179

Click here to load reader

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

1

BUNGE LA TANZANIA____________

MAJADILIANO YA BUNGE

___________

MKUTANO WA SABA

Kikao cha Hamsini na Sita – Tarehe 29 Juni, 2017

(Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua

SPIKA: Naomba tukae.

Waheshimiwa Wabunge tunaendelea na Mkutanowa Saba, Kikao cha Hamsini na Sita.

Katibu!

NDG. CHARLES MLOKA – KATIBU MEZANI:

HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI

Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:-

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU:

Taarifa ya Mwaka ya Mamlaka ya Usimamizi naUdhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa Mwaka 2015/2016(The Annual Report of Social Security Regulatory Authority forThe Year 2015/2016).

Page 2: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

2

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO:

Hati ya Uhamishaji Fedha Na. 1 ya mwaka 2016/2017(Statement of Reallocation Warrant No. 1 of 2016/2017); na

Hati ya Uhamishaji Fedha Na. 2 ya mwaka 2016/2017(Statement of Reallocation Warrant No. 2 of 2016/2017).

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Naibu Waziri Fedhana Mipango.

Katibu!

NDG. CHARLES MLOKA – KATIBU MEZANI:

MASWALI KWA WAZIRI MKUU

SPIKA: Maswali kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu;Mheshimiwa Waziri Mkuu karibu. (Makofi)

Swali la kwanza litaulizwa na Mheshimiwa Mbungewa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, ambaye niMheshimiwa Omary Tebweta Mgumba.

Mheshimiwa Mgumba!

MHE. OMARY T. MGUMBA: Mheshimiwa Spika,nashukuru kwa kunipa nafasi hii kumuuliza Mheshimiwa WaziriMkuu swali la kwanza.

Mheshimiwa Waziri Mkuu, wewe ndiye Kiongozi waSerikali yetu ya Chama cha Mapinduzi ndani ya Bunge, lakinipia ndiye kiranja mkuu wa Serikali hii ya Awamu ya Tano.Mheshimiwa Waziri Mkuu, kama unavyofahamu kunawazabuni wengi katika Halmashauri zetu tunakotoka ambaosisi ni wawakilishi wao pamoja na Serikali Kuu, walifanya kaziya kutoa huduma katika taasisi za Serikali na Serikali yenyewekwa muda mrefu, wengine wana miaka miwili, mitatu,wengine mpaka mitano, lakini mpaka sasa hawajalipwastahiki zao.

Page 3: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

3

Mheshimiwa Waziri Mkuu ukizingatia mnamo tarehe01 Juni ndani ya Bunge hili, uliliambia Bunge hili kwambamalipo yanachelewa ni kwa sababu wanafanya uhakiki,ambalo ni jambo zuri, kuwagundua wale ambao wanastahilikulipwa…

SPIKA: Swali Mheshimiwa Mgumba, moja kwa moja!

MHE. OMARY T. MGUMBA: Mheshimiwa Spika, natakakumuuliza Mheshimiwa Waziri Mkuu, watu hawa wamesubirikwa muda mrefu na ukaguzi umeshafanyika zaidi ya maratano, nini kauli ya Serikali, watawalipa lini wazabuni wotewaliotoa huduma ndani ya Serikali?

SPIKA: Majibu ya swali hilo muhimu Mheshimiwa WaziriMkuu tafadhali.

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibuswali la Mheshimiwa Mgumba, Mbunge wa Morogoro Vijijini,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, upo ukweli kwamba, Serikaliinadaiwa na wazabuni wetu waliokuwa wanatoa hudumakwenye maeneo mbalimbali. Wako ambao wametoahuduma kwenye Halmashauri za wilaya kwa maana yahuduma kwenye shule, kwenye magereza, lakini pia wakoambao wamefanya kazi za kutoa huduma kwenye Wizarambalimbali. Na kwa mara ya mwisho nilikuwa hapa nilipataswali la aina hii linalowahusu wadai/wazabuni wa pembejeo,wote hawa ni watoa huduma ndani ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba tumewezakugundua kwamba baadhi ya madeni na baadhi ya wadaiwachache miongoni mwao wametuletea taarifa za madaiambayo si sahihi sana. Na kweli, tulichokifanya tulitoamaagizo kwenye maeneo yote, ili kuhofu kupoteza fedha,kulipa fedha ambayo haikufanyiwa kazi kwa madai yale.

Kwa hiyo, tumeendesha zoezi la uhakiki chini yaWizara ya Fedha na taasisi yetu kupitia CAG, hasa kule kwenye

Page 4: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

4

madeni makubwa ili kujiridhisha viwango vinavyotakiwakulipwa kwa wazabuni hawa.

Mheshimiwa Spika, tuliweka utaratibu kwambaangalao kufikia mwishoni mwa mwezi huu tuwe tumemalizahilo zoezi la uhakiki halafu tuanze kulipa madeni haya. Kwahiyo ni matarajio yangu kwamba Wizara ya Fedha watanipataarifa, na Wizara zile zote ambazo zina madeni ya watoahuduma zitatoa taarifa ya viwango vya fedha, halafu sasatusimamie Wizara ya Fedha kuweza kuwalipa hawa watoahuduma.

Mheshimiwa Spika, nataka nitumie nafasi hii, kwanzaniwashukuru kwa uvumilivu wao wadeni wote wanaotudai,lakini pili tuwasihi waendelee kutuvumilia na taratibu hizi kwalengo lilelile nililokuwa nimelieleza awali la kuokoa fedhaambazo zinalipwa kwa watu ambao hawakutoa huduma.Hata hivyo bado tutaendelea kuwatumia watoa hudumakutoa huduma ndani ya Serikali kwenye maeneo ambayowameendelea kutoa huduma na tuwahakikishie tu kwambatutawalipa.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, Mheshimiwa Mbungekama wako watoa huduma kwenye eneo lako endeleakuwahakikishia kwamba Serikali tutlipa madeni. Ahsantesana. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Mgumba, kuna haja yanyongeza? Hebu tujaribu eeh, maana ahadi umeshapata!

MHE. OMARY T. MGUMBA: Mheshimiwa Spika,nashukuru sana. Kuna swali dogo tu la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze sanaMheshimiwa Waziri Mkuu kwa majibu mazuri ambayo kutokaSerikalini.

Swali dogo la tu la nyongeza, kwa kuwa kamaulivyosema kwenye majibu yako ya msingi, kwambammegundua kuna watu ambao wameleta madai ambayo

Page 5: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

5

si sahihi, lakini naamini pia kuna watu ambao watakuwamadai yao ni sahihi. Sasa nini kauli ya Serikali kwa waleambao madai yao ni sahihi ambao wamekaa muda mrefukiasi kwamba imewaongezea gharama kwa maana ya ribasehemu walizokopa, nani atalipa gharama hizi kwa ajili yausumbufu uliotokea na gharama zilizoongezeka kwenyemadeni hayo? (Makofi)

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swalila nyongeza la Mheshimiwa Mgumba, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kama ambavyo nimeelezakwenye jibu la awali kwamba kwanza tunathamini sana kaziwaliyoifanya katika kutoa huduma kwenye sekta zetu. Lakinimbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hikiambacho sisi tunafanya uhakiki. Baadhi ya wadai nimepatanafasio ya kukutana nao hapa Dodoma wakati huu waBunge na kuzungumza nao na kuwaambia kwa ninitumechelewa kuwapa fedha zao, wale ambao kweli wanamadai halali.

Mheshimiwa Spika, lakini bado nirudi tena kusemakwamba, hatuna namna nyingine ya kufanya zaidi yauchelewaji huu wa kulipa kwa sababu tuko kwenye zoezi lakuhakiki, ili tujiridhishe. Kama ingekuwa tumechelewa tu,kwamba hatuna kazi yoyote, tumeacha tu hapo kungekuwana swali ambalo naamini unacholenga kingeweza kupatamaelezo. Lakini bado niwahakikishie kwamba taratibuzinakamilika na tulisema tunakamilisha tarehe 30 Juni, yaanikesho tu tarehe 30 Juni, tunatarajia Wizara ya Fedha itapewataarifa kutoka kwenye Wizara mbalimbali, kwamba madaiyetu halali ni haya kwa ajili ya watu hawa kwa hudumawaliyoitoa, baada ya hapo tunalipa tu na tutaendeleakuwapa nafasi zaidi ya kutoa huduma.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo niwahakikishie kwambawataendelea kutoa huduma, hasa wale ambao niwaaminifu kwenye awamu ijayo hii ya mwaka wa fedhampya wa mwaka 2017/2018.

Page 6: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

6

SPIKA: Swali la pili kwa siku ya leo kwa MheshimiwaWaziri Mkuu linatoka kwa Mbunge wa Mbulu MheshimiwaFlatei Gregory Massay. Mheshimiwa Massay tafadhali swalifupi.

MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Spika, nashukurusana.

Mheshimiwa Waziri Mkuu, hivi karibuni Serikaliimefanya uhakiki wa vyeti fake na imeacha ma-gap namapengo katika maeneo yetu hasa ya vijijini kwa upandewa afya.

Je, lini sasa Serikali mtatusaidia ili vituo vyetu auzahanati ziweze kuendelea kutokana na nafasi hizo ambazosasa zimechwa wazi?

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba arudietena swali, maana kulikuwa na msikiko usio sahihi kwenyevipaza sauti vyetu.

SPIKA: Tafadhali, kwa kifupi!

MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Spika, Serikaliimefanya uhakiki wa watumishi ambao wana vyeti fake. Sasabaada ya uhakiki huo wengine wameacha vituo vya afyana zahanati zetu kule.

Sasa swali langu, je, lini mtaajiri sasa, ili watu wetukule wapate huduma, hasa kwenye maeneo ya afya ambakowatumishi wameshaacha kazi kutokana na kwamba,walikuwa wana vyeti ambavyo havistahili kuendeleakuwepo? Ahsante.

SPIKA: Kuziba mapengo ya mapungufu ya watumishiwaliopunguzwa kutokana na vyeti fake.

Mheshimiwa Waziri Mkuu, majibu!

Page 7: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

7

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibuswali la Mheshimiwa Flatei Massay, Mbunge wa Mbulu, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba tumepitisha zoezihili la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wetu na uhakiki huubaada ya kuwa tumekamilisha tulipata makundi matatu.Kundi la kwanza ni wale wenye vyeti fake moja kwa moja,kundi la pili ni wale wenye vyeti vinavyotumika na zaidi yamtu mmoja, lakini kundi la tatu uko utata wa majina ambaoumejitokeza kwenye vyeti hivi ambavyo wao wamepatanafasi ya kukata rufaa. Sasa wote hawa wameacha pengokwa sasa, na ndilo ambalo Mheshimiwa Mbungeamelizungumzia, lini tunatoa ajira.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais wetu Dkt. JohnPombe Magufuli ametoa nafasi za ajira zaidi ya 50,000 ilikuziba mapengo haya ambayo yamejitokeza kwa wenyevyeti fake, lakini vilevile ili kuongeza tu ajira kwenye sektanyingine kwa lengo la kuboresha utoaji huduma kwenye sektambalimbali.

Mheshimiwa Spika, tayari vibali vimeshatolewa naWizara ya Utumishi, tumeanza na idara ya elimu, tumeshaajiri walimu wa masomo ya sayansi wamekwenda kwenyevituo, tumetoa pia nafasi kwenye sekta ya afya na vibali hivivitaendelea kutolewa kadri ya nafasi ambazo MheshimiwaRais ameahidi kwa Watanzania.

Mheshimiwa Spika, ninaamini Rais wetu mpendwakwa ahadi yake nafasi hizi ataendelea kuzitoa ili tuzibemapengo na kuboresha pale ambako kuna upungufumkubwa. Na sasa ajira hizi zitaenda kitaaluma zaidi, ilikuweza kuleta ufanisi mkubwa kwenye sekta y ajira. Ahsante.(Makofi)

SPIKA: Ahsante sana, Mheshimiwa Munde Tambwe,Mbunge wa Tabora Viti Maalum. Mheshimiwa kuna swali lanyongeza tena kweli? Mheshimiwa Munde Tambwe kamahayupo tunaendelea. Mheshimiwa Martha Moses Mlata.

Page 8: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

8

MHE. MARTHA M. MLATA: Mheshimiwa Spika, ahsante;na mimi nashukuru kupata nafasi ili nimuulize MheshimiwaWaziri Mkuu swali.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwakuwa, tarehe 15/05/2017 Serikali ilitangaza rasmi kuivunjaMamlaka ya Ustawishaji wa Makao Makuu Dodoma namajukumu yake kuhamishiwa Manispaa ya Dodoma, kwahilo naipongeza Serikali. (Makofi)

Lakini kwa kuwa baadhi ya wananchi hataWaheshimiwa Wabunge pia walikuwa tayari wameshalipiaviwanja na walikuwa hawajakabidhiwa. Je, Serikali inatoatamko gani kuhusu jambo hili? Ahsante.

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibuswali la Mheshimiwa Martha Mlata, Mbunge wa Viti Maalum,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba Mheshimiwa Raisalitoa agizo la kuvunja Mamlaka ya CDA na mamlaka hiyona majukumu yake kuyahamishia Ofisi ya Rais – TAMISEMI,kupitia Manispaa ya Dodoma. Kazi hiyo imeshafanywa nazoezi linaloendelea sasa kwanza wale watumishi wote waCDA watahamishiwa Manispaa ya Dodoma, lakini tutafanyamchujo kidogo, wale ambao walikuwa na malalamiko,wanalalamikiwa na wananchi wale wote tutawawekapembeni, kwa sababu tunataka tupate timu mpya ambayoinafanya kazi vizuri.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, mbili, tunaendelea sasa na uhakikina ukaguzi wa kina kwenye masuala ya fedha na utumishiwenyewe ili tuweze kuanza vizuri, tujue CDA ilipoacha iliachana fedha kiasi gani na shughuli zake zilifikia hatua gani halafupia kuweza kuendelea, lakini majukumu yote yanabaki kamayalivyokuwa na CDA yataendelea kufanywa na Halmashauriya Manispaa ya Dodoma. Kinachobadilika pale ni maandishi,kama kwenye risiti zilikuwa zinasomeka CDA, sasa zitasomekaManispaa.

Page 9: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

9

Mheshimiwa Spika, baada ya kukamilisha utaratibuhuu mpango kazi wote utaendelea kama ulivyokuwa. Kamakuna mtu alilipa nusu anataka kumalizia, wataendelakukamilisha malipo yao, kama kuna mtu alishakamilihahajapata kiwanja, ataenda kukabidhiwa kiwanja chake nanamna yoyote ya utendaji wa kawaida utaendelea. Sasahivi akaunti zote zimefungwa kwa hiyo, huwezi kulipa mpakahapo tutakapofungua malipo.

Mheshimiwa Spika, tutamuagiza Mkurugenzi sasa waManispaa, atoe maelezo sahihi kwa Wana Dodoma na kwaWananchi, Waheshimiwa Wabunge mkiwemo ili kila mmojaaweze kujua, lakini kwa kauli hii ndio usahihi wa taarifa yaCDA kwa namna ambavyo tumeivunja na tumehamishiaMamlaka pale Manispaa ya Dodoma na watumishi wotesasa watawajibika kwa Mkurugenzi wa Manispaa nahakutakuwa na chombo kingine pale.

Mheshimiwa Spika, kwa namna ambayotumewaelekeza sasa pale CDA kwenye Idara ya rdhi, kwenyelile jengo lisomeke Idara ya Ardhi - CDA na huko ndani tume-plan sasa Wizara ya Ardhi ipeleke mtu anayeandika Hati.Tunataka pale ndani iwe One Stop Centre. Ukienda kuombaardhi, ukishapimiwa, ukishalipia, hati unapata humo humokwenye hilo jengo. Kwa hiyo, tunataka turahisishe upatikanajiwa hati na viwanja kwenye jengo hilohilo moja, ukiingia ndaniukitoka unatoka na hati yako badala tena kwenda mahalipengine. Ahsante. (Makofi)

SPIKA: Haya, Wana Dodoma, mambo mswano hayo.

Mheshimiwa Martha Mlata, bado kuna swali?

MHE. MARTHA M. MLATA: Mheshimiwa Spika, ndiyo.

Mheshimiwa Spika, kwanza namshukuru sana kwamajibu ambayo hakika yameponya nyoyo za watu ambaowalikuwa wanaguswa sana na suala hili la CDA. LakiniMheshimiwa Waziri Mkuu kwa kuwa umesema mamlakahaya; na umeeleza vizuri Halmashauri ya Manispaa ya

Page 10: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

10

Dodoma itakavyofanya kazi, naamini na Halmashaurinyingine nchi nzima zitafanya kazi kama ambavyo umetoamaelekezo.

Mheshimiwa Spika, kuna tatizo moja tu, kwambawanapokwenda kuchukua ardhi kutoka kwa wamiliki au kwawatu ambao wanahodhi zile ardhi zao, wanalipa fidia kwafedha ndogo sana, lakini wanapokuja kupima na kutakakuviuza wanauza kwa bei ambayo ni tofauti na ile gharamaambayo walinunulia.

Je, Serikali hapa inaweza pia ikatoa maelekezokwamba, angalau uwiano wake usipishane sana kwa ajiliya kuwanufaisha hata wale wahusika wa maeneo ambayoyanakuwa yamechukuliwa? Ahsante sana.

SPIKA: Hilo swali ni la nchi nzima. Mheshimiwa WaziriMkuu!

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibuswali la nyongeza la Mheshimiwa Mlata, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ziko sheria ambazo zinaongozafidia na ndizo ambazo tunazifuata. Fidia hizi kuna watuambao wamepanda mazao kwenye ardhi, lakini wenginehawajapanda chochote. Kwa hiyo, mabadiliko ya bei amatofauti ya bei inatokana na ambavyo mwenye ardhialivyoweza kuwekeza kwenye eneo lile. Kama kuna mazaoyoyote yanafanyiwa tathmini na tunalipa kwa mujibu wa beina taratibu zilizopo kisheria.

Kwa hiyo, bado tutasisitiza mamlaka zote zahalmashauri zote za Wilaya, Miji na Manispaa na Majiji kufutasheria zile ambazo zimeelekezwa katika kufanya fidia. Natumesemea ardhi ya mtu isichukuliwe bila fidia, kwa hiyo,bado hili litaende kuzingatiwa. Na agizo hili naombawazingatie maeneo yote haya ambayo nachukua ardhi yamtu, kwamba lazima alipwe kwanza ndipo uweze kuchukua,ili kuondoa migogoro ambayo siyo muhimu kwa sababusheria ipo na inatuongoza kufanya hivyo, ahsante. (Makofi)

Page 11: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

11

SPIKA: Swali la mwisho la Waziri Mkuu kwa siku yaleo. Linatoka kwa Mheshimiwa Ritta Esnepher Kabati.

MHE. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, nakushukurusana kwa kunipa nafasi i l i niweze kuuliza swali kwaMheshimiwa Waziri Mkuu.

Mheshimiwa Waziri Mkuu hivi karibuni Serikali imetoatamko la kutosafirisha chakula nje ya nchi, lakini kuna baadhiya mikoa ambayo imezalisha chakula cha kutosha cha ziadakinachoweza kusafirishwa hata nje ya nchi. Je, Serikali inatoaufafanuzi gani kuhusiana na utekelezaji wa tamko hilo?

SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Waziri Mkuu.

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibuswali la Mheshimiwa Ritta Kabati, Mbunge wa Iringa kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, jambo hili nimelizungumza siku yaIdd Mosi nikiwa kwenye sherehe ya Idd kwenye Baraza la Iddkule Mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro. Nilizungumza kwamsisitizo kwamba tumedhibiti na tumezuia usafirishaji wachakula na hasa mahindi nje ya nchi kwa sababu historiayetu sisi kuanzia mwaka wa jana mwezi Novemba, 2016mpaka Februari, 2017 nchi yetu ilikosa mvua za msimuunaotakiwa na tutapata usumbufu mkubwa ndani ya nchikwa maeneo mengi kukosa chakula cha kutosha.

Mheshimiwa Spika, na chakula kikuu sasa nchiTanzania naona utamaduni umebadilika, nil ikuwanazungumza pia na Mheshimiwa Mbatia hapa kwambautamaduni umebadilika, Wachaga, Wahaya sasa badala yakula ndizi wanakula ugali. Wamasai waliokuwa wanakulanyama tu pekee sasa wanakula ugali.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo utakuta mahindiyanatumika sana kuwa ni chakula kikuu nchini na kwa hiyolazima tuweke udhibiti wa utokaji wa mahindi ili yaendeleekutusaidia kama chakula kikuu hapa nchini kwetu.

Page 12: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

12

Kwa hiyo tumeweka zuio, na hasa baada ya kuwaKamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa Kilimanjaro ilitoa taarifakwamba kuna utokaji wa mahindi mengi kwenda nchi zanje kwenye mipaka yetu. Na siku ile nilipokuwa Kilimanjaromalori kumi yalikamatwa yakiwa na mahindi yakivushwakwenda nje ya nchi.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo lazima tuweke utaratibuna ninyi wote ni mashahidi kwamba uzalishaji huu haukuwawa uhakika sana kuanzia mwezi Machi mpaka mwezi Mei,kwa miezi mitatu. Maeneo machache yamezalisha sanakama ulivyosema Mheshimiwa Ritta Kabati lakini maeneomengine hayana chakula. Juzi nilikuwa Mwanza nikiwa paleUsagara, Kigongo Ferry nilisimamishwa na wananchi, mojakati ya tatizo walilolieza ni upungufu wa chakula. Nimeona,hata Sengerema mahindi yote yamekauka, Geita mahindiyote yamelimwa yamekauka. Kwa hiyo, bado tuna tatizo laupungufu wa chakula. Pia bei za chakula chetu iko juu sanahatuna namna nyingine ni kudhibiti chakula chetu.

Mheshimiwa Spika, na nilieleza kwamba nchi nyingiza jirani hazina chakula. Sisi tuna barua hapa kutoka Congo,South Sudan tumepata kutoka Somalia na nchi za jiraniwanaomba kupewa msaada wa chakula kutoka Tanzaniawakati sisi wenyewe hatuna chakula cha kutosha. Kwa hiyo,ni muhimu sana kwa Serikali na wananchi mkatuunga mkonokatika hili, kudhibiti utokaji wa chakula, na hasa mahindiyanayokwenda nje ya nchi.

Mheshimiwa Spika, nimeeleza kwamba sisitulichofanya ni kudhibiti kutoa mahindi nje bila kibali. Nakama kuna umuhimu wa kupeleka mahindi nje basi tunatakayasagwe ndani ili yapelekwe, kwa sababu ukisaga tunafaidazake, pumba tunazipata, tunazitumia kwa chakula chamifugo lakini pia mashine zetu ambako tuna msizitizo waviwanda vitafanya kazi ya kusaga, tutakuwa na ajira, lakinitunapotoa mahindi maana yake tunatoa kila kitu huku ndanitunakuacha tupu. Kwa hiyo, lazima tuwe na mpango ambaoutasaidia sasa, sisi wenyewe Watanzania kunufaika kupitiazao hili.

Page 13: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

13

Mheshimiwa Spika, bado msimamo ni ule ulekwamba tumezuia mahindi kutoka nje ya nchi na kama nilazima basi aende Wizara ya Kilimo akaombe kibali kama nilazima Wizara ikiona inafaa utapata kibali, lakini kibali hichoni cha kutoa unga na si mahindi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wote ni mashahidi, janatumepata taarifa malori zaidi ya 103 kwa siku nne kutokasiku ya Idd mpaka leo hii, malori 103. Je, kwa mwezi mzimatutakuta na mahindi hapa ndani?

Mheshimiwa Spika, tunazo taarifa kupita Kamati zaUlinzi na Usalama kwamba wengi wanaofanya biashara kujakuchukua mahindi Simanjiro, Kibaya kwa maana ya hapakatikati maeneo ya Kongwa ni watu kutoka nje ya nchi ndiowanaokuja kuchukua. Kwa hiyo hatuna faida sana haokuingia zaidi ya kwamba wanatuachia fedha. Hivyotunaitengeneza shida ambayo tutakuja kuanza kuulizatutapateje chakula ndani ya nchi.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo Watanzania kwa jambohili naomba mtuunge mkono kwa sababu tunachofanya nikwa maslahi ya nchi, hatimaye bei zitapanda tutashindwakununua mahindi na wote mnajua angalau sasa mahindiyamepungua kwenye masoko

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo tuendelee na hali hiyo ilichakula kiwe cha kutosha baada ya kuwa tumefanyatathimini tukijiridhisha kwamba chakula cha ndani chakutosha kipo na tuna akiba kutoka kwenye maeneoyanayozalisha sana basi vibali hivyo vinavyotolewa kwautaratibu vitaendelea kutoka, na wale ambao wanatakakufanya biashara nje ya nchi wataendelea kupata fursa yakufanya biashara nje ya nchi. Lakini kwa sasa tumezuia; naninataka nimpongeze sana Mkuu wa Mkoa ya Kilimanjaromama Anna Mghwira na Kamati yake ya Ulinzi na Usalamakwa kuendelea kusimamia.

Mheshimiwa Spika, tumeona malori yale agizolimebaki pale pale, mahindi yale ambayo yatakuwa

Page 14: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

14

yamaekamatwa; na tumejihisi kwamba yalikuwayamekwenda nje ya nchi, yote yataingizwa kwenye hifadhiya taifa, na hayo malori yanyofanya biashara hiyo yoteyatabaki kituo cha polisi. Lakini pia kwa namna ambavyowanaendelea na waendelee kwa utaratibu wote namaagizo yetu yatabaki vilevile ili tuweze kuwahudumiaWatanzania ndani ya nchi. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana tunakushukuru sana MheshimiwaWaziri Mkuu kwa majibu ya maswali haya. Katibutunaendelea na maswali.

NDG. CHARLES J. MLOKA:

MASWALI NA MAJIBU

Na. 462

Ahadi ya Ujenzi wa Nyumba za WatumishiWilaya ya Itilima

MHE. STANSLAUS H. NYONGO (k.n.y MHE. NJALUD.SILANGA) aliuliza:-

Wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka 2015,Mheshimiwa Rais aliahidi kujenga nyumba za watumishikatika Makao Makuu ya Wilaya ya Itilima katika Kijiji chaLangabidili.

Je, ni lini ahadi hiyo itaanza kutekelezwa?

NABU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisiya Rais - TAMISEMI naomba kujibu swali la Mheshimiwa NjaluDaudi Silanga, Mbunge wa Itilima kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Itilima ni kati ya Wilayatano zinazounda Mkoa wa Simiyu. Wilaya hii ilianzishwa

Page 15: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

15

mwaka 2012 kwa GN Na. 73, na Halmashauri yake ilianzishwamwezi Mei, 2013 kwa GN Na. 47. Wilaya ya Itilima imezaliwakutoka katika Wilaya ya Bariadi na kuunda Mkoa wa Simiyuwenye Wilaya tano na Halmashauri sita. Watumishi waHalmashauri wanalazika kuishi Bariadi Mjini na kusafiri umbaliwa kilometa 33 kila siku kutoka Bariadi hadi Makao Makuuya Wilaya kwa ajili ya kufanya kazi.

Mheshimiwa Spika, kutokana na usumbufu nagharama za usafiri Serikali ilitoa shilingi milioni 500 kwa mwakawa fedha 2014/2015 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba zawatumishi na kulipa fidia maeneo ya wananchi. Hadi sasaujenzi wa nyumba nne unaendelea katika hatua za mwisho.

Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2016/2017Serikali ilitenga shilingi milioni 230 kwa ajili ya ujenzi wa nyumbanne za wananchi. Aidha, Serikali imetoa shilingi milioni 500kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji. Ujenziunaendelea na unatekelezwa na Wakala wa MajengoTanzania (TBA).

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2017/2018, Serikali imetenga shilingi milioni 250 kwa ajili ya ujenziwa nyumba nyingine nne za watumishi. Serikali itaendeleakutenga fedha kidogo kidogo kwa kadri zitakavyopatikanaili kuweza kukamilisha nyumba za watumishi.

MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Spika,ahsante sana. Kwanza kabisa napenda kutoa pongezi kwaMheshimiwa Waziri kwa majibu mazuri. Nina maswali mawilitu madogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba ujenziunaendelea, lakini unaendelea kwa kasi ndogo sana.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwambawanatoa fedha kwa wakati na kuhakikisha ujenzi huounaendelea kwa haraka i l i ukamilike, kwa sababuwatumishi wanapata shida sana kusafiri kutoka Bariadi hadiLigangabilili?

Page 16: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

16

Mheshimiwa Spika, swali la pili, je, Serikali ina mpangogani juu ya kuikaribisha National Housing (Shirika la Nyumbala Taifa) kwenye Mkoa wa Simiyu kuweza kujenga nyumbaza National Housing katika mkoa nzima yaani katika wilayazake zote tano ili kuweza kuwasaidia wafanyakazi kupatamakazi mazuri ya kuweza kuishi? Ahsante sana.

NABU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, kwa ajenda ya kasindogo ya utendaji wa kazi naomba nichukue concern hiyo,tutafanya follow up kuangalia ni kinachoendea. Nilifika paleItilima, ni kweli changamoto kubwa ilikuwa ni tatizo la fedha.Tukaja kufanya uhangaikaji katika ofisi yetu ndiyo maanatukapata zile fedha nyingine zikaenda kule, ili kuwezakuongeza speed ya ufanyaji wa kazi pale. Vileviletutawasiliana na wenzetu wa Itilima ili kuangalia kuna kitugani ambacho kinakwaza. Nia ni kuongeza speed ya utendajiwa kazi ili hatimaye wananchi na hasa watumishi wa Itilimawaweze waweze kukaa katika mazingira rafiki.

Mheshimiwa Spika, kuhusu swali la National Housingkuweza kukaribia katika Mkoa wa Simiyu kwa ajili ya kujenganyumba; ni wazo nzuri, na niwashukuru sana wenzetu waNational Housing wamekuwa wakishiriki ujenzi wa nyumbakatika maeneo mbalimbali. Hata hivyo ninaamini kwambatutapata maelekezo vizuri juu ya nini cha kufanya kutokaWizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ambayoni Wizara yenye dhamana katika eneo hilo, hasa katika Mkoawa Simiyu.

Mheshimiwa Spika, mara nyingi sana wanaambiwakwamba watenge maeneo maalum kwa aji l i yakuwakaribisha National Housing. Hata hivyo kuna maeneomengine National Housing walijenga nyumba lakini matumiziya zile nyumba imekuwa ni changamoto kubwa na sanakatika Halmashauri zetu.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo tuchukue kama nichallenge nyingine katika upande wetu vilevile, kwambaendapo National Housing wanakuja kuwekeza basi lazima

Page 17: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

17

nisiamasishe Halmashauri tuwe tayari kuhakikisha kwambatunazitumia nyumba hizo, kwa sababu fedha hizi zisipotumikavizuri tutatengeneza gharama kubwa kwa Serikali yetu. Kwahiyo, ni wazo zuri Mheshimiwa Nyongo na mimi kama TAMISEMInitalichukua jambo hil i, nitaongea na dada yanguMheshimiwa Angelina, Naibu Waziri wa Ardhi tuangalienamna ya kufanya ili wananchi wa Simiyu waweze kufanyakazi kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa Simiyu.

SPIKA: Nimekuona Mheshimiwa Maryam Msabahaswali la nyongeza. Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ardhi kablaya Maryam Msabaha.

NAIBU WAZIRI WA ARDHI: Mheshimiwa Spika, Ahsantesana. Napenda kujibu swali la nyongeza na kumshukuru sanaMheshimiwa Naibu Waziri alivyojibu majibu yake mazurikuhusiana na suala la National Housing.

Kwa Mkoa wa Simiyu tayari National Housing wanamaeneo waliyopewa katika Wilaya mbili, Wilaya ya Busegapamoja na Wilaya ya Bariadi. Tatizo lililoko katika wilayazingine ni kwamba bado hawajawa tayari kutenga maeneo.

Mheshimia Spika, kwa maelekezo ambayo piaMheshimiwa Rais alitoa kwamba National Housing ili wawezekujenga na waweze kutoa nyumba zao kwa bei nzuri lazimaHalmashauri husika iwe imeshatenga eneo ambalo halinachangamoto kwa maana kwamba litahitaji fidia, litahitajimiundombinu. Kwa hiyo, wao wafanye maandalizi tayariviwanja waweke National Housing watakwenda kujenga.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, la pili pia, kuna Wilaya zaidi ya 30ambazo National Housing wamejenga na nyumba zilezinaharibika, ikiwemo Mkoa wa Rukwa, nyumba zimejengwalakini watu hawajaingia wala hawajapanga. Kwa hiyo,wakati mwingine ku-pull up resources katika maeneomengine inakuwa ni ngumu; na katikati hapa walisimamakwa ajili ya kuendeleza eneo la Iyumbu. Kwa hiyo halmashauriyoyote itakayokuwa tayari National Housing wataweza kuja,

Page 18: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

18

lakini tuwaombe pia mfanye maandalizi yale ya msingi iliNational Housing waweze kushiriki.

SPIKA: Mheshimiwa Maryam Msabaha.

MHE. MARYAM SALUM MSABAHA: Mheshimiwa Spika,ahsante sana kwa kunipa nafasi na mimi nipate kumuulizaMheshimiwa Naibu Waziri swali dogo la nyongeza.

Kwa kuwa watumishi wengi wa Serikaliwamehamishiwa Mkoa wa Dodoma, je, Serikali ina mkakatigani wa kuhakikisha watumishi wote wa Serikali wanapatanyumba na waache kuhangaika hangaika mitaani kwasababu nyumba za National Housing hazitoshi kwa watumishiwa Serikali waliohamishiwa Dodoma?

SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri TAMISEMI majibu yaswali hilo muhimu.

NABU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swalila mate wangu wa Bulombora dada yangu MheshimiwaMaryam Msabaha kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza ni kweli, ni nia njemaSerikali. Tumesema kwamba Serikali ya Awamu ya tano simlimila dole, kwamba inatekeleza kile ilichokiahidi; imesematunaamia Dodoma na tumehamia sasa hivi Dodoma.Naomba niwahakikishie kwamba Serikali imeweka mipangovizuri kupitia nyumba za TBA, National Housing na CDA.Mkiangalia kule kama mnapita Iringa Road zimekarabatiwa,lengo lake kubwa ni kwamba kuweza kuwa-accommodatewatumishi wote wa Serikali.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo tunashukuru sana kwasuala hili zuri, Serikali imeweka mpango vizuri. Niwaahakikishiewatumishi wote kwamba msiwe na hofu mtakapokujaDodoma, Serikali inapanga mipango mizuri, na ndiyo maanahata National Housing sasa wanajenga huu mji mpya pale.Hii yote ni kwa ajili ya kuhakikisha kwamba kwenye mchakato

Page 19: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

19

huu wa Mji Mkuu wa Serikali kuhamia Dodoma, Dodomaiweze ku-accommodate watumishi hawa wanaokuja hapa.

SPIKA: Tunaendelea na Ofisi ya Rais, Utumishi naUtawala Bora. Swali linaulizwa na Mbunge wa Ukerewe,Mheshimiwa Joseph Michael Mkundi.

Na. 463

Serikali kutoa Posho kwa Watumishi wa Maeneo yaPembezoni

MHE. JOSEPH M. MKUNDI aliuliza:-

Watumishi walio maeneo ya pembezoni mwa nchiikiwemo Wilaya ya Ukerewe wanafanya kazi katika mazingiramagumu, mfano walimu wa watumishi wa afya.

Je, Serkali ina mpango gani wa kutoa posho yamazingira magumu kwa watumishi wa maeneo yapembezoni?

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YAUTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, nakushukuru, naomba kujibu swalila Mheshimiwa Joseph Michael Mkundi, Mbunge wa Jimbola Ukerewe kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba watumishi waliokatika Halmashauri zilizo katika maeneo ya pembezoniikiwemo Wilaya ya Ukerewe hufanya kazi katika mazingiramagumu na upungufu mkubwa wa watumishi.

Mheshimiwa Spika, mwaka 2010 Serikali ilipitisha Seraya Malipo ya Mishahara na Motisha katika utumishi wa ummaambayo miongoni mwa malengo yake mahsusi ni kuwavutia,kuwapa motisha na kuwabakiza watumishi katika utumishiwa umma. Lengo ni kupunguza tatizo la uhaba wawatumishi katika Halmashauri za Wilaya.

Page 20: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

20

Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza sera hii mwaka2012/2013 Halmashauri 33 za Wilaya, ikiwemo Halmashauriya Wilaya ya Ukerewe ziliwezeshwa kuandaa miongozo yakutoa motisha kwa watumishi wake. Kutokana na zoezi hiloHalmashauri 29 ziliandaa na kuwasilisha katika ofisi yangumiongozo iliyoabainisha aina za motisha zinazohitajika kwaajili ya watumishi wake. Utekelezaji wa miongozo hiyo kwaHalmashauri zote 29 ulikadiriwa kugharimu jumla ya shilingibilioni 331.087 kwa mwaka, ambapo kati ya hizo kiasi chashilingi bilioni 314.372 kilihitajika kwa ajili ya miradi yamaendeleo na kiasi cha shilingi bilioni 16.761 kilihitajitaka kwaajili ya matumizi ya kawaida na utekelezaji wa miongozo hiiulitarajiwa kuanza katika mwaka wa fedha 2013/2014. Hatahivyo, utekelezaji wa miongozo hii haujaanza kutokana naufinyu wa bajeti ya Serikali.

SPIKA: Mheshimiwa Michael Mkundi swali la nyongeza.

MHE. MICHAEL J. MKUNDI: Mheshimiwa Spika,nashukuru sana kunipa fursa ya kuuliza maswali mawili yanyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Serikali inakiri kwambaUkerewe ni moja kati ya maeneo ambayo watumishi wakewanafanyakazi katika mazingira magumu na kwa kuwahuduma za elimu na afya visiwani Ukerewe hususan kwenyeVisiwa vya Ilugwa, Ukara, Bwilo na kwingineko zinaadhirikasana na changamoto zinazowakabili watumishi kwenyemaeneo haya.

Je, Serikali iko tayari kutoa fedha na kuwezesha serahii ya malipo ya mishahara na motisha katika utumishi waumma kuanza kutekelezwa ili kuokoa maisha na mazingiraya wakazi wa visiwa hivi?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, mwanzoni mwamwaka huu Serikali ilisambaza walimu kwenye Halmashaurizetu hasa walimu wa sayansi lakini kumekuwa namalalamiko mengi sana kutoka kwa walimu hawa kuishikatika mazingira magumu sana kwa sababu ya kutolipwa

Page 21: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

21

stahiki zao. Je, nini kauli ya Serikali juu ya tatizo hili? Nashukurusana.

SPIKA: Majibu ya maswali hayo mawili Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na UtawalaBora, Mheshimiwa Kairuki.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YAUTUMISHI WA UMMA NAUTWALA BORA: Mheshimiwa Spika,kwanza ni kweli ukiangalia si tu kwamba wananchi waUkerewe wanaadhirika kutokana na ukosefu wa huduma zaelimu na afya, lakini hata watumishi wenyewe walio katikamazingira magumu pia huduma ya elimu katika eneo lile naafya inapokuwa si nzuri inawafanya pia na wenyewewasivutiwe kufanya kazi katika maeneo hayo. Nimhakikishietu Mheshimiwa Mbunge kwamba tumeiona changamoto hii.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kwamba kwa ujumlawake mwongozo huu haujaanza kutekelezwa lakini kupitiaBajeti ya Serikali na kupitia bajeti za Halmashauri ambazozimepitishwa wameshaanza kutekeleza maeneo mbalimbaliikiwemo sekta ya elimu pamoja na afya.

Mheshimiwa Spika, niseme tu kwamba tutaendeleakulifanyia kazi kama Serikali kutoa msisitizo ili kuhakikishakwamba maeneo haya yanayokabiliwa na changamoto hizibasi yanaweza kutengewa fedha za bajeti za kutosha ilikuweza kutekeleza sera hii.

Mheshimiwa Spika, katika swali lake la pili kuhusianana walimu wa sayansi na hesabu walipangiwa vituo mwakahuu, kwamba hawajalipwa stahiki zao. Kwa kweli ni jamboambalo limetusikitisha, na haswa ukizingatia katikaHalmashauri moja unakuta mtu amepangiwa walimu 12 tu,inakuwaje Halmashauri inashindwa kuwahudumia kwawatumishi wake wapya waliopangiwa katika kituo kwamara ya kwanza.

Mheshimiwa Spika, niseme kupitia hadhara hii natoatamko au agizo kwa Halmashauri zote zilizopokea walimu

Page 22: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

22

wapya wa sayansi na hesabu lakini pia zilizopokea wataalamwa maabara za sayansi zihakikishe ndani ya siku sabazimewalipa watumishi hao stahiki zao zote. (Makofi)

SPIKA: Nimekuona Mheshimiwa Martha Umbulla swalila nyongeza.

MHE. MARTHA J. UMBULLA: Mheshimiwa Spika,nashukuru kwa kuniona.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa hamasa kubwa kwavijana waajiriwa katika shule zetu hasa za maeneo yapembezoni pamoja na vituo vya afya na zahanati, ni kulekuwepo kwa mitandao ya simu na umeme wa uhakika, kwakuwa vijana wetu kwa kweli wanapenda kutumia simu zamikononi katika mitandao hiyo kwa uhakika; na kwa kuwamaeneo yetu ya vijijini hasa katika Mkoa wetu wa Manyarana kwingineko maeneo ya pembezoni, huduma hiyo yaumeme na mitandao ya simu haipo.

Je, Serikali hasa Wizara ya Utumishi ina mikakati ganimahususi ya kuwa na mawasiliano ya karibu kuhakikishakwamba katika maeneo ya pembezoni katika shule hasa zasekondari na vituo vya afya kunakuwepo na umeme ili kutiahamasa ya waajiriwa waendelee kuishi maeneo hayo?(Makofi)

SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YAUTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika,nipende tu kusema kwamba kwa utafiti uliofanywa na bodiyetu ya mishahara katika utumishi wa umma mwaka 2014/2015, moja ya changamoto ambazo zilibainika, kwanzakatika mazingira haya magumu inategemeana na sekta kwasekta maeneo mengine jiografia, hali ya miundombinu,huduma za kijamii zilizopo; lakini pia nafurahi kwambaametaja suala zima la mitandao ya simu pamoja na umeme.(Makofi)

Page 23: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

23

Mheshimiwa Spika, nipende kumuhakikishia tukwamba kupitia ripoti ile ya utafiti tulitoa maelekezo kwaMamlaka za Serikali za Mitaa, lakini pia tumewasilisha katikaWizara husika ikiwemo Wizara ya Nishati na nyinginezokuhakikisha kwamba wanapopanga mipango yao yamaendeleo basi wanatoa vipaumbele katika maeneo hayayenye mazingira magumu.

SPIKA: Tunaendelea Waheshimiwa, lakini wakatitunaendelea Mheshimiwa Naibu Waziri TAMISEMI,Mheshimiwa Jaffo, hawa walimu wa sayansi ambaowalipangiwa kwenye Halmashauri mbalimbali wamekuwawakipangiwa huko kwa kupangwa moja kwa moja kutokaTAMISEMI; nafikiri jambo hili mliangalie lina matatizo makubwasana. Ni vizuri Halmashauri zenyewe zikaangalia maeneoambayo wana uhaba mkubwa zaidi wa walimu wakawezaku-allocate. Shule kadhaa hazina walimu kabisa, ukiuliza kwanini unaambiwa wanakuja wameshakuwa allocated kwendakwenye shule ambazo tayari zina walimu, kwa hiyo, tatizolinaendelea kuwa kubwa. (Makofi)

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, MheshimiwaMuhammed Amour Muhammed, Mbunge wa Bumbwini, kwaniaba yake Mheshimiwa Abdallah Mtolea.

Na. 464

Tatizo la Kuvuja Kwa Mitihani Nchini

MHE. ABDALLAH A. MTOLEA (K.n.y MHE. MUHAMMEDAMOUR MUHAMMED) aliuliza:-

Kumekuwa na tatizo la kuvuja kwa mitihani ya Taifahapa nchini hususani ile ya kidato cha nne (CSEE) haliinayoondoa ufanisi hasa ikizingatiwa matokeo yanayotokayamejaa udanganyifu.

Je, Serikali ina mpango gani wa kudhibiti tatizo hili?

Page 24: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

24

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIAalijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia napenda kujibu swali la MheshimiwaMuhammed Amour Muhammed, Mbunge wa Bumbwini kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali imeweza kudhibiti nakuondoa tatizo la kuvuja kwa mitihani ya kidato cha nne,ambapo kwa mara ya mwisho ilikuwa ni mwaka 2008 katikasomo la hisabati pekee. Changamoto inayoendeleakujitokeza ni kwa baadhi ya watahiniwa kujihusisha naudanganyifu wakati mitihani inapofanyika kwa kuingia katikachumba cha mtihani na vitu visivyoruhusiwa kama vile notesna simu ya mkononi kwa ajili ya kufanya mawasiliano ndaniya chumba cha mtihani.

Mheshimiwa Spika, Wizara yangu imeendeleakujidhatiti na kuikabili changamoto ya udanganyifu katikamitihani kwa kuimarisha usimamizi na kutoa elimu kwawatahiniwa kuhusu madhara ya kufanya udanganyifu. Wizaraimekuwa ikitoa adhabu ikiwa ni pamoja na kufutiwa matokeoya mitihani pale inapothibitika kuwepo kwa udanganyifu huo.Mfano, watahiniwa waliofutiwa matokeo ya mtihani wakidato cha nne mwaka 2011 ni 3,303, mwaka 2012 ni 789,mwaka 2013 ni 272, mwaka 2014 ni 184, mwaka 2015 ni 87 namwaka 2016 ni 126.

SPIKA: Mheshimiwa swali la nyongeza.

MHE. ABDALLAH A. MTOLEA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi na mimi niulize maswalimawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, umekuwa ni utaratibu wakati wamtihani wa kidato cha nne Serikali inapeleka askari tenaaskari wenye silaha kwenda kuwasimamia watoto wakatiwanafanya mtihani. Kitendo hiki kinawatia uoga wanafunzikwa sababu hawajazoea kusimamiwa na askari wakati

Page 25: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

25

wakifanya mitihani au wakati wanajisomea, hivyowanapoteza concentration katika mitihani na hiiinawapeleka wengine kufeli.

