92
TAASISI YA ELIMU TANZANIA MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE MAFUNZO ELEKEZI KWA WALIMU JAMII WASAIDIZI MWONGOZO WA MWEZESHAJI WA MAFUNZO 2015

TAASISI YA ELIMU TANZANIA MPANGO WA KUMUANDAA …€¦ · Matumizi ya Mwongozo: 3 Maeneo ya Umahiri 3 Matumizi ya Vitabu vya Hadithi 8 1)Hadithi 12 kwa wiki 12 8 2)Shughuli zitabuniwa

  • Upload
    others

  • View
    19

  • Download
    1

Embed Size (px)

Citation preview

  • TAASISI YA ELIMU TANZANIA

    MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    MAFUNZO ELEKEZI KWA WALIMU JAMII WASAIDIZI

    MWONGOZO WA MWEZESHAJI WA MAFUNZO

    2015

  • 2 MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Mwongozo huu umeandaliwa naTaasisi ya Elimu Tanzani (TET) kwa ushirikiano wa EQUIP-T, na Aga Khan Foundation (AKF). TET inashukuru EQUIP-T kwa kugharimia warsha ya kuandika mwongozo huu. Aidha TET inawashukuru wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine katika kuandika mwongozo huu. Shukrani za pekee ziwaendee wafuatao:

    Waandishi

    Vida Ngowi - Taasisi ya Elimu Tanzania (TET)Sharifa Majid - Aga Khan Foundation (AKF)Sultana Islam Karama - Aga Khan Foundation (AKF)Rose Chipindula - Taasisi ya Elimu Tanzania (TET)Laurence Kunambi - Taasisi ya Elimu Tanzania (TET)Samson Lumato - Songea Teachers’ CollegeOscar A. Ndalibamale - Mbuyuni Primary School Mollel Lumitu - Social Service WelfareOmary Patrick - Nachingwea Teachers’ College

    Mratibu wa Warsha ya UandishiVida Ngowi - Taasisi ya Elimu Tanzania (TET)

    Viongozi Dr. Wilberforce Meena - Mkurugenzi Idara ya Ubunifu na Uboreshaji wa Mitaala Ms. Fika Mwakabungu - Mkurugenzi Idara ya Mafunzo na Mitaala

    Ni matumaini kuwa mwongozo huu utakuwa na manufaa kwa Walimu Jamii Wasaidizi wanaofundisha katika Mpango wa Kumuandaa Mtoto kuwa Tayari Kuanza Shule.

    Dr. Leonard AkwilapoKAIMU MKURUGENZI MKUUTAASISI YA ELIMU TANZANIA

    SHUKURANI

  • 3MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    VIFUPISHO

    AKF - Aga Khan Foundation

    EQUIP-T - Education Quality Improvement Program - Tanzania

    MMJ - Mwalimu Msaidizi wa Jamii

    WWJ - Walimu Jamii Wasaidizi

    TET - Taasisi ya Elimu Tanzania

  • UTANGULIZI 2

    Malengo ya Mwongozo: 2

    Walengwa wa Mwongozo: 2

    Muundo wa Mwongozo 2

    Muda wa Mafunzo 2

    Mbinu za Kumwezesha MMJ Kufundisha. 2

    Vifaa/Zana Zitakazotumika katika Uwezeshaji 3

    Umuhimu wa Mwongozo 3

    Matumizi ya Mwongozo: 3

    Maeneo ya Umahiri 3

    Matumizi ya Vitabu vya Hadithi 8

    1)Hadithi 12 kwa wiki 12 8

    2)Shughuli zitabuniwa kutokana na hadithi 8

    Maendeleo ya Mtoto 9

    Hatua za Ukuaji kwa mtoto wa miaka 5 – 6 10

    Hatua za Ukuaji kwa mtoto wa miaka 7 – 8 11

    Mpango wa Shughuli kwa Wiki 11

    Mpangilio wa Hadithi. 12

    Maelekezo ya ufundishaji wa Hadithi 12

    Hadithi za Kusoma 12

    Umuhimu wa kusoma hadithi kwa sauti ni: 13

    Matumizi ya Vitabu Vikubwa 13

    Hatua za usomaji wa hadithi: 14

    Ratiba ya Siku 15

    Utekelezaji wa Ratiba ya Siku 16

    Hadithi ya siku husika 16

    Mambo ya Kuzingatia Wakati wa

    Kuandaa Igizo Dhima. 17

    Namna ya Kupanga Vibao Fumbo 18

    KIPINDI CHA MPITO 19

    MAPENDEKEZO YA UWIANO WA

    IDADI YA WATOTO NA WWJ 19

    WIKI YA TANO YA MAFUNZO 20 HADITHI YA KUKU NA KANGA

    WIKI YA SITA YA MAFUNZO HADITHI YA KUJIKINGA NA MALARIA 28

    WIKI YA SABAYA MAFUNZO HADITHI YA PUPA ZA NYIGU 36

    WIKI YA NANE HADITHI YA KODE NA KOLE 44

    WIKI YA TISA YA MAFUNZO HADITHI YA MOTO 51

    WIKI YA KUMI YA MAFUNZO HADITHI YA YANGE YANGE 59

    WIKI YA KUMI NA MOJA YA MAFUNZO 67

    WIKI YA KUMI NA MBILI YA MAFUNZO 75

    YALIYOMO

  • 1MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Elimu ya Awali ni msingi muhimu katika kumwezesha mtoto kuwa Tayari kwa ujifunzaji. Kutokana na umuhimu huu Taasisi ya Elimu Tanzania kwa Kushirikiana na Programu ya Uboreshaji wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-T) na mfuko wa Aga Khan wameandaa Mpango wa Kumwandaa Mtoto kuwa Tayari kuanza Shule. Mpango ambao unatekelezwa katika mikoa saba inayoratibiwa na EQUIP-T ambayo ni Dodoma, Lindi, Tabora, Kigoma, Shinyanga, Mara na Simiyu.

    Mpango huu, unatokana na tafiti mbalimbali zilizofanyika juu ya umuhimu wa mtoto kupata Mafunzo ya Elimu ya Awali kabla ya kuanza mfumo rasmi wa elimu ya msingi. Utafiti uliofanywa na Programu ya Uboreshaji wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-T) mwaka 2012 katika mikoa s aba wanayoiratibu unaonesha kuwa nusu ya watoto hawakupata Mafunzo ya Elimu ya Awali kabla ya kujiunga na darasa la kwanza, hii inasababisha watoto hawa kutokuwa na utayari wa kujifunza watakapoanza elimu ya msingi.

    Ili kufanikisha utekelezaji wa mpango huu wa kumwandaa mtoto kuwa tayari kuanza shule, Taasisi ya Elimu Tanzania imeandaa mwongozo wa Mwezeshaji utakaotumika kuwawezesha wawezeshaji ngazi ya wilaya pamoja na Mwalimu Msaidizi wa Jamii. Inatarajiwa kwamba Mwezeshaji atakapotumia mwongozo huu kikamilifu ataweza kumjengea mwalimu Msaidizi wa Jamii umahiri katika kuwawezesha watoto.

    Watoto watakaopata Mafunzo haya watajengewa stadi za msingi zitakazowasaidia kuwa tayari kumudu maisha ya Elimu ya Msingi.

    DIbAJI

  • 2 MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Mwongozo huu wa mafunzo umeandaliwa kwa kufuata kiunzi cha utekelezaji wa mpango wa Kumuandaa Mtoto kuwa Tayari Kuanza Shule. Mwongozo unatoa maelekezo ya namna ya kumjengea mtoto umahiri ufuatao: kuwasiliana kwa lugha ya Kiswahili, Utambuzi, Kuhusiana, Kujenga Mwili na Kuthamini Mazingira. Aidha mwongozo huu unatoa maelekezo ya kutumia hadithi 12 zilizoandaliwa ili kufikia umahiri uliobainishwa katika kiunzi. Mwongozo huu unazingatia mbinu shirikishi zikatakazotoa fursa kwa mtoto kuweza kujifunza kwa urahisi. Mwongozo huu pia unapendekeza shughuli, vifaa/zana ambazo mwezeshaji anaweza kuzitumia wakati wa mafunzo. Vile vile mwongozo unapendekeza mbinu zitakazotumika ili kupima ufanisi wa ujifunzaji wa mtoto.

    Malengo ya Mwongozo:Malengo ya mwongozo huu ni:i. Kumuongoza mwezeshaji namna ya kuwawezesha Walimu Jamii Wasaidizi kutekeleza mpango

    wa kumuandaa mtoto kuwa tayari kuanza shule.ii. Kumwongezea mwezeshaji stadi mbali mbali zitakazomsaidia kumuongoza mwalimu jamii

    msaidizi kuweza kutumia hadithi 12 katika kumjengea mtoto umahiri uliokusudiwa.iii. Kumjengea Mwalimu Jamii Msaidizi umahiri wa kutekeleza mpango wa kumuandaa mtoto kuwa

    tayari kuanza shule.

    Walengwa wa Mwongozo:Walengwa wa mwongozo huu ni hawa wafuatao:i. Wawezeshaji wa Walimu Jamii Wasaidizi.ii. Walimu Jamii Wasaidizi.iii. Wathibiti wa ubora wa elimu.iv. Waratibu Elimu Kata.v. Walimu wakuu.vi. Walimu wa darasa la kwanza.

    Muundo wa MwongozoMwongozo huu umegawanyika katika sehemu kuu tatu, sehemu ya kwanza ni utangulizi ambao unajumuisha maelezo mafupi kuhusu mwongozo wa mafunzo, sehemu ya pili ni mwongozo wa utekelezaji wa programu na sehemu ya tatu ni utekelezaji wa program ya Kumuandaa Mtoto kuwa Tayari kuanza Shule.

    Muda wa MafunzoMuda wa mafunzo wa utekelezaji wa mpango huu umegawanyika katika awamu mbili. Awamu ya kwanza ya mafunzo ni wiki nne ambayo tayari yamekwishafanyika kwa mikoa yote saba. Awamu ya pili, inatarajiwa kufanyika ambapo itajumuisha wiki nane (8). Mwongozo huu umebainisha shughuli zitakazofanyika kwa kipindi hiki cha wiki nane kwa ajili ya kumjengea mtoto umahiri tarajiwa.

    Mbinu za Kumwezesha MMJ Kufundisha. Mwezeshaji anashauriwakutumia mbinu shirikishi katika kuwezesha ili kumsaidia MMJ kuzitumia mbinu hizi katika kufundisha watoto. Baadhi ya mbinu hizo ni hadithi, igizo dhima, michezo, nyimbo, ziara, kumualika mgeni, matembezi ya galari, changanyaa kete, majadiliano ya vikundi, fikiri- jozisha-shirikisha, maswali na majibu.

    UTANGULIZI

  • 3MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Vifaa/Zana Zitakazotumika katika UwezeshajiMwanasesere, picha, vitabu vya hadithi, chati, kadi, vifaa vya TEHAMA, vitu halisi vinavopatikana kutoka katika mazingira yao na miongozo ya kufundishia.

    Umuhimu wa MwongozoMatumizi bora ya Mwongozo huu yatamjengea Mwalimu Jamii Msaidizi:• Uwezo wa kufundisha na kujifunza kwa udadisi na ufasini kwa watoto.• Uwezo wa kuwajengea watoto stadi na ujuzi wa kujitegemea. • Uwezo wa kushirikiana na watoto katika ufundishaji bora unaolenga katika kumjengea mtoto

    umahari unaotarajiwa.• Aidha kwa kutumia mwongozo huu vilevile utamuwezesha Mwalimu Jamii Msaidizi kufikiri na

    kubuni mikakati itakayoboresha ufundishaji wake wa kila siku darasani kwa kutumia hadithi nane (8) katika majuma manane ya mpango wa kumuandaa mtoto kuwa tayari kuanza shule.

    • Mwongozo huu pia umezingatia ufanisi wa ufundishaji wa hadithi nane katika maeneo ya:• Malengo mahususi yanayobainisha umahiri kwa kila hadithi• Njia na mbinu shirikishi za kufundishia na kujifunzia• Matokeo ya Mafunzo• Upimaji, tathmini na ufuatiliaji wa uhaulishaji wa maarifa ya watoto nyumbani na shuleni.

    Matumizi ya Mwongozo:Mwongozo huu utamsaidia Mwalimu Jamii Msaidizi katika: • Kuchambua kiunzi cha mpango wa kumwandaa mtoto kuwa tayari kuanza shule.• Kuandaa Mpango wa Kazi wa wiki nane (8) na andalio la somo lenye mwelekeo wa kumjengea

    mtoto umahiri tarajiwa.• Kuweka mikakati ya ufundishaji wa wiki nane(8) kwa ufanisi.• Kufanya upimaji na tathmini ya maendeleo ya watoto kwa kutumia mbinu zilizopendekezwa

    katika mwongozo.• Mwalimu Jamii Msaidizi kujipima mwenyewe.

    Maeneo ya UmahiriMwezeshaji awapitishe washiriki katika maeneo ya umahiri kwa kuwagawa katika makundi matano kulingana na uchanganuzi wa maeneo hayo kama yalivyo bainishwa kwenye jedwali lifuatalo. Kisha watumie igizo dhima kuonesha ni jinsi gani watakavyomjengea mtoto umahiri husika.

  • 4 MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Maeneo muhimu Umahiri Mahususi Shughuli za kutenda mwanafunzi

    Vigezo vya Upimaji

    Kuwasiliana Kwa Lugha ya Kiswahili

    Kukuza lugha ya mazungumzo

    Kusalimiana kwa kuzingatia umri, rika (kutokana na utamaduni)

    Usalimiaji umefanyika kwa usahihi kwa kuzingatia umri, rika na utamaduni wa mtoto

    Kujitambulisha na kuwatambulisha wengine

    Utambulishaji umefanyika kwa usahihi

    Kukaribisha na kuagana

    Ukaribishaji na uagaji umefanyika kwa usahihi

    Kuuliza, kuomba na kushukuru anapopewa kitu.

