3
© Boston University LANGUAGE PROGRAM, 232 BAY STATE ROAD, BOSTON, MA 02215 www.bu.edu/Africa/alp [email protected] 617.353.3673 Transcript: Haraka haraka. Kuluthumu: Amina huyo fundi wako anajua kushona nguo kweli? Amina: Ndiyo anajua. Kuluthumu: Maana hata hii nguo niliyoivaa kanishonea yeye anajua kweli. Kuluthumu: Je tukienda tutamkuta? Amina: Ndiyo tutamkuta, usikute ana kazi nyingi. Shikamoo fundi. Fundi: Marahaba, hamjambo? Amina: Nimekuletea mteja mwingine mshonee nguo vizuri. Kuluthumu: Fundi hivi vitambaa ni vya harusi naomba nishonee vizuri. Fundi: Hamna shaka. Ngoja nikupime, hapo unasemaje urefu ni sawa. Kuluthumu: Urefu, nataka iwe ndefu kabisa. Amina: Fundi fanya haraka basi nataka kwenda sokoni. Fundi: Usiwe na shida. Amina: Fundi mimi nina haraka, mbona unapima mara mbili mbili? Fundi: Mimi ni fundi. Amina: Mimi nachelewa fundi nataka kwenda sokoni. Fundi: Nataka nikushonee nguo upendeze. Amina: Mimi naenda fundi.

Transcript:+Haraka+haraka.+ - bu.edu · SubiraX!Uvumilivu!X!patience!!! Title: Microsoft Word - Swahili-Haraka Haraka.docx Author: Peter D. Quella Created Date: 5/14/2013 6:17:56

Embed Size (px)

Citation preview

 

©  Boston  University  

LANGUAGE  PROGRAM,  232  BAY  STATE  ROAD,  BOSTON,  MA  02215  www.bu.edu/Africa/alp  

[email protected]  617.353.3673  

Transcript:  Haraka  haraka.    

Kuluthumu:   Amina  huyo  fundi  wako  anajua  kushona  nguo  kweli?  

Amina:   Ndiyo  anajua.  

Kuluthumu:   Maana  hata  hii  nguo  niliyoivaa  kanishonea  yeye  anajua  kweli.  

Kuluthumu:    Je  tukienda  tutamkuta?  

Amina:       Ndiyo  tutamkuta,  usikute  ana  kazi  nyingi.  

Shikamoo  fundi.  

Fundi:         Marahaba,  hamjambo?  

Amina:   Nimekuletea  mteja  mwingine  mshonee  nguo  vizuri.  

Kuluthumu:         Fundi  hivi  vitambaa  ni  vya  harusi  naomba  nishonee  vizuri.  

Fundi:   Hamna  shaka.  

Ngoja  nikupime,  hapo  unasemaje  urefu  ni  sawa.  

Kuluthumu:   Urefu,  nataka  iwe  ndefu  kabisa.  

Amina:   Fundi  fanya  haraka  basi  nataka  kwenda  sokoni.  

Fundi:   Usiwe  na  shida.  

Amina:   Fundi  mimi  nina  haraka,  mbona  unapima  mara  mbili  mbili?  

Fundi:   Mimi  ni  fundi.  

Amina:   Mimi  nachelewa  fundi  nataka  kwenda  sokoni.  

Fundi:   Nataka  nikushonee  nguo  upendeze.  

Amina:   Mimi  naenda  fundi.  

 

  2  

Fundi:   Subiri  sijamaliza  kupima  bado.  

Amina:   Mimi  naenda  fundi,  sijaenda  kununua  mboga  za  jioni.  

Fundi:   Kwa  hiyo  mimi  ninavyokupima  siyo  fundi  tulia  basi  nimalize.  

Amina:   Nakuja  kuchukua  kesho  asubuhi  fundi.  

Fundi:   Watu  wengine  wanaharaka  kweli!  

Siku  ya  pili.  

Amina:   Shikamoo  fundi  nimekuja.  

Fundi:   Marahaba,  hujambo?  

Amina:   Fundi  umeshona  vizuri  kweli  nitapendeza?  

Fundi:   Ndiyo  utapendeza  nimeshona  vizuri.  

Amina:   Mimi  nakuamini  fundi  haya  asante  kwaheri.  

Fundi:   Haya  kwaheri  fundi.    

Siku  ya  tatu;  

Kuluthumu:     Habari  za  leo  fundi?  

Nadhani  unanikumbuka.  

Fundi:    Ndiyo  nakukumbuka.  

Kuluthumu:     Nimekuja  kuchukua  nguo  yangu  na  kama  umenishonea  vizuri,nitakuwa  nakuja  hapa  kila  siku.  

Fundi:   Usiwe  na  shaka  nimekushonea  vizuri.  

Kuluthumu:     Haya  fundi  asante.  

Fundi:   Haya  karibu  tena.  

Amina  :   Leo  kwenye  harusi  nitacheza  kweli.  

 

  3  

Kuluthumu:     Utacheza  wapi?  

Kwanza  nguo  yako  imebana,  hata  huwezi  kucheza  kwenye  harusi.  

Maana  ulivyokuwa  unamwuharakisha  yule  fundi  afanye  haraka  haraka.  

Amina:   Kweli  kabisa  subira  ya  vuta  heri.  

VOCABULARY   Msamiati.  

             

Shaka  =  Wasiwasi  =  worry  

Subira  -­‐  Uvumilivu  -­‐  patience