Je, Serikali haina njia mbadala ya kuhakikishakunakuwa na ulinzi lakini usiotisha kama vile kuweka askariambao hawana uniform na hawana silaha ili wawezekuwasimamia watoto hawa? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, tunaaminishwakwamba mtihani wa mwisho sio pekee ndiyo unaomfanyamtoto afaulu katika mitihani yake ya kumaliza kidato channe, kwamba continuous assessment inachukua asilimia 50na mitihani ya mwisho inachukua asilimia 50, kama hili nikweli kuna sababu gani ya kuweka ulinzi mkubwa wakatiwa mtihani wa mwisho wakati ule unachangia tu asilimia50? Je, ulinzi huo pia unawekwa kwenye zile continuousassessment ili kufanya usawa? (Makofi)

SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu Waziri,anachouliza Mheshimiwa watoto wa Kibiti wapi kule wakionabunduki zile mtihani watafanya kweli? Mheshimiwa NaibuWaziri. (Kicheko)

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Spika, kimsingi tunapoweka ulinzi lengo sikuwatisha watahiniwa bali kuhakikisha kwamba mazingirahayo yanakuwa salama kabisa. Kama ambavyoimeshuhudiwa katika siku za karibuni, hali ya uhatarishiimekuwa ikijitokeza katika aina tofauti tofauti. Kwa kwelisiamini kama wanafunzi wa Kitanzania wanawezawakamuogopa askari kwa sababu ni maisha yao ya siku zote,hawezi akawa hamuoni kabisa askari, karibu kila mahali nchihii imeimarisha ulinzi na askari kama polisi tuko nao siku zotetena kuna ulinzi jumuishi na shirikishi.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kwa misingi hiyo miminadhani kwamba lengo la muhimu lieleweke kwamba nikuhakikisha kwamba tunaweka mazingira salama kabisaambayo wanafunzi wale badala ya kuogopa askari kwao ni

Page 26: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

26

suala la usalama ili wafanye mitihani yao bila kupatauhatarishi wa aina yoyote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa kupimwa kwakufuata matokeo endelevu (continuous assessment), ni kwelitumekuwa tukifanya hivyo na hiyo haiwezi kuwa ndio sababuya kusema kwamba kwa sababu marks tunazozitegemeamwishoni ni asilimia 50 tu, basi tusiwawekee mazingira yausalama. Tutaendelea kufanya hivyo, na kwa sababu umetoahoja hiyo, tutafanyia kazi kama tukiona kweli mwanafunzianaogopa sana askari tutajua namna bora zaidi ya kufanya.

SPIKA: Nilikuona Mheshimiwa Waitara na MheshimiwaJames Mbatia.

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana, naomba niulize swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, mitihani ya kidato cha nne tunajuainatumika kwa lugha gani lakini kuna mitihani ya darasa lasaba ambapo mitihani hii inatungwa maswali ya kuchaguayote. Sasa nilikuwa naomba niiulize Serikali ni lini mtaanzakutunga mitihani ambayo si ya kuchagua, hasa katikamasomo ya hesabu ili watoto wetu wapimwe uelewa badalaya kuchagua na wengine wanabahatisha kufaulu kwendasekondari? Swali langu ni hilo.

SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri Elimu, majibutafadhali.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Spika, ahsante sana.

Mheshimiwa Spika, ni kweli kumekuwa na mtazamowa wadau tofauti tofauti katika maswali ya kuchagua hasakatika mitihani ya hisabati. Serikali nasi pia tumekuwatunaliangalia hilo japo katika utafiti uliofanyika ilioneshakwamba kuchagua peke yake hakumwezeshi mtu kufauluisipokuwa lazima kwanza awe ana msingi wa kujua swalianalolifanyia uchaguzi.

Page 27: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

27

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, kwa siku za nyumahasa kipindi chetu sisi, ni kwamba hata kama unakuwa namtihani wa kuchagua ilikuwa bado unakuwa na sehemuya kufanyia kazi ambayo na yenyewe inakuwa ni sehemu yakuiangalia. Kwa hiyo, tutaona namna gani tuweze kufanyahivyo ili yule anayekuwa amechagua tuweze pia kupatauthibitisho isiwe tu kwamba swali la mwisho ndio jibu lakuliangalia, lakini ni suala ambalo linafanyiwa kazi. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa James Mbatia swali la mwishokwa eneo hili.

MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Spika, nashukuru.

Mheshimiwa Spika, lengo la nne la maendeleoendelevu ya dunia ni elimu bora, sawa, shirikishi kwa wote.Suala la mitihani na udanganyifu ni mchakato mdogo to endproduct. Sasa Serikali ina weka lini au itaanzisha lini chombocha kudumu cha kuangalia mchakato mzima wa elimu yaaniubora wa elimu, kuwekeza kwenye miundombinu ya elimukwa walimu, ukaguzi, vyote yaani quality assuranceitaanzishwa lini chombo hiki ili elimu yetu, mitihani iwe nisehemu ndogo tu kama ilivyo nchi ya Finland ambapo asilimiakumi tu ndiyo ile mitihani lakini mchakato mwingine wote wakumuandaa mtoto unakuwa umeandaliwa naumesiamamiwa na chombo chenye mamlaka nakinachojitegemea? (Makofi)

SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu Waziri.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Spika, wizara imeliona hilo. Ni kwamba kwa sasahivi kwanza tunaiangalia upya Sheria yetu ya Elimu kwasababu ni ya muda mrefu na kuna mambo mengiyamejitokeza na hiyo tungependa iendane na uhalisia.Vilevile tunataka kuangalia mfumo mzima wa namna yaukaguzi. Kwa mfano mwanzo tulikuwa na ukaguzi katikasehemu za kanda na kwenye Halmashauri/kwenye Wilayazetu lakini sasa hivi baada ya kuongeza shule nyingi,inaonesha kwamba sasa kanda peke yake si sehemu sahihi

Page 28: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

28

badala yake tungeweza kuangalia mfumo mzima natukauboresha zaidi. Hii ni kwa sababu sasa shule za Serikalikwa mfano za sekondari zimeshaongezeka sana.

Mheshimiwa Spika, vilevile tunaona kwamba haitoshitu kuangalia shule ina walimu wangapi, madarasa mangapina vyoo vingapi, tunataka tuangalie mfumo mzima, na hivyowizara sasa hivi inaandaa Mfumo wa Uthibiti na Tathminikwa ujumla (National Schools Assurance Framework) ambayoitawezesha sasa hata kama unafanyika ukaguzi unakuwatayari una mwongozo unaokwambia ni nini unatakiwaufuatilie. Vilevile hata kushirikisha kamati za shule pamojana walimu na wananchi wenyewe kwa ujumla katikakudhibiti ubora wa elimu Tanzania. (Makofi)

Na. 465

Mkakati wa Kubadilisha Maji ya Bahari kwa Matumizi yaKawaida

MHE. FAIDA MOHAMED BAKAR aliuliza:-

Kumekuwa na upungufu mkubwa wa maji safi nasalama kutokana na kuongezeka kwa idadi kubwa ya watunchini na mpaka sasa nchi yetu bado inategemea majikutoka vyanzo vichache kama mabwawa, mito, maji yamvua na kadhalika.

Je, Serikali ina mkakati gani maalum wa kubadilishamatumizi ya maji ya bahari kwa ajili ya matumizi ya kawaidaili kupunguza au kuondoa kabisa tatizo la upatikanaji wamaji nchini?

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji naUmwagiliaji naomba kujibu swali la Mheshimiwa FaidaMohamed Bakar, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Page 29: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

29

Mheshimiwa Spika, nchi yetu kwa sasa kulingana natakwimu zilizopo ina maji juu ya ardhi na chini ya ardhiyanayofaa kwa matumizi mbalimbali kiasi cha kilomita zaujazo elfu 96.27, ambapo kila mwananchi ana uwezo wakupata maji wastani wa mita za ujazo 1,800 kila mwaka hadimwaka 2035 iwapo hatua madhubuti zitachukuliwa zakusimamia rasilimali za maji. Kiwango hicho cha maji kwakila mtu kwa mwaka ni kikubwa ukilinganisha na kiwangocha chini cha mahitaji ya maji kwa kila mtu kinachokubalikakimataifa cha mita za ujazo 1,700 kwa mwaka.

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na jitihada zakukabiliana na changamoto ya kupungua kwa rasilimali zamaji ikiwa ni pamoja na uhamasishaji wa uvunaji maji ya mvuaili nchi yetu isifike kiwango kikubwa cha uhaba wa maji nakusababisha athari kwa maendeleo ya nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa maji yaliyopoyanatosha, na gharama za uwekezaji katika maji ya baharikwa matumizi ya kawaida ni kubwa Serikali itaendeleakutumia vyanzo vingine vilivyopo, na endapo itabainikavyanzo hivyo vimepungua maji Serikali itajielekeza kuwekezakatika maji ya bahari kwa ajili ya matumizi ya kawaida.

SPIKA: Mheshimiwa Faida Mohamed Bakar swali lanyongeza.

MHE. FAIDA MOHAMED. BAKAR: Mheshimiwa Spika,ahsante sana kwa kunipatia nafasi ya kuuliza maswali mawiliya nyongeza. Pamoja na majibu mazuri ya MheshimiwaNaibu Waziri naomba kuuliza maswali yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Mheshimiwa NaibuWaziri amejibu hapa kwamba maji yanatosheleza kulinganana ujazo uliopo, lakini cha kushangaza ni kwamba maji hayohasa vijijini hayapatikani kwa ukamilifu.

Je, Serikali ina mkakati gani wa haraka wakuyasambaza hayo maji anayosema yapo, maana kuwepotu ardhini na juu ya ardhi si sababu ya kuyasambaza maji

Page 30: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

30

hayo ili yawafikie wananchi na kuwapunguzia matatizohususani wanawake? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa maji ya baharinitunayaona, hasa mvua ikinyesha maji ya mvua yanaelekeabaharini, mwisho wake ni baharini. Je, Serikali ina mkakatigani wa kujenga mabwawa yaliyo mengi katika nchi yetukila eneo ili kuyahifadhi maji hayo kwa matumizi yawananchi? Ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Majibu ya maswali hayo mawaili Naibu Waziriwa Maji na Umwagiliaji Mheshimiwa Engineer IsackKamwelwe.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:Mheshimiwa Spika, swali lake la kwanza ni kwamba kwelikuna kiwango kikubwa cha maji hapa nchini, lakini yapomaeneo hapa nchini ambayo hayana maji. Hilo ni kwelikabisa kwamba yapo maeneo na ndiyo maana Serikalikuanzia bajeti ya mwaka 2006/2007 ilianzisha Programu yaMaendeleo ya Sekta ya Maji. Malengo yake ni kuhakikishakwamba tumeyachukua haya maji na kuyafikisha maeneoambayo yana ukame. Programu hiyo imeenda mpaka Junimwaka 2015, na sasa hivi tumeingia kwenye awamu ya pili.

Mheshimiwa Spika, lakini matokeo ya programu hiyoni nini? Tayari tumesaini mikataba ya kutoa maji Ziwa Victoriakupeleka Shinyanga na sasa hivi tumesaini mkatabamwingine tunatoa Shinyanga kupeleka Nzega, Tabora hadiIgunga. Hiyo ndiyo tunaendelea utekelezaji wa kuichukuasasa hiyo hazina ya maji iliyopo ili tuweze kuyasambaza kwawananchi, na tunapoyapeleka tunapita kwenye vijijimbalimbali vingi kuhakikisha wananchi wanapata maji.

Mheshimiwa Spika, swali la pil i ni kweli mvuazinanyesha ni nyingi katika nchi yetu na maji haya yanapoteayanakwenda baharini, tunafanyeje? Tayaritumeshatengeneza utaratibu, tumeagiza kila Halmashaurikila mwaka kwenye bajeti zao watenge fedha ili kuhakikishawanavuna maji. Si hilo tu, ni kwamba kwenye maeneo

Page 31: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

31

ambayo Halmashauri wanahitaji hayo maji kwa ajili yawananchi kupata maji safi na salama, Wizara ya Maji naUmwagiliaji pia tunatoa fedha kwa ajili ya kujenga hayomabwawa madogo na ya kati. Pia tunaendelea sasakujenga mabwawa makubwa ya kimkakati ambayoyatazalisha umeme wakati huo huo tutapata maji kwa ajiliya umwagiliaji na tutapata maji kwa ajili ya matumizi yabinadamu. (Makofi)

SPIKA: Nilikuona Mheshimiwa Rhoda Kunchele naMheshimiwa Goodluck Mlinga.

MHE. RHODA E. KUNCHELA: Mheshimiwa Spika,ahsante. Mkoa wa Katavi bado una changamoto ya kupatamaji safi na salama, lakini kibaya zaidi katika Jimbo la Kataviambalo ni Jimbo la Mheshimiwa Waziri, katika maeneo yaSongambele, Kamsisi na Ilunde hakuna maji kabisa. SasaMheshimiwa Waziri ni lini utapeleka maji kwa sababuwananchi hawa umewatelekeza kwa muda mrefu? (Kicheko)

SPIKA: Hilo si swali, ni tuhuma. Hata hivyo MheshimiwaWaziri kwa kuwa upo ni vizuri ukasema kidogo jinsi ganiunawapenda wananchi wako.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:Mheshimiwa Spika, nijibu tu swali kwa ufupi kwa MheshimiwaRhoda Kunchela kwa sababu amechokoza jimbo langu.

Mheshimiwa Spika, Kamsisi wana visima vitatu tayarina wanapata maji. Songambele wana visima vinne na tayariwanapata maji, Ilunde tayari wana visima vitano na tayariwanapata maji, ndiyo tunaongeza vingine, kwa hiyo tayarijimbo langu linatendewa haki. (Makofi)

SPIKA: Safi sana, Mheshimiwa Mlinga.

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa Spika,ahsante sana. Kwa niaba ya Wanaulanga kwanza naombaniishukuru Serikali kwa ukamilishaji wa Daraja la MtoKilombero, haya ndiyo matunda ya Serikali ya CCM. (Makofi)

Page 32: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

32

Mheshimiwa Spika, maeneo ambayo yanazungukaMto Kilombero yana shida kubwa sana ya maji…

SPIKA: Mheshimiwa Mlinga, Daraja la Kilombero lipi?

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa Spika,Daraja la Mto Kilombero la kwenda Ulanga, limelamilika.

SPIKA: Lile kubwa kabisa?

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa Spika, lilelimekamilika, lile kubwa kubwa.

SPIKA: Limekamilika?

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa Spika,kabisa na tunapita pale. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana.

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa Spika, swalilangu ni hili, maeneo ambayo yanazunguka huu MtoKilombero yana shida kubwa sana ya maji kwa upandeWilaya ya Kilombero, kwa maana ya Ifakara Mjini, pamojana Tarafa ya Lupilo. Je, sasa Wizara ina mpango gani wakubadilisha matumizi ya Mto Kilombero ili uwe unatumika kwamatumizi ya binadamu, kwa maana ya maji ya kunywa nakupikia?

SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu Waziriwa Maji na Umwagiliaji.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:Mheshimiwa Spika, kwa bahati nzuri nimetembelea Morogorokwenye Majimbo yote na Halmashauri zote, nimefika mpakaMto Kilombero. Kwanza baada ya kuvuka Kilombero, Lupilopale tayari tulishaweka mfumo wa maji na wananchiwanapata maji safi na salama. Maeneo mengi tunaendeleakuhudumia kwa kutumia Bonde la Mto Kilombero, lakinimawazo yako pia pale itakapofika sasa inahitajika tutajenga

Page 33: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

33

bwawa kulingana na uwekezaji uliopo na idadi ya watuwaliopo. Tutajenga bwawa kubwa Mto Kilombero ili tuwezekuwahudumia wananchi. Lakini kwa sasa bado tunaendeleakutumia Bonde la Mto Kilombero, wananchi wote wanapatamaji safi na salama.

Na. 466

Mlundikano wa Viwanda vya Simenti Ukanda wa Pwani

MHE. ZAYNABU M. VULU (K.n.y. MHE. MARIAM N.KISANGI) aliuliza:-

Kumekuwa na mlundikano wa viwanda vingi vya ainamoja katika kanda moja, kwa mfano kumekuwa na viwandavingi vya saruji (cement) katika Mikoa ya Dar es Salaam,Pwani, Lindi na Mtwara.

Je, Serikali imejipanga vipi kukabiliana na tatizo hilo ilikuondoa changamoto za madhara ya athari kwa binadamuwanaoishi maeneo hayo?

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI (K.n.y.WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji, naomba kujibu swali la MheshimiwaMariam Nasoro Kisangi, Mbunge wa Viti Maalum, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, uamuzi wa wapi kiwandakijengwe kwa kiasi kikubwa hutegemea uwepo wa soko labidhaa itakayozalishwa na/au upatikanaji wa malighafi na/au teknolojia.

Mheshimiwa Spika, maeneo ya Ukanda wa Pwanikuanzia Tanga mpaka Mtwara wanayo faida ya kuwa namalighafi nyingi na yenye ubora wa hali ya juu wautengenezaji wa saruji. Lakini pia inapotokea malighafi hiyoinaagizwa kutoka nje ya nchi, viwanda vilivyoko Pwani

Page 34: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

34

vinakuwa na faida katika unafuu wa gharama za usafirishaji.Vile vile kihistoria soko kubwa la saruji na hata bidhaa nyingineni Ukanda wa Pwani na hasa Dar es Salaam, si kwa nia mbayaviwanda kulundikana katika eneo hilo.

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kuondoachangamoto za madhara ya shughuli za viwanda kuwandani ya makazi ya watu wanaoishi maeneo ya karibu kupitiaSera ya Mazingira, ambapo kwanza kabla ya kiwandakujengwa katika eneo husika, Tathmini ya Athari za Mazingira(Environmental Impact Assessment) hufanywa. Zoezi hilihufanywa na Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) kwakushirikiana na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na Wizarainayosimamia.

Mheshimiwa Spika, pili, baada ya kiwanda kuanzakufanya kazi Ukaguzi wa Athari za Mazingira (EnvironmentalAuditing) hufanyika kila baada ya mwaka mmoja. Tatu,Serikali huhamasisha matumizi ya teknolojia rafiki kwamazingira. Kwa mfano matumizi ya Electrostatic precipitator,west scraper ili kuzuia vumbi kusambaa hewani na kwenyemakazi ya watu. Wizara yangu kwa kushirikiana na Ofisi yaMakamu wa Rais, Muungano na Mazingira inaendelea kutoamafunzo na kusimamia Sheria ya Mazingira ili kuepushamadhara yatokanayo na shughuli za viwanda nchini.

MHE. ZAYNABU M. VULU: Mheshimiwa Spika, ahsantesana.

Mheshimiwa Spika, awali ya yote niipongeze Serikaliya Awamu ya Tano kwa juhudi zake za kuhakikisha viwandavinakuwa vingi nchini.

Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri yaMheshimiwa Naibu Waziri, nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, katika majibu yake ya swali lamsingi amegusia upatikanaji wa faida kwa kuhusisha kwakuwa na miundombinu rahisi kwa kufikisha malighafi kwenyeviwanda.

Page 35: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

35

Je, Mheshimiwa Waziri atakubaliana na mimikwamba hadi sasa baadhi ya maeneo miundombinu yabarabara si rafiki kwa magari yanayobeba bidhaa, halikadhalika miundombinu hiyo haileti ti ja kwawafanyabiashara wa viwanda na wanaokwenda viwandanikununua na kupelekea walaji kwa maana ya wananchikuwauzia?

Je nini mpango wa Serikali wa kuhakikishamiundombinu hiyo itaboreshwa na kuimarishwa ili kuwapanafuu wale wanaozalisha na wanunuzi wa hizo bidhaa?(Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, Mheshimiwa NaibuWaziri, ningependa kujua, viwanda vinapoanza kunakuwana utaratibu wa kuangalia hali ya mazingira rafiki kwawananchi. Viwanda vile vinapoongezwa kwa maana yawanavyopanua au kuongeza idadi ya miundombinu yauzalishaji mali.

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuangalia usalamawa raia wanaozunguka kiwanda, hali kadhalika na walewanaofanya kazi katika viwanda vile? Tumeshuhudia wengiwakiathirika, naomba majibu ya maswali hayo.

SPIKA: Majibu ya maswali haya Mheshimiwa NaibuWaziri Engineer Isack Kamwelwe.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI (K.n.y.WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI):Mheshimiwa Spika, ninaamini kwamba Mheshimiwa Mbungeyupo Tanzania. Serikali ya Chama cha Mapinduzi katika sualala miundombinu yeye mwenyewe ni shahidi, kila konazinajengwa barabara za lami ili kuunganisha Mikoa na Wilayakwa barabara imara zinazopitika mwaka mzima.

Mheshimiwa Spika, kuhusu upande wa umeme,maana mali ikishazalishwa inahitaji kusafirishwa kwenda kwawananchi inatumia barabara, lakini pia kuna miundombinuimara na Wizara ya Nishati na Madini inaendelea kuweka

Page 36: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

36

umeme wa msongo mkubwa ili viwanda visipate shida kwaajili ya kupata power, pia pamoja na matumizi ya gesi. Kwahiyo, suala la miundombinu, Mheshimiwa Mbungelinakwenda vizuri.

Mheshimiwa Spika, lakini pia ni mwaka huu tu kupitiaTAMISEMI tayari na ninyi Waheshimiwa Wabunge ni mashahidi,tumeunda Rural Road Agency ili kuhakikisha sasa utekelezajiwa barabara zile ndogo (feeder roads) zinafika kila kona ilimali zinazozalishwa viwandani ziweze kwenda kwawananchi.

Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la usalamaviwandani; kuna usalama kupitia kwenye mazingira, lakinikuna usalama wa watumishi wanaofanya kazi ndani yaviwanda. Suala hili linashughulikiwa vizuri sana na idara husikaya mazingira kuhakikisha kwamba matatizo yanayojitokezandani ya viwanda hayaathiri wananchi wanaoishi katikamazingira ya pembezoni mwa kiwanda kama tulivyojibukatika swali la msingi, lakini pia yapo masuala ya usalamayanayokuwa-addressed ndani ya watumishi kwenye viwanda.

SPIKA: Majibu ya nyongeza Mheshimiwa Naibu Waziri,Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS,MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Spika, nashukurukwa nafasi uliyonipa, lakini nimpongeze sana MheshimiwaNaibu Waziri kwa majibu mazuri na Mheshimiwa Vulu kwamaswali yake mazuri sana ya mazingira hapa Bungeni.

Mheshimiwa Spika, ameuliza swali l inalohusumiundombinu. Actually, kama Mheshimiwa Naibu Wazirialivyoeleza, kwamba tunafanya tathmini ya mazingira kablakiwanda hakijaanza ili kuona kwamba kiwanda hicho mahalikinapowekwa kama hakitakuwa na madhara yoyote katikamazingira au kwa wananchi wanaoishi katika eneo hilo.

Mheshimiwa Spika, sasa pale inapojitokeza kiwandakinataka kupanua miundombinu yake katika eneo husika,

Page 37: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

37

tunafanya tena tathmini ya athari kwa mazingira il ikujiridhisha, je, upanuzi na miundombinu inayoongezwahaitakuwa na athari yoyote ile kwa mazingira? Kwa hiyo,Mheshimiwa Vulu wala asiwe na wasiwasi, kila kiwandakinapopanua miundombinu huwa tunashiriki na kujiridhishakwamba hakuna athari yoyote ile kwa mazingira.

SPIKA: Mheshimiwa Lucy Magereli nilikuona swali lamwisho la nyongeza.

MHE. LUCY S. MAGERELI: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa fursa ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, katika Wilaya ya Kigamboni, Kataya Kimbiji, tuna Kiwada cha Saruji cha Nyati. Nimesikia majibuya Mheshimiwa Naibu Waziri kwamba kuna EnvironmentalImpact Assessment ambayo hufanyika lakini tunachangamoto kubwa sana ya vumbi linalotimka kutokakiwandani katika kata ile. Bahati mbaya kabisa kile kiwandakiko katikati ya makazi ya watu. Sasa hivi minazi yetu Kimbijihaizai, miembe haizai, michungwa haizai, mazao ya mahinditukilima kuvuna tunashindwa kwenda kulima kwa sababupanakuwa na vumbi kali sana ndani ya mazao ambayotunayalima.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Naibu Waziri,naomba utusaidie kwenye hili, ni kweli Environmental ImpactAssessment ilifanyika, na je ilitoa majibu sahihi? Mbonatunapata adha hii kubwa namna hii? Ahsante.

SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu waRais, majibu ya swali hilo.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS,MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Spika, Kiwandacha Nyati, nilipokea malalamiko ya kiwanda hiki na baadaya kuletwa, yalikuwa malalamiko mengi sana dhidi yauchafuzi wa mazingira ya kiwanda hiki. Kwanza, nimhakikishieMheshimiwa Mbunge kwamba Environmental ImpactAssessment ilifanyika katika kiwanda hicho na kiwanda

Page 38: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

38

kikajengwa, japokuwa katika utekelezaji wake zilijitokezachangamoto.

Mheshimiwa Spika, nilipokwenda kwenye ziara hiyokulikuwa na changamoto ya hilo suala la vumbi, lakini sualala vumbi NEMC walikwenda kushughulika pamoja nakiwanda na kuhakikisha kwamba changamoto hiyoimetatuliwa. Kulikuwa na changamoto ya kulipa fidiawananchi waliokuwa wanaishi karibu sana na kiwanda,wananchi hao wote wamekwisha kulipwa fidia mpaka sasahivi tunavyozungumza.

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na tatizo la yale makaaya mawe kwamba yalikuwa yako nje na yalikuwa mvuazikinyesha yanatiririka mpaka kwenye vyanzo vya maji nakuchafua vyanzo hivyo. Tatizo hilo lilishughulikiwa na sasamakaa hayo hayaendi tena kwenye vyanzo vya maji. Kamabado kuna tatizo hilo analolizungumza sasa hivi MheshimiwaMbunge, tutakwenda kujiridhisha kuona kama kiwanda hichobado kina tatizo hilo na kuchukua hatua stahiki.

Na. 467

Umeme wa Gridi ya Taifa – Mkoa wa Katavi

MHE. TASKA R. MBOGO aliuliza:-

Mkoa wa Katavi hauna umeme wa Gridi ya Taifa.

Je, ni lini Mkoa huo utapatiwa umeme wa Gridi yaTaifa?

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI (K.n.y.WAZIRI WA NISHATI NA MADINI) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nishatina Madini, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Taska RestitutaMbogo, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi, kamaifuatavyo:-

Page 39: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

39

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu waMikoa ya Kusini Magharibi ikiwemo Katavi, Kigoma na Rukwakuunganishwa na umeme wa Gridi ya Taifa. Serikali kupitiaTANESCO imeanza utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa njiaya kusafirisha umeme wa Gridi Msongo wa kilowati 400 yenyeurefu wa kilometa 1,080 kutoka Mbeya – Sumbawanga –Mpanda – Kigoma hadi Nyakanazi.

Mheshimiwa Spika, mtaalam mshauri amekamilishakazi ya kudurusu taarifa ya upembuzi yakinifu kwa ajili yakuhuisha mradi kutoka kilovoti 220 hadi kilovoti 400. Utekelezajiwa ujenzi wa mradi huu utaanza mwezi Desemba, 2017 nakukamilika mwaka wa fedha 2018/2019 ambapo Mkoa waKatavi utaanza kupata umeme wa Gridi ya Taifa. Gharamaza mradi ni dola za Marekani milioni 664.

SPIKA: Mheshimiwa Taska swali la nyongeza.

MHE. TASKA R. MBOGO: Mheshimiwa Spika, pamojana majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, ninaomba kuulizamaswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa umeme wa gridimpaka kufika Mkoa wa Katavi utachukua muda mrefu; nakwa kuwa umeme hautoshi Mkoani Katavi, lakini pia napendakuishukuru Serikali kwa kushirikiana na Serikali ya Uholanzi kwaujenzi wa jenereta mbili na jenereta hizo zimeanza kufanyakazi kutoka tarehe 27 Mei, 2017 , lakini jenereta hizo hazitoshi.

Mheshimiwa Spika, umeme unaotakiwa Mkoa waKatavi ni megawati tano, jenereta zinazalisha megawati 2.2.Je, Serikali haioni umuhimu wa kuongeza jenereta nyinginembili kwa Mkoa wa Katavi? Kwa sababu mahali pa kuzifungajenereta hizo tayaripameshajengwa, maana eneo la hizojenereta limejengwa sehemu za kufunga jenereta nne, lakiniSerikali pamoja na Serikali ya Uholanzi imefunga jenereta mbili,eneo hilo lipo. (Makofi)

Meshimiwa Spika, je, Serikali haioni umuhimu wakuongeza jenereta mbili?

Page 40: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

40

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili; kwa kuwajenereta hizi zinatumia mafuta ya dizeli na ni gharama zaidi,je, Serikali haioni kwamba matumizi ya jenereta kwa Mkoawa Katavi ni gharama zaidi kuliko kufunga umeme wa gridi?Naomba kuwasilisha. (Makofi)

SPIKA: Majibu ya maswali hayo kwa kifupi MheshimiwaNaibu Waziri.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI (K.n.y.WAZIRI WA NISHATI NA MADINI): Mheshimiwa Spika, kwanzakabisa, maswali yake ni mazuri na kwa faida ya Mkoa waKatavi ambao na mimi mwenyewe natoka kule siwezi kuahidilakini niseme kwamba nitalifikisha hili ili waweze kuongezajenereta nyingine mpya kuongeza umeme. Lakini pia hayamasuala ni ya kiuchumi. Ipo historia kwamba matumizi yaumeme katika mkoa wetu, hasa katika masuala ya viwandabado hatujawa na viwanda vingi, kwa hiyo umeme sehemukubwa unatumika majumbani tu na taarifa iliyopo nikwamba TANESCO imekuwa inatoa gharama kubwa zaidikuliko makusanyo yanayofanywa kutokana na matumizi yaumeme, lakini suala hili tutalifikisha.

Mheshimiwa Spika, kuhusu swali la pili linalozungumziadizeli. Ni kweli kabisa kwamba kutumia dizeli ni gharamakubwa kabisa na ndiyo maana sasa hivi Serikali nzima inatakakwenda kwa kutumia umeme ama wa gesi au wa maji, nandiyo maana sasa Serikali imeshalitambua hili, inaleta umemewa msongo mkubwa ambao sehemu kubwa utatumiauzalishaji kwa kutumia maji badala ya kutumia dizeli. Kwahiyo, mawazo yako Mheshimiwa Mbunge ni mazuri na tayariSerikali imeshaanza kuyatekeleza.

SPIKA: Mheshimiwa John Mnyika nilikuona.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru.

Mheshimiwa Spika, tatizo la umeme wa Gridi ya Taifakutokufika kwa wananchi haliko tu Mkoa wa Katavi, bali

Page 41: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

41

pia liko katika Jimbo la Kibamba, Jijini Dar es Salaam ambapokwenye Kata ya Mbezi maeneo kama ya Msumi kwa Londahayana kabisa miundombinu ya umeme. Kata ya Goba kunamitaa ambayo haina umeme, Kata ya Msigani kuna mitaaambayo haina umeme, Kata ya Kwembe kuna mitaa hainaumeme, Kata ya Saranga kuna mitaa haina umeme na Kataya Kibamba kuna mitaa haina umeme.

Sasa kwa kuwa TANESCO iko jirani kabisa na Jimbola Kibamba, je, Serikali iko tayari baada ya Mkutano huu waBunge kufanya ziara maalum kwenye kata hizi zote sitakwenda kuwaeleza wananchi ni lini hasa maeneo hayayatapata umeme?

SPIKA: Majibu ya swali hilo kwa kifupi MheshimiwaNaibu Waziri.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI (K.n.y.WAZIRI WA NISHATI NA MADINI): Mheshimiwa Spika, nisemekwanza Serikali iko tayari ndiyo maana imeanzisha REA III, natayari maeneo mengi miradi imezinduliwa kuhakikishakwamba vijiji vyote tulivyonavyo katika Tanzania vinapataumeme. Kwa hiyo, tayari imeshaanza, lakini nisemeMheshimiwa Mbunge mimi na wewe ni Madiwani tunauwakilishi ndani ya Bunge.

Mheshimiwa Spika, ni kazi yetu sasa kwamba wewekwasababu ni Mbunge uko ndani ya Bunge na matamshihaya ya Serikali umeyasikia, urudi kwenye Jimbo lakoukawaambie kuwa “jamani sasa Awamu ya Tatu ya REAinafika na kwetu tunapatiwa vijiji moja, mbili, tatu” na vijijivyako vimeainishwa kwenye hotuba ya Mheshimiwa Waziriwa Nishati, kwa hiyo uende ukatoe taarifa.

SPIKA: Waheshimiwa mtaona kwamba muda haukoupande wetu, naomba sasa tusikilizane.

Waheshimiwa Wabunge, kuhusiana na wageniwalioko katika jukaa la Spika. Ninao wageni 23 waMheshimiwa Naibu Spika ambao ni washiriki na waandaaji

Page 42: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

42

wa shindano la Miss Tanzania kutoka Mkoani Dodoma.Naomba msimame pale mlipokaa, ahsanteni sana nakaribuni sana ma-miss. Rafiki zangu Wasukuma hawa ni ma-miss kutoka Dodoma, kama na ninyi mnao hebu tuone sikumoja mlete ma-miss wa Mwanza, Shinyanga, Tabora. (Makofi/Kicheko)

Wageni wa Waheshimiwa Wabunge; wageni 35 waMheshimiwa Antony Mavunde, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisiya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na WenyeUlemavu na Mheshimiwa Juma Nkamia ambao ni wachezajiwa timu ya Area C United-Dodoma na bingwa wa Mkoawa Dodoma waliopanda ligi daraja la pili. Area C Unitednaomba msimame hapo mlipo, karibuni sana na hongerenisana kwa kutubeba Mkoa wa Dodoma kuweza kuingiakatika ligi daraja la pili. Naamini katika muda mfupi ujaomtakuwa katika ligi daraja la kwanza. Hongereni sana nakaribuni sana. (Makofi)

Wageni tisa wa Mheshimiwa Josephine Genzabukeambao ni Waheshimiwa Madiwani kutoka Wilaya ya KasuluMkoani Kigoma, Waheshimiwa Madiwani, karibuni sanaBungeni. (Makofi)

Wageni sita wa Mheshimiwa James Mbatia ambaoni wazee wa kutoka Jimbo la Arumeru Mashariki, Kata yaNgarenanyuki, Kitongoji cha Momela wakiongozwa na MzeeSenyael Nnko. Wazee kutoka Momela karibuni sana wazeewetu. (Makofi)

Wageni 30 wa Mheshimiwa Seif Gulamali ambao niwanafunzi 28 na walimu wawili kutoka Shule ya Sekondariya Ulaya iliyoko Ikungi, Wilaya ya Igunga, Mkoani Tabora,karibuni sana! Mmependeza kweli Wanyamwezi ninyi, karibunisana! (Makofi)

Wageni waliotembelea Bunge kwa ajili ya mafunzoni wanafunzi 81 kutoka Chuo Kikuu cha Dodomawakiongozwa na Ndugu Sadiki Nuru, UDOM!! Karibuni sana

Page 43: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

43

wanafunzi wa UDOM, tunawatakia kila la heri muongeze bidiikatika mafunzo. (Makofi)

Wanafunzi 89 kutoka Chama cha Wanafunziwanaosomea taaluma ya Manunuzi na Ugavi kutoka ChuoKikuu cha Dodoma, karibuni sana. (Makofi)

Wanafunzi 30 na walimu kutoka Chuo ca UalimuCapital cha Mkoa wa Dodoma; karibuni sana wanafunzi waualimu kutoka Capital. (Makofi)

Lakini pia tuna wanafunzi 80 kutoka Chuo chaKumbukumbu ya Hurbet Kairuki Jijini Dare es Salaam. (Makofi)

Karibuni sana wanafunzi wote ambaommetutembelea siku ya leo, na baadaye maofisa wanguwa Bunge watawapatia maelezo mbalimbali kuhusu Bungena namna ambavyo linafanya kazi na mnaweza mkawapamoja nasi kufuatilia ni shughuli gani zinazoendelea.(Makofi)

Mwenyekiti wa ibada chapel ya Bunge, AnnaLupembe anawataarifu Waheshimiwa Wabunge kwambabaada ya shughuli zetu saa 7:00 mchana anawaombawanamaombi mkutane basement leo ambapo patakuwana maombi ya kuliombea Taifa na kumuombea Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania na yataongozwa naMtumishi wa Mungu Mheshimiwa Dkt. Getrude Rwakatare;saa 7:00 baada ya shughuli zetu hapa, wanamaombi wotebasement. (Makofi)

Katibu wa Bunge ameomba niwataarifuWaheshimiwa Wabunge kwamba saa 7:00 tukimaliza hapakutakuwa na semina ya Red Cross, kwa hiyo tutaombwatubaki, wale ambao tutaona inafaa kufanya hivyo ili tuwezekusikiliza masuala yanayohusiana na Red Cross.

Naomba baada ya hapa tufanye shughuli mojainayofuata halafu kama kuna wanaotaka miongozo

Page 44: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

44

nitawapa nafasi mbele kidogo tu lakini tufanye shughuli mojakwanza ili na mimi niweke meza yangu vizuri hapa mezani.

Katibu!

NDG. CHARLES J. MLOKA – KATIBU MEZANI:

MISWADA YA SHERIA ZA SERIKALI

Muswada wa Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusuMasharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi wa Mwaka2017 [The Natural Wealth and Resources Contrats (Review andRe-Negotiations of Unconscieonable Terms)] Bill, 2017.

Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusianana Umiliki wa Maliasili wa Mwaka 2017 [The Natural Wealthand Resources (Permanent Sovereignty) Bill, 2017].

Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya SheriaMbalimbali wa Mwaka 2017 [The Written Ammendment Laws(Miscellaneous Amendments) Bill, 2017].

(Kusomwa Mara ya Kwanza)

SPIKA: Ahsante sana.

Palikuwa na baadhi ya Waheshimiwa Wabungeambao sijui ilikuwaje, lakini majina sikuwa nimeyapata hapamezani kwenye orodha yangu, lakini nitambue uwepo wawageni wa Mheshimiwa Taska Mbogo wakiongozwa namume wake Ndugu John Kilowoko na watoto wake palemlipo karibuni sana na watoto wa Mheshimiwa Taska wapopale, karibuni sana. Mume wake Mheshimiwa Taska anafanyakazi kule UNHCR Ethiopia sasa sijui Rukwa na Ethiopiamnafanyaje kazi! (Makofi)

Mheshimiwa Cecilia Paresso ana wageni wakewanafunzi 15 kutoka UDOM, wale pale, karibuni sana.(Makofi)

Page 45: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

45

Pia Mheshimiwa Lema ana wageni wake piasikuwanao kwenye orodha kama wapo popote walipowageni wa Mheshimiwa Lema. Ahsante sana, karibuni sana,sikuambiwa ni akina nani, kwa hiyo, nimeshindwakuwatambua vizuri zaidi.

MHE. GODBLESS J. LEMA: Ni watoto wangu.

SPIKA: Ni watoto? Oooh, basi karibuni sana watotowetu.

Waheshimiwa Wabunge, mtaona mmegawiwakaratasi ya ratiba na mtaona kwamba ratiba hii ni ratibaambayo ina mabadiliko tofauti na ratiba mliyokuwanayomwanzo. Kwa hiyo, nitaomba kila Mheshimiwa Mbungeaiangalie ratiba hii na naomba sana tusikilizane WaheshimiwaWabunge mnaoongeaongea ili twende pamoja katikabaadhi ya mambo haya, mtaongea baadaye tena.

Kamati ya Uongozi i l ikaa jana na kupitia nakupendekeza kwamba tulete ratiba hii ambayo kila mmojawenu nina uhakika ameshagawiwa, ambapo leotunaendelea na Maazimio baada ya shughuli zetu. Keshokutakuwa na maswali baada ya maswali tutatawanyikakwenda kwenye Kamati mbalimbali kama nitakavyoeleza nashughuli hiyo itaendelea hadi siku ya Jumatano ambapokutakutakuwa na Hoja ya Kuahirisha Bunge tarehe 5 Julai.

Waheshimiwa Wabunge, baada ya tangazo hilo lakazi za Kamati ya Uongozi sasa nieleze maelezo ya Spikakama ifuatavyo na naomba mnisikilize.

MAELEZO YA SPIKA

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kama mlivyosikiamuda mfupi uliopita Makatibu wangu hapa wamesoma kwamara ya kwanza kuna Miswada mitatu ya Sheria ya Serikali.Kwa mujibu wa Kanuni zetu, Miswada hiyo sasa nitaipelekakwenye Kamati za Kudumu za Bunge ili ikafanyiwe kazi kamaipasavyo kwa utaratibu ufuatao:-

Page 46: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

46

Kwanza, ule Muswada mmojawapo ambaounasomeka kama Muswada wa Marekebisho ya Sheriambalimbali wa mwaka 2017 (The Written Laws MiscellaneousAmendments, Bill 2017) utafanyiwa kazi na Kamati ya Katibana Sheria inayoongozwa na Mheshimiwa Mohamed OmaryMchengerwa. Huo ni ule Muswada mmoja.

Pili, kwa mujibu wa Kanuni ya 7(3) ya Nyongeza yaNane, nimeunda Kamati ya Pamoja ambayo itafanya kaziya kuchambua Miswada miwili ya sheria ifuatayo:-

(i) Muswada wa Sheria ya Mapitio na Majadilianokuhusu Masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi waMwaka 2017 (The Natural Wealth and Resources Contracts(Review and Re-Negotiations of Unconscionable Terms) Bill,2017.

(ii) Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusianana Umiliki wa Maliasili wa Mwaka 2017 (The Natural Wealthand Resources (Permanent Sovereignty), Bill 2017.

Waheshimiwa Wabunge, Kamati hii ya pamojaambayo nimeiunda itaongozwa na Mheshimiwa DotoMashaka Biteko na itajumuisha Kamati nne ambazo ni Kamatiya Nishati na Madini; Kamati ya Katiba na Sheria; Kamati yaArdhi, Maliasili na Mazingira na Kamati ya Sheria Ndogo.

Narudia tena, Kamati ya Nishati na Madini; Kamatiya Ardhi, Maliasili na Mazingira; Kamati ya Sheria Ndogo naKamati ya Katiba na Sheria. Hawa kwa pamoja watapitiaile Miswada miwili na Mwenyekiti wao atakuwa ni Mwenyekitiwa Kamati ya Nishati na Madini. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, Kamati ya Pamoja itafanyakazi kuanzia leo Alhamisi tarehe 29 Juni, 2017 baada yashughuli zetu kwisha saa 7.00 mchana katika Ukumbi wa PiusMsekwa mpaka siku ya Jumatatu tarehe 3 Julai, 2017. Hadiduza Rejea itakuwa ni kuchambua Miswada hiyo miwili nakuandaa taarifa ambayo itawasilishwa hapa Bungeni sikuya Jumanne tarehe 4 Julai, 2017. (Makofi)

Page 47: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

47

Waheshimiwa Wabunge, kufuatia Miswada hiyo,ratiba ya Bunge kama nilivyosema imebadilika kwa kuongezasiku tatu za kazi kutoka tarehe 30 Juni, 2017 hadi tarehe 5Julai, 2017 ambapo tutaahirisha Mkutano huu wa Saba waBunge. Ratiba mpya inayoonesha mabadiliko hayo tayariimeshasambazwa na iko mikononi mwenu.

Waheshimiwa Wabunge, aidha, napenda kutoataarifa kwenu Waheshimiwa Wabunge na wananchi wotekwa ujumla kwamba, Miswada hii mipya mitatututakayoifanyia kazi imeshawekwa kwenye tovuti ya Bungeambayo ni www.parliament.go.tz. Kwa maana hiyo, baadaya Miswada hii kwenda kwenye Kamati kama nilivyosemaimmediately baada ya saa 7.00 Kamati zitaanza kukutana,zinazohusika na Miswada hii; wao ndiyo watapanga utaratibuwa kuwaalika wadau na ratiba yao ya kukutana na wadauitakuwaje na jambo hilo litafanyika kama taratibu zetu zilivyona shughuli zitaendelea kwa utaratibu huo.

Waheshimiwa Wabunge, haya maelezo niliyokuwanayatoa ni maelezo yanayotokana na maamuzi ya Kamatiya Uongozi iliyokutana jana saa 1.00 jioni katika Ukumbi waSpika. Sasa kwa hatua hii kama kuna watu walitaka miongozona nini, haya, Katibu nipatie majina.

Mheshimiwa Flatei Massay ana wageni wake watanopopote pale walipo pia wasimame!! Karibuni sana Wageni,karibuni sana. (Makofi)

MWONGOZO WA SPIKA

SPIKA: Mheshimiwa Gekul.

MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kunipa nafasi, naomba mwongozo wako kuhusujambo ambalo limejitokeza mapema hapa Bungeni wakatiwa maswali kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu. Kuna swali ambaloliliulizwa na Mheshimiwa Ritta Kabati juu ya zao la mahindina Mheshimiwa Waziri Mkuu alisema kwamba katazo hilolipo na maana yake Wakulima wetu wa mahindi hawatauzazao hilo nje ya nchi.

Page 48: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

48

Mheshimiwa Spika, naomba nipate mwongozowako; kama ndio msimamo wa Serikali ni kwanini sasa Serikaliisituambie wazi kupitia Waziri wa Kilimo au Mheshimiwa WaziriMkuu au kauli ya Serikali kwamba wamejipanga kwa kiasigani kwa NFRA kununua mahindi hayo ya wakulima. Kwasababu wananchi wetu wanategemea zao la mahindi kamazao la biashara na zao la chakula pia na wengine pia wanaexcess. Naomba nipate mwongozo wako kwa nini Serikaliisitufafanulie kwa kina badala ya kusema tu wametoa katazo,watuambie wamejipanga kwa kiasi gani ili wananchi wetuambao wanategemea zao hilo la mahindi wasipate hasara.

