3
HakiElimu ni asasi isiyo ya kiserikali ambayo dira yake inalenga kufikia usawa, ubora, haki na demokrasia katika elimu na jamii. HakiElimu inawasaidia wananchi kujua haki na wajibu wao kwa kuwapa taarifa mbalimbali ili waweze kuchangia kuboresha elimu. Mojawapo ya nyenzo kuu zinazotumika kufanikisha ushiriki wa wananchi katika maamuzi yanayolenga kuboresha elimu na demokrasia ni “Harakati za Marafiki wa Elimu”. Hizi ni harakati za wananchi, mashirika na taasisi zenye nia na ari ya kuharakisha maendeleo ya elimu na demokrasia nchini. Harakati hizi zilianzishwa mwaka 2003 zikiwaunganisha pamoja wananchi wanaopenda maendeleo ya elimu. Ni fursa kwa wananchi kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala yanayohusu elimu na demokrasia. Ushiriki huu wa Marafiki wa Elimu katika mikakati ya kuboresha elimu na demokrasia unachagiza ushawishi mkubwa kwa serikali juu ya mwelekeo wa elimu Tanzania. Harakati za Marafiki wa Elimu mpaka sasa zina wanachama takribani 32,000 nchini kote. Marafiki hawa wanashiriki kwa namna mbalimbali shughuli za kuboresha elimu na demokrasia. Chapisho hili ni nafasi nyingine ya kujifunza mambo yanayoendelea katika harakati. Linalenga kumuongezea Rafiki na wadau wengine wa elimu mbinu bora zinazotumiwa na baadhi ya Marafiki kukuza ushiriki wa mwananchi katika shughuli za maendeleo hususani katika sekta ya elimu. Hizi ni harakati zetu wote. Kwa atakayesoma chapisho hili, tunamwacha na changamoto ya kutoa mwanga, kuihamasisha jamii kujiunga na harakati hizi. Asanteni na karibuni! Toleo la Pili, Julai - Decemba 2009 Marafiki wa Elimu watembelewa na wageni kutoka Afrika Kusini. Equal Education ni shirika lisilo la kiserikali linalofanya kazi katika mji wa Cape Town nchini Afrika ya Kusini. Shirika hili linaundwa na wanaharakati ambao ni wanafunzi, wazazi, walimu na wanajamii wenye nia ya kuimarisha ubora na usawa katika elimu nchini mwao. Mwezi Septemba mwaka 2009, wawakilishi wa shirika hili walitembelea ofisi za HakiElimu ili kujifunza shughuli za shirika hili ikiwemo Harakati za Marafiki wa Elimu. Katika kujifunza juu ya Harakati hizi, wageni walitembelea kikundi cha Marafiki wa Elimu cha MWAWODE kilichopo Mwananyamala mjini Dar es Salaam kinachoundwa na kina mama wapatao 60. Kikundi hiki kinajishughulisha na miradi ya kuinua kipato cha wanachama, na pia kuhamasisha umuhimu wa elimu kupitia machapisho na mijadala ya wazi. Kinatoa pia huduma kwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi ikiwemo kuwatetea kupata elimu bila kubaguliwa. Wakiwa MWAWODE, wageni walijifunza namna kikundi hiki kinavyo hamasisha baadhi ya wanachama wake na wananchi waliokosa elimu kujiunga na darasa la MEMKWA, na pia mbinu za kufuatilia matumizi ya fedha za Umma maarufu kama PETS kwenye shule za msingi na sekondari wilayani Kinondoni. Vilevile walijifunza namna kikundi kilivyofanikiwa kushawishi watu 160 kujiunga na Harakati za Marafiki wa Elimu. Ziara hii inatoa changamoto kwa vikundi vingine vya Marafiki wa Elimu kujibidisha katika shughuli zao. Mkutano wa kitaifa wa Marafiki wa Elimu wafanyika Morogoro Kati ya tarehe 12 hadi 14 Oktoba 2009, wawakilishi wa Marafiki wa Elimu wapatao 50 kutoka mikoa mbalimbali Tanzania Bara walikutana katika ukumbi wa Amabilis Centre (Mgolole Sisters), mjini Morogoro kwa ajili ya mkutano wao wa mwaka. Mkutano huu ni mojawapo ya mikakati ya makusudi ya kuimarisha uelewa na ushiriki wa wananchi katika shughuli za kuboresha elimu na demokrasia nchini. Mkutano huu unafuatia mikutano mingine ya Marafiki iliyofanyika mkoani Kigoma, Rukwa, Manyara na Lindi, kwa lengo la kutoa nafasi kwa Marafiki kubadilishana uzoefu, kufahamiana na kuimarisha mtandao wa Marafiki kutoka ngazi ya chini mpaka kitaifa. Mkutano huu ulitumika pia kuwajengea uwezo washiriki kwa kuwapa stadi za kufuatilia utekelezaji wa Ahadi za Serikali na Sera ya Elimu kwa ujumla. Marafiki hawa ni waraghbishi wa Harakati hizi katika maeneo wanayotoka. Wanasaidia kuimarisha ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo ya elimu na demokrasia kwa kuwahamasisha wananchi kuchangia nguvu zao na kushiriki kikamilifu kufuatilia utekelezaji wa sera ndani ya jamii zao. Kwa kutambua umuhimu wa ushiriki wao, Marafiki hawa wameahidi kuendeleza juhudi na ubunifu walioanzisha kwenye jamii zao kama vile huduma za maktaba za jamii na mijadala ya wazi ili kupigania mabadiliko chanya. Je wewe unafanya nini? Tafadhali tafakari na chukua hatua kujiunga na Harakati hizi za watu wanaopenda maendeleo ya elimu nchini. Pichani Washiriki wakikamilisha kazi ya kikundi