    Kuuliza, kuomba na kushukuru kumefanyika kwa usahihi

    Kufuata maelekezo anayopewa na watu wengine.

    Ufuataji wa maelekezo anayopewa umefanyika kwa usahihi

    Kuhesabu Kuhesabu idadi ya vitu vinavyopatikana katika mazingira ya shule na nyumbani.

    Uhesabuji wa vitu umefanyika kwa ufanisi

    Kutambua mlingano rahisi

    utambuaji wa milingano umefanyika kwa usahihi

    Maumbo rahisi (mraba. Mduara, pembe tatu)

    Ubainishaji wa maumbo rahisi umefanyika kwa usahihi

    Kuelezea hisia (anachopenda, asichopenda, furaha, huzuni, hasira, kuchanganyikiwa)

    Kusoma vitabu vya picha

    Usomaji vitabu vya picha umefanyika kwa usahihi

    Kusimulia hadithi kwa kuonesha hisia

    Usimuliaji wa hadithi kwa kuonesha hisia umefanyika kwa usahihi

    Kuchora picha na kujieleza kwa njia ya picha

    Uchoraji wa picha umefanyika kwa usahihi

  • 5MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Maeneo muhimu Umahiri Mahususi Shughuli za kutenda mwanafunzi

    Vigezo vya Upimaji

    Utambuzi Kuuliza na kujibu maswali

    Kusoma picha na kujibu maswali

    Usomaji picha na ujibuji wa maswali umefanyika kwa usahihi

    Ziara ya kutembelea maeneo ya historia au kwenye shamba la mifugo

    Ziara ya kutembelea maeneo ya historia na shamba la mifugo imefanyika kwa usahihi

    Kuchunguza mazingira Kuuliza na kujibu maswali

    Uulizaji na ujibuji wa maswali umefanyika kwa usahihi

    Kuchunguza vitu ndani ya darasa na kuvitaja

    Uchunguzaji wa vitu ndani na nje ya darasa umefanyika kwa usahihi

    Kuchunguza vitu nje ya darasa na kuvielezea

    Uelezeaji wa vitu vilivyochunguzwa nje ya darasa umefanyika kwa usahihi.

    Kuchunguza na kubuni Kuotesha mbegu za nafaka

    Uoteshaji wa mbegu za nafaka umefanyika kwa usahihi

    Kuunda vitu mbalimbali.

    Uundaji wa vitu umefanyika kwa usahihi

    Kutembelea maeneo ya kihistoria, shamba la mifugo/kilimo

    Uchunguzi kutokana na eneo liliokusudiwa umefanyika kwa usahihi

    Kucheza (Michezo ya Vibao)

    Uchambuzi wa vitu mbalimbali (sorting activities)

    Uchambuaji wa vitu umefanyika kwa usahihi

    Kucheza na vifaa mbalimbali vilivyoten-genezwa kwa mikono (kibao fumbo)

    Utumiaji wa vifaa mbalimbali vya michezo umefanyika kwa usahihi

    Kutumia vifaa vya michezo vya nje ya darasa (bembea mtel-ezo, kupanda ngazi .)

    Utumiaji wa vifaa vya michezo nje ya darasa umefanyika kwa usahihi

  • 6 MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Maeneo muhimu Umahiri Mahususi Shughuli za kutenda mwanafunzi

    Vigezo vya Upimaji

    Kuwa na mtazamo chanya katika kujifunza

    Kucheza katika kona ya nyumbani.

    Utumiaji wa kona ya nyumbani umefanyika kwa ufasaha

    Kuchagua shughuli wanayotaka kuifanya.

    Uchaguzi wa shughuli wanazotaka kufanya umefanyika kwa usahihi

    Kuimba nyimbo za shule

    Uimbaji wa nyimbo za shule umefanyika kwa usahihi

    Kuhusiana Kushirikiana Kucheza michezo mbalimbali pamoja na wenzie

    Uchezaji wa pamoja katika michezo umefanyika kwa usahihi

    Kufanya kazi katika jozi na kikundi

    Ufanyaji wa kazi katika vikundi na jozi umefanyika kwa usahihi

    Kutengeneza marafiki Utengenezaji wa marafiki umefanyika kwa usahihi

    Kusaidiana katika hali mbalimbali

    Kushiriki pamoja na wengine katika kazi.

    Ushiriki wa pamoja katika kazi umefanyika kwa usahihi

    Kuelekezana katika ujifunzaji.

    Uelekezanaji katika kujifunza umefanyika kwa usahihi

    Kumuhudumia mwingine anapohitaji msaada.

    Tendo la kuhudumia wengine limefanyika kwa usahihi

    Kubaini hisia za wengine.

    Ubainishaji wa hisia za wengine umefanyika kwa usahihi

    Kujitambua Kuelewa jina na jinsi yake

    Utambuaji wa jina na jinsi yake umefanyika kwa usahihi

    Kutambua haki zake Utambuaji wa haki zake umefanyika kwa usahihi

    Kutambua wajibu wake Utambuaji wa haki zake umefanyika kwa usahihi

  • 7MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Maeneo muhimu Umahiri Mahususi Shughuli za kutenda mwanafunzi

    Vigezo vya Upimaji

    Kukuza haiba Kujiheshimu na kuheshimu wengine

    Tendo la kutumia lugha ya upole limefanyika kwa usahihi

    Kutumia mikao inayokubalika na jamii

    Utumiaji wa mikao mbalimbali umefan-yika kwa usahihi

    Kuheshimu taratibu na tamaduni zinazokubalika na jamii

    Tendo la kuheshimu taratibu na tamaduni zinazokubalika limefanyika kwa ufanisi

    Kuonesha uadilifu katika maisha yake

    Uoneshaji wa uadilifu umefanyika kwa usahihi

    Kujenga mwili Kukuza misuli midogo midogo

    Kukata karatasi kwa kutumia mkasi

    Ukataji wa karatasi kwa kutumia mkasi umefanyika kwa usahihi

    Kupaka rangi maumbo bapa

    Upakaji wa rangi ume-fanyika kwa usahihi

    Kuunda vitu kwa kutumia udongo wa mfinyanzi

    Uundaji wa vitu kwa kutumia udongo ume-fanyika kwa usahihi

    Kutengeneza shanga kwa kutumia kamba

    Utengenezaji wa shanga kwa kutumia kamba umefanyika kama inavyopaswa

    Kufunga na kufungua vifungo

    Ufungaji na ufunguaji wa vifungo umefanyika kwa usahihi

    Kuweka pamoja vibao fumbo

    Umaliziaji wa kibao fumbo umefanyika kwa usahihi

    Kuimarisha afya Kukimbia kwenda mbele

    Ukimbiaji umefanyika kwa usahihi

    Kukimbia kurudi nyuma

    Ukimbiaji umefanyika kwa usahihi

    Kurusha na kudaka mpira

    Urushaji na udakaji wa mpira umefanyika kwa usahihi

    Kupanda na kushuka kwenye ngazi

    Upandaji na ushukaji kwenye ngazi umefan-yika kwa usahihi

  • 8 MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Maeneo muhimu Umahiri Mahususi Shughuli za kutenda mwanafunzi

    Vigezo vya Upimaji

    Kusimamia mguu mmoja

    Kusimama kwa mguu mmoja umefanyika kwa usahihi

    Kukuza ujasiri na ukakamavu

    Kutembea kwa kusimamia vidole vya miguu

    Utembeaji wa kusimamia vidole vya mguuni umefanyika kwa usahihi

    Kubembea Ubembeaji umefanyika kwa usahihi

    Kuendesha baiskeli Uendeshaji wa baiskeli umefanyika kwa usahihi

    Kuchezesha viungo kwa kufuatisha ala za muziki

    Ufuatiliaji wa ala za muziki kwa kuchezesha viungo umefanyika kwa usahihi

    Kuthamini Mazinigira Kubainisha vitu mbalimbali katika mazingira ya shule

    Kubainisha vitu vilivyo ndani na nje ya darasa

    Ubainishaji wa vitu ndani na nje ya darasa umefanyika kwa usahihi

    Kubainisha vitu hatarishi katika mazingira ya shule na nymbani namna ya kujikinga

    Ubainishaji wa vitu hatarishi katika mazingira ya shule nyumbani na njiani yamefanyika kwa usahihi

    Kubainisha aina mbalimbali za wanyama na mimea katika mazingira ya shuleni na nyumbani

    Ubainishaji wa wanyama na mimea katika mazingira ya shule na nyumbani umefanyika kwa usahihi

    Kutumia choo kwa usahihi

    Kuomba ruhusa anapotaka kwenda chooni

    Uombaji wa ruhusa anapotaka kwenda chooni umefanyika kwa usahihi

    Kuonesha matumizi sahihi ya choo.

    Matumizi ya utumiaji wa choo umefanyika kwa usahihi

    Kusafisha na kudumisha usafi wa mazingira ya choo.

    Usafi wa mazingira ya choo umefanyika kwa usahihi

  • 9MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Maeneo muhimu Umahiri Mahususi Shughuli za kutenda mwanafunzi

    Vigezo vya Upimaji

    Kuosha mikono baada ya kutoka chooni

    Uoshaji wa mikono baada ya kutoka chooni umefanyika kwa usahihi

    Kutambua maeneo salama na hatarishi

    Kuvuka barabara kwa uangalifu

    Uvukaji sahihi wa barabara umefanyika kwa usahihi

    Kutembea mkabala na magari pembezoni mwa barabara

    Utembeaji sahihi pembezoni mwa barabara umefanyika kwa usahihi

    Kubaini vitu na watu hatarishi katika mazingira ya shuleni, nyumbani na njiani.

    Ubainishaji wa maeneo hatarishi umefanyika kwa usahihi

    Matumizi ya Vitabu vya Hadithi

    Matumizi ya vitabu ni jambo la msingi sana katika utekelezaji wa mpango huu. Matumizi ya vitabu hivyo utafuata utaratibu ufuatao:

    1) Hadithi 12 kwa wiki 12

    Hadithi moja itasomwa kwa wiki, itasomwa wakati wa mduara wa asubuhi. Ni vema MMJ kubainisha umahiri uliokusudiwa wa mtoto baada ya kusoma hadithi kwa kutumia shughuli na mbinu mbalimbali katika ujifunzaji.

    2) Shughuli zitabuniwa kutokana na hadithi

    Toa shughuli kutegemeana na hadithi iliyosomwa ambayo itamwezesha mtoto kujenga umahiri uliokusudiwa. Shughuli zinaweza kuwa za kucheza igizo, au kuhadithia hadithi uliyowasomea.

    3) Upimaji

    Mwezeshaji amwongoze MMJ kubaini umahiri uliojengwa kwa kutumia zana mbalimbali za upimaji kama vile; orodha hakiki, shughuli, maswali na majibu na kazi za mikono.

  • 10 MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Umri Kipengele Yanayojitokeza

    Miaka 5-6 Ukuaji wa Mwili • Kupanda na kushuka ngazi• Kuruka kwa kutumia miguu yote• Kuongezeka kwa uwezo wa kuhimili mwendo wa misuli• Kuonesha kuwa anatumia mkono wa kulia au kushoto

    Miaka 5-6 Ukuaji wa Kijamii • Anaonesha hisia kali kwa familia na mambo ya nyumbani• Anaonesha ukuaji na kuanza kujitegemea• Anaweza kukubali maelekezo na kufuata taratibu• Anaweza kushirikiana vitu na wengine na hata

    kubadilishana • Anaweza kushiriki katika uzoefu wa shule

    Miaka 5-6 Ukuaji wa Akili (Ubongo)

    • Anaonesha usikivu mkubwa • Anaweza kuweka vitu katika mpangilio • Kutumia lugha kwa upana• Kujua majina ya vitu, rangi na maumbo

    Miaka 5-6 Ukuaji wa Kimaadili (Kiroho)

    • Kujua mema na mabaya• Kuathiriwa na tabia za watu wengine• Kujenga mitizamo sahihi ya kimaadili kama vile heshima,

    kuwa mkweli na kujenga imani au uaminifu

    Maendeleo ya Mtoto

    Ni muhimu MMJ kutambua kuwa kila mtoto ni wa kipekee japokuwa anaweza kufuata mfumo ulio sawa na mwingine katika ukuaji, maendeleo na makuzi yake akiwa mdogo kama vile kujifunza kuongea na kujifunza kutembea. Katika darasa moja unaweza kuwa na mtoto wa miaka 5 ambaye ana tabia kama za mtoto wa miaka 4 au akawana tabia kama za matoto wa miaka 6. Jedwali lifuatalo linaonesha hatua za maendeleo na makuzi ya mtoto wa miaka 5 – 8. Mwezeshaji awaongoze WWJ kujadiliana katika vikundi uzoefu wao katika makuzi na ukuaji wa watoto.

    Hatua za Ukuaji kwa mtoto wa miaka 5 – 6

    Umri Kipengele Yanayojitokeza

    Miaka 7-8 Ukuaji wa Mwili • Anaweza kupanda juu ya miti• Anaweza kuvaa na kuvua nguo yeye mwenyewe• Anaweza kushika mpira mikono yake ikiwa imesambaa• Anaweza kutembea kinyumenyume na kwa kutumia

    ncha za vidoleMiaka 7-8 Ukuaji wa Kijamii • Anaweza kucheza kwa ushirikiano na wezake

    • Anafahamu kuhusu jinsia na tofauti za rangi za watu• Anafahamu miiko ya jamii ambamo anaishi

    Hatua za Ukuaji kwa mtoto wa miaka 7 – 8

  • 11MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Umri Kipengele Yanayojitokeza

    Miaka 7-8 Ukuaji wa Kihisia • Anajenga uwezo wa kujihimili zaidi• Anaanza kuonesha hali ya ucheshi• Anaweza kuanza kuona mtizamo wa mtu mwingine, kwa

    kuongozwa• Anaanza kuonesha uwezo wa kutatua migogoro

    Miaka 7-8 Ukuaji wa Akili (Ubongo)

    • Anakuza msamiati haraka• Anaanza kutofautisha vitu kutokana na kazi zake• Anaanza kuonesha udadisi wa mambo na kuuliza

    “Kwa nini?” • Anaanza kufahamu thamani ya namba

    Miaka 7-8 Ukuaji wa Kimaadili (Kiroho)

    • Anafahamu vizuri matarajio ya watu wakubwa katika mazingira tofauti na anaeleza makosa yake inapotokea ameyafanya

    • Anafahamu kuwa matendo yanahukumiwa kwa matokeo yake

    • Anajua mambo ya kimaadili yanayokatazwa na jamii ambayo anaishi

    Mpango wa Shughuli kwa Wiki

    Mafunzo haya yatatolewa kwa watoto kwa muda wa wiki 12. Kila wiki moja itajumuisha siku 4 za mafunzo darasani na watoto. Siku 1 (siku ya 5) WWJ watakwenda katika shule ya msingi ya karibu kwa ajili ya kutafakari na kufanya maandalizi.