SPIKA: Nachukulia kama ni ushauri kwa Serikalikwamba unaiomba Serikali ingejipanga ije itoe kwa wakatiwake unaofaa ufafanuzi wa kina zaidi kuhusu suala la ununuziwa mahindi kutoka kwa wakulima wetu. Ni jambo jema,linapokelewa na ninaamini Serikali imelisikia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwita Waitara.

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru, mwongozo wangu ulikuwa unafanana naMheshimiwa Pauline Gekul, kwa hiyo naomba ni-withdraw.

SPIKA: Ahsante sana, Mheshimiwa Haonga.

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Spika,ninaomba muongozo wako kwa Kanuni ya 68(7) jamboambalo limetokea mapema.

Hivi karibuni kuna mchezaji wa Tottenham anaitwaVictor Wanyama aliingia Nchini kwetu na kwa bahati nzurisana akawa amepokelewa na Meya wa Ubungo NduguBoniface Jacob, wakati huo huo huyu mchezaji akawaameahidi kutengeneza ile barabara ya mtaa, akawaamepewa jina la mtaa lakini akasema kwambaatatengeneza barabara ya mtaa vizuri kwa kiwango chalami, atainua soka la nchini kwetu. Kwa bahati mbaya sanaMkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye tumekuwatukimlalamikia akaagiza kwamba…

Page 49: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

49

SPIKA: Samahani Mheshimiwa Haonga. Hilo jambolimetokea hapa Bungeni lini? (Kicheko)

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Spika,limetokea mapema siku za hivi karibuni. (Kicheko)

SPIKA: Tunaendelea Mheshimiwa Frank Mwakajoka.

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: Mheshimiwa Spika,ninashukuru sana kwa kunipa nafasi niweze kutoamwongozo wangu.

MBUNGE FULANI: Kuomba!

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: Kuomba Mwongozowako. Ninaamini kabisa kwamba wajibu wa Serikali nikuhamasisha wa Tanzania wengi na wananchi wengi waTanzania, kuhakikisha wanaingia kwenye mpango wa kilimona kuhakikisha wanazalisha chakula kwa wingi. Lakini Serikaliinawajibu wa kuhakikisha masoko yanapatikana ya chakulaambacho wanazalisha Watanzania hawa.

Mheshimiwa Spika, Watanzania hawa wanaofanyakil imo kama biashara ni wafanyabiashara kamawafanyabiashara wengine. Lakini wakulima hawa sasa hiviimetokea imekuwa ni tatizo na imekuwa ni kawaida yaSerikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kila wakatiinapofika kipindi cha mavuno, Serikali inatoa makatazowananchi wasitafute masoko…

SPIKA: Mheshimiwa Mwakajoka samahani, si ndio hilila Mheshimiwa Gekuli kwamba Serikali ije na maelezomapana zaidi.?

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: Mheshimiwa Spika,inatofautiana kidogo, huyu ameomba mimi siombi najaribukueleza hali halisi wakulima ni watu wa namna ganiMheshimiwa Spika.

Page 50: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

50

SPIKA: Kama huombi mwongozo basi kaa chini,ahsante sana. Mheshimiwa Heche. (Kicheko)

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Spika, mwongozowangu kwa sababu nipo kwenye boarder ya Sirari, nilikuwanataka kuongea suala la mahindi hilo hilo, sasa na withdraw.

SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Mnyika.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Spika, nashukuru,muda mfupi uliopita tumekabidhiwa hii ratiba ya Bunge namaelezo ambayo umeyatoa ya kwamba Mosi Serikali inaletamiswada mitatu kwa hati ya dharura. Lakini pili, katika hiyoMiswada mitatu kuna siku moja ambayo Miswada miwili yoteinajadiliwa kwa siku moja.

Mheshimiwa Spika, Bunge hili lina historia, mwaka 1997ilileta miswada ya madini na miswada ya kodi ikapitishwaharaka haraka hatimaye nchi imeingia kwenye matatizomakubwa ya madini ikiwemo hayo ya makinikia na madinikwa ujumla. Mwaka 2005, Bunge hili tena lilitewa miswadamitatu kwa siku moja kwa Hati ya Dharura, miswadailiyohusiana na masuala ya gesi, mapato na tasnia yauziduaji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kazi ya Bunge kwa Ibara ya 63 nikuishauri na kuisimamia Serikali, na Bunge ndio lenyemamlaka ya kutunga sheria na sisi Wabunge tulioko humundani, sisi ni wawakilishi wa wananchi. Kwa sababu sisiWabunge ni wawakilishi wa wananchi, na hii Miswadamitatu inayoletwa, Miswada kuhusu Mapitio ya Majadilianokuhusu Masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi,Muswada wa Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki waMaliasili na Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali.Miswada hii kwa umuhimu wake na kwa maslahi yake kwanchi ni vizuri sisi wananchi tukapata wasaa wa kukutana natunaowawakilisha ili tukapata maoni na mapendekezo yao.(Makofi)

Page 51: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

51

Mheshimiwa Spika, ni vema hii miswada ikasomwaleo kwa mara ya kwanza tu, Hati ya Dharura ikaondolewa,tukapata muda wa kurejea kwenda kukutana na wananchiwetu ili Miswada hii ikaletwa kwenye Bunge lijalo, Mkutanoujao wa Bunge tukaijadili na kuipitisha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukiondoa wananchi, Bunge hilivilevile linawategemea wadau. Kwa maelezo uliyoyatoa nikwamba wadau hawa sasa wanatakiwa kuitwa Dodomakwa short notice wafike Dodoma kuja kutoa maoni kwaKamati hapo Msekwa, kitu ambacho kitafanya wadau wengikukosa muda, sio tu wakuchambua haya maoni, bali kukosamuda wa kuja kutoa maoni. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sisi Wabunge vilevile, ni binadamu,Miswada mitatu inaletwa, tunatakiwa kwa muda mfupituichambue kifungu kwa kifungu, kipengele kwa kipengeletuweze kufanya marekebisho. Huu ni mtego, ni mtego wakutufanya tushindwe kutekeleza haki yetu ya Kibunge yakuishauri ya kuisimamia Serikali na haki yetu ya kibunge yakutunga sheria. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwahiyo, naomba mwongozowako kwamba, mapendekezo hayo ya kamati ya uongozi,kwa sababu Kamati ya Uongozi si Bunge ni sehemu tu yaBunge, sisi ndio Bunge. Mapendekezo haya ya Kamati yaUongozi yaweze kujadiliwa na Bunge hili, mapendekezo hayayaweze kutenguliwa, badala yake ratiba iondolewe hivi ilivyo,tupewe ratiba ambayo Muswada utasomwa kwa siku moja,tutakwenda kujadiliana. Naomba kutoa hoja kwambajambo hili li jadiliwe kama sehemu ya Haki, Kinga naMadaraka ya Bunge kwa mujibu wa Kanuni ya 51. Naombakutoa hoja.

SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Nchi nimekuona!

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Spika,kila jambo katika Bunge letu tukufu, linaongozwa na kanuniambazo tunazo. Masharti ya kutunga sheria na masharti ya

Page 52: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

52

jumla yanayoongoza mjadala unaohusu utungaji wa sheriandani ya Bunge letu Tukufu, yamewekwa katika Sehemu yaNane ya Kanuni za Bunge la Jamhuri ya Muungano waTanzania. Na masharti hayo, yanaongozwa na Kanuni ya 80na vifungu vyake vidogo na ukiendelea na Kanuni nyinginezilizopo.

Mheshimiwa Spika, Miswada ambayo tumeletambele ya Bunge lako Tukufu, imekuja kwa Hati ya Dharura.Na ili Bunge lako Tukufu lijiridhishe kama Miswada hii inastahilikujadiliwa na Bunge ama haistahili kujadiliwa na Bunge,kanuni ambazo zinatuongoza ni hizi zifuatazo na ninaombakwanza nizisome. Kanuni ya 80(4) inasema; Muswadawowote wa Sheria wa Serikali wa dharura hautaingizwakwenye shughuli za Bunge bila ya kuwa na hati iliyowekwasaini na Rais inayoeleza kuwa Muswada uliotajwa katika hatihiyo ni Muswada ambao unachukua sura hiyo kwambaunatakiwa uingie Bungeni Hati ya Dharura.

Mheshimiwa Spika, lakini Kanuni ya 80 (6) inaendeleakusema; iwapo kama Kamati ya Uongozi, itaona kuwaMuswada wa Sheria wa Serikali, iliowasilishwa kwa Hati yaDharura, haustahili kuwasilishwa kwa dharura, Kamati hiyoitaishauri Serikali ipasavyo. Lakini bado Kanuni hizozinaendelea kutupa maelezo; Muswada wowote ule ambaoumeletwa ndani ya Bunge lako na umekabidhiwa kwako namamlaka uliyonayo Mheshimiwa Spika, ili uweze kuonekanaunastahili kuingia ndani ya Bunge ama haustahili kuingiandani ya Bunge, utakwenda kutoa picha na muelekeo huo,baada ya kufika kwenye Kamati ya Bunge iliyopewa kazi yakujadili Muswada huo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kutoa maelezo hayo,naomba niseme mambo machache yafuatayo:-

La kwanza, sisi kama Serikali tumeshatimiza mashartiyote ya Miswada hii kuingizwa ndani ya Bunge lako Tukufu.Sababu za Miswada hii kuingizwa kwa Hati ya Dharuratumeshazikamilisha zote, Kamati ya Uongozi kwa mujibu wakanuni ilikuwa pia na wawakilishi wanaowakilisha Kambi ya

Page 53: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

53

Upinzani na tulijadiliana kwa pamoja umuhimu wa Miswadahiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini jambo ambalolitakaloendelea kutoka hapa, wanaoweza kulishauri Bungelako baada ya kuona uzito wa kazi iliyoletwa na Serikali,ukubwa wa Miswada, yaliyomo kwenye Miswada ni Kamatihusika zitakazopewa kazi ya kujadili Miswada hiyo. (Makofi)

La nne ambalo ni la mwisho nililolitaka kulisema hapa,haitakuwa ni busara na wala siamini kama ni utaratibu mzuri,sisi Wabunge kabla hatujaona maslahi mazito yaliyomokatika Miswada hiyo, tukajenga hoja ndani ya Bunge yakukataa maslahi mapana ya Taifa letu bila kuangalia kilekilichomo ndani ya Miswada hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwahiyo, nilikuwa naomba sana,tunapoendelea na jambo hili, tujue kwamba hata Wabungesisi tuliopo katika upande mwingine wa Bunge hili na sisitunawawakilisha wananchi na sio wenzetu tu peke yaowanawakilisha wananchi. Niliomba niyaseme hayo. (Makofi)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kama ilivyoelezwamwanzoni, kwa niaba yetu nilipokea Hati ya MheshimiwaRais, Hati ya dharula. Na kama ilivyo ada na wajibu,niwakumbushe Wabunge zamani kabla ya mwaka 2007 kwawale waliokuwepo wachache, ilikuwa Hati ya Dharurazinasemwa tu pale na Spika kwamba kuna Hati ya Dharura,Kamati ya Uongozi inaridhia na kadhalika. (Makofi)

Lakini tulipofanya mabadiliko ya Kanuni mwaka 2007,moja ya kitu tulichokiweka ni kwamba Hati ya Dharura yaMheshimiwa Rais itakuja hati yenyewe yenye sahihi yake ndaniya Kamati ya Uongozi. Kwa hiyo, baada ya kuipokea jana,Wajumbe wa Kamati ya Uongozi waliiona na pale ndanitukapewa na maelezo na sababu za kwa nini kuna haja yakufanyia jambo hili kazi katika udharura huo. Na nikisemaKamati ya Uongozi ni uwakilishi wa pande zote. Tulijadilianawote kwa pamoja, tukakubaliana kwamba tusonge mbele.(Makofi)

Page 54: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

54

Pia kama ambavyo Chief Whip ameeleza, kwa hatuahii tuliyofikia kwa taratibu zilivyo kwamba jambo hili liendekwenye Kamati na nimesema Kamati mbili zitahusika. Kamatimoja ni yale mambo ya kawaida (MiscellaneousAmendment) ambazo kwa taratibu zetu huwa inaendakwenye Kamati ya Katiba na Sheria ambayo Mwenyekiti wakeni Mheshimiwa Mchengerwa.

Kwa vile hiyo ndiyo kawaida, tukasema hiyoitaendelea na huo Muswada mmoja ambao kwa vyovyotevile huwa ni traditional tunapeleka kwenye Kamati hiyo. Lakinihii miswada miwili mingine ambayo ni midogo sananitakapoiangalia kwa maana vifungu vyake ni vichachevichache, lakini ni muhimu kwa Taifa letu. Tukasema kwambahii tupeleke Kamati nyingi zaidi kitu ambacho sio traditionyetu, lakini kwa ajili tu ya kuongeza uwazi, kuongeza uelewa,tukasema tupeleke kwenye Kamati nyingi zaidi, Kamati nnekwa mpigo, ambazo zenyewe zitafanya kazi kule MsekwaUkumbi wa Msekwa kuanzia leo mchana. Kulikuwa kunashida ya taa lakini sasa hivi wanafunga taa, kutakuwa namwanga wa kutosha. (Makofi)

Lakini pia Wabunge wengine wote kuanzia leomchana kuelekea huko jioni, kesho baada ya maswali,Jumamosi, Jumapili na kadhalika wote mnakaribishwakwenye kazi za Kamati hizo kushiriki kikamilifu. Kule ndikoambako tutajifunza na kuona kila kitu kwa nini kina umuhimugani na kwa sababu gani na kadhalika hatua kwa hatua yakila jambo. (Makofi)

Wakati Mheshimiwa Rais anapokea taarifa ya Kamatiya pili ya masuala yanayohusu madini kule Ikulu, Dar esSalaam, nilikuwa mmoja wa waliokuwepo pale na nilipewanafasi ya kuzungumza na kwa niaba yenu nilitoa ahadi pale,kwamba sisi Bunge hili kama kuna mambo mazito yenyemaslahi kwa nchi tutakuwa tayari kuyafanyia kazi kwauharaka wa kipekee. (Makofi)

Kwa hiyo, naziomba Kamati hizo zikaangalie, kwakawaida Spika hatawe za kupanga shughuli hapa isipokuwa

Page 55: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

55

Mwenyekiti wa Kamati amenitaarifu kwamba jambo hililimekamilika, ndio utaratibu wetu wa Kikanuni. Kwa hiyo,hatuwezi tena sisi Bunge tukawa Kamati maalum tena kujadili,inatakiwa sasa mambo haya yaende kwenye Kamati husika,Kamati zitajadili zitapitia kila kitu, halafu wao watanishaurimimi Spika, na mimi nitawaambia Kamati ya Uongozi. Sasakama linaingia Bungeni au haliingii itatokea kwenye Kamatisio hapa, ndio utaratibu wetu. (Makofi)

Kwa hiyo, kwa hatua hii, tukubaliane tu kwambalinaenda huko na nyie mnakaribishwa kwenye kamati hizombili kwenda kushiriki kujadili. Lakini kwa ujumla wake ni fursaambayo sio ya kuipoteza kirahisi. Nilisema neno moja tu janakwenye Kamati ya Uongozi labda ningerudia na hapa, sisiWabunge tumekuwa kwa muda mrefu tukipigania Bungehili liwe na nafasi fulani katika mchakato wa mikatabamikubwa inayohusiana na masuala ya madini na gesi. Liwena nafasi fulani ili Taifa lisije likatumbukia tena katika mikatabamikubwa ambayo inaweza ikatia hasara Taifa. (Makofi)

Moja ya mambo ambayo tunaenda kuyapata katikamikataba hii, ni kuliweka Bunge mahali ambapo litakuwana mkono fulani. Fursa kama hizo ni nadra, tumepigania kwamiaka mingi hatujawahi kupata fursa kama hiyo na mambohaya huwenda na upepo, tunaweza tukasitasita leo baadaya mwezi mmoja mawazo yamebadilika jambo hili tusipatetena.

Kwa hiyo, ndio maana nasema ipo haja ya kwendakule na kuona maudhui na nini kilichopo, na hakika wengihata hamjasoma, labda hata hamjaiona Miswada kwasababu ili muipate lazima isomwe mara ya kwanza. (Makofi)

Sasa baada ya kusomwa mara ya kwanza nina hakikakwenye pegionhole huko mtakapoanza kupitia mtapatanakala zake, na baada ya kusoma mara ya kwanza ndioimekuwa sasa public, kwa hiyo hata wadau sasa wanawezawaka acess kupitia internet Miswada hii kama tulivyokwishasema. Kwahiyo Mtanzania yoyote mwenye internet hivi sasa,ataipata miswada hii kupitia mitandao na ninyi Wabunge

Page 56: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

56

mtaipata mara moja na kwa hiyo tunaweza tukaendeleanakushauriana kadri tunavyoenda.

Baada ya maelezo haya naomba itoshe kusemakwamba, tukubali kwa hatua hii tuende hivyo, halafututaona kadri tunavyoenda tutazidi kushauriana vizuri. Baadaya maelezo haya sasa naomba nimkabidhi MheshimiwaMwenyekiti wa Bunge Mheshimiwa Zungu.

MBUNGE FULANI: Jambo la dharura.

Hapa Mwenyekiti (Mussa A. Zungu) Alikalia Kiti

MWENYEKITI: Katibu!

NDG.CHARLES MLOKA – KATIBU MEZANI:

HOJA ZA SERIKALI

MAAZIMIO

Azimio la Bunge kuridhia Marekebisho ya Mkataba waNairobi wa Hifadhi, Usimamizi na Uendelezaji wa

Mazingira ya Bahari na Ukanda wa Pwani ya Magharibiya Bahari ya Hindi (Amended Convention for the

Protection, Management and Development of Marine andCoastal Environment of the Western Indian Ocean)

Azimio la Bunge Kuridhia Itifaki ya Udhibiti wa Uchafuziwa Mazingira ya Bahari na Ukanda wa Pwani ya

Magharibi ya Bahari Hindi kutokana na vyanzo nashughuli zinazofanyika Nchi Kavu (Protocol for the

Protection of the Marine and Coastal Environment of theWestern Indian Ocean from Land-Based Sources and

Activities)

Azimio la Bunge Kuridhia Itifaki ya Nagoya ya KusimamiaUpatikanaji na Mgawanyo Sahihi wa Faida zitokanazo naMatumizi ya Rasilimali za ki-genetic (Nagoya Protocol on

Access to Genetic Resources and the Fair and Equitable

Page 57: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

57

Sharing of Benefits Arising from their Utilization to theConvention on Biological Diversity)

MWENYEKITI: Ahsante mtoa hoja upande wa Serikali.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaMwenyekiti, Tanzania ni nchi mwanachama wa Mkataba waKuhifadhi Usimamizi na Uendelezaji wa Mazingira ya Baharina Ukanda wa Pwani ya Afrika Mashariki uliopitishwa tarehe21 Juni, 1985 ukihusisha nchi tisa ambazo ni Comoro, Kenya,Somalia, Madagascar, Mauritians, Msumbiji, Ushelisheli,Reunion pamoja na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania iliridhia mkatabahuu tarehe 1 Machi, 1996 ikiwa ni nchi ya sita kuridhia. Mkatabahuu ulikuwa na lengo la kuhidhi mazingira ya bahari naUkanda wa Pwani kwa nchi wanachama tisa kwakushirikiana katika kuandaa mikakati na mipango yapamoja katika kuhifadhi, kusimamia na kuendeleza mazingirakatika Ukanda wa Pwani wa Mashariki ya Bahari ya Hindi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tangu mkataba huu kuanzakutekelezwa na nchi wanachama mwaka 1996 kulijitokezachangamoto kati ya nchi wanachama. Kati ya changamotohizo ni pamoja na ufumbuzi wa mazingira ya bahari naUkanda wa Pwani kutokana na shughuli za kibinadamuzinazofanyika katika nchi kavu.

Pili, ni utupwaji wa takataka zenye kemikali na sumubaharini na tatu ni athari za mabadilikio ya tabia nchi ikiwani pamoja na kuongezeka kwa kina cha bahari, kuongezekakwa joto la bahari na kuongezeka kwa asidini baharini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na changamotohizo nchi wanachama kupitia Mkutano wa Pili uliofanyikaPort Louis Mauritius mwaka 1999, zi l iamia kufanyamarekebisho kwenye baadhi ya vipengele vya mkataba waNairobi kwa lengo la kuwezesha na kuhifandi na kusimamiana kuendeleza mazingira ya Bahari na ukanda wa Pwani yamagharibi ya Bahari ya Hindi.

Page 58: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

58

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuweza kufikia Azimio lakufanya marekebisho ya mkataba huu nchi wanachama waNairobi ziliazimia kupitia mkataba huu kwa kuviboreshabaadhi ya vipengele na kuongeza vipengele vipya.Vipengele vilivyoboreshwa na kuongezwa vinahusu:-

(i) Kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi;

(ii) Kudhibiti utupwaji wa takataka zenye kemikali zasumu Baharini;

(ii i) Ufuatiliaji na uzingatiaji wa utekelezaji wamikataba;

(iv) Kuongezeka kwa nchi ya Afrika ya Kusini kamamwanachama mpya na kusababisha mabadiliko katika jinala mkataba na kuwa mkataba wa Nairobi kuhusu Hifadhi,Usimamizi na Uendelezaji wa Mazingira ya Bahari na Ukandawa Pwani ya Magharibi ya Bahari ya Hindi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, marekebisho ya mkatabahuu yalitiwa saini na nchi wanachama 10 badala ya tisa zaawali hii ilitokana nan chi ya Afrika Kusini kujiunga katikamkataba tarehe 1 Aprili, 2010 huko Nairobi nchini Kenya. Nchiwanachama kwa muundo pia ni Comoro, Reunion, Kenya,Madagascar, Mauritius, Msumbiji, Ushelisheli, Somalia, Jamhuriya Muungano wa Tanzania na nchi ya Afrika Kusini, sekretarietiya mkataba huu iko UNEP nchini Kenya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na maelezo yahapo juu kuna umuhimu wa nchi yetu kuridhia marekebishoya mkataba huu ili iendelee kunufaika na ushirikiano wakikanda na kimataifa katika kukabiliana na changamotompya za usimamizi na uhifadhi wa mazingira zinazokabilimaeneo ya Bahari na ukanda wa Pwani wa Bahari ya Hindi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mkataba huuuliorekebishwa pia umezingatia mikataba mingine baadhiya mikataba hiyo ni pamoja na mkataba wa mwaka 1982kuhusu Sheria ya Bahari, Mkataba wa mwaka 1992 Mabadiliko

Page 59: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

59

ya Tabianchi, Mkataba wa Basel Unaodhibiti Usafirishaji Bainaya Nchi na Utupwaji wa Takataka za Sumu, Mkataba waBamako unaopiga marufuku uingizaji na usafirishaji na utupajiwa takataka zenye sumu baharini na vilevile mkatabaunaoendelea kuzitambua itifaki zilizokuwa zimeridhiwa katikamkataba wa awali ili pamoja na itifaki kuhusu maeneoyaliyoundwa yenye viumbe pori pamoja na mimea wamwaka 1985 na itifaki kuhusu mashirikiano ya kuthibiti uchafuziwa bahari unaotokana na matukio ya umwagiaji wa mafutaama kemikali zenye madhara ya mwaka 1985.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mkataba huu unavipengele34 ambavyo vimefafanua maeneo mbalimbali ya mkatabaambayo nchi wanachama zinatakiwa kuyazingatia katikautekelezaji wake. Kimsingi maeneo hayo yamehusiana namawanda ya mkataba, ufafanuzi, wajibu wa nchiwanachama na ufafanuzi unaotokana na uchafunziutokanao na meli, utupaji taka hovyo, kazi zifanyikazo nchikavu toka taka hatarishi kutoka nchi moja kwenda nyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na maelezo hayovipengele muhimu ambavyo vinafanyiwa marekebishokwenye mkataba huu wa awali ni:-

(i) Utangulizi, nia ya nchi wanachama kuridhiamarekebisho; nchi wanachama zinatakiwa utekelezaji wamkataba kutekeleza mkataba kwa kutambua changamotoinayokabili mazingira ya Pwani ya Magharibi ya Bahari yaHindi na marekebisho yaliyofanywa kwenye aya ya tatu yautangulizi yametambua changamoto mpya zinazohusumasuala ya mabadiliko ya tabia ya nchi. Kwa kuwa baadhiya changamoto zinazokabili maeneo ya ukanda wa Pwaniwa Bahari zinasimamiwa na mikataba mingine ya kimataifaaya ya tisa ya utangulizi imetambua mikataba hiyo;

(ii) Ibara ya 7 ambayo ni uchafuzi wa kutoka vyanzovya nchi kavu Ibara hii inahusu udhibiti uchafuzi wa baharina ukanda wa Pwani utokanao na vyanzo vya nchi kavu.Marekebisho yaliyofanyika kwenye Ibara hii ni kuongeza

Page 60: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

60

masuala ya shughuli nyingine ambazo zinasababishia uchafuwa bahari;

(iii) Ibara ya 16 muundo wa kitaasisi, Ibara hii inahusumuundo wa kitasisi ambao shirika la kimataifa la mazingiralilipewa jumkumu la kusimamia masuala ya kitasisi pekee.Ibara hii kwa sasa inasomeka kama Ibara ya 17 na imempaMkurugenzi Mtendaji wa UNEP pia jukumu la kusimamiamasuala ya kifedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vipengele vipyavinavyoongezeka katika mkataba huu ni kama ifuatavyo:-

(i) Ibara ya 9 ambayo inaelezea uchafuzi unaotokanana usafirishwaji na umwagaji wa taka zenye kemikali za sumu.Ibara hii inahusu kuzuia uchafuzi wa bahari na Ukanda waPwani utokanao na usafirishwaji na umwagaji wa taka zenyekemikali na sumu zinazotoka nchi nyingine;

(ii) Ibara ya 11 bionuai ibara hii inahusu kuhifadhi nakulinda bionuai viumbe na mimea adimu vilivyo hatarinikutoweka na kuanzisha maeneo tengefu kama vile hifadhiza wanyama pori, misitu sanjali na kuzuia shughuli zinazowezakusababisha uharibifu wa viumbe hao pamoja na maeneoyao;

(iii) Ibara ya 27 uzingatiaji na utekelezaji wa sheria.Ibara hii inahusu nchi wanachama kuchukua hatuakulingana na uwezo wa nchi husika kutekeleza majukumuyaliyo aninishwa katika mkataba na kuzingatia Sheria husikaza kimataifa. Aidha, nchi wanachama kuanzisha taratibu zakutathimini utekelezaji i l i kuhamasisha uzingatiaji wamkataba ikiwa ni pamoja na kuwa na utaratibu wa waziwa kubadilishana taarifa baina ya nchi na nchi;

(iv) Marekebisho ya mkataba yatasaidia kuimarishahali ya uchumi wa nchi, kipato cha jamii za Ukanda wa Pwanina afya ya wananchi kwa ujumla.

Page 61: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

61

(v) Matokeo mengine mahususi ni pamoja nakuongezeka kwa bionuai za Bahari na Ukanda wa Pwani nakudhibiti wa uchafuzi unaotokana na shughuli zinazofanyikanchi kavu;

(vi) Kuongezeka kwa ubora wa maji kwenye Baharikwa kudhibiti utupaji wa taka zenye kemikali za sumuBaharini;

(vii) Kuongezeka kwa kipato cha jamii ukanda waPwani kutokana na kuongezeka kwa mazao ya Bahari,kuongezeka kwa uwezo wa jamii ukanda wa Pwani katikakuhimili athari za mabadiliko ya tabia nchi na kupunguzashughuli zinazosababisha mabadiliko ya tabia nchi;

(viii) Kuimarika kwa ushirikiano wa kikanda kutokanana mipango pamoja na programu za miradi ya kikandainayolenga hifadhi ya mazingira Bahari pamoja na ukandawa Pwani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili mkataba huu ili uwezekutekelezwa ni lazima nchi wanachama ziridhie. Aidha,utaratibu wa kuridhia mkataba huu unaoneshwa katika Ibaraya 30 ya mkataba wenyewe. Ibara hii inaeleza kuwa kila nchimwanachama inatakiwa kuridhia marekebisho ya mkatabana kuwasilisha ridhaa hiyo Serikali ya Jamhuri ya Kenyaambayo ni jukumu la kupokea na kuhifadhi ridhaa hizo. Tangumkataba huu usainiwe mwezi Aprili, 2010 nchi wanachamazipo katika hatua mbalimbali za kuridhia kulingana na Sheriana taratibu za nchi husika na utaanza kutekelezwa rasmibaada ya miezi sita baada ya kuridhia. Hadi kufikia Juni,2017 nchi ya Msumbiji, Mauritius, Ushelisheli ndizo zimeridhiamarekebisho ya mkataba huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maelezo hayasasa naomba kuwasilisha Azimio lenyewe kwa Bunge lakoTukufu ili liweze kuridhia kama ifuatavyo:-

Kwa kuwa mkataba wa Nairobi kuhusu hifadhi,usimamizi na uendelezaji wa mazingira ya bahari na Pwani

Page 62: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

62

ya kanda ya Afrika Mashariki ulipitishwa tarehe 21 Juni mwaka1985 ukihusisha nchi tisa ambazo ni Comoro, Kenya, Somalia,Madagasca, Mauritius, Msumbiji, Ushelisheli, Reunion naJamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Na kwa kuwa Tanzania iliridhia mkataba huu tarehe1 Machi, 1996.

Na kwa kuwa mkataba huu unalenga katikakudhibiti uchafuzi kutokana na vyanzo vya shughulizinazofanyika nchi kavu na nchi wanachama kushirikianakatika kuanda mipango na mikakati pamoja katika kuhifadhina kusimamia na kuendeleza mazingira Ukanda wa Pwanina Bahari.

Na kwa kuwa tangu mkataba huu ulidhiwe na nchiwanachama na kuanza kutekelezwa mwaka 1996kumejitokeza changamoto za mazingira ikiwa ni pamoja nauchafuzi wa mazingira ya Bahari na Ukanda wa Pwani tokavyanzo na shughuli zinazofanyika nchi kavu, uharibifu wamaeneo ya Pwani, utupwaji wa takataka zenye kemikali zasumu Baharini na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Na kwa kuwa katika Mkutano wa Pili wa nchiwanachama uliofanyika Port Louis Mauritius mwaka 1999 nchihizo ziliadhimia kufanya marekebisho kwenye baadhi yavipengele katika mkataba wa awali na kuongeza vipengelevipya.

Na kwa kuwa marekebisho yanahusu kuongezekakwa wigo wa vyanzo vya uchafuzi wa mazingira ya Baharina Ukanda wa Pwani kutoka nchi kavu na vipengelevil ivyoongezeka vinahusu kakabiliana na athari zamabadilikoya tabia nchi, kudhibiti utupwaji wa takatakazenye kemikali za sumu baharini, ufuatiliaji na uzingatiaji wautekelezaji wa mkataba na kuongezeka kwa nchi ya AfrikaKusini kama mwanachama mpya na hivyo kusababishamabadiliko ya jina la mkataba na kuwa Mkataba wa Nairobikuhusu Hifadhi, Usimamizi na Uendelezaji wa Mazingira yaBahari na Ukanda wa Pwani ya Magharibi ya Bahari ya Hindi.

Page 63: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

63

Na kwa kuwa marekebisho ya mkataba ya litiwa sainina nchi wanachama ikiwepo Tanzania tarehe 1 Aprili, 2010mjini Nairobi.

Na kwa kuwa marekebisho haya yatawezesha nchiwanachama kuchukua hatua zaidi katika utekelezaji wamkataba ikiwa ni pamoja na uandaaji wa mikataba yakikanda na katika kukabiliana na changamoto hizo.

Na kwa kuwa ni muhimu nchi yetu iridhia marekebishoya mkataba huu ili iendelee kunufaika na ushirikiano wakikanda na kimataifa katika kukabiliana na changamotompya za usimamizi na uhifadhi wa mazingira zinazokabilimaeneo ya Bahari na ukanda wa Pwani.

Na kwa kuwa hatua hii, itasaidia kuboredha hifadhina usimamizi na uendelezaji wa mazingira ya Pwani ya Bahariya Hindi.

Na kwa kuwa Tanzania kwa kutia saini mkataba huuna hatimaye kutelekeza itanufaika na mambo yafuatayo:-

(a) Kuimarisha hali ya uchumi wa nchi, kipato chajamii za ukanda wa Pwani na afya ya wananchi kwa ujumla.

(b) Kuwa na mpango wa pamoja na utekelezaji wamkataba ulioandaliwa.

(c) Kuimarisha mikakati na miongozo inayohusika nakuboresha na kuhifadhi na kusimamia mazingira ya Baharina ukanda wa Pwani.

(d) Kuongezeka kwa bionuai za Bahari na Ukandawa Pwani kwa kudhibiti uchafuzi kutokana na shughulizinazofanyika nchi kavu.

(e) Kuongezeka kwa ubora wa maji kwenye baharikwa kuthibiti utupaji wa taka zenye kemikali za sumu Baharini.

Page 64: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

64

(f) Kuongezeka kwa kipato cha jamii za ukanda waPwani kutokana na kuongezeka kwa mazao ya bahari.

(g) Kuongezeka kwa uwezo wa jamii za Ukanda waPwani katika kuhimili athari za mabadiliko ya tabia nchi nakupunguza shughuli zinazosababisha mabadiliko ya tabianchi.

(h) Kuimarika kwa ushirikiano wa kikanda kutokanana kuwa mipango ya pamoja na programu za miradi yakikanda inayolenga kuhifadhi mazingira ya bahari na ukandawa Pwani.

Hivyo basi kwa kuzingatia umuhimu na manufaa yamkataba huu kwa Tanzania Bunge hili katika Mkutano wakewa Saba na kwa mujibu wa Ibara ya 63(3)(e) ya Katiba yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1977 liliazimiakuridhia marekebisho ya mkataba wa Nairobi wa hifadhi,usimamizi na uendelezaji wa mazingira ya bahari na Ukandawa Pwani ya magharibi ya Bahari ya Hindi yaani AmendedConvention for the Protection Management andDevelopment of the Marine and Coastal Environment of theWestern Indian Ocean.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha naninaomba kutoa hoja.

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaMwenyekiti, naafiki.

MWENYEKITI: Ahsante hoja imeungwa mkono, sasanamuita Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheriaawasilishea taarifa yake. Sorry awasilishe yote. Waziri waMambo ya Ndani ya Nchi.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaMwenyekiti, Itifaki ya Udhibiti wa Uchafuzi wa Mazingira yaBahari na Ukanda wa Pwani wa Magharibi ya Hindi kutokana

Page 65: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

65

na vyanzo na shughuli zinazofanyika nchi kavu ni itifakiiliyoanzishwa chini ya Mkataba wa Nairobi kuhusu hifadhi,usimamizi na uendelezaji wa mazingira ya Bahari ukanda waPwani Magharibi ya Bahari ya Hindi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali mkataba ulijulikanakama Mkataba wa Kimataifa wa Hifadhi, usimamizi nauendelezaji wa mazingira ya Bahari na Ukanda wa Pwani yaAfrika Mashariki. Mkataba huu ulibadilishwa jina na kupewajina la sasa kwa kufanyiwa marekebisho mwaka 2010.Tanzania ilisaini itifaki hii sambamba na marekebisho yamkatba huu wa Nairobi tarehe 1 Aprili, 2010.

Mheshimiwa Mwenyekiti, madhumuni ya itifaki hii, nikudhibiti uchafuzi na uharibifu wa mazingira ya Bahari naukanda wa Pwani ya Magharibi ya Bahari ya Hindiunaotokana na vyanzo na shughuli za kibinadamuzinazofanyika nchi kavu. Nchi zinazohusika na itifaki hii, nizile zinazohusika na mkataba wa wa Nairobi yaani Comoro,Kenya, Somalia, Madagascar, Mauritius, Msumbiji, Ushelisheli,Reunion, Jamhuri ya Afrika Kusini na Jamhuri ya Muunganowa Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sababu za kuwa na itifakihii zinatokana na marekebisho yaliyofanywa katika mkatabawa Nairobi yaliyosababishwa na changamoto za mazingirazilizojitokeza wakati utekelezaji wa mkataba wa Nairobi waawali. Kujitokeza kwa changamoto hizo mpya ndiko kulikosababisha nchi wanachama kuazimia mkataba huourekebishwe na kuzijumuisha changamoto hizo,changamoto hizo ni pamoja na:-

(i) Uchafuzi wa mazingira ya Bahari na Ukanda waPwani toka vyanzo vya shughuli zinazofanyika nchi kavu;

(ii) Uharibifu wa maeneo ya Pwani; na

(iii) Utupwaji wa taka zenye kemikali za sumu baharini.

Page 66: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

66

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kukabiliana nachangamoto zilizojitokeza ususani suala la uchafuzi wamazingira Bahari na Ukanda wa Pwani toka vyanzo nashughuli zinazofanyika nchi kavu na kwa kuzingatia Ibara ya4(2) ya kataba wa Nairobi ambayo inazipa mamlaka nchiwanachama kuanzisha itifaki mbalimbali ili kutekelezamkataba. Nchi wanachama zilikubaliana kuanzishwa kwaitifaki iliyopendekezwa ili Bunge lako Tukufu la Jamhuri yaMuungano wa Tanzania liweze kuridhia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika utekelezaji wamkataba wa Nairobi Tanzania imeendelea kushirikiana nanchi wanachama wengine katika kubadilishana uzoefu wakitaalum wa masuala mbalimbali yanayohusu eneo laMagharibi ya Pwani ya Bahari ya Hindi, kuandaa na kutekelezamikakati, programu na miradi mbalimbali kuhusu hifadhi zaUkanda wa Pwani na Bahari. Aidha, mwaka 2008 Serikaliilipitisha mkakati wa hatua za haraka za kuhifadhi mazingiriaya Bahari Ukanda wa Pwani, Maziwa, Mito na Mabwawakwa lengo la kuhifadhi mazingira na bionuai zilizopo maeneohayo na kuongeza ubora wa maji i l i kuhakikishapanakuwepo na utumiaji endelevu wa rasilimali za bahari ilikuboresha hali ya maisha jamii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mafanikio yaliyopatikana nipamoja na kuimarisha vikundi vya kijamii katika kusimamiarasilimali za bahari ikiwemo kufanya doria za mara kwa mara,kuongeza uelewa wa jamii kuhusu hifadhi ya mazingira yaPwani na Bahari, kuimarisha utafiti, kuinua utalii endelevuna kuimarisha uvuvi endelevu. Pamoja na mafanikio hayokumekuwepo na uelewa mdogo wa kutozingatia masualaya uchafuzi kutokana na vyanzo na shughuli mbalimbalizinazofanyika nchi kavu zinavyoweza kuathiri mazingira yaBahari na Ukanda wa Pwani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii imepelekea kutodhibitikikamilifu shughuli zinazofanyika Nchi kavu ambazo zinaathirimazingira ya bahari kupitia mito inayoingiza maji baharini.

Page 67: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

67

Mheshimiwa Mwenyekiti, vipengele muhimu vya Itifakihii ni pamoja na:-

(i) Ibara 4 ambayo ni wajibu wa nchi wanachama,Ibara hii ni pamoja na mambo mengine inabainisha wajibuwa nchi wanachama kuchukua hatua madhubuti zakupambana na uhalibifu wa mazingira kulingana na Sheriaza Kimataifa, Mkataba na Itifaki yenyewe;

(ii) Ibara ya 5 ambayo ni vyanzo vya uchafuzi Ibarahii inahusu udhibiti wa umwagaji au utiririshaji taka kwenyemaji na uchafuzi wa hewa katika maeneo ya bahari naUkanda wa Pwani toka kwenye makazi, viwanda, vyombovya usafiri wa maji. Aidha, Ibara hii inazitaka nchi wanachamakuweka viwango vya kudhibiti uchafuzi na kuvisimamia;

(iii) Ibara ya 6 ambayo inaongelea udhibiti wa uchafuzikutokana na shughuli za kilimo. Ibara hii inazitaka nchiwanachama kuchukua hatua za kudhibiti uchafuziunaotokana na shughuli za kilimo zisizoendelevu ambazozinaweza kuathiri mazingira ya bahari na Ukanda waPwani;

(iv) Ibara ya 7 shughuli nyingine zinazoleta madharaIbara hii inazielekeza nchi wanachama kudhibiti shughulizinazoweza kuleta madhara kwa viumbe hai wa baharinina mazingira yao. Sambamba na kuchukua hatuazitakazosaidia jamii za Pwani kukabiliana na athari zamabadiliko ya tabia ya nchi;

(v) Ibara ya 8 uchafuzi unaovuka mipaka, Ibara hiiinazitaka nchi wanachama kudhibiti umwagaji wa takakwenye mito, inayopita nchi zaidi ya moja ambayo kwa njiamoja ama nyingine huathiri viumbe na maeneo ya Ukandawa Pwani na Bahari. Aidha, Ibara hii imeelezea umuhimuwa kushirikiana na nchi zisizo wanachama katika kudhibitiuchafuzi wa aina hii;

(vi) Ibara ya 13 ambayo ni tathimini ya athari kwamazingira na ukaguzi wa mazingira, Ibara hii inataka kilaNchi mwanachama kuwa na kanuni na miongozo ya ukaguzi

Page 68: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

68

na tathimini ya athari kwa mazingira kwa ajili ya programumiradi na shughuli ambazo utekelezaji wake unaweza kuwakwa namna moja ama nyingine kuathiri mazingira ya baharina Ukanda wa Pwani;

(vii) Ibara ya 14 ushirikiano katika masuala ya kitaalamna kujenga uwezo, Ibara hii inataka kila nchi mwanachamainapaswa kushirikiana na nchi nyingine katika masuala yasayansi na teknolojia zinazohusu udhibiti wa uchafuziunaotokana na shughuli zinazofanyika katika nchi kavu nakushirikiana katika kutekeleza program za kujenga uwezowa nchi wanachama;

(viii) Ibara ya 15 ambayo ni utoaji wa elimu kwa ummana ushirikishwaji wa jamii, Ibara hii inataka Nchi wanachamakuhamasisha upatikanaji wa taarifa na nyaraka muhimuzinazohusu uchafuzi toka nchi kavu. Aidha, nchi hizozinasisitizwa kukuza uelewa kwa jamii na kuhakikisha jamiiinashirikishwa katika kutoa maamuzi yanayohusu utekelezajiwa Itifaki;

(ix) Ibara ya 20 yenyewe inaongelea utaratibu wafedha kwa mujibu wa makubaliano. Kila nchi mwanachamakulingana na uwezo wake itatenga fedha za kutosha kwaajili ya utekelezaji wa programu na miradi inayolenga kudhibitiuchafuzi katika maeneo ya Ukanda wa Pwani ya bahari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo kwa upande waTanzania kuridhia Itifaki inayopendekezwa itakuwa katikanafasi nzuri kwa kushirikiana na nchi wanachamakukabiliana na changamoto zilizojitokeza chini ya mkatabahuo na haitaathiri shughuli za maendeleo ikiwa ni pamojana uchimbaji wa gesi na mafuta. Aidha, itaweza kutekelezamikakati na mbinu bora za kuhifadhi mazingira ya baharitukizingatia kuwa uchafuzi katika maeneo hayo haunamipaka. Mpaka sasa nchi ya Msumbiji, Ushelisheli, Mauritiuszimeridhia Itifaki hii na nyingine zipo katika hatua za kuridhiakulingana na taratibu za nchi husika.

Page 69: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

69

Mheshimiwa Mwenyekiti, faida za kuridhia itifaki hii nipamoja na kuhifadhi na kuongezeka bionuai ya kuboreshamazingira ya bahari na Ukanda wa Pwani ya Magharibi yaBahari ya Hindi, kutekeleza mipango ya kudhibiti uchafuziunaotokana na shughuli zinazofanyika nchi kavu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuongezeka kwa ubora wamaji kwenye mito, bahari na udhibiti wa uchafuzi,kuongezeka kwa kipato cha jamii za Ukanda wa Pwani nakuongezeka kwa mazao ya bahari na Ukanda wa Pwani,kuimarika kwa afya za wananchi kwa kuwa na mazingirabora, kuimarika kwa ushirikiano baina ya Tanzania na nchiwanachama kutokana na kuongezeka kwa hatua za kulindamazingira ya Pwani na Bahari, kupatikana kwa fursa zautekelezaji wa programu na miradi mbalimbali yenyeushirikiano na nchi nyingine inayolenga kudhibiti uchafuzi wamazingira katika bahari na Ukanda wa Pwani wa Magharibiya Bahari ya Hindi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maelezo haya,sasa naomba kuwasilisha azimio lenyewe kwa Bunge lakoTukufu, kuridhia itifaki ya udhibiti wa uchafuzi wa mazingiraya bahari na Ukanda wa Pwani ya Magharibi ya Bahari yaHindi kutokana na vyanzo na shughuli zinazofanyika katikanchi kama ifuatavyo:-

Kwa kuwa itifaki ya kudhibiti uchafuzi wa mazingiraya Bahari na Ukanda wa Pwani ya Magharibi ya Bahari yaHindi, kutokana na vyanzo vya shughuli zinazofanyika Nchikavu ilipitishwa na kusainiwa na nchi husika tarehe 01 Aprili,2010 Nairobi nchini Kenya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, waambie wanaoongeaWaziri wa Mambo ya Ndani anaongea hapo.

MWENYEKITI: Haya soma Azimio la tatu.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Na kwa kuwamadhumuni ya itifaki hii ni kudhibiti uchafuzi na uharibifu wamazingira ya Bahari na Ukanda wa Pwani wa Magharibi ya

Page 70: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

70

Bahari ya Hindi, unaotokana na vyanzo vya shughuli zakibinadamu ziinazofanyika nchi kavu;

Na kwa kuwa nchi wanachama zinazohusika naItifaki hii ni zile zinazopatikana Bahari ya Hindi ambazozinajumuisha Comoro, Kenya, Somalia, Madagascar,Mauritius, Msumbiji, Ushelisheli, Reunion Jamhuri ya Muunganowa Tanzania na Afrika ya Kusini;

Na kwa kuwa itifaki hii imeanzishwa chini ya Mkatabawa Nairobi uliofanyiwa marekebisho na nchi wanachamamwaka 2010 Mkataba wa Nairobi wa kuifadhi usimamizi nauendelezaji wa mazingira ya bahari ya Ukanda wa Pwaniwa Magharibi ya Bahari ya Hindi;

Na kwa kuwa utekelezaji wa Mkataba wa Nairobiunaohusu hifadhi, usimamizi na uendelezaji wa mazingira yaBahari na Pwani ya Kanda ya Mashariki ambayo Tanzaniaililidhia tarehe 01 Machi, 1996 inaonyesha kuwa zipochangamoto za kimazingira zil izojitokeza ambazozilisababisha nchi wanachama kuazimia Mkataba huourekebishwe;

Na kwa kuwa makubaliano ya kufanya mapitio yaMkataba wa Nairobi yalifikiwa katika Mkutano wa Pili wanchi wanachama uliofanyika Port Louis, Mauritius mwaka1999.