Toleo la Pili, Julai - Decemba 2009 - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/document164rafiki_elimu_2.pdfhuu ulitumika pia kuwajengea uwezo washiriki kwa kuwapa stadi za kufuatilia

  • Upload
    others

  • View
    10

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

HakiElimu ni asasi isiyo ya kiserikali ambayo dira yake inalenga kufi kia usawa, ubora, haki na demokrasia katika elimu na jamii. HakiElimu inawasaidia wananchi kujua haki na wajibu wao kwa kuwapa taarifa mbalimbali ili waweze kuchangia kuboresha elimu.

Mojawapo ya nyenzo kuu zinazotumika kufanikisha ushiriki wa wananchi katika maamuzi yanayolenga kuboresha elimu na demokrasia ni “Harakati za Marafi ki wa Elimu”. Hizi ni harakati za wananchi, mashirika na taasisi zenye nia na ari ya kuharakisha maendeleo ya elimu na demokrasia nchini. Harakati hizi zilianzishwa mwaka 2003 zikiwaunganisha pamoja wananchi wanaopenda maendeleo ya elimu. Ni fursa kwa wananchi kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala yanayohusu elimu na demokrasia. Ushiriki huu wa Marafi ki wa Elimu katika mikakati ya kuboresha elimu na demokrasia unachagiza ushawishi mkubwa kwa serikali juu ya mwelekeo wa elimu Tanzania.

Harakati za Marafi ki wa Elimu mpaka sasa zina wanachama takribani 32,000 nchini kote. Marafi ki hawa wanashiriki kwa namna mbalimbali shughuli za kuboresha elimu na demokrasia. Chapisho hili ni nafasi nyingine ya kujifunza mambo yanayoendelea katika harakati. Linalenga kumuongezea Rafi ki na wadau wengine wa elimu mbinu bora zinazotumiwa na baadhi ya Marafi ki kukuza ushiriki wa mwananchi katika shughuli za maendeleo hususani katika sekta ya elimu.

Hizi ni harakati zetu wote. Kwa atakayesoma chapisho hili, tunamwacha na changamoto ya kutoa mwanga, kuihamasisha jamii kujiunga na harakati hizi.

Asanteni na karibuni!

Toleo la Pili, Julai - Decemba 2009

Marafi ki wa Elimu watembelewa na wageni kutoka Afrika Kusini.Equal Education ni shirika lisilo la kiserikali linalofanya kazi katika mji wa Cape Town nchini Afrika ya Kusini. Shirika hili linaundwa na wanaharakati ambao ni wanafunzi, wazazi, walimu na wanajamii wenye nia ya kuimarisha ubora na usawa katika elimu nchini mwao.

