa Usimamizi wa Maafa
28
Uamuzi wa
Baraza 3.-(1) Swali linaloletwa katika Baraza litaamuliwa kwa
wingi wa kura za wajumbe waliohudhuria wakati wa upigaji
kura na kama kura zitakuwa sawa, mtu anayeongoza kikao
atakuwa na kura ya uamuzi.
(2) Bila kujali kifungu kidogo cha (1), uamuzi wa
Baraza unaweza kufanywa bila ya Mkutano kwa njia ya
mzunguko wa hati husika miongoni mwa wajumbe na
mwelekeo wa maandishi wa maoni ya wengi ya wajumbe ndio
utakaokuwa uamuzi wa wengi.
Kumbukumb
u za kikao 4.-(1) Baraza litasababisha kumbukumbu za mkutano
kuwekwa na kutunzwa na kumbukumbu zitatumiwa au
kurekebishwa na kuidhinishwa katika mkutano wa Baraza na
kusainiwa na mtu anayeongoza kikao.
(2) Kumbukumbu zilizosainiwa na mtu aliyeongoza
kikao cha Baraza kwa uthibitisho wa kutokuwepo kwa
makosa, zitachukulliwa kuwa kumbukumbu sahihi za kikao.
Kutokuhudh
uria
hakutaharami
sha kikao
5. Uhalali wa kikao au jambo lolote la Baraza
halitaathiriwa kwa sababu ya kutokuwepo kwa mmoja kati ya
wajumbe au kosa lolote la uteuzi wa mmoja wao.
Amri,
maelekezo,
matangazo
au hati
6. Amri, maelekezo, matangazo au hati
zilizotengenezwa au kutolewa kwa niaba ya Baraza
zitasainiwa na-
(a) Mwenyekiti au Mkurugenzi Mkuu au Ofisa
mwingine yeyote wa Wakala aliyeidhihishwa kwa
niaba ya Mkurugenzi Mkuu.
Lakili ya
Baraza 7. Lakili ya Baraza na itawekwa kwenye hati yoyote
isipokuwa mbele ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti au
Mkurugenzi Mkuu. Baraza
kuweka
taratibu zake
8. Kulingana na masharti ya Jedwali hili, Baraza
linaweza kuweka namna ya kuendesha taratibu zake.
Sheria ya Wakala wa Usimamizi wa Maafa
29
MADHUMUNI NA SABABU
______________
Muswada huu unapendekezwa kutungwa kwa Sheria ya Usimamizi
wa Maafa ya Mwaka, 2014.
Madhumuni ya Muswada huu ni kuzuia, Kujiandaa na kukabiliana
na maafa kwa madhumuni ya kuanzisha Wakala inayojitegemea ya
Menejimenti ya Maafa itakayokuwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Ofisi
ya Waziri Mkuu itakuwa ni kituo cha kuratibu menejimenti na usimamizi
wa maafa kati ya wadau na asasi mbalimbali zinazuhusiana na maafa.
Muswada unakusudia kuwaweka pamoja wadau wote wanaohusika na
masuala ya kuratibu,kuzuia, kujiandaa, kusimamia na kukabili maafa.
Muswada umegawanyika katika sehemu kuu Tisa. Sehemu ya
Kwanza ya Muswada inahusu mambo ya utangulizi, kama vile jina fupi la
Sheria, matumizi na tafsiri ya maneno mbalimbali yaliyotumika katika
Muswada.
Sehemu ya Pili ya Muswada inahusu uanzishwaji wa Wakala
inayojitegemea ya Menejimenti ya Maafa. Ofisi ya Waziri Mkuu
itasimamia Wakala, na itakuwa ni kituo cha kuratibu, kuzuia na
kusimamia masuala yatokanayo na maafa. Wakala utakuwa na Baraza
litakaloratibu na kumeneji kazi na masuala yote yatokanayo na maafa.
Sehemu ya Tatu ya Muswada inahusu mambo ya kiutawala ya
Wakala,inapendekezwa chini ya Sehemu hii kuteuliwa kwa Mkurugenzi
Mkuu atakayateuliwa na Mheshimiwa Rais. Ndani ya Sehemu hii
inapendekezwa kuanzishwa kwa Kamati za Kuratibu Masuala ya Maafa ya
Mikoa, Wilaya, Kata na Vijiji. Muudo na kazi za Kamati pia zimeainishwa
chini ya Sehemu hii. Miogozo ya Kamati, jinsi ya kuratibu shughuli za
kamati zimeainishwa na namna Kamati zitakavyotoa taarifa zake pia
zimeaanishwa.