Na kwa kuwa mapitio ya mkataba huo yalibainishachangamoto mbalimbali zikiwemo uchafuzi wa mazingiraya Bahari na Ukanda wa Pwani kutoka vyanzo vya shughulizinazofanyika nchi kavu, uharibifu wa maeneo ya Pwani,utupwaji wa takataka zenye kemikali za sumu baharini naathari za mabadiliko ya tabia ya nchi;

Na kwa kuwa katika kukabiliana na changamotozilizojitokeza hususani uchafuzi wa mazingira ya Bahari naUkanda wa Pwani toka vyanzo na shughuli zinazofanyika Nchikavu, marekebisho yamefanywa kwa kuzingatia Ibara ya 4(2)ya Mkataba wa Nairobi ambayo zinaipa nchi mamlaka

Page 71: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

71

wanachama kuanzisha itifaki mbalimbali ili kutekelezamkataba huo, na nchi wanachama zilikubaliana kuanzishwakwa itifaki inayopendekezwa kuridhiwa.

Na kwa kuwa Tanzania kuweka saini ya Itifaki hii,hatimaye kuitekeleza itanufaika na mambo yafuatayo:-

(a) Kuhifadhi na kuongezeka kwa bionuai yakuboresha mazingira ya Bahari na Ukanda wa Pwani yaMagharibi ya Bahari ya Hindi.

(b) Kutekeleza mipango ya kudhibiti uchafuziunaotokana na shughuli zinazofanyika nchi kavu.

(c) Kuongezeka kwa ubora wa maji kwenye mito nabahari kutokana na udhibiti wa uchafuzi.

(d) Kuongezeka kwa kipato cha jamii Ukanda waPwani kutokana na kuongezeka mazao ya Bahari na Ukandawa Pwani.

(e) Kuimarika kwa afya za wananchi kwa kuwamazingira ni bora.

(f) Kuimarika kwa ushirikiano baina ya Tanzania nanchi wanachama, kutokana na kuongezeka kwa hatua zakulinda mazingira ya Pwani na Bahari.

(g) Kuimarisha ushirikiano katika masuala ya kitaalamna kujenga uwezo katika masuala ya sayansi na teknolojiazinazohusu udhibiti wa ufafanuzi unaotokana na shughulizinazofanyika nchi kavu, na kushirikiana katika kutekelezaprogramu za kujenga uwezo kwa nchi wanachama.

(h) Kutoa elimu kwa umma na ushirikishwaji wa jamiikwa kuhamasisha upatikanaji wa taarifa na nyaraka muhimuzinazohusu uchafuzi wa Bahari kutoka nchi kavu.

(i) Kupatikana kwa fursa za utekelezaji kwa programuna miradi kwa ushirikiano na nchi nyingine inayolenga

Page 72: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

72

kudhibiti Uchafuzi wa Mazingira ya Bahari na Ukanda waPwani ya Mazingira ya Bahari ya Hindi.

Hivyo basi kwa kuzingatia umuhimu na manufaa yaItifaki hii kwa Tanzania, Bunge hili katika Mkutano wake waSaba na kwa mujibu wa Ibara ya 63(3)(e) ya Katiba yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 liliazimiakuridhia Itifaki ya Udhibiti wa Uchafuzi wa Mazingira ya Baharina Ukanda wa Pwani ya Magharibi ya Bahari ya Hindi,kutokana na vyanzo vya shughuli zinazofanyika nchi kavuyaani the Protocol for Protection of the Marine and CoastalEnvironment of Western Indian Ocean from land based sourcesand activities.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha nanaomba kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaMwenyekiti, naafiki.

MWENYEKITI: Ahsante. Hoja imetolewa imeungwamkono, maazimio matatu yote yamesomwa sasa namuitaMwenyekiti Kamati ya Katiba na Sheria na yeye aje kutoataarifa yake. Bado Azimio moja? Haya limalizie hilo.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaMwenyekiti, Tanzania ni nchi mwanachama wa Mkataba waKimataifa wa mwaka 1992 (The United Nations ConventionalBiological Diversity) uliopitishwa na Umoja wa Mataifa MjiniRio De Janeiro nchini Brazil wakati wa Mkutano wa Umojawa Mataifa kuhusu mazingira na maendeleo wa mwaka1992. Mkataba huu una malengo makuu matatu, ambayoni:-

(i) Hifadhi ya bionuai (Conventional of Bio Diversity);

(ii) Matumizi endelevu ya bionuai; na(iii) Usimamizi wa upatikanaji wa mgawanyiko wa

haki na sahihi wa faida zinazotokana na matumizi ya raslimaliza kijenetiki.

Page 73: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

73

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania iliridhia Mkatabahuu tarehe 8 Machi, 1996 chini ya Mkataba huu kuna Itifakitatu ambazo ni:-

(i) Itifaki ya Katagena ya mwaka 2000 inayohusuusimamizi wa mazingira dhidi ya athari zinazoweza kujitokezakutokana na matumizi ya ki-bio teknolojia ya kisasa. Tanzaniailiridhia Itifaki hii tarehe 16 Machi, 2003.

(ii) Itifaki ya kusimamia upatikanaji wa mgawanyosahihi wa faida zinazotokana na matumizi ya rasilimali zaasili, za kijenetiki Itifaki za ziada ya Nagoya, Kuala Lumpurkuhusu uwajibikaji wa kisheria na fidia katika kutekeleza Itifakiya Cartagena.

(iii) Itifaki ya Nagoya ilipitishwa na nchi wanachamawa Mkataba wa CBD katika kikao chake cha kumi mwaka2010 nchini Nagoya, Japan. Makubaliano haya yalifikiwabaada ya nchi wanachama wa CBD kujadiliana tangumwaka 2004 juu ya kuanzishwa kwa Itifaki hii yenye nguvu yakisheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo kuu la Itifaki hii nikuhakikisha kwamba kunakuwepo na mfumo wa kisheria,kiutawala na kitaasisi utakaosimamia upatikanaji warasilimali za kijenetiki kwa matumizi mbalimbali na piakuweka utaratibu wa mgawanyo sahihi wa faida zitokanazona matumizi ya rasilimali katika nchi zinazotoa rasilimali hizina zile zinazotumia rasilimali hizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mukhtadha huu Itifakihii itahamasisha utunzaji, uhifadhi, na matumizi endelevu yaraslimali za kijenetiki. Aidha, sehemu ya faida itokanayo narasilimali hizi itazifaidisha jamii ambazo rasilimali hizizinapatikana na hivyo kutoa motisha kwa jamii hizi kuzilindana kuhifadhi rasilimali hizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Itifaki ya Nagoya imeanzakufanya kazi mwezi Oktoba, 2014 katika Kikao cha Kumi naMbili cha Mkataba, kilichofanyika mjini Pyeongchang, Korea

Page 74: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

74

Kusini. Kwa mujibu wa utaratibu wa Mkataba huo Itifaki hiiilianza kutumika baada ya nchi 50 kuridhia. Katika Kikao chaKumi na Mbili cha Mkataba wa nchi 50 zilikuwa zimekwisharidhia Itifaki hii na kuwezesha nchi wanachama kuendeshakikao cha kwanza tarehe 13 hadi 17 Oktoba, 2014.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hadi mwezi Juni, 2017 nchi92 zimesaini ambapo nchi 100 duniani zimeridhia Itifaki hiyoya Nagoya. Katika Ukanda wa nchi za Afrika Mashariki nchiya Rwanda mwaka 2014, Kenya mwaka 2014, Ugandamwaka 2014 na Burundi mwaka 2014 tayari zimeridhia Itifakihiyo. Katika ukanda huu ni nchi ya Tanzania na Sudan Kusiniambazo bado hazijaridhia Itifaki hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo kwa Bunge lakokukubali kuridhia Itifaki hii Tanzania itakuwa imepiga hatuakatika kuimarisha usimamizi wa raslimali za kijenetiki kwakushirikiana na nchi za Ukanda huu na hatimaye kuchangiakatika uchumi wa nchi yetu na hifadhi ya utajiri ambayo nchiyetu ndiyo imejariwa kuwa nayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria ya Usimamizi waMazingira Sura Namba 191 ya mwaka 2014 inatambuaumuhimu wa rasilimali hizi katika uchumi wa nchi yetu nakuhifadhi bionuai. Sheria hii imetoa mamlaka kwa Wazirimwenye dhamana ya Mazingira kuandaa kanunizitakazosimamia mfumo na usimamizi wa kisheria katikamasuala ya upatikanaji wa raslimali za kijenetiki pamoja nakutoa muongozo wa mgawanyo sahihi wa faidazitakazotokana na matumizi ya rasilimali hizi. Ili kuwekamfumo huu wa kisheria tayari rasimu ya kanuni za kisheriazitakazosimamia masuala haya zimekwisha kuandaliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo basi kwa Bungekuridhia Itifaki hii, itakuwa linasaidia pia utekelezaji wa Sheriaya usimamizi wa Mazingira katika Masuala haya kwa vilesheria hii ilikwishaelekeza hivyo, hii ni kwa sababu maudhuiya Itifaki hii tayari yamekwisha, kuwekwa kwenye Sheria yausimamizi wa mazingira Sura Namba 191 ya mwaka 2004kifungu 230(2)(d).

Page 75: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

75

Mheshimiwa Mwenyekiti, msukumo mkubwa wakuridhia Itifaki hii unatokana na ukweli kwamba kwa mudamrefu raslimali za kijenetiki zimekuwa zikichukuliwa nakusafirishwa nje kwa matumizi mbalimbali kama vile utafiti,mafunzo, ama kutengenezea bidhaa za viwandani namadawa. Faida inayotokana na matumizi ya rasilimali hiziimekuwa hairudi kuzinufaisha nchi ambazo ndizo zenye umilikiwa rasilimali hizi. Kwa hiyo, nchi hizi zinaonekana kama vileshamba la bibi na rasilimali hizi kugeuzwa kuwa ni rasilimalizinazoweza kuchukuliwa wakati wowote bila ya utaratibuuliowekwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi wanachama na hasanchi za Afrika ambazo ndizo zenye utajiri wa raslimali zakijenetiki ziliona kuna umuhimu wa kudhibiti hali hii, ili nchizenyewe ziweze kunufaika na rasilimali za kijenetiki pamojana elimu ya asili ya rasilimali katika nchi zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, dhamira za kuridhia Itifakihii ni kwamba, endapo matumizi ya rasilimali za kijenetiki naelimu asili zinazohusisha matumizi ya rasilimali pamoja nakuimarisha fursa za mgawanyo sahihi wa faida zitokanazona matumizi ya rasil imali hizo, zitaimarishwa, nchiwanachama zinatarajia kwamba Itifaki hii itakuwa kichocheokatika kuhifadhi bionuai matumizi ya endelevu ya bionuaina bidhaa zinazotokana na bionuai na pia Itifaki itaimarishamchango katika maendeleo endelevu ya maisha yawananchi na uchumi wa nchi kwa ujumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, faida za kuridhia Itifaki hiikwa nchi yetu ni pamoja na kuwezesha nchi kuweka utaratibuwa kusimamia upatikanaji wa rasilimali za kijenetiki namgawanyo sahihi wa faida zitokanazo na matumizi yarasilimali za kijenetiki. Ofisi inayoratibu shughuli za mkatabahuu wa kuhifadhi mazingira itaimarisha utekelezaji waMkataba huu, pamoja na Itifaki ya Nagoya kikamilifu kwakuweka mfumo sahihi wa kusimamia rasilimali za kijenetikina matumizi ya watumiaji wa ndani na nje kwa kuzingatiataratibu zitakazokuwa zimewekwa.

Page 76: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

76

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuzingatia kwambamfumo wa sasa hauna utaratibu mzuri wa kudhibiti wageniwanaofanya utafiti kutoka nje, rasilimali zetu zinachukuliwana kusafirishwa bila kujua. Aidha, matokeo ya tafiti hizombalimbali pamoja na faida zake zimekuwa hazijulikani nawala nchi au jamii ambako jenetiki hizo zinatoka amazimechukuliwa hazifaidiki na tafiti hizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na faidaitakayotokana na tafiti kwa kuridhia itifaki hii itatusaidiamambo muhimu yafuatayo:-

(i) Kuweka misingi ya Kisheria na uwazi kwa utoaji nawatumiaji wa ndani na nje wa rasilimali za kijenetiki;

(ii) Baada ya kuweka utaratibu sahihi wa watumiajina watafiti wote watapaswa kuzingatia sheria za nchizonazohusiana na rasilimali;

(iii) Ada ya kuweka utaratibu sahihi wa kusimamiaupatikanaji wa rasilimali za kijenetiki jamii zenye elimu asilizinazohusiana na rasilimali za kijenetiki zitafaidika namgawanyo huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, huku nikiomba itifaki hii yoteiingie kwenye kumbukumbu sahihi naomba sasa baada yamaelezo haya kuwasilisha azimio lenyewe kwa Bunge lakokuridhia kama ifuatavyo:-

Kwa kuwa Tanzania ni nchi mwanachama waMkataba wa Mwaka 1992 unaohusu Hifadhi ya bionuai,matumizi endelevu ya bionuai pamoja na mgawanyo wafaida zinazotokana na matumizi ya bionuai ambao uliridhiwatarehe 8 Machi, 1996;

Na kwa kuwa chini ya mkataba huu kuna itifaki yaCartagena ya mwaka 2000 inayohusu usimamizi salama wamazingira dhidi ya athari zinazoweza kutokea kutokana namatumizi ya baionuai teknolojia ya kisasa ambayo Tanzaniaiiridhia tarehe 16 Machi, 2003;

Page 77: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

77

Na kwa kuwa katika Mkutano wa Sita wa Mkatabauliofanyika Johannesburg, Afrika ya Kusini mwaka 2002uliobaini kwa lengo la tatu la mkataba huo linahusumgawanyo sahihi wa faida zinazotokana na matumizi yarasilimali za kijenetiki halijafanikiwa kutokana na kukosekanakwa mfumo wa kusimamia utekelezaji wa mkataba huo;

Na kwa kuwa ili kuweka mfumo wa usimamizi wamkataba mchakato wa kuanzisha itifaki ya kusimamiaupatikanji wa mgawanyo sahihi wa faida zinazotoka namatumizi ya rasilimali za kijenetiki ulianzishwa na itifakiilipitishwa katika Mkutano wa Kumi wa nchi wanachamauliofanyika Nagoya, Japan mwaka 2010;

Na kwa kuwa Tanzania il ir idhia mkataba wabaionuai mwaka 1996 ambao umeanzisha itifaki yakusimamia upatikanaji wa mgawanyo sahihi wa faidazitokanazo na matumizi ya rasilimali ya kijenetiki;

Na kwa kuwa Tanzania kwa kuridhia itifaki hatimayekuitekeleza itanufaika na mambo yafuatayo:-

(a) Kuwa na misingi ya kisheria uwazi wa utoaji wawatumiaji wa rasilimali za kijenetiki.

(b) Sheria ya nchi zinazohusiana na rasilimali zakijenetiki zitazingatiwa.

(c) Jamii itanufaika na elimu na ujuzi wa siri warasilimali za kijenetiki.

(d) Udhibiti wa uhamishaji holela wa rasilimali zakijenetiki bila faida kwa nchi ama umma kwa ujumla.

(e) Kuongezeka kwa motisha ya hifadhi na matumiziendelevu kwa ajili ya ustawi wa jamii.

(f) Kupatikana kwa fursa za fedha kwa ajili yakutekeleza malengo ya itifaki,

Page 78: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

78

Na kwa kuwa Sheria ya usimamizi wa Mazingira SuraNa. 191 ya mwaka 2004 il iyopitishwa na Bunge hil iimeelekezwa kutungwa kwa kanuni na sheria zitakazowekamfumo wa kisheria, kiutawala na kitaasisi katika usimamiziwa masuala ya mazingira;

Hivyo basi kwa kuzingatia umuhimu wa manufaa yaitifaki hii kwa Tanzania, Bunge hili katika Mkutano wake waSaba kwa mujibu wa bara ya 63(3)(e) ya katiba ya Jamhuriya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 liliazimia kuridhiaitifaki ya kusimamia upatikanaji wa mgawanyo sahihi wafaida zinazotokana na matumizi ya rasilimali za ki-geneticyaani Nagoya Protocol on Access to Genetic Resources andFair and Equitable Sharing of Benefits Arising from theirUtilization of the Convention and Biological Diversity.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha nanaomba kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA:Mheshimiwa Mwenyekiti, naafiki.

MWENYEKITI: Ahsante, hoja imeungwa mkono.

AZIMIO LA BUNGE KURIDHIA ITIFAKI YA NAGOYA YAKUSIMAMIA UPATIKANAJI NA MGAWANYO SAHIHI WAFAIDA ZITOKANAZO NA MATUMIZI RASILIMALI ASILI ZA

KIJENETIKI NAGOYA PROTOCOL ON ACCESS TO GENETICRESOURCES AND THE FAIR AND EQUITABLE SHARING OF

BENEFITS ARISING FROM THEIR UTILIZATION TO THECONVENTION ON BIOLOGICAL DIVERSITY - KAMA

ILIVYOWASILISHWA MEZANI

Mheshimiwa Spika, Tanzania ni nchi mwanachama waMkataba wa Kimataifa wa Bioanuai wa mwaka 1992 (TheUnited Nations Convention on Biological Diversity) ambaouna malengo makuu (3) ambayo ni,Hifadhi ya bioanuai (Conservation of Biodiversity); Matumizi endelevu ya bioanuai(Sustainable Utilization of Biological resources); na Usimamizikatika upatikanaji na mgawanyo wa haki na usawa wa

Page 79: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

79

faida zitokanazo na matumizi ya rasilimali asilia za kijenetiki( fair and equitable sharing of benefits arizing from utilizationof genetic resources).

Mheshimiwa Spika, Tanzania iliridhia Mkataba huu tarehe 8Machi 1996. Chini ya Mkataba huu kuna Itifaki tatu ambazoni: Itifaki ya Cartagena ya mwaka 2000 inayohusu Usimamiziwa Mazingira Dhidi ya Athari zinaweza kutokea kutokanana Matumizi ya Biotekinolojia ya kisasa. Tanzania iliridhiaItifaki hii tarehe 16 Machi 2003; Itifaki ya kusimamiaupatikanaji na mgawanyo sahihi wa faida zitokanazo namatumizi ya rasilimali asili za kiejenetiki; na Itifaki ya ziadaya Nagoya – Kuala Lumpur kuhusu uwajibikaji kisheria nafidia katika kutekeleza Itifaki ya Cartagena.

Mheshimiwa Spika, Itifaki ya Nagoya ilipitishwa (adopted)na nchi wanachama wa Mkataba wa CBD katika kikaochake cha kumi (10) mwaka 2010 nchini Nagoya, Japan.Makubaliano haya yalifikiwa baada ya nchi wanachama waCBD kujadiliana tangu mwaka 2004 juu ya kuanzishwa kwaItifaki hii yenye nguvu ya kisheria (International Leagallybinding instrument on Access and Benefit Shairing).

Mheshimiwa Spika, Lengo kuu la Itifaki hii ni kuhakikishakwamba panakuwepo na mfumo wa kisheria na kitaasisiutakaosimamia upatikanaji wa rasilimali za kijenetiki kwamatumizi mbalimbali na pia kuweka utaratibu wamgawanyo sahihi wa faida zitokanazo na matumizi yarasilimali hizi kati ya nchi zinazotoa rasilimali hizi zinazotumiarasilimali hizi za kiejenetiki. Kwa muktadha huu, Itifaki hiiitahamasisha utunzaji wa rasilimali hizi pamoja na matumiziendelevu ya rasilimali za kiejenetiki.

Mheshimiwa Spika, Itifaki ya Nagoya imeanza kufanya kazi(entry into force) mwezi Oktoba, 2014 katika kikao cha kumina mbili (12) cha Mkataba wa Bioanuai kilichofanyika mjiniPyeongchang, Korea Kusini. Kwa mujibu wa utaratibu waMkataba wa Bioanuai(CBD), Itifaki hii ilianza kutumika baadaya nchi 50 kuridhia. Katika kikao cha 12 cha Mkataba waBioanuai nchi 50 zilikuwa zimekwisha ridhia Itifaki hii na

Page 80: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

80

kuwezesha nchi wanachama wa Itifaki kuendesha kikao chakwanza (COP-MOP 1) tarehe 13-17 Oktoba, 2014.

Mheshimiwa Spika, Hadi Januari, 2017 nchi 92 zimesainiambapo nchi 96 duniani zimeridhia Itifaki ya Nagoya.Katika ukanda wa nchi za Afrika Mashariki nchi za Rwanda(2014), Kenya (2014), Uganda (2014 na Burundi (2014) tayarizimeridhia Itifaki ya Nagoya ni Tanzania ambayo ilikuwabado haijaridhia Itifaki hii. Hivyo kwa Bunge lako kukubalikuridhia itifaki Tanzania itakuwa imepiga hatua katikakuimarisha usimamazi wa rasilimali za kijenetiki kwakushirikiana na nchi wanachama.

Mheshimiwa Spika,Tanzania tayari imeandaa Kanuni zakisheria zitakazosimamia mfumo mzima wa upatikanaji warasilimali za kijenetiki, matumizi yake na kuhakikishamgawanyo sahihi wa faida zitokanazo na matumizi yarasilimali za kijenetiki nchini.Mheshimiwa Mwenyekiti, Msukumo mkubwa wa kuridhia itifakihii unatokana na watafiti wengi wa kigeni kusafirisha nje yanchi rasilimali za kijenetiki bila kuzingatia mgawanyo sahihiwa faida zitokanazo na matumizi ya rasilimali hizi. Hivyo,nchi wanachama ziliona kwamba kuna umuhimu wakudhibiti hali hii ili nchi hizi ziweze kunufaika na rasilimali zakijenetiki pamoja na elimu asili ya rasilimali hizi katika nchizao. Vilevile utekelezaji wa Itifaki hii unawiana na utekelezajiwa Sheria ya Mazingira Cap 191 Kifungu cha 230 (2) (d)ambacho kinatoa fursa ya kuandaa kanuni ya kusimamiarasilimali za kijenetiki.

Mheshimiwa Spika, Dhamira za kuridhia Itifaki ni kwamba,endapo matumizi ya rasilimali za kijenetiki na elimu asilizinazohusisha matumizi ya rasilimali pamoja na kuimarishafursa za mgawanyo sahihi wa faida zitokanazo na matumiziya rasilimali hizo zitaimarishwa, nchi wanachama zinatarajiakwamba Itifaki hii itakuwa kichocheo katika hifadhi yabioanuai, matumizi endelevu ya bioanuai na bidhaazitokanazo na bioanuai na pia Itifaki itaimarisha mchangowa bioanuai katika maendeleo endelevu na maisha yawananchi kwa ujumla.

Page 81: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

81

Mheshimiwa Spika, Faida za kuridhia Itifaki hii kwa nchi yetuni kuwa itawezesha nchi kuweka utaratibu wa kusimamiaupatikanaji wa rasilimali za kijenetiki na mgawanyo sahihiwa faida zitokanazo na matumizi ya rasilimali asili zakijenetiki. Ofisi inayoratibu shughuli za Mkataba wa Hifadhiya Bioanuai itaimarisha utekelezaji wa Mkataba pamoja naItifaki ya Nagoya kikamilifu kwa kuweka mfumo sahihi wakusimamia rasilimali za kijenetiki kwa matumizi ya watumiajiwa ndani na nje kwa kuzingatia taratibu zitakazowekwa.

Mheshimiwa Spika, Kwa kuzingatia kwamba mfumo wasasa hauna taratibu nzuri za kudhibit i wageni nawanaofanya tafiti kutoka nje, rasilimali zetu muhimuzinachukuliwa na kusafirishwa bila kujua, na matokeo yatafiti hizo mbalimbali pamoja na faida zake zimekuwahazijulikani na wala nchi au jamii ambako jenetiki hizo zatafiti zimechukuliwa hazifaidiki na tafiti hizo pamoja nafaida itokanayo na tafiti. Nimatarajio yetu kuwa Itifaki hiiitatusaidia mambao muhimu yafuatayo:

i. Kuweka misingi ya sheria na uwazi kwa watoaji wawatumiaji wa ndani na nje wa rasilimali za kijenetiki;

ii. Baada ya kuweka utaratibu sahihi watumiaji na watafitiwote watapaswa kuzingatia sheria za nchi zinazohusianana rasilimaliasili za kijenetiki;

iii. Baada ya kuweka utaratibu sahihi wa kusimamiaupatikanaji wa rasilimali asili za kijenetiki jamii zenye elimuasili zinazohusiana na rasilimali za kijenetiki zitafaidika namgawanyo sahihi wa faida utakaozingatiwa katikamakubaliano ya kupata rasilimali husika;

iv. Kuwepo kwa sheria itayoweka utaratibu mzuri waupatikanaji wa rasilimali za kijenetiki utaimarisha udhibiti wawatumiaji hususan wageni kuhamisha holela rasilimali asili zakijenetiki kupitia vibali visivyozingatia faida ya matokeo yautafiti wa rasilimali za kijenetiki; na

v. Kutokana na utaratibu utakaowekwa wa kuhakikisha

Page 82: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

82

kuwa sehemu ya faida zitokanazo na matumizi ya rasilimaliza kijenetiki itarejeshwa kuendeleza hifadhi ya bioanuai,utaratibu huu utatoa motisha ya hifadhi na matumiziendelevu ya bioanuai na utabaoresha ustawi wa jamii kwaujumla.

Mheshimiwa Spika, Kutokana na mfumo wa uendeshaji waMkataba wa Hifadhi ya Bioanuai, nchi wanachama hupatafursa za kubadilishana mbinu na uzoefu wa kusimamia hifadhiya bionuai na pia fursa za kupata fedha kupitia vyanzombalimbali ikiwemo Mfuko wa Mazingira wa Dunia kwa ajiliya kutekeleza malengo ya Itifaki na Mkataba wa Hifadhi yabioanuai kwa ujumla. Hivyo, katika kuendeleza shughuli zahifadhi ya bioanuai na kuimarisha hali ya maisha kwa jamiikuna umuhimu wa kuridhia Itifaki hii.

Mheshimiwa Spika, Kutokana na kutokuwepo kwa sheriazinazodhibiti kikamilifu watumiaji wa rasilimali za kijenetikihususan wageni na watafiti mbalimbali kutoka nje, wagenina watafiti wengi wamesafirisha rasilimali asili za kijenetikinje ya nchi na kuziendeleza na kunufaika wao binafsi namataifa yao kwa ujumla. Mfano mmea ujulikanao kamaUsambara violate unaopatikana Milima ya Usambaraumesafirishwa nje ya nchi na sasa wauzaji wengiwanajipatia fedha kutokana na mauzo ya mmea huu bilaya Tanzania kufaidika. Hivyo, kutoridhia Itifaki hii kutatoamwanya zaidi kwa wageni na watafiti wengine kuendeleakukusanya na kusafirisha nje ya nchi mimea, wanyama, naviumbe wengine kwa faida yao na nchi zao.

Mheshimiwa Spika, Hasara za kuacha kuridhia Itifaki hiiitakuwa ni kulikosesha Taifa na wananchi mbalimbali fursaya kunufaika na rasilimali za kijenetiki pamoja elimu asili zaozinazohusiana na rasilimali asili za kijenetiki ambazo wagenina watafit i wengi wamekuwa wakizipata bila kutoamchango wowote. Hivyo, hasara ya kutoridhia Itifaki hii inasura mbili nazo ni:i. Kukosa faida zitokanazo na matumizi ya rasilimali zakijenetiki na zile elimu asili zinazohusiana na rasilimali zakijenetiki; na

Page 83: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

83

ii. Uhamishaji holela wa rasilimali za kijenetiki utaendelea nawageni na watafiti wataendelea kujinufaisha bila kusaidiahifadhi ya bioanuai.

Mheshimiwa Spika, Vipengele muhimu vya Itifaki hii nipamoja na:

Moja, Ibara ya 6: Utaratibu wa kupata idhini ya kuchukuarasilimali za kijenetiki. Ibara hii inahusu nchi kuweka taratibuza kupata idhini au vibali vya kukusanya mimea, wadudu,na wanyama kwa shughuli za kiutafiti au biashara ambapoidhini ya kupata rasiliami hizo lazima ipatikane kwa walewanaomiliki rasilimali husika kwanza.

Mbili, Ibara ya 7: Upatikanaji wa elimu asili inayohusuRasilimali za kijenetiki. Ibara hii inahusu nchi kuweka taratibuzitakazohakikisha kuwa elimu asili za jamii zinazohusiana narasilimali za kijenetiki zinazingatiwa na idhini ya kupatarasilimali inatolewa na jamii husika kabla ya kukusanya.

Tatu, Ibara ya 9: Uchangiaji wa Hifadhi na matumiziendelevu ya Bioanuai. Ibara hii inaelekeza nchi wanachamakuhimiza watumiaji na watoaji wa rasilimali za kijenetikikuchangia faida zitokanazo na rasilimali za kijenetiki.

Nne, Ibara ya 10: Mfumo wa kimataifa wa mgawanyosahihi wa faida zitokanazo na matumizi ya rasilimali zakijenetiki. Ibara hii inaelekeza nchi wanachama kuzingatiaumuhimu wa kuwa na mfuko wa dunia wa pamoja ambaoutazingatia namna ya kupata idhini na faida kwa rasilimaliza kijenetiki zilizoko mipakani ambazo zitahusisha jamii husikaza z anchi mbili au zaidi.

Tano, Ibara ya 13: Kuteua Mratibu wa kitaifa na mamlakazenye dhamana ya kusimamia rasilimali za kijenetiki. Ibarahii inaelekeza kila nchi wanachama kuteua Mratibu wakitaifa na mamlaka zenye dhamana ya kusimamia rasilimaliza kijenetiki kwa lengo la kufanya mawasilano na Sekretariatiya Mkataba ya bioanuai.

Page 84: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

84

Sita, Ibara ya 21: Kukuza uelewa wa wadau na jamii kwaujumla kuhusu Itifaki. Ibara hii inaelekeza nchi wanachamakukuza uelewa kuhusu umuhimu wa rasilimali za kijenetikina elimu asili inayohusiana na rasilimali za kijenetiki na faidazitokanazo na upataikanaji wa rasilimali za kijenetiki.

Saba, Ibara ya 22: Kujenga uwezo wa Taasisi na Rasilimaliwatu katika kusimamia na kutekeleza kikamilifu Itifaki.Ibara hii inaelekeza nchi wanachama kujenga uwezo wataasisi na rasilimali watu kwa ajili ya utekelezaji wa itifaki hiikatika ngazi ya kitaifa na kimataifa. Hatua za kujenga uwezoni pamoja na kujenga uwezo wa jamii asili na wananchihususan wanawake kuhusiana na upatikanaji wa rasilimaliza kijenetiki au elimu asili inayowiana na rasilimali zakijenetiki.

Mheshimiwa Spika, Matokeo ya kuridhia Itifaki hii nikuwezesha kuwepo kwa utaratibu wa upatinaji namgawanyo sahihi wa faida zitokanazo na matumizi yarasilimali asili za kijenetiki ikiwa ni pamoja na:

i. Kuweka misingi ya Sheria na uwazi kwa watoaji nawatumiaji wa rasilimali asili za kijenetiki;

ii. Kuwezesha uzingatiaji wa sheria za nchi zinazohusiana narasilimali asili za kijenetiki;

iii. Kuwezesha jamii kufaidika na elimu au ujuzi asili warasilimali za kijenetiki;

iv. Kuimarisha udhibiti wa uhamishaji holela wa rasilimali asiliza kijenetiki bila faida kwa nchi na jamii kwa ujumla;

v. Kutoa motisha ya hifadhi na matumizi endelevu yabioanuai kwa ajili ya ustawi wa jamii kwa ujumla; na

vi. Kupata fursa za fedha kwa ajili ya kutekeleza malengo yaItifaki.Mheshimiwa Spika; baada ya maelezo haya, sasa naombakuwasilisha Azimio la Bunge la kuridhia kama ifuatavyo;

Page 85: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

85

KWA KUWA, Tanzania ni Nchi Mwanachama wa Mkataba waBioanuai wa Mwaka 1992 unaohusu hifadhi ya bioanuai,matumizi endelevu ya bioanuai, na mgawanyo wa faidazitokanazo na matumizi ya bioanuai ambao uliridhiwatarehe 8 Machi, 1996;

NA KWA KUWA, Chini ya Mkataba huu kuna Itifaki yaCartagena ya Mwaka 2000, inayohusu Usimamizi Salama waMazingira Dhidi ya Athari Zinazoweza kutokea kutokana naMatumizi ya Biotekinolojia ya Kisasa ambayo Tanzania iliridhiatarehe 16 Machi, 2003;

NA KWA KUWA, katika Mkutano wa sita (6) wa Mkataba waBioanuai uliofanyika Johannesburg, Jamhuri ya Afrika KusiniMwaka 2002, ulibaini kwamba lengo la tatu la Mkataba huolinalohusu mgawanyo sahihi wa faida zitokanazo namatumizi ya rasilimali za kijenetiki halijafikiwa kutokana nakukosekana kwa mfumo wa kusimamia utekelezaji waMkataba huo;

NA KWA KUWA, ili kuweka mfumo wa usimamizi waMkataba, mchakato wa kuanzisha Itifaki ya KusimamiaUpatikanaji na Mgawanyo Sahihi wa Faida Zitokanazo naMatumizi ya Rasilimali za Kijenetiki ulianzishwa na Itifaki hiiilipitishwa katika Mkutano wa 10 wa Nchi Wanachama waMkataba uliofanyika Nagoya, Japan Mwaka 2010.

NA KWA KUWA, Tanzania iliridhia Mkataba wa BioanuaiMwaka 1996 ambao umeanzisha Itifaki ya KusimamiaUpatikanaji na Mgawanyo Sahihi wa Faida Zitokanazo naMatumizi ya Rasilimali za Kijenetiki (The Nagoya Protocol onAccess to Genetic Resources and the Fair and EquitableSharing of Benefits Arising From their Utilisation to theConvention on Biological Diversity) ambapo Ibara ya 33 yaItifaki hii, inaweka masharti ya kuridhiwa na NchiWanachama na kisha Hati ya kuridhia (Instruments ofAccession) kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja waMataifa;NA KWA KUWA Tanzania kwa kuridhia Itifaki hii na hatimayekuitekeleza itanufaika na mambo yafuatayo:

Page 86: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

86

(a)kuwa na misingi ya Sheria na uwazi kwa watoaji nawatumiaji wa rasilimali za kijenetiki kuwekwa;

(b)Sheria za Nchi zinazohusiana na rasilimali za kijenetikikuzingatiwa;

(c) jamii itanufaika na elimu au ujuzi asili wa rasilimali zakijenetiki;

(d)kudhibiti uhamishaji holela wa rasilimali za kijenetiki bilafaida kwa Nchi na Umma kwa ujumla;

(e)kuongezeka kwa motisha ya hifadhi na matumiziendelevu ya bioanuai kwa ajili ya ustawi wa jamii; na

(f) kupatikana kwa fursa za fedha kwa ajili ya kutekelezamalengo ya Itifaki.

HIVYO BASI, kwa kuzingatia umuhimu na manufaa ya Itifakihii kwa Tanzania, Bunge hili katika Mkutano wa Saba (7) nakwa mujibu wa Ibara ya 63(3)(e) ya Katiba ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania ya mwaka, 1977, linaazimia kuridhiaITIFAKI YA KUSIMAMIA UPATIKANAJI NA MGAWANYO SAHIHIWA FAIDA ZITOKANAZO NA MATUMIZI YA RASILIMALI ZAKIJENETIKI yaani Nagoya Protocol on Access to GeneticResources and the Fair and Equitable Sharing of BenefitsArising from their Utilization to the Convention on BiologicalDiversity.

Mheshimiwa Spika; naomba kuwasilisha na kutoa hoja.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, sasa namuitaMwenyekiti wa Kamati ya Biashara, ajiandae Msemaji waKambi ya Upinzani.

MHE. STANSLAUS H. NYONGO – KAIMU MWENYEKITIWA KAMATI YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA:Mheshimiwa Mwenyekiti, yafuatayo ni maoni ya Kamati yaKudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusuBunge Azimio la Bunge la Kuridhia Mkataba wa Marekebisho

Page 87: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

87

wa Nairobi wa Hifadhi, Usimamizi na Uendelezaji waMazingira ya Bahari na Ukanda wa Pwani ya Magharibi mwaBahari ya Hindi yaani Amended Convention for the Protection,Management and Development of the Marine and CoastalEnvironment of the Western Indian Ocean.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Kanuni ya53(6)(b) naomba kuwasilisha maoni ya Kamati ya Kudumuya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu Azimiola Bunge la Kuridhia Mkataba wa Marekebisho ya Nairobiwa Hifadi, Usimamizi na Uendelezaji wa Mazingira ya Baharina Ukanda wa Pwani wa Magharibi ya Bahari ya Hindi Itifakiya Udhibiti wa Uchafuzi wa Mazingira ya Bahari na Ukandawa Pwani ya Magharibi ya Bahari yaani AmendedConvention for the Protection, Management andDevelopment of the Marine and Coastal Environment of theWestern Indian Ocean.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuzingatia masharti yafasili ya 6(b), kifungu cha 53 ikisomwa pamoja na fasili ya1(b) ya kifungu cha 7, Nyongeza ya Nane ya Kanuni zaKudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016, Kamati ya Kudumuya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira inalo jukumu lakushughulikia mikataba inayopendekezwa kuridhiwa naBunge iliyo chini ya Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais,Mazingira. Naomba kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa hojaya Serikali kuhusu Bunge kuridhia marekebisho ya Mkatabawa Hifadhi, Usimamizi na Uendelezaji wa Mazingira ya Baharina Ukanda wa Pwani ya Magharibi ya Bahari ya Hindi yaaniAmended Convention for the Protection, Management andDevelopment of the Marine and Coastal Environment of theWestern Indian Ocean ililetwa kwenye Kamati ya Bunge yaViwanda, Biashara na Mazingira kwa mujibu wa Kanuni ya53 ya Kanuni za Bunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niongeleechimbuko la mkataba wa marekebisho. Tanzania ni mojaya nchi ya Ukanda wa Pwani ya Magharibi ya Bahari ya Hindizina utajiri mkubwa wa rasilimali za bahari zikiwemo madini(ikiwemo gesi asilia na mafuta), samaki na mimea. Rasilimali

Page 88: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

88

hizi zimekuwa na mchango wa pekee katika uchumi waukanda huu. Ili kutumia ipasavyo rasilimali zake ilionekana nivyema nchi mbalimbali kushirikiana katika kutunza mazingiraya bahari. Kwa lengo hilo mkataba wa awali wa Nairobiwa Hifadhi, Usimamizi na Uendelezaji wa Mazingira ya Bahariya Ukanda wa Pwani ya Magharibi ya Bahari ya Hindiuliridhiwa tarehe 21 Juni, 1985 huko Nairobi. Mkataba huoulilenga kuzuia au kukabiliana na uchafuzi wa mazingira yabahari unaotokana na:-

(i) Shughuli na vyombo vya usafirishaji baharini kamameli;

(ii) Utupaji wa taka;

(iii) Vyanzo na shughuli mbalimbali za kiuchumizilizoko nchi kavu;

(iv) Utafutaji na uchimbaji maliasili mbalimbali zilizopobaharini; na

(v) Usafirishaji wa taka zenye sumu unaovuka mipakaya nchi moja kwenda nchi nyingine na uchafuzi wa hewa/anga unaotokana na shughuli mbalimbali kama usafiri wandege wa angani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Marekebisho ya Mkataba waNairobi wa Hifadhi, Usimamizi na Uendeshaji wa Mazingiraya Bahari ya Ukanda wa Pwani ya Magharibi ya Bahari yaHindi kwa kifupi Marekebisho ya Mkataba yaani (AmendedConvention for the Protection, Management andDevelopment of the Marine and Coastal Environment of theWestern India Ocean) uliandikwa kwa kuzingatiachangamoto mpya zilizojitokeza tangu kusainiwa kwamkataba wa awali. Andiko la Mkataba wa Marekebisholilikubaliwa na mkutano wa nchi za Ukanda wa Pwani yaMagharibi ya Bahari ya Hindi tarehe 31 Machi, 2010 hukoNairobi. Moja ya nchi zilizokuwepo katika mkutano huo niNchi yetu ya Tanzania.

Page 89: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

89

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika andiko la Mkatabawa Marekebisho, nchi za Ukanda wa Pwani ya Magharibi yaBahari ya Hindi zilidhamiria kuendelea kuzuia au kukabilianana vyanzo vya uchafuzi vilivyoainishwa katika mkataba waawali (namba 1 - 6 ambavyo nimevitaja hapo juu). Zaidi yahayo, Mkataba wa Marekebisho umezingatia yafuatayo:-

(i) Haja ya kulinda na kudumisha bionuai ili kulindashughuli za kiuchumi kama uvuvi ambao umekuwaukidumaa kuanzia mwaka 2000;

(ii) Mabadiliko ya tabianchi na athari zake kwa viumbehai kama vile, ongezeko la halijoto na kina cha bahari,kupungua kwa alkali au ongezeko la tindikali kwenye majiya bahari, mabadiliko ya miongo na kadhalika;

(iii) Utambuzi wa haja ya kuwa na usimammizi wapamoja wa maendeleo ya sekta mbalimbali za uchumikatika Ukanda wa Pwani yaani intergrated coastal zonemanagement ya bahari ya Magharibi ya Bahari ya Hindi;

(iv) Makubaliano ya Mkutano wa Umoja wa Mataifajuu ya Mazingira na Maendeleo yaani outcomes and decisionsof the 1992 United Nations Conference on Environment andDevelopment;

(v) I l ikuwa ni mazingira maalum na hatarishiyanayojitokeza kwa nchi na visiwa hasa kutokana namadhara ya mabadiliko ya tabianchi;

(vi) Haja ya kuhamasisha utekelezaji kitaifa nakimataifa kwa mikataba mbalimabli ya kimataifa;

(vii) Nafasi ya taasisi zisizo za kiserikali yaani Non-Governmental Organizations – NGO’s, makundi ya kijamii nawanaharakati mbalimbali katika kuhamasisha utunzaji borawa mazingira;

(viii) Uwepo wa mikataba mbalimbali ya kimataifajuu ya mazingira ya bahari ambayo ukizingatia inapaswa hali

Page 90: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

90

halisi ya Ukanda wa Pwani ya Magharibi ya Bahari ya Hindina kadhalika; na

(ix) Ongezeko la ukubwa wa eneo la mkataba nakujumuisha pwani ya nchi ya Afrika Kusini iliyojikomboakutokana na ubaguzi wa rangi mwaka 1992.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati ilifanya kazi yaketarehe 14 Juni, 2017 na Kamati ilikutana na kupata maelezoya Serikali kuhusu pendekezo la kuridhia Mkataba waMarekebisho ya Nairobi. Aidha, tarehe 18 Juni, 2017 Ofisi yaBunge kupitia Mradi wa LSP iliiwezesha Kamati kupata uelewana stadi muhimu kuhusu utaratibu wa Bunge kuridhiamikataba ya kimataifa. Uelewa huu uliisaidia Kamati kuwakatika nafasi nzuri ya kuifanyia kazi hoja hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati ilipotekeleza jukumulake kuhusiana na hoja hii, ilizingatia masharti ya Kanuni ya117(8) na 117(9) kuhusu utaratibu wa Kamati pamoja nakuwaalika wadau. Katika hatua hii, Kamati iliwaalikawataalam kutoka Asasi za Serikali, Asasi za Kiraia (AZISE) nawadau wengine kwa ajili ya kupata maoni yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunawashukuru wadauwote waliowasilisha maoni yao kwa Kamati. Kwa namnaya pekee Kamati inakishukuru Chuo Kikuu cha Dar es Salaamkupitia Taasisi ya Sayansi ya Bahari kwa maoni na ushauriwao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati ilijiridhisha kuhusu haliiliyofikiwa katika mkataba huu kwa kuangalia nguvu yakisheria ya mkataba. Mkataba wa Marekebisho uliopitauliwapatia nguvu ya kisheria ya tarehe 1 Aprili, 2010 kwamujibu wa Ibara ya 29 kwa kuuweka wazi tayari kusainiwana nchi wanachama. Nchi wanachama na ambazo siowanachama zilizoalikwa na kuridhia kusaini kuanzia tarehe1 Aprili, 2010 hadi tarehe 1 Aprili, 2011.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utekelezaji wa Marekebishoya Mkataba huu utaanza siku 19 yaani mara baada ya nchi

Page 91: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

91

mwanachama wa sita kuwasilisha hati ya kuridhia, ni kwamujibu wa Ibara ya 32(2) ya Marekebisho ya Mkataba. Mpakasasa ni nchi mbili tu ndio zimekwisha wasilisha Hati ya kuridhiana nchi nyingine zipo katika hatua za kuridhia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaomba radhi kwa sababuya muda, baadhi ya mambo mengine yaingie kwenyekumbukumbu. Naomba sasa niende moja kwa moja kwenyemaoni na ushauri wa Kamati.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mwenyekiti, muda wako nimdogo na una maazimio matatu. Ungeyapitisha yote ilimengine yaingie kwenye Hansard. Umebakiwa na dakikatano tu.