Mwezi Septemba mwaka 2009, wawakilishi wa shirika hili walitembelea ofi si za HakiElimu ili kujifunza shughuli za shirika hili ikiwemo Harakati za Marafi ki wa Elimu. Katika kujifunza juu ya Harakati hizi, wageni walitembelea kikundi cha Marafi ki wa Elimu cha MWAWODE kilichopo Mwananyamala mjini Dar es Salaam kinachoundwa na kina mama wapatao 60. Kikundi hiki kinajishughulisha na miradi ya kuinua kipato cha wanachama, na pia kuhamasisha umuhimu wa elimu kupitia machapisho na mijadala ya wazi. Kinatoa pia huduma kwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi ikiwemo kuwatetea kupata elimu bila kubaguliwa.

Wakiwa MWAWODE, wageni walijifunza namna kikundi hiki kinavyo hamasisha baadhi ya wanachama wake na wananchi waliokosa elimu kujiunga na darasa la MEMKWA, na pia mbinu za kufuatilia matumizi ya fedha za Umma maarufu kama PETS kwenye shule za msingi na sekondari wilayani Kinondoni. Vilevile walijifunza namna kikundi kilivyofanikiwa kushawishi watu 160 kujiunga na Harakati za Marafi ki wa Elimu.

Ziara hii inatoa changamoto kwa vikundi vingine vya Marafi ki wa Elimu kujibidisha katika shughuli zao.

Mkutano wa kitaifa wa Marafi ki wa Elimu wafanyika MorogoroKati ya tarehe 12 hadi 14 Oktoba 2009, wawakilishi wa Marafi ki wa Elimu wapatao 50 kutoka mikoa mbalimbali Tanzania Bara walikutana katika ukumbi wa Amabilis Centre (Mgolole Sisters), mjini Morogoro kwa ajili ya mkutano wao wa mwaka. Mkutano huu ni mojawapo ya mikakati ya makusudi ya kuimarisha uelewa na ushiriki wa wananchi katika shughuli za kuboresha elimu na demokrasia nchini. Mkutano huu unafuatia mikutano mingine ya Marafi ki iliyofanyika mkoani Kigoma, Rukwa, Manyara na Lindi, kwa lengo la kutoa nafasi kwa Marafi ki kubadilishana uzoefu, kufahamiana na kuimarisha mtandao wa Marafi ki kutoka ngazi ya chini mpaka kitaifa. Mkutano huu ulitumika pia kuwajengea uwezo washiriki kwa kuwapa stadi za kufuatilia utekelezaji wa Ahadi za Serikali na Sera ya Elimu kwa ujumla.

Marafi ki hawa ni waraghbishi wa Harakati hizi katika maeneo wanayotoka. Wanasaidia kuimarisha ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo ya elimu na demokrasia kwa kuwahamasisha wananchi kuchangia nguvu zao na kushiriki kikamilifu kufuatilia utekelezaji wa sera ndani ya jamii zao. Kwa kutambua umuhimu wa ushiriki wao, Marafi ki hawa wameahidi kuendeleza juhudi na ubunifu

walioanzisha kwenye jamii zao kama vile huduma za maktaba za jamii na mijadala ya wazi ili kupigania mabadiliko chanya. Je wewe unafanya nini? Tafadhali tafakari na chukua hatua kujiunga na Harakati hizi za watu wanaopenda maendeleo ya elimu nchini.

Pichani Washiriki wakikamilisha kazi ya kikundi

Marafi ki wa Elimu wafanya mikutano kupitia simu za mkononiKufanya mkutano kupitia simu ni jambo ambalo halijazoeleka sana katika jamii yetu ya kitanzania. Ni kitu ambacho kimeibuka hivi karibuni kutokana na maendeleo ya teknolojia. Baadhi ya Marafi ki wa Elimu wa Kanda ya Ziwa wamekuwa wa mwanzo kabisa kuweza kuendesha mikutano kwa njia hii.

“Imeturahisishia kupanga mikakati kwa pamoja, kubadilishana uzoefu na kupeana taarifa mbalimbali zihusuzo maendeleo ya Harakati ndani ya maeneo yetu. Ni fursa nzuri ya kujifunza wenzako wanafanya nini ndani ya harakati” Anasema Rafi ki wa Elimu Juma Kalwani ambaye ni mmojawapo wa waanzilishi wa mtandao huu.

