8
Somo la 9 kwa ajili ya Agast 28, 2021

Somo la 9 kwa ajili ya Agast 28, 2021

  • Upload
    others

  • View
    3

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Somo la 9 kwa ajili ya Agast 28, 2021

Sabato hutukumbusha kwamba Mungu alituumba na kwambaanaweza kutuokoa na kutukomboa. Muumbaji Mwenyezialiyewaokoa Israeli kutoka utumwani Misri anaweza kutuokoa nasisi kutoka katika dhambi inayotutumikisha.

Tunapumzika siku ya Sabato pamoja na mibaraka ya Yeyealiyetuumba, Aliyetukomboa, Anayetutakasa, na Anataka kuwa naushirika na sisi.

Sabato ni kijito cha maji ya pumziko la kimbingu kwenye jangwakavu la huzuni na ulimwengu ulioharibiwa.

Uumbaji ulianza na ulimwengu mkavu, wenye giza, na usio naviumbe hai (Mwanzo. 1:1-2). Kidogo kidogo, vitu vingine kamanuru, hewa, nchi, na uoto viliumbwa.

Mara wakazi walipokuwa tayari, Mungu aliumba mahadhi ya ulimwengu mpya kwa kuweka“mianga”: jua, mwezi, na nyota.

Hatimaye, masha yaliujaza ulimwengu katika siku mbili zilizofuata. NdipoMungu aliumbua umbo la kipekee lenye uhai kwa mfano Wake kwa namnapekee: mwanamume (‘ish) na mwanamke (‘ishshah). Kila kitu ni “chemasana.” (Mwz. 1:31).

Uumbaji ulikuwa haujakamilikabado. Baada ya siku sita za kazi, Mungu alipumzika. Tambua kuwasiku ya pumziko inatambuka kamasehemu ya juma Uumbaji.

Siku ya mwisho ya Uumbaji ilibarikiwa na kutengwa kwa ajili ya viumbe waMungu kuwa na ushirika kamili na Yeye. Ingawa ulimwengu haukuwa nadhambi, wanadamu walihitaji kuyaacha majukumu ya kila siku na kutumiasiku yao nzima pamoja na Muumba wao.

Wakati dhambi ilipoingi ulimwenguni, maumivu, udhaifu, na ukali vikachukua nafasi ya furaha na amani. Kwahiyo, wanadamu walihitaji siku hiyo ya pumzikokutumia muda vizuri na Muumba wao kuliko kawaida.

Wakati Mungu alipoitoa Sheria yake katika Amri Kumi, aliijumuisha Sabato kwa ajili yetu kupumzika nakukumbuka kwamba alituumba (Kut. 20:8-11).

“Siku sita mtaokota; lakini siku ya saba ni Sabato, siku hiyo hakitapatikana.” (Kut. 16:26)

Musa aliwaasa wana wa Israeli kuitunza Sabato tena kabla yakutoka Misri. Hata hivyo, Farao alizuia (Kutoka 5:4-5).

Sabato inatajwa ghafla katika Kutoka16, kwahiyo Wana wa Israeli waliijuahata kabla. Mara walipokuwawamekombolewa kutoka Misri nakabla ya kufika Mlima Sinai, Mungualiwakumbusha umuhimu wapumziko la Sabato kupitia muujiza wamana.

Mungu alikuwa akiunganisha pumziko la Sabato na upendo Wake na kuwajali (Kumbukumbu la Torati 8:3).

Musa aliitaja Sabato tena kabla ya Waisraeli kuiingia Nchi ya Ahadi, akiihusinanisha na Ukombozi.

“Nawe utakumbuka ya kuwa wewe ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri, na ya kuwaBWANA, Mungu wako, alikutoa huko kwa mkono wenye nguvu, na mkono ulionyoshwa; kwa sababu hiyo BWANA, Mungu wako, alikuamuru ushke Sabato.” (Kumb. Torati 5:15)

Kizazi kipya kiliinuka takribani miaka 40 baada ya Amri Kumikufunuliwa pale Mlima Sinai. Kizazi hiki kilikuwa tayari kuingiaKanaani na ahadi ya pumziko (Ebr. 3:8-11, 16-19).

Kadri walivyokuwa wakiziacha Amri, wakati huu ndipo Sabatoilikuwa inazidi kuunganishwa na nguvu ya Mungu iokoayo (Kumb. 5:12-15).

Kwahiyo, Sabato imeunganishwa na wakati uliyopita[Uumbaji], uliopo [Ukombozi], na ujao [Uumbajimpya kwa waliokombolewa] (Isaya 66:23).

Sabato natuelekeza kwa Yesu, Muumbaji naMkombozi wetu. Tutaishi Naye milele.

SABATO NA PUMZIKO“Kama ukigeuza mguu wako usihalifu Sabato, usifanye anasa yako siku ya utakatifuwangu; ukiita Sabato siku ya furaha, na siku takatifu ya BWANA yenye heshima; ukiitukuza, kwa kuzifanya njia zako mwenyewe, wala kuyatafuta yakupendezayo, wala kusema maneno yako mwenyewe.” (Isaya 58:13)

Ni kwa namna ganinipumzike siku ya Sabatokulingana na Zaburi 92,

Kutoka 16:29, na

Isaya 58:13?

Mtukuze Mungu (Zab. 92: 1)

Mtangaze Mungu kwa wengine (aya. 2)

Mwimbie Mungu (aya. 3)

Shangilia katika Uumbaji wa Mungu (aya. 4-5)

Kumbuka haki ya Mungu (aya. 6-9)

Tafuta nguvu mpya katika Mungu (aya. 10)

Kutana na Mungu pamoja na Kanisa Lake (aya. 13)

Tumia muda pamoja na familia na marafiki zako (Kut. 16:29)

Usifanye yakupendezayo mwenyewe (Isa. 58:13)

Ifurahie Sabato (Isa. 58:13)

Usiwaze wala kuonelea kazi zako za kila siku (Is. 58:13)“Ndipo utakapojifurahisha

katika BWANA.” (Isa. 58:14)

“Sabato haikuwa kwa Waisraeli tu, balikwa ajili ya ulimwengu. Ilitambulishwakwa mwanadamu katika Edeni, na, kama ilivyo katika sheri zaingine zamaadili, ni sharti la kudumu […] Na kama vile edeni itakavyorejeshwa tena, siku ya pumziko takatifu la Munguitaheshimiwa na wote walio chini ya jua.”

E. G. W. (Matendo ya Mitume, sura. 29, p. 283)