MHE. STANSLAUS H. NYONGO – KAIMU MWENYEKITIWA KAMATI YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA:Mheshimiwa Mwenyekiti, sawa nashukuru. Nakwenda kwenyemaoni na ushauri moja kwa moja wa Kamati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kueleza yote hayanaomba sasa kutoa maoni ya mapendekezo ya Kamati kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkataba wa Marekebishoni muhimu kwa Tanzania na nchi nyingine za Ukanda waPwani ya Magharibi ya Bahari ya Hindi kutokana nachangamoto zilizojitokeza katika kutekeleza makubalianoya awali yaliyofanyika takribani miongo mitatu iliyopita.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkataba wa Marekebishoutaiwezesha Tanzania kama nchi na kwa kushirikiana na nchimajirani zake katika Ukanda wa Pwani ya Magharibi ya Bahariya Hindi kukabiliana na changamoto za uchafuzi namabadiliko mengine yanayoathiri mazingira ya bahari kwaukamilifu zaidi. Kama ilivyo kwa mkataba wa awali, mkatabawa Marekebisho pia umezingatia haja ya nchi za Ukandawa Pwani ya Magharibi ya Bahari ya Hindi kuwa na mtandaowa taasisi zake za utafiti ili kuimarisha mashirikiano katikatafiti, ufuatiliaji na ubadilishanaji wa taarifa. Kujumuika kwa

Page 92: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

92

Afrika Kusini katika Ukanda wa Pwani ya Magharibi ya Bahariya Hindi kunatoa fursa kubwa na ya pekee kwa maendeleoya sayansi na teknolojia ya mambo ya bahari. Kutokana naumuhimu huu Kamati inalishauri Bunge lako kuridhiaMarekebisho ya Mkataba huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na umuhimu wakuridhia, yapo baadhi ya maeneo ambayo ni vyematukachukua tahadhari katika utekelezaji wa mkataba huu.Ibara ya 26 ya Mkataba wa Marekebisho unaitaka nchiiliyokubaliana na mkataba iwe imesaini angalau moja yaitifaki zake kama ilivyoainishwa katika Ibara ya 4, na pia nchihaiwezi kuwa mjumbe wa Itifaki bila kuwa mjumbe waMkataba wa Marekebisho.

Aidha, Ibara ya 33 inayoelezea kujitoa katika Mkataba,yaani nchi haiwezi kujitoa kwenye Mkataba wa Marekebishoikabaki kwenye Itifaki au kinyume chake. Kamati inashauriSerikali kuzingatia mambo haya kwa ajili ya madhara yakiuchumi yanayoweza kujitokeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuzingatia umuhimuwa suala la mazingira na mabadiliko ya tabianchi, Kamatiinakubaliana na maelezo ya Serikali kuhusu faidazitakazopatikana na kuridhia Azimio hili, pamoja na ukwelikwamba Azimio hil i halikuletwa kwa wakati. Kamatiinaishauri Serikali kuleta Bungeni kwa wakati mikataba yoteya Kimataifa ili iweze kuridhiwa kwa wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati inaishauri Serikalikuwa makini na mikataba inayohusu mazingira ya baharikwa kuwa inaweza kuwa kikwazo katika uvunaji wa rasilimaliza baharini ikiwemo ugunduzi wa gesi asilia, uvuvi, kilimo,makazi na viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimpe mwenzanguambaye anakwenda sasa kutoa maoni ya Kamati kuhusianana Itifaki ya Mazingira na baada ya hapo atakuja mwingineatatoa maoni ya Itifaki ya Nagoya. Ahsante sana.

Page 93: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

93

MAONI YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA VIWANDA,BIASHARA NA UWEKEZAJI KUHUSU AZIMIO LA BUNGE LAKURIDHIA MKATABA WA MAREKEBISHO WA NAIROBI WAHIFADHI, USIMAMIZI NA UENDELEZAJI WA MAZINGIRA YA

BAHARI NA UKANDA WA PWANI YA MAGHARIBI MWABAHARI YA HINDI - KAMA YALIVYOWASILISHWA MEZANI

(Amended Convention for the Protection, Managementand Development of the Marine and Coastal Environment

of the Western Indian Ocean) __________

1.0 UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 53 (6) (b),naomba kuwasilisha maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bungeya Viwanda Biashara na Mazingira kuhusu Azimio la Bunge laKuridhia Mkataba wa Marekebisho wa Nairobi wa Hifadhi,Usimamizi na Uendelezaji wa Mazingira ya Bahari na Ukandawa Pwani ya Magharibi ya Bahari ya Hindi (AmendedConvention for the Protection, Management andDevelopment of the Marine and Coastal Environment of theWestern Indian Ocean).

Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia masharti ya fasili ya 6(b),Kifungu cha 53 ikisomwa pamoja na fasili ya 1(b) ya Kifungucha 7, Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge,Toleo la Januari, 2016, Kamati ya Kudumu ya Bunge yaViwanda, Biashara na Mazingira inalo jukumu la kushughulikiaMikataba inayopendekezwa kuridhiwa na Bunge iliyo chiniya Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira. Naombakuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa Hoja ya Serikali kuhusu Bungekuridhia Mkataba wa Marekebisho wa Hifadhi, Usimamizi naUendelezaji wa Mazingira ya Bahari na Ukanda wa Pwani yaMagharibi ya Bahariya Hindi (Amended Convention for theProtection, Management and Development of the Marineand Coastal Environment of the Western Indian Ocean), ililetwakwenye Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingirakwa mujibu wa Kanuni ya 53 (3) ya Kanuni za Bunge.

Page 94: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

94

2.0 CHIMBUKO LA MKATABA WA MAREKEBISHO

Mheshimiwa Spika, Tanzania ni moja ya nchi za Ukanda waPwani ya Magharibi ya Bahari ya Hindi zina utajiri mkubwawa rasilimali za bahari zikiwemo, madini (ikiwemo gesi asiliana mafuta), samaki na mimea. Rasilimali hizi zimekuwa namchango wa pekee katika uchumi wa ukanda huu. Ilikutumia ipasavyo rasilimali zake ilionekana ni vyema nchimbalimbali kushirikiana katika kutunza mazingira ya bahari.Kwa lengo hilo Mkataba wa awali wa Nairobi wa Hifadhi,Usimamizi na Uendeshaji wa Mazingira ya Bahari ya Ukandawa Pwani ya Magharibi ya Bahari ya Hindi uliridhiwa tarehe21 June 1985 huko Nairobi. Mkataba huo ulilenga kuzuia na/au kukabiliana na uchafuzi wa mazingira ya bahariunaotokana na:

i) Shughuli na vyombo vya usafirishaji baharini k.m. meli;ii) Utupaji wa taka;iii) Vyanzo na shughuli mbalimbali za kiuchumi zilizoko nchikavu;iv) Utafutaji na uchimbaji maliasili mbalimbali zilizopobaharini;v) Usafirishaji wa taka zenye sumu unaovuka mipaka yanchi moja kwenda nchi nyingine; navi) Uchafuzi wa hewa/anga unaotokana na shughulimbalimbali k.m. usafiri wa ndege angani.

Mheshimiwa Spika, Marehebisho ya Mkataba wa Mkatabawa Nairobi wa Hifadhi, Usimamizi na Uendeshaji wa Mazingiraya Bahari ya Ukanda wa Pwani ya Magharibi ya Bahari yaHindi (kwa kifupi – Marekebisho ya Mkataba) – (AmendedConvention for the Protection, Management andDevelopment of the Marine and Coastal Environment of theWestern India Ocean) uliandikwa kwa kuzingatiachangamoto mpya zilizojitokeza tangu kusainiwa kwamkataba wa awali. Andiko la Mkataba wa Marekebisholilikubaliwa na mkutano wa nchi za Ukanda wa Pwani yaMagharibi ya Bahari ya Hindi tarehe 31 March 2010 hukoNairobi. Moja ya nchi zilizokuwepo katika mkutano huo nakuridhia andiko hilo ni Tanzani.

Page 95: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

95

Mheshimiwa Spika, katika andiko la Mkataba waMarekebisho, nchi za Ukanda wa Pwani ya Magharibi yaBahari ya Hindi zil idhamiria kuendelea kuzuia na/aukukabiliana na vyanzo vya uchafuzi vilivyoainishwa katikamkataba wa awali (nambari 1-6 hapo juu). Zaidi ya hayo,Mkataba wa Marekebisho umezingatia yafuatayo:

i) Haja ya kulinda na kudumisha bayoanuai ili kulinda shughuliza kiuchumi kama uvuvi ambao umekuwa ukidumaakuanzia miaka ya 2000;

ii) Mabadiliko ya tabianchi na athari zake kwa viumbehai,kama vile, ongezeko la halijoto na kina cha bahari, kupunguakwa alkali au ongezeko la tindikali kwenye maji ya bahari,mabadiliko ya miongo n.k.;

iii) Utambuzi wa haja ya kuwa na usimammizi wa pamojawa maendeleo ya sekta mbalimbali za uchumi katikaukanda wa pwani (intergrated coastal zone management)ya bahari ya Magharibi ya Bahari ya Hindi;

iv) Makubaliano ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa juu yaMazingira na Maendeleo (Outcomes and decisions of the 1992United Nations Conference on Environment andDevelopment);

v) Mazingira maalum na hatarishi yanayojitokeza kwa nchiza visiwa hasa kutokana na madhara ya mabadiliko yatabianchi;

vi) Haja ya kuhamasisha utekelezaji kitaifa na kimataifa wamikataba mbalimabli ya kimataifa;

vii) Nafasi ya taasisi zisizo za kiserikali (non-governmentalorganisations – NGO), makundi ya kijamii na wanaharakatimbalimbali katika kuhamasisha utunzaji bora wa mazingira;

viii) Uwepo wa Mikataba mbalimbali ya kimataifa juu yamazingira ya bahari ambayo haikuzingatia ipasavyo hali halisiya Ukanda wa Pwani ya Magharibi ya Bahari ya Hindi; n.k.

Page 96: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

96

ix) Ongezeko la ukubwa wa eneo la mkataba na kujumuishapwani ya nchi ya Afrika Kusini iliyojikomboa kutokana naubaguzi wa rangi mwaka 1992.

3.0 NAMNA KAMATI ILIVYOSHUGHULIKIA HOJA HII

Mheshimiwa Spika, tarehe 14 Juni, 2017 Kamati ilikutana nakupata maelezo ya Serikali kuhusu pendekezo la kuridhiaMkataba wa Marekebisho wa Nairobi. Aidha, tarehe 18 Juni,2017 Ofisi ya Bunge kupitia Mradi wa LSP iliiwezesha Kamatikupata uelewa na stadi muhimu kuhusu Utaratibu wa Bungekuridhia Miakataba ya Kimataifa. Uelewa huu uliisaidia Kamatikuwa katika nafasi nzuri ya kuifanyia kazi hoja hii.

Mheshimiwa Spika, Kamati ilipotekeleza jukumu lakekuhusiana na hoja hii, ilizingatia masharti ya Kanuni ya 117(8) na 117 (9) kuhusu utaratibu wa Kamati pamoja nakuwaalika wadau. Katika hatua hii, Kamati iliwaalikawataalamu kutoka asasi za Serikali, asasi za kiraia (AZISE) nawadau wengine kwa aji l i ya kupata maoni yao.Tunawashukuru wadau wote waliowasilisha maoni yao kwaKamati. Kwa namna ya pekee Kamati inakishukuru ChuoKikuu cha Dar es Salaa kupitia taasisi ya Sayansi ya Baharikwa maoni na ushauri wao.

Mheshimiwa Spika, i l i kuliwezesha Bunge kutekelezamadaraka yake ipasavyo kwa mujibu wa Ibara ya 63(3) (e),Kamati ilizingatia mambo mbalimbali yaliyo muhimu katikakuifanyia kazi hoja ya Serikali iliyo mezani leo. Mambo hayoni pamoja na kuangalia Katiba ya Jamhuri ya Muunganowa Tanzania, baadhi ya Sheria za nchi zinazohusiana mojakwa moja na maudhui ya Mkataba unaopendekezwa,Uzoefu wa nchi nyingine katika masuala muhimu ya Mkatabana kutafakari kuhusu hasara au faida na kiwango chamanufaa au madhara yanayoweza kupatikana kwa kuridhiaau kutokuridhia Mkataba huu. Kamati ilijiridhisha pia iwapokuna umuhimu wa kuridhia Mkataba huu kama ulivyo aukuridhia baadhi ya vifungu vya Mkataba (Ratifying withreservation).

Page 97: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

97

Mheshimiwa Spika, Kamati ilijiridhisha kuhusu hali iliyofikiwakatika Mkataba huu kwa kuangalia nguvu ya kisheria yaMkataba. Mkataba wa Marekebisho ulipata nguvu ya kisheriatarehe 1 Aprili, 2010 kwa mujibu wa Ibara 29 kwa kuuwekawazi tayari kusainiwa na nchi wanachama. Nchiwanachama na ambazo siyo wanachama zilizoalikwa nakuridhia kusaini kuanzia tarehe 1 Aprili, 2010 hadi 1 Aprili, 2011.

Nanukuu: Article 29 “This convention shall be open forsignature at the Nairobi, Kenya from the 1 April, 2010 to 1April, 2011 by any Contracting party and non-contracting partythat has been invited to the conference of Plenipotentiaries”Mwisho wa kunukuu.

Kwa kuzingatia takwa la Ibara hiyo Mkataba wa Marekebishohuu ulisajiliwa tarehe 1 Aprili, 2010 na kupewa Namba UNEP(DEPI)/EAF/CPP.6/11/Suppl na Nchi Wanachama zote kumi(10). Kwa sasa Nchi Wanachama zinaendelea na taratibuza kuridhia.

Utekelezaji wa Mkataba wa Marekebisho huu utaanza sikukumi na tisa (19) mara baada ya nchi mwanachama wasita (6) kuwasilisha hati ya kuridhia hii ni kwa mujibu wa Ibaraya 32 (2) ya Marekebisho ya Mkataba.

Nanukuu: Article 32 (2) “This convention shall enter into forceon the ninetieth day following the date of the deposit of thesixth instrument of ratification, acceptance, approval oraccession to this Convention by the states and organizationsreferred to in article 30” Mwisho wa kunukuu.

Mpaka sasa ni nchi mbili tu ndio zimekwisha wasilisha Hatiya kuridhia na nchi nyingine zipo katika hatua za kuridhiakulingana na taratibu za nchi husika.

Mheshimiwa Spika, Aidha, kwa mujibu wa Ibara ya 33(1-5)ya Mkataba wa Marekebisho huu unaruhusu NchiMwanachama kujitoa katika Mkataba, ambapo inaelezakuwa, muda wowote baada ya miaka mitatu tangu

Page 98: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

98

Mkataba kuanza kutekelezwa, nchi inaweza kujitoa kwakutoa taarifa ya maandishi kwa mtunza nyaraka.

Nanukuu: Mfano, Article 33 (1) “At any time after three yearsfrom the date on which this Protocol has entered into forcefor a Party, that Party may withdraw from this protocol bygiving written notification to the Depositary “ Mwisho wakunukuu.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Tanzania ni moja ya nchiwanachama wa Mikataba mbalimbali, Kamati ilizingatiaumuhimu wa kulinganisha misimamo ya nchi hizi kwamustakabali wa ushirikiano wetu. Ibara ya 3 (1) ya Mkatabawa Marekebisho wa Nairobi inairuhusu nchi mwanachamakuingia mikataba mingine ya uhifadhi na usimamizi waPwani ya Bahari lakini Mikataba hiyo isikinzane na utekelezajiwa Mkataba huu.

Nanukuu: Mfano, Article 3(1) “The Contracting Parties mayenter into a bilateral or multilateral agreements, includingregional or sub regional agreements, for the protection andmanagement of the marine and costal environment of theConvention area. Such agreement shall be considered withthis Convention and Protocols made and in accordance withinternational law. Copies of such agreement shouldcommunicated to the organization and through theOrganization to all Contracting Parties” Mwisho wa kunukuu.

Mheshimiwa Spika, Mkataba wa Msingi kuhusu Mikataba yaKimataifa ni Mkataba wa Viena ambao Tanzania iliuridhiamwaka 1976. Mkataba wa Viena umeweka kanuni za msingikuhusu uridhiaji wa mikataba ya kimataifa. Kanuni hizomuhimu zilizngatiwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge yaViwanda, Biashara na Mazingira, wakati wa kuifanyia kazihoja iliyopo mbele ya Bunge hili kwa sasa.

Mheshimiwa Spika, Mkataba wa Marekebisho wa Nairobiya Hifadhi, Usimamizi na Uendelezaji wa Mazingira ya Baharina ukanda wa Pwani ya Magharibi ya Bahari ya Hindi ni

Page 99: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

99

Mkataba wa Nyongeza unaotokana Mkataba wa Nairobi(CBD..1996)

Mheshimiwa Spika, suala la Uhifadhi wa Mazingira ya Baharina ukanda wa Pwani kwa Tanzania linafahamika, Serikalikwa kushiriana na wahisani imechkua hatua mbalimbali ilikukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Hili linajidhihirishakatika miradi ya ujezi wa kingo za bahari Pangani, Oceanroad, Kigomboni na Kisiwa Panza Zanzibar.

4.0 MAONI NA USHAURI WA KAMATI

Mheshimiwa Spika, baada ya kueleza yote hayo, naombasasa kutoa maoni na mapendekezo ya Kamati kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Mkataba wa Marekebisho ni muhimukwa Tanzania na nchi nyingine za Ukanda wa Pwani yaMagharibi ya Bahari ya Hindi kutokana na changamotozilizojitokeza katika kutekeleza makubaliano ya awaliyaliyofanyika takriban miongo mitatu iliyopita. Mkataba waMarekebisho utaiwezesha Tanzania kama nchi na kwakushirikiana na nchi majirani zake katika Ukanda wa Pwaniya Magharibi ya Bahari ya Hindi kukabiliana na changamotoza uchafuzi na mabadiliko mengine yanayoathiri mazingiraya bahari kwa ukamilifu zaidi. Kama ilivyo kwa mkataba waawali, mkataba wa Marekebisho pia umezingatia haja yanchi za Ukanda wa Pwani ya Magharibi ya Bahari ya Hindikuwa na mtandao wa Taasisi zake za utafiti ili kuimarishamashirikiano katika tafiti, ufuatiliaji na kubadilishana taarifa.Kujumuika kwa Afrika Kusini katika Ukanda wa Pwani yaMagharibi ya Bahari ya Hindi kunatoa fursa kubwa na yapekee kwa maendeleo ya sayansi na teknolojia ya mamboya bahari. Kutokana na umuhimu huuKamati inalishauriBunge lako kuridhia Marekebisho ya Mkataba huu.

Mheshimiwa Spika, pamoja na umuhimu wa kuridhia, yapobaadhi ya maeneo ambayo ni vyema tukachukua tahadharikatika utekelezaji wa mkataba huu.

Page 100: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

100

Mheshimiwa Spika, Ibara ya 26 ya Mkataba wa Marekebishounaitaka nchi iliyokubaliana na mkataba pia iwe imesainiangalau moja ya itifaki zake kama ilivoainishwa katika ibaraya 4; na pia nchi haiwezi kuwa mjumbe wa Itifaki bila kuwamjumbe wa Mkataba wa Marekebisho. Aidha, Ibara ya 33inayoelezea kujitoa katika Mkataba, yaani nchi haiwezikujitoa kwenye Mkataba wa Marekebisho ikabaki kwenyeItifaki au kinyume chake. Kamati inashauri Serikali kuzingatiamambo haya ajili ya madhara ya kiuchumi yanayowezakujitokeza.

Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia umuhimu wa suala lamazingira na mabadiriko ya tabianchi, Kamati inakubalianana maelezo ya Serikali kuhusu faida zitakazopatikana kwakuridhia Azimio hili, pamoja na ukweli kwamba Azimio hilihalikuletwa kwa wakati. Kamati inaishauri Serikali kuletaBungeni kwa wakati mikataba yote ya Kimataifa ili iwezekuridhiwa kwa wakati;

Mheshimi Spika, Kamati inaishauri Serikali kuwa makini namikataba inayohusu mazingira ya bahari kwa kuwa inawezakuwa kikwazo katika uvunaji wa rasilimali za bahariniikiwemo ugunduzi wa Gesi asilia, uvuvi, kilimo, makazi naViwanda;

5.0 HITIMISHOMheshimiwa Spika, naomba nikushukuru sana wewe kwauongozi wako mahiri na kwakunipa ruhusa ya kuwasilishamaoni haya ya Kamati. Niwashukuru pia Mheshimiwa NaibuSpika na Wenyeviti wote wa Bunge kwa kuratibu nakusimamia shughuli za Bunge kwa umakini na umahiri.

Mheshimiwa Spika, Kamati inapenda kumshukuru Waziri waNchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mhe.January Makamba(Mb), Naibu Waziri wake Mhe. LuhagaJoelson Mpina (Mb) Makatibu Wakuu, pamoja na wataalamuwote wa Ofisi hii muhimu kwa ushirikiani walioutoa wakatiwa kujadili Azimio hili.

Page 101: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

101

Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee kabisa, napendakuwashukuru wajumbe wote wa Kamati ya Bunge yaViwanda, Biashara na Mazingira kwa ushirikiano walioutoawakati wa kupitia kuchambua na hatimaye kuwasilishamaoni yake juu ya Azimio hili mbele ya Bunge hili tukufu.Orodha yao ni kama inavyosomeka hapa chini na kwa ruhsayako naomba majina yao yaingie kwenye kumbukumbuRasmi za Bunge.

(i) Mhe. Stanslaus Haroon Nyongo Mb Mwenyekiti(ii) Mhe. Vicky Passcal Kamata, Mb Mjumbe(iii) Mhe. Salim Hassan Turky, Mb Mjumbe(iv) Mhe. Kalanga Julius Laizer, Mb Mjumbe(v) Mhe Dkt. Dalaly Peter Kafumu Mjumbe(vi) Mhe. Khatib Said Haji, Mb Mjumbe(vii) Mhe. Tauhida Cassian Gallos, Mb Mjumbe(viii) Mhe. Munira Mustafa Khaibu, Mb Mjumbe(ix) Mhe. Anthony Calist Komu, Mb Mjumbe(x) Mhe. Godbless Jonathan Lema, Mb Mjumbe(xi) Mhe. Dkt. Mary Machuche Mwanjelwa,Mb Mjumbe(xii) Mhe. Lameck Okambo Airo, Mb Mjumbe(xiii) Mhe. Hawa Subira Mwaifunga, Mb Mjumbe(xiv) Mhe. Balozi Dkt Diodorus Kamala, Mb Mjumbe(xv) Mhe. Jesca David Kishoa, Mb Mjumbe(xvi) Mhe. Mbarouk Salim Ali, Mb Mjumbe(xvii) Mhe. Mussa Ramadhani Sima, Mb Mjumbe(xviii) Mhe. Anatropia Lwehikila Theonest, Mb Mjumbe(xix) Mhe. Faida Mohammed Bakar, Mb Mjumbe(xx) Mhe. Suleiman Ahmed Sadick, Mb Mjumbe(xxi) Mhe Ibrahim Hassanali Raza, Mb Mjumbe(xxii) Mhe. Abdulaziz Mohamed Abood, Mb Mjumbe(xxiii) Mhe. Dkt. Raphael MMasunga Chegeni, Mb Mjumbe(xxiv) Mhe. Sylvestry Francis koka, Mb Mjumbe(xxv) Mhe. Gimbi Dotto Massaba, Mb Mjumbe(xxvi) Mhe. Martha Mosses Mlata, Mb Mjumbe(xxvii) Mhe. Joyce John Mukya, Mb Mjumbe

Page 102: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

102

Mheshimiwa Spika, napenda pia kumshukuru Katibu waBunge Dkt. Thomas D. Kashililah; Mkurugenzi wa Idara yaKamati Bw. Athumani Hussein; Mkurugenzi msaidizi Sehemuya Fedha na Uchumi Bw. Michael Chikokoto; Makatibu waKamati Bw. Wilfred Magova na Bi. Zainab Mkamba na Msaidiziwa Kamati Bi Paulina Mavunde kwa kuratibu shughuli zaKamati.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha na naunga mkonoAzimio.

Stanslaus Haroon Nyongo, (Mb)MWENYEKITI

KAMATI YA BUNGE YA VIWANDA, BIASHARA NAMAZINGIRA29 Juni, 2017

MWENYEKITI: Aaah! Mimi nilifikiri unamaliza wewe yotekwa sababu yote ilikuwa haifiki dakika 20.

MHE. STANSLAUS H. NYONGO – KAIMU MWENYEKITIWA KAMATI YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA:Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa ridhaa yako nadhani…

MWENYEKITI: Humalizi yote wewe?

MHE. STANSLAUS H. NYONGO – KAIMU MWENYEKITIWA KAMATI YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA:Mheshimiwa Mwenyekiti, hapana.

MWENYEKITI: Haya basi muite huyo. Muite.

MHE. STANSLAUS H. NYONGO – KAIMU MWENYEKITIWA KAMATI YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA:Ahsante sana.

MWENYEKITI: Dakika tano!

Page 103: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

103

MHE. DKT. MARY M. MWANJELWA - K.N.y. MWENYEKITIWA KAMATI YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA:Mheshimiwa Mwenyekiti, dakika tano au kumi?

MWENYEKITI: Mengine yataingia kwenye Hansard!Wewe toa kauli mengine yaingie kwenye Hansard.

MHE. DKT. MARY M. MWANJELWA - K.N.Y. MWENYEKITIWA KAMATI YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA:Mheshimiwa Mwenyekiti, maoni ya Kamati ya Kudumu yaBunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Kuhusu Azimio laBunge kuridhia Udhibiti wa Uchafuzi wa Mazingira ya Baharina Ukanda wa Pwani ya Magharibi ya Bahari ya Hindikutokana na vyanzo na shughuli zinazofanyika nchi kavu(Protocal for the Protection of the Marine and CoastalEnvironment of the Western Indian Ocean from Land-basedsources and activities).

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote kutokana namuda kuwa finyu sana naomba taarifa yangu yote iingiekwenye Hansard kama ilivyo na vilevile maeneo yoteyaliyoandikwa protokali naomba yasomeke kama itifaki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, muda ni mchache sanainabidi niruke maeneo mengine ndiyo maana nimesemayaingie kwenye Hansard kama ilivyo.

Naomba nisome maoni na ushauri wa Kamati; baadaya kueleza yote hayo naomba sasa kutoa maoni namapendekezo ya Kamati kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, itifaki hii ina umuhimumkubwa katika kulinda na kuhifadhi mazingira ya fukwe nayale ya bahari pamoja na rasilimali zake. Maeneo ya fukwena bahari yana rasilimali nyingi ambazo ni muhimu kwamaisha ya binadamu lakini pia kwa uchumi wa nchi. Maeneohaya yamekuwa yakiathiriwa sana na uchafu pamoja naathari zingine zitokanazo na shughuli za kibinadamu zikiwepomakazi, kilimo, viwanda na shughuli nyingine zinazozalishauchafu na vitu vingine vinavyoweza kuathiri mazingira ya

Page 104: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

104

bahari. Kutokana na umuhimu huo, Kamati inalishauri Bungelako kuridhia nyongeza ya Mkataba huu.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,Kuhusu Utaratibu.

MHE. DKT. MARY M. MWANJELWA - K.n.y MWENYEKITIWA KAMATI YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA:Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na ushauri huo wa kuridhia,yapo baadhi ya maeneo ambayo ni vyema tukachukuatahadhari katika utekelezaji wa mkataba huu.

MHE. JOHN J. MYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, KuhusuUtaratibu.

MHE. DKT. MARY M. MWANJELWA (K.n.y MWENYEKITIWA KAMATI YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA):Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo Kamati inaishauri Serikalikwamba wakati wa utekelezaji wa sharti la Ibara hii izingatiemustakaali wa uchumi wa wananchi watakaoathiriwa naitifaki hii. Aidha ni vyema Serikali ikatoa…

KUHUSU UTARATIBU

MWENYEKITI: Subiri! Mheshimiwa Mnyika.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,tumevumilia muda mrefu. Msomaji wa kwanza alikuwaanasoma hatuna Taarifa ya Kamati, msomaji wa pilianasoma hatuna Taarifa ya Kamati. Tungeweza kuvumiliana kusikiliza kama tu angekuwa anasoma ripoti yote sasakwa bahati mbaya mambo yote wanasema yameingiakwenye Hansard kwa hiyo, maana yake hata kusikiliza napohatuwezi kuyasikia. Sasa tutayasoma saa ngapi, tutachangiasaa ngapi. Naomba utaratibu kabla hajaendelea mbeletupewe nakala…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mnyika, hebu kaa kwanza.Mheshimiwa Mnyika hebu kaa. Taarifa zote zinasambazwasasa hivi. Mheshimiwa Mwanjelwa endelea.

Page 105: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

105

MHE. DKT. MARY M. MWANJELWA (K.n.y. MWENYEKITIWA KAMATI YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA):Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.Vilevile ili kuwezakutekeleza kikamilifu masharti ya Ibara hii upo umuhimu wakuainisha sheria, sera, programu na masuala mengine yausimamizi ya nchi zote zitakazo saini makubaliano haya,suala hili ni changamoto kwa nchi zote wanachama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hitimisho,naombanikushukuru sana wewe kwa uongozi wako mahiri na kwakunipa ruhusa ya kuwasilisha maoni haya ya Kamati,niwashukuru pia Mheshimiwa Naibu Spika na Wenyeviti woteMheshimiwa Spika mwenyewe ambaye ni jemedari wetu waBunge lako Tukufu katika kuratibu na kusimamia shughuli zaBunge kwa umakini na umahiri. (Makofi)

Kamati inapenda kumshukuru Waziri wa Nchi, Ofisiya Makamu wa Rais, Muungano na mazingira, MheshimiwaJanuary Makamba Mbunge, Makatibu wakuu pamoja nawataalamu wote wa Ofisi hii muhimu kwa ushirikianowalioutoa wakati wa kujadili Azimio hili bila kumsahauMheshimiwa Naibu Waziri, Mheshimiwa Luhaga Mpina.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa namna ya pekee kabisanapenda kuwashukuru wajumbe wote wa kamati ya Bungeya Viwanda, Biashara na Mazingira kwa ushirikiano walioutoawakati wa kupitia na kuchambua na hatimaye kuwasilishamaoni yake juu ya azimio hil i mbele ya Bunge hil iTukufu,orodha yao ipo hapo ni ndefu naomba nisiisome.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile naomba piakumshukuru Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah,Mkurugenzi wa Idara ya Kamati Bw. Athumani Hussein,Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Fedha na Uchumi BwanaMichael Chikokoto, Makatibu wa Kamati Bwana AlfredMagova na Bi. Zainabu Mkamba na Msaidizi wa Kamati Bi.Pauline Mavunde kwa kuratibu shughuli za Kamati. Naombakuwasilisha na ninaunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante.

Page 106: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

106

MAONI YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA VIWANDA,BIASHARA NA MAZINGIRA KUHUSU AZIMIO LA BUNGE

KURIDHIA ITIFAKI YA NAGOYA YA KUSIMAMIA UPATIKANAJIWA MGAWANYO SAHIHI WA FAIDA ZITOKANAZO NA

MATUMIZI YA RASILIMALI ZA KIJENETIKI - KAMAYALIVYOWASILISHWA MEZANI

(Nagoya Protocol on Access to Genetic Resources and theFair and Equitable Sharing of Benefits Arising from theirUtilization to the Convention on Biological Diversity)

_________________

1.0 UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika, kabla sijasoma Taarifa hii naombakufanya marekebisho katika nakala za hotuba yanguwalizogawiwa Waheshimiwa Wabunge kwa kuondoamaneno “Mkataba wa Nyongeza”, na badala yake kuwekaneno Itifaki. Naomba Taarifa yangu yote pamoja namarekebisho yake, iingie kwenye kumbukumbu ya TaarifaRasmi za Bunge.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 53 (6) (b),naomba kuwasilisha maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bungeya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu Azimio la Bungela Kuridhia Itifaki ya Nagoya ya kusimamia Upatikanaji waMgawanyo sahihi wa faida zitokonazo na Matumizi yaRasilimali za Kijenetiki (Nagoya Protocal on Access to GeneticResources and the Fair and Equitable Sharing of Benefits arisingfrom their utilization to the Convention on Biological Diversity).

Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia masharti ya fasili ya 6(b),Kifungu cha 53 ikisomwa pamoja na fasili ya 1(b) ya Kifungucha 7, Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge,Toleo la Januari, 2016, Kamati ya Kudumu ya Bunge yaViwanda, Biashara na Mazingira inalo jukumu la kushughulikiaMikataba inayopendekezwa kuridhiwa na Bunge iliyochini yaOfisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira. Naombakuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa Hoja ya Serikali kuhusu Bungekuridhia Itifaki ya Nagoya ya kusimamia Upatikanaji wa

Page 107: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

107

Mgawanyo sahihi wa faida zitokonazo na Matumizi yaRasilimali za Kijenetiki (Nagoya Protocal on Access to GeneticResouces and the Fair and Equitable Sharing of Benefits arisingfrom their utilization to the Convention on Biological Diversity)ililetwa kwenye Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara naMazingira kwa mujibu wa Kanuni ya 53 (3) ya Kanuni za Bunge.

2.0 CHIMBUKO LA MKATABA WA NYONGEZA

Mhesimiwa Spika, chimbuko na asili la Itifaki hii ni miongonimwa mambo muhimu katika kuridhia. Imeelezwa kuwaMkataba wa Bioanuai wa Mwaka 1992, una Itifaki tatuambazo ni Itifaki ya Cartagena ya mwaka 2000 inayohusuUsimamizi wa Mazingira Dhidi ya Athari zinaweza kutokeakutokana na Matumizi ya Biotekinolojia ya kisasa; Itifaki yakusimamia upatikanaji na mgawanyo sahihi wa faidazitokanazo na matumizi ya rasilimali asili za kiejenetiki; naItifaki ya ziada ya Nagoya – Kuala Lumpur kuhusu uwajibikajikisheria na fidia katika kutekeleza Itifaki ya Cartagena.

Mheshimiwa Spika, mkutano wa sita (6) wa nchiwanachama wa Mkataba wa Bioanuai uliofanyikaJohannesburg, Afrika ya Kusini mwaka 2002, ulibaini kusuasauakatika utekelezaji wa lengo la tatu la Mkataba huu. Lengohili linahusu mgawanyo sahihi wa faida zitokanazo namatumizi ya rasilimali za kijenetiki. Kutofikiwa kwa Lengo hilikunatokana na kutokuwepo mfumo rasmi wa usimamizirasimali za kijenetiki.

Mheshimiwa Spika, katika Mkutano huo ilikubaliwa kuanzishaItifaki kwa ajilli ya kusimamia rasilimali hizi. Mchakato huoulihusisha majadiliano yaliyofanyika katika mikutano tisakuanzia 2002 hadi 2010. Itifaki inayopendekezwa ilipitishwana nchi wanachama katika mkutano wa kumi uliofanyikaNagoya, Japani mwaka 2010.

3.0 NAMNA KAMATI ILIVYOSHUGHULIKIA HOJA HII

Mheshimiwa Spika, tarehe 14 Juni, 2017 Kamati ilikutanakatika na kupata maelezo ya Serikali kuhusu pendekezo la

Page 108: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

108

kuridhia Itifaki ya Nagoya ya kusimamia Upatikanaji waMgawanyo sahihi wa faida zitokonazo na Matumizi yaRasilimali za Kijenetiki (Nagoya Protocal on Access to GeneticResouces and the Fair and Equitable Sharing of Benefits arisingfrom their utilization to the Convention on Biological Diversity).Aidha, tarehe 18 Juni, 2017 Ofisi ya Bunge kupitia Mradi waLSP iliiwezesha Kamati kupata uelewa na stadi muhimukuhusu Utaratibu wa Bunge kuridhia Mikataba na Itifakimbalimbali za Kimataifa. Uelewa huu uliisaidia Kamati kuwakatika nafasi nzuri ya kuifanyia kazi hoja hii.

Mheshimiwa Spika, Kamati ilipotekeleza jukumu lakekuhusiana na hoja hii, ilizingatia masharti ya Kanuni ya 117(8) na 117 (9) kuhusu utaratibu wa Kamati pamoja nakuwaalika wadau. Katika hatua hii, Kamati iliwaalikawataalamu kutoka asasi za Serikali, asasi za kiraia (AZISE) nawadau wengine kwa ajili ya kupata maoni yao. Kamatiinawashukuru wadau wote waliotoa maoni yao kuhusu itifakihii. Aidha, Kamati inawashukuru sana Chuo Kikuu cha Dar esSalaam kupitia Taasisi ya Sayansi za Bahari ambao wametoamaoni kadhaa yaliyosaidia kuboresha maoni ya Kamatikuhusu itifaki hii.

4.0 MAMBO YA MSINGI YALIYOZINGATIWA NA KAMATI

Mheshimiwa Spika, i l i kuliwezesha Bunge kutekelezamadaraka yake ipasavyo kwa mujibu wa Ibara ya 63(3) (e),Kamati il izingatia mambo mbalimbali muhimu katikakuifanyia kazi hoja ya Serikali iliyomezani leo. Mambo hayo nipamoja na kuangalia Katiba ya Jamhuri ya Mungano, baadhiya sheria za nchi zinazohusiana moja kwa moja na maudhuiya Itifaki inayopendekezwa, uzoefu wa nchi nyingine katikamasuala muhimu ya Itifaki hii pamoja na kutafakari kuhusuhasara au faida na kiwango cha manufaa au madharayanayoweza kupatikana kwa kuridhia au kutokuridhia Itifakihii kama ulivyo.

Mheshimiwa Spika, pamoja na maelezo ya Mtoa hoja,Kamati ilitaka kujiridhisha kuhusu hali iliyofikiwa katikaMkataba huu kwa kuangalia kama una nguvu ya kisheria

Page 109: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

109

na kubaini kuwa Ibara ya 32 ya Itifaki, Ibara hii iliweka waziItifaki kwa ajili ya kusainiwa na Nchi Wanachama waMkataba kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, NewYork kuanzia terehe 2 Februari, 2011 hadi 1 Februari, 2012.

Nanukuu: Article 32 “This Protocal shall be open for signatureby paties to the Convention at the United NationsHeadquarters in New York, from 2 February 2011 to 1 February2012 Mwisho wa kunukuu.

Utekelezaji wa Itifaki hii ulianza terehe 29 Octoba, 2014 baadaya Nchi Wanacama 50 kuridhia. Hii ni kwa mujibu wa Ibaraya 33 (1-3) ya Itifaki ambayo inaeleza kuwa utekelezaji waItifaki utaanza siku ya kumi na tisa (19) mara baada ya nchimwanachama ya hamsini (50) kuwasilisha hati ya kuridhia.

Nanukuu: Article 33 (1) “This convention shall enter into forceon the ninetieth day following the date of the deposit of thefiftieth instrument of ratification, acceptance, approval oraccession of the state or regional economic integrationorganizations that are Parties to the Convention”. Mwishowa kunukuu.

Aidha, hadi kufikia Mei, 2016 nchi Wanachama 72 zilikuwazimekwisha ridhia Itifaki hii. Tanzania itaridhia Itifaki hii kwakuzingatia Ibara ya 63(3) (e) ya Katiba ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania ya Mwaka 1997.

Kwa mujibu wa Ibara ya 35 ya Itifaki hii inaruhusu NchiMwanachama kujitoa katika Itifaki, ambapo imeeleza kuwa,muda wowote baada ya miaka miwili tangu Itifaki imeanzakutekelezwa, nchi hiyo inaweza kujitoa kwenye Itifaki kwakutoa taarifa ya maandishi kwa mtunza nyarakazinazohusiana na uridhiaji Itifaki hii.

Nanukuu: Mfano, Article 35 “At any time after two years fromthe date on which this Protocol has entered into force for aParty, that Party may withdraw from this protocol by givingwritten notification to the Depositary “ Mwisho wa kunukuu.

Page 110: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

110

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Tanzania ni NchiMwanachama wa Mikataba mbalimbali ya Kimataifa,Kamati ilizingatia kipengele cha Itifaki hii kuhusu ushikikianowetu na mkiataba mingine. Ibara ya 4 ya Itifaki inaelezauhusiano kati ya Mkataba na Mikataba mingine ya kimataifa,kwamba masharti ya Itifaki hayatakinzana na haki na wajibuwa Nchi yoyote mwanachama anazozipata na kutokanana Mikataba mingine ya Kimataifa, isipokuwa pale ambapoutekelezaji wa haki na wajibu wa Mikataba hiyo mingineitasababisha hasara kubwa kwa Viumbe hai. Itifaki hii hailengikuweka madaraja kati ya Mkataba huu na Mikataba mingineya kimatafa.

Nanukuu: Mfano, Article 4 “The provision of this Protocol shallnot affect the right and obligation of any Party deriving fromany existing international agreement, except where theexercise of those rights and obligations would cause a seriousdamage or threat to biological deversity” Mwisho wakunukuu.

Mheshimiwa Spika, Mkataba wa Msingi kuhusu Mikataba yaKimataifa ni Mkataba wa Viena ambao Tanzania iliuridhiaMkataba mwaka 1976. Mkataba wa Viena umeweka kanuniza msingi kuhusu uridhiaji wa mikataba ya kimataifa. Kanunihizo muhimu zilizingatiwa na Kamati ya Kudumu ya Bungeya Viwanda, Biashara na Mazingira wakati wa kuifanyia kazihoja iliyopo mbele ya Bunge hili kwa sasa.

5.0 MAONI NA USHAURI WA KAMATI

Mheshimiwa Spiaka, Lengo kuu la Itifaki hii nikuimarisha ushirikiano wa haki na wa usawa juu ya faidazitokanazo na matumizi ya rasilimali za kijenetiki, ikiwa nipamoja na upatikanaji sahihi wa rasilimali hiyo, ikiwepoupatikanaji na uhamishaji wa teknolojia husika, na kwaufadhili wa kifedha unaokubalika, hivyo basi kuchangiauhifadhi wa bioanuai na matumizi endelevu ya rasilimalizitokanazo kwayo. Lakini hili litafikiwa tu ikiwa utekelezajiwa kikamilifu na wa haki wa vipengele mbali mbali vilivyomokwenye Itifaki hiyo utafanyika.

Page 111: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

111

Mheshimiwa Spika, baada ya kuipitia Itifaki hii imeonekanainahakikisha ulinzi na udhibiti wa kutosha wa rasilimali zakijenetiki zetu. Hata hivyo, ili Taifa linufaike ipasavyo na fursazitokanazo na uanachama wa Itifaki hii ya Mkataba waBioanuai kwa ujumla wake mambo kadhaayanapendekezwa kufanyika:

Mheshimiwa Spika, Itifaki inaopendekezwa inatoa fursamuhimu ya kuheshimiwa na kuzingatiwa masharti namatakwa ya sheria za ndani za nchi mwanachama husika,kwenye makubaliano yoyote ya utoaji/ubadilishanaji warasilimali za kijenetiki na mfumo wa ugawanaji wa faidizitokanazo na matumizi ya rasilimali hiyo. Hivyo basi, Kamatiinashauri kwamba Sheria za nchi ziimarishwe ili kutoa udhibitiwa kutosha wa rasilimali hiyo, ili kuhakikishwa kwamba Taifalinanufaika ipasavyo na rasilimali hiyo;

Mheshimiwa Spika, Itifaki inapendekeza kwamba upatikanajina matumizi ya Ujuzi Jadi, an mgawanyo wa faida itokanayona matumizi ya ujuzi huo, ufanyike kwa makubaliano katijamii za jadi husika na mtumiaji (muhitaji). Kamati inashauriSerikali kuandaa mfumo madhubuti wa kisheria na kiutendajikuhakikisha kwamba inajihusisha kikamilifu katikamazungumzo na makubaliano yoyote yakayofanyika kati yapande hizo mbili ili kulinda maslahi ya nchi;

Mheshimiwa Spika, Itifaki haijatoa ukomo wa aina walakiwango cha fidia anayotakiwa kupata mmiliki wa rasilimalihizi kwa matumizi (yakiwemo ya kibiashara) yatokanayo narasilimali hiyo. Ni maoni ya Kamati kuwa mapendekezo hayayanaweza kutumiwa vibaya na watumiaji wa rasilimali hii,kwa kuamua kwa makusudi kulipa fidia isiyostahiki kwammiliki wa rasilimali. Hivyo Kamati inaishauri Serikali kuwekautaratibu utakaoainisha aina na kiwango cha fidia kulingana aina ya raslimali hiyo na matumizi yake;

Mheshimiwa Spika, Itifaki inapendekeza fursa ya ujenzi nauendelezaji wa uwezo wa rasilimali watu na wa kitaasisikwenye Nyanja ya uhifadhi na usimamizi wa bioanuai narasilimali kijenetiki. Kamati inaishauri Serikali kuweka mfumo

Page 112: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

112

mzuri utakaohakikisha kuwa fursa hiyo inatumiwa ipasavyokwa manufaa ya nchi, ikiwemo kuainisha vipaumbele vyetukwenye nyanja mbalimbali;

Mheshimiwa Spika, Itifaki inapendekeza uwepo wawataalamu na Taasisi/mamlaka maalum ya kitaifa(Competent National Authority) kwa kila nchi mwanachamaitakayokuwa kitovu (focalpoint) cha utekelezaji wa shughuliza Itifaki. Kamati inaishauri Serikali kuhakikisha kwambainatumia umakini mkubwa kwenye uteuzi wa wataalamuna taasisi hiyo (hizo), ili kuhakikisha kwamba maslahi ya taifayanalindwa kuhusiana na ubadilishanaji wa rasilimali zakijenetiki, ikikumbukwa kwamba taasisi hiyo itakuwa namamlaka ya kuidhinisha ubadilishanaji wa rasilimali hiyo kwaniaba ya Serikali;

Mheshimiwa Spika, kumekuwepo na uporaji wa rasilimali zakijenetiki katika nchi hii kwa kisingizio cha utafiti, watafitihawa huwashirikisha wazawa katika hatua za mwanzo kwania ya kujua baadhi ya rasilimali za kijenetihi hususani mizizi,majani, mbegu au magamba ya miti ambayo inatibu baadhiya magonjwa. Wageni wamenufaika sana na rasilimali zakijenetiki kwa kujipatia ujuzi wa asili kutoka kwenye jamii zetubila malipo huku wao wakijinufaisha na rasilimali zetu. Kamatiinaishauri Serikali kubainisha maeneo yote yenye rasilimali hizina kuyawekea utaratibu wa uvunaji. Jambo hili la kubainimaeneo liende sambamba na utoaji wa elimu kwa jamii juuya matumkizi na faida zitakazopatikana kama rasilimali zetuzikitumika kwa kuzingatia utaratibu maalumu; na

Mheshimwa Spika, kumekuwepo na ucheleweshaji katikakuridhia Itifaki na Mikataba mbalimbali ya Kimataifa. Mfanoni Itifaki ya Nagoya iliyosainiwa tangu Oktoba, 2010, mpakasasa Juni 2017, takribani miaka minane(8). Kamati inaishauriserikali kuwasilisha Bungeni kwa wakati Mikataba yote yakimaifa pindi inaposainiwa.