Sehemu ya Nne ya Muswada inaainisha masuala ya usimamizi wa
haki za watu watakao athirika na maafa. Inapendekezwa ndani ya Muswada
kuwa Serikali ihusike au Wakala uhusishwe kwa ajili ya kutoa misaada
kwa wananchi mara yatokeapo maafa. Zaidi ya Serikali kutoa misaada pia
Sheria ya Wakala wa Usimamizi wa Maafa
30
wananchi wawe na jukumu la kuzuia, kujiandaa kumeneji na kukabili
maafa.
Sehemu ya Tano ya Muswada inapendekeza kuwepo na namna ya
kutoa tamko na ufafanuzi wa kazi zitakazohusika ama kufuatwa wakati
yatakapotokea maafa. Muswada pia unapendekezwa kuwepo na tamko la
kuteua au kutangaza sehemu iliyoadhirika na maafa, sababu ya kuitangaza
sehemu hiyo na mambo ya muhimu yatakayobidi yafanyike katika sehemu
yalipotokea maafa.
Sehemu pia inapendekeza kuwa Wakala waweze kutoa Tangazo
katika vyombo vya habari na katika Gazeti la Serikali iwapo Wakala
utaridhika kuwa kumetokea maafa ambayo yanapaswa yapewe kipaumbele.
Sehemu ya Sita inapendekaza kuwepo na utaratibu wa kuratibu,
kusimamia na kuandaa Mwongozo wa Taifa wa Kumeneji Maafa chini ya
usimamizi wa Wakala na hatimaye kupitishwa na Waziri.
Sehemu hii pia inapendekeza kuwa Serikali za Mitaa ziwe na
jukumu la kusaidia kutekeleza Mpango wa Taifa wa kuzuia, kujiandaa na
kukabili maafa. Muswada pia unapendekeza asasi za kiserikali na zisizo za
kiserikali kuandaa Mipango yao ya kukabiliana na masuala ya maafa ili
kuweza kutekeleza majukumu yao kama ilivyoainishwa ndani ya Mpango
wa isimamizi,uzuiaji na kukabili maafa.
Sehemu ya Saba ya Muswada inapendekeza kuanzishwa kwa Mfuko
wa Kumeneji na kusimamia Maafa. Mfuko huu utakuwa chini ya
usimammizi wa Wakala; pia Sehemu hii imeainisha matumizi ya fedha,
usimamizi na ukaguzi wa matumizi ya fedha.
Sehemu ya Nane inaainisha makosa na adhabu mbalimbali ambayo
pia yanahusu makosa yanayofanywa na mashirika.
Sehemu ya Tisa inahusu mambo ama masharti ya ujumla ambayo
yanahusu kuwepo kwa Jukwaa la Taifa la Kumeneji na Kusimamnia Maafa,
inazuia ama kusimamia iwapo kutatokea kitu chochote kitakachofanyika,
tendwa ama kutotendwa kwa nia njema ama kutodhamiriwa , kuondoa
masuala ya kodi wakati wa maafa. Sehemu hii inaongelea jinsi ya
kusimamia wataalamu wa kimataifa wanaokuja kusaidia wakati wa maafa,
majukumu ya Tawala za Mikoa na Wilaya na mambo yanayohusu fidia.
Sheria ya Wakala wa Usimamizi wa Maafa
31
Muswada, pia katika Sehemu hii unapendekeza masharti ya
kufuatwa wakati wa kutoa fidia iwapo kutatokea hasara au kuharibika kwa
vitu,utoajii wa fidia, kisasi na malipo. Muswada pia unapendekeza uwezo
wa Waziri wa kutengeneza Sheria ndogo kuhusiana na mambo ya Sheria
hii. Mwisho, Muswada unapendekeza kufutwa kwa Sheria ya Maafa na
Uratibu wa Misaada Sura 242 (Disaster Relief Coordination Act (Cap. 242).
Dar es Salaam, MIZENGO P. PINDA
10 Oktoba, 2014 Waziri Mkuu