    Kila kipindi kitakuwa na saa 2 hadi 3. MMJ anatakiwa kuzingatia shughuli zilizoainishwa kwa kila siku ili aweze kuzifanya ndani ya utaratibu ambao unaendana na elimu ya awali na mpango wa utayari wa shule.

    SIKU YA 1 SIKU YA 2 SIKU YA 3 SIKU YA 4

    Tafakuri na Maandalizi

    (kwenye shule ya msingi)

    WIKI MOJA

    SIKU YA 5

  • 12 MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Mpangilio wa Hadithi

    Mwezeshaji awaongoze WWJ kubaini mpangilio wa hadithi 12 zitakazosomwa kwa wiki 12 za mafunzo. Kila wiki MMJ atawasomea watoto hadithi moja kwa kufuata utaratibu uliooneshwa hapo chini:

    1. Napenda nyumbani2. Upendo3. Nyoka mkubwa4. Napenda kwenda shule5. Kuku na kanga6. Kujikinga na Malaria7. Pupa za nyigu8. Kode na Kole9. Moto10. Yangeyange11. Nani mshindi wa Rede12. Shule yangu

    Maelekezo ya ufundishaji wa Hadithi

    Zingatia mambo yafuatayo katika ufundishaji wa hadithi:

    i. Hakikisha kwamba msamiati mpya unafahamishwa kwa watoto, kwa kutumia mbinu na vifaa mbali mbali vikiwemo kadi za maneno na picha.

    ii. Anza na maelezo, yanayowahamasisha watoto kubashiri hadithi inahusu nini.iii. Soma hadithi kwa sauti na kwa namna nzuri ambayo ungependa mtoto aisome na kuielewa.

    Hadithi za Kusoma

    Kusimuliana hadithi ni njia nzuri sana ya kuwasaidia watoto kujifunza kusoma na kufurahia vitabu.

    Kusoma hadithi kwa sauti kunahamasisha watoto waongee kuhusu picha na kujihusisha na sehemu za hadithi ambazo wanazijua vizuri.

    Picha Kwa Hisani ya AKDN

  • 13MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Umuhimu wa kusoma hadithi kwa sauti ni:

    • Kunasaidia watoto kujenga stadi ya kusikiliza, usikivu, uwezo wa kutafakari na kukuza lugha ya mawasiliano.

    • Kuonesha hisia zao kutokana na hadithi hususani uhusika wa wahusika waliotumika katika hadithi.

    Matumizi ya Vitabu Vikubwa

    Kama jina linavyosawiri, vitabu hivi ni vikubwa kuliko vitabu vya kawaida vya kusoma. Vinaweza kutumiwa na watoto kugundua michoro na kubadilishana mawazo kuhusu hadithi, katika makundi.

    Picha kwa Hisani ya AKDN

  • 14 MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Hatua za usomaji wa hadithi:

    Zingatia hatua za usomaji wa hadithi kama ifuatavyo:

    Hatua ya 1: Unapaswa kukifahamu kitabu kikubwa ambacho unataka kusoma. Pia kuangalia kwenye picha zote kwani kwa kufanya hivyo, huongeza shauku ya watoto kujua zaidi kuhusu hadithi. Hakikisha umesoma hadithi kabla na uwe umeifahamu vizuri. Kuijua hadithi vizuri kutakupatia uwezo wa kujiamini wakati unawasilisha kwa watoto.

    Hatua ya 2: Yazoee maandishi ya Kiswahili ili kutambua hoja gani utazibainisha kwa kuangalia picha. Inatarajiwa kwamba watoto watatoa mawazo yao binafsi wakati wa kuangalia picha. Unapaswa kulisisitiza hili na uliza maswali ya wazi ambayo hayana jibu sahihi kama vile “Sauti gani hutolewa na ndege?”

    Hatua ya 3: Kabla ya kuanza kusoma unaweza kuzungumza na watoto juu ya eneo la ujifunzaji na kujiuliza ni maneno yapi tayari watoto wanayafahamu. Unahitaji kutambua watoto wanafahamu nini kabla ya kujifunza misamiati mipya kwa kutumia kitabu kikubwa.

    Hatua ya 4: Hakikisha watoto wote wanaweza kuona kitabu na picha vizuri. Kukaa chini katika mduara mkubwa, wakati ukiwa umekaa kwenye kiti kifupi huku ukiwa amefungua kitabu na kuelekeza kwa watoto, mara nyingi njia hii huwa na ufanisi zaidi.

    Hatua ya 5: Onesha jalada kwa watoto – kitabu kinahusu nini? Wahimize watoto wote kukubaliana na majibu hata kama siyo sahihi, wahimize watoto wote kuongea.

    Hatua ya 6: Fungua ukurasa wa kwanza na fuata maelezo ya picha, uliza maswali na kubaini taarifa za kutosha kutoka kwenye picha kwa kadri unavyoendelea kufungua kurasa. Katika hatua hii, usiwe na wasiwasi kuhusu maandishi, hii itakuja baadaye wakiwa wanajiamini kuhusu taarifa zinazobainishwa na picha.

    Hatua ya 7: Usiharakishe watoto wakati wa kusoma, badala yake, toa fursa kwa watoto ili watoe mawazo yao juu ya hadithi na maelezo ya picha. Tofautisha matamshi na toni wakati wa usomaji. Tumia sauti za wahusika wa kwenye hadithi kama unaweza.

    Hatua ya 8: Tumia vitendo na mifuatano/midundo ya sauti katika kuhadithia hadithi.

    Hatua ya 9: Fuatilia hadithi kwa kuuliza maswali ya wazi kupima ufahamu na uelewa.

    Hatua ya 10: Waongoze watoto kuchora picha kutokana na hadithi waliyosimuliwa, kisha kushirikishana kwa kuelezea picha walizochora.

  • 15MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Ratiba ya Siku

    Huu ni muhtasari wa ratiba ya siku itakavyokuwa katika kipindi chote cha mafunzo ya utekelezaji wa mpango wa utayari wa kuanza shule. Zifuatazo ni alama zinazoonesha taratibu mbalimbali zitakazofanyika kwa siku.

    Kusalimia (dk10)

    Hadithi (dk10)

    Hadithi ya siku husika

    Kazi 1 (dk30)

    Umahiri:

    Vifaa: Shughuli:

    Ufuatiliaji:

    kunawa Mikono / Uji (dk30) kucheza

    Kazi 2 (dk30)

    Umahiri:.

    Vifaa:

    Shughuli:

    Ufuatiliaji:

    Kuagana (dk10)

  • 16 MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Utekelezaji wa Ratiba ya Siku

    Mduara wa asubuhi – Mduara wa asubuhi unaweza kufanyika ndani au nje ya darasa kutegemeana na hali ya hewa na miundombinu iliyopo. Watoto wengi wanapokuwa wamefika, wakae kwa kufuata mtindo mmojawapo hapa chini.

    • Mduara kamili: Wakalishe watoto katika mduara mkubwa kwenye mkeka juu ya sakafu (kama unapatikana)

    • Nusu Mduara/Kiatu - farasi: Wakalishe watoto katika nusu mduara au mistari miwili ya nusu mduara.

    Anza kwa kubadilishana taarifa. Unganisha mduara wa asubuhi pamoja na ufuatiliaji wa shughuli za jana ambazo zilipaswa kufanywa na watoto walipokuwa nyumbani. Waulize watoto ikiwa walizifanya na badilishana nao uzoefu. Unaweza kuimba wimbo, kuna nyimbo nyingi sana za salamu ambazo zitakuwa sahihi kutumika. Unaweza pia kucheza mchezo rahisi kuchangamsha watoto kwa ajili ya kipindi. Ni muhimu mwalimu afanye ukaguzi wa afya usio rasmi kwa kujikita kwenye usafi binafsi na magonjwa. Watoto wanaweza kuhimizwa kufanya shughuli za usafi kuzunguka shule ili kuwa na mazingira safi na salama wakati wanasubiriana. Kumbuka – Toa fursa kwa watoto kuimba wimbo waliouzoea kwa siku ya kwanza iwapo watapenda kufanya hivyo. Wimbo wa jieleze au wimbo wowote wanaoufahamu katika mazingira yao wanaweza kuuimba kwani ni muhimu kwa kujitambulisha.

    Toa mfano kwa kuimba wimbo ukihusisha mazingira ya shule kwa kutaja majina ya sehemu mbalimbali na awaambie watoto vyoo viko wapi? Na wapi watoto wanaweza kunawa mikono. Kisha, andika kanuni kwenye bango na kutundika bango juu ya ukuta. Unaweza pia kufanya mapitio ya darasa pamoja na watoto, waulize kama wanafikiria kuongeza au kubadilisha mambo. Mfano wa kanuni unaweza kuwa:

    • Kuwa mnyenyekevu na unayejali wengine.• Ongea kwa sauti ya chini wakati uko darasani.• Omba ruhusa kabla ya kwenda chooni.• Tembea taratibu, unaweza kukimbia ukiwa nje ya darasa.

    Hadithi ya siku husika

    Waweke watoto wakae chini kwa utulivu (kama una tandiko/mkeka, wasaidie wakae katika mduara au kwenye nusu mduara) na endelea kusoma hadithi. Hakikisha kila mtoto anaweza kuona kitabu vizuri. Soma kwa kutumia kitabu kikubwa, kwa usahihi na polepole. Tumia sauti tofauti tofauti na badilisha toni ya sauti yako kwa kadri kitabu kinavyoeleza ili kufanya hadithi iwe na uhalisia.

    Umahiri: Umahiri utategemeana na hadithi husika, angalia kwenye jedwali la umahiri ili likuongoze, andika chini umahiri ambao shughuli zako zitahusiana.

    Matokeo ya mafunzo: Ni stadi mbalimbali ambazo watoto watazijenga baada ya mafunzo.

  • 17MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Vifaa: Hivi ni vitu ambavyo vinasaidia kufanikisha mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji katika mpango huu. Baadhi ya vifaa hivi ni kama vile: vitabu vya hadithi, karatasi/bango kitita, picha mbalimbali, vihesabio na penseli.

    Zoezi la kuchangamsha la darasani: Tambua kwamba kutoa mazoezi ya uchangamshi kwa watoto yana umuhimu wake. Mazoezi yanabidi yafanyike ndani ya darasa na nje ya darasa. Mazoezi haya yanapaswa kuwa ya viungo, chemsha bongo na kuimba.

    Shughuli: Ni kazi mbalimbali za vitendo zitakazofanyika wakati wa ufundishaji na ujifunzaji. Unatakiwa kutumia mbinu shirikishi katika kuwajengea watoto umahiri husika. Shughuli za wiki zitapangwa kuzingatia hadithi ya wiki husika.

    Ufuatiliaji: Weka kumbukumbu juu ya mambo ambayo watoto wanaweza kufanya nyumbani kama shughuli za nyongeza.

    Mduara wa kuagana: Wakati wa mzunguko wa kuagana, ni muda mzuri kupitia shughuli za siku kwa kuuliza watoto walijifunza nini katika siku hiyo. Wakumbushe watoto juu ya shughuli za ufuatiliaji ambazo wanaweza kuzifanya nyumbani kuongeza maarifa yao. Kama watoto wamefanya kazi, unaweza kuifafanua na kuionesha wakati wa mduara wa kuagana.

    Hitimisha siku kwa wimbo wa kuagana/muziki na mchezo (unaweza kuongozwa na mtoto). Kama wazazi wamekuja kuwafuata watoto wao, hii ni fursa ya kipekee kwa ajili yako kufanya mashauriano nao, juu ya watoto wao.

    Hakikisha watoto wana vitu vyao vyote. Wahamasishe wajaribu shughuli ya ufuatiliaji nyumbani na waje katika siku inayofuata kukupa taarifa. Waage kila mmoja na wahamasishe waagane pia. Baadhi ya watoto wanaweza kutembea wenyewe kwa hiyo hakikisha unawasaidia kuvuka barabara/mito kwa usalama.

    Tathmini ya Mafunzo:Fanya shughuli rahisi kupata mrejesho wa namna siku ilivyokwenda.

    Kumbuka: Kupitia shughuli za siku ya kwanza kwa kina. Japokuwa kila siku itakuwa na maudhui tofauti, mtiririko utakuwa uleule, kuwafanya watoto wazoee mwenendo wa kipindi na kufanya mazoezi juu ya tabia fulani, kama vile kuimba, kusikiliza hadithi, kucheza pamoja, kunawa mikono na kuagana mwisho wa kila kipindi.

    Mambo ya Kuzingatia Wakati wa Kuandaa Igizo Dhima:• Kulielewa vizuri lengo la igizo dhima kuzingatia hadithi ya wiki husika.• Hakikisha umewapa watoto uhusika kulingana na lengo na hadithi.• Tayarisha vifaa vinavyohitajika katika uigizaji.• Husianisha hadithi na mazingira yaliyowazunguka.• Waongoze watoto namna ya kutekeleza majukumu waliyopewa wakati wa uigizaji.