6.0 HITIMISHOMheshimiwa Spika, naomba nikushukuru sana wewe kwauongozi wako mahiri na kwa kunipa ruhusa ya kuwasilisha

Page 113: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

113

maoni haya ya Kamati. Niwashukuru pia Mheshimiwa NaibuSpika na Wenyeviti wote wa Bunge kwa kuratibu nakusimamia shughuli za Bunge kwa umakini na umahiri.

Mheshimiwa Spika, Kamati inapenda kumshukuru Waziri waNchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mhe.January Makamba(Mb), Naibu Waziri wake Mhe. LuhagaJoelson Mpina(Mb), Makatibu Wakuu, pamoja na wataalamuwote wa Ofisi hii muhimu kwa ushirikiani walioutoa wakatiwa kujadili Azimio hili.

Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee kabisa, napendakuwashukuru wajumbe wote wa Kamati ya Bunge yaViwanda, Biashara na Mazingira kwa ushirikiano walioutoawakati wa kupitia kuchambua na hatimaye kuwasilishamaoni yake juu ya Azimio hili mbele ya Bunge hili tukufu.Orodha yao ni kama inavyosomeka hapa chini na kwa ruhsayako naomba majina yao yaingie kwenye kumbukumbuRasmi za Bunge.

(i) Mhe. Stanslaus Haroon Nyongo Mb Mwenyekiti(ii) Mhe. Vicky Passcal Kamata, Mb Mjumbe(iii) Mhe. Salim Hassan Turky, Mb Mjumbe(iv) Mhe. Kalanga Julius Laizer, Mb Mjumbe(v) Mhe Dkt. Dalaly Peter Kafumu Mjumbe(vi) Mhe. Khatib Said Haji, Mb Mjumbe(vii) Mhe. Tauhida Cassian Gallos, Mb Mjumbe(viii) Mhe. Munira Mustafa Khaibu, Mb Mjumbe(ix) Mhe. Anthony Calist Komu, Mb Mjumbe(x) Mhe. Godbless Jonathan Lema, Mb Mjumbe(xi) Mhe. Dkt. Mary Machuche Mwanjelwa,Mb Mjumbe(xii) Mhe. Lameck Okambo Airo, Mb Mjumbe(xiii) Mhe. Hawa Subira Mwaifunga, Mb Mjumbe(xiv) Mhe. Balozi Dkt Diodorus Kamala, Mb Mjumbe(xv) Mhe. Jesca David Kishoa, Mb Mjumbe(xvi) Mhe. Mbarouk Salim Ali, Mb Mjumbe(xvii) Mhe. Mussa Ramadhani Sima, Mb Mjumbe(xviii) Mhe. Anatropia Lwehikila Theonest, Mb Mjumbe(xix) Mhe. Faida Mohammed Bakar, Mb Mjumbe(xx) Mhe. Suleiman Ahmed Sadick, Mb Mjumbe

Page 114: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

114

(xxi) Mhe Ibrahim Hassanali Raza, Mb Mjumbe(xxii) Mhe. Abdulaziz Mohamed Abood, Mb Mjumbe(xxiii) Mhe. Dkt. Raphael MMasunga Chegeni, Mb Mjumbe(xxiv) Mhe. Sylvestry Francis koka, Mb Mjumbe(xxv) Mhe. Gimbi Dotto Massaba, Mb Mjumbe(xxvi) Mhe. Martha Mosses Mlata, Mb Mjumbe(xxvii) Mhe. Joyce John Mukya, Mb Mjumbe

Mheshimiwa Spika, napenda pia kumshukuru Katibu waBunge Dkt. Thomas D. Kashililah; Mkurugenzi wa Idara yaKamati Bw. Athumani Hussein; Mkurugenzi msaidizi Sehemuya Fedha na Uchumi Bw. Michael Chikokoto; Makatibu waKamati Bw. Wilfred Magova na Bi. Zainab Mkamba na Msaidiziwa Kamati Bi Paulina Mavunde kwa kuratibu shughuli zaKamati.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha na naunga mkonoAzimio.

Stanslaus Haroon Nyongo, (Mb)MWENYEKITI

KAMATI YA BUNGE YA VIWANDA, BIASHARA NAMAZINGIRA29 Juni, 2017

MWENYEKITI: Mheshimiwa Chegeni, Waheshimiwakuna tangazo dogo kikao cha caucus cha Wabunge wotewa CCM, leo kutakuwa na kikao cha caucus Alhamisi tarehe29 saa 12.00 jioni, White House Wabunge wote wa Chamacha Mapinduzi mnaombwa kuhudhuria na mahudhurioyatazingatiwa.

MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI (K.n.y. MWENYEKITIWA KAMATI YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA):Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mwenyekiti wakamati naomba kuwasilisha maoni ya Kamati ya Kudumuya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu Azimio la Bungekuridhia itifaki ya Nagoya ya kusimamia upatikanaji wa

Page 115: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

115

mgawanyo sahihi ya faida zitokanazo na matumizi yarasilimali za kijenetiki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ya mudasitapenda kuwashukuru ila sitajikita kwenye maoni ya Kamati,maoni na ushauri wa Kamati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo kuu la itifaki hii nikuimarisha ushirikiano wa haki na usawa juu ya faidazitokanazo na matumizi ya rasilimali ya kijenetiki ikiwa nipamoja na upatikanaji sahihi wa rasilimali hiyo, ikiwepoupatikanaji wa uhamasishaji na teknolojia husika na kwaufadhili wa kifedha uliokubalika hivyo basi kuchangia hifadhina bionuai na matumizi endelevu ya rasilimali zitokanazo nakwayo. Lakini hili litafikiwa ikiwa utekelezaji wa kikamilifu nauhakika wa vipengele mbalimbali vilivyomo kwenye itifakihiyo utafanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kupitia itifaki hiiimeonekana inahakikisha ulinzi na udhibiti wa kutosha warasilimali wa kijenetiki zetu, hata hivyo ili Taifa linufaikeipasavyo na fursa hizi zifuatazo na wanachama wa itifaki hiipamoja na mkataba wa bionuai kwa ujumla wake mambokadhaa yanapendekezwa kufanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, itifaki inayopendekezwainatoa fursa muhimu ya kuheshimiwa na kuzingatiwamasharti na matakwa ya sheria ya ndani ya nchimwanachama husika kwenye makubaliano yote ya utoaji,ubadilishaji wa rasilimali wa kijenetiki na mfumo wa ugawajiwa faida zitokanazo na matumizi ya rasilimali hiyo. Hivyobasi Kamati inashauri kwamba sheria za nchi ziimarishwe ilikutoa udhibiti wa kutosha wa rasilimali hiyo ili kuhakikishakwamba Taifa linanufaika ipasavyo na rasilimali hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, it ifaki inapendekezakwamba upatikanaji wa matumizi ya ujuzi jadi na mgawanyowa faida itokanayo na matumizi ya ujuzi huo ufanyike kwamakubaliano kati ya jamii za jadi husika na mtumiaji aumuhitaji. Kamati inashauri Serikali kuandaa mfumo

Page 116: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

116

madhubuti wa kisheria na kiutendaji kuhaikisha kwambainajihusisha kikamilifu katika mazungumzo na makubalianoyote yatakayofanyika katika pande hizi mbili ili kulinda maslahiya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, itifaki haijatoa ukomo waaina wala kiwango cha fidia itayotakiwa kupata mmiliki warasil imali hizi kwa matumizi yakiwemo ya kibiasharayatokanayo na rasilimali hiyo. Ni maoni ya Kamati kuwamapendekezo haya yanaweza kutumiwa vibaya nawatumiaji wa rasilimali hii kwa kuamua kwa makusudi kulipafidia isiyostahiki kwa mmiliki wa rasilimali. Hivyo Kamatiinaishauri Serikali kuweka utaratibu utakaoainisha aina nakiwango cha fidia kulingana na aina ya rasilimali hiyo namatumizi yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, itifaki inapendekeza fursa yaujenzi na utekelezaji wa uendelezaji wa uwezo wa rasilimaliwatu na wa kitaasisi kwenye nyanja ya uhifadhi na usimamiziwa manuai na rasilimali kijenetiki. Kamati inaishauri Serikalikuweka mfumo mzuri utaohakikisha kuwa fursa hiyoinatumiwa ipasavyo kwa manufaa ya nchi ikiwemo kuainishavipaumbele vyetu kwenye nyanja mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, itifaki inapendekeza uwepowataalam na taasisi au mamlaka maalum ya kitaifa,(Competent National Authority) kwa kila nchi mwanachamaitakayokuwa kitovu (folk point) cha utekelezaji shughuli zaitifaki. Kamati inaishauri Serikali kuhakikisha kwamba inatumiaumakini mkubwa kwenye uteuzi wa wataalam na taasisihiyo au hizo au kuhakikisha kwamba maslahi ya Taifayanalindwa kuhusiana na ubadilishanaji wa rasilimali zakijenetiki ikikumbukwa kwamba taasisi hiyo itakuwa namamlaka ya kuidhinisha ubadilishaji wa rasilimali hiyo kwaniaba ya Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwepo na uporaji warasilimali za kijenetiki katika nchi hii kwa kisingizio cha utafiti,watafiti hawa hawashirikishi wazawa katika hatua za

Page 117: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

117

mwanzo kwa nia ya kujua baadhi ya rasilimali za kijenetikihususani mizizi, majani, mbegu au magamba ya miti ambayoinatibu baadhi ya magonjwa, wageni wamenufaika sanana rasilimali ya kijenetiki kwa kujipatia ujuzi wa asili kutokakwenye jamii zetu bila malipo huku wao wakijinufaisha kwarasilimali zetu. Kamati inaishauri Serikali kubainisha maeneoyote yenye rasilimali hizi na kuyawekea utaratibu wa uvunaji.Jambo hili la kubaini maeneo liende sambamba na utoajiwa elimu kwa jamii juu ya matumizi na faidazitakazopatikana kama rasilimali zetu zikitumika kuzingatiautaratibu maalum.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwepo ucheleweshajikatika kuridhia itifaki na mikataba mbalimbali ya kimataifa,mfano ni itifaki ya Nagoya iliyosainiwa tangu Oktoba, 2010mpaka sasa 2017 takribani miaka minane. Kamati inashauriSerikali kuwasilisha Bungeni kwa wakati mikataba yote yakimataifa pindi inaposainiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, naombanikushukuru wewe na uongozi wote mahiri wa Bunge, vilevilenaomba niwashukuru sana Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Mheshimiwa January Makamba,Naibu wake Mheshimiwa Luhaga Mpina, Makatibu wakuupamoja na wataalam wote wa ofisi hii muhimu kwaushirikiano waliotoa kwa Kamati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa namna ya pekee kabisanapenda kuwashukuru Wajumbe wote wa kamati kamaambavyo wameorodheshwa hapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayonaunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante.

Page 118: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

118

MAONI YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA VIWANDA,BIASHARA NA MAZINGIRA KUHUSU AZIMIO LA BUNGE

KURIDHIA ITIFAKI YA NAGOYA YA KUSIMAMIA UPATIKANAJIWA MGAWANYO SAHIHI WA FAIDA ZITOKANAZO NA

MATUMIZI YA RASILIMALI ZAKIJENETIKI

(Nagoya Protocol on Access to Genetic Resources and theFair and Equitable Sharing of Benefits Arising from theirUtilization to the Convention on Biological Diversity)

_________________

1.0 UTANGULIZIMheshimiwa Spika, kabla sijasoma Taarifa hii naombakufanya marekebisho katika nakala za hotuba yanguwalizogawiwa Waheshimiwa Wabunge kwa kuondoamaneno “Mkataba wa Nyongeza”, na badala yake kuwekaneno Itifaki. Naomba Taarifa yangu yote pamoja namarekebisho yake, iingie kwenye kumbukumbu ya TaarifaRasmi za Bunge.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 53 (6) (b),naomba kuwasilisha maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bungeya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu Azimio la Bungela Kuridhia Itifaki ya Nagoya ya kusimamia Upatikanaji waMgawanyo sahihi wa faida zitokonazo na Matumizi yaRasilimali za Kijenetiki (Nagoya Protocal on Access to GeneticResources and the Fair and Equitable Sharing of Benefits arisingfrom their utilization to the Convention on Biological Diversity).

Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia masharti ya fasili ya 6(b),Kifungu cha 53 ikisomwa pamoja na fasili ya 1(b) ya Kifungucha 7, Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge,Toleo la Januari, 2016, Kamati ya Kudumu ya Bunge yaViwanda, Biashara na Mazingira inalo jukumu la kushughulikiaMikataba inayopendekezwa kuridhiwa na Bunge iliyochini yaOfisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira. Naombakuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa Hoja ya Serikali kuhusu Bungekuridhia Itifaki ya Nagoya ya kusimamia Upatikanaji waMgawanyo sahihi wa faida zitokonazo na Matumizi ya

Page 119: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

119

Rasilimali za Kijenetiki (Nagoya Protocal on Access to GeneticResouces and the Fair and Equitable Sharing of Benefits arisingfrom their utilization to the Convention on Biological Diversity)ililetwa kwenye Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara naMazingira kwa mujibu wa Kanuni ya 53 (3) ya Kanuni za Bunge.

2.0 CHIMBUKO LA MKATABA WA NYONGEZA

Mhesimiwa Spika, chimbuko na asili la Itifaki hii ni miongonimwa mambo muhimu katika kuridhia. Imeelezwa kuwaMkataba wa Bioanuai wa Mwaka 1992, una Itifaki tatuambazo ni Itifaki ya Cartagena ya mwaka 2000 inayohusuUsimamizi wa Mazingira Dhidi ya Athari zinaweza kutokeakutokana na Matumizi ya Biotekinolojia ya kisasa; Itifaki yakusimamia upatikanaji na mgawanyo sahihi wa faidazitokanazo na matumizi ya rasilimali asili za kiejenetiki; naItifaki ya ziada ya Nagoya – Kuala Lumpur kuhusu uwajibikajikisheria na fidia katika kutekeleza Itifaki ya Cartagena.

Mheshimiwa Spika, mkutano wa sita (6) wa nchiwanachama wa Mkataba wa Bioanuai uliofanyikaJohannesburg, Afrika ya Kusini mwaka 2002, ulibaini kusuasauakatika utekelezaji wa lengo la tatu la Mkataba huu. Lengohili linahusu mgawanyo sahihi wa faida zitokanazo namatumizi ya rasilimali za kijenetiki. Kutofikiwa kwa Lengo hilikunatokana na kutokuwepo mfumo rasmi wa usimamizirasimali za kijenetiki.

Mheshimiwa Spika, katika Mkutano huo ilikubaliwa kuanzishaItifaki kwa ajilli ya kusimamia rasilimali hizi. Mchakato huoulihusisha majadiliano yaliyofanyika katika mikutano tisakuanzia 2002 hadi 2010. Itifaki inayopendekezwa ilipitishwana nchi wanachama katika mkutano wa kumi uliofanyikaNagoya, Japani mwaka 2010.

3.0 NAMNA KAMATI ILIVYOSHUGHULIKIA HOJA HII

Mheshimiwa Spika, tarehe 14 Juni, 2017 Kamati ilikutanakatika na kupata maelezo ya Serikali kuhusu pendekezo la

Page 120: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

120

kuridhia Itifaki ya Nagoya ya kusimamia Upatikanaji waMgawanyo sahihi wa faida zitokonazo na Matumizi yaRasilimali za Kijenetiki (Nagoya Protocal on Access to GeneticResouces and the Fair and Equitable Sharing of Benefits arisingfrom their utilization to the Convention on Biological Diversity).Aidha, tarehe 18 Juni, 2017 Ofisi ya Bunge kupitia Mradi waLSP iliiwezesha Kamati kupata uelewa na stadi muhimukuhusu Utaratibu wa Bunge kuridhia Mikataba na Itifakimbalimbali za Kimataifa. Uelewa huu uliisaidia Kamati kuwakatika nafasi nzuri ya kuifanyia kazi hoja hii.

Mheshimiwa Spika, Kamati ilipotekeleza jukumu lakekuhusiana na hoja hii, ilizingatia masharti ya Kanuni ya 117(8) na 117 (9) kuhusu utaratibu wa Kamati pamoja nakuwaalika wadau. Katika hatua hii, Kamati iliwaalikawataalamu kutoka asasi za Serikali, asasi za kiraia (AZISE) nawadau wengine kwa ajili ya kupata maoni yao. Kamatiinawashukuru wadau wote waliotoa maoni yao kuhusu itifakihii. Aidha, Kamati inawashukuru sana Chuo Kikuu cha Dar esSalaam kupitia Taasisi ya Sayansi za Bahari ambao wametoamaoni kadhaa yaliyosaidia kuboresha maoni ya Kamatikuhusu itifaki hii.

4.0 MAMBO YA MSINGI YALIYOZINGATIWA NA KAMATI

Mheshimiwa Spika, i l i kuliwezesha Bunge kutekelezamadaraka yake ipasavyo kwa mujibu wa Ibara ya 63(3) (e),Kamati il izingatia mambo mbalimbali muhimu katikakuifanyia kazi hoja ya Serikali iliyomezani leo. Mambo hayo nipamoja na kuangalia Katiba ya Jamhuri ya Mungano, baadhiya sheria za nchi zinazohusiana moja kwa moja na maudhuiya Itifaki inayopendekezwa, uzoefu wa nchi nyingine katikamasuala muhimu ya Itifaki hii pamoja na kutafakari kuhusuhasara au faida na kiwango cha manufaa au madharayanayoweza kupatikana kwa kuridhia au kutokuridhia Itifakihii kama ulivyo.

Mheshimiwa Spika, pamoja na maelezo ya Mtoa hoja,Kamati ilitaka kujiridhisha kuhusu hali iliyofikiwa katikaMkataba huu kwa kuangalia kama una nguvu ya kisheria

Page 121: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

121

na kubaini kuwa Ibara ya 32 ya Itifaki, Ibara hii iliweka waziItifaki kwa ajili ya kusainiwa na Nchi Wanachama waMkataba kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, NewYork kuanzia terehe 2 Februari, 2011 hadi 1 Februari, 2012.

Nanukuu: Article 32 “This Protocal shall be open for signatureby paties to the Convention at the United NationsHeadquarters in New York, from 2 February 2011 to 1 February2012 Mwisho wa kunukuu.

Utekelezaji wa Itifaki hii ulianza terehe 29 Octoba, 2014 baadaya Nchi Wanacama 50 kuridhia. Hii ni kwa mujibu wa Ibaraya 33 (1-3) ya Itifaki ambayo inaeleza kuwa utekelezaji waItifaki utaanza siku ya kumi na tisa (19) mara baada ya nchimwanachama ya hamsini (50) kuwasilisha hati ya kuridhia.

Nanukuu: Article 33 (1) “This convention shall enter into forceon the ninetieth day following the date of the deposit of thefiftieth instrument of ratification, acceptance, approval oraccession of the state or regional economic integrationorganizations that are Parties to the Convention”. Mwishowa kunukuu.

Aidha, hadi kufikia Mei, 2016 nchi Wanachama 72 zilikuwazimekwisha ridhia Itifaki hii. Tanzania itaridhia Itifaki hii kwakuzingatia Ibara ya 63(3) (e) ya Katiba ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania ya Mwaka 1997.

Kwa mujibu wa Ibara ya 35 ya Itifaki hii inaruhusu NchiMwanachama kujitoa katika Itifaki, ambapo imeeleza kuwa,muda wowote baada ya miaka miwili tangu Itifaki imeanzakutekelezwa, nchi hiyo inaweza kujitoa kwenye Itifaki kwakutoa taarifa ya maandishi kwa mtunza nyarakazinazohusiana na uridhiaji Itifaki hii.

Nanukuu: Mfano, Article 35 “At any time after two years fromthe date on which this Protocol has entered into force for aParty, that Party may withdraw from this protocol by givingwritten notification to the Depositary “ Mwisho wa kunukuu.

Page 122: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

122

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Tanzania ni NchiMwanachama wa Mikataba mbalimbali ya Kimataifa,Kamati ilizingatia kipengele cha Itifaki hii kuhusu ushikikianowetu na mkiataba mingine. Ibara ya 4 ya Itifaki inaelezauhusiano kati ya Mkataba na Mikataba mingine ya kimataifa,kwamba masharti ya Itifaki hayatakinzana na haki na wajibuwa Nchi yoyote mwanachama anazozipata na kutokanana Mikataba mingine ya Kimataifa, isipokuwa pale ambapoutekelezaji wa haki na wajibu wa Mikataba hiyo mingineitasababisha hasara kubwa kwa Viumbe hai. Itifaki hii hailengikuweka madaraja kati ya Mkataba huu na Mikataba mingineya kimatafa.

Nanukuu: Mfano, Article 4 “The provision of this Protocol shallnot affect the right and obligation of any Party deriving fromany existing international agreement, except where theexercise of those rights and obligations would cause a seriousdamage or threat to biological deversity” Mwisho wakunukuu.

Mheshimiwa Spika, Mkataba wa Msingi kuhusu Mikataba yaKimataifa ni Mkataba wa Viena ambao Tanzania iliuridhiaMkataba mwaka 1976. Mkataba wa Viena umeweka kanuniza msingi kuhusu uridhiaji wa mikataba ya kimataifa. Kanunihizo muhimu zilizingatiwa na Kamati ya Kudumu ya Bungeya Viwanda, Biashara na Mazingira wakati wa kuifanyia kazihoja iliyopo mbele ya Bunge hili kwa sasa.

5.0 MAONI NA USHAURI WA KAMATI

Mheshimiwa Spiaka, Lengo kuu la Itifaki hii nikuimarisha ushirikiano wa haki na wa usawa juu ya faidazitokanazo na matumizi ya rasilimali za kijenetiki, ikiwa nipamoja na upatikanaji sahihi wa rasilimali hiyo, ikiwepoupatikanaji na uhamishaji wa teknolojia husika, na kwaufadhili wa kifedha unaokubalika, hivyo basi kuchangiauhifadhi wa bioanuai na matumizi endelevu ya rasilimalizitokanazo kwayo. Lakini hili litafikiwa tu ikiwa utekelezajiwa kikamilifu na wa haki wa vipengele mbali mbali vilivyomokwenye Itifaki hiyo utafanyika.

Page 123: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

123

Mheshimiwa Spika, baada ya kuipitia Itifaki hii imeonekanainahakikisha ulinzi na udhibiti wa kutosha wa rasilimali zakijenetiki zetu. Hata hivyo, ili Taifa linufaike ipasavyo na fursazitokanazo na uanachama wa Itifaki hii ya Mkataba waBioanuai kwa ujumla wake mambo kadhaayanapendekezwa kufanyika:

Mheshimiwa Spika, Itifaki inaopendekezwa inatoa fursamuhimu ya kuheshimiwa na kuzingatiwa masharti namatakwa ya sheria za ndani za nchi mwanachama husika,kwenye makubaliano yoyote ya utoaji/ubadilishanaji warasilimali za kijenetiki na mfumo wa ugawanaji wa faidizitokanazo na matumizi ya rasilimali hiyo. Hivyo basi, Kamatiinashauri kwamba Sheria za nchi ziimarishwe ili kutoa udhibitiwa kutosha wa rasilimali hiyo, ili kuhakikishwa kwamba Taifalinanufaika ipasavyo na rasilimali hiyo;

Mheshimiwa Spika, Itifaki inapendekeza kwamba upatikanajina matumizi ya Ujuzi Jadi, an mgawanyo wa faida itokanayona matumizi ya ujuzi huo, ufanyike kwa makubaliano katijamii za jadi husika na mtumiaji (muhitaji). Kamati inashauriSerikali kuandaa mfumo madhubuti wa kisheria na kiutendajikuhakikisha kwamba inajihusisha kikamilifu katikamazungumzo na makubaliano yoyote yakayofanyika kati yapande hizo mbili ili kulinda maslahi ya nchi;

Mheshimiwa Spika, Itifaki haijatoa ukomo wa aina walakiwango cha fidia anayotakiwa kupata mmiliki wa rasilimalihizi kwa matumizi (yakiwemo ya kibiashara) yatokanayo narasilimali hiyo. Ni maoni ya Kamati kuwa mapendekezo hayayanaweza kutumiwa vibaya na watumiaji wa rasilimali hii,kwa kuamua kwa makusudi kulipa fidia isiyostahiki kwammiliki wa rasilimali. Hivyo Kamati inaishauri Serikali kuwekautaratibu utakaoainisha aina na kiwango cha fidia kulingana aina ya raslimali hiyo na matumizi yake;

Mheshimiwa Spika, Itifaki inapendekeza fursa ya ujenzi nauendelezaji wa uwezo wa rasilimali watu na wa kitaasisikwenye Nyanja ya uhifadhi na usimamizi wa bioanuai narasilimali kijenetiki.

Page 124: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

124

Kamati inaishauri Serikali kuweka mfumo mzuriutakaohakikisha kuwa fursa hiyo inatumiwa ipasavyo kwamanufaa ya nchi, ikiwemo kuainisha vipaumbele vyetukwenye nyanja mbalimbali;

Mheshimiwa Spika, Itifaki inapendekeza uwepo wawataalamu na Taasisi/mamlaka maalum ya kitaifa(Competent National Authority) kwa kila nchi mwanachamaitakayokuwa kitovu (focalpoint) cha utekelezaji wa shughuliza Itifaki. Kamati inaishauri Serikali kuhakikisha kwambainatumia umakini mkubwa kwenye uteuzi wa wataalamuna taasisi hiyo (hizo), ili kuhakikisha kwamba maslahi ya taifayanalindwa kuhusiana na ubadilishanaji wa rasilimali zakijenetiki, ikikumbukwa kwamba taasisi hiyo itakuwa namamlaka ya kuidhinisha ubadilishanaji wa rasilimali hiyo kwaniaba ya Serikali;

Mheshimiwa Spika, kumekuwepo na uporaji wa rasilimali zakijenetiki katika nchi hii kwa kisingizio cha utafiti, watafitihawa huwashirikisha wazawa katika hatua za mwanzo kwania ya kujua baadhi ya rasilimali za kijenetihi hususani mizizi,majani, mbegu au magamba ya miti ambayo inatibu baadhiya magonjwa. Wageni wamenufaika sana na rasilimali zakijenetiki kwa kujipatia ujuzi wa asili kutoka kwenye jamii zetubila malipo huku wao wakijinufaisha na rasilimali zetu. Kamatiinaishauri Serikali kubainisha maeneo yote yenye rasilimali hizina kuyawekea utaratibu wa uvunaji. Jambo hili la kubainimaeneo liende sambamba na utoaji wa elimu kwa jamii juuya matumkizi na faida zitakazopatikana kama rasilimali zetuzikitumika kwa kuzingatia utaratibu maalumu; na

Mheshimwa Spika, kumekuwepo na ucheleweshaji katikakuridhia Itifaki na Mikataba mbalimbali ya Kimataifa. Mfanoni Itifaki ya Nagoya iliyosainiwa tangu Oktoba, 2010, mpakasasa Juni 2017, takribani miaka minane(8). Kamati inaishauriserikali kuwasilisha Bungeni kwa wakati Mikataba yote yakimaifa pindi inaposainiwa.

Page 125: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

125

6.0 HITIMISHO

Mheshimiwa Spika, naomba nikushukuru sana wewe kwauongozi wako mahiri na kwa kunipa ruhusa ya kuwasilishamaoni haya ya Kamati. Niwashukuru pia Mheshimiwa NaibuSpika na Wenyeviti wote wa Bunge kwa kuratibu nakusimamia shughuli za Bunge kwa umakini na umahiri.

Mheshimiwa Spika, Kamati inapenda kumshukuru Waziri waNchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mhe.January Makamba(Mb), Naibu Waziri wake Mhe. LuhagaJoelson Mpina(Mb), Makatibu Wakuu, pamoja na wataalamuwote wa Ofisi hii muhimu kwa ushirikiani walioutoa wakatiwa kujadili Azimio hili.

Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee kabisa, napendakuwashukuru wajumbe wote wa Kamati ya Bunge yaViwanda, Biashara na Mazingira kwa ushirikiano walioutoawakati wa kupitia kuchambua na hatimaye kuwasilishamaoni yake juu ya Azimio hili mbele ya Bunge hili tukufu.Orodha yao ni kama inavyosomeka hapa chini na kwa ruhsayako naomba majina yao yaingie kwenye kumbukumbuRasmi za Bunge.

(i) Mhe. Stanslaus Haroon Nyongo Mb Mwenyekiti(ii) Mhe. Vicky Passcal Kamata, Mb Mjumbe(iii) Mhe. Salim Hassan Turky, Mb Mjumbe(iv) Mhe. Kalanga Julius Laizer, Mb Mjumbe(v) Mhe Dkt. Dalaly Peter Kafumu Mjumbe(vi) Mhe. Khatib Said Haji, Mb Mjumbe(vii) Mhe. Tauhida Cassian Gallos, Mb Mjumbe(viii) Mhe. Munira Mustafa Khaibu, Mb Mjumbe(ix) Mhe. Anthony Calist Komu, Mb Mjumbe(x) Mhe. Godbless Jonathan Lema, Mb Mjumbe(xi) Mhe. Dkt. Mary Machuche Mwanjelwa,Mb Mjumbe(xii) Mhe. Lameck Okambo Airo, Mb Mjumbe(xiii) Mhe. Hawa Subira Mwaifunga, Mb Mjumbe(xiv) Mhe. Balozi Dkt Diodorus Kamala, Mb Mjumbe(xv) Mhe. Jesca David Kishoa, Mb Mjumbe

Page 126: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

126

(xvi) Mhe. Mbarouk Salim Ali, Mb Mjumbe(xvii) Mhe. Mussa Ramadhani Sima, Mb Mjumbe(xviii) Mhe. Anatropia Lwehikila Theonest, Mb Mjumbe(xix) Mhe. Faida Mohammed Bakar, Mb Mjumbe(xx) Mhe. Suleiman Ahmed Sadick, Mb Mjumbe(xxi) Mhe Ibrahim Hassanali Raza, Mb Mjumbe(xxii) Mhe. Abdulaziz Mohamed Abood, Mb Mjumbe(xxiii) Mhe. Dkt. Raphael MMasunga Chegeni, Mb Mjumbe(xxiv) Mhe. Sylvestry Francis koka, Mb Mjumbe(xxv) Mhe. Gimbi Dotto Massaba, Mb Mjumbe(xxvi) Mhe. Martha Mosses Mlata, Mb Mjumbe(xxvii) Mhe. Joyce John Mukya, Mb Mjumbe

Mheshimiwa Spika, napenda pia kumshukuru Katibu waBunge Dkt. Thomas D. Kashililah; Mkurugenzi wa Idara yaKamati Bw. Athumani Hussein; Mkurugenzi msaidizi Sehemuya Fedha na Uchumi Bw. Michael Chikokoto; Makatibu waKamati Bw. Wilfred Magova na Bi. Zainab Mkamba na Msaidiziwa Kamati Bi Paulina Mavunde kwa kuratibu shughuli zaKamati.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha na naunga mkonoAzimio.

Stanslaus Haroon Nyongo, (Mb)MWENYEKITI

KAMATI YA BUNGE YA VIWANDA, BIASHARA NAMAZINGIRA29 Juni, 2017

MWENYEKITI: Mheshimiwa Msemaji Kambi ya UpinzaniDkt. Sware jiandae Mheshimiwa Gekul.

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI - MSEMAJI WAKAMBI RASMI YA UPINZANI WIZARA YA KILIMO, MIFUGO NAUVUVI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha maoniya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu kuridhia marekebisho yamkataba wa Nairobi wa hifadhi, usimamizi na uendelezaji

Page 127: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

127

wa mazingira ya bahari na ukanda wa Pwani ya Magharibiya Bahari ya Hindi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkataba wa Nairobi kuhusuHifadhi Usimamizi na Uendelezaji wa Mazingira ya Bahari naPwani ya Kanda ya Afrika Mashariki unalenga katikakusimamia mazingira ya Baharini na Ukanda wa Pwani.Tanzania ni nchi mwanachama kati ya nchi tisa zilizokatika Ukanda wa Pwani ya Magharibi ya Hindi kutokamwaka 1996.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa moja yamajukumu ya mkataba huu kwa nchi mwanachama nikutekeleza masharti ya mkataba huu (the contracting partiesshall cooperate in the formulation and adoption ofprotocols to facilitate the effective implementation of thisconvention).

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo basi Kambi Rasmi yaUpinzani Bungeni inashauri yafuatayo:-

(i) Serikali sasa ichukue hatua ya kutunga sheriamahususi ya kutekeleza hili ama kufanya marekebisho yasheria ya mazingira (Environmental Management Act) ilikuendana sambamba na matakwa ya mkataba huu mfano,katika mkataba huu umeainisha Ibara ya 5, 6 na 9 kusimamiauchafuzi wa mazingira kutoka kwenye meli (pollution fromships) na utupaji taka baharini hovyo. Serikali inatakiwakuchukua hatua mahususi ili kuhakikisha inadhibiti uchafuziwa mazingira baharini kwa kuzingatia sheria za kimataifa.Hivyo basi, Serikali inatakiwa kukiwezesha Kitengo cha Marinechini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ili kuwezakusimamia na kutekeleza sheria zake za utunzaji wa mazingirakama zipo.

(ii) Serikali itenge fedha mahususi kwa ajili ya udhibitina usimamizi wa uharibifu wa mazingira kwa kuwezeshakifedha Baraza la Usimamizi wa Mazingira chini ya NEMC ilikuweza kusimamia na kudhibiti uharibifu wa mazingira katikasekta mbalimbali ili kuhakikisha madhara ya uharibifu wa

Page 128: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

128

mazingira hayatokei katika bahari na Ukanda wa Pwani. PiaSerikali inabidi kuwezesha kifedha Mfuko wa Mazingira uliochini ya Ofisi ya Makamu ya Rais, Muungano na Mazingira ilikuweza kusimamia utunzaji wa usimamizi wa mazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mfano mwingine KatikaIbara ya 11 ya convention hii inataka kusimamia bionuai(Biological Diversity). Serikali inatakiwa kuhifadhi na kulindabionuai viumbe adimu au vilivyo hatarini kutoweka,kuanzisha maeneo tengefu kama vile hifadhi zawanyamapori na misitu sanjari na kuzuia shughuli zinazowezakusababisha uharibifu wa viumbe hao pamoja na maeneohayo. Je, hili litatekelezwaje ili hali sekta muhimu zakusimamia eneo hili hazijawezeshwa kifedha?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo basi, Kambi Rasmi yaUpinzani Bungeni inaishauri Serikali kutilia mkazo juu yaumuhimu wa kusimamia na kudhibiti mazingira yake hususaniya baharini kwa kuziwezesha taasisi husika kifedha ili ziwezekuendana na matakwa ya mkataba ukizingatia kuwa tangumkataba huu usainiwe nchi wanachama zipo katika hatuambalimbali za kuridhia kulingana na sheria na taratibu zanchi husika na utaanza kutekelezwa rasmi baada ya nchisita angalau kuridhia ambapo hadi sasa nchi za Msumbiji naAfrika Kusini ndizo zimeridhia marekebisho ya mkataba huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia mkataba waAfrika Mashariki na utunzaji wa mazingira ikiwemo baharimkataba huu hauna tofauti kubwa na matakwa ya jumlaya Ibara ya 111 na 112 ya Mkataba wa Jumuiya ya AfrikaMashariki ambayo kwa namna moja au nyingine unazitakanchi wanachama kuwa na mpango wa pamoja wausimamizi wa mazingira yakiwemo ya bahari. Kuingiakwenye mikataba ya kimataifa ni jambo moja na kutekelezamatakwa ya mikataba hiyo ni jambo jingine, izingatiwe kuwamkataba wa sasa wa Afrika Mashariki imekuwa kwenyeutekelezaji wa nchi wanachama kwa takribani miaka 16 sasa,na mkataba huu ambao unapitishwa kwa azimio la Bungehili leo ni wa tarehe 01 Aprili, 2010 ambapo ni miaka sitatoka kusainiwa kwake.

Page 129: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

129

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya Upinzaniinaitaka Serikali kulieleza Bunge lako Tukufu kuwa ni hatuagani ambazo zimechukuliwa kutekeleza matakwa yaMkataba wa Afrika Mashariki kuhusu masuala ya Bahari yaHindi huku ikizingatiwa kuwa nchi za Kenya na Tanzania ndiozinapakana na Bahari ya Hindi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya Upinzaniinahoji haya kwa sababu tunaweza kuwa na mikatabamingi ya kimataifa, lakini kama nchi na Serikali kwa ujumlabado hakuna hatua mahususi ya utekelezaji wa mikatabahiyo. Tumeweka mkataba huo wa Afrika Mashariki ili tuangaliemaudhui yake na siyo tu kuridhia mipya wakati tunashindwakutekeleza mikataba ambayo ipo tayari lakini haifanyiwi kazi.Kambi Rasmi ya Upinzani haipingani kabisa na mkataba huujambo la msingi ni kwa Serikali kuhakikisha inafuata ushauriambao tumeutoa hapo awali. Baada ya kusema hayonaomba kuwasilisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa ridhaa yako naombanimuite Naibu Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii atoe maoniya Kambi juu ya Azimio la Bunge Kuridhia Itifaki ya Udhibitiwa Uchafuzi wa Mazingira ya Bahari na Ukanda wa Pwaniya Magharibi ya Bahari ya Hindi pamoja na Azimio la BungeKuridhia Itifaki ya Nagoya ya Kusimamia Upatikanaji wamgawanyo sahihi wa faida zitokanazo matumizi ya rasilimaliza kijenetiki.

MAONI YA KAMBI RASMI YA UPINZANI KUHUSU KURIDHIAMAREKEBISHO YA MKATABA WA NAIROBI WA HIFADHI,

USIMAMIZI NA UENDELEZAJI WA MAZINGIRA YA BAHARI NAUKANDA WA PWANI YA MAGHARIBI YA BAHARI YA HINDI-

(AMENDED CONVENTION FOR THE PROTECTION,MANAGEMENT AND DEVELOPMENT OF THE MARINE AND

COASTAL ENVIRONMENT OF THE WESTERN INDIAN OCEAN) -KAMA YALIVYOWASILISHWA MEZANI

Yanatolewa kwa mujibu wa kanuni za Bunge, Kanuni ya86(6), Toleo la Januari, 2016"

Page 130: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

130

1. UTANGULIZI;Mheshimiwa Spika, Mkataba wa Nairobi kuhusu Hifadhi,Usimamizi na Uendelezaji wa Mazingira ya Bahari na Pwaniya Kanda ya Afrika Mashariki unalenga katika kusimamiamazingira ya Baharini na Ukanda wa Pwani

Tanzania ni nchi mwanachama kati ya Nchi tisa zilizo katikaukanda wa Pwani ya Magharibi ya Hindi kutoka mwaka 1996.

2. MAPITIO YA MKATABAMheshimiwa Spika, Kwakuwa moja ya majukumu yamkataba huu kwa nchi mwanachama ni kutekeleza mashariya mkataba huu ‘The Contracting Parties shall co-operate inthe formulation and adoption of protocols to facilitate theeffective implementation of this Convention’

Mheshimiwa Spika, Hivyo basi, Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni inashauri yafuatayo:

i. Serikali sasa ichukue hatua kwa kutunga sheriamahsusi ya kutekeleza hili, ama kufanya marekebisho yaSheria ya Mazingira (EMA-Environmental Management Act) ilikuendana sambamba na matakwa ya Mkataba huuMfano:

Ibara za 5, 6 na 9: Uchafuzi wa mazingira kutokana kwenyeMeli ‘Pollution from Ships, na utupaji taka bahariniSerikali inatakiwa kuchukua hatua mahsusi ili kuhakikishainadhibiti uchafuzi wa mazingira baharini kwa kuzingatiasheria za kimataifa. Hivyo basi, Serikali inatakiwa kuiwezeshakitengo cha Marine chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi naMawasiliano ili kuweza kusimamia na kutekeleza Sheria zakeza utunzaji wa Mazingira, kama zipo!

ii. Serikali itenge fedha mahususi kwa ajili ya udhibitina usimamizi wa uharibifu wa Mazingira kwa;

- Kuwezesha kifedha baraza la Usimamizi wa Mazingiria(NEMC- National Environmental Management Council) ilikuweza kusimamia na kudhibiti uharibu wa mazingira katika

Page 131: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

131

sekta mbalimbali ili kuhakikisha madhara ya uharibifu yamazingira hayatokei katika bahari na ukanda wa pwani

- Kuwezesha kifedha Mfuko wa Mazingira, ulio chini yaOfisi ya Makamu wa Rais-Wizara ya Muungano na Mazingiraili kuweza kusimamia utunzaji na usimamizi wa MazingiraMfano:Mheshimiwa Spika, Ibara ya 11: Bioanuai ‘Biological Diversity’,Serikali inatakiwa kuhifadhi na kulinda bioanuai, viumbeadimu au vilivyo hatarini kutoweka; kuanzisha maeneotengefu kama vile hifadhi za wanyamapori na misitu sanjarina kuzuia shughuli zinazoweza kusabisha uharibifu wa viumbehao pamoja na maeneo yao.

Je, hili litatekelezwaji ilhali Sekta muhimu za kusimamia eneohili hazijawezeshwa kifedha?

Mheshimiwa Spika, Hivyo basi, Kambi rasmi ya Upinzanibungeni inaishauri Serikali kutilia mkazo juu ya umuhimu yakusimamia na kudhibiti mazingira yake hususani ya Baharinikwa kuziwezesha Taasisi husika kifedha ili ziweze kuendanana matakwa ya Mkataba ukizingatia kuwa Tangu mkatabahuu usainiwe, Nchi wanachama zipo katika hatua mbalimbaliza kuridhia kulingana na sheria na taratibu za nchi husika nautaanza kutekelezwa rasmi baada ya nchi sita (6) kuridhia,ambapo hadi sasa ni nchi za Msumbiji na Afrika Kusini ndizozimeridhia marekebisho ya Mkaba huu.

3. MKATABA WA AFRIKA MASHARIKI NA UTUNZAJI WAMAZINGIRA IKIWEMO BAHARI

Mheshimiwa Spika, Mkataba huu hauna tofauti kubwa namatakwa ya jumla ya ibara ya 111 na 112 ya Mkataba waJumuiya ya Afrika Mashariki ambayo kwa namna moja amanyingine unazitaka nchi wanachama kuwa na mpango wapamoja wa usimamizi wa mazingira yakiwemo ya Bahari.

Mheshimiwa Spika, kuingia kwenye mikataba ya kimataifani jambo moja na kutekeleza matakwa ya mikataba hiyo nijambo lingine. Izingatiwe kuwa Mkataba wa sasa wa Afrika

Page 132: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

132

Mashariki umekuwa kwenye utekelezaji kwa nchiwanachama kwa takribani miaka 16 sasa. Na mkataba huuambao unapitishwa kwa azimio la Bunge hili leo ni wa tarehe01 Aprili, 2010 ambapo ni miaka sita toka kusainiwa kwake.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka serikalikulieleza Bunge lako tukufu kuwa ni hatua gani ambazozimechukuliwa kutekeleza matakwa ya Mkataba wa AfrikaMashariki kuhusu masuala ya Bahari ya Hindi huku ikizingatiwakuwa nchi za Kenya na Tanzania ndio zinapakana na Bahariya Hindi.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inahoji hayakwa sababu tunaweza kuwa na mikataba mingi yaKimataifa lakini kama nchi na serikali kwa ujumla badohakuna hatua mahususi za utekelezaji wa mikataba hiyo.

Mheshimiwa Spika, tumeweka Mkataba huo wa Afrika yaMashariki ili tuangalie maudhui yake, na sio tu kuridhia mipyawakati tunashindwa kutekeleza mikataba ambayo ipo tayarilakini haifanyikazi.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani haipinganikabisa na Mkataba huu. Jambo la msingi ni kwa Serikalikuhakikisha inafuata ushauri ambao tumeutoa hapo awali.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naombakuwasilisha.

Dr. Sware V. Semesi (Mb)K.n.y Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani-Ofisi ya

Makamu wa Rais Mazingira.29.06.2017

MWENYEKITI: Ahsante, huyo namuita mimi siyo wewe,Mheshimiwa Gekul.