Kwa kawaida wanamtandao huu huteua mmoja wao, ambaye hutumia simu yake kuwaunganisha wengine kupitia huduma za promosheni za makampuni ya simu hapa nchini ambazo huwapa wateja wake ofa ya kupiga simu kwa kiasi kidogo cha pesa kwa siku nzima. Mpaka sasa wameshafanya mikutano mitano (5) kupitia njia hii, ambayo ni rahisi na ya gharama nafuu na hivyo kuwapunguzia Marafi ki gharama za kukutana ana kwa ana. Kwa kutumia njia hii mshikamano baina yao umeongezeka na kufanya wigo wa shughuli zao kuwa mpana zaidi. Hii inatoa hamasa na changamoto kwa Marafi ki wengine kujifunza kutoka kwenye kundi hili.

Sauti ya Marafiki yahamasisha mabadiliko katika jamii Nampisi ni kijiji katika wilaya ya Ukerewe, Mkoani Mwanza. Ni mojawapo ya vijiji vilivyovunjwa mnamo mwaka 1974 kufuatia tamko la serikali la kuunda vijiji vya ujamaa nchini. Wanakijiji walilazimika kuhama makazi yao kwenda kuishi kwenye maeneo mapya ya vijiji vya ujamaa. Hata hivyo baada ya kutofanikiwa kwa vijiji vya ujamaa katika baadhi ya maeneo, wakazi wa Nampisi waliamua kurudi katika makazi yao ya zamani kuendeleza

mashamba na makazi yao.

Hata hivyo tangu kurudi katika maeneo yao haya, wakazi wa Nampisi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa baadhi ya mahitaji muhimu ya kijamii mfano shule, zahanati, na barabara. kutokuwepo kwa shule kunalazimisha watoto kutembea umbali mrefu kwenda ziliko shule vijiji vya jirani.Hali hii inaathiri maendeleo ya watoto kitaaluma. Wakati wa kipindi cha mvua watoto wenye umri chini ya miaka 7 hushindwa kuvuka mto uliopo kijijini hapo kwenda shule.

Msaho Mtaki ni kiongozi wa kikundi cha Marafi ki wa Elimu kijijini Nampisi. Kwa kutambua mapungufu yaliyopo, yeye na kikundi chake cha Marafi ki wapatao 30 kwa kutumia mijadala ya wazi na kukutana na viongozi wao wa Kata na Wilaya wamefanikiwa kuwashawishi wanajamii wa Nampisi na viongozi kufi kiria kuanzisha shule yao ya msingi. Katika kuonyesha nia, Marafi ki hawa wameweza kuanzisha darasa la awali lenye watoto zaidi ya 40. Wamefungua pia maktaba ya jamii ili kuhamasisha wananchi kujenga tabia ya kujisomea na kupenda elimu. Kutokana na kukubaliwa kwa ombi lao la kujenga shule na uongozi wa wilaya, sasa wanajipanga kufanikisha ujenzi huu.

Toka kuanzishwa kwa Harakati za Marafi ki wa Elimu mwaka 2003, HakiElimu imekuwa ikiwahamasisha Marafi ki kujiunga pamoja na kuchukua hatua kwa ajili ya kuboresha elimu na demokrasia. Wito huu umeitikiwa vizuri na baadhi ya Marafi ki, vikundi vingi vimeanzishwa kuimarisha juhudi za harakati. Mojawapo ya vikundi hivi ni Kikundi cha Marafi ki wa Elimu cha Mvumi, ambacho kipo kata ya Msowelo, Tarafa ya Mvumi, Wilaya ya Kilosa. Kikundi hiki kilianzishwa rasmi tarehe 27 Machi 2007, kikiwa na wanachama 23. Hadi kufi kia sasa kikundi kina wanachama 81.

Kikundi hiki kwa kutumia uhamasishaji na kwa kushirikiana na uongozi wa shule zilizopo katika eneo lao, kimefanikiwa kwa kiasi kikubwa kusaidia kupunguza tatizo sugu la utoro wa wanafunzi katika shule nyingi za Mvumi. Wanakikundi hutembelea shule na kuainisha majina ya wanafunzi watoro na kisha kuanza kuwafuatilia mmoja mmoja kujua tatizo, kuwashauri na kuwahamasisha kurudi shuleni. Sambamba na suala hili kikundi kinatoa elimu dhidi ya ukimwi, mimba kwa watoto wa shule, madawa ya kulevya na mambo mengine yanayokwamisha maendeleo ya elimu.