  • 18 MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Namna ya Kupanga Vibao Fumbo

    Maana ya kibao fumbo:

    Kibao fumbo ni kifaa kinacho husisha kupanga sehemu za picha, namba au herufi zilizokatwa ili kuifanya picha kamili.Vifaa vya kutengezea kibao fumbo: picha ya kuchora, picha kutoka kwenye picha kutoka kwenye majarida, magazeti, maboksi magumu, mikasi, gundi.

    Namna ya kutengeneza kibao fumbo:i. Tayarisha picha utakayoitumia katika utengenezaji wa kibao fumbo. Picha hio unaweza kuichora,

    kuikata katika gazeti au jarida.ii. Andaa kipande cha boksi/kibao/karatasi ngumu kulingana na picha uliyokusudia kuitengenezea

    kibao fumbo.iii. Paka gundi kwenye kipande cha boksi/kibao/karatasi ngumu ( sehemu ya kubandika picha)iv. Bandika picha kwa uangalifu sehemu uliopaka gundi katika boksi.v. Baada ya kukauka, kwa kutumia rula na penseli weka alama sehemu utakayokata.vi. Kata kibao fumbo kulingana na alama ulizoweka.vii. Idadi ya sehemu ziwe chache kwa watoto wadogo. Mfano kama kibao

    Kumbuka: Sehemu za kibao fumbo kimoja zihifadhiwe sehemu moja.

    Ufuatiliaji: Uendane au utokane na uchunguzi wa shughuli au vitendo vya ufundishaji na ujifunzaji vinavyofanywa na watoto ndani ya darasa, nje ya darasa na nyumbani.

    Kumbuka: • Kufuatilia mtoto mojamoja kulingana na uwezo wake.• Kumsaidia mtoto kile ambacho ameshindwa kukifanya ili aweze kuendana na wenzake.• Kumbuka kutunza kumbukumbu za watoto kwenye shajara ili kuweza kufuatilia maendeleo ya

    watoto hatua kwa hatua.

    Onesho Mbinu: Ni mbinu ambayo mwalimu huonesha uhalisia wa tendo maalumu hatua kwa hatua mbele ya watoto ili waweze kutenda ipasavyo.

  • 19MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    KIPINDI CHA MPITO

    Kipindi cha mpito: Ni kitendo cha kumwandaa mtoto kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine ili kuyamudu mazingira mapya atakayokutana nayo katika suala la ufundishaji na ujifunzaji. Mfano wa kipindi cha mpito kwa mtoto ni kutoka nyumbani kwenda shule ya awali, kutoka shule ya awali kwenda shule ya msingi. Kwa mtoto atakaeshiriki kati katika program hii, anatakiwa pia aandaliwe vizuri ili aweze kukabiliana na mazingira mapya ya shule ya msingi kwa kuanza darasa la kwanza. Kipindi cha mafunzo, mtoto atapata fursa ya kuonana na mwalimu wake wa darasa la kwanza, kuitembelea shule na kuona mazingira ya shule na ya darasa nje na ndani ni miongoni mwa vitu muhimu vinavyomsaidia mtoto kuyakubali na kuyazoea mazingira ya shule ya msingi. MMJ anatakiwa pia ashirikiane na wazazi wa watoto waliopo katika kipindi cha mpito.

    MAPENDEKEZO YA UWIANO WA IDADI YA WATOTO NA WWJ

    Waratibu Elimu Kata kwa kushirikiana na walimu wakuu, WWJ na jamii husika wanashauriwa kuhakikisha kuwa WWJ wanapata msaada wa kutosha kutoka kwa wanajamii wa kujitolea kulingana na idadi ya watoto walioko shule.

    Idadi inayopendekezwa ya wanajamii wa kujitolea kwa kuwasaidia WWJ ni kama ifuatavyo:

    WATOTO Mwanajamii wa kujitolea

    1-30 1

    31-50 2

    51-70 3

    71+.... 4

  • 20 MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    WIKI YA TANO YA MAFUNZOHADITHI YA KUKU NA KANGA

    Kusalimia (dk10)

    Mwezeshaji awaongoze WWJ kufanya yafuatayo: • Kuwakaribisha watoto mmoja mmoja na waelekeze wakae katika

    mzunguko.• Kuimba wimbo wa salamu kama vile Jieleze• Kupitia kanuni za darasa kwa pamoja (kwa mfano, tunashirikiana

    pamoja na kubadilishana vitu darasani) • Kuwapitisha katika mazingira ya shule.• Kuelezea mambo waliyofanya/yaliyotokea katika jamii zao wakati wa

    mapumziko mafupi.

    Hadithi (dk10)

    Kuku na KangaKuwasomea watoto hadithi kwa kutumia vikaragosi vya vijiti. (kuwaon-goza watoto kutaja idadi ya kuku, kanga, mayai na rangi zilizomo kwenye hadithi)

    Kazi 1 (dk30)

    Umahiri: Utambuzi, kuwasiliana kwa lugha ya Kiswahili na kujenga mwili.

    Vifaa: karatasi, kalamu, rangi, picha zilizochorwa

    Shughuli: Kuwaongoza watoto kufanya kazi wawiliwawili,elekeza kila kundi kuchora na kupaka rangi picha za kuku, kanga na vifaranga vyao. Kisha waelezee picha hizo na kuhesabu idadi ya kuku, kanga na vifaranga vyao.

    Ufuatiliaji: Chunguza kama watoto wameweza kuchora, kupaka rangi, kuhesabu na kuelezea picha walizozichora

    kunawa Mikono / Uji (dk30)

    Kucheza – Waongoze watoto kucheza mchezo wa kuendesha matairi ya vyombo tofauti, mfano: baiskeli, gari na mifuniko ya ndoo.

    Siku ya 1

  • 21MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kazi 2 (dk30)

    Umahiri: Utambuzi, Kuhusiana, Kuwasiliana kwa lugha ya Kiswahili na Kujenga mwili.

    Vifaa: Kalamu, karatasi, rangi za kuchorea, mikasi, maboksi, karatasi ngumu.

    Shughuli: Tumia onesho mbinu ya namna ya kupanga vibao fumbo kwa kutumia picha ulizochora au walizochora watoto wenyewe kipindi kilichopita.Wagawe watoto katika makundi ya 3 -5 wapangevibao fumbo,kisha kuelezea picha halisi walizozipanga.

    Ufuatiliaji: Kuhakikisha kuwa watoto wameweza kupanga picha kwa usahihi na kuzielezea.

    Kuagana (dk10)

    Mapitio:

    • Waulize watoto wanafikirinini kuhusu siku yao ya kwanza baada ya mapumziko mafupi.

    • Wanakumbuka majina ya rafiki zao?• Wakumbushe walindane na wawe makini wakati wanatembea kurudi

    nyumbani.• Watoto wachunguze ndege mbalimbali waliomo kwenye mazingira

    yao.

  • 22 MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kusalimia (dk10)

    Mwezeshaji awaongoze WJW kufanya yafuatayo:• Kukaribisha watoto, nakuimba nao wimbo wa ndege, ‘Sisi ndege

    twaruka twatafuta viota, atakayechelewa……….• Kuuliza watoto maswali ya yatakayowasaidia watoto kujieleza, mfano:

    ulipoamka asubuhi ulimsaidia mama kazi? wazi yatakayobainisha taarifa muhimu za watoto

    Hadithi (dk10)

    Kuku na KangaKuwasomea watoto hadithi kwa sauti kwa kuwapa uhusika, kwa mfano watoto waigize mlio wa kuku kila anapotajwa kuku wakati wa kusoma hadithi. Waongoze watoto hivyo kwa ndege wengine

    Kazi 1 (dk10)

    Umahiri: Kuwasiliakwa lugha ya Kiswahili, Kuhusiana na Utambuzi.Vifaa: Vitu vinavyopatikana nyumbani. ufagio, maji, sabuni, kizoleo.

    Shughuli: Katika vikundi waongoze watoto wajadili umuhimu wa kujali vitu vyao na vya wengine. Wahusianishe na hadithi wakati nyoka alipokula mayai ya kanga na mwewe alipokula vifaranga vya kuku.

    Ufuatiliaji: Chunguza kama watoto wameweza kujadiliana kuhusu umuhimu wa kujali vitu vyao na vya wengine.

    kunawa Mikono / Uji (dk30) Kucheza: - Kuwaongoza watoto kucheza mchezo wa kuendesha gari.

    Wagawe watoto katika makundi 2, mbele ya kila kundi aonekane dereva amekamata uskani

    Siku ya 2

  • 23MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kazi 2 (dk30)

    Umahiri: Utambuzi, kujenga mwili, kutathimini mazingira na Kuwasiliana kwa lugha ya Kiswahili

    Vifaa: karatasi ngumu, mifuko ya karatasi, magazeti ya zamani, penseli za rangi, viweka rangi, mikasi, gundi ya karatasi, vifaa chakavu.

    Shughuli: Utengenezaji wa vikaragosi. Waongoze watoto kupitia kitabu cha hadithi na kuchunguza picha, kisha wagawe katika makundi na wasaidianae kutengeneza vikaragosi vya kuku, mwewe na watoto wao na nyoka.

    Ufuatiliaji: Chunguza kama watoto wameweza kutengeneza vikaragosi vya ndege kama vile kuku mwewe na kanga.

    Kuagana (dk10)

    Mapitio• Waulize watoto nini walichojifunza leo• Tunza vikaragosi ambavyo wametengeneza shuleni kwa sababu

    watavihitaji tena.• Kuwaongoza watotokuimba wimbo wa Kanga wakati anaondoka na

    viranga vyake kama ulivyo kwenye hadithi.• Waagize watoto kuangalie ndege kama vile kuku, kanga, mwewe,

    kunguru, tetere, kware wakati wanatoka nyumbani kuelekea shuleni.• Fuatilia watoto kuhakikisha wamefika nyumbani salama.

  • 24 MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kusalimia (dk10)

    Mwezeshaji awaongoze WJW kufanya yafuatayo:

    • Kukaribisha watoto kwa wimbo.• Waulize watoto kuhusu walichojifunza siku iliyopita• Kuwaelekeza watoto kuimba wimbo waKanga na watoto wake, wa-

    toto wangu njooni tuondoke…..• Waulize watoto ikiwa waliwaona ndege mbalimbali nyumbani na

    kutaja ndege hao. • Waongoze watoto juu ya majibu wanayoyatoa.

    Hadithi (dk10)

    Kuku na KangaWasimulie watoto hadithi kwa kutumia picha zilizomo ndani ya hadithi.

    Shughuli 1 (dk30)

    Umahiri: Utambuzi, Kuhusiana na Kuwasiliana kwa lugha ya Kiswahili.

    Vifaa: Kadi za namba, vijiti, vifuniko vya chupa na chupa.

    Shughuli: Waongoze watoto kukaa katika vikundi , kisha wahesabu vitu halisi 1hadi 5 na kuvipanga kwa mpangilio kwa kuonesha idadi ya vitu 1 hadi 5. Waongoze kupanga kadi za namba 1-5.Waongoze watoto kupitia kwa usahihi.

    Ufuatiliaji: Chunguza kama watoto wameweza kuhesabu na kupanga vitu kwa usahihi,, kuanzia 1 hadi 5 kwa usahihi.

    kunawa Mikono (dk30)

    Uji/ Kucheza – Kucheza mchezo wa kuhesabu mfano: mdako au rede.

    Siku ya 3

  • 25MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Shughuli 2 (dk30)

    Ufuatiliaji: Kuuliza na kujibu maswali.

    Umahiri: Utambuzi, Kujenga Mwili na Kuwasiliana kwa Lugha ya Kiswahili.

    Vifaa: penseli, karatasi, magazeti, rangi za kuchorea na picha za ndege mbalimbali.

    Shughuli: Waongoze watoto kuimba wimbo unaohusu ndege, kuigiza sauti na miondoko ya ndege, mfano: Mabata madogo dogo…..Weka kadi za picha za ndege mbalimbali. Kisha waweke watoto katika vikundi kulingana na idadi ya watoto waliopo darasani, gawa kadi za picha za ndege mbalimbali na wasaidie watoto kutofautisha ndege wanaofugwa na wale wa porini.

    Ufuatiliaji: Chunguza jinsi watoto wanavyoshiriki katika kutofautisha ndege wanaofungwa na wale wa porini.

    Kuagana (dk10)

    Mapitio • Waulize watoto nini walichojifunza siku ya leo.• Kuwaongoza watoto kuimba wimbo wa kuagana• Wasiliana na wazazi kama kuna ujumbe wowote unaotaka kufikisha

    kwao • Fuatilia na hakikisha watoto wamefika nyumbani salama.

  • 26 MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kusalimia (dk10)

    Mwezeshaji awaongoze WJW kufanya yafuatayo:• Kukaribishana na kusalimiana na watoto.• Chagua mtoto mmoja aimbishe wimbo wowote anaoufahamu.• Waelekeze watoto kushirikishana kwenye zamu za usafi wa asubuhi

    pamoja na marafiki zao, pia kufanya ukaguzi wa usafi wa mwili.

    Hadithi (dk10)

    Kuku na Kanga – Kuwaongoza watoto kuigiza hadithi kwa kuvaa uhusika

    Kazi 1(dk30)

    Umahiri: kuthamini mazingira, Kuhusiana na utambuzi Kuwasiliana kwa lugha ya Kiswahili

    Vifaa: picha za ndege wanaopatikana katika mazingira yanayowazunguka, penseli, mpira rangi, karatasi.

    Shughuli: Waongoze watoto katika makundi kujadiliana ni namna gani kuku na kanga walitatua tatizo. Je kulikuwa na namna tofauti ya kutatua tatizo hilo?. Watoto waeleze namna wanavyoweza kutatua matatizo miongoni mwao. Katika vikundi watoto waigize wanacheza michezo mbalimbali, waoneshe kutofautiana miongoni mwao. Kisha waoneshe ni jinsi gani watakavyotatua tatizo hilo.

    Ufuatiliaji: Chunguza namna watoto watakavyotatua matatizo yatakayojitokeza.