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI - MSEMAJI WAKAMBI RASMI YA UPINZANI WIZARA YA KILIMO, MIFUGO NAUVUVI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. (Makofi)

Page 133: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

133

MHE. PAULINE P. GEKUL - MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI – OFISI YA MAKAMU WA RAIS -MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, yafuatayo ni maoni yaKambi Rasmi ya Upinzani kuhusu Kuridhia Itifaki ya Udhibiti yaUchafuzi wa Mazingira ya Bahari na Ukanda wa Pwani yaMagharibi ya Bahari ya Hindi kutokana na vyanzo na shughulizinazofanyika nchi kavu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, itifaki hii ya udhibiti wauchafuzi wa mazingira ya bahari ya Ukanda wa Pwani yaMagharibi ya Bahari ya Hindi kutokana na vyanzo na shughulizinazofanyika nchi kavu. Vyanzo na shughuli zinazofanyikanchi kavu maana yake ni kutokana na shughuli za kila sikuzinazofanywa na jamii mbalimbali katika kujitafutia riziki zakila siku.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mawanda ya Itifaki hiiyameelezwa kwa undani katika Ibara ya 2 na vifungu vyake,vinne lakini mkataba hauhusishi mito ambayo inaishiakwenye maziwa yetu ya ndani. Kwa maana nyingine nikwamba hauhusishi mito ambayo haimwagi maji yakekwenye bahari ya Hindi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ibara ya 5 inahusu udhibitiwa umwagaji au utiririshaji taka kwenye maji au uchafuziwa hewa katika maeneo ya bahari na Ukanda wa Pwanikutoka kwenye makazi, viwanda na vyombo vya usafiri wamajini. Aidha, Ibara hii inazitaka nchi wanachama kuwekaviwango vya kudhibiti uchafuzi na kuvisimamia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni ukweli kwamba miji mingiiliyopo Pwani mwa Bahari ya Hindi, mifumo ya maji takaimeunganishwa moja kwa moja kuingia baharini. Jambo hilini chanzo kimojawapo cha uchafuzi wa mazingira ya bahari,ni mtazamo wa Kambi Rasmi ya Upinzani kuondokana natabia hiyo ya kuelekeza maji taka baharini, sambamba nahilo kuacha kabisa ile tabia iliyozoeleka ya wakazi wa mijiniya kutapisha vyoo vyao hovyo.Kambi Rasmi ya Upinzanikatika mawasilisho yake, wakati wa kuchangia hoja ya Ofisiya Makamu wa Rais Mazingira ilishauri kufanyika kwa

Page 134: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

134

recycling ya taka maji hayo kwa matumizi mengine.Sambamba na hilo ni kwa viwanda vinavyotoa majimachafu vifunge mifumo ya kuyazungusha maji taka hayokwa matumizi ya kila siku.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ibara ya 6 inazitaka nchiwanachama kuchukua hatua za kudhibiti uchafuziunaotokana na shughuli za kilimo zisizo endelevu ambazozinaweza kuathiri mazingira ya bahari na Ukanda wa Pwani.Ibara hii ni pana mno kwani inagusa moja kwa moja nashughuli za kimaisha za jamii nyingi za kiasili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kilimo kisichoendelevukinachangiwa na aina ya kilimo kama vile matumizi yamitambo mikubwa ya kilimo kama vile matrekta makubwana hivyo kuifanya ardhi kuwa laini kuweza kuchukuliwa namikondo ya maji. Pia matumizi yasiyo sahihi ya mbolea namadawa ya mimea na kuulia wadudu. Aidha, madawa nambolea fake ni chanzo pia cha uchafuzi wa mazingira yabahari. Tukumbuke kwamba pale mvua nyingi zinaponyeshamikondo hiyo ya maji yaliyoharibika tayari inaishia baharinina hivyo kuwa chanzo cha uchafuzi wa mazingira ya bahari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ibara ya 15 inazitaka nchiwanachama kuhamasisha utapitakanaji wa taarifa nanyaraka muhimu zinazohusu uchafuzi toka nchi kavu. Aidha,nchi hizo zinasisitiza kukuza uelewa kwa jamii ma kuhakikishajamii zinazoshirikishwa katika kutoa maamuzi yanayohusuutekelezaji wa itifaki hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni ukweli pia jamii nyingizinazoishi kando kando mwa mito mikubwa, miaka yotewanatumia maji hayo kwa shughuli mbalimbali kama vilekufanya usafi binafsi wa mwili na nguo zao, makabilamengine yanatumia mito hiyo kwa uvuvi na wanatumiamadawa ya mashambani au sumu kwa shughuli hizo. Aidha,wengine wanatumia mito hiyo kama vyoo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo basi, elimu ya kutoshakwa jamii zilizo kwenye mito mikubwa ni muhimu sana

Page 135: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

135

kufanyika. Tukumbuke usemi usemao jasiri haachi asili, hivyokuondokana na tabia ya jadi ni jambo gumu sana bila yakutoa elimu ya kutosha kwa jamii husika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa ujumla Kambi Rasmiya Upinzani haipingani na mahudhui ya Mkataba huu balitunaitaka Serikali kuzingatia ushauri tulioutoa kwani kwa njiamoja au nyingine mkataba unaathiri maisha ya kila siku yajamii zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naombakuwasilisha kwa upande wa itifaki hii. (Makofi)

MAONI YA KAMBI RASMI YA UPINZANI KUHUSU KURIDHIAITIFAKI YA UDHIBITI WA UCHAFUZI WA MAZINGIRA YA

BAHARI NA UKANDA WA PWANI YA MAGHARIBI YA BAHARIYA HINDI KUTOKANA NA VYANZO NA SHUGHULI

ZINAZOFANYIKA NCHI KAVU- (PROTOCOL FOR THEPROTECTION OF THE MARINE AND COASTAL ENVIRONMENT

OF THE WESTERN INDIAN OCEAN FROM LAND-BASED SOURCEAND ACTIVITIES) - KAMA YALIVYOWASILISHWA MEZANI

Yanatolewa kwa mujibu wa kanuni za Bunge, Kanuni ya86(6), Toleo la Januari, 2016"

1. UTANGULIZIMheshimiwa Spika, Itifaki hii ya udhibiti wa uchafuzi waMazingira ya Bahari na Ukanda wa Pwani ya Magharibi yaBahari ya Hindi kutokana na vyanzo na shughuli zinazofanyikanchi kavu.

Vyanzo na shughuli zinazofanyika nchi kavu, maana yake nikutokana na shughuli za kila siku zinazofanywa na jamiimbalimbali katika kujitafutia riziki za kila siku.

Mheshimiwa Spika, chimbuko la Itifaki hii ni Mkataba waNairobi uliofanyiwa marekebisho na ambao ulitiwa saini nawanachama wake tarehe 1 Aprili, 2010 Nairobi, Kenya.

Page 136: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

136

2. MAPITIO YA ITIFAKI

Mheshimiwa Spika, mawanda ya Itifaki hii yameelezwa kwaundani katika Ibara ya 2 na vifungu vyake, vine lakinimkataba hauhusishi mito ambayo inaishia kwenye maziwayetu ya ndani. Kwa maana nyingine ni kwamba hauhusishimito ambayo haimwagi maji yake kwenye bahari ya Hindi.

Mheshimiwa Spika, Ibara ya 5 inahusu udhibiti wa umwagajiau utiririshaji taka kwenye maji au uchafuzi wa hewa katikamaeneo ya bahari na ukanda wa Pwani kutoka kwenyemakazi, viwanda na vyombo vya usafiri wa majini. Aidha,Ibara hii inazitaka nchi wanachama kuweka viwango vyakuthibiti uchafuzi na kuvisimamia.

Mheshimiwa Spika, ni ukweli kwamba miji mingi iliyopoPwani mwa bahari ya Hindi,mifumo ya maji takaimeunganishwa moja kwa moja kuingia baharini. Jambo hilini chanzo kimojawapo cha uchafuzi wa mazingira ya Bahari,ni mtazamo wa Kambi Rasmi ya Upinzani kuondokana natabia hiyo ya kuelekeza maji taka Baharini, sambamba nahilo kuacha kabisa ile tabia iliyozoeleka ya wakazi wa mijiniya kutapisha vyoo vyao.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani katika Wasilisholake, wakati wa kuchangia hoja ya Ofisi ya Makamu wa RaisMazingira ilishauri kufanyika kwa “recycling” ya taka maji hayokwa matumizi mengine. Sambamba na hilo ni kwa viwandavinavyotoa maji machafu vifunge mifumo ya kuyazungushamaji taka hayo kwa matumizi ya kila siku.

Mheshimiwa Spika,Ibara ya 6 inazitaka nchi wanachamakuchukua hatua za kudhibiti uchafuzi unaotokana nashughuli za kilimo zisizo endelevu ambazo zinaweza kuathirimazingira ya bahari na ukanda wa pwani. Ibara hii ni panamno kwani inagusa moja kwa moja na shughuli za kimaishaza jamii nyingi za kiasili.

Mheshimiwa Spika, kilimo kisichoendelevu kinachangiwa naaina ya kilimo kama vile matumizi ya mitambo mikubwa ya

Page 137: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

137

kilimo kama vile matrekta makubwa na hivyo kuifanya ardhikuwa laini kuweza kuchukuliwa na mikondo ya maji. Piamatumizi yasiyo sahihi ya mbolea na madawa ya mimeana kuulia wadudu. Aidha, madawa na mbolea feki ni chanzopia cha uchafuzi wa mazingira ya bahari. Tukumbukekwamba pale mvua nyingi zinaponyesha mikondo hiyo yamaji yaliaharibika tayari inaishia baharini na hivyo kuwachanzo cha uchafuzi wa mazingira ya bahari.

Mheshimiwa Spika, Ibara ya 15 inazitaka nchi wanachamakuhamasisha utapitakanaji wa taarifa na nyaraka muhimuzinazohusu uchafusi toka nchi kavu. Aidha nchi hizozinasisitizwa kukuza uelewa kwa jamii ma kuhakikisha jamiizinashirikishwa katika kutoa maamuzi yanayohusu utekelezajiwa itifaki hii.

Mheshimiwa Spika, ni ukweli pia jamii nyingi zinazoishi kandomwa mito mikubwa, miaka yote wanatumia maji hayo kwashughuli mbalimbali kama vile kufanya usafi binafsi wa mwilina ngua zao, makabila mengine yanatumia mito hiyo kwauvuvi na wanatumia madawa ya mashambani au sumu kwashughuli hizo. Aidha, wengine wanatumia mito hiyo kamavyoo. Hivyo basi, elimu ya kutosha kwa jamii zilizo kwenyemito mikubwa ni muhimu sana kufanyika. Tukumbuke usemiusemao “jasiri haachi asili”, hivyo kuondokana na tabia yajadi ni jambo gumu sana bila ya kutoa elimu ya kutosha kwajamii husika.

Mheshimiwa Spika, kwa ujumla Kambi Rasmi ya Upinzanihaipingani na mahudhui ya Mkataba huu bali tunaitakaSerikali kuzingatia ushauri tulioutoa kwani kwa njia moja aunyingine mkataba unaathiri maisha ya kila siku ya jamii zetu.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naombakuwasilisha.

Pauline P. Gekul (Mb)Msemaji Mkuu-Kambi Rasmi ya Upinzani-Ofisi ya Makamu

wa Rais Mazingira.29.06.2017

Page 138: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

138

MWENYEKITI: Ahsante Waheshimiwa tunaanzamjadala.

MHE. PAULINE P. GEKUL - MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI – OFISI YA MAKAMU WA RAIS -MAZINGIRA: Itifaki ya pili Mheshimiwa Mwenyekiti.

MWENYEKITI: Bado?

MHE. PAULINE P. GEKUL - MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI – OFISI YA MAKAMU WA RAIS -MAZINGIRA: Bado ya pili na ya mwisho.

MWENYEKITI: Haya malizia.

MHE. PAULINE P. GEKUL - MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI – OFISI YA MAKAMU WA RAIS -MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, yafuatayo ni maoni yaKambi Rasmi ya Upinzani kuhusu Kuridhia Itifaki ya Nagoyaya Kusimamia Upatikanaji na Mgawanyo Sahihi wa Faidazitokanazo na Matumizi ya Rasilimali za Kijenetiki. Naombayote yaingie kwenye Hansard lakini kwa kuokoa mudanisome maoni ya jumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maoni ya jumlakuingia kwenye Hansard Kambi Rasmi ya Upinzani inaitakaSerikali ilitilie mkazo haya yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza Serikali ihakikisheRasilimali za Kijenetiki za asili zinalindwa. Mfano, mbegu zanafaka na mazao mbalimbali, miti ya asili, mifugo yetu yaasili ambayo zimekuwa himilivu kwa magonjwa, ukame namabadiliko ya hali ya hewa. Aidha, pendekezo hili la KambiRasmi ya Upinzani halina maana ya kupuuza tafiti mbalimbalikatika maeneo haya bali ina lengo la kuikumbusha Serikali…

KUHUSU UTARATIBU

MWENYEKITI: Kuhusu Utaratibu.

Page 139: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

139

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,mpaka sasa hivi hatujapewa kitabu cha maoni ya Upinzani.

MWENYEKITI: Kitabu?

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, chamaoni ya Upinzani na akimaliza kusoma hapo tunaanzakuchangia, sasa tunachangia huku ambapo hatujasoma.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mnyika, nimekuambiavitabu vinakuja vyote, vilichelewa vya upande wa hukuvinakuja.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,vinakuja lini?

MWENYEKITI: Vinakuja, vyote vinakuja na msifanyeinterruptions ambazo hazinia nini. Endelea Mheshimiwa Gekul.

MHE. PAULINE P. GEKUL - NAIBU MSEMAJI WA KAMBIRASMI YA UPINZANI WIZARA YA MALIASILI NA UTALII:Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha pendekezo hili la Kambi Rasmiya Upinzani halina maana ya kupuuza tafiti mbalimbali katikamaeneo hayo bali yana lengo la kuikumbusha Serikali kulindana kuendeleza rasilimali zetu za kijenetiki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Pili, Serikali iwe makini nawatafiti wanaoingia nchini kufanya tafiti mbalimbali ilikuhakikisha kuwa rasilimali zetu za kijenetiki hazipotezwi kwamaksudi au kwa lengo baya kwa mwavuli wa utafiti. Mfanohalisi ni vyura wa kihansi wanaopatikana katikamaporomoko ya Udzungwa waliopelekwa nchini MarekaniChuo Kikuu cha Colorado kwa ajili ya utafiti lakini jambo lakushangaza baada ya vyura hao kurudishwa nchiniwameendelea kutoweka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tafiti zinaonyesha penginekutoweka kwa vyura hawa kunaweza kuwakumesababishwa na aina fulani ya fungus waitwao chytridhivyo ni muhimu sana Serikali ikawa makini na watafiti wa

Page 140: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

140

kigeni pamoja na aina mbalimbali ya rasilimali za kijenetikizinazopelekwa nje ya mipaka ya nchi yetu.

Tatu, Kambi Rasmi ya Upinzani inashauri pamoja nakazi zinazofanywa na watafiti wetu hapa nchini bado vyuovya utafiti vina hali ngumu sana jambo ambalo linaathiriufanisi wa utafiti au tafiti zetu za kufahamu thamani halisi yarasilimali zetu za kijenetiki. Vyuo hivi vinakosa fedha na hatapale zinapotoka fedha hizo hazitoki kwa wakati, hivyo basini rai ya Kambi Rasmi ya Upinzani kwamba Serikali kuwekezavizuri katika vyuo vyetu vya tafiti ili kuweza kunufaika narasilimali zetu za kijenetiki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho Kambi Rasmi yaUpinzani inasema jambo la msingi ni kuhakikishatunasimamia vema rasilimali zetu za kijenetiki ili zisijezikapotea kutokana na uingizwaji wa nguvu wa rasilimalikutoka kwa wenzetu wenye lengo la kuhakikisha vya kwetuvinapotea kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya Upinzanihaipingani na kuridhiwa kwa Azimio hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayonaomba kuwasilisha. (Makofi)

MAONI YA KAMBI RASMI YA UPINZANI KUHUSU KURIDHIAITIFAKI YA KUSIMAMIA UPATIKANAJI NA MGAWANYO

SAHIHI WA FAIDA ZITOKANAZO NA MATUMIZI YARASILIMALI ZA KIJENETIKI

(Nagoya Protocol on Access to Genetic Resources and theFair and Equitable Sharing of Benefits Arising from theirUtilization to the Convention on Biological Diversity) –

KAMA YALIVYOWASILISHWA MEZANI

“ Yanatolewa kwa Mujibu wa Kanuni ya 86(6) ya Kanuni zaBunge, Toleo la Januari, 2016”

Mheshimiwa Spika, Rasilimali za Kijenetiki ni vinasaba

Page 141: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

141

mbalimbali katika mimea, wanayama na viumbe haiwengine, vinasaba husika katika viumbe hai kwa ujumlawake ni muhimu katika utafiti wa mimea na wanyama namatumizi ya bioteknolojia ya kisasa.

Mheshimiwa Spika, Tanzania ni mwanachama wa Mkatabawa Bioanuai wa mwaka 1992, unaohusu hifadhi ya bioanuai;matumizi endelevu ya bioanuai; na mgawanyo wa faidazitokanazo na matumizi ya bioanuai. Tanzania ili sainimkataba huu tarehe 8 Machi,1996.

Mheshimiwa Spika, Mkataba huo wa Bioanuai una itifakimbili, moja ni Itifaki ya Cartegana ya mwaka 2000 naTanzania iliridhia Itifaki hii tarehe 16 Machi 2003. Itifaki ya pilini hii tunayoridhia sasa ambayo ilianzia rasmi kwenyemkutano wa sita (6) wan chi wanachama uliofanyika Afrikaya Kusini mwaka 2002 na kuhitimishwa na rasmi katikamkutano wa wanachama uliofanyika Nagoya Japanmwaka 2010.

Mheshimiwa Spika, Tanzania na Afrika nchiza ilikuwa narasilimali za kijenetiki nyingi sana, lakini kutokana na teknolojiainayoletwa rasilimali hizo zimeendelea kupotea na sasabaada ya wale waliozipoteza kuona hilo wanarudi tena namikataba kama hii.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inauliza ni naniau kabila gani lisilokuwa na aina yake ya mbegu au ninaasiyefahamu kuwa ng’ombe aina ya Zebu asili yake niTanzania? Na je ni kwanini ng’ombe aina hiyo wanafanyiwamkakati wa kuhakikisha wanapotea kabisa. Sababu kuu nimoja kwamba aina hiyo ya ng’ombe inavumilia sanamagonjwa na kwa sababu hiyo wale wanaotengenezamadawa ya mifugo watauza wapi madawa hayo?

Mheshimiwa Spika, si hilo tu mbegu zetu za asili inajulikanakwamba ni mbegu zilizokuwa zinavumilia sana mazingirayetu japokuwa hazikuwa zinazalisha sana, lakini kwa wenzetukuliona hilo wakaja na ujanja wa kutuaminisha kuwa zinamatatizo, na mbegu nyingi za asili kwa makabila mbali mbali

Page 142: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

142

zimepotea kabisa. Huo ulikuwa ni mkakati maalum wakuhakikisha masoko ya madawa yao ya kilimo na mbeguzao zinapata soko kwetu.

Mheshimiwa Spika, huo ulikuwa ni mtazamo wetu kuhusianana raslimali zetu za kijenetiki zinavyopotea na baadaetunaambiwa tuzilinde.

Mheshimiwa Spika,hiyo haiondoi ukweli kwamba kama nchitukiridhia mkataba huu, watanzania na jamii mbalimbali zakitanzania zitanufaika kwa Nyanja mbalimbali kamazilivyooneshwa katika Ibara ya Tano ya Itifaki, sambambana hilo ni kwenye utangulizi katika aya ya nne na tano. Faidazake zimeelezewa vizuri na zinaeleweka kwa wale wotewanaohitaji kuelewa.

Mheshimiwa Spika, pamoja na manufaa ya itifaki hii kwaTanzania na jamii nzima ya kitanzania, Kambi Rasmi yaUpinzani inaamini raslimali za kijenetiki ziko nchi nzima nakwa kila jamii, kwa msingi huo hatuna sababu yoyote yakupingana na uridhiwa wa azimio hili.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Serikali mara nyingi imekuwaikij ivuta katika suala zima la kutunga sheria za “ku-domesticate” itifaki zinazoridhiwa na Bunge ili kuwekauratatibu mzuri zaidi wa kiutendaji.

Mheshimiwa Spika, katika kukazia hoja hiyo, Ibara ya 15 yaItifaki inasema kuhusu “compliance with domestic legislationor regulatory requirements on access and benefit sharing”,

Mheshimiwa Spika, ni ukweli kwamba kwa kiasi kikubwaTanzania imekuwa ikipoteza rasilimali zake za kijenetiki katikasekta ya madawa ya asilia pale ambapo wanaojiita watafitiwanachukua mimea yetu kwa ajili ya kufanyia utafiti zaidikwa kigezo kwamba Tanzania haina maabara za kisasakuweza kutoa matokea tarajiwa. Hivyo basi kwa kifunguhicho na kama usimamizi na jutekelezaji wa sheria zetu zandani utakuwa imara ni dhahiri nchi yetu itanufaika zaidi narasilimali za kijenentiki.

Page 143: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

143

Mheshimiwa Spika, Ibara ya 17 inasema kuhusu ufuatiliaji wamatumizi ya rasilimali za kijenetiki, hoja ya msingi ni matumizihayo yanafuatiliwa wapi? Kwa kuwa rasilimali hizo zipo katikajamii yetu na kwa njia moja au nyingine jamii ndiyo mtumiajimkuu na muangalizi wa rasilimali hizo. Kambi Rasmi yaUpinzani inashauri kwamba; jambo la muhimu kwanza nikuzitambua raslimali ambazo inahitaji na kuziwekeautaratibu ili matumizi yake yawe endelevu, kinyume chahapo wananchi wanaweza kupata madhara kutoka kwenyevyombo vya dola bila ya wao kufahamu. Mfano mzuri nimatumizi ya mti wa Mpingo, watanzania wengi wanaufahamu ni kwanini mti huo unalindwa na Serikali.

Mheshimiwa Spika, kwa ujumla Kambi Rasmi ya Upinzaniinaitaka Serikali kwanza kutambua rasilimali hizi ziko wapina hivyo kutoa elimu kwa jamii mbalimbali za kitanzaniaambazo ndizo mmiliki wa rasilimali husika ili wazitunze nakuziendeleza kwa manufaa ya kizazi kilichopo na chabaadae. Hii imejitokeza katika Ibara ya 21, japokuwa ugumuunaweza kujitokeza kutokana na ukweli kwamba jambo hililinahitaji rasilimali fedha za kutosha ili itifaki hii iweze kutoamrejesho uliohitajika kwa taifa.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inatoa ushaurihuo kutokana na ukweli kwamba, mabadiliko ya tabianchiambayo yanaikumba Dunia yetu vile vile yanasababishakupotea kwa rasilimali nyingi za kijenetiki katika mimea,wanyama na viumbe hai wengine. Hivyo ni jukumu la nchikuhakikisha rasil imali zetu za kijenetiki zinaendeleakuhifadhiwa.

MAONI YA JUMLA

Mheshimiwa Spika, baada ya kueleza hayo, Kambi Rasmi yaUpinzani inaitaka Serikali iltilie mkazo haya yafuatayo:

i. Serikali ihakikishe rasilimali za kijenetiki za asilizinalindwa, mfano. Mbegu za nafaka na mazao mbalimbali,miti ya asili, mifugo yetu ya asili ambayo zimekuwa himilivukwa magonjwa, ukame na mabadiliko ya hali ya

Page 144: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

144

hewa.Aidha, pendekezo hili la Kambi Rasmi ya Upinzani halinamaana ya kupuuza tafiti mbalimbali katika maeneo hayobali lina lengo la kuikumbusha Serikali kulinda na kuendelezarasilimali zetu za kijenetiki.

ii. Serikali iwe makini na watafiti wanaoingia nchinikufanya tafiti mbalimbali ili kuhakikisha kuwa rasilimali zetuza kijenetiki hazipotezwi kwa makusudi au kwa lengo bayakwa mwavuli wa utafiti. Mfano halisi ni vyura wa kihansiwanaopatikana katika maporomoko ya Udzungwawaliopelekwa nchini Marekani (Chuo Kikuu cha Colorado)kwa ajili ya utafiti, lakini jambo la kushangaza baada ya vyurahao kurudishwa nchini wameendelea kutoweka. Tafitizinaonesha pengine kutoweka kwa vyura hawa(nectophrynoides asperginis) kunaweza kuwakumesababishwa na aina fulani ya fungus waitwao chytrid.Hivyo ni muhimu sana Serikali ikawa makini na watafiti wakigeni pamoja na aina mbalimbali ya rasilimali za kijenetikizinazopelekwa nje ya mipaka ya nchi yetu.

iii. Mheshimiwa Spika, pamoja na kazi zinazofanywa nawatafiti wetu hapa nchini bado vyuo vya utafiti vina halingumu sana, jambo ambalo linaathiri ufanisi wa tafiti zetuza kufahamu thamani halisi ya rasilimali zetu za kijenetiki.Vyuo hivi vinakosa fedha na hata pale zinapotoka hazitokikwa wakati. Hivyo basi ni rai ya Kambi Rasmi ya Upinzanikuwekeza vizuri katika vyuo vyetu vya tafiti ili kuwezakunufaika na rasilimali zetu za kijenetiki.

iv. Kambi Rasmi ya Upinzani inasema jambo la msingi nikuhakikisha tunasimamia vyema rasilimali zetu za kijenetiki ilizisije zikapotea kutokana na uingizwaji wa nguvu wa rasilimalitoka kwa wenzetu wenye lengo la kuhakikisha vya kwetuvinapotea kabisa.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani haipingani na

Page 145: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

145

uridhiwaji wa azimio hili, baada ya kusema hayo naombakuwasilisha.

…………………Pauline Philipo Gekul (Mb)

Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani –Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira

29.06.2017

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, nawashukurumaeneo yote mawili hakuna upande ambao umepingakuridhiwa kwa hiyo sasa tunaanza mjadala na tunaanza naMheshimiwa Dau, ajiandae Mheshimiwa Kitandula,Mheshimiwa Kuchauka na Mheshimiwa Lema kwa dakikatano.

MHE. MBARAKA K. DAU: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa fursa hii ya kuwa mchangiaji wakwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote nianze kwakuunga mkono itifaki ya Azimio hili na kwa namna ya kipekeekabisa niwaombe Waheshimiwa Wabunge wenzangutuunge mkono hili jambo muhimu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi natokea Mafia, kwakiasi kikubwa sana maisha ya watu wa Mafia ambayo nikisiwa maisha yetu ni bahari na bahari ndio watu wa Mafia.Chochote kile ambacho kinaelekea katika kulinda nakuhifadhi bahari kwa maana nyingine hicho ni chenye kutoamanufaa na nafuu kwa watu wa Mafia. Hali ya mazingira yabahari kwa sasa ni mbaya sana, kwa maana ya kwambakuna baadhi ya visiwa, Mafia ni kisiwa lakini ndani yake kunavisiwa vidogo vidogo. Vile visiwa vidogo vidogo vinginevimeshaanzwa kumezwa na bahari kutokana na uchafuziwa mazingira na mabadiliko ya masuala ya tabianchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulipokuwa wadogo kuleMafia tulikuwa tunakwenda kuvua katika maji usawa wamagoti, lakini sasa hivi unaweza ukaenda maji ya kina

Page 146: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

146

kikubwa kabisa na vyombo na ukarudi ukiwa na kikapukimoja au pengine ukarudi mikono mitupu. Kwa hiyo, ipohaja ya makusudi kabisa sisi Wabunge tukubaliane na tuliungemkono Azimio hili ambalo lina nia njema na nchi yetu namazingira yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, takwimu zinaonesha ifikapomwaka 2030 ndani ya bahari na hususan Bahari ya Hindikutakuwa na takataka nyingi zaidi kwa maana ya mifuko hiiya “rambo” na mifuko mingine ya plastiki kuliko samakiwenyewe. Kwa hiyo, hali ni mbaya sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata ilipotokea ile ndege yaMalaysia ikapotea na ikasemekana imeangukia baharinindipo wataalam wakaenda kugundua mambo makubwazaidi yaliyokuwepo chini ya bahari kutokana na uchafuzi wamazingira, wakakuta kuna takataka nyingi mno. Tuna kilaaina ya sababu kuhakikisha kwamba tunaunga mkonoAzimio hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mafia kuna taasisi maaluminayohusiana na masuala ya uhifadhi wa bahari maarufukama Marine Park. Ningeomba sana na sina uhakika kamaWaziri mwenye dhamana ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo yupohapa, lakini ningeomba sana watusaidie wenzetu wa Serikalikuhakikisha kwamba ile Taasisi ya Hifadhi ya Bahari inajikitana kujiingiza zaidi katika suala la uhifadhi. Kwa sasa hiviwamekuwa wana mambo mengi zaidi kuliko uhifadhiwenyewe. Wamejiingiza katika masuala ya ukusanyaji wamaduhuli, wamejiingiza katika masuala ya ujenzi, masualaya uwekezaji na uuzaji wa visiwa, wanajikuta mpaka kwenyethe core business yao wamekuwa diverted na sasawanashughulika zaidi na mambo ambayo hayawahusu nahayahusiani zaidi na uhifadhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba sana kama Waziriwa Kilimo, Mifugo na Uvuvi yupo hapa ahakikishe kwamba,anawaelekeza watu wa hifadhi ya bahari Mafia wajikitekwenye uhifadhi, hiyo ndiyo shughuli yao ya msingi waachanena habari ya kuuza visiwa, kuuza maeneo, mambo ya ujenzi,

Page 147: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

147

uwekezaji, ukusanyaji wa maduhuri hilo ni suala la TRA naHalmashauri ya Mafia tunaweza tukayafanya sisi wenyewe.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumze kidogo suala lambadala. Ndugu yangu Mheshimiwa Kitandula amekuwaakizungumza sana hapa, suala la ufugaji wa samaki. Baharinisamaki wa bahari pia wanafugwa. Sasa kutokana na hali…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Kitandula,ajiandae Mheshimiwa Kuchauka na Mheshimiwa Lema piaajiandae.

MHE. DUNSTAN L. KITANDULA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa fursa hii na mimi nichangie kwenyeitifaki hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kusema naiungamkono itifaki hii kwa sababu inazungumzia maisha ya sisiwatu wa Pwani na sisi watu wa Pwani bila bahari maishahayapo. Vilevile niseme kwamba itifaki hii itakuwa na maanatu kama itatuhakikishia watu wa Pwani maisha yetuyataboreka. Kama itifaki hii haitatusaidia maisha yetukuboreka haina maana, kama itifaki hii haitatuhakikishiakuboreka kwa maisha ya watu wa Pwani basi itifaki hii hainamaana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nayasema haya kwa sababumwaka 1996 tulisaini mkataba ule uliokuwa unazungumziaudhibiti wa bahari ukanda wa Afrika Mashariki. Mwaka 2010tukaiboresha itifaki ile tukasaini. Nataka tu nijiulize hivi tangu1996 tuliposaini watu wa Pwani maisha yamekuwa bora?Nini kinatuhakikishia leo kwa kusaini itifaki hii kwamba maishaya Pwani yataboreka? Utafiti umetuonyesha kwamba itifakihii katika utekelezaji wake tangu mwaka 1996 umekuwa nachangamoto kubwa ya kimfumo wa usimamizi wa taasisi

Page 148: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

148

za usimamizi, vilevile changamoto kubwa ya kifedha. Tafitihazifanyiki na zikifanyika zinafanyika kwa ufinyu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpaka leo watu wa Pwanizana tunazotumia kwenye uvuvi ni zana duni, tumekuwatukitamani tuyaone yanayofanyika kwenye sekta ya kilimokupewa pembejeo na vitu vya namna hii, yafanywe kwenyesekta ya uvuvi hayafanyiki. Tumekuwa tukitamani tuyaoneyanayofanyika kwenye sekta ya mifugo kwa watu wa sektaya uvuvi hayafanyiki. Ndiyo maana mnashuhudia watu walewanaendelea kutumia zana duni za tangu enzi ya Nabii Nuhu.Ndiyo maana mnashuhudia uvuvi wa kutumia mabomuunaendelea, ndiyo maana mnaona mazalia ya samakiyanaendelea kuharibika kwa sababu tumeitupa mkono sektaya uvuvi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilifurahi kwenye Ilani yetutuliposema kwamba katika kipindi hiki tutaleta meli tano zauvuvi. Nataka tu niikumbushe Serikali yangu, mwaka wa pilihuu sasa wa utekelezaji, tumebakia na miaka mitatu tujitahidiahadi ile itimie. Lakini hata ahadi hiyo ikitimia bado asilimiakubwa ya wavuvi watakuwa hawana zana za kisasa kwendakuvua, ndiyo maana leo unaona hata kwenye uuzaji wetuwa samaki tunategemea sana samaki wa kutoka ZiwaVictoria, uvuvi kwenye eneo la baharini uko duni. Twendenitukawekeze kwenye blue economy, twendeni tukahakikisheufugaji wa samaki unafanyika kwenye ukanda wa Pwani.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jarida la Sofia la FAOlinatuambia hivi takribani watu milioni 57 wana… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea na MheshimiwaKuchauka

MHE. DUNSTAN L. KITANDULA: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru.

Page 149: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

149

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante na mimi kunipa nafasi nitoe mchango wangu katikakuridhia hii itifaki ambayo imewasilishwa leo mbele yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote kamamwasilishaji alivyosema kwamba tunazo faida mbalimbaliameziainisha hapa, faida ambazo tungeweza kuzipataanasema kwamba ni kuimarisha uchumi, kuongeza mazaoya bahari pamoja na ushirikiano wa kikanda. Lakini wazolangu au maoni yangu ni kwamba kwanza kabisa niunganena Kambi Rasmi ya Upinzani yale maoni ambayo wameyatoanaishauri Serikali iendelee kuyazingatia kwa umakini kabisa,kwa sababu tatizo letu siyo tu kuridhia hii mikataba kwanzani mipango dhabiti ya utekelezaji wa mikataba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ya Tanzania imekuwana kawaida ya kusuasua sana kutekeleza mikatabambalimbali ambayo tunaingia ya Kimataifa. Kwa mfano,sasa hivi tunakwenda kuridhia hii it ifaki ambayotunaizungumzia leo, lakini je, Serikali iko tayari kuleta sheria,kutunga sheria za utekelezaji ambayo itasimamia kwauhalisia kabisa kulingana na matakwa ya mikataba hiiambayo tunakwenda kuiridhia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile ukiangalia tunayotaasisi ambayo kama msemaji aliyepita alisema Taasisi yaUhifadhi wa Mali/Bidhaa za Bahari. Lakini je, hii taasisi kamaSerikali mmeiwezesha kwa kiwango gani ili hayo matakwayaweze kutekelezeka kama ambavyo tumeridhia? Vilevilekwenye utafiti mara nyingi tumekuwa tukiibiwa rasilimali zetunyingi za baharini na nchi kavu na hawa watu wanaojiitawatafiti. Ni kweli kabisa mara nyingi watafiti wanapofanyautafiti wanaondoka na viumbe hai, wanaondoka na malizetu, lakini sisi wenyewe tumejidhatiti kwa kiwango gani, hizitafiti badala ya kufanyika na watu wa nje na wenyewetuweze kufanya hizi tafiti ili taasisi yetu kwa mfano, MaritimeInstitute pale Dar es Salaam sijui kwamba na yenyeweimeimarishwa kwa kiwango gani ili tafiti nyingine ziwezekufanyika hapa nchini badala ya kwamba hawa watuwanakuja kutuibia, wakati wenyewe tuna uwezo nalo.

Page 150: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

150

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile ukiangalia maranyingi Watanzania tumekuwa na kigugumizi sana. Mimisijaelewa Serikali inakuwaga na kigugumizi cha namna gani,kwa sababu ukiangalia mikataba mingi tuliyoridhia kwanzatunachukua muda mrefu sana kuiridhia na baada ya kuiridhiatunakuwa na kigugumizi sana katika utekelezaji. NaiombaSerikali izingatie ushauri ambao umetolewa na Kambi Rasmiya Upinzani na Wabunge mbalimbali ambao wanachangiahapa. Hili wote tunajua kwamba tunafanya hivi kwakuhifadhi mazingira yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kusema ukweli kwa upandewa baharini, kwa kweli Serikali tumesahau sana bahari, kwasababu ukiangalia uchumi Tanzania tumezungukwa naPwani kutoka Tanga mpaka Mtwara, lakini ni kiwango ganitunanufaika? Serikali inanufaikaje na fukwe hizi? Tumewekezakwa kiwango gani? Utakuta uwekezaji tuliouwekeza hukuni mdogo sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumesema hapa wakatitunachangia bajeti ya kilimo na uvuvi wakasema kwambasekta binafsi ndiyo wameachiwa wao ndiyo wanunue melikubwa za uvuvi ili tuweze kuvua na ndio jambo linalopelekeampaka leo hii tunakula samaki kutoka China. Hivi kweli kwautajiri huu tulionao Tanzania kuanzia Tanga mpaka Mtwaraleo hii hatuna hata meli moja ya uvuvi wa kisasa, hivitunategemea ulinzi huu wa hizi rasilimali zetu za baharini huyomlinzi atatoka wapi? Hivi ni kweli hawa Watafiti ambaotunawategemea kutoka nje ndiyo waweze kulinda mali zetu?Kwa kweli jambo hili silioni kama lina tija.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Serikali kwa dhatikabisa tutoke tuwekeze kwenye bahari ili nasi tuwezekunufaika nayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa hayomachache naunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Peter Msigwa,Mheshimiwa Lema ajiandae.

Page 151: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

151

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ninakushukuru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, in principle sina tatizo naitifaki zilizoletwa, lakini nilitaka tu tujitafakari kama Bunge.Hili Bunge letu la Bajeti ni Bunge la muda mrefu na Bungehuwa linajua ratiba itakuwaje. Lakini kumekuwa na mazoeakila siku mnapoleta itifaki hizi mnatuletea siku hiyo ya kupitishahizo itifaki. Hii inaonesha jinsi gani ambavyo Bungelinaonekana halitimizi wajibu wake na kwamba Serikaliinatuchukulia poa tu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi vifungu ukiwaulizaWabunge unavipitia saa ngapi, kila wakati itifaki zinapokujazinaletwa siku hiyo hiyo, hivi vifungu unavipitia saa ngapi?Unasoma saa ngapi? Unapewa dakika tano kuchangiawakati ingegaiwa mapema kwenye Kamati watuwangepitia tunapojua ratiba inavyokwenda tuje tusome,lakini imekuwa business as usual tunapiga makofi na Bungetunakubaliana mikono yetu na nguvu yetu ya Bungeinapungua nguvu kwa mambo kama haya ya kuridhiamambo ambayo hayawezekani, kwa sababu ni mambo yamsingi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Watalaam wanasema thepast is where you have learn the lesson and the future is whereyou apply the lesson. Asubuhi hapa tumejaribu hata kuombamiongozo, mambo ya Hati za Dharura tunarudia tena kanakwamba mambo ya nyuma hatujajifunza kwa sababutunaenda haraka haya mambo! Wabunge hebu tujiulize, hiviwananchi huko wakituona tunaondoka tumebeba mavitabuhaya, tunasoma saa ngapi? Tunasoma saa ngapi hivi vitabu!Tunaletewa muda mfupi! (Makofi)

Mheshikiwa Mwenyekiti, hii ni kulifanya Bunge liwecrippled, Bunge ambalo haliwezi kuisimamia Serikali, kwahiyo hapa sisi tumekuja ku-rubber stamp. Tukubalianekwamba, Bunge hili linaongozwa na Serikali, Bunge haliwezikuisimamia Serikali kwa sababu tunakuja hapa tuna-rubberstamp… (Makofi)

Page 152: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

152

MWENYEKITI: Mheshimiwa Msigwa kwa mujibu wataratibu za Kibunge baada ya Serikali kuwasilisha taarifa yakeupande wa Kamati umetoa taarifa yake umeridhia. Fursaimetolewa upande wa Upinzani na amesoma MheshimiwaDkt. Sware amesoma na Mheshimiwa Gekul, wote na waowameunga mkono Itifaki hii na Maazimio haya. Wote upandewa Upinzani na upande wa Kamati.

Ushauri uliotolewa ambao na wewe unayo nafasi yakusema, tunakubaliana na hiki kitu, lakini mna-reservationszenu, ushauri uwe ni huu ili tuende na wenzetu wa kimataifa.Sasa unapoanza lugha zingine Mheshimiwa Msigwa with duerespect, tumalizeni hii kazi ambayo iko mbele yetu. Somamaoni yako, ushauri unaotaka kutoa uutoe sasa hivi Serikaliiufanyie kazi, ndio kazi ya Bunge, kwa sababu haya menginesijui rubber stamping, wala si sehemu yake leo wala siku yoyotenyingine. Kwa hiyo, nakuomba tujielekeze kwenye Azimio.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakubaliana na unachokisema, lakini kumbuka Waziri Kivulianaletewa copy, lakini kama Wabunge tunatakiwa tuwe nacopy hizi tukae nazo tuzisome. Nimesema ratiba huwa inakujakabla! Hili Bunge tunakaa miezi mitatu hapa! Sasa kila sikutunaletewa, hebu tuwe wa kweli, umesoma saa ngapi?Aniambie Mbunge tumesoma saa ngapi hivi vifunguambavyo tunaridhia hapa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kama Wabungehatuwezi kuhoji haya mambo hapa, tutahojia wapi?Ninachozungumza lazima tuwe na Bunge strong, Bungelinaloweza kui-challenge Serikali.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU): Taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Chief Whip wa Serikali!

TAARIFA

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,

Page 153: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

153

KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU): MheshimiwaMwenyekiti, naomba kumpa taarifa Mheshimiwa Msigwa,kwa utaratibu wa Kibunge tunaoendelea nao na ambaondiyo utaratibu tunaoutumia ndani ya Bunge, ukiona Kambiya Upinzani inasoma taarifa hapa ndani ya Bunge ina maanajambo hilo ambalo linaendelea ndani ya Bunge upande huowa Upinzani walishalipata muda mrefu na ilikuwa ni wajibuwa kila kiongozi kwa upande husika anapopata hoja yaBunge kuikabidhi kwenye kambi yake il i Wabungewanaohusika waweze kuiangalia na kujiandaa. (Makofi)

Mheshikiwa Mwenyekiti, suala la pili, naomba nimpetaarifa Mheshimiwa Mbunge, ratiba ya Vikao vya Bunge tokasiku ya kwanza ilionesha tutakuwa na kazi ya Maazimio ndaniya Bunge ambayo kila Mbunge alipaswa kujiandaa.

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: MheshimiwaMwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Dkt. Sware kaa chinikwanza.

Mheshimiwa Msigwa, with due respect, Maazimio hayayameanza toka Bunge letu lianze miezi mitatu na nusuiliyopita. (Makofi)

Kwa hiyo, nakuomba na Kambi yenu ya Upinzaniimeeleza vizuri tu hapa, haipingani kabisa na Maazimioisipokuwa wanataka Serikali ipokee ushauri walioutoa. Sasana wewe elekea kwenye ushauri, unaposema hujasomainawezekana utaachwa peke yako humu. Wenziowamesoma!

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: MheshimiwaMwenyekiti, taarifa.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,sijui kwa nini tunashindwa kue…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Dkt. Sware taarifa.

Page 154: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

154

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: MheshimiwaMwenyekiti, nashukuru. Ningependa kuiambia Serikali na walewanao-represent Serikali, haya makabrasha menginetumeyasoma asubuhi na kuyafanyia kazi asubuhi,yamechelewa kufika kwenye Kambi. (Makofi)

MWENYEKITI: Mradi mmeweka Mezani taarifa zenu,ni Taarifa Rasmi za Serikali. Mheshimiwa Msigwa, tunakwendana procedure za Kibunge.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,sijui ni wapi tunashindana, mahali pako wazi kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunachokizungumza hataWaziri akisoma hotuba hapo haimaanishi kwamba Wabungewa CCM hawatakiwi kuchangia kwa sababu tu Waziriamesoma, ndiyo maana inaletwa humu ndani tutoe mawazoyetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachotaka kusema tunali-cripple Bunge kwa kuleta vitu hivi haraka! Tunatakiwa tupatemuda wa kusoma, tuyapitie, tujue vifungu, tuishauri Serikalitunapotoa haya Maazimio, ugumu uko wapi? (Makofi)

MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshikiwa Mwenyekiti,taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Nyongo, taarifa.

T A A R I F A

MHE. STANSLAUS H. NYONGO: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ni Mwenyekiti waKamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira. Taarifa hiitulipewa mapema na ndani ya Kamati ya Viwanda naBiashara kuna Wabunge wa Upinzani akiwemo MheshimiwaKomu ambaye tulipitia naye haya Maazimio. Tumepita tuka-digest kwa pamoja, wengine ni Mheshimia Lema ni Mjumbe

Page 155: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

155

wa Kamati yangu, lakini kwa bahati mbaya hajawahikuhudhuria hata siku moja. (Makofi)

Mheshikiwa Mwenyekiti, nashukuru sana. Naombaniwapatie taarifa hiyo. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Msigwa endelea.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshikiwa Mwenyekiti,nadhani Mheshimiwa Nyongo labda kwa sababu hanauzoefu…

MHE. ANTONY C. KOMU: Taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa kaa chini sasa, mnachukuamuda mwingi. Mheshimiwa Msigwa endelea.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,najaribu kumjibu Mheshimiwa Nyongo. Kwenye Kamati huwazinapewa, mimi nazungumza Bunge. Kamati huwa zinapewazote zinajadili, atapata uzoefu kidogo, nazungumzia Bungehizi document tusome ili tuje tupitishe vifungu tunavyovijua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunarudia makosa yaleambayo tunapewa sheria, tunapitisha, tena tunataka turudietena. Ninachoomba, hizi itifaki sio mbaya, lakini…

MHE. ANTONY C. KOMU: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Komu hebu kaa kwanza.Mheshimiwa Msigwa endelea, wewe endelea MheshimiwaMsigwa malizia. Mheshimiwa Mnyika mara nyingi hukaiBungeni humu.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Sikai au mnanitoa?