Kikundi kina maktaba ya jamii ambayo wanachama, wananchi na wanafunzi huitumia kupata taarifa na kujifunza mambo mbalimbali yakiwemo ya kitaaluma. Wanachama wa kikundi wanasema, “Nguvu ya kikundi inatokana na mahusiano mazuri ya kikazi na wananchi, viongozi wa shule na serikali za vijiji”. Kutokana na msingi huu, kikundi hiki kinatambulika kuanzia ngazi ya kijiji, hadi wilaya. Hii imesaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha Harakati kwa sababu imefi kia hatua watendaji wa Vijiji, Kata na Tarafa wanawashirikisha Marafi ki na kuwapatia nakala za taarifa mbalimbali za maendeleo. Hii inadhihirisha kuwa Marafi ki wanapokuwa katika kikundi ni rahisi kufanikiwa kuliko kuwa mtu mmoja mmoja.

Kikundi hiki kimeweza kujitengenezea vitambulisho kama njia ya kuwafanya wao watambulike na jamii yao. Hawakuishia hapo bali pia wamejitengezea fulana kama sare ambazo zimeandikwa Marafi ki wa Elimu Mvumi.

Ufuatiliaji wa Uwajibikaji wa kijamii waibua mengiMipango mibovu, mgawanyo mbaya wa rasilimali, usimamizi mbovu wa baadhi ya miradi, kutowajibika vizuri kwa baadhi ya watendaji, matumizi mabaya ya rasilimali na ufi sadi ni miongoni mwa mambo yaliyogunduliwa na Marafi ki wa Elimu katika zoezi la kufuatilia uwajibikaji wa kijamii uliofanyika katika wilaya za Ukerewe and Magu kati ya mwezi wa sita na wa saba ya mwaka huu.

Mojawapo ya ugunduzi wa Marafi ki wa Elimu wilayani Ukerewe ilikuwa ni pamoja na matumizi ya stakabadhi zisizo rasmi katika kukusanya ushuru na michango mbalimbali toka kwa wananchi unaofanywa na baadhi ya watendaji wa kata na vijiji. Wilayani Magu Marafi ki hawakuridhishwa na wasimamizi katika ujenzi wa jengo la Shule ya Msingi Fogofogo ambapo wajenzi/wasimamizi walidiriki kuweka nondo moja kwenye renta iliyopelekea jengo kuanguka kabla hata ya kumalizika kwa ujenzi. Pia Marafiki walishangazwa na bajeti ya halmashauri ya wilaya Ukerewe ambapo kulitengwa bajeti ya kujenga nyumba tano za walimu kwa gharama kubwa ya shilingi 450,000,000/- yaani milioni 90 kwa kila nyumba.

Haya ni baadhi tu ya mambo yaliyopatikana kutokana na zoezi lililofanywa na Marafi ki la kufuatilia uwajibikaji wa kijamii kwa kushirikiana na wadau wengine wa elimu wilayani Ukerewe na Magu. Huu ni mwanzo mzuri katika kuimarisha demokrasia, uwajibikaji ndani ya jamii, na dhana nzima ya utawala bora.

Usikubali ZawadiNa Alphonce L. KanaganwaKwa magoma na pambio, hututeka masikio,Gazetini sura zao, huwekwa kila toleo,Huongeza vichocheo, kusema wao chaguo,Usikubali zawadi, ukatoa yako kura.

Chaguliwa lengo lao, wawakilishe wenzao,Wapandishwe navyo vyeo,tuuone mwelekeo,Tusubiri matokeo, tungoje mwelekeo,Usikubali zawadi, ukatoa yako kura.

Kisha wapa kura zao. tunaona mambo yao,Hututupa kwa kombeo, husahau ndo pitio,Watufanya kingilio, cha yao maendeleo,Usikubali zawadi, ukatoa yako kura.

Hula ambavyo ni vyao, na kunywa yetu mafao,Hakika huwa tishio, hatuoni kimbilio,Twataka mafanikio, tufurahie mazao,Usikubali zawadi, ukatoa yako kura.