    Kunawa Mikono (dk30)

    Uji/ Kucheza – waongoze watoto kutengeneza tiara na kucheza nazo.

    Siku ya 4

  • 27MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kazi 2 (dk30)

    Umahiri: Kuhusiana, Kuwasiliana kwa lugha ya Kiswahili, Utambuzi

    Vifaa: Picha zinazoonesha hisia mbalimbali kama vile: furaha au huzuni

    Shughuli: waongoze watoto katika makundi kuigiza hisia mbalimbali kama vile hofu, furaha na kujali wengine. Kisha wengine watabiri hisia zilizojitokeza. Watoto wajadiliane jinsi wanavyojisikia na namna watakavyosaidiana wakati anapopata hofu au furaha.

    Mfano: kumsikiliza, kumfariji na kumpongeza. Husianisha na hadithi ya kuku na kanga.

    Ufuatiliaji: Chunguza kama watoto wameweza kuonesha hisia mbalim-bali kwa kuhusianisha na hadithi ya Kuku na Kanga. Wasaidie watoto kujenga tabia ya kusaidiana wanapopatwa na hisia mbalimbali kama vile furaha au huzuni.

    Kuagana 9 (dk10)

    Mapitio• Waulize watoto leo wamejifunza nini siku ya leo?• Wakumbushe watoto kwamba hakutakuwa na darasa kesho na

    watapaswa kurejea tena wiki inayofuata• Watakie watoto mapumziko mema ya mwisho wa wiki• Fuatilia kuhakikisha wamefika nyumbani salama• Chagua mtoto mmoja aimbishe wimbo wa kuagana

  • 28 MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    WIKI YA SITA YA MAFUNZOHADITHI YA KUJIKINGA NA MALARIA

    Kusalimia (dk10)

    Mwezeshaji awaongoze WWJ kufanya yafuatayo: • Kuwakaribisha watoto kwa wimbo unaohusu Malaria, “Malaria,

    Ugonjwa hatari.”• Waulize watoto leo ni siku gani?• Wakumbushe watoto kuhusu hadithi ya wiki iliyopita ya Kuku na

    Kanga. Watambulishe hadithi ya wiki hii ambayo ni Kujikinga na Malaria.

    Hadithi (dk10)

    Kujikinga na Malaria Soma hadithi ya Kujikinga na malaria kwa sauti, na uwaoneshe watoto picha. Kumbuka: Kama darasa lako lina idadi ya watoto wengi hakikisha watoto wote wapo karibu na wewe na wanaweza kuziona picha za hadithi.

    Kazi 1(dk30)

    Umahiri: Utambuzi, Kuwasiliana kwa lugha ya Kiswahili, kuthamini mazingira, kuhusiana.

    Vifaa: Picha inayoonesha mazingira machafu na safi, chombo cha kuwekea takataka fagio, kizoleo.

    Shughuli: Waongoze watoto wataje sababu za ugonjwa wa malaria wakiwa katika makundi yao.Waongoze watoto kuchora vitu mbalimbali vinavyosababisha malaria. (mf. Mbu, vifuu na vikopo vya maji, vidimbwi, taka zilizorundikana n.k.) Kisha watoto waelezee picha zao na kuzibandika ukutani au kutengeneza kitabu cha zig zaga kutegemeana na mazingira.

    Ufuatiliaji: Chunguza kama watoto wameweza kutaja sababu za malaria, kuchora picha za vitu vinavyosababisha malaria na kutengeneza kitabu chao.

    Kunaawa Mikono (dk 30)

    Uji/ kucheza – Waongoze watoto kucheza mpira wa miguu na michezo mingine wanayoipenda

    Siku ya 1

  • 29MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kazi 2 (dk30)

    Umahiri: Kuhusiana, utambuzi, kuwasiliana kwa lugha ya Kiswahili.

    Vifaa: Nguo za igizo dhima, beseni la maji, kitambaa cha kumkandia mgonjwa.

    Shughuli: Waongoze watoto kufanya igizo dhima kuonesha mtu anayeumwa ugonjwa wa malaria. Wape watoto uhusika mbali mbali kutokana na hadithi waliyoisoma, mfano mgonjwa, daktari, na watu wanaomsaidia mgonjwa. Mgonjwa awe amelala anateteneka wanaomuhudumia waoneshe huzuni, mmoja awe anamkanda paji la uso kwa maji na kitambaa.

    Ufuatiliaji: Chunguza kama watoto wameweza kuigiza kwa kuuvaa uhusika, mfano kutoa msaada wa mgonjwa, wameshukuru na wanakumbuka ushauri uliotolewa na daktari.

    Kuagana (dk10)

    Mapitio:• Wakumbushe watoto kufukia madimbwi yaliyotuwamisha maji. • Wakumbushe watoto kuokota makopo na vifuu vinavyohifadhi maji

    hasa wakati wa mvua.• Wakumbushe kunawa mikono baaada ya kuokota makopo na

    takataka nyingine. • Waongoze watoto kuimba wimbo wa kuagana

  • 30 MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kusalimia (dk10)

    Mwezeshaji awaongoze WWJ kufanya yafuatayo:• Kuwakaribisha watoto, na kuimba nao wimbo wa salamu• Waongoze watoto wataje siku ya leo.• Kagua usafi na afya za watoto • Waongoze watoto kuimba wimbo unaohusu Malaria, “Malaria,

    Ugonjwa hatari.”

    Hadithi (dk10)

    Kujikinga na MalariaMwezeshaji awaongoze WWJ kuismulia hadithi kwa kualika mgeni (unashauriwa kumwalika mwalimu wa darasa la kwanza kutoka shule ya msingi/mtaalamu wa afya au mtu yoyote mwenye uwezo wa kusimulia hadithi.

    Kazi 1(dk10)

    Umahiri: Kuwasiliana kwa lugha ya Kiswahili, Utambuzi, Kujenga Mwili, Kuthamini Mazingira.

    Vifaa: penseli, karatasi, penseli za rangi, picha za wadudu wanaoambukiza magonjwa na picha zinazoonesha magonjwa yanayosababishwa na mazingira machafu.

    Shughuli: Waongoze watoto kukaa wawili wawili na kujadiliana magonjwa mengine yanayosababishwa na mazingira machafu.

    Mfano: kipindupindu, kuharisha, ugonjwa wa ngozi na macho. Kisha washirikishane namna ya kuepuka magonjwa hayo.

    Ufuatiliaji: Chunguza kama watoto wameweza kutaja magonjwa mengine yanayosabishwa na uchafu.

    Kumbuka: Kuwakumbusha watoto watambue kituo cha afya kilicho karibu ya shule / nyumbani ambacho mtu akiumwa anapata tiba.

    Kunawa Mikono (dk30) Mwezeshaji awaongoze WWJ kuimba wimbo wa Malaria na kucheza

    michezo waipendayo.

    Siku ya 2

  • 31MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kazi 2 (dk30)

    Wahamasishe watoto wafuate njia sahihi za kuosha mikono kabla na baada ya kula.

    Umahiri: Utambuzi, Kuhusiana, Kukuza lugha ya Kiswahili na Kuthamini mazingira.

    Vifaa: picha mbalimbali za kujikinga na malaria mfano neti, dawa za kuulia mbu.

    Shughuli: Waweke watoto katika vikundi kulingana na idadi ya watoto waliopo. Waelekeze watoto kuzungumzia dalili mbali mbali za malaria na hatua za kuchukua ili kujikinga na ugonjwa huo. Kuwaongoza watoto kuimba wimbo wa “malaria ugonjwa hatari” uliomo katika kitabu cha hadithi.

    Ufuatiliaji: Fuatilia uhakikishe kama watoto wameweza kueleza na kutaja magonjwa mbalimbali yanayotokana na mazingira machafu, pamoja na kuweka mazingira kuwa safi na salama umuhimu wa kuweka mazingira safi na salama.

    Kuagana (dk10)

    Mapitio• Kuuliza watoto nini walichojifunza siku ya leo• Wasisitize watoto wafanye usafi wa mazingira shuleni na nyumbani.• Wakumbushe watoto umuhimu wa kutumia vyandarua wakati wa

    kulala.• Wakumbushe kuwa kinga ni bora kuliko tiba• Wakumbushe kwenda katika vituo vya afya au zahanati wanapohisi

    dalili za kuumwa.

  • 32 MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kusalimia (dk10)

    Mwezeshaji awaongoze WWJ kufanya yafuatayo:• Kuwaongoza watoto kuimba wimbo wa Malaria• Kuwauliza watoto leo ni siku gani? • Waulize watoto kutoa taarifa wanazozifahamu kuhusu ugonjwa wa

    malaria.• Waulize kama wamefanya usafi katika mazingira ya nyumbani kwao.

    Hadithi (dk10)

    Kujikinga na malaria Mwezeshaji awaongoze WWJ kusimulia hadithi kwa kutumia vikaragosi.

    Kazi 1(dk30)

    Umahiri: Utambuzi, Kuhusiana, Kuwasiliana kwa lugha ya Kiswahili, Kuthamini mazingira.

    Vifaa: Mavazi ya wahusika mfano mama, daktari, chombo cha kupimia joto bakuli, maji, sabuni, ufagio, kizoleo.

    Shughuli: Waongoze watoto kufanya igizo dhima juu ya hadidhi ya “kujikinga na malaria” kama ilivyo katika hadith. Hakikisha umewapa watoto uhusika kama ilivyoainishwa katika hadithi.

    Ufuatiliaji: Hakikisha kamawatoto wameweza kutaja kanuni za kujikinga na malaria na wahimize kuzifuata.

    Kunawa Mikono (dk30)

    Uji/ Kucheza - Mwezeshaji awaongoze WWJ kuimba wimbo wa “Kioo, Kioo alikivunja naniii…Waongoze watoto kuimba wimbo wa malaria a na kucheza michezo wanayoipenda

    Siku ya 3

  • 33MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kazi 2 (dk30)

    Umahiri: Utambuzi, Kujenga mwili, Kukuza lugha ya Kiswahili, Kuhusiana.

    Vifaa: Penseli, rangi, karatasi, picha za huzuni na furaha.

    Shughuli: Waongoze watoto kuonesha hisia za huzuni, furaha na kujali kwa kutumia onesho mbinu.Kisha waongoze watoto wachore picha zinazoonesha huzuni au furaha kwenye karatasi kwa vikundi. MMJ awaandikie watoto majina yao chini ya picha zao walizochora.

    Ufuatiliaji: Chunguza kama watoto wameweza kuchora picha zinazoonesha hisia mbalimbali.

    Kuagana (dk10)

    Mapitio• Kuwauliza watoto walichojifunza siku ya leo. • Waulize watoto nini kimewafurahisha zaidi katika siku ya leo.• Wasisitize kujali wenzao wanaopata matatizo.• Waongoze watoto kuimba wimbo wa vitendo na kuwaaga.

  • 34 MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kusalimia (dk10)

    Mwezeshaji awaongoze WWJ kufanya yafuatayo• Kuwakaribisha watoto katika siku yao ya nne ya wiki.• Kuimba wimbo wa kusalimiana• Kuwauliza watoto leo ni siku gani?• Waulize watoto kama kuna mtoto aliyewahi kuwasimulia wazazi wake

    hadithi ya Kujikinga na Malaria.

    Hadithi (dk10)

    Kujikinga na MalariaMwezeshaji awaongoze WWJ kusimulia hadithi kwa kusoma picha.

    Kazi 1(dk30)

    Umahiri: Kuhusiana, Utambuzi, Kujenga Mwili. Kukuza lugha ya mawasiliano, kuthamini mazingira.

    Vifaa: Kadi za rangi, visoda, mawe, karatasi, maua.

    Shughuli: Kwa kutumia onesho mbinu, waongoze watoto kupanga vitu mbali mbali kama maua, vifuniko vya chupa, visoda kwakuzingatia rangi na mpangilio ili kutengeneza nakshi.Waweke watoto katika vikundi na wasaidie watoto kupangavitu mbalimbali kwa nakshi wanazozipenda, watake waeleze walivyopanga na rangi walizotumia.

    Ufuatiliaji: Chunguza tabia ya watoto kama wanapenda kusoma vitabu kwa kuangalia vitabu na picha zilizopo kwenye eneo la hadithi.

    Kumbuka: kuwakumbusha watoto juu ya vitu na mazingira yanayoweza kusababisha kupata malaria.

    Kunawa Mikono (dk30) Uji/ Kucheza - Mwezeshaji awaongoze WWJ kuwaelekeza watoto kuimba

    na kucheza michezo wanayoipenda.

    Kuwahimiza watoto kunawa mikono kwa usahihi kabla na baada ya kula.

    Siku ya 4

  • 35MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kazi 2 (dk30)

    Umahiri: Kuhusiana, Kukuza lugha ya Kiswahili, Utambuzi, Kuthamini Mazingira

    Vifaa: Maji, bakuli, kadi za picha za matunda, matunda halisi.

    Shughuli: Waongoze WWJ kuelekeza watoto katika vikundi kutaja matunda na waeleze sifa za matunda kama rangi, umbo, harufu, ugumu na ladha. Kisha waseme ni matunda gani wanayoyapenda na kuelezea sababu zao.Waelekeze watoto kueleza umuhimu wa matunda (kulinda mwili dhidi ya maradhi.) kwa kuzingatia hadithi waliyoisoma.

    Ufuatiliaji: Chunguza kama watoto wameweza kutaja matunda na sifa zake.

    Kuagana (dk10)

    Mapitio

    • Waulize watoto wamejifunza nini siku ya leo• Wakumbushe watoto kutembea kwa usalama wakati wakirejea

    nyumbani kwa kuvuka barabara kama walivyojifunza.• Wakumbushe kusaidia shuhuli za nyumbani zinazoendana na umri

    wao.• Wakumbushe watoto kuwa hakutakuwa na darasa siku inayofuatia• Watakie watoto mapumziko memana waage kwa wimbo.