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ninachoomba hili Bunge letu, Serikali iwe inafanya vitu kwautaratibu, kwa sababu Serikali zote duniani huwa zinapenda

Page 156: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

156

kulifanya Bunge liwe kibogoyo ili zifanye mambo yake vizuri.Na sisi kama Wabunge tuna wajibu wa kuhakikishatunachukua role yetu kuisimamia Serikali. Hatuwezi kuchukuarole kama tunauziwa mbuzi kwenye magunia. Huku nikuletewa mbuzi kwenye magunia, halafu tunashangilia katikavitu ambavyo hatujasoma, na ni kukwepa wajibu wa Bunge.(Makofi)

Mheshikiwa Mwenyekiti, tunaposema mikataba nasheria ziletwe Bungeni hatumaanishi iletwe kama hivi itupwehapa! Tuna maana iletwe tupate muda wa kuisoma nakuitafakari ili tuone ni jinsi gani tunawawakilisha wananchiambao wametutuma, lakini ikiletwa tu hapa inakaa mezani,inaletwa hapa, halafu wanasema tunaazimia, watutunapiga makofi, tunasema ililetwa Bungeni, hiyo siyo maanahalisi ya kuletwa Bungeni. Hakuna kati yetu hapa aliyesomahapa tukisema lipi ambalo tunaazimia hapa, waliosoma niwachache sana kwenye Kamati idadi kubwa ya Wabungehatujasoma. (Makofi)

Mheshikiwa Mwenyekiti, hilo ndiyo naliomba tuliinueBunge letu kiwango. The more tutakuwa na Bunge dhaifu,the more tutakuwa na Serikali dhaifu. Hawa Mawaziri lazimatuwashughulishe wafanye kazi. Hawa Mawaziri hawatafanyakazi kama Wabunge tutakuwa weak. Ni lazima tuwe afterthem, watakuwa na nguvu ili kuishauri Serikali na ndiyo wajibuwetu. (Makofi)

Mheshikiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa kunipanafasi. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Enhee, Mheshimiwa Komuulikuwa unasemaje.

MHE. ANTONY C. KOMU: Mheshikiwa Mwenyekiti,nakushukuu sana. Alichosema Mheshimiwa Nyongo ni kwelikwamba tulipewa hizo taarifa mapema na tukazifanyia kazi.Lakini jana tulivyo-wind up nikataka kuondoka namakabrasha nikaambiwa na Katibu wa Kamatikwamba…

Page 157: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

157

MWENYEKITI: Sasa hiyo ni taarifa au unachangia?

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila mpangilio)

MHE. ANTONY C. KOMU: Mheshimiwa Mwenyekiti,nikaambiwa bado ni mali ya Kamati.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, miminazungumza na mhusika, mbona wengine mnaanzakunyoosha mikono, mnaanza ku-nini! Eeh vipi tena! Bado mnafever ya sikukuu? (Kicheko)

Mheshimiwa Komu haya malizia.

MHE. ANTONY C. KOMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwahiyo, ni kweli kwamba, taarifa zimefika kwenye Kambi yetuasubuhi. Na sisi kama Wajumbe wa Kamati, hatukuwa naruksa yoyote ya kwenda kuzisambaza kwa sababu kwanzakazi za Kamati ni siri kwa hiyo, mwenye kutoa ruhusa ni Katibuwa Kamati.

MWENYEKITI: Haya, umeeleweka ahsante.Mheshimiwa Rehani, ajiandae Mheshimiwa Mtulia.

MHE. SALUM MWINYI REHANI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante na mimi nashukuru kuweza kupata nafasi hii,ninakushukuru kwa kuweza kupewa haya makabrasha namaazimio haya yote matatu wakati mmoja kuwezakuyapitisha, tatizo moja tu lililokuwepo kwamba uelewa waWabunge wengi katika haya Maazimio ndiyo kitu kidogokinachoonekana ni tatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina-declare interestkwamba nimefanya kazi kwenye Marine Conservationkwenye Mradi wa MACEP chini ya World Bank miaka mitatu,naelewa haya maazimio yaliyokuwa yamepita huku nyuma.Lakini nilitaka kutoa ushauri tu sijui kama muda utatoshakatika hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja katika maazimio

Page 158: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

158

ambayo yalipendekezwa miaka mingi kwa nchi yetu hiiimegeuka dampo la kutupwa takataka nyingi kutoka nchiza nje. Wenzetu Kenya waliridhia mapema, baadae baadaya kuridhia wakawa wanachukua bidhaa kutoka viwandanimwao, zile by products zilizomalizika wanakuja kutupa katikabahari yetu kwa sababu tumeshindwa kuridhia mkataba huu,kwa hiyo shamba hili limekuwa kila mmoja anaweza kutupana kufanya anavyotaka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili katika bahari kunamambo mengi, moja katika vitu vinavyokuwa disturbed nibioanuai iliyopo katika bahari. Mazingira yetu ya bahariyanachafuliwa kwa vitu vingi, hali ya hewa inachangia, lakinimtiririsho wa bidhaa za kikemikali kutoka kwenye viwandaumekuwa ni mkubwa na hasa Watanzania wenyewetunaufanya. (Makofi)

Mheshikiwa Mwenyekiti, tuna viwanda vingi katikabelt hii ya bahari ambayo Wahindi na wengineo wanaomilikiviwanda vile wanatiririsha maji ambayo yana sumu nakemikali kutoka kwenye viwanda vyao, hawana mifumo yakuhifadhi maji machafu na ya kemikali ambayowanatengeneza bidhaa mbalimbali. Sasa sheria hii au Azimiohili liende likawabane hawa wote wenye viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunajua wazi kwambawengi wao wanawahonga wale watu wa mazingirawanaokwenda kufanya impact assessment katika maeneoyao na kusababisha uchafuzi wa mazingira uongezeke. Bahariyetu, beach zetu, kila siku, kila mwaka inaongezeka zaidi yamita moja, bahari inalika kutokana na destruction ambazozinafanyika za uchafuzi wa mazingira katika maeneo haya,ninaiomba Serikali hili tuweze kulisimamia. (Makofi)

Mheshikiwa Mwenyekiti, jingine ambalo linachangia,tumeweka uwekezaji wa mahoteli, tumezuwia wenyemahoteli kujenga ndani ya bahari, lakini yapo mahoteliwamejenga migahawa ndani ya bahari kitu ambachovilevile kinachangia kuharibu fukwe na kuharibu ule uoto waasili wa bahari uliokuwemo katika maeneo yale. Ninaishauri

Page 159: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

159

Serikali kwamba tatizo kubwa lililokuweko la nchi nyingi zanje…

MWENYEKITI: Waheshimiwa naongeza muda. EndeleaMheshimiwa Rehani.

MHE. SALUM MWINYI REHANI: MheshimiwaMwenyekiti, nchi nyingi za nje zinatumia eneo lile la baharikuu kupitisha na kumwaga bidhaa mbalimbali katikamaeneo hayo. Mfano mdogo nilionao ni meli nyingi zilizokuwazimezuiliwa kipindi kile na Al-Shabab zilikaa na bidhaa zilekwa muda mrefu zikiwa zimezuiliwa katika maeneo yao nabidhaa zile zilimwagwa katika ukanda huu wa bahari yetusisi.

Kwa hiyo, athari i l iyotokea samaki wengiwaliokuweko katika maeneo yale waliathirika, lakini watuambao walitumia wale samaki walipata matatizo ya ngozina wengine walipata matatizo ya cancer. Haya matatizoimekuwa sasa kwetu bila kuridhia mikataba kama hii aumaazimio kama haya hatutaweza kuweza kufanya usimamiziwa mazingira yetu. (Makofi)

Mheshikiwa Mwenyekiti, lingine lililokuweko katika nchipamoja na rasilimali nyingi tulizokuwanazo katika eneo letulakini hakuna doria ambazo zinakwenda kuangalia kitu ganikinafanyika katika ukanda wa bahari kuu, kitu ambacho kilammoja ana uwezo wa kufanya anachokitaka, mpaka silahambalimbali…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Mtulia, ajiandaeMheshimiwa Lema.

MHE. MAULID S. A. MTULIA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipa fursa hii na mimi kuchangia. Nashukurukwa michango mizuri iliyotolewa na wenzangu, lakini nawawakilishi wetu wa Kambi Rasmi ya Upinzani na hasa

Page 160: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

160

kuonesha tofauti kwa sababu mara nyingi watu wengiwanafikiri upinzani ni kupinga tu, lakini leo upinzaniumeonesha kabisa siyo lengo letu kupinga tu, mambomazuri tunayaunga mkono. Kwa hiyo, hili nashukuru sana.(Makofi)

Mheshikiwa Mwenyekiti, na mimi naunga mkono hiziitifaki, lakini nina maeneo ambayo nayaona lazimatuyaangalie na tuyarekebishe.

Mheshikiwa Mwenyekiti, eneo la kwanza, Wajumbewa Kamati na hata watu wa Kambi Rasmi ya Upinzaniwamelalamikia suala la muda, kwamba wakati mwingineSerikali inaingia itifaki muda mrefu takribani miaka sita, badohawajaleta Bungeni kwa ajili ya kuridhia hilo Azimio. Hili siyojambo zuri. Naiomba Serikali itambue kwamba, Wabungekwa ujumla wao wapo kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu.Tutajitajhidi kufanya lolote lile kwa maslahi ya nchi yetu, kwahiyo, hata jambo lolote wakiliona zuri wasihofie walatusiviziane, walete Bungeni na Wabunge huku kama kawaidayetu tutalichangia vizuri.

Kwa hiyo, hili jambo liangaliwe isiwe kawaida yaSerikali kuwa na wasiwasi wa kuleta jambo, jambo lolotelenye maslahi mapana ya nchi yetu wasiwe na kigugumizi,walilete tutalichangia, penye kasoro tutawaeleza, penyekuunga mkono tutaunga mkono, tuwe na utamaduni huo.(Makofi)

Mheshikiwa Mwenyekiti, wewe unajua sisi tuko Dar esSalaam pale, tunapozungumzia itifaki ya mambo haya yabahari mimi nakubaliana na itifaki, lakini nina mashaka nautekelezaji wetu wa kazi zetu wenyewe.

Mheshimiwa Mwneyekiti, wewe Jimbo lako la Ilalapamoja na Jimbo langu mimi la Kinondoni tunaungana paleSalender Bridge, tuna mikoko na Serikali tunayo pale Dar esSalaam. Wizara ya Mazingira iko pale Dar es Salaam, lakinimikoko yetu inakufa pale Jangwani na maeneo mengineyote! Sasa haya yataondoshwa kwa itifaki haya? (Makofi)

Page 161: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

161

Mheshimiwa Mwenyekiti, unajua kwamba, tuna mtowetu pale Msimbazi, tuna Mto Ng’ombe na mito mingine,inaleta uharibifu mkubwa wa mafuriko ni kwa sababu tu ilemito hatuiangalii. Kwa taarifa tu mwaka huu Jangwani paletumepita salama sana, nilitumia pesa zangu za Mfuko waJimbo kusafisha Mto na hatimaye mafuriko mwaka huuJangwani pale hayakutokea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama hatuna utaratibu wakulinda mito yetu hii, hizi itifaki sidhani kama zitatusaidia sana.Ni vizuri sasa kama Serikali yetu, kama Viongozi, tujikite katikakutatua matatizo yetu wenyewe, hizi itifaki ni jumla tu, itifakihaiwezi kuja kutuondolea matatizo yetu ya ndani ambayosisi wenyewe hatufanyi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeweka sheria ya mita 60,hivi hii sheria ya mita 60 kuiacha bahari, hii bahari anaisafishanani? Tunapokaa umbali wa mita 60 anayetegemewa sasaSerikali ndio ikafanye kazi za kusafisha mito. Je, inafanya?Tunapokaa umbali wa mita 60 inategemewa sasa bahariyetu Serikali ndio ikasafishe, matokeo yake bahari yetuinanuka. (Makofi)

Mheshikiwa Mwenyekiti, lakini ukienda nchizilizoendelea, Paris hata ukienda Dubai, watu sasa hiviwanajenga mpaka kwenye bahari. Hizi sheria sisi tunaangaliakulingana na hali ya sasa au sheria tunaleta tu ili mradi?Lazima tutoe sheria ambazo zitaendana na wakati. (Makofi)

Mheshikiwa Mwenyekiti, watu wetu waruhusiwekujenga kwenye bahari kwa lengo la kutunza hiyo bahariyenyewe. Watu wetu waruhusiwe kukaa karibu na mito kwalengo la kutunza hiyo mito yenyewe, kwa sababu hiyo Serikaliinayotaka watu wakae mbali, wao hawawezi kwenda hukowala hawawezi kwenda kutunza, badala yake tunakuwana fukwe chafu, tunakuwa na mito michafu ni kwa sababuya kutengeneza sheria ambazo wakati mwingine hatunauwezo wa kwenda kuzisimamia. (Makofi)

Mheshikiwa Mwenyekiti, mfano watu wangu wa

Page 162: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

162

mabondeni pale wanatakiwa wahame, hivi pale Jangwanimtu anahama vipi wakati watu Dubai wanakaa baharini?Wewe unamhamishaje mtu Jangwani! Una mhamisha mtuJangwani akakae Mabwepande wakati Jangwani anaendaPosta hata Kariakoo kwa mguu, Mabwepande anatumianauli shilingi 2,000 na anatumia saa matatu! Mimi nafikiri hiisiyo sawa, tutoke huko tuende katika ulimwengu wa kisasa.(Makofi)

Mheshikiwa Mwenyekiti, pale Dar es Salaam,Jangwani, watu wako wana uwezo wa kuendelea kukaapale hakuna madhara yoyote. Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Lema.

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshikiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana. Nikazie pale alipoishia MheshimiwaMsigwa na Waheshimiwa Wabunge wa Chama chaMapinduzi niwaombe sana, hili Bunge ndiyo think tank yanchi. Demand yetu ya kupata nyaraka muhimu kwa ajili yakuishauri Serikali ni kwa sababu ya kutoa opinion ambazozitawasaidia ninyi na Taifa letu na watoto wa watoto wetu.(Makofi)

Mheshikiwa Mwenyekiti, opinion zetu kila marazinaonekana ni uadui, na hii ndiyo inasababisha kuanzakususiana futari, hii ndiyo inasababisha uhasama unakuwani uhasama. Kwa sababu hakuna opinion yetu ya msingiambayo ninyi mtaichukua kama ni jambo muhimu katikaTaifa hili. Sisi sote ni Watanzania, mnapokuja na hizi nyarakasasa hivi naongea hapa hakuna hata hiyo hotuba ya Kambiya Upinzani haipo mezani. (Makofi)

Mheshikiwa Mwenyekiti, leo tu asubuhi hapatumeambiwa tutajadili habari ya Mikataba na Sheria zaMadini mpaka Jumatano mwisho. Sheria hizo mnaleta kwaHati ya Dharura. Wabunge wamekaa hapa miezi mitatu,wamechoka. Binadamu anapochoka ana-loose capacity yaku-focus, leo tunaenda emotionally. Kwa sababu makinikiana ripoti zimesomwa mbili kwa Rais, television mkapeleka

Page 163: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

163

nchi nzima kwenye masoko waone, sasa leo mnataka ku-implement jambo hilo ndani ya siku nne, kinachotokea ninini? Kitakachotokea mtafanya makosa yale mliyoyafanyakipindi cha mwanzo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninyi ndiyo Serikali, hayamambo kama yana umuhimu kwa kiwango hiki wapeniWabunge hizi nyaraka wazisome, wapeni Wabunge hizinyaraka wazipitie. Sasa kazi ya Mheshimiwa Jenista Mhagamahapa yeye, iko siku atatokea mtu huku aseme amegunduadawa ya UKIMWI, Mheshimiwa Jenista utasimama uombeutaratibu na ukatae kabisa, kama hiyo itakuwa inatibu kwasababu haiwezekani kila opinion yetu mnaikataa, tunasemahakuna nyaraka mnakataa, tunawaambia hivi mnakataa,sasa tuishauri, futeni basi upinzani tubaki chama kimoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kipindi kile CCM mko pekeyenu kulikuwa kuna G7 tukiwa wadogo, mlikuwamnashindana lakini mlikuwa hambaguani, sasa hivi tunaanzakupishana na tunaanza kubaguana. Narudia tena hikimnachoendelea kupanda kitatoka hapo nje ya Bunge,kitakwenda mitaani. Haya yanayotokea Kibiti msishangaesiku moja yakasambaa nchi nzima kwa sababu ya chukizinazojengwa ndani ya Bunge hili.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Lema jielekeze kwenyemjadala.

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, sasanakwenda kwenye mjadala nilikuwa najenga hoja.

MWENYEKITI: Nenda kwenye mjadala achana namambo ambayo hayapo mbele yako.

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kaziya Mbunge ni kutoa ushauri sasa nitoe ushauri gani zaidi yahuu? Huu ndiyo ushauri, nasema hizi chuki mnazojenga ndaniya Bunge ndiyo zitatoka hapo nje, zikitoka hapo njezitakwenda mitaani.

Page 164: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

164

Mheshimiwa Mwenyekiti, narudia tena itafika mahalinchi hii itakuwa ni sehemu mbaya ya kuishi kwa sababu ninyimlio wengi mmekataa kuchukua opinion zetu za msingi kwasababu tu tumeitwa Wapinzani, utafikiri tumetoka Sudan sasaleo tunajadili mambo ya itifaki. (Makofi)

Haya mambo ya mazingira, DC wa Hai alikwendaakavunja vunja shamba la Mheshimiwa Mbowe, Sea CliffHotel na Golden Tulip ziko baharini sasa kwa sababu issuehapa ni itifaki ya kuridhia mazingira bora ya bahari na hizihoteli basi zilizopo kando kando ya bahari zipigwe marufukukabisa, ziwe mita 120 kutoka ufukwe wa bahari, kwa sababuissue kama leo ni itifaki ya mazingira ya bahari ambayo leommeilete hapa, ipi ilikuwa ni muhimu? Kwenda kuvunjashamba la mboga ama kuondoa Sea Cliff iliyoko pale kandokando ya bahari ambapo vichungi vya sigaravinatumbukizwa mle ndani? (Makofi)

Kwa hiyo haya mambo ya itifaki nilikuwa nataka tuniwaambie tu hichi ninachowaambia hivi mnavyoishiendeleeni, ila nawaaambia iko siku kama ambavyo sasa hivihata issue za Kibiti mnaogopa kuzijadili utafikiri hamna kitukinachiendelea. Kila mtu anaogopa kujadili humu ndani,Waziri wa Mambo ya Ndani naye anaogopa, nani anaogopa,Usalama wanaogopa kwa sababu mkianza kujadili tu nikwamba jamaa wanaweza wakaja na hii inasababishwana hasira ya wananchi. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba sana hasira hiziambazo mnawapandikizia wananchi, mambo hayamnayotufanyia humu ndani ya Bunge, mnatuzuia tusiseme,mnatuzuia tusitoe opinion zetu, ninawashauri vunjeni siasaza vyama vingi katika Taifa hili mbaki wenyewe na familiazenu na wajukuu zenu. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Stephen Masele.

MHE. STEPHEN J. MASELE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa nafasi hii ya kuchangia hoja hii iliyopo mbeleyetu.

Page 165: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

165

Mheshimiwa mwenyekiti, kwanza nianze kwa kuungamkono hoja hii na nizungumze mambo mawili. Kwanza nikwenye eneo la utafiti, lakini la pili ni kwenye usimamizi nautekelezaji wa Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, itifaki hii ni muhimu sana kwaTaifa letu na itaweka ulinzi wa rasilimali zetu hasa za baharinina tafiti zinazoendelea kufanyika zinaonesha kwambakwenye bahari zetu tuna rasilimali zenye thamani kubwa sanainawezekana kuzidi rasilimali zilizopo nchi kavu. Kwa hiyo,ushauri wangu kwa Serikali ni kuongeza uwezo wa vyombovyetu vya utafiti hasa kupitia vyuo vikuu vyetu ili tuwe nauwezo mkubwa wa kibajeti na kitaalam na sisi tuwezekufanya tafiti hizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, ni kushirikiana navyombo vya utafiti va Kimataifa ili kujua kinachoendeleakwenye tafiti ambazo zinafanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zipo tafiti nyingi zinaendeleahapa nchini wakati mwingine unaweza kukuta hata kwenyeWizara Serikali haitambui kama tafiti hizi zinafanyika. Kwamfano, kuna taifiti moja inafanyika na Chuo Kikuu cha Floridacha Marekani wa kutafiti maji ya mito yetu kwa mfano MtoWami, Mto Mara, Mto Morogoro na Mito mingine miwili hapaTanzania lakini unakuta wale wanaotafiti hawanacoordination kabisa na Serikali, kwa hiyo mimi ombi langukwa Serikali kwamba baada ya kupitisha ikawa sheria basitusimamie na tuhakikishe tunasimamia na tunashiriki katikatafiti zinazofanywa ndani na Mashirika ama makampuni yaKimataifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tutimize wajibu wetu kamaWabunge wa kutunga Sheria na Serikali itimize wajibu wakewa kutekeleza haya ambayo tunayapitisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru, naunga mkonohoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Mnyika.

Page 166: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

166

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna mkataba mmojapamoja na Itifaki mbili na nimepata wasaa wa kuzisomasoma hapa, lakini kwa kuwa kuna dakika tano nitajielekezakwenye mambo machache tu.

Mheshimiwa Msigwa aliposema Bunge dhaifuhusababisha Serikali dhaifu amenikumbusha kauli ambayoniliisema Bungeni hapa tarehe 19 mwaka 2012. Na kinyumechake, Serikali dhaifu vilevile husababisha Bunge kuwa dhaifuna ndiyo hali ambayo tunayo hivi sasa. Bunge letu limefanywadhaifu sana na limefanywa dhaifu na Serikali na Serikali hiiingekuwa na nguvu ingejiamini sana, isingefanya Bunge kuwadhaifu, lakini kwa sababu Serikali ni dhaifu ni lazima na Bungenalo liwe dhaifu. (Makofi)

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa.

MWENYEKITI: Subiri Mheshimiwa Mnyika, kuna taarifa.

T A A R I F A

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba nimpe taarifa Mheshimiwa Mnyika kwa sababu yeyekatika Bunge hili hakuwepo kwa kipindi kirefu sana na hajuinini kinachoendelea Bungeni, naomba nimpe taarifa tu kuwaBunge lako siyo dhaifu kama anavyofikiria na Bunge letu likostrong.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mnyika endelea.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,namwombea Mwenyenzi Mungu Mheshimiwa Mlinga awezekubadilika hiyo tabia yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bunge hili limekuwa dhaifukwa kiwango ambacho miswada, mkataba mmoja na Itifaki

Page 167: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

167

mbili zinaletwa zote kwa siku moja wakati ambapo Bungelenye nguvu lingesema kwamba siku hii tunajadili mkatabahuu, tunaujadili vizuri vinatafakari hoja umetolewa. Siku hiitunajadili mkataba huu, siku hii tunajadili mkataba huu. Kwaudhaifu huu wa Bunge unaoendelea anasema sikuwepo sikunyingi. Hii siku nyingine sikuwepo si Mwenyekiti unajua mlinitoandiyo maana sikuwepo. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ya udhaifu huuWabunge Mheshimiwa Halima Mdee hatakuwepo kwa mudawote ambao hatakuwepo, akija kurudi mtamwambiamaneno haya haya. Mheshimiwa Ester Bulaya hatakuwepohakirudi mtamwambia maneno haya haya. Sasa hii hoja yauchafunzi wa mazingira upande wa bahari nizungumzie kwaniaba ya Mheshimiwa Mdee wa Jimbo la Kawe ambayebahari inazunguka eneo lake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mikataba hii Serikali iliisainimuda mrefu, lakini hakuna kinachofanyika kuzuia uchafuzi,hakuna kinachofanyika cha kutosha kunufaisha wavuvi.Nataka kusema nini hapa, kuridhia mikataba hii peke yakena Kambi ya Upinzani hapa inairidhia inaunga mkonokuridhiwa kwa hii mikataba haitoshi kama mwisho wa sikumasharti ya msingi yaliyoko kwenye Itifaki, masharti ya msingiyaliyoko kwenye mikataba hayatekelezwi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tutaruhusu Serikalikuendelea kuwa dhaifu na Bunge kuendelea kuwa dhaifu niwazi siku zote tutapitisha mikataba na sheria lakini utekelezajihakuna. Tuna Mkataba muhimu sana hapa, huu mkatabaunahusu rasilimali za kijenetiki ambao nchi iliuingia mwaka2010 tumeletewa leo kuridhia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, matajiri unaowakutaduniani iwe ni akina Bill Gates, iwe ni tajiri wa Apple aliyefarikimatajiri mnawakuta duniani walipata utajiri kwa sababu yaubunifu. Wenzetu wana ubunifu wa kiteknolojia sisitunawabunifu wengi sana ambao wangeweza kunufaika narasilimali za kijenetiki kwenye ugunduzi wa dawa, tiba, vitu

Page 168: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

168

na mbalimbali lakini kwa sababu mambo haya hatuyafanyivile inavyostahili ndiyo maana hatufiki pale ambazo tunafika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tumeingia katika sektaambayo wengine ndiyo tunadhani ina manufaa zaidi yamadini. Kumbe huku kuna madini kwenye jenetiki, lakinihatufanyi ipasavyo. Hata kwenye madini tumewaambiamuda mrefu leteni mikataba hapa Bungeni tumewaambiamuda mrefu leteni mikataba leteni mikataba, tumeimba kwamiaka mingi leteni mikataba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo mnatuletea hojamnasema kwamba tunaleta sheria ya kulipa Bunge mamlakajuu ya mikataba halafu mnataka propaganda kama vile sisiambao ndiyo tulikuwa tunasema mikataba iletwetunakataa, sisi tunachokataa ni kwamba ninyi wa kuziletasheria kwa Hati ya Dharura mnatunga sheria mbovu ambazomwisho wa siku hazileti tija ambayo inasukudiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama kweli ninyi mnatakakuisaidia nchi kwenye masuala ya madini, hata kamatukianzia na hapo ambapo nilisema Rais angekuwa makiniasingeanzia na makinikia angeanzia na madini. Hata kamatukiamua kuanzia na makinikia cha kwanza ambacho Bungeingetaka kwenye Bunge hili kabla hata kuletewa miswadakusoma kwa mara ya kwanza zile ripoti mbili zile, zile ripotializokabidhiwa Mheshimiwa Rais, ipaswa ziwasilishwe hapaBungeni Mawaziri wazisome tuzijadili Wabunge halafutuseme sasa Serikali kaandae mapendekezo ya muswadaya kuhusu hiki, kuhusu hiki, kuhusu hiki, iletwe hapa Bungeni.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nachotaka kusemahapa ni kuwa, badala ya kuanza kujadili Miswada ya Sheriakwa Hati ya Dharura, Bunge hili liletewe kwa udharura huohuo ripoti mbili za Rais kuhusu makinikia, zisomwe hapaBungeni, zijadiliwe hapa Bunge msipofanya hivyo ile kauliniliyosema kwamba Rais makini alipaswa kuanza na madinikabla ya makinikia kuna siku itakuja kuwatafuna.

Page 169: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

169

Mheshimiwa Lema amesema kwamba kamahamtasikia maoni yetu basi ni afadhali mfike hatua mfuteKambi ya Upinzani. Mheshimiwa Lema kabla hawajafutaKambi ya Upinzani kama wataendelea kutosikiliza maoni yetuimefikia hatua Watanzania waiondoe hii Serikali madarakani.(Makofi)

MBUNGE FULANI: Mmechelewa.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kamamnadhani tumechelewa, kama mnashindwa tu kuwadhibitiwale watu wa Kibiti, Mheshimiwa Mwigulu Nchemba, kamamnashindwa kuwadhibiti watu wa Kibiti wanaotumia silaha,ndugu zangu hamuwezi kuwadhibiti Watanzania hawawakiamua kutumia silaha yao, kadi yao kupigia kura kwenyesanduku la kura. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mnyika jielekeze kwenyehoja, mambo ya Kibiti hayahusiani na utafiti. Jielekeze kwenyehoja ambayo iko mbele yako. (Kicheko)

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ninasema haya kwa sababu kule Kibiti...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante muda wako umekwishakengele ilishapigwa. Mheshimiwa Musukuma mchangiajiwetu wa mwisho mjiandae watoa hoja kwa majibu. Waziri,Naibu Waziri na wengine nitawapa muda wenu.

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru sana kwa kunipa nafasi niweze kuchangia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme manenomachache sana kwa leo, hii safari tuliyonayo ya kuibadilishaTanzania hawa wenzetu hawako na sisi. Kwa hiyo, ni kamatunampigia mbuzi gitaa. Hakuna mtu aliye tayari kusafiri nahii kasi tuliyonayo. (Makofi)

Page 170: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

170

Mheshimiwa Mwenyekiti, amezungumza rafiki yanguhapa amechangia anasema tunaletewa Hati za Dharura,toka nimekuwa Bungeni taarifa zote za Kamati huwatunapewa hapa, zinasomwa tunaanza kuchangia, sijaonajipya wakisoma taarifa tunagawiwa na sisi hapa tunasomabaadaye tunaanza kuchangia. Sasa kama ninavyowaonahawa, mtu mwenye akili hata kama ungepewa siku kumihuwezi kuelewa ambaye huna akili. Lakini mwenye akili hayamasuala tumeshapewa leo na Kamati ya Uongozi imeshakaaimeshauriana sioni sababu ya kushindwa kuendelea nakujadili. (Makofi)

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa.

MWENYEKITI: Taarifa.

T A A R I F A

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushuruku sana. Ndugu yangu, shemeji yangu Musukumaalisha-declare kwamba shule hajaenda sana, kwa hiyo hataakipewa dakika mbili akapitia tu kichwa cha habari akaanzakuchangia ataogelea tu! Lakini watu wenye akili zaowanahitaji muda wa concentration, wanahitaji muda wakufanya reference point, duniani kote wenzetu walifanyajehiyo ndiyo taarifa muhimu. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waitara kaa chini.Mheshimiwa Musukuma endelea.

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti,Watanzania wamemsikia Mheshimiwa anayejiita shemejiyangu kwa kusema nilisha-declare mimi sijasoma. Ni boraukasema mimi ni darasa la saba kuliko kuwa na hivyo vyetiulivyo navyo wakati akili huna. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kuzungumza hayamaneno yanayozunguzwa humu ndani, yote haya nipropaganda kinacholengwa humu ni makinikia. Hawa watu

Page 171: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

171

wanachokitaka ni safari ya kurefusha mjadala kwambatusijadili hizi sheria ili tukabanane na wazungu tulipwe pesa,lengo lao ni kurefusha masafara ili wakatafute cross-cross kuleMorena walikokuwa wanakaa. Hatukubaliani nayo ngomaimeletwa tupige leo hii hii tumalize.

Nafahamu hawa wenzetu hawana uchungu na hiimiswada mara nyingi hawana uchungu, sisi wenzenutulioumia tunatamani hata ingepigwa siku moja hii sheriaambayo inataka kwenda kumbana mzungu atulipe pesa.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri tuende na ile sloganya juzi kwamba hela zikitoka hawa tusiwape, zije kwenyemajimbo yetu sisi wenye shida. Haiwezekani mtu anasimamahapa anazungumza anasema Wabunge tumekaa miezimitatu tumechoka kutafuta nini wakati tunalipwa pesa,tuongezwe hata wiki mbili. Watu wenyewe njaa humuzimetuua humu watu mkifukuzwa mnatoa macho, halafuunakuja kuanza kuzungumza vitu vya ajabu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nafikiria masuala hayayaende kama yalivyopangwa na hakuna mambo yakutishana mambo ya Kibiti kuna nini. (Kicheko)

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,Kuhusu Utaratibu.

MWENYEKITI: Kuhusu Utaratibu.

KUHUSU UTARATIBU

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,Mbunge anayezungumza amekuwa na tabia ya kuongealugha ambazo siyo za Kibunge. Kama sasa hivi anasematumetoa macho, tunalia na kwamba kuna watuwamehongwa Morena, na yeye ndiye anayekaa Morena sasatungeomba ili Bunge liwe na hadhi kama kuna watuwamechukua hela ana ushahidi awataje. Maana asikae anatisha tisha watu hapa watu. (Kicheko)

Page 172: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

172

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Musukumaendelea.

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ninakushukuru sana, unajua Waheshimiwa Wabunge Spikaanatuelekeza vizuri uwe na tabia ya kuwasiliza na wenziohuwa tunavumilia, wewe umesema hapa tumekuwa Bungela vibogoyo, kutoa macho unaumia? Na kweli umeyatoamacho! Tunawaona hapa mkifukuzwa mnavyotoa machokule mtaani. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo suala lakuzungumza kukodoa macho au watu wamehongwa nimaneno yako tu na vitendo vyako vinadhihirisha kwenyeUmma. Hivi kweli unategemea hiyo Serikali ya kuitoa CCMya ninyi mnaowatetea wezi kwa style hii! Serikali ya ninyimnaokataa kujadili Miswada ya kwenda kudai pesa zetu.Mimi nilikuwa nashauri tu kwamba hawa wenzetu hawapopamoja na sisi katika safari ya kuibadilisha Tanzania, hapowamekaa tu kizungumkuti lakini muda wowote walikuwawanaondoka nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana…...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mweyekiti, ahsante kwamjadala wako.

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Wewe bwana kaa chini. (Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Waziri mjadala umeuona kambizote wameridhika pokea ushauri, dakika tano.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS,MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza tunawashukuru sana Wabunge wote waliopata

Page 173: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

173

nafasi ya kuchangia ambao wamechangia vizuri sana kuhusuhoja hii na bahati nzuri wote Mkataba pamoja Itifaki zotembili zimeungwa mkono na Bunge hili na kwamba hakunaupande wowote ambao umepinga, tunaahidi kwamba yalemapendekezo waliyoyatoa Waheshimiwa Wabungetutayazingatia katika kuhakikisha kwamba tuna usimamizibora wa mkataba pamoja na itifaki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme moja la nyongezakatika hayo kwamba Serikali hapa imelaumiwa katika kuletanyaraka. Serikali inaonewa kwa vipi katika jambo hilo? Siyokazi ya Serikali kugawa nyaraka Bungeni. Kazi ya Serikalitulipoingiza kazi za Serikali katika Mkutano huu wa Sabatuliainisha kazi zote na nyaraka zote tuliwasilisha.

Kwa hiyo, siyo kazi ya Serikali tena kulaumiwa kuhusunyaraka na kwa Wabunge wanaojua kufuatilia nyarakakama rafiki yangu hapa amekuwa akilalamika na nimkongwe kabisa anajua, Serikali ikishaorodhesha kazi zakedocument zipo kwa Katibu wa Bunge. Hivyo, Serikali haihusikitena katika hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapoleta mikataba hii naitifaki hizi, haimaanishi kwamba Serikali haijafanya lolotekatika utekelezaji wa majukumu yake. Serikali tumefanyamambo mengi katika usimamizi wa Bahari Kuu pamoja naUkanda wa Pwani, hilo lazima lifahamike. Sheria na kanuninyingi zimetungwa na usimamizi wa usiku na mchanakuhakikisha kwamba Ukanda wa Pwani unalindwa katikauchafuzi, unalindwa katika uharibifu wa mazingira ambayoyanaweza yakafanyika Ukanda wa Pwani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa ufupi pia iongeleekuhusu baadhi ya hoja ambazo zimetolewa na WaheshimiwaWabunge. Tumeshauriwa kwamba mali zetu zimekuwazikiibiwa kwa utaratibu huu, wizi wa rasilimali za kijenetikikwa mfumo wa watu wanajifanya ni watafiti nawafanyabiashara na tukaombwa kwamba tuwekemwongozo mahsusi ambao utalinda rasilimali zetu zisiwezekuporwa tena.

Page 174: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

174

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuwaambiakwamba Kambi zote bahati nzuri imezungumzwa na Kamatiyenyewe ya Viwanda, Biashara na Mazingira naimezungumzwa na Kambi ya Upinzani na Serikali haina tatizokatika hili. Tutaandaa mkakati mahsusi ambao unadhibitiwizi wa aina yoyote katika eneo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, maisha ya Pwani yamekuwabora vipi toka mwaka tulivyoridhia. Amezungumza MakamuMwenyekiti wangu enzi hizo wa Kamati ya Uchumi, Viwandana Biashara kwamba wamenufaika vipi Pwani pamojakuridhia mwaka 1996. Wamenufaika kwa mengi, moja nikwamba miradi mingi sana inayojengwa sasa hivi tuna ujenziwa kuta katika Pwani kwa maana ya Pangani, Rufiji,Zanzibar, Pemba na Kilimani zinajengwa. Tunapanda mikokokatika maeneo yaliyoharibiwa ya pwani, tunaanda mikokoRufiji, Zanzibar na maeneo mengine ili kuhakikisha kwambatunanusuru. Pia tunajenga mifereji maene ambayoyanaathiriwa na kuongezeka kwa kina cha bahari ili kuwezakuhimili pia maji ya mvua ambayo yanaleta mafurikomakubwa kwa wananchi, kama kwa rafiki yangu hapaMheshimiwa Mtolea kule miradi mbalimbali inaendeleakujengwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia hatujakaa, tunachochuo kikubwa sana ambacho wamekisifu sana Kamati hapa,hiki chuo chetu cha Taasisi ya Sayansi ya Bahari ambachokinafanya kazi kubwa na kimejengwa Zanzibar kwa maanahiyo hiyo ya kuhakikisha kwamba ukanda wa pwaniunalindwa kwa nguvu zote na tafiti zinapatikana kwa wakatina kutumika kwa wakati. Sio hivyo tu, tumeanzisha sheriambalimbali nyingi za kulinda mazingira yetu katika ukandawa bahari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, taasisi za tafiti zinafanyavizuri tu, COSTECH na IMS katika kuhakikisha kwamba Ukandawa Pwani unanufaika hasa katika maeneo ya ufugaji wasamaki, mwani pamoja na mazao mengine ya bahari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchangiaji mmoja alisema

Page 175: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

175

kwamba Tanzania imegeuzwa kuwa dampo na sisihatusimamii. Ni kweli tuna haja tu ya kuongeza usimamizi,lakini ni kweli kabisa mipaka yetu yote tunailinda, ndani yaeneo la bahari yetu tunalilinda kwa nguvu zote na taasisi zaSerikali zipo kazini. NEMC, SUMATRA na TPA wapo kazinikuhakikisha kwamba kwa namna yoyote meli zinapongiandani katika eneo letu hili udhibiti wa uchafuzi wa mazingirahauruhusiwi kwa aina yoyote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata upande wa kemikalitupo vizuri, sawa zinaweza zikatokea kesi mbalimbaliambazo zipo hapa nchini za umwagaji wa sumu katikabahari yetu na katika kingo…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante, mambo mengine uwajibu kwamaandishi. Mheshimiwa Mtoa Hoja.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru sana kwa fursa na niwashukuruWabunge wote kwa umoja wao kwa kuridhia mapendekezohaya ya maazimio pamoja na itifaki tuliyoweka mezani. Kwakuwa wameridhia kama ulivyosema sitakuwa na mengi yakusema, niseme mawali tu ambayo yameleta sura za tofauti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja, Serikali strong, yenyenguvu ni Serikali inayochukua hatua, inatenda na siyo Serikaliinayosema na hiki ndicho kinachoendelea. MheshimiwaMnyika anaposema tumeongea sana kwenye mikataba naanajua ukubwa wa mambo yale, lakini Serikali jasiri na yenyenguvu imeenda kwenye kutenda, hicho ndicho ambachoWabunge na Watanzania wote wametamani muda mwingisana kukiona na ndicho ambacho Mheshimiwa Raisanakwenda kukitenda na analiomba Bunge lione umuhimuhuo kwa ukubwa wa rasilimali za nchi yetu na ukubwa wajambo lenyewe. (Makofi)

Page 176: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

176

Mheshimiwa Mwenyekiti, huu ukigeugeu ndiyo ambaohuwa unaweka mashaka kwamba mtu ambaye ameliongeakwa muda mrefu sana jambo, linapoletwa anageuka inaletamaswali kwamba huyu mtu amegeukaje. Nimemshukurusana ndugu zangu hapa walipokuja kuongelea kwamba siyokila kitu kupinga. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye hili jambo ambalolina maslahi ya Taifa, niwaambie Waheshimiwa Wabungehata kama ataunga mkono mtu mmoja tu, Serikali hatuwezitukarudi nyuma maadam tumepewa dhamana ya rasilimaliza nchi yetu. Wabunge na kama Serikali na Wasaidizi waRais tunawahakikishia kwamba nia na dira aliyonayo Rais ninjema sana kwenye rasilimali za nchi yetu. Nawaombenitwende tuunge mkono wala tusipepesuke kwa kuzingatiavitu vingine ambavyo haviko kwenye dira yetu visijevikatutoa kwenye dira. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mambo mengi sanaambayo yamo kwenye itifaki hizi yalishaletwa mbele yaWabunge na Wabunge wameshafuatilia na yamefanyiwakazi na watalaam ambao wana dhamana na wenyewekwenye Taifa letu, hatuna haja ya kuwa na mashaka,niwaombe tuende turidhie ili yaweze kwenda kufanyiwa kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mambo mengineWaheshimiwa Wabunge tunapoongelea ameongeaMheshimiwa Lema na Mheshimiwa Mnyika, ni vema sanatukawa makini sana tunapoongea. Nimemsikia akiongeleasuala la Kibiti, lakini ningekuwa nakuuliza maswali mengi,najua usingepata majibu yake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja, kama una uhusianona wale wahalifu hata ukadhani wameshinda, hebu waulizewalianza wangapi na sasa wapo wangapi. Mwenzio Lemakwa sababu alikuwa kule gerezani anaweza akawaonawengine kule, wewe Mheshimiwa Mnyika ambaye hujaendaunaweza ukatusaidia, wewe unayedhani wameshinda wapowangapi na wapo wapi? Lakini nikuhakikishie kwamba sisikama Serikali hatutaacha eneo hata moja la nchi yetu hii

Page 177: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

177

likatawaliwa na uhalifu. Tutashughulika na mmoja mmojana lazima haki ya watu wetu itasimama katika eneo lote lanchi yetu watasimama wakiwa wanafanya kazi kwamazingira yaliyo salama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, unaongea kimzaha mzaha,lakini taswira iliyopo ndani kabisa na niliisema mahali pengine,ina taswira hiyo ya siasa siasa. Leo hii ukituambia kwambayale yanayoendelea Kibiti yataenda na maeneo mengine,tunaendelea tu kutafuta connection unajuaje kwambayanaendelea na maeneo mengine. Kwa sababu kamaanauawa Mwenyekiti wa CCM, anauawa wa CCM,wanaruka nyumba ya yule asiye wa CCM na wewe unasemayataendelea na maeneo mengine, una haja ya kutusaidiakujua kwa nini yataendelea na maeneo mengine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini unadhani kwambawanashinda,kwa sababu sisi kwenye mpango kazi wetutuliopanga, tunaenda hatua kwa hatua kuhakikisha kwambawananchi wa maeneo yote ya nchi yetu wanakuwa katikamazingira salama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, sentensi kama hizipamoja na kwamba zimesemewa Bungeni nadhani kunaumuhimu sana ndugu zetu hawa watasaidia kujua kwambakumbe sisi tunavyotafuta sana kumbe kiini ama kinatokaBungeni au Serikalini, lakini sasa wanaenda kuhangaika nawananchi ambao ni very innocent, ndiyo maana sisitunakuwa very responsible.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ni kwa sababu kwenyemambo ya siasa tunatakiwa tupambane sisi wanasiasa nasiyo wananchi wengine ambao wanashughulika na shughulizao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa muda umeisha,ninaomba tu kutoa hoja kwamba Bunge lako sasa katikaMkutano wake wa Saba liridhie Maazimio tuliyoyaletapamoja na marekebisho na Itifaki tuliyoleta.

Page 178: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

178

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa hoja.(Makofi)

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA:Mheshimiwa Mwenyekiti, naafiki.

MWENYEKITI: Hoja hiyo imeungwa mkono. Sasanitawahoji kwa mujibu wa kanuni zetu za kibunge. KwambaBunge sasa liridhie marekebisho ya Mkataba wa Nairobi waHifadhi, Usimamizi na Uendelezaji wa Mazingira ya Bahari naUkanda wa Pwani ya Magharibi ya Bahari ya Hindi (AmendedConvention for the Protection Management andDevelopment of Marine and Coastal Environment of theWestern Indian Ocean).

(Hoja ilitolewa iamuliwe)(Hoja Iiiamuliwa na Kuafikiwa)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, sasanitawahoji Azimio lingine kuwa Bunge sasa liridhie Itifaki yaUdhibiti wa Uchafuzi wa Mazingira ya Bahari na Ukanda waPwani ya Magharibi ya Bahari ya Hindi kutokana na Vyanzona Shughuli zinazofanyika Nchi Kavu (Protocol For TheProtection of the Marine and Coastal Environment of theWestern Indian Ocean from Land base Sources and Activities).(Makofi)

(Hoja ilitolewa iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

MWENYEKITI: Azimio la mwisho, kuwa Bunge liridhieItifaki ya Nagoya ya Kusimamia Upatikanaji na MgawanyoSahihi wa Faida Zitokanazo na Matumizi ya Rasilimali zaKijenetiki (Nagoya Protocol on Access to Genetic Resourcesand The Fair and Equitable Sharing of Benefits Arising fromtheir Utilization to the Convention on Biological Diversity).(Makofi)

(Hoja ilitolewa iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

Page 179: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1510750928-29 JUNI 2017.pdf · mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

179

MWENYEKITI: Azimio hili nalo limepita. Nichukuenafasi hii kuwapongeza sehemu zote mbili za Bunge kwakupitisha Maazimio haya muhimu. Wengine hamjui, tunamabaharia wetu ambao wangeweza kupoteza kazi keshokama Maazimio haya yasingepita, wale Mabaharia ambaowanafanya kazi Kimataifa. Hivyo, nawapongeza wote.(Makofi)

Lakini Serikali chukueni ushauri mliopewa, kunareservations ambazo mkiingia kwenye itifaki, muhusika anayohaki ya kuingiza reservations zake ili zikubaliwe, bahari zetuzilindwe na bahari zetu zisimwagiwe sumu, kwa sababu sumuhizi zinaharibu mazingira na viumbe hai ndani ya bahari. Kwahiyo, nawapongeza wote, naipongeza Serikali na upandewa Vyama vyote kwa kupitisha Maazimio haya matatu, kazihaikuwa ndogo lakini tumevuka. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, kuna semina ya Red Crosssasa hivi, kwa hiyo nawaomba Waheshimiwa Wabungemsiondoke mhudhurie semina ya Red Cross ambayo nimuhimu sana na itaratibiwa na Tanzania Red Cross naitafanyika ukumbi huu wa Bunge kuanzia sasa.

Waheshimiwa Wabunge, ninaahirisha shughuli zaBunge mpaka kesho saa tatu asubuhi.

(Saa 7.30 Mchana Bunge liliahirishwa hadi Siku ya Ijumaa,Tarehe 30 Juni, 2017, Saa Tatu Asubuhi)