Mwalimu BoraNa Jadidi MjadiliHakiElimu njooni, njooni nitawambia,Mwalimu bora ni nani, swali mloulizia,Nawaondoa shidani, majibu kuwapatia,Hujiandaa mapema, mwalimu aliyebora.

Mwenye kufata kanuni, si somo kulipapia,Huwatoa mashakani, wanafunzi wenye nia,Kusoma wakatamani, udadisi kuwajia,Hutunza muda vizuri, mwalimu aliyebora.

Mwaminifu si muhuni, achukiaye kadhia,Mwenye kupenda maoni, bila hata kuchukia,Huamsha darasani, ari mijadala pia,Hana ubabaishaji, Mwalimu aliyebora.

Ana huruma na soni, upendo kwake ni njia,Ukali kwake si shani, bali diplomasia,Ajuaye ana deni, kwa Dira ya Tanzania,Hua ni karimu sana, Mwalimu aliyebora.

Njia nyingi atabuni, na mifano halisia,Wanafunzi kuauni, mazoezi kukazia,Huijali yake fani, nidhamu hufuatilia,Huzitunza kumbukumbu, Mwalimu aliyebora.

Yatokayo mdomoni, wote huyafurahia,Huhisi wana amani, anao wasimamia,Nao wakawa makini, ujuzi kujipatia,Huwa ni muadilifu, mwalimu aliyebora.

Si shule hata nyumbani, tabia yake sawia,Jamii hithamini, kwa wito kuitikia,Yatosha nilobaini. Beti saba naishia,Ni mzalendo halisi, Mwalimu aliyebora. M

AS

HA

IRI

Hula ambavyo ni vyao, na kunywa yetu mafao,

MA

SH

AIR

I

Hula ambavyo ni vyao, na kunywa yetu mafao,

“Kila mtanzania, kila mtu kijijini, kila mjumbe wa halmashauri ya wilaya, kila mbunge n.k lazima aweze kusema kwa uhuru bila hofu ya vitisho ama katika mkutano ama nje ya mkutano”

J. K. Nyerere (1974) kwenye Binadamu na Maendeleo

Nukuu

Kwa pamoja tunaweza: Funzo kutoka kwa Marafi ki wa Elimu Mvumi

Mkutano wa Marafi ki wa Elimu mkoa wa Kagera Februari 2010. Mkutano wa Marafi ki wa Elimu mkoa wa Singida Aprili 2010.

Rafi ki mwenye kiu ya kuona mabadiliko katika jamiiMussa Kamtande ni Rafi ki wa Elimu aliyejiunga na Harakati za Marafi ki wa Elimu mwaka 2003. Kilichomvutia hasa kujiunga, ni malengo ya Harakati ambayo yanakwenda sambamba na kiu yake ya kutaka kuiona jamii inashiriki kikamilifu katika kujiletea maendeleo.

Kamtande anakerwa sana na hali duni ya elimu katika mikoa ya kusini mwa Tanzania. Yeye ni mwenyeji na mzaliwa wa maeneo ya Mtwara. Haoni ni kwa sababu gani hali ya elimu iwe mbaya ukilinganisha na maeneo mengine ya Tanzania ili hali sera, mipango na sheria ni moja. Kamtande ameiangalia jamii yake na kuona maendeleo hafi fu ya kielimu yanasababishwa na mwamko mdogo wa wananchi, pamoja na ukosefu wa taarifa.

Rafi ki wa Elimu huyu ameamua kulivalia njuga tatizo hili na kuhakikisha kuwa jamii inazinduka na kuongeza ushiriki wao ili kupata maendeleo kwa kasi. Ameanza kukutana na wadau mbalimbali wa elimu wakiwamo walimu, wanafunzi na wananchi na kisha kujadili kwa kina matatizo na namna ya kuyapatia ufumbuzi. Matokeo ya mijadala hii yamekuwa wakiyawasilisha kwenye ngazi mbalimbali za uongozi na kwa jamii nzima kwa ajili ya utekelezaji.

Kamtande anatumia sana Redio Pride FM kufi kisha ujumbe na kutoa hamasa kwa jamii yake ili iweze kuhamasika na kushiriki kikamilifu katika mchakato wa maendeleo yake. Pia amekuwa akitumia fursa za barua kwa mhariri kutoa maoni, kero na changamoto mbalimbali. Kwa kushirikiana na kikundi cha WEMA alichokianzisha Masasi, amefungua maktaba ya jamii katika kijiji cha Mkalapa, Ndanda Masasi kwa lengo la kukabiliana na upungufu wa upatikanaji wa taarifa mbalimbali ili kuwawezesha wanajamii kuhabarika na kushiriki kikamilifu katika maendeleo yao.