  • 36 MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    WIKI YA SAbA YA MAFUNZO HADITHI YA PUPA ZA NYIGU

    Kusalimia (dk10)

    Mwezeshaji awaongoze WWJ kufanya yafuatayo• Kuwakaribisha watoto katika siku yao ya kwanza katika wiki ya saba• Waongoze watoto kuimba wimbo wa wadudu.• Jadiliana na watoto kuhusu wadudu wanaowafahamu.• Wajulishe kuwa wiki hii tuna hadithi mpya na wahusika wapya.•

    Hadithi (dk10)

    Pupa za Nyigu – Simulia hadithi kwa sauti kwa kutumia vikaragosi vya vijiti.

    Kazi 1(dk30)

    Umahiri: Utambuzi, kuhusiana, Kuwasiliana lugha ya Kiswahili na Kuthamini mazingira.

    Vifaa: Picha za hadithi

    Shughuli: Waongoze watoto kufanya majadiliano juu ya wanachokipenda kutokana na hadithi hiyo na ni kitu gani hawakipendi katika hadithi hiyo.Toa ufafanuzi juu ya majibu waliyoyatoa watoto.Waongoze watoto kuimba wimbo wa Maua mazuri….

    Ufuatiliaji: Chunguza kama watoto wametaja walichokipenda na wasichokipenda kutokana na hadithi.

    Kumbuka: Kuwaeleza watoto wasiwachezee wadudu hatari na pia waeleze wasiwaue wadudu.

    Kunawa Mikono (dk30)

    Uji/ Kucheza - Wacheze mchezo wa yai bovu na michezo mingine wanayoipenda.

    Siku ya 1

  • 37MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kazi 2 (dk30)

    Umahiri: Kujenga mwili, utambuzi na kuwasiliana kwa Lugha ya Kiswahili.

    Vifaa: Penseli, rangi na karatasi.

    Shughuli: Waoneshe watoto picha za wadudu mbalimbali kama inzi, nyuki, nyigu na mbu. Kisha waongoze kuonesha tofauti za wadudu mfano, ukubwa, udogo, rangi na upatikanaji wao. Katika vikundi watoto wachore picha za wadudu mbalimbali.

    Ufuatiliaji: Chunguza kama watoto wameweza kutaja wadudu, kuchora picha na kuonesha tofauti za wadudu hao.

    Kuagana (dk10)

    Mapitio

    • Wakumbushe watoto kutochezea wadudu ambao ni hatari.• Wasisitize watoto kutaja wadudu wanaopatikana katika mazingira yao.• Chagua mtoto mmoja aongoze wimbo wa kuagana.

  • 38 MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kusalimia (dk10)

    Mwezeshaji awaongoze WWJ kufanya yafuatayo

    • kuwaongoza watoto kukaribishana na kusalimiana. • Chagua mtoto/watoto wanaodumisha usafi ili akague usafi wa mwili

    na mavazi kwa wenzake.• Kutoa fursa kwa watoto kubadilishana taarifa kuhusu somo la siku

    iliyopita.• Kuwaongoza watoto kueleza faida za wadudu mbalimbali• Kuwaongoza watoto kutaja siku za wiki.

    Hadithi (dk10)

    Pupa za Nyigu Waongoze watoto kusimulia hadithi kwa kusoma picha za hadithi ya Pupa za Nyigu.

    Kazi 1(dk30)

    Umahiri: Utambuzi, Kuwasiliana kwa Lugha ya Kiswahili na Kuthamini mazingira na kuhusiana.

    Vifaa: Picha za wadudu mbalimbali.

    Shughuli: Waongoze watoto kutoka nje na kuchunguza wadudu mbalimbali. Wape watoto fursa ya kutoa maelezo juu yya wadudu waliowaona, faida/hasara zao na jinsi ya kuwalinda. Hamasisha watoto kuwa watulivu na wasiwaue wanyama au wadudu wadogo wadogo wasiokuwa na madhara.

    Ufuatiliaji: Chunguza kama watoto wamebaini wadudu wasio na madhara.

    Kunawa Mikono (dk30) Uji/ Kucheza - watoto wacheze mchezo wa kufukuzana: mfano: mchezo

    wa nyuki. Waimbe wimbo wa “maua mazuri….

    Siku ya 2

  • 39MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kazi 2 (dk30)

    Umahiri: kujenga mwili, utambuzi, Kuwasiliana kwa lugha ya Kiswahili.

    Vifaa: Penseli, karatasi, kamba, uzi na gundi.

    Shughuli: Wasimulie Watoto sehemu ya hadithi na waelekeze wachore picha kwa kufuata matukio, kisha wasaidie watoto kutengeneze kitabu kutokana na picha walizochora.

    Ufuatiliaji: Kuchunguza kama watoto wametengeneza kitabu kwa kufuata mtiririko wa matukio katika hadithi.

    Kuagana (dk10)

    Mapitio

    • Kuwaongoza watoto kuimba wimbo wa siku za wiki.• Waulize watoto wamejifunza nini siku ya leo.• Wasisitize watoto kuwa na uvumilivu wakiwa wanacheza na wenzao.• Chagua watoto wawili waimbe wimbo wa kuagana.

  • 40 MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kusalimia (dk10)

    Mwezeshaji awaongoze WWJ kufanya yafuatayo:• Kuwaongoza watoto kukaribishana na kusalimiana• Kukagua usafi wa mwili na mavazi (inapendekezwa kutoa fursa kwa

    watoto wanaodumisha usafi kukagua wenzao).• Kutoa fursa kwa watoto kubadilishana taarifa kuhusu somo la siku

    iliyopita• Waongoze watoto kuelezea matukio waliyoyaona jana walipokuwa

    njiani au nyumbani• Kuwaongoza watoto kutaja siku za wiki.

    Hadithi (dk10)

    Pupa za Nyigu –Kusimulia hadithi kwa kutumia vikaragosi

    Kazi 1(dk30)

    Umahiri: Kujenga mwili, Utambuzi, Kuwasiliana kwa Lugha ya Kiswahili.

    Vifaa: udongo, maji, ndoo, maboksi na vijiti, picha za sega, nyuki na Picha za wadudu mbalimbali.

    Shughuli: Waongoze watoto kutengeneza sega kwa kutumia udongo wa mfinyanzi. Wagawe katika vikundi kutengeneza masega, kisha wajadiliana kuhusu vitu vinavyohitajika ili kutengeneza asali.

    Ufuatiliaji: Fanya uchunguzi kuona kama watoto wameweza kutengeneza masega na kutaja vitu vinavyotumika kutengeneza asali.

    Kunawa Mikono (dk30) Uji/ Kucheza - kuigiza namna wadudu mbalimbali wanavyolia. Kucheza

    mchezo wa dama

    Siku ya 3

  • 41MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kazi 2 (dk30)

    Umahiri: Utambuzi, Kuwasiliana kwa Lugha ya Kiswahili Kujenga Mwili na Kuhusiana.

    Vifaa: Picha mbalimbali za wadudu

    Shughuli: Kwa kutumia igizo dhima watoto waigize namna wanavyosalimia wakubwa na matendo mbalimbali yanayoonesha tabia njema. Mfano kupoke mzigo, kusema asante, kuwa na subira, kuomba samahani wanapokosea. Waongoze watoto wazungumze juu ya subira na kuhusisha na hadithi ambapo nyuki alikuwa na subira ndio maana aliweza kutengeneza asali.

    Ufuatiliaji: Chunguza kama watoto wana tabia njema, mfano kuwa na uvumilivu.

    Kuagana (dk10)

    Mapitio

    • Waulize watoto wamejifunza nini siku ya Leo.• Wakumbushe wawasimulie wazazi wao hadithi ya Pupa za Nyigu.• Wakumbushe watoto wawasaidie wenzao wanapong’atwa na

    wadudu. • Chagua mtoto mmoja aongoze wimbo wa kusalimiana.

  • 42 MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kusalimia (dk10)

    Mwezeshaji awaongoze WWJ kufanya yafuatayo:

    • Kuchagua mtoto aliyewahi kufika akaribishe wenzake.• Waongoze watoto kutaja wadudu wanaojitengenezea mahali pa

    kuishi. • Waongoze watoto kuigiza sauti za wadudu mbali mbali• Kuwauliza watoto siku za wiki.

    Hadithi (dk10)

    Pupa za Nyigu – Kualika mgeni kusimulia hadithi

    Kazi 1(dk30)

    Umahiri: Utambuzi na Kuwasiliana kwa Kiswahili, Kuthamini Mazingira,

    Vifaa/zana: maua mbalimbali, maji, unga, Picha za maua

    Shughuli: Wapeleke watoto katika bustani nje ya darasa kuangalia maua ambayo ndio yanayotupatia asali. Kisha wachunguze mimea mbali mbali inayotoa maua. Pia unaweza kutumia picha za maua mbalimbali kuwaonesha watoto.

    Ufuatiliaji: Chunguza kama watoto wameweza kubaina miti mbali mbali na mimea inayotoa maua.

    Kunawa Mikono (dk30) Uji/ Kucheza - Kucheza michezo wanayoipenda kama kuruka kamba,

    rede, mpira, dama na michezo ya asili.

    Siku ya 4

  • 43MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kazi 2 (dk30)

    Umahiri: Utambuzi, Kuhusiana na Kuwasiliana kwa Lugha ya Kiswahili.

    Vifaa/zana: visoda, mawe, kokoto na kadi za namba.

    Shughuli: Waongoze watoto wacheze mchezo wa kutambua idadi ya vitu katika kopo. Weka vitu halisi kama mawe, vijiti, kokoto katika mifuko tofauti, elekeza mtoto achukue vitu bila kuhesabu kisha akisie ni vingapi, baada ya kukisia ahesabu kupata idadi sahihi ya vitu hivyo.

    Ufuatiliaji: Mwalimu ahamasishe kila mtoto kupanga vitu hivyo na kuhesabu 1-10.

    Kuagana (dk10)

    Mapitio

    • Wakumbushe na wahamasishe watoto kuhesabu vitu mbalimbali wanavyoviona wakiwa wanaelekea nyumbani.

    • Kuelekeza watoto kuimba nyimbo za matendo. • Wahamasishe watoto kutengeneza kitu chochote wanachopenda na

    walete Jumatatu.• Wakumbushe lini wanapaswa kuja kuendelea na shule.

  • 44 MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    WIKI YA NANE HADITHI YA KODE NA KOLE

    Kusalimia (dk10)

    Mwezeshaji awaongoze WWJ kufanya yafuatayo:• Kuwaongoza watoto kujitambulisha kwa kutumia wimbo wa Jieleze.• Kuwauliza watoto wataje leo ni siku gani?• Kutumia kipaza sauti cha ajabu kubadilishana taarifa mbalimbali

    walipokuwa nyumbani.• Waulize ikiwa yupo yeyote aliyetengeneza kitu chochote akiwa

    nyumbani ili aoneshe wenzake.• Waoneshe watoto Kitabu cha hadithi iliyopita. Wakumbuke hadithi

    ilikuwa juu ya nini

    Hadithi (dk10)

    Kode na kole Tambulisha hadithi mpya ya Kode na KoleSoma hadithi kwa sauti huku ukiwashirikisha watoto

    Kazi 1(dk30)

    Umahiri: Utambuzi, Kuhusiana, Kukuza lugha ya Kiswahili, Kuthamini mazingira

    Vifaa: Nguo za kuigizia na matunda halisi.

    Shughuli: Waongoze watoto kufanya igizo dhima linalohusu faida za matunda wakihusisha na hadithi ya Kode na Kole. Watoto waigize wanakula matunda ya aina mbalimbali, wapo shuleni wanafurahi na wanashiriki vizuri katika michezo na kujifunza. Pia kundi lingine liigize kuonesha kuwa wao hawali matunda, hivyo wanaonekana dhaifu na wagonjwa na hawawezi kushiriki kikamilifu katika ujifunzaji au michezo.

    Ufuatiliaji: Chunguza kama watoto wameweza kutaja faida za kula matunda.

    Kunawa Mikono (dk30) Kucheza - Watoto wacheze mchezo wa kulenga shabaha kwa kutumia

    chupa. (chupa zibandikwe picha mbalimbali za matunda)Watoto waimbe wimbo uliomo ndani ya hadithi ya Kode na Kole unaohusu matunda.

    Siku ya 1

  • 45MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Shughuli 2 (dk30)

    Umahiri: Kujenga mwili, Utambuzi, Kukuza lugha ya Kiswahili

    Vifaa: Vitu halisi, kadi za picha zinazoonesha thamani ya namba, vihesabio.

    Shughuli: Watoto wafanye mazoezi ya kuhesabu, kuonesha thamani, kuongeza na kupunguza kwa njia ya matendo na wimbo. (katika matendo ya kuongeza na kupunguza zao lisizidi 10)

    Ufuatiliaji: Chunguza kama watoto wameweza kuhesabu vitu mbalimbali, kutaja thamani, kuongeza na kupunguza

    Kuagana (dk10)

    Mapitio

    • Wakumbushe watoto umuhimu wa kula matunda kwa ajili ya kujikinga na maradhi.

    • Waongoze watoto kuimba wimbo wa matunda uliomo kwenye hadithi hii.

    • Waage watoto na kuwasisitiza watembee kwa uangalifu kando ya barabara.

  • 46 MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kusalimia (dk10)

    Mwezeshaji awaongoze WWJ kufanya yafuatayo• Kujitambulisha kwa kutumia wimbo wa jieleze.• Kukaribisha na kusalimiana.• Kukagua usafi wa mavazi na mwili.• Kuimba wimbo wa matunda

    Hadithi (dk10)

    Kode na Kole – Waongoze watoto kusimulia hadithi kwa kutumia igizo dhima.

    Kazi 1(dk30)

    Umahiri: Kujenga mwili, Utambuzi, Kukuza lugha ya Kiswahili na Kuhusiana.

    Vifaa: Penseli, rangi, karatasi, picha za matunda, matunda halisi.

    Shughuli: Wagawe watoto katika makundi waelekeze wachore picha za matunda mbalimbali na kuzipaka rangi.Kisha waelezee picha walizo zichora.

    Ufuatiliaji: Hakikisha watoto wamechora matunda, wamepaka rangi na kueleza juu ya picha walizo chora.

    Kunawa Mikono (dk30) Uji/kucheza - Waongoze watoto kuimba wimbo wa vitendo na wimbo wa

    pili waliofundishwa na babu yao Kode na Koleuliopo katika hadithi hii.

    Siku ya 2

  • 47MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kazi 2 (dk30)

    Umahiri: Kuhusiana, Kuthamini mazingira, Utambuzi, Kukuza lugha ya Kiswahili

    Vifaa: Visu, bakuli, maji, matunda

    Shughuli: Waongoze watoto katika vikundi kufinyanga maumbo ya matunda mbalimbali, na kuyaelezea matunda waliyofinyanga.

    Ufuatiliaji: Fuatilia kama watoto wameweza kufinyanga maumbo ya matunda mbalimbali.

    Kuagana (dk10)

    Mapitio

    • Waulize watoto wamejifunza nini siku ya leo.• Waongoze watoto kuimba wimbo wa matunda.• Wakumbushe watoto watembee kwa uangalifu wanapokuwa njiani.

  • 48 MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kusalimia (dk10)

    Mwezeshaji awaongoze WWJ kufanya yafuatayo:

    • Kukagua afya za watoto.• Kuwaongoza watoto kufanya majadiliano juu umuhimu wa kula

    matunda. • Waelekeze watoto kuimba nyimbo wanazozifahamu.• Kuuliza watoto walichojifunza siku iliyopita.

    Hadithi (dk10)

    Kode na Kole - kusimuia hadithi kwa kutumia njia ya kumwalika mgeni.

    Kazi 1(dk30)

    Umahiri: Kukuza lugha ya Kiswahili, Kujenga mwili, Utambuzi, Kuhusiana.

    Vifaa: Penseli, rangi, karatasi, penseli za rangi

    Shughuli: Kuwaongoza watoto kufanya igizo dhima kuhusu usafi na utunzaji wa mazingira. Kisha wataje na kuchora vifaa vinavyotumika katika kusafisha na kutunza mazingira.

    Ufuatiliaji: Hakikisha kama watoto wameweza kuchora, kupaka rangi na kuelezea picha zao.

    Kunawa Mikono (dk30)

    Uji/ kucheza - Watoto wacheza mchezo wa kutaja mwanzo wa jina la tunda wengine wamalizie kutaja jina la tunda mfano (“Mimi ni tunda jina langu linaanza na E mimi ni nani? Watoto wanajibu –Jina lako ni Embe)

    Siku ya 3

  • 49MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kazi 2 (dk30)

    Umahiri: Kuhusiana, Utambuzi, Kuthamini mazingira na Kuwasiliana kwa lugha ya Kiswahili.

    Vifaa: Matunda, picha mbalimbali za matunda na vitu vinavyopatikana darasani.

    Shughuli: Kwa kutumia igizo dhima waongoze watoto wajifunza tabia ya kupeana vitu na kushirikiana na kucheza kwa pamoja.

    Ufuatiliaji: Chunguza kama watoto wameweza kupeana na kutumia vitu kwa pamoja.

    Kuagana (dk10)

    Mapitio

    • Waulize watoto walichojifunza siku ya leo?• Wakumbushe watoto umuhimu wa kutunza miti katika maeneo yao

    yanayowazunguka.• Waongoze watoto kuimba wimbo wa matunda.• Wakumbushe watoto kuosha matunda kabla ya kula.• Waeleze watoto kuwakumbusha wazazi kuwa siku inayofuata

    watatembelea shule ya Msingi iliyokaribu.• Chagua mtoto mmoja aongoze wimbo wa kuagana.

  • 50 MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kusalimia (dk10)

    Mwezeshaji awaongoze WWJ kufanya yafuatayo:• Kuchagua mtoto mmoja aongoze wimbo wa kusalimiana.• Kukagua usafi wa mwili na mavazi• Kutoa fursa kwa watoto kubadilishana taarifa kuhusu kipindi

    kilichopita• Kuwaongoza watoto kuimba wimbo wa matunda uliomo kwenye

    hadithi hii.• Kuwaeleza kuwa leo tutatembelea shule ya msingi iliyo karibu kwa

    lengo la kujifunza mambo mbalimbali yaliyopo kwenye shule hiyo.Wakiwa katika shule hiyo watafanya yafuatayo:

    i. Kuchunguza mazingira ya ndani ya darasa.ii. Kuchunguza mazingira ya shuleiii. Kuimba na kucheza michezo mbalimbali.

    Kumbuka:• Baada ya ziara hakikisha kuwa watoto wanarudi nyumbani salama.• Waelekeze watoto kusimulia wazazi/walezi mambo waliyojifunza

    katika ziara hii.• Waelekeze watoto wachore picha ya shule waliyoitembelea na

    kuiwasilisha picha hiyo siku ya Jumatatu.

    Siku ya 4

  • 51MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    WIKI YA TISA YA MAFUNZO - HADITHI YA MOTO

    Kusalimia (dk10)

    Mwezeshaji awaongoze WWJ kufanya yafuatayo• Kuwakaribisha watoto katika siku yao ya kwanza. • Kuimba wimbo wa usafi wanaoufahamu.• Kukagua usafi wa mwili na nguo zao.• Kujadiliana na watoto juu ya usafi wa mazingira.

    Hadithi (dk10)

    Moto – Kusoma hadithi ya moto kwa kutumia picha zilizomo ndani ya hadithi

    Kazi 1(dk30)

    Umahiri: Utambuzi na Kuwasiliana kwa lugha ya Kiswahili.

    Vifaa: picha zinazoonesha kazi mbalimbali kama daktari muuguzi, mwalimu, dereva wa gari.

    Shughuli: Waongoze watoto kufanya kazi wawiliwawili, wajieleze wenyewe, wakitaja majina ya wazazi wao na kazi wanazofanya wazazi wao. Kisha katika vikundi waigize kazi hizo. Waulize maswali kama vile, wewe unaitwa nani? Mama yako anaitwa nani? Je wazazi/walezi wako wanafanya kazi gani?

    Ufuatiliaji: Hakikisha watoto wametaja majina yao, ya wazazi wao na kazi za wazazi wao.

    Kunawa Mikono (dk30)

    Uji/ Kucheza - Waongoze watoto kucheza ngoma za asili zenye ujumbe wa kutunza mazingira

    Kumbuka: Wakumbushe watoto juu ya utunzaji wa mazingira.

    Siku ya 1

  • 52 MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kazi 2 (dk30)

    Umahiri: Kuhusiana na Kuwasiliana kwa lugha ya Kiswahili, Utambuzi, Kuthamini mazingra

    Vifaa: Mavazi yanayovaliwa na wahusika tofauti

    Shughuli: watoto waigize mchezo unaonesha faida na hasara za moto. Watoto wavae uhusika wa watu waliotajwa katika hadithi kama vile wakulima, wapishi, watoto, mama, baba.

    Ufuatiliaji: Chunguza kama watoto wameweza kubaini hasara na faida za moto.

    Kuagana (dk10)

    Mapitio

    • Kuwaelekeza watoto kuchukua tahadhari ili kuepuka vitu vinavyoweza kusababisha hatari.

    • Wakumbuke wakirudi nyumbani kuuliza wazazi wao kazi wanzozifanya.

    • Wakumbushe watoto wawasimulie wenzao nyumbani hasara na faida za moto

    • Wakumbushe kulindanana wawe makini wakati wanatembea kurudi nyumbani.

  • 53MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kusalimia (dk10)

    Waongoze WWJ kufanya mambo yafuatayo

    • Kuwaelekeza watoto kuimba wimbo wa usafi wa mazingira.• Kuuliza watoto maswali ya wazi yatakayobainisha taarifa muhimu za

    nyumbani• Waongoze watoto wataje matarajio yao ya baadae watapokuwa

    wakubwa na kumaliza shule

    Hadithi (dk10)

    Moto - Simulia hadithi kwa kuwataka watoto waigize

    Kazi 1(dk30)

    Umahiri: Kuwasilina kwa lugha ya Kiswahili, Kujenga mwili, Utambuzi. Vifaa: Karatasi ngumu, mifuko ya karatasi, magazeti ya zamani, penseli za rangi, viweka rangi, mikasi, gundi ya karatasi, gundi ya maji.

    Shughuli: Waongoze watoto katika vikundi kujadiliana na kuchora picha za vitu hatarishi vinaavyoweza kusababisha moto nyumbani na maeneo ya shuleni.Katika kila kikundi watoto wakubaliana nani atakachora picha gani kisha kila kikundi kuelezea picha walizozichora.

    Ufuatiliaji: Fuatilia kama watoto wameweza kuchora picha za vitu vinavoweza kusababisha moto.

    Kunawa Mikono (dk30) Uji/ Kucheza - Waongoze kutaja michezo mbalimbali wanayoifahamu

    (watataja michezo iliyopo katika jamii wanayoishi) wapeleke watoto uwanjani kucheza michezo ya nje ya hiari chini ya uangalizi wa mtu mzima.

    Siku ya 2

  • 54 MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kazi 2 (dk30)

    Umahiri: Utambuzi, Kujenga mwili

    Vifaa: vichoreo, karatasi, rangi

    Shughuli: Wagawe watoto katika vikundi vidogo kulingana na idadi ya darasa. Waongoze kusimulia hadithi ya moto. Kisha wachore picha za matukio hatarishi wanayoyakumbuka wakizingatia tukio la moto lililotajwa katika hadithi.

    Ufuatiliaji: hakikisha kama watoto wamesimulia hadithi wamechora, wamepaka rangi na kusimulia picha zao.

    Kuagana (dk10)

    Mapitio

    • Kuwauliza watoto walichojifunza siku ya leo.• Tunza picha walizochora watoto kwa ajili ya kumbukumbu na kupima

    maendeleo yao.• Wakumbushe kujiepusha na matukio na vitu hatarishi• Chagua mtoto mmoja aongoze wimbo wa kuagana

  • 55MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kusalimia (dk10)

    Waongoze WWJ kufanya yafuatayo:• Kufanya mazoezi ya viungo yaliyoambatana na wimbo wa kuhesabu

    1 -10• Waulize watoto ikiwa waliona kitu chochote hatarishi njiani. • Jadiliana nao kuhusu taarifa ambazo wanataka kukujulisha.

    Hadithi (dk10)

    Moto – Simulia hadithi kwa mbinu ya kualika mgeni.

    Kazi 1(dk30)

    Umahiri: Utambuzi, Kuthamini mazingira

    Vifaa: Picha ya moto unaoteketeza msitu, karatasi, .

    Shughuli: kujadiliana katika vikundi madhara yanayoweza kusababishwa na upepo mkali. Mfano kuangusha miti, kuezua paa la nyumba na kupeperusha moto.

    Ufuatiliaji: Chunguza kama watoto wameweza kubainisha madhara ya upepo mkali.

    Kunawa Mikono (dk30) Uji/ Kucheza - kucheza mchezo wa Ukuti Ukuti.

    Siku ya 3

  • 56 MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kazi 2 (dk30)

    Vifaa: Mavazi kulingana na igizo, picha zinazoonesha hisia mbalimbali.

    Shughuli: Waongoze watoto kuigiza na kuonyesha hisia zao kama vile kuogopa au kuwa na hasira baada ya kutokea ajali ya moto ukihusisha na hadithi husika. Pia waigize namna watakavyowasaidia wenzao waliopata ajali na kushukuru baada ya kusaidia.

    Ufuatiliaji: chunguza kama watoto wameonesha hisia na kutoa huduma kwa wale waliopata ajali?

    Kuagana (dk10)

    Mapitio

    • Kuwauliza watoto wamejifunza nini siku ya leo• Wahimize watoto kutoa msaada kwa watu wanaopata ajali na

    kushukuru pale wanaposaidiwa.. • Wasiliana na wazazi kama kuna ujumbe wowote unaotaka kufikisha

    kwao. • Fuatilia na hakikisha watoto wamefika nyumbani salama.

  • 57MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kusalimia (dk10)

    Waongoze WWJ kufanya yafuatayo:

    • Kusafisha mazingira yao ya darasani nje na ndani• Waelekeze watoto kushirikishana kwenye zamu za usafi wa asubuhi.

    Hadithi (dk10)

    Moto – wasimulie hadithi kwa kutumia picha.

    Kazi 1(dk30)

    Umahiri: Kuthamini mazingira, kuhusiana na utambuzi.

    Vifaa: Katratasi ngumu, penseli, rangi, gundi.

    Shughuli: Waongoze watoto kuchora picha za hali ya hewa tofauti tafouti mfano mvua, jua, upepo. Waongoze watoto kubandika picha za hali ya hewa walizochora kwenye karatasi ngumu na ukutani na kuzielezea. Kisha wapeleke watoto nje wataje hali ya hewa iliyopo kwa wakati huo.

    Ufuatiliaji: Chunguza kama watoto wameweza kubaini hali za hewa tofauti.

    Kunawa Mikono (dk30) Uji/ Kucheza - Waongoze watoto kucheza michezo ya asili wanayoipenda.

    (michezo inayopatikana katika jamii yao)

    Siku ya 4

  • 58 MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kazi 2 (dk30)

    Umahiri: Kuhusiana. Kuthamini mazingira

    Vifaa: Vitu vinavyopatikana nyumbani na maeneo ya maigizo

    Shughuli: Waongoze watoto kuigiza matendo mbalimbali ya nyumbani bila kuzingatia jinsi zao. Mfano kusafisha nyumba, kupanda maua, kuosha vyombo na kufagia.

    Kumbuka: wakati wa kugawa matendo ya uigizaji usibague kati ya wasichana na wavulana, shughuli zifanye kwa usawa bila kubagua jinsi zao.

    Ufuatiliaji: Chunguza kama watoto wameweza kufanya kazi bila ya kujali jinsi zao.