Jitihada za Rafi ki huyu zimeanza kutoa matokeo chanya. Zinatufundisha kwa ujumla kuwa kila mtu ana wajibu na haki ya kutumia uwezo wake, utashi wake na kipaji chake katika kuisaidia jamii yake kuendelea. Wananchi wengi wana uwezo mbalimbali, lakini jamii zao hazinufaiki na chochote. Hima basi kila mwananchi aamke na kuanza kuchukua changamoto hii na kushiriki kikamilifu katika kuletea jamii yake maendeleo.

Rafi ki wa Elimu anayepigania Haki ya elimu kwa WalemavuSalum Ally ni Rafi ki wa Elimu aliyejiunga na Harakati mwaka 2008. Rafi ki huyu ni mwalimu wa Shule ya Msingi ya Viziwi mkoani Tabora, akiwa naye ni mlemavu (kiziwi). Alivutiwa kujiunga na Harakati ili aweze kuhamasisha watu wenye ulemavu kupata haki yao ya msingi ya elimu bila vipingamizi.

Amekuwa akifanya kazi ya kushauri na kushawishi wazazi wa watoto wenye ulemavu (viziwi) wasiwafungie watoto wao majumbani, bali wawapeleke shule kwani wana haki ya kupata elimu kama watoto wengine. Salum hufanya utafi ti kupitia walimu wenzie, wazazi na viongozi wa mitaa, na kuweza kujua wanapoishi watoto viziwi, ambao labda kutokana na wazazi wao kutokuelewa umuhimu wa elimu huamua kuwafi cha majumbani. Kwa juhudi zake, Salum ameweza kutembelea wazazi wengi wa watoto wenye ulemavu wa kusikia, kati yao tayari sita (6) wameweza kupelekwa shule.

Rafi ki huyu ameunda Klabu ya Marafi ki 12 ambao ni viziwi katika Shule anayofundisha. Klabu hii hujishughulisha na kuandaa mijadala mbalimbali inayohusu elimu. Anatoa rai kwa walimu wengine wa watu wenye ulemavu kufundisha kwa bidii na kwa kujituma ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi hawa.

Matukio yajayo

Harakati za Marafi ki wa Elimuc/o HakiElimu739 Mathuradas Street, UpangaSLP 79401 Dar es SalaamSimu (022) 2151852 / 3Faksi (022) 2152449Barua pepe: rafi [email protected]: www.hakielimu.org

Marafi ki wawezeshwa kutengeneza FilamuMarafi ki wa Elimu wa mikoa ya Kigoma, Mwanza na Mara wamewezeshwa kutengeneza fi lamu inayohusu shughuli mbalimbali wanazozifanya. Hii inatokana na sababu kubwa kuwa Marafi ki wanafanya shughuli nyingi na nzuri ambazo wengine wanaweza kujifunza kutokana nazo.

Filamu hii imekusanya baadhi ya visa mkasa vitokanavyo na utendaji wa baadhi ya Marafi ki kutoka katika mikoa hii. Visa mkasa hivi vinahusisha juhudi binafsi za baadhi ya Marafi ki katika kupigania haki ya mtoto kupata elimu, huduma za maktaba za jamii zinazosimamiwa na Marafi ki, kampeni dhidi ya mila zinazokandamiza maendeleo ya elimu, na pia juhudi ya Marafi ki kuwasaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu kupata elimu. Washiriki wakuu walioko katika fi lamu hii ni pamoja na Anna Shadrack na Mussa Gunda wa Kasulu Kigoma, Kikundi cha Nampisi na Toto vya Ukerewe; na pia kikundi cha Marafi ki wa Elimu cha Kimko wilayani Serengeti.

Filamu hii itatumika kuhamasisha wanachi kupitia mikutano, ziara na mkusanyiko mbalimbali ili waweze kujiunga zaidi kwenye Harakati, na pia kuwawezesha Marafi ki kujifunza kutokana na utendaji wa wenzao.