    Kuagana (dk10)

    Mapitio

    • Waulize watoto leo wamejifunza nini?• Kuimba wimbo wa hali ya hewa mfano nani kaona upepo?• Waulize watoto kama kesho watakuja shule au hawaji? Chunguza

    majibu yao na utoe ufafanuzi.• Kuwaongoza watoto kuimba wimbo wakuagana.

  • 59MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    WIKI YA KUMI YA MAFUNZO - HADITHI YA YANGE YANGE

    Kusalimia (dk10)

    Mwezeshaji awaongoze WWJ kufanya yafuatayo• Kuwasalimia watoto na kuwataka wataje siku ya leo• Kuimba wimbo unaohusu rangi.• Kuwataka watoto waeleze mambo mbalimbali yaliyotokea mwishoni

    mwa wiki iliyopita.• Kuwataka watoto wataje madhara ya uchaf• Wakumbushe hadithi ya wiki iliyopita ya Moto na watambulishe

    hadithi ya wiki hii ya Yange yange.

    Hadithi (dk10)

    Soma kwa sauti hadithi ya yange yange kwa kutumia vikaragosi, wakati wa kusoma, watoto waigize sauti za ndege wanaotajwa

    Kazi 1(dk30)

    Umahiri: Kuhusiana, Utambuzi, Kuwasiliana kwa lugha ya kiswahili.

    Vifaa: Picha za ndege na wadudu na kadi za herufi.

    Shughuli: Wagawe watoto katika makundi madogo dogo kulingana na idadi yao. Waongoze watoto wataje majina ya ndege na wadudu waliomo kwenye hadithi, ndege na wadudu wengine wanaowafahamu. Kisha wabaini sauti za ndege na wadudu waliomo katika hadithi.

    Ufuatiliaji: Chunguza kama watoto wameweza kuainisha majina ya ndege na wadudu, milio ya ndege na wadudu.

    Kunawa Mikono (dk30)

    Uji/ Kucheza - Waongoze watoto kucheza michezo ya kuruka kama ndege huku wakiimba nyimbo sisi ndege twaruka….au Mabata

    Siku ya 1

  • 60 MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kazi 2 (dk30)

    Umahiri: Kujenga Mwili,

    Vifaa: kadi za rangi, na vitu vya rangi mbali mbali, rangi

    Shughuli: Wagawe watoto katika vikundi na waongoze kubaini rangi zilizotajwa katika hadithi ya yangeyange. Kisha kulinganisha rangi za ndege na wadudu waliotajwa katika hadithi na wadudu/ndege wengine wanaowafahamu. Kisha waulize watoto kama wamewahi kuziona rangi hizo katika mazingira yao ya kila siku.

    Ufuatiliaji: kuchunguza kama watoto wameweza kutaja majina ya ndege na wadudu na kutofautisha Rangi za wadudu na ndege mbalimbali.

    Kuagana (dk10)

    Mapitio

    • Wakumbushe watoto kubaini rangi mbali mbali wakiwa njiani• Kuwauliza kama wapo wanaomjua kinyonga na sifa zake.• Kuimba wimbo uliomo kwenye hadithi na kuwaaga watoto.

  • 61MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kusalimia (dk10)

    Mwezeshaji awaongoze WWJ kufanya yafuatayo:

    • Kuimba wimbo wa kusalimiana• Kukagua afya za watoto • Kuwaelekeze watoto kuimba wimbo kuhusu hadithi ya Yangeyange.• Kuuliza rangi walizoziona wakiwa njiani.

    Hadithi (dk10)

    Yangeyange – Soma hadithi kwa sauti kwa kutumia picha zilizomo kwenye hadithi.

    Kazi 1(dk30)

    Umahiri: Kuwasiliana kwa lugha ya Kiswahili,Utambuzi, kujenga mwili

    Vifaa: Vihesabio

    Shughuli: Wagawe watoto katika makundi, wagawie vihesabio vya kutosha, waongoze watoto kufanya matendo ya hisabati ya kuongeza na kupunguza (idadi ya vitu isiyozidi 10) kwa njia ya mchezo. Elekeza kufanya matendo ya kuongeza kwanza, kisha wafanye matendo ya kupunguza, pita katika kila kundi kuangalia ushiriki wa kila mtoto na kutoa msaada.

    Ufuatiliaji: Chunguza watoto kama wameweza kuongeza na kupunguza idadi ya vitu isiyozidi kumi

    Kunawa Mikono (dk30) Uji/ Kucheza - Kuwaongoza watoto kucheza mchezo wa kujenga

    ushirikiano. Mfano: mchezo wa Ukuti ukuti au michezo mingine wanayoipenda.

    Siku ya 2

  • 62 MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kazi 2 (dk30)

    Umahiri: Utambuzi, Kuthamini Mazingira na Kuwasiliana kwa lugha ya Kiswahili.

    Vifaa: Picha ya Tausi na Yangeyange, udongo wa mfinyanzi, maji, beseni na boksi.

    Shughuli: Waongoze watoto katika vikundi kubaini picha za ndege wawili ambao ni tausi na yangeyange na kueleza ufanano na tofauti zao.

    Waongoze watoto wafinyange maumbo ya ndege wanaowafahamu na kisha wabadilishane ndege waliofinyanga na wenzao, wape fursa kila mmoja aelezee ndege wa mwenzake.

    Ufuatiliaji: Chunguza kama watoto wameweza kubaini tofauti na ufanano wa ndege hao na kufinyanga ndege. Vilevile hakikisha kama kila mtoto ameweza kuelezea ndege wa mwenzake.

    Kuagana (dk10)

    Mapitio

    • Wakumbushe watoto kutambua vitu vyenye maumbo tofauti kama unene wembamba ,urefu na upana.

    • Shiriki na watoto kuimba wimbo wa Kuagana watakaoupendekeza.

  • 63MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kusalimia (dk10)

    Mwezeshaji awaongoze WWJ kufanya yafuatayo:• Kukaribishana na kusalimiana • Kutaja sikuya leo• Kuwauliza mambo waliyojifunza siku iliyopita.• Waulize watoto juu ya rangi mbali walizoziona wakiwa njiani. • Kutaja ndege au wadudu waliowaona wakiwa njiani

    Hadithi (dk10)

    Yange yange – Soma kwa sauti hadithi ya ‘yange yange’ na wahamasishe watoto kuigiza wahusika kwenye hadithi (yange yange, tausi)

    Kazi 1(dk30)

    Umahiri: Kuwasilina kwa lugha ya Kiswahili, kuhusiana, Ukuaji wa mwili na Utambuzi.

    Vifaa: Karatasi ngumu, rangi, maboksi, kalamu, penseli

    Shughuli: Kwa kutumia vikaragosi waongoze watoto waruke juu na chini, kupepea mikono, kutembea kama tausi huku wakijieleza “mimi tausi, natembea kwa maringo…” Kisha waulize watoto ni nani anayefuga ndege nyumbani kwao. Wasaidie watoto kutoa majibu sahihi

    Ufuatiliaji: Wakumbushe watoto kuchunguza wadudu na ndege mbali mbali wanaopatikana katika mazingira yao.

    Kunawa Mikono (dk30) Uji/ Kucheza - shiriki pamoja na watoto kucheza ngoma za asili kulingana

    na mazingira, tumia vifaa vya muziki vinavyopatikana katika mazingira na tamaduni zao.

    Siku ya 3

  • 64 MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kazi 2 (dk30)

    Umahiri: Kuwasiliana kwa lugha ya Kiswahili.

    Vifaa: Karatasi, viweka alama na penseli, mavazi ya maigizo na vikaragosi

    Shughuli: Kuwaongoza watoto kufanya igizo dhima wakiwa wamevaa uhusika wa ndege na wadudu waliomo kwenye hadithi.

    Ufuatiliaji: Chunguza kama watoto wameweza kuigiza kwa kuuvaa uhusika wa ndege na wadudu.

    Kuagana (dk10)

    Mapitio

    • Kuwahamisisha watoto kuzingatia usafi wa mwili, mavazi na mazingira ukilinganisha na hadithi ya yange yange.

    • Kuhimiza kuwa na upendo na kupenda kusaidiana ukihusisha na hadithi ya yange yange.

    • Kuchagua watoto wawili waongoze wimbo wakuagana.

  • 65MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kusalimia (dk10)

    Mwezeshaji awaongoze WWJ kufanya yafuatayo:

    • Kukaribisha watoto na kusalimiana.• Kujadiliana wawiliwawili jinsi wanavyosaidiana na wenzao wakiwa

    nyumbani. • Kushiriki na watoto katika kuimba wimbo wa kusaidiana.

    Hadithi (dk10)

    Yange yange – Watoto wasimulie hadithi kwa kutumia picha zilizomo kwenye hadithi

    Kazi 1(dk30)

    Umahiri: Kuhusiana na Kujenga mwili.

    Vifaa: Karatasi ngumu, maboksi, kalamu, penseli, rangi na vitu halisi.

    Shughuli: Kuwaongoza watoto kuchora na kutengeneza vikaragosi vya ndege na wadudu. Kisha waigize namna ndege hao wanvyoruka, kutembea na kuigiza milio yao.

    Ufuatiliaji: Fuatilia kama watoto wameweza kuchora na kukata vikaragosi na baadae kuigiza tabia za ndege na wadudu.

    Kunawa Mikono (dk30) Uji/ Kucheza - Waongoze watoto katika makundi kucheza mchezo wa

    Mdako au Dama na michezo mingine wanayoipenda

    Siku ya 4

  • 66 MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kazi 2 (dk30)

    Umahiri: Kuthamini Mazingira, Utambuzi, Kuwasiliana kwa lugha ya Kiswahili.

    Vifaa: Vikaragosi vya ndege na wadudu.

    Shughuli: Kuwaelekeza watoto kutoka nje ya darasa, wasimamie wakusanye maua ya rangi mbali mbali na kutaja rangi za maua hayo. Walinganishe rangi za maua na rangi za picha zilizomo kwenye hadithi.

    Ufuatiliaji: Chunguza kama watoto wameweza kukusanya na kutaja rangi za maua na kulinganisha na rangi za picha zilizopo katika hadithi.

    Kuagana (dk10)

    Mapitio

    • Kuwaongoza watoto kukumbuka walichojifunza siku ya leo.• Kukumbusha watoto kutaja jina la shule ya msingi waliyoitembelea • Kukumbusha watoto kutembea kwa usalama wakati wa kurudi

    nyumbani.• Kuwaongoza watoto kuagana na kuwatakia mapumziko mema ya

    mwisho wa juma kwa kuimba wimbo.

  • 67MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    WIKI YA KUMI NA MOJA YA MAFUNZOHADITHI YA NANI MSHINDI WA REDE?

    Kusalimia (dk10)

    Mwezeshaji awaongoze WWJ kufanya yafuatayo• Kukaribishana na kusalimiana.• Kujadiliana wawili wawili juu ya matukio yaliyotokea walipokuwa

    katika siku za mapumziko, kisha washirikishane. • Kuwauliza watoto kama wamewahi kusikia neno “walemavu” Kisha

    jadiliana nao juu ya uelewa wao kuhusiana na neno ulemavu

    Hadithi (dk10)

    Nani mshindi wa rede? – soma kwa sauti na kuonyesha picha zilizopo katika hadithi

    Kazi 1(dk30)

    Umahiri: Utambuzi, Kuhusiana, Kuwasiliana kwa Lugha ya Kiswahili na Kujenga mwili.

    Vifaa: picha zinazoonyesha watoto wakicheza michezo mbalimbali, mpira.

    Shughuli: Kuwagawa watoto katika makundi kisha wajadiliane juu ya nini walichojifunza kuhusiana na hadithi hiyo. Waongoze kwa kuwapa maswali elekezi, mfano: nani aliyeshinda mchezo wa rede?, Kwa nini watoto walikataa kucheza rede na Doto? Hadithi hii inatufundisha nini?

    Ufuatiliaji: Chunguza kama watoto wameweza kujadilana mambo yaliyomo katika hadithi. (Ulemavu, ushirikiano, idadi ya vitu/watu)

    Kunawa Mikono (dk30) Uji/ Kucheza - Kuwaongoza watoto kucheza mchezo wa rede na michezo

    mingine wanayoipenda.

    Siku ya 1

  • 68 MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kazi 2 (dk30)

    Umahiri: Utambuzi, Kuwasiliana kwa lugha ya Kiswahili, Kuthamini Mazingira, Kuhusiana.

    Vifaa: Mavazi kulingana na wahusika.

    Shughuli: Kuwaongoza watoto kufanya igizo na kuonyesha matendo mengine yanayofanywa na walemavu wa aina mbalimbali kama yanavyofanywa na watu wasio na ulemavu. Kwa mfano; kundi la kwanza mtoto aigize anatembea akiwa na fimbo nyeupe anaelekea darasani kujifunza, anakaa kwenye nafasi yake anajifunza sawa na wenzake.

    Kundi la pili, mtoto mwngine aigize kama kiziwi yupo nje anapiga ngoma na kuimba.

    Kundi la tatu, mtoto mwengine na gongo lake anacheza mpira kwa kutumia gongo na mguu wake mmoja.

    Kumbuka: Walemavu wote wanauwezo wa kufanya kazi mbalimbali bila ya kujali ulemavu walionao. Isipokuwa wanahitaji upendo na kuthaminiwa kama watu wengine.

    Ufuatiliaji: Chunguza kama watoto wameweza kuigiza matendo yanayofanywa na watu wenye ulememvu wa aina mbali mbali.

    Kuagana (dk10)

    Mapitio

    • Kuwaongoza watoto waeleze walichojifunza siku ya leo.• Kusisitiza kuwapenda, kuwathamini, kuwasaidia na kuwajali watu

    wenye ulemavu.• Kuchagua mtoto aongoze wimbo wa kuagana.

  • 69MPANGO WA KUMUANDAA MTOTO KUWA TAYARI KUANZA SHULE

    Kusalimia (dk10)

    Mwezeshaji awaongoze WWJ kufanya yafuatayo:

    • Kukaribishana na kusalimiana.• Kutoa fursa kwa watoto